Pccb huduma

Page 1

Aidha, huduma hii inatoa fursa kwa TAKUKURU kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kwa wananchi kuhusu mapambano dhidi ya rushwa. Vilevile inaiwezesha TAKUKURU kupokea taarifa za vitendo vya rushwa kutoka sehemu mbalimbali ambazo isingekuwa rahisi kuzipokea na kuzishughulikia. JE, MWANANCHI ANA WAJIBU WA KUTOA TAARIFA? Ndiyo. Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya Mwaka 2007, Kifungu cha 39 kifungu kidogo cha (i), inamtaka kila mtu kutoa taarifa za vitendo rushwa kwa TAKUKURU. Kifungu hicho kinatamka kuwa …kila mtu anayefahamu juu ya kufanyika kwa au mpango wa kufanya kosa la rushwa, anapaswa kutoa taarifa TAKUKURU. JE, KUNA UTARATIBU WOWOTE WA KUMLINDA MTOA TAARIFA? Ndiyo. • Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007, kifungu cha 51 na kifungu cha 52 kinatoa ulinzi wa kisheria kwa mtu yeyote anayetoa taarifa au ushahidi mahakamani kuhusu kufanyika kwa vitendo vya rushwa. Ulinzi huo ni pamoja na kutotoa utambulisho wake kwa kutotajwa jina, makazi au anwani yake; kuzuia kulipiziwa kisasi au kutendewa vibaya; kutounganishwa kwenye mashtaka au kutofunguliwa kesi ya madai au jinai . • Endapo mtoa taarifa atatishiwa, kuumizwa au kulipiziwa kisasi na watu aliowataja au wanaohusiana nao, Serikali inaweza kumpa ulinzi au kumlipa fidia au kumpa msaada wa aina yoyote kulingana na madhara aliyoyapata. Kifungu cha 52 (3) kinatamka adhabu kwa mtu yeyote atakayemhujumu kwa aina yoyote ile mtoa taarifa ambayo ni kulipa faini isiyozidi shilingi laki tano ama kifungo kisichozidi mwaka mmoja au adhabu zote mbili. • Sheria ya kuwalinda Watoa Taarifa za Uhalifu na Mashahidi Na. 20 ya Mwaka 2015, inatoa ulinzi kwa mtu yeyote anayetoa taarifa za uhalifu wa makosa ya aina mbalimbali ikiwemo vitendo vya rushwa vilivyotokea, vinavyotokea au vinavyoweza kutokea. Vilevile Sheria hii inatoa ulinzi kwa mashahidi wanaotakiwa kufika mahakamani. • Ili kumlinda mtoa taarifa, inashauriwa mtoa taarifa atunze siri kuhusu nia yake na hatua ya kuwasilisha taarifa hiyo TAKUKURU.

• Mtumishi yeyote wa TAKUKURU, kwa mujibu wa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007, analazimika kutunza siri ya taarifa aliyopokea ikiwemo utambulisho wa mtoa taarifa na anaweza kuchukuliwa hatua za kisheria iwapo atavujisha siri hiyo. JE, KUNA NJIA NYINGINE ZA KUIFIKIA TAKUKURU? Ndiyo, zipo njia zifuatazo: • Kufika katika ofisi ya TAKUKURU iliyo karibu na muhusika. • Kuandika barua kwa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, 16 Mtaa wa Urambo, S.L.P 4865, Dar es Salaam. • Kupiga simu Ofisi ya Makao Makuu nambari: +255 22 2150043 -6 • Kuandika barua au kupiga simu kwa Wakuu wa TAKUKURU wa Mikoa au Wilaya kadiri ya eneo alipo mtoa taarifa. • Kutuma malalamiko kwa kujaza ‘fomu ya malalamiko’ iliyopo katika wavuti ya TAKUKURU - www.pccb.go.tz. • Kuandika baruapepe kwenda kwa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU:dgeneral@pccb.go.tz au kwa Wakuu wa TAKUKURU wa Mikoa au Wilaya. • Kutumia nukushi nambari: +255 22 2150047 HITIMISHO: TAKUKURU imeweka huduma ya simu ya dharura nambari 113 ili kurahisisha mawasiliano na wananchi. Tunamsihi mwananchi kutumia huduma hii kwa mujibu wa sheria za nchi na kadiri ya malengo yaliyokusudiwa ili kwa pamoja tuweze kutokomeza tatizo la rushwa nchini. Taarifa zinazotolewa zinapaswa kuwa za kweli na si zenye chuki binafsi au zenye nia ya kumkomoa mtu. Ikumbukwe ni kosa kisheria kutoa taarifa za uongo TAKUKURU au kwa mamlaka nyingine yoyote inayoshughulika na makosa ya jinai. Tuungane kuitokomeza rushwa kwa maendeleo, amani na usalama wa nchi yetu

MKURUGENZI MKUU TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA (TAKUKURU)

16 Mtaa wa Urambo, S.L.P 4865, 11102 Dar es Salaam, Tanzania. Simu: +255 22 215 0043 - 6, Nukushi: +255 22 215 0047, Barua pepe: dgeneral@pccb.go.tz Wavuti: www.pccb.go.tz, Simu ya Bure 113, *113#, SMS 113

KITUO CHA HUDUMA KWA MTEJA - TAKUKURU


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.