Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:37 PM
VIJANA NI HAZINA YA UISLAMU Kimeandikwa na: Jumuiya ya Maarifa na Utamaduni wa Kiislamu
Kimetarjumiwa na: Amiri Mussa Kea.
Page A
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
B
7/16/2011
12:37 PM
Page B
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:37 PM
©Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 - 512 - 85 - 0 Kimeandikwa na: Jumuiya ya Maarifa na Utamaduni wa Kiislamu Kimetarjumiwa na: Amiri Mussa Kea
Kimehaririwa na: Shaikh Haroon Pingili Kimepangwa katika Kompyuta na: Ukhti Pili Rajab Toleo la kwanza: April, 2011 Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info
Page C
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:37 PM
Page D
YALIYOMO Vijanani hazina ya Uislamu …….………………………………............2 Utangulizi…………………………………………………………............2 Sifa za Vijana wa Kiislamu……………………………………….............8 Vijana Katika Uislamu…………………………………………….............8 Mwenye Kujali, Kujidhibiti, Makini, Muongozaji na Mwenye Hekima ..10 Mwenye Kutumia Uwezo Wake, Dhamira Yake, Uchangamfu Wake na Nguvu Zake……………………………………………….......................12 Mwenye Wivu……………………………………………………….......13 Mwenye Haya………………………………………………………........14 Mwenye Kuunusuru Uislamu……………………………………............15 Hupenda Mambo ya Mustahabu na Sunna………………………............16 Kiigizo cha Vijana………………………………………………….........17 Pamoja na Kiongozi………………………………………………..........17 Kipindi cha Masomo……………………………………………….........18
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:37 PM
Page E
NENO LA MCHAPISHAJI Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kiitwacho, al-Shabaab Dhakhiratu ‘l-Islam. Sisi tumekiita, Vijana ni Hazina ya Uislamu. Kitabu hiki kimeandikwa na Jumuiya ya Maarifa na Utamaduni wa Kiislamu. Katika umma au taifa lolote, vijana ni mhimili mkubwa na nguvukazi ya taifa hilo. Hivyo, ili mhimili huu ufanye kazi yake vizuri na kwa maadili mema, ni lazima umma au taifa hilo lihakikishe kwamba vijana wanapata mafunzo na maelekezo ya kina ya majukumu yao kama vijana. Uislamu ukiwa kama umma, umeweka taratibu nzuri za kuwafundisha vijana wake ili wayafahamu majukumu yao, hii ikiwa ni pamoja na kuwapa elimu ya dini na elimu dunia (sekula). Kitu cha kusikitisha ni kwamba nchi nyingi za Kiislamu zimeacha utaratibu huu na kuupa mwanya utamaduni wa Magharibi kushamiri katika nchi zao. Na waathirika wakubwa ni vijana ambao ndio nguzo ya taifa. Kitabu hiki kinakumbusha Umma wa Kiislamu na vijana kwa ujumla juu ya jukumu lao hili muhimu. Mwandishi anaelezea sifa za vijana wa Kiislamu na wajibu wao katika taifa. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa utandawazi ambapo vijana wetu wametumbukia katika kuiga tamaduni za watu wa Magharibi na kusababisha maadili kuporomoka.
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:37 PM
Page F
Kutokana na ukweli huo, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili. Tunamshukuru ndugu yetu, Sheikh Amiri Mussa kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni changamoto kubwa kwa wasomaji wetu, hususan vijana wetu ambao ni waathirika wakubwa wa tamaduni hizi za Magharibi. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
G
7/16/2011
12:37 PM
Page G
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
1
7/16/2011
12:37 PM
Page 1
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:37 PM
Page 2
Vijana ni hazina ya Uislamu
VIJANA NI HAZINA YA UISLAMU Utangulizi: Mwenyezi Mungu (a.j) anasema:
“Vijana hao walipokimbilia katika pango na wakasema Mola wetu! Utupe rehema kutoka kwako, na ututengezee mwongozo katika jambo letu. Basi tukaziba masikio yao katika pango kwa muda wa miaka mingi. Kisha tukawafufua ili tujue ni lipi katika makundi mawili litalohesabu sawa sawa muda waliokaa. Sisi tunakusimulia habari zao kwa kweli, hakika wao ni vijana waliomwamini Mola wao, nasi tukawazidishia katika mwongozo. Na tukaziimarisha nyoyo zao waliposimama na wakasema: Mola wetu ni Mola wa mbingu na ardhi, kabisa hatutamwabudu mungu mwingine badala yake, bila shaka tutakuwa tumesema ubaya uliopita kiasi.” (18:10-14) Katika aya hiyo Mwenyezi Mungu anaeleza kisa cha watu wa pango (As’haabul-Kahf), ni vijana ambao walikuwa watumishi wa Mfalme aitwaye “Dakyanus” wa mji wa “Ifsus” miongoni mwa miji ya Roma, 2
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:37 PM
Page 3
Vijana ni hazina ya Uislamu ambayo hivi sasa upo katika nchi ya Uturuki, namna gani vijana hao walivyomwamini Mola wao kutokana na kufikiria hali zao na hali za dunia. Na jambo la msingi ni kwamba vijana hao walikuwa ni watu wa karibu wa Mfalme yule, na dunia ilikuwa mikononi mwao na walikuwa wakipata chochote wakipendacho, lakini wao pamoja na yote hayo walifikia daraja kubwa la imani juu ya Mwenyezi Mungu wakiomba msaada na nusura kutoka Kwake, na walipokuwa njiani walikutana na mchungaji wa mifugo wakamsimulia kisa chao, basi akaamini na akawa miongoni mwao, ikawa idadi yao ni watu saba wakiwa na mbwa wa mchungaji, na pindi Mfalme alipotambua kutoroka kwao aliwafuatilia nyuma yao yeye na jeshi lake hadi alipowagundua wakiwa katika pango, na Malaika wa kutoa roho alikuwa ameshachukua roho zao kwa amri ya Mwenyezi Mungu kabla ya kufika kwake, alipowaona wakiwa katika hali hiyo aliamuru uzibwe mlango wa pango kwa chokaa na mawe, akaliambia jeshi lake: “Waambieni na wao wamwambie Mola wao wa mbinguni awaokoe na awatoe mahala hapo.” Upembuzi wa kisa hicho ni kwamba hao walikuwa vijana waliomwelekea Mwenyezi Mungu (a.j) baada ya imani yao Kwake kwa ikhlas na ukweli, na hasa hasa vijana wana uwezo wa kuleta mabadiliko na mageuzi ndani ya nafsi zao kwa upeo mkubwa zaidi ya wengine, na huwawezesha wao kuzidi katika uongofu na maarifa kabla hawajafikwa na umri wa udhalili (umri wa uzee), ambapo nguvu zao za maarifa na utendaji hupungua. Kisa hicho ni kielelezo kizuri kwa vijana wa zama zote, ambapo hufunguka mbele yao katika umri huo milango yote ya matamanio. Kwa hivyo binadamu baada ya kupitia hatua ya utoto huingia hatua ya kubalehe ambayo ni nyeti mno katika maisha ya binadamu, kwa sababu umri huo huanza utambuzi wa kiakili na kufunguka juu ya dunia, na uwezo wa kimwili huwa katika mchakato wa ukamilifu, kisha huanza hatua mpya tunayoiita umri wa ujana, na hapo kijana huondokana na hali ya uthabiti 3
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:37 PM
Page 4
Vijana ni hazina ya Uislamu wa nafsi yake na uhakiki wa shakhsia yake ya kujitegemea, iwapo hatutakuwa na usimamizi na ukakosekana mwongozo na mwelekeo wake, kwa hivyo kijana atafeli kujidhibiti hususan jamii inayomzunguka ikiwa imeharibika na kuwa ya kifisadi pia kutokuwa nzuri, na ikawa kijana hakuhifadhika katika hatua ya kabla ya kubalehe kwa kupata malezi mazuri ya kiislamu. Zimepokewa hadithi chungu nzima ambazo kwa njia moja au nyingine zinatoa ishara kuhusu hatari ya kipindi hiki – kipindi cha ujana – Mtume (s.a.w.w) amesema: ?????? ???? ?? ?????? “Ujana ni aina ya uwendawazimu” Na imepokewa kutoka kwa Imam Swadiq (a.s.) amesema:
?? ????? ???? ???? ????? ?? ????? ???? ????? ????????? ??? ?? “Sipendi kumuona kijana miongoni mwenu ila awe katika hali mbili; msomi au mwanafunzi, na kama hakuwa hivyo basi atakuwa amefanya uzembe na kupoteza fursa, na iwapo atapoteza fursa atakuwa amefanya dhambi, na akifanya dhambi naapa kwa yule aliyemtuma Mtume Muhammad (s.a.w.w.) kwa haki kwamba ataishi mtu huyo motoni.” Imepokewa kutoka kwa Imam Baqir (a.s.) amesema: ?? ???? ???? ?? ???? ?????? ?? ????? ??????? “Lau nitaletewa kijana miongoni mwa vijana wa kishia hakujifunza dini nitamwadabisha.” Hapana shaka kwamba maandiko hayo hutoa ishara za wazi wazi kuhusu 4
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:37 PM
Page 5
Vijana ni hazina ya Uislamu hatari za kijana kuacha mambo ya msingi na kuingia katika mihangaiko ya maisha pasi na hifadhiko la kifikra, kiitikadi, kitabia na kimwenendo, kwani hayo yatampelekea kuangukia katika madhambi, maasi na upotevu kama alivyoapa Imam Swadiq (a.s) kwalo, Imam Baqir (a.s) amelitilia mkazo hilo kwa ibara “Nitakapojiwa na kijana hakujifunza mambo yake basi ningemtia adabu” na neno kujifunza hapa linakusudiwa kujifunza jambo lolote ambalo hushamili nyanja na pande zote za Uislamu, kwani huhusu elimu kwa upande mmoja na malezi kwa upande mwingine, hayo humwezesha kusimama katika mipaka na uthibiti wa sharia, na wala havuki mpaka kwani yeye anabeba silaha yenye kuzuia. Kwa mantiki hiyo tunazikuta hadithi nyingi ambazo humsifu kijana mwenye imani, mwenye kujituma na kuwajibika, kati ya hizo ni: Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) amesema:
“Hawi kijana ambaye anaacha dunia, starehe na upuuzi wake, na akazeeka akiwa katika kumtii Mwenyezi Mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu atampa malipo ya wakweli sabini na mbili.” Vile vile imepokewa hadithi kutoka kwake amesema:
“Hakika viumbe wapendwao zaidi na Mwenyezi Mungu ni kijana wa umri mdogo katika sura nzuri na akautumia ujana na uzuri wake katika kumtii yeye, Mwenyezi Mungu atajifaharisha kwa Malaika kwaye, atawaambia: huyu ndiye mja wangu wa kweli.”
