Mwanake Mkenya Toleo la 16

Page 1

1

Toleo Namba 16 • Aprili 2011

Toleo Namba 16 • Aprili 2011

Yanayojiri katiba mpya …Na Musa Radoli

Mizozo inayozembea katika utekelezaji wake

M

iezi sita baada ya katiba mpya kupitishwa ni hatua chache imefikiwa kuhusu kutekelezwa kwa katiba hiyo mpya kutokana na mizozo kila kuchao. Mashiriki kijamii yameeleza wasiwasi kuhusu jinsi wabunge watakavyoweza kukabiliana na kuharakishwa kwa utekelezaji wa katiba. Kinachovunja moyo zaidi ni mizozo kati ya vyama viwili vikuu Party of National Unity (PNU) na Orange Democratic Movement (ODM) ambavyo vyote vimekuwa vikivutana kisiasa. Mashirika hao ya kijamii yanahofu kwamba miezi sita tangu katiba mpya kupitishwa, migawanyiko ya msimamo wa kisiasa katika serikali ya muungano yanadhihirisha wazi kwamba huenda lengo hilo halitafikiwa kwa wakati unaofaa. Mashirika ya kijamii yanahuzunishwa kuona kwamba tangu katiba mpya kupitishwa, mgawanyiko ulioko katika serikali ya muungano ambapo pande zote mbili zimeendelea kulumbana, unatia wasiwasi kuwezesha utaratibu huo uweze kufanikiwa. Kwenye kikao ya hivi majuzi cha mashirika ya kijami mjini Nairobi, ilibainika kwamba karibu vifungu 700 vya kisheria vinapaswa kushughulikiwa na afisi za mkuu wa sheria ili vikabidhiwe kwa bunge vipitishwe.

Mizozo ya Kisiasa Tume ya utekelezaji wa katiba mpya (CIC), imelalamika kwamba mkondo unaofuatwa, ulikuwa mwendo wa kinyonga kutokana na mizozo na maluumbano ya kisiasa ndani na nje ya bunge. Mwenyekiti wa tume hiyo, Bw Charles Nyachae alisema: “Licha ya utaratibu wa utekelezaji kuwa kwenye mwendo wa polepole baada ya katiba kupitishwa mnamo Agosti 27, 2010, sisi katika CIC tumejitolea kwa moyo wetu wote kuhakikisha kwamba utaratibu huo utatekelezwa kama ipasavyo kwa muhula wa miaka mitano ijayo kama ilivyopendekezwa.” Akaongeza: “Pia ni lengo letu kujiepusha kabisa na tume nyinginezo za hapo awali ambazo zimekuwa zikishughulikia maswala mengine ya kitaifa, na baada yake kuwaleta pamoja wadau wote kutoka ngazi zote ili hatimaye kuhakikisha kuwa Wakenya wanafurahia utaratibu ulio wazi, wa uhakika na wa uzingativu, ambao haujawahi kuonekana kwenye historia ya taifa hili.” Mwenyekiti huyo alisema licha ya mizozo ya

“Tumejitolea kwa moyo wetu wote kuhakikisha kwamba tumewaleta pamoja wadau wote na wa ngazi zote, ili kuhakikisha kwamba Wakenya wanafurahia katiba iliyo na uwazi ambayo haija onekana katika historia ya nchi hii.” — Bw Charles Nyachae, Mwenyekiti CIC

Wakenya wakisherekea kuapishwa kwa katiba mpya uwanjani Uhuru Park mnamo Agosti, mwaka jana. (Picha ya ndani) Ni Mwenyekiti wa Kamati ya Utekelezaji Katiba, Bw Charles Nyachae. kisiasa na malumbano mengineyo kati ya pande zote mbili kwenye serikali ya muungano, ilikuwa ni dhamira ya makamishna wa CIC kuhakikisha kwamba utaratibu wa utekelezaji wa katiba mpya hautavurugwa ama kuingiliwa kwa njia yoyote ile na makundi ya kisiasa yanayopingana

