CDF Report / Ripoti ya CDF

Page 1

Ripoti ya CDF

Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika maeneo yao



Ripoti ya CDF Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika maeneo yao


Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika maeneo yao

Hazina hii ya CDF ni mpango wa Serikali ya Kenya iliyotenga shilingi milioni 20 kwa kila eneo la ubunge nchini kila mwaka. Dhamira ama lengo la hazina hii ni kurahisisha miradi ya maendeleo ama ustawi katika maeneo hayo. Huidhinishwa ama kupitishwa na sheria za Bunge kisha pesa hizo hutolewa kwa Kamati ya Kitaifa kupitia akaunti ya benki maeneo hayo.

Aina ya Miradi • Miradi yote ya maendeleo sharti iwe ni ile ya manufaa kwa jamii nzima • Pesa hizo pia zinaweza kutumiwa kugharamia ama kulipia ujenzi na uwekaji vifaa vya afisi hiyo ya miradi.(Haitapaswa 2 Ripoti ya CDF: Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika maeneo yao


Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika maeneo yao

iwe ni afisi ya kisisasa ya Mbunge). • Mradi wa ujenzi wa afisi, kadhalika vifaa vilivyomo humo kama viti, meza, kabati na kadhalika, vyote hivyo vitachukuliwa kama mradi wa maendeleo • Mpango wa kutoa msaada wa kifedha kwa elimu, utachukuliwa kama wa kimaendeleo, lakini hautapata zaidi ya asilimia 10% ya hazina ya kila mwaka kwa kila eneo la ubunge.

Miradi Inayoanzishwa na Jamii Hazina hii, KAMWE sio ya kufaidi makundi ama shughuli za kisiasa wala hata za kidi-

ni, ila tu pale kama iwapo makundi hayo yanatoa huduma kama wawakilishi. Miradi ya kufaidi watu binafsi, pia imeachwa nje ya mpango huu.

Utaratibu na Uandikishaji wa Mapendekezo ya Miradi Orodha ya mapendekezo ya miradi itakayopaswa kushughulikiwa, itapaswa itumwe kwa katibu mkuu wa bunge na Mbunge mhusika. Kuna fomu maalum itakayopaswa ijazwe kwanza. Hii itapaswa ifanywe kabla ya mwezi wa Februari, kila mwaka, ama mwezi mwingine wowote kama anavyoweza kuamua Waziri wa Fedha. 3

Ripoti ya CDF: Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika maeneo yao


Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika maeneo yao

Orodha hiyo itakuwa ni pamoja na miradi na gharama zao. Hayo yote, hata hivyo, yatachujwa na kamati ya Bunge na kamati ya hazina ya eneo la ubunge, ambazo baadaye zitapendekeza mapendekezo hayo yafikishwe kwa Waziri wa Fedha. Miradi hiyo yote, zitapewa nambari ili kuhakikisha kwamba kila mradi fulani unahifadhi namba ile ile hadi shughuli zake zimekamilika.

Kutekelezwa kwa Miradi Miradi yote iliyokusudiwa itapaswa kutekelezwa na idara za serikali wilay-

ani. Iwapo mradi fulani utahusu idara mbalimbali za serikali, idara iliyotajwa kwenye mapendekezo ya bajeti, itakuwa mstari wa mbele kwa utekelezaji wa mradi kama huo. Iwapo mradi utahusisha ununuzi wa vifaa, basi, vifaa hivyo vitabakia kwa utumizi mahsusi ya eneo hilo la ubunge. Kamati ndogo ya lokesheni pamoja na ingine ya ustawi zinaweza kuanzishwa kwa madhumuni ya kuchunguza jinsi kazi inavyondelea ama inavyofanya na kamati ya maendeleo katika sehemu kama hiyo.

4 Ripoti ya CDF: Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika maeneo yao


Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika maeneo yao

Kazi zote zinazohusiana na mradi zitapaswa kufuata utaratibu ulioko wa serikali wa ununuzi wa vifaa. Maombi yote ya tenda yatapaswa kuwasilishwa kwanza mbele ya kamati ya mipango wilayani ambapo wakuu wa idara ya wizara inayohusika katika kila wilaya watapaswa kuchunguza jinsi miradi iliyoko chini yao inayotekelezwa, kwa kuhakikisha kwamba wanahifadhi rekodi zote za matumizi ya fedha kwa miradi kama hiyo. Afisa wa maendeleo wilayani katika kila wilaya atapaswa kuweka rekodi ya risiti zote na jinsi fedha zilivyotumika kila mwezi na kwa kila mradi, kisha kuwasili-

sha akaunti yake kwa kamati ya kitaifa. Iwapo jamii itaomba, itaweza kuwateua wawakilishi wao kuangalia masilahi yao kwa mradi wowote ule unaoendelea katika sehemu yao.

Masharti Fedha zilizotengwa kwa minajili ya mradi fulani hazitapaswa kamwe zipelekwe kwingineko wakati wa msimu wa fedha za serikali kwa shughuli nyinginezo katika eneo la ubunge ama kwingineko. Iwapo mradi umefutiliwa mbali wakati wa msimu huo wa fedha za serikali, pesa hizo zitapaswa kurejeshwa kwenye hazina kuu ya serikali lakini kutakuwepo 5

Ripoti ya CDF: Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika maeneo yao


Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika maeneo yao

na rekodi ya kuonyesha mahali ambako pesa hizo zilitolewa. Gharama za kuwa na afisi maeneo ya ubunge na marupurupu mengineyo hazitapaswa ziwe zaidi ya asilimia 3% ya jumla ya fedha zinazotolewa kila mwaka, (Ksh.600,000). Asilimia 5% ama shilingi milioni moja ya jumla inayotolewa kwa kila eneo la ubunge hazitatengwa ila kubakia kama ‘hazina ya dharura’ ambapo pesa kama hizo zinaweza kutolewa iwapo kumezuka hali ya dharura inayohitaji msaada katika eneo la ubunge. Mpango ambapo mtu fulani atapaswa

kuzawadiwa kifedha ama kwa njia yoyote ile, hautaruhusiwa. Kamati ya CDF itahakikisha kwamba mashauri ya kufaa yanafanywa kati yake na idara za serikali zinazohusika kuhakikisha kuwa makadirio ya gharama zitakazohusika ni sahihi na ya ukweli. Cheki ama hundi zote za malipo zitapaswa zifuate utaratibu uliowekwa na serikali, kabla malipo yoyote kutolewa. Akaunti ya benki itakuwa tofauti na ile ya kawaida ya wilayani. Fedha zitatolewa tu wakati zinapohitajika baada ya rezolusheni ya kamati ya maendeleo ya CDF, kupitishwa. Fedha zote zitaba-

6 Ripoti ya CDF: Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika maeneo yao


Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika maeneo yao

kia kwenye akaunti ya CDF na hakuna uwekezaji mwingine wowote utaruhusiwa kwa dhamira ya kutumiwa kwa fedha kama hizo. Itapaswa ikumbukwe kuwa hakuna Mbunge wala Diwani yeyote atakuwa na saini yake kwenye hazina hiyo. Mtu yeyote yule ambaye atafuja fedha kama hizo atakuwa akivunja sheria ambayo adhabu yake ni kifungo cha hata kufikia miaka mitano gerezani ama faini Ksh 200,000 ama zote pamoja.

Wenye Kutia Saini Kwenye Cheki/Hundi Ni watu watatu tu ndio wanaoruhusiwa kutia saini ya malipo kwa cheki ama hundi za CDF. Kati ya hao ni mteuzi kutoka kwa kamati ya miradi wilayani na mwingine mteuzi wa CDF.

Kamati ya Maendeleo Eneo la Ubunge (CDC) • Kamati hii itapaswa ichaguliwe na Mbunge kwa muda wa siku 30 wakati wa kufunguliwa kwa bunge jipya • Wanachama wake hawatapaswa kuzidi idadi ya watu 15 7

Ripoti ya CDF: Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika maeneo yao


Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika maeneo yao

Wanaokusudiwa Kuwemo • Mbunge – akiwa kama mwenyekiti na mwenye mamlaka ya uteuzi • Madiwani wawili kutoka eneo lake • Afisa Tawala (DO) mmoja wa sehemu hiyo • Wawakilishi wawili wa kundi la kidini katika sehemu hiyo • Wawakilishi wawili wa kiume katika eneo hilo • Wawakilishi wawili wa kike sehemu hiyo • Mwakilishi mmoja wa vijana katika eneo hilo • Wateuzi wawili kutoka shirika

maarufu lisilo la kiserikali (NGO) kwenye eneo hilo.

Utendaji Kazi Mbunge wa kuchaguliwa atapaswa mara moja, kila mwaka kuandaa mikutano ya maendeleo sehemu za lokesheni • Kila lokesheni itapaswa ilete orodha ya miradi yake inayopaswa kushughulikiwa haraka mbele ya kamati hii • Kamati ya CDC itapaswa iwe ikijadili orodha kama hiyo kuona ni mradi gani utapaswa kupewa kipau mbele wakati huo na ni gani utashughulikiwa baadaye kisha

8 Ripoti ya CDF: Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika maeneo yao


Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika maeneo yao

kuwasilisha ripoti hiyo kwa bunge • Kushauriana na idara za serikali zinazohusika kuhakikisha kwamba makadirio ya fedha za mradi/miradi ni ya kweli

