1 minute read
STANDINGOUT IN NETWORKMARKETING
Farida ni kijana muhitimu wa ngazi ya Diploma katika kozi ya Electronic Engineering anayefanya biashara na kampuni ya watu wa Marekani. Muda wa ziada anafanya biashara ili kukidhi mahitaji yake ya kila siku. Anaamka kila siku saa kumi na moja alfajiri na kujiandaa kuingia chuoni na baada ya masomo hufanya biashara zake. Alianza kufanya biashara Desemba 2014 akiwa chuoni mwaka wa pilli, hivi karibuni atatimiza miaka miwili katika biashara yake. Shughuli zinazomuingizia kipato ni biashara . Kipato anachopata kinamsaidia kuendesha maisha yake mwenyewe yakuwa hategemei wazazi. Mfumo wa biashara anayofanya ni kushirikisha watu kwa njia mbali mbali ikwemo njia ya mtandao.Alipokuwa mwaka wa pili chuoni alitamani sana kufanya biashara na hakufaham ni biashara gani aanze nayo na kuanza biashara ya kuuza cheni ili kumsaidia katika maisha yake ya kila siku. “Rafiki yangu wa karibu ndiye aliniunganisha na mfanya biashara aliyefanya biashara hiyo kwa uzoefu zaidi na kunielezea namna ya kupata kipato, nilianza biashara ndani ya siku tatu baada ya kutangaziwa fursa ya biashara” Kilichomsukuma zaidi kuanza biashara ni pale alipokutana na kijana mdogo kama yeye aliyefanikiwa katika biashara hiyo alipokuwa akiingiza kiasi cha laki sita kwa mwezim kutokana na biashara hiyo. Farida alipoanza biashara wazazi wake hawakumkubalia kuchanganya biashara na masomo wakihisi kufanya hivyo kungemkwamisha katika pamoja, wazazi na waalimu wakapenda anachofanya na kumpa nguvu kwa pamoja.
VIKWAZO ANAVYOKUTANA NAVYO:
Advertisement
Kikwazo kikubwa anachokutana nacho ni baadhi ya watu kumkosoa kuwa atashindwa katika biashara yake ya kwamba walio wengi amabao wamefanya biasharahiyo. “kama mtu ana roho nyepesi na malengo madogo katika maisha yake anaweza kukata tama katika kufanya biashara ila naamini kabisa sio kila aliyefanya akashindwa namimi nikifanya ntashindwa la hasha!”
WITO KWA VIJANA
Farida amewaasa wanawake hasa wakinadada kujishughulisha na kutokuwa tegemezi kwa wanaume sababu wanadada wengi wanaolewa na wanaume ambao hawakuwapenda bali ni kutokana na kipato cha mwanaume kwa kupatiwa kila kitu. “Napenda kuwaambia vijana wenzangu hasa wakina dada wajitume ili waweze kufanya biashara yoyote nakujishughulisha na mambo mbalimbali ya kuongeza kipato sababu changamoto kubwa wanayokumbana nayo ni vijana kukosa ajira”