5
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:37 PM
Page 6
Vijana ni hazina ya Uislamu Hali kadhalika imepokewa hadithi kutoka kwake amesema: ???? ???? ???? ????? ?? ???? ???? “Hakika Mwenyezi Mungu humpenda kijana ambaye huumaliza ujana wake katika kumtii Mwenyezi Mungu.” Kwa hivyo kijana ana majukumu makubwa ambayo humwelekea yeye, kwani yeye ni mtu wa mwanzo mwenye kuwajibika kuulizwa kuhusiana na vitendo vyake, sawa ameandaliwa na kupata malezi mazuri utotoni na ujanani au hapana, kwani yeye anapofikia umri wa ujana huwajibika na huulizwa kulingana na matendo yake na amali zake, wala hana udhuru wowote mbele ya Mwenyezi Mungu lau ataghafilika kuipa nafsi yake malezi mazuri, kuifanya iwe na tabia njema na kuiadabisha, kwani yeye ni kama mwislamu mwingine hana budi kujua kwamba kuna mipaka na vidhibiti vya kisheria ambavyo haifai kwenda kinyume navyo au kupituka mipaka, kwa hakika atakabiliwa na maswali ya Mwenyezi Mungu (a.j) na atatakiwa kuyajibu. Yampasa kijana wa kiislamu kabla ya kitu chochote ajitambue yeye mwenyewe kwanza ili aikinge na kuifungamanisha nafsi yake na Mwenyezi Mungu, aidha aombe usaidizi kutoka Kwake na amtegemee yeye tu, kisha ajitume katika kushughulikia (uhai wake) uwe katika amani. Ama kwa njia ya kujifunza ili awe kiungo mtendaji katika jamii, kama vile daktari, mwandishi na wengineo miongoni mwa fani maalum ambazo huhitaji miaka mingi ya masomo yenye taabu na usumbufu, au anajifunza fani au taaluma fulani ili aweze kuitumikia jamii, kwani uhai wa watu wahitaji yote hayo, ama kijana kuishi bila kujifunza fani wala ujuzi wowote ambao kwa njia moja au nyingine utamwezesha kuishi vizuri na familia yake na jamii pia, na aishi bila kazi yoyote ile, hiyo ni hatari sana, kwani ukaaji bure huo utamuingiza katika mambo mengi maovu, ni dhahiri lazima faragha hiyo ijazwe na jambo lolote, asilani hapati mwanya wa 6
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:37 PM
Page 7
Vijana ni hazina ya Uislamu kufanya upuuzi na mambo machafu ila anapokuwa hana shughuli ya kujishughulisha kwayo, pamoja na wale ambao hufanana nao miongoni mwa vijana wasio na kazi, na hapo huanza mtandao wa uovu baina ya vijana ambao wengi wao hutumbukia katika dimbwi la uovu na uhalifu, na huenda uhalifu na uovu usiwahusu wao wenyewe pekee bali utawazoa wengi wa mfano wao, kama vile tunavyoyaona hayo katika jamii zetu, hususan katika jamii za kisasa ambazo zimepuuza suala la malezi na mafunzo mazuri, vijana wakaachwa katika mikono ya watu wenye itikadi potofu na mienendo mibaya katika nyanja zote za kifikra na kitabia. Kwa hivyo tunasema kuwa ujana ni hatua pambanuzi katika maisha ya binadamu ambayo hutoa mwelekeo wa mustakabali wa maisha yake kulingana na mtazamo, muono na mwenendo ambao huchukua nafasi katika kipindi hiki cha shida, iwapo chaguo lake litakuwa zuri bila shaka maisha ya sasa yatakuwa mazuri na yajayo pia, na ikiwa chaguo lake litakuwa baya basi atapata hasara hivi sasa na kuendelea, ameeleza vizuri Sayyid kiongozi naye si mwingine bali ni Ayatullah Khamenei katika ubainisho wake wa kipindi cha ujana katika khutba yake amesema: “Ama kuhusu kijana kwa hakika anaishi katika hali ya ukuaji wa kihisia, kimwili na kiroho, hupiga hatua mbele kuuelekea ulimwengu mpya kulingana na yeye, na aghlabu wale wenye kumzunguka yeye ikiwa wanandugu na wanajamii ima hawajui mabadiliko hayo na uhamaji huu mpya au hawajali mambo yake, miongoni mwa yale ambayo humsukuma kijana katika hisia ya kujitenga na kujiweka mpweke, na kijana katika kipindi hiki huelekea ulimwengu mkubwa ambao humpambazukia mara ya kwanza kwa namna ambayo hajawa na uzoefu wa changamoto za ulimwengu huu, aidha hukumbana na shakhsia mbali mbali ambazo ukabiliana nazo, na kwa hivyo huhisi haja ya mwongozo, mwongozaji na msaidizi wa kifikra, na asasi ambazo yapaswa zimsaidie kwalo hazimsaidii au hazimpi muda wa kutosha ambao anaouhitajia.”
7
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:37 PM
Page 8
Vijana ni hazina ya Uislamu Kwa mantiki hiyo vijana ni rasilimali na tegemeo la umma kwa ajili ya mustakabali wake, ni amana iliyopo shingoni mwa jamii ambayo anayoishi hususan hayo yapo shingoni mwa watu wenye uwezo wa kuongoza, wenye kutoa mwelekeo sahihi na wenye malengo, hali kadhalika vijana wao wenyewe wataulizwa kutokana na utafiti wa yale ambayo huwashika kwa mkono wao kuelekea nia ya imani sahihi na msimamo wa kifikra, mwenendo na maelekezo ya kivitendo katika maisha, ili wawe viongozi wa baadaye wachapakazi, wabunifu na wenye manufaa. Na baada ya utangulizi huo ambao hutengeneza njia katika kuingia katika mchakato huu, njooni tuingie katika mada ili tufanye utafiti juu ya sura ya kupigiwa mfano iliyowekwa na Uislamu kumuhusu kijana wa kiislamu kulingana na utafiti uliyofanywa kuhusu sifa za vijana wa kiislamu.
SIFA ZA VIJANA WA KIISLAMU Vijana katika Uislamu: Katika dini ya Mwenyezi Mungu vijana hubeba majukumu yote kumwelekea muumba wao, majukumu ambayo istilahi huitwa: Wajibu wa kisharia (Takliifu Shar’ii), huwa ni mahala pa kuelekea katika kufanya baadhi ya mambo na kuacha baadhi yake, kwa njia ya ulazima, na anapokwenda kinyume nayo anastahili kuadhibiwa duniani na akhera kwayo, na kati ya hayo ni kusimamia zamu na majukumu mbali mbali ya kijamii, ibada, uokoaji, kujitolea, mambo ya kisiasa, jihadi, utafutaji wa elimu, kusaidia, na aina zinginezo za majukumu ambayo kwa njia moja au nyingine huingia chini ya anwani: “Majukumu ya kisharia” pindi anapofikia umri wa kubalehe, uwezo na masharti mengineyo… Kwa hivyo kuanzia hapo humwezesha yule ambaye anapenda kujua maana na stadi katika hukumu za kiislamu za kiungu aone kwa uwazi na kijana achambue kwa mtazamo wa kiislamu, sio kama mtoto mdogo mwenye mtazamo finyu, lengo lake ni tumbo lake na utashi wake ni mchezo na 8
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:37 PM
Page 9
Vijana ni hazina ya Uislamu mambo ya upuuzi, na “kuupoteza bure wakati wake” na mwenye kufanya wepesi mambo yake, na kwa maelezo yao huitwa umri wa balehe anaishi katika ukingo wa maendeleo na mambo hatari ya maisha na mafikio ya umma wake. Bali hali ni kinyume na hivyo, vijana katika Uislamu wana nafasi ya mtendaji, mwenye uwezo wa kuamua na mwenye maendeleo, daima tunawaona wako mstari wa mbele katika uwanja wa vita, na kutangulia uwanjani hujua mambo mengi ya kimsingi yanayohusu umma, kama ilivyokuwa hivyo katika kikosi cha kwanza cha askari (hasa wapanda farasi) na historia yote ya Uislamu, mawalii na watu wema hadi siku zetu hizi, namna ambayo tumeshuhudia mahudhurio ya vijana uhudhuriaji ambao unakuwa ni uti wa mgongo wa mapambano ya kiislamu katika uwanja wa vita tangu katikati ya miaka ya themanini, na katika matendo yake yenye kupambanua mpaka siku hizi zetu baada ya kupata uhuru na ushindi, aidha kutokana na kuhudhuria vijana katika nyanja mbali mbali na wajibu ulio mwingi katika Uislamu. Na hilo sio jambo la ajabu na kushangaza ila kwa yule ambaye haujui Uislamu, mpingaji au yule ambaye ana chuki na dini ya Mwenyezi Mungu (a.j). Na kijana ambaye Uislamu wataka kumjenga ni:
Mwenye kijielewa na kujithibiti, makini, mtulivu na mwenye hekima: Huyu ni kijana ambaye halitumii umbo lake, muonekano wake, nywele zake, vuguvugu la harakati hatarishi na vitendo potofu…… Kama ilivyozagaa na kuenea, bali katika ulimwengu wetu wa sasa, na linalotakiwa katika ulimwengu wa leo wenye kujazwa mawazo ya uhuru wa kujiamulia, mpaka kufikia kiwango cha kuhatarisha uhai! Hadi kesho madai ya kuwa huru katika maovu na mambo ya kipuuzi na kuabudu kwa kila kitu kisichokuwa Mwenyezi Mungu. 9
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:37 PM
Page 10
Vijana ni hazina ya Uislamu Imepokewa hadithi katoka kwa Mtume (s.a.w.w.) juu ya vijana wetu kufanya kiigizo chao, Mtume (s.a.w.w) amesema: “Mbora wa vijana wenu ni yule mwenye kujifananisha na wazee wenu.”
Mwenye kujali na mwenye kuabudu: Kijana huhitajika kujituma katika kupata radhi za Mwenyezi Mungu aliyetuka, ambaye hutumia wakati wake katika yale ambayo atajifaharisha nayo akhera, wala asione aibu hapa duniani kwayo. Imepokewa hadithi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) amesema: ?? ?? ??? ??? ??? ?????? ?????? ????? ????? ?? ???? ???? ???? ????? ???? ??? ????? ?????? ?????? “Hawi kijana akaacha dunia pamoja na upuuzi wake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na akazeeka katika kumtii Mwenyezi Mungu, ila Mwenyezi Mungu atampa malipo ya wakweli sabini na mbili.” Na Amiirul-Mu’miniina Ali bin Abi Twalib (a.s.) alidhihirisha machungu yake kutokana na ufisadi wa zama hizo, na akatoa ishara kuhusu vijana wenye tabia mbaya, hakuna tofauti kati ya vijana hao na vijana wa hivi sasa, akidhihirisha suala la kukengeuka vijana na kupotoka ukiwemo upotoshaji wa nguvu na majukumu tarajiwa, kuhusu zama zetu, anasema: ?????? ??? ????? ???? ??????? ?? ????? ???? ... ???? ??????? ??? ??????? ??????? ??? ??????? ????? ???? “Wenye kusema kwa haki ni wachache, ukweli umetoeka… watu wake hupitisha muda mwingi katika maasi, hujishuhghulisha na mambo ya starehe, na wasichana wao wana tabia chafu.” Linganisha manemo hayo ya Imam Ali (a.s.) na mambo ambayo tunayo hivi leo.
10
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:37 PM
Page 11
Vijana ni hazina ya Uislamu
Mwenye kujishungulisha na kujifunza: Kijana hutafuta elimu yenye manufaa ambayo huhitajika mahala pengi maishani mwake, imepokewa hadithi kutoka kwa Amirul-Mu’miniina Ali (a.s) amesema: ?????? ?? ?????? ??????? ?? ????? “Elimu utotoni ni kama vile kuweka nakshi katika jiwe.” Kwa hivyo Uislamu humchukia kijana ambaye asiyejifunza, kwa mantiki hiyo, kijana wa kiislamu daima hutakiwa ama awe mtafutaji elimu au mtoaji elimu iwapo atakuwa na uwezo wa hilo. Imepokewa kutoka kwa Imam Baqir (a.s) amesema: ?? ???? ???? ?? ???? ?????? ?? ????? ??????? “Lau nitaletewa kijana miongoni mwa vijana wa Kishia hajifunzi basi ningelimuadabisha.” Imepokewa kutoka kwa Imam Swadiq (a.s) amesema:
“Hakika viumbe wapendwao zaidi na Mwenyezi Mungu ni kijana mwenye umri mdogo akiwa katika sura nzuri, akautumia ujana na uzuri wake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na katika kumtii Yeye, huyo ndiye ambaye anajionea fahari al-Rahmanu kwa Malaika wake akisema: huyu ndiye mja Wangu wa kweli.”
11
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:37 PM
Page 12
Vijana ni hazina ya Uislamu
Mwenye kutumia nguvu zake na uwezo wake kikamilifu: Kijana wa kiislamu hutumia vizuri nguvu na uwezo wake katika njia ya Mwenyezi Mungu (a.j), na dalili hiyo hudiriki maana ya shukrani ya kweli ambayo sio kusemasema tu kama baadhi ya watu wanavyodhani, bali hilo ni daraja la juu zaidi la kushukuru ambalo hudumisha neema, na hutumia kila ambacho amepewa na Mola Manani katika yale ambayo humridhisha Mwenyezi Mungu (a.j). Na hiyo ni alama miongoni mwa alama za imani ya hali ya juu kabisa, na kila kijana anapojiweka mbali na maasi na akashikamana na yale ambayo huyaridhia Mwenyezi Mungu na kuyatenda, basi imani yake huwa kubwa zaidi na hapo huthibiti kuwa yeye ni mtu wa peponi. Imepokewa hadithi kutoka kwa Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w.) amesema: ??? ???? ???? ?????? ???? ???? ????? ?? ???? ???? “Hakika Mwenyezi Mungu humpenda kijana ambaye huumaliza ujana wake katika kumtii Mwenyezi Mungu.” Tukichunguza kwa makini maelezo hayo ya Mtume (s.a.w.w.) hayakutaja ibara au neno “kuutumia ujana,” bali limetumika neno “kuumaliza” katika njia ya Mwenyezi Mungu. Vile vile Mtume (s.a.w.w.) amesema:
“Hakika viumbe wapendwao zaidi na Mwenyezi Mungu ni kijana mwenye umri mdogo akiwa katika sura nzuri, akautumia ujana na uzuri wake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na katika kumtii Yeye, huyo ndiye ambaye ana12
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:38 PM
Page 13
Vijana ni hazina ya Uislamu jionea fahari al-Rahmanu kwa Malaika wake akisema: huyu ndiye mja Wangu wa kweli.” Ni sahihi kwamba hadithi imetaja mandhari mazuri ambayo hayapingani na upendo wake, kwa hakika hadithi hizo zimetilia mkazo zaidi kufanya hilo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.
Mwenye Wivu: Kijana wa kiislamu huwa na wivu, asilani hakubali kufanyiwa uadui na kuvunjiwa heshima, utukufu na hadhi yake, kisha akae kimya bila kuchukua hatua yoyote ile seuze awe mwenye kuridhia au mwenye kutabasamu… kama yanavyotokea hayo katika jamii katika zama hizi, kwa hivyo kijana wa kiislamu haufumbii macho hata kidogo uadui wowote ule, hususan utukufu na heshima ya dini… kuhusiana na mchakato huu, ni mashuhuri kwamba zipo fat’wa za wanazuoni zinazoeleza wazi kwamba: “Mwenye kufa hali ya kutokubali udhalili basi mtu huyo ni shahidi.” Imepokewa hadithi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) amesema: ??? ???? ????? ?????? ???? ???? ?? ???? ??? ????? “Hakika Mwenyezi Mungu humchukia mtu ambaye huvamiwa nyumbani kwake wala hajihami.” Na Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) amesema:
“Baba yangu Ibrahimu alikuwa mtu mwenye wivu, na mimi nina wivu zaidi, Mwenyezi Mungu aigangamize pua ya asiye na wivu miongoni mwa waumini.”
13
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:38 PM
Page 14
Vijana ni hazina ya Uislamu Yote hayo ni miongoni mwa alama za watu wenye imani, na imekuja katika maandiko kwamba: ??? ?????? ?? ??????? “Hakika wivu ni katika imani.” Na labda wengi hawajui, hususan siku hizi kwamba wivu ni wajibu kwa wanaume, na la kusikitisha ni kwamba kutokuwa na wivu ni matokeo ya yale tunayoyaona kupitia vyombo vya habari, kukithiri uadui, mambo yasiyo ya kawaida na mitandao ya kifisadi, pia uenezaji wa hali ya kuchanganikana baina ya wanaume na wanawake katika vikao vya nyumbani au vya sehemu za umma, bali kwa njia za matangazo, pamoja na kuhifadhi Uislamu kwalo.
Haya: Haya ni miongoni mwa sifa nzuri za kijana wa kiislamu, nayo ndiyo sifa iliyobarizi zaidi kwa bwana Mtume (s.a.w.w.) hususan katika mazungumzo na mavazi, mambo hayo mawili huhitajika zaidi zama hizi. Kwa hivyo kukosekana haya na kwenda kinyume nayo kikauli ni hali iliyoenea sana katika jamii, kwa mfano; utukanaji, utoaji matusi, maneno machafu na ya haramu ambayo hutolewa wazi wazi barabarani na sehemu za umma kwa sauti ya juu pasi na haya, hali ya kuwa ipo hadithi inayoeleza kinaga ubaga kwamba: ??? ????? ??? ?? ???? ?? “Hana imani asiye na haya.” Na jumla ya mambo ambayo tunakumbana nayo aidha hutuingiza majaribuni kwayo, kwani baadhi ya maneno hayo tumeanza kuyaona yakienezwa na kutumiwa katika baadhi ya vipindi vya runinga na michezo ya kuigiza, 14
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:38 PM
Page 15
Vijana ni hazina ya Uislamu kwa namna ambayo vitu huitwa kwa majina yake, chini ya kivuli cha uhuru, ukweli na uwazi, na ufungukaji na kuchekesha watu… Na hilo huhusishwa na uovu wa ‘upotokaji na ujinga’ ama suala la kukosekana haya katika mavazi ni jumla ya mambo yanayodhihirika katika mavazi mafupi kwa wasichana na kurandaranda kwao masokoni au kusimama sehemu za wazi na kudhihirisha sehemu za miili au maungo kwa kuvaa nguo zilizobana na nyepesi, au kufungua vifungo ili kuonesha kifua… Ipo hadithi isemayo: “Asiyewaonea haya watu hawezi kumuonea haya Mwenyezi Mungu.” Kwa hivyo haya ni sifa miongoni mwa sifa za kijana wa kiislamu, kwa hakika Bwana Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na haya mno kushinda haya ya msichana, hata kama tupo katika zama ambazo baadhi ya watu huona kuwa haya ni kioja na ni uduni wa mawazo na kuchelewa, na kwamba kutokuwa na haya ndiyo ujanja na maendeleo! Kwa hakika Mwenyezi Mungu (a.j) anasema:
“Mlipoyanukuu kwa ndimi zenu bila ya kuthibitisha na kuzingatia na mkasema kwa vinywa vyenu msiyoyajua, na mlifikiri kuwa ni jambo dogo, kumbe mbele ya Mwenyezi Mungu ni kubwa.” (24:15)
Kuunusuru Uislamu: Kuunusuru Uislamu ni katika mambo ya msingi na ndiyo lengo kuu la kijana wa kislamu ambaye wakati wote huwa mwenye kujiandaa, kujitolea muhanga na kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu, naye anajua kwamba kwa kadri tunavyokuwa na uwezo zaidi ndivyo tuwezavyo kujilinda, kulinda haki zetu, uhuru wetu na kujitegemea kwetu… Na dini yetu ipo juu ya kila kitu, na katika umri wa ujana tuna fursa ya kuziandaa nafsi zetu kwa ajili ya jihadi na kujihami. 15
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:38 PM
Page 16
Vijana ni hazina ya Uislamu Imepokewa hadithi kutoka kwa Amirul-Mu’miniina Ali (a.s.) amesema: ??????? ??? ???? ?? ???? “Vaeni silaha hata kwa kipande kidogo cha chuma.” Na Imeelezwa kwamba Imam Ali bin Abi Twalib (a.s.) alikuwa na chumba hakukuwa humo na chochote ila msahafu… na upanga.
Anapenda Mambo ya Sunna: Kijana wa kiislamu hujihusisha na mambo ya sunna na huyapupia na kuyapa kipaumbele zaidi, na hilo linadhihirisha upendo wake kwa Bwana Mtume (s.a.w.w.) na ikiwa kijana wa kiislamu hakujihimiza wala kushikamana nayo basi ni nani atakayeshikamana nayo? Imekuja katika hadithi kwamba Mtume (s.a.w.w.) amesema: ?? ???? ????? ??? ?????? ??? ? “Mwenye kuhuisha sunna yangu kwa hakika amenihuisha mimi, na mwenye kunihuisha mimi atakuwa pamoja nami peponi.” Kwa hivyo mambo ya sunna na adabu mbali mbali huwa katika kusimama kwake na kukaa kwake, kama vile ulalaji wake, uamkaji wake wa mapema, ulaji wake, usimamaji wake, utembeaji wake na ufanyaji wake wa ibada … na muda wote huwa katika udhuu na huswali mwanzo wa wakati. - Je! Si jambo la heri kujizoesha hivyo! Na tuanze wakati gani kuzizoesha nafsi zetu katika mambo ya heri na kuacha maovu na shari? Imepokewa kutoka kwa Amirul-Mu’miniina Ali (a.s) amesema:
16
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:38 PM
Page 17
Vijana ni hazina ya Uislamu “… na fuateni uongofu wa nabii wenu, kwani huo ni uongofu bora zaidi, na shikamaneni na sunna zake kwani hizo ni sunna bora zaidi.” Aidha amesema:
“Ah! Juu ya ndugu zangu ambao wamesoma Qur’ani na wakaifanya ndiyo hakimu, wakazingatia faradhi na wakasimamisha, wakahuisha sunna na wakaitelekeza bid’aa, waliitwa katika jihadi wakaitikia, wakawa na imani na kiongozi na wakamfuata.” Hizo ni baadhi ya sifa za vijana wa kiislamu ambazo tunatarajia Mwenyezi Mungu ataleta ukombozi mkubwa kupitia mikono yao, na awaokoe wale wenye kudhulumiwa kutokana na kuhujumiwa na vitimbi vya makafiri, ada zao na mielekeo yao.
KIIGIZO CHA VIJANA Baada ya kueleza kwa ufupi sifa za vijana wa kiislamu, sasa njoo tuangalie mwenendo wa maisha wa kiongozi wa zama hizi na kiigizo chao chema naye si mwengine bali Imam kiongozi Ayatullah Sayyed Khamenei.
Pamoja na Kiongozi Kiongozi anakumbuka siku za ujana wake anasema: Sikumbuki lini nilianza kufikiria kuhusu mustakabali wangu pia kwamba napaswa niweje! Isipokuwa jambo nililolijua hali kadhalika familia yangu walilitambua tangu mwanzo ni kwamba; kila mmoja alikuwa anapenda niwe mmoja wa wanafunzi wa elimu ya dini, hilo ndilo lilikuwa kusudio la wazazi wangu, mimi binafsi kusudio langu na ndoto yangu ilikuwa ni masomo.
17
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:38 PM
Page 18
Vijana ni hazina ya Uislamu Haikutegemewa nivae pambo hilo tangu mwanzo wa umri wangu, ila upinzani na msimamo wa mzazi wangu aliokuwa nao dhidi ya kila lile ambalo lililokuwa likifanywa na nyumba ya Bahlawi, aliweka mikakati kabambe, kati ya mikakati hiyo ni kuvaa mavazi ya kidini, hakuruhusu katu kuvaa mavazi ambayo yanaondoa heshima ya nyumba kwa hali yoyote ile, namna ambayo watu walilazimishwa kutovaa nguo za kitaifa na kuvaa mavazi ya nchi za kimagharibi kama vile kofia ya pama na inayofanana na mavazi hayo, kuongezea hayo alikuwa mzazi wangu akipendelea zaidi niendelee na masomo yangu ya chuo cha elimu ya dini, mimi binafsi nilikuwa napenda kusoma chuo cha kidini.
