Adhan ni ndoto au ni wahyi

Page 1

Adhana ni Ndoto au ni Wahyi? ‫هل األذان رؤية أو وحي؟‬

Kimeandikwa na: Abdul-Karim Juma Nkusui



‫هل األذان رأية أو وحي ؟‬

‫التأليف‪:‬‬ ‫الشيخ عبدالكريم جمعة‬


©Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION

ISBN: 978 – 9987 – 17 – 072 – 2

Mtungaji: Sheikh Abdul-Karim Juma Nkusui

Kimehaririwa na: Ustadh Abdalla Mohamed Na Al-Hajj Ramadhani S. K. Shemahimbo

Kimepitiwa na: Mbarak Ali Tila

Kimepangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation

Toleo la kwanza: Agosti, 2014 Nakala: 1000

Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. - 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: www.alitrah.info


Yaliyomo Neno la Mchapishaji........................................................................1 Utangulizi.........................................................................................4 Maana ya Adhana.............................................................................7 Matamko ya Adhana........................................................................7 Kufuatiliza Adhana........................................................................10 Mwanzo wa Adhana....................................................................... 11 Uchambuzi wa Riwaya za Adhana................................................13 Shahada ........................................................................................21 Ushahidi wa Hadithi......................................................................23 Muamala wa Ahlus Sunnah Katika Adhana...................................28 Hayya A’laa Khayril A’mal............................................................30 Sababu za Kuondoa Ibara Hii........................................................41 Maangamio kwa Wenye Kubadilisha............................................42 v



Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

‫بسم اهلل الرحمن الرحيم‬

NENO LA MCHAPISHAJI

K

itabu ulichonacho mikononi mwako, Adhana ni Ndoto au Wahyi? asili yake ni kimeandikwa kwa Kiswahili na Sheikh Abdul-Karim Juma Nkusui. Katika mambo ambayo Waislamu wa madhehebu mbalimbali wamehitalifiana ni kuhusu suala adhana iwapo imekuja kwa ndoto au wahyi. Kama ilivyo kawaida, suala hili limeleta mabishano na mijadala mikubwa miongoni mwa wanachuoni na waumini. Mwandishi wa kitabu hiki amefanya juhudi kubwa kuthibitisha kutoka kwenye vyanzo mbalimbali na tafiti za kielimu na kuweka bayana ukweli wa suala hili. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni vitu ambavyo havina nafasi tena katika akili za watu. Kutoka na ukweli huu, taasisi yetu ya Al-Itrah imeamua k­ ukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumini yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili.

1


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

Tunamshukuru ndugu yetu mwandishi wa kitabu hiki, Sheikh Abdul-Karim Juma Nkusui kwa kazi kubwa aliyoifanya. Vilevile wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Allah awalipe wote malipo mema hapa duniani na kesho Akhera – Amin. Mchapishaji Al-Itrah Foundation

2


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

‫بسم اهلل الرحمن الرحيم‬ Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

َّ‫َو َم ْن أَ ْح َس ُن َق ْو اًل ِم َّم ْن َد َعا إلَى ه‬ ‫صالِ ًحا‬ َ ‫اللِ َو َع ِم َل‬ ِ َ ‫َو َق‬ َ ‫ال إِنَّ ِني ِم َن ْال ُم ْسلِ ِم‬ ‫ين‬ “Ni nani asemaye kauli bora zaidi kuliko anayeita kwa Mwenyezi Mungu…” (Fuswilat: 33)

“Hakika Adhana na Iqamah ni Sunnah mbili kwa ajili ya Swala tano na Swala ya Ijumaa” (Kauli ya Maimamu wane: Abu Hanifa, Malik, Shafi na Hanbali) 1

“Adhana na Iqamah ni Sunnahh mbili katika Swala tano za faradhi adaa na kadha, kwa mtu mmoja na kwa jamaa…”2

1 2

– Asha’araniy J: 1 uk: 125 – Al-Muhaqiqul – Hilly uk: 30 3


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

‫بسم اهلل الرحمن الرحيم‬ UTANGULIZI

A

dhana na Iqamah ni Sunnah muhimu sana katika Uislamu, Sunnah hizi mbili zimebeba ujumbe wa kuwafahamisha wanadamu nafasi ya Muumba wao katika nyanja zote za maisha ya kila siku hapa duniani na kesho akhera. Pia zinaeleza wazi wazi jukumu na nafasi ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kwa wanaadamu na wajibu wao kwake na kwa kizazi chake kitukufu (a.s.). Ibara za mwito huu mtukufu wa mbinguni zinawalingania viumbe na waja wa Mwenyezi Mungu katika kutimiza na kutekeleza wajibu wao kwa Mola wao, ili hali zikieleza wazi kwa ibara fupi na zenye kueleweka kwamba Swala ni amali bora mno miongoni mwa ibada na amali zingine anazozifanya mwanadamu. Mwito huu unamlingania mwanadamu kwenye kheri na kufaulu ambako hakuna kifani, kwani mtu anapoikosa kheri hii basi yote atakayoyafanya katika maisha yake yote hayatakuwa na thamani mbele ya Mwenyezi Mungu, kwani jambo la mwanzo kutazamwa na Mwenyezi Mungu katika amali za mja ni Swala yake. Kama itakubaliwa basi na amali zingine zitakubaliwa, na ikikataliwa basi na amali zingine pia zitakataliwa. Ndio maana tunakuta Hadithi za Mtume (s.a.w.w.) zinatueleza kuwa: “Swala ni nguzo ya dini, mwenye kuisimamisha swala amesimamisha dini, na mwenye kuiacha amevunja dini.” Kisha mwito huu mtukufu unamalizia kwa kumkumbusha na kumsisitiza mwanadamu nafasi ya Mola na umuhimu wake katika maisha yake ya kila siku ya kwamba Mwenyezi Mungu ni mkubwa kuliko kila kitu na wala hakuna Mungu isipokuwa yeye aliyetukuka. 4


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

Mwito huu unamjulisha kuwadia kwa wakati wa kumhimidi Mwenyezi Mungu na kabla ya kusimama na kutekeleza kile alichoitiwa hukumbushwa mwito huu kwa mara nyingine ambapo sasa mja hujiweka tayari kimwili, kiakili na kihisia hali ya kuwa tayari kasimama mbele ya hadhara ya Muumba Wake, hivyo huanza ibada yake hali ya kuwa fikra na mawazo yake yametawaliwa na mwito huu Mtukufu. Humwelekea Mwenyezi Mungu kwa mwili wake, akili yake na hisia zake zote huku akionyesha usikivu na unyenyekevu wa hali ya juu kabisa kwa Muumba Wake. Msomaji Mtukufu, tuwe pamoja sote katika kuifuatia Sunnah hii tukufu na mashuhuri kabisa miongoni mwa Sunnah za Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.). Safari yetu itakuwa ndani ya vitabu vya rejea vya madhehebu mbili kuu, Shia na Sunni ili tuone kwa pamoja vinaeleza nini kuhusu Sunnah hii tukufu, na hatimaye mwisho wa safari tuwe tumefikia natija muafaka inayokubaliana na Sunnah ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), kwani ni kwa njia hii tu ndio tunaweza kujua ukweli na hapo ndipo chuya itajitenga mbali na mchele safi. Yamezungumzwa mengi kuhusu Sunnah hii. Kuna wanaoinasibisha Sunnah hii na ndoto kwamba mmoja wa masahaba wa Mtume alioteshwa usingizini. Kwa madai ya wenye rai hii ni kwamba Mtume alipowasili Madina hakuwa anajua atawakusanya vipi Waislamu kwa ajili ya ibada na mengineyo, hivyo alishauriwa aweke kengele, wengine wakasema aweke tarumbeta n.k. Lakini Mtume hakuafiki hilo, na kwa uchungu wa dini aliokuwa nao mmoja wa maswahaba na kwa kumhurumia kwake sana Mtume ndipo alioteshwa adhana usingizini naye akaenda kumsimulia Mtume (s.a.w.w.) ambapo aliiafiki. Lakini tutakapokuwa katika safari yetu mambo hayakomei hapo, bali kuna na wengine waliooteshwa adhana ila hawakuwahi kum5


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

weleza Mtume hadi Abdullah bin Zaid alipomweleza Mtume. Mambo yanaendelea na kwenda mbali zaidi ya ndoto, wakati mwingine wanasema kuwa walimuona malaika na wakamsikia, lakini kubwa zaidi ni pale msimulizi wa adhana hii ya ndoto aliposema: “Kama si watu ningesema nilikuwa macho kabisa na wala sikuwa usingizini.” Ninaamini kabisa kuwa watu wengi wametosheka na kuwasikia masheikh tu katika suala hili bila ya wao kulifanyia uchunguzi, hivyo wakaamini pasi na shaka kuwa asili ya adhana ni ndoto ya mmoja wa masahaba. Lakini pia kuna watu ambao pengine hawajui chochote kuhusiana na suala zima la adhana, ama kwa kutokujali na ama kutokana na uhaba wa vitabu. Kijitabu hiki kinakuletea muhtsari wa uchambuzi wa kina uliofanywa na wanachuoni mbalimbali kuhusiana na maudhui haya ili ukupe mwanga na elimu juu ya suala hili. Sasa msomaji mtukufu kwa shauku kubwa ya kufahamu Adhana ni ndoto au ni wahyi, na kama ni wahyi ulishuka kwa Mtume au kwa swahaba? Ili ukate kiu ya kutaka kujua ukweli huu basi nakuomba tuwe sambamba ili tulibaini jambo hili kupitia vitabu vya madhehebu hizi mbili. Abdul-Karim J. Nkusui S.L.P. – 970, Singida. Tanzania. Barua pepe: abdulkarimjuma@yahoo.com

6


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

‫بسم اهلل الرحمن الرحيم‬ MAANA YA ADHANA

A

dhana - katika lugha, Qur’ani na Sunnah ni tangazo.

َ ُ‫َوأَ ِّذ ْن ِفي النَّاس ب ْال َح ِّج َي ْأت‬ َ ‫وك ِر َج اًال َو َعلَى ُك ِّل‬ ‫ضا ِم ٍر‬ ِ ِ ْ ‫َي‬ ِّ ‫ين ِم ْن ُك‬ َ َ ‫يق‬ ‫م‬ ‫ع‬ ‫ج‬ ‫ف‬ ‫ل‬ ‫ت‬ ‫أ‬ ٍّ َ ِ ِ ٍ “Watangazie watu Hija” (Suratul Haj: 27). Yaani wafahamishe wajibu wa kuhiji na waelimishe wajibu wa Hija.

“Akatangaza mtangazaji baina yao…” (Suratul A’araf: 44). Yaani alitangaza na kunadi mtangazaji baina yao. Na vivyo hivyo katika matumizi mengine. Hivyo adhana katika sharia ni tangazo la kujulisha kuingia kwa wakati wa Swala.

MATAMSHI YA ADHANA Allahu Akbar x 4 Ash’ hadu an laa ilaha illa llah x 2 Ash’ hadu anna Muhammadan Rasulullah x 2 Ash’ hadu anna A’liyyan waliyyullah x 2 3 Hayya a’laas- swalah x2 3

atika walioandika maudhui haya ni Al–Allammah As–Sayid Abdur-Razaq Al–Musawiy K Al–Muqarram, ameandika kitabu maalumu kuhusu nembo hii tukufu amekiita “Sirul– Imani” na ametaja humo majina yanayozidi sabini ya mafaqihi kati ya mafaqih wa sharia na maulamaa wa dini na wote wametoa fat’wa ya kujuzu shahada hii , kuwa kwake Sunnah au kuwa kwake wajibu. 7


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

Hayya a’laal- falah x 2 Hayya al’aa khayril – a’mali x 2 Allahu Akbar x 2 Laa ilaha illa llah x 2

4

Na katika Nailul–Autwar As–swalatu khayrum minan naumi x 2, kisha akasema: Katika AlBahar ameizua Umar, mtoto wake Ibnu Umar amesema: ‘’Hii ni bidaa.’’ Kutoka kwa Ali bin Abi Twalib amesema: “Msiongeze katika adhana yasiyokuwa adhana.’’ Kisha akasema baada ya kutaja hadithi ya Abu Mahudhurah na Bilal: “Tunasema kama ingekuwepo basi asingeipinga Ali, Ibnu Umar na Twausi...”5 Kutoka kwa Ibnu Juraiji amesema: “Ameniambia Hafsi kwamba Saad ni mtu wa kwanza kusema: “As–Swalatu khayrum minan naumi” katika zama ya ukhalifa wa Umar, akasema hii ni bidaa, na bora wangeiacha, Bilal hakuadhini kwa Umar.’’ Ameipokea AbdurRazak.6 Kutoka kwa Ibnu Umar ni kwamba, Umar alimwambia mwadhini wake ukifika (hayya a’laal-falah) wakati wa asubuhi sema: “As-Swalatu khayrum minan naumi.” Amepokea Daru-Qutniy, Ibnu Majah na Baihaqiy, na katika Muwatwa cha Malik ni kwamba mwadhini alimwendea Umar ili aadhini kwa ajili ya swala ya asubuhi akamkuta amelala akasema: “As-swalatu khairu mina naumi” Al–Istibswar Jz: 1, uk. 153 Nailul-Autwar Jz: 1, uk: 156. 6 Kanzul ummal: Jz: 4, uk : 270 4 5

8


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

basi akamwamuru aiweke katika adhana ya asubuhi.7 Kutoka kwa Mujahid amesema: “Nilikuwa pamoja na Ibnu Umar, akamsikia mtu anaadhini msikitini akasema: ‘’Nitoe kwa huyu mwanabidaa.” Ameipokea Abdur–Razaki.8 Mwenye kitabu cha Fiqihi a’laa madhaahibil-khamsah katika ufafanuzi Uk. 103 kuhusu (As-swalatu khayrum minan naumi) amenukuu kutoka kwa Ibnu Rushdi katika kitabu cha Bidayatul– Mujitahid wa nihayyatul–muqtaswid Juzuu ya 1, ukursa 103 chapa ya 1935: “Wamesema baadhi: Haisemwi As-swalatu khayrum minan naumi kwa sababu hii sio katika adhana, na kwayo amesema Shafii: Na sababu ya kuhitalifiana ni kwamba ilisemwa katika zama ya Nabii au katika zama ya Umar? Na katika kitabu, Mughni cha Ibnu Qudamah Jz. 1, uk. 408 chapa ya pili amesema: “Ondoa, hii imezuliwa na watu.”

IQAMAH NI MARA MBILI MBILI Amesema Ibnu Hajar katika (Naswibu rayah fiy takhirijil – ahadithil- hidayah) amepokea Twahawi katika njia ya Abdul-Aziz bin Rafii amesema: “Nilimsikia Abu Mahudhurah anaadhini mara mbili mbili na anakimu mara mbili mbili.” Na kutoka kwa Al-Asiwad bin Zaid kwamba Bilal alikuwa anaadhini mara mbili mbili na kukimu mara mbili mbili. Ameitoa Abdur-Razaki, Twahawi na Daru-Qutniy na Twabaraniy kwa lafdhi hiyo hiyo.9 Amesema As-Sayidu Murtadha katika Istibswar: “Ni karaha kusema (As-swalatu khayrum minan naumi) kisha akasema: ‘’Na kauli yenye kutegemewa ni haramu.’’10 7 Ibid 8 9

Ibid

Naswibu rayah uk. 60

10

Raudhatu Nadiyah Jz. 1, uk :53 9


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

Kutoka kwa Abu Abdillah (a.s.) amesema: “Adhana ni mara mbili mbili na Iqamah ni mara mbili mbili.”11

KUFUATILIZA ADHANA Kutoka kwa Abu Said amesema: ‘’Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.): “Mnaposikia adhana semeni kama anavyosema mwadhini.’’12 Nawawi amesema: ‘’Katika (hayya a’laa..) anasema: “Walaa haula wala quwata illa billahi”. Na katika Sharhul-Islami: Ni Sunnah kwa anayesikia adhana aikariri katika nafsi yake.13 Na katika maelezo, makusudio ni kwamba: Aseme kama anavyosema mwadhini kipengele kwa kipengele na katika (hayya a’laa …) imepokewa kwamba aseme badala yake: “Laahaula walaa quwata illa billahi”. Na katika Tanuwirul–Imani cha Muhammad bin Yaaqub Al-Kulaini kuna hadithi ya (Ash’ hadu anna A’liyyan amiru–muuminina wa Imamu–mutaqiyna). Na katika Maswahibur-Rashad cha Sayyid Muhammad Twabarasiy ni kwamba ilikuwepo katika zama za Nabii (s.a.w.w.) na ikaachwa katika zama ya utawala wa Bani Umayyah. Na katika Biharul–Anwar haiko mbali kwamba (shahadatu bil– wilayah) ni katika sehemu ya Sunnah ya adhana kwa ushahidi wa Sheikh Al-Allammah Shahidi wa kwanza na wengineo. Ama kupinga kwa mwenye kitabu cha (Man laa yahudhuruhul- faqihi) kauli yake sio yenye kutegemewa kwa sababu ni kauli yenye kupingwa, kama ambavyo imepingwa kauli yake kuhusu kusahau kwa Nabii kwa kauli za watu wa kweli. Al–Istibswar Jz.1, uk. 157 Sahih Muslim Jz. 1, uk. 166, Tirmidhiy Jz. 1, uk :29 13 An-Nawawi Jz: 1, uk: 166 11

12

10


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

Mwenye kitabu cha Fulkul-Najaat katika kuelezea kwake jambo hili amemalizia kwa kusema: “Ni juu ya Waislamu kutoichezea shere adhana ya Shia hata kama wanasema “Ash’ hadu anna A’liyyan waliyyullah” katika adhana, kwa sababu Mwenyezi Mungu amewatishia wanaocheza shere adhana kwa kauli yake: “Na unapolingania katika Swala wanaifanyia istihizai na upuuzi.” Na sisi katika kuthibitisha hii shahada tuna hoja tosha katika Qur’ani. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Na wale ambao ni wenye kusimamisha shahada zao” (Surat Ma’arij:33). Na katika watu wa fani ya lugha ni kwamba uchache wa wingi unaanza na tatu na katika adhana kuna shahada tatu, shahada ya Tauhid, shahada ya Utume na shahada ya Uimam. Hakika adhana na iqamah ni chimbuko la faradhi za kila siku na mwanzilishi wake ni mwanzilishi wa faradhi kwa hukumu ya mnasaba wa matamko na maana, hakika ni katika nembo kuu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ambayo kwayo mila ya Kiislamu imetofautiana na mila na dini zingine. Hivyo adhana na iqamah ni katika mambo ambayo kamwe hawezi akayaleta mwanadamu hata kama watajikusanya wote, tukiachilia mbali jambo la kuonwa katika ndoto.

MWANZO WA ADHANA Mwanachuoni mkongwe na mahiri As–Sayid Jaafar Murtadha katika kitabu chake As– Sahihu min Siratin Nabiyil – Aa’dham (s.a.w.w.) J: 3 uk: 80 – 98 amelichambua suala la adhana katika utafiti wake kama ifuatavyo: Hapa wanasema kuwa adhana imeanza mwaka wa kwanza hijiria na inasemekana kuwa ilianza mwaka wa pili hijiria. Ama vipi imeanza inasimuliwa kama ifuatavyo: 11


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

“Hakika Nabii (s.a.w.w.) aliijali sana Swala na vipi atawakusanya watu kwa ajili ya Swala, akaambiwa: ‘Simamisha bendera watakapoiona wataitana wao kwa wao,’ hilo halikumvutia, wakamtajia tarumbeta la wayahudi, hilo pia halikumpendeza, na akasema hilo ni katika mambo ya kiyahudi, wakamtajia kengele, akasema hilo ni katika mambo ya kinaswara, mwanzo alilichukia kisha akaamuru hivyo baadaye, basi ikatengenezwa kwa mbao. Abdullah bin Zaid akaondoka hali ya kuwa ni mwenye kujali sana jambo hili la Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) basi akaoteshwa adhana katika usingizi wake. Akasema asubuhi alimwendea Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na akamweleza, akamwambia: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hakika mimi nikiwa baina ya kulala na kuwa macho alinijia aliyenijia basi akanionyesha adhana. Akasema na Umar bin Khattab alikuwa ameshaiona kabla ya hapo basi akaificha kwa muda wa siku ishirini kisha akamweleza Nabii (s.a.w.w.). Akasema ni kipi kimekuzuia kunieleza? Akasema Abdullah bin Zaid ameniwahi basi nikaona haya.” Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akasema: ‘’Ewe Bilal, simama tazama atakayokuamuru kwayo Abdullah bin Zaid basi yafanye. Basi Bilal akaadhini.’’ (Al-Hadith). Hii ni moja ya riwaya za namna ya kuanza adhana, na riwaya ina lafidhi nyingi na zenye kutofautiana sana. Tazama: Sunanu Abi Daud Jz. 1, uk. 335 – 338 Al-Musnad cha Abdur-Razaq Jz. 1, uk. 455 - 456 As-Siratul Halabiyyah Jz. 2, uk: 93 – 97 Tarikhul-Khamis Jz. 1, uk. 359 Al-Muwatwa Jz. 1, na Sherhe yake, Zaraqaniy Jz. 1, uk. 120 -125 Al-Jamius-Sahih cha Tirmidhiy Jz. 1, uk. 358 –361 12


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

Musnad Ahmad Jz. 4, uk. 42 Sunan Ibnu Maajah Jz. 1, uk.124 Sunan Baihaqiy Jz. 1, uk. 390 na 391 Siratu Ibnu Hishaam Jz. 1, uk. 154 –156 na 125 Naswibu Rayah Jz. 1, uk. 259 –261 Fat-hul barri Jz. 3, uk. 63 – 66 Twabaqaati Ibnu Saad Jz.1, sehemu ya 2, uk. 8 Al-Bidayatu wan Nihayyah Jz. 3, uk. 232 – 233 Al-Mawahibu laduniyyah Jz. 1, uk. 71 Muntakhabu Kanzul Ummal Jz. 3, uk. l273 na 275 Hayatus-Swahabah Jz. 3, uk.131 - amenukuu kutoka katika Kanzul-Ummal Jz. 4 uk. 263 – 266. Pia amenukuu kutoka kwa Abu Shaikh, Ibnu Hiban, Ibnu Khuzaimah n.k.

UCHAMBUZI WA RIWAYA ZA ADHANA Sisi tunaitakidi kutosihi hilo, hiyo ni kwa kutegemea yafuatayo: Kwanza: Mgongano mkubwa wa riwaya kama inavyodhihirika kwa kurejea na kuzioanisha. Mfano: Riwaya iliyotangulia inasema kuwa Ibnu Zaid aliona adhana akiwa baina ya kulala na kuwa macho, na nyingine inasema: Aliiona akiwa usingizini. Ya tatu inasema kwamba Ibnu Zaid amesema: “Kama si kuchelea watu ningesema: Hakika mimi nilikuwa macho na wala sikuwa nimelala kabisa.” Na kuna riwaya inasema: Ibnu 13


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

Zaid ameiona basi akamweleza Nabii (s.a.w.w.), nyingine inasema kwamba: Jibril aliadhini katika mbingu ya dunia akaisikia Umar na Bilal, basi akamweleza Nabii (s.a.w.w.) kisha akaja Bilal, Mtume akamwambia amekutangulia Umar. Kuna riwaya inasema Ibnu Zaid ameiona, na nyingine inasema kwamba watu saba katika Answar wameiona na inasemekana ni watu kumi na nne, kuna riwaya inamuongeza Abdullah bin Abi Bakar. Aidha kuna riwaya inasema Bilal alikuwa anasema: “Ash ‘hadu an laa ilaaha illa llahu hayya a’las-swalah” Umar akamwambia: Ash’ hadu anna Muhammadan rasulullah. Nabii (s.a.w.w.) akamwambia Bilal: ‘’Sema kama anavyosema Umar.’’ Na mengine mengi kati ya ikhitilafu ambazo hakuna nafasi ya kuzitaja. Pili: Hakika Umar na Bilal kusikia kutoka kwa Jibril au Ibnu Zaid kuona adhana akiwa macho – haiwezi ikakubalika kwa sababu maana ya hilo ni kwamba watakuwa ni kati ya Manabii kwa sababu wao wamemuona Jibril ana kwa ana na kusikia kutoka kwake jambo la kisheria na hilo ni katika sifa mahsusi za Manabii. Na ikiwa sahihi ni kuona usingizini basi Al-Asqalaniy amekwishasema: “Ameshatia mushikeli kuthibiti hukumu ya adhana kwa ndoto ya Abdullah bin Zaid kwa sababu ndoto isiyokuwa ya Manabii haijengewi juu yake hukumu ya kisheria. Akajibiwa: Kwa kuwepo ihtimali ya uwiano wa wahyi na hilo.”14 Lakini jibu ni baridi sana kwani kuwepo kwa ihtimali hakutishi pamoja na kwamba riwaya inayotegemewa kwao haikutaja hilo, wala haikuashiria kwayo, bali inatosheka na amri yake (s.a.w.w.) kwa Bilal kujifunza kutoka kwa Ibnu Zaid, kisha kwa nini wahyi haukuteremka kwake tangu awali ambapo alikuwa na tahayyari, huzuni na hajui afanye nini? Swali linabaki kwamba: Kwa nini ni adhana tu ndio imekuwa ni mahsusi kuanza kwa namna hii bila ya 14

Fat-hul-Barri Jz. 2, uk: 62 14


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

hukmu zingine? Suhail amejibu kuwa: Katika adhana kuna kutukuza jambo lake na kunyanyua utajo wake, hivyo kama itakuwa kwa tamko la mtu mwingine kutakuwa na utukufu zaidi katika kutukuza jambo lake.15 Lakini jawabu hili pia ni baridi - ingawa amelipendelea Asqalaniy na wengineo – kwa sababu kama ingesihi ingekuwa ni wajibu hukumu ya swala, zaka, dua na uwajibu wa shahada mbili na mengineyo pia ingekuwa kwa tamko la mwingine. Kwa sababu ni kusifu utajo wake na kutukuza jambo lake kama vile kauli yake (s.w.t.): “Hakika wewe una tabia njema kabisa…” na mengineyo. Na baada ya yote yaliyotangulia ni lazima tuseme: Hakika hukumu ya Nabii (s.a.w.w.) kuifanyia kazi ndoto ya Ibnu Zayd itakuwa ni kutamka kwa matamanio, na kutotegemea wahyi na huku ni kupingana na kauli yake (s.w.t.): “Hatamki kwa matamanio yake.” Na Nabii kushauri masahaba katika jambo la dini ni mustahili kwa sababu hawahitajii wao kutokana na wahyi. Ndio, alikuwa anawataka ushauri katika mambo ya kidunia kwa kutaka kujua kwao hima ya kulifanya jambo hilo. Tatu: Kisha yeye alichukia kuwaafiki wayahudi na manaswara, kisha akarejea na akaridhia kwayo, je hilo lilikuwa baya kisha likawa zuri? Au alilazimika kuwaafiki pale alipokosa ufumbuzi? Na kwa nini asimuweke mtu wa kuita watu kwa ajili ya Swala, kama walivyokuwa wakifanya walipokuwa wakiwaita kwa ajili ya kukusanyika katika kila mnasaba uliohitajia hilo? Na kwa nini Mtume wa Mwenyezi Mungu amhitajie Abdullah bin Zaid wakati tatizo limekwishamalizika na haukubakia umuhimu wa hilo. Hakika wao wanapokea – ingawa sisi hatuafiki bali tunaamini kuwa hilo ni uongo 15

Raudhul–Anfi Jz. 2, uk. 285 15


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

- kwamba Mtume (saww) alikuwa anapenda kuwaafiki Ahlul Kitabu katika kila ambalo haujashuka kwalo wahyi. Kwa nini amechukia hilo hapa, akajali na kuhuzunika kwa ajili yake, ni wa nini huu mgongano mbaya katika yale wanayoyanasibisha kwa Nabii (s.a.w.w.) na kizazi chake? Nne: a.

Kutoka kwa As-Swibah Al-Maziniy, Sadir As-Sairaf, Muhammad bin Nuuman, Al Wahab na Umar bin Udhainah: Hakika wao walikwenda kwa Abu Abdillah (a.s.) akasema: ‘Ewe Umar bin Udhainah, unalionaje hili kwa wapinzani katika adhana yao na Swala yao?’ Akasema: “Niwe fidia kwako, hakika wao wanasema kwamba: Ubay bin Kaab Al–Answar aliiona usingizini. Akasema (a.s.): “Wamesema uongo. Naapa kwa Mwenyezi Mungu hakika dini ya Mwenyezi Mungu ni tukufu mno kuliko kuonwa usingizini.” Na kulingana na riwaya nyingine ni kwamba amesema (a.s.): “Unateremka wahyi kwayo kwa Nabii wenu kisha mnadai kuwa ameichukua kwa Abdullah bin Zaid.’’16

b.

Kutoka kwa Abul Alau amesema: “Nilimwambia Muhammad Al-Hanafia: Hakika sisi tunasema kuwa mwanzo wa adhana ulikuwa ni kutokana na ndoto aliyoiona mwanaume katika Answar usingizini mwake.” Akasema: ‘’Akashituka kwa hilo Muhammad bin Al-Hanafia mshituko mkubwa na akasema: ‘Mmefanya makusudi (kuacha) ambayo ni asili katika sharia ya Kiislamu na mafunzo ya dini yenu, hivyo mkadai kuwa ni ndoto aliyoiona mwanaume katika Answar usingizini mwake, ambapo yaweza kuwa kweli au uongo na inaweza kuwa ni ndoto ya uongo kabisa.’ Nikasema hii ni hadithi iliyoenea kwa watu.

16

iharul-Anwar Jz. 18, uk: 354 kutoka katika I’ilalis-Sharai uk. 112 na 113, B Nassu wal Ijtihad uk. 205. 16


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

Akasema: ‘Wallahi hii ni batili,’ kisha akasema: ‘Hakika baba yangu alinieleza kwamba: Jibril (a.s.) aliadhini katika BaitulMaqdis usiku wa Israi na akakimu, kisha akaadhini tena pale Nabii (s.a.w.w.) alipopanda mbinguni.’” 17 c.

Na Imam Al-Hasan (a.s.) alikwishapinga hilo vile vile, ambapo walimweleza adhana na wakataja kwake ndoto ya Ibnu Zaid Akasema: ‘’Hakika jambo la adhana ni tukufu mno kuliko hilo, Jibril aliadhini mbinguni mara mbili mbili na akamfundisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na akakimu mara moja moja akamfundisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.).”18 Lakini Iqama kuwa ni mara moja moja ni kinyume na yaliyothibiti kutoka kwa Ahlul bait (a.s.), kwani hashuku yeyote kwamba wao wanaona ni mara mbili mbili na hayo ndio maoni ya masahaba wengi, tabiina na wanachuoni wa Kiislam, na kuifanya kuwa ni mara moja moja ilikuwa ni katika zama ya watawala, kwani hilo ni jambo ambalo watawala waliona ni jepesi,19 vinginevyo Iqama ni mara mbili mbili.

Tano: Kutoka kwa Abdullah bin Zaid yeye mwenyewe: ‘’Nilisikia adhana ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), adhana yake na Iqama yake ilikuwa ni mara mbili mbili.’’20 Kama yeye ndio alioonyeshwa adhana basi yeye ndio atakuwa ni mwenye kujua zaidi kuliko mtu yeyote. 21 As-Siratul Halabiyyah J.2, uk. 96, Nassu wal Ijtihad uk. 205 Nassu wal Ijitihad uk. 205 kutoka katika Mushkeli al-Athar, Ibnu Marud’ wai na katika Kanzul Ummal Jz. 6, uk. 277. 19 Al-Musnaf cha Abdur-Razak Jz. 1, uk. 463, Sunan Al-Baihaqiy Jz. 1, uk. 425 20 Musnad Abi Awanah Jz. 1, uk. 331 na rejea Sunan Daru Qutuni Jz.1, uk. 241 17 18

21

(Vipi hapa anukuliwe kusikia adhana ya Mtukufu Mtume (saww) na ambapo huku tunaambiwa ndiye aliyemshauri Mtume kutokana na ndoto yake? Utasemaje kuhusu mgongano huu? – Mhariri.) 17


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

Sita: Dawi wadiy amesimulia kutoka kwa Is’haqa kwamba: Jibril alimjia Nabii (s.a.w.w.) na adhana kabla ya kumjia Abdullah bin Zaid na Umar kwa siku nane. Na inaunga mkono yale waliyoyapokea vilevile kwamba Umar alikwenda kununua kengele, akapewa habari kwamba: Ibnu Zaid ameshaona adhana akarejea kwenda kumweleza Mtume wa Mwenyezi Mungu, akamwambia wahyi umekuwahi kwa hilo. 22 Saba: Hakika sisi tunaona kuwa mwanzo wa adhana ulikuwa Makka na hiyo ni kwa yale yaliyotangulia kutoka kwa Ibnu Al-Hanafiyah na kwa yafuatayo: 1. Kutoka kwa Zayd bin Ali kutoka kwa baba zake (a.s.): “Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alifundishwa adhana siku aliyopelekwa Israi na akafaradhishiwa Swala.” Vivyo hivyo amepokewa kutoka kwa Amirul-Muuminina (a.s.), na kutoka kwa Ibnu Umar, Imamul Baqir na Aisha.23 - Na imekuja katika sanad sahihi kutoka kwa Imamul-Baqir (a.s.) yanayokaribiana na hayo.24 22

Musnaf cha Abdur-Razak Jz.1, uk. 456, Tarikhul-Khamis J. 1, uk. 360, al-Bi-

dayah wan Nihayyah Jz. 3, uk. 233, Siratul Halabiyah Jz. 2, uk. 96 na 97. Muntakhabu Kanzul Ummal katika hashiya ya Musnad Ahmad Jz. 3 uk. 273 kutoka kwa Twabari, Siratul Halabiyah Jz. 1, uk. 373 na Jz.2, uk. 93 na 95, Majimau Zawa’id Jz.1 uk. 329, Fatuhul Barri Jz. 2, uk. 63, Al-Bidayah wanNihayah Jz. 3, uk. 233. 24 Al-Kaafiy Jz. 3, uk. 302 23

18


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

2.

Kutoka kwa Anas: “Hakika Jibril alimwamuru Nabii (s.a.w.w.) kuadhini pale alipofaradhishiwa Swala.” 25 Suhaili amesema riwaya ya Imamul Baqir ambayo inaonyesha kuanza adhana wakati wa Israi na ambayo tumekwisha iashiria katika yaliyotangulia. Lakini wao wameipokea kwake kwamba yuko katika sanad yake Ziyad bin Al-Mundhir na humo kuna Shia 26 na kwamba Nabii hakuamuriwa adhana wakati wa hijira.27 Lakini upokezi wao wa kwanza na upokezi wao wa pili hauna mashiko kwani hapa ndio mahala pa mzozo. Haya, pia imepokewa kuwa Jibril aliadhini kwa Adam aliposhuka kutoka Peponi.28

Baada ya yaliyotangulia, hakika tunajua kutosihi yale waliyoyapokea kutoka kwa Ibnu Abbasi kwamba kufaradhishwa adhana ilikuwa pamoja na kushuka aya ya: “Enyi mlioamini inaponadiwa kwa ajili ya swala ya Ijumaa…”,29 ambapo adhana inakuwa imeanza wakati wa kushuka Surat Jumu’ah baada ya mwaka wa saba na baada ya kufariki Abdullah bin Zayd ambaye alikufa katika Uhdi au baada yake kwa muda mchache. Kwa ajili hiyo Al-Hakim amesema: “Hakika Masheikh wawili Bukhari na Muslim wameiacha hadithi ya Abdullah bin Zayd katika adhana ya ndoto kwa sababu ya kutangulia mauti ya Abdullah.”30 Lakini katika Durrul Manthur ibara iko hivi: “Adhana imeshuka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) pamoja na kufaradhishwa swala: “Enyi mlioamini inaponadiwa kwa ajili ya swala” kuna Al-Mawahibu laduniyah Jz. 1, uk. 72, Fatuhul Barri Jz. 2, uk. 63, Al-Bidayah wan-Nihayyah Jz. 3, uk. 233, Mustadrakul Hakim Jz. 3, uk. 171 26 Naswibu Rayah Jz. 1, uk. 261 27 Al-Bidayah wan-Nihayyah Jz. 3, uk. 233, Mustadrakul Hakim Jz. 3, uk. 171, Nasbu Rayah Jz. 1, uk. 261. 28 Fatuhul Barri Jz. 2, uk. 64, Siratul Halabiyah Jz. 2, uk. 92 29 Fatuhul Barri Jz. 2, uk. 64 na Siratul Halabiyah Jz. 2, uk. 93 30 Mustadrak Jz. 4, uk. 348 25

19


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

uwezekano wa kuwa makusudio yake ni kuwa adhana imeanza Makka pamoja na kufaradhishwa Swala, kisha akatoa ushahidi wa Aya kwa kuashiria adhana katika Qur’ani vile vile, kama haya yatasihi basi riwaya hii haipingi yaliyotangulia. Nane: Kutoka kwa Aisha, Ikrima, Qais bin Hazim na wengineo katika kauli yake (s.w.t.): “Na ni nani mwenye kauli nzuri kuliko anayeita kwa Mwenyezi Mungu na akafanya amali njema: Ni rakaa mbili baina ya adhana na iqamah.”31 Ni wazi kwamba aya hii imepokewa katika Surat Fuswilat nayo imeshuka Makka ambapo inaonyesha kwamba adhana na iqamah imeanza Makka na aya ilikuja ili kubainisha hukumu inayoambatana nayo. Na madai ya kwamba aya ni katika yale yaliyochelewa kushuka hakuna hoja kwayo isipokuwa riwaya ya Ibnu Zayd iliyotangulia, na tumeshajua kwamba haisihi kuitegemea bali hoja imesimama dhidi ya uongo wake.

MWISHO Imepokewa katika sanadi sahihi kutoka kwa Abi Abdillah As-Swadiq (a.s.) amesema: “Aliposhuka Jibril kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na adhana, Jibril aliadhini na kukimu na hapo ndipo Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimwamuru Ali amwitie Bilal akamwita, Mtume (s.a.w.w.) akamfundisha adhana na akamwamuru kuadhini. 32 31

32

Siratul Halabiyah Jz. 2, uk. 93, Durrul Manthur Jz. 5, uk. 364. 4 – Al Wasa’il

Jz. 1, uk. 366, Al Kafiy Jz. 3, uk. 302, Nassu wal Ijitihad uk. 205 Al Wasa’il Jz. 1, uk. 366, Al-Kafiy Jz. 3, uk. 302, An-Nassu wal Ijitaihad uk. 205 20


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

Kulingana na yaliyotokea Madina huenda iliyo karibu zaidi ni riwaya ambayo inasema: Wakati Waislamu walipohamia Madina walikuwa wanakusanyika kwa kungojea wakati wa swala na wala hawakuwa wanaitwa, siku moja wakamweleza hilo, baadhi yao walisema wekeni kengele mfano wa kengele ya manaswara wengine wakasema wekeni tarumbeta kama ya wayahudi, Umar akasema: ‘’Je, hamuwatumii watu wanadi Swala.” Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akasema: ‘’Ewe Bilal, simama uadhini.’’ 33 Riwaya hii ya mwisho inaonyesha kwamba: Waislamu ndio waliohitalifiana baina yao na wakapendekeza hilo baadhi kwa baadhi yao, Mtume wa Mwenyezi Mungu akatatua mzozo kwa kumwamuru Bilal kuadhini ambapo inadhihirika kuwa adhana ilikuwa imeshaanza kabla ya hapo wakati wa Israi.

