4 minute read

G. Ukumbusho

Next Article
D. Utambuzi

D. Utambuzi

(1) Utoaji wa maelezo: Kujua kile kilichotokea kupitia michakato ya uchunguzi ni sharti la utambuzi wa mahitaji ya haki. Uchunguzi kaburi la halaiki na ufukuaji wa maiti, kupitia maelezo wanayofichua, unaweza kuchangia kufanikiwa kwa ukweli na kuwa utangulizi wa malengo ya haki katika viwango kadhaa. Hasa, matokeo ya uchunguzi wa kaburi la halaiki na kumbukumbu zinaweza kusaidia katika kutoa: • Maelezo kuhusu matukio yaliyosababisha unyanyasaji wa haki za binadamu; • Kurudishwa kwa mabaki ya binadamu kwa madhumuni ya ukumbusho, na kutolewa kwa hati ya kifo (au hati inayolingana) ili kulinda hali ya kiuchumi wa familia, ikiwa ni pamoja na elimu na mahitaji ya kiafya; • Kutambuliwa kwa mwathiriwa na vile vile manusura; na • Kutambuliwa kwa wahusika. (2) Suluhisho: Kutoka kwa maelezo haya, haki zingine, haki za kufidiwa na madai ya kisheria yanaweza kufikiwa kwa: • Kuwezesha fidia, ikiwa ni pamoja na utambuzi rasmi, fidia, kuridhika na ukumbusho; • Kuwasilisha maombi chini ya masharti ya haki za binadamu ya ndani, kikanda na/au kimataifa; na • Kuwezesha mashtaka ya jinai. (3) Katazo na adhabu au uhamishaji: Uchunguzi wa kaburi la halaiki na uchunguzi wa uhalifu unaolenga uwajibikaji wa wahusika unapaswa kuimarishwa, na njia wazi za mawasiliano na waendesha mashtaka/mamlaka za mahakama ni muhimu. Thamani fulani ya uchunguzi wa kaburi la halaiki kwa michakato ya kimahakama inaweza kujumuisha: • Uthibitisho wa kumbukumbu ya mashahidi; • Idadi ya vifo; • Sababu, njia na tarehe/wakati wa kifo; • Jinsia, umri na kabila la waathiriwa; • Utambulisho wa waathiriwa; • Jaribio za kuficha uhalifu kwa kuhamisha miili kutoka makaburi ya msingi hadi ya makaburi ya pili; na • Muunganisho dhahiri na wahusika.74 Kukamilika kwa uchunguzi wowote wa kimahakama na mchakato wa mashtaka haipaswi kuathiri vibaya mwendelezo wa uchunguzi wa kaburi la halaiki na juhudi za ulinzi. (4) Kwa juhudi za Taifa zinazolenga haki na uwajibikaji,

kuripoti kwa uhuru na mamlaka kuhusiana na matokeo

ya uchunguzi, kama sehemu muhimu ya mchakato wa uchunguzi, inaweza kuchangia kutimiza haki ya mwathiriwa ya kujua nini kilitokea, kumbukumbu ya pamoja na usaidizi kwa Sheria. Matokeo ya uchunguzi wa kaburi la halaiki kwa hivyo yanapaswa kuripotiwa hadharani, isipokuwa kufanya hivyo itaathiri au kuhatarisha mashtaka ya jinai yanayoendelea au ya baadaye.

G. Ukumbusho

Kanuni za kimataifa

Haki ya kuzika wanafamilia kwa ujumla inaangaziwa kupitia ulinzi wa maisha ya kibinafsi na ya familia.75 Njia ya kuzika wafu inaweza kuunda jambo muhimu la mazoea ya kidini yanayolindwa chini ya uhuru wa mawazo, dhamiri na sheria za dini.76 Aidha, kuunda kumbukumbu kuhusu marehemu inaweza kuunda sehemu a dhamana ya juhudi za kutorudia.77 Kanuni za Orentlicher zinahitaji kwamba Taifa zihifadhi kumbukumbu ya pamoja ya matukio (Kanuni za Orentlicher, Kanuni ya 3).78 Kanuni ya 115 ya CIHL inasema kwamba ‘wafu lazima wazikwe kwa njia ya heshima na makaburi yao yaheshimiwe na kuhifadhiwa vizuri’.