KIPINDI CHA MASOMO Masomo ya dini nilianza rasmi baada ya kuhitimu elimu yangu ya msingi, nilijisomea mimi mwenyewe elimu ya shule ya upili bila ya kujiunga na shule ya akademia, azma na hamu yangu kubwa ilikuwa ni masomo ya dini, nasema wazi kwamba tangu nilipokuwa na umri wa miaka 12 nilianza kufikiri kwa makini kuwa mwanafunzi wa elimu ya dini. Kabla sijakwenda mji wa Qum nilihudhuria masomo yangu ya kidini kwa mzazi wangu – masomo ya ujumla katika mji wa Mashhad, na wakati wa likizo ya kiangazi mzazi wangu alikuwa akiniwekea ratiba ya masomo na alitufundisha yeye mwenyewe, kwa hakika hiyo sikusimama kimasomo tofauti na wanafunzi wengine ambao walikuwa wakisoma masomo ya jumla ambayo yalikuwa yakisimamishwa kwa miezi mitatu, mwezi wa Muharram, Swafar na mwezi mtukufu wa Ramadhani, na katika mapumziko ya kiangazi, nilimaliza masomo yote ya shahada ya kwanza, na hapo nikaanza masomo ya udhamiri na mimi nikiwa na umri wa miaka 16.
UFUNDISHAJI Nilianza kazi ya kufundisha katika siku za mwanzo za masomo yangu ya chuo cha kidini, namaanisha baada ya kumaliza elimu yangu ya msingi moja kwa moja nilianza kufundisha kitabu cha sarufi kwa wanazuoni 18
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:38 PM
Page 19
Vijana ni hazina ya Uislamu wakubwa wawili wenye umri wa makamo, hadi mwanzo wa mwaka 1958 AD nilikuwa mkazi wa Mashhad, nikawa huko nikifundisha vitabu vifuatavyo: Sarufi, lugha sanifu, fasihi, usuuli na sheria, vivyo hivyo nilipokuwa katika mji wa Qum nilikuwa nafundisha baada ya muda wa masomo yangu. Baada ya kurejea Mashhad mwaka 1964 AD, nilianza rasmi kazi ya ufundishaji, kwa hivyo kuanzia hapo hadi mwaka 1977 AD nilikuwa nafundisha elimu ya juu masomo ya sheria, tafsiri na itikadi.
NDOTO NA MATARAJIO YANGU Lakusikitisha ni kwamba siku hizo vijana hawakuwa na matarajio makubwa kama vile tunavyoyashuhudia zama zetu hizi, yalikuweko mabustani ya umma ya matembezi, isipokuwa zilikuwa bustani chache wala hazikukidhi haja, kwa mfano katika mji wa Mashhad ilikuwa sehemu ya matembezi ni moja tu, na kona zake zilikuwa zimetapakaa maovu kupita kiasi, familia yetu haikuruhusu kabisa tabia ya kwenda huko kwa ajili ya matembezi, kwa hakika kilikuwa ni kituo cha maovu na ufisadi. Na utawala wa wakati huo ulifanya kila liwezekanalo ili kueneza uovu katika sehemu za umma na kuchochea kwa njia za matamanio na ladha potofu, kwa hakika mambo hayo yalitimia kupitia mbinu na mikakati kabambe, hivyo ndivyo tulivyokuwa tunaitakidi, kisha tukapata yakini kwayo baada ya kujua na kutambua baadhi ya mambo hususan yale yaliyoingizwa, kwa mantiki hiyo tulikatazwa kabisa kutembelea mabustani kwa ajili ya mapumziko na kutastarehe. Starehe yangu na kuburudika kwangu katika mwezi wa Aban katika kipindi cha ujana nilikuwa pamoja na wanafunzi wenzangu wakati wa mapumziko nikijumuika nao na kuvutiwa na mazungumzo katika mambo mbali mbali, mazingira ya shule yaliandaliwa kwa jili ya vikao vya 19
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:38 PM
Page 20
Vijana ni hazina ya Uislamu majadiliano, na katika kuongezea hayo tulikuwa tukikusanyika msikitini “Kuhar Shad” baadhi ya wanazuoni wakubwa wenye fadhila pamoja na wanafunzi wa elimu ya dini, tulikuwa tukizungumza mambo mengi katika makongamano ya kielimu, utamaduni na dini, matembezi yangu yalikuwa ni hayo na burudani yangu ya wakati huo ndiyo hiyo. Nilikuwa nikifanya mazoezi na bado naendelea nayo hadi hivi sasa jambo hilo la kusikitisha kuona baadhi ya vijana wameacha mazoezi na hilo sio sahihi. Tulikuwa tukifanya mazoezi ya kutembea kwa miguu na kupanda milima, na nilikuwa nikitumia siku kadhaa kupanda milima ya mji wa Mashhad nikihama kutoka mlima mmoja hadi mwingine, na nilikuwa nikitembea kwa miguu kutoka kijiji kimoja hadi kingine na baadhi ya rafiki zangu waliongozana pamoja nami, uzuri ulioje kupanda milima ya mji wa Tehran ambayo ni mirefu sana. Mimi nahisi hali ya masikitiko kuhusu faragha hizi, fursa ambazo ni wajibu kwa vijana kuzijaza na kuzitumia ipasavyo, yawapasa wote kufanya mazoezi kwani hali hiyo ipo ndani ya dhamira ya vijana.
KUPENDA KUJISOMEA Wakati wa ujana wangu nilipendelea sana kujisomea na kudurusu vitabu mbali mbali, vitabu vya historia, sarufi, fasihi, tungo za mashairi, tenzi, visa na hadithi, nilikuwa napenda kusoma hadithi nyingi, na nilisoma hadithi nyingi zilizo mashuhuri wakati huo, na nilifurahishwa mno na hadithi za Mtume (s.a.w.w.) zenye mvuto na kupata athari nzuri kwa lunga ya kiarabu, kwa ubora wa masomo yangu na mfuatilio wangu katika masomo ya kiarabu. Na bado naendelea kukumbuka vizuri hadithi hizo ambazo nilizisoma katika zama za ujana, ambazo nilikuwa nikiziandika na kuzinakili ndani ya daftari dogo, na la kushangaza ni kwamba huenda nisizikumbuke baadhi 20
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:38 PM
Page 21
Vijana ni hazina ya Uislamu ya hadithi ambazo nimezidurusu wiki hii au juma la jana, lakini nazikumbuka zote nilizoziandika na kuzisoma zama hizo, yawapasa nyinyi kuzingatia kadhia hii, jueni kwamba mnayoyasoma leo hayafutiki katika kumbukumbu zenu abadani. Ni kweli kwamba umri wa ujana ni kipindi cha dhahabu ambacho katu hakilinganishwi na kipindi kingine katika umri wa mtu, hayo ni kwa upande mmoja, amma kwa upande mwingine mzazi wangu alikuwa na maktaba ya nyumbani, na humo nilidurusu na kujisomea vitabu mbali mbali, bila ajizi nilikuwa naazima baadhi ya vitabu hususan vitabu vya visa na riwaya kutoka katika maktaba ndogo iliyo jirani ya nyumba yetu ambayo ilikuwa ikiazimisha vitabu. Sikukosa kuhudhuria maktaba iliyokuwepo katika eneo takatifu la Imam Ridha (a.s.). Mwanzoni mwa masomo yangu ya chuo cha kidini nilikuwa na umri wa miaka 15 au 16, nilibobea katika kujisomea kitu ambacho kiliniwia vigumu kusikia adhana ambayo ilikuwa ikitolewa kwa sauti kubwa, nilikuwa karibu na upande wa spika lakini sikuweza kuisikia, nilishtuka baada ya kupita saa kadhaa tangu iadhiniwe adhana ya swala ya adhuhuri kwani nilikuwa nikifarijika na kupata raha kutokana na kujisomea vitabu. Jambo ambalo ni vema kulijua ni kwamba sijaacha kujisomea hadi hivi sasa, bali bado naendelea kujisomea maradufu ya kipindi cha ujana.
UTUNZI WA MASHAIRI Nilianza kutunga mashairi na kuyasoma tangu zama za ujana wangu, ila kutokana na baadhi ya sababu zilinifanya niache kusoma mashairi katika jumuiya ya malenga ambayo iliyokuwa imeasisiwa zama hizo katika mji wa Mashhad pamoja na kuwa kwangu mdau kwa muda wa miaka mingi kwalo.
21
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:38 PM
Page 22
Vijana ni hazina ya Uislamu Nilikuwa na uwezo mkubwa na hamu ya kufanya hivyo tangu nikiwa na umri wa miaka 20 au 21, niliendelea mpaka mwaka 1964 na 1966, hapo nilianza harakati za kisiasa ambazo zilinifanya niachane na utunzi wa mashairi.
HARAKATI ZA KISIASA Ama kuhusu uingiaji wangu katika uwanja wa mapambano pamoja na harakati za vuguvugu la kisiasa, nilianza nikiwa na umri wa miaka 16 hivi, wakati ambao marehemu Nuwabu Swafawi alikuja katika mji wa Mashhad na kuanza kazi ya kutoa hotuba zake za hamasa, ni jambo ambalo lilipenya na kuingia moyoni mwangu, sikuwa limbukeni kwalo kulinganisha na vijana wengine wa rika langu ambao walivutiwa naye, alikuwa akipendezwa zaidi na mimi kutokana na harakati zangu pamoja na uchamungu wangu niliyokuwa nao, ushujaa, kujituma, kujitolea kwangu, uwazi wangu uliochanganyika na ukweli na uaminifu. Na hapa naweza kusema kuwa tangu wakati huo nikaanza kushiriki moja kwa moja shughuli za kisiasa na vuguvugu la harakati za ukombozi. Nuwabu aliuawa kishahidi kando ya mji wa Mashhad kwa siku chache, mauaji yake yalichochea na kuleta hamasa zaidi ndani ya nyoyo za vijana waliokuwa wakimpenda na kumfanya kuwa ndiye kiongozi wao. Hivyo ndivyo nilivyochipukia katika siasa katika miaka ya 55 na kupata uzoefu na kukomaa kwangu katika medani ya kisiasa na kuendelea hadi hivi sasa. Katika harakati zangu za kisiasa nilikamatwa na kuingizwa korokoroni na kutolewa mara 6, na kuna kipindi niliswekwa jela nikikabilana na taabu na mateso kwa muda wa miaka mitatu, ni jambo lisilo na shaka kwamba zama zile Wairani walikuwa wakiishi hali ya ushubiki na dhiki mno. Tuliishi katika mazingira hayo na umma ulikuwa ukiishi katika hali tete na kuhatarisha mwamko na ari ya kutaka mabadiliko, hali iliyopelekea kufikiri na kudhani kuwa kupatikana mageuzi ya kisiasa huenda jambo hilo 22
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:38 PM
Page 23
Vijana ni hazina ya Uislamu likawa ni muhali, tukaamua kutumia njia ya kusambaza vipeperushi baina yao, lilikuwa ni jambo lisilo na shaka watu kuvamiwa na hilo kuwa ni jambo la kawaida, hali kadhalika uporaji wa mali, utekaji, utoroshwaji kutoka majumbani mwao watu na kupelekwa mahala pasipojulikana, na hilo lilitokea nyumbani kwetu mara nyingi, walipora kila kitu kilichokuwa changu ikiwa nyaraka, tafiti zangu za kielimu na za kitaalamu hawakuzirudisha, na iwapo walizirudisha basi walirudisha baadhi yake. Kisha mazingira ya kisiasa yakawa magumu mno na hasa hasa mbinu za vitisho na kuogofya, ambavyo vikitolewa na utawala wa wakati huo. Katika mwezi wa Aban nilikuwa nikijishughulisha na harakati za kisiasa kwa kutoa mihadhara mbali mbali katika somo la tafsiri nikiwahutubia vijana hasusan wanafunzi wa vyuo vikuu, na siku moja nilipokuwa nasoma aya zinahusiana na wana wa Israel, nilipokuwa nikitoa maelezo ya hali na mazingira ya wana wa Israel na mayahudi, basi sikuchukua muda ghafla nikakamatwa na kuingizwa korokoroni, bila shaka suala la msingi sio maelezo yangu niliyoyatoa bali walifungamanisha hilo na masuala mengine. Swali la kwanza nililokabiliana nalo lilikuwa: Kwa nini wazungumza dhidi ya mayahudi na wana wa Israel? Enyi watukufu wapendwa je! Mnatambua hilo? Yaani mwenye kutaka kutafsiri aya ambayo inaelezea wana wa Israel basi ajiandae kukabiliana na vitisho kutoka kwa wana usalama, utaulizwa kwa nini au jambo gani lililokusukuma hadi uzungumzie aya inayohusiana na mayahudi au kuwashambulia hao, wataka waonekane waovu kwa watu, enyi ndugu zangu wapendwa mara ngapi mmeweza kuleta picha kuhusu mazingira hayo magumu ya kisiasa katika kuelekea mchezo mchafu wa kisiasa ambao ulikuwa ukitekelezwa na serikali dhidi ya vijana. Wakati ule tulipokuwa katika uwanja wa mapambano tulikuwa tukifikiria kwa undani na makini sana, tulijitolea kwa hali na mali kadri tulivyoweza mpaka tuhakikishe kuwa vijana tunawatoa kutoka katika janga hilo la kutekeleza utamaduni wa utawala, kwa mfano mimi binafsi nilikuwa 23
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:38 PM
Page 24
Vijana ni hazina ya Uislamu nikienda msikitini kufundisha somo la tafsiri na kutoa hotuba baada ya swala na wakati mwingine nilikuwa nakwenda mikoani na huko nilikuwa nikitoa mihadhara mbali mbali, na lengo la msingi kutokana na harakati zangu lilikuwa kuwakomboa na kuwatoa vijana kutokana na utamaduni na fikra potofu ambazo zimejazwa na utawala, na ambacho niliweza kukivuka zama zile ni kile kilichoitwa “mtandao nyakuaji wa siri.”
