Hija katika usemi na ujumbe wa imam khomeini

Page 1

HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

Kimetarjumiwa na: Al-Haj Ramadhani S. K. Shemahimbo

Kimeandikwa na: Imam Khomeini

Kimetarjumiwa na: Al Haj Ramadhani S. K. Shemahimbo

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 1

11/3/2015 2:57:46 PM


‫ترجمة‬

‫الحج فى كالم و خطب اإلمام الخميني‬ ‫(قدس سره الشريف)‬

‫تأ ليف‬ ‫مؤسسة تنظيم ونشر آثار اإلمام الخميني‬

‫لنليزية الى اللغة السوا حلية‬

‫‪11/3/2015 2:57:46 PM‬‬

‫‪12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 2‬‬


©Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION

ISBN: 978 - 9987 – 17 – 092 – 0

Kimeandikwa na: Imam Khomeini

Kimetarjumiwa na: Al Haj Ramadhani S. K. Shemahimbo

Kimehaririwa na: Alhaji Hemedi Lubumba

Kimepangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation

Toleo la kwanza: Septemba, 2014 Nakala: 1000 Toleo la pili: Julai, 2016 Nakala: 1000

Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. - 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: www.alitrah.info

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 3

11/3/2015 2:57:46 PM


Yaliyomo Dibaji ......................................................................................... vi Neno la Mchapishaji........................................................................ 1 1. Sura ya Kiroho ya Hija................................................................ 3 2. Utukufu wa Makka na Nyumba Takatifu ya Mwenyezi Mungu........................................................................ 9 3. Falsafa ya Taratibu za Ibada za Hija.......................................... 13 4. Umuhimu wa Kusoma Qur’ani Wakati wa Hija........................ 17 5. Umuhimu wa Kujifunza kwa Makini Ibada za Hija.................. 17 6. Hija na Uimarishaji wa Umoja Miongoni mwa Waislamu........ 20 7. Hija, Wakati wa Kurekebisha na Kutatua Matatizo ya Waislamu................................................................ 29 8. Ulamaa wa Nchi za Kiislamu na Ibada ya Hija......................... 39 9. Dokezo la Jumla......................................................................... 44 10. Ufundaji na Uelimishaji Wakati wa Hija................................. 56 11. Hija na Kutangaza Mapinduzi ya Kiislamu............................. 61 12. Hija: Kitovu cha Mapambano Dhidi ya mafiduli wa dunia..................................................................... 69 13. Onyo Dhidi ya Njama za Viburi wa Dunia Katika Wakati wa Hija............................................................. 79 14. Wanachuoni Watumishi wa Vitala........................................... 85

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 4

11/3/2015 2:57:46 PM


15. Kuchukizwa Juu ya Wapagani................................................. 93 16. Wajibu wa Ujumbe wa Mafaqihi Kwenye Mambo ya Hija........................................................ 105 17. Umuhimu wa Ushirikiano wa Mahujaji na Ujumbe wa Faqihi Katika Mambo ya Hija............................ 108 18. Wajibu wa Ulamaa Katika Misafara ya Hija......................... 110 19. Wajibu wa Wasimamizi wa Misafara.................................... 116 20. Haja ya Mpangilio Makini Katika Hija................................. 118 21. Anasa na Matumizi Yasiyowiana na Hija.............................. 123 22. Mauaji ya Kikatili na Kumwaga Damu ya Mahujaji Katika Hija ya Mwaka 1987................................... 125

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 5

11/3/2015 2:57:46 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

DIBAJI

K

itabu hiki ni toleo la Kiswahili la taasisi ya Al Itrah Foundation. Chapisho lake limelenga kukidhi mahitaji ya kiroho ya zama hizi pamoja na Ubongo na fikra zinazokuwa za Muislam. Jitihada kubwa zimefanywa na Taasisi kuweka chapisho hili la Kiswahili ­katika msingi wa haki na wenye kukubalika katika Uislam. Unaombwa kwa Taadhima ukisome kitabu hiki katika malengo yaliyokusudiwa. Pia Unaombwa kuwasilisha kwetu maoni yako huru juu ya chapisho letu hili, jambo ambalo tutashukuru sana. Kutangaza ujumbe wa Uislam ni kazi ambayo inahitaji ushirikiano wetu sote. Taasisi inakuomba kuungana na kushirikiana kama ilivyoagizwa katika aya ya Qur’an: (Surat Saba’ 34:46). Na rehma za Allah ziwe juu yako. Wako katika Uislam Al Itrah Foundation Barua Pepe: alitrah@yahoo.com SMS: +255 778 300 140

vi

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 6

11/3/2015 2:57:47 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

NENO LA MCHAPISHAJI

K

itabu kilichoko mikononi mwako kinatokana na baadhi ya madondoo kutoka usemi na ujumbe wa Imam Khomeini S kwa mahujaji wa Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu huko Makka. Kitabu hiki kimetarjumiwa kutoka Kiingereza kutoka kitabu kiitwacho, Hajj in the Words & Messages of Imam Khomeini S. Sisi tumekiita, Hija katika Usemi na Ujumbe wa Imam Khomeini S. Tangu kufanikiwa kwa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Imam Khomeini alikuwa akitoa hotuba na ujumbe kwa mahujaji wote duniani katika msimu wa Hija. Suala muhimu kabisa alilokuwa akilizungumzia lilikuwa ni kuwazindua mahujaji wanapokwenda kuhiji wawe kuhiji kwao kuwe kunafuatana na Hija ya Nabii Ibrahim kama ilivyofundishwa na Mtukufu Mtume Muhammad 8 ili madhumuni na malengo ya Hija yawe yanabakia katika hali hiyo asili ya kimaanawi na kiroho kwa ajili ya kizazi hadi kizazi. Imam Khomeini amejaribu kuibadilisha taswira waliyokuwa nayo Waislamu ya kuichukulia Hija kuwa ni safari ya kitalii katika maeneo matukufu yenye kutekelezwa ibada zilizokuwa na sura za kimadhihirisho tu. Hivyo, ameelezea mambo muhimu ya kuzingatiwa ili kurudisha heshima na hadhi ya Hija asilia, mambo ambayo kwa uhalisia wa madhumuni ya Hija ni lazima yaguse vipengele vyote vya maisha ya mwanadamu kama vile masuala ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kadhalika. Ujumbe, hotuba na maneno hayo ya Imam Khomeini tumeyaona ni yenye kufaa sana katika kuwaamsha Waislamu katika utekelezaji madhubuti wa Hija. Hivyo, tumeona tuchukue baadhi ya madondoo 1

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 1

11/3/2015 2:57:47 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

hayo kwa faida hasa ya wale wanaokwenda Hija na kwa wengine kuyafahamu na kujiandaa vyema iwapo watakuja kujaaliwa, na pia kushirikiana kwa ufahamu katika kuleta mabadiliko na maendeleo kwa Uislamu na Waislamu duniani kote. Kwa hiyo, Taasisi yetu ya al-Itrah imeamua kuchapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu wote, hususan wazungumzaji wa Kiswahili. Tunamshukuru ndugu yetu al-Haji Ramadhani S. K. Shemahimbo kwa kufanya udondozi huu kwa mukhtasari kutoka kwenye lugha ya Kiingereza kwa faida ya Waislamu wazungumzaji wa Kiswahili. Aidha tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Mwenyezi Mungu awalipe wote malipo mema hapa duniani na kesho Akhera. – Amin. Mchapishaji Al-Itrah Foundation

2

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 2

11/3/2015 2:57:47 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬

1 SURA YA KIROHO YA HIJA

K

wa vile sasa tuko kwenye lengo la kutekeleza agizo letu la kheri la kidini la Hija, ni muhimu kuzingatia vipengele vyake vya kiirfani, kiroho, kijamii, kisiasa na utamaduni. Marafiki wengi waliojitolea, tayari wamekwisha kuelezea ubora wa vipengele mbalimbali vya Hija na sasa ningependa tu kufanya utajo wa kifupi wa baadhi ya vipengele vyake nikitarajia viwe kama ukumbusho. Kwa vile kuna vidokezo nyeti vya kiirfan na kiroho katika taratibu hizi za ibada, kuanzia mwanzo wa kuvaa vazi la hujaji ‘Ihraam’ kupitia “TALBIYA” au “LABBEIKA” (kwa maana ‘Mimi hapa katika utumishi Wako) hadi mwisho, ambazo maelezo yake hayatatolewa katika hotuba hii, nitataja tu baadhi ya dalili za “Talbiya.” Maneno ya kurudia kama haya ya “Labbeika” ni ya kweli kutoka kwa wale tu ambao wameutambua wito wa Mwenyezi Mungu kwa umaizi wao na hivyo wanaitikia mwito wa Mwenyezi Mungu kwa ukamilifu kabisa. Jambo halisi ni ule uwepo wetu mbele ya Mwenyezi Mungu na tafakari ya utukufu wake mpendwa, kiasi kwamba mtu anaweza kusema, mtamkaji amesafirishwa pamoja na hali ya roho kuungana na Mungu, na hivyo anarudia mwitikio wake kwenye 3

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 3

11/3/2015 2:57:47 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

mwito wa Kimungu, na hatimaye anakana uabudu masanamu katika maana yake kamili, katika namna ambayo inafahamika vyema kwa waumini wenye nyoyo safi. Hakika ukanaji wa mshiriki juu ya Mwenyezi Mungu una maana ya ukanaji wa daraja zote za ushirika, ikiwa ni pamoja na ulimwengu, kwa mtazamo wenye muono safi, na unajumuisha mazingatio yote ya yale yanayostahiki kusifiwa, kama: “Sifa ziwe juu Yako na rehema ni Zako…..,” inatenga sifa na rehema kwa ile Nafsi Kuu zaidi na inakanusha washirika wa namna yoyote ile, na hii ndio imani juu ya Mungu Mmoja ya hali ya juu kabisa ambayo ina maana kwamba kila sifa na rehema inayopatikana hapa kwenye dunia ya uhai ni utukufu kwa Mwenyezi Mungu na rehema Yake peke Yake, na huo ndio ukweli katika kila kituo, werevu, akili, mwendo, majibu na kitendo. Na jingine badala ya hilo ni uabudu masanamu katika maana yake ya jumla, na sisi sote, wale vipofu wa ndani kwa ndani, tumeathiriwa nao.” O  O  O Daraja za Hija, zikiwa ni rasilimali kwa ajili ya uhai wa milele, ambazo zinamleta mwanadamu karibu na peo za tawhidi na nyuradi za kumsifu Mwenyezi Mungu haziwezi kupatikana isipokuwa kama kanuni za Hija zinazingatiwa na kutekelezwa sawasawa na kwa usahihi kabisa, na waungwana Mahujaji na wahudumu wa misafara hiyo lazima wafanye juhudi zao za pamoja kufundisha na kufundishwa ibada hizo za Hija, na wenye elimu wanalazimika kuwa waangalifu wasije wafuasi wao wakavunja kanuni. Malengo ya kisiasa na kijamii ya Hija yanaweza yasifikiwe isipokuwa kama wajibu wa kiroho na kidini yakikamilishwa na “Labbeika” yenu iwe ni mwitikio wa kweli kwenye wito wa Mwenyezi Mungu. Kuweni na vaeni mavazi ya mahujaji kwa ajili ya kufikia kwenye kizingiti 4

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 4

11/3/2015 2:57:47 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

cha Mwenyezi Mungu; wakati mnapokariri “Labbeika” kanusheni uwepo wa mshirika yeyote wa Mwenyezi Mungu kwa hali yoyote ile, jitoeni kwenye nafsi zenu, ambazo ndio chanzo kikubwa cha uabudu masanamu na ushirikina na muondoke kuelekea kwake Yeye Mwenyezi Mungu Mtukuka, na kwa matumaini kabisa, vifo vya hawa wanaotafuta daraja hili vitakuwa ni baada ya kuondoka kwao, na kupata yale malipo wanayostahiki, kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Lakini kama vipengele vya kiroho vikipuuzwa, itakuwa ni vigumu sana kwenu kujitoa kwenye makucha ya tamaa za kimwili za nafsi zenu, na madhali mtakuwa mmefungwa kwenye ubinafsi wenu, hamtakuwa na uwezo wa kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu na kulinda mahali patakatifu pa Mwenyezi Mungu. Enyi wapendwa! Tahadharini! Angalieni wale wapiganaji mashujaa wa Jamhuri ya Kiislamu ambao walipata ushindi wa Mwenyezi Mungu unaoridhisha kwa ajili ya Uislamu na nchi ya Kiislamu na sasa, kikundi cha “Mashahidi wao Waliohai” wanaandamana nanyi katika taratibu za ibada ya Hija, na mnapaswa kupata somo kutoka kwenye mabadiliko makubwa ambayo yameleta ujitoaji muhanga wa nafsi ndani yao. Waislamu wanapaswa wajue kwamba isipokuwa pale tu watakapopitiwa na mabadiliko kama haya, mashetani wa ndani kabisa wa tamaa zao za kimwili, na kadhalika mashetani wa nje hawatawaruhusu kufikiria juu ya umma wa Waislamu na watu wanaodhulumiwa wa ulimwengu huu. O  O  O Mwote katika MIQAT Tukufu na katika vituo vya kutukuzwa, kwa Nyumba iliyobarikiwa ya Mwenyezi Mungu tekelezeni kanuni za ibada ya mahudhurio mbele ya utukufu wa Mwenyezi Mungu, na ziwekeni nafsi zenu huru kutokana na vifungo 5

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 5

11/3/2015 2:57:47 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

vyovyote vile mbali na Mwenyezi Mungu, na zisafisheni na chochote kisichokuwa Mwenyezi Mungu na zinururisheni na miale ya mianga ya mbinguni ili kwamba kanuni na ibada zenu katika hatua hii kuelekea kwa Mwenyezi Mungu iwe imepambwa na dhana za Hija ya Kiabraham na, baadaye kwa dhana za Hija ya Muhammad. Na mkiwa mmeachwa huru kutokana na vitendo vya kawaida, ninyi nyote, mkiwa mmesafishwa kutokana na ubinafsi na umimi, na mkiwa mmesheheneshwa kwa utambuzi wa Mwenyezi Mungu na mapenzi ya Mpendwa, rudini kwenye ardhi zenu za nyumbani na mikono yenu ikiwa imejaa hidaya za milele badala ya vitu vya kimada vinavyoisha na kutoweka. Jiungeni na marafiki zenu wenye kupenda muhanga mkiwa na mikono yenu iliyojaa mahadhi ya kibinadamu ya Kiislamu kwa ajili ya kazi ambayo, wale Manabii wakubwa – kuanzia Ibrahim Khalilullah, hadi kwa kipenzi cha Mwenyezi Mungu, Muhammad walipangiwa kuzifanya. Ni maadili haya na hamasa ambavyo vinaweza kumuokoa mwanadamu kutokana na inda na utegemezi wa Magharibi au Mashariki na kumuongozea kwenye mti uliobarikiwa wa “Hakuna MASHARIKI, Hakuna MAGHARIBI.”

O  O  O Tazama! Mapito ya Hija sio safari ya kawaida kwa ajili ya biashara na malengo ya kidunia: ni mapito kuelekea kwa Mwenyezi Mungu. Unatoka kuelekea kwenye Nyumba ya Mwenyezi Mungu. Yote unayoyafanya lazima yafanywe kimungu. Kutembea kwako tangu pale kunapoanzia, ni kuondoka kuelekea kwa Mwenyezi Mungu. Kama vile watakatifu wetu walivyotembea kuelekea kwa Mwenyezi Mungu, katika maisha yao yote, na bila kupotea hata hatua moja kutoka kwenye kile kilichoandaliwa kama mpango kwa ajili ya kuungana na Mwenyezi Mungu, wewe nawe pia sasa upo 6

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 6

11/3/2015 2:57:47 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

katika kupita kuelekea kwa Mwenyezi Mungu, unamwambia Allah “Labbeika” ambayo ina maana: “Tunaitikia mwaliko Wako.” Tahadhari, usije ukafanya jambo ambalo Mwenyezi Mungu anasema: “hapana, sikupokei wewe kwa sababu huna tabia ya Kiislamu.” Angalieni, msije mkaigeuza safari hii kuwa ni safari ya kibiashara; ninyi nyote, iwe viongozi wakuu wa misafara au mahujaji wa kawaida; hii ni safari kuelekea kwa Mwenyezi Mungu na sio kuelekea kwenye dunia. Msiipapatikie na mambo ya kidunia. O  O  O Miongoni mwa masharti muhimu ya matendo yote ya ibada ni unyofu katika utendaji. Kwa sababu, Mungu aepushie mbali, kama mtu atafanya jambo kwa riya na kujaribu kuonyesha kwa watu uzuri wa amali zake, matendo yake yatakuwa yameharibika. Waheshimiwa Mahujaji lazima wawe waangalifu sio kutafuta upendezaji usio wa Kimungu katika matendo yao. Vipengele vya kiroho vya Hija ni vingi sana na ni muhimu kwamba Hujaji afahamu ni wapi anakokwenda na ni mwaliko wa nani anaouitikia, anakuwa ni mgeni wa nani na ni nini utaratibu wa ukarimu huu. Anapaswa aelewe zaidi kwamba kila dalili ya umimi inapingana na uchamungu na ni upinzani kwenye kutembea kuelekea kwa Mwenyezi Mungu na kutatia dosari ile hali ya kiroho ya Hujaji. Lakini kama madhumuni haya ya ki-Irfaan na kiroho yakipatikana na ile “Labbeika” ikawa katika mfuatano halisi na mwaliko wa Mwenyezi Mungu, mwanadamu atakuwa mshindi katika nyanja zote za kisiasa, kijamii, kiutamaduni na hata kijeshi. Kwa mtu kama huyo kutakuwa hakuna kushindwa. Tumuombe Mwenyezi Mungu atuneemeshe kwa japo fungu dogo la safari ya kiroho kama hiyo na uondokaji wa kimbinguni. 7

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 7

11/3/2015 2:57:47 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

O  O  O Wale wanaosafiri kwenda Hija lazima wawe na hadhari wasije wakaitia dosari Hija yao kwa kufanya kitendo cha dhambi. Yote wanayoyafanya lazima yawe ya Kiislamu na ya kiibada. Maandamano lazima yawe ya kiibada na masafi, miito au mabango lazima yawe ya kiibada na masafi kadhalika; na katika namna ambayo inakuwa ni katika njia ya Mwenyezi Mungu; sio yafanywe tu kiholela, au mmoja kumkashifu mwingine kwa kujifurahisha. Mambo kama hayo ni lazima yapangwe vizuri kabla na lazima pia yafanywe kwa uangalifu vilevile.

8

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 8

11/3/2015 2:57:47 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

2 UTUKUFU WA MAKKA NA NYUMBA TAKATIFU YA MWENYEZI MUNGU

M

iongoni mwa nukta ambazo waheshimiwa Mahujaji lazima wazizingatie ni ule ukweli kwamba ile Makka yenye hadhi kubwa na yale maeneo ya makaburi yaliyotukuzwa ni vioo vya matukio yang’arayo ya matendo ya mitume na kunyenyekea kwenye mapenzi ya Mungu, na ile kazi ya kitume ya Mtume mkarimu mno wa Uislamu, amani iwe juu yake. Hatua kwa hatua, ardhi hii imekuwa mahali pa mashukio matakatifu ya mitume watukufu na ya Jibril mwaminifu, na kumbukumbu ya maumivu na mateso ambayo yule Mtume mkarimu kabisa wa Uislam 8 ameyapitia katika njia ya Uislamu na ubinadamu. Kuhudhuria kwenye sehemu hizi takatifu na maeneo ya makaburi yanayoheshimika na kufikiria zile hali ngumu kupindukia za ile kazi ya kitume ya Mtukufu Mtume wetu 8 kutatufanya sisi kuelewa vema wajibu wetu katika kulinda mafanikio ya matendo yetu na kazi tukufu, na kufahamu vema jinsi Mtukufu Mtume na Maimam maasumin (amani juu yao wote) walivyostahimili kwa ajili ya dini ya Mwenyezi Mungu na kufutilia mbali yale yasiyo na maana yoyote, na kamwe kutoogopa kwao shutuma, uzushi na ufidhuli wa ma-Abu Lahab, ma-Abu Jahal na ma-Abu Sufyan, na licha ya hali ngumu za mzingira, wakati wakiwa katika “Shi’b Abi Talib” kamwe hawakujizuia na kusalimu 9

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 9

11/3/2015 2:57:47 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

amri, na kisha wakavumilia machungu ya uhamaji na dhiki na kushiriki katika vita za mfululizo za majeshi yaliyolingana na kupigana dhidi ya maelfu ya njama na hujuma, wakafanya jitihada ya kuongoza na kuendeleza watu, kwa kiasi kwamba nyoyo za majabali, mawe, majangwa na milima na barabara na mitaa ya biashara ya Makka na Madina imejaa makelele ya ujumbe wao wa muongozo wao wa kitume, na kama wangeweza kuongea na kufichua zile siri za “Hivyo nyooka moja kwa moja kama ulivyoamrishwa” mahujaji wa Nyumba takatifu ya Mwenyezi Mungu wangeweza kutambua kiasi cha mateso ambayo Mtukufu Mtume 8 aliyapata kwa ajili ya mwongozo na wokovu, na ni uzito kiasi gani wa wajibu wa wafuasi wake ulivyokuwa. Taifa letu lenye kutoa muhanga, ingawa limepatwa na machungu makubwa na kutoa muhanga wapenzi wao katika njia ya Mwenyezi Mungu, hata hivyo, kiwango cha dhulma ambacho Maimam wetu Maasumin wamepitia, kwa kiasi kikubwa sana kinazidi kile cha kwetu. O  O  O Kaaba tukufu ndio kituo kikuu cha kumuangamizia sanamu. Nabii Ibrahim Khalilullah hapo mwanzoni, na Nabii Muhammad Habibullah na mjukuu wake Mahdi mwishoni mwa kipindi kile maalum walitangaza tawhidi kutoka kwenye Kaaba. Mwenyezi Mungu alimwambia Ibrahim: “Na watangazie watu Hija; watakujia kwa miguu na juu ya kila mnyama aliyekonda kutoka katika kila njia ya mbali.” Na akaendelea zaidi kusema: “Na uitakase nyumba Yangu kwa ajili ya wanaoizunguka na waliosimama na wanaorukui na wanaosujudu.” Usafishaji huu ni wa kila udhalili, juu ya yote ambao unasimama ushirikina kama ilivyoelezwa mwanzoni mwa aya hii tukufu na kama tunavyosoma 10

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 10

11/3/2015 2:57:47 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

katika Surat-Tawba: “(Tangazo la) Kujitoa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake kwa wale mlioahidiana nao miongoni mwa washirikina.” Ni tangazo kutoka kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake kwa wanadamu katika siku ya Hija Kubwa kwamba Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wanawachukia waabudu masanamu. O  O  O Nyumba iliyotakaswa ya Mwenyezi Mungu ndio Nyumba ya kwanza kujengwa kwa ajili ya umma. Hakuna mtu wala kabila au serikali yenye kipaumbele juu yake. Watu wote wanachukuliwa kuwa wako na hadhi sawa. Nyumba hii ni ya watu wote na imetolewa kwa ajili ya mwamko na harakati za watu na manufaa kwa umma. O  O  O Nyumba hii tukufu na misikiti mingine yote imekuwa ni vituo vya mikakati ya vita, utengenezaji wa sera na mambo ya kijamii na kisiasa. Msikiti wa Mtukufu Mtume 8 haukuwa wa kujadili mambo ya ibada tu kama vile swala, saumu bali mengi yaliyojadiliwa ni ya kisiasa. Kila walipotaka kutuma watu kwenda vitani walianzia misikitini. Makka ndio mahali ambapo Mitume walitekelezea majukumu yao kinyume na sasa hivi, wote kukaliwa na watawala tu na Waislamu kuridhika na hilo. Lakini Waislamu wanatambua wajibu wao, na jambo hili linapaswa kubakia hai kwao. O  O  O Mmepata fadhila ya kuwa Mahujaji kwenye Nyumba ya Mwenyezi Mungu ambayo ndio Nyumba ya kwanza aliyoitoa kwa 11

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 11

11/3/2015 2:57:48 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

watu wote kama alivyosema: “Nyumba ya kwanza iliyojengwa kwa ajili ya watu wote ni ile iliyokuwa Makka, mahali patakatifu na muongozo kwa watu wote.� Huu ni uthibitisho kwamba Mwenyezi Mungu aliwaita watu wote kwenye Uislamu na kuiweka Nyumba hii kwa watu wa ulimwengu wote tangu mwanzo wa kazi ya utume hadi mwisho. Sio Nyumba yenye kipaumbele kwa watu maalum bali watu wote wa dunia, Mashariki au Magharibi wanatakiwa kuwa Waislam na kuhiji kwenye Nyumba hii iliyowekewa wanadamu wote. Ni bahati kiasi gani mliyoipata ninyi, kwa kupewa heshima ya Uhujaji kwenye Makka tukufu na kituo cha wahyi, na Madina kituo cha Utume. Tumuombe Mwenyezi Mungu aitakabalie Hija yenu kwa kuwapongeza.

12

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 12

11/3/2015 2:57:48 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

3 FALSAFA YA TARATIBU ZA IBADA ZA HIJA

K

utufu Nyumba ya Mwenyezi Mungu kunaonyesha jambo la ukweli kwamba tusije kuvutiwa na mwingine asiyekuwa Mwenyezi Mu\ngu, na kule kutupa mawe pale Aqabat kuna maana ya kuwapiga mawe mashetani wa kibinadamu na majini. Kwa kuyapiga mawe mashetani, unapaswa kumuahidi Mwenyezi Mungu kuyafukuza mashetani ya kibinadamu na yale mataifa makubwa yenye mabavu kutoka kwenye nchi za Kiislamu zenye kupendwa. Siku hizi ulimwengu wa Kiislamu umekamatwa na Marekani. Ni lazima mfikishe ujumbe wa Mwenyezi Mungu kwa Waislamu wa mabara mbalimbali, wa kutomwabudu yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu. O  O  O Mnapokuwa mnarudia ile “Labbeika” semeni ‘HAPANA’ kwa masanamu yote na pigeni makelele ya “HAPANA” kwa wafalme wote wa mashetani na familia za kifamle za mashetani; na mnapotufu Nyumba ya Mwenyezi Mungu ambako kunaashiria mapenzi yenu Kwake, achanisheni nafsi zenu kutokana na mapumziko na takaseni nyoyo zenu kutokana na woga juu ya yeyote mbali na Mwenyezi Mungu, na sambamba na mapenzi yenu kwa Mwenyezi Mungu, 13

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 13

11/3/2015 2:57:48 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

funueni wazi chuki zenu juu ya masanamu madogo na makubwa na mashetani na washirika wao kama Mwenyezi Mungu na mawalii wake walivyoonyesha chuki juu yao, na watu wote waliokombolewa ulimwenguni wanawachukia. Na wakati mnapoligusa lile “Jiwe Jeusi” muahidini Mwenyezi Mungu kugeuka kuwa maadui dhidi ya maadui Wake, ambao pia ni maadui wa Mitume Wake, wale waliokombolewa na walio wachamungu, na kwamba hamtanywea mbele yao, bila kujali ni nani na wapi anakoweza kuweko, na futeni woga na udhalili kutoka nafsini mwenu juu ya maadui wa Mwenyezi Mungu, na juu yao wote, na yule shetani mkuu wenyewe hawana uwezo ingawa ni wenye hali ya juu sana katika kutenda mauaji ya binadamu na ukandamizaji na utekelezaji wa maovu. Wakati wa kukimbia baina ya Safa na Marwa, jaribuni kwa utiifu na uadilifu wote kumpata Mpendwa, kwani kwa kumpata Yeye mitandao yote ya kilimwengu iliyosukwa itapasuliwa na wasiwasi wote na dhana mbaya kuporomoka, tamaa zote za kimwili na matamanio kupita, vifungo vyote vya kimaada kugeuka na ukarimu wote kushamiri, na mahusiano na mafungamano yote na Shetani na dhalimu kutenguliwa. Elekeeni Mash’aril-Haram na Arafat katika hali ya utambuzi na irfaani, na katika kila kituo ongezeni kujiamini kwenu juu ya ahadi za Mwenyezi Mungu ya utambuzi wa miliki ya wale walionyimwa, na kimya kimya na utulivu tafakarini juu ya ishara za kimungu, dhamirieni kuwaokoa wale walionyimwa na walionyang’anywa, kutoka kwenye makucha ya mafidhuli wa ulimwengu na muombeni Mwenyezi Mungu katika vituo hivi vitukufu kufungulia ukombozi kwa watu wote. Kisha elekeeni Mina na tambueni matakwa ya haki, yaani kutoa muhanga vile vitu mnavyovipenda sana kwa ajili hasa ya Mwenyezi 14

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 14

11/3/2015 2:57:48 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

Mungu, na jueni kwamba isipokuwa pale mtakapotelekeza hivyo vitu mnavyovipenda, ambavyo ndimo yamesimama mapenzi yenu binafsi na ya dunia ni kutokana navyo hivyo, hamuwezi kupanda cheo kwa Mwenyezi Mungu Mpendwa. Ni katika hali hii kwamba ni lazima umfukuze shetani na umfanye akimbie kurudi nyuma huku mkizingatia amri tukufu, na kurudia kitendo cha kumfukuza shetani na wafalme wao, na kuwafanya warudi nyuma. Katika safari hii ya kimungu, mtakwenda kumpiga mawe Shetani. Kama, Mungu aepushilie mbali, mtakuwa wamojawapo miongoni mwa kundi la shetani, basi mtakuwa mnajipiga mawe wenyewe vilevile. Ni lazima muwe watu wa kimungu ili upigaji mawe wenu uwe upigaji wa Shetani wa kimungu. Hekalu la Makka na Kaaba tukufu vitapokea mahujaji wapendwa ambao wamehuisha ibada ya Hija kwa kukimbia kutoka kwenye siasa na upotovu wa msingi na kuifanya Hija ya ki-Ibrahim na ki-Muhammad, na waliobomoa masanamu yote ya Mashariki na Magharibi na kuonyesha maana ya mwamko wa umma na kutangaza kuwachukia wapagani. Moyo wa Miqat unadunda kwa hamu ukingojea kuwapokea mahujaji kutoka nchi zisizo na wito wa Mashariki wala Magharibi kuja kuitikia ulingano wa Mwenyezi Mungu kwenye njia iliyonyooka ya ubinadamu na kukana kwao utengano wa kimakundi na kuonyesha hisia za undugu, usawa na huruma kwa mataifa yote bila ya ubaguzu wa aina yoyote, wakijaribu kuimarisha umoja miongoni mwa Waislamu wote na kupigana dhidi ya maadui wa ubinadamu na wapenda dunia na madhalimu kwa kuungana pamoja. Na Jamarat nayo inasubiri wale wenye kujitoa muhanga ambao wamewafukuza mashetani wa kila kimo, wakubwa, wa kati na wadogo na ambao wametoa mikono yao kutoka kwenye mali ya 15

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 15

11/3/2015 2:57:48 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

nchi yao, na hapa mahali patakatifu watawafukuza mashetani kutoka Makka na ujirani wake, ikiwa ni dunia yote kwa kurusha mawe yao na kutamka miito yao kwa sauti kubwa. Na Arafat, Mash’ar na Mina zitawakaribisha wale ambao wameamka na kutambua maadili ya Kiislam kwenye nchi zote zinazokandamizwa, na kuwakashifu wanasiasa bandia ambao kwa ulaghai wao na hila wamewashambulia watu wanyonge wa dunia na kudokoa rasilimali zao. Ni lazima mtambue kwamba tiba ya msingi imo kwenye umoja wa Waislamu kwa jumla, na mkusanyiko wao wa jumla katika kukata mikono ya mataifa makubwa kutoka kwenye nchi za Kiislamu na kutimiliza zile ibada za vile vituo vitukufu na maeneo ya makaburi yaliyotukuzwa kwenye nchi zao wenyewe.

16

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 16

11/3/2015 2:57:48 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

4 UMUHIMU WA KUSOMA QUR’ANI WAKATI WA HIJA

N

ingependa kuwakumbusha wapendwa Mahujaji kwamba wakati wa safari yao hii tukufu kwenye mji mtukufu wa Makka na Madina yenye nuru na vituo vyote vitakatifu wasipuuze ushirikiano wao na Kitabu kitukufu cha mwongozo, Qur’ani kwa vile chochote walichokipata na watakachokipata baadaye ni kwa neema lukuki za Kitabu hicho Kitukufu. Na wanachuoni na wanasayansi pia wasikipuuze, kwani ndio kinachotamka kila kitu – Tibian Kulli Shayin. Na ambacho kina sifa zote na malengo na maandiko ya Majina ya Mwenyezi Mungu. Na kila aina ya elimu yenye manufaa kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiutamaduni, kiroho, amani na vita. Kisha wazifikishe elimu hizi kwa wale wenye kiu nazo. Ni lazima tujue kwamba sababu ya kwa nini Kitabu hiki cha milele kimeshushwa kwa ajili ya mwongozo wa binadamu, wa kila kabila na rangi na kwa kila ardhi na eneo, hadi milele, ni kudumisha thamani ya mambo muhimu na ya msingi, na kufanya iwe wazi kwamba masuala yote yaliyotajwa kwenye Kitabu hicho, hayahusiki na zama moja ama eneo moja na kamwe usije kudhani kwamba Ibrahim, Musa na Muhammad walikusudiwa kuwa ni wa zama moja maalumu. O  O  O 17

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 17

11/3/2015 2:57:48 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

5 UMUHIMU WA KUJIFUNZA KWA MAKINI IBADA ZA HIJJA

N

i muhimu kwa Mahujaji kujifunza mas’ala za Hija, zile za wajibu na yaliyokatazwa kutoka kwa Ulamaa maarufu ili kwamba kuwe hakuna uvunjifu wowote utakaotokeza ambao utavunja juhudi zao zote, au utakaoweza kuwafanya mahujaji wasiwe waliotahiriwa na kuwasababishia matatizo. Miongoni mwa mambo ya maana ambayo ni muhimu kwa waheshimiwa mahujaji na wakuu wa misafara ni kutumia muda wao wenye thamani kusomesha na kujifunza masuala ya Hija, kwani kuzembea kwenye wajibu huu kunaweza kusababisha matatizo mengi mazito kama vile ubatilikaji wa ibada za Hija, au kuweka kituo kwao kwenye hali ya Ihraam. Ulamaa mashuhuri wa misafara wanapaswa kuwaalika mahujaji wa misafara yao wanayoisimamia kwenye vipindi vya mafunzo juu ya taratibu za ibada za Hijj, na hao mahujaji wanatakiwa kwa bidii zote wasizembee hata kidogo, bali wajaribu kujifunza masuala hayo kwa moyo mkunjufu na watekeleze ibada hizo kwa utambuzi kamili. Wakati mwingi, Mungu aepushie mbali, utendaji wenu unaweza ukabatilishwa kwa ajili ya uzembe tu, na inawezekana msiweze kuyafidia hadi mwisho wa maisha yenu na kusimama kwenu katika hali ya Ihraam, na mrudi nyumbani mkiwa mmejibebea matatizo juu yanu na familia zenu. Hizo ni kanuni za kisheria ambazo hazipaswi 18

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 18

11/3/2015 2:57:48 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

kupuuzwa. Hivyo nawasihi wakuu wa misafara kwamba ni lazima wawe waangalifu kuwaangalia mahujaji hao wakati wa vitendo vyao na wawape mwongozo unaostahiki. O  O  O Kwa vyovyote vile, kazi hiyo ya kuwaongoza na kuwaelekeza mahujaji ni wajibu na jukumu la wakuu wa misafara. Namaanisha kwamba ni moja kati ya majukumu yao. Jambo jingine muhimu ni kuwazoelesha mahujaji mas’ala za Hija. Mara nyingi mtu anawaona mahujaji wanaofanya jitihada zao zote lakini hawana elimu juu ya mas’ala hayo ya Hija na kisha wanapata matatizo hapo. Miaka michache baada ya kurejea kwao wanauliza: “Tulifanya ibada zetu za Hija namna hii, je Hija yetu inakubalika?” Au hatukufanya hili na lile; je tuko sahihi ama la? Je bado sisi ni Muhrim au hapana?” Ulamaa lazima waitishe mikutano ya kuwafundisha watu kanuni na ibada za Hija, kuwaelezea zile kanuni za wajibu na matendo yaliyokatazwa katika mikusanyiko ya kila siku na watu lazima wahudhurie mikusanyiko kama hiyo kama ipo. Wanapaswa kwenda kujifunza masuala ya Hija ili wasije wakapata mzigo baadaye, wakiwa wamerejea nyumbani, wakiwa na shaka kuhusu iwapo kama ibada zao zilitendwa kikamilifu ama la. Wakati ukiwa umejifunza kanuni hizo, utekelezaji wako utakuwa hauna makosa. Msiseme kwamba mnataka kufanya safari ya Makka kwa vyovyote itakavyokuwa. Sasa, mtu anafanya Ziara kwenye makaburi matukufu. Hakuna tatizo iwapo Ziara yake itaishia bure tu. Hatapata tatizo kubwa wakati huo, lakini sio kwa mahali kama hapa, Makka na Madina ambapo atakabiliana na matatizo. Atapaswa kufanya Hija nyingine. Tafuta kujifunza kwa faida yako mwenyewe ili usije ukafanya makosa na kujiingiza kwenye matatizo baadaye. Hili ni jambo jingine la kutilia maanani. 19

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 19

11/3/2015 2:57:48 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

6 HIJA NA UIMARISHAJI WA UMOJA MIONGONI MWA WAISLAMU

W

aislamu wote wanaume kwa wanawake lazima wazingatie kwamba moja ya vipengele muhimu vya falsafa ya Hija ni uundaji wa kufahamiana na kuimarisha undugu miongoni mwa Waislamu. Kwa hiyo ni wajibu wa Ulamaa na wakuu wa misafara kujadili matatizo yao ya msingi ya kisiasa na kijamii pamoja na ndugu zao ili kuweza kutengeneza mpango wa kuyaondoa matatizo hayo ili kuwawezesha wale ndugu wengine kwenda kuyaweka wazi maazimio hayo kwa Ulamaa wao na wenye mamlaka wengine pale watakaporejea kwenye nchi zao husika. Hija ndio mahali bora pa kukutania kwa ajili ya kufahamiana kwa mataifa ya Kiislamu, ambapo wanaume kwa wanawake kutoka kote duniani wanaweza kukutana, katika Nyumba ambayo ni mali ya Waislamu wote na wafuasi wa Ibrahim Hanifa, na kupuuza tofauti zao binafsi za hadhi, rangi na utaifa au sifa za kimbari, na kurejea kwenye nchi zao za asili na kudhihirisha unyofu wao wa undugu wa Kiislamu kwa kutekeleza zile kanuni za maadili kubwa za Kiislamu na kuepuka magomvi na kujitukuza wenyewe. O  O  O Ni lazima tuzingatie kwamba falsafa muhimu ya kijamii ya kuitisha mkusanyiko mkubwa kama huo kutoka kote duniani, mahali 20

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 20

11/3/2015 2:57:48 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

hapa patakatifu na sehemu ya mashukio ya wahyi ni uunganishaji wa Waislamu wa dunia na kuimarisha umoja miongoni mwa wafuasi wa Mtume wa Uislamu 8 na wa Qur’ani tukufu katika mapambano yao dhidi ya madikteta wa ulimwengu, na kama, Mungu aepushilie mbali, matendo yenye dosari ya baadhi ya mahujaji yakiathiri umoja huu, na kusababisha kutopatana na mifarakano, hili litamuudhi Mtume wa Mwenyezi Mungu 8 na kusababisha ghadhabu na adhabu ya Mwenyezi Mungu. Waheshimiwa mahujaji wakati wanapokuwa karibu na mahali pa mashukio ya rehema, Nyumba ya Mwenyezi Mungu, ni lazima wawachukulie watu wote kama waja wa Mwenyezi Mungu, kwa huruma za Kiislam na undugu, na kuwaona wote kama ndugu, bila ya kujali tofauti zao za kimbari. Wote ni lazima waungane na kutenda kama mkono mmoja wa Qur’ani ili kuweza kuwashinda maadui wa Uislamu na ubinadamu. O  O  O Mahujaji watukufu kwenye Nyumba ya Mwenyezi Mungu, wa utaifa au madhehebu yoyote ile, lazima watii na kunyenyekea kwenye amri za Qur’ani Tukufu, kusimama dhidi ya gharika ya kishetani angamizi ya upinga Uislamu ya Mashariki na Magharibi na wafuasi wao wanaolindwa, huku mkishikana mikono ya kindugu, mkizingatia kabisa aya za Qur’ani zinazowalingania Waislamu kushikamana na “kamba ya Mwenyezi Mungu” kupiga vita harakati za mifarakano, na mchukue manufaa yaliyo makubwa zaidi kiroho na kisiasa kutoka kwenye wajibu huu wa kiibada-kisiasa mahali hapa patakatifu ambapo kwa hakika pamejengwa kwa ajili ya manufaa ya ulimwengu wa waabudu Mungu Mmoja (wanatawhidi), na tilieni maanani siri ya Ismail kutolewa muhanga na Nabii Ibrahim, 21

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 21

11/3/2015 2:57:48 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

jambo ambalo linaonyesha jinsi mtu anavyolazimika kustahimili kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Hili linaonyesha lile lengo kuu la Uislamu na kutetea upeo wa kiwango cha mtu kutoa muhanga tunda lake la maisha analolipenda sana. Mashetani wakubwa, wa kati na wadogo lazima wafukuzwe kutoka mahali patakatifu pa Uislamu na Ka’aba tukufu na kutoka kwenye nchi za Kiislamu na hivyo kuitikia “Labbeika” kwenye mialiko ya Mwenyezi Mungu. O  O  O Katika vituo hivyo vitakatifu, wekeaneni ahadi na kila mmoja wenu juu ya umoja na ushirikiano, mkimtegemea Mwenyezi Mungu, katika kusimama imara dhidi ya maaskari wa kikafiri na wenye fitna, na kuepuka mtengano na mikwaruzano. “…..Msigombane wenyewe kwa wenyewe, kwani hilo litakufanyeni muwe wadhaifu, na kuweni wenye subira, hakika Mwenyezi Mungu yuko na wenye subira.” Athari na manukato ya uaminifu wa Uislamu ambavyo ndio msingi wa ushindi na nguvu, vitakwisha kwa mifarakano na misimamo ya vikundi iliyoegemea kwenye matamanio ya kimwili na kinyume na amri za Mwenyezi Mungu. Wakati ambapo mkusanyiko katika shughuli za haki na umoja, na utangazaji wa tawhid (Mungu Mmoja) ambayo ndio chanzo cha heshima ya Waislamu kutaongozea kwenye ushindi. Enyi Waislamu wa ulimwengu! Inakuwaje? Mlikuwa na uwezo wa kuangamiza nguvu kubwa za wakati ule licha ya uchache wenu kiidadi, wakati wa siku za mwanzo za Uislamu na mkaleta taifa bora la Kiislam kubwa kiasi kile. Lakini sasa, pamoja na idadi zaidi ya bilioni moja duniani kote, na kumiliki rasilimali kubwa za utajiri wa nchi ambao unaweza kutumika kama silaha yenye nguvu sana ya kisiasa dhidi ya maadui, bado mmekuwa dhaifu mno na kufedheheka! 22

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 22

11/3/2015 2:57:48 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

Chunguzeni njia za kuleta umoja miongoni mwa Waislamu wa madhehebu na makundi yote, na kuhusu mambo ya kisiasa ambayo ni ya kawaida miongoni mwao, tafuteni ufumbuzi wa matatizo ambayo yanaletwa na maadui jeuri wa Uislamu, baya kabisa likiwa ni kupandikiza mbegu za migogoro miongoni mwa safu za Waislamu. Kama mjuavyo, kwa karne nyingi sasa, waliochochea moto katika uwanja huu wa mapambano ni wale waporaji wa Magharibi na Mashariki ambao wana hofu na hii idadi ya bilioni ya Waislamu, kwa nguvu zao zote na kwa msaada wa mawakala wao wapotovu ili kumiliki mustakabali wa Waislamu, na kuwatawala na kupora rasilimali zao zisizo na ukomo. O  O  O Ufumbuzi ni nini leo hii? Waislamu na watu walionyimwa wa dunia hii wafanye nini kuyapindua masanamu haya? Dawa ya msingi pekee wa kung’oa utatanishi wote na kuchoma dhulma na upotovu ni umoja sio tu wa Waislamu bali pia na wa walionyimwa na kufungwa minyororo wa dunia nzima, na umoja huu ambao juu yake Uislamu mtukufu na Qur’ani vinausisitiza lazima upatikane kupitia ulinganiaji mpana, na kituo cha ulinganiaji huu na miito ni Makka Tukufu wakati wa mkusanyiko wa mahujaji, mwito ambao ulianza na Nabii Ibrahim Khalilullah na Muhammad Mustafa 8 na utafuatwa na mtukufu aliyebakia wa Mwenyezi Mungu – Baqiyatullah – nafsi zetu ziwe muhanga kwa ajili ya hatua zake tukufu, wakati wa Mwisho wa Wakati. Ibrahim A aliamrishwa kuwaita watu kutoka pande zote, waje kukusanyika wote waje kung’amua manufaa yao, manufaa ya jumuiya, ya kisiasa, kijamii, kiuchumi na ya kiutamaduni, mje ili muone jinsi ninyi kama Mtume wenu, kwa hiari kabisa mlivyotoa 23

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 23

11/3/2015 2:57:48 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

muhanga tunda lenu la uhai lenye thamani kubwa kabisa, na kisha mkiri kwamba binadamu wote lazima wawaigize. Ninyi ambao mmetupilia mbali masanamu yote na kufuta kutoka akilini mwenu kila kitu isipokuwa Mwenyezi Mungu, chochote kile kingine, jua, mwezi, maumbo, wanyama na/au binadamu. Ulisema kwa uaminifu kabisa pale uliposema: “Na wote lazima waige kutoka kwa baba wa tawhid na baba wa mitume watukufu.” Katika Surat Tawbah, ambayo imeamriwa kusomwa katika mkusanyiko wa jumla hapo Makkh, tunasoma: Tangazo kutoka kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wa watu katika ile siku ya Hija Kubwa, kwamba Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wanachukizwa na waabudu masanamu. O  O  O Miongoni mwa wajibu wa Mahujaji katika mkusanyiko huu ni kuuita umma na jumuiya zote za Kiislamu kwenye umoja na usuluhishaji wa migogoro miongoni mwa makundi ya Waislamu, ambao lazima ufanywe na mubalighina, makhatibu na waandishi, na wanapaswa kufanya juhudi kuponya hili tatizo kubwa mno na kujaribu katika njia ya kuanzisha kundi la watu wanaodhulumiwa, kwani kwa umoja wa kundi na umoja wa maneno na kukamata wito wa “Hakuna Mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu – La – ilaha – ila – Llah,” wanaweza wakajikomboa wenyewe kutokana na utumwa wa mamlaka ya shetani wa kigeni na wakoloni na kuyamudu matatizo yao kwa undugu wa Kiislamu. O  O  O Uelezee ukweli huu kwa watu wote, kwamba maadui wa Uislamu wanajaribu, kwa nguvu zao zote, kupandikiza mbegu za migogoro miongoni mwa jamii za Kiislamu na wanafanya kila juhudi kusafisha 24

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 24

11/3/2015 2:57:48 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

njia kwa ajili ya umilikaji upya wa nchi zote za Kiislamu na kupora rasilimali zao. Kwa hiyo ni muhimu sana kuepuka vitendo vya mifarakano, na huu ni wajibu wa kidini na wa kimungu. Mnapaswa kuzingatia kwamba tiba ya msingi imo kwenye kuunganishwa kwa Waislamu wote na huu mkusanyiko uliopo sasa, na kukata mikono ya mataifa makubwa kutoka kwenye nchi za Kiislamu na kutimiliza katika nchi zenu wenyewe ibada zote za Kiislamu zinazotekelezwa katika vituo vitakatifu na makaburi yaliyotukuzwa. O  O  O Inategewa kwamba mahujaji watukufu wote wa nchi za Kiislamu watajaribu kudumisha umoja wao na hawatapuuza udugu wao ulioamriwa na Mwenyezi Mungu miongoni mwa Waislamu, na kuepuka umakundi ambao ni kazi na utaratibu wa Shetani na mashetani wa kibinadamu. O  O  O Ni muhimu kwa mahujaji wa Nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu kukemea kuchukizwa kwao dhidi ya madikteta na madhalimu kwenye mkusanyiko huu wa sasa na umati wa watu unaonguruma kwa sauti kubwa kabisa, kushikana mikono ya kindugu kati yao wote kwa nguvu na mkazo kabisa, na kuepuka kutoa muhanga manufaa mazuri ya Uislamu na ya Waislamu wanaoonewa kwenye mifarakano na uzalendo wa kitaifa, na wawaelimishe ndugu zao Waislamu kwa kiasi itakavyowezekana, juu ya umuhimu wa kudumisha umoja wao na kutupilia mbali Chuki zao za Zama za Jahiliya ambazo zitaishia kwenye faida na manufaa ya waporaji wa kilimwengu na washirika wao. Hili linakaribisha msaada wa Mwenyezi Mungu na ahadi Yake kwa matumaini kabisa itawajumuisha na wao. Lakini kama, Mungu 25

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 25

11/3/2015 2:57:48 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

aepushilie mbali, watafuata vitendo vya waporaji wa kiulimwengu, wabaya wao hasa wakiwa ni viongozi wa kidini wafuasi wa misimamo ya kivikundi na ya kubuniwa, basi watakuwa wametenda dhambi kubwa na watapatwa na laana ya Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu zote na kubakia kwenye minyororo ya mataifa makubwa, na ni lazima wote tukimbilie kwenye hifadhi ya Mwenyezi Mungu. O  O  O Enyi Waislamu wa ulimwengu, enyi wafuasi wa dini ya Mungu Mmoja, siri ya utatanishi wote wa nchi za Kiislamu imo kwenye kutengana kwao na kutokupatana, na siri ya ushindi wao imo kwenye umoja wao na kupatana. Mwenyezi Mungu amelisema hili katika mstari mmoja: “Shikamaneni katika kamba ya Mwenyezi Mungu kwa pamoja na wala msifarikiane.” Kushikamana kwenye kamba ya Mwenyezi Mungu yenye usalama kuna maana ya kudumisha umoja wa Waislamu wote kwa ajili ya Uislamu na manufaa ya Waislamu na kuepuka kutoelewana na umakundi ambako ndio msingi wa matatizo yote na ajizi. Tumuombe Mwenyezi Mungu awajaalie Waislamu na hadhi ya Uislamu na umoja na kupatana kwa Waislamu wa dunia nzima. Ni lazima mzingatie kwamba mkusanyiko huu mtukufu na mkubwa ambao unaitishwa kila mwaka katika ardhi hii takatifu, kama ilivyoagizwa na Mwenyezi Mungu, unawajibisha nchi za Kiislamu kufanya juhudi ya kutimiliza yale malengo matukufu ya Kiislamu na makusudio ya fahari kabisa ya dini hii halisi na kuendeleza na kuwaboresha Waislamu na kusaidia kuunganisha umma wa Kiislamu. O  O  O 26

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 26

11/3/2015 2:57:48 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

Tazameni! Enyi Waislamu wenye nguvu wa dunia hii! Amkeni, tambueni uwezo wenu na dunia itawatambueni. Nyenyekeeni kwenye amri za Mwenyezi Mungu na Qur’ani tukufu na tupilieni mbali migogoro yenu ya kimbari na kimaeneo iliyosababishwa na waporaji wa dunia hii na mawakala wao wakorofi ili kuwaporeni na kuikanyaga hadhi yenu ya kibinadamu na Kiislamu. Wafukuzeni wanazuoni mamluki, na wazalendo wasio na ujuzi ambao madhara yao kwa Uislamu hayana tofauti na ya wale waporaji wa kidunia. Wao wanaonyesha sura ya kubuniwa na wanawafungulia njia hao wanyang’anyi. O  O  O Enyi Waislamu wa ulimwengu huu, waumini wa kweli wa Uislamu, amkeni na muungane chini ya bendera ya Tawhid na kheri za Uislamu na muikate mikono ya udanganyifu ya mataifa makubwa kutoka kwenye nchi zenu. Telekezeni magomvi yenu na tamaa za kimwili, kwani kwa kweli ninyi mnacho kila kitu. Tegemeeni utamaduni wa Kiislamu, piganeni na Magharibi na umagharibi, simameni imara kwa miguu yenu, pambaneni na wanachuoni wenye umagharibi na umashariki na mrudishe utambulisho wenu halisi, kwani wanachuoni mamluki wameufanyia umma na nchi fitina kubwa ambayo, isipokuwa pale mtakapofuata Uislamu wa kweli na mkaungana, vinginevyo mtahangaishwa na upotovu ule ule kama uliokuwa nao hadi leo. Huu sasa ndio wakati wa umma kuwazindua wanachuoni wao na kuwaokoa kutoka kwenye udhalili na kusalimu amri wao wenyewe kwa Magharibi na Mashariki, kwani leo ndio siku ya harakati za umma na muongozo wa viongozi wa awali wa watu. Ni lazima mtambue kwa uhakika kwamba nguvu zenu za kiroho zitashinda 27

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 27

11/3/2015 2:57:48 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

nguvu nyingine zote na idadi yenu ya bilioni moja pamoja na hazina zenu zisizo na ukomo mnaweza mkazishinda nguvu zote kuu za dunia. Msaidieni Mwenyezi Mungu apate kuwasaidieni. Enyi bahari Kubwa ya Waislamu! Pingeni kwa makelele dhidi ya maadui wa ubinadamu na muwapindue, kwani wakati mtakapomzingatia Mwenyezi Mungu Mkuu, na mkafuata mafundisho ya kimbinguni, basi Mwenyezi Mungu pamoja na majeshi makubwa watakuwa upande wenu. O  O  O

28

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 28

11/3/2015 2:57:48 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

7 HIJA, WAKATI WA KUREKEBISHA NA KUTATUA MATATIZO YA WAISLAMU

S

asa kwa kuwa huu ni msimu wa Hija kwenye Nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu, na wakati ambapo Waislamu kutoka sehemu zote za dunia wamekusanyika hapa, ni muhimu kuzingatia moja ya sababu kuu kwa ajili ya mkusanyiko huu mkubwa na kuangalia hali za kijamii na kisiasa za nchi za Kiislamu, kujifunza kuhusu matatizo ya washirika wetu kidini na kufanya kila juhudi katika kuwasaidia kuyaondoa matatizo yao, kwa kiasi wajibu wa Kiislamu na kimaadili unavyomtaka afanye. Bidii na juhudi katika mambo ya Waislamu ni wajibu muhimu wa Kiislamu. Kwa mahujaji wote kwenye Nyumba takatifu Mwenyezi Mungu awasaidie. O  O  O

Sasa, kwa kuona kwamba kutokana na uzembe na unyonge wa mataifa ya Kiislamu, makucha ya kishetani ya ukoloni yamefika kwenye vina vya mbali sana vya nchi kubwa za watu wa Qur’ani na hazina zetu zinamiminwa vinywani mwao, chini ya jina la kisingizio cha utaifishaji, utamaduni wenye sumu wa kibepari umepenyeza hadi kwenye vijiji vya mbali vya nchi za Kiislamu na ukauzidi mwendo utamaduni wa ki-Qur’ani, makundi makubwa ya vijana 29

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 29

11/3/2015 2:57:48 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

wetu wanachukuliwa katika kuwahudumia wageni na kila siku, kwa jina jipya la kilaghai, vijana wetu wanapotoshwa; mataifa wapendwa wa Uislamu ambayo yamekusanyika kwenye ardhi hii ya wahyi kutekeleza ibada ya Hija yanatakiwa kutumia fursa hii na kutafuta ufumbuzi. Badilishaneni mawazo ya kutatua matatizo ya Waislamu na mkubaliane kwa pamoja. Zingatieni kwamba mkusanyiko huu mkubwa unaokutana kwenye ardhi tukufu kila mwaka, kama ilivyoagizwa na Mwenyezi Mungu unakuwajibisheni ninyi mataifa ya Kiislamu kufanya kila juhudi kwa ajili ya ufanikishaji wa malengo na makusudi matukufu ya dini halisi ya Uislamu na ya maendeleo na uinuaji wa Waislamu na vilevile umoja na mshikamano miongoni mwa jamii za Kiislamu. Patanisheni maoni yenu na mfikie ushirikiano kati yenu kwa ajili ya kung’oa saratani ya ukoloni. Tambueni vitatanishi vya kila taifa la Kiislamu kutoka kwenye ndimi za wananchi wake na msiache juhudi yoyote katika kutatua matatizo yao. Fikirieni kuhusu masikini na mafukara wa nchi za Kiislamu. Tafuteni ufumbuzi kwa ajili ya ukombozi wa ardhi ya Kiislamu ya Palestina kutoka kwenye makucha ya Wazayuni, adui mkaidi wa Uislamu na ubinadamu. Msiache kushirikiana na kusaidia watu wanaojitoa muhanga, ambao wanapigana kwa ajili ya ukombozi wa Palestina. Wasomi wanaoshiriki katika kongamano hili kutoka nchi yoyote ile, wanatakiwa kuyaelimisha mataifa yote kwa kutumia kauli zenye hekima, zinazogawanywa miongoni mwa Waislamu katika ‘ardhi ya wahyi,’ na kwenye nchi zao wakati wa kurejea nyumbani. Katika kauli zao wanapaswa kuwataka wakuu wa nchi za Kiislamu kutilia maanani malengo ya Uislamu, kuacha tofauti zao na kutafuta suluhisho kwa ajili ya wokovu wao kutoka kwenye makucha ya wakoloni.

30

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 30

11/3/2015 2:57:48 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

O  O  O Makusudio mengi ya kisiasa yanalenga katika kuitisha mikutano kama vile swala za jamaa za kila siku, Swala za Ijumaa na hususani mkusanyiko usiokadirika thamani yake wa Hija, miongoni mwayo ikiwa ni kujifunza kuhusu matatizo ya msingi na ya kisiasa ya Waislamu, ambayo yanaweza yakajadiliwa kupitia mikutano ya wanachuoni, wasomi na mahujaji watiifu kwenye Nyumba Takatifu ya Mwenyezi Mungu, na kutafuta ufumbuzi na kuuonyesha wazi kwa watu wa nyumbani kwao pale wanaporejea na kujaribu kuyaondoa. O  O  O Kwenye kongamano hili tukufu la Hija, kwanza jadilianeni kuhusu matatizo ya msingi ya ulimwengu wa Kiislam, na pili ndipo mjadiliane kuhusu matatizo maalum ya kila nchi ya Kiislamu, mjue ni nini mabepari na vibaraka wao walichokifanya katika nchi hizo dhidi ya ndugu zetu Waislamu. Katika kongamano hili tukufu, watu wa kila nchi lazima waeleze matatizo ya nchi yao wenyewe kwa Waislamu wa nchi zingine. Wakusanyeni pamoja mahujaji wa nchi nyinginezo, mjadiliane juu ya manufaa ya ulimwengu wa Kiislamu na matatizo ya Waislamu na mchukue vitendo vya kiuamuzi ili kutatua matatizo hayo na mkamilishe maadili matukufu ya Kiislamu. Chunguzeni juu ya njia ya kuyaunganisha madhehebu na makundi ya Kiislamu na mtafute tiba kwa ajili ya matatizo yao ya jumla yanayowakandamiza na ambayo yamesababishwa na maadui fidhuli wa Uislamu, baya zaidi kati ya hayo likiwa ni kutofautiana miongoni mwa safu za Waislamu. Kama tujuavyo wote, katika karne za hivi karibuni, wachochezi wa mgogoro huu walikuwa ni wale waporaji wa Magharibi na 31

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 31

11/3/2015 2:57:48 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

Mashariki, wanaohofia umoja wa Waislamu bilioni moja na wanajaribu, kwa nguvu zao zote, kuongeza tofauti hizo baina ya Waislamu ili kuweza kuwatawala Waislamu wa dunia nzima, kudhibiti mustakabali wao na kupora hazina zao zisizo na mwisho. O  O  O Mkusanyiko huu ambao umeandaliwa bila matata na Uislamu, unachukuliwa kama wajibu wa kidini kwa wale ambao wana uwezo, na zoezi lililokokotezwa kwa ajili ya Waislamu wote, kama tendo la utii kwa Mwenyezi Mungu. Jambo muhimu hapa ni kwamba Waislamu wote kwa namna moja, wakiwa huru kutokana na urasimu wa aina yoyote au hali ya anasa na starehe, wakitelekeza hadhi zote za kijamii, wakiwa wamejizingira kwenye shuka la kujifunika na nguo mbili, wanahudhuria kwenye vituo hivi vitukufu, na la muhimu zaidi ya hilo ni, ule uwezekano wa wao kuweza kuelezana kila mmoja wao juu ya matukio ya nchi zao katika kipindi cha mwaka uliopita na kufikiria juu ya namna ya kuondoa matatizo yanayoukabili ulimwengu wa Kiislamu. Hii ndio sababu kubwa na ya msingi ya mkusanyiko huu mkubwa wa Waislamu huko Hijaz. Kwa masikitiko makubwa kabisa, sisi Waislamu huwekwa mbali na Uislamu na kutengwa na ukweli wa Uislamu, kamwe tunakuwa hatuna hata wazo moja kwamba, kwanza kabisa wale wote wenye uwezo wa kumudu Hija, huwa hawaendi na wakapata hadhi hii ya Hija kwenye Nyumba ya Mwenyezi Mungu. Pili, wale wenye utambuzi, waandishi, wanachuoni na wasomi lazima wakusanyike pale kwa pamoja, wayaangalie matatizo ya Waislamu wa dunia nzima na wajaribu kutatua chochote kile watakachoweza. Kwa bahati mbaya sana, mafanikio yetu sasa kutoka kwenye kuhiji Makka ni ule mkusanyiko tu wa makundi ya 32

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 32

11/3/2015 2:57:48 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

umma wa kawaida tu, na wale wenye uwezo wa kuleta manufaa yatakiwayo, viongozi wa serikali na watu mashuhuri ambao wanaweza kuchunguza na kujifunza vikwazo na matatizo ya kisiasa na kijamii ya Waislamu wanapuuzwa na kuachwa nyuma. O  O  O Mikusanyiko yote inayoandaliwa katika nchi za Kiislamu, katika kila mji na kijiji, ni matamasha ya kijamii na kisiasa yanayoshughulika na kuwataka wakaazi wa kila mji kukusanyika pamoja na kujaribu kutatua matatizo ya mji wao. Swala za jamaa za kila Ijumaa pia ni ibada za kijamii na kisiasa zinazoitisha watu wengi na zinalengwa kutatua matatizo ya jamii. Mkusanyiko wa Makka ndio mkusanyiko mkubwa kabisa, ambao kuitishwa kwake huko kuko nje ya uwezo wa serikali yoyote ile. Na Mwenyezi Mungu ameamuru kwamba Waislamu, bila ulazimishaji mkubwa na kutwisha mzigo wa matumizi juu ya serikali zao, kukutana pale, lakini kwa bahati mbaya kabisa, jambo hilo halichukuliwi fursa yake kisawasawa. O  O  O Katika mwenendo mzima wa Hija, matatizo ya watu wa nchi ambazo mahujaji wake wamehudhuria lazima yatazamwe kwa undani. Hali za Waislamu katika mwaka uliopita lazima ichunguzwe. Jinsi uhusiano baina ya taifa na serikali yake, baina ya kila serikali na mamlaka za kishetani. Baina ya nchi moja na nyingine, baina ya wanachuoni wa nchi moja na nyingine, na mwishowe ni upi msimamo wao juu ya Hija. Haya ni mambo ambayo ni lazima yaangaliwe na kuchunguzwa, na hili ndio jambo ambalo kwalo Hija 33

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 33

11/3/2015 2:57:49 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

imekusudiwa. Hija imekusudiwa kwa ajili ya kuchunguza matatizo ya mwaka mzima ya Waislamu na kujaribu kuyaondoa. Wanachuoni wa mabaraza ya vitala wa eneo moja au nje ya eneo wanashauri kwamba Hija na ibada zake iko huru kutokana na mambo ya kisiasa. Hivyo basi wanamshutumu Mtume wa Mwenyezi Mungu 8, wanawashutumu makhalifa wa Uislamu na Maimam maasumin. Wao hawaelewi kwamba kuyatazama mambo haya kumekuwa ndio madhumuni makuu ya Hija; imekuwa ni kwa ajili ya mwamko wa watu, kwa ajili ya kujifunza matatizo ya Waislamu na kujaribu kuyaondoa na kwa ajili ya kujenga undugu na uchangamfu miongoni mwa Waislamu. O  O  O Kwa unyenyekevu kabisa napenda kuweka wazi kwa mahujaji kutoka nchi yoyote ile na taifa na madhehebu yoyote ile kuzingatia kwamba ninyi wote ni umma mmoja wa Kiislamu, wafuasi wa Mtukufu Mtume 8 na watiifu kwenye Qur’ani Tukufu. Wote mna maadui wadanganyifu wamoja, ambao kwa kupanda mbegu ya kutofautiana, kwa msaada wa watetezi na watendaji wao walijaaliwa maovu, vyombo vya habari na propaganda za ugawanishaji, katika historia yote hususan katika karne za hivi karibuni na hususan katika zama hizi wamezifanya serikali zote na mataifa ya Kiislamu kuwa watumwa wao na kupora rasilimali zenu tajiri na mapato ya kazi za wanaoonewa, na wanafanya juhudi zote kuzitwaa serikali hizo, kiupofu na kikamilifu kabisa kwenye huduma zao wenyewe, ili kuyafundisha mataifa kuwa walaji wa bidhaa zao, na kukwamisha ukuaji wa ubinadamu na uanzishwaji wa viwanda, na kuongeza utegemezi wao na mafungamano na Mashariki na Magharibi, na kuwanyima watu fursa ya kufikiri juu ya uhuru wao na kutumia 34

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 34

11/3/2015 2:57:49 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

ari zao za uvumbuzi, na kuwakaba wale ambao wana shauku ya kuelimisha mataifa. Dhiki zinazopiga mbizi zinazoonekana kwenye nchi za Kiislamu na nchi nyingine zinazokandamizwa zimetokana na njama hizo hizo za maadui wa pamoja wa Waislamu na mataifa yanayokandamizwa. Sasa kwa vile mmekutana katika kituo cha Uislamu unaoleta uhai, kama ilivyoagizwa na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake 8 bila kujali ni taifa gani au madhehebu gani unayotoka tafuteni tiba ya maradhi haya mabaya na saratani angamizi. O  O  O Katika kongamano hili kubwa ambalo haliwezi kuitishwa na yeyote isipokuwa kwa uwezo wa kudumu wa Mwenyezi Mungu, Waislamu lazima wayaangalie matatizo yao ya pamoja na kufanya juhudi za kuyaondoa kupitia mashauriano ya pamoja; moja kati ya matatizo makubwa na ya msingi ni mfarakano miongoni mwa Waislamu, ambao kwawo baadhi ya wale wanaoitwa ati viongozi wa nchi za Kiislamu wenyewe ndio chanzo, na katika uondoshaji wake hakuna hatua thabiti iliyokwisha kuchukuliwa mpaka sasa. Zaidi ya hayo wahalifu hao walanguzi, ambao wanafaidika kutokana na tofauti hizo baina ya mataifa na serikali zetu huwa wanachochea miali ya moto wa migogoro yetu, ambayo imetengenezwa na watendaji wao wapinga Mungu, na kila mara msingi wa umoja wa Waislamu unapojengwa, wao wanajaribu kwa nguvu zao zote kupinga na kupanda mbegu za faraka. Waislamu lazima wawe na fikra ya kuelimisha na kuwasahihisha wakuu wa nchi zetu ambao wamesalimu amri, na kuwazindua waamke, ama kwa kuwaasa au vitisho, kwani wanaweza kujiangamiza wenyewe na kutapanya maslahi ya nchi za Kiislamu. Waonyeni 35

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 35

11/3/2015 2:57:49 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

wale wahadimu wanyenyekevu kwa maarifa sana, jihadharini na vitisho vya wanafiki na watu wa kati wa nguvu za kibepari za kidunia. Msikae kimya na kubweteka, mkiangalia tu kushindwa kwa Uislamu na utekwaji nyara wa rasilimali na hazina na kukosewa kwa Waislamu wachamungu. O  O  O Leo hii kile Qibla cha kwanza cha Waislamu kimetwaliwa na Israili, saratani ya Mashariki ya Kati. Waisraili wanashambulia na kuua halaiki ya ndugu zetu Wapalestina na Walebanoni kwa nguvu zao zote. Leo hii Israili inajaribu, kwa kutumia njia zao zote za kishetani kutawanyisha majeshi ya Kiislamu. Ni wajibu kwamba Waislamu wote wajiandae kupigana kikamilifu kupigana dhidi ya Israili. Leo hii nchi za Kiislamu za Afrika zinatapatapa chini ya nira za utumwa wa Marekani na wageni wengine na wahadimu wao wanyenyekevu. Leo hii Waislamu Waafrika wananyanyua sauti zao zaidi na zaidi wakidai haki. Kwenda Hija lazima kujibu madai haya. Kuizunguka Ka’aba ni ishara kwamba hamtatafuta kumwendea yeyote mwingine. Kutupa mawe pale Aqaba maana yake ni kuwapiga mawe mashetani wote, wa kibinadamu na majini. Kwa kutupa mawe, mnamuahidi Mwenyezi Mungu kwamba mtawafukuza mashetani wa kibinadamu na mataifa makubwa kutoka kwenye nchi za Kiislamu. Leo hii ulimwengu wa Kiislamu umeingiliwa na kuzingirwa na Marekani. Mnapaswa kufikisha ujumbe kwa Waislamu wa mabara tofauti, utokao kwa Mwenyezi Mungu kwamba ni lazima wasimuabudu yeyote yule isipokuwa Mwenyezi Mungu tu. O  O  O 36

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 36

11/3/2015 2:57:49 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

Tafuteni ufumbuzi kwa ajili ya ukombozi wa ardhi ya Palestina kutoka kwenye makucha ya Wazayuni – adui muovu wa Uislamu na ubinadamu. Msishindwe kushirikiana na kuwasaidia wale wanaojitoa muhanga ambao wanapigana kwa ajili ya ukombozi wa Palestina. Mataifa ya Kiislamu lazima yafikirie juu ya ukombozi wa Palestina, na yautangazie ulimwengu kuchukizwa kwao kukubwa juu ya ufumbiaji macho na kuridhika kwa viongozi wanaotia aibu na kujisalimisha wenyewe, ambao kwa jina la Palestina wameharibu maadili ya watu wa ardhi iliyokaliwa kimabavu na Waislamu wa eneo hilo. Msiwaruhusu wasaliti hawa kuharibu hadhi na heshima ya taifa la kishujaa la Palestina kwa mazungumzo na kurudia mara kwa mara, kwani mapinduzi haya bandia na duni yana njia ya kupata msaada kwa Marekani na Israili kwa jina la ukombozi wa “Quds.” Kwa mshangao, kwa kila siku inayopita, tangu yale maangamizi ya kumwaga damu kwa wingi ya kuitwaa Palestina bila ya haki, wakuu wa nchi za Kiislamu wanazidi kuwa wakimya na wenye kuridhika, na ule mpango wa kubeza maendeleo na propaganda za Israili kwa wito wa kuikomboa Jerusalem hausikiki tena, na kama nchi kama Irani, ambayo yenyewe inateseka kutokana na vita na vikwazo, itajaribu kutoa sauti ya kuwaunga mkono watu wa Palestina, wao wataishutumu. Zaidi ya hayo wana hofu na suala la kwamba siku maalumu itukuzwe na kuitwa “Siku ya Quds.” Pengine wanaendelea kufikiri kwamba kwa kupita kwa wakati, nyakati zimebadilika na hali na sura ya maovu ya Israili na mbwamwitu wenye kiu ya damu wa Kizayuni wameachana na fikra zao za kiovu za kuingilia na kukalia ardhi za kuanzia mto Nile hadi mto Furati. Viongozi watukufu na watu wa Irani na mataifa ya Kiislamu hawataacha kamwe kupigana dhidi mti muovu na kuung’oa kabisa. Kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, juhudi zote lazima zifanyike kutumia vyema yale matone ya 37

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 37

11/3/2015 2:57:49 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

damu yaliyotawanyika ya wafuasi wa Uislamu, nguvu ya kiroho ya Waislamu na uwezo wa nchi za Kiislamu, na kwa kuunda majeshi ya upinzani ya Hizbullah kote duniani, kuifanya Israili itubie juu ya maovu yake yaliyopita na kuziacha huru zile ardhi za Waislamu walizozikalia kwa mabavu kutoka kwenye makucha yao. Kama nilivyoonya mara kwa mara, kabla na baada ya mapinduzi na katika mwaka uliopita, kwa mara nyingine tena ninawaonyeni juu ya uvimbe ambukizi wa Uzayuni ndani ya mwili wa nchi za Kiislamu na kutangaza kuwepo kwa uungaji mkono usio na unyimi, wangu binafsi na wa taifa la Iran na serikali yake kwa wapiganaji wote wa Kiislamu wenye ghera katika njia ya ukombozi wa Quds na kuonyesha shukurani zangu kwa vijana wapenzi wa Lebanoni ambao walisababisha kupatikana heshima na utukufu kwa Waislamu na aibu na fedheha kwa ulimwengu wa waporaji, na kuwaombea wale wapenzi wote, ambao ndani ya ardhi zinazokaliwa au mipakani mwake, wakitegemea silaha zao wenyewe na imani zao na jihadi, wanaharibu maslahi ya Israili, na ninawahakikishia kwamba watu wa Irani hawatawatupa mkono na kuwaacha peke yao. Mtegemeeni Mwenyezi Mungu, chukueni fursa ya nguvu za kiroho za Waislamu na muwashambulie maadui kwa kutegemea silaha zenu na uchamungu, jihadi na ustahimilivu. Enyi waumini, kama mtamsaidia Mwenyezi Mungu, Naye atawasaidieni na kukupitisheni kwenye hatua zenu. O  O  O

38

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 38

11/3/2015 2:57:49 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

8 ULAMAA WA NCHI ZA KIISLAMU NA IBADA YA HIJA

N

i muhimu kwa Ulamaa wanaokutana hapa kwenye kituo hiki kitukufu kutoka nchi yoyote ile iwayo, kuyaelimisha mataifa kwa kutumia maazimio yaliyotayarishwa kimantiki kupitia kubadilishana mawazo, na kuyagawanya hapo kwenye ardhi ya wahyi miongoni mwa Waislamu, na baadaye wakati wa kurejea, wakayachapishe kwenye nchi zao. Katika maazimio yao, wawatake viongozi wa nchi za Kiislamu kuweka mbele ya macho yao yale malengo ya Uislamu, waache tofauti zao na kutafuta dawa ama ufumbuzi kwa ajili ya ukombozi kutoka kwenye makucha ya mabepari. O  O  O Fursa iliyojipanga vyema na ya thamani mno kwa ajili ya wanachuoni ni ule uwezekano wa kukutana na wasomi, wanafikra, na wale wenye muono makini wa nchi za Kiislamu, ingawa mabepari wa dunia au baadhi ya viongozi wa serikali za nchi za Kiislamu wanahofia sana mawasiliano na mahusiano kama hayo, na huwa wanajaribu kuyazuia na kuyadhibiti. Hata hivyo, imekuwa ni matakwa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kutumia vizuri fursa inayofaa kama hii kwa ajili ya kubadilishana mawazo na fikra, kupitia mipango makini na kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya nchi za Kiislamu. 39

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 39

11/3/2015 2:57:49 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

O  O  O Maulamaa mashuhuri wa makhatibu wanapaswa kuwaelimisha Waislamu juu ya mtazamo wa kisiasa wa wajibu wao wa maana sana. Majukumu muhimu, ambayo kama yakitiliwa maanani kikamilifu na kutekelezwa, ule utukufu ambao Mwenyezi Mungu ameuagiza kwa ajili ya waumini wachamungu utapatikana, na heshima za kimbinguni na Kiislamu zitapatikana kama inavyostahiki, na Waislamu hapo ndipo watakapofaidi uhuru halisi wakiwa katika rehema ya Uislamu na chini ya bendera ya tawhidi na bango la “Hakuna apasaye kuabudiwa ila Mwenyezi Mungu,” na watakuwa na uwezo wa kukatilia mbali mikono ya madhalimu kutoka kwenye nchi za Kiislamu. O  O  O Inashangaza sana kwamba wanachuoni na Ulamaa wengi wa nchi za Kiislamu wanazembea juu ya wajibu wao muhimu na kazi ya kimbinguni na kihistoria katika zama hizi, wakati mwanadamu ana kiu juu ya maagizo na miongozo ya kiroho na yenye kung’ara ya Uislamu. Hawaitambui kiu ya mataifa, na hawana habari na shauku za jumuiya na tamaa yao juu ya thamani za wahyi. Wamedunisha ile nguvu yao ya kiroho ya mvuto, ambapo wanachuoni na makhatibu na viongozi wa swala za Ijumaa wanaweza kuileta dunia chini ya mamlaka ya ki-Qur’ani na muungano wao, umoja, na uwajibikaji na kufanya kazi yao katika kuelimisha na kuwaongoza watu, katika hali hii ya sasa ya umiliki wa ulimwengu kimada wa sayansi wenye rangi nyingi. Hivyo wanaweza wakazuia udhalimu wote huu, unyonyaji na dharau iliyowekwa juu ya Waislamu na kuzuia ukumbatiaji wa mashetani wadogo na wakubwa, hususan Marekani katika nchi za Waislamu. Na wanaweza pia kutamka na kuandika mapendekezo 40

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 40

11/3/2015 2:57:49 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

ya kipuuzi na yenye uamuzi, kuwasifu watawala madhalimu, kuwafanyia wanaoonewa ubeuzi ulioendelea kuhusiana na masuala ya Kiislamu na kusababisha kutoelewana miongoni mwa Waislamu. Hivi haifedheheshi kwa wanachuoni wa nchi za Kiislamu kuona kwamba kanuni na taratibu za kipagani zikiwa zinatekelezwa katika nchi za Kiislamu na maamuzi yakitamkwa na watumwa wa mali, mamlaka na unafiki, huku maadui halisi wa Uislamu wakitumiwa, wakati mkiwa na njia ya kuifikia Qur’ani, miongozo angavu ya Uislamu – Sunnah (mwenendo wa Mtukufu Mtume na Maimam Maasumin (amani juu yao wote), na hivi haifedheheshi kuwaachia uwezo wanasiasa wa Kremlin au Washington wa kutoa maelekezo kwenye nchi za Kiislamu? Wanachuoni wa nchi za Kiislamu lazima wajadili njia za kutatua shida na matatizo ya Waislamu na ukombozi wao kutoka kwenye umilikiwaji na mamlaka za kidhalimu, na kupigania manufaa ya Waislamu, kuzuia uvamizi wa tamaduni duni za magharibi na mashariki ambazo zinaishia katika kuharibu mbegu na mazao ya mataifa. Wanapaswa kuwaonyesha watu wao wenyewe yale matokeo maovu ya kujisalimisha wenyewe kwenye vivutio vyenye mapambo mengi vya Magharibi na Mashariki, kuyaonya mataifa na serikali dhidi ya ukoloni mamboleo na vitendo vya fitna vya mataifa makubwa ambayo yamechochea vita na mauaji ya umwagaji damu juu ya Waislamu. Kwa mara nyingine tena ninasisitiza kwamba dunia ina kiu na mambo mazuri na miongozo ya Kiislamu na hakuna kisingizio cha kufanywa na wanachuoni mbele ya Mwenyezi Mungu. Wakati vijana wa Kiislamu wanaelekea kwenye upeo wa kujitoa muhanga na kufa kishahidi, ili kutetea na kulinda sehemu zao takatifu, na kwa hiari kabisa wanakumbatia mawimbi ya mabalaa na maangamizi na vilevile kufungwa jela na mateso yake kama wale wapiganaji wapendwa wa Hizbullah wa Lebanoni na mashujaa wengine wa 41

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 41

11/3/2015 2:57:49 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

Kiislamu ambao wanastahimili na kupigana dhidi ya waporaji, basi ni ushahidi gani wenye nguvu unaoweza kuhitajika na ni kisingizio gani kinachoweza kutolewa kwa ajili ya kimya, kujishusha hadhi, kukimbilia majumbani na udanganyifu mwingi usio wa lazima. Ikiwa wanachuoni na Ulamaa watasita kuchukua hatua, itakuwa ni kuchelewa sana kufanya marekebisho tena. Ni wazi kwamba tunatambua juu ya upweke wa baadhi ya wanachuoni wenye ari ya kuwajibika ambao wamezungukwa na singe na chini ya mashinikizo ya vitisho na amri haramu za wanachuoni waovu wanaolindwa, hata hivyo, sisi tunawakumbusha wapendwa hawa juu ya ushauri wa Mwenyezi Mungu kwamba: “Sema ninakupeni onyo moja, kwamba simameni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wawili kwa wawili na mmoja kwa mmoja na kisha mtafakari.” Amkeni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na msiogope upweke na kutengwa. Misikiti ndio ngome za kijeshi bora, na swala za jamaa na swala za Ijumaa ndio viwanja vinavyofaa kabisa kwa ajili ya uandaaji na ufafanuaji wa manufaa ya Waislamu. Leo hii, ingawa serikali na wale watiifu wa mataifa makubwa yenye nguvu wanapigana kwa dhati kabisa dhidi ya Waislamu, na wanawauwa watu wasio na hatia, wapenda uhuru na wasio na ulinzi, hata hivyo hawathubutu kuifunga misikiti na sehemu tukufu za Waislamu za kudumu, wala wao hawataweza kuzima nuru ya kiroho ya mapenzi na mazingatio ya mamilioni ya Waislamu. Wakati huohuo, iwapo watafunga misikiti na duru za kidini na kisiasa za wanachuoni hao, au hata kuwanyonga hadharani, hii itatumika kama ushahidi wa ukosa hatia wa Uislamu na kuendeleza mvuto wa jumla wa umma kwa wanachuoni hao na kuamua kuwafuata. Hivi sio kwamba Mwenyezi Mungu amewalazimisha Ulamaa kutakaa kimya dhidi ya madikteta na dhulma ya wahalifu? Je, wanachuoni sio wawakilishi wa Mitume na Maimam M’asumin juu 42

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 42

11/3/2015 2:57:49 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

ya ardhi? Kwa sababu hiyo, ulamaa, wasomi na wataalamu lazima wajitokeze kuunusuru Uislamu na kuuokoa kutoka kwenye hali yake ya sasa ya kutengwa. Msivumilie aibu zaidi na ushushwaji hadhi. Angusheni sanamu la ubwana na ubora unaolazimishwa wa dunia ya waporaji, onyesheni wazi sura zenu ongofu na zenye mamlaka, wafukuzeni ndumila kuwili, wanachuoni bandia, waabudu utajiri muovu na wenye makelele na msiwaache wale wanachuoni waovu, watoa sifa na madhalimu kulazimisha mamlaka yao juu ya watu, mahali pa viongozi halisi wa Waislamu na twaeni fursa ya hali ya kiroho ya Ulamaa wa Uislamu. O  O  O

43

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 43

11/3/2015 2:57:49 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

9 DOKEZO LA JUMLA

M

oja ya falsafa muhimu za Hija imo kwenye mipaka ya kisiasa, kwa ajili ya ukandamizaji ambao mikono ya wahalifu imo kazini kutoka pande zote. Propaganda yao pana kwa masikitiko makubwa sana imewaathiri Waislamu kwa kiasi kwamba wanaiona Hija kama ni ibada ya kawaida tu bila kujali maslahi ya Waislamu. Kipengele muhimu cha Hija hakijapungua kuzidi kipengele cha ibada ya utiifu tangu mwanzo. O  O  O Katika vipengele vyote vya Hija, kilichotelekezwa zaidi ni kipengele cha kisiasa cha ibada hii tukufu ambacho kwa kuonekana kutofaa, mikono mingi isiyo ya uaminifu imekuwa na bado inaendelea kuwa kazini, na Waislamu leo hii, katika kipindi hiki cha sheria ya mwituni wana ulazima kuliko wakati wowote wa kutekeleza wajibu wao wa kisiasa na kuondoa shaka kuhusu malengo ya kisiasa ya Hija, kwani wadanganyifu wa kimataifa, kwa kuwalaghai na kuwakwamisha Waislamu, kwa upande mmoja, na watumishi wao walanguzi kwa upande mwingine, na wakosaji kwa kutokujua kwa upande mmoja, na wanachuoni wa bandia, na wanaojinyima starehe kwa ujinga kwa upande mwingine, kwa kujua au kwa kutokujua, wakiungana mkono wenyewe kwa wenyewe, wanafanya kazi ya kukomesha kipengele hiki cha 44

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 44

11/3/2015 2:57:49 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

majaaliwa cha Hija ambacho ndio mkombozi wa wanaoonewa na kukandamizwa. Ni muhimu kwa wale wenye kujali wajibu, walioamka na wale waliojawa na huruma juu ya upweke wa Uislamu na kutelekezwa kwa kipengele chake cha kisiasa miongoni mwa miongozo ya Uislamu, hususan wakati wa taratibu za ibada za Hija ambayo inapaswa kupewa mazingatio zaidi, lazima waamke na kuwaelimisha watu, kupitia kuandika makala na kutoa hotuba hasa wakati wa kipindi cha Hija, kwani baada ya kumalizika kwa vitendo maalum vya Hija, wakati Mahujaji wanaporejea majumbani kwao, wanaweza kuwaelimisha watu wao na kuwaamsha wale wanaoonewa wa ulimwengu kujikomboa wenyewe kutokana na ukandamizaji unaoendelea kuongezeka wa madhalimu “wenye kujifanya wapenda amani.” Ni dhahiri kabisa kwamba, katika mkutano huu mtukufu wa kidunia, ambamo matabaka mbalimbali ya Waislamu wanaokandamizwa, kutoka utaifa wowote ule, lugha, rangi, madhehebu na mawazo, wanakusanyika wote wakiwa kwenye vazi la sare ya aina moja wakiwa hawana doa au pambo lolote, basi ikiwa matatizo muhimu ya ulimwengu wa Waislamu hayatapatiwa ufumbuzi, na watawala jeuri wakafanywa wakimbie, basi bila shaka mikutano ya vikundi vidogo vya kieneo au vya kijimbo haitaweza kufanya cha ziada na kupata utatuzi mpana. Nyumba Takatifu ya Mwenyezi Mungu ndio nyumba ya kwanza kamwe kujengwa kwa ajili ya watu, umma wote kwa jumla. Hakuna mtu, hakuna utawala na wala hakuna kundi linaloweza kupendelewa juu ya wengine katika Nyumba hii. Mabedui, wakaazi wa kwenye majangwa na wasio na makazi wote wana hadhi sawa na wakaazi wa mji huo, watawala na wale waliojitenga ndani ya Ka’aba. Nyumba hii adhimu ilijengwa kwa ajili ya watu, kwa ajili ya harakati za umma 45

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 45

11/3/2015 2:57:49 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

na kwa ajili ya maslahi ya umma na maslahi ambayo yanaweza kuchukuliwa kama yaliyotukuka na ya fahari kama kukata umiliki wa madhalimu na madikteta kutoka kwenye nchi za wanaokandamizwa na kuokoa hazina zao kubwa kutumikia manufaa yao wenyewe. Nyumba iliyoasisiwa kwa ajili ya mapinduzi ya watu na kwa ajili ya watu, lazima iwe ndio uwanja kwa ajili ya lengo hili kubwa, na maslahi ya watu lazima yatimizwe kwenye vituo hivi vitakatifu na kuwapiga mawe mashetani wadogo na wakubwa lazima kukamilishwe kwenye vituo hivi. Kule kukabidhiwa tu funguo za Nyumba hii, kuwapatia mahujaji vinywaji au kukarabati Msikiti huu Mtukufu hakutoshi kupatikana kwa lengo hili. Urahisi wa Nyumba na Msikiti huu, kama ilivyokuwa wakati wa Ibrahim na mwanzoni mwa Uislamu, na muungano wa Waislamu safi, wasiotiwa nakshi, katika uwanja huu usio na mawaa, una thamani mara elfu kama kupamba Ka’aba na kusimamisha majengo marefu marefu, lakini huku mkipuuza lengo la asili ambalo ni kuamka kwa watu na kupatikana kwa masilahi ya watu. “Hivi mnahesabu kuwapa mahujaji maji na kufanya makazi ndani ya Msikiti Mtukufu kuwa ni sawa na kumuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na jitihada katika njia ya Mwenyezi Mungu? Haviko sawa mbele ya macho ya Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu hawaongozi madhalimu.” Inaelekea kana kwamba aya hii tukufu imeshushwa katika zama zetu hizi na inaelezea kuhusu hali yetu ilivyo. Ni kana kwamba aya hii inawasemesha kizazi hiki cha sasa na inawaona wale wanaojishughulisha wenyewe na kutoa vinywaji na chakula kwa mahujaji, na kuweka mapambo kwenye Msikiti Mtukufu, lakini wanapuuza imani yao ya kweli juu ya Mwenyezi Mungu na Siku ya Kiyama na mapambano kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kama watu makatili.

46

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 46

11/3/2015 2:57:49 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

O  O  O Mheshimiwa Mfalme Khalid bin Abdul-Azizi, Mfalme wa Saudi Arabia: Barua yako imepokelewa. Kile Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran ilichokisema ni sahihi kabisa. Mimi ninachukulia vizingiti na shida zote za Waislamu na serikali za nchi za Kiislamu kuwa ni kutokana na kutoelewana na migogoro miongoni mwao. Kwa nini serikali za Kiislamu zenye idadi ya watu ya takriban bilioni moja na zenye hazina ya chini ya ardhi hususan hifadhi za mafuta ambazo ndio pumzi ya uhai wa mataifa makubwa, na zenye kufaidi taasisi zenye kuleta uhai za kiibada na kisiasa za Mtukufu Mtume wa Uislamu 8 ambaye amewataka Waislamu kushikamana na “Kamba ya Mwenyezi Mungu” na kuepuka faraka na kutoelewana, na kuwa na njia ya kufika kwenye sehemu za hifadhi na kimbilio kama “AL-HARAMAIN AL-SHARIFAIN” yaani zile sehemu mbili takatifu – ambazo zilitumika kama vituo vya ibada na siasa wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume 8 na muda mrefu tu baada ya kifo chake, na ambapo mambo ya kisiasa na mapambano yalikuwa yakiundwa katika vituo hivi viwili vya kiibada na kisiasa, sasa hivi ifikie mahali ambapo masuala yoyote ya kisiasa na kijamii, ambayo ndio mahitajio muhimu ya Waislamu na yanayohitajika sana yaonekane kama dhambi, na polisi wa Saudia wakiwa wamevaa mabuti na silaha kamilifu wanadiriki kuingia kwenye Msikiti huo Mtukufu, mahali palipoagizwa na Mwenyezi Mungu na kuelezewa wazi na Qur’ani Tukufu kama kimbilio takatifu, hata kwa wapotovu, wawashambulie Waislam na kuwapiga na kuwaweka mahabusu. Kosa lao halikuwa lolote isipokuwa kupiga kelele dhidi ya Marekani na Israili, maadui wawili wa Mwenyezi Mungu na Mtume 8. Sijui kama unajulishwa juu ya matukio hayo na kile 47

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 47

11/3/2015 2:57:49 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

kinachotokea kwenye “Sehemu Takatifu” kwa uaminifu na ukweli, au yale mabango ya Wairani yaliyotolewa taarifa za uongo, ambayo yalikuwa yanajulikana kwa wote. Sijui jinsi viongozi wa swala wa Sehemu Tukufu zote mbili walivyoelewa dini na Hija ambayo yote inadhamiriwa kuwafanya watu wazinduke na kuamka kwa ajili ya haki na uondoshaji wa ukatili na uporaji kama ilivyokuwa sera maarufu ya Mitume, hususan wa mwisho wa Mitume, Muhammad 8. Kwa nini wanawazuia mahujaji kuingia kwenye masuala ya kisiasa, hata kupiga kelele dhidi ya Marekani na Israili na maadui wengineo wa Uislamu, bila kujali mienendo ya Mtukufu Mtume 8 na Waislamu wa siku za mwanzoni, na kwa makusudi kabisa au kwa kutojua au ujinga wanaandaa viwanja kwa ajili ya umiliki wa kigeni wa nchi za Kiislamu na hata hizo sehemu mbili tukufu, sehemu za mashukio ya wahyi na Malaika wa Mwenyezi Mungu. Kama serikali ya Hijazi ingetumia vizuri tukio hili la kila mwaka la mkusanyiko wa mamilioni ya Waislamu, isingekuwa na haja ya Marekani na AWACS yake, au taifa kubwa jingine, na matatizo ya Waislamu yangepatiwa ufumbuzi. Ni wazi kwamba Marekani imetoa ndege hizi kwa manufaa yake yenyewe na kwa ajili ya Israili, kama ilivyothibitishwa kwamba AWACS ya Marekani ilitoa taarifa za uongo kwamba “Irani imeshambulia kwa mabomu mitambo ya mafuta ya Kuwait,” kwa sababu tu ya kupandikiza mbegu za migogoro kati ya Iran na Waarabu Waislamu. Kwa masikitiko kabisa, upuuzaji na uzembe kama huohuo unakuwepo miongoni mwa nchi za Kiislamu, kiasi kwamba hayo mataifa makubwa dhalimu yanawazuia Waislam hasa hasa viongozi wao mashuhuri kuingia kwenye masuala ya kisiasa na kuonyesha kujali kuhusu mambo ya Waislamu, kwa kiasi kwamba katika kituo cha kisiasa cha Kiislamu, Waislamu wanawekwa jela na kuteswa, 48

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 48

11/3/2015 2:57:49 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

kwa fatwa za wahutubu wa vitala wanaolindwa, kwa kupiga kelele tu dhidi ya maadui wenye kiu ya damu wa Qur’ani na Uislamu adhimu. Je unatambua juu ya maovu yanayotendwa katika sehemu mbili hizi takatifu, patakatifu pa Mwenyezi Mungu na ukaribu wa hapo wa kaburi la Mtukufu Mtume 8, au huenda pengine unapewa taarifa za uongo, kama ulivyopewa taarifa potovu kuhusu mabango yale ya Wairani. Tulisimama ili kwamba kwa rehema za Mwenyezi Mungu, tukusanye Waislamu wa dunia nzima chini ya bendera ya tawhidi na kuwaunganisha kwenye amri zilizo mbele za Uislamu, kukata mikono ya mataifa makubwa kutoka kwenye nchi za Kiislamu, kurudisha ile heshima ya Waislamu wa siku za mwanzoni, kukomesha kabisa umiliki wa kionevu wa makafiri juu ya nchi za Waislamu na kurejesha uhuru na ukombozi wa Waislamu. Inatarajiwa kwamba serikali za Kiislamu, hususan serikali ya Saudi Arabia, ikiwa ipo katika kituo cha siasa za Kiislamu, zichukuane na kupatana na kuwa katika umoja nasi na kila moja katika nchi yake, ionje utamu wa uungaji mkono usio na kikomo wa mataifa yao na kufaidi neema za kimbinguni kama ile serikali ya watu ya Iran, na kufanya kama ilivyoamrishwa na Qur’ani Tukufu, kwa mapenzi na udugu kwa mataifa ya Kiislamu na serikali zao, na kuwa wagumu na wasionyenyekea kwa makafiri na waporaji. Kwa mara nyingine ninasisitiza kwamba wao wanakuletea taarifa potovu na zisizo sahihi, kama ulivyoandika kwamba mabango ya Wairani yamesababisha karaha na ukosefu wa furaha kwa mahujaji. Ni vyema uweke watu waaminifu wa kutoa taarifa na kuweka wazi kwamba mabango ya kupinga Marekani na Israili hayakusababisha chuki na karaha, bali vitendo vibaya vya watendaji wa Saudi Arabia katika kuwapiga na kuwafunga wageni wa Mwenyezi Mungu kwa kupiga kwao kelele dhidi ya Israili na Marekani vimewasababishia Waislamu wote wa dunia chuki na ukosefu wa furaha, hususan 49

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 49

11/3/2015 2:57:49 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

mahujaji kwenye Nyumba ya Mwenyezi Mungu na kaburi la Mtukufu Mtume 8. Namuomba Mwenyezi Mungu awaamshe Waislamu, azidishe heshima na muongozo, hasa kwa viongozi mashuhuri, wanasiasa, kwenye manufaa ya Uislamu na Waislamu. Hija ni jambo ambalo kipengele chake cha kisiasa kinazidi kile cha kiibada na ninyi mabwana na mabibi mnaokwenda Hija, lazima mchukue tahadhari ya kujisafisha wenyewe kutokana na hii fikra ya kikoloni. Zungumzeni wazi katika mikusanyiko yenu yote kwamba Uislamu sio huu tuliokuwa nao hadi sasa, kwamba mahujaji wanasafiri tu kwenda Makka, kufanya tawafu chache kuzunguka Nyumba Tukufu na kisha kufanya ‘WUQUUF’ na ibada hii na ile, lakini bila kujali ni nini wajeuri wanawafanyia Waislamu, na kumshutumu yoyote yule anayetaka kuzungumza juu ya manufaa ya Waislamu. Madhara ya wanachuoni wa vitala (Kasri za watawala) ni mabaya zaidi kuliko yale ya Marekani. Kwa sababu wao, kwa muonekano wao wa Kiislamu, wanaweza kunasibishwa na utelekezwaji wa Uislamu, wakati ambapo maadui hasa hawawezi hilo. Maadui ndio wanaowafanya watende hivyo. Waislamu wakati wanapokwenda Hija lazima wafanye Hija yenye uhai, Hija yenye pigo, Hija ambayo inashutumu Urusi ya kihalifu na Marekani mhalifu. Hija kama hiyo ni yenye kupata mapokezi ya kupendeza. Kwenda Hija bila kujali kuhusu maslahi ya Waislamu, bali kinyume chake mkafunika maovu yanayotendwa dhidi ya Waislamu, huo ni muonekano tupu wa nje wa Hija bila ya kuwa na kitu ndani yake. O  O  O Uislamu unakanganya, kila mahali, kuanzia katikati ya Ka’aba tukufu, mpaka sehemu ya mbali kabisa ya makazi ya Waislamu. 50

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 50

11/3/2015 2:57:49 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

Hawautambui vizuri. Hii ndio maana wakati Waislamu wanapokutana hapo Makka, mahali palipoamriwa na Mwenyezi Mungu kwa ajili ya mkusanyiko wa Waislamu, mkusanyiko wao wa kiroho, wao wanakuwa hawajui la kufanya. Hawapati manufaa ya Kiislamu kutoka kwenye mkusanyiko wao. Hatua ya kisiasa kama hiyo imegeuzwa na kuwa mahali pa purukushani tupu na uzembeaji wa matatizo yote ya Waislamu. Lazima muutafute Uislamu. Chimbueni mambo yote yahusuyo Hija, madhumuni ya kisiasa ya Hija. Kama Waislamu wakilitambua hili, basi litatosha kwao kutafuta uhuru wao. Lakini kwa masikitiko makubwa kabisa, tumeupoteza ule Uislamu wetu halisi na wa kweli. Tulionao sasa ni Uislamu ambao umetenganishwa na siasa moja kwa moja kabisa. Wameukata kichwa chake. Kile ambacho ndio sehemu ya msingi kimekatwa na tukaachiwa mabaki. Hilo ndio lililotuweka sisi kwenye hali mbaya ya kusikitisha. Mpaka pale tutakapouchimbua Uislamu, vinginevyo hatutaweza kurejesha hadhi yetu. O  O  O Siasa ya Hija sio jambo ambalo tumelipanga sisi wenyewe. Hija ni harakati ya kisiasa ya Kiislamu. Tulikuwa tumezingatia akilini tangu tulivyotoka kwenda Hija, kwamba tukaitekeleze kwa namna inavyostahiki kuwa, kama vile Mtukufu Mtume 8 alivyoyabomoa masanamu ndani ya Ka’aba, sisi tunapaswa kuvunja masanamu ya wakati wetu kama vilevile alivyovunja Mtume 8, masanamu ambayo ni maovu zaidi kuliko ya wakati ule. Ni lazima tutekeleze ibada za Hija kama tulivyofanya miaka miwili au mitatu iliyopita. Mahujaji lazima waandamane na kuonyesha kama walivyofanya kabla. Hija ifanywe kwa namna ile na serikali lazima zionyeshe ustahimilivu. Hatuwezi kukengeuka kwenye wajibu ambao Uislam na Qur’ani vimetuagiza juu yetu. Sera yetu juu ya 51

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 51

11/3/2015 2:57:49 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

Hija ni ile ile kama mwanzo. Kila tutakapokwenda tutafanya vivyo hivyo, labda watukataze kwenda Hija, hapo tena mambo yatakuwa tofauti. Nataraji kwamba mahujaji mwaka huu watatekeleza Hija yao kwa ubora zaidi na kwa wingi zaidi. Watu binafsi lazima wawe waangalifu kuhusu tabia na mwenendo wao na waungane kwa pamoja, na natumaini kwamba watu wa nchi nyinginezo za Kiislamu wameihisi maana hii pia. Waislamu zaidi ya bilioni moja hawapaswi kufuata kile anachokisema Marekani na Urusi. Lazima wasimame imara, bila kujali wengine, kama vile ambavyo idadi ya watu milioni arobaini wa Irani walivyosimama kwa umadhubuti wakipiga makelele ya “Hakuna Magharibi wala Mashariki.” Thamani ya hadhi ya nchi hii iko juu kabisa kuliko zile nchi zinazoungwa mkono na Magharibi au Mashariki, na heshima ya Muislam mmoja mmoja kwa ajili hiyo ni kubwa mno. Kwa hiyo mataifa yasihofie na kuogopa kile ambacho Marekani inaweza kufanya. Wao sio chochote bali ni ngoma tupu. O  O  O Salam za bashasha kwa mahujaji wa kwenye Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu – Mwenyezi Mungu awape kila aina ya msaada. Ni jambo lisilopingika na ni wazi kwamba Uislamu mtukufu ni dini ya tawhidi, Upweke wa Allah, mvunjaji wa ushirikina, uabudu masanamu na ubinafsi. Ni dini ya hali ya maumbile ya asili na yenye kumkomboa mwanadamu kutoka kwenye utumwa hadi kwenye vifungo vya asili na kutoka kwenye vishawishi vya kibinadamu na majini, kwa ndani na kwa nje. Dini inalazimisha siasa za dola na muongozo kuelekea kwenye njia iliyonyooka ya kukanusha “Umagharibi na Umashariki.” Ibada 52

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 52

11/3/2015 2:57:49 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

ya dini ya kweli imeunganishwa na siasa na matendo yake ya kisiasa yanahesabiwa kama ni ibada. Sasa kwa vile Waislamu kutoka nchi mbalimbali wanaelekea kwenye kituo chao cha matarajio na Hija kwenye Nyumba ya Mwenyezi Mungu kwenda kutekeleza wajibu ulioamriwa na Mwenyezi Mungu, na kuunda mkusanyiko mkubwa wa Waislamu, katika mahali palipobarikiwa, katika siku zilizobarikiwa, lazima wao kama wajumbe wa Mwenyezi Mungu, wafaidike kutokana na muktadha wake wa kisiasa na kijamii, kwa nyongeza ya vipengele vya kiibada, na sio kutosheka na kuridhika na utekelezaji wake usio na moyo. Ni dhahiri kwamba kuandaa mkusanyiko mkubwa kama huo ni jambo ambalo haliwezekani kwa mtu binafsi mtumishi au serikali. Limetokea tu kutokana na kutii amri ya Mwenyezi Mungu. Kwa masikitiko ni kwamba Waislamu hawakunufaika kikamilifu kutokana na nguvu hii tukufu kwa maslahi bora ya Uislamu na Waislamu. Sasa kwa kuwa mahujaji wanaondoka kwenye makazi yao ya kidunia na kuelekea kwenye Nyumba Takatifu ya Mwenyezi Mungu, na kutelekeza vyote bali hata wapendwa wao wa kweli, kwa vile hakuna yeyote mbali na Mwenyezi Mungu, kwa ndani na kwa nje, lazima wazingatie akilini kwamba ile Hija ya Ibrahim na Muhammad imeachwa siku nyingi, vyote, kiroho na kijamii. Mahujaji kutoka nchi zote za Kiislam lazima waiondolee Nyumba ya Mwenyezi Mungu upweke ilionao kwa maana zote. Ngoja siri zake za kimuujiza ziachwe kwa wale wanairfaan wasiowekewa mapazia au kufunikwa, na acha sisi tushughulike na maeneo ya kisiasa na kijamii ya Hija ambayo tumewekwa mbali mno nayo. Tunawajibika kufidia yale yaliyopotea. Mkusanyiko huu wote wa kisiasa ambao watu kutoka kila tabaka na kundi wanakutana, kama walivyoitwa na Ibrahim na Muhammad (Mwenyezi Mungu awape rehma na amani wote) ni kwa ajili ya kunufaisha umma kwa jumla na kuwafanya 53

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 53

11/3/2015 2:57:49 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

watu waamke kwa ajili ya haki, na ndio mwendelezo wa uvunjaji masanamu wa Ibrahim na Muhammad (amani juu yao wote) na uvunjaji wa upagani na upinduliwaji wa Firauni kutoka kwa Musa A, lakini ni sanamu lipi ambalo linaweza kufikia kiwango cha Shetani mkubwa (yaani, Marekani) na masanamu waporaji wa dunia na wapagani ambao wanathubutu kuwaita wanaokandamizwa wote duniani na kuwataka wawasujudie na kuwafanya watumwa wao wale viumbe huru wa Mwenyezi Mungu? Ibada ya Hija ambayo inajumuisha kuitika “Labbaika,” kwa Mwenyezi Mungu na kuondoka kutoka kwenye ubinafsi kwenda kuelekea kwa Mwenyezi Mungu, kwa mwongozo uliobarikiwa wa Ibrahim na Muhammad (amani juu yao wote) kwa kweli ni kituo cha kukanushia masanamu yote na madhalimu wa zama, na mashetani na vizazi vyao, lakini ni sanamu lipi ambalo baya zaidi kuliko yule Shetani mkuu, mporaji Marekani na mchokozi na mpagani Mrusi, na ni sanamu lipi la kiume au la kike ambalo ni baya zaidi kuliko madikteta wa zama zetu hizi? O  O  O Kwa bahati mbaya, Waislamu walio wengi wamekuwa hawatambui upana wa kisiasa wa ibada hii tukufu, kutokana na upotovu wao wenyewe au kutoelewa kwa baadhi yao ama njama za baadhi ya watendaji wataka makuu. Wasimamizi wa waheshimiwa mahujaji watumie umaizi wao wa kisiasa ili kuongoza mambo ya haja za mahujaji, kufufua desturi hii tukufu ya mbinguni kwa kuwaita Waislamu kwenye maafikiano na ushirikiano, kupitia kuwatolea hotuba na katika sherehe za kidini kuwafahamisha kile kinachoendelea huko Lebanoni, Irani inayojitahidi, na Afghastani inayokandamizwa na madikteta na 54

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 54

11/3/2015 2:57:49 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

waporaji wa kidunia na kuwazoelesha waheshimiwa mahujaji kutoka nchi tofauti wajibu wao mzito wa kupigana dhidi ya waporaji wa kimataifa na wateka nyara. O  O  O

55

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 55

11/3/2015 2:57:49 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

10 UFUNDAJI NA UELIMISHAJI WAKATI WA HIJA

E

nyi mubalighina! Enyi waandishi! Waelezeni ndugu zenu juu ya matatizo yenu ya kimajimbo ya kijamii na kisiasa kwenye mkusanyiko huu mkubwa na adhimu wa Arafa. Mash’ar, Mina, Makka yenye hadhi, na Madina yenye nuru na muombe usaidizi wa pande zote. Enyi mahujaji wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu! Fanyeni zijulikane kwa wakazi wote wa ulimwengu, zile njama za mkono wa Kulia na wa Kushoto, hususan mporaji na mchokozi Marekani na mhalifu Israili. Wapeni maelezo juu ya maadui zao na tafuteni msaada kutoka kwao walimwengu wapenda haki. Muombeni Mwenyezi Mungu rehema na fadhila kwa ajili ya uboreshaji wa hali za Waislamu na kukatika mikono ya wahalifu kutoka kwenye nchi za Kiislam. O  O  O Wajibu mkubwa wa Waislamu ni kufahamu vyema yale mambo ya uhakika kuhusu Hija, na kwa nini ni lazima daima watu watumie uwezo wao wa mali na kiroho kwa ajili ya kudumu kwake. Kile kilichoelezewa hadi sasa na wasiojua, wachambuzi wenye fitna au wanachuoni wa kulipwa kama ndio falsafa ya Hija ni kwamba, hiyo 56

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 56

11/3/2015 2:57:50 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

ni ibada tu ya mjumuiko wa watu na safari ya kuhiji (kwa maana ya kutembea na kujua nchi). Na yasiyopasa kwenye Hija ni, jinsi ya kuishi, jinsi ya kupigana na kusimama dhidi ya dunia ya kibepari na kikomunisti! Kisichopasa kwenye Hija ni kuwatetea Waislamu na wale wanaokandamizwa dhidi ya madikteta! Kisicho wajibu kwenye Hija ni kutafuta dawa kwa ajili ya kitulizo cha Waislamu kutokana na misongo na mikazo ya kiakili na kimwili! Kisichopasa kwenye Hija ni kwamba, Waislamu ni lazima wajithibitishe wenyewe kwamba wao ni watu wa dunia ya tatu! Kisichofaa kwenye Hija ni kuwachochea Waislamu kuasi dhidi ya serikali tegemezi! Bali Hija inachukuliwa kama safari ya kutembelea “Qiblah” yaani al-Ka’aba na Madina, hivyo tu basi! Ambapo Hija imekusudiwa kuwa katika kujikurubisha na kuungana na Mmiliki wa Nyumba hiyo. Hija sio tu utendaji wa baadhi ya kanuni za kiibada na utamkaji wa kiasi fulani cha maneno. Mtu hawezi kumfikia Mwenyezi Mungu kwa maneno na vitendo visivyo na maana yoyote. Hija ndio kitovu cha utambuzi wa kimbinguni ambamo maelezo ya siasa za Kiislamu katika hali zote za maisha lazima yapatikane. Hija ni mwasilisha ujumbe, mtengenezaji na mjenzi wa jamii huru kutokana na uovu wa kimada na kiroho. Hija ni udhihirisho na urudiaji wa mandhari zote zinazopendeza za maisha ya mwanadamu aliyekamilika na jamii yenye kuamini kwamba ina uwezo wa kushindana katika ulimwengu huu, na kanuni za ibada za Hija ndio kanuni za maisha na kutokana na ukweli kwamba jamii ya Waislamu wa ulimwengu, wa rangi au taifa lolote wanakoweza kutokea, lazima wawe wa kiIbrahim ili waweze kuungana na umati wa Muhammad kwa ujumla wake. Hija ni mahali pa kupanga, kutenda na kuunda maisha haya ya kitawhid. Hija ni mandhari iliyowekwa kwa ajili ya maonyesho, na ni kioo cha tathmini ya uwezekano na uwezo wa kimali na kiroho 57

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 57

11/3/2015 2:57:50 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

wa Waislamu. Hija inabeba ufanano wa Qur’ani kwa kuwa kila mtu anaweza kufaidika kutokana nayo, na bado kama wanafikra, wenye kujitahidi kwa bidii na wazamia lulu wa umma wa Waislam wakijitosa kwenye bahari ya utambuzi, bila kuhofia kuendea na kuingia kwenye miongozo na sera zake, watapata kutoka kwenye chaza wake lulu za hekima, mwongozo, ukuaji na ukarimu na kuwa wenye kukinai na hekima na utambuzi wake angavu. Lakini sisi ni lazima tufanye nini, na tutaipeleka wapi huzuni hii, kwamba Hija imetelekezwa kama ilivyotelekezwa Qur’ani Tukufu, na kwa kiwango hicho hicho kwamba hicho Kitabu cha uhai, ukamilifu na uzuri kimevikwa pazia kwa mapazia tuliyoyatengeneza sisi wenyewe, na hazina hii ya siri za maumbile kuzikwa chini tani kadhaa za udongo wa welewa wetu mbaya wa kimakosa na lugha yake tamu ya kupendeza ya urafiki na muongozo na falsafa yenye kuleta uhai imeshushwa hadi kwenye lugha ya kitisho, kifo na kaburi. Hija vilevile imezongomezwa kwenye hali mbaya kwa majaliwa hayo hayo tu kutokana na majaaliwa haya ya mamilioni ya Waislamu wanaofanya Hija ya kila mwaka kwa kwenda Makka, wakakanyaga pale Mtukufu Mtume Muhammad 8, Ibrahimu, Isma’il na Hajjar walipokanyaga, lakini hakuna mtu anayejiuliza mwenyewe kwamba Ibrahim na Muhammad walikuwa kina nani, walifanya nini, malengo yao yalikuwa yapi, na walitutarajia sisi tuje kufanya nini? Kana kwamba jambo pekee ambalo halikufikiriwa ni hili. Bila shaka Hija isiyokuwa na uhai, bila hamasa ya kuamka na kuonyesha kuchukizwa na kukerwa na wapagani, kuazimia juu ya umoja wa Waislamu na ubomoaji wa upagani na uabudu masanamu, hiyo kwa hakika sio Hija hata kidogo. Ujumla wote wa Waislamu lazima ufanye kila jitihada ili kuhuisha Hija na Qur’ani Tukufu na kuviingiza kwenye uhai wao, na watafiti waliojitolea kwa dhati ni lazima wajaribu kutupilia mbali uzushi wote unaoshutumiwa na 58

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 58

11/3/2015 2:57:50 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

sura zote za itikadi ya kudhania za ulamaa watumishi wa kitala kwa kuwasilisha maelezo sahihi na halisi ya falsafa ya Hija. Ni muhimu kwa waheshimiwa wanachuoni na waandishi waliojitolea kwa dhati na wasemaji kutetea na kulinda Uislam katika makabiliano na propaganda yenye sumu ya vyombo vya habari vitiifu kwa Marekani na Israili, dhidi ya Uislamu na Jamhuri ya Kiislamu ya Irani na kuwasilisha kwa wakaazi wa dunia ile sura yake halisi na ya kweli, na mafanikio ya taifa la Irani lililojitolea kwa dhati, licha ya vikwazo vingi na vipingamizi vilivyowekwa na maadui wa Uislam wa ndani na wa nje kwa njia zao zote, ili kuwahamasisha Waislam wa dunia kutokata tamaa. Waelimisheni watu na fichueni zile shutuma zisizo za kweli zinazoletwa na matarumbeta ya propaganda dhidi ya Uislamu na kutoa sura na sifa mbaya juu ya Irani ya Kiislamu ili kuvunja moyo wa mapinduzi kwa mataifa mengine. Fichueni njama za Marekani na washirika wake na waelimisheni Waislamu juu ya nini kilichoufika Uislamu na Waislamu kwa mikono ya watawala waliojazwa kasumba ya kimarekani, na baya zaidi ni kule kuitambua Israil baada ya uvamizi wa kikatili kwenye nchi ya Kiislamu ya Lebanoni na kuwauwa kishahidi na kuwatia vilema makumi ya maelfu ya watu wasio na hatia wala ulinzi. Huenda mataifa yanazuia matukio ya kimsiba kama haya, ambayo yanaleta aibu juu ya Waislamu mbele ya dunia ya sasa na kwa vizazi vijavyo na kuutoa Uislamu na Waislamu kutoka kwenye dharau hii mbaya na kujitoa wao wenyewe kutoka kwenye udhalilishaji na dharau hii yenye kuchukiza, ukumbusho ambao kwamba utawatingisha Waislamu wenye ghera. O  O  O

59

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 59

11/3/2015 2:57:50 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

Katika tukio hili la thamani, wanachuoni waheshimika na waunganishaji wa Hija lazima wachukue wajibu wenye nguvu na athari katika kupitisha uzoefu wa mapinduzi na kuwasilisha taratibu za kisiasa, kwa utukufu wa aya za Qur’ani, na wajibu wenye nguvu kwa kiasi kikubwa wa watumishi wa Kiislamu katika uongozi wa jamii.

60

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 60

11/3/2015 2:57:50 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

11 HIJA NA KUTANGAZA MAPINDUZI YA KIISLAM

W

aheshimiwa mahujaji lazima wazingatie kwamba wanatoka kwenye nchi ya Kiislamu, nchi iliyojitolea kwa dhati na ya kimapinduzi, na kwamba wote, marafiki na maadui wanawaangalia wao. Marafiki ni ili kuona iwapo kama mahujaji hawa bado wamejifunga katika misimamo yao ya Kiislamu, je, wanahifadhi ile hadhi ya mapinduzi matukufu ya Kiislamu katika maneno na vitendo vyao na katika kujishughulisha kwao na Waislamu wengine. Je, wanaonyesha subira na uvumilivu wanapokabiliwa na matatizo na shida ambazo hazitenganishiki na safari hii tukufu, je wanakubali juu wa kuwepo daima utazamaji wa Mwenyezi Mungu katika matukio yote yanayotokea na je watarejea nyumbani pamoja na heshima na fahari na kuwa ni njia ya utangazaji na uenezaji wa mapinduzi au, Mungu aepushilie mbali, wanaweza wakasema jambo, bila kujali ni dogo kiasi gani, kinyume na sifa na desturi ya Kiislamu kwenye muonekano huu kwa Waislamu wengine, jambo ambalo litaaibisha Uislamu na Jamhuri ya Kiislamu, ambalo ni kosa lisilosameheka. Na kwa upande wa maadui, ni ili kugeuza vitendo vyao na maneno yao, na kujaribu kutafuta makosa, bila kujali yatakuwa madogo kwa kiasi gani, kuyaongeza na kuyakuza kisha kuyatangaza ili kuonyesha kwa wageni muonekano uliogeuzwa wa Uislamu na Mapinduzi hayo na kuwatafsiri vibaya Waislamu wa Irani kama watu wasio na simile, 61

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 61

11/3/2015 2:57:50 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

na Uislamu kama dini ambayo imetoka nje ya maadili matukufu ya kibinadamu, na Wairani waungwana kama watu wanaotia aibu na walio mbali na ustaarabu na upandaji hadhi. Waheshimiwa mahujaji lazima watambue ukweli wa kwamba wajibu wao mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya taifa tukufu la Iran ambalo linajitahidi kwa ajili ya Uislamu na mafundisho yake ya kibinadamu ni mkubwa sana na unaohitaji umakini. Msichukulie mwaka huu – wakati tunafahamu wote kwamba mataifa makubwa yenye nguvu pamoja na washirika wao wamekita makucha yao kwenye nchi za Kiislamu na zinazodhulumiwa za ulimwengu huu kwa nguvu zaidi kuliko hapo kabla, na damu za vijana wasio na hatia zinadondoka kutoka kwenye ncha za kucha zao za vidole – kuwa ni mzito sawa na wa mwaka uliopita. Leo hii yale mataifa yenye nguvu kubwa yanauogopa Uislamu na “ufutaji wake wa programu za Magharibi na Mashariki,” na yule shetani mkubwa amewaita mashetani wadogo na kuingia kwenye kila aina ya njama ili kuzima nuru ya Mwenyezi Mungu. O  O  O Mahujaji watukufu wa Iran na mahujaji wengine kwenye “maeneo mawili matukufu ya ibada” lazima wazingatie akilini kwamba wanasafiri kwenda kwenye Nyumba ya Mwenyezi Mungu na kaburi tukufu la Mtukufu Mtume 8 na eneo tukufu la makaburi ya kizazi kitukufu cha Mtume, kutoka kwenye nchi ambayo umma wake umesimama kwa ajili ya malengo ya Uislamu na kuwafukuza madikteta kutoka kwenye nchi yao nzuri wanayoipenda, na kwamba ndugu zao Waislamu kutoka kote duniani wana macho maangalifu juu yao, na waandishi wa habari na wazushi wa uwongo wa matarumbeta ya propaganda na maadui wanaopotosha fununu ndogo ndogo kama 62

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 62

11/3/2015 2:57:50 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

mawe mazito wamejiandaa kwa uvamizi wa habari, wakiangalia kwa makini vitendo na maneno yao na wakidhamiria kueneza uvumi wa udaku duniani kote. Kwa hali hiyo, upotovu japo mdogo kabisa na makosa ni lazima yaepukwe kabisa, kwa kuwa hayo mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya Mtume Wake 8 na mahujaji wengine wa kwenye sehemu mbili hizo tukufu huonekana kama kosa na dhambi kubwa kwa kuzingatia matokeo yake hasi ya baadaye. Kwa sababu baadhi ya vitendo na maneno kwa nyongeza ya kuwa kwao kinyume na utukufu wa sehemu hizo mbili pia husababisha aibu kwa Uislamu na hasa kwa Jamhuri ya Kiislam ambayo imejitoa kwa ajili ya utukufu wa mbinguni na utekelezaji wa amri za Qur’ani Tukufu na kufuata kwa vitendo Hadithi za Mtukufu Mtume 8. Na kwa sababu tabia fulani mbaya zinaweza kugeuzwa na watafuta makosa wenye fitna, ambao wanangojea tu kupata fursa ya kueneza uvumi wa uzushi dhidi ya Uislamu na kuitafsiri vibaya sura nzuri ya Uislamu na ya Jamhuri ya Kiislamu na makosa hayo yakaingizwa kwenye kumbukumbu zao za matendo, wakati ambapo wao wamesafiri kwa ajili ya ibada na kutimiza wajibu wao wa Hija. O  O  O Mnasafiri kutoka kwenye nchi yenye ushindi ambayo imejitahidi kwa miaka kadhaa chini ya utawala kandamizi wa wafalme lakini, kwa fadhila za Mwenyezi Mungu na kwa rehema za mkumbushaji wa Mwenyezi Mungu 8 nafsi zetu ziwe fidia kwa ajili yake, tumekata utumwa na vifungo wakati tukistahamili shida na dhiki na mateso na kutoa kwa Uislamu maelfu ya mashahidi wafiadini na vilema katika kupigania lengo la mwisho. Mnabeba ujumbe wa ummah ambao umetumikia taifa ambalo lilikuwa karibu ya kuzama katika uovu, upujufu na uasi unaoibukia 63

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 63

11/3/2015 2:57:50 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

kutoka kwenye umashariki, na baya zaidi kuliko hilo mataifa yenye umagharibi, na kubadilisha serikali dhalimu kwa ile ya Kiislamu. Ni watu haohao ambao wamedhamiria kueneza mapinduzi yao ya Kiislamu, sio tu kwa nchi za Kiislam, bali pia kwa watu wanaokandamizwa wa duniani kote, pamoja na Uislamu mpendwa na mfumo wa Kiislamu wa utawala wa haki. Mnawakilisha umma ambao mapinduzi yake ya Kiislamu, licha ya kuwa na umri mchanga, na licha ya vipingamizi vya kuangamiza vinavyotokana na kukabiliana kwao na mataifa makubwa ya kote, Magharibi na Mashariki na vitendo vya hujuma vya magaidi wao wa kukodishwa, bado yameziamsha nchi za Kiislamu za Mashariki na Magharibi na vilevile watu wanaokandamizwa wa duniani kote, yakawavutia kwenye Uislamu na kufanikiwa kuwafanya wakazi wa ulimwengu kuisikia sauti ya Uislamu kwa kiasi inavyowezekana na kupata upendeleo wao. Ninyi mahujaji kwenye Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu mnabeba ujumbe wa umma huu na mnawakilisha nchi hii. Nafasi yenu kwa hiyo ni nyeti sana na wajibu wenu ni mkubwa mno. Ama mtafanya kama ilivyotarajiwa, kujaribu kuwa uvutiwaji wa wote, kwa tabia zenu njema na mwenendo wa Kiislamu na wa kimapinduzi na kuonyesha kwa mataifa ya dunia ile sura halisi ya mapinduzi ya Kiislamu na kuvuta nadharia zao kwenye mapinduzi matukufu ya Irani kwa tabia yenu ya kindugu na upendo na kivitendo hasa kuwabatilishia walionyimwa, ile propaganda ya waovu ya mbiu zao za uenezaji, kwa hali ambayo ibada za Hija yenu zitapata mapokezi mazuri na malipo mema, ambapo iwapo kama, Mungu aepushilie mbali, baadhi ya watu wajinga watafanya kinyume cha haya yaliyotangulia kusemwa, jambo ambalo nataraji hawatalifanya, vinginevyo watakuwa wamefanya kosa kubwa sana mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya Nyumba Yake, mbele ya kibla 64

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 64

11/3/2015 2:57:50 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

cha Waislamu wa dunia nzima, watakuwa wametoka nje ya safu za mahujaji wa kwenye Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu na eneo la kaburi la Mtukufu Mtume 8 na Maimamu Maasumin wengine hapo Baqii na kurejea nyumbani wakiwa na gunia la maovu. O  O  O Hata hivyo, mahujaji wa Irani lazima wazingatie akilini kwamba vitendo vyao na tabia zao katika kila hatua ya Hija zitakuwa zinaangaliwa kwa karibu na kwa udadisi sana na wote, maadui na marafiki wa mapinduzi yetu. Maadui wanajaribu kutafuta kisingizio, kiwe kidogo vipi, kuweza kutafsiri vibaya uchamungu na heshima tukufu ya watu wetu, na marafiki na wapenzi wa mapinduzi yetu wao wana shauku ya kujifunza kuhusu tabia na habari za kina za umma huu ambao umaarufu wake, kwa fadhila za Mwenyezi Mungu umekamata nadhari ya dunia nzima, na Hija ndio makutano bora kwa ushirikiano wa mataifa ya Kiislamu, ambapo Waislamu kutoka pande zote za dunia watafahamiana kati yao katika Nyumba ambayo ni mali ya jumuiya zote za Kiislamu na wafuasi wa Ibrahim A na kutelekeza tofauti zao za kimimbari, rangi, utaifa na shakhsia binafsi, na watakaporejea majumbani kwao kwa asili kuonyesha kwa ulimwengu taswira ya msimamo wa jumuiya ya Muhammad na uzuri wa undugu wa Kiislamu kwa kutekeleza maadili matukufu ya Kiislamu na kuepuka migogoro na hali ya anasa. O  O  O Nawaomba mahujaji waheshimiwa kutoka Iran kufikiria wametoka kwenye nchi gani na wanaelekea kwa nani. Wanaondoka kutoka kwenye nchi ambayo umma wake umesimama kwa ajili ya njia ya Mwenyezi Mungu na Uislamu adhimu na kubadilisha amri 65

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 65

11/3/2015 2:57:50 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

za kidhalimu kwa maagizo yang’arayo ya Uislamu, ambayo kwayo, wanaume na wanawake, na wakongwe na vijana wametoa muhanga mali zao; vijana wapendwa waliojitoa – ambao thamani yao tukufu hatuwezi kuitambua – waliuawa kishahidi na wengine kufanywa vilema au mateka; umma ambao, kwa hiari kabisa waliacha mali zao na uhai wao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na wakakaribisha misiba ya kufiwa na wapendwa wao. Wanaelekea kwenye Nyumba ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, lengo kuu la matumaini ya Mitume watukufu na mawalii waliotukuka na sehemu ya wahyi na mashukio ya Malaika Jibril mwaminiwa, na Malaika wengine wa Mwenyezi Mungu; wanasonga kuelekea kwa Mwenyezi Mungu, hivyo kila hatua na mapumziko yao yawe ya ki-Mungu, kuelekea kwenye madhabahu ya mpendwa Isma’il A ambaye ametuelekeza sisi jinsi ya kutoa kafara kila kitu tulichonacho kwa ajili ya Mwenyezi Mungu; kuelekea Madina ya Muhammad, ili kuwa wa Muhammad na kujifunza jinsi ya kuishi, jinsi ya kufanya jitihada na jinsi ya kupita kuelekea kwa wapendwa; kuelekea kwenye viwanja vya makaburi ya Mtume Mtukufu 8 na Mawalii waliotukuzwa sana ambao hawakuujali ulimwengu na mapambo yake japo kwa kiasi kidogo, wala hawakufikiria juu ya chochote kile isipokuwa amri za Mwenyezi Mungu na hawakutafuta chochote isipokuwa radhi Zake; hivyo tahadharini huko mnakokwenda! Wajibu wenu ni mkubwa kabisa, vitendo na amali zenu ni kwa nyongeza ya kuwa mbele ya Mwenyezi Mungu na mkiangaliwa na mawalii na Malaika wa Mwenyezi Mungu, mbele ya macho ya maelfu ya mahujaji kutoka nchi za Kiislamu ulimwenguni kote, na kuwa uwezekano wakati mwingine wakaathiriwa na uenezi mkubwa wa maadui wa Uislamu na Iran, ambao wamo shughulini mchana na usiku wakiwa na uzushi unaodaiwa kuhusu Uislamu na umma wa Irani na watumishi wake, wakiwaelezea kwa ubaya watu walioamka wa nchi hii, wakitegemea ama kuwafanya baadhi ya 66

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 66

11/3/2015 2:57:50 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

Waislamu wa ulimwengu waamini au kuwatupia mkanganyiko juu yao. Na miongoni mwa watu wetu wapendwa, kuna walemavu, mashahidi walio hai, waliopona katika vita na familia za mashahidi, ambao wametoa macho maangalifu kwenye vitendo vyenu, na sasa, mpo hapo pamoja na wajibu wenu mzito na dhamana tukufu, majukumu yenu ya Kiislamu na dhamira zenu, na silika zenu za asili. Mtakuwa ama – shukrani kwa damu ya mashahidi na heshima ya Uislamu na umma wenu mpendwa usio na hatia – watangazaji wenye fahari wa haki na uadilifu, wajumbe wa Uislamu na Jamhuri ya Kiislamu kwa vitendo na maneno, na kwa nyongeza ya kupata malipo ya kiroho ya Hija kwenye Nyumba ya Mwenyezi Mungu na makaburi ya Mawalii wa Mwenyezi Mungu, hususan Mtume aliyetukuka 8 mtaneemeshwa kwa rehema za Mwenyezi Mungu na baraka zinazotunukiwa na bakisho la Mwenyezi Mungu – roho zetu ziwe kafara kwa ajili ya kudhihiri kwake – na kuzamishwa katika neema za Mwenyezi Mungu na rehema Zake mwote katika dunia hii na hiyo ijayo. Au, Mungu aepushilie mbali, mtakuwa watangazaji wa shetani na waenezi wa matangazo ya maadui wa Uislamu na sababu ya fedheha kwa Uislamu na Jamhuri ya Kiislamu na mashahidi na watesekaji wa umma wenu, kwa hali ambayo mtakataliwa kama watu wasioaminiwa. Mwenyezi Mungu atulinde na kutuongoza kwenye Hija yenye kukamilika na kukubalika, Insha’Allah. Sasa, enyi wapendwa, mnakabiliwa na chaguzi kati ya kutafuta ustawi wa milele na kupata radhi za Mwenyezi Mungu na wapenzi Wake, au uovu na kukoseshwa au kunyimwa kwa milele. Nataraji kwa rehema ya muda wenye thamani na kwa vituo vitukufu na du’a za watu walionyimwa ambazo zinakusindikizeni, mtakuwa watu wa daraja la kwanza na kuleta heshima na fahari kwa Uislamu, kwa 67

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 67

11/3/2015 2:57:50 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

mashahidi, walemavu na wasiojiweza, na kwa taifa na nchi yenu, mtawafukuza maadui wa Uislamu na Waislamu, mtawakatisha tamaa adui zenu na kuwaweka kwenye aibu na dharau wakati mkiwachangamsha marafiki. Ingawa ninyi mnajua nini cha kufanya na nini cha kuepuka kufanya, lakini mimi ninadokeza yale mambo muhimu kabisa kama kutekeleza wajibu wangu na kama kauli ya mwisho: Chungeni kwa umadhubuti hasa sifa na tabia za Kiislamu na kibinadamu kwa mahujaji wote, kutoka kwenye tabaka lolote lile, la rangi, lugha, nchi, makundi ya kimimbari au kiutamaduni litakalokuwa; onyesheni subira wakati wote, hali na matukio; mtendeeni kila mtu kwa ukarimu; kuweni wapole na wenye amani pale mtakapokabiliwa na machukizo na muwe na upendo dhidi ya kutendewa mabaya na kwa kumridhisha Mwenyezi Mungu, kuweni wavumilivu katika baa au bahati mbaya yoyote itakayotendwa na yoyote yule awaye, kwa moyo mkunjufu na ukarimu, kwa vile vituo hivyo vitukufu na makaburi adhimu sio mahali pa migogoro na mapigano. Kuweni na tabia kwa namna ambayo mtaonyesha kwamba mnatoka kwenye nchi ya Imam Ja’far as-Sadiq (amani iwe juu yake) ambayo peke yake ni huduma kwa Uislamu na kwa Jamhuri ya Kiislamu na kwa wananchi wenzenu, na kuweni na uhakika kwamba mtapata shukurani za utaratibu huu mtakaporejea nyumbani, kwa nyongeza ya kupata radhi za Mwenyezi Mungu na za Mtume mtukufu 8 na Hujja wa Allah aliyebakia (nafsi yangu iwe muhanga kwa kudhihiri kwake), ambaye yuko hadhiri na anashuhudia.

68

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 68

11/3/2015 2:57:50 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

12 HIJA: KITOVU CHA MAPAMBANO DHIDI YA MAFIDHULI WA DUNIA

K

wa kushirikiana na mahujaji wengine kutoka kote duniani, igeuzeni Makka tukufu kuwa kitovu kwa ajili ya kutoa sauti dhidi ya madhalimu, kwani hii ni mojawapo ya siri za Hija na Mwenyezi Mungu hana haja na ibada za kibinadamu na “Labbeyka� nyingi tu. Napenda niwapongeze Waislamu wote wa dunia katika wakati huu wa sikukuu hii kubwa ya Kiislamu ya Makafara; sikukuu ambayo inawakumbusha wale wenye utambuzi kuhusu ile madhabahu ya Ibrahim, madhabahu ambayo inawafundisha kizazi cha Adam na wateule wa Mwenyezi Mungu na mawalii, kule kujitoa muhanga na vita au mapambano dhidi ya maovu katika njia ya Mwenyezi Mungu. Hakuna wengine isipokuwa wale Manabii watukufu, Mawalii waliotukuka kabisa na waja ama watumishi wa Mwenyezi Mungu watakatifu wanaoweza kutambua kina cha vipengele vya kitawhid na kisiasa vya tendo hili. Huyu baba wa Tawhid na mvunjamasanamu ya dunia alitufundisha sisi na binadamu wengine wote, kwamba kutoa muhanga katika njia ya Mwenyezi Mungu kuna thamani yake ya kisiasa na kijamii kabla ya kipengele cha kiibada na kitawhid. Alitufundisha sisi na wote kutoa kafara yale matunda yetu ya maisha yanayopendeza sana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kusherehekea. 69

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 69

11/3/2015 2:57:50 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

Jitoeni muhanga ninyi wenyewe na wale muwapendao ili kuthibitisha na kutangaza dini ya Mwenyezi Mungu na haki ya kimbinguni. Alitufundisha sisi sote kwamba Makka na Mina ni madhabahu za wafuasi walioambatana, na mahali pa kutangaza imani ya Mungu Mmoja na kukanusha ushirikina, kwani kujiambatanisha mtu na maisha yake na wapenzi wake pia kunahesabiwa kama ni ushirikina. Aliwafundisha kizazi cha Adam A kupambana kwa ajili ya haki na kuwasilisha kwa wakazi wa ulimwengu, kutoka mahali hapa palipotukuzwa, lile somo la ibada na kujitoa muhanga; kuwaambia kwamba mtu lazima apoteze mali yake anayomiliki katika njia ya haki na utekelezaji wa uadilifu wa kimbinguni na kukata mikono (nguvu) ya wapagani, na kuachilia kila kitu na hata kutoa kipenzi chake kama vile Isma’il (Dhabihullah) ili kwamba haki iwe ya kudumu milele. Huyu mvunja-masanamu na mwanawe kipenzi, mvunjamasanamu wa pili, bwana wa mitume, Muhammad Mustafa 8 walifundisha wanadamu kwamba masanamu yote, ya aina yoyote, ni lazima yavunjwe na Ka’aba kama makao makuu na popote palipopanuliwa kutoka hapo, mpaka kwenye sehemu ya mwisho ya ardhi, hadi siku ya mwisho ya dunia, lazima pasafishwe kutokana na uchafu wa masanamu ya aina yoyote, iwe ni kinyago cha kuchongwa, jua, mwezi, mnyama au binadamu; bado ni sanamu gani linaweza kuwa baya na la hatari sana kuliko dhalimu, dikteta, mwote katika historia, kuanzia wakati wa Adamu mpaka wakati wa Ibrahim na hadi wakati wa Muhammad 8 hadi kwenye wakati wa mwishoni ambapo mvunja-masanamu wa mwisho atatoa sauti na kulingania juu ya tawhid – imani ya Mungu Mmoja tu? Hivi haya mataifa makubwa yenye nguvu ya zama zetu hizi sio masanamu makubwa ambayo yanawaita wakaazi wa ulimwengu 70

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 70

11/3/2015 2:57:50 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

kwenye kuwatii na kuwaabudu? Je, hawalazimishi utawala wao kwa mabavu, unafiki au fedha? Ka’aba tukufu ndio kituo pekee cha kuvunja masanamu kama hayo. Ibrahim, mwandani wa Mwenyezi Mungu katika nyakati za mwanzoni na Muhammad 8 kipenzi cha Mwenyezi Mungu, na mwana mpenzi wa Mtume (saww), Mahdi, aliyeahidiwa (nafsi yangu iwe kafara kwa ajili yake) mwishoni mwa zama walitamka na watakuja kutamka ule mwito kwa ajili ya Tawhid. Mwenyezi Mungu alimwambia Ibrahim: “Na watangazie watu Hijja; watakuja kwa miguu na juu ya kila mnyama aliyekonda kutoka kila njia ya mbali.” Na akasema tena: “…..na uitwaharishe nyumba Yangu kwa ajili ya wanaozunguka na wakaazi na wanaorukui na wanaosujudi.” Ina maana usafishaji wa uchafu wote, ambao mbaya zaidi juu ya wote ni ushirikina ambao unatajwa katika sehemu ya aya hii tukufu. Na tunasomo katika Surat-Tawba: “Na ni tangazo litokalo kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wa watu siku ya Hijja kubwa ya kwamba Mwenyezi Mungu amejitoa na washirikina na pia Mtume Wake.” Wao wanawachukia washirikina. Mahdi, mtarajiwa, anasemekana, katika dini tofauti na kwa Waislamu wote kwa ujumla wao, kuja kunyanyua wito wa Tawhid kutoka kwenye al-Ka’aba. Wote wananyanyua sauti zao kutoka alKa’aba na Makka na sisi lazima tuwafuaishe na kuwaiga wao na kunyanyua sauti zetu kwa umoja wa maneno na kudai juu ya imani ya Mungu Mmoja – Tawhidi kutoka mahali pale palipotukuzwa na kuvunja masanamu kwa sauti zetu na miito na kwa kutoa manung’uniko yetu na uwazi wetu na kuwafukuza mashetani ambao juu yake yuko yule ibilisi mkubwa, ili tuwe tumetekeleza ibada za Hija kama vile Ibrahim, Muhammad na Mahdi walivyofanya, 71

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 71

11/3/2015 2:57:50 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

vinginevyo tutahusika kwenye ule usemi kwamba: “Ni idadi kubwa kiasi gani ya waombolezaji na ni wachache kiasi gani hao mahujaji wa kweli.” O  O  O Enyi wote, wapendwa mahujaji kwenye Nyumba Takatifu ya Mwenyezi Mungu! Enyi mliokimbilia kuelekea kwenye Nyumba ya Mwenyezi Mungu, kituo cha Tawhidi, mahali pa wahyi, kituo cha Ibrahim na Muhammad – wale wavunja-masanamu wawili wenye uwezo usio kifani na wapinzani dhidi ya madhalimu wakandamizaji – na mkaweza wenyewe kufikia vituo hivi vitukufu ambavyo vilikuwa ardhi za kiu na ardhi zilizoinuka zisizo na maji katika zama za wahyi lakini zilikuwa ni mahali pa mashukio ya Malaika wa Mwenyezi Mungu na sehemu ya kukimbilia ya wapiganaji wa Mwenyezi Mungu na kituo cha Mitume wa Mwenyezi Mungu na waja Wake wachamungu. Ni lazima muwatambue vema wamaizi wakubwa hawa, jiandaeni wenyewe katika kituo hiki cha uvunjaji masanamu, kwa ajili ya kuvunja masanamu makubwa makubwa ambayo yameendelezwa kama nguvu ya kishetani na waporaji wala nyama za watu na kamwe msiziogope nguvu hizi zisizo na imani. Mtegemeeni Mwenyezi Mungu, kuleni kiapo cha utii wa umoja dhidi ya nguvu za ushirikina na fitna na epukeni kufarakana na migogoro. Na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na msigombane wenyewe kwa wenyewe na hivyo mkavunjika moyo, na nguvu yenu kuwaondokeni; na kuweni na subira, hakika Mwenyezi Mungu yupo na wale wenye subira. O  O  O

72

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 72

11/3/2015 2:57:50 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

Katika mantiki ya wenye kiburi wa dunia, yule atakayeonyesha kukirihishwa na wapagani, yeye atashutumiwa kwa upagani, na “mamufti” na watoto wa “mamufti” wale wa kizazi cha Bal’am Ba’ura watamhukumu kifo. Si ajabu kwamba, katika historia ya Uislamu, upanga ule ule wa upagani na ukafiri ambao ulikuwa umefichwa chini ya vazi la hujaji la ma-Yaziid na watendaji wa kukodishwa wa Bani Umayyah – laana ya Mwenyezi Mungu iwe juu yao – kwa ajili ya mauwaji ya watoto wakweli bora wa Mtukufu Mtume 8, Abu Abdillah al-Husayn A na wafuasi wake waaminifu, kwa mara nyingine tena unatoka kwenye mavazi ya warithi wa BANI-SUFYAN na wanakata shingo za wafuasi wasafi na halisi wa Imam Husein A katika maeneo yenye joto yanayozunguka Karbala ya Hijaz, katika madhabahu takatifu, na kuwashutumu na uzushi uleule kama wale ma-Yaziid walivyofanya dhidi ya watoto waaminifu wa Uislamu, kama walivyowaita wa mataifa, wakana-Mungu, washirikina na ambao damu zao zinaweza kumwaga bila hofu ya kuadhibiwa. Wamewashutumu wafuasi wao kama vivyo hivyo. Tunataraji, Mungu akipenda, kutuliza maumivu ya mioyo yetu, kwa wakati wake, kwa kulipiza kisasi wenyewe juu ya Amerika na ufalme wa Saudi na tusiache hata kovu moja la hali ya kunyimwa kutoka kwenye muonjo wa uhalifu huu mkubwa, kwenye mioyo yao, na baada ya hapo, tutauingia Msikiti Mtukufu baada ya kusherehekea ushindi wa haki dhidi ya kufuru na ukafiri na ukombozi wa al-Ka’aba kutoka kwenye makucha ya wasiojiweza na wasioaminika. O  O  O Waislamu, wakati wanapokwenda Hijja, ni lazima watekeleze hijja ambayo imechangamka, kuitwanga na kuilaani Urusi ya 73

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 73

11/3/2015 2:57:50 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

kihalifu na Amerika. Hiyo itakuwa ni hijja yenye kukubalika kabisa. O  O  O Mahujaji wa kwenye Nyumba ya Mwenyezi Mungu na wenye shauku ya kukutana na Mwenyezi Mungu wanaondoka kutoka kwenye majumba yao ya ubinafsi kuelekea kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake mpendwa katika wakati ambapo ile Makka tukufu imejiandaa kuwapokea wale Waislamu wanaosaka haki na uadilifu, na kukaribisha sauti zao zinazoponda dhidi ya madhalimu wakubwa na wateka nyara wakubwa wa zama hizi, na inangojea kwa hamu kuwapokea. O  O  O Mahali pa kutupia mawe panawangojea kwa hamu kuwapokea wenye kujitoa kafara ambao wanakuja kutoka kwenye nchi ambayo mashujaa wake wamewafukuza bila woga mashetani wakubwa, wadogo na wa kati, na sasa wakiwa mahali hapa, watalitupia mawe na kulifukuza lile kundi la mashetani kutoka kwenye makao makuu na maeneo yake yanayozunguka hapo ambayo ni dunia nzima. O  O  O Ni lazima mzingatie akilini kwamba tiba ya mwisho imo katika muungano wa Waislamu wote, na kukubaliana kwao kwa pamoja, kukata mikono (nguvu) ya mataifa yenye nguvu kutoka kwenye nchi za Kiislamu na kukamilisha ile miito iliyotolewa katika vituo hivi vitukufu na maeneo ya makaburi yaliyopewa heshima, wakati wanaporejea nyumbani. 74

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 74

11/3/2015 2:57:50 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

O  O  O Mwenyezi Mungu akipenda hatutaiacha sauti ya maafikiano na Marekani na Urusi, kufuru na ushirikina iwe inasikika masikioni mwetu kutokea al-Ka’aba, mimbari kuu na tukufu iliyowekwa kwenye kilele cha ubora wa mwanadamu, ambapo huzuni za wale wanaokandamizwa lazima zitangazwe hapo badala yake na wito wa imani ya Mungu Mmoja – Tawhidi upaze sauti na kutoa mwangwi. Tunamuomba Mwenyezi Mungu atujaalie na nguvu ya kupaza sauti ya kifo cha Marekani na Urusi, sio tu kutoka kwenye Ka’aba ya Waislamu, bali pia kutoka kwenye kengele za makanisa duniani kote. Acha Waislamu na wale wanaokandamizwa ulimwenguni wajisikie huru na wajivunie ile hatari isiyo na mwisho ambayo mapinduzi yetu ya Kiislamu yameijenga kwa ajili ya waporaji madhalimu, na watangaze ukombozi wao na uhuru wa kusimamia maisha yao wenyewe na hatima zao na wapate kufidia huzuni zao, kwani kipindi cha mkwamo na maudhi na kuvuta hewa katika mazingira ya upujufu kimefikia mwisho na vitalu vya maua (mafanikio) vya mataifa vimefunuliwa. Na nina matumaini kwamba Waislamu wote watawaza na kukisia uchanuaji wa uhuru, hewa yenye manukato ya majira ya kuchipua, maua mapya ya mapenzi na upendo na ujaaji wa chemchem safi za uchangamfu wa hiari zao wenyewe. Ni lazima sisi wote, tujitoe kwenye kinamasi cha ukimya na kutotingishika ambamo wanasiasa wa Marekani na Urusi wamepanda mbegu za kifo na utumwa, tuanze safari kuelekea kwenye bahari ambayo kutoka humo imechimbuka “Zamzam” na kusafisha kwa machozi yetu lile pazia la Ka’aba na sehemu takatifu ya Mwenyezi Mungu ambayo imetiwa doa na mikono michafu ya Marekani isiyoaminika, na kizazi chao cha kimarekani. 75

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 75

11/3/2015 2:57:50 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

Enyi Waislamu wa nchi zote kote duniani! Kwa vile mmewekwa kwenye kifo cha taratibu chini ya umiliki wa kigeni, ni lazima muishinde hofu yenu ya kifo na mnufaike kutokana na vijana wenye shauku ya kutafuta Shahada, ambao wako tayari kuivunja mipaka ya wapagani. Msijaribu kuendeleza hali zenu za sasa hivi, bali fikirieni kuepuka kutekwa, na ukombozi kutokana na utumwa na shambulieni dhidi ya maadui wa Uislamu, kwani heshima na uzima wenu unategemea mapambano na hatua yenu ya mwanzo ni utashi na dhamira ya kujitoa wenyewe kwenye umiliki wa wapagani na washirikina, hususani Marekani. Tukiwa tuko Makka au laa, nyoyo na nafsi zetu ziko pamoja na Ibrahim na ndani ya Makka. Watufungie milango ya Madina ya Mtume ama laa, mafungamano ya mapenzi kwa Mtukufu Mtume 8 kamwe hayatavunjika au kudhoofika. Tunaswali tukielekea Ka’aba, na kunafariki tukielekea Ka’aba na Alhadulillahi, tunabakia imara katika utiifu wetu kwa Mwenyezi Mungu, kwa vile tuliweka msingi wa kuonyesha kuwachukia wapagani, kwa damu ya maelfu ya vipenzi vyetu waliouawa kishahidi na hawakutarajia msaada wa watawala waovu wa nchi za Kiislamu na zisizo za Kiislamu. Sisi tulionyimwa na tulio pekupeku bila viatu ndio watu tuliokandamizwa daima katika historia. Hatuna mwingine isipokuwa Mwenyezi Mungu, na kamwe hatutaacha kuwapiga vita madikteta na madhalimu, hata kama tutakatwakatwa viungo mara elfu. O  O  O Wapendwa kaka zangu na dada zangu! Katika nchi yoyote mtakakokuwa, lindeni Uislamu wenu na heshima ya taifa lenu dhidi ya maadui zenu, yaani, Marekani, Uzayuni wa kimataifa, na nchi kubwa zenye nguvu za Magharibi na Mashariki bila ya kuangalia huku na huko na fichueni dhulma za maadui wa Uislamu. Ndugu 76

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 76

11/3/2015 2:57:51 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

zangu Waislam, mabibi na mabwana! Mnatambua kwamba maslahi yetu yote ya kimada na kiakili yanatekwa nyara na mataifa makubwa ya Magharibi na Mashariki yakituacha sisi katika umasikini na utegemezi kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni na kijeshi. Zindukeni na mrudishe shakhsia yenu ya Kiislamu. Msisalimu amri kwenye ukatili na fichueni njama ovu za husuda za waporaji wa kimataifa, ambao juu yao anasimama Marekani. O  O  O Tunao wajibu wa kutamka kuchukizwa kwetu na wapagani kama hatua yetu ya kwanza ya kupigana na kuendelelea kwenye hatua inayofuata, na katika kipindi chochote kile inahitajia mtindo wake unaofaa wa kudhihirisha na kupanga. Ni lazima tuone ni nini tunachopaswa kufanya kwa wakati kama huu wa leo ambapo wakuu wa upagani na ushirikina wanatishia uwepo wa Tawhidi (imani juu ya Mungu Mmoja) na wamechezea uwakilishaji wote wa kitaifa, kiutamaduni, kidini na kisiasa wa mataifa. Hivi tukae tumebweteka majumbani mwetu na kuvumilia hivihivi mashetani na kizazi cha mashetani hawa, kwa uchambuzi wa kimakosa, kudhalilisha binadamu, na kutia msukumo wa moyo wa kukosa uwezo na kutokujiweza katika akili za Waislamu, na kuizuia jamii kupata utakaso ambao ndio lengo la juu na ukamilifu wa hali ya juu kabisa, na kujiridhisha wenyewe kwamba yale mapigano ya Mitume F dhidi ya masanamu na uabudu masanamu ulikuwa unakomeshea kwenye vinyago vya miti na mawe visivyo na uhai, na fikiria kwamba, Mwenyezi Mungu aepushilie mbali, Nabii kama Ibrahim ambaye aliasisi uvunja masanamu alitelekeza uwanja wa mapambano wakati alipokabiliwa na madhalimu? Ambapo uvunjaji masanamu wake wote na mapambano dhidi ya akina Nimrodi, na 77

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 77

11/3/2015 2:57:51 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

waabudu mwezi, jua na nyota vilikuwa ni utangulizi wa uhamaji na uhamaji wote, mateso, kuishi ndani ya jangwa kavu, kuijenga Nyumba na kumtoa kafara Ismail vilikuwa ni utangulizi wa kazi ya kitume, ambamo yule mwisho wa Mitume 8 anayarudia maneno ya warasimishaji wa mwanzo na wa mwisho wa Ka’aba na anatangaza kazi yake ya milele kwa kusema: “Ninamchukia yule ambaye mnashirikiana naye.” Endapo tutawasilisha uchanganuzi wa namna nyingineyo, tutapaswa kuamua kwamba kwa wakati huu wa sasa hakuna sanamu wala uabudia masanamu kabisa, lakini ni mwanadamu gani mwenye busara aliyepo ambaye hakuutambua uabudia masanamu wa kisasa katika miundo yake maalum, mvuto na shere zake, na akawa hana habari kuhusu umiliki wa majumba ya sanamu kama vile White House, Ikulu ya Marekani, juu ya nchi za Kiislamu na maisha na heshima za Waislamu na wa nchi za dunia ya tatu? Leo hii kilio chetu cha kuchukizwa na wapagani ni kelele dhidi ya ukatili wa madhalimu, na ni kelele ya watu ambao wamo kwenye machungu ya upitukaji mipaka wa Mashariki na Magharibi, ambao juu yake kabisa kuna Marekani na washirika wake, watu ambao ardhi yao na mali zao vimetekwa nyara na kuporwa. Kilio chetu cha kukarahika na kelele ya taifa ni juu ya taifa linalokandamizwa na kuonewa la Afghanistani, na ninasikitika kwamaba Urusi haikufuata ushauri wangu kuhusiana na Afghanistan na ikavamia nchi hii ya Kiislamu. Kwa mara nyingine tena ninawaonya waachane kabisa na taifa la Afghanistan, kwani sasa wanaweza kujiamulia wenyewe hatima yao na kuhakikisha usalama wa uhuru wao. Hawahitajii ulezi wa Kremlin au Marekani, na kwa uhakika wa kutosha kabisa, kwa kuondoka majeshi ya kigeni kamwe hawatanyenyekea kwenye tawala nyinginezo, na watamuangusha Mmarekani kama atajaribu kuingilia kati. 78

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 78

11/3/2015 2:57:51 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

O  O  O

13 ONYO DHIDI YA NJAMA ZA VIBURI WA DUNIA KATIKA WAKATI WA ­HIJJA

W

aislamu wanaohudhuria kwenye vituo hivi vitakatifu, wa kutoka taifa lolote lile au madhehebu yoyote yale yanayoweza kuwa, ni lazima watambue vyema kwamba adui mkubwa wa Uislamu na Qur’ani na Mtume Mtukufu 8 ni yale mataifa makubwa, hususan Marekani na mwanae dhalimu Israili ambao wana mtazamo wa uchu juu ya mataifa ya Kiislamu, na hawaachi uhalifu wowote ule na njama za kupora hazina ya chini ya ardhi na ya juu ya ardhi kadhalika, na siri yao ya mafanikio ni kupandikiza mbegu ya chuki na migogoro miongoni mwa Waislamu kwa njia yoyote inayowezekana. Wanaweza wakatumia mamullah wao wa kukodi kusambaratisha na kuwatenganisha Shi’ah na Sunni wakati wa ibada za Hijja, na kuchochea moto wa mpango huu wa kishetani kwa kiasi kwamba watu wenye akili nyepesi wanaweza wakawaamini, na hivyo kusababisha mfarakano na vurugu. Ndugu zetu mabibi na mabwana wa madhehebu zote lazima wawe na tahadhari na wajue kwamba 79

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 79

11/3/2015 2:57:51 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

wale mamluki wa kulipwa wenye mioyo mipotovu wananuia kuuchukua Uislamu, Qur’ani na hadithi za Mtukufu Mtume 8 kwa jina la Uislamu au angalau kuzipotosha. Kaka zetu na dada zetu lazima wazingatie akilini kwamba Marekani na Israili wako dhidi ya kiiini cha Uislamu kwa sababu wanauona Uislamu, Kitabu kitukufu na hadithi za Mtukufu Mtume 8 ni vikwazo katika njia yao ya uporaji, na Iran kwa kufuata Kitabu hicho hicho imesimama na kufanya mapinduzi na kupata ushindi. Leo hii, njama dhidi ya Iran na Hizbullah kwa hakika zimelenga katika kuufuta Uislamu, Kitabu na hadithi za Mtume 8 na Irani sio chochote zaidi ya kisingizio. Walikuwa wameridhika sana na Iran katika wakati ambapo Shah alikuwa mtiifu na mnyenyekevu kwao, wakaifanya Iran iwategemee wao katika kila kitu na ikafuata mipango na mbinu zao za kuufuta Uislamu. Lakini wanaipinga Iran ya leo ambayo imekata mikono yao kutoka kwenye maslahi yake na ikawafukuza washauri wao wa kijeshi na washirika wao kutoka kwenye nchi hiyo. Kwa upande mwingine, wao wanajua kabisa kwamba Uislamu ndio adui yao halisi isipokuwa ule Uislamu uliobuniwa na baadhi ya serikali na wale mamullah (wanachuoni wa bandia) wabaya zaidi. Wanaukubali Uislamu kama huo na kwa kukubaliana wanawaunga mkono na kulinda maslahi yao na inaanzia kwenye msimamo ambao ni kuwasonga na kukaba vilio vya utetezi vya Mahujaji wa Iran kwenye kituo cha wahyi na mahali pa mashukio ya: Tangazo kutoka kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, kwa wanadamu katika siku ya Hijja Kubwa: “Mwenyezi Mungu amejitoa na washirikina na pia Mtume Wake.” Wanawachukia washirikina. Na watajeni kwamba ni wenye kumkufuru Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo, katika mwanya wa wakati huu, ni wajibu mtukufu wa Mahujaji kukataa kila usemi watakaoweza kusikia kutoka kwa wazungumzaji, ambayo unaweza kuleta muonjo wa kusababisha faraka na utengano miongoni mwa 80

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 80

11/3/2015 2:57:51 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

safu za Waislamu na wafikirie kupiga kelele ya kuwachukia wapagani kama wajibu wao, ili Hijja hiyo iwe ya ki-Ibrahim (Abul-Anbiya), na Muhammad Mustafa 8 vinginevyo ule usemi wa: “Ni idadi kubwa kiasi gani ya waombolezaji na ni wachache kiasi gani hao mahujaji wa kweli” utatumika kwao wao. O  O  O Katika baraza la mkusanyiko wa Waislamu wa ulimwengu na wakati wa maafikiano ya jumla ya makundi mbalimbali ya Waislamu kwa ajili ya uokoaji wa nchi zao kutoka kwenye makucha machafu ya mataifa makubwa na katika baraza la kuondoa mikono ya Mashariki na Magharibi kwa maafikiano ya maneno na kumtegemea Mwenyezi Mungu, chini ya bango la Uislamu na Tawhidi – upweke wa Mungu, shetani mkuu amewakusanya watoto wake ili kupanda mbegu za utengano miongoni mwa Waislamu, kwa kila ujanja unaoweza kufikirika, na kuwaingiza watu wa Tawhidi na ndugu wanadini katika utesi na uhasama na kusafisha njia kwa ajili ya umiliki na uporaji wao unaoongezeka. Shetani mkuu anahofia kuenezwa kwa mapinduzi ya Kiislamu nchi zingine, za Kiislamu na zisizo za Kiislamu na uondoshwaji wa mikono yake michafu kutoka kwenye nchi alizokwisha kuzimiliki. Kwa vile hakunufaika na vikwazo vya kiuchumi na uvamizi wa kijeshi, alijaribu mbinu nyingine ili kuyatafsiri vibaya mapinduzi yetu ya Kiislamu mbele ya Waislamu wa dunia na kusababisha Waislamu wapigane wenyewe kwa wenyewe, ili aweze kuendeleza udhalimu wake na uporaji. Ndio sababu katika wakati muafaka wa jitihada za Iran kwa ajili ya maafikiano ya kauli miongoni mwa Waislamu wa duniani, kushikamana kwenye Uislamu mtukufu na hali ya umoja, mmoja wa watu wafitina wabaya wa Marekani na 81

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 81

11/3/2015 2:57:51 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

rafiki wa Shah aliyevuliwa taji na kuangamizwa aliagizwa kutafuta fatwa kutoka kwa mafaqihi (mamufti wa kununuliwa) wa madhehebu ya Sunni ya kuwahukumu Wairani kuwa ni wapagani, na baadhi ya watu hawa wakasema: “Uislamu ambao Iran inauanzisha ni tofauti na Uislamu wetu.” Subhanallah! Ni kweli, Uislamu wetu ni tofauti na ule Uislamu wa wale wanaowaunga mkono Wamarekani, watu kama Sadat na Begin na kushikana mikono na maadui wa Uislamu, licha ya amri ya Mwenyezi Mungu, na hawaachi juhudi yoyote au uzushi na usingiziaji kwa ajili ya kuwagawanya na kuwatenganisha Waislamu. Waislamu wa dunia lazima wawafanye watu hao wachochezi wafahamike na kuzimisha njama zao za kifitna zenye madhara. O  O  O Katika ibada zote hizi na vituo vitakatifu hivi, sharti la kupata matumaini ya kawaida na malengo ya kibinadamu ni uunganishaji wa Waislamu wote, katika hatua hizi, na neno la maafikiano ya pamoja ya Waislamu wa makundi yote, bila kujali lugha zao za kikabila, nchi zao, rangi zao au hisia za chuki za kipagani za makabila, na kupiga makelele ya pamoja dhidi ya adui yao wote ambaye ndiye adui wa Uislamu na kuhakikisha yamechapa usoni mwake katika kipindi hiki cha wakati. Anauchukulia kama ni kikwazo dhahiri kwenye uporaji wake na anajaribu kuuondoa kwa njia ya uchochezi kupitia mawakala wake wa kulipwa ambao juu yao ni wale wanachuoni bandia wa kidunia wenye wivu na watumishi wa mabaraza ya kifalme (maakhundi) ambao wameajiriwa kutekeleza dhamira zake za kisirani mahali popote na wakati wowote hususan wakati wa msimu wa Hijja na ibada zake tukufu. Katika hatua zote na vitendo vyote vya ibada hii ambayo imekusudiwa hasa kwa ajili ya mkusanyiko wa 82

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 82

11/3/2015 2:57:51 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

Waislamu kutoka kote ulimwenguni kwa manufaa ya faida ya watu walionyimwa wa ulimwenguni – na ni manufaa gani yanaweza kuwa juu zaidi ya uondoshaji wa mikono ya waporaji kutoka kwenye nchi za Kiislamu…..Mahujaji lazima wawe na tahadhari ya kutosha juu ya vitendo pinzani vya Uislamu na Qur’ani vya mawakala hawa wafitini na maakhundi wachochezi, na kuwafukuza wale ambao hawaujali Uislamu na maslahi ya Waislamu – haidhuru washauriwe kiasi gani – kwa sababu wao ni mashetani na waovu zaidi kuliko wapagani. Ni dhahiri kabisa kwetu sisi na kwa wanafikra na wachunguzi ambao wanatambua dhamira za kifitna za utawala wa Aali-Saud kwa nini wanatushutumu sisi na vurugu na kutuita sisi kuwa ni watenganishaji, ambao tangu ushindi wetu tumekuwa tukipiga kelele juu ya umoja na uunganishwaji wa Waislamu kujiona wenyewe ni wenye huruma kwa Waislamu katika machungu na mafanikio pia, na baya kuliko hilo, wanawashutumu mahujaji ambao wamesafiri kwa mapenzi kabisa kuja kuhiji kwenye eneo la kaburi la Mtukufu Mtume 8 na sehemu takatifu ya Mwenyezi Mungu, kwa tuhuma za kuhamasisha na kuandaa kuikalia Ka’aba, kuchoma mahali patakatifu pa Mwenyezi Mungu na kuibomoa Madina, na wanadai uwepo wa majeshi yetu na maafisa wa kiraia kama ushahidi na msingi wa madai yao. Kwa mantiki ya Aali al-Saud, mtu mwanajeshi, walinzi wa mapinduzi (sepah pasdaran) na maafisa watumishi wa dola wa Iran lazima watenganishwe na Hijja na mahujaji wanaotokana na maafisa wa kijeshi au dola wanawashangaza wao na kuwachukulia kama wenye njama. Kwa mtazamo wa wenye makuu na kiburi wa dunia maafisa waandamizi wa nchi za Kiislamu lazima wasafiri tu kuelekea Magharibi. Hijja sio shughuli yao. Wafanyakazi wa kuajiriwa na Marekani wanachukulia uchomaji wa bendera ya Marekani kama uchomaji wa sehemu takatifu ya Mwenyezi Mungu 83

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 83

11/3/2015 2:57:51 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

na mwito wa “Ianguke Urusi, ianguke Marekani na ianguke Israili,” kama ni uadui kwa Mwenyezi Mungu, Qur’ani na Mtukufu Mtume 8 na wanawatafsiri au kuwachukulia maafisa wetu wa kijeshi waliovalia vazi la hujaji kama viongozi wa njama fulani. O  O  O

84

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 84

11/3/2015 2:57:51 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

14 WANACHUONI WATUMISHI ­WA VITALA

S

ikukuu yenye kheri na baraka kwa hakika ni ile siku ambapo, kwa utambuzi wa Waislamu na uchamungu wa wanachuoni wa kidini, Waislamu wote wa dunia nzima wanaokolewa kutoka kwenye utawala wa madhalimu na wateka nyara wa dunia, na lengo hili tukufu linafikiwa tu pale vipengele mbalimbali vya sheria za Kiislamu vinaweza kuwasilishwa kwa mataifa yanayodhulumiwa na mataifa hayo yakaufahamu ule Uislamu usiotambulika, alimuradi fursa kwa ajili ya matukio ya majaaliwa kama hayo hazipotezwi. Na ni fursa gani ya juu na ya fahari kabisa kuliko mkusanyiko wa Hijja tukufu ulioandaliwa na Mwenyezi Mungu kwa ajili ya Waislamu? Lakini kwa masikitiko makubwa vipengele tofauti vya wajibu huu wa kidini mtukufu na wa majaaliwa umebakia katika hali ya utata kutokana na upotovu wa genge la watawala wa Kiislamu wasio na haki na wanachuoni waovu watumishi wa mabaraza ya watawala na uelewa wenye mapungufu wa baadhi ya watu wenye vilemba na wanafiki wenye kujifanya watakatifu katika nchi zote za Kiislamu; watu wasio na busara ambao wanapinga hata kuanzishwa kwa serikali ya Kiislamu na wanaiona ni mbaya kuliko serikali yenye kiburi na majivuno; mafidhuli ambao wameuwekea mipaka finyu wajibu wa kidini wa Hijja na kuwa utendaji wa ubabaishaji mtupu, na wanaona kwamba kuzungumzia matatizo ya Waislamu na ya nchi za 85

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 85

11/3/2015 2:57:51 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

Kiislamu kama kusiko halali na kunakokwenda sambamba na kufuru; wategemezi wa serikali chochezi na za kidikteta ambao wanaoamulia vibaya vilio vya watu wanaokandamizwa ambao wamekusanyika katika kituo cha kupigia makelele ya kudai haki kama ni vilio vichafu na vya kinyume na Uislamu wenye kughushi ambao wameubana Uislamu kwenye mipaka ya kuishia misikitini na sehemu za ibada na kutangaza shughuli yoyote inaoonyeshwa kwa ajili ya mambo ya Waislamu kama isiyo ya Kiislamu na ni kinyume na wajibu wa Waislamu na Ulamaa wao. Lakini kwa masikitiko makubwa kabisa, upeo wa propaganda yao ya kichochezi imefika na bado inaendelea kwenda mbali zaidi kiasi kwamba uingiliaji wowote katika masuala ya kijamii na kisiasa ya ummah wa Waislamu unaonekana kuwa kinyume na wajibu wa wahudumu na ulamaa wa kidini na uingiliaji katika siasa ni dhambi isiyosameheka. Vilevile wameishusha ile swala ya jamaa ya siku ya Ijumaa hadi kuwa ni utendaji usio na maana na wakachukulia kwamba kuvuka mipaka hii ni kuukiuka Uislamu. Inafaa kusemwa kwamba Uislamu ni mkiwa na usiotambuliwa na mataifa ya Kiislamu yanatenganishwa na kufanywa kutofahamu mambo ya ukweli wa Uislamu. O  O  O Sharti la kupata matumaini ya kimaumbile na maadili ya kibinadamu ni kuhakikisha uunganishaji wa Waislamu wote, katika hatua hizi, na neno la maafikiano ya pamoja ya Waislamu wa makundi yote katika ibada na hatua zote za Hijja, bila kujali lugha zao za kikabila, nchi zao, rangi zao au hisia za chuki za kipagani za makabila, na kupiga makelele ya pamoja dhidi ya adui yao wote ambaye ndiye adui wa Uislamu na kuhakikisha yamemchapa 86

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 86

11/3/2015 2:57:51 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

usoni mwake katika kipindi hiki cha wakati. Anauchukulia kama ni kikwazo dhahiri kwenye uporaji wake na anajaribu kuuondoa kwa njia ya uchochezi kupitia mawakala wake wa kulipwa ambao juu yao ni wale wanachuoni bandia wa kidunia wenye wivu na watumishi wa mabaraza ya kifalme (ma-akhundi) ambao wameajiriwa kutekeleza dhamira zake za kisirani mahali popote na wakati wowote hususan wakati wa msimu wa Hijja na ibada zake tukufu. Katika hatua zote na vitendo vyote vya ibada hii ambayo imekusudiwa hasa kwa ajili ya mkusanyiko wa Waislamu kutoka kote ulimwenguni kwa manufaa ya faida ya watu walionyimwa wa ulimwenguni – na ni manufaa gani yanaweza kuwa juu zaidi ya uondoshaji wa mikono ya waporaji kutoka kwenye nchi za Kiislamu…..Mahujaji lazima wawe na tahadhari ya kutosha juu ya vitendo pinzani dhidi ya Uislamu na Qur’ani vya mawakala hawa wafitini na vibaraka wachochezi, na kuwafukuza wale ambao hawaujali Uislamu na maslahi ya Waislamu – haidhuru washauriwe kiasi gani – kwa sababu wao ni mashetani na waovu zaidi kuliko wapagani. O  O  O Mahujaji wa nchi mbalimbali ambao kwa hakika wamesafiri chini ya udhibiti mkali na vitisho vya serikali zao watawakosa marafiki zao wa kweli, ndugu, waungaji mkono na wapiganaji wenzao. Ukoo wa Kifalme wa watawala wa Saudia, ili kufunika jinai yao kubwa ya mwaka uliopita na pia ili kuhalalisha kosa lao la “Kipingamizi kwenye njia ya Mwenyezi Mungu” na uzuiaji wa mahujaji wa Iran kutofanya Hijja, watawafululizia mahujaji propaganda yao endelevu, na wanachuoni wa vitala na mamufti wa kulipwa – laana iwe juu yao – katika nchi za Kiislamu, hususan 87

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 87

11/3/2015 2:57:51 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

Hijaz, watafanya ulaghai na kutoa hotuba za uongo kupitia vyombo vya habari, ili kuwabana mahujaji katika nafasi mbaya, wakikosa uwezo wa kufikiri na kuchunguza kuhusu falsafa halisi ya Hijja na/au kugundua kuhusu mpamgo uliokwisha kupangwa wa mauaji ya halaiki ya wageni wa Mwenyezi Mungu uliopangwa na shetani mkuu, suala ambamo kazi hasa ya mahujaji hao, bila shaka ni kuingia makaburini (baada ya kuuliwa). O  O  O Kwa masikitiko sana, kuzembea huku ni kwa kawaida miongoni mwa serikali za nchi za Kiislamu kwa kiasi kwamba mikono ya fitna ya mataifa makubwa yenye nguvu imewazuia watu wao kujiingiza kwenye masuala ya kisiasa kiasi cha kwamba uingiliaji wa Waislamu katika siasa au hata kutamka miito dhidi ya maadui wa Uislamu na Qur’ani wenye kiu cha damu, wao watashutumiwa na wahubiri wa mabaraza ya vitala kama wahalifu, na wanafungwa na kuteswa. O  O  O Mwenyezi Mungu swt. na Mtume Wake Mtukufu wametangaza katika Siku ya Hijja, kwamba wao wanachukizwa na wapagani na wamejitenga nao, tangazo kutoka kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake kwa wanadamu katika Siku ya Hijja Kubwa: “Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wamejitoa na waabudu masanamu.” Marekani na marafiki zake, na wanachuoni wa kulipwa wa vitala, ambao wanalinda maslahi ya shetani mkuu, hawakuwepo hapo wakati huo, kuhukumu kwamba, Mwenyezi Mungu aepushilie mbali, Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wanakwenda kinyume na ibada sahihi za Hijja na kwamba Hijja ilipaswa kuwa mbali na 88

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 88

11/3/2015 2:57:51 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

mambo hayo. Siku ambapo yule Walii kipenzi cha Mwenyezi Mungu, yule Imam Mtukufu wa zama hizi (Mola aharakishe kudhihiri kwake kutukufu) atakapodhihiri na akalingania haki na makelele dhidi ya madhalimu na wapagani, wanachuoni haohao wa vitala watakuwa wajitenge naye na kuwaunga mkono hao madhalimu madikteta. O  O  O Waislamu lazima wayajaze mazingira yote na mapenzi kwa Mwenyezi Mungu na chuki na unyarafu au kukarahika kwa dhahiri juu ya maadui wa Mwenyezi Mungu na kamwe wasisikilize vishawishi vya hao mashetani na wasiwasi wa wenye kushuku na wa walioondolewa uwezo wa kufikiri na wa waliopotoshwa na kamwe wasiitelekeze dini hii tukufu ya kiulimwengu ya imani ya Mungu Mmoja ya Kiislamu, kwani wateka nyara wa duniani na maadui wa mataifa hawatashikilia amani yao kuanzia hapo na watakimbilia kwenye hila na vitimbi vya aina zote na ulaghai kwa sura mbalimbali na wanachuoni wa bandia na wahubiri wa vitala na wale wa kulipwa, wazalendo na wanafiki wote watakimbilia kwenye falsafa zisizo sahihi na mawazo ya uchochezi na watajishughulisha na kufikiria kuwanyang’anya silaha Waislamu na kuuvunja mshikamano, utukufu na nguvu ya ummah wa Waislamu – na wakati mwingine inawezekana baadhi ya wakana mungu wajinga wakasema kwamba utakatifu wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu, hii Ka’aba tukufu utakuja kuvunjwa kwa kaulimbiu, maandamano, matembezi na kutangaza chuki kwa wapagani, na kwamba Hijja ni mahali pa ibada pekee na sio uwanja wa mapambano. Au wakati mwingine, wanachuoni madhalili wanaweza wakashauri kwamba vita na kupambana na chuki ni kazi ya watafuta dunia, na kuingilia kwenye siasa hususan wakati wa Hijja 89

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 89

11/3/2015 2:57:51 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

ni chini ya nafasi ya wanachuoni na ulamaa. Mapendekezo haya ni sehemu ya njama na uchochezi wa wateka nyara wa dunia ambao kwawo Waislamu lazima wakabiliane kwa bidii kabisa kwa uwezo wao wote na njia zote, na walinde maadili matukufu na maslahi ya Waislamu, na waunganishe na kuimarisha safu zao kwa ajili ya kupigana na ulinzi mtukufu, na msiwape wale wajinga na wenye nyoyo dhaifu fursa ya kushambulia mipaka ya Waislamu ya imani na heshima. O  O  O Kati ya Mahujaji wa kwenye Nyumba ya Mwenyezi Mungu, kwa masikitiko makubwa kabisa, baadhi ya wanachuoni wa vitala wajinga kabisa au wenye fitna kubwa wanapatikana miongoni mwao, ambao katika muda huu wa baina ya matukio ya ibada, wao wameandika makala na kuchapisha makaratasi ambamo wamewafedhehesha Maimam wa Shi’ah na Sunni, katika wakati ambapo wasomi na watu wenye elimu wa madhehebu mbalimbali wanakutana kufikiria juu ya mipango ya manufaa ya Uislamu. Katika wakati kama huo, wao wanachapisha makaratasi kama hayo kana kwamba wanahisi hatari kwa Marekani na wanapiga makelele kwa ajili ya kutaka msaada. Mwanachuoni huyo mpumbavu ambaye anadhalilisha mambo matukufu ya Shi’ah katika muda huu, huyo anakusudia kuwachochea watu wasimame na kusema jambo katika makabiliano na kusababisha mfarakano, katika wakati ambapo juhudi zinafanywa kwa ajili ya kuimarisha umoja wa Waislamu. Uislamu unaweza kufanya nini na mawazo kama hayo na vitendo kama hivyo? Uislamu ufanye nini na mashekhe kama hao ambao wanaoendeleza muonekano wa kiungwana wa wanachuoni na wametawanyika na kuenea miongoni mwa watu? Ni jambo kubwa 90

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 90

11/3/2015 2:57:51 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

kabisa la kikorofi kwamba katika hali kama hii, mtu anasema, tangu nilipoona kwamba vijana wamevutiwa na mkusanyiko huu na juu ya Iran, nilijihisi binafsi kuwa na wajibu wa kutangaza kwamba wao ni washirikina, wao ni Majusi na wao ni hivi na vile na kadhalika, na wanakufurisha haya maeneo matakatifu. Huyo anawahudumia wakoloni tu, anayahudumia mataifa makubwa yenye mabavu na anakwamisha maendeleo ya Waislamu. Lazima sisi tufikirie juu ya matatizo kama hayo na watu kama hao wanaojaribu kuvunja umoja wa Waislamu. O  O  O Miongoni mwa mambo yanayofaa kunasihiana, ingawa limetajwa hapo kabla, ni kwamba, wakati tunapopiga makelele juu ya kuwachukia wapagani na madhalimu katika wakati wa matembezi na maandamano, ili kufanya vilio vya Waislamu wanaoonewa na mataifa yanayokandamizwa yawafikie wakaazi wa dunia na kuwaamsha wale waliolala na kuwachangamsha wale walio kimya ili kuamka dhidi ya madhalimu na madikteta, na wakati tukijaribu kuwanyamazisha wahubiri bandia, ambao kinyume na maamrisho ya Mwenyezi Mungu na Qur’ani na hadithi za Mtukufu Mtume 8 wanawaunga mkono madhalimu wenye kiu ya damu, hususan wale mashekhe wa kulipwa wa mabaraza ya watawala ambao wanashusha kalamu zao juu ya makaratasi au kutoa hotuba wakijaribu kuzima nuru ya Mwenyezi Mungu na mwenge uliowashwa kwa ajili ya ukombozi wa wale wanaokandamizwa na madhalimu, mahujaji lazima wawe waangalifu kuangalia tabia makini na mwenendo wa Kiislamu na kuepuka miito na mabango ya utungo binafsi wa kizushi ambayo yanaweza yakaanzia kutoka kwenye mapendekezo ya kichochezi ya wahujumu ili kuvunja hadhi na hesima ya Mahujaji hususan wale wa kutoka Iran. 91

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 91

11/3/2015 2:57:51 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

O  O  O Kupanda mbegu za migogoro baina ya madhehebu ya Waislamu ni kosa kubwa mno linalotendwa na wenye maguvu ambao wananufaika kutokana na kutoelewana miongoni mwa Waislamu, na watendaji wao wasiomjua Mungu, ikiwa ni pamoja na mashekhe wahubiri wa vitala ambao wana aibu kubwa zaidi kuliko hao wafalme wenyewe, na wanachochea miali ya moto wake kila siku, na kuunda njama mpya kila wakati wakitegemea kubomoa msingi wa umoja miongoni mwa Waislamu. O  O  O Mashekhe wachamungu lazima wawaonye Waislamu juu ya hatari kubwa inayotishia jumuiya za Kiislamu, itokanayo kwa mashekhe wenye fitna na wanachuoni watumishi wa vitala, kwa vile ndio wanajaribu kuhalalisha ukatili wa madikteta hao na kuwazuia wale wanaoonewa katika kudai haki zao stahiki, na wakati wowote wanapoweza, huwa wanawatenga wale wapambanaji wanaopigania uhuru. Tunamuomba Mwenyezi Mungu ayaokoe mataifa ya Kiislamu kutokana na fitna na mitihani ya watu waovu na wasiomcha Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu Mtukufu awasaidieni kupata ushindi katika makabiliano na propaganda za kichochezi za vyombo vya habari na mbaya zaidi kuliko hizo, zile za mashekhe watumishi wa vitala vya watawala ambao wanaishambulia Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kalamu na maneno yao. O  O  O 92

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 92

11/3/2015 2:57:51 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

15 KUCHUKIZWA JUU YA WAPAGANI

K

utangaza kuchukizwa na wapagani, ikiwa ni nguzo ya Tawhidi na haja muhimu ya kisiasa ya Hijja, lazima kutekelezwa kwa utukufu na heshima kubwa kiasi iwezekanavyo. Mahujaji kutoka Iran na wasiotoka Irani bali kwenye nchi za Kiislamu wanapaswa kuambatana na wakuu wa Hijja (kwa wakati ule, pamoja na muwakilishi wake H.E. Hujjatul-Islam Karrubi) katika kushiriki kwenye kanuni zote za kidini na wafanye sauti yao kubwa yenye kuponda ya unyarafu na kuchukizwa viburi wa dunia, wapagani na makafiri pamoja na Marekani ikiwa mbele kuwaongoza, sauti hiyo ikivuma kutoka upande wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu, na msipuuze kuonyesha chuki na mfundo dhidi ya maadui wa Mwenyezi Mungu na viumbe Wake. Hivi uchamungu unaweza kupatikana bila ya kuonyesha mapenzi na uaminifu kwenye haki na ghadhabu na mfundo dhidi ya batili? Hasha, sio hivyo! kwamba usafi wa mwanaTawhidi upatikane isipokuwa kwa chuki kamili dhidi ya wapagani na wanafiki na ni nyumba gani inayofaa zaidi kuliko al-Ka’aba, sehemu takatifu ya usalama na utakaso, ambapo mtu anaweza akaupinga uvamizi, ukatili, unyonyaji, utumwa, akili-finyu na unyama, kwa vitendo na maneno, na kutoa upya kiapo cha utii na kuvunja masanamu ya miungu wa kike na mabwana wengi tofauti na kuhuisha ukumbukaji wa ukale wa harakati kubwa ya kisiasa ya Mtukufu Mtume 8 kwa sababu hadithi za Mtume za kutangaza chuki kwa wapagani 93

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 93

11/3/2015 2:57:51 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

hazitakuwa zilizopitwa na wakati, na sio tu chuki kwa wapagani kwamba haikuwekewa mipaka kwenye kanuni za ibada ya Hijja, bali pia Waislamu lazima wajaze eneo lote kwa mapenzi na heshima kwa Mwenyezi Mungu na chuki na unyarafu kwa maadui wa Mwenyezi Mungu na wasisikilize vishawishi vya mashetani na wasiwasi wa wenye kushuku na walioondolewa uwezo wa kufikiri na waliopotoka, na kamwe wasipuuzie ule wito wa kidunia wa tawhid tukufu ya Uislamu. Na waunganishe ukakamavu wao mtukufu, kutoka kwenye nchi yoyote iwayo, na hususan kutoka kwenye Ka’aba ya Mwenyezi Mungu, watukufu mahujaji wanapaswa kuelekea kwenye kaaba ya juu zaidi kutoka kwenye ardhi hii tukufu ya upendo na hekima na “Jihadi,” na kama yule Bwana wa mashahidi, mtukufu Abi Abdillah al-Husein A, waondoke kutoka kwenye vazi la Hijja na kuingia kwenye vazi la vita, na kutoka kwenye kuizunguka Ka’aba na kwenda kumzunguka Mmiliki wa Nyumba hiyo, na kutoka kwenye udhuu wa Zamzam kwenda kwenye udhuu wa shahada na kubadilika kuwa watu wasioshindwa na ngome imara, kwa kiasi kwamba, sio mataifa makubwa ya Mashariki wala Magharibi yanayoweza kukabiliana nao, kwani bila shaka msukumo na ujumbe wa Hijja sio chochote kile isipokuwa kwamba Waislamu wachukue masomo yao kwa ajili ya vyote, vita vya ndani na vilevile vita dhidi ya ukafiri na uabudu masanamu. O  O  O Kutangaza kuchukizwa na wapagani wakati wa Hija ni wito wa kisiasa-kiibada ambao umeamriwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu 8. Sasa lazima tumuulize yule mwanachuoni wa kulipwa ambaye anaona ile miito ya “Hatuitaki Marekani, Israili na Urusi” 94

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 94

11/3/2015 2:57:51 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

kuwa ni kinyume na Uislamu: Je, kumfuata Mtukufu Mtume 8 na kutii amri za Mwenyezi Mungu ni kinyume na utekelezaji wa Hija? Ninyi wanachuo watumishi wa Marekani na wenzenu kama ninyi, je mnashutumu kitendo cha Mtukufu Mtume na amri ya Mwenyezi Mungu? Na kuona kwamba kumfuata Mtukufu wa daraja na kutii amri ya Mwenyezi Mungu kama ni dhambi au kosa? Na kisha mnadai kwamba mnazitakasa kanuni za Hija za kuchukizwa na wapagani? Na kuzifanya amri za Mwenyezi Mungu kuangukia kwenye kusahaulika kwa sababu ya maslahi yenu ya kidunia tu? Na kujitenga na hali ya kuwachukia mate na kuwalaani maadui wa Uislam na wasimamisha vita dhidi ya Waislamu? Tunataraji kwamba serikali ya Saudi Arabia haitavitegea masikio vishawishi hivi vya wanachuoni (maakhundi) hawa wa kipagani na itakubaliana na Waislamu na kuwaacha – hasa Wairani, Wapalestina, Walebanoni na Waafghani wakimbizi ambao wamefanyiwa uhalifu na wapagani – wawe huru kutangaza kuchukizwa kwao na wapagani hao na kumtambulisha adui wa jumla wa watu walioonewa duniani kote. Kutangaza kuchukizwa na wapagani hakuishii kwenye tukio moja tu. Ni agizo la kudumu, ambapo wapagani wa Hijazi ya kale wamekwisha kuangamizwa. Na kuamka kwa watu hakukuwekewa mipaka ya mahali pamoja tu. Ni andiko kwa ajili ya wakati wote na kwa sehemu zote, na katika mkusanyiko huu mkuu wa mwaka kama ibada muhimu daima hadi Siku ya Kiyama. Na ni kwa sababu hiyohiyo lile agizo la Ma’sumiin G la kutekeleza daima maombolezo juu ya Bwana wa wanaokandamizwa na kulia kwa ajili ya hali ya kudhulumiwa ya nyumba ya Mtukufu Mtume 8 na hali ya udhalimu wa Bani Umayyah, ingawa hao Bani Umayyah walikwisha kuangamizwa. 95

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 95

11/3/2015 2:57:51 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

Ni makelele ya wanaodhulumiwa dhidi ya madhalimu. Makelele na vilio hivi lazima dhidi ya Ma-Yazidi. Ni muhimu kwa mahujaji wa kwenye Nyumba ya Mwenyezi Mungu kutoa sauti zao za kukirihishwa na wapagani katika mkusanyiko huu mkubwa na umati wenye sauti kubwa, kwa sauti kubwa zaidi kiasi iwezekanavyo na kushikana mikono yao ya kindugu kiasi kinachowezekana na wasitoe muhanga manufaa haya makubwa ya Uislamu na Waislamu kwenye umakundi na utaifa na wayavute mazingatio na nadhari za ndugu wa Kiislamu kwenye umoja wa maneno na kutelekeza chuki za kipagani ambazo zinatumikia maslahi ya wateka nyara wa dunia na washirika wao. Hivyo, wanaweza wakapata na kupokea msaada wa Mwenyezi Mungu, na ahadi Yake, kwa matumaini makubwa kabisa, itawajumuisha na wao pia. Lakini kama, Mwenyezi Mungu aepushilie mbali, watawafuata watendaji wa wateka nyara wa dunia, ambao juu yao wamo hao wanachuoni wa kununuliwa, watakuwa wametenda dhambi kubwa sana na watastahili ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, na watabakia wamefungwa minyororo na vifungo vya mataifa makubwa, na ni lazima tuombe hifadhi ya Mwenyezi Mungu kutokana na hilo. O  O  O Shukurani kwa Mwenyezi Mungu, leo hii Wairani na Waislamu kutoka mataifa mengine ya Kiislamu wameiona njia yao, na mkusanyiko mkubwa wa mahujaji kutoka nchi za Kiislamu wamekusanyika kuuzunguka Msikiti Mtukufu, kitovu cha mvuto kwa Waislamu, mahali pa mashukio ya Malaika wa Mwenyezi Mungu na mahali pa mashukio ya wahyi ili kutekeleza wajibu wao wa Kiislamu na wa ki-Qur’ani ambao ni kutoa sauti kubwa ya kuonyesha kukarahishwa kwao na wapagani, ambao ulitekelezwa na Mtume wa Mwisho 8 wakati wa Hija Kubwa, kupitia 96

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 96

11/3/2015 2:57:51 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

kwa Bwana wetu, Imam Ali ibn Abi Talib A. Na kama, Mungu akipenda, wengi wa mahujaji kutoka kundi lolote lile na madhehebu yoyote, ambao wamekutana mahali hapa patakatifu, wakiitikia wito wa Mwenyezi Mungu, na wote kwa umoja wakalaani ukatili na maonevu ya madhalimu, basi makasiri ya madikteta yataporomoka. Kama wawakilishi wa Waislamu bilioni moja wa dunia watatoa sauti dhidi ya waingiliaji haki za wenye kuonewa na pia nchi za Kiislamu, kwa majina na sifa zao na kudai kuondoa kwao uhalifu wao, hakuna nguvu itakayoweza kupinga hilo. Kama mataifa na serikali za Kiislamu, zikiwa nyingi sana kwa idadi, na zikiwa na hazina kubwa ambazo ni za umuhimu mkubwa kwa hayo mataifa makubwa, zikiwakabili kwa nguvu zote na bila kuhofia porojo na makelele ya wakazi wa makasiri, na zisisalimu amri kwenye propaganda bandia za uongo za vyombo vya habari vya kukodiwa vyenye uhalifu wa hali ya juu, na zikitegemea nguvu isiyo na mwisho ya Mwenyezi Mungu Mwenye kudura na wakiwa wenye kushukuru neema Zake, wakapiga makelele dhidi ya mataifa maovu ya dunia, na nchi hizo zikayatishia mataifa hayo kwa kufunga mipaka yao na kuwakatia upatikanaji wa mafuta na vitu vinginevyo, bila shaka mataifa hayo yatasalimu amri kwenye nguvu na uwezo tulionao bali sisi wenyewe hatulitambui hilo. O  O  O Jambo la kuzingatiwa sana hapa ambalo linapaswa kusisitizwa ni kwamba mahujaji waeleze kukarahishwa kwao na wapagani kwa nguvu na bidii sana kupitia matembezi na maandamano, kwa namna ambayo kwamba vilio vya Waislamu na mataifa yanayokandamizwa vinayafikia masikio ya wakazi wa dunia na kuwaamsha waliolala na kuwatikisa wakimya kusimama dhidi ya madhalimu na kujaribu 97

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 97

11/3/2015 2:57:51 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

kuwazima wahubiri waongo ambao, kinyume na amri za Mwenyezi Mungu na Qur’ani, na hadithi za Mtukufu Mtume 8, wao wanawaunga mkono madhalimu wa kimataifa wenye kiu cha damu, hususan wale wanachuoni wa kukodiwa wa mabaraza ya watawala, ambao wanaandika makala na kutoa hutuba zenye kulenga kuzima nuru ya Mwenyezi Mungu na taa iliyowashwa kwa ajili ya wokovu wa wale wanaodhalilishwa na madikteta wa dunia. Chukueni tahadhari ya kuheshimu tabia ya adabu na mwenendo wa Kiislamu na jiepusheni na kutangaza miito ya kuzusha binafsi ambayo inaweza kuanzia kutoka kwenye mapendekezo ya kichochezi ya baadhi ya wahujumu ili kuvunja heshima ya mahujaji hususan wale kutoka Iran. O  O  O Ni lazima tutekeleze wajibu wetu wa Hija kwa namna ileile kama tulivyofanya hapo kabla. Mahujaji lazima watembee na kuandamana kama walivyofanya Wairani miaka mitatu iliyopita. Ibada za Hija ni za kutekelezwa kama vilevile zilivyo, na serikali zetu zinapaswa kulivumilia hilo. Hatuwezi kukengeuka kutoka kwenye wajibu ambao Qur’ani imeagiza kwetu sisi. Sera zetu juu ya Hija ni ileile kama ilivyokuwa kabla. Kila wakati tunapokwenda Hija tutafanya vivyo hivyo, isipokuwa labda wakituzuia kuhudhuria ambalo hilo ni suala tofauti. Ninataraji kwamba mahujaji kwa mwaka huu ni wengi zaidi na watatekeleza wajibu wao vizuri zaidi. O  O  O Mwaka huu, Mwenyezi Mungu akipenda, mahujaji takriban mia moja na hamsini elfu kutoka Iran watakwenda kuhiji Makka na watafanya wajibu wao wa kutamka kwa sauti kubwa kuhusu kukerwa 98

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 98

11/3/2015 2:57:51 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

na wapagani, Marekani na Israili. Haiwezekani kwamba mahujaji wetu waende Hija na wasishiriki katika maandamano dhidi ya mafidhuli wa ulimwengu. Kimsingi, kuchukizwa na wapagani ni moja ya kanuni za kisiasa za Hija na bila hiyo, Hija zetu hazitahesabiwa kama ni Hija kamilifu. Ukoo wa Kifalme wa watawala wa Saudia lazima uelewe kwamba, kama watafanya vinginevyo, basi watakabiliwa na Waislamu wote wa ulimwenguni, na kama wakitenda sawa, hiyo itakuwa hasa ni kwa manufaa yao wenyewe. O  O  O Tunasisitiza kwa nguvu zote kwamba Waislamu ni lazima pale wanapokuwa kwenye Nyumba ya Mwenyezi Mungu na eneo takatifu, wajione wako huru, waliokombolewa kutokana na kila aina ya utumwa na vifungo vya madhalimu, na waweze kutamka kukirihishwa kwao na wapagani kupitia matembezi makubwa na kutumia kila uwezekano uliopo kwa ajili ya ukombozi wao. Kwa kutangaza karaha kwa wapagani tunanuia kuweka huru zile nguvu za ulimwengu wa Kiislamu zilizobanwa na kugandamizwa, ambako kutafanyika siku moja, kwa msaada wa Mwenyezi Mungu na mikono ya watoto wa Qur’ani, na insha’Allah siku moja Waislamu wote na wale wote wenye kuteseka ulimwenguni watapiga makelele dhidi ya madhalimu na kuthibitisha kwamba hayo mataifa makubwa pamoja na watumishi wao wa kukodi ndio viumbe wa dunia hii wanaochukiza mno. O  O  O Kutangaza kuchukizwa kwetu ni makelele ya Waislamu wa Afrika, makelele ya ndugu zetu wa kidini mabibi na mabwana, 99

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 99

11/3/2015 2:57:51 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

ambao wanateswa na kuumizwa kikatili sana na wabaguzi wasio na aibu wala akili, kwa sababu tu kwamba ndugu zetu hao walikuwa ni weusi. Kutangaza kuchukizwa kwetu ni makelele ya ndugu zetu wa Lebanoni, Wapalestina na mataifa yote ambayo hazina zao, yale mataifa makubwa, hususan Marekani na Israili yanazitazama kwa jicho la tamaa, wameteka nyara rasilimali zao na wakawekea watumishi wao kwa lazima juu yao, wakazikamata nchi zao na wakazikalia ardhi zao na mipaka ya baharini kwa mabavu. Kutangaza kuchukizwa kwetu ni makelele ya binadamu wote ambao hawawezi tena kuvumilia ujeuri wa Marekani na uwepo wao wa kikandamizi, na ambao hawapendi kilio chao cha ghadhabu na chuki kibakie kimekandamizwa na kuzimwa, na wamedhamiria kuishi maisha huru na kufa wakiwa huru na kuwa wapiga makelele ya ghadhabu kwa ajili ya vizazi. Makelele yetu ya kuchukizwa ni makelele ya kulinda maadili, heshima na usafi wetu, na ni makelele kwa ajili ya kulinda mali, utajiri na rasilimali zetu. Ni makelele ya uchungu ya mataifa ambayo yamechomwa mkuki na wanafiki kwenye moyo. Makelele yetu ya kuchukizwa ni makelele ya umasikini na ufukara wa wenye njaa, walionyimwa, na watembea pekupeku bila viatu, ambao matunda ya kazi zao na matokeo ya kazi ngumu za sulba yameporwa na wateka nyara na wenye kuhodhi hazina, ambao wamenyonya kilafi damu ya wakulima masikini na wafanyakazi, ama kwa jina la ubepari au kwa jina la usoshalisti na ukomunisti, wale ambao wameunganisha njia ya uchumi wa kilimwengu kwao wao wenyewe na kuyazuia mataifa kutokana na kupokea haki zao stahiki.

100

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 100

11/3/2015 2:57:52 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

O  O  O Sasa, kuhusu wapendwa mahujaji wa Iran, kwa kweli wameonyesha heshima yao na akili, na ukuaji wao kisiasa na kijamii, katika Hija ya miaka ya hivi karibuni na kwa hiyo kuipatia heshima Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Mwaka huu pia, kwa nyongeza ya kuzingatia na kujali ibada muhimu za Hija na utekelezaji wake na kunufaika na rehema kubwa ya kuhiji Makka tukufu na Madina yenye nuru na maeneo ya kaburi la Mtukufu Mtume 8. Mtakatifu Bibi Fatimah Zahra I na Maimam Ma’sumiin nao watashiriki katika matembezi haya mazito kwa ajili ya kuchukizwa na wapagani, kwa ushirikiano kamili na uimara thabiti, na kutoa miito na kuhudhuria programu zilizopangwa, na kutumia vizuri mkusanyiko huu mtukufu wa kiibada-kisiasa ambao unaonyesha nguvu na hadhi ya Waislamu na wale watokao Iran pia. Na kwa kukutana na watu wa nchi nyingine mbalimbali, au hata na wafanyakazi wa Saudia kwa uchangamfu mzuri na tabia za kibinadamu, wakati wa matembezi haya, ni lazima watawaelimisha juu ya umuhimu wa kuhudhuria mikusanyiko kama hii. Mahujaji lazima waepuke kushikilia maoni yao tu na maslahi binafsi ambayo yanaweza yakaleta uvunjaji wa heshima katika mkusanyiko huu mkuu, au mgogoro wowote na ufidhuli. Ingawa waheshimiwa mahujaji kwa tahadhari kabisa watabatilisha hila na njama, hata hivyo, wakati mwingi wanaweza wakawepo watu, ambao kwa kujaribu kuvuruga fahari na utukufu wa mikusanyiko ya Hija na kuharibu sura ya mapinduzi na kufanya vitendo vya vurugu. Bila shaka haiyumkini kwa serikali ya Saudia au wafanyakazi wake kwamba wakati wakiwakaribisha mahujaji kwenye Nyumba ya Mwenyezi Mungu na maeneo ya kaburi la Mtukufu Mtume 7 watayazuia maandamano ya nguvu ya Uislamu na Waislamu dhidi 101

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 101

11/3/2015 2:57:52 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

ya upagani na ari ya siasa kivitendo ya taifa letu kwa ajili ya fahari ya Waislamu. O  O  O Inatarajiwa kwamba serikali ya Saudia itashirikiana vizuri na mahujaji kutoka Iran ambao hawafanyi lolote isipokuwa kutoa malalamiko juu ya madhalimu waovu ambao wanaingilia pasi na haki kwenye nchi za Kiislamu, na kwa umoja pamoja nao, wanawalaani wapagani wanaoingilia utukufu wa Uislamu. ili kwamba maadhimisho ya Hija yatekelezwe katika mwaka huu kwa njia ambayo inakubalika kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake

7. Polisi wa Saudia, maafisa wa serikali ya Saudia na serikali ya Saudia yenyewe lazima watambue kwamba mahujaji kutoka Iran, ambao wanatoka kwenye nchi ya kimapinduzi, ambayo hapo mwanzo ilikandamizwa na kuporwa na mataifa ya Mashariki na Magharibi na wamesimama, kwa rehema ya Mwenyezi Mungu, wakajikomboa wenyewe kutoka kwenye makucha ya mataifa makubwa, wakapata uhuru na ukombozi wao na wakaubadilisha udikteta wa ufalme wenye sura ya Kimarekani kwa kuweka mfumo wa watu wa Kiislamu, na wakawafukuza au kuwafunga washauri wa Kimarekani na Kirusi, sasa ni wageni wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na kwamba jeuri yoyote kwao hao itakuwa ni jeuri kwa wenyeji wao wakubwa, hususani kwamba wageni hawa wamekuja kusema: “Labayka” kwa Ibrahim na Muhammad (amani juu yao wote) ambayo kwa kweli ni Labayka kwa Mwenyezi Mungu swt. Watendeeni wale ambao wamezihama nchi za mbali kabisa na kuelekea kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake kwa mapenzi na 102

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 102

11/3/2015 2:57:52 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

upendo na hali ya udugu wa Kiislamu, hivyo msiwadhuru wageni wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Wao wamekuja kutekeleza ibada za Hija na kutamka kukerwa kwao na washirikina na wapagani ambao hata Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wanawachukia. Onyesheni heshima kwa wageni hawa wachamungu. Chukueni fursa ya mfumo wa Kiislam wenye nguvu katika kuizimisha Israili, adui mkuu wa Uislamu na Waislamu, na kuiondoa Marekani kiongozi mkuu wa maadui wa nchi za Kiislamu na kuibadilisha Makka tukufu kuwa kitovu cha sauti kuu dhidi ya madhalimu kupitia ushirikiano na mahujaji kutoka duniani kote, kwani hii ni mojawapo ya siri za Hija, na Mwenyezi Mungu si mhitaji wa chochote kutoka kwa wenye kuitikia “Labayka” na ibada za wanadamu. O  O  O Baadhi ya watu walikuwa hawajatambua misingi kwa ajili ya usisitizaji juu ya uandaaji wa matembezi ya kukarahishwa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mpaka lile tukio chungu, na kwa namna nyingine tamu na zuri la mwaka wa jana. Walijiuliza wao wenyewe na wengineo kuhusu umuhimu wa kuandamana na kupaza sauti wakati wa msimu wa Hija katika hali ya joto kama ile, na kwamba kutaleta madhara gani kwa wajeuri wa dunia? Na wakati mwingi, watu wenye akili za kawaida wanaweza wakawa wamedhania kwamba hao wanaoitwa wateka nyara wa dunia iliyoendelea sio tu wanaweza kuvumilia maandamano ya kisiasa kama hayo bali pia kuwaruhusu wapinzani wao kuendelea hata zaidi ya hapo, na kutoa sababu za maandamano ya umma yaliyoandaliwa na zile zinazoitwa nchi huru za Magharibi kama ushahidi. Lakini ni lazima ieleweke wazi kwamba aina hizo za maandamano huwa haziyadhuru hayo mataifa makubwa. 103

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 103

11/3/2015 2:57:52 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

Ni maandamano ya Makka na Madina ambayo yanaweza kufuatiwa na uzuiaji na ukatishaji wa kutoa mafuta wa Saudi Arabia. Ni yale matembezi ya kukerwa ya Makka na Madina ambayo yanaweza kuishia katika kuwabomoa wafuasi watiifu wa Urusi na Marekani, na hivyo ndio hasa kwa nini inakatazwa kwa kuwauwa kwa halaiki watu waungwana wenye akili huru, wanawake kwa wanaume, na ni kwa baraka za haya maandamano ya kukerwa ambapo kwamba wale wenye nyoyo za ukweli watatambua kwamba hawapaswi kusalimu amri kwa Urusi na Marekani.

104

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 104

11/3/2015 2:57:52 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

O  O  O

SEHEMU YA NNE MAELEKEZO NA MAPENDEKEZO YA IMAM KHOMEINI KUHUSIANA NA MAADHIMISHO YA HIJA

16 WAJIBU WA UJUMBE WA MAFAQIHI KWENYE MAMBO YA HIJA

M

heshimiwa Hujjatul-Islam Hajji Sheikh Muhyiddin Anwar na Mheshimiwa Hujjatul-Islam Sheikh Fadhlullah Mahallat – Mwenyezi Mungu arefushe uenezaji wao: Kwa vile msimu wa kutekeleza moja ya maagizo makubwa ya Kiislam na utukufu wa maudhui zake za kibinadamu, kiroho, kisiasa na kijamii, yaani kwenda kuhiji Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu umekaribia, ni muhimu kwamba wajibu huu mtukufu usafishwe kutokana na dalili za masazo ya kipagani na kuurudisha kwenye asili yake halisi ya Kiislamu. Kwa hiyo ninakuteuweni kuwasimamia mahujaji wa kwenye Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu. Hivyo mnapaswa kuchagua chombo cha wachamungu na kusimamia mambo yote yanayoruhusiwa kwenye Hija, ili kwamba, 105

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 105

11/3/2015 2:57:52 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

Mungu akipenda, ibada hii tukufu iwe inatekelezwa kwa maudhui ya kiroho, wakati Mfumo wa Jamhuri ya Kiislam ukiwa uko madarakani. Mheshimiwa Hujjatul-Islam Hajji Sheikh Mohammad Reza Tavassuli Mahallati – Mwenyezi Mungu arefushe uenezaji wake: Unateuliwa kuwa msimamizi wa mahujaji kwenye Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu kuhakikisha kunakuwa na utendaji bora wa ibada hii tukufu na kuendesha mambo yote yanayofaa kwenye wajibu huu wa ki-mungu na kuifanya misafara na shughuli zao kuwa ya Kiislamu, na kwa kushirikiana na Mheshimiwa Hajji Sayyed Ali Hashemi Gulpaygani na wengine wenye mamlaka, kuchagua timu ya watu wachamungu na watiifu na kuongoza mambo yote yanayopasa kwenye Hija. Pia iwapo jambo lolote litahitaji ushirikiano wa taasisi kama “Hilal Ahmar” (Hilali Nyekundu) na kadhalika, uteuzi wa maafisa wake lazima uwe unakuridhisha wewe na unapaswa kuteua wafuasi waaminifu kwa ushirikiano kama huo. O  O  O Kwa masikitiko kabisa wengi wa Waislamu wamekitelekeza kipengele au sura ya kisiasa ya ibada hii tukufu – Hija – kwenye kusahaulika, kwa sababu tu ya kupotoka kwao au kutoelewa baadhi ya vipengele, au kwa njama zilizofanywa na baadhi ya wanaojitafutia mamlaka binafsi. Nakuteua kama mwakilishi wangu katika kuwasimamia wapendwa mahujaji wa Iran, ili kwamba, kwa kuzingatia umaizi wako mkubwa wa kisiasa, uyatawale mambo yote ya mahujaji katika shughuli zote na uwalinganie Waislamu kwenye umoja na mshikamano katika hotuba zako na katika taratibu za kidini, kwa ajili ya uhuishaji wa mila hii yenye utukufu mkubwa. Wajulishe juu ya kile kinachotokea huko Lebanoni, juu ya Iran 106

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 106

11/3/2015 2:57:52 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

inayopambana na Afghastani inayokandamizwa na madhalimu na waporaji wa kidunia na uwazoeze na kuwakumbusha juu ya wajibu wao wa kukabiliana na waporaji na wateka nyara wa kimataifa. O  O  O Natarajia kwamba utazingatia akilini maudhui za ubinadamu, za kiroho, kisiasa na kijamii za Hija na uwaelimishe mahujaji kuhusu sura ya “Mkusanyiko wa Kimapinduzi wa kila Mwaka” wa Uislamu. Inaaminiwa kwamba ni muhimu kutamka kwamba dalili za mabaki yote ya kipagani lazima ziondolewe kwenye mwanzo wa safari hii tukufu. Tunamuomba Mwenyezi Mungu awape kila msaada. O  O  O

107

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 107

11/3/2015 2:57:52 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

17 UMUHIMU WA USHIRIKIANO WA MAHUJAJI NA UJUMBE WA FAQIH KWENYE MAMBO YA HIJA

N

inahitaji kwa dhati kabisa kwamba mahujaji wote wa Iran na mahujaji wengine vilevile kuwa na tabia ya adabu njema na amani, kutenda kwa mujibu wa mwakilishi wangu Mheshimiwa Hujjatul-Islam Muusavi Khoiniha, kuwachukulia Waislamu wote kama ndugu zenu na muwatendee kama Mwislamu mchamungu anavyostahili kutenda. Na ninawaomba mahujaji waheshimiwa na viongozi wao wapendwa kushirikiana ipasavyo pamoja na wewe na kutenda mambo kwa mujibu wa maelekezo yako. O  O  O Ni muhimu kuwa waangalifu katika kuepuka vitendo vyovyote kinyume na utaratibu na hotuba zisizofaa, na kila mmoja kuchunga sana juu ya marafiki na wenzake kwa makini, kushiriki katika mipango iliyopangwa na mwakilishi wangu, Mheshimiwa HujjatulIslam Muusavi Khoiniha na msizivunje hizo ratiba vinginevyo itaishia kwenye machafuko na kuwasumbua mahujaji. Kwa vile ni lazima katika safari hii iliyobarikiwa kwamba misafara na makundi yanashughulika kwa ushirikiano na upatanifu katika ratiba zao za Kiislamu-kisiasa na kuepuka ghasia na 108

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 108

11/3/2015 2:57:52 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

tabia zisizo za Kiislamu, watukufu mahujaji na hiyo misafara pia wanatakiwa kufuata mapendekezo ya mkurugenzi wa Hija, Mheshimiwa Hujjatul-Islam Muusavi Khoiniha, vinginevyo, na Mwenyezi Mungu aepushilie mbali, kama kila msafara na kila kundi litajiendesha kwa kujitegemea lenyewe bila ya kushirikiana, inaweza ikaleta machafuko na kutokea baadhi ya upotovu ambao utatafsiri vibaya mapinduzi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ambayo itakuwa ni kosa kubwa mno na linafuatiliwa na uwajibikaji mkubwa mbele ya Muumba na viumbe, na ninatarajia kwamba wapendwa mahujaji – Mwenyezi Mungu awasaidie – kujidhibiti wenyewe na wenzao katika kulinda ibada hii tukufu ya Mwenyezi Mungu kutokana na madoa ya uovu na makosa. O  O  O Maulamaa watukufu wakiwemo katika safari hii, wote wale waliosafiri kwa maombi yangu na wale wengineo bila shaka watakuthibitisheni, na mahujaji wanatakiwa kujali na kuzingatia maelekezo yenu na kufuata taratibu zenu, ili kwamba ibada hii tukufu itekelezwe kwa kuzingatia maudhui zote na idadi kubwa ya vipengele vyake. Ni dhahiri kwamba wakuu wote ambao wanahusika na wajibu huu wa kidini wa Hija na mambo ya mahujaji watashirikiana nanyi na kuthamini maelekezo yenu. Viongozi wa kitaifa ambao wanahusika na Hija, kwa sababu yoyote ile, wanatakiwa kuchukua hatua yoyote ile kwa kushirikiana na kwa idhini ya mabwana hawa. O  O  O

109

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 109

11/3/2015 2:57:52 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

18 WAJIBU WA VIONGOZI (MASHEIKH) KATIKA MISAFARA YA HIJA

N

apenda kuwakumbusha viongozi na vilevile waandalizi wa misafara, na mahujaji wote wa kwenye Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu kwamba Hija ya mwaka huu ni tofauti na zile za miaka iliyopita. Katika miaka iliyopita, hususan miaka ya hivi karibuni, mahujaji walisafiri pamoja na misafara ya kipagani au ile iliyokusanywa na kuhudumiwa na dhalimu. Kwa hiyo, tendo lolote ovu au vurugu, iwe lilitendwa na Ulamaa au waandalizi, lilihesabiwa kuwa ni hatia ya dhalimu huyo. Halikuudhuru Uislamu, bali lilisababisha uimarishaji zaidi wa Uislamu. Mwaka huu, kama vile tu ambavyo uendeshaji na utawala wote lazima ubadilike na kuwa katika hali ya Kiislamu, ni muhimu sana kwamba misafara ya Hija iwe na tahadhari na uangalifu sana. Macho yote yanatazama kwa makini sana kuona tofauti iliyopo kati ya mwaka huu na miaka iliyopita. Watu wanataka kujua iwapo kama wale wanaodai kwamba dola la kipagani limeangamia na Jamhuri ya Kiislamu imekuja badala yake, wale ambao wamechaguliwa na maulamaa wa miji mbalimbali na wale ambao wametumwa na serikali ya Kiislamu, je ni kweli wanathibitisha kuwa kama vyeo vyao vinavyohitajia wawe? Au ni madai yasiyo na msingi na visingizio tu? Leo ni lazima mthibitishe kutimiza wajibu mkubwa kabisa, wajibu wa kulinda na kuhifadhi hadhi na heshima ya Uislamu. 110

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 110

11/3/2015 2:57:52 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

Wakati wa utawala fidhuli uliopita, kama mtu mwenye kilemba angefanya kosa lingehusishwa kwa huyo dhalimu. Lakini leo hii, wao hawasemi kuwa ni wa kutoka kwenye ule utawala wa kifidhuli. Wanasema huyo anatokana na Uislamu au ni Mwislamu huyo. Endapo kama, na Mwenyezi Mungu aliepushe mbali hili, katika Hija hii mnayokwenda, kila wakati mnapotokeza mbele ya macho ya Waislamu kutoka duniani kote, muonekano wenu ukawa hauna tofauti na ule wa wakati wa wana wa wafalme wa mashetani, itatangazwa duniani kote kwamba kisingizio ni cha Kiislam lakini maana ni ya kipagani! Hivyo basi, mnaweza ama mkauaibisha na kuufedhehesha Uislamu au, Mwenyezi Mungu akipenda, mkaweza kuilinda heshima yake. O  O  O Kwa mintarafu ya Hija hiyo na waungwana ambao wanakwenda pamoja na misafara ya Hija, uhalisi na uhakika wa Hija ni kwamba ni lazima muende mkajifunze matatizo na maumivu ya watu. Muone masikini wanajisikiaje, na myahisi matatizo yao. Kama kuhiji ni kukufanya wewe utegemee kupata maisha ya anasa zaidi, basi hiyo sio Hija ya kweli. Hija ambayo Mwenyezi Mungu ameamuru ni ile ya kwamba mnakwenda pale na kuona jinsi watu wengine wanavyoishi. Hapo nyuma kabla ya sasa, wakati mmoja tulipokwenda huko tuliona mambo ambayo mahujaji wa leo hawayaoni. Katika kusafiri kati ya Makka na Madina, wakati mwingine gari yetu ilisimamishwa katikati ya jangwa hame, na wakichomoza kutoka kwenye vichaka, walikuwa ni watoto waliokuwa uchi na wanawake wakiwa wamefunika sehemu tu ya miili yao na wanaume wakiwa katika hali duni isiyoelezeka ambao walikuwa wakiomba msaada. Kwa kutambua dhiki kama hizo, mtu lazima asitegemee faraja kubwa zaidi kutoka kwenye misafara hiyo. Hapo zamani mahujaji 111

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 111

11/3/2015 2:57:52 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

walikuwa wakisafiri kwa punda. Hakuna nyumba za kuishi ambazo walikuwa wamepatiwa na walilazimika kujitafutia wenyewe sehemu za makazi. Na safari yao ya mzunguko wa kwenda na kurudi iliwachukua miezi kumi na nne. Sasa hivi, ndani ya saa mbili au tatu unawasili huko kwa ndege yenye kustarehesha na mahali pako pa kufikia pakiwa pameandaliwa kabla hujafika. Sasa ninyi ni Mahujaji na ni Waislamu, munao wajibu mkubwa wa kuwaokoa wale wanaoonewa na kukandamizwa wa duniani humu. Msijiwekee matarajio makubwa kupita kiasi kwamba Mwenyezi Mungu azikatae huduma zenu, na kisha kutakuwa na matatizo ya kimitego. Waheshimiwa Ulamaa, ninyi ni lazima muwashauri mahujaji kuyasamehe na kutoyatilia maanani mapungufu yoyote watakayokutana nayo. Wasimamizi wa Hija wamefanya kila waliloweza, wamefanya juhudi nzuri kabisa na bado wanaendelea kujaribu, licha ya matatizo yote huko, kuwapatieni makazi yaliyo bora kabisa kiasi iwezekanavyo. Sio kwamba wameshindwa kujaribu zaidi na zaidi. Bali ni kwamba hawakuweza kufanya zaidi ya hapo. Wasingeweza kuwaambieni kwamba msiende Hija kwa sababu hawakuweza kuwaandalieni makazi ya daraja la juu, hapana, mnapaswa kwenda na kufikiri zaidi juu ya mateso na dhiki za walio mafukara. Vyovyote iwavyo, ni jukumu la Ulamaa wanaoandamana na misafara. Nina maana kwamba ni moja ya majukumu yao. Wajibu wao mwingine ni kuwafahamisha juu ya masuala ya Hija. Wakati mwingi watu wanakwenda kuhiji, wanafanya juhudi zote, lakini hawana ufahamu wa masuala ya Hija. Huko wanapatwa na matatizo na wakati wanaporejea nyumbani, baada ya miaka michache kupita, wanaanza kuulizia kama ibada yao ya Hija ilikuwa haina makosa ama vipi. Iwapo wanachukuliwa kama ni maalhaji au hapana? 112

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 112

11/3/2015 2:57:52 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

Ninyi waheshimiwa viongozi lazima mtengeneze vikao vya hotuba na maongezi kwa ajili ya watu na muwapime juu ya vitendo vya Hija vya wajibu na vile vilivyoharamishwa, sio lazima sana tu kwa adabu za kawaida. Hizo sio lazima mno. Na watu wana wajibu wa kuhudhuria vikao hivi, wasikilize kwa makini na kujifunza mas’ala za Hija, ili wasije kupata matatizo baadaye, na kubakia na shaka kuhusu usahihi wa ibada zao. Mtakapoyajua mas’ala ya Hija, kila jambo litafanyika kwa ukamilifu wa uhakika kabisa. Huu ni wajibu mwingine wa Ulamaa wa kutekelezwa huko. Na watu lazima wafuatilie kuzielewa mas’ala za Hija, sio waridhike tu kuwa wamehiji na hiyo iwe ndio basi. Hapana, hapa ni mahali tofauti na sehemu nyinginezo. Unapofanya ziara kwenye makaburi matukufu hutakuwa unaingia kwenye matatizo. Lakini hapa ni tofauti kabisa. Unaweza ukabakia kuwa Mahrim na utapaswa kurudia Hija yako. Kutojua kuhusu masuala ya Hija kunasababisha matatizo. Hivyo, jaribu kujifunza masuala hayo kwa faida yako mwenyewe na kuepukana na makosa. Hili ni moja ya mambo hayo. Jambo jingine linafaa kutajwa hapa ni kwamba hao Ulamaa wa misafara ni lazima wawapime mahujaji kwa harakati zao za kisiasa katika Hija, lazima ziwe na mpango makini. Maoni binafsi ya kishupavu yataishia kwenye vurugu na wakati wote yameonekana kutokuwa sahihi. Kila jambo lazima lifanywe kwa mpango fulani. Kwa mfano, wanataka kukusanyika kwa lengo fulani, sawa, kuna mtu ambaye ni msimamizi wa mambo ya Hija. Yeye lazima atengeneze utaratibu na wao lazima waufuate huo. Vitendo vya maoni binafsi ya kishupavu ya mtu mmoja au ya kundi, pamoja na tofauti iliyopo katika maoni, vitasababisha migogoro, na baya zaidi kuliko hilo ni kwamba, vinaweza wakati mwingine vikafedhehesha Jamhuri ya Kiislamu. Ni lazima waepuke mambo ambayo yanaivunjia heshima Jamhuri ya Kiislamu, wana propaganda wengi duniani kote kwa sasa 113

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 113

11/3/2015 2:57:52 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

wanajishughulisha mno katika kueneza uvumi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu. Kwa nini basi sisi tuwapatie kisingizio na kuwafanya waweze kuongeza propaganda yao ya kifitna? Hili ni jambo jingine muhimu ambalo linapaswa kuzingatiwa na kila mmoja, yaani ni kusema, watu wote lazima wafanye mambo kwa mpango na nidhamu, ili kwamba ibada zao zisichanganyike na uovu; zote ziwe za Kiislam, na zote zifanywe kiibada na kiutiifu; matembezi na miito iwe yote ni ya kiibada na sio ya kipotofu; kila kitu kiwe ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, sio kila mtu afanye kama anavyotaka na kumtusi anayemtaka. Hapana, hiyo sio njia iliyo sahihi. Mambo haya lazima yaende kwa kulingana na mipango na taratibu zilizopangwa vizuri. O  O  O Enyi Ulamaa wapendwa, jaribuni kuwafahamisha mahujaji wajibu wao ili Hija itekelezwe kama ilivyoagizwa kwenye sheria tukufu. Ningependa kuwashauri ndugu mahujaji kwenye Nyumba ya Mwenyezi Mungu kwamba wajaribu kujifunza taratibu na kanuni hizo kutoka kwa masheikh wao wanaoandamana na misafara na wasifanye kitendo chochote bila ya muongozo wao. Wakati mwingi ibada zenu zinaweza zikawa batili kutokana na kupuuza na kamwe usijifanye uko tayari kwa ibada hizo au mnabakia katika hali ya ihram na mkajiweka ninyi wenyewe na ndugu zenu katika matatizo. Huu ni wajibu wa kidini ambao haupaswi kupuuzwa. Na ningependa kuwaeleza watukufu masheikh kwamba kwa ziada ya kuwafundisha mas’ala hayo kwa mahujaji kwa uwazi kabisa, na kueleweka kwa ujumla, kupitia vikao kadhaa, wao pia wanapaswa kuwaangalia wakati wanapotekeleza ibada hizo na kuwaongoza pale inapobidi. 114

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 114

11/3/2015 2:57:52 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

O  O  O Waheshimiwa Ulamaa, mameneja, na wasimamizi wa misafara na viongozi wakuu wengine, kwa kuzingatia wajibu wao mkubwa katika kuwasimamia na kuwaongoza mahujaji na kwa kuzingatia hali ya kipekee ya Jamhuri ya Kiislamu, wanapaswa kufanya kila juhudi kufanya ibada hizo za Hija kutekelezwa kikamilifu na kwa utaratibu mzuri, wafundisheni kanuni za Hija na mas’ala zake kwa ukarimu na fanyeni mipango kwa ajili ya shughuli zao, wote wasomi na wasio na elimu. Msisahau majukumu yenu yenye kujenga na athari za kudumu za Hija katika mustakbali wa binadamu, kwani katika mazingira ya kiroho, nyoyo zote zimejiandaa kwa ajili ya mabadiliko na utambuzi wa ukweli. Kwa hiyo, hali ya kushikilia maoni binafsi katika mambo ya Hija, hasa katika masuala yake na taratibu zake za kiibada lazima iepukwe, na masuala za Hija lazima kwa ufahamu kabisa zifafanuliwe, na inapobidi, kwa kuboresha ufahamu, rejea lazima zifanywe kwenye vyanzo, kwa sababu katika kaida za Hija masuala mapya ni mengi, na Mwenyezi Mungu aepushilie mbali, maelezo ya mas’ala hayo yasiyokamilika vizuri yanaweza kufanya juhudi zote kuwa bure tu, na kusababisha shida kwa mahujaji. Waheshimiwa masheikh/viongozi wakati wanapoelezea kwa uwazi kabisa mas’ala na maelekezo ya kidini wanapaswa kuepuka kusitasita ambako kunaweza kuwaweka mahujaji kwenye hali ya kutokuwa na uhakika na kuwa na shaka, na wakumbuke kwamba urefushaji zaidi katika kaida za kidini na ibada kutasababisha taklifu na uzembe katika majukumu muhimu. O  O  O

115

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 115

11/3/2015 2:57:52 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

19 WAJIBU WA WASIMAMIZI WA ­MISAFARA

N

i lazima muwe mfano bora wa matendo mazuri, mkiiwakilisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ima mkiwa mashekh, wakuu wa misafara au mahujaji wa kawaida. Mwaka huu Hija yenu ni ya mfano wa Jamhuri ya Kiislamu. Hija ya kweli, sio Hija ya utawala wa kipagani. Mnayo heshima kubwa na wajibu ulio mkubwa zaidi. Sisi sote tunawajibika mbele ya Uislamu. Leo hii sio ninyi tu, bali pia tabaka lote la taifa na serikali vina wajibu mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na Uislamu. Tunadai kwamba ule utawala wa kipagani umefutwa na Jamhuri ya Kiislamu imechukua mahali pake. Ni lazima tuthibitishe kwamba mambo yamebadilika. Kila kitu kimepitiwa na mabadiliko kamili. Kama tunaona kwamba hakuna mabadiliko yaliyotokea kwenye serikali, katika misafara ya Hija na masheikh na ndani yenu wenyewe, na masheikh wa misafara, basi kuna tofauti gani iliyopo? Itakuwa mambo ni yaleyale basi; utawala uleule wa kipagani lakini kwa jina jingine tofauti tu. Ni lazima tuhakikishe kwamba maudhui zimebadilika Insha’Allah. Ule utawala wa kipagani umebadilika na kuwa utawala wa Kibinadamu wa Kiislamu, yote katika yote. Jichungeni ninyi wenyewe kwa makini kabisa, ichukulieni safari hii kama ni safari kuelekea kwa Mwenyezi Mungu na zingatieni akilini kwamba, mnaweza mkapata heshima kubwa zaidi mbele ya Mwenyezi 116

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 116

11/3/2015 2:57:52 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

Mungu, au, Mwenyezi Mungu aepushilie mbali, mkapotelea kwenye kuoza tu. O  O  O Masheikh/viongozi, wakuu na wasimamizi wa misafara ya Hija, kwa kuzingatia wajibu mkubwa waliouchukua wa kusimamia na kuwaelekeza mahujaji, na kwa kuzingatia hali za kipekee za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, lazima wafanye juhudi za hali ya juu kabisa za kupanga na kuendesha Hija, kwa ukarimu kabisa wafundishe ibada na masuala ya Hija kwa mahujaji, wote, wasomi na wasio na elimu. Ni lazima wasisahau majukumu yao yenye ujenzi na matokeo ya kudumu ya Hija katika maisha ya wanadamu, kwa sababu katika mazingira ya kiroho kama hayo, nyoyo zinakuwa zimejiandaa kubadilika na kupokea ukweli. Kwa hiyo, epukeni hali ya kushikilia maoni binafsi katika mambo ya Hija, hususani katika kufundisha mas’ala na kanuni, na mzieleze kwa ufahamu kamili na mrejee kwenye vyanzo au vitabu vya kisheria na wanatheolojia wasomi ikibidi lazima, kwa sababu wakati mwingi mas’ala mpya huibukia wakati wa Hija na maelezo yenye dosari na ya kimakosa, Mwenyezi Mungu aepushilie mbali, yanaweza kubatilisha ibada na kuwatatiza mahujaji.’ Masheikh wapendwa wanapaswa kuwa waangalifu ili wasije wakawatia wasiwasi mahujaji wakati wanapofafanua mas’ala hizo, kwani wanaweza wakaingiwa na shaka zisizo na lazima, na wazingatie akilini kwamba kurefusha katika ibada za kidini kutasababisha kusita kwenye wajibu muhimu wa kidini. O  O  O

117

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 117

11/3/2015 2:57:52 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

20 HAJA YA MPANGILIO MAKINI ­KATIKA HIJA

N

i muhimu kuwa na mpangilio makini katika kutekeleza ibada za Kiislamu vizuri zaidi, na kuepuka miito iliyobuniwa binafsi ambayo inaweza kuanzia kwenye mapendekezo ya wapotovu ili kusababisha vurugu, na kuwafedhehesha mahujaji wanaoshiriki kutoka nchi za Kiislamu, hususani Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Na fuateni miito inayoelekezwa moja kwa moja na wenye mamlaka hasa Hujjatul-Islam Karrubi, mwakilishi wangu, Mwenyezi Mungu amsaidie, na kamwe msiikengeuke hiyo. Msiwafuate wale ambao wanajaribu kutoa miito yenye vurugu; washaurini, na kama waking’ang’ania basi wafukuzeni. Msifanye matembezi ya kikaidi, na mnapaswa kujua kwamba madhara yoyote yatakayofanywa kwenye sifa njema za mahujaji kupitia upotokaji kwenye mipaka, kutawafanya muwe wa kulaumiwa kabla na kukemewa na Mwenyezi Mungu. Mnapaswa kujua kwamba falsafa muhimu ya mkusanyiko huu mtukufu wa Waislamu kutoka pande zote za dunia, kwenye kituo hiki kitakatifu na mahali pa mashukio ya wahyi ni mwingiliano wa Waislamu wa dunia na uunganishaji wa wafuasi wa Mtukufu Mtume 7 na wale wenye kuamini Qur’ani Tukufu, dhidi ya wapagani wa ulimwengu. Na kama, Mwenyezi Mungu aepushilie mbali, tabia ya baadhi ya mahujaji ikivuruga umoja huu na kusababisha mfarakano, hilo litamkasirisha Mtukufu Mtume 7 na kusababisha adhabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu. 118

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 118

11/3/2015 2:57:52 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

O  O  O Ningependa kwa nia njema, kuwataka mahujaji wa kwenye Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu kuzingatia utaratibu mzuri na amani, na kufuata maagizo ya mwakilishi wangu Mheshimiwa Hujjatul-Islam Musawi Khoiniha. Wachukulieni Waislamu wote kama ndugu zenu na watendeeni kwa tabia ambayo inategemewa kutoka kwa Mwislam wa dhati, mchamungu. Ningependa kuwashauri wapendwa mahujaji wa Iran ambao wanabeba ujumbe wa Uislamu na Qur’ani na vilevile ujumbe wa Mapinduzi ya Kiislamu kwamba waonyeshe mwenendo wa wastani kwa Waislamu wote, hata kwa wafanyakazi wa Saudia wawapo kwenye vituo hivyo vitukufu, huko Makka na Madina na msikabiliane nao kwenye maeneo hayo matakatifu. Watendeeni wote kwa tabia ya Kiislamu na kibinadamu, wavuteni kutoka kwenye tabia ya ukali kwa kuwapa ushauri wa kirafiki na mawaidha ya amani, na kama ilivyoamriwa na Mwenyezi Mungu, kuweni na busara kwa watu wajinga, na wekeni macho ya uangalifu kwenye mienendo yenu wenyewe na utulivu wenu, na ule wa marafiki zenu. Na kama wapinzani wenu wakiwatendea kinyume na amri za Qur’ani Tukufu ninyi msilipize ili muweze kuonekana kama watiifu na wenye kuheshimika mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na mnapaswa kujua kwamba kwenye mikusanyiko kama ile ya matembezi ya kisiasa, mtu anaweza akataharuki, na wakati mwingi anaweza akahamaki na kukasirika na akafuata mwito usiofaa ambao umetolewa na wapotofu wataka shari bila kujijua katika matembezi na maandamano ya Hija ambayo yanapaswa kufanywa kimya kimya na kwa amani kabisa, na hili ni kinyume na vigezo vya Kiislamu, lakini wao, kupitia muonekano wao wa kihisia wanasababisha upotovu miongoni mwa watu. Ni muhimu kwamba wapendwa mahujaji 119

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 119

11/3/2015 2:57:52 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

wa Iran wayachukulie kwa uangalifu mambo haya, na waandaaji wa maandamano hayo waitengeneze kwa makini miito yao, na wale wenye elimu kuhusu mambo ya kisiasa na kijamii waanzishe miito inayofaa, kupitia mashauriano na mwakilishi wangu HujjtulIslam Muusawi Khoiniha na kuwaelimisha watu kufuata miito hii tu na kuepuka kuitika miito isiyodhibitiwa, na lazima wadumishe utaratibu wao na amani. O  O  O Miongoni mwa mambo mengine yanayohusiana na watu kutoka kwa Maulamaa ni lile suala la kwamba maandamano ya kisiasa yanayofanyika wakati wa Hija lazima yaratibiwe kwa mpangilio wenye utaratibu mzuri. Ikiwa kila mmoja, kwa makusudi, atafanya vile atakavyo, hiyo ni vurugu na wakati wote hili ni kosa. Kila jambo lazima lifanywe kwa mpango. Kama wanataka kukusanyika pamoja kwa lengo fulani, hilo ni sawasawa. Lakini ni lazima washirikiane na mamlaka zinazosimamia mambo ya Hija. Kwa sababu kila mtu mmoja mmoja ana upendeleo wake binafsi, na mapendo yanatofautiana, na hilo ndio linalosababisha matatizo na aibu kwa Jamhuri ya Kiislamu. Ni lazima tuepuke vitendo vya vurugu na ghasia ambavyo vinaweza vikaivunjia heshima Jamhuri ya Kiislamu. Wana propaganda takribani kila mahali duniani kote wanajishughulisha kueneza minon’gono ya uzushi dhidi yetu na dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu. Sasa kwa nini sisi tufanye jambo ambalo litawapa wao kisiingizio kwa ajili ya uenezaji wa propaganda? Hili ni tatizo jingine ambalo lazima lionyeshwe kwa mahujaji, ili kwamba kila jambo liweze kuandaliwa vizuri kwa mujibu wa vigezo sahihi.

120

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 120

11/3/2015 2:57:52 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

O  O  O Katika matembezi na maandamano hayo, fuateni maelekezo ya wale walio na mamlaka kwa ajili ya upangaji wa muda, mipango, miito na kadhalika. Dumisheni taratibu na adabu za Kiislamu na msimruhusu mtu yoyote kutoa miito ya kuzusha yeye mwenyewe na isiyodhibitika kwa vile maadui wa Uislamu na wa Jamhuri ya Kiislamu wanaweza wakajipenyeza kwenye safu zenu ili kusababisha mfarakano miongoni mwenu, na wakakuchafulieni heshima yenu na kulifedhehesha taifa lenu na dini yenu kwa kupendekeza miito mibovu na isiyo ya Kiislamu. Kwa hali yoyote mnatakiwa kusikiliza maelekezo na kufuata miito inayoshauriwa na mwakilishi wangu Hujjatul-Islam Karrubi na maafisa wengineo na kuwaepuka wote waliobakia. O  O  O Katika safari hii iliyobarikiwa, ni muhimu kwamba uratibu kamili na ushirikiano unakuwepo miongoni mwa misafara yote na makundi yote pia, ili katika ushughulikaji na mambo ya kisiasa, vurugu zozote na tabia na mwenendo usio wa Kiislam viwe lazima vinaepukwa. Wapendwa waheshimiwa mahujaji na wakuu wa misafara wanatakiwa kufuata mafundisho ya Meneja ama msimamizi wa mambo ya Hija, Hujjatul-Islam Musa Khoiniha. Kama, na Mwenyezi Mungu aepushilie mbali, kila kundi na msafara watafanya kila moja kivyake bila kupatana kiuratibu, basi linaweza likatokea balaa na baadhi ya upotofu kutokea ambao utaitafsiri vibaya sura ya Jamhuri ya Kiislam na mapinduzi ya Iran, na hii ni dhambi kubwa inayobeba uwajibikaji mkubwa mbele ya Mwenyezi Mungu na viumbe Wake.

121

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 121

11/3/2015 2:57:52 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

Na ninataraji wapendwa mahujaji (msaada wa Mwenyezi Mungu uwe juu yao), watachukua uangalifu kamili ili wasiichanganye ibada hii tukufu na maovu na utenda makosa. O  O  O Ni muhimu kwa wote kuwa waangalifu wasije kuruhusu vitendo vya vurugu kufanyika au maneno yasiyo na msingi wa maana kusemwa. Kila mmoja lazima awe macho kumwangalia mwenzie wa karibu, na kufuata mipango ya kibinadamu ya Kiislam kama ilivyoratibiwa na mwakilishi wangu Hujjatul-Islam Musavi Khoiniha na msiikengeuke mipango hiyo ili kusije kujitokeza hali ya vurugu na kuwe hakuna taklifu yoyote inayosababishwa juu ya mahujaji. O  O  O

122

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 122

11/3/2015 2:57:52 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

21 ANASA NA MATUMIZI ­YASIYOWIANA NA FALSAFA YA HIJA

M

iongoni mwa bidhaa zinaonyeshwa kwa mahujaji huko Hijaz, zile ambazo ni za kimarekani ziko kinyume na maadili ya Kiislamu, na kimsingi kuzinunua ni kinyume na Uislamu, na ni kuwasaidia maadui wa Uislamu na kueneza maovu, na ni lazima kufanya hivyo kuepukwe. Sio haki kuwaacha vijana wetu wapendwa kujitoa muhanga kwenye mipaka wakati mnawasaidia wahalifu wa kivita na kuidhihaki Jamhuri ya Kiislamu na taifa la Iran lililokandamizwa. Mnaweza mkanunua vitu vinavyokufaeni ninyi wenyewe pamoja na jamaa zenu kutoka Iran ili iwe hamuwasaidii maadui wa Uislamu. Mimi nimetimiza wajibu wangu tu na sasa inakubidini kuwa waangalifu na kutambua kwamba hamuwaungi mkono na kuwasaidia maadui wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wakati mnakwenda kuhiji Nyumba ya Mwenyezi Mungu, hivyo mkaliaibisha taifa lenu na nchi yenu, haya ni mambo ambayo yalikwisha kuelezwa hapo kabla na sasa yanarudiwa tena kutokana na umuhimu wake. O  O  O Wale ambao wanatumia kiasi kikubwa cha fedha, bila ya ulazima wowote, kwa ajili ya hidaya au mapokezi ya kianasa, bora watumie aina hii ya matumizi, wakati wanaporejea nyumbani, katika 123

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 123

11/3/2015 2:57:52 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

kuwasaidia wasio na uwezo na mafukara, ili Mwenyezi Mungu aje kuwalipa thawabu na kuwarehemu. O  O  O Oh! Enyi Maulamaa na viongozi wa misafara na mahujaji wote! tahadharini msije mkaifanya safari hii kama ni safari ya biashara. Safari ya kuelekea kwa Mwenyezi Mungu na sio kuelekea vitu vya kidunia, msiitie madoa kwa mambo ya kidunia. O  O  O Mwaka huu, kwa vile ndugu wanaume kwa wanawake wakiwa wameteseka sana kutokana na hasara na dhiki zilizolazimishwa juu yao na utawala wa kipagani katika wakati wa mapinduzi, na wanamapinduzi wengi walemavu wako katika haja kubwa ya msaada, inafaa zaidi sana kwamba wale wanaotaka kutekeleza ile Hija iliyopendekezwa (Umrah), watumie gharama hizo zinazohusika katika kutatua shida na haja za ndugu kama hao, jambo ambalo linachukuliwa kwamba ni lenye thawabu na malipo bora zaidi kwa Mwenyezi Mungu kuliko kufanya hiyo Hija isiyo ya lazima kiwajibu. O  O  O

124

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 124

11/3/2015 2:57:52 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

22 MAUAJI YA KIKATILI NA KUMWAGA DAMU YA MAHUJAJI KATIKA HIJA YA MWAKA 1987

N

itakachofanyia tathmini leo hii ni lile tukio la msiba wa kusikitisha na la kuomboleza lililotokea ndani ya mji wa Makka. Tangu mwanzo wa mwamko kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na kwa ajili ya ukombozi wa taifa – Mwenyezi Mungu aridhishwa nalo hili – tumekuwa na watu wengi waliokufa shahidi, kabla na baada ya mapinduzi. Tulikuwa na mashahidi wakubwa wakati wa utawala dhalimu wa kinasaba na baadaye, kama mlivyoona, tulikuwa na mashahidi ambao ni watu wenye thamani sana. Lakini lile janga baya la Makka ni jambo jingine kabisa, tofauti na balaa nyinginezo. Wakati ule sisi tulipiga na tukapigwa. Tumepata kuwa na mashahidi kila mahali. Wakati wa utawala wa Riza Shah, kwa wale wanaokumbuka, wanaweza wakasimulia ni mateso gani ambayo tuliyapata. Na katika wakati wa Muhammad Reza, wote mnaweza kukumbuka hali mbaya tuliyokuwa nayo wakati ule na mashahidi gani tuliokuwa nao wakati huo. Lakini yote hayo yalikuwa ni vifo vya kishahidi, yote katika yote ilikuwa ni hatari kubwa vilevile. Lakini suala la Hijazi ni jambo jingine kabisa. Tuliona kilichotokea katika Siku ya Quds, lakini ile Ijumaa ya umwagaji damu ya Makka ni jambo jingine kabisa. Katika kadhia ya Siku ya Quds sisi tulijaribu kuikomboa Quds tukufu kutoka katika mikono ya waporaji na wao 125

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 125

11/3/2015 2:57:53 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

walidai kuimiliki. Lakini wao hawakufanya kufuru juu yake. Kwa kweli Quds lazima isiachwe mikononi mwao, ni lazima ikabidhiwe kwa wamiliki halali. Wapendwa wengi, ambao vumbi la miguu yao lina thamani mno kuliko miili yote ya wakazi wa kwenye makasiri, wameuawa kishahidi katika milipuko na mauaji ya hivi karibuni. Wakati wa vita vilivyolazimishwa na Saddam, vilevile tulipoteza wapendwa wetu wengi na tukapata kiasi kikubwa cha uharibifu. Lakini tena, yote hayo ni tofauti na ile kadhia ya Hijazi. Sisi bado hatutambui kwa ukamilifu hasa juu ya kile kilichotokea, na dunia pia bado haijatambua. Ndani ya Hijazi, utakatifu wa kituo kitukufu zaidi cha ulimwengu wa Kiislamu na usio wa Kiislamu umevunjwa. Ka’aba inaheshimiwa sio tu na sisi Waislamu wa dunia, bali pia hata na mataifa yote yanayoamini juu ya dini. Ka’aba imekuwepo tangu mwanzo. Mitume wote wamefanya ibada ndani yake. Kuivunjia heshima Ka’aba sio kitendo kidogo cha kupuuzwa vivi hivi. Kama tusipozingatia na kujali msiba wa Quds, kama tusipojali uhalifu wa Saddam, kama tusipojali juu ya wale wote ambao wametutendea mabaya, lakini hatuwezi kupuuza suala la Hijazi. Lile ni jambo jingine kabisa, ni tofauti na masuala mengine yoyote. Na ni muhimu kuiweka siku hii kuwa hai siku zote; siku ambayo waliusaliti Uislamu. Na sasa mwezi wa Muharram unakaribia. Muharram ni mwezi wetu wa maombolezo juu ya kuuliwa kishahidi kwa Bwana wa mashahidi, ambaye aliondoka Makka ili kulinda utakatifu wa Makka – wote tuwe muhanga kwa ajili ya Makka. Na sasa eneo hili takatifu linatwaliwa na kundi la watu wenye kukufuru ambao hawajui ni lipi wanalopaswa kufanya na hawawezi kuelewa ni nini kilicholazimishwa juu yao na juu ya Waislamu. Hii ni aibu na fedheha juu ya Waislamu wote kuuacha utakatifu wa Makka, mahali patakatifu na kituo kitukufu cha Mungu kiwe kimevunjwa kiasi hicho na Waislamu wawe wamekaa kimya kabisa namna hiyo. Ni juu ya 126

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 126

11/3/2015 2:57:53 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

Waislamu kuiweka kumbukumbu hiyo kuwa hai. Katika Muharram, wahutubu wote, waombolezaji na watembeaji wa maombolezo ni lazima washughulike na jambo hili kama suala lao la hali ya juu la mihadhara kwamba Imam Husein A aliuliwa shahidi katika njia ya haki ya ki-Mungu, utii kwa Mwenyezi Mungu, utimilifu wa ibada ya Hija na ulinzi wa utakatifu wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu. Na sasa tumebakia tumekaa kimya tukiangalia nini? Tunapaswa kufanya nini? Bila shaka, ni lazima nieleze kwamba sina maana kamwe kwamba ni lazima tuwasumbue wale walioko hapa, Wasaudi, Wakuwaiti au wengineo. Wao wamepewa makazi na sisi ni lazima tuhakikishe wako salama, na nina hakika vijana wetu wana nia nzuri. Lakini ngojeni niwaambie kwamba wanaweza wakawepo wengine miongoni mwenu wenye nia mbaya, na wanaotaka kulitia doa taifa na serikali ya Iran. Ni lazima muwe waangalifu sana. Wasaudi na wengine kama wao sio wale ambao sisi tunataka kuwaadhibu. Tatizo liko zaidi ya hapo. Sisi ni lazima kwa nguvu zetu zote, na Waislamu wenzetu ni lazima kwa nguvu zao zote, na watu wengine, wale ambao wanamwamini Mwenyezi Mungu, ni lazima kwa nguvu zao zote wakabiliane na kupigana dhidi ya tatizo hili, katika njia ambayo wanaiona inafaa. Ni lazima tufe kwa aibu kwamba uhalifu huu mkubwa ulitendeka mbele ya macho yetu, na hata hivyo, wao wanadai kwamba wako katika haki. Njama hii, bila shaka ilikuwa imepangwa mapema. Wameilazimisha juu ya ukoo wa Kifalme wa utawala wa Saudia kufanya jambo la kipuuzi kama hili na kujifedhehesha wenyewe duniani, ingawa walikwisha kujiaibisha na wataendelea kujiaibisha, na tunashangaa na kujiuliza, tutafanya nini? Mwenyezi Mungu Mtukufu atailinda Mwenyewe Nyumba Yake, na watatwezwa kwa dharau na Waislamu, na waumini na watu wa Hijazi. Watu wa Hijazi 127

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 127

11/3/2015 2:57:53 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

hawakushiriki na kutia mkono katika hilo. Lilifanywa na watu wa makundi yenye uhusiano na kundi hili potovu na serikali hii potovu. Njama hii ilibuniwa mapema kabla ya hapo. Ilikuwa ni jambo lisilo na kifani, ambalo halijawahi kutokea kwamba Mfalme wa Saudia anitumie mimi ujumbe na kunishukuru kwa kusema kwamba mambo yatakuwa shwari huko. Hajawahi kamwe kufanya hivyo hapo kabla. Amefanya hivyo mwaka huu tu. Kwa nini? Kwa nini alinitumia ujumbe huu mwaka huu? Ilikuwa ni onyesho. Yeye kwa hiyo alijaribu kunionyesha nia yake njema. Ushahidi ulio bora kabisa kwamba njama yao ilikuwa imepangwa kabla ni namna ya utendaji wao. Wilikiri hilo wao wenyewe. Walisema: “Wairani walitaka kuichoma moto al-Ka’aba na kupanga Qum kuchukua nafasi mahali pa Ka’aba”, madai ya kipuuzi kama hayo! Hivyo inajionyesha wazi kwamba njama hiyo ilikuwa imepangwa kabla ya hapo. Kisingizio chao pekee kilikuwa kwamba Wairani wamekuja kuibomoa al-Ka’aba. Sisi tumejiandaa kulipiza kisasi chetu. Tatizo sio kule kuwauwa halaiki ya mahujaji wasio na hatia tu; tatizo hasa ni kule kuinajisi kwao Makka. Msiba wa Hijazi una sura nyingi, lakini iliyokuwa kubwa mno ni kule kuvunja heshima ya mahali patakatifu na Waislamu hawatabakia kimya tu. Baada ya hapa, Fahad na wale wa aina yake watakuja kutambua kwamba ni nini kilichopandikizwa juu yao, na ni balaa gani lililokuwa limejitokeza. Wairani wanajua njia yao sahihi ya kufuata. Watu wa Hijazi wanajua vizuri sana vilevile. Hili lingetokea huko Ta’if, lingeweza kuvumilika, lakini sio kwenye Haram ya Mwenyezi Mungu. Tumewahi kuwa na mashahidi wengi mno katika vita nyingi na kadhalika, na tutakuwa na kama hao hapo baadaye pia. Lakini hili limetokea katika sehemu takatifu, mahali patakatifu (Haram) ambapo Mwenyezi Mungu ameamuru pawe hivyo kutoka mwanzoni, ambapo sasa pameporwa na wao. Walikuja ili kuwa watumishi wa 128

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 128

11/3/2015 2:57:53 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

Haram mbili hizi, lakini sasa wamekuwa wasaliti kwenye Haram hizo tukufu. Ni nani aliyewateua kuwa watumishi wa Haram hizo mbili? Wamethubutu vipi kubadili jina la Hijazi kuwa Saudi Arabia? Yote haya ni matatizo yenye utata na hatujui ni jinsi gani tutajisafisha wenyewe kutokana na dosari hizi. Kwa kweli nimekuwa mwenye subira kuhusu matatizo hayo, matatizo ya vita na kwa kila jambo. Lakini hili limenifanya nikose subira! Hili ni jambo tofauti kabisa. Tuna matumaini kwamba Mwenyezi Mungu atayatatua matatizo haya. Ninamuomba Mwenyezi Mungu atusaidie sisi tusiwe ni wenye kupuuza kwenye suala hili katika mwezi huu wa Muharram. O  O  O Kile ambacho ni lazima nikielezee kwa wapendwa mahujaji ni kwamba Marekani na ukoo wa al-Saud wamelionyesha tukio hili la Makka kama ni mgogoro wa kimadhehebu, na kugombea madaraka kati ya Shi’ah na Sunni na wakawatafsiri vibaya viongozi wa Iran kama ni watu wanaoota kupata utawala juu ya himaya kubwa, hivyo, wengi ambao hawatambui ile mielekeo ya kisiasa katika ulimwengu wa Kiislamu na zile njama za kisirani na uovu za ulimwengu wa waporaji, watadhani kwamba vilio vyetu vya kukerwa na wapagani na jitihada zetu kwa ajili ya ukombozi wa mataifa kwamba kwa kweli ni jaribio la kupata nguvu zaidi za kisiasa na kupanua mamlaka yetu ya kijiogorafia ya Kiislamu. Sio jambo la kushangaza kwetu sisi na kwa wanafikra wote na watu wenye elimu ambao wanatambua madhumuni ya kifitna ya al-Saud kama wakiishutumu serikali ya Iran, ambayo tangu siku za mwanzoni za ushindi wake imekuwa ikipiga mbiu kwa ajili ya umoja wa Waislamu na inashiriki katika huzuni na furaha za Waislamu duniani kote, wakiishutumu juu ya kujaribu kuwatenganisha Waislamu, au 129

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 129

11/3/2015 2:57:53 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

zaidi ya hayo, kuwashutumu mahujaji ambao kwa mapenzi kabisa wamekwenda kuhiji kwenye eneo takatifu na kaburi la Mtukufu Mtume 7, na kwa msafara wa kijeshi eti kwenda kuiteka Ka’aba, kuchoma maeneo matukufu ya Mwenyezi Mungu na kuuharibu Mji wa Mtukufu Mtume, Madina, wakitoa kama ushahidi wao, ule ushiriki wa maafisa wetu wa kijeshi na kiraia katika msafara huo wa Hija. Kwa mantiki ya ukoo wa al-Saud, hao watumishi wa kijeshi lazima wawe ni wageni kwenye mambo ya Hija. Kuhiji kama huko kwa maafisa wakubwa wa kijeshi na kiraia ni kwenye mashaka kwao wao, na wanashuku kwamba wana njama. Katika macho ya wenye kiburi, hao maafisa wa juu wa nchi za Kiislamu ni lazima wasafiri tu kwenda Ulaya na sio kwenda Hija. Hao wafuasi wenye kulindwa na Marekani wanachukulia kuchoma bendera ya Marekani kama kuchoma sehemu hiyo takatifu, na kutoa miito dhidi ya Marekani, Urusi na Israili kama ni uadui kwa Mwenyezi Mungu na Qur’ani na pia kwa Mtukufu Mtume 7 na watumishi wetu walio kwenye mavazi ya Hija kama ndio viongozi wa njama hizo. O  O  O Na wale waliohama katika njia ya Mwenyezi Mungu, na waliouawa, au waliokufa, Mwenyezi Mungu atawaruzuku ujira bora, na kwa hakika Mwenyezi Mungu Ndiye Mbora wa kuruzuku. Mheshimiwa Hajj Sheikh Mahdi Kurrubi uenezaji wake uwe mrefu zaidi: Nimesikia ujumbe wako wenye uhifadhi na ule wa mahujaji wapendwa kuliko nafsi zetu, kutoka upande wa Ka’aba iliyofanyiwa ubaya na eneo takatifu la Mwenyezi Mungu lililopakazwa damu. Fikisha salamu zangu za ukweli na zile za taifa la Iran kwa wapendwa 130

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 130

11/3/2015 2:57:53 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

wote ambao katika ujirani na Nyumba ya Mwenyezi Mungu na hifadhi yake waliudhishwa kifidhuli na mawakala wa kukodishwa wa Marekani shetani mkuu, na mhalifu mkubwa. Tukio hili baya halikujeruhi taifa la Iran tu peke yake, bali kwa hakika limejeruhi wapenda uhuru wote na mataifa ya Kiislamu ya ulimwengu mzima. Lakini kwa watu mashujaa na mahodari kama Wairani, ambao kama taifa, wamepita katika miaka mingi ya uzoefu wa kimapinduzi na wametupilia mbali barakoa la kidanganyifu la wasaidizi wa Marekani kama vile Shah na Saddam ambaye alifanya shambulizi kwa waombolezaji wa Imam Husein A na kuchoma misikiti, maovu kama hayo sio yasiyowahi kutokea ama kutotarajiwa. Hivyo kwa mara nyingine tena, mikono michafu ya Marekani na Israili ilichomoza kutoka kwenye mikono ya mavazi ya wakuu wa unafiki wa Arabia na wasaliti wa Haram mbili hizo na wakalenga katika nyoyo za Waislamu wapendwa mno na wageni wa Mwenyezi Mungu na wadai wa “SIQAYATUL-HAJJ WAIMARATUL MASJIDILHARAM” yaani kuwanywesha mahujaji na kuimarisha maadili ya Msikiti Mtukufu, na wakamwaga damu ya Waislamu katika mitaa ya mji wa Makka. Wakati tukiwa na huzuni sana na maombolezo kwa ajili ya tukio hili lisilo na kifani la mauwaji ya halaiki ya Waislamu na wafuasi wa Ibrahim Hanifa, na weledi wa Qur’ani, tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwamba maadui zetu na wapinzani wetu wa kisiasa ni miongoni mwa wapumbavu na wajinga, kwa sababu hawakuweza kutabiri au kuona yajayo mbele ya jinsi vitendo vyao vya kiupofu vilivyotuimarisha sisi na kutangaza mapinduzi yetu, na kudhihirisha jinsi taifa letu lisivyokuwa na hatia na lilivyodhulumiwa, katika namna isiyo na mfano kwa mamia ya njia za uenezaji au maelfu ya ulamaa na mubalighina waliotumwa kwenye sehemu za mbali kabisa za ulimwengu kwenda kuonyesha tofauti kati ya serikali za 131

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 131

11/3/2015 2:57:53 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

haki na zile za kidhalimu, kwa dhahiri na uwazi kabisa. Ni kwa ubora gani ambao sisi tungeweza kufunua zile nyuso mbaya za watumishi wa Marekani na kuthibitisha kwamba hakuna tofauti kati ya Muhammad Reza Shah na Saddam na viongozi wakuu wa serikali ya Kiarabu isiyopenda mabadiliko, katika kupigana dhidi ya Uislamu na Qur’ani, na kwamba wote ni watumishi wa Marekani na walioteuliwa kuvunja misikiti na sehemu zinazofaa kuswalia, na kuzima miale ya vilio vya haki vya mataifa? Ni kwa vizuri kiasi gani sisi tungeweza kuuthibitishia ulimwengu wote kwamba wale ambao kwa sasa wameaminishwa kushika funguo za al-Ka’aba hawafai kuwa wenyeji wa waja na wageni wa Mwenyezi Mungu, na kwamba hawawezi kufanya chochote isipokuwa kuhakikisha maslahi ya Marekani na Israili, na kuwatunukia wao maslahi ya nchi yao wenyewe? Kama tungetaka kuudhihirishia ulimwengu kwamba serikali ya Ukoo wa Kifalme wa Saud, wale mawahabi wasio na Mungu ni kama kisu ambacho siku zote kimekuwa kikipenya kwenye nyoyo za Waislamu kutoka migongoni mwao, tusingeweza kufanya hivyo kwa uzuri hasa kama wale maafisa wakuu wa Saudia wanyonge na waliodhaifika walivyofanya hilo kikatili kabisa na kwa nguvu zote, na kwa hakika wao ndio warithi wa Abu Sufyan na Abu Lahab, na wao kama wafuasi wa “Yazid” wao wanayashinda mahalifu yake. Alhamdulillah, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetengeneza marafiki wengi wakweli na waaminifu na waungaji mkono kutoka makabila na mataifa mengi, ikiwa ni pamoja na wa Kiarabu, ambao wanashuhudia uadilifu wetu na wanatoa ushahidi juu ya mauaji ya umwagaji damu ya halaiki ya Waislamu yaliyofanywa na wale wanaoitwa eti ni watumishi wa Haram mbili (Haramain) na wanaweza kuyatangaza yale mambo machungu ya siku ile ya tukio kwa ulimwengu. Na baya zaidi kuliko yote, ni ule uungwaji mkono 132

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 132

11/3/2015 2:57:53 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

wa mara moja wa Saddam, Mfalme Huseini wa Jordan na Mfalme Hassan wa Morocco juu ya jinai za Ukoo wa Kifalme wa Saud, kana kwamba Arabia imepiga ngome kubwa sana na kupata ushindi mnono kwa kuwapiga risasi za bombom (machine-gun) maelfu ya watu wasio na hatia, wasio na ulinzi wala silaha za kujikinga nazo, na kukanyaga na kushetasheta miili yao mitukufu. Hivyo wanajipongeza wenyewe kwa wenyewe wakati ambapo dunia inaomboleza na Mtukufu Mtume 7 amevunjika moyo kwa huzuni. O  O  O Serikali ya Ukoo wa Kifalme wa Saud imechukua udhibiti wa mahujaji ambao unatupa sisi sote imani kwamba lile tukio la Makka haliko mbali ya sera kuu ya msingi ya waporaji wa kilimwengu ya kuwaangamiza Waislamu wapenda uhuru wa duniani kote. Mwenyezi Mungu kwa hakika ametimiza ahadi aliyoitoa kwa Mtume Wake kwa ukweli: “Utauingia Msikiti Mtukufu, kama Mwenyezi Mungu akipenda, kwa usalama kabisa.” Licha ya kupita mwaka tangu yale mauaji ya kuangamiza na ya kikatili ya Mahujaji wasio na ulinzi na mahujaji wachaji waumini juu ya Mungu Mmoja yaliyofanywa na watumishi wa Marekani, ule ukoo muovu mno wa Ukoo wa Kifalme wa Saud, mji wa Mwenyezi Mungu na viumbe wa Mwenyezi Mungu bado wamejawa na fadhaa. Ukoo wa Kifalme wa Saud, kwa kuwauwa wageni wa Mwenyezi Mungu na kumwaga damu ya waja wema wa Mwenyezi Mungu, sio tu wameitia doa sehemu hiyo takatifu, bali pia na ulimwengu mzima wa Kiislamu, kwa damu za mashahidi wafiadini na kuwaweka Waislamu na watu walio huru katika maombolezo. Mwaka uliopita, Waislamu duniani, kwa mara ya kwanza walisherehekea Eid al-Qurban (sikukuu ya kafara) kwa wafiadini 133

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 133

11/3/2015 2:57:53 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

wa watoto wa Ibrahim G– ambao walikuwa wamerejea kutoka kwenye makumi ya vita na wateka nyara wa dunia na wafuasi wao – kwenye madhabahu hizi za upendo na “Mina” ya ridhaa ya mbinguni. Mahali ambapo Marekani na Ukoo wa Kifalme wa Saud, kinyume na namna na desturi ya uungwana waliuwa idadi kubwa ya wanaume na wanawake miongoni mwa mababa na mama wa mashahidi na walemavu, na katika dakika za mwisho wakaichapa mijeledi ile miili ambayo ilikuwa nusu maiti, ya watu wazee na vinywa vyenye kiu vya wale waliokandamizwa, ili kulipiza kisasi juu yao! Lakini ni juu ya nani na kwa hatia gani? Kulipa kisasi juu ya watu ambao walikuwa wametoka majumbani kwao wenyewe kwenda kwenye Nyumba ya Mwenyezi Mungu na Nyumba ya watu! Kisasi kwa watu ambao walikuwa wamebeba shanta la hazina ya Mungu ya jitihada juu ya mabega yao! Kisasi kwa watu ambao, kwa mfano wa Ibrahim wamerejea kutoka kwenye uvunjaji masanamu! Wale ambao walikuwa wamemvunja Shah! ambao waliivunja Urusi na Marekani! na wakauponda upagani na unafiki! hao hao ambao baada ya kusafiri kupita kwenye njia ndefu, wamekuja vichwa wazi na miguu pekupeku kuja kutoa kilio chao: Ili kumfurahisha na kumridhisha Ibrahim   A wao wamekuja kwenye karamu ya Mwenyezi Mungu, ili kuosha vumbi lililomo nyusoni mwao kwa maji ya Zamzam na kuzima kiu chao kwa ibada angavu za Hija ili kupata nguvu mpya kwa ajili ya wajibu na majukumu mengine na katika kuendelea mbele kwa daima, sio tu kwenye ‘Miqaat’ ya Hija bali pia katika ‘Miqaat’ ya vitendo vyao, na kujivua wenyewe na mapazia ya kujifungamanisha na dunia. Wao hao, ambao ili kuwaokoa wale walionyimwa na waja wa Mwenyezi Mungu, walijikatalia wenyewe kuwa watafuta anasa za dunia, wakajivisha wenyewe vazi la ufiadini (shahada) na wakaamua kwa akili zao kutokuwa watumwa wa Marekani na Urusi, wala kukubali 134

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 134

11/3/2015 2:57:53 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

utumwa wa yeyote yule isipokuwa Mwenyezi Mungu. Wamekuja kumwambia Mtukufu Mtume 7 kwamba wao hawajachoka kujitahidi na kwamba wanajua vizuri kwamba Abu Lahab na Abu Jahl wanawavizia kwa ajili ya kulipa kisasi. Wanashangaa na hawajui kama Lata na Hubal bado wako ndani ya Ka’aba? Ndio, kuna maadui wabaya zaidi kuliko masanamu hayo, lakini wakiwa kwenye kisingizio na udanganyifu na hila mpya. Wao wanajua kwamba leo hii Haram hiyo sio mahali kwa ajili ya watu, bali kwa ajili ya Marekani, na yeyote ambaye hatasema “Labbayka” kwa Marekani bali akasonga mbele kuelekea kwa Mwenyezi Mungu huyo anastahili kufanyiwa kisasi. Wanalipiza kisasi kwa mahujaji ambao kuwepo kwao kote na harakati za kimapinduzi zinahuisha ibada za Ibrahim A na kwa hakika watakwenda kunukisha angahewa la nchi yao na maisha yao kwa manukato ya sauti changamfu ya “Labbayka Allahuma-Labbayk.” Ndiyo, katika mantiki ya kilimwengu ya upagani, yeyote yule anayejaribu kuonyesha kukerwa na kuwachukia wapagani, huwa anashutumiwa kama mwabudu masanamu, na “Ma-Mufti” wao watamhukumu kifo. Hata hivyo, panga zilezile za ukafiri na unafiki ambazo zilikuwa zimefichwa chini ya mavazi ya udanganyifu ya Hija ya watu wa Yazid na wale waliokodiwa na Bani Umayyah – laana ya Mwenyezi Mungu iwe juu yao – kuja kuuwa watoto watukufu kabisa wa Mtukufu Mtume 7, yaani Imam Husein A na wafuasi wake waaminifu, lazima sasa zitoke tena kuja kukata makoo safi na yaliyotakaswa ya wafuasi wa Imam Husein A katika majira ya joto ya Karbala ya Hijaz katika madhabahu ya Haram, na kuwashutumu watoto halisi wa Uislamu na wakawatafsiri vibaya kama ndumilakuwili, wakana mungu, watu wa mataifa, na ambao damu yao inaweza kumwagwa tu. Tunataraji, Insha’allah, kwamba tutakuja kuchukua kisasi dhidi yao 135

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 135

11/3/2015 2:57:53 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

katika muda ujao na kuacha kwenye nyoyo zao kovu la ukoseshwaji, kutoka kwenye utamu wa uhalifu huu mkubwa na mbaya, na kisha tutaingia kwenye Msikiti Mtukufu baada ya kusherehekea ushindi wa haki na uadilifu juu ya kufuru na ukafiri, na kuikomboa al-Ka’aba kutoka kwenye mikono ya watu wasiojimudu na wasioaminika. O  O  O Na kwa mahujaji kutoka nchi nyinginezo, ambao kwa hakika wamehiji chini ya udhibiti na vitisho vya serikali zao, hawatawaona tena marafiki zao, ndugu zao, waungaji mkono wao na wapiganaji wenza. Ukoo wa Kifalme wa Saud, ili kufunika maovu yao mabaya ya mwaka uliopita, na kuhalalisha kosa lao la “kuweka kipingamizi kwenye njia ya Mwenyezi Mungu” kwa kuwazuia mahujaji wa Iran kuingia Hija, watawashambulia mahujaji kwa propaganda zao endelevu, na ulamaa wao na Mamufti wa kukodiwa katika nchi za Kiislamu, hasa huko Hijaz, watafanya visingizio na hotuba za uongo wakitumia vyombo vya mawasiliano ya habari, kwa jitihada ya kuwabana mahujaji na kuwaondolea uwezo wa kufikiri na kujifunza falsafa ya Hija na kuhoji kuhusu misimamo iliyopangwa kabla ya shetani mkuu katika kuuwa wageni wa Mwenyezi Mungu. Na wajibu na majukumu ya mahujaji katika mazingira kama haya kwa kweli ni mazito mno. Maumivu makubwa ya jumuiya za Kiislamu ni kwamba wao bado hawajatambua ile falsafa halisi ya maagizo mengi ya Mwenyezi Mungu, na Hija, pamoja na siri zake zote, na utukufu wake, imebakia bado kama ibada ya bandia na harakati isiyo na matunda.

136

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 136

11/3/2015 2:57:53 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

Orodha Ya Vitabu Vilivyo Chapishwa Na Al-Itrah Foundation 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24. 25. 26. 27. 28. 29. 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38.

Qur’an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu Ya Kwanza Mpaka Thelathini Uharamisho Wa Riba Uharamisho Wa Uwongo Juzuu Ya Kwanza Uharamisho Wa Uwongo Juzuu Ya Pili Hekaya Za Bahlul Muhanga Wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo Iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab Vazi Bora Ukweli Wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu Imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini Katika Swala Misingi Ya Maarifa Kanuni Za Ndoa Na Maadili Ya Familia Bilal Wa Afrika Abudharr Usahihi Wa Historia Ya Uislamu Na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur’an Na Hadithi Elimu Ya Nafsi Yajue Madhehebu Ya Shia Ukusanyaji Na Uhifadhi Wa Qur’an Tukufu Al-Wahda Ponyo Kutoka Katika Qur’an Uislamu Mfumo Kamili Wa Maisha Ya Kijamii Mashukio Ya Akhera Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu Kwa Mujibu Wa Kitabu Na Sunna. Haki Za Wanawake Katika Uislamu Mwenyezi Mungu Na Sifa Zake Kumswalia Mtume (S) Nafasi Za Ahlul Bayt (A.S) Adhana 137

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 137

11/3/2015 2:57:53 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

39. 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52. 53. 54. 55. 56. 57. 58. 59. 60. 61. 62. 63. 64. 65. 66. 67. 68. 69. 70. 71. 72. 73. 74. 75. 76. 77. 78. 79. 80.

Upendo Katika Ukristo Na Uislamu Tiba Ya Maradhi Ya Kimaadili Maana Ya Laana Na Kutukana Katika Qur’ani Tukufu Kupaka Juu Ya Khofu Kukusanya Swala Mbili Bismillah Ni Sehemu Ya Qur’ani Na Husomwa Kwa Jahara Kuwaongoza Vijana Wa Kizazi Kipya Kusujudu Juu Ya Udongo Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (S) Tarawehe Malumbano Baina Ya Sunni Na Shia Kupunguza Swala Safarini Kufungua Safarini Umaasumu Wa Manabii Qur’an Inatoa Changamoto As-Salaatu Khayrun Mina -’N Nawm Uadilifu Wa Masahaba Dua E Kumayl Sauti Ya Uadilifu Wa Binadamu Umaasumu Wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake Umaasumu Wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata Umaasumu Wa Mitume - Umaasumu Wa Mtume Muhammad (S) Nahju’l-Balaghah - Juzuu Ya Kwanza Nahju’l-Balaghah - Juzuu Ya Pili Kuzuru Makaburi Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu Ya Kwanza Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu Ya Pili Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu Ya Tatu Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu Ya Nne Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu Ya Tano Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu Ya Sita Tujifunze Misingi Ya Dini Sala Ni Nguzo Ya Dini Mikesha Ya Peshawar Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu Ubora Wa Imam ‘Ali Juu Ya Maswahaba Na Ushia Ndio Njia Iliyonyooka Hukumu Za Kifikihi Zinazowahusu Wanawake Liqaa-U-Llaah Muhammad (S) Mtume Wa Allah Amani Na Jihadi Katika Uislamu Uislamu Ulienea Vipi? Uadilifu, Amani Na Mtume Muhammad (S) 138

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 138

11/3/2015 2:57:53 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

81. Mitala Na Ndoa Za Mtume Muhammad (S) 82. Urejeo (Al-Raja’a ) 83. Mazingira 84. Utokezo (Al - Badau) 85. Hukumu Ya Kujenga Juu Ya Makaburi 86. Swala Ya Maiti Na Kumlilia Maiti 87. Uislamu Na Uwingi Wa Dini 88. Mtoto Mwema 89. Adabu Za Sokoni 90. Johari Za Hekima Kwa Vijana 91. Maalimul Madrasatain Sehemu Ya Kwanza 92. Maalimul Madrasatain Sehemu Ya Pili 93. Maalimul Madrasatain Sehemu Ya Tatu 94. Tawasali 95. Imam Mahdi Katika Usunni Na Ushia 96. Hukumu Za Mgonjwa 97. Sadaka Yenye Kuendelea 98. Msahafu Wa Imam Ali 99. Ngano Ya Kwamba Qur’ani Imebadilishwa 100. Idil Ghadiri 101. Kusoma Sura Zenye Sijda Ya Wajibu 102. Hukumu Zinazomuhusu Mkuu Wa Kazi Na Mfanyakazi 103. Huduma ya Afya katika Uislamu 104. Sunan an-Nabii 105. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) 106. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) 107. Shahiid Mfiadini 108. Kumsalia Nabii (s.a.w) 109. Ujumbe -Sehemu ya Kwanza 110. Ujumbe - Sehemu ya Pili 111. Ujumbe - Sehemu ya Tatu 112. Ujumbe - Sehemu ya Nne 113. Mariamu, yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu 114. Hadithi ya Thaqalain 115. Ndoa ya Mutaa 116. Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza 117. Ukweli uliopotea sehemu ya Pili 118. Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu 119. Ukweli uliopotea sehemu ya Nne 120. Ukweli uliopotea sehemu ya Tano 121. Mkutano wa Maulamaa wa Baghdad 122. Safari ya kuifuata Nuru 139

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 139

11/3/2015 2:57:53 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

123. Fatima al-Zahra 124. Myahudi wa Kimataifa 125. Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi 126. Visa vya kweli sehemu ya Kwanza 127. Visa vya kweli sehemu ya Pili 128. Elimu ya Ghaibu ya Maimamu 129. Mwanadamu na Mustakabali wake 130. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) 131. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) 132. Khairul Bariyyah 133. Uislamu na mafunzo ya kimalezi 134. Vijana ni Hazina ya Uislamu 135. yafaayo kijamii 136. Tabaruku 137. Taqiyya 138. Vikao vya furaha 139. Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 140. Visa vya wachamungu 141. Falsafa ya Dini 142. Azadari-Kuhuzunika na Kuomboleza 143. Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah 144. Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu 145. Kuonekana kwa Allah 146. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) 147. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) 148. Ndugu na Jirani 149. Ushia ndani ya Usunni 150. Maswali na Majibu 151. Mafunzo ya hukumu za ibada 152. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1 153. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2 154. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 155. Abu Huraira 156. Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. 157. Mazingatio kutoka katika Qur’an - Sehemu ya Kwanza 158. Mazingatio kutoka kaitka Qur’an - Sehemu ya Pili 159. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza 160. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili 161. Qur’ani Tukufu – Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili 162. Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) 163. Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani 164. Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu 140

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 140

11/3/2015 2:57:53 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

165. Uislamu Safi 166. Majlisi za Imam Husein Majumbani 167. Je, Kufunga Mikono 168. Uislam wa Shia 169. Amali za Makka 170. Amali za Madina 171. Asili ya Madhehebu katika Uislamu 172. Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi 173. Ukweli uliofichika katika neno la Allah 174. Uislamu na Mifumo ya Uchumi 175. Umoja wa Kiislamu na Furaha 176. Mas’ala ya Kifiqhi 177. Jifunze kusoma Qur’ani 178. As-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah 179. Hayya ‘Alaa Khayri’l-’Amal Katika Adhana 180. Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura 181. Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na Ramadhani) 182. Uadilifu katika Uislamu 183. Mahdi katika Sunna 184. Maswali ya Uchunguzi Kuhusu Uislam 185. Kazi na Bidii ni njia ya maendeleo 186. Abu Talib – Jabali Imara la Imani 187. Ujenzi na Utakaso wa Nafsi 188. Vijana na Matarajio ya Baadaye 189. Usalafi – Historia yake, maana yake na lengo lake 190. Ushia – Hoja na Majibu 191. Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) 192. Maombolezo – Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) 193. Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu 194. Takwa 195. Upotoshaji dhahiri katika Turathi (Hazina) ya Kiislamu 196. Amirul Muuminina (‘as) na Makhalifa 197. Uongozi na Utawala katika Mwenendo wa Imam ‘Ali (‘a) 198. Kuvunja hoja iliyotumika kutetea Uimamu wa AbuBakr 199. Adabu za vikao na mazungumzo 200. Hija ya Kuaga 201. Uwazi baina ya Maslahi na Vikwazo 202. Fadhila za watukufu watano katika Sahih Sita 203. Mdahalo baina ya Mwanachuoni wa Kisunni na Mwanachuoni wa Kishia (Al-Muraja’aat) 204. Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (as) 205. Mjadala wa Kiitikadi 141

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 141

11/3/2015 2:57:53 PM


HIJA KATIKA USEMI NA UJUMBE WA IMAM KHOMEINI

206. Mtazamo kuhusu msuguano wa Kimadhehebu 207. Nchi na Uraia – Haki na wajibu kwa Taifa 208. Mtazamo wa Ibn Taymiyyah juu ya Imam Ali (as) 209. Uongozi wa Kidini – Maelekezo na Utekelezaji wa Kijamii 210. Maadili ya Ashura 211. Mshumaa – Shahidi na Kifo cha Kishahidi 212. Mizani ya Hekima – Hadithi za Ahlul Bait (as) – Sehemu ya Kwanza 213. Imam Ali na Mambo ya Umma 214. Imam Ali na Mfumo wa Usawa 215. Mwanamke na Sharia 216. Mfumo wa Wilaya 217. Vipi Tutaishinda Hofu? 218. Kumswalia Mtume ni Ufunguo wa Utatuzi wa Matatizo 219. Mahali na Mali za Umma 220. Nahjul-Balagha – Majmua ya Khutba, Amri, Barua, Risala, Mawaidha na Semi za Amirul-Muuminin Ali bin Abu Talib (a.s.) 221. Mukhtar – Shujaa aliyelipiza kisasi dhidi ya wauaji wa Imam Husein (as) hapo Karbala 222. Uimamu na Tamko la Kutawazwa 223. Imam Husain ni Mfumo wa Marekebisho na Mageuzi 224. Saada Kamili – Kitabu cha Kiada cha Maadili 225. Maeneo ya Umma na Mali Zake 226. Imam Hasan na Mfumo wa Kujenga Jamii 227. Adhana ni Ndoto au ni Wahyi? Kopi Nne Zifuatazo Zimetafsiriwa Kwa Lugha ­Kinyarwanda 1. 2. 3. 4.

Amateka Na Aba’Khalifa Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya Shiya na Hadithi Orodha Ya Vitabu Vilivyo Chapishwa Na AL-Itrah ­Foundation Kwa Lugha Ya Kifaransa

1.

Livre Islamique

142

12_15_HAJJ KATIKA MANENO_3_Nov_2015.indd 142

11/3/2015 2:57:54 PM


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.