SHAHADA Shahada ni kushuhudia kutokana na elimu inayopatikana kwa njia ya kuona na kufahamu, hivyo inazingatiwa katika shahada iwe kwa kujua, kwani shahada kwa dhana na shaka haizingatiwi. Mfano kama mtu atasema nashuhudia kwamba kitabu hiki ni cha Zayd kisha akaulizwa: Unajua? Kama atasema hapana, nadhani, ushahidi wake haukubaliwi. Elimu hii wakati mwingine inakuwa kwa njia ya kuona au kufahamu, mtu anaona kwa macho yake kwamba kitabu hiki amekinunua Zaiyd dukani, hivyo ni milki yake, na wakati mwingine mtu anashuhudia kitu lakini kitu hicho hakionekani bali anakiona kwa utambuzi wake, hivyo anashuhudia, kama hali ilivyo katika kushuhudia upweke wa Mwenyezi Mungu, Miadi, Qiyama n.k. katika mambo ambayo mwanadamu anajua kwa elimu isiyo na shaka hivyo anashuhudia mambo hayo. 33

Sunan Daru-Qutny Jz. 1, uk. 237 21


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

SHAHADA YA WILAYAH (UONGOZI) WA ALI (A.S.) Shahda ya wilayat Ali ni kushuhudia juu ya haki ya uongozi wake kwa watu baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) moja kwa moja bila ya utenganisho. Tazama tunapounganisha mambo haya matatu. Tunatangaza katika adhana, tunatangaza na kutoa habari kwa watu habari ya jumla kwamba sisi tunaitakidi uongozi wa Ali kwa watu punde tu baada ya kuondoka Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.). Hii ndio maana ya uongozi wa Ali katika adhana. Tunawaambia watu, tunauambia ulimwengu kuwa sisi tunaitakidi uongozi wa Ali na juu ya ubora wake kwa watu baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kauli hii ni kauli ya jumla tunaitangaza katika adhana na tunawasikilizisha walimwengu juu ya itikadi hii. Na itikadi hii haikuja tu hivi hivi kimchezo bali kuna hoja zinazotia nguvu itikadi hii na kuunga mkono itikadi hii, hivyo tunatangaza itikadi hii kwa ulimwengu na adhana tunaichukulia kuwa ni wasila wa kutangaza itikadi hii. Na kama kutangaza kwetu uongozi wa Ali katika adhana hatukusudii kuwa sehemu hii ni katika adhana, ni kitu gani kinazuia hilo? Swali litakuja ikiwa huyu mwadhini hakukusudia kuwa shahada hii ni sehemu ya asili katika sehemu za adhana bali anataka kutangazia ulimwengu juu ya itikadi yake juu ya ubora wa Ali kwa watu baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, kuna kizuizi gani kwa hili? Kinachozuia ni Kitabu, Sunnah au Akili? Hivyo anayedai kuwa kuna kizuizi alete dalili. Ndio Maulamaa wetu wamekiri kuwa kumtaja Mwenyezi Mungu kama anavyostahiki katika shahada ya kwanza na kumtaja Nabii baada ya shahada ya kwanza kwamba kusema “Aswalatu wasalam alaihi� ni Sunnah na kwamba mwadhini kuzungumza maneno ya kawaida wakati wa adhana inajuzu na wala 22


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

haidhuru adhana yake. Sasa itakuwaje ikiwa maneno yake na makusudio yake ni kutangaza uongozi wa Amirul-Muuminina Ali (a.s.), naye anaitakidi kuwa shahada na Ujumbe wa Mtume wa Mwenyezi Mungu kama haukuambatanishwa na shahada ya uongozi wa Ali utakuwa na upungufu? Hivyo anataka kwa tangazo hili kukamilisha shahada yake kwa ujumbe wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na kwa Uungu wa Mwenyezi Mungu. Kama kizuizi hakijathibiti hata kama tusingekuwa na dalili ya kujuzu basi asili ni kutokuwepo na kizuizi, na kwa asili ya uhalali inatosha kanuni hii ya kielimu, kiakili na ya kunukuu juu ya kujuzu tangazo hili katika adhana. Wakati huo mwenye kukataza na mwenye kudai kizuizi alete dalili ya kutojuzu, na hapo mwenye kukanusha na mpingaji wa kutangaza shahada ya uongozi wa Ali katika adhana anageuka kuwa ni mwenye kudai baada ya kuwa ni mpingaji, na wajibu wake ni kuleta dalili juu ya madai yake kutoka katika Kitabu au Sunnah n.k.

USHAHIDI WA HADITH Ushahidi wa Hadith juu ya Sunnah ya shahada ya wilayat Ali katika adhana katika baadhi ya vitabu vya jamaa zetu: Kutoka katika Kitabus Salafah fiy amril khilafah cha Abdul Maraagh Al Masri: Hakika Salman Al Farsi alitaja katika adhana na iqama shahada ya Ali baada ya shahada ya Mtume katika zama za Nabii (s.a.w.w.) basi mtu aliingia kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu nimesikia jambo sijalisikia kabla ya leo.” Mtume akasema lipi hilo? Akasema: “Salman ametaja katika adhana yake baada ya shahada ya utume shahada ya wilayat (uongozi wa) Ali.” Akasema (s.a.w.w.): “Mmesikia kheri.” 23


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

Na kutoka katika kitabu cha salafah vile vile ni kwamba mwanaume aliingia kwa Mtume (s.a.w.w.) Akasema: ‘’Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hakika Abu Dhari anataja katika adhana baada ya shahada ya utume, shahada ya wilayat Ali anasema: “Ashahadu anna Aliyan waliyulllah.” Akasema: “Hivyo ndivyo, je mmesahau kauli yangu siku ya Ghadir khum: ‘Man kuntu maulahu fa Aliyun maulahu?’ atakayetengua ahadi hakika anatengua kwa ajili ya nafsi yake.” Na katika kitabu cha Ihtijaji katika hoja za Amirul Muuminina kwa Muhajirina na Answar, Maulamaa wetu wanatoa ushahidi wa riwaya hii bali wameitolea hoja katika vitabu vyao vya fiqihi. Amepokea Qasim bin Muawiya amesema: “Nilimwambia Abu Abdillah (a.s.): hawa (yaani Ahlus Sunnah) wanapokea Hadith kwamba Mtume alipopelekwa Israi aliona maandishi katika Arshi: ‘Laa ilaha illa llahu Muhammadu rasulullah Abu bakar swidiq’, akasema: ‘Subhanallah! Wamebadilisha kila kitu hata hili pia?’ Nikasema ndio, akasema (a.s.): ‘Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu alipoumba Arshi akaandika juu yake: ‘Laa ilaha illa llahu Muhammad Rasulullah Aliyun Amirul-Muuminina’, na alipoumba Kursiyu akaandika katika nguzo zake‘Laa ilaha illa llahu Muhammad rasulullah Aliyun Amirul muuminina’ vivyo hivyo alipoumba Lauhu, alipomuumba Jibril, alipoumba Ardhi n.k. Mwisho akasema alipoumba Mwezi akaandika juu yake “Laa ilaha illa allahu Muhammad rasulullah Aliyun Amirul muuminina nayo ndio weusi mnaouona.” Riwaya hii ipo katika kitabu cha Ihtijaj cha Sheikh Abi Mansur Twabarsi uk: 158. Na kutoka kwa Abu Huraira kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) amesema: ‘’Nilipopelekwa mbinguni nilikuta Arshi imeandikwa “Laa ilaha ila llah Muhammadur Rasulluhi ayadtuhu bi Aliyyi.” Imeandikwa hivi katika Arshi, na tumeshapata katika riwaya hii vile vile kwamba arshi imeandikwa jina la Amirul muuminina, riwaya 24


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

hii ipo katika Kitabu Shifaa cha Ayyad Jz. 1, uk. 138 chapa ya Istambul, Al Manaqib cha Ibnul Maghazi uk. 39, Riyadh Nadhar fiy Manaqil Asharatil Mubasharah Jz. 2, uk. 172, Nudhumu Durar Simtwain uk.120, Majmau Zawa’id Jz. 9, uk. 121, Khaswaiswil Kubra Jz. 1, uk. 7, Durul Manthur Jz: 4, uk. 153, riwaya hii ipo katika rejea hizi na nyinginezo. Ikiwa riwaya inakubaliwa na pande mbili zinazozozana bila shaka mtu atapata matumaini ya kupokewa riwaya hii. Kundi miongoni mwao wameipokea riwaya kwa sanadi kutoka kwa Jabir bin Abdillah Answar amesema: Amesema Mtume (s.a.w.w.) katika mlango wa Pepo imeandikwa: Muhammadur Rasullulahi Aliyun bin Abi Twalib akhur-Rasullillah, hii ni kabla ya kuumbwa mbingu na ardhi kwa miaka 2000. Riwaya hii ya Twabarani na wengineo, wameipokea kwa sanad ambayo humo kuna baadhi ya maimamu wakubwa wenye kuhifadhi, ipo katika rejea zaidi ya moja, Kanzul Ummal Jz: 11, uk: 624, Al-Manaqib cha Al Khawazirimi uk: 87 n.k. Kutoka kwa Ibnu Masud, kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.): “Alinijia Malaika akasema: ‘Ewe Muhammad: Waulize tuliowatuma kabla yako’ Surat Zukhuruf: 45 kwa kitu gani walitumwa?’ Nikasema: kwa kitu gani walitumwa? Akasema walitumwa juu ya uongozi wako na uongozi wa Ali bin Abi Talib.” Mitume waliotangulia walitumwa juu ya uongozi wa Mtume na Amirul muuminina baada yake yaani walipewa jukumu la kutangaza jambo hili muhimu. Hadithi hii mtaikuta katika kitabu “Maarifat ulumil Hadith” uk: 96 cha Al-Hakim Anisabur mweye kitabu cha Mustadrak, na amesema kuwa wapokezi wake ni wakweli, vile vile katika Tafsir Tha’alab kuhusu aya tukufu, pia ameipokea Abu Nua’im Al-Isfahan katika Manqabatul Mutwahirina na wengineo. Kutoka kwa Hudhaifa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Kama watu wangejua ni lini Ali aliitwa 25


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

Amirul-Muuminina basi wasingekanusha fadhila zake. Ameitwa Amirul-Muumunina kabla ya kuumbwa Adam. Amesema Mwenyezi Mungu: Mola Wako alipochukua ahadi kwa wanadamu na akashuhudisha juu ya nafsi zao, kwamba Mie si ndio Mola Wenu… Surat A’araf: 172. Malaika wakasema: Ndio. Akasema: Mimi ni Mola Wenu, Muhammad ni Nabii wenu na Ali ni kiongozi wenu.” Riwaya hii inapatikana katika Firdausil Akhibar cha Dailami Jz. 3, uk. 399. Nimetaja riwaya hizi kutoka katika vitabu vya Ahlus’Sunnah ili ziipe nguvu riwaya ya Ihtijaj baada ya kuchunguza sanad zake na hoja zake. Riwaya nyingine katika Ghayyatul Marami kutoka kwa Ali bin Babawaihi Asuduq kutoka kwa Al-Baraq kutoka kwa Fadhil bin Mukhutar huyu ni mkweli na Baraq ni mkweli na Ibnu Babawaihi ni maarufu kutoka kwa Abu Jaafar Al-Baqir (a.s.) kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Ewe Ali, hakunikirimu kwa utukufu (yaani Mwenyezi Mungu) isipokuwa amekukirimu kwa mfano wake.” Na riwaya inaonyesha kuwa ni ya jumla na kumtaja Mtume katika adhana ni katika Mwenyezi Mungu kumtukuza Mtume kwa kuweka shahada yake katika adhana “na hakunitukuza kwa utukufu isipokuwa amekutukuza kwa mfano wake” matokeo ni kwamba: Mwenyezi Mungu amemtukuza Ali katika kumtaja kwake na kushuhudia uongozi wake katika adhana. Amepokea Assayid Niimatillah Al-Jazair kutoka kwa sheikh wake Al-Majilis marufuu kwa Nabii (s.a.w.w.): “Ewe Ali hakika mimi nimeomba kwa Mwenyezi Mungu akutaje katika sehemu anayonitaja, ameniitikia na amenikubalia.” Katika kila sehemu anayotajwa Mtume wa Mwenyezi Mungu Ali yuko pamoja nae na adhana ni katika sehemu hizo.

26


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

Ushahidi katika vitabu vya Ahlus Sunnah: Kauli yake (s.a.w.w.) kwa Ali: “Sikumuomba Mwenyezi Mungu kitu katika Swala yangu isipokuwa amenipa, na sikuiombea nafsi yangu kitu ila nimekuombea na wewe.” Al-Khaswais uk: 262 chapa ya Al Mahamuud cha Anasai, Majmau Zawa’id Jz: 9, uk: 110 na Riyadh nadhar Jz: 2, uk: 213. Hadith nyingine “Nakupendelea ambacho naipendelea nafsi yangu na nachukia kwako ambacho nakichukia kwa ajili ya nafsi yangu.” Sahihi Tirmidhiy Jz: 2, uk: 79 chapa ya Swawiy ya Misri. Na katika riwaya ambazo amezipokea Sheikh Suduq katika Amaal kwa sanad yake kutoka kwa Imam As-Swadiq (a.s.) amesema: “Hakika sisi ni Ahlul Bait wa kwanza ambao Mwenyezi Mungu ametukuza majina yetu, alipoumba mbingu na ardhi alimwamuru mwenye kunadi akanadi: Ash hadu an laa ilaha illa llahu mara tatu, ash hadu anna Muhammadan Rasulullah mara tatu, ash hadu anna aliyan Amirul muuminina haqan haqan mara tatu” (Al amaal cha Sheikh As-Suduq uk: 701. Katika shahada ya uongozi wa Amirul-Muumina kuna neno haqan haqan na hii ni kwa kuwajibu wapinzani. Na katika Al-Bihar kutoka kwa Kulain kutoka kwa Ibnu Abbas amesema: “Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.): ‘’Mwenye kusema laa ilaha illa llahu inafunguka kwake milango ya mbingu, na mwenye kufuatiliza kwa Muhammad Rasulullahi unakunjuka kwake uso wa haki na kufurahishwa na hilo, na mwenye kufuatiliza kwa Aliyun waliyullah Mwenyezi Mungu anamsamehe dhambi zake hata kama zikiwa kama idadi ya matone ya mvua.” (Biharul-Anuwar Jz: 38, uk: 318 ).