USIA WA IMAM KHOMENI KWA VIJANA Ewe mwanangu! Faidika na ujana wako na ishi umri wako wote kwa kumtaja Mwenyezi Mungu pamoja na kumpenda Yeye, aidha rudi katika maumbile ya Mwenyezi Mungu. Yamekithiri mengi miongoni mwa yale ambayo shetani huyatumia katika kuidanganya nafsi, sisi ni wezee na nyinyi ni vijana – zipo nyenzo tofauti ambazo sisi wazee tunakabiliwa na changamoto na silaha yake ya ukataji tamaa kutokana na uhudhuriaji na kufanya dhikri basi hunadi: Hakika mmefikwa na umri wa uzee na mmepitwa na wakati wa kutenda mema, siku za ujana wenu ambapo mlikuwa mna uwezo na nguvu ya kutenda mema… Enyi vijana! njia ambayo huitumia kwetu sisi hiyo hiyo huitumia kwenu, yeye huwaambia: “Nyinyi ni vijana na wakati wa ujana ndiyo huu, ndiyo wakati wa kujirusha, kufanya starehe na kujiburudisha na ladha mbali mbali” na ushawishi huo na unaofanana na huo ni mwingi sana ambao huuingiza sikioni mwa binadamu… Ewe mwanangu! Zinduka na uamke kwa ajili ya mapambano, na wewe ni kijana unamiliki nguvu kubwa, na waweza kuepuka kila kitu ila Mola Muweza aliyetukuka, jitahidi kadri uwezavyo kuainisha mafungamano yako na Mola Manani ikiwa unayo mafungamano hayo. Ama ikiwa hauna – jilinde kwa Mwenyezi Mungu – basi jitume kadri ya uwezo wako ili kuyapata hayo, jitahidi katika kuyakuza na kuyaimarisha, hakuna kitu una24
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:38 PM
Page 25
Vijana ni hazina ya Uislamu chostahili kama kufungamana Naye… Ewe mwanangu! Nazungumza na wewe hivi sasa hali ya kuwa wewe u kijana, yakupasa uzinduke kutubia, nalo ni jambo rahisi kwa kijana kama vile ilivyo rahisi kuitengeneza nafsi yake na kuipa malezi mazuri, kwani hilo hutimia haraka sana, nyoyo za vijana ni laini, nyepesi na rahisi kuongoka, basi kijana anaweza kwa njia rahisi – kwa mnasaba fulani - kujiepusha na shari ya nafsi ya kuamrisha maovu na kuelekea upande wa mambo ya kiroho… Basi vijana wazinduke, kwani kifo kipo karibu na vijana na wazee kwa hali sawa, na kijana gani ambaye anaweza kujihakikishia kuwa atafikia umri wa uzee?! Ewe mwanangu! Jifungamanishe na tajiri halisi asiyefilisika hata kidogo, ili utosheke na asiyekuwa yeye, na omba uwezeshwaji kutoka kwake ili nafsi yako ivutike na kuachana na wote ila Yeye tu, na akuidhinishe kuingia na akukaribishe kuhudhuria kwake… Ewe mwanangu! Jitahidi mwenendo wako uwe katika njia iliyonyooka – njia ya Mwenyezi Mungu – jihangaishe hadi moyo wako uwe wenye harakati, utuliaji wako na viungo vyako vingine katika mchakato wa kufikia hali ya juu na mafungamano na Mwenyezi Mungu… Ewe mwanangu! Fanya uwezalo ili kuitambua nafsi yako iliyoumbwa katika maumbile ya Mwenyezi Mungu, na iokoe kutoka katika lindi la upotevu, mawimbi ya majivuno, umimi na ubinafsi, panda “jahazi la Nuhu” ambalo ni “utawala na uongozi wa Mwenyezi Mungu” kwa hakika mwenye kupanda amenusurika na mwenye kuliacha kwa kutolipanda ameangamia”… Mwanangu mpendwa! Hakika Mwenyezi Mungu (a.j) Yeye ni wa mwanzo na wa mwisho ‘alfa na umega’ wa dhahiri na wa batini… Yeye ni dhahiri na kila kilicho dhahiri humdhihirisha Yeye, vipo vizuizi katika dhati zetu, umimi na ubinafsi wetu ndiyo vikwazo ambavyo hutuzuia sisi, basi 25
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:38 PM
Page 26
Vijana ni hazina ya Uislamu tushikamane Naye na tumuombe Yeye hali ya kuwa wanyenyekevu na wenye shauku ya kupata nusura kutokana na vizuizi… Ewe mwanangu! Hakika jambo ambalo huchukiwa msingi na chanzo chake ni aina zote za maovu, nayo husababisha adhabu na maangamizi, kichwa cha yote hayo ni makosa na madhambi, na jambo hilo sio lingine isipokuwa ni “kupenda dunia” ambayo imeanza kutokana na “kupenda nafsi.” Dunia ni kitu kinachochukiwa nayo ipo ndani yako, na kujifungamanisha na asiyekuwa na moyo nayo hupelekea kuanguka… Ewe mwanangu! Ijue Qur’ani – ni kitabu chenye maarifa makubwa… kwa hivyo kitabu hiki ni kitabu kitokacho kwa mpendwa hadi kwako na watu wote, na kitabu cha mpendwa pia hupendwa… na tambua kuwa lau sisi tutautoa umri wetu wote kusujudu sajda moja ya shukrani kwa kuwa Qur’ani ni kitabu chetu, tusingelitekeleza neema hii na kuipa haki yake na kushukuru… Ewe mwanangu! Jitahidi, fanya kila uliwezalo kuweka mpaka wa matamanio ya nafsi ambayo hayana mpaka wala wigo, omba msaada kwa Mwenyezi Mungu aliyetukuka kwani mtu hafikii kitu bila ya msaada Wake, swala – ni Miiraji yako wewe katika kumjua, na ni safari ya wenye ashki – ni njia ya kufikia makusudio haya… Ewe mwanangu! Hakika dua na maombi ambayo yametufikia sisi kutoka kwa Maimamu maasumina (a.s.) ni dalili tosha katika kumjua Mwenyezi Mungu (a.j) nazo ndio funguo bora za ibada, na hunyanyua zaidi mafungamano baina ya kiumbe na muumba wake, kama vile hushamiri na kuenea katika kupiga hatua mbele kuelekea maarifa ya kiungu, vile vile hufananishwa na njia iliyobuniwa na watu wa nyumba ya Wahyi ili kupata liwazo kwa Mwenyezi Mungu (a.j) – basi usiweke kizuizi kwa vishawishi vya wajinga katika kushikamana au kupata liwazo kwalo…
26
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:38 PM
Page 27
Vijana ni hazina ya Uislamu Ewe mwanangu! Jitahidi kujiepusha na vikao ambavyo humuingiza binadamu katika kughafilika kumtaja Mwenyezi Mungu, kwani kushiriki vikao hivyo na vinavyofanana na hivyo huenda vikamsababisha mtu kukosa uwezeshwaji, na jambo hilo ambalo huhesabiwa kwa dhati yake ni hasara haiwezekani kulibadilisha … Ewe mwanangu! Hakika tumaini la wote ni kuzima mioto ya nafsi iliyoasi na huweka mpaka kutokana na kuibembeleza na kutaka izidi katika utafutaji, si lingine ila kumfikia Mola Manani. Na utajo au dhikri ya hakika ni Yake Yeye tu… Ukiwa wewe sio miongoni mwa watu wenye cheo kikubwa cha mambo ya kiroho, jitahidi usikanushe cheo cha kiroho na maarifa, kwani ukanushaji ni miongoni mwa mitego hatari ya shetani na nafsi inayoamrisha maovu ambayo humzuia binadamu kufikia madaraja yote ya kibinadamu na vyeo vya kiroho… Ewe mwanangu! Chaguo lako kati ya watu liwe baina ya wale watu wema, washikadini na wenye kujali mambo ya kiroho, aidha hawadanganywi na starehe za dunia wala hawashikamani nayo… na miongoni mwa wale ambao madhambi hayachafui vikao vyao, vile vile ni miongoni mwa wale ambao wenye tabia nzuri, hakika utoaji athari moja kwa moja katika pande mbili kutokana na kufanya wema, na kuleta ufisadi ni jambo ambalo halina shaka katika kutokea kwake… Ewe mwanangu mpendwa! Sikiliza nasaha za baba asiye na raha mwenye kutingwa wala usiichokeshe nafsi yako kuhama njia katika mlango huu au mlango ule ili ifikie cheo au ipate umashuhuri ambao nafsi yautamania, na wewe cheo chochote utakachofikia utapata machungu yake na majuto yako yatazidi, na kuiadhibu roho yako kutokana na kutofikia kwako ni zaidi ya hayo…
27
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:38 PM
Page 28
Vijana ni hazina ya Uislamu Ewe mwanangu! Haifai ikusukume dunia na ikugeuze wewe na kuielekea hiyo, na kuihakikishia yale yashibishayo matamanio yako mpaka ufanye kiburi na kujifaharisha kwa waja wa Mwenyezi Mungu, mengi ambayo wayaona wewe kuwa ni heri na hali ya kuwa ni shari kwako… Ewe mwanangu! Mtazamo wako ufanye uwe katika vitu vyote vilivyopo, hususan binadamu, kwa mtazamo wa huruma na upendo, au sio kwamba viumbe wote wako chini ya rehema za Mola wa viumbe kwa pande mbali mbali… Vivyo hivyo katika mambo muhimu ambayo yameusiwa kwayo; kupupia katika kuwasaidia waja wa Mwenyezi Mungu hasa hasa wanyonge, masikini na wenye kudhulumiwa, toa uwezalo kutoa katika kuwahudumia wao, kwani kufanya hivyo ni kujiandalia masurufu mazuri, nalo ni miongoni mwa matendo bora mbele ya Mwenyezi Mungu (a.j), jitume katika kutoa huduma kwa waliodhulumiwa, aidha wahami hao na mabeberu na madhalimu… Ewe mwanangu! Uzuri uliyoje kuiambia nafsi yako na kuikinaisha juu ya uhakika mmoja, nao ni kwamba sifa za wasifiaji na maelezo ya waelezaji, aghlabu humwangamiza mtu na humweka yeye mbali dhidi ya kuifanya nafsi yake iwe nzuri, tena umbali mkubwa mno… Ewe mwanangu! Madhambi ambayo hata kama kwa mtazamo wako ni madogo, usiyafanye mepesi na sio kitu, “angalia yule ambaye unayemuasi,” na kwa mtazamo huu madhambi yote ni makubwa na mazito… Ewe binti yangu! Jua kwamba ipo siku utabebeshwa mgongoni kwako mbebesho mzito wa masikitiko (utakumbwa na masikitiko makubwa) juu ya vijana, kwani utakuja kuona hapo baadaye msafara wa wenye ashki na wenye kumpenda Mwenyezi Mungu umekupita Mwenyezi Mungu aepushe hilo… kwa hivyo msikilize mzee huyu aliyechoka na aliyekata tamaa ambaye anabeba mzigo huu (yaani amekuwa kikongwe) kwa hakika aliponda umri wake katika siku za ujana wake na akasahau na kudan28
