Huyu ndiye bilal

Page 1

HUYU NDIYE BILAL (Uchunguzi juu ya Sira ya Sahaba Mtukufu na Uhusiano Wake na Bwana Mtume na Ahlul Bayt Wake)

‫هذا هو بالل‬ .‫قراءة في سيرة الصحابي الجليل وعالقته بالنبي وأهل بيته عليهم السالم‬

Kimeandikwa na: Sheikh Nabil Qawuq

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 1

4/23/2016 2:45:49 PM


‫هذا هو بالل‬

‫قراءة في سيرة الصحابي الجليل وعالقته بالنبي وأهل بيته عليهم السالم‪.‬‬

‫تأليف‬ ‫الشيخ نبيل قاووق‬

‫من اللغة العربية إلى اللغة السواحلية‬

‫‪4/23/2016 2:45:49 PM‬‬

‫‪10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 2‬‬


©Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 – 17 – 040 – 1 Kimeandikwa na: Sheikh Nabil Qawuq Kimetarjumiwa na: al-Haj Ustadh Hemedi Lubumba Kimehaririwa na: Al-Haj Ramadhani S.K. Shemahimbo Kimepitiwa na: Al-Haji Mujahid Rashid Kimepangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation
 Toleo la kwanza: Septemba, 2016 Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation
 S.L.P. - 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: www.alitrah.info

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 3

4/23/2016 2:45:49 PM


Yaliyomo Hadiya .......................................................................................... 1 Dibaji .......................................................................................... 2 Neno la Mchapishaji........................................................................ 3. Utangulizi......................................................................................... 5. Bilal na uaminifu wa historia........................................................... 5. Uturi wa Bilal ni mali yetu............................................................... 6. Ni kigezo chema cha pekee.............................................................. 7. Faslu za Kitabu................................................................................ 8. FASLU YA KWANZA:.............................................................. 10 Taarifa Binafsi................................................................................ 10 Jina lake na nasaba yake................................................................ 11 Kuzaliwa kwake............................................................................. 11 Ndugu zake.................................................................................... 12 Umbile lake.................................................................................... 13 Tabia yake tukufu........................................................................... 14 FASLU YA PILI:........................................................................ 16 Kusilimu Kwake na Kuteswa Kwake............................................ 16 Kusilimu kwake na mateso aliyoyapata......................................... 16 Aya zilizoteremka kumhusu yeye.................................................. 19 Kukombolewa kwake na kuachwa huru........................................ 25

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 4

4/23/2016 2:45:49 PM


FASLU YA TATU:...................................................................... 27 Swahaba Mwema........................................................................... 27 Ukaribu wake na Mtume wa Mwenyezi Mungu ....................... 28 Alikuwa miongoni mwa watu wa mwanzo kumhudumia Mtukufu Mtume .................................................. 29 Alikuwa mhazini wa Mtukufu Mtume ...................................... 32 Bilal akiwa kati ya utiifu na mapenzi........................................... .40 Anatangaza sharia na maamrisho ya Mtukufu Mtume ............. 43 Alikuwa ni mmoja kati ya wateule wa Mtukufu Mtume .......... 46 Labayka ........................................................................................ 47 Mwadhini wa Mtukufu Mtume , ............................................... 48 Bilal, katika Hadithi za Mtukufu Mtume....................................... 51 Hadithi ya Mtukufu Mtume  kuhusu riziki ya Bilal................... 56 Usia wa Mtukufu Mtume  kwa Bilal.......................................... 57 Ni mpokezi wa Hadithi za Mtukufu Mtume ............................. 58 Nafasi ya Bilal katika kisa cha kupumzika usiku safarini............. 60 Adhama nyingine ya Adhana ya Bilal........................................... 64 FASLU YA NNE:........................................................................ 66 Mwenendo wa Jihadi Yake............................................................ 66 Bilal na safari ya jihadi.................................................................. 66 Mwenyezi Mungu anampa uwezo dhidi ya aliyekuwa akimtesa... 67 Ushujaa wake na kujitolea kwake.................................................. 71 Kuhamia kwake Madina................................................................ 73 Kurudi kwake Makkahh kwa kishindo.......................................... 74 Adhana ya Bilal yafunga ukurasa wa masanamu.......................... 77

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 5

4/23/2016 2:45:49 PM


HUYU NDIYE BILAL

Mpiganaji katika Nchi ya Sham..................................................... 79 Bilal anamdhibiti Khalid bin Walid kwa kilemba chake............... 80 FASLU YA TANO:..................................................................... 82 Utu wa Bilal................................................................................... 82 Sin ya Bilal..................................................................................... 82 Bilal ni kama nyuki....................................................................... .85 Bustani ya elimu katika hadithi ya Bilal........................................ 86 Tunachojifunza kutoka katika Hadithi hii..................................... .91 Hebu tuzungumzie roho yake yenye hisia za kweli....................... 94 Beti zinazonasibishwa na Bilal...................................................... 97 Mtu mweusi hataingia peponi........................................................ 98 Ni nani aliyeshinda?....................................................................... 99 Ni miongoni mwa waliomsadiki.................................................. 100 Kupata kwake medali ya ukweli.................................................. 103 Kuoa kwake................................................................................. 104 Mtukufu Mtume anamwozesha Bilal........................................... 107 Ubaguzi warudi upya................................................................... 109 FASLU YA SITA:..................................................................... 114 Bilal na Ahlul-Bayt ............................................................ 114 Mapenzi yake kwa Ahlul-Bayt..................................................... 115 Bilal alizuru kaburi la Mtukufu Mtume  na akutana na Husein .................................................................. 118 vi

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 6

4/23/2016 2:45:49 PM


HUYU NDIYE BILAL

Bilal atoa Adhana kwa ajili ya Fatimah na Husein ............... 119 Bilal ajitolea kumhudumia Fatimah ...................................... 120 Bilal ashiriki katika kuandaa walima wa ndoa ya Fatimah na Ali .................................................................. 120. Bilal aenda kumnunulia manukato Fatimah .......................... 121 Bilal asikia Hadithi ya Mtukufu Mtume  kuhusu nafasi ya Fatimah ............................................................... 122 Bilal ahudhuria mbele ya Mtukufu Mtume  wakati wa maradhi yake. Na awaleta Hasan na Husein ......................... 123 Ufuasi wa Bilal kwa Ali ......................................................... 124 Huzuni ya Bilal kutokana na kifo cha Fatimah...................... 125 Habari njema kwa wenyekumlilia Mtukufu Mtume ............... 126 Bilal anapokea habari njema za wenyekuwapenda Ahlul-Bayt ............................................... 126 Mtukufu Mtume  anamtetea Bilal............................................ 128 Imam Ali  anamtetea Bilal................................................... 130 Imam as-Sadiq  anamtetea Bilal............................................. 131 FASLU YA SABA:.................................................................... 133 Kuanza kwa Adhana.................................................................... 133 Je Adhana ilianza baada ya Hijra kwa njia isiyokuwa wahyi?.... 133 Adhana ilianza kwa njia ya wahyi............................................... 142 Maimamu wa Ahlul-Bayt wanautetea wahyi katika Adhana....... 145 Adhana ilianza lini?..................................................................... 147 Wakati ilipoanzwa kutangazwa Adhana...................................... 149 vii

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 7

4/23/2016 2:45:49 PM


HUYU NDIYE BILAL

Bukhari na Muslim wamezipuuza Hadithi za ndoto.................... 150 Vipengele vya Adhana ya Bilal.................................................... 152 Adabu za Adhana ya Bilal na sifa zake........................................ 153 Tupe raha ewe Bilal..................................................................... 158 Adhana katika upande wake wa kisiasa na kiibada..................... 159 Adhana ya Bilal inawachukiza wanafiki na mushrikina.............. 160 FASLU YA NANE:................................................................... 162 Maandalizi na Safari.................................................................... 162 Aghani kwa kukumbuka mauti.................................................... 162 Katika ardhi ya maandalizi.......................................................... 164 Maneno mengine kuhusu kuhamia kwake Sham......................... 166 Hitimisho lisilo na mwisho.......................................................... 166 Kaburi lake ni kibla cha wenyekumzuru..................................... 168 KIAMBATISHO...................................................................... 170 Je Bilal alimrudisha Makkahh Mtukufu Mtume ?................... 170 Kisimamo kifupi katika kisa cha Bilal na Jamanah..................... 178

viii

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 8

4/23/2016 2:45:49 PM


HUYU NDIYE BILAL

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬

HADIYA

H

ii ni hadiya kwa Mrithi wa Manabii na Mitume… mwakilishi wa Mwenyezi Mungu ardhini……badiri itoayo nuru…. taa iangazayo…al-Hujah mwana wa Hasan, Imam Mahdi…sala za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na juu ya wahenga wake watoharifu. Naitoa roho yangu fidia kwake, nikitaraji mapokezi mema na uombezi kutoka kwake. Nabil.

1

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 1

4/23/2016 2:45:49 PM


HUYU NDIYE BILAL

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬

DIBAJI

K

itabu hiki ni toleo la Kiswahili la taasisi ya Al Itrah Foundation. Chapisho lake limelenga kukidhi mahitaji ya kiroho ya zama hizi pamoja na Ubongo na fikra zinazokuwa za Muislam. Jitihada kubwa zimefanywa na Taasisi kuweka chapisho hili la Kiswahili katika msingi wa haki na wenye kukubalika katika Uislam. Unaombwa kwa Taadhima ukisome kitabu hiki katika malengo yaliyokusudiwa. Pia Unaombwa kuwasilisha kwetu maoni yako huru juu ya chapisho letu hili, jambo ambalo tutashukuru sana. Kutangaza ujumbe wa Uislam ni kazi ambayo inahitaji ushirikiano wetu sote. Taasisi inakuomba kuungana na kushirikiana kama ilivyoagizwa katika aya ya Qur’an: (Surat Saba’ 34:46). Na rehma za Allah ziwe juu yako. Wako katika Uislam Al Itrah Foundation Barua Pepe: alitrah@yahoo.com SMS: +255 778 300 140

2

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 2

4/23/2016 2:45:49 PM


HUYU NDIYE BILAL

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬

NENO LA MCHAISHAJI

K

itabu ulichonacho mikononi mwako asili yake ni cha lugha ya Kiarabu kwa jina la, Hadha Huwa Bilal. Sisi tumekiita, Huyu Ndiye Bilal. Jina la Bilal ni maarufu sana katika historia ya Uislamu. Kwa mujibu wa kitabu hiki, Bilal alikuwa na asili ya Uafrika kutoka Uhabeshi (Ethiopia ya sasa), na alikuwa akiishi Uarabuni kama mtumwa. Bilal pamoja na kuwa yeye mtumwa alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kabisa kusilimu na kutokana na imani yake hiyo alipata mateso makubwa sana kutoka kwa bwana wake. Lakini hatimaye alikombolewa na kuungana Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) huko Madina alikohamia na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamfanya kuwa muadhini wake. Huu ni wasifu wa mtu mkubwa sana na maarufu katika Uislamu, hivyo, fuatana na mwandishi ili ujionee mwenyewe umaarufu wa bwana huyu Sahaba mtukufu wa Mtume (s.a.w.w.). Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa makubwa hususan wakati huu wa sayansi na tekinolojia kubwa ambapo ngano, hadithi za kale na upotoshaji wa historia ni vitu ambavyo havina nafasi kwa watu wa sasa. Taasisi yetu ya Al-Itrah imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili. Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni chenye manufaa makubwa kwao. 3

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 3

4/23/2016 2:45:49 PM


HUYU NDIYE BILAL

Tunamshukuru ndugu yetu al-Haj Ustadh Hemedi Lubumba kwa kufanikisha tarjuma ya kitabu hiki katika lugha ya Kiswahili, pia na wale wote waliosaidia kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Allah awalipe wote malipo mema hapa duniani na Akhera pia. Amin! Mchapishaji: Al-Itrah Foundation Dar es Salaam.

4

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 4

4/23/2016 2:45:50 PM


HUYU NDIYE BILAL

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬

UTANGULIZI Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

K

ila sifa njema ni ya Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu. Swala na salamu zimwendee Bwana wetu Muhammad, na ziwaendee Aali zake watoharifu. Bilal na uaminifu wa historia: Hakika historia yenyewe, ndio kikwazo kikubwa katika zoezi la ­kuzama katika historia na katika vipindi vya wakati uliopita ili kutafuta sura halisi ya mtu fulani. Hiyo ni kutokana na ugumu uliopo katika baadhi ya vipengele, au kukosekana na kutokuwepo viunganishi ­vyenye kuunganisha matukio yake na vipindi vyake, ili hatimaye, mwisho wa utafiti upatikane mwanzo na mwisho wa utu na historia yake. Kitabu kilichomo mikononi mwetu ni juhudi za kutaka kupanua wigo wa maarifa, pamoja na kuangazia na kutupia macho maeneo yaliyosahaulika na kupuuzwa katika sira ya Swahaba Mkubwa Bilal (ra), maeneo ambayo yamepuuzwa kutokana na mchoko wa utafiti au kutokana na makosa au sababu nyinginezo. Lakini kusimama katika historia yake ilikuwa kama makutano yenye furaha kutokana na majibu yaliyopatikana. Lakini pia ilikuwa ni kujaza ombwe na kujaribu kujibu majumui ya maswali yaliyosaidiana kuongeza kiwango cha dhulma aliyofanyiwa Bilal 5

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 5

4/23/2016 2:45:50 PM


HUYU NDIYE BILAL

katika moja ya pande za sira yake. Namaanisha katika yale yanayohusiana na mafungamano yake na watu wa nyumba ya Mtukufu Mtume F. Na la kuzingatia hapa ni kwamba, hakika jamii ya Bilal ilikuwa imejaa watu wazito na mabwana wa makabila, viongozi wa koo, matajiri na wenye ushawishi katika jamii. Na mara nyingi historia ilitua mizigo yake mbele ya hawa, na ikaweka darubini yake kwao, ikifuatilia nyenendo zao, ikizingatia kwamba wao ndio chanzo na ala ya matukio. Na Bilal si katika hawa (watu wazito), na wala huwezi kukuta mfanano baina yake na wao. Pamoja na hayo lakini hali hiyo haikuondoka bila kufuta utajo wao katika daftari la kumbukumbu, na wala haikuzuia mja huyo mwema kutoka Uhabeshi, kupanda juu katika kilele cha utukufu kwa imani yake, kujitokea kwake na kwa fadhila zake. Na hatimaye jina lake litaendelea kutamkwa katika kila kinywa na ulimi mpaka siku ya Kiyama. Na maana ya msimamo uliobebwa na utu wake itaendelea kuwa mfano wa kuigwa na kila muumini aliye huru. Kudumu kwake kunatosha kuwa dalili ya upekee wake. Uturi wa Bilal ni mali yetu: Ijapokuwa historia katika kuwasilisha sura kamili na sira ya Bilal haijakusanya taarifa za kutosha katika kiwango tulichotaraji, bali imepuuza, lakini hata hivyo imekuwa ni vigumu juu ya historia kutomtendea haki hata kidogo, kwa sababu taarifa tulizokusanya kutoka katika sira yake, na yale tuliyochuma kutoka katika bustani ya umri wake, ijapokuwa ni kiasi kidogo lakini yanatoa sura ya wazi inayojibu maswali mengi, na kuondoa utata mwingi, na yanafungua njia ya kufikia hitimisho la haki lenye kubeba sifa ya umakinifu katika maudhui. Kwani uturi mchache unaosambaa kutoka kwa muuza uturi hufichua sehemu kubwa ya uhalisia wake.

6

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 6

4/23/2016 2:45:50 PM


HUYU NDIYE BILAL

Ni kigezo chema cha pekee: Hakika utu wa Bilal ni utu wa pekee katika haki. Alimwandama Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 mpaka kufa kwake 4. Alichukua kutoka kwake masomo makubwa na akaishi pamoja naye katika matukio, vipindi na majaribu mbalimbali, hatimaye akatoka humo akiwa tajiri wa maadili na tabia, mkomavu wa imani na adabu. Kumzungumzia Bilal ni kumtweza kila mwenye kubeba fikra ya ubaguzi, fikra ambayo inatekelezwa kivitendo leo hii na majabari na majeuri ulimwenguni. Bila shaka wanafanya hivyo ili kuiimarisha fikra hiyo upya katika jamii zetu kwa malengo mabaya, na kwa uchache kabisa ni kwa lengo la kutufarakisha, kutugawa makundi na kutugombanisha. Na kwa neno jingine ni kwamba, Bilal anaweza kutengeneza mfano wa kuigwa kwa ajili ya vizazi vya Waislamu, katika kujituma, subira, elimu na kujinyima, kwani maisha yake ni zaidi ya maarifa tuliyoyazoea kumhusu yeye, yana kina cha mvuto, yanashtua na kustaajabisha zaidi. Na sina budi kuashiria kwamba, katika juhudi zetu za kutaka kuyafikia madhumuni kwa ukamilifu, hatukutumia zaidi mtindo wa maneno uliozoeleka. Kwa sababu ukweli wa mambo ni kwamba kinachotakiwa ni haki kujulikana kama ilivyo. Anachojali mwenye kiu ni maji na si birika tupu lisilo na maji, zuri lenye mapambo. Hivyo hata kama kuna sehemu tumeongeza ubainishaji wakati wa kuwasilisha na kufafanua, tumefanya hivyo si kwa lengo la kutafuta uzuri au kulazimisha mtazamo, bali ni katika jaribio la kutaka kupoza baadhi ya maneno makali yanayokuja kutoka katika jangwa hilo lenye kutisha.

7

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 7

4/23/2016 2:45:50 PM


HUYU NDIYE BILAL

FASLU ZA KITABU

K

atika kitabu hiki tumefaidika sana na vyanzo vya historia, vya Hadithi, vya Fiqhi, vya elimu ya wapokezi na vya elimu nyingine zinazotegemewa kwa Sunni na Shia. Na tumegawa yaliyomo katika kitabu hiki, katika faslu kadhaa ili kukamilisha uchunguzi katika pande zake mbalimbali, na ili kufungamanisha fikra katika namna ambayo itamrahisishia msomaji kufika katika lile analolitaka. Na hiyo ni kupitia mtindo ufuatao: Faslu ya Kwanza: Inawasilisha muhtasari wa utambulisho wa B ­ ilal, upande wa jina, nasaba, umbile na tabia. Faslu ya Pili: Inawasilisha safari yake ya kuelekea katika uongofu wake, na mateso aliyoyapata wakati wa kuelekea katika uhuru wake. Faslu ya Tatu: Inawasilisha mazungumzo kuhusu tabia ya mahusiano yake na Mtume wa Mwenyezi Mungu 4. Faslu ya Nne: Inawasilisha sira yake na jihadi yake, kuanzia pale alipoweza kulipiza kisasi huko Badri dhidi ya yule aliyekuwa akimtesa, mpaka siku ya ushindi wa Makkah, na hatimaye kutulia kwake katika nchi ya Sham. Faslu ya Tano: Inawasilisha baadhi ya mwanga utakaochangia kutambua maeneo muhimu ya utu wa Bilal (ra). Faslu ya Sita: Inawasilisha uhusiano na mapenzi yake kwa watu wa nyumba ya Mtume F. Na inaonesha majumui ya matukio yenye kubainisha kina cha mafungamano yake na wao F kidini, na jinsi wao walivyokuwa radhi naye. Faslu ya Saba: Inawasilisha ubainifu juu ya sharia ya Adhana na Iqamah. 8

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 8

4/23/2016 2:45:50 PM


HUYU NDIYE BILAL

Faslu ya Nane: Inawasilisha na kugusa mateso halisi yaliyompata Bilal baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu 4, na alivyojiandaa na kifo na kukutana na Mwenyezi Mungu. Na mwisho wa kitabu hiki tumeongeza baadhi ya mada na nukuu ambazo tumeona kwamba zinafaa kumfikia mpendwa msomaji, na ambazo kwa namna moja au nyingine zinaweza kufungamana na lengo la kitabu hiki. Na mwisho ni kwamba, sisi hatudai kuwa tumejumuisha kila kitu, lakini tunaitakidi kwamba, bila shaka tumewasilisha angalau kitu ambacho kinafaa kutiliwa umuhimu, katika yale yanayohusu maeneo mbalimbali ya sira ya Swahaba huyu mkubwa (ra).

9

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 9

4/23/2016 2:45:50 PM


HUYU NDIYE BILAL

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬

Faslu ya Kwanza TAARIFA BINAFSI Tutazungumzia: 1.

Jina lake na nasaba yake.

2.

Kuzaliwa kwake.

3.

Ndugu zake.

4.

Umbile lake.

5.

Tabia yake tukufu.

Nasaba yake na kuzaliwa kwake: Yeye ni Bilal Mhabeshi, mwadhini wa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4.1 Jina lake linapendwa na kila nafsi ya Mwislamu, linapotajwa tu, haraka sana kujitolea kwake, mateso yaliyompata na kutangulia kwake kutoa adhana, ni mambo ambayo humjia Mwislamu katika ubongo wake. Kuna wakati hutajwa kwa nasaba ya ubabani kwake, huitwa: Bilal bin Rabah. Na kuna wakati hutajwa kwa nasaba ya umamani kwake, huitwa: Bilal bin Hamamah. Mzazi wake wa kiume alikuwa ni Mhabeshi na mtumwa.2   Tahdhibul-Asmai Wa lughat, Juz. 1, uk. 136. Rijal Swahih Bukhar, Juz. 1, uk. 120. AlKamal Fii Asmair-Rijal, Juz. 4, uk. 288. 2   Ansabul-Ashraf, Juz. 1, uk. 136. Aayanus-Shiah, Juz. 3, uk. 605. Al-Kamil Fii Taarikh, Juz. 2, uk. 45. 1

10

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 10

4/23/2016 2:45:50 PM


HUYU NDIYE BILAL

Mama yake, Hamamah, huitwa pia kwa jina la Sukaina. Yeye alikuwa ni mtumwa wa mmoja kati ya watu wa ukoo wa Bani Jamhi. Kujitolea kwa familia hii hakukukomea kwa Bilal tu, bali kulimjumuisha hata mama yake ambaye aliteswa mateso makali kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kabla hajanunuliwa na kuachwa huru.3 Jina lake la ubaba: Anaitwa; Abu Abdul-Karim. Na pia huitwa Abu Amru. Na pia huitwa Abu Abdurahman.4 Historia haijakusanya taarifa za kutosha kuhusu maisha ya wazazi wake, bali imefupisha sira yao hadi kupelekea sehemu kubwa ya sira hiyo kutojulikana. Na hasa upande unaohusu utumwa wao na jinsi walivyofika katika Bara Arabu. Inasemekana kwamba: Wao walifika Bara Arabu na Jeshi la Abraha mwaka wa Tembo, ambapo walikuwa wanafanya kazi ya kupika chakula na kufunga mahema. Na kwamba walichukuliwa mateka Makkah baada ya jeshi hili kushindwa.5 Isipokuwa huu ni uwezekano tu, sisi hatujapata njia ya kuweza kuhakiki usahihi na kusihi kwa madai haya. Kuzaliwa kwake: Alizaliwa takriban miaka 43 kabla ya Mtume kuhamia Madina, hiyo ni kwa mujibu wa vyanzo vingi. Na imesemekana kinyume na hivyo, ijapokuwa kuna namna fulani ya mwafaka kwamba alizaliwa baina ya mwaka wa 42 na mwaka wa 50 kabla ya kuhama kwa Mtume 4.6   Ikhtiyar Maarifat Rijal, Juz. 1, uk. 989. Darajatur-Rafiah, uk. 362. Tahdhibul-Kamal, Juz. 4, uk. 288. Tabaqatul-Kubra cha Ibn Saad, Juz. 7, uk. 385. Ansabul-Ashraf Juz. 1, uk. 184. Siyaru Aalamin-Nubalai, Juz. 1, uk. 351. Tahdhibut-Tahdhib, Juz. 1, uk. 502. 4   Rijal Swahih Muslim, Juz. 1, uk. 95. Swahih Bukhar, Juz. 1, uk. 120. Majmauz-Zawaid, Juz. 9, uk. 300. Al-Istiiba, Juz. 1, uk. 141. Tanqihul-Maqal, Juz. 1, uk. 182. UsudulGhabah, Juz. 1, uk. 206 5   Simay Bilal Habashiy cha Kiajemi, uk. 33. Aayanus-Shiah, Juz. 14, uk. 152. 6   al-Bidayat Wanihayat, Juz. 7, uk. 102. Tahdhibut-Tahdhib, Juz. 1, uk. 503. Ansabul3

11

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 11

4/23/2016 2:45:50 PM


HUYU NDIYE BILAL

Dhuria wake: Maelezo ya kihistoria yametofautiana kuhusu dhuria wake, Ibn Athir katika kitabu chake cha historia, ametaja kwamba: “Mnamo mwaka 519 alifariki Hilal bin Abdurahman bin Sharih bin Ahmad, naye ni kutoka katika kizazi cha Bilal bin Rabah mwadhini wa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4.”7 Na katika kitabu as-Siratul-Halabiyyah imeandikwa: “Abu Yusuf wa madhehebu ya Shafi, aliamuru kuletwa mbele yake watoto wa Bilal na watoto wa waadhini wengine wa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4, akawauliza: Ni kwa njia ipi mlipokea Adhana na Iqamah kutoka kwa baba zenu?”8 Na wengine wametaja kuwa hakuwa na dhuria.9 Ndugu zake: Ana ndugu wa nasaba anayeitwa Khalid.10 Na huyu si yule Abu Ruwayha ambaye imetajwa kwamba, Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 aliunganisha udugu baina yake na Bilal. Na kauli ya kwamba Abu Ruwayha ni jina la ubaba la Khalid,11si kauli sahihi, na inapingana na maelezo kadhaa yanayojulisha kwamba ni ndugu yake katika imani. Na hebu tuashirie hapa maelezo yaliyokuja katika kitabu Usudul-Ghabah kutoka kwa Abu Dardai: Kwamba Umar bin Khattab alipoingia katika mji wa Jabiyah wakati wa kuikomboa Baytul-Maqdas, Bilal alimuomba amwache Sham, Ashraf, Juz. 1, uk. 193. Tahdhibu Taarikhu Damashqiy al-Kabir, Juz. 3, uk. 304. Tahdhibul-Asmai Walughat, Juz. 1, uk. 137. Aaayanus-Shiah, Juz. 3, uk. 601 – 602. 7   Al-Kamil Fii Taarikh, Juz. 8, uk. 319. 8   As-Siratul-Halabiyyah, Juz. 2, uk. 100. 9   Usudul-Ghabah, Juz. 1, uk. 209. Tahdhibu Taarikhu Damashqiy al-Kabir, Juz. 3, uk. 304. 10   Tahdhibul-Kamal, Juz. 4, uk. 290. Siyaru Aalamin-Nubalai, Juz. 1, uk. 351. UsudulGhabah, Juz. 1, uk. 290. Tahdhibut-Tahdhib, Juz. 1, uk. 502. Al-Istiaab, Juz. 1, uk. 142. 11   Al-Iswabah, Juz. 2, uk. 89. Tahdhibu Taarikhu Damashqiy al-Kabir, Juz. 5, uk. 35. 12

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 12

4/23/2016 2:45:50 PM


HUYU NDIYE BILAL

naye akakubali. Bilal akasema: “Na ndugu yangu Abu Ruwayha, ambaye Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 aliunga udugu baina yangu na yeye.” Umar akasema: “Sawa, na ndugu yako.”12 Kisha ni kwamba Abu Ruwayha huyu, kwa mujibu wa vyanzo vingi, jina lake ni Abdullah bin Abdurahman al-Khathaamiy.13 Hivyo inabainika kwamba Abu Ruwayha si Khalid, hivyo hilo si jina lake la ubaba. Bilal ana dada anayeitwa Ghufrah au Ufrah, au Ghufayrah.14 Naye alikuwa mtumwa wa Umar bin Abdullah.15 Na huenda alikuwa na ndugu wengine ukiacha hawa tuliowataja, lakini hazijatufikia habari zao. Umbile lake: Imepokewa kutoka kwa Makuhul kwamba alisema: Alinisimulia yule aliyewahi kumuona Bilal, kwamba alikuwa ni mtu mweusi sana, mwembamba mrefu, mwenye mgongo wa kupinda, mwenye nywele nyingi, mwenye mashavu membamba, mwenye nywele nyingi nyeupe zilizochanganyikana na nyeusi.16 Na imepokewa kwamba alikuwa mwenye sauti nzuri.17 Na ameeleza umbile lake yule aliyemuona wakati wa uzee wake kwam  Usudul-Ghabah, Juz. 1, uk. 208. Al-Swabah, Juz. 2, uk. 89, na Juz. 7, uk. 70.   Siratun-Nabawiyyah cha Ibn Hisham, Juz. 2, uk. 506. Ansabul-Ashraf, Juz. 1, uk. 192 – 193. Tabaqatul-Kubra cha Ibn Saad, Juz. 3, uk. 51 na 234. Al-Istiaab, Juz. 1, uk. 141. Aayanus-Shiah, Juz. 3, uk. 602. 14   Usudul-Ghabah, Juz. 1, uk. 209. Al-Istiaab, Juz. 1, uk. 141. Tahdhibul-Asmai Wa-lughat, Juz. 1, uk. 137. 15   Tahdhibul-Kamal, Juz. 4, uk. 290. Siyaru Aalamin-Nubalai, Juz. 1, uk. 351. UsudulGhabah, Juz. 1, uk. 209. Tahdhibul-Asmai Walughat, Juz. 1, uk. 137. Tahdhibut-Tahdhib, Juz. 1, uk. 502. 16   Tahdhibul-Asmai Walughat, Juz. 1, uk. 137. Ansabul-Ashraf, Juz. 1, uk. 193. UsudulGhabah, Juz. 1, uk. 209. Tabaqatul-Kubra cha Ibn Saad, Juz. 3, Uk. 238 – 239. AayanusShiah, Juz. 2, Uk. 602. 17   Al-Bidayat Wan-Nihayat, Juz. 7, uk. 102. 12 13

13

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 13

4/23/2016 2:45:50 PM


HUYU NDIYE BILAL

ba: Alikuwa ni mzee mrefu, mweusi sana, weusi wa kung’aa, mwenye nywele na ndevu nyeupe. Alikuwa na nguo mbili, moja nyeusi na nyingine nyeupe.18 Tabia zake tukufu: Bilal alijifundisha masomo mengi kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4, katika sifa, mwenendo na tabia. Jambo ambalo lilitengeneza kwake hali ya uwelewa kamili juu ya Uislamu, mambo yake na vipengele vyake, hasa vile vinavyohusu malezi ya nafsi ya mwanadamu. Hivyo misimamo yake na maneno yake vilikuwa ni muhtasari wa maarifa haya aliyoyachukua kutoka kwa Nabii wake. Maneno ya sifa aliyokuwa akisifiwa kutokana na ubora wake, wala kheri aliyopewa kutokana na kuwa karibu na Mtume wa Mwenyezi Mungu 4, vyote hivi havikubadili chochote katika matendo yake, wala havikudhihirisha kutoka kwake aina yoyote ya kujiona, kujisikia, maringo na kujihisi yeye ni bora, bali hata hakuonekana ni mwenye kufurahishwa na kusifiwa huko. Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alituliza woga wa yule aliyepatwa na woga kutokana na haiba yake 4, akamwambia: “Mimi si chochote bali ni mtoto wa mwanamke aliyekuwa akila chakula huko Makkah.” Na huyu ndiye Bilal aliyekunywa kutoka katika chemchemu tamu ya Mtume wa Mwenyezi Mungu 4, anawajibu wale waliokuwa wakienda kwake na kutaja fadhila zake na kheri aliyogaiwa na Mwenyezi Mungu, anawaambia: “Mimi si chochote bali ni Mhabeshi ambaye jana tu nilikuwa mtumwa…”19 Ijapokuwa kwa upande mmoja yeye anaonesha unyenyekevu uliyomo ndani ya nafsi yake, na anawakumbusha wenye kumsifu, ile 18 19

Amaliy cha Swaduq, Majlisi ya 38, uk. 175.   Tahdhibu Taarikhu Damashqiy al-Kabir, Juz. 3, uk. 318. Tabaqatul-Kubra cha Ibn Saad, Juz. 3, uk. 238. Ansabul-Ashraf, Juz. 1, uk. 190. 14

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 14

4/23/2016 2:45:50 PM


HUYU NDIYE BILAL

historia yake ambayo haimpi nafasi ya kujifakharisha na kujigamba, lakini kwa upande mwingine anawasilisha ujumbe wa thamani ya juu, wenye kufichua mbele ya wale wenye kumsifu, kwamba ni Uislamu pekee ndio uliomhamisha Bilal kutoka katika historia hiyo na sifa hizo, mpaka katika hali hii ya sasa aliyonayo kwa sifa zake zote.

15

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 15

4/23/2016 2:45:50 PM


HUYU NDIYE BILAL

Faslu ya Pili KUSILIMU KWAKE NA KUTESWA KWAKE Tutazungumzia: 1.

Kusilimu kwake na mateso aliyoyapata.

2.

Aya zilizoteremka kumhusu yeye.

3.

Kukombolewa kwake na kuachwa huru.

Kusilimu kwake na mateso aliyoyapata: Aliingia katika Uislamu mwanzoni mwa daawa, pamoja na kundi dogo la waliotangulia kuingia katika Uislamu:20 Ammar, Yasir, Sumaiyyah, Mikidad, Hamamah mama yake na Bilal……ambao walidhoofishwa na mabeberu wa sharki wa Makkah. Ambao waliwafanyia uadui kwa kuwatesa kwa kila aina ya mateso ili wawazuie kuendelea na dini. Hivyo kila kabila likawakamata Waislamu waliyomo ndani ya kabila lao, wakawachukua na kuwavisha minyororo ya chuma na kuwaunguza kwa jua. Na wakawa wanawatesa kwa kuwapiga, na kwa njaa na kiu. Umayya bin Khalaf, baada ya kumwacha Bilal na njaa na kiu kwa muda wa siku nzima kutwa kucha, alikuwa akimtoa wakati wa 20

Baadhi ya maelezo yametaja kuwa aliingia katika Uislamu baada ya Ali, Khadija, na Zaydi bin Harith. Na katika maelezo mengine imetajwa kinyume na hivyo. Rejea Biharul-An’war, Juz. 18, uk. 228. 16

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 16

4/23/2016 2:45:50 PM


HUYU NDIYE BILAL

adhuhuri ya jua kali, na kwenda kumlaza chali juu ya mchanga wenye moto ambao kama kipande cha nyama kitawekwa juu yake basi kitawiva. Kisha anaamuru kuletwa jiwe kubwa na kuliweka juu ya kifua chake, kisha anamwambia: “Utaendelea kuteseka hivyo mpaka ufe au umkane Muhammad na uabudu Lata na Uza.” Lakini Bilal alikuwa akikataa kumpa anachotaka, na alikuwa akisema: “Ahadun, Ahadun (Mungu Mmoja wa pekee, Mungu Mmoja wa pekee).” Na alikuwa akiwapa changamoto wenye kumwadhibu kwa kuwaambia: “Wallahi laiti ningekuwa ninalijua neno lenye kuwachukiza zaidi kuliko hili, basi ningelisema.” Yeye ni mtu huru ambaye hadhoofishwi na misukosuko. Na yeye ni mwenye imani thabiti ambaye mijeledi haimpokonyi imani yake. Hivyo utamuona akidharau ujabari wao na ujeuri wao na akikataa kuwapa hata chembe ya imani yake, hata kama anakaribia kifo. Bali anawapa changamoto na kupambana nao katika imani yake, jambo ambalo haliwazidishii isipokuwa hasira, nao wanaongeza na kupanua mateso yao juu yake, mpaka wakamvisha kitanzi shingoni kisha wakawaamuru vijana wao wamburuze kwa kuzunguka naye katika mitaa ya Makkah. Lakini yeye hakuacha kusema: “Ahadun, Ahadun (Mungu mmoja wa pekee, Mungu mmoja wa pekee).”21 Nao ni msimamo imara na mkali ambao uliyashinda malengo ya Mushrikina, na hivyo hata kama waliweza kuuteka mwili wake na kuufunga kwa minyororo isipokuwa ni kwamba wao hawakuweza kuteka roho yake. Na hata kama mijeledi iliweza kuchukua nyama yake na damu yake, lakini ilishindwa kuchukua uimara wa imani yake, au kusambaratisha subira na uthabiti wake. 21

Siratun-Nabawiyyah cha Ibn Hisham, Juz. 1, uk. 317 – 318. Siratul-Halabiyyah, Juz. 1, uk. 299 – 300. Siyaru Aalamin-Nubalai, Juz. 1, uk. 347 na 348. Usudul-Ghabah, Juz. 1, uk. 209. Ansabul-Ashraf, Juz. 1, uk. 184 na 185. Tabaqatul-Kubra cha Ibn Saad, Juz. 3, uk. 232 na 233. Tanqihul-Maqal,, Juz. 1, uk. 182. 17

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 17

4/23/2016 2:45:50 PM


HUYU NDIYE BILAL

Walikusudia kuzima sauti yake kwa anuai mbalimbali za adhabu, lakini mara wito wake umefika kila sehemu na kila zama, unazitikisa dhamira zilizo hai, na kwa wito huo wanaongoka wale wenye itikadi safi, na kwa wito huo wanachukua azma na msimamo mbele ya majabari wapetuka mipaka. Imebaki kuashiria kwamba, nukuu zinazohusu kusilimu kwake na kuteswa kwake ni nyingi, nazo katika maeneo mengi zinakaribiana upande wa madhumuni, licha ya kuwepo tofauti katika baadhi ya maeneo. Miongoni mwazo ni ile iliyokuja katika kitabu as-Siratul-Halabiyyah, ambapo anasema: “Bilal alikuwa ni mtoto wa kulea wa Abdullah bin Jadian, alikuwa ni miongoni mwa watoto waliolelewa Makkah, na alikuwa ni miongoni mwa watumwa wake mia moja wa kulea. Mwenyezi Mungu alipomleta Nabii wake 4, Abdullah aliwaamuru watoke Makkah, akikhofia kwamba wasije wakaingia katika Uislamu. Nao wakatoka isipokuwa Bilal. Yeye alikuwa akichunga kondoo wake, hivyo Bilal alisilimu na akaficha Uislamu wake. Siku moja Bilal akayamwagia uchafu masanamu yaliyokuwa yameizunguka Kaaba. Na inasemekana kuwa alikuwa akiyatemea mate huku akisema: ‘Ameshindwa na kupata hasara yule mwenye kukuabuduni.’ Makuraishi wakagundua, wakamshitaki kwa Abdullah. “Wakamwambia Abdullah: ‘Umegeuka mtoto?’ Akawaambia: ‘Mtu mfano wangu mnaweza kuniambia hivyo?’ Wakasema: ‘Hakika mtumwa wako mweusi amefanya hivi na vile…’ basi akawapa ngamia mia moja wazichinje kwa ajili ya masanamu, na akawakabidhi Bilal hivyo wakawa wanamtesa… Na inawezekana ikawa Abdullah bin Jadian alimmilikisha Umayya bin Khalaf baada ya tukio hilo, kwani Umayya bin Khalaf ndiye aliyekuwa akimwadhibu Bilal…”22 22

Siratul-Halabiyyah, Juz. 1, Uk. 298. Siratun-Nabawiyyah Wal-Athar al-Muhammadiyyah, Juz. 1, Uk. 240. 18

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 18

4/23/2016 2:45:50 PM


HUYU NDIYE BILAL

Aya zilizoteremka kumhusu yeye: Aya za Qur’ani zilizoteremka kumhusu Bilal na kumgusia yeye, zimemzidishia na kumwongezea nafasi, upendo na heshima katika nafsi za Waislamu. Na bila shaka huu ni ukarimu na neema ya Mungu, ambaye anaashiria utukufu wa imani yake na kusilimu kwake kwa moyo mmoja, na kwa ukarimu huo Bilal anapata yenye kupendwa na nafsi yake, yenye kuponya majeraha yake na kutuliza maumivu yake, na yenye kumpa pole kutokana na mateso na adhabu alizopata. Miongoni mwa matukufu makubwa aliyoyapata Bilal, ni kwamba Mwenyezi Mungu alimtazama na akateremsha Aya mbalimbali katika moyo wa Nabii Wake 4, Aya ambazo zimeubakisha na kuufanya msimamo wake udumu na kuendelea katika muda wote wa historia, na zimeufanya kuwa somo kwa mataifa na vizazi vingine. Na hapa tunataja sehemu ya Aya zilizopokewa kumhusu yeye: 1.

Siku moja Mtukufu Mtume 4 alikuwa ameketi pamoja na Bilal, Salman, Shuaybu, Ammar na wanyonge na mafakiri wengine. Mara likaingia kundi miongoni mwa Mushrikina, wakamwambia Mtukufu Mtume 4: “Kama watajitenga na wewe hawa, watakujia mabwana wa kaumu yako na watasilimu.” Maneno hayo yalikuwa ni hadaa yao dhidi ya Mtume, na Mwenyezi Mungu alikuwa anajua siri na undani wao. Na hakika wao walilenga kwa maneno hayo kuwadharau. Ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha juu ya Nabii Wake:

ْ ‫ك َعلَ ْي ِه ْم ِم ْن َش ْي ٍء فَت‬ ‫َط ُر َدهُ ْم‬ َ ِ‫ك ِم ْن ِح َسابِ ِه ْم ِم ْن َش ْي ٍء َو َما ِم ْن ِح َساب‬ َ ‫َما َعلَ ْي‬ َ‫فَتَ ُكونَ ِمنَ الظَّالِ ِمين‬

19

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 19

4/23/2016 2:45:50 PM


HUYU NDIYE BILAL

“Wala usiwafukuze wale wanaomwomba Mola Wao asubuhi na jioni kwa kutaka radhi Yake; si juu yako hisabu yao hata kidogo, wala hisabu yako si juu yao hata kidogo, kwamba uwafukuze na uwe miongoni mwa madhalimu.”23

2.

Imepokewa kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu:

َ‫ك َم َع الَّ ِذينَ أَ ْن َع َم للاهَّ ُ َعلَ ْي ِه ْم ِمنَ النَّبِيِّين‬ َ ِ‫َو َم ْن ي ُِط ِع للاهَّ َ َوال َّرسُو َل فَأُو ٰلَئ‬ ‫ك َرفِيقًا‬ َ ِ‫َوالصِّ دِّيقِينَ َوال ُّشهَدَا ِء َوالصَّالِ ِحينَ ۚ َو َحسُنَ أُو ٰلَئ‬ “Na wenye kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume, basi hao (watakuwa) pamoja na wale aliowaneemesha Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii na wasadikishaji na mashahidi na watu wema. Na hao ndio marafiki wema.”24 Kwamba mashahidi ni Ali, Ja’far, Hamza, Hasan na Husein F, hawa ndio mabwana wa mashahidi. Na watu wema ni Salman, Abu Dhari, Mikidad, Ammar, Bilal na Khabab.25

3.

Kutoka kwa Ibn Abbas, amesema: “Bilal, Khabab, Abis, Ammar na marafiki zao, waliteswa mpaka wakasema baadhi ya yale waliyoyataka Mushrikina. Kisha wakaachiwa, na ni kwao wao iliteremka Aya hii:

‫َوالَّ ِذينَ هَا َجرُوا فِي للاهَّ ِ ِم ْن بَ ْع ِد َما ظُلِ ُموا لَنُبَ ِّوئَنَّهُ ْم فِي ال ُّد ْنيَا َح َسنَةً ۖ َو أَلَجْ ُر‬ َ‫آْال ِخ َر ِة أَ ْكبَ ُر ۚ لَوْ َكانُوا يَ ْعلَ ُمون‬ ‘Na wale waliohama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu baada ya kudhulumiwa, hakika tutawaweka katika dunia kwa wema. Na ujira wa Akhera ni mkubwa zaidi, lau wangelikuwa wanajua.’” (Sura Nahli; 16:41).   Sura Al-An’am: 52. Tafsir Tabariy, Juz. 7, uk. 128. Al-Mizan, Juz. 7, uk. 109. Tafsir Ibn Kathir, Juz. 2, uk. 134. Tibyan cha Tusi, Juz. 4, uk. 143. 24   Sura Nisai: 69. 25   Safinatul-Bihar, Juz. 1, uk. 104 na 105. Biharul-An’war, Juz. 9, uk. 74. 23

20

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 20

4/23/2016 2:45:50 PM


HUYU NDIYE BILAL

4.

Ibn Asakir amesema:26 Aya hizi ziliteremka kuwahusu Bilal, Suhaybu, Khabab na wengine miongoni mwa wanyonge: “Wala usiwafukuze wale wanaomwomba Mola Wao asubuhi na jioni kwa kutaka radhi Yake; si juu yako hisabu yao hata kidogo, wala hisabu yako si juu yao hata kidogo, kwamba uwafukuze na uwe miongoni mwa madhalimu.”27 Na

‫َب َربُّ ُك ْم َعلَ ٰى نَ ْف ِس ِه‬ َ ‫َوإِ َذا َجا َء‬ َ ‫ك الَّ ِذينَ ي ُْؤ ِمنُونَ بِآيَاتِنَا فَقُلْ َسلاَ ٌم َعلَ ْي ُك ْم ۖ َكت‬ ‫َاب ِم ْن بَ ْع ِد ِه َوأَصْ لَ َح فَأَنَّهُ َغفُو ٌر‬ َ ‫الرَّحْ َمةَ ۖ أَنَّهُ َم ْن َع ِم َل ِم ْن ُك ْم سُو ًءا بِ َجهَالَ ٍة ثُ َّم ت‬ ‫َر ِحي ٌم‬

“Na wanapokufikia wale wanaoamini Ishara Zetu waambie: Amani iwe juu yenu (Assalam alaykum), Mola Wenu amejilazimisha rehema; ya kwamba atakayefanya miongoni mwenu uovu kwa ujinga, kisha akatubu baada yake na akatengenea, basi Yeye ndiye Mwingi wa maghufira Mwenye kurehemu.” (Sura al-An’am; 6:54).

Na

‫ك َم َع الَّ ِذينَ يَ ْد ُعونَ َربَّهُ ْم بِ ْال َغدَا ِة َو ْال َع ِش ِّي ي ُِري ُدونَ َوجْ هَهُ ۖ َو اَل تَ ْع ُد‬ َ ‫َواصْ بِرْ نَ ْف َس‬ ‫ك َع ْنهُ ْم تُ ِري ُد ِزينَةَ ْال َحيَا ِة ال ُّد ْنيَا ۖ َو اَل تُ ِط ْع َم ْن أَ ْغفَ ْلنَا قَ ْلبَهُ ع َْن ِذ ْك ِرنَا َواتَّبَ َع‬ َ ‫َع ْينَا‬ ‫هَ َواهُ َو َكانَ أَ ْم ُرهُ فُ ُرطًا‬ “Na isubirishe nafsi yako pamoja na wanaomuomba Mola Wao asubuhi na jioni, wakitaka radhi Yake; wala macho yako yasiwaruke kwa kutaka mapambo ya maisha ya dunia; wala usimtii tuliyemghafilisha moyo wake asitukumbuke na akafuata matamanio yake na mambo yake yakawa yamepita kiasi.” (Sura Kahfi; 18:28).   Tahdhibu Taarikhu Damashqiy al-Kabir, Juz. 3, uk. 308.   Sura al-An’am: 52.

26 27

21

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 21

4/23/2016 2:45:50 PM


HUYU NDIYE BILAL

Na Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alipokuwa akiketi msikitini walikuwa wakiketi mbele yake wanyonge miongoni mwa Maswahaba zake: Ammar, Suhaybu, Bilal, Abu Fakiha, Amir bin Fuhayrah na mfano wao miongoni mwa Waislamu. Makuraishi wakawa wanaambizana wao kwa wao: Hawa ndio wanaoketi naye kama mnavyowaona. Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu amewafadhili miongoni mwetu. Mwenyezi Mungu akateremsha:

َ ِ‫َو َك ٰ َذل‬ ُ َّ‫ْس للاه‬ َ ‫ْض لِيَقُولُوا أَ ٰهَ ُؤ اَل ِء َم َّن للاهَّ ُ َعلَ ْي ِه ْم ِم ْن بَ ْينِنَا ۗ أَلَي‬ َ ‫ك فَتَنَّا بَ ْع‬ ٍ ‫ضهُ ْم بِبَع‬ َ‫بِأ َ ْعلَ َم بِال َّشا ِك ِرين‬ “Na namna hii tumewajaribu wao kwa wao ili waseme: Je, hao ndio ambao Mwenyezi Mungu amewafadhili miongoni mwetu? Kwani Mwenyezi Mungu hawajui wanaoshukuru?” (Sura al-An’am; 6:53).

Na akateremsha kuwahusu wao:

‫َوالَّ ِذينَ هَا َجرُوا فِي للاهَّ ِ ِم ْن بَ ْع ِد َما ظُلِ ُموا لَنُبَ ِّوئَنَّهُ ْم فِي ال ُّد ْنيَا َح َسنَةً ۖ َو أَلَجْ ُر‬ َ‫آْال ِخ َر ِة أَ ْكبَ ُر ۚ لَوْ َكانُوا يَ ْعلَ ُمون‬ “Na wale waliohama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu baada ya kudhulumiwa, hakika tutawaweka katika dunia kwa wema. Na ujira wa Akhera ni mkubwa zaidi, lau wangelikuwa wanajua.” (Sura Nahli; 16:41).

Na pia akateremsha kuwahusu wao:

‫ك‬ َ َّ‫ك َوأَصْ لَحُوا إِ َّن َرب‬ َ ِ‫ك لِلَّ ِذينَ َع ِملُوا السُّو َء بِ َجهَالَ ٍة ثُ َّم تَابُوا ِم ْن بَ ْع ِد ٰ َذل‬ َ َّ‫ثُ َّم إِ َّن َرب‬ ‫ِم ْن بَ ْع ِدهَا لَ َغفُو ٌر َر ِحي ٌم‬ 22

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 22

4/23/2016 2:45:50 PM


HUYU NDIYE BILAL

“Kisha hakika Mola Wako kwa waliotenda uovu kwa ujinga kisha wakatubu baada ya hayo na wakatengenea, hakika Mola Wako ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.” (Sura Nahli; 16:119).

5.

Kutoka kwa Mujahid kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu: “Watasema: Mbona hatuwaoni wale watu ambao tukiwahesabu ni katika waovu? Je, tuliwafanyia maskhara, au macho yamewakosa?”28 Amesema: “Abu Jahli atasema: ‘Yuko wapi Bilal? Yuko wapi fulani na fulani? Tulikuwa tukiwahesabu duniani kuwa ni katika waovu, mbona hatuwaoni motoni. Au wao wako katika sehemu ambayo hatuwezi kuwaona. Au wako motoni lakini hatuoni sehemu yao?”’29

6.

Kutoka kwa Muhammad bin Umar, amesema: Alinisimulia Uthman bin Muhammad, kutoka kwa Abdul-Hakim bin Suhaybu, kutoka kwa Umar bin al-Hakam, alisema: Ammar bin Yasir alikuwa akiadhibiwa mpaka anashindwa kutambua ayasemayo. Na Suhaybu alikuwa akiadhibiwa mpaka anashindwa kutambua ayasemayo. Na Abu Fakiha alikuwa akiadhibiwa mpaka anashindwa kutambua ayasemayo. Na pia Bilal, Amir bin Fuhayrah na watu wengine miongoni mwa Waislamu. Na ni kuwahusu wao iliteremka Aya hii: “Kisha hakika Mola Wako kwa waliotenda uovu kwa ujinga kisha wakatubu baada ya hayo na wakatengenea, hakika Mola Wako ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.”30

7.

Kutoka kwa Ibn Abbas, amesema: “Bilal, Khabab, Abis, Ammar na marafiki zao, waliteswa mpaka wakasema baadhi ya yale

Sura Swad: 62 – 63.   Tafsirul-Qurtubiy, Juz. 16, uk. 432. Tafsir al-Baydhawiy, Juz. 1, uk. 380. Tafsir Zamakhshariy, Juz. 1, uk. 453. Ansabul-Ashraf, Juz. 1, uk. 187. Tafsir Ibn Kathir, Juz. 2, uk. 134. Tafsir Shawkaniy, Juz. 2, uk. 115. 30   Sura Nahli: 119.Tabaqatul-Kubra, Juz. 4, uk. 248. 28 29

23

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 23

4/23/2016 2:45:50 PM


HUYU NDIYE BILAL

waliyoyataka Mushrikina. Kisha wakaachiwa, na ni kwao wao iliteremka Aya hii: ‘Na wale waliohama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu baada ya kudhulumiwa, hakika tutawaweka katika dunia kwa wema. Na ujira wa Akhera ni mkubwa zaidi, lau wangelikuwa wanajua.’”31 8.

31 32

Katika kitabu Ansabul-Ashraf imeandikwa kwamba: Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alipokuwa akiketi msikitini walikuwa wakiketi mbele yake wanyonge miongoni mwa Maswaha zake: Ammar, Suhaybu, Bilal, Abu Fakiha, Amir bin Fuhayrah na mfano wao miongoni mwa Waislamu. Makuraishi wakawa wanaambizana wao kwa wao: Hawa ndio wanaoketi naye kama mnavyowaona. Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu amewafadhili miongoni mwetu. Mwenyezi Mungu akateremsha: “Na namna hii tumewajaribu wao kwa wao ili waseme: Je, hao ndio ambao Mwenyezi Mungu amewafadhili miongoni mwetu? Kwani Mwenyezi Mungu hawajui wanaoshukuru?” Na akateremsha kuwahusu wao: “Wala usiwafukuze wale wanaomwomba Mola Wao asubuhi na jioni kwa kutaka radhi Yake; si juu yako hesabu yao hata kidogo, wala hesabu yako si juu yao hata kidogo, kwamba uwafukuze na uwe miongoni mwa madhalimu.” Na pia akateremsha kuwahusu wao: “Na wale waliohama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu baada ya kudhulumiwa, hakika tutawaweka katika dunia kwa wema. Na ujira wa Akhera ni mkubwa zaidi, lau wangelikuwa wanajua.” Na pia akateremsha kuwahusu wao: “Kisha hakika Mola Wako kwa waliotenda uovu kwa ujinga kisha wakatubu baada ya hayo na wakatengenea, hakika Mola Wako ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.”32

Swafayni, uk. 325.   Ansabul-Ashraf, Juz. 1, uk. 198. 24

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 24

4/23/2016 2:45:51 PM


HUYU NDIYE BILAL

Kukombolewa kwake na kuachwa huru: Mtukufu Mtume 4 alijali na kutilia umuhimu mambo ya wenye kuadhibiwa na kuteswa. Hivyo alijituma na kufanya juhudi kuhakikisha kwamba anawaokoa na kuwakomboa kutoka katika utumwa wao na kutoka katika mateso na adhabu wanazozipata. Na alionesha umuhimu mahususi kwa kumkomboa Bilal kama ilivyopokewa katika baadhi ya riwaya. Ambapo aliwataka baadhi ya Waislamu wamnunue kwa kusema: “Kama ningekuwa na chochote basi ningemnunua Bilal.”33 Bali tunakuta zaidi ya hilo kwamba, yeye mwenyewe Mtukufu Mtume 4 ndiye aliyempa uhuru wake. Al-Iskafiy amesema: “Ama Bilal na Amir bin Fuhayrah, hawa walipewa uhuru na yeye mwenyewe Mtukufu Mtume 4. Amepokea hilo al-Waqidiy na Ibn Is’haqa.”34 Na kuna tofauti kubwa katika nukuu kuhusu namna alivyoachiwa huru na kukombolewa, na kuhusu aliyemnunua, na thamani iliyotolewa.35 Imepokewa kwamba Abbas bin Abdul-Muttalib ndiye aliyemnunua.36 Pia imepokewa kwamba Abu Bakr ndiye aliyemnunua na kumwacha huru.37 Vyovyote iwavyo ni kwamba fadhila za kukombolewa kwake na kuachwa huru zinarejea kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4,38 sawa iwe ni yeye mwenyewe ndiye aliyemkomboa na kumwacha   Usudul-Ghabah, Juz. 1, uk. 207. Siyar Aalamun-Nubalai, Juz. 1, uk. 352.   Siratun-Nabawiyyah Wal-Athar al-Muhammadiyyah, Juz. 1, uk. 243. 35   Tahdhibu Taarikhu Damashqiy al-Kabir, Juz. 3, uk. 307. Siyaru Aalamin-Nubalai, Juz. 1, uk. 352. Taarikhul-Khamis, Juz. 2, uk. 245. Usudul-Ghabah, Juz. 1, uk. 206. SiratulHalabiyyah, Juz. 1, uk. 298. 36   Usudul-Ghabah, Juz. 1, uk. 207. Siyaru Aalamin-Nubalai, Juz. 1, uk. 352. Al-Istiaab, Juz. 1, uk. 143. 37   Siratun-Nabawiyyah Wal-Athar al-Muhammadiyyah, Juz. 1, uk. 243. 38   Tahdhibu Taarikhu Damashqiy al-Kabir, Juz. 3, uk. 307. Siyaru Aalamin-Nubalai, Juz. 1, uk. 352. Taarikhul-Khamis, Juz. 2, uk. 245. Usudul-Ghabah, Juz. 1, uk. 206. SiratulHalabiyyah, Juz. 1, uk. 298. 33 34

25

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 25

4/23/2016 2:45:51 PM


HUYU NDIYE BILAL

huru, au iwe aliagiza hilo. Na ni kuanzia hapa ndipo akahesabiwa miongoni mwa huria wa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4,39 na ni kwa jina hilo alikuwa akitambulika na kunasibishwa. Na miongoni mwa dalili juu ya hilo ni Hadithi ya adhana, kwamba mpokezi wa Hadithi hiyo aliulizia habari za Bilal na hakuwa anajua jina lake, watu wakamjibu: Huyu ni Bilal, huria wa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4.40

39 40

Al-Manaqib, Juz. 1, uk. 1715.   Qamusir-Rijal, Juz. 2, uk. 237. Tanqihul-Maqal, Juz. 1, uk. 182. Biharul-An’war, Juz. 81, uk. 123. 26

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 26

4/23/2016 2:45:51 PM


HUYU NDIYE BILAL

Faslu ya Tatu SWAHABA MWEMA Tutazungumzia: 1.

Ukaribu wake na Mtume wa Mwenyezi Mungu 4.

2.

Alikuwa miongoni mwa watu wa mwanzo kumhudumia Mtukufu Mtume 4.

3.

Alikuwa mhazini wa Mtukufu Mtume 4.

4.

Bilal akiwa kati ya utiifu na mapenzi.

5.

Anatangaza sharia na maamrisho ya Mtukufu Mtume 4.

6.

Alikuwa ni mmoja kati ya wateule wa Mtukufu Mtume 4.

7.

Labayka.

8.

Mwadhini wa Mtukufu Mtume 4, Bilal, katika Hadithi za Mtukufu Mtume.

9.

Hadithi ya Mtukufu Mtume 4 kuhusu riziki ya Bilal.

10. Usia wa Mtukufu Mtume 4 kwa Bilal. 11. Ni mpokezi wa Hadithi za Mtukufu Mtume 4. 12. Nafasi ya Bilal katika kisa cha kupumzika usiku safarini. 13. Adhama nyingine ya Adhana ya Bilal. 27

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 27

4/23/2016 2:45:51 PM


HUYU NDIYE BILAL

Ukaribu wake na Mtume wa Mwenyezi Mungu 4: Mara tu alipomjua Mtume wa Mwenyezi Mungu 4, Bilal alipata hadhi ya kumtilia umuhimu na kuwa karibu naye. Na Mtume 4 alikuwa akimtafuta yeye mwenyewe na kuketi pamoja naye na kuzungumza naye. Alikuwa akimlinda na kuandamana naye nyumbani na safarini, na akimtegemea katika mambo mengi. Historia imetunukulia ushahidi mwingi, na nukuu nyingi kuhusu undani wa maisha yake na kusuhubiana kwake na Mtukufu Mtume 4, sisi tutataja zile zilizo maarufu zaidi. Nukuu hizo zinatoa kielelezo cha wazi juu ya uhusiano wake na ukaribu wake na Mtukufu Mtume 4. Na yeye ndiye aliyemfanya ndugu yake katika maisha yake nyumbani na safarini.41 Na alikuwa karibu naye katika hatua na vipindi vyote, kuanzia mwanzo wa daawa yake mpaka kufa kwake 4. Yaani kipindi cha zaidi ya miongo miwili. Navyo ni vipindi ambavyo vilishuhudia mazingira tofauti na changamoto ngumu katika historia ya kulingania Uislamu, na katika historia ya Dola ya Kiislamu. Ambapo ni pamoja na mazingira magumu ya vikwazo, vita na mashambulizi ya kijeshi yaliyojitokeza kabla, wakati na baada ya dola hiyo. Pia ni pamoja na matukio yote yaliyoandamana na vipindi hivyo katika viwango mbalimbali vya kisiasa, kijamii, kiuchumi na vinginevyo. Na kupitia matukio dhahiri ya vipindi hivyo vigumu, na pia kupitia maelezo yaliyowasilishwa na nukuu za kihistoria, tunaweza kuipata tabia halisi ya mafungamano na mahusiano imara ya kiroho ya Bilal kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4. Na yeye ndiye aliyeishi katika ulinzi wa Mtukufu Mtume 4, na akapata heshima ya kuwa mhudumu wake 4. Na akajua mengi kutoka katika vipengele na matukio ya maisha yake 4, na akasikia kutoka kwake baadhi ya yale yenye kufungamana na mustakabali wa dini hii. 41  Rejea Usudul-Ghabah, Juz. 1, uk. 207. 28

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 28

4/23/2016 2:45:51 PM


HUYU NDIYE BILAL

Imepokewa kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alimwambia Bilal: “Niwapeni habari njema?” Wakasema: Ndiyo, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Wakati huo walikuwa wanatembea safarini. Mtume akasema: “Hakika Mwenyezi Mungu amenipa mamlaka mbili: Urumi na Uajemi…”42 Alikuwa miongoni mwa watu wa mwanzo kumhudumia Mtukufu Mtume 4: Mtukufu Mtume 4 alimbakisha Bilal karibu yake na karibu na nyumba yake. Alikuwa miongoni mwa wale aliowateua kwa ajili ya mambo yake mahususi, msaidizi wake katika majukumu na mambo mbalimbali. Na kwa sababu hiyo alipata fursa ya kuwa miongoni mwa wenye kujitolea katika kutekeleza mahitaji ya Mtume 4. Mtume alikuwa anapouliza: “Yuko wapi Bilal?” Haraka alikuwa akijibu: “Labayka niko hapa kwa ajili yako.”43 Na ushahidi juu ya hilo ni mwingi, nasi hapa tunataja sehemu tu ya ushahidi huo: 1.

Katika Swala ya Iddi na katika Swala ya Istiskaa alikuwa akimbebea Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 fimbo yake na kuisimika pale patakaposwaliwa Swala husika.44

2.

Wakati Mtukufu Mtume alipokuwa anatoka kwenda kupambana na Mayahudi wa Bani Nadhir, alimwamuru Bilal kufunga hema.45

3.

Alisuhubiana na Mtukufu Mtume 4 nyumbani na safarini, na alikuwa akimtengenezea kivuli kwa nguo yake licha ya kutoombwa kufanya hivyo na Mtukufu Mtume 4. Na wanapoku-

Al-Maghaziy, Juz. 3, uk. 101.   Nahjus-Saadah, uk. 18. 44   Tabaqatul-Kubra cha Ibn Saad, Juz. 3, uk. 235. Ansabul-Ashraf, Juz. 1, uk. 188. 45 Al-Maghaziy, Juz. 1, uk. 371. 42 43

29

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 29

4/23/2016 2:45:51 PM


HUYU NDIYE BILAL

wa wanafanya maandalizi ya kivita yeye alikuwa akimjengea Mtume hema, akimchinjia na kumchomea nyama Mtume wa Mwenyezi Mungu 4.46 4.

Alikuwa akikinga maji yanayodondoka kutoka katika udhu wa Mtume 4 na kuwapelekea watu. Yeyote anayekutana naye alikuwa akichukua sehemu ya maji hayo na kujipaka uso, na yule anayekosa chochote kutoka katika maji hayo alikuwa anauchukua mkono wa rafiki yake na kupaka uso wake kwa mkono huo. Na ni kama hivyo walifanya kwa maji yaliyokuwa yakidondoka kutoka katika udhu wa Kiongozi wa Waumini B.47

5.

Imepokewa kutoka kwa Jabir bin Abdillah kwamba, siku moja Mtukufu Mtume 4 alisimama akaswali Swala ya Idil-Fitri. Alianza kwa Swala kisha ndipo akahutubia, alipomaliza aliteremka kutoka katika mimbari. Mara wakaja wanawake, akawa anawakumbusha ilihali ameegemea mkono wa Bilal.48

6.

Mtukufu Mtume 4 alikuwa akimwambia Bilal: “Ewe Bilal! Simama, wafuate wanafiki mpaka uwatoe msikitini….” Naye Bilal alikuwa akifanya hivyo.49

7.

Alikuwa akiwaandalia chakula wageni wa Mtukufu Mtume 4 na kuwakirimu. Alikuwa akimchinjia ngamia na kumchomea nyama Mtukufu Mtume 4, hasa maini na sehemu ya nundu.50

Taarikhul-Islam, uk. 280, cha al-Maghaziy.   Musnad Imam Ridhaa, uk. 15. Safinatul-Bihar, Juz. 1, uk. 104. Mustadrak SafinatilBihar, Juz. 1, uk. 420. 48   Sahih Bukhari, Juz. 2, uk. 9. Sahih Muslim, Juz. 3, uk. 18. 49   Taarikhul-Madinat al-Munawarah cha Ibn Shibah, Juz. 1, uk. 375. 50   Taarikhul-Islam, uk. 554. al-Maghaziy, Juz. 3, uk. 978. 46 47

30

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 30

4/23/2016 2:45:51 PM


HUYU NDIYE BILAL

8.