27


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

Imekuja katika Siratul Halabiyah kutoka kwa Abi Yusuf, mwanafunzi wa Abu Hanifa Imam wa Hanafia: “Sioni ubaya mwadhini kusema katika adhana yake As-salaam alaika ayuhal Amiru warahamatullah wabarakatuhu.” Anakusudia khalifa wa wakati ule yeyote awaye. Tazama ibara iliyobakia: “Sioni vibaya mwadhini kusema katika adhana yake As salaam alaika ayuhal Amir warahamatullahi wabarakatuhu. Haya alaa swalah, Haya alaal falaha, as swalatu yarham kumullahu.” Ndio maana mwadhini wa Umar bin Abdul Azizi alikuwa anaadhini hivyo na kumsalimia Umar bin Abdul Aziz katika adhana kwa kusema: Allahu akbar Allahu akbar, ash haadu an laa ilaha illa llahu ash hadu anna Muhammadan rasulullah asalam alaikum yaa ayuhal amiru warahamatullahi wabarakatuhu, hayya alaa swalah haya a’lal falaha. Sioni ubaya katika hili.” Kama hakuna ubaya mwadhini kumwambia Khalifa wa wakati huo na Amir wa waumini katika adhana kwa maneno haya basi kusema “Ash’hadu anna Amiral muuminina haqan” sioni kama humo kuna ubaya bali ni kati ya mambo yanayopendeza sana kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) na kama tutatoa fat’wa ya kwamba ni sehemu ya wajibu basi tutakuwa na fursa pana, ingawa kauli hii imepingwa na watu mashuhuri.

MUAMALA WA AHLUS SUNNAH KATIKA ­ADHANA. Muamala wa Ahlus Sunnah katika adhana ni kama ufuatao: 1.

Kuondoa hayya a’laa khairil a’mali

2.

Kuongeza As swalatu khairun minan naumi 28


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

Na wala hawajatoa dalili juu ya hayo, hayo yapo katika Sharhi Tajirid cha Qaushaji (Sharhi Tajirid Mabhathul Imamah). Hii inadhihiri kwamba “hayya a’laa khairil a’mal” ilikuwa ni katika asili ya adhana wakati wa Mtume wa Mwenyezi Mungu na Umar akaikataza kama alivyokataza mut’a mbili kama tulivyoeleza hilo hapo mwanzo. Ama “As swalatu khairu mina naumi” wana riwaya nyingi zinazosema kuwa ni bidaa. Rejea Kanzul Ummal Jz. 8, uk. 257 – 356 pia rejea ushahidi tulioutaja huko mwanzo. Pamoja na kwamba shahada ya wilayati Ali ni Sunnah katika adhana ila imeshakuwa ni nembo na alama ya madhehebu ya Shia na kuiacha kwake ni madhara kwa madhihab na kila ambacho kimekuwa ni alama na nembo ya madhihab hii, basi Sunni wamekiacha si kwa kingine bali ni kwa kuwa kimekuwa ni alama ya Ushia. Tazama katika kitabu cha Al-Wajiz cha Al-Ghazal katika fiqihi, vilevile katika Sharhi al-Wajizi nacho ni (Fatuhul aziz fiy sharhil wajiz), katika fiqihi ya Shafi wanasema kwamba kusawazisha kaburi ni bora kuliko kulinyanyua lakini kwa kuwa kusawazisha imekuwa ni alama ya Shia basi ni bora kuwakhalifu (fatuhul Aziz) katika Sharhul Wajiz chapa ya Al-majumuu cha Nawawi Jz. 5, uk. 229. Sunnah ya kuvaa pete - Sunnah ya Mtume ni kuvaa pete mkono wa kulia lakini Shia walipoivaa mkono wa kulia na kuwa ni alama yao basi Sunni wakajilazimisha kuvaa pete mkono wa kushoto na wa kwanza kuvaa pete mkono wa kushoto ni Muawiya (Rabiul abrar Jz. 4, uk:24). Vile vile kuvaa kilemba (ammamah) wameacha kwa kuwa kimekuwa ni alama ya Maulamaa wa Kishia ili wasifanane nao (Sharhu al mawahib laduniyah Jz. 5, uk. 13 n.k. Tazama ibara hii: “Amepokea An-Nasai kutoka kwa Said bin Jubair amesema: Ibn Abbas alikuwa Arafa akasema: Ewe Said vipi 29


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

mbona sioni watu wakisoma talbiyah? Nikasema wanaogopa. Ibn Abbas akatoka katika hema lake akasema: Labaika Allahumma labaika hata kama Muawiya atachukia, Ee Mwenyezi Mungu walaani hakika wameacha Sunnah kwa kumchukia Ali” (Sunanu An-Nasai J. 5, uk. 253, Sunanu Baihaq Jz. 5, uk. 43), Sandiy amesema katika maelezo ya An Nasai yaani kwa ajili ya chuki yake kwani alikuwa anamchukia sana na hawa wanaiacha kwa kumchukia Ali. Hivyo ikiwa jambo fulani ni Sunnah kisha likawa ni alama ya Shia wanajilazimisha kuliacha jambo hilo kwa sababu ya kuwa kwake ni alama ya Ushia pamoja na kujua kwao kuwa ni Sunnah, vivyo hivyo katika shahada ya tatu ni kupiga vita Shia na Ushia kwa sababu shahada ya tatu ni alama ya Shia na Ushia na hii ni kuwatumikia wasiokuwa Mashia na kuwafuata wasio kuwa Shiatul Imamiyah katika kupinga Sunnah na nembo hii. (imenukuliwa kutoka katika makala ya As Sayyid Ali Al-Hussein Al Milaan).

HAYYA A’LAA KHAIRIL A’MALI KATIKA ADHANA Imamu Sharaf Diyn amefanya uchambuzi mzuri na wa kina katika suala hili katika kitabu chake (An-Nasu wal – ijitihadi uk. 197 – 205 kama ifuatavyo: “Hakika katika mambo ambayo kumetokea ikhitilafu humo baina ya wanaothibitisha na kukanusha ni kusema ‘hayya a’laa khairul a’mali’ katika adhana mara mbili baada ya kusema hayya a’laalfalaha. Kundi moja kwa kufuata maimamu wao wanasema kwamba kipengele hiki: “Hayya alaa khairul a’mali” haisihi kukitaja katika adhana na hawa ni kundi la Ahlus Sunnah wal Jama’ah na baadhi yao wanasema ni makuruhu kwa kutoa sababu kwamba hilo 30


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

halikuthibiti kutoka kwa Nabii (s.a.w.w.) na ziada katika adhana ni makuruhu. 34 “Na Ahlul Bait na wafuasi wao wanasema kwamba kipengele hiki ni sehemu ya adhana na iqamah, na wala haisihi bila ya kuwepo na hukumu hii ni ya ijamai kwao,35 hupati humo kamwe mwenye kupinga na wanatoa dalili kwa hilo kwa ijmai na kwa riwaya nyingi kutoka kwa Ahlul Bait (a.s.) katika hilo kama vile riwaya ya Abi Rabii, Zurarah, Al-Fadhil bin Yasir na Muhammad bin Muhammad kutoka kwa Abu Abdillah (a.s.) na riwaya ya Fiqihi Ridhaa kutoka kwa Imamu Ridhaa (a.s.). “Na riwaya ya Ibnu Sanan, Maaliy bin Khamis, Abu Bakar bin Al-Hadharamiy, na Kulainiy bin Al as-Sadi kutoka kwa Abu Abdillah (a.s.), na riwaya ya Abu Baswiri kutoka kwa mmoja wao, na riwaya ya Muhammad bin Umair kutoka kwa Abu Hassan, na riwaya ya Ali na Muhammad bin Al Hanafiya kutoka kwa Nabii (s.a.w.w.), na riwaya ya Ikrimah kutoka kwa Ibnu Abbas. 36 “Na sisi katika ikhitilafu hii hatuna njia ila kuchukua kutoka katika madhehebu ya Ahlul Bait (a.s.) na wafuasi wao na wala hatutotegemeza katika hayo kamwe ijimai iliyotajwa na kwa yaliyopokewa kutoka kwa Ahlul Bait ambao wao ni moja ya Vizito Viwili na ambao Mwenyezi Mungu amewahifadhi kutokana na uchafu, bali na kutokana na dalili na hoja nyingi zingine ambazo tunazikuta kwa wengine wasiokuwa wao vile vile.” Katika jumla ya hayo kwa mfano baadhi yake yamepokewa kwa sanadi sahihi kutoka kwa: Sunan Baihaqiy Jz. 1, uk: 5425, Baharu raiq Jz.1, uk: 275 katika Sharihu ya Mashihab Al-Intiswar cha Sayid Al Murtadhaa uk. 39 36 Rejea Wasa’il na Jaamiul ahadith Shiah, Biharul Anwar, Mustadrak wasa’il Shiah Abuwabul adhana 34 35

31


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

1.

Abdullah bin Umar

2.

Ali bin Al Husein Zainul Abidin (a.s.)

3.

Sahal bin Hanif

4.

Bilal bin Rabaha

5.

Ali Amirul muuminina (a.s.)

6.

Abu Mahudhurah

7.

Ibnu Abi Mahudhurah

8.

Zayd bin Arqam

9.

Al-Baqir (a.s.)

10. As-Swadiq (a.s.) Ama Abdulla bin Umar imepokewa kutoka kwake na:

37 38 39

1.

Malik bin Anas kutoka kwa Nafii amesema: Ibnu Umar wakati mwingine alikuwa anaposema: Hayya a’laal-falaah anasema baada ya hapo: Hayya a’laa khayril a’mali. 37

2.

Kutoka kwa Laith bin Saad kutoka kwa Nafii amesema: Ibnu Umar alikuwa anaadhini katika safari yake na alikuwa Anasema: Hayya a’laal falah na wakati mwingine alikuwa anasema: Hayya a’laa khayiril a’mali. 38

3.

Kutoka kwa Laith bin Saad kutoka kwa Nafii amesema: Ibnu Umar alikuwa anazidisha katika kuadhini kwake: Hayya a’laa khayril a’mali. Ameipokea Abdullah bin Umar, kutoka kwa Nafii. 39

Sunanu Baihaqiy J. 1 Uk. 424

Ibid

Ibid uk. 465 na Dalail Swidiq Jz. 3 sehemu ya 2, uk. 155 32


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

4.

Kutoka kwa Muhammad bin Sirin kutoka kwa Ibnu Umar kwamba: Yeye alikuwa anasema hivyo katika kuadhini kwake. 40

5.

Vile vile ameipokea Nasir bin Dhahiq kutoka kwa Ibnu Umar, na amesema katika safari. 41

6.

Kutoka kwa Abdur Razak kutoka kwa Ibnu Juraih kutoka kwa Nafii kutoka kwa Ibnu Umar kwamba: “Yeye alikuwa anakimu katika safari anasema mara mbili au mara tatu, anasema: ‘Hayya a’laal falaah hayya a’laa khayril amal.’” 42

7.

Kutoka kwa Abdur Razak kutoka kwa Maamar kutoka kwa Yahya bin Abi Kathir: “Hakika Ibnu Umar alikuwa anaposema katika adhana: Hayya a’laal falaah’ anasema ‘Hayya alaa khayril a’mal’ kisha anasema ‘Allahu akbar laa ilaha illa llahu’.43 Na amepokea Abu Shaibah44 kwa njia ya Ibnu Ajalaan, Abu Abdillan na Nafii kutoka kwa Ibnu Umar. Na amepokea Ibnu Abi Shaibah katika njia ya Ibnu Ajalaan na Ubaidullah bin Nafii kutoka kwa Ibnu Umar.

Ama yaliyopokewa kutoka kwa Ali bin Husein (a.s.): 8.

40

Kutoka kwa Hatim bin Ismail kutoka kwa Jafar bin Muhammad kutoka kwa baba yake kwamba: Ali bin Husein alikuwa anasema katika adhana yake anapofika katika hayya

Ibid uk. 425

Sunanu Baihaqiy Jz. 1, uk. 425 Musnaf Abdur Razaq Jz.1, uk. 464 43 Ibid uk. 460 44 Kutoka katika Musnaf Abiy Shaibah Jz. 1, uk. 145 na katika Hamishi ya Musnaf Abdur Raq Jz. 1, uk: 460. 41 42

33


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

a’laal-falah anasema: Haya alaa khairil amali na anasema hii ndio adhana ya awali.45 Na haijuzu kuchukuliwa kauli yake: Ndio adhana ya awali isipokwa ni adhana ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.). 46 9.

