Historia na Sira za Viongozi Waongofu Sehemu ya Pili
Imamu Hasan bin ‘Ali bin Abi Talib (‘a) Imamu Husain bin ‘Ali bin Abi Talib (‘a) Imamu ‘Ali bin Husain as-Sajjad (‘a)
Kimeandikwa na: Jopo la Waandishi wa Vitabu vya Kiada
Kimetarjumiwa na: Hemedi Lubumba Selemani
Kimehaririwa na:: Ustadh Abdalla Mohamed
ﺗﺮﺟﻤﺔ ﺗﺮﺟﻤﺔ ﺗﺮﺟﻤﺔ ﺗﺮﺟﻤﺔ ﺗﺮﺟﻤﺔ ﺗﺎرﻳﺦ وﺳﻴﺮة اﻟﻘﺎدة اﻟﻬﺪاة ﺗﺎرﻳﺦ وﺳﻴﺮة اﻟﻘﺎدة اﻟﻬﺪاة اﻟﻘﺎدةاﻟﻬﺪاة وﺳﻴﺮةاﻟﻘﺎدة ﺗﺎرﻳﺦوﺳﻴﺮة ﺗﺎرﻳﺦ اﻟﻬﺪاة اﻟﻬﺪاة اﻟﻘﺎدة وﺳﻴﺮة ﺗﺎرﻳﺦ ﺗﺄﻟﻴﻒ ﺗﺄﻟﻴﻒ ﺗﺄﻟﻴﻒ ﺗﺄﻟﻴﻒ ﺗﺄﻟﻴﻒ ﻟﺠﻨﺔ ﺗﺄﻟﻴﻒ اﻟﻜﺘﺐ اﻟﺪراﺳﻴﺔ ﻟﺠﻨﺔ ﺗﺄﻟﻴﻒ اﻟﻜﺘﺐ اﻟﺪراﺳﻴﺔ اﻟﺪراﺳﻴﺔ اﻟﻜﺘﺐ ﺗﺄﻟﻴﻒ ﻟﺠﻨﺔ اﻟﺪراﺳﻴﺔ اﻟﻜﺘﺐاﻟﺪراﺳﻴﺔ ﺗﺄﻟﻴﻒاﻟﻜﺘﺐ ﻟﺠﻨﺔﺗﺄﻟﻴﻒ ﻟﺠﻨﺔ ﻡﻦ اﻟﻠﻐﺔ اﻟﻌﺮﺑﻴﺔ اﻟﻰ اﻟﻠﻐﺔ اﻟﺴﻮا ﺣﻠﻴﺔ ﻡﻦ اﻟﻠﻐﺔ اﻟﻌﺮﺑﻴﺔ اﻟﻰ اﻟﻠﻐﺔ اﻟﺴﻮا ﺣﻠﻴﺔ ﺣﻠﻴﺔ اﻟﺴﻮا اﻟﻠﻐﺔ اﻟﻰ اﻟﻌﺮﺑﻴﺔ اﻟﻠﻐﺔ ﻡﻦ ﺣﻠﻴﺔ اﻟﺴﻮا اﻟﻠﻐﺔ اﻟﻰ اﻟﻌﺮﺑﻴﺔ اﻟﻠﻐﺔ ﻡﻦ ﻡﻦ اﻟﻠﻐﺔ اﻟﻌﺮﺑﻴﺔ اﻟﻰ اﻟﻠﻐﺔ اﻟﺴﻮا ﺣﻠﻴﺔ 2 2
©Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION
ISBN: 978 - 9987 –512 – 51 – 5
Kimeandikwa na: Jopo la Waandishi wa Vitabu vya Kiada
Kimetarjumiwa na: Hemedi Lubumba Selemani
Kimehaririwa na: Ustadh Abdalla Mohamed
Kimepangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation
Toleo la kwanza: Machi, 2014 Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. - 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: www.alitrah.info
YALIYOMO Neno la Mchapishaji........................................................................................... 01 Utangulizi............................................................................................................ 02 Somo la ishirini.................................................................................................. 08 Imam Hasan Al-Mujtaba (a.s.) ....................................................................... 08 Nasaba yake ing’aayo......................................................................................... 08 Tarehe ya kuzaliwa kwake.................................................................................. 08 Maumbile yake.................................................................................................... 10 Vipindi vya maisha yake..................................................................................... 11 Makuzi yake........................................................................................................ 12 Muhtasari............................................................................................................ 13 Maswali............................................................................................................... 14 Somo la ishirini na moja................................................................................... 15 Mwonekano wa utu wa Imam Hasan Al-Mujtaba (a.s.)............................... 15 Imam mteule ndani ya Aya za Qur’ani tukufu.................................................... 15 Nafasi ya Imam Hasankwa Mtume wa mwisho (s.a.w.w.)................................. 18 Nafasi ya Imam kwa watu wa zama zake........................................................... 19 Muhtasari............................................................................................................ 20 Maswali............................................................................................................... 21 Nafasi ya Imam Hasan (a.s.) kwa wasomi na wanahistoria................................ 22 Somo la ishirini na mbili.................................................................................. 25 Sifa za Imam Hasan na mwonekano wake..................................................... 25 Ibada yake........................................................................................................... 25 Uvumilivu na msamaha wake............................................................................. 26 Ukarimu wake..................................................................................................... 27 Unyenyekevu na utawa wake.............................................................................. 28 Muhtasari............................................................................................................ 30 Maswali............................................................................................................... 31 Kwa ajili ya kujisomea........................................................................................ 31 Somo la ishirini na tatu.................................................................................... 35 Urithi wa Imam Hasan Al-Mujtaba (a.s.)....................................................... 35 v
Elimu na akili...................................................................................................... 35 Qur’ani Tukufu................................................................................................... 36 Hadithi za Mtume (s.a.w.w.)............................................................................... 37 Utawala wa Ahlul-Baiti (a.s.).............................................................................. 38 Muhtasari............................................................................................................ 39 Maswali............................................................................................................... 40 Kwa ajili ya kujisomea Mawaidha yenye hekima.............................................. 40 Miongoni mwa hekima zake za thamani............................................................ 42 Somo la ishirini na nne..................................................................................... 44 Bwana wa Mashahidi Imam Husein bin Ali (a.s.).......................................... 44 Nasaba yake ing’aayo......................................................................................... 44 Mazazi yaliyobarikiwa........................................................................................ 44 Tarehe ya kuzaliwa............................................................................................. 46 Maumbile yake.................................................................................................... 46 Lakabu na kuniya zake........................................................................................ 47 Nakshi ya pete zake............................................................................................ 48 Vipindi vya maisha yake..................................................................................... 48 Muhtasari............................................................................................................ 49 Maswali............................................................................................................... 49 Kwa ajili ya kujisomea........................................................................................ 50 Somo la ishirini na tano.................................................................................... 53 Fadhila za Imam Husein na mwonekano wake.............................................. 53 Nguvu ya maamuzi............................................................................................. 53 Kukataa udhalili.................................................................................................. 53 Ushujaa............................................................................................................... 54 Uwazi wa maneno............................................................................................... 55 Ushupavu katika haki.......................................................................................... 56 Subira.................................................................................................................. 56 Muhtasari............................................................................................................ 56 Maswali............................................................................................................... 58 Kwa ajili ya kujisomea........................................................................................ 59
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Fadhila za Husein (a.s.) na mwonekano wake.................................................... 59 Usamehevu.......................................................................................................... 59 Unyenyekevu...................................................................................................... 59 Huruma na upole................................................................................................. 60 Ukarimu.............................................................................................................. 60 Ibada zake na uchamungu wake......................................................................... 63 Khofu dhidi ya Mwenyezi Mungu...................................................................... 63 Wingi wa Swala na funga zake........................................................................... 63 Kuhiji Kwake...................................................................................................... 64 Sadaka zake......................................................................................................... 64 Kipaji cha elimu.................................................................................................. 64 Somo la ishirini na sita..................................................................................... 67 Urithi wa Imam Husein (a.s.)........................................................................... 67 Muhtasari............................................................................................................ 72 Maswali............................................................................................................... 72 Somo la ishirini na saba.................................................................................... 73 Imam Ali bin Husein (a.s.)................................................................................ 73 Nasaba ing’aayo.................................................................................................. 73 Kuzaliwa na kufariki kwake............................................................................... 73 Kuniya, lakabu na nakshi ya pete yake............................................................... 74 Vipindi vya maisha yake..................................................................................... 74 Mwonekano wa utu wa Imam Zaynul-Abidiin (a.s.).......................................... 76 Muhtasari............................................................................................................ 78 Maswali............................................................................................................... 79 Kwa ajili ya kujisomea........................................................................................ 79 Somo la ishirini na nane................................................................................... 81 Fadhila namwonekano wa Imam Zaynul-Abidiin (a.s.)................................ 81 Uvumilivu........................................................................................................... 81 Ukarimu wake..................................................................................................... 82 Huruma yake kwa mafakiri................................................................................. 83 Heshima yake na kukutaa udhalili...................................................................... 85 vii
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Utawa.................................................................................................................. 85 Ibada zake na kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu......................................... 86 Muhtasari............................................................................................................ 87 Maswali............................................................................................................... 87 Kwa ajili ya kujisomea........................................................................................ 88 Sadaka zake......................................................................................................... 88 Somo la ishirini na tisa..................................................................................... 92 Urithi wa Imam Zaynul-Abidiin (a.s.)............................................................ 92 Hekima zake........................................................................................................ 92 Dua yake katika kujikinga na ubaya, maadili mabaya na matendo maovu........ 94 Dua yake ya kutaka shauku ya kuwa mwenye kuomba maghfira kwa Mwenyezi Mungu....................................................................................... 95 Dua yake ya kuomba kimbilio kwa Mwenyezi Mungu...................................... 96 Dua yake kuomba mwisho mwema.................................................................... 97 Muhtasari............................................................................................................ 98 Maswali............................................................................................................... 98 Somo la thelathini............................................................................................. 99 Urithi wa Imam Zaynul-Abidiin (a.s.)............................................................ 99 Risala ya haki ya mtu kwa mtu........................................................................... 99 Muhtasari wa haki na viwango vyake............................................................... 101 Haki kwa ufafanuzi........................................................................................... 102 Muhtasari.......................................................................................................... 105 Maswali............................................................................................................. 106 Kwa ajili ya kujisomea...................................................................................... 106
viii
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
NENO LA MCHAPISHAJI
K
itabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kiitwacho Tarikh wa Sirati ‘l-Qadati ‘l-Hudaah. Sisi tumekiita, Historia na Sira ya Viongozi Waongofu. Kitabu hiki ni matokea ya kazi ya kielimu iliyofanywa na wanavyuoni wa Kiislamu waliomo kwenye Jopo la Waandishi wa Vitabu vya Kiada katika Taasisi ya Kimataifa ya Hawza na Madrasa. Kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili za watu. Kutokana na ukweli huu, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kuchapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili, ili kuongeza ujuzi wao katika masuala ya dini na ya kijamii. Tunamshukuru ndugu yetu, Hemedi Lubumba Selemani kwa kukubali kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Mchapishaji Al-Itrah Foundation.
1
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
UTANGULIZI
H
amna shaka kuwa historia ya mwanadamu ndio chemchemu na chanzo cha maarifa, chanzo ambacho mataifa yanakihitaji katika safari yake yenye kuendelea. Na ndicho chanzo pekee chenye uwezo wa kuhuisha na kulisukuma taifa mbele na kulipa sifa na hadhi maalumu huku kikilifunganisha taifa hilo na mizizi yake ya ustaarabu ambayo hulizuwia taifa dhidi ya mmong’onyoko. Qur’ani imemhimiza kila mwanadamu ikamtaka azame ndani ya historia ya mwanadamu na azingatie yaliyomo ili awaidhike na kuongoka, hivyo Mwenyezi Mungu akasema: “Je, hawatembei katika ardhi ili wapate nyoyo za kufahamia au masikio ya kusikia?”1 Baada ya Mwenyezi Mungu kutoa historia ya Aad, Thamud, Firaun, watu wa miji iliyopinduliwa na watu wa Nuh akasema: “Ili tuifanye ukumbusho kwenu na sikio lisikialo lisikie.”2 Historia ya ujumbe mbalimbali wa Mwenyezi Mungu imejaa masomo na mazingatio, masomo ambayo yameonyesha jinsi manabii watukufu walivyojali mataifa yao ili kuyaokoa toka kwenye matatizo mbalimbali. Pia ujumbe huo umeonyesha lengo na mwelekeo wake wenye kujaa nuru na manufaa. Kwa ajili hiyo sera ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kizazi chake huwa ni tafsiri ya kivitendo ya misingi na sheria za kiislamu. Hivyo, kusoma sera yao na historia ya maisha yao ni chanzo muhimu cha kuifahamu Qur’ani na Sunna, na ni chemchemu ya maarifa ya wanadamu wote, kwa sababu ni ujumbe wa Mwenyezi Mungu alioutuma kwa wanadamu huku Nabii wa mwisho na mawasii wake wateule wakiwa ni viongozi wa wanadamu wote bila kubagua. 1 2
Al-Haji: 46. Al-Haqah: 12. 2
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Tumeona ni vizuri tuweke silabasi kwa ajili ya kusoma historia ya kiislamu kwa kufuata hatua moja baada ya nyingine, kwani masomo ya historia ya nukuu hutangulia kabla ya masomo ya uchambuzi. Na kwa kuwa umma wote umekongamana juu ya wema na utakaso wa viongozi wa ujumbe wa Mwenyezi Mungu basi inafaa tuingize historia ya maisha yao ndani ya maisha ya wanafunzi, kwani Qur’ani imetamka wazi kuhusu umaasumu na utakaso wao ili wawe ni kiigizo chema kwa yule anayetarajia fadhila za Mwenyezi Mungu na malipo mema ya siku ya Kiyama. Lengo la silabasi ya kitabu hiki Kitabu Masomo ya utangulizi katika historia na sera ya viongozi wema kimetungwa ili kiwe hatua ya mwanzo ya kuelekea kwenye masomo mbalimbali ya lengo la kina zaidi, huku kikitegemea kufikia lengo hilo kwa kutumia wepesi wa ibara, usalama wa nukuu na vyanzo vyenye kukubalika ili kitowe picha ya wazi isiyokuwa na utata, shaka au hisia ambazo huenda zikamchanganya msomaji wa sera na historia mwanzoni tu mwa safari yake hii. Masomo haya sitini yataanza kuzungumzia historia na sira kwa mtazamo wa Qur’ani, kisha yatatoa maisha binafsi na ya kijamii ya kila mmoja kati ya maasumina kumi na wanne (a.s.), na mwisho yataishia kwenye uwanja kati ya viwanja vya urithi wao wenye kunukia manukato. Mwisho kabisa tutatoa faida ya maisha yao ya ujumbe huku tukionyesha mavuno ambayo yamepatikana ndani ya karne tatu bali ni zaidi ya karne kumi na nne za mapambano yenye kuendelea kwa ajili ya kuuokoa umma wa kiislamu na jamii ya wanadamu toka kwenye yale yaliyowapata na waliyonasa ndani yake. Na ili yawe maandalizi mema yenye kuenea na mapinduzi ya kiulimwengu ambayo yanamsubiri kiongozi wake wa kiroho, Imamu 3
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
angojewaye Al-Mahdi (a.s.) ambaye Mwenyezi Mungu aliwaahidi watu wa mataifa yote, ili aje kuunganisha nguvu na kuzifanya vizuri hali zao huku akiwaokoa wanadamu toka kwenye upotevu na kutimiza matarajio ya manabii na akitimiza wema wa ubinadamu, wema ambao bado binadamu anaendelea kuutolea juhudi zake usiku na mchana. Hivyo mafunzo ya historia yamegawanywa katika sera binafsi na sera ya kijamii, huku yakiwa hayana uchambuzi wa matukio ya kihistoria wala kuzama sana ndani ya matukio makuu ya kihistoria, hiyo ni ili baadae yafuatiwe na masomo mapana zaidi kuliko mafunzo haya. Pia tumejiepusha na urudiaji huku tukikomea kwenye historia ya ujumbe wenyewe na yale yaliyopita katika mzunguko na vipindi vya ujumbe na kwenye matokeo yaliyopatikana ndani ya karne zilizopita ambazo ziliupitia Uislamu na Waislamu. Mada hizi zimetimia kwa kufuata uchambuzi wa kielimu dhidi ya matukio yaliyosajiliwa ndani ya vitabu vya historia au yaliyogunduliwa na watafiti. Katika hali zote mbili tumejaribu kutegemea juhudi za wale waliotutangulia, ambazo ni masomo ya waandishi na watafiti ili kupata matunda ya juhudi zao na kuunganisha kati ya watu wa zamani na kizazi cha sasa. Pia ili tuwafunze vijana dharura ya kurejea kwenye rejea za kutegemewa za zamani na za sasa bila kudhulumu haki za waliyotangulia bali ili zionekane juhudi zao na jinsi walivyochangia katika uwanja wa elimu na maarifa ya jamii, na ili kuijua nafasi waliyonayo katika kunukuu urithi na kuvipelekea vizazi vijavyo. Waandishi wa zama hizi tutakaowataja ni Sheikh Baqir Sharif Al-Qarashiy, Sayyid Murtaza Al-Askariy, marehemu Sheikh Asad Haydar, mashahidi wawili: Sayyid Muhammad Baqir Sadr na Sayyid Muhamad Baqir Al-Hakim. Kisha Sayyid Jafar Murtaza Al-Amiliy, Sheikh Muhamad Had Al-Yusufiy Al-Gharawiy na wengine ambao 4
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
tumegusia vitabu vyao mwishoni mwa kila mada ambayo tumenukuu toka kwao. Ni wajibu wetu kusema: Kitabu hiki ni mjumuisho wa mada mbalimbali na utunzi unaolenga mafunzo ambayo yamezagaa ndani ya vitabu maalumu vilivyoteuliwa kufundisha sera ya kizazi cha Mtume (s.a.w.w.) ili iwe ni mali kwa mtafiti, mwanafunzi, mhutubu, mhubiri, mlezi na mlelewa ili ajiandae na masomo ya juu zaidi katika historia ya Uislamu kwa ajili ya kupambana mapambano ya kielimu dhidi ya matukio ya kihistoria na kijamii, na ili tuzame ndani huku tukipata mafunzo toka humo ili yawe ni mazingatio kwa msomaji na mawaidha kwa mwenye mazingatio inshaallah. Kutokana na maelezo yaliyopita kwa muhtasari tunatoa matokeo yafuatayo: Kwanza: Katika hatua hii mwalimu anapofundisha historia asitegemee kukutana na mafunzo ya kihistoria yenye mtiririko wa kuungana na kufuatana kwa maana iliyozoeleka. Kwa kuanzia jografia na historia ya Bara la Uarabu, kisha utume wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na dola yake, kisha dola ya makhalifa ambao walitawala kwa utaratibu maalumu. Hiyo ni kwa sababu sisi hatukusudii isipokuwa kusoma sera ya viongozi wema maasumina ambao ni lazima kuwaiga ili mwanafunzi afuate nyayo zao, awafuate na kuongoka kwa uongozi wao na sera yao katika maisha yake binafsi na ya kijamii. Pili: Mwanafunzi anaweza kupata mafunzo muhimu ya kihistoria kupitia njia ya kutoa hatua za maisha ya kila mmoja kati ya maasumina kumi na nne kwa kiwango kinachonasibiana na hatua ya mwanzo ya utangulizi ambayo imeishia kugusia nafasi na sehemu ya kizazi cha Mtume katika historia na harakati za Uislamu, kwa kuanzia nafasi yao maalumu ya kipekee aliyowapa Mwenyezi Mungu na 5
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
kumalizia hali halisi ya kihistoria ambayo imetoa harakati zao na mwenendo wao muda wa karne tatu na zaidi. Tatu: Kwanza hakika mafunzo ya historia ya Bara la Uarabu hayaingii yote katika historia ya Uislamu ispokuwa huwa kama utangulizi tu. Pili hutumiwa katika sehemu ya uchambuzi, jambo ambalo hatulikusudii katika hatua hii ya masomo haya. Zaidi ya hapo ni kuwa maelezo ya kizazi cha Mtume (s.a.w.w.) kama vile kauli za Imam Ali (a.s.) toka kwa Mtume (s.a.w.w.) na maelezo ya Zahra (a.s.) ndani ya hotuba yake mashuhuri aliyoitoa baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.w.) yameelezea vizuri hali ya waarabu kabla ya Uislamu. Na pia imeunganisha kati ya yaliyopita na yaliyopo ambayo aliyatimiza Mtume (s.a.w.w.), na majukumu makubwa yaliyofuatia yaliyopo juu ya waislamu ambao walitolewa na Uislamu toka kwenye shimo la ujinga mpaka kwenye nuru ya mwanga wa Uislamu. Nne: Hakika anayemaliza kusoma kitabu hiki inampasa azalishe mafunzo ambayo yatampa njia ya kufikia malengo yanayokusudiwa katika kusoma historia ndani ya hatua zote mbili, na wala asitosheke na haya yaliyopo kwenye masomo ya hatua ya utangulizi. Hatutaki kurudia mafunzo mara juu juu au mara nyingine kwa upana na undani zaidi, kwa ajili hiyo tunategemea waheshimiwa walimu wetu watazingatia malengo ya masomo kabla ya kuhoji silabasi ya kitabu. Na watatilia maanani silabasi ya kitabu kabla ya kuzama ndani ya vipengele vidogo vidogo vya historia ambavyo tumeviteua kwa ajili ya hatua hii. Pia watazingatia kikomo cha wakati na dharura ya kupangilia mafunzo kulingana na ubora ambao ni lazima kuzingatiwa katika silabasi ya mafunzo. Na kwa kuwa hiki si kitabu cha ziada bali kimeandaliwa kama kitabu cha kiada basi walimu watafundisha kulingana na silabasi ya mafunzo iliyopangwa. 6
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Hatuna budi kusema kuwa kitabu hiki kilichapishwa mwanzo kwa jina la: “Dondoo za sera za viongozi wema.” Lakini baada ya kupitia upya mafunzo ya kitabu, kilibadilishwa jina na kuitwa: Masomo ya utangilizi katika historia na sera ya viongozi wema.” Mwisho tunatoa shukurani za dhati kwa ndugu zetu kamati ya elimu katika taasisi ya kimataifa inayosimamia vituo vya elimu na shule za kiislamu kwa msaada na juhudi walizozitoa. Pia tunatoa shukurani za dhati kwa mwandishi wa kitabu hiki Ustadh Sayyid Mundhir Al-Hakim (Heshima yake idumu). Tunamuomba Mwenyezi Mungu ampe uongofu na nguvu, hakika Yeye ndiye kiongozi bora na Mwenye kunusuru. Jopo la Kamati ya Waandishi wa Vitabu vya Kiada 1425 A.H.
7
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Somo la Ishirini Imam Hasan Al-Mujtaba (a.s.) Nasaba yake ing’aayo: Imam Hasan ni mjukuu wa Mtume (s.a.w.w.) na ni mjukuu wake mkubwa, ni mmoja wa mabwana wa vijana wa peponi, na ni mmoja kati ya wawili ambao kizazi cha Mtume (s.a.w.w.) kimetokana na wao tu. Na ni mmoja kati ya wanne ambao wameondolewa uchafu na wametakaswa kabisa, ni mmoja kwenye kati ya vizito viwili ambavyo Mtume (s.a.w.w.) aliamrisha kushikamana navyo. Pia yeye ni wa pili katika orodha ya Maimamu kumi na wawili ambao Mtume (s.a.w.w.) aliwaacha kwa umma wake baada yake. Baba yake ni Ali (a.s.) mbora wa mawasii, kiongozi wa waumini na mama yake ni mbora wa wanawake wote wa ulimwenguni Fatimah mtakasifu, aliyeipa dunia mgongo, hakika ni nasaba tukufu sana. Tarehe ya kuzaliwa kwake: Ulipofika wakati wa Az-Zahrau (a.s.) kujifungua ndani ya nusu ya mwezi wa Ramadhani mwaka wa tatu hijiriya, Mtume (s.a.w.w.) alimtuma Asmaa binti Umays na Ummu Ayman wakaenda kumsomea Aya Kursiyyi na kinga mbili (Sura An-Nas na Sura Al-Falaq). Furaha zilijaa moyo wa Mtume (s.a.w.w.) baada tu ya kutangazwa habari ya kujifungua kwake, hivyo akaharakisha kwenda nyumbani kwa binti yake ili kumpa hongera kwa kizazi chake kipya. - Akampongeza ndugu yake na mtoto wa ami yake Ali (a.s.). 8
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Akamwita Asmau: “Ewe Asmau niletee mwanangu.” Akamleta huku akiwa ndani ya kitambaa cha njano, Mtume (s.a.w.w.) akakitupa na kusema: “Hivi sikuwaambia kuwa msimuweke mtoto ndani ya kitambaa cha njano?” Hapo Mtume (s.a.w.w.) akasimama kisha akamkata kitovu na kumnywesha mate yake, akamkumbatia kifuani, akainua mikono yake na kumwombea dua kwa kusema: “Ewe Mola Wangu, hakika mimi namkinga kwako yeye na kizazi chake dhidi ya shetani aliyelaniwa……”.3 Kisha Mtume (s.a.w.w.) akamtekelezea sunna ya Uislamu juu ya mtoto mchanga hivyo akafanya yafuatayo: a. Akamwadhinia sikio la kulia na akakimu la kushoto,4 kwani kufanya hivyo ni kumkinga mtoto dhidi ya shetani aliyelaniwa.5 b. Mtume (s.a.w.w.) akamuuliza ndugu yake kuhusu jina alilopewa mtoto. Akajibu: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu siwezi kukutangulia.” Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Siwezi kumtangulia Mwenyezi Mungu. Hapo ukashuka wahyi ukamnong’oneza Mtume (s.a.w.w.) huku ukibeba jina toka kwa Mwenye haki, hivyo Jibril akasema: “Mpe jina Hasan.”6 c. Mjukuu wa Mtume (s.a.w.w.) akatimiza siku saba tangu azaliwe, hapo Mtume (s.a.w.w.) akaelekea nyumbani kwa Fatimah (a.s.) ili akamfanyie baadhi ya takrima na sherehe, ndipo Dairatul-Maarif cha Bustaniy, Juz. 7, Uk. 38. Musnad Ahmad, Juz. 6, Uk. 391. Sahih Tirmidhiy, Juz. 1, Uk. 286. 5 Hayatul-Imam Hasan bin Ali, Juz. 1, Uk. 61. 6 Tarikhul-Khamiis, Juz. 1, Uk. 470. Humo imepokewa kuwa Jibril mwenye dhamna na Wahyi aliteremka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kumwambia: “Hakika Mola wako anakusalimu na anakwambia kuwa: Ali kwako ni sawa na Harun kwa Musa lakini hakuna nabii baada yako, basi mpe mwanao huyu jina la mtoto wa Harun.” Hapo Mtume akamuuliza: “Ni lipi jina la mwana wa Harun ewe Jibril?” Akasema: “Shubbar.” Mtume (s.a.w.w.) akasema: Lugha yangu ni kiarabu.” Akamwambia: “Mwite Hasan.” Ndipo Mtume akafanya hivyo. 3 4
9
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
akamjia na kilicho bora na kizuri zaidi kuliko vyote alivyo navyo kulingana na hali yake, akamfanyia akika kwa kumchinjia kondoo mmoja, hivyo akampa mkunga paja zima. Kuanzia hapo kitendo hicho kikawa sunna kwa umma wake baada ya Hasan.7 a. Akamnyoa kichwa chake na kumtolea sadaka kwa kutoa kiasi fulani cha madini ya fedha kwa masikini,8 kisha akapaka manukato kichwani kwa mtoto.9 b. Siku ya saba akamtahiri,10 hakika kumtahiri mtoto ndani ya wakati huo ni safi na tohara zaidi.11 c. Mtume (s.a.w.w.) akampa kuniya, akamwita: Abu Muhammad.12 Wala hana kuniya nyingine zaidi ya hiyo. d. Akapewa lakabu kwa kuitwa: Sibtu, Zakiyyu, Mujtaba, Sayyid na Taqiyyu. Maumbile yake: Sifa zake za kimaumbile zilikuwa zikionyesha maumbile ya Mtume (s.a.w.w.w). Anas bin Malik amesimulia kwa kusema: “Hakuna mtu arikhul-Khamiis, Juz. 1, Uk. 470. Hilyatul-Awliyai, Juz. 7, Uk. 116. Mushkilul-Athar, T Juz. 1, Uk. 456. 8 Tarikhul-Khamiis, Juz. 1, Uk. 470. Nurul-Absar, Uk.107. Sahih Tirmidhiy, Juz. 1, Uk. 286. 9 Biharul-An’war, Juz. 10 Uk. 68. 10 Nurul-Absar, Uk.108. 11 Jawahirul-Kalam, kitabu cha ndoa. Humo amepokea kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Wafanyieni tohara wanenu wa kiume siku ya saba, kwani kufanya hivyo ni usafi mno na utohara zaidi na kunaharakisha kuotesha nyama na hakika ardhi hunajisika siku arubaini kwa mkojo wa mwenye govi.” 12 Usudul-Ghaba, Juz. 2, Uk. 9. 7
10
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
aliyeshabihiana sana na Mtume (s.a.w.w.w) kama Hasan bin Ali (a.s.).”13 Alikuwa anafanana na babu yake kwa sura na kimaumbile hivyo alifanana naye katika maadili bora ya hali ya juu ambayo yalimtofautisha na manabii wengine.14 Wapokezi wa hadithi wameungana kuwa Hasan bin Ali (a.s.) alirithi maadili bora mazuri ya babu yake. Haikupokewa kuwa alilipa ubaya kwa ubaya au dhambi kwa dhambi, isipokuwa alikuwa akiwakirimu maadili yake bora huku akiwastarehesha kwa wema wake na uzuri wake. Vipindi vya maisha yake: Imam Hasan aliishi miaka arubaini na saba. Aliishi na babu yake zaidi ya miaka saba, akaishi na baba yake baada ya babu yake miongo mitatu, akaishi mwongo mmoja baada ya baba yake, hivyo tunaweza kugawa vipindi vya maisha yake kama ifuatavyo: a. Maisha yake chini ya kivuli cha babu yake kuanzia mwaka wa tatu mpaka wa kumi na moja hijiriya. adhailul-Asw’hab 166. Na ndani ya Sahih Tirmidhiy, Juz. 2, Uk. 307 imepokewa kuF toka kwa Ali (a.s.) kuwa: “Hasan ameshabihiyana sana na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) eneo la kati ya kifua na kichwa. Husein ameshabihiyana sana na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) eneo la chini ya hapo.” Ama ndani ya kitabu Al-Isabah imepokewa kutoka kwa Al-Bahayyu amesema: “Tulijiuliza ni nani anayeshabihiyana mno na Mtume kati ya ahli zake? Ndipo akaingia Abdullah bin Zubayr akasema: Mimi nitawaambia ni nani anayeshabihiyana naye sana na ampendaye sana, ni Hasan bin Ali.” Riwaya hiyo kaipokea pia Al-Haythamiy ndani ya kitabu chake Al-Majmau, Juz. 9, Uk. 175. 14 Tarikh Yaaqubiy, Juz. 2, Uk. 210. Imepokewa kutoka kwa Al-Ghazaliy ndani ya kitabu Ihyaul-Ulum kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu alimwambia Hasan: “Umechukua maumbile yangu na tabia zangu.” 13
11
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
b. Maisha yake chini ya kivuli cha uimamu wa baba yake kuanzia mwaka wa kumi na moja mpaka wa arubaini hijiriya. c. Maisha yake baada ya baba yake kuanzia mwaka wa arubaini mpaka mwaka wa hamsini hijiriya. Makuzi yake: i. Imam Hasan (a.s.) kakulia mikononi mwa babu yake, Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akala toka kwenye chemchemu ya utume wake maadili yake, adabu yake na heshima yake. Akawa chini ya kivuli cha malezi yake mpaka Mwenyezi Mungu alipomchagulia nyumba ya kudumu baada ya kuwa kishamrithisha maadili yake, heshima yake, haiba yake na uongofu wake. Tayari kishamwandaa kwa uimamu ambao ulikuwa ukimsubiri baada ya baba yake, hivyo babu yake alitamka wazi wazi katika minasaba mbalimbali kuhusu uimamu wake akasema: “Hasan na Husein ni maimamu, wakisimama au wakikaa, ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nawapenda, mpende atakayewapenda.�15 ii. Baada ya babu yake Imam akabakia chini ya malezi ya baba yake, mbora wa mawasii na mama yake Az-Zahrau mkweli mtakasifu, isipokuwa hakukaa sana ukawa umefunikwa ukurasa wa pili wa maisha yake kwa kuondokewa na mama yake Az-Zahrau (a.s.). iii. Wakati wa utawala wa Umar Imam akawa amefikia kipindi cha ujana, hivyo akaenda na baba yake kuwafundisha watu na kutatua matatizo yao. 15
Al-Manaqib cha Ibnu Shahru Ashuub, Juz. 3, Uk. 381-385. 12
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
iv. Wakati wa utawala wa Uthman Imam alisimama bega kwa bega na baba yake huku akiweka kikomo cha uharibifu ambao kipindi hicho ulikuwa umeenea ndani ya umma na dola ya kiislamu. v. Imam Hasan bin Ali (a.s.) alisimama bega kwa bega na baba yake katika kila alilosema na kulitenda. Akashirikiana naye katika vita vyote huku akitamani baba yake amruhusu kuendeleza mapambano na aingie vitani pindi vita vinapopamba moto. Lakini baba yake alikuwa mwangalifu juu yake na juu ya ndugu yake Husein akihofia kizazi cha Mtume (s.a.w.w.) kisikome kwa kuuawa wao wawili.16 Hasan (a.s.) alibaki bega kwa bega na baba yake mpaka sekunde ya mwisho huku yakimpata toka kwa Wairaki yale yaliyokuwa yakimpata baba yake, akiumia kama anavyoumia huku akimuona Muawiya ambaye ni mtumwa akieneza wanapropaganda wake, huku akiwarubuni viongozi wa jeshi la baba yake kwa mali na madaraka mpaka akafanikiwa kuwafarakisha wengi wao. Imam Ali bin Abu Twalib akawa akitamani afarikiane nao kwa kuuawa au kifo cha kawaida mpaka Imam alipokufa shahidi na Hasan akarithi uimamu na uwasii katika zama hizo na katika vitisho hivyo. Muhtasari: Hasan (a.s.) mjukuu ni tawi la mti wa unabii, mti ambao Mwenyezi Mungu aliupanda kwa rehema Zake, Mtume (s.a.w.w.) akaukuza kwa kuujali na kuutilia umuhimu. Alizaliwa mwanzoni mwa uasisi wa Uislamu huko Madina, tena ndani ya mapambano makali kati ya Uislamu na ukafiri, kwenye vita vya kuuhami Uislamu, vita ambavyo vilikuwa vikiongozwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). 16
Hayatul-Imam Hasan bin Ali, Juz. 1, Uk. 497 13
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Mtume (s.a.w.w.) alifika kilele cha mwisho katika kumjali mjukuu wake, hivyo akamtekelezea sunna ya kuzaliwa ambayo ikawa ni sunna ya Waislamu wote baada yake. Mtume (s.a.w.w.) alionyesha uhusiano wa Hasan na Mwenyezi Mungu tangu alipozaliwa, hivyo hakumpa jina mpaka wahyi uliposhuka na jina lake la Hasan. Mtume (s.a.w.w.) akatangaza wazi wazi uimamu wake sehemu mbali mbali mbele ya Waislamu wote huku akiwahimiza wampende na kumtii. Imam Hasan (a.s.) alichukua uimamu katika mazingira magumu yaliyojaa uasi, tofauti na yenye kukatisha tamaa. Baba yake alimkabidhi uimamu na kumuusia, hivyo akaongoza kwa siasa, ujuzi, hekima na utatuzi sahihi, kisha akalazimika kufanya suluhu na Muawiya na kundi lake potevu, alifanya hivyo kwa ajili ya kulinda dini na umma mzima. Maswali: 1. Ni sunna ipi Mtume (s.a.w.w.) alimfanyia mjukuu wake Hasan alipozaliwa? 2. Ni uhusiano upi uliyopo kati ya Hasan (a.s.) na babu yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)? 3. Ni ipi kuniya ya Imam Hasan (a.s.)? 4. Taja lakabu zake na elezea zinamaanisha nini? 5. Elezea vipindi vya maisha yake kwa ufupi? 6. Taja mambo muhimu yaliyompata Imam Hasan (a.s.) toka alipozaliwa mpaka alipofariki baba yake? 14
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Somo la ishirini na moja Mwonekano wa utu wa Imam Hasan Al-Mujtaba (a.s.) Imam mteule ndani ya Aya za Qur’ani tukufu: Waislamu hawajakubaliana katika jambo kama walivyokubaliana kuhusu fadhila za kizazi cha Mtume (s.a.w.w.) na nafasi yao ya juu ya kielimu na kiroho na kujumuisha kwao sifa zote za ukamilifu ambazo Mwenyezi Mungu alimtaka mwanadamu ajipambe kwazo. Bila shaka Imam Hasan ni mmoja wa kizazi cha Mtume (s.a.w.w.) waliotoharishwa dhidi ya uchafu17 na yeye ni mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa mujibu wa maelezo ya Aya ya maapizano. Qur’ani imedumisha maelezo ya tukio hili kwa maelezo ya kina kwa kusema:
ع ُ اجكَ فِي ِه ِمنْ بَ ْع ِد َما َجا َء َك ِم َن ا ْل ِع ْل ِم فَقُ ْل تَ َعالَ ْوا نَ ْد فَ َمنْ َح ﱠ س ُك ْم ثُ ﱠم َ ُسنَا َوأَ ْنف َ ُسا َء ُك ْم َوأَ ْنف َ ِسا َءنَا َون َ ِأَ ْبنَا َءنَا َوأَ ْبنَا َء ُك ْم َون نَ ْبتَ ِھ ْل فَنَ ْج َع ْل لَ ْعنَتَ ﱠ ين َ ِﷲِ َعلَى ا ْل َكا ِذب “Na atakayebishana nawe katika hili baada ya ujuzi uliokujia, basi waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake wetu na wanawake wenu, na nafsi zetu na nafsi zenu, kisha tuombe kwa unyenyekevu na tuiweke laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie wenye kusema uwongo.”18 17 18
Al-Ahzab: 33. Al Imran: 61. 15
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Wanahadithi wote wamepokea kuwa Aya hiyo ilishuka kwa ajili ya kizazi cha Mtume (s.a.w.w.) nao ni: Mtume wa Mwenyezi Mungu, Ali, Fatimah, Hasan na Husein. Watoto hapo ni Hasan na Husein. Pia hadithi nyingi zimepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) zikimaanisha kuwa wao ndio wabora kuliko watu wote wa ardhini na wao ndio wabora wao mbele ya Mwenyezi Mungu. Kwa ajili hiyo Mtume (s.a.w.w.) alitaka kuapizana kupitia kwao. Hapo askofu wa Najrani akakiri hilo kwa kusema: “Naona nyuso ambazo laiti zitamwomba Mwenyezi Mungu auhamishe mlima toka sehemu yake basi ataondoa.”19 Hivyo ndivyo tukio lilivyoonyesha na zikaonyesha Aya nyingine cheo chao na utukufu wa nafasi yao na ubora wao, na wao ni viumbe wapendwao sana na Mwenyezi Mungu na Mtume wake (s.a.w.w.) kuliko vingine, kwani hakuna yeyote anayewakaribia katika ubora. Qur’ani haijaleta maelezo ya utakaso wa yeyote ukiacha Mtume (s.a.w.w.) isipokuwa ni ya utakaso wa kizazi chake tu kitakasifu ambacho Mwenyezi Mungu amekitakasa dhidi ya kila aina ya uchafu.20 Wala Waislamu hawajatofautiana kuhusu kuingia Ali, Az-Zahrau, Hasan na Husein katika madhumuni ya Aya tukufu.21 Na hapa tunafahamu sababu ya ulazima wa kuwapenda na dharura ya kushikamana na njia yao na wala si ya wengine. Ibnu Abbas amesema: “Iliposhuka Aya ya kuwapenda ndugu wa mtume, baadhi ya Waislamu urul-Absar 100. Rejea Tafsirul-Jalalayni, Ruhul-Bayan, Al-Kashafu, Al-Baydhawiyyu, N Ar-Raziy, Sahih Tirmidhiy, Juz. 2, Uk. 166. Sunanul-Bayhaqiy, Juz. 7, Uk. 63. Sahih Muslim, kitabu cha fadhila za masahaba. Musnad Ahmad, Juz. 1, Uk. 85. MaswabihusSunna, Juz. 2, Uk. 201. 20 Al-Ahzab: 33. 21 Tafsir Al-Kabir cha Ar-Raziy. Tafsir Nisabur; Sahih Muslim, Juz. 2, Uk. 33. KhasaisunNasaiy Uk. 4. Musnad Ahmad, Juz. 4, Uk. 107. Sunanul-Bayhaqiy, Juz. 2, Uk. 150. Mustadrakul-Hakim, Juz. 2, Uk. 416. Usudul-Ghaba, Juz. 5, Uk. 521. 19
16
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
walimuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu kuhusu mfano halisi wa ndugu ambao mapenzi yao yamewajibishwa kwa Waislamu wote. Hivyo Mtume (s.a.w.w.) akajibu: “Hao ni Ali, Fatimah na wana wao wawili.”22 Ndani ya Sura Ad-Dahri Qur’ani imeashiria sababu zilizopelekea ubora huu, Sura ambayo ilishuka kubainisha ikhlasi waliyo nayo Ahlul-Baiti katika kumtii na kumwabudu Mwenyezi Mungu hapo ikasema: “Tunakulisheni kwa ajili ya radhi ya Mwenyezi Mungu tu, hatutaki kwenu malipo wala shukurani.* Hakika sisi tunaogopa kutoka kwa Mola wetu siku yenye shida na taabu.* Basi Mwenyezi Mungu atawalinda katika shari ya siku hiyo na kuwakutanisha na neema na furaha.* Na atawapa mabustani na hariri kwa sababu walisubiri.”23 Wafasiri na wanahadithi wote kwa ujumla wao wamepokea kuwa Sura hii tukufu imeshuka kwa ajili ya fadhila za Ahlul-Baiti baada ya Hasan na Husein kuugua kisha Imam Ali (a.s.) na Az-Zahrau wakaweka nadhiri kuwa watafunga siku tatu kumshukuru Mwenyezi Mungu iwapo watapona, hivyo wakatekeleza nadhiri yao huku wakionyesha upendeleo wa hali ya juu kwa wengine kuliko nafsi zao mpaka ikashuka: “Hakika watawa watakunywa katika kikombe kilichochanganyika na kafuri.* Chemchemu watakayoinywa waja wa Mwenyezi Mungu wataitiririsha mtiririko.* Wanatimiza nadhiri na wanaiogopa siku ambayo shari yake itaenea.* Na huwalisha chakula masikini na yatima na mfungwa hali ya kuwa wanakipenda.”24 Mwenyezi Mungu akashukuru juhudi zao juu ya upendeleo huo na utimizaji wa nadhiri ambao uliwarithisha nafasi ya kupendeza afsir Al-Kabir cha Ar-Raziy. Ad-Durul-Manthur, Juz. 7. Tafsirut-Tabar, Juz. 5, Uk. 16. T Ad-Dahri: 9 – 12. 24 - Ad-Dahri: 5 – 8. 22 23
17
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Siku ya Kiyama, na kuwapa nafasi ya juu ya uongozi kwa Waislamu hapa duniani mpaka itakapotanduka ardhi na vilivyomo. Nafasi ya Imam Hasan kwa Mtume wa mwisho (s.a.w.w.): Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwapa wajukuu zake Hasan na Husein sifa maalumu zinazoelezea ukubwa wa nafasi zao kwake akasema: a. “Hasan na Husein ni manukato yangu duniani,25 na Hasan na Husein ni manukato yangu ndani ya umma huu.”26 b. “Hasan na Husein ndio wabora kwa watu wa ardhini.”27 c. “Hasan na Husein ni mabwana wa vijana wa peponi.”28 d. “Hasan na Husein ni maimamu, wakisimama au wakikaa.”29 e. Wao wawili ni kizazi cha Mtume ambacho hakiachani na Qur’ani mpaka siku ya Kiyama, hivyo umma hautopotea iwapo tu utashikamana nao.30 f. “Mfano wa Ahlul-Baiti wangu ni sawa na safina ya Nuh atakayeipanda ataokoka na atakayeiacha atazama.”31 g. Wao ni miongoni mwa wale aliyowazungumzia babu yao kwa kusema: “Nyota ni kinga ya watu wa ardhini wasizame na AhlulBaiti wangu ni kinga ya watu wa ardhini ili wasitofautiane.”32 Sahih Bukhari, Juz. 2, Uk. 188. Sunanut-Tirmidhiy, Uk. 539. 27 Uyunul-Akhbar-Ridha, Juz. 2, Uk. 62. 28 Sunan Ibnu Majah, Juz. 1, Uk. 56. At-Tirmidhiy, Uk. 539. 29 Al-Manaqib cha Ibnu Shahru Ashuub, Juz. 3, Uk. 163, amenukuu kutoka kwenye Musnad Ahmad, Jaamiut-Tirmidhiy na Sunan Ibnu Majah. 30 Jaamiut-Tirmidhiy, Uk. 541. na Mustadrak Al-Hakim, Juz. 3, Uk. 109. 31 Hilyatul-Awliyai, Juz. 4, Uk. 306. 32 Mustadrak Al-Hakim, Juz. 3, Uk. 149. 25 26
18
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
i.
Imepokewa kutoka kwa Anas kuwa Mtume (s.a.w.w.) aliulizwa: Kati ya Ahlul-Baiti wako ni yupi umpendaye sana? Akajibu: “Hasan na Husein.” Alikuwa akimwambia Fatimah (a.s.): “Niitie wanangu wapendwa,” kisha anawabusu na kuwakumbatia.33
Nafasi ya Imam kwa watu wa zama zake: i. Muawiya aliwauliza waliyokuwa wamekaa naye: Ni nani aliye bora, mwenye baba, mama, babu, bibi, ami, shangazi, mjomba na mama mdogo, wote wabora? Wakasema: Kiongozi wa waumini anajua kuliko sisi. Hapo akashika mkono wa Hasan bin Ali na kusema: “Ni huyu hapa: Baba yake ni Ali bin Abu Twalib, mama yake ni Fatimah binti wa Muhammad, babu yake ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, bibi yake ni Khadija, ami yake ni Jafar, shangazi yake ni Halat binti wa Abu Twalib, mjomba wake ni Qasim bin Muhammad na mama yake mdogo ni Zaynab binti wa Muhammad.”34 ii. Abu Huraira alikuwa akisema: “Sikumwona Hasan isipokuwa macho yangu yalitoka machozi, kwa sababu mimi nilimwona Mtume wa Mwenyezi Mungu akiingiza mdomo wake ndani ya mdomo wake Hasan, kisha akisema: “Ewe Mwenyezi Mungu mimi nampenda na wewe mpende na mpende ampendaye.” Alikuwa akisema hivyo mara tatu.35 Akasema: Sikuacha kumpenda mtu huyu tokea nilipomwona Mtume (s.a.w.w.) akimfanyia hivyo.”36 Sunanut-Tirmidhiy, Uk. 540. Tazama Al-Aqdu Al-Farid, Juz. 3, Uk. 283. 35 Tazama Mukhtasar Tarikh Damashki cha Ibnu Asakir, Juz. 7, Uk. 10. 36 Tazama Nurul-Absar, Uk. 171. 33 34
19
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
iii. Alipoharakisha Mar’wan bin Al-Hakam kubeba mwili mtakasifu wa Hasan, Husein alimshangaa na kumwambia: “Hivi leo unabeba mwili wake ilihali ulikuwa ukimnywesha matatizo?!” Mar’wan akajibu: “Nilikuwa namfanyia ambaye uvumilivu wake unalingana na mlima.”37 iv. Abu As’wad Ad-Duuliy amemzungumzia kwa kusema: “Hakika yeye ni mstaarabu, amekuwa maarufu kwa waarabu kwa uhalisi wake, utukufu wake, na uzuri wa asili yake.”38 v. Amru bin Is’haqa amesema: “Hakuna mtu aliyezungumza kisha nikatamani asinyamaze, mfano wa Hasan bin Ali, wala sikusikia neno la ubaya kutoka kwake.”39 vi. Abdullah bin Zubayr amesema: “Naapa kwa Mwenyezi Mungu kuwa wanawake hawakumnyanyukia yeyote kwa haiba yake na utukufu wa nafsi yake kama walivyomnyanyukia Hasan bin Ali.”40 Muhtasari: Qur’ani tukufu ambayo ni muujiza na katiba ya kudumu ya maisha imetoa maelezo kuhusu utakaso wa kizazi cha Mtume (s.a.w.w.), ulazima wa kuwapenda, kuwafuata na kuamini utawala wao ambao ndio kuendelea kwa utawala wa Mtume (s.a.w.w.), hivyo kupitia wao Mwenyezi Mungu alileta dini yake aliyoiteuwa kwa viumbe wake. Kama ambavyo Qur’ani imethibitisha ubora wa kizazi cha Mtume (s.a.w.w.), nafasi yao ya juu, na nia yao safi kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake (s.a.w.w.). Imam Hasan alikuwa miongoni Tazama Tahdhibut-Tahdhib, Juz. 2, Uk. 298. Hayatul-Imam Hasan bin Ali, Juz. 2, Uk. 247. 39 Tazama Biharul-An’war, Juz. 43, Uk. 357. 40 Tazama Al-Bidayatu Wan-Nihayah, Juz. 8, Uk. 37. 37 38
20
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
mwa watu maalumu waliopewa nafasi maalumu na Qur’ani tukufu huku akiwa yeye na Ahlul-Baiti wengine. Mtume (s.a.w.w.) aliainisha kuwa kusalimika kwa imani na kufaulu kwa dola ya kiislamu kunategemea utiifu kwa kizazi cha Mtume (s.a.w.w.). Pia kuokoka dhidi ya moto kunategemea mapenzi yao na utawala wao. Akawaamrisha Waislamu kuwatii wao kwa kutoa maelezo ya wazi yanayoonyesha uimamu wao, na akatoa maelezo mahususi juu ya uimamu wa mjukuu wake Hasan (a.s.). Hasan mjukuu wa Mtume (s.a.w.w.) alipata nafasi ya juu kwa wanadamu kwani alikuwa anatokwa na nuru, uongofu, maadili bora na fadhila mpaka ikalazimika maadui wake kukiri hilo kabla ya rafiki yake. Hivyo alikuwa ni jua ling’aalo katika mbingu ya utukufu, hadhi na heshima. Maswali: 1. Ni Aya ipi inayothibitisha utukufu wa Imam Hasan (a.s.)? 2. Elezea jinsi Aya ya maapizano inavyoonyesha fadhila za Imam Hasan? 3. Elezea jinsi Sura Ad-Dahri inavyoonyesha nafasi maalumu ya kizazi cha Mtume (s.a.w.w.)? 4. Je, mapenzi ya Mtume (s.a.w.w.) kwa mjukuu wake yalitokana na uhusiano wa upendeleo wa mzazi kwa mwanae? Fafanua kwa nini? 5. Taja maelezo aliyotoa Mtume (s.a.w.w.) yakionyesha cheo na nafasi ya Imam Hasan (a.s.) na sehemu yake katika maisha ya kiislamu? 21
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Kwa ajili ya kujisomea Nafasi ya Imam Hasan (a.s.) kwa wasomi na wanahistoria: i. Muhammad bin Is’haq amesema: “Hakuna mtu aliyefikia sharafu ya juu baada ya Mtume (s.a.w.w.) kama Hasan, alikuwa akitandikiwa busati mlangoni kwake kisha anatoka na kuketi, na ghafla njia inajifunga, kwa ajili ya kumheshimu hakuna yeyote kati ya viumbe wa Mungu anayepita tena. Anapogundua hilo husimama na kuingia ndani, hapo watu huanza kupita tena. Nilimuona akitembea kwa miguu katika njia ya Makka, hakuna aliyemuona ila na yeye alishuka juu ya kipando chake na kutembea kwa miguu, mpaka nikamuona Saad bin Abu Waqqas na yeye akitembea kwa miguu.”41 ii. Msomi wa karne ya nne Al-Hafidh Abu Nu’aim Al-Ispahaniy amesema kuhusu Imam Hasan kuwa: “Ni bwana wa vijana, msuluhishi wa jamii na wapendanao, shabihi wa Mtume wa Mwenyezi Mungu na kipenzi chake, ni mtoto wa uongofu na sehemu ya wachamungu, ni wa tano kati ya watu wa kishamiani, ni mtoto wa mbora wa wanawake, yeye ni Hasan bin Ali bin Abu Twalib.”42 iii. Ibnu Abdul-Barri amesema: “Hakuna jeusi lililotoka kwa yule aliyeitwa bwana na Mtume, yeye alikuwa mvumilivu, mchamungu mwenye fadhila, uchamungu wake na fadhila zake zilimpelekea kuacha ufalme na dunia kwa kutamani yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu, hivyo akasema: “Naapa kwa Mwenyezi Mungu sikutamani kupuuzia jambo la umma wa kiislamu tangu nijue linalonidhuru na linaloninufaisha, sikuacha damu imwagike kwa ajili ya jambo hilo.””43 Tazama Al-Manaqib cha Ibnu Shahari Ashuub, Juz. 2 Uk. 148. Rejea Akhbar Isbahan, Juz. 1, Uk.44, chapa ya Lidan mwaka 1931. 43 Al-Istiaab, Juz. 1, Uk. 385. 41 42
22
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
iv. Ibnu Athir amemzungumzia kwa kusema: “Ni bwana wa vijana wa peponi na manukato ya Mtume (s.a.w.w.), na yeye ni kati ya watu watano wa kishamiya.”44 v. Sibtu Ibnul-Jawziy amesema: “Alikuwa kiongozi wa wakarimu wakubwa na mwenye uelevu mkubwa. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), alikuwa akimpenda sana.”45 vi. Al-Hafidh Ibnu Kathir Ad-Damashqiy amesema: “Abu Bakr alikuwa akimheshimu, akimtukuza, akimkarimu na akimthamini, na hivyo ndivyo alivyokuwa Umar bin AlKhattab, Ibnu Abbas alikuwa akiandaa kipandwa kwa ajili ya Hasan na Husein huku akiona hii ni neema kubwa juu yake.”46 vii. Al-Hafidh Ibnu Asakir As-Shafiiyyu amesema: “Ni mjukuu wa Mtume na manukato yake, ni mmoja wa mabwana wawili wa vijana wa peponi.”47 viii. Al-Hafidh As-Suyuutiy amesema: “Ni mjukuu wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, manukato yake na khalifa wake mwingine kwa maelezo yake.”48 ix. Muhammad bin Talha As-Shafiiyyu amesema: “Mwenyezi Mungu alikuwa amemruzuku maumbile hodari katika kufafanua makusudio yake. Akampa mtazamo wa kutengeneza misingi ya dini na nguzo zake.”49 Usudul-Ghaba, Juz. 2, Uk. 9. Tadhkiratul-Khuwwas, Uk. 111. 46 Al-Bidayatu Wan-Nihayah, Juz. 8 Uk. 37. 47 Mukhtasar Tarikh Damashqi cha Ibnu Asakir, Juz. 7, Uk. 5. 48 Taarikhul-Khulafai, Uk. 188. 49 Matwalibus-Suul, Uk. 65. 44 45
23
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
x. Abdul-Qaadri Ahmad Al-Yusuf amesema: “Hakika Hasan bin Ali ni mtoto wa binti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), na ni miongoni mwa maimamu maasumina ambao wanajiona kuwa ndio wenye haki zaidi kuliko wengine, bali wao wamelazimishwa kueneza Uislamu baada ya Mtume (s.a.w.w.) na kulinda sunna na sheria ya Muhammad, hilo ni kutokana na ukaribu wao, usafi wa nafsi zao, na kuitambua kwao Qur’ani kama inavyostahili.”50
50
Al-Hasan bin Ali cha Abdul-Qaadir Ahmad Al-Yusuf, Uk. 42. 24