Alisuhubiana na Mtukufu Mtume 4 siku ya kuukomboa mji wa Makkah, na akaketi katika kizingiti cha nyumba yake akingojea kutoka kwake 4.51

9.

Mtukufu Mtume 4 alikuwa akimwamuru kuwakusanya Muhajirina, Answari na Waislamu wengine.52

10. Wakati Mtukufu Mtume 4 alipotaka kulisha chakula katika ndoa ya binti yake Fatimah I na Kiongozi wa Waumini B, alimwita Bilal na kumpa jukumu hilo, naye alilitekeleza vizuri.53 Kama ambavyo yeye ndiye aliyemnunulia Fatimah I manukato.54 11. Na alikuwa akimlinda Mtukufu Mtume 4.55 12. Imepokewa kutoka kwa Anas kwamba; Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alisema: “Nimetishwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na hakuna atakayetishwa kuliko mimi. Nimeudhiwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na hakuna atakayeudhiwa kuliko mimi. Na nilifikwa na siku tatu, mchana na usiku, nikiwa sina chakula isipokuwa kilichohifadhiwa na kwapa la Bilal.”56 13. Imepokea kutoka kwa Auni bin Abu Hujayfah, kutoka kwa baba yake, kwamba alisema: “Nilipelekwa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 pindi alipokuwa Abtahi katika hema. Ilikuwa ni wakati wa jua kali la adhuhuri. Bilal akatoka akanadi Swala, kisha akaingia ndani akatoka na maji yaliyodondoka kutoka katika udhu wa Mtume wa Mwenyezi   Sahih Muslim, Juz. 5, uk. 193.   Al-Maghaziy cha al-Waqidiy, Juz. 1, uk. 326. Sahih Bukhari, Juz. 4, uk. 15. Musnad Ahmad, Juz. 2, uk. 3. 53   Nahjus-Saadah, uk. 18. Biharul-An’war, Juz. 121, uk. 222. 54   Biharul-An’war, Juz. 43, uk. 94. Al-Amaaliy cha Tusiy, uk. 40. 55   Al-Ghadir, Juz. 7, uk. 102. 56   Swafuwatus-Swafuwah, Juz. 1, uk. 438. 51 52

31

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 31

4/23/2016 2:45:51 PM


HUYU NDIYE BILAL

Mungu 4, watu wakamzunguka wakichukua sehemu ya maji hayo. Kisha akaingia na kutoa fimbo ya Mtume….”57 14. Na imepokewa kutoka kwa Ummu Huswayni, amesema: Nilikwenda Hijja pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 katika Hijja ya kuaga. Nikamuona Usamah na Bilal, mmoja wao ameshikilia hatamu ya mnyama wake, na mwingine amenyanyua nguo yake akimkinga na joto, mpaka alipomaliza kutupa vijiwe katika Jamaratul-Aqabah.58 15. Imepokewa kutoka kwa Abdurahman Fahriy, amesema: Nilikuwa pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 katika vita vya Hunayni. Tulitembea katika siku yenye jua na joto kali, tukateremka chini ya vivuli vya miti. Jua lilipopinduka nikavaa kofia yangu, nikampanda farasi wangu, nikaenda kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4. Wakati huo alikuwa ndani ya hema lake. Nikamwambia: ‘Asalamu Alayka ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Muda wa kuondoka umewadia.’ Akasema: “Ndio umewadia. Ewe Bilal!” Ghafla Bilal akatoka juu ya mti huku akiwa ametengeneza kivuli kama kivuli cha mabawa ya ndege, akasema: “Labayka niko hapa kwa ajili yako. Na mimi ni fidia kwako.” Mtume akasema; “Nitengenezee kitanda cha farasi wangu.” Akatoa kitanda ambacho migongo yake miwili imetengenezwa kwa majani ya mitende, haikeri wala kuumiza.59 Mhazini wa Mtukufu Mtume 4: Mtukufu Mtume 4 alimpa jukumu la kuwahudumia mafakiri tangu alipoletwa kuwa Mtume 4. Na alikuwa akimuusia kwamba asil  Sahih Bukhari, Juz. 4, uk. 16.   Sahih Muslim, Juz. 4, uk. 79. 59   Siratun-Nabawiyyah cha Ibn Kathir, Juz. 3, uk. 629. Tabaqatul-Kubra cha Ibn Saad, Juz. 2, uk. 156. Majmauz-Zawaid, Juz. 6, uk. 181. 57 58

32

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 32

4/23/2016 2:45:51 PM


HUYU NDIYE BILAL

imbikize mali, na akimhimiza kufanya haraka kuitoa kwa ajili ya mahitaji ya wasiojiweza. Na ilikuwa Mwislamu anapokwenda kwa Mtukufu Mtume na akamuona kuwa hana mavazi, alikuwa akimwamuru Bilal kukopa mali na kumnunulia mavazi na chakula. Mwenyezi Mungu anasema:

َّ‫آ ِمنُوا بِ ه‬ ‫اللِ َو َرسُولِ ِه َوأَ ْنفِقُوا ِم َّما َج َعلَ ُك ْم ُم ْست َْخلَفِينَ فِي ِه ۖ فَالَّ ِذينَ آ َمنُوا ِم ْن ُك ْم‬ ‫َوأَ ْنفَقُوا لَهُ ْم أَجْ ٌر َكبِي ٌر‬ “Mwaminini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake; na toeni katika alivyowafanyia nyinyi kuwa ni waangalizi Wake. Basi walioamini miongoni mwenu, na wakatoa, wana malipo makubwa.”60

Alikuwa ni mhazini wa Mtukufu Mtume 4, na mwakilishi wake katika sadaka za matunda. Na alikuwa ana jukumu la kukusanya mali na kuzigawa kwa mujibu wa maelekezo ya Mtukufu Mtume 4.61 Hapa tunataja baadhi ya nukuu zilizopokewa katika upande huu: 1.

60 61

Imepokewa kutoka kwa Abu Abdullah Hawzaniy, amesema: Nilikutana na Bilal mwadhini wa Mtukufu Mtume 4 huko Halab, nikamwambia: Ewe Bilal! Nisimulie ni vipi ulikuwa utoaji wa Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu 4. Akasema: “Hakuwa akifanya hivyo yeye mwenyewe, bali mimi ndiye nilikuwa nikitekeleza hilo kwa maelekezo yake, tangu alipoletwa na Mwenyezi Mungu kuwa Mtume mpaka kifo chake. Alikuwa anapojiwa na Mwislamu na akamuona kuwa hana mavazi, alikuwa akiniamuru, nami

Sura Hadid: 7.   Al-Iswabah, Juz. 1, uk. 165. Swafuwatus-Swafuwah, Juz. 1, uk. 434. Dairatul-Maarif al-Islamiyyah, uk. 73. 33

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 33

4/23/2016 2:45:51 PM


HUYU NDIYE BILAL

nakwenda kukopa na kumnunulia mhusika nguo na chakula, namvisha na kumlisha, mpaka siku moja mmoja kati ya Mushrikina akanikabili na kuniambia: ‘Ewe Bilal! Hakika mimi nina wasaa wa mali hivyo usikope kutoka kwa yeyote isipokuwa kutoka kwangu.’ Nami nikafanya hivyo. Siku moja nilichukua udhu na nikasimama kwa ajili ya kutaka kutoa adhana na kuwaita watu katika Swala. Mara nikamuona Mushrik yule akiwa pamoja na kundi la wafanyabiashara. Aliponiona akasema: ‘Ewe Mhabeshi!’ Nikamwambia: Labayka. Basi akanitazama kwa uso wa hasira kwa kunikunjia uso, na akanitamkia maneno mazito, akasema: ‘Unajua zimebaki siku ngapi mwezi kufika?’ Nikamwambia: Karibu. Akasema: ‘Tokea sasa zimebaki siku nne. Nami nitakuchukua kutokana na deni ninalokudai, kwani hakika mimi sikukupa nilichokupa eti kutokana heshima yako kwangu, wala si kwa heshima ya rafiki yako. Lakini nilikupa ili uje kuwa mtumwa wangu, nikurudishe katika uchungaji wa kondoo kama ulivyokuwa hapo kabla.’ Nikapatwa katika nafsi yangu hali ambayo huwapata watu wengine. Nikaondoka, kisha nikaadhini, mpaka namaliza kuswali Swala za usiku tayari Mtukufu Mtume 4 alikuwa amesharejea nyumbani kwake. Nikamuomba idhini ya kuingia kwake, naye akanipa idhini, nikamwambia: ‘Ewe Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu! Baba na mama yangu ni fidia kwako, hakika Mushrik ambaye nilikwambia kuwa mimi hukopa kutoka kwake, amesema hivi na vile. Na mimi wala wewe hatuna cha kuweza kumlipa deni lake, na yeye ni mwenye kunifedhehesha. Nipe idhini niende kwa baadhi ya hawa walio hai miongoni mwa waliosilimu ili Mwenyezi Mungu amruzuku Mtume Wake kile kitakachoweza kunilipia deni.’ Nikatoka mpaka nyumbani kwangu, nikaweka upanga wangu, ala yangu, mkuki wangu na viatu vyangu upande wa kichwa chan34

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 34

4/23/2016 2:45:51 PM


HUYU NDIYE BILAL

gu. Nikaelekea juu kwa uso wangu, kila nilipolala na kushtuka kutoka usingizini nilikuta bado usiku ungalipo. Niliendelea kulala mpaka ilipopambazuka asubuhi ya kwanza, wakati nataka kutoka kwenda, mara akaja mtu na kuita: Ewe Bilal! Itikia wito wa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4. Nikatoka mpaka kwa Mtume, nikakuta ngamia wanne wakiwa na mizigo. Nikaomba idhini kwa Mtume 4, nikaingia kwake, Mtume 4 akaniambia: ‘Furahia habari njema. Mwenyezi Mungu amekuletea cha kukulipia deni.’ Nikamhimidi Mwenyezi Mungu, kisha akaniambia: ‘Haujawaona ngamia wanne wenye mizigo?’ Nikasema: Nimewaona. Akasema: ‘Ngamia hao na walivyobeba, vyote ni vyako, vichukue na ulipe deni lako.’ Walikuwa wamebeba mavazi na chakula ambayo Mtume alizawadiwa na chifu wa eneo la Fadaki. Nilifanya alivyoelekeza. Nikashusha mizigo iliyokuwa juu ya migongo yao, kisha nikawafunga. Kisha nikaenda kuadhini kwa ajili ya Swala ya Subhi. Baada ya Mtume 4 kumaliza kuswali nilitoka hadi Baqii, nikaweka vidole vyangu masikioni, nikanadi na kusema: ‘Yeyote aliyekuwa akimdai Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 deni, basi na aje.’ Nileendelea kuuza na kulipa madeni hadi nikamaliza madeni yote na halikubaki deni lolote juu yaMtume wa Mwenyezi Mungu 4 katika ardhi. Bali ilibaki mali kidogo wakia mbili au wakia moja na nusu. Kisha nilikwenda msikitini na mara nikamkuta Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 ameketi msikitini peke yake. Wakati huo sehemu kubwa ya mchana ilikuwa imepita. Nilimtolea salamu, akaniambia: ‘Umefanya nini kwa mali iliyokufikia?’ Nikamwambia: ‘Mwenyezi Mungu amemlipia Mtume Wake 4 madeni yote aliyokuwa nayo, hakuna deni lililobakia.’ Akaniuliza kuna chochote kilichobakia? Nikamwambia ndiyo. Akasema: ‘Endelea kuwangojea wengine, hadi uniondolee dhima 35

