Mienendo ya soko la mazao ya Horticulture kwa mwaka
Utangulizi.
M
azao ya horticulture hujumuisha mazao yote ya mboga, matunda, viungo, maua na mazao ya mizizi. Kwa kawaida mengi ya mazao haya hudumu kwa muda mchache sana baada ya kuvunwa. Hivyo maandalizi ya soko kabla ya kupanda ni muhimu ili kujua yatakapopelekwa baada ya kuvunwa. Kujua mienendo au kalenda za mazao haya katika misimu yote ya mwaka kunasaidia sana kupunguza
hatari za kuangukia kwenye kipindi cha mafuriko ya bidhaa na bei duni. Kwa upana wake, inasaidia kuimarisha usalama wa chakula nchini kwa kuwezesha upatikanaji wa bidhaa kwa walaji katika vipindi vyote vya mwaka tofauti na kuegemea miezi fulani tu. Ifuatayo ni jinsi mienendo ya bei za baadhi ya mazao hayo ilivyokuwa kuwa kwa kipindi cha mwaka 2016:
1 Vitunguu
Vitunguu
Miezi ya bei nzuri.
itunguu ni moja ya mazao yanayodumu sana baada ya kuvunwa ukilinganisha na mazao mengine ya horticulture. Inakisiwa kuwa vitunguu vinaweza kutunzwa kwa kuhifadhiwa vizuri mpaka miezi sita au zaidi baada ya kuvunwa. Ni zao ambalo kwa miaka 3 mitatu tangu 2014 bei zake zimekua zikiimarika hata kipindi cha mavuno mengi.
Kwa takwimu za masoko makubwa ya walaji ya Tanzania, kuanzia mwezi Januari hadi Juni ya mwaka 2016 bei za vitunguu zimekuwa juu ukilinganisha na miezi mingine. Katika kipindi hiki, bei ilikuwa kati ya wastani wa Tsh. 146,000 hadi 240, 000 kwa gunia la kilo 120. Bei zimekuwa zikipanda kwa haraka kuanzia Januari kuelekea Juni. Sababu za kupanda kwa bei ni kwamba,
V
wakulima wengi wanapanda kuanzia miezi ya Aprili na Mei na kuvuna kuanzia miezi ya Julai na Agosti. Hivyo kipindi cha Januari hadi Juni huwa kina upungufu mkubwa wa vitunguu. Vilevile, nchi za jirani kama Uganda, Kenya na Sudani Kusini na nyinginezo zimekuwa na uhaba mkubwa wa vitunguu katika kipindi hiki na hivyo kupelekea kiasi kikubwa kuelekea huko. Miezi ya bei ndogo Kwa kuwa wakulima wengi hupanda mwezi Aprili na Mei, bei ilikuwa chini kuanzia mwezi Julai walipoanza kuvuna hadi mwanzoni mwa Disemba. Mwishoni mwa Disemba bei huanza kupanda taratibu kwa sababu ya uhaba wa vitunguu unaanza.
Chanzo: TAHA
2 Nyanya
Nyanya
T
ofauti na vitunguu, nyanya ni miongoni mwa mazao ambayo yana muda mfupi sana wa kuishi baada ya kuvuna. Inalazimika kuchumwa ikiwa nusu mbichi ili ifike sokoni ikiwa nzuri. Grafu hapo chini inaonesha bei zilivyokuwa kwa mwaka 2016. Miezi ya bei nzuri za nyanya. Kutoka kwenye grafu hapo juu, kuanzia mwezi Februari hadi Juni ya mwaka 2016 bei za nyanya zimecheza kati ya wastani wa Tsh 30,000 hadi 58,000 (hadi Tsh 70,000 kwa Dar es salaam na Arusha) kwa kreti ya kg 40 kwa bei ya sokoni.
Bei hupanda haraka kuelekea Juni. Kipindi hiki kimekuwa na uhaba mkubwa wa nyanya kwa kuwa wakulima wengi wamekuwa wakianza kupanda kwa kutegemea mvua kuanzia mwezi Aprili na kuvuna mwezi Julai. Kipindi cha bei ndogo Baada ya wakulima waliopanda Aprili kwa kutegemea mvua kuanza kuvuna , kuanzia mwezi Julai bei za nyanya ziliporomoka kwa kasi sana toka Tsh 25000 hadi Tsh 7,000 kwa kreti ya kg 40 kwa bei ya sokoni.
Wakulima wengi sana hulima kipindi hiki cha kuanzia Aprili hata ambao wametoka kuvuna mpunga nao humwaga mbegu za nyanya kwenye mashamba yao. Hali hii ya bei ndogo ilidumu hadi mwanzoni mwa mwezi Disemba. • Kama inavyoonekana kwenye grafu, bei zimeanza kupanda taratibu kuanzia mwezi Novemba 2016. Inatarajiwa mwishoni mwa Januari 2017 hadi kufikia mwanzoni mwa Juni bei kuwa nzuri kwa sababu zilizotajwa hapo juu. • Bei zinatarajiwa kuwa ndogo hadi chini ya TSH 15000 baada ya Julai hadi mwanzoni mwa Disemba 2017
Chanzo: TAHA
3 Pilipili Hoho ya kijani
Pilipili Hoho ya kijani
100,000 hadi 200,000 kwa gunia la kilo 100 katika kipindi hiki.
oho za kijani pia ni zao ambalo kukaa muda mfupi sana baada ya kuvunwa, pengine muda mfupi zaidi ya nyanya. Inatakiwa ifike sokoni ndani ya masaa 24 baada ya kuchumwa ili iwe katika hali nzuri kama hakuna vihifadhio vya baridi.
Bei za chini:
H
Baada ya Juni 2016 bei zilishuka kwa kasi hadi kufikia karibu na Tsh 50,000 baada ya wakulima wengi waliopanda kwa mvua za Aprili kuanza kuanza kuvuna. • Bei zinatajiwa kupanda kuanzia Januari 2017 hadi Mei 2017 kwa sababu zilizotajwa hapo juu. • Bei zinatarajiwa kushuka baada ya mwezi Mei 2017.
Kipindi cha bei nzuri za Hoho za kijani: Hoho za kijani imekuwa na bei nzuri kuanzia mwezi Januari kuelekea Mei 2016. Katika kipindi hiki hoho ziliadimika mno maeneo yote ya nchi. Zilikuwa zikipatikana kwa uchache sana maeneo ya mikoa ya kaskazini. Kiasi kidogo pia kilikuwa kikitokea Iringa. Hii ilifanya bei zipande kuanzia wastani wa Tsh
Chanzo: TAHA
4 Karoti
Karoti
K
aroti ni miongoni mwa mazao ya mboga ambayo hustawi sana katika hali ya hewa ya baridi. Kiasi cha karoti kilichopo sokoni na bei kinategemea msimu uliopo kama ni wa joto au baridi.
kwa gunia la kilo 100. Kipindi hiki kina hali ya hewa ya baridi ambayo hufaa sana kwa uzalishaji wa karoti hivyo kuifanya iwe nyingi sokoni na kupelekea kushuka kwa bei.
Kipindi cha bei nzuri: Hali ya hewa ya baridi inapokuwa inakwenda mwishoni kuanzia mwezi Septemba hadi mwishoni Novemba, bei za karoti nazo zilipanda kutokana na kupungua kwa uzalishaji. Bei ilifika hadi wastani wa Tsh 85,000 kwa gunia la kilo mia moja mwaka 2016. Kipindi cha bei ndogo: Kuanzia mwezi Aprili hadi Agosti 2016, bei za karoti zilishuka nchini mpaka wastani wa Tsh 60,000
Chanzo: TAHA
5 Matango
Matango
Bei ndogo
laji wa matango huathiriwa na hali ya hewa. Kipindi cha baridi, ulaji wa matango nchini hupungua kwa kiasi kikubwa sambamba na bei zake katika masoko. Walaji hawapendelei sana matango wakati wa baridi.
Kwa kuwa wakulima wengi hulima matango baada ya mvua za Aprili hali inayopelekea kuongezeka kwa kiasi cha matango masokoni na kushuka kwa bei kuanzia Juni hadi Septemba hadi kufikia Tsh 80,000 kwa gunia la kilo 100. Hali ya baridi pia huchangia ulaji wa matango kushuka, hivyo kushuka kwa huhitaji.
U
Bei nzuri Bei za matango zilianza kupanda kuanzia Januari hadi Mei 2016 na kuanzia Oktoba hadi Disemba 2016 katika kipindi cha joto na ukame. Katika kipindi hiki kiasi cha matango masokoni kilipungua na ulaji kuongezeka. Hali ya hewa ya joto huchangia sana kuongezeka kwa ulaji wa matango. Hali hii ilisababisha bei kuongezeka toka Tsh 100,000 hadi kufikia Tsh 180,000 kwa gunia la kilo 100.
Chanzo: TAHA
6 Viazi mviringo
Viazi mviringo
K
una maeneo makuu mawili maarufu kwa kilimo cha viazi mviringo nchini Tanzania. Maeneo hayo ni Nyanda za juu Kusini na Kaskazini.