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Somo la ishirini na mbili Sifa za Imam Hasan na mwonekano wake: Ibada yake: i. Al-Mufadhil amepokea kutoka kwa Imam Jafar bin Muhammad As-Sadiq (a.s.) kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake kuwa: “Hasan bin Ali bin Abu Twalib alikuwa ni mfanya ibada mno kuliko watu wote wa zama zake, ni mbora wao na aliyeipa mgongo dunia. Alikuwa anapohiji huenda kuhiji kwa miguu na huenda akatembea bila kiatu. Kinapotajwa kifo na kutajwa kaburi hulia, pia unapotajwa ufufuo na Kiyama hulia. Yanapotajwa mapito ya njia ya siku ya Kiyama hulia, kinapotajwa kisimamo cha mbele ya Mwenyezi Mungu hulia mpaka mwisho huzimia. Asimamapo kwa ajili ya Swala viungo vyake hutetemeka mbele ya Mwenyezi Mungu. Pepo na moto vinapotajwa hutikisika kama unavyotikisika mkia wa ng’e huku akimwomba Mwenyezi Mungu pepo na akimwomba amkinge na moto. Alikuwa hasomi: “Enyi mlioamini” isipokuwa atasema: “Nimekubali ewe Mwenyezi Mungu. Nimekubali ewe Mwenyezi Mungu”. Hajaonekana katika hali yoyote isipokuwa atakuwa anamtaja Mwenyezi Mungu. Alikuwa ni mkweli na mfasaha wa maneno…”51 ii. Pindi anapotawadha viungo vyake hutetemeka na kubadilika rangi ya njano. Akaulizwa kuhusu hilo. Akajibu: “Ni haki ya kila 51
Tazama Al-Amaali cha As-Swaduq, Uk. 150. Na Biharul-An’war, Juz. 43, Uk. 331. 25
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
anayesimama mbele ya Mola wa Arshi abadilike rangi ya njano na viungo vyake vitetemeke.” iii. Alikuwa afikapo mlango wa msikiti huinua kichwa chake na kusema: “Mgeni wako yuko mlangoni kwako ewe Mwema. Muovu amekujia, hivyo nisamehe mabaya niliyo nayo kwa kunipa mazuri uliyo nayo ewe Mkarimu.”52 iv. Anapomaliza Swala ya alfajiri alikuwa haongei mpaka lichomozapo jua hata kama atasumbuliwa.”53 v. Kutoka kwa Imam Muhammad bin Ali Al-Baqir amesema: “Hakika Hasan alisema: “Mimi naona aibu kukutana na Mola wangu kabla sijakwenda nyumbani Kwake.” Hivyo akaenda mara ishirini kwa miguu yake akitokea Madina.”54 vi. Ali bin Jadh’an amesema: “Hasan bin Ali alitoka ndani na mali yake mara mbili, na akamgawia Mwenyezi Mungu mali yake mara tatu.”55 Uvumilivu na msamaha wake: Imam Hasan (a.s.) alifahamika kwa uvumilivu wake mpaka Mar’wan bin Al-Hakam akasema: “Uvumilivu wake ulikuwa unalingana na mlima.” Dalili ya wazi juu ya uvumilivu wake ni suluhu yake dhidi ya Muawiya ambaye alichukua haki ya Ali (a.s.) akatumia mlango huo kupata cheo na madaraka. Baada ya suluhu akavumilia lawama kali kutoka kwa maswahaba zake waaminifu lakini alikuwa akiwaelekea kwa subira na uvumilivu. Alivumilia aina ya ususaji dhidi ya Mwenyezi Mungu Al-Manaqib, Juz. 3, Uk. 180. Biharul-An’war, Juz. 43, Uk. 339. Biharul-An’war, Juz. 43, Uk. 339. Akhbar Isbahan, Juz. 1, Uk. 44. 54 Al-Manaqib, Juz. 3, Uk. 180. Biharul-An’war, Juz. 43, Uk. 339. 55 Al-Manaqib, Juz. 3, Uk. 180. Biharul-An’war, Juz. 43, Uk. 339. 52 53
26
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
kutoka kwao, ilihali yeye ni mvumilimu mwenye subira. Hakusikika akitamka neno la kuudhi isipokuwa mara moja tu ambapo kulikuwa na madai kati yake na Amru bin Uthman kuhusu ardhi, hivyo Hasan akasema: “Amru hana kitu kwetu isipokuwa kinachomdhalilisha.”56 Mar’wan bin Al-Hakam alimkashifu Hasan bin Ali (a.s.), alipomaliza Hasan akamwambia: “Hakika naapa kwa Mwenyezi Mungu sifuti chochote kuhusu wewe, lakini namwomba Mwenyezi Mungu akubali udhuru wako, iwapo ni mkweli basi Mwenyezi Mungu akulipe kwa ukweli wako, na iwapo ni mwongo basi Mwenyezi Mungu akulipe kwa uongo wako, na hakika Mwenyezi Mungu ndiye mkali wa malipo ya adhabu kuliko mimi.” Imepokewa kuwa kijana wake alitenda kosa linalostahiki adhabu, Imam akaamuru aadhibiwe. Kijana akasema: “Ewe bwana wangu, mwenye kuwasamehe watu.”57 Imam akasema: “Nimekusamehe.” Kijana akasema: “Ewe bwana wangu, na Mwenyezi Mungu huwapenda wenye kufanya ihsani.”58 Imam akasema: “Upo huru kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na unastahiki mara mbili ya yale niliyokuwa nikikupa.”59 Ukarimu wake: Ukarimu wa kweli ni kutoa heri kwa lengo la heri na kutoa ihsani kwa lengo la ihsani. Sifa hii ilidhihirika kwa maana yake ya juu kwa Imam Hasan (a.s.) mpaka akapewa lakabu ya Mkarimu wa kizazi cha Mtume (s.a.w.w.). Alikuwa hathamini mali isipokuwa kwa kiwango kinachozuwia njaa ya mwenye njaa au kinachomvisha aliye tupu, au kinachomsaidia mwenye matatizo, au kinachokidhi kulipa deni la mwenye kudaiwa. Biharul-An’war, Juz. 43, Uk. 344. Al Imran: 134. 58 Al Imran: 134. 59 Biharul-An’war, Juz. 43, Uk. 352. 56 57
27
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Alikuwa ana bakuli kubwa pana aliloliandaa kwa ajili ya wageni. Aliulizwa kwa nini hatuoni ukimnyima mwombaji? Akajibu: “Hakika mimi namwomba Mwenyezi Mungu na ninatamani aliyo nayo, naona aibu mimi kuwa mwombaji kisha nimnyime mwombaji mwenzangu, na hakika Mwenyezi Mungu amenizowesha kwa kunimiminia neema Yake na nimemzowesha kwa kumimina neema Yake kwa watu, hivyo nahofia nikiacha mazoea na mimi nitazuiliwa nilichozoeshwa.”60 Siku moja alimkuta mtumwa mweusi akiwa na kipande cha mkate huku akila tonge moja na tonge lingine akimlisha mbwa, hapo Imam akamuuliza: ‘Ni kitu gani kimekupelekea kufanya hivyo?” Kijana akajibu: “Naona aibu kula bila kulisha.” Basi hapo Imam akaona maadili mazuri toka kwa mtumwa huyo na akatamani amlipe mazuri kwa wema anaotenda. Imamu akamwambia: “Usitoke hapo ulipo”, hivyo akaenda kwa mmiliki wake na kumnunua kisha akanunua bustani aliyokuwemo mtumwa yule na kumwachia huru huku akimmilikisha ile bustani.”61 Unyenyekevu na utawa wake: Unyenyekevu ni dalili ya ukamilifu na utukufu wa nafsi, unyenyekevu haumzidishii mja isipokuwa hadhi ya juu. Imam Hasan (a.s.) alifuata nyayo za babu yake na baba yake katika maadili yake mazuri. Hakika historia imesajili mifano mingi halisi ambayo inaashiria maadili ya hali ya juu aliyokuwa nayo Imam (a.s.), hivyo hapa tunadokezea baadhi tu: i. Imam (a.s.) alikuta kundi la mafakiri likiwa limeweka vipande vya mikate ardhini huku wakiwa wamekaa wakiviokota na kula, 60 61
Tazama Asbabul-Ashraaf, Juz. 1, Uk. 319. At-Tabaqat Al-Kubra, Juz. 1, Uk. 23. Al-Bidayatu Wan-Nihayah, Juz. 8, Uk. 38. 28
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
wakamwambia: “Ewe mtoto wa binti wa Mtume karibu tujumuike kwenye chakula.” Akateremka kisha akasema: “Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wenye kiburi.” Akaanza kula nao mpaka walipomaliza huku kwa baraka zake chakula kikiwa vilevile bila kupunguka. Kisha akawakaribisha kwake akawalisha na kuwavisha.62 ii. Siku moja alipita sehemu akawakuta watoto wanakula chakula huku wakimwita ashirikiane nao. Akawakubalia, kisha akawabeba nyumbani kwake akawapa wema wake, kisha akasema: “Wema ni ule wa kwao kwa sababu wao hawana kingine zaidi ya kile walichonilisha lakini sisi tunapata zaidi ya yale tuliyowapa.”63 iii. Na miongoni mwa utawa wake ni ule aliouzungumzia Mudrik bin Ziyad alisema: “Tulikuwa kwenye bustani ya Ibnu Abbas akaja Hasan na Husein wakazunguka bustani hizo kisha wakaketi pembeni mwa baadhi ya wahudumu. Hasan akasema: “Ewe Mudrik je, una chakula?” Nikamwambia: Ndio. Kisha nikatoka nikamletea mkate, chumvi na mboga mboga. Alipokula akasema: “Ewe Mudrik chakula kitamu mno!!!” Baada ya hapo kikaletwa chakula kingine kitamu zaidi, hapo Imam (a.s.) akamgeukia Mudrik na kumwamuru awakusanye watumwa na awape chakula kile. Mudrik akawaita wakala chakula kile huku Imam akiwa hajakula hata chembe katika chakula kile. Mudrik akamwambia: Kwa nini huli? Imam akajibu: “Hicho ni chakula nikipendacho sana.”64 Awalimul-Uluum, Uk. 123. Al-Manaqib, Juz. 3, Uk. 187. Hayatul-Imam Hasan bin Ali, Juz. 1, Uk. 313, kutoka kwa As-Swabban pambizoni mwa Nurul-Absar, Uk. 176. 64 Mukhtasar Taarikh Damashqi, Juz. 7, Uk. 21. 62 63
29
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Muhtasari: Historia imethibitisha kuwa Hasan (a.s.) alikuwa na moyo mkunjufu katika kumtii na kumwabudu Mwenyezi Mungu, alikuwa mjuzi na mtaalamu wa sharia na kanuni zake. Maelezo tuliyo nayo ni ishara juu ya maarifa ya ajabu na nafsi yenye bidii imnong’onezayo Mola wa ulimwengu, hivyo ibada yake haikuwa ya kujitenga na jamii bali alikuwa akishirikiana na kila kundi la kijamii kama kiongozi wao na mlezi wao. Kwa nafsi yake pana na sifa zake nzuri alijiepusha na maadui zake, kama alivyojiepusha na kila aliyeshindwa kujua nafasi yake, hivyo hakusikika akitamka kauli chafu, wala hakumtukana au kumkashifu mtu. Kwa kutumia akili zake za juu toka kwa Mola wake huku akiwa na uvumilivu uliyopindukia aliweza kuukomboa umma dhidi ya upotevu kutoka ndani ya mawimbi ya uasi. Hivyo akameza machungu makubwa kwa ajili ya kulinda masilahi ya sharia ya kiislamu na umma wa babu yake bwana Mtume (s.a.w.w.). Hakika Imam Hasan (a.s.) ni tawi la mti wa Hashimiya, watu ambao walifahamika kwa ukarimu, hakika alifanya ukarimu wake wote ni kwa ajili ya kumtii Mwenyezi Mungu na ni mfumo wa kimalezi ambao utafuatwa na umma. Hasan (a.s.) alikuwa ni kiongozi wa umma na ni mlinzi wa ujumbe wa Mwenyezi Mungu, hivyo katika sekta zote za maisha yake utakuta akiwapa watu uongofu wa Mwenyezi Mungu, akidhihirika kwa unyenyekevu, ukarimu na heshima yake, ilihali akihimiza uchamungu na utawa, huku akiwalea watu juu ya fikira ya: Akhera ndio nyumba ya kudumu.
30
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Maswali: 1. Je, unaweza kutoa sura halisi ya wazi kuhusu ibada za Imam Hasan (a.s.)? 2. Taja tukio linalowakilisha uvumilivu wa Imam Hasan (a.s.)? 3. Kwa nini Imam Hasan (a.s.) hakumnyima mwombaji wa aina yeyote? 4. Taja tukio ambalo linawakilisha utawa na unyenyekevu wa Imam Hasan (a.s.)? Kwa ajili ya kujisomea Imam Hasan (a.s.) ana dua ambazo zimekusanya baadhi ya maarifa, zikabeba adabu ya kumtakasa Mwenyezi Mungu, kumnyenyekea na kujidhalilisha kwake, hivyo hapa tutazitaja baadhi tu kama mfano. Imam amesema: “Ewe Mwenyezi Mungu wewe ndiye mbadala kuliko viumbe Wako wote, wala katika viumbe wako hakuna mbadala mfano wako. Ewe Mola Wangu atakayetenda mazuri basi ni kwa rehema zako, na atakayekosea basi ni kwa makosa yake, wala atendae wema haachi kuhitajia msaada wako na wala aliyekosea hajampata badala yako wala hajatoka nje ya nguvu zako. “Ewe Mola wangu kupitia Wewe nimekujua, kupitia Wewe nimefuata amri Yako, na laiti kama si Wewe basi nisingekujua wewe ni nani. Ewe ambaye uko hivyo wala hayuko hivyo mwingine, mpe rehema na amani Muhammad na kizazi cha Muhammad, na niruzuku moyo mkunjufu katika matendo yangu na nipanulie riziki yangu. Ewe Mola Wangu, fanya mwisho wangu uwe kwa matendo mema, na ubora wa hali yangu awe mwishoni, na siku yangu bora 31
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
iwe ni siku nitakayokutana na wewe. Ewe Mola Wangu, nimekutii ilihali wewe umenineemesha kunipa vitu uvipendavyo sana: Kukuamini na kumkubali Mtume wako. Wala sijakuasi kwa kutenda mambo uyachukiayo sana: Kukushirikisha na kumkanusha Mtume wako. Nisamehe yaliyo kati ya hayo mawili, ewe mbora wa kurehemu.”65 Imepokewa kutoka kwa Ibnu Kathir kuwa: “Kila siku usiku akiwa kitandani kabla ya kulala Hasan (a.s.) alikuwa akisoma Sura Kahfi kwenye ubao ulioandikwa, alikuwa akizunguka nao jinsi azungukavyo nyumba za wakeze.”66 Hakika Imam Hasan (a.s.) alikula asili ya maarifa na jauhari ya imani akawa ni mtu mwenye imani mno na mkunjufu mno wa moyo na utiifu kwa Mwenyezi Mungu.67 Al-Mubarrid na Ibnu Aisha wamepokea kuwa: Mtu wa Sham alimwona Hasan (a.s.) akiwa juu ya kipando chake basi akaanza kumlaani ilihali Hasan (a.s.) hamjibu kitu. Alipomaliza Hasan akamwendea, akamsalimia na kucheka kisha akasema: “Ewe mzee nadhani wewe ni mgeni, inawezekana umefananisha, hivyo laiti ungeuliza tungekujibu, laiti ungetuomba tungekupa, laiti ungetaka tukuongoze tungekuongoza, laiti ungetaka tukubebe tungekubeba, kama ni mwenye njaa tutakulisha, kama hauna mavazi tutakuvisha, kama una haja na kitu tutakutimizia haja yako, kama umefukuzwa tutakunusuru, kama ni mwenye haja tutakutajirisha, kama utaamsha mnyama wako kuja kwetu ili uwe mgeni wetu mpaka utakapoondoka basi hili ni bora zaidi kwako, kwa sababu sisi tuna nafasi, cheo, wasaa na mali nyingi.” Mahjud-Daawat, Uk. 144. Al-Bidayatu Wan-Nihayah, Juz. 8 Uk. 42, chapa ya Daru Ihyait-Turath Al-Arabiy 1408 A.H. 67 Hayatul-Imam Hasan bin Ali, Juz. 1, Uk. 326. 65 66
32
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Mzee yule aliposikia maneno yale akaanza kulia kisha akasema: “Nakiri hakika wewe ni khalifa wa Mwenyezi Mungu ardhini na Mwenyezi Mungu anajua mahali pakuweka ujumbe wake, wewe na baba yako mlikuwa viumbe mnaochukiwa mno kwangu mimi kati ya viumbe wa Mwenyezi Mungu, hivi sasa wewe ni kiumbe nikipendacho mno….”68 Imepokewa kuwa: Kijakazi alimsalimia kwa kumpa fungu la maua yenye harufu nzuri. Imam akamwambia: “Tangu sasa wewe uko huru kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.” Hapo Anas akamlaumu kwa hilo, Imam akajibu: “Hakika Mwenyezi Mungu ametufunza adabu akasema: “Na mnaposalimiwa kwa maamkizi yoyote basi itikieni kwa yaliyo bora kuliko hayo.” Na kilicho bora zaidi kuliko maamkizi yake ni kumpa uhuru.”69 Miongoni mwa maadili yake bora ni kuwa hakununua bustani toka kwa mtu kisha baadae muuzaji akafilisika isipokuwa ni lazima atamrudishia bustani yake au atampa nyingine na kumwongezea thamani. Alijiwa na fakiri akimlilia hali huku Imam akiwa hana chochote siku hiyo, hivyo mambo yakawa magumu kwake akaona aibu kumrudisha bila kitu, Imam akamwambia: “Hakika mimi nakuonyesha jambo ambalo litakupatia kheri.” Fakiri akasema: “Ni lipi ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu?” Akasema: “Nenda kwa khalifa hakika binti yake kafariki na khalifa ameumia sana kwa kifo cha binti yake, lakini hajasikia pole ya maana kutoka kwa yeyote, hivyo nenda kampe pole kupitia maneno haya hakika yatakupatia kheri”. Fakiri akasema: “Ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, nihifadhishe maneno hayo.” Imamu akasema: “Mwambie: Kila sifa njema ni ya Mwenyezi Mungu ambaye amemsitiri binti kwa kitendo 68 69
Al-Awalim, Uk. 121, amenukuu kutoka kwenye kitabu Al-Manaqib, Juz. 3, Uk. 184. Al-Manaqib, Juz. 2, Uk. 18. Aya ni ya Surat An-Nisai: 86 33
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
cha wewe kukaa juu ya kaburi lake, wala hajamvunjia heshima kwa kitendo cha yeye kukaa juu ya kaburi lako.” Fakiri akahifadhi maneno haya na kwenda nayo kwa khalifa, kisha akampa pole kutumia maneno hayo. Hapo khalifa akaondokwa na huzuni kisha akaamrisha apewe zawadi huku khalifa akisema: “Je haya ni maneno yako mwenyewe?” Akajibu: “Hapana isipokuwa ni maneno ya Imam Hasan.” Khalifa akasema: “Umesema kweli hakika ni maneno fasaha ya chimbuko la ufasaha.” Na hapo akaamrisha apewe zawadi nyingine. Hakika Hasan (a.s.) alikuwa akiwapa mafakiri wema wake kabla hawajataja shida zao huku akiwasifu ili udhalili wa kuomba usidhihirike kwao.70
70
Hayatul-Imam Hasan bin Ali, Juz. 1, Uk. 324. 34
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Somo la ishirini na tatu Urithi wa Imam Hasan Al-Mujtaba (a.s.) Elimu na akili: i.
“Jifunzeni elimu hakika hivi sasa nyinyi ni watoto katika jamii na ni wakubwa wao kesho, na yule asiyeweza kuhifadhi basi aandike.”71
ii.
“Kuuliza vizuri ni nusu ya elimu.”72
iii. “Wafunze watu na ujifunze elimu za wengine kwani kufanya hivyo utakuwa umeimarisha elimu yako na umejua uliyokuwa huyajui.”73 iv. “Yakini ni kinga ya imani.” v.
“Nawausia kumcha Mwenyezi Mungu na kufikiri daima, hakika kufikiri ndio baba wa kila jambo la kheri.”74
vi. “Akili ni moyo kuhifadhi kila ilichoomba kihifadhiwe.”75 vii. “Asiye na akili hana adabu, asiye na hima hana mapenzi, asiye na dini hana aibu, na kilele cha akili ni kuishi na watu vizuri. Kupitia akili wema wa dunia na Akhera hupatikana, hivyo atakayenyimwa akili kanyimwa vyote viwili.” viii. “Akili haimhadai atakayeiomba nasaha.” Al-Fusulul-Muhimmah cha Ibnu As-Swabbagh Al-Malikiy, Uk. 142. Nurul-Absar, Uk. 110. 73 Al-Ithnaashariyyah, Uk. 37. 74 Hayatul-Imam Hasan bin Ali, Juz. 1, Uk. 343 na 346. 75 Imam Hasan bin Ali, Juz. 1, Uk. 343 na 346. 71 72
35
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Qur’ani Tukufu: i. “…Ni kitabu cha Mwenyezi Mungu chenye ufafanuzi wa kila kitu, hakina batili hivi sasa wala baadae na ni tegemeo katika kila kitu. Tafsiri yake haitupotoshi bali tunajua ukweli wake kwa yakini, hivyo tutiini sisi kwa sababu utiifu kwetu umewajibishwa, kwani utiifu kwa Mwenyezi Mungu, Mtume wake na wenye madaraka umeunganishwa pamoja……” ii. “Hakika ndani ya Qur’ani hii mna taa za nuru na tiba ya vifua, hivyo kwa mwanga wake aangaze mwenye kuangaza……Hakika kufikiri ni uhai wa moyo wa mtu mjuzi kama anavyotembea gizani huku akijiangazia kwa nuru.”76 iii. “Hii hapa Qur’ani ifanyeni imam. Mwenye kuitendea haki ni yule anayeifanyia kazi hata kama atakuwa hajaihifadhi. Aliye mbali mno nayo ni yule asiyeifanyia kazi hata kama atakuwa anaisoma.”77 iv. Alikwenda mtu msikiti wa Mtume kuuliza tafsiri ya Aya: “Na kwa shahidi na kwa anayeshuhudiwa”.78 Akawaona watu watatu kila mmoja kazungukwa na kundi la watu huku akiwasimulia aliyoyasikia kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.). Akamuuliza mmoja wao, akajibu: “Shahidi ni siku ya ijumaa na mwenye kushuhudiwa ni siku ya Arafa.” Kisha akamuuliza mwingine, akajibu: “Shahidi ni siku ya ijumaa na mwenye kushuhudiwa ni siku ya kuchinja.” Kisha akamuuliza wa tatu, akajibu: “Shahidi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na mwenye kushuhudiwa ni siku ya Kiy ayatul-Imam Hasan bin Ali, Juz. 1, Uk. 343 na 346 – 347. Amenukuu kutoka kwenye H kitabu Kashful-Ghummah na Irshadul-Quluub. 77 Hayatul-Imam Hasan bin Ali, Juz. 1, Uk. 343 na 346 – 347. Amenukuu kutoka kwenye kitabu Kashful-Ghummah na Irshadul-Quluub. 78 Al-Buruj: 3. Tazama tafsiri Majmaul-Bayan. 76
36
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
ama kwa kuwa Mwenyezi Mungu anasema: “Ewe nabii kwa hakika sisi tumekutuma shahidi na mtoaji wa habari nzuri na mwonyaji.”79 Na Mwenyezi Mungu akasema kuhusu Kiyama: Hiyo ni siku yenye kushuhudiwa.”80 Akauliza wa kwanza ni nani? Akaambiwa ni Abdullah bin Abbas. Akauliza wa pili? Akaambiwa ni Abdullah bin Umar. Akauliza wa tatu ni nani? Akaambiwa ni Hasan bin Ali bin Abu Twalib. Hadithi za Mtume (s.a.w.w.): Imam Hasan (a.s.) alitilia umuhimu suala la kueneza hadithi za Mtume (s.a.w.w.), maadili bora na mwenendo wake, kwani Bani Umaiyya walikuwa wakifanya juhudi kupoteza sera hii ya Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) na kuficha ulazima wa kizazi cha Mtume kuongoza umma baada ya Mtume (s.a.w.w.). Hivyo hapa tutachagua baadhi ya hadithi alizopokea Imam Hasani (a.s.) kutoka kwa babu yake. i. “Popote mtakapokuwepo nitakieni rehema na amani kwani hakika rehema na amani zenu zitanifikia.” ii. Ewe mwislamu, nihakikishie mambo matatu nitakuhakikishia Pepo: Iwapo utatenda yale uliyofaradhishiwa ndani ya Qur’ani basi wewe utakuwa ni mfanya ibada mno kuliko watu wengine. Ukitosheka na kile ulichoruzukiwa basi wewe utakuwa ni tajiri kuliko watu wote. Ukijiepusha na yale aliyoharamisha Mwenyezi Mungu basi wewe utakuwa mchamungu kuliko watu wote.” iii. “Hakika miongoni mwa mambo yanayowajibisha usamehewe madhambi yako ni wewe kuingiza furaha moyoni mwa ndugu yako mwislamu.” 79 80
Al-Ahzab: 45. Hud: 103. 37
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
iv. “Atakayeswali Swala ya alfajiri kisha akaketi kwenye msala wake mpaka kuchomoza kwa jua, basi Mwenyezi Mungu atamsitiri mtu huyo dhidi ya moto.” v. “Mwanamke alikwenda kwa Mtume (s.a.w.w.) akiwa na wanae wawili. Akamwomba Mtume (s.a.w.w.), hapo Mtume akampa tende tatu. Kisha mwanamke yule akampa kila mwanae tende moja. Walipomaliza kula wakamtazama mama yao, hapo mama yao akawaonea huruma akapasua tende iliyobaki vipande viwili na kumpa kila mmoja kipande cha tende. Hapo Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Mwenyezi Mungu amsamehe mwanamke huyu kwa kuwaonea huruma wanae.”81 Utawala wa Ahlul-Baiti (a.s.): i. Imam Hasan (a.s.) amesema: “Jueni kwa yakini kuwa nyinyi hamuwezi kujua uchamungu mpaka mjue sifa za uongofu, wala hamuwezi kushika ahadi za Kitabu mpaka mumfahamu aliyezivunja, wala hamtokisoma Kitabu kwa uhakika mpaka mumjue aliyekipindisha. Mtakapojua hayo mtajua bidaa na uzushi na mtaona uwongo anaozushiwa Mwenyezi Mungu na mtaona jinsi anavyopotea mwenye kupotea. Wala wasiwapotezeni wasiojua. Chukueni hayo toka kwa wenyewe, hakika wenyewe ni watu maalumu nao ni nuru inayowaangazia watu na ni maimamu waongozao. Kupitia wao elimu huishi na ujinga hutoweka, na wao ndio ambao uvumilivu wao umewapa habari kuhusu elimu yao, na maneno yao yakawapa habari kuhusu ukimya wao, na dhahiri yao kuhusu undani wao. Hawakhalifu haki wala hawatofautiani katika haki, hakika wametangulia wa mwanzo toka kwa Mwenyezi Mungu kwa ajili yao na imepita kati yao hu81
Hayatul-Imam Hasan bin Ali, Juz. 1, Uk. 361 na 333 – 334. 38
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
kumu toka kwa Mwenyezi Mungu, hakika katika hayo kuna ukumbusho kwa wenye kukumbuka.”82 ii. Siku moja akatoa hotuba, akazungumzia filosofia ya sheria na mahusiano kati ya hukumu na kizazi cha Mtume (s.a.w.w.), kisha akasema: “Laiti kama si Muhammad na mawasii wake mngekuwa hamjui chochote, mngekuwa hamjui faradhi yoyote kati ya faradhi za Mwenyezi Mungu na hamuwezi kuingia ndani ya nyumba isipokuwa ni lazima mpitie kwenye mlango wake.” Baada ya kuthibitisha ukamilifu wa dini na ukamilifu wa neema akaashiria haki za mawasii wa Mwenyezi Mungu na nafasi yao katika usalama na maendeleo ya maisha, na kuwa bahili ni yule anayefanya ubahili katika kuwapenda ndugu wa karibu wa mtume…….. Akasema: “Nilimsikia babu yangu akisema: “Mimi nimeumbwa kutokana na nuru ya Mwenyezi Mungu na kizazi changu kimeumbwa kutokana na nuru yangu na wawapendao wameumbwa kutokana na nuru yao na watu wengine kutokana na wengine.”83 Muhtasari: Maimamu (a.s.) walifanya kazi ya kujenga misingi ya akida ya kiislamu ndani ya nafsi za umma. Wakajaribu kutekeleza hukumu za Mwenyezi Mungu ndani ya maisha yao ya kila siku huku wakitumia njia mbalimbali katika kutimiza hilo. Katika hatua ya kuulinda umma wa kiislamu dhidi ya kupotea maimamu walijenga kundi la watu wema wanaomwamini Mwenyezi Mungu, Mtume wake na kizazi cha Mtume. Na wakawa wameeneza kanuni za kiislamu ndani ya umma kadiri walivyoweza. Pia wakafanya kazi ya kueneza mawazo salama ya kiislamu, kufafan82 83
Hayatul-Imam Hasan bin Ali, Juz. 1, Uk. 361. Hayatul-Imam Hasan bin Ali, Juz. 1, Uk. 361. 39
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
ua hukumu kwa sura sahihi na kuainisha maadili ya mwanadamu mwislamu, maadali ambayo sheria ya Uislamu inataka kuyafunza na kuyazalisha kwa wanadamu. Katika hadithi za Imam Hasan (a.s.) tunapata hayo yote kwa uwazi. Hakika yeye alikunywa elimu na maarifa toka ndani ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu, babu yake Mtume (s.a.w.w.) na baba yake Ali (a.s.), kisha akasimamia jukumu la uimamu na uongozi wa umma baada ya baba yake ili kipindi cha mfano bora alichokitaka Mwenyezi Mungu kwa ajili yake kitimie. Maswali: 1. Ni elimu ipi iliyo kinga ya imani? 2. Elezea mahusiano ya akili na wema? 3. Elezea tunavyoangaziwa na nuru ya Qur’ani? 4. Je Imam Hasan (a.s.) alitilia umuhimu suala la kueneza hadithi za babu yake? Fafanua. 5. Ni maadili yapi bora yanayomnufaisha mwanafunzi katika maisha yake ya kielimu na kikazi? Kwa ajili ya kujisomea Mawaidha yenye hekima: i. Imam Hasani (a.s.) amehimiza uchamungu akasema: “Mwenyezi Mungu hakuwaumba bila malengo wala hajawaacha hivi hivi bila kitu. Amewaandikia muda wa kifo chenu, akagawa maisha yenu kati yenu ili kila mmoja ajue nafasi yake, na kuwa kila alichokadiriwa atakipata, na kila alichotengwa nacho hatokipata. Amewatimizia mahitaji ya duniani akawapa muda wa kumwabudu, akawahimiza kumshukuru, akawafaradhishia utajo 40
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
wake, akawausia kumcha yeye, akafanya uchamungu ndio kilele cha ridhaa yake na uchamungu ndio mlango wa kila toba na kiongozi wa kila hekima na utukufu wa kila tendo. Kwa uchamungu amefaulu yule aliyefaulu kati ya wachamungu, Mwenyezi Mungu akasema: “Hakika wachamungu wamewekewa kufuzu.”84 Na akasema: “Na Mwenyezi Mungu atawaokoa wale wamchao kwa ajili ya kufaulu kwao, hautawagusa ubaya wala hawatahuzunika.”85 Mcheni Mwenyezi Mungu enyi waja wa Mwenyezi Mungu, jueni kuwa atakayemcha Mwenyezi Mungu atapewa utatuzi dhidi ya fitina, atamwongoza katika amri yake na atamwandalia njia ya uongofu, na atamfanya afaulu kupitia dalili yake. Atang’arisha uso wake, atamtekelezea matamanio yake pamoja na wale ambao Mwenyezi Mungu amewaneemesha miongoni mwa manabii, wasema kweli, mashahidi na watu wema, Na hao ndio waliyopata urafiki mwema.86 ii. Alikwenda tajiri mmoja akamwambia: “Ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, mimi naogopa kifo”. Imam akamwambia: “Lazima iwe hivyo kwa sababu wewe umechelewesha mali zako, na laiti ungezitanguliza ungefurahia kukutana nazo.”87 iii. Alizungumzia utafutaji wa riziki akasema: “Usipigane na utafutaji mapigano ya mtu aliyeshinda, wala usiuletee hoja uwezo wa Mwenyezi Mungu hoja ya mtu aliyeshindwa, hakika kutafuta riziki ni sunna na kutopindukia katika utafutaji ni kujiheshimu, wala kujiheshimu si kuifukuza riziki, wala pupa si kuivuta riziki kwani riziki imegawanywa na kutumia pupa ni kutumia makosa.”88 An-Nabai: 31. Az-Zumar: 61. 86 Tuhaful-Uquul, Uk. 55. 87 Taarikh Al-Yaaqubiy, Juz. 2, Uk. 202. 88 Tuhaful-Uquul, Uk. 55. 84 85
41
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
iv. Akahimiza kushikamana na misikiti akasema: “Atakayedumisha kwenda msikitini mara kwa mara atapata vitu nane: Aya yenye hekima, ndugu mwenye faida, elimu ya kutosha, rehema zinazosubiriwa, neno linaloonyesha uongofu au linalozuwia upotevu na ataacha dhambi kwa ajili ya kumwonea aibu au kumwogopa Mwenyezi Mungu.”89 v. Akaiwekea siasa kipimo sahihi kilichokusanya maana kamili akasema: “Ni kulinda haki za Mwenyezi Mungu, haki za watu hai na wafu. Ama haki za Mwenyezi Mungu ni kutekeleza aliyotaka na kujitenga na aliyokataza. Ama haki za walio hai ni kutekeleza wajibu wako kwa ndugu zako, wala usichelewe kuhudumia jamii yako, uwe na moyo safi kwa mwenye madaraka kama alivyo na moyo safi kwa umma wake, uinue sauti yako mbele ya uso wake pale aendapo kinyume na njia sahihi. Ama haki ya wafu ni kutaja mazuri yao na kufumbia macho mabaya yao, hakika wao wana Mola atakayewalipa.”90 Miongoni mwa hekima zake za thamani: i.
“Atakayetafuta ibada basi itamtakasa.”
ii.
“Matatizo ni ufunguo wa malipo.”
iii. “Neema ni zawadi, hivyo ukishukuru inakuwa na thamani yenye kuhifadhiwa na ukikufuru inakuwa na adhabu.” iv.
“Jambo liumizalo mno kuliko msiba ni tabia mbaya.”
v.
“Akumbukaye umbali wa safari hujiandaa.”
vi.
“Fedheha ni udhalili kuliko moto.”
89 90
Uyunul-Akhbar cha Ibnu Qutaybah, Juz. 3, Uk. 3. Hayatul-Imam Hasan bin Ali, Juz. 1, Uk. 351na 367 – 370. 42
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
vii. “Mali bora ni ile inayohudumia familia.” viii. “Mwombwaji yuko huru mpaka atakapoahidi na atabakia na deni la ahadi mpaka atakapotekeleza.” ix.
“Fedheha ya kifo ni dunia, hivyo ulichokitafuta hapa duniani na hujakipata jalia sawasawa na kile kisichogonga fikira zako.”
x.
“Kupitwa na mahitaji yako ni bora zaidi kuliko kuyatafuta kwa asiyestahiki.”91
91
Hayatul-Imam Hasan bin Ali, Juz. 1, Uk. 351na 367 – 370. 43
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Somo la ishirini na nne Bwana wa Mashahidi Imam Husein bin Ali (a.s.) Nasaba yake ing’aayo: Imam Husein (a.s.) ni mjukuu wa pili wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), na ni mmoja wa mabwana wa vijana wa peponi na wa tatu katika orodha ya maimamu kumi na mbili, na ni wa tano katika mjumuiko wa watu wa kishamiya. Ni baba wa maimamu tisa wema (a.s.). Hakika yeye ni tunda la mti wa utume na uimamu, mti wa haki na uadilifu hapa duniani. Baba yake ni mlango wa jiji la elimu ya Mtume (s.a.w.w.) na mama yake ni mbora wa wanawake wote wa ulimwenguni Fatimah Az-Zahrau (a.s.). Na yeye Husein (a.s.) ni miongoni mwa kizazi cha Mtume (s.a.w.w.) ambacho Mwenyezi Mungu amekitakasa dhidi ya uchafu. Mazazi yaliyobarikiwa: Ummul-Fadhli binti wa Al-Harith,92 mke wa Abbas bin Abdul Muttwalib aliota ndoto ya ajabu ambayo hakujua tafsiri yake, hivyo akakimbilia kwa Mtume (s.a.w.w.) na kumwambia: “Mimi nimeota ndoto mbaya, kipande cha mwili wako kimekatwa kisha kikawekwa Ndiye mwanamke wa kwanza kusilimu Makka baada ya Khadija binti Khuwaylid. Alikuwa akipewa nafasi ya kwanza kwa Mtume (s.a.w.w.) hivyo alikuwa akimzuru na kukaa nyumbani kwake. Amepokea hadithi nyingi kutoka kwake. Rejea wasifu wake kwenye kitabu Al-Istiaab na Al-Iswabah, Juz. 4, Uk. 464.
92
44
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
mapajani mwangu.” Mtume (s.a.w.w.) akamwambia: “Umeona jambo zuri, Inshaallah Fatimah atajifungua mtoto wa kiume na mtoto huyo atakuwa mapajani mwako.” Siku zikaenda haraka na hapo Fatimah (a.s.) akajifungua Husein naye akawa mapajani mwa UmmulFadhli kama alivyoeleza Mtume (s.a.w.w.).93 Imepokewa kuwa zilipomfikia Mtume (s.a.w.w.) habari za kuzaliwa mjukuu wake wa pili aliharakisha kwenda nyumba ya kipande cha nyama yake Fatimah (a.s.) huku akihuzunika. Alikwenda kwa upole kisha akatamka kwa sauti hafifu yenye huzuni: “Ewe Asmau niletee mwanangu.” Akampa mjukuu wake akamkumbatia, akaanza kumbusu, kisha akaanza kulia. Asmau akashtuka akamwambia: “Nimekufidia baba na mama yangu, kitu gani kinachokuliza?” Mtume akamjibu huku macho yake yamelowa kwa machozi: “Mwanangu huyu mpendwa ndiye anayeniliza.” Asmau akastaajabu, hakufahamu maana ya tukio hilo, hivyo akaendelea kusema: “Hakika yeye amezaliwa punde tu.” Mtume (s.a.w.w.) akamjibu kwa sauti iliyotanguliwa na huzuni, akasema: “Kundi ovu litamuuwa baada yangu, sintoliombea kundi hilo kwa Mwenyezi Mungu.”94 Kisha akasimama akiwa mzito ilihali ana huzuni na kumwambia Asmau: “Usimwambie Fatimah, hakika yeye katoka kujifungua punde tu muda si mrefu.”95 Mustadrakus-Sahihayn, Juz. 3, Uk. 127. Musnadul-Imam Zayd, Uk. 468. Ndani ya Amaal cha As-Swaduq, Uk. 120 imepokewa kuwa: Mtume (s.a.w.w.) alimchukua Husayn baada ya kuzaliwa kwake akampa Swafiyyah binti Abdul-Muttwalib ilihali akilia na kusema: “Mwenyezi Mungu amewalaani watu watakaokuua ewe mwanangu mpendwa.” Alisema hivyo mara tatu. Swafiyyah akasema: “Nimekufidia mama na baba, ni nani atakayemuuwa?” Akasema: “Litamuuwa kundi ovu kutoka ukoo wa Umaiyyah..” 95 Kashful-Ghummah, Juz. 2, Uk. 216. Ali (a.s.) amepokea kuwa: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.w.) alisema: “Atakayepata mtoto basi amwadhinie sikio la kulia na kukimu la kushoto, kufanya hivyo ni kumkinga dhidi ya shetani aliyelaniwa. Na aliniamuru kufanya hivyo kwa Hasan na Husein. Na pamoja na adhana na ikama amsomee pia sura Al-Fat’ha, Aya Kurusiyi, mwishoni mwa sura Al-Hashri, sura Ikhlas na kinga mbili.” Hilo limepatikana ndani ya kitabu Daaimul-Islam, Juz. 1, Uk. 178. 93 94
45
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Tarehe ya kuzaliwa: Mashuhuri ni kuwa kazaliwa huko Madina mwaka wa nne, maarufu ni kuwa kazaliwa tarehe tatu ya mfungo kumi na moja (Shaabani). Mtume (s.a.w.w.) yeye mwenyewe akamfanyia sunna kama zile alizomfanyia mjukuu wake Hasan (a.s.).96 Akampa jina la Husein kama alivyompa kaka yake jina la Hasan.97 Wakati wa ujahiliya waarabu walikuwa hawayajui majina haya, hata wawaite wana wao, hivyo Mtume (s.a.w.w.) aliwaita majina haya baada ya kuletwa kwa njia ya wahyi.98 Mtume (s.a.w.w.) akasimamia malezi ya Husein usimamizi maalumu hivyo akamjali sana. Akachanganya roho yake na roho yake, matakwa yake na matakwa yake, mpaka akawa anaweka kidole gumba chake kinywani mwake. Imepokewa kuwa baada ya kuzaliwa alimchukua kisha akaweka ulimi wake kinywani mwake ili amlishe mate ya unabii huku akimwambia: “Ewe Husein, Mwenyezi Mungu amekataa isipokuwa analolitaka, nalo liko kwako na kwa kizazi chako…….”99 Maumbile yake: Maumbile ya Husein yalikuwa yakionyesha maumbile ya babu yake, kama yalivyokuwa maadili yake yakionyesha maadili ya Mtume ya kipekee ya juu kuliko ya mitume wote. Baadhi ya askari wa Ibnu Ziyad wameelezea haiba ya Imam (a.s.) kwa kusema: “Hakika nuru ya uso wake na uzuri wa haiba yake vilituondolea wazo la kumuuwa.” Biharul-An’war, Juz. 43, Uk. 238. Usudul-Ghabah, Juz. 2, Uk. 11. Ndani ya kitabu Taarikhul-Khulafai, Uk. 188 amepokea kuwa: Irman bin Sulayman alisema: “Hasan na Husein ni majina miongoni mwa majina ya peponi, waarabu hawakuyasikia majina hayo zama za ujahiliya.” 98 Al-Manaaqib, Juz. 3, Uk. 50. 99 Ansabul-Ashraaf cha Al-Baladhariy, Juz. 1, S. 1. Hapo anaashiria uimamu uliyoendelea kwenye kizazi cha Husein (a.s.). 96 97
46
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Kichwa chake kitukufu kilipoletwa mbele ya shetani Ibnu Ziyad, aliangaziwa na nuru ya uso wa Husein akasema: “Sijaona uzuri mfano wa huu.” Anas ibnu Malik akamjibu ilihali kachukizwa: “Hakika yeye alikuwa anashabihiyana sana na Mtume wa Mwenyezi Mungu.”100 Lakabu na kuniya zake: Baadhi ya sifa za Imam Husein zinadhihirika katika lakabu zake tukufu nazo ni: Shahid, msafi, bwana wa vijana wa peponi, mjukuu wa Mtume,101 mwongozaji, mtekelezaji, mbarikiwa, mfuasi wa radhi za Mwenyezi Mungu,102 alama ya Mwenyezi Mungu, mtakaswa, mwema na mzuia hasira.103 Kuniya yake ni Abu Abdillah.104 Wanahistoria wengi wamesema kuwa hana jina lingine la heshima zaidi ya hilo.105 Inasemekana alikuwa akiitwa kwa jina lingine la heshima nalo ni Abu Ali.106 Baada ya kifo chake watu wakamwita kwa jina la heshima nalo ni AbusShuhadau na Abu Ahrari. Nakshi ya pete zake: Alikuwa na pete mbili moja ya akiki ilikuwa imeandikwa: “Hakika Mwenyezi Mungu ni mfikishaji wa jambo lake.” Ama ya pili ambayo iliporwa siku ya Ashura ilikuwa imeandikwa: “Hapana Mola wa haki isipokuwa Allah. Ni maandalizi ya kukutana na Allah.”107 ayatul-Imam Hasan bin Ali, Juz. 1, Uk. 38 kutoka kwenye Tuhfatul-Azhaar H Wazilalul-Anhaar. 101 Nurul-Absaar, Uk. 114. Jawharul-Kalami Fimadhis-Saadatil-Aaalam, Uk. 116. 102 Dalalilul-Imamah, Uk. 73. 103 Al-Irshad, Uk. 103. 104 Al-Fusuulul-Muhimmah, Uk. 176. Nurul-Absaar, Uk. 152. 105 Al-Manaaqib, Juz. 4 Uk. 717. Ansaabul-Ashraaf, Juz. 1 S. 1 106 Dalalilul-Imamah, Uk. 76. 107 Kashful-Ghummah, Juz. 3, Uk. 6. 100
47
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Vipindi vya maisha yake: Imam Husein aliishi chini ya kivuli cha babu yake zaidi ya miaka sita. Akaishi na mama yake karibu miaka saba. Akaishi na baba yake zaidi ya miaka thelathini na sita. Akaishi na kaka yake Hasan zaidi ya miaka arubaini na sita. Karibu muda wa miaka kumi alikuwa peke yake katika uimamu na jukumu la kuongoza umma baada ya babu yake, baba yake na kaka yake. Alikuwa aking’oa dhulma ya Bani Umaiyya kwa ulimi wake na maneno yake mpaka ukweli ukadhihirika kwa aliye mbali na karibu kuwa watoto wa Abu Suf’yani wanajificha kwa pazia ya Uislamu ilihali wao ni maadui wakubwa wa Uislamu, hawana dini wala imani, hivyo akasimama kama mlima imara dhidi ya ubeberu wa Yazid, na nia yake na dharau yake dhidi ya maadili ya Uislamu. Kwa damu yake, damu ya kizazi chake na damu ya maswahaba zake wema akaandika kiwango cha juu cha kujitolea na kufidia njia ya imani ya haki na kuhuisha sheria ya babu yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na hapo yakatimia maelezo ya babu yake aliposema: “Husein anatokana na mimi na mimi natokana na Husein.”108 Amani iwe juu yake siku aliyozaliwa, siku ya kufa kwake shahidi, na siku atakayofufuliwa akiwa hai. Muhtasari: Matakwa ya Mwenyezi Mungu yalitaka kizazi cha Mtume (s.a.w.w.) kikomee kwa kizazi cha Ali na Fatimah (a.s.). Mtume (s.a.w.w.) na watu wa nyumba yake waliishi kwa furaha kwa kuzaliwa Hasan, haukupita mwaka mmoja Mtume (s.a.w.w.) akabashiriwa kuzaliwa kwa mjukuu wake wa pili Husein (a.s.). Huzuni zilifuata furaha ya mazazi ya Husein, hivyo Mtume (s.a.w.w.) akahuzunika sana alipo108
Tazama Sunan Ibnu Majah, Juz. 1, Uk. 51. Amaalil-Murtadha, Juz. 1 Uk. 219. 48
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
jua kuwa matatizo makubwa yatampata mwanae Husein huku akiwa ni Imam na Khalifa, kwani umma uliopotea utasimama kidete kumuuwa. Kati ya Husein (a.s.) na babu yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuna mambo mengi ya kushabihiana. Anashabihiana nae katika sura, mwonekano wake na maadili yake. Pia alishabihiana nae katika msimamo kwani Mtume (s.a.w.w.) alianzisha mapinduzi katika ulimwengu wa wanadamu pindi alipotangaza Uislamu, na Husein (a.s.) alianzisha mapinduzi ndani ya umma wa kiislamu, akatikisa nyoyo za wanadamu ili zisimame na kutekeleza jukumu lao mbele ya dini yao na ujumbe wa Mola wao. Imam Husein (a.s.) alipambana na tatizo la utawala kupindishwa na hatari dhidi ya Uislamu, akafuata njia ya baba yake na kaka yake katika mapambano hayo, kisha akasimamisha mapinduzi huku akijitoa muhanga yeye mwenyewe, watu wa nyumba yake na maswahaba zake wema ili kuamsha dhamira za umma na kuhuisha utashi wake, hivyo akafa shahidi katika njia ya haki, akijisalimisha kwenye matakwa ya Mwenyezi Mungu akiwa mshindi aliyekataa udhalili, mwenye subira na mvumilivu. Utu wa Imam Husein (a.s.) ulikuwa wa hali ya juu, hivyo uliathiri sana umma wa kiislamu na mpaka leo bado unaendelea kuangazia katika mbingu ya ubinadamu. Maswali: 1. Imam Husein (a.s.) alizaliwa lini na ilikuwa wapi? 2. Imam Husein aliishi miaka mingapi akiwa na babu yake, baba yake na kaka yake?
49
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
3. Je, Mtume (s.a.w.w.) alikuwa anajua yatakayompata mwanae Husein (a.s.), na alisema nini kuhusu hilo? 4. Elezea kwa muhtasari sifa na mwonekano wa Imam Husein? 5. Taja hadithi ya Mtume inayotoa maelezo kuhusu uimamu wa Imam Husein (a.s.)? Kwa ajili ya kujisomea i.
Umar bin Al-Khattab alimwambia Husein: “Hakika aliyeotesha unayoyaona katika vichwa vyetu ni Mwenuyezi Mungu kisha wewe.”109
ii.
Uthman bin Affan alisema kuhusu Hasan na Husein: “Walijitofautisha kwa elimu, wakapata kheri na hekima.”110
iii.
Husein alikuwa akisindikiza jeneza, ghafla akaketi chini kwa kuchoka, Abu Hurayra akaanza kupangusa udongo kwenye miguu yake kutumia nguo yake. Imam akamwambia: “Ewe Abu Hurayra, hivi na wewe unafanya hivi?” Akajibu: “Niache, naapa kwa Mwenyezi Mungu laiti watu wangejua kutoka kwako yale ninayoyajua basi wangekubeba juu ya mabega yao.”111
iv.
Abdullah bin Abbas aliwaletea Hasan na Husein vipando vyao. Watu wakamlaumu wakamwambia: “Wewe ni mkubwa kiumri zaidi yao.” Akajibu: “Hawa wawili ni watoto wa Mtume, hivi hamuoni kuwa ni wema kwangu kuwaletea vipando vyao.”112 Baada ya kifo cha Hasan Muawiya alise-
Al-Iswabah, Juz. 1, Uk. 333, amesema njia yake ya upokezi ni sahihi. Al-Khiswal, Uk. 136. 111 Al-Khiswal, Uk. 136. 112 Taarikh Ibnu Asaakir, Juz. 4, Uk. 322. 109 110
50
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
ma: “Ewe Ibnu Abbas, umekuwa bwana wa watu wako.” Akajibu: “Ama muda huu ambao bado Mwenyezi Mungu amembakisha Abu Abdillah mimi si bwana.”113 v.
Abu Barzatu Al-Aslamiy alipomwona Yazid akichezea meno ya Husein alimwambia: “Hivi unachezea meno ya Husein kwa fimbo yako? Hakika fimbo yako imechukua nafasi niliyomwona Mtume (s.a.w.w.) akiibusu midomo yake. Hakika wewe Yazid utakuja siku ya Kiyama ilihali Ibnu Ziyad ndiye mwombezi wako, na atakuja huyu ilihali Muhammad (s.a.w.w.) ndiye mwombezi wake.”114
vi.
Muawiya alimwambia Abdullah bin Jafar: “Wewe ni bwana wa Bani Hashim.” Akamjibu: “Bwana wa Bani Hashim ni Hasan na Husein.”115 Abdullah bin Jaafariy alimwandikia Husein: “Iwapo ukifariki leo basi nuru ya Uislamu itakuwa imetoweka, hakika wewe ni bendera ya waongokao na matarajio ya waumini.”116
vii.
Mtu mmoja alimuuliza Abdullah bin Umar kuhusu damu ya mbu inayokuwa kwenye nguo, je, aswali na nguo hiyo? Abdullah akamuuliza: “Wewe umetoka wapi?” Akajibu: “Kutoka Iraki.” Akasema: “Jamani mtazameni mtu huyu, eti ananiuliza kuhusu damu ya mbu huku wamemuuwa mtoto wa Mtume ilihali nilimsikia Mtume (s.a.w.w.) akisema: “Wao wawili ni manukato yangu hapa duniani.”117
viii. Muhammad bin Al-Hanafiyya amesema: “Huseini ni mjuzi kielimu kuliko sisi, ni mvumilivu kuliko sisi, na kiundugu 113 114
Hayatul-Imam Hasan bin Ali cha Al-Qarashiyyu, Juz. 2, Uk. 500.
Al-Hasan Wal-Husein Sibta Rasulillah Uk. 198.
Al-Hasan bin Ali cha Kamil Sulayman, Uk. 173. Al-Bidayatu Wan-Nihayah, Juz. 8, Uk. 167. 117 Taarikh Ibnu Asaakir, Juz. 4, Uk. 314. 115 116
51
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
yeye ni wa karibu mno na Mtume (s.a.w.w.) kuliko sisi, alikuwa ni Imam na mjuzi wa sheria.”118 ix.
Imam Husein alipita ilihali Amru bin Aas akiwa ameketi kwenye kivuli cha Al-Kaaba, hapo Amru akasema: “Huyu ni wa ardhini aliye kipenzi mno leo kwa watu wa ardhini na kwa watu wa mbinguni.”119
x.
Muawiya alimwambia mwanawe Yazid: “Sikuacha kutamani kumtia dosari Husein lakini naapa kwa Mwenyezi Mungu sioni kwake sehemu ya dosari.”120
xi.
Hotuba ya Yazid bin Mas’ud An-Nahshaliyu: “Huyu ni Husein bin Ali mtoto wa Mtume, mwenye sharafu na sifa asili, fadhila zake hazisifiki, elimu yake haizuiliki, yeye ndiye anayestahiki jambo hili kwa umwanzo wake katika Uislamu na ukaribu wake kwa Mtume, kuhurumia watoto na kuheshimu wakubwa. Muheshimuni sana, yeye ni Imam wa kaumu hii, Mwenyezi Mungu ametimiza hoja kupitia yeye na akafikisha nasaha kupitia yeye.”121
xii. Ibnu Sirin amesema: “Mbingu haijamlilia yeyote baada ya Zakaria ila Husein. Alipouawa mbingu ilififia na nyota zikawaka mchana mpaka nyota ya Jawzau ikaonekana wakati wa alasiri, udongo mwekundu ukadondoka huku mbingu ikabakia kama kipande cha damu kwa siku saba usiku na mchana.”122 Biharul-An’war, Juz. 10, Uk. 140. Taarikh Ibnu Asaakir, Juz. 4, Uk. 322. 120 Aayanus-Shiah, Juz. 1, Uk. 583 na 590. 121 Aayanus-Shiah, Juz. 1, Uk. 583 na 590. 122 Taarikh Ibnu Asaakir, Juz. 4, Uk. 339. 118 119
52
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Somo la ishirini na tano Fadhila za Imam Husein na mwonekano wake: Kuna sifa mbalimbali za ukamilifu zilizoonekana kwa Imam Husein (a.s.), hivyo hapa tutaashiria baadhi ya sifa hizo: Nguvu ya maamuzi: Imam mjukuu shahidi alisimama kidete dhidi ya utawala wa Bani Umaiyya, akatangaza kupinga kumtii Yazid, akaondoka kwenda uwanja wa mapambano akiwa na wafuasi wachahe ili ainue haki na aangamize batili. Dola ya Umaiyya ikakusanya jeshi kubwa la kutosha lakini hakulijali bali alitangaza azma yake na maamuzi yake kwa neno lake la kudumu: “Hakika mimi sioni kifo isipokuwa ni wema, na kuishi na madhalimu isipokuwa ni uovu.”123 Akaondoka kuelekea uwanja wa heshima na utukufu akiwa yeye na familia yake watu wa nyumba yake na maswahaba zake ili ainue bendera ya Uislamu, na autimizie umma wa kiislamu ushindi mkubwa, mpaka alipokufa kishahidi huku akiwa na nguvu ya maamuzi na azma imara na shupavu ilihali hatetemeshwi na matatizo yaliyompata ambayo huchanganya akili na kuogopesha. Kukataa udhalili: Kati ya lakabu zake zilizoenea kwa watu ni Abu Dhaymi “Mkataa udhalili.” Alikuwa ni mfano bora wa sifa hii kwani yeye aliinua mbiu ya heshima na akachora njia ya sharafu na heshima, mpaka Ibnu 123
Al-Wathaiqur-Rasmiyyah Lithawratil-Imam Husayn, Uk. 112. 53
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Abul-Hadid Al-Muutaziliy akamzungumzia kwa kusema: “Yeye ni bwana wa wakataa udhalili, aliwafundisha watu hasira na kifo chini ya kivuli cha mapanga ili kuchagua cha thamani na kuacha cha udhalili. Yeye na maswahaba zake walitangaziwa usalama, akakataa udhalili, akahofia Ibnu Ziyad asimsababishie aina yoyote ya udhalili japokuwa hatomuuwa. Hivyo akachagua kifo badala ya udhalili.”124 Maneno yake siku ya Karbala ni miongoni mwa maneno bora ya waarabu katika kutoa taswira halisi ya heshima, kupinga udhalili na kujitegemea hivyo akasema: a. “Fahamuni kuwa hakika mtuhumiwa wa nasaba, mtoto wa mtuhumiwa wa nasaba amenihakikishia moja kati ya haya mambo mawili: Kati ya sumu ya upanga na udhalili, na kamwe hatutochagua udhalili, Mwenyezi Mungu hataki hilo kwetu, wala Mtume wake na waumini, na hata akili safi zilizotakasika, nyoyo na nafsi zenye heshima zinakataa kutanguliza utii wa muovu kuliko mapigano yenye heshima.”125 b. Naapa kwa Mwenyezi Mungu sitotoa mkono wangu kwenu utoaji wa mtu dhalili, wala sitokimbia ukimbiaji wa mtumwa, mimi najikinga kwa Mola wangu na Mola wenu msije mkanishinda.”126 Ushujaa: Historia haijamshuhudia mtu shujaa, jasiri, wala mkakamavu kama Imam Husein siku ya Ashura, alisimama msimamo ambao ulishangaza na kushtua akili hadi mataifa yaliyofuata yakawa yakizungumzia kwa ajabu na upana kuhusu ushujaa wake. Aliwachosha maadui zake kwa ukali wa nguvu zake, kwani hakudhoofika mbele Sharhu Nahjul-Balagha cha Ibnu Abul-Hadid, Juz. 1, Uk. 302. Biharul-An’war, Juz. 45, Uk. 8. Ithbatul-Waswiyyah cha Al-Mas’udiy, Uk. 142. 126 Al-Kamil Fit-Tarikh, Juz. 3, Uk. 287. Iilamul-Waraa, Juz. 1, Uk. 459. 124 125
54
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
ya makundi ya kutisha ambayo yalikuwa yakilundikana kwake, bali alizidi kuchangamka na kuwa mshupavu kila balaa na tatizo linavyoongezeka. Baada ya kuondokewa na watu wa nyumba yake na maswahaba zake, jeshi lilimzunguka likiwa na watu kama elfu thelathini, lakini alipambana nao peke yake mpaka akaingiza na kumilikisha khofu na uoga ndani ya nyoyo zao. Hivyo wakawa wakidondoka mbele yake kama kondoo waliozidiwa na mbwa mwitu, akabaki imara kama mlima huku akipokea mashambulizi ya mishale toka kila eneo ilihali akiendelea na mapambano kwa ajili ya kutaka na kutojali kifo. Imam Husein (a.s.) alivuka hali ya kawaida ya mwanadamu katika ushujaa wake, akadharau mauti kiasi kwamba pindi mishale ya maadui ilipozidi dhidi yake pale kabla ya vita kuanza, alisema kuwaambia maswahaba zake: “Simameni kiendeeni kifo ambacho ni lazima kukiendea hakika Mwenyezi Mungu atawarehemu. Kwani hakika mishale hii ni ujumbe wa watu hawa kwenu…”127 Uwazi wa maneno: Uwazi katika kauli na ujasiri katika vitendo ni matunda ya ushujaa, na Husein (a.s.) alijulikana kwa uwazi huu na ujasiri ule, kwani hakupita njia yoyote yenye maficho bali ilikuwa ni njia ya wazi ambayo inalingana na dhamira yake iliyo hai ilihali akijiepusha na mabonde ambayo hayakubaliani na dini yake na maadili yake. Miongoni mwa mifano ya uwazi wake ni kuwa: Al-Walid gavana wa Madina alimwita usiku akampa habari za kuhiliki kwa Muawiya, kisha akamtaka ampe Yazid kiapo cha utii kwa siri. Imam (a.s.) alikataa na kumuwekea wazi kuwa: “Ewe kiongozi, sisi ni kizazi cha Mtume (s.a.w.w.) na chimbuko la Uislamu, kupitia sisi Mwenyezi 127
Aayanus-Shiah, Juz. 1, Uk. 603. Al-Luhuuf, Uk. 65. 55
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Mungu alifungua na kuhitimisha, na Yazid ni fasiki muovu, mnywa pombe, muuwaji wa nafsi zilizoharamishwa na mwenye kudhihirisha ufasiki na uovu wake, hivyo mtu kama mimi siwezi kutoa kiapo cha utii kwa mtu kama yeye.”128 Ushupavu katika haki: Imam Husein (a.s.) alitetea haki kwa viwango vyake vyote na sehemu zake zote, akaenda kwenye viwanja vya mishale ili asimamishe haki katika ardhi. Imam (a.s.) aliona umma umezamishwa na batili wala nasaha za maneno haziufai, hivyo akaenda kwenye viwanja vya muhanga na kujitolea ili ainue bendera ya haki. Imam (a.s.) alitangaza lengo hili mwanzoni tu mwa hotuba yake aliyoitoa mbele ya maswahaba zake huko Makka, akasema: “Hivi hamuoni kuwa haki haifanyiwi kazi wala batili haikatazwi, basi muumini atamani kukutana na Mwenyezi Mungu…”129 Subira: Imam Husein (a.s.) alijitofautisha kwa subira dhidi ya misukosuko ya dunia na matatizo ya kila siku, alimeza uchungu wa subira tangu alipokuwa mtoto, hivyo akapatwa na msiba wa babu yake na mama yake, akashuhudia matukio ya kutisha yaliyompata baba yake baada ya kifo cha babu yake. Akapatwa na matatizo na misukosuko iliyomfanya ameze uchungu wa subira zama za kaka yake. Alikuwa akiona jinsi jeshi likimsaliti na kumtosa kaka yake mpaka akalazimika kufanya suluhu, wakabaki pamoja akishirikiana naye katika matatizo na maumivu yake mpaka Muawiya alipomuuwa kwa sumu. Na alipotaka kuzika mwili mtakatifu wa ndugu yake 128 129
Ansabul-Ashraaf, Juz. 1, S. . Biharul-An’war, Juz. 44, Uk. 381. Yanabiul-Mawaddah, Uk. 406. 56
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
karibu na kaburi la babu yake, Banu Umayya walimzuwia, nalo hilo likawa ni tatizo juu yake. Miongoni mwa misiba mikubwa aliyovumilia ni ile hali ya kuona jinsi misingi ya Uislamu inavyotenguliwa na hadithi za uwongo zinazopingana na sheria ya Mwenyezi Mungu zikinasibishwa na babu yake mtukufu (s.a.w.w.) ilihali yeye akijaribu kusawazisha kwa kila nguvu aliyokuwa nayo. Miongoni mwa misukosuko iliyompata ni kuwa alikuwa akisikia matusi ya Banu Ummaya dhidi ya baba yake, wakimkashifu waziwazi juu ya mimbari huku muovu Ibnu Ziyad akiwauwa na kuwatesa wafuasi wao na vipenzi vyao. Matatizo magumu na makubwa yalimfika siku ya kumi ya mfungo nne mwaka sitini na moja hijiriya, hivyo kabla hajamaliza matatizo akazungukwa na kundi la misiba na machungu, akawa akisimama kwenye nyota zing’aazo ambazo ni wanawe na watu wa nyumba yake ilihali panga na mikuki vikiwa vimeshawagombania, akawa akiwaita kwa uhakika na kujiamini: “Kuweni na subira enyi watu wa nyumba yangu, kuweni na subira enyi wana wa ami zangu, kwani hamtoona udhalili baada ya siku hii.”130 Alipomuona Zaynab (a.s.) kachanganyikiwa na msiba ilihali machungu yamepasua moyo wake, alimwendea kumtaka awe na subira na aridhike na alichokigawa Mwenyezi Mungu. Miongoni mwa uchungu wa matatizo aliyovumilia Husein (a.s.) ni kuwa alikuwa akiwatazama wanawe na familia yake wakipiga kelele kwa ukali wa kiu ilihali wakimuomba msaada, lakini alikuwa akiwataka wasubiri na wawe na msimamo huku akiwapa habari kuhusu malipo bora yanayofuata jinsi yanavyowasubiri baada ya matatizo haya. Alikuwa na subira kwa kukutana na maadui ambao walijaza ardhi kwa makundi yao ilihali yeye akiwa mmoja peke yake, akapokea 130
Al-Wathaiqur-Rasmiyyah Lithawratil-Imam Husayn, Uk. 229. 57
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
mapigo na mashambulizi ya mishale toka kila sehemu. Ini lake liliungua kwa kiu lakini hakutetereka kwa hilo. Msimamo wake siku ya Ashura ulikuwa imara kuliko msimamo wowote anaoufahamu mwanadamu, mpaka mwanahistoria Al-Arballiy akasema: “Ushujaa wa Husein ni wa mfano, na subira yake katika vita haikuwezekana kwa waliyotangulia wala haitowezekana kwa wale watakaofuatia.”131 Muhtasari Imam Husein (a.s.) amekusanya kila sifa na fadhila zinazomwinua mwanadamu. Vipi itashindikana kuwa hivyo ilihali kalelewa mikononi mwa mlezi mkuu wa mwanadamu huku akisuhubiana na utume wake, hivyo akanywa uongofu toka chemchemu yake mpaka Mtume (s.a.w.w.) akamzungumzia kwa kusema: “Husein anatokana na mimi na mimi natokana na Husein.” Ujumbe wa Muhammad (s.a.w.w.) uliendelea kwa baraka za damu ya Husein (a.s.), damu ya watu wa nyumba yake na damu ya maswahaba zake. Husein (a.s.) alikuwa mshupavu wa maamuzi, mwenye azma imara, mwenye yakini ya kweli huku akitetea ujumbe wa Uislamu na hadhi ya haki na uadilifu. Alifanya hivyo kwa maneno mazuri na upanga mkali. Pia hakukubali udhalili bali alikuwa mtukufu wa nafsi, shujaa na jasiri ilihali wingi wala kelele havimtishi, hivyo hakuficha wala hakujali kutelekezwa, na kusita kwa wengine, bali hakutetemeka wala hakukata tamaa mbele ya mng’ao na mwanga wa mapanga. Maswali: 1. Elezea mahusiano yaliyopo kati ya nguvu ya maamuzi na kutokukubali udhalili? 131
Kashful-Ghummah, Juz. 2, Uk. 20. 58
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
2. Toa ushahidi juu ya nguvu ya maamuzi aliyokuwa nayo Husein (a.s.) kwa kupitia maneno yake yanayoonyesha nguvu ya maamuzi na kukataa kwake udhalili? 3. Elezea uhusiano uliyopo kati ya uwazi na ushujaa? 4. Onyesha msimamo wa Husein (a.s.) unaodhihirisha uwazi wake katika kauli ya haki? 5. Toa sura tatu zinazoonyesha subira ya Imam Husein? Kwa ajili ya kujisomea Fadhila za Husein (a.s.) na mwonekano wake Usamehevu: Kati ya sifa nzuri alizokuwa nazo Husein (a.s.) ni usamehevu. Kati ya mambo waliyokubaliana wapokezi wa hadithi kuhusu yeye ni kuwa halipizi ubaya kwa ubaya, wala dhambi kwa dhambi, isipokuwa anastarehesha kwa wema wake ilihali hali yake katika hilo ni hali ya babu yake ambaye aliwafikia watu wote kwa maadili yake na tabia zake. Alifahamika kwa sifa hii huku ikienea kutoka kwake, mpaka baadhi ya vijakazi na watumwa wake wakawa wanatumia mwanya huu, hivyo wakawa wakimkosea makusudi ili waneemeshwe kwa wema wake. Unyenyekevu: Imam Husein (a.s.) aliumbwa katika hali ya unyenyekevu na kujiepusha na majivuno na kiburi. Sifa hii nzuri aliirithi kutoka kwa babu yake ambaye alisimamisha misingi ya maadili bora na fadhila hapa duniani.
59
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Huruma na upole: Imam Husein (a.s.) alikuwa akiwahurumia sana watu akimsaidia kila mwenye haja. Akimhudumia kila mwenye tatizo, anamsogelea kila anayetaka kusogelewa. Mar’wan bin Al-Hakam alishangazwa na Husein na ndugu yake Hasan pindi alipochukuliwa mateka baada ya vita vya Jamal. Aliwaomba wamwombee msamaha kwa baba yao. Wakaongea na baba yao Ali (a.s.) kuhusu Mar’wan wakamwambia: “Ewe kiongozi wa waumini, atakupa kiapo cha utii.” Imam Ali (a.s.) akajibu: “Kwani hakunipa kiapo cha utii baada ya Uthman? Sihitaji kiapo chake hakika yeye ni kiganja cha kiyahudi, hivyo laiti akinipa kiapo cha utii kwa mkono wake atakivunja kwa siri, ana utawala kama mbwa alambavyo kwa pua yake, na yeye ni baba wa kondoo wanne, na umma utapata siku nyekundu toka kwenye kizazi chake.”132 Walioendelea kumlainisha baba yao mpaka akamsamehe, isipokuwa Mar’wan hakuthamini wema huu, hivyo akawalipa wajukuu wawili hawa kila shari na ubaya anaoumiliki. Ukarimu: Husein (a.s.) alikuwa kimbilio la mafakiri na wasio na kitu, na kimbilio la yule ambaye siku ngumu zimempitia. Alikuwa akipoza nyoyo za wanao mkimbilia kwa kuwazawadia na kuwapa. Kamalud-Diin bin Twalha amesema: “Ni mashuhuri kuwa alikuwa akimkarimu mgeni, akimpa mtafutaji, akiunga undugu, akimpa huduma ya kwanza mwombaji, akimvisha asiye na mavazi, akimshibisha mwenye njaa, akimlipia mwenye deni, akimpa nguvu aliye dhaifu, akiwahurumia yatima, akimtosheleza mwenye haja. Na kila alipopata mali aligawa na hiyo ndio tabia na asili ya mkarimu, alama 132
Nahjul-Balagha, hotuba ya 73. 60
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
ya mwenye kujali watu na sifa yenye kukusanya maadili bora, hivyo vitendo vyake vilivyotajwa ni ushahidi tosha juu ya ukarimu wake na vinaelezea kuwa yeye alipambika na maadili bora.”133 Wanahistoria wanasema kuwa alikuwa akibeba gunia usiku akijaza vyakula na pesa akiwapelekea wajane, yatima na masikini majumbani mwao, mpaka akakutwa na alama mgongoni.134 Alikuwa akiletewa vyakula vingi lakini hasimami mpaka akung’ute chombo kilichokusanya. Muawiya mwenyewe aliitambua sifa hii kwa Husein hivyo akamtumia zawadi kama alivyowatumia zawadi wengine miongoni mwa watu wa Madina. Akaanza kuwaeleza waliomzunguka jinsi kila mmoja atakavyofanya juu ya zawadi hizo. Akasema kuhusu Husein (a.s.): “Ama Husein huanza kwa mayatima waliofiwa na wazazi wao katika vita vya Suffin, na kama zitabakia basi huchinjia wanyama na kunyweshea maziwa.” Kisha akatuma mfuatiliaji aone watakavyofanya wale waliotumiwa zawadi, akakuta ni kama alivyoeleza, Muawiya akasema: “Mimi ni mtoto wa Hindu, mimi nawafahamu makurayshi kuliko wanavyojifahamu.”135 Bedui mmoja alikwenda kwa Husein (a.s.) akamsalimia kisha akamwomba haja yake ilihali akisema: “Nilimsikia babu yako akisema: “Mkiomba haja zenu ziombeni kutoka kwa watu wanne: Kutoka kwa mwarabu sharifu, au bwana mkarimu au mbeba Qur’ani au mwenye uso ung’aao.” Ama waarabu wamepata sharafu kupitia babu yako. Ama ukarimu ni asili yenu na mwenendo wenu. Ama Qur’ani yenyewe iliteremka majumbani mwenu. Ama uso ung’aao, hakika mimi nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akisema: “Mkitaka kunitazama mtazameni Hasan na Husein.’” Matwalibus-Suul, Uk. 73. Rayhanatur-Rasuul, Uk. 71. 135 Uyunul-Akhbar, Juz. 3, Uk. 40. 133 134
61
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Husein (a.s.) akamwambia: “Unahitaji nini?” Hapo bedui akaandika haja yake aridhini. Husein (a.s.) akamwambia: “Nilimsikia baba yangu Ali akisema: “Wema ni kwa kiwango cha maarifa.” Hivyo mimi nakuuliza mambo matatu iwapo utajibu moja nitakupa theluthi ya nilichonacho, na ukijibu mawili nitakupa theluthi mbili ya nilichonacho, na ukijibu yote matatu nitakupa chote nilichonacho. Na tambua kuwa nimeletewa fuko la fedha kutoka Iraki.” Bedui akasema: “Uliza hakuna nguvu wala ujanja isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu.” Imam Husein (a.s.) akasema: “Ni amali gani iliyo bora mno?” Akajibu: “Kumwamini Mwenyezi Mungu.” Akamuuliza: “Ni kitu gani kinachomwokoa mja asiangamie?” Akajibu: “Kumtegemea Mwenyezi Mungu.” Akamuuliza: “Kitu gani kinachompamba mtu?” Akajibu: “Elimu yenye hekima.” Akamuuliza: “Akikosa hilo?” Akajibu: “Mali yenye ukarimu.” Akamuuliza: “Akikosa hilo?” Akajibu: “Ufakiri wenye subira.” Akamuuliza: “Akikosa hilo?” Akajibu: “Kimondo kitokacho mbinguni na kumuunguza.” Hapo Imam (a.s.) akacheka na kumpa fuko la fedha.136 136
adhailul-Khamsa minas-Swahahis-Sittah, Juz. 3, Uk. 268. Tarikh ibnu AsaaF kir, Juz. 4, Uk. 323. 62
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Ibada zake na uchamungu wake: Imam Husein (a.s.) alimwelekea Mwenyezi Mungu akiwa amejaa mapenzi Yake na amejielekeza Kwake tu huku akimwogopa, alitenda kila litakalomkurubisha kwa Mwenyezi Mungu. Alikuwa ni mwingi wa swala, funga, hija, sadaka na matendo ya kheri.137 Hapa tutagusia baadhi ya yale yaliyopokewa kuhusu ibada zake. Khofu dhidi ya Mwenyezi Mungu: Imam (a.s.) alikuwa kinara wa wale wanaomjua Mwenyezi Mungu. Alikuwa akimwogopa sana, akijitahadhari sana kumkhalifu, mpaka baadhi ya maswahaba zake wakamwambia: “Kwa nini unamwogopa mno Mola wako?” Akajibu: “Hatosalimika mtu Siku ya Kiyama isipokuwa yule aliyemwogopa Mwenyezi Mungu hapa duniani.”138 Wingi wa Swala na funga zake: Alikuwa akijishughulisha sana na Swala na funga139 muda wake wote mpaka akawa akiswali jumla ya rakaa elfu moja usiku na mchana. Haya ni kama alivyoeleza mwanae Zaynul-Abidiin.140 Alikuwa akihitimisha Qur’ani ndani ya mwezi wa Ramadhani.141 Ibnu Zubayri amezungumzia ibada ya Imam (a.s.) akasema: “Naapa kwa Mwenyezi Mungu hakika wamemuuwa ambaye kisimamo chake usiku kilikuwa kirefu, funga yake mchana ilikuwa nyingi.”142 Tahdhibul-Asmai, Juz. 1, Uk. 163. Rayhanatur-Rasuul, Uk. 58. 139 Tahdhibul-Asmai, Juz. 1, Uk. 163. 140 Taarikhul-Yaaqubiy, Juz. 2, Uk. 219. 141 Siratul-Aalamun-Nubalai, Juz. 3, Uk. 193. 142 Taarikhut-Tabariy, Juz. 6, Uk. 273. 137 138
63
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Kuhiji Kwake: Husein (a.s.) alikuwa mwingi wa hija, alihiji hija ishirini na tano akienda kwa nyayo zake.143 Alikuwa akiishika nguzo nyeusi na kumwomba Mola wake: “Ewe Mola wangu, umenineemesha ilihali hujanikuta nikikushukuru, umenipa mitihani hujanikuta nikivumilia. Hujaninyang’anya neema kwa kuacha kukushukuru, wala hujanidumisha ndani ya shida kwa kuacha kuvumilia. Ewe Mola wangu, hayatoki kwa mkarimu isipokuwa ukarimu.”144 Sadaka zake: Alikuwa mwingi wa wema na sadaka. Alirithi ardhi na vitu mbalimbali lakini akavitoa sadaka kabla hajaviweka mikononi.145 Alikuwa akibeba chakula usiku na kuwapelekea masikini wa Madina146 ilihali hatafuti chochote katika hayo isipokuwa ujira toka kwa Mwenyezi Mungu na kujikurubisha Kwake. Kipaji cha elimu: Hakuna yeyote aliyemkaribia Husein (a.s.) katika fadhila na elimu yake, aliwashinda wengine kwa kipaji cha elimu yake. Tangu alipokuwa mtoto alianza kunywa elimu kutoka kwenye mrija wa elimu ya babu yake ambayo iliangaza ulimwengu huu. Pia alikunywa elimu ya baba yake, mlango wa jiji la elimu ya Mtume (s.a.w.w.), mjuzi kuliko umma wote na maswahaba wote, na mjuzi wa sheria ya dini kuliko wao. Abdullah bin Abbas amesema: “Husein alitokana na nyumba ya utume na wao ndio warithi wa elimu.”147 Tarikh ibnu Asaakir, Juz. 13, Uk. 254. Al-Kawakibud-Duriyyah, Juz. 1, Uk. 58. 145 Daaimul-Islam, Juz. 2, Uk. 337. 146 Tadhkiratul-Khuwwas, Uk. 264. 147 Hayatul-Imam Husayn bin Ali, Juz. 1, Uk. 135. 143 144
64
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Imam Husein (a.s.) alikuwa ni marejeo ya fatwa katika ulimwengu wa kiislamu. Maswahaba wakubwa walikuwa wakirejea kwake katika maswala ya dini. Miongoni mwa watu waliorejea kwake ni Abdullah bin Zubayr aliyemuuliza Husein: “Ewe Abu Abdillah, unasemaje kuhusu kumwachia mateka, ni nani mwenye jukumu hilo?” Akajibu: “Ni la watu aliowasaidia au aliopigana pamoja nao.” Akamuuliza tena: “Ewe Abu Abdillah, ni muda gani nalazimikiwa na matumizi ya mtoto?” Akajibu: “Atakapotoa sauti wakati wa kuzaliwa basi ni lazima kumpa fungu lake na riziki yake.” Akamuuliza swali la tatu kuhusu kunywa wima. Imamu akaomba ngamia wake, akakamuliwa maziwa kisha akanywa wima, kisha akampa muulizaji.148 Kikao chake kilikuwa cha heshima na elimu, alijichanganya na wahitaji elimu kati ya maswahaba zake, huku wakichukua hekima na adabu anayowapa, wakisajili hadithi anazowasimulia kutoka kwa babu yake. Imepokewa kuwa watu walikuwa wakikusanyika kwake kumsikiliza ilihali wametulia kama vile juu ya vichwa vyao kumetua ndege, wanasikiliza elimu pana na simulizi za kweli.149 Kikao chake kilikuwa ni ndani ya msikiti wa babu yake huku akiwa na kipindi maalumu kuhusu babu yake. Kuna mkurayshi mmoja alimuuliza Muawiya: “Nitampata wapi Husein?” Akamjibu: “Ukiingia msikiti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, kisha ukaona kundi la watu kama vile juu ya vichwa vyao kuna ndege basi hilo ndilo darasa la Abu Abdillah Husein.”150 Imam Husein (a.s.) alikuwa kiongozi wa wasomi na wanamitazamo wa zama zake. Alijitahidi na kushiriki kwa uimara katika kueneza elimu ya kiislamu. Akatandaza na kueneza maarifa na adAl-Istiab iliyochapwa pambizoni mwa Al-Iswabah, Juz. 2, Uk. 283. Hayatul-Imam Husayn bin Ali, Juz. 1, Uk. 136 - 137. 150 Tarikh ibnu Asaakir, Juz. 4, Uk. 222. 148 149
65
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
abu kwa watu. Maswahaba wengi, wakubwa kwa wadogo, wao na watoto wao wote walipata elimu kupitia mrija wa maarifa na elimu yake.
66
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Somo la ishirini na sita Urithi wa Imam Husein (a.s.)
M
wenyezi Mungu alimpa Husein (a.s.) hekima na ufasaha wa kuongea, hivyo hekima na mawaidha vilikuwa vikibubujika toka ulimini mwake. Zifuatazo ni baadhi ya hekima zake: i.
“Mwenye akili hamsimulii anayekhofia upingaji wake, wala hamuombi anayekhofia unyimi wake, wala hamwamini asiye na uwaminifu, wala katika matatizo hamtarajii asiyeaminika.”151
ii.
Alimwambia mwanae Ali (a.s.): “Ewe mwanangu mpendwa, jiepushe na kitendo cha kumdhulumu asiye na msaidizi juu yako ila Mwenyezi Mungu.”152
iii. “Mwenyezi Mungu hakuchukua nguvu ya mtu isipokuwa alimpunguzia utiifu wake, wala hakuchukua uwezo wake isipokuwa alimpunguzia majukumu.” 153 iv.
“Jiepushe na jambo litakalokupelekea kutoa udhuru, hakika muumini wa kweli hafanyi kosa wala hatoi udhuru, na mnafiki kila siku hufanya kosa na hutoa udhuru.”154
v.
“Acha yanayokutia shaka ufanye yasiyokutia shaka, hakika uwongo ni shaka na ukweli ni utulivu wa moyo.”155
Rayhanatur-Rasul, Uk. 55. Tuhaful-Uquul, Uk. 46. 153 Tuhaful-Uquul, Uk. 46. 154 Tuhaful-Uquul, Uk.248. 155 Hayatul-Imam Husayn bin Ali, Juz. 1, Uk. 181, kutoka kwenye kitabu Ansabul-Ashraf. 151 152
67
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
vi. vii. viii.
ix.
x.
xi. xii.
“Ewe Mwenyezi Mungu usinishushe daraja kwa wema, wala usiniadabishe kwa balaa.”156 “Ambaye hatokuwa na vitu vitano basi hatostarehe: Akili, adabu, dini, aibu na tabia njema.”157 “Atakayejaribu kupata jambo kwa njia ya kumwasi Mwenyezi Mungu basi atakosa anachotarajia na haraka sana atapata anachokikimbia.”158 “Miongoni mwa dalili za kuwa na alama za kukubalika ni: Kukaa na wenye akili. Na miongoni mwa alama za ujinga ni kupingana na wasio makafiri, na miongoni mwa alama za mwenye elimu ni kufuata maneno yake na kujua ukweli wa fani za utafiti.”159 “Hakika muumini humfanya Mwenyezi Mungu ngome yake, na kauli Yake kioo chake. Mara huchunguza sifa za waumini na mara nyingine huchunguza wasifu wa wenye kiburi, hivyo hupata tawfiki kutoka Kwake na hujitambua kupitia nafsi yake, na kutokana na ufahamu wake huwa na yakini, na kutokana na utakasifu wake huweza kuimarika.”160 “Ukisikia yeyote anatoa aibu za watu basi jitahidi asikujue…”161 Alimwambia mtu mmoja aliyemteta mwenzake mbele yake: “Ewe ndugu acha utesi (usengenyaji), hakika wenyewe unawafaa mbwa wa motoni.”162
Kashful-Ghummah, Juz. 2, Uk. 243. Rayhanatur-Rasul, Uk. 55. 158 Tuhaful-Uquul, Uk. 246 - 248. 159 Tuhaful-Uquul, Uk. 246 - 248. 160 Tuhaful-Uquul, Uk. 246 - 248. 161 Rayhanatur-Rasul, Uk. 55. 162 Tuhaful-Uquul, Uk. 245. 156 157
68
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
xiii.
Kuna mtu aliongea mbele yake akasema: “Hakika wema akifanyiwa asiyefaa hupotea bure.” Imam (a.s.) akasema: “Si hivyo, lakini wema huwa kama mvua humpata mwema na muovu.”163
xiv.
Akaulizwa kuhusu tafsiri ya Aya: “Na neema ya Mola wako Mlezi izungumze.”164 Akajibu: “Amemwamuru azungumzie neema aliyomneemesha ndani ya dini yake.”165
xv.
“Kufia katika jambo la heshima ni bora kuliko kuishi ndani ya udhalili.”166
xvi.
“Kulia kwa ajili ya kumwogopa Mwenyezi Mungu ni kuepukana na moto.”167
xvii.
“Atakayekosa rai na ujanja ukamwishia basi upole ni ufunguo wake.”168
xviii.
“Atakayekubali ulichotoa basi amekusaidia kuwa mkarimu.”169
xix.
“Ikifika siku ya Kiyama atanadi mwenye kunadi: “Enyi watu, mwenye malipo kwa Mwenyezi Mungu asimame.” Hapo hawatosimama isipokuwa wenye kheri…” 170
xx.
“Hakuna amali yoyote katika umma huu inayotendwa kuanzia asubuhi isipokuwa inawakilishwa kwa Mwenyezi Mungu.”171
Tuhaful-Uquul, Uk. 245. Sura Ad-Dhuha: 11. 165 Tuhaful-Uquul, Uk. 246. 166 Hayatul-Imam Husayn bin Ali, Juz. 1, Uk. 183. 167 Hayatul-Imam Husayn bin Ali, Juz. 1, Uk. 183. 168 Taarikh Ibnu Asakir, Juz. 4, Uk. 323. 169 Hayatul-Imam Husayn bin Ali, Juz. 1, Uk. 183. 170 Hayatul-Imam Husayn bin Ali, Juz. 1, Uk. 183. 171 Hayatul-Imam Husayn bin Ali, Juz. 1, Uk. 183. 163 164
69
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
xxi.
Kuna mtu alimwambia Husein bin Ali (a.s.): “Ewe mtoto wa Mtume, mimi ni kati ya wafuasi wenu.” Akasema (a.s.): “Mche Mwenyezi Mungu, wala usidai jambo ambalo Mwenyezi Mungu atakwambia: “Umeongopa na umezua katika dai lako.” Hakika wafuasi wetu ni wale ambao nyoyo zao zimesalimika na kila aina ya utapeli, khiyana na chuki. Lakini sema: Mimi ni miongoni mwa wanaowatawalisha na kuwapenda.”172
xxii.
Amesema (a.s.): “Mwenye kutupenda ni yule ambaye hajatupenda kwa ajili ya udugu uliyopo kati yetu na yeye, wala kwa wema tuliyomtendea, isipokuwa katupenda kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hivyo atakuja nasi siku ya Kiyama tukiwa naye kama hivi viwili”. Hapo akakutanisha vidole vyake vya shahada.173
xxiii.
“Haifai kwa nafsi ya muumini kumwona anayemwasi Mwenyezi Mungu kisha asichukie.”174
xxiv.
Kuna mtu aliandika barua kwa Husein: “Ewe bwana wangu niambie kheri ya dunia na Akhera.” Husein akamwandikia: “Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu. Ama ba’d, hakika atakayetafuta ridhaa ya Mwenyezi Mungu japo watu wanachukia basi Mwenyezi Mungu atamtosheleza dhidi ya mambo ya watu. Na atakayetafuta ridhaa ya watu japo anamuudhi Mwenyezi Mungu basi Mwenyezi Muungu atamtelekeza kwa watu, wassalam.”175
Tafsirul-Burhan, Juz. 4, Uk. 22. Biharul-An’war, Juz. 68 ,Uk. 156. Biharul-An’war, Juz. 27, Uk. 128. 174 Kanzul-Ummal, Juz. 3, Uk. 85, hadithi ya 5614. 175 Amalis-Swaduq, Uk. 167. 172 173
70
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
xxv.
“Ukweli ni ushindi, uwongo ni kushindwa, siri ni amana, ujirani ni udugu, msaada ni urafiki, kitendo ni uzoefu, tabia njema ni ibada, ukimya ni pambo, ubakhili ni ufukara, ukarimu ni utajiri na upole ni akili.”176
xxvi.
“Asiyejiweza mno ni yule asiyeweza kuomba dua, na bakhili mno ni yule mbakhili wa salamu.”177
xxvii.
“Tabia mbaya mno kati ya tabia za watawala ni kuwaogopa maadui, kuwa na roho ya ukatili kwa madhaifu na kuwa bakhili wakati wa kutoa.”178
xxviii. “Jiepushe usiwe mtu anayeogopa adhabu isiwapate waja kutokana na dhambi zao huku anaruhusu adhabu kutokana na dhambi yake. Kwani hakika Mwenyezi Mungu hadanganywi kuhusu pepo Yake, wala hakipatikani kilichopo Kwake ila kwa kumtii inshaalallah.”179 xxix.
“Ulikutwa ubao chini ya ukuta wa mji mmoja kati ya miji umeandikwa: “Mimi ni Allah, hapana Mola wa haki isipokuwa Mimi, na Muhammad ni Nabii Wangu. Nashangaa inakuwaje mwenye yakini na kifo anafurahi?!! Nashangaa inakuwaje mwenye yakini na majaliwa anahuzunika?!! Nashangaa inakuwaje aliyeitahini dunia anakuwa na imani nayo?!! Nashangaa inakuwaje mwenye yakini na malipo anatenda dhambi?!!”.180
Taarikh Yaaqubiy, Juz. 2, Uk. 246. Biharul-An’war, Juz. 93, Uk. 294. Makarimul-Akhlaq, Uk. 284. 178 Biharul-An’war, Juz. 44, Uk. 189. 179 - Tuhaful-Uquul, Uk. 170. 180 - Uyunu Akhbarir-Ridha, Juz. 2 Uk. 48. 176 177
71
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Muhtasari Hakika maneno yaliyopokewa kutoka kwa Imam Husein (a.s.) ni shule iliyokusanya elimu, maarifa na malezi. Maneno yake kuhusu mapinduzi yake matukufu yanadhihirisha heshima, kutokubali udhalili, kujitolea kwa ajili ya dini na kuifadhilisha dini kwa kila maana yake.Maneno yake yamedhihirisha jinsi anavyojali mambo ya umma na jamii ya kiislamu. Imam Husein (a.s.) hakuishia kubainishia ukweli kuhusu mapinduzi yake, sababu zake na matunda yake tu, bali alizidi kubainisha misingi ya elimu na malezi, na misingi ya utamaduni wa kiislamu ambao utazaa vizazi vyema vyenye kujua nafasi zao na majukumu yao mbele ya dini muda wote wa maisha yao. Maswali: 1. Ni vitu gani vinavyojenga nguvu ya utu wa muumini? 2. Elezea maadili bora yaliyomo kwenye maneno ya Imam Husein (a.s.)? 3. Kwa mujibu wa maelekezo ya Imam Husein (a.s.) ni kwa kitu gani mtu ataweza kupata kheri ya dunia na Akhera? 4. Taja maelekezo ya Imam Husein (a.s.) yanayohusu kuitengeneza nafsi na jamii nzima? 5. Ni vitendo vipi vinavyoonyesha akili ya mwenye kuvitenda? 6. Ni ipi sifa mbaya sana kwa mwanadamu?
72
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Somo la ishirini na saba Imam Ali bin Husein (a.s.) Nasaba ing’aayo:
N
i wa nne katika orodha ya maimamu wa Ahlul-Baiti (a.s.) ambao Mwenyezi Mungu amewatakasa na kuwaondolea uchafu. Babu yake ni kiongozi wa waumini, Imam wa wachamungu Ali bin Abu Twalib. Bibi yake ni Fatimah Az-Zahrau kipande cha nyama ya Mtume mwaminifu wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na yeye ni mbora wa wanawake wote. Baba yake ni bwana wa vijana wa peponi, mjukuu wa mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na manukato ya Mtume (s.a.w.w.), ambaye alikufa shahidi huko Karbala kwa ajili ya kutetea heshima ya Uislamu na Waislamu. Mama yake ni binti wa Yazdajardi mfalme wa mwisho kati ya wafalme wa kiajemi. Na yeye alijibu wito wa Mola wake akiwa bado yumo katika siku za nifasi yake na wala hakuzaa mwingine asiyekuwa yeye (a.s.). Kuzaliwa na kufariki kwake: Alizaliwa siku ya tano ya mfungo kumi na moja (Shaabani) mwaka wa thelathini na nane hijiriya, na inasemekana mwaka wa thelathini na sita. Alifia Madina mwaka wa tisini na nne au tisini na tano hijiriya akiwa na umri unaokaribia miaka hamsini na saba. Hivyo akaishi miaka miwili akiwa na babu yake, miaka kumi na mbili akiwa na 73
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
ami yake, miaka ishirini na tatu akiwa na baba yake Husein (a.s.), akaishi karibuni miaka thelathini na tatu baada ya baba yake na huo ndio muda wa uimamu wake. Kuniya, lakabu na nakshi ya pete yake: Kuniya aliyopewa ni Abu Muhammad, Abul Hasan na Abu Abdillah. Lakabu aliyopewa ni Zaynul-Abidiina, Dhuthafanati, SayyidulAbidina, Qud’watuz-Zahidina, As-Sajad, Sayyidul-Muttaqina, AlAmin, Az-Zakiyyu, Zaynus-Swalihina, Manarul-Qanitina, Al-Bakkau. Na lakabu maarufu sana kwake ni As-Sajad na Zaynul-Abidiina. Nakshi ya pete yake ilikuwa ni: “Katika kila tatizo Mwenyezi Mungu ni tegemeo langu.” Na katika nyingine: “Nguvu zote ni za Mwenyezi Mungu”. Na katika ya tatu: “Ushindi ni wa Mwenyezi Mungu.” Na katika ya nne: “Kila sifa njema ni ya Mwenyezi Mungu wa juu.” Na katika ya tano: “Dhalili na mwovu ni muuwaji wa Husein. Na katika ya sita: “Hakika Mwenyezi Mungu ni mfikishaji wa jambo lake.” Na katika ya saba: “Umejua basi tenda.”181 Vipindi vya maisha yake: Maisha ya Imam huyu mtukufu yamegawanyika katika vipindi viwili: Cha kwanza kinaanzia pale alipozaliwa na kinakomea alipofariki baba yake siku ya Ashura mwaka wa sitini na moja hijiriya ambacho ni kipindi cha miaka ishirini na tatu. Kipindi cha pili kinaanza siku ya Ashura na kukomea alipofariki mwaka wa tisini na nne au tisini na tano, na hiki ni kipindi cha miaka thelathini na tatu. 181
- Tazama Al-Irshad. Iilamul-Wara. Na Hayatul-Imam Zaynul-Abidina, Juz. 1, Uk. 21 – 43. 74
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Imam (a.s.) alipita njia bora katika uongozi kisiasa, kijamii na kifikira ilihali akiwa katika mazingira magumu ambayo yaliupata umma wa kiislamu muda wote wa uimamu wake. Kipindi ambnacho ni cha utawala wa Bani umayya, yaani kizazi cha Suf’yani na Mar’wani. Katika ulingo wa elimu na dini Imam (a.s.) alichomoza akiwa Imam katika dini, taa katika elimu, marejeo katika halali na haramu na mfano bora katika uchamungu na ibada. Waislamu wote wanakiri kuhusu elimu yake, msimamo wake na ubora wake, na wenye akili walifuata uongozi wake, elimu yake na wakarejea kwake. Imani ya umma kwa Imam Zaynul-Abidiin haikuishia upande wa sheria na mambo ya kiroho tu, bali umma ulikuwa unaamini kuwa yeye ndiye marejeo, kiongozi na kimbilio katika matatizo ya maisha na mambo yake. Kwa kuwa yeye ndiye mwendelezo wa baba zake watakasifu. Ndio maana tunamkuta Abdul-Malik bin Mar’wani anamtaka ushauri Imam Zaynul-Abidiin kuhusu ufumbuzi wa tatizo la sarafu ya kiislamu yenye kujitegemea dhidi ya Rumi baada ya vitisho vya mfalme wa Rumi kwa lengo la kuwadhalilisha Waislamu. Imam (a.s.) aliinua harakati za kielimu ili kuweka msingi imara wa Uislamu kupitia mbegu za ijtihadi. Pia akafanya dua kuwa msingi wa kutibu matamanio ya ladha za maisha, hivyo kitabu SahifatusSajadiah kikawa ni maelezo ya kweli na fasaha kuhusu matendo ya kijamii na kimalezi, kwani kwa hakika hali halisi ya kipindi alichoishi Imam (a.s.) ndiyo iliyomlazimisha kuelekeza hayo.182 Imam Zaynul-Abidiin alilea vizazi vyenye mwamko wa mstari sahihi wa Uislamu halisi wa Muhammad (s.a.w.w.) unaowakilishwa na maimamu wa Ahlul-Baiti (a.s.) ambao walisimamia jukumu la 182
- Tazama dibaji ya Sahifatus-Sajadiyyah ya Shahid Sayyid Muhammad Baqir As-Sadri (q.s.). 75
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
kuhifadhi na kutetea jamii ambayo polepole ilikuwa imeanza kwenda nje ya msitari waliowekewa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Mwonekano wa utu wa Imam Zaynul-Abidiin (a.s.): i.
Suf’yan bin Al-Uyaynah alimwambia Az-Zahriy kuwa: “Je ulimdiriki Ali bin Husein?” Akajibu: “Ndiyo nilimdiriki na wala sikukutana na mtu mbora kama yeye, wala sikumjua rafiki yake wa siri wala adui yake wa dhahiri.”183
ii.
Pia imetoka kwa Suf’yani kuwa: “Sikumwona Hashimiya mbora kuliko Ali bin Husein.” Abu Hazim akasema: “Sikumwona mwenye elimu kuliko yeye.”184
iii. Az-Zahriy amesema: “Sikumwona mkurayshi mbora kuliko yeye.”185 iv. Said bin Al-Musayyab amesema: “Huyu ndiye ambaye haiwezekani kwa mwislamu kutokumfahamu.”186 v.
Na akasema: “Katu sikumwona yeyote mbora kuliko Ali bin Husein, na katu sikumwona isipokuwa nilichukizwa na nafsi yangu, na wala hakuna siku niliyomwona katika hali ya kucheka.”187
vi. Siku moja Umar bin Abdul-Aziz alisema baada ya Ali bin Husein (a.s.) kusimama na kuondoka kwake: “Hakika mtu mbora 183
Masailus-Shia, Juz. 5, Uk. 541. Ilalus-Sharaiu, Uk. 88. Biharul-An’war, Juz.
184
Tadhkiratul-Khuwas cha Sibtu Ibnul-Jawziy, Uk. 331 chapa ya maktaba mpya
46, Uk. 64.
ya Naynawa Tehran.
Tahdhibut-Tahdhib, Juz. 7, Uk. 305. 186 Aayanus-Shia. 187 Taarikh Yaaqubiy, Juz. 2, Uk. 46. 185
76
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
sana ni huyu aliyesimama punde tu kabla yangu. Mtu ambaye watu wanatamani watokane na yeye na wala yeye hatamani kutokana na yeyote.”188 vii. Pia alipokuja kumuomboleza Imam (a.s.) alisema: “Imeondoka taa ya dunia, uzuri wa Uislamu na pambo la wafanya ibada.”189 viii. Abdul-Malik bin Mar’wan alimwambia: “Umepewa fadhila, elimu, dini na uchamungu, hakuna yeyote aliyepewa mfano wako.”190 ix. Jabir bin Abdullah Al-Answari alisema: “Katika watoto wa manabii hakuna yeyote mwenye sifa kama zilizoonekana kwa Ali bin Husein.”191 x.
Ibnu Saad katika kitabu chake At-Tabaqat amesema: “Ali bin Husein alikuwa mwaminifu, mkweli, mwenye hadithi nyingi, mwenye hadhi ya juu, mchamungu na mwenye kuheshimika.”192
xi. Al-Waqidiy amesema: “Ali bin Husein alikuwa mchamungu na mfanya ibada mno kuliko watu wote na mtiifu mno kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.”193 xii. Shaikhu Al-Mufid amesema: “Alikuwa mbora mno kuliko viumbe wengine wa Mwenyezi Mungu baada ya baba yake, kielimu na kivitendo.”194 iharul-An’war, Juz. 46, Uk. 3 – 4. Muhadharatul-Udabai cha Ar-Raghib Al-Isfahaniy, B Juz. 1, Uk. 166. 189 Taarikh Yaaqubiy, Juz. 2, Uk. 48. 190 Biharul-An’war, Juz. 46, Uk. 75. 188
191
Hayatu Imam Muhammad Al-Baqir, Juz. 1, Uk. 34.
At-Tabaqat Al-Kubra, Juz. 5, Uk. 222. 193 Al-Bidayatu Wan-Nihayah, Juz. 9, Uk. 104. 194 Al-Irshad cha Al-Mufid, Uk. 254. 192
77
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Muhtasari Imam Ali bin Husein (a.s.) alizaliwa kipindi cha mapambano kati ya haki na nguvu yenye kupinga Uislamu. Akashuhudia kipindi cha ukhalifa kwenda kombo kwa Muawiya bin Abu Sufyani na Bani Umayya kushika madaraka ya dola ya kiislamu. Kwa huruma ya Mwenyezi Mungu Imam Ali bin Husein (a.s.) aliokoka dhidi ya mauwaji baada ya kuuwawa baba yake, watu wote wa nyumba yake na maswahaba zake bora katika tukio la Karbala, tukio ambalo huonyesha jinsi umma ulivyoharibika na kufa kidhamira ilihali ukipotea kifikra na kimaarifa. Sifa ya kipekee ya zama za Imam Zaynul-Abidiin (a.s.) ni kuenea kwa sauti za ulimwengu wa kiislamu, kubadilika kwa ukhalifa wa kiislamu na kuwa ufalme wa kurithiana, jaribio la watawala kutaka kuitenganisha dini ya kiislamu na serikali na maisha ya kisiasa ilihali Waislamu wakifikiwa na mporomoko wa hadhi ya Uislamu na kushuka kwa imani mbele ya mbinyo huku jamii na tamaduni nyingine mpya zikipatikana, pia hali ya anasa na kung’ang’ania dunia iliyo mbali na imani ya Mwenyezi Mungu ikishamiri. Imamu As-Sajjad (a.s.) alitoa juhudi zake zote katika kujenga jamii safi na kupanua kanuni ya kijamii kwa ajili ya kuhifadhi dini ya kiislamu na kulinda umma wa kiislamu dhidi ya upotevu huku akipambana na vishawishi vya dunia. Imam (a.s.) alifanikiwa kuimarisha utu wake na kuuweka ndani ya jamii ya kiislamu, hivyo historia ikathibitisha elimu yake, uchamungu wake na dini yake.
78
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Maswali: 1. Imam Zaynul-Abidiin (a.s.) alizaliwa lini? Alifariki lini? Na alizikwa wapi? 2. Kwa nini Imam Zaynul-Abidiin (a.s.) alipewa lakabu ya As- Sajjad? 3. Taja mambo aliyoyafanya Imam Zaynul-Abidiin (a.s.) kwa ajili ya kuhudumia dini? 4. Ni wakati gani Imam Zaynul-Abidiin (a.s.) alikuwa akiingilia kati kutatua matatizo ya serikali ya kidhalimu? 5. Elezea ni zipi lakabu muhimu za Imam As-Sajjad huku ukielezea zinajulisha nini? Kwa ajili ya kujisomea As-Shahid Sayyid Muhammad Al-Baqir As-Sadri amesema: “Waislamu wote walikuwa wakimpenda mno Imam huyu na kumjali sana. Miongozo yake ya kijamii ilikuwa imefika kila sehemu ya ulimwengu wa kiislamu kama linavyoonyesha tukio kubwa la mahujaji. Alipohiji Hisham bin Abdul-Malik kisha akatufu akataka kushika jiwe jeusi lakini hakuweza kulishika kutokana na msongamano wa watu. Hivyo akawekewa mimbari akabaki akilitizama. Muda si mrefu akatokea Zaynul-Abidiin na yeye akaanza kutufu, hivyo ikawa kila afikapo sehemu ya jiwe watu wanampisha na kumuachia nafasi mpaka anapolishika. Walifanya hivyo kutokana na wanavyojua ukubwa wa nafasi yake na mapenzi yao kwake bila kujali miji yao na mataifa yao. 79
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Farazdaqi amesajili tukio hili la kupendeza kwa kaswida yake mashuhuri:195 “Ewe mwenye kuniuliza ni wapi ukarimu umekaa? Ninalo jibu bainifu iwapo watafuta jibu watakuja. Huyu ndiye ambaye Makka inajua nyayo zake, na Nyumba {Kaaba}, Haramu, na eneo la nje ya Haramu vyote vinamjua. Huyu ni mtoto wa mbora wa waja wote wa Mwenyezi Mungu. Huyu ni mchamungu, msafi, mtakasifu ajulikanaye mno. Makurayshi wakimuona, msemaji wao husema: Kwa ukarimu wa huyu ndio kilele cha ukarimu. Huyu ni mwana wa Fatimah ikiwa kweli humjui. Manabii wa Mwenyezi Mungu wamehitimishwa kupita babu yake. Wala kauli yako: Ni nani huyu, haimdhuru chochote. Waarabu na wasio waarabu wanamjua uliyejifanya humjui. Akaendelea mpaka akasema: “Yeye ni miongoni mwa kundi ambalo kuwapenda ndio dini na kuwachukia ni ukafiri. Kujikurubisha kwao ndio kiokoleo na kizuwizi. Katika kila faradhi baada ya utajo wa Mwenyezi Mungu hutangulizwa utajo wao, na kwa utajo wao huhitimishwa maneno.196 Tazama dibaji ya Sahifatus-Sajadiyyah ya Shahid Sayyid Muhammad Baqir As-Sadri (q.s.). 196 Tazama Nihayatul-Adab, Juz. 21, Uk. 327- 331. Zuhrul-Adab, Juz. 1, Uk. 103. 195
Aayanus-Shia, sira ya Ali bin Husein. Taarikh Damashqi, Juz. 36 Uk. 161. Shar’hul- Uyun cha Ibnu Nabatah, Uk. 390. 80
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Somo la ishirini na nane Fadhila na mwonekano wa Imam Zaynul-Abidiin (a.s.)
I
mam Zaynul-Abidiin (a.s.) alikuwa mbora kuliko watu wa zama zake, mjuzi kuliko wao, mjuzi wa sheria, mchamungu, mfanya ibada, mkarimu, mvumilivu, mwenye subira, mfasaha, mwenye tabia njema, mtoaji sana wa sadaka, mwenye huruma sana kwa mafakiri na mwenye kuwanasihi sana Waislamu. Alikuwa mheshimiwa mwenye haiba kwa mtu wa karibu hadi wa mbali, kwa rafiki hadi kwa adui.197 Tunakuletea taswira halisi ya baadhi ya sifa zake nzuri na mwonekano wa utu wake. Uvumilivu: Imam (a.s.) alikuwa mvumilivu mno na mwenye kuzuwia hasira zake, hivyo miongoni mwa sura halisi ya uvumilivu wake ni hili tukio lililopokewa na wanahistoria: i. Kijakazi wake alikuwa akimmiminia maji, ghafla birika likamdondoka na kudondokea uso Mtukufu wa Imamu na kumjeruhi, hapo kijakazi akaharakisha kusema: “Hakika Mwenyezi Mungu amesema: Na wenye kuzuwia hasira.” Haraka Imam akasema: “Nimezuwia hasira zangu.” Kijakazi akatamani uvumilivu wa Imam (a.s.) akaendelea kutafuta nyongeza akasema: “Wenye kusamehe watu.” Imam akasema: “Mwenyezi Mungu akusame197
- Aayanus-Shia, sira ya Ali bin Husein (a.s.). 81
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
he.” Kisha kijakazi akasema: “Mwenyezi Mungu anawapenda wafanyao ihsani.” Akamwambia: “Nenda hakika wewe uko huru.”198 ii. Muovu mmoja alimtukana. Imam akaondoa uso wake kwake. Muovu akamwambia: “Nakulenga wewe.” Imam akaharakisha kumwambia: “Ninakuvumilia ………..Imam akamuacha wala hakumrudishia kisasi.”199 iii. Kati ya uvumilivu wake mkubwa ni kuwa kuna mtu alimzushia uwongo na kumtukana sana. Imam (a.s.) akamwambia: “Ikiwa tupo kama ulivyosema basi tunamuomba Mwenyezi Mungu atusamehe, na kama hatuko kama ulivyosema basi Mwenyezi Mungu akusamehe.”200 Ukarimu wake: Wanahistoria wote wamekubali kuwa alikuwa mkarimu mno, mwepesi wa mkono, mwema kwa mafakiri na madhaifu. Wamenukuu mifano mingi halisi kuhusu mafuriko ya ukarimu wake. Kati ya mifano hiyo ni: i. Muhammad bin Usama aliugua, Imam (a.s.) akamtembelea, punde baada ya Imam kutulia Muhammad akaanza kulia. Imam akamuuliza: “Unalizwa na nini?” Akajibu: “Ninadaiwa.” Imam akamwambia: “Kiasi gani?” Akajibu: “Dinari elfu kumi na tano.” Imam akamwambia: “Nitakulipia.” Imam hakuinuka mpaka alipompa.201 Taarikh Damashqi, Juz. 36, Uk. 155. Nihayatul-Urbi, Juz. 21, Uk. 326. Aya ni ya Sura Al Imran: 134. 199 Al-Bidayatu Wan-Nihayah, Juz. 9, Uk. 105. 200 Swaf’watus-Swaf’wah, Juz. 2 , Uk. 54. 201 Al-Bidayatu Wan-Nihayah, Juz. 9 Uk. 105. Siyaru Aalamun-Nubalai, Juz. 4, Uk. 239. 198
82
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
ii. Miongoni mwa ukarimu wake ni kuwa alikuwa akiwalisha watu mlo kamili kila siku huko Madina wakati wa sala ya adhuhuri na nyumbani kwake.202 iii. Alikuwa akibeba matumizi ya nyumba mia moja kwa siri.203 Huruma yake kwa mafakiri: i. Alikuwa akijichanganya na mafakiri ilihali akichunga hisia zao, hivyo alikuwa ampapo mwombaji humbusu ili athari za udhalili na uhitaji zisionekane.204 Alikuwa atembelewapo na mwombaji humkaribisha na kumwambia: “Karibu kwa yule anayebeba mahitaji yake kuelekea Akhera.”205 i. Alikuwa akiona fahari kuhudhuria chakula cha mayatima na masikini wasio na ujanja. Alikuwa akiwapelekea chakula au kuni huku akibeba mwenyewe mgongoni na kwenda kwenye kila mlango kati ya milango yao na kuwapa.206 ii. Abu Hamza At-Thumaliy amesema: “Nilisali na Ali bin Husein (a.s.) Swala ya alfajiri siku ya Ijumaa huko Madina, alipomaliza kusali aliondoka kwenda nyumbani kwake nikiwa nae. Akamwita kijakazi wake aitwaye Sukayna akamwambia: “Asivuke mwombaji yeyote mlangoni kwangu isipokuwa mumlishe, hakika leo ni Ijumaa.”Abu Hamza akamwambia: “Si kila mwombaji anastahiki kupewa.” Imam (a.s.) akasema: “Nakhofia isiwe baadhi ya wanaotuomba ni wastahiki kisha ikawa hatukuwalisha tukawanyima, Hayatul-Imam Zaynul-Abidin, Juz. 1 Uk. 84. Biharul-An’war, Juz. 46, Uk. 88. 204 Hilyatul-Awliyai, Juz. 3 Uk. 137. 205 Swaf’watus-Swaf’wah, Juz. 2 Uk. 53. 206 Biharul-An’war, Juz. 46, Uk. 62. 202 203
83
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
hivyo tukashushiwa aliyoshushiwa Yaqub na ndugu zake, walisheni walisheni. Hakika Yaqub kila siku alikuwa akichinja kondoo, hutoa kipande sadaka na kingine hula yeye na familia yake. Siku moja muombaji muumini mwenye fungu, mstahiki mwenye hadhi mbele ya Mwenyezi Mungu akapita mlangoni kwa Yaqub siku ya Ijumaa wakati wa kufuturu. Akaanza kugonga mlango wake akisema: “Nilisheni chakula chenu muombaji mgeni mwenye njaa”, huku wao wakimsikia hawajui kama anastahili wala hawaamini kauli yake, basi alipokata tamaa na usiku ukazidi akajiondokea akalala na njaa ilihali akimuelezea Mwenyezi Mungu njaa yake. Yaqub na ndugu zake wakalala wameshiba wamejaza matumbo yao huku wakiwa na chakula cha ziada, hivyo asubuhi ya usiku huo Mwenyezi Mungu akateremsha wahyi kwa Yaqub: “Umemdhalilisha mja wangu na balaa langu litakuwa juu yako na juu ya kizazi chako. Ewe Yaqub, nabii nimpendae sana na mbora mno Kwangu ni yule awahurumiaye maskini wa waja Wangu, akawakurubisha kwake, akawalisha na yeye akawa ni kimbilio lao. Namrehemu mja Wangu mwenye juhudi katika ibada zake, mwenye kutosheka na malipo ya siri kuliko dhahiri ya dunia. Naapa kwa utukufu Wangu kuwa nitakushushia balaa na nitakufanya wewe na kizazi chako ni shukio la matatizo.” Abu Hamza akasema: “Niko chini ya miguu yako, ni lini Yusuf aliona ndoto yake?” Akajibu: “Ni katika usiku ule ambao Yaqub na ndugu zake walilala wameshiba na akalala muombaji fakiri bila kitu akiwa na njaa.”207
207
Darus-Salam, Juz. 2, Uk. 141. 84
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Heshima yake na kukataa udhalili: Imam Zaynul-Abidiina alirithi toka kwa baba yake tabia ya heshima na kukataa udhalili, baba yake ambaye ni Husein bwana wa mashahidi ambaye aliwaita viburi wa zama zake kwa kusema: “Naapa kwa Mwenyezi Mungu sitotoa mkono wangu kutoa kwa dhalili wala sitowakubali kukubali kwa mtumwa.”208 Sifa hii ilidhihirika katika kauli yake: “Sipendi neema nyekundu zidhalilishe nafsi yangu.”209 Akasema kuhusu heshima ya nafsi: “Ambaye nafsi yake imekamilika basi dunia huwa dhalili kwake.”210 Wanahistoria wanasema: Mmoja wao alichukua haki yake bila kuomba idhini toka kwake. Kipindi hicho Imam (a.s.) alikuwa Makka na Al-Walid bin Abdul-Malik akiwa ndio khalifa huku akiwa amehudhuria hija. Akaambiwa: “Ungemwomba Al-Walid akurudishie haki zako.” Akawajibu kupitia neno la kudumu lenye kulinda heshima na kupinga udhalili kwa kusema: “Je ndani ya sehemu takatifu ya Mwenyezi Mungu nimwombe asiye Mwenyezi Mungu, ikiwa mimi siwezi kuomba dunia toka kwa muumba wake, vipi nije kuomba dunia toka kwa kiumbe mfano wangu.”211 Kutokana na heshima yake katu hakuwahi kula hata dirham moja kinyume, eti kwa ajili ya ukaribu wake na Mtume (s.a.w.w.).212 Utawa: Katika zama zake alikuwa mashuhuri kwa kuipa dunia kisogo kuliko watu wote, hayo ni kama alivyoelezea Az-Zahriy. Alipomuona Hayatul-Imam Zaynul-Abidin, Dirasatu watahlil, Uk. 80. Al-Khiswal, Uk. 24. 210 Biharul-An’war, Juz. 78, Uk. 135. 211 Biharul-An’war, Juz. 46, Uk. 64. 212 Majalis Thaalab, Juz. 2, Uk. 462. 208 209
85
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
muombaji akilia alipatwa na uchungu akaenda huku akisema: “Laiti dunia ingekuwa mikononi mwa huyu kisha ikamdondoka isingepasa kwake kuililia.”213 Ibada zake na kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu: Hakika kuvuma kwa lakabu ya ‘Pambo la wafanya ibada’ [ZaynulAbidiina] na ‘Mbora wa wenye kusujudu’ [Sayyidus-Sajidina] ni ishara ya wazi juu ya sifa ya kujielekeza kwa Mwenyezi Mungu na kujikurubisha kwake katika maisha yake na mwenendo wake, japokuwa kitabu Sahifatus-Sajadiah ni dalili nyingine juu ya ukweli huu. Tukipitia haraka haraka anuani za dua za kitabu hiki tutaona jinsi Imam (a.s.) alivyojielekeza kwa Mwenyezi Mungu. Hakuna sehemu yoyote isipokuwa Imam ana dua na ibada. Imam (a.s.) aliishia katika kumpenda Mwenyezi Mungu akawa na moyo mkunjufu Kwake, jambo hilo lilijiakisi katika harakati zake zote, utulivu wake wote na hali zake zote. Miongoni mwa mambo waliyoyapokea wanahistoria ni kuwa: Alimkuta mtu kakaa mlangoni kwa tajiri. Hapo Imam akamwambia: “Kitu gani kinakukalisha kwenye mlango wa huyu tajiri mwenye kiburi?” Akajibu: “Ukata.”Imam (a.s.) akamwambia: “Simama nikuelekeze mlango bora kuliko wake na kwa Mola wako ni bora kwako kuliko kwake……….” Hapo Imam (a.s.) akasimama na yule mtu akaenda nae msikiti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, kisha akamfunza sala, funga, dua, kusoma Qur’ani, kuomba haja toka kwa Mwenyezi Mungu na kukimbilia kwenye ngome Yake yenye kukinga.”214 213 214
Al-Fusulul-Muhimmah, Uk. 192. Hayatul-Imam Zaynul-Abidin, Uk. 93 – 94. 86
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Muhtasari Imamu Zaynul-Abidiin (a.s.) alijenga maadili ya hali ya juu, hivyo akawa kiongozi bora na dalili bora inayoongoza kwenye wema na kufaulu ilihali akibeba taa ya ujumbe wa kiislamu na kuutetea na kuupandikiza ndani ya nafsi za Waislamu. Imamu Zaynul-Abidiin (a.s.) alikuwa akiishi ndani ya nyoyo za umma na kati ya umma wa kiislamu, anashirikiana nao katika machungu yao na matarajio yao kwa mwamko asili wa Uislamu ili adhihirishe utukufu wa ujumbe wa kiislamu na uwezo wake katika kujenga jamii njema yenye mfano bora wa kutatua kila gonjwa linalokumba maisha. Hakika mwonekano wa utu wa Imamu Zaynul-Abidiin (a.s.) ulikuwa unaendana na zama ambazo ziliupitia umma wa kiislamu, hivyo akamsamehe muovu na akamuongoza kwenye njia ya haki. Akawahurumia mafakiri na kuwasaidia katika matatizo ya maisha yao. Akamhurumia dhaifu ilihali akiimarisha muungano wa akida na jamii ya kiislamu. Akatoa sadaka kwa siri na kwa dhahiri ili awafunze watu majukumu ya kijamii. Amali zake zote akaziunganisha na ridhaa ya Mwenyezi Mungu na kufaulu kwa kujikurubisha Kwake ili watu wamuabudu Mwenyezi Mungu mmoja Mwenye nguvu na wala wasiabudu kitu kingine‌‌..Akadhihirisha heshima na kukataa udhalili kwa kiwango kinacholingana na nafsi yake na utakasifu wake ilihali katika hali zote hizo akiwa ni zaidi kuliko viumbe wote wa Mwenyezi Mungu, kiibada na kiuchamungu. Maswali: 1. Toa taswira mbili kuhusu uvumilivu na msamaha wa Imam Zaynul-Abidiin (a.s.)? 87
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
2. Ni kitu gani alichokuwa anakitaka Imam As-Sajjad (a.s.) kutokana na kuwasaidia mafakiri? 3. Toa taswira tatu kuhusu kutoa kwa Imam (a.s.)? 4. Ni uhusiano upi uliopo kati ya kukataa udhalili kwa Imam (a.s.) na kuipa kisogo dunia? 5. Toa mfano halisi wa Imamu kuipa kisogo dunia na mfano mwingine kuhusu kuukataa udhalili? Kwa ajili ya kujisomea Said bin Al-Musayyib amesema: “Ali (a.s.) alikuwa akiwapa mawaidha watu na akiwahimiza kuipa dunia kisogo huku akiwatamanisha kutenda amali za Akhera. Alikuwa kila siku ya Ijumaa akiwahutubia kwa maneno haya ambayo yalihifadhiwa na kuandikwa toka kwake, alikuwa akisema: “Enyi watu mcheni Mwenyezi Mungu, na muwe na yakini kuwa mtarejea Kwake. Ewe mwanadamu, hakika kifo chako ndicho kitu kijacho haraka sana kwako. Kimefika kwako kikikutafuta na karibu kitakupata na ninaona muda wako umekwisha huku malaika wa kifo kachukua roho yako na sasa umo kaburini peke yako, kisha kakurudishia roho yako ilihali wamekuzunguka malaika wawili: Munkara na Nakiiri ili wakuulize na mtihani wako ni mgumu……… “Mcheni Mwenyezi Mungu enyi waja wa Mwenyezi Mungu na mjue kuwa Mwenyezi Mungu hapendi mapambo ya dunia yawe ya mmoja kati ya vipenzi vyake. Wala hajawatamanisha dunia, mapambo yake ya haraka, wala furaha yake isiyo na thamani, bali ameumba dunia na watu wake ili awatahini ndani yake ni yupi mwenye matendo mema kwa ajili ya Akhera yake. 88
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
“Hakuna shaka hakika Mwenyezi Mungu amewatoleeni mifano, akawatambulisha alama kwa watu wenye akili, wala hakuna nguvu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, hivyo yapeni kisogo yale aliyotaka Mwenyezi Mungu muyape kisogo ambayo ni maisha ya dunia. Wala msizame kwenye mapambo ya dunia na yaliyomo duniani kwa kufanya dunia ndio nyumba ya kudumu na ya kuishi, hakika yenyewe ni nyumba ya kupita na ya kung’oka na ya matendo. “Hivyo humo jiandalieni matendo mema kabla siku za kuishi humo hazijaisha na kabla Mwenyezi Mungu hajaidhinisha kutolewa………Mwenyezi Mungu atujalie sisi na nyinyi tuwe kati ya waipao kisogo dunia na mapambo yake, wanaotamani malipo yachelewayo ambayo ni thawabu za Akhera.”215 Sadaka zake: Miongoni mwa makubwa aliyokuwa akiyafanya Imam Zaynul-Abidiin (a.s.) katika maisha yake ni kutoa sadaka kwa mafakiri ili kuwapa maisha bora na kuondoa hali ngumu kwao. Imam (a.s.) alikuwa akihimiza kutoa sadaka kutokana na malipo mazuri yanayopatikana katika hilo, akasema: “Hakuna mtu yeyote atakayetoa sadaka kwa fakiri dhaifu kisha masikini yule akamwombea chochote ndani ya saa hiyo isipokuwa ni lazima dua yake itajibiwa.”216 Hapa tunatoa baadhi ya mifano kuhusu sadaka zake: Wakati wa kiangazi alikuwa akivaa nguo ya sufi, ifikapo masika huitoa sadaka au kuiuza na thamani yake huitoa sadaka.217 Wakati wa masika alikuwa akivaa nguo mbili za kimisri, kisha ifikapo kiangazi huzitoa sadaka. Alikuwa akisema: “Hakika mimi namuonea aibu Mwenyezi Mungu kula thamani ya nguo ambayo nimemwabuRejea Al-Kafiy, Juz. 8, Uk. 72 – 76. Tuhaful-Uquul, Uk. 249 – 252. Wasailus-Shia, Juz. 6, Uk. 296. 217 Taarikh Damashqi, Juz. 36, Uk. 161. 215 216
89
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
dia Mwenyezi Mungu.” Alikuwa akitoa sadaka ya sukari na aina fulani ya matunda, na anapoulizwa kuhusu hilo hujibu: “Hamtopata wema mpaka mtoa yale myapendayo.”218 Imepokewa kuwa alikuwa akitamani zabibu huku amefunga, hivyo wakati wa kufuturu kijakazi wake akamletea mkungu wa zabibu, ghafla akatokea muombaji. Imam (a.s.) akamwamuru kijakazi ampe muombaji mkungu ule, kisha kijakazi akaenda kununua mkungu ule toka kwa muombaji na kumpa Imam (a.s.). Ghafla akatokea muombaji mwingine, hapo Imam (a.s.) akaamuru apewe mkungu ule, kisha kijakazi akaenda kuununua toka kwa yule muombaji na kumletea Imam (a.s.). Ghafla muombaji mwingine wa tatu akagonga mlango, Imam (a.s.) akampa mkungu ule.219 Imam (a.s.) aligawana mali yake na masikini na mafakiri akagawa mafungu mawili: Fungu kwa ajili yake na lingine akatoa sadaka kwa mafakiri na masikini.220 Jambo alilolipenda sana (a.s.) ni kutoa sadaka kwa siri ili yeyote asimjue, hivyo alikuwa akihimiza sadaka ya siri akisema: “Hakika inazima ghadhabu za Mola Mlezi.”221 Alikuwa na mtoto wa ami yake, basi Imam (a.s.) alikuwa akimuendea usiku na kumpa baadhi ya dinari. Ndugu yake yule akaanza kulalamika akisema: “Hakika Ali bin Husein hanijali,” huku akimuombea dua mbaya. Imam (a.s.) akawa anasikia lawama zake huku akiendelea kujificha bila ya kujitambulisha kwake. Imam (a.s.) alipofariki na ndugu yake yule akakosa mahitaji aliyokuwa akihudumiwa ndipo akajua kuwa aliyekuwa akimuhudumia ni Ali bin Husein (a.s.), hivyo akawa akienda katika kaburi lake ilihali akilia na kumuomba msamaha.222 Nasikhut-Tawarikh, Juz. 1, Uk. 67. Al-Mahasin, Uk. 547. Furuul-Kafiy, Juz. 6, Uk. 350. 220 Khulaswatut-Tahdhibil-Kamal, Uk. 231. Al-Hilyah, Juz. 3, Uk. 140. Jamharatul-Awliyai, Juz. 2, Uk. 71. 221 Taz. Tadhkiratul-Huffadh, Juz. 1, Uk. 75. Akhbarud-Duwal, Uk. 110. Nihayatul-Urbi, Juz. 21, Uk. 326. 222 Biharul-An’war, Juz. 46, Uk. 100. 218 219
90
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Ibnu Aisha amesema: “Niliwasikia wakazi wa Madina wakisema: “Hatukuikosa sadaka ya siri mpaka alipofariki Ali bin Husein (a.s.) .”223 Imam (a.s.) hakutaka chochote kupitia wema na ihsani yake kwa mafakiri isipokuwa radhi za Mwenyezi Mungu siku ya mwisho. Az-Zahriy amesema: “Nilimuona Ali bin Husein ndani ya usiku wenye baridi akiwa amebeba unga mgongoni. Nikamwambia: “Ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, kitu gani hiki?” Akajibu: “Nataka kusafiri naandaa matumizi nitakayoyabeba, naenda nayo sehemu ya kuhifadhia.” Az-Zahriy akasema: “Kijana wangu huyu hapa akubebee.” Hapo Imam (a.s.) akakataa. Al-Zahriy akanyenyekea na kumbembeleza ambebee yeye mwenyewe, isipokuwa Imam (a.s.) aliendelea kukataa na kumwambia: “Lakini mimi siondoi nafsi yangu kwenye kile kitakachoniokoa safarini na kutengeneza vizuri mafikio yangu ambayo nataka kufikia, nakuomba kwa utukufu wa Mwenyezi Mungu uendelee na haja yako.” Az-Zahriy akaenda zake na kumuacha Imam (a.s.). Na baada ya siku akakutana na Imam (a.s.) huku akidhani yuko safarini kwani hakuelewa makusudio ya Imam (a.s.). Az-Zahriy akamwambia: “Ewe mtoto wa Mtume, sioni athari yoyote ya ile safari uliyoiacha. Imamu akamjibu: “Ewe Az-Zuhriy si kama ulivyodhania lakini safari ni kifo na mimi najiandaa kwa kifo, kwani kwa hakika kujiandaa na kifo ni kujiepusha na haramu na kueneza umande katika jambo la kheri.”224
223 224
Swaf’watus-Swaf’wah, Juz. 2, Uk. 54. Al-Ittihaf Bihubil-Ashraf, Uk. 49. Ilalus-Sharaiu, Uk. 88. Biharul-An’war, Juz. 46, Uk. 65- 66. 91
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Somo la ishirini na tisa Urithi wa Imam Zaynul-Abidiin (a.s.) Hekima zake:225 i.
“Kheri yote ni mwanadamu kujilinda mwenyewe.”
ii.
“Kuridhia lichukizalo litokanalo na majaliwa ni kiwango cha juu cha daraja la yakini.”
iii.
“Ambaye nafsi yake imekamilika dunia huwa dhalili kwake.”
iv.
“Tajiri mno ni yule anayetosheka na alichogaiwa na Mwenyezi Mungu.”
v.
“Upatikanapo uchamungu matendo hayapungui, itakuwaje kipungue kinachokubalika?!!”
vi.
Aliambiwa: Mtu hatari sana ni nani? Akajibu: “Ni yule asiyeona dunia kuwa ni hatari kwa nafsi yake.”
vii. Mtu mmoja akasema mbele yake: “Ewe Mwenyezi Mungu nitosheleze dhidi ya viumbe wako.” Imam (a.s.) akamwambia: “Si hivyo, hakika watu huwahitajia watu wengine, lakini sema: Ewe Mwenyezi Mungu, nitosheleze dhidi ya viumbe wako wabaya.” 225
ekima zote hizi zinapatikana ndani ya kitabu Tuhaful-Uquul, Uk. 200 – 205, tumenH ukuu kutoka humo. 92
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
viii. “Jiepusheni na uwongo, mdogo na mkubwa, katika mzaha na ukweli, hakika mtu anaposema uongo katika kidogo huwa jasiri wa kuongopa kikubwa.” ix. “Ni msaada tosha wa Mwenyezi Mungu kwako kumuona adui yako akimuasi Mwenyezi Mungu kwa kukulenga wewe.” x.
Mtu mmoja akamuuliza nini maana ya kuipa dunia kisogo? Akajibu: “Kuipa dunia kisogo kuna mafungu kumi: Hivyo daraja la juu kabisa la kuipa dunia kisogo ndio daraja la chini la uchamungu. Na daraja la juu la uchamungu ndio daraja la chini la yakini. Na daraja la juu la yakini ndio daraja la chini la ridhaa. Na hakika kuipa dunia kisogo kumezungumziwa ndani ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu: Ili msihuzunike juu ya kitu kilichokupoteeni, wala msifikiri kwa alichokupeni.”226
xi. “Ewe mwanadamu utaendelea kuwa katika kheri iwapo tu utakuwa na mawaidha toka ndani ya nafsi yako, na kujitathmini kukawa ndio lengo lako, na hofu ikawa ndio mbiu yako, na tahadhari ikawa ndio shuka lako. Ewe mwanadamu wewe ni mwenye kufa na utafufuliwa na kusimama mbele ya Mwenyezi Mungu hivyo muandalie majibu.” xii. “Hakuna ubora wa nasaba kwa mkurayshi wala kwa mwarabu isipokuwa kwa unyenyekevu, wala hakuna ubora isipokuwa kwa uchamungu, wala hakuna amali isipokuwa kwa nia, wala ibada isipokuwa kwa elimu. Fahamuni kuwa mtu achukiwaye sana na Mwenyezi Mungu ni yule afuataye mwenendo wa kiongozi wala hafuati matendo yake mwenyewe.”
226
Sura Al-Hadid: 23. 93
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Dua yake katika kujikinga na ubaya, maadili mabaya na matendo maovu “Ewe Mwenyezi Mungu, mimi najikinga Kwako dhidi ya hasira ya pupa na ukali wa ghadhabu, nguvu za husuda, udhaifu wa subira, uchache wa kukinai, ugumu wa tabia na mhimizo wa matamanio, uwezo wa kujipenda, kufuata matamanio, kukhalifu uongofu, usingizi wa mghafiliko, utoaji wa kulazimishwa na kutanguliza batili kuliko haki. “Najikinga dhidi ya kukazania madhambi, nidharau maasi na kukuza utii, kuwafakharisha wenye mali na kuwadhalilisha mafakiri, kumtawala vibaya yule aliyomo mikononi mwetu na kuacha kumshukuru yule aliyetutendea wema. Au kumsaidia dhalimu, au kumtelekeza mwenye matatizo, au kutaka tusichokuwa na haki nacho, au kusema tusichokuwa na elimu nacho. “Tunajikinga kwako dhidi ya kula njama za kumtapeli mtu, au kujivuna kwa matendo yetu, na kurefusha matarajio yetu. Tunajikinga Kwako dhidi ya nia mbaya, kudharau kichache, au kutawaliwa na shetani, au muda usitupoteze au mtawala asitudhulumu. Tunajikinga Kwako dhidi ya kuchukua uharibifu na kukosa cha kutosheleza. Tunajikinga Kwako dhidi ya furaha ya maadui. Ututoe toka kwenye ufakiri mpaka tuweze kujitosheleza, ututoe kwenye maisha magumu na kifo cha bila maandalizi. Tunajikinga Kwako dhidi ya majuto makubwa, msiba mkubwa, uovu wa kupindukia, mafikio mabaya, kunyimwa thawabu na kupatwa na adhabu. “Ewe Mwenyezi Mungu, mrehemu Muhammad na kizazi cha Muhammad, nikinge na hayo yote kwa rehema zako, na wakinge waumini wote wa kiume na wakike, ewe Mbora wa wenye kurehemu.” 94
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Dua yake ya kutaka shauku ya kuwa mwenye kuomba maghfira kwa Mwenyezi Mungu “Ewe Mwenyezi Mungu mrehemu Muhammad na kizazi chake. Tupeleke kwenye toba uipendayo na utuepushe na kung’ang’ania ulichukialo. Ewe Mwenyezi Mungu tutakaposimama kati ya mapungufu mawili: Katika dini au dunia basi weka upungufu kwenye lile la kuondoka haraka, na weka toba kwenye lile lenye kubakia muda mrefu. “Na tutakapokusudia makusudio mawili ilihali moja likikuridhisha na jingine likikukasirisha basi tuegemeze kwenye lile likuridhishalo, na udhoofishe nguvu zetu kwenye lile likuchukizalo, wala usiache mwanya katika hilo kati ya nafsi zetu na hiyari zetu, kwa sababu nafsi zetu huchagua batili isipokuwa pale unapozipa taufiki, huamrisha mabaya isipokuwa pale unapozirehemu. “Ewe Mwenyezi Mungu, hakika Wewe umetuumba kutokana na udhaifu, ukatuimarisha juu ya udhaifu ukatuanzisha kutokana na maji dhalili, hivyo hatuna ujanja isipokuwa kwa nguvu Zako, wala hatuna nguvu isipokuwa kwa msaada Wako. Tuunge mkono kwa taufiki Yako na tuimarishie njia kwa uimara Wako. Pofusha macho ya nyoyo zetu kwenye yale yaliyopingana na mapenzi Yako, wala usifanye sehemu yoyote ya viungo vyetu itekeleze maasi dhidi Yako. “Ewe Mwenyezi Mungu mrehemu Muhammad na kizazi chake, jalia sauti za nyoyo zetu, harakati za viungo vyetu, mtazamo wa macho yetu na lahaja za ndimi zetu vyote katika vinavyowajibisha thawabu Zako, ili usitupite wema wowote tunaostahili kwao malipo, wala tusibakie na baya lolote tunalostahili kwalo adhabu Yako.”
95
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Dua yake ya kuomba kimbilio kwa Mwenyezi Mungu “Ewe Mola Mlezi! Ukipenda tusamehe kwa fadhila Zako na ukipenda utatuadhibu na hiyo itakuwa kwa uadilifu Wako. Hivyo basi tufanyie wepesi msamaha Wako kwa huruma Yako. Tuepushe na adhabu Yako kwa subira Zako. Kwa kuwa hatuna uwezo wa kuukabili uadilifu Wako wala hakuna anayeokoka bila ya msamaha wako. “Ewe Mwenye kujitosha kuliko matajiri wote. Tu waja wako mbele Yako, nami ni fakiri kuliko mafakiri wote Kwako basi urekebishe ufakiri wetu kwa wasaa Wako. Usikate matumaini yetu kwa zuio Lako, utakuwa umemdhalilisha mwenye kukuomba kheri na umemnyima aliyekuomba fadhila Zako. Kwa hiyo tugeukie kwa nani zaidi Yako, twende wapi kama si mlangoni Kwako, hakika utukufu ni Wako, sisi ni wenye dhiki ambao umewajibisha kuwakubalia, ni wenye uovu uliowaahidi kuwaondolea uovu wao. “Ni kitu chafanana sana na utashi Wako na ni bora kulingana na utukufu Wako kumhurumia aliyekuomba umuhurumie na kumsaidia aliyekuomba msaada. Hurumia ungamo letu Kwako na tutosheleze tujitupapo mbele Yako. “Oh! Mola wetu Mlezi! Hakika shetani ametusimanga kwa kuwa tumemfuata katika kukuasi wewe. Mrehemu Muhammad na kizazi chake, usimuache atusimange baada ya kuwa tumemwacha kwa ajili Yako. Tumemtelekeza na kuelekea Kwako.” Dua yake kuomba mwisho mwema “Ewe ambaye utajo wake ni heshima kwa wamtajao. Ewe ambaye shukurani yake ni ufanisi kwa wenye kumshukuru. Ewe ambaye utii wake ni uokovu kwa wenye kumtii. Mrehemu Muhammad na kizazi chake. 96
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
“Zihangaishe nyoyo zetu katika kukutaja Wewe na kuziweka mbali na utajo mwingine wote. Na zihangaishe ndimi zetu katika kukushukuru na ziwe mbali na shukuru zingine zote. Na viungo vyetu vya miili vihangaike kukutii Wewe na kuwa mbali na utii mwingine wowote. “Ukitupangia wakati wa faragha basi jalia faragha iliyo salama. “Tusifuatwe na lipizo baya wala usituambatanishe humo na kuchoshwa ili watuondokee waandishi wa maovu na nyaraka tupu zisizotaja chochote katika maovu yetu. Na warudi waandishi wa mema kutoka kwetu wakiwa na furaha na waliyoyaandika miongoni mwa mema yetu. Na ziishapo siku za maisha yetu na kumalizika kwa muda wa umri wetu na kutufikia wito Wako ambao hapana budi utufikie na pia hapana budi kuujibu, basi umrehemu Muhammad na kizazi chake. “Na ujaalie matokeo ya hesabu ya waandishi wa mabaya yetu kuwa toba yenye kukubaliwa. Usitusimamishe na dhambi tuliyotenda baada yake wala maasi tuliyoyafanya. Wala usifichue sitara uliyotusitiri nayo mbele ya mashahidi siku zitakapojaribiwa habari za waja Wako. Hakika Wewe ni mpole kwa akuombaye na ni mwenye kuitikia kwa akuitaye.”227 Muhtasari Maimamu wa Ahlul-Baiti (a.s.) walijitofautisha kwa elimu yao na maarifa yao ya hali ya juu. Wanahistoria wote wamesema kuwa walizama ndani ya elimu, na wao ndio watu wenye elimu kuliko wengine. Ahlul-Baiti (a.s.) ambao Mtume (s.a.w.w.) aliwafanya pacha wa Qur’ani kwa amri ya Mwenyezi Mungu walifuata njia ya Qur’ani 227
- Tazama As-Swahifatus-Sajadiyyah. 97
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
katika kuchimbua maarifa ya Mwenyezi Mungu katika jamii ya kiarabu na ya kiislamu. Wakapiga vita kwa namna kali sana kila jaribio la kijalihiya lililolenga kuvuruga misingi na mafunzo ya mapinduzi haya ya Mwenyezi Mungu. Wala harakati zao hazikukomea kwenye sekta fulani tu ya kimaarifa, kimaadili na kimwenendo bali zilijumuisha sekta zote. Kuanzia hapo kitabu Sahifatus-Sajadiah kikawa ni hazina ya urithi huu wa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kumjenga mwanadamu kuanzia mtu mmoja mmoja hadi jamii nzima. Wala urithi wa Imam Zaynul-Abidiin (a.s.) haukomei kwenye kitabu hiki Sahifatus-Sajadiah tu, bali kuna urithi mwingine kama zinavyotuwekea wazi suala hilo rejea za Imam Zaynul-Abidiin (a.s.). Maswali: 1. Kwa mujibu wa maneno ya Imam (a.s.) tajiri mno ni nani? 2. Mtu hatari mno ni nani? 3. Kwa nini uwongo haufai hata wakati wa mzaha? 4. Ni nani achukiwaye sana na Mwenyezi Mungu? 5. Ni mambo gani ambayo mwanadamu inampasa kuyaomba toka kwa Mola wake Mlezi?
98
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Somo la thelathini Urithi wa Imam Zaynul-Abidiin (a.s.) Risala ya haki ya mtu kwa mtu: Kitabu Risalatul-Huquq kimebeba jukumu la kuratibu aina mbalimbali za mahusiano ya mwanadamu ndani ya maisha haya kuanzia ya mtu mmoja mmoja hadi ya kijamii kwa namna ambayo yatamhakikishia mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla mahusiano salama na kuwakusanyia sababu za kujitegemea, kufaulu na kustawi. Hakika kuratibu mahusiano ya kijamii kwa msingi wa kuainisha makundi ya haki kwa umakini ndio lengo la kwanza la nidhamu ya jamii ya Kiislamu, na ndio msingi wa kiakili wa sheria zote za kiislamu, hivyo atakayefahamu kwa undani ujumbe wa kitabu hiki, na akasoma kwa undani haki za muumba na haki za viumbe mbele ya viumbe wengine ataweza kufahamu siri za sheria ya kiislamu na falsafa ya hukumu ambazo zimeletwa na sheria ya kiislamu kwa ajili ya kupangilia maisha ya mwanadamu kuanzia mtu mmoja mmoja hadi jamii nzima. Tunajua kuwa Imam (a.s.) aliwatangulia wasomi na waweka kanuni wote katika ulimwengu wa kiislamu bali katika ulimwengu wa mwanadamu katika uwanja huu ambao kwa misingi yake inajengeka misingi ya maadili, malezi na nidhamu ya jamii. Imamu Zaynul-Abidiin (a.s.) aliandika ujumbe huu wa dhahabu, akawapa baadhi ya maswahaba zake na ukapokewa na Thiqatul-Islam Thabit bin Abi Swafiyah, aliye maarufu kwa jina la Abu Hamza At-Thummaliy ambaye ni mwanafunzi wa Imam (a.s.). Pia 99
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
umepokewa na mwanazuoni wa hadithi As-Swaduq ndani ya kitabu chake Al-Khiswal. Pia kaupokea Thiqatul-Islam Al-Kulayni ndani kitabu Al-Kafiy. Na ameupokea Al-Hasan bin Ali bin Shaabah AlHarraniy ndani ya kitabu Tuhaful-Uquul, na kitabu hiki ni kati ya vitabu vya zamani mno vinavyotegemewa na wanazuoni. Imam (a.s.) kabla hajaanza kubainisha haki ameanza kuashiria kuwa kuna haki zilizomzunguka mwanadamu ambazo ni lazima azijue. Kisha akabainisha haki kubwa, nayo ni ile inayomfungamanisha mwanadamu na Mwenyezi Mungu, kisha anazalisha haki za mwanadamu zilizofaradhishwa kwa mwanadamu dhidi ya nafsi yake. Hivyo anabainisha aina za mahusiano ya mwanadamu na nafsi yake kwa mtazamo wa Mwenyezi Mungu kisha anaishia kubainisha aina za mahusiano kati ya mwanadamu na mazingira yamzungukayo ambayo yanajumuisha watawala na watawaliwa, raia na viongozi, ilihali akibainisha aina za maimamu na maamuma na daraja zao. Kisha anabainisha mahusiano mengine pamoja na udugu wa damu, familia na matawi yake, kisha familia inajumuisha watwana na vijakazi. Kisha Imam (a.s.) anagusia wengine wenye haki kama mwadhini, imamu wa sala, mshirika, mwenzio, mwenye deni, mgomvi, mwomba ushauri na mwombwa ushauri, mtaka nasaha na mwombwa nasaha, mwombaji na mwombwa, mdogo, na mkubwa. Mpaka anaishia kwa yule anayeshirikiana na mwanadamu katika dini yake kati wa wanadamu. Kisha haki za yule anayeshirikiana na mwanadamu katika ubinadamu na anayeshirikia nae katika muundo wa kisiasa ambaye anautii japokuwa si katika watu wa mila yake na dini yake. Hivyo kifuatacho ni maelezo kamili ya ujumbe kama ulivyo ndani ya kitabu Al-Khiswal.228 228
l-Khiswal cha Shaikh As-Swaduq, tazama chapa iliyohakikiwa na jopo la wahadhiri A au Darul-Maarif. 100
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Muhtasari wa haki na viwango vyake: “Fahamu kuwa Mwenyezi Mungu anazo haki fulani juu yako zenye kukuzunguka kila uendapo au kila ukaapo, katika kila sehemu uwayo, na katika kila kiungo ukisogezacho au kila zana unayoitumia, baadhi ya haki hizi ni kubwa kuliko nyinginezo. Na iliyo kubwa zaidi kuliko zote ni ile haki aliyo nayo Mwenyezi Mungu mwenyewe juu yako ambayo ndiyo mzizi wa haki zote. Kisha ameziweka haki ambazo viungo vyako tofauti tofauti zinavyo juu yako toka kichwani hadi miguuni. Hivyo aliupa haki ulimi wako, macho yako masikio yako, mikono yako, miguu yako, tumbo lako, na viungo vya siri. Haki hizi zinahusu viungo saba ambavyo hutoa shughuli zako zote za maishani mwako. Kisha Mwenyezi Mungu ameweka haki ya matendo juu yako, hivyo akayawekea haki matendo yako ya sala yako, funga yako, zaka yako, kafara yako, sadaka zako, na matendo mengine ya ibada. Baada ya hapo hufuata haki walizo nazo watu wengine juu yako, hivyo zilizo muhimu zaidi ni haki za mkuu wako, wanaokutegemea na ndugu zako. Na hizi aina tatu za haki zimezaa matawi mengi ya haki. Hivyo haki za wakuu wako ni za aina tatu: Haki ya mfalme, haki ya mwalimu wako na haki ya mwajiri wako na kila mkuu ni kiongozi. Na haki za wanaokutegemea ni za aina tatu: Haki ya raia zako, haki ya mwanafunzi wako kwani hakika mwanafunzi humtegemea mwalimu, kisha ni haki za unaowamiliki: Wake zako na vijakazi wako. Na haki za ndugu zako wa damu ni nyingi mno kutegemeana na ukaribu wa udugu huo. Hivyo iliyo muhimu sana kati ya hizo ni haki ya mama yako, kisha baba yako, kisha watoto wako, kisha ndugu zako, kisha ndugu wengine kufuatana na ubora wa udugu wake, hivyo awe ndugu wa karibu kwanza, kisha ndugu wa mbali. 101
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Kisha kuna haki ya mkubwa wako wa kazi na ya mtumishi wako, kisha haki ya mfadhili wako, kisha haki ya mwadhini anayekuita kwenye sala, na haki ya imamu anayekuongoza katika sala, kisha haki ya mfuasi wako, kisha haki ya jirani yako, kisha haki ya wenzi wako na washirika wako. Kisha haki ya tajiri kuliko wewe, kisha haki ya mdaiwa wako, kisha haki ya aliyekukopesha, kisha haki ya rafiki yako na haki ya mwenye malalamiko juu yako, kisha haki ya mtu unayelalamika juu yake, kisha hufuata haki ya mtu anayekutaka ushauri na anayekushauri, kisha haki ya yule anayetaka nasaha toka kwako na yule anayekunasihi. Kisha kuna haki ya mtu aliyekuzidi umri na ya mtu uliyemzidi umri, kisha haki ya anayekuuliza jambo na ya unayemuuliza jambo. Kisha haki ya mtu uliyemkosea kwa maneno au kwa matendo kwa bahati mbaya au kwa kudhamiria. Kisha ni haki ya Waislamu wenzio kwa ujumla, kisha haki ya wale wasio Waislamu ambao wako katika hifadhi ya Waislamu, kisha ni haki nyinginezo zilizo wajibu katika hali bali na kwa sababu mbalimbali. Hivyo basi, aliyebarikiwa ni yule ambaye Mwenyezi Mungu humsaidia kuzitimiza haki zote zilizo wajibu juu yake.� Haki kwa ufafanuzi: Hivyo haki ya Mwenyezi Mungu ni umwabudu yeye tu bila ya kumuwekea mwenza. Na kama ukiutimiza wajibu huu kwa uaminifu basi Mwenyezi Mungu ameahidi kukutosheleza katika mambo ya ulimwengu huu na kesho Akhera. Na haki ya nafsi yako kwako ni kuwa uitumie kikamilifu kumtii Mwenyezi Mungu. Na haki ya ulimi ni kuwa uupe heshima kwa kutokuzungumza mambo machafu, na kuufundisha kuzungumza mam102
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
bo mazuri, na kuuambaza na mambo yasiyo na faida, na kusema maneno yenye faida na kusema mazuri na yenye wema. Haki ya masikio ni kuyaepusha kusikia utesi na yale yasiyo halali kusikilizwa. Na haki ya macho ni kuyafumba yasione ambayo hayaruhusiwi kuyaona, na kujifunza kupitia muono wake. Na haki ya mkono wako ni kuwa usiunyooshe kwenye kitu kilichokatazwa. Na haki ya miguu yako ni kuwa usiitumie kwenda kwenye sehemu ulizokatazwa kwenda. Kwani utasimama kwenye njia ya Mwenyezi Mungu kwa kutumia miguu hiyo, hivyo jihadhari isikutelezeshe ukaja angukia ndani ya moto. Na haki ya tumbo lako ni kuwa usiligeuze mtungi wa chakula haramu, na wala usile hadi ukavimbiwa. Ama haki ya via vyako vya siri ni kuwa uvilinde visije vikazini, na uvisitiri visije vikaonekana. Haki ya sala ni kuwa ni lazima utambue kuwa ni baraza la Mwenyezi Mungu na kuwa wakati wa Sala unasimama mbele ya Mwenyezi Mungu. Utakapotambua hivyo basi kusimama kwako kutakuwa kule kwa mja wa Mwenyezi Mungu aliye mnyenyekevu, ilihali ukiwa na hamu kubwa, ukiogopa, ukihofia ghadhabu yake ukitegemea kupata na ukiwa mkata mwenye kuomba huku ukimheshimu yule ambaye uko mbele yake kwa utulivu na ukimya, ukiheshimu haki zake na mipaka yake ilihali ukitoa roho yako kwake. Haki ya hija ni utambue kuwa ni baraza la Mola wako Mlezi na ni kumkimbilia dhidi ya dhambi zako na hapo ndipo panakubaliwa toba yako na kutekelezwa faradhi aliyowajibisha Mwenyezi Mungu kwako. Na haki ya Funga ni utambue kuwa ni pazia la Mwenyezi Mungu aliloliweka katika ulimi wako, masikio yako, macho yako, tumbo lako na via vyako vya siri ili akulinde dhidi ya moto, hivyo ukiacha funga utakuwa umepasua pazia ya Mwenyezi Mungu aliyokuwekea. 103
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Haki ya sadaka ni utambue kuwa ni akiba yako uliyoiweka kwa Mwenyezi Mungu na amana yako ambayo haihitajii ushahidi, hivyo utakapotambua hilo utakuwa na imani sana na ile amana uliyoiweka kwa siri kuliko ile uliyoiweka kwa dhahiri. Na tambua kuwa inakuondolea mabalaa na magonjwa hapa duniani na itakuondolea moto huko Akhera. Na haki ya mnyama wa kafara ni kuwa atolewe kwa nia safi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na wala si kwa kuwakusudia viumbe Wake huku ukiwa hautaki isipokuwa kupata rehema za Mwenyezi Mungu na kuiokoa roho yako siku ya kukutana nae. Na haki ya mtawala wako ni lazima utambuwe kuwa wewe ni jaribio kwake na wewe unajaribiwa kwa madaraka aliyonayo juu yako, hivyo ni lazima usimuasi ili usije ukajiangamiza hivyo ukawa mshiriki mwenza katika ubaya unaokufika toka kwake. Na haki ya mwalimu wako ni kumheshimu na kuheshimu baraza la wasikilizaji wake, umsikilize kwa makini na uwepo kwake kifikra. Usiinue sauti mbele yake kuliko sauti yake wala usimjibu yeyote aliyemuuliza kabla hajajibu. Usizungumze na yeyote kwenye baraza lake wala usimtete yeyote mbele yake. Umtetee iwapo katajwa vibaya mbele yako, ufiche aibu zake, udhihirishe fadhila zake. Usikae na adui wake wala usimfanyie uadui rafiki yake. Basi ukitimiza hayo ujue kuwa malaika watakutolea ushahidi kuwa kweli ulimkusudia na ulijifunza elimu yake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na wala si kwa ajili ya watu. Na haki ya tajiri wako ni kumtii na wala usimuasi ila katika yale yanayomchukiza Mwenyezi Mungu, kwani hakika hakuna kumtii kiumbe katika jambo la kumuasi muumba. Na haki ya raia ni lazima utambue kuwa wamekuwa raia wako kutokana na kuwashinda kwa nguvu zako, hivyo ni lazima uwe 104
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
mwadilifu kwao na uwe kama mzazi mwenye huruma kwao, usamehe ujinga wao na wala usiharakishe kuwaadhibu. Na umshukuru Mwenyezi Mungu kwa kukupa nguvu Zake mpaka ukaweza kuwashinda. Ama haki ya mwanafunzi ni lazima utambue kuwa Mwenyezi Mungu kakufanya bwana wao kwa kukupa elimu na kukufungulia hazina zake, hivyo iwapo utakuwa mkarimu kwa kuwafundisha watu bila kuwafanyia kiburi wala kuwakashifu basi Mwenyezi Mungu atakuzidishia fadhila Zake. Na iwapo utawanyima watu elimu yako au ukawafanyia kiburi wakati wa kutafuta elimu toka kwako, basi itakuwa ni haki kwa Mwenyezi Mungu kukunyang’anya elimu yake na heshima yake na aondoe nafasi yako kwenye nyoyo za watu.” Muhtasari Kitabu Risalatul-Huquq kimechukua jukumu la kuweka muundo wa mahusiano ya mwanadamu kwa namna isiyo na mfano kuanzia mahusiano ya mtu mmoja mmoja hadi ya kijamii. Imam (a.s.) alitibu maradhi ya kinafsi na kimatendo kwa kupitia dua zake nzuri na maneno yake ya busara, maradhi ambayo yalikuwa yameikumba jamii yake baada ya kupatwa na tatizo la kuacha njia sahihi ya uongozi baada ya Mtume (s.a.w.w.), jambo lililopelekea kidogo kidogo kuharibika mazingira ya kidini na kifikra na kushuka kiwango cha maadili na mwenendo mwema kwa Waislamu wote. Kuanzia hapo zikawa harakati za Imam As-Sajjad (a.s.) zinalenga jambo moja nalo ni kuasisi jamii imara ya kielimu na kuweka vizuizi vya kinafsi na kiroho vitakavyosimama mbele ya mawimbi ya mmong’onyoko wa maadili ambao ulianza kuingia ndani ya umma 105
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
kupitia mmong’onyoko wa maadili ya watawala wa kibani Umayya na kupitia mapinduzi ya mataifa yaliyokuwa yakiendelea kujiunga na Uislamu. Maswali: 1. Haki muhimu na kubwa kuliko zote ni ipi? 2. Ni haki gani ambayo haki nyingine zote zinatokana na yenyewe? 3. Ni ipi haki ya Mwenyezi Mungu iliyopo kwa viumbe wake? 4. Ni ipi haki ya nafsi na viungo iliyopo kwa mwanadamu? 5. Ni ipi haki ya sala kwa mwanadamu? 6. Ni ipi haki ya ulimi kwa mwanadamu? 7. Ni ipi haki ya mwalimu kwa mwanafunzi? 8. Ni ipi haki ya mwanafunzi kwa mwalimu? Kwa ajili ya kujisomea Ama haki ya mkeo ni kuwa ni lazima utambue kuwa Mwenyezi Mungu amemfanya kuwa utulivu na starehe kwako, hivyo ni lazima ufahamu kuwa hiyo ni neema kubwa kwako, basi mhurumie na kumheshimu japokuwa haki zako ni kubwa kwake. Yeye ana haki kwako ya kuhurumiwa kwa sababu ni mateka wako na chakula chake na mavazi yake ni wajibu juu yako. Ama haki ya mtumishi wako ni lazima utambue kuwa ni kiumbe wa Mola wako, ni mwana wa baba yako na mama yako, na ni nya106
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
ma yako na damu yako, hivyo hujammiliki kwa kuwa umemuumba kinyume na Mwenyezi Mungu, au umeumba kiungo kati ya viungo vyake, wala kwa kuwa umemuumbia riziki yake bali Mwenyezi Mungu ndiye aliyefanya yote hayo, kisha akamfanya kuwa mwenye kukutegemea huku akiwa dhamana kwako na amana yake kwako ili Mwenyezi Mungu akuhifadhie kheri unayompa. Hivyo mtendee wema kama Mwenyezi Mungu akutendeavyo wema, na kama ukichukizwa nae badilisha mwingine bila kuadhibu viumbe wa Mwenyezi Mungu. Na hakika hakuna nguvu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu. Ama haki ya mama yako ni kuwa ni lazima utambue kuwa alikubeba kiasi ambacho hakuna mtu yeyote yule mwingine awezaye kukubeba. Akakulisha matunda ya moyo wake ambayo hakuna yeyote awezaye kukulisha, akakulinda kwa viungo vyake vyote. Alivumilia njaa ili akulishe, akavumilia kiu ili akunyweshe, akavumilia kubaki bila mavazi ili akuvishe, akapigwa na jua huku akikukinga kwa kivuli chake na akikosa usingizi kwa ajili yako. Alikukinga na joto na baridi ili uwe kwa ajili yake. Hakika wewe huwezi kumshukuru isipokuwa kwa msaada wa Mwenyezi Mungu na taufiki Yake. Ama haki ya baba yako ni lazima utambue kuwa yeye ni mzizi wako na laiti kama si yeye usingekuwepo, hivyo kila unapoona kinachokupendeza basi tambua kuwa baba yako ndiye chanzo cha zawadi hiyo uliyonayo, hivyo muhimidi Mwenyezi Mungu na kumshukuru baba yako kwa kadiri ya mchango wake. Hakuna nguvu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu. Ama haki ya mtoto wako ni lazima utambue kuwa anatokana na wewe, na kuwa unahusika kwa matendo yake mazuri na mabaya katika ulimwengu huu, na kuwa wewe unapaswa kumfundisha tabia nzuri na kumuongoza kuelekea kwa Mola wake huku ukimsaidia katika kuzifuata amri Zake. Hivyo ni lazima ujitahidi kumuelimisha 107
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
kama vile afanyavyo mtu mwenye kutambua kuwa atalipwa mema kwa kumtendea wema na ataadhibiwa kwa kumtendea mabaya. Ama haki ya ndugu yako ni lazima utambue kuwa yeye ni mkono wako, mgongo wako unaoutegemea na nguvu yako ambayo kwayo unashambulia, hivyo usimfanye silaha ya kumuasia Mwenyezi Mungu wala chombo cha kuwadhulumia viumbe wa Mwenyezi Mungu. Usiache kumnasihi na kumsaidia dhidi ya adui yake. Kama atamtii Mola wake ni bora na kama si hivyo basi mchague Mwenyezi Mungu badala ya ndugu yako. Hakuna nguvu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu. Ama haki ya aliyekupa uhuru ni kuwa ni lazima utambue kuwa alitumia mali yake kwa ajili yako, kisha akakutoa katika fedheha na ukiwa wa utumwa na kukuweka katika heshima na furaha ya uhuru. Amekupa uhuru toka kifungo cha utumwa huku akikufungua minyororo ya utumwa. Akakutoa jela ya udhalimu na amekufanya wewe mwenyewe kuwa bwana wa nafsi yako, amekupa nafasi ya kumuabudu Mola wako, hivyo tambua yeye ni mbora kwako katika maisha yako na kifo chako kuliko mtu mwingine yeyote. Hivyo ni wajibu kwako kumsaidia na kumtimizia haja yake anayohitajia toka kwako. Hakuna nguvu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu. Ama haki ya uliyempa uhuru ni lazima utambue kuwa Mwenyezi Mungu amefanya huko kumpa uhuru kuwa ni njia ya kuelekea Kwake na kinga yako dhidi ya moto, na kutakuletea thawabu Siku ya Akhera, na amekufanya umrithi kama hana ndugu wa damu kufidia mali yako uliyotoa na Siku ya Kiyama ni peponi. Ama haki ya mfadhili wako ni lazima umshukuru na kukumbuka wema wake na mtangaze kwa maneno mazuri na muombee kwa uaminifu uwapo wewe na Mwenyezi Mungu. Hakika ukifanya hivyo 108
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
utakuwa umemshukuru kwa siri na dhahiri, kisha kama inawezekana kumlipa fadhila zake kwa matendo yako basi fanya hivyo. Ama haki ya mwadhini ni lazima utambue kuwa anakukumbusha Mola Wako na anakuita kupata fungu lako na yeye ni msaada kwako katika kutekeleza wajibu uliyo juu yako. Hivyo ni lazima umshukuru mtu huyo kama vile unavyomshukuru mtu aliyekufanyia huruma. Ama haki ya Imamu wa Sala yako ni lazima utambue kuwa amechukua jukumu la kuwa balozi wako mbele ya Mwenyezi Mungu. Amezungumza kwa niaba yako lakini wewe hukuzungumza kwa niaba yake, kakuombea lakini wewe hukumuombea, amekuokoa katika fadhaa ya kusimama mbele ya Mwenyezi Mungu. Hivyo kama upo upungufu wowote katika matendo hayo basi ni yeye atakayeulizwa wala si wewe. Na kama yametimia basi unakuwa mshiriki mwenza katika malipo ingawa wewe ni mbora kuliko yeye. Hivyo ameokoa nafsi yako kwa nafsi yake na Sala yako kwa Sala yake basi mshukuru kwa kadiri ya mchango wake. Ama haki ya mwenzi wako ni kuwa uwe mpole kwake na kumtendea haki katika mazungumzo na wala usiinuke kutoka katika kikao chake isipokuwa kwa idhini yake, na kama yeye atakuja kukaa pamoja na wewe basi anao uhuru wa kuchagua kwenda au kutokwenda bila idhini yako. Sahau makosa yake, hifadhi kheri yake na usimsikilizishe isipokuwa la kheri. Ama haki ya jirani yako ni kuyalinda mambo yake awapo hayupo na kumheshimu awapo mbele yako, umsaidie adhulumiwapo na usizipeleleze aibu zake, hivyo iwapo kwa bahati mbaya ukigundua aibu zake msitiri. Na ukitambua kuwa anakubali nasaha zako basi mnasihi ukiwa wewe na yeye tu. Usimtelekeze wakati wa shida, msamehe makosa yake na yabeue maneno yake 109
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
na uishi nae kwa wema. Hakuna nguvu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu. Ama haki ya rafiki ni lazima uishi nae kwa uadilifu na heshima, umheshimu kama anavyokuheshimu na uwe rehema kwake na wala usiwe adhabu kwake. Hakuna nguvu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu. Ama haki ya mshiriki mwenza ni kuwa ni lazima uchukue jukumu lake awapo hayupo na akiwepo mkabidhi jukumu lake. Usiamue jambo bila idhini yake, usitekeleze mawazo yako kabla ya kupata mawazo yake. Muokolee utajiri wake na wala usimfanyie khiyana katika jambo lake dogo au kubwa. Hakika baraka za Mwenyezi Mungu ziko juu ya washiriki kwa kadiri wabakiavyo bila kufanyiana khiyana. Hakuna nguvu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu. Ama haki ya utajiri wako ni kuwa usiupate isipokuwa kwa njia halali na wala usiutumie isipokuwa matumizi ya halali. Usimrithishe ambaye hawezi hata kukushukuru, hivyo utumie katika kumtii Mola wako na wala usiufanyie ubahili kwa kuishi maisha magumu na kuishia kujuta. Hakuna nguvu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu. Ama haki ya mwia ambaye anataka umlipe deni ni kuwa kama una uwezo mlipe na kama una matatizo basi ni lazima umridhishe kwa maneno ya upole na umrudishe kwa ukarimu na upole. Ama haki ya mshirika ni kuwa usimlaghai au kumpunja na wala usiseme uwongo kwake na mche Mwenyezi Mungu katika jambo lake. Ama haki ya mdai ni kuwa kama dai lake dhidi yako ni la haki basi kuwa shahidi wake dhidi yako mwenyewe, wala usimdhulumu na umpe haki yake. Na kama dai lake si la haki basi zungumza nae kwa upole na wema na wala usiache kumlainisha na wala usimuudhi 110
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Mola wako katika dai lake. Hakuna nguvu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu. Ama haki ya mtuhumiwa unayemtuhumu ni kuwa iwapo dai lako ni haki zungumza nae kwa ukarimu kwa kulieleza wazi wazi dai lako. Usikanushe haki yake iliyomo ndani ya dai lako. Na kama dai lako ni la batili basi mche Mwenyezi Mungu na utubu kwake na uache dai lako. Ama haki ya mtu anayetaka ushauri ni kuwa kama una ushauri wowote kwake basi mpe kwa uaminifu na kama hauna ushauri wowote basi muongoze kwa mtu mwenye ushauri. Ama haki ya mtu anayekupa ushauri ni kuwa usimdhanie mabaya kama ushauri wake hauafikiani na maoni yako. Na kama ushauri wake unaafikiana na maoni yako basi mshukuru Mwenyezi Mungu. Ama haki ya mtu anayekutaka nasaha basi ni lazima umnasihi na mwenendo wako katika kumnasihi uwe ni rehema tupu na upole. Ama haki ya mtu anayekunasihi ni kuwa ni lazima uwe mnyenyekevu kwake na umsikilize kwa masikio yako. Yatazame mazungumzo yake kwa uangalifu, kama ni sahihi mshukuru Mwenyezi Mungu na kama hukuona usahihi basi mhurumie na wala usimtuhumu na ujue kuwa kakosea bahati mbaya, wala usimtuhumu kwa hilo isipokuwa atakapostahili kweli kutuhumiwa, hivyo hapo usimsikilize katika hali yoyote ile. Hakuna nguvu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu. Ama haki ya mkubwa aliyekuzidi umri ni lazima umheshimu kwa umri wake na umfadhilishe kwa kukutangulia ndani ya Uislamu, usibishane nae katika mazungumzo, usijaribu kutaka kumpita uwapo naye katika matembezi na usimtangulie utembeapo naye njiani, usiwe mfidhuli kwake na umvumilie awapo mfidhuli kwako na endelea kumuheshimu kwa sababu ya Uislamu na umri wake. 111
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
Ama haki ya uliyemzidi umri ni kuwa umpende kwa kumuelimisha, kwa kumsamehe, kwa kumsitiri kwa kumhurumia na kumsaidia. Ama haki ya anayeomba ni kumpa kadiri ya mahitaji yake. Ama haki ya aombwaye ni kuwa akikupa basi ipokee zawadi hiyo kwa kuithamini na kushukuru na akikunyima basi kubali udhuru wake. Ama haki ya aliyekufurahisha kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ni kuwa kwanza mshukuru Mwenyezi Mungu kisha mshukuru mtu huyo. Ama haki ya aliyekudhulumu ni kumsamehe na iwapo ukiona kumsamehe kutakudhuru basi chukua kisasi kwani Mwenyezi Mungu amesema: “Na ajikingaye baada ya kudhulumiwa basi hao ndio juu yao hakuna lawama.�229 Ama haki ya Waislamu wenzio ni kuwadhamiria amani na usalama na rehema, kuwa mpole kwa wakosefu miongoni mwao na kuwakosoa na kuwafanya wakupende, kumshukuru mwema wao, kuzuwia maudhi dhidi yao, wapendelee yale unayopendelea kwa ajili ya nafsi yako na uchukie kwao yale unayochukia kwa ajili ya nafsi yako. Waweke watu wazima katika cheo cha baba yako na vijana katika cheo cha ndugu yako, waweke maajuza katika cheo cha mama yako na wadogo katika cheo cha wanao. Na haki ya wasio Waislamu waliyo chini ya himaya za Waislamu ni ukubali toka kwao kile ambacho Mwenyezi Mungu amekipokea toka kwao wala usiwadhulumu bali ni lazima utimize wajibu ambao Mwenyezi Mungu amewawekea. Na kila sifa njema ni ya Mwenyezi Mungu. 229
- Sura As-Shura: 41. 112
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1. Qur’an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thelathini 2.
Uharamisho wa Riba
3.
Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza
4.
Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili
5.
Hekaya za Bahlul
6.
Muhanga wa Imamu Husein (A.S.)
7.
Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.)
8.
Hijab vazi Bora
9.
Ukweli wa Shia Ithnaashariyyah
10.
Madhambi Makuu
11.
Mbingu imenikirimu
12.
Abdallah Ibn Saba
13.
Khadijatul Kubra
14. Utumwa 15.
Umakini katika Swala
16.
Misingi ya Maarifa 113
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
17.
Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia
18.
Bilal wa Afrika
19. Abudharr 20.
Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu
21.
Salman Farsi
22.
Ammar Yasir
23.
Qur’an na Hadithi
24.
Elimu ya Nafsi
25.
Yajue Madhehebu ya Shia
26.
Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur’an Tukufu
27. Al-Wahda 28.
Ponyo kutoka katika Qur’an.
29.
Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii
30.
Mashukio ya Akhera
31.
Al Amali
32.
Dua Indal Ahlul Bayt
33.
Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna
34.
Haki za wanawake katika Uislamu
35.
Mwenyeezi Mungu na sifa zake
36.
Kumswalia Mtume (s)
37.
Nafasi za Ahlul Bayt (a.s)
38. Adhana 114
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
39.
Upendo katika Ukristo na Uislamu
40.
Tiba ya Maradhi ya Kimaadili
41.
Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu
42.
Kupaka juu ya khofu
43.
Kukusanya swala mbili
44.
Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara
45.
Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya
46.
Kusujudu juu ya udongo
47.
Kusherehekea Maulidi Ya Mtume (s)
48. Tarawehe 49.
Malumbano baina ya Sunni na Shia
50.
Kupunguza Swala safarini
51.
Kufungua safarini
52.
Umaasumu wa Manabii
53.
Qur’an inatoa changamoto
54. as-Salaatu Khayrun Mina -’n Nawm 55.
Uadilifu wa Masahaba
56. Dua e Kumayl 57.
Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu
58.
Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake
59.
Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata
60.
Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mtume Muhammad (s) 115
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
61.
Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza
62.
Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili
63.
Kuzuru Makaburi
64.
Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza
65.
Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili
66.
Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu
67.
Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne
68.
Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano
69.
Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita
70.
Tujifunze Misingi Ya Dini
71.
Sala ni Nguzo ya Dini
72.
Mikesha Ya Peshawar
73.
Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu
74. Ubora wa Imam ‘Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliyonyooka 75.
Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake
76. Liqaa-u-llaah 77.
Muhammad (s) Mtume wa Allah
78.
Amani na Jihadi Katika Uislamu
79.
Uislamu Ulienea Vipi?
80.
Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s)
81.
Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s)
116
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
82.
Urejeo (al-Raja’a )
83. Mazingira 84.
Utokezo (al - Badau)
85.
Hukumu ya kujenga juu ya makaburi
86.
Swala ya maiti na kumlilia maiti
87.
Uislamu na Uwingi wa Dini
88.
Mtoto mwema
89. Adabu za Sokoni 90.
Johari za hekima kwa vijana
91.
Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza
92.
Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili
93.
Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu
94. Tawasali 95.
Imam Mahdi katika Usunni na Ushia
96.
Huduma ya Afya katika Uislamu
97.
Sunan an-Nabii
98.
Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza)
99.
Shahiid Mfiadini
100. Ujumbe - Sehemu ya Kwanza 101. Ujumbe - Sehemu ya Pili 102. Ujumbe - Sehemu ya Tatu 103. Ujumbe - Sehemu ya Nne 117
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
104. Kumswalia Nabii (s.a.w) 105. Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu 106. Hadithi ya Thaqalain 107. Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza 108. Ukweli uliopotea sehemu ya Pili 109. Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu 110. Ukweli uliopotea sehemu ya Nne 111. Ukweli uliopotea sehemu ya Tano 112. Safari ya kuifuata Nuru 113. Fatima al-Zahra 114. Myahudi wa Kimataifa 115. Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi 116. Visa vya kweli sehemu ya Kwanza 117. Muhadhara wa Maulamaa 118. Mwanadamu na Mustakabali wake 119. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) 120. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) 121. Khairul Bariyyah 122. Uislamu na mafunzo ya kimalezi 123. Vijana ni Hazina ya Uislamu. 124. Yafaayo kijamii 118
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
125. Tabaruku 126. Taqiyya 127. Vikao vya furaha 128. Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 129. Visa vya wachamungu 130. Falsafa ya Dini 131. Kuhuzunika na Kuomboleza - Azadari 132. Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah 133. Kuonekana kwa Allah 134. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) 135. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) 136. Ushia ndani ya Usunni 137. Maswali na Majibu 138. Mafunzo ya hukmu za ibada 139. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1 140. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2 141. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 142. Abu Huraira 143. Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. 144. Mazingatio kutoka katika Qur’an - Sehemu ya Kwanza 145. Mazingatio kutoka kaitka Qur’an - Sehemu ya Pili 146. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza 119
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
147. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili 148. Qur’ani Tukufu – Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili 149. Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) 150. Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani 151. Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu 152. Uislamu Safi 153. Majlisi za Imam Husein Majumbani 154. Uislam wa Shia 155. Amali za Makka 156. Amali za Madina 157. Asili ya Madhehebu katika Uislamu 158. Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi 159. Ukweli uliofichika katika neno la Allah 160. Uislamu na Mifumo ya Uchumi 161. Umoja wa Kiislamu na Furaha 162. Mas’ala ya Kifiqhi 163. Jifunze kusoma Qur’ani 164. As-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah 165. Hayya ‘Alaa Khayri’l-’Amal Katika Adhana 166. Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura 167. Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na Ramadhani) 168. Uadilifu katika Uislamu 120
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
169. Mahdi katika Sunna 170. Kazi na Bidii ni njia ya maendeleo 171. Abu Talib – Jabali Imara la Imani 172. Ujenzi na Utakaso wa Nafsi 173. Vijana na Matarajio ya Baadaye 174. Usalafi – Historia yake, maana yake na lengo lake 175. Ushia – Hoja na Majibu 176. Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) 177. Maombolezo – Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) 178. Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu 179. Takwa 180. Amirul Muuminina (‘as) na Makhalifa 181. Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.) 182. Kuelewa Rehma ya Mwenyezi Mungu 183. Mtazamo kuhusu msuguano wa kimadhehebu 184. Upotoshaji Dhahiri katika Turathi (Hazina) ya Kiislamu 185. Nchi na Uraia – Haki na wajibu kwa Taifa 186. Mtazamo wa Ibn Taymiyyah kwa Imam Ali (a.s.) 187. Uongozi wa kidini – Maelekezo na utekelezaji wa Kijamii 188. Huduma ya Afya katika Uislamu 189. Historian a Sira za Viongozi Waongofu – Sehemu ya Pili 190. Uwazi baina ya Maslahi na Vikwazo 121
Historia na Sira za Viongozi Waongofu
KOPI NNE ZIFUATAZO ZIMETAFSIRIWA KWA LUGHA KINYARWANDA 1. Amateka Na Aba’Khalifa 2. Nyuma yaho naje kuyoboka 3
Amavu n’amavuko by’ubushiya
4. Shiya na Hadithi
122