Makaburi ya halaiki yanaweza kuwa matata, yenye changamoto na/au ya kutatanisha katika mazingira ya kijamii, kisiasa na kijiografia. Wakati wa kuchunguzwa na kuchimbwa, makaburi yote ya zamani ya halaiki na sehemu mpya za mazishi na ukumbusho zinaweza kuwa maeneo ya ukumbusho binafsi na/au pamoja; maonyesho ya mazoea ya kitamaduni, dini na siasa; na kuunda sehemu ya fidia. Kwa hivyo makaburi mengi yanaweza kuwa vyanzo vya: • Kuendeleza kumbukumbu ya kihistoria; • Kuchangia kwenye mazungumzo ya kitaifa kuhusu matukio ya zamani; • Mifumo ya usaidizi wa kisaikolojia na kijamii; • Kuathiri sera za baadaye; na/au • Kuwezesha hali ya msingi ya jamii yenye haki. Makaburi ya halaiki yaliyochimbiwa yanaweza kuhitaji utambuzi na ulinzi wa kisheria kama maeneo ya ukumbusho. Maeneo ya makaburi ya halaiki ambayo hayawezi kuchunguzwa pia yanaweza kuwa mahali pa ukumbusho na yanapaswa kutambuliwa kisheria na kulindwa kwa kiwango kinachowezekana ili kuhakikisha uadilifu wa ushahidi ikiwa kuna uwezekano wa uchunguzi utakaokea baadaye.

74 Kama ilivyotolewa kutoka kwa uzoefu wa ICTY na kesi kama vile Prosecutor v Mladić, Hukumu, IT-09-02-T-117281 (22 Novemba 2017) na Prosecutor v Karadžić,

Toleo la Hukumu la Umma lililohaririwa na kutolewa mnamo 25 Machi 2016, IT-95-5 / 18-T (25 Machi 2016). 75 Kama ilivyoonyeshwa, kwa mfano, katika Sabanchiyeva and others v Russia, Hukumu, Maombi ya ECtHR Nambari 38450/05 (6 Juni 2013) 76 Johannische Kirche & Peters v Germany, Uamuzi, Maombi ya ECtHR No 41754/98 (10 Julai 2001). 77 Kwa mfano, ‘Las Dos Erres’ Massacre v Guatemala, Hukumu ya Mapingamizi ya Awali, Ustahiki, Malipo na Gharama, IACtHR Mfululizo wa C Nambari 211 (24 Novemba 2009), aya ya 265 na Pueblo Bello Massacre v Colombia, Hukumu kuhusu Ustahiki, Malipo na Gharama, Mahakama ya Kimarekani ya Haki za

Binadamu Mfululizo wa C Nambari 140 (31 Januari 2006) aya ya 278. 78 Uzingatiaji wa uhuru wa haki za kujieleza unaweza kutokea katika muktadha wa ukumbusho kama huo au maeneo ya mauaji kama ilivyoonyeshwa katika

Faber v Hungary, Hukumu, Maombi ya ECtHR Nambari 40721/08 (24 Julai 2012) ambapo Mahakama inakubali ‘kwamba onyesho la ishara isiyo wazi katika maeneo mahususi ya mauaji ya halaiki yanaweza katika hali fulani kuelezea utambulisho na wahusika wa uhalifu huo; ni kwa sababu hii kwamba hata ujielezaji uliolindwa vinginevyo hauruhusiwi sawa katika sehemu zote na nyakati zote’ (katika aya ya 58).

This article is from: