Bilal wa afrika

Page 1

©Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 9987-427-03-0 Kimeandikwa na: Husayn Malika Ashtiyani

BILAL WA AFRIKA Kimetarjumiwa na: Al-Akh Salman Shou S. L. P. 19701 Email:info@alitrah.org Website:www.alitrah.org Kimeandikwa na: Husayn Malika Ashtiyani

Kupangwa katika kompyuta na: Ukhti Pili Rajabu. Toleo la kwanza: Agosti 2005 Nakala: 1000

Kimetajumiwa na: Al-Akh Salman Shou S. L. P. 19701 Email:info@alitrah.org Website:www.alitrah.org

Kimetolewa na kuchapishwa na: Al-Itrah Foundation P. O. Box 19701 Dar-es-Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Fax: +255 22 2113107 Email: info@alitrah.org Website: www.alitrah.org


YALIYOMO

Aaa!Aaa!Naungua..........................................................................38 Bilal amefariki dunia.....................................................................41

Maisha ya Bilal .................................................................................i

Chungu kuliko sumu ....................................................................43

Mazingira ya Kipindi hicho..........................................................iv

Abu Bakar anakutana na Bwana wa Bilal ...................................49

Hadhi ya Mwanamke wa jamii ya Makkah kipindi hicho. ........1

Bilal ashinda na kuwa huru..........................................................51

Nuru iliyoangaza kwenye giza .......................................................3

Utumwa au Uhuru.........................................................................54

Bilal akiwa mwangalizi wa hekalu la Masanamu.........................4

Tabia ya kishenzi...........................................................................57

Mfadhaiko wa Bilal .........................................................................6

Uzuri wa kustaajabisha wa jiji la Madina ...................................61

Kuelekea bahati njema ...................................................................9

Tatizo kubwa..................................................................................63

Mwislamu wa kwanza kutoka Ethiopia ......................................10

Maombi ya dua ya Mtukufu Mtume (s.a.w.) ..............................64

Sura ya ukweli................................................................................12

Moyo wa undugu katika Uislamu................................................68

Mkutano wa Maadui .....................................................................15

Wito mkubwa wa Uislamu ...........................................................71

Uchunguzi kutoka kwa Bilal........................................................18

Ubora wa adhana na muadhini ....................................................76

Dini ni jambo la hiyari .................................................................22

Mwongo achomwa moto hadi kufa .............................................82

Njozi za kishetani ..........................................................................25

Bilal ashutumiwa ...........................................................................83

Kwenye upeo wa matumaini........................................................27

Bilal kwenye vita vya Badr ...........................................................86

Jela na kazi ngumu ........................................................................28

Bilal analipa kisasi.........................................................................88

Utulivu kwenye makucha ya minyororo ....................................30

Bilal mbele ya Imamu Ali.............................................................92

Uimara na kujitolea mhanga........................................................32

Kuelekea mahali alipozaliwa........................................................94

Shukrani kwa Bilal ........................................................................36

Wanangojea hatima yao ................................................................99


Bilal kwenye paa la Al-Ka’aba ...................................................101

Mahja - Muadilifu sana...............................................................147

Wimbi la upinzani.......................................................................103

Luqman -mtumwa muadilifu.....................................................147

Ubaguzi wa rangi kwa mara nyingine.......................................106

Yasir - shahidi wa khaibar..........................................................148

Masanamu yaporomoshwa chini ...............................................108

Yasir - mswalihina ......................................................................149

Mtukufu Mtume anaugua kitandani.........................................109

Mabur Al- Hahi ...........................................................................150

Bilal afanya upelelezi ..................................................................111

Mahir ............................................................................................150

Madina yatoa rambi rambi ya kifo cha Mtukufu Mtume .......112

Abu Rafi Ibrahim Qibty .............................................................150

Nyumba ya huzuni ......................................................................114

Usama bin Zaidi bin Haritha kamanda ....................................151

Tukio la Saqifa.............................................................................115

Abaidullah Ibn Abu Rafi mwandishi........................................153

Jukumu la Imamu katika kulinda Uislamu .............................122

Ali ibn Abu Rafi ..........................................................................153

Bilal afanya mgomo.....................................................................123

Watoto wa Fizzah ........................................................................154

Bilal anafukuzwa .........................................................................128

Abu Naisar - Sahaba wa Imamu Ali ..........................................154

Adhana ya mwisho ......................................................................133

Nasir Ibn Abu Naisar..................................................................155

Wakati wa kujitoa mhanga .........................................................135

Jaun bin Huwi - Mtumwa wa Abudhar ....................................155

SEHEMU YA PILI

Hajjaj Ayman Ubayd - Kutoka Ethiopia ..................................158 Mariya Qibtiyya - mama wa Waumini......................................158

Utangulizi.....................................................................................138 Mariya bin Shamim Qibtiyya -msichana mtumwa wa Ibrahim bin Muhammad............................................................141 Mtume...........................................................................................159 Asmaha Najjashi - Mfalme wa Ethiopia ...................................142 Sirin - Mke wa Mshairi...............................................................159 Ayman bin Ubaid - shahidi wa Hunain....................................146 Umme Ayman - Mama wa Mtukufu Mtume ...........................160


Fizzah - Hifadh wa Qur’an Tukufu...........................................163 Shohra- mjukuu wa kike wa Fizzah ..........................................168


NENO LA MCHAPISHAJI Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza, kwa jina la “Bilal of Africa” kilichoandikwa na Mwanachuoni, mwanahistoria na mtafiti, Husayn Malika Ashtiyani kwa Kifarsi na kisha kikatarjumiwa kwa lugha ya Kiingereza na Al-Akhy Muhammad Fazal Haq. Kitabu hiki kinahusu maisha ya Bilal muadhini na mhudumu wa Mtukufu Mtume. Yeye alikuwa ni Muafrika kutoka Ethiopia lakini mzaliwa wa Makka. Bilal ni mashuhuri sana katika historia ya Uislamu, alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kabisa kumkubali Mtukufu Mtume Muhammad (saww) na Uislamu. Kama alivyokuwa baba yake mzee Rabah, na yeye pia alikuwa mtumwa, na mmiliki wake alikuwa ni Umayyah bin Khalaf. Bwana huyu alikuwa katili sana na alimtesa sana Bilal. “Ahad, Ahad, Ahad.” Haya ni maneno aliyokuwa akiyatoa Bilal wakati alipokuwa anateswa na kulazimishwa na bwana wake kuukana Uislamu; maneno yenye maana ya: Mmoja, Mmoja , Mmoja, yaani Mungu ni Mmoja tu na hana mshirika. Maneno haya yalimkasirihsa sana bwana wake na akamtesa kwa mateso makali sana, lakini Bilal hakubadilisha msimamo wake, wakati wote yeye alikwa akisema : “Ahad, Ahad, Ahad.” Kutokana na umashuhuri wa Bilal katika historia ya Uislamu, tumeona ni vizuri tukitoe kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili

ili kuzidisha mwanga wa elimu kwa Waislamu wazungumzaji wa Kiswahili. Na hili likuwa ndilo lengo kubwa la Taasisi yetu ya ‘Al-Itrah Foundation’ katika kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili. Tunamshukuru Ndugu yetu Salman Shou kwa kukubali jukumu hili la kukifanyia tarjuma kitabu hiki. Vile vile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki. Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni mwanga kwa wasomaji wetu na kuzidisha upeo wao wa elimu katika dini.

Mchapishaji: Al-Itrah Foundation S. L. P. 19701 Dar-es-Salaam. Tanzania.


MAISHA YA BILAL Mojawapo ya sehemu zenye vilima zinazopakana na Makkah liliishi kabila la Bani Jumuh. Watu wote wa kabila hili walikuwa waabudu masanamu na walikuwa wafugaji na wakulima kama makabila mengine katika ufugaji na ukulima. Desturi na mila fulani zilikuwa wazi miongoni mwao. Kuua, kunyang’anya na kuiba ni mambo yalionekana kwa hawa watu. Kabila hili lenye utajiri na uwezo liliweza kuwateka watu na kutumia huduma zao kama watumwa, na miongoni mwa watumwa hao walikuwemo vijakazi. Kwa ufupi, kabila hili lilikuwa na uadilifu mdogo sana na halikuwa na dalili ya wema na tabia nzuri, mambo ambayo hayakuonekana katika maisha yao. Miongoni mwa watumwa waliomilikiwa na kabila hili alikuwapo mtu mmoja aliyeitwa Rabah ambaye aliwazidi wenzake wote kwa uadilifu, tabia na hadhi. Mtumwa huyu alipewa dhamana ya kuwa mwangalizi wa mali ya kabila hilo na alipendwa na wote. Jeshi la Tembo1 lilipowasili Makkah kwa lengo la kuvunja AlKa’bah, Hamamah, mpwawe Abraha (binti wa dada yake), Mkuu wa jeshi, alikwenda kwenye mlima uliokuwa karibu ili ajipumzishe na kuwinda. Punde baadhi ya watu wa kabila la Khath’am liliokuwa linaishi pembezoni mwa Makkah, kama ilivyo kawaida ya makabila

1

Kwa maelezo zaidi kuhusu tukio hili la kuchochea fikra na la kimuujiza, angalia kitabu kiitwacho “Stories from Qur’an” uk. 171, Islamic Seminary Publicatios i

yasiyostaarabika na katili, lilifanya shambulizi dhidi ya wapiganaji wa Abraha. Kwa mujibu wa jinsi na mila za Kiarabu, mwanamke huyu alishambuliwa na hatimaye gari la kifalme la kukokotwa na ngamia alimokuwa, lilitekwa na maadui. Kwa kuwa palikuwepo na urafiki baina ya makabila haya mawili – Bani Katham na Bani Jumuh wao – Bani Katham walichukua gari la kifalme la kukokotwa na ngamia pamoja na vito vya madini na kadhalika na waliwapa huyo mwanamke Bani Jumuh kama zawadi. Katika hali hii mtu mmoja zaidi aliongezeka kwenye kundi la watumwa wasichana wa kabila hili. Hamamah aliishi na kabila hili kwa muda fulani. Alikuwa na matumaini kwamba mambo fulani yangetokea na kumwezesha yeye kuungana tena na jeshi la Abraha. Hata hivyo, jinsi muda ulivyopita, alitambua kwamba hangeweza kuandokana na utumwa kwa hiyo, alilazimika kuendelea kuishi nao. Wakati wa kipindi alichokuwa anaishi na kabila hili alipendezwa sana na maadili na mwenendo mzuri wa tabia ya Rabah ambaye alifikiriwa kuwa mlezi wake kwa kiwango fulani. Kufuatana na upatanifu wao, Mkuu wa kabila alitoa ruhusa aolewe na Rabah.2 Mateka hawa wawili walianza maisha yao mapya na waliishi kwa miaka mingi wakipendana na kuaminiana. Wakati wa kipindi hiki walijaaliwa kupata watoto wawili wa kiume na mmoja wa kike. Majina ya watoto wa kiume ni Bilal na Khalid na jina la mtoto wa kike, Ghufrah. Kama wao, watoto wao pia 2

Qiblah -e- Islam, uk. 688. ii


MAZINGIRA YA KIPINDI HICHO

walichukiliwa kama watumwa na mjakazi wa kabila hili. Khalaf ambaye alikuwa mkuu wa kabila, alikufa baada ya miaka michache. Aliacha watoto wa kiume, mkubwa kati yao walikuwa Umayyah. Mtu huyu alikuwa kijana mrefu. Alionekana kuwa na kiburi sana na mkali. Watu wote wa kabila lake walikuwa wanamuogopa na walimheshimu sana. Baada ya muda Fulani, Rabah naye pia akafariki, na Bilal na mama yake, ndugu na dada yake waliendelea kuishi na kabila hili. Bilal alikuwa mrefu kwa kimo na rangi ya uso wake ilikuwa kahawia iliyoelekea kuwa nyeusi zaidi. Alipewa hadhi ya mzaliwa –mweusi wa kabila hilo, na watu wa kabila, hususan Umayyah, walikuwa wapole sana kwake.3 Kabila lote walimpenda Bilal, walimpenda sana hivyo kwamba walimpa cheo cha marehemu baba yake na wakamkabidhi dhamana ya uangalizi wa mali yao pamoja na hekalu lao la masanamu. Umayyah alikuwa na desturi ya kutembelea jiji akiwa na watumwa kama baba yake. Ilitokea akampenda Bilal kwa namna ya pekee, ambaye alikuwa hawezi kulinganishwa na wengine.

Kwa muda wa miaka mingi jua lilikuwa linang’ara juu ya mataifa mawili makubwa na yaliyostaarabika yaani Iran na Rumi. Dola hizi zilitawala nchi zote ndogo za wakati huo isipokuwa Bara la Arabuni na mkoa wa Makkah ambao pamoja na rekodi yao ndefu ya kihistoria, hazikuwa na mvuto kwa himaya hizi, kwa sababu Makkah ilikaliwa na makabila ya Mabedui mbayo hayakustahili kuangaliwa kwa umakini.4 Watu walioishi kwenye ukanda huo walikuwa katika hatari ya kupata matatizo na wasi wasi wa aina zote na dalili za ujinga, chuki bila sababu, na ukandamizaji, ni mambo yaliyofanywa sana, na watu hao hawakuwa na sifa za ubinadamu. Katika hao kila nyumba walitayarisha sehemu maalum kwa ajili ya ibada ya masanamu na kila kabila lilikuwa na sanamu lake maalum. Pia walitengeneza masanamu kadhaa yaliyo nakshiwa kwa dhahabu na fedha yaliyowekwa katikati ya jiji. Zaidi ya hayo, walichonga masanamu yao ambayo idadi yao ilikuwa sawa na siku za mwaka mmoja na wakayaweka ndani ya Al- Kabah Tukufu, yaani masanamu 360 yaliyomilikiwa na makabila mashuhuri ya Kiarabu.5 Moto mharibifu wa kivita uliwaka mfululizo kwenye mazingira hayo ya kuhuzunisha na idadi kubwa ya vijana walipoteza maisha yao. Wakati mwingine vita hivi viliendelea kwa muda mrefu sana hivyo kwamba amani na starehe vilitoweka na mtu

3

Qiblah- e- Islam, uk. 688 na Tafsiri -e- Ithna ‘Ashari, juzuu ya pili, uk. 157. iii

4 5

Tafsiri -e-Surah wal-Asr. History of Civilization, Gustar Le Bon uk. 103 iv


aliweza kuona kama vile anaishi Jahanamu. Wizi ulifanywa kama sifa ya ujuzi wa kazi. Waporaji ambao hawakumjua Mwenyezi Mungu walinyang’anya misafara iliyopita karibu na pia waliwanyanyasa na kuwakandamiza watu.

v


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

HADHI YA MWANAMKE WA JAMII YA MAKKAH KIPINDI HICHO Makabila yote ya Bedui ya kiarabu yaliwachukia wanawake na kuwadharau sana hivyo kwamba kama mtoto aliyezaliwa alikuwa mwanamke alizikwa angali hai! Mwanamke bora sana alikuwa yule aliyemuua na kumzika mtoto wake mchanga wa kike kwa lengo la kumridhisha mumewe. Jambo hili lilikuwa ni sehemu ya shughuli zao na halikuathiri nyoyo zao hata kidogo. Heshima na utu ni tabia ambazo hazikuwepo miongoni mwao. Ni watu wa ukoo bora na watemi tu ndio waliokuwa na maisha ya furaha na starehe. Hawakuwa na hisia za wema na ubinadamu na waliendekeza mamlaka ya kulazimisha heshima. Waliwateka wageni na watu wanyonge, na kuwafanya watumwa na kuwakandamiza. Hata katika hali ya utumwa waliendeleza uovu wao kwa kiasi kwamba waliwanyang’anya upendeleo na uhuru wao wote na wao (watumwa masikini) hawakuwa na mamlaka ya namna yoyote. Wao walikuwa watumwa waliomilikiwa na mabwana zao ambao waliwafanyia vituko kadiri walivyotaka. Siku moja waliambiwa kufanya kazi, siku ya pili walipigana kwa ajili ya kumuunga mkono bwana wao, na siku ya tatu walishindana kwa lengo la kumfurahisha bwana wao. Mathalani watumwa wawili waliamuriwa kushambuliana na mmoja wao kuuawa, ili bwana wao afurahie kuona tukio hilo.

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Kwa ufupi mazingira ya wakati huo yalijaa ukatili, ujinga, ufisadi, wizi, kamari na chuki za kijamii na kikabila, mila zisizovutia na sherehe na majivuno yasiyo na mpaka. Ukweli, uaminifu, unyoofu, utakatifu, uhisani na hisia zenye wema ni maneno ambayo hayakuwa na maana katika jamii hiyo. Wote, ama vijana au wazee, walivunjika nyoyo zao na kudhikika kwa sababu ya uharibifu wa vita ambayo ilikuwa inaendelea miongoni mwao kwa miaka mingi. Matendo maovu yalikithiri na vijana wote walijitolea kuwa fisadi kwa sababu ya kutokuwepo uadilifu na maovu mengi ya kijamii yaliyoenea miongoni mwao. Ni dhahiri kwamba katika jamii kama hizo watoto wengi wa nje ya ndoa walizaliwa. Takwimu za matendo machafu na upotofu huongezeka. Mauaji, uporaji na ukandamizaji yanazidi kuenea na maadili mema husahauliwa. Haiwezekani kuishi katika mazingira kama hayo na kifo ni kizuri zaidi kuliko maisha kama hayo kwa sababu hakuna kingine isipokuwa kifo cha polepole ndicho huwepo katika jamii ambayo utawala wa sheria (katika uhalisi wake) haupo na kila kundi hutengeneza sheria zake kufuatana na matakwa yake na huongoza watu, na jamii ambamo sheria ni kwa ajili ya watu wa chini na watu fulani fulani hivyo kwamba kama mmojawapo wa ndugu wa watengeneza sheria au wale wanaoshurutisha utiifu wa sheria anafanya kosa kubwa wala hawajibishwi na sheria.

Katika mazingira kama hayo wanawake waovu walianzisha madanguro kwa uhuru kabisa na walijishughulisha wazi wazi kuwavutia wateja kwa kutumia njia mbali mbali.

Kipindi ambacho wezi wanaweza kuiba wazi wazi, rushwa inatolewa na kuchukuliwa na kupewa jina la mapato; ni watu wachache sana hufurahia upendeleo wa maisha, na maelfu hulala bila kula na hapana mtu anayetambua hali yao na watu

1

2


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

wengi hawawezi kuendesha maisha yao na jasho lao na utu wao havikuthaminiwa, kifo kwa uhakika ni kizuri zaidi kuliko uhai na watu wanayo dalili ya kutamani kifo.

NURU ILIYOANGAZA KWENYE GIZA Ilikuwa kwenye giza hilo, jamii iliyochafuka, iliyosongwa na maovu na kuwa nyuma, ghafla ilichomoza nyota ya uadilifu, uhuru, na amani ya Mungu mmoja iliyong’ara na kueneza nuru kwenye dunia ya giza ya wakati huo. Mtume mkuu wa Uislamu, Muhammad (s.a.w.) aliteuliwa na Mwenyezi Mungu kwa uongofu na mwongozo wa watu ili aweze kuwaongoza kwenye mafanikio ya Utukufu wa Dini, kuondosha mila zao potofu na chuki zisizo na msingi, kuwaonyesha njia ya maendeleo, kupata ubora, ujuzi na uadilifu, kuondosha pazia la ujinga, kuvunja minyororo ya mateka, kuigeuza jamii chafu, kuwaondosha watu kutoka kwenye utumwa na kuwaelekeza kwa Mwenyezi Mungu, Muumba wa Ulimwengu. Hakika kwenye jamii iliyoko gizani kama hii ambayo ilinyang’anywa neema ya Mitume ya Mwenyezi Mungu kwa muda mrefu sana, jicho la kutafuta ukweli liliangamia na hawangeweza kutumia mwanga haraka. Na fikra ambazo zilipata lishe katika makunjo ya pazia nene la ujinga, kutokujua kusoma na upotofu havingeweza kuwafanya watambue kwamba pia palikuwepo njia nyingine zaidi ya hiyo waliokuwa wanaifuata. Na kwa hakika ilikuwa vigumu kwa jamii, ambayo imekuwa inapita kwenye njia isiyo sahihi kwa kipindi kirefu sana, kurudi kwenye njia iliyonyooka.

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

BILAL AKIWA MWANGALIZI WA HEKALU LA MASANAMU Pindi Mtume wa Uislamu alipotangaza tablighi yake ya Utume hadharani na kuwaita watu katika kumwabudu Mwenyezi Mungu, makelele ya kushangaza yalitokea katika jiji la Makkah na katika kipindi kifupi sana, imani hii mpya iliwavutia watu wengi. Watu waliokuwa bado wanao uadilifu, ubinadamu na uelewa katika nyoyo zao, walitoa jibu la kukubali wito huu. Ingawa idadi yao ilikuwa ndogo sana, imani yao ilikuwa imara. Watemi wa Makabila na watu wengi waliokuwa wanapinga wito huu, waliamua kukomesha mapema iwezekanavyo. Qur’an tukufu inasema: (61:8)

% & ! " # $ Ni kawaida kwamba ambapo watu wenye kiburi ambao waliwatawala watu kwa kipindi kirefu waliona jinsi uwezo na mamlaka yao yalivyokuwa hayana nguvu na kuona kwamba watu hawakujali matendo yao maovu na hawakuyatilia umuhimu na wakaamua kumpinga Mtukufu Mtume ambaye aliwaita ili waokoe maisha yao. Pale ambapo waporaji dhalimu na mabwana ambao walivamia maisha na mali na heshima ya watu kwa kipindi kirefu sana na hawakuacha kufanya matendo kama hayo wakaona kwamba palijitokeza mtu ambaye alitaka kukomesha shughuli zao na kuzifuta athari zake za kuchukiza kutoka kwenye jamii ya binadamu, hawakutaka kuruhusu kwa njia yoyote kwamba angeishi kwa amani na kufuatilia lengo lake. Kundi hili la upinzani, lilikusanyika kutoka sehemu zote

3

4


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

kutaka kumwondosha mlezi na kiongozi wa wito huu wa Mungu na walishirikiana kutekeleza lengo lao. Walifanya mikutano na kutoa hotuba, na hata baada ya mikutano walizungumzia jambo hili majumbani mwao au pembezoni mwa barabara na njia panda za barabara kuu. Kila mmoja alitoa maoni yake, kufuatana na uwezo wake, kuhusu kumuua Mtume wa Uislamu. Kwa kweli, upinzani na uadui wao wote ulifanikisha sana kupata matokeo yaliyo tarajiwa kuhusu kuwafanya watu wajue ujumbe wa dini hii ya Mungu na wakawa sababu ya matabaka yote ya jamii kujifunza kwa uangalifu makusudio na sera ya Mtume. Kinyume chake watu waliokuwa masikini na kukandamizwa ambao hawakuwa na hadhi katika jamii walitambua jambo hili na kulizungumzia wao kwa wao. Wakati wa ghasia hizi za kushangaza na mazungumzo yasiyo na mantiki ya watu wa Makkah, Bilal, msimamizi wa hekalu la masanamu naye pia akaanza kutafakari.6 Ilikuwa sahihi Bilal kufikiria kuhusu jambo hili, kwa sababu alikuwa anashirikishwa na masanamu kwa muda wa miaka mingi na alikuwa anayaomba msaada na aliyafikiria kuwa ni miungu yake, na sasa baada ya kusikia wito huu, mageuzi mapya yalifanyika katika mawazo yake na kwa hiyo, alitafakari ni imani ipi kati ya hizi mbili ilikuwa bora na kuwa karibu zaidi na ukweli. Ingawa Bilal alikwisha kuwa na mazoea ya hawa miungu –

6

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

masanamu kwa kipindi kirefu sana na alikuwa na kawaida ya kulalamika mbele yao wakati akiwa peke yake na aliyaomba kumtimizia mahitaji yake, lakini sasa, aliposikia wito huu alifadhaika na akatafakari kama ingewezekana kwamba haya masaanamu yasiyo na uhai na yasiyoweza kusogea na hayangeweza hata kujilinda yenyewe kama ni Mungu na pia kwamba haya masanamu ambayo yalikuwa yanasafishwa na kufutwa vumbi kila siku na Bilal yangeweza kuwa waumbaji wa dunia, anga, jua na nyota? Akateta akingali peke yake. “Hivi hizi nyota nzuri za kupendeza, makundi ya nyota, misimu hii na mabadiliko ya usiku na mchana kweli hutegemea kuwepo kwao kwa uwezo na nguvu za haya masanamu yasiyo na uhai?” Hata hivyo, tangu Bilal alipozaliwa aliona masanamu yanaheshimiwa. Aliwajibika kukubali maneno ya waabudu masanamu lakini hakutosheka na roho yake haikuwa na raha. Kila siku alikuwa na huzuni na kufadhaika alipoyafikiria na hiyo ilimfanya awe na mawazo zaidi.

MFADHAIKO WA BILAL Kila siku jua lilipochomoza kutoka nyuma ya milima na kuwa mkabala na shughuli na ghasia za binadamu ambao kila mmojawao alishika njia yake. Hata hivyo, mfadhaiko na maovu ni hali ambayo haikuwaacha watu wa Makka kwani akili zao ziliendelea kutafakari. Walifikiri wakati wa usiku, walikusanyika wakati wa mchana na kusambaa jioni. Hakuna kingine isipokuwa uchovu na huzuni hali ambazo zilizidi kuwasumbua. Bilal hakukaa pembeni mwa mikusanyiko hii, alitafakari wakati wote wa saa alizokuwa peke yake. Kuna wakati alifikiria

Tafsiri -e-Ithna ‘Ashari, Juz. 12, uk. 157. 5

6


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

kwa makini sana wito wa Mtukufu Mtume na wakati mwingine pia alifikiria kuhusu imani yake pamoja na ile ya wengine. Bilal alifadhaika kisaikolojia na hakujua afanye nini na achague njia ipi. Kuna wakati fulani alisema: “Huu wito wa Muhammad (s.a.w.w) unatosheleza akili ya mtu. Hata hivyo, haiwezekani kwa jamii ambayo imekuwa inapiga magoti kuyaabudu masanamu kwa muda mrefu sana inaweza kuacha kukiabudu kitu hiki?” wakati mwingine alisema: “Endapo washindani wanaruhusu, inawezekana imani hii ikaendelea. Hata hivyo, mtu mmoja anaweza kufanya nini mbele ya dunia ya waabudu masanamu?” Baada ya muda fikra yenye nuru iliangaza na kupenya kwenye akili ya Bilal, roho ya ubinadamu iliamshwa mwilini mwake, dhamira yake ikachochewa na akateta peke yake: “Inaonekana Mjumbe wa Mwenyezi Mungu yu sahihi. Analosema lazima liwe sahihi.” Dhoruba iliamshwa kutoka kwenye kina cha moyo wake. Ilionekana kama vile Bilal alifika kwenye dunia nyingine na roho yake ikaruka na kwenda juu kwenye upeo wa anga, kwenye milima na majangwa, na pembezoni mwa makonde na viunga, misitu midogo ya mitende ya kijani na ikaleta taarifa kwamba anga hizi na nyota zing’arazo, mikusanyiko ya makundi ya nyota na mfumo huu mdogo unavyovitawala, kuchomoza na kuchwa kwa jua na mwezi, hii miti ya kijani na mashamba haya mapya na kuwepo kwa misimu minne na kuumbwa kwa binadamu, wanyama na mimea, havitegemei masanamu yale yasiyo na uhai na kwa uhakika Mola wao Mlezi ni mwingine.

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

akasema: “Nimepata! Nimepata! Nimepata kitu ambacho kimeweka mawazo yangu katika shughuli ya muda mrefu. Loo, nimekosea kiasi gani!” Haya masanamu yasiyo na uhai yanaweza kuwa waumbaji wa ulimwengu huu mzuri? Mawe haya ambayo yamechongwa kwa mikono yetu yanaweza kuwa waumbaji wetu wa dunia na mbingu zote? Inawezekana sanamu likaleta mchana na usiku, masanamu haya yanaweza kutimiza mahitaji yetu? Masanamu haya yasiyo na uhai yanaweza kuingilia kati mfumo hata ulio mdogo sana wa dunia hii? Hapana! Hapana kabisa. Masanamu haya hayana uwezo wa namna yoyote. Nimekosea. Dunia imekosea. Lazima niende nimuone mjumbe wa Mungu ambaye ametangaza wito huu wa kutia moyo kwa wanadamu. Ninaweza kusoma ukweli huu kwenye uso unaong’ara kimalaika wa Mtume. Ninampenda kwa dhati ya moyo wangu. Ni mtu muadilifu ambaye amejitenga na jamii chafu ya leo. Ndiye tu mtu ambaye hajaanguka mwenye tope la fikra chafu inayonuka vibaya. Mikono ya kihalifu ya jamii haijamshinda nguvu. Ndiye tu mtu ambaye hajashika njia na tabia za jamii na kwa ujasiri amejitenga na watu waovu na ametumia muda wake mwingi akiwa pangoni huko mlimani! Inaonyesha kwamba aliiona jamii imechafuliwa sana hivyo kwamba hakutaka kuishi miongoni mwao na akapendelea maisha ya pango la mlima kuliko yale ya wakosaji na hali ya mazingira machafu ya jiji.

Bilal alinyanyua kichwa chake na kutazama juu mbinguni na

Alijua kwamba mtu bora hawezi kuishi katika jamii chafu na yeye ambaye amejitenga na fitina na matendo maovu, ndiye tu mtu ambaye anaweza kuongoza jamii hii yenye maovu.

7

8


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

KUELEKEA BAHATI NJEMA Jua lilichomoza polepole na kuashiria kuwa siku hiyo ni ya joto sana. Kwa sababu ya joto kali sana watu waliketi kwenye kivuli cha kuta za nyumba. Taratibu mitaa ilipungua wapita njia na baadaye hawakuonekana kabisa barabarani. Mara chache ombaomba au wahamahamaji ambao walikuja mjini walionekana wakishughulika na mambo yao. Bilal alitoka nje ya hekalu la masanamu akiwa na matumaini kwamba wakati huu wa upweke huenda angekutana na rafiki yake. Dalili za uchovu zilionekena wazi wazi usoni mwake na ilithibitika kwamba mawazo mapya yaliingia akilini mwake. Joto kali halikumwathiri. Ilionekana kama vile hakuhisi kwamba hali ya hewa ilikuwa ya joto kali. Alipita kwenye mitaa, mtaa moja baada ya mwingine, alivuka barabara na akawasili msikiti wa Masjidul Haram. Alikwisha sikia kwamba wakati wa adhuhuri Mtukufu Mtume alikuwa akimwomba Mwenyezi Mungu pembezoni mwa Al-Kaabah, na hii ilikuwa sehemu nzuri ya kumuona bila watu wengi kujua. Bilal alipoingia Masjidul Haram alimwona Mtukufu Mtume (s.a..w.w) akiwa na binamu yake Imam Ali (a.s) wakiwa wamesimama bega kwa bega huku wakisali. Bilal akashusha pumzi. Mapenzi kwa Mtukufu Mtume yalifunika kiwiliwili chake chote. Machozi ya furaha yalitiririka na kudondoka. Alitamani kwenda karibu naye na kumkumbatia, lakini ilionekana kama vile mtu fulani alikuwa anamwambia kwenye kina cha moyo wake: “Ngoja. Uwe mvumilivu. Inawezekana kwamba mtu fulani anaweza kukuona na jambo hili linaweza likachukua hali nyingine ya hatari!” Moto wa mapenzi ulikuwa unawaka ndani wake. Hakutosheka 9

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

na kutazama uso wa Muhammad wenye hali ya kimbingu. Hakutazama kuelekea upande mwingine wowote. Alikuwa anateta ndani ya moyo wake miongoni mwa mioyo: “Huyu ni mtu anayeweza kutuongoza sisi watumwa kuelekea kwenye ustawi. Ni mtu ambaye ameleta habari za Muumbaji wa ulimwengu huu mzuri na ni yeye ndiye mwenye ujumbe wangu kuhusu kile nilichokipoteza…” Bilal alikuwa amezama kwenye mawazo na macho yake wakati wote yalikuwa yanamwelekea Mtume (s.a.w.w). Mtukufu Mtume na Imam Ali walinyanyuka baada ya kumaliza kuswali lakini Bilal alibakia pale pale alipokuwa. Inawezekana kusema kwamba alipoteza fahamu kwa kumwangalia Mtukufu Mtume. Baada ya muda alikwenda kumwona na akaushika mkono wa Mtukufu Mtume na akaubusu. Aliukubali Uislamu kwa kutamka ‘Shahadatayn’ (akishuhudia kumwabudu Mungu mmoja na Utume wa Muhammad)7 na kwa hiyo idadi ya Waislamu iliongezeka kwa mtu mmoja.

MWISLAMU WA KWANZA KUTOKA ETHIOPIA Kabla ya kupita siku nyingi tangu Mtukufu Mtume alipotangaza wito wa Uislamu kwa watu, na idadi ya Waislamu ilikuwa haijazidi arobaini, pale Bilal, mtumwa wa kutoka Ethiopia, alipokubali wito wa kuingia kwenye Uislamu na akakanyaga mguu wake kwenye njia ya kweli na yenye ubora.

7

Ash-hadu an la ilaha illa lah wa ashhadu anna Muhammadar-Rasulullah. (Nashuhudia kwamba hakuna Mungu ila Allah na Muhammad ni Mjumbe Wake.) 10


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Washindani wa Mtukufu Mtume pia waliogopa sana kuhusu Uislamu kupenya kwenye nyoyo za watu wengi. Kila siku walichukua watu wapya na hawakutegemea kabisa. Kwamba pamoja na matusi yote na kukandamizwa mkuu wa wito huu angeendelea kuwepo katika jamii kwa muda wa siku chache, kwa sababu watu walikwisha kuwa na tabia ya vitendo viovu na hawakuelekea kukubali ukweli na uhalisi kwa haraka hivyo na kutii mwongozo kutoka mbinguni. Palikuwepo na kundi dogo tu la watu katika jamii hii ilioyochafuliwa ambalo liling’ara na halikuzama kwenye tope la jamii iliyo na maovu. Maadili yao yaliongezeka kila siku na walikubali uhalisi wa jambo hili kama dhahabu isiyochanganyika na metali nyingine. Palikuwepo na vito ving’aravyo vya ubinadamu. Hivi vilikuwa mifano kwa ubinadamu. Ingawa idadi yao ilikuwa ndogo walikubali wito wa Mtukufu Mtume wa Uislamu kwa uaminifu kamili. Walipatwa na shida, walikabiliana nazo kishujaa kwa ajili ya imani yao na wakalinda utukufu huu kwa ajili yao kwa nyakati zote zijazo. Roho zao zineemeshwe kwani pamoja na matatizo yote, walifuata mwongozo huo wa peponi na ukamkomboa mwanadamu asiangamie. Kama mambo yalivyo, mtu wa kwanza kukubali wito wa Mtukufu Mtume wa Uislamu alikuwa binamu yake Imam Ali alikuwa mwarabu, na wa kabila la Quraishi na baada ya kukubali Uislamu watu wengine walifuata. Hawa ni pamoja na Salman Farsi (Iran), Sohayb kutoka Rumi,

11

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Bilal kutoa Afrika na Khubab kutoka Nabat.8 Ingawa Bilal alinasa kwenye makucha ya mmojawapo wa maadui sugu wa Mtukufu Mtume wa Uislamu na alikuwa anafuatilia nyendo zake kwa kila njia, mapenzi yake kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.) na dini ya Uislamu halikuwa jambo lisilo na thamani, hivyo kwamba angeacha imani yake kirahisi. Inawezekana kusemwa kwamba Bilal alibeba mabegani mwake bendera ya uhuru wa watu wote walio weusi na machotara. Alikuwa mtu wa kwanza kunyanyua sauti yake kwa ajili ya uhuru wa watu weusi, na alilidhihirisha jambo hilo kwa ulimwengu uliojaa ukandamizaji na ukatili kwamba hakuna tofauti kati ya mtu mweupe na mweusi. Mwenye uso mweusi na uso ulio elimika na moyo unaong’ara, na wasi wasi na mateso ambayo ilibidi ayapitie na kuyastahamili, alisema ukweli kwa sauti pana na aliufanya ujumbe wa Uislamu ufike kwenye kila sikio. Ujumbe ulisikika sana hivyo kwamba aliwashangaza wale waliokuwa wanaupinga Uislamu, na nyumba ambayo ndimo alimofanya kazi kama mtumwa kwa ajili ya imani yake iliyo thabiti na imara.

SURA YA UKWELI Tangu Bilal alipokubali kuwa Mwislamu alizidi kujitenga na watu na alitumia muda wake mwingi kutafakari juu ya imani hii mpya. Alipenda kuomba dua kwa Mwenyezi Mungu na akaendeleza hali ya akili ya kiroho. Alifikiri yeye mwenyewe: “Ni kiasi gani watu wamekosea 8

Rijal Ma maqzani uk. 182; Nafasur Rahman; sura ya 10; Ayanush Shiah uk. 147 na Tabafat bin Sa’d Juz. ya tatu, uk. 165. 12


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

hivyo kwamba wanaabudu masanamu haya badala ya Mwenyezi Mungu na kutoa sadaka na vitu vingine, ingawa hayawezi kufanya lolote!”

fumbo: “Labda Mtume wa Mwenyezi Mungu anasema ukweli. Yupo mtu ambaye amekwisha sikia uongo kutoka kwake hadi sasa?”

Bilal aliona ufukara na bahati mbaya ya watu na alistaajabu sana kuhusu jambo hili, kwa sababu hakujua afanye nini ili watu waweze kwenda kwa Mtukufu Mtume na kukubali wito wake kwa Mungu.

Mazingira machafu ya jiji yaliyojazwa uovu na kutokuwa na uwezo wa kujizuia ambayo yalifurika kila sehemu na yalikuwa yanawaingiza kwemye uovu vijana kila siku, na wenye kuendesha sehemu za kufanyia uovu kwa ujasiri walikuwa wanayaweka mawazo ya watu, miili yao na roho zao kwenye hatari mbali mbali na kwa hiyo walikuwa wanaitendea jamii mambo yasiyofaa9 walimhuzunisha sana Bilal na alijisemea mwenyewe: “Ee Mola wetu Mlezi! Lini watu hawa watakuwa wazingativu? Ee natamani wote wangekuwa huru! Kwa nini iwe kwamba wote wanaochafua jamii wawe huru, lakini Mtume wa Mwenyezi Mungu na marafiki zake waingizwe kwenye matatizo? Hali hii haitaendelea kuwepo.”

Kila aliposikia kwamba wazee wa jiji walikuwa wanafanya upinzani dhidi ya Mtukufu Mtume na walikuwa na uhasama naye alishusha pumzi na alisikitika sana na alishangaa kwa nini watu hao (wapinzani) hawakuweza kutambua ukweli. Wakati wowote alipokutana na wazee na mabwana wamiliki wa watumwa wenye kupenda umwagaji damu aliwaangalia kwa jicho la kinyongo. Wakati wowote alipowaona mabwana, na malodi lofa wenye mvuto, moyo wake ulijaa chuki na maudhi dhidi yao kwa sababu ya wao kuwa na uhasama dhidi ya Mtukufu Mtume na wafuasi wake, walifanya maisha ya watu wote kuwa ya taabu. Walizuia njia ya watu na hawakuruhusu watu kupata ustawi na uongofu. Akajisemea mwenyewe: “Hawa wazee na watemi wa makabila wanataka nini kutoka kwenye maisha ya watu? Kwa nini wasiache tabia zao za ubinafsi na kuwa sababu ya watu kubakia kwenye umasikini na uovu uliokithiri? Watu wamekosea nini hivyo kwamba wameangukia kwenye fumbato la hawa wababe wenye kupenda umwagaji damu.”

“Kusema ukweli moyo wangu unapwita na kufa kwa ajili ya huzuni ninapoona kwamba wezi na fisadi wapo huru lakini Mtume wa Mwenyezi Mungu anao maadui wengi kweli, na watu wenye akili bora na tabia yao kuwa taa zinazoangaza wanateswa na watu wabaya. Ole wao wanaozima taa ya mwongozo na wanapambana katika giza la ujinga.” Bilal alitafakari na kuumia sana na hakutaka kushuhudia makosa, ukatili na uovu, kwani kama alivyosema mshairi: “Jicho lenye haki haliwezi kuona chochote isipokuwa ukweli.”

