Mwanamke Mkenya Toleo 20

Page 1

1

Toleo Namba 20 • Agosti 2011

Toleo Namba 20 • Agosti 2011

Mwaka mmoja baadaye Kutazama utekelezaji wa sheria kwa darubini ya jinsia

…Na Odhiambo Orlale

W

anawake wana kila sababu ya kusherehekea maadhimisho ya mwaka wa kwanza tangu kuzinduliwa rasmi kwa katiba. Milango ambayo hapo awali ilikuwa imeshika kutu nzito isiweze kufunguka imeanza kutiwa mafuta ya kuilegeza na kufunguka, yote hayo sababu yake ikiwa ni mafuta yanayojulikana kama sheria hii mpya. Mnamo siku ya kuanzishwa rasmi kwa katiba, Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mwai Kibaki, aliitia saini katiba hiyo na akawaahidi Wakenya kwamba aitailinda na kuitetea sheria hiyo mpya. Kunako siku hii kadhalika Wakenya waliwashuhudia Waziri Mkuu Raila Odinga na Makamu wa Rais Kalonzo Musyoka wakiahidi kuwatumikia Wakenya chini ya katiba hii mpya na kadhalika kuilinda. Watunga sheria ambao ni Wabunge pia walikula viapo vya kuitetea katiba huku mawaziri na majaji pia wakiapa kuitetea katiba hiyo mpya. Hiyo ikiwa na maana ya kuheshimu kila neno lililomo ndani ya katiba hiyo yakiwemo mafanikio ambayo yanapendelea haki za wanawake na kupewa uwezo miongoni mwao, kupewa nafasi zaidi katika ulingo wa siasa na katika ngazi za utoaji maamuzi. Hata hivyo, uamzi wa hivi majuzi wa Baraza la Mawaziri la kutangaza kanuni ya thuluthi moja katika katiba kuwa isiyoweza kutekelezwa ni uzandiki wazi wa ubaguzi wa kijinsia na kutumiwa vibaya kwa manufaa ya wanawake katika sheria hiyo mpya. Hata ingawa baraza hilo la mawaziri lilipendekeza kuundwa kwa jopo kazi la kuchunguza kanuni hiyo ambayo imezusha mgogoro, na kuwasilisha matokeo ya uchunguzi wake kwao, wanawake wana hofu kwamba kama katika hatua hizo za awali za utekelezaji wa katiba unazusha mgogoro, haitachukua muda mrefu tena kabla ya mafanikio ya wanawake kuondolewa kabisa.

Matarajio mema Hata hivyo, Wakenya na wanawake kwa ujumla wanasubiri roho mkononi huku wanawake wakitazamia kwamba mzozo huo utasuluhishwa haraka iwezekanavyo na kwa manufaa yao. Tangu kuanza kutumiwa kwa katiba mpya, wanawake wamefanikiwa kupata kazi za mamlaka makubwa kwenye utekelezaji wa katiba mpya. Kwa mfano Nancy Baraza alipitia moja ya taratibu ngumu za mahojiano ya hadhara ya uteuzi wa Naibu wa Jaji Mkuu, kabla ya kuteuliwa kwenye mamlaka hayo ili kufanyia matengenezo idara hiyo ya mahakama. Ama kwa kweli manufaa ambayo wanawake wamepata kuanzia wakati wa Tume ya Marekebisho ya Katiba ambayo ilijulikana kwa jina maarufu la Bomas miaka mitano iliyopita na kushirikishwa kwenye katiba mpya, yanatekelezwa kikamilifu kwa dhati ya moyo wa katiba hiyo. Uteuzi wa aliyekuwa Mbunge Maalumu Njoki Ndung’u kama mmoja wa majaji saba wa mahakama kuu ni moja ya mafanikio ya wanawake ingawa bado kuna kesi inayopinga urari wa kijinsia katika idadi ya majaji wa mahakama hiyo kuu. Kulingana na wengi wa viongozi wanawake, tatizo kubwa hapa ni kwamba hawako tayari

Picha ya juu aliyekuwa Mkuu wa Sheria, Bw Amos Wako (mwenye wigi kichwani) akishuhudia Rais Mwai Kibaki akitia sahihi stakabadhi kuidhinisha rasmi katiba mpya mnamo Agosti 27, mwaka jana. Kulia, Rais Kibaki akionyesha kwa hadhara stakabadhi hiyo ya kuidhinishwa katiba mpya. Sherehe hii ilifanywa katika bustani ya Uhuru Park, Nairobi. kuwaruhusu viongozi wa kisiasa kuitekeleza katiba kuanza na utekelezaji usiofaa huku kukiwa na udhaifu mkubwa katika kushughulikia maswala ya kijinsia. Jaji Mkuu, Dkt Willy Mutunga alianzisha utangulizi bora wakati alipowaambia wanasiasa kwamba wanahitajika kusikiliza kwa makini na kuelewa kwamba Kenya ina wanawake ambao wana elimu na wenye uwezo wa kufikisha idadi ya thuluthi moja ambayo katiba inapendekeza

izingatiwe, wakati alipowateua wanawake kumi na watatu kati ya watu ishirini na wanane kuchukua nyadhifa za mahakimu wa mahakama kuu ambao wameteuliwa hivi punde. Lydia Achode ambaye ni msajili mkuu wa mahakama anayeondoka ni miongoni mwa majaji walioteuliwa pamoja na Pauline Nyamweya. Wengine ni Mumbi Ngugi, Beatrice Angalia Uk.2


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.