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:38 PM
Page 29
Vijana ni hazina ya Uislamu ganyika na ladha na raha za dunia ambazo zaisha haraka. Ewe binti yangu! Madamu ujana upo mkononi mwako basi jitahidi katika amali utengeneze moyo wako na funga makufuli na ondoa vizuizi, kwani kuna maelfu ya vijana ambao wao wapo karibu zaidi kufikia zoni za ufalme wa mbinguni na hufanikiwa kuifikia, na wala haifikii mzee mmoja. Makufuli ya shetani yakisahauliwa katika umri wa ujana, hukita mizizi yake kila siku ya umri na hatimaye huwa na nguvu zaidi… Na kutokana na mitego mikubwa ya shetani na nafsi iliyo hatari zaidi kutoka kwake, kwamba hayo mawili humwandaa binadamu katika kufanya wema mwishoni mwa umri wake na zama za uzeeni na huchelewesha hayo katika kuitakasa nafsi na kutubia kwa Mwenyezi Mungu hadi zama ambazo huwa ni mti muovu na mti mchungu wenye nguvu ya utashi na uwezo wa kuzisafisha nafsi mbili dhaifu bali zilizokufa… Ewe binti yangu! Weka kando majivuno na matarajio potofu danganyifu ya kishetani…na kuwa makini katika matendo na kutakasa nafsi yako na kuilea katika malezi mazuri, hakika safari ipo karibu sana… na kila siku inayopita na hali ya kuwa umeghafilika, yakufanya wewe kubakia nyuma… Ewe binti yangu! Jali na azimia kuondoa vizuizi, na sio ukusanyaji wa vitabu… hakika kujilimbikizia elimu wala haipunguzi vizuizi bali huzidisha na humhamisha mwenyewe kutoka vizuizi vidogo hadi vikubwa. Sisemi ukimbie na uache kupata elimu, maarifa na falsafa na kuupitisha umri wako katika ujinga, kwa hakika upo utoaji huu… nasema jitume na jitahidi ili uwe msukumo wa kiungu… Ewe binti yangu! Njiani kuna maafa mengi… ulimi huu mwekundu huponza kichwa na hufanikisha, aidha humfanya yeye kuwa ni chezeo la shetani, na nyenzo ambayo huharibu roho na moyo. 29
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:38 PM
Page 30
Vijana ni hazina ya Uislamu Usighafilike na uadui mkubwa wa binadamu na mambo haya ya kiroho… hesabu makosa makubwa uwezavyo kwa kiungo hiki kidogo, na angalia unafanya nini ndani ya saa katika umri wako, yakupasa kuutumia vizuri ili kupata radhi ya Mola kipenzi! Ni masaibu gani ambayo husababisha hayo, kwani moja ya masaibu hayo ni kumsengenya kaka na dada… Ewe binti yangu! Kujishughulisha katika kutafuta elimu hata elimu ya kumjua Mungu na tawhiid ikiwa zinaleta istilahi mbali mbali – ndilo litakiwalo – au kwa ajili ya elimu hizo, kwani hazimuweki karibu mtafutaji kutokana na lengo, bali humweka mbali yeye kwalo (elimu nayo ni kizuizi kikubwa). Na ikiwa utafiti kuhusiana na haki na kuwa na ashki naye – na hilo ni nadra sana - ndiyo taa ya njia na nuru ya uongofu…
KIIGIZO CHA VIJANA KWA VIJANA Roho ya ujana kwa kiongozi Ayatullah Ali Huseini Khamenei anasema: Mimi hivi sasa bado umri wa ujana haujaisha kabisa, kwa hivyo bado nahisi ndani ya dhati yangu roho ya ujana, na katu sitaruhusu kwa nafsi yangu – namshukuru Mwenyezi Mungu – na siruhusu hilo – na sitoruhusu kamwe katika mustakabali kuporomoka na kuangukia katika makucha ya mitindo ya kisasa ya uzee, ama wale ambao wamezisalimisha nafsi zao mikononi mwa uzee, ni dhahiri shahiri hawapati ladha kwa yale ambayo wanapata ladha vijana katika mambo yote ya maisha.
UHALISIA WA UJANA NA UMUHIMU WAKE Kwa hakika ujana ni mmea uliyolala umefichikana kwa undani sifa nyingine za heri, hung’aa na kutoa nuru, na usafi huu na upendo ambao hutoa alama kwenu – enyi wapendwa – hakika chanzo chake ni nyoyo zenu safi zilizotoharika, na mimi nawabadilishia kwenu upendo huu, hakika moyo wa baba yenu mzee mwenye kujali upendo wenu enyi vijana. 30
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:38 PM
Page 31
Vijana ni hazina ya Uislamu Kwa hali yoyote ile ukipatikana ujana hupatikana furaha, raha na utakaso, kwa hivyo kijana ni dhihirisho la uchangamfu na uhai, naye anamiliki uwezo na maandalizi ya kinafsi, yaani uchangamfu wa kijana, uwezo wake, vipaji vyake na ngozi yake kwa uwezekano huo hufanya miujiza, ikiwa utawepo upuuziaji wa hilo ila silka na ufahamu husifika kwa sifa ya ulegevu na upotokaji.
MANENO YA KIONGOZI KWA VIJANA Usia kwa Ujumla: Yale ambayo naweza kuwausia ni kama ifuyatavyo: Mosi: Hakika kijana lazima ahisi kuwa na majukumu, ajielewe kuwa ni mtu mwenye majukumu na mwenye kuwajibika, analazimika aweke bayana njia ya maisha yake, wala asiwe kama bendera mfuata pepo na matukio. Pili: Ajishughulishe maishani mwake kwa kuongozwa na mwongozo wa imani, kwani imani ina nafasi kubwa katika kupata maendeleo katika nyanja zote, na kwa kila ambalo hukumbana nalo katika harakati zake. Tatu: Awe mwenye mwamko na muono wa mbali katika mambo. Yatakapotimia mambo hayo matatu kwa kijana – nayo sio kazi rahisi, lakini inawezekana kufikia kiwango kikubwa – na itikadi kwamba ana uwezo wa kushughulikia suala la afya kwa msimamo wake, pamoja na maendeleo yote ambayo hupatikana ulimwenguni kuhusiana na maendeleo katika nyanja za mawasiliano, na kudhihiri tamaduni mpya ulimwenguni, na kutokea nguvu kubwa katika ramani ya ulimwengu.
UTAFUTAJI ELIMU Nyinyi bado mngali katika umri wa ujana, bado hazina yenu nzuri ingalipo hapana budi kufaidika na sehemu ya hazina hiyo kwa ajili ya mustakabali wenu, hali kadhalika yale ambayo hufungamana na umri wa ujana wenu, 31
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:38 PM
Page 32
Vijana ni hazina ya Uislamu inafafana na mbegu ya mustakabali; Basi ni juu yenu kupanga mikakati mizuri na thabiti kwa ajili ya maisha yenu, na kuna mambo mengi ambayo humfaa mtu hadi mwisho wa uhai wake, na miongoni mwa hayo ni yale ambayo manufaa yake huendelea hadi baada ya maisha haya, yaani maisha ya akhera, na kati ya hayo ni yale yenye kumnufaisha mtu pindi anapopatwa na matukio, na namna kwamba umri wenu utarefushwa miaka mingi katika maisha ya dunia hii, na huongezewa nyinyi elimu. Hayo ni jumla ya mambo yenye faida na manufaa kwa binadamu hadi mwisho wa umri wake, na amali njema isipoleta matunda kwake kwa hakika manufaa yake yataendelea hadi baada ya kifo. - Kwa hivyo kutafuta elimu ni wajibu wa msingi kwenu nyinyi.
MWAMKO Zifanyeni nafsi zenu ziwe zenye kuona mbali na kuwa na uwezo wa uchambuzi wa mambo, ili itengezwe picha kamili katika ubongo wenu kutokana na mambo ya kijamii, hakika uwezo wa kuchambua na kuchanganua mambo ni suala lenye umuhimu mkubwa mno, na kila tunalokutana nalo sisi waislamu kutokana na matatizo limekuja kwa sababu ya udhaifu wa uwezo wetu wa upembuzi yakinifu wa mambo, hali kadhalika hiyo ndiyo sababu ya vipigo ambavyo tulivyokumbana navyo mwanzoni mwa Uislamu na hatua zilizofuata. Kwa uhakika huo yapo maelezo mengi na maoni mbali mbali kuhusiana na mchakato huo, na adui haachi kuutumia mwanya huo kuangamiza muono na utambuzi wetu, na hudhihirika kwetu mambo mbali mbali yaliyogeuzwa uhalisia wake. Mimi naamini kwamba vijana hasa hasa wawepo ndani ya jamii, si vibaya kwao kufanya utafiti na majadiliano, lakini majadiliano hayo lazima yawe katika kuangazia hali halisi na yenye kueleweka, na kwa maana nyingine yawe yamefanyiwa utafiti wa kina na upembuzi yakinifu, hilo suala la kwanza, ama suala la pili ni kwamba majadiliano hayo lazima yasiishie 32
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:38 PM
Page 33
Vijana ni hazina ya Uislamu katika ugomvi, kwani ugomvi na mizozano ni mbinu chafu zichukiwazo, nayo ni ile ambayo imeelezwa na hadithi takatifu kwa ibara ya majigambo.
KUFAIDIKA NA UZOEFU Ni lazima kujua thamani ya uzoefu pamoja na watu wenye uzoefu, ni jambo la kawaida kutegemea uzoefu, na hii haimaanishi kwamba ifungwe milango ya uwezo wa vijana.
