Uwahabi kwenye njia panda

Page 1

UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

Mwandishi: Ayatullah Nasir Makarim Shirazi

Kimetarjumiwa na: Salman Shou

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 1

5/31/2016 7:38:06 PM


©Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 – 17 – 047 – 0 Mwandishi: Ayatullah Nasir Makarim Shirazi Kimetarjumiwa na: Salman Shou Kimehaririwa na: Al-Haj Ramadhani S. K. Shemahimbo Kimesomwa Prufu na: Al-Haji Hemedi Lubumba Selemani Kimepitiwa na: Mujahid Rashid Kimepangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation Toleo la kwanza: Oktoba, 2016 Nakala: 2000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. - 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: www.alitrah.info

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 2

5/31/2016 7:38:06 PM


YALIYOMO Utangulizi......................................................................................... 1 Neno la Mchapishaji........................................................................ 2 Dibaji ya Mchapishaji...................................................................... 4 Dibaji .......................................................................................... 7 SEHEMU YA 1:............................................................................ 9 Sababu za Kuangamia:..................................................................... 9 Ukatili uliopindukia....................................................................... 11 Jeshi la Masahaba (Sipah-e-Sahaba............................................... 11 Ukatili nchini Iraq.......................................................................... 20 Ukatili ndani ya Taifa lao wenyewe (Saudi Arabia)...................... 20 Mizizi ya Ukatili Iliyotiwa Kwenye Mafundisho ya Muasisi wa Uwahhabi.................................................................... 22 Ruhusa kufanya Ukatili.................................................................. 22 Ukatili na Shambulizi la Kutisha Kwenye Nguzo za Uislamu:.................................................................................... 29 Hitilafu za Kustaajabisha............................................................... 30 Tunatangaza Waziwazi.................................................................. .31

SEHEMU YA 2:.......................................................................... 33 Kulazimisha Imani......................................................................... 33 Kumbukumbu Isiyovumilika......................................................... 33 Wapo Kimya kwa sababu Hawana Jibu......................................... 36

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 3

5/31/2016 7:38:07 PM


Wajibu Mkuu wa Walinzi wa Nyumba ya Mungu......................... 37 Muundo Mbaya sana wa Kulazimisha Imani................................. 38 Wahhabi Wasomi na wenye mtazamo wa Kiasi............................ 42 SEHEMU YA 3:.......................................................................... 44 Ushabiki Uliozidi na Mbaya.......................................................... 44 SEHEMU YA 4:.......................................................................... 48 Kutokujua Thamani ya Utamaduni................................................ 48 Uharibifu wa Kumbukumbu za thamani za Uislamu..................... 48 Hitilafu Nyingine........................................................................... 50 Kwa nini Mahali Patakatifu pa Mtukufu Mtume  bado panadumishwa?..................................................................... 50 SEHEMU YA 5:.......................................................................... 53 Ukaidi katika kukubali bidaa yoyote............................................. 53 Hitilafu Nyingine........................................................................... 58 Sababu za kushindwa kwa Bin Taymiah........................................ 58 SEHEMU YA 6:.......................................................................... 64 Dhana Isiyo na Mantiki na Usahihi .............................................. 64 Kuhusu istilahi sita za Ki-Qur`ani................................................. 65 Ukosoaji na Uchambuzi................................................................. 66 Imani ya Ushirikina (Shirk)........................................................... 66 Ilah (Mungu).................................................................................. 71 Ibada ........................................................................................ 76

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 4

5/31/2016 7:38:07 PM


Uombezi ........................................................................................ 78 Kisingizio kisichofaa..................................................................... 82 Maombi (Du’a).............................................................................. 83 Hitimisho....................................................................................... 90 Bidaa ni ya aina tatu....................................................................... 90 SEHEMU YA 7:.......................................................................... 98 Miito ........................................................................................ 98 1.  Wito uliopazwa kutoka Makka............................................... 98 Yusuf bin Alawi na ukosoaji wake wa kijasiri............................... 98 Mapitio tahakiki ya kitabu hiki...................................................... 99 Maudhui ya kitabu hiki................................................................ 100 Eneo la kwanza............................................................................ 102 Eneo la pili…………………………………………................... 104 Eneo la tatu………………………………………….................. 105 Ukumbusho Muhimu................................................................... 106 A) Tabaka jipya la Wahhabi......................................................... 107 B) Hatari ya wakereketwa wa kupindukia................................... 109 2.  Wito mwingine kutoka kwa mwandishi mwingine jasiri...................................................................... 110 Kitabu “Mwanada’awa na Sio Mtume!”...................................... 110 Mukhtasari wa Kitabu “Mwanada’awana sio Mtume”................ 110 Sura ya kwanza:........................................................................... 117 Tahakiki ya “Kashf-ul-Shubahat”................................................ 117 Utiaji chuku na chumvi kuhusu Watukufu................................... 117

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 5

5/31/2016 7:38:07 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

Sura ya Pili:.................................................................................. 119 Tahakiki ya Al-Durarul-Saniyyah................................................ 120 Kukinzana katika maneno ya Sheikh........................................... 121 Sura ya Tatu:................................................................................ 122 Katika kufuatilia njia yake........................................................... 122 Sura ya Nne:................................................................................. 125 Mtazamo wa Waislamu................................................................ 125 Shutuma muhimu sana dhidi ya viongozi wa Uwahhabi!.................................................................................... 127 Neno la Mwisho! Tamko lililotolewa na Baraza la Ulama Waandamizi la Saudi Arabia likilaani uchokozi wa Mawahhabi........................................................... 129 Uchambuzi wa tamko la baraza la Ulama waandamizi (wanazuoni wa kidini) wa Saudi Arabia...................................... 134 Uchambuzi Mfupi wa tamko hili................................................. 136 Ushauri wa kirafiki kwa wanazuoni wa Kiislamu wa Hijaz........ 136

vi

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 6

5/31/2016 7:38:07 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬

UTANGULIZI

K

itabu hiki ni toleo la Kiswahili la taasisi ya Al Itrah Foundation. Chapisho lake limelenga kukidhi mahitaji ya kiroho ya zama hizi pamoja na Ubongo na fikra zinazokuwa za Muislam. Jitihada kubwa zimefanywa na Taasisi kuweka chapisho hili la Kiswahili katika msingi wa haki na wenye kukubalika katika Uislam. Unaombwa kwa Taadhima ukisome kitabu hiki katika malengo yaliyokusudiwa. Pia Unaombwa kuwasilisha kwetu maoni yako huru juu ya chapisho letu hili, jambo ambalo tutashukuru sana. Kutangaza ujumbe wa Uislam ni kazi ambayo inahitaji ushirikiano wetu sote. Taasisi inakuomba kuungana na kushirikiana kama ilivyoagizwa katika aya ya Qur’an: (Surat Saba’ 34:46). Na rehma za Allah ziwe juu yako. Wako katika Uislam Al Itrah Foundation Barua Pepe: alitrah@yahoo.com SMS: +255 778 300 140

1

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 1

5/31/2016 7:38:07 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬

NENO LA MCHAPISHAJI

K

itabu ulichonacho mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza kiitwacho, Wahhabism at the Crossroad, kilichoandikwa na mwanachuoni na mfasiri mashuhuri wa Qur’ani, Ayatullah Nasir Makarim Shirazi. Sisi tumekiita, Uwahabi kwenye Njia Panda. Sote tunaijua madhehebu ya Wahabi na jinsi ilivyojipenyeza hapa Afrika ya Mashariki kati ya miaka ya 50 na 60 na kueneza fitna kubwa miongoni mwa Waislamu na kufanikiwa kupandikiza chuki baina ya Umma huu wa Waislamu pamoja na kuwakufurisha wale wote ambao hawafuati itikadi zao. Leo Mawahabi wamekuwa ni wakiukaji wakubwa wa haki za binadamu kwa kuua watu hovyo na kuwakandamiza kwa mateso makubwa wale wote walio kinyume nao. Mwandishi wa kitabu hiki anajaribu kuchambua kwa kina uhalisia na udhalimu wa madhehebu hii potofu. Haihitaji kusoma sana ili kuwatambua wauaji hawa wanaotumia jina zuri la Uislamu ili kufikia malengo yao ya kidhalimu. Taarifa zao za ukatili zimeenea kila mahali ulimwenguni kiasi kwamba hata watoto wadogo wanawaelewa na kuwaogopa. Hii ni moja kati ya kazi kubwa zinazofanywa na Taasisi ya Al-Itrah katika kuwahudumia kielimu wasomaji wake wazungumzaji wa Kiswahili. Na kwa maana hiyohiyo imeamua kuchapisha kitabu hiki chenye hazina kubwa kwa lugha ya Kiswahili kwa lengo lake lilelile la kuwahudumia Waislamu hususan wanaozungumza Kiswahili. 2

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 2

5/31/2016 7:38:07 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

Hivyo, ni matumaini yetu kwamba wasomaji wetu watanufaika vya kutosha kutokana na kitabu hiki, kwani tumekiona ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni vitu ambavyo havina nafasi tena katika akili za watu. Tunamshukuru mwandishi wa kitabu hiki Ayatullah Nasir Makarim Shirazi kwa kazi kubwa aliyoifanya kwa ajili ya Umma huu wa Waislamu, Allah Azza wa Jallah amlipe kila la kheri na amuingize Peponi kwa salama na amani insha’Allah. Halikadhalika tunamshukuru ndugu yetu Salman Shou kwa kukitarjumi kwa Kiswahili kitabu hiki, insha’Allah na yeye Allah Azza wa Jallah amlipe kila la kheri hapa duniani na Akhera pia, bila kuwasahau na wale wote waliochangia kwa namna mmoja au nyingine mpaka kufanikisha kuchapishwa kwake. Allah awalipe wote malipo mema hapa duniani na Akhera pia. Mchapishaji Al-itrah Foundation

3

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 3

5/31/2016 7:38:07 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬

DIBAJI YA MCHAPISHAJI “Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwenye kurehemu, Mwingi wa Rehema.”

U

rithi wa thamani kubwa mno wa Nyumba (Ahlul-Bayt) ya Mtukufu Mtume (amani iwe juu yao wote), kama unavyotunzwa na wafuasi wao, ni madhehebu yenye maarifa mengi ambayo inakumbatia matawi yote ya elimu ya Kiislamu. Madhehebu haya yamezalisha wanazuoni wengi wazuri sana ambao wamepata msukumo kutoka kwenye rasilimali hii yenye neema nyingi na safi. Madhehebu haya yametoa wanazuoni wengi kwa Umma wa Waislamu ambao, kwa sababu ya kufuata nyayo za Maimamu wa Nyumba ya Mtukufu Mtume , wamefanya kadiri ya uwezo wao kuondoa mashaka ambayo yameletwa na itikadi mbalimbali na mawimbi ndani na nje ya umma wa Waislamu na kujibu maswali yao. Wakati wa karne zote zilizopita, wanazuoni hao wamekuwa wakitoa majibu yenye mantiki na ufafanuzi kuhusu maswali na mashaka hayo. Ili kuweza kufanikisha wajibu ambao limepewa, Baraza la Ahlul Bayt la Ulimwengu (ABWA) limeanzisha ulinzi wa utakatifu wa ujumbe wa Kiislamu na ukweli wake, ambao mara kwa mara hufichwa na wafuasi wenye ari wa madhehebu na itikadi mbalimbali na pia fikra za kileo ambazo ni adui wa Uislamu. Baraza hilo linafuata nyayo za Ahlul-Bayt  na wanafunzi wa madhehebu yao katika utayari wao wa kukabiliana na changamoto hizi na kujaribu kuwa katika mstari wa mbele katika kulingana na mahitaji ya kila zama. 4

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 4

5/31/2016 7:38:07 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

Hoja zilizomo katika kazi (vitabu) za wanazuoni wa Madhehebu ya Ahlul Bayt ni zenye umuhimu wa kipekee. Hiyo ni kwa sababu kazi hizo zimeegemezwa kwenye utaalamu halisi na kukubalika akili na huepuka upendeleo na chuki. Hoja hizi zinaelekezwa kwa wanazuoni na wanafikira katika namna ambayo inavutia akili zenye busara na asili ya binadamu kwa ujumla wake. Katika kuwasaidia watafutaji wa ukweli Baraza la Ahlul Bayt la Ulimwengu limejaribu kuwasilisha sura mpya ya hoja hizi zilizomo kwenye uchunguzi na tarjuma za kazi za waandishi wa Madhehebu ya Shia wa zama za leo na wale ambao wameyakubali madhehebu haya matukufu kupitia neema za Kimungu. Pia Baraza la Ahlul Bayt linafanya kazi ya kuhariri na kuchapisha kazi zenye thamani za wanazuoni mashuhuri wa Madhehebu ya Shia wa zama zilizopita katika kuwasaidia wale watafutao ukweli katika kugundua ukweli wote ambao Madhehebu ya Watu wa Nyumba ya Mtukufu Mtume  imeutoa kwa ulimwengu wote. Baraza la Ahlul Bayt linatarajia kunufaika kutokana na maoni ya wasomaji na ushauri wao na ukosoaji wenye kujenga katika eneo hili. Pia tunawaalika wanazuoni, wanaofanya kazi ya kutarjumi na taasisi zingine katika kutusaidia kutangaza mafundisho halisi ya Kiislamu kama yalivyolinganiwa na Mtukufu Mtume Muhammad . Tunamwomba sana Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka Sana, kukubali juhudi zetu duni na atuwezeshe sisi kuzidisha juhudi hizi chini ya usimamizi wa Imamu al-Mahdi, ambaye ni Mwakilishi Wake hapa duniani. (Mwenyezi Mungu Mtukufu auharakishe ujio wake). Tunatoa shukurani zetu kwa Ayatullah Nasir Makarim Shirazi, mwandishi wa kitabu hiki, na Mustafa Muhammadi, mtarjumi wa 5

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 5

5/31/2016 7:38:07 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

kitabu hiki. Pia tunawashukuru wenzetu ambao wameshiriki katika kufanikisha kazi hii, hususani wafanyakazi wa Ofisi ya Tarjuma. Kitengo cha Mambo ya Utamaduni Baraza la Ahlul Bayt la Ulimwengu

6

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 6

5/31/2016 7:38:07 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬

DIBAJI

A 1.

ina mbili za Wahhabi – Wakereketwa wa kupindukia na Wenye Mtazamo wa Wastani:

Wafuasi wa Madhehebu ya Salafi ambao wanao ukereketwa wa kupindukia na wenye msimamo mkali wanawachukulia Waislamu wote isipokuwa wao, kuwa ni Makafiri (Kafr) na Washirikina (Mushrik) na huchukulia kwamba kumwaga damu zao na kuchukua mali zao ni rukhsa. Ukaidi katika fikira, ukatili katika matamshi na vitendo na dharau kwa mazungumzo ya kimantiki na busara ni miongoni mwa tabia zao ambazo ni dhahiri kabisa.

Nchini Afghanistan, Iraq, Pakistan, na nchini mwao wenyewe, Saudi Arabia, unyama wao umeifanya dunia kuwachoka watu hawa. Sura yao mbaya ya Uislamu kama unavyowasilishwa na watu hawa duniani, itachukua miaka mingi ya jitihada kuzitengua. Matokeo yake, sasa hivi wamekaribia sana kwenye mwisho wa uwepo wao na baada ya muda mfupi watabaki kuwa ni historia. 2.

Mawahabi wenye msimamo wa wastani na walioelimika ni watu wa mantiki, mijadala na mazungumzo (Hiwar), na huwaheshimu wanazuoni wengine na huingia kwenye mazungumzo ya kirafiki na Waislamu wengine. Wala hawaamuru kuuawa mtu wala hawamchukulii Muisalmu yeyote kuwa mshirikina au kafiri, ama kufikiri ni ruhusa kuchukua utajiri na rasilimali za watu wengine. Kundi hili la Wahhabi hupata masapota kila 7

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 7

5/31/2016 7:38:07 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

siku. Haya ni mapambazuko mazuri kwa ulimwengu wa Kiislamu, ambayo ishara zake zinaonekana katika vitabu ambavyo vimechapishwa hivi karibuni nchini Hijaz, katika majarida na mazungumzo yao kwenye runinga. Kitabu hiki kitakupa maelezo ya kina kuhusu mambo hayo hapo juu.

8

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 8

5/31/2016 7:38:07 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬

SEHEMU YA 1 SABABU ZA KUANGAMIA

J

e Uwahhabi unakaribia ukomo wake?

Miaka kumi kabla ya kuvunjika kwa iliyokuwa Shirikisho la Kisovieti (Soviet Union), mwandishi wa kitabu kiitwacho: “The end of Marxism`s life” Kiswahili: “Mwisho wa uhai wa Umaksi,” aliandika: “Kwa jinsi nionavyo mimi, ni lazima tuukubali ukweli huu, ambao unaweza kuwa haupendezi na mchungu kwa baadhi ya watu, na wakustaajabisha kwa wengine, kwamba Umarksi - na zao lake Ukommunisti -unajongelea kifo chake na sasa hivi upo katika kuanguka. Kwa udhahiri zaidi, napaswa kusema Umaksi - kufuatana na mchunguzi mwanafikirahuru - ni mafundisho ya zamani ambayo hatimaye lazima yawekwe kwenye kumbukumbu za historia. Umaksi umetumia ustadi wake wote na umeshindwa katika kutimiza wajibu wake kwa mintarafu ya jamii ya wanadamu. Kimantiki na kifalsafa Umaksi si mafundisho ya kuchangamsha tena na ndoto walizokuwa nazo akina Marx, Angles na Lenin zilitafsiriwa vibaya au ziligeuzwa na kuonekana ni udanganyifu; na udhanifu wake kuangamizwa. Umaksi unaelekea kwenye kutengwa na kuvunjika vipande mbali na aina nyingi zinazotekelezwa katika nchi 9

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 9

5/31/2016 7:38:07 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

mbalimbali duniani kote. Umaksi wa Mao1 haufanani na Umaksi wa Brezhnev,2 na Ukommunisti wa Tito3 ni tofauti na Ukommuinisti wa Enver Hoxha,4 na hizi aina mbili zinatofautiana na tafsiri ya Fidel Castro, na zingine tatu hazihusiani nazo …”5 Kwa kweli, kama ilivyotabiriwa, Shirikisho la Kisovieti (Soviet Union) ya Umaksi, pamoja na madai yote makubwa kwamba Dola ya Ubepari ingeelekea kwisha baada ya muda si mrefu na Umaksi ungeshinda dunia yote, ghafla ulivunjika na kujumuika kwenye kumbukumbu za historia! Utabiri kama huo wala haukuwa ubashiri ama kubahatisha, lakini ni matokeo ya Umaksi wenyewe. Leo hii, ushahidi na uthibitisho wote unaashiria kwamba tegemeo kuu la muundo wa madhehebu ya Uwahhabi wenye msimamo uliovuka mpaka umefika mwisho wake na kupoteza watetezi na wafuasi wake kwa kasi kubwa. Leo hii, ishara za kuangamia huku zimekuwa za  ������������������������������������������������������������������������������� Mao Zedong (Desemba 26, 1893 - Septemba 9, 1976) (pia Mao Gi-dong katika mwandiko wa herufi kwa herufi wa Wade Giles) alikuwa kiongozi na mwandishi wa kijeshi na kisiasa wa Umaksi wa China, ambaye aliongoza Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) hadi ushindi dhidi ya Kuamintang (KMT) katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vya China na kupelekea kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China mnamo Octoba, 1, 1949 jijini Beijing. 2   Leonid Ilyich Brezhnev (Januari 1, 1907 - Novemba 10, 1982) alikuwa mtawala mwenye nguvu wa Soviet Union kuanzia 1964-1982, mwanzoni alikuwa akiongoza kwa kushirikiana na wengine. Alikuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha Soviet Union kutoka 1964-1982, na aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Supreme Soviet (Mkuu wa Nchi), mara mbili, kutoka 1960-1964 na kuanzia 1977-1982. 3   Josip Bros Tito (Mei 7, 1892 - Mei 4, 1980) alikuwa kiongozi wa Yugoslavia mnamo katikati ya mwisho wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia na kifo chake mnamo 1980. 4   Enver Hoxha (en-ver hoj-e) (Octoba 16, 1908 - Aprili 11, 1985) alikuwa kiongozi wa Kikomunisti nchini Albania kuanzia mwisho wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia hadi kifo chake. 5   Mwisho wa uhai wa Umaksi, uk. 10,11 kitabu hiki kama ambavyo imekwishatajwa hapo juu kilichapishwa mnamo 1360 (kufuatana na Kalenda ya Jua ya Uajemi) takribani miaka kumi kabla ya kuvunjika kwa Shirikisho la Kisovieti (Soviet Union) na kilichapishwa na taasisi ya “Nasl-e-Javan”. 1

10

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 10

5/31/2016 7:38:07 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

kuonekana dhahiri, kwa sababu kuna baadhi ya kanuni za misingi za tegemeo kuu la Uwahhabi wa msimamo mkali ambazo haziwezi kudumu katika ‘kijiji cha ulimwengu’ wa karne ya 21. Kanuni hizi ni kama zifuatazo: 1.

Ukatili uliopindukia

2.

Imani zinazolazimishwa kwa wengine

3.

Ushabiki uliokithiri

4.

Ukaidi wa kutokukubali jambo lolote geni

5.

Uelewa usio na mantiki na usahihi juu ya istilahi sita za Qur`ani Tukufu.

Ukatili uliopindukia: Ukatili wa Wahhabi wenye ukereketwa uliopindukia si kitu kilichofichikana kwa mtu yeyote. Mauaji ya kinyama ya halaiki ya Waislamu – sio wale wasioamini – yanayofanywa na ma-Wahhabi katika maisha yao yote ni ya kuogofya kupindukia. Mafuriko ya damu ya Shia iliyomwagika katika mji wa Karbala, uporaji wa mali na uharibifu ni mambo yanayokumbukwa na wote. Ya kushtusha zaidi ya hilo, ni mauaji ya kutisha sana na umwagaji wa damu wa wafuasi wa madhehebu ya Sunni huko Ta`if. Ukatili ndio msingi wa Madhehebu ya Wahhabi, na sababu yake ni utambuzi wenye dosari wa maana ya Kufuru (Kufr), Imani, Tawhid na Shirk. Wao humlaumu mtu yeyote kwa urahisi sana kwa imani ya ushirikina inayofuatiwa na dhana ya kanuni ya sheria yenye kunyambulika uruhusiwaji wa kutoa uhai na kupora mali. (Kama ilivyokuwa kwa madhehebu fulani ya Kikristo nchini Ujerumani yaliyodai kuwa 11

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 11

5/31/2016 7:38:07 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

Wakristo hawawajibiki katika kufuata sheria ya kimaadili mnamo 1535). Kiongozi wa Wahhabi anawachukulia Waislamu wa zama za leo kuwa ni wabaya zaidi kuliko makafiri wa zama za ujahiliya. Miongoni mwa matunda machungu ya mti huu usiostaarabika katika zama zetu ni “Taliban”, “Sipah-e-Sahaba”, na “Al-Qa`idah”, na tumeona sifa yenye kuchukiza inayochorwa na kila moja ya makundi haya katika akili za jamii ya ulimwengu, na madhara yaliyosababishwa kwa dini ya Uislamu inayoendelea kwa amani mno. Taliban: Kundi hili liliundwa na Mulla Mohammed Omari mnamo 1994, sehemu za kusini mwa Afghanistan katika mji wa Kandahar, na kutoka 1996 hadi 2001 walitawala sehemu kubwa ya Afghanistan. Afghanistan ilivamiwa na Shirikisho la Kisovieti (Soviet Union) na watu wa Afghanistan waliungwa mkono na Marekani (U.S.A.), kwa hiyo utawala wa Russia nchini Afghanistan haukudumu muda mrefu. Baada ya majeshi ya Urusi kuondoka katika miji ya Uzbek na Tajik mnamo 1986, makundi mengine madogo yalipata kiasi fulani cha nguvu. Ni wakati huu ambapo majeshi ya Taliban yalijitambulisha kwamba wao walikuwa Wanawaita watu kwenye Uislamu. Ambapo wao walitokana na asili ya Pashtuun, Taliban waliamua kuchukua udhibiti wa serikali na walikuwa wanaungwa mkono na kupewa silaha na Marekani! Mwanzoni mwa tapo hili maelfu ya vijana wakimbizi, yatima na watoto wa mtaani walijiunga na kundi hili. Hao Taliban walijitambulisha kama jeshi la amani! Watu wengi ambao zaidi walikuwa Pashtuun na ambao walichoshwa na vita na hali ya machafuko yaliyochukua nafasi kubwa nchini humo, waliunga mkono kundi 12

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 12

5/31/2016 7:38:07 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

hili, ambapo viongozi wengi wa Taliban walipata makuzi yao katika shule za Wahhabi. Taliban walianza mapigano mnamo 1994 katika sehemu za kusini na magharibi ya Afghanistan, na wakatwaa Kandahar, Herat, na miji mingine ya jirani. Mnamo 1995 walifika kwenye vitongoji vya Kabul lakini walirudishwa nyuma na majeshi ya serikali. Taliban waliendelea na mapigano hadi wakaitwaa Kabul mnamo 1996, baada ya kusababisha vifo vya watu 50,000! Burhanuddin Rabbani na Gulbadin Hikmatyar walikimbilia kaskazini mwa nchi kutafuta hifadhi. Baada ya Taliban kutwaa mji wa Kabul walimuua Mohammad Najib-Allah ambaye alikuwa anatawala Afghanistan kwa kuungwa mkono na Shirikisho la Kisovieti (Soviet Union). Mulla Mohammad Omari, ambaye alikuwa kiongozi wa majeshi ya Taliban, alianzisha Baraza la viongozi wa Taliban, alianzisha na kuweka fatwa za Wahhabi wenye ushabiki uliopindukia na hatua ya mwisho ya utekelezaji wa sheria ilikuwa chini ya uthibitisho wake tu! Kupitia redio ya Kabul na vipaza sauti vilivyosimikwa kwenye magari, Taliban walitangaza sheria zao kwa raia. Walifunga sinema na kumbi za maonyesho, wanamume walikuwa wanalazimishwa kwenda kuswali swala misikitini kwa kuchapwa viboko. Walifunga shule za wasichana, na waliharamisha ajira ya wanawake, matokeo yake pakawepo na upungufu wa wafanyakazi mahospitalini. Jambo hili lilifanywa wakati ambapo wanawake wengi walikwisha poteza waume zao waliokufa vitani na walikuwa hawana namna ya kujikimu kimaisha. Taliban walizuia kabisa elimu kwa wanawake, na walifanya kampeni dhidi ya aina yoyote ya maonyesho ya zama za leo hata 13

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 13

5/31/2016 7:38:07 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

kama yangekuwa na manufaa na ya kujenga kwa namna yoyote. Waliyaona yote hayo ni bidaa (bid`ah). Wakati waliwalaumu watu na hata kuwafunga jela wengine kwa kuacha kufuga ndevu ndefu, walihimiza kupanua mashamba ya bangi nchini Afghanistan na waliunga mkono umuhimu wa ulanguzi wa vitu vyenye dawa za kulevya, pamoja na kwamba walitangaza kwamba kuvuta sigara ni kinyume cha sheria. Na hii ilikuwa kwa sababu walipata mapato makubwa ya fedha kutokana na kilimo na ulanguzi wa bangi, na fedha hizo ndizo walizotumia kununua silaha ambazo zilitumika kuwaua ndugu zao katika imani. Hakuna anayejua jinsi walivyo halalisha hitilafu hii ya mambo ya kidunia inayohusiana na matokeo ya vitendo vyao; kwamba: ni haramu kuvuta sigara, ni lazima kufuga ndevu ndefu, lakini kilimo cha bangi na kulangua bangi ni halali! Bila ya mlolongo wowote wa kimahakama, Taliban waliwatesa watu na kuwachinja kama kondoo. Hayo yaliwapata Waislamu wa madhehebu ya Sunni na Shia; yeyote aliyewapinga alichinjwa. Kwa kuwa Osama bin Laden alifanikisha misheni nyingi mnamo miaka ya 1980 dhidi ya serikali ya Ki-Sovieti kwa manufaa ya Afghanistan, serikali ya Taliban ilitayarisha mahala salama kwa ajili yake. Na ilikuwa baada ya vita hii ndipo Osama bin Laden alianzisha kundi la “Al-Qa`idah�, ambalo lilifanya kazi kubwa katika kudumisha Taliban na liliwasaidia wao katika vita dhidi ya majeshi ya muungano ya kasikazini mwa Afghanistan. Bin Laden ni mtu ambaye Marekani ilikwisha mtambua kwamba alikuwa mtaalamu na alikuwa na kipaji cha ugaidi tangu aliposhambulia balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania mnamo 1998, na kusababisha vifo vya watu 250 na 190 na kujeruhi zaidi ya watu 1400! 14

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 14

5/31/2016 7:38:07 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

Kufuatana na msimamo wa Marekani, walidai kwamba shambulio la tarehe 11, Septemba, 1999, lilitekelezwa na Bin Laden, kwa hiyo ni dhahiri kwamba Marekani iliomba serikali ya Taliban kumpeleka Bin Laden nchini Marekani. Hata hivyo, Taleban hawakukubali ombi hilo, kwani Taliban walikuwa na deni kwa Bin Laden na walimchukulia yeye kuwa ni kiongozi wa maslahi yao. Mnamo mwezi wa Octoba mwaka huohuo Marekani na Uingereza wakaanza vita dhidi ya ugaidi na walielekeza mashambulizi yao kwa Taliban na Al-Qa`idah. Wakati Taliban walipokuwa kwenye kilele cha nguvu za kiutawala nchini Afghanistan, walipata uungwaji mkono kutoka nchi kama Pakistan, Saudi Arabia na Marekani. Hata hivyo, msaada huu haukudumu kwa muda mrefu. Chama cha Taliban kilihitaji dola za Kimarekani milioni 70 (milioni sabini) kila mwaka mnamo 1995 na 1996, ili kiweze kuendelea na shughuli zake. Kufuatana na jarida la India liitwalo “Strategic Analysis” Kiswahili: “Uchambuzi wa kistratejia,” sehemu kubwa ya bajeti hiyo ilikuwa ikitolewa na serikali ya Saudi Arabia. Jarida la “News Week” la Marekani liliandika katika mojawapo ya taarifa zake kuhusu suala hili: “Riyadh (serikali ya Saudi Arabia) ndiye mtoaji mkubwa wa fedha kwa chama cha Taliban.” Katika mojawapo ya safari zake za kuzulu Saudi Arabia, Mulla Mohammad Omari alifanya mazungumzo na maofisa wa ngazi za juu nchini humo, na serikali ya Saudi Arabia ilitoa dola za Kimarekani milioni kumi kama msaada kwa kundi lake analoliongoza ili waendeleze ukatili wao usio na mwisho. Hata hivyo, baadaye kila mtu aliigeuzia kisogo Taliban na utawala wa Taliban ulifurushwa kwenye kumbukumbu za historia16 6

Taarifa hii inapatikana kutoka kwenye maeneo yenye kupendwa na Umma na kwenye Majarida ya dunia. 15

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 15

5/31/2016 7:38:07 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

Kwa sababu ya ukatili wa kufedhehesha wa Taliban hakuna aliyejitokeza kuwatetea wakati waliposhambuliwa na Marekani, badala yake walisaidia katika kuanguka kwao, na pamoja na matatizo ambayo Marekani iliyasababisha kwa watu wa Afghanistan, raia wa Afghanistan waliiona Marekani ni afadhali kuliko Taliban, baada ya kutambua kwamba ukatili wa Taliban ulikuwa mkubwa zaidi kuliko wa Marekani. Jeshi la Sipah-e-Sahaba: Katika sehemu kubwa ya bara la India, wafuasi wa madhehebu ya Shia na Sunni waliishi pamoja kama ndugu katika Uislamu, hadi wakati madhehebu ya Wahhabi yenye ushabiki uliopindukia, wafuasi wake wakajisingizia kuwa ni jeshi la sahaba, wakaanza mauaji ya wafuasi wa madhehebu ya Shia wakimudu vilivyo kufanya mauaji ya kinyama. Walimwaga damu ya kundi hili la Waislamu wanamume, wanawake na watoto. Katika matukio fulani walisababisha malipizo ya kisasi na usalama ulikosekana kila mahali. Kufuatana na vyombo vya habari vya dunia, uundwaji wa kundi hili ulikuwa kama ifuatavyo: Jeshi hili linalodai kwamba ni wafuasi wa dini ya Mtukufu Mtume wa Uislamu  ni kundi lenye ushabiki uliopindukia, ambalo linajumuisha mojawapo ya madhehebu ya Sunni. Kundi hili lilianzishwa mwanzoni mwa miaka ya 1980 na mwanazuoni wa madhehebu ya Sunni, Maulana Haq Nawaz Jhangavi, wakati wa baada ya mapinduzi ya Iran yalipofanyika. Sababu ya kuunda kundi hili ilikuwa ni kuzuia athari za mapinduzi ya Kiislamu ya Iran kwa watu wa Pakistan. Madhumuni muhimu sana ya kundi hili yalikuwa ni kulaani sherehe za kumbukumbu za kifo cha Imamu Hussain ď ‚ na kuyaum16

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 16

5/31/2016 7:38:07 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

bua mapinduzi ya Imamu Khomeini. Jarida la “Khilafat-e-Rashid” lilitamka lengo hili mara nyingi katika kipindi chote cha uchapishaji wake, na liliiomba serikali ya Pakistan kufunga misikiti yote ya Shia na vituo vyote vya Shia, na kuzuia sherehe za kumbukumbu za matukio ya Ashura zisifanyike katika shule yoyote au chuo kikuu. Hata hivyo ombi hili kamwe halikukubaliwa na serikali ya Pakistan. Lengo jingine la kundi hili lilikuwa ni kukampeni dhidi ya kundi la Shia lililoanzishwa nchini Pakistan mnamo 1979 lililoitwa “Tehrik-e-Ja`faria”. Sababu nyingine kuu ya kuasisiwa “Jeshi la Sahaba” ilikuwa ni kuzuia tishio la kukua kwa nguvu ya madhehebu ya Shia katika jeshi, siasa na dini katika kanda hiyo. Kufuatana na takwimu zilizotolewa na Parvez Musharraf, watu 400 waliuawa kutoka katika makundi yote mawili katika kushambuliana kwao katika kipindi cha mwaka moja tu. Licha ya mashambulizi yao dhidi ya Shia, Jeshi hili la Sahaba liliwashambulia raia wa Iran waliokuwa wakazi wa Pakistan kwa kisingizio kwamba walikuwa wanaungwa mkono na serikali ya Shia nchini Iran ambayo lazima iondolewe. Lengo lao halisi lilikuwa ni kuifanya Pakistan itangazwe rasmi kuwa ni nchi ya Kiislamu ya madhehebu ya Sunni. Ngome ya kijeshi ya kundi hili ipo hasa zaidi katika mkoa wa kusini ya Pakistan, hasa zaidi katikati na sehemu zenye wakazi wengi za Punjab na sehemu za pembezoni mwa Karachi. Idadi ya vituo vya shughuli na ofisi za kundi hili ni zaidi ya 500, na katika kila wilaya ya mkoa wa Punjab lipo tawi la kundi hili. Takribani watu laki moja wamesajiliwa kama wanachama wa kundi hili na pia kundi hili limefungua vituo vya shughuli nchi za nje, kama vile: Falme za Kiarabu (United Arab Emirates), Saudi Arabia, Bangladesh, Canada, Yemen, India na kadhalika. 17

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 17

5/31/2016 7:38:07 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

Shule nyingi na seminari za theolojia katika mkoa wa Punjab zinaendeshwa na kundi hili na taarifa zilizopo ni kwamba shule nyingi za madhehebu ya Sunni nchini Pakistan, huendeshwa chini ya usimamizi wa walimu na wafanyakazi wa Jeshi la Sahaba, na kama sehemu ya programu yao, huwafundisha wafanyakazi wao kuua wapinzani wote. Maulana Jhangavi aliuawa mnamo mwaka 1990. Ni mwaka huo ndiyo alioshiriki katika uchaguzi wa kugombea kiti cha Baraza la Kitaifa (National Council) lakini hakuchaguliwa. Baada yake Maulana A`zam Tariq alishika nafasi ya kuongoza kundi hili. Jeshi la Sahaba liliungwa mkono na wanamgambo wa Taliban na Maulana A`zam Tariq alikuwa akisema hadharani kwamba yeye alikuwa anamuunga mkono kiongozi wa Taliban. Pia alitangaza kuharamisha sinema na runinga. Mwanzoni, A`zam Tariq alikuwa anaunga mkono Jeshi la Jhangavi (Lashkar-e-Jhangavi), lakini mnamo mwezi wa Februari, 2003, alikana ushirikiano wake na jeshi hilo, kwamba baadhi ya wanachama wachokozi wa Jeshi la Sahaba walichoshwa na chama chao cha amani kwa sababu ya kuweka sheria ya Kiislamu nchini humo, na kwa hiyo walianzisha Jeshi la Jhangavi. Lilisitisha ushirikiano wowote na wao mara moja A`zam Tariq alijulikana kwamba aliongoza mauaji ya viongozi mashuhuri wa madhehebu ya Shia takribani 103. Chanzo cha mapato ya fedha ya kundi hili wakati mwingine kilipatikana kutoka kwa matajiri wa madhehebu ya Sunni wenye ukereketwa uliopindukia wa Saudi Arabia na Ghuba ya Ajemi, na wakati mwingine vyama vya kiraia vyenye msimamo mkali kama vile “Jama`at-e-Islam” (Jumuiya ya Kiislamu), “Jamiatul Ulemae Islam” (Baraza la Ulama wa Kiislamu) na makundi mengine yaliyokuwa na imani inayofanana. 18

