JUNIOUR ENTREPRENEUR MAGAZINE DRAFT

Page 10

Schools Business Club

Jangwani Sec Xcul

H

ivi karibuni serikali na wadau wa maendeleo wamekua wakijadili kuhusu tatizo sugu la ajira kwa vijana ambalo ukubwa wake unaongezeka kwa kasi. Serikali kwa kushirikiana na taasisi zisizo za kiserikali kama Junior Achievement imekua ikijaribu njia mbalimbali kutatua tatizo hili. Serikali imekua ikiimba wimbo kuhusu ujasiriamali kwa vijana ingawa walengwa wamekuwa wakipuuzia fursa hiyo sababu hawana msingi wowote kuhusu ujasiriamali pia Jamii haiungi mkono ujasiriamali. Baadhi ya familia tajiri huwa na mawazo hasi kwa mwana familia kama anataka kuwa mjasiriamali, familia huwa ya kwanza kumvunja moyo kwa kuwa wengi hufikili wanaofanya ujasiriamali ni watu walioshindwa kimaisha. Hii inadhihirishwa pale ambapo mtu anashindwa kabisa kupata kazi ndipo atafikiria kuhusu biashara, Watu wengi wanaamini kuwa ukiajiriwa ndio utakuwa na mafanikio. Mashirika yasio ya kiserikali yameanza kutengeneza msingi mbao utawajenga wajasiriamali wa kizazi kijacho kwa kuwaandaa wanafunzi katika shule za sekondari kwa kuwapa mafunzo ya ujasiriamali, na kuwaongoza kupitia kampuni ambazo zinatumika kama darasa. Kupitia kampuni hizo, Wanafunzi watajifunza jinsi biashara zinavyoendeshwa katika maisha halisi. Junior Achievement Company Program ni Programu inayoendeshwa katika shule za sekondari nchini Tanzania na shirika lisilo la kiserikali liitwalo Junior Achivement, shule ya sekondari Jangwani ni moja kati ya shule tisa zilizopata fursa hii. Wanafunzi wa Shule hiyo wamewezeshwa kufungua kampuni iitwayo Green Innovation Enterprise inayotengeneza bidhaa za thamani kwa kutumia vifuu vya nazi na madafu. Bidhaa zinazotengenezwa ni vikombe, upawa, Majagi, vibakuli n.k

Mwanzo

Junior Achievement Company Program ni mpango unaoendeshwa katika shule za sekondari na taasisi isiyo ya kiserikali inayotoa mafunzo ya ujasiriamali kwa vitendo. Wanafunzi wanakaa vikundi na kuunda kampuni kwa kutafuta wazo la biashara, na kulitekeleza. Taasisi hii ya Junior Achievement inatoa mafunzo jinsi ya kuendesha kampuni ambayo itakuwa imeundwa na wanafunzi wanapokuwa shuleni.

“Junior Achievement walipo kuja kujitambulisha na kutueleza kuhusu mpango wa ujasiriamali tulikuwa wanafunzi wa kawaida tu ambao hatujui nini tufannye tuliambiwa tufikirie bidhaa za kutengeneza yakapatikana mawazo tofauti na mwisho likapatikana wazo kuu la kuutengeneze bidhaa kutumia vifuu vya nazi na madafu ” alisema Lillian Kilave mwanafunzi wa shule ya sekondari Jangwani. Jacqueline Chitomwa ni kiongozi wa Green Innovation Enterprises katika shule ya sekondari Jangwani ambaye alitoa wazo la kutengeneza bidhaa kwa kutumia vifuu ya nazi na madafu . “Nilifikiri kuhusu vifuu vya nazi na madafu kwasababu madafu yakiliwa yanatupwa ovyo mitaani hivyo husababisha uchafuzi wa mazingira , nikapata wazo nikafikiria ni jinsi gani tuna weza kutumia hizi taka kutengeneza vitu vya thamani,” alisema Jacqueline Chitomwa. Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwa ni wanaounda Green Innovation

Enterprise walikubaliana na wazo la kutengeneza bidhaa kutumia vifuu vya nazi na madfafu sababu vifuu vinauwezo wa kutunza joto kwa masaa manne. Walitumiaa wazo lao katika vitendo na bidhaa ya kwanza kutengeneza ilikuwa jagi kama jaribio, baada ya jagi walifanikiwa kutengeneza bidhaa nyingine zikiwemo vikombe, bakuli, upawa nk.

MTAJI

Kupitia mafunzo waliyoyapata kutoka kwa wahamasishaji wa Junior Achievement. waliamua kuuza hisa kama njia mojawapo ya kukusanya mtaji...kampuni iliuza hisa zenye jumla ya laki moja na nusu, kila kipande kiliuzwa kwa thamani ya shilingi 1000/= Baada ya kupata mtaji walifikiria waanze kuuza bidhaaa mbazo mzunguko wake ni waharaka hapo shuleni. Wakaanza kuuza vifaa vya shule ikiwemo madaftari, peni, vitabu, chokleti, keki na ubuyu. Pesa waliyoipata iliwawezesha kutengeneza bidhaa zao kwa kutumia vifuu vya nazi na madafu. Wateja wakuu wa bidhaa hizo ni


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.