HEKAYA NA FIKRA
حكاية و فكرة
Kimeandikwa na: Mahdi Ja’far Sulail
Kimetarjumiwa na: Abdul-Karim Juma Nkusui
03_15_Hekaya na fikira_22_July_2015.indd 1
7/22/2015 12:30:23 PM
حكاية و فكرة
تأليف مهدي صليل
من اللغة العربية الى اللغة السوا حلية
7/22/2015 12:30:23 PM
03_15_Hekaya na fikira_22_July_2015.indd 2
HEKAYA NA FIKRA
Yaliyomo Mchapishaji...................................................................................... 1 Utangulizi......................................................................................... 2 Ufukweni.......................................................................................... 3 Safari ya angani................................................................................ 5 Katika bustani.................................................................................. 7 Ramadhani ni mwezi wa Qur’ani.................................................... 9 Marafiki watatu.............................................................................. 11 Katika meza ya chakula................................................................. 13 Mpira wa Nasri.............................................................................. 15 Nampenda baba yangu................................................................... 17 Samiru na mtende.......................................................................... 19 Samiru na mafakiri......................................................................... 21
iii
03_15_Hekaya na fikira_22_July_2015.indd 3
7/22/2015 12:30:23 PM
03_15_Hekaya na fikira_22_July_2015.indd 4
7/22/2015 12:30:23 PM
HEKAYA NA FIKRA
NENO LA MCHAPISHAJI
K
itabu hiki kiitwacho, Hekaya na Fikra ambacho kimeandikwa na Sheikh Mahdi Ja’far Sulail kimetarjumiwa kutoka lugha ya Kiarabu na anwani yake ni Hikayatun wa Fikratun. Kitabu hiki kimeandikwa kwa ajili ya watoto na hujifundisha mambo mbalimbali yanayohusu dini ya Kiislamu kwa kuelezea visa na hekaya zenye kuelimisha, kuchangamsha na kuimarisha misingi ya malezi bora. Sisi kama wachapishaji tunakiwasilisha kitabu hiki kama kilivyo kwa wasomaji wetu (hususan watoto wa Kiislamu) na kuwashauri wasome yaliyomo humo, wayafanyie kazi na kuyazingatia na kufaidika na hazina iliyomo ndani yake. Hivyo, ni matumaini yetu kwamba wasomaji (watoto) wetu watanufaika vya kutosha kutokana na kitabu hiki, kwani tumekiona ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote za elimu, sayansi na tekinolojia. Tunamshukuru mwandishi wa kitabu hiki Sheikh Mahdi Ja’far Sulail kwa kazi kubwa aliyofanya kwa ajili ya Umma huu wa Waislamu, Allah ‘Azza wa Jallah amlipe kila la kheri na amuingize Peponi kwa salama na amani insha’Allah. Halikadhalika tunamshukuru Ndugu yetu Abdul-Karim Juma Nkusui kwa kukitarjumi kwa Kiswahili kitabu hiki, insha’Allah na yeye Allah ‘Azza wa Jallah amlipe kila kheri hapa duniani na Akhera pia. Aidha hatuwasahau wale wote waliochangia kwa namna mmoja au nyingine mpaka kufanikisha kuchapishwa kwake. Allah Mwenye kujazi awalipe wote malipo mema hapa duniani na Akhera pia. Mchapishaji
1
03_15_Hekaya na fikira_22_July_2015.indd 1
7/22/2015 12:30:23 PM
HEKAYA NA FIKRA
UTANGULIZI
M
kusanyiko wa visa hivi kwa ajili ya watoto, unalenga kuimarisha misingi ya malezi na tabia njema katika nafsi za wanaokua, kwa namna nyepesi yenye kuambatana na michoro ambayo inazatitifikira na kuziimarisha, ambapo watoto watafanya kazi ya kuikoleza rangi michoro hiyo katika vibao katika hali ya furaha, kucheza na kuchangamka kutokana na fikira zake. Na taraji kwamba watoto wapendwa watafaidika na kupata maisha mazuri na yenye furaha. Mahdi Ja’far Sulail Rajabu 1435 Hijiria.
2
03_15_Hekaya na fikira_22_July_2015.indd 2
7/22/2015 12:30:23 PM
HEKAYA NA FIKRA
UFUKWENI
W
atoto walikuwa wanacheza katika mchanga ufukweni, Ahmad anajenga nyumba ya udongo, Hasan anamsaidia, Sadiq anachimba shimo na analijaza maji. Ama Zahra yeye amekaa kando ya mama yake anasoma kisa kizuri, na katika umbali wa mita chache baba alikuwa anachoma nyama kwa ajili ya wote. Mama akamwambia binti yake Zahra: “Unaonaje, utamsaidia baba yako au utacheza pamoja na kaka zako?” Zahra akajibu: “Nitamsaidia baba yangu.” Akaenda haraka kwa baba yake na kumwambia: “Nataka nikusaidie ewe baba yangu.” Baba akasema: “Nenda kacheze pamoja na kaka zako.” Zahara akarejea kwa mama yake ilihali amehuzunika. Mama akasema: “Unanini?” Akasema: “Baba hataki nimsaidie! Anasema: Nenda na ukacheze pamoja na ndugu zako.” Mama akatabasamu na akasema: “Baba yako anahofia usije kupatwa na cheche za moto, yeye anakupenda.” Zahra akadhihirisha alama za kuridhia na akaenda kucheza pamoja na ndugu zake. Je, unamsaidia baba yako na mama yako katika kazi za nyumbani? Je, unashirikiana na ndugu zako katika michezo yenye kuburudisha?
3
03_15_Hekaya na fikira_22_July_2015.indd 3
7/22/2015 12:30:23 PM
HEKAYA NA FIKRA
4
03_15_Hekaya na fikira_22_July_2015.indd 4
7/22/2015 12:30:23 PM
HEKAYA NA FIKRA
SAFARI YA ANGANI
K
asim anaangalia filamu za katuni katika runinga, mara anafungua daftari lake anaandika na anachora. Watu wote nyumbani wanamwangalia akiandika na kuchora, lakini wao hawajui anafanya nini! Sara akamuuliza mama yake: “Mama, kaka yangu anafanyanini? Yeye anaagalia filamu za katuni kisha anaandika na kuchora vitu na hatuonyeshi!” Mama akajibu: “Kaka yako anapenda kuchora tangu alipokuwa katika darasa la kwanza.” Wakati mmoja Kasim alisahau daftari lake sebuleni na akaenda kurejea masomo yake, Sara akachukua daftarina akakuta humo michoro lakini hakufahamu chochote. Akachukua daftari kwenda kwa baba yake na akamuuliza: “Kasim anafanya nini katika daftari hili?” Baba akasema: “Je, umeomba ruhusa kwa kaka yako kabla hujachukua daftari?” Sara akasema kwa mshangao: “Kwani yeye hapendi tuangalie!?” Baba akasema: “Ni wajibu wetu kutaka ruhusa ewe mwanangu kabla ya kuchukua vitu vya wengine.” Kisha baba akamwita Kasim na akamuuliza kuhusu siri ya michoro hiyo. Kasim akasema: “Mimi napanga safari ya kwenda angani na ninanufaika na filamu za katuni. Je utanisaidia ewe baba yangu?” Tunafaidika nini kwa kuangaliafilamu za katuni?
5
03_15_Hekaya na fikira_22_July_2015.indd 5
7/22/2015 12:30:23 PM
HEKAYA NA FIKRA
6
03_15_Hekaya na fikira_22_July_2015.indd 6
7/22/2015 12:30:23 PM
HEKAYA NA FIKRA
KATIKA BUSTANI YA WANYAMA
K
atika mshangao uliowafurahisha wanafunzi wa shule ya msingi, ni pale mwalimu Abbas alipowachukua wanafunzi wake kwenda kutembelea bustani ya wanyama, hivyo walipaza sauti zao kwa hamasa na vifijo, na walipofika kwenye bustani wakatembea kwa furaha na bashasha. Ahmadi akaulizia kuhusu tembo na mkonga wake mrefu, na Sadiq akataka kumkaribia twiga na kutazama urefu wa shingo yake kwa mshangao, na Husein akapanda juu ya mti ili aangalie wanyama wote. Lakini mguu wake ukaning’inia baina ya matawi na akawa hajui namna gani atajinasua na tatizo hilo. Akawa anawaita marafiki zake, lakini wao walikuwa wamekwenda katika sehemu ya ndege pamoja na mwalimu Abbas. Walipomaliza ziara yao na wakataka kupanda basi mwalimu akawa anawaita majina yao na akafika katika jina la Husein. Akawa anamwita Huseini, Husein uko wapi ewe Husein? Wanafunzi wakasikia sauti ya Husein juu ya mti, mimi niko huku, wote wakacheka na wakaenda kwake na wakamsaidia kuteremka kutoka kwenye mti. Nini maoni yako katika kitendo cha Husein?
7
03_15_Hekaya na fikira_22_July_2015.indd 7
7/22/2015 12:30:23 PM
HEKAYA NA FIKRA
8
03_15_Hekaya na fikira_22_July_2015.indd 8
7/22/2015 12:30:24 PM
HEKAYA NA FIKRA
RAMADHANI MWEZI WA QUR’ANI
Z
ainabu anafurahia mwezi mtukufu wa Ramadhani. Anakwenda kwenye nyumba ya babu yake na bibi yake, huko anakutana na wanafamilia wote. Kila usiku anakutana na kaka zake na dada zake, wanasoma Qur’ani tukufu na wanasimuliana hadithi nzuri na hekaya zenye kuliwaza. Zainabu alimwambia mama yake: “Naupenda mwezi wa Ramdhani ewe mama yangu, natamani mwaka mzima uwe ni Ramadhani.” Mama akasema: “Je, unataka kufunga mwaka mzima?” Zainabu akacheka na akasema: “Nataka kusikiliza hekaya nzuri za bibi yangu.” Bibi akasema: “Njoo ewe kipenzi changu Zainabu.” Akamkumbatia kwenye kifua chake huku akisema: “Sisi tuna furaha kubwa sana kwa ziara yenu. Baada ya mwezi mtukufu wa Ramadhani nitamwambia baba yako aje kwetu kila wiki ili tupate matumaini na hali zenu.” Zainabu akafurahi na akaenda haraka kwa ndugu zake na watoto wa ami yake akinadi: “Habari mpya, habari mpya. Baada ya mwezi mtukufu wa Ramadhani tutakutana hapa kila wiki inshaallah.” Wote wakafurahi kwa fikira hii na wakahamasika kwayo. Vipi unadhihirisha mapenzi yako kwa babu yako na bibi yako?
9
03_15_Hekaya na fikira_22_July_2015.indd 9
7/22/2015 12:30:24 PM
HEKAYA NA FIKRA
10
03_15_Hekaya na fikira_22_July_2015.indd 10
7/22/2015 12:30:24 PM
HEKAYA NA FIKRA
MARAFIKI WATATU
S
aidi anaangalia runinga.
Mama yake akamwambia: “Kipenzi changu Saidi, safisha meno yako na uende kwenye kitanda chako, sasa hivi ni saa tatu!” Saidi akasema: “Ninamsubiri baba yangu.” Mama akasema: “Huenda atachelewa.” Akasema: “Kwa nini atachelewa? Mimi nampenda baba yangu, sipendi kulala ila baada ya kumuona.” Mama akasema: “Amenipigia simu akasema kuwa Ana kazi pamoja na marafiki zake.” Saidi akasema ilihali akitabasamu: “Nitakuwa miongoni mwa marafiki wa baba yangu ili akae pamoja na mimi kwa muda mwingi zaidi.” Mama akasema: “Na mimi vilevile. Na hivi sasa ni wajibu wako uende kwenye kitanda chako, na atakapokuja baba yako nitamwambia fikira yako, tutakuwa marafiki wema ewe Saidi.” Saidi akasimama akabusu kichwa na mkono wa mama yake na akaenda kwenye kitanda chake huku akisema: “Nitawaota marafiki watatu katika usingizi wangu.” Je, unasuhubiana na baba yako na unacheza pamoja naye?
11
03_15_Hekaya na fikira_22_July_2015.indd 11
7/22/2015 12:30:24 PM
HEKAYA NA FIKRA
12
03_15_Hekaya na fikira_22_July_2015.indd 12
7/22/2015 12:30:24 PM
HEKAYA NA FIKRA
KATIKA MEZA YA CHAKULA
A
li na Hashim wanacheza. Sara anaangalia runinga. Mama anaandaa chakula cha usiku, Baba amekaa mezani anasubiria watoto wake. Baada ya mama kumaliza kuandaa meza, baba akawa anawaita watoto, lakini wao wakachelewa kuja. Sara akahisi kukasirika kwa mzazi wake naye akiita kwa sauti ya juu. Akaenda haraka lakini akasahau kuosha mikono yake. Ama Ali na Hashim wakamwambia mama yao: “Sisi hatutaki kula chakula cha usiku, tutaendelea kuangalia sehemu ya mwisho ya mchezo.�
Kosa liko wapi katika kisa hiki?
13
03_15_Hekaya na fikira_22_July_2015.indd 13
7/22/2015 12:30:24 PM
HEKAYA NA FIKRA
14
03_15_Hekaya na fikira_22_July_2015.indd 14
7/22/2015 12:30:24 PM
HEKAYA NA FIKRA
MPIRA WA NASRI
N
asri aliingia nyumbani naye analia kwa sauti ya juu, na nguo zake zimechafuka! Mama yake akamsikia, akafanya haraka kwenda kwake: “Una nini ewe kipenzi changu?” Akasema: “Mtoto wa jirani (Jasim) amenipiga na amechukua mpira wangu na amekimbia kwenda kwenye nyumba yao!” Mama akasema: “Nenda ukaoshe uso wako na ubadilishe nguo, nitamwambia baba yako suala hili.” Baba alipokuja akamweleza kisa. Baba akasema: “usijali, ewe mwangu nitamwendea sasahivi na nitampigana kukurudishia mpira wako.” Nasri akafurahi kwa maneno ya baba yake. Ama mama akasema: “Ni bora ukazungumze na baba yake na kumweleza yaliyotokea na usikilize kutoka kwa mtoto wakeJasim kisa kamili.” Nasri akasema: “Hapana mama. Acha baba ampige na kunirudishia mpira wangu.” Mama akasema: “Wewe na Jasim ni marafiki tangu miaka minne, ni bora msuluhishane.” Baba akaenda kwenye nyumba ya jirani yake akapokelewa na mzazi wa Jasim kwa moyo mzuri na akampa kikombe cha kahawa na akasikiliza maneno yake kwa makini, kisha akamwita mtoto wake Jasim na akamuuliza juu ya kisa chake na Nasri. Jasim akawa anasimulia kisa chake: “Nikiwa nacheza pamoja na rafiki yangu Nasri huwa anagombana na mimi na kunipiga na mimi namsamehe kila mara, lakini leo amenipiga sana, hivyo nilichukua mpira wake ili ami yangu baba Nasri aje na nimweleze kisa.” Ni kwa namna gani inapasa rafiki kuamiliana na rafiki yake ?
15
03_15_Hekaya na fikira_22_July_2015.indd 15
7/22/2015 12:30:24 PM
HEKAYA NA FIKRA
16
03_15_Hekaya na fikira_22_July_2015.indd 16
7/22/2015 12:30:24 PM
HEKAYA NA FIKRA
NAMPENDA BABA YANGU
H
asan aliangalia picha ya mzazi wake iliyotundikwa sebuleni na kutafakari vizuri. Akaelekea kwa mama yake na akamwambia kwa sauti ya huzuni: “Mimi nampenda baba yangu ewe mama yangu.” Mama: “Sote tunampenda, alikuwa ni mpole anapenda kheri kwa watu wote, msomee Qur’ani na umuombee maghfira ewe kipenzi changu.” Hasan: “Nataka niwe mwanaume kama baba yangu, ili afurahie naye akiwa peponi.” Mama: “Sawa ewe mwanangu, utakua na utakuwa mtu mwema unayewasaidia wenye haja na kuwahurumia mafakiri kama alivyokuwa baba yako.” Hasan: “Nitakwenda kwenye biashara ya ami yangu ili nifanye kazi pamoja naye na ili nijitegemee.” Mama: “Na vipi utarejea masomo yako na kufanya wajibu wako?” Hasan: “Baada ya kurudi shuleni, nitamaliza kazi zangu zote kabla sijakwenda pamoja na ami yangu.” Mama: “Hili ni jambo zuri, nitamwambia ami yako juu ya kupenda kwako kazi na atafurahia inshaallah.” Ami yake alipojua hilo akamkaribisha na akawa anamwita mfanyabiashara mdogo. Je, unapenda kuwasaidia watu kama Hasan mfanyabiashara?
17
03_15_Hekaya na fikira_22_July_2015.indd 17
7/22/2015 12:30:24 PM
HEKAYA NA FIKRA
18
03_15_Hekaya na fikira_22_July_2015.indd 18
7/22/2015 12:30:24 PM
HEKAYA NA FIKRA
SAMIRU NA MTENDE
S
amiru anakwenda pamoja na mzazi wake kwenye swala ya jamaa kila siku, na imamu wa jamaa anapotoa khutba yake na mawaidha, Samiru anatoa karatasi na kalamu na kuandika busara na mawaidha. Siku moja alisikia khatibu anasema: “Mkirimuni shangazi yenu mtende.” Samiru akaandika ibara katika karatasi huku akistaajabu. Aliporejea nyumbani akamuuliza baba yake: “Vipi mtende utakuwa shangazi yetu?” Baba akasema: “Hii ni hadithi iliyopokewa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu Muhammad (saww), mtende ni mti wenye baraka unatupa tende, nacho ni chakula bora kwa mwili kama ambavyo baba na mababu wananufaika kutokana na majani yake na miti yake katika kujengea nyumba zao na kutengenezea zana zao.” Samiru akasema: “Nini rai yako ewe baba yangu, tupande mtende katika nyumba yetu na tule matunda yake, kwani tende mbichi na tende mbivuni bora zaidi kuliko haluwa na vilivyotengenezwa viwandani.” Baba akasema: “Nani atauangalia na kuumwagilia?” Samiru akasema: “Mimi ewe baba yangukwani imepokewa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) kwamba amesema: ‘Mkirimuni shangazi yenu mtende.’” Mtende ni mzuri na unafaida…….Taja faida za mtende.
19
03_15_Hekaya na fikira_22_July_2015.indd 19
7/22/2015 12:30:24 PM
HEKAYA NA FIKRA
20
03_15_Hekaya na fikira_22_July_2015.indd 20
7/22/2015 12:30:24 PM
HEKAYA NA FIKRA
SAMIRU NA MAFAKIRI
M
zazi wa Samiru alipanda miche ya mitende katika bustani ya nyumba, na Samiru akawa anaiangalia na kuimwagilia kila siku. Ilipokua na kutoa matunda akawa anachuma matunda yake na kuyaweka kwenye vikapu safi. Samiru akamwambia mzazi wake: “Nini maoni yako ewe baba yangu, tumpe babu yangu kikapu kimoja na jirani yetu kikapu kimoja na sisi tuchukue kikapu kimoja?” Baba akasema: “Hili ni jambo zuri, vipi imekujia fikira hii?” Samiru akasema: “Nitakusimulia kisa. Siku moja sisi tulikuwa katika uwanjawa shule nilimuona mwanafunzi mdogo analia, nikamwambia: Kwa nini unalia? Je, amekupiga yeyote? Akasema: ‘Hapana, lakini mimi nina njaa na sina fedha.’ Nikamwambia: Kwa nini huchukui matumizi yako kwa baba yako? Akasema: ‘Baba yangu ameshafariki, na mama yangu hana fedha.’ Nikawa nampa masurufu yangu kila siku. Na nikamwambia: Unaonaje kama tutapanda miti katika nyumba yenu ili uuze matunda yake na kupata faida kubwa? Mtoto akafurahia fikira hiyo na mimi nikafurahi kwa sababu nawasaidia mafakiri na wenye haja ili Mwenyezi Mungu anipende na aniingize peponi.” Nini faida za kuwasaidia mafakiri na wenye shida?
21
03_15_Hekaya na fikira_22_July_2015.indd 21
7/22/2015 12:30:24 PM
HEKAYA NA FIKRA
22
03_15_Hekaya na fikira_22_July_2015.indd 22
7/22/2015 12:30:25 PM