KUMCHA MWENYEZI MUNGU NA KUITAKASA NAFSI Na huenda ikasemwa kuwa ubadilikaji wa kitabia ni suala ambalo huwa gumu zaidi, na kwa hivyo muelewa wa amali hubakia yeye mwenyewe, na muulizwa wa kwanza katika kadhia ya ubadilikaji wa kitabia ni vijana wenyewe, namna ambayo matendo yote huwa ni rahisi kulingana na wao. Hakika vijana nyoyo zao ni safi na maumbile yao ni salama wala hayajachafuliwa na mafungamano, starehe za dunia, viburudisho, na anasa zake, kwani hukokotwa na kamba ya idadi ndogo ya vijana, ya kupenda mali na cheo, na utawala ambao hushika hatamu ya mambo yote ya watu, pamoja na udhaifu, na kwa hivyo mabadiliko ya kitabia baina ya vijana huwa rahisi, bila shaka haifai kwa wenye umri wa makamo kukata tamaa kuhusiana na mabadiliko ya kitabia ndani ya nafsi zao. Sisi tunataka kizazi kipya cha kijana ambaye ni mshika dini, mwema na mchamungu, asifike ndani ya dhati yake kwa uchangamfu, ubunifu na kupambika na tabia njema, vile vile awe mfanyakazi, aidha ajiepushe na uvivu na uzembe, na kaulimbiu yake iwe uchamungu – na naamini kwamba nimezungumza mara moja katika hotuba ya swala ya Ijumaa yale yanayohusiana na kadhia hii – na hushika hatamu ya nafsi yake, na huipoteza bure nguvu hii yenye kuogopesha ambayo huitwa nguvu ya 33
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:38 PM
Page 34
Vijana ni hazina ya Uislamu ujana katika njia ya kupata ukamilifu na kutoa huduma kwa nchi yake na familia yake. Hilo ndilo tumaini letu kwa vijana kama vile yatakiwayo hayo kwake nyakati zote, na ikiwa nchi haitozama katika vita tunataraji kutoka kwa vijana mchango fulani, na ikiwa nchi itakuwa katika hali ya kujijenga na kujiimarisha tunataraji kutoka kwao kitu kingine. Kwa hakika kupatia ni pale kijana anaposhikamana na mfumo wa kiislamu katika maisha, yeye akiwa mshikadini daima huchunguza anapokuwa na afya au anapokosa afya kuhusu kitendo chake, nyendo zake, masomo yake, mahusiano yake na ufahamu wake katika mambo. Na ufikiriaji – katika afya au ugonjwa katika nyendo zake – kwa wigo wa dhati yake ambayo huwa na nguvu. Suala la utoharishaji wa nafsi zenu husuniwa hilo kwa vijana kutokana na njia ya kuingiza maarifa ya kidini ya kiungu na njia za milango ya elimu ya kibanadamu na amali ya dini iliyosalimika, kwani ambalo Uislamu hulitaka ni kuteremsha yale yaliyopo kwetu kutokana na nguvu zilizopo hadi kikomo cha kitendo. Katika Qur’ani tukufu ipo dondoo muhimu ya kimsingi, si vibaya kuielewa hiyo kwani wahusika ni nyinyi vijana wapendwa, na huko ndiko kushikamana na uchamungu. Na pindi mtu anapotaka aweke sura ya uhalisia kutokana na uchamungu, humjia haraka katika ubongo wake maana za swaumu, swala, ibada, dhikri na dua. Ni sahihi kwamba maana hizi kwa ujumla wake hufungamana na nadharia ya uchamungu, isipokuwa yote kati ya hayo hayaakisi kwa umoja wa maana yake. Kwa mantiki hiyo uchamungu humaanisha uchungaji wa dhati, na binadamu atambue kila tendo katika matendo yake liwe na shabaha, lengo 34
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:38 PM
Page 35
Vijana ni hazina ya Uislamu fikra, utashi, azma na hiari, kwa hivyo mtu ambaye anamwendesha farasi na hushika kamba yake kwa mkono wake na anajua anakotaka kuelekea, hiyo ndiyo nadharia ya uchamungu. Ama yule ambaye amekosa uchamungu, vitendo vyake, mikakati yake na mustakabali wake havienei mkononi mwake, hufananishwa hilo na moja ya hutba za Nahjul-Balaghah kwa yule ambaye anapanda farasi hali ya kuwa hajui kuendesha farasi – na sio kulipenda hilo – bali ni vigumu kukaidi hata kama atapanda kwa kupenda kwake hali ya kuwa yeye hajui kushika kamba yake…hajui pa kwenda naye farasi, popote atakapokwenda hana hiari nyingine, mfano wa mtu huyo hawezi kunusurika wala kuokoka. Kwa hakika kijana kimaumbile huelemea katika mashindano, nalo hilo ni jambo zuri. Bila shaka suala la kushindana ni jambo ambalo tunatamani kwalo na tunalolitarajia wawe nalo vijana, aidha waepukane na nafsi inayoamrisha maovu ambayo humfanya kuwa duni, mwenye tabia mbaya na kumzuia kutokana na kupata ukamilifu, na kudumaa nafsi hiyo, na vijana hutakiwa kusimama kidete dhidi ya propaganda ya vishawishi vya matamanio na vichocheo vyote ambavyo huwasukuma wao katika machafu hayo. Mzunguko wa maisha hauwezi kueleweka kwa urahisi huu. Hakuna kazi muhimu na makini ambayo hufanywa kwa urahisi, na mtu akiwa hatakuwa na shabaha kwa kupata chochote chenye thamani hapana budi kwake kutoa kitu kwa juhudi na kustahamili mashaka na matatizo.
HIFADHINI SWALA Enyi wapendwa wangu jueni kwamba hakika binadamu huwa na lengo la kudumu… na hapana budi kwa mwanadamu, awe mdogo au mkubwa, kijana au mzee hufanya kosa, au husahau kutenda jambo fulani au hufanya dhambi fulani, na atakapotaka mtu apite njia ya kufaulu maishani mwake, 35
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:38 PM
Page 36
Vijana ni hazina ya Uislamu basi swala ndiyo itayomwezesha kufikia hali hiyo. Ipo aya ya Qur’ani tukufu inasema: “Na simamisha swala katika sehemu mbili za mchana na nyakati za usiku hakika mema huyaondoa maovu…” (11:114) Kwa hivyo swala huondoa giza na maovu, aidha hufuta athari ya dhambi moyoni, basi mtu huenda akachafuka kwa maasi na akaifunga mikono yake kwa minyororo ya dhambi, isipokuwa anaposhikamana na swala, nuru hiyo hubakisha uwepo wa binadamu, wala hawezi kuruhusu maasi yapate nafasi ndani ya nafsi yake. Ombi langu kwenu ni kwamba angalieni swala uangaliaji wa makini, ni jambo la kawaida kwenu, kwani nyote mnahudhuria katika swala, lakini litakiwalo kwenu ni muondokane na hali ya uvivu na uzembe, na ikiwa swala haitatufanya tuondokane na hali ya kubwabwaja hivyo, na urudiaji wa maneno kama wa kasuku, itakuwa ni kwa sababu ya uvivu, kwa maana kwamba mtu anainuka na kuchukua udhuu na hatimaye hajui ni ipi amali aitekelezayo! Na lau mtachunguza maana ya maneno ya swala mtayakuta hayasababishi wala kuleta uvivu, bali hupanda ndani ya nafsi mbegu ya shauku na upendo, aidha humuhimiza mtu kufanya haraka kuelekea kutekeleza swala, na huthibiti kwayo maana ya “Hayya’ala swalaat” yaani njooni katika swala. Mimi sitaki kutoka kwenu mjue maana zote za swala, kwani kazi hii ni kazi ya watu maalum na mahsusi waliobobea kwayo, na huenda isiwe rahisi hata kwetu sisi kuwa hivyo, lakini inalazimu kwa uchache kusoma sehemu ya swala kwa kutambua na kuhudhurisha moyo, kwa maana kwamba kumwelekea yule ambaye unayezungumza naye kwa maana ya maneno ambayo mnazungumza naye kwayo.
36
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:38 PM
Page 37
Vijana ni hazina ya Uislamu
KATIKA KUKABILIANA NA VITA VYA KITAMADUNI KUWENI KIIGIZO WALA MSIWAFUATE WATU WA MAGHARIBI Mwenyezi Mungu anasema kinaga ubaga kwa ulimi “Na utujaalie kuwa viongozi kwa wamchao (Mwenyezi Mungu)” 25:74. Kwa hivyo ni juu ya kila mtu akuze ndani ya nafsi yake uwezo ili awe kiigizo kwa wengine katika hali yoyote itavyokuwa, wala hilo halihusu tu uigizaji katika swala ya jamaa, bali huvuka hadi kwa matendo, fikra na mwenendo. Nawaambia vijana: Enyi wapendwa wangu, enyi watoto wangu, acheni ufuataji na fikirini juu ya mfumo na njia ambayo ndani yake mna nguvu kwa akili zenu, utashi wenu, kutoharika na kuhifadhika na tabia zenu. Kwa hakika muda umepita watu wamefumbwa macho kwa kufuata tamaduni za kimagharibi, wametekwa nyara mawazo yao yote, kila kitu ni cha kimagharibi, hivi ni kitu gani watu hawa wakijuacho kutoka kwa watu wa Magharibi? Ni faida gani waipatayo kutoka kwa watu wa Ulaya! Nalo ni hatarisho ambalo lilikuwa ni mchakato wa kufanikiwa kwalo, je! Wale waliotekwa nyara na fikra za kimagharibi wajua hilo? Na haina maana kwamba ni kukataa moja kwa moja utalaamu, maendeleo, elimu na uzoefu wa watu wa Magharibi, na hakuna yeyote mwenye akila timamu asemaye hivyo, kuwakataa watu wa Magharibi maana yake ni kwamba kutokubali kutawaliwa na wamagharibi ikiwa katika njanja za kisiasa, uchumi na utamaduni. Na hapa nitawaeleza kitu kwa ufupi kutokana na kutawaliwa na utamaduni wa kimagharibi, huenda mkafaidika kwacho.
37
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:38 PM
Page 38
Vijana ni hazina ya Uislamu Tofauti Kati ya Vita vya Kitamaduni na Ubadilishanaji wa Utamaduni Kwa hakika nimeeleza zaidi ya mara moja tofauti baina ya vita vya kitamaduni na ubadilishanaji wa utamaduni. Kwa hivyo vita vya utamaduni ni jambo baya, ama ubadilishanaji wa utamaduni ni jambo zuri… mara nyingine mtu mwenyewe hutafuta chakula au dawa muafaka ambayo huziba mapungufu katika mwili wake na humfaa kwayo, basi anaitumia na huingia tumboni mwake, na wakati mwingine tunaitumia kwa hiari yetu, bali wao hutudanganya, hutughiribu na huingiza katika miili yetu wayatakayo na sio tuyatakayo sisi, au si hivyo… Ni juu yetu kufanya kazi kwa uwezo wetu na uono wetu, sote kwa pamoja na kuhifadhi juu ya… na juhudi zetu zisikomee katika tarjuma, na wapo baadhi hawako katika maandalizi hata katika uainishaji wa fikra ya mtarjumu katika michakato mbali mbali, wenye kudai kutokuwepo uwezekano wa kujadiliana nayo, kwani fikra au ulinganisho hutokea kwa msomi wa nafsi au mtaalamu wa mambo ya kijamii au mwanauchumi mwandamizi, na mwenye kwenda kinyume nalo kana kwamba amekufuru! Lakini wao baada ya siku kadhaa hurejea kutoka katika maoni yao na hushikamana na kauli nyingine, aidha huikubali kauli ya pili bila ya uchanganuzi na upembuzi yakinifu! Kwa hakika hilo lina mashaka kulingana na nchi yoyote ile.
KUJUA DHAMIRA YAKE Hakika mambo ya umuhimu ambayo kijana huyahitaji ni kujua dhamira na lengo lake, inalazimu kwanza ajijue yeye ni nani, na kazi yake na harakati zake zina lengo gani? Kwa hivyo adui hujaribu kuondoa dhamira ya kijana na kufuta malengo yake ambayo humlenga na kuyakusudia, na hushika upeo wa macho mbele yake na kufunua kwake kwamba, hakika wewe ni kiumbe dhalili.
38
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:38 PM
Page 39
Vijana ni hazina ya Uislamu
CHAGUENI KIIGIZO Sisi ndio ambao tunawajibika kuchagua kiigizo chetu kwa nafsi zetu, yaani tuangalie kwa upeo wa mbali na itikadi yetu ya haki, aidha tuchunguze picha ambayo tuiridhiayo katika nafsi zetu kati ya picha hizo… hivyo ndivyo inakuwa picha hiyo na shakhsia kuwa ndio kiigizo chetu, wala siamini kuwepo ugumu wa kupatikana kwa kijana wa kiislamu mtambuzi juu ya maisha ya Maimamu na Ahlul-Bayt mwanzo wa Uislamu, ikiwa ndio kiigizo chake, na watu wa kuigwa hawana idadi.
MFANO WA KUIGWA Hakika nyinyi leo mnahamasika na mnafuatilia mambo ya Palestina, na binti yetu mpendwa amesema: ‘Ee laiti muono wetu ungelifikia hadi Palestina’ je! mnajua yale wayajuayo Wapalestina? Palestina imeporwa tangu miaka ya hamsini, na katika muda wote huo ilikuwa Palestina inalenga vijana, lakini miongoni mwa yale ayajuayo kijana huyu wa Kipalestina ambaye amekumbana katika uwanja wa picha hiyo, ameiga kutoka kwa nani? Kiigizo chake ni kijana wa Kilebanoni mpiganaji muumini mwenye ikhlas, na hilo silisemi mimi bali wao hueleza hilo wazi wazi, wao ndio hunyanyua picha za Sayyed Hasan Nasrullah katibu mkuu wa kikundi cha Hizbullah cha Lebanoni katika mchakato ambao hupangwa katika Ghaza na Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan – nayo ni sehemu ya Palestina – na hakika wamechomeka bendara ya Hizbullah juu ya Qubba la msikiti wa Aqswa, wameichomeka kwa lengo la kuwazuia wazayuni, na hicho kimekuwa ni kiigizo cha vijana wa Kipalestina, na wengi wa wafuasi hufuatilia kituo cha luninga cha Al-Manaar cha Hizbullah cha Lebanoni – ambacho hurusha matangazo yake saa ishirini na nne – hao hutokana na ardhi za Wapalestina na zilizoporwa! Wao hukisikiliza kituo hicho kana kwamba ni wanakunywa maji matamu, na hawatosheki tu kukisikiliza bali huyapokea maneno yake mfano wa yule mwenye kiu. 39
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:38 PM
Page 40
Vijana ni hazina ya Uislamu
JIHADI Miongoni mwa usia wa kiongozi Khamenei kwa vijana hubainika matarajio makubwa mangapi ambayo hukumba kizazi hiki cha vijana katika njanja za elimu, amali na jihadi namna ambayo anasema: Jemadari wa jeshi la Uislamu ni wao wapiganaji bora katika mstari wa mbele.
KUJISOMEA Katika mwenendo wa kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hubainika kwamba yeye ni miongoni mwa watu wengi ambao hudurusu na kujisomea, anasema: “Hakika kitabu kina anwani, utamaduni na roho ya binadamu, na mwili wake hula kwa baraka ya kitabu.”
KUSHIRIKI KATIKA HARAKATI MBALI MBALI Hakika harakati ambazo huzifanya vijana huidhihirisha shakhsia yao na mustakabali uangazao, na mimi nausia familia kuwasaidia watoto katika kushiriki katika zile harakati zinazowahusu wao, na nawapa usia wasichana kutoangalia utashi wa familia zao kana kwamba ni mzigo mzito. Nawausia vijana kushiriki katika mambo ya kijamii, lakini kwa sharti kwamba harakati hizo za kijamii zisiwe kizuizi kinachozuia kuelewa masomo, na ni juu yao kuzipa kipaumbele harakati za kijamii zenye nembo za kidini zilizo wazi, kwani harakati za kijamii zenye nembo za kidini aghlabu humwepusha mtu na madhara, au ni zenye madhara machache kushinda nyinginezo iwapo zina madhara, zaidi ya hayo ni mambo mazuri yapatikanayo katika harakati za kijamii.
40
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:38 PM
Page 41
Vijana ni hazina ya Uislamu
KUFANYA MAZOEZI Mimi nazingatia kuwa mazoezi ni wajibu kwa watu wote, suala la ufanyaji mazoezi linawahusu vijana, wazee na wanawake. Na hii ina maana kwamba ikiwa mazoezi ni wajibu kwa vijana, vile vile ni wajibu juu yetu, kwa wale wenye umri usio wa uzee na utoto hulinda afya zao na huboresha usalama wa maisha yao au vifo vyao, hii ina maana kuwa mtu atakapofanya mazoezi ataishi maisha ya salama, wala hapatwi na maradhi wala huzuni. Ama umuhimu wake kulingana na vijana, hilo huwapa usalama, uchamungu, furaha na uzuri kwalo, na katika mwangaza ambao umetangulia hapo kabla nazingatia kwamba mazoezi ni wajibu kwa watu wote, wanaume na wanawake, na kwa yale ambayo yanayohusiana na umri wao. Na kwa kuwa mazungumzo haya yatapeperushwa na kusikilizwa na vijana, kwa hivyo nawausia watu wote kufanya mazoezi. Na wakati fulani asubuhi nakwenda milima iliyopo Kaskazini mwa mji wa Tehran, napata kuzikuta sehemu hizo tupu wala hakuna watu, nahisi vibaya pindi ninapohitaji kuburudika na wakati mwingine ninapokwenda huko siku za Ijumaa nakuta idadi kubwa ya watu.
FAIDIKENI NA WAKATI Hatujapata maneno ya kuhitimisha mchakato huu yasiyokuwa ibara ambazo mheshimiwa kiongozi anaeleza kuhusiana na mambo ya kiroho ambayo huwapatia vijana wa kizazi kipya wa umma wake, kiongozi amesema: Ninapokuwa pamoja na vijana kwa hakika hisia zangu zinakuwa ni kana kwamba ni upepo mwanana wa asubuhi, nahisi kukunjukiwa na furaha, aghlabu hunijia akilini mwangu kitu fulani ninapokutana na vijana, na huenda nikalifikiria hilo mara kwa mara nalo ni je! hivi vijana wanajua kuwa ni nyota gani hung’aa katika mapaji ya nyuso zao? 41
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:38 PM
Page 42
Vijana ni hazina ya Uislamu Mimi naiona nyota hiyo, je! pia wao huiona? Nyota ya vijana inatoa mwanga mzuri mkubwa, iwapo vijana watahisi kitu hicho cha thamani kisichokuwa na mfanowe….. Hakika mimi naamini kwamba wao watafaidika kwacho kwa aina kubwa akipenda Mwenyezi Mungu.
42
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:38 PM
Page 43
Vijana ni hazina ya Uislamu
ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24. 25. 26.
Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thalathini Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudharr Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur'an na Hadithi Elimu ya Nafsi Yajue Madhehebu ya Shia Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu 43
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:38 PM
Page 44
Vijana ni hazina ya Uislamu 27. 28. 29. 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52. 53. 54. 55. 56. 57.
Al-Wahda Ponyo kutoka katika Qur'an. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii Mashukio ya Akhera Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyeezi Mungu na sifa zake Amateka Na Aba'Khalifa Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana. Upendo katika Ukristo na Uislamu Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya Kupaka juu ya khofu Kukusanya swala mbili Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kusujudu juu ya udongo Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) Tarawehe Malumbano baina ya Sunni na Shia Kupunguza Swala safarini Kufungua safarini Umaasumu wa Manabii Qur’an inatoa changamoto as-Salaatu Khayrun Mina -'n Nawm Uadilifu wa Masahaba Dua e Kumayl Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu 44
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:38 PM
Page 45
Vijana ni hazina ya Uislamu 58. 59. 60. 61. 62. 63. 64. 65. 66. 67. 68. 69. 70. 71. 72. 73. 74. 75. 76. 77. 78. 79. 80. 81. 82. 83. 84. 85. 86.
Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mitume Muhammad (s) Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili Kuzuru Makaburi Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita Tujifunze Misingi Ya Dini Sala ni Nguzo ya Dini Mikesha Ya Peshawar Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliyonyooka Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake Liqaa-u-llaah Muhammad (s) Mtume wa Allah Amani na Jihadi Katika Uislamu Uislamu Ulienea Vipi? Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) Urejeo (al-Raja’a ) Mazingira Utokezo (al - Badau) Sadaka yenye kuendelea Msahafu wa Imam Ali 45
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:38 PM
Vijana ni hazina ya Uislamu 87. 88. 89. 90. 91. 92. 93. 94. 95.
Uislamu na dhana Mtoto mwema Adabu za Sokoni Johari za hekima kwa vijana Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu Tawasali Imam Mahdi katika Usunni na Ushia
96.
Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu
97.
Hukumu ya kujenga juu ya makaburi
98.
Swala ya maiti na kumlilia maiti
99.
Shiya na Hadithi (kinyarwanda)
100.
Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu
101.
Hadithi ya Thaqalain
102
Fatima al-Zahra
103.
Tabaruku
104.
Sunan an-Nabii
105.
Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza)
106.
Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili)
107.
Mahdi katika sunna
108.
Kusalia Nabii (s.a.w)
109.
Ujumbe -Sehemu ya Kwanza
110.
Ujumbe - Sehemu ya Pili
111.
Ujumbe - Sehemu ya Tatu
112.
Ujumbe - Sehemu ya Nne
113.
Ngano ya kwamba Qur’ani imebadilishwa 46
Page 46
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:38 PM
Vijana ni hazina ya Uislamu 114.
Iduwa ya Kumayili
115.
Maarifa ya Kiislamu.
116.
Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza
117.
Ukweli uliopotea sehemu ya Pili
118.
Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu
119.
Ukweli uliopotea sehmu ya Nne
120.
Ukweli uliopotea sehmu ya Tano
121.
Johari zenye hekima kwa vijana
122.
Safari ya kuifuata Nuru
123.
Idil Ghadiri
124.
Myahudi wa Kimataifa
125.
Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi
126.
Visa vya kweli sehemu ya Kwanza
127.
Visa vya kweli sehemu ya Pili
128.
Muhadhara wa Maulamaa
129.
Mwanadamu na Mustakabali wake
130.
Imam Ali binamu ya Mtume Sehemu ya Kwanza
131.
Imam Ali binamu ya Mtume Sehemu ya Pili
132.
Khairul Bariyyah
133.
Uislamu na mafunzo ya kimalezi
134.
Vijana ni Hazina ya Uislamu.
135.
Yafaayo kijamii
136.
Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu
137.
Taqiyya
138.
Vikao vya furaha
139.
Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 47
Page 47
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:38 PM
Page 48
Vijana ni hazina ya Uislamu 140.
Uislamu na Mazingatio Sehemu ya Kwanza
141.
Uislamu na Mazingatio Sehemu ya Pili
142.
Azadari-Kuhuzunika na Kuomboleza
143.
Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah
144.
Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu
145.
Kuonekana kwa Allah
146.
Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza)
147.
Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili)
148.
Ndugu na Jirani
149.
Ushia ndani ya Usunni
150.
Maswali na Majibu
151.
Mafunzo ya hukmu za ibada
152.
Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisusunni No1
153
Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisusunni No 2
154.
Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisusunni No 3
155.
Abu Huraira
156.
Kati ya Alama kuu za dini Swala ya Jamaa, na Adabu za Msikiti na Taratibu zake.
48
Vijana ni
hazina ya Uislamu check Lubumba.qxd
7/16/2011
12:38 PM
Page 49
Vijana ni hazina ya Uislamu
BACK COVER Imepokewa kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w.) kwamba amesema: “Hawi kijana ambaye anaacha dunia, starehe na upuuzi wake, na akazeeka akiwa katika kumtii Mwenyezi Mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu atampa malipo ya wakweli sabini na mbili.” Vilevile imepokewa hadithi kutoka kwake akisema: “Hakika miongoni mwa viumbe wapendwao zaidi na Mwenyezi Mungu ni kijana wa umri mdogo katika sura nzuri na akautumia ujana na uzuri wake katika kumtii Yeye. Mwenyezi Mungu atajifakharisha kwa malaika kwaye, atawaambia: ‘Huyu ndiye mja wangu wa kweli.’” Hali kadhalika imepokewa hadithi kutoka kwake akisema: “Hakika Mwenyezi Mungu humpenda kijana ambaye huumaliza ujana wake katika kumtii Mwenyezi Mungu.” Uislamu ukiwa kama umma au taifa umeweka taratibu nzuri za kuwafundisha vijana wake ili wayafahamu majukumu yao, hii ikiwa ni pamoja na kuwapa elimu ya dini na elimu dunia (sekula). Kitu cha kusikitisha ni kwamba nchi nyingi za Kiislamu zimeacha utaratibu huu na kuupa mwanya utamaduni wa Magharibi kushamiri katika chi zao. Na waathirika wakubwa ni vijana ambao ndio nguzo ya taifa. Kitabu hiki kinakumbusha Umma wa Kiislamu na vijana kwa ujumla juu ya jukumu lao hili muhimu. Mwandishi anaelezea sifa za vijana wa Kiislamu na wajibu wao katika taifa kwa vile wao ni waathirika wakubwa wa tamaduni za Magharibi. Kimetolewa na kuchapishwa na: Al -Itrah Foundation 49