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 18

5/31/2016 7:38:07 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

Dola ya Pakistan iliamua kukomesha vyama vyote vyenye makundi yenye ukereketwa uliopindukia mnamo Augosti, 14, mwaka 2001. Miezi mitano baada ya uamuzi huu, kundi la Sahaba (Jeshi la Sahaba) lilikuwa bado linaendelea na shughuli zake za siasa kali. Matokeo yake Parvez Musharraf alitangaza kwamba shughuli za kundi hilo zimeharamishwa na akalishambulia kundi hilo na watu wengi walikamatwa mnamo Januari, 12, 2002. Baada ya tukio hili A`zam Tariq alianzisha tena shughuli za kundi hili kwa kutumia jina lingine, “Taifa la Kiislamu” (Millat-e-Islamiyah) na alipokea fedha nyingi sana kutoka kwa mapromota wake wa nchi za nje. Mnamo Novemba, 15, 2003 serikali ya Pakistan ilitangaza kwamba kundi hili lilikuwa haramu na ikawakamata wanachama wake wakuu, ikataifisha akaunti zake za benki na ikashambulia sehemu za mikusanyiko yao kwenye makazi yao, misikiti na sehemu zingine. Serikali ya Pakistan iliwahukumu watu 600 miongoni mwa wale waliokamatwa kulipa faini ya Rs. 100,000 kila mmoja, kwa lengo la kuzuia shughuli zozote za kundi hilo chini ya jina lingine katika siku za usoni. Mnamo mwanzoni mwa mwezi wa Octoba, 2001, “A`zam Tariq” alikamatwa. Wakati yupo jela alishiriki katika uchaguzi mkuu wa mwezi Octoba, 2001, na alichaguliwa kama mbunge wa kujitegemea wa Bunge la Shirikisho kutoka jimbo la Punjab na aliachiwa huru kutoka jela mnamo Octoba, 30, 2001. Miezi michache tu baada ya kuachiwa huru, alianza kuunga mkono serikali iliyochaguliwa ya Zafarullah Khan Jamali na akaendelea na vitendo vyake vya ukereketwa wa kupindukia dhidi ya wafuasi wa madhehebu ya Shia. Aliuawa mnamo Octoba 6, 2003. Baada ya kifo chake vikosi vya usalama viliwekwa katika hali ya tahadhari katika mkoa huo na siku 19

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 19

5/31/2016 7:38:08 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

iliyofuata wafuasi wake walifanya mazishi yake kwa hamaki kubwa mbele ya jengo la bunge. Baada ya hapo kundi hilo lilishambulia maduka, mahoteli na nyumba za sinema chache, na kuzichoma moto na kusababisha uharibifu mkubwa sana.7 Ukatili nchini Iraq: Katika miaka ya hivi karibuni, Wahhabi wenye msimamo mkali na ukereketwa wa kupindukia, walivuka mipaka yote ya ukatili nchini Iraq. Waliwachinja wanamume, wanawake, wazee, vijana, wafuasi wa Sunni, wafuasi wa Shia, na wa-Kurd. Ardhi ilitapakaa rangi ya damu ya wahanga na vipande vya miili yao (wahanga) ilitapakaa kwenye mitaa na majangwa. Walioshtushwa si Waislamu tu bali watu wote duniani walishtuka na kuogopeshwa na vitendo hivi vya kikatili na wakawa wanauliza kama watu hao walikuwa washenzi wenye kiu ya damu. Jamii ya dunia ilitamani kujua malengo yao yalikuwa nini na walikuwa wanatangaza dini gani. Baadhi ya watu wanasisitiza kuihusisha tabia hii ya kikatili na chama cha Ba`th. Fikra hii si sahihi kwa sababu mbinu ya mashambulizi ya kujilipua kamwe haikutumiwa na chama cha Ba`th. Shughuli hii inafanywa na Wahhabi wenye msimamo mkali ambao wanajifikiria kwamba wao kama Waislamu na wengine ni waabudu miungu mingi na washirikina ambao wao wanajipa ruhusa kuwaua. Ukatili Katika Nchi yao Wenyewe: Jambo la kushtusha na kuogopesha zaidi kuliko kitu chochote ni kwamba Wahhabi wenye msimamo mkali hawaoneshi huruma hata kwa Wahhabi wenzao, na wameeneza eneo la ukatili kwenye hali ambapo, kwa kutumia milipuko mingi sana katika jiji la Riyadh, 7

  Imechomolewa kutoka kwenye vyombo vya habari vyenye kupendwa na wengi na ­Ensaklopidia ya Encarta. 20

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 20

5/31/2016 7:38:08 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

Jeddah na mikoa mingine, wamewaua na kuwachinja kundi la raia wenzao wasio na hatia. Mnamo mwaka wa 1425 A.H. wakati wa Hijja, wahutubu wa swala ya Ijumaa walihutubia mikusanyiko mikubwa sana ya Waislamu. Walifanya mijadala mingi, walililaumu kundi hili, walilaani mwenendo wao wa kikatili na wakaanzisha kauli-mbiu “Hakuna kuwatangaza wengine kuwa ni waasi, hapana kufanya ugaidi.” Serikali ya Saudi Arabia ililazimika kuitisha kongamano muhimu (Irhab) dhidi ya “Ugaidi” na ilialika nchi mbalimbali kupanga na kuratibu mpango wa kukampeni dhidi ya ugaidi. Kwa hatua hii serikali ya Saudi Arabia ilitaka kujitoa kwenye lawama kwamba haina uhusiano wowote na kundi hilo na kutafuta njia inayofaa kukomesha ugaidi. Kwa bahati mbaya, hii ilisababisha Uislamu kuhusishwa na ukatili, na maadui wa Uislamu walipata kisingizio cha kuchafua dini kwa kiasi kwamba hadi leo hii katika nchi nyingi Waislamu wanatambulishwa kama jumuiya ya kujilipua. Kampeni ya udanganyifu ya Marekani, hususani Wazayuni, ilisaidia kutangaza suala hili, ambapo Uislamu ni dini ya amani, haki na huruma na upendo kwa wote. Sote tunajua kwamba zipo Sura mia moja na kumi na nne katika Qur`ani Tukufu na zote isipokuwa moja, huanza na jina la Mola wa Neema na Mrehemevu, ambalo linarejelea: Bismillah ar-Rahmanir Rahiim - Kwa Jina la Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu. Na tofauti ya ile Sura moja inahusiana na tangazo la vita dhidi ya wale waliovunja mkataba wa amani na Waislamu. Qur`ani Tukufu inamwambia Mtukufu Mtume  kwa dhahiri kwamba yeye hakuumbwa awe mkali na moyo mgumu kwa sababu tabia hiyo ingewafanya watu wamkimbie.

ۖ‫ك‬ َ ِ‫ب اَل ْنفَضُّ وا ِم ْن َحوْ ل‬ ِ ‫َولَوْ ُك ْنتَ فَظًّا َغلِيظَ ْالقَ ْل‬ 21

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 21

5/31/2016 7:38:08 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

“Lau ungelikuwa mkali mwenye moyo mgumu bila shaka ­wangelikukimbia.” (3:159)

Hadithi za Kiislamu zimejaa ufafanuzi wa dini kama huu, “Hivi dini ni kitu kingine chochote isipokuwa upendo?” 2 ; upendo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mtukufu Mtume  watu waadilifu, na viumbe vyote vya Mwenyezi Mungu Mtukufu; lakini vitendo vya Wahhabi vimewapatia kisingizio kibaya sana maadui ambao wanaudhalilisha na kuuchafua Uislamu. Mizizi ya Ukatili Iliyotiwa Kwenye Mafundisho ya Muasisi wa Uwahhabi: Naomba fursa ya kuwasilisha wasifu mfupi wa muasisi wa madhehebu ya Wahhabi kupitia maandishi ya mabingwa wa historia wa nchi za Mashariki na Magharibi. Kiongozi wa imani ya Wahhabi Mohammad bin Abdul-Wahhab alizaliwa mnamo mwaka wa 1115 A.H sehemu iitwayo Uyaynah, mji mdogo nchini Hijaz (Saudi Arabia ya leo) na alifariki dunia mnamo 1207 A.H. Baba yake alikuwa mmojawapo wa wanasheria wa madhehebu ya Hanbali, pia alikuwa ndiye mwalimu wake wa utotoni. Mwandishi wa kitabu kiitwacho “Ezalat-o-shobahat” ameandika: “Mohammad bin Abdul-Wahhabi aliathiriwa sana na Ibn Taymiyah na Ibn Zayyem Jawzi na wote hawa wawili waliishi katika karne ya nane, na alichomoa viambato vikuu vya fikra za watu hao wawili. Waandishi wengi wameandika kwamba baba yake alipata usumbufu kufuatana na fikra za mwanae huyu za mwanzo. Alitambua kwamba aina hiyo ya fikra ilikuwa na dosari kubwa mno ya kiitikadi, na akawa na wasiwasi kuhusu msimamo wake kiimani katika siku za usoni. Kwa hiyo baba yake alikuwa anamlaumu mara kwa mara kwa sababu ya ukorofi wake wa kiitikadi. 22

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 22

5/31/2016 7:38:08 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

Mohammad bin Abdul-Wahhab alisafiri hadi Makka na Madina. Alikaa huko kwa kipindi fulani na halafu alikwenda Iran na akachukua mafunzo kutoka kwa mwanazuoni mmoja aliyeitwa Mirza Jan-e-Isfahan. Halafu alikwenda Qum ambako alikaa kwa kipindi kifupi sana na akaendelea na safari yake hadi kwenye utawala wa Uthmainia nchini Syria na Misri, na hatimaye alirudi Najd katika rasi ya Arabia na kuanza kutangaza imani yake. Mwanzoni kundi fulani lilipinga fikra zake na likamfukuza kutoka Harimele, kwa hiyo alikwenda Ayineh. Habari za itikadi yake potovu zilifika kwa Suleiman bin Mohammad, mtawala wa Ehsa na Qatif, na alimuamuru Othman, gavana wa Ayineh, kumchinja, lakini kwa kuwa Othman hakutaka mikono yake kuchafuliwa na damu ya Mohammad bin Abdul-Wahhab, aliamuru mtu huyo afukuzwe mjini hapo. Hatimaye aliomba hifadhi katika mji wa Dar`iyeh. Gavana wa jimbo hilo alikuwa Mohammad bin Saud wa kabila la Ghanizeh. Sheikh Mohammad alikutana naye na akawasilisha itikadi yake kwake na akamchochea kwa matumaini kwamba, kwa msaada wake, angeweza kutawala Najd yote. Mohammad bin Saud, mhenga wa wafalme wa Saudi Arabia, alihisi kwamba angeweza kunufaika na uwepo wa Mohammad bin Abdul-Wahhab katika kupanua udhibiti wa nchi, kwa sababu alikusanya kundi kubwa la vijana wenye shauku na uchu ambao tayari walikwisha jihusisha naye na walikuwa wanatayarishwa na bin Saud kama jeshi la kufanikisha tamaa yake. Bin Saud aliahidi kumuunga mkono na kumtetea Sheikh kwa masharti mawili. Kwanza Sheikh asiwe na mawasiliano na mtu mwingine yeyote isipokuwa yeye tu, na sharti la pili ni kuendelea kupokea msaada wa fedha aliokuwa anapokea kutoka kwa watu wa 23

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 23

5/31/2016 7:38:08 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

Dar`iyeh! Sheikh alikubali sharti la kwanza lakini alikataa sharti la pili moja kwa moja na akasema: “Kwa matumaini ushindi mwingi na ngawira nyingi sana, ambayo ni zaidi ya fedha ya msaada kutoka Dar`iyeh, zitakuwa hazina yako.” Hata isisahaulike kwamba ngawira ambazo Sheikh Mohammad alikuwa anategemea zilikuwa kwanza kabisa ni utajiri wa Waislamu wa Hijaz, Makkah na Madina, na baada ya hapo, nchi zingine za Waislamu ambazo hazikumtii yeye, kwa sababu alimchukulia kila mtu isipokuwa wafuasi wake kuwa ni waabudu miungu mingi na alifikiri kwamba ilikuwa ruhusa yeye kuwaua na kuchukua rasilimali zao. Wafuasi wa Mohammad bin Abdul-Wahhab walishambulia miji kadhaa ya Hijaz, ikifuatiwa na mauaji makubwa, umwagaji damu na kupora mali kwa lengo la kutangaza imani ya Wahhabi, au kwa kweli, kupata nguvu kupitia na ushindi. Baada ya kifo cha Mohammad bin Abdul-Wahhab wafalme wa Saudi Arabia waliendeleza mpango wake na walipanua eneo la utawala wao, wakatawala Najd yote na Hijaz. Miongoni mwa vitendo vya kutisha sana ambavyo vimerekodiwa katika historia ya madhehebu ya Uwahhabi, na ambavyo pia wanahistoria wa madhehebu hayo wamekiri kwamba vilifanyika, ni mauaji ya kinyama ya watu wa “Ta`if”. Kitendo cha kutisha zaidi ya hivyo ni mauaji ya kinyama ya watu wa Iraq na Karbala mara kadhaa. Watu wengi miongoni mwa wakazi wa Karbala walikuwa wakizuru Najaf kama Ziyarahh kwenye Kaburi la Imamu Ali B1. Utawala wa Saudi Arabia ulifanya mashambulizi ya kushutukiza hapo Karbala. walivunja ukuta wa jiji, wakaingia mjini, wakaua maelfu ya watu kinyama kwenye mitaa na masoko bila kujali kama ni wanawake au watoto. Na wakapora mali yote waliyoona. 24

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 24

5/31/2016 7:38:08 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

Wakashambulia Kaburi la Imamu Husain , ambalo lilipambwa kwa vipande visivyohesabika vya ufundistadi bora sana. Wakaharibu Kaburi na wakachukua mapambo yote na vitu vya thamani. Baadhi ya watu wamearifu kwamba watu laki moja na hamsini elfu walikufa! Vijito vya damu vilitiririka kwenye mitaa ya Karbala, na sehemu ya kuvutia ni kwamba wao (Wahhabi) wanakiita kitendo hiki ‘Kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na kueneza ‘Tawhid’ katika ummah wa Waislamu!’ Matukio ya Karbala yameandikwa na wanahistoria wengi. Unaweza kufanya rejea kwa ajili ya maelezo ya kina kwenye kitabu kiitwacho “The history of the Arabian Saudi State” mwandishi: mwanazuoni wa mashariki ya kati Nasi Lif, na Miftah al-Karamah na Sayyid Jawad Ameli, na vitabu vingine ambavyo vimeandikwa kuhusu mada hii.8 Kwa vyovyote vile, Mohammad bin Abdul-Wahhab ameandika vitabu kadhaa vyenye maelezo mafupi ambamo ametaja waziwazi imani yake. Alikuwa na kisomo kidogo sana na alikuwa na elimu ndogo ya elimu za Kiislamu kwa sababu kamwe hakusoma kwenye seminari kubwa za Kiislamu na kwa wanazuoni mashuhuri wa zama za kale. Kwa sababu hii, mfumo wa imani yake ulikuwa na dosari kubwa sana na wenye makosa. Kwa bahati mbaya yeye alisisitiza kuendelea kwenye makosa ambayo alikwishaoneshwa na wanazuoni. Mojawapo ya vitabu vyake ni kinachoitwa ‘Kashif al-Shubuhat’ (Kuondoa shaka). Kitabu hiki kidogo kimeandikwa kwa lengo la kujibu ukosoaji ulioelekezwa kwake hasa zaidi na wanazuoni wa madhehebu ya Sunni.9 9

‫ عنوان المجد في تاريخ نجد‬,‫ تاريخ العربية السعودية‬,‫  تريخ المملكة السعودية‬8

Miongoni mwa wale ambao wameandika ufafanuzi wao ya tasnifu hii ni Muhaamad bin Sale Al-Othman )‫ ( محمد ابن صالح العشيمين‬ambaye kwa kiasi fulani alikuwa mtu wa kiasi na msomi lakini kwa bahati mbaya, ama kwa sababu ya tishio la kupoteza cheo 25

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 25

5/31/2016 7:38:08 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

Nukta zifuatazo zinatengeneza mfumo wa imani ya madhehebu ya Uwahhabi na zinatosha kuonesha chimbuko la ukatili lilianzia wapi: 1.

Muhammad bin Abdul-Wahhab alikuwa na dhana potovu ya Tawhid (imani ya uwepo wa Mungu Mmoja) na Ushirikina wa kuabudu miungu mingi (Shirk)3. Aliwaona wote wale wanaosihi maombezi kutoka kwa Mtukufu Mtume wa Uislamu  licha ya kutoka kwa Mola wao - ambayo yanaendana kwa dhahiri na Qur`ani Tukufu na Hadithi – kwamba ni kama makafiri na wabudu miungu mingi - Washirikina (Mushirk) na anafikiria kuwaua na kupora mali yao ni rukhusa, ni halali.

Kuwashirikisha miungu mingine na Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwa hakika Waislamu wote, pamoja na Shia na Sunni huomba msaada wa maombezi kutoka kwa Mtukufu Mtume  zaidi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwa hiyo uhai wao rasilimali zao na wake zao ni rukhusa kuuawa na kuporwa na Wahhabi! 2. Wahhabi wamekwenda mbali zaidi ya hapo kwamba wanasema kwa dhahiri: “Kwa sababu mbili waumini wa zama zetu ni wabaya zaidi kuliko wasiomini wa zama za Mtukufu Mtume , ambao alipigana dhidi yao. Kwanza, wasioamini wa zama za Mtukufu Mtume  walikimbilia kwenye miungu mingine na si kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu tu wakati walipokuwa katika hali ya raha, lakini kufuatana na Aya za Qur`ani Tukufu - walimuita Mwenyezi Mungu Mtukufu pale tu walipopatwa na majanga (kwa mfano walipokumbwa na ghasia ya mawimbi ya bahari.) chake au kudanganya )‫(تقيه‬, alijaribu kuwa mtetezi. 26

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 26

5/31/2016 7:38:08 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

‫صينَ لَهُ ال ِّدينَ فَلَ َّما نَجَّاهُ ْم إِلَى ْالبَ ِّر إِ َذا هُ ْم‬ ِ ِ‫فَإِ َذا َر ِكبُوا فِي ْالفُ ْل ِك َد َع ُوا للاهَّ َ ُم ْخل‬ َ‫يُ ْش ِر ُكون‬ “Na wanapopanda katika jahazi, humwomba kwa kumsafia dini, lakini anapowaokoa wakafika nchi kavu mara wanamshirikisha.” (Sura Al-A`nkabut, 29:65)

Lakini wasioamini (waabuduo miungu mingi) wa zama za leo hukimbilia miungu mingine isiyo Mwenyezi Mungu Mtukufu wakiwa katika hali mbili kwa pamoja, yaani wakati wa raha na wakati wa majanga. Pili, washirikina wa zama za Ujahiliya waliabudu sanamu ya mti na jiwe, vitu ambavyo vilikuwa viumbe vya Mwenyezi Mungu Mtukufu na vilikuwa vinamtii Muumba wao, lakini wasioamini wa zama za leo wanawaabudu wakosaji (inaonesha kama vile wanarejelea kwa baadhi ya Ulama wa Sufi)10 kwa hiyo damu yao, utajiri wao na wanawake zao kwa hakika zaidi ni halali yao. 3.

mwingine wa ukatili wao ni namna yao isiyo na heshima ya kuwaita kundi la wanazuoni mashuhuri wa madhehebu ya Sunni wakati wa mazungumzo, hutumia majina ya kuchukiza na kifedhuli, kwa mfano:

Ewe mshirikina11   Anasema: Tambua kwamba, Shirki ya watu wa mwanzo ni nyepesi zaidi kuliko Shirki ya watu wa zama zetu. Hiyo ni kutokana na mambo mawili: Jambo la Kwanza: Watu wa mwanzo hawakuwa wakimshirikisha Mungu na kuwaomba Malaika na Mawalii na masanamu isipokuwa wakati wa raha, lakini wakati wa shida walikuwa wakimuomba Allah kwa moyo mmoja. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu: ‘Wanapopanda katika merekebu…..’ Jambo la Pili: Watu wa mwanzo walikuwa wakiwaomba pamoja na Allah, watu waliowekwa karibu na Allah….ama watu wa zama zetu, wao wanawaomba pamoja na Allah, watu ambao ndio waovu zaidi kuliko watu wote. (Sharhu Kashfu Shubhat, Uk. 100). 11   Ufafanuzi wa Kashf al-Shubuhat, uk.77 10

27

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 27

5/31/2016 7:38:08 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

Maadui wa Mungu!12 Wasioamini wanayo mashaka mengine!13 Wale wasioamini majahilia!14 Maadui wa Tawhid15 Mtu mmoja mjinga na asiye na elimu anawashinda wanazuoni elfu moja wa wasioamini (Waislamu wanaoamini katika maombi -Shafaah)16 Kiongozi wa imani hii amepata elimu kidogo sana kutoka kwenye elimu za Kiislamu na inaonekana kwamba kwa sababu ya kukasirika baada ya kukosolewa na wanazuoni mashuhuri, huwaita wanazuoni hawa kwa majina mbalimbali mabaya na humshutumu kila mtu kuwa ni jahiliya, muabudu miungu mingi, mshirikina na asiyeamini, ambapo Qur`ani Tukufu inasema kwa dhahiri:

‫ض ْال َحيَا ِة ال ُّد ْنيَا‬ َ ‫َو اَل تَقُولُوا لِ َم ْن أَ ْلقَ ٰى إِلَ ْي ُك ُم الس اَ​َّل َم لَسْتَ ُم ْؤ ِمنًا تَ ْبتَ ُغونَ َع َر‬ “…..wala msimwambie mwenye kuwapa salaam: Wewe si muumini. Mnataka mafao ya duniani.....” (Surah Nisaa, 4:94).

Rukhusa ya kuendeleza Ukatili: Baada ya kufikiria hayo hapo juu inaweza kueleweka kwa nini Taliban, Al-Qa`idah na Wahhabi wengine wenye msimamo mkali hum  Ufafanuzi wa Kashf al-Shubuhat, uk. 79   Ufafanuzi wa Kashf al-Shubuhat, uk. 109 14   Ufafanuzi wa Kashf al-Shubuhat, uk. 120 15   Ufafanuzi wa Kashf al-Shubuhat, uk. 65 16   Ufafanuzi wa Kashf al-Shubuhat, uk. 68 12 13

28

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 28

5/31/2016 7:38:08 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

waga damu ya Waislamu wengine na kupora mali zao kwa urahisi katika sehemu mbalimbali duniani. Mauaji ya kinyama yaliyofanywa na Taliban nchini Afghanistan zaidi yalikuwa kwa Waislamu (kujumuisha Sunni na Shia) na mauaji ya kinyama yaliyofanywa na Al-Qa`idah na Wahhabi wenye msimamo mkali wa Pakistan na Iraq bila kufikiri, waliouawa wote ni Waislamu. Nani aliyesababisha makundi haya kukosa huruma? Ni mtu yuleyule aliyesema Waislamu wasio Wahhabi ni katika wasioamini na waabuduo miungu mingi, na akatangaza kwamba ni rukhusa (Mubah) Waislamu hao kuuawa na kuporwa mali zao. Haishangazi kwamba damu ambayo wamemwaga kwa kiwango kikubwa ni damu ya Waislamu na utajiri wote waliopora ni utajiri wa Waislamu. Ukatili na Shambulizi la Kutisha Kwenye Nguzo za Uislamu: Katika historia yote hakuna mtu ambaye amesababisha madhara kwa Uislamu kuliko Wahhabi wenye msimamo mkali, Uislamu ambao umekuwa ni dini ya rehema na huruma, dini ambayo inamshauri kila mtu anapotaka kufanya kila kitendo cha halali kuanza na jina la Bismillah Rahmanir Rahim;17 dini inayosema kwamba hata kama wasioamini wakikujia wewe kukuuliza maswali kuhusu Uislamu wape hifadhi ili kwamba waweze kusikia Aya za Qur`ani Tukufu, halafu wasindikizwe wafike salama kwenye makazi yao (hata kama wameukubali Uislamu au hapana);18 dini ambayo inawasihi sana watu kuonesha ukarimu kwa uchoyo ili kwamba maadui jeuri wawe wanaweza kushawishika na kuwa marafiki;19 dini ambayo huuliza:   Jambo lolote ambalo hufanywa bila kwanza kutaja jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kweli halina manufaa. (Tafsiir al-Bayaan, uk. 461. 18   Surah Tawbah, 9:6. 19   Surah Fussilat; 41:34. 17

29

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 29

5/31/2016 7:38:08 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

“Hivi dini ni kitu kingine chochote isipokuwa kupendana sisi kwa sisi?”20 Wao waliwasilisha dini (Uislamu) mkali na wa kuogofya sana ambao ulimfanya rafiki na adui kuchoshwa nao! Chimbuko la kweli la Uislamu siku zote ni kwamba upo tayari kutekeleza kazi yake na kuwafanya binadamu “Kuingia kwenye dini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu”21 makundi kwa makundi, lakini kwa bahati mbaya, vitendo vya kundi hili katili na lenye msimamo mkali vimekuwa tishio kwa uenezi wa Uislamu na Waislamu duniani kote. Ewe Mola wape mwongozo watu hawa! Hitilafu ya Kustaajabisha: Serikali yao ambayo imeingia kwenye utawala kwa msaada wa imani hii, imeanzisha uhusiano kisiasa kiuchumi na kiutamaduni na serikali zote duniani - za Kiislamu na zisizo za Kiislamu. Hii ni ishara kwamba wao ni marafiki wa wote wasioamini - waabuduo miungu mingi! Zaidi ya hayo, wamebadilisha Makkah yote na Madina yote kuwa mkusanyiko wa hoteli nzuri sana kwa ajili ya kuwafurahisha Waislamu waabuduo miungu mingi, ambao kila mwaka hutekeleza Hijja na Umrah huko Makkah na huhudumiwa kwa ukarimu mkubwa? Kwa nini? Unaona hawa Waislamu Waabuduo miungu mingi hujaza hazina yao. Qur`ani Tukufu inasema kwamba Wale Waabuduo miungu mingi sio safi, yaani ni Najisi (Najis) na ni haramu kuwaruhusu watu hao katika Masjid-ul-Haram, hata kama mnaogopa umasikini Mola atawatajirisha kwa fadhila Yake akitaka.   “Khisal,” kimeandikwa na Saduuq, uk. 21 (Imesimuliwa kutoka kwa Imamu Sadiq  – [Dini si chochote ila mahaba] 21   Surah Nasr; 110:2 (wataingia kwenye dini ya Mwenyezi Mungu makundi kwa makundi). 20

30

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 30

5/31/2016 7:38:08 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

‫ْج َد ْال َح َرا َم بَ ْع َد عَا ِم ِه ْم‬ ِ ‫يَا أَيُّهَا الَّ ِذينَ آ َمنُوا إِنَّ َما ْال ُم ْش ِر ُكونَ نَ َجسٌ فَ اَل يَ ْق َربُوا ْال َمس‬ ‫ٰهَ َذا ۚ َوإِ ْن ِخ ْفتُ ْم َع ْيلَةً فَ َسوْ فَ يُ ْغنِي ُك ُم للاهَّ ُ ِم ْن فَضْ لِ ِه إِ ْن َشا َء ۚ إِ َّن للاهَّ َ َعلِي ٌم َح ِكي ٌم‬ “Enyi mlioamini! Hakika washirikina ni najisi, kwa hivyo wasiukaribie Msikiti Mtakatifu baada ya mwaka wao huu. Na kama mkihofia umasikini, basi hivi karibuni Mwenyezi Mungu atawatajirisha kwa fadhila Yake akitaka. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye hekima.” (Surah AT-Tawba, 9:28)

Inakuwaje waabudu miungu mingi wanatokeza kuwa waumini wa imani ya uwepo wa Mungu Mmoja na hupokelewa kwa ukunjufu kwa upendo na huruma kama “Wageni wa Rahmaan”, na mikataba mikubwa na midogo ya kuwaazimisha nyumba zao?! Tunatangaza Waziwazi: Mwenye saini yake hapo chini, kama mja wa sayansi za Kiislamu, anasema kwa sauti ya juu na kwa dhahiri kwamba huu mchezo wa Wahhabi wa kuigiza Uislamu kwa namna yoyote ile si Uislamu wa kweli. Ni dhana ya watu binafsi ambao wana elimu ndogo ya elimu za Uislamu, na Ulama wa Kiislamu walio wengi wamepinga kwa pamoja kile kinachotangazwa na Wahhabi. Katika sehemu ya mwisho ya kitabu hiki tutafafanua kupitia na Aya za Qur`ani Tukufu zilizo wazi na hadithi za Kiislamu kuhusu walivyokosea dhana yao ili kwamba watu binafsi miongoni mwao ambao wanahisi wamefungwa kiwajibu na mantiki na hoja waweze kujua kwamba njia iliyonyooka ipo mahali pengine. Ningependa kumwomba kila mmoja kuungana pamoja na kutoa wito kwa sauti pana kwamba hili kundi dogo lenye msimamo mkali haliwasilishi Uislamu wa kweli. Ni dhahiri kwamba itikadi kama hiyo haiwezi kudumu katika dunia hii ya sasa, na ipo katika kupun31

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 31

5/31/2016 7:38:08 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

gua nguvu. Lazima tuwasilishe Uislamu ambao ni dini ya rehema katika dhati yake ya kweli ili iweze kukubalika na iweze kuendeleza mageuzi yake hapa duniani na kuathiri akili na nyoyo. La kushangaza zaidi kuliko chochote ni kwamba ukatili wa kundi hili hudhibiti serikali ambayo wao wenyewe ndiyo walioiweka kwenye mamlaka (serikali ya dhuria ya Saudi) na limeweka mauaji ya kutisha katika ufalme wa Saudi. Serikali ya Saudi Arabia imekiri kwamba wao mawahhabi ni tishio kwa raia wake na imeamua kuwazuia wafuasi wa madhehebu ya Wahhabi wasiendeleze ghasia. Serikali ya Saudi Arabia imefikiria upya mafundisho ya kidini ya madhehebu ya Wahhabi na imewahamisha Wahhabi wenye siasa kali na msimamo mkali wasipewe uongozi katika misikiti, hii ni hatua ambayo ni ishara nyingine ya mwisho wa madhehebu ya Wahhabi, kwa kuwa sasa madhehebu haya hayana nafasi hata mahali pale yalipoanzishwa.

32

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 32

5/31/2016 7:38:08 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

SEHEMU YA 2 KULAZIMISHA IMANI

U

islamu umeagiza kwamba ushirikiano wa madhehebu mbalimbali za Kiislamu zinazotofautina lazima ufanyike kupitia njia ya mazungumzo ya kirafiki na kimantiki tu, hata na wale wasio Waislamu:

ُ ‫ا ْد‬ ۚ ‫ك بِ ْال ِح ْك َم ِة َو ْال َموْ ِعظَ ِة ْال َح َسنَ ِة ۖ َو َجا ِد ْلهُ ْم بِالَّتِي ِه َي أَحْ َس ُن‬ َ ِّ‫يل َرب‬ ِ ِ‫ع إِلَ ٰى َسب‬ َ‫ض َّل ع َْن َسبِيلِ ِه ۖ َوهُ َو أَ ْعلَ ُم بِ ْال ُم ْهتَ ِدين‬ َ َّ‫إِ َّن َرب‬ َ ‫ك هُ َو أَ ْعلَ ُم بِ َم ْن‬ “Waite kwenye njia ya Mola Wako kwa hekima na mawaidha mazuri na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora. Hakika Mola Wako ndiye anayemjua zaidi aliyepotea njia yake na Yeye ndiye anayewajua zaidi walioongoka.” (Surah Al-Nahl, 16:125)

Na pia Anasema:

‫ب إِ اَّل بِالَّتِي ِه َي أَحْ َس ُن إِ اَّل الَّ ِذينَ ظَلَ ُموا ِم ْنهُ ْم ۖ َوقُولُوا‬ ِ ‫َو اَل تُ َجا ِدلُوا أَ ْه َل ْال ِكتَا‬ َ‫اح ٌد َونَحْ ُن لَهُ ُم ْسلِ ُمون‬ ِ ‫آ َمنَّا بِالَّ ِذي أُ ْن ِز َل إِلَ ْينَا َوأُ ْن ِز َل إِلَ ْي ُك ْم َوإِ ٰلَهُنَا َوإِ ٰلَهُ ُك ْم َو‬ “Wala usijadiliane na watu wa Kitabu isipokuwa kwa njia iliyo nzuri kabisa; isipokuwa wale waliodhulumu miongoni mwao. Na semeni: Tumeamini yaliyoteremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwenu. Na Mungu wetu na Mungu wenu ni Mmoja na sisi ni wenye kusilimu kwake.” (Surah Al-Ankabut; 29:46) 33

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 33

5/31/2016 7:38:08 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

Uislamu haumruhusu yeyote kumuita mpinzani kwa majina mabaya kama “jahiliya, waabuduo miungu mingi” “maadui wa Mungu” “maadui wa Tawhiid; na kujifikiria yeye kama mhimili wa Uislamu, na kushambulia kila kitu na kila mtu kwa madai ya kwamba Waislamu wenzao wanaotoa salaam wamewaweka kwenye kundi la wasioamini na wanaoabudu miungu mingi, kitendo kinachofanyika kwa ukatili katika vitabu vingi sana vinavyochapishwa na jumuiya hii. Waislamu wote wana kanuni zinazofanana katika mafundisho na imani ya Kiislamu, na wanazuoni wote wa Kiislamu, sheria zao za mambo ya mafundisho zinafanana pamoja na kwamba panakuwepo na upotovu katika kutafsiri kanuni fulani. Tofauti hizi katika fikra hazitakiwi kusababisha migongano, ugomvi na umwagaji damu; badala yake wanatakiwa kufanya mazungumzo yanayofaa kupitia fikra ya kimantiki na njia tulivu za kufikiri. Wahhabi (masalafi) wenye msimamo mkali wanapinga mazungumzo ya Kiislamu katika njia ya haki na kimantiki. Wao huamini katika kutekeleza dhana yao kwa kulazimisha katika mambo ya shiriki na tawhidi kwa wengine, hata kama utekelezaji huo unapatikana kwa njia ya kumwaga damu na kupora rasilimali, na uthibitisho wa hayo upo kwenye vitabu vya waasisi wa imani hii. Tunapowaambia wanazuoni wao kwamba kama wao wameelimika, na sisi pia tumeelimika, tena sisi tumeelimika zaidi kuliko ninyi, na tumeandika vitabu vingi zaidi kuliko ninyi. Kama ninyi ni Mujtahid,22 sisi pia ni Mujtahid. Wanazuoni waliosoma hapo AlAzhar na seminari za Damascus, Jordan na nchi zingine wanao mujtahid miongoni mwao. Kwa nini watu wengine walazimishwe kukubali imani yenu ambayo kufuatana na msimamo wetu imani hiyo 22

Mujtahid: Mwanachuomi ambaye ni mwanasheria wa shariah za kidini, ambaye anayo mamlaka ya kufasiri na kutoa fatwa za kidini kutokana na sheria za kimumgu. 34

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 34

5/31/2016 7:38:08 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

bila shaka ina dosari? Wao wanasisitiza kwamba kile wanachosema ndio Uislamu!! Wao wana manufaa gani kwa wanazuoni wengine wa Kiislamu kwamba nia yao ni kulazimisha utekelezaji wa imani yao kwa wanazuoni hao, na kwa nini huwachapa viboko watu wengine? Hawana jibu la kimantiki! Kwa dhahiri wao hudhani kwamba wapo kwenye kilele cha elimu na ucha Mungu, na kwa mtazamo wao kila mtu ameangukia kwenye kina kirefu cha ujinga. Hiki ni kitu ambacho hakuna mtu anayekipenda katika ulimwengu wa leo, na kitu hiki hakina nafasi miongoni mwa Waislamu. Ni kwa sababu hii sisi tunadai kwamba wao sasa wapo ukingoni mwa muhula wao katika dunia hii. Kumbukumbu ya Kusikitisha na Inayotia Uchungu! Siwezi kusahau miaka ya kwanza nilipojaaliwa kuzuru Nyumba ya Mungu, niliona tukio la kushangaza sana hapo Madina ambalo lilinifanya mimi nitafakari kwa kina sana. Kundi liitwalo “Makamanda wa maadili” (lililoundwa na Wahhabi wenye msimamo mkali) wenye ndevu lilizunguka kaburi la Mtukufu Mtume . Kila mmojawao alikuwa na kiboko mkononi mwake na kila mtu aliyesogea karibu ya kaburi la Mtukufu Mtume  alichapwa kiboko na kuambiwa: “Sanamu hii si lolote isipokuwa ni kipande cha chuma na mbao, hiki unachofanya wewe ni Shiriki!” Wao hawakutambua kwamba hakuna kiumbe mwenye mantiki anabusu mbao na chuma kwa sababu ya kitu hicho ni mbao au chuma, badala yake tabia kama hiyo ni kitendo cha ishara ya kuonesha utiifu, upendo na hisia kwa mintarafu ya mwenye kaburi hilo, kama vile ambavyo Waislamu wote, kujumuisha Wahhabi wenyewe, hubusu jalada la Qur`ani Tukufu, ambalo linaweza kuwa limetengen35

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 35

5/31/2016 7:38:08 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

ezwa kwa ngozi, kadibodi, nguo au ubao. Hivi kuonesha upendo na utiifu kwa Qur`ani Tukufu na Mtukufu Mtume  ni shiriki? Hakuna mantiki inayokubaliana na imani kama hiyo. Watu wote duniani hubusu bendera za nchi zao na huonesha heshima kwa bendera hizo. Hivi nia yao ilikuwa ni kuonesha utiifu kwa kipande cha nguo kisicho na thamani ambacho kilikuwa sehemu ya bolti iliyokerezwa, kipande ambacho kimekuwa bendera na sehemu iliyobaki ikashonwa mashati na suruali? Kwa hakika sio hivyo! Shauku yao ni kuonesha heshima kwa kujitawala kwa nchi yao na huo ni mfano wa uzalendo.23 Hivi yupo mtu yeyote anayefikiria kuheshimu nchi yake kwamba ni shiriki?! Kinachoshangaza ni kwamba Wahhabi wote huonesha heshima kwa mintarafu ya (Hajar-ul-Aswad) lile Jiwe Jeusi na kulibusu. Tunaposema kwamba hili si chochote isipokuwa ni jiwe na hatima yetu haipo katika uwezo wake, wao hujibu kwa kusema: “Mtukufu Mtume  alikuwa na tabia ya kubusu jiwe hili kwa hiyo sisi tunapobusu jiwe hili tunafuata sunnah yake!” Sisi husema: Hivi mnamaanisha kwamba Mtukufu Mtume  aliwaruhusu kutenda dhambi ya Shiriki, na hili ni jambo la pekee kwa hiyo ni aina ya Shiriki iliyoruhusiwa, au hasa kubusu jiwe hilo sio Shiriki? Wao hunyamaza kimya kwa sababu hawana jibu: Sisi tunatamka kwamba ninyi nyote huwa mnabusu ‘jalada la Qur`ani Tukufu’ na kuchukulia kwamba kitendo hicho ni cha kuonesha heshima kilichoruhusiwa. Hiki kipande cha ngozi na karatasi nene kina thamani gani kwamba mpaka mnakibusu? Wao 23

Safinat-ul-Bihar, chini ya chimbuko la neno; watwani (nchi ya nyumbani),

imesimuliwa kwenye hadithi kutoka kwa Imamu Ali  ambaye alisema kwamba: ujenzi wa taifa huja kupitia kuipenda nchi. Mizan-ul-Hikmah, Juz. 4, uk. 3566. Katika kuhama Mtukufu Mtume  kutoka Makkah kwenda Madina hadithi inayofanana na hiyo imesimuliwa katika al-Dar-ul-Manthuur Juz. 1, uk. 300.

36

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 36

5/31/2016 7:38:08 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

hujibu: Nia ni kuonesha hisia na heshima kwa mintarafu ya Qur`ani Tukufu! Sisi tunasema: Hivi hii haifikiriwi kuwa ni Shiriki? Wao hujibu: Masahaba wa Mtukufu Mtume  walikuwa na mazoea ya kubusu Qur`ani Tukufu.24 Sisi tunasema: Hivi Mtukufu Mtume  amewaruhusu ninyi kuwa watu wenye kuabudu miungu mingi? Pamoja na kwamba haiwezekani katika njia ya ushirikina kupambana na jambo la kipekee:

َّ‫ك لِ َم ْن يَ َشا ُء ۚ َو َم ْن يُ ْش ِر ْك بِ ه‬ َ ِ‫ك بِ ِه َويَ ْغفِ ُر َما ُدونَ ٰ َذل‬ َ ‫إِ َّن للاهَّ َ اَل يَ ْغفِ ُر أَ ْن يُ ْش َر‬ ِ‫الل‬ ‫َظي ًما‬ ِ ‫فَقَ ِد ا ْفتَ َر ٰى إِ ْث ًما ع‬ “Hakika Mwenyezi Mungu hasamehi kufanyiwa mshirika, lakini husamehe yasiyokuwa hayo kwa amtakaye. Na mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu hakika amezusha dhambi kubwa.” (Surah An-Nisaa, 4:48)

Mtanguo wa Shiriki ni amri safi ya kimantiki ambayo haitoi mwanya. Hawana jibu. Kwa ufupi, wao wamezama chini ya machafuko ya kuhitilafiana. Wajibu Mkubwa wa Watunzaji wa Nyumba ya Mungu: Sehemu Tukufu na Nyumba Takatifu ya Mungu ni sehemu za ­Waislamu wote duniani: 24

Katika Insaikolopidia ya Kuwait, kidahizo cha neno Taqbil tunasoma: ni maarufu miongoni mwa wafuasi wa Hanbali na pia wafuasi wa Hanafi kwamba kubusu Qur`ani Tukufu inaruhusiwa na imesimuliwa kutoka kwa Umar kwamba alibusu Qur`ani Tukufu kila siku asubuhi. Na pia imesimuliwa kutoka kwa Uthman kwamba alikuwa na mazoea ya kubusu Qur`ani Tukufu na kupangusa uso wake kwa Qur`ani Tukufu. 37

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 37

5/31/2016 7:38:08 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

ۚ ‫ي َو ْالقَ اَلئِ َد‬ َ ‫اس َوال َّش ْه َر ْال َح َرا َم َو ْالهَ ْد‬ ِ َّ‫َج َع َل للاهَّ ُ ْال َك ْعبَةَ ْالبَيْتَ ْال َح َرا َم قِيَا ًما لِلن‬ ‫ض َوأَ َّن للاهَّ َ بِ ُك ِّل َش ْي ٍء‬ َ ِ‫ٰ َذل‬ ِ ‫ك لِتَ ْعلَ ُموا أَ َّن للاهَّ َ يَ ْعلَ ُم َما فِي ال َّس َما َوا‬ ِ ْ‫ت َو َما فِي أْالَر‬ ‫َعلِي ٌم‬ “Mwenyezi Mungu amefanya Al-Kaaba Nyumba tukufu, kuwa ni kisimamo cha watu na miezi mitukufu na wanyama wa kuchinja na vigwe. Hayo ni kwamba mjue kuwa Mwenyezi Mungu anayajua yaliyomo mbinguni na yaliyomo ardhini na kwamba Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa kila kitu.” (Surah Ma`idah, 5:97)

Kila mtu kutoka karibu na mbali anatakiwa kunufaika kwa ulinganifu katika matumizi ya Nyumba ya Mungu;

ُ ‫َس َوا ًء ْال َعا ِك‬ ۚ ‫ف فِي ِه َو ْالبَا ِد‬ “…..kwa ajili ya watu wote sawa sawa, kwa wakaao humo na wageni…” ( Surah Hajj, 22:25).

Hivyo wajibu wa watunzaji wa Nyumba ya Ka`abah ni kuweka nidhamu na usalama, na kutoa viambajengo vinavyotolewa kwa mahujaji, si kukifanya kituo hiki cha Kiislamu kama sehemu ya kuhubiri imani na kulazimisha imani yao kwa wengine. Wao (Wahhabi) hawana haki ya kulazimisha kwa mahujaji ufahamu wao mahususi juu ya mambo ya Kiislamu ambayo yanapinga elimu (Ijtihad) na dhana za wanazuoni wa nchi zingine. Hata katika zama za ujahiliya, kazi ya wantuzaji ilikuwa si zaidi ya ile ambayo imetajwa katika Qur`ani Tukufu; viambajengo vinavyotolewa kwa mahujaji na kukarabati Msikiti Mtukufu:

‫ْج ِد ْال َح َر ِام‬ ِ ‫أَ َج َع ْلتُ ْم ِسقَايَةَ ْال َحاجِّ َو ِع َما َرةَ ْال َمس‬ 38

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 38

5/31/2016 7:38:08 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

“Je, mnafanya kuwanywesha mahujaji na kuimarisha msikiti mtukufu…..” ( Surah Tawbah, 9:19)

Kwa hiyo kama wanazuoni wa kanda hii wanayo maoni mahususi kuhusu suala la Tawhiid, hawana haki ya kulazimisha imani yao kwa wengine, hususani ambapo wanazuoni wengine mashuhuri Waislamu wanapofikiria kwamba ufahamu huo ni batili. Mathalani kundi hili linafikiri kuwa ni kufuru kule “kutaka uombezi - Shufaa” kutoka kwa Mtukufu Mtume wa Mungu  na ambapo maana yake ni kwamba huomba kwa niaba ya waja, ambapo wengine wanaona hili ni Tawhiid kamili. Mara nyingi wao huona kitu hiki ni Uasi wa kidini ambapo wengine hufikiria hilo ni sunnah. Sio Wahhabi au kundi lingine lolote, ambalo lina haki ya kulazimisha fikira na dhana zao juu ya wengine. Ninasisitiza nukta hii: wao wanalazimika kushughulika na nidhamu na usalama na kuimarisha sehemu hiyo tukufu, sio kufanya iwe kituo cha kuhubiri imani yao. Na inashangaza kwamba mfalme wa Saudi Arabia anajiona yeye kuwa ‘Mtumishi wa Sehemu Takatifu Mbili’ na si ‘mtawala wa Sehemu Takatifu Mbili’ hizo. Iweje wanazuoni wa Salafi-Wahhabi ambao ni wakereketwa wa kupindukia kujifikiria kuwa wao kama “watawala wa Sehemu Mbili Takatifu.” Ingawa wao wanaamini kwamba utii kwa Watawala wao ni lazima kwao. Kwa hakika lazima wazuie vitendo ambavyo vimeharamishwa kufuatana na makubaliano ya wanazuoni wa Uislamu. Kwa ufupi, ulazimishaji wa fikra unaofanywa na kundi dogo ambalo lipo kwenye kiwango cha chini cha elimu, kwa Waislamu walio wengi haukubaliki kimantiki. Hata hivyo, Salafi wenye msimamo mkali hutumia aina mbaya zaidi za mbinu katika kulazimisha itikadi yao kwa mahujaji, na hiyo ni bahati mbaya sana.

39

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 39

5/31/2016 7:38:08 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

Aina Mbaya zaidi ya Kulazimisha Imani: Wahhabi wenye msimamo mkali katika siku za hivi karibuni wameandika baadhi ya vitabu vinavyokataa baadhi ya kanuni za imani za Kiislamu na wakavisambaza vitabu hivyo kwa mahujaji. Vitabu hivi vimejaa lugha isiyo na adabu na msamiati mchafu, vyenye aina zote za uongo na kashifa. Vinawashutumu wengine kwamba ni washirikina wanamkufuru Mungu. Hii katika hali ambapo kama jibu moja tu la kimantiki na lenye upole likiandikwa kujibu vitabu hivi vyenye sura mbaya, haingewezekana kuruhusu kuchapisha hata toleo moja la vitabu hivyo. zo?

Hivi hii ndiyo maana iliyokusudiwa katika Aya Tukufu zifuata-

ۚ ُ‫فَبَ ِّشرْ ِعبَا ِد الَّ ِذينَ يَ ْستَ ِمعُونَ ْالقَوْ َل فَيَتَّبِعُونَ أَحْ َسنَه‬ “….. Basi wabashirie waja Wangu. Ambao husikiliza maneno, wakafuata mazuri yake zaidi. …..” (Surah Zumar, 39:17-18).

Ni dhahiri kwamba imani kama hiyo yenye utamaduni kama huo haina nafasi katika dunia ya leo, ambapo kufuatana na waonavyo wasomi, ni jambo lenye thamani muhimu sana kuheshimu imani ya watu wengine. Ukweli huuhuu umetayarisha uwanja kwa ajili ya kujitenga na kuanguka kwa imani hii, kwa sababu hakuna Muislamu anayeweza kuvumilia madai ya kuwa mshirikina na kafiri, ambayo watunzaji wa Nyumba ya Mungu wanatangaza waziwazi. Sehemu Takatifu ya Mtume na makaburi yaliyopo katika Baqi ni ya Waislamu wote na wajibu wa waangalizi hawa ni kuhakikisha mahali pale ipo nidhamu na usalama, kuwapa mahujaji viambajengo na kuzuia kile ambacho ni kinyume na maafikiano ya Waislamu wote, na si zaidi ya hayo. 40

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 40

5/31/2016 7:38:08 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

Ni lazima waheshimu imani ya Waislamu wote wa dunia na wajizuie katika kumkufuru Mungu na kutoa maneno ya dharau kuhusu mwambatano wao mtakatifu na wasijipanue hadi kuvuka mpaka, kwani si Mwenyezi Mungu wala Mja wa Mungu wanafurahishwa, na kitendo hiki hakina matokeo ya kusifika. Masikani salama ya Mungu lazima yawe salama kwa vyovyote vile. Ni aina gani ya usalama ambayo Waislamu ambao sio Wahhabi wakienda hatua moja mbele na huku nyuma wanashutumiwa kuwa wanamkufuru Mungu? Kamwe sitaweza kusahau ziara yangu ya kwanza kwenye Nyumba ya Mungu, nilipoona Waislamu kutoka nchi mbalimbali wanataka kubusu mimbari ya Mtukufu Mtume  na wakawakasirisha polisi. Wakala mmoja wa “wakufunzi wa maadili” alisimama na kutamka kufuru hii: “Ninaapa kwa jina la Mungu kwamba inaruhusiwa kulishambulia kundi hili kwa upanga (na kumwaga damu yao)” Kuna tofauti gani?! Ninyi mnabusu jalada la Qur`ani Tukufu na wao wanabusu mimbari ambayo kwa miaka mingi ilikuwa ni mahali pa uongozi na Mtukufu Mtume  wa Uislamu alikuwa anafundishia Qur`ani Tukufu hapo. Kwa nini unatoa amri ya kuuawa hawa wanaobusu mimbari ya Mtukufu Mtume  na si kwa wafuasi wenu?! Ninyi mnafikiria kitendo cha kubusu mimbari ya Mtukufu Mtume  kuwa ni uzushi katika dini lakini kitendo chenu ninyi ni ibada. Sasa tumeelewa kwa nini Taliban na Al-Qa`idah, ambao ni Wahhabi haohao ambao ni wakereketwa wa kupindukia, waliwaua watu mia moja na hamsini wasio na hatia na kuwajeruhi watu mia tatu, miongoni mwao wakiwepo watoto wadogo, watoto wachanga, wanawake na wazee huko Najaf (miaka miwili iliyopita). Haya ni 41

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 41

5/31/2016 7:38:08 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

matokeo yanayoumiza na machungu ya njia potovu ya kufikiri ambayo imeharibu taswira ya Uislamu hapa duniani na imefanya kuwa kila watakapokanyaga Waislamu hawatakuwa salama, hata katika ufalme wa Saudi, ambapo ni mahali pa chimbuko lao. Hivi itikadi kama hii inaweza kudumu?! Wahhabi Wasomi na wenye msimamo wa wastani: Hivi karibuni mwelekeo kwa mintarafu ya msimamo wa wastani na ishara za kutathimini tena fikira za nyuma umeonekana kutokana na serikali ya Saudi Arabia na baadhi ya Wahhabi wasomi na wanazuoni. Mwelekeo huu umeimarika barabara kabisa, kwa hiyo yapo matumaini kwamba mazungumzo na maelezo ya pande mbili baada ya muda si mrefu yatachukua nafasi ya migongano, vita, mifarakano, kashifa na lawama ya kukufuru Mungu na shiriki. Pamoja na kwamba hii haijafika kwenye kiwango cha kimataifa lakini mifano mingi sana inaashiria kuchipua kwa mti huu mchanga wenye ahadi Habari ambazo zimepokelewa ni kwamba baadhi ya Ulama wa Shia waliopo Hijaz (Saudi Arabia) wamekaa kwenye mazungumzo na baadhi ya wanazuoni wa Wahhabi wenye msimamo wa wastani na matangazo yao kutangazwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari. Jambo hili ndilo hasa ambalo Wahhabi wakereketwa kupindukia wanafikiria kuwa ni kumkufuru Mungu na uasi na wamekasirika sana kuhusu mwelekeo huu. Wao wanaona kuwa sasa huo ni mfumo wa kupindisha Uislamu, ambapo, kama mwenendo huu wa suluhu ya kirafiki, ambao unawaamuru Waislamu “kuzungumza kwa namna iliyo nzuri sana�, 1 ukivuka mpaka na kuwa wa ulimwengu wote, Uislamu utaondosha wagomvi kwa Waislamu wenzao na uwanja utaandaliwa kwa ajili ya 42

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 42

5/31/2016 7:38:08 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

taswira ya kweli ya Uislamu kuweka kiini chake duniani, Uislamu ambamo ipo mantiki, akili na mazungumzo ya kirafiki ndiyo utakao chukua nafasi ya ule wa mawasiliano na matusi, umwagaji damu na uporaji rasilimali, na Uislamu katika Hijaz utarudi kwenye njia yake ya kweli. Kundi la waandishi wenye msimamo wa wastani wa nchi hii wamepita kwenye njia hii na kupanga kalamu zao. Mathalani yupo mwanazuoni aitwaye Yousef-ibn-Alavi,25 hivi karibuni ameandika kitabu kiitwacho “Ideas that Need to be Re-examined and Corrected”2 yaani: “Mawazo yanayohitaji Kuchunguzwa upya na Kusahihishwa.” Kitabu hiki kinafikiriwa kama mojawapo ya maajabu ya aina yake na tunayo matumaini ya kukichunguza, Inshallah, mwishoni mwa kitabu hiki.

25

Yousef-ibn-Alavi ni mmojawapo wa wanazuoni wa Makka wenye kuheshimika na cheo cha juu ambaye alikuwa na seminari kubwa na amefariki dunia katika siku za hivi karibuni. Ameandika vitabu vya aina mbalimbali ambavyo vimewavutia watafiti wengi, miongoni mwa vitabu hivyo ni hiki cha “Mawazo yanayohitaji Kuchunguzwa upya na Kusahihishwa.” 43

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 43

5/31/2016 7:38:08 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

SEHEMU YA 3 USHABIKI ULIOPINDUKIA NA KWENDA UPANDE MWINGINE ­KABISA NA USIO NA HURUMA

U

shabiki uliopindukia leo hii umerejelewa kama ‘imani iliyotoka upande mmoja na kwenda hadi upande mwingine, au mwenendo unaohusiana na kitu.’ Ama kuhusu chimbuko au hapana, kuhusu suala la maadili, aina fulani ya desturi na mila ya taifa au jumuiya, au hata katika utetezi wa mtu mahususi. Amiri wa waumini Imamu Ali  amesema katika NahajulBalaghah katika Hotuba ya Kushusha hadhi amegawanya ushabiki uliopindukia katika aina mbili: ushabiki uliopindukia wa kujenga na wa kusifiwa, na ushabiki uliopindukia wa kukanusha na ulio haramishwa. Kuhusu ushabiki uliopindukia wa kukanusha anataja ushabiki uliopindukia wa Iblis ambao ulimzuia asimsujudie Adam. Imamu Mtukufu Ali  anamuita Iblis kuwa ni kiongozi wa wale wenye msimamo mkali katika viumbe vyote, na anasema: “Adui wa Mungu (Iblis) ndiye kiongozi wa wote wale wenye msimamo mkali na ishara ya wale wenye kiburi.” Na kuhusu ushabiki uliopindukia wa kudharaulika, anasema: “Endapo huwezi kuepuka kuwa na ushabiki uliopindukia, basi huo ushabiki wako uwe kwa ajili ya sifa ya uadilifu na vitendo vinavyofaa kusifiwa.”26 26

Nahjul-Balaghah, Hotuba ya 192. 44

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 44

5/31/2016 7:38:08 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

Ushabiki uliopindukia na wa kudharauliwa siku zote umekuwa ukihusishwa na ukaidi wa kiitikadi, mtazamo wa upande mmoja na kutoa hukumu isiyo na mantiki, na siku zote - hususani katika zama zetu - imekuwa sababu ya chuki na kurudisha nyuma maendeleo. Ishara ya aina hii ya ushabiki uliopindukia na kuchukua misimamo isiyo na huruma na iliyovuka mpaka, mara kwa mara ya kuchukulia kusihi umwagaji damu na kupora rasilimali, kuwadhalilisha wengine, na kukimbilia kwenye utetezi wa kutumia maneno machafu, hamaki na kushambulia. Waumini wenye msimamo mkali kama huo hawana thamani kwa maoni ya watu wengine, hawasikilizi hoja za wapinzani wao, na ni watu wenye dharau na majivuno. Yote haya yanaonekana kwenye matamshi na vitendo vya Wahhabi wenye ukereketwa wa kupindukia na pia kwa bahati mbaya kwenye vitabu vya kiongozi wa kundi hili. Sampuli ya tabia yao inaonekana dhahiri kutokana na ukweli kwamba kwa kisingizio kidogo sana huwaita Waislamu wenzao Watu Wasioamini au Waabudu miungu mingi: Washirikina na hufikiria kumwaga damu yao na kupora rasilimali zao ni halali. Wale wanaowaita wanazuoni mashuhuri wanaojitokeza kuwapinga kama “jahiliya” na kuwapa salaam kwa kusema: “Ewe mshirikina, na kumfikiria yeyote anayekataa kukubaliana na imani yao kuwa mlengwa wa mashambulizi, hivi daima wanaweza kuwa tayari kwa mazungumzo na maelezo ya kimantiki au ‘kujadiliana katika namna iliyo nzuri sana?” Qur`ani Tukufu haiwafikirii wale wenye msimamo mkali, ambao hawasikilizi maoni ya watu wengine, miongoni mwa waja wacha Mungu, kama Asemavyo:

45

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 45

5/31/2016 7:38:08 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

ۖ ُ َّ‫ك الَّ ِذينَ هَدَاهُ ُم للاه‬ َ ِ‫فَبَ ِّشرْ ِعبَا ِد الَّ ِذينَ يَ ْستَ ِمعُونَ ْالقَوْ َل فَيَتَّبِعُونَ أَحْ َسنَهُ ۚ أُو ٰلَئ‬ ‫ب‬ َ ِ‫َوأُو ٰلَئ‬ ِ ‫ك هُ ْم أُولُو أْالَ ْلبَا‬ “….. Basi wabashirie waja wangu. Ambao husikiliza maneno, wakafuata mazuri yake zaidi. Hao ndio aliowaongoza Mwenyezi Mungu, na hao ndio wenye akili.” (Surah Zumar, 39:17-18)

Qur`ani Tukufu inawaonya kabisa wale wanaoweka vidole vyao kwenye masikio yao wakati wa wito wa mitume waliopita na inadhihirisha malalamiko ya Nuh kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu:

‫صابِ َعهُ ْم فِي آ َذانِ ِه ْم َوا ْستَ ْغ َشوْ ا ثِيَابَهُ ْم‬ َ َ‫َوإِنِّي ُكلَّ َما َدعَوْ تُهُ ْم لِتَ ْغفِ َر لَهُ ْم َج َعلُوا أ‬ ‫صرُّ وا َوا ْستَ ْكبَرُوا ا ْستِ ْكبَارًا‬ َ َ‫َوأ‬ “Na hakika kila nilipowaita ili upate kuwaghufiria, walijiziba masikio yao kwa vidole vyao, na wakajigubika nguo zao, na wakakamia, na wakafanya kiburi kingi!” (Nuh; 71:7)

Mnamo siku za nyuma, nchini Saudi Arabia kila aina ya upinzani wa kimantiki, busara za kisayansi dhidi ya imani ya Wahhabi ulipigwa marufuku. Na sensa kali ilifanyika wakati huo, na bado inaendelea kuhusu uingiaji wa kitabu cha aina yoyote hata kinachotoka kwenye nchi ya Kiislamu kama Misri. Kitu chochote mbali ya kanuni hii, ni jambo la pekee. Kwa dhahiri, kamwe hawatatulia kutokana na hali yao ya ukaidi wala wakati wowote hawatafaidika na ukosoaji wa kimantiki ambao ungesaidia katika maendeleo yao ya kinadharia. Nukta ya kuvutia ni kwamba maktaba zetu sisi Shia zimejaa na zinafurika vitabu vilivyoandikwa na Ahlus-Sunna na Wahhabi na hatuhisi hatari yoyote katika imani yetu kwa sababu ya kuwepo vitabu hivi, ambapo ni vigumu sana kuona maktaba yoyote katika 46

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 46

5/31/2016 7:38:08 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

ufalme wa Saudi yenye vitabu vya Shia (hata kitabu kimoja) ukiacha vitabu vinavyohusu ukosoaji wa Wahhabi! Kwa nini wanaogopa sana na sisi Shia hatuna hofu kabisa? – Dhamira ya msomaji aliye mkweli, mwenye kujiheshimu itajibu swali hili! Siasa kali kama hizo kamwe hazipendwi katika zama zozote, achilia mbali wakati huu na zama za leo. Wanaounga mkono siasa kali kama hizi wanatakiwa kufungasha virago waende kwenye kumbukumbu za historia! Vijana wa ki-Wahhabi wanayo haki ya kuwauliza wazee wao kwa nini vitabu vya imani zingine za Kiislamu na pia vitabu vinavyohusu ukosoaji wa kisayansi na kimantiki kuhusu madhehebu ya Wahhabi havipatikani?! Hata hivyo kama ilivyotamkwa mwanzoni, tabaka la Wahhabi wenye msimamo wa wastani na walioelimika limeonesha kukubali mazungumzo, na hii ni hali ya mapambazuko yenye neema kwa ajili ya ulimwengu wa Kiislamu.

47

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 47

5/31/2016 7:38:08 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

SEHEMU YA 4 KUTOKUJUA THAMANI YA ­UTAMADUNI Uharibifu wa athari za ukumbusho za Kiislamu zenye thamani kubwa.

H

ivi inawezekana katika nchi chache kuwepo na athari za kale zinazohusiana na karne za mwanzo wa Uislamu kama ilivyo nchini Hijaz, ufalme wa Saudi Arabia ya leo? Inaeleweka kwamba hapo ni mahali palipozaliwa Uislamu, athari za ukumbusho za thamani sana za historia ya Uislamu zinaweza kuonekana kila mahali katika nchi hii. Sehemu takatifu na makaburi, mahali pa kuzaliwa, ushahidi wa viapo vya masahaba na wafuasi wao na alama zenye thamani sana za ukumbusho za Maimamu wa Nyumba ya Mtukufu Mtume , wanazuoni na mabingwa wa sheria (mafaqihi), na hata watawala na vituo vyao vya uhuru wao, kazi za kiusanifu majengo na kisanaa, na kadhalika, lakini Wahhabi wenye msimamo mkali wa kiimani na wenye uadui waliharibu ishara nyingi sana za ukumbusho miongoni mwa zile zilizokuwepo tangu mwanzo, wakitumia kisingizio kisicho na msingi kinachofanana na uthibitisho wa shirki! Na dalili za ukumbusho chache sana miongoni mwa zilizokuwepo zimebaki na inafaa kwamba Waislamu walie machozi ya damu, kwa ajili ya kuharibiwa kwa athari hizi zenye thamani. Leo hii, sote tunajua kwamba kila taifa, kwa ajili ya ushahidi wa chimbuko lake, hutegemea kwenye historia yake ya siku zilizopita, 48

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 48

5/31/2016 7:38:08 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

na huifikiria alama muhimu tangu siku za zamani kuwa ni uthibitisho na ushahidi wa jambo lao. Kufuatana na mtazamo huu, kwa uangalifu mkubwa huilinda alama zao za ukumbusho wa kihistoria. Lakini kundi hili liliharibu takribani alama zote za kihistoria ya Kiislamu na kubakisha michache sana katika nchi hii takatifu, na waliiharibu na kuondosha yote, alama za ukumbusho ambazo haziwezi kukadiriwa thamani yake. Mfano ulio dhahiri ni ule wa makaburi ya Baqii. Uwanja wa makaburi wa Baqii ni uwanja wa makaburi ambao ni muhimu sana katika Uislamu, ambao unashikilia sehemu muhimu ya historia ya Kiislamu na ni kitabu kikubwa na chenye maelezo mengi ya historia ya Waislamu. Makaburi ya wake, watoto na Maimamu wa Nyumba ya Mtukufu Mtume wa Uislamu , mabingwa wa sheria na wanazuoni mashuhuri, masahaba wa daraja la juu, mashahidi mashuhuri, mashujaa jasiri wa Uislamu, wote wamezikwa hapo Baqii; labda wanaweza kufika masahaba zaidi ya elfu kumi ambao wamezikwa hapo. Kwa maneno mengine, kipande kikubwa cha historia ya Kiislamu kimelala kwenye maficho ya hapo Baqii. Lakini leo hii, tunapoingia Baqii, utaona vunjiko la mahali hapo lisilopendeza kutazamwa, la kuchukiza na mikunjokunjo, bila ya jina lolote, bila alama au ishara inayoonekana, kitu ambacho kinasababisha mtu kutokwa na machozi. Wahhabi hawa wenye msimamo mkali na wakali, kwa bahati mbaya sana wameondoa alama hizi za thamani ya kihistoria kwa kutumia kisingizio kisicho na msingi cha “mapambano dhidi ya ushirikina” na wameuweka ulimwengu wa Kiislamu mufilisi wa historia, kitendo ambacho hakisameheki. Kwa kweli, hivi ndivyo muumini mwenye msimamo mkali anaweza kuwa wa hatari, na jinsi ambavyo anaweza kufuja rasili49

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 49

5/31/2016 7:38:09 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

mali zenye thamani sana za nchi, rasilimali ambazo ni haki ya kila mtu, watu wa leo, jana na kesho! Hitilafu nyingine: Kwa nini sehemu takatifu ya Mtukufu Mtume  bado inadumishwa? Kwa wale ambao wamefika Makkah na Madina, wanajua kwamba pamoja na uharibifu wa uwanja wote wa makaburi ya Baqii na makaburi ya mashahidi wa vita vya Uhud na mengineyo, kaburi na sehemu takatifu ya Mtukufu Mtume  bado ipo na Waislamu kutoka kila sehemu ya dunia hutamani kwa shauku kubwa kuzuru sehemu hiyo, mandhari hiyo huingiza swali muhimu sana katika akili zao: Kwa nini kundi hili halikuharibu sehemu takatifu ya Mtukufu Mtume ?! Ukweli ni kwamba wao walijiona ni wenye hasara kufanya kazi kama hiyo na kuifanya dunia yote ya Kiislamu kuwakasirikia wao. Kwa kweli Wahhabi wenye msimamo mkali walijaribu, lakini walishindwa kuondosha sehemu takatifu ya Mtukufu Mtume  na kubomoa lile Quba la kijani na kuteketeza kabisa Kaburi Tukufu. Walipoulizwa kwamba imekuwaje ambapo waliondosha sanamu na vyumba vya makaburi ambavyo vilikusanywa juu ya makaburi ya Maimamu hapo Baqii na mashahidi wa vita vya Uhud na wengineo katika uwanja huo wa makaburi, lakini wakaliacha Kaburi na Sehemu Tukufu ya Mtukufu Mtume  kama ilivyokuwa? Kuna maana gani ya hitilafu hii? Kama hizi ni alama za kuabudu masanamu na kuabudu miungu wengi kwa nini basi wamebakiza “alama hii mashuhuri mno” ambayo ipo karibu kabisa na Msikiti huu wa mtukufu sana na bora sana? Na kama hiyo si alama, sasa kwa nini wameondosha alama zingine? 50

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 50

5/31/2016 7:38:09 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

Hawana jibu kwa swali hili, na kwa kweli wanashikwa pabaya. Katika mojawapo ya safari zangu za kidini ambayo ilifanyika siku nyingi za nyuma, nilikwenda kumtembelea Imamu wa Madina, ambaye alikuwa nii mtu mwenye busara na mwaminifu na nilimuuliza swali hilo. Alijaribu kuvuta fikira zangu ili tuendelee na mazungumzo ya kitu kingine badala ya kujibu swali langu ambalo lilikuwa la kukasirisha na lisilo na jibu kwa kuanza kutoa maelezo ya tukio la kihistoria. Hadithi hiyo ilikuwa inahusu wakati wa Naser-ud-Dawlah, kuhusu Wayahudi wawili ambao walichimba mtaro kutoka kwenye nyumba zilizopo pembezoni mwa sehemu takatifu ili wafike kwenye kaburi la Mtukufu Mtume . Naser-ud-Dowlah aliota kwenye ndoto kwamba Mtukufu Mtume  alikuwa anamwomba amuokoe kutokana na hao watu wawili! Ndoto hii ilimjia mtu huyu kila usiku kwa siku kadhaa. Alishangaa ni kitu gani kilikuwa kinaendelea hapo Madina. Alikuja Madina na akawapanga watu wote wa hapo mjini, na akawaona watu hao wawili ambao alikuwa anawaona kwenye ndoto yake mara kwa mara. Aliagiza watu hao wakamatwe na akasitisha ukamilishaji wa mpango wao muovu. Halafu akawaelekeza watu wake kuchimba mtaro kuzunguka sehemu takatifu na kujaza chuma kilichoyeyushwa na kutengeneza ukuta wa chuma ili kwamba iwe hakuna mtu atakayethubutu kufanya kitu kama hicho katika siku za usoni. Jibu hili lingeweza kuhalalisha ujenzi wa sehemu ya chini ya kaburi tukufu, lakini halingeweza kuhalalisha ukarabati wa kaburi maalum la kuhifadhi maiti wa jamii moja, Sehemu Takatifu na Kaburi kubwa zuri. Hata hivyo, adabu na hisia kwamba mtu huyo hakuwa na lolote zaidi la kusema na angeweza kuhisi kufedheheshwa, hivyo nilijizuia kuendelea na mazungumzo hayo. 51

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 51

5/31/2016 7:38:09 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

Hivi karibuni imesikika kwamba mmojawapo wa Wahhabi wenye msimamo mkali amesema kwamba watabomoa Sehemu Takatifu na Kaburi kubwa zuri la Mtukufu Mtume  katika siku za usoni. Pamoja na kwamba usemi huu unaendana na misingi yao ya kinadharia ya ushabiki uliopindukia, ni hakika kwamba kamwe hawataweza kuwa na ubavu wa kufanya hivyo, hususani wakati ambapo Wahhabi wenye msimamo wa wastani wamejitokeza. Ni jambo la kushangaza kwamba baadhi ya watu wanahusisha usemi huu kwa kiongozi wa Wahhabi Mohammad ibn AbdulWahhab. Lakini amefikiria taarifa hii ni ya uongo katika baadhi ya usemi wake, pamoja na kwamba Hasan ibn Farhan Maleki kwenye kitabu chake “Ni Madai tu lakini sio Mtume” (Pretention and not a Prophet) anaamini kwamba rejea ya usemi huu: ‘Kama ninao uwezo, nitaharibu Sehemu Takatifu ya Mtukufu Mtume ’ upo kwenye maneno ya Sheikh Mohammad (Ibn-Abdulwahhab)!

52

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 52

5/31/2016 7:38:09 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

SEHEMU YA 5 UKAIDI KATIKA KUKUBALI BIDAA YOYOTE

M

uasisi wa imani ya Wahhabi alifanya kampeni dhidi ya aina yoyote ya uasi wa kidini, kitu ambacho kimsingi hakikukanushwa na madhehebu mengine ya Kiislamu, kwa sababu wote kwa pamoja walikataa uasi katika dini. Lakini muasisi wa imani ya Wahhabi alifanya kosa baya sana katika kufafanua maana ya uasi wa kidini, na kwa sababu hii aliongoza kampeni dhidi ya chochote kile kilichokuwa kipya. Nini maana ya uasi wa kidini? Hivi kila suala jipya ni uasi katika dini, kila ugunduzi mpya ni uasi katika dini? Hivi tunatakiwa kukampeni dhidi ya kila kitu kilichogunduliwa na binadamu na tuiite baiskeli ni chuma cha Shetani kwa hiyo tujizuie kuwa nayo, na nyaya za simu zinazounganisha ikulu ya mfalme wa Saudi na makao makuu ya jeshi la nchi hiyo zikatwe vipande vipande. Kwenye hadithi kutoka kwa Mtukufu Mtume  tunasoma: Waasi ni viumbe wabaya kabisa wa Mungu. Kanz-ul-Ummal, hadithi na. 10951. Na kwenye hadithi kutoka kwa Imamu Ali ď ‚ imesimuliwa kwamba alisema: (Uasi haukutokea isipokuwa pale ambapo ibada ilitelekezwa; Sharh Nahj-ul-Balaghah ya Ibn Abial-Hadid, Jz. 9, uk. 93; na hadithi zingine zinazofanana na hii kuhusu mada hii zinaonekana kwa wingi kwenye vitabu vya madhehebu zote.

53

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 53

5/31/2016 7:38:09 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

Wao waliiona kamera ya kupiga picha kuwa ni haramu na wakakataza kununua na kuuza kamera hadi hivi karibuni, na kiongozi wa Taliban Mulla Omari, kamwe hakutaka kupigwa picha. Alipinga kuelimisha wasichana na wanawake hata katika shule zake maalum. Alikataza wanawake kuendesha magari hata kama wamevaa Hijabu kamili. Alifikiri na akazuia kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtukufu Mtume  na matukio mengine yanayofanana na hilo kwamba ni uasi wa kidini! Wanalaani Waislamu wengine wote wa madhehebu ya Sunni na Shia kwa sababu ya kutekeleza kitendo hiki cha kimantiki na ubinadamu! Kwa hakika, kufuatana na mtazamo wa wanasheria-washauri mashuhuri na wanazuoni wa falsafa ya sheria 1, uasi wa kidini una maana tofauti. “Bidaa” ina tafsiri yake maalum, ambayo ni: “Bidaa maana yake ni kujumuisha kile ambacho hakitokani na dini na kukiingiza katika dini”273 Kwa hakika hakuna mtu ambaye hutumia ugunduzi mpya kama baiskeli, simu, kamera ya kupiga picha na kompyuta…… kwa kuwa ni jambo la wajibu1 au utekelezaji wa kidini uliopendekezwa2 lakini kama tu jambo la kawaida, kama vile aina mbalimbali za vyakula, nguo na majengo vitu ambavyo hubadilika kufuatana na mabadiliko ya wakati na hubadilika na kuwa kitu chenye muundo mwingine. Vitendo vingine ambavyo sisi huvitekeleza ni vitendo vya kawaida, ambavyo havihusiani na dini, vinavyofanana na mifano ili27

Bidaa maana yake ni kujumuisha kile ambacho hakitokani na dini na kukiingiza

katika dini Ghanaam al-Ayaam (‫ (غنائم اآليام‬Juz. 1, uk. 277 Katika al-Bihar alRaaq kilichoandikwa na mtu wa Misri (Ibn Najiim) bidaa ya kidini imefafanuliwa kama ifuatavyo: Matumizi yake yanaoongoza yamo katika kusababisha dosari au yale ambayo ni ya ziada katika dini na katika kitabu )‫ )فيض القدير‬kilichoandikwa na Mannawi imetajwa kama ifuatavyo: Tukio katika dini baada ya ukamilishwaji wake, na ufafanuzi wote huu unarejelea nyuma katika maana ya muunganiko. 54

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 54

5/31/2016 7:38:09 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

yotajwa hapo juu: tofauti katika mitindo ya mavazi, njia za usafiri, bidhaa za nyumbani, vyakula, ibada na tabia. Uzushi (Bid`ah) unaomaanisha mambo mapya yenye manufaa katika mambo haya kwa hakika ni kitendo cha kupendeza sana na ni ishara ya maendeleo ya ustaarabu wa binadamu. Kwa hiyo baiskeli wala si chuma cha Shetani au kamera ya kupiga picha si jicho la Shetani. Wala aina mbalimbali za simu si sababu ya upotovu na ufisadi, wala zile sherehe za kuadhimisha kumbukumbu za kuzaliwa watu mashuhuri katika dini hazifikiriwi kama ni dhambi. Sherehe ya kuzaliwa kwa kila mtu katika familia, mwanazuoni mashuhuri wa kidini, au maadhimisho makubwa kwenye kasri ya kumbukumbu ya kuzaliwa Mtufuku Mtume  na watu mashuhuri katika dini si dhambi. Hatuna sababu ya kuharamisha utekelezaji wa hayo hapo juu isipokuwa kutokuelewa maana ya uasi katika dini na kutokuwa na elimu ya kifalsafa ya sheria ya maana ya neno hili, na kuelewa vibaya mambo ya kimila kama ni fatwa za kidini. Hatuhusiki na sehemu takatifu na kaburi kubwa zuri la waasisi wa kidini tu, ambalo ni somo la mazungumzo mengine, lakini pia na viwanja vya kawaida vya makaburi. Nchini Saudi Arabia makaburi ni maeneo yenye sura mbaya sana na ya kuudhi yanayofanana na jangwa kame, miamba iliyopangana kama mbavu, yenye mikunjokunjo na isiyo na mpangilio, bila kuwa na hata jiwe moja lililonyooka juu ya kaburi lolote! Ujenzi wa kawaida wa makaburi ni kitendo cha kimila miongoni mwa mataifa yote na viumbe hai vinavyotekeleza mambo kimantiki hapa duniani, ambavyo hujaribu kujenga makaburi katika namna ambayo huweka heshima yao, na huzuia wasidhalilishwe na 55

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 55

5/31/2016 7:38:09 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

kukashifiwa waziwazi. Na kupanda mimea na miti kwenye eneo kwa lengo la kuleta utulivu na amani kwa masalia yao. Kwa washairi na waasisi katika elimu na usomi, vyumba vinavyofaa kwa maziko hujengwa kufuatana na heshima ya tabaka la marehemu, na kwa kila mtu kufuatana na nafasi yake. Hiki ni kitendo cha ubinadamu na cha kawaida. Kitendo hiki wala si uasi wa kidini ama imani ya kuabudu miungu wengi, ama kuabudu masanamu, lakini ni utaratibu wa kiheshima wa ubinadamu, ambapo, bidaa ya kidini1 iliyoharamishwa maana yake ni kuongeza kitu kwenye fatwa za kidini. Siku hizi kila mahali hapa duniani katika kila miaka mia moja hufanyika sherehe za kuadhimisha kumbukumbu ya viongozi, washairi, wagunduzi, na wanadamu mashuhuri ili kuwatia motisha vijana kwa mintarafu ya elimu na sayansi na maendeleo yake. Hivi mtu yeyote mwenye busara anaweza kuita kitendo hicho ni uasi wa namna yoyote, au ni ufuasi wa imani ya kuabudu miungu wengi, au kitu fulani kinaongezwa kwenye dini?! Hata hivyo, kama kitendo hicho kinafanywa kwa watu mashuhuri kidini kwa lengo la kuwavuta watu kwa mintarafu ya fikra zao, mafundisho yao na ajenda zao, na kutengeneza mapatano ya umoja baina yao, inawezekanaje kitendo hiki kiitwe uasi wa kidini na ufuasi wa imani ya miungu wengi? Desturi zilizoanzishwa upya wakati mwingine huwa zinaendana na mambo ya kidini na bila kuunganishwa nayo hupewa jina la uasi wa kidini. Kwa mfano leo hii tunaona minara mingi katika Masjidul-Haram na Masjid-ul-Nabi ambayo kwa hakika haikuwepo wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume . Mihrab28 ya Mtukufu Mtume  imepambwa kwa mitindo mizuri ya kisanii, na Aya nyingi za Qur`ani Tukufu zimeandikwa kwa kaligrafia nzuri sana kwenye uku28

Mihrabu shubaka la swala ndani ya Msikiti. Ni kitu ambacho kama alama inayoelekezea upande wa Ka`bah hapo Makkah. 56

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 56

5/31/2016 7:38:09 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

ta na ndani ya milango ya Msikiti wa Mtukufu Mtume . Jina la Mtukufu Mtume  na Maimamu  wote wa Nyumba ya Mtukufu Mtume  na baadhi ya sifa zenye umaarufu za Uislamu zinaonekana upande wa mbele wa viwanja vya Msikiti. Vyote hivi havikuwepo wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume . Kwa hiyo, vitu hivyo vinachukuliwa kuwa ni uasi wa kidini na vinaharamishwa? Kama jibu ni ndiyo, kwa nini basi Wahhabi hawaviondoi vitu hivyo vyote? Hata hivyo, vitu hivi vipo chini ya udhibiti wao, na kama si uasi wa kidini, sasa kwa nini hawaruhusu vitu kama hivyo mahali pengine? Kwa hakika hakuna mtu aliyeanzisha vitu hivi kwa nia ya kuvifanya sehemu ya fatwa za kidini, lakini vitu hivi ni matokeo tu ya mlolongo wa vitendo vya kawaida kwa ajili ya kuwapenda na kuwaheshimu watu. Wale ambao wanapinga utaratibu huu wa kijamii unaofanywa na Waislamu na wasio Waislamu, kwa sababu ya ukaidi wa kiitikadi, hawana nafasi katika dunia ya leo na lazima washughulikiwe haraka, hadi hapo ambapo kundi lenye msimamo wa wastani miongoni mwao lisahihishe na iwe kama malipo ya fidia kwa makosa haya makubwa. Tunarudia kusema kwamba uasi wa kidini uliokatazwa na haramu ni wakati ninapodai kwamba ninafanya kitu kwa kudhani kwamba kitu hicho ni fatwa ya kidini ambapo hakuna chochote kuhusu kitu hicho katika sheria za kawaida na sheria mahususi. Uasi wa kidini maana yake ni kuongeza baadhi ya sehemu katika swala au saumu au kaida za dini na taratibu zote za kawaida za Hijja au nidai kwamba dini imependekeza sisi kufanya sherehe ya kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtukufu Mtume wa Uislamu . 57

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 57

5/31/2016 7:38:09 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

Kwa bahati mbaya ukaidi na kutokuwa na taarifa ni mambo ambayo yamesababisha haya masomo mawili: “Kuanzishwa kwa mambo mapya” na “ uasi wa kidini” kutokueleweka. Hitilafu Nyingine: Miongoni mwa hitilafu za kustaajabisha za kundi hili ni kwamba watu haohao ambao, siku moja hufikiria baiskeli ni “chuma cha Shetani” na kufikiria matumizi yake kuwa ni uasi wa kidini, leo hii wanaendesha motokaa za mtindo wa kisasa za Kimarekani na Kijapani na hakuna mtu anayelalamika kuhusu wao kufanya hivyo. Na wale ambao, siku moja walifikiri ni kitendo cha uasi kutumia simu ya waya ya ikulu ya mfalme wa Saudia iendayo kwenye makao makuu ya jeshi na ilikuwa inafaa kukatakata waya huo, leo hii wanaonekana wanamiliki ‘Jawwal’ simu za mkononi! Hivi huu si ushahidi wa mgeuko wa nyuzi 180 unaotosha kuonesha kwamba fikra za Wahhabi zipo katika kufeli? Na jambo la ajabu ni kwamba serikali yao, ambayo haisikilizi fikra hizi zisizopenda mabadiliko, ipo mbele zaidi katika kusimamia maendeleo ya viwanda nchini humo, na imeshinikizwa katika kutegemea mapato yake kutokana na viwanda hivi. Sababu zilizopelekea Ibn Taymiah kufeli: Watu wenye ufahamu wanajua kwamba Imamu wa imani ya Wahhabi - kufuatana na yeye mwenyewe kukubali makosa - amekuwa akiketi kwenye meza ya Ibn Taymiyah. Ibn Taymiyah alikuwa na fikra kama za kwake kuhusu imani ya kuabudu miungu wengi, imani ya uwepo wa Mungu Mmoja, maombezi na kadhalika, lakini hakuweza kueneza fikra zake nchini Damascus (ambacho ndicho kilikuwa kituo cha shughuli zake) na hatari hii iliepushwa kutoka Syria, lakini mwanafunzi wake Mohammad Abdul-Wahhab alifaulu, kwa nini? 58

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 58

5/31/2016 7:38:09 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

Ni muhimu kuangalia kwa ufupi wasifu wa Ibn Taymiyah. “Ahmad ibn Abdul-Halim ibn Taymiyah Hanbali,” alizaliwa mnamo mwaka wa 661 A.H. na akafariki dunia mnamo mwaka 728 A.H. Alizaliwa katika mji wa Haran nchini Syria na kwa sababu ya utawala wa Tartar, aliondoka Haran akifuatana na familia yake na akaenda Damascus. Kwa kuwa alikuwa muumini wa imani ya Hanbali, aliamua kuhubiri imani hiyo na alishutumu sayansi ya Theolojia na akawafikiria wanatheolojia kama waasi! kuhusu somo la ubora wa sifa za Mwenyezi Mungu Mtukufu ambazo zimetajwa kwenye maandiko ya dini bila ya aina yoyote ya dharura. Kwa kuzingatia yote haya, alilaani aina yoyote ya falsafa mantiki. Aliunga mkono mbinu na kanuni za muhadithina na aliongeza kanuni zingine fulani kwenye taratibu ya maadili ya imani yao ambazo zilikuwa hazijasikika kabla yake. Mathalani, alisema kwamba nia ya kuzuru Sehemu takatifu ya Mtukufu Mtume , na kuomba idhini na kukimbilia kwa Watu wa Nyumba ya Mtukufu Mtume  kwa ajili ya maombezi, kitendo kile kilifanana na imani ya kuamini miungu wengi! Alikana sifa za watu wa Nyumba ya Mtukufu Mtume  ambazo zimetajwa kwa uwazi katika vitabu vya Ahlus-Sunnah na hata kwenye Musnad wa Imamu wake mwenyewe Ahmad ibn Hanbal na alijaribu, kama vile walivyofanya Bani Umayyah, kutweza hadhi na msimamo wa Imamu Ali  na dhuria wake. Lakini uchochezi wa Ibn Taymiyah haukukubaliwa na wanazuoni wa madhehebu ya Sunni, na isipokuwa wanafunzi wake wachache kama “Ibn Qaym”, wengine wote walipingana naye na waliandika vitabu vingi mbalimbali vilivyomfedhehesha yeye na uasi wake. Miongoni mwao alikuwa “Dhahabi” kutokana na wanazuoni wa zama zake mwenyewe ambaye alimwandikia barua ya kumlaumu na akamtaka akubali ukweli wa mapokeo. 59

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 59

5/31/2016 7:38:09 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

“Dhahabi” ameandika katika barua yake: “Sasa hivi upo katika muwongo wako wa saba wa maisha yako na muda wa wewe kuondoka hapa duniani unakaribia, hivi huu si wakati wako mwafaka wa kutubu na kuwa mtu aombaye toba?” Hakimu mwenye mamlaka ya juu wa madhehebu manne ya imani ya Sunni nchini Misri alitangaza kwamba fikra za Ibn Taymiyah ni zenye hitilafu na uzushi wa kidini. Lakini mnamo karne ya kumi na mbili, Mohammad ibn Abdul-Wahhab alitokeza na kuunga mkono fikra za Ibn Taymiyah, na alisisitiza sana fikra zake mpya. Zaidi ya imani hizo zilizotajwa hapo juu, Ibn Taymiyah alikuwa anaamini fikra zingine fulani. Mnamo mwaka wa 698 A.H.29, alikuwa na mazoea ya kuingia waziwazi katika mazungumzo ya kiitikadi, na kuhojiana na wapinzani wake. Rejea inafanywa hapa chini kama ifuatavyo kuhusu baadhi ya imani zake na misimamo yake:

29 30

1.

Alikuwa na mazoea ya kutekeleza mipaka ya kidini yeye mwenyewe.

2.

Alikuwa na mazoea ya kuwanyoa watoto nywele.

3.

Alikuwa tayari kupigana nao wale waliompinga.

4.

Aliwakataza watu kutoa sadaka kisheria.

5.

Aliamini katika uwezekano wa kumuona Mungu katika umbo la kimwili.

6.

Kuhusu Makhawariji aliandika: “Pamoja na kwamba Makhawariji walitengwa kwenye dini licha ya hayo walikuwa watu wa kweli sana katika dini!”30

Kufuatana na kalenda hii ya Mwezi ya Kiislamu sasa tupo katika mwaka wa 1437.   Kulikuwepo na kundi la watu waliokuwa katika jeshi la Imamu Ali  katika

vita vyake dhidi ya Muawiyah, lakini baadaye walimtenga Imamu Ali  na kuanza kupigana dhidi yake katika vita vijulikanayo kwa jina la Nahrawan, na 60

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 60

5/31/2016 7:38:09 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

Miongoni mwa vitendo vyake vya kujenga ilikuwa kwamba alifanya mapambano dhidi ya wa-Mongoli mnamo mwaka wa 702 A.H. Allamah Amini, baada ya kutaja shutuma zilizofanywa na Ibn Taymiyah katika kukataa hadithi ya “mwanzo wa wito wa Mtukufu Mtume ” (Waonye watu wa karibu yako, Surah Al-Shu`ara, 26:214) na kusema kwamba yeye hathibitishi ushahidi wa hadithi hii, anasema: “Hili ni tamko lililotarajiwa kutoka kwake kwa sababu yeye ni shabiki ambaye anasisitiza katika kukanusha ukweli ulio dhahiri na huwatenga Waislamu. Huyu ni mkali katika kukanusha lolote linalohusu sifa za watu wa Nyumba ya Matukufu Mtume ”31 Mahali pengine ameongeza: “Hii ndiyo sababu ya yeye kushutumiwa kwa mfululizo na Ulama mashuhuri wa madhehebu ya Sunni, miongoni mwao ni Shukani, ambaye anasimulia kutoka kwa Mohammed Bukhari Hanafi kwamba alimtenga yeye na kusema: “Yeyote anayemuita Ibn Taymiyah kwa cheo cha Sheikh wa Uislamu (Shaikh-ul-Islam), ni kafiri”32 Miongoni mwa wale wanaomuunga mkono kwa moyo wote Ibn Taymiyah alikuwa ni Ibn Kathir, mwandishi wa kitabu kiitwacho “Al-Bidayah and Al-Nihayah” (alikufa mwaka wa 744 A.H), ambaye amemtetea na kumsifu Ibn Taymiyah katika kitabu chake chote. Miongoni mwa Ulama wa wakati wa uhai wa Ibn Taymiyah, mmoja ambaye amemtetea na matokeo yake amedharauliwa na jumuiya yake ni mhafidhina Abu Al-Hajjaj Mezi, mwenye kitabu kiitkatika vita hivyo wote walipelekwa jahannam na Imamu Ali  na jeshi lake.

Al-Ghadir, Juz. 2, uk. 280 32   Al-Ghadir, Juz. 1, uk.247 (kwenye tanbihi) 31

61

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 61

5/31/2016 7:38:09 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

wacho “Tahdhib ul-Kamal,” ambaye alifariki dunia mnamo mwaka wa 742 A.H. Miongoni mwa wanafunzi wa Ibn Taymiyah ni Ahmad ibn Mohammed Meri Lebli33 ambaye kufuatana na asemavyo Ibn Hajar, alikuwa anampinga Ibn Taymiyah mwanzoni, lakini baada ya kumtembelea akawa rafiki yake na mwanafunzi wake na aliandika maandiko yake na akamtangaza na kumuunga mkono katika ‘suala la kukataza ruhusa ya kusafiri kwa ajili ya kuzuru Kaburi kubwa la Mtukufu Mtume . Hatimaye, jaji Ikhnayyee wa Maliki alimuita mahakamani na akamchapa viboko sana, hivyo kwamba mwili wake wote ukatapakaa damu na halafu akawaagiza wafanya kazi wampandishe kwenye mgongo wa nyumbu kichwa chini miguu juu na kumzungusha mjini kwa lengo la kumfedhehesha. Mwanafunzi mashuhuri sana na anayemuunga mkono kwa bidii Ibn Taymiyah, bila shaka alikuwa Ibn Qayyim Al-Jauziyah, ambaye katika matangazo yote na imani alikuwa na mwambatano na utetezi, na aliwajibika na uchapishaji na uenezaji wa imani ya Ibn Taymiyah wakati wa uhai wake na baada ya kifo chake. Alikuwa akienda jela na Ibn Taymiyah mara kwa mara, na kwa sababu hii tu walimchapa viboko na kumfedhehesha na kumzungusha mjini akiwa juu ya ngamia, na halafu wakamfunga jela na Ibn Taymiyah katika bandari ya Damascus.34 Sasa tunarudi tena kwenye mada kuu ya mazungumzo, ambayo ilikuwa ni: kwa nini Ibn Taymiyah hakufaulu kupanga dhifa ya Salafi   Ahmad ibn Mohammed Meri Lebli: Na kwa ajili hiyo, amekuwa ni shabaha ya mishale ya ukosoaji wa maulamaa wakubwa wa ki- Ahlus Sunnah tangu ulipodhihiri upotovu wake mpaka leo hii. Yakutosha kauli aliyoisema Shawkani katika kitabu al-Baduru atwaliu Jz. 2, uk. 260: Muhammad Bukhari Mhanafi aliyefariki mwaka wa 841 ametamka wazi kuwa (Lebli) alikuwa mzushi wa mambo. Kisha alimkufurisha na akawa anatamka wazi katika vikao vyake kwamba: Yeyote atakayemuita Ibn Taymiyyah kuwa ni Sheikhul-Islam basi ajue uitaji huu ni wa mtu kafiri. 34   Imekusanywa kutoka vyanzo mbalimbali, kwa rejelea tazama kwenye bibliografia. 33

62

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 62

5/31/2016 7:38:09 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

nchini Syria, lakini Mohammed ibn Abdul-Wahhab aliweza kufanya hivyo katika mkoa wa Najd, na pia aliweza kueneza mpango huo katika rasi yote ya Arabia na akaandika imani hizi katika historia chini ya jina lake chini ya jina la “Uwahhabi.” Palikuwepo na sababu mbili kuu kwa ajili ya hilo: Kwanza, Damascus ilikuwa mojawapo ya vituo vya elimu ya Kiislamu katika zama hizo, na kituo hiki kilikuwa na wanazuoni mashuhuri wengi sana na seminari za Kiislamu nyingi sana; pamoja na kwamba alikuwa amepata idadi ya kutambulika ya wale waliokuwa wanamuunga mkono, fikra za Ibn Taymiyah zilizoeleweka vibaya, zilipingwa vikali. Na pamoja na kwamba alikuwa amepata watu wengi wa kumuunga mkono, walibomoa ufuasi wake kwa hoja za kimantiki, ambapo wakati huo mkoani Najd hapakuwepo wanazuoni mashuhuri wengi, vituo vya sayansi ya Kiislamu na seminari za Kiislamu…na kwa hiyo, mashaka ambayo yaliingizwa na kundi hili hayakukutana na upinzani mkubwa. Hivyo basi, kwa haraka yalienezwa miongoni mwa watu wa kawaida. ‘Kila mkoa ambao ulikuwa na wanazuoni na wanasayansi ulibaki salama kutokana na madhara ya kundi hili.’ ‘Zaidi ya hayo, zama hizo palikuwepo na mapambano ya kweli ya mamlaka miongoni mwa makabila ya Najd. Kufuatana na historia ya sasa Mohammed ibn Abdul-Wahhab alinufaika kutokana na mazingira haya na akaandikiana mkataba na wahenga wa ufalme wa Saudi Arabia kwamba wao watangaze fikra zake, na yeye Mohammed ibn Abdul-Wahhab angeawaunga mkono wahenga wa ufalme wa Saudi Arabia wapate ushindi katika mapambano yao na makabila mengine ya kushika mamlaka.’

63

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 63

5/31/2016 7:38:09 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

SEHEMU YA 6

K

Uelewa usio na mantiki na usio sahihi kuhusu utambuzi sita wa Qur`ani Tukufu:

iini kikuu cha imani hii kipo kwenye suala la Tawhiid na Shirk ambayo inapatikana kutoka kwenye imani za Ibn Taymiah Damishki. Mohammed ibn Abdul-Wahhab katika mazungumzo marefu ya Kashf-ul-Shubahat amewasilisha suala lake kuhusu mazungumzo haya, ufupisho wake ni kama ifuatavyo: 1.

Tawhiid - Imani ya uwepo wa Mungu Mmoja ambayo Uislamu umetangaza ni Umoja katika Ibada, kwa sababu Waarabu waliokuwa wanaabudu miungu wengi waliamini katika Umoja wa Muumbaji na walitangaza kwamba ulimwengu wote uliumbwa na Mungu.

‫ض لَيَقُولُ َّن َخلَقَه َُّن ْال َع ِزي ُز ْال َعلِي ُم‬ َ َ‫َولَئِ ْن َسأ َ ْلتَهُ ْم َم ْن َخل‬ َ ْ‫ت َو أْالَر‬ ِ ‫ق ال َّس َما َوا‬ “Na ukiwauliza: Nani aliyeumba mbingu na ardhi? Bila shaka watasema: Kaziumba Mwenye nguvu, Mjuzi.” (Surah Al-Zukhruf, 43:9)

Na mahali pengine Anasema:

ُ ِ‫ض أَ َّم ْن يَ ْمل‬ ‫صا َر َو َم ْن ي ُْخ ِر ُج‬ َ ‫ك ال َّس ْم َع َو أْالَ ْب‬ ِ ْ‫قُلْ َم ْن يَرْ ُزقُ ُك ْم ِمنَ ال َّس َما ِء َو أْالَر‬ ْ‫ت َوي ُْخ ِر ُج ْال َميِّتَ ِمنَ ْال َح ِّي َو َم ْن يُ َدبِّ ُر أْالَ ْم َر ۚ فَ َسيَقُولُونَ للاهَّ ُ ۚ فَقُل‬ َّ ‫ْال َح‬ ِ ِّ‫ي ِمنَ ْال َمي‬ َ‫أَفَ اَل تَتَّقُون‬ Sema: Ni nani anayewaruzuku kutoka mbinguni na ardhini? Au ni nani anayemiliki usikizi na uoni na ni nani amtoaye hai kutoka maiti 64

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 64

5/31/2016 7:38:09 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

na akamtoa maiti kutoka aliye hai na ni nani anayedabiri mambo yote? Watasema ni Mwenyezi Mungu. Waambie: Basi je hamuwi na takua?” (Surah Yunus, 10:31)

Kufuatana na Aya hizi Waarabu waliokuwa wanaabudu miungu wengi, mmoja tu na ni Mungu tu ndiye Muumba wa ulimwengu na mwenye Kufadhili waja Wake na Msimamizi na Mpangaji wa dunia. Sasa basi kwa nini wao walikuwa wanaabudu miungu mingi? Tatizo lao moja tu lilikuwa ni Umoja katika Ibada, maana yake ni kwamba wao waliabudu masanamu na baadhi ya watu waadilifu. Kwa maneno mengine, Waarabu waliokuwa waabudu miungu wengi kamwe hawakukanusha Umoja wa Muumba, Mfadhili na Mola wa walimwengu, lakini wao walikuwa wanaabudu miungu wengi katika ibada ya Mungu Mmoja na kwa njia hii Uislamu uliwaita katika kumwabudu Mungu Mmoja tu. 2.

Fikra ya Imani ya kuabudu miungu wengi ina maana kwamba binadamu huomba msaada kwa kitu kingine cha kiroho badala ya Mungu Mmoja na kukimbilia kwenye hifadhi ya kitu hicho kwa ajili ya kutatua matatizo (mathalani wakati anapomuita Mjumbe wa Mungu  au Imamu Ali , kama isemavyo Qur`ani Tukufu:

‫فَ اَل تَ ْد ُعوا َم َع للاهَّ ِ أَ َحدًا‬ “…….basi msimuombe yoyote pamoja na Mwenyezi Mungu” (Surah Al-Jinn, 72:18)

3.

Kama mtu anatafuta maombezi kutoka kwa Mtukufu Mtume wa Uislamu  au kutoka kwa kiongozi yeyote mkubwa na watu waadilifu, kitendo chake hiki ni kitendo cha kuabudu miungu wengi! Uhai wake na rasilimali zake ni halali ya wale 65

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 65

5/31/2016 7:38:09 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

Wamuabuduo Mungu Mmoja! Kwa sababu yeye ni wale wanaoabudu miungu wengi na ni halali kumwaga damu yake, kuchukua rasilmali, mke wa kila anayeabudu miungu wengi. Qur`ani Tukufu inashauri:

ُ ‫قُلْ للِهَّ ِ ال َّشفَا َعةُ َج ِميعًا ۖ لَهُ ُم ْل‬ َ‫ض ۖ ثُ َّم إِلَ ْي ِه تُرْ َجعُون‬ ِ ‫ك ال َّس َما َوا‬ ِ ْ‫ت َو أْالَر‬ “Sema: Uombezi wote uko kwa Mwenyezi Mungu. Ni wake ufalme wa mbingu na ardhi. Kisha mtarejeshwa Kwake.” (Surah Az-Zumar, 39:44)

4.

Zaidi ya hayo, wakati waliposhutumiwa Waarabu waliokuwa wanaabudu masanamu, walisema:

ِ َّ‫َما نَ ْعبُ ُدهُ ْم إِ اَّل لِيُقَرِّ بُونَا إِلَى للاه‬ “….Sisi hatuwaabudu ila wapate kutujongeza tu kumkaribia Mwenyezi Mungu…..” (Sura Al-Zumar, 39:3).

Na Mtukufu Mtume  kamwe hakukubali madai yao. Hivyo wao waliabudu masanamu si kwa sababu masanamu hayo yalikuwa Waumbaji au Wafadhili, lakini ni kama waombezi tu. Hivyo mtu yeyote aliyekifikiria kitu kingine zaidi ya Mungu kama mwombezi alikuwa kama Waarabu waliokuwa wanaabudu masanamu na damu na rasilimali yake vilikuwa halali!! Haya yalikuwa maelezo yao mafupi ya matamko yao kuhusu suala la Imani ya uwepo wa Mungu Mmoja na imani ya kuabudu miungu wengi. Ukosoaji na Uchambuzi: Katika hali halisi, chanzo cha Uwahhabi katika vitabu vyao mbalimbali kuhusu imani ya uwepo wa Mungu Mmoja na imani ya kuabudu 66

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 66

5/31/2016 7:38:09 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

miungu wengi ni aya chache tu ambazo zimetajwa hapo juu, ambazo zinarejelea kila mahali, na zinajaribu kukwepa Aya zingine za Qur`ani kwa urahisi, na kufikiria aya hizo kama vile hazionekani, hivyo kuwa wachaguzi kabisa kwa mintarafu ya Qur`ani Tukufu. Zaidi ya hayo, ili kuweza kuwavunja nguvu wanazuoni wapinzani, ambao hufichua makosa yao kupitia Aya zingine za Qur`ani Tukufu, wao hudai kwamba Aya zote ambazo watu wengine huzirejelea katika kukanusha fasiri hii ya imani ya uwepo wa Mungu Mmoja na imani ya kuabudu miungu wengi, zote ni Aya zenye utata! Katika uchambuzi mfupi, fasiri isiyo sahihi na yenye makosa ya “maneno sita ya Qur`ani Tukufu” imemsababishia yeye kuwafikiria Waislamu wote isipokuwa wafuasi wa imani yake kama watu wanaoabudu miungu wengi. Kwa nini hawataki kukaa na wanazuoni wa Al-Azhar, Damascus, Qum na Najaf kwa ajili ya mazungumzo ya kimantiki kwa lengo la kufafanua ukweli? Kwa nini hawako tayari kuanzisha mjadala wa kirafiki kufuatana na maagizo ya Qur`ani Tukufu:

‫َوالَّ ِذينَ اجْ تَنَبُوا الطَّا ُغوتَ أَ ْن يَ ْعبُ ُدوهَا َوأَنَابُوا إِلَى للاهَّ ِ لَهُ ُم ْالبُ ْش َر ٰى ۚ فَبَ ِّشرْ ِعبَا ِد‬ ‫ك هُ ْم‬ َ ِ‫ك الَّ ِذينَ هَدَاهُ ُم للاهَّ ُ ۖ َوأُو ٰلَئ‬ َ ِ‫الَّ ِذينَ يَ ْستَ ِمعُونَ ْالقَوْ َل فَيَتَّبِعُونَ أَحْ َسنَهُ ۚ أُو ٰلَئ‬ ‫ب‬ ِ ‫أُولُو أْالَ ْلبَا‬ “Na wale wanaojiepusha na kuabudu Taghut, na wakarejea kwa Mwenyezi Mungu, watapata bishara njema. Basi wabashirie waja Wangu. Ambao husikiliza maneno, wakafuata mazuri yake zaidi. Hao ndio aliowaongoza Mwenyezi Mungu, na hao ndio wenye akili.” (Surah Zumar, 39:17-18).

Kama wangefanya hivyo, damu yote safi ya Waislamu haingemwagika wala rasilimali zao zisingeporwa; maadui wa Uislamu ha67

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 67

5/31/2016 7:38:09 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

wangewashinda na Wazayuni wachache hawangechezea hatima yao. Haijulikani wametayarisha jibu la aina gani mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu mnamo Siku ya Hukumu? Hata hivyo, maoni sita makubwa sana ni kama yafuatayo: 1.

Shirki na Mshirikina (katika Qur`ani Tukufu).

2.

Ilah (Mungu katika Qur`ani Tukufu).

3.

Ibada (katika Qur`ani Tukufu).

4.

Maombezi (katika Qur`ani Tukufu).

5.

Du’a (katika Qur`ani Tukufu).

6.

Bida’a (katika Qur`ani Tukufu).

1. Shirki: Neno la kwanza muhimu ni ‘Shirki’ na ‘Mshirikina’. “Shirki” ni lugha ya Kiarabu inaendana na kitu na “Shariik” ni mwenza. Lisan al-Arab, kwa ajili ya maana ya neno “Ishtirak” inasema: (Kumuwekea Mungu mshirika katika Ufalme Wake) na kwa ajili ya maana ya “Shirk” inasema: (Kumuwekea Mungu mshirika katika Umola Wake) na inaelezea Shirk kama kushirikisha kitu kingine na Mungu katika Mamlaka Yake na Utawala Wake. Raghib anatamka katika Mufradat yake: “Katika dini Shirki ni ya aina mbili: aina ya kwanza ni ‘Shirki Kuu’ pale ambapo binadamu hushirikisha kitu na mwenza kwa Mungu, jambo ambalo litamzuia kupata Pepo.35 Aina ya pili ni ‘Shir35

������������������������������������������������������������������������� Mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote, Mwenyezi Mungu amemharamishia Pepo Yake. 68

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 68

5/31/2016 7:38:09 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

ki Ndogo’ nayo ni pale ambapo binadamu anajishughulisha na baadhi ya vitu vingine badala ya kujishughulisha na mambo yahusuyo Mungu, jambo ambalo linafanana na majivuno au unafiki. Qur`ani Tukufu inashauri:

َّ‫َو َما ي ُْؤ ِم ُن أَ ْكثَ ُرهُ ْم بِ ه‬ َ‫اللِ إِ اَّل َوهُ ْم ُم ْش ِر ُكون‬ “Na wengi wao hawamwamini Mwenyezi Mungu pasi na kuwa ni washirikina.” (Surah Yusuf, 12:106)

Kwa hiyo, ukweli halisi wa ‘Shirki Kuu’ ni kumfikiria mtu fulani anayefanana na Yeye au kitu fulani kinachofanana na Yeye au anayelingana na Yeye au kinacholingana na Yeye katika Uumbaji na Umiliki, Mamlaka na Kuabudiwa. Lakini kama tukisema, Mtukufu Isa aliponya magonjwa sugu kwa idhini ya Mungu, na aliwafufua wafu kwa idhini ya Mungu, na kupitia ujuzi ambao alikwishapata kutoka kwa Mungu alitabiri yale yasiyojulikana na yaliyokuwa siri, wala hatujapita njia ya shirki ama kusema uongo. Hivi Qur`ani Tukufu haisemi katika jina la Isa :

ً‫َو َرس ا‬ ُ ُ‫ُول إِلَ ٰى بَنِي إِ ْس َرائِي َل أَنِّي قَ ْد ِج ْئتُ ُك ْم بِآيَ ٍة ِم ْن َربِّ ُك ْم ۖ أَنِّي أَ ْخل‬ َ‫ق لَ ُك ْم ِمن‬ ِّ ‫ال‬ ُ ‫ين َكهَ ْيئَ ِة الطَّي ِْر فَأ َ ْنفُ ُخ فِي ِه فَيَ ُك‬ ‫ص‬ ُ ‫ون طَ ْيرًا بِإِ ْذ ِن للاهَّ ِ ۖ َوأُب ِْر‬ َ ‫ئ أْالَ ْك َمهَ َو أْالَ ْب َر‬ ِ ‫ط‬ ‫َوأُحْ يِي ْال َموْ ت َٰى بِإِ ْذ ِن للاهَّ ِ ۖ َوأُنَبِّئُ ُك ْم بِ َما تَأْ ُكلُونَ َو َما تَ َّد ِخرُونَ فِي بُيُوتِ ُك ْم ۚ إِ َّن فِي‬ َ‫ك لآَ يَةً لَ ُك ْم إِ ْن ُك ْنتُ ْم ُم ْؤ ِمنِين‬ َ ِ‫ٰ َذل‬ “Na Mtume kwa wana wa Israeli (awaambie): Mimi nimewajia na Ishara kutoka kwa Mola Wenu, hakika mimi nitawafanyia kama namna ya ndege katika udongo; kisha nimpulizie awe ndege kwa 69

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 69

5/31/2016 7:38:09 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

idhini ya Mwenyezi Mungu na niwaponye vipofu na wenye mbalanga. Niwafufue wafu kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na niwaambie mnavyovila na mtakavyoweka akiba. Hakika katika haya ipo Ishara kwenu ikiwa ni wenye kuamini.” (Surah Al-Imran, 3:49).

Kwa hiyo, kama tukimuomba Mtukufu Mtume  na baadhi ya waja wa Mungu ambao ni waadilifu kama vile Maimamu  wa Nyumba ya Mtukufu Mtume  kwa mambo kama hayo kwa namna ileile, kwa maana kwamba “kwa idhini ya Mungu”, si tu kwamba hiyo si Shirki bali ni Tauhidi kamili, kwa sababu sisi kamwe hatuwaweki wao katika kiwango kimoja na hadhi moja, wala kuwafanya wao kama washirika wa Mungu, au wasiomtegemea Mungu katika kusababisha. Kwa kweli, tunawaona wao kama ni waja watiifu na watekelezaji wa amri Zake. Ni jambo la ajabu kwamba viongozi wa Uwahhabi wamefasiri kimakosa neno “Shirki”, na wao wanafikiri kuwa ni “Shiriki” kwa kila maombi kupitia kwa waja waadilifu wa Mungu ambao wao hawatekelezi isipokuwa kwa idhini ya Mungu, fikra ambayo ni dhidi ya maamuzi dhahiri ya Qur`ani Tukufu!? Na hebu tudhanie kwamba mtu fulani anammliki mtumwa ambaye hujituma katika kutekeleza kazi anazopewa na bwana wake, na kamwe hafanyi kitu bila idhini ya bwana wake. Kama mtu anamuomba mtumwa huyo ampelekee ombi lake kwa bwana wake kwa ajili ya kitu fulani, hivi yule mtu anayemuomba mtumwa kufanya hivyo anamfikiria mtumwa huyo kuwa analingana na bwana wake au analingana na bwana wake kwa hadhi, au kama mshirika wa bwana wake, au katika huduma yake!? Hivi dhamira yeyote yenye utambuzi inaweza kukubali tamko hilo, kwamba kitendo hiki ni “Shirki”? Hitilafu inaanzia kwenye nukta hii: bado hawajaweka na hawataweka Aya za Qur`ani Tukufu kando ya kila moja ili maana yake ya kweli idhihirike, lakini wao husisitiza kukubaliana na hayo tu ambayo yanaendana na tafsiri yao. 70

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 70

5/31/2016 7:38:09 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

2. Ilah (Mungu). Kufuatana na Uwahhabi, neno “Ilah” linamaanisha yule tu mungu anayeabudiwa. Tamko lisemalo “hapana mungu ila Mungu”, ambalo ni tamko litumikalo katika kushuhudia, la Mtukufu Mtume wa Uislamu  na Waislamu wote wa dunia, ni kufikiria tu “Tauhidi (umoja) katika ibada.” Wao wanamaanisha kwamba hakuna anayeabudiwa isipokuwa Mmoja na ni Mungu tu. Waabudu masanamu waliamini katika Ummoja Wake kama Muumba, Mtunzaji na Mola. Kinyume cha hiki, Waarabu waabudu masanamu hawakuathiriwa na masanamu tu katika ibada na “Ilah” si siku zote ina maana ya mungu anayeabudiwa, lakini wakati mwingine inamaanisha “Muumba”. Qur`ani Tukufu inasema:

ۚ ‫ض هُ ْم يُ ْن ِشرُونَ لَوْ َكانَ فِي ِه َما آلِهَةٌ إِ اَّل للاهَّ ُ لَفَ َس َدتَا‬ ِ ْ‫أَ ِم اتَّ َخ ُذوا آلِهَةً ِمنَ أْالَر‬ َ‫صفُون‬ ِ َ‫ش َع َّما ي‬ ِ ْ‫فَ ُس ْب َحانَ للاهَّ ِ َربِّ ْال َعر‬ “Au wamepata waungu katika ardhi wafufuao? Lau wangelikuwemo humo waungu wengine isipokuwa Mwenyezi Mungu basi zingefisidika. Ametakasika Mwenyezi Mungu, Mola wa Arsh, na hayo wanayoyasifu.” (Al-Anbiyaa, 21:21-22).

Katika Aya hizi ‘Aliha’ wingi wa ‘Ilah’ kwa dhahiri inaleta maana ya ‘Muumbaji.’ Katika Aya nyingine maana hii hii inaonekana katika namna ya dhahiri zaidi:

‫ق َولَ َع اَل‬ َ َ‫َب ُكلُّ إِ ٰلَ ٍه بِ َما َخل‬ َ ‫َما اتَّ َخ َذ للاهَّ ُ ِم ْن َولَ ٍد َو َما َكانَ َم َعهُ ِم ْن إِ ٰلَ ٍه ۚ إِ ًذا لَ َذه‬ ‫ب َوال َّشهَا َد ِة فَتَ َعالَ ٰى‬ ُ ‫بَ ْع‬ ِ ‫صفُونَ عَالِ ِم ْال َغ ْي‬ ِ َ‫ْض ۚ ُس ْب َحانَ للاهَّ ِ َع َّما ي‬ ٍ ‫ضهُ ْم َعلَ ٰى بَع‬ َ‫َع َّما يُ ْش ِر ُكون‬ 71

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 71

5/31/2016 7:38:09 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

“Mwenyezi Mungu hakujifanyia mwana, wala hanaye mungu mwingine. Ingelikuwa hivyo basi kila Mungu angelichukua alivyoviumba. Na baadhi yao wangeliwashinda wengine. Ametakata Mwenyezi Mungu na wanavyomsifu. Mjuzi wa ghaibu na dhahiri. Ametukuka juu ya hayo wanayomshirikisha nayo.” (Surah Al-Mu`minun, 23:91-92).

Katika Aya hizi uwepo wa muumbaji mwingine yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu Mmoja umekanushwa (na hilo linapatikana kwa neno ‘Ilah’) kwamba kama pangekuwepo muumbaji mwingine yeyote zaidi ya Yeye, mpangilio wa ulimwengu ungeteketezwa. Aya hii inafafanua imani ya Kiarabu ya kuabudu miungu wengi katika wingi wa waumbaji, kwani inasema: “Yeye ametukuka juu ya hayo wanayomshirikisha nayo.” Kwa hiyo Uislamu umepewa kazi ya kuwaita watu kwenye “Tawhidi (ummoja) katika ibada” na kutokufuata matawi mengine ya Tawhidi, ni dhambi kubwa na ni kinyume na Qur`ani Tukufu. Shauku kubwa ya Uwahhabi kwa uelewa wao wa dhana ya “imani ya uwepo wa Mungu Mmoja” na “imani ya kuabudu miungu wengi” iliwaongoza wao kuzikwepa Aya hizo katika Qur`ani Tukufu ambazo zinaunga mkono uelewa wao na kwa makusudi hawazitilii maanani, pamoja na kwamba wengi wao ni mahafidhi wa Qur`ani. Kwa bahati mbaya kuhifadhi Qur`ani Tukufu haina maana kwamba siku zote ni kuielewa Qur`ani Tukufu! Zaidi ya hayo, imechukuliwa kutoka kwenye Aya zingine za Qur`ani Tukufu kwamba kundi la waabuduo masanamu waliamini katika “mamlaka” ya masanamu na athari ya hatima yao. Kundi hilo lenye ushirikina lilisadiki kwamba ghadhabu ya masanamu iliangukia kwa wale waliokuwa wanayapinga masanamu, na waliwapa mambo mazuri na bahati nzuri wale walioamni masanamu. Mathalani, katika kipindi cha Hud, waabudu masanamu walisema: 72

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 72

5/31/2016 7:38:09 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

‫ك بَعْضُ آلِهَتِنَا بِسُو ٍء ۗ قَا َل إِنِّي أُ ْش ِه ُد للاهَّ َ َوا ْشهَ ُدوا أَنِّي بَ ِري ٌء‬ َ ‫إِ ْن نَقُو ُل إِ اَّل ا ْعتَ َرا‬ َ‫ِم َّما تُ ْش ِر ُكون‬ “Hatuna la kusema ila baadhi ya miungu yetu imekutia balaa. Akasema: Hakika mimi ninamshuhudisha Mwenyezi Mungu, na nyinyi shuhudieni kwamba niko mbali na hao mnaowashirikisha,” (Hud; 11:54).

Shairi mashuhuri lililotungwa na mshairi Mwarabu katika kulishutumu “kabila la Hanifah” katika zama za upagani ni ushahidi kwa dai hili! Wakati palikuwepo na njaa watu wa kabila hili walikula sanamu ambalo walilitengeneza kwa tende: “Kabila la Hanifah lilimla Mungu wao katika mwaka wa njaa na matatizo, Hivi hawakuogopa karipio la Mola wao?” Shairi limepachika neno Mola (Rabbi) kwa masanamu, na kwa hiyo limewaonya wale waliokula sanamu dhidi ya matokeo yenye madhara kwa kitendo chao isijekuwa wakadhuriwa na masanamu. Shairi lingine linasema: “Hivi mola wao ni lile sanamu ambalo mbweha hulikojolea?” Katika kipindi chote cha historia ya ibada ya masanamu, pamekuwepo na kupachikwa neno “Mola” ) ِّ‫ ( َرب‬na mola ) ّ‫ (أرباب‬kumaanisha masanamu, ni ushahidi kwamba waabudu masanamu waliamini kwamba sehemu ya usimamizi wa mambo ya ulimwengu ulikuwa mikononi mwa masanamu. Hivyo, wakati Yusufu  alipotaka kuwaita wafungwa waabudu masanamu kwa mintarafu ya Tauhidi (imani ya uwepo wa Mungu Mmoja), alisema:

73

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 73

5/31/2016 7:38:09 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

‫اح ُد ْالقَهَّا ُر‬ َ ‫يَا‬ ِ ‫احبَ ِي السِّجْ ِن أَأَرْ بَابٌ ُمتَفَرِّ قُونَ َخ ْي ٌر أَ ِم للاهَّ ُ ْال َو‬ ِ ‫ص‬ “Enyi wafungwa wenzangu wawili! Je, waungu wengi wanaofarikiana ni bora au Mwenyezi Mungu Mmoja Mwenye nguvu? (Yusuf, 12:39).

Angalia neno miungu katika aya hii, wingi wa Mungu. Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu  aliwahubiria watu wa Kitabu waabuduo miungu wengi kufuatana na Aya za wazi za Qur`ani Tukufu:

‫ك‬ َ ‫ب تَ َعالَوْ ا إِلَ ٰى َكلِ َم ٍة َس َوا ٍء بَ ْينَنَا َوبَ ْينَ ُك ْم أَ اَّل نَ ْعبُ َد إِ اَّل للاهَّ َ َو اَل نُ ْش ِر‬ ِ ‫قُلْ يَا أَ ْه َل ْال ِكتَا‬ ‫ون للاهَّ ِ ۚ فَإِ ْن تَ َولَّوْ ا فَقُولُوا ا ْشهَ ُدوا‬ ُ ‫بِ ِه َش ْيئًا َو اَل يَتَّ ِخ َذ بَ ْع‬ ِ ‫ضنَا بَ ْعضًا أَرْ بَابًا ِم ْن ُد‬ َ‫بِأَنَّا ُم ْسلِ ُمون‬ “Sema: Enyi watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno la usawa baina yetu na baina yenu. Kwamba tusimwabudu yoyote ila Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote; wala baadhi yetu tusiwafanye baadhi kuwa waungu zaidi wasaidizi wangu kwa Mwenyezi Mungu. Wakikataa, semeni: Shuhudieni kuwa sisi ni Waislamu.” (Surah Al-Imran, 3:64).

Matumizi ya neno “mungu” kwa dhahiri linaonesha kwamba pia walishawishika kuabudu miungu wengi juu ya suala la mamlaka ya Mwenyezi Mungu. Katika Aya nyingine kutoka katika Surah hii tunasoma:

‫َو اَل يَأْ ُم َر ُك ْم أَ ْن تَتَّ ِخ ُذوا ْال َم اَلئِ َكةَ َوالنَّبِيِّينَ أَرْ بَابًا ۗ أَيَأْ ُم ُر ُك ْم بِ ْال ُك ْف ِر بَ ْع َد إِ ْذ أَ ْنتُ ْم‬ َ‫ُم ْسلِ ُمون‬ 74

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 74

5/31/2016 7:38:09 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

“Wala hatawaamrisha kuwafanya Malaika na manabii kuwa waungu. Je, atawaamrisha ukafiri baada ya kuwa nyinyi Waislamu?” (Al-Imran, 3:80).

Kuhusu waabudu masanamu wa zama za upagani Qur`ani Tukufu inasema:

َ‫صرُون‬ َ ‫ون للاهَّ ِ آلِهَةً لَ َعلَّهُ ْم يُ ْن‬ ِ ‫َواتَّ َخ ُذوا ِم ْن ُد‬ “Na wameishika miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu wapate kusaidiwa!” (Yasin; 36:74).

Kwa hiyo walishawishiwa na ibada ya miungu wengi katika tawi lake la Mamlaka na wakawafikiria masanamu kama kwa kweli yalikuwa yenye kuwasababishia matokeo yanayotarajiwa katika bahati mbalimbali. Ibrahim  mwanzoni alipeleka maombi yake kwa mwezi, jua na nyota na akasema, “Huyu ndiye mungu wangu,” hadi hapo alipoona kosa la imani yao. Msisitizo wake kwa mamlaka unaonesha kwa dhahiri kwamba waabudu masanamu wa Babyloni, walifikiria mwezi, jua na nyota kama watawala wa maisha yao. Matamko yake mbele ya Nimrod yanazungumzia fikira hizohizo. Hitimisho ni kwamba llah haina maana ya mungu anayeabudiwa tu, lakini wakati mwingine linatumika kama muumbaji na wakati fulani kama mola. Hivyo, waabuduo miungu wengi hawakuwa wameshawishiwa na imani ya miungu wengi tu katika ibada bali pia waliamini masanamu yao kuwa waumbaji na ma-mola. Ikifikiriwa uelewa wa juujuu walionao waumini wa Uwahhabi wa Aya za Qur`ani, hususani wa neno “llah”, hivi wanaweza kuamua kwamba ni ruhusa wao kumwaga damu na wanaweza kupora mali ya mtu gani? Kwa kweli, ni jinsi gani ambavyo uhai wa Muislamu 75

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 75

5/31/2016 7:38:09 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

umekuwa hauna thamani na rasilimali ya Muislamu ambavyo imekuwa haina thamani!! Ibada: Ibada ni neno la tatu la Qur`ani Tukufu ambalo wafuasi wa Uwahhabi wamelielewa kimakosa. Wao wanasema kwa dhahiri: kama mtu akiwaomba waadilifu kuwa waombezi wao mbali ya Mwenyezi Mungu, hao ni marejeo ya Aya hii Tukufu:

ُ ‫أَ اَل للِهَّ ِ الد‬ ‫ِّين ْالخَالِصُ ۚ َوالَّ ِذينَ اتَّ َخ ُذوا ِم ْن ُدونِ ِه أَوْ لِيَا َء َما نَ ْعبُ ُدهُ ْم إِ اَّل لِيُقَ ِّربُونَا‬ ‫إِلَى للاهَّ ِ ُز ْلفَ ٰى إِ َّن للاهَّ َ يَحْ ُك ُم بَ ْينَهُ ْم فِي َما هُ ْم فِي ِه يَ ْختَلِفُونَ ۗ إِ َّن للاهَّ َ اَل يَ ْه ِدي َم ْن‬ ‫هُ َو َكا ِذبٌ َكفَّا ٌر‬ “Ehee! Dini halisi ni ya Mwenyezi Mungu. Na wale wanaofanya wenginewe kuwa ni walinzi badala Yake, (husema): Sisi hatuwaabudu ila wapate kutujongeza tu kumkaribia Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu atahukumu baina yao katika wanayohitilafiana. Hakika Mwenyezi Mungu hamwongozi aliye mwongo, kafiri.” (Az-Zumar, 39:3.).

Wale wanaoabudu miungu wengi wanalaaniwa kwa kutafuta uombezi kupitia kwa masanamu yao ambayo wanayasujudia, wanayaomba na pia huyaabudu. Tunapokwenda Hijja kwenye Sehemu Tukufu ya Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu  na kuomba msaada kutoka kwake ili awe muombezi wetu hapa duniani na akhera, hivi huwa tunamuabudu yeye? Hivi sisi huwa tunaanguka chini kifudifudi na kumsujudia? Hivi kuomba msaada wa kuombewa una uhusiano gani na kuabudu? Yeyote yule ambaye anao uzoefu na lugha na desturi ya 76

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 76

5/31/2016 7:38:09 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

matendo, anajua kwamba kama mtu alimwendea Nabii Isa  na akamkabidhi mtoto wake ambaye ni kipofu na akasema, ‘Kama wewe unadai kwamba unaweza kuwatibu vipofu kwa idhini ya Mungu, mtibu mtoto wangu kwa idhini ya Mungu,’ ni sehemu gani ya kitendo hiki ni ibada?! Huu ni utaratibu ambao Qur`ani Tukufu inaona unakubalika. “Ibada” kama neno na kama kitendo cha desturi kinarejelea kwenye unyenyekevu wa juu kabisa mbele ya mtu fulani, kama kusujudia na kupiga magoti (kurukuu katika swala), lakini kumwomba mtu akusaidie ni kitendo ambacho hakina uhusiano na jambo hili. Raghib anasema katika Mufradat: Utumwa ni kuonesha unyonge, na ibada ni bora kuliko hilo kwa sababu ni unyenyekevu wa juu kabisa.” Tunasoma katika Lisan al-Arab: “Msingi wa utumwa ni udhalili na unyenyekevu.” Ni jambo la kuvutia kwamba kiongozi wa imani ya Uwahhabi ameelekeza usikivu wake mkubwa kwa sentensi isemayo: “ila wapate kutujongeza tu kwa Mwenyezi Mungu,” lakini hakuwa msikivu na ameruka mwanzo wa sentensi usemao, “Sisi hatuwaabudu ili …..,” (Al-Zumar, 39:3.) kwa hiyo tatizo lipo kwenye kuabudu, wenginewe zaidi ya Mungu, si kwa “kuomba msaada wa uombezi kwa ajili ya kuwa karibu na Mwenyezi Mungu” na huo ni msaada wa uombezi kwa idhini ya Mungu. Kwa kweli, wakati mtu anapoingiza somo kwa uamuzi usio sahihi, huona kile tu kinachoendana na nia yake. Na yule anayepinga, wakati mwingine kamwe haoni hilo na wakati mwingine hukanusha kwa makusudi na hutoa fatwa kwa ajili ya kifo cha mamilioni ya Waislamu hao ambao yeye huamua kuwa ni washirikina! Halafu 77

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 77

5/31/2016 7:38:09 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

huchukulia kumwagika kwa damu yao na kuporwa rasilimali zao na kushushiwa heshima yao ni kitendo cha halali! Maombezi: Maombezi ni neno la nne la Qur`ani Tukufu ambalo madhehebu hii imetafsiri kimakosa, na kama ambavyo tayari nimekwisha sema, wamepitisha fatwa ya ukafiri dhidi ya wote wale wanaotaka msaada wa maombezi kutoka kwa Mtukufu Mtume  na Maimamu wa Nyumba ya Mtukufu Mtume  au waja wengine waadilifu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na wakawaita wao ni watu waabuduo miungu wengi. Ushabiki wao uliopindukia ni wa dhahiri kutokana na ukweli kwamba kiongozi wao, katika risala ndefu ya mada moja tu kwenye “Kashf al-Shubahat”, inawachukulia hawa washirikina waliojiamulia wenyewe, ni wabaya zaidi kuliko waabuduo masanamu wa zama za upagani kwa sababu mbili. Anasema kwa dhahiri kabisa kwamba pamoja na kwamba waabudu masanamu kamwe hawakuamini katika ufufuo, wala hawakuwa wakiswali au ibada zingine zozote za Kiislamu, na walimchukulia Mtukufu Mtume  kuwa ni mwanamazingaombwe na ilimlazimu kuua, na Qur`ani Tukufu kama uchawi, bado wanao ubora juu ya waabuduo miungu wengi wa zama zetu ambao hukubali kama ni kweli kila kitu kilicholetwa kwao na Uislamu, lakini hutaka msaada wa uombezi kutoka kwa Mtukufu Mtume !! Hii inathibitisha kwamba imani ya kuabudu miungu wengi ya waabuduo masanamu ni nyepesi zaidi kuliko ya kwao! Kwa nini?! Kwa sababu, wao wanasema, ni wakati fulani fulani tu wa ustawi wao hao waliabudu masanamu, lakini wakati wa dhiki, walipokuwa 78

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 78

5/31/2016 7:38:09 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

kwenye dhoruba na kuzingirwa na mawimbi hatari ya bahari, walimuita Mungu kwa imani! Inawezekanaje mtu kutokutenda haki kiasi hicho? Ni nani anayeweza kudai kwamba watu hao wa dini ambao wanaamini katika kanuni zote za Uislamu, hutenda kufuatana na mafundisho yake yote na ibada, hujizuia kutenda dhambi zote, hutoa zaka, na kodi zote za kidini kwa uangalifu. Huenda Hijja kwenye nyumba ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kutoka sehemu mbalimbali za dunia, huhifadhi Qur`ani Tukufu na wao ni wenye elimu katika kanuni zote za Kiislamu, wawe wabaya kuliko waabudu masanamu, walevi wa vileo na wauaji na wajinga washenzi ambao kamwe hawakuamini katika kitu chochote na waliathiriwa na kila aina ya dhambi. Inawezekanaje mtu yeyote kukubaliana na mantiki hii katika ulimwengu wa leo?! Hivi Sheikh Al-Islam amefanya uvumbuzi mpya katika jambo hili ambalo lilikuwa bado halijavumbuliwa kwa ajili ya wanazuoni wote wa Kiislamu katika historia yote isipokuwa kwake yeye na mheshimiwa Ibn Taymiyah?! Ukweli ni kwamba msingi wa fikra ya uombezi imethibitishwa katika Aya nyingi za Qur`ani Tukufu, na kufuatana na maafikiano ya wanazuoni wa Kiislamu ni dhana inayokubalika hata wafuasi wa Uwahhabi hawakanushi bali wanakiri waziwazi. Nukta nyingine ni kwamba kutokutekelezeka kwa uombezi wa waombezi bila idhini ya Mwenyezi Mungu pia ni dhana inayokubalika kwa sababu imetamkwa kwa dhahiri katika zaidi ya Aya tano za Qur`ani Tukufu; miongoni mwa Aya hizo ni Ayatul-Kursi ambayo inasomeka ifuatavyo:

‫َم ْن َذا الَّ ِذي يَ ْشفَ ُع ِع ْن َدهُ إِ اَّل بِإِ ْذنِ ِه‬ 79

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 79

5/31/2016 7:38:09 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

“…..Ni nani huyo awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini Yake?…….” (2:255)

Tawhiid ya Vitendo yasema kwamba kila kitendo katika ulimwengu lazima kitokee kwa idhini ya Mungu na hapana yeyote ambaye ni mwenza wake katika utendaji huo. Na kama uombezi unafanyika, ni kwa amri na idhini Yake, na kwa kuwa Yeye ni Mwenye Hekima, amri na idhini Yake hutokea kufuatana na hekima. Na ni kwa wale tu ambao amewapa idhini ya uombezi ndio ambao wana ujuzi wa uombezi, na hawakuunguza madaraja nyuma yao kwa njia ya ukaidi. Hivyo hadi hapo, yapo makubaliano katika mambo yote, sasa basi tofauti inatokea wapi? Tofauti ipo pale ambapo wanazuoni wa Kiislamu wanasema kwamba kumuomba msaada Mtukufu Mtume  wa kutuombea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu jambo ambalo limewekwa katika wadhifa wake (yaani hadhi ya uombezi) ni kitendo kizuri na si tu kwamba ni hakipo kinyume cha Tauhidi lakini kinathibitisha jambo hili. Lakini wafuasi wa Uwahhabi wanadai kwamba kama ukiomba msaada wa uombezi kutoka kwake basi wewe unakuwa kafiri na muabudu miungu wengi na ni halali wewe kuuawa na rasilimali zako kuporwa!! Hivi kitendo cha uombezi hufikiriwa kama vile ni jambo batili? Hapana, kwa sababu jambo hili ni halali kufuatana na makubaliano ya wanazuoni wote. Hivi Mtukufu Mtume  hana hadhi ya uombezi? Kila mtu anashikilia kwamba kwa kweli Mtukufu Mtume  anayo hadhi ya uombezi. Sasa basi tatizo liko wapi? Wafuasi wa Uwahhabi wanasema kwamba Mtukufu Mtume  anayo hadhi ya uombezi lakini mtu akiomba msaada wa uombezi kutoka kwake atakuwa kafiri! Wao hunukuu Aya ya Qur`ani Tukufu ambayo inasema kwamba Waarabu 80

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 80

5/31/2016 7:38:09 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

waliokuwa wanaabudu miungu wengi walidai kwamba waliabudu masanamu ili kwamba wangekuwa waombezi wao mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwa hiyo kitendo chako ni sawa kabisa kama kile cha Waarabu waabuduo miungu wengi. Au sivyo?! Sisi tunashikilia kwamba Waarabu hao waliabudu masanamu, lakini sisi kamwe hatumuabudu Mtukufu Mtume  na dhuria wa Nyumba yake  na kuomba msaada wa uombezi bila kuabudu ni vitendo viwili vinavyotofautiana kabisa. Wao wanasisitiza kwamba kile wasemacho wao ndicho kilicho sahihi! Sisi tunasema: Qur`ani Tukufu yenyewe inawaelekeza wenye dhambi waende kwa Mtukufu Mtume  na wamsihi awaombee msamaha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ili wapate kusamehewa dhambi zao na Mwenyezi Mungu Mtukufu:

‫ك فَا ْستَ ْغفَرُوا للاهَّ َ َوا ْستَ ْغفَ َر لَهُ ُم ال َّرسُو ُل‬ َ ‫َولَوْ أَنَّهُ ْم إِ ْذ ظَلَ ُموا أَ ْنفُ َسهُ ْم َجا ُءو‬ ‫لَ َو َج ُدوا للاهَّ َ تَ َّوابًا َر ِحي ًما‬ “…….Na lau kwamba wao walipojidhulumu wangekujia wakaomba maghufira kwa Mwenyezi Mungu na wakaombewa maghufira na Mtume, wangelimkuta Mwenyezi Mungu ni Mwenye kutakabali toba Mwenye kurehemu.” (Surah An-Nisaa, 4:64)

Na inayoashiria zaidi ya hiyo tunasoma hadithi ya Yaquub  wakati ambapo baada ya watoto wa Yaquub  kukiri kosa la mwenendo wao mbaya na hatia kwa Yusuf , walimsihi baba yao (ili awafanyie uombezi) ili wapate maghufira kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, wakasema:

81

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 81

5/31/2016 7:38:10 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

ُ‫َاطئِينَ قَا َل َسوْ فَ أَ ْستَ ْغفِ ُر لَ ُك ْم َربِّي ۖ إِنَّه‬ ِ ‫قَالُوا يَا أَبَانَا ا ْستَ ْغفِرْ لَنَا ُذنُوبَنَا إِنَّا ُكنَّا خ‬ ‫َّحي ُم‬ ِ ‫هُ َو ْال َغفُو ُر الر‬ “Wakasema: Ewe baba yetu! Tuombee maghufira kwa dhambi zetu, hakika sisi tulikuwa ni wenye hatia. Akasema: Nitawaombea maghufira kwa Mola Wangu. Hakika Yeye ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.” (Yusuf; 12:97-98)

Nabii Yaquub  si tu kwamba hakulikataa ombi hili ambalo lilikuwa ombi la msaada wa uombezi kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, bali alilipokea ombi hilo vizuri. Hivi Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu anaweza kuwaita wanawe kwenye imani ya kuabudu miungu wengi na uasi? Kisingizio kisichofaa: Nukta ya kuvutia ni kwamba Wahhabi wenye msimamo mkali, hubadili maneno yao wanapofika kwenye nukta hii, kwa sababu hawana uthibitisho. Wao wanasema kwamba hizo aya mbili zilizonukuliwa hapo juu zinahusu wakati wa uhai wa hao Mitume wawili, lakini baada ya Mitume hao kufariki dunia na kuwa mavumbi, hakuna chochote wanachoweza kufanya.!! Hivyo kumsihi Mtume  kuhusu msaada wa uombezi baada ya kifo chake ni kitendo kisicho na thamani! Ona kwa kinaganaga kwamba hapo kwenye nukta hii mambo ya kuabudu miungu wengi na uasi yanaondolewa kwenye taswira, na suala la kutokuwa na thamani limejitokeza. Na wanaseama kwamba kama ilikuwa wakati wa uhai wao, haingekuwa imani ya kuabudu miungu wengi au uasi, lakini kama ilikuwa baada ya vifo vyao, ni kitendo kisicho na thamani. Na hii ni dalili ya kukanusha madai yao yote ya nyuma. Sisi tunasema kwamba suala hili wala si uasi 82

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 82

5/31/2016 7:38:10 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

ama kutokuwa na thamani, kwa kuwa hapana Muislamu ambaye anajiruhusu kutangaza kwamba cheo cha Mtukufu Mtume wa Uislamu  kilikuwa cha thamani ndogo kuliko mfiadini wa kawaida katika vita vya Badr na Uhud, kwani wao ni:

َ‫بَلْ أَحْ يَا ٌء ِع ْن َد َربِّ ِه ْم يُرْ َزقُون‬ “…..bali wako hai mbele ya Mola wao wanaruzukiwa.” (Al-Imran, 3:169).

Lakini Mtume anakuwa mavumbi? Ni mtu katili wa aina gani anaweza kusema kitu kama hicho?! Inaonekana kwamba kosa lao linatokeza pale ambapo Qur`ani Tukufu inawaambia Mitume:

َ‫ك اَل تُ ْس ِم ُع ْال َموْ ت َٰى َو اَل تُ ْس ِم ُع الصُّ َّم ال ُّدعَا َء إِ َذا َولَّوْ ا ُم ْدبِ ِرين‬ َ َّ‫إِن‬ “Kwa hakika wewe huwezi kuwasikilizisha wafu wala kuwasikilizisha viziwi wanapogeuka kurudi nyuma.” (Al-Naml, 27:80)

Ambapo Aya hii inarejelea kwa watu wa kawaida na si Mitume au watu waadilifu na watakatifu. Basi ni lazima waulizwe, kwa nini basi huwa mnapeleka salamu zenu kwa Mtukufu Mtume  wakati wa swala “Asalaam alayka Ayuha Nabiiyu wa rahamatullah.” Hivi mnaomba rehma na amani kwa mtu ambaye (Mungu apishe mbali) haelewi kitu chochote? Hivi ninyi mnaiamini Aya isemayo:

‫صلُّوا َعلَ ْي ِه َو َسلِّ ُموا‬ َ ‫صلُّونَ َعلَى النَّبِ ِّي ۚ يَا أَيُّهَا الَّ ِذينَ آ َمنُوا‬ َ ُ‫إِ َّن للاهَّ َ َو َم اَلئِ َكتَهُ ي‬ ‫تَ ْسلِي ًما‬

83

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 83

5/31/2016 7:38:10 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

“Hakika Mwenyezi Mungu na malaika Wake wanamswalia Nabii. Enyi ambao mmeamini Mswalieni na mumsalimu kwa salamu.” (Surah Al-Ahzab, 33:56)

Mungu na wale mlioamini, wewe unampelekea nani neema na rehema zako? Je, Unampelekea mtu ambaye (Mungu apishe mbali) haelewi kitu chochote?! Kwa nini mmeweka Aya hii iwe alama juu ya Sehemu Takatifu ya Mtukufu Mtume ?

ُ‫ت النَّبِ ِّي َو اَل تَجْ هَرُوا لَه‬ َ ْ‫يَا أَيُّهَا الَّ ِذينَ آ َمنُوا اَل تَرْ فَعُوا أَصْ َواتَ ُك ْم فَو‬ َ ‫ق‬ ِ ْ‫صو‬ َ‫ْض أَ ْن تَحْ بَطَ أَ ْع َمالُ ُك ْم َوأَ ْنتُ ْم اَل تَ ْش ُعرُون‬ ِ ‫بِ ْالقَوْ ِل َك َجه ِْر بَع‬ ٍ ‫ْض ُك ْم لِبَع‬ “Enyi mlioamini! Msinyanyue sauti zenu kuliko sauti ya Nabii, wala msiseme naye kwa kelele kama mnavyosemezana ninyi kwa ninyi, visije vitendo vyenu vikaanguka, na hali hamtambui.” (Al-Hujurat; 49:2)

Kwa nini hamruhusu mtu yeyote kunyanyua sauti yake pembezoni mwa Sehemu Takatifu ya Mtukufu Mtume ? Kama mnaamini kwamba baada ya kifo cha Mtukufu Mtume  haelewi kitu chochote (Mungu apishe mbali),1 hivi vitendo na matamshi ya ukinzani maana yake ni nini?! Dua: Neno lingine ambalo wafuasi wa Uwahhabi wenye ukereketwa wa kupindukia walifasiri kimakosa ni Dua katika Qur`ani. Wao wanaamini kwamba mtu yeyote anayemuita Mtukufu Mtume  au mmojawapo wa watakatifu au waadilifu wa Mungu, mtu huyo ni mkana Mungu au mpagani, na ni halali mtu huyo kuuawa na mali yake kuporwa. Sa`nani, mmojawapo wa waunga mkono wa fikra za Mohammad Ibn Abdul-Wahhab katika kitabu kiitwacho: “Tanziih ul-i`tiqad” 84

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 84

5/31/2016 7:38:10 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

anasema: “Mungu ameona dua kama ni kuabudu na amesema: “Mola Wenu anasema, ‘Niiteni, na Mimi nitaitikia (dua zenu)!’ Kwa kweli wale wenye kudharau ibada Yangu wataingia jahannam wakiwa wamefedheheka kabisa.” Hivyo yeyote anayemuita Mtukufu Mtume  au mtakatifu wa Mungu kutaka kupata kitu fulani, au kuomba msaada wa maombezi kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu toka kwao ili wafanikiwe matakwa yao, kama vile unafuu wa deni au tiba ya maradhi, na kadhalika, ameomba dua (ameomba msaada kwa) Mtukufu Mtume  au mtakatifu huyo, na dua inachukuliwa kama ibada, na kwa kweli dua ni kiini cha ibada. Mtu kama huyo ameabudu kitu kingine zaidi ya Mungu na amekuwa mkana Mungu, kwa sababu “Tauhidi” haikamiliki isipokuwa mtu amuone Mungu ni pekee katika uungu. Katika kuwa Muumbaji na Mfadhili (Mpaji). Na anajizuia kufikiria kitu kingine chenye uhai kama Muumbaji au Mfadhili (Mpaji), na haabudu kitu kingine isipokuwa Yeye. Hapana yeyote anaweza kutekeleza baadhi ya maombi kwa kiumbe kingine isipokuwa Mungu.” (Tanziih al-Itqaad) Matamko kama kwa ufasaha ni yale ambayo yanarudiwarudiwa katika vitabu vyao. Marejeleo yao ya fatwa ambayo yanatangaza ukafiri wa wale ambao hukiomba kitu kingine pamoja na Mungu, ni Aya ya Qur`ani Tukufu ambayo imetajwa hapo juu katika maneno ya San`ani, na pia Aya zingine kama hizi zifuatazo:

‫اج َد للِهَّ ِ فَ اَل تَ ْد ُعوا َم َع للاهَّ ِ أَ َحدًا‬ ِ ‫َوأَ َّن ْال َم َس‬ “Na hakika misikiti yote ni ya Mwenyezi Mungu, basi musimuombe yoyote pamoja na Mwenyezi Mungu.” (Surat Al-Jinn; 72:18).

ِّ ‫لَهُ َد ْع َوةُ ْال َح‬ ‫ق ۖ َوالَّ ِذينَ يَ ْد ُعونَ ِم ْن ُدونِ ِه اَل يَ ْست َِجيبُونَ لَهُ ْم بِ َش ْي ٍء‬ 85

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 85

5/31/2016 7:38:10 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

“Kwake ndiyo maombi ya haki. Na hao wanaoomba badala Yake hawajibiwi chochote……..” (Surah Al-Ra`d; 13:14).

‫ون للاهَّ ِ ِعبَا ٌد أَ ْمثَالُ ُك ْم ۖ فَا ْد ُعوهُ ْم فَ ْليَ ْست َِجيبُوا لَ ُك ْم إِ ْن ُك ْنتُ ْم‬ ِ ‫إِ َّن الَّ ِذينَ تَ ْد ُعونَ ِم ْن ُد‬ َ‫صا ِدقِين‬ َ “Hakika hao mnaowaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, ni waja mfano wenu. Hebu waombeni nao wawaitikie kama ikiwa ninyi mnaseama kweli.” (Al-A`araf, 7:194)

Wao huhitimisha kutokana na aya hizi, kwa ufasaha hiki ndicho kilichotajwa katika tamko la Sa`nani. Kufuatana na waonavyo wao, hapana mtu mwenye haki ya hata kusema: “Ewe Mjumbe wa Mungu, nakuomba uniombee kwa Mungu”, kwani akifanya hivyo tayari amekwishakuwa mkana Mungu na ambaye ni halali kuuawa. Kwa hukumu hii, wanaua maelfu kwa maelfu ya watu na kupora rasilimali zao. Sasa tunarudi ndani ya Qur`ani Tukufu, na kuuliza kuhusu maana ya dua kutoka katika Qur`ni Tukufu, na inatufafanulia kwamba dua na kuwaita wengine pamoja na Mungu kwa wakati mwingine ni uasi na wakati mwingine ni uaminifu; lakini watu hawa kwa sababu ya kupungukiwa elimu au tafsiri zisizo sahihi, wamepotoka mno. Hata hivyo, neno dua limetokea katika Qur`ani Tukufu likiwa na maana zilizotofauti: 1.

Dua inayomaanisha ibada katika aya ya 18 ya Surah AlJinn:

‫فَ اَل تَ ْد ُعوا َم َع للاهَّ ِ أَ َحدًا‬

86

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 86

5/31/2016 7:38:10 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

“…..basi msimuombe yoyote pamoja na Mwenyezi Mungu.” Al-Jinn, 72:18

Fungu la maneno ‘pamoja na Mwenyezi Mungu’ linaonesha kwamba hii aya tukufu inawaamuru watu wasimchukulie mtu yeyote kama mshirika wa Mungu wala kumuabudu yeyote pamoja na Yeye. Shahidi wa madai haya ni Aya ya 20 ya Surah hii hii ambayo inatenganishwa na aya moja katikati, ambayo inasema:

ُ ‫قُلْ إِنَّ َما أَ ْد ُعو َربِّي َو اَل أُ ْش ِر‬ ‫ك بِ ِه أَ َحدًا‬ “Sema: Hakika mimi namwomba Mola Wangu tu, wala simshirikishi na yoyote.” (Surah Al-Jinn, 72:20)

Kila Muislamu anatambua kwamba dua katika maana hii, ni mahususi kwa Mungu, na Yeye hana mshirika, na hakuna nafasi ya shaka na tuhuma. 2.

Dua katika maana ya kuita kwa mintarafu ya kitu, uitaji wa aina ile kama kile kinacho taarifiwa kuhusu Nabii Nuh , ambapo Qur`ani Tukufu inasema:

ُ ْ‫قَا َل َربِّ إِنِّي َدعَو‬ ‫ت قَوْ ِمي لَي اًْل َونَهَارًا فَلَ ْم يَ ِز ْدهُ ْم ُدعَائِي إِ اَّل فِ َرارًا‬ “Akasema: Ee Mola Wangu! Hakika mimi nimewalingania watu wangu usiku na mchana. Lakini mlingano wangu haukuwazidisha ila kukimbia.” (Surah Nuh; 71:5-6)

Ni dhahiri kwamba ulinganiaji huu na kuwaita watu, ni sawa na kuwaita watu kwenye uaminifu, na wito kama huu unafanana na ule wa uaminifu na utekelezaji wake ni wajibu wa Mitume wa Mungu. Na vivyo hivyo, Mungu anamwambia Mtume wa Uislamu:

87

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 87

5/31/2016 7:38:10 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

ُ ‫ا ْد‬ ۚ ‫ك بِ ْال ِح ْك َم ِة َو ْال َموْ ِعظَ ِة ْال َح َسنَ ِة ۖ َو َجا ِد ْلهُ ْم بِالَّتِي ِه َي أَحْ َس ُن‬ َ ِّ‫يل َرب‬ ِ ِ‫ع إِلَ ٰى َسب‬ “Waite kwenye njia ya Mola Wako kwa hekima na mawaidha mazuri na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora…..” (Surah An-Nahl, 16-125)

3.

Dua katika maana ya kuomba kwa ajili ya haja, mathalani:

ۚ ‫ب ال ُّشهَدَا ُء إِ َذا َما ُد ُعوا‬ َ ْ‫َو اَل يَأ‬ “…..Na mashahidi wasikatae waitwapo…..” (Surah Al-Baqarah, 2:282 )

Wito na ulinganiaji kama huo hufanywa katika mambo ya kawaida, na kwa hakika yeyote anayetekeleza haiwezekani awe kafiri, lakini kwa kweli atakuwa anatii amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Wakati mwingine inakuwa kwa njia isiyokuwa ya kawaida, miujiza, ambayo inaweza kuwa ya aina mbili: Inaweza kuambatana na imani katika manufaa kutoka kwa Mungu bila kutegemea kitu kingine, na inaweza kuwa maombi ya msaada kupitia kwa mtu mashuhuri kumwomba Mungu kwa niaba yetu kwa kile tunachokitaka. Aina ya kwanza ni namna ya Shirki, kwa sababu mategemeo pekee katika athari ni kutoka kwa utakatifu hasa wa Mungu; sababu zote za kawaida na athari hupata yote kutoka kwa Mungu na hutekeleza kwa idhini yake tu. Juu ya msimamo huu Qur`ani Tukufu inasema:

ً‫قُ ِل ا ْد ُعوا الَّ ِذينَ َز َع ْمتُ ْم ِم ْن ُدونِ ِه فَ اَل يَ ْملِ ُكونَ َك ْشفَ الضُّ ِّر َع ْن ُك ْم َو اَل تَحْ ِو ا‬ ‫يل‬ 88

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 88

5/31/2016 7:38:10 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

“Sema: Waombeni hao mnaodai badala Yake, hawawezi kuwaondolea madhara wala kuyabadilisha.” (Surah Bani Israil; 17:56)

Hakuna muumini mwenye kuelewa au Muislamu aliye mwaminifu anashikilia imani kama hiyo kuhusu yeyote miongoni mwa Mitume au watakatifu wa Mungu. Kuhusu aina ya pili, ni Tauhidi ambapo mtu humchukua mtu mwingine kuwa muombezi na mpatanishi kwenye mlango wa Mungu. Na anaona kuwa Mungu ndiye msababishaji wa visababishi vyote na anafahamu kila kitu chini ya ukuu Wake na mamlaka Yake, bado kukimbilia kwa watakatifu wa Mungu, huwaomba wao wamuombee kwa Mungu, na hii ndiyo Tauhidi na imani sahihi katika Ufadhili Mkuu wa Mungu. Qur`ani Tukufu inasema: Wana wa Israil walimwendea Nabii Musa  na wakamuomba amuombe Mungu awape vyakula vya aina mbalimbali (badala ya manna na kituitui):

ُ ‫اح ٍد فَا ْد‬ ‫ك ي ُْخ ِرجْ لَنَا ِم َّما‬ َ َّ‫ع لَنَا َرب‬ ِ ‫َوإِ ْذ قُ ْلتُ ْم يَا ُمو َس ٰى لَ ْن نَصْ بِ َر َعلَ ٰى طَ َع ٍام َو‬ ُ ِ‫تُ ْنب‬ ‫ت أْالَرْ ضُ ِم ْن بَ ْقلِهَا َوقِثَّائِهَا‬ “Na mliposema: Ewe Musa! Hatuwezi kuvumilia kwa chakula cha namna moja tu. Basi tuombee Mola wako atutolee vile vinavyooteshwa na ardhi miongoni mwa mboga zake, na matango yake…….” (Surah Al-Baqarah, 2:61)

Nabii Musa  kamwe hakulalamika kuhusu maelezo yao kwake! Hakugeuka na kusema: ‘Kwa nini msimuombe Mungu ninyi wenyewe moja kwa moja, kwa sababu kitendo hiki mnachokifanya ni kumkufuru Mungu, na kwamba mnaabudu miungu wengi.’ Kinyume chake, alimuomba Mungu kwa ajili ya ombi lao. Na ombi hilo lilikubaliwa. “kwa kweli mtapata kile mlichokiomba!” Licha ya 89

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 89

5/31/2016 7:38:10 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

hayo aliwaambia kwamba waliacha vyakula bora na kutaka vyakula duni. Hitimisho: Kundi hili la Uwahhabi, badala ya kurejelea Qur`ani Tukufu na kuona matumizi kadhaa ya ‘Dua’ na kuyaweka pembezoni mwa kila moja na kugundua kina cha mafundisho ya Qur`ani Tukufu juu ya suala la dua, wao walifanya uchunguzi wa Aya chache tu na kuchezea mambo kwa maslahi yao, na halafu wakawahukumu Waislamu walio wengi kama makafiri na wanaoabudu miungu wengi. Na hata la kusikitisha zaidi ya hilo, walitekeleza hilo kwa vitendo, na wakawaua idadi kubwa ya Waislamu waaminifu na kupora rasilimali zao. Bidaa: Neno la sita la Qur`ani Tukufu ambalo limetafsiriwa kimakosa na kundi hili la Uwahhabi, ni ‘Bid`ah’ (au kuanzisha jambo upya). Wakati Qur`ani Tukufu inashutumu na kulaumu suala la mfumo wa utawa, inasema:

‫ان للاهَّ ِ فَ َما‬ ِ ‫َو َرحْ َمةً َو َر ْهبَانِيَّةً ا ْبتَ َد ُعوهَا َما َكتَ ْبنَاهَا َعلَ ْي ِه ْم إِ اَّل ا ْبتِغَا َء ِرضْ َو‬ َّ ‫َرعَوْ هَا َح‬ ۖ ‫ق ِرعَايَتِهَا‬ “…..Na utawa wameuzua wao. Hatukuwaandikia hayo, ila kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu. Lakini hawakufuata inavyotakiwa kuufuata…..” (Surah Al-Hadid, 57:27)

Wakristo walianzisha aina ya mfumo wa utawa na kanusho, mambo ambayo hawakupewa na Mungu, hata hivyo kamwe hawakuambatana nayo. Maana ya Aya ni kwamba Mungu hakuwaele90

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 90

5/31/2016 7:38:10 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

keza kuanzisha mfumo wa utawa (lakini hilo lilikuwa ni jambo jipya la kwao wenyewe). Mwenyezi Mungu Mtukufu alipendekeza ‘Kutafuta radhi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu,’ jambo ambalo hawakulizingatia kamwe. Kwa vyovyote vile, Aya hii inalaumu aina hii ya bidaa, ambayo kufuatana na baadhi ya wanahistoria, ilitokeza karne chache tu baada ya Nabii Isa , kwa sababu ya matukio fulani ya kihistoria ambayo yalikuwa matokeo ya kushindwa kwa Wakristo. Wakristo waliposhindwa walilazimika kukimbilia milimani na majangwani na kupata kimbilio la hifadhi katika maisha ya upweke, hatimaye mfumo wa utawa ukachukua vazi la kidini. Mwanzoni watawa wanamume Wakristo (Anchorites) walianzisha ‘makazi ya watawa.’ Baadaye, waliungana na watawa wanawake Wakristo (anchoresses) na mfumo wa utawa ukaanzishwa. Miongoni mwa hadithi ambazo zilikuwa sambamba na mfumo wa utawa kimakosa ni kanusho kamili la ndoa, ambalo lilikuwa kinyume na msingi wa asili wa binadamu na ndiyo umekuwa msingi wa kufisidi mfumo huo. Will Durant (1885-1981) mwanahistoria mashuhuri wa nchi za Magharibi amezungumzia kuhusu watu wanaotawa, jambo ambalo linashika usikivu. Anakiri kwamba watawa wanawake kuungana na watawa wanamume ni tukio ambalo lilianza mnamo karne ya nne na mafanikio ya mfumo wa utawa yalifika kileleni mnamo karne ya kumi.36 Pamoja na kwamba watawa wanamume na watawa wanawake walifanya huduma nyingi mbalimbali za kijamii, lakini ufisadi wa kijamii na kimaadili ambao ulijitokeza miongoni mwao ulikuwa wa kufedhehesha hasa, na yeye anadhani ni bora zaidi kuacha kuzun36

Hadithi ya Ustaarabu (The Story of Civilization, vol. 13, pg. 443.) 91

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 91

5/31/2016 7:38:10 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

gumzia mfumo huo. Hili limeandikwa kwenye vitabu vilivyoandikwa na wanahistoria Wakristo. Kwa kweli, matokeo ya bidaa yamepotoka hasa. Hata hivyo, kwa nyongeza ya Aya iliyotajwa hapo juu, zipo hadithi nyingi zinazolaumu bidaa ambazo zimehadithiwa na vyanzo vya Kiislamu. Miongoni mwa hadithi hizo ni ile hadithi mashuhuri kutoka kwa Mtukufu Mtume : ‘Kila Bidaa ni upotovu,’! ambayo imetajwa kwenye vitabu vingi kama vile Musnad Ahmad Jz. 4, uk.126, Mustadrak al-Sahihayn Jz. 1, uk. 97, Sunan al-Baihaq Jz.10, uk.114, al-Mu`jam al-wasat Tabrani Jz. 1, uk. 28 na Sunan ibn Majah Jz. 1, uk.16. Wafuasi wa Uwahhabi wenye ukereketwa wa kupindukia, wanaposoma hadithi kama hizo, bila ya kuelewa maana ya bidaa, mwanzoni walipinga jambo lolote jipya, hadi wakaiita baiskeli chuma cha Shetani, na walipinga hata simu. Walipoona dunia inakwenda mbele haraka sana kwa mintarafu ya viwanda, hatimaye walikubaliana na jambo la viwanda vya nchi za Magharibi. Si tu kwamba walikubaliana na jambo hilo, walishinikizwa ndani ya jambo hilo, na leo hii tunaona Saudi Arabia imejaa mitindo mbalimbali ya aina za motokaa za kisasa, vifaa vya kisasa vya uingizaji hewa, samani za makazi za kuvutia sana na hata aina mbalimbali za maduka makubwa (supermarkets) na vyakula vya nchi za Magharibi, ambavyo kila mtu anakula, watu wazima, watoto, wasomi na wasio wasomi. Kwa sasa, wameacha kupinga ujio wa haya mambo mapya yaani bidaa, na wameelekeza upinzani wao kwa ujio wa mambo mapya kwamba, kufuatana na maoni yao, mambo hayo mapya (bidaa) ni katika dini. Mathalani, kujenga kaburi maalum la kuhifadhi maiti ya jamii moja, sherehe ya kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa (Maulid) Mtukufu Mtume  na watakatifu wa kidini, kumbukumbu za 92

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 92

5/31/2016 7:38:10 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

kuomboleza mashahidi wafia dini na mengine yafananayo na hayo yanalaaniwa kama bidaa. Yeyote anayetekeleza shughuli hizi anachukuliwa kuwa anafanya jambo jipya (bidaa) ambalo halipo katika dini na anastahili kukosolewa vikali. Lakini ni muhimu kujua maana ya bidaa (jambo jipya) na linaharamishwa katika mifano ipi? “Bid`ah” maana yake halisi ni kitu chochote kizuri au kibaya ambacho kimeongezwa katika dini, na kufuatana na wanazuoni wa falsafa ya sheria ni, “kuingiza jambo lisilo la dini na kuliweka katika dini.” Kama tukiambatanishia jambo ambalo si la dini na kuliweka katika dini, na kuliona jambo hilo kama amri ya Mungu, tutakuwa tumefanya uzushi yaani bidaa. Hii inafanyika katika njia mbili: kugeuza jambo la wajibu na kuwa jambo lililoharamishwa au kugeuza jambo ambalo limeharamishwa na kuwa jambo la wajibu. Na kugeuza kitendo ambacho kimeharamishwa na kuwa kitendo kilichohalalishwa au kugeuza kitendo ambacho kimehalalishwa na kukifanya ni kitendo kilichoharamishwa. Mathalani: kusema kwamba riba ni kitu kisichoepukika katika mfumo wa kibenki wa kisasa, kwa hiyo ni jambo ambalo linakubalika. Au amri ya kidini ya mwanamke kuvaa Hijabu ni jambo linalohusiana na mambo ya kizamani lakini leo hii ni ruhusa mwanamke kuacha kuvaa Hijabu, ni mifano ya bidaa kwa sababu haiendani na amri za Mungu na kutangaza kwamba jambo lililoharamishwa ni halali. Wakati fulani huwa tunafikiria kama ni sehemu ya dini jambo ambalo halikutajwa katika fatwa za kidini au katika Kitabu na hadithi; mathalani, kuchukulia kama mwenendo wa kitamaduni kama sehemu ya dini, kama vile shughuli ya maombolezo ya mazishi ya 93

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 93

5/31/2016 7:38:10 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

marehemu ndani ya siku ya tatu, saba na arobaini (baada ya kifo cha marehemu), au kuchukulia maadhimisho na kufurahi sana mnamo Idi (Eid) ya Kiislamu kama jambo ambalo limewajibishwa kidini. Bidaa ni za aina tatu: 1.

Bidaa katika mambo ambayo hayahusiani na mambo ya kidini, kama vile viwanda, ugunduzi wa kisayansi na sayansi asili pia ni mambo ambayo yalikuwepo wakati wa Mtukufu Mtume . Maendeleo ya sayansi na ugunduzi ni bidaa zenye manufaa na hujenga, na wasomi wote wa dunia walilikaribisha jambo lolote lenye manufaa - bila ubaguzi, bila kujali jambo hilo lilitoka mbari ipi au taifa gani.

2.

Bidaa zinazohusu mambo ya kidini, bila ya kuyahusisha na dini, kama vile kujenga msikiti kwa mtindo maalumu; Mihrabu, mpangilio wa marumaru ya sakafuni, nakshi za chini ya dari, kutumia vipaza sauti wakati wa kuadhini, na mamia ya bidaa kama hizo.

Kwa uhakika hakuna hata mojawapo ya mambo haya lililokuwapo wakati wa Mtukufu Mtume , lakini hakuna anayeyalaani kama ni Bidaa na mambo ambayo yameharamishwa, na misikiti yote ya Waislamu, hata nchini Saudi Arabia, vituo vya Uwahhabi na msikiti wa Mtukufu Mtume  imejaa vitu hivi. Pia mabadiliko makubwa, ambayo yamefanyika katika Masjid ul-Haram, kwa vyovyote vile yanafanana na yale ya wakati wa Mtukufu Mtume , kama vile kujenga ghorofa ya pili juu ya eneo la Sa`i (ibada ya kukimbia) baina ya Safa na Marwa, na mabadiliko mapya yasiyokuwa ya kawaida katika Jamarat, na uhamisho wa mahali pa machinjio na kuyapeleka nje ya Mina na mengine kama hayo. 94

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 94

5/31/2016 7:38:10 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

Bidaa hizi zipo pale kwa ajili ya kurahisisha kazi ngumu na kupunguza matatizo na hatari na hayachukuliwi kama fatwa maalumu za kidini wala hayachukuliwi kama Bidaa (katika maana ya kidini). Kupanga vikao vya mashindano ya kughani Qur`ani Tukufu na kuchagua washindi wazuri katika kughani, kuhifadhi na kufasiri Qur`ani Tukufu. Haya ni mambo ambayo hayakuwepo wakati wa Mtukufu Mtume ; haya mambo ni bidaa ambazo zinachukuliwa ni zenye kuleta maendeleo katika malengo na makusudio ya kidini, bila madai kwamba mambo haya ni sehemu ya dini. Vivyo hivyo, heshima inaoneshwa kwa marehemu kwa kufanya kumbukumbu yao katika mahali maalum na muda mwafaka. Licha ya kupanga makongamano haya na semina za kidini na kumbukumbu kwa ajili ya wanazuoni wa dini, kusherehekea siku za kuzaliwa voingozi wa dini na maadhimisho ya vifo vya mashahidi au vifo vya kawaida. Matukio kama haya hutumikia Uislamu na Waislamu katika kupigania njia ya haki, na husaidia katika kutengeneza utambuzi miongoni mwa Waislamu. Desturi hizi huamsha utambuzi na tahadhari miongoni mwa vijana, na mvuto kwa mintarafu ya elimu ya Qur`ani Tukufu na mambo ya kidini, na kusitisha mipango kama hii inaweza kusababisha hasara kubwa kwa Waislamu. Huu ni mlolongo wa desturi ambazo hakuna mtu anayezichukulia kama amri zitokazo kwa Mungu au Mjumbe Wake wakati zinapotekelezwa. Kwa maneno mengine, kujumuisha zile ambazo sio sehemu ya dini na kuziingiza katika dini bila kufikiria kama zimeamriwa kimungu. Kwa hiyo, ni makosa kusema kwamba desturi hizi ni Bidaa kwa dhana kwamba ‘Kila Bidaa ni mkengeuko,’ hivyo inatakiwa kuchukuliwa kama upotovu. 95

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 95

5/31/2016 7:38:10 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

3.

Ipo aina nyingine ya bidaa, kama bidaa iliyoharamishwa, ambayo ilirejelewa mwanzoni; kuvunja mahali patakatifu pa kidini pasipostahili kuvunjwa na kuanzisha fatwa dhidi ya fatwa ya kidini, au kuongeza au kupunguza fatwa bila ya kuwepo sababu yoyote ya kufanya hivyo katika dini.

Lakini wafuasi wa Uwahhabi wenye ukereketwa wa kupindukia, kwa sababu ya wao kutokuwa na elimu ya kutosha ya falsafa ya sheria ya Kiislamu na kanuni za falsafa ya sheria, (mbinu za kuelewa sheria kutoka kwenye vyanzo vya Kiislamu) hushindwa kutofautisha baina ya hizi aina tatu za bidaa, na kwa sababu ndogo sana wao huwashutumu ndugu zao Waislamu kwa ajili ya Bidaa, kwa urahisi sana kama wanavyowashutumu kwa kuabudu miungu wengi. Tunamalizia mazungumzo haya kwa kuonesha semi kutoka kwa mwanazuoni mashuhuri wa Masjidul-Haram, Yusuf bin Alawi Maleki: Yafuatayo chini ni maelezo yake mafupi ya Bidaa yaliyopo katika kitabu chake kiitwacho: “The Concepts That Need to be Corrected” chini ya kichwa cha habari: Good and Bad Innovations: Baadhi ya wafuasi wa Uwahhabi wenye ukereketwa uliopindukia ambao ni dhalili, wajinga na wenye akili finyu ambao bila ulazima hujihusisha kwa masalafi waadilifu, hukampeni na kukataa kila ugunduzi unaofaa kwa dhana kwamba hiyo ni bidaa na kila bidaa ni upotovu, bila kutofautisha baina ya bidaa sahihi na uasi37 au kutofautisha baina ya bidaa nzuri na bidaa mbaya. Utofautishaji huu unathibitishwa na akili ya kawaida na akili ya kisomi, na wanazuoni mashuhuri wa kanuni za falsfa ya sheria kama vile Nawawi, Suyuuti, Ibn Majar na Ibn Hazm wamekubaliana na utofautishaji huu. Wakati tunapoweka pamoja hadithi za Kitume ambazo hujitafsiri 37

Bidaa katika dini ambayo haikuegemezwa kwenye Qur`ani Tukufu au Sunnah. 96

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 96

5/31/2016 7:38:10 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

zenyewe, na kuzipitia upya kwa pamoja, hitimisho hilo hilo ndilo litakalopatikana. Miongoni mwa hadithi hizi ni: Kila Bidaa ni upotovu, ambayo inalaani zile bidaa zilizo potovu ambazo huja bila kuwa chini ya kanuni za dini. Anaongeza: bidaa katika maana yake halisi (yaani kitendo au mlolongo wa kugundua au kuanzisha kitu kipya), haijaharamishwa, kile ambacho kimeharamishwa na kuchukuliwa kama upotovu ni bidaa katika maana yake ya kidini kama “Kuongeza kitu katika fatwa ya kidini na kukipatia hadhi na muonekano wa kidini” kwa dhana kwamba kimeingizwa na mwenye dini, kwa lazima kikubalike na kutekelezwa. Lakini kidunia kwa vyovyote vile, bidaa hazijaharamishwa. Kwa hiyo, kugawanya bidaa katika matawi mawili; bidaa nzuri na bidaa mbaya, ni maana isiyo na uvumbuzi. Kwa hakika, bidaa ya kidini ni ya aina moja tu, ambayo ni ile iliyoharamishwa, na kama wale wanaopinga mgawanyo huu wangekuwa wanajua maana ya chanzo cha mgawanyo, hawangepinga na wangetambua kwamba upinzani ni wa kimisamiati tu. Kwa kweli, miongoni mwa bidaa za kidunia, mambo mengi yenye manufaa yanaonekana ambayo lazima yafuatiliwe, ambapo yapo mambo ambayo si chochote isipokuwa fitina na ufisadi. (Ifanywe rejelea kwenye baadhi ya ubadhirifu wa kijamii)38

38

‘Dhana zinazohitaji kusahihishwa’ uk. 102 na kuendelea 97

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 97

5/31/2016 7:38:10 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

SEHEMU YA 7 WITO 1.

Wito ulionyanyuliwa kutoka Makka. Yusuf bin Alawi na ukosoaji wake wa kijasiri:

Yusuf bin Alawi alikuwa mwanazuoni jasiri, ambaye aliishi Makka na alikuwa na kundi la aina ya pekee la wanazuoni na wasomi. Watu ambao ni mabingwa wa kisiasa nchini Saudi Arabia katika kuongoza shughuli za kiserikali walimheshimu sana. Amefariki dunia hivi karibuni na wimbi la huzuni na majuto lilijaa katika kanda yote. Yeye alijiita mtumishi wa elimu takatifu katika Jiji Takatifu na alikuwa mfuasi wa imani ya Maliki. Alikuwa dhuria wa Zahra  mtoto wa kike wa Mtukufu Mtume Muhammed  na aliona fahari kuremba jina lake kwa cheo cha Al-Husna (Mzuri) Mduara wake wa mafunzo katika Masjid-ul-Haram ulikuwa na watu wengi sana katika Msikiti, na pia aliandika vitabu vingi juu ya sayansi za Kiislamu. Kwa kweli yeye alikuwa anapinga Uwahhabi uliovuka mpaka, waumini wenye msimamo mkali na hatimaye aliandika kitabu kiitwacho “The Concepts That Need to be Rectified” 39 akikosoa fikra zao na imani yao. Yeye alikosoa msingi muhimu sana wa kiitikadi wa kundi hili lenye ukereketwa wa kupindukia katika njia nzuri ya kiwanazuoni 39

Kitabu hiki kilichapishwa mara kumi katika kipindi cha miaka kumi. Katika kipindi cha mwaka moja tu kitabu hiki kilichapishwa mara nne na kikawa na mvuto mkubwa miongoni mwa watu katika nchi nyingi za Kiislamu, pamoja na Saudi Arabia! 98

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 98

5/31/2016 7:38:10 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

na katika namna ya upole. Na yeye alitegema zaidi katika Aya za Qur`ani na Hadithi za Mtukufu Mtume  zilizosimuliwa na vyanzo thabiti, uthibitisho wa hadithi hizo ambao, hata wafuasi wa Uwahhabi wenye ukereketwa uliopindukia hawakuweza kukanusha. Alikuja kwenye jukwaa kwa dhana kwamba katika akili za kundi hili palikuwepo na mlolongo wa fikra ambazo zilihitaji kusahihishwa, kwa sababu kundi hili lilikuwa linawatangaza Waislamu kuwa makafiri na lilijiruhusu kuwaua na kupora rasilimali zao, na kuharibu umoja wa Waislamu. Anastahili kupewa shukurani nyingi kwa juhudi zake zisizo na ukomo, aliweza kulishughulikia jambo hili vizuri kabisa. Kitabu hiki ni cha pekee kwa sababu fulani kadhaa: 2.

Idadi kubwa ya wanazuoni mashuhuri wa madhehebu ya Sunni nchini Misri, Morocco, Sudan, Bahrain, Pakistan, Falme za Kiarabu (the Emirates) na nchi zingine, ziliandika mapitio ya kuthibitisha juu ya kitabu hiki zikisifu ujasiri wake katika kuwasilisha fikra zake katika kitabu hiki ambacho kimefanyiwa mapitio 23 yenye kurasa 70 yaliyotangulia mswada wake.

3.

Kitabu hiki kilichapishwa “Dubai” na pamoja na kuwepo na udhibiti mkali ambao Salafi walilazimisha kuhusu mauzo ya kitabu hiki katika ufalme wa Saudi ambamo hawakuruhusu kitabu chochote kinachokosoa fikra zao kuingia nchini humo, kitabu hiki kilikuwa kinauzwa waziwazi katika masoko ya Makkah ambapo ndipo sisi tulipata fursa ya kukinunua. Hii inaonesha kwamba tabaka jipya la Uwahhabi haliungi mkono fikra za Salafi wenye msimamo mkali, na wanachukulia kuwa ni muhimu kuyafikiria upya. 99

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 99

5/31/2016 7:38:10 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

Mapitio ya kitabu hiki: Hapa yapo mapitio matatu tu ambayo yaliandikwa juu ya kitabu hiki na wanazuoni mashuhuri, kuonesha dunia ya Kiislamu inafikiria nini juu ya tabaka la wafuasi wa Uwahhabi lenye msimamo mkali: 1.

Dkt. Abdul Fattah Barakah, ambaye ni katibu mkuu wa Kongamano la Mjadala wa Kiislamu, ameandika katika mapitio yake:

“Katika kitabu hiki chenye thamani, jaribio kubwa sana na juhudi imefanywa kwa niaba ya mwanazuoni msomi aliye mwangalifu katika kuwaunganisha Waislamu waliotawanyika na kuondosha ishara zote za ushabiki uliopindukia kutokana na mambo madogo, na maamuzi ya kibinafsi, katika kuwashutumu Waislamu kwamba wana imani ya kuabudu miungu wengi na kumkufuru Mungu, kuhusu suala la kuomba msaada wa maombezi, kuhiji Sehemu Takatifu ya Mtukufu Mtume , na masuala mengine muhimu. Inatumainiwa kwamba kitabu hiki chenye thamani kitasaidia katika kuunganisha Waislamu na kuondoa hoja zinazobishaniwa”40 2.

Sheikh Ahmad Al-Ewadh, kiongozi wa Kongamano la Fatwa za Kidini nchini Sudan ameandika katika mapitio yake:

“Kwa bahati nzuri nilipata taarifa kuhusu kitabu ambacho kimeandikwa na msomi mheshimiwa Bin Alawi Maliki Makki Hasani - mtumishi wa elimu katika Sehemu Mbili Tukufu - kiitwacho Concepts That Need to be Rectified (‘Dhana zinazohitaji kusahihishwa’). Kitabu hiki kinazungumzia kuhusu masahihisho ya fikra za kimakosa ambazo zinahusiana na mambo matatu: Kwanza ni mjadala wa kiitikadi ambapo amethibitisha kupitia akili yenye mantiki na uthibitishaji kwa haki kwamba viwango vili40

‘Dhana zinazohitaji kusahihishwa’ uk. 29-30 (pamoja na mukhtasari kidogo) 100

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 100

5/31/2016 7:38:10 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

vyochaguliwa na kundi la Uwahhabi kuhusu kumkufuru Mungu na upotovu ni rubuni. Pili ni mazungumzo yanayohusu Mtukufu Mtume wa Uislamu  na uhalisia wa Utume. Akiwa na sababu zenye msimamo, amethibitisha dhana ya kumtakia mtu heri kupitia kwa Mtukufu Mtume  kuwa ni sahihi na matokeo yake yanayofuata. Mjadala wa tatu unahusu dunia ya usuluhishi41 na uhalali wa kuzuru Sehemu Takatifu ya Mtukufu Mtume  na mambo mengine yanayohusiana na hayo. Mwanazuoni huyu amesahihisha kwa uangalifu na kufuzu, fikra potovu.’42 3. Abdul Salam Johran, kiongozi wa Kongamano la Kisayansi la Kikanda nchini Morocco, pamoja na wajumbe wa Kongamano hilo, kwa pamoja wameandika mapitio yenye kueleweka ya kitabu hiki. Sehemu ya mapitio hayo ni kama yafuatayo: “Kitabu hiki kilipoingia mikononi mwa wanazuoni weledi, wote waliidhinisha na kumsifu mwandishi kwa kutekeleza wajibu huu mbele ya Mungu, Mtukufu Mtume  na ummah wa Kiislamu, ambao ni wajibu wa wanazuoni wote…. Kwa hiyo wajumbe wa Kongamano la Kisayansi la Morocco chini ya uongozi wa kiongozi wa Kongamano hilo walitangaza uthibitisho wao juu ya kitabu chote, walitoa shukurani zao kwa mwandishi huyu mashuhuri, na kumpongeza kwa kuelewa kazi hii muhimu.”43   Kipindi cha mpito baina ya kifo na ufufuo.  ‘Dhana zinazohitaji kusahihishwa’ uk. 37 43  ‘Dhana zinazohitaji kusahihishwa’ uk. 68 41 42

101

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 101

5/31/2016 7:38:10 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

Zaidi ya hayo, katika kukisifu kitabu hiki, beti za mashairi za kusisimua na kugusa hisia zilitungwa na washairi mashuhuri, ambazo miongoni mwao tutagusia beti tatu tu. Beti hizi tatu, zinatokana na shairi ambalo Sheikh Muhammad Salem Adood, aliyekuwa Kiongozi wa Mahakama ya Sheria nchini Mauritania na mjumbe wa Jumuiya ya Kongamano la Falsafa ya Sheria la Umma wa Kiislamu1 lililoundwa Makkah: “Kutatiza, iliyokosewa na tata; Dhana hubainishwa na yeye kwa ajili yetu; Udanganyifu upumbavu na uwongo hutoweka; Wakati ambapo matumizi safi ya akili na furaha ya ushahidi; Jinsi gani Alawi ameweza kuziweka dhana hizi kwa wazi kwa urahisi; Hapajatokea mwanazuoni mashuhuri kufanya hivi katika kipindi cha karne nyingi”44 Yaliyomo katika kitabu hiki: Kitabu hiki kimekosoa imani za wafuasi wa Uwahhabi wenye ukereketwa wa kupindukia katika maeneo matatu makuu na kimebainisha udhaifu wao kwa njia ya rejea kwenye Aya za Qur`ani Tukufu na Hadithi zilizothibiti. Eneo la kwanza: Masuala yahusuyo imani na yasiyohusu imani. Anabainisha: “Watu wengi (Salafi wenye msimamo mkali), Mwenyezi Mungu Mtukufu naawajalie wajisahihishe, wamepotoka katika kuelewa kanuni ambazo humtenganisha mtu na Uislamu, kwa kiasi ambacho 44

‘Dhana zinazohitaji kusahihishwa’ uk. 55 102

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 102

5/31/2016 7:38:10 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

kwamba yeyote anayekataa kukubaliana nazo, ni kwamba, takribani Waislamu wote hapa duniani - isipikuwa walio wachache sana - huchukuliwa na wao kama wasioamini!” Yeye anaamini kwamba kiongozi wa imani hii hakuwa anapenda ukereketwa wa kupindukia kama huo. Amerejelea Hadithi mashuhuri ya Mtukufu Mtume  isemayo: “Kuwatukana Waislamu ni ufisadi wa kupindukia na kuwaua Waislamu ni kutosadiki.” Na inakaripia vikali kuwakashfu na kuwalaumu Waislamu. Ametoa sababu za kutosha katika kubainisha mipaka ya kuamini na kutokuamini. Tokea hapo na kuendelea, anaonesha hoja zao zenye hitilafu ambazo zimewaelekeza kwenye dhana zilizokosewa. Ni jambo la kuvutia kuona kwamba wakati fulani sauti yake dhidi ya waumini wa Salafi inakuwa kali, na mara nyingi yenye hasira pale ambapo msamiati wa dharau unatumiwa na wao. Mathalani, ananukuu kutoka kwenye kazi zao: “Wakati mwingine watu huomba vitu kutoka kwa Mitume na Watakatifu wengine kwamba hapana yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye Mwenye uwezo wa kufadhili na hii ni Imani ya kuabudu miungu wengi (kutokusadiki),” Katika kujibu amesema: “Usemi huu unatokana na kutokuwa na elimu ya kutosha na uelewa wa desturi ambayo imekuwepo miongoni mwa Waislamu tangu mwanzo. Watu huwasihi watu hao wenye huruma wawaombee kwa Mungu na kuomba Utukufu Wake kutatua tatizo lisilowezekana kutatuliwa, na mifano mingi isiyo na hesabu ya uombezi huu kwa Mitume inaonekana katika hadithi thabiti za Kiislamu; kama vile, tiba ya maradhi yasiyo na tiba, kuomba mvua inyeshe, kububujika kwa maji ya chemchem kutoka kwenye ncha za vidole vya Mtukufu Mtume , kiasi kidogo cha chakula kuweza kuwatosha kabisa kundi kubwa la watu, na mifano mingine mingi kama hiyo.” 103

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 103

5/31/2016 7:38:10 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

Mwishoni mwa eneo hili anashauri: “Hivi hawa wafuasi wa Salafi wanaelewa maana ya Tauhidi na Kufuru (Ukafiri) vizuri zaidi kuliko Mitume ? Hiki ni kitu ambacho hakuna Muislamu mjinga achilia mbali wanazuoni, anayeweza kuthubutu kufikiria.”45 Sauti ya mtu huyu ni yenye upole katika maelezo yake yote, lakini lugha yake imekuwa kali dhidi ya vurugu zao, mashitaka ya ufisadi wa kupindukia na matamko ya kutukana. Eneo la Pili: Katika eneo hili, Alawi anabainisha cheo cha juu cha Mtukufu Mtume wa Uislamu  kufuatana na Qur`ani Tukufu na Hadithi za Kiislamu. Halafu anaelezea dhana ya kupata baraka kutoka kwenye dalili za Mtukufu Mtume  na jinsi gani upatikanaji huu wa baraka usivyohusiana na imani ya kuabudu miungu wengi. Baada ya hapo anaelezea matukio mengi yaliyotajwa katika hadithi na matamko ya wanazuoni kuhusu idhini ya kupata baraka kwa kubusu mkono wa Mtukufu Mtume . Kupata baraka kutoka kwenye chombo alichokuwa akinywea maji Mtukufu Mtume . Kupata baraka kutoka Nyumba yake Tukufu, kutoka Mimbari yake Tukufu na Kaburi lake Tukufu, na kutakasa kumbukumbu za Watukufu Watakatifu na Mitume wa kabla yake . Amenukuu ushahidi wake zaidi kutoka katika vitabu mashuhuri vya wanazuoni wa Sunni ili pasiwepo na mwanya wa shaka yoyote, na halafu anataja masahaba ambao walipata baraka kutoka katika kumbukumbu za Mjumbe wa Mungu . Yeye anashangaa kawa nini pamoja na kuwepo hadithi zote hizi zilizowazi na ushahidi uliothibiti, kundi la watu wenye masikio na 45

‘Dhana zinazohitaji kusahihishwa’ uk. 181 104

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 104

5/31/2016 7:38:10 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

macho yaliyofumbwa, linakataa ukweli huu na kuulaani kama aina fulani ya ujinga na fitina.46 Eneo la Tatu: Sehemu ya kitabu hiki inashughulikia masuala mengi ya ubishani. Suala muhimu kuliko yote ni hili la pendekezo la kuzuru Kaburi Takatifu la Mtukufu Mtume  na kuomba dua pembezoni mwa kumbukumbu hiyo takatifu wa ukumbusho, na kupata baraka kutoka katika dalili zake Mtukufu Mtume . Alawi anaunga mkono hoja yake kwa kurejelea nukuu nyingi kutoka kwa wanazuoni mashuhuri wanaokubalika wa zama za kale. Mwishoni anabainisha nukta ambayo inakanushwa vikali sana na wafuasi wa Uwahhabi wenye ukereketwa wa kupindukia, na nukta hii ni, maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtukufu Mtume , siku ya kuhama kutoka Makkah kwenda Madina, siku ambapo Mtukufu Mtume  alikabidhiwa Utume, kuteremshwa kwa Qur`ani Tukufu, ushindi wa Waislamu katika vita vya Badr (vita ya kwanza ya Mtukufu Mtume , na usiku wa Katikati ya mwezi wa Shaaban. Wafuasi wa Uwahhabi wenye ukereketwa uliopindukia wanaamini kwamba vitendo hivi ni uzushi ulioharamishwa na hivyo wao huzuia utekelezaji wa maadhimisho na kumbukumbu za tarehe hizo kikatili. Katika busara iliyorahisi, Bin Alawi ametoa jibu la kimantiki kwa kuwaambia kwamba maadhimisho haya ni mambo ya kawaida, na hapana yeyote anayeyatekeleza kama fatwa ya kidini na, kwa hiyo, mambo haya hayahusiani na kuingiza jambo geni au kutokuin46

Ufupisho kutoka kwenye kitabu: “Dhana Zinazohitaji Kusahihishwa” uk.194-242. 105

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 105

5/31/2016 7:38:10 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

giza jambo geni katika dini. Lakini kwa hakika yanahusisha athari za maana sana ambazo zinatakiwa kuzingatiwa. Kwa namna yoyote ile ujumbe wa Uisalmu unatakiwa kuwasilishwa kwa watu katika makongamano haya matukufu. Anamalizia kwa kusema: “makongamano haya, katika hali halisi, ni matukio yenye thamani sana, ambayo lazima yalindwe na kupata manufaa yake katika namna iliyo nzuri, na wale wanaoyapinga na kujitahidi kuyafutilia mbali, ni wajinga na akili zao ni finyu.” Kumbukumbu Muhimu: Lengo la kuwasilisha dondoo kutoka kwenye kitabu hicho ni kushauri kwamba msingi wa matamko yake ambayo yamesokotana na busara, mantiki, heshima na ujasiri ni ya kweli na yanakubaliwa na sehemu kubwa ya wanazuoni mashuhuri wa Kiislamu wa nchi mbalimbali, pamoja na ufalme wa Saudi. Inaonesha kwamba wafuasi wa Uwahhabi wenye msimamo mkali wamemaliza muhula wao, ukizingatiwa ukweli kwamba kitabu ambacho kinashughulika katika kukaripia Uwahhabi wenye ukereketwa uliopindukia kinashangiliwa na ummah wa Kiislamu. Hata hivyo, ikiwa kama faida kwa ajili ya zawadi hii kubwa kwa ummah wa Kiislamu na hata kwa wafuasi wa Uwahhabi wenye msimamo wa kati walipokea tuzo yake. Kundi hilohilo la wafuasi wa Uwahhabi wenye msimamo mkali lilichapisha vitabu, ambamo mbinu ileile ya zamani na isiyo na adabu ya kutenganisha ilitumika na fatwa kwa ajili ya ukafiri wake ilitolewa. (Vitabu kwa jina la “Discourse with Maliki” na “Refutation to Maliki on his Misguidance and Indecency.”) Si tu kwamba vitabu hivi vililaaniwa na wasomaji lakini vilifikiriwa na mkusanyiko wa wanazuoni wa Al-Azhar kama vilikuwa 106

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 106

5/31/2016 7:38:10 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

vinahudumia Uzayuni na shambulio kwa umoja wa Uislamu. Bin Alawi alikuwa bado anaheshimiwa sana na watu wa Saudi Arabia, na makumi kwa maelfu ya watu walihudhuria maandamano ya mazishi yake, na viongozi wa Saudi walizuru makazi yake mara kadhaa kutoa mkono wa rambirambi kwa familia yake. Kiitikio hiki cha ummah kilionesha maoni ya jumla ya watu dhidi ya wafuasi wa Uwahhabi wenye ukereketwa uliopindukia na silaha yao ya kutenga na kuleta machafuko! Hata hivyo, mwanasheria mkuu wa Makkah alimuita katika mahakama ya Riyadh na akamtia hatiani. Alitetea maandishi yake kwa saa chache lakini na hatimaye alisema: “Huu ni uamuzi wangu binafsi. Hasa zaidi wewe ni mwanasheria Muislamu na hakuna mwanasheria anayeweza kulazimisha maoni yake kwa mwanasheria mwingine yeyote.” Mahakama ilimuachia huru! A.  Tabaka jipya la wafuasi wa Uwahhabi Kinachoanguka sasa ni kundi la wafuasi wa Uwahhabi lenye msimamo mkali, lenye imani kali na hatari ambalo linawachukulia Waislamu wote, isipokuwa lenyewe, kama wenye kuabudu miungu wengi. Lakini lipo kundi linajilotokeza lenye msimamo wa wastani na kutekelezeka. Tabaka hili linao vijana waliosoma na wahadhiri wa chuo kikuu kwa kushirikiana na wanazuoni mashuhuri. Wanaonesha tabia zifuatazo: 1.

Wanaheshimu imani za watu wengine, hawawalaumu Waislamu kama wenye kuabudu miungu wengi, kukufuru Mungu na bidaa, na hawapendi umwagaji damu.

2.

Wanakaribisha mazungumzo na maelezo ya kimantiki miongoni mwa imani za Kiislamu na wanasikiliza yale yanayosemwa na wengine, na wanasoma vitabu vilivyoandikwa na wengine. 107

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 107

5/31/2016 7:38:10 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

3.

Hawachukulii kama jambo la haramu mtindo mpya wa maisha ya kisasa wenye kujenga, ambapo hakuna sababu ya kuharamishwa kwao, na hawakatai kuadhimisha siku za watakatifu mashuhuri wa dini, wala hawachanganyi mambo ya kidini na ya kawaida.

4.

Wanawaruhusu wanawake kusoma, na kushiriki katika shughuli za ujenzi wa kijamii, almuradi wanazingatia vazi la Kiislamu na viwango vya usahili.

5.

Wapo tayari kushirikiana na madhehebu mengine ya Kiislamu na wanaelekeza chuki yao kwa wale wanaolenga kuwaharibu Waislamu. Kwa polepole watawahamisha Salafi wenye msimamo mkali mno na wenye matusi. Mtanuko wa kundi hili upo dhahiri katika mikusanyiko ya kisayansi na kitamaduni wakati wa hijja na msukumo wake umeonekana katika vitabu ambavyo vimechapishwa hivi karibu. Tunaamini kwamba kufutika kwa kundi hilo na kutokeza kwa kundi hili jipya, kunaweza kuchora taswira inayofaa ya Uislamu hapa duniani, na kurudisha gharama ya imani hii safi ambayo imehatarishwa na mfumo wa imani unaofuatwa bila kusaili na chokozi ya wafuasi wa Salafi wa zama zilizopita, na Inshallah, kutayarisha uwanja kwa ajili ya kuingia dini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu katika makundi, na kuweka jukwaa kwa ajili ya Uislamu kupata mahali pake halisi hapa duniani. Waislamu hapa duniani wanakaribisha ujio wa kundi kama hilo, na kuchukulia kama kipengele muhimu katika kuimarisha nguzo kuu za udugu wa Kiislamu na kuwaunganisha Waislamu dhidi ya maadui ambao hujitahidi kuwaona ni wapumbavu na kuwatukana Waislamu. Maoni mengi ambayo yameandikwa na wanazuoni wa Kiislamu kuhusu kitabu cha Alawi, ni ushahidi mwingine kwa ukweli huu. 108

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 108

5/31/2016 7:38:10 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

Ni juu ya viongozi wa Saudia kuendeleza maendeleo haya kwa kufungua mipaka yao ambayo imefungwa kwa ajili ya vitabu vya Kiislamu na maandishi ya Waislamu wengine wa nchi zingine za Waislamu, kutayarisha uwanja kwa ajili ya mazungumzo baina ya imani za Kiislamu na kutia moyo wa maingiliano baina ya wanazuoni wa nchi hizi. Jambo hili litakuwa na manufaa kwao na kwa ummah wa Kiislamu! B.  Hatari ya wakereketwa Wakupindukia:47 Kipengele kimojawapo kinachoelekeza kwenye fikira ya wafuasi wa Uwahhabi wenye ukereketwa uliopindukia ni kundi la Waislamu, wajinga na wasio na elimu ambao hutia chuku kuhusu Watakatifu wa dini na huwanyanyua kutoka kwenye daraja la utumwa na kuwaweka kwenye daraja la uungu na kuwafanya kuwa washirika wa Mungu. Bila shaka tishio lao halijawa na kamwe halitakuwa pungufu ya tishio la wafuasi wa Uwahhabi wenye ukereketwa uliopindukia, na kama ingekuwa si kwa ajili yao, hapangekuwepo na kisingizio chochote kwa ajili ya wafuasi wa Uwahhabi. Usemi ambao hauendani na mtazamo wa imani ya uwepo wa Mungu Mmoja na kamwe haukutajwa katika Maandiko Matakatifu na Hadithi, kama vile “Muumbaji wa Mbingu na Dunia” na “Mwingi wa Rehema na Mrehemevu” na sifa zingine zinazofanana na hizo ambazo ni mahsusi kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, hazitakiwi kutumika kwa ajili ya Watakatifu wa Mungu kwani wala haiendani na mafundisho ya Kiislamu. Msisitizo wa baadhi ya watu wajinga juu ya mambo haya umesababisha kundi ambalo ni sawa na kundi lenye ukereketwa uliopindukia katika ujinga, kupinga na kutangaza kwamba Mtukufu Mtume  (Mungu na apishe mbali) hana uwezo wa kufanya lolote baada 47

Ghulat 109

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 109

5/31/2016 7:38:10 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

ya kifo chake, ikiwa ni pamoja na uombezi na swala kwa ajili ya waumini na hata kwenda kuzuru Kaburi lake ni bidaa. Na hii ndiyo sababu Amiri wa Waumini Imamu Ali  anasema: “Aina mbili za watu wameangamia kwa ajili yangu: marafiki ambao hutengeneza maoni yaliyotiwa chumvi kuhusu mimi na maadui waovu ambao hufikiri mimi kuwa dhaifu”48 Khawarij na Nasibi walitengeneza uwanja kwa ajili ya wafuasi wenye Ukereketwa uliopindukia, na kwa upande wao wafuasi wenye ukereketwa uliopindukia waliwaendeleza Ukhawarij. Ni wajibu wa wanazuoni wa Kiislamu kufanya kila jitihada kuwaongoza hawa wafuasi wenye ukereketwa uliopindukia, na kwa upande mwingine wanatakiwa kutoa majibu kwa maneno ya hila ya wafuasi wa Uwahhabi wenye msimamo mkali. Ni vigumu kuuweka mshikamano wa ummah usio na elimu katika mambo kama hayo, lakini inakuwa ni vigumu zaidi wakati mwingine pale baadhi ya watu wenye elimu wanapojikwaa na kuwa katika pande zote mbili. “Mwenyezi Mungu Mtukufu na atuepushe na ukereketwa uliopindukia na atuongoze kwa mintarafu ya njia iliyonyooka.” 1.

Wito Mwingine kutoka kwa mwandishi mwingine jasiri: Kitabu “Mmishenari na sio Mtume”!

Kitabu “Mmishenari na sio Mtume” ni tathimini ya ukosoaji kilichoandikwa na kiongozi wa imani ya Uwahhabi kuhusu suala la kutenga na kuwatangaza Waislamu wengine kama makafiri, ambacho kimechapishwa hivi karibuni na umaarufu wake umeenea katika Hijaz (Saudi Arabia) yote na nchi zingine. Sifa pekee za kitabu hiki ni kama zifuatazo: 48

Nahjul-Balaghah, Semi fupi na.117 110

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 110

5/31/2016 7:38:10 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

1.

Mwandishi wa kitabu hiki, Sheikh Hasan bin Farhan Maliki, ni msomi mashuhuri wa madhehebu ya Sunni nchini Saudi Arabia na yeye ni mfuasi wa imani ya Maliki ambaye hujiita mfuasi wa Uwahhabi mwenye msimamo wa wastani.

Mtu huyu anamheshimu kiongozi wa madhehebu ya Uwahhabi, Sheikh Mohammad bin Abdul-Wahhab, lakini anakosoa vikali sana matangazo yake, hususani juu ya kutenga Waislamu (Taqfiir), anasema kwa dhati: ‘Pamoja na kwamba ninamheshimu yeye (Mohammad bin Abdul-Wahhab), bado si tu kwamba nimemuona mwenye uelekeo wa kukosa, lakini ninaamini amefanya makosa mengi.’ 2.

Mbinu yake ya kukosoa ni yenye upole na kimantiki, lakini inapotokeza kukosoa dhamira ya kiongozi wa Uwahhabi, yeye hashughuliki na kitu chochote kabisa; hata hatilii maanani vitisho vingi vinavyomuogopesha yeye kwa niaba ya wafuasi wa Uwahhabi wenye ukereketwa uliopindukia, kama awaitavyo yeye.

3.

Anao uelewa mzuri wa imani ya Kiislamu na vyanzo vya kidini, na hasa zaidi anao uwezo mzuri wa kutumia misamiati inayotumiwa na upande wa upinzani dhidi yao. Na kwa namna ya burudani ameweka wakfu sehemu ya kitabu chake kwa “hitilafu na kutofautiana utaratibu katika matamko ya Mohammad bin Abdul-Wahhab.”

4.

Yeye anaamini kwamba wafuasi wa Uwahhabi wenye ukereketwa uliopindukia, ambao wanachukulia kuwa ni sahihi wao kuwaua, kupora utajiri na kutweza hadhi ya Waislamu wasio wafuasi wa Uwahhabi, wamekumbwa na ushabiki uliopindukia na ni tishio kwa Uislamu, Waislamu na kanda. 111

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 111

5/31/2016 7:38:10 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

5.

Ameelekeza ukosoaji wake zaidi kwenye vitabu viwili “Kashfu-Shuhabat” na “Kitab-u-Tawhiid” vilivyoandikwa na Muhammad bin Abdul-Wahhab, na anaelezea vyanzo vingi vya maelezo yake kwenye kitabu kiitwacho “Al-Durar-u-Sunniyah”.

Al-Durar-u-Sunniyah kimekusanywa na Abddur-Rahman bin Muhammad binTasim Al-Hanbali, ambaye naye amekusanya seti ya vitabu, makala na barua zilizoandikwa na Muhammad bin AbdulWahhab na kundi la watemi wafuasi wa Uwahhabi tangu wakati wa uhai wake hadi leo hii. Alifariki dunia mnamo 1392 AH. Bin Baz Mwanasheria mashuhuri wa madhehebu ya Uwahhabi ambaye amefariki dunia hivi karibuni, alikitumia kitabu hicho kama kitabu cha kufundishia. Kitabu hiki chenye juzuu kumi ni chanzo kizuri sana cha taarifa zihusuzo Uwahhabi. 6.

Mwandishi wa “Mmishenari na sio Mtume” hakuwa salama katika kutishwa na kushinikizwa na wafuasi wa Uwahhabi wenye ukereketwa ulopindukia na fatwa za kutengwa kwake zimewasilishwa, kama ilivyofanyika kwa Bin Alawi Maliki, na haijulikani kwa dhahiri ni hatima ya aina gani inayomngojea yeye. Hata hivyo, ameufanyia Uislamu upendeleo mkubwa kupitia kitabu hiki na amethibitisha kwamba umwagaji damu na matusi ni mambo mageni kwenye Uislamu na ni matokeo ya tafsiri zilizokosewa za mafundisho ya Kiislamu.

7.

Katika maelezo ya utangulizi wa kitabu chake anasema: “Ukweli ni kwamba nilitayarisha somo hili jipya la vitabu vya Muhammad bin Abdul-Wahhab kabla ya tukio la kulipuliwa kwa majengo pacha ya Kituo cha Bishara cha Kimataifa nchini Marekani mnamo tarehe 11, mwezi Septemba, 1999 na baada ya tukio hilo sikuwa makini sana kuhusu uchapishaji wake (kwani nilidhani ingekuwa ni sababu ya kushutumiwa kwa Waislamu 112

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 112

5/31/2016 7:38:11 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

wakati wa tukio hilo). Lakini jinsi nilivyotazama wafuasi wa Uwahhabi wenye ukereketwa uliopindukia walivyokuwa wanafanya semina na makongamano kwa mfululizo kwa lengo la kumsafisha kiongozi wa Uwahhabi, Sheikh Muhammad, na kumtangaza yeye kuwa hana hatia ya uhalifu wowote, niliona ilikuwa muhimu kufichua ukweli ili kwamba waweze kushughulikia jambo hili kwa ulinganifu na kukiri makosa yaliyofanywa na Sheikh katika kutoa fatwa za kutenga.”49 8.

Ameanza kwa kusema: “Mohammad bin Abdul-Wahhab alikuwa mrekebishaji sio Mtume! Halafu anabainisha: ‘Tupo katikati ya makundi mawili yenye ukereketwa uliopindukia; baadhi ya watu humuona yeye kama kafiri, na wengine huchukulia misemo yake na hotuba zake kama mafungu ya maneno ya kitume ambayo hapana mtu yeyote anayeweza kuyakaripia; pande zote mbili zimekosea.

9.

Katika sehemu yake nyingine ya hotuba yake anasema: “Sheikh hakuwa na upekee katika kuzungumza na kuita” anashauri: “Baadhi ya wafuasi wa Sheikh wanamuona yeye kama ana upekee katika elimu na maarifa, na kulaani nchi zote za Kiislamu ambazo hazikuitikia wito wa Uwahhabi kama maeneo ya ukafiri na waabudu miungu wengi. Na zaidi ya hayo, huwachukulia wanazuoni wote wa nchi hizo kuwa wajinga wasiojua lolote kuhusu Uislamu”50

Halafu anaongeza: “Kwa bahati mbaya, niliona chimbuko la kuwatenga Waislamu na msingi wa kuzichukulia nchi zao kuwa nchi za kikafiri, na wanazuoni wao wote kuwa makafiri, kwa maneno ya Sheikh mwenyewe, na hivi punde nitataja vyanzo vya hayo.” 49 50

Mmishenari na sio Mtume, uk. 28   Mmishenari na sio Mtume, uk. 13 113

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 113

5/31/2016 7:38:11 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

Halafu anasema: “Kwa hakika, Sheikh na wafuasi wake hawakufuata njia iliyonyooka katika mafundisho haya. Baadhi ya makosa ambayo Sheikh na baadhi ya wafuasi wake waliyafanya, hususani kuhusu kuwatenga Waislamu, walinasa kwenye mtego wengi wa watu wapenda elimu - ama kwa sababu ya ukereketwa uliopindukia au kuiga - na kama matokeo vitendo vingi vya mikwaruzo vilitekelezwa hivi karibuni, (katika sehemu mbalimbali za dunia) na kundi hili, kwa kutumia hoja hizohizo zilizotumiwa na Sheikh lilifanya matukio ya kuogopesha (na kufanya mauaji ya kutisha sana na bado yanaendelea hadi leo)� 10. Mwanazuoni yeyote nchini Saudi Arabia, kwa kutaja makosa ya kijinga ya Sheikh, ni matokeo ambayo yasingeepukika katika kuvunjiwa heshima na kuaibishwa. Hivyo kukosoa imani hizi ikawa kazi ya kuamuru na ikanifanya mimi niingie katika mazungumzo haya. Ni wajibu wa kila mwanazuoni na kila raia katika nchi ya Saudi Arabia kufanya kila wawezalo katika kutuweka huru kutokana na uchokozi huu na kutengwa, na kujizuia katika kuendeleza kile ambacho matokeo yake ni kuumiza nchi yetu na watu wake kwa kipindi kirefu, (baadhi ya watu wanaweza kudhani). Hali hii inaweza kuwa na manufaa ya muda mfupi. Lazima tuisafishe nchi yetu na dini yetu kutokana na uchafu wa ukandamizaji wa kutengwa na kumwaga damu ya watu wasio na hatia. Mapema katika kipindi hiki, hakuna hata siku moja ambayo hatupati habari za ukatili za uchokozi wa kutisha unaofanywa nchini Iraq. Kila siku, makumi, na wakati mwingine hata mamia ya watu wanasakwa kupitia mabomu yaliyotegwa kwenye motokaa. Na katika mifano mingi zaidi unaona malengo ya kujilipiua katika vurugu hizi ambazo zinaonesha kwamba hii ni kazi ya wale ambao wao wa114

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 114

5/31/2016 7:38:11 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

najiona ni Waislamu na Waislamu wengine ni makafiri ambao uhai wao na rasilimali zao ni halali yao. Haya ndio matokeo ya mafundisho ya madhehebu ya Sheikh, ambaye alihama kutoka Hijaz na kwenda Jordan na kutoka huko kwenda Iraq. Katika hatua fulani kwenye tanbihi katika sura hii mwandishi anapendekeza kwamba watu wa Magharibi hususani Marekani, kupitia sera za kisiasa, kijeshi na kiuchumi na misaada yenye kuhusisha pande mbalimbali inayopelekwa kwa dhalimu Israel, wamekuwa ndio chanzo cha ukandamizaji huu. Katika sehemu nyingine ya semi zake ameendelea kuelezea ni mahali gani ukaidi huu wa kutengana, ambao unasababisha machafuko, hata nchini Saudi Arabia, umeanzia?! Na hatimaye anahitimisha kwamba mafundisho ya Sheikh na madhehebu yake ndio sababu kuu ya uchokozi huu. Vurugu zote; kuanzia kwenye uchokozi unaofanywa na kundi la Ikhwan katika kanda ya Najd na baada ya hapo katika mji mtakatifu wa Makkah, na shughuli zingine za uchokozi na milipuko ya mabomu sehemu zingine katika mikoa mbalimbali ya Saudi Arabia, ni matokeo ya mafundisho ya Sheikh. Halafu anaongeza: “Kwa kuwa wale walioanzisha uchokozi huu na milipuko ya mabomu, sio watu wa kutoka nchi za nje ya Hijaz, kama tukidai kwamba wanaofanya hayo wamepata msukumo kutokana na utamaduni na mafundisho ya Sheikh, hatutakuwa mbali na ukweli, na kama mtu anarejelea matamko ya watu hao kwa kweli mtu anaweza kukiri ukweli huu.” Ufupisho wa Kitabu: “Mmishenari Na Sio Mtume” Hasan Ibn Farhan Maliki, katika kitabu chake “Mmishenari Na Sio Mtume!” hasa zaidi kinahusika na kukosoa misemo na imani za kiongozi wa Uwahhabi juu ya suala la kuwatenga Waislamu na kuwa115

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 115

5/31/2016 7:38:11 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

tangaza wale ambao wamekataa mafundisho yao, kama waabuduo miungu wengi na makafiri. Katika sura ya kwanza ameanza kwa kukosoa kitabu kiitwacho “Kashf-ul-Shubahat” katika namna ya dhahiri. Katika sura ya pili anakosoa vitabu vyake vingine juu ya masuala ya Tauhidi na Imani ya kuabudu miungu wengi - Shirk. Katika sura ya tatu anaendelea kwenye suala muhimu sana la kuwatenga Waislamu. Halafu anafichua kipande mashuhuri cha hitilafu yake katika namna ya kisayansi. Katika sura ya nne anazungumzia kama wafuasi wake walimfuata yeye katika kuwatenga Waislamu wakiwa wameziba masikio na kufumba macho, au walijishughulisha katika kukosoa fikira za Sheikh? Na hatimaye katika sura ya tano anakosoa fikira za wale wanaompinga Sheikh na amewatenganisha wafuasi wenye ukereketwa uliopindukia na wale wenye msimamo wa wastani, na yeye anajiegemeza upande wa wale wenye masimamo wa wastani. Na kwa namna ya kushangaza, mwishoni amesema: “Ufupisho wa mazungumzo ni kwamba Sheikh amepotoka kuhusu suala la kuwatenga Waislamu. Akikiri kuhusu jambo hili, mbele ya hoja tulizonazo, ni kazi rahisi kwa mtu mwenye akili isiyo na upendeleo. Wala Uislamu haujaharibiwa kwa kitendo hiki cha kukiri ama jua halitachomoza kutoka Magharibi. (ni kwamba huyu ni binadamu mwenye kuweza kufanya makosa na alifanya makosa.)”51 Kwa hakika ukosoaji huu utasafisha imani hii kutokana na uchokozi wa kutisha sana na unyama ambao wamekuwa wakifanya katika jina la Uislamu. Kwa uchache sana kile kinachoweza kutokea ni kuwaweka wafuasi wa Uwahhabi wenye msimamo wa wastani mahali pa wafuasi wa Uwahhabi wenye ukereketwa uliopindukia. 51

“Mmishenari Na si Mtume” uk. 28-29 116

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 116

5/31/2016 7:38:11 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

Sura ya Kwanza: Ukosoaji wa “Kashf-ul-Shubahat” Kitabu kiitwacho Kashf-ul-Shuhabat kinajulikana kama ni kitabu kinachopendwa sana katika vitabu vilivyoandikwa na Sheikh. Ibn Farhan ameona mapingamizi muhimu thelathini na tatu ndani ya kitabu hiki, na anazikosoa pingamizi hizo, hususani zile zinazohusu kuwatenga Waislamu. Anaelezea mshangao wake kwamba ni vipi wanazuoni wa Uwahhabi kuwa wanapuuza makosa yote haya makubwa ambayo yametamkwa na Sheikh na huyatupilia mbali kwa urahisi. Halafu anaongeza: “Endapo baadhi yao tu wangehoji makosa yake machache tu, nisingeona ulazima wa kuandika kitabu hiki. Lakini natakiwa nifanye nini wakati kila mtu amenyamaza kimya.” Upigaji chuku na utiaji chumvi kuhusu Watu wema: Mohammed bin Abdulwahhab anasema mwanzoni mwa kitabu kiitwacho: Kashf-ul-Shubahat: “Tauhidi ni dini ya Mitume ambao Mwenyezi Mungu Mtukufu amewatuma kwa waja Wake, wa kwanza miongoni mwao ni Nuh . Muweza wa Yote alimpeleka kwa ummah wake wakati ambapo watu hao walikuwa wametia chuku kuhusu Watu wema.” Baada ya hapo Ibn Farhan anatoa maoni yake: Mwanzo wa usemi huu ni sahihi, lakini unaishia kimakosa na labda ndio utangulizi wa kuanza kuwatenga Waislamu! Muweza wa Yote alimpeleka Nuh , kuwaita watu kwa mintarafu ya Mungu Mmoja na kuacha kuabudu miungu wengi, kwa sababu watu hao walikuwa wanaabudu masanamu yaliyoitwa Wadd na Suwa na kadhalika….. Tatizo lao halikuwa katika kutia chuku kuhusu Watu wema tu. Kutia chuku na kutia chumvi inaweza kuwa sababu ya watu kuabudu miungu wengi (au kutokuamini), lakini kwa kweli si kila kinachotiwa chumvi ni 117

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 117

5/31/2016 7:38:11 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

imani ya kuabudu miungu wengi wala hapana yeyote mwenye haki ya kumwaga damu ya Waislamu akiegemeza kitendo chake katika kisingizio hiki! Halafu anaendelea kusema: “Mimi sina madai yanayofanywa kuhusu Watu wema na watu mashuhuri katika dini au ibada fulani za ushirikina kuwa ni sahihi. Mimi ninadai kwamba kufanya hivyo ni makosa lakini vitendo hivyo haviwezi kuitwa kufuru.” Baadhi ya watu walimkosoa Sheikh wakisema kwamba wale watu aliowatenga na akapigana nao vita na kuwaua, walikuwa Waislamu waliosimamisha swala, waliofunga saumu, na waliokwenda hijja. Yeye alijibu kwa kusema kwamba kwa kuwa wanatia chuku kuhusu watu mashuhuri katika dini, wote hao ni watu wasioamini na wao ni wabaya hata kuliko waabudu masanamu wa zama za upagani.52 Ibn Farhan anashangazwa kwamba wapinzani utiaji chuku wao wenyewe wanatajwa katika utiaji chuku usioaminika kuhusu Sheikh Mohammad bin Abdul-Wahhab kwa kumchukulia yeye kama mtu mtakatifu ambaye hawezi kufanya kosa lolote, wakimuita yeye kuwa mkuu wa uwepo.”53 Msamiati ambao wao wala hawaruhusu kutumiwa kwa ajili ya Mtukufu Mtume . Na katika ukosoaji wa mwisho (nukta ya thelathini na tatu ya ukosoaji), anamwambia Sheikh na kusema kwamba katika ukurasa wa 70 wa kitabu chake, jambo moja tu la pekee ambalo amefanya juu ya suala la kufuru (au kuwatenga Waislamu) ni kwa wale ambao “hawana ari” (hawapo tayari), maana yake ni wale ambao wanalazimishwa kutoa matamko ya kukufuru. Halafu amerejelea katika Aya ya Qur`ani Tukufu ya “Isipokuwa yule ambaye alilazimishwa.” 52 53

“Mmishenari Na sio Mtume” uk. 33 (kwa ufupisho).   “Mmishenari Na sio Mtume” uk. 14 118

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 118

5/31/2016 7:38:11 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

Ibn Farhan ametaja sehemu nyingine ambayo imetajwa katika Qur`ani Tukufu, ambaye alitokeza kukana baadhi ya mambo ya kidini (ambapo walikuwa wanaamini katika misingi ya Uislamu), kwa sababu ya kutokuwa na utambuzi na ujinga, au kama matokeo ya uelewa usio sahihi wa aya ya Qur`ani Tukufu na simulizi za hadithi. Watu kama hao, kufuatana na Qur`ani Tukufu, wamesamehewa na hawachukuliwi kama wasioamini. Halafu anahitimisha: ‘Mojawapo ya dosari za mbinu za Sheikh ipo katika utaratibu wake wa kuchukua aya moja ya Qur`ani Tukufu au hadithi moja na kuacha pembeni aya au hadithi zingine, na hili ni kosa baya sana.’ Sura ya Pili: Ukosoaji wa Al-Durar-ul-Sunniyah: Katika sura ya pili ya kitabu hicho, anahoji maoni ya Sheikh yaliyopo katika Al-Durar-ul-Sunniyah na anaonesha makosa arobaini, pamoja na tamko katika kitabu hiki:54 ‘hakuna mwanazuoni yeyote wa Najd wala wanasheria wa mkoa huo ambao wanajua maana ya “ Laa ilaha ilallah” (Hapana mungu ila Mwenyezi Mungu Mtukufu), na hawawezi kutofautisha baina ya dini iliyoletwa na Muhammad  na dini ya Amr ibn Lahi (muabudu masanamu mashuhuri wa zama za upagani). Wao wanachukulia dini ya Amr ibn Lahi kuwa ni bora na kwamba ndiyo dini iliyo sahihi.’ Matokeo yake anatangaza kwamba wanazuoni, wanasheria na mahakimu wa mkoa huo ni waabudu miungu wengi na makafiri. Halafu Ibn Farhan anatoa tamko kuhusu vitabu vilivyoandikwa kuhusu wanazuoni na wanasheria wa mkoa huu kuonesha kwamba Sheikh Mohammad alikuwa anaelekea upande usio sahihi wakati wa kuwatenga Waislamu. Miongoni mwa mifano ambayo alionesha kuhusu utiaji chuku katika kuwatenga Waislamu, kitendo kilichoku54

Al-Durar ul-Sunniyah” Juz. 10, uk. 51 119

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 119

5/31/2016 7:38:11 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

wa kinafanywa na kundi la Uwahhabi wenye ukereketwa uliopindukia, ni mifano miwili ifuatayo: 1.

Kuwatenga Waislamu wa madhehebu ya Shia: Sheikh Mohammad bin Abdul-Wahhab anashauri kwamba yeyote anayetilia shaka ukafiri wa Shia na yeye ni kafiri.55 Ibn Farhan anaendelea kusema: ‘Hii ni wakati ambapo Ibn Taymiyah, pamoja na utiaji chuku wake na uhasama dhidi ya Shia anawachukulia wao kama Waislamu (pamoja na kwamba anawachukulia Shia kama watu wa bidaa ambazo zimeharamishwa), lakini yeye anasema kwa dhahiri kwamba Shia sio makafiri.’56

Halafu mwandishi anashauri: ‘Ilikuwa ni baada tu ya hizi fatwa za unyama na zisizo na hisia za Uislamu ambapo kwamba mauaji ya Shia yalianza na kuendelea hadi leo. Ambapo hawa Shia ndio walioweka misingi iliyoendelezwa sana kwa ajili ya mafundisho ya Tauhidi (Imani ya uwepo wa Mungu Mmoja) katika Uislamu. 2.

Sheikh anasema: “Yeyote anayemlaani sahaba wa Mtukufu Mtume  (yeyote yule awaye) ni kafiri!57

Ibn Farhan Maliki anasema kwa uwazi, ‘Mu`awiyah, kufuatana na maelezo yaliyo dhahiri katika Sahih Muslim aliamuru watu wake kumlaani Imam Ali B 3.

Alimwambia Sa`d Ibn Abi Waqqas, ‘Inawezekanaje (pamoja na amri yangu yoyote) wewe humlaani Ali? Sa`d akajibu. ‘Kwa sababu ya sifa tatu ambazo nilisikia Mtukufu Mtume  akisema kuhusu ubora wa Ali . (Halafu akataja hizo sifa tatu) ambazo zimetajwa katika Sahih Muslim katika sehemu juu ya ‘Uadilifu

Al-Durar ul-Sunniyah” Juz. 10, uk. 369   Mmishenari Na sio Mtume” uk. 86 57 Al-Durar ul-Sunniyah, Juz. 10, uk. 369 55 56

120

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 120

5/31/2016 7:38:11 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

wa Sahaba’, katika sura juu ya ‘Uadilifu wa Ali ibn Abu Talib’, kama hadithi ya tatu. Kwa taarifa zaidi kuhusu kumlaani na kumwapiza Imam Ali  kama alivyofanya Mu`awiyah rejelea katika juz. ya 4, uk. 52 na 188, (na kwa miongo mingi Imam Ali  alilaaniwa kwenye mimbari na wahutubiaji). Pamoja na haya; hivi Sheikh huyu alimuita Mu`awiyah kafiri?58 Huyu mwanazuoni wa madhehebu ya Sunni, Maliki anasema: ‘Imeonekana kwamba Sheikh Mohammad, anajitetea yeye kama ifuatavyo: “Maadui wanadai kwamba mimi nina watenga watu juu ya tuhuma, ninawachukulia watu wajinga ambao hawajapewa uthibitisho kama makafiri. Huu ni usingiziaji mkubwa. Watu hawa wanayo nia ya kuwafarakisha watu wengine kutoka katika dini ya Mungu na Mtukufu Mtume Wake .”59 Ibn Farhan anasema: ‘Madai haya yenyewe ambayo yamefanywa na Sheikh ni yenye maana ya kujitenga bila kutajwa waziwazi katika uhusiano na wale ambao hawajakubali Uwahhabi, kwani kwa kuwa ana maana kwamba dini ya Mungu na Mtukufu Mtume Wake , kwamba wana nia ya kuwatoa watu kutoka kwenye dini, ndiyo imani ya Uwahhabi. Kwa hiyo, wale wanaopinga imani ya Uwahhabi, hawaamini dini ya Mungu na Mtukufu Mtume .’60 Hitilafu katika maneno ya Sheikh: Ibn Farhan anarejelea katika misemo mingine ya dhahiri ya Sheikh na anasema: “Zipo dosari nyingi na makosa mengi ambayo yanasababisha kulaumiwa kwa Sheikh na yeye hujiepusha nayo, ambapo dosari na makosa hayo mengi yapo katika usemi wake!” Halafu anataja mifano ishirini na tano ya dosari na makosa hayo kwa kurejelea   Mmishenari Na sio Mtume, uk. 86   Al-Durar ul-Sunniyah” Juz. 10, uk. 113. 60   Mmishenari Na sio Mtume, uk. 86 58 59

121

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 121

5/31/2016 7:38:11 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

vyanzo vyake na ushahidi, pamoja na hayo ambayo Sheikh anayakanusha kuhusu haya yafuatayo: 1.

Anazichukulia sehemu nne za imani ya Sunnah kama batili.

2.

Yeyote anayeomba uombezi kutoka kwa Watu wema ni kafiri.

3.

Akiwa na nguvu na uwezo atabomoa Kaburi na Sehemu Tukufu ya Mtukufu Mtume ! (Na sehemu zingine tukufu za Maimamu wa nyumba ya Mtukufu Mtume  na watu wengine mashuhuri katika uwanja wa makaburi wa Baqii, atasawazisha na kuwa tambarare.)

4.

Anachukulia kitendo cha kuzuru Kaburi la Mtukufu Mtume  kuwa ni haramu.

5.

Yeye anamchukulia kila mtu kama kafiri isipokuwa wale wanaomfuata!

Amekanusha matamko yake mengi na mengine yanayofanana na haya, ambapo ama yanaonekana waziwazi katika vitabu vyake au yamesikika katika hotuba zake. Na hitilafu hii ya kushangaza inamstajabisha yeyote ambaye amesoma vitabu vyake bila upendeleo. Sura ya tatu: Anafuatilia njia yake: Hasan Ibn Farhan Maliki, katika sura ya tatu ya kitabu chake anasema: “Kwa bahati mbaya wanafunzi na wafuasi wa Sheikh walifuata njia yake ya kuwatenga Waislamu, na walitangaza makabila mengi ya Waarabu wengi na wasio Waarabu, wafuasi wengi wa imani za Kiislamu, na kundi la wanazuoni mashuhuri Waislamu, kama ni makafiri.61 61

Kwa maneno mengine walitangaza mara kwa mara kwamba Waislamu wengine

walikuwa makafiri, na waliwaburuza Waislamu wote chini ya ubapa mkali wa ukafiri. 122

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 122

5/31/2016 7:38:11 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

1.

Walitamka kwa dhahiri kabisa kwamba watu wote wa Makka na Madina ni makafiri (ambao wakati huo walikuwa hawajakubali madhehebu ya Uwahhabi.)62

2.

Yeyote ambaye amekubali wito wa Mohammad Ibn Abdulwahhab lakini bado anaamini kwamba baba yake alifariki dunia kama Muislamu, huyu ni kafiri! Lazima alazimishwe kutubu. Yeyote anayekataa kutubu, lazima auawe kwa kukatwa kichwa! Rasilimali yake itataifishwa na hazina ya serikali ya Kiislamu! Kama mhusika ametekeleza Hijja kabla ya hapo lazima arudie utekelezaji wa Hijja mara ya pili, kwani Hijja yake ya kwanza ilikuwa kabla hajakubali Uwahhabi na kwa hiyo bado alikuwa muabudu miungu wengi.63

3.

Ufalme wote wa Uthmainia (Ottoman) ulikuwa wa kikafiri, na yeyote ambaye hakuichukulia serikali hiyo kuwa ni ya kikafiri yeye mwenyewe alikuwa kafiri.64

4.

Wafuasi wa imani ya Ash`aria walikuwa makafiri kwani wao walikuwa hawatambui shahada mbili;65 wafuasi wa Mu`tazilah pia walikuwa makafiri.66

5.

Mtu anayeshikilia Zaka ni kafiri.67

6.

Wale ambao waliwaajiri wasio Waislamu katika ofisi zao na makazini kwao, wale ambao hawakutilia maanani wajibu wa kidini na ambao walitekeleza mambo mengi yaliyoharamishwa, wale ambao hawakujua lolote kuhusu shahada

  Al-Durar ul-Sunniyah, Juz. 9, uk. 285. Al-Durar ul-Sunniyah, Juz. 10, uk. 138, 143. 64 Al-Durar ul-Sunniyah, Juz. 10, uk. 429. 65 Al-Durar ul-Sunniyah, Juz. 1, uk. 364. 66 Al-Durar ul-Sunniyah, Juz. 1, uk. 357. 67 Al-Durar ul-Sunniyah, Juz. 10, uk. 177. 62 63

123

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 123

5/31/2016 7:38:11 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

mbili isipokuwa kutamka tu, wote walikuwa makafiri na walioritadi!68 Hasan Ibn Farhan, baada ya kutaja makosa ishirini na saba ambayo wanafunzi na wafuasi wa Sheikh waliyafanya katika kuwatenga Waislamu, anaendelea kwa kusema: “Baada ya kujidekeza sana katika jambo la kuwatenga Waislamu, ambao watu kama wewe asingeona mahali popote, kundi la wanazuoni wa Uwahhabi wakielekeza uchokozi wao wa mashambulizi ya kutenganisha kwa Sayid Khutbi, Maududi, Ikhwan ul-Muslimiin na Hisb ul-Tahrir. Ni kweli kwamba watu hawa walipata pigo kali kwa kupita kiasi katika uwanja wa siasa, lakini mtazamo wao kwa namna yoyote ile haukufika kwa Wahhabi wasio na wastani katika vipengele vyote, ama kisiasa, kitheolojia, falsafa ya kisheria, kitamaduni au kijamii; kwa hakika hapa hakuna haki.”69 Halafu anaongeza: “Ikifikiriwa kuhusu matamshi yaliyopita, hivi kuna kitu chochote kilichobaki, wa kile kiitwacho mpango tukufu wa mapambano (na mashambulizi dhidi ya Waislamu) ambayo Wahhabi wamesahau kuyataja?”70 Na mwishoni mwa mazungumzo haya anaonesha kwamba baada ya Mohammad Ibn Abdul-Wahhab wimbi kubwa la kuwatenga Waislamu liliwaelemea Wahhabi wenyewe, ambapo baadhi waliwatenga wengine na kuwateka nyara wake zao! Halafu anataja matukio kadhaa akirejelea katika kitabu cha AlDurar ul-Sunniyah.71 Anamalizia sura hii kwa maelezo yenye matumaini na anasema: ‘Mtoto wa kiume wa muasisi wa imani ya Uwahhabi, Abdullah Ibn Mohammad, alihama na kwenda Misri baada ya   Al-Durar ul-Sunniyah, Juz. 15, uk. 486.   Mmishenari Na sio Mtume, uk. 117 70   Mmishenari Na sio Mtume, uk. 117 71   Mmishenari Na sio Mtume, uk. 123 na kuendelea 68 69

124

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 124

5/31/2016 7:38:11 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

anguko la mji wa “Darieyah” (mji katika nchi ya Hijaz), na alihamishwa kutoka kwenye mazingira yenye msimamo mkali na kwenda kwenye mazingira yaliyo wazi zaidi, ambako alipata kiasi cha utambuzi mpya, na akakimbilia kwenye kundi lenye wastani, akapinga tamko la kuyatenga makundi mbalimbali ya Waislamu kwa sababu za bidaa za kidini ambazo baba yake alikuwa anaziamini. Na akatangaza kwamba hapana mtu yeyote ambaye atatengwa isipokuwa kama anakanusha mojawapo ya wajibu wa dini au angefanya kitendo ambacho kufuatana na makubaliano ya Uislamu ni sababu ya mtu huyo kutengwa.72 Sura ya nne: Msimamo wa Waislamu. Katika sura ya nne anazungumzia kuhusu wapinzani wa Sheikh ambao walimtenga yeye (Sheikh) na wafuasi wote wa Uwahhabi. Halafu anaendelea kutetea hoja yao na anasema: Jambo hili la kuwatenga Waislamu halina manufaa yoyote, ni lazima wakubaliwe kama ni kutokana na kosa lao (hususani yanayohusu kutengwa kwao). Katika sura hii, amewataja watu ishirini na mbili miongoni mwa wanazuoni wa madhehebu ya Sunni, wengi wao walitoka Najd na Makkah, na baadhi ya wanazuoni wa Damascus, Iraq, Tunis na Morocco, ambao wote walisimama dhidi ya Sheikh, na baadhi yao hata waliandika vitabu wakipinga yale aliyoyasema Mohammad ibn Abdul-Wahhab.73 Kwa kufanya hivyo, anaonesha kwamba upinzani wake zaidi ulitoka mkoani kwake au wengine walikuwa ndugu zake! Madai Muhimu zaidi dhidi ya viongozi wa Uwahhabi! Ibn Farhan amefupisha ukosoaji mkuu ulioelekezwa dhidi ya Sheikh na wanazuoni mashuhuri wa madhehebu ya Sunni, katika nukta nne kuu: 72 73

Al-Durar ul-Sunniyah, Juz. 10, uk. 244, na Mmishenari Na sio Mtume, uk. 125   Mishenari Na sio Mtume uk. 127-133. 125

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 125

5/31/2016 7:38:11 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

1.

Kuwatenga Waislamu

2.

Yeye kudai utume (kwa njia ya mzunguko si moja kwa moja)

3.

Aliamini katika kumfyonza Mungu na kuwa ndani Mwake anakuwa kitu.

4.

Kukanusha vitendo vya kimwujiza vya watu wema na watu mashuhuri wa dini.

Halafu anasema: ‘Dai kuu ni lile la kwanza ambalo hakuna anayeweza kukanusha.’ Baada ya hapo, amenukuu kutoka kwenye maandishi ya mwandishi mashuhuri wa kitabu kiitwacho “Da`wa al-Munawi`in”, Sheikh Ahmed Zaini Dahlan, kwamba: Wahhabi hawamchukulii yeyote kama mwenye imani ya uwepo wa Mungu Mmoja, isipokuwa yule anayefuata kila neno wanalolisema wao”74 Amemnukuu mwanazuoni mwingine mashuhuri, Zahawi, ambaye alisema, kama mtu angemuuliza imani ya Uwahhabi ilikuwaje na ilikuwa na lengo gani, katika kujibu maswali yote mawili angesema: “Uwekaji uamuzi wa kisheria kwamba Waislamu wote duniani ni makafiri! Jibu hili fupi linatosha kwa ajili ya aina hii ya maswali.” Hasan Ibn Farhan amejaribu kumtoa hatiani Sheikh kuhusu shutuma zingine tatu. Hata hivyo, shutuma ya kwanza ambayo ameikubali wala si shutuma ndogo hata kidogo, katika kufikiria ukweli kwamba Qur`ani Tukufu kwa kweli imeharamisha kuwashutumu Waislamu wengine na kuwaita makafiri pamoja na wale ambao hujifanya kuwa Waislamu:

‫يل للاهَّ ِ فَتَبَيَّنُوا َو اَل تَقُولُوا لِ َم ْن أَ ْلقَ ٰى إِلَ ْي ُك ُم‬ َ ‫يَا أَيُّهَا الَّ ِذينَ آ َمنُوا إِ َذا‬ ِ ِ‫ض َر ْبتُ ْم فِي َسب‬ 74

Da`wa al-Munawi’in, uk. 166. 126

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 126

5/31/2016 7:38:11 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

ۚ ٌ‫ض ْال َحيَا ِة ال ُّد ْنيَا فَ ِع ْن َد للاهَّ ِ َمغَانِ ُم َكثِي َرة‬ َ ‫الس اَ​َّل َم لَسْتَ ُم ْؤ ِمنًا تَ ْبتَ ُغونَ َع َر‬ “Enyi mlioamini! Mtakaposafiri katika njia ya Mwenyezi Mungu, basi hakikisheni wala msimwambie mwenye kuwapa salaam: wewe si muumini. Mnataka mafao ya duniani na kwa Mwenyezi Mungu kuna ngawira nyingi!.....” (Surah Al-Nisa, 4:94)

Ikifikiriwa jinsi Aya hii Tukufu ilivyosema kwa dhahiri, hivi upo mwanya wowote ulioachwa kwa ajili ya kuwatenga Waislamu?! Mahali pengine Muweza wa Yote anasema:

ُ‫ب للاهَّ ُ َعلَ ْي ِه َولَ َعنَه‬ َ ‫َض‬ ِ ‫َو َم ْن يَ ْقتُلْ ُم ْؤ ِمنًا ُمتَ َع ِّمدًا فَ َجزَا ُؤهُ َجهَنَّ ُم خَالِدًا فِيهَا َوغ‬ ‫َظي ًما‬ ِ ‫َوأَ َع َّد لَهُ َع َذابًا ع‬ “Na mwenye kumuua muumini kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannam, ni mwenye kudumu humo; na Mwenyezi Mungu amemghadhibikia na amemlaani na amemwandalia adhabu kubwa.” (Surah Al-Nisa, 4:93).

Aya hii inapeleka mtetemko kwenye uti wa mgongo wa muumini yeyote wa kweli; akiogopeshwa na moto wa jahannam, na kwamba hiyo ni adhabu ya milele ikiunganishwa na ghadhabu na laana ya Mungu. Ni maelezo ambayo hayajatajwa kwa dhambi yoyote kuu -isipokuwa kwa dhambi ya mtu kuua kwa kukusudia. Ikielezea adhabu ya Mungu kuwa ni ya milele - kufuatana na nukta kwamba adhabu hii kubwa ni mahususi kwa wasioamini - inaonesha kwamba wauaji wa Waislamu kwa hakika watakufa wakiwa sio waumini, na makazi yao ya milele huko Jahannam ni ya uhakika. Sasa fikiria kuhusu hadhi ya wale walioua kwa visingizio visivyo na msingi, waumini waliosimamisha swala, walifunga saumu, na waliotekeleza ibada zote za Kiislamu. Halafu wakawakamata wa127

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 127

5/31/2016 7:38:11 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

nawake zao na kupora rasilimali zao. Haya yalifanywa sio kwa mtu mmoja bali kwa mamia au hata maelfu ya watu pamoja na wanamume, wanawake, watoto wachanga, wazee, na vijana wote hawa waliangamizwa. Na wao wanaita hiyo ni dini ya Uislamu na Tawhidi ya Muhammad, na wao wanajifikiria kuwa ni waokoaji! “Kimbilio letu ni kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu” ambapo wao ni marejeo ya Aya hii Tukufu:

ُ َ‫َو َزيَّنَ لَهُ ُم ال َّش ْيط‬ َ‫يل فَهُ ْم اَل يَ ْهتَ ُدون‬ َ َ‫ان أَ ْع َمالَهُ ْم ف‬ ِ ِ‫ص َّدهُ ْم ع َِن ال َّسب‬ “….Na Shetani amewapambia vitendo vyao na akawazuilia njia. Kwa hiyo hawakuongoka.” (Surah An-Naml, 27:24).

Kwa bahati nzuri, wengi wa wafuasi wa imani hii hivi karibuni wamegundua kosa lao na sasa wanachukulia kitendo cha kuwatenga Waislamu kama dhambi kuu, hata kama kufuatana na waonavyo wao, hao ni watu wa bidaa. Kwa matumaini, hali hii itasafisha Uislamu na hapatakuwepo na uchokozi na vitisho. Mwishoni - kwa hitimisho lenye matumaini - tutafanya mapitio juu ya tangazo moja muhimu sana ambalo liliandikwa hivi karibuni na likachapishwa na kundi la wanazuoni, wanasheria na muhadithina wa Saudi Arabia: Tangazo hili lilichapishwa katika magazeti mengi sana, lakini tunanukuu tangazo hili kutoka kwenye kitabu “ (faharasa ya orodha ya wanatheolojia).

128

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 128

5/31/2016 7:38:11 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

NENO LA MWISHO Tamko Lililotolewa na Baraza la Ulama Waandamizi la Saudi Arabia Likilaani Uchokozi wa Wahhabi: Tafsiri ya tamko lililoandikwa na baraza la Ulamaa waandamizi wa kidini wa Saudi Arabia. “Sifa zote ni stahiki Yake Mwenyezi Mungu Mtukufu, na salaam za kumtakia rehma Mjumbe wa Mungu  na pia watu wa Nyumba yake na masahaba wake na wale walioongozwa nao baadaye. Katika kikao chake cha arobaini na tisa cha kongamano la baraza la “wanzuoni waandamizi” ambalo lilifanyika Ta`if mnamo tarehe 2 ya mwezi wa Rabi-u-Thani 1419 A.H., lilipima matukio yanayotokea katika nchi za Kiislamu na sehemu zingine kuhusu kuwatenga Waislamu. Milipuko ya mabomu, umwagaji damu na uharibifu wa taasisi. Kufuatana na mtazamo wa umuhimu wa jambo hili na matokeo yake, mauaji ya watu wasio na hatia, uharibifu wa rasilimali, kusababisha hofu miongoni mwa watu na kusababisha hali isiyo ya usalama. Kutokuwepo uimara na uwepo wa wasiwasi katika jamii, kongamano limeamua kufafanua uamuzi kuhusu jambo hili kwa ajili ya wema wa kimungu, kwa ajili ya waja wa Mungu na utimizaji wa wajibu, ili kuweza kufutilia mbali namna yoyote ya kutokueleweka kwa dhana za Kiislamu. “Katika msingi huu, nukta zifuatazo zimetajwa na kumwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu ajalie ufaulu wa utimilifu wake. 1.

Kuwatenga Waislamu (kumchukulia mtu mwingine kuwa Kafiri) ni fatwa ya kidini inayohitaji kigezo fulani ambacho kinatakiwa kuteuliwa na Mungu na Mjumbe Wake, kama vile ilivyo 129

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 129

5/31/2016 7:38:11 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

kwa yaliyohalalishwa na yaliyoharamishwa, na fatwa za faradhi lazima ziwekwe na Mwenyezi Mungu Mtukufu. Zaidi ya hayo, kuwatenga Waislamu na matamko na vitendo ambavyo wakati mwingine vinafikiriwa kuwa kufuru havifikii kiwango cha kufuru kuu ambayo itasababisha mtu kufukuzwa katika dini ya Uislamu. “Kwa hiyo, kwa kuwa fatwa ya kuwatenga Waislamu lazima iwe kwa niaba ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mjumbe Wake hairuhusiwi kumtenga mtu isipokuwa pale ambapo upo uthibitisho ulio dhahiri kutoka kwenye Kitabu na Hadithi unaoshuhudia kufuru yake. Kwa hiyo, tuhuma na dhana kamwe havitoshi, kwa sababu fatwa nzito sana zitawekwa katika hukumu hii. Wakati ambapo tunaamini kwamba kufuatana na kanuni ambayo inasema “adhabu za kisheria hukataliwa kupitia na kutiliwa shaka” hatutakiwi kufanya bila ya kuwa na uhakika kuhusu suala la “kuwatenga watu”, kwa sababu ya msukumo muhimu ambao unashirikisha, hata ni muhimu zaidi kuliko adhabu zilizokongomewa na hivyo Mtukufu Mtume  alitahadharisha kila mtu kuhusu kumtenga mtu ambaye kwa kweli sio kafiri na akasema; “Kama mtu anamuita ndugu yake Muislamu hivi: Ewe Kafiri! Na anasema kweli, upande wa pili utakuwa umekamatwa katika malipo ya maovu, lakini kama anasema uwongo malipo ya uovu yatamrudia yeye.” “Wakati mwingine mafungu fulani ya maneno yanaonekana katika Kitabu na hadithi ambayo hufichua kwamba neno fulani au kitendo fulani au imani fulani italeta matokeo ya kufuru, ambapo vipo vizingiti fulani ambavyo huzuia fatwa hii. Hii inafanana na fatwa zingine ambazo hazikuhakikiwa bila ya mkusanyiko wa sababu zote za kisheria na masharti na kuondosha vipingamizi. Mathalani, urithi ni mojawapo ya fatwa za kimungu ambayo huja 130

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 130

5/31/2016 7:38:11 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

kufuatana na undugu, lakini wakati mwingine vikwazo fulani huzuia ufanikishaji wa fatwa hii, kama vile katika dini. Pia, ipo mifano ambapo mtu analazimishwa kutamka maneno ya kukufuru lakini hayamfanyi yeye kuwa kafiri (kama ambavyo amelazimishwa). Wakati mwingine mtu anaweza kutamka neno la kukufuru akiwa katika shinikizo la furaha au hasira (wakati mtu anakuwa hawezi kudhibiti hisia zake), na hali hiyo haiwezi kumwelekeza yeye kwenye ukafiri. Hali hii inafanana sana na ile hadithi mashuhuri ambapo mtu alisema wakati akiwa katika hali ya raha mustarehe iliyopindukia: Ewe Mungu! Wewe ni mja wangu na mimi ni Mola wako!” “Matokeo muhimu na yanayotishia huendelea kutokana na haraka katika kuwatenga watu, miongoni mwao ni kutangaza uhai na rasilimali za mtu kuwa ni halali kwa sababu ya uhalifu. Kuzuia urithi wake na kutangaza utengano wake na mke wake, ambayo ni miongoni mwa matokeo ya kuritadi. Inawezekanaje Muislamu kuruhusiwa kumshtaki Muislamu mwenzake bila kuwa na uhakika kabisa na kutokuwa na hata shaka ndogo sana (na kuchukua jukumu la yote haya?) “Haraka katika kuwatenga watu ina hatari kubwa, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

ِّ ‫ال ْث َم َو ْالبَ ْغ َي بِ َغي ِْر ْال َح‬ ‫ق‬ َ ‫اح‬ ِ ‫قُلْ إِنَّ َما َح َّر َم َربِّ َي ْالفَ َو‬ ِ ْ‫ش َما ظَهَ َر ِم ْنهَا َو َما بَطَنَ َو إ‬ َّ‫َوأَ ْن تُ ْش ِر ُكوا بِ ه‬ َ‫اللِ َما لَ ْم يُنَ ِّزلْ بِ ِه س ُْلطَانًا َوأَ ْن تَقُولُوا َعلَى للاهَّ ِ َما اَل تَ ْعلَ ُمون‬ “Hakika Mola Wangu ameharamisha mambo machafu yaliyodhihirika na yaliyofichika. Na dhambi na dhulma bila ya haki. Na kumshirikisha Mwenyezi Mungu na ambacho hakukiteremshia dalili. Na kusema juu ya Mwenyezi Mungu msiyoyajua.” (Surah Al-A`araf, 7:33). 131

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 131

5/31/2016 7:38:11 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

“Kufuatana na Aya hii Tukufu aina yoyote ya kitendo kisicho na heshima, uchokozi, imani ya kuabudu miungu wengi, na shutuma zisizo za kweli, na matamko yasiyo na msingi kuhusu Mungu yanachukuliwa kama mambo yaliyoharamishwa. 2.

Matokeo ya itikadi hii ya uwongo (kuwashutumu Waislamu kwamba wanaabudu miungu wengi), hiyo ni kuchukulia uhai wa mtu kwa ajili ya uhalifu, kutowaheshimu na kutowajali watu wengine na kupora rasilimali zao, na kulipua majengo, magari, biashara na vituo vya biashara. Kufuatana na makubaliano ya Waislamu wote hivyo ni vitendo vilivyoharamishwa na viovu, kwani vitendo hivyo vitasababisha kutoheshimu uhai na rasilimali na vitavuruga amani na usalama wa watu ambao husafiri kila siku asubuhi hadi jioni kutoka majumbani kwao kwenda ofisini kufanya kazi.

“Vitendo hivi visivyopendeza, pia vitasambaratisha maslahi ya watu katika jamii ambapo bila ya shughuli hizo maisha hayatavumilika. Uislamu umeheshimu rasilimali, vikorokoro na uhai wa Waislamu na haumruhusu mtu yeyote kuingia katika eneo bila ruhusa. Na miongoni mwa masuala ya mwisho ambayo Mtukufu Mtume  aliwatangazia Waislamu wote wakati wa Hijja yake ya mwisho alisema kwamba: “Uhai wenu, rasilimali zenu na vikorokoro vyenu lazima viheshimiwe na ninyi wote, kama ambavyo mnaheshimu mwezi huu (mwezi ulioharamishwa vita) na Ardhi hii Tukufu ya (Makkah).” Halafu akarudia: “Ewe Mola Wangu! Uwe shahidi kwamba nilisema (kile ambacho nilitakiwa kusema)!” “Hadithi hii imethibitishwa na wasimuliaji wote kwa pamoja. Na aliendelea kusema: “Muislamu ameharamishwa kunyang`anya vikorokoro vya Muislamu mwenzake, kumuua bila haki, kupora rasilimali zake, kukamata wake zao, na kuwavunjia heshima.” Pia 132

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 132

5/31/2016 7:38:11 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

alisema: “Jizuieni vitendo vya dhulma kwani mtu dhalimu atakuwa mpweke katika giza mnamo Siku ya Hukumu.” Zaidi ya hayo Mola aliyetukuka amewatishia wale wanaoua watu wasio na hatia, kwamba atawaadhibu adhabu kali sana:

ُ‫ب للاهَّ ُ َعلَ ْي ِه َولَ َعنَه‬ َ ‫َض‬ ِ ‫َو َم ْن يَ ْقتُلْ ُم ْؤ ِمنًا ُمتَ َع ِّمدًا فَ َجزَا ُؤهُ َجهَنَّ ُم خَالِدًا فِيهَا َوغ‬ ‫َظي ًما‬ ِ ‫َوأَ َع َّد لَهُ َع َذابًا ع‬ “Na mwenye kumuua muumini kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannam, ni mwenye kudumu humo; na Mwenyezi Mungu amemghadhibikia na amemlaani na amemwandalia adhabu kubwa.” (Surah Al-Nisa, 4:93).

“Na pia kuhusu kumuua mtu asiye muumini kwa kughafilika, ambaye anaishi maisha ya kuhifadhiwa na Waislamu, alisema: “Aliyeua lazima alipe fedha ya kufidia damu kwa familia ya marehemu.”75 “Kufuatana na yote haya, pangekuwepo na fatwa ipi kwa ajili ya kuua kwa kukusudia? Kwa hakika uhalifu huu ungekuwa mkubwa zaidi na adhabu yake ambayo ni kali zaidi. “Katika hadithi iliyothibiti kutoka kwa Mtukufu Mtume , imetamkwa kwamba mtu anayemuua mtu asiye muumini ambaye yupo katika hifadhi ya Waislamu kamwe hatanusa manukato ya pepo! 3.

75

Baraza hili linawatangazia watu wote wa ulimwengu kwamba Uislamu unakataa aina hizi za imani zilizo batili na linachukulia yale yote yanayofanywa sasa katika baadhi ya mataifa, kama vile kuua watu wasio na hatia, kulipua majengo na magari, vituo vya miji na rasilimali za watu binafsi na kuharibu sehemu za kufanyia kazi, kama ni uhalifu wa kuchukiza.

Imedondolewa kutoka kwenye aya ya 92 ya Surah Al-Nisaa. 133

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 133

5/31/2016 7:38:11 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

Vivyo hivyo, kila Muislamu anayemwamini Mungu na Siku ya Hukumu amechoshwa na vitendo hivi. Vitendo hivi vinatekelezwa na wale ambao fikira zao zimekengeuka na kupotoka, kwa hiyo lawama ya uhalifu huu inawaangukia wao tu na isifungamanishwe na Uislamu wala na Waislamu ambao wanaongozwa na Uislamu na kuambatana na Qur`ani Tukufu na Hadithi. Vitendo hivi ni vitendo vichafu vya kifisadi na mauaji ya kikatili, ambavyo havikubaliki katika sheria za dini ya Kiislamu na misingi ya asili ya utu wa binadamu. Hivyo hadithi za Kiislamu kwa kweli zimekataza kabisa vitendo hivi, na kuharamisha usuhuba na aina hii ya watu…. Tamko hili limemalizia kwa kunukuu aya na hadithi kadhaa ambazo zinaonesha kwamba Uislamu ni dini ya upendo, urafiki, mshikamano katika wema na uadilifu, imani ya kimantiki na mazungumzo yenye busara, dini ya uzuiaji kabisa aina yoyote ya vurugu na uchokozi.76 Uchambuzi wa Tamko hili kwa Ufupi: Tamko hili lilisainiwa na mwanazuoni wa cheo cha juu kidini wa Uwahhabi wa Saudi, Abdul-Aziz bin Abdullah bin Baz, na wanazuoni wengine wa cheo cha juu ishirini na lilitolewa siku chache kabla ya kifo cha ibn Baz. Tamko hili lina nukta kadhaa muhimu, baadhi ya nukta hizo zinawasilishwa kama ifuatavyo: 1) Pamoja na kwamba tamko hili lilitakiwa kuchapishwa kabla ya umwagaji damu wote na upotevu wa uhai wenye thamani, rasilimali na hadhi, ni kama vile ni tiba ambayo imekuja kwa kuchelewa sana. Lakini, katika hatua yoyote ya hatari, kuzuia hali hiyo kuen76

Tamko hili lilichapishwa kwennye magazeti mengi na majarida ya Saudi Arabia, lakini tunanukuu kutoka kwenye kitabu kiitwacho “Tabaqat al-Mutaqalimin” Juz. 4, uk. 100 134

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 134

5/31/2016 7:38:11 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

delea ni kupiga hatua na manufaa, ambayo inastahili kupewa shukurani na kuzingatiwa. Hatimaye, sharti la mwisho madhubuti na la maana lilitolewa dhidi ya wale wenye msimamo mkali, ambao walidai kuwa ni vipenzi wa Mtunga sheria za dini, na bado walionesha iwe wazi kwa yote hayo kwamba hawakukubaliana na tamko hili, na walifuata matamanio yao wenyewe na hamu zao na sio fatwa za Kiislamu. 2.

Tamko hili limeandaa njia kivitendo kwa ajili ya kukosoa fikira na imani za Sheikh Mohammad bin Abdul-Wahhab na hata wafuasi wa Uwahhabi wanaweza kumkosoa kwa namna ya heshima, na wakawasili katika matokeo ya msimamo wa wastani zaidi katika imani yao ili waweze kufanya kazi kwa kushirikiana na Waislamu wenzao.

3.

Tamko hili ambalo limesheheni maneno yaliyotumiwa kwa uangalifu, liliwatangazia wale wenye msimamo mkali kwamba zama za kuwatenga Waislamu sasa zimefika tamati, na kwamba wasingemshutumu mtu yeyote ambaye hakukubaliana na fikira zao, za kufuru na kuharibu maisha yao, utajiri wao na hadhi zao, kwa sababu kitendo hiki kingeweza kumfanya mtekelezaji kuwa kafiri.

4.

Tamko hili liliboresha taswira ya Uislamu ya kuchukiza sana na ya kichokozi ambayo ilikwishachorwa na kundi hili kuhusu Uislamu kwa dunia nzima na kuonesha kwamba Waislamu halisi walichoshwa na vitendo hivi, hususani kwa kuwa vitendo hivyo viliwapatia kisingizio kizuri sana mabwana wa kanisa na Wazayuni, kuwasilisha taswira hii mbaya kama ndiyo sura halisi ya Uislamu na kuogopesha dunia kwa kutumia taswira hiyo. Sisi kimbilio letu ni kwa Mungu kutokana na madhara ya wajinga, na kuomba kwamba Mungu anamuongoza kila mtu 135

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 135

5/31/2016 7:38:11 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

kwa mintarafu ya njia iliyonyooka na kuwasaidi kutokana na mitego ya Shetani. Ushauri wa kirafiki kwa wanazuoni wa Kiislamu wa Hijaz: Tunatoa ushauri wetu wa kirafiki na unyenyekevu kwa wanazuoni wote wa Uwahhabi ambao wanatafuta njia ya msimamo wa wastani wasipoteze fursa hii yenye thamani kupima upya kanuni za Uwahhabi na kuondoa ufa mpana kwa uangalifu baina yao na Waislamu wengine, ambao maadui wanautumia kwa manufaaa yao. Tunaweka maoni ya kirafiki kama ifuatavyo: 1.

Tunalaani kuwatuhumu Waislamu kuhusu imani ya kuabudu miungu wengi na kufuru kwa mambo ambayo ni ya falsafa ya kisheria ya juu sana, na kuwashauri wafuasi wao kuambatana na amri hii ya Qur`ani Tukufu; “…..basi hakikisheni wala usimwambie mwenye kuwapa Salaam: wewe si muumini….”

2.

Tunalaani vikali uchokozi wowote wa kidini ambao umetokea katika vitisho vya kushtua sana Iraq, Pakistani, Afghanistan na hata Saudi Arabia na sehemu zingine za dunia.

Chokochoko hizo huchafua jina la dini tukufu ya Uislamu, ambayo kwa uhakika ni imani ya dunia nzima. Na vitendo hivyo vinatoa njia nzuri sana ya propaganda kwa maadui wa Uisalmu, na inaangamiza juhudi zote ambazo wanafikira wa Kiislamu na wamishenari na waandishi weledi wa Kiislamu ambazo wamezitekeleza katika njia ya kutangaza Uislamu. Tunalaani ukiukaji wote wa haki na tunauchukulia kama mfano wa kufutilia mbali kimbari na uzao,77 ambao umetajwa katika Qur`ani Tukufu. 77

al-Hujurat; 49:13 136

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 136

5/31/2016 7:38:11 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

3.

Kutengeneza uwanja kwa ajili ya mazungumzo ya kirafiki na kimantiki na wanazuoni wengine wa Kiisalmu katika misingi ya kuheshimiana na bila ya utovu wa adabu na tuhuma za kuabudu miungu wengi na ujinga, na kukubali kile ambacho wanakiona ni cha kweli kufuatana na aya hii: “Wale wanaosikiliza neno (la Mwenyezi Mungu Mtukufu) na kufuata uelewa wake ulio mzuri sana.”

4.

Kufungua mipaka yao ya kiitikadi na kijiografia ili waweze kupokea vitabu vya kisayansi na kimantiki vya imani za Kiislamu bila wao kujiona wapo kwenye hatari katika kufanya hivyo, na kubadilishana wanafunzi wa seminari wa nchi zingine za Kiislamu.

5.

Kuvunja ukuta wa kutokuaminiana, kutuhumiana na nia mbaya baina yao wenyewe na Waislamu wengine na kuwa katika mawasiliano na kuzuru seminari za kila upande, na kuwa tayari kushiriki kwenye makongamano yahusuyo mambo mbalimbali ya Kiislamu mahali popote katika ulimwengu wa Kiislamu.

6.

Kuwaonya marafiki zao dhidi ya kuyachukulia katika dharura masuala ya sheria ya dini juu ya mambo makubwa na madogo kama ndiyo uhalisi wa Uislamu, na kuchukulia mambo mengine zaidi ya hayo kuwa ni kufuru, kutenda dhambi na bidaa zilizoharamishwa, na kusikia ujumbe wa Aya Tukufu isemayo: “Hatuwapeni elimu yote isipokuwa kidogo tu” Popote pale ambapo kanuni hizi zinapofanyiwa kazi yapo matumaini kwamba mshikamano miongoni mwa safu za Waislamu utakuwepo na tamaa ya mafaniko ya kufika kwenye kamba ya Mwenyezi Mungu Mtukufu itakuwepo, na lengo la Uislamu “kushinda dini zingine zote” litafanikiwa. MWISHO. 137

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 137

5/31/2016 7:38:11 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

ORODHA YA VITABU VILIVYO ­CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1. i) Qur’ani Tukufu – Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili ii) Qur’an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thelathini 2. Uharamisho wa Riba 3. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza 4. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili 5. Hekaya za Bahlul 6. Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) 7. Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (a.s.) 8. Hijab vazi Bora 9. Ukweli wa Shia Ithnaashari 10. Madhambi Makuu 11. Mbingu imenikirimu 12. Abdallah Ibn Saba 13. Khadijatul Kubra 14. Utumwa 15. Umakini katika Swala 16. Misingi ya Maarifa 17. Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia 18. Bilal wa Afrika 19. Abudhar 20. Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu 21. Salman Farsi 22. Ammar Yasir 23. Qur’an na Hadithi 24. Elimu ya Nafsi 25. Yajue Madhehebu ya Shia 26. Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur’an Tukufu 138

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 138

5/31/2016 7:38:11 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

27. Al-Wahda 28. Ponyo kutoka katika Qur’an 29. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii 30. Mashukio ya Akhera 31. Al Amali 32. Dua kwa Mujibu wa Ahlulbayt (a.s) 33. Udhuu kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna 34. Haki za wanawake katika Uislamu 35. Mwenyezi Mungu na sifa zake 36. Kumswalia Mtume (s) 37. Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) 38. Adhana 39. Upendo katika Ukristo na Uislamu 40. Qur’ani na Kuhifadhiwa Kwake 41. Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu 42. Kupaka juu ya khofu 43. Kukusanya Sala Mbili 44. Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara 45. Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya 46. Kusujudu juu ya udongo 47. Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) 48. Tarawehe 49. Malumbano baina ya Sunni na Shia 50. Kupunguza Swala safarini 51. Kufungua safarini 52. Umaasumu wa Manabii 53. Qur’an Yatoa Changamoto 54. as-Salaatu Khayrun Mina -’n Nawm 55. Uadilifu wa Masahaba 56. Dua e Kumayl 57. Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu 139

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 139

5/31/2016 7:38:11 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

58. Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake 59. Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata 60. Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mtume Muhammad (s) 61. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza 62. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili 63. Kuzuru Makaburi 64. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza 65. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili 66. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu 67. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne 68. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano 69. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita 70. Tujifunze Misingi Ya Dini 71. Sala ni Nguzo ya Dini 72. Mikesha Ya Peshawar 73. Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu 74. Ubora wa Imam ‘Ali na Ushia ndio njia iliyonyooka 75. Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake 76. Liqaa-u-llaah 77. Muhammad (s) Mtume wa Allah 78. Amani na Jihadi Katika Uislamu 79. Uislamu Ulienea Vipi? 80. Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) 81. Dhana ya Ndoa ya Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) 82. Urejeo (al-Raj’ah) 83. Mazingira 84. Utokezo (al - Badau) 85. Hukumu ya kujenga juu ya makaburi 86. Swala ya maiti na kumlilia maiti 87. Uislamu na Uwingi wa Dini 88. Mtoto mwema 140

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 140

5/31/2016 7:38:11 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

89. 90. 91. 92. 93. 94. 95. 96. 97. 98. 99. 100. 101. 102. 103. 104. 105. 106. 107.

Adabu za Sokoni Na Njiani Johari za hekima kwa vijana Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu Tawasali (AT- TAWASSUL) Imam Mahdi katika Usunni na Ushia Hukumu za Mgonjwa Sadaka yenye kuendelea Msahafu wa Imam Ali Maimamu wa Ahlul Bait – Ujumbe na Jihadi Idi Al-Ghadir Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu Hukumu zinazomuhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi Huduma ya Afya katika Uislamu Sunna za Nabii Muhammad (saww) Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) Shahiid Mfiadini

108. 109. 110. 111. 112. 113. 114. 115. 116. 117. 118. 119.

Mwanamke Na Sharia Ujumbe -Sehemu ya Kwanza Ujumbe - Sehemu ya Pili Ujumbe - Sehemu ya Tatu Ujumbe - Sehemu ya Nne Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu Hadithi ya Thaqalain Ndoa ya Mutaa Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza Ukweli uliopotea sehemu ya Pili Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu Ukweli uliopotea sehemu ya Nne 141

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 141

5/31/2016 7:38:11 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

120. Ukweli uliopotea sehemu ya Tano 121. Mkutano wa Maulamaa wa Baghdad 122. Safari ya kuifuata Nuru 123. Fatima al-Zahra 124. Myahudi wa Kimataifa 125. Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi 126. Visa vya kweli sehemu ya Kwanza 127. Visa vya kweli sehemu ya Pili 128. Elimu ya Ghaibu ya Maimamu 129. Mwanadamu na Mustakabali wake 130. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) 131. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) 132. Khairul l’Bariyyah 133. Uislamu na mafunzo ya kimalezi 134. Vijana ni Hazina ya Uislamu 135. Adhana ni Ndoto au ni Wahyi? 136. Tabaruku 137. Saada Kamili – Kitabu cha Kiada cha Maadili 138. Vikao vya furaha 139. 140. 141. 142. 143. 144. 145. 146. 147. 148. 149. 150.

Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? Visa vya wachamungu Falsafa ya Dini Kuhuzunika na Kuomboleza Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah Mjadala wa Kiitikadi Kuonekana kwa Allah Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) Ndugu na Jirani Ushia ndani ya Usunni Maswali na Majibu 142

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 142

5/31/2016 7:38:11 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

151. 152. 153. 154. 155. 156. 157. 158. 159. 160. 161. 162. 163. 164. 165. 166. 167. 168. 169.

Mafunzo ya hukmu za ibada Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1 Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2 Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 Abu Huraira Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. Mazingatio kutoka katika Qur’an - Sehemu ya Kwanza Mazingatio kutoka kaitka Qur’an - Sehemu ya Pili Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili Shia na Qur’ani – Majibu na Maelezo Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu Uislamu Safi Majlisi za Imam Husein Majumbani Je, Kufunga Mikono Uislam wa Shia Amali za Makka

170. 171. 172. 173. 174. 175. 176. 177. 178. 179. 180. 181.

Amali za Madina Asili ya Madhehebu katika Uislamu Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi Ukweli uliofichika katika neno la Allah Uislamu na Mifumo ya Uchumi Umoja wa Kiislamu na Furaha Mas’ala ya Kifiqhi Jifunze kusoma Qur’ani as-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah Hayya ‘Alaa Khayri’l-’Amal Katika Adhana Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na Ramadhani) 143

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 143

5/31/2016 7:38:11 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

182. Uadilifu katika Uislamu 183. Mahdi katika Sunna 184. Maswali Ya Uchunguzi Kuhusu Uislam 185. Kazi na Bidii ni njia ya maendeleo 186. Abu Talib – Jabali Imara la Imani 187. Ujenzi na Utakaso wa Nafsi 188. Vijana na Matarajio ya Baadaye 189. Historia maana na lengo la Usalafi 190. Ushia – Hoja na Majibu 191. Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) 192. Maombolezo – Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) 193. Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu 194. Takwa 195. Upotoshaji Dhahiri katika (Turathi) Hazina ya Kiislamu 196. Amirul Muuminina (as) na Makhalifa 197. Tawheed Na Shirki 198. Kuvunja hoja iliyotumika kutetea Uimamu wa AbuBakr 199. Adabu za vikao na mazungumzo 200. Hija ya Kuaga 201. 202. 203. 204. 205. 206. 207. 208. 209. 210. 211. 212.

Uwazi baina ya Maslahi na Vikwazo Fadhila za watukufu watano katika Sahih Sita Mdahalo baina ya Mwanachuoni waKisunni na Kishia (Al- Muraja’aat) Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (as) Imam Husain ni Mfumo wa Marekebisho na Mageuzi Mtazamo kuhusu msuguano wa Kimadhehebu Nchi na Uraia – Haki na wajibu kwa Taifa Mtazamo wa Ibn Taymiyyah juu ya Imam Ali (as) Uongozi wa Kidini – Maelekezo na Utekelezaji wa Kijamii Maadili ya Ashura Mshumaa – Shahidi na Kifo cha Kishahidi Mizani ya Hekima – Hadithi za Ahlul Bait (as) – Sehemu ya Kwanza 144

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 144

5/31/2016 7:38:11 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

213. Imam Ali na Mambo ya Umma 214. Imam Ali na Mfumo wa Usawa 215. Uimamu na Tamko la Kutawazwa 216. Mfumo wa Wilaya 217. Vipi Tutaishinda Hofu? 218. Kumswalia Mtume ni Ufunguo wa Utatuzi wa Matatizo 219. Maeneo ya Umma na Mali Zake 220. Nahju ‘L-Balagha– Majmua ya Khutba, Amri, Barua, Risala, Mawaidha na Semi za Amirul-Muuminin Ali bin Abu Talib (a.s.) 221. Mukhtar – Shujaa aliyelipiza kisasi dhidi ya wauaji wa Imam Husein (as) hapo Karbala 222. Mazingatio Katika Swala 223. Imam Hasan na Mfumo wa Kujenga Jamii 224. Vyakula Na Vinywaji 225. Kuelewa Rehema ya Mwenyezi Mungu 226. Imam Mahdi na Bishara ya Matumaini 227. Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu 228. Shia Na Sahaba - Majibu na Maelezo 229. Majanga Na Jukumu la Jamii 230. Shia Na Hadith - Majibu na Maelezo 231. Upotofu Ndani ya Kitabu cha Mitaala kwa Shule za Sekondari 232. Ugaidi Wa Kifikra Katika Medani Ya Kidini 233. Yafaayo kijamii 234. Uswalihina Dhahiri Na Batini Yake 235. Mkakati wa Kupambana na Ufakiri 236. Mwanamke Katika Harakati Za Mageuzi 237. Jihadi 238. Hija Katika Maneno Na Ujumbe Wa Imam Khomeini (R.A) 239. Tiba Ya Maradhi Ya Kimaadili 240. Yusuf Mkweli 241. Taqiyya Kwa Mujibu Wa Sheria Ya KIISLAMU

145

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 145

5/31/2016 7:38:12 PM


UWAHABI KWENYE NJIA PANDA

242. Imam Mahdi (A.S) Imam Wa Zama Hizi Na Kiongozi Wa Dunia 243. Talaka Tatu 244. Safari Ya Kuelekea Kwa Mwenyezi Mungu 245. Hotuba Za Kiislamu Juu Ya Haki Za Binadamu 246. Mashairi Ya Kijamii 247. Ngano Ya Kwamba Qur’ani Imebadilishwa 248. Wito Kwa Waumini: “Enyi Mlioamini” 249. Imam Husain (a.s) ni Utu na Kadhia 250. Imam Husain ni Kielelezo cha Kujitoa Muhanga na Fidia 251. Imam Mahdi ni Tumaini la Mataifa 252. Kuchagua Mchumba 253. Mazungumzo ya Umoja – Ukosoaji na Usahihishaji 254. Utamaduni wa Mwamko wa Kijamii 255. Hekima za kina za Swala 256. Kanuni za Sharia za Kiislamu 257. Utamaduni kufuatana na Qur’ani na Utekelezaji wa Kivitendo (Sehemu ya Kwanza) 258. Kauli sahihi zaidi katika kufafanua Hadithi

146

05_16_UWAHABI KWENYE_31_May_2016.indd 146

5/31/2016 7:38:12 PM


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.