Kamati ya Miradi Wilayani Wajibu: • Kushirikisha utekelezaji wa miradi iliyonufaika na fedha za CDF na shughuli nyinginezo ambazo zimependekezwa na kamati ya Kitaifa. • Kamati ya miradi wilayani, inaweza wakati wa kutekeleza shughuli zake chini ya Kanuni hii ya bunge,

kuzuru kwa ghafla sehemu ambako miradi kama hiyo ya maendeleo inashughulikiwa

Wanachama • Wabunge wote wilayani aidha wa kuchaguliwa ama kuteuliwa. • Wenyeviti/Mameya wa mabaraza ya wilaya. • Mkuu wa wilaya (DC) • Afisa wa maendeleo wilayani (DDO) ambaye atakuwa ndiye katibu wa kamati ya miradi wailayani • Mwenyekiti wa kamati ya maendeleo eneo la ubunge (CDC) ambaye atapaswa awe ni Mbunge 9

Ripoti ya CDF: Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika maeneo yao


Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika maeneo yao

• Mhasibu mkuu wa wilaya. Wakuu wa idara ya serikali wanaweza pia kuhudhuria mikutano kama maafisa waalikwa • Muda wa kuhudumu miongoni mwa Wabunge ama Madiwani waliochaguliwa kwa kipindi cha miaka miwili hadi mwisho wa msimu wa bunge • Kila Mbunge atapaswa awe akiorodhesha orodha ya miradi atakayotaka zishughulikiwe • Kamati ya miradi wilayani itapaswa kuhakikisha kwamba miradi zitakazoshughulikiwa hazifanani katika eneo moja na kwamba kila

mradi utakuwa manufaa kwa jamii nzima wilayani. • Kupendekeza orodha ya miradi kwa katibu mkuu wa bunge kupitia kwa Mbunge kutoka kila eneo na ambaye hatapaswa kukalia mapendekezo kama hayo bila sababu

Kamati Teule ya Bunge kuhusu Hazina Kamati hii ilibuniwa chini ya sheria za bunge kama kamati teule

Uanachama Wanachama wake watakuwa sawa na kamati zingine teule za bunge, kwa

10 Ripoti ya CDF: Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika maeneo yao


Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika maeneo yao

mfano, kuwepo kwa mwenyekiti na sio zaidi ya Wabunge 10 ambao si mawaziri/ wasaidizi wa mawaziri. Uwakilishi wa usawa kwa vyama vya kisiasa bungeni, utapaswa kuwepo.

Utendaji Kazi • Kufikiria juu ya mapendekezo ya miradi sehemu za wilayani kisha kutoa mapendekezo hayo kwa katibu mkuu wa bunge • Kutoa mapendekezo ya majina ya watu watakaohitajika na ambao wataidhinishwa na bunge chini ya sheria za CDF • Kuhakikisha kuwa sheria hiyo ime-

fuatwa, na kuweza pia kupendekeza kufanywa kwa mabadiliko kisha kuwasilisha ripoti kwa bunge kila baada ya miezi sita • Kuchunguza kuona kuwa maongozi yaliyowekwa ya kutekelezwa kwa mipango hii yameshughulikiwa haraka

Wanachama wa Kamati ya Kitaifa ya Usimamizi ya Ustawi Maeneo ya Ubunge • Mwenyekiti (kutoka Wizara ya Fedha), Katibu Mkuu Wizara ya Mipango ya Uchumi • Katibu Mkuu wa Wizara ya Ustawi wa Mikoa 11

Ripoti ya CDF: Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika maeneo yao


Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika maeneo yao

• Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo • Katibu Mkuu wa Bunge • Watu wanane walioteuliwa na waziri kutoka Kenya Farmers Union na Institute of Engineers of Kenya • Kenya National Chamber of Commerce, Kanisa Katoliki, KNUT, Baraza la Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO), Baraza Kuu la Waislamu nchini (SUPKEM), afisa mmoja mtumishi wa umma kusimamia hazina (kama mteule na vile vile katibu) • Majina na maelezo ya wanachama wa kamati ya kitaifa yataidhinishwa na rais.

Wajibu wao Kuhakikisha kwamba fedha zimetolewa kwa usawa kwa kila eneo la ubunge na kwamba kuna usimamizi bora Kutayarisha ripoti na rekodi zote kutoka maeneo ya ubunge kisha kuziwasilisha kwa bunge. Katibu wa kamati hii atachunguza na kuhakikisha kwamba anasimamia vilivyo shughuli za siku hadi siku za matumizi ya fedha hizo huku akihakikisha kuwa rekodi zote za kifedha ziko sawa kabla hatimaye kuzituma kwa mkaguzi mkuu wa hesabu za fedha serikalini.

12 Ripoti ya CDF: Jinsi jamii inavyoweza kuelewa na kutumia CDF kuondoa umasikini katika maeneo yao



Imehaririwa na kuchapishwa na AWC Feature Service. Imedhaminiwa na shirika la Swedish International Development Cooperation Agency (SIDA).


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.