Wakati wowote alipokutana na marafiki zake na jamaa zake, alitamani kuwaongoza. Hata hivyo hakuweza kuwa na ujasiri wa kuzungumza nao moja kwa moja, lakini alisema kwa 9

13

World ina danger of decline, uk. 51. 14


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

MKUTANO WA MAADUI Kama ilivyosemwa hapo juu, wazee wa Makka walifadhaika sana waliposikia kuhusu wito wa Mtume (s.a.w.w.) na sura mpya ilifunguliwa katika maisha yao yenye uchungu. Walizungumza wao kwa wao: “Juu ya Muhammad kuja kwenye uongozi wa mambo na dini yake ya kuamini Mungu Moja kunavyozidi kusonga mbele, tutapoteza heshima na nafasi katika jamii ya watu wa Makkah na sehemu zingine, na baada ya muda mfupi hali ya jamiii itabadilika. Lazima tuchukue hatua ili kwamba sauti hii ya kuabudu Mwenyezi Mungu Mmoja ina nyamazishwa na tatizo hili linaweza kutatuliwa!” Walikuwa na lengo hili katika mtizamo, wazee wa Makkah walikusanyika mahali kila siku na kubadilishana mawazo ili waweze kupata ufumbuzi wa tatizo hili kwa msaada wa kila mmoja wao. Sehemu hii (darun Nadwah) lilikuwa bunge la wakati huo ambapo matatizo yote ya makabila ya Waarabu na wazee wa Makkah walikutana hapo na mawazo yaliyotolewa na kila mtu yalipewa uzito unaostahili.10 Ni watu hao tu ambao umri wao ulikuwa chini ya miaka 4011 na walioamini kanuni za ujahilia na ibada ya masanamu na wakumpinga Mtume wa Uislamu wangeweza kuhudhuria mikutano hii mara nyingi sana hivyo kwamba hapangekuwepo na mtu yeyote katika familia zao ambaye alikubali kuwa Mwislamu. Umayyah, bwana mmiliki wa Bilal, alikuwa mmojawapo wa 10 11

History of Civilization by Georgie Zaidan, uk. 20. History of Civilization by Georgie Zaidan, uk. 20. 15

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

watu waliohudhuria mikutano hii bila kukosa na mara nyingi alikuwa akitoa hotuba kali na zenye vitisho vya kumwangamiza Mtukufu Mtume (s.a.w.w), kwa sababu alikuwa miongoni mwa maadui sugu wa Mtume wa Uislamu. Siku moja wakati walipokuwa wamefanya mazungumzo na kila mmoja wao alisema kuhusu jambo hili au lile na maamuzi mbali mbali yalifanywa na mawazo yalikuwa yanabadilishwa miongoni mwa wawakilishi, Umayyah alikuwa mkali zaidi kuliko wenzake wote katika kutafuta njia ya kuuzima Uislamu. Wakati huo mtu moja alimwendea akaketi karibu naye kimya kimya na alimwambia kwa kumnong’oneza sikioni mwake: “Niruhusu nikwambie jambo, kwa sababu ninaona kwamba unaongea kwa nguvu sana na unaonekana kuwa makini zaidi ya wengine.” Umayyah alikubali na akamjibu: “Hakuna madhara. Tafadhali sema. Tunatakiwa kufanya juhudi zaidi kuliko hivi sasa ili tuweze kukomesha hali hii isiyopendeza, katika muda mfupi ujao.” Mgeni alianza kuzungumza kwa kusema: “Ninaelewa kwamba sharti la kumfanya mtu ahudhurie na kushiriki kikao hiki ni kwamba watu wanaohusika lazima wawe waabudu masanamu na pia pasiwepo hata na mtu mmoja katika familia zao ambaye amekubali Uislamu.” Umayyah akamwangalia Mwarabu huyo kwa hasira na kusema: “hivi mimi ninao upungufu wowote kuhusu jambo hili au mtu yeyote ambaye ana uhusiano na mimi amekuwa na upungufu huu?” Mpelelezi akasema: “Nimepata taarifa kwamba mmojawapo wa 16


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

watumwa wako amekubali kuwa Mwislamu!” Umayyah akasema: ‘Nyumbani mwangu? Mtumwa wangu? Ni kweli nyumbani mwangu? Mtumwa yupi kwani ninao wengi? Umesikia habari hizi kutoka kwa nani? Endapo taarifa hii ni sahihi adhabu ya mhusika ni uhai wake, lakini kama si sahihi nitakuadhibu haraka sana kwa kukata kichwa chako kwa mashataka yasiyo ya kweli! Ninao uhakika si kweli. Hapana yeyote nyumbani kwangu anaweza kufanya hivyo kwa ujasiri.” Mpelelezi akasema: “Mambo kama yalivyo jambo hili limefanyika nyumbani mwako na ni mtumwa wako ambaye amefanya hivi. Mimi sisemi uongo. Ni kawaida yake kukutana na Muhammad wakati wa mchana na usiku.” Umayyah alisimama, akaunyanyua mkono wa mpelelezi na akaondoka mkutanoni huku akisema: “Ni vema tungezungumzia jambo hili nje, isije mtu mwingine akasikia.”

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Heshima yangu imetiwa dosari. Kama siwezi kuwa makini na mambo ya nyumba yangu nitawezaje kuwakosoa wengine?” Umayyah alikwenda nyumbani kwake akiwa amevunjika moyo, mwenye hasira na wasi wasi.

UCHUNGUZI KUTOKA KWA BILAL Akiwa njiani anakwenda nyumbani kwake na fikira zinazoashiria kejeli, akitetemeka kimya kimya: “Huu ni uongo ulioje! Bilal anaweza kuwa na ujasiri wa kufanya hivi? Hata kama angekuwa amefikiria tu, pindi tu ambapo angetambua kwamba jambo hili halifurahishi, angeaecha. Anatambua tabia yangu!” Umayyah alipofika nyumbani kwake aliita kwa sauti ya kishindo: “Bilal…… Bilal!”

Mpelelezi akajibu: “Ndio, Bilal. Mimi mwenyewe nimemuona kwamba hukutana na Muhammad katika faragha na ana uhusiano mzuri naye.”

Aliposikia sauti ya mmiliki wake, Bilal alikwenda kwake haraka, akamsalimia na kusimama wima. Watumwa wengine walikuwa wanaangalia huku na kule. Bilal aliwahi kumuona bwana wake akiwa katika hali hiyo mara chache sana. Akatambua kwamba Umayyah alikwisha sikia kuhusu yeye kuwa Mwislamu. Uso wake ulisawajika na akaanza kutetemeka na kuingiwa na woga. Akanong’ona peke yake. “Ee Mola wangu Mlezi! Njoo unisaidie sasa, kwa sababu mtu huyu mkali amekwisha gundua siri yangu.”

Dalili za hasira zilionekana usoni mwa Umayyah na rangi yake ikabadilika. Macho yake yakageuka kuwa mekundu. Akatetemeka na kulalamika na akajisemea mwenyewe: “Inawezekanaje mtumwa akawa jasiri na kuonyesha imani kwa Muhammad? Kama habari hizi ni sahihi basi atalipa kwa kifo.

Umayyah akasema kwa sauti ya kutetemeka na kali: “Bilal! Haya ni mambo gani ambayo watu wananiambia kuhusu wewe? Nasikia kwamba umeingia kwenye dini ya Muhammad, mtoto yatima. Umefuata mambo haya ya kipumbavu? Unawezaje kudiriki yote haya? Hujui kwamba wewe ni

17

18

Mgeni huyo akafuatana na Umayyah na alisema: “Kama mambo yalivyo, mmoja wapo wa watumwa wako aitwaye Bilal amemwamini Muhammad!” Umayyah alishangaa kusikia habari hi na kusema: “Bilal?”


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

mtumwa wangu? Hujui kwamba huna uhuru wa chaguo?” Pole pole sauti ya Umayyah ilizidi kwenda juu zaidi. Wote wale waliokuwepo nyumbani walianza kutetemeka kwa hofu na woga. Rangi ya Bilal ilififia, kama vile dunia ilikuwa nyeusi kwenye macho yake na akakabiliana uso kwa uso na mlima wa matatizo. Hata hivyo, alisimama kwenye kona akiwa kimya. Umayyah aliendelea kutamka maneno makali na akasema: “Kwa haraka iwezekanavyo lazima ukane ambalo umelifanya na utubu na umtukane yatima Muhammad ambaye ni mwendawazimu. Umenivunjia heshima yangu. Hakuna mtu yeyote ndani ya nyumba yangu angekuwa jasiri hadi kuweza kufanya hivi.” Ingawaje Bilal hadi wakati huo alikuwa bado hajajipa moyo kuwa na ujasiri wa kusema na hakuweza kutoka jibu kwa kusema na hakuweza kutoa jibu kwa yale aliyokuwa anasema bwana wake, lakini kwa kuwa alikwisha onyesha hakumuogopa yeyote isipokuwa Yeye, na aliona uwezo wote dhaifu si lolote ukilinganishwa na uwezo wa Mwenyezi Mungu, alijitikisa na kusema: “Nimekwisha toa tamko la imani na siogopi na sitaikana imani yangu. Mimi ni mtumwa wako, lakini kuhusu jambo la imani nipo huru.”12 Maneno ya Bilal ya kusisimua yalikuwa hayajaisha ambapo Umayyah alimwendea haraka na kwa hasira na kuingilia kati sauti dhaifu ya Bilal kwa mikono yake yenye nguvu. Aligandamiza koo lake kwa nguvu sana hivyo kwamba alikuwa karibu ya kufa! Halafu akamvurumishia mapigo mengi sana.

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Upande wowote alikogeukia Bilal, alipata pigo kali mwilini mwake. Muda mfupi baadaye muumini wa kwanza wa imani ya Mungu Mmoja kutoa Ethiopia alizirai na kuanguka chini kwenye kona. Umayya alionyesha dalili za wasiwasi na alizunguka na kusema: “Alaah! Huyu Muhammad amefanya nini? Amepenya majumbani mwa watu na watumwa kwa nini wazee wa Makkah hawachukui hatua ya kukomesha janga hili: endapo Muhammad huyu ataendelea kuwepo atayafanya maisha ya watu kuwa machungu. Alaaah! Ni muda ulioje uliopo sasa! Mtumwa amekusanya nguvu nyingi sana hivyo kwamba anasema mbele yangu na kutamka imani yake. Mtu huyu mnyonge hajui kwamba hatakiwi kusema na mimi.” Watu wote waliokuwa ndani ya nyumba walikimbia na kujificha sehemu mbali mbali huku wakitetemeka kwa hofu. Wakati mwingine walimlaani Bilal kwa sauti za chini chini kwa kumuudhi mmiliki wao. Waliogopa hivyo kwamba walidhani watumwa wengine pia wangeuawa. Kimya cha kifo kilitawala hapo nyumbani. Ni mrindimo wa kuhofisha sana wa Umayyah na wakati mwingine kilio cha kurarua moyo cha masikitiko ya huzuni ya Bilal ambaye alikuwa amelala kwenye kona kutokana na maumivu makali, yalivunja kimya hiki na kudhihirisha hofu kwenye nyumba hiyo. Hapana mtu aliyeweza kusema. Kwa mara nyingine tena Umayyah alivunja kimya na kusema kwa sauti ya hasira: “Ninaapa kwa jina la Lat na Uzza13 kwamba kama mtumwa

12

Stories from the Qur’an about the Holy Prophet uk. 330 19

13

Lat na Uzza walikuwa masanamu mawili makubwa waliowekwa kwenye 20


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

huyu hatakanusha alichosema nitamuua kwa njia mbaya kupita njia zote ili wengine watambue kwamba hawana uwezo wa aina hiyo.” Dalili za uchovu na kero zilionekana wazi usoni mwa Umayyah. Kwa sababu ya unyong’onyevu mkubwa alijilaza kwenye kona. Hali ya hewa ya joto ilikuwa inamsumbua na hasira ilizidi kuwa kali katika kiwiliwili chake na kumchochea zaidi. Hata hivyo, hakuwa na nguvu zaidi za kutosha kuendelea kufanya lolote. Akajisemea mwenyewe: “Endapo mtumwa huyu hatakufa, hakika atakana kile alichosema. Bila shaka atakana. Hata hiyvo, jambo hili lazima lipewe uzito wake unaostahili na wazee wote wa Makkah lazima wapewe tathmini ya hatari iliopo ili waweze kujua kitu ambacho Muhammad amekifanya.” Wakati mwingine alitafakari: “Kitu hiki si kizuri kwangu, kwa sababu watu watang’amua kwamba mimi sina mamlaka ndani ya nyumba yangu. Hata hivyo, baada ya Bilal kurudi kwenye imani yake ya zamani au akiuawa, watatambua kwamba utawala wangu upo ndani ya nyumba yangu.” Umayyah alitaka kupumzika lakini mawazo yake yaliyomsumbua na fikra na hisia kali zilizokuwa zinagongana akilini mwake hazikumruhusu kulala. Watumwa wote na wasichana watumwa walipokwenda kazini kwao. Mtu mmoja tu asiyekuwa na msaada, Bilal alikuwa amelala kwenye kona na alikuwa analia. Damu ilikuwa Al-Kabah walikuwa wanaheshimiwa na waabudu masanamu (Tafsir - ewal- Asr, uk. 84). 21

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

inamtoka kwenye kichwa chake na uso na hakuna mtu aliyeonyesha kuhusika hata kidogo. Watu wote walisema: “Bilal amejiua kwa mikono yake mwenyewe. Wakati huu si wa kufanya mambo kama haya. Ukiacha mtumwa kama Bilal, hata wakuu wa Kiarabu hadi sasa hawakubali dini hii.” Kila mmojawapo alisema na kutamka maoni yake kuhusu suala hili.

DINI NI JAMBO LA HIYARI Baada ya saa kadhaa Bilal alijitikisa na akapoteza fahamu zake tena. Aliporudiwa na fahamu zake, machozi yalitiririka kutoka machoni mwake. Alitazama huku na kule lakini hakuona mtu yeyote ambaye angemsaidia. Kila upande wa hapo nyumbani alimuona shetani wa uoga amesimama kwa kilachi zake za moto na kujigamba. Mwili wote wa Bilal ulitapakaa damu. Ilionyesha kama vile mifupa yake yote ilivunjwa na hakuwa na nguvu za kutosha kumwezesha kwenda popote. Angefanya nini? Angekata rufaa kwa nani? Alinyanyua macho yake yaliyofunuka nusu na yaliyojaa machozi na kutazama mbinguni na kusema huku akiwa na moyo wa majonzi makubwa: “Ee Mwenyezi Mungu! Njoo unisaidie. Ee Mwenyezi Mungu wa watu! Ee Muumbaji wa ulimwengu! Mimi sina hatia. Ee Mweza Mola wetu Mlezi …..” Bilal alilia mfululizo. Machozi yalikuwa yanamtoka lakini hakuweza kusogea kutoka pale alipokuwa. Alikuwa anangojea kuona nini kingetokea kwake. Umayyah alinyanyuka kutoka pale alipokuwa na nyusi za macho yake zikiwa zimenyanyuka na macho yake kama vikombe viwili vya damu na akamwendea Bilal. Alikuwa 22


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

anategemea kwamba Bilal angesema haraka sana: “Ewe bwana wangu: najisalimisha kwako. Najuta kwa kile nilichofanya. Nina mwamini Lat na Uzza! Baada ya hapa sitakwenda kwa Muhammad.” Alimkodolea macho Bilal na akangojea kuona angesema nini baada ya kurudiwa na fahamu. Alifumbua macho yake yaliyojaa machozi na wakati machozi yakiwa yanatiririka kutoka machoni mwake alijitikisa na kusema: “Mpendwa bwana wangu” na akapoteza fahamu zake kwa mara nyingine. Umayyah akaonekana kufurahi na akasema: “Inaonyesha kama vile amekwisha rudi kwenye imani yake ya zamani na anataka kutubia. Hata kama akirudi kwenye imani yake ya zamani lazima apigwe kwa gongo ili kwamba asije akafikiria kutamani kufanya kitendo hiki tena. Bilal akarudiwa na fahamu na akasema: “Bwana! Imani yangu haihusiani chochote na wewe. Imani yangu kwa Muhammad si dhambi na haikuleta dosari yoyote kwenye kazi yangu.” Umayyah hakutegemea kusikia maneno haya na yaliingia kwa kishindo kikubwa masikioni mwake hivyo kwamba ilionekana kama vile dunia iliingia giza machoni mwake. Akasema kwa sauti ya mshindo: “Ewe mtu mwenye bahati mbaya! Hujui ya kwamba wewe ni mtumwa wangu? Akili zako, roho yako, na mwili wako vyote hivi ni mali yangu. Moyo wako hauruhusiwi kuonyesha imani nyingine yoyote kama uipendayo. Fikra zako hazina uhuru wa kuendelea upande wowote zinakotaka.” Bilal akasema: “Ni kweli kwamba mimi ni mtumwa wako na mimi pia sikatai jambo hili. Sana tena sana hivyo kwamba ukiniamuru kutembea kwenye majangwa wakati wa usiku

Bilal Wa Afrika

nitafanya hivyo. Na kama ukiniamuru kwamba wakati wa mchana lazima nibebe mawe mazito mabegani kwangu wakati wa joto la mchana, nitafanya hivyo bila kuonyesha uchovu wowote. Hata hivyo, akili zangu, fikira zangu na imani yangu hivi si vitu vyako, na si vitu ambavyo vinaweza kumilikiwa na wewe. Lazima nifanye kazi zangu ingawa imani yangu inaweza kuwa tofauti na imani ya bwana wangu. Imani ni hiyari.” Umayyah ambaye alikuwa anatetemeka kwa hasira akasema: “Hapana! Hapana! Kila kitu chako ni mali yangu! Imani yako na fikra zako ni mali yangu na hata matamshi ya ulimi wako yapo kwenye udhabiti wangu. Nitakupa kipigo kikali sana ili uondoshe imani hi kutoka kwenye moyo wako na akili.” Baada ya kusema hivi Umayyah alimshambulia Bilal kama ibilisi na akampiga sana hivyo kwamba alionekana kama maiti.14 Kweli madhalimu wanataka kufanya nini na watu wasio na msaada? Hawa watu wakali wanatamani nini kutoka kwenye uhai wa taifa? Hadi kwenye kiwango gani hawa watu wenye ubinafsi wamejitayarisha kufanya fujo kuwafutilia mbali watu wanyonge? Ni kosa limefanywa na Bilal na wengine kama yeye? Je, kuonesha imani kwenye utakatifu ni dhambi na kwa sababu hiyo mtu apate adhabu ya kifo? Je, ni muhimu kwamba kusema kweli na kuitetea kweli lazima igharimu uhai wa mtu? Bilal alifanya uovu gani na alifanya kosa gani hivyo kwamba

14

23

Bilal Wa Afrika

Stories from the Qur’an kuhusu Mtukufu Mtume uk. 330. 24


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

alilazimika kuteswa hivyo? Kama mambo yalivyo ambavyo madikteta na watu wa koo bora ambao wamekuwa wana wagandamiza watu tangu zama za kale walipoona mamlaka yao na ubwana wao upo hatarini na hawangeweza kuwatawala watu wasio na msaada kama mwanzo na hawakuweza kutawala maisha yao, mali zao heshima ya watu, walijionyesha kwa njia hii na walifanya maovu dhidi ya watakatifu na watu wa kimungu.

NJOZI ZA KISHETANI Kwa sababu ya wasiwasi mkubwa sana, bwana wa Bilal hakuweza kupata amani na raha na alionyesha kama vile alikua anapigana na milango na kuta na ardhi na mbingu. Popote alipokanyaga alihisi shinikizo zito zaidi na dunia ilionekana yenye giza kwake. Umayyah alijisemea peke yake; “Ni mateso makubwa yalioje yameikumba jamii! Hata mtumwa anafanya madai yasio na busara kutoka kwa bwana wake. Ni dini gani hii? Muhammad huyu anasema nini?” wakati mwingine pia alijisemea mwenyewe: “Nitamuua mtumwa huyu ili niweze kupata raha na wengine watatambua pia ninao uwezo kiasi gani!” Alipohisi wasi wasi mkubwa aliamua kuondoka nyumbani kwake na kwenda kukutana na wazee na watemi wa jiji na wawakilishi wa bunge na kuwaarifu kuhusu nini kinachoendelea. Kwa kutoka nje pia alikuwa anaondoa uchovu na wasi wasi kwa kiasi fulani na kupata nguvu mpya ya kumtesa mtu mnyonge.

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

wasiwasi huu. Alikwenda kuwaona wazee wa jiji na kuwapa tathmini ya hatari hii kubwa na halisi. Alikwenda kutafuta jinsi ya kumwangamiza Muhammad, Mtume wa Uislamu na wafuasi wake. Alikwenda kutoa maelezo kwa watu wa tabaka lake wenye ujasiri dhidi ya watumwa wanyonge ili kwamba watu wengine wangeweza kumpa msaada wa kupata suluhu ya tatizo lake. Baada ya saa chache ambapo Umayyah aliwaona wazee wa Makkah na kuwaeleza kuhusu wasi wasi wake, alirudi nyumbani na kumuona Bilal bado amelala kwenye kona kama maiti. Alitikisa kichwa na akamwambia Bilal: “Unamwamini Muhammad?” Halafu akaingia nyumbani mwake ili apumzike. Hapana mtu yeyote ambaye angekuwa jasiri na kuanza kusema. Kimya cha kifo kilitawala hapo nyumbani! Hata hivyo, Umayyah alikuwa anasema maneno yasiyoeleweka akiwa usingizini. Wakati mwingine alipiga kelele na kuingilia kimya kilichotanda hapo nyumbani kwake na wakati mwingine pia aliota jinsi Bilal alivyojuta na kukana imani yake kwa Muhammad. Ndoto hii ilimfurahisha Umayyah sana na aliamka kutoka usingizini lakini hakumwona mtu yeyote karibu naye. Hali hii ilimpa wasi wasi zaidi na akalala tena! Kabla ya kupatwa na usingizi mzito tena alimuona Bilal akitetemeka na kulia na akimtukana Muhammad na alimwomba bwana wake kukubali toba yake na amsamehe kosa lake.

Aliondoka nyumbani kwake ili atafute njia ya kuondoa

Umayyah aliruka haraka sana akiwa amefurahi sana lakini aliona kwamba hizo zilikuwa ndoto za kishetani na si zaidi ya hiyo. Hali hi iliongeza uchovu wake na kero kwake na akasema: “Natamani mtumwa huyu aniruhusu nilale

25

26


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

inavyostahihili. Ni ndoto za kishetani zilioje hizi ninazoziota?

Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema.15

Masikini mtu huyu aliketi na akakumbuka ule uamuzi wake mkali aliochukua dhidi ya Bilal na akasema: “Lazima nimwadhibu Bilal kwa tendo lake kwa sababu amefanya maisha, usingizi na kuwa macho yawe ni mambo yasiovumilika. Ni mateso yalioje ninayoyavumilia? Ni vipi kwamba kipande cha nguo yangu kimeshika moto kwanza? Ni maendeleo gani haya ambayo yamenitokea mimi tu?

Lakini! Kiasi gani mabwana na watu wajinga waliwagandamiza wale wanao wamiliki na hapana yeyote anayeweza kuja kuwaokoa! Kiasi gani wachoyo na wenye uwezo wamecheza na maisha, mali na imani ya watu na makosa mangapi wanayatenda kwa lengo la kukidhi tamaa zao za kimwili na kuishi maisha ya starehe! Na kiasi gani cha damu ya watu wasio na hatia imemwagika! Kila siku nafasi ya wakuu wa makabila na Waarabu wanaoishi kwa starehe inazidi kuwa na nguvu na uungwana wa kibinadamu unaendelea kwenye hatari.

KWENYE UPEO WA MATUMAINI Akiwa na taabu kubwa sana ambayo Bilal alipata kwa mara ya kwanza katika njia hii, akajitayarisha kwa mateso yasiyo na ukomo na akatambua kwamba huu ulikuwa mwanzo wa kujitoa mhanga. Alitambua kwamba kama alitaka kubeba bendera ya uhuru mabegani kwake na kupinga madikteta na majahiliya kwa mara ya kwanza hapakuwepo na lingine kuhusu yeye isipokuwa mateso, dhiki na wasiwasi. Hata hivyo, alikubali kuyapata yote haya kwa sababu ya mfumo wa mawazo yake na mapinduzi yenye thamani na hakuacha imani yake katika hali yoyote ile. Nguzo za imani ya Bilal zilikuwa imara sana hivyo kwamba dharuba hizi hazingezitikisa au kuziharibu. Mapenzi yake kupata uhuru hayakumruhusu kuacha imani yake kwa sababu ya shinikizo la muda mfupi na akubaliane na fikra za kipumbavu za Umayyah. Hata hivyo, kitu kimoja tu kilichomsikitisha na kumtesa Bilal ilikuwa upungufu wa hisia na kutokuwepo kwa uwajibikaji miongoni mwa watu wake ambao waliacha njia iliyonyooka na kuabudu masanamu yasiyo na uhai na mabwana zao dhalimu badala ya kumwabudu 27

Bila shaka Bilal aliweza kuona kwamba jamii iliwekwa kwenye poromoko la uharibifu na kila kitu kilikuwa katika hatari na katika hali ya kudhoofika. Kwa hakika mateso haya na mengine kwa mamia yalimuudhi Bilal na alitamani jambo moja tu kwamba watu wanyonge wangekomesha hali yao ya kusikitisha. Ilikuwa kwa sababu hii hivyo kwamba matamanio yake ya kutimiza azma hii, alivumilia mateso yote kwa ustahamilivu.

JELA NA KAZI NGUMU Umayyah aliamua kutekeleza mpango wake alioutayarisha wa kumwadhibu Bilal kwa uadui aliokuwa nao moyoni mwake dhidi ya Muhammad na wafuasi wake ili aweze kukidhi utashi wake na kufanikisha lengo lake. Alianza kumwadhibu Bilal kwa kumnyima chakula, kumpa

15

World in danger of decline uk. 33. 28


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

kazi ngumu za kufanya, na kumtoa nje ya nyumba. Pia alitoa amri kwamba hapana mtu aliyeruhusiwa kuwasiliana na Bilal au kumsikitikia.

wanamapinduzi wa Iran kusalimu amri, tuliona kwamba walisonga mbele wakiwa wameazimia zaidi na wakaupa pigo la nguvu ubeberu na unyonyaji.

Alidhani kwamba hii ilikuwa ni njia fupi sana kuweza kutimiza lengo lake na kama Bilal angenyimwa chakula na kama Bilal angepewa kazi ngumu na kama asingekutana na mtu yeyote, angejuta na kutubu na hakika angeacha imani yake, na angewajibika kumheshimu bwana wake na kumtaka amsamehe kwa makosa yake ya nyuma. Zaidi ya haya, ilikuwa ni wajibu kwa Bilal kufanya kazi alizofanya na kama angeshindwa angeadhibiwa. Kwa ujumla labda haya ni mateso makubwa zaidi ambayo yangeweza kumfanya mkosaji kusalimu amri na kumweka kwenye shinikizo kali.

Vyovyote vile, kinyume na matumaini yao, mbinu hii pia haikumwathiri Bilal. Aliendelea kustahamili kwenye jela yake na kazi ngumu na alidhihirisha imani yake ya Uislamu kwa ufasaha na kwa sauti ya kupaza zaidi.

Kama mambo yalivyo, madikteta na makabaila kila mara huishi kwenye vitendo vya aina hii ili kuweza kutawala jamii na taifa na kulinda uatawala wao na pia kupata matokeo yanayo ridhisha, kwa sababu njia moja tu ya kutawala mataifa yasiyo na uwezo ni kuzidi kuyafanya yawe dhaifu zaidi na kuyawekea shinikizo, njaa na umasikini, ili kwamba yaweze kufuata utashi wa makabaila, kuyadanganya, kufanya kwa mujibu wa utashi wa makabaila, na kuwa watumwa wao ili waweze kujaza matumbo yao. Wanafanya wanachosema na hupata wanachotaka na kwa programu hii huweza kufanikisha mipango yao ya uovu. Lakini Je, mpango wa uovu kama huo umewahi kupenya kwenye umma wa kiislamu pia? Wanaweza kulifanya taifa likajisalimisha pamoja na maadili yake na imani kwa njia ya shinikizo la kiuchumi? Hakika hapana, kwa sababu tumechunguza mfano unaofanana na vikwazo vya kiuchumi dhidi ya dunia inayoendelea. Walitaka kuwafanya Waislamu na 29

UTULIVU KWENYE MAKUCHA YA MINYORORO Bilal wa Ethiopia alipomaliza kazi zake ngumu na nzito, Umayyah aliamuru kwamba badala ya kupumzika na kula chakula, mikono na miguu yake lazima ifungwe kwa minyororo na atupwe miongoni mwa wanyama, na apewe chakula kidogo sana. Ni dhahiri kwamba Bilal aliteseka sana kwenye sehemu hizi zenye unyevu na giza na miongoni mwa mazizi ya wanyama na labda alikanyagwa kwa hiyo alipata maumivu makali sana na dhiki. Umayyah alidhani kwamba hii ilikuwa mbinu nzuri zaidi ya kumuua mtu kwa sababu mtu ambaye alifanya kazi nyingi sana wakati wa mchana akiwa na njaa na mwili uliochoka na akapitisha usiku wake wote akiwa amechanganikana na wanyama huku mikono na miguu yake ikiwa imefungwa kwa minyororo, haingekuwa rahisi kuendelea kuishi. Wakati mwingine Umayyah aliamuru kwamba miguu ya Bilal ingefungwa kwa kamba na aliwapa ncha ya kamba watoto ili wakimbie huku wanamvuta Bilal. Watoto walimvuta Bilal na 30


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

kumpeleka kushoto kulia, na mbele na kurudi nyuma, na pia alikimbia nao kwani kama angesimama angeanguka na watoto wangeendelea kumvuta na kumtupia mawe na mchanga.16 Lakini! Kiasi gani aliumizwa na kuteswa na ni udhalimu mkubwa na ukatili ulioje kwamba watu hao walifanya uhalifu wa aina hiyo ili waweze kulinda mambo yao! Palikuwepo na uhalali gani wa kumwadhibu mtu kiasi hicho kwa sababu hakuwa tayari kuwaheshimu watu sugu na masanamu yasiyo na uhai na kukubali fikra zao potofu na kupenda anasa? Kwa nini mtu aliumizwa sana kwa sababu tu alielewa ukweli na hakuwa tayari kupiga magoti mbele ya masanamu? Kwani imani si hiyari? Ni dhambi kuelewa ukweli? Kwa kweli hali ya hewa ya kunyonga iliyo tawala Hijaz na mafumbato ya wagandamizaji ilifika chini kwenye makoo ya watu pamoja na Bilal na hawakuweza kuvuta hewa kwa uhuru. Bilal alifanya nini? Kosa lake ilikuwa nini? Alifanya jambo gani baya? Ni uhalifu kukataa udikteta wa watu wengine na kukataa kuanguka chini mbele yao? Hivi jamii haitawaliwi na sheria? Ni sheria ipi inayoruhusu mtu akamatwe na makucha ya watu wenye ubinafsi kwa sababu ya kutangaza dini na kusema kweli na wagandamizaji wana kuwa huru kumuonea kwa njia zote za kikatili na udhalimu? Hakika, sheria na dhamiri hazitawali kwenye hali ya woga na hofu. Hata kama jambo linasemwa kuhusu sheria ni kuchochea tu na kulinda sheria na ubwana wa watu wachache. Na katika hali kama hiyo inashangaza kutegemea utekelezaji wa sheria.

16

Qiblah - e- Islam, uk. 691. 31

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Katika jamii za namna hiyo kama mtu anasema kitu ambacho hata kama ni sahihi, lakini hakiafikiani na matakwa ya watu fulani, bila kukawia anakamatwa, anafungwa jela, anapelekwa uhamishoni, anateswa na mamia ya maumivu na usumbufu!

UIMARA NA KUJITOLEA MHANGA Pamoja na dhiki zote, ambazo mtu huona aibu kusimulia, na ambazo Bilal alikutana nazo moja baada ya nyingine, aliendelea kuwa mgumu na imara kama mlima na alijua kwamba kufuzu hufuata uvumilivu. Pamoja na mateso yote mtu huru wa Afrika alipaisha roho yake kwa kutamka maneno matamu na swala. Na si hiyo tu kwamba matatizo na mateso haya hayakudhoofisha imani yake, lakini yaliongeza uimara wake na kujitolea. Ingawa mwili wake ulijeruhiwa na tumbo lake lilikuwa na njaa na alilia kwa sababu ya wasi wasi roho yake ilikuwa madhubuti na kuelimika. Hakika, Bilal, mbeba bendera ya uhuru aliendelea kuwa mvumilivu ili Waislamu wenye moyo wangetambua ni hadi kiwango gani wanatakiwa kuwa imara katika njia ya imani yao na wasiondoke katika uwanja kwa maelezo ya ahadi au tishio, na wasiogopeshwe na wagomvi hao wenye kulewa, ambayo ilitoka kwenye makoo ya watu wakali na wadhalimu. Wasije wakaacha imani yao kwa lengo la kuwafurahisha watu wengine na lazima wasimame imara mbele ya watu hao kama milima migumu na lazima wajue kwamba ushindi ni wao. Uimara na kujitolea mhanga kwa Bilal ulimweka bwana wake mbali na uvumilivu. Alionyesha ishara za wasi wasi mkubwa sana hivyo, kwamba uso wake ulibadilika na akarindima: “Ujeuri ulioje wa mtu huyu? Nifanye nini? Nimemtesa kadiri 32


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

ya uwezo wangu. Hayupo tayari kuacha maoni yake potofu na imani yake. Hata hivyo, ninaapa kwa jina la Lat na Uzza kwamba lazima afe katika hali hii. Nitafanya kitu fulani hivyo kwamba atazikwa chini ya vumbi na mawazo yake yote.”

wake ulikuwa wa kikatili sana na wa hatari. Hapana mtu aliyeweza kuwa na nguvu ya kuvumilia kuweza kuhimili azma yake. Mpango huu ulikuwa unakaribia kuwa sawa na kifo cha Bilal!

Bilal alikuwa mkimya mvumilivu kwa maneno yote haya. Alipata msukumo na kutiwa moyo kutoka kwa marafiki zake wengine na akasema kwa roho iliyojaa mapenzi ya dini ya Uislamu na Mtukufu Mtume: “Kitu kimoja tu ambacho unaweza kufanya ni kwamba unaweza kuniuwa mimi.

Hali ya hewa ilikuwa joto na jua liliwaka kwenye kanda ya Hijaz. Mchanga wa jangwa ulikuwa kama Jahanamu!

Hata hivyo, siogopi kuuawa. Kwa upande mwingine nitajivuna zaidi kama nikiuawa kwa sababu ya kumfuata Mtume wa Mwenyezi Mungu na kuwaondoa watu katika ukatili na ukandamizaji. Ni vizuri zaidi kufa kwa heshima kuliko kuishi katika udhalili. Ni watu hao tu wenye ubinafsi na hawaamini siku ya Hukumu ndio huogopa kifo. Hata hivyo, kwangu mimi kifo cha aina hii ni heshima na ukamilifu!” Umayyah akawa anatafakari kila siku na akajisemea mwenyewe: “Nifanye nini zaidi ya hilo? Nimetekeleza mipango yangu yote katika vitendo. Nimemfanyia mateso makubwa sana ………” Kama ilivyotarajiwa, alimfunga Bilal jela. Akampa kazi nzito za kuchosha. Akampiga kwa gongo! Akamnyima chakula. Hata hivyo, hakuna hata kimoja wapo ya vitu hivyo ambacho kimemuathiri Bilal isipokuwa vimemfanya kuwa imara na kumpa nguvu ya kulia na kusema mambo ambayo lazima yasemwe na kufedhehesha watu fulani. Hatimaye, Umayyah aliamua kutekeleza mpango wake wa kishetani ili kwamba Bilal afe au aache imani yake. Mpango 33

Umayyah alishika mkono wa Bilal mwenye huzuni na kuumia na akatembea jangwani hadi akafika kwenye kanda ambapo mchanga wake ulikuwa unaunguza. Hapo alimvua nguo Bilal aliye dhaifu na kukonda na akamuamuru alale kwenye mawe yenye joto kali sana na pia akaweka mawe mazito juu ya kifua chake. Ngozi yake ilikuwa inaungua na alikuwa anapumua kwa taabu. Baada ya muda mfupi akahisi mapigo ya kiboko cha bwana wake. Heshima kubwa zaidi ya zote kwa wale waliofuatana na Umayyah ilikuwa kwamba kila mmoja wao alimchapa viboko Bilal aliye dhoofu naye alijibu kwa tabasamu la ushindi. Kwa bahati mbaya hata hivyo, watu hawa walikuwa viziwi na vipofu kwa sababu kilio cha mateso ya Bilal kilikuwa kilio cha mamia ya maelfu ya watu wasio na hatia ambao walikuwa wanateswa bila haki na kilio cha umma ambao ukamilifu wao, matumaini yao, na matamanio yao ilikuwa ushindi wa mfumo wa Uislamu na kuondoa imani ya kuabudu masanamu, udikteta, unafiki, ukabaila na unyonyaji. Wakati mwingine Bilal alipoteza fahamu kwa sababu ya maumivu makali na alipopata fahamu alikabiliwa na sauti kali yenye hasira ya bwana wake ambaye alitaka amkane Muhammad na Mola wake Mlezi. Hata hivyo, Umayyah alisema kwa kushangaa kwamba Bilal alisema pole pole akiwa

34


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

amefumba macho na sauti yake ikitetemeka: “Ahad. Ahad.17 (Mmoja, mmoja). Kutamka kwa maneno “Ahad, Ahad’ sahaba mwaminifu wa Mtukufu Mtume na mtumwa muumini na kipenzi cha Mwenyezi Mungu, alisababisha mwili wote wa adui kuwaka hasira na hakutaka kujiruhusu kuamini kwamba alikuwa na Bilal huyo huyo wa zamani. Hakuweza kuvumilia kwamba mtumwa kama huyo angeweza kuwa amepata hadhi kubwa na ya juu kiasi hicho kwamba anaweza kuwa tayari kujitoa mhanga kwa ajili ya imani yake ya kumwamini Mungu Mmoja. Hata hivyo, Umayyah alisema kwa moyo mchafu usio na huruma: “Ama lazima ufe au umkane Mola wa Muhammad.” Lakini Bilal mgumu na jasiri ambaye alikwisha jaa mapenzi makubwa kwa ajili ya Mtukufu Mtume hakutaka kujisahau hata kwa sekunde moja na aliendelea kurudia lile neno fasaha lenye athari ya kudumu ‘Ahad, Ahad’. Umayyah alichoka. Wakati mwingine alirudi jijini peke yake na alimwacha Bilal peke yake na mara nyingine alikwenda naye jijini.18 Siku zilipita na Bilal aliendelea kuteswa na kuumizwa. Historia haiweki kumbu kumbu za uimara wa aina hii. Na waandishi wa historia, wameshindwa kuandika kumbu kumbu ya ustahamilivu na uimara unaofanana na ule ulioonyeshwa na Bilal na hawajaamini hata kidogo kwamba masanamu yanaweza kushindwa na uongofu ukapatikana kama zawadi. 17 18

Huu ni wito wa wanaoamini Allah mmoja tu. Al -Kamil bin Athir, Juz. ii, uk. 45, Rijal Ma MAdhana uk. 182, Babul Ba, Tabaqat ibn Sad, Juz. ii, uk. 185, Nasikhut- ul- Tawarikh, Hubut uk. 579, Tafsir - e- Ithna Asheri Juz. xii, uk. 157, Usul Ghabah Juz I, uk. 207. 35

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Hapana. Hapana. Kwani ninasema kwamba si tu wataalamu wa historia lakini watu waliokuwa wanaishi na Bilal na walikuwa na mawasiliano ya karibu naye na walisikia kuhusu mateso yake makubwa na walishuhudia kwa macho yao, walistaajabu na hawakuweza kuamini uimara, kujitolea na umadhubuti kama ulivyoonyeshwa na Bilal.

SHUKRANI KWA BILAL Kila siku jua lilichomoza asubuhi kutoka nyuma ya mlima na jinsi lilivyozidi kuonekana, liliunguza mwili wa Bilal kwa joto lake lisilovumilika. Haiwezekani ni joto la kiasi gani la mchanga na mawe makubwa yaliyo unguza mwili wa Bilal, hakuathirika. Ilionekana kama vile mawe magumu na yenye joto yalimfundisha Bilal ustahamilivu na imani yake ikazidi kuwa madhubuti. Usiku ulipoingia, mwezi uliangaza kwenye jangwa la Makkah na uliweka utakaso maalum mlimani, vichaka na jangwa. Bilal alifurahia kuona hali hiyo na alisali kimya kimya kwa Mola wake Mlezi – Mola Mlezi Ambaye kwa ajili ya ukuu wake alikuwa anavumilia dhiki zote hizo na mateso yote hayo ambayo yaliathiri mwili wake wote. Baadhi ya watu walipokwenda jangwani kuona hali ya kusikitisha ya Bilal, Umayyah alizidi kuwa mkorofi na alizidisha mateso kwake. Hata hivyo, Bilal alionyesha imani yake kwa kutamka ‘Ahad. Ahad’. Watu wote hao walistaajabu na kumkodolea macho yaliyokuwa yanamsifu na kuhimili uimara wake. Lakini uimara huu haukuwaathiri na hawakujifunza lolote kutokana na yaliyokuwa yanaendelea 36


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

hapo. Waraqah mtoto mwanamume wa Nawfal alipopita hapo alisimama na akatokea kumpenda Bilal sana na akataka kumkumbatia mara moja. Alimsogelea zaidi na akamwambia kwa sauti ya kupaza: “Bilal unafanya vema! Mimi pia nimesema kwamba Mwenyezi Mungu ni Mmoja tu. Na pia ninakubali mantiki yako.” Halafu akamgeukia Umayyah na akasema: “Ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba endapo Bilal atafariki dunia katika hali hii nitatengeneza kaburi lake na kulifanya sehemu ya kuhiji mimi na nitaomba neema kutoka kwenye vumbi lake, na sehemu hii hakika itakuwa ni mahali ambapo neema za Mungu zitateremka.”19 Bila shaka watu wenye busara na waadilifu ambao hujitolea maisha yao katika njia ya Mwenyezi Mungu na kujitoa mhanga kwa ajili ya imani yao na dini huendelea kuwa hai daima milele na kifo kwao hakina maana. Kama mambo yalivyo, vumbi la makaburi yao linakuwa sehemu ya hija ya watu waadilifu. Makaburi yao yanakuwa sehemu ya neema zisizo na ukomo za Mola Mlezi wa ulimwengu. Ni hao viumbe hai, ambao hufundisha jamii ya binadamu somo la maisha, na kwa uimara wao na uvumilivu huwafundisha wanyonge wanaogandamizwa somo la jihadi katika njia ya imani na uhuru. Udongo wa makaburi na vumbi lao takatifu huweka kujitoa mhanga na uimara kuwa sifa hai daima milele, hutia mkazo 19

Al- kamil ibn Athir, Juz. ii. uk. 45, Sirah ibn Hisham Juz. I, uk. 340, Rijal Ma Maqani Babul Ba uk. 182, usudul Ghabah, Juz. I, uk. 206. 37

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

moyo wa ujasiri na ushujaa kwa kila mwanadamu wa kila jamii na hutoa wito kwa jamii kuendea uchaji Mungu na wema. Hii ni siri ya kutoa heshima kwa makaburi ya makamanda, viongozi na wapiganaji wasiojulikana ambao ni wahanga wa dunia ya ubinadamu.

AAA! AAA! NAUNGUA Uzito wa mawe, mapigo ya kiboko joto linalobabua la mchanga, havikumwathiri Bilal ambaye ushupavu wake ulikuwa madhubuti kama chuma. Umayyah alichukua uamuzi wa hatari zaidi. Aliamua kutengeneza kiboko cha chuma kwa lengo la kukiingiza kwenye musuli wa paja la Bilal baada ya kukipasha moto na kuwa chekundu kama kaa la moto. Ilitokea Bilal alikuwa amelala chali na jiwe kubwa lilikuwa kifuani mwake ambalo lilimzuia asione walitaka kufanya nini na mguu wake. Bilal aliona tu kwamba walitengeneza kipande cha chuma – mfano wa kiboko ambacho kilikwisha pashwa moto na kuwa chekundu. Ghafla alihisi mguu wake unaungua moto. Ilionekana kama vile moto huo ulipenya ndani ya mwili wake wote na alikuwa anaungua. Aliutikisa mwili wake na alipokuwa anaelekea kupoteza fahamu, alipiga kelele ya kuhisi maumivu makali na isiyo na matumaini ya kupata msaada: “Ooh! Nimechomwa moto!” mara baada ya hapo hakuweza kusema kitu. Wale wote waliokuwa hapo walisema kwamba Bilal alifariki dunia.20 Hayo yalikuwa mateso makali sana. 20

Abu Jahl ndiye aliyefanya kitendo hiki. Alimwomba Umayyah ampe kazi hiyo aifanye yeye na alifanya hivyo. Imeandikwa pia kwamba kwanza alikata paja la Bilal kwa kisu na halafu akaingiza chuma kupitia hapo. (Ghaftar -e- Wuaaz, uk. 456). 38


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Mtu ambaye ameteswa kwa siku kadhaa hawezi kuhimili maumivu kama haya. Wote wale waliokuwepo hapo walishangaa kuona tukio hilo. Hata jua pia lilitunduwaa lilipoona tukio hili. Kimya cha kifo kilitawala kwenye jangwa lote. Uso wa bwana wa Bilal ulikuwa wa kuogofya. Ilionekana kama vile alijutia kwa kile alichokifanya na mchanga wa jangwa ulikuwa una mlaani.

Hapana. Usikosee. Imani kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake imepenya na kuenea kila mahali na mapenzi yangu kwake yameota mizizi hadi kwenye kina cha roho yangu. Huwezi kuyachukua na kuyaharibu kwa njia ya minyororo hii na viboko hivi. Lazima ujue uhakika kwamba hutaweza kunishinda mimi na kudhoofisha imani yangu kwa matendo haya ya kikatili.�

Muda ulikuwa unakwenda pole pole. Bilal mstaahamilivu, anayegandamizwa, na kadiri alijitikisa. Machozi yalitiririka kutoka machoni mwake. Alipumua pole pole. Rangi yake nyeusi ilibadilika kuwa nyeupe. Alikuwa hawezi kusogea. Hakuwa na nguvu za kumwezesha kusema. Yeyote aliyekuwa karibu hapo aliweza kutambua kwamba Bilal alikuwa analia kwa sauti za chinichini na alilalamika kwa Mwenyezi Mungu. Baada ya muda mrefu akasema pole pole Ahad Ahad yaani Mwenyezi Mungu ni Mmoja tu halafu tena akapoteza fahamu. Kimya cha jangwa kilisitishwa na maneno ya Bilal na wale wote waliokuwa hapo walishangaa na kila mtu alikuwa anamsema yeye.

Kusema kweli, maneno haya yaliyotamkwa na Bilal, kama hayangewaathiri hao watu wenye majivuno, kiburi na wavamizi, ili waweze kutambua kwamba hawawezi kuzuia imani ya watu kwa nguvu, mateso, udanganyifu na utajiri? Hawawezi kufikiria kwamba moyo wa dini na imani makazi yake ni kwenye mishipa ya damu ya Ateri na vena ya Waislamu, hususan Waislamu waaminifu na hawawezi kuvumilia kwamba kitu kingine kikae hapo?

Baada ya muda mfupi alifungua mdomo wake tena.akayafumbua macho yake kidogo na akayazungusha pande zote na akamuona bwana wake mwenye moyo mgumu mfano wa jiwe na akamwashiria dalili na kuanza kusema polepole: “Unadhani kwamba imani yangu imejificha kwenye msuli wa paja langu kwa hivyo, unataka kuichoma kwa chuma chenye moto mkali na uiharibu na uyaondoe mapenzi ya Mwenyezi Mungu Mmoja kutoka humo? Unadhani kwamba imani yangu kwa Mwenyezi Mungu na mimi kushikamana Naye ipo kwenye kiwiliwili changu hivyo kwamba unaweza kuiharibu kwa kuiumiza na kuitesa? Hapana. 39

Maadui wa ubinadamu hawawezi kudhoofisha imani ya watu kutumia sumu ya maneno yasiofaa na yasiyo na maana katika kueneza propaganda yao. Lazima watambue kwamba imani, mapenzi na mfumo wa fikra zinazomwelekea Mwenyezi Mungu ni mchanganyiko uliopo kwenye damu yao. Wale wanaofikiri kwamba wanaweza wakaondosha imani na itikadi ya mtu binafsi kutoka kwenye nyoyo zao wanakosea na hapo hukata mizizi yao. Qur’an Tukufu inasema: (61:8).

% & ! " # $ “Wanataka kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao. Na Mwenyezi Mungu atakamilisha nuru yake ijapokuwa makafiri watachukia.� Imani haiwezi kushindwa na itikadi haiwezi kuharibiwa. 40


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Kinyume chake misimamo hiyo huzidi kung’ara siku hadi siku. Kwa ufupi, Bilal, bingwa wa Afrika mpenda uhuru na ujuzi hakuitelekeza imani yake na akasema akingali kwenye mateso makali kwamba: “Mwenyezi Mungu ni Mmoja” Jinsi yoyote alivyoteswa zaidi ndivyo alivyozidi kuwa mvumilivu na imara. Kusema kweli, mtu anastaajabu kuona ni vipi binadamu anaweza kujitolea kiasi hicho kwa sababu ya imani na itikadi kwa Mwenyezi Mungu na ili aweze kupata uhuru na haki. Ni nani hao ambao huishi namna hii na kukumbatia kifo kwa heshima? Wameumbwa kwa vitu gani, na hutazama upande gani, nani ambaye ametengeneza umadhubuti huu na hadhi hii katika dhamiri zao hivyo kwamba hata hawaogopi migongo ya hatari sana na iliyofika upeo wa kutokuvumilika na husimama pasipo hofu mbele ya madikteta na wakandamizaji na hawaachi imani yao? Kwa kweli, hufundisha somo maisha kwa dunia ya binadamu.

BILAL AMEFARIKI DUNIA Hali ya kusikitisha ya Bilal ilifanyiza tukio la kuhuzunisha kwa wapita njia. Watu wote waliopita karibu na tukio hilo walipata wasi wasi kuhusu hali yake na mateso aliyofanyiwa na bwana wake. Siku moja Amr bin Aas alikuwa anapita karibu na tukio hilo, akamuona Umayyah anamwambia Bilal maneno makali. Alisogea karibu akamuaona Bilal amelala chini mikono na miguu yake ikiwa imefungwa, na Umayyah alikuwa anamwambia: Mkane Mungu wa Muhammad na Udhihirishe imani kwa Lat na Uzza. Hata hivyo, Bilal alikuwa anasema: 41

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

“Mwenyezi Mungu ni Mmoja. Mwenyezi Mungu ni Mmoja.” Amr anasema: “Ghafla niliuona uso wa Umayyah umebadilika na macho yake yakiwa mekundu kwa hasira. Aliunguruma na kumsogelea Bilal kama jini mbaya, akaketi kifuani mwake na akamkaba koo lake kwa nguvu sana nilidhani amekufa. Nilisikitika sana kwamba sikutamani kuendelea kuwa hapo na kuona tukio hilo la kuhuzunisha. Nilipoondoka Umayyah alikuwa hajali nikasemea mwenyewe: “Ole wao hawa watu ambao ni wakali sana, katili na madhalimu. Bilal amekufa. Bila shaka wamekuwa katili sana kwake.” “Nilikwenda nikafanya kazi yangu. Hata hivyo, wakati wote huu nilikuwa nasumbuliwa sana na hali mbaya ya kusikitisha ya Bilal iliendelea kuwepo machoni mwangu hadi niliporudi. Sasa nilifikiria kwamba naweza kwenda na kuona hali ya Bilal ilivyokuwa. Nilikwenda nikamuona alikuwa bado amelala chini. Nilijisemea mwenyewe: masikini mtu huyu amekufa. Ghafla niliona anajitikisa na Umayyah alikimbia na kwenda hapo na akasema: “Sema: Ninamwamini Lat na Uzza.” Hata hivyo, kwa kuwa Bilal alikuwa amedhoofu sana, hakuweza kusema badala yake alionyesha kidole kuelekea juu angani na kujulisha kwamba Mola wake Mlezi alikuwa Mola wa walimwengu.* Kama mambo yalivyo, huu ni uimara katika dini na huku ndio kujitolea katika njia ya imani na itikadi. Hawa ndio watu ambao, kwa kulala chini maisha yao, hulinda mambo ya kiroho na ubinadamu kwa ajili ya wanadamu. Hawa ni watu ambao wamewafundisha wengine somo la kujitoa mhanga na uhuru.

*

Tafsir - e - Ithna Ashari, Juz xii,uk.157 42


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Amani iwe juu yao hawa wamuabudio Mwenyezi Mungu! Salaamu zao hawa wapenda uhuru wa historia ya mwanadamu! Kweli, huyu Umayyah katili alifanya nini? Shughuli yake iliishia wapi? Alitaka nini kutoka kwa maisha yaa Bilal? Kwa nini hakuambatanisha maadili yoyote kwa maisha ya Bilal? Kwa kweli inaonekana kama vile hakuwa nazo sifa zozote za kibinadamu. Ilikuwa mbwa mwitu aliyevaa joho la binadamu na alichezea maisha ya watu waaminifu. Endapo watu kama hao wanasema kuhusu ubinadamu, amani na starehe katika jamii wanasema uongo na wanasema mambo haya kudanganya na kuwapumbaza watu. Watu kama hawa ni adui wa mwanadamu na ubinadamu. Hawa ni watu wanaofanya uhalifu kwa watu wanyonge wasio na uwezo ili kulinda mamlaka yao. Hawa ni watu wanaoua maelfu ya binadamu ili waweze kutekeleza malengo yao binafsi. Walaaniwe hawa mbwa mwitu wenye umbile la mwanadamu, ambao wamekuwepo wakati wote na uthibitisho wa matone ya damu yanapoonekana katika kizazi chao ili waweze kutimiza njama zao za uovu.

CHUNGU KULIKO SUMU Wakati mwingine Bilal alichoka sana na alikuwa na wasi wasi kwa sababu ya maumivu makali na alilalamika na kusema: “Nifanye nini? Ufumbuzi wake ni nini.” Hakuweza kufikiria kitu chochote! Bilal aliona njia zote za ukombozi zilifungwa. Kwa hiyo, jambo la muhimu alilofanya sasa ni wakati fulani alifanya maombi kwa Mweza Mwenyezi Mungu na wakati mwingine alizungumza na nafsi yake. Wakati fulani alitazama huku na huko na alionekana kwamba kama vile alikuwa analalamika kwa milima na misitu na majangwa kwa kutumia macho yake. Na usiku ulipoingia alielekeza macho yake mbinguni na alifungua moyo wake na kuzikaribisha nyota 43

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

nzuri na zinazopendeza. Alisema kwa lugha yake ya ububu: “Wakati huu kilicho kichungu kuliko sumu kitapita. Usiku huu wa giza utapita. Kipindi cha dhiki kitapita. Mikono hii iliyojificha itakatwa. Sauti hizi za kuunguruma zitanyamazishwa na hali haitaendelea kuwanufaisha watu jeuri na wakandamizaji. Jua litachomoza kutoka nyuma ya mawingu manene na meusi. Miguu ya jamii iliyozidi na visivyo na manufaa na kupe wenye kudukiza ambao ni kama povu juu ya maji vitaondoka na havitakuwepo na mwanzo wa ushindi utadhihiri.* “Watu wapumbavu na wajinga, kila mara wamekuwa wanashambulia ukweli na hali halisi. Si mimi tu ambaye nimeteswa kwa sababu ya jambo hili. Ninatambua kwamba wakati wote ushindani huenda kwa wamwabuduo Mwenyezi Mungu na watafutao ukweli na maangamizo ya wagandamizaji huanza. “Mola Mlezi Mwenye Uwezo usio wezwa anajua kuhusu matendo maovu ya wagandamizaji na anatambua kuhusu udikteta na udhalimu wao. Amempa kipindi hiki kifupi cha wazi zaidi uovu wao kwa watu, na watu pia lazima wawakatae baada ya kujua, waonyeshe imani yao kwa Mwenyezi Mungu Mola Mlezi, na wajue kwamba Mwenyezi Mungu amewapa adhabu na fedheha ya milele wagandamizaji na waabudu masanamu.” Bilal alivumilia dhiki na mateso lakini kamwe hakufanya uzembe wa kutomkumbuka Mwenyezi Mungu na kudhikiri Jina Lake. Wakati wote alifanya maombi kwa Mola wake Mlezi *

Tafadhali rejea Qur’an Tukufu. 44


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

pekee akisema: “Ee Muumbaji wa ulimwengu! Hadi lini maisha ya watu yataendelea kutekwa nyara na watu asherati wenye ubinafsi?” “Ee Mola Mlezi Mwenye uwezo usiowezwa! Muda haujawadia ambapo Utawapindua watu wadhalimu na wenye kiburi na uvute pua zao hadi kwenye vumbi la fedheha na ukaushe mzizi wao mchafu na uwaokowe wanyonge na waadilifu kutoka kwenye makucha yao ya ufisadi na uwape miliki kwenye nchi Yako ilio neemeshwa? “Ee Mola Mlezi Mweza wa Yote! Hadi lini udikteta na udhalimu huu utaendelea? Hadi lini wanyonge wataendelea kufedheheshwa na hadi lini haki zao zitaendelea kukandamizwa? Ee Mola Mlezi Uliye Mwema! Sina kimbilio lingine isipokuwa Kwako; popote ninapoona uovu, moyo mgumu, mauaji, uhalifu, uporaji na usaliti. Ee Mkombozi na Kimbilio la wanyonge! Sina mwingine wa kunisaidia isipokuwa wewe! Njoo unisaidie. Ee Mola wangu Mlezi! Njoo unisaidie kwani nimejisalimisha kwenye kifo na ninaona aibu kuishi maisha ya fedheha na ninatamani kujitoa mhanga kwa hiyari yangu katika kupigania Uislamu, Mtume wako na yote hayo Unayoyapenda. Ee Mola Mlezi wa walimwengu! Nimechagua kifo lakini nihurumie kwa kunipa muda mfupi wa kupumua ili niweze kuona uhuru wa wahenga wangu, uhuru wangu na uhuru wa wanyonge na niweze pia kuona ushindi wa Mtume Wako Muhammad na bendera ya Hapana mungu ila Mwenyezi Mungu imetundikwa kwenye kilele kirefu kuliko vyote. 45

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Mimi ninatamani ukombozi wa watu wa Makkah tu na wanaokandamizwa duniani pote na ushindi wa Uislamu, ingawa naweza kufa, kwa sababu nafikiria kifo changu kuwa ni kuzaliwa upya na damu yangu kuwa mhuishaji wa roho zilizo kufa za watu na kilio changu kuwa mwanzo wa upinzani dhidi ya ibada ya masanamu na kufuru. Na ujumbe wangu ambao ni ujumbe wa vizazi vyote vilivyoloweshwa kwenye damu, umma wote uliofungwa minyororo, na kwa imani ya watu wote waaminifu na wenye kuwajibika unaendelea milele na kuheshimiwa. Ufichue nyuso za wanafiki na makafiri katika historia daima, milele na kuacha alama yao chafu kama kumbu kumbu kwa vizazi vijavyo! “Ee Mola wangu Mlezi! Ee Mola Mlezi Mkuu! Nakuomba unipe muda wa kupumua!” Siku ziliendelea kupita na hali ya Bilal ilizidi kuwa ya kusikitisha. Alikuwa karibu afe na kuondokana na makucha ya kiuaji ya Umayyah. Kila mtu alisimulia habari kuhusu yeye. Mtukufu Mtume wa Uislamu alisumbuliwa sana. Angefanya nini? Angewaokoaje hawa watu bora na wenye hekima wa jamii kutoka kwenye makucha ya wakandamizaji? Alilifikiria sana jambo hili lakini hakufanikiwa kupata ufumbuzi. Pia aliwasiliana na watu wengine lakini wote hawakuwa na matumaini. Si Mtume tu wa Uislamu ambaye hakufurahishwa, lakini Waislamu wote walihuzunika na walikuwa wanajaribu kufuata njia ya kumkomboa Bilal na wengine kama yeye. Bilal alikuwa binadamu na pia Mwislamu na kama asemavyo Sadi: “Binadamu ni viungo vya kila mmojawao kwa sababu wameumbwa kutokana na chimbuko moja. Kiungo kimoja kikipata maumivu, viungo vingine vinahisi maumivu.”

46


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Je! Bilal hakuwa mmojawapo katika jamii? Uislamu unafuata misingi ya upendo na huruma. Endapo Mwislamu mmoja anaumizwa au ameumia maana yake ni kwamba Waislamu wengine wote wameumia. Uislamu unasema kwamba jamii ni kama mwili. Kama kiungo kimoja cha mwili kinauma viungo vingine pia vina dhikika. Kwa namna ile ile kwamba kama Mwislamu moja anasumbuliwa, Waislamu wengine pia wanasumbuliwa.21 Waislamu wote wapo kama roho mmoja na mwili mmoja, na kama jengo moja madhubuti, wameshika mikono ya wengine na wengine wamefanya hivyo ili kufanyiza jamii ya Waislamu na roho zao zimeunganishwa.22

Kwa upande mwingine wataweza kuzuia kwa mikono isiyohusika ambayo huelekezwa kwenye Qur’an Tukufu na Uislamu, kwa hiyo, bendera ya kutoa uhuru ya Uislamu itapepea kwa utukufu mkubwa daima katika kanda zote za dunia na maadui jeuri wa Uislamu wataangamizwa na jamii mpya itajengwa.

Kama mambo yalivyo, hii ndio mantiki ya Uislamu. Inasema: Mwislamu akipitisha usiku mmoja bila kufikiria ustawi wa waislamu wengine, si Mwislamu.”23

Tukirudi nyuma kidogo na kuchunguza historia ya kutia moyo ya makamanda na wajumbe wawajibikaji, tunajua kwamba wakati wa siku za mwanzo wa Uislamu, Waislamu, ambao walikuwa wachache kwa idadi, waliishinda dunia ya ukafiri na ibada ya masanamu, na waliweza kwenye uwezo wao, kupeleka ujumbe wa Utume na kumuabudu Mwenyezi Mungu kwa dunia ya ushirikina.

Pia inasema: “Waislamu ni ndugu wa kila mmoja.” Inawataka watembee kwenye njia moja na wasimame imara dhidi ya maadui kama ngome madhubuti. Tunaamini kwamba endapo Waislamu wa dunia wakihuisha mantiki hii miongoni mwao na wote washikamane na kutoa mkono wa udugu, mshikamano na umoja kwa njia hii kwamba wanafikiria maumivu ya ndugu Mwislamu kuwa sawa na maumivu yao wenyewe, mantiki na utaratibu wa Uislamu kamwe hautashindwa katika hali yoyote ile.

21

22

23

Muumini ni ndugu wa muumini kama mwili mmoja, kama kiungo kimoja kimeumia viungo vyote vitaathirika. Mwislamu kwa Mwislamu ni kama ukuta mgumu ambao matofali yake yameshikamana inavyostahili. Mtu anayeamka asubuhi na anakuwa hahusiki na mambo ya Waislamu, si Mwislamu. 47

Endapo Waislamu wa dunia wanaamsha miongoni mwao ukweli kwamba chimbuko la wao wote ni moja na wao ni ndugu wa kila mmoja wao, hapana mtu ambaye angeingia, kati yao na kuanzisha makoloni kwenye makazi yao.

Kama mambo yalivyo, Mtukufu Mtume wa Uislamu alisumbuliwa sana kwa sababu Mwislamu aliyeitwa Bilal alikuwa anateswa na makafiri na Waislamu pia walihuzunika na wote walikuwa wanafikiri jinsi ya kufanya. Baada ya kufikiri kwa muda kuhusu tukio hili, Mtukufu Mtume alisema: “Kama yeyote miongoni mwenu anaweza kumnunua Bilal na kumwacha huru, inawezekana kwamba huo utakuwa ndio ufumbuzi wa tatizo hili.” Abu Bakar alikubali pendekezo hili na akaamua kufanya hivyo.24

24

Al-Kamil, Ibn Athir, Juz. ii, uk. 45 48


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

ABU BAKAR ANAKUTANA NA BWANA WA BILAL Abu Bakar alikwenda nyumbani kwa Umayyah na alikuwa anafikiri mwenyewe vipi Umayyah angempokea ama angefaulu kufanya kazi hiyo kama ilivyotegemewa na kama Umayyah angekuwa tayari kumuuza Bilal kwake. Alikuwa anatafakari kuhusu mambo haya alipofika nyumbani kwa Umayyah na akamwita. Walipoonana, walisalimiana na kuonyeshana mapenzi na huba. Umayyah akasema: “Muda mrefu umepita tangu ulipoacha kuwa mwema na uliacha kuja kututembelea. Umeshusha hadhi yetu.” Abu Bakar alijibu: “Natumaini kuendeleza mawasiliano ya karibu na wewe siku zijazo.”

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

mmojawapo wa watumwa wangu ambaye ni mfuasi wa dini yako.” Umayyah alisema: “Unamaanisha Bilal?” Abu Bakar alijibu: “Ndio, Bilal.” Sura ya Umayyah ilibadilika. Alimtupia Abu Bakar jicho kali na alisema kwa mshangao: “Umekuja kwa lengo hili? Hana maana. Amekuwa mwasi na mtu muovu. Amekosa busara. Amekanganya hali za maisha yetu. Yeye sasa ni mtu wa kufa tu. Lazima nimuue kwa namna mbaya sana ili niweze kupata furaha na pia inaweza kuwa fundisho kwa wengine. Usimruhusu mtu huyu aingie katika maisha yako!” Abu Bakar alisema: “Nipo tayari kumnunua bei yoyote na kama unataka mtumwa anayeabudu masanamu nitakupatia mmoja tubadilishane.”

Umayyah akasema: “Ninaishi katika hali mbaya sana. Huyu Muhammad ambaye umemfuata inaonyesha kama vile ataiharibu jamii yetu baada ya muda mfupi na si mimi tu isipokuwa wazee wote wa Kiarabu wana wasiwasi huu. Na uwezo wote nilionao umeshindwa kumlazimisha mtumwa wangu kukana imani ya Muhammad.”

Umayyah alitoa jibu kali zaidi na alisema: “Hapana. Siwezi kukubali pendekezo lako. Lazima afe katika hali hii. Kwa njia hii nitapata furaha na wengine pia watajifikiria wenyewe.”

Abu Bakar aliingilia kati na akasema: “Mambo haya yatarekebishwa. Nimekuja kukutua mzigo wa tatizo hili.”

Umayyah alisema: “Hujui huyu mtu mweusi amenifanya nini. Maumivu ya moyo wangu hayawezi kupona kwa kumuuza yeye!”

Umayyah alisema: “Kweli unaweza kuliondoa tatizo hili? Muhamad ameacha mahubiri yake?” Abu Bakar alisema: “Nimekuja kumnunua kutoka kwako mtumwa ambaye ana kutia wasiwasi au tubadilishane na 49

Abu Bakar alisema: “Badala ya kufanya mambo yote haya na kujipa wasi wasi ni vema umuuze kwangu na wewe upate amani.”

Abu Bakari alisema kwa Usipomuuza utaumia zaidi.”

sauti

ya

chini;

Umayyah alisema: “Usisisitize. Hafai kuuzwa.” 50

“Unakosea.


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Abu Bakar alisema huku akitupa jicho la kulalamika: “Nimekuomba na pia nimekuambia kwamba ninaye mtumwa ambaye ana nguvu zaidi kuzudi Bilal na nipo tayari kukupatia mtumwa huyo. Kwa nini unajisumbua hivi?”

ilionyesha kwamba alisahau majanga yote na usumbufu wote. Abu Bakar alifurahi sana kwa kuibuka mshindi na akampa uhuru Bilal hapo hapo mbele ya Mtukufu Mtume kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.∗

Hatimaye Abu Bakar alimnunua Bilal kwa namna fulani kutoka kwa Umayyah. Alikata kamba alizofungwa Bilal miguuni kwake kwa mikono yake na akamshukuru Umayyah na akaondoka.

Bilal aliangalia huku na kule kwa kukodoa macho. Alitupa jicho la haraka juu mbinguni na halafu akamgeukia Mtukufu Mtume. Wakati anashusha pumzi na machozi ya furaha yakitiririka machoni mwake kwenye uso wake mweusi na alianguka chini, alisema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Hadi leo nilikuwa ninateswa. Nilivumilia na nilikuwa mwangalifu nisije nikasema kitu chochote kinyume na radhi ya Mwenyezi Mungu. Hivi nipo kwenye njia iliyonyooka?”

BILAL ASHINDA NA KUWA HURU Bilal alitoka kwenye makucha ya utekaji nyara wa mmiliki wake wa kuogofya kama ndege ambaye manyoya yake yalipitishwa haraka kwenye moto. Hata hivyo, hakuweza kutembea. Alama za mateso zilionekana kwenye ngozi yake nyeusi. Mifupa ya kifua chake ilidhoofu. Dalili za uchovu na njaa zilionekana katika Umbile Lake. Alikuwa hawezi kusema. Hata hivyo alikuwa anasema peke yake: Hivi nimekuwa huru? Mola Mlezi wa ulimwengu amenikomboa kutoka kwenye makucha ya huyu mtu katili? Hivi nimepata ushindi haraka hivi? Ee Mola wangu Mlezi! Ninakushukuru …” Mkono wa Bilal ulikuwa umeshikwa na mkono wa Abu Bakar na alikuwa anatembea pole pole. Wakati mwingine aliketi chini. Wakati mwingine alipoteza fahamu na kuanguka chini. Abu Bakar aliketi karibu na kuanza kupapasa uso wake. Bilal alihisi mkono mwingine ulikuwa unapapasa si ule wa kwanza. Halafu alipata nguvu, alisimama na kuanza kutembea. Kwa matatizo sana Abu Bakar alimfikisha Bilal kwa Mtukufu Mtume wa Uislamu. Alipouona uso unaong’ara na wa peponi wa Mtukufu Mtume matumaini mapya yalimwingia Bilal na 51

Mtukufu Mtume akasema: “Ndio, iliyonyooka.” Na akamwombea.

upo

kwenye

njia

Bilal mgumu na anayependa, alikuwa mvumilivu na imara ingawa alipata mateso makubwa, hadi, hatimaye alipata uhuru na ustawi na kufuzu. Alionyesha kwa dunia inayopita jinsi wakati ujao wa Kiislamu unavyoweza kuzaa matunda kwa njia ya ustahamilivu, uimara na kampeni na jinsi ilivyowezekana kushinda masanamu na ukafiri na kulifanya kuwa tukio la kihistoria ambalo lilichangia katika upatikanaji wa ushindi na uhuru wa wakandamizwaji. Siku ya kwanza ya Bilal kuanza kutangaza Uislamu alikuwa

Imeandikwa katika Tarekh Ibn Sa’d kwamba Abu Bakar alimnunua Bilal kwa ushirika na Mtukufu Mtume (s.a.w.) na akaachwa huru na Mtukufu Mtume (s.a.w.) (Tabaqat Ibn Sa’d J.3,uk.169) Na baadhi ya wengine wameandika kwamba Abu Bakr alimnunua na akamuacha huru yeye mwenyewe. 52


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

hana haki za kibinadamu na upendeleo. Hakuwa na hadhi yoyote katika ile iliyoitwa jamii ya binadamu ya wakati huo na alitendewa kama mnyama. Alikuwa mtumwa wa mwonevu na dikteta na hakuwa na uhuru wowote. Alikuwa mateka. Lakini sasa kwa kukubali Uislamu alifanya kunyimwa yote hayo kuwa ni batili na akaweka mguu wake kwa mara ya kwanza kwenye uwanja wa maisha ya kibinadamu na akatambua kwamba yeye pia alikuwa binadamu kama wengine. Na sasa alianza maisha mapya kwenye paja la bahati njema na akaibuka mshindi. Aliondokana na mateso yote na usumbufu wote, mambo ambayo aliyapenda kwa uvumilivu na ustahamilivu. Alipata ushindi na kufaulu na hadhi maalum na sifa mbele ya Mtukufu Mtume na Waislamu. Kwa kweli, Bilal alipotambua kwamba yeye pia alikuwa binadamu na alikuwa na haki katika jamii na angeishi kama wengine, maisha ya mtu huru. Hakufikiria kuabudu masanamu na ubinafsi kuwa sahihi na akadhihirisha imani kwa Mwenyezi Mungu Mweza na akaasi dhidi ya uovu na ufisadi akiwa na matumaini kwamba Mwenyezi Mungu ndiye kimbilio la wanyonge na mkombozi wa wanaokandamizwa na akiwa na matumaini kwamba ukweli wakati wote hushinda na hudumu milele na udanganyifu wakati wote unatakiwa kufutwa na kutoweka,* akaanza maisha mapya. Aliingia kwenye uwanja wa maisha na kujitolea akiwa na matumaini kwamba giza la usiku halitaendelea kudumu milele na kufunika sura ing’aayo ya mapambazuko. Alichagua uvumilivu na uimara kama ndio kazi yake na *

Rejea Surah Bani Israil 53

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

akavumilia usumbufu wote na akabeba bendera ya uhuru mabegani mwake na akawa mshindi. Alitoa mwongozo kwa wote. Kwa viongozi wanaojitokeza kwa ajili ya ukombozi wa mataifa na nchi kutoka kwenye makucha ya mabeberu, kwa watu huru ambao wana shauku ya kupata uhuru wa umma, na haki za mwanadamu; kwa wanachuoni, kwa wanafunzi ambao wanahatarisha maisha yao kwa ajili ya maendeleo na mageuzi ya dola yao ya kimapinduzi; kwa wapiganaji na walinzi, ambao huyatoa mhanga maisha yao kwa ajili ya sifa njema, heshima na kwa ajili ya wapigananji na walinzi, ambao hujitolea maisha yao kwa ajili ya sifa njema, heshima na kwa Uislamu wao, ubinadamu na viwango vya kimapinduzi, na kupigana kijasiri, na kwa matabaka yote yanayokandamizwa ya mataifa mbali mbali ambayo yamekuwa mateka ya wauaji, na wabaguzi, wapenda mauaji kwa ajili ya kosa lao moja tu la weusi. Huleta matumaini ya kuishi chini ya ulinzi wa mafundisho bora sana ya Kiislamu na kuelekea kwenye maisha ya binadamu na kuanzisha utawala wa Haki ya Mungu, ushindi, uvumilivu na kujitoa mhanga. Kusema kweli, kama watu wote wa dunia wangejua kwamba waweza kupata uhuru kwa ajili ya uvumilivu, ustaarabu na juhudi, mikono ya wahalifu wachafu ingekatwa na mbwa mwitu waliovaa joho la binadamu, ambao wanatafuta uhai wa watu na kuwatafuna wangefedheheshwa na fikra zao za kuchukiza zingeng’olewa na watu wangeendelea kuishi katika utakaso, uadilifu, bahati njema starehe na amani.

UTUMWA AU UHURU Lengo la kila mwanadamu ni kuwa huru katika maisha yao na uhuru huu una thamani kubwa sana kwao hivyo kwamba wapo tayari kutojali uhai wao ili waweze kuupata, na wapo tayari kuweka dhamana uhai wao ili wapate uhuru. Wanaona kufa 54


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

kwa ajili ya uhuru ni vizuri kuliko kuishi kama mateka, kwa sababu maisha ambayo hayana uhuru si maisha.25 Utukufu mkubwa wa mwanadamu ni kwamba ajitolee maisha yake ili apate uhuru. Bila shaka mwanadamu ana uhasama na utumwa na wakati wote anauchukia na kuwalaani wale wanaowanyang’anya wanadamu uhuru. Ni mahali pamoja tu ambapo utumwa unakubalika kwa mwanadamu na huo utumwa ni uhusiano baina yake na Mola Mlezi wa ulimwengu. Ni hapa tu ambapo utumwa si jambo la fedheha, lakini ni utukufu mkubwa kuliko wote na heshima ya mwanadamu. Watu mashuhuri sana miomngoni mwa wanadamu ni wale wanao fikiria kuwa ni heshima kuwa mtumwa wa Mwenyezi Mungu Mweza wa Yote. Angalia jinsi Imamu Ali (a.s) alivyosema jambo hili kwa ufasaha mkubwa. “Ee Mola Mlezi uliye Mwema! Ni heshima kubwa sana kwangu mimi kwamba ni mtumwa wako.” Kuwa mtumwa wa Mola Mlezi Mweza wa Yote wa ulimwengu wenyewe huo ndio uhuru. Unampa mwanadamu umashuhuri na humfikisha kwenye kituo cha juu sana. Hata hivyo, utumwa kwa mwanadamu, ashiki, masanamu, hisia kali, utajiri kwa vitu hivyo ni fedheha kubwa sana. Wakati wote watu huru wamekuwa wanajaribu kukomesha kutoka kwenye makucha ya utumwa wa madhalimu.

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

na mwenye majivuno. Alimtaka Bilal ayaabudu mawe na masanamu. Ni kitu hiki, ndicho kilicho mfanya Bilal akatae katakata na akaurudisha utukufu wake. Bilal alitaka kuwa mtumwa wa Mwenyezi Mungu na sio mtumwa wa viumbe vyake. Bila shaka ni jambo lililo mchukiza Bilal sana kujiweka chini ya masanamu na mabwana zake madhalimu na akajitoa mhanga ili aweze kupata uhuru ili kwamba badala ya kuwa mtumwa wa wengine, awe mtumwa wa Mwenyezi Mungu. Akili inasema: Uwe na furaha na mafanikio Upendo unasema: Uwe mtumwa wa Mwenyezi Mungu na uwe huru.26 Baada ya mashauriano kidogo tunatambua kwamba uaminifu na nia ya Bilal ilikuwa kumnyenyekea na kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu na kwa hiyo alisimama imara ili apate uhuru kamili wa mwanadamu na jina lake litang’ara wakati wote katika kumbu kumbu za historia ya Kiislamu, kwani wakati huo palikuwepo na vita vya kumwaga damu baina ya imani ya Mungu mmoja na ushirikina na ambapo hatimaye imani ya Mungu Mmoja ilipata ushindi. Watu kama hao wanatambua uhalisi na thamani ya ubinadamu wakati wote wamekuwa hai na wakati wote wamepata ushindi mkubwa katika njia ya Mwenyezi Mungu na kundi lake, chini ya bendera ya unyenyekevu Kwake.

Bilal alikuwa mtumwa wa Umayyah- mtumwa wa mtu muovu 25

Imamu Hussein alisema: “Ni afadhali kufa kifo cha heshima kuliko kuishi kwenye fedheha na madhalimu. 55

26

Payam-e- Jawanan, uk. 69. (The messege of Alama Dr. Mohammad Iqbal). 56


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

TABIA YA KISHENZI Muda ulipita na Bilal aliondokana na Umayyah na alikuwa anashiriki katika shughuli nyingi mbali mbali pamoja na Waislamu wengine. Wakazi walio wengi wa Makkah walimjua na walikuwa wanatambua historia ya maisha yake na waliyona uimara wake wakati alipokuwa anateswa na Umayyah. Wazee wa kabila la Quraysh na wawakilishi wao walimuumiza Bilal katika namna ile ile waliyokuwa wanamuumiza Mtukufu Mtume (s.a.w.) na Waislamu wengine. Wakati wowote walipomuona walimkejeli; walimshambulia na kumpiga mijeledi kwa pamoja. Wakati mwingine waliingia nyumbani mwake na wakati mwingine walimdhihaki na kumtukana. Hatimaye mikono ya wahalifu haikuruhusu kwamba Bilal na Waislamu wengine waishi kwa amani. Mipango kisirani ilifanywa dhidi yao na tabia ya kishenzi ilitumika. Hivyo, Waislamu walijikuta wamo katika hali ngeni ya mashaka.27 Ilikuwa wakati huu ambapo baadhi ya watu wa Madina waliongoka, walikwenda kumuona Mtukufu Mtume na wakamualika ahamie humo ili aweze kuondokana na mateso ya Maquraishi. Habari hizi zilipoenea Makkah, makafiri miongoni mwa Maquraishi waliongeza mateso kwa Waislamu na waliudhi sana hivyo kwamba Mtukufu Mtume aliwajibika kuwatuma watu fulani Madina.

Bilal Wa Afrika

Kwa hiyo, Waislamu wachache waliondoka kwenda Madina kwa kukubali agizo la Mtukufu Mtume. Baada ya watu hawa kundi lingine la muhajirina liliundwa na Bilal akiwemo humo na wakaondoka Makkah kama alivyo amuru Mtukufu Mtume (s.a.w.).28 Ilikuwa usiku na giza nene lilienea kila mahali. Nuru iliyoangaza ilikuwa ni ya nyota tu zilizoko angani ambazo zilimeremeta kwa utulivu. Watu wengi walikwisha lala. Wakati fulani sauti ya wazururaji na walevi wenye kupenda ugomvi ilisikika mbali na karibu. Watu wenye kukubali walioteuliwa na watu wa Makkah walikwisha lala. Ghafla lango la makazi ya baadhi ya Waislamu na mahali pa kuishi lilifunguliwa pole pole na wakiangalia kuelekea kila upande kwa uangalifu sana wakazungumza na wakaondoka. Kishindo cha mwendo wa watembezi kilivunja kimya cha sehemu ya jiji na kusababisha woga zaidi. Walitembea kwenye mtaa moja hadi mwingine kimya kimya na hatimaye walitoka nje ya lango la jiji la Makkah. Baada ya kuondoka kwenye jiji la Makkah kwa kiwango fulani walifurahi. Hata hivyo, palikuwepo na uwezekano kwamba mtu fulani alitambua kuhusu mpango wao na angeweza kuwafuata na kuvuruga lengo lao likiwa katika hatua ya mwanzo kabisa. Msafara huu ulisumbuliwa sana na ulikuwa na wasi wasi. Kila mara baada ya kutembea hatua chache waliangalia nyuma na kuchunguza kama jambo lolote lilkuwa linatokea kwenye lango la jiji. 28

27

Tafsir-e-Surah Wal’Asr uk. 309 57

Bilal Wa Afrika

Tabaqat Ibn Sa’d Juz. iii, uk. 268; Nasikh al-Tawarikh Hazrat -i- rasul, uk. 33. 58


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Jinsi walivyozidi kuwa mbali na jiji ndivyo walivyozidi kuwa na matumaini mema na walitembea kwa kasi ya haraka zaidi. Muda ulikuwa unapita haraka. Waliambizana: “Lazima twende haraka na tuondokane na makucha ya watu hawa waovu.� Uchovu, usumbufu wa akili na woga, vilichosha. Kwa hiyo, waliwajibika kuamua kuwa wakae kwenye kilima cha mchanga na wapumzike na pia wapate fursa ya kuchunguza endapo mtu alikuwa anawafuata. Walipo angalia kwenye sehemu za mbali na hawakuona mtu yeyote, walifurahi na walitafakari kwa sekunde chache kuhusu jiji la Makkah, nyumba ya Mwenyezi Mungu, Mtukufu Mtume, masahaba wa Mtukufu Mtume na nyuso za kuogofya na kuchukiza za makafiri miongoni mwa watu wa kabila la Quraishi. Dakika chache zilipita na halafu wakaendelea na safari kwa huzuni. Walitembea hadi mapambazuko na mwanga ulianza kuenea. Hali ya hewa ilikuwa angavu na upepo mwanana uliotia nguvu ulikuwa unavuma. Anga ilikuwa ng’aavu sana. Msafara wa muhajirina uliamua kumwomba Mola wao Mlezi. Wote walianza kuomba dua. Roho ya kila mmoja wao ilikuwa imebadilishwa. Ilionekana kama vile mchanga wa jangwa nao pia ulishiriki kutoa sauti pamoja nao na ulikuwa umsifu Mwenyezi Mungu. Walijishughulisha sana na kumwabudu Mwenyezi Mungu na kumsikiliza Yeye kwa namna ambayo kwamba ilionekana kama walisahau kila kitu na walikuwa wanaruka angani kuelekea kwenye mbingu isio na ukomo.

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

ulimwengu. Ambapo hali ya hewa ilikuwa inaelekea kuwa ng’aavu, waliendelea na safari yao. Kila siku ambapo msafara huu mdogo ulizidi kuwa mbali na Makkah na kuwa karibu zaidi na Madina wasafiri walizidi kufurahi na matumaini ya kufuzu yaliongezeka katika nyoyo zao. Bilal na wenzake walikuwa wanaondoka kutoka kwenye nchi yao na sehemu walikozaliwa, na walikuwa wanakwenda kuwa wakimbizi ‘katika nchi ya ugeni,’ na hili lilikuwa jambo gumu kwa kila mtu, lakini kwa mtu jasiri kama Bilal ambaye alikwishapata mateso makali sana katika njia hii, uchovu na umbali huu, kwake haukuwa na maana kabisa na si muhimu. Wakati wowote ambapo wasafiri wenzake Bilal walilalamika kwa uchovu na kuondoka kwao, aliwafariji na kusema: “Na wanaofanya juhudi kwa ajili yetu, Sisi tutawaongoa kwenye njia zetu. na hakika Allah yu pamoja na watu wema.� (29:69).

2 + 3 4 5 6 5 1 ) * % +, - . /+ + % + % 0 ' () Wakati wote Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kumcha na wafanyao matendo mema.

Walisali sala na kuomba dua kwa Mola wao Mlezi wa

Ili waweze kufanya kazi yao kwenye njia ya kweli na kusadikisha imani yao ya Mungu mmoja, watu jasiri wa nyakati mbali mbali wakati wote walitumia uhajirina na kufuata nyayo za kiongozi, walistahamili matatizo yote, na walikuwa katika uhajirina wao walichukua hatua zinazofaa kuhuisha maadili ya Mungu, na kwa kujitoa kwao mhanga waliimarisha mambo ya roho na ukweli wa mabadiliko yao. Walisema ‘hapana’ kwa viwango vyote na udhibiti wa

59

60


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

kishetani, walijiondoa kwenye hatua ya majaribu na kwenda kwenye hatua ya kujitosheleza na walifanya bidii yao kuwa mfumo wa maisha yao na walionyesha hamasa na akili yao kwenye uwanja wa vita kwa kuhatarisha maisha yao na walipigana kwa ushupavu sana ili wawaokoe wapendwa wao.

UZURI WA KUSTAAJABISHA WA JIJI LA MADINA Msafara mdogo wa Waislamu kwa namna fulani ulimaliza safari ya kuchosha kati ya Makkah na Madina na ulifika karibu ya Madina. Kila mmoja wao alikuwa anatafakari atakuwa na nafasi gani katika nchi ile ya ugenini. Walisemeshana wenyewe kwa wenyewe: “Tutaweza kuishi bila hao tuwapendao na marafiki. Hakuna mtu yeyote katika sehemu hii ambaye anaweza kutusumbua?” Inawezekana Bilal alikuwa anajuliza mwenyewe: “hivi hapa tunaweza kumuabudu Mola Mlezi wa ulimwengu bila kizuizi chochote na kutayarisha mazingira ya kuasisi utawala wa Mungu?” wote walizama kwenye mawazo yao ambapo ghafla ajabu ya jiji la Madina lilivutia macho yao. Wakati huo huo jua lilikwishachomoza kutoka katikati ya mitende na lilikwisha sambaza miale yake ya rangi ya dhahabu kwenye milima na miti ya jiji la Madina na kufanyiza mandhari nzuri sana na ya kusisimua. Upepo mwanana mtulivu ulikuwa unavuma na kusukuma matawi ya mitende upande huu na ule. Shani hii ya Madina ilikuwa nzuri sana na kupendeza. Walihisi harufu tamu ya amani na uaminifu kutoka kila sehemu sana sana hivyo kwamba watu wote wa msafara walisahau uchovu wa safari na 61

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

wakapeana habari njema za kukutana na kuungana. Walifurahi kufika kwenye sehemu iliyofanana na Pepo katika uso wa ardhi. Wote walifurahia shani hii nzuri. Wakati mwingine pia waliangalia mbinguni kwa kukaza macho na walimshukuru Mwenyezi Mungu Mweza wa Yote na wakamwomba Yeye kutoka yakini ya mioyo yao: “Ee Mola Mlezi! Ifanye nchi hii iwe kituo cha dini Yako na utupatie nguvu hivyo kwamba, kwa kufuata nyayo za Mtume wako, tutundike na kuinyanyua juu bendera adhimu ya Uislamu na tuweze kueneza nuru na mantiki ya Uislamu duniani pote na tuweze kufanya mapinduzi ya Kiislamu kuwa mwelekeo wa wale wote wanaokandamizwa.” Walipoona kwamba wamefika karibu na jiji na walikuwa hawajapata madhara yoyote kutoka kwa maadui wa Uislamu, Bilal na wasafiri wenzake walifurahi sana na walisahau usumbufu wote. Hata hivyo, walihisi, hali ya hewa ya jiji la Madina ilikuwa nzito. Walisema: “Hakika tumechoka na taratibu tutazoea. Baada ya muda mfupi waliingia kwenye jiji la Madina. Baadhi ya waislamu karimu na waadilifu wa Madina walijitokeza kuwapokea. Waliwakumbatia na kuwakaribisha na wakafika nyumbani kwa baadhi ya Answari.”29

TATIZO KUBWA Hali ya hewa ya jiji la Madina ilikuwa nzito. Wakati mwingine palikuwepo joto kali na upepo ulivuma uliosababisha msongo 29

The Book, “Come with me to the House of Allah,” uk. 2; Tabaqat bin Sad, vol 2, uk. 169 ameandika kwamba Bilal na wenzake walisali kwenye nyumba ya Sad bin Khatima. 62


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

wa pumzi. Watu walikuwa majeruhi wa maradhi kama kipindupindu, homa na kadhalika. Watu wengi walikufa kila mwaka. Hasa zaidi wageni ambao hawakuweza hali ya hewa ya Madina waliungua zaidi kuliko wengine.

Ee Mola Mlezi! Ni Wewe ndiye uliyenikomboa kutoka kwenye makucha ya Umayyah na ulinisaidia hadi nikafika katika nchi hii. Wakati huu, pia, niokoe kutoka kwenye hali ya hewa hii nzito na chafu.

Ukosefu wa furaha kwa sababu ya upungufu wa uwezo wa kujikimu kimaisha, kukaa mbali na wapenzi wao na tatizo kuwa mgeni Madina zilikuwa sababu zilizo tengeneza mazingira ya Waislamu wengi kuugua hususan Bilal. Hili lilikuwa tatizo kubwa sana ambalo Muhajirina walikabiliwa nalo kwa mara ya kwanza.

Ee Mola Mlezi Mweza wa Yote! Katika matatizo yangu yote nilikugeukia Wewe na Ulinikomboa. Ulinifundisha uvumilivu. Nilihamia kwenye nchi Yako na sina mwingine isipokuwa Wewe. Kwa wema Wako nakuomba ulitatue tatizo hili na kunikomboa mimi na Waislamu wote wasiendelee kupata maradhi.”

Bilal ambaye alikuwa amedhoofika sana na muda mfupi tu uliopita aliopndokana na makucha ya waabudu masanamu na wakandamizaji aliugua haraka sana baada ya kufika Madina. Hakuwa na furaha. Wakati mwingine Waislamu walikwenda kumuona. Walimfariji na kumwombea apone haraka.

Kufuatana na hali ya Bilal na Waislamu wengine, mambo yaligeuka hivyo kwamba Waislamu hawakuwa na furaha hapo Madina na waliishi kwa majonzi. Kila siku walikumbuka mahali walipozaliwa, Makkah. Wote walimwomba Mwenyezi Mungu kwamba Anaweza kufungua njia ya kuondokana na mahali hapa.

Wakati mwingine Bilal alikuwa hana furaha hata kidogo kwa sababu ya homa na maumivu alilia na kulalamika kwa Mwenyezi Mungu Mweza wa Yote akisema:

MAOMBI YA DUA YA MTUKUFU MTUME (s.a.w.)

“Mwenyezi Mungu na amlaani Athbah, Shibah na Umayyah bin Khalaf, ambaye ndio wametuleta hapa. Wakati mwingine Bilal alikariri Aya kwa kukumbuka hali ya hewa ya Makkah na kusema: Hivi utafika wakati ambapo nitabadili usiku wangu huko Makkah kuwa asubuhi na kuona maua yapendekezayo na kuinukia vizuri pande zote. Na nitaona siku ambayo nitakunywa maji yote ya nchi hiyo na milima mirefu ya Makkah ikiwa mbele yangu?

63

Mtukufu Mtume (s.a.w.) wa Uislamu alihuzunika sana kwa sababu ya hali ya kusikitisha ya Waislamu. Alitafakari angefanyaje. Zaidi ya hapo, hakuna linaloweza kufanyika kuhusu hali ya hewa ya jiji. Hapana mtu mwenye uwezo kubadili hali ya hewa ya jiji. Hata hivyo, inafahamika pasi na maelezo kwamba katika matatizo na shida zote Mtukufu Mtume wa Uislamu alimgeukia Mwenyezi Mungu na akayaweka matatizo yake yote mbele Yake. Kwenye dharura hii pia alimgeukia Mwenyezi Mungu Mweza wa Yote na akasema: “Ee Mola Mlezi! Wapunguzie Waislamu mateso haya na 64


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

uyaponye magonjwa yao. Ee Mola Mlezi! Watu wanaonekana hawaridhiki na nchi hii. Hali ya hewa ya Makkah na kupenda nchi walikozaliwa haifutiki akilini mwao kabisa. Ee Mola Mlezi Mweza wa Yote! Wewe unao uwezo wa kubadilisha hali hii ya hewa nzito na chafu na utusaidie tuondokane na tatizo hili. Ee Mola Mlezi! Isafishe hali ya hewa ya jiji na yaondoshe magonjwa mbali mbali kutoka katika nchi hii.

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

kuaminika vya historia, inakubalika na tatizo hili la kimwujiza linaweza kueleweka kama limetatuliwa. Mola Mlezi Mweza wa Yote ambaye alimsaidia kipenzi Chake, Mtume wakati wote na alikuwa msaidizi wake katika matatizo yote alikuwa na uwezo (wakati huu, pia, ambapo Mtukufu Mtume alikabiliwa na tatizo kubwa) kubadili hali ya hewea ya jiji na huu ulikuwa mojawapo wa muujiza ya Mtume Mkuu, kwa sababu mambo kama haya na mabadiliko ya namna hii hii yaliyonyeshwa na Mitume wa Mwenyezi Mungu hayawezi kuhusishwa na watu wengine isipokuwa Mitume.

Ee Mola Mlezi! Wafanye Waislamu walipende jiji hili kwa yakini ya mioyo yao kama wanavyopenda Makkah.

Mojawapo ya matatizo katika njia ya Waislamu liliondolewa kwa njia ya maombi ya dua ya Mtukufu Mtume. Hata hivyo, walikuwa bado wanakabiliwa na tatizo kubwa zaidi.

Maombi ya dua ya Mtukufu Mtume wa Uislamu ilikuwa bado inaendelea hivyo kwamba hali ya hewa ya Madina ilibadilika kuwa safi na kupendeza. Wagonjwa waliokuwa wamelala vitandani walipona maradhi yao. Walishusha pumzi ya faraja. Sasa waliambatana na nchi hii na hawakukumbuka tena walikozaliwa, Makkah.

Muhajirina walioacha nyumba zao, wake zao na watoto wao, na walichokoza mateso makubwa ya uhamiaji, hawakuwa na fedha. Hawakuwa na nyumbani kwao wala uwezo wa kutosha wa kuendesha maisha ya furaha.

Tangu siku ile na kuendelea, Madina ilianza kuitwa Madina – e- Tayyabah na hali ya hewa yake ilikuwa tulivu sana na safi. Hali ya hewa ya jiji ilibadilika kama matokeo ya maombi ya dua ya Mtukufu Mtume kwa Mwenyezi Mungu.30 Endapo sehemu hii ya historia haingeandikwa, lingekuwa tatizo kubwa kwa wote. Hata hivyo kama ambavyo waandishi wa historia ya maisha ya Mtukufu Mtume wameandika kuhusu tukio hili na pia limenukuliwa kwenye vitabu vingi vya 30

Ni dhahiri kwamba kwa watu kama hawa, kukaa mbali na ndugu zao, kuwa mbali na nchi walikozaliwa na kutokuwa na uhusiano wa kijamii lilikuwa tatizo lisilovumilika. Hapana mtu aliyekuwa tayari kuanzisha mawasiliano na wao isipokuwa watu wachache ambao siku chache za nyuma walikubali kuwa Waislamu. Mauaji ya kikatili, mashambulizi ya mtu na mtu na ubaguzi wa kitabaka, bado ulikuwa unatawala jamii. Wengi wao miongoni mwa Muhajirina waliishi maisha ya upweke kwenye mitaa na vibanda vilivyokuwa karibu na msikiti wa Mtukufu Mtume. Usikivu wao wote ulielekezwa kwa Mwenyezi Mungu na

Qiblah-e-Islam, uk. 699. 65

66


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

walikuwa na matumaini kwamba Mola Mlezi wa ulimwengu angetatua matatizo yao.

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

MOYO WA UNDUGU KATIKA UISLAMU

Ni jambo lisilopingika kwamba watu ambao humgeukia Mwenyezi Mungu katika hali zote na huweka matatizo yao yote Kwake kamwe hawapotezi matumaini au kukasirishwa Mwenyezi Mungu Mweza wa Yote anasema: “Na wanaofanya juhudi kwa ajili yetu, sisi tutawaongoa kwenye njia zetu (29: 69).

Ili kuweza kuweka msingi wa jamii nzuri na iliyostaarabika, ni muhimu kupita katika njia nyingi na kuweka sheria bora na muhimu. Mojawapo ya njia ambayo Mtukufu Mtume Muhammad alipita ili aweze kustaarabisha dunia ilikuwa kwanza kabisa aliunganisha na kuwashirikisha watu wa jamii moja na nyingine na akatengeneza upendano miongoni mwa matabaka mbali mbali.

Mambo kama yalivyo, panapokuwepo na watu ambao kuacha jiji lao na mahali walipozaliwa na kwenda kukaa kwenye nchi ya ugenini ili waweze kumuabudu Mola Mlezi wa ulimwengu na kukataa kuabudu masanamu, ukatili na ukandamizaji, Mola Mlezi Mweza wa Yote pia huwafanya waheshimike na kuondoa matatizo yote kwenye njia yao.

Aliondoa tofauti za matabaka, wivu, husuda na ubaguzi kwa sababu jamii inaweza tu kuwa huru na kujitegemea ambapo kwanza kabisa inajibadilisha na kujitakasa yenyewe na halafu inachukua hatua za kusonga mbele na kujitegemea kwa watu wake na kwa njia hii hulinda mipaka yake dhidi ya mashambulizi ya adui.

Hapana mtu ambaye angefikiria kuhusu mageuzi ya jamii ambayo ilitiwa najisi na aina zote za upotovu na uchafu, lakini Mola Mlezi wa ulimwengu alilitatua tatizo hili kwa urahisi sana kwa kuweka sheria ya mbinguni. Ilikuwa sheria ambayo ilitia mwamko katika jamii ya wakati huo, na ambayo bado hai na itaendelea daima milele. Ilikuwa sheria ya udugu na moyo wa ushirikiano. Ilipoanzishwa na kuanza kutekelezwa sheria hii, Bilal na Muhajirina wengine walipata utulivu na amani ya kimawazo.

Jamii inaweza kuwa kiongozi wa msafara wa ustaarabu ambapo watu wake wote wanao ubinadamu na wanafanyiana wema na wanajitahidi kuwafurahisha wenzao na kutekeleza maadili ya kweli ya Kiislamu. Taifa linaweza kuishi katika amani na utulivu ambapo kwanza kabisa huondoa uovu na tofauti za ndani kwa ndani halafu watu wake huishi maisha ya ushirikiano na kupendana. Taifa na jamii inayoharibu tofauti za matabaka na ambayo watu wake ni waaminifu na hufanyiana wema na kuvunja minyororo ya mateka na utumwa, hupata mafanikio na kufuzu. Mambo kama yalivyo, ni jamii hiyo tu ambayo watu wake ni waaminifu na wanajali ustawi wa kila mmojawao inaweza kufuzu na kupata utukufu.

67

68


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Dini ya Mungu ya Uislamu ilianza kufahamika kwenye jamii ambayo ilipoteza maadili yote ya kweli na halisi ya maisha ya kibinadamu na yalikwisha fanana na yale ya hayawani. Kitu kilichokosekana katika jamii hiyo ni wema na kuhurumiwa. Hata hivyo, Uislamu ulitatua matatizo yote ya siku hizo moja baada ya lingine na kusitisha sheria nyingi zisizofaa. Kwa ufupi, mpango huu wa kuvutia ulianzisha kipindi cha mafanikio na bahati njema katika maisha ya Waislamu. Kama ilivyoamuriwa na Mwenyezi Mungu, Mtukufu Mtume wa Uislamu aliwakusanya Waislamu pamoja kwenye msikiti na akakariri udugu baina yake na Imamu Ali Amiri wa waumini, na baina ya wawili wa Waislamu wote wengine na kuwafanya kuwa ndugu ya kila mmoja. Siku moja Bilal na Ubaydah, mtoto mwanamme wa Harith walishikana mikono kama ndugu.31 Tangu hapo na kuendelea Waislamu wote wakawa ndugu ya kila mmojawao32 na kwa utekelezaji wa mpango huu, tatizo la pili ambapo liliwakabili Waislamu Muhajirina lilikoma kwa maana kwamba walishiriki katika furaha ya kila mmoja wao na katika huzuni ya kila mmoja wao na wakawa kama mwili moja na roho moja. Maumivu ya Muislamu moja yalihisiwa kama maumivu ya

31

32

Qamus-ur- rijal, uk. 243; Al-Isabah, uk. 169; Usud-ul-Ghabah, juz.i, uk. 208.Baadhi ya sera zimetaja kwamba Bilal alifanywa ndugu wa Abu Doyah. Hakika waumini wote ni ndugu, (Surah Hujurat, 49:10); Tabaqat bin Sad, Juz. iii, uk. 165. (Baadhi ya wengine wameandika kwamba Bilal alifanywa ndugu na Abdulla bin A. Rahman Khat’an, Nasikh uk.35). 69

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Waislamu wote. Muislamu mmoja alipopata shida na alikuwa na matatizo, Waislamu wote waligawana tatizo lake. Na ilikubalika kwamba wasingefanyiana uhaini au kusingiziana uwongo na wangependana wao kwa wao. Kipengele kikubwa sana kilichokuwa njia ya maendeleo ya kundi hili dogo ilikuwa ni huu mkataba wa udugu. Mfano wa madai haya yanaweza kuonekana kwenye maisha ya baadaye ya watu hawa. Kwenye vita ya Badr waumini 313 walipigana na makafiri 1,000 na wakapata ushindi. Kipengele kimoja tu kilichosababisha huu ushindi wao ni kwamba waliungana kikamilifu na walikuwa wanapigana kwa sababu moja. Kwenye mojawapo ya mapambano, watu kumi walikufa kwa sababu ya kiu, ingawa maji yalikuwepo. Ilitokea hivyo kwa sababu waliwapendelea ndugu zao kwanza. Mamia ya matukio mengine mengi ya aina hii yameandikwa kwenye historia na yote yalitokea kama matokeo ya ushirikiano na udugu. Ni sawa kabisa kama tukisema hapa kwamba nchi za Kiislamu na kupata nguvu na watu wote waoneane huruma na kushirikiana na kila mmoja ili kwamba tatizo la Muislamu mmoja walione la kwao wote na kama wanao uaminifu wanapo sema kwamba wao ni ndugu, basi kwa hakika watapata maendeleo yao, ustaarabu na kujitegemea hapa duniani na wataweza kumwangamiza adui yao mkubwa sana katika kipindi kifupi sana. Endapo makubaliano ya udugu na ushirikiano miongoni mwa Waislamu ungeendelea kubakia kamili, mabeberu wangewezaje kuona njia yao ya kuingia kwenye nchi za Kiislamu na 70


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

kuwafanya wapigane wao kwa wao na halafu kufanya Uzayuni (Zionism) kuwatawala? Mabeberu wangewezaje kuingilia kati hatima ya Waislamu na kuwaonea polepole? Mabeberu wangewezaje kuzitupa pembeni sheria za mbinguni za Waislamu na kutekeleza sheria zao zisizo na msingi miongoni mwao? Kwa kweli, Wazayuni wangewezaje kukalia sehemu ya nchi za Kiislamu na kuwaonea Waislamu sana hivyo kwamba hawawezi kulala usingizi kwa amani? Ni dhahiri kwamba mapigo haya yanaendeshwa dhidi ya Waislamu na watu hao ambao wamelifanya jina la Uislamu chombo cha kulinda maslahi yao. Tunasema kwamba mambo yaliyo endeleza jamii ya wakati huo iliyokuwa nyuma na Waislamu wakaweza kufika upeo wa juu sana wa dunia chini ya bango la ushirikiano na kutundika bendera tukufu ya Uislamu katika kanda hizo ni udugu na usawa. Tunasema tena kwamba udugu na upatanifu ndio tu njia ya kusonga mbele na kuendelea. Mwafaka wa udugu maana yake ni kufuta ubaguzi wa tabaka, kuharibu mizizi ya fitina na undumilakuwili, kukazia mafunzo ya imani na upendo katika kuwaendeleza wanadamu, na kuwatayarisha kwa kampeni dhidi ya ubeberu na uzayuni kwa ajili ya ushindi wa Uislamu na Waislamu.

Bilal Wa Afrika

walipohamia Madina na kujenga msikiti mkubwa huko, uamuzi ulifanywa kwamba wasikose Swala ya jamaa, hususan Swala ya Ijumaa. Hata hivyo, kwa kuwa hapakuwepo na namna ya kutangaza wakati wa Swala (adhana), watu walikwenda msikitini katika makundi makundi. Watu wengine waliwahi kufika na wengine walichelewa. Wakati mwingine ilitokea kwamba baadhi yao walikosa neema ya Swala ya jamaa au waliweza kushiriki kwenye sehemu ndogo tu ya Swala. Kwa upande mwingine Mtukufu Mtume wa Uislamu alisema mara nyingi kuhusu ubora na thawabu za kiroho za Swala ya Ijumaa hivyo kwamba watu walitiwa moyo kwenda kusali Swala za jamaa na walitaka kushiriki kwenye Sala za jamaa kadiri ilivyo wezekana. Kwa mfano, siku moja ambapo Mwislamu ambaye hakuweza kushiriki kwenye sehemu ya Swala ya jamaa mathalani Takbiratul Ihram alimuuliza Mtukufu Mtume: “Nitastahili kupata thawabu za kiroho nyingi endapo nikimwacha huru mtumwa?”33 Waislamu walipata shauku ya kupata wepesi wa kuwaita watu msikitini katika muda uliopangwa. Kila mtu alishauri na Mtukufu Mtume alisema kwamba ili ushauri uliotolewa uweze kuchunguzwa, Waislamu wakusanyike msikitini ili 33

WITO MKUBWA WA UISLAMU Wakati wa miaka kumi na tatu ambayo Waislamu walikaa Makkah, hawakuweza wakati wowote kukusanyika pamoja na kuunda jamii kwa uhuru na kuswali sala za jamaa. Hata hivyo, 71

Bilal Wa Afrika

Inasemekana kwamba mtu huyo alikuwa Abdullah Bin Mas’ud ambaye alisema: Nimesahau kutamka Takbiratul-Ihram. Ninaweza kupata thawabu zinazolingana na kumwachia mtumwa kuwa huru?” Mtukufu Mtume alijibu: “Hapana,” Akasema: itakuwaje endapo nikiwaachia huru watumwa wawili?” Mtukufu Mtume alijibu: “Ewe bin Masud! Hata kama utatumia vyote vilivyopo katika uso wa ardhi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, hutaweza kupata ubora (ulioambatanishwa naTakbir ambayo ulisahau kutamka.)” 72


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

wabadilishane mawazo. Ilikuwa muhimu kwamba mapendekezo yote yaliyotolewa yafikiriwe na Mtukufu Mtume. Watu wengine walisema: “Ingekuwa vizuri kama pembe lingepulizwa wakati wa swala ili watu wajue kwamba muda wa swala umefika.” Mtukufu Mtume akasema: “Kupuliza pembe ni jambo linalofanywa na Wayahudi pekee na sisi hatuwezi kuwa wafuasi wa Wayahudi.”

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Mtukufu Mtume akamuagiza Bilal kutangaza saa ya Swala kwa watu kwa kutamka maneno hayo hapo juu. Kila siku Bilal alikuwa anatamka kwa sauti ya kupaza Assalat Jamiah wakati wa Sala na kwa hiyo aliwaita watu waende msikitini. Ingawa Waislamu walikwenda msikitini baada ya kusikia sauti ya Bilal, hata hivyo, kutamka maneno hayo tu kwa ajili ya Waislamu kukusanyika pamoja kwa ajili ya kusali haikutosha, ilihitajika mbiu nyingine imara, yenye athari na hamasa.

Mtu mwingine alisema: “Itakuwa vizuri kama tukinunua kengele kama ile ya Wakristo na tuitumie.”

Siku moja Mtukufu Mtume alipokuwa nyumbani kwa Imam Ali, Amiri wa Waumini, Malaika Mkuu Jibrili alishuka na akaleta ‘Adhana’ na akaikariri mbele ya Mtukufu Mtume.

Mtukufu Mtume alisema: “Njia ya Wakristo haikidhi matakwa yetu. Lazima tujitegemee.”

Mtukufu Mtume alimuuliza Imamu Ali: “Umesikia Adhana?” Ali alijibu “Ndio.”

Kundi la tatu lilitoa penedekezo kwamba muda wa Swala utakapokaribia, moto mkubwa sana uwashwe ili kwamba watu wauone na waende msikitini.

Halafu Mtukufu Mtume alisema: Mfundishe Bilal namna ya kutamka Adhana ili siku zijazo anaweza kuitamka wakati wa sala”.34

Mtukufu Mtume akasema: “Moto unaweza kuwashwa wakati wa usiku. Zaidi yake kuwasha moto ni dini ya Magi”

Baada ya hapo mfumo wa Adhana’ ulionekana kuwa mzuri sana na njia iliyo bora ya kutangaza wakati wa Swala na kuwakusanya Waislamu.

Wakati huo huo mtu akasimama akasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu itakuwa vema kama wakati wa Swala mtu mwenye sauti ya kupaza anatangaza hivyo kwamba, inaposikika sauti yake, watu waende msikitini.” Mtukufu Mtume alipenda pendekezo hili na akaliboresha kwa namna ifuatayo: wakati wa Swala ukifika mtu atamke kwa sauti ya kupaza ‘As-Salat Jamiah.’

73

Wakati wa Swala Bilal alikuwa akipiga Adhana kwa sauti yake tamu na ya kupaza kutoka kwenye paa la msikiti. Moyo wa imani na hamasa ya kuboreka na kukombolewa ulupulizwa kwenye dhamira ya Waislamu na haraka walielekea msikitini.

34

Furu’ul Kafi Juz. 3, uk. 302, Qamusur Rijal, uk. 1 Majma’ul Bayan uk. 268, Majalisul Muminin uk. 268, chapt. ‘Muslims gathering. 74


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Ni lazima ieleweke kwamba Adhana si sauti tu. Si sauti isiyo na mantiki, isiyo na maana na hafifu ambayo kazi yake ni kuwakusanya watu kwa ajili ya propaganda kama ilivyo kwenye dini zingine. Kwa upande mwingine ni alama ya kanuni na mambo yafuatayo ya Uislamu. Ni mbiu ya kutia moyo. Inamfanya mtu ahamasike kutenda. Ni shauku, hamasa, matumaini na utafiti. Adhana ni wito unaowaita watu waende kwenye ushirikiano na mshikamano na maafikiano chini ya kivuli cha Upweke wa Mungu na huwaita waende kwenye ubora na maendeleo chini ya uongozi wa Utume wa Mtukufu Mtume wa Uislamu.

na kampeni dhidi ya ukandamizaji na dhuluma ilienea katika dunia yote ya Arabuni

Mambo kama yalivyo, pale ambapo sauti ya kuchangamsha ya Bilal ilitokeza kutoka kwenye kona ya msikiti wa Mtume na kuvuma kwenye anga ya Madina ilisisimua hisia za watu na kuwavuta waende msikitini kusali kwa hamasa kubwa.

Abdullah bin Ali anasema: “Nilipokuwa nabeba bidhaa kutoka Basra kwenda Misri, nilikutana na mzee mmoja njiani ambaye nywele zake nyeupe ziliongezeka kung’aa kwake na sura yake takatifu na nuru ya imani na ukuu ilikuwa inang’ara usoni mwake. Alikuwa na nguo mbili tu mwilini mwake, mojawapo ilikuwa nyeusi na nyingine nyeupe.

Watu walifurahia sana Adhana na maneno yake hivyo kwamba walikuwa wanangojea ile sauti ya mbinguni itokeze kutoka kwenye koo la muandini wa Mtukufu Mtume wa Uislamu na kuwaita waende kwa Mungu. Adhana ya Bilal ilipomalizika, Waislamu walijipanga kwenye safu bega kwa bega na Mtukufu Mtume aliongoza Swala.35 Mkusanyiko wa Waislamu waliosimama katika safu, ulimfanya adui atetemeke na kuyafanya macho ya kila mtazamaji yatunduwae.

Maadui wa Uislamu waliogopa isije siku moja mapinduzi haya mazuri kabisa yakaweza kuvutia mioyo na roho za watu wote na kuwa ya ulimwengu wote na kuangusha dunia yao nyepesi na chafu. Kwa hivyo, walipanga mpango mpya kila siku na walitumia njama mbaya sana ili waharibu mapinduzi na wanamapinduzi wa Kiislamu.

UBORA WA ADHANA NA MUADHINI

Niliwauliza watu: “Mtu huyu ni nani?” Walijibu: “Huyu ni Bilal muadhin wa Mtukufu Mtume” Nilifurahi sana kujua hilo na niliamua kunufaika na ujuzi wake. Nilinunua nyenzo za kuandika na nikamwendea. Nilimsalimia naye akaitikia.

Umashuhuri wa Uislamu na jamii mpya ya Waislamu ambao ulidhibitiwa na moyo wa adui, usawa, imani ya Mungu mmoja

Nilisema: “Mwenyezi Mungu na akurehemu. Wewe ni mmojawapo wa masahaba wa Mtukufu Mtume na umefaidika kuwa sahaba wake. Ningependa unisimulie hadithi na maneno ambayo uliyasikia kutoka kwake.”

35

Halafu Bilal akasema: “Umenijuaje?”

Safinatul Bihar Juz. I, uk. 165. The life of the Holy Prophet uk. 261. Muntahul Amal uk. 87. 75

76


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Nikasema: “Wewe ni Bilal muadhin wa Mtukufu Mtume wa Uislamu.” Nilipotamka maneno haya machozi yalianza kutiririka kutoka machoni mwake na mimi pia nikalia na watu waliokuwa wamekusanyika nao pia walilia. Bilal akauliza: “Wewe unatoka wapi?”

Bilal Wa Afrika

Nilimsikia Mtukufu Mtume wa Uislamu anasema: “Yeyote anaye Adhin Adhana kwa siku arobaini kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, mnamo Siku ya Hukumu atafika katika hali kwamba matendo yake mema arobaini yatakuwa yamekubaliwa, matendo ambayo hayataachanishwa naye mnamo siku hiyo.” Nikasema: “Mwenyezi Mungu na akusamehe. Sema zaidi.” Bilal aliendelea na kusema: “Andika”

Nikamjibu: “Natoka Iraq.” Alifurahi kwa taarifa hiyo na baada ya kutafakari kwa sekunde chache akasema: “Ewe ndugu wa Iraq! Andika kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu, nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu anasema: ‘Wale wanaotoa Adhana ni wadhamini wa sala na saumu ya watu.’ Nyama iliyonunuliwa kutoka kwenye soko ambamo humo husikika sauti ya Adhana ni safi na halali; na kupigana na watu wa jiji ambamo humo sauti ya Adhana inasikika si halali.36 Waadhini hawaombi kitu chochote kutoka kwa Mwenyezi Mungu ila hupewa na hawamuombei mtu yeyote isipokuwa kwamba maombezi yao hukubalika.” Abdullah anasema: “Nilifurahia maneno ya Bilal na nikasema: ‘Mwenyezi Mungu akuneemeshe. Sema zaidi.” Bilal akasema: “Andika”

36

Bilal Wa Afrika

Lazima itamkwe hapa kwamba vita inayoendeshwa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haikuwa dhidi ya taifa linaloteseka la Iraq isipokuwa ilikuwa dhidi ya Chama cha Bath cha Iraq ambacho kilikuwa kinapigana kwa msaada wa Marekani (U.S.A) Urusi na mataifa mengine yanayopinga maendeleo. Katika hali hiyo ilikuwa ni kujilinda si vita. 77

“Nilisikia Mtukufu Mtume wa Uislamu anasema: ‘endapo mtu anaadhini kwa miezi ishirini, Mola Mlezi wa ulimwengu atamfufua Siku ya Hukumu akiwa na nuru ambayo itakuwa sawa na mbingu (ni dokezo la zaidi ya nuru ya kawaida). Endapo mtu ana Adhini kwa miaka kumi Mwenyezi Mungu atampa nafasi ya Peponi sawa na ile atakayopewa Mtume Ibrahim.’ ” “Pili nilimsikia Mtukufu Mtume anasema: ‘Kama mtu ana Adhini Adhana kwa mwaka moja Mwenyezi Mungu atamfanya Siku ya Hukumu afike katika hali ambayo dhambi zake zote zitakuwa zimesamehewa hata kama zitakuwa kubwa kama Mlima Uhud.’ ” Abdullah akasema: “Tafadhali endelea kusema zaidi.” Bilal alisema: “Sawa kabisa. Weka katika kumbu kumbu yako na utekeleze kwa mujibu wa taarifa hii. Mtukufu Mtume alisema: ‘Kama mtu ana adhin Adhana kwa ajili ya Sala moja kwa imani ya Mwenyezi Mungu atamsamehe dhambi zake na humfanya kuwa mwenzi wao na wahanga katika pepo.” Abdullah anasema: “Nikaanza kudadisi. Nikasema kwa jazba

78


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

kubwa na hamasa: “Usifiwe wewe. Tafadhali nukuu maneno mazuri kuliko yote ambayo uliyasikia kutoka kwa Mtukufu Mtume.” Akasema: “Ah! Umegusa nyuzi za moyo wangu” na akaanza kulia kwa namna ambayo kwamba hata mimi nililia. Halafu akasema: “Andika: Nilimsikia Mtukufu Mtume anasema; “Siku ya Hukumu Mwenyezi Mungu atawakusanya watu pamoja na atawatuma malaika ambao watabeba bendera za nuru mikononi mwao na watakuwa wamepanda farasi ambao hatamu zao zitakuwa za fuwele na viti vyao vya nyuma vitakuwa vya maski. Wataingia Uwanja wa Siku ya Hukumu wakingali wamesimama juu ya farasi hao na wata Adhini Adhana kwa sauti ya kupaza. “Ninaapa kwake Yeye ambaye ameniteua mimi kwenye tabligh ya Kitume kwamba Ufufuo utakapofanyika waadhini watakuwa wamepanda farasi wa thamani na watapita mbele ya watu huku wanasema. ‘wataadhini (Mwenyezi Mungu mkubwa). “Watakapotamka maneno haya wafuasi wangu watalia. Na watakaposema: ‘Ninashahidili ya kwamba hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu.’ Wafuasi wangu watasema: ‘Tulikuwa tukimuabudu Mwenyezi Mungu Mmoja duniani’. Na watakaposema: ‘Ninashuhudia kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu.’ Wafuasi wangu watasema: ‘Sisi ni wafuasi wa Mtume huyu huyu ambaye hatukumuona lakini tulimwamini.’ Halafu wataongeza: ‘Ni Mtume huyu huyu ambaye ameelekeza kazi yake kikamilifu kama Mjumbe wa Mwenyezi Mungu.’

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Abdullah anasema: “Halafu Bilal alinitazama na akasema: ‘Kama inawezekana usiache Adhana na jaribu kwamba usifariki dunia bila kuwa Muadhini.’ ”37 Kuadhini Adhana ilikuwa zawadi maalum ya Bilal. Wote walimjua vizuri na walimheshimu. Huyu mtu Bilal na heshima aliyoifurahia iliamsha wivu miongoni mwa baadhi ya watu. Hawa ni watu ambao kabla ya hapo hawakumthamini Bilal. Hawakuweza kuona watu wengine wa matabaka ya chini wakifurahia nafasi kama hiyo. Pole pole walifikiria mkakati wa kumwondoa Bilal asiwe Muadhini wa Adhana na walikuwa wanatafuta kisingizio kwa ajili ya utekelezaji huu. Ili kuweza kutimiza lengo hili watu walitengeneza na kutekeleza mipango mbali mbali. Mathalan, walimwendea Mtukufu Mtume na wakamwambia: “Nafasi hii ya muadhini ni ya juu sana na inayothaminiwa na haistahili apewe mtu ambaye kabla ya hapo alikuwa mtumwa. Ni vizuri kwamba muadhini wa Mtume awe ni mmojawapo wa watu mashuhuri wanaojulikana kwa Waarabu.” Siku nyingine walikwenda kwa Mtume na kusema: “Sauti ya Bilal si nzuri hata kidogo. Muadhini anatakiwa kuwa na sauti nyororo ili aweze kuwavuta watu wengi iwezekanavyo.” Silaha yao ya tatu na ya muhimu sana dhidi ya Bilal ilikuwa walisema kwamba:

“Halafu ni Mola Mlezi Mweza wa Yote ambaye atawakusanya nyinyi na Mitume. Halafu waadhini watakwenda kwenye nafasi zao na kuna zawadi hapo ambazo hakuna jicho ambalo limeziona au sikio ambalo limezisikia.’ “

“Bilal alikuwa hatamki maneno ya Kiarabu kwa usahihi kwa

79

80

37

Al-Wafi, Juz. ii, uk. 87; Amali As Saduq p. 127, Nafasur Rahman. Juz. 10. uk. 127.


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

mfano husema ‘sin’ badala ya ‘shin” (As-hadu an lailaha Ilalah badala ya Ash-hadu an lailaha illalah) na hii ni dosari kubwa sana ambayo lazima itafutiwe ufumbuzi.”38 Kwa ufupi makusudio ya pingamizi, ambazo wakati mwingine zilielezewa kwa shauku na wakati mwingine kwa ukali, haikuwa lolote isipokuwa Bilal asiwe muadhini. Kwa mujibu wa maoni yao, Adhana ambayo ilisikika kwa Waislamu na wasio Waislamu, ingeadhiniwa na mtu mwenye sauti nyororo ambaye hakusema ‘sin’ badala ya ‘shin’. Wakati mwingine walimdhihaki Bilal moja kwa moja na walisema kwa lengo la kuhalalisha kitendo chao: “Tunasema hivi kwamba ili tulinde heshima ya Uislamu na Qur’an.” Wapinzani wa Bilal ambao idadi yao ilikuwa kubwa, walifanya shughuli zao za upinzani na walitoa hoja kwa kiasi kwamba Mtukufu Mtume, pamoja na umashuhuri wake, alianza kutafakari ama akubaliane na mapendekezo yao na amzuie Bilal asiendee na kazi yake. Hapa ndipo Jibril alishuka na akampa taarifa Mtukufu Mtume kuhusu mipango ya uovu ya maadui na ubaguzi wao wa kipindi cha ujahiliya na akamthibitisha Bilal kuwa muadhini na akasema: “Mwenyezi Mungu Muweza wa Yote anakubali ‘sin’ ya Bilal badala ya ‘Shin’ kwa kuwa Bilal hawezi kutamka ‘shin’ kwa usahihi ‘sin’ yake imekubaliwa badala ya ‘shin’.39 38 39

Muntahul Amal uk. 87; Safinatul Bihar uk. 105 Mtu alikuja kwa Imam Ali na akasema: “Mtu anatafuta na kumuona Bilal kuwa na makosa na kumshutumu kuhusu jambo la matamshi ya 81

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Kwa hiyo jibu la mkato lilitolewa kwa washindani wa Bilal na aliendelea na kazi yake ya ngazi ya juu. Kama mambo yalivyo wapinzani na maadui wa mapinduzi na Uislamu walifanya bidii sana kutaka kumzuia Bilal asiwe muadhini lakini Mwenyezi Mungu aliwafedhehesha na alifichua mpango wao mbaya na akahakikisha kwamba kwa kisingizio hiki walikuwa wanaunga mkono ubaguzi wa rangi na kijamii na walitaka kuleta vurugu za kijamii. Baadaye watu hawa walifichua tabia yao kwenye historia ya Uislamu na baadhi yao walifikiriwa kuwa wafitini maarufu.

MWONGO ACHOMWA MOTO HADI KUFA Sauti ya Adhana ya Bilal ilisikika katika jiji la Madina kila asubuhi na jioni. Waislamu walipenda kuisikia na maadui wa Mtukufu Mtume hawakuipenda. Kila adui alisema kitu kimoja au kingine kuhusu Adhana na maneno yake ya kusisimua. Mmojawapo wa maadui, ambaye kwa upande mmoja hakuweza kufichua upinzani wake na chuki yake na kwa upande mwingine alihuzunika sana kwa sababu maendeleo ya Uislamu na Waislamu alionyesha dalili za usumbufu anaposikia Adhana. Na hasa zaidi Bilal alipofika sehemu ya jina takatifu la Mtukufu Mtume na kushahidilia Utume wake, uso wa mtu huyo ulibadilika na alisema kwa hasira na kinyongo: “Ona jinsi huyu mwongo mweusi anavyotukuza jina la Muhammad kama ‘sin’ na ‘shin’. Imam alisema: Maneno tunayotamka ni ya kuweka imara matendo mema. Kama mtu anatamka maneno kwa usahihi lakini matendo yake ni maovu na dhalimu, matamshi ya maneno hayamsaidii kitu. ‘sin’ na ‘shin’ ya Bilal haina madhara, kwa sababu matendo yake ni mema na sahihi. (Nafasur Rahman. sura I) 82


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Mtume! Angalia kwa maneno haya jinsi anavyowakusanya watu mahali pamoja!”

Kwa hiyo , alimwita Bilal na alisema: “Hivi huruma na upendo vimekutoka hata ukafanya hivyo?”40

Hatimaye wito wa mnafiki huyu ambaye alikuwa na desturi ya kutamka kwa ajili ya Bilal aliyekandamizwa ulikubalika kwa ajili yake mwenyewe. Siku moja alipokuwa anawasha taa wakati wa Adhana ya Swala ya jioni na alikuwa anasema: “Huyu mwongo na aungue moto” ghafla mwale wa moto ulimchoma kidole chake na polepole moto ulifika kwenye vidole vyake vingine. Ingawa alijaribu sana kuzima moto huo, hakuweza. Hatimaye moto ulienea kwenye kiwiliwili chake chote na akaanza kulia na kupambana katikati ya miale ya moto. Majirani na ndugu zake walijaribu sana kuuzima moto huo mkali lakini hawakuweza.

Bilal alikuwa mmojawapo wa masahaba ambao Mtukufu Mtume alikuwa anawapa heshima maalum. Alifikiriwa kuwa mtunza hazina na mfanyakazi wa Mtume naye Mtukufu Mtume alikuwa anamtambua vema kuhusu jitihada zake na kujitolea kwake lakini hapana hata kimoja ya vitu hivyo vingeweza kumzuia Mtume asimlaumu na kumshutumu Bilal kwa kufanya kinyume cha haki.

Kwa hiyo, hatimaye mwongo na adui wa Mtukufu Mtume wa Uislamu alisimama kwenye kona na baada ya muda mfupi aliungua mwili wote na kuwa majivu mbele ya watu.

BILAL ASHUTUMIWA Wakati ambapo jeshi la Uislamu liliteka ngome za Khaybar chini ya uongozi wa Imamu Ali Amiirul Muuminiina na kurudi Madina kituo cha Uislamu likiwa limeshinda, baadhi ya watu walichukua ngawira na mateka miongoni mwa watu hao, Bilal alikuwepo ambaye aliwachukuwa mateka wanawake wawili. Bilal aliwapitisha hao mateka wa kike katikati ya uwanja wa vita na katikati ya maiti za wapiganaji waliouawa vitani. Wanawake hao walionekana katika hali ya kusikitisha sana kwa kulia kwa uchungu sana, na kukwaruza nyuso zao na kupasua nguo zao.

Bilal alikuwa sabaha wa Mtukufu Mtume na siku zote alikuwa anasifiwa na kufanyiwa wema naye, lakini wema wote huo na upendeleo ulikuwa kwa mema na endapo alibadili tabia yake na kupotoka kutoka kwenye njia yake alipaswa kulaumiwa vikali. Ingawa Bilal hakufanya dhambi kubwa na tendo lake lingeeleweka tu kama kinyume cha tabia njema na haki, Mtukufu Mtume alitaka maelezo yake mwenyewe ili aweze kuweka wazi kwamba alikuwa hayuko tayari kuvumilia upotovu hata uwe mdogo sana kutoka kwenye njia ya Uislamu hata kwa upande wa masahaba wake wa karibu sana. Uislamu ni dini, ambayo imekamilika kama mfumo wa maisha na nidhamu na haivumilii upotovu wowote kwa upande wa waumini wake. Si sawa na mifumo mingine na dini zingine ambamo makosa ya ndugu na watu wa karibu sana kufumbiwa macho. Hapa ni amri ya Mwenyezi Mungu ambayo inatakiwa itekelezwe, na Mwenyezi Mungu hutaka kwamba Uislamu 40

Mtukufu Mtume alipata taarifa ya tukio hilo na hakufurahi. 83

Zindaghi -e- Payambar Juz. 2, uk. 81; Safinatul Bihar Juz. I, uk. 104; Muhamad wa Yaman uk. ii, uk. 69. 84


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

lazima uwachukue watu wote katika kiwango kimoja na sheria, na Mtume lazima aizingatie sheria hii na aitekeleze kwa mujibu wake. Kama mambo yalivyo katika dini hii utaratibu wa kawaida inawezekana usifuatwe kuhusu matendo ya Bilal- Bilal huyo huyo ambaye yupo karibu sana na familia ya Mtukufu Mtume kwamba humsaidia binti ya Mtume katika kazi zake kwa kuwabembeleza watoto na kufanya kazi yake kwa uzuri unaopendeza. Huhakikisha kwamba Bibi Fatimah Zahra anasaga shayiri kwa kutumia kinu cha kusukuma kwa mkono na afanyapo hivyo hawezi kuwaangalia watoto, wanalia. Halafu Bilal humwomba Bibi Fatimah Zahra ama awabembeleze watoto au asage shayiri yeye mwenyewe. Binti wa Mtukufu Mtume alijibu: “Hapana, ninaweza kuwaangalia watoto vizuri zaidi, kwa hiyo, wewe saga shayiri.” Katika hali iliyo wavutia wengi, siku hiyo Bilal alichelewa kufika msikitini kwa ajili ya Adhana isivyo kawaida na akakutana na macho ya Mtukufu Mtume na Waislamu yaliyokuwa yanamdadisi. Baadaye Bilal alimtaarifu Mtukufu Mtume kuhusu jambo hilo na alisikia jibu hili: Mwenyezi Mungu na awarehemu wewe na Fatimah.”41 Hata hivyo, pamoja na haya yote, Mtukufu Mtume alionyesha kosa lake ili kwamba wote wajue kwamba mbele ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake hakuna mtu anayeheshimiwa au kufedheheshwa bila sababu na bila kujali nafasi yoyote aliyo nayo mtu, lazima ajieleze kuhusu kushindwa kwake kufuata kanuni.

Bilal Wa Afrika

BILAL KWENYE VITA VYA BADR Bilal hakuwa tu mwenye kuabudu ili aweze kuadhini Adhana wakati wa sala kwa hiyo asiwe na kazi nyingine yoyote ya kufanya. Kwa upande mwingine alikuwa mtu mwenye juhudi kwa jamii, na alitoa mchango muhimu katika kuunda jamii mpya na kueneza Uislamu. Alikuwa na ari kubwa ya kujituma na ushupavu. Katika vita vilivyofanyika baina ya Waislamu na Makafiri baada ya Waislamu kuhamia Madina, pamoja na vita vya Badr, Uhud na khandak,42 Bilal alikuwa msitari wa mbele kwenye uwanja wa vita na nguvu zake na ustahamilivu wake vilisifiwa na wote.43 Baada ya Mtukufu Mtume kuhamia Madina, hali ya Waislamu ilibadilika na walianza kuhubiri Uislamu kwa uhuru. Uislamu ulianza kuenea. Mfumo wa jamii ulianzishwa na Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu aliamuriwa, kinyume na sera yake ya Makkah, kusimama kidete dhidi ya makafiri na hata kupigana nao endapo upo umuhimu. Vita ya Badr ilikuwa vita ya kwanza ya muhimu ambayo ilikuwa pambano baina ya Waislamu na Makafiri. Jambo lenyewe lilikuwa kwamba mnamo nusu ya pili ya mwezi wa Jamadul Awwal taarifa ilipokelewa Madina kwamba kulikuwa na msafara uliotoka Makkah kwenda Syria kwa lengo la kufanya biashara. Mtukufu Mtume aliufuatilia msafara huo 42 43

41

Safinatul Bihar, Juz. I, uk. 104. 85

Bilal Wa Afrika

Muntahul Amal, uk. 119. Qamus ur Rijal uk. 238; Tabaqat bin Sa’d uk. 170; Safinatul Bihar Juzl. I, uk. 105; Jame’ur Ru’at, uk. 131; Rijal- e- Ma Maqani uk. 182; Life of the Holy Prophet uk. 697. 86


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

hadi Zatuk Ashira. Na akakaa hapo hadi mwanzoni mwa mwezi uliofuata. Hata hivyo hakuona msafara na alirudi. Taarifa iliyopokelewa ilikuwa kama ifuatayo: (i)

Ni msafara mkubwa na wakazi wote wa Makkah wanao mgawo wao humo.

(ii)

Kiongozi wa Msafara ni Abu Sufyani na watu watano wanayo kazi ya kuulinda msafara huo.

(iii)

Bidhaa zimebebwa na ngamia elfu moja na thamani yake ni takriban dinari elfu hamsini.

Mtukufu Mtume aliondoka Madina wakati wa mwezi wa Ramadhani wa mwaka wa pili baada ya kuhamia Madina akiwa na watu mia tatu kumi na tatu kwa lengo la kutaifisha rasilimali ya Quraishi na akapiga kambi karibu na Badr. Abu Sufyan ambaye alikwisha pata taarifa kwamba msafara wake ulikuwa unafuatiliwa na wapiganaji wa Uislamu, wakati wa kurudi kutoka Syria hakushindwa kuchukua hatua ya kuwa mwangalifu zaidi na alitambua baada ya wapelelezi kwamba safari hii hangeweza kuwakwepa Waislamu. Kwa hiyo, alipeleka ujumbe Makkah awaeleze Quraishi kuhusu nia ya Mtukufu Mtume na kutaka msaada kutoka kwao. Wakati huu hisia za watu wa Makkah ziliamshwa na watu wote jasiri na wapiganaji, isipokuwa Abu Lahab, walijitayarisha kwenda kupigana. Pia yeye (Abu Lahab) alimweka Abi bin Hisham badala yake na akampa ‘dirham’ 4000. Umayyah bin Khalaf, ambaye alikuwa mmojawapo wa wazee wa Quraishi hakutaka kushiriki katika matayarisho haya ya jumla kwa sababu ilitaarifiwa kwamba Muhammad alisema: 87

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

“Umayyah atauawa na Waislamu.” Watu matajiri miongoni mwa makafiri waliona kwamba kutoshiriki kwa mtu kama huyo kungeleta madhara kwao. Kwa hiyo, waliwapa watu wawili sinia na sanduku la losheni ya macho na wakawaomba wampelekee Ummayah. Watu hao wawili walifika kwa Ummayah ambaye alikuwa ameketi ndani ya msikiti wa Masjid-ul-Haram na wenzake na wakamwambia: Sasa basi wewe umekataa kulinda utajiri wako na biashara na umeamua kuwa kama wanawake, kuishi maisha ya upweke, badala ya kupigana kwenye uwanja wa vita, ni vizuri zaidi utumie losheni ya macho kama wanawake na labda jina lako litafutwa kutoka kwenye orodha ya watu jasiri na wapiganaji. Maneno haya yalimchoma sana Ummayah hivyo kwamba alikusanya vifaa muhimu katika safari na haraka akaondoka na Maquraishi kwenda kulinda msafara wa Abu Sufyan. Baada ya siku chache hatimaye, jeshi la makafiri lilifika hapo Badr. Hapo vita ilifanyika baina ya majeshi yanayotetea ukweli na uwongo. Kwenye vita hii wafuasi wa ukweli walishinda. Majeshi ya Maquraishi yalipata pigo la kufedhehesha. Wengi miongoni mwao ama walikimbia au walitekwa. Baadhi yao pia waliuawa.44

BILAL ANALIPA KISASI Baada ya jeshi la Maquraishi kukimbia, baadhi ya Waislamu walikwenda kuchukua ngawira. Miongoni mwao alikuwa Abdur Rahman bin Awf ambaye alikwenda kwenye kituo 44

Kamil bin Athir Juz. ii, uk. 82. 88


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

kilichotumiwa na maadui kwa lengo hilo. Kabla ya kukubali Uislamu alikuwa rafiki wa Umayyah bin Khalaf, lakini baada ya hapo uhusiano wao ulikatika. Umayyah, ambaye alitambua kwamba baada ya muda mfupi angekuwa mateka alikuwa amesimama kwenye kona na mwanae wakiwa na woga. Ghafla alimwona rafiki yake wa zamani Abdur Rahman, ambaye alikuwa anawaendea. Umayyah alipomuona Abdur Rahman, alifurahi sana na alifikiri kwamba ingekuwa vema kujisalimisha kwa rafiki yake wa zamani kwa hiyari yake na kuwa mateka wake ili baadaye angeweza kuwa huru tena. Akiwa na lengo hili katika fikra zake alilia. “Ewe Abdul Uzza! (Kabla ya kusilimu Abdur Rahman alikuwa anaitwa Abdul Uzza). Abdur Rahman, ambapo alikuwa ameshika lulu mikononi mwake, alikwenda haraka pale walipokuwa. Umayyah alisema kwa sauti ya kutetemeka: “Tupa vitu hivyo na utuchukue sisi mateka kwa sababu ukilinganisha na vitu hivyo, sisi tutakuwa na manufaa zaidi kwenu.” Aliposikia maneno haya ya Umayyah, Abdur Rahman bila kuanzisha mazungumzo na yeye, alimfunga mikono yake pamoja na ya mwanae na akaamua kuwapeleka kwenye kambi ya Waislamu. Hata hivyo, kabla hawajatembea hatua nyingi walikutana na Bilal. Bilal alipomuona Umayyah, mmiliki wake wa zamani, ambaye alimtesa sana, alisema kwa sauti ya ukali: “Enyi Waislamu! Umayyah huyu hapa mtoto wa Khalaf, mmojawapo wa viongozi wa makafiri na adui jeuri wa Mtukufu Mtume. Amekamatwa. Mwenyezi Mungu anaweza asiniache niendelee kuishi kama nitamwacha aendekee kuishi!” 89

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Abdul Rahman alisema: “Ewe Bilal! Unataka kumuua mateka wangu?” Bilal akajibu: “Ndio. Siwezi kumruhusu mkandamizaji wa kishetani na adui mwovu wa Mwenyezi Mungu kuendelea kuishi.” Abdur Rahman alisema kwa hasira: “Ewe mtoto wa kijakazi! Unajua unachokisema?” Bilal alisema kwa sauti ya juu zaidi: “Ndio, najua!” Halafu akawageukia Waislamu na alisema: “Enyi Masahaba wa Mtukufu Mtume! Njooni haraka iwezekanavyo na muoneni huyu adui yake Mwenyezi Mungu. Nina maanisha Umayyah bin Khalaf. “Kama hamtamtambua lazima mjue kwamba huyu ni mtesaji wangu pamoja na wengine. Lazima auawe!” Waislamu wote walikuwa wanamjua Umayyah na walisikia hadithi kuhusu uadui wake dhidi ya Uislamu na mateso yasiyo vumilika aliyoyapata Bilal kutoka kwake. Kwa hiyo, baada ya kusikia sauti ya mithili ya ngurumo ya Bilal, baadhi yao walikusanyika na kumzunguuka Umayyah na mtoto wake. Abdur Rahman alijaribu kumtetea mateka wake wasiumizwe kwa namna yoyote na awafikishe kwa Mtukufu Mtume wakingali hai. Hata hivyo, sauti kali ya hasira ya Bilal ilizimua jitihada zake. Inawezekana Mungu aliridhia kwamba Umayyah asiepuke kifo. Mmoja wapo wa Waislamu alichomoa upanga wake kwa ushupavu mkubwa na kumkata kabisa mguu mtoto wa Umayyah kwa namna ambayo ulitenganishwa na mwili wake na alianguka chini. Alipoona hivi Umayyah alipiga unyende kwa kiruu ambao hakuna mfano wake uliowahi kuonekana au kusikika. Abdur 90


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Rahman alimgeukia Umayyah na akasema: “Sasa ndio mwisho kuhusu mwanao. Sasa wewe ukimbie ili kwamba yawezekana ukaponya maisha yako.” Umayyah ambaye alihuzunika sana kwa sababu ya kifo cha mwanae aliendelea kusimama bila kusogea kwa namna yoyote. Inaweza kusemekana kwamba alikuwa anataka kufa. Ambapo Abdur Rahman alikuwa anajaribu kumponya rafiki yake wa zamani, Mwislamu alimshika pua Umayyah wakati anamwangalia mwanae aliyejeruhiwa, na alimfanya aanguke chini, na pigo la upanga la Mwislamu mwingine lilimmaliza. Kwa hiyo, matamanio ya Bilal ya siku nyingi yalitimia, aliangalia juu angani na kumshukuru Mwenyezi Mungu.45 Umayyah ambaye aliwatesa Waislamu akiwa na moyo mgumu mno na aliupinga Uislamu na mapinduzi ya Mtukufu Mtume hadi mwisho wa uhai wake, aliuawa mbele ya watu wengi. Alikuwa ni Umayyah huyo huyo ambaye alikuwa na chuki dhidi ya Mtukufu Mtume, Uislamu na Waislamu kwa njia nyingi tofauti na alikuwa bado hajaacha dharau, kutukana mashtaka na usengenyi dhidi yao. Na alikuwa Bilal huyo huyo, Mwafrika ambaye wakati fulani alivumilia mateso makali sana kutoka kwa Umayyah. Na kwa nini asingevumilia? Ilikuwa si Uislamu uliompa uhuru na utu wake, Uislamu

45

Al-Kamil Juz. ii, uk. 89; tarikh -e- Tabari, Juz. ii uk. 135; The life of the Holy Prophet p. 310; Muhamad Rasul Akram uk. 223; Who is Ali? uk. 27; Sirah bin Hisham Juz. ii, uk. 272; Stories from Qur’an p. 372; Biographies of tha Prophets p. 372. 91

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

ambao ulimnyanyua kutoka kwenye kiwango cha chini sana cha jamii hadi kwenye upeo wa juu sana wa maendeleo? Ulimpeleka kwenye paa la Al-Kaabah na ulimfanya yeye kuwa mtangazaji wa imani ya Mungu Mmoja. Uislamu huunga mkono wanyonge na kuwaangaza wenye kiburi. Umayyah hakufikiria hata kidogo kwamba haiwezekani kupigana na Radhi ya Mwenyezi Mungu na watu, na iliwezekana kwamba mkono ambao unao nguvu nyingi zaidi kuzidi wa kwake pia ungetokeza.

BILAL MBELE YA IMAMU ALI Tangu wakati Bilal alipopata uhuru na kuungana na Waislamu wengine, wakati wote alionyesha mapenzi maalum kwa Imamu Ali (a.s) na kwa kawaida alikuwa karibu naye na alinufaika. Kwenye mikutano na mazungumzo alimsifia sana Imamu Ali. Desturi hii ya Bilal ilidhihirika sana hivyo kwamba watu wote walijua kwamba alimheshimu Imamu Ali kuliko mtu mwingine, na hili likawa jambo la kushangaza na mara nyingi ikawa mada ya mazungumzo miongoni mwa watu. Baadhi ya watu walisema: “Bilal lazima ampe heshima hii Abu Bakr kwa sababu ni Abu Bakr sio Ali aliye mwondoa kwenye makucha ya wakandamizaji.” Bilal alitambua tatizo hili na mazungumzo ya watu. Siku moja alipokaribia mkusanyiko wa watu ambapo jambo hili lilikuwa linazungumzwa, alitoa jibu lifuatalo: “Kama inakubalika kwamba nimheshimu mtu kwa sababu ya wema alio nifanyia nitalazimika kumheshimu Abu Bakr zaidi ya Mtukufu Mtume, kwa sababu hata Mtukufu Mtume 92


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

hajanifanyia hilo ambalo Abu Bakr amefanya. Mnasemaje kuhusu hili?” wote walisema kwa sauti moja: “Tumesema kuhusu Imam Ali ikilinganishwa na Abu Bakr. Kuhusu Mtukufu Mtume, jambo hili lipo tofauti. Ni wajibu kwa kila mmoja kumheshimu Mtume wa Mwenyezi Mungu.” Bilal alijibu: “Suala ni kwamba endapo heshima apewe mtu kwa sababu ya kumfanyia mtu hudumu au kwa sababu ya kuwa bora na mtakatifu zaidi. Endapo heshima itatolewa kwa sababu ya huduma, hali ni kama ambavyo nimekwisha sema yaani nitalazimika kumheshimu zaidi Abu Bakr kuliko Mtukufu Mtume, ingawa Abu Bakr alininunua mimi na akanipa uhuru kwa kufuata amri aliyopewa na Mtukufu Mtume, ambapo Mtukufu Mtume ni mbora zaidi na mpenzi mno machoni mwangu.” Wale waliokuwepo walisema: “Hatuhoji ukweli kwamba Mtukufu Mtume ni mtu wa kuheshimiwa zaidi miongoni mwa wanadamu na anastahili kuheshimiwa kadiri iwezekanavyo.” Bilal akasema: “Vema sana, Ali, pia ni mtu mkubwa sana baada ya Mtukufu Mtume kwani yeye yu ‘ndani mwake’ na ‘roho yake’46 Abu Bakr mwenyewe anatambua kwamba Ali ni bora zaidi yake. Kwa hiyo Ali hufurahia haki zaidi kwangu kuliko Abu Bakr. Abu Bakr alinitoa mimi kutoka kwenye mateso ya Umayyah na ninamshukuru kwa kufanya hivyo. Hata hivyo, endapo hangenipa uhuru na ningekufa katika hali ile, 46

Inahusu Aya inayozungumzia habari za Mubahila (Surah Al-Imran, 3:61) 93

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

ningepata neema za Mungu zisizo na ukomo na endapo ningeishi katika mateso ya dunia hii, ningekuwa mdogo na nisingedumu. Hata hiyvo, Imamu Ali hufurahia nafasi hiyo kwamba urafiki wake ni njia ya ukombozi kutoka kwenye moto wa Jahanamu na kuhakikisha maisha ya milele huko Peponi. Ni kwa sababu hii ninamuona Ali ni mpendwa wangu zaidi.”47 Bilal alipata matatizo ili apate imani na njia ya bahati nzuri na kuboresha, na hakuweza kuvumilia maumivu yote hayo na shida bila kunufaika. Aliunga mkono ukweli na kama ambavyo tutasoma baadaye, hakujisalimisha kwa mamlaka ya ukhalifa pamoja na watu hao ambao waliendekeza mazungumo yasiyofaa na hakuacha urafiki na Imamu Ali hatimaye aliondoka hapa duniani akiwa katika imani hii.

KUELEKEA MAHALI ALIPOZALIWA Mnamo mwaka wa nane wa Hijiria, Mtukufu Mtume alipokea amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu ya kuiteka Makkah. Kazi hii ilidhaminiwa kwa Mtukufu Mtume wakati ambapo makafiri miongoni mwa Maquraishi na watu wa Makkah walivunja mkataba uliofanywa na Waislamu miaka miwili iliyopita na kwa kiwango fulani hii ilikuwa ni sababu ya shambulizi hili. Kwa upande mwingine Waislamu, ambao waliwashinda maadui wa ndani walio wengi zaidi, walitaka kuiteka na kuiweka Makkah chini ya udhibiti wao. Hii ilikuwa ni sehemu ya kati na nchi walikozaliwa ambayo ilikuwa na Qibla (Al47

Safinatul Bihar, Juz. I, uk. 104. 94


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Ka’abh) ambako huelekea wakati wa Swala.

kustawi.

Sababu nyingine ya shambulizi hili ni kwamba maadui halisi wa Uislamu walikuwa Makkah. Jiji hili lilikwisha kuwa kituo cha kati cha ujasusi, uadui, hila na majungu na mipango ya njama michafu kupindukia ilitayarishwa katika kituo hiki kitakatifu cha imani ya Mungu Mmoja.

Baada ya safari ya siku chache, Waislamu walifika sehemu iliopo pembezoni kwa jiji la Makkah. Mtukufu Mtume aliwaamuru wapiganaji wa Kiislamu kukoka moto katika sehemu nyingi. Kwa upande mwingine, kwa sababu ya hofu ya Waislamu, watu wa Makkah waliteua watu wa kujitolea kufuata barabara ya kwenda Madina.

Ilikuwa ni muhimu kwa wafuasi wa jumuiya ya Uislamu kuichukua sehemu hiyo na kuwa chini ya udhibiti wao na kukomesha ibada za masanamu, kufanya dhambi, ukandamizaji, matumizi ya nguvu, uonevu na ubaguzi wa kijamii. Ilikuwa ni haki isiyovumilika kwa Waislamu kuiona Nyumba ya Mwenyezi Mungu, kumbukumbu ya Mtume Ibrahim na kituo cha kati cha ibada ya Mungu Mmoja kibakie hapa duniani kama mahali pa uovu na viongozi wa ukafiri, imani ya kuabudu miungu wengi na kuabudu masanamu kama Abu Sufyan afanye maamuzi ya mambo ya kisiyasa, kiuchumi na kijamii ya Makkah. Ilikuwa ni kwa sababu hii kwamba Mtukufu Mtume alitayarisha jeshi la wapiganaji elfu kumi na mbili walio waaminifu na jasiri na wakaelekea Makkah.

Wakati huo huo Abu Sufyani ambaye alikuwa mmojawapo wa maadui wakubwa wa Uislamu na Waislamu alitoka nje ya Makkah na baadhi ya wenzake ili waweze kutumia hali halisi na kupata ufumbuzi wa jinsi majeshi yake ambavyo yangefanya upinzani dhidi ya jeshi kali na lenye nguvu la Uislamu. Miale ya moto ilimvutia na alisema: “Moto huu mkubwa umewashwa na jeshi kubwa ambalo linatujia.” Akiwa na hofu alisogea mbele kidogo na alimuona Abbas, mjomba wake Mtukufu Mtume, akiwa amepanda nyumbu na akiwaendea wao. Abbas alipokutana na Abu Sufyan na wasaidizi wake aliwaambia Waislamu wamekusudia kuendelea hadi Makka. Abu Sufyani na wenzake ambao waliogopa sana alisema: “tufanye nini?” Abbas alimjibu: “Ingieni katika Uislamu.”

Jambo kubwa na la muhimu sana ambalo limejificha kwenye jumuiya hii na linastahili tafakuri ni kwamba matayarisho haya na jumuiya hii iliyofanywa na Mtukufu Mtume haikuwa kwa nia ya kupigana, kumwaga damu na kuteka. Kwa upande mwingine lengo lake ilikuwa kuipatia uhuru jamii iliyokuwa kwenye makucha ya ukafiri na ushirikina, na badala yake kueneza imani ya Mungu Mmoja na kuunda jamiii yenye

Abu Sufyani alipoona kwamba hapakuwepo na chaguo lingine alisema kwa shingo upande kwamba alikuwa tayari kuingia kwenye Uislamu. Kwa hiyo, alimwendea Mtukufu Mtume wa Waislamu na kwa nje alikubali Uislamu na akawa Mwislamu.

95

96

Abbas alitazama alikokuwa Mtukufu mtume na alisema: “Abu Sufyan amekuwa Muislamu na anatamani apate daraja itakuwa vema kama atatiwa moyo kwa maslahi ya Waislamu.”


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Mtukufu Mtume alisema: “Mtu ambaye ataingia nyumba ya Abu Sufyani au anabakia ndani na anafunga lango la nyumba yake au anaingia msikiti wa Masjidul Haram atakuwa salama.”

wengine, hadi alilazimika kutoka katika jiji mnamo usiku moja. Sasa baada ya kuona kuanguka kwa Makkah alianza kukumbuka matukio ya zamani.

Abu Sufyani alifurahi kusikia hivi. Baadaye alirudi Makkah na akawaeleza watu kuhusu hali halisi.

Alishusha pumzi na kunyanyua kichwa chake kuelekea mbinguni na alimshukuru Mwenyezi Mungu kwa furaha, kwa sababu matumaini ya moyo wake yalitimia na akawa ameiona ile kambi ya maadui wa Uislamu ikiwa imekaliwa na jeshi la Uislamu.

Watu wote walifadhaika na kuhuzunika na kila mtu alikuwa anasema kitu hiki au kingine. Baadhi waliuliza: “Sasa tufanye nini?” Abu Sufyani alirudia maneno ya Mtukufu Mtume kuhusu kupewa msamaha wa jumla. Watu waliudhika na walikuwa katika hali mbaya sana. Walikuwa wanangojea tukio fulani, ambapo jeshi la Uislamu lililojipanga na zuri lilifika kwenye lango kuu la jiji la Makkah na likaingia ndani ya jiji bila kipingamizi au upinzani wa adui.48 Jiji la Makkah ambalo ndilo lilikuwa kituo kikubwa cha maadui wa Uislamu na kituo cha njama zote dhidi ya Uislamu na ujasusi lilitekwa.

KUMBUKUMBU YA YALIYOPITA Akiwa katikati ya ndugu zake Waislamu, Bilal alianza kukumbuka siku hizo ambapo alikuwa mateka na mtumwa kwenye makucha ya wakandamizaji na watu wenye majivuno katika nchi hii na hata baada ya kukombolewa kutoka kwenye mateka na mateso kutoka kwa wanawake, alitiwa uchungu na

Kama mambo yalivyo, palikuwepo wakati ambapo Bilal hakuweza kuwa na ujasiri wa kutamka neno katika jiji hili kwa sababu ya kuogopa maadui lakini leo kutokana na neema ya Uislamu na msaada wa Mwenyezi Mungu Mweza wa Yote, alikuwa anaingia mama wa majiji akiwa na ushindi na uhuru kamili. Jua liliangaza jiji la Makkah kwa kulikaribisha jeshi la Uislamu na lilieneza miale yake ya rangi ya dhahabu kwenye milango yake na kuta zake ambapo Bilal na Waislamu wengine waliingia jijini. Shani nzuri na ya kupendeza ya Al-Kaabah ilivutia macho ya Waislamu. Bilal alikuwa analia machozi ya furaha na matendo yake yalionyesha kwamba alikuwa amefurahia sana ushindi wa ukweli dhidi ya ukafiri. Alijiambia mwenyewe. Wako wapi watu hao, ambao walikuwa na desturi ya kutuita sisi na kiongozi wetu mpendwa kwamba hatukuwa na busara, na wenye wazimu, na mafundisho ya dini yetu ya mbinguni kuwa; hadithi za watu wa kale?” “Na yu wapi bwana wangu mkandamizaji na mwenye majivuno, ili aweze kuona ukubwa na ushindi wa Mola wangu

48

Nasikhut Twarikh, uk. 283. 97

98


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Mlezi kwa macho yake mwenyewe na angeweza kufanya jaribio yeye mwenyewe kwamba yale masanamu aliyokuwa anatualika tuyaabudu hayana thamani yoyote.” Inaweza kusemwa kwamba Bilal alikuwa ameketi juu ya mawingu na alikuwa anawaambia watu wa Makkah kutokea hapo: “Enyi wakandamizaji! Ni nyinyi mliotufanya sisi tutangetange nje ya jiji letu na nchi tulipozaliwa na mkayafanya maisha yetu ya taabu sana hivyo kwamba tulihuzunika kuondoka wakati wa usiku na tulikwenda kwenye hatima tusioijua. Enyi watu ambao mlitufikiria sisi kuwa wanyonge na tuliostahili dharau, oneni sasa ni nani aliye mshindi. Sasa Mola wetu Mlezi ametimiza ahadi Yake na amewafanya wanyonge kuwa washindi dhidi ya watu wenye majivuno.”

WANANGOJEA HATIMA YAO Jua lilichomoza polepole. Hofu ya watu ilizidi kuongezeka jinsi wakati ulivyozidi kupita. Walikuwa wanasimama au kuketi majumbani kwao, kando ya barabara, na kwenye kona za mitaa na wakingojea hatima yao isiyotabirika. Si tu kwamba hawakujikuta kwenye nafasi ya kufanya upinzani dhidi ya jeshi kubwa la Uislamu lakini walikuwa na wasiwasi hata na maisha yao. Wanawake walikuwa wanaketi majumbani mwao wakiwa wamezielekeza nyuso zao zilizosawijika chini na walikuwa wanajaribu kuwabembeleza watoto wao waliokuwa wanalia. Wakati mwingine watu walijilaumu wenyewe na kujutia sana kuhusu ukatili waliomfanyia Mtukufu Mtume wa Uislamu na 99

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

masahaba wake siku za nyuma. Jiji lote lilikumbwa na huzuni na simanzi. Watu walikuwa kwenye ukomo wao wa kuweza kuelewa nini kilichokuwa kinafanyika na wafanye nini. Kundi la watu lilighani aya za Qur’an Tukufu ambazo zilionyesha majuto yao na woga wao na wakajishutumu wenyewe kwa njia hii. Baadhi ya watu walikimbia na kwenda milimani na kuishi huko na wenye wasi wasi mkubwa.49 Na baadhi yao ambao hawakuwa na hatia walijitenga pembeni na kuwalaani wazee na watemi wa Makkah, kwa sababu ni wao ndio waliowachochea watu kumpinga Mtukufu Mtume, wakati wa siku za mwanzo wa Uislamu, na wao ndio, walikuwa watu wa kwanza kuingia kwenye Uislamu. Watu wengine walijiambia wenyewe: “Muhammad atatufanya nini? Tutaepuka kifo, kwa sababu tulifanya kila tuliwezalo kumchanganya yeye. Hata hivyo, baada ya kipindi kifupi ukimya na usumbufu wa akili ulisitishwa na taarifa ya kufurahisha. Muislamu aliyekuwa anamwakilisha Mjumbe wa Mwenyezi Mungu aliwauliza watu kwa sauti ya kupaza: “Sasa mnatumaini nini?” Wote walimjibu: “Tunatumaini kusamehewa, kuwiwa radhi na ukarimu.” Mtukufu Mtume alisema: “Tangaza hilo na walisikie wote kwamba wasiwe na wasiwasi. Wote nimewapa

49

Tarikh-e- Yaqubi, uk. 46. 100


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

uhuru!”50 Vurumai isiyotegemewa ilitokea. Vilio vya furaha vilisikika kutoka kila upande. Tangazo hili ambalo lilikuwa tangazo la Uislamu, lilitia ari mpya kwenye miili ya watu waliokuwa nusu maiti ya watu wa Makkah. Machozi ya furaha yalitiririka machoni mwao kwa sababu ya wema na ukarimu wa Mtukufu Mtume. Hususan baadhi ya maadui wa zamani wa Uislamu walishangaa sana walipoona upendeleo na msamaha huu uliofanywa na Mtukufu Mtume. Waliondoka kuelekea nyumbani mwao huku wakiwa na aibu kubwa na walijuta kwa matendo yao ya zamani. Mmojawao alisikika anasema: “Muhammad mkweli wakati wote amekuwa mwema na mkarimu. Hata sasa ametuacha huru kwa sababu ya ukarimu wake.51

BILAL KWENYE PAA LA AL-KAABAH Jua lilifika katikati ya anga na ilikuwa muda wa joto kali sana katika siku hiyo. Makkah ilikuwa chini ya ushindi wa Waislamu. Wakati huo huo Mtukufu Mtume aliamuru Bilal apande kwenye paa la Ka’abah na Adhini Adhana kuashiria kufika kwa muda wa Sala ya adhuhuri, ili kwamba watu wajitayarishe kwa Sala hiyo. Kwa hiyo, Bilal Mwafrika, mtumwa na mtu mweusi wa jana na leo msemaji wa tablighi ya Mtukufu Mtume alipanda juu ya paa la Ka’abah yaani juu ya nyumba ya kwanza takatifu ya 50 51

Tarikh-e- Yaqub, uk. 46; Qibla-e-Islam, uk. 567. Muhamad Rasul Akram, uk. 488. 101

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

ibada ya Mungu Mmoja ili aweze kutangaza Utume wa Mjumbe wa Mwisho wa mbinguni, afanye itikadi ya kuendelea kuliko zote isikike na watu wote, na awaambie kwa hizo kaulimbiu za kimapinduzi kwamba Sala ya jamaa ya kwanza ilikuwa ifanyike Makkah. Bilal ambaye alifurahishwa sana na kumshukuru Mwenyezi Mungu kila sekunde, aliifanya sauti yake ya kutia moyo isikike hadi kwenye upeo wa jiji kutoka kwenye paa la Nyumba ya Mwenyezi Mungu ikitamka sentensi nzuri na adhimu ya ‘Allahu Akbar’ (Mwenyezi Mungu Mkubwa). Kaulimbiu ya ‘Allahu Akbar’ ni alama ya kuanzishwa kwa utawala wa Mwenyezi Mungu, mwangamizaji wa mamlaka ya Shetani. Watu wa Makkah walitoka nje ya nyumba zao wakati huo huo wa joto kali kuelewa mambo yalivyokuwa. Walinyoosha shingo zao ili wamuone mtangazaji. Walisikia kaulimbiu za Uislamu zinatoka mdomoni mwa Bilal, walipeana ishara kwa macho yao na walisema; “Ni huyo Bilal mtumwa mweusi. Sasa anafikiriwa kuwa mmojawapo wa sahaba wa karibu na Muhammad.” Dalili za mshangao na hofu zikiwa zimechanganyika na matumaini ya siku za usoni ziliweza kuonekana kwenye nyuso za watu. Pamoja na tangazo la msamaha wa jumla wa Mtukufu Mtume baadhi ya watu walikuwa na wasi wasi walihofia kuanza kwa vita. Wanawake waliowengi waliogopa walisimama kwenye mapaa ya nyumba wakitegemea jambo fulani kutokea. Pande zote za Nyumba ya Mwenyezi Mungu zilikuwa na msongamano wa watu kuliko sehemu zingine. Macho yalielekezwa kwa Bilal kutokea sehemu za karibu na mbali. Palikuwepo na kelele sana hivyo kwamba sauti ya Bilal ilikuwa

102


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

haisikiki. Hata hivyo, aliendelea kuadhini Adhana.52

WIMBI LA UPINZANI Sauti ya Bilal ilikuwa ya kutia moyo kwa Waislamu kama ilivyokuwa ya kuchukiza kwa makafiri na washirikina. Nafasi ya Bilal iliwakasirisha waabudu masanamu na wanafiki miongoni mwa Waislamu na ilikuwa kisingizio cha upinzani wao. Ilikuwa jambo lisilo kubalika kwamba mtu mweusi na mtumwa angepewa nafasi hiyo au astahili kushika nafasi hiyo. Ilikuwa kwa sababu hii kwamba walifikiri kwamba endapo Uislamu ulikuwa dini kubwa ya Mungu kwa nini watumwa wale walikubali kuwa Waislamu, kwa sababu walizowezwa kwayo na walidhani kwamba utu ulikuwa kitu pekee kwa mtu mwenye ngozi nyeupe, mabepari, wale wenye kupenda anasa na watu wenye majivuno. Hawakujua kwamba hivyo havikuwa vipimo vya kutathmini utu wao kwenye Uislamu. Baada ya Bilal kumaliza kuadhini Adhana watu hao hawakufurahishwa. Waliinamisha vichwa vyao na kwa sababu waliudhika sana, nyuso zao zilifadhaika na mishipa ya shingo zao ilionekana sana hivyo kwamba walikaribia kufa kwa sababu ya huzuni. Upinzani mbali mbali ulitolewa na wao na kila mmojawao alikuwa anasema kitu hiki au kile. Harith bin Hakim alisema: “Ooo! Hivi Muhammad hakuwa na mtu mwingine wa kumkabidhi kazi hii isipokuwa huyu kunguru mweusi?” Mtu alilalamika na alisema: “Ooo! Kifo ni kizuri zaidi kuliko maisha haya. Dunia hii si mahali panapostahili kuishi.” 52

Tabaqat bin Sad, juz iii, uk. 169; Qamusr Rijal, Juz. ii, uk. 234; Sirah bin Hisham. Juz. iv, uk.33 103

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Kundi la watu ambamo binti yake Abu Jahl pia alikuwepo lilipiga ukelele kwa pamoja: “Wahenga wetu walikuwa na bahati kwa sababu walikufa na hawakuona kioja kama hiki kwamba Bilal atoe Adhana ili waende kusali. Wahenga wetu wako wapi ili kwamba waone siku nyeusi kama hii iliyotujia. Lau na sisi tungeuawa pia kwenye vita kama wao, tusingeiona siku kama hii” Baadhi yao walisema: “Lau kama dunia hii ingefunua mdomo wake na kututafuna kwa sababu ikilinganishwa na maisha haya ya fedheha ni afadhali kuzikwa kwenye vumbi ukingali hai.”53 Baadhi ya watu kama Abu Sufyani na Sohayl bin Umar ambao walikasirika sana walisema: “Sasa hivi hatutaki kusema kitu chochote kwa sababu inawezekana kwamba Muhamad anaweza akatambua kuhusu suala hili na akaudhika.” Kwa kutafakari haya maneno yasiyo na maana ambayo yalitoka kwenye makoo ya watu wasio na fikra na wajinga, tunatambua ni kiwango gani ubaguzi wa rangi ulikuwepo kwenye jamii hiyo. Baada ya kuona uhuru na uwezo wa mtu mweusi walikasirika sana hivyo kwamba walitamani kufa kuliko kuvumilia kumuona Bilal, mtumwa anafanya kazi kama hiyo. Bila shaka ni vigumu kufanya mabadiliko kwenye fikra kama hizo. Watemi wa makabila na watawala madhalimu, kwa miaka mingi walifanya matabaka ya chini watumwa wao na kujipatia wenyewe maisha ya starehe kwa gharama ya umasikini wao, mateso, ujinga na njaa. Walidai kutoka kwao mambo yasiyo na mantiki na walihodhi 53

Tabaqat bin Sad, Juz. iii, uk. 169; Safinah Juz. I, uk. 105; Tabikh -eYaqubi, Juz.i, uk. 46; Tafsir Abul Futuh Razi Juz. ix, uk. 193. 104


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

utajiri, na walifikiria maisha yao ya fedheha kuwa ni ukweli usio na shaka na kitu cha heshima sana. Ilikuwa ni ugumu ulioje kupigana na aina hii ya kufikiri na kuondoa fikra zote hizo zisizo na maana na zilizo kinyume na utu wa mwanadamu kutoka kwenye akili zao? Kwa hali ya mambo yalivyokuwa wakati watu wa Makkah walikuwa wanatoa mawazo kama haya, Malaika Jibriil alikwenda kumuona Mtukufu Mtume na akampa Aya yenye amri kuhusu usawa wa binadamu “Enyi watu! Hakika sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni yule aliye mchamungu zaidi katika ninyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kujua, Mwenye habari.” (49:13). Katika mtazamo wa Uislamu hakuna tofauti baina ya mtu mweupe na mweusi, mtu maskinni na tajiri na mwarabu na asiye Mwarabu kuhusu asili ya ubinadamu. Wale wanaofikiria kuwa weusi ni jambo la aibu na watu weusi kuwa duni na kutaka kuwafukuza kutoka kwenye jamii wamekosea. Mtu mweusi pia ni binadamu. Mwili wake na roho yake ni vitu vinavyohitaji mahitaji sawa na mtu mweupe. Mtu ambaye hana mali au ngozi yake ni nyeusi haina dosari yoyote kuhusu ubinadamu na utu wake na wala haja fanya uhalifu wowote. Na umbo la kiwiliwili baya au zuri wala si dosari ama sifa ya mtu. Ni utakatifu wa roho tu, ambao unatokana na uchaji Mungu wa mtu, na mtu wa namna hii ni mwenaye kuheshimiwa mbele ya Mwenyezi Mungu, Muumbaji wa Ulimwengu.

105

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Aya hii ya Qur’an Tukufu na sheria ya mbinguni ni mkataba wa usawa wa wanadamu na sheria iliyo na haki kupita zote ambazo ubinadamu umeshuhudia. Ni sheria ambayo walipewa wanadamu kwenye mojawapo ya vipindi vya hatari sana katika historia na katika tukio hilo ilitambua rasimi haki za watu weusi na watu wengine machotara na pia iliwafungulia njia za juhudi, shughuli na maendeleo. Ni Uislamu tu ndio unaofaidi heshima hii katika historia ya mwanadamu kwamba katika siku zake za mwanzo ulikomesha ubaguizi wa rangi na hata leo haiwezi kulinganishwa sheria za kijamii za hapa duniani kwani katika maudhui yake Waislamu hawaruhusu ubaguzi wowote kuhusu watu wenye rangi tofauti ya ngozi. Kama mambo yalivyo, ufunuo wa Aya iliyonukuliwa hapo juu ilitoa jibu imara na la kuondoa kiini cha tatizo kwa watu walio mlaumu Bilal au waliosema kwa mshangao kwa nini watu weusi kama huyo,watumwa na masikini wapewe kazi ya hadhi kama hiyo.

UBAGUZI WA RANGI KWA MARA NYINGINE Ingawa katika Uislamu ubaguzi wa rangi haukuwa na maana yoyote tangu siku ulipoanza na Mtukufu Mtume aliwaona Waislamu wote wa mataifa mbali mbali kwa mtazamo mmoja, bado fikra za wakati wa kijahiliya na ushirikina ziliendele kuwepo kwenye akili za baadhi ya watu hadi miaka michache baada ya kuja kwa Uislamu na kujitokeza mara moja moja. Walikuwepo watu waliojivunia wahenga wao, makabila yao na mataifa yao na waliwafikiria watu wengine kuwa duni na wanyonge. 106


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Mtukufu Mtume alijaribu kufuta mawazo ya aina hiyo kutoka kwenye akili za watu ili kwamba mambo ya kuaibisha yakomeshwe kabisa. Ili kuthibitisha yale ambayo yamesemwa kwenye kurasa za nyuma tunafikiri ni muhimu tusimulie tukio ambalo lilitokea baina ya Salman, Bilal na Sohayb wa Rumi kwa upande mmoja na Mwarabu mmoja kwa upande mwingine ili kwamba tuweze kuona kilele cha majivuno. Siku moja Salman al-Farsi, Suhayb wa Rumi na Bilal wa Afrika walikuwa wameketi pamoja kwenye mkusanyiko. Mwarabu aliyeitwa Qays pia alifika hapo. Alikasirishwa sana kuona jinsi walivyo komesha unyonge na ukandamizaji chini ya nguvu ya Uislamu na walipata heshima, umashuhuri na uhuru. Aliwaambia: “Aus na Khazraj wamemfanya Mtume wa Uislamu kuwa mashuhuri. Hawa wageni wanasema nini?” Ni dhahiri kwamba walihangaika baada ya kusikia maneno haya lakini hawakumjibu Qays. Hata hivyo, Mtukufu Mtume alifahamu nini kilichotokea na kwa hiyo alisema kwenye mkusanyiko wa Waislamu: “Acheni upendeleo huu usiofaa. Mwenyezi Mungu wenu ni Mmoja. Dini yenu ni moja. Na chimbuko lenu linatokana na baba mmoja na mama mmoja, nasaba yako ya Kiarabu ambayo unajivunia hivi sasa wala si ya baba yako ama mama yako, lakini kwa kweli ni mfano wa kuumiza.”54

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

umbile, urefu au ufupi wa umbile na kadhalika ni kwamba wanaweza kutofautishwa na mpangilio na mambo ya jamii hayawezi kupangiliwa, na hii ndani mwake ni Hekima ya Mungu.

MASANAMU YAPOROMOSHWA CHINI Sauti changamfu ya Bilal ilisikika kwenye upeo wa mipaka ya Makkah na kugusa masikio ya waabudu masanamu ambao walibaki wachache baada ya kutekwa jiji. Sauti ya Adhana ya Bilal iliashiria tukio la mageuzi katika historia iliyojaa matukio ya Makkah na ikatangaza kwamba: “Kipindi cha ushirikina na kuabudu masanamu kimekwisha na imani ya Mungu Mmoja na udhibiti wa kibinadamu wa Kiislamu umefika kileleni.” Inasemekana kwamba Bilal alipotamka ‘Takbir’ kutoka kwenye paa la Nyumba ya Mwenyezi Mungu, masanamu ambayo yalikuwa yamewekwa ndani ya Ka’abah Tukufu yalianguka chini.55 Jiji ambalo lilikuwa linaendeshwa na washirikina, waabudu masanamu na watawala madhalimu kwa miaka mingi sana lilitekwa chini ya uongozi wa kiongozi mkuu wa mbinguni na kelele ya ‘Allahu Akbar’ kaulimbiu ya Upweke wa Mungu na imani ya Mungu Mmoja ilijaa kwenye mazingira yote na anga ya Makkah.

Kwa hiyo, kila wakati Mtukufu Mtume alitangaza ubaguzi wa rangi kuwa ni upuuzi. Kwa kweli hawakujua kwamba tofauti ya wanadamu na kuhusu taifa, rangi, utaifa, rangi ya ngozi,

Kama mambo yalivyo, baada ya kufika ukweli ukafiri uliondolewa, masanamu yalianguka chini na shetani akatoweka; watawala madhalimu wenye kiburi walilazimika kujitweza na nafasi yao ya utawala wa aibu ilikomeshwa.

54

55

Tabizat-e-Najadi,uk. 137 107

Safinatul Bihar, Juz. I, uk. 105. 108


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Bendera ya ukafiri iligeuzwa chini juu na bendera ya ukweli na haki inaendelea kupepea na upepo mwanana imara wa imani ya Mungu Mmoja unairudisha jamii kwenye maisha.

MTUKUFU MTUME ANAUGUA KITANDANI Jua lenye mwanga unaong’ara wa Utume uliangaza dunia yote ya mwanadamu kwa miaka ishirini na tatu. Jamii iliyoganda, iliyooza, na kusimama kimaendeleo ilianza tena kuwa kwenye msogeo kwa msaada wake wa fikra za juu sana na ikaendelea kwenye njia ya maendeleo na kuboreka. Ilikuwa jamii iliyokuwa na watu wasiojua kusoma na kila siku ilikumbwa na matukio mbalimbali kama vita, mauaji kwa ajili ya sababu ndogo sana, wizi, uporaji mkubwa na kadhalika. Mtukufu Mtume alijaribu kwa miaka ishirini na tatu kuanzisha jamii ya Kibinadamu miongoni mwa watu hao hao na akafaulu. Na mwishoni mwa maisha yaliyojaa mapambano, jitihada na baada ya kuwasilisha ujumbe wake kwa watu na kuwasogeza karibu na Mwenyezi Mungu Mweza wa Yote na kuwapa sheria zilizo bora sana kwa mtu binafsi na umma wote wakati anarudi kutoka kwenye Hija yake ya Mwisho na akalala kitandani kwa sababu ya kuugua. Wakati wa siku ambapo maradhi ya Mtukufu Mtume yalizidi, jiji la Madina lilimezwa na simanzi na hofu ya tukio la kuogofya na lisiloelezeka ilionekana kwenye nyuso za watu.

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Siku hizo Waislamu walikuwa wanafanya kampeni dhidi ya Warumi kwenye mpaka wa Magharibi. Mtukufu Mtume aliagiza jeshi liondoke Madina chini ya uongozi wa Usamah bin Zayd ili kuimarisha majeshi ya Uislamu. Inasemekana kwamba watu fulani wangeambatana na jeshi na wasingebaki Madina kwani yeye alitaka kwamba kama ingetokea akatawafu Madina ingekuwa haina aina yoyote na migongano na njama ili kwamba mrithi wake na khalifa Ali bin Abi Twalib angeweza kuimarisha misingi ya Ukhalifa. Maradhi ya Mtukufu Mtume yaliongezeka siku hadi siku na rangi ya uso wake ilisawijika. Wakati mwingine hali yake ilipokuwa nafuu aliweza kwenda Msikitini kusali na wakati mwingine alimtuma Imam Ali kusalisha badala yake. Siku moja ambapo Mtukufu Mtume alikuwa na nguvu kidogo alikwenda Msikitini. Baada ya Swala alipanda kwenye mimbari na akasema maneno yake ya mwisho kwa watu na akatoa mapendekezo yake. Pia aliacha kama kumbukumbu yake hadithi maarufu ya Thaqalayn akasema: “Mimi ninaondoka kutoka miongoni mwenu na ninawaachieni vitu viwili vya thamani sana. Kama mkivishikilia hamtapotoka kamwe: mojawapo ya vitu hivyo ni Qur’an na kingine ni watu wa Nyumba Yangu. Baada ya kurudi kutoka msikitini, maradhi ya kiongozi mkuu wa Waislamu yalizidi na hali yake ikazidi kuwa mbaya.

Shujaa Bilal alihuzunika sana kwa sababu ya ugonjwa wa Mtukufu Mtume na hakuweza kupata fursa katika kipindi hiki cha wasi wasi mkubwa sana kwake.

Hali mbaya zaidi ya Mtukufu Mtume iliongeza wasi wasi wa watu. Watu wale ambao wangeungana na jeshi la Usammah kwa mujibu wa amri ya Mtukufu Mtume, walibaki Madina kwa kisingizio cha ugonjwa wake, na wale waliokwisha ondoka, walirudi ili wapate taarifa kuhusu hali yake. Kwa hiyo sababu

109

110


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

ya msokotano wa pamoja wa Waislamu kuwa hafifu, na uwanja wa upotovu ukaanza kutayarishwa kuhusu suala la urithi wa Mtukufu Mtume.

BILAL AFANYA UPELELEZI Mtukufu Mtume alikuwa anaugua kitandani na Bilal aliendelea kuadhini Adhana kama kawaida wakati wa Swala na halafu anakwenda kwenye mlango wa nyumba ya Mtukufu Mtume na kutangaza wakati wa Swala. Kama hali ya Mtukufu Mtume ilikuwa nafuu yeye mwenyewe alikwenda msikitini na kuongoza Swala. Vinginevyo alimuagiza Imamu Ali kuongoza Swala. Asubuhi ya usiku ambapo baadhi ya watu pamoja na Abu Bakr waliporudi kutoka kwenye jeshi la Usamah na kwenda Madina Bilal aliadhini Adhana, halafu akaenda kwa Mtukufu Mtume. Hali ya Mtukufu Mtume haikuwa nzuri wakati huo. Aisha alijipatia fursa na akatuma ujumbe kwa Abu Bakr akimwomba aongoze sala badala ya Mtukufu Mtume. Bilal alipofika msikitini akamuona Abu Bakr yupo kwenye sehemu ya kuongozea Swala akisema kwamba aliambiwa na Mtukufu Mtume aongoze Swala. Hata hivyo, watu walikuwa wanapiga kelele sana na kuuliza maswali mbali mbali. Kila mtu alikuwa anapendekeza hiki au kile na palikuwepo na uwezekano wa tofauti kutokeza miongoni mwao. Kwa haraka Bilal aliwaashiria wamsikilize na alisema: “Tulieni kimya na acheni tofauti zenu. Mtukufu Mtume bado mzima na yupo miongoni mwetu. Sasa hivi ninakwenda kuleta taarifa sahihi.”

111

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Bilal aliondoka msikitini mara moja na alikwenda nyumbani kwa Mtukufu Mtume na akamtaarifu kuhusu suala hilo. Mtukufu Mtume alikasirika sana na alimwambia Imamu Ali na bin Abbas: “Nishikeni. Ninyanyueni nisimame. Ninaapa kwa jina lake, Ambaye mikononi Mwake uhai wangu upo, hii ni dharura katika Uislamu dharura kubwa na vurugu. Imamu Ali na bin Abbas walimsaidia Mtukufu Mtume na wakaelekea msikitini na Bilal akiwepo. Walipofika msikitini Mtukufu Mtume mwenyewe aliongoza Swala na akanyamazisha makelele yote na kilio chote. Halafu akatoa hotuba mashuhuri sana ambayo imeandikwa kirefu kwenye vitabu vya historia. Alifanya mapendekezo muhimu na baada ya hapo alirudi nyumbani. Kwa kweli, Bilal mtu mwenye akili bora na muumini, alizuia hali ya mfarakano mnamo hatua za mwanzo, na kwa kitendo cha kimapinduzi aliwafahamisha watu utambulisho wa hao watu ambao wangeweza pia kufanya njama siku zijazo. Bilal alikuwa na desturi ya kufanya kazi yake ya kudumu na baada ya kuadhini Adhana, alimtaarifu Mtukufu Mtume kuhusu wakati wa Sala kwa kusema “Asalat ya rasula-llah” (ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu wakati wa Swala umewadia.) siku moja, wakati wa ugonjwa wake, Mtukufu Mtume alimwambia Bilal baada ya kusikia sauti yake. “Ewe Bilal! Mwenyezi Mungu na akurehemu wewe kwani umefanya kazi kwa uzuri wa kupendeza.”

112


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

MADINA YATOA RAMBI RAMBI YA KIFO CHA MTUKUFU MTUME

walitoka mitaani na kuelekea nyumbani kwa Mtukufu Mtume katika makundi mbali mbali.

Mtume mashuhuri wa Waislamu alitawafu ambapo alikuwa na wasiwasi sana kuhusu hali ya baadaye ya Uislamu na Waislamu.

Wanawake waombolezaji walitoka nje ya nyumba zao na wakiwa wanasikitika wakielekea nyumbani kwa Bibi Fatimah Zahra, binti mpendwa wa Mtukufu Mtume, kumliwaza.

Baada ya kutawafu Mtukufu Mtume matendo yasiyo halali yalifanywa na watu na matatizo mbali mbali yalijitokeza kwenye jamii mpya kabisa ya Kiislamu.

Bilal alihuzunika sana kwa sababu ya janga hili. Alikuwa anasikitika akiwa pembeni mwa nyumba ya Mtukufu Mtume na alisema: “Ooo! Mtume wa Mwenyezi Mungu ametawafu! Mgongo wangu umevunjika na matumaini yangu kuharibika! Afadhali nisingezaliwa ili nishuhudie siku hii!�

Maadui wakubwa kama vile Ajemi na Rumi na vile vile Wayahudi na wanafiki walikuwa wanaingojea siku hii kwa shauku kubwa. Walikuwa wameridhia matumaini na walifanya mipango ya siku zifuatazo, maadui wa hatari kuzidi wote ni wale watu ambao hawakubadilika miongoni mwa Waislamu wenyewe ambao walikuwa na matumaini ya kuanzisha tena njia na tabia za kipindi cha ujahilia na kupata vyeo na kazi kubwa. Baada ya Mtukufu Mtume walianza kutekeleza mipango yao ya kisaliti ili kuweza kutimiza uovu wao. Matukio yasiyopendeza yalielekea kufanyika. Njama za chini chini na shughuli ambazo zilikuwa zinafanywa ili kufanya hali kuwa mbaya zaidi. Waislamu walipata usumbufu sana kwa sababu ya kumpoteza kiongozi wao mkuu. Jiji lote la Madina lililalamika. Machozi yalikuwa yanatirirka kutoka machoni mwa waombolezaji kama mvua za majira ya kuchipua na mawingu mazito yamefunika mbingu ya jiji. Inawezekana kusemekena kwamba ardhi na mbingu zilikuwa zinaomboleza kifo cha Mtukufu Mtume.

NYUMBA YA HUZUNI Imamu Ali na baadhi ya masahaba wa karibu wa Mtukufu Mtume walikuwa wameketi karibu na mwili wake wakiwa na simanzi kubwa. Vilio vya kugumia na masikitiko vilifika kileleni. Kwa mujibu wa wasia wa Mtukufu Mtume Imamu Ali alianza kuosha maiti yake tukufu baada ya saa chache. Baada ya hapo walingoja hadi hapo tukio hilo litakapotangazwa hadharani, ndipo maiti ya Mtukufu Mtume itakapozikwa, na watu watakuwa wamekwisha fika mahali palipo pendekezwa kwa kusudio hilo. Katika hatua hii ya kutafakari katika historia ya Uislamu baadhi ya watu walikusanyika mahali paitwapo Saqifah Bani Saidah na wakaanza shughuli ya kumteua mtu wa kumrithi Mtume wa Uislamu.

Watu walishtuka na kushangaa. Waliacha kazi zao za kila siku,

Ni dhahiri kwamba kitendo hiki kilikuwa kinyume na

113

114


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

mapendekezo na maagizo ya Mtukufu Mtume kuhusu Imamu Ali kuwa Wasii wake na Khalifa kwa sababu Khalifa wa Mtume alikwishateuliwa huko Ghandr Khum kwa amri ya Mwenyezi Mungu iliyotekelezwa kupitia kwa Mtukufu Mtume. Idadi ya watu waliokusanyika hapo Saqifah ilikuwa ndogo sana kwani ingehesabiwa kwa vidole. Wakati ambapo mwili mtakatifu wa Mtukufu Mtume ulikuwa bado haujazikwa na maneno ya Mtukufu Mtume kuhusu uteuzi wa Khalifa baada yake bado hayajafutika katika akili za watu, na binti yake na mkwe wake walikuwa bado wanaomboleza na kumwaga machozi, baadhi ya watu wajulikanao sana walikuwa wanazungumzia kuhusu uteuzi wa Khalifa! Ni dhahiri kwamba mkutano huu lazima ueleweke kama una dosari, si wakati wake na unapingana na uamuzi wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Zaidi ya hayo, mtu mashuhuri zaidi kuliko wote miongoni mwa Waislamu na mwenye jitihada katika kufuata njia ya Uislamu ni Imamu Ali bin Abi Talib hakushiriki katika shughuli hii ya mkutano huu usio stahili kufanywa na haukuwa na uthibitisho wa Waislamu wa Madina na masahaba waaminifu wa Mtukufu Mtume kama vile Bilal, Miqdadi, Abu Dharr, Salman, Ammar na kadhalika. Kusema kweli, mtu anaposoma historia ya Uislamu kwamba watu hao waliofanyiza halimashauri hiyo ya kumteua Khalifa, hawakungoja hata baada ya maziko ya Mtukufu Mtume, na waliendelea na utafutaji wao wa mamlaka atastaajabu.

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

kumpata Khalifa na kuwatawala watu walitia sahihi hati ya mfarakano wa daima milele na maafa ya Waislamu hadi siku ya Hukumu.

TUKIO LA SAQIFAH Siku hiyo, watu wachache wa kabila la Aws walimleta Sa’d bin Ubadah Ansari mtu mzee sana, hapo Saqifah na wakamteua yeye kuwa mgombea wa ukhalifa kutoka miongoni mwa Ansari. Kwa upande mwingine ambapo baadhi ya watu wa kabila la Khazraj walipata taarifa kwamba halimashauri iliundwa huko Saqifah kumteua mrithi wa Mtukufu Mtume, wao pia walikwenda huko haraka. Inasemekana kwamba baadhi ya watu mahsusi walikwishadokezwa na walialikwa hapo. Kwenye mkutano kila mtu alikuwa anazungumza kwa maslahi yake mwenyewe na kutamani kwamba yeye mwenyewe au mtu anaye muunga mkono awe Khalifa. Baadhi ya watu walikuwa wanasema kwamba Ansar walikuwa na haki zaidi ya kurithi Ukhalifa na khalifa lazima atoke miongoni mwao, kwa sababu ni wao ndio waliomkaribisha Mtukufu Mtume na Muhajirina wengine katika jiji lao na wakawasaidia. Baadhi ya watu walikuwa wanasema kwamba Ukhalifa ungerithiwa na Muhajirina kwa sababu ni wao ndio walioacha nyumba zao kwa ajili ya Uislamu.

Kweli, watu hao walimwacha Imamu Ali peke yake akiwa ameketi karibu na mwili wa Mtukufu Mtume na ili waweze

Mmojawapo wa Ansar alisema: “Khalifa lazima atoke miongoni mwa kabila la Quraishi, kwa sababu kama kujitolea na mtu kujitolea muhanga nafsi yake ni kigezo ni nani ambaye anastahili zadi kurithi ukhalifa ikilinganishwa na Imamu Ali”?

115

116


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Mmojawapo wa watu waliohudhuria alikasirishwa aliposikia neno ‘Ali; na alisema kwa hasira: “Nyamaza!” Palitokea kelele na sauti za kugumia. Kila kundi la watu liliengua kundi la watu wengine na kuona kasoro ya kundi hilo. Pingamizi juu ya pingamizi zilifika kileleni. Wakati huo huo Abu Bakar aliingilia kati hotuba za wengine na alisema: “Maoni yangu ni kwamba Ukhalifa urithiwe na Muhajirina na ninafikiri Abu Ubaydah na Umar wanasifa za kufanya kazi hiyo na mimi nipo tayari kwa yeyote kati yao.” Umar ambaye alikuwa anangojea fursa hii na alikusanya ujasiri wake na alisema: “Nilimsikia Mtukufu Mtume akisema kwamba viongozi wa dini watatoka miongoni mwa Quraishi.” Abu Bakr alifurahi na alisema: “Umenena vema.” Kwa hali ya mambo yalivyokuwa Abu Ubaydah na Umar walisema kwa sauti moja: “Tunaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba kamwe hatutakutangulia wewe katika jambo hili kwa sababu wewe umekuwa sahaba bora kuliko wote na rafiki mwaminifu wa Mtukufu Mtume na hapana yeyote ambaye anaweza kuwa bora zaidi yako.” Ansari walitambua kwamba kutokana na mazungumzo haya kwamba walikuwa wananyang’anywa Ukhalifa. Kwa hiyo, haraka walibadili msimamo wao na wakapiga kelele za kaulimbiu za kumpendelea Amir wa Waumini na wakasema: “Ali bin Abi Talib ndiye awe Khalifa wa Mtukufu Mtume.” Kaulimbiu hii ilisababisha wakubwa wengine watetemeke, kwa sababu walitambua kwamba kama Imamu Ali angekuwa huru baada ya kumaliza shughuli za maziko ya Mtukufu Mtume na akahudhuria mkutano wa Saqifah, watu wote wangetoa kiapo cha utii kwake na angepata kura za watu wengi. 117

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Ilikuwa ni kwa sababu hii Umar aligeukia kwa Abu Bakr haraka na kusema: “Nipe mkono wako ili kwamba nitoe kiapo cha uaminifu kwako, kwani wewe ni mzee wa taifa na unastahili nafasi hii,” Halafu akanyoosha mkono wake na akaushika mkono wa Abu Bakr kwa njia ya kutoa kiapo. Baada ya hapo isipokuwa watu wawili au watatu, wote wale waliokuwepo walitoa kiapo cha uaminifu kwa Abu Bakr bin Abu Quhafaha. Kwa hiyo, halimashauri ya uteuzi wa Khalifa ilimaliza kazi yake na watu walio hudhuria walirudi jijini na kutangaza kwamba walimteua bin Abu Quhafa kumrithi Mtukufu Mtume. Jambo moja tu ambalo halikutamkwa kwenye mkutano wa halimashauri ni kuhusu Ahlul Bait Nyumba ya Mtukufu Mtume. Jina moja lililotamkwa kidogo sana ni lile la Imamu Ali na jambo moja tu ambalo halikuzungumziwa ni mapendekezo na usemi wa Mtukufu Mtume kuhusu urithi na Ukhalifa wa Imamu Ali. Masahaba na watu waliokaribu naye Mtukufu Mtume kama Bilal, Salman, Abu Dharr, Miqdad na kadhalika hawakuwepo huko na hata kama wangekuwepo hakika wangekataa hili. Baada ya kuimarisha kutoa kiapo cha utii kwa Abu Bakr, kundi la watu la ukoo wa Bani Umayyah, walipoona kwamba Imamu Ali hangeridhika, waliondoka kuelekea nyumbani kwake wakiongozwa na Abu Sufyan. Lengo la kundi hili na hususani Abu Sufyan ilikuwa kwamba kwa msaada wao Imamu Ali achukue haki yake kutoka kwa Bani Tamim. Na moyoni mwake hasa hasa Abu Sufyani alitaka 118


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

kwamba baada ya msaada huo yeye mwenyewe angepata umashuhuri na yeye mwenyewe pamoja na watu wa karibu naye wangekuwa sehemu muhimu katika utawala halisi wa nchi za Kiislamu na serikali ya Imamu Ali. Au alitaka kuendesha uadui wake wa zamani dhidi ya Uislamu na Waislamu na aweze kupata malengo yake yenye uovu kwa kuanzisha vita vya wenyewe kwa wenyewe. Abu Sufyani alisema kwenye mkusanyiko wa marafiki zake: “Enyi Bani Abdul Muttalib! Ukhalifa umeondoka mikononi mwa Bani Hashim na umehamishwa kwa Abu Bakr. Na kesho huyu mtu (Umar) atatutawala. Simameni ili kwamba twende kwa Ali na baada ya kuzungumza kuhusu jambo hili na yeye tunaweza kutoa kiapo cha utii kwake na tunaweza kumuua kila mtu anayetupinga.” Akiwa na lengo hili katika fikra zake, Abu Sufyani alimwendea Imamu Ali siku hiyo na alimwambia kwamba endapo yeye (Imamu Ali) angeamua kurudisha haki yake yeye angefanya kila njia ya kumsaidia.

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

“Kuuendea Ukhalifa kwa njia iliyo pendekezwa na wewe, hakuna tofauti na maji machungu. Kwa hiyo, upinzani wa kivita katika hali kama hii mimi sipendelei kwa sababu mtu anayechuma tunda ambalo halijawiva ni sawa na mtu anayelima kwenye ardhi ya mtu mwingine. “Kama nikisema kuhusu haki yangu na kwamba mimi ninastahili kuwa kiongozi, itasemekana kwamba mimi nina tamaa ya utawala na endapo nina nyamaza itasemekana kwamba ninaogopa kuuawa, ingawa mtoto wa Abu Talib anapenda kifo zaidi ya mtoto apendavyo titi la mama yake. Kwa hiyo kimya changu kuhusu jambo la Ukhalifa si kwa sababu ya kuogopa kifo au kushindwa au kurudi nyuma, lakini ni kwa sababu ya kitu ambacho ninakitambua, na ambacho kinanizuia mimi kutaka Ukhalifa katika hali ya sasa. Na endapo ninafichua kile ninachokitambua, utatetemeka na kutikisika kama kamba kwenye kisima chenye kina kirefu. “Kwa hiyo, kitu unachotaka nifanye si kwa maslahi yangu au maslahi ya Uislamu na Waislamu. Nyanyukeni na mwondoke.”

Amiri wa Waumini alimwangalia Abu Sufyani na ilionekana kama vile alisoma lengo lake kwenye uso wake na aligundua kwamba alikuwa anatafuta fursa ya kuuangamiza Uislamu. Kwa sababu hii alimkatalia na alimwambia: “Enyi watu! Yakatisheni mawimbi ya ghasia kwa kutumia boti za ukombozi na mzivuke. Weka mguu wako nje ya njia ya uadui na uvue taji la ubinafsi kutoka kichwani mwako na ulitupe ardhini. Yeyote atakaye nyanyuka akiwa na manyoya (marafiki na wanao muunga mkono) anao utulivu na amani, na yeyote atakaye salimu amri kwa kulazimishwa au madhumuni mazuri ajipwekeshe.

Bilal na mamia ya Waislamu wengine walikusanyika karibu na nyumba ya Mtukufu Mtume na walikuwa wanalia. Walikuwa hawajapata kuona siku yenye huzuni kama siku hiyo ya kifo cha Mtukufu Mtume. Simanzi na uzito wa janga iliwaathiri sana hivyo kwamba hawangeweza kuyaona matatizo yaliyokuwa yanatokea wakati huo humo jijini.

119

120

Ghafla habari zilipokelewa kwamba kundi la watu ambao walikusanyika Saqifah Bani Saidah wamemteuwa Abu Bakr kama mrithi wa Mtukufu Mtume. Bilal na waombolezaji wengine walistaajabu kusikia habari hiyo. Walisema: “Hii ina maana gani? Tendo hili baya na lisilo na mantiki limefanywa


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

wakati mwili mtakatifu wa Mtukufu Mtume haujazikwa na machozi ya wale waliobaki bado hata hayajakauka? Khalifa wa Mtukufu Mtume hakuteuliwa Ghadir Khum na Amri ya Mungu? “Inawezekana kwamba mtu ambaye si Imamu Ali akamrithi Mtukufu Mtume? Si watu hawa hawa walitoa kiapo cha utii kwa Imamu Ali huko Ghadir Khum kama Khalifa? Tukio la Ghadir bado bichi na mapendekezo ya Mtukufu Mtume bado yanasikika masikioni mwetu!” Hata hivyo, taratibu zilikamilishwa na Abu Bakr alianza kufanya kazi ya Khalifa. Watu hawa ambao walipanga mpango huu miaka mingi kabla ya hapo, waliutekeleza baada ya kifo cha Mtukufu Mtume. Hawangefanya hivi, kwa sababu kwa hili tendo lao, umoja na ulinganifu wa Waislamu ulivunjika na mbegu ya tofauti ilipandwa katika jamii na Mwenyezi Mungu anatambua matatizo ambayo wameyafanyiza kwa Waislamu. Kundi dogo la utawala lilipeleka watu kadhaa kama wawakilishi, magavana wakusanyaji, kwenye nchi za Kiislamu. Hawa ni watu ambao walikuwa wanajitayarisha kwa fursa kama hii tangu muda mrefu na sasa wamekuwa na bidii ya kupata kiapo cha utii kutoka kwa watu na kuimarisha kiti cha Ukhalifa. Wakati mwingine baadhi ya watu walisema vitu vya kumpendelea Imamu Ali lakini sauti yao ilinyamazishwa haraka kwa ahadi, vitisho na udanganyifu na hali kama hiyo ilitengenezwa hivyo kwamba endapo mtu yeyote alifanya upinzani wowote jina lake liliingizwa kwenye orodha maalumu na faili lilifunguliwa kwa ajili yake na alifanyiwa usumbufu na kuteswa. 121

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Wapelelezi na waungamkono wa Ukhalifa walisababisha hali kuwa ya wasi wasi hivyo kwamba endapo mtu yeyote alisema kuhusu tukio la kutawafu kwa Ukhalifa, shutuma na vitisho vilimngojea.

JUKUMU LA IMAMU KATIKA KULINDA UISLAMU Kufika kwa Abu Bakr kwenye kilele cha mambo ni jambo lililoanzisha hali nyeti kwa dunia ya Uislamu. Ni dhahiri kwamba katika hali hii, mgogoro wa wenyewe kwa wenyewe wa mapambano ya kivita ungeharibu Uislamu na Qur’an kabisa, kwa sababu himaya ya Ajemi na Rumi kwa upande moja na maadui wa ndani – Wayahudi na Wakristo kwa upande mwingine walikuwa wanangojea siku kama hizo ili kwamba pindi vita vya wenyewe kwa wenyewe vikianza, wao wangepata fursa ya kushambulia Uislamu na kuuharibu kabisa ukingali katika hatua zake za Mwanzo. Idadi ya wanaomuunga mkono Imamu Ali walimwendea mnamo kipindi hicho hicho na walimwomba waanzishe maasi. Hata hivyo, Mtukufu Imamu hakusita hata kwa nukta moja katika kuamua kwamba hatua kama hiyo haikuwa na maslahi kwa Uislamu na Waislamu. Alikuwa anatambua nia halisi ya maadui wa nje na ndani. Alimsikia Mtukufu Mtume akisema: “Ewe Ali! unafaidi nafasi ya Ka’abah. Watu wanatakiwa kuja kwako na wala si wewe uende kwao kwa ajili ya uongozi.” Wakati wa hali ile nyeti; Mtukufu Imamu hakutaka kulinda haki yake kwa nguvu ya kupigana ili kwamba Uislamu uendelee kudumu katika hali ya usalama na angetoa mchango wake wa kuujenga na kuuokoa Uislamu siku za usoni. 122


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Imamu Ali alichagua uvumilivu na kimya kama ndio kazi yake kwa kipindi cha miaka ishirini na tano na aliishi maisha ya upweke kama ndege asiye na mabawa ya kurukia na kwa njia hii alionesha umashuhuri wake wa kiroho na ujasiri kwa manufaa ya Uislamu na Waislamu na aliwaongoza watu akiwa nyuma ya pazia. Haikuwa tu kwamba aliitekeleza haki yake, lakini aliamua kuwa kimya kuulinda Uislamu kutoka kwenye balaa la tofauti za ndani, ingawa kimya hiki kilikuwa kilio cha aina yake.

BILAL AFANYA MGOMO Tangu siku ambapo Mtukufu Mtume na Waislamu wengine walipohamia Madina hadi siku alipokuwa yu hai, Bilal alikuwa na desturi ya kuwaita watu na kukusanyika msikitini yaani wakati wa sala na kukusanya jeshi au kama palitokea tatizo ambalo lilihitaji ufumbuzi, alikuwa na utaratibu wa kuadhini Adhana na watu walimiminika msikitini na kukusanyika.

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Mtume na hii ilikuwa mbinu nyeti sana, kawaida sana na wakati huo huo ya hatari sana ambayo Bilal aliitumia dhidi ya Ukhalifa. Na tangu hapo, na kuendelea, Bilal hakushiriki kwenye mkusanyiko wowote rasmi ulioitishwa na ‘wao’ Kutoshiriki kwa Bilal, ambaye alikuwa na wadhifa nyeti kutoka kwenye jukwaa na jamii iliweza kuwafanya watu wafikirie tatizo la siku hiyo. Waungaji mkono wa Khalifa walidhani kwamba kama Bilal angepiga Adhana sauti za kugumia na kilio cha wapinzani wa Khalifa kingekwisha na watu wangekwenda msikitini kama walivyozoea kufanya baada ya kusikia sauti ya Bilal. Adhana iliyoadhiniwa na Bilal, ingeweza kufunika pazia kwenye – njama za uendeshaji wa Ukhalifa na kuwadanganya watu wenye akili finyu na wa kawaida. Wakiwa na mawazo haya akilini mwao walimuona Bilal baada ya kumfuata sana na wakamwomba Adhini Adhana kwa ajili ya Swala.

Hata hivyo, baada ya Mtukufu Mtume, Abu Bakr alipopata Ukhalifa aliamua kwenda msikitini akiwa na cheo hicho, na alisimama kwenye mimbari ya Mtukufu Mtume ili kwamba kwa njia hii angeweza kuimarisha nguzo za serikali yake na kuwasiliana na watu moja kwa moja. Hatua ya kwanza ya kufanya taarifa ya mkusanyiko na watu kwenda msikitini hadi hapo Mtukufu Mtume alipokuwa yu hai, ilikuwa ni Bilal kuadhini Adhana kwa sababu ya kuwaita watu msikitini. Hata hivyo, Bilal aliacha kuadhini Adhana baada ya kutawafu

Bilal alipata mafundisho ya Uislamu na kulelewa na Uislamu kwa muda wa miaka ishirini na tatu. Na alikuwa anahusika moja kwa moja na matukio mbalimbali ambayo yalifanyiza historia ya taifa jipya. Aliutambua na kuukubali Uislamu kwa uaminifu na alisikia aliyoyasema Mtukufu Mtume kuhusu kiongozi na uongozi. Hususan alikuwa anatambua matamshi ya Mtukufu Mtume yasiyo na utatanishi kuhusu Ukhalifa wa Imamu Ali na alijua kwamba uendeshaji wa utawala ulichukua kazi hiyo kinyume na maagizo ya Mwenyezi Mungu na Mtukufu Mtume. Kwa mujibu wa imani yake, aliyestahili kupata kazi hiyo ya Ukhalifa ni Amiri wa Waumini, Ali tu. Katika hali hiyo, ni dhahiri kwamba angetoa jibu gani kwa wale watu walio mwendea.

123

124

Watu wote walikuwa wameizoea sauti ya Bilal na kila wakati walingojea kusikia sauti hii ya kuvutia ambayo iliwaita kwa Mwenyezi Mungu na habari njema.


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Wajumbe wa Khalifa walisisitiza sana lakini Bilal alirudia jibu hilo hilo, kila mara na hakutaka kutilia maanani maneno yao.56 Kwa kukataa kuadhini Adhana, Bilal alitaka watu waone wajibu wao katika kufikiria hilo na wajikumbushe pole pole wakati wa Mtukufu Mtume na mapendekezo yaliyotolewa naye kuhusu Imamu Ali na Uimamu wake. Ilikuwa ni kwa sababu hii kwamba watu walimuuliza kwa nini hakuadhini Adhana, aliwajibu: “Baada ya Mtukufu Mtume wa Uislamu sintaadhini Adhana kwa ajili ya mtu mwingine.” Kwa upande mwingine kutohudhuria kwa Amiri wa Waumini, Salman, Abu Dhar, Zubayr, Bilal, Miqda, Suhayb na kadhalika kwenye mikuanyiko ambayo kwa kawaida ilifanywa msikitini, ni jambo ambalo liliimarisha msimamo wa Bilal na ikawa sababu ya watu kutilia shaka uhalali wa kisheria wa kundi lililokuwa linatawala wakati huo na hata kuukataa. Utawala wa Ukhalifa uliogopa na kuwa na wasiwasi kwa sababu ya msimamo wa Bilal na ulijaribu kumfanya yeye na wapinzani wengine wasalimu amri. Ilikuwa katika hali hii ya woga kwamba khalifa aliwatuma rasmi baadhi ya watu kwenda kwa Bilal kumfanya huyo mtu mweusi mbishi asiyeyumbishika57 ajisalimishe kwa Khalifa kwa gharama yoyote kwa njia ya ahadi au vitisho kishawishi cha fedha na cheo. 56

57

Nafasus Rahman sura. 10, Majalisul Mu’minin Juz. I, uk. 268; Jame’ur Ruwat, Juz. I, uk. 131; Majma’ul Bahrain Babul Lam; Muntahul Amal, uk. 78; Usudul Ghabah Juz. I, uk. 209; Rijal Ma Maqani, uk. 192; Qamusr Rijal Juz. ii, uk. 243. Hiki ni cheo ambacho utawala wa Ukhalifa na wafuasi wa fikra hiyo wamempa Bilal katika historia. 125

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Hata hivyo, Bilal hakuwa tayari kutojali ukweli na ‘kufanya wafanyavyo Waumini.’ Bilal aliuona Uislamu umo ndani ya Imamu Ali na aliamini kwamba hata kama pendekezo la Mtukufu Mtume halingekuwepo pale, hapana mwingine isipokuwa Imamu Ali ndiye aliyekuwa anastahili kwa Ukhalifa. Alikuwa anasadiki kwamba Uislamu wa kweli ulikuwa ule ulioonyeshwa na Imamu Ali na marafiki zake ingawa walikuwa wachache kwa idadi. Yeye huyo, ambaye alistahili shida na kupata mateso kwa ajili ya Uislamu huo huo sasa hakutaka kuuona kama kitu cha kuchezea cha matamanio ya kimwili na kuwa ni kitu kinacho milikiwa na utawala wa Ukhalifa. Kwa hivyo, Bilal alitoa jibu la mkato kwa wakilishi wa Khalifa kwa kusema: ‘Sitaadhini Adhana kwa mwingine yeyote isipokuwa mtu ambaye Mtukufu Mtume alimteua kama mrithi wake.” Hatimaye, Umar ambaye alikuwa rafiki wa karibu wa Khalifa (Abu Bakr) na alifikiriwa kuwa wakala muhimu sana kwa kuchanguliwa kwake kuwa khalifa na muungaji mkono mkubwa wa kuendelea kwake kuwa katika cheo hicho aliamua kujadili suala hili na Bilal mwenyewe binafsi. Umar alipomuona Bilal, alikuwa anafikiri: “Sasa nitamfanya asalimu amri na na kumtoa kwenye kundi la wapinzani wa Khalifa.” Baada ya kusalimiana na kubadilishana vishamirisho, Umar alisema: “Ewe Bilal! Kwa nini umetuacha sisi peke yetu siku hizi? Nilikuwa napenda sana kwamba ungekuwa na sisi ili kwamba tungekupa kazi fulani. Kwa nini hufiki msikitini tunakutegemea uadhini Adhana na uwaite watu waende 126


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

msikitini wakasali na Khalifa wa Mtukufu Mtume. Naealewa kwamba umeamua kwamba hutaadhini Adhana. Kwa nini? Unakumbuka kwamba ni huyu huyu Abu Bakr aliyekukomboa kutoka kwenye utumwa na mateso ya mmiliki wako katili. Unadhani kwamba ni vema umwache sasa na usiadhini Adhana kwa ajili yake?

kuniacha huru siku hiyo na ningelikufa katika hali hiyo, kwa sababu wakati huo nilikwisha kuwa muumini wa kweli ningekwenda peponi. Lakini kwa mazingira ya sasa ambapo mnataka nishiriki katika jambo hili sielewi hatima yangu ni kwenda Peponi au Jahanamu, na ama ndivyo au sivyo ninaweza kulinda imani yangu.”

Bilal alianza kukumbuka matukio yaliyopita ya historia kama mateso na kipindi cha kufukuzwa kwake na kukosa makazi, kuhamia kwake Madina, mapigano ya kivita na makafiri na washirikina, kutekwa kwa Makkah na kutawafu Mtukufu Mtume. Alimwambia Umar: Ni furaha iliyoje wakati wa siku ambapo Mtukufu Mtume alikuwa miongoni mwetu na aliwaita watu waende kwa Mwenyezi Mungu na haki. Na aibu hizi zimekuwa ngumu kiasi gani zenye giza na msiba mkubwa? Tunakabiliwa na hali gani?”

Umar alikasirika sana aliposikia maneno haya na alimtupia Bilal jicho kali na la hasira lililojaa dharau. Baada ya dakika chache alinyanyuka na kuondoka kwenda zake akiwa amefadhaika.58

Bilal aliyarejesha mazungumzo kwenye jambo husika na ambapo machozi yalikuwa yanatirirka kwenye mashavu yake aliendelea kusema: “Na tuangalie kama Abu Bakr alininunua mimi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na akanipa uhuru kwa ajili ya Mwenyezi Mungu au alikuwa na lengo lingine. Kama alifanya yote haya kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, hana haki yoyote juu yangu na kama hakufanya haya kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, basi bado mimi ni mtumwa wake na chini ya miliki yake, lakini mimi ni huru kuhusu jambo la imani. Na kama ambavyo nimekwisha sema, sitaadhini Adhana kwa ajili ya mtu mwingine yeyote baada ya Mtukufu Mtume. Zaidi ya hayo nitatoa kiapo cha heshima kwa mtu huyo tu ambaye wajibu wangu ni kumtii. Ninamkubali mtu huyo kama Khalifa ambaye ameteuliwa na Mtukufu Mtume kama mrithi wake. Halafu ninakwambia: Kama Abubakr hangeninunua na 127

BILAL ANAFUKUZWA Mipango yoye ya utawala wa Ukhalifa ya kumfanya Bilal ajisalimishe ilikuwa ya kuvunja moyo na haikuweza kusababisha uharibifu hata kidogo kuhusu uamuzi wake imara. Alivumilia bila woga, hakuafiki ahadi zilizofanywa na Umar na akawa hatishiki kwa vitisho. Na hakujisalimisha. Kwa sababu ya msimamo wa Bilal na unyeti uliokuwa umetengenezwa katika jamii kwa sababu ya kukataa kwake kutoa kiapo cha utii kwa Abu Bakr, utawala ua Ukhalifa ulitengeneza mpango wake wa mwisho wa kumwadhibu. Kama ilivyohofiwa kwamba angeungwa mkono na watu wengine na tatizo lingeongezeka mmoja wapo wa watu waliokuwepo hapo alishauri kwamba ingekuwa vema endapo Bilal angefukuzwa kutoka Madina na kupelekwa sehemu ya mbali na makao makuu ili kwamba kwa njia hii sauti za kugumia na kilio kingekoma na watu wangemsahau.

58

Majalisul Muminin juz, I, uk. 268; Qamurs Rijal, Juz. ii, uk. 243. 128


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Hata hivyo, washauri wa Khalifa wakasema: “Endapo tukimfukuza wazi wazi tutalaumiwa sana. Inawezekana kwamba Imam Ali anaweza akakataa. Kufuatia tukio hilo, kitendo chetu kitasababisha matokeo kinyume na vile tunavyotaka sisi. Kwa hiyo, ni vema kama angetishiwa na kutekwa ili alazimike kuondoka Madina yeye mwenyewe. Njia hii ‘nzuri sana’ watu wote watasema kwamba ameondoka Madina kwa chaguo lake Mwenyewe. Mpango huu ulithibitishwa kwa wingi wa kura na kwa hiyo Bilal aliteswsa wakati wa mchana na usiku na kutishwa kuuawa. Hatimaye alipokea ujumbe ufuatao: “Ama utoe kiapo cha utii kwa Abu Bakar na uadhini Adhana au uondoke Madina.”* Baadhi ya wana historia wameandika: Umar alimwambia Bilal: “Sasa wewe hutaki kuadhini Adhana, hutakiwi kuendelea kuwepo Madina ili usije ukawa sababu ya uovu kwa wengine.” Na alimshinikiza Bilal.59 Hivyo msemaji mkuu wa Uislamu aliwekwa kwenye hali ngumu ya kushangaza. Kwa upande moja ilimwia vigumu kwake kuondoka kwenye ‘jiji la Mtume’ na kwa upande mwingine ilikuwa haiwezekani pia yeye kuendelea kuishi hapo. Alitafakari ama aendelee kuishi hapo Madina au astahamili shinikizo. Hata hiyvo, angeondokaje na kuacha Madina na kaburi la Mtukufu Mtume bwana wake, kwa kuwa hilo lilikuwa jiji la rafiki yake lenye kumbu kumbu nyingi? Hata hivyo, * 59

Rijal Ma Maqani, uk. 182. Majalisul Mu’minin J.1,uk 268; Qamusur Rijal, J.2, uk.243 129

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

alilazimika kuondoka hapo ili angeweza kuwashawishi watu kutafakari zaidi kuhusu jinsi mambo ya wakati huo ambayo yalikuwa hayaridhishi na pia wangefanya upinzani, shutuma na mara kwa mara wasingetii, na labda ingewezekana haki iliyoporwa ingerudi kwa mwenyewe. Ilikuwa ifanyiwe hivyo kwa sababu hapakuwepo na marekebisho mengine. Endapo Bilal angeendelea kuishi Madina angelazimika kukubaliana na watawala na angeeleza hali ilivyo wakati huo na msimamo wake mwenyewe. Endapo angeendeleakuishi, angelazimika kuthibitisha matendo ya serikali na Bilal hangeweza kufanya hivyo, kwa sababu maoni yake ni kwamba matendo haya hayakuwa ya haki. Aliamua kwennda Syiria na alijitayarisha kwa kufukuzwa, na kwa lolote lile. Kabla ya kuamua kuondoka Madina Bilal alionana na familia ya Mtukufu Mtume kwa ushauriano. Alipokuwa tayari kuondoka, kwanza alikwenda kumuona na kumuaga Amiri wa Waumini, Imamu Ali. Mkutano huu ulifanyika katika hali ya kuchanganyikiwa sana na Mtukufu Imamu alishangaa sana. Machozi yalikuwa yanatiririka kwenye mashavu maeusi ya Bilal kama lulu na labda alikuwa anasema: “Endapo ningekuwa na chaguo kamwe nisingeondoka kutoka kwako na karibu na Mtume. Ni matumanini yangu kwamba nitarudi. Halafu akazuru kaburi la Mtukufu Mtume akiwa katika huzuni kubwa na aliendelea kulia kwa muda mrefu. Alisema: “Ewe Mtukufu Mtume wa Uislamu! Wewe mwenyewe unatambua jinsi tunavyopita kwenye siku za huzuni na pigo kubwa ambalo limetia kwenye dini yako. Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Kwa kweli umelazimika kama matokeo ya shinikizo linaloongezeka wakati wote kutoka kwa utawala wa Ukhalifa niondoke kutoka kwenye jiji lako niende Syria.” 130


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Wakati wa mapambazuko wa usiku huo Bilal aliondoka kutoka Madina kuelekea Syria. Hatimaye baada ya kupita kwenye matatizo mbali mbali aliyokutana nayo njiani kati ya Madina na Dameski, Bilal alimaliza safari. Alipokaribia Dameski alisimama kwa muda mfupi na akalitazama jiji kwa mshangao na akajisemea mwenyewe: “Jiji gani hili lililo fifia na kuhuzunisha! Inaonyesha kama vile kifo kimetupa kivuli chake kila mahali. Ee Mola Mlezi! Nitawezaje kuishi hapo? Nimekuwa nikifikiria kwamba safari imefika mwisho wake na ninaweza kupumzika kwa muda mfupi, lakini sasa nahisi nimechoka zaidi na kuhuzunika zaidi. Ee Mola Mlezi! Nifanye nini?” “Inanibidi nikubaliane na hali yao na nibakie kuwa mvumilivu wakati nikiwa niko mbali na bwana wangu, Imam Ali na wafuasi wake waaminifu. Wakati ninavumilia usumbufu wote huu ninawezaje kuishi hapa kama zamani?” Bilal alielekea kwenye lango la jiji akiwa amekata tamaa na akachagua sehemu yake baada ya kupita hapa na pale. Bilal alifurahishwa na kuridhika kwa sababu aliweza kuhimili manyanyaso na nguvu za watu wenye uwezo na akasema ukweli. Alimshukuru Mwenyezi Mungu na akajivunia kuwepo kwake kwa kuona kwamba uhai wake ulikuwa hatari kwa watawala na waliogopa hata kimya chake. Bilal aliishi Dameski kwa muda fulani. Ingawa yeye mwenyewe alikuwa Dameski, lakini roho yake ilikuwa Madina. Kwa mfululizo alikuwa anafikiria ufumbuzi fulani wa tatizo. Hatimaye alishindwa kuendelea kuvumilia na aliamua kurudi Madina ili aione familia ya Mtukufu Mtume na Imamu wake mheshimiwa kwa mara nyingine. Pia alidhani kwamba hali ya 131

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

kisiasa ya serikali haingefikiria kurudi kwake kuwa na manufaa na ilikuwa inawezekana kwamba wangemrudisha. Hata hivyo, kwa kuwa alikwisha amua alijiambia mwenyewe: “Nitasafiri hata kama nitatoweka hapa duniani.” Bilal aliondoka Dameski akiwa na ujasiri mkubwa, hamasa na mwambatano maalum kwa familia ya Mtume. Njia ambayo ilionekana kuwa ndefu alipoanza safari aliimaliza haraka. Alifika karibu na Madina na aliona shani iliyotulia ya jiji. Aliona kuta za msikiti wa Mtukufu Mtume kutoka hatua kitambo na alikumbuka kumbukumbu za kufurahisha za matukio ya zamani. Alishusha pumzi na machozi yalianza kumtoka machoni mwake. Baada ya kufika humo jijini, haraka Bilal alizuru kaburi la Mtukufu Mtume. Wapelelezi pia walimwona Bilal na walitaka kumkamata. Hata hivyo, waliona haingefaa kufanya hivyo, lakini walitoa taarifa kwa mamlaka kuhusu kuwasili, kwa Bilal hapo jijini. Watawala waliogopa na upande mwingine habari hizi zilifika kwa Bibi Fatimah Zahra, binti mpendwa wa Mtukufu Mtume na wakati huo Bilal alipata taarifa kwamba hakuwa na afya njema. Taarifa hii ilimsikitisha sana na akaanza kuleta dhikri pembeni mwa kaburi la Mtume: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Baada yako, dunia imeingia giza na Uimamu umebadilishwa kuwa Ukhalifa na umeporwa na watu ambao hawafai kwa kazi hii.” “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Nimepata taarifa kwamba binti yako afya yake si nzuri.” “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Mrithi wako Ali anakaa nyumbani. Kwa njia ya kimya chake analinda utukufu wa 132


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Uislamu na umoja wa Waislamu.” “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Punde tu nimewasili kutoka safari yangu kutoka Syria. Nilihamishwa huko.” Halafu kwa sababu ya kuvurugikiwa sana na akili, Bilal alianguka chini na akazirai.

ADHANA YA MWISHO Baada ya kutawafu Mtukufu Mtume, binti yake ambaye alikuwa huyo mmoja tu Fatimah ambaye kwa mapenzi makubwa alihisi kuondokewa na baba yake mpendwa, pole pole aliugua. Na aliposikia kwamba Bilal amerudi Madina alionyesha nia ya kutaka kumsikia anaadhini Adhana kwa mara nyingine. Muda wa swala ya adhuhuri ilikaribia. Muadhini wa Mtukufu Mtume alikwenda kwenye paa la msikiti wa Mtukfu Mtume na aliaza kuadhini kwa sauti yake ya kupaza kama ilivyokuwa kawaida yake kipindi kilichopita. Alisema: “Allahu Akbar.” Waliposikia sauti ya Bilal, muadhini wa kwanza wa Mtukufu Mtume, watu wa Madina walitoka nyumbani mwao na kuelekea msikitini. Watu wote walishangaa kwa jinsi gani Bilal alikuwa anaadhini Adhan tena baada ya kutawafu Mtume (s.a.w.). Muda mfupi baadaye idadi kubwa zaidi ya watu ilikusanyika msikitini na Bilal aliendelea kuadhini Adhana. Bilal alipotamka ‘takbir’ kwa sauti kubwa na bibi Fatimah aliisikia akiwa nyumbani kwake alikumbushwa siku tukufu na za kupendeza zilizopita wakati wa uhai wa baba yake. Alishusha pumzi na kuanza kulia. Watoto wake pia walianza 133

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

kulia. Bilal aliposema’Ashhadu al la illalah’ Bibi Fatimah alilia kwa uchungu zaidi. Hata hivyo, Adhana ilipofikia sehemu nyeti alipoteza fahamu kwa sababu ya majonzi. Kwa hiyo, Bilal aliamriwa kuacha kuendelea kuadhini mara moja, kwa sababu uhai wa Bibi Fatimah Zahraa ulikuwa hatarini. Watu ambao walikusanyika karibu na msikiti na mitaani na barabarani, na kwenye macho yao hamasa ya pekee na ari ilikuwa inabiringika, ghafla walijitambua Bilal alipoacha kuadhini Adhana, na kustaajabu kwa nini ilitokea hivyo. Kama mambo yalivyo, Bilal aliadhini Adhana ya mwisho kwa yakini yake yote na imani yake kwa Mtukufu Mtume na kuupenda mfumo wa fikra yake. Bilal ambaye alikuwa hataki tena kuishi kwa sababu ya shinikizo la matatizo, alijitayarisha kutoa mchango wa kuelimisha na kuwataarifu watu kuhusu shughuli zake za kisiyasa. Aliwakusanya watu na kuwashawishi waanzishe harakati za kuwapinga watu wenye mamlaka serikalini kwa njia za mazungumzo na hotuba kali kwa namna ambayo walianza kusababisha upinzani na kutamka kaulimbiu kali zenye kupinga serikali na ilihofiwa kwamba wangesababisha machafuko. Mawakala wa serikali kwa hiyo walimiminika msikitini, walimkamata Bilal na kumhamisha kwenda Syria kwa mara nyingine tena. Baada ya uhamisho huu wa pili, Bilal hakuruhusiwa hata kuchukua ruhusa kutoka kwenye kaburi la Mtume kwa sababu maofisa walikuwa wanamfuatilia kila mahali na yeye mwenyewe alitambua hali hiyo vyema. Kwa hivyo, aligeuzia uso wake upande wa kaburi la Mtukufu Mtume na akauweka wazi moyo wake kwa muda mrefu kidogo baada ya kumsalimia. 134


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Bilal alifika Dameski na alikuwa na masikitiko sana kwa sababu ya hali iliyotengenezwa kwa ajili yake. Aliombea Uislamu na Waislamu mchana na usiku na alikuwa na huzuni sana alipoona maumivu yaliyochukuliwa na Mtukufu Mtume kwa miaka mingi, yalikuwa hatarini Kwa kweli Bilal alikuwa anaishi Dameski chini ya shinikizo zito sana kutoka serikalini. Watu walimuona mara chache sana na wakati wote aliishi peke yake. Mambo yalifika mahali ambapo alipata taabu sana kwa sababu ya kuishi peke yake.

WAKATI WA KUJITOA MHANGA Bilal alizaliwa namna hii na aliishi namna hii na hatimaye alipanda mimbari ya upendo. Ulikuwa mpao uliompeleka kwenye kilele cha juu zaidi cha utukufu na kujitoa mhanga. Sasa yupo kwenye dunia kuu yenye ukuu wa dunia! Marafiki zake wote walikuwa wanalia kwa sababu ya kujitoa mhanga. Alikuwa Bilal mtumwa mweusi aliandika historia na aliukunja mpango wa kikabaila wa kipindi cha ujahilia na akaanza kung’aa kama uso wa daima milele ambao utaonyesha kama mfano katika kumbukumbu za historia ya mwanadamu. Ni kweli kwamba Bilal yu hai. Amekuwa mfano bora wa uchaji Mungu na utakatifu. Watu walikuwa wanajaribu sana kutukuza na kuhudhuria mazishi yake. Wale wote waliokuwa wanashiriki katika ibada ya mazishi walikuwa wanalia kwa uchungu sana. Dameski kilikuwa mojawapo ya vituo muhimu vya ukabaila wa Umayyah na uwanja wa maonyesho wa Ukhalifa ulioporwa na warithi wasiohalali wa mapinduzi ya Kiislamu, hata hivyo, pamoja na ukatili na utawala wa dikteta wa Bani Umayyah, 135

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

idadi kubwa ya watu walihudhuria maziko. Kwenye miji mingine ya nchi za Kisilamu hususan Madina, watu walihuzunika na kusikitika sana. Waliomboleza kifo cha Bilal kwa muda mrefu. Bilal alikuwa moja wapo wa watu wachache waliotetea ukweli hadi dakika ya mwisho wa uhai wao. Alihubiri Uislamu wa kweli. Wala mateso ya aina mbali mbali hayakudhoofisha uamuzi wake imara ama kushawishiwa, ama kuhofishwa na vitisho, ama kutoa kiapo cha utii kwa mtu asiyestahili, ama autoe kafara Uislamu na ukweli kwa manufaa ya dunia, jina na utajiri. Baada ya kuishi maisha ya uhuru na kujitoa mhanga katika njia ya Uislamu, Bilal alifariki dunia katika hali ambayo hakuwa na rasilimali. Waislamu waliobora walimzika kwenye kiwanja cha makaburi kiitwacho ‘Saghir’ (kidogo) kilichoko Dameski60 na waliomboleza kifo chake kwa siku kadhaa. Kaburi la Bilal ni sehemu ya hija ya Waislamu na watu wapenda uhuru wa dunia nzima tangu wakati huo hadi sasa. Ni kaburi ambalo masomo ya uhuru, ukweli, uaminifu, kujitoa mhanga na uimara watu hujifunza na ambalo hutufundisha sisi vipi mtu anatakiwa aishi na afikiri dunia vipi. Wanahistoria wote wa Kiislamu, wa madhehebu yoyote, wanapowataja masahaba wa madhehebu yoyote yale, wanapowataja masahaba wa karibu na waumini wa kiongozi mkuu wa Uislamu, wametaja Bilal kuwa mmoja wao na wamemweka kwenye kundi la wale waliokuwa karibu naye. Kwa hiyo, imeonekana kwamba kwa sababu ya Uislamu na 60

Usudul Ghabah, Juz. I, uk. 209; Majalisul Muminn Juz. I, uk. 268; Nafusus rahman.Sura ya. 10; Jame’ur Ruwat Juz. I, uk. 131; Al-Isabah, uk. 169; Muntahul Amal, uk. 87. 136


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

utekelezaji wa amri zake na mafundisho ya maana, Bilal ambaye alikuwa mtumwa kabla ya kuja kwa Uislamu, alipata daraja ambalo alitegemewa kwamba alikuwa mmojawapo wa masahaba ambao walikuwa waaminifu sana, waliojitolea sana na waliokuwa karibu sana na Mtukufu Mtume (s.a.w.). Muda ambapo Bilal alikuwa hai alijaribu kuuendeleza Uislamu na alijitolea kwa uaminifu kwa familia ya Mtukufu Mtume hadi dakika ya mwisho ya uhai wake. Waandishi wengine wamesema kwamba Bilal alifia huko Alepo na alizikwa huko Babul Arba’in. kwa kawaida inasemekana kwamba alifariki dunia huko Syria kwa ugonjwa wa tawni na akazikwa Babu Saghir. Marehemu Sheikh Abbas Qummi ameandika alitembelea kaburi la Bilal huko Dameski.

kwamba

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

wa Uislamu na tunatamani kwamba mnamo siku ya Hukumu tuwe karibu na wewe na tuwe tayari kwa uombezi wako ambao kwa hakika utakubaliwa na Mwenyezi Mungu Mweza wa Yote. Amina!

SEHEMU YA PILI UTANGULIZI Hata kama Afrika haikuleta hata Muisilamu mmoja tangu mwanzo wa Uislamu hadi leo, bado hatungeweza kuacha kujali huduma kubwa iliyotolewa na Waafrika kwa Uislamu ambapo waliwapatia bila kinyongo hifadhi Waislamu ambao walihamishwa nyumbani kwao Arabuni.

Salamu, Ewe Bilal, ewe mtoto wa Rabah . . . . Ni kwa namna bora ilioje na imani uliutangaza kwa uamninifu Uislamu na ulihatarisha maisha yako kwa kujitolea hivyo katika njia hii! Salam kwako ewe muadhini wa Mtukufu Mtume! Salamu kwako ewe muadhini wa Adhana ya kwanza! Kama ungekuwa hai sasa kuona kwamba baada ya kupita karne nyingi hayo maneno matakatifu yaliyotamkwa kwa mara ya kwanza Madina kwa sauti yako ya kusisimua sasa yanatangazwa duniani pote kila siku kutoka kwenye minara ya mamilioni ya misikiti na huwakusanya Waislamu humo kwa ajili ya swala zao za faradhi kila siku.

Wana wa Kiislamu hao walikuwa katika hali ya kukata tama kabisa. Maisha yao yalitishiwa kwa kuteswa kikatili na Maquraishi. Ilikuwa ni wakati huu wa kuogofya ambapo Bilal na Waislamu wengine walipambana na kila aina ya dhiki. Zaidi ya hayo, Mtume Muhammad (s.a.w.) alitupwa katikaki ya tatizo lote. Alikuwa lengo la njama nyingi dhidi ya uhai wake na maadui wake waliomtupia mawe na takataka. Walikuwa tayari kumuuwa wakati wowote kama wangeweza kupata nafasi hiyo. Lakini ilikuwa kwa sababu ya mfano unaong’ara na ujasiri mkubwa wa Abu Talib, ami wake Mtukufu Mtume na baba yake Imamu Ali, kwamba hawakuthubutu kutekeleza matakwa yao ya kumuuwa kwa vitendo. Ulinzi ambao Abu Talib alimpa Mtukufu Mtume uliwazuia Maquraishi wasimdhuru Mtume.

Salamu kwako ewe Bilal! Kwa wito wa Adhana takatifu inayokuwa mfano wa jina lako kwenye macho yetu wote, kujitoa kwako na kazi uliyoifurahia mbele ya Mtukufu Mtume

Wakati huu wa mateso ambayo yalikuwa hayavumiliki, nchi moja tu iliyokuwepo ya kuwapa hifadhi Waislamu nayo ilikuwa Afrika. Nia kubwa kwa kweli ilikuwa Waafrika ndio waliokuwa

137

138


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

wa kwanza kuvumilia mateso. Watu wa kwanza kufia dini ya Uislamu ni Sumayyah na mume wake Yasir, (angalia: Ammar Yasir, Islamic Seminary Publication) ambao walichagua kufa kuliko kukufuru. Ilianza hapo ambapo Mtume Muhammad alihubiri Uislamu na akapata wafuasi Makkah. Washirikina wa Maquraishi hawakufurahishwa na jambo hilo. Kwanza walijaribu kumshawishi Mtukufu Mtume asiendelee na tabligh yake. Baadaye walijaribu kumtishia. Lakini, hakukubali bila woga, alisema: “Siwezi kuacha hata kama wangeweza kuweka jua kwenye mkono wangu mmoja na halafu mwezi waweke mkono mwingine, kwa sababu ninayohubiri ni dini ya kweli.” Kwa hiyo aliporidhika na ujasiri na uamuzi wake, ulio thabiti, walianza kuwatesa Waislamu, kwani wangefanya kidogo sana kumdhuru Mtukufu Mtume mwenyewe kwa sababu ya ulinzi aliopewa na ami wake Abu Talib. Mateso yao yalikuwa makali sana na yalitofautiana na baadhi ya masahaba wa Mtukufu Mtume waliuawa.

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

kutoka kabila la Maquraishi na 7 kutoka makabila mengine. Walikuwa kama kundi la kwanza la wahamiaji, walipewa hifadhi na ulinzi na Najash- Mfalme wa Ethiopia. Washirikina walipeleka ujumbe Ethiopia kwa lengo la kumshawishi mfalme wa Ethiopia awafukuze Waislamu wakimbizi kutoka kwenye nchi yake, lakini mfalme alikataa na aliendelea kuwahifadhi na kuwalinda, kwa hiyo akajipatia nafasi ya pekee kwa Afrika katika kipindi hiki cha historia ya Uislamu. Zaidi ya haya, Afrika inayo heshima ya kumhesabu Ummu Ayman kama binti wa Kiafrika. Alikuwa yaya wa Mtukufu Mtume wakati akiwa mtoto mchanga na alimbembeleza. Mtukufu Mtume alikuwa na tabia ya kumwita ‘mama’. Sifa nyingine ambayo inakwenda Afrika tu ni kwamba baada ya Khadija kama kuna mwanamke yeyote alizaa mtoto na mtukufu Mtume ni mwanamke wa Kiafrika aliyeitwa Mariya Qibtiyya.

Sasa, ilipoonekana mateso yaliyokuwa yanaongezeka hayangedhibitiwa na kuvumiliwa Mtukufu Mtume aliwaeleza Waislamu kuondoka Makkah na kuhamia Habash (leo hii Ethiopia). Kwa hiyo kundi la kwanza la Waislamu, weakiwemo wanaume 11 na wanawake 14, waliweza kupanda meli kwenda Ethiopia, ambako Waafrika waliwapa hifadhi na kuwakirimu.

Zaidi ya hapo, ni Afrika ndio yenye heshima ya kudai kwamba Bilal akiwa muadhini na mtunza hazina wa mtukufu Mtume. Afrika pia inajivunia haki yake ya kumtukuza sana Asmaha, mfano bora wa mfalme Habasha, ambaye alikuwa wa kwanza miongoni mwa wafalme wa dunia kukubali ukweli wa Uislamu na mafundisho ya Mtume Muhanmmad (s.a.w.).

Washirikina wa Makkah walipotambua kuhusu mpango wa kuhamia walianza kuwashambulia upya Waislamu waliobaki Makkah. Mtukufu Mtume akamwelekeza Jafar bin Abu Talib, kaka yake Ali, kuhamia Ethiopia. Yeye pia alifika Ethiopia na kundi la Waislamu 103, kati yao wanaume 85 na wanawake 11

Haya ndio mambo yanayoongeza ufahari wa historia ya Afrika; ufahari ambao sehemu zingine za dunia zinakosa.

139

Tumejaribu kuonyesha mambo yanayojulikana kuhusu maisha ya hawa Waislamu Waafrika wakati wa mwanzo wa historia ya Kiislamu. Tunayo nia ya kutambulisha historia fupi ya 140


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Waislamu hao ambao walikubali kuwa Waislamu wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume, ambao kwa namna moja au nyingine walikua na uhusiano na Afrika, na ambao maisha yao yataonyesha ukweli wa ujumbe wa Uislamu duniani. Muhtasari ya maisha yao imepangwa kwa mfuatano wa jinsi walivyoingia kwenye Uislamu, lakini wako ambao miaka yao ya kukubali Uislamu haijulikani habari zao zimeandikwa mwishoni mwa kitabu.

mnamo mwaka wa 10 wa Hijiria, Ibrahim alifariki dunia akiwa na umri wa miezi 18.

Waafrika wengi ambao walikuwa ni Waislamu walikuwa wamepata nguvu na utakaso wa kiroho hivyo kwamba wasifu wao utawatia moyo Waisilmau wote wafuate nyayo zao, kwa Neema za Mwenyezi Mungu.

ASMAHA NAJJASHI –MFALME WA ETHIOPIA

Wachapishaji.

IBRAHIM BIN MUHAMMAD Mnamo mwaka wa 8 wa Hijiriya, Ibrahim, mtoto wa Mtukufu Mtume alizaliwa na Mariya Qibtiyya. Mama yake alikuwa mtu wa Misri na alikuwa (mkristo mzalendo wa Misri) wa madhehebu ya Copt (mtu wa asili ya Misri) kabla hajaingia kwenye Uislamu na kuolewa na Mtukufu Mtume wa Uislamu.

Mtukufu Mtume aliathiriwa na huzuni kubwa na masikitiko kutokana na kifo cha Ibrahim. Kwenye maziko yake, Mtume alisema: “Macho yangu yamelowa na moyo wangu umejaa huzuni, lakini nitasema yale yatakayo mfurahisha Mwenyezi Mungu tu . . . Ewe Ibrahim! Ninahuzunishwa na kifo chako!

Mateso yalipofika kilele cha juu sana Mtukufu Mtume aliwaashauri baadhi ya wafuasi waondoke waende Abysinia. Mnamo mwaka wa tano wa mahubiri yake, wanaume 11 na wanawake 14 waliondoka Makkah kwenda Abyasinia (sasa Ethiopia) na waliishi maisha ya amani huko chini ya hifadhi ya mfalme Asmaha, (jina halisi la mfalme huyo lilikuwa Asmaha na cheo chake Najjash ambacho kwa kiingereza mara nyingi huandikwa ‘Negus’)

Ibrahim alifanana na Mtukufu Mtume sana na Mtume alimpenda sana. Alikuwa na kawaida ya kumbeba mabegani mwake na akipita anamwonyesha kwa wake zake wengine kwa fahari kubwa.

Baada ya muda walirudi Makkah. Lakini waliporudi; washirikina wa Makkah waliongeza mateso na waliwatesa watu walioingia kwenye Uislamu siku hizo za karibuni. Mtukufu Mtume aliwashauri wahamie Ethiopia wapate hifadhi huko kwa mara nyingine. Kundi la wanaume 85 na wanawake 11 kutoka kabila la Maquraishi na watu 7 kutoka makabila mengine walikwenda Ethiopia na kupata hifadhi huko na wakaishi maisha ya amani na salama.

Mama yake Ibrahim alikuwa na afya isiyoridhisha kwa hiyo hangeweza kumnyonyesha mtoto wake. Kwa hiyo, Mtukufu Mtume alinunua kondoo ambaye maziwa yake alinyonyeshwa Ibrahim. Pamoja na hayo, mtoto hakuishi muda mrefu na

Washirikina wa Makkah walipopata taarifa hii, waliwatuma wawakilishi wawili,’Amr bin Al-As na Amara bin Walid wakiwa na zawadi za kumpa Mfalme na ombi kwamba Waislamu warudishwe Makkah.

141

142


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Walipopata ruhusa ya kumuona mfalme, walimpatia zawadi na walimwambia awarudishe Waislamu kwani walidai kwamba ni watu wenye kusababisha ghasia. Mfalme huyo aliwajibu kwamba hangefanya hivyo hadi hapo upelelezi kamili ungefanywa na yeye mwenyewe. Kwa hiyo, mfalme alimwita Jaafar bin Abu Talib, kaka (ndugu) yake na Imamu Ali, ambaye alikuwa kiongizi wa wakimbizi, aende barazani kwake na alimuuliza aeleze kuhusu imani yao mpya. Jaafar alitoa hotuba ndefu akielezea walikuwa katika hali gani kabla ya kukubali Uislamu na Uislamu umewafundisha nini. Halafu akakariri Surah Maryam ya Qur’an Tukufu ambayo inayo Aya zifuatazo kuhusu kuzaliwa kwa Mtume Isa (yesu): Na mtaje Mariamu katika Kitabu, pale alipo jitenga na jamaa zake mahali upande wa mashariki; na akaweka pazia kujikinga nao. Tukampelekea Roho wetu, akajifananisha kwake sawa na mtu. (Mariamu) akasema: Hakika mimi najikinga kwa Mwingi wa Rehema aniepushe nawe, ukiwa ni mchamungu. (Malaika) akasema: Hakika mimi ni mwenye kutumwa na Mola wako ili nikubashirie tunu ya mwana aliye takasika. Akasema nitampataje mwana hali mwanadamu yeyote hajanigusa, wala mimi si kahaba? (Malaika) akasema: Ndio hivyo hivyo! Mola wako amesema: Haya ni mepesi kwangu! Na ili tumfanye kuwa Ishara kwa watu, na Rehema itokayo kwetu, na hilo ni jambo lilio kwisha hukumiwa. Basi akachukua mimba yake, na akaondoka nayo mpaka mahali pa mbali. Kisha uchungu ukampeleka kwenye shina la mtende; Akasema: Laiti ningelikufa kabla ya haya, na nikawa niliye sahaulika kabisa! Pakatangazwa kutoka chini yake: Usihuzunike! Hakika Mola wako amejaalia chini kijito kidogo cha maji! Na litikise kwako hilo shina la 143

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

mtende, utakuangushia tende nzuri zilizo mbivu. Basi kula, na kunywa, na litue jicho lako. Na pindi ukimuona mtu yeyote basi sema: Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu ya kufunga; kwa hiyo leo sitasema na mtu. akaenda naye (mwanawe) kwa jamaa zake amembeba. Wakasema: Ewe Mariamu! Hakika umeleta kitu cha ajabu! Ewe dada yake Harun! Baba yako hakuwa mtu muovu, wala mama yako hakuwa kahaba. Akawaashiria (mtoto). Wakasema: Vipi tumsemeze aliye mdogo yumo katika susu? (Mtoto) akasema: Hakika mimi ni mja wa Mwenyezi Mungu. Amenipa Kitabu, na amenifanya Nabii. Na amenijaalia ni mwenye kubarikiwa popote pale niwapo. Na ameniusia Sala na Zaka maadamu ni hai. Na nimtendee wema mama yangu. Wala hakunifanya niwe jeuri, muovu. Na amani iko juu yangu siku niliyozaliwa, na siku nitakayo kufa, na siku nitakayo fufuliwa kuwa hai. Huyo ndiye Isa mwana wa Mariamu. Ndiyo kauli ya Haki ambayo wanaifanyia shaka. (19:16- 34). Aliposikia hotuba ya Ja’far na hizi Aya za Mungu zilizomo kwenye Qur’an Tukufu kutoka kwenye Sura iitwayo ‘Maryam,’ Mfalme alishtuka na alisema: “kwa jina na Mungu Mkuu, ukweli ni kwamba uamuzi huu na yale yaliyofunuliwa kwa Musa na Isa yametoka kwenye chanzo kimoja.” Halafu, aliwageukia wale wawakilishi wawili wa washirikina, alisema: “Ninaapa kwamba kamwe sitawarudisha watu hawa kwenu na nitawasaidia kadiri ya uwezo wangu.” Wawakilishi hao wa washirikina walimwambia Mfalme Najjashi kwamba Waislamu walimfikiria Isa (Yesu) Mjumbe wa Mungu na si Mungu mwenyewe kama inavyo aminiwa na Wakristo. 144


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Kiongozi wa wakimbizi wa Waislamu, Jaffar bin Abu Talib, alijibu kwamba Waislamu wanaamini kwamba Isa ni mja wa Mwenyezi Mungu na Mjumbe wake. Mfalme Najjashi alivutiwa na hoja iliyowasilishwa na Ja’far na baada ya hotuba ya Ja’far alisema: “Ipo tofauti ndogo baina ya mambo ninayojua kuhusu Kristo na yale ambayo yameelezwa na ninyi Waislamu.

Aymah

“Rehma iwe juu yenu pamoja na mtu aliyewatuma, nina shuhudia ukweli kwamba Muhammad (s.a.w.) ni mjumbe wa Mungu.”

Nafe

Halafu aliwageukia washirikina na akawarudishia zawadi walizompa na akawaaga na kuwaamuru waondoke nchini humo. Waliondoka wakiwa wamekasirika na walikwenda Arabuni bila wakimbizi, ambapo jaafar na wakimbizi wenzake waliendelea kuishi Abyssinia kwa amani. Baada ya kutambua ukweli wa Waislamu kwa mujibu wa mahubiri ya Jaffar bin Abi Talib, Mfalme alikubali kuwa Mwislamu na matokeo yake Wakristo kadhaa katika himaya yake waliingia kwenye Uislamu pia. Watu arobaini katika hao waliosilimu waliomba ruhusa kutoka kwa Mfalme watembee Arabuni ili wakutane na Mtukufu Mtume wa Uislamu. Mfalme aliwaruhusu na aliwapa zawadi za nguo na watumwa wanawake kwa ajili ya Mtukufu Mtume. Viongozi wa kundi hili wametajwa katika historia kama: Abraha Idrisa

Bilal Wa Afrika

Buhaira Taman Tameem na

Aya ya Qur’an Tukufu ifuatayo inazungumza habari za watu hawa: (28:52). Walifika Madina ambako walikutana na Mtukufu Mtume na hatimaye walishiriki katika Vita ya Uhud. Mfalme Najjashi mwenyewe alifariki dunia akiwa Muisilamu katika himaya yake kabla ya Makkah kutekwa na Mtume mnamo mwaka wa 8 Hijiria. Mtukufu Mtume alisali Salatul Mayyit (Swala ya kusalia Maiti) kwa ajili yake.61

AYMAN BIN UBAID –SHAHIDI WA HUNAIN Ayman alikuwa mtoto wa kiume wa Ummme Ayman mtumwa mwanamke wa mtukufu Mtume, na alikuwa ni kaka yake Usammah bin Zaid kwa upande wa mama yake. Wakati wa kipindi cha Ujahiliya Ubaid bin Amarah alimuoa Umme Ayman wa Ethiopia na alihamia Madina kutoka Makkah akiwa na mumewe. Alimzaa Zaidi alipokuwa Madina. Mume wake alipofariki dunia, alirudi Makkah. Ayman alikuwa Muislamu imara ambaye aliyatoa maisha yake

Ashraf

61

145

Tarikh -e- Baghdad, Juz. I, cha Khatib Baghdad. 146


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

kwa ajili ya Uislamu wakati anapigana kwenye vita ya Hunain.

YASIR – SHAHIDI WA KHAIBAR

Wakati ambapo Waislamu wengi walishikwa na hofu katika Vita ya Hunain na walikimbia na kuondoka kwenye uwanja wa mapigano, Ayman bin Ubaid alikuwa mmojawapo wa watu wanane waliobaki pamoja na Imamu Ali na Abbas, ami wa Mtukufu Mtume, kuendeleza mapigano na Mtume. Aliuawa, akawa shahidi aliyekufa kwa kupigania Uislamu.

Yasri alikuwa mtumwa wa Myahudi aliyeitwa Kamir na aliishi Khaibar. Alikuwa mchungaji wa kondoo wa bwana wake. Wakati jeshi la Waislamu lilipozunguka baadhi ya ngome za Khaibar, Yasir alimwendea Mtume na alimuuliza amweleze kuhusu Uislamu. Mtukufu Mtume alimuelimisha kuhusu Uislamu na akakubali kuwa Muisilamu.

Hata hivyo, Waislamu walishinda vita hii na baada ya kwisha vita Abbas bin Abdul Muttalib, mmmojawapo wa ami zake Mtukufu Mtume, alitunga beti za shairi katika kusifu ujasiri na uimara ulioonyeshwa na Ayman bin Ubaid na akimpa heshima ya kufa kwake shahidi .62

Yasir baada ya kuwa Muislamu, aliungana na jeshi la Waislamu lakini alikuwa na wasi wasi kuhusu kazi yake ya kuchunga kondoo wa bwana wake. Kwa hiyo, alimuuliza Mtume, “Nitafanya nini na hawa kondoo ambao mwenyewe amenikabidhi mimi na chini ya uangalizi wangu?” Mtukufu Mtume akamjibu: “Zielekeze nyuso zao kuelekea nyumba ya bwana wao na kabla ya muda mrefu watakwenda huko.”

Ayman bin Ubaid alikuwa mfugaji wa Kondoo na pia alikuwa akiwatunza mbuzi wanane wa maziwa wa Mtukufu Mtume.

MAHJA- MUADILIFU SANA Mahja alikuwa mmojawapo wa watumwa wa Mtukufu Mtume. Alikuwa mmojwapo wa waadilifu sana. Mmojawapo wa masahaba wa Mtume alisema kwamba miongoni mwa Waislamu wa kutoka Afrika Mahja, Luqman na Bilal walikuwa waadilifu sana.*

LUQMAN – MTUMWA MUADILIFU Luqman alikuwa mmojawapo wa watumwa watatu wa Mtume. Alifikiriwa kuwa mmojawapo wa watu waadilifu sana. 62 *

Al-Istiab cha Abdul Bir Al- Istiab cha Ibn Hajar Al-Asqalani 147

Kwa hiyo, Yasir alichukua mchanga uliojaa kiganja chake na akautupa kwenye nyuso za kondoo hao huku anasema: “Rudini nyote kwa bwana wenu. Kwa jina la Mwenyezi Mungu sitarudi nanyi!” Baada ya tukio hili kondoo wote walirudi kwenye ngome bila mchungaji. Ilikuwa kama vile mchungaji asiyeonekana kwa macho alikuwa anawaongoza. Halafu Yasir alijiunga na jeshi la Waislamu na akafa shahidi wakati anapigana. Alipigwa na jiwe kubwa ambalo lilitupwa kutoka kwenye mojawapo ya ngome ambazo zilizungukwa na Waislamu. Mtukufu Mtume alikwenda haraka kwenye maiti hiyo iliyo takasika na alimvesha sanda yeye mwenyewe na kufanya ibada ya mazishi. Hapo makaburini Mtukufu Mtume (s.a.w.w) alisema: “Yeye sasa anao hao wanawake wa peponi kama wake zake.”

148


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Kwa hiyo Uislamu ulimpa heshima na mara tatu, alikuwa mtu wa muujiza, alikufa shahidi na aliwapokea wanawake wa peponi ili wamtunze huko peponi.63

YASIR- MSWALIHINA. Yasir huyu alikuwa mojawapo wa watumwa wa Mtukufu Mtume. Alikuwa anawatunza ngamia wa maziwa kumi wa Mtume. Kujinyima kwake starehe za dunia, uchaji Mungu wake na kuambatana sana na Swala ni mambo ambayo yalimpendeza sana Mtukufu Mtume hivyo kwamba alimwacha huru. Alikwenda kuishi sehemu iiitwayo Hira, ambako pamoja na kuwa huru, aliendelea kuwachunga ngamia wa Mtume ambao walikuwa huko naye.

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

paitwapo Quba, ambapo hatimaye alizikwa hapo.64

MABUR AL- HAHI Mabur alikuwa ni Mkibti. Na alipelekwa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.) na akiwa pamoja na Mariya Qibtiyya na Mfalme wa Misri. Alikubali kuwa Muisilamu wakati wa uhai wa Mtume. Kwa mujibu wa taarifa fulani, alikuwa mmojawapo wa binamu wa Mariya Qibtiyya.65

MAHIR Mahir naye alikuwa Mkibti. Na alitumwa kwa Mtukufu Mtume na Mfalme wa Misiri.66 Baadaye alikubali kuwa Muisilamu lakini hakuna maelezo zaidi kuhusu mtu huyu.

ABU RAFI IBRAHIM QIBTY

Watu fulani kutoka kabila la Umayyah walikwenda kwa Mtume na wakaingia kwenye Uislamu. Watu hao wote walikuwa wanayo shida ya kwashakoo na matumbo yalikuwa yamevimba.

Abu Rafi Ibrahim alikuwa Mkibti. Na mtumwa wa Abbas bin Muttalib, mmojawapo wa ami zake Mtume (s.a.w.).

Mtume aliwaambia waende kwa Yasir hapo walikunywa maziwa ya ngamia na baada ya muda, matumbo yao yalirudi katika hali yao ya kawaida.

Pia alijulikana kama Aslam. Abbas alimtambulisha kwa Mtukufu Mtume ambaye alimpa uhuru alipompa taarifa ya kufurahisha ya Abbas kuingia kwenye Uislamu.

Ni jambo la kusikitisha kiasi gani! Watu hawa, baada ya kupona na kuwa na afya njema, waliingiza vyuma vidogo kwenye macho ya Yasir na walimuua. Baada ya mauaji yake, mwili wa Yasir ulipelekwa kwa Mtukufu Mtume, mahali

Abu Rafe alikuwa mmojawapo wa wakimbizi walioondoka Makkah na kwenda kutafuta hifadhi Madina. Alishiriki kwenye vita vya Uhud na Khandaq na alikuwa mfawidhi wa

64 65 63

Usudul Ghabah, Juz. v, cha Ibn -e-Athir al-Jaziri; astiab; Isabah 149

66

Usudul Ghabar, vol. 2 Usudul Ghabar, Juz. iv. Isabah, Juz. i. 150


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

chakula cha Mtume. Mtume alimwambia: “Ewe Abu Rafi utaendeleaje ambapo watu wengi watapigana na Ali bila kujali kwamba Ali (mrithi halali wa Mtukufu Mtume) atakuwa upande wa haki na wao upande wa dhuluma na watu watawajibika kuanzisha vita Vitakatifu dhidi yao, na mtu ambaye atakuwa hana uwezo wa kupigana kwa maneno yake na endapo atashindwa kupigana hata kwa maneno yake, atapaswa aumie moyoni mwake kuwachukia ili asilaumiwe?� Abu Rafi alimwomba Mtume amwombee ili aishi na apate fursa ya kuona tukio hilo, Mwenyezi Mungu angemsaidia kumpa nguvu na apigane nao. Abu Rafe anasimulia kwamba watu walipotoa kiapo cha utii kwa Imamu Ali, na Muawiyah (Gavana wa Syria) alianza kukusanya kundi lake la kumpinga Imamu Ali, aliyakinisha katika akili yake kwamba hawa ndio watu ambao Mtukufu Mtume aliwasisitizia waanzishe Vita takatifu dhidi yao. Kwa hiyo Abu Rafi haraka sana aliuza viunga vyake vya Khaibar, na pamoja na familiya yake alikwenda kuishi na Imamu Ali na aliendelea kuwa naye hadi Imamu Ali alipokufa shahidi. Halafu alirudi Madina na Imamu Hussein.67 Alikuwepo wakati wa ushindi wa Waislamu Misiri.

USAMA BIN ZAIDI BIN HARITHA- KAMANDA Usama bin Zaid bin Haritha alikuwa mtoto wa Umm Ayman ambaye aliwahi kumpakata Mtukufu Mtume mikononi mwake wakati angali mchanga.

Bilal Wa Afrika

alimteua Usama ambaye wakati huo alikuwa na umri wa miaka ishirini, kuwa kamanda wa jeshi la Waislamu lipigane vita na Warumi wa Syria ambao walimuua baba yake Usama. Hata hivyo, jeshi halikuondoka Madina kwa sababu ya maradhi ya Mtume. Mtume alitawafu kabla ya jeshi halijaanza kazi. Abu Bakr alilituma jeshi hili baada ya kutawafu Mtukufu Mtume.68 Kwa sababu ya umri wake mdogo, Usamah alikuwa hashawishiki na aliungana na wapinzani wa Imamu Ali. Walimlaghai kwa kumpa heshima kubwa ya kinafiki. Hata hivyo, baadaye alitambua kosa lake na akatubu. Mnamo mwaka wa 35 A.H alikula kiapo cha utii kwa Imamu Ali alipoteuliwa kuwa Khalifa na Umma wa Kiislamu. Lakini hakushiriki kwenye vita alivyopigana Imamu Ali. Katika maisha yake ya baadaye, alijuta kuhusu jambo hili na alitubu kwa kutoshiriki kuwa upande wa Imamu Ali.69 Wakati fulani aliugua sana na Imamu Hussein (mtoto wa Imamu Ali) alikwenda kumuona. Imamu Hussein alimkuta amefadhaika sana. Imamu Hussein alimuuliza kwanini alikuwa katika hali hiyo, ambayo Usama alimjibu kwamba alikuwa na deni la vipande vya fedha (dirham) elfu sitini na alikuwa na wasiwasi kwamba angekufa kabla deni hilo halijalipwa. Imamu Hussein alimwahidi kwamba angelipa deni hilo kabla ya kifo chake Imamu alitimiza ahadi yake.70

68

Mwishoni mwa maisha yake, alipokuwa anaugua, Mtume

69

67

70

Arjahul Matalib cha Ubaidullah Amratsari Hindi. 151

Bilal Wa Afrika

Al-Isabah Juz. I, uk. 31. Manaqib -e- Ali Abi Talib, Juz. iii, uk. 221. cha Allama Rashiduddin Ibn-e-Shahr -a-Shob. Tangihul Maqal, Juz. I, uk. 169 cha Allama Shaikh Ma Mqani. 152


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Imamu Muhammad Biqir, Imamu wa tano wa Waislamu wafuasi wa dhehebu la Shia, alisema kwamba “Usama bin Zaid alitubu kwa hiyo napenda akumbukwe kwa maneno mazuri .”71 Alifariki dunia mwaka wa 54 A.H.

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Alihifadhi moyoni hadithi nyingi sana. Aliandika vitabu vingi sana kuhusu vipengele vingi vya sheria za Kiislamu kama vile Swala na wudhu.74

WATOTO WA FIZZAH UBAIDULLAH IBN ABU RAFI –MWANDISHI Ubaidullah alikuwa mmojawapo wa watoto wa kiume wa Abu Rafi Ibrahim Qibty na alikuwa mmojawapo wa masahaba wa Mtukufu Mtume. Aliteuliwa kuwa mwandishi rasmi na Imamu Ali wakati alipokuwa Khalifa.72 Ubaidullah anahesabika kuwa miongoni mwa waandishi wa mwanzo kabisa wa Waislamu. Aliandika vitabu kadha, mojawapo ya vitabu hivyo ni Hukumu za Imamu Ali.73 Ni sifa kubwa kwa Ubaidullah kwamba alianza kuandika vitabu ambapo hakuna Muisilamu aliyekuwa na tahadhari ya ulazima huo. Pia ni Muhadithi (msimuliaji wa hadithi) na baadhi ya hadithi za Mtukufu Mtume zimeandikwa naye kwenye maandishi ya Kiislamu. Alikuwa na mtoto wa kiume aliyeitwa Awn ambaye alikuwa miongoni mwa watu wenye akili sana Madina.

ALI IBN ABU RAFI Ingawa hakuhesabika kuwa miongoni mwa masahaba wa Mtukufu Mtume, Ali Ibn Rafi alizaliwa wakati wa uhai wa Mtume. Alikuwa mfuasi wa Imamu Ali na mmojawapo wa waandishi rasmi.

71 72 73

Tanqihul Mqal, Juz.i. Tanqihul Maqal, Juz. ii, uk. 237. Tanqihul Maqal, Juz. ii, uk. 237.

Daudi, Muhammad, Mussa na Yahya wanatajwa katika wasifu wa Bibi Fizzah (Mwishoni mwa kitabu hiki) kwamba ni watoto wake, lakini hakuna, maelezo zaidi yajulikanayo kuwahusu wao.

ABU NAISAR –SAHABA WA IMAMU ALI Abu Naisar alikuwa mmojawapo wa ukoo wa Najjash, mfalme wa Ethiopia. Wakati akiwa na umri mdogo alivutiwa na Uislamu na alisilimu na alikwenda kumuona Mtukufu Mtume. Aliishi na Mtume ambaye alimlea, na baada ya kutawafu Mtume, alikwenda kuishi na Bibi Fatima binti yake Mtukufu Mtume. Aliungana na Imamu Hussein kwenye vita ya Karbala na akafa shahidi. Amezikwa na mashahidi wengine wa Karbala (Iraq) karibu na kaburi la Imamu Husein. Kila mwaka wakati wa kwanza wa kalenda ya Kiislamu, mamia ya maelfu ya Waislamu wa madhehebu ya Shia hutembelea makaburi hayo ya mashahidi kutoa heshima zao.75

74 75

153

Tanqihul Maqal, Juz. ii, uk. 263. Tarjuma ya Absorul Ain. 154


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

NASIR IBN ABU NAISAR Nasir alikuwa mtoto wa Abu Naisar ambaye maelezo yake yametolewa kwenye ukurasa uliopita. Aliungana na kundi lililokuwa linasafiri na Imamu Husein kutoka Madina na alikuwa naye hadi alipofika Karbala. Vita ilipoanza hapo Karbala, alikuwa mmojawapo wa watetezi wa kwanza wa kweli na kufa shahidi kwenye pambano la kwanza. Miguu yake ilikatwa alipokuwa anapanda farasi. Alizikwa karibu na kaburi la baba yake miongini mwa mashahidi wengine wa Karbala.76

JAUN BIN HUWI- MTUMWA WA ABUDHAR Jaun bin Huwi alikuwa mtumwa wa Abu Dharr ambaye historia ya maisha yake inaonyesha mafunzo ya Abu Dharr. Kwa mujibu wa Ma Maqani, nasaba ya Jaun ni kama ifuatayo: Jaun bin Huwi bin Qatadah bin Awar bin Saidah bin Awf bin Kab bin Huwi Habashi.77 Imerekodiwa kwenye historia ya Uislamu kwamba asili yake alikuwa Mwafrika na alikuwa anamilikiwa na Fazl bin Abbas bin Abdul Muttalib, ambako Ali alimnunua kwa vipande vya dhahabu 150 na akampa Abu Dharr kama zawadi. Kwa hali hii Imamu Ali alitaka Jaun kumhudumia Abu Dharr. Kwa hiyo, Jaun alitoa huduma bora sana kwa Abudhar ambaye alifurahishwa sana naye. Jaun alimuhudumia Abu Dharr na 76 77

Tarjuma of Absarul Ain. Tanqihul Maqal, J. l. i. 155

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

alipata manufaa ya kuwa naye. Alichunguza kila kipengele cha tabia ya Abu Dharr kwa uangalifu sana na akapendezewa nayo sana. Kama mambo yalivyo, Jaun hakubakisha kitu katika kumhudumia Abu Dharr. Pia hakuna sehemu ambapo alikosa heshima ya kuwa karibu na Abu Dharr isipokuwa huko Rabzar ambako hakuna kitabu cha historia kinachoaminika chenye kuonyesha kuwepo kwake sehemu hiyo. Pamoja na hayo, Jaun alimhudumia Abu Dharr vizuri kuondoka kwenda Rabzah, yeye alibaki na aliendelea kumhudumia Imamu Ali. Baada ya kifo cha Imamu Ali, aliendelea kumhudumia mwanae Imamu Hassan na Imamu Hasan alipokufa shahidi mnamo mwaka wa 50 A.H, aliendelea kumhudumia kaka yake Imamu Husein. Kwa ufupi, alitoa huduma kwa uaminifu kwa watu waadilifu sana katika maisha yake yote. Imamu Husein alipoondoka kwenye mji wa nyumbani kwake kwanza alikwenda Makkah na halafu Karbala wakati wa Rajab mnamo mwaka wa 60 A.H Jaun pia alikuwa naye wakati wa safari hii. Allamah Majlisi na Allamah Samawi wameandika kwa ruhusa ya mamlaka ya Sayyid Razi Daudi kwamba mapigano yalipoanza Karbala mnamo terehe 10 ya mwezi wa Muharam mwaka wa 61. A.H. Jaun alikwenda kwa Imamu Husein na akamwomba yeye apigane. Imamu Hussein alisema: “Unaruhusiwa. Lakini ewe Jaun! Umekaa na mimi na umeishi kwa amani na sasa unataka kuuawa!” baada ya kusikia maneno haya, Jaun alianguka chini ya miguu ya Imamu Husein na alisema: “Ewe bwana wangu, mimi si miongoni mwa wale wanaokulaghai wakati wa amani na starehe, na kukukimbia wakati wa dhiki. Ewe bwana wangu! Hapana shaka kwamba jasho langu linalo harufu mbaya, nasaba yangu si ya watu bora, 156


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

na rangi yangu ni nyeusi lakini kwa baraka zako jasho langu litakuwa manukato, nasaba yangu itakuwa bora na rangi yangu itakuwa nyeupe huko Peponi. Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sitakuacha wewe hadi hapo damu yangu itakapochanganyika na damu yako.” Hatimaye Imamu Husein alimruhusu. Jaun aliingia kwenye uwanja wa vita na alianza kupigana na alikariri aya za tenzi zifuatazo: “Enyi mliolaaniwa! Mliona mapigano ya mtumwa mwafrika? Oneni anavyopigana kwa kuwaunga mkono watu wa Nyumba ya Mtume wa Uislamu!” baada ya kukariri tenzi hizo, Jaun alifanya shambulizi kali dhidi ya adui akapigana mfululizo hadi akawaua maadui ishirini na tano na akafa shahidi.78 Muhammad bin Abi Talib Makki ameandika kwamba Jaun alipokufa shahidi Imamu Husein alikwenda kwenye maiti yake akaweka kichwa chake kwenye mapaja yake na akamwomba Mwenyezi Mungu, “Ee Mwenyezi Mungu! Ung’arishe uso wa Jaun, fanya jasho lake linukie vizuri na umweke pamoja na waadilifu huko Peponi, hivyo kwamba aweze kuwa naye Mtukufu Mtume na Ahlul Bait.” Wanachuoni wamemnukuu Imamu Muhammad Baqir ambaye humnukuu baba yake Imamu Zaynul Abidin akisema kwamba siku chache baada ya Bani Asad walipozika miili ya mashahidi wa Karbala na kuondoka, walikuta mwili wa Jaun ambapo uso wake ulikuwa unang’ara na mwili wake ulitoa harufu nzuri ya

Bilal Wa Afrika

manukato.79 Kwa ufupi, mtumwa huyu mwaminifu wa Abu Dharr alitoa maisha yake kwa ajili ya bwana wake Imamu Husein, alipigana na Yazid bin Muawiyyah, dikteta wa ukoo wa Umayya, kwa ujasiri ukakamavu na ushujaa na akafa shahidi.

HAJJAJ AYMAN UBAYD- KUTOKA ETHIOPIA Bibi yake Ummu Ayman (mama yake Ayman), alikuwa mtumishi wa kike wa Mtukufu Mtume. Ayman alikufa shahidi kwenye vita ya Hunain mnamo mwaka wa 8 A.H. mtoto wa kiume wa Ayman- Hajjaj alizaliwa wakati Mtukufu Mtume akiwa hai. Hadithi nyingi za Mtukufu Mtume zimenukuliwa kutoka kwa Hajaj kwenye maandishi ya Kiislamu.80

MARIYA QIBTIYYA- MAMA WA WAUMINI Mtawala wa Alexandria (Misiri) alimpeleka Mariya Mkristo wa Copt. dada yake Sirin na kama yake Mabur, pamoja na Mithqal 1000, nguo laini 20, nyumbu aliyeitwa ‘Duldul’ na punda aliyeitwa ‘Yafur’ kama zawadi kwa Mtukufu Mtume. Mariya na dada yake Sirin walisilimishwa na Habib Ibn Baltara ambaye aliwapeleka kwa Mtukufu Mtume, kabla ya kufika Madina. Kaka yao Mabur, hata hivyo hakusilimu hadi muda fulani baadaye lakini ilikuwa wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume, alipokubali kuwa Muisilamu.

79

78

Muntahul Amal by Shaukh Abbas Qummi. 157

Bilal Wa Afrika

80

Absarul Ain, uk. 165 kimechapishwa Deccan mwaka wa 1357 A.H; Biharul Anwwar, Juz. i Al-Isabah, Juz. I, uk. 367 158


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

UMME AYMAN-MAMA WA MTUKUFU MTUME

Mariya aliolewa na Mtukufu Mtume na kwa hiyo akawa mmojawapo wa mama wa Waumini kaka ilivyoandikwa kwenye Quran Tukufu: (33:6) Alikwenda Madina akaolewa na Mtume mnamo mwaka wa 7. A.H. mnamo mwaka wa 8. A.H. alizaa mtoto wa kiume aliyeitwa Ibrahim lakini mtoto huyu alifariki akiwa na umri wa miezi 18.81

MARIYA BINT SHAM’UN QIBTIYYAMSICHANA MTUMWA WA MTUME Mariya binti wa Sham’un alikuwa Mkibti. Ambaye baadaye alisilimu. Alikuwa mmojawapo wa watumwa wawili, mwingine alikuwa Rihana, bint yake Zayd waliotolewa zawadi na mtawala wa Alexandria kwa Mtukufu Mtume.82

SIRIN –MKE WA MSHAIRI Sirin alikuwa dada yake na Mariya Mkibti, mmojawapo wa wake zake Mtukufu Mtume, na alipelekwa kama zawadi kwa Mtume na mtawala wa Alexandria (Misri). Aliolewa na Hasan bin Thabit, sahaba wa Mtukufu Mtume na mmojawapo wa Waarabu maarufu sana kwa umahiri wake.83

Bilal Wa Afrika

Jina lake alikuwa Barka na alikuwa na asili ya Ethiopia. Alikuwa mtumwa wa Abdullah, baba yake na Mtukufu Mtume. Alikuwa yaya wa Mtukufu Mtume wakati alipokuwa mchanga na alipokuwa mkubwa akampa uhuru. Alikuwa mmojawapo wa watu wa mwanzo kusilimu na aliungana na watu waliohamia Ethiopia na kutoka huko alikwenda Madina. Kabla ya Uislamu aliolewa na Ubayd bin Umar hapo Makkah. Alizaa mtoto aliyeitwa Ayman kwa hiyo aliitwa Umme Ayman (mama yake Ayman). Baada ya kifo cha Ubayd, aliolewa na Zayd bin Harith ambaye alizaa naye mtoto mwingine aliyeitwa Usama ambaye habari zake zimeandikwa kwenye kurasa za nyuma. Mtukufu Mtume alimwita ‘mama’ na mara nyingi alimtembelea na kumpa heshima zake.84 Binti yake Mtume, Bibi Fatimah alipoolewa na Imamu Ali mnamo mwaka wa 12. A.H, Umme Ayman alikabidhiwa sherehe ya harusi na Mtukufu Mtume. Alishuhudia harusi ya Mtukufu Mtume alipomwoa Bibi Khadija, mmojawapo wa wanawake matajiri sana Arabuni na alipoona mahari ya kudunduliza na sherehe nyepesi ya harusi ya Bibi Fatima (binti yake Mtume na Bibi Khadija) alilia sana. Mtume alimliwaza.85 Baada ya kifo cha Mtukufu Mtume, ushindani uliotokea kati ya Khalifa Abu Bakr na Bibi Fatima, unaojulikana kama ‘Kesi ya

81

82 83

Al-Isabah, Juz. iv; Usudul Ghabah, Juz. v; Manaqib -e- Ali Abi Talib, Juz i. Manaqib -e-Ali Abi Talib, Juz.i Usudul Ghabah 159

84 85

Al-Isabah; Usudul Ghabah. Manaqib -e- Ali Abi Talib, juz. iv. 160


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Fidak.’ Fidak ni kiunga alichopewa Bibi Fatimah na Mtukufu Mtume. Baada ya kifo cha Mtukufu Mtume, haki yake ya kumiliki kiunga hicho ilisitishwa na khalifa Abu Bakr. Bibi Fatima alikwenda kwenye Mahakama ya Khalifa kuwasilisha madai yake. Alitakiwa apeleke mashahidi kuonyesha kwamba Mtukufu Mtume alimpa kiunga hicho. Bibi Fatimah aliwaonyesha mashahidi wake kuwa mume wake Imamu Ali watoto wake wawili Imamu Hasan na Imamu Huseini na Ummu Ayman. Imamu wa sita wa Shia, Imamu Jafar –as-Sadiq amesema kwamba Ukhalifa wa Abu Bakr, ulipoanzishwa na akasitisha haki ya Bibi Fatimah, kumiliki Fidak, Fatimah alikwenda kwa Khalifa kutaka kujua sababu za wakala wake kuondolewa toka Fidak. Alisema, Fidak ilikuwa mojawapo ya viunga ambavyo Mtume alinipa . . . . .” Abu Bakr alisema. “Lete mashahidi kuhusu hilo”. Hapo hapo Fatima alimpeleka Ummu Ayman kama shahidi. Umme Ayman alisema: “Abu Bakr! Sitatoa ushahidi wowote, mpaka uthibitishe maelezo ya Mtume kuhusu mimi.” Halafu alisema: “Mtume hajasema kwamba Umme Ayman ni mwanamke wa Peponi?” Abu Bakr alijibu: “Ndio, Mtume alisema.” Halafu Umme Ayman alisema: “Ninashuhudia kwa kusema kuhusu ukweli kwamba Mwenyezi Mungu alileta ufunuo kwa Mtume Wake: “Na mpe jamaa yako haki yake...” (17:26) mara baada ya kusikia amri hii ya Mwenyezi Mungu, Mtume alimpa Fatima Fidak.” Imamu Ali alifuata, naye alitumia mkondo huo huo wa hoja.

Bilal Wa Afrika

Baada ya kusikia ushahidi huu Abu Bakr aliandika ‘agizo’ kwamba Fidak irudishwe kwa bibi Fatima. Wakati huo huo Umar (ambaye baadaye alikuja kuwa Khalifa wa pili) aliwasili hapo na alimuuliza Abu Bakr hati hiyo ilihusu nini. Alijibu: “Fatima alilalamika kuhusu Fidak na Ummu Ayman na Imamu Ali walitoa ushahidi, kwa hiyo niliamuru kwa maandishi Fidak irudishwe kwake”. Umar alimnyang’anya Abu Bakr amri hiyo ya maandishi na akaipasua vipande vipande. Bibi Fatimah alilia wakati anarudi nyumbani.86 Allama Shaykh Abdullah Ma-Maqazi, mmojawapo wa wanazuoni maarufu wa Waislamu wa Sunni, ameandika kwa kurejea tukio hili: Ummu Ayman ni mtu huyo huyo ambaye Fatima, msema kweli mkubwa sana alipeleka ushahidi kuhusu ushindani wa Fidak, na ambaye alikataliwa kwa sababu hakuwa Mwarabu. Kutokana na ukweli kwamba Umme Ayman alichukuliwa kuwa shahidi na Bibi Fatima, ninahitimisha kwamba lazima alikuwa mwanamke wa kutegemewea na kuaminiwa, kwani haiwezekani kuishawishi akili ya kawaida kwamba mwanamke wa hadhi ya Fatima angemtaja shahidi ambaye ni dhalimu na asiyeaminika. Nukta nyingine inayomfanya aonekane kusadikika na kuaminika ni kwamba washindani wa Fatimah walimkataa Ummu Ayman kwa sababu ya kutokuwa Mwarabu na si kwamba hakuwa mwaminifu au dhalimu.87 Inasimuliwa kwamba baada ya kifo cha Bibi Fatima, hakutaka kuishi Madina, alikwenda Makkah. Alipofika mahali paitwapo Hajafa (Julifa) alizidiwa na kiu na akatazama juu mbinguni na 86 87

161

Bilal Wa Afrika

Biharul Anwar, Juz. viii, cha Allamah Majlisi. Man la Yahzuruhul Faqih, cha Shaykh Saduq 162


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

kuomba. Jibu la maombi yake, watu waliona ndoo ya ngozi iliyojaa maji ikiteremka kutoka mbinguni na akakata kiu. Athari ya tukio hili ni kwamba hakuona kiu wala njaa kwa miaka mingi.

“Ee uliye Peke Yako, Ambaye hana afananaye Naye, Ambaye husababisha kila mtu kufa, husababisha kila kitu kuangamia; ambaye yu Peke Yake, tu huko mbinguni; Ambaye wala hasinzii ama kulala.”

(Mwandishi ameshindwa kupata kumbukumbu ya kifo chake kwenye vitabu vya Historia ya Kiislamu).

Fizzah amesimulia kwamba kazi nyingi ngumu zilirahisishwa kwa kukariri dua hii.

FIZZAH – HAFIDH WA QUR’AN TUKUFU Fizzah alikuwa Mnubi na alikwenda Arabuni kama mtumwa. Aliwasili Arabuni muda mfupi baada ya Hijiriya ya Mtukufu Mtume Madina. Alipewa jina la Fizzah na Mtukufu Mtume na binti yake mpendwa Mtume, Bibi Fatima alipomwomba mtumishi, Mtume alimpa Fizzah. Kwa mujibu wa mafundisho ya baba yake, Mtukufu Mtume Bibi Fatima hakumpa daraja la msichana mtumwa. Aligawa kazi za nyumbani sawa baina yake na Fizzah na kazi zingine walizifanya kwa kupokezana.88 Fizzah aliolewa na Abu Thalaba mtu wa kutoka Ethiopia na alizaa naye mtoto mmoja wa kiume. Baada ya kifo cha mume wake, aliolewa na Abu Malik Ghaftani. Mwanae wa kiume wa kwanza pia alifariki dunia. Hata hivyo, alizaa watoto kadhaa na Abu Malik. Mtukufu Mtume alimfundisha Fizzah dua maalum za kuhifadhi moyoni kwa ajili ya kukariri wakati wowote alipoona kazi yoyote ‘nzito’ kama ifuatavyo:

88

Anayo heshima yakuwa mmoja wapo katika ‘Saumu ya siku tatu’ ambayo ilisababisha sura nzima ya Qur’an Tukufu kushuka kutoka mbinguni kwa ajili ya kuwatukuza. ( 76:5-31). Inasimuliwa kwamba wakati fulani Imamu Hasan na Imamu Huseini wajukuu wawili wa Mtume (s.a.w.) waliugua. Mtukufu Mtume (s.a.w.) alikwenda nyumbani kwa binti yake Fatima kutaka kujua hali yao na akashauri Imamu Ali aweke nadhiri ya kufunga (Saumu) siku tatu kwa ajili ya nafuu ya watoto. Watoto walipopona Imamu Ali, bibi Fatima, Imamu Hasain, Imamu Husein na Bibi Fizzah walifunga saumu. Mikate ya bofulo ya shayiri ilitayarishwa na mara tu walipoketi tayari kuanza kufuturu, mtu alipiga hodi mlangoni huku akiomba chakula akisema: “Enyi watu wa nyumba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, mimi ni mtu masikini nipeni chakula.” Kila mmojawao pamoja na Fizzah, alitoa mkate wake wakampa. Wakafuturu kwa kunywa maji na wakalala bila kula chakula. Siku iliyofuata walifunga saumu na Bibi Fatimah alitayarisha mikate mitano kwa mara nyingine tena, walipokuwa wanaketi ili wafuturu, mtu alitokea mlangoni kwao akalia “Enyi watu wa nyumba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, mimi ni yatima, nina njaa, sina chakula, nipeni chakula. Wote walimpa mikate na wao wakabaki na njaa.

Al-Isabah, Juz. iv. 163

164


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Siku ya tatu ya saumu yao na jioni mara tu walipoketi, kufuturu, mtu alitokea na akasema, “Enyi watu wa nyumba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, mimi sina msaada na ni mateka, nina njaa, nipeni chakula.” Kwa mara nyingine tena wakampa mikate yao na walifuturu kwa maji. Wao kukubali kubaki na njaa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kutoa msaada chote kile walichotaka kula, Mwenyezi Mungu aliteremsha sura ya 76 kwa Mtukufu Mtume kwa kuwasifia. Sura hi inayo Aya 31 baadhi ya hizo ni kama zifuatazo: “Wanatimiza ahadi, na wanaiogopa siku ambayo shari yake inaenea sana. Na huwalisha chakula, juu ya kukipenda kwake, masikini, na yatima, na wafungwa. Hakika sisi tunakulisheni kwa wajihi wa Mwenyezi Mungu. Hatutaki kwenu malipo wala shukrani. Hakika sisi tunaigopa kwa Mola wetu hiyo siku yenye shida na taabu. Basi Mwenyezi Mungu atawalinda na shari ya siku hiyo, na atawakutanisha na raha na furaha. Na atawalipa Bustani za Peponi na enzi, hawataona humo jua kali wala baridi kali.” (76:6-12). Fizzah alikuwa mtumishi wa ndani ya nyumba ya watu wa Ahlul Bait (watu wa nyumba ya Mtukufu Mtume yaani Imamu Ali, Bibi Fatima, Imamu Husein Imamu Hasani ambao walikwua watakatifu sana na walio heshimiwa baada ya Mtukufu Mtume Muhammad s.a.w.w). Fizzah aliishi kwenye mazingira haya matakatifu ambayo yalimfanya kuwa na bidii. Alihifadhi Qur’an Tukufu yote na kwa miaka ishirini ya maisha yake hakusema hata neno moja ila kwa kutumia aya za Qur’an Tukufu katika mazungumzo yake. Tukio la kuvutia sana limesimuliwa na Abul Qasim Qushairi. 165

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Anasema: Wakati fulani niliachwa na msafara wangu peke yangu kwenye mbuga. Nilimuona mwanamke ambaye nilimuuliza, “wewe ni nani?” alijibu; “…Nasema Salam” (yaani ‘amani’ salamu ya maamkizi ya Kiislamu). Kwani baada ya muda mfupi watajua!” (43:89). Kwa hiyo nilimsalimia kwa njia ya Kiislamu kwa kutamka maneno “Salam Alaikum’ (Amani iwe kwako) na nilimuuuliza, “Unafanya nini hapa?” Alinijibu: “Na ambaye Mwenyezi Mungu anamwongoa hana wa kumpotoa (39:37). Niliposikia jibu lake, nilimuuliza: “Wewe ni katika wanadamu au majini? Akajibu: “Enyi wanadamu chukueni pambo lenu kwenye kila pahala wakati wa ibada” 7:31. Nikamuuliza: “Unatokea wapi?” Akasema:.. “Hao ndio watakaoitwa kutoka mahali pa mbali.” Nimuuliza: “Unakusudia kwenda wapi?” Akajibu: “...... Na ni haki ya Mwenyezi Mungu juu ya watu kuhiji Nyumba hiyo .......” Nilimuuliza : unakusudia kwenda wapi? Alisema: “...Na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu imewajibikia watu wahiji kwenye nyumba hiyo...” 3:97. “Nilimuuliza: Nilini uliwachwa na msafara?” Alijibu: “Na bila shaka sisi tumeziumba mbingu na ardhi na vilivyomo baina yao kwa muda wa siku sita...” 50:38. Nilimuuliza: “Je wasikia njaa?” Alijibu: “Wala hatukuwafanya miili isiyokula chakula...” 21:8. Nilimpa chakula nilimwomba akaze mwendo ili tuufikie msafara lakini si kukimbia. Alijibu: “Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadri ya iwezavyo (2:286). Nilimshauri aketi juu ya ngamia nyuma yangu. Alijibu: “Lau wangelikuwemo humo miungu wengi isipokuwa Mwenyezi Mungu basi bila shaka hizo mbingu na ardhi zingelifisidika (21:22). 166


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Niliposikia hivi nilishuka kutoka kwenye ngamia wangu na kumpandisha yeye. Alipopanda juu ya ngamia, alisema: “Ili mkae vizuri migongoni mwao (43:13). Wakati tulipoupita msafara, nilimuuliza: “ Je kuna yeyote katika msafara ambaye ni jamaa yako?” Alijibu: (i) “Ewe Daudi! hakika Sisi tumekufanya wewe khalifa katika nchi...” 38:26 (ii) ‘Na hakuwa ila ni Mtume tu...” (iii) Ewe Yahya kishike kitabu kwa nguvu...” 19:12 (iv) Ewe Musa Hakika mimi ndiye Mola wako...” 27:9 (Haya ni majina ya Mitume) nilianza kuita majina haya manne ambayo kwayo vijana wanne walitoka nje ya msafara na kumkimbilia Fizzah. Nilimuuliza ni nani hawa vijana wanne’ akajibu: Mali na watoto ni pambo la maisha ya dunia...” 18:46. Wakati vijana wale walipokaribia mama yao alisema: “...Ewe baba yetu muajiri huyu. Hakika mbora wa kumuajiri ni mwenye nguvu na muaminifu” 28:26. Hapo vijana wale walinipa pesa ambapo Bibi Fizzah alisema: “... Na Mwenyezi Mungu humzidishia amtakaye....” 2:261 Vijana waliongeza juu ya kile walichokwisha nipatia. Niliwauliza vijana hao huyo mwanamke mwenye kuheshimika na muungwana ni nani? Walijbu: “Ni mama yetu, Fizzah, mtumishi wa ndani wa Bibi Fatima bint yake Mtukufu Mtume. Hazungumzi isipokuwa kwa Aya za Qur’an Tukufu kwa miaka ishirini.”

Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

Fizzah alifuatana na mabibi wa nyumba ya Imamu Husein wakiwa mateka na alitabika na kudhalilishwa pamoja nao na uonevu kwenye mikono ya askari wa Yazid na wafuasi wake. Hatimaye aliachiliwa pamoja na watu wengine wa familia ya Imamu Husein na alikwenda Madina nao. Kila mwaka, Waislamu hususan Shia huadhimisha kumbu kumbu ya kufa shahidi Imamu Husein wakati wa miezi miwili ya kwanza ya Kalenda ya Kiislamu (Muharaamu na Safar) na wasomaji hutaja jina la Fizzah kwa uchaji Mungu wake, ujuzi wake, moyo wa ibada na kujitolea katika kuitumikia familia Mtukufu Mtume. Jina lake na kujitolea kwake ni maneno yanayo tamkwa katika kila nyumba ya Shia.

SHOHRA – MJUKUU WA KIKE WA FIZZAH Shohra alikuwa mmojawapo wa wajukuu wa kike wa Bibi Fizzal. Pia alijaliwa uwezo wa muujiza na Mwenyezi Mungu. Tukio limesimuliwa na Malik bin Dinar kuhusu Shohra. Anasema kwamba wakati fulani alimuona mwanamke mzee amepanda ngamia aliyedhoofu akienda Hija Makkah. Njiani, ngamia alizidi kudhoofu na hakuweza kuendelea na safari. Mwanamke aliyekuwa amepanda ngamia huyo jike alinyanyua macho kuelekea mbinguni na alisema: “Ee Mwenyezi Mungu! Hukuniacha nibaki nyumbani kwangu wala huniachi nifike kwenye Nyumba Yako (Kaabah). Kama mtu mwingine (asiye wewe) angenifanyia hivi mimi, ningekuja Kwako kulalamika.”

Bibi Fizzah aliungana na Imamu Hussein katika safari ya kwenda Karbala (Iraq) mahali ambapo Imamu na wafuasi wake walikufa mashahidi. Imamu Husein alipokwenda kuaga mnamo siku ya Ashura (tarehe 10 Muharam, 60 A.H) aliita majina ya dada zake, wake zake, mabinti zake na Fizzah.

Baada ya sekunde chache mwanamke huyo kutamka maneno haya, ghafla alitokea mtu kutoka jangwani akiwa ameshika pua ya ngamia jike. Alikwenda kwa huyu mwanamke bora na alisema; “Bibi! Panda ngamia huyu.” Alipanda juu ya ngamia

167

168


Bilal Wa Afrika

Bilal Wa Afrika

jike na alitoweka kwa kasi ya kimuujiza. Nilipofika Makkah, nilimuona mwanamke huyo anafanya Tawaf ya Kaaba (kuzunguuka Nyumba Takatifu ya Makkah). Nilitaka aniambie kwa kiapo kwamba yeye ni nani na alijibu kwamba yeye alikuwa mjukuu wa kike wa Bibi Fizzah.89

89

Manaqib-e-Ali Abi Talib, juz. iv. 169


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.