Kipindi cha bei ndogo Baada ya Mikoa ya Kaskazini kuanza kuvuna kuanzia Julai hadi Disemba, bei za viazi ilishuka hadi Tsh 82000 kwa gunia la kilo 100. Kipindi hiki kinakuwa na mavuno mengi kwa kuwa viazi huvunwa karibu kutoka maeneo yote inayozalisha.
Kipindi cha bei nzuri Bei ya Viazi mviringo ilikuwa nzuri kuanzia Januari hadi June 2016. Miezi hii viazi vingi hutokea Nyanda za juu Kusini.Wakati huu Mikoa ya Kaskazini inakuwa bado haijaanza kuvuna hivyo kusababisha uhaba mkubwa wa bidhaa hii na hivyo kuongezeka kwa bei hadi kufikia wastani wa Tsh 160,000 kwa gunia la kilo 100 Chanzo: TAHA
7 Tikiti maji
Tikiti maji
T
ikiti maji ni tunda ambalo huliwa sana kipindi cha joto kuliko kipindi cha baridi kwa mujibu wa takwimu toka katika masoko mbalimbali nchini. Mbegu iliyofanya vizuri kwa mwaka 2015/16 ni ya tikiti aina ya Pundamilia, mfano, Sukari F1, King, Queen, nk.
Miezi ya bei mbaya. Ijapokuwa kipindi cha joto huwa na bei nzuri, kuanzia Mwishoni mwa Disemba hadi Februari bei za tikiti hushuka kutokana na kufurika kwa matunda yanayopendwa zaidi na walaji kama maembe, mananasi, nk. Hivyo, bei ya tikiti maji kwa kipindi hiki hudorora. Pia bei mbaya ziko katika mwezi wa Juni hadi Agosti ambapo ni kipindi cha baridi.
Miezi ya bei nzuri: Kipindi cha kuanzia mwezi Oktoba hadi Novemba mwaka 2015 na 2016 kimekuwa na bei nzuri kwa tikiti ikiuzwa kwa bei ya wastani ya karibu Tsh 700 kwa kilo. Vilevile kipindi cha Machi hadi Mei kilikuwa na bei nzuri kama kinavyoonyeshwa kwenye grafu. Vipindi vya bei nzuri vimeangukia katika kipindi ambacho kina hali ya joto.
Chanzo: TAHA
Miezi sahihi ya kupanda na kuvuna ili kupata bei nzuri Zao
Wakati mzuri wa kuvuna
Kipimo
Bei (TZs)
Wakati Mbaya Bei (TZs) wa kuvuna
Muda sahihi wa kupanda
Nyanya
Jan - May
40 Kg Kreti
35,000 – 52,000
June - Dec
Sept -Dec
Kitunguu
Jan - june
120 kg Gunia
136,000 – 200,000 Jully - Dec
90,000 – 13,5000 Sept - Feb
Pilipili hoho
Feb - April
100 kg Gunia
110,000 – 200,000 May - Jan
52,000 – 110,000 Oct - Nov
Matango
Feb-May
50 kg Gunia
46,000 – 67,000
June - Jan
34,000 – 45,000
Dec - Jan
Karoti
Oct - March
100 kg Gunia
70,000 – 95,000
April - Dec
57,000 -70,000
Jully - Oct
Viazi mviringo
March - June
120 kg Gunia
91,000 – 116,000
Jully - Feb
77,000 – 90,000
Dec - Feb
17,800 - 34000
Hitimisho Miezi ilikuwa na bei nzuri ya mwaka 2016 inatarajiwa kubaki karibu sawa kwa mwaka 2017. Hivyo, wakulima wanashauriwa kufuata mienendo ya bei kwenye ripoti hii ili kupunguza hatari ya kuangukia kwenye mafuriko ya bidhaa na bei duni.
Reach out to us Tanzania Horticultural Association (TAHA) Head Office, Kanisa Road, House No.49 P.O. Box 16520, Arusha-Tanzania Tel/Fax: +255 27 2544568 info@taha.or.tz www.taha.or.tz FB: https://www.facebook.com/TanzaniaHorticulturalAssociationTaha?fref=ts Twitter: taha_tanzania View our photos through: https://www.flickr.com/photos/tahacommunications
Dar es Salaam
Zanzibar
Morogoro
Rita Tower, Makunganya Street, PLOT NO. 727/11 Floor 21 P. O. Box 7666, DAR ES SALAAM Tel/Fax +255 22 211 2943
Road Fund Building, Kikwajuni Gofu P. O. Box 2834, Zanzibar.
Morogoro Regional Hospital Road, Posta Building, First Floor.