11 minute read

Lengo na wupeo wa Itifaki

Next Article
Kiambatisho cha 6

Kiambatisho cha 6

Yaliyomo

Lengo na wupeo wa Itifaki........................................................ 3 Kanuni kuu za utendaji katika ulinzi na uchunguzi wa makaburi ya halaiki...................................................................... 6 A. Ugunduzi na kuripoti salama............................................... 8 B. Ulinzi ............................................................................................ 8 C. Uchunguzi................................................................................... 9 D. Utambuzi..................................................................................... 12 E. Kurejeshwa kwa mabaki ya binadamu ............................. 14 F. Haki ............................................................................................... 15 G. Ukumbusho................................................................................ 16 Kiambatisho cha 1........................................................................ 17 Kiambatisho cha 2........................................................................ 18 Kiambatisho cha 3........................................................................ 19 Kiambatisho cha 4........................................................................ 20 Kiambatisho cha 5........................................................................ 21 Kiambatisho cha 6........................................................................ 22

Lengo na upeo wa Itifaki

Makaburi ya halaiki ni historia ya mara kwa mara inayotokana na migogoro na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu. Kwa walionusurika, hitaji la kujua hatima na mahali walipo wapendwa wao, na kupokea mabaki ya mauti kwa ajili ya mazishi na/au ukumbusho wa heshima, yanaweza kuwa makubwa sana. Kwa kuongezeka hitaji hili linatambuliwa kama haki ya kisheria ya kujua ukweli. Makaburi ya halaiki yana ushahidi ambao ni muhimu kwa utimilifu madhubuti wa ukweli, haki na uwajibikaji wa wahusika. Sheria na taratibu madhubuti za ulinzi, utunzaji na uchunguzi wa makaburi ya halaiki ni muhimu sana. Kwa sasa, hata hivyo, ingawa kuna mbinu kadhaa bora za utendaji zinazotumika miongoni mwa wahusika mbalimbali katika uwanja, hakuna viwango vya jumla vilivyopo, vya pamoja au vya kawaida. Kupitia mchakato shirikishi na wa mashauriano, Itifaki hii inajaza pengo hilo. Hairudufu wala kuchukua nafasi ya hati zilizopo kuhusiana na kanuni na mazoea mazuri1. Badala yake inatoa mbinu ya kuunganisha ya ndani na nje ya utaalamu kwa ulinzi wa kaburi la halaiki na uchunguzi. Inafuata mpangilio wa michakato hii kwa ukamilifu pamoja na washikadau, taaluma na mifumo mingi inayoungana kwa madhumuni ya pande mbili, na yanayoimarisha pande zote za kukuza ukweli na haki, kwa kutoa:

(1) Itifaki ya Kimataifa kuhusu Ulinzi na Uchunguzi wa

Makaburi ya Halaiki, yenye msingi wa sheria zinazohusika, na kuchanganya na kuunganisha matawi ya sheria ya kimataifa ya haki za binadamu, sheria ya kimataifa ya kibinadamu na - pale inapofaa - sheria ya kimataifa ya uhalifu; na

1 Angalia orodha ya hati husika katika Kiambatisho cha 1.

(2) Maoni ya Kielimu kuhusu Itifaki, yanayozingatia msingi na majadiliano ambayo yalisababisha sheria mbalimbali zilizomo. Maoni ya Kielimu, yaliyochapishwa kando, yanaangazia na kupanua mitazamo tofauti na mahitaji ambayo yanatokea katika mchakato wa ulinzi wa kaburi la halaiki na uchunguzi ili kuhakikisha kuwa, katika utekelezaji, yanatarajiwa na, inapowezekana, kupunguzwa. Watumiaji: Itifaki imekusudiwa kutumiwa na wataalamu, ikiwa ni pamoja na lakini sio tu: maafisa wa serikali na taifa, watekelezaji sheria, wawakilishi wa sheria, wataalamu wa uchunguzi, wataalamu wa afya, wataalamu wa usalama na wahusika wataalamu wa mashirika ya kijamii.2

Upeo na matumizi ya Itifaki: kulingana na kisa maalum

Msamaha wa muktadha wa Itifaki hii umewekewa kikomo kwa makaburi ya halaiki ambayo huibuka katika muktadha wa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na migogoro, ya ndani na ya kimataifa. Hii haiondoi, hata hivyo, Itifaki hiyo kuwa ya umuhimu kwa makaburi ya halaiki yanayotokana na hali tofauti.3 Waathiriwa katika makaburi ya halaiki wanaweza kuwa wanaume, wanawake na/au watoto. Wanaweza kuwa raia na/au wapiganaji wenye silaha kutoka pande zote za mgogoro. Itifaki imekusudiwa kutumika bila ubaguzi na bila kujali maoni ya kisiasa au maoni mengine, ushirikiano na wachache katika kitaifa, jinsia, mwelekeo wa kijinsia, utambulisho wa jinsia, dini au imani, umri, mbari, rangi, lugha, kabila, tabaka, asili ya kitaifa au kijamii, ulemavu wa mwili au akili, hali ya afya, mali, kuzaliwa, hali ya ndoa, au sababu nyingine yoyote inayotambuliwa na vyombo vya kisheria vya kimataifa. Hakuna jambo kama uchunguzi au ufuakuaji wa kaburi la halaiki wa ‘kawaida’. Uchunguzi kaburi la halaiki unazingatia muktadha mahususi. Hii inaweza kuwa kwa sababu kama vile mamlaka ya kijiografia na ya muda na pia mazingira ya kisiasa. Kwa sababu hiyo, Itifaki hii haikusudiwi kuwa kama maelekezo kulingana na mazoea bora katika visa vyote vya makaburi ya halaiki. Badala yake, Itifaki inatoa mazingatio maalum ambayo yamekusudiwa kusaidia na kuwaelekeza wahusika wanaposhughulika na mchakato wa uchunguzi katika uwezo wao mbalimbali na katika hatua zote. Kufikia mwisho huu, inapaswa kutambuliwa kuwa huenda mazingatio yaliyomo katika Itifaki yasiweze kutumika kwa kikamilifu kwa kila uchunguzi. Ijapokuwa Itifaki imeundwa kusaidia kwa msingi jumla, ubainishaji wa matumizi ya mambo mahusuzi ya Itifaki unapaswa kufanywa na mtaalam kwa msingi wa kila kisa. Kando na hayo, kwa kiwango cha chini, na kulingana na njia, viwango vya uchunguzi na ulinzi vinavyotumika kwa hali yoyote vinapaswa kutosha kutimiza malengo ya ukweli na haki, yaani, vinapaswa kuhimili uchunguzi wenye mamlaka.

Mbinu

Yaliyomo katika Itifaki yameundwa kutokana na uzoefu na maoni ya wataalam walioalikwa, ikiwa ni pamoja na wataalam wa uchunguzi, wachunguzi, majaji, waendesha mashtaka, wahudumu wa usalama/polisi, wawakilishi wa asasi za kiraia na wasomi, wakiangazia kuhusu uzoefu wa ulinzi na uchunguzi wa makaburi ya halaiki, utaalamu katika haki za binadamu, sheria za kibinadamu na/au uhalifu, pamoja na utofauti wa kijiografia.4

Ufafanuzi

Kwa madhumuni ya Itifaki, tunatoa ufafanuzi ufuatao unaotumika: • Neno kaburi la halaiki, ambalo halijafafanuliwa katika sheria ya kimataifa, linatumika hapa kumaanisha ‘eneo au mahali palipobainishwa penye watu wengi (zaidi ya mmoja) wa waliozikwa, waliozama au sehemu iliyo na mabaki ya wanadamu yaliyotawanyika (ikiwa ni pamoja na mabaki ya mifupa, yaliyochanganyika na kugawanyika), ambapo hali kuhusiana na vifo na/au njia ya utupaji mwili inahitaji uchunguzi juu ya uhalali wake’. • Watu waliopotea inamaanisha ‘watu waliopotea kutokana na migogoro, ukiukwaji wa haki za binadamu na/au vurugu zilizopangwa.’5 • Kwa mwathiriwa Itifaki inamaanisha ‘watu ambao, mmoja au kwa pamoja, wameumia, ikiwa ni pamoja na kuumia kimwili au kiakili, mateso ya kihisia, kupoteza uchumi au kuathiriwa pakubwa kwa haki zao za kimsingi, kupitia vitendo au ukiukaji ambavyo vinakiuka sheria za uhalifu zinazotumika katika Taifa au kutokana na vitendo ambavyo ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za haki za binadamu za kimataifa au ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa sheria ya kibinadamu’.6 Sambamba na sheria za kimataifa, ufafanuzi wa mwathiriwa uliotumiwa katika Itifaki haujumuishi tu watu walio katika kaburi la halaiki (‘msingi’ Au waathiriwa wa ‘moja kwa moja’), lakini pia familia zao na, pale inapofaa, jamii (‘ wa pili’ au

‘wahanga’ wasio wa moja kwa moja). Kwa ajili ya uwazi,

Itifaki hii pia inarejelea ‘familia’, ‘wanafamilia’ na ‘jamii zilizoathiriwa’ ambapo sheria fulani zinawahusu.7

2 Hii inaweza kujumuisha mipango ya uchunguzi wa kiraia ambapo inakuwa chini ya udhamini wa shirika lililoidhinishwa la utaalamu wa asasi ya kiraia.

Mipango ya kisiasa pia inaweza ‘kuhalalisha’ manusura ambao wanaweza kushiriki katika mchakato wa uchunguzi na ufukuaji wa maiti na ambao huenda si wataalamu lakini wanatekeleza ufukuaji. Kwa majadiliano zaidi, angalia Maoni ya Kielimu yaliyoambatishwa. 3 Mfano, majanga, ikiwa ni pamoja na majanga yanayotokana na wanadamu na vifo vinavyotokana na utekelezaji wa mipaka au usafirishaji haramu. 4 Maelezo kuhusu mbinu ya sampuli ya ushiriki wa wataalam inaweza kupatikana katika Maoni ya Kielimu. 5 Imechukuliwa kutoka kwa Muungano wa Mabunge na ICRC (2009), Watu Waliopotea -Mwongozo wa Wabunge katika ukurasa wa 9 na kulingana na jukumu la

Tume ya Kimataifa ya Watu Waliopotea. Kama ilivyo kwa makaburi ya halaiki, hakuna fasili moja ya watu waliopotea. Ufafanuzi uliopendekezwa hapa ni finyu katika dhana kuliko ile inayopatikana katika Azimio la Baraza la Usalama la UN la 2019 kuhusu Watu Waliopotea kutokana na Vita vya Silaha, ambayo inaunga mkono ufafanuzi wa UNHCR wa 2010 wa watu ‘wasiowajibikiwa kutokana na vita vya silaha vya kimataifa au visivyo vya kimataifa’ tu (aya ya 9). Wakati huo huo ufafanuzi hapa haujumuishi kwa uwazi wahamiaji waliopotea, mada ambayo haiwezi kuangaziwa kikamilifu na Itifaki. 6 Huu ni ufafanuzi uliojumuishwa kutoka Azimio la Umoja wa Mataifa la Kanuni za Msingi za Haki kwa Waathiriwa wa Uhalifu na Matumizi Mabaya ya Mamlaka, kwenye Kiambatisho cha A, 1, na Kanuni za Msingi za UN na Miongozo juu ya Haki ya Suluhisho na Malipo kwa Waathiriwa wa Ukiukaji Mkubwa wa Sheria ya

Kimataifa ya Haki za Binadamu na Ukiukaji Mkubwa wa Sheria ya Kimataifa ya Kibinadamu, Kiambatisho cha V, 8, na inaunga mkono kifungu cha 24(1) cha

Mkataba wa Kimataifa wa Ulinzi wa Watu Wote kutokana na Upoteaji Unaotokana na Mamlaka. 7 Ambapo kuna rejeleo dhahiri kwa ‘familia’, ‘wanafamilia’ au ‘jamii zilizoathiriwa’, hii haikusudiwi kwa njia yoyote kuashiria kwamba wao pia sio waathiriwa.

Aidha, inatambuliwa kuwa familia binafsi na wanajamii wanaweza kuwa waatjiriwa wa moja kwa moja wa madhara mengine yaliyosababishwa katika muktadha mpana wa ukiukaji unaochunguzwa, ambapo makaburi ya halaiki ni sehemu yake.

• Neno familia, ambalo halina ufafanuzi katika sheria ya kimataifa, limetumika hapa kama dhana inayohusiana na mazoea ya jamii katika muktadha mahususi.8

Kwa madhumuni ya Itifaki hii, ushirika wa familia ni muhimu kwa kubaini, kwa mfano, jamaa wa karibu9 , mpokeaji anayefaa ya mabaki ya mauti na utoaji wa hati za hali ya kisheria kwa heshima ya mtu aliyepotea.

