Hekima za kina za swala

Page 1

HEKIMA ZA KINA ZA SWALA (Profundities of the Prayer)

Hotuba za: Ayatullah Sayyid Ali Khamenei

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 1

8/12/2015 6:35:10 PM


‫ترجمة‬

‫من أعماق الصالة‬

‫تأ ليف‬ ‫أية هللا السيد علي الخامنئي‬

‫من اللغة اإلنجليزية الى اللغة السواحلية‬

‫‪8/12/2015 6:35:10 PM‬‬

‫‪06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 2‬‬


©Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 –17 – 028 – 9 Hotuba za: Ayatullah Sayyid Ali Khamenei Kimetarjumiwa na: al-Haj Ramadhani S. K. Shemahimbo Kimehaririwa na: Alhaji Hemedi Lubumba Kimepitiwa na: Mubarak A. Tila Kimepangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation Toleo la kwanza: Agosti, 2015 Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. - 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: www.alitrah.info

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 3

8/12/2015 6:35:10 PM


‫َّح ِيم‬ ِ ‫بِس ِْم للاهَّ ِ الرَّحْ ٰ َم ِن الر‬ Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehma Mwenye kurehemu

Kitabu hiki ni mukhtasari wa maelezo ya baadhi ya hotuba fupi zilizotolewa baada ya swala za jamaa za jioni katika Msikiti wa Karamat – Mashhad - na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislam, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei mwaka 1972. Kitabu cha Kifursi “Az-Zharfai-Namaz,” ambacho ndio msingi wa tafsiri yetu, kilichapishwa na Daftar-e-Nashr Farhang-e-Islami, Tehran.

‫َّح ِيم‬ ِ ‫بِس ِْم للاهَّ ِ الرَّحْ ٰ َم ِن الر‬ “Na wale wanaoshikamana na Kitabu na wakasimamisha Swala, hakika Sisi hatupotezi ujira wa watendao mema.” (7:170).

Mtukufu Mtume amesema: “Kupiga hodi kwenye lango la majaaliwa, pamoja nadhati nzima ya ndani kunawezekana tu kupitia Rukuu na Sujuud. Yeyote anayefanikiwa kugonga kwenye lango hili tukufu atapokea utajiri wote na ustawi papo kwa papo. Mawlavi

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 4

8/12/2015 6:35:11 PM


Yaliyomo Dibaji ......................................................................................... vi Neno la Mchapishaji........................................................................ 1 Utangulizi......................................................................................... 3 Wasifu wa Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, kiongozi wa ............ 10 Mapinduzi ya Kiislam ya Iran........................................................ 10 Mlango wa Kwanza....................................................................... 14 Falsafa ya Swala katika Uislam..................................................... 14 Mlango wa Pili............................................................................... 25 Sura ya al-Hamd (Fatiha)............................................................... 25 Mlango wa Tatu............................................................................. 42 Sura Al-Ikhlaas............................................................................... 42 Mlango wa Nne.............................................................................. 49 Tasbihatul-Arbaa (Sifa tukufu nne)............................................... 49 Mlango wa Tano............................................................................. 58 Rukuu – Kuvunja goti ................................................................... 58 Mlango wa Sita.............................................................................. 60 Kusujudu........................................................................................ 60 Mlango wa Saba............................................................................. 63 Tashahudi....................................................................................... 63 Mlango wa Nane Salaam............................................................... 70

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 5

8/12/2015 6:35:11 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

DIBAJI

K

itabu hiki ni toleo la Kiswahili la taasisi ya Al Itrah Foundation. Chapisho lake limelenga kukidhi mahitaji ya kiroho ya zama hizi pamoja na Ubongo na fikra zinazokuwa za Muislam. Jitihada kubwa zimefanywa na Taasisi kuweka chapisho hili la Kiswahili ­katika msingi wa haki na wenye kukubalika katika Uislam. Unaombwa kwa Taadhima ukisome kitabu hiki katika malengo yaliyokusudiwa. Pia Unaombwa kuwasilisha kwetu maoni yako ­huru. Juu ya chapisho letu hili, jambo ambalo tutashukuru sana. ­Kutangaza ujumbe wa Uislam ni kazi ambayo inahitaji ushirikiano wetu sote. Taasisi inakuomba kuungana na kushirikiana kama ­ilivyoagizwa katika aya ya Qur’an: (Surat Saba’ 34:46). Na rehma za Allah ziwe juu yako. Wako katika Uislam Al Itrah Foundation Barua Pepe: alitrah@yahoo.com SMS: +255 778 300 140

vi

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 6

8/12/2015 6:35:11 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬ NENO LA MCHAPISHAJI

K

itabu ulichonacho mikononi mwako ni cha mafunzo juu ya swala, hekima na falsafa yake. Kitabu hiki kilichotarjumiwa kutoka lugha ya Kiingereza kwa jina la Profundities of the Prayer, ni mkusanyiko wa khutba za Ayatullah Sayyid Ali Khamenei – Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. Swala ni nguzo muhimu sana ya dini; na inasemekana kwamba Siku ya Hesabu kitu cha kwanza kuangaliwa ni swala. Kama swala itatakabaliwa na Mwenyezi Mungu, basi huchukuliwa kwamba matendo yote hutakabaliwa pia. Matokeo yake, mtu huyo hupitishwa moja kwa moja kwenye Sirati na kuingizwa Peponi. Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Swala ni nguzo ya dini, mwenye kusimamisha swala amesimamisha dini, na mwenye kuicha swala hakika ameiangusha dini.” Mtume (s.a.w.w.) akaendelea kusema: “Tofauti baina yetu na ukafiri ni kuacha (taariku) swala.” Yaani kinachotutofautisha sisi Waislamu na ukafiri ni kuacha swala. Swala ndiyo inayotutofautisha na ukafiri kwa sababu kafiri yeye huwa haswali. Hadithi nyingine kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) inasema kwamba: “Kila kitu kina uso, na uso wa dini (ya Uislamu) ni swala.” Kitu cha kwanza kuonekana katika kila kitu ni uso wake, kama uso ni safi huchukuliwa kwamba kitu chote ni safi, kama uso ni mchafu huchukuliwa kwamba kitu chote hicho ni kichafu. Kwa hivyo, hadithi inatuhimiza kuswali ili kuuweka uso wa dini katika hali ya usafi na dini yetu kwa ujumla iwe safi.

1

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 1

8/12/2015 6:35:11 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

Tumekiona kitabu hiki ni kizuri sana na chenye manufaa makubwa kwa Waislamu wote kwa ujumla. Sisi kama wachapishaji ­tunakiwasilisha kitabu hiki kama kilivyo kwa wasomaji wetu na ­kuwashauri wasome yaliyomo humo, wayafanyie kazi na kuyazingatia na kufaidika na hazina iliyoko ndani yake. Ni matumaini yetu kwamba wasomaji wetu watanufaika vya kutosha kutokana na kitabu hiki, kwani tumekiona ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote za elimu. Shukurani zetu za pekee zimuendee Ayatullah Sayyid Ali Khamenei kwa kazi kubwa anayofanya kwa ajili ya Umma huu wa Waislamu, Allah ‘Azza wa Jallah amlipe kila la kheri na amuingize Peponi kwa salama na amani insha’Allah. Halikadhalika tunamshukuru ndugu yetu al-Haj Ramadhani S. K. Shemahimbo kwa kukitarjumi kwa Kiswahili kitabu hiki, insha’Allah awalipe wote kila la kheri hapa duniani na Akhera pia, bila kuwasahau na wale wote waliochangia kwa namna mmoja au nyingine mpaka kufanikisha kuchapishwa kwake. Allah Mwenye kujazi awalipe wote malipo mema hapa duniani na Akhera pia. Amin. Mchapishaji Al-Itrah Foundation

2

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 2

8/12/2015 6:35:11 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬ UTANGULIZI

T

unashuhudia kipindi chenye ghasia kubwa kabisa cha huu unaoitwa ustaarabu wa kisasa, ambamo mfumo wa dunia unabadilika kwa haraka sana. Mpaka hivi karibuni tulikuwa na Taifa kubwa la Mashariki, U.S.S.R. (Jamhuri ya Kisoshalisti ya Kisovieti ya Urusi) Kubwa yenye nguvu ambayo ilitangaza ukomunisti kama itikadi ya kimapinduzi yenye nguvu hai. Ghafla ikatoweka kwenye mandhari ya dunia, bila hata ya risasi moja ama kombora lililorushwa kutoka nje. Kuanguka kwake kunafanana na kufa maji kwa Firauni. Qur’ani inasimulia kisa cha kuanguka kwa Firauni, ambaye kwa ajili yake hakuna hata kiumbe kimoja ulimwenguni kilichomlilia machozi. Kadhalika hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa taifa kubwa la mashariki, ambalo lilikandamiza na kuuwa mamilioni ya watu wasio na hatia katika kipindi cha utawala wake wa vitisho, na vita vyake visivyofanikiwa dhidi ya uwepo wa Mwenyezi Mungu Muumba, na dhidi ya dini za kimbinguni. Kama kwa Mkandamizaji wa Mashariki na itikadi yake ya kikomunisti, Ufidhuli wa Magharibi na itikadi yake ya ubaguzi wa rangi na ubepari vilevile umeshindwa kuleta hiyo pepo iliyoahidiwa kwa binadamu, na badala yake umewafikisha binadamu mahali ambapo hawawezi kugeuka na kuangalia nyuma tena. Bila ya shaka yoyote ile, mifumo na itikadi zilizotengenezwa na binadamu haina uwezo wa kuuongoza msafara huu wa binadamu uliopotea. Ni Mwenyezi Mungu tu na Mfumo Wake Mtukufu ambao wanaweza kuuokoa 3

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 3

8/12/2015 6:35:11 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

msafara huu uliopotea na kuuongoza kuelekea kwenye njia iliyonyooka ya ukamilifu wote na furaha. Kwa karne nyingi sasa, Uislamu umekuwa mgeni hata kwa Waislam wenyewe kwa sababu ya propaganda ya kinyume ya majeshi ya kibeberu yanayotafuna ulimwengu kwa ulafi. Rasilimali kubwa za kifedha na kiuchumi za ulimwengu wa Kiislamu ziliporwa na wakoloni. Nchi za Kiislamu zilihujumiwa kiuchumi na kiutamaduni kwa uingiliaji wa moja kwa moja kwenye mambo ya ndani ya nchi zao. Kwa bahati nzuri, kwa ule ushindi wa Mapinduzi ya Kiislam mnamo Februari, 11 mwaka 1979, chini ya uongozi wa kielimu wa Mwanahekima bora wa zama hizi, ambaye jina lake na ambaye neno lake linakonga nyoyo za Waislam, Imam Ruhollah al-Musavi alKhomeini , kazi ya kuunda dola ya Kiislam ilikamilika. Alimuradi Iran ya Kiislam inabakia kuwa “Ummul-Qura” au kitovu cha Uislam, na bendera yake ya utukufu wa Mwenyezi Mungu ikiwa inapepea juu kabisa hewani, Ummah wa Kiislam wenye zaidi ya watu bilioni moja utabakia umezindukana, na damu mpya itakuwa inaingizwa kwenye mishipa yake na mirija yake. Leo, watu wanadai utekelezwaji wa sharia ya Kiislamu huko Bosnia Herzegovina, Algeria, Kashmiir, Uturuki, Misri, Sudani, Palestina, Chechnia, Tajikistan na kote ulimwenguni. Huku kuenea kwa ‘Uislamu wa Siasa kali,’ kama magharibi yenye hofu inavyopenda kuuita, kumeutokomeza mbali ule usingizi wa wavamizi wa Palestina na kugeuza ndoto zao kuwa majinamizi. Kwa hiyo vita vinaendelea dhidi ya itikadi ya Kiislamu. Wakati mwingine kubomoa nchi nzima kama Bosnia, ambako utaratibu wa mauaji makubwa umekuwa unaendelea kwa miaka mitatu iliyopita. Na wakati mwingine huchukua muundo wa ubomoaji uliopangwa wa Msikiti wa Babri huko Uttar Pradesh, jimbo lililoko India (Desemba 6, 1992), au hivi karibuni kabisa, mauaji ya kinyama ya mamia ya Waislam wasio na hatia waliokuwa wana 4

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 4

8/12/2015 6:35:11 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

saumu wakiwa kwenye hali ya kusujudu kwenye wakati wa Swala ya Ijumaa katika mwezi wa Ramadhani katika uwanja wa makaburi ya Nabii wa Mwenyezi Mungu, Ibrahim  katika mji wa al-Khalil. Kwa nini adui anahofia sana Msikiti na Swala? Kwa nini anajiingiza kwenye jinai kama hizo kwenye sehemu tukufu za ibada? Jibu liko wazi dhahiri. Nguvu za giza zinauhofia tu ung’araji wa Uislamu na athari za uelimishaji wake juu ya binadamu. Swala au ile ibada ya mara tano kwa siku ndio udhihirisho wa kina kabisa wa undugu wa Uislam wa ulimwengu mzima. Kwa vile kuna haja ya kuutambulisha umuhimu wa hekima na natija za nguzo hii ya dini kwa sehemu za ummah zinazozungumza Kiingereza, nimefanya tafsiri ya kitabu cha sasa (“Profundity of the Prayers) cha Ayatullah Khamenei kutoka kwenye lugha ya ki-Farsi kwenda kwenye Kiingereza,1 kama mchango wangu kwa ajili ya uelewa wa wajibu huu muhimu wa Kiislamu. Swala katika Uislamu inaweza kugawanywa katika miundo minne ya msingi. Swala, du’a, nyiradi na dhikri. Mtu anaweza akasema huo wa kwanza katika muundo wake wa wajibu unaweza kidogo kulinganishwa na kile kinachomaanishwa katika Ukristo kama misa au komuniyo, ingawa aina hii ya swala katika Uislamu ni ya kipekee na haiwezi kulinganishwa na kitu kingine chochote kile. Hii ya pili, du’a ni sawasawa na maombi binafsi au kwa kawaida, ni maombi kama kwa jumla Wakristo wanavyotumia neno hilo. Swala ya wajibu lazima iswaliwe na mtu binafsi au kwa jamaa, mara tano kwa siku na kwa mujibu wa kanuni zilizofafanuliwa kwa umadhubuti hasa. Swala za sunna (nawafil) nazo pia zinafuata mkondo huo huo wa swala za wajibu. Lakini kwa upande mwingine, mtu anaweza kumuomba Mwenyezi Mungu wakati wowote na 1

Chapa ambayo sisi al-Itrah Foundation ndio tuliyoitafsiri kwa Kiswahili na kukufikishia mikononi mwako msomaji wetu wa Kiswahili. 5

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 5

8/12/2015 6:35:11 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

katika mazingira yoyote yale, bila ya utaratibu au kanuni yoyote ile. Du’a ni za hiari na zisizo rasmi. Nyiradi na dhikri, yaani usomaji wa aya za Qur’ani au jina moja au zaidi kati ya majina ya Mwenyezi Mungu kama du’a ni za uchaguzi wa hiari. Kitabu hiki cha sasa kinashughulika na Swala na kinafafanua vina vyake vya ndani kabisa katika utaratibu maalum. Mbali na muundo wake wa nje wa kiibada, swala ina miujiza ya ndani yenye mipaka isiyo na ukomo. Ni kama maji ya bahari yasiyofikika chini ambayo mtu anaweza kuyatumia tu kwa mujibu wa haja zake au uwezo wake. Katika Siku ya Kiyama wakaazi wa Motoni wataulizwa: “Ni kipi kilichowapeleka Motoni? Watasema: ‘Hatukuwa miongoni mwa waliokuwa wakiswali.’” (74:42-43) Jambo la muhimu sana katika swala ni uaminifu, nia safi na kuhudhurisha moyo kwani mtu yupo rasmi mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Qur’ani tukufu inasema: “Basi ole wao wanaoswali, ambao wanasahau swala zao.” (107:4-5). Kwa hiyo, wakati wa utekelezaji wa swala za kila siku, kuyadhibiti mawazo na kupata mahudhurio ya moyo na akili kwa ajili ya Mwenyezi Mungu tu, badala ya kushughulishwa na mambo ya kidunia ni jambo muhimu sana. Ili swala yako iweze kuwa na maana na kukubaliwa na Mwenyezi Mungu, ni muhimu sana kwamba milango yote ya kutokea kwenda kwenye mambo yote ya nje iwe imefungwa barabara kabisa wakati wa swala. Bila shaka kuipata hali ya utulivu wa akili na moyo iliyotajwa hapo juu kunahitajia subira kwa wingi na jitihada kubwa. Kama mtu amezama katika mapenzi na tamaa ya dunia hii, kwa kawaida moyo wake utakuwa umezongwa katika mambo ya kawaida kabisa, ya kidunia. Mpaka hapo unakua mti huu wa shauku na tamaa za kidunia ndani yake na moyo wake utakuwa na tabia kama ya ndege ukiruka kutoka tawi hadi tawi ndani ya swala. Ikiwa kwa mapambano, mazoezi, juhudi na kufikiri kuhusu matokeo ma6

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 6

8/12/2015 6:35:11 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

baya na hasara, mtu anaweza akafanikiwa kuukata mti huu wa hawaa au tamaa ya dunia, na kisha moyo utakuwa umepata utulivu na amani. Moyo huo utapata hatua ya ukamilifu wa kiroho. Angalau kila anavyojitahidi mtu kujinasua mwenyewe kutoka kwenye vishawishi vya kidunia, ndio anavyozidi kufanikiwa katika kukata baadhi ya matawi ya mti ule, na uhudhurishaji zaidi wa nafsi utapatikana kwa kuwiana. Kwa kiasi mapenzi ya dunia hii yanavyohusika, kuna watu ambao hawana kitu chochote kabisa lakini bado wanaweza kuwa ni watu ambao wamezama jumlajumla kabisa kwenye mapenzi ya dunia hii. Ambapo kwa upande mwingine mtu anaweza akawa kama Nabii Suleiman, mfalme wa wafalme na anayemiliki hazina zote za ulimwengu huu, lakini wakati huohuo anaweza asiwe ni mtu wa dunia hii, aliyejitenga kabisa kutoka kwenye vishawishi na tamaa za uhai wa dunia hii. Inasimuliwa kutoka vyanzo mbalimbali vya kuaminika kwamba kama mtu ataweza kuswali swala ya rakaa mbili tu katika muda wa uhai wake wote kwa utii mkamilifu, uaminifu na kuhudhurisha akili, Mwenyezi Mungu ataikubali swala hiyo na atamkirimu na pepo. Kuhusu sajida, inasimuliwa kwamba katika uhai wake wote mtu, kama atafanikiwa wakati wa sajida moja tu kupata fungamano halisi na Muumba, hiyo itakuwa fidia kwa ajili ya mapungufu yote ya siku za nyuma. Atapokea baraka za kimbinguni na atakuwa amekingwa na vishawishi vya kishetani daima. Kinyume chake, kama wakati wa sajida, ambayo ni hali ya unyenyekevu, kama moyo wake utakuwa unashughulishwa na jambo jingine mbali na Yeye swt. huyo ataorodheshwa miongoni mwa kundi la wanafiki na waliopotoka. Mtu lazima ajikinge kwa Mwenyezi Mungu kutokana na hila za Shetani na nafsi yake mwenyewe, wakati atakapokuwa mbele ya Mwenyezi Mungu mnamo siku ya Kiyama. 7

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 7

8/12/2015 6:35:11 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

Ili kusisitizia umuhimu wa swala katika kumuunganisha kiumbe wa kidunia dhaifu asiyejiweza, masikini asiye na thamani, kuwa pamoja na Chanzo Kikuu cha Mamlaka, tunaweza kunukuu hapa riwaya mbili sahihi zifuatazo: Mwenyezi Mungu anasema: “Ewe mja wangu! Nitii Mimi, mpaka nikujaalie uwe kama mfano Wangu.” – Mysteries of Prayers cha Maliki Tabrizi uk. 4. Na hadithi ifuatayo inasimulia hivi:

ُ‫ب إِلَ َّي بِالنَّ َوافِ ِل َحتَّى أُ ِحبَّه‬ ُ ‫َما يَ َزا ُل َع ْب ِدي يَتَقَ َّر‬ ْ َ‫س ْم َعهُ الَّ ِذي ي‬ ُ‫ص َره‬ َ َ‫س َم ُع بِ ِه َوب‬ َ ُ‫فَإِ َذا أَ ْحبَ ْبتُهُ ُك ْنت‬ ‫ش بِ َها‬ ُ ‫ص ُر بِ ِه َويَ َدهُ الَّتِي يَ ْب ِط‬ ِ ‫الَّ ِذي يُ ْب‬ “Kwa kuswali swala za Sunnah, mja wangu anakuwa karibu sana na Mimi kiasi kwamba ninaanza kumpenda. Wakati hili linapotokea, Mimi ninakuwa masikio yake anayosikilizia kwayo, ninakuwa macho yake ambayo kwayo anaonea, na ninakuwa mikono yake anayofanyia kazi zake…...”