Na amenukuu hayo kutoka kwa Ali bin Husein Al Halabiy, Ibnu Hazim na wengineo kama itakavyokuja. Amesema Sahal bin Hanif:

10. Amepokea Baihaqiy kwamba: Ametaja hayya a’laa khairil amal katika adhana, na amepokea kutoka kwa Abi Umamah na Sahal bin Hanif. 47 11. Na amenukuu Ibnul-Wazir kutoka kwa Al-Muhibu Twabari As-Shafii katika kitabu chake Ahkamul-Ahkaam: “…ametaja hai’alah kwa hayya alaa khairil amal. Kutoka kwa Saduq bin Yasir kutoka kwa Sahali bin Hanif: Kwamba yeye alikuwa anapoadhini alikuwa anasema: Haya alaa khairil amal, ameipokea Said bin Mansur. 48 Vile vile kutoka kwa Bilal: 12. Kutoka kwa Abdullah bin Muhammad bin Ammaar kutoka kwa Ammaar na Umar watoto wa Hafsi bin Umar kutoka kwa baba zao kutoka kwa babu zao kutoka kwa Bilal: Kwamba yeye alikuwa ananadi asubuhi na anasema: Hayya a’laa khairil amal basi Nabii akamwambia aweke mahala pake: Aswalatu khairu minan naumi, akaacha hayya a’laa Sunan Baihaqiy Jz. 1, uk: 425 na Dalailus Swidiq Jz. 3 sehemu 2, uk. 100 Dalailus Swidiq Jz. 3, sehemu 2, uk. 100 kutoka katika Mabadiul–Islaamiy uk. 38 47 Sunan Baihaqiy Jz. 1, uk. 425 48 Dalailus Swidiq Jz. 3 sehemu 2, uk: 100 kutoka katika Mabadiul–Islaamiy uk. 38 45 46

34


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

khayril amali.49 Lakini mwisho wa riwaya huenda ni katika ziada ya riwaya, hiyo ni kwa sababu ibara (aswalatu khayrum minan naumi) iliongezwa katika adhana baada ya zama ya Nabii (s.a.w.w.) kama zilivyosema hayo riwaya nyingi. 50 13. Kutoka kwa Bilal: Bilal alikuwa anaadhini asubuhi anasema: Hayya a’laa khairil amal. 51 Yanaongezwa katika yote hayo: 14. Aliyoyasema Al-Qaushaji na wengineo: Kwamba Umar alihutubia watu akasema: “Enyi watu, mambo matatu yaliyokuwa katika zama ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) mimi ninayakataza, ninayaharamisha na nitaadhibu kwayo nayo ni: Mut’a ya wanawake, Mut’atul Haji na Hayya a’laa khairil a’mal..” 52 Al-Qaushaji msemaji wa Ashairah ametoa udhuru juu ya hilo kwa kauli yake: “Hakika mujitahidi kumkhalifu mujitahidi mwingine sio bidaa.53 (Ajabu yaani Mtume ni mujtahidi na Umar ni mujtahid) na udhuru huu sio sahihi tukizingatia kuwa Nabii (s.a.w.w.) hatamki kwa matamanio bali ni 9 – Majimau Zawa’id J. 1, uk: 330 kutoka kwa Twabarani katika Al Kubra na Musnaf Abdur Razak Jz. 1 uk. 460, Sunanu Baihaqiy Jz.1, uk. 425, Kanzul Ummal Jz. 4, No: 5504, Muntakhabul Kanzu hamishi ya Musnad Jz. 3, uk. 272 kutoka kwa Abi Sheikh Kitabul Adhana, Dalailus Swidiq Jz. 3 sehemu 2, uk. 99. 50 Muwatwa Jz. 1, uk: 93, Sunanu Dar qutuni, Kanzul Ummal Jz. 4 No: 5562 na Muntakhabu yake katika hamishi musnad Jz. 3, uk. 278 na humo amesema ni bidaa, Timidhiy, Abu Daud na wengineo. 51 Muntakhabu Kanzul ummal hamishi ya musnad Jz. 3, uk. 276, Dalailus Swidiq Jz. 3, sehemu 2 , uk. 99 kutoka katika Kanzul Ummal Jz. 4, uk. 266. 52 Sharhu tajirid cha Qaushaji bahathul Imamah Uk: 484, kanzul umal Jz. 2, uk. 158 kutoka kwa Twabari katika Al Mustaniri, al-Ghadir Jz. 6 uk. 213 amesema ameitoa Twabar katika Mustabin kutoka kwa Umar na amesimulia kutoka kwa Twabar Sheikh Ali al bayadh katika kitabu chake Aswiratwal Mustaqimah na Jawahirul Akhibar wal Athar Jz. 2, uk. 192 kutoka kwa Taftazan katika hamishi ya sharhul Adhid. 53 Sharihu Tajirid cha Al Qaushaji uk: 484 49

35


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

wahyi unaofunuliwa na nyinginezo kati ya aya. Lakini udhuru sahihi ni kwamba khalifa wa pili aliona - kwa mtazamo wake – kwamba watu watakaposikia kwamba swala ni amali bora basi wataijali zaidi swala na kuacha jihadi, kama ambavyo khalifa mwenyewe ataeleza hayo katika yafuatayo: 15. Al-Halabi amesema: “Imenukuliwa kutoka kwa Ibnu Umar na kutoka kwa Ali bin Husein (r.a.): Hakika wao walikuwa wanasema katika adhana yao baada ya hayya a’laal–falaah: Hayya a’laa khayril a’mal.”54 16. Amesema Alau Diyni Al-Hanafiy katika kitabu Tal wih katika sharhi ya Al-Jami’us -Sahihi: Na ama hayya a’laa khayril a’mal ameitaja Ibnu Hazim kwamba imesihi kutoka kwa Abdullah bin Umar, Abi Umamah na Sahal bin Hanif: Kwamba wao walikuwa wanasema: Hayya a’laa khayril a’mal, kisha akasema: Na Ali bin Huseini alikuwa akifanya hivyo. 55 17. Amesema As-Sayid Al–Murtadhaa: Na wamepokea wengine kwamba hayo ni kati ya yaliyokuwa yanasemwa katika baadhi ya zama ya Nabii (s.a.w.w.) lakini imedaiwa: Kwamba yamefutwa na kuondolewa na mwenye kudai hayo ni juu yake alete dalili, na wala haipati. 56 18. Kutoka kwa Abdur-Razak kutoka kwa Maamar kutoka kwa Ibnu Hamad kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake kutoka kwa Nabii (s.a.w.w.) katika hadith ya miraji amesema: ‘’Kisha akasema Jibril akaweka kidole chake cha shahada cha mkono wake wa kulia katika sikio lake basi Siratul Halabiyah chapa ya 1382H Babul adhana Jz. 2, uk. 105 Dalailus Swidiq Jz. 3, sehemu 2, uk. 100 kutoka katika Mabadiul fiqihi l’Islaamiy cha Uruf uk. 38, Al Hiliy Jz. 2, uk. 160 56 Al Intiswar uk. 39 54 55

36


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

akaadhini mara mbili mbili anasema katika mwisho wake: Hayya a’laa khayril a’mal mara mbili. 57 19. Ibnu Nabaha alikuwa anasema katika adhana yake: Hayya a’laa khayril a’mal. 20. Amesema Said Al-Arafii: “Ama Hayya a’laa khayril a’mal, madhehebu ya Ahlul bait ni kuiweka baina ya hayya a’laalfalah na Allahu akbar, na dalili zao juu ya hilo ni nyingi katika vitabu vyao kama ifuatavyo: Amepokea Baihaqiy… 58 Kisha baadhi wametaja ambayo tumeyaashiria kwayo hapo mwanzo, na baada ya haya haisihi kauli ya baadhi: Kwamba hiyo ni makuruhu kwa sababu haikuthibiti kutoka kwa Nabii (s.a.w.w.).59 Kwani umeshajua kwamba madhehebu ya Ahlul-Bait ambao wao ndio moja ya vizito viwili, na kauli ya hayya alaa khairil amal imebakia kuwa ni nembo ya Al-Alawiyina, Ahlul–Bait na wafuasi wao kwa muda wote hadi kwamba thaura ya Husein bin Ali Swahibul-Fakh ilikuwa ni kwamba: 21. Abdullah bin Hasani Al Afutwasi alipanda mnara ambao uko mbele ya kichwa cha Nabii (s.a.w.w.) akamwambia mwadhini: Adhini Hayya a’laa khayril a’mal, alipoangalia upanga uliopo mkononi mwake akaadhini na Maamar akasikia (yaani gavana wa Madina kutoka kwa Mansur), akahisi shari akashangaa na akapiga kelele: Fungieni baghali mlango na nipeni maji. 60 Saad Suud uk. 100, Al Bihar Jz. 4, uk. 107, Jamiul Ahadithis Shiah Jz. 2, uk. 221 Dalais Swidiq Jz. 3, sehemu 2, uk. 100 kutoka katika Mabadiul–Islaamiy cha Al Uruf uk.38 59 Al-Baharu raiq Jz. 1, uk. 275 kutoka katika Sharhil–Madhihab na Sunanu Baihaqi 60 Maqaatil Twalibiyna uk. 446 57 58

37


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

22. Tanukh ametaja kwamba: Abu Faraj amempa habari kwamba yeye alisikia katika zama yake wanasema katika adhana kipande hiki cha Hayya a’laa khayril a’mal. 61 23. Al Halabi amesema: “Na baadhi yao wamesema kwamba katika dola ya Buwaihi Shia walikuwa wanasema: Baada ya hayya a’laa mbili, Hayya a’laa khayril a’mal. Walipokuja Saljuqiyah wakawakataza waadhini hilo na wakawaamuru waseme katika adhana ya asubuhi badala ya hilo As -swalatu khayrum minan naumi mara mbili na hiyo ilikuwa mwaka 448 H. 62 24. Imepokewa kutoka kwa Ali (a.s.) alisema nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) anasema: ‘’Jueni kwamba amali zenu bora ni Swala na akamwambia Bilal aadhini: Hayya a’laa khayril a’mal, ameeleza katika Shifaa. 63 25. Amepokea Muhammad bin Mansur katika kitabu chake Al-Jamiu kwa isnadi yake kutoka kwa watu wanaoridhiwa kutoka kwa Abu Mahudhura moja wa waadhini wa Mtume (s.a.w.w.) kwamba amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu aliniamuru niseme katika adhana: Hayya a’laa khayril a’mal. 64 26. Imepokewa kutoka kwa Muhammad bin Mansur kwamba Abul Qasim (a.s.) alimwamuru aadhini na aseme hivyo (yaani Hayya a’laa khayril a’mal ) katika adhana yake, 61

Nashawarul Muhadharat Jz. 2, uk. 133

Siratul Halabiyah chapa ya mwaka 1382 babul adhana Jz. 2, uk. 105 Jawahirul Akhibar wal Athar ameitoa katika Bahar Zakhir Jz. 2, uk: 191, Imam Swadiq wal Madhaahibil Arubaah Jz. 5, uk. 284 64 Al Bahru Zakhir Jz. 2 uk.192, Jawahirul Akhibar wal Athar ameitoa katika Bahar Zakhir Jz. 2, uk: 191 62 63

38


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

akasema: Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ameamuru hayo, hivi ndivyo ilivyo katika Shifaa. 65 27. Kutoka kwa Abu Bakar Ahmad bin Muhammad As-Sairiy: Hakika yeye amemsikia Mussa bin Haruna kutoka kwa AlHaman kutoka kwa Abu Bakar bin Ayashi kutoka kwa Abdul-Aziz bin Rafii kutoka kwa Abu Mahudhura amesema: Nilikuwa kijana Nabii (s.a.w.w.) akaniambia: Jaalia katika mwisho wa adhana yako Hayya a’laa khayril a’mal. 66 28. Na katika Shifaa, kutoka kwa Hadhil bin Bilal Al-Madain amesema: ‘’Nilimsikia Ibnu Mahdhura anasema: Hayya a’laa khayril a’mal.’’ 67 29. Kutoka kwa Zayd bin Arqam kwamba yeye aliadhini kwa Hayya a’laa khayril a’mal. 68 30. Amesema Shaukany kwa kunukuu kutoka katika KitabulAhkami: ‘’Imeshasihi kwetu: Hayya a’laa khayril a’mal ilikuwepo katika zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ikiadhiniwa kwayo, na haikuondolewa isipokuwa katika zama za Umar.’’69 31. Na hivi ndivyo alivyosema Al-Hasan bin Yahya.70 32. Tumepokea kutoka kwa Ali bin Al-Husein (a.s.): Kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuwa anapomsikia mwadhini husema kama anavyosema, na anaposema: Jawaihirul Akhbar wal Athar Jz. 2, uk. 191 Mizanul Itidal cha Dhahabi Jz. 1, uk. 139, Lisanul Mizan cha Al Asqalaan Jz. 1, uk. 268. 67 Ibid 68 Imams Swadiq wal Madhaahibil Arubaah Jz. 5, Uk: 283 69 Nailul Autar Jz. 2, uk. 321. 70 Ibid 65 66

39


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

Haya a’laas-swala, hayya a’lal-falaah, hayya a’laa khayril a’mal, husema: Laa haula walaa Quwata illaa billahi.71 33. Kutoka kwa Muhammad bin Ali kutoka kwa baba yake Ali bin Al-Husein (a.s.) kwamba yeye alikuwa anaposema: Haya a’laal-falah kisha husema: Hayya a’laa khayril a’mal.72 34. Amesema Zarkishi katika Bahrul Muhit: “Na miongoni mwayo ni ambayo humo kuna ikhitilafu kama ambavyo ipo katika mengineyo, Ibnu Umar ambaye ndiye tegemeo la watu wa Madina alikuwa anaona kuwa vipengele vya adhana na kuadhini ni Hayya a’laa khayril a’mal. 73 35. Na katika kitabu cha As-Sana’ani kwa matamshi yake: “Ni sahihi kwamba adhana ilianza kwa Hayya a’laa khayril a’mal”. 74 36. Na katika Raudhu Nadhar: “Na wamesema wengi wa maulamaa wa madhehebu ya maliki, hanafi, na shafii: Kwamba Hayya a’laa khayril a’mal ilikuwa ni katika matamko ya adhana.” 75 37. Amesema Ibnu Qasim Anuriy Al-Iskindariy: “Alipowasili Al-Ghazal Misri aliamuru iadhiniwe katika msikiti wa Ijumaa wa Ibnu Twahina kwa Hayya a’laa khayril a’mal. Ikadumu hivyo katika adhana hadi ilipomalizika dola ya Al-Abidiyna mwaka 567, hapo ikamalizika kutajwa Hayya a’laa khayril a’mal kwa kumalizika dola yao. Aliondoa hilo Da’aimul–Isalaam Jz.1, uk. 145, Al Bihar Jz. 84, uk. 179 Jawahirul-Akhibari wal Athar cha Saadiy Jz. 2, uk. 192 73 Raudhu Nadhir Jz. 1, uk. 542 71 72

74 75

Ibid Ibid

40


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

Swalahu Diyn Yusufu bin Najim Diyn Ayub.76 Na amesema: Kwamba Al–Abidiyna wanaodai kuwa wao ni wafuasi wa Fatima walikuwa ni Shia, katika adhana yao baada ya hayya alalfalah, wanasema Hayya a’laa khayril a’ma,l wanaisema mara mbili kama wanavyosema Zaidiyya katika adhana yao Makka na Madina katika siku zisizokuwa za Hijja, vile vile katika Sa’adat na sehemu zingine katika nchi ya Yemeni. 77

SABABU YA KUONDOA IBARA HII Ama ni kwa nini ibara hii imeondolewa katika adhana, Khalifa wa pili mwenyewe alikwishasema wazi siri ya hilo. Ibnu Shadhan amesema aliwaeleza Ahlus Sunnah wal Jamaa: 38. Na wamepokea kwa Abu Yusuf Al–Qadh, amepokea Muhammad bin Al–Hasan na As-habi zake na kutoka kwa Abu Hanifa wamesema: “Adhana zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na zama za Abu Bakr na mwanzo wa ukhalifa wa Umar ilikuwa ikiadhiniwa humo: Hayya a’laa khayril a’mal. Umar bin Khattab akasema: “Hakika mimi ninahofia watu kuijali sana Swala inaposemwa: Hayya a’laa khayril a’mal.” 78 39, 40 na 41 – Na yamepokewa mfano wa hayo kutoka kwa Abu Abdillah As-Swadiq, Abu Jafar, Al-Baaqir na Ibnu Abbas (a.s.). 79 76

Al–Ilimam bil–I’laam fiyma jarat bihi Al–Ahkaam Jz. 4, uk: 34

Ibid uk. 32, 40 na 41 Al-Idhaha cha cha Ibnu Shadhan uk. 201 na 2021 79 Da’aimul – Islaam Jz. 1, uk. 142, Al-Bihar Jz. 84, uk. 156, Ilalu Sharaiu Jz. 1 uk. 56 n.k 77 78

41


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

KAULI KUHUSU RAI HII Sisi hata kama tunaona kuwa: Jambo la jihadi katika zama za Mtume (s.a.w.w.) ni tukufu mno na watu walikuwa na haja nalo zaidi kuliko zama za Umar, ila sisi hatuwezi tukasema kwamba ijitihadi ya Khalifa wa pili ilikuwa na nguvu na yenye kutosheleza; kama ambavyo hapakuzingatiwa pande zote na sababu za kadhia hii kwa namna inayotosheleza na kukubalika, ila sisi wakati huo huo tunapata kwamba sababu ya kisingizio cha Umar kilichotangulia kuonyesha kuacha kipengele hiki cha adhana kilikuwa ni cha muda tu. Kilipelekea hivyo kwa mtazamo wake na huenda hakufikiria – kamwe – kutoa kipengele hiki cha adhana milele, bali ni kwa muda maalum tu aliouona unahitaji maamuzi haya. Kama hivyo ndivyo ilivyotokea, basi sisi hatuwezi kufahamu kisingizio cha kuendelea kuacha kipengele hiki katika adhana katika wakati huu ambao hakuna tena kisingizio hicho. Kwa nini sote haturejei katika Sunnah ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Ahlul Bait wake watoharifu?

MAANGAMIO KWA WENYE KUBADILISHA Umma wa Kiislaam ni umma bora kuliko umma zote zilizowahi kuja hapa duniani na Nabii wa umma huu ni Nabii bora kuliko Manabii wote, na kwamba yeye ndiye aliyefunga pazia la Manabii wa Mwenyezi Mungu. Mtume wetu ndio kipenzi cha Mwenyezi Mungu, na ni rehema kwa walimwengu wote. Hakika alijitahidi kwa uwezo wake wote kuuandaa umma huu ili kufikia upeo wa juu katika kumnyenyekea na kumtii Mwenyezi Mungu. Aliwaandalia mazingira mazuri yanayowafanya wawe karibu na Mwenyezi Mungu na 42


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

hakuna jambo linalowafanya wawe karibu na Mwenyezi Mungu na linalowafanya waingie Peponi ila aliwaonyesha. Na wala hakuna jambo linalowaweka mbali na Mwenyezi Mungu na kuwapeleka motoni ila aliwaonya na kuwahadharisha kwalo. Kama zilivyokuwa umma zilizotangulia kwamba hawakosekani watu wema na waovu, hivyo kwa muda wa miaka 23, Nabii aliwaandaa wafuasi wake na waumini kwa ujumla na walipatikana wafuasi bora na wema kwa kiwango cha juu kabisa mfano wa Imam Ali bin Abu Talib, Abu Dharr, Salman, Ammar, Miqidad n.k. Lakini sambamba na hao pia walipatikana watu walioshindwa kufaidika na malezi na mafunzo mazuri ya Nabii (s.a.w.w.), na hawa sio wengine bali ni wanafiki ambao walidhihirisha Uislam katika ndimi zao na kuficha ukafiri katika nyoyo zao. Hali hii haikuwa katika umma wa Kiislam tu, bali ni hali ya kawaida katika jamii ya binadamu, kwani Manabii waliotangulia walikabiliwa na hali kama hii vile vile. Mfano mzuri hapa na uliowazi ni ule wa Nabii Nuhu na kaumu yake. Pamoja na kwamba walipata wafuasi ila walikabiliwa na upinzani mkali katika kaumu zao, na hasa upinzani wa ndani kama vile watoto, wake n.k. ambao ndio walikuwa waharibifu wakubwa wa da’awa ya Manabii hao. Vile vile Mtume (s.a.w.w.) alikabiliwa na upinzani wa aina hii katika umma wake. Mtume (s.a.w.w.) katika kipindi cha Makka alipambana zaidi na washirikina wa kikuraishi, lakini alipohamia Madina na kuunda dola ya Kiislaam alikabiliwa na upinzani wa ndani yaani wanafiki, watu ambao walidhihirisha kuunga mkono harakati za Kiislam lakini ndani ya nyoyo zao walikuwa wakifanya kila hila na njama za kuizima na kuididimiza dola changa ya Kiislamu. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kupitia wahyi mara kwa mara alikuwa akizifichua njama hizo za wanafiki na kuwaeleza bayana yale wanayoyadhamiria katika nyoyo zao. Jambo hili lilisaidia 43


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

kwa kiasi kikubwa kuwatambua baadhi ya wanafiki, hivyo Mtume (s.a.w.w.) aliwafahamu na waumini pia wakawatambua. Kisha Mwenyezi Mungu alizidi kumweleza Nabii wake kuwa kuna wanafiki anaowafahamu na kuna ambao hawafahamu. Lakini kwa kusoma Qur’ani tukufu tunaweza kupata vielelezo ambavyo vinaweza kutusaidia kuwatambua watu wa aina hii kufuatana na matendo yao. Katika vita ya Uhud masahaba walipotimua mbio na kumwacha Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ila wale waliohifadhiwa kwa Usmah Mfano wa Ali bin Abi Twalib.80 Inasimuliwa kuwa mmoja kati ya waliokimbia alikuwa analia sana kila anapokumbuka tukio hilo la kusikitisha na kusema: “…..nilikuwa wa mwanzo kurejea siku ya Uhud basi nikamuona mtu anapigana pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) nikasema na awe Twalha kwani yamenipita yaliyopita, awe ni mtu kutoka katika kaumu yangu.”81 Katika tukio hilo Mwenyezi Mungu aliteremsha Aya kali kushutumu hali hii mbaya ya masahaba kwa kusema:

ٌ ‫ُح َّم ٌد إ اَّل َر ُس‬ ‫الر ُس ُل أَ َفإِ ْن‬ ُّ ‫ول َق ْد َخلَ ْت ِم ْن َق ْبلِ ِه‬ ِ َ ‫َو َما م‬ َ ‫َم‬ ‫ات أَ ْو ُق ِت َل ا ْن َقلَبْتُ ْم َعلَى أَ ْع َق ِاب ُك ْم َو َم ْن َي ْن َقلِ ْب َعلَى‬ َّ‫ض َّر ه‬ َّ َُّ‫اللَ َشي ًْئا َو َس َي ْجزي الله‬ ُ ‫َع ِق َب ْي ِه َفلَ ْن َي‬ َ ‫الشا ِك ِر‬ ‫ين‬ ِ “Hakuwa Muhammad ila ni Mtume na wameshapita kabla yake Mitume. Je, akiuliwa au akifa mtarejea tena katika ukafiri? Na atakayerejea katika ukafiri hatomdhuru Mwenyezi Mungu kwa chochote na Mwenyezi Mungu atawalipa wenye kushukuru.” (Al-Imran: 144.) 80 81

Hayatu Muhammad cha Hasanaini Haikal uk: 298 na 299. Twabaqat Ibnu Saad Jz. 3, uk. 155, Siratul Halabiyah Jz. 3, uk. 58, Tarikhul Khamis Jz. 1, uk. 431, Al-Bidayatu wan Nihayyah Jz. 4, uk. 29 44


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

Hii ni kwa kuwa baadhi ya masahaba waliokimbia, walikwishadhani kuwa Mtume amekwishauliwa na tayari walishaanza kutafuta mtu atakaye waombea msamaha kwa Abu Sufiyan ili warudi katika dini yao ya zamani yaani ukafiri. “Wakuu wa Muhajirina waliokimbia waliokuwa juu ya jabali hawakumpinga yule aliyesema kuwa anataka kumfanya Ibnu Ubayyi kuwa wasila kwa Abu Sufiyan na kuomba kwao arejee katika dini yao ya awali au mfano wa hayo, ambapo inaonyesha raghaba yao ya kuritadi na kutoka katika Uislam, kumili kwao kwa washirikina na kuafikiana nao.”82 Msukosuko huu ulibainisha aina ya imani ya baadhi ya masahaba kwamba wao wapo na Mtume kwa masilahi tu, na endapo watayapata au Mtume atakapouliwa au kufa basi wao watarejea tena katika ukafiri wao, na historia ni shahidi mzuri, pale tu Mtume alipofariki baadhi yao waliritadi. Aidha Mwenyezi Mungu katika Suratul Hujurat amekemea vikali sana muamala mbaya waliokuwa nao baadhi ya masahaba kwa Mtume wao na kuwatishia wale wote wenye muamala kama huo kufutilia mbali amali zao zilizotangulia:

َّ‫َيا أَُّي َها ال‬ َّ‫ْن َي َدي ه‬ ِّ ‫ين آ َمنُوا اَل تُ َق‬ َ َ ‫اللِ َو َر ُسولِ ِه‬ ‫ي‬ ‫ب‬ ‫ُوا‬ ‫م‬ ‫د‬ ‫ذ‬ َ ِ ِ َ َّ َّ‫اللَ إ َّن ه‬ َّ‫َّ ُ ه‬ َ ‫اللَ َس ِمي ٌع َعلِي ٌم َيا أ ُّي َها ال ِذ‬ ‫ين آ َمنُوا اَل‬ ِ ‫َواتقوا‬ ‫ص ْو ِت النَّ ِب ِّي َو اَل َت ْج َه ُروا‬ ْ َ‫َت ْر َفعُوا أ‬ َ ‫ص َوا َت ُك ْم َف ْو َق‬ ُ ِ ‫لَ ُه ب ْال َق ْول َك َجهْر َبع‬ ‫ْض أَ ْن َت ْح َب َط أَ ْع َمالُ ُك ْم‬ ِ ِ ٍ ‫ْضك ْم لَِبع‬ ِ َ ‫ُر‬ ‫ون‬ ُ ‫َوأَ ْنتُ ْم اَل َت ْشع‬ 82

As-Sahihu min Siratin Nabiyil a’adham Jz. 4, uk: 285. 45


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

“Enyi mlioamini! Msimtangulie Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, muogopeni Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia na Mjuzi. Enyi mlioamini! Msinyanyue sauti zenu juu ya sauti ya Nabii wala msiseme naye kama mnavyosemezana baadhi kwa baadhi yenu, amali zenu zisije zikaporomoka hali ya kuwa nyinyi hamjui….” (Suratul Hujurat: 1 – 2).

Aya zinazoendelea zinazungumzia kumjadili Mtume katika maamuzi yake na kumpinga, mambo yote haya ni mabaya sana kumfanyia Mtume na yanasababisha kuporomoka kwa amali zote za mtu alizozifanya katika maisha yake. Kwa mtazamo wa haraka haya yanaonekana ni mambo ya kawaida lakini kwa mtu ambaye ni kiongozi tena kiongozi aliyeteuliwa na Mwenyezi Mungu kwa viumbe Vyake mambo ni tofauti kabisa, hayo huhesabiwa kuwa ni kosa kubwa mno kwani hilo linaonyesha utovu wa nidhamu na kutomtii kiongozi. Kama hali ni hii katika mambo kama haya, mambo yatakuwaje kwa mtu ambaye ameondoa ya Mtume na akaweka ya kwake? Bila shaka mambo yatakuwa kama alivyoeleza Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) katika Sahih Bukhari: “Sa’ad amesema: “Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Mimi nitawatangulia katika hawdh (birika) atakayenifikia atakunywa kwayo na atakayekunywa kwayo hatapata kiu kamwe baada yake. Watanijia watu nawajua na wananijua kisha kutawekwa kizuizi baina yangu na wao. Akasema nilimsikia akiongezea: Akasema: Hakika wao ni katika watu wangu: Itasemwa: Hakika wewe hujui waliyoyabadilisha baada yako, basi nitasema: Awe mbali aliyebadilisha baada yangu. 83 83

Sahih Bukhari Jz. 9, uk: 114 kitabul fitina babu fitani 46


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

Amesema Abdillah kwamba amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.): “Mimi nitawatangulia katika hawdh, hakika wataletwa wanaume miongoni mwenu mpaka nitakapowakaribia ili niwapatie (maji) watazuiwa dhidi yangu basi nitasema: Ewe Mwenyezi Mungu, masahaba wangu. Atasema: Hujui waliyoyazua baada yako. 84 Kutoka kwa Abu Huraira kwamba yeye alikuwa anasimulia kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Litanijia Siku ya Kiyama kundi kati ya masahaba wangu litazuiliwa kufikia hawdh, nitasema: Ewe Mola Wangu! Masahaba wangu. Atasema: Hakika wewe hujui waliyoyazua baada yako, hakika wao waliritadi na kurudi nyuma.’’ 85 Kuna riwaya nyingine inasema: “Baada ya masahaba kuingizwa motoni Nabii atasema: Sioni akiwaacha isipokuwa kama mfano wa hamalu (yaani ngamia) wasio na mchungaji.86 Ibnu Hajar amesema: ‘’Hamalu kwa fataha mbili, ni ngamia asiye na mchungaji, na maana yake ni kwamba: Hawataingia katika hawdh miongoni mwao isipokuwa wachache kwa sababu ngamia wasiokuwa na mchungaji kati ya ngamia ni wachache ukilinganisha na wengine2.87 Pia imekuja katika kamusi “Lisanul Arab na Nihaaya ya Ibnu Athir: ‘’Yaani watakaofaulu kati yao ni wachache kwa maana ya uchache wa ngamia wenye kupotea.” 88 Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu atujaalie kuwa miongoni mwa wanaoshikamana na Mtume na kizazi chake chema na atufufue pamoja na Mtume Muhammad (s.a.w.w.) na kizazi chake Sahih Bukhari Jz. 9, uk: 114 kitabul fitina babul fitani Ibid 86 Sahih Bukhari Kitabur-Riqaaq babu fiyl hawdh. 87 Fat-hul Barri Jz. 11, uk: 401 88 Lisanul Arab Jz 15, uk: 135, Nihayyatu fiy ghariybil Hadith Jz. 5, uk. 274. 84 85

47


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

na atuingize Peponi pamoja nao naye ni mwenye kusikia maombi. Rehema na amani zimwendee Mtume Muhammad na kizazi chake kitukufu. Wabillahi Tawfiq. Wasalaam Abdul karim J. Nkusui 27 Mei 2005 / Rabiul - Akhir 1426 A.H.

48


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1. Qur’an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka ­Thelathini 2.

Uharamisho wa Riba

3.

Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza

4.

Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili

5.

Hekaya za Bahlul

6.

Muhanga wa Imamu Husein (A.S.)

7.

Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.)

8.

Hijab vazi Bora

9.

Ukweli wa Shia Ithnaashari

10. Madhambi Makuu 11. Mbingu imenikirimu 12. Abdallah Ibn Saba 13. Khadijatul Kubra 14. Utumwa 15. Umakini katika Swala 16. Misingi ya Maarifa 17. Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia 49


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

18. Bilal wa Afrika 19. Abudharr 20. Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu 21. Salman Farsi 22. Ammar Yasir 23. Qur’an na Hadithi 24. Elimu ya Nafsi 25. Yajue Madhehebu ya Shia 26. Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur’an Tukufu 27. Al-Wahda 28. Ponyo kutoka katika Qur’an 29. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii 30. Mashukio ya Akhera 31. Al Amali 32. Dua Indal Ahlul Bayt 33. Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. 34. Haki za wanawake katika Uislamu 35. Mwenyezi Mungu na sifa zake 36. Kumswalia Mtume (s) 37. Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) 38. Adhana 39

Upendo katika Ukristo na Uislamu 50


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

40. Tiba ya Maradhi ya Kimaadili 41. Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu 42. Kupaka juu ya khofu 43. Kukusanya swala mbili 44. Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara 45. Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya 46. Kusujudu juu ya udongo 47. Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) 48. Tarawehe 49. Malumbano baina ya Sunni na Shia 50. Kupunguza Swala safarini 51. Kufungua safarini 52. Umaasumu wa Manabii 53. Qur’an inatoa changamoto 54. as-Salaatu Khayrun Mina -’n Nawm 55. Uadilifu wa Masahaba 56. Dua e Kumayl 57. Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu 58. Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake 59. Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata 60. Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mtume Muhammad (s)

51


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

61. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza 62. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili 63. Kuzuru Makaburi 64. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza 65. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili 66. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu 67. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne 68. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano 69. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita 70. Tujifunze Misingi Ya Dini 71. Sala ni Nguzo ya Dini 72. Mikesha Ya Peshawar 73. Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu 74. Ubora wa Imam ‘Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia ­iliyonyooka 75. Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake 76. Liqaa-u-llaah 77. Muhammad (s) Mtume wa Allah 78. Amani na Jihadi Katika Uislamu 79. Uislamu Ulienea Vipi? 80. Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) 81. Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s)

52


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

82. Urejeo (al-Raja’a ) 83. Mazingira 84. Utokezo (al - Badau) 85. Hukumu ya kujenga juu ya makaburi 86. Swala ya maiti na kumlilia maiti 87. Uislamu na Uwingi wa Dini 88. Mtoto mwema 89. Adabu za Sokoni 90. Johari za hekima kwa vijana 91. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza 92. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili 93. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu 94. Tawasali 95. Imam Mahdi katika Usunni na Ushia 96. Hukumu za Mgonjwa 97. Sadaka yenye kuendelea 98. Msahafu wa Imam Ali 99. Ngano ya kwamba Qur’ani imebadilishwa 100. Idil Ghadiri 101. Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu 102 Hukumu zinazomuhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi 103. Huduma ya Afya katika Uislamu 53


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

104. Sunan an-Nabii 105. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) 106. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) 107. Shahiid Mfiadini 108. Kumsalia Nabii (s.a.w) 109. Ujumbe -Sehemu ya Kwanza 110. Ujumbe - Sehemu ya Pili 111. Ujumbe - Sehemu ya Tatu 112. Ujumbe - Sehemu ya Nne 113. Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu 114. Hadithi ya Thaqalain 115. Ndoa ya Mutaa 116. Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza 117. Ukweli uliopotea sehemu ya Pili 118. Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu 119. Ukweli uliopotea sehemu ya Nne 120. Ukweli uliopotea sehemu ya Tano 121. Mkutano wa Maulamaa wa Baghdad 122. Safari ya kuifuata Nuru 123. Fatima al-Zahra 124. Myahudi wa Kimataifa 125. Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi 54


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

126. Visa vya kweli sehemu ya Kwanza 127. Visa vya kweli sehemu ya Pili 128. Elimu ya Ghaibu ya Maimamu 129. Mwanadamu na Mustakabali wake 130. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) 131. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) 132. Khairul Bariyyah 133. Uislamu na mafunzo ya kimalezi 134. Vijana ni Hazina ya Uislamu 135. Yafaayo kijamii 136. Tabaruku 137. Taqiyya 138. Vikao vya furaha 139. Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 140. Visa vya wachamungu 141. Falsafa ya Dini 142. Azadari-Kuhuzunika na Kuomboleza 143. Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah 144. Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu 145. Kuonekana kwa Allah 146. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) 55


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

147. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) 148. Ndugu na Jirani 149. Ushia ndani ya Usunni 150. Maswali na Majibu 151. Mafunzo ya hukmu za ibada 152. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1 153 Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2 154. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 155. Abu Huraira 156. Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. 157. Mazingatio kutoka katika Qur’an - Sehemu ya Kwanza 158. Mazingatio kutoka kaitka Qur’an - Sehemu ya Pili 159. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza 160. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili 161. Qur’ani Tukufu – Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili 162. Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) 163. Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani 164. Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu 165. Uislamu Safi 166. Majlisi za Imam Husein Majumbani 167. Je, Kufunga Mikono 168. Uislam wa Shia 56


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

169. Amali za Makka 170. Amali za Madina 171. Asili ya Madhehebu katika Uislamu 172. Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi 173. Ukweli uliofichika katika neno la Allah 174. Uislamu na Mifumo ya Uchumi 175. Umoja wa Kiislamu na Furaha 176. Mas’ala ya Kifiqhi 177. Jifunze kusoma Qur’ani 178. As-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah 179. Hayya ‘Alaa Khayri’l-’Amal Katika Adhana 180. Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura 181. Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na ­Ramadhani) 182. Uadilifu katika Uislamu 183. Mahdi katika Sunna 184. Maswali Ya Uchunguzi Kuhusu Uislam 185. Kazi na Bidii ni njia ya maendeleo 186. Abu Talib – Jabali Imara la Imani 187. Ujenzi na Utakaso wa Nafsi 188. Vijana na Matarajio ya Baadaye 189. Usalafi – Historia yake, maana yake na lengo lake

57


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

190. Ushia – Hoja na Majibu 191. Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) 192. Maombolezo – Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) 193. Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu 194. Takwa 195. Upotoshaji dhahiri katika Turathi (Hazina) ya Kiislamu 196. Amirul Muuminina (‘as) na Makhalifa 197. Uongozi na Utawala katika Mwenendo wa Imam ‘Ali (‘a) 198. Kuvunja hoja iliyotumika kutetea Uimamu wa AbuBakr 199. Adabu za vikao na mazungumzo 200. Hija ya Kuaga 201. Uwazi baina ya Maslahi na Vikwazo 202. Fadhila za watukufu watano katika Sahih Sita 203. Mdahalo baina ya Mwanachuoni wa Kisunni na Mwanachuoni wa Kishia (Al-Muraja’aat) 204. Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (as) 205. Mjadala wa Kiitikadi 206. Mtazamo kuhusu msuguano wa Kimadhehebu 207. Nchi na Uraia – Haki na wajibu kwa Taifa 208. Mtazamo wa Ibn Taymiyyah juu ya Imam Ali (as) 209. Uongozi wa Kidini – Maelekezo na Utekelezaji wa Kijamii 210. Maadili ya Ashura

58


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

211. Mshumaa – Shahidi na Kifo cha Kishahidi 212. Mizani ya Hekima – Hadithi za Ahlul Bait (as) – Sehemu ya Kwanza 213. Imam Ali na Mambo ya Umma 214. Imam Ali na Mfumo wa Usawa 215. Mwanamke na Sharia 216. Mfumo wa Wilaya 217. Vipi Tutaishinda Hofu? 218. Kumswalia Mtume ni Ufunguo wa Utatuzi wa Matatizo 219. Mahali na Mali za Umma 220. Nahjul-Balagha – Majmua ya Khutba, Amri, Barua, Risala, Mawaidha na Semi za Amirul-Muuminin Ali bin Abu Talib (a.s.) 221. Mukhtar – Shujaa aliyelipiza kisasi dhidi ya wauaji wa Imam Husein (as) hapo Karbala 222. Uimamu na Tamko la Kutawazwa 223. Imam Husain ni Mfumo wa Marekebisho na Mageuzi 224. Saada Kamili – Kitabu cha Kiada cha Maadili 225. Maeneo ya Umma na Mali Zake 226. Imam Hasan na Mfumo wa Kujenga Jamii 227. Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

59


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

KOPI NNE ZIFUATAZO ­ZIMETAFSIRIWA KWA LUGHA KINYARWANDA 1.

Amateka Na Aba’Khalifa

2.

Nyuma yaho naje kuyoboka

3.

Amavu n’amavuko by’ubushiya

4.

Shiya na Hadithi

60


Adhana ni Ndoto au ni Wahyi?

ORODHA YA VITABU VILIVYO ­CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION KWA LUGHA YA KIFARANSA 1.

Livre Islamique

61


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.