Ushirika wa familia unapaswa kubainishwa kulingana na sheria za eneo, mila na/au mazoea. • Uchunguzi wa kisheria (sawa na maana yake halisi

‘katika korti wazi’ au ‘umma’) inamaanisha eneo la kisayansi, kisheria na kijamii kwa kuleta maswala katika na mbele ya korti za kisheria na/au njia zingine za kimahakama (kama vile afisa mchunguzi wa vifo).

Muundo wa Itifaki

Hati inajumuisha michakato mbalimbali ya mpangilio inayotumika kwa ulinzi na uchunguzi wa kaburi la halaiki wakati huo huo ikifuata mbinu ya kawaida, kwa hivyo yaliyomo kwenye Itifaki yana msingi wazi katika sheria na kanuni za kisheria za kimataifa. Kila sehemu kwa hivyo itaanza na kisanduku cha bluu kikielezea sheria za msingi zaa kanuni kutoka kwa sheria ya kimataifa10 (kanuni za kimataifa) na hivyo kutoa mantiki ya kisheria kwa yaliyomo yaliyopendekezwa ya Itifaki.

Msingi wa kisheria

Sehemu ya kuanza kwa Itifaki kwa ujumla ni wajibu wa Mataifa kutafuta na kuchunguza. Wakati tukikubali kwamba makaburi ya halaiki yanaweza kuwa katika mazingira yenye vifaa finyu au yasiyo na upatikanaji wa mbinu, mahakama iliyolemewa, ukosefu wa usalama na idadi kubwa ya mahitaji tofauti, ya wakati mmoja, kuna mahitaji wazi ya sheria ya ndani na uanzishwaji wa taasisi mahususi. Sheria na taasisi kama hizo zinachukuliwa kama sharti la jibu madhubuti kwa visa vyote vya watu waliopotea.

Kanuni za kimataifa Wajibu wa kutafuta na kuchunguza

Chini ya sheria za haki za binadamu, Mataifa yana wajibu wa kutafuta na kuchunguza wakati haki ya mtu binafsi, na ulinzi wake, umekiukwa. Haki ya kuishi na marufuku ya mateso au matendo mengine ya kikatili, yasiyo ya kibinadamu au ya kudhalilisha ni pamoja na utaratibu unaohitaji uchunguzi madhubuti (ICCPR11, Kifungu cha 6 na 7). Chini ya sheria za kieneo za haki za binadamu, uchunguzi lazima uwe wa haraka, huru, kamili, bila upendeleo na wenye uwazi. Matokeo yake lazima yawe na msingi ‘kulingana na uchambuzi wa kina, madhubuti na usio na upendeleo wa mambo yote muhimu.’12 Kifungu cha 24(3) cha Mkataba wa Kimataifa wa Kulinda Watu Wote kutokana na Upoteaji Unaotokana na Mamlaka (CED13) kinahitaji Washirika wa Taifa ‘kuchukua hatua zote zinazofaa ili kutafuta, kupata na kuwaachilia watu waliopotea na, katika tukio la kifo, kupata, kuheshimu na kurudisha mabaki yao’. Ni wajibu unaoendelea hadi hatima na/ au mahali walipo wale waliopotea pamegunduliwa (Kanuni za Kuongoza za CED14, Kanuni ya 7). Kwa ujumla, jukumu la kufanya uchunguzi madhubuti ni wajibu wa njia na sio wa matokeo.15 Sheria ya kimataifa ya kibinadamu inahitaji kutafutwa kwa wafu (kwa mfano, GC I, Kifungu cha 15; GC II, Ibara ya 18 na 21; GC IV, Kifungu cha 16; Itifaki ya Ziada ya I, Kifungu cha 17(2)) na waliopotea (Itifaki ya Ziada ya I, Kifungu cha 33 (2))16. Sheria ya kitamaduni ya kibinadamu ya kimataifa inapendekeza kila mshirika kwenye mgogoro, uwe wa kimataifa au wa ndani, ana wajibu wa ‘kuchukua hatua zote zinazowezekana kuwajibika kwa watu walioripotiwa kupotea kutokana na vita vya silaha’ (Kanuni za CIHL17 2006, Kanuni ya 117).

