Yajue madhehebu ya shia

Page 1

Yajue Madhehebu ya Shia

Kimeandikwa na Mohammad Ali Shomali

Kimetarjumiwa na: Al-Akhy Salman Shou

Kimehaririwa na: Dr. M. S. Kanju


ŠHaki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION

ISBN: 9987 - 9022 - 8 – 6

Kimeandikwa na Mohammad Ali Shomali

Kimetarjumiwa na: Al-Akhy Salman Shou

Kimehaririwa na: Dr. M. S. Kanju

Asomwa na prufu: Mbarak A. Tila Kimepangwa katika Komputa na: Al-Itrah Foundation Toleo la Kwanza: Desemba 2005 Nakala: 1000 Toleo la pili: Machi 2015

Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv.com Katika mtandao: www.alitrah.info


Neno La Mchapishaji Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza, kwa jina la “DISCOVERING SHI’I ISLAM” kilichandikwa na Mohammad Ali Shomali. Kitabu hiki ni matokeo ya muda mrefu ya uchunguzi wa masuala muhimu ya Uislamu kwa ujumla, na hususan Madhehebu ya Shi’a sambamba na madhehebu nyingine za Kiislamu. Lengo kubwa la kitabu hiki ni kujaribu kuziba mianya iliyopo baina ya madhehebu, na ili kuwafanya Waislamu wazielewe vizuri madhebu hizo, waepukane na dhana na upotoshaji wa watu wasioutakia mema Uislamu, na kubwa sana kuleta umoja na mshikamano baina ya Waislamu wote bila kujali hitilafu zao za madhehebu. Kama alivyoelezea mwandishi wa kitabu hiki kwamba: mambo yanayowaunganisha Waislamu ni mengi mno, tena ni yale ya msingi, kuliko yale wanayohitilafiana ambayo wala sio katika misingi mikuu ya Uislamu. Tumekiona kijitabu hiki ni chenye manufaa sana, na kitawafaa sana Waislamu wa rika zote na wa jinsia zote. Hivyo, kama ilivyo ada yetu tumeona tukitoe kijitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa nia ile ile ya kuwahudumia Waislamu wazungumzaji wa Kiswahili. Tunamshukuru Ndugu yetu al-Akh Salman Y. Shou kwa kukubali jukumu hili la kukifanyia tarjuma kitabu hiki. Vile vile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki. Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni chenye manufaa kwa wasomaji wetu, na chachu ya kuleta umoja na mshikamano katika dini yetu hii ya Uislamu, hususan katika kipindi hiki ambapo maadui zetu wameungana ili kutuangamiza. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation


Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu. Sifa zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu wote.

Utangulizi. Kitabu hiki sehemu yake kubwa ni mukhtasari wa kitabu kiitwacho; Shi’i Islam Origins, Faith and Practices (2003 ICAS Press). Ambacho kimeandikwa na mwandishi wa kitabu hiki. Toleo hili fupi linalenga kwenye kushughulikia kwa ufupi masuala muhimu yanayohusu Uislamu kwa ujumla na hususan Uislamu wa madhehebu ya Shi’a. Vitabu hivi viwili vinaonesha jaribio la wastani kuziba mianya iliyopo kwenye uwanja wa mafunzo ya Kislamu kwa ujumla na hasa zaidi mafunzo ya madhehebu ya Shi’a. Licha ya kwamba vitabu hivi vimeandikwa kwa urahisi na kwa uwazi, ni matokeo ya zaidi ya miaka ishirini ya kujihusisha na mafunzo ya Kiislamu, na ambayo yametegemezwa kwa kiasi fulani kwenye mfululizo wa seti mbili za mihadhara kuhusu Uislamu wa madhehebu ya Shi’a iliyotolewa kwa wasikilizaji wa Kingereza: Seti ya kwanza ya mihadhara hamsini iliyotolea hapo Jamiat az-Zahra (Seminari inayoongoza ya Kiislamu ya wanawake) katika jiji la Qum, Iran, mnamo mwaka wa 1995 na 1996 na seti ya pili ni mihadhara thelathini iliyotolewa huko ‘Manchester Islamic Institute‘ na ‘Shi’a Welfare Center in Manchester,’ Uingereza mnamo mwaka wa 1998 na 1999. Sura ya kwanza imeanza kwa kueleza maana ya maandishi na istilahi ya neno ‘Shi’a na rejea za masomo mashuhuri kuhusu somo hilo zimeoneshwa. Halafu inaendelea kuchunguza chimbuko la Uislamu wa madhehebu ya Shia na jinsi ulivyoanza na kuwepo. Sura ya pili inachunguza chanzo cha fikira ya Shia, yaani Quran, Sunna, sababu na maridhiano. Katika mazungumzo kuhusu hadhi ya Quran, sura hii inaendelea kuthibitisha kwamba Shi’a kama Waislamu wengine wanaamini kwamba Quran ilioyopo leo ni mfano halisi wa ufunuo wa Mungu kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w). Sura inaendelea kwa kueleza chanzo cha pili ambacho ni muhimu sana, yaani Sunna ambacho kinajumuisha matamshi na matendo ya Mtume Muhammad (s.a.w.w). Quran yenyewe inawataka Waislamu kumchukua Mtume na kumweka kwenye nafasi ya mfano wao, kurejea kwake kuamua na kusuluhisha migongano yao, na inasema kuhusu Mtume kuwa ndiye ambaye hukariri, hufundisha na kuieleza Quran. Kwenye sura hii pia yapo mazungumzo kuhusu watu wa Nyumba ya Mtume (a.s) (Ahlul bait) na nafasi yao katika kuonesha Sunna. Halafu unafuata mjadala kuhusu umuhimu wa sababu na nafasi yao katika kuwasilisha sunna. Halafu yanafuata mazungumozo kuhusu umuhimu wa sababu na nafasi yake katika kuelewa imani za Kislamu, maadili na kanuni za ibada. Mwishowe kuna mjadala kuhusu uhalali wa ‘makubaliano ya wote pamoja’ (al-Ijma) na jinsi yanavyo onekana kuhusiana na Sunna katika mtizamo wa madhehebu ya Shi’a. Sura ya tatu, inachunguza msingi wa mafundisho ya imani ya madhehebu ya Shi’a. Pamoja na Upweke wa Mungu, Utume na Ufufuo vipengele vinavyofanyiza kanuni za Dini (Uislamu na dini zingine za ki-Mungu), baadhi ya mafundisho muhimu ya ziada kama vile haki ya ki-Mungu na uimamu yanachunguzwa. Mafundisho haya, sehemu fulani inaweza kuafikiwa na Waislamu wengine, lakini madhehebu ya Shi’a ndio wale wanaoamini mafundisho hayo yote. Sura ya nne, ni maelezo mafupi sana ya ibada za madhehebu ya Shi’a sambamba na marejeo mafupi kwenye malengo na kanuni zilizomo humo. Utekelezaji huu kimsingi unaafikiwa na Waislamu wote, ingawa kunawezekana kuwepo na tofauti fulani hususan miongoni mwa madhehebu za Kiislamu. Sura ya tano na ya mwisho ni mazungumzo mafupi kuhusu ulimwengu wa leo wa ki-Shi’a. Sura hi inaanza na maelezo mafupi ya takwimu za hivi karibuni kuhusu idadi iliyopo ya Waislamu kwa ujumla na idadi ya Mashi’a hapa duniani. Pia upo mchanganuo wa mahusiano ya kidini wa baadhi ya nchi zenye historia ndefu ya Shi’a uliopo humo. Ingawa hakuna takwimu sahihi na zilizo thibitishwa kwa wakati huu kuhusu idadi ya Shi’a hapa duniani, juhudi imefanywa hapa kukusanya zile nzuri zaidi zilizopo.


Pia lazima nitamke kwamba mwandishi kwa uaminifu na moyo wote amejifunga kwenye umoja wa Kiislamu na ana matumaini kwamba kazi hii inaweza kuwa kama hatua ya adabu kuelekea kwenye udugu wa Waislamu. Kwa kweli, njia mojawapo iliyo nzuri sana katika kufanikiwa kupata umoja na udugu huu ni kufahamiana na kushinda chuki za kihistoria ambazo huzuia lengo la kuelewana kati ya wenyewe kwa wenyewe. Kwa mujibu wa methali ya Kiarabu, ‘watu ni maadui wa kile wanachokidharau.’ Uchunguzi makini wa madhehebu zote kubwa za Kiislamu unaonesha kwamba mambo ambayo wanafanana ni mengi zaidi kuliko yale wanayo tofautiana. Waislamu wote wanamuamini Mungu huyo huyo, Mtume yule yule na Quran ile ile. Waislamu wote wanamini Siku ya Ufufuo na malipo ya Mungu na adhabu. Wote wanasali Swala za kila siku na kibla ni moja, na hiyo ni Makkah. Wote wanafunga Saumu mwezi wa Ramadhani. Wote wanakwenda Hija Makkah katika wakati mmoja. Wote wanaamini kutoa sadaka, kuamrisha mema na kukatazana mabaya. Wote wanaamini kwamba wanatakiwa kufanya urafiki na watu wa imani na nia njema na kuachana na maadui wa Mungu. Wote wanashikilia wema ule ule na maadili yale yale. Kwa mujibu wa Quran waumini wote ni ‘ndugu.’ Bila kujali rangi, utaifa, jinsia na madhehebu, kuna majukumu maalum kwa kila mmoja ambayo ndugu wa imani lazima amfanyie mwenziwe. Wakati moja Mu’alla bin Kunays alimuuliza Imamu Sadiq (a.s) kuhusu kitu gani Mwislamu anamuwia Mwislamu mwenzake. Imamu alijibu; “Kuna majukumu saba yanayo muajibikia juu yake. Kama akidharau moja miongoni mwa majukumu hayo yeye si rafiki au mja wa Mungu, na kwa kweli atakuwa hajafanya lolote kwa ajili ya Mungu.” Kisha Imamu alitaja mambo yafuatayo: Mfanyie nduguyo yale unayotaka wewe ufanyiwe na usitamani yamfike ndugu yako yale ambayo hungetamani yakupate. Usimuudhi nduguyo isipokuwa mridhishe na utii matakwa yake. Msaidie kwa moyo wako, ulimi wako, mkono na miguu yako. Uwe macho yake kuona mwongozo wake na kiapo chake. Usile ukashiba wakati yeye ana njaa, wala usinywe na kuvaa ambapo yeye ana kiu na yu uchi. Kama hana mtumishi, lakini wewe unaye, ni wajibu wako kumpa mtumishi wako afue nguo zake, ampikie chakula na atandike kitanda chake. kubali ahadi yake na mwaliko wake; mtembelee wakati anaugua, hudhuria maziko yake na umtimizie mahitaji yake kabla hajakuomba, mtimizie haraka kama unaweza. (Muzaffdar, uk. 76 na 77) Kwa bahati mbaya, kila mara pamekuwepo na watu wasioona mbali kiakili miongoni mwa kila kundi au madhehebu na wamejaribu kukuza tofauti na wametaka mfarakano badala ya mshikamano na udugu. Hufanya haraka kutafuta visingizio fulani kumwita yeyote anayepingana naye kafir (asiye amini) au mushrik (mshirikina) na tendo lolote ambalo haliwapendezi wao huliita bida’ah. (uzushi). Naam hakika, kuna wasioamini (kafir), na kuna wazushi (waasi), lakini mtu lazima awe mwangalifu sana katika kuyatumia maneno haya. Viongozi wakubwa wa Kiislamu na wanachuoni, Sunni au Shi’a, kamwe hawajaitana majina haya. Kwa njia hii, wamewasilisha katika fatwa zao, misemo na matendo yao moyo halisi wa Uislamu, ujumbe huu wa upatanifu wa wakati wote, wa amani, haki, umoja na huruma. Uislamu ulileta umoja na mshikamano kwa wale walio teseka sana kwa chuki na uadui. (3:103) Kitendo hiki cha kuwafanya watu washikamane kinaheshimiwa sana kama kitendo cha Mungu. (8:63). Kinyume chake, kilikuwa kitendo cha Farao kuwatenganisha watu (28:4) Quran inaonya waumini kwamba kama wakianza kugongana wao kwa wao watakuwa dhaifu na kwa hiyo watashindwa (8:46). Kwa kweli, wito wa umoja haukuishia kwa Waislamu tu. Quran inawalingania watu wote wa imani kama vile Wakristo na Wayahudi kuunganisha jitihada zao na kuongeza nguvu kwenye jambo moja (3:64) Na tuwe na matumanini kwamba siku hadi siku akili hii ya muungano na umoja inakuwa imara na kuzidi.


Na mwisho ningependa kuchukua fursa hii kuwashukuru watu wote binafsi na mashirika ambayo yamenipa moyo, hususan Ayatullah Muhsin Araki, Islamic Collage for UK. na Jamhuri ya Ireland hapo Uingereza. Pia ningependa kutoa hisia zangu za shukurani ya dhati kwa Mungu kwa upendeleo wake wote ambao Ametupatia siku za nyuma na sasa. Mohamad A.Shomali, Ramadhani 1423, November, 2002.

Sura Ya Kwanza: Chimbuko La Uislam Wa Shi’a Maana Ya Neno Shia. Kwa lugha ya Kiarabu neno ‘Shi’ah’ kwa asili maana yake ni Mfuasi moja, wawili au kundi la wafuasi. Kwenye Quran Tukufu, neno hili limetumiwa mara kadhaa kwa maana hii. Mathalan, kwenye Aya ya 28:15 Mwenyezi Mungu anasema kuhusu mmojawapo wa wafuasi wa Musa kuwa ni mmojawapo wa Shi’a wake. Mahali pengine, Ibrahim ametambulishwa kama Shi’a wa Nuhu (37:83). Mwanzoni mwa historia ya Uislamu, neno ‘Shi’a lilitumiwa katika asili yake au maana halisi kwa wafuasi wa watu tofauti. kwa mfano, baadhi ya Hadith zinasema kuhusu Shi’a wa Ali bin Abi Talib na wengine Shi’a wa Mu’awiyah bi Abi Sufyani. Hata hivyo pole pole neno hili lilipata maana ya pili au istilahi, yaani wafuasi wa Ali wale walioamini Uimamu wake (uongozi wa KiMungu). Shahrestani (alifariki 548 A.H) kwenye al-Milal wa al-Nihal yake ambacho ni chanzo mashuhuri kuhusu madhehebu mbali mbali za Uislamu, ameandika; ‘Shi’a ni wale waliom fuata Ali hasa na walioamini Uimamu na ukhalifa wake kwa mujibu wa mafundisho yaliyo wazi na wosia wa Mtume Muhammad (s.a.w.w).1 Hii ni maana sahihi kabisa, kwani Shi’a wenyewe wanaamini kwamba sababu ya kumfuata Ali ni kwamba ilitakiwa iwe hivyo na Mtume na huu haukuwa ni uamuzi wao binafsi kuamua wamfuate nani; tofauti na wale ambao si Shi’a ambao baada ya kutawafu kwa Mtume Muhammad, walimfuata yule aliyechaguliwa kule Saqifa na waliamini kwamba Mtume aliliacha hilo kwa watu wenyewe waamue nani wa kumfuata. Naam hakika, Abu Bakr bin Abi Quhafah, Khalifa wa kwanza, ambaye alichaguliwa kwa njia hii, aliamini kwamba lazima amteue mtu wa kushika nafasi yake baada yake. Na Khalifa wa pili Umar bin Khattab, aliteua jopo la watu sita kumteua mmojawapo miongoni mwao kwa mujibu wa utaratibu wa nidhamu kali uliowekwa naye. Inavutia kuona kwamba ni Ali, Khalifa wa nne ambaye alichaguliwa na kwa kweli alilazimishwa na takriban Waislamu wote baada ya kuuawa Khalifa wa tatu, Uthman bin Affan, kushika nafasi ya Ukhalifa. Mwnachuoni maarufu wa madhehebu ya Shi’a, al-Hasan bin Musa al Nawbakhti (alikufa 313 A.H) ameandika kwenye kitabu chake Firaq as-Shi’a, “Shi’a ni kundi la Ali bin Abi Talib. Waliitwa Shi’a wa Ali wakati na baada ya uhai wa Mtume na wanajulikana kama wafuasi wa Ali na waumini wa Uimamu wake.’2 Shaykh al-Mufid (alikufa 413 A.H), mmojawapo wa wanavyuoni mashuhuri sana wa siku za mwanzo wa Shi’a, ameeleza maana ya Shi’a kama watu wanaomfuata Ali na wanaamini kuwa yeye alikuwa ndiye mrithi wa Mtume mara tu baada ya kifo chake. 3 Akielekeza kwa nini Shi’a pia wanaitwa ‘Imamiyah’ anasema: “Hili ni jina la wale wanaoamini umuhimu wa Uimamu na mwenendo wake, katika vipindi vyote na kwamba kila Imamu lazima awe kwa dhahiri ameteuliwa, na lazima pia awe na kinga ya kutokutenda dhambi na aliye bora.’ 4 Hivyo, inasemekana kwamba Waislamu walioko kwenye madheheubu ya Shi’a ni wale ambao 1 Shahrestani, Juz.1, uk. 146.

2 Al-Nabakhti, uk. 17 3 Angalia al-Mufid, uk. 36. 4 Ibd, uk. 38.


wanazo itikadi zifuatazo kuhusu urithi kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w): 1. Urithi kwa Mtume ni cheo kitokanacho na Mungu. 2. Kwa kuwa Mtume aliteuliwa na Mungu, mrithi wake au Imamu pia lazima ateuliwe na Mungu na halafu adhihirishwe na Mtume. 3. Mrithi wa mara moja wa Mtume (s.a.w.w) baada yake alikuwa ni Ali (a.s).

Ushi’a Ulianza Lini? Bila shaka swali linajitokeza kwamba Ushia ulianza lini. Zipo Hadith nyingi ambazo zimesimuliwa na Shi’a na wale wasio Shi’a kuhusu suala la Uimamu ambalo litachunguzwa baadaye wakati wa kuzungumzia mafundisho ya Shi’a. Hata hivyo, kifuatacho ni kuchunguza tu baadhi ya Hadith ambamo Mtume Muhammad (s.a.w.w) alilisema kundi la watu fulani kama “Shi’a” (wafuasi) wa Ali na kisha akataja baadhi ya sababu za ziada kutoka kwenye Hadith na historia ya Uislamu ambazo zinaweza kurahisisha kueleweka zaidi somo linalozungumziwa. Hadith zote zilizotajwa hapo chini zimechukuliwa kutoka kwenye vyanzo vya Sunni vyenye kuheshimiwa. Hata hivyo, hizi ni chahe tu miongoni mwa simulizi ambazo ni muhimu, na zipo nyingi zaidi zinazo patikana kwenye vyanzo vilivyotajwa hapa pamoja na zingine: Bin Asakir (alikufa 571 A.H) alisimulia kutoka kwa Jabir bin Abdillah al-Ansar kwamba alisema: “Wakati moja tulikuwa na Mtume Muhammad, ambapo Ali aliwasili hapo, wakati huo Mtume alisema, ‘Ninaapa kwa jina lake ambaye uhai wangu uko mikononi mwake kwamba kwa kweli mtu huyu na Shi’a (wafuasi) wake watafurahi mnamo siku ya Ufufuo’ na halafu Aya isememayo; “Hakika walioamini na wakatenda mema, hao ndio bora wa viumbe’ iliteremshwa. Baadaye, wakati wote masahaba wa Mtume Muhammad walipomuona Ali anakuja walisema ‘Mbora katika watu amekuja.’ (Bin Asakir, Juz. 2, uk. 442 na al-Suyuti, Juz. 6, uk. 5890). Bin Hajar (alikufa 974) alisimulia kutoka kwa Bin Abbas kwamba wakati ilipoteremshwa aya ya (98:7), Mtume alimwambia Ali; “Hao ni wewe na Shi’a (wafuasi) wako. Wewe na Shi’a (wafuasi) wako mtakuja Siku ya Ufufuo mkiwa na furaha na mkimfurahisha Mungu na maadui wenu watakuja wakiwa wamekasirika na kukabwa shingo zao.”5 (Bin Hajar, sehemu ya 11, Sura 1, Aya ya 11). Bin al-Athir (alikufa 606) alisimulia kamba wakati anamwambia Ali, Mtume alisema: “Ewe Ali! Wewe na Shi’a (wafuasi) wako mtafika kwa Mungu mkiwa mnafurahishwa. Naye na nyinyi mtamfurahisha Yeye, na maadui wenu watafika Kwake wakiwa wamekasirika na watakabwa shingo zao.” Halafu Mtume akaonesha mfano itakavyokuwa kwa kuweka mkono wake kwenye shingo (Ibn al-Athir, Al-Nihayah, ingizo “qa-maha”) Zipo Hadith zingine ambamo Mtume Muhammad (s.a.w.w) alipomwambia Ali, alitumia usemi ‘Shi’a wetu.’ Hii inaafikiana na usemi wa hapo juu kwamba Shi’a ni wale wanao mfuata Ali, kufuatana na mafundisho ya Mtume (s.a.w.w) na si kwa sababu ya uamuzi wao wenyewe. Kwa mfano, Bin Asakir alisimulia kwamba Mtume (s.a.w.w) alisema; “Kwa kweli ipo chemchemu Peponi ambayo ni tamu kuzidi maji matamu katika maua, nyororo kuliko siagi, baridi kuzidi barafu, na hunukia vizuri kuliko manukato. Kwenye chemchemu hiyo upo udongo wa mfinyanzi (tinah) ambao kutokea humo sisi (Mimi na watu wa Nyumba yangu) tumeumbwa na Shia (wafuasi) wetu wametengenezwa kutoka kwenye udongo huo huo.” (Bin Asakir, Juz. 1, uk. 129, na 180). Bado zipo Hadith zingine ambamo Mtume alimwambia Ali, alitumia usemi: ‘Shi’a wa nasaba wako.’ Hii inathibitisha kwamba kile kilichodokezwa hapo juu, kwamba Shi’a ni wale wanaomfuata Ali kwa sababu wameamini taasisi ya Uimamu iliendelea kwa dhuria wa Ali na Fatimah kwamba waliteuliwa

5 Kwenye kitabu hicho hicho, Bin Hajar pia amesimulia kutoka kwa Umm Salamah kwamba siku moja mnamo muda wa usiku ambapo Mtume alikiwa Nyumbani kwa Umm Salamah, bint yake Fatimah alifika hapo akiwa amefuatana na Ali Halafu Mtume alisema: Ewe Ali! Wewe na masahaba wako mpo Peponi. Wewe na Shi'a (wafuasi) wako mpo Peponi."


na Mungu na kutambulishwa na Mtume. Mathalani, Zamakhshari (alikufa 528 A.H) kwenye maandishi yake ‘Rabi al-Abrar’ anataarifu kwamba Mtume (s.a.w.w) alisema: “Ewe Ali! Siku ya ufufuo itakapowadia, mimi nitamshikilia Mungu, wewe utanishikilia mimi, dhuria wako watakushikilia wewe na Shi’a (wafuasi) wao watawashikilia wao. Halafu utaona huko tutakopelekwa.”6 Inaonekana kwamba kwa mujibu wa Quran Utume ulirithiwa-Quran inasema: {26}

َ ‫ب‬ ‫سللبناَ بنوححاَ بوإكلببراَكهيِبم بوبجبعللبناَ كفيِ بذرريوتككهبماَ اَلننببووةب بواَللككبتاَ ب‬ ‫بولبقبلد أبلر ب‬

“Na bila shaka tulimtuma Nuhu na Ibrahim na tukaweka katika dhuriya zao Unabii na Kitabu” (57:26). Hii ina maana kwamba wale ambao walikuwa na sifa za kuteuliwa na Mungu kama mitume walijumuishwa kwenye dhuria zao. Kwa nyongeza ya Hadith zilizotajwa hapo juu na zile zinazofanana nazo, na zile Hadith zinazozungumzia Uimamu ambazo zitatajwa baadaye, zipo sababu zingine ambazo zinafanyiza kutokeza kwa kundi la watu kama Shi’a wakati wa uhai wa Mtume (s.a.w.w) kuwa ni jambo la kawaida sana, na hata kuwa la muhimu. Kwa mfano mwanzoni mwa Uislamu ambapo Mtume (s.a.w.w) alitakiwa na Mungu kuanza kuhubiri Uislamu hadharani kwa kuwaita ndugu zake wa karibu, aliwaalika ndugu zake kwenye karamu. Baada ya chakula Mtume (s.a.w.w) alisema kuhusu ujumbe wake na aliwalingania wageni waingie kwenye Uislamu na alisema kwamba yeyote miongoni mwao ambaye angeingia kwenye Uislamu na kumsaidia yeye angekuwa mrithi wake. Wote walinyamaza kimya. Mmoja tu ambaye alikubali mwito wa kumsaidia yeye ni Ali, ambaye alikuwa bado ni kijana mdogo wakati huo. Mtume alimsihi aketi chini na alirudia tena wito kwa mara ya pili na ya tatu. Tena na tena alikuwa ni Ali tu ndiye aliyeonesha kuwa tayari kumuunga mkono Mtume. Mtume (s.a.w.w) alikubali kutii kwa Ali utashi wa Mungu na akatekeleza amri ya kumteua yeye (Ali) kuwa mrithi wake. tukio hili limeandikwa kwenye vyanzo vingi.7 Kwenye usemi muhimu sana, Mtume alithibitisha wazi wazi kwamba Ali alikuwa mkweli na hakuwa na imani za uwongo na matendo mabaya, iwe katika mwenendo wake binafsi au matendo yake na maamuzi yake, na alithibitisha kwa kuwataka Waislamu wamfuate yeye. Umm Salamah alinukuliwa akisema kwamba, Mtume alisema: “Wakati wote Ali yu mkweli (al-haqq), na Quran na ukweli wakati wote viko na Ali, na hadi Siku ya Ufufuo havitatengana.” Hadith hii mahususi imesimuliwa na Bin Abbas, Abu Bakr, Aisha, Abu Said al-Khuddari, Abu Layla na Abu Ayyub al-Ansari pia.8 Pia Mtume amenukuliwa anasema; “Mungu na ambariki Ali. Mola wangu Mlezi ifanye kweli iwe naye kila mara.”9 Pia Mtume alitangaza katika nyakati kadhaa kwamba Ali alikuwa na ujuzi zaidi miongoni mwa watu wake katika mambo yanayohusu elimu ya Kiislamu. Kwa mfano, Mtume aliposema; “Hekima imegawanywa sehemu kumi; Sehemu tisa amepewa Ali na sehemu moja imegawanywa miongoni mwa watu waliosalia.”10 Baadaye Khalifa wa pili alithibitisha kwa mara nyingine misemo ya Mtume

6 Yamechukuliwa kutoka kwenye Subhani, Juz. 6, uk. 104. 7 Miongoni mwa vyanzo visivyo vya KiShi'a, mtu anaweza kurejea kwenye Tarikh al-Umam wa al-Muluk, mwandishi Tabari (alikufa 310 A.H) Juz. 3, uk. 62, 63; Al-Kamil fi al Tarikh mwandishi Bin al-Athir alikufa mwaka 630 A.H) Juz. 2, uk. 40, 41 na Musnad ya Ahmad b. Hanbali na Musnad al-asharali ya mwandishi alMubashsharin bin al-Jamah, Sakhr toleo na. 841. 8 Kwa mujibu wa Ghafari, uk. 10 Hadith hii imesimuliwa kupitia vyanzo 15 visivyo va KiShi'a, kama vile Mustadrak mwandishi al-Hakim al-Nishaburi, al-Sawaiq mwandishi bin Hajar, Kanzul -Ummal na Yanabi alMawaddah. 9 Angalia kwa mfano al-Tirmidhi, Kitab al-Manaqib, Sakhr toleo Na. 3647. 10 Al-Bidayah wa an-Nihayah mwandishi bin Kathir (alikufa 774 A.H), Juz. 7, uk. 359.


kwa kusema, “Mungu na asinitese kwa kunipambanisha na kazi ngumu ambapo Ali hayupo.” 11 Mtu pia lazima afikirie huduma kubwa na muhimu za manufaa na za kujitolea za Ali ili kuweza kutambua nafasi yake miongoni mwa Waislamu. Mathalani, wakati makafiri wa Makka walipopanga kumuua Mtume na Mungu akamtaarifu kuhusu njama zao, Mtume alimwambia Ali kama angekuwa tayari kulala kitandani pake ili wapagani wangedhani kwamba bado yupo nyumbani, ili aweze kuondoka Makkah Salama. Ali alikubali kazi hii, na wakati huo Aya ifuatayo iliteremshwa: {207}

‫ت و‬ ‫اك ِهَّلل‬ ‫س بملن يب ل‬ ‫سهب اَلبتكبغاَبء بملر ب‬ ‫شكريِ نبلف ب‬ ‫ضاَ ك‬ ‫بوكمبن اَلوناَ ك‬

“Na miongoni mwa watu ni hao wanaouza roho zao ili wapate radhi ya Mungu.”(Sura 2:207). Kuhama kwa Mtume kutoka Makkah kwenda Madina inaonesha mwanzo wa Kalenda ya Kiislamu. Ali alijitolea katika njia ya Uislamu kwa kupigana kwenye vita ya Badr, Uhud Khaybar, Khandaq na Hunain, ambamo alitoa mchango mkubwa. Yote haya yameandikwa kwenye vitabu vingi mno vya kihistoria na mkusanyiko wa Hadith zilizo simuliwa na wanavyuoni wasio Shi’a. Ilitajwa hapo mwanzoni, Hadith za Mtume kuhusu suala la Uimamu kwa ujumla na kuhusu hasa zaidi Ali, kwamba zitachunguzwa baadaye. Hata hivyo, ningependa kuhitimisha mazungumzo hapa kwa kurejea Hadith inayojulikana sana ya Ghadir Khum. Alipokuwa anarudi kutoka kwenye Hija yake ya mwisho Makkah, Mtume (s.a.w.w) aliwataka maelfu ya Waislamu waliokuwa pamoja naye kusimama njiani. Alisimama kwenye mimbari iliyotayarishwa kwa kutumia mito ya kukalia kwenye ngamia na akasema; “Yeyote anaye kubali kwamba mimi ni mawla wake, Ali sasa ni mawla wake.” Halafu watu waliokuwa hapo, akiwepo Khalifa wa kwanza na wa pili walisimama kutoa kiapo cha uaminifu kwa Ali na kumpongeza. Hadith hii imesimuliwa na zaidi ya vyanzo mia moja. Kwa orodha kamili ya vyanzo vya wasio Shi’a vya Hadith hii tazama Abaqat al-Anwar mwandishi Muz Hamid Kusayn al-Hindi (alikufa 1306 A.H) na Al-Ghadir mwandishi Abd al-Husayn al-Amini (alikufa 1390 A.H). Baada ya kuthibitisha ukweli wa Hadith hii, baadhi ya waandishi wa Sunni wametafsiri neno mawla lililotumika kwenye Hadith hii vinginevyo. Kufuatana na waonavyo wao, neno mawla limetumika hapa kumaanisha urafiki. Kama tafsiri hii itakubaliwa au hapana, hapana shaka kwamba Hadith hii na tukio vimempa Ali nafasi ya pekee na ya katikati miongoni mwa Masahaba wa Mtume. Hivyo, inaonesha kwamba seti tofauti za Hadith pamoja na uthibitisho wa kihstoria uliotajwa hapo juu zinaondoa shaka kwamba wakati wa uhai wa Mtume (s,a,w.w) Waislamu wengi walimpenda Ali sana na walitaka kuwa naye na walikuwa wamenuia kumfuata yeye baada ya Mtume (s.a.w.w) (kufariki). Watu hawa mara nyingi sana na kwa maana sana walijulikana kama Shi’a (wafuasi) wa Ali, hivyo kwamba pole pole neno ‘Shi’a’ peke yake likawa linalingana na Shi’a wa Ali. Muhimu zaidi ya hili ni ukweli kwamba fikira ya Uimamu wa Ali kwa hakika ilianza wakati wa uhai wa Mtume muhamad (s.a.w.w). Kifo cha Mtume (s.a.w.w) bila shaka kilileta jambo hili kwenye kitovu na kubainisha wale ambao bado walikuwa wanaamini umuhimu wa kumfuata Ali kutoka kwenye Waislamu wengine, ambao baada ya muda si mrefu, waliamini kuanzishwa kwa ukhalifa kama ndio urithi kwa Mtume katika kutawala jamii ya Kiislamu, na kwamba sio nafasi ya ki-Mungu. Akielezea matukio baada ya kifo cha Mtume Al-Masudi (alikufa 345 A.H) mwandishi mashuhuri wa historia wa madhehebu ya Sunni ameandika; “Kwa kweli Imamu Ali na wale ambao ni Shi’a wake ambao walikuwa naye walikaa ndani ya nyumba yake wakati huo ambapo kiapo cha utii kilikuwa kinatolewa kwa Abu Bakr.” 12 11 Angalia kwa mfano Al-Isabah fi Tamyiz as-Sahabah mwandishi bin Hajar, Juz. 2, uk. 509 na Al-Bidayah waal-Nihayah mwandishi bin Kathir, Juz. 7, uk. 36. 12 Ithbat al-Wasiyah, uk. 121


Baadaye matukio fulani kama vile vita vilivyotokea wakati wa ukhalifa wa Ali tukio la Karbala ambapo Husein Imamu wa tatu wa Shi’a na watu 72 wa familia yake na masahaba waliuawa, waliwafanya Shi’a wa Ali kutambulika zaidi na kubaini utambulisho wa Shi’a dhahiri zaidi. Mathalani tunaona kwenye mojawapo ya maandishi ya mwanzo kwamba Ali akiwalaani Talha na Zubair, alisema: “Kwa kweli wafuasi wa Talha na Zubair huko Basra waliwauwa Shi’a wangu na wawakilishi wangu.”13 Abu Mikhnaf (alikufa 158 A.H) anataarifu kwamba baada ya kifo cha Mu’awiyah, Shi’a walikusanyika nyumbani kwa Sulayman bin Surad na akawaambia; “Mu’awiyah amekufa na Husein amekataa kutoa Kiapo cha utii kwa Banu Umayya na ameondoka kuelekea Makkah na nyinyi ni Shi’a wake na Shi’a wa baba yake.” 14

Shia Wa Mwanzo Bila shaka madhehebu ya kiislamu ya Shia yalianzia Hijaz miongoni mwa masahaba wa Mtume. Rejea kwenye maandishi ya Kiislamu ya kihistoria na wasifu zinaonesha kwamba orodha ya Shi’a miongoni mwa masahaba wa Mtume (s.a.w.w) inajumuisha Bani Hashim maarufu wafuatao (kizazi cha Hashim babu wa babu wa Mtume Muhammad) Abdullah bin al-Abbas, al-Fadl bin al-Abbas, Ubaydullah bin al-Abbas, Qiththam bin al-Abbas, Abd al-Rahman bin al-Abbas, Tamim bin al Abbas, Aqil bin Abi Talib, Abu Sufyani bin al-Harith bin Abd al-Mutalib, Naufil bin al-Harith, Abdullah bin Jafar bin Abi Talib, Awn bin Jafar, Muhammad bin Jafar, Rabiat bin al-Harth bin Abd al-Mutalib, al-Tafayl bin al-Harith,al-Mughayrat bin Nawfil bin al-Harith, Abdullah bin al-Harith bin Abi Sufyani bin al-Abas bin Rabiat bin al-Harith, al-Abas bin Utbah bin Abi Lahab, Abd al-Mutalib bin Rabiat bin al-Harthi, Jafar bin Abi Sufyani bin al-Harth. Orodha ya Shi’a miongoni mwa masahaba hao wa Mtume ambao hawakuwa Bani Hashim inajumuisha; Salman, Miqdad, Abudhar, Ammar bin Yasir, Hudhayfah bin al-Yaman, Khuzaymah bin Thabit, Abu Ayyub al-Ansari, Abu al-Haytham Malik bin al-Tiham, ubayy bin Kab, Quys bin Sad bin Ubadah, Adiy bin hatam ubadah bin al-Samit, Bilal al-Habash, Abu rafi, Hashim bin Utbah, Uthman bin Hunayf, Sahl bin Hunayf, Hakim bin Jibilah al-Abdi, Khalid bin Said bin al-Aas, bin Husayb Aslami, Hind bin Abi Halah al-Tamimi Judah bin Hubayrah, Huyr bin Adiy al-Kindi, Amr bin alHama al-Khuzai, Jabir bin Abdullah al Ansari, Muhammad bin Abi Bakr (mtoto wa khlaifa wa kwanza) Aban bin Saidi bin al-Aas, Zayd bin Sauhan. 15

Sura Ya 2 :Vyanzo Vya Madhehebu Ya Shi’a. Kabla ya kuchunguza itikadi au ibada za Shi’a ni muhimu kujua vyanzo ambamo Shi’a hutegemea kwa ajili ya kuelewa Uislamu kutoka humo. Kinachofuata ni kwamba tutachunguza vyanzo vinne vya fikira ya Shi’a, kwa maneno mengine vyanzo vinne, ambamo humo kutokana na mtazamo wa Shi’a, uchunguzi wowote kuhusu Uislamu unategemea humo; Quran Tukufu, Sunna, akili na makubaliano ya wote pamoja.

Qur’an Tukufu

13 Waqat Seffin mwandishi Nass bin Muzalim (alikufa 212 A.H). 14 Maqtal al-Imam al-Husein, mwandishi Abu Mukhnaf, uk. 15.

15 Kwa mfano tazama Buhuth fi al-Milal wa al-Nihal mwandishi J. Subhani, Juz. 6, uk. 109 na 110. Sayyid Ali al-Madani (alikufa 1120 A.H) kwenye maandishi yake al-Dayat al-Rafiat fi Tabaqat al-Shi'a al-Imamiyah, anataja majina ya masahaba 69 wa Mtume ambao walikuwa Shi'a. Sayyid Abdi al-Husayn Sharafd al-Din (1377 A.H) kwenye maandishi yake Al-Fusul al Muhima fi Talif al-Ummah ametaja majina zaidi ya mia mbili ya masahaba wa Mtume Muhammad ambao walikuwa Shi'a katika mpangilio wa A-Z. Kuanzia na Abu Rafi na kuShi'a na Yazid bin Hautharah al-Ansari Yusuf bin Abdilah (aliokufa 456) kwenye Taarifa yake al-Istiab, bin al-Athir kwenye taarifa yake Usd al-Ghabah na Bin Hajar (alikufa 852 A.H) kwenya taarifa yake al-Isbah ni baadhi ya wanachuo wasio Shi'a ambao wametaja baadhi ya waanzilishi wa Shi'a.


Inajulikana kwamba Quran ni chanzo muhimu zaidi kwa Waislamu wote, pamoja na Shi’a. Pia Quran hufanya kazi kama chombo cha umoja miongoni mwa Waislamu. Bila kujali tofauti za kimadhehebu na asili zao za kimila, Waislamu wote hurejea kwenye kitabu hicho hicho kama mwongozo wa Mungu wa kutawala maisha yao. Kama ilivyo katika wakati wowote, leo hii katika ulimwengu wote wa Waislamu ipo Quran moja tu bila ongezeko au mabadiliko yoyote. Mtazamo hasa wa Shi’a kuhusu Quran unaweza kuonekana kwenye maandiko yafuatayo: “Tunaamini kwamba Quran ilikuwa mwongozo wa ki-Mungu na ilidhihirishwa na Mwenyezi Mungu kwa ulimi wa Mtume Wake mtukufu, ikieleza kila kitu wazi, muujiza wa daima milele. Mwanadamu hawezi kuandika kitu chocote kifananacho na kitabu hiki kwa sababu ya ufasaha wa lugha yake uwazi ukweli na ujuzi, na hakuna mabadiliko yanayoweza kufanywa humo. Quran tuliyonayo ni ile ile iliyoteremshwa kwa Mtume, na yeyote anayedai vinginevyo ama ni muovu, mpotoshaji au vinginevyo amekosea, na wote wamekengeuka kwa sababu ni maneno ya Mwenyezi Mungu, na; {42}

َ ‫بل يبألكتيِكه اَللبباَكطبل كملن ببليِكن يببدليكه بوبل كملن بخللفككه‬

“Hautakufikia, upotofu mbele yake au nyuma yake.” (41:42). ... Pia tunaamini kwamba lazima tuipatie heshima hadhi Quran Tukufu na yote hii katika matamshi na matendo, kwa hiyo, haitakiwi kabisa inajisiwe kwa makusudi, hata mojawapo ya herufi zake na isiguswe na mtu ambaye hana tohara! Imeandikwa kwenye Quran: {79}

‫سهب إكول اَللبم ب‬ ‫طوهبروبن‬ ‫بل يببم ن‬

“Hapana akigusaye ila walio tohara.” (56:79) (Muzaffar, uk. 26).

Shi’a Wanakataa Kuwepo Mabadiliko Yoyote Kwenye Qur’an Kama ilivyotamkwa hapo juu, Shi’a wanakataa kuwepo mabadiliko yoyote kwenye Quran na wanaamini kwamba Quran iliopo leo ni ile ile iliyoteremshwa kwa Mtume Muhamamd (s.a.w.w). Quran imekamilika. Hapana yeyote anbaye ameona nakala ya Quran tafauti na hii iliyo mhimili mahali popote katika dunia ya Kiislamu. Ipo miswada ya Quran leo ambayo inaonesha kuwepo tangu wakati wa Maimam wa Shi’a na hazitofautiani hata kidogo na zile za sasa. Quran Tukufu yenyewe inasema wazi kwamba Mungu mwenyewe huilinda Quran isibadilishwe na isiharibiwe. {9}

‫إكوناَ نبلحبن نبوزللبناَ اَلرذلكبر بوإكوناَ لبهب لببحاَفك ب‬ ‫ظوبن‬

“Hakika sisi ndio tulioteremsha ukumbusho huu na hakika sisi ndio wenyekuulinda. (15:9). 16 Kuhusu Aya hii, Allamah Tabatabai katika tafsir yake mashuhuri Al-Mizani fi Tasifri al-Quran, mmoja wa wafasiri wakubwa wa Quran Tukufu anasema: Quran ni ukumbusho ulio hai na utakuwepo daima milele ambao hautakufa kamwe na kuangukia kwenye kusahaulika. Inayo kinga ya kuzuia kuongezwa au kupunguzwa. Inayo kinga na imesalimika dhidi ya mabadiliko yoyote ya muumbo na mtindo ambayo yangeathiri unyoofu wake na wajibu wake, na hiyo ni kama Ukumbusho wa Mwenyezi Mungu unaodhihirisha ukweli wa kiungu na ujuzi. Kwa sababu hii, Aya 16 Lazima ifahamike kwamba dai la imani katika mabadiliko hukomea kwenye baadhi ya aya zinazodaiwa kufutwa, vinginevyo si shi’a wala Sunni hakuna aliyewahi kushutumiwa kuwa na imani ya kubadilika kwa Qur’an. Kwa hiyo mtu anaweza kkuhoji kutoka kwenye aya zozote za Qur’an kukanusha wazo la mabadiliko katika Qur’an.


iliyonukuliwa hapo juu inaonesha kwamba kitabu cha Mungu kila mara kimekuwa kinalindwa na kitaendelea kulindwa dhidi ya uharibifu wowote na mabadiliko yoyote.

Sunna Baada ya Quran Tukufu chanzo muhimu zaidi cha kuelewa Uislamu na kwa hiyo fikira ya Shi’a, ni Sunna ya Mtume Muhammad (s.a.w.w), pamoja na semi zake na matendo yake. Quran yenyewe inampa Mtume nafasi ya juu kiasi hicho, kama alivyotajwa, kwamba ndiye mwenye wajibu wa kuelezea Quran (16:44) na kufundisha Quran na hekima (62:2). Mtume ni mfano ulio bora kwa walio amini (33:21). Kamwe hasemi kufuatana na matamanio yake (53:3). Waislamu wanatakiwa kushikilia chochote anachowapa na kuacha chochote anachowakataza (59:7). Wakiwa wanajua Aya zilizotajwa hapo juu na Aya zingine nyingi kuhusu hadhi ya Mtume na huzingatia umuhimu wa kuwa Mtume wa Mungu aliyeteuliwa moja kwa moja na Mungu na akasemeshwa Naye, Shi’a pamoja na Waislamu wengine, waliendeleza hali ya mapenzi ya kweli ya kujitolea kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Watu Wa Nyumba Ya Mtume. Inaonesha hakuna kutokuelewana miongoni mwa Waislamu kuhusu uhalali wa kufuata mafundisho ya watu wa Nyumba ya Mtume katika kuelewa Uislamu, hususan kwa mujibu wa Sunni ambao huwaona masahaba wote wa Mtume kama vyanzo vya kuaminika katika kuelewa Uislamu. 17 Hapana shaka, basi, kwamba watu wa Nyumba ya Mtume ni wa kutegemewa na kuaminiwa katika kuwasilisha Uislamu. Ukweli huu unakuwa wazi zaidi wakati tunaporejea kwenye Hadith kutoka kwa Mtume kuhusu watu wa Nyumba yake, na kupima semi za wanachuoni wa Sunni kuhusu ujuzi wa Ali na watu wa Nyumba ya Mtume. Kwa mfano, Imamu Malik anasema; “Hapana macho ambayo yameona, hapana masikio ambayo yamesikia na hakuna ambacho kimekuja kwenye moyo wa mwanadamu yeyote bora zaidi ya Jafar bin Muhamamd katika ujuzi wake, ucha Mungu wake, kujinyima kwake anasa na utumwa wake kwa Mungu.” Bin Taymiyah anataarifu kuhusu jambo hili kutoka kwa Imamu Malik kwenye kitabu chake.18 Katika uchunguzi kuhusu watu hao waliosimulia kutoka kwa Imamu Sadiq (a.s), Shaykh al-Mufid (alikufa 413) kwenye taarifa yake iliyomo kwenye al-Irshad, anasema kwamba wale ambao walikuwa wanaaminika miongoni mwao kutoka kwenye madhehebu mbalimbali idadi yao ilifika 4000. Hivyo, hakuna utata hapa, na hii ndio maana wanachuo wengi wa Sunni kama vile marehemu Shaykh Shaltut wamaonesha wazi wazi kwamba kila Mwislamu anaruhusiwa kutekeleza ibada kwa mujibu wa mojawapo ya madhehebu tano za fiqh (sharia). Ja’far, Hanafi, Malik, Shafi’i na Hanbal, Sababu ipo wazi kwa sababu kama Imam Ja’far Sadiq au watu wengine wa Nyumba ya Mtume hawakuwa na ujuzi zaidi au njia bora zaidi ya kufikia kwenye elimu ya Mtume kuzidi wengine, basi mtu lazima akubali kwamba lazima angekuwa angalau sawa na wengine, hususan kama ambavyo amewafundisha wao, kama vile Abu Hanifa, Imamu wa Waisalmu wa madhehebu ya Hanafi ambaye alihudhuria mafunzo ya Imamu Sadiq kwa miaka miwili. Watu waliosoma au ambao wanatafuta ukweli wanatarajiwa, kwa hiyo, kupima vyanzo vyote vya Kiislamu vilivyopo na hapo kufikia hitimisho kuhusu njia ambazo Waislamu wanaweza kuishi maisha ya kuigwa. Kwa hakika chanzo kimoja ambacho ni hazina ni mafundisho ya watu wa Nyumba ya Mtume.

17 Waislamu wa Sunni huchukulia kwamba yeyote aliyekutana na Mtume na huku akiwa anamuamini, anachukuliwa kama sahaba wa Mtume na anaweza kutegemewa katika kujipatia elimu ya kuhusu Uislamu. Kwa hiyo, jamaa wa nyumba ya Mtume kama vile Ali na Fatima, ambao siku zote walikuwa na Mtume na wana uhusiano wa karibu wa kindugu na Mtume wanaweza kutegemewa bila kuhojiwa 18 Al-Tawassul wa al-Wasilah, uk. 52, toleo la kwanza


Sasa, na tuangalie kama ni muhimu kurejea kwenye Nyumba ya Mtume au hapana katika kuuelewa Uislamu. Katika kutoa jibu, mwelekeo wangu utakuwa kwenye baadhi ya Hadith za Mtume mwenyewe ambazo zimesimuliwa na wanahadith mashuhuri wa Sunni na zimekubaliwa na wasomi wa madhehebu zote mbili; Suni na Shi’a. Lakini kabla ya hilo lazima ifahamike kwamba mafundisho yote ya watu wa Nyumba ya Mtume kila mara yalitegemezwa kwenye Quran Tukufu na Sunna ya Mtume (s.a.w.w). Hapana mtu ambaye angefikiria kwamba, kwa mfano Imam Sadiq (s.a) alikuwa anasema jambo kuhusu Uislamu kufuatana na fikra zake binafsi. Lolote walilosema lilikwa ni kama vile walivyopokea kutoka kwa Mtume (s.a.w.w). Zipo Hadith nyingi kuhusu suala hili. Mathalani kwenye Usul al-Kafi tunaona kwamba Imamu Sadiq alisema kwamba chochote alichosema ni kile alichopokea kupitia kwa wahenga wake kutoka kwa Mtume (s.a.w.w). Mojawapo ya Hadith hizi ni ile Hadith maarufu ya Thaqalayn. Hadith hii ilitamkwa na Mtume katika nyakati mbali mbali, pamoja na siku ya Arafah wakati wa Hija yake ya Mwisho na tarehe 18 ya mwezi wa Dhul-Hijjah hapo Ghadir Khum. Licha ya tofauti ndogo ndogo katika maneno lakini kiini cha jambo kinabakia hicho hicho katika matokeo yote ya Hadith. Mathalan kwenye toleo moja la Hadith hii Mtume alisema; “Enyi watu! Ninawaachieni vitu viwili miongoni mwenu; Kitabu cha Mungu na watu wa Nyumba yangu. Kama mkishikamana navyo hamtapotea.”

Au katika Hadith nyingine Mtume alisema: “Ninawaachieni vitu viwili vya thamani miongoni mwenu, ambavyo kama mkivishikilia hamtapotea baada yangu; Kitabu cha Mwenyezi Mungu ambacho ni kama kamba iliyonyooka kati ya mbingu na ardhi, na watu wa Nyumba yangu. Vitu hivi viwili havitaachana hadi vitakapo nijia karibu ya Haudhi Siku ya Hukumu. Angalieni na mtahadhari jinsi mtakavyo vizingatia baada yangu.”

Hii inaonesha kwamba Mtume alikuwa na wasi wasi kuhusu jinsi Waislamu au baadhi yao, wangeichukulia Quran na watu wa Nyumba yake. Kwenye Hadith nyingine amesema: “Ninawaacha warithi wawili; kwanza Kitabu cha Mungu ambacho kipo kama kamba iliyonyoka baina ya mbingu na ardhi na pili watu wa Nyumba yangu. Vitu hivi havitaachana hadi vitakapo kuja kwangu karibu na Haudhi ya Kawthar.”

Hadith hizo hapo juu zinapatikana kwenye vyanzo vikuu vya Sunni, kama vile (Sahih Muslim Juz. 8, uk. 25, na 2408) Musnad Mwandishi Imamu Ahmad (Juz 3, uk. 388 na 10720) Sunnan mwandishi Darimi Juz. 2, uk. 432) na Sahih Mwandish Tirmidh Juz. 5, uk. 6432 na 3788. Pia zimetajwa kwenye vitabu kama Usd al –Ghabah mwandishi Bin Athir Juz. 2, uk. 13, Al-Sunnan al-Kubra mwandishi Bayhaqi Juz. 2, uk. 198. na Kanzul al-Ummal Juz. 1, uk. 44. Sasa na tutafakari kuhusu yale yaliomo kwenye Hadith, yaani ukweli kwamba Mtume ameacha miongoni mwa Waislamu vitu viwili vizito; Quran na watu wa Nyumba yake, na kwamba almradi watu wanashikilia vitu hivi viwili, hawata kengeuka. Hii inaonesha kwamba vitu hivi viwili lazima kila mara viwe katika mlingano, na kwamba kamwe havitahitilafiana. Vinginevyo, Mtume hangetoa maelekezo ya kuvifuata vyote viwili. Aidha, watu wangekanganyikiwa kuhusu wafanye nini kama watu wa Nyumba ya Mtume wangewaambia waelekee upande mmoja na Kitabu cha Mungu kinasema waelekee upande mwingine. Pamoja na kwamba ukweli huu umeeleweka kwa uthabiti tangu mwanzo wa Hadith, Mtume mwenyewe baadaye alithibitisha kwa ukamilifu ukweli huu kwa kusema; “Vitu hivi havitaachana hadi vije kwangu karibu na Haudhi ya Kawthar.” Hivyo Hadith hii katika matoleo yote inaonesha kwamba; 

Tangu wakati wa Mtume hadi mwisho wa dunia, Kitabu cha Mungu na watu wa Nyumba ya Mtume wakati wote vitakuwa pamoja.


Hapana mtu anayeweza kusema kwamba Kitabu cha Mungu kinatosha na kwamba hatuhitaji watu wa Nyumba ya Mtume, au kinyume chake, kwani Mtume alisema wazi; Ninaacha vitu viwili vya thamani ambavyo lazima mvishikilie na kama mkifanya hivyo hamtapotea.

Watu wa Nyumba ya Mtume kamwe hawangefanya kosa na kila mara wao ni wa kweli.

Ni jambo la kuvutia pia kwamba kwa mujibu wa Hadithi hii watu wa Nyumba ya Mtume, kama ilivyo Quran yenyewe, inaeleweka kuwa inaendelea, itaendelea hadi Siku ya Hukumu na Pepo. Hivyo, watu wa Nyumba ya Mtume kamwe hawatatoweka, hata kwa kipindi kifupi.

Hadith nyingine ni ile ya Safinah (jahazi). Waislamu wote wamesimulia kwamba Mtume (s.a.w.w) alisema: “Chungeni kwamba kwa hakika mfano wa watu wa Nyumba yangu miongoni mwenu ni sawa na mfuno wa Safinah ya Nuhu. Yeyote aliyepanda safinah ya Nuhu aliokolewa na yeyote aliyekataa kuingia kwenye Safina ya Nuhu alikufa maji.”

Hadith ya Safinah kwenye matoleo yake mbali mbali inasisitiza ukweli huo huo na inaonekana kwenye vitabu mbali mbali vya Sunni. Kwa mfano, inaweza kuonekana kwenye Mustadrak mwandishi Hakim Nishapuri, Juz. 3, uk. 149 na 151, Arbaun Hadiuth mwandishi Nabahani, al-Sawaiq al-Muhriqah mwandishi Bin Hajar miongoni mwa vyanzo vingine. Hivyo kwa mujibu wa seti hizi za Hadith matakwa ya mwongozo wa watu wa Nyumba ya Mtume ni ya muhimu mkubwa sana. Yafaa ifahamike; Hadith ya Thaqalayn imetajwa kwenye vyanzo vya pande zote mbili, Sunni na Shi’a, kwa hiyo, ni jambo la makubaliano miongoini mwa Waislamu wote. Hata hivyo, lipo toleo moja la Hadith ambamo Mtume amenukuliwa akisema: “Sunna zangu’ badala ya ‘watu wa Nyumba yangu’. Licha ya kwamba toleo hili linaweza kupatikana kwenye baadhi ya vyanzo vya Suni tu, si vigumu kuelewa Hadith hii ina maana gani, alimradi toleo hili pia nalo linaweza kuhakikishwa. Kwenye Hadithi nyingi zilizosimuliwa na Waislamu wote, Mtume amesema: “Ninaacha vitu viwili vya thamani, na vitu hivyo ni Quran Tukufu na watu wa Nyumba yangu.” Na kwenye Hadith chache zilizosimuliwa na kundi pekee la Waislamu, amesema; “Qurani Tukufu na Sunna zangu.” Ni dhahiri kwamba matoleo yangelikuwa kwa vile upande mmoja wa mlingano uko sawa sawa, yaani Quran, upande moja lazima ufanane. Kwa hiyo, ‘Sunna zangu’ na watu wa Nyumba yangu’ pia lazima ufanane; vinginevyo mtu anaweza kusema kwamba hakuna ulinganifu katika yale aliyoyasema Mtume. Hivyo, kitendo cha kukimbilia mafundisho na ushauri wa watu wa Nyumba ya Mtume ni kitendo hicho hicho cha kukimbilia kwenye Sunna za Mtume. Hivyo, njia moja tu ya kutufikisha kwenye Sunna ilikuwa na inaendelea kuwa kurejea kwa watu hawa ambao wamekuwa na uhusiano wa karibu sana na Mtume na ambao walijua vizuri zaidi kuliko mwingine yeyote yale aliyosema au aliyofanya au aliyoyathibitisha.

Ni Nani (Ahlul Bayt) Watu Wa Nyumba Ya Mtume? Suala lingine linahusu maana sahihi ya ‘watu wa Nyumba ya Mtume’ Kufuatana na Hadith nyingi tunaambiwa kurejea kwa watu wa Nyumba ya Mtume; “Ahlul Bait’ au ‘Itrah’. Maneno haya yana maana gani? Hapana shaka kuhusu hadhi ya watu wa Nyumba ya Mtume katika Uislamu, lakini inawezekana kuwepo na haja ya kuchunguza kumbu kumbu ya neno hili kuona inajumuisha yeyote ambaye alikuwa ndugu yake Mtume au hapana. Naam, hapana shaka miongoni mwa Waislamu kwamba hakika Fatima, bint yake Mtume (s.a.w.w), Imamu Ali na watoto wao Imamu Hasan na Imamu Husein ni watu wa Nyumba ya Mtume. tatizo moja tu ni kwamba ndugu wengine wa Mtume, wamejumuishwa au hapana, na kama ndio, kwa kiasi gani.


Waislamu wa Sunni wanaamini kwamba ndugu wote wa Mtume wamejumuishwa. Kwa hakika, wanawatenga wale ambao hawakuingia kwenye Uislamu, kama vile Abu Lahab, mmojawapo wa ami zake Mtume (s.a.w.w), na wakati huo huo alikuwa mmojawapo wa maadui zake aliyekuwa anamchukia sana, ambaye amelaaniwa kwenye Quran. Waislamu wa Shi’a wanaamini kwamba Ahlul Bait ni wale ambao wana viwango vinavyo stahili vya imani na ujuzi, jambo ambalo limewezesha wao kutajwa pamoja na Quran kwenye Hadith ya Thaqalain na zingine. Aidha, wanaamini kwamba Mtume mwenyewe amewatambulisha wazi wazi. Katika yanayofuata, nitataja baadhi ya Hadith zilizosimuliwa na vyanzo vikuu vya Sunni: Muslim anasimulia kutoka kwa Aisha, Umm al-Muminin: Mtume alitoka akiwa amevaa joho jeusi la sufi, ambapo Hasan mtoto wa Ali alikuja kwake, hivyo Mtume alimruhusu Hasan aingie kwenye joho lake. Halafu Husein alikuja naye pia aliingia. Halafu Fatima naye alikuja, Ali naye pia aliingia kwenye joho, hivyo kwamba joho lilimfunika Mtume, Ali, Fatima, Hasan na Husein. Halafu Mtume alikariri aya ya Quran ifuatayo: {33}

‫إكنوبماَ يبكريبد و‬ َ‫ت بويبطبرهبربكلم تبلطكهيِحرا‬ ‫ب بعلنبكبم اَلررلج ب‬ ‫اب لكيِبلذكه ب‬ ‫س أبلهبل اَللببليِ ك‬

“Hakika Mwenyezi Mungu anataka kuwaondoleeni uchafu enyi watu wa Nyumba ya Mtume, na kukusafisheni barabara.” (33:33)19 Muslim alisimulia kutoka kwa Sad bin Abi Waqqas kwamba aliulizwa na Mu’awiyah kwa nini alikataa kumtukama Ali kwa mdomo. Sad alijibu: “Nina kumbuka semi tatu za Mtume kuhusu Ali ambazo zilisababisha mimi nisiseme kitu chochote kibaya kuhusu yeye. Kama mimi ningekuwa na hata sifa moja tu miongoni mwa sifa hizi ingekuwa bora zaidi kwangu kuliko ngamia wekundu. 20 Usemi huu wa kwanza ilikuwa hapo Mtume alipotaka kuondoka kwenda kwenye vita vya Tabuk, alimwacha Ali Madina. Ali alihuzunika sana kwa kutokuwa na bahati njema ya kujumuika kwanye jeshi na kupigana kwa ajili ya Mungu. Alikwenda kwa Mtume alisema: “Mnaniacha mimi na watoto na wanawake?” Mtume akajibu: Huoni furaha kuwa na mimi kama Haruni alivyokuwa kwa Musa isipokuwa hapatakuwepo na Mtume baada yangu? Usemi wa pili, nilisikia kutoka kwa Mtume siku tuliposhinda vita vya Khaybar; alisema: “Hakika nitampa bendera ya Uislamu mtu ambaye humpenda Mungu na Mjumbe Wake na yeye anapendwa na Mungu na Mjumbe Wake.” Tulikuwa na matumanini ya kupewa bandera, lakini Mtume alisema; “Mwiteni Ali aje kwangu! Ali alikuja wakati anaumwa macho. Mtume alimpa yeye bendera na kwa uwezo wake Mungu alitupatia ushindi. Usemi wa tatu ni pale ambapo Aya ya Mubahalah ilipoteremshwa, Mtume alimwita Ali, Fatima, Hasan na Husein na alisema: “Mola wangu Mlezi! Hawa ni watu wa Nyumba yangu.” 21 Imamu Ahmad bin Hanbal amesimulia kutoka kwa Anas bin Malik kwamba wakati Aya ya Tatihir (33:33) ilipoteremshwa, kwa kipindi cha miezi sita Mtume alikuwa na kawaida ya kwenda Nyumbani kwa Ali na Fatima kila siku asubuhi wakati anakwenda msikitini kwa Sala ya Alfajiri na kusema; “Swala, Enyi watu wa Nyumba.”22 Pia zipo Hadith kuhusu maana ya Qurba (watu wa karibu) ambayo imetajwa mara kadhaa kwenye Quran. Kwa mfano, kwa mujibu wa Qurani Mtume (s.a.w.w) hakuomba malipo yoyote kama ujira wa kuwafundisha watu. Yeye alitaka tu watu wawapenda watu wa karibu yake kwa faida yao. Kwa hiyo, ni nani hawa watu wa karibu? Zamakhshari, mwanachuo na mufasir mashuhuri wa Quran wa Sunni, anasema kwamba Aya hii ilipoteremshwa, Mtume aliulizwa ni nani hao walio maanishawa na aya hii, na ambao wanatakwia waheshimiwe na watu wote. Mtume alijibu: Ali, Fatima, Hasan na Husein.” 23

19 Sahih Muslim, Juz. 4, uk. 1883, na. 2424. (Kitab Fadhail al-Sahabah, Bab Fadhail Ahlul Bayt, Sakhr Na. 4450) 20 Ngamia wekundu walikuwa wanachukuliwa kama wenye thanmani sana zama hizo. 21 Sahih Muslim, Juz. 4, uk. 1871, Na. 2408 (Kitab Fadhail al-Sahaba, Sakhr na. 4420)

22 Musnad mwandishi Imamu Ahmad bin Hanbal, Na. ya kimataifa 13231.Pia angalia Sunnan, mwandishi alTirmihi, na./ ya kimataifa 3130. 23 Al Kashshaf mwandishi Zamakhshari Fasili ya Aya 42:23, Juz. 4, uk.220.


Akili Shi’a wanaamini kwamba akili ni chanzo cha ujuzi cha kutegemewa sana na kinacho ulinganifu kamili na wahyi. Kwa mujibu wa baadhi ya Hadith, Mungu anavyo vithibitisho viwili (hujjah) ambavyo kwavyo wanadamu wanaweza kuelewa utashi wake. Aina ya ndani ambayo ni akili (al-aql) na ya nje ambayo ni mitume. Wakati mwingine akili huitwa ‘mitume wa ndani’ na mitume huitwa ‘akili ya nje’. Ipo kanuni iliyoanzishwa miongoni mwa wanasheria wa Shi’a kwamba uamuzi wowote unaofanywa na akili ni sawa na ule ambao umefanywa na dini (Shar’) na kinyume chake. Pia inakubalika kwa pamoja kwamba mojawapo ya masharti ya wajibu wa kimaadili au kisheria ni kuwa na akili timamu. Kama mtu anao wazimu, hafikiriwi kuwajibika kwa yale anayoyatenda. Yale yanayo tarajiwa kutoka kwa watu kwenye dini pia hutofautiana kufuatana na uwezo wa akili na busara. Wale watu ambao ni hodari sana na wenye akili wanatarajiwa kuwa waliotayarishwa zaidi, kuwa wacha Mungu zaidi na watiifu zaidi ya wale ambao si wataalam au wasio jua. Kwa mujibu wa Quran, Mungu huwataka binadamu wote kutumia uwezo wa busara na kutafakari ishara Zake na mawasiliano ya ulimwengu. Mara nyingi wasioamini hulaaniwa na kukosolewa kwa sababu ya kushindwa kwao kutumia akili au kutenda kufuatana na inavyohitajika busara. Kwa mfano, hulaaniwa kwa sababu ya kuiga mambo ya wahenga wao bila kutumia akili na zipo Aya nyingi zenye maswali yasiyohitaji majibu, ambayo huwataka watu kufikiria, kama: {68}

‫أبفببل يبلعقكبلوبن‬

“Basi je hawazingatii? (36:68),

َ ‫أبفببل يبتببدبوبروبن اَللقبلرآْبن‬ “Hebu hawazingatii hii Quran?” (4:82, 47:24),

‫ذ‬ ‫ت لكقبلومم يبلعقكبلوبن‬ ‫إكون كفيِ بذلكبك بلبياَ م‬ “Hakika katika hayo zipo ishara kwa watu wanaotia mambo akilini.” (13:4; 16:67, 30:28). Kwa jumla, akili huchangia kwenye mafundisho ya kidini katika maeneo matatu makuu: Mtu anatakiwa kuelewa ukweli wa dunia, kama vile kuwepo kwa Mungu, ukweli wa dini na mambo ya kisayansi. Eneo la pili ni kuanzisha kanuni za manufaa ya maadili na kanuni za sharia, kama vile ubaya wa ukandamizaji na uadilifu wa haki. Eneo la tatu ni kuweka viwango vya mfuatano wa mantiki ya akili na hitimisho. Huu ni wajibu wa aina tatu wa akili ambao unatambulika na kwa kweli unasisitizwa na Uislamu. Katika kuonesha tofauti wajibu wa ufunuo au maandiko matakatifu kwenye uchunguzi wa kidini unaweza kufupishwa ifuatavyo:   

Uthibitisho wa mambo ambayo tayari yanajulikana kiakili. Kuanzisha masomo mapya ambayo hayajulikani kiakili, kama maelezo ya kina kuhusu ufufuo na maelezo ya kina ya maadili na mifumo ya kisharia. Kutoa idhini kupitia mfumo wa kidini wa malipo na adhabu.

Mwishowe, ningependa kusema kwamba hakuna kitu kisicho na uwiano katika Uislamu. Naam hakika, mtu lazima abainishe kati ya hakika na hukumu za wazi za kimantiki, na kukisia kwa mtu au maoni binafsi. Kama kuna kesi ambayo inaonekana kwamba uamuzi wake wa kimantiki unagongana na misimamo fulani ya kidini, mtu lazima athibitishe kwamba, lazima kuwe na kosa angalau kwenye upande moja; ama haikuwa hukumu ya kweli ya akili au haikuwa sharia ya kidini.


Mungu kamwe hapotoshi watu kwa kuwaambia wafanye jambo kupitia kwa Mitume, na kinyume cha kitu kupitia akili yetu tuliyopewa na Mungu. Wakati wote pamekuwepo na baadhi ya hukumu ambazo zimehusishwa na akili na kuchukuliwa kama zinazopinga na misimamo ya dini, kwamba baada ya kufikiri kwa undani zaidi imethibitika kuwa kinyume cha kauli za wazi za mantiki.

Makubaliano Ya Wote Pamoja. Kimapokeo chanzo kimojawapo cha kuelewa Uislamu inafikiriwa kuwa makubaliano ya wote pamoja (ijma). Kwa mujibu wa utaratibu (methodolojia) wa/ya fikira ya Shi’a, makubaliano ya wote pamoja ya watu wote au kundi, kama vile wanavyuoni wenyewe hautoshi kama thibitisho (hujjah); kwa sababu mtu mmoja anaweza kukosea, watu wawili au watatu au hata maelfu au wote wanaweza kufanya hivyo. Hata hivyo, pale ambapo yapo makubaliano miongoni mwa Waislamu wote au wanavyuoni wa Waislamu katika njia ambapo hudhihirisha Sunna, inaweza kutumika kama uthibitisho, kama chombo cha kuweka wazi utashi wa Mungu. Kwa mfano, tunapoona kwamba kila Muislamu wakati wa uhai wa Mtume aliswali Swala yake kwa namna fulani, tunatambua kwamba Mtume aliwaelekeza wafanye hivyo; vinginevyo hapangekuwepo na kipengele cha kuunganisha kitendo chao. Haiwezekani kudhani kwamba wote walifanya hivyo, bila tahadhari na bila mwelekeo au kwamba wote walikosea na Mtume hakuwasahihisha. Hivyo, kwa upande wa Shi’a, makubaliano ya wote pamoja yenyewe si uthibitisho. Hufanya kazi tu yanapoelekeza kwenye kugundua Sunna. Kwa hiyo, kama Waislamu leo hii wanakubaliana kuhusu suala fulani, ambapo mwanachuoni anao wasiwasi kuhusu hukumu ya Kiislamu kuhusu suala hilo, kiutaratibu hawezi kusema kwamba; kwa sababu kila mtu anasema hivyo, na mimi pia ninasema hivyo. Pamekuwepo na masuala mengi katika historia ambapo wanaadamu wote waliamini kwa njia moja na baadaye waliona kwamba walikosea, kwa mfano, ardhi kuwa bapa. Ni Quran tu na Sunna ambazo ukweli wao haupingiki na zinazo kinga ya kukosea au kufikiria visivyo. Msimamo huu huridhia aina ya nguvu kwa fikira ya Shi’a, ili kwamba kila kizazi cha wanavyuoni na hata msomi yeyote anaweza na kwa kweli anahitajika kurejea moja kwa moja kwenye Quran na Sunna na kuendesha mtindo wa kwanza wake mweyewe wa ijtihad, yaani uchunguzi na hukumu ya kujitegemea. “Ijitihad’ kamwe haijapigwa marufuku katika ulimwengu wa Shi’a. Shi’a wanaamini maoni ya kwamba, hakuna mwanavyuoni, hata angekuwa na cheo cha juu cha kiwango chochote, (kwamba) anayo kinga ya kutokuhojiwa kisayansi au kupewa changamoto. Naam hakika, kama ilivyo katika somo lingine lolote, kila mwanachuoni wa dini anahitaji kutafuta maoni na kupima kwa uangalifu kazi za wenzake waliopita.

Sura Ya Tatu: Itikadi Katika historia ya Uislamu, Waislamu licha ya tofauti zao, wamekuwa na makubaliano makubwa, si tu kwenye kanuni nyingi za Uislamu, lakini pia katika nyingi ya ibada zake. Quran na shakhisia kubwa ya Mtume kwa upande moja, na upendo wa kweli na mapenzi ya Waislamu wote kwavyo, vimewaunganisha Waislamu na kutokana humo wamefanyiza taifa la kweli ambalo lina utambulisho wake, urithi wake, madhumuni na malengo na hatma yake. Chuki ya maadui wa Uislamu, ambao kila mara wamekuwa wanajaribu kuung’oa Uislamu kabisa, pamoja na changamoto za zama hizi, pia ni mambo ambayo yamesaidia kuamsha na kuimarisha moyo wa mshikamano na udugu miongoni mwa Waislamu. Quran na wito wa kitume wa umoja na udugu umekuwa mwangi wa kila mara wa viongozi mashuhuri wa Kiislamu wa madhehebu tofauti ya Uislamu. Kuhusu imani, Waislamu wote wanashirikiana katika imani ya Mungu na Upweke Wake, katika mitume kwa ujumla na hususan ujumbe wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) ambao ni kufikisha ujumbe wa mwisho wa Mungu kwa wanadamu, pamoja na kila mtu kutendewa haki sawa mnamo Siku ya Hukumu. Hizi ni kanuni muhimu zaidi za msingikatika Uislamu ambazo zinakubaliwa na Waislamu wote.


Mtazamo wa nje kuhusu kiasi cha makubaliano baina ya Waislamu wa Shi’a na Sunni umeoneshwa kwenye maandiko yafuatayo: “Tangu Mapinduzi ya Iran kila mtu anajua kwamba Shi’a ni Waislamu, kama Suni wanaheshimu kiini cha imani ya Upweke wa Mungu, maandishi hayo hayo matakatifu ya Quran Mtume Muhammad huyu huyu, Imani ile ile kuhusu ufufuo inayofuatiwa na Hukumu ya Mwisho na wajibat za msingi hizo hizo, Swala, Kufunga, Kuhiji, Kutoa sadaka na Jihad (vita vitakatifu). Nukta hizi zinazofanana kwa wote ni muhimu zaidi kuliko tofauti zilizoko. Sasa hivi hakuna tena upinzani wa kinadharia kuhusu Shi’a kuswali Swala na Sunni, au kinyume chake, ingawa matatizo mengi yamekuwepo siku za nyuma na kiutekelezaji bado yapo.” (Richard, uk. 5; na ufupisho).

Katika haya yafuatayo, tutaendelea kueleza kwa mukhtasari kanuni za dini au masharti ya imani. Baadhi ya sifa bainifu ya itikadi za Shi’a zitafanyiwa uchunguzi hapo baadaye. 24

Kanuni Za Dini. Upweke Wa Mungu Imani ya Kiislamu imeundwa na tangazo la kweli mbili mambo mawili; yaani kwamba hapana mungu (yaani hapana yeyote anayestahiki kuabudiwa) isipokua Mungu (Mwenyezi Mungu) na kwamba Muhammad ni mjumbe Wake. (LA ILAHA ILLALLAH MUHAMADU RRASULULLAH). Waislamu wanaamini kwamba Mwenyezi Mungu ni Yeye Peke Yake. Hana mshirika au watoto. Yeye ni Mwanzo na Yeye ni Mwisho. Yeye ni Mwenye uwezo juu ya vyote, Yeye ni Mwenye ujuzi wote, Yeye Alikuwepo, Yupo na Ataendelea Kuwepo. Quran inasema kamba Yeye Yu karibu zaidi na mwanadamu kuliko mshipa wake wa shingo lakini haiwezekani kuonekana kwa macho au kutambuliwa na akili ya binadamu. Katika kuomba dua Imamu Ali anasema: “Ee Allah, hakika nakuomba Wewe kwa Jina lako, kwa jina la Allah, Mwingi wa Rehema Mwenye kurehemu, Ee Mwenye Ufalme wa milele, hapana mungu isipokuwa Wewe.”

Uadilifu Wa Mungu Miongoni mwa sifa za Mungu ambazo Shi’a wamesisitiza sana ni uadilifu. Naam hakika, Waislamu wote wanamini kwamba Mungu ni muadilifu (Aa‘dil); kwa kuwa Mungu kamwe hatendi udhalimu kwa waja wake, kamwe Hamkandamizi yeyote. Ukweli huu unadhihirishwa na Quran kwa wazi wazi kabisa:

‫بوأبون و‬ ‫س بكظبولمم لكللبعكبيِكد‬ ‫اب لبليِ ب‬ “... Na kwamba Mwenyezi Mungu si mwenye kuwadhulumu waja.” (3:182 na 8:51 na 22:10). {46}

‫بوبماَ برنببك بكظبولمم لكللبعكبيِكد‬

“...Wala Mola Wako Mlezi si mwenye kuwadhulumu waja.” (41:46) {40}

‫إكون و‬ َ ‫اب بل يبلظلكبم كملثبقاَبل بذورمة‬

“Hakika Mwenyezi Mungu hadhulumu hata chembe moja.” (4:40). {44}

‫إكون و‬ ‫سبهلم يبلظلكبموبن‬ ‫س ب‬ ‫س أبلنفب ب‬ ‫شليِحئاَ بو ذلبككون اَلوناَ ب‬ ‫اب بل يبلظلكبم اَلوناَ ب‬

24 Mojawapo ya vyanzo vikuu vya mazungumzo yafuatayo kuhusu kanuni na utekelezaji wa Uislamu ni 'An Introduction to Islamu kilichoandikwa na Bashir Rahim. Kwa toleo la mukhtasari wa ibara hii, tazama WWW.al.islam.org/begin/index/html.


“Hakika Mwenyezi Mungu hawadhulumu watu kitu chochote lakini watu wenyewe wanajidhulumu nafsi zao.” (10:44) Zaidi ya umuhimu wa haki ya Mungu yenyewe, sababu nyingine ya kusisitiza katika kanuni hii na Shi’a, ni kwamba Ashariyah, kundi la wanachuoni/wanatheolojia wa Sunni, wanaamini kwamba hakuna kiwango chenye upendeleo wowote kwa ajili ya matendo mema au maovu kimaadili. Mungu hufanya matendo mema au chochote kinachoamriwa na Mungu. Kwa hiyo chochote anachofanya Mungu au anachoamuru ni kitu kizuri na cha haki katika ufafanuzi Wake. Wanaamini kwamba kama Mungu angetutaka sisi tuseme uwongo, kusema uwongo lingekuwa tendo jema na kama Mungu angewapeleka wacha Mungu jahanamu hiyo ingekuwa haki. Hakika, wanaamini kwamba Mungu kamwe hafanyi matendo hayo,sio kwamba wenyewe wanakosea, bali kwa sababu kiutendaji Amesema kwamba matendo hayo ni makosa. Ashaira vile vile huamini kwamba mwanadamu hana utashi wake mwenyewe na kwamba ni Mungu ndiye ambaye huumba matendo yao bila ya wao kuwajibika na lolote ndani yake. Wao ni wapokeaji tu wa matendo ya Mungu. Shi’a na baadhi ya wanachuoni wa Sunni, kama vile Mu’tazila, wanaamini kwamba wema na uovu au haki na dhuluma ni vitendo vyenye kukusudiwa, na kwamba vipo vigezo vya wazi kwa ajili ya hukumu za mema na mabaya. Kwa maneno mengine, wanaamini kwenye asili ya wema na uovu. Wanaamini kwamba kwa kweli ipo tofauti baina ya, haki na uoevu na sio holela kwamba Mungu ametuamuru kuwa waadilifu na tusimkandamize yeyote hata maadui zetu. Pia wanaamini kwamba wanadamu wapo huru na wanawajibika na matendo yao. Kwa hakiaka, Mu’tazila wanaamini katika ‘Tafwid’ yaani, kwamba Mungu amewapa wanadamu mamlaka Yake juu ya matendo yao ya hiyari na wanao udhibiti kamili juu ya matendo yao. Lakini Shi’a wanaamini kwamba ingawa jabr (itikadi ya kwamba matukio yote, pamoja na matendo ya mwanadamu huamuliwa na sababu zinazo chukuliwa kama nje ya utshi ) kwamba ni kosa na kinyume cha uadilifu wa Mungu, na kwamba wanadamu wapo huru, uhuru na uwezo wao umewekewa mpaka, na Mungu anayo mamlaka yote juu ya matendo yao. Ukweli huu umetamkwa na Imamu Jafar al-Sadiq (a.s) kwenye maelezo yake: “Hakuna shurutisho (jabr) wala uwakilishi kamili wa uwezo (tawfid), bali msimamo halisi ni baina ya ncha mbili (yaani, jabr na tawfid).” Kwa ajili ya msingi muhimu wa somo hili kwa faida ya mfumo ya mfumo wowote, kila mara Shi’a wametia mkazo juu ya suala la uadilifu wa Mungu na mara kwa mara wameutambulisha pamoja na tawhid (Upweke wa Mungu), Utume, Uimamu (uongozi wa ki-Mungu) na ufufuo kama mojawapo ya kanuni tano za Imani (Usul al –madhhab) ikilinganishwa na tawhid, Utume na ufufuo, ambazo huhesabiwa kama kanuni tatu za Dini (Usul al-Din), ambazo Waislamu wote wanashiriki kuziamini. Msisitizo huu juu ya suala la uadilifu wa Mungu si tu kwamba lina mchango wake kwenye kipengele cha nadharia ya Ushi’a. Hakika, Shi’a wanaona suala la uadilifu kama kipengele cha msingi wa Uislamu kwamba kila mara wametoa wito wa utekelezaji wa kanuni ya uadilifu katika kiwango cha jamii pia. Mashirika ya Shi’a ambayo yameanzishwa kila mara yamekuwa yanatoa wito wa uadilifu.

Utume Mungu alimuumba mwanadamu kwa hekima na kwa madhumuni (51:56). Amempa mtu akili na utashi atafute njia yake kuelekea kwenye ukamilifu na furaha. Pia Ameiongezea akili ya mwanadamu ufunuo wa Mungu. Kwa busara Zake na uadilifu Hakumuacha mtu yeyote au sehemu yoyote ya dunia bila mwongozo; Amepeleka Mitume kwenye mataifa yote kuwaelekeza na kuwaongoza watu hao. (10:47 na 16:36). Mtume wa kwanza alikuwa Adamu (a.s) na wa mwisho alikuwa Muhammad (s.a.w.w), mwisho wa mitume (33: 40). Quran imetaja mitume ishirini na watano miongoni mwa mitume na nchi kwamba walikuwa wengi zaidi (40:78). Kupitia maelekezo ya Hadith, Waislamu wanaamini kwamba walikuwepo mitume


124,000. Miongoni mwa wale waliotajwa kwenye Qurani n: Adam, Idris, Nuhu, Hud, Saleh, Ibrahim, Ismail, Is’haq, Lut, Yaqub, Yusuf, Ayub, Musa, Harun, Yunus, Zakaria, Dawud, Suleiman, Yunus, Zakaria, Yahya, Issa na Muhammad. Miongoni mwao, Nuhu, Ibrahim, Musa, Isa na Muhammad walikuwa na ujumbe unaofanana na walileta kanuni mpya ya sharia. wanaitwa “Ulul al-Adhma” maana yake, wale wa maazimio makubwa. Mbali na Quran yenyewe, Quran inazungumzia vitabu vine : Kitabu cha Ibrahim (87:19); Zaburi ya Dawudi (4:163) na (17:55); Torati ya Musa (2:87, 3:3 & 4, 6:91 & 154) na Injili ya Issa (5:46). Mwislamu lazima aamini vitabu vyote vitakatifu (2:4 na 285) na mitume wote. Kama tutakavyoona baadaye, Shi’a pia wanaamini kwamba mitume wote wana kinga ya kutokutenda dhambi na hawakuwa na dhambi kabla na baada ya kupewa utume. Shi’a kama Waislamu wengine, wanampenda sana Mtume Muhammad (s.a.w.w). Wanaona kwamba Mtume Muhammad (s.a.w.w) ni kigezo kikamilifu na mategemeo yote kwa Mungu, elimu ya kina kuhusu Mungu, msingi wa upendo kwa Mungu, utiifu wa kweli kwa utashi wa Mungu, tabia tukufu zaidi, mapenzi na rehema kwa wanadamu wote. Haikuwa kwa bahati kwamba aliteuliwa na Mungu kufikisha ujumbe Wake wa mwisho na bora sana kwa wanadamu. Ili kuweza kupokea wahyi wa Mungu na kuitwa kwa jina na cheo cha mbingu inahitaji mtu kuwa na tabia bora sana, na zaidi ya hayo kuweza kupokea wahyi ulio kamili zaidi kwa kweli inahitaji mtu kuwa na tabia bora zaidi sana. Tabia na mwenendo binafsi wa Mtume ni sifa zilizochangia sana kuendelea kwa Uislamu. Alijulikana kuwa mnyofu, muaminifu na mcha Mungu tangu alipokuwa mtoto. Wakati wa utume wake, kila mara aliishi kwa kuzingatia kanuni zake na maadili yake. Wakati wa utulivu na matatizo, usalama na woga, amani na vita, ushindi na kushindwa, kila mara alionesha unyenyekevu, haki na kujiamini. Alikuwa mnyenyekevu mno hivyo kwamba kamwe hakujipenda, kamwe hakuhisi kuwa yeye ni bora kuliko wengine na kamwe hakuishi maisha ya anasa. Vipindi vyote viwili alipokuwa peke yake na bila uwezo, na alipotawala rasi ya Arabu na waislamu, walikuwa wanamfuata kwa moyo ni mmoja, hakubadili tabia. Aliishi maisha ya kawaida sana na wakati wote alikuwa na watu, hususan mafukara. Hakuwa na ikulu ya kifalme au baraza au walinzi. Alipoketi na masahaba wake hakuna mtu ambaye angebainisha kati yake na watu wengine kwa kigezo cha kiti chake au nguo. Ilikuwa maneno yake na msimamo wake wa kiroho tu ndizo sifa zilizomtofautisha na watu wengine. Alikuwa muadilifu sana hivyo kwamba kamwe hakudharau haki ya mtu yeyote hata kama walikuwa maadui zake. Maisha yake yalikuwa mfano wa maamrisho ya Quran:

‫ب‬ ‫بياَ أبنيبهاَ اَلوكذيبن آْبمبنواَ بكوبنواَ قبوواَكميِبن كولك ب‬ ‫سكط َ بوبل يبلجكربمنوبكلم ب‬ ‫شبهبداَبء كباَللقك ل‬ ‫شبنآَبن قبلومم بعلبذى أبول تبلعكدبلواَ َ اَلعكدبلواَ بهبو أبلقبر ب‬ ‫اب َ إكون و‬ ‫كللتولقبوذى َ بواَتوبقواَ و‬ {8}‫ن‬ ‫اب بخكبيِرر بكبماَ تبلعبمبلو ب‬ “Enyi mlioamini! Kuweni wasimamizi madhubuti kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mkitoa ushahidi kwa haki. Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu. Hivyo ndio kuwa karibu mno na ucha Mungu.” (5:8). Kabla ya vita kila mara alitoa maelezo kwa wapiganaji wake wasiwaumize wanawake, watoto, wazee na wale waliojisalimisha wenyewe, wasiharibu mashamba na bustani, wasiwafukuze wale waliotoroka kutoka kwenye uwanja wa vita, na kuwatendea wema mateka wao. Muda mfupi kabla ya kifo chake alitangaza Msikitini: “Yeyote anayenidai au sikumtimizia haki yake, tafadhali ajitokeze na adai haki yake.” Waislamu walipiga makelele, walikumbuka huduma zote ambazo Mtume aliwapa na matatizo ambayo alipata kwa ajili ya kuwaongoza wao. Walijua kwamba kamwe hakujipendelea kuhusu mahitaji yake na kamwe hakupenda kupumzika na kuwasumbua wengine. Kwa hiyo walisema maneno ya kutoa shukrani nyingi sana na heshima kwake. Lakini mtu mmoja alisimama na kusema; “Ninakudai kitu. Kabla ya moja wapo ya vita, wewe ulikuwa unawapanga wapiganaji kwenye msitari na fimbo yako ilinipiga. Sasa nataka kulipa kisasi.” Bila


kuuliza swali lolote Mtume alimwambia mmojawapo wa masahaba wake wa karibu kwenda Nyumbani kwake na kuleta fimbo hiyo hiyo na akamtaka mtu huyo kulipa kisasi na ampige lakini mtu huyo alisema; “lakini fimbo yako ilimpiga kwenye ngozi ya tumbo.” Kwa hivyo Mtume alifunua tumbo lake ili ampige ngozi yake, ambapo ghafla mtu huyo alibusu mwili wa Mtume. Labda, sababu yote ya kufanya hivi ilikua anatafuta fursa ya kumbusu kwa sababu ya mapenzi ya kumheshimu.

Uimamu Kama ilivyotamkwa mwanzoni, Shi’a wanaamini kwenye Imamah kama mwendelezo wa utume. Kwa Kiarabu neno “Imam” maana yake hasa ni ‘uongozi.’ Neno “Imam” katika matumizi ya kawaida ya kiistilahi anaweza kuwa mzuri au mbaya, na eneo la uongozi wake linaweza kuwa pana sana kama vile kuongoza taifa lote, au uongozi wenye mpaka kama vile kuongoza jamaa msikitini. Hata hivyo, katika imani ya Shi’a, Imamu katika maana yake finyu zaidi, ni mtu ambaye ni mfawidhi wa mambo yote ya kisiasa na kidini katika taifa la Kiislamu. Kwa usahihi zaidi, Imamu ni mtu ambaye ameteuliwa na Mungu na kutambulishwa na Mtume na halafu na kila Imamu aliyetangulia kwa uteuzi wa wazi (nass) kuongoza umma wa Waislamu, kufafanua na kulinda dini na sharia (Shari’ah), na kuongoza umma katika mambo yote. Imamu ni mwakilishi wa Mungu hapa duniani (Khalifat Allah) na mrithi wa Mtume. Lazima asiwe na dhambi na awe na elimu ya ki-Mungu ya dhahiri na ya ndani ya maana ya Quran.

Mtizamo Wa Sunni. Waislamu wa madhehebu ya Sunni hutumia neno Imamu kama lililo sawa sawa na neno ‘Khalifah’. Kwa Kiarabu neno ‘Khalifah’ maana yake ni mrithi. Neno hili limetumiwa kama cheo kwa yeyote aliyechukuwa mamlaka na kutawala nchi ya Kiislamu baada ya kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w). Khalifa anaweza kuchaguliwa, au kuteuliwa na aliyemtangulia, au kuchaguliwa na kamati, au anaweza hata kuchukua madaraka kwa kutumia nguvu za kijeshi. Khalifa si lazima awe hana dhambi. Wala hahitaji kuwa bora zaidi kuhusu sifa zake, kama vile imani na ujuzi. Shi’a Ithna-Sheria ambao ndio wengi katika Waislamu wa Shi’a wanaamini kwamba Mtume alirithiwa na Maimamu kumi na wawili.25 Hawa ni: 1. 2. 3. 4. 5. 6.

Imamu Ali bin Abi Talib26 - Alikufa Shahidi 40/659. Imamu Hasan bin Ali - Alikufa Shahidi 50/669. Imamu Husein bin Ali - Alikufa shahidi 61/680. Imamu Ali bin Husein - Alikufa shahidi 95/712. Imamu Muhammad bin Ali-Alikufa shahidi 114/732. Imamu Jafar bin Muhammad ª Alikufa shahidi 148/765.

7. Imamu Musa bin Jafar ª Alikufa shahidi 183/799 8. Imamu Ali bin Musa-Alikufa shahidi 203/817. 9. Imamu Muhammad bin Ali-Alikufa shahidi 220/835 25 Upo mlolongo wa Hadith ambamo Mtume (s.a.w.w) alisema kwamba pangetokeza viongozi kumi na wawili baada yake. Kwa mfano, Bukhari anataarifu kwamba Mtume (s.a.w.w) alisema; Watatokeza viongozi kumi na wawili (amiri) baada yangu. halafu msimuliaji anaendelea kusema kwamba Mtume alisema kitu ambacho hakusikia. Alimuuliza baba yake, ambaye naye alikuwepo wakati huo, amwambie Mtume alisema nini. Baba akasema kwamba Mtume alisema; "Viongozi wote hawa kumi na wawili watatokea kwenye kabila la Quraishi." Muslim pia ametaarifu Hadith hii kwa kusema kwamba msimulizi wa Hadith hii alikuwenda na baba yake mahali alipokuwa Mtume, na Mtume alisema; "Dini hii haitafika mwisho wake hadi watokeze makhalifa warithi kumi na wawili." Halafu msimuliaji anasema; Mtume alisema kitu ambacho sikuelewa na nikamuulizi baba yangu. Alisema ,'Mtume alisema; wote watatokea Quraishi.' " 26 Kama ambavyo tumeona humo kurasa za nyuma, Imamu Ali alikuwa binamu wa Mtume na mkwe wake (mume wa Fatima). Alikuwa mwanaume wa kwanza kukubali Uislamu.


10. Imamu Ali bin Muhammad-Alikufa shahidi 254/868/ 11. Imamu Hasan bin Ali ª Alikufa shahidi 260/872. 12. Imamu al-Mahdi-Alizaliwa 255/868. Imani ya kuja mkombozi inashirikisha dini nyingi sana (kama si zote). Katika Uislamu, fikira ya mkombozi imetambulishwa kwa makusudi katika mafundisho ya al-Mahd (Kiongozi) ambaye atatokeza akiwa na neema za Mungu na kujaza dunia haki baada ya kujazwa udhalimu na uonevu. Fikira ya mkombozi au mwisho mzuri wa dunia inaoneshwa kwenye aya nyingi za Quran na Hadith za Kiislamu. Kwa mfano, tunasoma kwenye Quran: {105}

‫صاَلكبحوبن‬ ‫يِ اَل و‬ ‫ض يبكرثببهاَ كعبباَكد ب‬ ‫بولبقبلد بكتبلببناَ كفيِ اَلوزببوكر كملن ببلعكد اَلرذلككر أبون اَللبلر ب‬

“Na hakika tulikwishaandika katika Zabur baada ya kumbukumbu, ya kwamba nchi watarithi waja wangu walio wema.” (21:105). {5}

‫ض بونبلجبعلببهلم أبئكومةح بونبلجبعلببهبم اَللبواَكركثيِبن‬ ‫ستب ل‬ ‫بونبكريبد أبلن نببمون بعبلى اَلوكذيبن اَ ل‬ ‫ضكعبفواَ كفيِ اَللبلر ك‬

“Na tukataka kuwafadhili waliodhoofishwa katika nchi hiyo na kuwafanya wawe waongozi na kuwafanya ni warithi.” (28:5). Ifuatayo ni baadhi tu ya mifano ya Hadith zinazozungumzia fikira hiyo hiyo ya mkombozi zilizosimuliwa na vyanzo vya pande zote mbili Suni na Shi’a: Mtume (s.a.w.w) alisema: “Hata kama muda wote wa kuwepo kwa dunia tayari umekwisha, na iwe imebaki siku moja tu (kabla ya Siku ya Hukumu) Mungu atairefusha siku hiyo kuendelea kwa muda mrefu ambao utaipatia nafasi ya ufalme wa mtu wa kutoka kwenye watu wa Nyumba yangu ambaye ataitwa jina langu.27 Pia Mtume alisema: “Al-Mahdi ni mmoja wetu, watu wa Nyumba yangu (Ahlul Bait). Mungu atatayarisha mambo yake katika muda wa usiku moja. Zaidi ya hayo, mtume alisema: “Al-Mahdi atakuwa wa familia yangu, wa dhuria ya Fatima.28 Pia imesimuliwa kutoka kwa Jabir bin Abdillah al-Ansari kwamba alisikia Mtume wa Mungu (s.a.w.w) anasema: “Kundi la taifa langu litapigana kwa ajili ya ukweli hadi karibu na Siku ya Hukumu ambapo Isa mwana wa Mariam, atashuka na kiongozi wao atamtaka aongoze Swala, lakini Isa atakataa, atasema: “Hapana, hakika miongoni mwenu Mungu ameweka viongozi kwa ajili ya wengine ili kuheshimu taifa hili”. 29 Hivyo, al-Mahdi atakuwa na ujumbe wa dunia nzima kuanzia Arabuni. Jina lake litakuwa sawa kama jina la Mtume Muhammad (s.a.w.w) na atatokea kwenye uzao wa Bibi Fatimah. Shi’a wanaamini kwamba ni mtoto mwanaume wa Imam Hasani al-Askari. Alizaliwa mwaka 255 A.H. Mnamo mwaka wa 260 A.H alikwenda mafichoni. Bado yu ngali hai, lakini analindwa na Mungu katika hali ya maficho hadi hapo matayarisho yatakapofanyika kwa ajili ya kujitokeza kwake. Imani hii hii wanayo baadhi ya wanachuoni wa Sunni, lakini wanachuoni wengine wa Sunni wanaamini kwamba bado hajazaliwa.

Sayyid Muhsin al-Amin kwenye maandishi yake Ayan al ªShi’ah ametaja mifano kumi na tatu ya wana chuo wa Suni ambao wamekubali kwamba al-Mahd ni mtoto wa Imamu Hasan na tayari alikwisha zaliwa kama vile Muhammad bin Yousufa al-Kanji al-Shafii kwenye taarifa yake al-Bayan 27 Sunnan cha Bin Majah, Kitab al-Fitah, Sakhr, Na. 4075 na Musnad cha Ahmad, Musnad al-Asharah al Mubashsharim bin al-Jannah Sakhr na. 610. 28 Sunan, cha Abu Dawudi, Kitab al-Mahdi, Sakhr Na. 3755. Tazama pia; Kitab al-Fitan, Sunan mwandishi bin Majar, Kitab al-Fitan, Sakhr na. 4076. 29 Sahih cha Muslim, Kitab al Iman, Sakhr, na. 225 na Musnad cha Ahmad, Baqi Musnad al-Mukthirin, Sakhr na. 14193 na 14595.


fi Akhbar Sahib al-Zaman na Kifayat al-Talib fi Manaqib Ali bin Abi Talib; Mus al-Bin Ali bin Muhammad al-Maliki kwenye taarifa yake al-Fusul al-Muhimuh fi Marifal al-Aimmah na Bin alJawzi kwenye maandishi yake maarufu Tadhikrat al-Khawass.

Ufufuo Dunia itafika mwisho mnamo Siku ya Ufufuo (Qiyama), Siku ya Hukumu. Watu wote watafufuliwa na kusimamishwa mbele ya Mungu Ambaye ataamua kuhusu hatma ya kila mtu binafsi kwa mujibu wa itikadi na matendo yao hapa duniani. Watu wema watapata thawabu na waovu wataad hibiwa (22:6-9 na 1-2; 3:185, 6:62) Mungu atawatendea watu haki lakini jambo litakalotawala katika kuendesha haki Yake litakuwa Huruma Yake (6:12).

Maelezo: Ingawa Waislamu wote wanaamini katika kanuni za Uislamu zilizotajwa hapo juu, ipo tofauti ndogo katika maelezo yao kuhusu imani na matendo ya ibada. Waislamu wa madhehebu ya Shi’a wanazielezea imani zilizotajwa hapo juu, kama kanuni au nguzo za dini (Usul ud-Din) na matendo ya ibada kufuata kama ibada au matawi ya dini (furu ud-Din). Sababu ya maelezo kama hayo, ni kwamba imani hizo ndio kipengele cha msingi wa dini na kigezo cha mtu kufikiriwa kuwa Mwislamu. Hata hivyo, matendo ya ibada yaliyoidhinishwa ni vidokezo vya mtu kuwa ni mwenye imani, kwani imani halisi hujionesha kwenye utekelezaji wa ibada. Waislamu wa Sunni kwa kawaida huwasilisha tamko la Uislamu (kalimah) lenye kushuhudia kwamba hapana mungu ila Mungu (Allah) na Muhammad ni Mjumbe Wake, pamoja na matendo manne ya ibada yani; Sala tano, kufunga Saumu, kwenda Hija (Makkah) na kutoa Zaka, kama nguzo tano za Imani. Wanafikiria matendo mengine ya ibada kama kuamurisha mema na kukataza mabaya, na jitihada kama matendo ya wajibu, lakini hayakujumuishwa kwenye Nguzo za Imani.

Sura Ya 4: Ibadah Matendo makuu ya lazima ya ibada yanayokubaliwa na Waislamu wote wa Sunni na Shi’a, ni haya yafuatayo:

Swala Za Kila Siku. Kila Muislamu tangu anapo balekhe huswali Swala tano kila siku. Ili mtu aweze kusali lazima kwanza ajitoharishe kwa kutawadha kwa jinsi ilivyoagizwa. Halafu mtu husimama na kuelekea Makkah na hutia nia ya kuswali Swala ya wakati huo ili aweze kumkaribia Mungu. Nia hii lazima iwepo wakati wote wa Swala. Kama mtu anasahau anachofanya mwanzoni mwa Swala au baadaye, au anaswali ili ajioneshe kwa watu au kwa sababu nyingine za kibinafsi, Swala yake haiswihi. Swala halisi kuanza pale ambapo mtu hutamka; Allahu Akbar (Mungu Mkubwa). Baada ya kutamka hivi ndipo huingia kwenye Swala ambamo huendelee hadi mwisho wa Swala yake. Kila Swala ina rakaa mbili hadi nne.30 Kila rakaa inayo yafuatayo: Kisomo cha Sura ya kwanza ya Quran Tukufu (Al-hamdu) ikifuatiwa na Sura nyingine kama Tawhid au Qadr.31 Kurukuu na kumsifu na kumtukuza Mungu katika hali hiyo, kufanya sijda mbili (sajdah) na kisha 30 Sala ya Alfajiri ambayo kusaliwa kati ya mapambazuko na mawio ya jua ina rakaa mbili, Swala ya Adhuhuri na Alasiri kila moja inazo rakaa nne, Swala ya Magharibi inayo raka tatu na Swala ya Ishai inayo rakaa nne. 31 Kwenye Sala ya rakaa tatu na nne, rakaa ya tatu na ya nne ina kiso mo cha sura ya kwanza ya Qur'an Tukufu au badala yake kisomo maalum cha dhikiri kiitwacho !al-tasbihat al-arbiah! na halafu hurukuu na kwenda sijda. Katika Swala hizi kukiri kwa upweke wa Mungu na utume wa Mtume Muhammad na kumuamkia yeye na watu wa Nyumba yake hufanyika katika rakaa ya pili na rakaa ya mwisho baada ya sijda mbili.


kumsifu na kumtukuza Mungu. Swala humalizika kwa kushuhudia kwamba Mungu ni Moja na hana mshirika, na Muhammad ni mtumishi na Mjumbe Wake, pamoja na kumtolea salamu juu yake yeye na watu wa Nyumba yake, na kumtakia amani mtume, watu wote wema na wote ambao wanasali. Swala ya kila siku ni muundo muhimu sana wa ibada na kumbu kumbu ya Mola Mlezi. Quran Tukufu inasema: {45}

‫اك أبلكبببر ِهَّلل بو و‬ ‫شاَكء بواَللبملنبككر ِهَّلل بولبكذلكبر و‬ ‫صنببعوبن‬ ‫صبلةب تبلنبهذى بعكن اَللفبلح ب‬ ‫اب يبلعلببم بماَ تب ل‬ ‫إكون اَل و‬

“Hakika Swala inazuilia mambo machafu na maovu. Na kwa yakini kumdhukuru Mwenyezi Mungu ndilo jambo kubwa kabisa. Na Mwenyezi Mungu anayajua mnayo yatenda. (29:45) .

Kufunga Saumu Ibada ya pili ni kufunga Saumu mwezi wa Ramadhani, mwezi wa tisa katika kalenda ya Kiislamu. Katika mwezi huu kila Mwislamu baleghe anaacha kula, kunywa na tendo la ndoa tangu mapambazuko hadi machweo. Kama lilivyo tendo lingine lolote la ibada, kufunga Saumu lazima itiliwe nia kamili, ni kwamba kufanywa kwa ajili ya Mungu tu na kuwa karibu Naye. Pamoja na ukaribu kwa Mungu na kupata starehe Yake, yapo manufaa mengine mengi yatokanayo na kufunga Saumu, kama vile kuimarisha dhamiri kuwakumbusha watu kuhusu neema za Mungu, kama vile chakula ambacho hufurahia kila siku ambacho huchukulia kama kitu cha kawaida, kumkumbusha njaa na kiu ya Siku ya Hukumu, kuwasaidia matajiri kuelewa yanayo wapata mafukara ili kuamsha hisia yao ya ukarimu na huruma, kudhoofisha ladha na matamanio ya ovyo, na kufanya uwiano wa kuelewa na hadhari ya kustawi kiroho. Kwa ujumla Quran inasema: {183}

‫ب بعبلى اَلوكذيبن كملن قبلبلكبكلم لببعلوبكلم تبتوبقوبن‬ ‫ب بعلبليِبكبم اَل ر‬ ‫صبيِاَبم بكبماَ بكتك ب‬ ‫بياَ أبنيبهاَ اَلوكذيبن آْبمبنواَ بكتك ب‬

“Enyi mlioamini! Mmefaradhishiwa kufunga, kama waliyofaradhishiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu” (2:183).

Kwenda Hija Makka. Kila Mwislamu aliyefikia baleghe na ana uwezo wa kifedha lazima aende Hija Makkah, angalau mara moja katika maisha yake katika mwezi wa Dhul-Hijjah, mwezi wa kumi na mbili katika kalenda ya Kiislamu. Makkah upo Msikiti muhimu sana kwa Waislamu wote duniani, unaoitwa Masjid al-Haram, ambapo ni sehemu takatifu ya Al-Ka’abah. Waislamu wote huelekeza nyuso zao na miili yao upande iliko Ka’abah wakati wanaposwali. Al-Ka’abah ni mjengo wa chumba ulio jengwa na Mtume Ibrahim na mwanae Islamil, kwenye misingi ambayo hapo mwanzo ilijengwa na Mtume Adamu. Hakika, kwa kiasi kikubwa, kwenda kuhiji Makkah ni kujenga upya pale mahali ambapo Mtume Ibrahim, mtetezi mkuu wa imani ya Mungu Mmoja alimopitia takriban miaka elfu nne (4,000) iliyopita. Baada ya safari ndefu, Ibrahim alipofika Makkah Mungu alimwambia atayarishe mahali pa watu kuhiji Makkah. Quran inasema;

‫شليِحئاَ بوطبرهلر ببليِتكبيِ كلل و‬ ‫سبجوكد‬ ‫بل تب ل‬ ‫شكرلك كبيِ ب‬ ‫طاَئككفيِبن بواَللبقاَئككميِبن بواَلنروككع اَل ن‬ {27} ‫ق‬ ‫س كباَللبحرج يبألبتوبك كربجاَحل بوبعلبذى بكرل ب‬ ‫بوأبرذلن كفيِ اَلوناَ ك‬ ‫ضاَكممر يبألكتيِبن كملن بكرل فبجج بعكميِ م‬ ‫ب‬ ‫ل‬ ‫سبم و‬ {28} ‫هلم‬ ‫لكيِب ل‬ ‫شبهبدواَ بمبناَفكبع لببهلم بويبذبكبرواَ اَ ل‬ ‫ت بعلبذى بماَ بربزقب ب‬ ‫اك كفيِ أوياَمم بملعبلوبماَ م‬ {26}

“Usinishirikishe na kitu chochote; na isafishe Nyumba yangu kwa ajili ya wanaoizunguka kwa kutufu, na wanaokaa hapo kwa ibada, wanaorukuu, na wanaosujudi. Na watangazie watu Hija, watakuja Kwa miguu na juu ya kila ngamia aliyekonda, wakija kutoka katika kila njia ya mbali. Ili washuhudie manufaa yao na walitaje jina la Mwenyezi Mungu katika siku maalum juu ya wanyama hao Aliowaruzuku.” (22:26-28).


‫س لبلوكذيِ بكببوكةب بمبباَبرحكاَ بوبهحدى لكللبعاَلبكميِبن‬ ‫إكون أبووبل ببليِ م‬ ‫ت بو ك‬ ‫ضبع كللوناَ ك‬ ‫ستب ب‬ ‫سكبيِحل َ بوبملن بكفببر‬ ‫ت ببيِربناَ ر‬ ‫كفيِكه آْبياَ ر‬ ‫ت بمكن اَ ل‬ ‫طاَبع إكلبليِكه ب‬ ‫س كحنج اَللببليِ ك‬ ‫ت بمبقاَبم إكلببراَكهيِبم َ بوبملن بدبخلبهب بكاَبن آْكمحناَ ِهَّلل بوكولك بعبلى اَلوناَ ك‬ ‫ب‬ ‫ب‬ ‫ل‬ ‫و‬ ‫ب‬ {97} ‫ن‬ ‫فإ كون اب غنكييِ بعكن اَلبعاَلكميِ ب‬ {96}

“Hakika Nyumba ya kwanza waliowekewa watu kwa ibada ni ile iliyoko Makkah iliyobarikiwa na yenye uwongofu kwa walimwengu wote. Ndani yake zipo Ishara zilizo wazi, sehemu ya kusimama ya Ibrahim, na mwenye kuingia humo anakuwa katika amani. Na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu imewajibikia watu wahiji kwenye Nyumba hiyo, kwa yule awezaye njia ya kwenda. Na atakayekanusha basi Mwenyezi Mungu si mhitaji kwa walimwengu.” (3:96-97). Hijja ya kwenda Makkah imejaa matukio yasiyosahaulika. Labda miongoni mwa hayo makubwa kuliko yote ni ukarimu, udugu, usawa na urahisi. Kila mwaka mamilioni ya Waislamu kutoka mabara mbali mbali huacha familia, nyumba zao, biashara zao na chochote wakipendacho na husafiri kuelekea Makkah, iliyoko jangwani. Kila mmoja wao anatakiwa awepo sehemu mbali mbali katika wakati uliowekwa wote wakiwa wamevaa vazi la aina moja na kutekeleza matendo ya aina moja. Matajiri na mafukara mfalme na mtu wa kawaida, msomi na asiye msomi wote wanatakiwa kusimama bega kwa abega na kuvaa vipande viwili vya nguo nyeupe. Hili ni jambo ambalo kila mtu angelipitia angalau mara moja katika maisha yake, na halafu ajaribu kutelekeza katika maisha yake ya kila siku.

Kutoa Zaka Kutoa sadaka ni jambo lililonasihiwa sana ndani ya Quran na Sunna na thawabu za vitendo vya sadaka ni kubwa. Licha ya kwamba kila kitu pamoja na fedha alizo nazo mtu ni mali ya Mungu, Quran inatambulisha kutoa sadaka sawa na kumkopesha Mungu: {11}

‫ض و‬ ‫ضاَكعفبهب لبهب بولبهب أبلجرر بككريرم‬ ‫بملن بذاَ اَلوكذيِ يبلقكر ب‬ ‫سحناَ فبيِب ب‬ ‫ضاَ بح ب‬ ‫اب قبلر ح‬

“Ni nani atakayemkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mwema, ili amrudishie maradufu, na apate malipo ya ukarimu.” (57:11). Zaidi ya kutoa sadaka za hiyari zimo aina fulani za sadaka ambazo ni wajibu kutoa. Kwa mfano aina moja ya sadaka ni Zaka, kodi ya utajiri ya asilimia ndogo (kwa kawaida ni 2.5%). Kutoa Zaka si kutoa zawadi kwa fukara lakini hususan hiyo ni haki yao ambayo inatakiwa kuangaliwa kwa makini: {19}

‫ساَئككل بواَللبملحبروكم‬ ‫بوكفيِ أبلمبواَلككهلم بح ي‬ ‫ق كلل و‬

“Na katika mali yao ipo haki ya mwenye kuomba na asiyeomba” (51:19). Pia Imamu Ali alisema: “Mungu Atukuzwe ameweka riziki ya yule anayeomba kwenye utajiri wa tajiri. Kwa hiyo, wakati wowote fukara anapoona njaa, ni kwa sababu watu fulani walio matajiri wamemnyima mgawo wake.32 Wale ambao rasilimali zao za idadi fulani za ngano, shayiri, tende, zabibu kavu, dhahabu, shaba, ngamia, ng’ombe na kondoo, huzidi kiasi fulani walipe Zaka kwa kila mwaka kwa fukara miongoni mwa ndugu zake, yatima, wanaoomba, msafiri na kadhalika. Zaka inaweza kutumiwa kwa chakula, hifadhi, elimu, afya, mayatima na huduma zingine za jamii.

Inafaa kuangalia kwamba Aya nyingi zimesema kuhusu kutoa Zaka inafuatia baada ya Swala za mtu na kama ishara ya imani na itikadi kwa Mungu. Kutoa Zaka ni kitendo cha ibada, kwa lazima 32 Makundi kadhaa ya watu yamesamehewa, kama vile wagonjwa au wale wanaosafiri.


kitekelezwe kwa ajili ya Mungu. Kwa hiyo, si tu kwamba inasaidia fukara na kuchangia kuanzisha haki ya jamii na maendeleo, lakini pia hutakasa roho ya watu wanaolipa kutoka kwenye ubakhiri na ulafi. Quran inasema: {103}

‫صبدقبةح تب ب‬ َ ‫صرل بعلبليِكهلم‬ ‫طرهبربهلم بوتببزركيِكهلم بكبهاَ بو ب‬ ‫بخلذ كملن أبلمبواَلككهلم ب‬

“Chukua sadaka katika mali zao, uwasafishe Na uwatakase kwazo, na waombee rehema.” (9:103).

Khums Waislamu wa madhehebu ya Shi’a wanaamini katika wajibu mwingine wa kodi iitwayo Khums. Kwa Kiarabu maana yake halisi ni moja ya tano. Ni kodi ya asilimia 20 kutoka kwenye faida inayopatikana kwa mwaka wa fedha wa mtu, hulipa asilimia ishirini (20%) ya pato baada ya kutoa matu mizi ya nyumbani na biashara.33 Wajibu wa kulipa Khums umetajwa kwenye Quran:

‫سكبيِكل إكلن بكلنتبلم‬ ‫بواَلعلببمواَ أبنوبماَ بغنكلمتبلم كملن ب‬ ‫ساَككيِكن بواَلبكن اَل و‬ ‫سهب بوكللور ب‬ ‫سوكل بولككذيِ اَللقبلرببذى بواَلليِببتاَبمذى بواَللبم ب‬ ‫شليِمء فبأ بون كولك بخبم ب‬ ‫آْبملنتبلم كباَولك بوبماَ أبلنبزللبناَ بعلبذى بعلبكدبناَ يبلوبم اَللفبلربقاَكن يبلوبم اَللتببقى اَللبجلمبعاَكن ِهَّلل بو و‬ {41} ‫ر‬ ‫اب بعلبذى بكرل ب‬ ‫شليِمء قبكدي ر‬ “Na jueni kwamba ngawira mnayopata basi Khums (sehemu moja katika tano) ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume, na jamaa na mayatima, na maskini na wasafiri, ikiwa nyinyi mnamuanini Mwenyezi Mungu na tuliyoyateremsha kwa mja wetu siku ya kipambanuo.” (8:41). Waislamu wa madhehebu ya Sunni kwa kawaida huamini kwamba Aya hii inazungumzia kuhusu kile wanachopata Waislamu baada ya kushinda vita na kufikiria hiyo kuwa aina fulani ya Zaka. Kwa mujibu wa maarifa ya sharia za Shi’a, nusu ya Khumus anapewa Imamu wa Kumi na mbili, kwa sasa anapewa Marjaa watu wengine wa Nyumba ya Mtume na mrithi wake, na nusu nyingine wanapewa uzao wa Mtume walio fukara, waitwao ‘Sayyids.’ Khumus lazima itumike chini ya uangalizi mamlaka ya kidini ya Shi’a (marji al-taqlid) marija, yaani mwanasheria mkuu ambaye hufuatilia masuala katika utekelezaji wake. Hii ni kuhakikisha kwamba inatumika katika njia ambayo Imamu Mahdi anaridhika nayo. Sehemu ya Imamu kwa kawaida hutumika kwenye seminari za Kiislamu na miradi mingine ya kielimu kama vile kuchapisha vitabu vifaavyo au kujenga Misikiti na mashule.

Jitihada Kwa Ajili Ya Mungu Kila Mwislamu anatakiwa kujitahidi kwa bidii ili ajaribu kwa ajili ya Mungu katika njia mbali mbali ili kuendeleza maisha ya mwanadamu kwa ujumla, na hasa zaidi maisha yake binafsi. Quran inasema: {61}

َ‫ستبلعبمبربكلم كفيِبها‬ ‫بهبو أبلن ب‬ ‫ض بواَ ل‬ ‫شأ ببكلم كمبن اَللبلر ك‬

“Yeye ndiye aliyekuumbeni katika ardhi na akakuwekeni humo.” (11:61). Kutokujali mabalaa ya binadamu au mtu kuwa mzembe katika maisha yake binafsi ni sifa inayo 33 Ipo mifano mingine iliyotajwa kwenye sharia za Shi'a ambamo Khums huwa wajibu. Yale yaliyosemwa hapo juu ndio yanayojulikana zaidi.


laaniwa. Kwa upande mwingine mtu anayefanya bidii kupata fedha ili azitumie kwa familia yake na kuendeleza hali ya misha yao anaonekana kama shujaa katika kujitahidi kwa ajili ya Mungu, mtu kama huyu ni mujahidi. Mfano mmoja maarufu na muhimu wa jitihada hii (jihadi) ni kulinda haki za binadamu, kama vile uwezo wa kujiamulia na kufanya uhuru, na maadili ya Kiislamu na kibinadamu kama vile haki, hadhi na ukamilifu wa taifa la Waislamu. Quran inasema: {61}

َ‫ستبلعبمبربكلم كفيِبها‬ ‫بهبو أبلن ب‬ ‫ض بواَ ل‬ ‫شأ ببكلم كمبن اَللبلر ك‬

“Wameruhusiwa kupigana wale wanaopigwa vita kwa sababu wamedhulumiwa, na kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuwasaidia wale ambao wametolewa majumbani mwao pasipo haki, kwa kuwa wanasema: Mola wetu Mlezi Mwenyezi Mungu …….” (22:39-40).

‫سكبيِكل و‬ ‫ساَكء بواَللكوللبداَكن اَلوكذيبن يببقوبلوبن بربوبناَ أبلخكرلجبناَ كملن ذبهكذكه‬ ‫ستب ل‬ ‫اك بواَللبم ل‬ ‫ضبعكفيِبن كمبن اَلرربجاَكل بواَلنر ب‬ ‫بوبماَ لببكلم بل تببقاَتكبلوبن كفيِ ب‬ ‫اَللقبلريبكة اَل و‬ {75} َ‫را‬ ‫صيِ ح‬ ‫ظاَلككم أبلهلببهاَ بواَلجبعلل لببناَ كملن لببدلنبك بولك يحيِاَ بواَلجبعلل لببناَ كملن لببدلنبك نب ك‬ “Na mna nini msipigane katika njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanaoonewa, wanaume na wanawake na watoto, ambao husema: “Mola Mlezi wetu tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhaalimu, na tuyaache tuwe na mlinzi anayetoka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anaye toka kwako.” (4:75). Kwa hakika, jihadi pia inajumuisha zaidi masuala ya kibinafsi ambayo familia ya mtu, rasilimali au sifa huwa katika hatari kuporwa au huharibiwa. Kwa mujibu wa Hadith za Kiislamu, mtu anayeuawa akiwa analinda familia yake au ardhi, anafikiriwa kuwa yu sawa na mpiganaji ambaye anakufa shahidi akiwa katika uwanja wa vita. Jihadi lazima iendelee hadi hapo ambapo njia ya haki inapatikana. Quran inasema: {193}

‫فبإ ككن اَلنتببهلواَ فببل بعلدبواَبن إكول بعبلى اَل و‬ ‫ظاَلككميِبن‬

“Piganeni dhidi ya wavamizi hadi hapo udhalimu utakapo komeshwa.” (2:193). Kwa hakika, katika kiwango kikubwa zaidi, jihadi ya kweli imekuwepo wakati wote, tangu mwanzo wa kuumbwa kwa binadamu, baina ya wema na uovu, ukweli na uwongo na kati ya kundi la Mungu na kundi la shetani. vita hii itaendelea takriban hadi mwisho wa muda ambapo Dunia itajazwa haki na mgawanyo usio na upendeleo wa mali yote kwenye serikali ya al-Mahdi. Jihadi, iwe ni kwa kalamu, ulimi, silaha au njia nyingine yoyote ile, ni kitendo cha ibada, na lazima kifanywe kwa nia safi, ni kwamba iwe kwa ajili ya Mungu tu na njia za haki. Hapana mtu anayeruhusiwa kupigana au kupambana kwa ajili ya anasa za kidunia, kwa ajili ya utukufu wa mtu binafsi au kuonea, kama vile kukalia ardhi ya watu wengine kimabavu na kuwa tajiri zaidi au uwezo wa mamlaka makubwa zaidi. Hakika, kwanza kabisa jihadi huanzia ndani ya nafsi ya mtu, yaani mujitahidi. (mtu anayejitahidi kupambana). Kuhakikisha kuwa mtu anaweza kushinda vita ya nje dhidi ya uovu, lazima kwanza mtu apigane dhidi ya matamanio yake mabaya na ashiki ya mwanamke, na kwanza aunasue moyo wake kutoka kwenye makazi ya shetani na apate tena hadhi na heshima ambayo Mungu Mweza wa Yote Amewapa wanadamu. Quran inasema:

‫س اَللبملطبمئكنوةب‬ ‫بياَ أبيوتببهاَ اَلنولف ب‬ {28} ‫ضيِ وةح‬ ‫ضيِبةح بملر ك‬ ‫اَلركجكعيِ إكلبذى بربركك براَ ك‬ {29} ِ‫عبباَكدي‬ ‫بفاَلدبخكليِ كفيِ ك‬ {30} ِ‫جن وكتي‬ ‫بواَلدبخكليِ ب‬ {27}


“Ewe nafsi iliyotua! Rejea kwa Mola wako Mlezi umeridhika na umemridhisha. Basi ingia miongoni mwa waja wangu, Na ingia katika Pepo yangu.” (89:27-30). Kwa mujibu wa Hadith maarufu sana, wakati fulani Mtume Muhammad (s.a.w.w.) aliwaambia kundi la masahaba wake ambao walishinda vita: “Mmefanya vizuri. Karibuni kwa watu ambao wamekamilisha jihadi ndogo (al-Jihad alasghar) na ambao bado wanaowajibu wa kukamilisha jihadi kubwa (al-jihad al-akbar).” Wakiwa wameshangaa, masahaba ambao waliwashinda maadui na walikuwa tayari kuwapatia kitu wanachokipenda sana, yaani maisha yao ili walinde Uislamu waliuliza; “Jihad kubwa ni ipi?” Mtume Muhammad (s.a.w.w) akajibu: “Jihadi kubwa ni kupigana na nyinyi wenyewe au nafsi zenu. Hivyo kujizuia dhidi ya majaribu na kuizuia roho isiingie kwenye uovu, na kujitakasa wenyewe hiyo ni jihadi kubwa sana na jihadi ngumu sana.” Mwishoni, na turejee kwenye baadhi ya sifa za hao wanao jitahidi kwa ajili ya Mungu kma ilivyoelezwa na Mungu Mwenyewe: {20}

‫سكهلم أبلعظببم بدبربجةح كعلنبد و‬ ‫سكبيِكل و‬ ‫اك َ بوبأو ذلبئكبك بهبم اَللبفاَئكبزوبن‬ ‫اَلوكذيبن آْبمبنواَ بوبهاَبجبرواَ بوبجاَبهبدواَ كفيِ ب‬ ‫اك بكأ بلمبواَلككهلم بوأبلنفب ك‬ {21} ‫م‬ ‫يببب ر‬ ‫شبربهلم برنببهلم بكبرلحبممة كملنهب بوكر ل‬ ‫ضبواَمن بوبجوناَ م‬ ‫ت لببهلم كفيِبهاَ نبكعيِرم بمكقيِ ر‬ ‫ب‬ ‫ب‬ ‫و‬ ‫ل‬ ‫ب‬ {22} ‫م‬ ِ‫ظي‬ ‫ع‬ ‫ر‬ ‫ج‬ ‫أ‬ ‫ه‬ ‫د‬ ‫ن‬ ‫ع‬ ‫ا‬ ‫ن‬ ‫إ‬ َ َ‫دا‬ ‫ب‬ ‫أ‬ َ‫ها‬ ِ‫في‬ ‫ن‬ ‫دي‬ ‫ل‬ َ‫خا‬ ‫و‬ ‫ب‬ ‫ب‬ ‫ح‬ ‫ب‬ ‫كك ك ب ب ك‬ ‫ب ك ب ل ر ك ر‬

“Wale walioamini, na wakahama, na wakapigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali yao na nafsi zao, hao wana cheo kikubwa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu, na hao ndio wenye kufuzu. Mola wao Mlezi anawabashiria rehema zitokazo Kwake, na radhi na Bustani ambazo humo watapata neema za kudumu. Watadumu humo milele. Hakika kwa Mwenyezi Mungu yapo malipo makubwa.” (9:20-22).

Kuamrisha Mema Na Kukataza Mabaya. Kuamrisha mema (al amr bi ul-ma’rif) na kukataza mabaya (al-nahy ‘an al-munkar) ni matendo mawili ya ibada ambayo kila Mwislamu balekhe anatakiwa kuyatekeleza popote inapowezekana. Hapana Mwislamu anayeweza kutojali yale yanayotokea katika mazingira yake hapa duniani., Sehemu ya majukumu ya jamii ya kila Mwislamu, ni kuzingatia maadili ya kibinadamu na kidini, na wakati wowote ambapo lolote kati ya hayo linapuuzwa au kukiukwa, lazima atoe ushauri na kuelekeza wale wenye wajibu wa kufanya mema na dhidi ya kutenda maovu na matendo ya dhambi. (3:103; 109, 113; 7:199; 9:71; 112; 22:41).

Sura Ya 5: Shi’a Waliopo Duniani Kwa mujibu wa UNFPA (The United Nations, Population Fund) na vyanzo vingine mnamo mwaka wa 1999 idadi ya watu duniani ilizidi bilioni sita.34 Takriban asilimia ishirini ya idadi hii (yaani bilioni 1.2) ni Waislamu. Uainishaji takwimu wa idadi ya Waislamu waliokuwepo duniani mnamo katikati ya mwaka wa 1998 inakadiriwa kama ifuatavyo: 35 Afrika: 315,000,000. Asia: 812,000,000. Ulaya: 31,401,000.

34 Idadi ya watu duniani ya tarehe 1/1/2002 inakadiriwa kuwa 6,196,141,294. (Tazama U.S Census Bureau Official Website ya www.census.gov). 35 Britimaca 2002. Kwa mujibu wa chanzo hiki, idadi ya Waislamu wote duniani katikati ya 1998 ilikuwa 1,164,622,000. Hiyo ni 19.6.% ya idadi ya watu wote duniani.


Amerika ya kusini: 624,000. Amerika kaskazini: 4,349,000. Sehemu zinginezo: 248,000. Waislamu huishi kila mahali duniani. Idadi ya nchi ambamo Waislamu huishi ni 208. 36 Takriban asilimia 85 ya Waislamu huishi nje ya Bara Arabu. 37 Waislamu walio wengi wapo Mashariki ya mipaka ya Iran, hususani Pakistani, India, Bangladesh, Malaysia na Indonesia. Indonesia ni nchi yenye Waislamu wengi zaidi duniani. Miongoni mwa Waislam wanaofanyiza watu wachache katika idadi ya watu ya dunia yote, Shi’a wanafanyiza asilimia kumi (10%) ya Waislamu wote, ambayo kwa mujibu wa idadi ya sasa ya dunia idadi yake ni 120,000,000. 38 Kwa mfano, Britannica 2002 (Deluxe Edition) inasema: “Kwa kipindi cha karne nyingi kundi la Shi’a limeathiri sana Waisalmu wote wa Suni, na wafuasi wake wanaofika takriban milioni 60 au 80 mwishoni mwa karne ya 20 au moja ya kumi ya Uislamu wote. UShi’a (Kiarabu Shi’a au Uislamu wa madhehebu ya Shi’a) wapo wengi katika imani hii Iran, Iraq na labda Yemen. (San’a) na kuna wafuasi Syria, Lebanon, Afrika Mashariki, India na Pakistani. Kwa mujibu wa vyanzo vingine, tarakimu ni 11%. 39 Hivyo idadi iliopo ya Shi’a hapa duniani lazima iwe takriban milioni 132,000,000.40 Mchanganuo wa idadi ya Shi’a katika baadhi ya nchi za Asia pamoja na idadi ya Shi’a au pamoja na asilimia kubwa ya idadi ya Shi’a yaweza kufupishwa kama ifuatavyo: 41.42 Afghanistan: Idadi ya watu (1998) 24,792,000. ushirikishaji wa dini (1990): Waislamu wa Sunni 36 Britimaca 2002, Deluxe version. 37 Kwa mfano tazama: Islam outside the Arab World by D. Westerland and I. Svanberg 38 Wengi waliobakia, zaidi ni Waislamu wa madhehebu ya Suni wakiwa ni Hanafi (wamo Misri, Lebanon, Syria, Jordani, Iraq, na Uturuki), wa Malik (walio wengi wamo Moroco na Sudan), wa Shafi (tapo la shafii linatumika Syria, Yemen, Oman, Muungano wa falme za Kiarabu, Bahrain na Kuwait, na yapo matapo mengine Jordan na Misri) na wa Hanbal. Kwa mujibu wa MEDEA, neno 'USUNI', tapo la Hanbal ni tapo rasmi Saudia Arabia na Qatar. 39 Yann Richard (1991 tarjumi ya Kiingereza 1995), uk. 2 kwa kutumia zaidi matarakimu yaliyowekwa Md-R. Djalili, Religion et revolution, Paris, Economica, 1981, uk. 234 na M. Momen, An Introduction to Shii Islam, New Haven na London, Yale University Press 1985, uk. 264 ff. Hivyo tarakimu za Richard hazihusiki kipindi cha miaka ya 80. mmeng'enyo wake ni kama ufuatao: Iraq; 55% au milioni 18,000,000; Bahrain; 70% au takriban 170,000; Kuwait; 240 ya raia wa Kuwa au 137,000; Qatar; 20% ya idadi ya watu au 50,000; Muungano wa Falme za Kiarabu; 6% au 60,000; Saudi Arabia: 7% ya raia wa Saudi Arabia au 440,000; Lebanon 1/3 au 1,000,000; India 15% au 20% ya idadi ya Waislamu ambayo inafika milioni 80 au 12% jumla ya idadi yote (Imamis na Ismailis) pakistani; 12,000,000; Afghanistani; 15% au takriban 2.3 milioni, Azebaijani; Jamii kubwa ya Shi'a (4.5 milioni; Uturuki; 1,500,00 mbali na tapo la Alawiyah; Syria; 50,000 mbali ya tapo la Alawiyah (kumbuka; Shi'a na Alawiyah kwa pamoja ni milioni 4,900,000)

40 Kwa bahati mbaya hakuna takwimu sahihi zinazoonesha idadi kamili ya Waislamu kwa ujumla na hususan Shi'a. Dokezo hilo hapo juu ni kwa mujibu wa vyanzo vingi sana zilivyomo kuhusu somo hili. Hata hivyo, imependekezwa kwamba Waislamu wa madhehebu ya Shi'a wanafanyiza asilimia 23 ya Waislamu, ambapo madhehebu ya Hanafi wanafanyiza 31% madhehebu ya Maliki wanafanyiza 25% madhehebu ya Shafii 16% na madhehebu ya Hanbal wanafanyiza 4%. Rejea S.M Qazwini, uk. 4 iliyochukuliwa kutoka kwenye Bulletin of Affliation: Al-Madhhab School of Thought, Juz. 17, Na. 4 (Desemba 1998, uk. 5). 41 Tarakimu zilizotajwa kwenye maandishi ni kwa mujibu wa Britannica 2002 Deluxe Edition. Tarakimu zinahusu mwaka wa 1998. Kwa hiyo, idadi ya watu lazima iliongezeka katika kipindi cha miaka michache iliyopita. Hata hivyo, asilimia zingebakia zile zile.

42 Lazima ifahamike kwamba orodha hiyo hapo juu haimaanishi kuweka jumla zote pamoja; ni uteuzi uliotegemezwa kwenye taarifa iliyo kusanywa kutoka kwenye chanzo kuhusu kila nchi. Mathalani, Qatar haipo ambapo kufuatana na MEDIA, 10% ya idadi ya watu wa nchi hiyo ni Shi'a.


84%;. Waislamu wa Shi’a 15%; wengine 1%. 43 Azerbeijan: Idadi ya watu (1998): 765,000/ Ushirikishaji wa kidini (1991): Waislamu wa madhehebu ya Shi’a 70%; Sunni 30%. Bahrain: Idadi ya watu (1998) 633,000/Ushirikishaji wa kidini: (1991). Waislamu 81.8% miongoni mwao Shi’a wapo 61.3%, Sunni 20.5%, Wakristo 8.5%; wengineo 9.7%. 44 India: Idadi ya watu (1998): 987,004,000/ ushirikishaji wa kidini (1995); Hindu 81.3%, Waislamu 12 % ambao miongoni mwao Sunni wapo 9%, Shi’a 3%; Wakristo 2.3% ambao miongoni mwao WaªProtestant 1.1% Wakatoliki 1%, Sikh 1.9% Budha 0.8%; Jain 0.4%; Zoroesta 0.01%; wengine 1.3%. Iran: Idadi ya watu (1998):61,531,000/ Ushirikishwaji wa kidini (1995) Waislamu 99%; Shi’a 93.4%; Sunni 5.6% Wakristo 0.3%, Zotoesta 0.05%; Yahud 0.05%. 45 Iraq: Idadi ya watu (1998); 21,722,000; Ushirikishwaji wa kidini (1994); Shi’a 62.5%; Sunni 34.5%; Wakristo (hususan wafuasi wa ibada ya Chaldean, na ya wasyria, wakatoliki na Nestory) 2.7% wengineo (hususan Yazid Ayncretist) 0.3%. 46 Jordan: Idadi ya watu (1998): 4,682,000. Ushikishaji wa kidini (1995); Waislamu wa Sunni 96.5% Wakristo 3.5%. 47 Lebanon: Idadi ya watu (1998); 3506,000 ushirikishwaji wa kidini (1995); Waislamu 55.3% miongoni mwao 34.0% ni Shi’a, 21.3% Sunni, wakristo 37.6% miongoni mwao, Wakatoliki 25.1% (Maronite 19% Wakatoliki wa kigiriki au Malachite 4.6%), Orthodox 11.7% (Greek Orthodox 6%, Armenian Apostolic (5.2%), Protestant 0.5%; Druze 7.1%. 48 Oman: Idadi ya watu (1998); 2,364,000. Ushirikishwaji kidini (1993): Waislamu 87.7% miongoni

43 CIA World Factbook ni kitabu chenye taarifa inayokisia idadi ya watu wa Afghanistani mnamo Julai, 2001 kama ifuatavyo; Waislamu wa madhehebu ya Sunni wapo milioni 26,813,057 sawa na 84% Waisilamu wa madhehebu ya Shi'a wapo 15%, wengine 1%. Chini nitarejea kwenye chanzo hiki kwa Acwf. Kwa mujibu wa Westerlund na Swanberg (1999; uk. 177, takriban 18% ya idadi ya watu wa Afghanistani inafikiriwa kuwa na wafuasi wa Ithna Asharia na kidogo chini ya 2% ni Ismailia. 44 Kwa mujibu wa CWF, Shi'a wa Bahrain wanafanyiza 70% ya Idadi ya Waislamu. Kwa mujibu wa MEDIA (European Institute for Research on Mediterenian an Euro-Arab (cooperation) 85% ya idadi ya Waislamu ambao miongoni mwao 1/3 ni Suni na 2/3 ni Shi'a (katika wingi wa Waarabu lakini pia wapo Wairan 70,000) Kwa mujibu wa Fuller and Franke (1999, uk. 120), Shi'a wanafanyiza takriban 70% miongoni mwa idadi ya wazalendo wa Bahrain. 45 Kwa mujibu wa CWF, Shi'a wanafanyiza 89% katika idadi ya watu ya nchi nzima. 46 Kwa mujibu wa CWF, Shi'a wanafanyiza 60%-65% na Sunni 32%37% katika idadi yote ya watu. Kwa mujibu wa MEDIA, Waislamu wa Iraq ni 97%, miongoni wmao Shi'a ni 65% na Sunni 32%. Kwa mujibu wa Fuller and Fraknke (1999, uk. 87), Shi'a wanafanyiza 50%-60% ya idadi ya watu wa Iraq. Taarifa hii inaongezea kwamba tangu mwishoni mwa miaka ya 1970 Shi'a wa Iraq wamekuwa wanaondoka Iraq kwa idadi kubwa kwenda kuishi Iran, Syria, Uingereza na nchi nyingine. 47 Kufuatana na CWT, Waislamu wa madhehebu ya Sunni ni 92% Wakristo na 6% (walio wengi, zaidi na Orthodox wa Ugiriki, lakini baadhi ni Wakatoliki wa Ugiriki, Wakatoliki wa Rumi, Orthodox wa Syria, Orthrodox wa Coptic, Orthodox wa Armenia na madhehebu ya Protestant) na wengineo ni 2%. (Idadi ndogo kadhaa za Waislamu wa Shi'a na Druze) ilitolewa mwaka 200. 48 Kwa mujibu wa CWF, Waislamu wanafanyiza 70% (idadi hii inajumuisha Shi'a, Sunni, Druze, Ismaili, Alawiya au Nusayri). Kwa mujibu wa MEDIA, Waislamu ni 70% (makundi matano ya Kiislamu yanayotambuliwa kisheria ni Shi'a, Sunni Druze, Ismailia, Alawiya au Nusayri) na Wakristo ni 30% (makundi 11 ya Kikristo yanayo tambuliwa kisharia: Wakristo wa Orthodox makundi 4, Wakatoliki makundi 6, Waprotestanti kundi moja). Wayahudi asilimia yao ni ndogo. Kwa mujibu wa Fuller ana Francke (1999, uk. 203), Shi'a wanafanyiza 30%40% ya idadi ya watu na akilisha kundi moja kubwa zaidi la kimadhehebu nchini Lebanon.


mwao Waislamu wa madhehebu ya Ibaadhi ni 75% (makundi makuu ya Waislamu ni Sunni na Shi’a); Hindu 7.4%; Wakristo 3.9%; Budha 0.5%; wengineo 0.5%.49 Pakistani: Idadi ya watu (1998); 141,900,000; Ushirikishwaji wa kidini: (1993); Waislamu wapo 95% (walio wengi zaidi ni Suni, na Shi’a ambao wanafanyiza 20% ya idadi yote ya watu); Wakristo 2% Hindu 1.8%; wengineo (pamoja na Ahmadiya) 1.2%. 50 Saudia Arabia: Idadi ya watu (1998) 20,786,000. Uwakilishwaji wa Kidini (1992); Suni 93.3% na Shi’a ni 3.3%.51 Syria: Idadi ya watu (1998). 15,335,000. Uwakilishwaji wa kidini (1992); Waislamu ni 86% miongoini mwao Suni ni 74%, Alawiyah (Shi’a) 12%; Wakristo 8.9%; Druze 3% wengineo 1%. 52 Tajikistani: Idadi ya watu (1997): 6,112,000. Uwakilishwaji wa kidini (1995): Sunni 80%, Shi’a 5%, Orthodox wa Kirusi 1.5%; Wayahudi 0.1; wengineo (zaidi wasio na dini )13.4%. Uturuki: Idadi ya watu (1998): 64, 367,000. Uwakilishaji wa kidini (1994): Sunni 80%; Shi’a 19.8% ambao kwamba Wasio orthodox ªAlevi (onorthodox) ni 14.8%; ni 14%; Wakristo 0.2%. 53 Muungano wa Falme za Kiarabu: Idadi ya watu (1998): 2,744,000. Uwakilishwaji wa kidini (1995): Waislamu 96% (Sunni 80% Shi’a! 6%); wengineo hasa zaidi Wakristo na Hindu) 4%. Yemen: Idadi ya watu (2000): 18,260,000.54 Uwakilishaji wa kidini 1995). Waislamu ni 99.9% Sunni 60% Shi’a 40%) wengineo 0.1%.55 Idadi ya Shi’a kwenye nchi zingine hubishaniwa. Baadhi ya watu huamini kwamba idadi ya Shi’a ni kubwa zaidi kuliko idadi rasmi, kwa sababu ya kutokuwa na takwimu sahihi au kwa sababu ya matizo ya kisiasa.

Back Cover: Je, madhehebu za Kiislamu zinazuia mshikamano na umoja wa Kiislamu? ‘Yajue madhehebu ya Sh ’a’ ni kitabu kinachoelezea kwa mukhtasari kuhusu madhehebu ya Shi’a sambamba na madhebu nyingine za Kiislamu. Kitabu hiki ni matokeo ya uchunguzi wa muda mrefu kuhusu masuala muhimu ya Kiislamu kwa

49 Kwa mujibu wa CWF, Waislamu wa dhehebu la Ibadhi ni 75% na yaliyobakia ni Sunni, Shi'a na Hindu. Kwa muijibu wa MEDIA, Waislamu ni 75% miongoni mwao ¾ ni wa madhehebu ya Ibadhi. 50 Kwa mujibu wa CWF, Waislamu wamo 97% (Sunni 77% na Shi'a 20%) Wakristo, Hindu na wengineyo ni 3%. Kwa mujibu wa Westerlind na Svanbeg (1999, uk. 225); Waislamu wanafanyiza zaidi ya 96% ya jumla yote ya idadi ya watu. Miongoni mwa Waislamu 15%-20% wanakisiwa kuwa Shi'a. 51 CWF haioneshi asilimia ya idadi ya Shi'a Saudia Arabia, licha ya kwamba wapo wengi zaidi kuliko waliopo kwenye nchi zingine hapo juu. Taarifa hii inasema tu kwamba Waislamu wanafanyiza 100% ya jumla ya idadi ya watu. Kwa mujibu wa MEDIA, Shi'a ni 2.5% na Suni ni 97%. Kwa mujibu wa Fuller and Francke (1999, uk. 180) serikali ya Saudia imesema Shi'a ni 2,%-3% kutoka kwenye jumla ya idadi ya watu, takriban 300,000, lakini vyovyote vile inawezekana tarakimu kuwa nusu milioni. 52 Kwa mujibu wa CWF, Sunni ni 74%. Alawiya, Druze na madhehebu mengine ya Kiislamu ni 16%. Wakristo (madhehebu mbali mbali) ni 10% na Wayahudi ni jamii ndogo sana katika Dameski, Al-Qamishi, na Aleppo. Kwa mujibu wa MEDEA, Sunni ni 75%, Alawiya ni 11%, Wakristo (wa idadi zote) 10% na Druze 3%. 53 CWF inasema tu kwamba 99.8 % ni Waislamu (hasa zaidi Sunni) na mengineo (Wakristo na Wayahudi) ni 0.2%. Inashangaza kuona kwamba taarifa ya MEDIA haikuwatilia maanani idadi ya Shi'a walipo Uturuki na inasema; "Dini: Waislamu 99% Sunni, wengineo 1% (Wakristo na Wayahudi)" (http://www.media.be/en/index059.htm). Kwa mujibu wa Wasterlund and Svanberg (1999, uk. 133), Waislamu wa Sunni wanafikiriwa kuwa 70%-80% kutoka kwenye jumla ya idadi ya watu na waliobaki 30-30% ni Alawiya. 54 Hii ni kwa mujibu wa SESRTCIC iliyounganishwa kwenye Organisation of Islamic Conference (OIC) 55 CWF inaelezea tu: "Waislamu wakiwemo pamoja na Shafi'i (Sunni) na Zaydiya (moja katika madhehebu ya Shi'a), idadi ndogo ya Mayahudi, Wakristo na Wahindu." Kwa mujibu wa MEDEA, Sunni ni 55% Waislamu wa Zaydiya ni 44% na Wakristo ni 1%.


ujumla. Vile vile mwandishi katika kitabu hiki amelishughulikia kwa makini sana suala la umoja na mshikamano wa Waislamu, na kuonesha kwa kutumia elimu, mantiki na hoja kwamba, umoja ni dharura kubwa sana, na pia ni jambo linalowezekana kabisa pamoja na kuwepo kwa tofauti hizi za kimadhehebu, ambapo nyingi kama si zote hazihusiani na misingi mikuu ya Kiislamu kama wanavyoijua Waislamu wenyewe. Mohammad Ali Shomali ni mhitimu wa Islamic Seminaries of Qum, na vile vile anayo shahada ya BA na MA katika filosofia ya Magharibi kutoka chuo kikuu ca Tehran. Alipata shahada ya udaktari katika filosofia kutoka chuo kikuu cha Manchester. Jimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.ibn-tv.org


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.