Hukumu zinazomhusu mkuu wa kazi na mfanyakazi

Page 1

Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi ‫أحكام المدير والعامل‬

Kimeandikwa na: Jumuiya ya Maarifa na Utamaduni wa Kiislamu

Kimetarjumiwa na: Hemedi Lubumba (Abu Batul)



‫ترجمة‬

‫أحكام المدير والعامل‬

‫تأليف‬ ‫جمعية المعارف اإلسالمية الثقافية‬

‫من اللغة العربية الى اللغة السوا حلية‬


©Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION

ISBN: 978 – 9987 –17 – 070 – 8

Kimeandikwa na: Jumuiya ya Maarifa na Utamaduni wa Kiislamu

Kimetarjumiwa na: Hemedi Lubumba (Abu Batul)

Kimepangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation

Toleo la kwanza: Agosti, 2014 Nakala: 1000

Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. - 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: www.alitrah.info


Yaliyomo Neno la Mchapishaji........................................................................1 Utangulizi.........................................................................................3 Kazi ..........................................................................................5 Kazi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu................................................5 Unawezaje kufanya kazi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu?..............6 Je Lengo huhalalisha Njia?..............................................................8 Dharura ya Kuwepo Nidhamu.......................................................10

1. Kufuata kanuni:....................................................................10

2. Kufanya kazi kulingana na nafasi ya mtu: ......................... 11

3. Kutii amri za ...................................................................... 11 Muda wa Kazi.......................................................................14

Kuheshimu muda wa Kazi.............................................................15 Kujishughulisha..............................................................19 Kujishughulisha.............................................................................19 Kujishughulisha huku huonekana kupitia mambo yafuatayo...........................................................................20

1. Kutimiza majukumu:...........................................................21 v


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

2. Kuhisi uzembe:....................................................................21

3. Kufanya kazi ndani ya wakati:.............................................21

4. Kufanya kazi yenye ubora:..................................................22 Mahusiano ya Kibinadamu (1)....................................26

Uhusiano na Wengine....................................................................26

1. Kuwadhania vizuri:..............................................................26

2. Kuwataja wenzako kwa kheri: ............................................27

3. Kuongea na watu kwa adabu na heshima: ..........................28

Mgawanyo wa Majukumu.............................................................29 Uhusiano wa Mfanyakazi kwa Mkuu wake...................................31

1. Kumnasihi:...........................................................................31

2. Kumsaidia:...........................................................................31

3. Kutii maamuzi na sheria za ofisi:.........................................32 Mahusiano ya Kibinadamu (2)....................................34

Uhusiano wa Mkuu kwa Mfanyakazi wake...................................34 Ewe Ndugu yangu Kiongozi..........................................................35

vi


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

Ni lipi jukumu la Kiongozi............................................................36

1. Mfano mwema: ...................................................................36

2. Kuwatia moyo: ....................................................................37

3. Kutokuwa na maringo na masimango: ...............................38

4. Kumlipa mazuri yule aliyefanya vizuri:..............................38

5. Kumwadhibu mwenye kosa:................................................39

6. Kuzuia udhalilishaji:............................................................40

7. Kusamehe:............................................................................41 Vifaa na Vitendea Kazi..................................................43

Vifaa vya Kazi ni Amana...............................................................43 Kuheshimu Amana ni kipimo cha Uchamungu.............................44 Vifaa vitumike kwa Kazi tu...........................................................45 Kutokufanya Ubadhirifu na Ufujaji...............................................45 Mali ........................................................................................48. Mali ........................................................................................48 Madhara ya Mali............................................................................48

vii


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

Mipaka ya Matumizi......................................................................49

1. Kwanza: Haki ya kutumia mali:.........................................49

2. Pili: Dharura ya kuitumia katika kukidhi mahitaji: .............49

3. Tatu: Kuitumia katika maeneo yaliyopitishwa kisharia:......49

Uwiano na Kuheshimu vipaumbele...............................................50

viii


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

‫بسم اهلل الرحمن الرحيم‬ NENO LA MCHAPISHAJI

K

itabu ulichonacho mikononi mwako asili yake ni cha lugha ya Kiarabu kwa jina la, Ahkamul Mudir wal A’amil kilichoandikwa na Jumuiya ya Maarifa na Utamaduni wa Kiislamu. Sisi tumekiita, Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi. Uislamu ni dini na ni mfumo kamili wa maisha. Kwa maana hiyo Uislamu mbali na kuwaaendeleza waumini wake kiroho, huangalia pia na maendeleo ya waumini wake kimaisha katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na ustawi wa jamii kwa ujumla. Ili mwanadamu apate kuishi maisha bora lazima afanye kazi. Uislamu unahimiza waumini wake kufanya kazi kwa bidii na ufanisi ili kuishi maisha mazuri kama yanavyoainishwa katika mafundisho ya Kiislamu. Katika kitabu hiki tutaona umuhimu wa kufanya kazi kwa mtazamo wa Kiislamu ili kupata pato halali kwa maendeleo ya maisha, halikadhalika maisha ya kiroho. Vilevile tutaona mgawanyo wa majukumu ya kazi na wajibu wa kila mfanyakazi katika nafasi yake, na pia jinsi ya kuchunga nidhamu kazini. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni vitu ambavyo havina nafasi tena katika akili za watu.

1


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

Kutoka na ukweli huu, taasisi yetu ya Al-Itrah imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumini yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu hususan wazungumzaji wa Kiswahili. Tunamshukuru ndugu yetu Hemedi Lubumba (Abu Batul) kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kukitarjumi kitabu hiki kwa Kiswahili kutoka lugha ya asili ya Kiarabu. Aidha tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Allah awalipe wote malipo mema hapa duniani na kesho Akhera – Amin. Mchapishaji Al-Itrah Foundation

2


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

‫بسم اهلل الرحمن الرحيم‬ UTANGULIZI Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.

M

wenyezi Mungu amesema: “Na sema: Tendeni vitendo Mwenyezi Mungu na Mtume wake na waumini wataviona vitendo vyenu na mtarudishwa kwa Mjuzi wa ghaibu na dhahiri, naye awaambie mliyokuwa mkiyatenda.” (Sura Tawba: 105) Hakika muumini anapofanya kazi huifanya kwa ustadi, hivyo kazi tutakayozungumzia ndani ya kijitabu hiki kilichomo mikononi mwako ni ile yenye kupambika kwa sifa mbili za msingi: Imani na ustadi. Imani ndio wigo unaopasa kudhibiti harakati za mfanyakazi na roho yake, kwani yenyewe huakisi hukumu ya kisharia na hivyo hunadhimu harakati zake na hudhibiti utendaji wake ili unasibiane na roho, imani, ufahamu na hukumu za Uislamu Mtukufu. Na ustadi ndio tunda ambalo mfanyakazi aliye muumini hulichuma kutokana na sifa za ikhlasi, kujituma, muono na maarifa aliyonayo katika jambo lake na kazi yake. Na ili ziweze kupatikana sifa hizi mbili (imani na ustadi) kuna masharti ambayo yamebainishwa na riwaya na maandishi ya kisharia na yamefafanuliwa na Marjaa wetu adhimu kama fatwa ambazo 3


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

ni wajibu kuzifuata ili kwamba ziweze kunadhimu sifa za kazi ya kibinadamu ambayo hupatikana kutokana na mwanadamu, muda, vitendea kazi na mali. Haya ndio tutakayoyajua punde tu kupitia faslu zifuatazo:

4


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

‫بسم اهلل الرحمن الرحيم‬ KAZI KAZI KWA AJILI YA MWENYEZI MUNGU:

M

iongoni mwa wasia wa Amirul-Muuminin (a.s.) kwa wanawe Hasan na Husain (a.s.) ni: “Nawaasa kumcha Mwenyezi Mungu, na kwamba msiitafute dunia hata kama yenyewe itawatafuta, na wala msihuzunishwe na chochote kile mlichoepushiwa toka humo. Semeni haki na tendeni kwa ajili ya malipo (ya Akhera).”1 Watu kwa jumla wanachoka na kutoa juhudi zao huku wakitoa mihanga mikubwa ili kutimiza malengo yao, katika hilo hakuna tofauti baina ya muumini na asiyekuwa muumini. Lakini tofauti iliyopo baina ya mfanyakazi muumini na asiyekuwa muumini ni kwamba muumini anataka kupata radhi za Mwenyezi Mungu kupitia kazi yake huku akitaraji kupata matokeo ya kazi yake huko Akhera. Anajua kwamba yeye ataiacha dunia hivyo hafanyi kazi kwa ajili yake na wala haipi wakati wake na juhudi zake. Anaamirisha Akhera yake kwa kuwa ndio makazi yake ya kudumu, na hivyo dunia si hima yake kubwa kwa sababu ni nyumba ya kupita. Hali hii hujiakisi katika tabia yake na mwenendo wake, Imam Ali (a.s.) anasema: “Fanyeni kazi, kazi ya mtu anayejua kwamba hakika Mwenyezi Mungu atamlipa kwa mabaya yake na mazuri yake.”2 Ama asiyekuwa muumini dunia imetawala akili yake na kuushughulisha moyo wake mpaka haoni kitu kingine ila dunia, hivyo ata1 2

Nahjul-Balagha, Barua ya 47. Mizanul-Hikma, Hadithi ya 14361. 5


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

juta siku ambayo ataona roho yake ikitoka, anaiacha dunia nyuma ya mgongo wake na yote aliyowekeza humo, anapokea maisha mapya ambayo hakuyaandaa kupitia kazi zake. Hali hii ndio iliyogusiwa na Aya Tukufu: “Anayetaka mapato ya Akhera tutamzidishia katika mapato yake, na anayetaka mapato ya dunia tutampa, lakini katika Akhera hana sehemu yoyote.” (Sura Shura: 20).

UNAWEZAJE KUFANYA KAZI KWA AJILI YA MWENYEZI MUNGU? Amirul-Muuminin (a.s.) anasema: “Ni uzuri ulioje! Kwa mtu mwenye kukumbuka marejeo, akatenda kwa ajili ya hisabu (ya Akhera) na akakinai na kinachomtosha.”3 Muumini hafanyi kazi isipokuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa ajili ya kutafuta radhi Zake na kujiandaa kwa ajili ya hisabu ya Akhera. Hali hii hujiakisi katika mwenendo wake na matarajio yake, hivyo anachongojea kutokana na kazi yake ni: 1.

3

Anayefanya kazi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu hatizami chochote isipokuwa radhi za Mwenyezi Mungu, malengo mengine yoyote si kitu kwake mbele ya radhi Zake (s.w.t.), Mwenyezi Mungu anasema: “Hakika tunawalisheni kwa ajili ya radhi ya Mwenyezi Mungu tu.” (Sura al-Insan: 9). Lengo lake la msingi ni jinsi gani Mwenyezi Mungu ataitazama kazi yake na je itakubaliwa na kuridhiwa na Mwenyezi Mungu? Kwani Mwenyezi Mungu anasema: “Mwenyezi Mungu na Mtume wake na waumini wataviona vitendo vyenu...” (Sura Tawba: 105)

Nahjul-Balagha, Hikima ya 41.. 6


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

2.

Anayefanya kazi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu hana msukomo wa dunia katika kazi yake: “Hatutaki kwenu malipo wala shukurani.” (Sura al-Insan: 9), hivyo kazi yake na ari yake haviathiriwi na shukurani za watu au kudhulumiwa haki yake.

Anayefanya kazi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu utamkuta ni mwenye ari, mwenye kujituma na mwenye kufanya haraka katika kufanya kazi. Mwenyezi Mungu anasema: “Na harakisheni kuomba msamaha kwa Mola wenu na pepo ambayo upana wake ni mbingu na ardhi imeandaliwa wamchao.” (Sura Aali Imran: 133).

3. Anayefanya kazi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu hawasimbulii waja wa Mwenyezi Mungu kazi yake, bali anaona kuwa kazi yake hii ni neema na rehema kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu anasema: “Wanakusimbulia kwa kuingia kwao Uislamu. Sema msifanye kuwa ni ihsani kwangu kusilimu kwenu, bali Mwenyezi Mungu ndiye aliyekufanyieni ihsani kwa kukuongozeni katika Uislamu, ikiwa nyinyi ni wakweli.” (Sura Hujurat: 17).

4

Kwani hakika utiifu wake haumnufaishi Mwenyezi Mungu chochote wala kuasi kwake hakumdhuru chochote. Imam Ali (a.s.) anasema: “Hukuwaumba viumbe ili ujiondolee woga na wala hujawaamrisha ili unufaike. Hakupiti umtafutaye wala hakuponyoki uliyemkamata, hapunguzi mamlaka Yako yule mwenye kukuasi wala haongezi mamlaka Yako yule mwenye kukutii, na wala hana uwezo wa kuzuia amri yako yule mwenye kuchukizwa na majaaliwa Yako.”4

Nahjul-Balagha, Hotuba ya 109. 7


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

4.

Anayefanya kazi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu hujitahidi kumshinda mwingine katika kutaka kupata thawabu. Mwenyezi Mungu anasema: “Yaendeeni upesi (mambo ya kukupatieni) msamaha wa Mola wenu na Pepo ambayo upana wake ni kama upana wa mbingu na ardhi, iliyowekewa wale waliomwamini Mwenyezi Mungu na Mitume Wake, hiyo ni fadhili ya Mwenyezi Mungu, humpa amtakaye, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhili kuu.” (Sura al-Hadid: 21). Na huchelea Mwenyezi Mungu asije kumuweka mwingine nafasi yake, Imam Ali (a.s.) anasema: “Hakika kheri na shari vina watu wake, wakati wowote mtakapoviacha watachukua nafasi zenu watu wake.”5

Chunga mambo yote haya ndani ya nafsi yako na jitahidi kuyatimiza ili uwe miongoni mwa kundi la Mwenyezi Mungu kweli na mwandani wake, kwani hakika kundi la Mwenyezi Mungu ni wale wenye kumwogopa Mwenyezi Mungu huku hima yao duniani ni kumtii Yeye na kumridhisha. Mwenyezi Mungu anasema: “….Mwenyezi Mungu amekuwa radhi nao, na wao wamekuwa radhi naye, hao ndio kundi la Mwenyezi Mungu, Sikilizeni! Hakika kundi la Mwenyezi Mungu ndilo linalofaulu.” (Sura al-Mujadilah: 22).

JE LENGO HUHALALISHA NJIA? Mwenyezi Mungu anasema: “Sema: Hakika swala yangu na ibada zangu na uzima wangu na kufa kwangu, ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mola wa ulimwengu wote.” (Sura An’am: 162). 5

Nahjul-Balagha, Hikima ya 414. 8


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

Hakika Uislamu haujamfunga mwislamu katika malengo yake ambayo yampasa mwenyewe kuyatimiza, na wala haujamwacha afuate njia aitakayo katika kutimiza lengo lake, bali umeingilia kati katika suala la njia ya kufikia malengo. Kuanzia hapa ndipo maisha yote ya muumini, ikiwa ni pamoja na malengo yake na njia za kuyafikia vimekuwa ni lazima viwe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Sifa hii ameizungumzia Amirul-Muuminin (a.s.) kwa kauli yake: “Wallahi Muawiya si mjanja kushinda mimi, isipokuwa yeye huhadaa na kufanya uovu. Laiti si kuchukia hadaa basi ningekuwa mjanja kushinda watu wote, lakini ni kwamba kila hadaa ni uovu na kila uovu ni ukafiri, na wahadaaji siku ya Kiyama watakuwa na bendera yao itakayowatambulisha.”6 Muumini kama ambavyo lengo lake ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kadhalika utendaji wake na njia ya kufikia lengo lake haiwezi kuwa isipokuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kwani hakika Mwenyezi Mungu hapasi kutiiwa katika njia ya kuasiwa. Hili ndilo alilosisitiza Amirul-Muuminin (a.s.) kwa kusema: “Hivi mnaniamrisha niutafute ushindi kwa njia ya uovu? Hapana, wallahi sintafanya hivyo muda wote ambao jua litaendelea kuchomoza na nyota zitaendelea kung’aa mbinguni.” Hivyo ni lazima mfanyakazi atambue njia ya kumtii Mwenyezi Mungu katika kazi yake, mipaka na hukumu za kisharia za kazi husika, hukumu ambazo tutazibainisha ndani ya jaribio lifuatalo inshaallah, na ambazo ni kufuata nidhamu na kanuni, muda wa kazi, kufanya kazi ndani ya muda wa kazi, mahusiao ya kibinadamu, hukumu za vitendea kazi na hukumu za mali. Tunamuomba Mwenyezi Mungu atujaalie tuwe miongoni mwa wenye kufanya kazi katika njia yake wenye kuwafikishwa kwa kupata radhi Zake. 6

Nahjul-Balagha, Hotuba ya 191. 9


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

DHARURA YA KUWEPO NIDHAMU: Amirul-Muuminin (a.s.) anasema: “Nawaasa ninyi wawili, wanangu wote, ndugu zangu na kila atakayefikiwa na maandishi yangu, kumcha Mwenyezi Mungu na kuwa na nidhamu katika mambo yenu.”7 Hebu tazama jinsi ambavyo Amirul-Muuminin (a.s.) hakuishia kuwaasa wanawe na ndugu zake tu bali amezingatia kuwa ni wasia kwa ajili ya kila atakayefikiwa na maandishi haya. Hii inamaanisha kuwa uchamungu na nidhamu katika mambo ni mambo ambayo mwanadamu anapasa kuwa nayo katika kila zama na sehemu yoyote aliyopo. Nidhamu si jambo makhususi kwa ajili ya kundi fulani au tabaka fulani, bali ni la kila muumini mwenye kufuata njia ya Amirul-Muuminin (a.s.), bali ni kwamba tunamkuta Amirul-Muuminin (a.s.) mahala pengine anaonyesha adhama na umuhimu wa nidhamu, pale anapoijumuisha miongoni mwa malengo ya Qur’ani Tukufu, anasema katika wasifu wake kwa Qur’ani: “Ah! Hakika humo mna yatakayokuja na habari kuhusu yaliyopita, dawa ya magonjwa yenu na nidhamu inayopasa baina yenu.”8 Nidhamu si neno la kutamkwa tu, bali nidhamu ni njia ya kazi ambayo hutokana na mambo mbalimbali ya kikazi ambayo bila hayo haipatikani nidhamu. Miongoni mwa mambo hayo ni: 1. Kufuata kanuni: Kila kazi yenye nidhamu ina sheria na kanuni makhususi ambazo ni wajibu ziheshimiwe na kufuatwa na wafanyakazi, kwa sababu kanuni hizi ndizo zenye dhamana ya kuzaa ufanisi na ukamilifu, kuibua uwezo na kuutumia kwa faida kwa namna sahihi. Imam Khamenei 7 8

Nahjul-Balagha. Nahjul-Balagha, Hotuba ya 158. 10


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

anazungumzia umuhimu wa kufuata nidhamu katika Serikali ya Kiislamu, anasema: “Miongoni mwa mambo ambayo ni wajibu kushikamana nayo ni kufuata nidhamu na kanuni zilizotolewa, kwani kuheshimu kanuni na amri si dhulma, bali utiifu wa namna hii una thamani tukufu mno.”9 2. Kufanya kazi kulingana na nafasi ya mtu: Hakika miongoni mwa mambo yasiyoachana na nidhamu ni kugawa kazi na majukumu kulingana na nafasi ya mtu, na kumpa kila mmoja nafasi yake kulingana na jukumu analopasa kulitimiza. Hivyo nidhamu maana yake ni kugawa kazi, na kugawa kazi maana yake ni kuainisha nafasi, hivyo ni wajibu kuheshimu nafasi kwa ukamilifu ili kwamba ipatikane kivitendo ile maana ya nidhamu katika kazi. Kufanya kazi bila kuheshimu nafasi hata kama lengo lake litakuwa sahihi lakini njia yake si sahihi, ni sawa na mtu anayeiba ili akatoe sadaka. Hivyo ni lazima mfanyakazi ajue nafasi yake, akomee hapo na wala asiivuke, Amirul-Muuminin (a.s.) anasema: “Ameangamia yule mwenye kudai na amekula hasara yule mwenye kuzusha…… Ni ujahili tosha mtu kutokujua nafasi yake.”10 3. Kutii amri za juu: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Msikieni na mtiini yule aliyepewa mamlaka na Mwenyezi Mungu, kwani kufanya hivyo ndio nidhamu ya Uislamu.” Nidhamu ambayo huleta mshikamano, umoja na nguvu ni ile ya kumtii kiongozi, na utii huo kwa upande mwingine huleta ushindi, nguvu na mafanikio. Mwenyezi Mungu anasema: “Na atakayem9

Hadithil-Wilayat Juz. 5/ 8222. Nahjul-Balagha, Hotuba ya 16.

10

11


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

tawalisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale walioamini, basi kundi la Mwenyezi Mungu ndio watakaoshinda.� (Sura al-Maida: 56). Hukumu: Katika Serikali ya kiislamu na taasisi za kiislamu, ni wajibu kufanya kazi kulingana na kanuni na sheria husika, wala si ruhusa kuzikhalifu. Swali na jibu: 1.

Mzazi wangu amefariki, hivyo familia imebaki chini yangu kwa kuwa mimi ndiye mtoto wake mkubwa, na nilianza kazi ya ulinzi (wa taifa) huku nikidhani kuwa nitaweza kuitunza familia kwa chakula, lakini kazi ya ulinzi hainipi muda wa kufanya hivyo, na nina ndugu yangu mdogo kwangu lakini yeye hajali suala la kuitunza familia kwa chakula, na nilipoingia kwenye kazi ya ulinzi nilichukua mkataba wa kufanya kazi miaka mitano, lakini sasa baada tu ya miezi minne ya huduma nimepanga kuacha kazi ya ulinzi ili nikafanye kazi itakayonihakikishia chakula cha familia, je, ni upi mtazamo wenu katika hilo?

Jibu: Ni wajibu kutenda kulingana na sheria ya ulinzi (wa taifa).11 2.

11

Mimi nafanya kazi katika wakala wa habari wa Jamuhuri ya Kiislamu na katika kandarasi ya ujenzi ya Jihadi, na nina haja inayonisukuma kuchukua mshahara toka asasi zote mbili, kwa kuzingatia kwamba dola imekataza kuchukua mshahara toka asasi mbili pamoja za dola, ni ipi fatwa yenu kuhusu suala hili?

Istiftaat Juz. 3, Uk. 484, Mas’ala ya 2. 12


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

Jibu: Haja si mizani, bali maudhui inafuata sheria husika, si ruhusa kama kufanya hivyo ni kwenda kinyume na sheria.12

12

Istiftaat Juz. 3, Uk. 533, Mas’ala ya 151. 13


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

MUDA WA KAZI

H

akika kujituma na kuharakisha kwenda kwenye kazi ya halali ni jambo la kawaida kwa mwanadamu muumini, apatapo kazi ambayo ni kumhudumia Mwenyezi Mungu na waja wake, huhisi kuwa ni fursa aliyoneemeshwa na Mwenyezi Mungu, hivyo huitumia ipasavyo kwa shauku kabla haijamtoka na humshukuru Mwenyezi Mungu kwa tawfiki hii. Kazi ya halali ni neema lakini wakati huo huo ni dhima, unapochukua nafasi ya kufanya kazi fulani basi unakuwa mwenye dhima mbele ya Mwenyezi Mungu kuhusu utekelezaji wake ambao unapasa uwe katika kiwango cha ukamilifu na katika njia bora, kwa sababu wewe unapochukua nafasi hiyo ya kufanya kazi fulani na kuitumia nafasi hiyo unakuwa umemzuia mwingine miongoni mwa waumini kuitumia nafasi hiyo na kushughulika na nafasi hiyo, hivyo usipotekeleza kazi kwa kiwango kinachopasa na kuhitajika unakuwa umemzibia mwenzio njia na kumzuia kufaidika na neema ya kuihudumia dini ya Mwenyezi Mungu na waja wake, na upande wa pili unakuwa umeikosesha kazi hali ya kufaidika na uwezo wa watu wengine. Kuanzia hapo ndipo kwa uchache tunapasa kutimiza angalau kiwango cha chini kabisa cha haki za kazi na kubeba dhima, kiwango hiki cha chini kinawakilisha kiwango cha kisharia ambacho ni wajibu kushikamana nacho na ambacho lau ikitokea mwanadamu kukiacha basi atakuwa mwenye kutenda kosa na mwenye kufanya dhambi na hivyo ni mwenye kustahili ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na adhabu ya Akhera. Tunamuomba Mwenyezi Mungu atuepushie mbali hilo.

14


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

Kuwepo daima kazini ndani ya muda wa kazi ni miongoni mwa mambo muhimu na ya dharura.

KUHESHIMU MUDA WA KAZI: Hakika kufanya kazi ndani ya muda maalumu mkabala na malipo na mshahara wa kila mwezi, maana yake ni kwamba mtumishi anachukua mali mkabala na saa hizi ambazo anazitoa kwa ajili ya kazi, hivyo saa hizi za kazi, juhudi zake na nguvu zake katika kazi hiyo si milki yake bali ni milki ya kazi, na hivyo upungufu wowote au dosari yoyote inayopatikana katika utoaji wake (wa muda, juhudi na nguvu) unamaanisha kuwa anakula mali asiyo na haki nayo. Amirul-Muuminin (a.s.) alikuwa akikutana na hali hizi ambazo ni kuacha kazi na kupoteza kazi na alikuwa akizizingatia kuwa si uaminifu, hivyo katika maandishi yake kwenda kwa al-Mundhir bin al-Jarud alimwambia: “Imenifikia habari kwamba hakika wewe unaacha kazi zako nyingi na unatoka kwenda kwenye upuuzi, matembezi na mawindo…….. na hakika mimi naapa kwa Mwenyezi Mungu ikiwa hilo ni kweli basi tambua ngamia wa mkeo na mkanda wa kiatu chako ni bora kushinda wewe mwenyewe, na hakika mchezo na upuuzi havimridhishi Mwenyezi Mungu. Kuwasaliti waislamu na kupoteza kazi zao ni mambo yamchukizayo Mola wako, na mtu ambaye yuko hivyo hafai kulinda mipaka na kukusanya ngawira na wala kuaminiwa mali za Waislamu.”13 Hukumu: Ni wajibu kufanya kazi kulingana na sheria husika kwa kuwepo kazini muda wa kazi, kuanzia mwanzo wa muda wa kazi mpaka mwisho 13

Ansabul-Ashraf Uk. 163. 15


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

wake. Umbali wa makazi au matatizo ya usafiri au baridi kali ‌‌ hayo yote hayamhalalishii mtu kuchelewa kufika kazini mwanzo wa wakati ikiwa kuchelewa huko ni kwenda kinyume na sheria husika. Ni wajibu kuheshimu sheria kuhusu wakati wa kula chakula na kusali na kuhusu sehemu za kufanyia vitendo hivyo. Ikiwa suala la kuheshimu muda wa kazi ni wajibu kwa mujibu wa sheria ya kazi husika basi ni wajibu kuheshimu muda hata kama hakuna kazi. Watumishi ambao huwa hawapo kazini saa moja au saa kadhaa, hawastahiki kuchukua mali mkabala na saa hizi ikiwa kufanya hivyo (kutokuwepo kazini) ni kwenda kinyume na mkataba wa kazi. Maswali na majibu kuhusu muda wa kazi: 1. Kuna mfanyakazi ambaye kwa mujibu wa sheria ni wajibu awepo kazini mwanzo wa muda wa kazi, lakini kwa sababu ya umbali wa makazi yake au kwa sababu ya baridi kali ya majira ya masika au kwa sababu ya ugumu wa usafiri huchelewa saa moja au saa mbili siku za jumamosi tu kufika kazini, je huyu kisharia anaruhusiwa kufidia upungufu huu ndani ya siku hii au ndani ya siku nyingine za wiki? Jibu: Ni wajibu kufanya kazi kulingana na sheria husika.14 2.

14

Mimi ni mfanyakazi kwenye shirika la serikali, ambapo kazi husitishwa kwa muda wa nusu saa ili kutoa fursa ya kusali sala ya Adhuhuri, lakini kwa kuzingatia kuwa mimi husalia kwenye msikiti uliyopo mbali kidogo na sehemu yangu ya kazi, nahitaji zaidi ya nusu saa ili niweze kushiriki sala ya

Istiftaat (ya Kiajemi) Juz. 3, Uk. 499, Swali la 51. 16


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

jamaa katika msikiti husika, je kuna kizuizi chochote cha kisharia katika hilo? Jibu: Hakuna kizuizi iwapo tu kufanya hivyo si kwenda kinyume na mkataba wa kazi.15 3.

Ufikapo wakati wa sala husitishwa kazi ofisini muda wa nusu saa ili kutoa fursa ya kutekeleza sala, hebu sasa tujaalie kwamba nyumba yangu ipo karibu na kazini kwangu kiasi kwamba naweza kwenda nyumbani nikasali, nikala chakula cha mchana na nikarejea ndani ya nusu saa, je kisharia naruhusiwa kufanya hivyo?

Jibu: Ni wajibu kufanya kazi kulingana na sheria husika.16 4.

Katika baadhi ya taasisi ndani ya baadhi ya siku huwa hakuna kazi anayopasa mfanyakazi kuitekeleza, je mfanyakazi anaruhusiwa kutokuwepo sehemu ya kazi ndani ya siku hizi? Au kuhudhuria saa moja au saa mbili tu za mchana? Kwa jumla ni kwamba je mfanyakazi ana haki ya kutoka sehemu yake ya kazi kabla ya kwisha kwa muda wa kazi kwa sababu yoyote aliyonayo?

Jibu: Ni kulingana na mkataba wa kazi.17 Maswali na majibu kuhusu kukatwa mshahara: 1.

Mimi ni mfanyakazi katika taasisi ambayo inategemea kadi ambayo unaiingiza ndani ya mashine ya elektroniki na moja kwa moja inasajili muda wa kuingia kazini, na hivyo hivyo

Istiftaat (ya Kiajemi) Juz. 3, Uk. 523, Swali la 118. Istiftaat (ya Kiajemi) Juz. 3, Uk. 523, Swali la 119. 17 Istiftaat (ya Kiajemi) Juz. 3, Uk. 526, Swali la 129. 15 16

17


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

muda wa kutoka, na mwisho wa mwezi unapoonekana upungufu wa saa za kuwepo kazini, hukatwa mshahara, ile thamani ya kazi niliyopasa kufanya ndani ya saa zilizopunguka. Lakini tambua kuwa upungufu huo kuna wakati unasababishwa na kule kusahau kwangu kuingiza kadi ndani ya mashine, je kitendo chao hiki (cha kunikata mshahara) kinaruhusiwa kisharia? Jibu: Ni wajibu kuheshimu sheria za serikali ya Kiislamu.18 2. Baadhi ya wafanyakazi kutokana na sababu maalumu huwa hawafiki kazini siku moja au siku mbili ndani ya mwezi, je kisharia mkuu wa kazi anaruhusiwa kumpa mfanyakazi malipo ya siku hii ambayo hakuwepo kazini? Jibu: Ni kulingana na mkataba wa kazi.19 1.

Katika ofisi mbalimbali kuna wafanyakazi ambao husitisha kazi zao na kurudi majumbani kwao kabla ya kumalizika saa nane (muda wa kazi kiserikali), na husema kwamba wao wanatekeleza kazi zao haraka ili warudi mapema majumbani kwao, kitu ambacho huwaondolea umakini katika kazi zao, je kwa mtazamo wenu mtukufu hakuna tatizo la kisharia katika haki ambazo wao wanazichukua kiukamilifu? Na je ni halali kwao mali wanazozichukua mkabala na saa za kazi ambazo huwa hawapo kazini?

Jibu: Si ruhusa kwao kuchukua mali mkabala na saa hizi ikiwa kitendo chao hiki ni kwenda kinyume na mkataba wa kazi.20 Istiftaat (ya Kiajemi) Juz. 3, Uk. 507, Swali la 74. Istiftaat (ya Kiajemi) Juz. 3, Uk. 525, Swali la 128. 20 Istiftaat (ya Kiajemi) Juz. 3, Uk. 529, Swali la 140. 18 19

18


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

KUJISHUGHULISHA KUJISHUGHULISHA:

H

akika kuwepo kazini muda wa kazi si tu kupatikana eneo la kazi bali ni kutumia muda kwa ajili ya kazi husika na kufanya kila lililo wajibu kwako bila kuzuiliwa na jambo jingine. Hivyo muda wa kazi ni utangulizi wa kazi na ni wajibu juu yako kuutumia kwa kazi kwani wakati unaokwenda bure utageuka majuto huko Akhera. Imam as-Sadiq (a.s.) amesema: “Hakuna siku inayomfika mwanadamu ila humwambia: Ewe mwanadamu mimi ni siku mpya nami ni shahidi juu yako, nitendee kheri na tenda humu kheri nitakutolea ushahidi siku ya Kiyama kwani hakika hutaniona tena baada ya leo.”21

Amirul-Muuminin (a.s.): “Tambua kwamba hakika dunia ni nyumba ya kutoweka, yeyote atakayeacha saa iende bure basi muda huo utageuka majuto kwake siku ya Kiyama.”22 Na anasema sehemu nyingine: “Mcheni Mwenyezi Mungu, mcheni Mwenyezi Mungu enyi waja mngali salama katika siha kabla ya maradhi, na mngali katika nafasi kabla ya mbano. Fanyeni juhudi katika kujikomboa kabla hatamu haijafungwa, kesheni macho, punguzeni matumbo yenu, zitumikisheni nyayo zenu, toweni mali zenu na chukueni toka kwenye miili yenu kile mtakachozikirimu kwacho nafsi zenu na wala msizinyime hicho.”23 Mizanul-Hikma, Hadithi ya 7413. Nahjul-Balagha, Barua ya 59. 23 Nahjul-Balagha, Hotuba ya 237. 21 22

19


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

Wakati ni neema hivyo ni wajibu juu yako kufaidika na wakati huo kwa ajili ya Akhera yako, ukiupoteza utakuwa sawa na fakiri ambaye amepewa mali ili ajenge nyumba yake na kuboresha maisha yake kisha akachukua mali hiyo na kuiharibu kwa kuitupia baharini. Wakati na siha vyote viwili ni neema, ni wajibu wetu kuvitumia kwa faida na kwa kuandaa masurufu yetu, kwani sisi ni wahitaji wa Akhera na hatuwezi kuondoa uhitaji wetu ila kwa kutumia wakati wetu katika kumtii Mwenyezi Mungu na kujenga makasiri ya Akhera na mabustani yake. Amirul-Muuminin (a.s.) amesema: “Mwenyezi Mungu amrehemu mja …… ambaye ametumia muda, akakiwahi kifo na akajiandalia masurufu toka katika kazi.”24

KUJISHUGHULISHA HUKU HUONEKANA KUPITIA MAMBO YAFUATAYO:

24 25

1.

Kutimiza majukumu: Hamtegemei mwingine katika hilo, vipi muumini anaweza kuwa mtu asiyetimiza wajibu na mwenye kumtegemea mwingine katika kazi zake na hali anajua kwa yakini kwamba kazi yake hii ndio rasilimali yake huko Akhera. Amirul-Muuminin (a.s.) anasema: “Kuzembea katika kazi kwa yule anayeamini kuwa atapata thawabu kwa kazi hiyo ni kujiibia.”25

2.

Kuhisi uzembe: Hakika mfanyakazi aliye muumini huhisi daima kuwa hajatimiza wajibu, na ni vipi asihisi hivyo mtu ambaye kazi yake ni moja ya milango ya kutolea shukurani zake kwa Mwenyezi Mungu au milango ya kujiandalia

Nahjul-Balagha, Hotuba ya 75. Mizanul-Hikma, Hadithi ya 2792. 20


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

Akhera yake. Ni kazi ipi inayolingana na malipo ya Akhera au ni utiifu gani unaotimiza haki ya Muumba au kutimiza shukurani anayostahiki? Kwa ajili hiyo utamkuta muumini huyo ni mwenye kazi nyingi huku daima akiwa katika kujishughulisha, kana kwamba anaona kuwa kihalalishi cha uwepo wake ni kazi, pamoja na juhudi zote hizo bado anaona kuwa kazi zake ni chache, Amirul-Muuminin (a.s.) anawasifu kwa kusema: “Hawaridhishwi na amali zao chache, wala zile nyingi hawazioni kuwa ni nyingi, ni wenye kuzituhumu nafsi zao na ni wenye kuzihangaikia kazi zao.”26 Na katika barua yake kwa mmoja wa magavana wake alimwambia: “Jitumeni katika njia Yake kadiri alivyowajibisha juu yenu, kwani hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ametutendea wema sisi na nyinyi ili tumshukuru kwa juhudi zetu na tumtetee kwa kadiri ya nguvu zetu.”27 3.

Kufanya kazi ndani ya wakati: Wakati ni miongoni mwa mambo ambayo yakishampita mwanadamu hawezi kufidia, kwa sababu wakati haukubali kurudi nyuma, siku inayokwisha leo haiwezi kurudi, na ni miongoni mwa semi za hekima zilizo mashuhuri kuwa: “Wakati ni kama upanga usipoukata utakukata.” Basi tutawezaje kufaidika kikamilifu na wakati huu? Amirul-Muuminina (a.s.) anasema: “Itekelezee kila siku kazi yake kwani hakika kila siku ina mambo yake…..Jihadhari kuharakisha mambo kabla ya wakati wake au kuakhirisha yanapowezekana au kupinga humo usilolijua au kuwa goigoi unapolijua, weka kila jambo sehemu yake na tekeleza kila jambo kwa wakati wake.”28 Na anasema katika barua yake kwa mmoja wa

Nahjul-Balagha, Hotuba ya 184. Nahjul-Balagha, Barua ya 51. 28 Nahjul-Balagha, Barua ya 53. 26 27

21


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

magavana wake: “Jihadharini kuakhirisha kazi na kufukuza kheri, kwani hakika hilo lina majuto.”29 4.

Kufanya kazi yenye ubora: Hakika kufanya kazi yenye ubora ni miongoni mwa sifa ambazo zinamtofautisha mfanyakazi mwenye ikhlasi na yule asiye na ikhlasi, maadamu kazi ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu basi inazungukwa na msaada wa Mwenyezi Mungu basi itakuwa imara na bora, na maadamu mfanyakazi anafanya kazi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na anataraji thawabu basi kazi yake itakuwa na ubora kadiri atakavyo thawabu. Amirul-Muuminin (a.s.) anasema: “Kutotimiza wajibu katika kazi kwa yule anayeamini kuwa atapata thawabu kwa kazi hiyo ni kujiibia.”30

Ni wajibu kwa muumini kutilia umuhimu ubora wa kazi yake na ustadi wake kuliko wingi wake na idadi yake. Amirul-Muuminin (a.s.) anasema: “Kichache chenye kudumu ni bora kushinda kingi kisichodumu.”31 Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimwambia mmoja wa masahaba wake: “Ewe Ibnu Masuud! Utakapofanya kazi yoyote ifanye kwa elimu (ujuzi) na akili, jihadhari kufanya kazi bila mazingatio na elimu kwani Mtukufu aliyetukuka anasema: ‘Wala msiwe kama yule mwanamke aliyekata uzi wake vipande vipande, baada ya kuusokota na kuwa mgumu.”32 Na anasema tena (s.a.w.w.): “Hakika Mwenyezi Mungu anapenda mmoja wenu anapofanya kazi yoyote aifanye kwa ustadi.”33 Biharul-Anwar, Juz. 72, Uk. 355. Nahjul-Balagha, Hekima ya 376. 31 Nahjul-Balagha, Hekima ya 432. 32 Mizanul-Hikma, Hadithi ya 14360. 33 Mizanul-Hikma, Hadithi ya 14371. 29 30

22


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

Hukumu: Mfanyakazi akikataa kufika kazini na kutekeleza jukumu lake ambalo ameajiriwa kwa ajili yake, hastahiki malipo na anatakiwa kulipa mali aliyoichukua bila kuifanyia kazi, hivyo ni wajibu juu yake kuirejesha. Mfanyakazi asipotekeleza kazi alizopewa, hata kama atakuwa amefika kazini na katimiza baadhi ya kazi, ni wajibu juu yake kurudisha mali ambayo amechukua mkabala na kazi hizi ambazo hajazitekeleza, tena airudishie ofisi ileile iliyomkabidhi. Yule ambaye kazi yake ni udereva haruhusiwi kwenda kwenye matembezi yake binafsi ndani ya muda wa kazi maadamu tu kufanya hivyo ni kwenda kinyume na sheria husika na ni bila idhini ya mkuu wake wa kazi. Ni ruhusa ndani ya muda wa kazi kujishughulisha na mambo kama kuhifadhi Qur’ani Tukufu na Hadithi Tukufu, ikiwa tu kufanya hivyo hakusababishi matokeo hasi kwenye kazi. Ruhusa ya kufanya kazi binafsi ndani ya muda wa kazi ndani ya saa ambazo hakuna kazi inategemea sheria husika. Maswali na majibu: 1.

Mimi ni mfanyakazi wa muda mrefu serikalini, na kutokana na baadhi ya sababu maalumu katika baadhi ya hali nilikuwa sifanyi kiukamilifu na kwa usahihi kazi zangu nilizopewa, na nilikuwa nachukua mshahara, sasa ili niweze kutatua mushkili huu je naweza kufanya kazi sehemu yoyote iliyo chini ya serikali ili nifidie upungufu huu au ni wajibu juu yangu kufanya kazi kwenye asasi ileile? Na je nikipen23


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

da kurejesha mshahara niliochukua kwa kuwa sikutekeleza kazi, ni vipi naweza kurejesha mali hii na ni kwa anwani ipi? Na je naruhusiwa kuikabidhi mali hii kwenye ofisi ya Imam huko Qum? Jibu: Ikiwa hukutekeleza kazi ulizokabidhiwa basi ni wajibu juu yako kurudisha mali uliyochukua mkabala na kazi hizi, uirudishie ofisi ileile iliyokupa.34 2.

Kuna baadhi ya wafanyakazi ambao huchukua mali na wala hawafanyi kazi tangu mwanzo, na hata wakiitwa na wakuu wa kazi waje wafanye kazi huendelea kutoa sababu mbalimbali zinazowazuia kufika kazini na kujishughulisha na kazi, basi ni ipi hukumu ya mali hizi ambazo wanachukua licha ya kuwa wamekataa kufika kazini? Je asasi husika ina wajibu wa kuheshimu nafasi yao ya kazi licha ya kuwa hawafiki kazini? Na ni ipi hukumu ya mali hizi ambazo walikuwa wakichukua kipindi chote ambacho walikuwa hawafanyi kazi?

Jibu: Mfanyakazi akikataa kutekeleza jukumu lake ambalo kaajiriwa kwalo hastahiki mshahara, na ana wajibu wa kulipa mali aliyochukua bila kufanyia kazi (ni wajibu juu yake kuirejeshea ofisi husika mali hiyo).35 3. Mfanyakazi wa shirika la ulinzi au taasisi nyingine ya serikali au isiyo ya serikali, anatoka kwenda kutekeleza kazi aliyotumwa na wakati wa kurudi anapitia nyumbani kwa wazazi wake ili kuwajulia hali muda wa dakika kumi na tano hivi, je kuna kizuizi chochote cha kisharia? 34 35

Istiftaat (ya Kiajemi) Juz. 2, Uk. 51, Swali la 140. Istiftaat (ya Kiajemi) Juz. 2, Uk. 212, Swali la 43. 24


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

Jibu: Ni kulingana na sheria husika, hakuna tatizo ikiwa amepata ruhusa ya wakuu wa kazi wanaohusika.36 4.

Je inaruhusiwa kusoma Qur’ani Tukufu na dua ndani ya muda wa kazi ikiwa kufanya hivyo hakuathiri mwenendo wa kazi wala hakusababishi kazi kusimama?

Jibu: Hakuna tatitizo kama tu ni katika hali kama hiyo iliyokuja katika swali.37 5.

Tujaalie kuwa kuna wakati usio na kazi kwa wafanyakazi kwa sababu hakuna kazi au hakuna wateja, je inaruhusiwa ndani ya wakati huo usio na kazi kufanya kazi binafsi?

Jibu: Ni kulingana na sheria ya taasisi husika ambayo wewe unafanya kazi.38

Istiftaat (ya Kiajemi) Juz. 2, Uk. 498, Swali la 47. Istiftaat (ya Kiajemi) Juz. 2, Uk. 528, Swali la 128. 38 Istiftaat (ya Kiajemi) Juz. 2, Uk. 522, Swali la 149. 36 37

25


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

MAHUSIANO YA KIBINADAMU (1) UHUSIANO NA WENGINE:

U

islamu umeainisha aina ya uhusiano unaopasa kuwa baina ya waumini kwa neno moja:

“Kwa hakika wenye kuamini tu ndio ndugu, basi patanisheni baina ya ndugu zenu na mcheni Mwenyezi Mungu, ili mrehemewe.” (Sura Hujurat: 10), hivyo jambo la msingi katika uhusiano na wengine sehemu yoyote watakapokuwa ni undugu na wala si jambo jingine. Kama ambavyo sifa nyingine na mitizamo mingine havina nafasi baina ya wanandugu kadhalika havina nafasi baina ya waumini katika maadili yao ya kuamiliana na jamii.

Moyo huu wa kuamiliana ambao Mwenyezi Mungu amewaamuru waumini wawe nao huonyesha ni kwa kiwango gani mwanadamu husika amefungamana na Mwenyezi Mungu. Amirul-Muuminin (a.s.) anasema: “Yule atakayeboresha uhusiano wake na Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu ataboresha uhusiano wake na watu.”39 Kadiri mwanadamu anavyozidi kushikamana na dini yake na kufungamana na Mwenyezi Mungu, ndivyo moyo wa undugu unazidi kuimarika katika uhusiano wake na wengine. Hivyo kuna mambo ya kitabia ambayo ni wajibu kuyaheshimu katika uhusiano wake na waumini, sawa wawe ni watawala au watawaliwa, marafiki au wateja, mambo hayo kwa muhtasari ni: 1.

39

Kuwadhania vizuri: Hakika kuwadhania vibaya waumini ni miongoni mwa maradhi mabaya mno ambayo anaweza kujaribiwa kwayo muumini mfanyakazi, kwa sababu hum-

Nahjul-Balagha, Hekima ya 415. 26


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

sababishia hali ya kutowaamini wengine, jambo ambalo hupelekea kuzorota kwa kazi , kupoteza uwezo wa kufanya kazi na kutofaidika na rasilimali hizo. Pia hupelekea kutoelewana kazini na katika asasi kwa namna ambayo hupelekea kushindwa kufanya kazi na kukosekana ule moyo wa Uislamu katika kazi. Mwenyezi Mungu anasema: “Enyi mlioamini! Jiepusheni sana na dhana, kwani dhana ni dhambi wakati mwingine…….” (Sura Hujurat: 12). 2.

Kuwataja wenzako kwa kheri: Hakika ni kosa kubwa sana kukazania dosari za waumini na kuzichunguza kwa nia isiyokuwa ya kuwanasihi na kuwarekebisha bali kwa ajili ya kuwatia dosari na kuwateta, mtu mwenye kufanya hivyo ana sura mbaya ya kutisha ambayo itamfedhehesha mhusika mbele ya mkusanyiko mkuu mbele ya Manabii, Mitume na Malaika wakuruba. Sura hii mbaya ameiashiria Mwenyezi Mungu kwa kauli yake: “Wala msipeleleze, wala baadhi yenu wasiwatete wengine. Je mmoja wenu anapenda kula nyama ya nduguye aliyekufa? Mnalichukia hilo…..” (Sura Hujurat: 12).

Hakika matendo yetu yana sura na umbile ambalo linanasibiana nayo, hivyo vitadhihiri huko Akhera katika sura na maumbile hayo ili virudi kwetu. Mtesi anafanana na mbwa mwenye kuwinda kutokana na kushambulia kwake heshima za watu na nyama zao, na atadhihiri katika sura hii ya mbwa mwenye kutafuna nyama ya maiti ndani ya moto wa Jahanam. Imekuja katika riwaya kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipompopoa mtu mawe kwa kuzini, mtu mmoja alimwambia rafiki yake: “Huyu ameuawa kama mbwa.” Basi Mtukufu Mtume (s.a.w..w) akapita nao karibu na mzoga, akasema (s.a.w.w.): “Tafuneni kipande chake.” Wakasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mun27


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

gu tutafune mzoga?” Akasema (s.a.w.w.): “Mlichokitafuna toka kwa ndugu yenu ni kichafu kushinda mzoga huu.”40 Hakika Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kutokana na nguvu ya nuru ya unabii isiyoonekana aliyonayo yeye, ameshuhudia kitendo cha watesi na kugundua kuwa ni mzoga mchafu kuliko maiti, na sura halisi ya utesi ni mbaya kushinda ubaya wa sura ya maiti. Imekuja katika riwaya nyingine kuwa hakika mtesi ataliwa nyama yake siku ya Kiyama, Amirul-Muuminin (a.s.) amesema: “Jiepusheni na utesi, hakika wenyewe ni chakula cha mbwa wa motoni.”41 3.

Kuongea na watu kwa adabu na heshima: Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Mola wangu ameniamuru kuongea na watu kwa adabu kama alivyoniamuru kutekeleza sala za faradhi.”42

Imam as-Sadiq (a.s.) amesema kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu “Na semeni na watu vizuri” (Sura al-Baqara: 83) “Yaani watu wote, waumini na wasiokuwa waumini. Ama waumini unawakunjulia uso, na ama wasiokuwa waumini unaongea nao kwa adabu ili uweze kuwavuta kwenye imani.”43 Hivyo kuongea na watu kwa adabu ni wema huko Akhera na ni fadhila mbele ya Mwenyezi Mungu, na wakati huo huo hurahisisha utendaji wa kazi na husababisha taufiki hata katika mambo ya kidunia. Imam Ali (a.s.) amesema: “Usalama wa dini na dunia uko katika kuwa na adabu kwa watu.”44 Muhujatul-Baydhai, Juz. 5, Uk. 253. Wasailus-Shia, Jz. 8, Mlango wa 152, Hadithi ya 16. 42 Mizanul-Hikma, Hadithi ya 5490. 43 izanul-Hikma, Hadithi ya 5495. 44 Mizanul-Hikma, Hadithi ya 5509. 40 41

28


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

Qur’ani Tukufu imesisitiza kwamba kauli kali haiwezi kufanikisha mambo, Mwenyezi Mungu anasema: “Kwa sababu ya rehma itokayo kwa Mwenyezi Mungu, umekuwa mpole kwao, lau ungelikuwa mkali mwenye moyo mgumu bila shaka wangelikukimbia. Basi wasamehe na uwaombee maghfira na ushauriane nao katika mambo.” (Sura Aali Imran: 159). Na katika riwaya nyingine Amirul-Muuminin (a.s.) anabainisha njia kuu anayopaswa muumini kupita, anasema katika ibara fupi: “Hapo zamani nilikuwa na ndugu katika njia ya Mwenyezi Mungu, kwa mtazamo wangu alikuwa akimtukuza (Allah) huku dunia ikiwa duni kwa mtazamo wake… alikuwa akitenda asemalo na wala hasemi asilotenda….. alikuwa anapendezwa na kusikia kuliko kuongea, na ilikuwa anapotokewa na mambo mawili basi huchunguza ni lipi lililo karibu na matamanio, hilo hulikhalifu. Ni juu yenu kuwa na tabia hizi, shikamaneni nazo na shindaneni katika hizo.”45

MGAWANYO WA MAJUKUMU: Hakika fahari ya kweli ambayo hasa mwanadamu anaweza kujivunia ni kule kuwa na sira hii ya kimungu, kuwa nayo yote au sehemu tu. Thamani ya kitu inayotokana na kitu chenyewe hailingani na ile inayokipata kwa kunasibiana na kitu kingine, kitambaa kikuukuu kilichogusa mwili wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) thamani yake ya kimaana haiwezi kulingana na kito chochote cha ulimwengu huu kilichopo juu ya taji la mtawala au mfalme yeyote aliyewahi kupatikana katika dunia hii. Hivi hutamani kuwa mtumishi mwenye kuihudumia haki? Au umepotoshwa na sifa za kidunia na mapambo yake? 45

Nahjul-Balagha, Hukima ya 281. 29


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

Hakika mgawanyo wa majukumu ni sharti la msingi katika kutekeleza kazi kwa ukamilifu, wala mtu mmoja hawezi kufanya kazi zote, bali ni lazima kila mfanyakazi atimize jukumu lake ndani ya safari hii yenye baraka, hiyo ni kama ilivyo ndani ya riwaya ambazo zinasisitiza dharura na ulazima wa kila kundi kuwa na kiongozi hata kama litakuwa ni la watu watatu tu. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Watu watatu wakiwa safarini wamfanye mmoja wao kiongozi.”46 Hivyo ni lazima apatikane kiongozi na mwongozwa, si kwa ajili ya kuwafanya wengine bora kushinda wengine bali ni kwa ajili ya nidhamu ya kazi na kuondoa mapungufu. Imam Khamenei anasema: “Cheo humaanisha nidhamu makini, na nafasi yake ni kubainisha majukumu na uhusiano baina ya wahusika.”47 Hivyo kiongozi na muongozwa kila mmoja anamkamilisha mwenzake ili waweze kufikia katika hali ya kumtii Mwenyezi Mungu, kupata radhi Zake na kutimiza amri yake. Imam Khomein alikuwa akijizingatia kuwa ni msimamizi na ni mtumishi, alikuwa akisisitiza aitwe mtumishi na akipendezwa na jina hilo. Imam Khomein anasema: “Kuitwa mtumishi ni bora kwangu kuliko kuitwa kiongozi, uongozi si muhimu bali kilicho muhimu ni utumishi na Uislamu, jukumu letu ni kuwatumikia.” Ili hilo liweze kutimia kwa ukamilifu ni lazima kujua uhusiano uliopo baina ya mkuu na mfanyakazi. Hakika uhusiano wao una pande mbili: Mmoja ni uhusiano wa mfanyakazi kwa mkuu wake, na wa pili ni uhusiano wa mkuu kwa mfanyakazi wake.

46 47

Mizanul-Hikma, Juz. 2 Hadithi ya 8609. Itilaat 30/ 11/ 69. 30


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

UHUSIANO WA MFANYAKAZI KWA MKUU WAKE: Hakika uhusiano wa mfanyakazi kwa mkuu wake unapasa uwe ndani ya anwani zifuatazo:

48

1.

Kumnasihi: Hakika kutoa nasaha na ushauri ni jambo analopaswa kulifanya kila mtu mwenye fikra na uwezo wa kufanya hivyo. Amirul-Muuminin (a.s.) anasema: “Ni juu yenu kupeana nasaha katika hilo (la kutekeleza haki za Mwenyezi Mungu) na kusaidiana vizuri juu ya hilo. Yeyote yule hata awe na uchu kiasi gani wa kutaka radhi za Mwenyezi Mungu au na juhudi kiasi gani katika kazi, hawezi kufikia kiwango halisi cha utiifu anaostahiki Mwenyezi Mungu. Lakini miongoni mwa haki za Mwenyezi Mungu alizowajibisha juu ya waja ni kupeana nasaha kwa kadiri ya juhudi zao na kusaidiana katika kusimamisha haki baina yao. Mtu yeyote hata awe na haki kubwa kiasi gani, na awe na ubora kiasi gani katika dini, haachi kuhitajia msaada katika kutekeleza haki za Mwenyezi Mungu alizombebesha. Na mtu yeyote hata awe duni kiasi gani ndani ya nafsi za watu na kudharauliwa na macho kiasi gani, haachi kuwa na nafasi ya kusaidia juu ya hilo (la kutekeleza haki za Mwenyezi Mungu) au kusaidiwa juu ya hilo.”48

2.

Kumsaidia: Hilo tunalipata ndani ya riwaya iliyotangulia: “Na kusaidiana vizuri juu ya hilo.” Riwaya inasisitiza kuwa haitoshi tu kusaidiana bali ni lazima iwe kusaidiana vizuri, yaani kazi tunayoifanya iwe kazi bora yenye ustadi, kwani miongoni mwa sifa za mtu mukhlis ni kazi yake kuwa bora, kwani hutoa nguvu zake na hujaribu kwa kila hali kupa-

Nahjul-Balagha, Hotuba ya 207. 31


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

ta sababu za kufanikisha kazi iliyomo mikononi mwake. Hakika moyo wa kusaidiana ndio unayopaswa kuwepo baina ya wafanyakazi. 3.

Kutii maamuzi na sheria za ofisi: Kutii sheria na kanuni ndio sharti la msingi la kufanikiwa na kufaulu katika kazi, uasi na kutokutii ni maradhi hatari sana ambayo yanaweza kuipata taasisi yoyote, ndio maana Amirul-Muuminin (a.s.), yule kiongozi mkuu anasimama mbele ya jeshi lake baada ya kuwa limevunja matumaini yake, analiambia: “Namuomba Mwenyezi Mungu akuuweni, hakika mmeujaza moyo wangu machungu na mmejaza kifua changu hasira…. Na mmeuharibu uamuzi wangu kwa kuniasi na kunitelekeza, mpaka imefikia maquraishi kusema: “Hakika mtoto wa Abu Talib ni mtu shujaa lakini hana ujuzi na vita.” Ole wao! Hivi kuna yeyote miongoni mwao mzoefu wa vita na mwenye kutangulia mbele vitani kushinda mimi?! Lakini hana uamuzi yule asiyetiiwa.”49

Tatizo kubwa lililoikumba serikali yake (a.s.) halikuwa nidhamu, hivi kuna nidhamu bora kushinda Uislam?! Wala halikuwa kiongozi, kwani yeye mwenyewe Amirul-Muuminin (a.s.) ndiye aliyekuwa kiongozi wao. Tatizo zima lilikuwa katika kutomtii, kwani kutokutii kuna uwezo wa kuharibu ubora na kusababisha kushindwa miradi mingi ya muhimu. Hukumu: Ni wajibu mfanyakazi kuwatii wakuu wake wa kazi na wakubwa wake wa kazi katika mambo ya kiofisi kulingana na sheria husika. 49

Nahjul-Balagha, Juz. 1, Uk. 70, Hotuba ya 27. 32


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

Maswali na majibu: 1.

Tangu nilipoanza kazi mpaka leo nafanya kazi kitengo cha utawala kama alivyoamuru mkuu wa ulinzi wa taifa, na wala sijafanikiwa kwenda kwenye medani ya vita kupambana, na kila ninapoomba hilo (la kwenda kwenye medani ya vita) wakuu wa kazi hawanikubalii, je ninabeba dhamana ya kutokushiriki kwenye medani ya vita au ni juu yangu kuwatii wakuu wangu wa kazi kwa hali yoyote?

Jibu: Ni wajibu kuheshimu sheria ya ulinzi wa taifa.50 2. Mkuu wa ofisi alimtaka mmoja wa wafanyakazi wa ofisi kufanya kazi fulani, basi ni kwa kiwango gani anawajibika huyu mfanyakazi kutekeleza amri ya mkuu? Na itakuwaje iwapo hatatii amri yake? Jibu: Ni wajibu mfanyakazi kuwatii wakuu wake wa kazi walioainishwa, awatii katika mambo ya ofisi kulingana na sheria ya dola ya Kiislamu.51

50 51

Istiftaat, Juz. 2, Uk. 506, Mas’ala ya 72. Istiftaat cha Kiajemi, Juz. 2, Uk. 484, Swali la 1. 33


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

MAHUSIANO YA KIBINADAMU (2) UHUSIANO WA MKUU KWA MFANYAKAZI WAKE:

I

mam Zainul-Abidin (a.s.) amesema: “Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi najikinga Kwako na……… na kuwaongoza vibaya wale walio chini yangu.”52 Kuna nukta mbili za msingi katika uhusiano wa kiongozi kwa wale walio chini yake, ni wajibu kiongozi azitazame kwa makini nukta hizi, nazo ni: Kwanza: Hakika kuwepo mfanyakazi anayefanya kazi chini yako haimaanishi kuwa wewe ni bora kushinda yeye katika ustawi wa kiroho, bali huenda yeye ni bora kushinda wewe mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na huenda wewe utahitaji uombezi wake huko Akhera kutokana na ukamilifu wake na upungufu wako. Pili: Wewe ni mkuu wake ili unadhimu kazi zake tu na si mkuu wake katika kila kitu, hivyo hauna ruhusa wa kumtumikisha katika mambo yako binafsi, na hata katika mambo ambayo si binafsi iwapo yako nje na mipaka ya kazi na cheo chako ulichonacho kinidhamu. Amirul-Muuminin (a.s.) anasema: Hakika kazi yako si chakula chako lakini ni dhamana iliyo shingoni mwako, na wewe uko chini ya uangalizi wa yule aliye juu yako, hivyo huna ruhusa ya kuwakandamiza raia.”53 Yaani kumtumikisha kwako mtu ni kukiwa kwa namna ya lazima na nguvu basi jua ni utumikishaji usio wa haki na 52 53

Sahifatus-Sajjadiyyah Uk. 57. Nahjul-Balagha Juz. 2, Uk. 6. 34


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

ni haramu, bali yapasa ujihadhari kumtumikisha mtu kwa njia ya soni, kwani kinachochukuliwa kwa njia ya soni ni sawa na kinachochukuliwa kwa wizi. Imepokewa riwaya kuwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Yeyote kati yenu akialikwa kwenye chakula asiandamane na mwanaye, kwani hakika kama atafanya hivyo atakuwa (mtoto) amekula haramu na ameingia (nyumba hiyo) kwa njia ya wizi.”54

EWE NDUGU YANGU KIONGOZI! Ewe mtawala! Chukua tahadhari kwani hakika uongozi ni mtihani mgumu ambao wengi watashindwa kufaulu huko mbele, na wala hawatabakia ila mawalii wa Mwenyezi Mungu ambao hawajatetemeshwa na mapambo ya dunia wala sauti ya wingi wa viatu vya walio nyuma yao. Hivyo cheo chako kiwe ni njia ya kupatia radhi za Muumba na kupata daraja za juu, na si njia ya kuzama ndani ya dunia na kuwadharau waumini. Mwenyezi Mungu aepushie mbali hilo. Kumbuka wasia wa Amirul-Muuminin (a.s.) kwa Malik alAshtar radhi za Allah ziwe juu yake: “Wala usiseme mimi ni kiongozi basi ni lazima nitiiwe, kwani kufanya hivyo ni kuuharibu moyo, kuharibu dini na ni kujiweka karibu na mwingine (asiyekuwa Mwenyezi Mungu). Ukipatwa na kiburi au majivuno kutokana na mamlaka uliyonayo basi tazama adhama ya ufalme wa Mwenyezi Mungu uliopo juu yako na uwezo Wake kwako juu ya lile ambalo huwezi kuliepusha na nafsi yako, hakika hali hiyo itakupunguzia uasi wako na kukuzuia usitende kwa msukumo wa hasira yako na itakurejeshea ile sehemu ya akili iliyokutoka.”55 54 55

Al-Kafiy Juz. 6 Uk. 27. Barua kwenda kwa Malik al-Ashtar. 35


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

NI LIPI JUKUMU LA KIONGOZI: Hakika mwenendo wa viongozi, harakati zao na namna yao ya kuamiliana na wale walio chini yao vina mchango mkubwa na wa msingi katika kazi, mchango ambao huonekana katika utendeaji wa mfanyakazi na taasisi nzima. Kiongozi hubeba jukumu kubwa la kuwahimiza walio chini yake kufanya kazi, kuibua nguvu yao iliyojificha, kuzioanisha juhudi zao na kuzifikisha katika kiwango cha kuchuma matunda kwa njia fupi na gharama ndogo katika kiwango cha kimada na kiroho, ndani ya mazingira ambayo Mwenyezi Mungu anayaridhia na ambayo ramani yake imechorwa na Uislam Mtukufu. Hivyo inawapasa viongozi katika mtindo wao wa kuamiliana na wale walio chini yao wasiusahau Uislamu na mafunzo yake ya asili na sahihi, hivyo wanawajibika kujipamba na sifa zifuatazo: 1. Mfano mwema: Kiongozi anatakiwa kuwa mfano mwema kwa anaowaongoza, anakuwa msitari wa mbele na kutoa mfano wa kivitendo ili awe mfano wa kuigwa ambao watauweka mbele yao ili uweze kuwasaidia kutekeleza mipango kwa ari ya juu na kwa njia ya wazi. Imam Khamenei anasema: “Ni wajibu kwa viongozi katika harakati zao zote wawe wenye kufaa na mfano mwema kwa wengine, wawafunze nidhamu na uchamungu kupitia utendaji wao.”56 Usitende baya ambalo wewe wawakataza wale uwaongozao, wala usiwatake watende jema lolote kabla wewe mwenyewe hujailazimisha nafsi yako kulitenda, wala usijitofautishe na wao isipokuwa kwa wingi wa kazi, uungwana na juhudi… haya ni mambo ambayo unawajibika kuwashinda kwayo. 56

Jamhuriy Islamiy 70/ 6 / 26. 36


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

Amirul-Muuminin (a.s.) anasema: “Usiwe mmoja wa wale wanaotaraji Akhera bila amali na wanaakhirisha toba kwa kujipa matumaini ya kuishi muda mrefu. Duniani anasema kauli ya wenye kujinyima (dunia), lakini anatenda humo matendo ya wenye kuipenda. Akipewa chochote toka humo hashibi na akinyimwa hakinai…. anakataza bila kujikataza na anaamuru asiyoyatenda. Anawapenda watu wema bila kutenda amali zao, na anawachukia watenda dhambi na hali angali ni mmoja wao.”57 Anasema tena (a.s.): “Atakayejipa uongozi wa kuwaongoza watu basi ni wajibu juu yake aanze kuifunza nafsi yake kabla ya kumfunza mwingine, amfunze adabu kwa vitendo vyake kabla ya kumfunza kwa ulimi wake.”58 Njia hii ndiyo yenye mafanikio ambayo huleta hamasa kwa wanaoongozwa, maelekezo ya maneno tu huondoa hamasa ya kazi. Amirul-Muuminin (a.s.) anasema: “Anayelingania bila vitendo ni sawa na anayejaribu kurusha mshale bila upinde.”59 2.

Kuwatia moyo: Hakika kuwadharau ndugu zako wafanyakazi, kuwadhihaki, kudharau kazi zao, kutozijali na kuzitafutia dosari si kwa nia ya kutengeneza na kumtia moyo bali ni ili umtie doa mfanyakazi, hayo yote ni maradhi hatari ambayo ni wajibu kiongozi kujiepusha nayo. AmirulMuuminin (a.s.) anasema: “Hazitamfaa mtu juhudi zake hata ziweje au kitendo chake hata kiwe na ikhlasi kiasi gani, kama atatoka duniani kwenda kukutana na Mola wake na hali ana moja kati ya sifa hizi na hajatubia…… na kuitafutia doa kazi aliyoifanya mwenzake.”60

Nahjul-Balagha, Hikima ya 142. Nahjul-Balagha, Hikima ya 70. 59 Nahjul-Balagha, Hikima ya 330. 60 Nahjul-Balagha, Hotuba ya 152. 57 58

37


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

3.

Kutokuwa na maringo na masimango: Imam Ali anasema: “Jiepushe kuwatendea raia wako vitendo vya masimango kwa hisani yako au vya kujikweza, au kuwaahidi bila kuwatimizia ahadi yako. Hakika masimango huharibu hisani na kujikweza huondoa nuru ya haki, na uvunjaji wa ahadi hupelekea kuchukiwa na Mwenyezi Mungu na watu pia. Mwenyezi Mungu anasema: “Ni chukizo kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu kusema msiyotenda.” (Surat as-Swaf: 3)61

Imam (a.s.) hakuzuia tu masimango na kujikweza, mambo ambayo ni harakati za kivitendo, bali pia ameingia ndani zaidi katika nia ambazo hubaki ndani ya siri ya mwanadamu, na amefika mpaka kwenye hisia za mambo hayo. Anasema (a.s.): “Jiepushe na maringo na kutegemea kile kinachokufanya uringe na kupenda sifa. Hakika hiyo ni fursa nzuri aliyonayo shetani inayomwezesha kuharibu hisani ya muhisani.”62 4.

Kumlipa mazuri yule aliyefanya vizuri: AmirulMuuminin (a.s.) anasema: “Kisha tambua kila mtu miongoni mwao ana chumo lake, wala usiongeze chumo la huyu kwa yule, wala usishindwe kufikia mwisho wa chumo lake. Sharafu ya mtu isikufanye ukuze chumo lake licha ya kuwa dogo, wala uduni wa mtu usikufanye upunguze chumo lake licha ya kuwa kubwa.”63

Hakika kumlipa mazuri yule aliyetenda mazuri ni jambo lenye athari kubwa katika kumtia mfanyakazi hamasa na kumsukuma kutoa uwezo wake wa juu alionao ili kuziba mapengo yaliyopo. Malipo haya humfanya aone kuwa kazi yake imethaminiwa Nahjul-Balagha, Barua ya 53. Nahjul-Balagha, Barua ya 53. 63 Nahjul-Balagha, Barua ya 53. 61 62

38


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

na waumini kama ilivyothaminiwa pia na Mwenyezi Mungu. Allah anasema: “Na sema: Tendeni vitendo, Mwenyezi Mungu na Mtume wake na waumini wataviona vitendo vyenu na mtarudishwa kwa Mjuzi wa ghaibu na dhahiri, naye awaambie mliyokuwa mkiyatenda.” (Sura Tawba: 105). Imam Khamenei anasema: “Miongoni mwa kanuni ambazo ni wajibu viongozi kuzitilia umuhimu ni kanuni ya kuheshimu sifa na vigezo ndani ya taasisi ya kijeshi. Hapo namaanisha suala la motisha na vitisho, ni juu yenu kutekeleza jukumu hili kiukweli.”64 Hivyo kutoa motisha ni jukumu na wajibu wa kiongozi, anawajibika kumtimizia wajibu huo yule aliye chini yake, hiyo ni kwa sababu binadamu ni roho yenye hisia na si jiwe, hivyo ni lazima kuheshimu upande huu wa kibinadamu kupitia motisha na malipo ambayo yatamtia ari na kumsukuma kutafuta kikubwa zaidi. 5.

Kumwadhibu mwenye kosa: Ukiachilia mbali motisha pia kuna adhabu ambayo haipasi kiongozi kuisahau ili kutimiza utekelezaji wa kazi na kuheshimu nidhamu yake na ili kusipatikane fujo, uholela na dharau. Amirul-Muuminin (a.s.) anasema: “Kuheshimu haki ya mtu kusiwazuieni kumwadhibu adhabu ambayo ni haki yake.”65 Jambo hili alilitekeleza Imam (a.s.) zama za serikali yake.

Imam Khamenei anasema katika moja ya hotuba zake kwa majeshi ya ulinzi ya Jamuhuri ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran: “Amirul-Muuminin (a.s.) alimwadhibu yule mtu ambaye hakutii amri yake….nanyi ni juu yenu kufanya hivyo, msiseme: ‘Hakika fulani ni mtu mwema na mzuri basi hafai kuadhibiwa nasi kwa tendo 64 65

Jamhuriy Islamiy 5/ 8/ 70 Mizanul-Hikma Juz. 1, Uk. 659. 39


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

lake baya alilolitenda.’ Msipotekeleza amri hii basi tambueni jeshi la ulinzi litajimaliza lenyewe.”66 Ndiyo, kufumbia macho makosa na uhalifu, hususan ule mkubwa husababisha athari mbaya kwenye kazi. Imam Khamenei anasema: “Enyi viongozi! Msipopambana na makosa na uhalifu ndani ya umoja mnaoutawala basi umoja huu utavunjika na kutoweka.”67 Utekelezaji huu si kwenda kinyume na Uislamu bali ndio Uislamu wenyewe kimatendo, ambao unaendana na mazingira na unaweka sheria kwa masilahi ya umma. Imam Khamenei anasema: “Pindi kiongozi anapomwamuru mmoja ya waandamizi wake kwenda kujaza ndoo maji chini ya anga lenye makombora yanayorushwa na adui, na anamwambia: ‘Ni wajibu juu yako kwenda na kurudi mbio, wala hupasi kupumzika njiani utakapochoka, na kama ukifanya hivyo (ukipumzika) nitakuadhibu.’ Kiongozi akifanya hivyo si kosa, kwani hii ni moja ya aina za nidhamu kubwa na ulinzi mkali tunaoweza kuutumia, wala kufanya hivyo si ushetani bali ni Uislamu timilifu.”68 6.

Kuzuia udhalilishaji: Yote tuliyoyataja katika maudhui ya adhabu hayamaanishi kumwondolea heshima muumini na kumdhalilisha, bali ni wajibu kujiepusha na udhalilishaji, na ni wajibu kuheshimu mipaka sahihi ya Uislamu hata katika kazi za kijeshi na amri za kijeshi. Imam Khamenei anasema: “Ni wajibu kuung’oa udhalilishaji kwenye vikosi vya kijeshi. Udhalilishaji ni jambo lisiloruhusiwa kufanywa na yeyote na dhidi ya yeyote yule, na yeyote atakayetenda hilo atachukuliwa hatua za kinidhamu, na jambo hili halip-

Mizanul-Hikma Juz. 1, Uk. 659. Jamhuriy Islamiy 5/ 8/ 70 68 Bayam Inqilab, Toleo la 112, Uk. 54. 66 67

40


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

ingani na hali ya kumkaripia mtu ambaye katenda kosa, lakini ni wajibu iwe kwa ibara munasaba.”69 Amirul-Muuminin (a.s.) anasema: “Wapendelee raia wako wote lile unalolipenda kwa ajili ya nafsi yako na watu wa nyumba yako, na chukia kuwatendea lile unalochukia kutendewa wewe na watu wa nyumba yako. Hakika hilo hukupa hoja tosha na ndilo linalowafaa raia.”70 7.

Kusamehe: Tulipozungumzia suala la kumwadhibu mkosaji hatuna maana kwamba hali ya kazi igeuke na kuwa baadhi ya kanuni za adhabu na nguvu iwe ndio mtawala mkuu katika kuamiliana na walio chini yako. Bali sehemu ya msamaha na ulaini inapasa kuwepo kwa kiwango ambacho hakitasababisha fujo na uholela, yaani usipoteze nafasi ya msamaha na kutoa fursa nyingine kwa mhusika. AmirulMuuminin (a.s.) anasema:

“Wape msamaha wako na usamehevu wako kwa kiwango kile cha msamaha na usamehevu unachotamani upewe na Mwenyezi Mungu na utakachoridhika nacho. Hakika wewe ni mkuu wao, na aliyekupa mamlaka ni mkuu wako, na Mwenyezi Mungu ni mkuu wa yule aliyekupa mamlaka, naye amekutaka umwakilishe katika jambo lao na amekutahini kupitia wao.”71 Hukumu: Ni wajibu kwa waajiri kutekeleza mikataba yote inayohusu haki za wafanyakazi na watumishi kulingana na kanuni na sheria rasmi. Na wafanyakazi wana haki ya kuomba haki zao za kisheria. Dhamimatu Ruwaydiha, Toleo la 325. Al-Amaal cha Shaikh al-Mufid Uk. 269. 71 Nahjul-Balagha, Barua ya 53. 69 70

41


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

Maswali na majibu: 1.

Ni ipi hukumu lau ikitokea wamiliki wa taasisi na mashirika fulani wakigoma kutoa baadhi ya stahili na haki za wafanyakazi zilizopo kwenye sheria ya kazi iliyopendekezwa na Bunge la Jamhuri ya Kiislamu na ikapitishwa na Bunge la katiba.

Jibu: Ni wajibu kwa waajiri kutekeleza mikataba yote inayohusu haki za wafanyakazi na watumishi kulingana na kanuni na sheria rasmi. Na wafanyakazi wana haki ya kuomba haki zao za kisheria.72

72

Ajwibatul-Istiftaat Juz. 2 Uk. 205, Swali la 576. 42


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

VIFAA NA VITENDEA KAZI VIFAA VYA KAZI NI AMANA:

H

akuna shaka kwamba kazi inahitaji baadhi ya vitendea kazi, vifaa vya lazima vinavyomsaidia mfanyakazi kutekeleza jukumu lake kwa ukamilifu na ubora tena kwa njia rahisi kadiri iwezekanavyo. Vitendea kazi hivi ni mjumuiko wa vitu mbalimbali kama vile vifaa vya mawasiliano, vifaa vya usafirishaji, vifaa vya utendaji wenyewe, samani, sehemu ya kufanyia kazi na mengineyo. Mambo yote haya lazima yawe chini ya utendaji wa mfanyakazi ili kwamba aweze kutimiza vizuri kazi yake na jukumu lake, lakini cha muhimu ni lazima mfanyakazi mwenyewe ajiulize, je anavichukuliaje vifaa hivyo vilivyo chini ya utendaji wake, je ni dhamana iliyo chini yake na kwamba atawajibika iwapo vitaharibika? Au anachukulia kuwa vimekuwa milki yake binafsi na hivyo ana haki ya kuvitumia atakavyo yeye, kwa kuviharibu na kutovitunza ipasavyo na hivyo kuvitumia katika lenye faida na lisilo na faida? Ukweli ni kwamba vifaa hivi si milki binafsi ya mfanyakazi wala si mali iliyotupwa bali ni amana iliyopo katika shingo ya mfanyakazi na siku ya Kiyama ataulizwa kuhusu kila sehemu ya vifaa hivyo. Imam Ali (a.s.) anasema: “Naapa hakika nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akiniambia mara tatu punde tu kabla ya kifo chake: ‘Ewe Abu Hasan! Heshimu amana ya mwema na ya muovu, ndogo na kubwa, hata katika uzi na sindano.”73

73

Mizanul-Hikma Juz. 1 Uk. 214. 43


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

KUHESHIMU AMANA NI KIPIMO CHA ­UCHAMUNGU: Hakika kuheshimu amana ni miongoni mwa sifa za msingi za mtu muumini, sifa ambazo kazitaja Mwenyezi Mungu ndani ya Kitabu chake Kitukufu, anasema: “Na ambao kwa amana zao wanazihifadhi.” (Sura Muuminun: 8). Bali ni kwamba riwaya zinatusimulia kuwa kuheshimu amana ndio imani bora. Amirul-Muuminin (a.s.) anasema: “Imani bora ni uaminifu, na tabia mbaya zaidi ni kuvunja uaminifu.”74 Hakika uchamungu wa kweli huonekana katika vitendo katika kuheshimu miko ya kisharia katika kazi, vitendo hivi ndio hudhihirisha iwapo ibada za muumini, sala na saumu ni za kweli au ni sura tu ya nje iliyokosa madhumuni yake halisi. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) anasema: “Msitazame wingi wa sala zao na funga zao na wingi wa hija zao na sadaka zao na kusimama kwao usiku, lakini tazameni ukweli wa mazungumzo yao na kuheshimu kwao amana (uaminifu).”75 Zinduka ewe mfanyakazi na jihadhari, kwani bila shaka Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amejitenga mbali na kila mtu ambaye haheshimu amana wala haijali na hatimaye husababisha kuharibika. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: “Si miongoni mwetu yule asiyeheshimu amana mpaka anaiharibu pindi anapokabidhiwa amana.”76

Mizanul-Hikma Juz. 1, Uk. 214. Mizanul-Hikma Juz. 1, Uk. 214. 76 Mizanul-Hikma Juz. 1, Uk. 215. 74 75

44


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

VIFAA VITUMIKE KWA KAZI TU: Hakika kutunza vifaa si kutoviharibu tu, bali ni zaidi ya hilo, ni pamoja na namna ya kuvitumia, vifaa hivi vimewekwa ili vitumike eneo maalumu hivyo ni lazima kuheshimu hilo. Imenukuliwa kuwa Amirul-Muuminin (a.s.) aliingia siku moja ndani ya Baytul-Mali usiku akawa anaandika mgawanyo wa mali, ghafla Talha na Zubair wakafika, Imam (a.s.) akazima taa iliyokuwa mbele yake na akaomba iletwe taa nyingine kutoka nyumbani kwake. Wakamuuliza kuhusu kitendo hicho, akasema (a.s.): “Mafuta yake yalitokana na mali ya Baytul-Mali, haipasi niandamane nanyi katika mwanga wake.”77 Hakika taa ambayo Amirul-Muuminin (a.s.) alikuwa akiitumia ilitokana na Baytul-Mali hivyo hakuwa anaitumia isipokuwa katika mambo ambayo inapasa itumike, hivyo alipoingia katika kazi binafsi aliizima taa hii na akatumia taa nyingine ambayo ni milki binafsi ya Imam (a.s.). Na hii inaonyesha kiwango cha ukamilifu katika kutunza mali za ofisi, lakini hii haiwakilishi mpaka wa kisharia ambao si ruhusa kuuvuka. Kutumia vifaa vya kazi katika mambo binafsi ni jambo linalowezekana iwapo tu ni ndani ya masharti ambayo yataonekana ndani ya hukumu za kisharia zifuatazo.

KUTOKUFANYA UBADHIRIFU NA UFUJAJI: Hakika ubadhirifu na ufujaji ni moja ya maradhi ambayo huondoa baraka, hupoteza nguvu na hupoteza kipato bure bila faida. Qur’ani Tukufu imeonyesha madhara yake katika tangazo la Mwenyezi Mungu: “Wala msifanye ufujaji, hakika Yeye hawapendi wafujaji.” (Sura An’am: 141). Hakika Mungu Mwenyezi kutokupenda 77

Al-Imam Ali (a.s.) cha Ar-Rahmaniy al-Hamdaniy Uk. 669. 45


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

ubadhirifu si bila sababu, bali hali hiyo inaonyesha madhara ya ubadhirifu. Imam Ali (a.s.) alimwandikia mmoja wa magavana wake: “Chongeni kalamu zenu na ibananisheni misitari yenu. Mnaponiandikia ondoeni lisilo na maana na andikeni lile lenye maana. Jiepusheni kukithirisha (maandishi), kwani hakika mali za Waislamu hazivumilii ufujaji.�78 Amirul-Muuminin (a.s.) ametuandikia usia mzuri sana nasi tunataraji kuwa miongoni mwa wenye kuufanyia kazi. Hukumu: Vifaa vya kazi ambavyo ni amana iliyopo mikononi mwa mfanyakazi iwapo ikitokea kuharibika bila kukusudia au uzembe, mfanyakazi hatalipa thamani yake, isipokuwa kama kuna sheria makhususi, hapo ni wajibu kutenda kwa mujibu wa sheria husika. Hakuna kizuizi kutumia vifaa vya kazi kwa matumizi binafsi ya kawaida ambayo wakuu wa kazi hawakatazi. Si vibaya kutumia simu kwa lengo binafsi kama utalipa thamani ya mawasiliano na kuruhusiwa na wakuu wa kazi. Maswali na majibu: 1.

78

Kabla ya miaka mitatu na nusu nilitumia gari lililo chini ya Hazina Kuu kufanya kazi fulani, lilipokuwa njiani liliacha njia na kupinduka, wachunguzi rasmi na wataalamu walisema kuwa kuacha njia huko kulitokana na tatizo la kiufundi, je kisharia ni wajibu kulipa gharama za hasara iliyoipata Hazina Kuu au hapana? Na kama ni wajibu ni nani

Mizanul-Hikma , Hadithi ya 19441. 46


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

anawajibika kulipa, ni dereva au mimi ambaye nilimtuma kwenda kutekeleza jukumu hilo? Jibu: Iwapo amana imo mikononi mwake na ikaharibika bila kukusudia wala uzembe halipi, isipokuwa kama kuna sheria makhususi iliyowekwa na dola ya kiislamu kuhusu jambo hili, hapo itawajibika kutenda kulingana na sheria husika.79 2.

Katika baadhi ya taasisi za dola kuna kawaida ya kwamba anayetumia simu kwa mambo yake binafsi hulipa riyali hamsini katika sanduku maalumu lililowekwa kwa ajili ya jambo hili, je kuna tatizo katika hilo?

Jibu: Hakuna tatizo kama limeruhusiwa na wakuu wa kazi wahusika.80 3. Ni ipi hukumu ya kutumia mali za dola katika baadhi ya matumizi madogomadogo ya kawaida ambayo wakuu wakazi hawakatazi, kama vile kutumia kalamu na karatasi kuandikia nukta muhimu binafsi, au kunywa chai (ya ofisi), na mengineyo mfano wa hayo? Jibu: Hakuna kizuizi katika matumizi madogomadogo ya kawaida.81 4. Je mfanyakazi ana haki ya kusamehe baadhi ya haki zake za kikanuni asizichukue toka serikalini, na mkabala na kitendo hicho akatumia mali za dola kama simu, kinakilishi na mfano wake kadiri ya thamani ya haki zake? Jibu: Hana haki ya kufanya hivyo. 82

Istiftaat cha Kiajemi Juz. 2, Uk. 25, Swali la 2. Istiftaat cha Kiajemi Juz. 2, Uk. 288, Swali la 15. 81 Istiftaat cha Kiajemi Juz. 2, Uk. 288, Swali la 16. 82 Istiftaat cha Kiajemi Juz. 2, Uk. 522, Swali la 114. 79 80

47


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

MALI MALI:

M

wenyezi Mungu anasema: “Akasema (Yusuf): Nifanye mweka hazina wa nchi, hakika mimi ni mlinzi, mjuzi.” (Sura Yusuf: 55). Hakika Aya hii Tukufu licha ya ufupi wake lakini inatoa mukhtasari wa njia nyoofu katika maudhui ya mali, njia ambayo inatokana na misingi miwili: Kwanza: Uaminifu na kutofanya usaliti, msingi huo umeelezwa kwa neno: ‘mlinzi.’

Pili: Kutambua mipaka ya matumizi, sehemu zake na vipaumbele vyake, msingi huo umeelezwa kwa neno: ‘mjuzi.’

MADHARA YA MALI: Mwenyezi Mungu ameitaja mali ndani ya Qur’ani Tukufu na kuizingatia kuwa ni mapambo ya dunia, amesema: “Mali na watoto ni pambo la maisha ya dunia….” (Sura Kahfi: 46). Hili ni onyo kwetu, yule ambaye moyo wake una sehemu yoyote ya mapenzi ya dunia basi mali yake itakuwa mtihani na majaribu kwake na itampeleka kutenda maasi kila siku na kila sekunde maadamu mali ipo mbele ya macho yake. Hivyo anayebeba majukumu ya mali anapasa awe yule ambaye ni miongoni mwa watu wa Akhera ambao wanalijua fungu la Akhera ndani ya Aya iliyotangulia: “….Na vitendo vizuri vibakiavyo ndi48


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

vyo bora mbele ya Mola wako kwa malipo na tumaini bora.” (Sura Kahfi: 46). La sivyo atakuwa mawindo rahisi ya shetani mlaaniwa na nafsi iamrishayo maovu. Imam as-Sadiq (a.s.) amesema: “Hakika shetani humwendesha mwanadamu katika kila kitu, akichoshwa naye humfunga kwenye mali na kumwinamisha shingo yake.”83 Ni wajibu daima tukumbuke yale maneno aliyokuwa akiyakariri Amirul-Muuminin (a.s.) kuhusu dhahabu na fedha: “Ee njano (dhahabu), ee nyeupe (fedha), hamtanihadaa, muhadaeni mwingine….. ewe dunia, usijionyeshe kwa ajili yangu wala usinitamani na wala usinidanganye, nimeshakutaliki talaka tatu, siruhusiwi kukurejea.”84

MIPAKA YA MATUMIZI: Hakika matumizi ya mali yana mipaka ambayo imetajwa na Imam as-Sadiq (a.s.) katika riwaya fupi, anasema (a.s.): “Ibilisi laana ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake anasema: ‘Yapo yanayonichosha kwa binadamu, lakini halitanichosha kwake moja kati ya matatu: Kupata mali kwa njia isiyo ya halali, au kuzuia haki yake (yaani ya mali hiyo), au kuitumia pasipo mahali pake.”85 Riwaya hii tukufu inatufunza mambo matatu ya msingi katika suala la mali kazini na ofisini, nayo ni: Kwanza: Haki ya kutumia mali: Hakika kutumia mali bila kuwa na haki ya kuitumia ni sawa na kupata mali kwa njia isiyo ya halali, kama pale anapotumia mali iliyowekwa amana kwake aihifadhi kama amana bila kuwa na haki ya kuitumia. Mali iliyowekwa amana inatofautiana na ile aliyo na mamlaka nayo, hivyo tangu Mizanul-Hikma, Hadithi ya 19322. Biharul-Anwar Juz. 41 Uk. 103. 85 Mizanul-Hikma, Hadithi ya 19324. 83 84

49


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

mwanzo ni lazima ajue je mali hii ana mamlaka nayo? Na je ana haki ya kuitumia au hana haki ya kuitumia? Hili litambainishia uhalali wa kuitumia au uharamu wake. Pili: Dharura ya kuitumia katika kukidhi mahitaji: Kama ana mamlaka ya kuitumia ndani ya mipaka ya kiofisi basi ni lazima aitumie katika sehemu za lazima, kwa sababu mali hazikuwekwa mikononi mwake ila ni kwa ajili ya kukidhi mahitaji na kuondoa mahitaji yaliyopitishwa kisharia, hivyo kutozitumia katika mahitaji halali yanayostahiki ni moja ya aina za ubahili wenye madhara, na ni usaliti na kutokuheshimu amana za wenyewe. Hili ndilo lililoashiriwa na Imam as-Sadiq (a.s.) katika kauli yake: “Kuzuia haki yake.” Hilo linaashiriwa na Amirul-Muuminin (a.s.) katika kauli yake: “Kuwa mkarimu usiwe mbadhirifu, kuwa mkadiriaji usiwe bahili.”86 Tatu: Kuitumia katika maeneo yaliyopitishwa kisharia: Ni wajibu kuitumia katika maeneo makhususi ambayo mali imewekwa kwa ajili yake, matumizi yoyote yaliyo nje na maeneo husika na bila ruhusa ni moja ya usaliti na ni mfano halisi wa kauli ya Imam Ali (a.s): “Kuiweka sehemu isiyo yake.”

UWIANO NA KUHESHIMU VIPAUMBELE: Hakika mambo hapa duniani yana mipaka kwa jumla, na mahitaji na maeneo yanayopasa kutumia mali ni mengi na hayaishi, hivyo ni lazima kuchunga vipaumbele katika matumizi na kutokuacha kilicho na umuhimu zaidi na kuzitumia katika chenye umuhimu mdogo, ambapo pia ni lazima kuwepo na uwiano na uadilifu wa matumizi baina ya mambo muhimu, mambo haya mawili ni lazima kuyachunga. 86

Nahjul-Balagha, Hikima ya 33. 50


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

Amirul-Muuminin (a.s.) anasema: “Wallahi, nilimuona Aqil akiwa amedhikika mpaka akaniomba pishi moja toka katika mali yenu, na nilimuona kijana wake ameishiwa nguvu na kabadilika rangi kutokana na ufukara wao kana kwamba nyuso zao zimefifizwa na giza. Alinitaka msaada kwa msisitizo na akarudia kauli mara kwa mara, nilimsikiliza, naye akadhani nitamuuzia dini yangu na kufuata hatamu yake kwa kuacha njia yangu, ndipo nikakipasha moto chuma kwa ajili yake, kisha nikamsogezea karibu na mwili wake ili apate mazingatio kwacho, akapiga kelele kutokana na maumivu yake kama mtu aliyezidiwa na maradhi, na alikaribia kuungua kutokana na joto lake. Nikamwambia: Wakuomboleze waombelezaji, ewe Aqil! Unalalamika kutokana na chuma kilichopashwa moto na mwanadamu kwa mchezo wake, lakini wewe wanikokotea kwenye moto uliowashwa na Jabari kwa ghadhabu zake, wewe unalalamika kwa adha je mimi nisilalamike kwa ladhwa.�87 Kwa mujibu wa riwaya ni kwamba Aqil hakuwa tajiri wala mbadhirifu bali yeye na familia yake walikuwa wahitaji, lakini Imam Ali (a.s.) aliheshimu uwiano katika matumizi. Ni sahihi kwamba Aqil ni muhitaji lakini yupo mwingine muhitaji kama yeye, hivyo inapasa kugawa matumizi kwa uwiano katika maeneo yote yaliyopitishwa kisharia, bila kuingiza hisia na mambo binafsi katika kutoa kipaumbele. Hukumu: Matumizi yote ya pesa yanayohusu kubadili pesa, kuchenji na kufaidika nazo lazima yawe chini ya sharia husika. Si haki mfanyakazi kuchukua mali bila ruhusa ya wakuu wa kazi mkabala na simu na mafuta binafsi anayotumia katika kazi. 87

Biharul-Anwar Juz. 40, Uk. 347. 51


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

Maswali na majibu: 1.

Kuna baadhi ya mali zinazotumwa na baadhi ya taasisi‌. Na kuna mtu aliyetumwa kufikisha pesa hizi, na mtu huyu akafanya biashara ya kubadili pesa na amepata faida kutokana na ubadilishaji huo, je mtu huyu anaweza kuchukua yeye binafsi theluthi ya faida na theluthi na iliyobaki kuiongeza kwenye mtaji wa asili?

Jibu: Kubadili pesa kunahitaji ruhusa ya mmiliki wa pesa, na faida inayopatikana ni milki ya mwenye pesa na ni wajibu kuitumia katika eneo lilelile aliloainisha mwenyewe. Mtu wa kati haruhusiwi kuitumia bila ridhaa ya mmiliki.88 2.

Ni ipi hukumu ya mtu aliyefaidika na mali za dola kwa manufaa yake binafsi au mengine kinyume na sheria na kanuni?

Jibu: Kufaidika na mali za dola kinyume na sheria kunawajibisha kulipa na nilazima kulipa mbadala kwa kurudisha kwenye sanduku lile lile alilochukulia.89 3.

Mimi nafanya kazi hazina ya soko la Hamdani, na hupokea pesa kila baada ya muda toka ofisini ili nizitumie katika mambo ya hazina na mambo mengineyo ya kiofisi, na kuna pesa hubaki nazo kama amana mpaka wakati wa kufunga mahesabu ya mwaka, je ni ipi hukumu kama nitatumia pesa hizi na kufaidika nazo kwa kununua na kuuza?

Jibu: Kutumia na kufaidika na pesa na miliki nyinginezo za dola kuko chini ya sheria za dola. 88 89

Istiftaat Juz. 2, Uk. 233, Mas’ala ya 4. Istiftaat Juz. 2, Uk. 499, Mas’ala ya 50. 52


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

4.

Mtu anayetumia mali zake binafsi kama simu na mafuta kwa ajili ya kazi za dola, je ana haki ya kuchukua alichotumia au thamani yake toka katika mali za dola?

Jibu: Hana haki ya kufanya hivyo bila kupata ruhusa ya wakuu wahusika. 5.

Kuna shirika maalumu linafanya kazi ya uwakala wa mashirika ya nje wa kuuza bidhaa za mashirika hayo, na mkabala na kazi hiyo linachukua asilimia fulani ya thamani ya bidhaa, je hilo linaruhusiwa kisharia kuchukua asilimia hiyo? Na kama mfanyakazi wa dola akiwa na usaidizi maalumu na shirika hilo, je anaruhusiwa kuchukua asilimia hiyo au la?

Jibu: Kama asilimia hii ni malipo ya uwakala wa kuuza bidhaa za mashirika ya nje au ya ndani ya serikali au yasiyo ya serikali, hakuna kizuizi wakala kuchukua asilimia hiyo. Lakini mtumishi wa serikali ikiwa mshahara anaochukua kila mwezi ni kutokana na kazi ya kuuza bidhaa za serikali basi hana haki ya kuchukua malipo mengine au zawadi mkabala na utumishi wake serikalini.90

90

Ajwibatul-Istiftaat Juz. 2, Uk. 107. 53


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

ORODHA YA VITABU VILIVYO ­CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1. Qur’an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka ­Thelathini 2.

Uharamisho wa Riba

3.

Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza

4.

Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili

5.

Hekaya za Bahlul

6.

Muhanga wa Imamu Husein (A.S.)

7.

Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.)

8.

Hijab vazi Bora

9.

Ukweli wa Shia Ithnaashari

10. Madhambi Makuu 11. Mbingu imenikirimu 12. Abdallah Ibn Saba 13. Khadijatul Kubra 14. Utumwa 15. Umakini katika Swala 16. Misingi ya Maarifa 17. Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia

54


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

18. Bilal wa Afrika 19. Abudharr 20. Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu 21. Salman Farsi 22. Ammar Yasir 23. Qur’an na Hadithi 24. Elimu ya Nafsi 25. Yajue Madhehebu ya Shia 26. Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur’an Tukufu 27. Al-Wahda 28. Ponyo kutoka katika Qur’an 29. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii 30. Mashukio ya Akhera 31. Al Amali 32. Dua Indal Ahlul Bayt 33. Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. 34. Haki za wanawake katika Uislamu 35. Mwenyezi Mungu na sifa zake 36. Kumswalia Mtume (s) 37. Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) 38. Adhana 39

Upendo katika Ukristo na Uislamu 55


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

40. Tiba ya Maradhi ya Kimaadili 41. Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu 42. Kupaka juu ya khofu 43. Kukusanya swala mbili 44. Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara 45. Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya 46. Kusujudu juu ya udongo 47. Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) 48. Tarawehe 49. Malumbano baina ya Sunni na Shia 50. Kupunguza Swala safarini 51. Kufungua safarini 52. Umaasumu wa Manabii 53. Qur’an inatoa changamoto 54. as-Salaatu Khayrun Mina -’n Nawm 55. Uadilifu wa Masahaba 56. Dua e Kumayl 57. Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu 58. Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake 59. Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata 60. Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mtume Muhammad (s) 61. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza 56


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

62. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili 63. Kuzuru Makaburi 64. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza 65. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili 66. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu 67. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne 68. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano 69. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita 70. Tujifunze Misingi Ya Dini 71. Sala ni Nguzo ya Dini 72. Mikesha Ya Peshawar 73. Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu 74. Ubora wa Imam ‘Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliyonyooka 75. Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake 76. Liqaa-u-llaah 77. Muhammad (s) Mtume wa Allah 78. Amani na Jihadi Katika Uislamu 79. Uislamu Ulienea Vipi? 80. Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) 81. Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) 82. Urejeo (al-Raja’a )

57


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

83. Mazingira 84. Utokezo (al - Badau) 85. Hukumu ya kujenga juu ya makaburi 86. Swala ya maiti na kumlilia maiti 87. Uislamu na Uwingi wa Dini 88. Mtoto mwema 89. Adabu za Sokoni 90. Johari za hekima kwa vijana 91. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza 92. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili 93. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu 94. Tawasali 95. Imam Mahdi katika Usunni na Ushia 96. Hukumu za Mgonjwa 97. Sadaka yenye kuendelea 98. Msahafu wa Imam Ali 99. Ngano ya kwamba Qur’ani imebadilishwa 100. Idil Ghadiri 101. Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu 102 Hukumu zinazomuhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi 103. Huduma ya Afya katika Uislamu 104. Sunan an-Nabii 58


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

105. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) 106. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) 107. Shahiid Mfiadini 108. Kumsalia Nabii (s.a.w) 109. Ujumbe -Sehemu ya Kwanza 110. Ujumbe - Sehemu ya Pili 111. Ujumbe - Sehemu ya Tatu 112. Ujumbe - Sehemu ya Nne 113. Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu 114. Hadithi ya Thaqalain 115. Ndoa ya Mutaa 116. Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza 117. Ukweli uliopotea sehemu ya Pili 118. Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu 119. Ukweli uliopotea sehemu ya Nne 120. Ukweli uliopotea sehemu ya Tano 121. Mkutano wa Maulamaa wa Baghdad 122. Safari ya kuifuata Nuru 123. Fatima al-Zahra 124. Myahudi wa Kimataifa 125. Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi 126. Visa vya kweli sehemu ya Kwanza 59


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

127. Visa vya kweli sehemu ya Pili 128. Elimu ya Ghaibu ya Maimamu 129. Mwanadamu na Mustakabali wake 130. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) 131. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) 132. Khairul Bariyyah 133. Uislamu na mafunzo ya kimalezi 134. Vijana ni Hazina ya Uislamu 135. Yafaayo kijamii 136. Tabaruku 137. Taqiyya 138. Vikao vya furaha 139. Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 140. Visa vya wachamungu 141. Falsafa ya Dini 142. Azadari-Kuhuzunika na Kuomboleza 143. Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah 144. Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu 145. Kuonekana kwa Allah 146. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) 147. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) 60


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

148. Ndugu na Jirani 149. Ushia ndani ya Usunni 150. Maswali na Majibu 151. Mafunzo ya hukmu za ibada 152. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1 153 Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2 154. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 155. Abu Huraira 156. Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. 157. Mazingatio kutoka katika Qur’an - Sehemu ya Kwanza 158. Mazingatio kutoka kaitka Qur’an - Sehemu ya Pili 159. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza 160. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili 161. Qur’ani Tukufu – Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili 162. Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) 163. Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani 164. Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu 165. Uislamu Safi 166. Majlisi za Imam Husein Majumbani 167. Je, Kufunga Mikono 168. Uislam wa Shia 169. Amali za Makka 61


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

170. Amali za Madina 171. Asili ya Madhehebu katika Uislamu 172. Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi 173. Ukweli uliofichika katika neno la Allah 174. Uislamu na Mifumo ya Uchumi 175. Umoja wa Kiislamu na Furaha 176. Mas’ala ya Kifiqhi 177. Jifunze kusoma Qur’ani 178. As-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah 179. Hayya ‘Alaa Khayri’l-’Amal Katika Adhana 180. Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura 181. Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na Ramadhani) 182. Uadilifu katika Uislamu 183. Mahdi katika Sunna 184. Maswali Ya Uchunguzi Kuhusu Uislam 185. Kazi na Bidii ni njia ya maendeleo 186. Abu Talib – Jabali Imara la Imani 187. Ujenzi na Utakaso wa Nafsi 188. Vijana na Matarajio ya Baadaye 189. Usalafi – Historia yake, maana yake na lengo lake 190. Ushia – Hoja na Majibu 191. Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) 62


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

192. Maombolezo – Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) 193. Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu 194. Takwa 195. Upotoshaji dhahiri katika Turathi (Hazina) ya Kiislamu 196. Amirul Muuminina (‘as) na Makhalifa 197. Uongozi na Utawala katika Mwenendo wa Imam ‘Ali (‘a) 198. Kuvunja hoja iliyotumika kutetea Uimamu wa AbuBakr 199. Adabu za vikao na mazungumzo 200. Hija ya Kuaga 201. Uwazi baina ya Maslahi na Vikwazo 202. Fadhila za watukufu watano katika Sahih Sita 203. Mdahalo baina ya Mwanachuoni wa Kisunni na Mwanachuoni wa Kishia (Al-Muraja’aat) 204. Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (as) 205. Mjadala wa Kiitikadi 206. Mtazamo kuhusu msuguano wa Kimadhehebu 207. Nchi na Uraia – Haki na wajibu kwa Taifa 208. Mtazamo wa Ibn Taymiyyah juu ya Imam Ali (as) 209. Uongozi wa Kidini – Maelekezo na Utekelezaji wa Kijamii 210. Maadili ya Ashura 211. Mshumaa – Shahidi na Kifo cha Kishahidi 212. Mizani ya Hekima – Hadithi za Ahlul Bait (as) – Sehemu ya Kwanza 63


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

213. Imam Ali na Mambo ya Umma 214. Imam Ali na Mfumo wa Usawa 215. Mwanamke na Sharia 216. Mfumo wa Wilaya 217. Vipi Tutaishinda Hofu? 218. Kumswalia Mtume ni Ufunguo wa Utatuzi wa Matatizo

219. Mahali na Mali za Umma 220. Nahjul-Balagha – Majmua ya Khutba, Amri, Barua, Risala, Mawaidha na Semi za Amirul-Muuminin Ali bin Abu Talib (a.s.) 221. Mukhtar – Shujaa aliyelipiza kisasi dhidi ya wauaji wa Imam ­Husein (as) hapo Karbala 222. Uimamu na Tamko la Kutawazwa 223. Imam Husain ni Mfumo wa Marekebisho na Mageuzi 224. Saada Kamili – Kitabu cha Kiada cha Maadili 225. Maeneo ya Umma na Mali Zake

64


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

KOPI NNE ZIFUATAZO ­ZIMETAFSIRIWA KWA LUGHA KINYARWANDA 1.

Amateka Na Aba’Khalifa

2.

Nyuma yaho naje kuyoboka

3.

Amavu n’amavuko by’ubushiya

4.

Shiya na Hadithi

65


Hukumu Zinazomhusu Mkuu wa Kazi na Mfanyakazi

ORODHA YA VITABU VILIVYO ­CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION KWA LUGHA YA KIFARANSA 1.

Livre Islamique

66


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.