![](https://static.isu.pub/fe/default-story-images/news.jpg?width=720&quality=85%2C50)
1 minute read
KWA AJILI YA MAREHEMU
Ee Mungu wangu ! Ewe msameheaji wa dhambi, mjalia thawabu, muondoa mateso ! Hakika, nakusihi kusamehe dhambi za wale walioacha vazi la kimwili na wamepaa kwenye ulimwengu wa kiroho.
Ee Bwana wangu ! Uwatakase kutokana na makosa, ondoa huzuni zao, na Ugeuze giza lao kuwa mwanga. Wafanye waingie bustani ya furaha. Uwatakase kwa maji safi kabisa, na Uwajalie wauone utukufu Wako kwenye mlima ulio bora kabisa.
‘Abdu’l-Baha