Kanuni za kimataifa: Sheria ya Watu Waliopotea na Mamlaka mahususi ya Watu Waliopotea

CED inahitaji mamlaka husika kuwa na rekodi na sajili rasmi za watu wote walionyimwa uhuru wao (Kifungu cha 17 (3)). Usimamizi wa sajili na hifadhidata unapaswa kuheshimu faragha ya wahasiriwa na usiri wa maelezo (Kanuni ya Kuongoza ya CED, 11(8)).

8 Sheria ya Mfano ya ICRC kuhusu Waliopotea hutumia neno ‘jamaa wa watu waliopotea’ kwa kurejelea, na kwa mujibu wa, masharti ya sheria ya ndani inayotumika (Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) (2009), Kanuni za Kuongoza/Sheria ya Mfano kuhusu Waliopotea, Kifungu cha 2(2)) (kwa kifupi Sheria ya Mfano ya ICRC kuhusu Waliopotea). 9 Ikiwa ni pamoja na uhusiano wa kijeni na jamaa wa karibu (Pueblo Bello Massacre Colombia, Hukumu kuhusu Ustahiki, Malipo na Gharama, Mahakama ya

Kimarekani ya Haki za Binadamu Mfululizo wa C Nambari 140 (31 Januari 2006) aya ya 273 na 274. 10 Orodha ya masharti ya kawaida inaweza kuwa ya kuonyesha tu. 11 Mkataba wa Kimataifa kuhusu Haki za Kiraia na Kisiasa (uliopitishwa 19 Disemba 1966, ulianza kutumika tarehe 23 Machi 1976) 999 UNTS 171 (kwa kifupi

ICCPR). Angalia pia Kamati ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa (HRC), Maoni ya jumla nambari 36, Kifungu cha 6 (Haki ya Kuishi) CCPR/C/GC/35 (3 Septemba 2019) aya ya 58. 12 Kukhalashvili and others v Georgia, Hukumu, Maombi ya ECtHR nambari 8938/07 na 41891/07 (2 Mei 2020) aya 130. 13 Mkataba wa Kimataifa wa Ulinzi wa Watu Wote Kutoka kwa Upoteai Unaotokana na Mamlaka (uliopitishwa 12 Januari 2007 ulianza kutumika 23 Disemba 2010) Hati ya UN ya A/RES/61/177 (20 Disemba 2006) (kwa kifupi CED). 14 Kamati ya Umoja wa Mataifa kuhusu Upoteaji Unaotokana na Mamlaka, Kanuni za Kuongoza katika kutafuta watu waliopotea (8 Mei 2019) Hati ya UN ya

CED/C/7, Kanuni ya 7 (baadaye hapa ni Kanuni za Kuongoza za CED). 15 Da Silva v United Kingdom, Hukumu ya Baraza Kuu, Maombi ya ECtHR Nambari 5878/08 (30 Machi 2016) vifungu vya 231-238, inatoa muhtasari kamili wa

Baraza Kuu wa mahitaji ya uchunguzi madhubuti. 16 Mkutano wa Geneva (I) kwa Uboreshaji wa Hali ya Waliojeruhiwa na Wagonjwa katika Vikosi vya Wanajeshi Vitani (iliyopitishwa 12 Agosti 1949) 75 UNTS 31 (kwa kifupi GC I); Mkutano wa Geneva (II) wa Uboreshaji wa Hali ya Wanajeshi Waliojeruhiwa, Wagonjwa na Wahasiriwa wa Jeshi wa Meli Zilizovunjika

Baharini (iliyopitishwa 12 Agosti 1949) 75 UNTS 85 (kwa kifupi GC II); Mkutano wa Geneva (IV) unaohusiana na Ulinzi wa Wananchi katika Wakati wa Vita (iliyopitishwa 12 Agosti 1949) 75 UNTS 288 (kwa kifupi GC IV); na Itifaki ya Ziada ya Mikataba ya Geneva ya tarehe 12 Agosti 1949, na Kuhusiana na Ulinzi wa

Wahasiriwa wa Migogoro Vita vya Silaha ya Kimataifa (Itifaki I) (iliyopitishwa tarehe 8 Juni 1977, ilianza kutumika tarehe 7 Disemba 1979) 1125 UNTS 17512 (kwa kifupi Itifaki ya Ziada). 17 Henckaerts J-M. na Doswald-Beck L., (2006) Sheria ya Kimila ya Kibinadamu ya Kimataifa,Toleo la 1: Kanuni (kwa kifupi Kanuni za CIHL).

This article is from: