![](https://static.isu.pub/fe/default-story-images/news.jpg?width=720&quality=85%2C50)
2 minute read
Kiambatisho cha 2
Utaalamu unaofaa wa uchunguzi na uchunguzi wa kisheria unaweza kujumuisha wahusika au taaluma zifuatazo za wataalam:
Msimamizi wa vifo vya halaiki anachukua jukumu la jumla kwa usimamizi wa uendeshaji shughuli katika makaburi ya halaiki ikiwa ni pamoja na, lakini sio tu, kuzingatia makubaliano ya mamlaka na Taratibu za Kawaida za Uendeshaji; kudumisha ushirikiano na jamii, afya, usalama na ustawi kwenye eneo; utekelezaji wa miundo ya kuripoti na mkakati wa mawasiliano; na uratibu wa utambulisho na mchakato wa urejeshwaji wa mabaki ya binadamu.
Wachunguzi wa eneo la uhalifu/maafisa wakuu
wa eneo ni watu waliofunzwa kutambua, kuweka kumbukumbu, kukusanya na kuhifadhi ushahidi halisi kwa uchambuzi zaidi wakati huo huo wakidumisha mfululizo wa kumbukumbu. Wataalamu wa data dijitali ili kuchunguza na kutoa ushahidi na data kutoka kwa simu za mkononi, kadi za hifadhi, kompyuta au mitandao ya jamii. Anthropolojia ya uchunguzi wa kisheria inahusika na urejeswahji na uchunguzi wa mabaki ya binadamu (ikiwa ni pamoja na yanayooza, mifupa, yaliyotengenishwa au kuchomeka) ili kujibu maswali ya sheria na kimatibabu, ikiwa ni pamoja na yale ya utambulisho. Akiolojia ya uchunguzi wa kisheria inaashiria utumiaji wa njia zilizotumika katika utafutaji wa mabaki ya zamani na vitu kwa madhumuni ya kisheria, ili kurekodi, kuchimba, kurejesha, kujenga upya na kutathmini eneo la uhalifu.
Uchunguzi wa kisheria wa makombora/Wataalamu wa silaha na alama baada ya kutumia zana
wanahusika katika uchunguzi wa alama zilizoachwa kwenye maonyesho na kulinganisha hizi pamoja na vifaa/zana/silaha zinazowekana kusababisha, na kutoa hitimisho la thamani ya uchunguzi wa kisheria kuhusiana na majeraha ya risasi na roketi zilizopatikana kutoka kwao. Entomolojia ya uchunguzi wa kisheria ni uchunguzi wa wadudu katika mazingira ya uchunguzi wa kisheria, mara nyingi kama sehemu ya patholojia ya uchunguzi wa kisheria, kama kiashiria cha wakati mdogo zaidi tangu kifo. Odontolojia ya uchunguzi wa kisheria ni uchunguzi wa meno kuhusiana na sheria, haswa katika uchunguzi wa kifo, haswa kwa utambulisho wa mabaki ya binadamu. Dawa za uchunguzi wa kisheria zinahusu kanuni na mazoea ya dawa kama zinavyotumika kwa mahitaji ya sheria na mahakama.
Mwanapatholojia wa uchunguzi wa kisheria au
daktari wa uchunguzi wa kisheria ni mtaalam aliyeidhinishwa wa matibabu ambaye ameidhinishwa kufanya uchunguzi wa kisheria wa baada ya kufa. Uchunguzi wa kisheria wa athari ya sumu ni sayansi ya dawa na sumu inayotumika kwa mahitaji ya kisheria na mahakama.
Wataalamu wa utambulisho wa wanadamu
wakiwemo wataalamu wa jeni, wataalam wa alama za vidole, wanabiolojia wa molekuli/wataalam wa uchunguzi wa kisheria wa DNA, au madaktari wa meno wa uchunguzi wa kisheria.
(Chanzo: ilitolewa kutoka Itifaki za Minnesota, ukurasa wa 30 na 53)
Kila moja ya taaluma/wataalamu hawa watasimamiwa na kanuni husika na zinazofaa za za maadili. Vyeo vyao vinaweza kutofautiana.