2 minute read

Innovative Jangwani SS Find the treasure in Coconut Shells

Schools Business Club

Jangwani Sec Xcul

Advertisement

Hivi karibuni serikali na wadau wa maendeleo wamekua wakijadili kuhusu tatizo sugu la ajira kwa vijana ambalo ukubwa wake unaongezeka kwa kasi. Serikali kwa kushirikiana na taasisi zisizo za kiserikali kama Junior Achievement imekua ikijaribu njia mbalimbali kutatua tatizo hili. Serikali imekua ikiimba wimbo kuhusu ujasiriamali kwa vijana ingawa walengwa wamekuwa wakipuuzia fursa hiyo sababu hawana msingi wowote kuhusu ujasiriamali pia Jamii haiungi mkono ujasiriamali. Baadhi ya familia tajiri huwa na mawazo hasi kwa mwana familia kama anataka kuwa mjasiriamali, familia huwa ya kwanza kumvunja moyo kwa kuwa wengi hufikili wanaofanya ujasiriamali ni watu walioshindwa kimaisha. Hii inadhihirishwa pale ambapo mtu anashindwa kabisa kupata kazi ndipo atafikiria kuhusu biashara, Watu wengi wanaamini kuwa ukiajiriwa ndio utakuwa na mafanikio. Mashirika yasio ya kiserikali yameanza kutengeneza msingi mbao utawajenga wajasiriamali wa kizazi kijacho kwa kuwaandaa wanafunzi katika shule za sekondari kwa kuwapa mafunzo ya ujasiriamali, na kuwaongozakupitia kampuni ambazo zinatumika kama darasa. Kupitia kampuni hizo, Wanafunzi watajifunza jinsi biashara zinavyoendeshwa katika maisha halisi. Junior Achievement Company Program ni Programu inayoendeshwa katika shule za sekondari nchini Tanzania na shirika lisilo la kiserikali liitwalo Junior Achivement, shule ya sekondari Jangwani ni moja kati ya shule tisa zilizopata fursa hii. Wanafunzi wa Shule hiyo wamewezeshwa kufungua kampuni iitwayo Green Innovation Enterprise inayotengeneza bidhaa za thamani kwa kutumia vifuu vya nazi na madafu. Bidhaa zinazotengenezwa ni vikombe, upawa, Majagi, vibakuli n.k

“Junior Achievement walipo kuja kujitambulisha na kutueleza kuhusu mpango wa ujasiriamali tulikuwa wanafunzi wa kawaida tu ambao hatujui nini tufannye tuliambiwa tufikirie bidhaa za kutengeneza yakapatikana mawazo tofauti na mwisho likapatikana wazo kuu la kuutengeneze bidhaa kutumia vifuu vya nazi na madafu ” alisema Lillian Kilave mwanafunzi wa shule ya sekondari Jangwani. Jacqueline Chitomwa ni kiongozi wa Green Innovation Enterprises katika shule ya sekondari Jangwani ambaye alitoa wazo la kutengeneza bidhaa kwa kutumia vifuu ya nazi na madafu . “Nilifikiri kuhusu vifuu vya nazi na madafu kwasababu madafu yakiliwa yanatupwa ovyo mitaani hivyo husababisha uchafuzi wa mazingira , nikapata wazo nikafikiria ni jinsi gani tuna weza kutumia hizi taka kutengeneza vitu vya thamani,” alisema Jacqueline Chitomwa. Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwa ni wanaounda Green Innovation

baadhi ya bidhaa zilizo zalishwa na wanafunzi wa jangwani ni thermos Flask... chupa unayo weza kutunza joto kwa masaa 8

Enterprise walikubaliana na wazo la kutengeneza bidhaa kutumia vifuu vya nazi na madfafu sababu vifuu vinauwezo wa kutunza joto kwa masaa manne. Walitumiaa wazo lao katika vitendo na bidhaa ya kwanza kutengeneza ilikuwa jagi kama jaribio, baada ya jagi walifanikiwa kutengeneza bidhaa nyingine zikiwemo vikombe, bakuli, upawa nk.

This article is from: