3 minute read

E. Kurejeshwa kwa mabaki ya binadamu

Next Article
Kiambatisho cha 1

Kiambatisho cha 1

Kanuni za kimataifa

Kifungu cha 24(3) cha CED kinasisitiza wajibu wa kurudisha mabaki ya binadamu waliopotea kwa wanafamilia walio hai; na kifungu cha 15 kinachohitaji Mataifa kutoa ushirikiano na usaidizi katika juhudi zao za kutafuta na kurudishwa. Kanuni ya 2(4) ya Kanuni za Kuongoza za 2019 inabainisha kuwa ‘kurudishwa [kwa mabaki ya binadamu] kunapaswa pia kuhusisha njia na taratibu zinazohitajika kuhakikisha mazishi yenye heshima yanayolingana na matakwa na mila ya kitamaduni ya familia na jamii zao.’ Hili linaweza kujumuisha kugharamia ada za uhamishaji kati ya mipaka wa mabaki ya binadamu. Maarifa ya sheria kutoka kwa Mahakama ya Kimarekani ya Haki za Binadamu inasema: ‘Wakati mabaki ya mwili yanapatikana na kutambuliwa, Taifa lazima iyarudishe kwa jamaa zake haraka iwezekanavyo, baada ya kudhibitisha uhusiano wa jeni, ili aweze kuheshimiwa kulingana na kanuni zake. Taifa pia inapaswa kulipia gharama za mazishi, kwa makubaliano na jamaa wa karibu.’64 Kutorejeshwa kwa mabaki ya binadamu na mazishi katika maeneo ambayo hayajabainishwa kutakuwa ukiukaji wa haki ya familia na maisha ya kibinafsi; uingiliaji ambao unaruhusiwa tu panapokubaliwa na sheria, ni kutafuta lengo halali (kama vile usalama wa umma, kuzuia machafuko au haki na uhuru wa wengine) na kunahitajika katika jamii ya kidemokrasia.65 Katika sheria ya kimataifa ya kibinadamu, ‘kurudishwa kwa mabaki ya binadamu kwa ombi na mshirika au ndugu wa karibu, kama ishara ya kuheshimu maisha ya familia na kuhusiana na haki za mwathiriwa, inatumika wakati wa vita vya kimataifa na visivyo vya kimataifa’ (CIHL, Kanuni ya 114). Sheria ya Mfano ya ICRC kuhusu Kifungu cha 21(4) cha Waliopotea inasema kwamba ‘[m]abaki ya binadamu na vifaa vya kibinafsi zitarejeshwa kwa familia’.

Baada ya kukamilisha michakato ya uchunguzi, utambulisho na haki, mabaki ya binadamu, sehemu husika za mwili na vifaa vya kibinafsi zinapaswa kurudishwa kwa wanafamilia, na kuwaruhusu kuzika marehemu kulingana na imani zao.

Ambapo utambulisho na kurudishwa kwa mabaki ya binadamu kunawezekana:

• Baada ya uchunguzi wa baada ya kufa, mabaki yanapaswa kutolewa kwa familia mapema iwezekanavyo. • Mchakato wa kurudisha mabaki ya binadamu unapaswa kutekelezwa na kufuatwa. Inapaswa kujumuisha mkakati unaofaa wa mawasiliano, na, inapowezekana, pendekezo la, au rufaa, rasilimali kwa usaidizi kwa familia na jamii zilizofiwa.

Ambapo mwili umetambuliwa lakini haujadaiwa na mwanafamilia:

• Mabaki ya binadamu na rekodi zote husika zinaweza kuhifadhiwa/kudumishwa; AU • Mabaki ya binadamu yanaweza kuzikwa katika makaburi yaliyotiwa alama kulingana na mila ya kitamaduni au mila mwafaka za kidini za marehemu na rekodi husika zinaweza kuhifadhiwa. Kwa chaguo lolote linalopendelewa, mipango inapaswa kujumuisha utoaji wa uhifadhi unaoweza ufuatiliaji, wa muda mrefu au uzikaji wa maiti. Mipango inapaswa kufaa utamaduni, na uzingatiaji inapaswa kutolewa kwa mahali mpya pa kuzikwa kama eneo lenye umuhimu na ukumbusho kwa familia na jamii. Hali za ziada zitajumuisha maswala ya umiliki wa ardhi, hali iliyopo ya udongo na urefu wa meza ya maji ya chini ya ardhi katika eneo lililokusudiwa. Kama ilivyo kwa miili ambayo haijatambuliwa (angalia hapo juu, kifungu cha D kuhusu utambulisho), na kuwezesha urekebishaji wa utambulisho wa kimakosa na kurudishwa kwa kimakosa kwa mabaki ya binadamu, ufuatiliaji unapaswa kuhakikishwa kupitia mbinu kama vile: • Uwekaji wa kumbukumbu na kuambatisha eneo, ikiwa ni pamoja na kuambatisha eneo la miili ya kibinafsi ndani ya eneo; • Kuweka nambari na alama kwa kila mwili na mfuko/ jeneza kwa kurejelea nambari ya sampuli ya DNA na uhifadhi; • Matumizi ya ishara kuweka alama kwenye eneo; na • Uhifadhi salama wa maelezo ili kuhakikisha usalama wake. Kutekekeza maiti kunapaswa kuepukwa.

Viungo husika vya mwili na ushahidi

Njia zinazofaa kitamaduni za kushughulikia vifaa binafsi ambavyo havijadaiwa na sehemu za mwili ambazo hazijatambuliwa au hazijadaiwa zinapaswa kukubaliwa na jamii zilizoathiriwa.66 Hii inaweza kujumuisha ukumbusho, maonyesho nyeti, mazishi, maeneo maalum ya ukumbusho au mahali pa uhifadhi wa mifupa ya wafu.

64 Pueblo Bello Massacre Colombia, Hukumu kuhusu Ustahiki, Malipo na Gharama, Mahakama ya Kimarekani ya Haki za Binadamu Mfululizo wa C Nambari 140 (31 Januari 2006) aya ya 273. 65 Sabanchiyeva and others v Russia, Hukumu, Maombi ya ECtHR Nambari 38450/05 (6 Juni 2013) aya za 117-134. 66 Mwongozo wa Utambulisho wa Waathiriwa wa Maafa ya Majanga wa Interpol, Kiambatisho cha 17: Jukumu na Wajibu wa Mwanaanthropolojia wa DVI unapendekeza ‘ukaguzi wa mwisho wa uchunguzi wa kisheria wa anthropolojia na kukagua mabaki ya mwili katika matukio yaliyo na mabaki yaliyogawanyika na/au yaliyobadilishwa. Kabla ya kutolewa kwa mabaki kwa ndugu wa karibu, ukaguzi wa mwisho ya anthropolojia unaongeza safu ya ziada ya uhakikisho wa ubora na udhibiti ambao unadumisha kiwango cha juu cha uaminifu na familia za waathiriwa’ (katika ukurasa wa 3).

This article is from: