Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
Kimeandikwa na: Ali Swalah
Kimetarjumiwa na: Alhaji Hemedi Lubumba (Abul Batul)
Kimehaririwa na: Alhaji Ramadhani S. K. Shemahimbo
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 1
7/5/2013 9:06:10 AM
ﺗﺮﺟﻤﺔ ﺗﺮﺟﻤﺔ الحكم واالدارة في نھج االمام علي )ع( الحكم واالدارة في نھج واالدارة الحكم نھج )ع( االمامفيعلي االمام علي )ع( ﺗﺄ ﻟﻴﻒ ﻋﻠﻲ ﺻﻼح
ﺗﺄ ﻟﻴﻒ ﺻﻼح ﻋﻠﻲ ﻟﻴﻒ ﺗﺄ ﻋﻠﻲ ﺻﻼح ﻣﻦ اﻟﻠﻐﺔ اﻟﻌﺮﺑﻴﺔ إﻟﻰ اﻟﻠﻐﺔ اﻟﺴﻮاﺣﻠﻴﺔ 7/5/2013 9:06:10 AM
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 2
©Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION
ISBN: 978 - 9987 - 17 - 034 - 0
Kimeandikwa na: Ali Swalah
Kimetarjumiwa na: Hemedi Lubumba Selemani (Abul Batul)
Kimehaririwa na: Alhaji Ramadhani Saleh Kanju Shemahimbo
Kimepangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation
Toleo la kwanza: Septemba 2013 Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. - 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: w.w.w.alitrah.info
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 3
7/5/2013 9:06:11 AM
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 4
7/5/2013 9:06:11 AM
YALIYOMO Neno la Mchapishaji...............................................................................01 Utangulizi...............................................................................................03 Hebu tusimame pamoja na msomaji.....................................................06
Faslu ya Kwanza: Dhana za kitume kutoka ndani ya Nahjul-Balaghah.........................09 Kwa nini tunajiweka karibu na Nahjul-Balaghah?.............................09 Kwanza: Upande wa Utu wa Kitume:................................................10 Pili: Upande wa Jamii yenye Imani:................................................. 11 Tatu: Upande wa madhumuni ya Dhana za Uislamu:.......................12 Nne: Upande wa Siasa ya Kiislamu:..................................................13 Siasa ni Sehemu ya Uislamu?................................................................15 Kwanza: Maana ya siasa katika Uislamu...........................................17 Pili: Sifa za kiongozi mwenye kuwasimamia waja............................17 Siasa katika Nahjul-Balaghah.................................................................20 Kwa Raia wa Mataifa ya Kiislamu:.....................................................20 Kwa Viongozi na Magavana:..............................................................24 Kwa Maadui zake na Makundi ya Upinzani:.....................................29
v
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 5
7/5/2013 9:06:11 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
Faslu ya Pili: Waraka wa Imam kwenda kwa Malik al-Ashtar.................................35 Mamlaka ambayo Imamu (as) alimkabidhi al-Ashtar:......................35 Kwanza: Shughuli za Kiuchumi:........................................................36 Pili: Shughuli za Kijeshi:....................................................................37 Tatu: Shughuli za Kijamii:..................................................................38 Nne: Shughuli za Kimaendeleo:........................................................38 Ulazima wa Mtawala kuidhibiti Nafsi yake............................................40 Sifa za Uongozi.......................................................................................42 Kwanza: Uchamungu:........................................................................42 Pili: Uwezo wa Kielimu:.....................................................................43 Tatu: Uwezo wa Kivitendo:................................................................44 Kufaidika na uzoefu wa waliotangulia:..................................................45 Kutosukumwa na matamanio na ubinafsi:............................................47 Muamala wa Mtawala kwa raia:.............................................................48 Tiba ya kiburi:........................................................................................53 Kushikamana na uadilifu:......................................................................54 Dhulma lazima imwangushe:................................................................56 Baina ya raia wa kawaida na tabaka la wasaidizi wa Mtawala:..............57 vi
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 6
7/5/2013 9:06:11 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
Tabaka la watu wa kawaida:...................................................................61 Mtawala na namna ya kutatua matatizo ya Kijamii..............................63 Mtawala na wizara mpya.......................................................................69 Muamala mzuri ndio njia ya kuufikia uhuru:.......................................72 Umuhimu wa kuufanyia kazi urithi:......................................................74 Kuwajali wasomi:...................................................................................76 Mtazamo wa Imamu (as) kuhusu matabaka ya kijamii:........................77 Nafasi ya Jeshi katika Umma.................................................................79 Sifa anazolazimika kuwa nazo mtu ili kubeba Jukumu la Uongozi.......81 Uongozi wa jeshi:...............................................................................82 Uteuzi wa Kadhi:................................................................................84 Uhusiano uliyopo baina ya Mtawala na Kadhi:.................................85 Uhusiano uliopo baina ya Mtawala na watendaji wake:...................86 Kodi........................................................................................................88 Mshauri wa Mtawala:.............................................................................90 Majukumu ya Mtawala mbele ya wafanyabiashara na Wamiliki wa Viwanda........................................................................93 Tabaka la chini na msimamo wa Uislamu kuhusu tabaka hilo.............96 Wajibu alionao mtawala wa Kiislamu....................................................99 Mtawala na msimamo wake kwa wandani wake:................................103 vii
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 7
7/5/2013 9:06:11 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
Nchi na uhusiano wake na nchi nyingine...........................................106 Mtawala na umwagaji damu................................................................ 110 Onyo kwa mtawala............................................................................... 112
viii
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 8
7/5/2013 9:06:11 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
NENO LA MCHAPISHAJI
U
tawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.) ni kitabu kinachotoa mwongozo kwa ajili ya viongozi wote wawe wa dini au wa kisiasa (kiserikali). Mwandishi wa kitabu hiki ametumia mfano wa Imam Ali bin Abu Talib (a.s) jinsi alivyoongoza Umma wakati alipokuwa Imam na wakati alipokuwa Khalifa. Na katika kuwasilisha mada yake hii ametumia sana hotuba, barua na semi za hekima za Imam Ali (a.s) ambazo zimekusanywa katika kitabu maarufu cha siku nyingi kinachoitwa, Nahju ‘l-Balaghah. Nahju ’l-Balaghah ni kitabu maarufu sana katika ulimwengu wa Kiislamu na kinatumiwa na Waislamu wote kama rejea katika masuala yao mbalimbali. Kitabu hiki kama ilivyoelezwa hapo juu ni mkusanyiko wa hotuba, barua na semi za hekima za Imam Ali (a.s). Ni mkusanyo wa mwanzo kabisa wa kimaandishi ya mwenyewe Imam Ali (a.s), na kwa Mashia hiki ni kitabu sahihi baada ya Qur’ani Tukufu, hakuna kitabu kingine chochote walichokiita sahihi. Hata hivyo, kwa mtazamo wa Kishia kitabu cha pekee kilicho sahihi kabisa, bila ya kuwepo dosari, ziada au kasoro yoyote ndani yake ni Qur’ani Tukufu tu peke yake. Sisi kama wachapishaji, tunakiwasilisha kitabu hiki kama kilivyo kwa wasomaji wetu na kuwashauri wasome yaliyomo humo, wayafanyie kazi na kuyazingatia na kufaidika na hazina iliyoko ndani yake. Hii ni moja kati ya kazi kubwa zilizofanywa na Taasisi ya Al-Itrah katika kuwahudumia kielimu wasomaji wake wazun1
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 1
7/5/2013 9:06:11 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
gumzaji wa Kiswahili. Na kwa maana hiyohiyo imeamua kukichapisha kitabu hiki chenye manufaa makubwa kwa lugha ya Kiswahili kwa lengo lake lilelile la kuwahudumia Waislamu, hususan wanaozungumza Kiswahili. Hivyo, ni matumaini yetu kwamba wasomaji wetu watanufaika vya kutosha kutokana na kitabu hiki, kwani tumekiona ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni vitu ambavyo havina nafasi tena katika akili za watu. Tunamshukuru mwandishi wa kitabu hiki Ali Swalah kwa kazi kubwa aliyoifanya kwa ajili ya Umma huu wa Waislamu, Allah ‘Azza wa Jallah amlipe kila kheri na amuingize Peponi kwa salama na amani insha’Allah. Halikadhalika tunamshukuru Ndugu yetu Alhaj Hemedi Lubumba Selemani (Abul Batul) kwa kukitarjumi kwa Kiswahili kitabu hiki, insha’Allah na yeye Allah ‘Azza wa Jallah amlipe kila kheri hapa duniani na Akhera pia, bila kuwasahau na wale wote waliochangia kwa namna moja au nyingine mpaka kufanikisha kuchapishwa kwake. Allah awalipe wote malipo mema hapa duniani na huko Akhera pia. Mchapishaji Al-Itrah Foundation
2
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 2
7/5/2013 9:06:11 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
Utangulizi MWANZO WA MAZUNGUMZO
T
umechoshwa na matukio yenye kuumiza na kuishi kwa mateso na adhabu, hebu tuacheni tutoke kishujaa toka ndani ya minyororo ya ubinafsi ili tutambue yale yaliyomo ndani ya umma wetu wa Kiislamu, umma ambao bado unakumbana na vita angamizi dhidi ya misingi ya itikadi huku maradhi angamizi yakiendelea kusambaa ndani ya jengo lake lililo mong’onyoka na ndani ya mwili wake uliooza, kama ambavyo maradhi ya kifikra na kijamii yameendelea kusambaa ndani ya jamii yetu yenye kuharibika siku baada ya siku. Katika umma huu wenye kukabiliwa na mazingira ya ukatili na ugaidi, na ambao ni muda mrefu sasa umehamwa na furaha, je yupo mwenye kumiliki uwezo na ushujaa wa kuweza kutufuta machozi yenye kuumiza au kumliwaza mwenye huzuni aliyomo katika himaya ya maisha duni yaliyoenea katika umma uliodhoofishwa? Katika giza za magereza kumejaa watu wasio na hatia ambao wamenyimwa utamu wa maisha na raha zake. Katika kila kona kati ya kona za umma huu kuna watoto mayatima wasiojiweza huku wajane wakilia. Achia mbali wale wanaokanyagwa na minyororo ya vifaru na miili yao ikiteketezwa kwa makombora, zaidi ya hapo ni mamilioni ya watoto ambao wanauzwa katika ulimwengu wa mbali katika vizimba vya soko jeusi, na si ajabu kusikia au kusoma kuwa katika ulimwengu 3
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 3
7/5/2013 9:06:11 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
wa tatu kuna watoto karibuni milioni mia moja wanauzwa kwa njia ya mauzo kamili katika muda wote wa maisha. Kwa kweli yote haya ni maumivu yaliyo ndani ya umma wa Kiislamu. Lakini hebu tusimame kidogo ili tuzitazame nafsi zetu kwa mtazamo wa kweli na hakika‌. Je inatosha tu kuainisha maeneo yenye majeraha na pale palipo na maumivu bila kuhisi hilo kiundani, na bila kuwa na nia thabiti katika utendaji kwa lengo la kubadili hali hiyo na kuitengeneza? Hapana, hiyo ni kwa sababu ushujaa haukomei tu katika mtu kujua chanzo cha maumivu yake au mipasuko ya majeraha yake, bali ushujaa ni mtu kuyashinda matamanio yake dhaifu ili mtu huyu aweze kufika kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa roho yake. Na ili uwe mikononi mwetu ule uwezo wa kutatua matatizo yetu ya kuwepo au kukosekana jambo fulani, na kwa ushujaa wa dhati zetu, ni juu yetu kwa mara nyingine tena kusimama pamoja na nafsi zetu kisimamo cha kutaamali na kuchunguza matukio yenye kuendelea pembezoni mwetu, na kisha tuyachambue uchambuzi wenye kujenga, wenye kutamka waziwazi athari zake kwa lengo la kuimarisha kasri la dola yetu ya Kiislamu juu ya nguzo imara zilizojengwa kutokana na haki na uongofu. Lazima tujue kwa ukweli kabisa kuwa siri ya matatizo yetu inarejea kwetu wenyewe na imejificha ndani ya nafsi zetu zilizokufa, ambazo zimesahau kufaidika na ujumbe wa ustaarabu katika kila anuai zake na sura zake, na hatimaye zimesahau kuelekea kwenye shubaka la nuru itokayo mbinguni na kutupilia mbali hali ya masanamu, hali ambayo hainufaishi chochote bali ipo karibu zaidi na madhara. 4
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 4
7/5/2013 9:06:11 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
Je sisi ni madhaifu upande wa ujumbe na maadili? Fuateni dini na misingi! Hapana sisi ni imara kama mlima bali ni imara hata kuushinda mlima, kwa sababu mlima huwa unamegwa lakini muumini hamegwi, lakini tukirejea kwenye maumbile yetu safi, kwenye urithi wetu wa asili, kwenye malengo ya kweli na kwenye mantiki salama isiyo na makosa, na tukaweza kuumiliki ushujaa wa dhati yenye imani na yenye kumtawakali Mwenyezi Mungu Mtukufu, na tukaweza kuufahamu mwenendo wa Ali (as) na Aali zake, wahitimu wa chuo cha Mtukufu Mtume (saww) ambaye ni Jiji la elimu na maarifa, basi hatutopatwa na udhaifu na hali ya kushindwa katika medani ya jihadi dhidi ya maadui waovu. Hakika hatuwezi kupasua njia itakayotufikisha katika utatuzi sahihi wa matatizo yetu leo bila kurejea kwenye uwanja wa fikra ya kiungu, na kurudi kwenye ustaarabu wa maadili yetu ya asili yenye lengo maalumu. Kuanzia hapa, masomo haya yanayowasilishwa baina ya vidole vyako yamekuwa ni jaribio la dhati kabisa la kutatua baadhi ya matatizo yaliyopo katika zama zetu, kupitia mwenendo wa uongozi na utawala kwa mujibu wa Imam Amirul-Muuminina Ali (as). Namuomba Mwenyezi Mungu masomo haya yawe mwangaza wenye kuangazia njia ya umma huu ili kuweza kuurudishia utu wake na utambulisho wake uliopotea, na kuuondolea matatizo uliyonayo na hali ya kubaki nyuma yenye kuchukiza. Ali Swalah
5
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 5
7/5/2013 9:06:11 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
HEBU TUSIMAME PAMOJA NA MSOMAJI Msomaji mpendwa! Amani iwe juu yako. Baada ya salamu, nasema:
W
akati mambo yanapomchanganya mja aliyechoshwa na maisha, wakati anaposhambuliwa kwa makombora yenye kuacha maumivu ya ulemavu, wakati anapokuwa mbali na maadili ya mbinguni, mbali na itikadi safi, hapo ni juu yake kuazimia kurudi kwa Mwenyezi Mungu Mmoja Mwenye kukusudiwa, atazame upya itikadi zake kwa jicho la utambuzi la mtu mchunguzi mwenye uwelewa. Hiyo ni kwa sababu kufuata kwetu Uislamu ni lazima kutokane na sura halisi ya malengo na madhumuni yaliyoelezwa na Uislamu, ili tuweze kuutambua kwa utambuzi sahihi na kamili usiochanganyikana na udanganyifu, hivyo tuweze kutambua ni upi Uislamu wa mwamko, Uislamu wa mapambano na kukataa batili, bali ni wajibu kwetu kupasua njia kwa kuvumilia magumu yake yote na machungu yake yote ili tuweze kufika katika Uislamu huo. Na njia ya kuweza kufikia shabaha hiyo ni sisi kuazimia toka ndani ya nafsi zetu kurudi katika ustaarabu wake (Uislamu) na kutenda kwa mujibu wa mipaka yake na nuru yake tu. Hakika wenyewe ndio mfumo wa maisha ya mtu katika nyanja zake zote, unamwekea taratibu za maisha yake, unanadhimu matendo yake, unaweka mipango ya uchumi wake na unarasimu siasa yake, hivyo tunakuta Uislamu una 6
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 6
7/5/2013 9:06:11 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
mfumo wake wa kumlea Mwislamu kwa mujibu wa maadili ya kiutu ya kweli na kwa malengo matukufu. Unaweza kuuliza: Unawezaje kutimiza hilo? Ndiyo, hakika Uislamu unampa mtu fikra salama ambazo zinafanya kazi ya kumtengeneza mwanadamu, kumpa ufaulu na mafanikio, na zinamfungua toka kwenye kamba na minyororo ya kifikra, kama vile ujinga na kufuata kibubusa, na unamkinga dhidi ya upotovu wa kinafsi na dhidi ya maradhi ya kimaadili kama vile uwongo, usaliti na unafiki. Na hii ndio mantiki ya Uislamu asili, na kwa kweli hakuna kitu bora kama kuilinda safari ya mwanadamu mpaka katika lengo. Hapa mazungumzo yanahusu hali halisi ya umma wetu wa Kiislamu, katika wakati tulionao sasa umma wetu una haja kubwa ya kutambua vyanzo vya ustaarabu wake wa thamani wa asili uliopo katika Uislamu huu, na kuweza kuchota toka kwenye chanzo hiki adhimu, kwani inapasa tutambue kuwa chanzo hiki adhimu ndio silaha yetu katika vita vyetu vya kitamaduni dhidi ya maadui wa ubinadamu wenye chuki na sisi. Hivyo ni lazima turejee kwenye chanzo hiki na tunywe kutoka kwenye maji yake matamu ili tuweze kutimiza matarajio yetu na malengo yetu matukufu ambayo ni taabiri ya uwepo wetu kama umma katika tumbo la ulimwengu huu wenye kutoweka licha ya ukubwa wake na urefu wake, na tuweze kutengeneza utu wake uliotoweka. Ama Nahjul-Balaghah: Yenyewe ndio fikra hai zinazoweza kutatua suala hili katika vipengele vyake vyote na mifano yake yote, hivyo njooni sote kwenye chemchem hii tukufu ili tuweze kupata mtazamo wa ustaarabu na nuru, mtazamo wa maisha na matendo, kwani msemaji wake ni mtu ambaye 7
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 7
7/5/2013 9:06:11 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
ameigusa hali halisi ya umma wenye kusikitisha, amejitolea kwa juhudi zake zote katika kupambana na changamoto za wakati wake na za baadaye kwa mtazamo wake mpana, na ametufumbulia vidole vya fikra zake kwa kutupa mtazamo wa uongozi na utawala na yote yanayojumuisha uongozi wa mwanadamu.
8
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 8
7/5/2013 9:06:11 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
FASLU YA KWANZA DHANA ZA KITUME KUTOKA NDANI YA NAHJUL-BALAGHAH Kwa nini tunajiweka karibu na Nahjul-Balaghah?
K
wa sasa jamii ya Kiislamu iko mbali na utamaduni wake wa asili uliomo ndani ya Qur’ani na Sunnah tukufu ya Mtume (saww), na pia urithi safi wa kifikra wa Maimamu maasumina (as) ikiwemo Nahjul-Balaghah ambayo ni maneno yaliyo chini ya maneno ya Muumba na juu ya maneno ya viumbe, nayo haijulikani isipokuwa jina tu, na haijabaki isipokuwa maandishi yake tu na kwamba inanasibishwa tu na Imam Ali (as), na si zaidi ya hapo. Haijulikani kwa Waislamu wote, bali ni kwamba lililo baya zaidi na lenye kuumiza ni kwamba imekuwa mbali hata na vituo vya elimu ambavyo vinapaswa vichukue maarifa yake na fikra zake kutoka humo moja kwa moja. Na bahati mbaya sana tuliyonayo sasa ni kwamba yule mwenye kuijua basi maarifa yake hukomea kwenye kufafanua misamiati yake na maneno yake tu na si zaidi ya hapo. Kwa kweli ni maganda bila kiini. Zaidi ya hapo ni yale mashambulizi ya makusudi na vita vya kifikra vinavyolazimishwa, ambavyo vinailenga njia nyoofu na ambavyo miongoni mwa shabaha zake ni kuitenga mbali nasibu yake (Nahjul-Balaghah) na Imam 9
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 9
7/5/2013 9:06:12 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
Ali (as) ili isiwe na faida tena na ili iwe na manufaa kidogo. Hivyo ukichunguza mambo na sababu nyingine zinazoihusu Nahjul-Balaghah, ukiongezea mambo manne yafuatayo, yote hayo yanatutaka sisi tujiweke karibu zaidi na kivuli cha Nahjul-Balaghah aminifu. Mambo hayo manne ni:
Kwanza: Upande wa Utu wa Kitume: Katika upande huu imebainisha kwa uwazi kabisa vita vikali vinavyoendelea toka kwa maadui ambao wanashambulia kwa nguvu zote katika kiwango cha fikra na ustaarabu, vita ambavyo kwa chuki nzito vinalenga kuunyima Utu wa Mwislamu nguzo zake na misingi yake imara ambayo ni: Itikadi, historia na ustaarabu. Pindi Mwislamu wa sasa anapojitenga mbali na fikra safi ambayo inawakilisha itikadi yake katika maisha yake, anapojitenga mbali na historia yake ng’aavu ambayo inahusu hatima yake na mwenendo wake, na anapojitenga mbali na ustaarabu wake ambao ndio kilele cha utukufu wake na cha heshima yake, basi Mwislamu huyo anakuwa hana uwezo wa kuibadili nafsi yake na mazingira yake, yaani hatafakari tena katika kutumia uwezo na nyenzo za mafanikio kwa matumizi mazuri yenye faida, matumizi yatakayomfikisha katika ukamilifu wake wa juu kabisa katika maisha yake. Kwa sababu hii kusoma kwetu Nahjul-Balaghah kunalenga kujenga Utu wa Kiislamu wa Kitume kwa nguzo zilizo juu ya misingi na mihimili sahihi.
10
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 10
7/5/2013 9:06:12 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
Pili: Upande wa Jamii Yenye Imani: Kwa sasa tunaona mawingu mazito meusi yamejaa katika anga la jamii hiyo, hiyo yote ni ili yaeneze machafuko, dhulma na matatizo kila kona, kwa lengo la kupora uwezo wake imara na rasilimali zake hai, ili yaifanye jamii hiyo kuwa dhaifu isiyo na uwezo wa kupambana na maadui zake madhalimu, yenye kuitupilia mbali bunduki yake angamizi kwa kutoa kaulimbiu za kuvutia chini ya kivuli cha udhalili na unyenyekevu, ili tuishi katika sauti za mivumo ya mijeledi itoayo moto, na katika sauti za panga na za kuyatukuza na kuyasifu majina ya madikteta na madhalimu. Mazingira haya yamekuja yakiwa ni matokeo ya hali ya ujinga na kukosekana uwelewa sahihi juu ya mambo ya maisha, kiasi kwamba Waislamu wa leo hawajui namna ya kuchukua misimamo na hatua sahihi mbele ya matukio yenye kuendelea, hivyo badala ya kuyapeleka na kuyaelekeza upande wa kheri na maendeleo, wao wanayapeleka kinyume na dhidi ya inavyotakikana, kwani utawaona wanayaelekeza upande wa masilahi ya wakoloni kwa kuwatumikia wao bila kujua. Miongoni mwa mifano halisi na dhahiri ya hali hii ni ugomvi uliopo baina ya Uislamu na Uzayuni (Izraeli). Kujiweka karibu na Nahjul-Balaghah kupitia kifua hiki cha kijamii kutawezesha kupata suluhisho na mfumo sahihi utakaoyapeleka maisha ya kijamii katika hali nzuri zaidi na katika sura ya kupendeza zaidi. Hakika Nahjul-Balaghah imeujaza upande huu mtazamo wa Kitume wa kutosha ili kurudisha uhusiano na mshika11
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 11
7/5/2013 9:06:12 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
mano katika kiwiliwili cha jamii yenye mwamko, ili ichukue nafasi yake baina ya jamii za kibinadamu zilizopo.
Tatu: Upande wa Madhumuni ya Dhana za Uislamu: Upande huu tunakuta Mwislamu wa sasa, msomi na asiyekuwa msomi, aliyeelimika na asiyeelimika, wote wamezitafsiri dhana hizi kwa tafsiri hasi isiyoafikiana na makusudio halisi, tafsiri ambayo imezitenga mbali na harakati za historia, na hatimaye imezifanya zijiweke kando na kujijali zenyewe, na kusalimu amri mbele ya hali yake mbaya yenye kuchukiza. Unamkuta mtu anatafsiri Majaaliwa na Makadara kwa maana ya kukosa hiyari katika maisha yake, na kwa tafsiri hii ya makosa anapoteza moja kati ya nguzo zake za kimaumbile, nayo ni utashi wa kujichagulia mambo, na hivyo anafanya kila tukio kuwa ni kutokana na utashi wa Mwenyezi Mungu na si vinginevyo, na hivyo mtu hana mapungufu katika vitendo vyake na mambo yake – vyovyote vile vitakavyokuwa – na hakika tafsiri hii imeleta udumavu katika roho ya umma wenye mwamko. Na kosa lingine ambalo liliyeyusha harakati za umma tangu zamani ni dhana ya kumtawakali Mwenyezi Mungu Mtukufu, pale walipopotosha maana yake halisi hadi wakaifikisha katika moja ya daraja za tawakali. Matokeo yake yakawa ni kuuondoa uwezo halisi wa mwanadamu katika medani ya vitendo, na matokeo ya kufuata dhana hizi kimakosa ikawa ni kupatikana usufi (Zuhdi), na hakika masufi walichangia sehemu kubwa katika kuifuta maana yake sahihi na hatimaye wakaigeuza kuwa ni 12
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 12
7/5/2013 9:06:12 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
mwelekeo wa Akhera tu, na hatuna la kufanya duniani isipokuwa utawa na ibada. Wamesahau ukweli muhimu nao ni kwamba: Zuhdi ni wewe kumiliki kitu na si kitu kukumiliki wewe. Watu hawa hawakuishia hapo bali waliharamisha dhana muhimu sana ambayo kwayo ujumbe wa mbinguni husimama na kujilinda wakati wa kuutekeleza kimatendo, nayo ni dhana ya Taqiyyah. Dhana hizi za asili zimedhulumiwa maana zake na kupotoshwa hadi katika maana nyingine zenye mapungufu. Na bahati mbaya sana ni kwamba dhana hizi zilikuwepo kivitendo huku zikihifadhi roho ya umma, na tafsiri hizi katika hali halisi ziko mbali na vipimo sahihi vya Uislamu.
Nne: Upande wa Siasa ya Kiislamu: Katika ulimwengu huu tulionao, vipimo vya akili na dhamira vimegeuka na hatimaye matamanio yametawala, kiasi kwamba siasa imekuwa ni sifa mbaya na kosa katika jamii yetu iliyo nyuma kimaendeleo, na kila anayezungumzia siasa au kuingilia masuala ya usimamizi na utawala anazingatiwa kuwa ni mtu aliyekwenda nje ya njia nyoofu na nje ya msitari wa misingi na itikadi, bali hali ni zaidi ya maamuzi haya yanayotolewa, kwani yule mwenye kumiliki uwezo wa kisiasa au mwelekeo wa kiutawala wa kuweza kunadhimu maisha ya watu huchukuliwa kuwa ni mtu aliyetenda dhambi kubwa na kosa kubwa lisilosameheka, hivyo huwa wanamwekea kizuizi imara na kumzuia yeye asiweze kusoma magazeti na majarida ya kisiasa, na asiweze kusikiliza habari za kisiasa kupitia redio na runinga. 13
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 13
7/5/2013 9:06:12 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
Kwa kweli kwa mtazamo wa majahili, hayo yote ni haramu katika kanuni zao na rai zao, wamesahau kuwa dini tukufu ni mfumo kamili na jumuishi usioridhia nadharia hizi za vipande vipande. Yenyewe inapinga nadharia duni ya matamanio, na inawasilisha nadharia tukufu katika usimamizi na utawala, na inaitazama siasa kwa mtazamo wa ukamilifu na unaijumuisha miongoni mwa mitazamo ya Kiislamu, na hivyo katika Nahjul-Balaghah kuna uwanja mpana kuhusu usimamizi, utawala na siasa iliyoletwa na Uislamu kutoka kwenye chanzo chake cha asili.
14
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 14
7/5/2013 9:06:12 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
SIASA NI SEHEMU YA UISLAMU
U
islamu ni dini ya maisha, harakati na ukamilifu, nayo inaonesha uwepo wake halisi kupitia jinsi inavyoamiliana na matukio na maendeleo (mabadiliko) ya kila siku ya kimaisha na kijamii, hivyo yenyewe ni dini ya siasa na ibada, na wala haipasi kuyazingatia haya mambo mawili kuwa ni mambo mawili yaliyoachana, isipokuwa ni kwamba baadhi ya watu na kutokana na taathira ya mtazamo hasi wa vitendo vya kisiasa vilivyotokea katika historia ya Uislamu vikiwa mbali kabisa na siasa, vimewafanya waufunge Uislamu katika duru ya ibada tu. Na hatimaye kila anayetekeleza jukumu lake la kidini la kisiasa wanamtuhumu kwa upotovu, lakini ukweli ni kwamba nadharia hii ya kutenganisha (dini na siasa) haina mashiko mbele ya ukweli ufuatao: Kwanza: Hakika Uislamu umekuja kumwokoa mwanadamu kutoka kwenye hali zote za kijahiliya na za kubaki nyuma, na majaribio yote ya maadui, ya jana na ya leo, yalikuwa yakilenga na bado yanalenga kufuta maadili bora ya Mwislamu na kumzuia kuunda chombo chake cha kijamii na cha kiustaarabu cha kipekee. Hivyo ili Mwislamu aweze kupambana na hatari hii hana budi kuingia kwa kila nguvu katika kazi za kisiasa ili aweze kuthibitisha ustaarabu wake halisi. Pili: Kazi ya siasa haikomei tu katika kuwakamata maadui, bali ni kwamba wajibu wa kimaisha, na wajibu wa kidini unawajibisha kuingia katika mapambano ya kisiasa, la sivyo maisha ya umma yatakuwa katika fujo, kwa sababu yatakosa kitu muhimu ambacho ndio msingi wa mfumo wa kijamii, nacho ni usimamizi na utawala. 15
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 15
7/5/2013 9:06:12 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
Tatu: Hakika dini ina mtazamo wake kamili kuhusu maisha unaohusu pande zake zote za kimada na za kiroho. Na siasa si kitu kinachotengana na pande hizi, na dini ya Uislamu ina mitazamo yake kamili kuhusu usimamizi na utawala kama sehemu mbili muhimu miongoni mwa sehemu za siasa. Hivyo siasa haiachani na dini, bali yenyewe ni sehemu isiyoachana na Uislamu, na hakika kutilia umuhimu mambo ya kisiasa na kiutawala, na kuchukua hatua na maamuzi ya kila siku kuhusu mambo na matukio mbalimbali ni wajibu wa Kiislamu (wa kidini). Na hakika jaribio lolote la kutaka kutenganisha dini na siasa litatujumuisha katika kundi la wachukua sehemu na kuacha sehemu, ambao wanaamini sehemu ya Kitabu na wanakufuru sehemu nyingine ya Kitabu. Uislamu ni dini inayokusanya dunia na Akhera, ibada na siasa. Manabii (as), Maimamu (as) na viongozi wa umma wote walikuwa wanazingatia kuwa kuwasimamia waja ni katika jukumu lao la kwanza la kisiasa. Katika dua iliyopokewa kutoka kwao imekuja ibara inayowasifu Maimamu (as) kuwa: “Nyinyi ni wasimamizi wa waja na nguzo za nchi.” Na katika hadithi ni kwamba Wana wa Israeli: “Wanasimamiwa na Manabii wao.” Na katika Nahjul-Balaghah katika barua ya Imam Ali (as) kwenda kwa Malik al-Ashtar an-Najafiy imekuja: “Kwa ajili ya kusimamia kazi zako wachague wale wenye ujuzi, uchamungu na uwezo wa kuendesha mambo.” Na amesema (as): “Uadilifu ndio siasa bora.” Na akasema (as) katika barua yake kwa Muawiyah bin Abu Sufiyan: “Tangia lini ewe Muawiya nyinyi mmekuwa wasimamizi wa raia na watawala wa mambo ya umma?” 16
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 16
7/5/2013 9:06:12 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
Hivyo tunapokusanya hadithi hizi na nyinginezo na kuzidurusu kwa kina na kwa kulingana na maudhui husika, na kuzisoma kwa mapana tutazikuta zinaainisha dhana mbili:
Kwanza: Maana ya siasa katika Uislamu: Siasa ni namna ya kuendesha na kunadhimu mambo ya watu kwa namna nzuri zaidi na bora zaidi itakayowafikisha katika saada ya milele. Uislamu una mtazamo wake bayana ambao haukubali kubadilishwa wala kutiliwa shaka, bali ni kwamba mtazamo huu ni miongoni mwa misingi ya Uislamu, kwa sababu ujumbe wote wa mbinguni ulikuja kwa ajili ya kuelezea lengo moja, nalo ni kunadhimu na kuendesha maisha ya watu, ili kwa uwendeshaji huo wafikie katika kiwango cha maumbile ambayo kwayo watu wameumbwa.
Pili: Sifa za kiongozi mwenye kuwasimamia waja: Hakika uongozi wa kitume wa kisharia pamoja na sifa za kiimani na kimaadili zilizo njema anazojipamba nazo Mtume, huakisi ustaarabu wa umma na mwonekano wake, na hufanya kazi ya kunyoosha mwenendo wake katika maisha. Kwa ajili hii ni wajibu tuchague uongozi wa kitume ambao utawakilisha umma wetu wa Kiislamu kwa yote unayojumuisha ikiwemo maana zake, desturi zake, kanuni zake na mtazamo 17
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 17
7/5/2013 9:06:12 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
wake. Na pia ikiwemo maadili ya msingi na ya haki katika vyanzo na sababu za mapinduzi ili kubadili mazingira yaliyo kinyume katika maisha na kujenga jamii ya Kiislamu iliyokamilika. Na kwa kuwa roho ya Uislamu ni siasa, unadhimu na uendeshaji, na kwa kuwa msingi huu una dhamana ya kuwapangia watu maisha yao ya kijamii na ya mtu mmoja mmoja, na kwa kuwa watu huathiriwa na utu wa viongozi wao kwa hasi au chanya, ndio maana ikawa ni lazima kwa Uislamu kuangazia kwa nguvu zote hali halisi ya utu wa kiongozi, sifa na vigezo vya kinafsi alivyonavyo. Kwa sababu utu wa kiongozi, kwa namna moja au nyingine huakisi hali ya watu, na hivyo ikiwa kiongozi ni mtu mwema basi fikra za wema huenea katika jamii, na hivyo kiongozi akiwa na maadili mema na sifa nzuri alizonazo anakuwa kiungo bora katika maisha ya raia wake na jamii yake, mwenye kuipeleka katika ukamilifu wa kiroho na kitabia na katika saada ya kweli. Saada ya mwanadamu ni matokeo ya kitabia ya jinsi mtu anavyoamiliana na maadili ya Mwenyezi Mungu na misingi ya ujumbe wa mbinguni, ikiwemo uadilifu, staha, kujizuia, uchamungu, elimu na upole, na hatuwezi kuyatimiza hayo isipokuwa baada ya kuzitakasa nafsi na kuzilea mpaka imani yake ifikie katika kiwango cha tabia za kitume. Na hatuwezi kufika katika kiwango cha tabia za kitume isipokuwa kwa viongozi ambao roho ya ujumbe inaonekana kwao kivitendo, hiyo ni kwa sababu ujumbe unahitaji utekelezaji wa kivitendo na mifano ya kibinadamu, binadamu ambao watautekeleza kivitendo, ili kwamba utoke kwenye hatua ya nadharia mpaka kwenye medani ya utekelezaji wa nje wa kivitendo. 18
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 18
7/5/2013 9:06:12 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
Na kwa ajili hiyo kuzungumzia sifa za uongozi wa Kiislamu na kuziainisha kwa umakini kunaziba njia kwa kila ambaye nafsi yake inamshawishi kutaka uongozi wa umma wetu wa Kiislamu, kama walivyo viongozi wengi ambao wanatawala nchi za Kiislamu, na wao hawana chochote isipokuwa kukidhi matamanio yao na starehe zao za kimatamanio katika maisha.
19
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 19
7/5/2013 9:06:12 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
SIASA KATIKA NAHJUL-BALAGHAH
N
ahjul-Balaghah kati ya mambo yake mengi iliyonayo imekusanya pia mtazamo na miongozo kuhusu hali ya utawala na majukumu ya Mtawala na maadili ya Kiislamu ambayo yanapasa kuwa kigezo katika kuwateua Makadhi, kuwachagua Mawaziri, Manaibu na Maafisa. Kama ambavyo pia imekusanya miongozo mingi ya majukumu ya ulamaa na wasomi, na uhusiano wa Mtawala na raia wake na wandani wake. Na waraka wa Imam kwenda kwa Malik al-Ashtar umekusanya sehemu kubwa ya dhana hizi, japokuwa si waraka huu tu peke yake pia kuna barua nyingi, usia na nyaraka nyingi zenye kubeba dhana zote hizi. Hakika barua, usia na nyaraka zilizotufikia kutoka kwa Imam Ali (as) na ambazo zinabeba madhumuni haya ya kisiasa na kiutawala tunaweza kuzigawa katika aina tatu kulingana na wale waliotumiwa: Kwanza: Kwa raia wa mataifa ya Kiislamu. Pili: Kwa viongozi na magavana. Tatu: Kwa maadui zake na makundi ya upinzani.
Kwa Raia wa Mataifa ya Kiislamu: Barua na usia wa kisiasa ambao Imam Ali (as) aliuelekeza kwa raia wa mataifa ya Kiislamu umekusanya falsafa ya AmirulMuuminina (as) katika uendeshaji wa mambo ya nchi na mambo ya kiutawala, na njia ya kuamiliana na mazingira ya 20
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 20
7/5/2013 9:06:12 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
kawaida na yasiyokuwa ya kawaida yanayojitokeza katika ngazi ya jamii. Na kwa ufafanuzi ni kwamba barua na usia ulioelekezwa kwa raia umekuja ili kutatua mambo kadhaa, nayo ni: Kwanza: Baadhi umekuja ukiwa ni ufafanuzi wa baadhi ya mambo yasiyoeleweka kwa raia au ni jibu dhidi ya vita vya propaganda ambazo kawaida adui huzieneza, au ni pigo dhidi ya fikra za makosa zilizoenea au zinazoenea katika jamii. Kama ambavyo pia kupitia mawasiliano haya Amirul-Muuminina (as) alikuwa anajaribu kusahihisha mtazamo wa jamii kuhusu baadhi ya mambo na kuweka wazi ukweli wake, na katika baadhi ya barua Imam anajaribu kuondoa mkanganyiko ambao ulizuka zama za ukhalifa wake na utawala wake. Kwa mfano tu tunamkuta akisema katika barua moja akiwaambia watu wa Kufah: “Ama baada ya hayo, kwa hakika mimi nakupasheni habari kuhusu suala la (kuuwawa) Uthman mpaka iwe kulisikia ni kama kuliona dhahiri shahiri. Hakika watu walimkosoa na wakanipa kiapo cha utii bila kulazimishwa wala kutumia nguvu.� (Hotuba ya 1). Baada ya kuuwawa Uthman kulitokea aina fulani ya sintofahamu ndani ya jamii, na maadui wa Imam wakajaribu kutumia mwanya huo kwa maslahi yao binafsi, na wakaelekeza tuhuma za kuuwawa Uthman kwa Amirul-Muuminina, kiongozi wa wachamungu Ali bin Abu Talib (as), ili wafanye hilo kuwa kigezo cha kuhalalisha uasi wao dhidi yake na kutangaza vita dhidi yake. Kuanzia hapa ndipo Imamu (as) akaandika barua hii kwenda kwa watu wa Kufah akiwafafanulia humo ukweli na matukio ya kifo cha Uthman. 21
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 21
7/5/2013 9:06:12 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
Na katika barua nyingine alioipeleka kwa watu wa miji mbalimbali, humo anaelezea yaliyotokea baina yake na watu wa Siffin, akibainisha humo makosa ya fikra zilizoenea kati yao huku akijaribu kutengeneza mwenendo wao na kurekebisha hali yao ya kijamii na kuwaita wote katika kushikamana na kuzima fitina na kutuliza hali kwa watu wote kutulia na kumtii kiongozi wao, ili kwa njia hiyo iwezekane kuifichua haki na kuiweka sehemu yake sahihi. Hivyo anasema (as): “Jambo (kuhusiana na imani yetu) ni moja, isipokuwa tofauti yetu kuhusu damu ya Uthman ni kwamba sisi hatukuhusika nayo! Tukasema njooni tugange lisilofikiwa hii leo kwa kuizima hii fitina yenye kuenea, na kuwatuliza watu, mpaka mambo yaimarike na tupate nguvu ya kuiweka haki mahali pake.” (Hotuba ya 58). Kadhalika barua yake kwenda kwa watu wa Misri na kwa Malik al-Ashtar alipompa ugavana wa Misri. Hapa Imam anaweka wazi sababu husika zitokanazo na mitazamo ya kiitikadi na kiimani zilizompelekea kuchukua usimamizi na utawala na kuupa kipaumbele pindi alipokosa njia ya kujiepusha nao. Abdullah bin Abbas anasema: “Niliingia kwa Kiongozi wa Waumini (as) alipokuwa katika kitongoji cha Dhuqaar, naye akiwa anashona ndara zake, akaniuliza: ‘Nini thamani ya ndara hizi?’ Nikamwambia: ‘Hazina thamani yoyote.’ Akasema (as): ‘Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu! Hizi ndara nazipenda zaidi kuliko uamiri wenu (ukhalifa) ila tu endapo nitatenda haki au kuzuia batili.’” Amesema (as): “Alipoondoka (as) – yaani Mtume wa Mwenyezi Mungu - Waislamu walikhitilafiana kuhusu Ukhalifa baada yake….Nikasimama katika matukio yale mpaka ba22
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 22
7/5/2013 9:06:13 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
tili ilitoweka na kuyeyuka, na Dini ikabaki katika amani na salama.� (Hotuba ya 62). Pili: Barua na usia mwingine umekuja ukiwaelekea raia kwa lengo la kuwatahadharisha hatari inayouzunguka umma, ili kwamba ujiepushe nayo usiweze kutumbukia katika hatari husika, na Imamu aliuchorea umma mfumo kamili wa ustaarabu ili umma uweze kunyanyuka mpaka katika kiwango cha matukio na kusimama kwa ujasiri na kwa moyo shupavu mbele ya changamoto zinazoelekezwa dhidi ya umma na dhidi ya utu wake, ili kwamba umma ujiandae kwa maandalizi kamili na ukusanye nguvu kwa ajili ya kupambana na hatari ambazo zinauzunguka toka kila upande. Katika kifungu hiki cha aina hii ya barua, Imamu pia amebainisha namna ya kujiandaa kupambana na ustaarabu unaoenezwa na maadui, hivyo akafanya kazi ya kuandaa nguvu zilizopo katika jamii na kuziamsha kwa ajili ya jihadi na kazi, hivyo katika barua yake kwenda kwa watu wa Kufah imekuja: “Jueni kwamba nyumba ya hijra (Madina) imewaondoa watu wake na wameihama, na imechemka uchemkaji wa chungu, na fitina imeibuka dhidi ya mhimili (dhidi yake mwenyewe (as)), hivyo basi harakieni kwa amiri jeshi wenu na harakieni kumpiga vita adui yenu, Mwenyezi Mungu akipenda.� (Hotuba ya 1). Tatu: Na ili Imamu (as) apandishe ari ya umma na kuuamsha hadi kwenye utekelezaji wa kivitendo utakaoleta mabadiliko yenye kuupeleka kwenye hali nzuri zaidi na bora zaidi, Imamu (as) anatumia lugha ya ukali na ya mashambulizi makali dhidi ya uvivu wa raia, kuganda kwao na kufara23
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 23
7/5/2013 9:06:13 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
kiana kwao. Hii hapa barua yake kwenda kwa watu wa Basra akibainisha hilo: “Kufunguka kwa kamba yenu (kuparaganyika kwa nguvu) na kufarakana kwenu ni jambo lisilofichika kwenu..….. Ikiwa mambo yaangamizayo yamewazidi, na rai dhaifu zilizo mbali na haki zimekufikisheni katika kunipinga na kufanya kinyume na mimi, hapo jueni kwamba farasi wangu nitakuwa nimemuweka karibu, na nimetandika tandiko la ngamia wangu. Na endapo mtanifanya nilazimike kufanya safari kuja kwenu basi nitawafanyieni tukio ambalo ukililinganisha na Siku ya Ngamia, yenyewe itakuwa ni kama mrambo wa mwenye kuramba…..simsamehe mtuhumiwa kiasi cha kumfanya asiwe na hatia wala kiasi cha kumzingatia mwenye kuikiuka ahadi kuwa ni mtekelezaji.” (Barua ya 29).
Kwa Viongozi na Magavana: Hakika barua za Imam (as) na nyaraka zake kwenda kwa magavana wa miji mbalimbali zililenga kutimiza mambo kadhaa: Kwanza: Ili aufanye uendeshaji wa serikali kuwa ni njia salama yenye kuelekea kwenye uongofu sahihi wa Mwenyezi Mungu, na ili aufanye kuwa ni shule ya kifikra iliyokamilika iliyosimama juu ya misingi ya maadili, Imam (as) anatumia onyo kali dhidi ya makosa na anasisitiza kuwa ni lazima Gavana asielemee kwenye makosa au kunasa katika mitego yake na kamba zake. Kwa maana ya kwamba ni lazima awe mfuatiliaji wa mazingira yenye kuendelea uwanjani, ufuatiliaji kamili, 24
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 24
7/5/2013 9:06:13 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
na awe katika tahadhari kubwa kwa kuogopa asije kutumbukia katika makosa, afuatilie hilo hata katika mambo madogo madogo ambayo mmoja wetu anaweza kudhani kuwa hayastahiki kupewa umuhimu mkubwa wala tahadhari kubwa. Lakini mambo haya ambayo kwa mtazamo wetu ni mambo madogo madogo, yanapojitokeza kwa Mkuu wa eneo au Mtawala wake, katika mtazamo wa Imam Ali (as) yenyewe yanapata sifa makhususi katika kuzuia na kuharamisha. Anasema (as): “Ama baada ya hayo! Ewe mwana wa Hunayf! Imenifikia habari kuwa mtu miongoni mwa vijana wa Basra alikualika kwenye karamu, ukaharakia kwenda huko, ukawa unaletewa aina kadhaa za vyakula, na kusogezewa bilauri. Sikudhani kuwa ungeitika kwenye karamu ya watu ambao mtu masikini miogoni mwao hufurushwa kikatili, na tajiri miongoni mwao hualikwa….” Pili: Alichora ramani pana ya siasa yote ambayo Mtawala au kiongozi anapaswa kuifuata kulingana na mazingira ya wakati wake yanavyomtaka, kulingana na miongozo ya Kiislamu. Sawa iwe ni katika kuamiliana na raia, kuwapanga na kuwagawa, au iwe ni katika siasa ya nje katika kuamiliana na adui, rafiki au asiyekuwa hao. Kwa mujibu wa siasa ya Kiislamu Mtawala hana haki ya kutotimiza mahitaji ya watu na maombi yao, au kuwavuta kwa kuwazuia wasineemeke na utawala na mamlaka, kwani hakika wao ni ndugu katika dini na ni wasaidizi katika kutoa haki mbalimbali. Imam anasema: “Ama baada ya hayo! Kwa kweli wakuu wa mji wako wamelalamikia ukali na ugumu wa tabia yako, dharau na ufedhuli…..Basi wavalie joho la upole ukichanganya na ukali, na wabadilishie kati ya ugumu na huruma. Wachanganyie 25
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 25
7/5/2013 9:06:13 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
kati ya kuwa karibu na mbali na kuwaweka mbali na karibu. Mwenyezi Mungu akipenda.” (Hotuba ya 19). Na anasema: “Na wateremshie bawa lako, walainishie upande wako, na wakunjulie uso wako, na washirikishe katika mtupo wa jicho, ili wakubwa wasitamani udhalimu wako kwao (raia), na wala wanyonge wasikate tamaa na uadilifu wako kwao.” (Hotuba ya 27). Na pia anasema: “Wala usiikatae suluhu aliyokuitia adui yako ambayo ndani yake kuna ridhaa ya Mwenyezi Mungu, kwa kweli katika suluhu kuna raha kwa askari wako, na pumziko la majonzi yako, na amani kwa nchi yako. Lakini tahadhari yote iwe kwa adui yako baada ya kufanya naye suluhu, kwa kuwa huenda adui akawa amejikurubisha kwa suluhu ili akughafilishe, kwa hivyo kuwa thabiti..” (Hotuba ya 52). Tatu: Tahadhari dhidi ya kutumia madaraka kwa ajili ya kutimiza masilahi binafsi au kwa ajili ya kudhibiti mali za Waislamu, au kwa ajili ya kufaidika na neema anazozipata kupitia nafasi yake ya kijamii, na wakati mwingine hufikia hadi kuwatisha watu na kuwafukuza. Binti ya Ammarah al-Hamdaniyyah amepokea kwamba yeye aliingia kwa Muawiya baada ya kifo cha Ali (as), Muawiya akaanza kumlaumu kwa kitendo cha kuwahimiza watu dhidi yake siku ya Siffin, kisha Muawiya akamwambia: “Ni ipi haja yako?” Akasema: “Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kukuuliza kuhusu jambo letu na kuhusu haki yetu aliyofaradhisha juu yako. Bado unaendelea kutuletea kutoka kwako mtu anayejifakharisha kwa nafasi yako na anatumia nguvu ya mamlaka yako, anatuvuna kama mashuke na anatukan26
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 26
7/5/2013 9:06:13 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
yaga kama Harmalu, anatudhalilisha na kutuonjesha mauti, huyu Basru bin Artatu amekuja kwetu, akawauwa wanaume wetu na kuchukua mali zetu. Ukimuuzulu tutakushukuru la sivyo tutakukufurisha.” Muawiya akasema: “Hivi unanitishia mimi jamaa zako ewe Sawdah, na nimekusudia kukubeba juu ya usafiri mbaya ili nikurudishe kwake akapitishe hukumu yako.” Sawdah akasoma beti za mashairi kwa kusema: “Mungu aisalie roho iliyomezwa na kaburi hatimaye uadilifu ukawa umezikwa humo. Hakika ilishikamana na haki bila kutafuta mbadala, hivyo haki na imani vikawa mapacha wasioachana.” Muawiya akasema: “Ni nani huyu (mwenye sifa hizi) ewe Sawdah?” Akasema: “Wallahi huyo ni Amirul-Muuminina Ali bin Abu Talib (as), Wallahi nilikwenda kwake kumlalamikia kuhusu mtu mmoja aliyekuwa amempa usimamizi wa sadaka zetu lakini mtu huyo akafanya dhulma, nilipokwenda nilimkuta amesimama akisali, aliponiona alikatisha Sala yake na akanigeukia kwa huruma, upole na upendo, akasema: ‘Je una haja yoyote?’ Nikasema: Ndiyo. Nikampa habari, akalia kisha akasema: ‘Ewe Mungu Wangu wewe ni shahidi juu yangu na juu yao kuwa hakika mimi sikumwamrisha awadhulumu viumbe wako.’ Kisha akachukua kipande cha ngozi na kuandika humo: ‘Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu. Imekwisha kufikieni hoja ya wazi kutoka kwa Mola Wenu Mlezi. Basi timizeni sawasawa vipimo na mizani, wala msiwapunje watu vitu vyao, wala msifanye uharibifu katika nchi, baada ya kuwa imekwishatengenea. Hivi ndivyo bora kwenu ikiwa nyinyi ni Waumini. Utakaposoma tu barua yangu hii hifadhi kilichomo mikononi mwako miongoni 27
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 27
7/5/2013 9:06:13 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
mwa amali yetu mpaka atakapowajieni yule atakayeichukua kutoka kwako. Wasalam.’ Kisha akanikabidhi barua, Wallahi hakuipiga muhuri wa udongo wala hakuihifadhi, nikaenda na barua mpaka kwa mhusika, naye akaondoka akiwa ameuzuliwa.” Na anasema (as): “Kwa hakika kazi uliyopewa sio funda la mlo, lakikni ni amana shingoni mwako, na wewe ni mwenye kuangaliwa na aliye juu yako. Haupaswi kuwafanyia raia udikteta, wala kujihatarisha ila kwa lenye msingi. Mkononi mwako mna mali ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na wewe ni miongoni mwa wahifadhi wake, hadi utakapo nikabidhi. Na huwenda mimi nisiwe miongoni mwa Watawala wako wabaya mno kwako. Wasalam.” (Namba 5). Na anasema tena: “Kwa hakika mimi naapa kwa Mwenyezi Mungu kiapo cha kweli! Ikinifikia habari kwamba wewe umefanya khiyana katika nyara za Waislamu katika kitu kidogo au kikubwa, nitakupa adhabu kali ambayo itakuacha ukiwa mchache wa mali, mwenye mgongo mzito na mwenye kudharauliwa.” (Namba 15). Nne: Kuainisha maeneo ya siasa ya uchumi na mali, na kutoa tahadhari dhidi ya uharibifu na ubadhirifu, na kuelekeza kwenye kutilia umuhimu ujenzi na uzalishaji na kuimarisha harakati za uchumi katika umma. Anasema (as): “Acha kufanya israfu, kuwa wa wastani…Izuwie mali ile iliyo kadiri ya dharura yako… Je unamtarajia (Mwenyezi Mungu) akupe ujira wa wanyenyekevu na hali wewe kwake Yeye ni miongoni mwa wenye kiburi!...na wewe ni mwenye kuogelea katika neema ambayo unaizuia isimfikie mnyonge na mjane...” (Namba 21). 28
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 28
7/5/2013 9:06:13 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
Na anasema tena: “….Mazingatio yako yawe zaidi kwenye uendelezaji wa ardhi (kilimo) kuliko ukusanyaji wa kodi, kwani hilo (la kodi) halipatikani isipokuwa kwa kilimo, na mwenye kutaka mapato bila ya kilimo atakuwa ameiharibu nchi, na kuwaangamiza waja….” (Namba 53). Tano: Ni mafunzo ya kivita kwa askari na makamanda wa jeshi, Imamu anayafanya mwongozo kutoka kwake kwa kutoa nasaha na maelekezo ya kiaskari. Kama pia anavyosisitiza sifa ambazo ni lazima askari wajipambe nazo, kama vile werevu, tajiriba, ujanja wa kiaskari na yanayofanana na hayo miongoni mwa mbinu na fikra za kiaskari. Imamu (as) anasema: “Wakirejea kwenye kivuli cha utii hilo ndilo tulipendalo. Na kama utashi wa kaumu utaafikiana na kufikia kwenye mfarakano na maasi basi inuka na wanaokutii kuwaendea wanaokuasi. Na tosheka na anayeongoka pamoja na wewe dhidi ya anayechelewa nyuma, kwani hakika mwenye kulazimishwa, kughibu kwake ni bora kuliko kuhudhuria kwake, na kukaa kwake kunatosha zaidi kuliko kuinuka kwake.” (Namba 4). Barua namba 11, namba 13 na namba 14, zote zina madhumuni haya.
Kwa Maadui zake na Makundi ya Upinzani: Imam Amirul-Muuminina (as) katika barua zake kwenda kwa maadui na makundi ya upinzani alikuwa anakusudia mambo kadhaa, muhimu kati ya hayo ni: 29
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 29
7/5/2013 9:06:13 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
Kwanza: Kugusia propaganda zilizokuwa zikitolewa na kuondoa kitambaa kwenye nyuso zilizokuwa zikiendesha propaganda hizo na kuzitambulisha nyuso hizo mbele ya jamuhuri, ili raia wachukue msimamo wa wazi dhidi yao, na watambue ni wapi penye maradhi ili iwe rahisi kwao kutoa tiba muwafaka. Na suala la msingi kabisa ambalo Imamu (as) alishughulika nalo kwa undani zaidi katika aina hii ya barua lilikuwa ni suala la: Kuuawa Uthman bin Affan, kwani ukweli wa jambo hili ulikuwa haujawafikia raia wa mataifa ya Kiislamu kwa sura ya ukweli, hiyo ni kutokana na umbali wa zama uliojitokeza, na umbali uliokuwepo baina ya sehemu ya matukio ya suala hili na walipo wao. Kuanzia hapa Imamu akawa ana haja kubwa ya kufafanua ukweli kwa sura kamilifu kwa wanaumma wote. Ili wasije kudanganyika na fikra ya makosa aliyotuhumiwa kwayo Imamu ya kwamba alikula njama ya kumuuwa Uthman, na hatimaye waifanye sababu ya kukataa kutii ukhalifa wake wa kisharia. Hakika kifo cha Uthman kiligeuka mlango mkubwa ambao maadui wenye chuki waliingia kupitia hapo ili kutimiza masilahi yao machafu. Na mbele ya maadui wa Imamu (as) na wapinzani wake, kama vile Muawiya, Talha na Zubair, damu ya Uthman iligeuka njia ya kuyapoteza makundi makubwa katika umma ili waweze kufikia matakwa yao ya kisiasa na malengo yao ya kupata utawala, malengo ambayo yalikuwa yanapingana na kitendo cha kuridhia ukhalifa wa Imam Ali (as) na kumpa kiapo cha utii. Ibn Athir anasema katika Juzuu ya Tatu, katika Ukurasa wa 203: â€œâ€Ś.Ulipofika mwezi wa tatu tangu Uthman alipouwawa katika mwezi wa Safar, Muawiya alimwita mtu mmoja 30
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 30
7/5/2013 9:06:13 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
kutoka katika kabila la Bani Absi, aliyekuwa akiitwa Qubaydhah, akamkabidhi bahasha iliyokuwa imefungwa, anuani yake ikisomeka ‘Sabaiyyah kutoka kwa Muawiya kwenda kwa Ali.’ Mjumbe akaingia kwa Ali na kumkabidhi, alipoifungua hakukuta barua, akamwambia mjumbe: ‘Kuna nini nyuma yako?’ Akasema: ‘Nitasalimika mimi?’ Ali (as) akasema: ‘Ndiyo, hakika mjumbe hauwawi.’ Akasema: ‘Hakika yaliyo nyuma yangu ni kwamba mimi niliteremka kwa watu ambao hawaridhii isipokuwa kwa kisasi.’ Akasema (as): ‘Kutoka kwa nani?’ Akasema: ‘Kutoka kwenye mishipa ya shingo yako. Na nimewaacha wazee sitini elfu wakilia chini ya kanzu ya Uthman, nayo imewekwa kwa ajili yao, wameivisha kanzu hiyo mimbari ya Damascus.’ Akasema: ‘Niamini hakika wanatafuta damu ya Uthman, wewe si umeshindwa kuchukua kisasi cha damu ya Uthman? Ewe Mungu wangu! Nakimbilia kwako kwa kujikinga mbali na damu ya Uthmani.’” Katika barua yake kwenda kwa Muawiya, Imam Ali (as) aliandika: “Wamenipa kiapo cha utiifu watu waliompa kiapo cha utiifu Abu Bakr, Umar na Uthman, na ni juu ya misingi ileile. Aliyekuwepo hakuwa na hiyari ya kuchagua, wala kukataa yule ambaye hakuwepo. Bali Shura ni ya Muhajirina na Maanswari… Naapa kwa umri wangu! Ewe Muawiya! Ukiangalia kwa akili yako sio kwa utashi wako, utanikuta mimi ni mtu niliyeepukana mbali na damu ya Uthman. Na kwa hakika utajua kuwa nilikuwa nimejitenga mbali naye kabisa, isipokuwa ikiwa utasingizia, basi singizia utakalo. Wasalamu.” (Barua ya 6). Na pia aliandika barua yenye madhumuni haya haya kwenda kwa Talha na Zubair baada ya kuwa wamevunja kiapo cha utii, hiyo ni baada ya wao kumuomba Ali (as) 31
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 31
7/5/2013 9:06:13 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
awape ugavana wa miji miwili, Basra na Kufah, lakini Ali (as) alikataa ombi lao na akawaambia: “Ridhikeni na mgao wa Mwenyezi Mungu kwenu mpaka nitakapotazama upya rai yangu. Na tambueni kuwa hakika mimi simshirikishi katika amana yangu sahaba yangu yeyote isipokuwa yule ambaye nimeridhika na dini yake na uaminifu wake na nimeshajua undani wake.” Msimamo huu kutoka kwa Imam Ali (as) uliwafanya waanze kufikiria kutoka Madina na kwenda Makka ambako ndipo makundi ya wapinzani na maadui yalikuwa yamejikusanya. Walimwendea Aisha na wakamshawishi kutoka na hivyo alikwenda mpaka Basra akiwa pamoja na Talha na Zubairi, wakiwa na kundi kubwa la watu. Jamaa hawa walipita katika eneo moja la maji linaloitwa “Maji ya Haw’abu”, hapo wakabwekewa na majibwa, Aisha akasema: “Yanaitwaje maji haya?” baadhi miongoni mwao wakasema: “Ni maji ya Haw’abu.” Aisha akasema: “Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na hakika kwake Yeye tutarejea! Nirudisheni, haya ni maji ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu aliniambia kuwa: ‘Usiwe mwanamke ambaye utakuja kubwekewa na majibwa ya Haw’abu.’” Lakini jamaa wakamletea wanaume arubaini wakaapa kwa Mwenyezi Mungu (kiapo cha uwongo) kuwa maji hayo si maji ya Haw’abu, na hatimaye jamaa wakafika Basra, na Amirul-Muuminina naye akafika hapo na hatimaye vikatokea Vita vya Ngamia (Jamali) sehemu inayoitwa alHaribah ikiwa ni mfunguo nane (Jamadul-Uwla), mwaka wa 36 A.H. Pili: Kuwatahadharisha maadui na makundi ya wapinzani kuhusu hatima ya jambo hili, na kuwatisha kuwa atakabiliana nao kwa nguvu zote ili kuitetea haki na ukweli. 32
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 32
7/5/2013 9:06:13 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
Hakika msimamo wa mtu katika maisha huainisha sura ya ujumbe anaouamini na uwezo wake katika kuendesha mambo yake na kutatua matatizo yake. Na nguvu ya msimamo huonekana kupitia uwazi wa maneno anayoyaongea mtu, hivyo Imam (as) hapa anakabiliana na changamoto za maadui zake kwa vitisho na vita, na kupitia hilo anaainisha imani yake ya kitume ya kweli. Anasema (as): “Tangu lini ewe Muawiya nyinyi mmekuwa wasimamizi wa raia na watawala wa mambo ya umma? Bila ya kuwa na ubora wenye kuonekana hapo nyuma, wala utukufu wa ziada. Na ninakutahadharisha juu ya kuendelea kudanganywa na utashi tofauti, wa wazi na wa siri.” Na anasema pia: “Umewaita watu kwenye vita, basi waache watu kando na uje kwangu (tupambane), na yaepushe makundi mawili mbali na mapigano, ili ujuwe ni yupi kati yetu mwenye moyo mzoefu na aliyefunika macho yake. Basi elewa kwamba hakika mimi ni Abu Hasan muuwaji wa babu yako, ndugu yako na mjomba wako, kwa kuwakatakata siku ya Badri. Na upanga ule bado ninao, na kwa moyo ule ule namkabili adui yangu…” (Barua ya 10). Tatu: Kupitia barua zake kwenda kwa wapinzani na maadui zake, Imamu (as) alikuwa anaelekeza kwao wito unaowataka wafanye taamuli, watafakari na kutumia akili, na wito wa kweli unaowataka waache kuugawa umma na kuufarakisha. Bali ulikuwa ni wito wa wazi unaozitaka dhamira zilizokufa ambazo zinajaribu kugeuza ukweli na kuficha ukweli mbele za watu kuhusu matukio husika, zirudi kwenye uongofu wake na akili yake na zifuate njia ya haki na imani. 33
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 33
7/5/2013 9:06:13 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
Kwa sababu mfarakano unaougawa umma na kuondoa roho ya kusaidiana na umoja baina ya raia, ndio zana kuu inayoyapa nguvu makundi ya kidhalimu kudhibiti hatamu za mambo. Na hili ndilo lililomtokea Imam Ali (as) pindi kundi lake lilipofarakana kuhusu suala la mahakimu wawili, jambo ambalo lilimpa nguvu Muawiya ya kujiandaa kudhibiti hatamu za mambo. Kadhalika lilimtokea Imamu Hasan (as) pindi kundi lake lilipogawika katika makundi tofauti, jambo ambalo pia lilimpa nguvu Muawiya ya kudhibiti hatamu za serikali kwa ukamilifu. Imamu (as) anasema: “Umekiangamiza kizazi kikubwa cha watu ambao umewahadaa kutokana na upotofu wako, na kuwaingiza katika mawimbi ya bahari yako, wanafunikwa na giza, na kupigwa na shubha (batili iliyoshabihiyana na ukweli), basi wamepotea mbali na njia ya sawa na kurejea nyuma ya visigino vyao na kugeuka nyuma ya migongo yao (wameasi maamrisho ya Mola Wao), na wakategemea juu ya nasaba zao, isipokuwa wale wenye uoni miongoni mwa wanaotambua, kwani wao walijitenga nawe baada ya kukutambua, wakati ulipowaingiza katika mashaka na kuwatoa katika lengo (la kumuabudu Mola Wao), basi ewe Muawiya, mche Mwenyezi Mungu kwa ajili ya nafsi yako, na jiepushe na kuongozwa na Shetani, kwani dunia ni yenye kukukatikia, na Akhera ipo karibu nawe. Wasalamu.� (Barua ya 32).
34
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 34
7/5/2013 9:06:13 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
FASLU YA PILI WARAKA WA IMAM KWENDA KWA MALIK AL-ASHTAR
W
araka huu unazingatiwa kuwa ni miongoni mwa maandiko muhimu sana aliyoyaandika Imam Ali (as) kuhusu usimamizi na utawala, bali ni miongoni mwa nguzo za kifikra za kisiasa na miongozo ya kiutawala ambayo Kiongozi aliipeleka kwa mmoja kati ya Magavana wake. Waraka huu umejumuisha mchoro wa mfumo mpana wa siasa ya jamii ambayo Mtawala anapaswa kuifuata katika kila zama na katika kila mji, kwa kufuata misingi ya maadili ya Kiislamu ambayo yanalenga kunadhimu maisha ya Kijamii kwa mpangilio makini, na kujenga mahusiano ya ndani katika jamii ya Kiislamu juu ya msingi imara na wa sawa, sawa iwe katika namna ya Mtawala kuamiliana na raia na wandani wake, kwa kufuata siasa yenye kuleta uhuru na maendeleo kwa jamii, au iwe katika nyanja ya mahusiano ya nje pamoja na adui na rafiki, kwa namna ambayo itahifadhi heshima ya umma, nguvu yake na uhuru wake kamili.
Mamlaka ambayo Imamu (as) alimkabidhi al-Ashtar: Waraka umejumuisha mambo kadhaa ya msingi ambayo ni wajibu Mtawala kuyatilia umuhimu, nayo ni manne: 35
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 35
7/5/2013 9:06:13 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
Kwanza: Shughuli za Kiuchumi: Waraka unasisitiza wajibu wa Mtawala kufaidika na vyanzo vya Kiuchumi na rasilimali, na kuvikuza kwa njia salama kwa kufuata misingi yenye faida na yenye kujenga, ili nguvu hii iweze kuutumikia umma katika njia ya kuleta msukumo wa ustaarabu wa Kiislamu ulio mbali na nguvu za kibeberu, na wenye kuafikiana na utashi wa Mwislamu. Kama ambavyo pia kufaidika na vyanzo vya Kiuchumi ni wajibu iwe kwa namna ambayo italinda uhuru wa umma na utu wake, na kutokufuata nguvu za nje, na hiyo itatimia kwa njia ya kujijengea uwezo wa kujitegemea kwa kuweka njia na mifumo ya Kiuchumi yenye kutoa dhamana hiyo. “Mhitajie yeyote umtakaye utakuwa mateka wake. Usimhitajie yeyote umtakaye utakuwa mfano wake. Na mtendee wema yeyote umtakaye utakuwa amiri wake.” Kwa kufaidika na kheri zilizomo ndani ya umma na kuzielekeza kwenye mwelekeo sahihi kwenye lengo tukufu, na kuziweka katika mazingira ya kuihudumia jamii na ubinadamu. Imam Ali (as) anamtaka Malik kufaidika na kila nguvu ya kimada na kibinadamu iliyotelekezwa, na afanye kazi ya kuitumikisha na kuishughulisha kwa ajili ya kunyanyua kiwango cha uchumi wa nchi, na hili kwa msisitizo kabisa ndilo linalosisitizwa na riwaya nyingi, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) anasema: “Ibada ina sehemu sabini, iliyo bora zaidi (kati ya hizo sabini) ni kutafuta halali.” Na anasema tena (saww): “Ewe Mungu Wangu tubarikie mkate wetu na wala usitutenganishe nao. Na bila mkate tusingesali wala kufunga, na wala tusingetekeleza faradhi za 36
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 36
7/5/2013 9:06:13 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
Mola Wetu.” Na anasema tena (saww): “Ufakiri umekaribia kuwa ukafiri.”
Pili: Shughuli za Kijeshi: Waraka unasisitiza wajibu wa kulinda kiukamilifu uhuru wa umma na kutetea kwa nguvu zote haki zake, heshima yake na nguvu yake, na kumdhibiti kila anayejaribu kutaka kuzua machafuko na mtikisiko katika safu za umma. Kisha ni wajibu kufanya kazi ya kuimarisha ulinzi wa nchi kwa njia ya kukuza na kuendeleza rasilimali za umma, kuendeleza na kuhuisha nguvu zake. Uislamu unatumia silaha ya kutoa changamoto mbele ya kila anayeupa Uislamu changamoto, na unajitokeza mbele ya maadui zake kwa nguvu zake zote za kimada na kimaanawiya ambazo huzikuza ndani ya nafsi za watu wake. Mwenyezi Mungu anasema:
ُون َ َوأَعِ ُّدوا َل ُھ ْم َما اسْ َت َطعْ ُت ْم ِمنْ قُوَّ ٍة َو ِمنْ ِربَاطِ ْال َخي ِْل ُترْ ِھب ﷲ َو َع ُدوَّ ُك ْم ِ َّ َِّب ِه َع ُدو “Basi waandalieni nguvu kama muwezavyo, na kwa farasi waliofungwa tayari-tayari, ili kuwatishia maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu..” (Sura An’fal: 60).
Hakika kulikuwa na mazingira tete huko Misri, mazingira ambayo yalionekana kupitia hujuma zenye kufuatana, na mashambulizi ya kidhalimu kutoka kwa maadui, dhidi ya 37
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 37
7/5/2013 9:06:14 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
umma na mipaka yake salama, mpaka mazingira hayo yakafanya mapambano kuwa ni suala la lazima, na mazingira haya yakaainisha aina ya mapambano, nayo yalikuwa ni mapambano ya kijeshi. Mwenyezi Mungu anasema: “Wafanyieni uadui kwa kadiri walivyokufanyieni uadui.” Hivyo Uislamu ni amani kwa anayeishi nao kwa amani, ni vita kwa anayeupiga vita, na ni jihadi dhidi ya adui wake.
Tatu: Shughuli za Kijamii: Ni lazima kukidhi mahitaji ya dharura ya jamii kwa ajili ya kuhakikisha saada ya jamii inapatikana, kama vile amani ambayo ni kizuizi kinachozuia kutenda jinai, na kama vile siha ambayo inazuia kuenea kwa maradhi na kutoa tiba kwa wagonjwa, na kama vile elimu ili kufuta ujinga katika maisha ya jamii, na kuhakikisha fursa za kazi zinapatikana ili kutokomeza ukosefu wa kazi, na kuhakikisha huduma za kijamii zinapatikana kwa watu ili kuzuia ufakiri na udhaifu. Imamu Ali (as) anasema: “…..Na kuwafanyia mema watu wake….”
Nne: Shughuli za Kimaendeleo: Kama vile kutilia umuhimu ujenzi kwa kuweka miundombinu ya miji, kujenga makazi, maeneo ya huduma za umma (Masoko, hospitali, vituo vya mafuta, nk), kuendeleza ardhi kwa kilimo, na kushajiisha viwanda vya ndani kwa ajili ya kujijengea uwezo wa kujitegemea na hatimaye kutokomeza matatizo ya kimada na kuendeleza miundombinu ya kimai38
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 38
7/5/2013 9:06:14 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
sha kwa ajili ya kuupeleka umma katika msafara wa ustaarabu na maendeleo, na kwa ajili hiyo utapatikana ukamilifu katika taasisi za maendeleo ya kijamii. Imamu (as) anasema: “….Na kuiendeleza miji yake….”
39
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 39
7/5/2013 9:06:14 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
ULAZIMA WA MTAWALA KUIDHIBITI NAFSI YAKE
H
akika kuipiga vita nafsi na kung’oa matamanio na kuyapa kisogo kwa ajili ya kuelekea upande wa uongofu wa Mwenyezi Mungu, ndio maana yenyewe ya Mtawala kuidhibiti mwenyewe nafsi yake, na hali hii ni lazima itajiakisi katika hali ya umma na katika safari ya maisha ya umma, mpaka Mtawala na umma watakuwa kama kitu kimoja. Kila mmoja anaelezea hali ya mwingine, hivyo umma ambao unamfuata Mtawala mwenye imani, mwenye yakini na aliye safi, mara nyingi ni lazima na wenyewe utajivisha utu wake na utachukua kutoka kwake sifa zake na mwenendo wake, kwa sababu watu hufuata dini za wafalme wao. Kwa ajili hii inampasa Mtawala awe alama ya ustaarabu wa kweli katika dhana zote zinazobebwa na ustaarabu wa kitume, na katika maadili yote bora ya kibinadamu, autendee umma kheri na wema katika dunia na Akhera, bali ni wajibu awe kiigizo na mfano wa juu kabisa wa watu wa taifa lake na umma wake, na hiyo ni kwa kutabikisha mtazamo wa Uislamu, dhana za haki na majukumu na wajibu uliofaradhishwa na Uislamu, na kuweza kuutelekeza kwanza katika nafsi yake na katika maisha yake ya kimatendo kabla hajautoa na kuuwasilisha wajibu huo katika jamii, Imam Ali (as) anasema: “….Na nimekukunjulieni mema kwa kauli yangu na vitendo vyangu, na nimekuonyesheni tabia njema za hali ya juu kutoka kwangu mimi mwenyewe binafsi….”
40
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 40
7/5/2013 9:06:14 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
Zaidi ya hapo ni wajibu Mtawala asikomee tu kwenye kuijali nafsi yake, bali anapaswa kwenda hadi kwenye medani ya matendo na utekelezaji wa nje ili kunusuru misingi na dini ya Mwenyezi Mungu, na kunusuru maadili yake (ya dini) kwa kuhakikisha yanatekelezwa katika umma, na si kuwaelekeza tu watu katika maadili hayo bali pia ni kuunda mazingira yanayofaa yatakayowezesha maadili hayo kutekelezwa, na hiyo ni kwa njia ya kuyaimarisha maadili hayo katika jamii na kuyafanya kuwa ndio maamuzi ya mwanzo na mwisho.
41
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 41
7/5/2013 9:06:14 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
SIFA ZA UONGOZI
K
uanzia hapa ndipo linapojitokeza swali: Ni nani anayefaa kuchukua uongozi wa umma?
Uongozi ni sawa na akili yenye kuuelekeza umma, kwani wenyewe ni dharura ya kimaisha kwa ajili ya kuipangilia jamii, hivyo si kila mtu ana uwezo wa kutambua majukumu ya dhamana hii kubwa, bali kuna vipimo na vigezo ambavyo kwa msingi wake uongozi huchaguliwa, na vilivyo muhimu kati ya hivyo ni:
Kwanza: Uchamungu: Moyo usiyokuwa na uchamungu ni moyo mfu, hauna harakati wala nguvu, kwa ajili hiyo ndio maana uchamungu umezingatiwa kuwa ndio sharti la kwanza na muhimu zaidi ambalo ni lazima litimie kwa Mtawala, kwa sababu uchamungu ni sawa na ngome imara ambayo inamzuia Mtawala kwenda nje ya njia sahihi. Imamu (as) anasema: “Hakika uchamungu ni nyumba iliyo ngome imara.� Ama mtu aliyekosa sifa hii ya msingi hataweza kuyashinda mashinikizo ya nafsi yake na matamanio yake, na kusimama imara mbele ya matatizo na magumu ya maisha ambayo hujitokeza katika njia ya maisha. Kuanzia hapa sifa hii ya uchamungu inakuwa ndio nguzo ya msingi ambayo ni wajibu ipatikane katika utu wa Mtawala, kwa sababu watu wengi wapo katika hatari ya kuteleza na kupotoka kwa sababu ya nafasi zao za kiuongozi katika umma, 42
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 42
7/5/2013 9:06:14 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
kwani mamlaka ya juu, mamlaka ya kisiasa, nguvu ya kijeshi na kiuchumi, vyote vimo mkononi mwake na chini ya amri yake. Na iko wazi jinsi mambo haya yalivyo na mchango mkubwa katika kumwangusha mtu katika maporomoko ya upotovu na udikteta.
Pili: Uwezo wa Kielimu: Inamaanisha maarifa kamili kuhusu mambo ya dini, na uwezo wa kutoa hukumu zake kutoka ndani ya vyanzo vyake vyote, kama vile Qur’ani, Sunnah, Akili na Ijmai, na kuwa na uwelewa kamili kuhusu mambo ya maisha ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kimaendeleo, kwa sababu yote hayo ni mambo ya kimaisha na ya dharura ambayo ni lazima yawepo kwa Mtawala. Na ni kwa sababu kwa upande mmoja ni lazima pia Mtawala awe mjuzi mwenye kutambua maadili ya Kiislamu ya kimbingu, na matukio ya nje kwa upande mwingine, ili aweze kuwaelekeza watu katika njia sahihi. Imam (as) anasema: “…Lakini wamtazame mtu miongoni mwenu ambaye amepokea hadithi zetu, amechunguza halali yetu na haramu yetu na ametambua hukumu zetu, wamridhie awe hakimu, kwani hakika mimi nimemfanya hakimu juu yenu. na iwapo atahukumu kwa hukumu yetu kisha mtu akaikataa kutoka kwake, basi mtu huyo atakuwa ameidharau hukumu ya Mwenyezi Mungu na ametupinga sisi. Na kutupinga sisi ni kumpinga Mwenyezi Mungu, na kumpinga Mwenyezi Mungu ni sawa na kumshirikisha Mwenyezi Mungu.” 43
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 43
7/5/2013 9:06:14 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
Tatu: Uwezo wa Kivitendo: Inamaanisha uwezo wa kufahamu mambo ya maisha na kuamiliana na matukio yaliyopo kwa mtazamo wa Mwenyezi Mungu na kulingana na mtazamo wa Uislamu. Na kusimama imara na thabiti mbele ya changamoto zinazoukabili umma, na kuwa na uwezo wa kuwaongoza watu na kusahihisha mwenendo wao katika maisha, na kuwaelekeza upande wa amani na uokovu wakati wa matatizo, na kuulinda umma dhidi ya njama ambazo zinaukabili umma kila wakati. Imamu (as) anasema: “Ama kuhusu matukio yanayojitokeza rejeeni kwa wapokezi wa hadithi zetu, hakika wao ni hoja yangu juu yenu, na mimi ni hoja ya Mwenyezi Mungu juu yao.�
44
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 44
7/5/2013 9:06:14 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
Kufaidika na uzoefu wa waliotangulia:
I
li Mtawala awe kiongozi wa kuigwa, mwenye uwelewa katika uendeshaji wa mambo yake na mwenye mafanikio katika kuwaongoza kwake watu, ni juu yake kurudi kwenye historia na kuchukua mazingatio na maarifa kutoka kwa waliotangulia, kwa sababu kumiliki kwake uzoefu wa watawala na viongozi wengine waliomtangulia, na kutambua msimamo wa jamhuri kuhusu viongozi hao, kutamsaidia sana kugundua udhaifu ulipo (sababu zinazopelekea utawala wake kuanguka) na kujitenga nao mbali, na kutambua ukamilifu ulipo (sababu zinazopelekea utawala wake kubakia) na kuutilia mkazo, ili ajenge uhusiano wake na raia juu ya msingi imara usiotetereka, na ili asitumbukie ndani ya makosa ambayo walitumbukia humo wale waliomtangulia. Kwa sababu uzoefu wa waliomtangulia utampa mtazamo kamili wa njia inayofaa katika kuamiliana na watu, na kwa ajili hiyo uzoefu huu utakuwa kioo atakachotumia kurekebishia misimamo yake na kunyooshea njia yake, na hatimaye uongozi wake utaoana na kuafikiana na matarajio na uwelewa wa raia ambao yeye alikuwa ni mmoja wao. Raia hawawezi kuyakubali yaliyo nyuma ya fikra zinazowasilishwa na kiongozi katika jamii, isipokuwa watakapojiridhisha kuwa zinafaa kuzitabikisha kwake mwenyewe na kwamba zitamletea kheri na kudhamini saada yake na raha yake katika maisha. Kwa ajili hiyo ni wajibu na lazima kwa kiongozi kuthibitisha kivitendo faida zitokanazo na sera ana45
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 45
7/5/2013 9:06:14 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
zoziwasilisha katika jamii, ili raia wapate matumaini kwamba fikra na sera hizo zinaafikiana na matarajio wanayoyatamani na wanayotaka yatimie katika maisha yao. Hiyo ni kwa sababu mara nyingi raia wamezoea kusikia sera zisizo na kitu ambazo huwasilishwa na viongozi wao wenye kufuatana, na ambao hutoa nadharia kama sera zenye kuvutia wakati ambapo umma huwa haupati utekelezaji wa nje katika kiwango cha jamii. Hivyo suala limejificha katika utekelezaji wa sera hizi ambazo ni kama sera mpya, na jinsi gani raia watakavyozipokea kutokana na zitakavyowafaidisha. Imamu Ali (as) anasema: “Halafu elewa ewe Malik kwamba, nimekupeleka kwenye eneo ambalo zimepita serikali mbalimbali kabla yako, miongoni mwa serikali adilifu na zile za kidhalimu, na kwa hakika watu watakuwa wanayaangalia mambo yako kama vile ulivyokuwa ukiyaangalia mambo ya watawala waliokuwa kabla yako. Na watakuwa wanakukosoa kama ulivyokuwa ukiwakosoa. Kwa kweli hutambulika watu wema kwa yale ayapitishayo Mwenyezi Mungu katika ndimi za waja, hivyo basi hazina uipendayo zaidi iwe ni hazina ya matendo mema‌â€?
46
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 46
7/5/2013 9:06:14 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
Kutosukumwa na matamanio na ubinafsi:
P
indi matamanio yanapomdhibiti mtu hugeuka na kuwa sababu yenye kuathiri mwenendo wake, na huporomosha tabia zake zote na maadili yake ya kiutu ndani ya nafsi yake, kiasi kwamba huwa mtumwa duni asiyefaa. Hiyo ni kwa sababu kudhibitiwa na matamanio huwa kunamfanya mtu awe kama mnyama aliyefungwa ambaye lengo lake ni chakula, au mnyama aliye huru ambaye hudhalilishwa na shughuli yake, kiasi kwamba nafsi yake huwa ndio kigezo ambacho hutumia kupimia kila kitu, huifanya ndio mizani na kipimo, hivyo kila kinachoafiki matamanio ya nafsi yake hukiamini, la sivyo hukikhalifu. Kwa ajili hiyo ni wajibu juu ya Kiongozi wa Kiislamu kwanza aanze na nafsi yake, yaani ajinasue toka kwenye mashinikizo ya nafsi na udanganyifu wake, ili baada ya hapo aweze kubadili hali halisi na kuiathiri jamii. Hivyo jambo lenye kushughulisha fikra ya Kiongozi wa Kiislamu ni lazima liwe ni jambo la Mwenyezi Mungu na watu, jambo la dini na jamhuri, si jambo la nafsi yake na matamanio yake. Hivyo hapaswi kufikiria manufaa yake binafsi kwa kadiri anayofikiria mambo ya raia, na ajitolee kwa kila kitu chake na kwa juhudi zake zote katika kuwatumikia raia. Imamu (as) anasema: “Udhibiti utashi wako, inyime nafsi yako yasiyo halali kwako, kwani kuinyima nafsi ni miongoini mwa kuifanyia uadilifu katika inayoyapenda au kuyachukia.� 47
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 47
7/5/2013 9:06:14 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
Muamala wa Mtawala kwa raia:
H
akika muamala wa Mtawala kwa raia ni lazima uwe muamala wa kiusimamizi na ulio juu ya msingi wa huruma, upendo na upole, ili kuleta mazingira ya kimaanawiya yenye kuungana na kutengeneza mshikamano wa kisaikolojia baina ya raia na Mtawala, hivyo inapasa kujiepusha kabisa na muamala wa kidikteta, bali ni wajibu Mtawala kuheshimu hisia za wengine na ajaribu kadiri awezavyo kujitenga mbali na maeneo ambayo yatajeruhi hisia zao na kuzitibua.
Yeyote atakaye kuwaongoza watu ni lazima ajifunze namna ya kudhibiti hisia zake katika kuamiliana na jamii, na ajitume kwa juhudi zake zote katika kutatua matatizo yake kwa njia iliyo mbali kabisa na udikteta, ili kwamba watu wasimkimbie, hivyo Mtawala wa Kiislamu ni yule ambaye anabeba matatizo ya watu na kuyaweka katika daraja la kwanza miongoni mwa matatizo yake, hivyo anakuwa baba mwema mwenye moyo mpana kwa raia, na mpole mvumilivu. Qur’ani mpana kwa raia, na mpole mvumilivu. Qur’ani inaashiria inaashiria upande huu kwa kusema:
upande huu kwa kusema:
ْ َو ين َ ِاح َك لِ َم ِن اتﱠبَ َعكَ ِم َن ا ْل ُم ْؤ ِمن ْ ِاخف َ َض َجن “Na watwae kwa upole wanao kufuata miongoni mwa “Na watwae kwa upole wanao kufuata Waumini.” (Sura Shuaraa: 215).
miongoni mwa Waumini.” (Sura Shuaraa: 215). Na Na
◌ۖ ضوا ِمنْ َح ْولِ َك ب َال ْنفَ ﱡ ِ 48َولَ ْو ُك ْنتَ فَظًّا َغلِيظَ ا ْلقَ ْل “Na lau ungelikuwa mkali, mwenye moyo mgumu, bila ya shaka wangelikukimbia.”
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 48
7/5/2013 9:06:14 AM
“Na watwae kwa upole wanao kufuata miongoni mwa Waumini.” (Sura Shuaraa: 215).
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
Na
◌ۖ ضوا ِمنْ َح ْولِ َك ب َال ْنفَ ﱡ ِ َولَ ْو ُك ْنتَ فَظًّا َغلِيظَ ا ْلقَ ْل “Na lau ungelikuwa mkali, mwenye moyo mgumu, bila ya “Nashaka lau wangelikukimbia.” ungelikuwa mkali,(Sura mwenye moyo Imran: 159).
mgumu, bila ya shaka wangelikukimbia.” (Sura Imran: 159). Katika upande huu Imamu Ali (as) anasisitiza misingi
mitatu ambayo ni wajibu Mtawala kuifuata katika kuamiliana
Katika upande kwake na watu:huu Imamu Ali (as) anasisitiza misingi mitatu ambayo ni wajibu Mtawala kuifuata katika kuamiliana kwake Kwanza: Hakika watu ima ni ndugu zako katika dini au na watu: ni mfano wako katika ubinadamu, mtazamo huu ndio unaomzuia Mtawala kujikweza juu ya wengine na kuwafanyia Kwanza: Hakika watu ima ni ndugu zako katika dini au ni kiburi watu. Hiyo ni kwa kuwa tofauti zote za kimada kama mfano wako katika ubinadamu, mtazamo huu ndio unaomzuia vile rangi, lugha, na ubaguzi, zote huyeyuka katikati ya Mtawala kujikweza juu ya wengine na kuwafanyia kiburi maadili ya Kiislamu, na Uislamu unazingatia kuwa tofauti watu. ni yenye kwa kuwa tofauti zote za vile hizo niHiyo sababu kubomoa muundo wakimada jamii, nakama ni zana rangi, na ubaguzi, zoteyahuyeyuka katikati ya ajili maadili yenyelugha, kuvunja mahusiano kibinadamu, kwa hiyoya Kiislamu, na Uislamu dharura unazingatia kuwa tofautimahusiano hizo ni sababu Uislamu umesisitiza ya kuimarisha ya yenye kubomoa muundo wa jamii, na ni zana yenye kuvunja kibinadamu kupitia kiunganishi cha msingi, nacho ni kiunmahusiano kibinadamu, hiyo umesisitiza ganishi chaya imani na udugukwa wa ajili imani ya Uislamu kweli. Imamu (as) dharura kuimarisha mahusiano ya aina kibinadamu kupitia anasema:ya“Kwani wao (raia) wako katika mbili: Ama ni kiunganishi cha msingi, nacho ni kiunganishi cha imani ndugu yako katika Dini au ni mfano wako katika kuumbwana (ni binadamu kama wewe)….” Pili: Kwa kuwa cheo cha Mtawala katika jamii ya Kiisla54 mu si zana ya kujikwezea na kuwafanyia kiburi watu, bali ni kituo cha huduma na kuvumilia joho la majukumu yote, na kwa kuwa Mtawala anawaongoza raia kwa msingi wa maadili ya Mwenyezi Mungu na kwa ajili ya maslahi yao na saada yao, hivyo ni wajibu katika siasa yake kwenda kulingana na amri za Mwenyezi Mungu, hivyo asikhalifu sharia ya Mwe49
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 49
7/5/2013 9:06:15 AM
zanahuduma ya kujikwezea na kuwafanyia kiburi watu,yote, bali na ni kituo cha na kuvumilia joho la majukumu kwa cha huduma na kuvumilia joho la majukumu yote, na kuwa Mtawala anawaongoza raia kwa msingi wa maadilikwa ya kuwa Mtawala anawaongoza raia kwa msingi wa maadili ya Mwenyezi Mungu na kwa ajili ya maslahi yao na saada yao, Mwenyezi Mungu na kwa yakwenda maslahikulingana yao na saada yao, hivyo ni wajibu katika siasaajili yake na amri Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.) hivyo ni wajibu katikahivyo siasa yake kwenda kulingana na amri za Mwenyezi Mungu, asikhalifu sharia ya Mwenyezi za Mwenyezi Mungu, shariakanuni ya Mwenyezi Mungu kwa dhulma na hivyo ujeuri. asikhalifu Kiasi kwamba zote za Mungu kwa dhulma na ujeuri. Kiasi kwamba kanuni zote za nyezi Mungu kwa zitoke dhulmandani na ujeuri. Kiasi asili, kwamba kanuni serikali ya Mtawala ya Uislamu si Uislamu serikali Mtawala zitoke na ndani yandani Uislamu asili, si Uislamu zote za ya serikali ya Mtawala zitoke ya Uislamu asili,wa si wa ubinafsi na matamanio, serikali itokane na uchaguzi wa ubinafsi na matamanio, na serikali itokane na uchaguzi wa Uislamu wa ubinafsi na matamanio, na serikali itokane na umma wa Waislamu wenyewe na si iwe inayotokana umma wa Waislamu na si iwe inayotokana na uchaguzi wa umma wawenyewe Waislamu wenyewe si iwe inayotomabavu kwa kurithishana au mapinduzi yanakijeshi, au kwa mabavu kurithishana auyanapokosekana mapinduzi ya kijeshi, auhaya kwa kana nakwa mabavu kwahivyo kurithishana au mapinduzi ya kijeshi, shinikizo la ukoloni, masharti shinikizo la ukoloni, hivyo hivyo yanapokosekana haya au kwa shinikizo la ukoloni, yanapokosekana masharti katika serikali iliyopo madarakani, serikali hiyo masharti kwa mtazamo katika serikali iliyopo madarakani, serikali hiyo kwa mtazamo haya katika serikali iliyopo madarakani, serikali hiyo kwa wa raia huzingatiwa kuwa ni serikali haribifu isiyo ya mtazamo wa raia huzingatiwa kuwa ni serikali haribifu isiyo wa raia huzingatiwa kuwa ni serikali haribifu isiyo ya Kiislamu. ya Kiislamu. Kiislamu. Mwenyezi Mungu anasema: Mwenyezi Mungu anasema: Mwenyezi Mungu anasema:
ق ۚ ُھ َو َخ ْي ٌر ثَ َوابًا َو َخ ْي ٌر ُع ْقبًا ُھنَالِ َك ا ْل َو َاليَةُ ِ ﱠ�ِ ا ْل َح ﱢ َ ْ َ َ ق ۚ ُھ َو خ ْي ٌر ث َوابًا َوخ ْي ٌر ُعقبًا ُھنَالِ َك ا ْل َو َاليَةُ ِ ﱠ�ِ ا ْل َح ﱢ
“Hakuna hukumu isipokuwa ya Mwenyezi
“Hakuna hukumu isipokuwa ya Mwenyezi Mungu.” “Huko “Hakuna hukumu isipokuwawa ya Mwenyezi Mwenyezi Mungu.”“Huko usaidizi usaidizi ni wa Mwenyezi Mungu,niMkweli. Yeye ni Mbora Mungu.”“Huko usaidizi ni wakwa Mwenyezi Mungu, Mkweli. Yeye Mbora (Suramalipo Kahfi: 44). kwa malipo na mbora wanimatokeo.”
Mungu, Yeye ni(Sura Mbora kwa44). malipo na mboraMkweli. wa matokeo.” Kahfi: na mbora wa matokeo.” (Sura Kahfi: 44).
َو َمنْ لَ ْم يَ ْح ُك ْم بِ َما أَ ْن َز َل ﱠ ون َ ﷲُ فَأ ُ ٰو ٰلَئِ َك ُھ ُم ا ْل َكافِ ُر َو َمنْ لَ ْم يَ ْح ُك ْم بِ َما أَ ْن َز َل ﱠ ون َ ﷲُ فَأُولَئِ َك ُھ ُم ا ْل َكافِ ُر
“Na wasiohukumu kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio55 Makafiri.” (Sura Maidah: 44).
55
Imamu Ali (as) amesema: “Wala usijisimamishie vita kwa kupigana na Mwenyezi Mungu kwani huna mkono (nguvu) mbele ya kisasi Chake, na hujitoshelezi bila ya msamaha Wake na huruma Yake…” Tatu: Ni wajibu Mtawala asifikirie kuwa wajibu wake ni tu kutoa maagizo yasiyo na maswali, bali ni lazima katika hilo aheshimu mazingira waliyomo raia wake, na awe na 50
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 50
7/5/2013 9:06:15 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
utambuzi kamili juu ya mazingira yanayowazunguka raia wake, hivyo aoanishe baina ya fikra zinazotolewa na uwezo uliyopo, na kisha afaidike na rai zote ili kutoa maagizo bora zaidi, kwa sababu Kiongozi mwenye busara ni yule ambaye rai zake zinaoana na kukubaliana na mazingira yaliyopo katika jamii. Imamu Ali (as) anasema: “Wala usiseme kuwa mimi ni mwenye kuamrisha, hivyo naamrisha nitiiwe…” Udikteta wa mawazo na kutozingatia mambo haya, husababisha: a. Huleta matatizo ya kisaikolojia kwa watu: “Kufanya hivyo ni kuuingiza ufisadi moyoni..” kwa sababu hali za kijamii, kisiasa na kiuchumi hutegemea misingi ya kisaikolojia ya umma, ikiwa hakuna uwiano baina ya misingi ya kisaikolojia na mambo hayo, umma huwa katika hali ya kuyumba na kuhangaika, jambo ambalo husababisha kukosekana mshikamano, siasa, uchumi na mengineyo kwa upande mmoja, lakini pia kukosekana raha, kuwepo na mashaka na matatizo ya kisaikolojia kwa upande mwingine. Hakika Dr. Shakhty wa Ujerumani aliiwekea Ujerumani mipango ya kiuchumi na akafanikiwa katika sehemu kubwa ya mipango hiyo, wakati ambapo Dr Shakhtiy huyo huyo aliiwekea Indonesia mipango hiyo lakini ikafeli katika sehemu kubwa ya mipango hiyo, licha ya kwamba Indonesia ni miongoni mwa nchi za Mwenyezi Mungu zenye ardhi yenye rutuba nyingi, na ni miongoni mwa nchi zilizoendelea kwa mikono ya vibaraka. Kufeli huku kwa mipango hii hakukutokana na sababu nyingine isipokuwa ni kwa sababu hali ya kisaikolojia ya jamii ya Indonesia ilikuwa inatofautiana na hali ya kisaikolojia ya jamii ya Ujerumani. Na sisi Waislamu 51
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 51
7/5/2013 9:06:15 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
tulipobaki nyuma kiuchumi kwa namna hii ya aibu ni kwa sababu mipango iliyowekwa kwa ajili ya uchumi wetu ilikuwa inatofautiana na hali ya kisaikolojia iliyopo kwetu.1 Hivyo udikteta wa mawazo mwisho wake ni kuleta mpasuko wa kisaikolojia baina ya matakwa ya raia na matakwa ya Kiongozi, jambo ambalo huleta mkinzano na mgongano baina yao, na hatimaye hutokea yenye kutokea, na kwa ajili hiyo wamesema: “Uongozi bora na wenye umri mrefu ni ule utokao ndani ya umma wenyewe.” b. Huchafua sura halisi ya dini ya Uislamu, hiyo ni kwa kuudhihirisha Uislamu kwa sura ya ukatili na matumizi ya nguvu, na kuwa wenyewe hauna huruma na upole, hiyo ni kwa sababu utekelezaji wa dhana za dini ni lazima uonekane kwa viongozi, hivyo kitendo cha viongozi kukiuka maadili ya Uislamu kunapelekea watu kutokuwa na imani na serikali, na uhalali wake kuondoka machoni mwao, hivyo Imam Ali (as) anasema: “…Na kuidhoofisha Dini…” c. Kiongozi kuanguka, hiyo ni kwa sababu kitendo cha Kiongozi kuharakisha kuchukua hatua juu ya raia bila kuheshimu mazingira ya kisaikolojia na kijamii, na jinsi hatua hizo zinavyoweza kutekelezwa katika jamii, kutaleta athari mbaya na hatua hizo zitakataliwa na kutokutekelezwa. Si kwa sababu fikra na hatua husika si sahihi, hapana, isipokuwa ni kwa sababu ya mazingira iliyomo jamii husika, na jambo hili huongeza mpasuko baina ya raia na Kiongozi wao, mpasuko mkubwa na hatimaye huwa ni mapinduzi dhidi yake, Imamu Ali (as) anasema: “…Na kujikurubisha kwenye maangamizi.” 1
Fiqhul-Iqtisad Uk. 85 cha Ayatullah al-Udhma Sayyid Muhammad Shiraz. 52
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 52
7/5/2013 9:06:15 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
Tiba ya kiburi:
H
akika tiba pekee ya maradhi ya kiburi ambacho huanza kwa Mtawala kwa kutaka kujikweza kwa mamlaka yake, ni kukumbuka adhama ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, jambo hilo linatosha kumfanya mdogo Kiongozi huyo mbele ya adhama hiyo, na hatimaye atarudi katika akili yake na uongofu wake, Imamu Ali (as) anasema: “Na ikiwa mamlaka uliyonayo inakusababishia majivuno au kiburi, angalia utukufu wa mamlaka ya Mwenyezi Mungu juu yako, na uwezo Wake kwako, ambao usio uweza nafsini mwako, hilo litaishusha tamaa yako, na kuzuia ukali wako, na kukurejeshea yaliyoghibu mbali na akili yako!�
53
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 53
7/5/2013 9:06:15 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
Kushikamana na uadilifu:
M
iongoni mwa sifa ambazo ni lazima awe nazo Kiongozi ni uadilifu, na autumie katika pande mbili:
Ya kwanza: Katika uhusiano wake na Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa maana ya kwamba ni wajibu juu ya Kiongozi kumfanyia Mwenyezi Mungu uadilifu, Imamu (as) anasema: “Mfanyie uadilifu Mwenyezi Mungu..” hiyo ni kwa kuilazimisha nafsi yake kumtii Yeye, kutekeleza vipengele vya sharia na kutekeleza wajibu wake kiukamilifu kama mmoja katika jamii na kama Kiongozi, na kadhalika kuilinda nafsi yake isiweze kuasi na kujiingiza katika mambo ya kimada na starehe za maisha ya duniani, mambo ambayo yatamzuia kupangilia mambo ya raia na kutekeleza mahitaji yao ya dharura, Imam Ali (as) anamsifu muumini mchamungu kwa kusema: “Amejiambatanisha binafsi na uadilifu, na ukawa uadilifu wake wa kwanza ni kujiondolea utashi binafsi.” Ya pili: Katika uhusiano wake na watu, ambapo majukumu ya Kiongozi ya kidini, kijamii na kiutu yanamlazimisha kuwafanyia uadilifu kivitendo raia na umma (Uadilifu wa Kijamii), kuwafanyia raia wote bila ubaguzi kwa kuheshimu haki zao na kuwapa uhuru wao kamili, na kuwatimizia nyenzo za maisha mazuri, na kuwatazama kwa mtazamo mmoja bila kuelemea upande mmoja na bila ubaguzi. Imamu Ali (as) anasema: “…Na wafanyiye watu uadilifu kutokana na nafsi yako na kutokana na jamaa zako walio makhsusi..” Hakuna ubora wala upendeleo isipokuwa kwa imani na uchamungu. Mwenyezi Mungu anasema:
54
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 54
7/5/2013 9:06:15 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
إِنﱠ أَ ْك َر َم ُك ْم ِع ْن َد ﱠ ۚ ﷲِ أَ ْتقَا ُك ْم “Hakika mtukufu zaidi yenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni
“Hakika mtukufu yenu aliyezaidi na takua zaidimbele yenu…”ya(Sura Hujurat: 13). Mwenyezi Mungu ni aliye na takua zaidi yenu…” (Sura HataHujurat: Kiongozi 13). hana ubora wa asili kuliko watu wengine, wa-
najamii wote wako sawa mbele ya kanuni, na wala Kiongozi a Kiongozi hana hana kinga uboradhidi wa ya asili kulikobali watu wengine, kanuni, kanuni inawajumuisha watu najamii wotewote, wako sawa mbele ya kanuni, na wala hivyo iwapo mtu atamshitaki atapaswa kusimama pamoja ngozi hanana kinga ya kanuni, bali kanuni mgomvidhidi wake mbele ya Kadhi ili mwenye haki kati yao ajuwajumuisha likane, watu wote, hivyohukumu iwapo zinawahusu mtu atamshitaki kwa sababu wote bila ubaguzi.
paswa kusimama pamoja na mgomvi wake mbele ya Kadhi mwenye haki kati yao ajulikane, kwa sababu hukumu awahusu wote bila ubaguzi.
ulma lazima imwangushe:
di dhulma inapoenea juu ya jamii na kuufunika uadilifu na ru kwa giza lake, huku Kiongozi akiwa amezifunga nyoyo watu kamba na kuwakandamiza wanajamii kwa nguvu ya ma na moto, hakuna kitakachofuata isipokuwa ni raia mkataa na kumpindua, mpaka serikali iliyopo ianguke na oweka kwa sababu ya msingi huu wa ukandamizaji na wa lma.2 Imamu Ali (as) anasema: “Na hapana kitu
ama tulivyoshuhudia hali hii hivi karibuni kwa kuanguka Serikali yingi za kidhalimu na za ukandamizaji ambazo zilijengwa juu ya isingi ya unyonyaji na ukandamizaji dhidi ya raia, kwa vibaraka wa chi za Magharibi kuwakandamiza raia wake na kuwanyonya mali zao a rasilimali za nchi zao, kwa kutumia nguvu ya dola. Lakini mwisho wa ku dunia imeshuhudia Zainul-Abidin bin Ali huko Tunisia, Husni ubaraka huko Misri na wengineo, waking’olewa madarakani kwa guvu ya umma na serikali zao kuanguka. Hiyo ni mifano tu, bado 55 wamko wa mageuzi katika nchi nyingine unakuja muda si mrefu – Mtarjuma 07_Uongozi na_05_July_2013.indd 55
7/5/2013 9:06:15 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
Dhulma lazima imwangushe:
P
indi dhulma inapoenea juu ya jamii na kuufunika uadilifu na uhuru kwa giza lake, huku Kiongozi akiwa amezifunga nyoyo za watu kamba na kuwakandamiza wanajamii kwa nguvu ya chuma na moto, hakuna kitakachofuata isipokuwa ni raia kumkataa na kumpindua, mpaka serikali iliyopo ianguke na kutoweka kwa sababu ya msingi huu wa ukandamizaji na wa dhulma.2 Imamu Ali (as) anasema: “Na hapana kitu kinachosababisha kuibadili neema ya Mwenyezi Mungu na kuharakisha adhabu Yake kama kubakia katika dhulma, kwa sababu Mwenyezi Mungu ni Msikivu mno wa maombi ya wenye kukandamizwa, Naye yuko kwenye lindo kwa ajili ya madhalimu.”
2
Kama tulivyoshuhudia hali hii hivi karibuni kwa kuanguka Serikali nyingi za kidhalimu na za ukandamizaji ambazo zilijengwa juu ya misingi ya unyonyaji na ukandamizaji dhidi ya raia, kwa vibaraka wa nchi za Magharibi kuwakandamiza raia wake na kuwanyonya mali zao na rasilimali za nchi zao, kwa kutumia nguvu ya dola. Lakini mwisho wa siku dunia imeshuhudia Zainul-Abidin bin Ali huko Tunisia, Husni Mubaraka huko Misri na wengineo, waking’olewa madarakani kwa nguvu ya umma na serikali zao kuanguka. Hiyo ni mifano tu, bado mwamko wa mageuzi katika nchi nyingine unakuja muda si mrefu – Mtarjuma 56
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 56
7/5/2013 9:06:15 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
Baina ya raia wa kawaida na tabaka la wasaidizi wa ÂMtawala:
H
akika nukta ya mwanzo katika kutengeneza tabaka la watawala au ambao huitwa wandani, ilikuwa ni ili kufanya kazi kwa lengo hili, yaani kufika katika madaraka kwa kuwa pamoja na Mtawala na bega kwa bega na yeye. Lakini pindi wanapofika katika nafasi hii, achilia mbali kuwa kwao na uwezo au kutokuwa na uwezo, hakika wao kwa kuzingatia historia yao bila shaka watapata baadhi ya nafasi ambazo zitawapa fursa ya kulazimisha rai zao kwa raia moja kwa moja au kwa njia ya kumshawishi Mtawala. Hivyo kwa kuwa kila muwamba ngoma huvutia kwake, wakati kundi hili linapofanya kazi ya kutimiza matakwa yake ya kimatamanio, upande mwingine raia hujituma na kujibidisha kwa ajili ya haki zao, hivyo hutokea mgongano baina ya maslahi ya viongozi na maslahi ya raia wa kawaida, na wakati huo Mtawala huwa baina ya kingo mbili kama mwendo wa mikondo miwili yenye kupingana. Wa kwanza: Ni mkondo wa maslahi ya tabaka la wandani (viongozi). Wa pili: Mkondo wa haki za raia kama jamii. Na hapa ndipo yanapojiainisha mambo mawili ya namna ya kuamiliana katika jamii kutokana na uwepo wa mikondo hii miwili tuliyotangulia kuitaja, mambo hayo ni: 57
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 57
7/5/2013 9:06:15 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
Kwanza: Ni kupita katikati katika mambo yenye mgongano, kwa sharti iwe ni haki, ili asidhulumu haki ya yeyote kati ya makundi hayo mawili. Imamu Ali (as) anasema: “Na yawe mambo yapendwayo sana na wewe ni yale ya wastani katika haki…” Na anasema pia: “Mambo bora kabisa ni ya wastani.” Pili: Ni kupata ridhaa ya raia, kwa sharti raia wawe na uwelewa juu ya maslahi yao na wasiwe wenye kuendeshwa na kundi fulani au mkondo fulani, baada ya hapo si muhimu tena tabaka lenye kumzunguka Mtawala kuridhia au kutokuridhia. Imamu (as) anasema: “…na makasiriko ya walio makhsusi husameheka waridhiapo walio wengi.” Na hapa ndipo linapojitokeza swali ndani ya mada hii, nalo ni kwa nini anasisitiza kuwa ridhaa ya watu makhususi si muhimu maadamu tu watu wa kawaida wameridhia, wakati tunajua kuwa watu makhususi hutengeneza kundi lenye nguvu ya kibinadamu na kiuchumi, na linaweza kundi hilo kuupa umma kitu fulani, ikiwa hivi ndivyo ni kwa nini basi anachukua msimamo huu hasi dhidi yao? Haya yote ni haki na kweli, lakini watu makhususi huwa na sifa ambazo huwazuia kuupa umma kitu fulani, na kwa msingi huo hupatikana msimamo huu hasi, na sifa hizo ni: Kwanza: Huwa na kipato cha ziada walichopewa na Mtawala aliyetangulia, na hutumia fursa hiyo kutaka kuongezewa zaidi ya zile haki wanazozipata raia wa kawaida. Imamu (as) anasema: “Na ni mwenye uzito zaidi juu ya gavana wakati wa raha ya maisha..” Pili: Huwa hawako tayari kutoa na kujitolea katika kuutetea umma au kumtetea Mtawala wakati wa hatari na matatizo, kwa sababu hujiweka katika nafasi ya mwenye 58
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 58
7/5/2013 9:06:16 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
kushindana na Mtawala na kufaidika na umma. Imamu (as) anasema: “Na mwenye msaada kidogo kwake katika balaa.” Tatu: Kwa sababu kundi hili husimama nafasi ya mtu mwenye kushindana na Mtawala na kutaka kufaidika na umma, hivyo hujaribu kwanza kabla ya kila kitu, kutimiza maslahi yake binafsi bila kujali haki za watu wengine. Imamu (as) anasema: “Na mwenye kuuchukia mno uadilifu, na king’ang’anizi mno katika kuomba.” Nne: Hujikita katika starehe, na hiyo ndio tabia ya kundi hili makhususi katika mahusiano yake ya kiuchumi na umma, wao huwa hawashukuru neema za Mwenyezi Mungu walizopewa na wala huwa hawatosheki. Imamu (as) anasema: “Na mchache mno wa shukrani wakati wa kupewa.” Tano: Huwa hawatazami mazingira ya kimaisha ya umma, hivyo wao huwa hawakomei katika kiwango hiki tu bali huvuka hadi katika maeneo makubwa bila kuuhurumia umma wala kuzingatia mazingira yake ya kimaisha, daima wao hutaka kuongezewa mali ili kukidhi matakwa yao, hivyo Mtawala anaposhindwa kuwatimizia hilo kwa sababu ya uchache wa kipato cha serikali, utawaona wanamtenga kwa kuwa amezuia hilo, bali huutendea umma kwa namna ya upofu na ya mtu asiyejua, huwa hawajali matatizo na misukosuko watakayoisababisha katika umma, na hatimaye wanaweza kuutumbukiza umma katika shimo la moto. Imamu (as) anasema: “Na mwenye udhuru goigoi mno wakati wa kunyimwa.” Sita: Hukosa roho ya uvumilivu, hiyo ni kwa sababu muungano wa kundi hili na umma, na pia mahusiano ya kundi hili na umma, vimesimamia juu ya msingi wa masla59
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 59
7/5/2013 9:06:16 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
hi tu, hivyo huwa hawana kabisa roho ya kujitolea, na wao hawako tayari kusimama kwa uvumilivu mbele ya matatizo yanayoukabili umma. Imamu (as) anasema: “Na mwenye Subira dhaifu mno wakati wa shida za zama.�
60
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 60
7/5/2013 9:06:16 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
Tabaka la watu wa kawaida:
T
abaka hili ndio la watu wengi katika umma, nalo ni sawa na umbile kubwa ambalo ni juu ya msingi wake jengo la serikali hujengwa na harakati zake kupatikana, hivyo iwapo uongozi utaweza kupata ridhaa ya jamhuri basi jambo hilo hupelekea utawala kutulia juu ya msingi thabiti na imara. Na hakika kuupuuza upande huu huufanya utawala uwe katika hatari ya kuanguka wakati wowote, kwa sababu ni kama tulivyotangulia kusema kuwa raia hawana mbadala wala hakuna serikali inayoweza kusimama bila wao. Kama ambavyo pia jamhuri wanapofanya mapinduzi dhidi ya Mtawala huwa kama bahari yenye mawimbi makali hakuna wa kuweza kuwazuia wala hakuna nguvu yoyote iwezayo kusimama mbele yao. Umuhimu wa tabaka hili unatokana na mambo yafuatayo: Kwanza: Wao wanatengeneza sehemu kubwa ya dini, na kwa kushikamana nao dini inapata nguvu kupitia nguvu yao, kwani bila wao dini inakuwa ni fikra tu na dhana zilizoganda zisizo na athari ya kimatendo kwa nje. Imamu Ali (as) anafafanua ukweli wa fikra hii kwa kusema: “Kwa hakika watu wa kawaida katika jamii ndio nguzo ya Dini na nguvu ya Waislamu…” Pili: Wao wanaunda ngome imara ya umma, na yenye kutetea rasilimali zake, heshima yake na utu wake, kwa sababu wao wanatengeneza nguvu dhidi ya maadui. Imamu (as) anasema: “Na walinzi dhidi ya maadui.” 61
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 61
7/5/2013 9:06:16 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
Kwa ufupi ni kwamba uongozi ni sawa na safina katikati ya bahari ya jamhuri, hivyo iwapo itapoteza mwelekeo na kuyumba basi bahari itaipiga kwa mawimbi yake katika pande zake zote na hatimaye itaizamisha. Hivyo basi ni wajibu juu ya Mtawala kutumia juhudi zake zote katika kutafuta na kupata ridhaa ya jamhuri, kwa gharama yoyote ya matatizo na ya kujitolea, kwa sababu wao ndio uti wa mgongo wa umma na ni juu yao husimama kila kitu. Imamu Ali (as) anasema: “Basi usikivu wako uwe kwao, na muelemeo wako uwe kwao.�
62
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 62
7/5/2013 9:06:16 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
MTAWALA NA NAMNA YA KUTATUA MATATIZO YA KIJAMII
H
akika kupatikana matatizo ni jambo la kawaida katika maisha, hakuna jamii isiyo na matatizo ya namna moja au nyingine, lakini hiyo haimaanishi kwamba kuwepo na matatizo ni jambo linalopendeza, kwa sababu kukithiri kwa matatizo kunaweza kupelekea muundo wa jamii kudhoofika na hatimaye jamii kusambaratika, jambo ambalo litawafanya raia waelekeze macho yao kwa uangalifu katika matatizo yenye kujitokeza katika jamii yao, na kwa hilo watajikuta wanabaki nyuma kimaendeleo. Na kama sisi tupo katika kutatua matatizo yaliyopo katika safari yetu ya maisha, au yale tunayotaraji kuwa yatatokea, basi inatulazimu tuwe makini katika kujua suluhisho litakaloleta mafanikio upesi kabla matatizo hayajakomaa na mazingira hayajakuwa magumu, ili maisha yasiwe moto usiozimika. Kwa sababu kuchukua tahadhari kubwa ni miongoni mwa fikra za wenye akili, ambapo tahadhari huzuia na kuepusha matokeo yasiyokuwa mazuri, hivyo ili Mtawala aweze kufanikiwa kutatua matatizo yaliyojitokeza katika jamii ni lazima afanye mambo mawili ambayo Imamu Ali (as) anayafafanua ndani ya maneno yake: Kwanza: Kudhibiti athari: Yaani kutatua matatizo yaliyoanza kujitokeza kwa kuondoa athari zake katika jamii, na hilo litatimia kwa njia mbili: A. Kuyazika matatizo na kuyaficha iwapo kuyadhihirisha kutapelekea watu kuathirika nayo. Lakini si kukomea hapa tu bali ni wajibu wake kung’oa kabisa mizizi yake. 63
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 63
7/5/2013 9:06:16 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
Imamu Ali (as) anasema: “Kwani kati ya watu kuna mambo ya aibu, na Mtawala ndiye mwenye haki zaidi ya kuzisitiri. Hivyo basi, usizifichue zilizofichika mbali na wewe katika hizo..” B. Baadhi ya matatizo huenda tayari yameshadhihiri, basi hapa Mtawala anawajibika kufanya haraka na kuharakisha kutatua matatizo haya yaliyodhihiri kwa kuyadhibiti katika sehemu finyu na kuyang’oa kabla hayajatapakaa katika jamii nzima na kuwafanya watu wayaelekee, jambo ambalo linaweza kuwafanya walete vurugu na kulikuza tatizo katika jamii. Imamu Ali (as) anasema: “Bali ni wajibu wako kuzirekebisha zilizo kudhihirikia..” Pili: Kudhibiti chanzo husika: Yaani kutatua tatizo kwa namna ambayo halitajirudia tena, na zoezi hili hufanikiwa kwa kutazama chanzo chake na ambacho mara nyingi na katika matatizo mengi hutokana na vitu viwili: Mwanadamu na mazingira, hivyo hapa Mtawala analazimika kuchukua njia mbili katika kutatua tatizo: A. Kutokomeza mazingira na sababu iliyopelekea tatizo kujitokeza, ili kwamba lisiendelee kukua na kuongezeka na hatimaye likasambaa. Imamu Ali (as) anasema: “Wafungue watu vifundo vyote vya chuki, na ziweke mbali na wewe sababu zote za uadui..” B. Kumkatia njia kila anayenufaika na uwepo wa tatizo husika au kuendelea kwake na kukua kwake, kwani huenda uwepo wa tatizo ni faida kwa mtu fulani, au huenda ni mwanya unaotumiwa na baadhi ya watu kuiharibu jamii na kueneza uchafu na kuleta madhara kwa wanajamii, na hatimaye jamii inakosa chembechembe muhimu ka64
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 64
7/5/2013 9:06:16 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
tika kuleta mshikamano, upendo, huruma, kusaidiana na mengine miongoni mwa sifa njema na nzuri. Hivyo ili tuiepushe jamii na hatari ni lazima kukabiliana na tatizo na kumfukuzia mbali kila mwenye manufaa na uwepo wa tatizo husika ili tuepukane na athari zake za kuzuia mambo yasiende kama yanavyopasa katika jamii. Imamu Ali (as) anasema: “Wala usiharakiye kumsadiki chakubimbi mfanya ghushi, hata kama atajishabihisha na watoao nasaha.� Na wakati wa zoezi la kutatua tatizo lolote lile na pia wakati wa kuweka suluhisho muwafaka, ni lazima Mtawala ajiepushe mbali na udikteta na ukandamizaji wa mawazo, hivyo achukue rai, fikra na ushauri kutoka kwa watu wenye uzoefu na maarifa, kisha kutokana na mjumuiko mzima wa ushauri aweze kuzalisha rai moja na msimamo wa dhati. Lakini atamtaka nani ushauri? Swali hili tutalijibu katika kurasa zifuatazo. Washauri: Kutaka ushauri ni jambo la dharura, kwa sababu humuonesha mtu ni wapi palipo na makosa na ni wapi palipo sahihi, na humshika mtu mkono mpaka katika njia sahihi, na kwa sababu binadamu ni mwenye fikra finyu basi huenda akaliweka jambo pale pasipofaa, na huenda akachukua uamuzi ambao kupitia ushauri anaweza kugundua makosa ya fikra zake na hatima yake, na hivyo wengine wanaweza kumuonesha maeneo yenye makosa katika ufumbuzi wake. Hivyo kwa ushauri huo itajengeka kwake fikra kamili ya kutatulia tatizo gumu, na kwa fikra hizo atafanikiwa kuiokoa jamii kab65
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 65
7/5/2013 9:06:16 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
la matatizo na machungu yake hayajaongezeka, na hatimaye atatibu majeraha mabaya ya tatizo na athari zilizojitokeza, na atazuia kuongezeka kwa madhara mabaya ambayo hayaachi manufaa wala usalama. Kwa ajili hiyo Uislamu umesisitiza wajibu wa kutaka ushauri na umuhimu wake katika jamii ya Kiislamu, na zimekuja riwaya kadhaa kusisitiza hilo. Mwenyezi Mungu anasema: “Na shauriana nao katika jambo.” Na pia anasema: “Na mambo yao ni kwa ushauri baina yao.” Na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) amesema: “Hababaiki mwenye kumtaka Mwenyezi Mungu ushauri, na wala hakosi kufanikiwa mwenye kuomba ushauri, na hakuna msaada mkubwa kama ushauri.” Na amesema tena: “Mwenye akili ni yule mwenye kujumuisha akili za watu kwenye akili yake.” Mtukufu Mtume (saww) alitekeleza hili kivitendo pindi alipowataka ushauri Maswahaba zake katika namna ya kupambana na nguvu ya vikosi vya muungano wa makafiri, Swahaba maarufu Salman Farsiy akampa ushauri wa kuchimba handaki litakalouzunguka mji wa Madina, Mtukufu Mtume (saww) akachukua ushauri wake na akachimba handaki na hatimaye ushindi ukapatikana. Leo hii katika serikali za kisasa suala la ushauri limechukua hatua nyingine zaidi baada ya kuwa ni idara na kitengo chenye kujitegemea, na ni wadhifa kama wadhifa mwingine wa kiserikali, na jambo halijaishia hapo tu bali kumekuwa na mikondo mingi ya ubobezi katika suala hili, na hatimaye limezunguka pande zote za maisha ya jamii, hivyo tunamuona yupo mshauri wa mambo ya kijeshi, mwingine ni mshauri wa mambo ya kiuchumi, mwingine ni mshauri katika mambo ya utawala bora, mwingine ni mshauri katika 66
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 66
7/5/2013 9:06:16 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
mambo ya kijamii, hivyo hivyo mpaka mwisho wa sekta za kiserikali. Na iko wazi kwa kila mwenye akili athari ya watu hawa katika jamii yao, ima hasara iwapo wenyewe wameharibika, na ima faida iwapo wao wenyewe wametengemaa, hivyo uharibifu wa jamii na kutengemaa kwake kunategemea pia hali yao. Na kutokana na tuliyoyataja linajitokeza swali muhimu, nalo ni, ni mshauri gani anayefaa? Mshauri anayefaa ni lazima awe na sifa za kiroho zifuatazo: Kwanza: Kujitolea: Kwa sababu kupitia sifa hii ya kiroho anaweza kutoa na kujitolea kwa ajili ya lengo, nalo ni kutatua tatizo gumu, na hapa ni kinyume na endapo ni bakhili ambaye anachojali na kutizama ni kiasi gani cha gharama atakachotumia, na si je lengo litatimia au hapana. Imamu Ali (as) anasema: “Usimwingize katika mashauri yako mtu bakhili, kwani atakuweka nyuma usiwe mkarimu, na atakukhofisha ufakiri.” Pili: Ushujaa: Katika kuchukua maamuzi muwafaka ndani ya muda muwafaka wakati wa kupambana na vyanzo vya tatizo, sawa chanzo kiwe ni watu fulani au mazingira fulani ya muda mfupi, au ni mila na desturi za kijamii au kitu kingine. Na kwa muhtasari sana ni kwamba mshauri anahitaji ushujaa wa kimaadili na kiroho ili kuweza kupambana na tatizo na kulitatua. Bila sifa hii tatizo halitatatuka, kwani anayeiogopa jamii yake hawezi kutatua tatizo. Imamu (as) anasema: “Wala (usimtake shauri) mtu mwoga, atakufanya uhisi udhaifu kwenye mambo.” Tatu: Asiwe mtu wa maslahi binafsi au ubinafsi: Anayeuza utu wake kwa thamani ya mali au kipande cha ardhi, 67
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 67
7/5/2013 9:06:16 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
hivyo unamuona anamhamasisha Mtawala kuendelea na siasa yake ya kimakosa ambayo kiuhalisia iko dhidi ya raia. Imamu Ali (as) anasema: “Wala mwenye pupa atakupambia shari kwa dhulma.” Sifa hizi zisizotakiwa: Ubahili, uwoga na tamaa, pamoja na kutofautiana kwa sifa hizi lakini zinakusanywa pamoja na sifa moja nayo ni kumdhania vibaya Mwenyezi Mungu, yaani ni kutetereka kwa maadili ya kiroho na kuwa na udhaifu katika kushikamana na dini, kwa sababu muoga husema: “Nikiingia nitauawa.” Na bakhili husema: “Nikitoa nitafakirika.” Na mwenye tamaa husema: “Nisipotumia juhudi zangu sintajenga mustakbali wangu.” Imamu Ali (as) anasema: “Kwa sababu ubakhili, woga, na pupa ni tabia tofauti zinazokusanywa na (jambo moja), nalo ni kumdhania vibaya Mwenyezi Mungu.” Tiba pekee ya sifa hizi tatu mbaya imejificha katika sifa ya kumdhania vizuri Mwenyezi Mungu na kutengeneza muamala wa kiroho baina yake na Uislamu, na hiyo ni kupitia utaratibu wa kiroho wenye kutibu maradhi hayo. Kwa sababu sifa hiyo ya kumdhania vizuri Menyezi Mungu ina uwezo wa kuzalisha itikadi thabiti ya kwamba mwanamume anaweza, ufakiri na utajiri vyote vinawezekana, na kila kinachotokea katika maisha haya ni kwa amri ya Mwenyezi Mungu na ni kwa utashi na taufiki yake.
68
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 68
7/5/2013 9:06:16 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
MTAWALA NA WIZARA MPYA
H
akika miongoni mwa mambo magumu sana ambayo Mtawala hukutana nayo baada ya kukaa kwenye kiti cha utawala na baada ya kushika hatamu ya mambo ni suala la kuunda Baraza la Mawaziri na kugawa mabegi ya wizara katika nchi, na kuziwezesha wizara kwa kuzipa watu wenye kufaa wenye uwezo wa kuendesha mambo ipasavyo. Kuanzia hapa ndipo vyeo vingi vya wizarani hubakia vitupu bila watu, na Mtawala wa Kiislamu hutumia muda mrefu kutafuta Mawaziri watakaobeba jukumu la wizara kwa dhati na kwa uaminifu na ambao wataleta manufaa makubwa kwa uepo wao. Kwani wao huwa sawa na mishipa ya damu yenye kuunganisha moyo na viungo vingine, hivyo iwapo yenyewe itaacha kufanya kazi basi na moyo utapoteza nafasi yake katika safari ya uhai na ukuaji, kwa sababu kuendelea kuwa hai kwa serikali kunategemea mwenendo wa Mawaziri. Na hapa ndipo linapojitokeza swali zito, nalo ni utatumiaje uteuzi wa Mawaziri? Kwanza: Ni mwenye historia nzuri: Ni wajibu kumteua Waziri asiye na historia mbaya, na ambaye hajashiriki katika dhulma za kijamii zilizotangulia, na wala hajawahi kuingia katika serikali au wizara dhalimu. Imamu Ali (as) anasema: “Waziri wako mbaya ni yule aliyekuwa waziri wa waovu kabla yako, na aliyeshirikiana nao katika dhambi. Wala asiwe mwandani wako, kwani wao ni wasaidizi wa watenda dhambi, na ni ndugu wa madhalimu.� Lakini linaweza kujitokeza tatizo nalo ni, katika hali kama hii hivi huoni tunataka kuuwa ujuzi na uzoefu wa wataalamu 69
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 69
7/5/2013 9:06:16 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
waliotangulia ambao walikuwa wanafanya kazi za kiwizara katika miaka ya serikali zilizotangulia? Jibu lake ni kwamba: A. Kuna watu wengi wenye uwezo katika jamii ambao walipuuzwa au walitengwa na serikali dhalimu, kwa sababu ilikuwa inataka Mawaziri watakaokidhi masilahi yake na kuhalalisha matendo yake na kufuata siasa yake, wala haikutaka Mawaziri wenye uwezo wa kiutendaji ambao watabeba majukumu yao ipasavyo na watafanya kazi katika msingi wa kuwahudumia na kuwatumikia raia na kutekeleza kanuni, bali ilihitaji lile kundi la watu watakaounga mkono siasa yake ya kidhalimu na kukidhi matamanio yao maovu. B. Hakika Mawaziri waliotangulia waliokuwa chini ya msingi wa kutekeleza maslahi yao binafsi kwa njia ya kuwadhulumu raia, hawawezi kubadilika mara moja ghafla, na miongoni mwa raia wapo watu waumini wa kweli waadilifu ambao wanatenda kwa ajili ya raia, na wanajituma kwa juhudi zao zote ili kuihakikishia jamii na raia kwa ujumla raha na heshima yake. Na raia hawako tayari kudanganyika tena kwa propaganda na uwongo na ahadi hewa, kwa sababu tayari wameshaujua uhalisia wao na hali yao hapo kabla kupitia utendaji wao wa kidikteta. Na raia wanajua vizuri kuwa wao ni watu wa maslahi binafsi na ubinafsi hivyo wanavuma na upepo kule maslahi yalipo. Imamu Ali (as) anasema: “Na wewe unaweza kuwapata badala yao wengine wema, ambao watakuwa kama wao, katika rai zao na ushawishi wao, na juu yake hana dhambi kama zao, na mizigo kama yao, miongoni mwa ambao hawa70
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 70
7/5/2013 9:06:16 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
jamsaidia dhalimu katika udhalimu wake, wala mweye dhambi katika dhambi zake.” Pili: Ni kuwaondoa Mawaziri wanafiki ambao hufanya kazi ya kuvipamba vitendo vya Mtawala na kuvihalalisha, hivyo ni lazima kuwatenga mbali wasiweze kumuathiri, na kisha kuwachagua watu waumini majasiri ambao katika haki hawaogopi lawama ya mwenye kulaumu wala nguvu ya Mtawala, ambao wao kawaida yao ni kumzindua Mtawala, kumwamsha na kumuonesha mapungufu yake na makosa yake, na hata kama kufanya hivyo kutamkera kiasi gani Mtawala. Imamu Ali (as) anasema: “Kisha iwe athari yao kwako ni kauli zao za haki zilizochungu kwako, na mchache mno miongoni mwao wa uliyonayo miongoni mwa ayachukiayo Mwenyezi Mungu kwa mawalii wake, hali yakiwa katika upendo wako.” Tatu: Kuyasogeza karibu makundi mema ambayo yana uchamungu na ukweli, kama msingi wa muamala katika kupambana na vichocheo vya ndani na mashinikizo ya nje. Imamu Ali (as) anasema: “Jiambatanishe na wachamungu na wa kweli.”
71
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 71
7/5/2013 9:06:16 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
Muamala mzuri ndio njia ya kuufikia uhuru:
H
akika kuna dharura ya kuwepo na kipimo kwa Mtawala kinachotokana na athari za kimatendo, kwa ibara nyingine ni kwamba ni uwepo wa kipimo maalumu kwa Mtawala kitakachompelekea kuchukua msimamo sahihi dhidi ya watu, na misimamo hii ndio inayoainisha kiwango cha hatua wanazopaswa kuchukuliwa. Imamu Ali (as) anasema: “Wala mwema na muovu wasiwe daraja sawa kwako, kwani hilo huwatia unyonge watendao wema wa kutenda wema, na kuwatia motisha waovu kutenda uovu.” Na msimamo sahihi maana yake ni Mtawala aainishe msimamo wa mtu na kazi yake na amchukulie hatua kulingana na amali aliyoitenda, kwani bila kipimo na kigezo jamii haiwezi kupata amani na kupata uhuru. Na wala hawezi kupiga hatua kwenda mbele katika njia ya maendeleo na ustawi wa kijamii, bali atabaki nyuma na kurudi nyuma kutokana na vizuizi vingi. Imamu Ali (as) anasema: “Muambatanishe kila mmoja kati yao na lile alilojiambatanisha nalo.” Lakini swali linalojitokeza hapa ni, vipi Mtawala ataweza kuaminiwa na raia na kupata mapenzi yao? Ili mwanadamu apite njia kwa uwelewa na maarifa kamili, ni juu yake kuainisha alama za njia anayotaka kupita. Na ili Mtawala apate kuaminiwa na raia na kupendwa na wao na aingie ndani ya nyoyo zao, ni wajibu kwake kupita njia zenye dhamana ya kufanikisha hayo, na njia hizo ni mambo yafuatayo: 72
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 72
7/5/2013 9:06:16 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
1. Kuwatendea hisani raia: Nako ni Mtawala ajitahidi kutimiza mambo yatakayowafanya raia waridhike kikamilifu, na kutobagua baina ya makundi yao. Na hisani hapa haimaanishi kuwapa mahitaji ya kimada tu bali ni kutimiza hatua zinazoitangulia, kwa maana nyingine ni kwamba, kutoa na kuiridhisha nafsi ndio hatua zinazotengeneza na kuzaa hisani. Imamu Ali (as) anasema: “Na tambua kwamba hapana kitu kinachomfanya Mtawala adhaniwe vizuri na raia wake kuliko kuwatendea kwake wema..” 2. Kuwapunguzia mzigo wa maisha, na kujaribu kuwapatia mahitaji ya lazima hata kama kutimiza hilo kutagharimu na kupoteza mambo mengine, kwa sababu raia ndio lengo. Imamu Ali (as) anasema: “Na kuwapunguzia kwake shida..” 3. Rai iliyodurusiwa na hatua yenye hekima, kwa neno jingine ni kwamba ni lazima kutokuwalazimisha raia kutekeleza rai na hatua zilizo juu ya uwezo wao na zisizo katika uwezo wao, kwa sababu kufanya hivyo kutatengeneza mpasuko mkubwa baina ya raia na Mtawala, raia wataanza kuhisi ndani ya nafsi zao kwamba katika njia yake hii Mtawala anaelekea katika ukandamizaji na udikteta. Imamu Ali (as) anasema: “Na kuacha kuwalazimisha kwa wasilokuwa nalo.”
73
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 73
7/5/2013 9:06:16 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
Umuhimu wa kuufanyia kazi urithi:
H
akuna umma wowote unaoweza kujihakikishia uhuru wake kamili katika nyanja zote za kisiasa, kiuchumi, kijamii, kitamaduni na kiustaarabu, eti kwa kuwafukuza tu wakoloni kutoka katika ardhi ya nchi husika, bali ni lazima izifukuze na fikra zao na kufanya mapinduzi ya kifikra na kitamaduni yenye kulilenga taifa kimaadili na kifikra. Hiyo ni kwa sababu ukoloni ulipotaka kututawala na kututumikisha ulitupokonya utamaduni wetu wa asili na wakaubadili kuwa utamaduni wa uzalishaji uliotutenga mbali na hali nzima ya kubeba majukumu yetu ya kidini na kijamii. Hivyo ili tujikomboe kutoka kwenye udhalili wa utumwa na umilikiwaji ni juu yetu kukata mawasiliano yote na tamaduni zile za kikoloni na fikra za kijahiliya, tamaduni za uhuru usio na mipaka na usio na majukumu, na tuitenge mbali kwa akili zetu na maarifa yetu mipango yote na njama zote za kikoloni ambazo zinatulenga sisi na kututaka tuwe nyuma na wenye kuwafuata wao. Hivyo ili tumiliki falsafa ya kukataa kikamilifu fikra zao zenye sumu mbaya, ni lazima turudi upande wenye uokovu na salama, kwenye misingi ya Uislamu wa kweli na tufanyie kazi fikra zake na elimu yake iliyojaa, ambayo inakwenda sawia na mwanadamu na maendeleo yake, na inafanya kazi ya kunadhimu maisha ya jamii katika kila zama. Hivyo kuachana na fikra hizi za asili na kufanyia kazi fikra za nje na kuchukua kanuni zao katika kutatua matatizo yetu ya kijamii, kimalezi, kiuchumi na mengineyo, ndio njia ya kuendelea kuku74
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 74
7/5/2013 9:06:16 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
lia ndani ya mikono ya ukoloni mbaya. Kwa sababu ukoloni si chochote bali ni matokeo mabaya ya kuachana na Uislamu, Imamu Ali (as) anasema: “Wala usiutengue mwenendo mwema uliofanywa na wa mwanzo katika umma huu, ambao kwa mwenendo huo umepatikana upendo, na kwa huo raia wamekuwa na hali njema. Na wala usizushe mwenendo utakaodhuru kitu chochote miongoni mwa mienendo ile iliyopita, ujira uwe kwa walioufanya, na dhambi juu yako kwa vile umeutengua.�
75
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 75
7/5/2013 9:06:16 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
Kuwajali wasomi:
K
wa kiwango kile kile tunachopaswa kushikamana na urithi wetu ndivyo tunavyopaswa kuwajali wasomi waliobeba urithi wetu na wenye kuutafsiri kivitendo, nao ni ulamaa na wenye busara. Kwa sababu uwepo wao katika kuendesha nchi humaanisha uhai wa nchi, ustawi na uvumbuzi, kwa sababu ulamaa huungana na sehemu kubwa ya raia, kwa ajili hii ni lazima kuwashirikisha katika kutengeneza maamuzi na maazimio, na katika kupata ufumbuzi na suluhisho sahihi la matatizo ya watu yenye kujitokeza. Kwa sababu wajibu wa aalimu ni kufanyia kazi kile anachokijua, la sivyo hatakuwa na hali nzuri kuliko mjinga ambaye hajui chochote, bali yeye atakuwa na mzigo mzito zaidi kuliko mjinga. Imamu Ali (as) anasema: “Inapojitokeza bidaa ni wajibu juu ya aalimu kuonesha elimu yake, la sivyo laana ya Mwenyezi Mungu itakuwa juu yake.” Na pia anasema: Na kithirisha kuongea na wanachuoni, na wadodose wenye hekima katika kuimarisha lile litakalosababisha suala la nchi yako kuwa jema, na kuimarisha lile walilokuwa nalo daima watu kabla yako.”
76
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 76
7/5/2013 9:06:16 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
Mtazamo wa Imamu (as) kuhusu matabaka ya kijamii:
K
una usemi usemo: “Hakuna jamii isiyo na matabaka.� Hivyo Imamu (as) anamwandikia Maliki msingi huu kama utangulizi wa mwanzo katika kuamiliana na jamii, kama ambavyo mtu mmoja mmoja anavyotofautiana na mwenzake katika kiwango cha fikra, kipato na aina ya maisha, ndivyo hivyo hivyo makundi ya watu yanavyotofautiana. Lakini swali hapa ni, je Uislamu unatambua uwepo wa matabaka na je unawagawa watu katika msingi wa matabaka? Jibu ni hapana na ndiyo. Tunaposema ndiyo Uislamu unatambua uwepo wa matabaka ni kwa sababu huo ndio uhalisia uliyopo na hivyo ni kama tulivyosema kuwa hakuna jamii isiyokuwa na matabaka, hivyo wasomi hutengeneza tabaka lao tofauti na wale wasiokuwa wasomi, na wenye kipato kikubwa hutengeneza tabaka tofauti na wale wenye kipato kidogo, na watawala hutengeneza tabaka tofauti na raia wa kawaida. Na tunaposema hapana, ni kwa maana hii: Ndiyo ni sahihi kuwa Uislamu unatambua uwepo wa matabaka mbalimali ya kijamii lakini hauamiliani na watu kwa msingi huu wa matabaka, yaani hauchukui msimamo wa kumthamini mwenye mali kushinda asiye na mali, au mwenye cheo kushinda asiye na cheo, na hivyo hivyo kwa upande wa matabaka ya chini. Imamu Ali (as) anasema: “Na tambua ya kwamba raia wako katika matabaka tafauti, baadhi ya matabaka hayapati 77
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 77
7/5/2013 9:06:16 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
ufanisi ila kwa ushirikiano na baadhi ya matabaka mengine, wala baadhi yao hayajitoshelezi bila ya mengine;�
78
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 78
7/5/2013 9:06:16 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
NAFASI YA JESHI KATIKA UMMA
N
afasi ya jeshi inatofautiana kulingana na uwanja wake wa kazi, hivyo nafasi ya jeshi imegawanyika katika sehemu mbalimbali, mara hufanya kazi ya kulinda raia, na mara hufanya kazi ya kumlinda Mtawala na mara hufanya kazi za kifikra. Ili kufafanua hilo tunasema: Ni yapi majukumu ya jeshi? Kwanza: Kulinda raia: Hiyo ni kwa sababu kama kila raia atakuwa mwanajeshi basi sekta nyingine za kijamii zitabaki bila watendaji, hivyo kuanzia hapa ndipo jukumu la kwanza muhimu la jeshi likawa ni kuwalinda na kuwahami raia, na kwa namna hii raia wengine watapata fursa ya kufanya kazi katika sekta nyingine, na kila mmoja atafanya kazi katika sekta yake na nyanja yake. Imamu Ali (as) anasema: “Wanajeshi kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, wao ndio ngome ya raia, na ni pambo la mtawala, na ni nguvu ya Dini, na ni sababu ya kuwepo kwa amani. Na raia hawawezi kuishi (kwa amani) bila ya wao.� Pili: Kumlinda Mtawala na kiongozi wa nchi: Jukumu hilo ni miongoni mwa majukumu ya lazima ambayo kuyapuuza huhesabika ni hatari kubwa, kutokana na madhara makubwa na yasiyokubalika yanayoweza kujitokeza, hiyo ni kwa sababu Mtawala asingepata huduma hiyo isipokuwa ni ili kwanza awe mfano hai wa mtu mwema ambaye anajituma yeye mwenyewe katika kutumikia dini na nchi. Na pili ni kwa sababu yeye ni mmoja kati ya raia na ni kiongozi wao, na ni kwa ajili ya kumpa nguvu ya kisiasa yenye kuendelea kutoka kwenye nguvu ya jeshi analolimiliki, hiyo ni sawa iwe 79
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 79
7/5/2013 9:06:17 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
wakati wa mizozo au wakati wa kuchukua hatua na maamuzi magumu. Kwa ajili hii jeshi kumlinda Mtawala ni jambo la lazima ili aweze kufanikisha hayo. Tatu: Kuhami na kulinda imani ya umma: Kulinda njia ambayo inafuatwa na umma katika maisha. Yaani wakati jeshi linapowalinda na kuwahami raia na Mtawala lina wajibu pia wa kuitetea dini kama lengo la kwanza ambalo jeshi linapaswa kulitumikia. Nne: Kupambana na uharibifu wa ndani: Kupambana na makundi ambayo huleta fujo na ghasia katika safu za kijamii. Na lijaribu kumtizama mkuu wa nchi na kumlinda ili asiweze kutekwa na makundi ya maadui. Hivyo kwa kuwa jeshi hubeba majukumu haya makubwa na mazito ambayo ni wajibu juu ya jeshi kuyatimiza na kutumia wakati wake wote katika majukumu haya, basi ni jambo lisilowezekana kwa mwanajeshi kujitimizia mahitaji yake na ya familia yake na ya wale walio chini yake, hivyo ni lazima atengewe mshahara, na hili ndilo wanalofanyiwa wanajeshi wa serikali katika zama hizi. Imamu Ali (as) anasema: “Kisha askari hawawezi kuhifadhiwa ila kwa mfuko ulioainishwa na Mwenyezi Mungu katika mapato, kupitia huo wanakuwa na nguvu za kupigana dhidi ya adui yao. Na ambao wanautegemea kwa ajili ya ufanisi wao, na unakuwa kwa ajili ya haja zao.�
80
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 80
7/5/2013 9:06:17 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
SIFA ANAZOLAZIMIKA KUWA NAZO MTU ILI KUBEBA JUKUMU LA UONGOZI 1. Kuhisi majukumu yeye mwenyewe, ajue vizuri kwamba yeye ana wajibu wa kuongoza matabaka tofauti kwa makundi yake yote ya kijamii. Kutokana na hisia hii inapatikana hali ya kutilia umuhimu mazingira ya jamii na hali zake. 2. Kushikamana na Mwenyezi Mungu daima, na kumkabidhi mambo Yeye, na kuwa na imani kwamba kuongoza umma ni jambo jepesi na dogo maadamu tu ameshikamana na nguvu isiyo na mipaka na isiyokwisha. Kitendo tu cha kujua kwamba ameegemea kwenye nguvu itakayomnusuru na kumpa msaada wa hali na mali wakati wa matatizo makubwa, kitamfanya ajitume na kutenda katika upande huu kwa mafanikio makubwa. Imamu Ali (as) anasema: “Ila kwa kutilia hima na kuomba msaada kwa Mwenyezi Mungu.” 3. Sifa za kinafsi, hasa zile zinazohitajika sana upande huu, kama vile kuwa na utashi wa dhati na maandalizi ya kinafsi ya kuweza kukabiliana na matatizo ya njiani, na kuendelea na safari kivitendo mpaka afikie katika lengo. Imamu (as) anasema: “Na kuutuliza moyo wake katika kujiambatanisha na haki, na kuvuta subira kwa hilo, liwe jepesi au zito.”
81
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 81
7/5/2013 9:06:17 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
Uongozi wa jeshi: Kwa kuzingatia kwamba jeshi hutengeneza nguvu isiyodharaulika katika kushughulikia mambo ya kisiasa na kijamii, sawa iwe ni katika mambo yenye matokeo chanya kama vile kupambana na makundi mabaya ya ndani na ya nje, au iwe ni katika mambo yenye matokeo hasi kama vile kushika madaraka kwa njia ya mapinduzi ya kijeshi, hivyo kwa kuzingatia nafasi hii kubwa lililonayo jeshi, suala la uongozi wa jeshi nalo pia huendelea kuwa jukumu hatari. Hivyo ni juu yetu kujua ni mtu mwenye sifa zipi ndiye anayefaa kuwa kiongozi wa jeshi? Sifa ya kwanza: Ikhlasi: Sifa hii haiwezi kupatikana kwa mtu isipokuwa pale inapoimarika nafsini mwake sifa ya takua, na hapa ndipo Imamu (as) akasema: “Mpe uongozi wa wanajeshi wako yule mwenye kunasihika sana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na kwa Imamu wako.� Uwepo wa serikali na kuanguka kwake unategemea sifa hii, hasa kama hatuwezi kuhakikisha anakuwa chini ya kiongozi na anatii uongozi wa juu, ikiwa hatuwezi kuhakikisha hilo basi ni nani anaweza kuhakikisha kiongozi wa jeshi hauzi utu wake kwa thamani ndogo ya kukidhi na kuitikia wito wa matamanio yake binafsi na sauti za starehe mbaya, bali ni nani anaweza kuhakikisha kiongozi huyo hauzi nchi na serikali yake, je kuna nguvu yoyote inayoweza kumzuia? Hakuna zaidi ya takua na ikhlasi. Sifa ya pili: Hii inahusu kazi yenyewe, ni sifa ya kinafsi inayohusu utendaji na namna ya kukabiliana na upinzani unaotibua nafsi ya kiongozi, kitendo cha kiongozi kutenda 82
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 82
7/5/2013 9:06:17 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
kulingana na mtibuko wa nafsi kunaweza kuuweka umma katika hatari ya kutoweka, na hili ni jambo lililo wazi kabisa, kwa ajili hiyo kiongozi ni lazima awe kama alivyosema Imamu (as): “Miongoni mwa wale wasio na haraka ya kughadhibika, na wenye utulivu kwenye udhuru, wenye huruma kwa wanyonge. Wanaoumuka dhidi ya wenye nguvu, vurugu haziwachochei, unyonge hauwafanyi wabweteke.” Sifa ya tatu: Awe na nafasi katika jamii: Ambayo inaweza kumzuia na kumbana asiweze kufanya uhaini na kuasi, kwa kuhofia kuporomoka nafasi yake ya kijamii aliyonayo. Ufafanuzi wa hilo ni kama vile awe anatokana na nasaba kubwa yenye nafasi kijamii, hali hii inaweza kumzuia kwenda kinyume bali inaweza kutengeneza kizuizi cha kijamii kitakachomzuia kukiuka sheria. Imamu (as) anasema: “Kisha jiambatanishe na wenye hadhi, na waliotoka ukoo mwema, na waliotanguliwa na sifa njema.” Kwa kupitia shakhsiya yenye nafasi kubwa kijamii anaweza kuvuna nguvu ya raia ambayo kupitia nguvu hiyo atafanikiwa kuyakusanya pamoja sehemu kubwa ya makundi ya jamii na matabaka yake. Sifa ya nne: Kukubalika na askari: Hii inamaanisha kiongozi ni lazima awe anakubalika na kupendwa na wale anaowaongoza, Imamu (as) anasema: “Mkuu bora wa jeshi lako kwako awe yule anayewasaidia wanajeshi kwa uadilifu, na ambaye ni bora kwao kwa nguvu zake kwa kinachowatosha, na kuwasaidia wanaobaki nyuma, miongoni nwa jamaa zao waliobaki nyuma, ili hima yao iwe moja katika Jihadi dhidi ya adui. Kwa hakika wema wako juu ya wakuu wa jeshi utazifanya nyoyo zao ziwe na huruma na wewe.” 83
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 83
7/5/2013 9:06:17 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
Uteuzi wa Kadhi: Kwa kuzingatia kwamba Kadhi anawakilisha upande wa sheria katika umma, na kutokana na kazi nzito na hatari iliyonayo idara hii katika kuainisha hatima ya umma, ni kwa sababu hii suala la kumteua Kadhi linaendelea kuwa jukumu kubwa, hivyo basi ni ipi misingi ya kufuatwa wakati wa kuteua Kadhi? Imamu (as) anaainisha msingi unaotakiwa kufuatwa ambao ni sifa ambazo anapaswa kuwa nazo huyo mwenye kuteuliwa kuchukua nafasi ya ukadhi, hiyo ni kwa sababu uteuzi wa Kadhi yeyote unapaswa kuzingatia sifa kadhaa, nazo ndio misingi yenye kutegemewa, na Kadhi anapaswa kuteuliwa kupitia misingi hiyo. 1. Uwezo wa kutoa hoja na dalili: Awe na uwezo wa kutoa hoja na kujibu hoja, na awe mwepesi wa kujinasua katika mitego ya kimatamshi, pamoja na hili haruhusiwi kuingia katika mjadala ambao hautamrejesha kwenye haki ikiwa anaijua haki. Imamu (as) anasema: “Kisha mchague mtu wa kupitisha hukumu (hakimu) kati ya watu, yule aliye mbora kati ya raia wako katika nafsi yako ambaye mambo hayatombana, wala uhasama wa mahasimu hautomuingiza kwenye ukaidi, asiyeng’ang’ania katika makosa, asiyeshindwa kurejea kwenye haki pindi anapoitambua, ambaye nafsi yake haimsukumi kwenye tamaa.” 2. Awe ana uwezo wa kuhakiki mambo na kufuatilia kwa undani: Awe na utashi wa kufanya uhakiki na kufuatilia mambo kiundani, kumhoji mhusika na kumjibu, na awe mwingi wa umakini wakati wa utata, na wala 84
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 84
7/5/2013 9:06:17 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
asiwe mwepesi wa kukimbilia kutoa hukumu. Imamu (as) anasema: “Asiyetosheka na ufahamu wa karibu bila ya mbali, na mwenye kusimama sana kwenye jambo ambalo hukumu yake haiko wazi, mwenye kushikamana na hoja, mchache mno wa kuchoshwa kumrejea hasimu, mwenye subira zaidi pindi mambo yanapofichuka.” 3. Asiwe na mzaha katika kazi: Awe na utashi wa kufanya kazi ipasavyo, hivyo kwa mfano asifuate matamanio au mambo mengine miongoni mwa vishawishi vinavyoweza kujitokeza, hivyo hapaswi kubadili au kugeuza chochote katika hukumu kwa kushawishiwa na chochote, bali anapaswa kuwa jasiri na imara wakati wa kutoa hukumu. Imamu (as) anasema: “Na mkataji shauri mno pindi hukumu inapokuwa wazi, asiyepunguzwa na sifa nyingi, hapindishwi na chombezo, kwa kweli watu wa aina hiyo ni wachache.”
Uhusiano uliopo baina ya Mtawala na Kadhi: Ukiwa ni Mtawala na chini ya mamlaka yako kuna Kadhi, mahusiano yako na yeye yanapaswa kuwa vipi? Kwanza: Ni upande wa kipato: Unapaswa kumpa kile kitakachokidhi mahitaji yake na maisha yake. Imamu (as) anasema: “Kisha kithirisha kufuatilia maamuzi yake, na mfanyie nafasi katika kumpa kiwezacho kumuondolea shida zake, kimpunguziacho haja yake kwa watu.” 85
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 85
7/5/2013 9:06:17 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
Pili: Ni upande wa kijamii: Ni lazima umheshimu na kumthamini. Imamu (as) anasema: “Na mpe daraja kwako, asiyoweza kuitamani yoyote miongoni mwa watu mahsusi kwako.” Hiyo ni kwa sababu, kutokana na nafasi yake hatari na muhimu, Kadhi huwa katika hatari kubwa ya kushambuliwa na vishawishi ikiwemo mali na shakhsiya zenye nafasi katika jamii, hivyo akiwa na upungufu upande huu basi ataziba upungufu huo kupitia watu wengine na kinyume na maslahi ya Mtawala. Imamu (as) anasema: “Ili awe katika amani dhidi ya kudhuriwa kwako na watu.”
Uhusiano uliopo baina ya Mtawala na watendaji wake: Mtendaji wa serikali au kila anayejishughulisha na jukumu muhimu ni lazima awe katika kiwango sawa na jukumu husika, bali ni wajibu kumteua mtendaji huyu kwa kutazama uwezo wake kiutendaji na maarifa yake, lakini ni pamoja na sifa ya kuwa miongoni mwa watu wema. Imamu (as) anasema: “Kisha angalia mambo ya wafanyakazi wako, wape kazi baada ya majaribio, usiwachague kwa upendeleo au ufadhili.” Kama ambavyo sifa hii pekee haitoshi, bali inapasa pia kupitia wapelelezi kufuatilia na kuchunguza mazingira ya utendaji wake ili kujua raia wanapokeaje kazi yake. Imamu (as) anasema: “Kisha chunguza kazi zao, tuma waangalizi miongoni mwa watu wakweli na watekelezaji juu yao.” Lakini hapa panaweza kujitokeza tatizo jingine nalo ni yule aliyetumwa na Mtawala kwenda kuchunguza anaweza 86
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 86
7/5/2013 9:06:17 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
asifanye uaminifu, na akaridhika na kazi ya mtendaji huyo kwa kuhofia kupoteza cheo chake au mshahara wake, au kwa tamaa ya kutaka kupata maslahi mengi zaidi, hivyo Imamu (as) anasema huyo anayetumwa ni lazima awe miongoni mwa watu wakweli waaminifu. Pia baada ya kukusanya taarifa zake kutoka kwa wapelelezi wake, haitoshi tu kumuuzulu mtendaji husika bali anatakiwa kumfanya fundisho na mawaidha kwa wengine, bali amfanye njia atakayopitia kuwadhibiti wengine, na hiyo ni kwa Mtawala kumwadhibu adhabu itakayouadhibu mwili wake, na kumnyang’anya kile alichokipata kinyume na sheria kupitia kazi yake. Imamu (as) anasema: “Kisha muweke mahali pa udhalili, na kumuorodhesha kuwa ni miongoni mwa watu wabaya, na mvishe kidani cha aibu.”
87
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 87
7/5/2013 9:06:17 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
KODI Ni upi mtazamo wa kwanza wa Mtawala kuhusu maudhui hii?