Utekelezaji Hofu ya jinsi utaratibu wa polepole wa utekelezaji wa katiba mpya inavyoendelea ni jambo lililozungumziwa kwa mapana na wadau kwenye mkutano huo kwa dhamira ya

kuchunguza ni ufanisi gani umepatikana tangu kuapishwa kwa katiba mpya. Mkutano huo uliofanywa chini ya mada: “Kuchunguza hali: Miezi sita ya katiba” ulidhaminiwa na mashirika ya Bridge Africa, Medeva Africa na Oxfam miongoni mwa mashirika mengineyo ya kijamii kukiwepo na lengo la kuboresha na kuchunguza jinsi katiba inavyopaswa kutekelelzwa na wale wasio serikalini. Wajibu mkubwa wa mpango huo ni kuchunguza kwa hisibati ustawi uliofanywa hadi sasa kwa utekelezaji wa katiba na kuchunguza Angalia uk.4

TAHARIRI

M

Akina mama wajitokeze kunyakua viti vikuu

namo Januari, mwaka huu, mashirika kadha wa kadha ya akina mama, yalilalamikia vikali hatua ya rais ya kufanya uteuzi wa vyeo kadhaa vikuu mahakamani. Katika kesi iliyowasilishwa kwenye mahakama kuu, akina mama hao, walieleza kuwa rais hakuzingatia usawa wa kijinsia alipowateua jaji mkuu, mkuu wa sheria, mkurugenzi wa mashtaka ya umma na cheo kile cha msimamizi wa bajeti. Hata hivyo, miezi miwili baadaye na hasa baada ya rais sasa kuamua

kutangaza nafasi ya vyeo hivyo mahakamani, majaji na mawakili wengine wamejitokeza kujaza nafasi hizo. Wagombezi ishirini na wanne walijitokeza kwa vyeo vya mkuu wa sheria na naibu wake. Hata hivyo, ilifedhehesha kwamba wanawake hawakutuma maombi kwa cheo kile cha mkurugenzi wa mashtaka ya umma. Matarajio yapo kuwa kati ya wale waliotuma maoimbi kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na jaji mkuu aliyeondoka, Bw Evan Gicheru, kama iwapo mwanamke hatajaza na-

fasi hiyo, hapana shaka kile kiti cha naibu jaji mkuu, hakitawaponyoka. Kwenye maazimio ya katiba mpya, nafasi za kazi zitatangazwa, hivyo basi, wanawake sharti wawe macho na tayari kuhakikisha kuwa hawaachwi nyuma. Jambo la kutia moyo zaidi kwenye katiba hii ni kule kukumbatia jinsia katika afisi za utumishi wa umma. Hii inamaanisha kuwa kuajiriwa kwa maafisa serikalini kuanzia ngazi za chini hadi zile za juu, sio tu unazusha ushindani kati ya wake na waume, ila ni kwamba theluthi tatu ya

kazi hizo ni sharti kutengwa wa jinsia ya akina mama. Hata hivyo, kwa kazi ya ngazi za juu kwa afisi za umma, wanawake watapaswa kuwa na stakabadhi za kuhitimu za juu ili waweze kuajiriwa kulingana na uwezo wao kikazi. Zaidi ya hayo, wanawake watapaswa kuboresha uwezo wao wa kushirikiana kwenye nyanja za kitaalamu miongoni mwao. Hadi sasa maongozi ya kuhakikisha kuwa haki inatendeka katika zoezi la uajiri wa kamishna, imefanywa kwa uwazi. Wakati umewadia kwa wanawake

wale walio na ari za viti vikuu vya kisiasa kujitokeza na kuhesabiwa kama alivyofanya aliyekuwa waziri wa sheria, Bi Martha Karua. Hawatapaswa kujikalia kitako hadi dakika za mwisho kisha kuwalaumu waume kwa madai wamekuhujumu juhudi zao za kutaka kuwakilisha wapiga kura wao. Ni jambo la kuvunja moyo kwamba hadi wakati huu, ni wanawake wachache tu wamejitokeza hadharani kutangaza nia ya kugombea viti vya magavana 47 ambavyo vitagombaniwa kwenye uchaguzi mkuu ujao.


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.