– Mysteries of Prayers cha Maliki Tabrizi uk. 5. Jinsi mtu anavyozidi kufanikiwa katika kupata ukamilifu kwenye utii kwa Mwenyezi Mungu ndio yatakavyozidi matendo na amali kuanza kuakisi sifa takatifu za hali ya juu kabisa, na bila shaka hizi hatua za ukamilifu na utakatifu huwa zinapatikana kwa kuwa mwamimifu katika swala ambayo imeitwa: Swala ndio safari takatifu ya muumini.

8

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 8

8/12/2015 6:35:11 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

Mwishoni tafsiri hii inasadifiana na taarifa za kuhuzunisha za mauwaji ya mamia ya Waislamu wasio na hatia waliofunga wakati wa kitendo hasa cha swala ndani ya uwanja wa makaburi wa Nabii Ibrahim katika mji wa al-Khalil kutoka kwa Wazayuni wakatili. Kwa hiyo, inafaa kutabaruku tafsiri hii kwa ajili ya roho tukufu za wahanga, wafiadini wa al-Khalil. Napenda niwashukuru wale wote ambao wamechangia katika kufanikisha tafsiri hii, hususan Ayatullah Amini, mwanachuoni msomi na faqihi maarufu kutoka kwenye Kituo cha Masomo ya Kidini cha Qum, Dkt. Ali Naqi Baqir Shahi na Bw. Ansariyan kwa msaada na uhimizaji wao mkubwa. Kwa kweli ninapaswa kumshukuru sana Bw. Asghar Hashembeiki kwa kuhariri na kuhakiki maandishi haya; Hujjatul Islam Sayyid Muhammad Taqi Hakim kwa ajili ya kuhakiki maandishi ya Kiarabu, na Bibi Irafan Parviz kwa kuchukua usumbufu wote wa kuyapanga kwenye Kompyuta maandishi haya. Maelezo yaliyoongezwa na mfasiri yameashiriwa kwa alama (tr). Kwa makosa yoyote ya kamisheni, mimi ninachukua dhima. Sayyid Hussein Alamdar Tehran Ramadhan 1414 / Machi, 1994

9

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 9

8/12/2015 6:35:11 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬ WASIFU WA AYATULLAH SAYYID ALI KHAMENEI Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Irani

A

lizaliwa mwaka 1939 katika mji mtukufu wa Mashhad jimboni Khorasani, Kaskazini mashariki mwa Iran. Wazazi wake wote walitokana na familia za kiwanachuoni wa kidini naye alipitisha miaka ya ujana wake katika mazingira ya kiroho. Alihitimu masomo yake ya theolojia kwa mafanikio kabisa katika kile Kituo cha Masomo ya Kidini maarufu cha Qum mwaka 1964 na hatimaye alifuatilia masomo ya kidini katika Chuo cha Theolojia hapo Mashhad hadi mwaka 1968.

Wakati wa utawala wa Pahlavi aliyeondoshwa, Bw. Khamenei alikuwa mmoja wa wanafunzi wanaopendwa sana na wenye kung’ara sana wa Imam Khomeini , na alichukuliwa kuwa mmoja wa viongozi mashuhuri na waaminifu sana wa harakati za Kiislamu, ambazo ziliingia kwenye awamu mpya muhimu sana mnamo tareha 5 Juni, 1963 (15 Khordad 1342 S.H.), baada ya kusimama kihistoria kwa Imam Khomeini dhidi ya utawala wa Shah. Wakati wa mapambano hayo yeye alikamatwa mara kwa mara na kuwekwa kizuizini na akakaa gerezani kwa muda wa miaka mitatu kati ya 1964 na 1978. Baadye alifukuzwa nchini kwa muda wa 10

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 10

8/12/2015 6:35:11 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

takriban mwaka mmoja kwenda mahali ambapo pana hali ya hewa mbaya kupindukia. Katika mwaka wa 1978, wakati wa kurejea kwake kutoka uhamishoni na wakati wa kilele cha harakati za mapinduzi ya Waislam wa Iran, Bwana Khamenei pamoja na wachache kati ya washirika wake wa karibu waliongoza mapambano ya watu wa Khorasan. Baadaye katika mwaka huo huo wakati Imam Khomeini alipoongoza vuguvugu za mapinduzi ya Kiislam kutoka Neauphle Le Chateau huko Paris, yeye aliteuliwa kuwa mjumbe wa Baraza la Mapinduzi. Baada ya kuanguka kwa ufalme huo na kuundwa kwa serikali ya mapinduzi, yeye alikabidhiwa wajibu wa kuliwakilisha Baraza la Mapinduzi katika Jeshi. Yeye pia alihudumia kama Makamu wa Mambo ya Mapinduzi katika Wizara ya Ulinzi, na baadaye akateuliwa kama Kamanda wa Kundi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislam (IRGC). Alichaguliwa pia na Kiongozi wa Mapinduzi Imam Khomein kuongoza Swala za Ijumaa mjini Tehran, na aliteuliwa kwenye Bunge la Kwanza la Ushauri kama mwakilishi wa Tehran mnamo mwaka 1980. Baada ya kuundwa kwa Baraza Kuu la Ulinzi (Supreme Defence Council), Khamenei aliteuliwa kuwa mwakilishi wa Kiongozi wa Mapinduzi. Mheshimiwa Khamenei alikuwa mmoja wa waasisi wa chama cha Islamic Republic Party nchini Iran na akateuliwa kuwa Katibu Mkuu wa kwanza. Alikuwa mwathirika wa jaribio la mauwaji lisilofanikiwa mnamo tarehe 27 June, 1981. Hotuba yake kwenye Baraza la Ushauri ilisaidia sana katika kuwaondoa Bani Sadr katika uraisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na wakati alipokuwa akihutubia mkusanyiko baada ya kuongoza swala katika msikiti huko Tehran, bomu la kutegwa lililipuka karibu yake likamuumiza vibaya sana mkono wake, uso na kifua. Alikimbizwa hospitali mara moja na watu waliojitoa wa 11

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 11

8/12/2015 6:35:11 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

Tehran na akasalimika na kupona kimuujiza. Mkono wake wa kulia hata hivyo bado haujaweza kufanya kazi vizuri. Mnamo mwaka 1981, kufuatia kuuliwa shahidi kwa Muhammad Ali Rajaei, Rais wa pili wa Jamhuri ya Kiislamu ya Irani, yeye akawa mgombea na alichaguliwa kwenye uraisi kwa asilimia 95% ya kura zilizopigwa kwa ajili yake kutoka kwa watu wa Iran (Idadi kamili ya kura zilizopigwa ilikuwa ni 16,847,717). Alichaguliwa tena kama Rais mnamo 1985 kwa kipindi cha pili cha miaka minne tena. Vilevile aliliongoza Baraza Kuu la Kijeshi na Baraza la Mapinduzi ya Kiutamaduni. Wakati wa vile vita vya kulazimishwa, Rais Khamenei alitembelea kwenye maeneo mbalimbali ya vita na akiendelea kukagua mistari ya mbele ya mapambano ili kuwaongezea hamasa zaidi wapiganaji wa Kiislam na kutoa ushauri juu ya mambo ya kiutendaji. Baada ya kifo cha kuhuzunisha cha Imam Khomeini, Baba wa Mapinduzi ya Kiislam, Baraza la Wanataaluma lilimchagua yeye kama Kiongozi anayefuatia wa Mapinduzi ya Kiislamu mnamo tarehe 4 Juni, 1989. Ana ujuzi mzuri wa Kiajemi, Kiarabu na lugha za Azeri za Kituruki na pia anao ufahamu mzuri wa Kiingereza. Ayatullah Khamenei ni mwanachuoni na faqihi mashuhuri na anaweza kupewa daraja kama mmoja wa makhatibu fasaha kabisa katika ulimwengu wa Kiislam kwa wakati huu. Kwa nyongeza ya uandishi, anao utambuzi juu ya kazi za vitabu na mashairi. Ametafsiri na kutunga idadi kadhaa ya vitabu juu ya Uislamu na juu ya historia. Tafsiri zake ni pamoja na Future of the Islamic Lands, An Indictment Against the Western Civilazation, and Imam Hasan’s Peace Treaty. Kutoka miongoni mwa maandishi yake, mtu anaweza akataja: The Role of Muslims in the Independence Struggle 12

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 12

8/12/2015 6:35:11 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

of India, General Pattern of Islamic Thoughts in the Qur’an, Discourse on Patience, Understanding Islam Properly, Imam Sadiq’s Life, Profundities of Prayer, and a collection of lectures about Wilayat. Vilevile alikuwa mwandishi mshirika wa jarida maarufu la Our Positions ambalo lilisaidia maendeleo ya kisiasa, kijamii na ya kifalsafa ya Chama cha Jamhuri ya Kiislamu. (Wachangiaji wengine walikuwa ni Shahid Ayatullah Beheshti, Shahid Hujjatul Islam Dr. Bahonar, na Hujjatul Hashemi Rafsanji).

13

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 13

8/12/2015 6:35:11 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬ MLANGO WA KWANZA Falsafa ya Swala Katika Uislamu

S

wala na kutukuza ndio mawasiliano makuu ya karibu sana baina ya mwanadamu na Mwenyezi Mungu, kati ya kiumbe na Muumba. Swala inaleta utulivu na amani kwenye nyoyo zilizochoka, zenye wahaka na kusumbuka, na ndio nishati ya utakaso wa kina na nuru kwa ajili ya nafsi ya mwanadamu. Ni kifungo, uhamasishaji kwa ajili ya kitendo, na ukusanyaji, na ni tangazo kwa ajili ya utayari katika njia ya uaminifu zaidi, mbali kabisa na udanganyifu au uongo, kwa ajili ya kukanusha aina zote za uovu, utovu wa adabu na uimarishaji wa kila jema na zuri. Ni mpango kwa ajili ya kuigundua nafsi, na hatimaye kuijenga kiroho, au kwa kifupi, ni uhusiano endelevu wenye manufaa pamoja na chanzo cha wema wote yaani Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwa nini swala inachukuliwa kama wajibu muhimu sana na wa msingi mno? Kwa nini swala imeelezewa kama ndio msingi na kiini cha imani? Kwa nini bila ya swala hakuna chochote kitakachokubaliwa? Ili kupata majibu ya maswali haya, hebu tuchambue na kutathmini maeneo na vipengee mbalimbali vya swala. Kwa kuanzia, ingefaa kuweka mazingatio kwenye nia na malengo ya kuumbwa kwa mwanadamu, ambako kunachukuliwa kama moja ya mihimili mikuu ndani ya mtazamo wa kidunia wa Itikadi ya Kiislamu. Kama mwanadamu ni kiumbe kilichoumbwa, na kama tunaamini mkono wenye nguvu kuu na hekima, ndio umemleta kwenye uhai, 14

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 14

8/12/2015 6:35:11 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

basi ni kawaida kwa hiyo, kufikiri kwamba lazima kuwe na makusudio na malengo nyuma ya kuumbwa huku na kuwa hai. Makusudio haya yanaweza kuitwa kama upimaji, barabara inayoelekezea kwenye mwisho wa safari au Mwenyezi Mungu, kusafiri kwenye barabara hiyo kwa mujibu wa ramani halisi na nyenzo zilizoainishwa, ili hatimaye kufika kwenye mwisho wa safari uliokusudiwa. Katika hali hii ni muhimu kuainisha ile njia inayoelekea kwenye mwisho wa safari, tafuta njia, na wakati wote zingatia lengo ili kuweza kupata matokeo yanayotakiwa. Yule mtu ambaye anaianza safari hii lazima atembee moja kwa moja kuelekea mbele; apasike wakati wote kuendelea kuweka akilini kile kituo cha mwisho wa safari, asije akaondolewa na michepuko ya njiani, au kupoteza nadharia kwenye shughuli zisizo na maana; vilevile ili kuendelea, shikilia ile nafasi sahihi katika muelekeo ulioainishwa, na usipotoke kwenye maelekezo yaliyoagizwa na Kiongozi wake yaani, Mtukufu Mtume [s.a.w.w.]. Lengo hilo ni hatua kuelekea kwenye utukufu na ukamilifu wa mtu usio na kipimo. Ni marejeo kwa Mwenyezi Mungu na kwenye maadili mema. Ugunduzi wa nguvu za kimaumbile na uwezo ndani mwake mwenyewe, na kuvitumia katika njia iliyo sahihi, kwa ajili ya ustawi wake mwenyewe, na ule wa binadamu wenzie na wa ulimwengu mzima. Kwa hiyo ni lazima tuhusishe uwepo wa Mwenyezi Mungu, na ile njia ambayo ameiagiza Yeye kwa ajili ya hali ya utukufu wa wanadamu, na lazima tusonge mbele katika mwelekeo huo bila ya kusitasita na ulegevu. Kufanya shughuli ambazo zinampeleka mtu karibu na lengo, kujitenga na mambo ambayo yanaleta hasara na madhara, na kuweka maana kwenye maisha, hiyo ndiyo iwe falsafa ya maisha, vinginevyo maisha yanakuwa hayana maana bila ya maridhiko yoyote. Kwa maneno mengine, maisha ni darasa ama maabara ambamo tunapas15

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 15

8/12/2015 6:35:11 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

wa kushughulika kulingana na sharia na kanuni ambazo zimeagizwa kwetu na Mwenyezi Mungu Muumba wa dunia na uhai wote, ili kupata na kukamilisha matokeo mazuri yanayotakikana. Ni lazima tuzihusishe sharia hizo, hadithi tukufu na kanuni za kimaumbile, na tujenge maisha yetu kulingana nazo hizo. Kwa hiyo, mtu lazima kwanza aihusishe nafsi yake, na mahitaji ya nafsi hiyo, ambayo inachukuliwa kama moja ya majukumu na wajibu wa mwanadamu. Ni mara tu baada ya utekelezaji wa wajibu huu mkubwa ambapo kwamba binadamu atakuwa anaweza kusonga mbele kwa uangalifu zaidi na mafanikio, vinginevyo atachukuliwa kama aliyebweteka, mjinga na asiyefanikiwa. Dini sio inaamua tu juu ya malengo, mwelekeo, njia na nyenzo za safari hiyo, bali pia inatoa kwa binaadamu uwezo wa muhimu na mahitaji kwa ajili ya kuifanya safari hiyo iwe njia kuelekea kwenye ukamilifu, bila shaka, mahitaji muhimu zaidi ambayo yanabebwa na wasafiri katika njia hii si mengine bali ni “kumbukumbu juu ya Mwenyezi Mungu.” Mbawa zenye nguvu zaidi katika msafara huu ni kutafuta, matumaini na kujiamini ambayo ni matokeo ya kulekule “kumkumbuka Mwenyezi Mungu.” Kwa upande mmoja inatufanya wenye kutambua lengo la kujiambatanisha na Yeye, Ukamilifu Kamili, na wakati huohuo kuzuia mikengeuko, na kumweka msafiri katika tahadhari na muangalifu kuhusiana na hizo njia na mahitaji. Kwa upande mwingine inaleta ujasiri, furaha na kujiamini juu yake na kumlinda na vurugu na kukata tamaa, anapokabiliwa na mazingira magumu na yasiyofaa. Jamii ya Kiislamu, na kila kikundi au mtu mmoja, wanaweza kusonga mbele kwa uhakika katika njia hii iliyowekewa mpangilio na Uislamu na kutangazwa na Mitume wote, bila kuivunja safari 16

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 16

8/12/2015 6:35:11 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

au kurudia katikati ya njia, pale tu kama hawasahau kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo, ni kwa sababu ya mazingatio haya kwamba dini inajitahidi iwezekanavyo, kwa kushauri njia mbalimbali na maandalizi katika kuhuisha kumbukumbu juu ya Mwenyezi Mungu katika nyoyo za waumini katika nyakati zote. Kitendo kimoja kama hicho, ambacho kimekifu hamasa ya kumbukumbu ya Mwenyezi Mungu, na ambacho kinamuwezesha mtu kujizamisha kikamilifu ndani yake, kinamfanya kujitambua na kuwa mgunduzi wa nafsi yake, na ambacho kinasimama kama mbao ya alama ya njia ya hiyo njia iliyonyooka kwa wale wanaopita kwenye njia hiyo ya Mwenyezi Mungu, kumkinga na mizingile (njia zenye utata), na kuzuia uzembe, si chochote kingine bali ni Swala. Mwanadamu, kwa sababu ya mishughuliko yake anakuwa hana wasaa wa kufikiri na kutafakari kuhusu yeye mwenyewe, juu ya lengo la maisha, na kuhusu kupita kwa nyakati, saa, na siku. Ni kwa nadra sana kwamba siku zinapita na kuingia usiku, siku mpya inaanza, na majuma na miezi inapita bila ya mwanadamu kuwa na nafasi ya kutambua kuhusu kupita kwa wakati, maana zake, na kupotea kwake bure. Swala ni kama king’ora kwa ajili ya kuamshia, onyo katika saa tofauti za mchana na usiku, ambalo linatoa utaratibu kwa ajili ya mwanadamu, na kuhitaji kujitoa kwake kwa ajili ya utekelezaji wake, hivyo kuweza kuleta maana kwenye nyakati za mchana na usiku na kumfanya awajibike kwa kupita kwa nyakati. Mwanadamu anapokuwa amezama sana katika mambo yake ya kidunia, bila kuzingatia kupita kwa wakati, na utuuzima unaomnyemelea, swala inamrudisha na kumfanya aelewe kwamba siku imepita na siku mpya imekwishaanza. 17

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 17

8/12/2015 6:35:11 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

Lazima ajishughulishe kwa kuchukua jukumu kubwa kwa kufanya kazi muhimu, kwa sababu sehemu ya maisha tayari imekwisha kutumika. Kwa hiyo mtu lazima ajaribu sana, na achukue hatua kubwa mbele kwa sababu lengo hilo ni la kutukuka sana hadi panapokuwa na fursa, mtu anapaswa kujaribu kulipata kabla hajachelewa. Kwa upande mwingine, kusahau lengo na mwelekeo kwa sababu ya shinikizo la maisha ya siku hadi siku au kujihusisha na uyakinifu, hilo ni jambo la kawaida na la dhahiri. Uwezekano wa kuangalia upya wajibu wote uliowekwa juu ya mwanadamu, ili kukamilisha lengo linalotakikana, katika kila siku kiasi ni kugumu na karibu na kutowezekana. Kwa nyongeza juu ya hilo, muda wa kutosha kwa ajili ya kuangalia upya masharti na maadili yote ya madhehebu ya Kiislamu, ambayo yanaleta hali ya utukufu na ustawi kwenye maisha ya binadamu, kamwe unakuwa haupo na fursa kama hiyo kamwe haitokezi. Swala kwa yenyewe inakuwa na mukhtasari mfupi wa kanuni zote za madhehebu hii, kwa sababu maneno, na matendo yaliyokadiriwa na yaliyopangwa hasa na yenye utulivu ambayo yamo ndani yake, swala inaweza kwa usahihi kabisa kuitwa udhihirisho kamili wa Uislamu. Au, kwa maneno mengine, tunaweza kulinganisha swala na wimbo wa taifa wa nchi, bila shaka pamoja na baadhi ya tofauti katika maana na vigezo vinginevyo. Nchi, ili kufanya kanuni na maadili yake yawe yamewekwa kwenye kumbukumbu ya kudumu katika akili na mawazo ya raia zake, na kuweka hai uzalendo wao kwenye itikadi hiyo, hutunga wimbo wa taifa, wenye mukhtasari wa maadili hayo na kufanya kuimbwa kwake kuwa ni wajibu wa lazima. Uimbaji wa kurudiwa wa wimbo wa taifa unakuwa ni njia ya kuwafanya raia wake kubakia wamejizatiti kwenye maadili hayo, vilevile kama ukumbusho kwao kwamba wao ndio raia wa nchi hiyo na walinzi na watetezi wa maadili hayo yaliyotungwa ndani ya wimbo huo. Vinginevyo, kusahau kanuni na 18

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 18

8/12/2015 6:35:11 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

maadili hayo kunaweza kumaanisha kwamba wameyakengeuka, na hawamo tena katika kujifunga kwayo katika maisha yao. Kwa hiyo, marudio haya yanawafanya wawe tayari na hadhiri kwa ajili ya kazi na huduma kwa ajili ya nchi yao, yanawafundisha utaratibu unaofaa, yanawapangia majukumu na wajibu, kuweka hai kanuni hizo kwenye akili zao, yanawasaidia katika kazi zao na mwisho kabisa yanalea ndani ya nafsi zao ujasiri na uwezo wa kutenda katika kutekeleza majukumu yao kwa mafanikio kabisa. Kama wimbo wa taifa kwa nchi, swala kwa kifupi ni mukhtasari kamili wa itikadi ya Kiislam ambayo kwa uwazi kabisa inaonesha njia ya Muislam, na inabainisha wazi wajibu wote na majukumu, njia na matokeo. Ni swala ambayo ndio inamwita Muislam mwanzoni mwa siku, wakati wa mchana na jioni, na inamfanya aelewe kanuni, mwelekeo, malengo na matokeo kwa ulimi wake mwenyewe, ikimhimiza kutenda kwa kumpa nguvu ya kiroho. Swala ndio ambayo hatua kwa hatua inamuongoza muumini kufikia kilele cha ukamilifu, yenye kuwa na imani na vitendo, na inamtengeneza na kuwa kitu cha thamani kubwa, yaani mfano kamili wa Mwislamu. Ni kwa sababu ya sifa hizi kwamba Mtukufu Mtume ameiita swala: ni ngazi ya muumini, inayompandisha juu zaidi kuelekea mbinguni. Mwanadamu ana barabara ngumu na ndefu mbele yake, barabara ambayo inamuongoza kuelekea kwenye uadilifu halisi na ustawi. Kusafiri kwenye barabara hii ya ukamilifu kumekuwa ndio lengo la asili la kuumbwa kwa mwanadamu na uhai. Lakini analokabiliana nalo sio tu hii barabara moja peke yake, bali anapaswa kuepuka njia za giza na nyembamba, michepuko, na njia za hatari ambazo zimezagaa karibu tu na barabara kuu iliyonyooka. Wakati mwingine njia hizi huwa zinashawishi sana na zimejaa vivutio ambavyo 19

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 19

8/12/2015 6:35:11 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

kwavyo msafiri huwa anachanganyikiwa na kuchagua njia isiyo sahihi, kwa makosa tu. Kwa hiyo, ili kuepuka mitego hii, msafiri anapaswa kung’ang’ania kwenye mpango wa asili, yaani kuhakikisha ule mwelekeo sahihi, na kusonga mbele kuelekea kwenye lengo lenye thamani sana na mwisho bora kabisa (mwendo kuelekea kwa Mwenyezi Mungu), kwa kufuata ramani iliyoelekezwa inayoonyesha njia, na lengo. Swala sio chochote zaidi ya mazingatio endelevu kuelekea kwa Mwenyezi Mungu na ramani yenye maelekezo ya kina yanayoonyesha hiyo njia kuu muhimu. Ni mkondo unaotoa mawasiliano ya kudumu na kiungo madhubuti na Mwenyezi Mungu kwa sababu una mukhtasari kamili wa itikadi za Kiislamu katika ibada zake. Kwa maelezo hayo hapo juu, inakuwa dhahiri kwa hiyo kwamba ni sababu gani iliyoko katika kuamrisha swala mara tano kwa siku na ni muhimu kwa kiasi gani? Inaweza ikalinganishwa na mahitaji ya chakula ya mwili wa binadamu katika nyakati tofauti za kupishana katika kipindi cha saa 24. Mbali na ukweli kwamba swala ina mukhtasari kamili wa malengo na maadili ya Kiislamu, na kwa vile usomaji wa Qur’ani ni wa lazima katika nyakati za ibada zake, kwa kawaida swala inamfanya mwenye kuiswali kuwa na ujuzi wa sehemu ya Qur’ani na kwa hiyo inamtia moyo na kumhimiza kutafakari na kufikiria kuhusu maana za Kitabu hicho Kitukufu, ambapo kidogo kidogo mwisho inakuwa ni tabia yake. Matendo ambayo yanaagizwa ndani ya swala ni utambuzi kamili na wa jumla wa Uislamu katika muundo mdogo. Katika mfumo wa kijamii, Uislamu unashirikisha mwili, akili na nafsi za wanadamu na kuzifanya zishughulike, kuleta ustawi na furaha kwa ajili yao. Jambo hilohilo linatimizwa hasa pale mtu anaposwali swala zake, kwa sababu hivi vyote vitatu, mwili, akili na nafsi vinafanyishwa kazi na kuhusishwa kama ifuatavyo: 20

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 20

8/12/2015 6:35:11 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

Mwili: Mikono, miguu na ulimi viko kwenye mshughuliko kwa vile swala inahitaji namna tatu za usimamaji, kurukuu na kusujudu. Akili: Kufikiria juu ya yaliyomo na maneno ya swala ambako kwa kawaida ndio kiashirio kuhusu malengo na njia; na ni kama kukamilika kwa mafunzo mafupi kuhusu mbinu za kufikiri katika itikadi za Kiislamu. Nafsi: Kumkumbuka Mwenyezi Mungu, na upaaji wa kiroho kuelekea kwenye mawanda matukufu yaliyo juu kabisa, kwa kutupilia mbali matukio yote ya kidunia ya nafsi kwa kuyafanya ni upuuzi usio na idadi na burudani, na kujaribu kupata mahudhurio ya nafsi kwa kutafakari kwa makini, na vilevile kustawisha mbegu za unyenyekevu na hofu juu ya Mwenyezi Mungu katika moyo wa mwanadamu. Ni ukweli unaokubalika kwamba swala ya kila dini au itikadi inaakisi mukhtasari mfupi wa dini au itikadi hiyo. Vivyo hivyo ndio ukweli kwa swala katika Uislamu yaani, inakusanya nafsi na mwili, mada na maana, dunia na akhera, katika maneno, maudhui na katika usogevu ambao ndio utaalamu wa swala katika Uislamu. Mwislamu, kwa kuswali swala kamili anaweza akatumia nguvu zake zote mwenyewe kwa ajili ya kupata utukufu, yaani papo kwa papo anaziamuru nguvu zake zote za kimwili na za kiroho kuelekea kwenye lengo hili. Muumini anayeswali, akiitafuta njia ya Mwenyezi Mungu kwa nguvu zote za umakinikaji wa kimwili na kiakili hufanikiwa katika kuzishinda dhamira zote za uovu, uonevu na udhalilishaji, akijifanya mwenye kukingwa na aina zote za athari za maovu. Baadhi ya aya za Qur’ani zinaelezea usimamishaji swala kama ishara ya uwanadini, wakati ambapo aya nyingine nyingi zinaweka msisitizo kwa ajili ya jambo hili. Kwa hiyo, inaelekea kwamba mfumo wa swala unakwenda ndani zaidi kuliko kule kuiswali tu. 21

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 21

8/12/2015 6:35:12 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

Haitoshi kwa muumini kuswali kirahisi tu swala yake, bali anawajibika pia kufanya jitihada ya kutimiza makusudio na malengo na kufuata ile njia inayoelekezwa nayo kwa ajili yake, na vilevile kuwahimiza wengine kuambatana naye katika mwelekeo huo. Kwa maneno mengine ni kwamba, inaelekea kwamba kule kuswali kuna maana kwamba mtu lazima afanye jitihada zake zote kwa ajili ya kuanzisha mazingira ya kumtafuta Mwenyezi Mungu pamoja na uchamungu kwa ajili yake mwenyewe na kwa ajili ya wengine pia, na kuisogeza mbele jamii kwa ujumla wake kuelekea katika huo mwelekeo wa swala. Kwa hiyo muumini ama jamii ya waumini, kwa kule kusimamisha swala huwa wanachoma mizizi ya upotofu, dhambi na ufisadi ndani mwao na ndani ya mazingira ya kijamii, na pia kwa wakati huohuo wanatangua kabisa aina zote za mawazo ya dhambi na dhamira za ndani na za nje za uovu ima wa binafsi au wa mkusanyiko wowote utakaokuwa. Kwa hakika swala inamlinda mtu binafsi na jamii vilevile kutokana na vitendo visivyopendeza na vyenye kufedhehesha.

َّ ‫إِ َّن ال‬ ‫صلاَ ةَ تَ ْنهَ ٰى َع ِن ْالفَحْ َشا ِء َو ْال ُم ْن َك ِر‬ “…..Hakika swala inakataza maovu na machafu…..” (29:45)

Wakati wa mapambano muhimu ya maisha, wakati ambapo nguvu za kishetani zimeandaliwa kikamilifu na kuhamasishwa kwa ajili ya ubomoaji wa dhamira zote, vichocheo vya wema na uadilifu ndani ya kila mtu na kila mahali, ngome kuu inayoshambulia inajumuisha pamoja na dhamira ya mwanadamu na nguvu ya kiroho. Kwa sababu mara kizingiti hiki kitukufu kinapoondolewa, kukaliwa na kubomolewa kwa ngome inayowakilisha utu wa mwanadamu, ngome ambayo ndio hazina ya uungwana wote wa asili, na limbikizo 22

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 22

8/12/2015 6:35:12 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

la ujuzi na elimu, kunakuwa kwenye kuwezekana. Kwa hiyo, wale wanaotangaza ujumbe mpya na wa asili kwa ajili ya kipindi chao wao wanashambuliwa kwa ukali zaidi kuliko wengine na wanahitaji kuulinda kwa nguvu zote uwekaji ngome huu usiozuilika kwa kiasi kidogo zaidi kuliko wengine. Swala ya Uislamu kwa msukumo na marudio ya kumkumbuka Mwenyezi Mungu inamuunganisha yule mtu aliye na kikomo na udhaifu kwenye nguvu isiyo na ukomo na ya dhahiri kabisa na kumfanya yeye ategemee juu ya chanzo hicho. Kwa kumuunganisha mwanadamu na hiyo nguvu ya dhahiri na mwendeshaji wa ulimwengu wote, kunampatia nguvu isiyopimika wala kuvunjika, ambayo inaweza kuchukuliwa kama ndio tiba bora kabisa kwa ajili ya udhaifu wa mwanadamu na dawa yenye nguvu sana yenye kudukiza azma na dhamira yenye nguvu. Mtukufu Mtume wa Uislamu mwanzoni mwa uhuishaji mkubwa wa Uislamu, na akikumbana na mkabiliano kamili na wapagani, alihisi mzigo mzito kabisa wa wajibu na majukumu juu ya mabega yake, aliagizwa na Mwenyezi Mungu kuswali swala ya usiku (swalatil-Layl) na kumtukuza Yeye kama ifuatavyo:

ً‫يَا أَيُّهَا ْال ُم َّز ِّم ُل قُ ِم اللَّ ْي َل إِ اَّل قَلِ ا‬ ْ‫يل نِصْ فَهُ أَ ِو ا ْنقُص‬ ً‫آن تَرْ تِ ا‬ ً‫ِم ْنهُ قَلِ ا‬ ‫يل إِنَّا‬ َ ْ‫يل أَ ْو ِز ْد َعلَ ْي ِه َو َرتِّ ِل ْالقُر‬ ‫ك قَ ْو اًل ثَقِيل‬ َ ‫َسنُ ْلقِي َعلَ ْي‬ “Ewe uliyejizongazonga nguo! Simama usiku, ila kidogo tu. Nusu yake, au ipunguze kidogo, au izidishe, na soma Qur’ani kwa utaratibu. Hakika tutakuteremshia kauli nzito.” (73:1-5).

Sasa, tungeiangalia upya maudhui ya swala kwa namna, bila kuzama zaidi kwenye tafsiri na maelezo mapana. Juhudi zitafanyika 23

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 23

8/12/2015 6:35:12 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

kuwaongoza wasomaji hatua moja karibu zaidi na lengo la swala. Swala huwa inaanza kwa Jina la Mwenyezi Mungu na ukumbusho wa utukufu Wake mkubwa usio na kiwango wa nguvu Zake, na umiliki na ukubwa usiopimika kutoka kwenye kiwango cha juu kabisa cha fikra za mwanadamu: (Allahu-Akbar – Mungu Mkuu). Muumini anaanza utukuzaji wake kwa maneno hayo hapo juu, na kwa ajili ya tendo bora, anaanza sura ya ufunguzi iliyokifu utukufu. Mungu ni Mkuu – Mkubwa kuliko chochote kinachoweza kuingizwa kwenye ubora au sifa -. Mkuu kuliko kulinganishwa na wenye kudai utukufu na miungu midogo yote katika historia, na Mkuu kuliko mamlaka zote na vyote vya asili vidhihirikavyo na kuonekana ambavyo kwamba mwanadamu anaweza akaviogopa au kuweza kushawishika navyo, na ni Mkuu kuliko yeyote anayeweza kuthubutu kupingana na sharia Zake tukufu na za kimaumbile. Ikiwa mja wa Mwenyezi Mungu tayari ametambua desturi hizi za kimungu, na kulingana nazo hizo akachagua njia, na anajitahidi katika mwelekeo huo, kisha pamoja na ukumbusho huu kwamba “Mungu Ndiye Mkuu zaidi,” basi hupata uwezo mkubwa kabisa katika uhai wake na anakuwa amekifu matumaini kikamilifu kabisa. Kwa uhakika kamili, yeye anajua kwamba juhudi zake zote zimekuwa zenye mafanikio na hatimaye mwisho wake utakuja kuwa mwema. Uhakika wa namna hizi unamfanya awe mwenye matumaini na kuridhika kuhusu njia aliyoichagua, akitaraji mustakabali wenye matumaini mema. Baada ya kutamka maneno haya, mwenye kuswali anaingia kwenye taratibu za swala kivitendo. Ni lazima asome ile aya ya Himidi (sura ya ufunguzi) na baada ya hapo anakamilisha sura kutoka kwenye Qur’ani Tukufu katika hali ya kusimama.

24

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 24

8/12/2015 6:35:12 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

MLANGO WA PILI Sura al-Hamd (Sura ya Kifunguzi)

‫َّح ِيم‬ ِ ‫بِس ِْم للاهَّ ِ الرَّحْ ٰ َم ِن الر‬

K

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

wa jina la Mwenyezi Mungu, ambaye ndiye mmiliki wa neema zote na Mtoaji wa huruma ya milele. Aya hiyo hapo juu ndio aya ya kwanza ya sura zote za Qur’ani Tukufu, (isipokuwa Sura Tawba au Barrat, sura ya tisa ya Qur’ani) ndio kifunguzi cha swala, na vilevile kifunguzi cha vitendo na shughuli zote za mwislamu, yaani kazi zote huwa zinaanza tu na jina la Mwenyezi Mungu, kila kitu kilichoko kwenye miliki ya mwanadanmu – mwanzo wa uhai wa mwanadamu na pia udhihirisho wote wa kuwa kwake hai uko katika jina la Mwenyezi Mungu-. Mwislamu anaanza siku zake na kusimamisha shughuli zake za kila siku, anafumba macho yake kudumu kutoka kwenye ulimwengu huu na kuwa sehemu ya akhera.

‫ين‬ َ ‫ْال َح ْم ُد لِهَّلِ َربِّ ْال َعالَ ِم‬ “Sifa njema (zote) ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa viumbe (vyote).” (Qur’ani 1:2)

25

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 25

8/12/2015 6:35:12 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

Sifa njema zote na shukrani ni Zake Yeye makhsusia, kwa sababu Yeye Ndiye chanzo na asili ya Neema Kubwa zote. Yeye Ndiye mkusanyiko wa sifa na tabia zote zinazostahiki kutukuzwa, wema na uadilifu wote ambao unamiminika kutoka kwenye chemchem Yake ya asili. Kwa hiyo, kumsifia Mwenyezi Mungu maana yake ni kusifia matendo yote mema na adilifu. Yeye Ndiye anayetoa muelekeo (au lengo) kwenye juhudi zote zinazosaidia wema na uadilifu. Kama tukiangalia baadhi ya sifa zinazostahiki kusifiwa na tabia katika nafsi zetu wenyewe, ni lazima tuzizingatie kama ni huruma, fadhila na neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwa sababu kwa hakika Mwenyezi Mungu ameshirikisha uwezo kwa ajili ya wema ndani ya maumbile ya mwanadamu, na ameiandaa asili yake kwa namna ambayo wakati wote anatafuta ubora wa hali ya juu. Na amejaalia juu ya mwanadamu uwezo wa kujiamulia kama chombo kingine kwa ajili ya utendaji wa matendo adilifu na ya kiungwana. Utambuzi huu wa kupewa na Mwenyezi Mungu sio tu unafunga mlango wa kuwa mtu mwenye umimi na mwenye kujivuna, bali pia kwa wakati huohuo unazuia vitendo vya hasara na vichafu ya uwezo wa ujuzi na ubunifu ndani ya maumbile ya mwanadamu. Mola wa ulimwengu wote anaelezea uwepo wa sayari zingine na kutoa hisia kwamba sayari hizo na makundi ya nyota zinahusiana kwa pamoja na kutengeneza kitu kimoja. Hivyo muumini anagundua kwamba mbali na dunia hii, na uoni wake wenye mipaka na mfinyu, nje ya mipaka anayoidhania yeye kwa maisha yake, kuna matufe mengine ya mbinguni, sayari na makundi ya nyota na Mwenyezi Mungu vilevile Ndiye Mola wa ufalme mkubwa wote huu mtukufu. 26

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 26

8/12/2015 6:35:12 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

Akiangalia kutoka kwenye pembe nyingine atagundua kwamba viumbe wote yaani wanadamu, wanyama, mimea, viumbe visivyosogea, anga na makundi kadhaa ya nyota ya ulimwengu vyote viko kwenye utii wa Mwenyezi Mungu, ambaye Ndiye Mola Wao na anaudhibiti ulimwengu mzima. Anakuja kuelewa kwamba Mungu wake sio Mungu wa kabila lake tu, au nchi yake au kwa binadamu tu, bali vilevile wa yule mdudu chungu mdogo kabisa na mmea dhaifu pia. Yeye vilevile ni Mungu wa anga na mbingu, makundi ya nyota na nyota moja moja pia. Kwa utambuzi huu, yeye huwa anagundua kwamba kumbe hayuko peke yake, bali anahusiana na chembechembe ndogo zote za ulimwengu huu, na viumbe vyote vidogo au vikubwa. Ameshirikishwa na kuhusishwa na wanadamu wa namna zote, wote ni ndugu na wasafiri wenza, na msafara mkubwa huu wa binadamu unaelekea kwenye lengo moja. Utambuzi huu wa ushirikiano na mahusiano na uwiano inamfanya awajibike na kujitolea kuhusiana na viumbe vyote. Kuhusu wanadamu ana jukumu la kuonyesha wajibu wake, miongozo na usaidizi, ambapo kuhusu viumbe wengine anawajibika kwenye utambulisho wao halisi, na matumizi katika njia ya usawa na usahihi kwa mujibu wa malengo na maelekezo ya kimbinguni.

‫َّح ِيم‬ ِ ‫الرَّحْ ٰ َم ِن الر‬

“Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.” (Qur’ani 1:3) Rehema za jumla za Mwenyezi Mungu katika muundo wa uwezo wa ubunifu, sharia zenye kuleta uhai na vyanzo vya nishati zenye kuendelea zilizoumbwa kwa ajili ya kuimarisha ulimwengu, zinavizunguka viumbe vyote; na kila kitu na kila mtu mpaka muda wa mwisho vinahitajia neema (Rehema) hii. Kwa upande mwingine, rehema Zake maalum – rehema kwa ajili ya muongozo na usaidizi, 27

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 27

8/12/2015 6:35:12 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

kwa ajili ya malipo, na upendo – ni kwa ajili ya waja Wake waadilifu na wachamungu. Rehema hii maalum (Huruma) kama njia yenye kuangazia inakuwa ni sehemu ya uhai wa viumbe hawa adhimu na wema na inabakia pamoja nao hadi wakati wa kifo, na kutoka kwenye kifo hadi wakati wa kufufuliwa; na kwenye makazi ya mwisho ya kudumu milele. Hivyo, Mwenyezi Mungu Ndiye Mpaji wa rehema za jumla, ambazo ni kwa ajili ya wote lakini ni za muda, na rehema maalum kwa ajili ya vikundi maalum ambayo ni ya kudumu na ya milele. Kwa hiyo, kule kukumbuka sifa za huruma za Mwenyezi Mungu, katika utangulizi wa Qur’ani Tukufu kwa ajili ya kuanza kwa swala, na mwanzoni mwa kila Sura kunaashiria kwamba upendo na fadhila za Mwenyezi Mungu ni nyingi sana na zenye kuonekana waziwazi kwenye mandhari ya maumbile kulinganisha na ghadhabu na adhabu Zake, ambazo zimehifadhiwa tu kwa ajili ya maadui, wakaidi, madhalimu na wahalifu, ambapo rehema Zake zinazunguka kila kitu mahali pote.

‫ين‬ ِ ‫َمالِ ِك يَ ْو ِم ال ِّد‬ “Mwenye kumiliki Siku ya Malipo.” (Qur’ani 1:4)

Siku ya ufufuo ndio hatima ya mwisho ya matendo yetu katika maisha yetu ya kidunia. Tunajaribu kwa uwezo wetu wote kupata kuwa na mwisho mwema, na tunatamani kupata hatima njema. Katika jitihada hizo, wote – wayakinifu (wapenda dunia zaidi), na wale wanaomwamini Mwenyezi Mungu, wote katika juhudi zao wanatafuta hatimaye kupata hatima njema. Tofauti inakuja kwamba kila mmoja ana tafsiri tofauti kuhusu huo mwisho wenyewe. Kwa wayakinifu mwisho huo maana yake ni, saa in28

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 28

8/12/2015 6:35:12 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

ayokuja, siku inayofuata, mwaka ujao, au miaka michache ijayo, na hatimaye kuwa mzee na kuchakaa kwa kupita kwa wakati, lakini kwa mtazamo wa mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu matokeo ya mwisho ni ya kina zaidi na mapana zaidi kuliko ilivyoelezwa hapo juu. Kwa mtazamo wa mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu, dunia haikufungika kwenye mipaka yenye ukomo, bali mustakabali wake hauna mipaka, ambao unaibua ndani ya nafsi yake matumaini makubwa mno yakimtia moyo wa kufanya kazi kwa bidii bila ya kuchoka kamwe. Mtu kama huyo, ambaye kamwe hakati tamaa na kupoteza matumaini, kwa ajili ya kuja kulipwa thawabu, na kuona matokeo ya vitendo vyake hata baada ya kufariki, anaweza kuendeleza matendo yake mema kwa ajili ya kupata radhi za Mwenyezi Mungu kwa msisimko sana hadi muda wa mwisho kabisa wa uhai wake. Ukumbusho wa kwamba Mwenyezi Mungu Ndiye Mmiliki wa mwisho, na amri zote ni Zake Yeye mnamo Siku ya Kiyama na malipo, huwa unatoa uwezo kwa mwenye kuswali kutembea kuelekea upande sahihi, na kufanya vitendo vyake vyote na juhudi zake kuelekezwa upande wa Mwenyezi Mungu. Maisha na udhihirisho wote wa kuwa hai unakuwa ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na njia Yake. Kila kitu anachokimiliki na juhudi zake zote na vitendo vinatumika katika uelekeo wa ukamilifu na ubora wa mwanadamu, mwelekeo pekee unaoridhisha kwa Mwenyezi Mungu. Kwa upande mwingine, mlango wa kutegemea dhana potovu na matarajio yasiyo ya kweli umefungwa kwake yeye, na matumaini ya kweli kwa ajili ya vitendo inadukizwa ndani ya uhai wake wa ndani kabisa. Katika dunia hii, ile mifumo isiyo sahihi na serikali potofu na za kidhalimu zimetoa fursa kwa watu wenye akili vivu na uwezo wa kujishughuli29

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 29

8/12/2015 6:35:12 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

sha katika utekaji nyara na uporaji, bila ya kupata taabu yoyote au kufanya juhudu yoyote kwa kutumia kirahisi tu udanganyifu, uongo na mbinu za utapeli; katika dunia ijayo ambako juhudi zote zinasimamiwa na kudhibitiwa kwa makini kabisa na Mungu Mwenye hekima na uadilifu, udanganyifu na ulaghai kama huo utakuwa hauwezekani, na hakuna atakayelipwa thawabu kwa mambo ambayo yeye hakushiriki humo. Hapa ile nusu ya kwanza ya Sura al-Fat-ha ambayo ndani yake mna utukufu wa Mwenyezi Mungu, Mola wa ulimwengu wote, na inaelezea baadhi ya sifa za Dhati Zake, inafikia kwenye ukamilifu wake. Nusu ya pili ambayo inakusanya kukubali utumwa (kujifunga) na kuwa na haja ya muongozo inatoa ufafanuzi juu ya baadhi ya kanuni muhimu za itikadi ya Kiislam.

ُ ‫ك نَ ْستَ ِع‬ ‫ين‬ َ ‫ك نَ ْعبُ ُد َوإِيَّا‬ َ ‫إِيَّا‬ “Wewe tu tunakuabudu na Wewe tu tunakuomba msaada.” (Qur’ani 1:5)

Uwezo wetu wote wa kimwili, kiroho na kiakili wa uhai wetu upo mikononi mwa Mwenyezi Mungu, na uko tayari kwa ajili ya amri Zake na maelekezo Yake. Yule mwenye kuswali, kwa kutamka sentensi hii anakata mnyororo wa fungamano na yeyote yule asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na anaiweka huru mikono yake, nyayo zake na shingo yake na kwa hiyo anakataa madai ya miungu wa bandia – wadai utukufu wenye kiburi – ambao daima wamekuwa wakihusika na kuunda matabaka ya watu wa chini na watu wa juu katika jamii yote katika historia, na wakawafanya wengi wa binadamu kuwa wenye kuonewa, kunyimwa na wakawaweka kwenye nyororo za utumwa. 30

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 30

8/12/2015 6:35:12 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

Mwenye kuswali anajipeleka yeye mwenyewe na wenye kumaumini Mwenyezi Mungu wengine pia, mbali zaidi kutoka kwenye mipaka ya utii na utumwa kwa yeyote yule mbali na Mwenyezi Mungu, na mfumo wowote mbali na serikali ya kimungu. Kwa mukhtasari, kwa kukubali utumwa kwa Mwenyezi Mungu kunatupilia mbali utumwa kwa viumbe wenzetu, na kwa kufanya hivyo kunaunganisha safu za watumishi wa kweli halisi wa madhehebu ya tawhid. Kukiri na kukubali kwenye ukweli kwamba fungamano na utii unaruhusiwa tu mbele ya Mwenyezi Mungu na Kwake tu, ni moja ya kanuni muhimu sana (kwa matamshi na vilevile kwa vitendo) ya itikadi na imani ya Kiislamu na dini nyingine zote, ambayo ina maana kwamba utukufu na majaaliwa ni vya Mwenyezi Mungu peke Yake, yaani ni Yeye peke Yake anayo haki ya kuabudiwa na hakuna mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu, na kwa hiyo hakuna mwingine mbali na Yeye anayepaswa kutukuzwa au kuabudiwa. Kwa bahati mbaya walikuwepo baadhi ya watu ambao tafsiri yao haikuwa sahihi na yenye mipaka, hawakuweza kuelewa maana yake sawasawa, na kwa hiyo bila kujijuwa wanakuwa mawindo kwenye utumwa mbali na ule wa Mwenyezi Mungu. Wao walidhani kwamba ibada ya Mwenyezi Mungu inaishia kwenye kumtukuza na kumuabudu Yeye, na kwa vile wameswali mbele ya Mwenyezi Mungu na kumtukuza, basi kwa kufanya hivyo wanaridhika kwamba hawakuwa wamemuabudu mwingine yeyote zaidi, kinyume na Mwenyezi Mungu. Ujuzi wa maana pana ya ibada kutokana na mtazamo wa Qur’ani Tukufu na hadithi unakosoa msingi wa tafsiri iliyotajwa hapo juu. Kwa mujibu wa istilahi ya Qur’ani Tukufu na hadithi, ibada inaweza kuelezwa kama ni: utiifu, kujisalimisha, na unyenyekevu halisi kabisa kwenye amri, taratibu na mifumo ya kanuni iliyotolewa ku31

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 31

8/12/2015 6:35:12 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

toka kwa mwenye kushikilia madaraka au kitovu cha mamlaka, na yamelazimishwa juu ya binadamu, iwe unyenyekevu na utii huo umeambatana na hali ya utakasaji wa sifa au vinginevyo. Kwa hiyo, kwa mujibu wa ufafanuzi huo hapo juu, wale wote waliojisalimisha kwenye kanuni, mifumo na amri zilizotolewa na mamlaka yoyote kinyume na Mwenyezi Mungu wanakuwa ni waabudia wake, watumwa na udhihirisho wake. Licha ya hivyo, kama bado kuna nafasi iliyobakia kwa ajili ya amri za Mwenyezi Mungu, na katika baadhi ya sehemu au maeneo katika maisha yao binafsi au ya kijamii, wakitii sharia na maagizo ya Mungu wataitwa wanafiki – yaani wale ambao pamoja na kumuabudu Mwenyezi Mungu wanaabudu wengineo pia; na kama hakuna kilichobakia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu basi wanaitwa makafiri wasioamini (yaani wale ambao hawaoni ule ukweli wa wazi wenye kung’ara kabisa kuhusu uwepo wa Mwenyezi Mungu na wanaukana katika imani na vitendo vyao). Kwa hoaja hizo za Kiislamu hapo juu, inaweza kueleweka kwa urahisi kwamba ni kwa nini dini zote za ki-Mungu haya maneno “Hapana mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu”2 yalikuwa ndio wito wao mkuu. Ukweli huu – ukweli wa maana ya swala – katika nyaraka za Kiislamu, ndani ya Qur’ani Tukufu, na katika Sunnah umetajwa kwa kurudiwa rudiwa na kwa uwazi zaidi, kiasi kwamba kwa wanafikra na wasomi kusiwe kumebakia uwezekanao japo mdogo kabisa wa kupingana au shaka. Kama mfano, tutarejelea kwenye aya mbili za Qur’ani zifuatazo na hadithi iliyosimuliwa na Imam Ja’far as-Sadiq  kama ifuatavyo:

2

Rejea kwenye Qur’ani Tukufu, Surat al-Araf , aya ya 59 hadi 158; Surat Hud aya ya 50 hadi 84 ambamo wito huo umelinganiwa na baadhi ya Manabii wakubwa. 32

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 32

8/12/2015 6:35:12 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

ِ َّ‫ون للاه‬ ِ ‫اتَّ َخ ُذوا أَحْ بَا َرهُ ْم َو ُر ْهبَانَهُ ْم أَرْ بَابًا ِم ْن ُد‬ ‫َو ْال َم ِسي َح اب َْن َمرْ يَ َم َو َما أُ ِمرُوا إِ اَّل لِيَ ْعبُ ُدوا إِ ٰلَهًا‬ ‫ون‬ َ ‫اح ًدا ۖ اَل إِ ٰلَهَ إِ اَّل هُ َو ۚ ُس ْب َحانَهُ َع َّما يُ ْش ِر ُك‬ ِ ‫َو‬ “Wamewafanya makuhani wao na watawa wao kuwa ni miungu badala ya Mwenyezi Mungu, na Masih mwana wa Maryamu. Wala hawakuamrishwa isipokuwa wamwabudu Mungu Mmoja tu. Hakuna mungu ila Yeye. Ametakata na wanayomshirikisha nayo.” (Qur’ani 9:31)

َ ‫ين اجْ تَنَبُوا الطَّا ُغ‬ ‫وت أَ ْن يَ ْعبُ ُدوهَا َوأَنَابُوا إِلَى‬ َ ‫َوالَّ ِذ‬ ‫للاهَّ ِ لَهُ ُم ْالبُ ْش َر ٰى ۚ فَبَ ِّشرْ ِعبَا ِد‬ “Na wale wanaojiepusha na kuabudu taghut, na wakarejea kwa Mwenyezi Mungu, watapata bishara njema. Basi wabashirie waja Wangu. (Qur’ani 39:17)

Abu Basir anasimulia yafuatayo kutoka kwa Imam Ja’far asSadiq  ambaye aliwahutubia Mashia wa kweli wa wakati wa kipindi chake:

‫ ومن أطاع جباراً فقد عبده‬،‫أنتم هم‬ “Ninyi ndio wale waliokataa kuwaabudu miungu wa bandia. Na yeyote ambaye ametii amri ya jabari au dhalimu kwa hakika amemuabudu yeye.”3

3

Tafsiir Nuur-al-Thaqalayn, Jz. 5, uk. 481, vilevile rejea kwenye aya ya 17 ya Surat-Zumar 33

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 33

8/12/2015 6:35:12 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

ُ ‫ك نَ ْستَ ِع‬ ‫ين‬ َ ‫َوإِيَّا‬ “…..Na Wewe tu tunakuomba msaada.” (Qur’ani 1:5)

Hatutegemei aina yoyote ya msaada au tegemeo lolote kutoka kwa wapinzani Wako na wenye kudai utukufu. Kwa sababu ya kukataa kwao kukubali utukufu wa Mwenyezi Mungu, hawawezi kuwa ni wenye msaada wowote kwa wale watafutaji na wafuasi wa njia ya Mwenyezi Mungu. Hiyo njia ya Mwenyezi Mungu ni njia ambayo iliyofuatwa na Mitume  – ndio chanzo kwa ajili ya kuukamilisha ukweli, uadilifu, undugu, na kuwepo kwa pamoja kwa wanadamu katika muda mmoja uleule, na kuleta utukufu kwa wanadamu wakati wakishutumu na kulaani na kukanusha aina zote za chuki, uonevu na utendewaji usiolingana (au upendeleo unaooneshwa kuelekezwa kwa tabaka fulani au kundi Fulani). Ni vipi basi, hao maadui wa Mwenyezi Mungu na wenye kudai utukufu ambao wamejitolea moja kwa moja kwenye uhai huu wa kidunia wenye fedheha, na ambao kwa tabia yao ya uporaji hawakuacha kufanya juu chini katika juhudi zao za kubomoa na kuharibu maadili halisi yote ya mwanadamu, wao waweze kuwa wa msaada wowote ule kwa waja watumwa wa Mwenyezi Mungu? Wao wamo kwenye vita vya kudumu na wanabeba ghadhabu kali yenye kuchoma dhidi ya watumwa (waumini) wa Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo, sisi tunatafuta msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu tu, uwezo wa akili na kufanya uamuzi, uliowekwa na Mwenyezi Mungu pamoja na asili ya maumbile yetu, njia na nyenzo zilizotolewa kwa ajili ya kuisha maisha haya; sharia za asili na kihistoria, ambazo kama zikiweza kueleweka vizuri zinaweza kusimama kama mwongozo kwa ajili ya mawazo na vitendo vyetu; na vilevile kutoka kwenye ziada zote za uwezo wa mbinguni ambazo ni askari Wake wenye nguvu katika kuwahudumia binadamu. 34

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 34

8/12/2015 6:35:12 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

‫ا ْه ِدنَا الصِّ َراطَ ْال ُم ْستَقِي َم‬ “Tuongoze njia iliyonyooka” (Qur’ani 1:6)

Kama mwanadamu angekuwa na lengo kubwa na la muhimu (suala la kufa na kupona) kuliko huo “Mwongozo,” kwa kweli hilo lingejumuishwa katika Sura al-Fatiha – Sura ambayo ndiyo kifunguzi cha Qur’ani Tukufu na inayounda sehemu muhimu ya swala – na ingekuwa ikisomwa kama dua kwa ajili ya kupata kukubaliwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Ni kwa njia ya maelekezo au mwongozo Wake kwamba akili na uzoefu viliwekwa mkondo wake katika mwelekeo sahihi, wenye manufaa, na nafasi inayofaa, na kupanua njia ya msafiri kwa miguu. Vinginevyo, bila ya huo, akili na uzoefu vingegeuka kuwa ni mwanga mikononi mwa mwizi, au kipande cha ubapa mkali katika mkono wa mtu kichaa. Hiyo njia iliyonyooka ni uleule mpango wa kimaumbile uliokusudiwa, ambao umeandaliwa kulingana na makisio sahihi kabisa kuhusiana na vyanzo vilivyopo, mahitaji, na mapungufu ndani ya mipaka ya uwezekano wa asili kwa ajili ya mwanadamu. Ni njia iliyofunguliwa kuelekea kwa binadamu na Mitume wa Mwenyezi Mungu ambao wenyewe walikuwa ni watafutaji watangulizi na wasafiri kwa miguu juu ya njia hii. Njia hiyo, kama ikifuatwa na mwanadamu inaweza kulinganishwa kama mtiririko endelevu wa maji ulionyooshwa juu ya eneo laini na lililonyooka, ambalo kwa lenyewe na bila kuingiliwa kokote, bila ya kuonyesha ulazimishaji au nguvu, unatiririka kuelekea mwisho wa safari, ambao sio lolote bali ile bahari ya milele ya hali ya utukufu wa mwanadamu. Ni mpango ambao kama ungeweza kutekelezwa na kukamilishwa chini ya utawala adilifu kusimamia maisha ya watu, ungeleta uhuru, usalama, manufaa, ushirikiano, utoshelezaji binafsi, mapenzi undugu na utakomesha na kumaliza ajali zote mbaya na misiba 35

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 35

8/12/2015 6:35:12 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

yote iliyohusiana na binadamu katika maisha yao yaliyopita. Lakini njia hii na mpango huu unapaswa kuwa ni nini? Kila mmoja katika mtaa huu wa biashara ni mdai na kila kundi linalaumu jingine. Kwa hiyo ni lazima kuwe na ishara kwa mujibu wa utangulizi huu mfupi, kuhusiana na hii njia iliyonyooka, na kuieleza bayana kutoka kwenye mtazamo wa Qur’ani Tukufu.

َ ‫ين أَ ْن َع ْم‬ ‫ت َعلَ ْي ِه ْم‬ َ ‫ص َراطَ الَّ ِذ‬ ِ “Njia ya wale uliowaneemesha…..” (1:7)

Ni watu gani ambao walikuwa na uwezo wa kupokea zawadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu na walineemeshwa kwa fadhila maalum? Hakuna shaka kwamba hili halimaanishi mafanikio ya kimaada, cheo na mamlaka. Kwa sababu hivi ni vitu ambavyo vilikuwa vinamilikiwa na watu maarufu kabisa wa historia, ambao wakati huohuo walikuwa ni maadui wabaya wa Mwenyezi Mungu na wa watu pia. Kwa hiyo zile fadhila na rehema ambazo zilitamaniwa lazima ziwe ni jambo la ndani zaidi kuliko vivutio vya kidunia. Neema hiyo ni fadhila maalum, msaada na muongozo wa Mwenyezi Mungu. Neema ya utambuzi wa thamani halisi ya nafsi na kugundua tena ile nafsi ya ndani kabisa. Qur’ani Tukufu inaielezea neema hiyo maalum kama ifuatavyo:

‫ين أَ ْن َع َم‬ َ ‫ك َم َع الَّ ِذ‬ َ ِ‫َو َم ْن ي ُِط ِع للاهَّ َ َوال َّرسُو َل فَأُو ٰلَئ‬ ‫ين َوال ُّشهَ َدا ِء‬ ِّ ‫ِّين َوال‬ َ ِ‫ص ِّديق‬ َ ‫للاهَّ ُ َعلَ ْي ِه ْم ِم َن النَّبِي‬ ۚ ‫ين‬ َ ‫َوالصَّالِ ِح‬ 36

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 36

8/12/2015 6:35:12 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

“Na wenye kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume, basi hao (watakuwa) pamoja na wale aliowaneemesha Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii na wasadikishaji na mashahidi na watu wema…..” (Qur’ani 4:69).

Hivyo, mwenye kuswali katika aya hii anaomba mwongozo kuelekea kwenye ile njia ya Manabii, mawalii, mashahidi, na watu wema. Ile njia kuu ya historia yenye nuru, njia nyeupe yenye kuonekana yenye malengo yaliyofafanuliwa kikamilifu na yaliyo imara pamoja na watafiti mashuhuri na maarufu. Kinyume na hili, kuna njia nyingine iliyofafanuliwa vizuri na wasafiri wake wametambulishwa kwa ukamilifu. Kwa kuzingatia hili, mwenye kuswali anajionya mwenyewe asiifuate njia ile na katika kuendeleza kisomo chake cha awali, anasoma yafuatayo:

‫ب َعلَ ْي ِه ْم‬ ِ ‫َغي ِْر ْال َم ْغضُو‬ “…..Sio ya wale waliokasirikiwa…..” (Qur’ani 1:7)

Walikuwa ni watu gani walipokea ghadhabu ya Mwenyezi Mungu? Wale ambao waliamua kufuata njia minghairi ile ya Mwenyezi Mungu sio tu kwamba walichagua njia hii potofu, bali pia waliweza kuwaongoza, pamoja na wao wenyewe, kwa mabavu, kundi la watu wajinga, wasio na maamuzi na wavivu, na pia baadhi ya watu watambuzi na imara, lakini mikono yao ilikuwa imetiwa minyororo katika kutekwa, wafuate njia hiyo. Hawa walikuwa ndio watu, ambao wote katika historia walifanikiwa kudhibiti hali ya mambo ya ummah. Wakati mwingine ilipatikana kwa kutumia ukatili wa kinyama au wakati mwingine kwa kutumia hila mbaya, ufitini na ulaghai. Lengo lilikuwa ni kuwalazimisha watu kuwa kama viumbe wasio na maamuzi au 37

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 37

8/12/2015 6:35:12 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

kama zana tu iliyogandamizwa kwenye mikono ya wakandamizaji na madhalimu. Wale walikuwa ndio watu ambao, kwa kupitia njia za kupenda mno, walijiweka wenyewe juu ya umma wa watu na hivyo wakafanikiwa kumiliki rasilimali kwa ajili ya mambo yao maovu na machafu ya hisia kali za utafutaji starehe na anasa. Kwa maneno mengine, watu hawa walichagua njia ya uovu sio kwa sababu ya ujinga, bali waliasi huku wakijua, kwa ajili tu ya tamaa zao za ubinafsi na choyo. Hali halisi ya kihistoria inaonyesha kwamba malengo ya kidini wakati wote yalichukua hatua za mwanzo kuandamana dhidi ya matabaka ya juu yenye nguvu za kidunia na utajiri, na wakaikataa falsafa ya kuwepo kwao (kwa sababu kulikuwa kunagongana na malengo na madhumuni ya kidini). Mbali na makundi haya mawili – yaani lile lililopokea mwongozo wa Mwenyezi Mungu, na lile lililopatwa na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, kulikuwepo na kundi jingine la tatu, ambalo hatimaye lilifuata njia ileile iliyofuatwa na hili kundi la pili.4 Aya ya mwisho ya Sura Fatiha inalielezea kundi hili kama ifuatavyo:

‫ين‬ َ ِّ‫َو اَل الضَّال‬ “…..wala ya wale waliopotea.” (Qur’ani 1:7).

Wale ambao kwa sababu ya ujinga wao na kwa ushawishi wa viongozi waliopotoka, walichagua njia mbali na ile ya Mwenyezi Mungu na haki, lakini wakadhani kwamba wamechagua njia ya haki na iliyonyooka. Wakati kwa hali halisi wao walikuwa wanatembea 4

Maudhui hii imeelezwa kwa mtindo uliojaa maana katika matukio tofauti katika aya za Qur’ani Tukufu zifuatazo: Surat Shuaraa, aya ya 91 hadi 102; Surat Ibrahim, aya ya 2122; Surat Swad, aya ya 58-61, Surat Ghafiir, aya ya 47-48. 38

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 38

8/12/2015 6:35:12 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

juu ya njia hatari na yenye kupoteza, hatimaye kuwaongozea kwenye mwisho mchungu na uliojaa maangamizi. Hebu tuliangalie hili kundi lililotajwa hapo juu kwa kuangalia nyuma kihistoria. Hawa ndio watu ambao chini ya mifumo ya kipagani, wakiwa wamekunja mikono na kwa upofu, walijiachia wenyewe kabisa chini ya mamlaka ya viongozi wao wapotovu, waliokengeuka, na kwa ajili ya manufaa yao walisimama dhidi ya wajumbe wa Mwenyezi Mungu – watangazaji wa haki na uadilifu – hivyo kuharibu nafasi zao; na kwa kufanya hivyo, kamwe hawakujiruhusu wenyewe kutafakari japo kwa kitambo kidogo na kufikiri upya kuhusu vitendo vya kijinga.. Hivyo vitendo vyao hapo juu vinaweza kuitwa vya kukosa busara au vya kijinga, kwa sababu vilikuwa moja kwa moja ni kwa manufaa ya matabaka ya juu na kinyume chake ni hasara kwa wale waliokengeuka; kinyume tu na ulingano wa Manabii watukufu, ambao ulikuwa wenye manufaa na faida kwa wale watu walionyimwa ikijumlisha na hawa waliokengeuka, ambapo wakati huohuo uling’oa uwepo, na hadhi ya wale watu wanaochukiza kutoka kwenye mizizi. Mwenye kuswali kwa kukumbuka mielekeo na njia mbili zinazotofautiana (yaani njia ya walioongozwa na njia ya wale wanaochukiza) lazima apekue ndani ya nafsi yake ya ndani kabisa, na aamue kwa uangalifu,usahihi na kwa hisia za utambuzi ile njia ambayo ni lazima aifuate na msimamo ambao unapaswa kuchukuliwa na yeye kwenye ujumbe unaookoa maisha ya Manabii wa Mwenyezi Mungu. Hivyo katika wakati huo, kwa kushuhudia ishara za ukomaavu na muongozo (wa Mwenyezi Mungu) katika maisha yake mwenyewe, kwa mara nyingine tena anafungua ulimi wake kwa ajili ya kutoa asante na shukurani kwa neema kubwa ya Mwenyezi Mungu kwa kusema (mwishoni mwa Sura al-Fatiha) kama ifuatavyo: 39

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 39

8/12/2015 6:35:12 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

‫ين‬ َ ‫ْال َح ْم ُد لِهَّلِ َربِّ ْال َعالَ ِم‬ “Sifa njema (zote) ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa viumbe (vyote).” (Qur’ani 1:2).5

Na kwa njia hii huwa anakamilisha kipande muhimu cha swala yake. Huu ulikuwa ndio utangulizi wa Qur’ani Tukufu (ambao ulisomwa) na unaitwa pia kama Fatihatul-Kitab, kifunguzi cha Kitabu. Utangulizi wa Qur’ani Tukufu kama utangulizi wa kila kitabu unaashiria asili ya jumla ya yaliyomo yote ya Maandiko hayo Matakatifu. Kwa kuwa swala ni mukhtasari au picha ya kutazama kutoka juu ya Uislamu, na inawakilisha mingi ya mipaka au mawanda ya itikadi ya Kiislamu; hali kadhalika Sura ya “Kifunguzi” inaorodhesha zile nukta muhimu na muelekeo halisi wa elimu ya Qur’ani na kwa kifupi ina mukhtasari wa miongozo muhimu kwa namna ifuatayo: Ulimwengu na viumbe vyote au spishi ni kitu kimoja pekee – vyote kabisa vimeumbwa na Mwenyezi Mungu – “Mola wa walimwengu wote. Kila mmoja na kila kitu kipo chini ya upole na upendo wa Mwenyezi Mungu. Lakini waumini wameneemeshwa kwa fadhila maalum na huruma za Mwenyezi Mungu – Mwingi wa rehema na Mwenye kurehemu.” Maisha ya mwanadamu baada ya dunia hii yanaendelea na kuwepo katika akhera, ambako mamlaka yote kabisa ni ya Mwenyezi Mungu – “Mmiliki wa Siku ya Malipo.” Mwanadamu anapaswa kujikomboa mwenyewe kutoka kwenye utumwa wa mwingine mbali na wa Mwenyezi Mungu. Anapaswa kujitahidi kuishi chini ya kivuli cha mpango wa Mwenyezi Mungu kwa dhamira na maadili mema ya kibinadamu, juu ya njia hiyo kwa uhuru na heshima na atake kupata 5

Kuisoma aya hii mwishoni ni kwa hiari. 40

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 40

8/12/2015 6:35:12 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

msaada kutoka Kwake tu basi – “Wewe tu tunakuabudu na Wewe tu tunakuomba msaada.” Mwanadamu lazima atafute mpango kwa ajili ya ustawi na mafanikio kwa kutembea juu ya njia iliyonyooka ya maisha itokayo kwa Mwenyezi Mungu - “Tuongoze njia iliyonyooka.” Lazima azitambue safu za mbele za maadui na marafiki pia. Awe na utambuzi kuhusu maoni yao na nafasi zao. Achukue uchaguzi angalifu kuhusu njia yake mwenyewe – yaani “Njia ya wale ulio-

waneemesha. Sio ya wale waliokasirikiwa wala ya wale waliopotea.”

41

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 41

8/12/2015 6:35:12 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

MLANGO WA TATU Sura al-Ikhlaas (Uaminifu)

B

aada ya kuisoma Sura “Alhamdu” ambayo imejaa elimu na maana za kina kabisa – mwenye kuswali lazima asome sura moja nyingine nzima kutoka kwenye Qur’ani Tukufu. Hii inachangamsha kumbukumbu yake kwa ajili ya sehemu ya maandiko matukufu yaliyochaguliwa kwa uamuzi na hiari yake mwenyewe, au kwa maneno mengine inafungua sura nyingine ya elimu ya Kiislamu mbele yake.

Wajibu wa kusoma Qur’ani Tukufu wakati wa swala umeelezewa katika hadithi na Imam Ali ibn Musa ar-Ridhaa . Imam alimwambia Fadhl bin Shazan kwamba ule usomaji wa Sura za Qur’ani Tukufu wakati wa swala umekikinga Kitabu Kitukufu hicho kutokana na kutelekezwa, kutozingatiwa na kumeyaweka hai maudhui yake kwenye mawazo na akili. Katika mazungumzo yetu itatosha kuzungumzia Sura al-Ikhlaas6 ambayo kwa kawaida inasomwa katika swala baada ya kusoma Sura al-Fatihah.

‫َّح ِيم‬ ِ ‫بِس ِْم للاهَّ ِ الرَّحْ ٰ َم ِن الر‬ 6

Al-Ikhlaas “ ” ambayo pia inajulikana kama “al-Tawhiid” inachukua jina kutokana na maudhui yake. Imeitwa vilevile msingi wa Qur’ani Tukufu. Baadhi ya vyanzo vinaihusisha Surah hii kushuka katika kipindi cha Madina, na wanadhani kwamba ilipokelewa katika kujibu swali la baadhi ya waganga wa Kiyahudi kutokana na asili ya Mwenyezi Mungu. Kwa jumla inachukuliwa kama ni katika Surah za mwanzoni kabisa za Makkah. (Tr.) 42

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 42

8/12/2015 6:35:12 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

”‫“قُل‬ “Sema (Ewe Mtume)”

Lijue hili wewe mwenyewe na ni lazima ufikishe ujumbe huu kwa watu wengine kwamba:

”‫“هُ َو هللا أ َح ٌد‬ “Yeye Mwenyezi Mungu ni wa Pekee”

Tofauti na miungu wa itikadi potofu za dini nyingine, Yeye hana washirika wala wapinzani, au walio sawa na Yeye. Ina maana maumbile yako huru kutokana na mgogoro baina ya miungu tofauti. Bali desturi na sharia zote za ulimwengu zinatokana na chanzo kimoja cha nguvu ya nje, kwa uamuzi mmoja. Ni kwa sababu ya nguvu hii kwamba nidhamu iliyoratibiwa na yenye ulinganifu inadumishwa kote ulimwenguni. Sheria zote na mabadiliko na usogevu wa asili wa ulimwengu vyote vinakwenda kuelekea upande mmoja kuelekea kwenye lengo moja. Miongoni mwa viumbe wote ni mwanadamu tu ndiye aliyepewa uwezo wa kuamua na haki ya kuazimia. Ana uwezo wa kutotii nidhamu hii tukufu, na anaweza akapiga muziki, kwa mgongano na kutoratibiwa na zana nyingine za kimuziki, au anaweza kuimba wimbo kama muimbaji mpweke. Vile vile anao uwezo wa kuchagua kuishi maisha yake kwa mujibu wa amri hizi tukufu za Mungu.

43

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 43

8/12/2015 6:35:12 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

َّ ‫للاهَّ ُ ال‬ ‫ص َم ُد‬ “Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kukusudiwa kwa haja.”

Mwenyezi Mungu yu huru, hahitajii kutoka kwa yoyote au kwa chochote. Mwenyezi Mungu ambaye tunamuabudu, tunamtukuza na tunayemheshimu sio kama hao miungu wa kubuniwa ambao kuumbwa kwao, kuendelea kwa maisha yao, nguvu na kuishi kunahitajia msaada, kuungwa mkono na upendeleo wa mtu mwingine. Mungu kama huyo ni sawa na binadamu au mnyenyekevu zaidi au chini kidogo. Mwanadamu – huyu kiumbe mwenye fahari ya kina – atasalimu amri mwenyewe, na ataabudu na kutukuza mamlaka kuu tu, ambayo haihitajii haja yoyote kutoka kwenye chanzo au kitu chochote. Dhati Yake ilikuwepo, yenye nguvu, na ya milele, vyote vinategemea juu ya asili Yake Mwenyewe.

‫لَ ْم يَلِ ْد‬ “Hakuzaa…..”

Sio hivyo! kwa namna ilivyodhaniwa kiajabu ajabu miongoni mwa dini zilizopotoka au itikadi za kishirikina. Yeye swt., hayuko kama mungu (wa kubuniwa) wa Wakristo na washirikina ambaye anaweza kuwa baba au mwana. Yeye ni Mmoja, ambaye anaumba kila kitu na kila mtu – na wala sio baba yao. Viumbe wote hawa wa ulimwengu (viwe vya kimbinguni au vya kidunia) ni watumwa Wake – na sio watoto Wake, wa kike au wa kiume. Ni kwa sababu ya uhusiano huu maalum (utumwa dhidi ya utakatifu) kati ya Mwenyezi Mungu na mwanadamu, ambao unawakomboa waja Wake wa kweli kutokana na utumwa wa kila kitu na wa kila mtu. Kwa sababu mtumwa kwa wakati mmoja hawezi akamilikiwa na mabwana wawili. 44

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 44

8/12/2015 6:35:12 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

Wale waliomdhania Mwenyezi Mungu kama namna ya baba wa mwanadamu na viumbe vingine na hawakufikiria ule uhusiano (mtumwa dhidi ya utukufu) kati ya mwanadamu na Mwenyezi Mungu kama ni jambo lenye thamani ya kutosha kwa nafasi ya utukufu wa mwanadamu, kwa uhalisia wamejifungulia wenyewe mlango kwa ajili ya utumwa kwa mwingine asiyekuwa Mungu, na kwa kufanya hivyo, wanakuwa watumwa wa wamiliki watumwa wengi wa dunia hii wasio na huruma, kwa kugeuka kuwa zana za mkono na mali ya wamiliki-watumwa na wazalishaji watumwa.

‫َولَ ْم يُولَ ْد‬ “…..wala hakuzaliwa.”

Yeye sio kitu ambacho hakikuwepo siku moja, na ambacho kitakuja kuwa chenye kuonekana katika huu ulimwengu wa uhai siku inayofuatia. Yeye hakuzaliwa kimwili na mtu yoyote yule wala sio matokeo ya ziada ya mawazo au dhana za mtu. Wala Yeye hakutengenezwa na nguvu kuu ya kijeshi ama tabaka la juu, wala hafanani na muundo wowote wa uhai wa mwanadamu. Yeye Ndiye Mamlaka Kuu na uhalisia unaotukuzwa mno na Mmoja wa milele, ambaye alikuwepo kabla na atakuwepo daima milele.

‫َولَ ْم يَ ُك ْن لَهُ ُكفُ ًوا أَ َح ٌد‬ “Wala hana anayefanana naye hata mmoja.”

Hawezi kufananishwa na yeyote au chochote na hakuna anayeweza kupatikana kuwa kama mpinzani Wake au wa kulingana Naye. Haiwezekani kugawanya miliki ya uwezo au ufalme Wake, 45

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 45

8/12/2015 6:35:12 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

ambao unajumuisha ulimwengu wote, kati Yake na mtu mwingine yoyote, yaani kuchukulia kwamba sehemu ya dunia au sehemu ya maisha ya mwanadamu ni ya Mwenyezi Mungu na inayobakia ni ya mtu mwingine mbali na Yeye. Au kugawa sehemu ya ulimwengu na hatua ya maisha ya binadamu kati Yake na wengineo, kati ya miungu ya walio hai na miungu ya wafu; au kuzigawa kwa wadai bandia wa umungu na mamlaka. Kama jina linavyoashiria, Surah hii kwa uhalisia wake ni Surah ya tawhid, upweke wa Mwenyezi Mungu. Falsafa ya tawhid, ambayo imeelezewa kwa namna nyingi na mitindo tofauti, katika mamia ya Surah ndani ya Qur’ani yote; katika Surah hii, imewasilishwa katika muundo ufupisho finyu na utaratibu wa dhahiri kabisa usio na shaka ambao unapuuza na kuweka pembeni ile fikra ya ajabu na ya kishirikina iliyokuwapo wakati ule, kuwakataa na kuwakanusha waziwazi wote wenye kudai uungu wa bandia – kwa mara ya mwisho katika maandiko ya Kitabu kitakatifu. Surah hii inatambulisha sifa za Mwenyezi Mungu ambazo kwa mtazamo wa Uislamu anastahiki kutukuzwa na kuabudiwa, sio tu na Waislamu, bali pia na binadamu wote wanaoishi katika ufalme Wake. Mungu ambaye sio wa kipekee, na mamia ya maelfu ya wenzie anaofanana nao wako wengi sana miongoni mwa wanadamu hastahili utukufu wala uungu. Mtu mwenye nguvu, au chanzo cha nguvu, kinachohitajia msaada na uungwaji mkono na vyanzo vingine kwa ajili ya kudumu kwake, huyo hastahili, na hapaswi kuwekwa kwa kulazimishwa juu ya binadamu. Yule anayeinamisha kichwa chake mbele ya mungu kikaragosi, kiumbe kilichoumbwa, chenye kuhitajia, na mwenye kufanya makosa, kwa hakika ameaibisha na kushusha hadhi ya ubinadamu, na amekwenda hatua moja kurudi nyuma. Hiki ndio kipimo chanya cha uhakika cha Sura ya Tawhid (au Ikhlaas), ambayo inaashiria na kupambanua sifa za Mola wa 46

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 46

8/12/2015 6:35:13 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

ulimwengu, na wakati huohuo inakanusha uwepo wa miungu vikaragosi mwote katika historia. Kwa upande mwingine Surah hii inawaonya wale wenye kuabudu Mungu Mmoja na waumini wa Kiislamu wasiwe wadadisi na wenye kujiendekeza kwenye midahalo ya kiakili na kimantiki kuhusu sifa za Mwenyezi Mungu na asili, ambayo itawaingiza kwenye shaka na vishawishi vya kiovu, bali wanapaswa kumtafuta Mwenyezi Mungu na kumkumbuka kwa maneno mafupi ili kuwaondosha hawa wadai uungu wa bandia na kuwatoa kwenye maongezi yao yasiyo na msingi. Badala ya kunasa kwenye mtengo wa mkanganyo wa kifalsafa wanapaswa kutafakari juu ya wajibu unaojitokeza kwenye itikadi na imani ya kitawhid. Kwa mujibu wa hadithi iliyosimuliwa na Imam Ali ibn al-Husein, Zaynul-Abidin , kwa vile Mwenyezi Mungu alikuwa anatambua kwamba kipindi cha baadaye cha historia kitazalisha watu wenye udadisi, na kwa hiyo alishusha aya za Sura al-Hadid7 mpaka aya ya “…..Yeye ni mwenye kuyajua yaliyomo vifuani,” ili kuelezea mipaka kwa ajili ya uchunguzaji wa asili na sifa Zake. Kwa hiyo yeyote aliyejipa uhuru wa kutafakari nje ya mipaka hii iliyowekwa ana uhakika wa kuangamia. Kana kwamba Surah hii: “Sema Mwenyezi Mungu ni Mmoja,” inamwambia mwenye kuswali kwamba: Mwenyezi Mungu ni Nguvu Kuu ya kipekee, Aliye Juu Kabisa, asiyehitajia, Dhati Yake iko nje ya kuweza kuelezwa, kamwe hakuzaa wala hakuzaliwa, na hakuna yeyote anayefanana Naye au aliye sawa Naye. Mwenye ujuzi, Anayeona, Mwenye hekima…….na kadhalika, na sifa nyingine za Dhati ya Mwenyezi Mungu ambaye elimu na kumtambua kwake ni wajibu juu ya Waislamu, ambazo zinachukuliwa kama ni zenye uwezo na nguvu katika kutengeneza maisha yao, na kupanda 7

Al-Hadid; 57:1-6 47

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 47

8/12/2015 6:35:13 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

kwa ari zao, zimerudiwa katika Surah nyinginezo za Qur’ani Tukufu. Usifikiri kuvuka mipaka kama ilivyokwisha kuelezwa katika Surah hii kuhusu Dhati ya Mwenyezi Mungu na ujuzi kuhusu sifa Zake. Badala yake mkazo unapaswa uwe unatiliwa nguvu kwenye utekelezaji wa vitendo ambavyo hatimaye vitamtaalimisha muumini katika kumjua Mwenyezi Mungu vizuri zaidi. Usidhani kwamba kwa kujiingiza kwenye midahalo mirefu ya kiakili kuhusu asili Yake ndio utapata maalumati zaidi. Laa, sivyo hivyo! Badala yake jaribu kupata ujuzi huo unaohitajika kwa kuleta utakaso na uchamungu zaidi kwenye nafsi yako ya ndani kabisa, na kwa kujizoesha kanuni za tawhidi katika matendo yako na amali zako, na hiyo ndio sunna ya Manabii, mawalii na waja wema wa Mwenyezi Mungu, wanatawhid wa kweli na wana-Irfaan waliyokuwa nayo.

48

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 48

8/12/2015 6:35:13 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

MLANGO WA NNE Tasbihi Nne (Tasbihatul-Arba)

K

abla ya kuzungumzia hizi nyuradi na sifa maalum zinazosomwa wakati wa kurukuu na kusujudu, tutazungumzia vifungu vinavyosomwa katika rakaa ya tatu na ya nne kwenye swala katika hali ya kisimamo (Itidal). Vifungu hivi vinakuwa na usomaji wa dhikiri nne zenye kuelezea uhalisia, namna nne kuhusu Mwenyezi Mungu:

َ ِ‫سبحـان هللا‬ Subhanallah “Utakatifu ni wa Mungu”

‫َوال َح ْمدهلل‬ Wal hamdu lillahi “Na Sifa njema ni ya Mwenyezi Mungu.”

‫َوالَإلهَ إالّ هللا‬ “Wala ilaha ilallahu” “Wala hakuna mungu ila Allah”

‫َوهللا اَ ْكبَ ُر‬ “Wallahu Akbar.” “Na Mwenyezi Mungu ni Mkuu.” 49

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 49

8/12/2015 6:35:13 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

Utambuzi kuhusu sifa tukufu hizo nne hapo juu unasaidia sana, na una athari kubwa kabisa kuhusu uelewa sahihi na kamilifu wa tawhid, kwa sababu kila moja kati ya hizo inaashiria umbo moja na picha moja la muundo wa tawhid. Madhumuni ya kurudia mistari hiyo ya sifa sio tu kuongeza ufahamu wa kiakili tu, au elimu, bali uelewa wa sifa tukufu hizi na muendelezo wa kuzirudia kwake kunazalisha hali ya uwajibikaji, ambapo mtu anaweza kutekeleza wajibu na majukumu yote kwa umuhimu wa ukweli halisia anaougundua yeye. Kwa jumla, mbali na mipaka ya kiakili, itikadi za Kiislamu zinapaswa kutoa hamasa kwa ajili ya vitendo katika maisha halisi. Kwa sababu bila ya kujali mpanuko wake wa nadharia ya kiakili, zinathibitishwa katika Uislamu kwa kutekeleza wajibu muhimu kabisa katika kusimamia maisha ya wanadamu katika vitendo vya kijamii vya mtu mmoja mmoja na vilevile vya pamoja vya jamii husika. Ni kweli kwamba kila itikadi au imani ya Kiislamu ina maana ya utambuzi wa ukweli fulani, lakini ni zile itikadi tu za Kiislamu ambazo katika hali ya kuzikubali kwake na kuzishika kunaweza kuanzisha dhima juu ya mtu kwa kumwekea jukumu la nyongeza ndio zinazofanywa ni lazima. Hiyo ndio namna ambavyo uwepo wa Mwenyezi Mungu unapaswa kuwa. Uwepo wa Mwenyezi Mungu au kutokuwepo, kila moja katika njia maalum inaleta fursa mpya kwa ajili ya utendaji katika maisha. Mtu binafsi au jamii ikiwa kwa kweli wanaamini juu ya uwepo wa Mwenyezi Mungu huwa wanaishi maisha yao katika namna maalum kuliko wale ambao wanaukanusha ukweli huu. Kama mtu aliamini kwamba yeye pamoja na ulimwengu huu wameumbwa na chanzo chenye uwezo mkubwa ulioegemea kwenye hekima na elimu Yake, basi hana hiari bali kukubali kwamba uumbwaji huu una madhumuni fulani na lengo la hali ya juu kabisa. Hivyo 50

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 50

8/12/2015 6:35:13 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

anatambua kwamba yeye pia anao wajibu mkubwa wa kufanya, na anapaswa kutwaa majukumu fulani, kwa ajili ya kutimiza lengo hilo. Utambuzi huu wa dhima na wajibu unamhamasisha yeye kujitahidi kwa kukubali mzigo wa juu zaidi, na kwa kufanya hivyo huwa anajihisi mwenye furaha na kuridhika. Kadhalika imani juu ya ufufuo, utume, na uongozi wa Maimam Ma’sumin (Wilayat…..) na kadhalika, kila moja inabeba dhima na inabebesha mzigo wa jukumu kubwa mabegani mwa muumini, na kwa ujumla, hiyo njia, mpango na mwelekeo wa jumla wa maisha vinafanywa kuonekana tofauti kwa ajili yake. Kama kwa nje inaonekana kwamba wale wanaoamini kanuni hizi za kiitikadi, na wale ambao hawajui kabisa au hawaamini kabisa, wanaishi maisha ya kufanana na yaleyale bila ya tatizo hata kidogo au mgogoro, hiyo ni kwa sababu ya ukweli kwamba hili kundi la mwanzo linakosa uelewa sahihi, kiwango chao cha imani sio thabiti, na hawaamini kwa namna inavyopaswa kuamini. Katika nyakati nyeti na katika hatua muhimu za maisha, njia ya waumini wa kweli inajitenga na ile ya wafuasi wasiojua kitu, wanatafuta maslahi binafsi na waumini bandia. Kwa kuzingatia haya akilini tunarudi kuzungumzia maana na maudhui ya hizo Sifa Nne (Tasbihatul-Arba) zilizotajwa hapo juu kama ifuatavyo:

‫ان هللا‬ َ ‫ُس ْب َح‬ Subhanallah “Utakatifu ni wa Mungu”

Mwenyezi Mungu ni Mtakatifu, aliye huru kutokana na mshirika yeyote, huru kutokana na dhulma au ukandamizaji, kutokana na kuwa ameumbwa, kutokana na kufanya mambo kinyume na hikma, 51

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 51

8/12/2015 6:35:13 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

huru kutokana na mapungufu na dosari, na huru kutokana na uchafu wote uliopo miongoni mwa viumbe vilivyoumbwa na sifa zote zinazohusiana navyo. Kwa kukisoma kifungu hiki, mwenye kuswali anaelewa na kujikumbusha mwenyewe kwamba ni kwa aina gani ya mamlaka makubwa na matakatifu – yenye kustahiki kutukuzwa – ambayo amenyenyekea kwayo na kusujudu. Anatambua kwamba amejinyenyekeza mbele ya nguvu ambayo ni chanzo cha uadilifu na ukamilifu halisi. Hivi inawezekana mtu ambaye ameheshimu chanzo cha ukamilifu halisi wa wema wote, uadilifu na ubora, kwamba anaweza kuhisi utovu wa adabu juu ya chanzo hicho? Hivi ndivyo ambavyo swala ya Kiislamu inavyotakiwa kuwa. Ni kuonyesha unyenyekevu na heshima mbele ya dhati ambayo ni kama bahari kubwa mno ya ukamilifu, wema na dalili. Sio unyenyekevu ambao utamfanya mtu asikitike, au utashusha kiwango cha hadhi na heshima yake – huu hautamfanya adharaulike au kufedheheka. Je mwanadamu anaweza kuelezewa kama ni kitu mbali na mtafutaji na mridhiaji wa uzuri halisi na ukamilifu hasa. Kwa hiyo ni jambo la kawaida tu kwamba mwanadamu lazima aweke paji lake la uso juu ya udongo mbele ya chanzo kama hicho cha ukamilifu halisi, na lazima atukuze na kuabudu dhati hiyo kwa uwepo wake wote. Utukuzaji huu na ibada hii vinamuongoza yeye kuelekea kwenye njia ya wema, ubora na ukamilifu, na yeye kwa hiyo anapanga harakati za maisha yake katika mwelekeo wa upande huo. Wale waliodhania swala na ibada za Kiislamu kwamba zinahusika juu ya kufedheheka na ufukara wa mwanadamu, na wakazilinganisha na utukuzaji wa vyanzo vya mamlaka ya kimaada, kwa bahati mbaya wao hawakutambua na kuelewa hii nukta nyeti: kutukuza na kupenda sana wema na utakatifu kwa zenyewe tu ndio hamasa zenye nguvu sana kwa ajili ya kupata sifa hizi ndani ya mwenye kuswali, 52

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 52

8/12/2015 6:35:13 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

kwa hiyo, kule kusoma “utukufu ni wa Mwenyezi Mungu” kunatukumbusha sisi kuhusu sifa na ubora huu katika maisha yetu vilevile.

‫َوال َح ْم ُد ل‬ “Wal hamdu lillahi.” “Na Sifa njema ni ya Mwenyezi Mungu.”

Mwote katika historia ya mwanadamu ya kusikitisha, mwanadamu kwa sababu ya kupata fursa ndogo ama kubwa, kwa ajili ya kuishi siku chache za ziada, na katika masuala mengi ni kwa ajili tu ya kuishi kutoka mkononi hadi kinywani, ameuruhusu ulimi wake kwa ajili ya kutukuza na kujisalimisha mwenyewe kwa unyenyekevu mbele ya wale ambao walikuwa hasa ni sawa na yeye, na kwa namna yoyote ile hawakuwa ni wamiliki wa ubora au heshima juu yake. Kwa sababu mwanadamu alidhania kwamba neema kwa hakika zilikuwa ni miliki ya watumiaji wa neema hizo. Katika kutafuta utajiri na mali hizi, yeye amekubali kuwa mtumwa wa wamiliki wa vitu hivyo, ima iwe kimwili au kiroho au katika muundo wa kiakili. Ukumbusho wa kwamba shukurani zote ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu tu (na sio kwa ajili ya mwingine yeyote yule) unatufanya tuelewe kwamba neema zote (utajiri, uwezo, zawadi, upendeleo na tuzo) vyote hivi vinatoka Kwake Yeye. Hivyo, kwa uhalisia, hakuna mwingine mbali na Mwenyezi Mungu ambaye ndiye mmiliki wa vitu ambavyo vitamuidhinisha yeye kumfanya mwanadamu mwenzie kuwa mtumwa. Kwa hiyo inatoa fundisho hata kwa wale ambao ni wenye nia dhaifu, na ambao nyoyo zao na macho yao yanashawishika kwa ajili ya utajiri na fadhila, wasitilie umuhimu kwenye fadhila zisizo na 53

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 53

8/12/2015 6:35:13 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

maana na milki zinazotolewa na wenye kushikilia mamlaka ya kidunia, vyeo na mali. Wasifikirie vitu hivi vinavyozawadiwa na wao, bali kile chanzo cha neema na fadhila au tuzo mbalimbali, wasivumilie kunyimwa ama ukosaji kwa ajili ya mahitaji haya halisi, na mnapaswa kuwaona wenye kuhodhi neema hizi kama wanyang’anyi au wavamizi.

‫َوالَإلهَ إالّ هللا‬ “Wala ilaha ilallahu” “Wala hakuna mungu ila Allah”

Huu ni wito wa Uislamu – wito ambao kwa uwazi na dhahiri kabisa unaakisi kwa ujumla falsafa ya maisha na ya kiitikadi Kiislamu – unakuwa na kanusho moja na uthibitisho mmoja. Kwanza kabisa unakanusha miungu yote ya bandia, au mamlaka nyinginezo mbali na ya Mwenyezi Mungu. Unamuweka huru kila mmoja kutokana na dhamira ya utumwa wa mamlaka zote za kishetani na unakata kila mkono na bega linalojaribu kumvuta kwa hila tofauti kuelekea kwenye njia upotofu. Unamuweka mtu mbali na vyanzo na mifumo ya mamlaka mbali na ile ya Mwenyezi Mungu na kutokana na hamasa yoyote mbali na ile iliyounganishwa na Yeye. Kwa mkanusho huu mkubwa, yeye anajiweka huru kutokana na aina zote za fedheha, udhalili, ufukara na utumwa wa aina mbalimbali. Halafu anairuhusu nafsi yake ya ndani kabisa kutawaliwa kwa mujibu wa ridhaa ya Mwenyezi Mungu na amri Zake, ambazo bila shaka zinaweza kuhisiwa na kutekelezwa chini ya utawala Wake katika jamii ya Kiislamu yenye maadili mema. Kukubali kama huku na utumwa mbele ya Mwenyezi Mungu haulinganishiki na aina nyingineyo ya utumwa. 54

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 54

8/12/2015 6:35:13 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

Utumwa kwa Mwenyezi Mungu maana yake ni mtu kupanga maisha yake kwa mpangilio wa kimantiki kwa mujibu wa hekima yake na kuishi chini ya utawala Wake katika jamii ya kimaadili ya Kiislamu, ambayo uelekeo wake halisi umefikiwa kwa mujibu wa amri za Mwenyezi Mungu na pia kujitahidi kwa nguvu na uwezo alionao mtu kwa ajili ya utekelezaji wa utawala wa Mwenyezi Mungu mkamilifu kama huu. Kwa vile mifumo mingine iliyoundwa kwa fikra ya kiakili ya wanadamu, haiko huru kutokana na mambo kama ujinga wa kibinadamu, ukosefu wa elimu, hali ya upotofu na hasa hasa kwa sababu za ubinafsi; haiwezi kumsaidia mwanadamu katika kufanikiwa na kujiongoza mwenyewe kuelekea kwenye ukamilifu unaotakikana. Ni utawala wa Mwenyezi Mungu pekee na Jamii ya Kiislamu, iliyobarikiwa kwa hekima tukufu na majaaliwa ambao umepangiliwa kulingana na haja na mahitaji ya mwanadamu, ndio unaoweza kutoa mazingira yanayofaa na yenye kutumainiwa kwa ajili ya ukuaji wa huo uumbaji maalum unaoitwa “mwanadamu.” “Sisi sio maadui wa mifumo mingine, bali sisi ni wenye kuwahurumia wao;” haya ni maneno ya Mitume wa Mwenyezi Mungu ambao ndio watu wenye kujali na wenye huruma ya kibaba kimalezi kwa ajili ya wanadamu. Wao wanawafundisha wajenzi na wasanifu wa majengo ya makazi ya kukaliwa na binadamu, au kwa maneno mengine, wanatoa mafunzo kwa viongozi na waasisi wa mifumo ya kijamii kwamba: “Mwanadamu hajafanikiwa kamwe, na wala hatakuja kufanikiwa au kufanikisha matakwa yake katika muundo wowote wa utawala isipokuwa wa Mungu Mmoja – mfumo wa Tawhid unaosimamiwa na Mwenyezi Mungu Mwenyewe.” Historia imethibitisha, na sisi tumeshuhudia kwamba katika utawala usio wa

55

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 55

8/12/2015 6:35:13 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

kimungu,8 ni jinsi gani mwanadamu ameteseka na ni mbaya za kutisha na duni kiasi gani zilivyokuwa hali za binadamu chini ya tawala zao kandamizi.

‫َوهللا اَ ْكبَ ُر‬ “Wallahu Akbar.” “Na Mwenyezi Mungu ni Mkuu.”

Baada ya kuwakana miungu wote wa bandia, mtu wa kawaida akiwa bado anatatanishwa na mielekeo ya kipagani, huwa anajihisi upweke, mgeni na mwenye hofu. Kwa upande mmoja anashuhudia kuporomoka kwa ghafla kwa miundombinu yote ya kipagani yenye nguvu, ambayo ilikuwa imara hadi wakati huu hasa, na kwa upande mwingine, upagani kama kilele madhubuti cha mlima unajitokeza wenyewe kama mbadala unaowezekana, na unajaribu kila uwezavyo kukamata mazingatio na nadharia yake. Mambo yaleyale ambayo ameyakanusha na kuyakataa yanaonyesha uwepo wake mbele ya macho yake na kumfanya awe mwenye hofu. Ni kufikia hapa hasa ambapo kwamba anatamka: “Mungu ni Mkuu,” Mkuu na Mkubwa kuliko yeyote au chochote, Mkuu kuliko mamlaka zote na udhihirisho wao na Yeye yuko mbali na maelezo. 8

Kwa sasa hivi tunashuhudia kipindi cha kuvutia sana cha historia wakati mpango wa dunia ukiwa unabadilika kwa haraka sana. Mpango wa kiuchumi wa kikomunisti ambao ulitenda aina mbaya sana za udhalimu na kuuwa mamilioni ya watu, na wakati fulani ulitangazwa kama itikadi ya kimapinduzi yenye nguvu sana, ghafla ikapotea kutoka kwenye mandhari ya dunia. Walitoa miito bora na wakafanikiwa katika kutia kasumba na kughilibu mamilioni ya vijana duniani kote. Kama Qur’ani Tukufu inavyoelezea kuanguka kwa Firauni mwenye maguvu, kwamba hakuna jicho katika ulimwengu mzima lililomwaga machozi kwa kufa maji kwa Firauni huyo mwenye nguvu, katika zama zetu, kadhalika hali ilikuwa hivyo kwa kuanguka kwa Urusi yenye nguvu. Katika kutoweka kwake, kuna somo kwa binadamu kwamba mbali na mfumo wa Mwenyezi Mungu ambao ni madhubuti, mifumo mingine yote ni dhaifu kama nyumba ya buibui. (Tr. – mfasiri kwenye Kiingereza) 56

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 56

8/12/2015 6:35:13 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

Yeye Ndiye msanifu na muumba wa taratibu zote za kimaumbile asili na kihistoria, na sharia tukufu za uumbaji wa ulimwengu huu. Hivyo, ushindi wa juu kabisa umo katika mchukuano na sharia hizi za kimungu na hadithi, na unaweza kupatikana tu kwa kujizatiti katika amri za Mwenyezi Mungu. Ni waja wema wa Mwenyezi Mungu tu ndio waliokuwa kundi la ushindi mwote katika mapambano ya kihistoria ya mwanadamu. Mtukufu Mtume  alifahamu na kuamini uhalisia wake wa kihistoria kwa usahihi kabisa, na aliuhisi na kuuzoea kwa nguvu zake zote za uhai wake. Ilikuwa ni kwa sababu kwamba yeye alisimama peke yake na sio tu dhidi ya watu wote waliopotoka wa mjini Makka, bali alipingana na ulimwengu mzima. Na kama ilivyokuwa ikitarajiwa kwa uhalisi kutoka kwa mtu mtukufu kama huyu, alipinga na akabakia imara kwa kiasi kwamba alikuwa na uwezo wa kuukomboa msafara potofu wa mwanadamu kutoka kwenye utumwa wa mamlaka bandia za kidunia, na akauelekeza kwenye njia yake ya asili – njia ya ukamilifu na utukufu wa mwanadamu. Mtu ambaye anajiona kama ni dhaifu, asiyejiamini, na asiye na maamuzi dhidi ya wenye mamlaka ya kidunia, kama ataweza kutambua kwamba mamlaka kuu ni ya Mwenyezi Mungu, huwa anapata kutulia, kuwa na uhakika, na anagundua muwako wa aina ya moto usio na mfano ndani ya uhai wake, ukimbadili kuwa mtu mashuhuri sana na mwenye nguvu na uwezo papo kwa papo. Huu ulikuwa ni mukhtasari wa yale yaliyomo katika maudhi ya sentensi hizo zinazosomwa katika hali ya kisimamo wakati wa rakaa ya tatu na ya nne katika swala.

57

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 57

8/12/2015 6:35:13 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

MLANGO WA TANO Rukuu (Kuinama, hali ya kushika ­magoti)

B

aada ya kuwa umesoma aya za Qur’ani Tukufu (katika rakaa ya kwanza na pili) au zile sifa nne (Tasbihatul-Arba’a) (katika rakaa ya tatu au ya nne), katika hali ya kisimamo, mwenye kuswali anaingia katika hali ya kurukuu – yaani anainamisha kichwa huku ameshika magoti, kwa heshima kwa Mwenyezi Mungu – ambaye uwepo Wake ndio kilele cha ubora wote mkubwa, uliotukuka na wa kiadilifu, ambao unaweza kutamaniwa na kufanywa ndio lengo na mwanadamu. Kurukuu kunaakisi unyenyekevu wa mwanadamu mbele ya nguvu, ambayo anaiona kuwa ni kuu na bora zaidi kuliko yeye mwenyewe. Kwa sababu Mwislamu anamuona Mwenyezi Mungu kuwa ndio nguvu na mamlaka kuu zaidi, huwa anarukuu mbele Yake, na kwa vile hamfikirii yeyote mbali na Mwenyezi Mungu kuwa mbora kwake, kamwe hainamishi kichwa chake mbele ya yeyote au chochote. Wakati huohuo, akiwa ameinamisha kichwa chake kwa unyenyekevu mbele ya Mwenyezi Mungu, kadhalika anauachia huru ulimi wake kusoma zile sifa Zake kama ifuatavyo:

‫العظيم َو بِ َح ْم ِده‬ ‫ان َربِّي‬ َ ‫سُب َح‬ ِ Subhana rabbiyal’adhiim wa bihamdih Ametakasika Mola Wangu, na himidi ni Yake

58

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 58

8/12/2015 6:35:13 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

Kitendo hiki kikiambatana na kusoma maneno hayo hapo juu huleta hisia za utumwa na unyenyekevu mbele ya Mwenyezi Mungu ndani ya mwenye kuswali, na vilevile kwa wengine ambao wanashuhudia kitendo hicho. Na kwa vile mtumwa wa Mwenyezi Mungu hawezi kuwa wa mtu yeyote yule, huwa anatangaza kwa uwazi na dhahiri kabisa heshima, hadhi na uhuru wake wa kutokuwa mtumwa wa watu wengine.

59

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 59

8/12/2015 6:35:13 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

MLANGO WA SITA SIJIDA (Sujuud)

B

“Ametakasika Mola Wangu, utukufu na himidi ni Yake.”

aada ya kunyanyua kichwa chake kutoka kwenye hali ya Rukuu, anakuwa amejitayarisha kujinyenyekesha mwenyewe kwa hali ya juu kabisa mbele ya Mwenyezi Mungu kwa kuweka paji la uso wake chini juu ya ardhi katika hali ya kusujudu. Mtu kuweka paji la uso wake chini ni kiwango kikubwa sana cha unyenyekevu wa mwanadamu, na mwenye kuswali anauona unyenyekevu huu mkubwa kuwa ni wenye kufaa na kustahiki mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwa sababu utumwa wa hali ya juu mbele ya Mwenyezi Mungu ni sawa na kutoa heshima na kuinama mbele ya uadilifu halisi usio onekena na wema wa hali ya juu, unyenyekevu na utii kama huo mbele ya mtu mwingine mbali na Yeye hautakiwi na umepigwa marufuku kabisa. Kwa vile kwa kitendo hiki kila kitu au kiini cha ubinadamu, bidhaa yenye thamani sana katika duka la uhai wa mwanadamu inakuwa imepondwapondwa na kumfanya mwanadamu kuwa duni na kufedheheka. Wakati katika hali ya Sajida, na kichwa chake kikiwa juu ya vumbi, mawazo yake yakiwa yamezama katika utukufu na hadhi ya Mwenyezi Mungu, ulimi wake pia unaungana kwa kusoma mstari ufuatao wa sifa ya utukuzaji – ukitangaza tafsiri ya kitendo hiki.

60

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 60

8/12/2015 6:35:13 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

‫ان َربِّي االَعلَى َوبِحم ِده‬ َ ‫ُس ْب َح‬ “Subhana rabbiyal a’laa wabihamdih.” “Ametakasika Mola Wangu na himidi ni Yake.”

Inastahiki tu kwa mwanadamu mbele ya “Dhati” yaani Mwenyezi Mungu, ambaye Ndiye Mkuu kabisa, Aliyepambika hasa, Mtukufu bila kifani…..na kadhalika, kumtukuza na kumuabudu, na kujishusha mwenyewe hadi kwenye hali ya Sajida. Hivyo Sajida wakati wa swala sio kuanguka chini kwenye vumbi mbele ya kiumbe dhaifu, mwenye mwisho na asiyekamilika, kama kuinama mbele ya mamlaka za kidunia nyepesi na zilizodorora; bali Sajida maana yake ni kuweka paji lako la uso juu ya udongo mbele ya mamlaka iliyo Kuu, Tukufu na Bora zaidi. Mwenye kuswali, kwa kitendo hiki anatangaza utii wake na kujisailimisha kwa Mwenyezi Mungu Mwenye hekima na Mwenye kuona, na kwa kweli, kabla ya kutangaza kwa wengine, huwa anajipa moyo na kuikumbusha nafsi yake ya ndani kabisa juu ya kutekeleza kujisalimisha na utii huu katika mambo yake. Ni kwa kukubali huku: “utumwa kamili mbele ya Mwenyezi Mungu” ambao kwao mwanadamu anajiweka huru kutokana na utumwa na kifungo cha kila kitu na kila mtu na anajikinga mwenyewe kutokana na aina yoyote ya utumwa wa kulazimishwa na fedheha. Athari muhimu kabisa inayotarajiwa kutokana na utamkaji wa sifa wakati wa hatua ya kurukuu na kusujudu ni kwamba kunamfundisha mwenye kuswali kwamba: ni mbele ya nani ambapo ni lazima asalimu amri kikamilifu na kuabudu, na kwa wakati huohuo akimuamrisha kukanusha na kukataza vitendo hivi dhidi ya yeyote na chochote isipokuwa kwa Dhati hiyo moja tu. Kuna riwaya iliyosimuliwa na Imam  inayoelezea uhusiano baina ya Mwenyezi Mungu Muumba na kiumbe aliyeumbwa katika hali ya kusujudu: 61

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 61

8/12/2015 6:35:13 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

“Mahali mja anapokuwa na mawasiliano ya karibu sana na Mwenyezi Mungu ni katika hali ya Sajida.” – Safinatul-Bihar, Jz. 1, mada ya Sajida.

62

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 62

8/12/2015 6:35:13 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

MLANGO WA SABA Kushuhudia – Tashahud

K

atika rakaa ya pili na ile ya mwisho ya kila swala, baada ya kunyanyua kichwa kutoka kwenye sajida ya pili, mwenye kuswali katika hali ya kukaa anasoma mistari mitatu, kila mmojawapo unaakisi uhalisia wa msingi wa imani. Kitendo hiki cha kusoma mistari hii mitatu kinaitwa “Tashahud” – kushuhudia. Mstari wa kwanza unahusika na kutamka “nashuhudia kwamba:” Upweke wa Mwenyezi Mungu:

‫اشهَ ُد اَن ال اِلهَ اِالَّ هللا‬ “Ashhadu an la ilaha ilallahu.” “Nashuhudia kwamba hakuna mungu ila Allah.”

ُ‫َوحْ َده‬ “Wahdahu.” “Mmoja Peke Yake (Ndiye Mola wa Ulimwengu).

Ambayo kwa maneno mengine inaelezewa kama ifuatavyo:

ُ‫ك لَه‬ َ ‫ال َش ِري‬ “La sharika lahu” “Hana mwenza wala mshirika” 63

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 63

8/12/2015 6:35:13 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

Vivutio vyovyote vile, viwe vya kimwili au mali za kimada, au vitu ambavyo vinafanikisha katika kumuingiza mtu katika nira ya kifungo, na kumlazimisha kwenye utumwa na utiifu, haviwezi kwa usahihi kabisa kuelezewa kama ni “mungu” kwa ajili ya mtu huyo. Mawazo ya ajabu ajabu, ashiki, tamaa za kinyama, ulafi na anasa, mawasiliano na mifumo ya kijamii, kila moja ya hayo katika njia maalum hufanikiwa katika kumtega mwanadamu na kumuingiza katika utumwa wake kwa ajili ya kutoa huduma; na hivyo kulazimisha umungu bandia wake9 juu ya yule mtu duni ambaye ametegewa mtego. Hakuna mungu ila Allah inakanusha aina zote hizi za utumwa na utumikishaji, na kwa kitendo cha Tashahudi, huyo mwenye kuswali anatoa ushahidi wake kuhusiana na ukanushaji huu, yaani huwa anakubali kwamba kuna Mungu Mmoja tu, ambaye peke yake ndiye mwenye haki ya kudai utumwa na utii kamili, na kwamba mwingineo yoyote yule mbali na Yeye hana kabisa haki kama hizo juu ya shingo yake. 9

Kuhusiana na hili tafadhali rejea kwenye aya ya Qur’ani Tukufu:

‫ك‬ َ ‫َم ْن ي ُِط ِع ال َّرسُو َل فَقَ ْد أَطَا َع للاهَّ َ ۖ َو َم ْن تَ َولَّ ٰى فَ َما أَرْ َس ْلنَا‬ ‫َعلَ ْي ِه ْم َحفِيظًا‬ “Mwenye kumtii Mtume ndio amemtii Mwenyezi Mungu, na mwenye ­kukataa, basi hatukukupeleka kuwa mlinzi juu yao.” (4:80)

َ‫صلاَ ة‬ َّ ‫ون ال‬ َ ‫ين يُقِي ُم‬ َ ‫ين آ َمنُوا الَّ ِذ‬ َ ‫إِنَّ َما َولِيُّ ُك ُم للاهَّ ُ َو َرسُولُهُ َوالَّ ِذ‬ ‫ُون‬ َ ‫ون ال َّز َكاةَ َوهُ ْم َرا ِكع‬ َ ُ‫َوي ُْؤت‬ “Hakika walii wenu hasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wale walioamini ambao husimamisha swala na hutoa Zaka wakiwa wamerukui.” (5:55) 64

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 64

8/12/2015 6:35:13 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

Kama mantiki hiyo hapo juu ikikubaliwa na mtu, basi bila shaka kwa kawaida atakuwa hakubali kamwe kusalimu amri mbele ya yeyote na hatakubali pia uungu wa kiumbehai kingine chochote, yaani tamaa na mapenzi ya kibinadamu, kinyama, kimalaika, kimahuluku au vinginevyo vya nafsi yake. Kwa kweli haina maana kwamba mwabudu Mungu Mmoja yuko kinyume na majukumu na wajibu wote wa kijamii, au kwamba haamini juu ya kuwepo sharia au mamlaka yoyote kabisa. Kwa sababu ni dhahiri kwamba maisha ya kijamii yameundika juu ya wajibu na utii usiopingika. Bali ina maana kwamba mwabudia Mungu Mmoja haamini na kuvumilia amri au utawala ambao hautegemei juu ya amri za Mwenyezi Mungu. Katika maisha yake ya binafsi au ya kijamii, huwa anazingatia maagizo ya Mwenyezi Mungu na mara kwa mara, kwa mujibu wa amri za Mwenyezi Mungu umuhimu unaohusika kwa ajili ya maisha ya binadamu katika mfumo wa pamoja wa kijamii, ni wajibu juu yake kutii mtu aliyeko madarakani, na pia anapaswa kuwajibika na kujituma kwenye wajibu na majukumu ya kijamii. Hivyo utii na kujihusisha kama ndio sifa ya maisha binafsi na ya kijamii hakutenganishiki katika maisha ya Muamini Mungu Mmoja. Lakini hajisalimishi kwenye tamaa na matamanio ya nafsi yake yenye kuasi au kwenye maslahi ya kichoyo na umimi wa watu ambao wako sawa kama yeye. Badala yake, utiifu wake uko mbele ya amri za Mwenyezi Mungu, Mwenye hekima, Mwenye kuona. Kwa sababu Yeye Ndiye mwenye kuagiza sharia na kanuni ambazo zinapaswa kutekelezwa, na huteua wenye kushika mamlaka, ambao nao hutoa amri kwa mujibu wa maagizo ya mbinguni kwa ajili ya waja wa Mwenyezi Mungu. Aya ya Qur’ani Tukufu ifuatayo inafafanua kwa uwazi kabisa jambo hilo hapo juu: 65

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 65

8/12/2015 6:35:13 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

‫ين آ َمنُوا أَ ِطيعُوا للاهَّ َ َوأَ ِطيعُوا ال َّرسُو َل‬ َ ‫يَا أَيُّهَا الَّ ِذ‬ ۖ ‫َوأُولِي أْالَ ْم ِر ِم ْن ُك ْم‬ “Enyi mlioamini! Mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume na wenye mamlaka katika ninyi….” (4:59).

Na bila shaka ni kwa ajili ya kuakisi ukweli huu kwamba tunasoma ile sentensi ya pili katika Tashahudi kama ifuatavyo:

ُ‫َواَ ْشهَ ُد اَ َّن ُم َح َّمدا َع ْب ُدهُ َو َرسُولُه‬ “Wa ash’hadu anna Muhammadan abduhu wa rasuluhu.” “Na ninashuhudia kwamba Muhammad  ni mja wake na Mtume Wake.”

Kumkubali Muhammad  kama ndiye Mtume ni kukubali uwakilishi wa Mwenyezi Mungu au Wilaya au kwa maneno mengine, kutafuta njia ya Mwenyezi Mungu kwa kufuata nyayo za Muhammad  na kupokea amri za Mwenyezi Mungu kupitia kwa mtumishi Wake. Walikuwepo wenye kumuabudu Mungu wengi, ambao kwa bahati mbaya walifanya makosa katika kuitambua njia aliyoipenda Yeye. Kumkubali Muhammad  kama Mtume Wake kwa uwazi kabisa kunafafanua maelekezo juu ya vitendo na jitihada. Mwenendo kama huo unatakiwa katika maisha ya muumini ili kuthibitisha wajibu wake katika kumwabudu Mwenyezi Mungu. Katika sentensi hiyo hapo juu, kwa kutumia neno mtumishi au mtumwa kabla ya neno Mtume, msisitizo maalum umeambatanishwa kwenye utumishi wa Muhammad . Inaelekea kana kwamba lengo lilikuwa ni kutambulisha sifa kuu na muhimu sana ya Uislamu ambayo kwa hakika ni: “Wema wote wa binadamu unaweza kufu66

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 66

8/12/2015 6:35:13 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

pishwa kwa kuwa mtumwa mkweli halisi wa Mwenyezi Mungu. Kwa mujibu wa itikadi za Kiislamu, yule ambaye amewatangulia wengine katika nyanja hii, huyo ndiye mzito zaidi katika mizani au kipimo cha ubinadamu.” Yule ambaye anatambua maana za kuwa mtumwa wa Mwenyezi Mungu, huwa hahitaji maelezo ya kimantiki au kibusara ili kuunga mkono ukweli huo hapo juu. Kama utumwa kwa Mwenyezi Mungu ni kujisalimisha mbele ya hikma kubwa mno, umaizi, rehema, uadilifu na wema, na kunaambatana na uhuru kutokana na utumwa wa nafsi na kutokana na kila kitu na kila mtu mbali na Mwenyezi Mungu, kunaweza kuwepo na ubora mkubwa kuliko huu. Kwani sio kweli kwamba maovu yote, udhalilishaji, hali duni, roho mbaya, woga na mambo ya gizani yanatokana na utumwa wa mtu kwenye nafsi yaka yenye kuasi? Hivi sio kweli kwamba utumwa kwa Mwenyezi Mungu unaharibu na kuchoma mizizi ya aina nyingine zote za utumwa? Sentesi mbili zilizotajwa hapo juu ambazo zinasomwa kwenye Tashahudi zina nukta nyeti sana na za dhahiri kabisa, ambazo mwenye kuswali anashuhudia kuhusu Upweke wa Mwenyezi Mungu na kuhusu Utume, yaani anashuhudia kwamba “Hapana mungu ila Allah, na anaendelea kuthibitisha utumwa na utume wa Muhammad . Ushuhuda huu kwa kweli unamaanisha kukubali kujihusisha kote na wajibu wote unaohusiana na itikadi hizo mbili hapo juu. Kana kwamba mwenye kuswali, kwa ushuhuda huu anataka kusema: “Niko tayari kuanza kubeba wajibu wote huu unaotokana na itikadi hizo mbili hapo juu kwenye mabega yangu; Upweke wa Mwenyezi Mungu (Tawhiid), na Utume (Nubuwwat). Elimu isiyovutia, iliyofunikwa bila kujifunga, imani na vitendo inakuwa haina thamani yoyote kwa mtazamo wa Kiislamu. Kuushuhudia ukweli kuna maana ya kusimama kwa ajili yake na kukubali wajibu na majukumu 67

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 67

8/12/2015 6:35:13 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

yake yote na ulazima utokanao humo, ukubalifu unaochipukia kutoka kwenye imani safi, aminifu na ya kweli. Hivyo kule kusoma Tashahudi ndani ya swala ni kama kutoa kiapo cha utii kwa mwenye kuswali mbele ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake . Sentesi ya tatu ya Tashahudi ni ombi na du’a kama ifuatavyo:

‫آل ُمح َّمد‬ َ ‫اَللَّهُ َّم‬ ِ ‫صلِّ َعلَى ُمح َّمد َو‬ “Allahumma swali’ala Muhammadin wa aali Muhammad.” “Ewe Mola mpe rehema Muhammad na kizazi chake Muhammad.”

Muhammad  na kizazi chake kitukufu ndio udhihirisho kamili wa madhehebu hii. Mwenye kuswali, kwa kusoma dua hii anakumbusha akili yake kuhusu watu hawa ambao ni mifano kamilifu, na kwa kuwatukuza huwa anaimarisha muungano wake wa kiroho na wao hao. Wafuasi wa kila madhehebu ya kiitikadi, kama hawaoni watu wa mifano halisi ya kuigwa au udhihirisho kamili wa madhehebu hiyo husika, basi wana muelekeo wa kufuata njia potofu na wanaweza kupotea. Kwa hiyo ni muhimu kutenda kwa uwasilishaji hai wa udhihirisho halisi, ambao umelinda ile hali ya kudumu ya madhehebu ya Mitume watukufu katika mpito wote wa wakati. Historia inashuhudia kwamba walikuwepo wanaitikadi au wanafikra wengi, ambao kwa kuhakikisha ubora na ustawi wa maisha ya mwanadamu wamewasilisha mipango na usanifu wa “mji wa kinjozi” (MadinaFadhila), na wameandika vitabu vikubwa vikubwa katika kuunga mkono mapendekezo yao. (Rejea aya za Qur’ani – 45:23, 9:31 na 28:38) Lakini Mitume watukufu, badala ya kujishughulisha na mijadala ya kifalsafa, wao waliwasilisha mipango yao kwa njia ya vitendo 68

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 68

8/12/2015 6:35:13 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

vyao. Kwa kujiwasilisha wenyewe kama mifano bora, na vilevile kuonyesha vitendo vitukufu vya wafuasi wao bora kabisa, Mitume walifanikiwa katika kutengeneza wanadamu wa mfano kamili (Insan al-Kamil), ambao juu ya mabega yao ndimo ulimokuwemo uandalizi wa madhehebu za kidini, na hii ndio iliyokuwa sababu ya madhehebu za Mitume zimebaki hai milele, ambapo hakuna chochote zaidi ya baadhi ya maandishi na maoni kwenye kurasa za vitabu yaliyobakia kutoka kwenye mipango na usanifu wa wale wanafalsafa na wanafikra wakubwa. Mwenye kumswalia Muhammad  na kizazi chake kitoharifu, ambao walikuwa ndio udhihirisho bora kabisa wa madhehebu hii, anaomba dua kwa ukweli kabisa. Anatuma salamu kwa wale ambao waliishi maisha yao yote kama mifano ya kuigwa ya madhehebu hii, na walitoa na kuwasilisha wanadamu wa Kiislamu waliokamilika sawia kwenye historia. Mwenye kuswali anawatumia salamu za amani na rehema kwa ajili yao na anamuomba Mwenyezi Mungu Naye pia kufanya vivyo. Kwa namna hii yeye anajaribu kuimarisha muungano wa kiroho pamoja nao, muungano ambao unaleta uwezo wenye nguvu sana na kumhamasisha kufuata njia na maadili yaliyothaminiwa na kuhifadhiwa na wao. Kumswalia Mtukufu Mtume  na kizazi chake kitoharifu kuna maana ya kutoa heshima kwa watu bora kabisa, wakamilifu na wateule wa Uislamu. Kwa udhihirisho wa watu hawa bora na wakamilifu mbele ya macho yake, Mwislamu wakati wote anaweza akaitambua njia ambayo angeifuata na kujifanya mwenywe kuwa tayari kutembea kuelekea upande huo.

69

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 69

8/12/2015 6:35:13 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

MLANGO WA NANE Kutoa Salaam (Salaam)

S

alam katika swala ni kutuma maamkizi matatu (katika salamu tatu hizi, ya mwisho ndio ya wajibu) na kwa kawaida yanaandamana na Jina na ukumbusho (dhikr) wa Mwenyezi Mungu. Hivyo, swala inaanza Kwa Jina la Mwenyezi Mungu na inamalizika pia kwa Jina la Mwenyezi Mungu, na kati ya mwanzo na mwisho wake, hakuna chochote isipokuwa ukumbusho wa Mwenyezi Mungu na Jina Lake. Kama kuna mstari unaomsifu Mtukufu Mtume na kizazi chake, hata hiyo pia inaambatana na ukumbusho wa Mwenyezi Mungu na kuomba msaada wake kupitia neema na fadhila Zake. Sentesi ya kwanza ni salamu za mwenye kuswali kwa Mtume  na Mwenyezi Mungu swt., akiomba neema na fadhila Zake zishuke juu yake:

‫السالم عليك أيها النبي ورحمة هللا وبركاته‬ “Assalamu alayka ayyuhan’nabiyyu wa rahmatullahi wa barakatuh” “Amani iwe juu yako, ewe Mtume, na rehema na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.”

Mtume ndio mwanzilishi wa Uislamu. Yeye ana wajibu juu ya vitendo vyote, juhudi na bidii kwa ajili ya harakati hii, mambo ambayo pia yanathaminiwa na mwenye kuswali. Yeye alikuwa ndiye mtangazaji wa Tawhid – imani ya Mungu Mmoja – na aliitingisha dhamira ya ulimwengu, na akaweka msingi wa maisha ya heshima 70

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 70

8/12/2015 6:35:13 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

ya milele kwa ajili ya mwanadamu. Yeye alikuwa ndiye msanifu wa binadamu kamili wa Kiislamu, na jamii kamilifu ya Kiislamu ambayo itaendelea kuzalisha watu bora kama hao. Sasa mwenye kuswali, kwa swala yake na masomo yanayohusika na muongozo ndani yake, anaakisi wito huo huo katika maisha yake mwenyewe kwa ajili ya mazingira na kipindi chake. Anachukua hatua kubwa kuelekea kwenye ile jamii bora na kamilifu iliyoagizwa na ile shakhsia iliyotukuka (Mtukufu Mtume). Kwa hiyo, ni kawaida kwamba, wakati mwenye kuswali anakaribia kumaliza kitendo hiki, anamkumbuka Mtukufu Mtume  kwa salamu na heshima, ambaye amemuongoza kuelekea kwenye njia hii na amekuwa kiongozi wake kwenye safari yote, na kwa namna hii anatangaza uwepo wake pamoja naye, na katika njia yake. Katika sentensi ya pili ya salamu, mwenye kuswali anatoa heshima zake na salamu juu yake mwenyewe, wapiganaji wenziwe na juu ya waja wema wote Mwenyezi Mungu.

‫السالم علينا وعلى عباد هللا الصالحين‬ “As salamu alayna wa ala ibadillahis swalihin.” “Amani iwe juu yetu na juu ya waja wema wa Mwenyezi Mungu wote.”

Kwa hiyo kwa njia hii anaiweka kumbukumbu ya waja wema na waadilifu wa Mwenyezi Mungu katika akili yake; na ile hisia ya uwepo wao na uhai wao inampatia yeye nguvu na nishati. Katika dunia ambamo udhihirishaji wa uovu na dhambi; ufukara, ubaya wa kupindukia, ukatili udikteta, ubakaji na uchafuzi vimezidi kila mahali na kwa kila mtu, ambamo ukiangalia kwa jicho la 71

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 71

8/12/2015 6:35:14 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

mtu mwenye akili timamu, mwenye kujua na mtambuzi wa mambo, mazingira ya sasa yanatoa picha ya kuporomoka na kufilisika kabisa kwa maadili ya binadamu. Ambamo hali ya unafiki mtupu na udanganyifu wa wazi imefichwa kwa mng’aro wa bandia. Katika dunia ambamo sauti za kutafuta haki na ukweli zinazimwa na kunyamazishwa kwa vitendo vya kudhalilishwa vya watu wachoyo na wenye tamaa ya kujiendeleza, ambamo nafasi zilizoshikwa na watu watukufu kama Imam Ali , Imam Husein , Imam as-Sadiq  zinajazwa makelele ya kifitna ya watu kama Mu’awiyah, Yazid na Mansuur, na kwa kuhitimisha, katika ulimwengu ambamo watoto wastahifu wa Shetani wamekalia sehemu zote ambazo mwanzoni zilikaliwa na waja waadilifu wa Mwenyezi Mungu. Katika hali ya mambo kama hiyo, kuna matumaini au matarajio kwamba uadilifu na wema utaweza kuwa na nafasi yoyote ile ya kuwepo na kuenea? Je, kuna kitu chochote mbali na uovu, ufukara, kukata tamaa, na dhulma kinachoweza kutegemewa kutoka kwa binadamu? Mtu ni lazima atarajie kwamba kama kuna uwezekano wa kubadili mambo hauwezi kufanyika kwa urahisi hivyo. Maamkuzi na salamu kwa waja wema na waadilifu wa Mwenyezi Mungu, ambao katika mazingira ya giza kiasi hicho bado wanatoa maliwazo na wanachukua uangalizi wa watu wasio na matumaini, na waliovunjika mioyo. Inakuwa kana kwamba ni bishara njema ya mwanga unaong’ara unaotokea kwenye moyo wa kiza kinene kabisa. Inamuahidi mwenye kuswali kuhusu uhai na uwepo wa wapiganaji wenza wengine. Inamwambia: Wewe huko peke yako katika jangwa hili kavu na kame, unaweza kuona uoto wenye manufaa na wenye kudumu muda mrefu. Kama ilivyo kawaida wakati wote katika historia, kwamba zile jamii zilizopotoka kupita kiasi na kuharibika, zilikuwa pia ndio mahala pa kuzaliwa wanamageuzi wenye dhamira hasa wenye utashi na maarufu, ambao waliweka msingi 72

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 72

8/12/2015 6:35:14 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

kwa ajili ya itikadi mpya zenye kuchangamsha na kuleta uhai, na wakaanzisha mifumo mipya katikati ya ule ukosa matumaini na giza lote lililokuwepo. Hata wakati huu wa sasa, kwa mujibu ya ahadithi tukufu za kihistoria, nguvu kama hizo hizo zilizotaalimika za uadilifu na wema, katikati ya dunia hii iliyojaa giza na dhulma zimo zikishughulika kwa bidii kabisa. Ndio! waja wema wa Mwenyezi Mungu, ambao wanamuona Mwenyezi Mungu kama mwenye kufaa na kustahiki kuabudiwa, wanafuata amri Zake na kukabili na kuwakataa wadai bandia wa uungu (Twaghuut). Ni akina nani waja hawa wastahifu wa Mwenyezi Mungu na ni wapi wanapoweza kupatikana? Halipasi kusomeka somo kutoka kwao na je haipasi kufuatana nao hao katika kusonga mbele kwao? Ndio. Wakati mwenye kuswali anapojiweka mwenyewe sambamba pamoja na watu hawa waaminifu na akatuma salamu kwa ajili yake mwenyewe na kwa ajili yao, mwale wa fahari, heshima, na uhakikisho huwaka katika moyo wake. Hujaribu kwa uwezo wake kujiunga nao kwa ukweli kabisa katika safu zao ili kujiweka mwenyewe pamoja nao, na kwa vile asingeweza kutembea hatua kwa hatua pamoja nao, huhisi kusikitika kuhusu hilo. Hisia hii humwekea ndani yake ahadi na wajibu mpya. Ni aina gani ya waja hawa wa Mwenyezi Mungu wastahiki na waaminifu, na ustahiki unapaswa kuwa ni nini? Uaminifu hauna maana ya kutekeleza ibada ya swala tu hivi. Mtu mwadilifu ni yule anayeweza kutekeleza majukumu mazito ya kimbinguni katika namna sahihi inayofaa kama inavyopasa na kama inavyotegemewa kutoka kwa mja mwaminifu wa Mwenyezi Mungu. Kwa maneno mengine, anaweza akalinganishwa na mwanafunzi bora katika darasa. Mwanafunzi bora wa mfano anapaswa kufanya kazi za shule zifanywazo nyumbani (homework) vizuri. 73

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 73

8/12/2015 6:35:14 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

Mwishoni katika sentensi ya tatu, mwenye kuswali anatoa salamu kwa waja wema wale wale (kwa malaika au wenye kuswali wengineo) kama ifuatavyo:

‫السالم عليكم ورحمة هللا وبركاته‬ Assalaamu ’alaykum wa rahmatullahi wa barakatuh “Amani iwe juu yenu na rehema na baraka za Mwenyezi Mungu.”

Kwa hiyo kwa namna hii mwenye kuswali anajikumbusha kuhusu wema na ustahili (au sifa za kimalaika ua umoja pamoja na wenye kuswali wengine), na kwa hiyo anamalizia swala yake kwa kuomba dua na salamu kwa ajili ya hadhara yake ya heshima.

74

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 74

8/12/2015 6:35:14 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

ORODHA YA VITABU VILIVYO ­CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1. Qur’an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thelathini 2. Uharamisho wa Riba 3. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza 4. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili 5. Hekaya za Bahlul 6. Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) 7. Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) 8. Hijab vazi Bora 9. Ukweli wa Shia Ithnaashari 10. Madhambi Makuu 11. Mbingu imenikirimu 12. Abdallah Ibn Saba 13. Khadijatul Kubra 14. Utumwa 15. Umakini katika Swala 16. Misingi ya Maarifa 17. Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia 18. Bilal wa Afrika 19. Abudharr 20. Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu 21. Salman Farsi 22. Ammar Yasir 23. Qur’an na Hadithi 24. Elimu ya Nafsi 25. Yajue Madhehebu ya Shia 26. Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur’an Tukufu 27. Al-Wahda 28. Ponyo kutoka katika Qur’an 29. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii 30. Mashukio ya Akhera 31. Al Amali 32. Dua Indal Ahlul Bayt 33. Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. 34. Haki za wanawake katika Uislamu 35. Mwenyezi Mungu na sifa zake 36. Kumswalia Mtume (s) 37. Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) 38. Adhana 39 Upendo katika Ukristo na Uislamu 40. Tiba ya Maradhi ya Kimaadili 41. Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu 42. Kupaka juu ya khofu 43. Kukusanya swala mbili 44. Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara 45. Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya 46. Kusujudu juu ya udongo 47. Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) 48. Tarawehe 49. Malumbano baina ya Sunni na Shia 50. Kupunguza Swala safarini 51. Kufungua safarini 52. Umaasumu wa Manabii 53. Qur’an inatoa changamoto 54. as-Salaatu Khayrun Mina -’n Nawm 55. Uadilifu wa Masahaba 56. Dua e Kumayl

75

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 75

8/12/2015 6:35:14 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

57. Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu 58. Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake 59. Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata 60. Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mtume Muhammad (s) 61. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza 62. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili 63. Kuzuru Makaburi 64. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza 65. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili 66. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu 67. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne 68. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano 69. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita 70. Tujifunze Misingi Ya Dini 71. Sala ni Nguzo ya Dini 72. Mikesha Ya Peshawar 73. Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu 74. Ubora wa Imam ‘Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliyonyooka 75. Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake 76. Liqaa-u-llaah 77. Muhammad (s) Mtume wa Allah 78. Amani na Jihadi Katika Uislamu 79. Uislamu Ulienea Vipi? 80. Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) 81. Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) 82. Urejeo (al-Raja’a ) 83. Mazingira 84. Utokezo (al - Badau) 85. Hukumu ya kujenga juu ya makaburi 86. Swala ya maiti na kumlilia maiti 87. Uislamu na Uwingi wa Dini 88. Mtoto mwema 89. Adabu za Sokoni 90. Johari za hekima kwa vijana 91. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza 92. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili 93. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu 94. Tawasali 95. Imam Mahdi katika Usunni na Ushia 96. Hukumu za Mgonjwa 97. Sadaka yenye kuendelea 98. Msahafu wa Imam Ali 99. Ngano ya kwamba Qur’ani imebadilishwa 100. Idi Al-Ghadir 101. Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu 102 Hukumu zinazomhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi 103. Huduma ya Afya katika Uislamu 104. Sunan an-Nabii 105. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) 106. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) 107. Shahiid Mfiadini 108. Kumsalia Nabii (s.a.w) 109. Ujumbe -Sehemu ya Kwanza 110. Ujumbe - Sehemu ya Pili 111. Ujumbe - Sehemu ya Tatu 112. Ujumbe - Sehemu ya Nne 113. Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu 114. Hadithi ya Thaqalain 115. Ndoa ya Mutaa 116. Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza 117. Ukweli uliopotea sehemu ya Pili 118. Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu

76

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 76

8/12/2015 6:35:14 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

119. Ukweli uliopotea sehemu ya Nne 120. Ukweli uliopotea sehemu ya Tano 121. Mkutano wa Maulamaa wa Baghdad 122. Safari ya kuifuata Nuru 123. Fatima al-Zahra 124. Myahudi wa Kimataifa 125. Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi 126. Visa vya kweli sehemu ya Kwanza 127. Visa vya kweli sehemu ya Pili 128. Elimu ya Ghaibu ya Maimamu 129. Mwanadamu na Mustakabali wake 130. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) 131. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) 132. Khairul Bariyyah 133. Uislamu na mafunzo ya kimalezi 134. Vijana ni Hazina ya Uislamu 135. Yafaayo kijamii 136. Tabaruku 137. Taqiyya 138. Vikao vya furaha 139. Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 140. Visa vya wachamungu 141. Falsafa ya Dini 142. Azadari-Kuhuzunika na Kuomboleza 143. Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah 144. Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu 145. Kuonekana kwa Allah 146. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) 147. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) 148. Ndugu na Jirani 149. Ushia ndani ya Usunni 150. Maswali na Majibu 151. Mafunzo ya hukmu za ibada 152. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1 153 Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2 154. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 155. Abu Huraira 156. Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. 157. Mazingatio kutoka katika Qur’an - Sehemu ya Kwanza 158. Mazingatio kutoka kaitka Qur’an - Sehemu ya Pili 159. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza 160. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili 161. Qur’ani Tukufu – Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili 162. Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) 163. Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani 164. Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu 165. Uislamu Safi 166. Majlisi za Imam Husein Majumbani 167. Je, Kufunga Mikono 168. Uislam wa Shia 169. Amali za Makka 170. Amali za Madina 171. Asili ya Madhehebu katika Uislamu 172. Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi 173. Ukweli uliofichika katika neno la Allah 174. Uislamu na Mifumo ya Uchumi 175. Umoja wa Kiislamu na Furaha 176. Mas’ala ya Kifiqhi 177. Jifunze kusoma Qur’ani 178. As-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah 179. Hayya ‘Alaa Khayri’l-’Amal Katika Adhana 180. Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura

77

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 77

8/12/2015 6:35:14 PM


HEKIMA ZA KINA ZA SWALA

181. Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na R ­ amadhani) 182. Uadilifu katika Uislamu 183. Mahdi katika Sunna 184. Maswali Ya Uchunguzi Kuhusu Uislam 185. Kazi na Bidii ni njia ya maendeleo 186. Abu Talib – Jabali Imara la Imani 187. Ujenzi na Utakaso wa Nafsi 188. Vijana na Matarajio ya Baadaye 189. Usalafi – Historia yake, maana yake na lengo lake 190. Ushia – Hoja na Majibu 191. Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) 192. Maombolezo – Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) 193. Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu 194. Takwa 195. Upotoshaji dhahiri katika Turathi (Hazina) ya Kiislamu 196. Amirul Muuminina (‘as) na Makhalifa 197. Uongozi na Utawala katika Mwenendo wa Imam ‘Ali (‘a) 198. Kuvunja hoja iliyotumika kutetea Uimamu wa AbuBakr 199. Adabu za vikao na mazungumzo 200. Hija ya Kuaga 201. Uwazi baina ya Maslahi na Vikwazo 202. Fadhila za watukufu watano katika Sahih Sita 203. Mdahalo baina ya Mwanachuoni wa Kisunni na Mwanachuoni wa Kishia (Al-Muraja’aat) 204. Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (as) 205. Mjadala wa Kiitikadi 206. Mtazamo kuhusu msuguano wa Kimadhehebu 207. Nchi na Uraia – Haki na wajibu kwa Taifa 208. Mtazamo wa Ibn Taymiyyah juu ya Imam Ali (as) 209. Uongozi wa Kidini – Maelekezo na Utekelezaji wa Kijamii 210. Maadili ya Ashura 211. Mshumaa – Shahidi na Kifo cha Kishahidi 212. Mizani ya Hekima – Hadithi za Ahlul Bait (as) – Sehemu ya Kwanza 213. Imam Ali na Mambo ya Umma 214. Imam Ali na Mfumo wa Usawa 215. Mwanamke na Sharia 216. Mfumo wa Wilaya 217. Vipi Tutaishinda Hofu? 218. Kumswalia Mtume ni Ufunguo wa Utatuzi wa Matatizo 219. Mahali na Mali za Umma 220. Nahjul-Balagha – Majmua ya Khutba, Amri, Barua, Risala, Mawaidha na Semi za Amirul-Muuminin Ali bin Abu Talib (a.s.) 221. Mukhtar – Shujaa aliyelipiza kisasi dhidi ya wauaji wa Imam Husein (as) hapo Karbala 222. Uimamu na Tamko la Kutawazwa 223. Imam Husain ni Mfumo wa Marekebisho na Mageuzi 224. Saada Kamili – Kitabu cha Kiada cha Maadili 225. Maeneo ya Umma na Mali Zake 226. Imam Hasan na Mfumo wa Kujenga Jamii 227. Adhana ni Ndoto au ni Wahyi? 228. Maimamu wa Ahlul Bait – Ujumbe na Jihadi KOPI NNE ZIFUATAZO ZIMETAFSIRIWA KWA LUGHA KINYARWANDA 1. 2. 3. 4.

Amateka Na Aba’Khalifa Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya Shiya na Hadithi.

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION KWA LUGHA YA KIFARANSA 1.

Livre Islamique

78

06_15_Hekima Za Kina Swala_12_August_2015.indd 78

8/12/2015 6:35:14 PM


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.