K
wanza: Ni kujielekeza kikamilifu katika kuiendeleza ardhi na kuihuisha kabla ya kutazama ukusanyaji wa kodi na kabla ya kutazama vyanzo vya mapato. Kwa sababu mtazamo huu wenyewe ulivyo utawasukuma na kuwashawishi raia katika kuijali ardhi na kuendeleza rasilimali za asili, jambo ambalo litaleta maendeleo ya nchi na ustawi wake na mafanikio kwa raia wake. Imamu (as) anasema: “Mazingatio yako yawe kwenye uendelezaji wa ardhi (kilimo) zaidi kuliko ukusanyaji wa kodi, kwani hilo (la kodi) halipatikani isipokuwa kwa kilimo, na mwenye kutaka mapato bila ya kulima atakuwa ameiharibu nchi, na kuwaangamiza waja, na suala lake halitokuwa imara ila kidogo.” Pili: Kutokana na mtazamo huu Mtawala anaweza kuwapunguzia raia mzigo wa kodi wakati wa majanga kama vile ukame au upungufu wa maji na mfano wa hayo, jambo ambalo hupunguza uzalishaji. Hiyo ni kwa sababu uhusiano uliopo baina ya Mtawala na watawaliwa si uhusiano wa Mtawala kuchukua, hapana, ni uhusiano wa kushirikiana na kuungana na kupeana baina ya pande mbili, na hivyo kupunguza kodi kutaimarisha mahusiano baina ya raia na Mtawala wao ambaye anawasaidia wakati wa matatizo. Imamu (as) anasema: “Endapo watalalamikia uzito (wa kodi) au ugonjwa, au kuka88
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 88
7/5/2013 9:06:17 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
tika kwa unyweshelezeaji au ubichi au kubadilika kwa ardhi iliyofunikwa na mafuriko, au ukosekanaji wa mvua, basi wapunguzie kiasi unachoona kitawaboreshea mambo yao.�
89
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 89
7/5/2013 9:06:17 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
Mshauri wa Mtawala:
K
wa kuwa usalama wa nchi na siri za Mtawala zina mahusiano ya karibu na kundi hili, na kwa kuzingatia hatari ya cheo hiki ambacho kinaweza kuwa silaha dhidi ya Mtawala mwenyewe kwa kuwa anazijua siri zake, na anajua udhaifu wake na upungufu wake, basi sifa anazozitaja Imamu (as) zinaainisha mtu anayefaa katika cheo hiki, mwenye nia njema na Mtawala na umma, anayeweza kung’oa mapungufu yaliyopo serikalini, Imamu (as) anasema: “Kisha waangalie makarani wako, wape mamlaka kushughulikia mambo yako wale walio bora kati yao, na barua zako ambazo unaingiza humo mikakati (ya kupambana na maadui) yako na siri zako mpe mwandishi maalumu kati ya wale wenye tabia bora zaidi kuliko wote.” Lakini swali ni: Ni sifa zipi anazopasa kuwa nazo mtu anayeteuliwa kuwa mshauri wa Mtawala? Kwanza: Unyoofu katika kila jambo: Kiasi kwamba hawezi kuathiriwa na matukio ya nje, wala kuchezewa na mabadiliko ya kinafsi, asiyeathirika kwa faida wala hasara, asiyetolewa nje ya msitari wa haki, yule aliye imara na thabiti asiyetikiswa na kimbunga wala mafuriko. Imamu (as) anasema: “Ambaye hafurahishwi kupita kiasi kwa kukirimiwa, ili asije akathubutu kusema dhidi yako mbele ya halaiki.” Pili: Uangalifu wenye kumwajibisha: Hiyo ni kwa sababu mtu anapokuwa katika sehemu adhimu kama hii na katika nafasi muhimu kama hii ni wajibu awe mwangalifu na mwenye tahadhari kubwa, na wala asitoe maamuzi isipokuwa 90
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 90
7/5/2013 9:06:17 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
baada ya kushauriana na Mtawala katika hilo, Imamu (as) anasema: “Na wala asiwe mzembe wa kuleta mawasiliano ya maofisa wako mbele yako, wala mughafiliko haumzuwii kutambua yanayoingia miongoni mwa maandishi ya wafanyakazi wako kwako, na kutoa majibu yake yaliyo sahihi kutokana na wewe katika anayochukua kwa ajili yako na kutoa kutoka kwako, asifanye makubaliano mabaya kwa niaba yako, wala asishindwe kukataa makubaliano yaliyofanyika dhidi yako.” Tatu: Kujitambua na kuitambua nafasi yake: Hiyo ni kwa sababu atakapojua jambo hili hatoongea au kutenda isipokuwa kulingana na nafasi yake hii, kwa sababu kujishusha na kusahau nafasi yake kutamfanya asihisi majukumu, na hatimaye atatenda kwa kupuuza na ujinga. Imamu (as) anasema: “Wala asiwe hajui kiwango cha nafasi yake katika mambo, kwani asiyejua kiwango cha nafasi yake mwenyewe hatajua kabisa kiwango cha nafasi ya mwingine. Nne: Historia nzuri: Ambayo inaelezea shakhsiya yake na utu wake kupitia mwenendo wa tabia njema, mfano ukweli, uaminifu, upendo wake kwa raia na nyinginezo miongoni mwa tabia hizi za kiutu ambazo anatakiwa kujipamba nazo Mwislamu. Imamu (as) anasema: “Lakini wajaribu walivyo watendea watu wema kabla yako. Chukua maamuzi kutoka kwa mwenye jina miongoni mwa watu wa kawaida na aliye maarufu kwa uaminifu. Hiyo ni dalili ya kuwa nasaha zako ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kwa ambaye kwa niaba yake umetawalia mambo yake.” Mtawala anawajibika na kila linaloendelea miongoni mwa matukio na ukiukwaji wa taratibu unaofanywa na watu kwa jumla, na ule unaofanywa na mtu ambaye ana mahusiano 91
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 91
7/5/2013 9:06:17 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
na yeye, sawa awe ni mtu katika familia yake au mtu nje ya familia yake. Kwa ajili hii jambo lolote litakalofanywa na Mtawala na likawa si sahihi basi yeye ndiye atakayewajibika nalo na kuhukumiwa kwalo, kama pale atakapotilia maanani familia yake na ndugu zake ambao ni mafakiri na masikini huku akiwapuuza watu wengine. Katika hali kama hiyo utetezi wowote hautamfaa bali utakuwa ni maneno matupu, kama vile kudai hawa ni katika familia yangu, au jamaa zangu wa karibu au wafanyakazi, kwa sababu huo ni utetezi usiyo na tija usiokuwa sahihi. Kwa ajili hiyo Imamu (as) anasema: “Na aibu yoyote utakayoipuuza kwa maofisa wako itakulazimu wewe (itakuganda).�
92
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 92
7/5/2013 9:06:17 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
MAJUKUMU YA MTAWALA MBELE YA WAFANYA BIASHARA NA WAMILIKI WA VIWANDA
L
eo hii biashara na viwanda vimekuwa alama inayoonesha kiwango cha maendeleo ya nchi na ustawi wake, bali ndio mambo yanayoainisha nafasi ya nchi baina ya nchi nyingine katika ulimwengu wa sasa, je yenyewe ni katika nchi tajiri au masikini? Na kwa ajili hiyo ndio maana tunakuta nchi za ulimwengu wa sasa zimeiundia wizara kila moja kati ya kazi hizi mbili: ya biashara na viwanda, wizara makhususi inayojishughulisha na kunadhimu na kuratibu mambo ya biashara na ya viwanda katika nchi, au kutengeneza mahusiano ya kibiashara na nchi nyingine. Na hapana shaka kwamba biashara na viwanda ni mihimili muhimu inayotegemewa katika uchumi wa nchi, kama ambavyo ni mihimili pia kwa mtu binafsi. Mtume (saww) amesema: “Tisa ya kumi ya riziki inapatikana katika biashara.” Na kwa ajili hii ndio maana tunamkuta Imamu (as) akiainisha majukumu ya Mtawala mbele ya wafanyabiashara na wamiliki wa viwanda, na majukumu hayo ni: 1. Kuwajali: Sawa awe anajishughulisha na biashara za nje au za ndani, na sawa awe ni mjasiriamali ambaye anafanya kazi katika viwanda vidogo vidogo vya uzalishaji wa kutumia mikono. Hiyo ni kwa kuwa wote wanafanya kazi ya kuiletea jamii mahitaji yake, na wanavumilia usumbufu wa kuleta bidhaa kutoka nje, na kwa biashara yao hii ndogo na kazi yao hii ndogo, utawaona wamepambika 93
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 93
7/5/2013 9:06:17 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
kwa sifa nzuri na wanaipenda jamii, na hivyo jamii haitarajii kudhurika kupitia tamaa yao. Imamu (as) anasema: “Kisha wausie mema wafanyabiashara na wenye viwanda, mkaazi (mwenye maduka) kati yao au anayetembeza biashara yake au kibarua, kwa hakika watu hao ndio chimbuko la manufaa na njia ya faida, na waletaji wake (wa bidhaa) kutoka mbali na maeneo ya mbali zaidi, nchi kavu na majini, ardhi tambarare na ya milimani, maeneo ambayo watu hawathubutu kwenda maeneo hayo, kwa hakika wao (wafanyabiashara na wenye viwanda) ni watu wa amani hauhofiwi kwao uasi, na ni watu wema ambao hauhofiwi kwao uhaini.” 2. Kufanya ziara za uvumbuzi: Kwa kuendelea kuchunguza mazingira ya biashara na namna ya kuamiliana na jamii, kwa sharti kwamba ziara hizi zifanyike maeneo yote ya nchi hata yale ya mbali. Imamu (as) anasema: “Na yachunguze mambo yao mbele yako na popote wawapo kwenye maeneo yako.” Wakati ambao Imamu (as) anasisitiza sifa nzuri za wafanyabiashara wa kiwango cha kawaida, anarudi tena na kubainisha kwamba kuna wafanyabiashara wengi na wamiliki wengi wa viwanda wenye sifa mbaya, wanazitumia sifa hizi pale serikali inapowapuuza, na sifa hizo ni: A. Huwa na muamala mbaya na jamii, Imamu (as) anasema: “Na elewa kwamba, pamoja na hayo wengi miongoni mwao wana ufinyu wa kutisha wa mawazo.” B. Huwa mabahili, wabinafsi na kupenda mali, Imamu (as) anasema: “Na ubakhili mbaya.”
94
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 94
7/5/2013 9:06:17 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
C. Huhodhi bidhaa na kuziuza kwa bei ya juu, Imamu (as) anasema: “Na ufichaji wa vitu vya manufaa.” D. Hudhibiti soko la bidhaa na bei zake, Imamu (as) anasema: “Na upandishaji wa bei za bidhaa.” Katika hali ya kawaida iwapo wafanyabiashara na wamiliki wa viwanda wenye sifa kama hizi wataamiliana na jamii, basi sifa hizi zitaiathiri jamii na kuidhuru sana, na wakati huo huo zitamuweka mahali pabaya Mtawala kwa kushindwa kuchukua hatua zinazopasa katika mipaka ya uadilifu na kwa bei sahihi, ambazo zitakuwa ni njia ya kati ambayo haitakuwa juu kiasi cha kuidhuru jamii, na wala haitakuwa chini kiasi cha kuwadhuru wafanyabiashara. Hivyo iwapo Mtawala atafafanua na kuweka wazi uwiano huu kisha akaona ukiukwaji unaofanywa na wafanyabiashara au watu wengine, ni wajibu juu yake kuwateremshia adhabu kali ambayo itawazuia wao na walio mfano wao, lakini hatua hizo lazima zichukuliwe ndani ya mipaka ya sheria ya Uislamu. Imamu (as) anasema: “Hii ni sababu ya madhara kwa walio wengi, na ni aibu kwa watawala, hivyo basi, zuia ufichaji wa bidhaa, kwani Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (saww) amekataza hilo, na biashara inabidi iwe ya nafuu, kwa vipimo na mizani za kiadilifu, na bei isiyodhulumu pande zote mbili kati ya muuzaji na mnunuzi. Basi mwenye kuficha bidhaa baada ya kuwa umemkataza, mpe fundisho, lakini sio adhabu kali ya kupita kiwango.”
95
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 95
7/5/2013 9:06:17 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
TABAKA LA CHINI NA MSIMAMO WA UISLAMU KUHUSU TABAKA HILO
T
abaka hili linaundwa na watu wahitaji, mafakiri, masikini, wenye ulemavu, wenye kipato kidogo, wajasiriamali wa kazi za mikono, wakulima na wengineo. Na hawa wanaunda kundi kubwa la raia, na katika lugha ya leo hawa wanajulikana kama tabaka la walalahoi, na katika mtazamo wa Imamu (as) wanajulikana kama tabaka la chini, Imamu (as) anasema: “Kisha kuwa mwangalifu na watu wa tabaka la chini, miongoni mwa ambao hawana hila, na masikini na wahitaji, na ambao ni hohehahe na wenye ulemavu, kwani katika tabaka hili kuna anayeomba na asiyetosheka.” Na tunapotembea katika safari ya historia ya zamani na ya sasa, tunakuta hili ndio tabaka ambalo lilisimama pamoja na Manabii (as) na watu wema katika kupambana na mabeberu na madhalimu, na ndio tabaka ambalo hudhulumiwa na huteseka kwa kunyimwa, kwa kunyang’anywa haki zao na serikali za kidhalimu, kwa ajili hiyo ndio maana tunawakuta daima wakiwa ni kuni za mapinduzi ya wananchi dhidi ya madhalimu na mabeberu. Kwa ajili ya yote haya inampasa Mtawala au serikali ya Kiislamu kulijali sana tabaka hili, na kutumia juhudi zake zote kuhakikisha watu wa tabaka hili wanapata saada yao na anaboresha maisha yao kwa njia ya: Kwanza: Kuwatengea fungu kutoka katika pato la ardhi, ili kwamba waweze kukidhi mahitaji yao, na wagawie kwa uadilifu na usawa katika sehemu zote za nchi na vijiji vyake 96
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 96
7/5/2013 9:06:17 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
vyote. Imamu (as) anasema: “Na wajaalie sehemu kutoka katika mfuko wa hazina ya mali yako, na sehemu kutoka katika mazao ya ardhi ya ngawira ya Kiislam katika kila mji, kwani aliye mbali miongoni mwao ni sawa na aliye karibu, na wote kila mmoja haki yake imewekwa chini ya uangalizi wako.” Pili: Mtawala awajali muda wote, na wala asidanganyike na mali kwa kujitenga na wao, na miongoni mwa aina za kuwajali ni kuwa mnyenyekevu kwao, na kutumia sehemu ya wakati wake katika kutatua matatizo yao na kuyafanyia kazi, na kuwatumia watu waaminifu ili kwenda kumchukulia Mtawala habari zao na kumpelekea taarifa za mazingira yao na mahitaji yao, pale anaposhindwa kwenda kwao yeye mwenyewe. Na aifanyie kazi taarifa iliyomfikia ya mazingira yao, kwa kutekeleza mahitaji yao, kwani kufanya hivyo ni kumridhisha Mwenyezi Mungu, Imamu (as) anasema: “Hivyo basi mkorofi asikuzuie kujishughulisha nao, kwa kweli wewe hutopewa udhuru kwa kupoteza jambo hafifu, eti kwa sababu ya kutilia maanani mengi yaliyo muhimu kwa hivyo usiiondoe hima yako mbali nao.” Tatu: Awajali na kuwatilia umuhimu mayatima na wazee kwa njia ya kuanzisha asasi zenye kuwahudumia, na kuwarahisishia mahitaji yao ya kimaisha kama ilivyo leo katika baadhi ya nchi, na kama ilivyo katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusu familia za mashahidi na wanyonge miongoni mwa raia. Kwa kweli Mtawala anaweza kupata uzito katika hilo, lakini Imamu (as) anamuweka Mtawala njiapanda pindi anapomuainishia kwamba haki yote ni nzito. Imamu (as) anasema: “Na waangalie mayatima na wenye umri mkubwa miongoni mwa ambao hawana hila (njia ya kupata riziki), 97
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 97
7/5/2013 9:06:17 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
wala hawako tayari kuomba, na hilo ni zito kwa watawala, na kwa kweli haki yote ni nzito.” Nne: Ni wajibu kwa Mtawala kutenga sehemu ya wakati wake kwa ajili ya kupokea watu kutoka katika tabaka hili la wahitaji katika kikao cha kawaida bila kuwepo na vitisho vya wanajeshi, walinzi na askari, ili kila mmoja aweze kuwasilisha mahitaji yake yote kwa Mtawala bila khofu yoyote. Na ni wajibu juu ya Mtawala katika hali kama hii kuvumilia kila kitakachotoka kwao miongoni mwa ukali, awatulize na kuwapa matumaini, na hivyo iwapo atatekeleza mahitaji yao basi asiwasimange, na kama hataweza basi aongee nao kwa upole na kuwaomba radhi kwa kutokuwa na uwezo wa kuwatekelezea. Imamu (as) anasema: “Na watengee wenye kudhulumiwa sehemu ya muda utakaokuwa kwa ajili yao wewe mwenyewe, na ukae kikao cha wote, basi uwe mnyenyekevu katika kikao hicho kwa ajili ya Mwenyezi Mungu aliyekuumba, waweke kando askari wako na wasaidizi wako, ili msemaji wao aseme na wewe, bila ya woga.”
98
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 98
7/5/2013 9:06:18 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
WAJIBU ALIONAO MTAWALA WA KIISLAMU
K
wanza: Kuna mambo muhimu katika nchi ambayo Mawaziri na wengineo miongoni mwa watendaji wa serikali wanaweza kushindwa kuyatatua serikalini, hivyo katika hali kama hii analazimika Mtawala wa Kiislamu kuingilia kati moja kwa moja ili kuweza kutatua tatizo husika. Imamu (as) anasema: “Kisha miogoni mwa mambo yako huna budi ila kuyafanya mwenyewe.” 1. Kuitikia maombi ya wafanyakazi na kusikiliza matatizo yao na kufanya kazi ya kuyatatua, Imamu (as) anasema: “Miongoni mwayo, kuwajibu wafanyakazi wako yale ambayo makarani wako wanashindwa.” 2. Yampasa Mtawala afanye haraka kutimiza mahitaji ya watu, na kuwadhibiti Mawaziri walio wazito katika kutekeleza wajibu wao mbele ya raia, ambao wanatafuta manufaa na faida na kwa ajili hiyo wanazembea katika kutekeleza kazi zao, hiyo ni kwa upande mmoja, na kwa upande mwingine asiwategemee moja kwa moja katika kushughulikia mambo ya raia. Imamu (as) anasema: “Na miongoni mwayo, kuondoa shida za watu siku zinapokufikia ambazo vifua vya wasaidizi wako vinapata shida.” Pili: Ni wajibu juu ya Mtawala aweke ratiba yenye kueleweka na ajichukulie ahadi ya kutekeleza ratiba hiyo kikamilifu kadiri atakavyoweza, kwa njia ya kutekeleza kila kazi ndani ya siku yake husika na ndani ya wakati wake ulioainishwa. Na iwapo Mtawala atatimiza hilo basi matokeo yake 99
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 99
7/5/2013 9:06:18 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
yatakuwa mazuri na yenye matunda kuliko kama atakwenda bila ratiba iliyopangiliwa. Imamu (as) anasema: “Na ikamilishie kila siku kazi yake, kwani kila siku ina kazi yake.” Na ndani ya ratiba hiyo ni wajibu kwake kuchagua wakati unaofaa na mzuri ili aweze kuihudumia nafsi yake, kumwabudu Mola Wake na kujitathmini, Imamu (as) anasema: “Na jaalia kwa ajili yako sehemu nzuri na kubwa ya muda kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ingawa muda wote ni wa Mwenyezi Mungu, endapo nia itakuwa njema, na raia kubaki salama.” Tatu: Ni wajibu juu ya Mtawala wa Kiislamu kutekeleza haki tatu: 1- Haki ya Mwenyezi Mungu peke yake. 2- Haki ya raia. 3- Haki ya Mwenyezi Mungu na raia. Ama haki ya Mwenyezi Mungu peke yake yenyewe inapatikana katika kutekeleza faradhi zote alizoziweka Mwenyezi Mungu juu ya waja wake, azitekeleze kikamilifu na kwa usahihi bila dosari yoyote, bila kujali mchoko na taabu itakayompata. Imamu (as) anasema: “Na jambo maalumu umpwekeshalo Mwenyezi Mungu katika Dini yako liwe ni kutekeleza wajibu wake ambao ni maalumu kwa ajili Yake, basi mpe Mwenyezi Mungu uyatendayo kwa mwili wako wakati wa usiku wako na mchana wako. Na yatekeleze uliyotenda kwa ajili ya kutaka ukaribu kwa Mwenyezi Mungu kikamilifu bila ya dosari, wala upungufu, na kwa kiwango chochote kifikacho mwilini mwako.” 100
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 100
7/5/2013 9:06:18 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
Ama haki za raia anazopaswa Mtawala kuzitekeleza ni kutojificha muda mrefu mbali na raia, bali anapasa kujitokeza hadharani kwa raia wake katika nyakati tofauti, hiyo ni kwa sababu kujitenga mbali na raia kwa muda mrefu huchukuliwa kama kiburi na majivuno na ni tabia mbaya. Kama ambavyo hali hiyo itamfanya asijue hali za raia wake, zaidi ya hapo ni kwamba kujificha mbali na raia kwa muda mrefu kutamaanisha kujiweka karibu na kundi tu fulani la wahudumu wake na kujiweka mbali na watu wenye fikra na ubora zaidi yake, na hii ni kuwatukuza wadogo na kuinua nafasi yao na kuwadharau wakubwa na kushusha hadhi yao, na matokeo yake ni kutokea mchanganyiko wa haki na batili. Imamu (as) anasema: “Na ama baada ya hayo: Usirefushe kutoonekana kwako mbali na raia wako, kwani kutoonekana kwa Mtawala ni tawi miongoni mwa matawi ya dhiki na uchache wa elimu juu ya mambo. Na kutoonekana kwao pia kunawazuia wao kujua vitu ambavyo hawavijui, kwa minajili hiyo, kubwa wanalifanya dogo na dogo wanalifanya kubwa, na uzuri unakuwa ubaya na ubaya kuwa wema, na haki huchanganywa na batili.” Nne: Kwa kuwa Mtawala ni mtu kama watu wengine na si mungu, na kwa kuwa mara zote raia humhukumu mtu kwa mtazamo wa nje, basi hatarajiwi kwa raia kumdhania vizuri iwapo atajificha mbali na wao kwa kuda mrefu, hiyo ni kwa sababu haki haina alama za wazi zenye kuonesha sababu iliyomfanya Mtawala ajifiche mbali na wao. Imamu (as) anasema: “Na mtawala ni binadamu hajui waliyojitenga nayo watu miongoni mwa mambo. Na wala haki haina alama ambayo kwayo aina za ukweli na uwongo hujulikana.” 101
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 101
7/5/2013 9:06:18 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
Na hapa ndipo linapojitokeza swali, nalo ni Mtawala ni nani? Na ni upi msimamo wake katika haki? Kwa kweli Mtawala ni mmoja kati ya hawa wawili hakuna wa tatu, Imamu (as) anasema: “Na wewe ni mmoja kati ya watu wawili.” 1. Mwenye kufuata haki na kuifanyia kazi, hawi bahili kwa raia wake kwa kuwanyima haki zao, bali anafanya lililo ndani ya uwezo wake katika kutekeleza haki zao, na katika hilo hujitolea kila anachokimiliki miongoni mwa nguvu na uwezo wa hali na mali. Imamu (as) anasema: “Ama ni mtu ambaye nafsi yake imekuwa karimu kwa kutoa katika haki, basi kwa nini unajificha katika kuwapa haki wanayostahiki, au kuwatunukia kitendo chema?” Na katika hali kama hii Mtawala haogopi kukutana na raia wake na wala hafanyi ubahili katika kutimiza maombi yao. 2. Mwenye kwenda kinyume na haki, anawanyima raia wake haki zao na anakataa kujibu maombi yao, katika hali kama hii raia hawajihangaishi kuomba haki zao bali huanza mchakato wa kutaka kuchukua haki zao hata kama ni kwa nguvu, kwa sababu haki hizo hazitoki mfukoni mwa Mtawala bali ni zao na ni haki yao kuzichukua. Imamu (as) anasema: “Au umepatwa na mtihani wa kunyimwa, basi mikono ya watu itajitenga mbali nawe kukuomba pindi watakapokata tamaa na utowaji wako, pamoja kwamba haja nyingi za watu kwako hazina ugumu wowote kwako, kama vile malalamiko dhidi ya dhulma, au maombi ya kutaka kutemdewa uadilifu.” 102
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 102
7/5/2013 9:06:18 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
Mtawala na msimamo wake kwa wandani wake:
K
wanza: Tangu zamani mpaka leo hii huwa kuna kundi ambalo huwa karibu zaidi na Mtawala na katika mtandao wake, hao ni wale wandani ambao wanatokana na watu wake wa karibu na wenye manufaa na yeye. Kundi hili la wandani hujaribu kwa juhudi zote wakati wowote lipatapo fursa, na hasa Mtawala anapokuwa dhaifu, au mwenye kukandamiza haki za raia, kumtumia yeye na vyombo vya dola katika kujipatia maslahi binafsi, na kundi hili hujitambulisha kwa sifa mbaya, nazo ni: 1. Kujipendelea rasilimali za umma na kheri zake, Imamu (as) anasema: “Kisha kwa hakika mtawala anakuwa na watu maalumu na wasiri, kati yao kuna wanaojitwalia.” 2. Kuwashambulia raia na kuwanyang’anya haki zao, Imamu (as) anasema: “Na kudhulumu.” 3. Huwa na muamala wa mtu dhalimu katika kuamiliana na raia katika muamala wowote ule, ambapo daima wao huiweka haki upande wao dhidi ya raia mnyonge. Imamu (as) anasema: “Na kuwa na uchache wa uadilifu katika matendo.” Hivyo kutokana na sifa walizonazo, Imamu (as) anamtaka Mtawala kuchukua msimamo madhubuti dhidi ya watu hawa kwa: A. Kung’oa mizizi ya tatizo linalosababishwa na watu hawa, kwa kuwakatia njia na kuwatenga mbali na idara yoyote 103
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 103
7/5/2013 9:06:18 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
ya serikali, Imamu (as) anasema: “Basi kata chimbuko (la shari yao) lao kwa kukata sababu za hali hizo.” B. Kuwaweka hawa sawa na raia wengine wa kawaida, hivyo Mtawala asiwape upendeleo wowote wala asimkatie yeyote kipande cha ardhi kwa upendeleo, kwani kufanya hivyo ni kuwadhuru raia kwa upande mmoja, na kwa upande mwingine ni kwamba wao ndio wenye kufaidi na si wengine. Na tatu kwa matendo haya Mtawala atakuwa ni dhalimu kwa mtazamo wa raia hapa duniani, na pia kwa mtazamo wa Mwenyezi Mungu kesho Akhera. Imamu (as) anasema: “Wala usimkatie (usimpe) yoyote miongoni mwa wapambe na wasaidizi wako kipande cha ardhi. Na wala asitamani yeyote kwako umiliki (wa ardhi) ambao utamdhuru aliye karibu miongoni mwa watu katika kunywesheleza, au katika kazi ya ushirikiano ambao wataubebesha mzigo wake juu ya wengine, hatimaye ikawa manufaa yake ni ya kwao na si yako, na aibu yake itakuwa juu yako duniani na Akhera.” Pili: Mtawala ana wajibu wa kuwatimizia haki raia wake wote bila ubaguzi wala upendeleo, sawa wawe wandani wake au wa kawaida, na wala katika haki asiogope lawama ya mwenye kulaumu, hata kama kufanya hivyo kutawaathiri jamaa zake wa karibu na wandani wake. Na kwa kweli katika kutekeleza hilo anaweza kukutana na maudhi na madhara na uzito juu yake, hivyo analazimika kuwa na subira na kumtegemea Mwenyezi Mungu, kwani hatima njema huko Akhera itakuwa ni ya yule mwenye kutekeleza haki na kuifuata. Imamu (as) anasema: “Iambatanishe haki kwa wale wanao jilazimisha nayo, kwa aliye karibu na wewe au aliye mbali, na kuwa mwenye subira ukitarajia thawabu, hata 104
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 104
7/5/2013 9:06:18 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
kama itawahusu ndugu zako wa karibu na watu maalumu kwako, na taka matokeo yake kwa jambo zito kwako, kwani matokeo yake ni yenye kuhimidiwa.” Tatu: Tumetaja huko nyuma kwamba raia humhukumu Mtawala kwa kutazama dhahiri ya mambo yake, na hapo raia wanaweza kumdhania vizuri Mtawala wao na wanaweza kumdhania vibaya na kumtuhumu kwa dhulma, hivyo katika hali kama hii anapotuhumiwa na raia kwa dhulma, ni wajibu juu ya Mtawala abainishe udhuru wake na kujitetea na awawekee wazi raia wake uhalisia wa hali ilivyo, kwa kufanya hivyo hali ya kuaminiana baina ya raia na Mtawala itajitokeza, na hapo anyenyekee na unyenyekevu huo umuongoze katika haki na uadilifu. Imamu (as) anasema: “Endapo raia wako watakudhania umetenda dhulma jidhihirishe kwa udhuru (utetezi) wako kwao, na ziweke sawa dhana zao kwa kujiweka wazi. Kwa kweli katika hilo kuna mazoezi kwako kwa ajili ya nafsi yako, na kuwatendea upole raia wako, na kueleza udhuru, kwa hayo utaifikia haja yako ya kuwanyoosha kwenye haki.”
105
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 105
7/5/2013 9:06:18 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
NCHI NA UHUSIANO WAKE NA NCHI NYINGINE
N
i jambo lisilo na shaka kwamba dola ya Kiislamu haiwezi kujitenga peke yake bila kuhitaji ushirikiano na nchi nyingine, bali hulazimika kuwa na mahusiano na nchi nyingine kwa namna yoyote ile, hivyo inaweza kuwa na mahusiano chanya na nchi nyingine kama vile ya kusaidiana na kubadilishana bidhaa. Au yanaweza kuwa ni mahusiano hasi kama vile ya kuwekeana mikataba, makubaliano, na sulhu baina ya pande mbili. Lakini swali ni: mikataba hii inapaswa kuwaje? Na katika misingi ipi? Na ni kwa maslahi ya nani? Hili ndilo linalojibiwa na Imamu (as) katika waraka wake kwa Malik Ashtar Nakhaiy (r.a). 1. Imamu Ali (as) anaweka sharti kwamba katika makubaliano yoyote yanayofanywa baina ya nchi ya Kiislamu na adui, sharti la msingi ni lazima makubaliano haya yawe ni yenye kumridhisha Mwenyezi Mungu na si yenye kumridhisha Mtawala au adui. Kwani ridhaa ya Mwenyezi Mungu hutokana na ridhaa ya raia ambao ndio wenye kuathirika moja kwa moja na matokeo ya makubaliano, kwa madhara au faida. Imamu (as) anasema: “Wala usiikatae suluhu aliyokuiitia adui yako ambayo ndani yake mna ridhaa ya Mwenyezi Mungu.� Sulhu yenye ridhaa ya Mwenyezi Mungu huwa na ridhaa na maslahi kwa raia, nayo ni sulhu yenye kudhamini amani yao na uhuru wao, na kulinda haki zao na kuwapumzisha askari dhidi ya vita, na Mtawala dhidi ya 106
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 106
7/5/2013 9:06:18 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
mashaka na huzuni. Imamu (as) anasema: “Kwa kweli katika suluhu kuna raha kwa askari wako, na pumziko la majonzi yako, na amani kwa nchi yako.” 2. Baada ya makubaliano ya sulhu na adui, ni wajibu juu ya Mtawala wa Kiislamu muda wote awe katika kufuatilia harakati na mwenendo wa adui, kwani huenda amefanya sulhu na yeye ili tu apate fursa ya kumshambulia na kukiuka makubaliano. Imamu (as) anasema: “Lakini tahadhari yote iwe kwa adui wako baada ya kufanya naye suluhu, kwa kuwa huenda adui akawa amejikurubisha kwa suluhu ili akughafilishe, kwa hivyo kuwa thabiti, na katika hilo ituhumu dhana njema.” 3. Kutekeleza ahadi na makubaliano, pia kuheshimu amana, ni miongoni mwa mambo ambayo wamekongamana kwayo watu wote bila kujali tofauti ya fikra zao na mielekeo yao, wote wamekongamana juu ya kuheshimu mambo hayo na kuyatukuza kuliko faradhi nyingine za Mwenyezi Mungu, hata mushrikina ambao wao ni duni kuliko Waislamu, japo baadhi yao walikiuka kwa kutokuwa kwao na dini wala akida. Lakini kwa jumla watu wote huheshimu na kushikamana na maadili haya matukufu, na kwa ajili hii tunamkuta Imamu (as) akimsisitiza Mtawala kwamba atekeleze ahadi na aheshimu amana, asifanye hadaa wala asivunje ahadi, wala asivunje uaminifu, bali ni wajibu kwake kutekeleza yale aliyoahidi kutekeleza. Imamu (as) anasema: “Na endapo utakuwa umefunga ahadi kati yako na adui yako, au umemvisha dhimma (umekubaliana na asiye Mwislamu kuishi katika dola ya Kiisalmu, na yeye kukubali kulipa stahiki zote za dola), basi tekeleza ahadi yako, na chunga ahadi yako kwa ua107
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 107
7/5/2013 9:06:18 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
minifu. Ihifadhi ahadi uliyoifanya kwa nafsi yako. Kwa hakika watu hawajakongamana kwenye jambo la faradhi miomgoni mwa faradhi za Mwenyezi Mungu zaidi kushinda walivyokongamana katika kuheshimu utekelezwaji wa ahadi, pamoja na kutofautiana upendo wao na kutawanyika kwa rai zao, kiasi kwamba hata washirikina wamejilazimisha kutekeleza ahadi kati yao na Waislamu, kwa vile wamekuta matokeo ya kuangamiza kwa kutotekeleza ahadi, hivyo basi, kabisa usiifanyie khiyana dhima yako wala usiitengue ahadi yako. Wala usimdanganye adui yako, kwani mtu hawezi kuthubutu kumchukiza Mwenyezi Mungu isipokuwa aliye jahili muovu.� 4. Maadili ya Kiislamu, na maadili ya kimungu ni deraya yenye kuwakinga wanadamu na kuwapa himaya na amani iwapo tu watashikamana na maadili hayo, wasikiuke maadili hayo wala wasiyaharibu au kudanganya katika utekelezaji wake. Kama ambavyo Mtawala wa Kiislamu anavyotakiwa kujiepusha na usiri na upotoshaji katika kila mkataba na makubaliano anayoingia, bali ni wajibu mkataba na makubaliano yawe wazi kikamilifu. Haruhusiwi kufanya udanganyifu na hadaa katika makubaliano. Imamu (as) anasema: “Mwenyezi Mungu amezijaalia ahadi na dhima Zake kuwa ni amani, ameieneza kati ya viumbe kwa rehema Zake, na ni miiko ambayo viumbe wanaitumia kukaa kwenye hifadhi Yake na kukimbilia karibu Yake, kwa hivyo hapana ufisadi wala khiyana wala hadaa humo, wala usifanye mapatano ambayo yataruhusu tafsiri tofauti ndani yake, wala usibadilishe tafsiri ya maneno yasiyo wazi baada ya kuhakikishwa na kuthibitishwa.� 108
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 108
7/5/2013 9:06:18 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
5. Hakika anapaswa kufanya subira wakati wa kutekeleza makubaliano, hata kama utekelezaji huo utamsababishia matatizo mengi, kufanya hivyo ni bora kuliko kukiuka makubaliano na kudanganya, hiyo ni kwa sababu kutekeleza makubaliano na ahadi kutakuwa na matokeo mazuri katika hali yoyote ile. Ama kukiuka makubaliano na ahadi kutakuwa na matokeo mabaya duniani na Akhera. Imamu (as) anasema: “Wala shida ya jambo lililokulazimu ndani yake ahadi ya Mwenyezi Mungu isikufanye utake kulibatilisha bila ya haki, kwani subira yako kwenye jambo la shida ambalo unataraji faraja yake na fadhila za matokeo yake, ni bora kuliko usaliti unaohofia baadaye kuwajibishwa. Na ukuzunguke ufuatiliaji kutoka kwa Mwenyezi Mungu, kwani hutoweza kuomba msamaha hapa duniani wala Akhera.�
109
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 109
7/5/2013 9:06:18 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
MTAWALA NA UMWAGAJI DAMU
H
akuna jambo lenye thamani kwa mwanadamu kushinda damu yake, mwanadamu anaweza kusamehe kila kitu chenye thamani kwake lakini hawezi kusamehe damu yake kirahisi, na Mwenyezi Mungu Mtukufu amempa mwanadamu heshima na nafasi ambayo haijafikiwa na kiumbe kingine chochote, na ameipa heshima damu yake. Lakini leo hii madhalimu wa zama zetu hawatambui heshima ya mwanadamu na hadhi yake, hivyo wamwagaji damu katika kila kona wanamwaga damu za watu wasio na hatia, huku silaha za maangamizi na uharibifu, vifaru vya watu makatili, na bunduki za watu wenye chuki zikiendelea kumkandamiza mwanadamu mnyonge bila kujali nafasi yake na heshima yake huko Iraq, Kusini mwa Lebanon, Palestina, Eritria, Afghanistani, Filipino na katika kila ardhi aliyopo dikteta mkoloni. Imamu Ali (as) anamtahadharisha Mtawala wa Kiislamu na umwagaji damu pasipo na haki, kwa sababu kufanya kitendo hiki kutazalisha upinzani wa kisasi kizito kutoka kwa raia dhidi ya Mtawala, kwani kitaamsha chuki ya raia dhidi ya Mtawala, na hatimaye chuki hii itageuka na kuwa mapinduzi yatakayobomoa nguzo za serikali na utawala wake kama tulivyoshuhudia hilo katika Iran ya zamani (ya Shah). Zaidi ya hapo ni kwamba matokeo yake yatakuwa mabaya juu ya Mtawala ikiwa ni pamoja na kuondokewa na neema, kuwa na maisha mafupi duniani, na kupata adhabu ya moto huko Akhera. Imamu (as) anasema: “Jihadhari sana na damu kwa kutozimwaga bila ya uhalali wake, kwani hakuna kitu kinacholeta adhabu kwa haraka zaidi, wala dhambi kubwa zaidi, 110
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 110
7/5/2013 9:06:18 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
wala kitu kiondoacho neema kwa haraka zaidi na kukatisha muda (uhai) haraka zaidi, kushinda kumwaga damu bila ya haki yake.” Na iwapo Mtawala atajaribu kuupa nguvu utawala wake kwa kumwaga damu za wapinzani wake na kuwateketeza, basi ajue huko ni kujiharakishia udhaifu na hatimaye ni kuanguka na utawala kuhamia kwa mtu mwingine, kama tulivyoshuhudia hilo katika Iran ya Shah, pale marehemu Shah alipojaribu kutaka kung’ang’ania utawala wake kwa njia ya kumwaga damu za raia wake, matokeo yake ilikuwa ni kukimbia uchi kwa kuogopa kushikwa na raia, kisha akafariki kwa kuihuzunikia na kuijutia dunia yake ambayo haikumhurumia kwa kumzuia na kifo na adhabu ya kaburi, hii ni duniani, na kesho huko Akhera atakuwa katika adhabu maarufu na iliyo bayana. Na kama itatokea Mtawala kumuuwa mtu bila kudhamiria bali kwa bahati mbaya, ni wajibu juu yake katika hali kama hii kuwapa haki yao warithi wa aliyeuawa. Imamu anasema: “”Hivyo basi musiimarishe utawala wenu kwa kumwaga damu ya haramu, kwani hilo ni miongoni mwa mambo yanayoudhoofisha na kuutweza utawala, bali kuondoa na kuupeleka kwa wengine. Hutakuwa na hoja kwa Mwenyezi Mungu wala kwangu kwa kuuwa makusudi, kwani katika hilo kuna kisasi cha mwili (kuuwawa kama ulivyouwa). Na ukipatwa na hilo kwa makosa (ukiuwa bila ya kukusudia), kama vile kupiga mjeledi kupita kiasi, au upanga wako, au mkono wako, au kuadhibu kwa nguvu, kwani hakika katika kumpiga mtu ngumi na zaidi yake pengine husababisha mauwaj, hivyo basi kiburi cha mamlaka yako kisikukuzuie kuwapa ndugu wa aliyeuawa haki yao (wape fidia).” 111
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 111
7/5/2013 9:06:18 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
ONYO KWA MTAWALA
I
mamu aliuanza waraka wake kwa kumpa nasaha Mtawala ili ziwe kinga yake ya kinafsi itakayomzuia kwenda nje ya njia sahihi. Na Imamu anahitimisha waraka wake kwa kumtahadharisha Mtawala na baadhi ya sifa mbaya ambazo kama zitapatikana kwa Mtawala basi zitamuondoa haraka katika njia sahihi, na miongoni mwa sifa hizo mbaya ni: 1. Maringo, majivuno na kupenda sifa. Imamu (as) anasema: “Na jihadhari kujifakharisha mwenyewe na kujiamini na unalojifakharisha nalo, na kupenda sifa, kwani kwa hakika hizo ni tabia anazoziamini Shetani nafsini mwake, ili afutiliye mbali mema ya watenda mema.” 2. Kuwasimanga raia pindi anapowatekelezea haki zao, Mtawala akifanya hivyo atakuwa amepoteza malipo yote na thawabu zote za matendo yake. Imamu (as) anasema: “Na jihadhari kuwasimbulia raia wako kutokana na wema wako, kwa hakika masimbulizi yanabatilisha wema.” 3. Kujionesha kwamba ni mchapakazi sana ilihali si kweli, kwa lengo la kutaka kuwapotosha raia na kuwadanganya kuwa amefawanyia mambo mengi, wakati katika hali halisi anajipoteza mwenyewe na anajiondolea nuru ya haki. Imamu (as) anasema: “Au kudhihirisha ziada katika vitendo vyako, kwani kudhihirisha kufanya ziada kunaondoa nuru ya haki.” 4. Kuvunja ahadi aliyowekeana na raia kama inavyotokea leo kwa Watawala madhalimu, pale wanapowaahidi wananchi miradi ya maendeleo na mabadiliko, lakini baada 112
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 112
7/5/2013 9:06:18 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
ya hapo hawatekelezi chochote. Jambo hili huamsha hasira za Mwenyezi Mungu juu ya Mtawala husika, na huamsha pia hasira na ghadhabu za raia dhidi yake, Imamu (as) anasema: “Au kuwaahidi kisha usitekeleze ahadi yako, na kutotekeleza ahadi kunasababisha chuki mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya watu, Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: Yanachukiza mno kwa Mwenyezi Mungu kuwa mnasema msiyoyatenda.’’ 5. Ni wajibu juu ya Mtawala kutumia hekima katika kila jambo na katika kila kitu kinachohusu nchi, hivyo asitende jambo kabla ya wakati wake, na wala asizembee kutenda kitu ndani ya wakati wake wa kutekelezwa jambo husika, na wala asitumbukie ndani ya mambo yasiyo bayana lakini ayatekeleze baada ya kumuwia bayana. Imamu (as) anasema: “Jihadhari kuharakia mambo kabla ya wakati wake, au kuyachukua pole pole yanapokuwa tayari, au kung’ang’ania yanapokosa kujulikana uhalisia wake, au kuonesha udhaifu yanapokuwa wazi, basi weka kila jambo pahala pake, na fanya kila jambo kwa wakati wake.” 6. Kwa kuwa Mtawala ni mmoja kati ya raia, kwa kuwa raia wengi wako sawa katika haki, basi Mtawala hana haki ya kujipendelea chochote katika haki, bali awe kama mmoja wao mwingine yeyote, awe sawa na wao, Imamu (as) anasema: “Jihadhari kujizidishia nafsi yako kwenye ambacho watu wako sawa (wanatakiwa wapate sawasawa).” 7. Uongozi ni dhamana kabla haujakuwa heshima, hivyo inamlazimu Mtawala kutokughafilika wala kuzembea hata sekunde moja katika kutekeleza majukumu yake, kama Mtawala atashindwa kufanya hivyo na akakiuka taratibu za uongozi, basi ajue matokeo yake yatakuwa mabaya, 113
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 113
7/5/2013 9:06:18 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
kwani raia watamhukumu na watamwadhibu kwa ukiukaji wake. Imamu (as) anasema: “Na kujighafilisha na linalotiliwa muhimu miongoni mwa ambayo yamekuwa wazi mbele ya macho, ikiwa utaghafilika basi litachukuliwa kutoka kwako na kupewa mwengine. Na punde mambo yatakufichukia, na utafanyiwa uadilifu kutokana na mwenye kudhulumiwa.” 8. Ni wajibu juu ya Mtawala kuidhibiti nafsi yake na kushikamana na maadili mema, hata katika mazingira magumu na katika hali ngumu, hivyo asiwafanyie kiburi watu, asitumie nguvu, wala asikate tamaa, wala asighadhibike, kutekeleza yote haya kutamfanya Mtawala muda wote amkumbuke Mwenyezi Mungu na kutafakari Akhera. Imamu (as) anasema: “Imiliki nafsi yako wakati wa ghadhabu, na ukali na mlipuko wa ukali wako, na nguvu za mkono wako, na ulimi wako mkali. Na jiepushe mbali na yote hayo kwa kujizuia na lile linalojitokeza (ulimini wakati wa ghadhabu), na chelewesha ukali mpaka ghadhabu yako itulie kuitamalaki hiyari, wala hilo hutalimakinisha nafsini mwako, mpaka utakapokithirisha majonzi yako kwa kukumbuka marejeo kwa Mola Wako.” 9. Ili mwanadamu aweze kupasua njia yake kwa mafanikio katika maisha, ni juu yake kuchagua kiigizo chema kinachomfaa, na afaidike na uzoefu wake, hivyo na Mtawala wa Kiislamu naye pia anapotaka kwenda kwa unyoofu na uadilifu katika utawala wake, ni juu yake kufaidika na uzoefu wa serikali adilifu zilizotangulia, pia kwa sura makhususi kabisa anaweza kufaidika na uzoefu wa Mtukufu Mtume (saww) katika masuala ya kuendesha serikali, na pia uzoefu wa Imamu Ali (as), kwani katika 114
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 114
7/5/2013 9:06:18 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
uzoefu wa hawa wawili Uislamu ulitabikishwa kikamilifu. Imamu (as) anasema: “Na lililo wajibu juu yako ni kujikumbusha yaliyopita ya waliokutangulia miongoni mwa serikali adilifu, au Sunnah bora, au athari kutoka kwa Nabii wetu (saww), au wajibu katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na ufuate uliyoyaona katika yale tuliyoyafanya. Na ujitahidi mwenyewe kufuata niliyokuagiza katika hati yangu hii, na hoja yangu mwenyewe niliyokuthibitishia, ili usiwe na sababu wakati nafsi yako inapoharakia utashi wake.�
115
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 115
7/5/2013 9:06:18 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1. Qur’ani Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thelathini 2.
Uharamisho wa Riba
3.
Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza
4.
Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili
5.
Hekaya za Bahlul
6.
Muhanga wa Imamu Husein (A.S.)
7.
Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.)
8.
Hijab vazi Bora
9.
Ukweli wa Shia Ithnaashari
10.
Madhambi Makuu
11.
Mbingu imenikirimu
12.
Abdallah Ibn Saba
13.
Khadijatul Kubra
14. Utumwa 15.
Umakini katika Swala
16.
Misingi ya Maarifa
17.
Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia 116
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 116
7/5/2013 9:06:18 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
18.
Bilal wa Afrika
19.
Abu Dharr
20.
Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu
21.
Salman Farsi
22.
Ammar Yasir
23.
Qur’ani na Hadithi
24.
Elimu ya Nafsi
25.
Yajue Madhehebu ya Shia
26.
Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur’ani Tukufu
27. Al-Wahda 28.
Ponyo kutoka katika Qur’ani.
29.
Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii
30.
Mashukio ya Akhera
31.
Al Amali
32.
Dua Indal Ahlul Bayt
33.
Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunnah.
34.
Haki za wanawake katika Uislamu
35.
Mwenyeezi Mungu na sifa Zake
36.
Kumswalia Mtume (s)
37.
Nafasi za Ahlul Bayt (a.s)
38. Adhana. 39
Upendo katika Ukristo na Uislamu 117
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 117
7/5/2013 9:06:19 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
40.
Tiba ya Maradhi ya Kimaadili
41.
Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu
42.
Kupaka juu ya khofu
43.
Kukusanya swala mbili
44. Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara 45.
Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya
46.
Kusujudu juu ya udongo
47.
Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s)
48. Tarawehe 49.
Malumbano baina ya Sunni na Shia
50.
Kupunguza Swala safarini
51.
Kufungua safarini
52.
Umaasumu wa Manabii
53.
Qur’ani inatoa changamoto
54.
as-Salaatu Khayrun Mina -’n Nawm
55.
Uadilifu wa Masahaba
56.
Dua e Kumayl
57.
Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu
58.
Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake
59.
Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata
60. Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mtume Muhammad (s) 118
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 118
7/5/2013 9:06:19 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
61.
Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza
62.
Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili
63.
Kuzuru Makaburi
64.
Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza
65.
Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili
66.
Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu
67.
Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne
68.
Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano
69.
Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita
70.
Tujifunze Misingi Ya Dini
71.
Sala ni Nguzo ya Dini
72.
Mikesha Ya Peshawar
73.
Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu
74. Ubora wa Imam ‘Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliyonyooka 75.
Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake
76. Liqaa-u-llaah 77.
Muhammad (s) Mtume wa Allah
78.
Amani na Jihadi Katika Uislamu
79.
Uislamu Ulienea Vipi?
80.
Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s)
81.
Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s)
119
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 119
7/5/2013 9:06:19 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
82.
Urejeo (al-Raja’a )
83. Mazingira 84.
Utokezo (al - Badau)
85.
Hukumu ya kujenga juu ya makaburi
86.
Swala ya maiti na kumlilia maiti
87.
Uislamu na Uwingi wa Dini
88.
Mtoto mwema
89.
Adabu za Sokoni
90.
Johari za hekima kwa vijana
91.
Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza
92.
Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili
93.
Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu
94. Tawasali 95.
Imam Mahdi katika Usunni na Ushia
96.
Hukumu za Mgonjwa
97.
Sadaka yenye kuendelea
98.
Msahafu wa Imam Ali
99.
Ngano ya kwamba Qur’ani imebadilishwa
100. Idil Ghadiri 101. Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu 102
Hukumu zinazomuhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi
103. Huduma ya Afya katika Uislamu 120
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 120
7/5/2013 9:06:19 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
104. Sunan an-Nabii 105. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) 106. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) 107. Shahiid Mfiadini 108. Kusalia Nabii (s.a.w) 109. Ujumbe -Sehemu ya Kwanza 110.
Ujumbe - Sehemu ya Pili
111.
Ujumbe - Sehemu ya Tatu
112. Ujumbe - Sehemu ya Nne 113. Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu 114. Hadithi ya Thaqalain 115. Maarifa ya Kiislamu 116. Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza 117. Ukweli uliopotea sehemu ya Pili 118. Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu 119. Ukweli uliopotea sehemu ya Nne 120. Ukweli uliopotea sehemu ya Tano 121. Johari zenye hekima kwa vijana 122. Safari ya kuifuata Nuru 123. Fatima al-Zahra 124. Myahudi wa Kimataifa
121
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 121
7/5/2013 9:06:19 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
125. Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi 126. Visa vya kweli sehemu ya Kwanza 127. Visa vya kweli sehemu ya Pili 128. Muhadhara wa Maulamaa 129. Mwanadamu na Mustakabali wake 130. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) 131. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) 132. Khairul Bariyyah 133. Uislamu na mafunzo ya kimalezi 134. Vijana ni Hazina ya Uislamu. 135. Yafaayo kijamii 136. Tabaruku 137. Taqiyya 138. Vikao vya furaha 139. Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 140. Visa vya wachamungu 141. Falsafa ya Dini 142. Azadari-Kuhuzunika na Kuomboleza 143. Sunnah katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah 144. Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu 145. Kuonekana kwa Allah 122
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 122
7/5/2013 9:06:19 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
146. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) 147. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) 148. Ndugu na Jirani 149. Ushia ndani ya Usunni 150. Maswali na Majibu 151. Mafunzo ya hukmu za ibada 152. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1 153
Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2
154. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 155. Abu Huraira 156. Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. 157. Mazingatio kutoka katika Qur’ani - Sehemu ya Kwanza 158. Mazingatio kutoka kaitka Qur’ani - Sehemu ya Pili 159. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza 160. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili 161. Qur’ani Tukufu – Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili 162. Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) 163. Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani 164. Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu 165. Uislamu Safi 123
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 123
7/5/2013 9:06:19 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
166. Majlisi za Imam Husein Majumbani 167. Mshumaa. 168. Uislam wa Shia 169. Amali za Makka 170. Amali za Madina 171. Asili ya Madhehebu katika Uislamu 172. Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi 173. Ukweli uliofichika katika neno la Allah 174. Uislamu na Mifumo ya Uchumi 175. Umoja wa Kiislamu na Furaha 176. Mas’ala ya Kifiqhi 177. Jifunze kusoma Qur’ani 178. As-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah 179. Hayya ‘Alaa Khayri’l-’Amal Katika Adhana 180. Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura 181. Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na Ramadhani) 182. Uadilifu katika Uislamu 183. Mahdi katika Sunnah 184. Jihadi ya Imam Hussein (‘as) 185. Kazi na Bidii ni njia ya maendeleo 186. Abu Talib – Jabali Imara la Imani
124
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 124
7/5/2013 9:06:19 AM
Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.)
187. Ujenzi na Utakaso wa Nafsi 188. Vijana na Matarajio ya Baadaye 189. Usalafi – Historia yake, maana yake na lengo lake 190. Ushia – Hoja na Majibu 191. Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) 192. Maombolezo – Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) 193. Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu 194. Takwa 195. Mwonekano wa Upotoshaji katika Hazina ya Kiislamu 196. Amirul Muuminina (‘as) na Makhalifa 197. Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.) 198. Kuelewa Rehma ya Mwenyezi Mungu 199. Mtazamo kuhusu msuguano wa kimadhehebu
MATOLEO MANNE YAFUATAYO YAMETAFSIRIWA KWA LUGHA KINYARWANDA 1.
Amateka Na Aba’Khalifa
2.
Nyuma yaho naje kuyoboka
3.
Amavu n’amavuko by’ubushiya
4.
Shiya na Hadithi
125
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 125
7/5/2013 9:06:19 AM
MUHTASARI
126
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 126
7/5/2013 9:06:19 AM
MUHTASARI
127
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 127
7/5/2013 9:06:19 AM
MUHTASARI
128
07_Uongozi na_05_July_2013.indd 128
7/5/2013 9:06:19 AM