Elimu ya ghaibu

Page 1

Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:35 PM

Page A

ELIMU YA GHAIBU YA MAIMAMU Kimeandikwa na: Sayyid Abdul Rahim al-Musawi

Kimetarjumiwa na: Shaikh Haroon Pingili


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:35 PM

Page B

B


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:35 PM

Page C

|

ŠHaki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 - 512 - 96 - 6 Kimeandikwa na: Sayyid Abdul Rahim al-Musawi Kimetarjumiwa na: Shaikh Haroon Pingili Kimehaririwa na: Hemedi Lubumba Seleman Kimepangwa katika Kompyuta na: Hajat Pili Rajab Toleo la kwanza: Januari, 2010 Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:35 PM

Page D

YALIYOMO Utangulizi..........................................................................................2 MLANGO WA KWANZA: Mwanadamu na haja yake ya kujiambatanisha na ghaibu............8 MLANGO WA PILI: Uhusiano wa Umaasumu na elimu ya ghaibu.............................16 MLANGO WA TATU: Msimamo wa Qur’ani na Sunna kuhusu elimu ya ghaibu.........25 MLANGO WA NNE: Elimu ya ghaibu na Elimu ya falsafa ya Saikolojia (Phisycological Philosophy).................................................................................51 MLANGO WA TANO: Elimu ya ghaibu kwa wengine ambao sio Imamiya...................59 MLANGO WA SITA: Historia ya Mas’ala hii na mwelekeo wake kitafsiri katika maoni ya imamiyya................................................................................65 Daraja la Kwanza: Zama za Maimam........................................................................68 Daraja la Pili: Baada a kughibu kwa Maasumu (a.s)..........................................73 Daraja la Tatu: Kwa wanachuoni wa mwishoni....................................................78 Natija ya Utafiti...............................................................................93


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:35 PM

Page E

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu

NENO LA MCHAPISHAJI Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kiitwacho, ‘Ilmu Aimmah Bi ‘l-Ghayb, kilichoandikwa na Sayyid Abdul Rahim al-Musawi. Sisi tumekiita, Elimu ya Ghaibu ya Maimamu. Ghaibu (ghayb) maana yake - yasioonekana. Sharti moja la imani katika Uislamu ni kuamini yasiyoonekana ambayo kwa kweli ni mengi sana, lakini kwa kutaja machache ni kama vile, malaika, majini, Pepo, moto wa Jahannam, roho, n.k. Hivi vyote havionekani katika macho yetu lakini vipo na lazima tuamini hivyo. Qur’ani Tukufu inasema: “Hicho ni Kitabu kisicho na shaka ndani yake, ni mwongozo kwa wamchao (Mungu), ambao huyaamini yasiyoonekana...” (2: 2-3). Mwandishi wa kitabu hiki ameelezea kwa kina maana halisi ya ghaibu kwa kutumia vyanzo vitukufu - Qur’ani Tukufu, Sunna na hoja za kielimu. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili za watu. Kutokana na ukweli huo, taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili.

E


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:35 PM

Page F

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Tunamshukuru ndugu yetu, Sheikh Harun Pingili kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni chenye manufaa sana kwa wasomaji wetu na Waislamu wote kwa ujumla. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation S. L. P. 19701, Dar-es-Salaam.

F


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:35 PM

Page G

NENO LA JUMUIYA Hakika mirathi ya Ahlul-Bait ambayo imehifadhiwa na kambi yao na wafuasi wao dhidi ya upotovu inaonyesha kambi iliyokusanya aina mbalimbali za taaluma za kiislamu. Kambi hii imeweza kulea nafsi mbalimbali zilizo tayari kunywa kutoka kwenye chemchemu hiyo, na kuupa umma wa kiislamu wanavyuoni wakubwa wenye kufuata nyayo za ujumbe wa Ahlul-Bait. Wanavyuoni waliokusanya vidodosa na maswali mbalimbali ya madhehebu na mitazamo tofauti ya kifikira kuanzia ndani ya desturi ya kiislamu hadi nje ya desturi hiyo, huku wao wakitoa majibu na utatuzi makini juu ya maswali hayo ndani ya karne zote. Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bait imefanya hima kutetea tukufu za ujumbe wa Uislamu na ukweli wake ambao umechafuliwa na makundi, madhehebu na wanaharakati mbalimbali wenye chuki na Uislamu. Jumuiya imefuata nyayo za Ahlul-Bait na za wafuasi wa kambi yao njema ambayo imefanya hima kujibu madai yenye kuendelea na daima ikajaribu kubaki ndani ya msitari wa mapambano kwa kiwango kinachohitajika ndani ya kila zama. Hakika uzoefu ambao umehifadhiwa ndani ya vitabu vya wanavyuoni wa kambi ya Ahlul-Bait katika dhamira hii ni wa aina ya pekee, kwa sababu una akiba ya kielimu inayotegemea akili na hoja, huku ukijiepusha na matamanio na upendeleo uliokatazwa.

G


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:35 PM

Page H

Unazungumza na wasomi na wanafikra wenye fani maalumu, mazungumzo ambayo yanakubalika kiakili na yanapokewa na maumbile yaliyo salama. Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bait limekuja kuwapa watafuta ukweli hatua mpya ya uzoefu wa thamani katika ulingo wa mazungumzo na maswali na kujibu hoja za utata zilizotolewa zama zilizopita au zinazotolewa leo kwa njia ya Tovuti, na hasa kwa kupewa nguvu na baadhi ya duru zenye chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu. Ikijiepusha na uchochezi uliokatazwa, na ni yenye kuhangaikia kuzishauri akili zenye kufikiria na nafsi zenye kutafuta haki, ili ziweze kufikia kwenye haki ambayo inatolewa na Kambi ya Ahlul-Bayt ulimwengu mzima, ndani ya zama ambazo akili inaerevuka na nafsi na roho zinaboreka kwa kasi ya pekee. Ni lazima tugusie kuwa mfululizo huu wa tafiti hizi umeandaliwa na Kamati maalumu toka jopo la wanavyuoni watukufu, hivyo tunatoa shukurani njema kwa hawa wote na kwa wasomi na wahakiki kwa kila mmoja miongoni mwao kupitia sehemu ya tafiti hizi na kutoa mchango wao wa thamani kuhusu tafiti hizi. Na sote tunategemea na kutaraji kuwa tutakuwa tumetoa kile tulichokiweza katika juhudi za kutekeleza baadhi ya wajibu tulionao mbele ya ujumbe wa Mtukufu Mola wetu Mlezi ambaye alimtuma Mtume Wake na uongofu na dini ya haki ili aipe ushindi dhidi ya dini zote. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi. Jumuiya ya kimataifa ya Ahlu-Bait Kitengo cha utamaduni

H


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:35 PM

Page I

I


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:35 PM

Page 1


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:36 PM

Page 2

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu

UTANGULIZI Ameumbwa mwanadamu na vitu viwili: Mada na Roho na kila kimoja kina taathira kwa mwenzake, tafiti katika elimu ya tiba imethibitisha kuwa maradhi mengi na hasa kidonda na Sukari na ambayo yajulikana kuwa ni maradhi ya al’juhdu yanarejea kwenye vyanzo vya kisaikolojia; kwa hiyo maradhi kama haya hayatibiki kwa tembe na mtu kuchanguka kwa kutumia vidonge au aina nyingine ya dawa, bali mara nyingi hutibiwa kwa njia za tiba za kisaikolojia. Na matokeo ya kuendelea kwa utafiti wa kielimu katika uwanja huu na majaribio ya kugundua kiwango cha taathira ya kila upande na ya uingilianaji kati ya limwengu mbili za mwanadamu, wa maada na wa kiroho wameasisi elimu kwa ajili ya uwanja huu kwa jina la (Caracterolohgie), elimu ya tabia. Na lengo lilikuwa kuielekeza nguvu ya mtu na ya jamii kwenye lengo la urekibishaji na kuadabisha mahusiano yake na wengine na yake binafsi, baada ya kumaliza kuutambua uwezo alionao na nguvu zake kiroho, ili asijibebeshe asiloliweza, na likamilike adabisho la huo uwezo na kabilia kwa njia ya yeye mwenyewe, ili baada ya hapo iwezekane kumwelekeza mtu na kumlea mpaka kwenye yanayomrekibisha, na kumhadharisha asifanye yasiyo mema kwake, haya ni kwa upande mmoja. Ama kwa upande mwingine tunaona kuwa mwanadamu anahusika na kuathirika na kuathiri kwa ghaibu ijayo, nasema hata kwa kufichua undani zaidi wa yaliyopita kama ule ambao Qur’ani tukufu imemhadithia Rasuli, ikiwa ni kama nyongeza inayompa nguvu katika tendo la urekibishaji. Mfano wa visa vya Bani Israeli na Musa (a.s.) na njama za mayahudi na misimamo yao kuwaelekea manabii (a.s.), na yaliyomkumba Nabii Isa (a.s.). Kisha aliyopambana nayo Nabii Yusufu (a.s.), kiasi kwamba visa vya Qur’ani vinatofautiana katika kufichua yaliyopita mbali na vingine miongoni mwa riwaya zinazonakiliwa na mayahudi na zile ambazo zipo katika vitabu vya mbinguni vilivyopotoshwa. 2


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:36 PM

Page 3

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Amesema (s.w.t.):

“Hizo ni katika habari za ghaibu tunazokufunulia. Hukuwa ukizijua, wewe wala watu wako kabla ya hii. Basi vuta subira, hakika mwisho mwema ni kwa wamchao Mungu.� (Sura Hudi:49) Mtu hufanya juhudi kuijenga jamii ya kitawhidi hujikuta binafsi ahitaji kuwa na utambuzi wa kitakachokuwa mfano wa sura ya mwisho ya ulimwengu, akitaka harakati zake zilizopo ziwe zinalenga na kutiririka sawa na alikusudialo. Na anapoanza anakuwa amejiegama kwenye misingi madhubuti na utangulizi sahihi, si kwenye msingi wa dhana na mawazo au uwongo na upotoshaji. Na kwa upande mwingine: Kwa kweli maongezi kuhusu ghaibu au lililokuwa na litakalokuwa sio maongezi ya anasa yasiyoambatana na ukweli, bali tunayakuta yameingia kwenye kina cha historia, na mwanadamu amekuwa nayo kwa sura tofauti. Bali ni kusudio la ushirika la mtu, hakuna taifa la kidini au lingine ila litachukua kwa njia yake mahsusi wala halikatai kamwe, ila mwenye tabia ya pekee au mwenye lengo la kisiasa lisilo wazi. Na utaratibu huu umekubaliwa na risala ya kiislamu, huku kukiwa na tofauti katika kuanzia na lengo. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuwa anapoelekea kwa ajili ya vita vyake kwa washirikina huwaahidi waislamu nusra ya kiungu. Ni jambo ambalo mpiganaji wa kiislamu alikuwa analitendea kazi kwa uaminifu wa moja kwa moja. Na hilo Qur’ani tukufu imeliunga nguvu pindi ilipoahidi kuwa nusra haina budi katika baadhi ya matukio.

3


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:36 PM

Page 4

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Amesema (s.w.t.):

“Kwa hakika Mwenyezi Mungu amemhakikishia Mtume Wake ndoto yake ya haki. Lazima nyinyi mtaingia katika Msikiti Mtukufu” (Sura Fat’hu:27) Na urithi wa kiislamu umekuja na milango yake ya ghaibu na maelezo kuhusu habari za mwisho wa zama na dola ya Imam Mahdi ili uelekee mwelekeo ule ule. Na katika urithi wetu wa kiislamu kuna habari zinazohusu matukio ya ghaibu ya aina hii yenye dalili za kihistoria na za kiitikadi. Nabii (s.a.w.w.) amesema akimwambia Ammar: “Ewe Ammar kitakuuwa kikundi kiovu.”1 Na ambalo humshangaza msomaji miongoni mwa upashwaji habari na yanayovuka mipaka, yale ya ghaibu ambayo yanahadithiwa na vitabu vya urithi wetu wa kiislam usio wa Kiimamiya, ni kuwa imekuja ndani ya kitabu Karamatul-Awliyai kwamba Abaa Madyan alikuwa limjiapo wazo basi hulikuta limeonesha alama kwenye upande wa nguo yake, ikiwa ni kuamrishwa au kukatazwa.2 Na pia imekuja habari katika kitabu kilichotajwa: Kuwa miongoni mwao kuna wanaofichua kutoka ulimwengu huu wa hisi ulimwengu wa ghaibu, hivyo hazuiliwi na kuta wala na giza mbali na wayatendayo viumbe ndani ya nyumba zao.3 Na miongoni mwao kuna ambaye mtu akiingia kwake ikiwa ametoka kufanya zinaa, kulewa au kuiba au kutukana au alitembea kwenda kwenye 1 Kanzul-Ummal cha al-Mutaqi Al-Hindiy Juz. 11, Uk. 727. Hadithi ya 33561. Ibnu Asakir ameitaja katika Tarikh yake Juz. 6, Uk. 203. Na ad-Durul-Manthur cha Suyutiy Juz. 4, Uk. 371. 2 Karamatul-Awliyai cha an-Nabhaniy Juz.1, Uk. 53. 3 Karamatul-Awliyai cha an-Nabhaniy Juz.1, Uk. 53. 4


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:36 PM

Page 5

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu maasi au dhulma kwa mfano, huonekana kwenye kiungo cha mwili ambacho kilitenda tendo, mchoro mweusi.4 Naam, yote hayo yanawezekana na yametokea yanayoafikiana nayo nje, yaani kimatendo. Lakini endapo itokee wafuasi wa madrasa ya Ahlul-Bayt wanakili habari kutoka kwa Imam Ali bin Abu Talib na wanawe walio maasumu (a.s.) zinazoelezea kupatikana kwa habari ya ghaibu, walioipata kutoka kwa Nabii (s.a.w.w.) kutoka kwa Allah (s.w.t.) au kwa Il’ham kutokana naye (s.w.t.), wafuasi hawa hupewa sifa ya Ghulatu. Yapendeza kutaja kuwa thamani ya mustakabali wa kidini unathibiti kwa utangulizi mfupi ambao wategemea kuambatana na ghaibu ya moja kwa moja ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.). Imekuja katika Al-Mazamiir: “Uvukapo maji basi mimi ni pamoja nawe katika mito wala hayakuzamishi, na endapo utatembea katika moto hautokuunguza.”5 Na wamesema: Kumtumainia Mwenyezi Mungu ndiko ambako yambidi akudhihirishe daima kuwa mtu mchamungu. Yaweza ikaelezwa hiyo kuwa hata kwenye dhoruba kali hatoishakia kudra ya Allah na kuwa atamuokoa bila shaka.6 Na kwa mwelekeo uleule mwandishi wa kitabu Karamatul-Awliyai ametilia mkazo, aliposema: “Na miongoni mwao – katika mawalii – kuna anayetunukiwa nafasi ya kufahamu kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.), na usahihi wa kusikia ishara zake (s.w.t.), hivyo huwa asikia tamko la visivyokuwa na uhai kwenye utaratibu wa utamkaji wao katika mema na mabaya.”7 4 Karamatul-Awliyai cha an-Nabhaniy Juz.1, Uk. 53. 5 Al-Masihi Fii Maswadiril-Aqaidil-Masihiya cha Ahmad bin Abdul’Wahhabi Uk. 213. 6 Al-Masihi Fii Maswadiril-Aqaidil-Masihiya cha Ahmad bin Abdul’Wahhabi Uk. 213. 7 Karamatul-Awliyai cha an-Nabhaniy Juz. 1, Uk. 53. 5


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:36 PM

Page 6

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Na miongoni mwao kuna anayefichuliwa mwendo wa ulimwengu wa uhai katika viumbe hai, na miongoni mwa siri apewazo katika kila dhati kulingana na utayarifu wa dhati, na jinsi ibada zinavyokuwa kwa daraja katika huu mwendo. Na miongoni mwao kuna anayefichuliwa ratiba ya elimu ya nadharia na fikra zilizo salama na kuyafahamu makosa yanayoingia kwenye fahamu.8 Na safu ya Ahlul-Bayt (a.s.) imejibidisha kutendea kazi uwelewa wa elimu ya ghaib kwa Imam kulingana na taswira ya Qur’ani na lile ambalo Nabii (s.a.w.w.) amelitilia mkazo. Lakini sisi hatujui hoja ya wakanushao elimu ya ghaibu kwa Maimam (a.s.), na kuwatuhumu wafuasi wa madrasa yao kuwa ni Ghulatu japokuwa madrasa hiyo inashikilia na kujibidisha kwao na safu ya Rasuli (s.a.w.w.). Na kuwa Maimamu wao wanajua kama ajuavyo Rasuli sio ila ni elimu ya kutunukiwa kutoka kwake Aliyetukuka. Yapatikana kutokana na utangulizi huu mambo kadhaa: Kwa kweli upashaji habari wa ghaibu ni eneo ambalo ubinadamu umejipa muda wote wa zama, na kwa sura tofauti. Na jambo lingine ni kuwa wenyewe ni mahali ambapo pamefaidika na uthamani wa kimatendo na malezi. Na tatu ni kuwa suala la upashaji habari wa mambo ya ghaibu hauachani na kitendo cha kuwa na mwambatano wa kiroho na Mwenyezi Mungu, kwa ajili hiyo tunawakuta wasimulizi wakubwa katika mlango huu, wametoa sharti la uchamungu na usafi wa moyo na kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, japokuwa kuna tofauti kuhusu njia za kujiambatanisha. Na ili tuwe mbali na kuzama ndani zaidi na ili tukidhi utashi wa muhtasari, tunasema: Haiwezekani kuingia katika ufafanuzi wa maudhui hii na upeo wa mpaka wake, faida yake, na kadiri ambayo fikra ya kiislamu inavyochukua katika medani hii, ila baada ya kumaliza itikadi ya umaasumu 8Karamatul-Awliyai cha an-Nabhaniy Juz. 1, Uk. 53. 6


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:36 PM

Page 7

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu kulingana na mtazamo wa Shi’ah, ambao ndani yake mna elimu ya kutunukiwa. Kadhalika haiwezekani kupanda katika utafiti huu kabla ya kusalimu amri kuwa Khalifa wa Rasuli hapana budi awe afaidika na sifa zilezile za Rasuli (s.a.w.w.) ila bila ya kupata wahyi. Hivyo basi unakuja utafiti wa maudhui ya elimu ya ghaibu ya Maimam katika ngazi ya mwisho ya utafiti wa uimam na utafiti wa umasumu. Hivyo kutokea katika msingi huu, na mbali na mgubiko uliogubikwa kwenye maudhui hii na ghasia ya kelele za majahili na wenye malengo, na utafiti wa maudhui hii kwa njia ya mada iliyo mbali na uislam, na kutotambua tija kubwa za kielimu zilizodhibitiwa na wanazuoni wa madrasa ya Ahlul-Bayt (a.s.) katika uwanja huu, ambao semi zinashindwa kutambua falsafa yake kikamilifu, ndio maana kwa juhudi tumejaribu kuzileta karibu ncha zake na kuifanyia muhtasari baadhi misamiati yake. Kwa hiyo njia yetu ya utafiti ndani ya milango ni uliyopita unauandalia unaofuata. Mzunguko wa maneno katika mlango wa kwanza utahusu haja ya mwanadamu kuwa na mawasiliano na ghaibu pamoja na dharura ya kuizunguka elimu ya ghaibu ya kutunukiwa kutoka kwake Yeye (s.w.t.), ili ufahamike mchango wa kiungu ulio kamili kuizunguka elimu hii. Ama katika mlango wa pili tumetupia mwanga kwenye uhusiano kati ya umaasumu na elimu ya kutunukiwa, ambayo kwa njia yake maasumu hufahamu kanuni za maisha na sababu zake katika ulimwengu wa ghaibu na wa hadhiri katika hali iliyo sawa. Ama katika mlango wa tatu: Maneno yamejiri kuhusu Aya ambazo zimetaja elimu ya ghaibu katika maisha ya manabii na watu wema. Na baada yake tumeziendea Aya ambazo zinathibitisha uwezekano wa elimu ya ghaibu kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.). Kisha zimetajwa Aya ambazo zimethibitisha kumpa elimu ya ghaibu Hitimisho la Manabii (s.a.w.w.). Na katika mlango wa nne: Tumejishughulisha na kuonesha dalili za elimu ya ghaibu kwa njia ya elimu ya saikolojia ya kifalsafa. 7


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:36 PM

Page 8

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Na katika mlango wa tano: Tumehoji ndoto ya elimu ya ghaibu katika nadharia isiyo ya Imamiya. Na mwishowe mlango wa sita: Ambao unadhamini kuiweka wazi historia ya suala hili na mielekeo ya kitafsiri katika mtazamo wa Kiimamiya, na kwayo lapatikana hitimisho la muhtasari wa uwelewa sahihi.

MLANGO WA KWANZA MWANADAMU NA HAJA YAKE YA KUJIAMBATANISHA NA GHAIB Qur’ani tukufu inaitia watu kwenye utafutaji wa elimu, kwa kuwa umerudiwa rudiwa utajo wa neno lake katika Aya mia saba.9 Wala haukuwa wito wa Qur’ani wa kujielimisha na umuhimu wake ni semesho mahsusi lenye kuengua aina maalumu ya watu, bali wito wa kuitafuta: “Je, wanaweza kuwa sawa wale wanaojua na wale wasiojua?” (Sura Zummar: 9), ni wa watu wote, ukiongeza kuwepo kwa wingi wa zana za kujielimishia na zilizo rahisi kwa wote. Lakini je ni elimu gani hii ambayo Qur’ani inaitia? Bila shaka ni elimu ambayo ina maslahi kwa mwanadamu na kwayo unathibiti ujenzi na ukazi. Lakini hilo lapatikana kwa kuchuma na juhudi, kwa minajili hiyo imesifika kwa kadiri ya kiwango: ‘’Mwenyezi Mungu atawainua wale walioamini miongoni mwenu na waliopewa elimu daraja za juu.” (Sura al-Mujadila:11.) tofauti na elimu ya kutunukiwa ambayo hatunukiwi yeyote kutoka kwa Yeye Sub’hanahu ila aliyemridhia miongoni mwa waja wake. 9 Al-Muujamu Al-Mufahris Lil-Qur’ani Al-Kariim cha Muhammad Fuadi AbdulBaaqiy Uk. 469 -481. Msamiati Ilmu. 8


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:36 PM

Page 9

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Kama ambavyo elimu iliyokusudiwa mtu ajielimishe haibanwi na masafa ya ulimwengu unaoshuhudiwa, kadhalika haiishii kwenye elimu ile inayochumwa kupitia vyombo vinavyohisiwa, bali duru yake inapanuka ili ienee ulimwengu mwingine, huo ni ulimwengu wa ghaibu. Qur’ani haikutenganisha kati ya dunia hizi mbili ya ghaibu na ya hadhiri, hivyo imehesabu elimu ya ghaibu na ile ya yaliyomo nyuma ya yanayohisiwa kuwa ni elimu, kama ilivyomuita mtu ambaye anayemiliki sehemu fulani ya elimu ya ulimwengu mmoja wapo au ya dunia mbili hizo zote mbili kuwa ni alimu. Na kwa ibara nyingine ni kuwa: Elimu ya ghaibu ni jina la elimu ya kukijua kilicho ghaibu mbali na hisi tano, kwa njia yeyote ipatikanayo. Kwa hiyo huenda ikapatikana elimu ya ghaibu kwa njia ya thibitisho ya kiakili au kwa dalili ya nukuu. Mfano wake elimu ya kumjua Muumba na kuwa ni Mmoja (s.w.t). Kama ambavyo hujulikana kuwa ni elimu ya ghaibu ile iliyo ghaibu mbali na hisi na akili. Mfano wake hali za Barzakh na siku ya Kiyama na yatakayojiri ndani ya siku hiyo. Na mwishowe: Na huitwa kuwa ni ya ghaibu ile elimu ya Istiqlal yaani elimu iliyo ghaibu mbali na hisia za watu wote. Na ni wazi kuwa elimu ya ghaibu ile ya aina ya kwanza na ya pili mtu anaweza kuipata, ama elimu ya aina ya tatu haiwezi kupatikana. Ukweli wathibitisha kupatikana elimu za aina mbili za mwanzo kwa waumini wote, bali hata kwa wasiokuwa wao, na kupatikana kwake kwatimia kwa njia ya dalili za kiakili za hisi, kama ambavyo imani ya ghaibu inalazimu kuijua hiyo ghaibu. Hivyo basi wachamungu wanaoamini ghaibu wanaijua, kama ambavyo wao wanajua baadhi ya ghaibu kwa njia ya upashaji habari wa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) katika kitabu chake. Mfano wa ushindi wa warumi kabla ya wakati wake, na kama vile elimu yao ya matukio yaliyopita, ambayo hisi zao haziwezi kuyapata, ambayo Qur’ani 9


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:36 PM

Page 10

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu tukufu imeyafichua. Na kwa kweli amesema swt:

“Hizo ni katika habari za ghaibu tunazokufunulia. Hukuwa ukizijua, wewe wala watu wako kabla ya hii.” (Sura Hudi:49) Kisha Qur’ani haikuitaka miongoni mwa elimu ila elimu inayoongoza kwenye maslahi na kupitia hiyo yakini hupatikana:

“Kwa hakika wanaomwogopa Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja wake ni wale tu wenye elimu.’’ (Sura Faatir: 28) Na inachombeza kufanya kazi na kuwa na mwenendo mwema:

“Ni kosa kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu kusema msiyoyatenda.” (Sura Swaf: 3). Lakini je! Ni katika uwezo wa mwanadamu kuzijua siri kwa ukamilifu na yaliyofichikana ya ulimwengu wote, na yaliyoazimiwa kwa kanuni inayoingiliana yenye kuathirika na kuathiri kati yao katika kuchukua umbo la dhahiri. Anabaki mwanadamu – kundi au mmoja – ndani ya mipaka hawi na uwezo wa kuyazunguka yaliyomzunguka, yaliyompita na ya mustakabali wake, wala uzoefu haumsaidii wala tafiti kuweza kumfikisha kwenye ila kamili na sababu ambazo zinahukumu majaliwa ya dunia mbili zenye maingiliano na maisha ya wanadamu wote, japokuwa hilo linaingia chini ya duru ya uwezekano wa kiakili kama tulivyokwishasema.

10


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:36 PM

Page 11

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Wito wa Qur’ani unatilia mkazo kuujenga msingi wa imani juu ya kuamini ghaibu na kujiambatanisha na sababu ambazo kwazo wahyi umeasisiwa:

“Ambao huyaamini yasiyoonekana na husimamisha swala na hutoa katika yale tuliyowapa.” (Sura Baqarah: 3) Na kumfunga mwanadamu kwenye msingi huo, kwa kuwa utamaduni wa mwanadamu daima hauendi juu ila kwa chanzo cha asili kilicho juu mbali na ardhi, au sema kilicho mbali na ulimwengu unaoshuhudiwa. Kwa kuwa kujichanganya kwenye ulimwengu unaosifika kuwa ni wa hali ya chini, eti kwa kuwa anajitosha mwenyewe binafsi, ni kauli isiyo sahihi, kwa sababu ya historia kumtegemea mwanadamu na mwanadamu kuitegemea historia. Hivyo mwanadamu katika hali hiyo anabaki amezuilika ndani ya historia hiyo hiyo. Kwa hiyo hilo linapelekea kuporomoka kwa maendeleo, kama ambavyo yaonekana katika historia ya maendeleo na uporomokaji wake, hivyo ni kwa sababu ya kutegemea kwake upeo wenye kikomo. Mwenyezi Mungu asema:

“Wa-Iram, wenye majumba marefu marefu. Ambao mfano wao haukuumbwa katika miji. Na Thamudi waliochonga majabali bondeni. Na Firaun mwenye majeshi. Ambao walifanya maovu katika miji. Kisha walizidisha humo ufisadi. Kwa hiyo Mola wako Mlezi akawateremshia namna ya adhabu.” (Sura Fajri: 7-13) 11


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:36 PM

Page 12

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Kisha ni kuwa maendeleo yanalazimu mhitaji auchukue ukamilifu wake kutoka kwa mwenye ukamilifu wa moja kwa moja. Kwa minajili hiyo haiwezekani kumweka mbali mtu huyu na ulimwengu huu mkunjufu, kwa sababu ya kuwepo kiungo thabiti cha milele na mwambatano wa kimaumbile wa asili:

“Basi nitakapomkamilisha na kumpulizia roho yangu, basi mumwangukie kwa kumtii.” (Sura Hijri: 29) Je, mwanadamu ni kiumbe aliye karibu na ghaibu? La hasha bali yeye ni gao moja la ghaibu. Qur’ani imeuzungumzia ukaribu huu na uhusiano kwa shuhuda nyingine, mna maongezi kati ya ghaibu tupu – Allah – na mwanadamu:

“Na Mola wako Mlezi alipowaleta katika wanadamu kutoka miongoni mwao kizazi chao, na akawashuhudilisha juu ya nafsi zao: Je mimi siye Mola wenu Mlezi? Wakasema: Ndiye, tunashuhudia. Msije mkasema siku ya Kiyama, hakika sisi tulikuwa tumeghafilika nayo.” (Sura Aaraf: 172). Kwa ajili hiyo yatosha kuwa mawaidha kwa mwanadamu anapolinganiwa kuamini tawhidi, tumueleze ukumbusho, kama zilivyo njia za manabii na ulinganiaji wao wa tawhid. Kwa sababu ya kumiliki kwake akiba ya kiroho iliyotangulia na kuwa amekiri kwa maumbile yake itikadi hii. Kwa 12


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:36 PM

Page 13

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu minajili hiyo haukubaliwi udhuru wowote kutoka kwa mshirikina mbishi wa kuhalalisha ushirikina wake kama mghafala kwa mfano. Na maadamu mwanadamu ameazimia njia, haiwezekani kumtenga na ulimwengu wa ghaibu kama ulimwengu mwingine anaojiambatanisha nao, kwa sababu ya mwambatano huu kati ya hizi dunia mbili. Na taathira ya kila viumbe hawa na wenzao, na kwa alichotunukiwa huyu kiumbe mwanadamu hali ikiwa ni aina ya ustahiki na uwezo wa kuvitumikisha viini vya ghaib vilivyowekwa ndani yake mwenyewe na ndani ya ulimwengu kwa ajili ya makazi na ujenzi, hali ikiwa ni jukumu ambalo amelichukua mabegani mwake; basi kwa ajili hiyo yeye ni muhitaji wa kuelewa, na kuwa na mkazo wa elimu ya ulimwengu huu, kwa sababu ya hayo kuhusika kwake na ukhalifa. Qur’ani tukufu imehimiza kujielimisha kanuni za kiulimwengu ikiwa ni njia, inatufichulia ukweli wa mustakabali ambao haujatukia bado, na watoa mchango wa kuendelea mtu kuuelekea kwenye ukamilifu. Kwa sababu kuyajua hayo na sharti zake humuweka mtu mkao utakaomuwezesha kuitengeneza hali ya baadae, na kuwa juu yake, na mwenye kujihukumu katika kuchagua ambalo lafaa kwa maisha yake, kwa hiyo atafanya juhudi kwa uelewa ili kuandaa na kuzikusanya sharti zake na sababu zake kwa kutegemea kanuni za kiulimwengu zilizothibiti, zenye kufichua kutoka kwenye wahyi. Hivyo basi elimu ya kanuni za kiulimwengu na sharti zake ni jambo la kujipatia kwa kuchuma, ila tu ni mojawapo miongoni mwa ghaibu, au kuwa ni kanuni ya kiulimwengu yenye mafungamano na imani ya ghaibu kwa kutaraji ukaribu au kubisha, na yaendelea mpaka kwenye nia na maksudio ya kiroho ya utambuzi na hisia katika maisha ya umma:

13


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:36 PM

Page 14

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu

“Uharibifu umedhihiri barani na baharini kwa sababu ya yale iliyoyafanya mikono ya watu.” (Sura Rum: 41)

“Na kama watu wa miji wangeamini na kumcha (Mwenyezi Mungu), lazimsa tungewafungulia baraka za mbingu na ardhi, lakini walikadhibisha” (Sura Aaraf: 96) Kama ambavyo Qur’ani haikubaliani na njia ya utendeaji kazi wa kanuni za kiulimwengu wa kiupofu, na ule ambao usiotegemea uelewa na elimu katika kuchagua, kutokana na mchango wake na umuhimu wake katika kuchunguza hali ya baadae ya mwanadamu. Kwa upande mmoja huenda mtu hafikii maarifa ya kina au ya moja kwa moja ya kanuni za kiulimwengu, na huenda ameifikia na kuizunguka kivitendo kanuni hii ya kiulimwengu au ile, na katika hali hii au ile, ila tu ni kuwa yeye anabaki ni mwenye kuhemewa kuielewa muda wote na katika msitari wote, na hubaki ni mwenye kuhemewa kuyaelewa muda wote maarifa ya kiungu yenye maingiliano na maisha ya kiwanadamu kwa jumla, na kwayo zinafungamana harakati za kuwepo pande zake mbili zote, ya ghaibu na ya hisi, kwa kuelekea malengo makubwa, kwa njia ya elimu ya kujielimisha ya kuichuma, yenye uelewa. Hayo ni kwa sababu elimu ya aina hii – ya kuchuma – haina yaliyofichika na siri zinazojiri katika ulimwengu huu mpana, hususan wa kimaumbile, sio wa kisheria peke yake. Kwa sababu kuzizunguka siri hizo hakutimii ila kwa kujulishwa na Yeye (s.w.t.). Kwa kuwa kujielimisha kwa njia ya kuchuma ambako mtu mmoja 14


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:36 PM

Page 15

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu akufanyako au jamaa kunabaki ni chombo na ni cha muda kilichopo katika mabano ya zama, ni chenye kuhemewa kuizunguka kikamilifu siri hiyo, hivyo basi yenyewe ni pungufu, hivyo haitupi tija ila mchango pungufu, na hali utashi wa kiungu wakusudia ukamilifu. Hii ni hata kwa mpaka wa ulimwengu ushuhudiwao basi itakuwaje kwa upeo wa ghaibu na ulimwengu wake mpana. Hivyo basi mwanadamu ni aina inayohitajia elimu ya kutunukiwa, lakini yeye haipati elimu hii ila kwa kuichukua kupitia nyenzo za Kiungu kama wahyi au Il’ham, au kuandikwa moyoni, au kujielimisha kupitia kwa anayefunuliwa, kwa lengo la kuzijua vilivyo harakati zote za historia. Katika vifungu vya maneno vijavyo vya utafiti na vifungu vitakavyofuatia, mchango wa mfano huu wa Mola utakuwa wazi, ukiongezea kule kuwa wazi kwa dharura ya elekezi lake kupitia utoaji wake wa uwezo na elimu makhsusi inayotekeleza mchango wake uliowakilishwa kwake kwa namna kamili, na hatimaye huyu aliyekabidhiwa elimu yake ya kutunukiwa anaweza kumfikishia mwenye kustahiki kuibeba, kulingana na lazima za ukazi na ujenzi katika ulimwengu wa dunia.

15


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:36 PM

Page 16

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu

MLANGO WA PILI UHUSIANO WA UMAASUMU NA ELIMU YA GHAIBU Hadithi katika kipande hiki haikufanya utafiti kuhusu umaasumu na dharura yake kuwa ni makhsusi kwa Imam mwenyewe, ila tu tunayakata maongezi katika ufafanuzi wake na tunaifanya kwa mfano inakubali katika shakhsia ya Imam, kwa sababu utafiti katika elimu ya ghaibu kwa maasumu uko nyuma kidaraja kuliko utafiti wa umaasumu, au waingiliana, kwa minajili hiyo tunajikita kwenye kiungo kati ya umaasumu na elimu ya kutunukiwa kwa Imam, kwa kuzingatia kuwa nukta hii dhati yake inafanya msingi wa vipengele vifuatavyo. Viumbe katika huu ulimwengu havikuumbwa kwa namna ya kujitegemea, bali walizingatiwa viumbe wengine wanaomzunguka, hivyo basi ulimwengu wote ni wenye mafungamano na unafanya harakati kwa njia iliyo katika nidhamu na kwa mwongozo wa kiungu wenye kukadiriwa:

“Yule aliyekipa kila kitu umbo lake kisha akaongoza.” (Sura Taha:50) Na (s.w.t.) amesema:

“Na jua linapita kuendea kituoni pake hicho ni kipimo cha Mwenye nguvu, Mwenye kujua. Na mwezi tumeupimia vituo mpaka ukarudia 16


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:36 PM

Page 17

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu kuwa kama kole la mtende kuukuu. Haliwi jua kuufikia mwezi, wala usiku kuupita mchana, na vyote vinaogelea katika njia.” (Sura Yasin:38-40) Kwa mujibu huo viumbe waliopo katika jumla ya ulimwengu baadhi yao wana taathira kwa wengine, na mwanadamu hayuko nje ya kanuni hii, yeye ni kiumbe yuko ndani ya kanuni hizi. Na hatimaye ni mtii wa kanuni yake. Na kwa upande wa kuwa yeye anaathirika katika ulimwengu huu ni wazi, kwa kuwa jua likipanda au kuwa karibu litaathiri maisha yakiwemo ya mwanadamu. Na upande wa pili ni kuwa mwanadamu anaviathiri viumbe vilivyomzunguka. Hivyo basi upande huu unahitaji ubainifu zaidi. Amesema (s.w.t.):

“Na Mwenyezi Mungu amepiga mfano wa mji uliokuwa na amani na utulivu, riziki yake ikaufikia kwa wingi kutoka kila mahala, lakini ukazikufuru neema za Mwenyezi Mungu kwa hiyo Mwenyezi Mungu akauonjesha vazi la njaa na khofu kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyafanya.” (Sura Nahli: 112) Linalofahamika kutokana na Aya hii ni kuwa amani na utulivu, harakati zinazolenga uhusiano kati ya jamii ya watu, kazi, uzalishaji, raha na kuwepo bidhaa kwa wingi, na kutawala kwa amani kwa sura zake zote, mambo yote haya na mengine yanayofanya mambo yawe salama, yamekuja kwa sababu watu wa mji wamejibidiisha kushukuru kwa vipengele vyake kiutendaji, mfano wa uadilifu, upendo na usawa. Lakini mara tu mji ulipotupilia mbali kanuni hizi na wala haukumfanya Mwenyezi Mungu kuwa 17


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:36 PM

Page 18

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu mhimili wa nguvu na uhai wake, mji ukakufuru tawhidi iliyochomoza ya hapo mwanzo na kuibadilisha tawhidi kwa miungu mingi, kama kumfuata mtu mwenye nguvu, au kuitii nafsi na Shetani, kupenda mali, madaraka, basi viambato hivi viliishia kwenye mgao mbaya na dhuluma kuchukua nafasi na kukosa utulivu na kuenea kwa hofu, ufakiri na utabaka, na haitohesabiwa kuishi katika mji huu kama kuna maisha ya furaha kabisa. Ukafiri, ufasiki, unafiki na msimamo wowote kifikra au kimwenendo kutoka kwa mwanadamu, ni natija ya kuendelea kwa taathira ya yanayomzunguka, wala si sahihi kuyabana mas’ala upande wa maada wa matendo ya mwanadamu. Bali pia inaingia misimamo ya kiroho na ya kiitikadi katika wigo huu pia, kwa kuwa itikadi ni kitendo, hivyo basi ukafiri ambao ni tendo la ndani kwa ndani lina taathira yake nje kwa wale waliozunguka miongoni mwa viumbe wengine, na mwenendo wa binadamu uko chini ya utii wa maamuzi yake ya kiitikadi ya ndani, kwa ajili hiyo malaika wanauliza kuhusu kiumbe huyu mpya Adam kupitia uambatanaji wake kati ya ufasiki na tendo la kumwaga damu, ambayo ni natija ya utashi, na jinsi atakavyokuwa, kuanzia uhai wake na harakati zake ardhini hadi jinsi ya kuamiliana kwake na ulimwengu kwa jumla, kwa kuwa wao ndani ya maalumati zao ni kuwa ulimwengu uko chini ya utii wa nidhamu moja ya kilimwengu, kulingana na wote wanavyofanya kazi. Na hapana budi huyu kiumbe aliyetokea ulimwenguni awe na uwiano na nidhamu yake. Na maadamu ameazimia njia itakayomfanya awe mwenye kuweza kwenda kinyume na nidhamu ya kilimwengu, hivyo italeta natija ya umwagaji damu uharibifu na maangamizi katika ulimwengu huu, kwa kuwa vurugu huwa kwa kuwepo utashi ambao pengine husababisha kufuru na uwezekano wa kuirarua nidhamu na kujitanda nayo. Hivyo huyu kiumbe mpya ni hatari si kwa nafsi yake tu, bali kwa ulimwengu wote:

18


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:36 PM

Page 19

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu

“Je, utamweka humo atakayefanya uharibifu humo na kumwaga damu” (Sura Baqarah: 30) Lakini Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alirekebisha ishkali na swali hili ambalo malaika waliibainisha wakikinza kutawalishwa kiumbe huyu hatamu za ukhalifa, akasema:

“Hakika Mimi najua msiyoyajua. Na akamfundisha Adamu majina yote.” (Sura Baqarah: 30-31) Alimtengeneza kiumbe huyu na alimpa baadhi ya elimu yenye uiano na mambo muhimu ya kiungu ambayo yanamsaidia kuthibitisha malengo, hivyo elimu ya mwanadamu ya majina yote ni hiba kutoka Kwake (s.w.t.). Alimjulisha ukweli wa vitu na kumjulisha ulimwengu wote na nidhamu zinazohukumu humo. Kisha ni nini nafasi yake katika kuwepo huku na anaathiri vipi ili kuutumia kwa lengo la kuutumikisha kwa ajili ya malengo na shabaha yake njema

“Na kila kitu tumekihifadhi katika daftari lenye kubainisha.” (Sura Yaasin: 12) Na kuiweka elimu hii kwa ambaye atakuwa baada yake mpaka msululu wa manabii (a.s.) na kumfikia wa mwisho wao Muhammad (s.a.w.w.) na baada yake mlolongo wa walio tohara miongoni mwa Aali zake (a.s.). 19


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:36 PM

Page 20

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Kwa elimu hii maasumu huudiriki ukweli wa vitu kama vilivyo, na kwa uoni wa wazi, na kwa sura isiyo na shaka. Hivyo basi elimu yenye sifa hii pembuzi lazima inafikisha kwenye umaasumu. Ili kuileta karibu taswira hii mfano wake ni: Kanuni ya mvutano – gravitation, ni moja ya kanuni zilizopo ulimwenguni, hapa ina uhusiano na mwanadamu, kwa hiyo ni juu ya mwanadamu afanye kulingana nayo na ajihadhari kufanya kinyume chake, kama ambavyo uhusiano kati ya kanuni hii na mwanadamu watofautiana na uhusiano wake na baadhi ya viumbe mfano wa ndege, kwani ndege huirarua kanuni hii kwa ajili ya maslahi, au sema kuwa: Kanuni hii kwa upande mwingine ina uhusiano na ndege unaotofautiana na wa mwanadamu. Hivyo mwanadamu hujiepusha afanyavyo ndege kwa kurarua kwake kanuni hii, kwa kuwa athari zilizo kwenye ratiba ya mwanadamu sio zile zilizopo kwenye ratiba ya ndege. Hivyo basi elimu ya mwanadamu ya kanuni hii na upande wa kuirarua kwake ndiyo ambayo imemtunukia umaasumu ili asifanye kinyume chake, vinginevyo mwanadamu ana utashi katika kukhalifu na kufanya mfarakano. Kisha kuna kanuni zingine zina kinyume chake kwa maisha ya mwanadamu, huenda mwanadamu akazitambua, lakini huenda asitambue athari zake na kinyume chake, kwa kuwa yeye hamiliki elimu na uoni wa athari zitokanazo na kitendo cha kuziendea kinyume. Mfano wa kula mali ya yatima. Qur’ani tukufu inasema:

“Hao hawali matumboni mwao ila ni moto.” (Surat al-Baqarah:174). Maasumu anamiliki elimu anaona kuwa katika mali ya yatima kuna moto, na asiye maasumu huiona kuwa ni mali anajipatia ladha kwayo wala haoni kuwa ni moto uunguzao. Kwa maasumu kuna elimu na uwazi wa kuwa tendo hili lina athari kama ambavyo sisi tunaona na kutambua kanuni ya 20


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:36 PM

Page 21

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu mvutano –gravitation - ambayo imetufanya sisi tujizuie kuikhalifu pamoja na kuwepo katika sisi uwezo wa kuikhalifu. Ama athari zitokanazo na kula mali ya yatima, hatuzijui, yaani hakika sisi hatumiliki elimu ambayo kwayo tunaziona kanuni za vitu vyote vilivyopo. Yusufu (a.s.) alikuwa anaweza kufanya ufuska kwa kuwa alikuwa anamiliki utashi ulio huru wa kutenda, ila tu ni kuwa Yusufu alikuwa anaiona zinaa kuwa ni ufuska, kwa mujibu wa uwazi wake na elimu yake ya kanuni hii, maana yake sio kuwa yeye alikuwa hamiliki ladha ya kujamiana, wala utashi kama vile ukuta, bali yeye anayo elimu ya athari ya kanuni hizi, kwa hiyo kamwe hafanyi kinyume. Kutokana na hali hiyo tunawakuta wafuasi wa Ahlul-Bayt (a.s.) wanasema kuwa maimamu wao wote ni maasumu wamehifadhika, akiwemo Imam al-Jawwad (a.s.) japo alikuwa bado yu mdogo, kijana wa miaka saba. Yeye alikuwa mjuzi wa kila kitu, sio mjuzi wa hukumu za swala, Hijja peke yake, bali ni wa kila kitu, wala hamuasi Mwenyezi Mungu (s.w.t.). Wala maadui zake waliokuwa wanamiliki utawala wakati ule hawakukosea walikuwa wanajua kuwa Shia wa Ahlul-Bayt (a.s.) wana rai hii, yaani hiyo si itikadi ya siri au ya kifichoficho, walikuwa wanajua kuwa Shia wa Ahlul-Bayt (a.s.) wanasema kuwahusu Maimamu wao (a.s.) kauli hii. Dola na vyombo vyake pamwe na majaribio yake, kila ilipojaribu kuukadhibisha ukweli huu haikufanikiwa. Walimleta Imam al-Jawad (a.s.) naye akiwa ni mtoto na waliwakusanya wanazuoni wakuu miongoni mwao Kadhi Yahya bin Akhtam, na akaketi mahali pake (kama Kadhi) na akamgeukia Imam al-Jawadu (a.s.) akisema: “Ewe mwana wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) nikuulize?” Imam (a.s.) akamwambia: “Simama na ukae ukaaji wa muulizaji kwa amuulizaye!” Yahya Bin Aktham akasimama na mmvi zake, na akakaa kwa adabu mbele ya Imam (a.s.) ukaaji wa muulizaji kwa muulizwa.

21


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:36 PM

Page 22

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Yahya Bin Aktham alifikiri nini amuulize Imam (a.s.)? Je amuulize kuhusu swala na hukumu zake? Hali akiwa anajua kuwa Imam (a.s.) na famili yake wanatekeleza wajibu wa swala kila siku. Kwa hiyo, hivyo basi yeye atakuwa ajua swala na hukumu zake. Alifikiri kuwa je huyu mtoto yuko Baghdadi hajaenda Hijja, kwa kuwa faradhi ya Hijja mtu huitekeleza mara moja kwa umri wake ikiwa wajibu, na akipewa tawfiki ataifanya – kwa mfano – mara kumi. Kisha kwa kweli Imam (a.s.) angali mtoto hajapata kwenda Hijja, akamwambia: “Ewe mwana wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) wasema nini kuhusu mtu aliye katika Ihramu na ameua windo?” Imam (a.s.) alimjibu: “Aliua akiwa nje ya Haram10 au ndani ya Haram, huyu aliyehirimia alikuwa anajua au hajui, alimuuwa makusudi au kwa bahati mbaya. Aliyehirimia alikuwa huru au mtumwa, mtoto au mkubwa, kuuwa kwake ni kwa mara ya kwanza au anarudia, ni katika ndege kilikuwa kiwindo au kitu kingine, kilikuwa kiwindo kikubwa au kidogo, ni mwenye kuendelea na alilofanya au mwenye kujuta. Uuwaji wa kiwindo ulifanyika usiku au mchana, alikuwa amehirimia Umra au Hija?”11 Yahya Bin Aktham alitahayari na hali ya kushindwa ilibainika usoni kwake na kuhemewa, kisha Imam alijibu mas’ala kama ilivyofafanuliwa katika vitabu. Tukio hili linaashiria kuwa Imam (a.s.) anamiliki umaasumu ulioelekezwa vyema uliodhamini elimu ya kutunukiwa.12 Na elimu ambayo Imam maasumu anamiliki na kwayo anadhibiti maarifa ya vitu, na kwayo yanatimia malengo ya Risala, ni ya kutunukiwa na Yeye 10 Ni eneo maalumu linalouzunguka msikiti mtakatifu huko Makka. Eneo hili lina sheria zake kutokana na utakatifu wake. 11 Biharul-Anwar cha al-Majlisiy Juz. 5, Uk. 76, nukuu kutoka al-Ihtijaj. 12 Rejea Al-Ismatu Washurutul-Hifadh Alan-Nidham. Utafiti wa Sayyid Mahdi al-Hakiim. Na uchunguzi kuhusu uimam, wa Sayyid Kamalu al-Haydariy. Na uchunguzi kuhusu uimamu na uwalii, wa kundi la wanazuoni. 22


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:36 PM

Page 23

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu (s.w.t.), bila ya Imam kuichuma, kwa lengo la Imam awe na uwezo timilifu wa kulifanya lengo la kiungu litimie, lengo ambalo yapasa litekelezwe kwa namna iliyo kamili mno, na ishinde dini zote.

“Ni mjuzi wa siri wala hamdhihirishii yeyote siri yake. Isipokuwa Mtume aliyemridhia, basi hakika yeye humuwekea walinzi mbele yake na nyuma yake.” (Surat Al-Jinni: 26 -27) Na elimu apewayo Imam kwa sababu yeyote iwayo, sawa iwe kwa Ilham au kwa kusikilizishwa au kwa kuelimishwa na Rasul – na yaenda mpaka kwenye maarifa ya ghaibu – hiyo sio elimu ambayo ni mahsusi Kwake (s.w.t.). Hiyo inapatikana hata kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu na hata malaika waliokurubishwa na manabii waliotumwa na hiyo ndiyo ghaibu ya moja kwa moja. Kwa ajili hiyo elimu ya kupewa hutimia imma kwa sura ya kujielimisha isiyo ya kawaida, kama ilivyo katika vitabu vya kiungu vilivyoteremshwa kwa Mitume wake kupitia Malaika wa wahyi, navyo vinadhamini hukumu na kuhabarishwa matukio yaliyopita na yaliyopo hata na yajayo kwa kila Nabii kulingana na aina ya risala yake. Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anasema:

“Hao Mitume tumewatukuza baadhi yao kuliko wengine. Katika wao wako ambao Mwenyezi Mungu alisema nao, na baadhi yao amewatukuza daraja nyingi.” (Surat al-Baqarah 253.). Au itimie kwa njia ya matendo mfano wa miujiza, hivyo hutendeka mkononi mwake, wala Mtume hapati ila thamani yake kimatendo. Ama 23


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:36 PM

Page 24

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu ukweli wake kielimu huenda asiumiliki wala kuufahamu, na huenda akaupata kama vile ukweli wa kuhuisha maiti, wenyewe ni miongoni mwa ghaibu mahsusi Kwake (s.w.t.), lakini haizuiliki kumwelimisha mwingine na kuwapatia baadhi ya Mitume wake, kama ilivyokuja kumhusu Ibrahiim Khalili (a.s.). Amesema (s.w.t.): “Na Ibrahim aliposema: Mola wangu Mlezi nioneshe jinsi unavyohuisha mauti…’’ (Surat Al-Baqarah:260). Elimu ya Imam inatofautiana na elimu ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwa kuwa elimu Yake (s.w.t.) ni ya milele na ni yenye kuvitangulia vijulikanavyo, nayo ni dhati yake. Ama elimu ya kutunukiwa ya Imam haishirikiani na elimu ya Mwenyezi Mungu kwa lolote miongoni mwa mambo haya, kwa kuwa elimu ya Imam ni ya kutukia na ni yenye kutanguliwa na vijulikanavyo. Nayo siyo dhati katika yeye, kuhudhuria kwake kwa Imam maana yake ni kufichuka kwa vijulikanavyo kivitendo mbele yake, wala hashirikiani na Mwenyezi Mungu katika elimu yake. Na kauli ya kushirikiana na kuwa kitu kimoja kati ya elimu hizi mbili ni miongoni mwa kauli ya ushirikina na uvukaji mipaka, ambayo hawaisemi Maimamu wenyewe (a.s.) sembuse wafuasi wao. Na muhtasari wa kauli ni kuwa elimu Yake (s.w.t.) ni ya dhati na elimu ya Imam ni ya kuzuka na ya hiba na ya kutunukiwa kutokana na Yeye (s.w.t.), hakuna umoja kati ya elimu mbili hizi. Ikiwa elimu ya ghaibu ya moja kwa moja ni Yake (s.w.t.) na huitoa hiba kwa ampendae kwa waja wake mahsusi. Je kuna yeyote miongoni mwa hao mahsusi aliepata elimu ya ghaibu na kuitendea kazi? Jibu la swali hili na lingine litakuwa katika kifungu cha maneno kijacho.

24


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:36 PM

Page 25

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu

MLANGO WA TATU MSIMAMO WA QUR’ANI NA SUNNA KUHUSU ELIMU YA GHAIBU Elimu ambayo Imam maasumu anaimiliki na kadiri yake na sanadi yake haiwezi kuthibitishwa ila kwa njia ya nukuu iliyokuja katika Kitabu na Sunna sharifu. Kwa kuwa si katika uwezo wa akili peke yake kuipata kwa kuikanusha na kuithibitisha, kwa kuwa kuthibitisha inalazimu kuelezea habari za ghaibu. Kutokana na hali hiyo tutaijadili mas’ala hii katika mipaka yake ya nukuu kupitia mambo kadhaa: Jambo la kwanza: Aya zinazohadithia elimu ya ghaibu katika maisha ya manabii na watu wema: Qur’ani tukufu inauchukua ukweli huu katika maisha ya manabii na watu wema kwa maelezo na kwa mkazo. Kwa kuwa tunawakuta wao (a.s.) walimiliki uwezo wa kuijua elimu ya ghaibu kwa idhini Yake (s.w.t.) na waliitumikisha kwa maslahi ya Risala, na mifano katika hiyo yakujia: 1. Yusufu (a.s.) aliwaambia ndugu zake: “Nendeni na kanzu yangu hii na mumwekee usoni baba yangu, atakuwa mwenye kuona” (Sura Yusufu: 93). Halafu (s.w.t.) alitoa habari ya yaliojiri baada ya hivyo, amesema:

“Basi alipofika mtoaji wa habari njema, akaiweka mbele ya uso wake, mara aliona.” (Sura Yusufu: 96). 25


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:36 PM

Page 26

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Kwa kweli dhahiri ya Aya hii inajulisha kuwa Nabii Ya’qub (a.s.) alirudisha uoni wake kikamilifu kwa uwezo wa ghaibu ambao aliufundisha Yusuf (a.s.) na aliutumikisha kwa lengo hilo. Na ni wazi kuwa kuurudisha Ya’qub (a.s.) uoni wake haikuwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa sura ya moja kwa moja, bali hilo lilitimia kwa idhini Yake (s.w.t.) kupitia Nabii Yusuf (a.s.). Kwa hakika Nabii Yusuf (a.s.) alikuwa ndio sababu ya kurudi kwa uoni wa macho ya baba yake, lau si hivyo asingewaamuru ndugu zake waende na kanzu yake na waitupe usoni kwa baba yao, bali ilikuwa inamtosha Yusuf (a.s.) amuombe Mwenyezi Mungu tu (s.w.t.) kwa hilo. Kwa kweli kitendo hiki cha ghaibu kimetoka kwa mmoja wa mawalii wa Mwenyezi Mungu, naye ni nabii Yusuf (a.s.), aliibadilisha njia ya kawaida kwa idhini Yake (s.w.t.), na hawezi kufanya kitendo kama hiki ila yule ambaye Mwenyezi Mungu amemtunukia mamlaka ya ghaibu. 2. Tunasoma kuwa Musa (a.s.) kwa fimbo yake analipiga jiwe, kutokana na kipigo hicho zimeibuka chemchemu kumi na mbili. Amesema (s.w.t.):

“Tukasema: Lipige jiwe kwa fimbo yako, mara zikabubujika humo chemuchem kumi na mbili” (Sura Baqarah:60). Kama ambavyo Musa aliutumikisha uwezo wake wa ghaibu mara nyingine alipopiga bahari kwa fimbo yake ili afungue chini ya mkondo wa bahari na katika ardhi yake njia kavu kumi na mbili kwa ajili ya wana wa Israeli, ili waipite na kuivuka bahari. Amesema (s.w.t.):

26


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:36 PM

Page 27

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu

“Mara tulimpelekea wahyi Musa: Piga bahari kwa fimbo yako. Mara ikatengana, na kila sehemu ikawa kama mwamba mkubwa.” (Sura Ash-shuraa-: 63). Katika sehemu mbili hizi Nabii Musa (a.s.) alifaidika na uwezo wake wa ghaibu aliotunukiwa na ambao wote ulitimia kwa idhini ya Mwenyezi Mungu na irada yake. 3 . Nabii Sulayman alikuwa anafaidika na uwezo wake mbalimbali wa ghaibu, na alikuwa na mamlaka juu ya majini, ndege, na alikuwa ajua matamshi ya ndege na lugha za wadudu wadogo wadogo. Anasema (s.w.t.):

“Na Sulaiman alimrithi Daud na akasema: Enyi watu! Tumefundishwa usemi wa ndege na tumepewa kila kitu, hakika hii 27


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:36 PM

Page 28

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu ndiyo fadhili dhahiri. Na alikusanyiwa Sulaiman majeshi yake kutoka katika majini na watu na ndege, nayo yakawekwa makundi makundi. Hata walipofika katika bonde la wadudu chungu, akasema mdudu chungu: Enyi wadudu chungu! Ingieni majumbani mwenu, asikupondeni Sulaimani na majeshi yake, hali hawatambui. Basi akatabasamu akichekea kauli yake, na akasema: Ee Mola wangu Mlezi! Nipe nguvu nishukuru neema yako uliyonineemesha mimi na wazazi wangu, na nipate kufanya vitendo vizuri uvipendavyo, na uniingize kwa rehema zako katika waja wako wema.” (Sura Namli: 16-19) Na Nabii Suleyman alikuwa na uwezo wa ghaibu yenye uwezo wa kuushinda upepo kwani ulikuwa unakwenda kwa amri yake apendako. Amesema (s.w.t.):

“Na kwa Sulaiman upepo wa nguvu uendao kwa amri yake kwenye ardhi ambayo tumeibarikia, nasi ndio tunaokijua kila kitu.” (Sura Anbiyai: 81) Mwenye kuchunguza ataona kuwa upepo waenda kwa amri yake, hii ni dalili ya kuwa Sulayman (a.s.) anayo mamlaka katika mwenendo na mapito ya upepo.13 Je hii elimu ya ghaibu ambayo Mwenyezi Mungu aliwatunukia manabii na watu wema miongoni mwa waja wake, aliwapa kwa ajili ya jambo muhimu tu makhsusi na la maslahi yenye kikomo, halafu huenguliwa elimu hiyo mbali nao? Au ni kwamba elimu hii ya ghaibu iliyotunukiwa Imam au Rasuli anaimiliki kwa namna ya kuendelea na kudumu kulingana na kudumu kwa umuhimu alionao na wingi wa majukumu ya risala yake? 13 Al-Wahabiya Fil-Mizaan Uk. 323. 28


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:36 PM

Page 29

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Baadhi wanatambua kuwa kwa Mitume kumetokea muujiza, na kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amewapa miongoni mwa elimu ya ghaibu ambayo kwayo watathibitisha usahihi wa risala. Ila tu upewaji huu ni tukizi na wa kikomo watokea pindi maslahi yapo, na hauwi thabiti daima. Na baadhi wameushabihisha na bomba la maji ambalo hufunguliwa pindi yanapokuwepo maslahi na baada ya hapo hufungwa. Ni sahihi kwao ni kuwa Rasul anao uwezo wa ghaibu na tendo la muujiza ila tu ni makhsusi kwa tukio maalumu. Ama wakati mwingine hamiliki uwezo huu. Lakini sahihi ni kuwa uwezo wa manabii na kumiliki kwao elimu ya ghaibu waliyotunukiwa unakuwa wa namna ya kudumu na kuendelea, na kuna Aya zaidi ya moja zathibitisha hilo, miongoni mwazo ni kauli Yake (s.w.t.):

“Hakika mimi nimewajieni na dalili itokayo kwa Mola wenu. Mimi nakufanyieni katika udongo kama namna ya ndege, kisha napulizia ndani yake anakuwa ni ndege kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na nawapoza vipofu na wenye mbalanga, nawafufua wafu kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. (Sura Ali Imran: 49) Aya hii inathibitisha kuwa uwezo wa Isa (a.s.) kufanya miujiza na kuwezeshwa kwake, hayo sio mahsusi kwenye tukio maalum, kwani yeye hakusema: Nilikuumbieni ndege na nilikuponyesheeni kipofu wa kuzaliwa na mwenye ukoma na nimekuhuishieni maiti, ili tufahamu kuwa anakusudia tukio maalumu, lililotokea wakati uliopita. Kadhalika hakusema nitakuumbieni ndege na nitakuponyesheeni kipofu wa kuzaliwa na mwenye ukoma na kukuhuishieni maiti, ili tufahamu kuwa yeye atafanya matendo haya katika wakati maalumu, wakati ujao kwa namna ya tukio lisilotazamiwa. 29


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:36 PM

Page 30

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Bali alieleza kwa kitenzi cha wakatis wa kawaida – present simple – na akajaalia wahusika ni jinsi ya ndege na kipofu wa kuzaliwa, mkoma na maiti. Yeye (a.s.) alisema:

Mimi nakufanyieni katika udongo kama namna ya ndege, kisha napulizia ndani yake anakuwa ni ndege kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na nawapoza vipofu na wenye mbalanga, nawafufua wafu kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. (Surat Ali Imran: 49) ifidishayo kuwa yeye ni mwenye kuivaa hali hii kwa kudumu, na kuwa yeye ni muweza wa kutenda vitu hivi wakati wowote aupendao.14 Na amesema (s.w.t.) akielezea kumhusu Sulayman (a.s.).

“Akasema: Mola wangu Mlezi! Nisamehe na unipe ufalme, asiupate yeyote baada yangu, bila shaka wewe ndiye Mpaji. Basi tukamtiishia upepo ukaenda pole pole kwa amri yake anakotaka kufika.’’ (Sura Swad: 35 - 36) Hivyo kuufanya upepo umtii Sulayman (a.s.) ni jibu la dua na ombi lake.

14 Al-Wilayatut-Tak’winia Baynal-Kitabi Was-Sunna cha Hisham Shariy alAamiliy Uk. 107. 30


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:36 PM

Page 31

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Aliposema: “Na unipe ufalme, asiupate yeyote baada yangu’’ (Sura Swad: 35 - 36) Na ni kawaida kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) hakuipatia jibu dua ya Sulayman (a.s.) kwa ajili ya muda mmoja mfupi na katika tukio moja maalumu. Hivyo kuutiisha upepo ilikuwa ni katika jumla ya ufalme ambao Mwenyezi Mungu alimtunukia Sulayman (a.s.), ikiwa ni natija ya dua yake na ni ile ambayo Mwenyezi Mungu aliitaja baada ya hivyo kwa kauli yake: “Hiki ndicho kipawa chetu bila ya hesabu, basi fanya ihsani au zuia.”

(Sura Swad: 39) Kwa mujibu huo uwezo wa Sulayman (a.s.) juu ya harakati na mienendo ya upepo ulikuwa kwa amri yake, ilikuwa imethibiti kwake daima kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.). Na amesema (s.w.t.): “Na tukamlainishia chuma.” (Sura Sabai: 10). Kwa kweli kumlainishia chuma Daudi (a.s.) hakukuwa kwa namna isiyotazamiwa na wala sio tukio maalumu, na si kwa sababu makhsusi, bali hiyo ilikuwa fadhila ya daima Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alimpa. Na hilo ndilo Aya tukufu imelisema waziwazi: “Na kwa hakika tulimpa Daudi fadhila kutoka kwetu, enyi milima

nyenyekeeni pamoja naye, na ndege, na tukamlainishia chuma.” (Sura Sabai: 10) Imebaki tujue kuwa je hii haiba ya kiungu ya daima ya elimu ya ghaibu, je hiba yake ni kwa ajili ya manabii tu, au inawaenea wasiokuwa wao miongoni mwa waja wake wema? Qur’ani tukufu imesema waziwazi kuwa hii hiba ya kiungu haiishii kwa manabii tu, bali Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amewatunukia awaridhiao miongoni mwa waja wake wema, amesema 31


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:36 PM

Page 32

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu (s.w.t.): “Akasema: Enyi wakuu wa baraza! Ni nani atakayeniletea kiti chake

cha enzi kabla hawajafika kwangu, hali ya kuwa wamekwishakusilimu? Akasema Ifriti katika majini: Mimi nitakuletea hicho kabla hujasimama kutoka mahala pako, na mimi bila shaka ninazo nguvu za hayo, mwaminifu. Akasema yule aliyekuwa na elimu ya Kitabu: Mimi nitakuletea hicho kabla ya kupepesa jicho lako.”(Sura Namli: 38 – 40) Kwa kweli Aswifu alikuwa anatoa khabari ya uwezo wake juu ya hilo kwa kauli Yake (s.w.t.): “Mimi nitakuletea hicho”, yaani mimi ni muweza wa kukileta, hasa pamoja na kulizingatia swali la Sulayman (a.s.) na ombi lake kwa awezaye kufanya hivyo, kwa kauli yake: “Ni nani atakayeniletea kiti chake cha enzi”. Zaidi ya hapo ni kuwa Mwenyezi Mungu amemtaja kwa sifa yake, aliposema: “Akasema yule aliyekuwa na elimu ya Kitabu”, kumtaja kwa sifa hii kunaleta mwanga wa kuwa sababu ya uwezo ni ile ile elimu ya kitabu. Na hilo ndilo linalotiliwa mkazo na riwaya za Ahlul-Bayt (a.s.), endapo Aswifu hajasahau elimu hii basi yeye ni muweza juu ya hilo daima na kila apendapo.15

Jambo la pili: 15 Al-Wilayatut-Tak’winia Baynal-Kitabi Was-Sunna Uk. 107. 32


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:36 PM

Page 33

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu

Aya ambazo zinaifunga elimu ya ghaibu kwake Yeye tu (s.w.t.), na kukanusha kuwanayo mwingine yeyote asiyekuwa Yeye: Tumesema katika yaliyotangulia kuwa elimu ya ghaibu inafanya jambo linalotambulika katika maisha ya manabii na watu wema. Basi Aya zinazoweka mabano kuwa elimu ya ghaibu ni Yake tu (s.w.t.) na zinakanusha kuwanayo wengine zinamaanisha nini? Amesema (s.w.t.): “Sema: Hakuna aliyoko katika mbingu na ardhi ajuaye ghaibu ila

Mwenyezi Mungu tu, na wao hawajui ni lini watafufuliwa.” (Sura anNaml: 65). Na amesema: “Na ziko kwake funguo za ghaibu, hakuna azijuaye ile Yeye.’’ (Sura

An’aam:59). Na amesema:

“Wala sikuwambieni kuwa nina hazina za Mwenyezi Mungu, wala kuwa najua ghaibu.” (Sura Hud: 31).

33


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:36 PM

Page 34

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Na amesema:

“Na ni vya Mwenyezi Mungu tu vyote vilivyo ghaibu katika ardhi na mbingu, na mambo yote yatarejeshwa kwake.” (Sura Hud: 123) Na amesema (s.w.t.)

“Siku ambayo Mwenyezi Mungu atawakusanya Mitume awaambie: Mlijibiwa nini? Watasema: Hatujui, bila shaka wewe ndiye ujuaye ghaibu.” (Sura Maida:109). Sehemu hii ya Aya ambazo zinaibana elimu ya ghaibu kwake Yeye tu (s.w.t.) hazipingani na Aya ambazo zinathibitisha elimu ya ghaibu kwa asiyekuwa Yeye (s.w.t.), kwa kuwa utaratibu wa Qur’ani ulioenea katika kubainisha vitendo vya kiungu mfano wa kuumba, kuruzuku, umauti, huwa wategemea kukanusha upande na kuthibitisha upande mwingine. Mfano wa hayo ni kauli Yake (s.w.t.): “Mwenyezi Mungu hupokea roho wakati wa mauti yao” (Sura Zumar: 42) inavyomaanisha kulingana na dhahiri ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) hutenda mwenyewe. Na hapo hapo aonyesha kuwepo kiunganishi kwa kauli Yake (s.w.t.): “Sema: Atakufisheni Malaika wa mauti aliyewakilishwa kwenu” (Sura Sajdah:11), ambayo yajulisha kuwepo na njia au kiunganishi, ila mazingatio yanatufanya tuitakidi kuwa Aya ya kwanza inathibitisha upande, na ya pili yathibitisha upande mwingine. Hivyo kupingana hakupo, wala kuthibitisha na kupinga hakupo.

34


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:36 PM

Page 35

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Kwani Aya ya kwanza inathibitisha kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anazifisha nafsi kwa namna ya asili na Aya ya pili yathibitisha kuwa malaika wa umauti anazifisha nyoyo kwa namna ya kumfuatia Mwenyezi Mungu (s.w.t.), Mwenyezi Mungu ndiye anayezifisha nyoyo kwa njia ya malaika wa umauti kwa mujibu wa Aya mbili pamoja. Suala liko hivyo kuusiana na elimu ya ghaibu. Hivyo lile kundi la Aya linaloibana elimu ya ghaibu kwa Mwenyezi Mungu tu (s.w.t.) hilo linaangalia kwenye elimu yake ya dhati ya milele ambayo ni makhsusi kwa Mwenyezi Mungu tu (s.w.t.). Ama kundi linalozungumzia elimu ya ghaibu kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) hilo lazungumzia elimu isiyo ya dhati, nayo ni ile anayoigawa Mwenyezi Mungu kutoka katika elimu ya ghaibu kwa anayemchagua miongoni mwa waja wake, ili amjulishe baadhi ya hakika, hivyo basi hakuna kupingana kati ya haya makundi mawili. Jambo la tatu: Aya ambazo zinathibitisha uwezekano wa elimu ya ghaibu kwa asiyekuwa Yeye (s.w.t): Limekuja kundi la Aya katika Qur’ani tukufu linaongelea kuhusu uwezekano wa elimu ya ghaibu kwa asiyekuwa Yeye (s.w.t.), mfano wa kauli Yake (s.w.t.)

“Je, nikufuate ili unifundishe katika ule mwongozo uliofundishwa?” (Sura Kahf: 66) Na amesema:

35


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:36 PM

Page 36

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu

“Akasema: Hakika wewe huwezi kuvumilia kuwa pamoja nami. Na utawezaje kuvumilia yale usiyoyajua hakika yake?” (Sura Kahf: 67-68 ). Na amesema:

“Na lau kama ningelijua ghaibu bila shaka ningejizidishia wema mwingi.” (Surat A’araf: 188) Na amesema:

“Na sema: Ewe Mola wangu Mlezi nizidishie elimu.” (Sura Twaha: 114) Hivi punde tulifikia kuwa elimu ya ghaibu ni makhsusi Kwake (s.w.t.) na Yeye huwapa hiba miongoni mwayo amtakaye, wala hapana kupingana katika kukanusha na kuthibitisha kati ya elimu mbili hizo, kwani kwa uchambuzi huu kupingana kunatoweka kati ya Aya ambazo zinaiwekea wigo elimu ya ghaibu Kwake tu (s.w.t.), na zile ambazo zinaongelea uwezekano wa elimu ya ghaibu kwa asiyekuwa Yeye (s.w.t.). Kwa hakika Aya ambazo zinaongelea kutoa kwake elimu ya ghaibu kwa asiyekuwa Yeye, zinafidisha kuwa elimu hupatikana kwa idhini yake na irada yake na kwa ridhaa yake, wala haiko nje ya mambo Yake (s.w.t.) kwa hali yoyote ile.

36


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:36 PM

Page 37

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu

Jambo la nne: Aya zinazothibitisha kumpa elimu ya ghaibu Hitimisho la Mitume (s.a.w.w.): Tulitaja kundi la Aya linalothibitisha uwezekano wa kupatikana kwa elimu ya ghaibu kwa baadhi ya waja, na pia tukasema linalothibitisha kuitoa kwake elimu ya ghaibu kwa asiyekuwa Yeye (s.w.t.), mfano wa kauli Yake (s.w.t.):

“Na akamfundisha Adamu majina yote.” (Surat Baqarah: 31) Na kauli yake:

“Akasema: Hakitakufikieni chakula mtakachopewa isipokuwa nitakuambieni hakika yake kabla hakijakufikieni.” (Sura Yusufu: 37) Na kauli yake:

“Na hakuna ajuaye tafsiri yake ila Mwenyezi Mungu na wale waliozama katika elimu tu. “(Sura Imran:7) Kwa muktadha huu huu kuna kundi la Aya zinataja kumpa elimu ya ghaibu Hitimisho la Manabii (s.a.w.w.), mfano wa kauli yake:

37


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:36 PM

Page 38

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu

“Wala hasemi kwa matamanio. Hayakuwa haya ila ni Wahyi uliofunuliwa.” (Sura Najmi: 3-4) Na kauli Yake (s.w.t.):

“Tutakusomesha wala hutosahau.” (Sura Aala: 6) Na kauli yake:

“Hizo ni habari za ghaibu tunazokufunulia.” (Sura Aali Imran: 44) Na kutoka kwa Imam al-Baqir (a.s.) kuwa yeye alisema: “La wallahi mwanachuoni hawi mjinga kamwe. Mjuzi wa kitu na si mjuzi wa kitu (kingine). Mwenyezi Mungu ni Mtukufu na Mwenye nguvu mno si wakufanya faradhi ya utii wa mja ambaye anamficha mbingu zake na ardhi zake.”16 Na kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s.), alisema: “Kwa kweli Mwenyezi Mungu amemfunza adabu Nabii wake, akaifanya adabu yake kuwa nzuri, na alipomkamilishia adabu akasema: “Na bila shaka una tabia njema, adhimu.” (Sura Qalam: 4). Kisha alimwachia suala la dini na la umma ili awachunge waja Wake, akasema: “Na anachokupeni Mtume basi pokeeni, na anachokukatazeni basi jiepusheni.” (Sura Hashri: 6). Kwa kweli Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa mwenye kuwekwa sawa na mwenye kupewa taufiki na Roho mtakatifu, hatelezi wala hakosei kitu 16 Usulul-Kafiy Juz. 1 Uk. 262 Hadithi ya 6. 38


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:36 PM

Page 39

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu ambacho kwacho anawaongoza watu, kwa hiyo alikuwa na adabu kwa adabu ya Mwenyezi Mungu.”17 Na hii ikiwa ndio hali ya Rasul (s.a.w.w.) na Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amemtunukia elimu ya ghaibu kwa ajili ya kukamilisha risala na siasa kwa waja, na kueneza uadilifu, na alimweka sawa kwa Roho mtakatifu. Je Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ametoa hiba uwezo huu na alitoa elimu ya ghaib kwa Makhalifa wake aliowaridhia ili kukamilishia mwendo wake kutoka kwa Maimamu wa Ahlul-Bayt wake (a.s.), kutokana na lengo lile lile? Kwa kweli hili tutalieleza katika kifungu kifuatacho.

Jambo la tano: Maelezo ambayo yanathibitisha kuwapatia elimu ya ghaibu Maimamu wa Ahlul-Bayt (a.s.): Tulisema kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amewapa elimu ya ghaibu manabii wake na walio wema miongoni mwa waja wake. Na maimamu wa Ahlul-Bayt (a.s.) ndio ambao Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amewaondolea uchafu na amewatoharisha usafi kwa tamko la Kitabu na Sunna iliyo sahihi. Na kuwa wao ni makhalifa wa Mtume Wake katika kuthibitisha majukumu ya risala na malengo yake, na hii yalazimu wawe wajuzi wa yaliyo ghaibu kama alivyokuwa Mtume (s.a.w.w.) ajua hayo. Kwa mujibu huo tunamkuta Amirul-Mu’min Ali (a.s.) anasema: “Tambua, hakika elimu ambayo aliteremka nayo aridhini Adamu toka mbinguni, na yote yaliyowafanya manabii mpaka hitimisho la manabii wawe bora, yapo katika kizazi cha Hitimisho la manabii.”18 Imekuja kutoka kwa Abdillah bin Al-Waliid as-Samani, kuwa alisema: Abu Ja’far (a.s.) aliniambia: “Ewe Abdullah! Shia wanasemaje kuhusu Ali, 17 Usulul-Kafiy Juz. 1 Uk. 266 Hadithi ya 4. 18 Tafsirul-Qumiy Juz. Uk. 367. Nurut-Thaqalayn Juz. Uk. 523. 39


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:36 PM

Page 40

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Musa na Isa (a.s.)?” “Akasema: Nilisema: ‘Nimejitoa muhanga kwako; katika hali gani waniuliza?’ Alisema (a.s.): ‘Nakuuliza kuhusu elimu, amma katika ubora wao wako sawa.’ “Akasema: Nilisema: ‘Nimejitoa muhanga kwako, basi nitasema nini kuwahusu?’ Hapo (a.s.) alisema: ‘Ni yeye Allah mjuzi mno kuliko wao wawili.’ Halafu alisema: ‘Ewe Abdullah hawasemi kuwa: Ali ana yale aliyokuwa nayo Mtume miongoni mwa elimu?’ “Akasema: Nilisema: ‘Ndiyo.’ Akasema (a.s.): ‘Basi hasimiana nao katika hilo. Hakika Mwenyezi Mungu Mtukuka alimwambia Musa “Na tukamwandikia katika mbao mawaidha ya kila namna” (Sura A’araf:145). Akatujulisha kuwa hakumbainishia jambo lote. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu alimwambia Muhammad (s.a.w.w.): “Na tukakuleta wewe kuwa ni shahidi juu ya hawa?” (Sura Nisai: 41). Na akamwambia: “Na tumekuteremshia Kitabu kielezacho kila kitu.” (Sura Nahlu:89). Na amesema (s.w.t.):

“Akasema yule aliyekuwa na elimu ya Kitabu: Mimi nitakuletea hicho kabla ya kupepesa jicho lako.”(Sura Namli: 40) “Kwa kweli sababu ya uwezo wa Aswifu Bin Barkhiya kufanya yanayovuka desturi ya maumbile ya kawaida ni ile elimu ya Kitabu aliyokuwa nayo. Na hii yajulisha kuwa sababu yake ni elimu ya Kitabu wala si kitu kingine. Hivyo uwalii wake wazunguka mzunguko wa elimu ya Kitabu. Hivyo maadamu anayo elimu ya Kitabu uwalii wake unabaki imara kwake kwa kadiri hii. Na ikiwa hii ndio hali ya ambaye ana sehemu tu ya elimu ya Kitabu, basi itakuwa vipi hali ya mwenye elimu yote ya Kitabu?”

40


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:36 PM

Page 41

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Na kwa makusudi haya Imam as-Sadiq (a.s.) anampa habari Sadiiru kuhusu elimu yao ya yaliyomo katika Kitabu, akisema: “Ewe Sadiiru, haujasoma Qur’ani?” Sadiiru amjibu akimwambia: “Ndiyo nimesoma.” Imam as-Sadiq (a.s.) anamwambia: “Je umekuta katika uliyosoma miongoni mwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu: “Sema Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi kati yangu na kati yenu, na yule mwenye elimu ya Kitabu.” (Sura Raad: 43)” Akasema: Nilisema: “Nimeisoma, nimejitoa muhanga kwako.” Alisema (a.s.): “Je mwenye elimu ya Kitabu chote ni mwenye kufahamu zaidi, au mwenye baadhi ya elimu ya Kitabu?” Nilisema: “Hapana bali ni yule mwenye elimu ya Kitabu chote.” Akaashiria kifuani kwake kwa mkono wake na akasema: “Elimu ya Kitabu wallahi tunayo sisi.”19 Na Mwenyezi Mungu amesema:

“Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu watu wa nyumba, na kukutakaseni sanasana. “ (Surat Ahzab: 33) Pia amesema:

“Hakika Mwenyezi Mungu amemchagua Adam na Nuhu na kizazi cha Ibrahim na kizazi cha Imran juu ya walimwengu.” (Surat Ali Imran: 33) Kwa kuuzingatia uenezi wa kuondolewa uchafu wa maada, itikadi na wa kimatendo, na kutoharishwa mbali na aina zote za upungufu ulio dhahiri na ulio batini, na kuwa mbali na mchanganyiko uliotibuka na giza la ujinga na 19Usulul-Kafiy Juz. 1 Uk. 257 41


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:36 PM

Page 42

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu kusahau, wajulisha uenezi wa elimu yao na utendewaji kazi wake.20 Kutoka kwa Abdul Aala Bin Aayan alisema: “Nilimsikia Abu Abdillah (a.s.) akisema: ‘Kwa hakika amenipa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na mimi ni mjuzi mno wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu, ndanimwe kuna mwanzo wa kuumbwa viumbe na ambacho kipo mpaka siku ya Kiyama. Na ndanimwe kuna habari ya mbingu na ardhi, habari ya Janna, habari ya moto, habari ya yaliyokuwa na ambayo yapo. Nayajua hayo kama niangaliavyo kiganja changu, kwa hakika Mwenyezi Mungu anasema: “Humo mna ubainifu wa kila kitu.”21 Kutoka kwa Abu Baswir, kutoka kwa Abu Abdillah (a.s.) katika Hadithi. Alisema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu alimwelimisha Ali (a.s.) milango elfu, kila mlango katika hiyo wafungua milango elfu, mpaka alifikia kusema kuwa: ‘Sisi tuna Al-Jamia. Sahifa urefu wake dhiraa sabini kwa dhiraa ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), na kwa imla ya mdomo wake na hati ya Ali (a.s.) ya mkono wake wa kulia. Ndani yake mna halali zote na haramu, na kila kitu ambacho watu wanahitajia hata fidia ya kwaruzo.’ Na alinipiga kwa mkono wake, na aliniambia: ‘Waniidhinisha ewe Abu Muhammad?’ Nikasema: Nimejitoa kwako muhanga. Kwa kweli mimi ni wako, fanya upendavyo. Alinibonyeza kwa mkono wake, kisha alisema: ‘Hata fidia ya hiki (kitendo cha kukubonyeza), kama ikiwa (mtu) amekasirishwa (na kitendo hiki).”’22 Kutoka kwa al-Husain Bin Abil-Alaa. Alisema: “Nilimsikia Abu Abdillah (a.s.) akisema ‘Kwa kweli mimi nina al-Jufru nyeupe.’ Nilisema: ‘Ni kitu 20 Al-Maarifu As-Sulaymaniyah cha Ayatullahi Sayyid Abdul Husain an-Najafiy al-Lariy Uk. 60. 21 Al-Kafiy Juz. 1, Uk. 61. Kitabu cha fadhila za elimu. Mlango wa 20. Hadithi ya 8. 22 Al-Kafiy Juz. 1, Uk. 238. Kitabu cha hoja. Mlango wa kutaja Sahifa. Hadithi ya 1. 42


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 43

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu gani kipo humo?’ Alisema: ‘Zaburi ya Daud, Taurati ya Musa, Injili ya Isa na Suhufu Ibrahim, halali na haramu na msahafu wa Fatima. Sidhanii kama ndani yake kuna Qur’ani.23 Ndani yake kuna ambayo watu wanayahitajia kwetu. Wala hatumhitajii yeyote, ndani yake mna hata (fidia ya) ngozi na nusu ya ngozi, na robo ya ngozi, na fidia ya kwaruzo “24 Kutoka kwa Rub’iy bin Abdillah, kutoka kwa Abu Abdillah (a.s.) kuwa yeye alisema: “Mwenyezi Mungu amekataa kupitisha vitu ila kwa sababu, akakifanyia kila kitu sababu, na ameifanyia kila sababu ufafanuzi, na ameufanyia ufafanuzi wote elimu, na ameijalia elimu yote mlango utamkao, wameujua wenye kuujua na wamejingikiwa nao waliojingikiwa nao, mjuzi huyo ni Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na sisi.”25 Kutoka kwa Bakrun Bin Karbi as-Swayrafiy, alisema: “Nilimsikia Abu Abdillah (a.s.) akisema: ‘Kwa kweli sisi tunayo ambayo hatuhitajii kwa watu kitu pamoja nayo, na kwa hakika watu wanatuhitajia sisi, na kwa kweli sisi tuna kitabu ambacho ni imla ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na hati za Ali (a.s.), ni Sahifa ndani yake mna halali zote na haramu zote.”’26 Kutoka kwa Hisham Bin al-Hakam. Kutoka kwa Abu Abdillah (a.s.) katika Hadith ndefu, alisema: “Kwa hakika Mwenyezi Mungu hamfanyi hoja 23 Yaani: Sisemi kuwa ndani yake kuna Qur’ani, bali ndani ya al-Jufru mna elimu ya yaliyokuwa na yatakayokuwa mpaka siku ya Kiyama. 24 Al-Kafiy Juz. 1, Uk. 240. Kitabu cha hoja. Mlango wa kutaja Sahifa. Hadithi ya 3. 25 Al-Kafiy Juz. 1, Uk. 238. Kitabu cha hoja. Mlango wa kumtambua Imam. Hadithi ya 7. 26 Baswairud-Darajaat. Juz. 1, Uk. 142. Mlango wa 12 mlango usemao kuwa Maimam wanayo Sahifa al-Jamia…

43


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 44

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu katika ardhi yake aulizwe kitu na aseme sijui.”27 Kutoka kwa Suratu Bin Kulaybi, alisema: “Nilimwambia Abu Abdillah (a.s.): ‘Kwa kitu gani Imam hutoa fatwa?’ Alisema: ‘Kwa Kitabu.’ Nilisema: ‘Na ambalo halipo ndani ya Kitabu?’ Akasema: ‘Kwa Sunna.’ Nikasema: ‘Ambalo halipo ndani ya Kitabu na Sunna?’ Akasema: ‘Hakuna kitu ila kipo katika Kitabu na Sunna.’ Nilikariri mara moja au mbili, alisema: ‘Anawekwa sawa na kuafikishwa.28 Ama unayodhania hapana.”’29 Kutoka kwa al-Harth Bin al-Mughira, kutoka kwa Abu Abdillah (a.s.) alisema: “Nilimsikia akisema: ‘Hakika ardhi haiachwi bila alimu, watu wanamuhitajia wala (yeye) hawahitajii, anajua halali na haramu.”’30 Kutoka kwa Hisham Bin Salim, alisema: “Nilimwambia Abu Abdillah (a.s.): ‘Nini haki ya Mwenyezi Mungu juu ya viumbe wake?’ Akasema: ‘Waseme wanayoyajua na wajizuie na wasiyoyajua, wakifanya hivyo watakuwa wametekeleza kwa Mwenyezi Mungu haki Yake.’”31 Abu Abdillah (a.s.) alisema: “Haiwi wepesi kwenu katika yanayokuteremkieni miongoni mwa msiyoyajua, ila ni kujizuia na kuwa thabiti na kufanya rejea kwa Maimamu waongofu, ili wawachukueni humo kwenye makusudio na wawatandue humo upofu, na wawatambulisheni humo haki. Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amesema: “Basi waulizeni wenye 27 At-Tawhidu 270:1. Mlango wa 37. Mlango wa kujibu. 28 Yaani hutoka kwa Mwenyezi Mungu na si kwake yeye (a.s.). 29 Baswairud-Darajaat. Juz. 1, Uk. 387. Mlango wa maimamu huwekwa sawa na kuafikishwa 30 al-Mahasinu Juz. 1, Uk. 234. Kitabu cha taa za kuangazia giza. Mlango wa 21. Hadithi ya 194. 31 al-Mahasinu Juz. 1, Uk. 204. Kitabu cha taa za kuangazia giza. Mlango wa 4. Hadithi ya 53. 44


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 45

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu ukumbusho ikiwa nyinyi hamjui.” (Surat an-Nahl:43).”32 Kutoka kwa Abu Is’haq an-Nahawiy, alisema: “Niliingia kwa Abu Abdillah (a.s.) nilimsikia akisema: ‘Kwa kweli Mwenyezi Mungu amemfunza adabu Nabii Wake kwa mahaba Yake, akasema: “Na bila shaka una tabia njema, adhimu.” (Sura Qalam: 4). Kisha alimwachia suala la dini na la umma, akasema: “Na anachokupeni Mtume basi pokeeni, na anachokukatazeni basi jiepusheni.” (Sura Hashri: 6). Na akasema Azza wajala: “Mwenye kumtii Mtume kwa kweli atakuwa amemtii Mwenyezi Mungu.”’ “Akasema: Kisha alisema: ‘Nabii wa Mwenyezi Mungu alimwachia Ali (a.s.) suala la dini na la umma, na alimwamini, nyinyi mkakubali na watu wakapinga. Wallahi tunawapenda mseme tusemapo na mnyamaze tukinyamaza. Na sisi tuna dhamana ya yaliyopo kati yenu na Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu hakujaalia kheri kwa yeyote akiwa kinyume na amri yetu.”’33 Kutoka kwa Is’haq Bin Ammar, kutoka kwa Abu Abdillah (a.s.) alisema: “Nilimsikia akisema: ‘Hakika ardhi haitoacha kuwa na Imam, ili waumini wakiongeza kitu awazuie, na iwapo wakipunguza kitu awatimizie.”34 Kutoka kwa Ibnu Tayyar, kutoka kwa Abu Abdillah (a.s.) alisema: “Hakika Mwenyezi Mungu aliweka hoja juu ya watu, kwa yale aliyowapa na kuwatambulisha.”35 32 Al-Kafiy Juz. 1, Uk. 50. Hadithi ya 10. Mlango wa mambo ya nadra. 33 Al-Kafiy Juz. 1, Uk. 265. Hadithi ya 1. Mlango wa kuacha mambo mikononi mwa Mtume wa Mwenyezi Mungu. Kitabu cha hoja. 34 Al-Kafiy Juz. 1, Uk. 178. Kitabu cha hoja. Hadithi ya 2. Mlango wa ardhi huwa haikosi hoja. 35 al-Kafiy Juz. 1, Uk. 162. Kitabu cha Tawhidi. Mlango wa kubainisha na kutambulisha ulazima wa Hoja. Hadithi ya 1. 45


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 46

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu

Jambo la sita: Imam Ali bin Abu Talib (a.s.) na elimu ya ghaibu: Maadam Imam Ali (a.s.) ni Khalifa aliyeagizwa baada ya Rasul (s.a.w.w.) kulingana na dalili za kiakili na za kunakili zilizothibiti mahali pake, basi Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amempa Imam Ali (a.s.) sehemu ya elimu yake ya ghaibu kama alivyompa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), ili awe muweza wa kutekeleza yaliyo muhimu ya risala. Na kwa lengo hili tunataja kundi la maelezo ambayo yanatilia mkazo umiliki wake (a.s.) wa sehemu ya elimu ya ghaibu. Miongoni mwayo ni: 1. Kauli Yake (s.w.t.): “Na yule mwenye elimu ya Kitabu.” (Sura Ra’adu: 42) Kwa kuwa Jamhuri ya Ahlu Sunna wameeleza riwaya kuwa mlengwa wa Aya hiyo ni Imam Ali bin Abu Talib (a.s.).36 2. Kauli Yake (s.w.t.) “Kisha tumewapa Kitabu wale tuliowachagua miongoni wa waja wetu.” (Sura Fatir: 32) Imeelezwa kuwa ni Ali (a.s.).37 Naye ni miongoni mwa vielelezo vya wazi mno vya ambao Mwenyezi Mungu amewachagua miongoni mwa waja wake. 3. Kauli Yake (s.w.t.): “Na sikio lisikialo lisikie.” (Sura al-Haqah: 12). Jamhuri wameeleza kuwa pia imeteremka kumhusu Ali (a.s.).38 36 Shawahidut-Tanzil Juz.1 Uk. 307 cha al-Hakim al-Haskaniy. Na TawdhihudDalaili Uk. 163 cha Allama Shihabu diin as-Shiiraziy. Na an-Nuru Al-Mushtailu Uk. 125 cha al-Hafidhu Abu Nuaim Ahmad bin Abdillah as-Shafi’iy. Na TanziilulAyati Uk. 15 cha al-Hafidhu Husain al-Hibariy. Na Yanabiiul-Mawadda Uk. 103 cha Allama al-Qunduziy al-Hanafiy. Chapa ya Istanbul. Na Arjahul-Mataalib Uk. 86 na 111. Chapa ya Lahore, cha Allama Sheikh Abiidullahi al-Hanafiy. Na alJamiu Liahkamil-Qur’ani Juz. 9, Uk. 336 cha Allama Abu Abdillah Muhammad bin Ahmad al-Answariy. Na al-Itqan Juz. 1, Uk. 32 cha as-Suyutiy. 37 Shawahidut-Tanziil Juz. 2, Uk. 103. Na Yanabiiul-Mawadda Uk. 103. Chapa ya Istanbul. 38 Tafsirul-Kabiiru Juz. 30, Uk. 107. Na Tafsiru Tabariy Juz. 29, Uk. 31. Na Asbabun-Nuzul Uk. 249. Na Tafsiru Ibnu Kathiir Juz. 4, Uk. 413. Na DurulManthur Juz. 6, Uk. 260. Na Ruhul-Maaniy Juz. 29, Uk. 43. Na YanabiiulMawadda Uk. 120. Na Nurul-Abswar Uk. 105. Na Kanzul-Ammal Juz. 6, Uk. 408. 46


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 47

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Na kuwa yeye (a.s.) amesema: “Sikusikia kitu kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu nikasahau.”39 Hivyo basi ambaye anamiliki elimu ya Kitabu naye ni miongoni mwa wateule ambao wamerithishwa Kitabu ni lango la elimu ya Rasul (s.a.w.w.). Na elimu hii ndiyo ambayo ndanimwe mna elimu za ghaibu na zingine. Na ametunukiwa Imam Ali (a.s.) kwa mujibu wa maelezo hayo. 4. Amesema (a.s.) akitoa habari za matukio ya ghaibu “Wallahi lau ningependa nimpe habari kila mtu miongoni mwenu, matokeo yake na maingilio yake na hali yake yote ningefanya, lakini nahofia mtakufuru kunihusu mimi (mkidhania) kuwa ndiye Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.). Fahamuni mimi ni mwenye kuitoa kwa watu makhsusi wanaoamini. Naapa kwa yule aliyemtuma kwa haki, na akamteua awe juu ya viumbe, hakika hakutamka ila ni kweli, na ameniusia mimi hayo yote. Mwenye kuangamia anaangamia na mwenye kuokoka anaokoka, na matokeo ya jambo hili. Wala hakubakisha kitu kinapita juu ya kichwa changu ila amekimiminia sikioni mwangu na amenipa.”40 5. Ameishiria (a.s.) na kutoa habari za matukio ambayo yalitendwa na alQaramitwa kwa kauli yake: “Wanajichukua kutupenda na kututaka na wanaficha dhidi yetu chuki, na alama ya hilo ni kuwaua kwao warithi wetu na kuyagura kwao matukio yetu.” Ibnu Abil Hadid amesema: “Ni sahihi habari aliyoitoa, kwa sababu Qaramitwa wamewaua katika Aali Abu Talib (a.s.) watu wengi.”41 6. Imekuja katika hotuba ya Imam Amirul-Mu’miniin (a.s.) kuwa yeye amesema: “Niulizeni kabla hamjanikosa, Wallahi hamuniulizi kuhusu kikundi kitakachowapoteza watu mia na kuwaongoza mia ila nitawapa 39 Majmaul-Bayan cha Tabarasiy Juz. 10, Uk. 345. Ameipokea kupitia njia za Masunni na Mashia. 40 Sharhu Nahjul-Balagha cha Ibnu Abil’ Hadid Juz. 10, Uk. 10. 41 Sharhu Nahjul-Balagha cha Ibnu Abil’ Hadid Juz. 10, Uk. 14. 47


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 48

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu habari ya mwitaji wake na mchungaji wake mpaka siku ya Kiyama.” Basi mtu mmoja alisimama na kumuuliza: “Nipe habari kuna mashimo ya nywele mangapi katika ndevu na nywele zangu?” Akasema (a.s.): “Wallahi hakika alinipa habari zake Mtume wa Mwenyezi (s.a.w.w.) hilo ulilouliza, kwa kweli katika kila shimo la nywele kichwani mwako kuna malaika anakulaani, na katika kila shimo la unyele katika ndevu zako kuna Shetani anakuchochea, na kwamba ndani ya nyumba yako kuna mtoto atamuua mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), na lau si kuwa uliyoyauliza uthibitisho wake ni mgumu ningeyaeleza. Lakini alama yake ni hiyo laana niliyokwambia na mtoto wako aliyelaaniwa.” Na mwanawe wakati ule alikuwa mdogo, nae ndiye ambaye alitawalia kumuua Husein (a.s.) hapo baadae.42 7. Imam Amirul-Mu’miniin alikuwa na hukumu ngeni na za ajabu hazihesabiki. Nazo upande wake zinafichua elimu ya Imam aliyotunukiwa na Mwenyezi Mungu (s.w.t.). Kwa kuwa tunamkuta anajibu hukumu za Mwenyezi Mungu baada ya kushindwa wengine. Mfano wa amri ya kumpasua mtoto nusu mbili mpaka wanawake wawili waliokuwa wakidai waliporudi upande wa haki.43 Na mfano wa mgao wa Dirham kwa wenye mikate wawili.44 Na kuileta hukumu ya Khuntha.45 Na hukumu ya Bughatu mpaka Shafi’iy alisema: “Tulizitambua hukumu za Bughatu kutoka kwa Ali (a.s.)”46 42 Sharhu Nahjul-Balagha Juz. 2, Uk. 448 na Juz. 1, Uk. 208. Ameeleza kutoka kitabu al-Gharatu cha Ibnu Hilal at-Thaqafiy. Na Sinanu bin Anas an-Nakh’iy ni miongoni mwa walioshiriki kumuua Husein (a.s.). Rejea Tahdhiibut-Tahdhiibu Juz. 7, Uk. 337. Na Kanzul-Ummal Juz.1, Uk. 228. Na Yanabiiul-Mawadda Uk. 73. 43 Kanzul-Ummal Juz. 3, Uk.179. 44 Dhakhairul-Uq’ba Uk. 84. Na Swawaiqul-Muhriqa Uk. 77. 45 Nurul-Abswar Uk. 71. Na Manaqibu Ahmad al-Khawarzamiy Uk. 60. Na Matalibus-Suul Uk. 13. 46 Kitabul-Ummu Juz. 2, Uk. 233 katika mlango wa tofauti kuhusu kuwauwa Bughatu. 48


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 49

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu 8. Katika Usudul-Ghaba imekuja katika wasifu wa Ghurfatul-Azdiy, kuwa: Yeye alikuwa miongoni mwa Swahaba wa Mtume (s.a.w.w.). Na ni miongoni mwa wenye sifa. Naye ndiye ambaye Nabii (s.a.w.w.) alimuombea abarikiwe katika patano lake la kibiashara. Ghurfatu alisema: “Shaka iliniingia kuhusu Ali (a.s.), hivyo nilitoka naye kwenye ukingo wa mto wa Furat, alichepuka njia na alisimama na tulisimama kumzunguka. Alionesha kwa mkono wake: ‘Hii ni sehemu ya mapumziko yao na ya kuketi wanyama wao na pa mwagikio la damu yao. Naapa ni mtu asiye na wa kumnusuru ardhini wala mbinguni isipokuwa Allah.’ Husein (a.s.) alipouliwa nilitoka mpaka mahali walipomuulia, ikawa kama alivyosema hakukosea kitu. Nilistaghfiru kwa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya shaka niliyokuwa nayo na nikajua kuwa Ali (a.s.) haliendei ila lile aliloagizwa.”47 9. Imam Ali bin Abu Talib (a.s.) alitoa habari ya kuuliwa Dhi Thudayyah, ambaye ni miongoni mwa Khawarij, na habari za kutovuka kwa Khawarij mto baada ya kuwa aliambiwa: Wamekwishavuka.48 10. Na alitoa habari (a.s.) ya kuuliwa yeye mwenyewe binafsi.49 11. Na alitoa habari kuwa Maghul watachukua ufalme kutoka kwa Bani Abbasi.50 12. Na alitoa habari ya kusulubiwa kwa Miitham at-Tammariy na kuchomwa kwake mkuki. Na alimuonesha mtende ambao juu ya kigogo chake atasulubiwa. Abdullah bin Ziyad alimfanyia hivyo, juu ya wawili hawa laana ishuke.51 47 Rejea Usudul-Ghaba Juz. 4, Uk. 169. 48 Murujud-Dhahab Juz. 2, Uk. 305. Na al-Kamil cha Ibnu Athiir Juz. 3, Uk. 174 na Uk. 175. 49 Lisanul-Mizan Juz. 3, Uk. 439. Na Usudul-Ghaba Juz. 4, Uk. 35. Na Muntakhabu Kanzul-Ammal Juz. 5, Uk. 59. Na Musnadu Ahmad Juz. 1, Uk. 156. 50 Sharhu Nahjul-Balagha Juz. 2, Uk. 125. na Uk. 241. Na Tahdhiibut-Tahdhiib Juz. 7 Uk. 358. 51 Sharhu Nahjul-Balagha Juz. 1, Uk. 210. 49


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 50

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu

Jambo la saba: Riwaya ambazo zinaelezea elimu ya maimamu na utoaji habari wao wa yaliyo ghaibu: Imekuja katika Hadithul-Qudsiyi: “Ewe mwanadamu, mimi ni tajiri siwi fakiri, nitii mimi katika nililokuamuru nitakufanya tajiri hautokua fakiri. Ewe mwanadamu, mimi ni hai sifi, nitii katika nililokuamuru nitakufanya hai hautokufa. Ewe mwana wa Adamu, mimi hukiambia kitu kuwa na kinakuwa, nitii mimi katika nililokuamrisha nitakufanya ukiambie kitu kuwa na kitakuwa.”52 Na Maimamu walimtii Mwenyezi Mungu (s.w.t.) mpaka akawathibitishia umaasumu, hivyo wao ni bora wasadikishwao na hii Hadithul-Qudsiy. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Mimi ni Jiji la elimu na Ali ni lango lake.”53 Kutoka kwa Ibn Atwai al-Makiy, alisema: “Nilikuwa na shauku ya Abu Ja’far nami nikiwa Makka nikaenda Madina, sikuiendea ila kwa shauku yake, nilipatwa na baridi kali nikaishia mlangoni kwake nusu ya usiku. Nilisema: Je niugonge mlango saa hii au ningojee mpaka asubuhi? Mimi nikiwa nafikiria hilo punde nilimsikia akisema: ‘Ewe kijakazi, mfungulie mlango Ibnu Atwau, amepatwa na baridi kali huu usiku.’ Kijakazi akafungua mlango.”54 Abu Kahmas alisema: “Nilishuka mji wa Madina katika nyumba ndani yake kuna binti mrembo, alikuwa ananipendeza, nikatoka usiku, niliomba nifunguliwe mlango, alinifungulia nikamshika mikono yake. Ilipofika asubuhi niliingia kwa as-Sadiq (a.s.), akasema: ‘Ewe Abu Kahmas, tubu kwa Allah kwa uliyofanya jana usiku.”’55 52 Biharul-Anwar Juz. 90, Uk. 376. 53 Kanzul-Ummal Juz. 11 Uk. 614 Hadithi ya 32978 na 32979. Lisanul-Miizan Juz. 1 Uk.432. 54 Baswairud-Darajati Juz. 5 Uk. 277. Biharul-Anwar Juz. 46 Uk. 235. 55 Baswairud-Darajati Juz. 5 Uk. 262. 50


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 51

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu

MLANGO WA NNE ELIMU YA GHAIBU NA ELIMU YA FALSAFA YA SAIKOLOJIA (PSYCOLOGICAL PHILOSOPHY) Si sahihi kuwa Maimamu hawajui elimu ya ghaibu kwa sababu ya kuwa uwepo wao ni wenye mpaka maalumu, uwepo ambao upo katika wigo wa uwezekano, na kuwa sio uwepo wa milele, hali ikiwa ghaibu uwepo wake sio wa mpaka maalumu, na chenye mpaka maalumu hakiwezi kukizingira kisicho na mpaka maalumu, kwa mujibu wa hukumu ya kiakili. Kwa ajili hiyo elimu ya ghaibu imekuwa mahsusi kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ambaye hawekewi mpaka. Na Nabii na Imam kuwa na mpaka ni jambo halina shaka ndani yake wala kupatwa na utata, kadhalika elimu ya ghaibu kuwa mahsusi kwa Allah (s.w.t.) ni jambo lililothibiti halijakanushwa na yeyote miongoni mwa waislamu. Lakini linalodaiwa hapa ni kuwa Allah (s.w.t.) amewakirimu na amewafanya kuwa mahsusi kwa baadhi ya habari za ghaibu na kuwatunukia elimu yake, hivyo basi kwa idhini Yake na amri Yake wameijua hiyo, na hayo yakawa ni hadhiri kwao, japokuwa kwa wengine ni ghaibu isiyojulikana, Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amewatunukia hilo, kwa kuwa kwao karibu na Yeye (s.w.t.) kwa matendo mema na nia ya ukweli na kuwa na ikhlasi, taq’wa na bidii. Hawakupewa hayo kwa kulazimishwa na kukirihishwa, bali ni kwa njia ya kumiliki kwao sababu inayowawezesha kuzifikia daraja na kustahiki nafasi ambazo wamethibitishiwa na fitna, balaa, mitihani na taabu ya muda mrefu.

51


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 52

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Kwa kweli suala la kuona mbali na kukanusha uwezekano wa elimu ya ghaibu kwa Maimamu inayoenea wakati uliopita na uliopo na wa baadae, uoni huo utanywea pindi ikifahamika kuwa si kwa kujitegemea, bali ni kwa njia ya Wahyi wa kiungu uteremshwao kwenye moyo wa Rasuli (s.a.w.w.), na kupitia ilhamu kwa Aali zake watoharifu. Na madamu imethibiti kupitia uhakiki wa nukuu kuwa wao walihodhi vipaji hivyo, na tunukio la kiungu la elimu ya ghaibu katika utafiti uliotangulia, basi hapa tutajihusisha na mas’ala hii kwa wigo wake wa kifalsafa. Na aina ya uhakiki katika mas’ala hii haitimii ila kwa misingi ya kiakili itumikayo katika thibitisho za kifalsafa, nayo ni misingi isiyohitaji dalili. Kwa mfano ili tujue uhakika wa elimu kuwa ni nini? Je ni kitu cha mada material, miongoni mwa vitu vya mwili wa mwanadamu? Au ni jambo lihisiwalo la ngazi ya juu zaidi kuliko zoni ya mada – material, na ni kitu kiko mbali nayo, kufuatia hivyo ni kitu mahsusi upande wa vitu ambavyo sio mada kwa mwanadamu, na uhusiano wake na yeye ni nini? Na hujulikanaje, bali kimsingi nini kazi yake? Na ipi mipaka yake ambayo juu yake yasimama? Maswali haya yote haiwezekani kujua majibu yake ila kwa misingi yakinifu ya kiakili. Sasa je elimu hii inatupa nini sisi ili tunufaike kwenye hali hii tuliyonayo? 1. Elimu ya maarifa inatilia mkazo kuwa elimu hakika yake inajificha katika kufichua kwake ukweli, hivyo basi inadhihirisha ukweli na kutufichulia, ni jambo ambalo tunalijua kwa uwazi. 2. Kuufichua ukweli ni miongoni mwa mambo mahsusi ya uwepo wa mwanadamu, kwa kiwango ambacho ni muhali kuwa na dhana ya kuutenga mbali na yeye, vinginevyo ingekuwa ni kujitenga mwenyewe binafsi.

52


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 53

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu 3. Elimu au kuufichua ukweli ni jambo lililo juu mbali na mada, kwa sababu sifa zake haziafikiani nayo, kama vile kugawanyika na kutoweka, kubadilika na mengine, hivyo basi hizo ni sifa zilizopo ambazo ni mbali na mada, kwa mujibu huo nafsi ni jambo lililo nyuma ya mada. 4. Elimu hutokea na ukweli hufichuka kwa njia ya mawasiliano ya uwepo, na ya uhakika kati ya nafsi - ya mjuzi – na kitu kikusudiwacho kutambuliwa, na bila ya mawasiliano haya dhana ya kutokea ufichukaji na kuthibiti elimu ni muhali, kwa kuwa hakuna sababu yake. 5. Njia za kuwasiliana elimu na ukweli ni tatu: Kuwasiliana kupitia hisi zinazohusiana na matukio ya mada. Kuwasiliana kupitia akili inayowakilisha utambuzi wa mambo kwa jumla yake (kuliyati). Uwasilianaji wa moja kwa moja na kitu bila ya njia ya akili au hisi, na huitwa maarifa ya kushuhudiwa au ya kiroho. 6. Kuwasiliana na kuutambua ukweli ulio mbali na mada ni jambo lililorahisishiwa nafsi ya mwanadamu. Kwa kuwa hiyo katika daraja yake haitengwi na kitu, kwa kuwa vizuizi vya elimu na ufichukaji wake ni suala la nje, na huwakilishwa na zama na mahali, hali ni yenye kuambatana na hali ya kimwili, na miongoni mwayo ni ile ijulikanayo kwa maana tu si ya kimwili. Na inakuwa katika hali ya mshughuliko usiozindukana. Na ilipothibiti kuwa nafsi na vidirikiwa vyake viko mbali na mada, kwa hiyo vitenganishi vya kiwakati havihusiani nayo. Vinaambatana tu na upande wake wa kimwili ambao hauna uhusiano na elimu na ufichuaji wa ukweli. Hivyo basi kinabakia kitenganishi cha kimaana, nacho ni kujishughulisha na yanayookotwa na hisi na hatimaye kuwa nayo, na kutupilia mbali yaliyo nyuma yake miongoni mwa ukweli wa mambo. 53


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 54

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Jambo ambalo pia limejulishwa na Kitabu kitukufu, katika kauli Yake (s.w.t.):

“Wanajua hali ya dhahiri ya maisha ya dunia, nao ndio wameghafilika mbali na Akhera.” (Sura Rum:7) Ni lawama kwa anayeweka matumaini ya elimu yake kwenye maumbile haya ya dhahiri wala hateremki batini yake. Lau angekuwa hana fursa hiyo lawama ingekuwa si mahali pake. Tumefikia tija kuwa kuitambua kweli iliyo mbali na mada kwa aina fulani miongoni mwa aina za utambuzi, ni jambo lipo kwenye uwezo wa nafsi ya mwanadamu, wala si jambo ambalo liko juu ya uwezo wa nafsi, na lililo nje ya uwezo wake. Hii kwa upande wa kwanza. Ama upande wa pili, ambao mas’ala hii inauelekea ni upande wa kupatia kwa mwanachuoni, na katika maudhui ya mas’ala anakuwa ni Imamu salamu’llahi Alayhi. Na yeye ana sehemu mbili: Sehemu moja anashirikiana na binadamu wengine. Na kwa ibara ya undani zaidi: Ni sehemu ya upande wa elimu, nayo ni sehemu tukufu ambayo inashabihiana na nafsi zingine upande wa kuwa ni nafsi. Na sehemu ya pili ni ile anayotofautiana na watu wengine na anapanda na uwepo wake mpaka zoni ya juu kwenye nafasi ya uwalii mkuu. Na kwa mara nyingine tunalazimika kuikimbilia ibara ya undani zaidi, nayo ni: Upande wa jinsi ya uwanachuo na ukubwa wake wa zoni ambao nafsi yake inatofautiana na nafsi za watu wengine. Na kwa uhakiki huu ndiyo elimu ya kuitambua nafsi, ya kifalsafa, na sio ya uchambuzi ambao madrasa za elimu ya falsafa za kisasa inajiambatanisha nayo. Hivyo tofauti ya msingi iliyopo kati ya elimu ya saikolojia ya 54


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 55

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu uchamuzi na kati ya elimu ya falsafa ya kisaikokolojia ambayo ni moja ya matawi ya elimu ya falsafa ya kiislamu, ni kuwa ya kwanza inafumbia macho kufanya utafiti katika nafsi na inajiimarisha kudurusi dhahiri zake zilizopo katika sifa zake na vitendo vyake. Hali ikiwa nyingine inaidurusi nafsi upande wa kuthibitisha kuwepo kwake na jinsi ilivyokuwa na hali zake za ndani baada ya umauti na kukusanywa kwake na kurudi kwake hai. Na mengine miongoni mwa mas’ala yanayoambatana nayo. Hebu sasa tuitake ushauri elimu hii katika hali tuliyonayo ili tuone inachotupa: 1. Kwanza yanayothibitishwa na uhakiki ndani ya nafsi ya mwanadamu ni kuwa nafsi ina daraja na nafasi kwa upande wa kujiweka mbali sana na mada na kupaa kwenye ulimwengu wa juu zaidi, na kupungua kwake. Na ya kuwa uchache wa kuzingatia na wingi wake warejea kwenye hali hiyo. Na maadamu kudiriki sio mada na ni kitu mahsusi cha nafsi ya mwanadamu hivyo kudurusu kiwango cha kuepukana kwake na mada kunajulisha kiwango cha kuepukana kwa nafsi. Na somo hili linasanifu daraja ya kuyadiriki yanayohisiwa kutokea daraja dhaifu mno ya kuepukana. Yakurubia kuwa haiachani na mada bali haiwi ila kwa kuungana nayo, nayo ni daraja ambayo mnyama anashirikiana na mwanadamu. Na huenda akamzidi na kusanifu daraja ya kuzidiriki kuliyati. Nao ni upande ambao mwanadamu anapanda kumzidi mnyama katika zoni ya kuwa mbali akitokea daraja za wastani. Ama daraja ya juu mno ya kudiriki kwa kujiweka mbali na kuenea ni daraja iitwayo kudiriki kwa kiroho au kwa shuhuda, na maelezo ya kifalsafa ni elimu iliyo hadhiri kwenye ukweli wa jambo. Nayo pia ina ngazi na daraja, na iliyo dhaifu mno kati ya ngazi hizo ni njozi za kweli, na ya kati ni ilhamu na maneno ya malaika. Na ya hali ya juu katika ngazi ya elimu na kudiriki kwa mwanadamu kwa urefu wake ni kufanikiwa kuupata wahyi na kukutana nao. 55


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 56

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Njia ambayo nafsi ya Imam inatofautiana na nafsi zingine ni hii, yaani upande ule wa wasaa wa kudiriki na kuuzunguka kwake ukweli wa mambo, na kuwa mbali kikamilifu na mada, kwa hali ambayo haombi auni kwa njia ya hisi au akili kwa ajili ya kufichukiwa na kupata elimu, nayo ni dalili ya wasaa wa nafsi na daraja yake kuwa juu na kuinuka kwa nafasi yake na daraja yake. Na utafiti wa Qur’ani pia watilia nguvu tulilofikia. Katika kauli Yake (s.w.t.):

“Na tukawafanya miongoni mwao maimamu wanaoongoza kwa amri yetu waliposubiri, na walikuwa wakiziyakinisha Aya zetu.” (Sura Sajdah:24). Na kwa hakika ameuratibu uimamu ambao ni uongozi kwa amri ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) juu ya subira, na ameiratibu subira juu ya yakini ya Aya. Na yakini ni daraja ya juu mno miongoni mwa daraja za kudiriki, kwa sababu mwambatano wake ni katika zoni iliyo mbali mno na mada, hiyo ni kwa tamko lake (s.w.t.): “Na kadhalika tukamwonyesha Ibrahim ufalme wa mbingu na ardhi, na ili awe miongoni mwa wenye yakini.” (Sura An’aam:75). Na amesema: “La hasha! lau mngelijua kwa elimu ya yakini. Hakika mtauona Moto.’’ (Sura at-Takaathur: 56). Hivyo basi imebainika kuwa mas’ala ya nafsi kufichukiwa na ukweli ambao sio maada upatikanao kwenye nafasi ya uimamu yazingatiwa kuwa ni miongoni mwa dharura za nafasi yake ya uwepo. Upande wa tatu, ambao mas’ala hii inaambatana na mikia yake ni Kinachojulikana au Kinachoambatana na udiriki, yaani ukweli unaokusudiwa ujulikane na kuupata. Kwa upande huu mas’ala hii inaangukia kwenye mapaja ya maarifa ya uwepo wa vitu na daraja zake, na kwa hesabu ya ibara ya undani zaidi iliyorudiwa rudiwa kutajwa ni: Kukijua kitu na sababu zake. 56


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 57

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Ni dharura kuutambua upeo huu wa mas’ala pia ili tuone kuwa kujua matokeo kwa namna ya ufafanuzi nafasi yake huwa wapi katika uhakiki na vipi kwayo elimu hupatikana? 1. Kulingana na nidhamu ya sababu na kisababishwa inayotawala maumbile, ni kuwa mas’ala ya kupatikana shaka ya kuwepo kwa vitu huainishwa na uthibitisho. Kwa hiyo ambalo lipo katika ngazi ya mada ya vitu yatokana na ya kabla yake, bali ni rangi miongoni mwa rangi ya kuwepo kwake kulikonyauka na kwenye ukomo. Hivyo basi vitu vina uwepo mwingine ulioepukana na mada na zama, upo katika eneo la mtengano na zama, na kuona huko kunalingana na uoni kamilifu na timilifu. 2. Ama matukio yatukiayo katika hali ya hiyari ya mwanadamu na ambayo si katika vitu vya mada kuzijua sababu zake ni kuyajua yenyewe kulingana na ilivyohakikiwa mahali pake, kuwa: Kuijua sababu ni kukijua kisababishwa. Hivyo basi kujua utashi ambao ni mojawapo ya hizo sababu za ujuzi timamu, hivyo hivyo kuzijua sababu zingine zinazoleta tija ya ukweli wa mambo, ni hakikisho la tukio la ufichukaji na kutokea kwa elimu. 3. Na hakika daraja ya juu mno ya kuwepo kwa vitu vyote ikiwemo tukio lililo chini ya hiyari ya kibinadamu, ni kule kuwepo kwake kwenye uwanja wa elimu yake kamili (s.w.t.). Hivyo kwa kupitia njia yake na kwa kutoa habari Yeye (s.w.t.), elimu hutimia kwa ajili yake. Hakika haya ambayo tumeishia, Kitabu kitukufu kimeyaeleza. Kwa kweli kimevithibitishia vitu vingine aina ya uwepo ulio mbali na mada na kimeufanya uwepo wa mada upo chini yake, ni kana kwamba Yeye (s.w.t.) anathibitisha uwepo mmoja wa vitu ulio na tofauti, kama ilivyo katika kauli Yake (s.w.t.): “Na hakuna chochote ila tunayo khazina yake, wala hatukiteremshi isipokuwa kwa kipimo maalumu.” (Sura Hijri: 21) Hivyo kadiri yenye ukomo ya kitu ndiyo ukweli wa chombo cha uteremshaji, na wala sio kitu timilifu, na katika kauli Yake (s.w.t.): 57


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 58

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu

“Wala punje katika giza la ardhi, wala kilichorutubika wala kilichoyabisika, ila yamo katika Kitabu kidhihirishacho.” (Sura An’aam:59). Hivyo basi kuna aina ya uwepo wa sura ya jumla wa vitu, Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ameueleza kuwa ni Kitabu kidhihirishacho bayana. Na ni wazi kuwa bayana hapa haimrejelei Muumba (s.w.t.) kwa kuzingatia kuwa kila kitu Kwake (s.w.t.) kipo, hivyo wala hapana maana kuielezea bayana kumhusu. Na Aya za Kitabu kitukufu zimeeleza kuwa kitabu hiki au uwepo wa jumla wa vitu unakubali kupata sehemu ya elimu, na kuwa kunakipa kitu aina fulani ya uwezo. Kama ilivyo katika kauli Yake (s.w.t.):

“Akasema yule aliyekuwa na elimu ya Kitabu: Mimi nitakuletea hicho kabla ya kupepesa jicho lako.” (Sura Naml:40). Na mwishowe Qur’ani imeeleza kuwa uwepo huu wa jumla wa vitu umedhibitiwa kwa hesabu katika:

“Na kila kitu tumekihifadhi katika daftari lenye kubainisha.” (Sura Yasin: 12). Japo wafasiri watofatiane katika kuainisha mpaka wa daftari lenye kubainisha, lakini bado uhakiki wetu kuihusu mas’ala hii upo katika kituo makini.56 56 Ilmul-Imam Wanahdhwatu Sayyidus-Shuhadai cha Muhammad Husein Tabatabaiy Uk. 30 – 32. 58


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 59

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu

MLANGO WA TANO ELIMU YA GHAIBU KWA WENGINE AMBAO SIO IMAMIYA Mwelekeo mwingine unaohitilafiana na kambi ya Ahlul-Bayt (a.s.) unalifanyia istilahi nyingi suala la elimu ya ghaibu katika maisha ya manabii na watu wema na mawalii. Miongoni mwa istilahi hizo ni: Kufichukiwa, Karama na Farasa57, kuwa ni vitu ambavyo hutunukiwa watu hawa. Hivyo tunakuta umashuhuri wa mwelekeo huu unathibitisha hili. Isipokuwa tu hitilafu kati yao imetokea katika misingi na majengeo ya kitafsiri na dalili za kisheria za kuthibitisha jambo hili. Udhaifu na mbabaiko umevuka mpaka kwenye tafsiri hizo, kama inavyoonesha kuwa mas’ala hii iliachwa bila kufanyiwa darasa na kuangaliwa kwa kina kwa upande wa mwelekeo huu. Na huenda suala hili linarejea kwenye hali ya kutoitakidi uimamu ambao ni ukhalifa wa unabii, ambao unalazimu umaasumu, kwa namna ambayo itikadi hii inadhihirisha kuwa maasumu ana elimu ya ghaibu, kiasi kwamba likawa kwenye hatari ya kujadiliwa, kudodoswa, na kuongelewa kwa kina kulikotoa mchango wa kuliimarisha jengo lake kwa ustadi wa hali ya juu. Ama mwelekeo mwingine usiotambua umaasumu kwa yeyote baada ya Rasuli (s.a.w.w.) umeichukuwa mas’ala hii juu juu haukuingia kwenye mizizi yake na wala haukuunganisha peo zake. Amechanganya kati ya Kufichukiwa na Farasa na Karama na elimu ya kutunukiwa ya Maasumu. Kutokana na hali hii tutafahamu majaribio muhimu ya kitafsiri ya jambo hili.

57 Farasa: Maono na ujuzi uingiao akilini bila kufikiri. 59


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 60

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu

Jaribio la Shawkaniy: Shawkaniy ameleta dalili ya kuthibitisha mas’ala hii kwa njia ya nukuu, hivyo akaidhania elimu ya ghaibu kuwa ni Farasa58, kwa mujibu huo aliitolea dalili kauli yake (s.a.w.w.): “Icheleeni Farasa ya muumini kwa kuwa yeye anaona kwa nuru ya Mwenyezi Mungu.” Na anatolea mfano kwa elimu aliyokuwanayo sahaba Hudhaifa Bin al-Yamani, kuwa yeye alikuwa anawatambua wanafiki kwa Farasa. Na usahihi ni kwamba Farasa sio elimu aliyokuwa nayo Hudhaifa, kwa kuwa elimu yake kuwahusu watu hao alikuwa ameichukua kutoka kwa Nabii (s.a.w.w.) kwa stahiki aliyokuwa nayo Hudhaifa, na hiyo ni hiba kutoka Kwake (s.w.t.), kwa hiyo elimu ya aina hii sio Farasa, japokuwa Farasa ni aina ya kipaji cha kiungu. Kisha unajitokeza mchangayo mwingine ndani ya maneno ya Shawkaniy, anadai kuwa Karama au Kufichukiwa, kunakumbwa na Shetani. Kwa minajili hiyo tunasema: Mwenye elimu ya kutunukiwa itolewayo hiba kwa maasumu haikumbwi na Shetani, hivyo basi elimu yake sio Karama wala Kufichukiwa, kukusudiwako ndani ya maneno ya Shawkaniy. Ama kudai kuwa kufaidika kwake na usahihi wa uwalii au Karama kwa kutoa habari zinazoafikiana na ukweli kuwa ni dalili ya kufichukiwa, hilo liko mbali, kwa sababu elimu aliyokuwa nayo Hudhaifa inahitilafiana na elimu aliyonayo mtu mwingine. Hudhaifa hakuwajua wao kwa kufichukiwa, japokuwa utoaji habari wake unaafikiana na ukweli kama ilivyo kwa mwenye elimu ya kutunukiwa au ambaye anaimiliki kwa kadiri. Na hayo kwako aliyoyasema Shawkaniy: “Kwa hakika Kufichukiwa ni jambo linalowezekana kutokea, si jaizi kwa yeyote kulikanusha. Na miongoni mwa mifano ya hilo ni Sahaba Hudhaifa 58 Farasa: Maono na ujuzi uingiao akilini bila kufikiri. 60


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 61

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Bin al-Yaman kuwatambua kwake wanafiki; kwa minajili hiyo tunasema: Mkanushaji asikanushe yatokeayo kwao miongoni mwa kufichukiwa kwenye ukweli kunakoafikiana na hali halisi. Katika hilo kuna Hadithi ya Nabii (s.a.w.w): “Icheleeni Farasa ya muumini kwa kuwa yeye huona kwa nuru ya Mwenyezi Mungu.”59 Lakini hapana budi kuugemeza Kufichukiwa huku kwenye sheria ili kuuthibitisha. Huenda mchanganyo wa Shetani ukawasukuma baadhi ya watu pindi utashi wao unapokithiri na kuchemka utashi wa nafsi, na kuwafikisha kwenye aina ya uoni na harakati za kipekee ambazo haziafikiani na hukumu za kiislamu, ambazo huitwa Shatahati, na kwa hao hiyo ni ishara, na kuwa dhahiri yao haielezei ukweli wa hali yao. Lakini mwenendo huu uitwao Shatahati ndio ulioharibu itikadi za wengi, kwa hiyo iliwasukumia kwenye kuritadi mbali na Uislamu.60 Ama jaribio la Ibnu Taymiyya ni kuwa: Amevigawa vitendo vinavyovuka hali ya kawaida na kuviweka kwenye sehemu ya Kufichukiwa, ambayo ni aina ya elimu na sehemu ya utendaji ambao ni katika jinsi ya uwezo na kumiliki. Na sehemu ya matendo haya kuna yanayorejea kwenye jinsi ya utajiri.61 Na mahali pengine amesema: “Na yote Mwenyezi Mungu ampaye mja wake katika mambo haya, endapo atajisaidia nayo kwa anayopenda Mwenyezi Mungu na kuyaridhia na yanayomkurubisha kwake na kunyanyua daraja yake kwa hayo, basi atazidi kupanda na kuwa karibu na Allah na Mtume Wake. Na endapo atajisaidia kwayo kwa ajili ya aliyoy59 Qutrul-Wali Alal-Hadithil-Wali cha Shawkaniy. Uhakiki na kutolewa na Ibrahiim Hilal. Chapa ya Ihyau Turath Al-Arabiy Biduni Tariikh Uk. 249- Beiruti. 60 Rejea ileile iliyotangulia. 61 Ibnu Taymiyya, Kitabu Taswawufu Uk. 298, nukuu kutoka kwa Dkt. As’ad alSahamraniy Uk. 155. 61


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 62

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu akataza Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, kama ushirikina, dhulma na yanayochukiza, basi kwa hayo atastahili lawama na adhabu. Hivyo sana huadhibiwa watu wa vioja, mara kwa kuvipokonya kama anavyoenguliwa mfalme kwenye ufalme wake na kupokonywa mwanachuoni elimu yake. Na mara huteremshwa na kuwa kwenye daraja ya mafasiki na pengine huritadi kwa kuacha Uislamu.”62 Mgao huu wa matendo yanayovuka kiwango cha kawaida au yanayoitwa Kufichukiwa yanatofautiana kabisa na madhehebu ya Ahlul-Bayt (a.s.), kwa kuwa Mwenyezi Mungu haupokonyi umaasumu kutoka kwa maasumu, ambao ndanimwe mna elimu ya kutunukiwa baada ya kustahiki kwa makadirio Yake (s.w.t.). Na umaasumu kama ilivyo elimu ya kutunukiwa iliyotolewa hiba ambayo imedhamini umaasumu unakataa kutenda kinyume na irada ya Kiungu. Kwa kuwa ni elimu ambayo maasum amestahiki kuhifadhiwa nayo, na Mola anamtunukia Imam mwenye ainisho kutoka kwa Nabii (s.a.w.w.), kwa lengo la kuusadikisha unabii na kutekeleza uliyoyaleta na kuyaongoza kupitia Imam, kwa hiyo kuipokonya elimu kunakinzana na lengo la Kiungu ambalo hapana budi litekelezwe kwa njia ya kuwepo kwa maasum baada ya Nabii (s.a.w.w.). Lakini yawezekana kuyachukulia maneno ya Ibnu Taymiyya kuhusu mambo yasiyo ya ada, kuwa ni katika aina nyingine na si elimu iliyotunukiwa ambayo ni juu ya ada, na ambayo ni miongoni mwa yalazimianayo na umaasumu, kulingana na madhehabu ya Ahlul-Bayt (a.s.). Ama kukiri kwa Ibnu Abul-Hadiid mas’ala ni kuwa hakuzungumzia mas’ala hii kwa ufafanuzi, bali tu ameishia kukanusha kuwepo kupingana kati ya kauli Yake (s.w.t.): “Na nafsi yoyote haijui ni nini itakayochuma kesho..” (Sura Luqman: 34) na kujua kwake fika (s.a.w.w.) ushindi wa 62 Al-Farqu Bayna Awliyair-Ridha Waauliyais-Shaytani cha Ibnu Taymiyya Uk. 151. 62


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 63

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Makka, na itakavyokuwa baadae ikiwemo kuwaua Nakithina na Mariqiina. Anasema: “Upeo ambao Aya yajulisha ni kukanusha elimu ya yatakayokuwa kesho, ama ikiwa ni kwa kujulishwa na Allah, silo lililokanushwa, kwani bila shaka ni jaizi Allah (s.w.t.) amwelimishe Nabii wake yatakayokuwa.”63 Na kuifikia mas’ala hii kwa kadiri hii haitoshelezi kadiri itakiwayo, ila ni kuwa mkusanyo wake kwa njia hii haupingani na mwenendo wa wafuasi wa madrasa ya Ahlul-Bayt (a.s.). Ama Ibnu Khaldun anautambulisha Uwalii, Kufichukiwa, Ilmu ya ghaibu na kusifika na mambo haya, kuwa hakuhitaji kupata elimu wala kusifika na mwenendo wa sawa unaoendana na amri za risala na katazo zake. Kwa minajili hiyo anatilia nguvu kuwa Mwenyezi Mungu amewatunukia Uwalii huu, Kufichukiwa, na kuijua ghaibu watu vichaa, na miongoni mwa hao ni: “Kaumu ya Mabahaluli waliochanganyikiwa, wanaoshabihiana zaidi na wendawazimu kuliko wenye akili. Wao pamoja na hayo imesihi kuwa wametunukiwa nafasi za Uwalii na hali za wasema kweli. Wamejua hilo kutokana na hali zao wale wanaowafahamu miongoni mwa wenye uelewa japokuwa wao sio mukalafina. Na hupatikana kwao miongoni mwa khabari za ghaibu za ajabu kwa kuwa wao hawana mwiko. Kwa hiyo wanayaachia maneno yao katika hayo na wanaleta maajabu, na huenda wanafiqhi wakafikiri kuwa wao wana kitu miongoni mwa makamu, kwa waonavyo kuwa taklifu haipo kwao, na Uwalii haupatikani ila kwa ibada. Na hilo ni kosa kwani fadhila za Mwenyezi Mungu humpa amtakae wala kupatikana kwa Uwalii hakutegemei ibada wala jingine.”64 63 Sharhun-Nahji Juz. 1, Uk. 427. 64 Tariikhu Ibn Khaldun Juz.1, Uk. 110. 63


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 64

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Ni kawaida kuwa Uwalii na Kufichukiwa akusudiako Ibnu Khaldun katika maneno yake, sio Uwalii na elimu aliyonayo maasum, ambayo hakuna mwachano kati ya elimu yake aliyotunukiwa kutoka Kwake (s.w.t.) na mwenendo wake na matendo yake. Kwa kuwa sababu yenye kuzalisha mwenendo ni elimu na kukata shauri kuwa kitu kipo na kufichuka kwake. Kisha haja ya kukipata kwake huzua mwenendo na harakati za kukifikia, na si sahihi kuwa mwenendo huja kwa sababu ya kukosa elimu, au kuwa mwenendo wake unahitilafiana na elimu yake, wa ila yeye ni kama ambaye akatae shauri kuwa maji yapo nyuma yake naye akiwa anayahitaji, kisha anakwenda si kwenye mwelekeo wake. Ama maelezo ya Fakhru Razi ndani ya tafsiri yake65, hilo ni jaribio la usogezaji karibu wa kuthibitisha karama ndani ya Qur’ani na si zaidi. Na ambalo tulikusudialo ni kuthibitisha elimu ya kutunukiwa kutoka Kwake (s.w.t.) kama sifa inayolazimiana na maasum. Na ambayo inatunufaisha sisi kuitafiti ni uwezekano tu wakupatikana karama kwa asiye maasum. Kama ambavyo karama haifai kuwa kama mahali pa kumthibitishia yeyote Uwalii katika watu. Na jengo hili linahitilafiana na madhehebu yetu katika kuthibitisha Uwalii ambao hauthibiti ila kwa tamko kutoka kwa Rasul (s.a.w.w.) linayofichua kwa upande wake umaasumu unaodhamini elimu ya kutunukiwa. Kwa minajili hiyo karama haijawa kama njia ya kuthibitisha Uwalii kwetu.

65 At-Tafsiri Al-Kabiir cha Fakhru Razi Juz. 21, Uk. 91. 64


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 65

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu

MLANGO WA SITA HISTORIA YA MAS’ALA HII NA MWELEKEO WAKE KITAFSIRI KATIKA MAONI YA IMAMIYYA Wafuasi wa madrasa ya Ahlul-Bayt (a.s.) wamejilazimisha bila ya utafiti wa ziyada kuwa Nabii (s.a.w.w.) hapana budi awe mjuzi wa yote ambayo umma unahitajia. Kwa sababu ujinga ni upungufu na hapana budi Nabii (s.a.w.w.) awe mkamilifu mno miongoni mwa raia ili astahiki kutiiwa. Hivyo hivyo Imam hapana budi awe mjuzi kwa mfano huo hata awe anastahiki ukhalifa wa Nabii (s.a.w.w.) katika kutiiwa na kufuata athari zake na ili awe kigezo. Baada ya haya utafiti umetokea kuhusu duru ya elimu ambayo Nabii (s.a.w.w.) yalazimu asifike nayo au Imam (a.s.). Je elimu hiyo ni ya hukumu tu? Au elimu ya maudhui za nje, na matukio mengine ya kilimwengu, yakiwemo mambo ya ghaibu yaliyopita na yajayo? Hivyo Imamia wamejilazimisha na uwezekano wa elimu hii kwa namna ya moja kwa moja na kutokuwa mahsusi au kuifunga na kitu mbali na kingine miongoni mwa maalumati yenyewe binafsi, isipokuwa yale ambayo dalili ya kata shauri imejulisha kuitoa. Na kumepingwa kujilazimisha huku kwa njia kadhaa, tunazichagua miongoni mwazo njia mbili, kwa kuwa mbili hizo ni mihimili miwili ambayo kwayo jiwe la mjadala na mazungumzo linazunguka katikati ya Imamiyya. Ya kwanza: Nabii na Imam ikiwa wanajua ghaibu hapana budi watakuwa wanajua yanayowadhuru na kuwaumiza. Akili na sheria zinahukumu kuwa ni wajibu kujiepusha na kuwa mbali na yanayosumbua na kudhuru. Hali ikiwa tunakuta kuingia kwa Nabii na Imam katika yaliyowadhuru na kuwaudhi. 65


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 66

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Na umekuja uwazi wa ukweli huu katika ulimi wa Nabii katika usemi wake (s.w.t.):

“Na lau kama ningelijua ghaibu bila shaka ningejizidishia mema mengi, wala isingenigusa dhara, mimi si chochote ila ni mwonyaji na mbashiri tu kwa kaumu wanaoamini.” (Sura Aarafu:188). Lau Maimam wangekuwa wanajua ghaibu wasingefanya matendo yaliyosababisha kuuliwa na umauti wao, na kuwaingiza kwenye ubaya dhidi yao. Kama Amiirul-Mu’miniina alivyoanza kwenda msikitini usiku wa dharuba ya Ibnu Muljim na alikufa shahidi kutokana na dharuba yake. Na kama alivyoanza kwenda al-Husain (a.s.) Karbala alikouliwa na wanawake wake kuchukuliwa mateka na msafara wake kuporwa, kwa kuwa hayo yote lau angekuwa ana elimu nayo, basi yangekuwa miongoni mwa vielelezo vya wazi vya kuiingiza nafsi kwenye maangamizi, ambako Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amekataza kwa kauli Yake (s.w.t.):

“Wala msizitie nafsi zenu katika maangamizo, na fanyeni wema. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema.” (Sura alBaqara: 195). Kwa kweli upinzani huu umechochewa zamani sana hata kwa kweli sisi tunakuta umedhihiriswa mbele ya Maimam wenyewe (a.s.), na tunaukuta umewekwa katika karne zilizofuata ukirudiwa. Na majibu yake yamekuja kwa idadi nyingi hivyo hivyo kupitia karne nyingi.

66


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 67

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Pili: Lau tufanye mfano kuwa kuna taklifu ya kifichifichi inayomtaka kujiingiza kwenye maangamizi pamwe na kuthibiti elimu yake kuhusu matokeo ya baadae, basi kusimama kwa Imam Husein (a.s.) kungekuwa sawa na mmoja yoyote miongoni mwa Maimamu ambao wanamiliki elimu ya ghaibu iliyoporomoka maana yake, kwa sababu hakuwa na hiyari ila kwenda kuelekea majaliwa yake. Hii ikiwa kinyume na hali ya kutojua majaliwa yake, hapo basi kusimama kwake kutakuwa miongoni mwa hiyari imuiayo rahisi kwake, na tofauti kati ya mambo hayo mawili ni kubwa. Na kabla ya kuingia katika utafiti wa kihistoria wa mas’ala hii na yaliyopelekea tafsiri yake, hapana budi kuthibitisha utangulizi utakaokuwa mahali pa jibu linalokata msingi wa mjadala. Hii ni kuwa uimamu ukimthibitikia mtu, basi hapana budi sharti zake za msingi ziwepo kwa mtu huyo, na miongoni mwa sharti zake kwa Imamiya ni umaasumu. Nao maana yake ni kuzuilika mbali na dhambi na maasi kwa hiyari, na miongoni mwa umaasumu ni kuwa na elimu ya hukumu za kisheria kwa ufafanuzi. Na ambaye uimamu wake umesihi na kukusanya sharti zake, haiji katika taswira kuhusiana na yeye awe atenda haramu kama kuiingiza nafsi kwenye maangamizi kulikokatazwa katika Aya. Kadhalika hawezi kufanya kitendo kinachobatilisha maana. Hapo basi hapana budi litokalo kwake liwe katika sura ya kisheria. Hivyo basi haiwezekani kuegemeza kwake uharamu wa kujiingiza katika maangamizi au matendo yasiyo kuwa na maana, ili kumkanushia elimu ya ghaibu, kwa kuwa kuijadili elimu yake ya ghaibu huwa baada ya kuukubali uimamu wake, nao wamkanushia kujiingiza katika haramu. Na hii yamaanisha kuwa analofanya ni halali na sheria, sawa awe ajua ghaibu au hajui. Hivyo basi haiwezekani kukanusha elimu yake ya ghaibu kwa uharamu wa kujiingiza katika maangamizi, na hivyo hivyo kufanya kwake kitendo chenye maana batili. 67


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 68

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Kwa minajili hiyo tumefikia kuwa pinzani mbili hizi zote hazitoki kwa anayeitakidi sharti za uimamu wa haki unaokubalika na kuthibiti katika vitabu vya theiolojia na uimamu. Na yaliyopo katika sura ya pinzani hizi mbili au zingine katika turathi yetu, huo ni mfano uliofanywa kwa lengo la kuondoa utata wa wapinzani na kujibu upinzani wao.

DARAJA LA KWANZA: ZAMA ZA MAIMAM (A.S.) Sura ya maudhui ya elimu ya Maimamu ya ghaibu wakati wa uhai wao katika kitovu cha Imamia ni kama jambo la kiitikadi na la kimatendo, kwani ilikuwa ni maudhui ya mjadala na ushindani na kuulizana kati yao. Kwa mwenye kuzingatia Hadithi ambazo zinanakiliwa na vitabu vya hadithi atavikuta vinafichua ukubwa wa umuhimu wa maudhui hii kwa mtazamo wa Maimamu (a.s.), na Umma unavihitajia kwa upande wa malezi na dharura ya kuelewa maana yake kikamilifu kwa utashi wa kutendea kazi kwa uelewa kamili. Kwa ajili hiyo majibu ya Maimamu hasa katika maudhui hii yalikuwa na sura tofauti, yakitaka kwa wakati huo huo kuondoa ukungu ulioyazingira na kuhofia kuyafanyia vibaya. Hivyo katika jumla ya maswali hayo ni yale aliyojibu Imam Ridha (a.s.). 1 – Kutoka kwa Hasan Bin al-Jaham alisema: “Nilimwambia Ridha (a.s.) kuwa Amiirul-Mu’minina (a.s.) alimtambua muuwaji wake na usiku ambao atauliwa na mahali atakapouliwa. Na kauli yake aliposikia kelele za bata ndani ya nyumba: ‘Kelele za bata zitafuatiwa na vilio vya kina mama.’ Na kauli ya Ummu Kulthum: ‘Lau ungeswali usiku huu ndani ya nyumba, na ungemwamuru mtu mwingine awaswalishe watu.’ Lakini alimkatalia. Na kuingia na kutoka kulikithiri usiku ule akiwa bila ya silaha! Na alitambua (a.s.) kuwa Ibnu Muljim, Mwenyezi Mungu amlaani, ni muuwaji wake kwa upanga. Haya yalikuwa miongoni mwa yasiyofaa kuguswa?” 68


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 69

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Akasema (a.s.): “Hayo yote yalikuwa lakini yeye alihiyarishwa usiku ule ili kudra ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ipite.”66 Na kutokana na Hadithi hii faida inapatikana kwa mambo kadhaa: La kwanza: Mushkeli huu ulikuwa umeletwa mbele toka zama za Maimamu na kwa kiwango cha juu, pale mmoja miongoni mwa wapokezi wakubwa alipouleta mbele. Nae ni al-Hasan Bin al-Jaham Bin Bakiir Bin A’ayan, Abu Muhammad az-Zurariy as-Shiibaniy, ambaye ni miongoni mwa wanandani wa Imam Ridha (a.s.). Na imepokewa Hadithi kutoka kwa Imam Al-Kadhim (a.s.) na kutoka kwake yeye limepokea Hadithi kundi miongoni mwa waaminifu wa madhehebu haya. Na uaminifu wake umeelezwa wazi. Naye anacho kitabu maarufu, watu wa enklopedia wameeleza riwaya kutokana na kitabu hicho, na anazo Hadithi nyingi katika vitabu vinne.67 Na yeye ni miongoni mwa wakuu wa Aali Zurara, nyumba ya kishia iliyo maarufu kwa kushikamana na madhehebu hii. Pili: Elimu ya Imam na utambuzi wake wa wakati wa kuuliwa kwake, na yaliyotajwa katika riwaya miongoni mwa kauli na vitendo vijulishavyo kuchagua kwake kuuliwa na kukuendea kwake. Hayo yote ni mambo yalikuwa yanakubalika kutokea na ni maarufu katika zama za muulizaji. Tatu: Kwa kweli mpokezi aliuliza sababu ya Imam kuyaendea kwake mambo haya, na yeye akiwa ajua yatafikia kuuliwa kwake, vipi inakuwa jaizi yeye kujipeleka binafsi kwenye kifo? Nayo ndiyo madhumuni ya upinzani wa kwanza. Nne: Ni kuwa jibu la Imam Ridha (a.s.) kwa kauli yake: “Hayo yote yalikuwa” ni sadikisho la yote yaliyojiri katika swali kuhusu habari ya 66 Al-Kaafiy: Juz. 1, Uk. 359. 67 Muujamul-Aalam Min Aali Aayan al-Kariim Uk. 204. Namba 12. 69


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 70

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu elimu ya Imam, kauli na vitendo alivyovitaja muulizaji. Na kutopinga kwa Imam Ridha (a.s.) kitu chochote katika hayo na kutokukanusha kwake, yote hayo ni dalili ya kuafiki kwake Imam Ridha (a.s.) itikadi ya muulizaji kuhusu elimu ya Imam wakati wa kuuliwa kwake. Tano: Jibu la Imam Ridha (a.s.) la swali kwa kuelekeza ujasiri wa Imam, na kutopinga asili ya dhana ya elimu ya ghaibu, ni dalili ya kuikubali dhana hii, na kutothibiti upinzani wa mwanzo. Sita: Kauli ya Imam katika jibu: “Lakini yeye alihiyarishwa” ni wazi kuwa Imam (a.s.) alipewa hiyari kuhusu suala la umauti wake, hivyo alichagua kuuliwa ili mambo yajiri katika makadirio yake yalioainishwa katika ghaibu, na iwe yajulisha utii wake mno wa irada Yake Allah (s.w.t.) na kufuata kwake makadirio yake. Na hii ni maana ya wazi mno na yenye uwiano mno na anwani ya mlango. Na katika nakala nyingine alioitaja al-Majlisiy badala ya neno “Alihiyarishwa” kuna neno “Aliwekewa wakati”. Ambalo maana yake ni kuwa kuuliwa kuliainishwa wakati ule, kwa ajili ya makadirio ambayo Mwenyezi Mungu alikadiria yapite na yathibiti. Hivyo inakuwa dalili ya Hadithi juu ya anwani ni kuthibiti elimu ya Imam tu wakati wa kuuliwa kwake na kujipeleka kwake, na kutokataa kwake na kutojihami kwake binafsi. Na hilo ladhamini kuwa Imam aliafiki makadirio na alifanya kulingana nayo. Ama nakala “Alifadhaishwa” haina maana, kwa sababu kufadhaishwa kwa Imam hakuna maingiliano na kujipeleka kwake kuuliwa akiwa anajua, bali hilo linaitangua dhana hii, hailingani na anwani ya mlango huu. Hivyo dhana yake inakataliwa. Na huenda ikawa limekosewa kutoka neno (khubbira ) likiwa na maana ya alijulishwa, kwa hiyo inakuwa kwenda sawa na makadirio na kuyapitisha ni sababu ya Imamu kupewa khabari na kujulishwa. Lakini hii haiachwi bila kuzingatiwa.

70


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 71

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Maana iliyo bora na inayolingana na anuwani ni (Khuyyira) “Alihiyarishwa” kama tulivyofafanua. Hivyo dalili ya Hadithi kuhusu kuthibiti wa elimu ya Imam ya wakati wa umauti wake, na kuchagua kwake katika hilo, ni wazi kabisa. Na jibu la upinzani wa kujiingiza katika maangamizi ni kuwa: Imam aliuchagua umauti na kuuliwa kwa namna ambayo juu yake imejiri kadari, ili afichue upeo wa utii wake kwa Allah na kufuata kwake utashi Wake na kumpenda kwake na kwisha kwake humo, na kuwa kwake na shauku Naye na upendo wake wa kukutana Naye, kama ilivyonakiliwa kauli kutoka kwao (a.s.): “Ridhaa kwa ajili ya ridhaa Yako. Kusalimu amri Yako. Hapana mwabudiwa wa haki asiye kuwa Wewe.” 2. Kwa sanad yake kutoka kwa aliyeingizwa kwa Musa al-Kadhim (a.s.), basi (a.s.) akatoa habari kuwa amenyweshwa sumu na kesho atakuwa katika hali ya kifo na kesho kutwa atakufa. Hivyo dalili ya elimu ya Imam juu ya wakati wa umauti wake ni wazi.68 3. Kutoka kwa Imam Ja’far as-Swadiq (a.s.) kutoka kwa baba yake alBaqir (a.s.): Kuwa yeye alimjia baba yake Ali Bin al-Husain as-Sajjad (a.s.). Alimwambia: Usiku huu ndio ambao atafishwa. Nao ni usiku ambao alifishwa humo Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.).69 Na kuwa ni dalili juu ya elimu ya Imam ya usiku wa kufa kwake ni wazi. 4. Sanad yake kwa Abul-Hasan ar-Ridha (a.s.), kuwa yeye alimwambia msafiri mpokezi: Kuwa yeye alimuona Mtume wa Mwenyezi Mungu akimwambia: Ewe Ali! Tuliyonayo ni bora kwako.70 68 Biharul-Anwar Juz. 48, Uk. 247. Madhumuni ya Hadithi ya 56. 69 Biharul-Anwar Juz. 49, Uk. 313. na Sharhuz-Ziyara al-Jaamia Uk. 117. 70 Biharul-Anwar Juz. 49, Uk. 54. 71


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 72

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Na ni wazi kuwa kauli hii ni wito kwa Imam ayaelekee yaliyo kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, na hiyo ni kinaya ya wazi imaanishayo umauti na Imam Ridha (a.s.), amefananisha uwazi wa hilo na uwazi wa kuwepo kwa samaki katika mfereji ambao aliuishiria mwanzo wa hadithi. 5. Sanadi yake kutoka kwa Abu Abdillah as-Swadiq (a.s.): Kuwa baba yake alimuusia vitu katika ghusli yake na katika sanda yake na katika kuingizwa kwake kaburini mwake, hali hakuna juu yake athari ya umauti. Al-Baqir (a.s.) alisema: “Ewe mwanangu haukumsikia Ali Bin al-Husein (a.s.) akinadi nyuma ya ukuta: ‘Ewe Muhammad, njoo, fanya haraka.’”71 Na kujulisha kwake ni kama Hadithi ya kwanza, kuwa wito ni wa nyumba ya akhera, na hapa muktadha upo wazi mno, Imam alipousia kumwandaa. Na Hadithi mbili hizi kujulisha kuwa hiyari ni ya Imam kupo wazi mno, kwa kuwa ni wito peke yake hakuna lazima ya kuutekeleza, bali utekelezaji wasimama juu ya itikio la hiyari la wito huo. 6. Sanadi yake kutoka kwa Abdul-Maliki Bin Aayan kutoka kwa Abu Ja’far (a.s.). Alisema: Mwenyezi Mungu (s.w.t.) aliteremsha nusra juu ya Husain (a.s.) mpaka ikawa kati ya mbingu na ardhi,72 kisha alihiyarishwa kupata nusra au kukutana na Allah (s.w.t.). Na kujulisha kwake humo kuhiyarishwa halafu Imam kuchagua kwake kukutana na Mwenyezi Mungu ni wazi mno.

71 Al-Kafiy Juz. 1, Uk. 260. Hadithi ya 7. 72 Tarikh Aliz-Zararah Uk. 124. Na katika lafudhi nyingine ni kutoka kwa asSadiq, tazama Kalimatul-Imam as-Sadiq Uk. 473. 72


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 73

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu

DARAJA LA PILI: BAADA YA KUGHIBU KWA MAASUMU (A.S.) Tunaanza kuleta mbele rai ya baadhi ya wanachuoni wa mwanzo miongoni mwa ambao wameguswa na mas’ala hii. Sheikh Mufiidu: Rai ya Sheikh Mufidu ni kuwa elimu ya Ghaibu ya Maimamu (a.s.) ni thabiti kwa ajili yao, bila ya kuwa ni sifa ya dhati kwao, wala kuwa ni wajibu kiakili kwake, bali yenyewe ni karama kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa ajili yao, na kuwa kusikia kumekuja na hilo. Kauli hii imenasibishiwa jamaa watu wa uimamu, hakuwaengua ila wasio wa kawaida miongoni mwa ghulatu. “Kuwa Maimamu kutoka Aali Muhammad (a.s.) walikuwa wanajua dhamiri za baadhi ya waja na walijua kitakachokuwa kabla hakijawa, na hilo si wajibu katika sifa zao wala si sharti ya Uimamu wao. Ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amewakirimu hilo na kuwaelimisha nalo, kwa ajili ya wema katika ibada yao na kushikamana na uimamu wao. Na hilo sio wajibu kiakili lakini limekuwa wajibu kwao kwa njia ya kusikia. “Ama kuiachia kauli juu yao kuwa wao wanajua ghaibu ni jambo lisilokubalika mbele ya mafisadi, kwa kuwa sifa hiyo anayestahiki ni mwenye kujua vitu mwenyewe, sio kwa elimu ya kufaidika, na hawi hivyo ila Allah. Na wapo katika kauli yangu hii jamaa watu wa uimamu, ila walio nje ya utaratibu miongoni mwa Mufawidhwa na waliojiambatanisha nao miongoni mwa Ghulatu.”73 Na amethibitisha katika kitabu chake al-Irshad mifano miongoni mwa riwaya zilizokuja katika uelezaji wao wa habari za ghaibu, sawa iwe 73 Awailul-Maqalati Uk. 77.chapa ya Muutamaru Sheikh Mufiidu. 73


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 74

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu kuhusu zilizopita au zijazo, hata kuhusu habari za wasemeshwa na wayafichayo nafsini mwao. Ametaja hayo katika dalili za kila mmoja miongoni mwa Maimamu (a.s.) katika kufafanua hali zao. Haya hapa kwako aliyoyasema Sheikh baada ya kuleta swali linalokujia: “Kwetu sisi Imam anajua yatakayokuwa, basi imekuwaje AmirulMu’miniin (a.s.) alitoka kwenda msikitini hali akijua kuwa ni mwenye kuuawa na alimjua muuaji wake, wakati na muda? Na imekuwaje Husein (a.s.) aliwaelekea watu wa Kufa akiwa anajua kuwa watamtelekeza wala hawatomnusuru, na kuwa yeye ni mwenye kuuliwa katika safari yake ile, na kwa nini alipozingirwa na alikuwa anajua kuwa maji yapo lau angechimba dhiraa kidogo hakuchimba. Kwa nini aliwasaidia dhidi ya nafsi yake mpaka aliangamia kwa kiu? Na Hasan (a.s.) alimpa ahadi Muawiya, hali akiwa anajua kuwa ataihini wala hatotekekeza na atawauwa Shia wa baba yake (a.s.)? “Jibu: Imam anajua litakalokuwa kwa ijmai yetu, kwa kweli suala lipo kinyume na alivyosema na walivyoafikiana Shia wote juu ya kauli hii. Lakini kuafikiana kwao kupo thabiti kuwa Imam anajua hukumu ya kila litakalokuwa, bila ya kuwa anajua litakalokuwa lenyewe na ufafanuzi wa ndani wa lile litakalokuwa. Jibu hilo linaidondosha asili iliyojengewa maswali haya yote. “Na sisi hatukatai Imamu kujua kiini cha matukio ikiwa kwa kuelimishwa na Mwenyezi Mungu (s.w.t.). Ama kauli ya kuwa yeye anajua kila linalokuwa, sisi hatuitoi wala kumuona amesema sawa msemaji wa madai hayo panapokuwa hapana hoja wala ubainifu.”74 Na Sheikh Mufiidu kwa kauli yake hii hatofautishi kati ya elimu ya Imamu ya hukmu za kisheria na elimu yake ya maudhui, madamu hilo limetimia kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.). 74 Muswanafatu Shaikh al-Mufiid 6:69. 74


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 75

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Na usahihi ni kwamba Imamu hajui litakalokuja kuwa moja kwa moja. Sheikh Tusi: Ama rai ya Sheikh Tusi kuhusu mas’ala hii inakuwa wazi kupitia swali aliloulizwa baada ya kuchukulia kuwa Maimamu wana elimu ya ghaibu, na kuwa Imamu Ali bin Abi Talibi (a.s.) alikuwa anamjua atakayemuua usiku ule, kadhalika Imamu Husain (a.s) ila tu wawili hawa waliamriwa wavute subira kwa hayo? Alijibu, rehema ya Mwenyezi Mungu imfikie: “Imesemwa: Swahiba zetu wamehitilafiana katika hilo: Miongoni mwao kuna aliyejuzisha hilo.”75 Na amesema: “Haizuiliki ifanywe ibada hii kwa subira katika mfano kama huu, kwa kuwa mauaji yaliyotokea – ingawaje kwa aliyefanya ni vibaya lakini kulifanyia subira hilo ni vyema, na thawabu yake ni kubwa. Bali huenda ikawa nyingi zaidi, kwa kuwa pamoja na ujuzi wa kupatikana mauaji - bila kizuizi – lakini subira ni jambo zito mno inapouvuka ushindi na ikilifikia lengo. “Na miongoni mwao kuna wale waliosema: ‘Si jaizi kufanya hivyo, kwa kuwa kuilinda nafsi isipatwe na madhara ni wajibu wa kiakili na wa kisheria, wala haijuzu kuitekeleza ibada ya subira kwenye jambo baya, kwa kweli hutekelezwa tu ibada ya subira kwenye jambo jema, na hapana kuhitilafiana kuwa yaliyotokea katika mauaji yalikuwa mabaya, bali ni miongoni mwa mabaya mno’. “Msemaji huyu amefanya ta’awili yaliyoelezwa kutoka kwa AmirulMu’minina (a.s.) miongoni mwa habari zinazojulisha kuwa alijua atauliwa, msemaji anasema: ‘Alikuwa anajuwa kwa njia ya jumla, wala hakuwa anajua wakati wenyewe hasa, na kadhalika alijua usiku wenyewe atakaouawa, ila tu ni kwamba alikuwa hajui wakati ambao tukio la mauaji litatokea.’ 75 Ameyafafanua maelezo hayo muhakiki mwandishi wa kitabu Talkhiisus-Shafii: “Kwa hilo anawakusudia Masheikh wawili al-Mufiidu na al-Kaylaniy”. 75


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 76

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Mwenendo huu ndio aliouchagua al-Murtadha (Mwenyezi Mungu amrehemu) katika mas’ala hii. Na mimi (Tusi) nina maoni katika mas’ala hii.”76 Sheikh Tusi ameziwekea wigo kauli za wafuasi wa kambi ya Ahlul-Bayt (a.s.) katika mas’ala ya elimu ya ghaibu ya Maimamu, kati ya kauli mbili tu, wala hawajahitilafiana katika asili ya elimu ya ghaibu ya Maimamu, bali wamehitilafiana kuhusu maarifa ya wakati wa kuuliwa kati ya ufafanuzi na sura ya jumla, na wameafikiana juu ya elimu isiyokuwa ya hilo, kuwa wanajua kwa ufafanuzi, kwa kuwa inabidi Imamu awe anajua hukumu. Kuinasibisha Sheikh Tusi kauli ya elimu ya sura ya jumla kwa Sayyid Murtadha ni miongoni mwa yanayolazimu kutohitilafiana kwake na kundi kuhusu ulazima wa Imam kuwa na elimu katika mengine yasiyokuwa haya, na miongoni mwa hayo ni hukumu. Allama Hilli: Baada ya kuvurumishiwa swali lililotajwa hapo kabla, alijibu: “Yawezekana kuwa yeye (a.s.) alipewa habari ya kutokea uuwaji usiku ule, na alikuwa hajui kuwa ni wakati gani katika usiku ule! Au alikuwa hajui mahali gani atauliwa! Au ni kuwa taklifu yake (a.s.) inatofautiana na taklifu yetu, hivyo ikawa inajuzu aikalifu damu yake tukufu (s.a) katika dhati ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.), kama ambavyo ni wajibu kwa mpiganaji vita kubakia thabiti japo kubaki kwake thabiti kutamletea kuuliwa, na wala halaumiwi kwa hilo.”77 Ni dhahiri kuwa Allama alizingatia katika majibu yake, ile hali ya kumchukulia muulizaji kuwa swali lake la utata halitoki kwa anayeitakidi uimamu na lazima zake, bali ni kutoka kwa mtu miongoni mwa wapinzani 76 Talkhisus-Shaafiy cha Tusi Juz. 4, Uk. 188-190. Na mhakiki wake ametoa maoni yake. Rejea ufafanuzi wa mlango katika Mir’atul-Uquli cha al-Majlisi Juz. 3, Uk. 123. Na Biharul-Anwar Juz. 42, Uk. 259. Na ad-Duratu an-Najafiyah cha al-Bahraniy Uk. 58 na vingine. 77 Ajwibatul-Masailil-Mahnaiyah Uk. 148. 76


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 77

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu haitakidi uimamu wa Imam (a.s.), wala hajiambatanishi na sharti zake zijulikanazo kama vile umaasumu na elimu na zinginezo. Kwa mujibu huo, lau ikitakiwa muulizaji alazimishwe kuamini elimu ya Imam na sadikisho la habari zijulishazo kujua kwake kuwa atauliwa – ambazo zimekuja na hazikukanushwa – hapana budi tutatoka na tija mojawapo ya zile alizozitaja Allama: Imma kuziwekea mabano habari zilizomfikia, kuwa awe anajua asili, yaani kuwa atauliwa, na awe anamjua mtu atakaye muuwa, lakini hajui muda uliopangwa. Au anajua kuuliwa kwake bila ya kujua mahali maalum. Kulingana na vigezo hivi viwili, kujipeleka kwa Imam kwenye kuuliwa kwake hakukanushiki, kwa kuwa yeye hakupewa habari ya wakati wala mahali mahsusi, kiasi cha kuwa apewe taklifu ya kujiepusha na viwili hivyo, kwa hiyo haelekezewi lawama ya kuwa alijipeleka mwenyewe kwenye kuhiliki. Ama jibu la tatu, ni muwafaka hata kwa muulizaji anayeitakidi uimamu, ambalo ni awe Imamu anatekeleza ibada ya taklifu mahsusi, nayo ni mfano wa taklifu ya mwanajihadi aliyeamriwa na mwenye taklifu ya jihadi mpaka aipate shahada. Hivyo Imamu ni kama mujahidu ambaye anaipokea shahada, halaumiwi wala kukemewa, kwa kuwa kitendo chake ni utii, si haramu wala si maasi, wala haitosemwa kumhusu kuwa kwa mkono wake amejiingiza katika maangamizi.

77


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 78

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu

DARAJA LA TATU: KWA WANACHUONI WA MWISHONI Wanachuoni waliokuja mwishoni wameifanyia uchambuzi na ubainifu wa ziada mas’ala hii, na hapa tunautaja kwa muhtasari: Imamu Kashiful-Ghita: Imethibiti kwa Imamu Husein salamu’llahi alayhi alijua matokeo yake kwa namna ambayo inairuhusu kanuni ya badau kuingilia kati, kwenda nayo na kuigeuza. Kwa ibara nyingine: Kwa kweli rangi iliyopayuka na sura iliyositushwa kuhusiana na hali ya mambo iko wazi kwake, anasema: “Hapana shaka kuwa wao salamullahi alayhim walikuwa wanajua yote hayo kwa kupewa habari na Nabii (s.a.w.w.) kwa njia ya wahyi, lakini wanatazamia huenda badau ikachukuwa nafasi itakayokuwa miongoni mwa ubao wa kufuta na kuthibitisha, itakayokuwa kinyume chake ndicho kilichothibiti katika elimu iliyohifadhiwa iliyofichwa, ambayo Mwenyezi Mungu ameifanya mahsusi Kwake binafsi.”78 Lakini aina hii ya elimu ambayo inawezekana ikabadilika na kuwa ujahili, na ukweli ukawa kitu kingine, haiwezekani iitwe elimu ila kimsamaha (kama ilivyo katika kanuni za matumizi ya lugha), kwa kuwa hapana elimu ila ni ile inayofichua ukweli, ama inayoonwa hivi sasa kuwa ni miongoni mwa ukweli, na ya kwamba yenyewe ni elimu (kumbe kihalisi yenyewe sivyo ilivyo), hiyo inaingia kwenye daraja ya dhana, wala haipandi na kuifikia daraja ya elimu ila kama itabadili njia yake na kutoka bila ya kuingiliwa na kanuni ya badau. Zingatia kwa umakini. Tuliyoyapata ni kuwa uangalizi uliotajwa huwezi ukasema ni wa aina ile ya kielimu ili kuirejesha mas’ala nyingi kwenye umoja. 78 Jannatul-Maawa Uk. 42. 78


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 79

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Sayyid as-Shahiid as-Swadri: Anakwenda na kuitolea sababu mas’ala ya elimu ya ghaibu ya Imamu Husain (a.s.) na hatma ya mauaji yake Karbalaa. Anaona kuwa maamuzi ya kisiasa na ya kijamii hayaachi kuwa ni maamuzi ya ghaibu, nayo (maamuzi hayo) ni mfuasi wake. Wala hatenganishi kati ya matukio mawili: Ukweli wa ghaibu na ukweli wa kijamii. As-Shahiid as-Swadri amebainisha kuwa Imamu Husain (a.s.) ameitoa mas’ala hiyo ya elimu ya ghaibu kupitia kauli mbiu kadhaa, na alifanya juhudi katika kuuelimisha umma wakati ule ili uwe na uelewa mzuri juu ya mas’ala hiyo. Kauli mbiu ya kwanza: Hatma ya mauwaji: Imamu Husain (a.s.) alikuwa anapingwa, na huambiwa: Kwa nini unatoka? Abdullah bin Zubair na wengine wanampinga. Na yeye (a.s.) anawaambia: “Kwa hakika mimi nitauliwa kwa hali yeyote sawa niwe nimetoka au sikutoka. Kwa hakika Bani Umayyah hawatoniacha hata kama nitafichama kwenye tundu la mdudu miongoni mwa wadudu hawa, lazima wangenitoa na wangeniua. Kwa kweli Bani Umayyah wananifuatilia popote niwapo, hivyo mimi ni maiti kwa hali yoyote ile, sawa nibakie Makka au nitoke humo, na ni vyema nisiuawe nikiwa Makka, ili isitanguliwe heshma ya Haram hii shariifu.” Waona yeye ameleta kauli mbiu hii, na kauli mbiu hii pamoja na ukweli wake inalingana na tabia ya umma unaoishi pia. Kwani tabia ya kushindwa ambayo umma wa kiislamu unaishi nayo, haupati tamko la kupenya humo ili kutoa ibara ya kukinza mfano wa harakati kama hizi kutoka kwa Imamu Husain, alayhi swalatu wasalaam. Hivyo yeye (a.s.) asema: “Mimi ni mwenye kuuawa kwa hali yeyote ile.” Na dhahiri yatoa ushahidi juu ya hayo. Dalili, ishara na msongamano wa mambo watoa ushahidi kuwa Bani Umayyah waliazimia kumuua Imamu Husein (a.s.) japo kwa njia ya kumvizia hata kama atakuwa amejiangika kwenye pazia za Kaaba. Hivyo basi kuileta kauli mbiu kama hii kwa ajili 79


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 80

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu ya kutoa tafsiri ya msimamo huu ilikuwa ni hali yalingana mno na hali ya kukinaika kwa tabia ya kushindwa, na wakati huo huo ni kauli mbiu ya kweli. Kauli mbiu ya pili: Ughaibu wa maamuzi ya safari: Watu wengine wanamjia wanamkinza, wanasema: Kwa nini unakwenda! Muhammad bin al-Hanafiyah anakuja mwanzo wa usiku na nasaha nyingi, na anamwambia: “Naangalia na ninafikiria usemayo.” Basi Muhammad Bin al-Hanafiya anakwenda, na katika mwisho wa usiku anasikia kuwa Imamu Husein (a.s.) ameondoka. Anamwendea, anakuja na kumshika mnyama wake wa safari na anamwambia: “Ewe ndugu yangu, uliniahidi kuwa utafikiri.” Imam anasema: “Ndiyo, lakini mimi nimelala usiku huu nikamuona Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akasema: ‘Kwa hakika wewe ni mwenye kuuawa.”’ Wamuona yeye (a.s.) anajibu jibu hili kwa maamuzi ya ghaibu yaliyotoka juu. Na uamuzi huu wa ghaib ni kutoka ngazi ya juu, haiwezekani tabia ya kushindwa iyakatae maadamu mwenye tabia hii anamwamini Husain na anaamini njozi ya Husein. Ndiyo yeye hajamwambia njozi hii Abdullah bin Zubair ambaye hakuwa muumini wa njozi ya Husain, bali alimhadithia hiyo Muhammad bin al-Hanafiyya na walio mfano wa Muhammad bin alHanafiyya. Na hii ni kauli mbiu nyingine alikuwa anaitoa nayo ni kauli mbiu ya umauti hauna budi juu yake, na kuwa kuna maamuzi ya juu yanayomfaradhia afe, ajitoe muhanga, ajitose, aikabili safari hii inayoishia kwenye kuuawa. Na kauli mbiu hii pia ilikuwa pamoja na ukweli wake, inaendana na tabia ya kushindwa, nayo wakati huohuo ni kauli mbiu ya kweli. Kauli mbiu ya tatu: Dharura ya kujibu wito wa wakazi wa mji wa Kufa:

80


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 81

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Na mara ya tatu analeta kauli mbiu ya tatu. Alikuwa anawaambia watu anaopishana nao akiwa njiani kutoka Makka akielekea Iraq, kwenye mafikio yake ambayo yalikuwa idadi kadhaa, walipokuwa wanamnasihi asiende Iraq, alikuwa anawaambia:” Kwa kweli mimi nimepata wito kutoka kwa watu wa Kufa niende kwao, na hali ya mambo yakiwa yamekuwa tayari katika mji wa Kufa, ili niende na ili niimarishe haki na niiondoe batili.” Hivyo alikuwa anaakisi na kuifasiri safari yake kwa msingi kuwa yenyewe ni kuitika na ni jibu kwa kitendo, na yenyewe ni ufafanuzi wa jibu la utashi, na kwamba umma umefanya harakati na umetaka, na kwamba hoja imesimama dhidi yake, kwa hiyo yeye hana budi aende. Imamu Husain (a.s.) hakuwa kwa ukweli wake anaishia katika daraja yake hii ya jihadi awe anangoja umma umuombe ndio aende, lau ingekuwa hivyo asingekuwa hapo mwanzo anaandikiana na wakuu wa ngome za Shia huko Basra akiwataka kwenda. Lakini yeye wakati huo huo alikuwa anaakisi upande huu zaidi kuliko alivyokuwa akiakisi upande ule. Kwa kuwa upande huu uko karibu mno na una uwiano zaidi na tabia ya kushindwa. Inasemaje tabia ya kushindwa mbele ya mtu anayeiambia: “Kwa hakika mimi nimepata wito, na kuwa hali ya mambo ya wito huu inalingana na hali ya kuukubali wito na kuondoka kumuelekea muhitaji.” Na kwa kawaida kuna tofauti kubwa kati ya mtu afanyaye harakati tokea mwanzo na mtu afanyaye harakati za kuuitika umma uliomwamini na ambao umeamini uongozi wake na ukuu wake. Katika harakati za tangu mwanzo kuna kauli ya tabia ya kushindwa: Na kwa kweli huyu mtu ni mwenye haraka, na kwa kweli huyu hafikirii matokeo, na kwamba yeye amejiingiza mwenyewe kwenye hatari.

81


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 82

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Ama tendo linapokuwa ni jibu la wito kutoka kwa umma uliyoandaa hali zote za lazima kwa ajili ya wito huu, tabia hizi za kushindwa hazisemi kuhusiana na kazi hii na uendaji huu kwamba: Ni tendo la kutia haya, na kuwa ni tendo la kitoto, na kwamba ni tendo lisilodurusiwa. Kauli mbiu hizi ambazo Imamu Husain (a.s.) amezileta, zote zilikuwa ni za uhakika, na wakati huohuo zilikuwa zinaafikiana na tabia za umma ulioshindwa kiroho, kifikra na kinafsi. Kauli mbiu ya nne: Dharura ya kupambana dhidi ya Sultani dhalimu: Na pia alikuwa anaweka pambizoni mwa kauli mbiu hizo zote kauli mbiu ya ukweli hasa alipokuwa anatilia mkazo kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Mwenye kumuona Sultani dhalimu na wala hakumrekibisha kwa kitendo wala kauli, itakuwa haki kwa Mwenyezi Mungu amuingize mahali pake.� Pembeni mwa kauli mbiu hizo ambazo zinatimiza chapa ya kisheria katika kazi yake kwa kiwango cha tabia ya umma, pia alikuwa anatoa kwa muendelezo na daima kaulimbiu ya kweli iliyo hai, ambayo hapana budi iwe ndio msingi wa tabia mpya ambayo alikuwa anaijenga katika dhati ya umma huu wa kiislamu.79 Sayyid Muhammad Husain Tabatabai: Alijibu baada ya kuletwa swali lifuatalo: Je hivi Sayyidu Shuhadaa (a.s.) alikuwa ajua katika safari yake kutoka Makka mpaka Kufa kuwa atakufa kishahidi au hapana? Kwa ibara nyingine, hivi yeye (a.s.) alielekea Iraq kwa kusudi la shahada au kwa kusudi la kuunda serikali ya kiislam adilifu? Kwa kweli Sayyid Shuhadaa kulingana na itikadi ya Shia ni Imamu ambaye kumtii ni faradhi wajibu, naye ni watatu wa makhalifa wa Rasulil79 Al-Fikru Al-Islamiy, toleo la kumi na saba Uk. 70. 82


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 83

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Akram (s.a.w.w.), na yeye ndiye mwenye mamlaka yote wakati huo. Hakika elimu ya Imamu ya vitu halisi vya nje na matukio ya ukweli, huwa kwa idhini ya Allah (s.w.t.), hiyo ni juu ya hakika zote za ulimwengu uliopo, na katika sharti zake zote, hiyo ni pamoja na zile ambazo hujulikana kwa njia ya hisia tano, na kadhalika ni pamoja na zile zilizo nje ya hisia tano, kama vile yaliyomo mbinguni, matukio yaliyopita na matukio yatakayokuja. Hayo tunayatolea dalili zijazo: Kwanza: Njia za kuthibitisha elimu hiyo kwa kunakili hutimia kwa riwaya mutawatir zilizo katika vitabu vinavyokusanya Hadithi za Shia, mfano wa kitabu al-Kafiy, al-Baswairu, vitabu vya Swaduq, al-Biharu na vingine. Kwa hiyo kwa mujibu wa riwaya hizi ambazo haiwezekani kuziwekea kipimo na kuziwekea wigo, inabainika kuwa Imamu (a.s.) hupata elimu yake kwa njia ya hiba ya kiungu, sio kwa njia ya kujifunza toka kwa mtu. Hivyo anafahamu kila kitu na anavijua, na kila akitakacho hukijua kwa idhini ya Mwenyezi Mungu na kwa kiasi kidogo cha kuzinduka. Kuna Aya kadhaa ndani ya Qur’ani tukufu ambazo zinaiwekea wigo elimu ya ghaibu, kuwa ni ya Mwenyezi Mungu tu Aliye juu kwa daraja, na ni katika uwanja Wake Mtakatifu. Lakini enguo liliopo katika Aya tukufu:

“Ni mjuzi wa yaliyo ghaibu wala hamdhihirishii yeyote ghaibu yake. Isipokuwa Mtume aliyemridhia, basi hakika yeye humuwekea walinzi mbele yake na nyuma yake.” (Sura Jinni: 26 - 27). limebainisha kuwa elimu ya ghaibu kuwa mahsusi kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ni kwa maana hii: Ni kwamba ghaibu inayojitegemea na umiliki wa dhati ni Wake, hauwi kwa yeyote asiye Mwenyezi Mungu (s.w.t.), lakini yawezekana kwa Manabii wateuliwa wakaijua kwa kuelimishwa na Mwenyezi Mungu, na 83


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 84

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu yawezekana pia wateuliwa wengine wakajua kwa kuelimishwa na Manabii. Kwa hiyo katika riwaya nyingi zimekuja kuwa Rasul na pia kila Imamu atakayekuwa baada yake, hukabidhi elimu yake kwa Imamu anayekuja baada yake, katika sehemu ya mwisho ya uhai wake. Pili: Ama kwa njia ya akili kuna thibitisho ambazo kulingana nazo Imamu (a.s.) kulingana na nafasi yake yenye nuru, ni mtu mkamilifu mno wa zama zake, na ni dhihirisho kamili la majina na sifa za kiungu, na ni mjuzi kwa vitendo wa matukio yote ya kibinafsi, na kulingana na asili yake kokote aelekeako ukweli wa mambo wote humfichukia, na tunaona kuwa thibitisho hizi zimefungwa na mlolongo wa maswali ya kiakili, upeo wake ni wa juu mno kuliko upeo wa insha hii, kwa minajili hii tunaihamishia kwenye maudhui nyingine. Na hapa kuna suala ambalo ni wajibu tulitupie jicho, nalo ni: Elimu kama hii iliyo thabiti, kwa mujibu wa dalili za kiakili na za nukuu haikabiliwi na tatizo la kuwa kinyume au kubadilika, na kwa istilahi ni elimu ambayo imethibiti katika Lawhul-Mahfudh na ni habari ambazo zimeambatana na makadiri ya Allah. Na dharura ya kubainisha yaliyotangulia ni kuwa hakuna uhusiano wowote kati ya aina yeyoye ya taklifu na uambatano wa elimu ya aina hii, kadhalika hakuna mafungamano na kitendo cha mwanadamu kuikusudia au kuiomba, kwa kuwa wakati ambao taklifu huwa inaambatana na tendo kwa njia ya uwezekano, na hali kutenda na kuacha, mawili hayo yote yapo katika hiyari ya mukalafu, wakati huo viwili hivyo huwa viko kwenye njia ya uombaji wake. Ama upande wa kuwa yenyewe ni lazima ithibiti na kwamba yaambatana na makadiri ya lazima, ni muhali upande huo kuwa ni mahali pa takliifu. Mfano, ni sahihi Mwenyezi Mungu amwambiye mja wake: “Tendo ambalo kulitenda na kutolitenda yawezekana kwako, na ambalo liko katika hiyari yako, ni wajibu ulitende.� Lakini ni muhali aseme: “Tendo ambalo 84


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 85

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu ni wajibu liwe kwa mujibu wa utashi Wangu wa uumbaji na makadiri Yangu ya lazima, na ambalo kuthibiti kwake hakuna taradudi, ni wajibu juu yako utekeleze au usitekeleze.” Kwa kweli mfano wa amri na katazo kama hii haina athari. Ni kama hivi, mtu anaweza kuwa na utashi katika jambo ambalo lina uwezekano kutokea na kutotokea, na alifanyie kusudi au lengo na afanye juhudi ili lithibiti. Lakini haitowezekana awe na utashi katika jambo ambalo kwa yakini kabisa litatokea, na ni muhali kulibadilisha na kutotokea na linalokuwa katika makadiri ya lazima ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.), hivyo utashi wa mwanadamu hautokuwa na uwezo wa kuliomba au kulipuuza jambo la aina hii ambayo haina budi kutokea. Inakuwa wazi kutokana na ubainifu huu: 1. Kwa kweli elimu hii ya Imamu (a.s.) ya kutunukiwa haina athari katika amali yake na taklifu yake mahsusi. Na kimsingi ni kwamba kila jambo ambalo ni faradhi kwa upande wa kuambatana kwake na makadara ya lazima, halina mafungamano na amri na katazo au utekelezaji wa mwanadamu au kusudio lake. Ndio, kuambatana kwa makadara ya lazima ya Mwenyezi Mungu na utashi Wake (s.w.t.) wa kata shauri, huwa ni mahali pa ridhaa yake (a.s.), kama alivyosema Sayyidu Shuhadaa katika saa ya mwisho ya maisha yake na hali yeye akiwa kati ya mchanga na damu, alisema: “Kwa ajili ya kuridhia makadara Yako na kujisalimisha kwenye amri Yako, hakuna apasaye kuabudiwa asiyekuwa Wewe.” Na kama alivyosema katika hotuba yake alipokuwa anatoka Makka: “Kuridhika kwa Mwenyezi Mungu ndio ridhaa yetu Ahlul-Bayt” 2. Kwa kweli tendo la mwanadamu kuwa ni la lazima kwa upande wa kuambatana kwake na makadiri ya Mwenyezi Mungu haizuii tendo hilo kuwa la hiyari kwake kwa upande wa vitendo vya hiyari, kwa kuwa 85


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 86

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu makadiri ya kiungu ya kitendo yana mafungamano na fafanuzi zake zote na sio kwa kitendo peke yake. Mfano: Mwenyezi Mungu amemtaka mtu fulani afanye kitendo cha hiyari kwa hiyari yake, katika sura hii kuthibiti nje kwa kitendo hiki cha hiyari kwa kuwa kinaambatana na utashi wa lazima wa Mwenyezi Mungu hakiwezi epukwa, wakati huo huo ni cha hiyari kwa mtu, na nisba ya kitendo kwake ni nisba ya uwezekano. 3. Kwa kweli kabiliya ya dhahiri ya matendo ya Imamu (a.s.) ya kutafsiri kwa kutumia sababu za dhahiri, haiwezi kuwa dalili ya kutokuwepo elimu hii iliyotolewa hiba, au iwe ndio ushahidi wa kutojua kwake tukio, kwa mfano isemwe: Ikiwa Sayyidu Shuhadaa (a.s.) anayo elimu ya tukio, basi ni kwa nini alimtuma Muslim bin Aqiil huko Kufa akiwa wakili wake? Na ni kwa nini Swaidawiy alituma barua yake kwa watu wa Kufa? Na kwa nini alijitia binafsi kwenye maangamizi hali ikiwa Allah (s.w.t.) anasema: “Wala msijiingize kwa mikono yenu kwenye maangamizi”? Na kwa nini? Na kwa nini? Kwa kweli tuliyoyataja ni jibu la maswali hayo yote wala hapana maana ya kukariri. Mtume (s.a.w.w.) kwa mujibu wa tamko la Qur’ani tukufu, kadhalika Maimamu (a.s.) miongoni mwa dhuria zake walio tohara, wote ni binadamu mfano wa binadamu wengine, na matendo wayatendayo katika muda wa uhai wao ni mfano wa matendo ya watu wengine, yanatendeka kwenye nyanja za hiyari yao na kwa msingi wa elimu ya kawaida. Imamu Ali (a.s.) ni kama wengine wanaiona kheri na shari, manufaa na madhara, na matendo yote haya ni kwa njia ya elimu ya kawaida. Ayaonayo yamfaa miongoni mwa matendo haya yeye huyataka na hufanya juhudi kuyatekeleza. Na wakati ambao sababu, vitendea kazi, hali ya mambo na hali ilivyo nje ni ya kufaa ndipo malengo yake huthibiti, na kati86


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 87

ka hali ambayo sharti hazifai basi malengo yake hayawi. Na elimu ya Imamu (a.s.) kwa idhini ya Mwenyezi Mungu zikiwemo sehemu zake zote, matukio yaliyopita na yajayo, haiathiri matendo yake ya hiyari, hivyo ni kama ulivyotimia ubainifu wake. Imamu ni sawa na wanadamu wengine, ni mja wa Mwenyezi Mungu, apaswaye kuwajibika na sheria, na ana wadhifa wa maamuzi na lazima za kidini, na kulingana na nafasi yake kiuongozi aliyopewa na Mwenyezi Mungu Mtukufu, itakuwa wajibu juu yake atekeleze kwa vipimo vya kibinadamu vya kawaida, na atumiye upeo wa juhudi yake ili kuhuisha neno la haki na kuihifadhi dini.80 Kikao na al-Kafiy kuhusu riwaya: “Na kwamba wao hawafi ila kwa hiyari kutoka kwao wenyewe”: Na muhtasari wa aliyoufaidisha Kulayniy kwenye kichwa cha habari ya mlango “Na kwamba wao hawafi ila kwa hiyari kutoka kwao wao wenyewe” anamaanisha kuwa umauti wa kiungu ambao Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amewashurutisha waja wake na wasiokuwa Yeye, bila ya kuachwa yeyote, na amejitenga Yeye kuwa ndiye wa kubaki sio wao, hapana budi uwaingize wao (a.s.) bila kizuizi, wala wao hawana kimbilio mbali nao. Ila tu wamekuwa wapekee kati ya viumbe wengine, kuwa Mwenyezi Mungu amejaalia hiyari ya kufa kwao ni juu yao wao wenyewe, na hii yafahamisha: Kwanza: Kuwa wao wana hiyari ya kuchagua wakati wa umauti, kwa hiyo wanachagua wakati uliopangwa ulioangikwa, kabla haujakatiwa shauri, hivyo hilo huwa kwa utashi kutokana na wao, kwa hiyari na ujuzi, upendo utokanao na wao katika kuharakia kukutana na Allah, na kuthibitisha athari kubwa iliyopangika kwa ajili ya shahada yao katika wakati ule ulioteuliwa. 80 Ilmul-Imamu Wanahdhwatu Sayyidish-Shuhadaa cha Tabatabai Uk. 45 – 49 87


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 88

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Na hii yalingana mno na usemi wa kwamba kuliendea kwao jambo huwa kwa hiyari yao kamili, na kuwa sio jambo lililolazimishwa juu yao, na inafaa mno kuwa hiyo inaafikiana na makadara ya Allah na uamuzi wake. Hivyo yeye anakusudia kwamba ni utashi wa Allah kutoka kwao kwa lile waliloliendea, bila ya kuwa suala ni la lazima. Kama si hivyo na ikiwa ni makadara ya lazima yaliyokwisha kupitishwa na ni muda uliopangwa wa lazima, vipi watakuwa na hiyari humo?! Na nini maana ya kuafiki kwao juu ya ambalo hawawezi kulitoka na kwenda kweye lingine.?! Pili: Wao wana hiyari ya kuchagua aina ya umauti ambao watakaokufa nao, miongoni mwa kuuliwa na upanga kwa pigo moja, kama alivyochagua hilo Imam Amirul-Mu’miniin (a.s.), au kwa kunywa sumu au kula kilichotiwa sumu, kama walivyochagua Maimamu wengi (a.s.), au kwa kukatwakatwa viungo vya mwili, na kwa kukatwa koo na kuivumilia mikuki na mishale na machungu ya vita na mikuki, na kuvumilia kiu, kama ilivyojiri kwa Imam Sayyid Shuhadaa (a.s.). Wala tamko la jumla la anuwani halikatai kulibebesha yote hayo. Hali ikiwa katika maana ya pili kuna upeo muhimu wa kijamii, nao ni kuwa Maimamu walio tohara (a.s.) walikuwa wanajua kupitia hali ya mambo, matukio, ishara na mambo yanayojiri na kuwazunguka, bila hata ya haja ya kuitegemea ghaibu na utoaji wake habari, kwamba makhalifa wadhalimu, na majahili walioshinda juu ya serikali ya waja na nchi, watakuja wazitoe roho zao takatifu kwa kila njia itakayowawezesha, kwa kuwa wao hawawezi kuvumilia kuwepo kwa Maimamu wanaozikataa serikali za kidhalimu na za kifisadi, na ambazo zinahukumu na kushinikiza hukumu zake kwenye shingo kwa batili, na kwa jina la uislamu, ili kuchafua utajo wake ulio safi kwa matendo yao mabaya. Maimamu (a.s.) waliotohara ili kuuleta kimwili upinzani wa haki ulio hai, japo kuwa wao walikuwa katika hali ya ukimya, na bila ya kunyoosha 88


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 89

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu mkono kwenye silaha za chuma, lakini kuwepo kwao kutukufu kulikuwa ni kama makombora yaliyo tayari kulipuka wakati wowote! Na mafunzo yao yalikuwa yanawakilisha vilio vinavyofanya mwangwi kwa watu watendao batili, darasa zao na sera zao zilikuwa zinawakilisha cheche dhidi ya serikali hizo! Basi vipi zitaweza nidhamu za kifisadi kuuvumilia uwepo wa hao Maimamu (a.s.) japo kwa mtupo mmoja wa jicho?! Na Maimamu (a.s.) walikuwa wanajua kuwa mwisho wao ni umauti, na wanatambua kuwa madhalimu wanawafanyia vitimbi, na wanawavizia kwenye mzunguko wa hali ya mambo, na wanawafanyia mpango wa kuwaua na kujinasua mbali na uwepo wao, na wanafanya juhudi ili watimize uovu wao wakiwa siri kifichoficho, ili wasibebe jukumu la kuulizwa kwa hayo, wala wasihesabiwe dhidi yao katika historia! Na lau watawala waovu wangekamilisha kuwamaliza hawa Maimamu kwa siri na kwa njia waipendayo, ingekuwa ni jambo lenye manufaa mno kwao na bora kwa malengo yao! Lakini Maimamu (a.s.) hapana budi wavizime vitimbi hivi vya wadhalimu wauaji, wachukue kwa mikono yao hatamu za kuuingilia kati uwanja huu muhimu na hatari. Na wachague wao wenyewe namna bora ya umauti, ambayo itakayotangaza kudhulumiwa kwao, na wapige kelele ya kuomba msaada wa kudhulumiwa kwao, na kuwafedhehesha wauaji wao, na watangaze uovu na vitimbi vilivyojiri dhidi yao, wala nafsi zao zisizo na hatia zisipotee bure, wala damu zao tohara zisimwagike bure. Lau Imamu Amirul-Mu’miniin (a.s.) angeuliwa nyumbani mwake, au katika baadhi ya vichochoro na njia, nje ya msikiti, nani basi angeweza kuyapuuza madai ya uzushi ambayo Bani Umayyah waliyaeneza kati ya watu wa Shamu ya kuwa Ali (a.s.) haswali?! Basi pindi waliposikia kuwa yeye aliuliwa msikitini walitanabahi na kuutambua uwongo wa madai hayo potoshi.

89


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 90

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Lau Imamu Husain (a.s.) angeuliwa Madina, basi ni nani angelijua suala lake?! Hata kama angeuliwa Makka. Ongeza kuwa angechukuliwa kuwa amefanya tendo la aibu, kwa kuwa mwiko wa Haram umekiukwa kwa kuuliwa kwake! Ingekuwa damu yake yapotea kati ya sauti za juu za mahujaji na kelele zao! Lakini Husain (a.s.) akiuliwa katika ardhi si Karbala, basi ni wapi?! Na vipi?! Na itakuwa nini tafsiri ya maelezo yote yaliyonakiliwa na vitabu, na habari zote kutoka kwa babu yake Nabii mteuliwa (s.a.w.w.) kuhusu mto Furat, Karbalaa na udongo wake mwekundu?! Hivyo uchaguzi huu wajulisha uratibu wa mwenye hekima na ujanja wa kisiasa, na mtazamo unaopenya, na jambo lililoshikwa lililo thabiti, ambalo kwalo Maimamu (a.s.) kwa ajili yake walisimama kidete katika maisha yao ya kisiasa kuwahusu wadhalimu wenye kutwaa vipimo vyote, na ambao wameupokonya umma uhuru wake wote, hata uhuru wa kuuchagua umauti, kiwango chake na jinsi yake, wakati na mahali. Kwa kuwa kusimama kwa Maimamu (a.s.) wakiwa na mpango wao wenye hekima dhidi ya utawala uliokuwa katika mapambano haya, na kuuvuka kwa utashi wao, na kuichukua hatamu ya hiyari mikononi mwao, na kuchagua kwao njia iliyo bora ya umauti wao, kwahesabika kuwa ni ushindi mkubwa, katika mazingira yale ya shida kandamizi. Je kuihifadhi nafsi, na utashi wa kutomwaga damu, na hofu ya kuuawa, ni mambo yanayozuia kutekeleza wajibu?! Na je kwazuia sera ya majukumu makubwa, ambayo ni kuuhifadhi uislamu na miko yake, na kutimiza hoja juu ya umma baada ya kuufikishia wito na msaada wa mfululizo?! Kisha je yaingia akilini kuihifadhi nafsi, baada ya kuzivuka daraja hizo za kimapambano, na ambayo natija yake inayongojewa ni kuuliwa?! 90


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 91

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Kwa kuwa Yazidu aliazimia kumuuwa Imamu (a.s.) ambaye alikuwa anamwona kizingiti pekee mbele yake kimzuiacho kupata matunda ya juhudi ya baba yake kuelekea njia ya ufalme wa Kibani Umayyah wenye kuuma, hivyo hapana budi amuondoe njiani. Utawala wa Bani Umayyah unatamani lau Husain (a.s.) angesimama akiwa kimya mtulivu, japo kwa kadiri ya mtupo mmoja wa jicho, ili aimarishe lengo lake, na umuuwe!! Uzuri ulioje lau kufa kwa Husain (a.s.) kungekuwa kwa njia ya kumteka, ili damu yake ipotee na suala lake liwe bila faida!! Na Husain (a.s.) alifichua utashi wao wa kumuua kama hivi, na kuwa wao wamedhamiria hilo hata kama watamkuta kwenye shimo la wadudu! Yazid aliwaelekeza mamluki wake kuwa wafanye kila wawezalo kumuua Husain popote wamkutapo japo awe amejiangika kwenye pazia ya Kaaba! Basi ni kwa nini Imam (a.s.) asiwatangulie kwa kuchagua zama iliyo bora mno, na mahali palipo bora mno, na aina iliyo bora mno ya kuuliwa?! Zama ni Ashura iliyosajiliwa katika ulimwengu wa ghaibu, na iliyothibitishwa katika Sahifa za mwanzo, na zilizofuata miongoni mwa habari za ghaibu, ambayo tutaidhihirisha. Mahali ni Karbalaa, ardhi ambayo jina lake limetajwa na ndimi toka zama za Manabii. Ama aina ya kuuliwa aliyoichagua ni mapambano ya kishujaa yautafutao umauti, ambayo mwangwi wake umebaki. Mwangwi wa ushujaa wake, sauti za mgongano wa panga zake na kilio cha Husein (a.s.) vinafichua malengo yake na kudhulumiwa kwake, vinatoa mwangwi katika masikio ya historia muda wote, vinabatilisha walikolalia madhalimu na wanaopotosha ukweli. Kwa kweli Imam Husain (a.s.) na kwa mfano wa ambayo ameyafanya kwa kujipeleka, kumethibitisha kudumu kwa utajo wake, na kuzungumziwa kuuawa kwake katika sahifa za dahari, ili kuuliwa kwake kusipatwe na 91


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 92

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu khiyana za wapotoshaji, wala upinzani wa wakanushaji, wala ubadilishaji wa wapotoshaji, lakini kunadumu kudumu kwa haki na dini.81 Na mwishowe kwa kweli Shaikh Kulayniy, naye ni mwaminifu mno miongoni mwa watu katika Hadithi na mdhibiti mno, kama ambavyo anNajashiy alivyotoa ushahidi kumhusu, hakika amejengea utunzi wa kitabu chake juu ya msimgi madhubuti. Na miongoni mwa shuhuda za umadhubuti humo ni kuwa yeye Mwenyezi Mungu amrehemu, ameweka mlango kwa anuani: “Nadra katika kuitaja ghaibu.” Humo ameleta Hadithi zinazotanzua mushkili wa upinzani wa kwanza juu ya elimu ya ghaibu ya Maimamu (a.s.). Ndanimwe mna jibu safi la kauli ya muulizaji aliyewauliza Maimamu (a.s.): “Je mnaijua ghaibu?” Na ameifanya natija ya mlango huu kuwa ndio asili iliyowekwa kwa ajili ya milango ifuatayo. Na miongoni mwa Hadithi hizo ni Hadith ya Humran Bin A’a’yan, alimuuliza Abu Ja’far (a.s.): “Umeiona kauli yake Jalla dhikruhu “Ni Mjuzi wa yaliyo ghaibu wala hamdhihirishii yeyote ghaibu yake.” (Sura Jinni: 26)” Abu Ja’far (a.s.) akasema: “Isipokuwa Mtume aliyemridhia, na Muhammad Wallahi alikuwa miongoni mwa aliowaridhia.”82 Hivyo Kulayniy alikuwa anachunga kuratibu milango ya kitabu chake uratibu wenye mfumo wa kidalili na hoja, ili hatima yake izae tija zenye mantiki na zenye kukubalika. Hivyo akakifanya kitabu chake al-Kafiy kuwa ni kizibo cha tundu lenye kuielekea dini kwa malengo mabaya, hawawezi walahidi kuiondolea heshima kupitia tundu hilo kwa utata wao na mashaka yao, wala hawawezi kuitia dosari wale wakanusha dini.

81 Al-Husayn Simatuhu Wasiratuhu Uk. 112. 82 Al-Kafiy Juz. 1, Uk. 256, Hadithi ya 2. Wafasiri wengi wa Kisunni na Kishia wameafiki maana hii. 92


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 93

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu

NATIJA YA UTAFITI Imethibiti kupitia mwendo wa utafiti kuwa mwanadamu ni aina iliyoumbwa kwa njia ambayo hawezi kujitosha kiasi cha kuwa hana mafungamano na ghaibu, kwani majukumu yake ya kirisala yanategemea kuambatana kwake na ghaibu, kwanza. Pili, kuijua kwa lengo la kuamiliana nayo, hali hiyo ni kwa sababu kutimia malengo ya kiungu kunategemea kuwa na elimu ya ulimwengu huu mpana. Wala hapana kupingana kati ya anayoyamiliki mwanadamu miongoni mwa uhuru na utashi, na kati ya miyenendo ya kuwepo inayosimama juu ya misingi ya kutokuwa na hiyari, kwa sababu mwanadamu ameongezewa elimu ambayo kwayo amezitambua siri za kuwepo na harakati zake zinazofanya sababu ya kuwa kitu, matokeo yake na mwisho wake. Na elimu hii haiachani na umaasumu ambao wamzuia kuchezea siri hizi. Kwa sababu umaasumu wamaanisha kuwa maasum kwa elimu hii anadiriki ukweli wa vitu kama vilivyo kwa uoni wa wazi na kwa namna isiyokubali shaka, jambo ambalo lamfanya awe anastahiki kupewa wadhifa wa mambo ya risala na malengo yake. Na makusudio hayakuwa elimu ile ipatikanayo kwa kuchuma, kujifunza na kwa juhudi, kwa sababu hii ni pungufu na ni yenye ukomo, hali ikiwa risala yahitajia duru kamili. Hivyo basi ikusudiwayo ni elimu ya kutunukiwa, aliyotunukiwa kutoka Kwake (s.w.t.). Elimu ya Imam (a.s.) inatofautiana na elimu ya Allah (s.w.t.), kwa sababu elimu Yake (s.w.t.) ni ya milele na ni yenye kuyatangulia maalumati na yajulikanayo. Nayo ni dhati Yake (s.w.t.). Ama elimu ya kutunukiwa kwa Imam (a.s.) haishirikiani chochote na elimu ya Allah katika mambo haya, kwa kuwa elimu ya Imam (a.s.) ni ya kutokea na hutanguliwa na maalumati nayo si ya dhati ya Imam. Hivyo basi elimu ya Imam ni ya 93


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 94

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu kuzuka na ni ya kutunukiwa ya kupewa na Yeye Azza Wajallah, hivyo hapana uwiano kati ya elimu mbili hizo. Aya nyingi zimeongelea elimu ya ghaibu katika maisha ya Manabii na watu wema, kama vile Nabii Yusuf, Nabii Suleyman, Nabii Isa na Nabii Daudi alayhimu salaam. Kisha yapasa ijulikane kuwa hapana mgongano kati ya Aya ambazo zinaiwekea wigo ilimu hii kuwa ni ya Mwenyezi Mungu tu (s.w.t.) na yakanusha kuhusika nayo wengine, na Aya zile ambazo zinaithibitisha kuwa huwanayo wengine wale wasiokuwa Allah (s.w.t.). Aya ya kwanza inaithibitisha katika hali ya msingi na asili ya elimu, na ya pili inaithibitisha kwa kufuatia. Na zaidi ya hiyo ni kuwa elimu ya kutunukiwa iliyopo kwa maasum husifika kuwa ni ya kuendelea na kubaki, na likusudiwalo ni uwezo, sio ile elimu iliyo tupu mbali na uwezo. Kama ambavyo elimu ya maarifa inavyotilia nguvu kuwa elimu ukweli wake ni katika kufichua kwake ukweli, na kwamba elimu au kufichua ukweli ni jambo la hali ya juu lililo mbali na mada, kwa sababu ya kutoafikiana sifa zake na elimu. Hivyo elimu na kufichukiwa na ukweli havipatikani isipokuwa kwa mawasiliano ya uwepo wa ukweli na ya uhalisia kati ya nafsi na kitu kikusudiwacho kutambuliwa, na ni maarufu kuwa nyenzo za mawasiliano ya kielimu na ukweli wa tukio, ima ni njia tano za fahamu au akili au mawasliano ya ana kwa ana na kitu bila ya kiunganishi cha njia za fahamu au akili, jamabo ambalo huelezwa kwa ibara ya: AlMaarifatushuhudiya au al-Qalbiyah au al-Fuadiyah. Na nyenzo hizi za kuipata elimu ni fursa kwa wote bila ya wengine kuenguliwa. Upande wa nafsi ya mwanadamu kulingana na yanayothibitishwa na elimu ya falsafa ya saikolojia ni kuwa ina viwango na daraja. Na yasifika kuwa na uwezo wa kuzidiriki kuliyati, hivyo daraja ya juu mno ndanimwe huitwa utambuzi wa kimoyo, au wa 94


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 95

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu kutunukiwa au hiba ya kutunukiwa uhalisia wa vitu. Lakini daraja hizi pia zina viwango, na daraja ya chini mno miongoni mwazo ni, njozi za kweli, na kiwango cha katikati ni Ilhamu na semesho la malaika. Na yenye nguvu zaidi katika ngazi hii na kwa urefu wake ni kufanikiwa kuupata wahyi. Kwa minajili hiyo, kwa kweli nafsi ya Imam inatofautiana na nafsi zingine, kwa upande wa wasaa wa kudiriki, na maarifa yake kuuzunguka ukweli na kuwa mbali kikamilifu na mada. Na nidhamu ya sababu na kisababishwa inayohukumu ulimwengu huwa hadhiri kwa Imam (a.s.) na hapo anakuwa ameitambua kikamilifu, na ni wazi kuwa kuijua sababu kunamaanisha kukijua kinachosababishwa na sababu hiyo, hivyo Imam (a.s.) huwa anajua utashi ambao ni mojawapo ya hizo sababu, na kadhalika sababu zingine anakuwa na maarifa nazo kamili. Na kuwa daraja ya juu mno ya kutokea vitu, ikiwemo tukio lililo chini ya hiyari ya mwanadamu, kuwepo kwake kunategemea elimu kamili ya (s.w.t.) kuhusiana navyo. Hivyo kwa kupitia njia yake na kwa utoaji wake wa habari elimu ya hivyo vitu huwa. Ama mtizamo wa wasiokuwa Imamiya kuihusu mas’ala hii unaipa nguvu kupitia yale ambayo hayakubali shaka, kuwa elimu ya ghaibu wametunukiwa si manabii peke yao, bali pia watu ambao sio maasumu. Lakini elimu au kufichukiwa ambako walikokusema hakuthibitishi Uwalii, kwani Uwalii huthibiti kwa Nassu tu, huu ni upande mmoja, na kwa upande mwingine wao wameichukua elimu ya ghaibu kwa anuani ya karama na kufichukiwa, na sio elimu ya kutunukiwa ambayo yafuatana na umaasumu kulingana na mtazamo wetu. Na mwisho ni kuwa Imamiya muda wote wamejilazimisha, kuwa elimu hii ambayo ni wajibu Nabii au Imam asifike nayo, ni elimu ya maudhui za nje na matukio mengine ya kilimwengu, kuongezea elimu ya hukumu.

95


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 96

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Umejadiliwa baadhi ya upinzani uliojitokeza katika mas’ala hii zama za Maimam (a.s.), kiasi kwamba majibu yao yote yanatilia nguvu kumiliki kwao elimu ya kutunukiwa ambayo haigongani na usemi wa kujitia katika maangamizi au kutokuwa na faida katika matendo yao. Kama ambavyo hapana tofauti kati ya mwenendo anaokwenda nao Sheikh Mufiidu au Sheikh Tusi au Allama Hilli, na kadhalika wanachuoni wengine waliokuja nyuma, bali tofauti imetokea katika tafsiri tu ya mas’ala wala si vinginevyo.

96


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 97

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24. 25. 26.

Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thalathini Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudharr Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur'an na Hadithi Elimu ya Nafsi Yajue Madhehebu ya Shia Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu 97


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 98

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu 27. 28. 29. 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52. 53. 54. 55. 56. 57.

Al-Wahda Ponyo kutoka katika Qur'an. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii Mashukio ya Akhera Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyeezi Mungu na sifa zake Amateka Na Aba'Khalifa Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana. Upendo katika Ukristo na Uislamu Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya Kupaka juu ya khofu Kukusanya swala mbili Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kusujudu juu ya udongo Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) Tarawehe Malumbano baina ya Sunni na Shia Kupunguza Swala safarini Kufungua safarini Umaasumu wa Manabii Qur’an inatoa changamoto as-Salaatu Khayrun Mina -'n Nawm Uadilifu wa Masahaba Dua e Kumayl Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu 98


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 99

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu 58. 59. 60. 61. 62. 63. 64. 65. 66. 67. 68. 69. 70. 71. 72. 73. 74. 75. 76. 77. 78. 79. 80. 81. 82. 83. 84. 85. 86.

Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mitume Muhammad (s) Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili Kuzuru Makaburi Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita Tujifunze Misingi Ya Dini Sala ni Nguzo ya Dini Mikesha Ya Peshawar Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliyonyooka Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake Liqaa-u-llaah Muhammad (s) Mtume wa Allah Amani na Jihadi Katika Uislamu Uislamu Ulienea Vipi? Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) Urejeo (al-Raja’a ) Mazingira Utokezo (al - Badau) Sadaka yenye kuendelea Msahafu wa Imam Ali 99


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 100

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu 87. 88. 89. 90. 91. 92. 93. 94. 95.

Uislamu na dhana Mtoto mwema Adabu za Sokoni Johari za hekima kwa vijana Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu Tawasali Imam Mahdi katika Usunni na Ushia

96.

Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu

97.

Hukumu ya kujenga juu ya makaburi

98.

Swala ya maiti na kumlilia maiti

99.

Shiya na Hadithi (kinyarwanda)

100.

Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu

101.

Hadithi ya Thaqalain

102

Fatima al-Zahra

103.

Tabaruku

104.

Sunan an-Nabii

105.

Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza)

106.

Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili)

107.

Mahdi katika sunna

108.

Kusalia Nabii (s.a.w)

109.

Ujumbe -Sehemu ya Kwanza

110.

Ujumbe - Sehemu ya Pili

111.

Ujumbe - Sehemu ya Tatu

112.

Ujumbe - Sehemu ya Nne

113.

Ngano ya kwamba Qur’ani imebadilishwa 100


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 101

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu 114.

Iduwa ya Kumayili

115.

Maarifa ya Kiislamu.

116.

Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza

117.

Ukweli uliopotea sehemu ya Pili

118.

Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu

119.

Ukweli uliopotea sehmu ya Nne

120.

Ukweli uliopotea sehmu ya Tano

121.

Johari zenye hekima kwa vijana

122.

Safari ya kuifuata Nuru

123.

Idil Ghadiri

124.

Myahudi wa Kimataifa

125.

Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi

126.

Visa vya kweli sehemu ya Kwanza

127.

Visa vya kweli sehemu ya Pili

128.

Muhadhara wa Maulamaa

129.

Mwanadamu na Mustakabali wake

130.

Imam Ali binamu ya Mtume Sehemu ya Kwanza

131.

Imam Ali binamu ya Mtume Sehemu ya Pili

132.

Khairul Bariyyah

133.

Uislamu na mafunzo ya kimalezi

134.

Vijana ni Hazina ya Uislamu.

135.

Yafaayo kijamii

136.

Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu

137.

Taqiyya

138.

Vikao vya furaha

139.

Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 101


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 102

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu 140.

Uislamu na Mazingatio Sehemu ya Kwanza

141.

Uislamu na Mazingatio Sehemu ya Pili

142.

Azadari-Kuhuzunika na Kuomboleza

143.

Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah

144.

Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu

145.

Kuonekana kwa Allah

146.

Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza)

147.

Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili)

148.

Ndugu na Jirani

149.

Ushia ndani ya Usunni

150.

Maswali na Majibu

151.

Mafunzo ya hukmu za ibada

152.

Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisusunni No1

153

Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisusunni No 2

154.

Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisusunni No 3

155.

Abu Huraira

156.

Kati ya Alama kuu za dini ni Swala ya Jamaa na Adabu za Msikiti na Taratibu zake

102


Elimu ya Ghaibu.qxd

7/1/2011

12:37 PM

Page 103

Elimu ya Ghaibu ya Maimamu

BACK COVER Ghaibu (ghayb) maana yake - yasioonekana. Sharti moja la imani katika Uislamu ni kuamini yasiyoonekana ambayo kwa kweli ni mengi sana, lakini kwa kutaja machache ni kama vile, malaika, majini, Pepo, moto wa Jahannam, roho, n.k. Hivi vyote havionekani katika macho yetu lakini vipo na lazima tuamini hivyo. Qur’ani Tukufu inasema: “Hicho ni Kitabu kisicho na shaka ndani yake, ni mwongozo kwa wamchao (Mungu), ambao huyaamini yasiyoonekana...” (2: 2-3). Mwandishi wa kitabu hiki ameelezea kwa kina maana halisi ya ghaibu kwa kutumia vyanzo vitukufu - Qur’ani Tukufu, Sunna na hoja za kielimu. Kimetolewa na kuchapishwa na: Al -Itrah Foundation P. O. Box 19701, Dar-es-Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Fax: +255 22 2131036 Email:alitrah@raha.com Website: www.alitrah.org www.alitrah.info

103


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.