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 35

4/23/2016 2:45:51 PM


HUYU NDIYE BILAL

ya mali hiyo. Sintaingia kwa mke wangu yeyote mpaka uniondolee dhima ya mali hiyo.’ Hakutujia yeyote mpaka ulipoingia usiku. Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 aliposwali Swala ya usiku aliniita, akasema: ‘Umefanya nini kwa mali iliyokufikia?’ Nikamwambia: ‘Bado ninayo hajakuja yeyote.’ Basi akalala msikitini mpaka asubuhi, na akaendelea kuwepo msikitini katika siku ya pili, mpaka ilipofika jioni ndipo walipofika watu wawili na vipando vyao. Nikaenda nikawapa mavazi na chakula. Aliposwali Swala ya usiku aliniita, akasema: ‘Umefanya nini kwa mali iliyokufikia?’ Nikasema: ‘Mwenyezi Mungu amekuondolea dhima ya mali hiyo ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu.’ Akatoa takbira na kumhimidi Mwenyezi Mungu, kwani alikuwa anakhofia kwamba mauti yasije yakamfika ilihali bado ana mali hiyo. Kisha nilimfuata mpaka alipoingia kwa wake zake, akamsalimu mmoja baada ya mwingine mpaka akafika katika chumba chake. Hili ndilo uliloniuuliza.62 2.

Ibn Mas’udi amepokea kwamba: Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 aliingia kwa Bilal na kumkuta ana chane la tende. Akasema: “Kitu gani hiki Bilal?” Bilal akasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, niliweka hili kwa ajili yako na wageni wako.” Mtume akasema: “Hivi hauogopi chane hili kuwa na moshi kesho motoni? (Hivi hauogopi chane hili kuwa na miale kesho motoni?)63 Gawa na wala usiogope kwamba Mmiliki wa Arshi ataishiwa.”64

3.

Abu Said Khidriy amepokea kutoka kwa Bilal kwamba alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alisema: “Ewe

As-Sunanul-Kubra, Juz. 6, uk. 81. Swahih Ibn Habban, Juz. 14, uk. 264. Hilyatul-Awliyai, Juz. 1, uk. 149. 63   Hilyatul-Awliyai, Juz. 1, uk. 149. 64   Swafuwatus-Swafuwah, Juz. 1, uk. 438. Al-Ghadir, Juz. 8, uk. 374. 62

36

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 36

4/23/2016 2:45:51 PM


HUYU NDIYE BILAL

Bilal! Kufa fakiri na wala usife tajiri.” Nikamwambia: Nitawezaje kufanya hivyo ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: “Usiweke akiba unachoruzukiwa. Na usizuie unachoombwa.” Nikamwambia: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Nitakuwaje? Akasema: “Ni hivyo, au moto.”65

65 66

4.

Kutoka kwa Abu Awfa, amesema: Tulikuwa tumeketi kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4, na mara akajiwa na kijana, akasema: “Mimi ni kijana yatima na dada yangu ni yatima. Na mama yangu ni mjane. Tulishe katika vile alivyokulisha Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu atakupa yaliyopo Kwake mpaka uridhike.” Mtume akasema: “Mazuri sana uliyonena ewe kijana. Bilal nenda katuletee kilichopo kwetu.” Bilal akaja na tende ishirini na moja. Mtume akasema: “Saba ni zako. Saba nyingine ni za dada yako. Na saba nyingine ni za mama yako.”66

5.

Kutoka kwa Ibn Hisham, amesema kwamba: Wakati Jabir alipomchukua ngamia aliyenunuliwa na Mtume 4 kutoka kwake, na kwenda kumkalisha karibu na nyumba ya Mtume 4, Mtume aliuliza: “Ngamia mwenyewe ndiye huyu?” Jabir akasema: “Ndiyo ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, yule uliyemnunua.” Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 akamwita Bilal na kumwambia: “Nenda kampe wakia. Na mchukue ngamia wako ewe mwana wa ndugu yangu (Jabir), huyo ni wa kwako.” Jabir anasema: Nilikwenda pamoja na Bilal, Bilal akaniambia: “Wewe ndiye mtoto wa mmiliki wa shamba?” Nikasema ndiyo. Akasema: “Wallahi nitakupa na nyongeza.” Basi akaniongezea karati moja au mbili. Ngamia huyo aliendelea kuzaa huku Mwenyezi

Hilyatul-Awliyai, Juz. 1, uk. 150. Al-Ghadir, Juz. 8, uk. 375.   Majmaul-Bayan, Juz. 1, uk. 506. 37

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 37

4/23/2016 2:45:51 PM


HUYU NDIYE BILAL

Mungu akituongezea kupitia kwake, na sisi tukaendelea kutambua nafasi yake, mpaka alipopatwa na mauti (yaani ngamia) hapa karibu yenu.67 6. Al-Waqidiy ametaja baadhi ya zawadi ambazo Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alizitoa kwa baadhi ya misafara. Anasema: Naiona baadhi ya misafara siku hiyo ikichukua zawadi zao kwa Bilal, wakia kumi na mbili na nusu.68 Bilal aliendelea kuwa mhazini wa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 mpaka kifo chake. Alipofariki 4 alikuja Abubakri mwanzoni mwa ukhalifa wake, akamwambia Bilal: “Ulikuwa mwadhini wa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4. Na mikononi mwako una riziki za Mtume na ya wageni wake. Hivyo basi, kuwa mwadhini kama ulivyokuwa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4. Na kuwa mwadhini wangu kama ulivyokuwa.” Lakini Bilal hakukubali ombi lake, akamwambia: “Niache mimi na Mola Wangu.”69 7.

Na katika Sunan Daramiy imeandikwa kwamba: Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alianza kwa Swala kabla ya hotuba siku ya Iddi. Kisha ndipo akahutubia, ikaonekana kwamba wanawake hawakumsikia, akawafuata akawakumbusha, akawawaidhi na kuwaamuru kutoa sadaka. Bilali alikuwa ameshika nguo yake, hivyo akawa anakuja mwanamke na gramu ya dhahabu au chochote na kukitupia katika nguo ya Bilal.70

8.

Kutoka kwa Jabir bin Abdullah, amesema: Nilimkamata kichwa ngamia na kuja naye kwa Mtukufu Mtume 4,

Al-Maghaziy, Juz. 1, uk. 400.   Al-Maghaziy cha al-Waqidiy, uk. 980. 69   Darajat ar-Rafiah, uk. 366. 70   Sunan Daramiy, Juz. 1, uk. 376. Sahih Bukhariy, Juz. 2, uk. 9. 67 68

38

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 38

4/23/2016 2:45:51 PM


HUYU NDIYE BILAL

9.

akasema kumwambia Bilal: “Ewe Bilal! Mpe dinari ishirini kutoka kwenye ghanima.”71 Imepokewa pia kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alikuwa anapopata ghanima, humwamrisha Bilal awaite watu mara tatu. Na watu hao huja na ghanima zao na hatimaye huzigawa na kutoa khumsi yake. Siku moja baada ya zoezi hilo alikuja mtu mmoja na hatamu iliyotengenezwa kwa nywele, akasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Hii ndio ghanima tuliyoipata.” Mtume akamwambia; “Hivi hukumsikia Bilal akinadi mara tatu?” Akasema: “Nilimsikia.” Akamuuliza: “Ni kipi kilichokuzuia usije nayo?” Akajitetea kwa kutoa udhuru, Mtume 4 akamwambia: “Naomba uwe ambaye utakuja nao Siku ya Kiyama, nami sintaukubali kutoka kwako.”72

10. Ummu Malik al-Answariyyah alikuja na chombo chenye samli kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4, Mtume akamwamuru Bilal kukikamua, kisha akamrudishia chombo chake. Alipokichunguza akakikuta kikiwa bado kimejaa. Akaja kwa Mtume na akamwambia: “Kuna chochote kilichoteremka dhidi yangu?” Mtume akasema: “Kwanini?” Akasema: “Umeikataa zawadi yangu.” Mtume akamwita Bilal na kumuuliza, akasema: “Naapa kwa Yule aliyekutuma na haki, nimekamua mpaka nikaona aibu.” Mtume akasema: “Hongera. Hii ni baraka ewe Ummu Malik. Hii ni baraka, Mwenyezi Mungu ameanza kukulipa hapa hapa thawabu zake.” Kisha akamfundisha kwamba asome kila baada ya Swala: Subhanallah mara kumi. Alhamdulilahi mara kumi. Na Allahu Akbaru mara kumi.”73   Sunan Ibn Majah, Juz. 2, uk. 743.   Sahih Ibn Hayyah, uk. 198. 73   Al-Iswabah, Juz. 8, uk. 277. Al-Muswannaf, Juz. 7, uk. 437. Al-Ahadiy Wal-Mathaniy, Juz. 6, uk. 177. 71 72

39

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 39

4/23/2016 2:45:51 PM


HUYU NDIYE BILAL

Bilal akiwa kati ya utiifu na mapenzi: Hakika Mtukufu Mtume 4 baada ya kupewa habari ya mauti yake, alimwamuru Bilal anadi Swala ya jamaa. Wakakusanyika Muhajirina na Answari katika msikiti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, Mtume akawaswalisha watu, kisha akapanda mimbari na kuanza kuwahutubia hotuba ambayo ilizihuzunisha nyoyo na kuyaliza macho. Akawaambia: “Enyi Waislamu! Nakuapizeni kwa Mwenyezi Mungu, na kwa haki yangu iliyo juu yenu, kwamba yeyote niliyemtendea dhulma yoyote basi asimame na aje kulipiza kisasi kwangu, kabla ya kisasi cha siku ya Kiyama.” Miongoni mwa Waislamu waliokuwepo alisimama mzee kikongwe, aliyeitwa Akashah, akawapita Waislamu mpaka akasimama mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu 4, akasema: “Wazazi wangu baba na mama ni fidia kwako. Kama si kutuapiza kwako ulikotuapiza mara kwa mara basi nisingefanya chochote kama hiki. Nilikuwa pamoja na wewe vitani, Mwenyezi Mungu alipotupa ushindi sisi na Mtume wake tulianza kuondoka, na mara ngamia wangu alikuwa akitembea usawa wa ngamia wako. Niliteremka kutoka katika ngamia na nikasogea karibu yako ili nibusu paja lako. Ukainua fimbo yako nayo ikanipiga, na sijui ilikuwa ni kwa kukusudia au ulitaka kumpiga ngamia.” Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 akasema: “Nakukinga kwa utukufu wa Mwenyezi Mungu, kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu hawezi kukupiga makusudi. Ewe Bilal! Nenda nyumbani kwa Fatimah na uniletee fimbo.” Bilal akatoka msikitini huku kaweka mikono yake juu ya kichwa chake akinadi: “Mtume wa Mwenyezi Mungu anajilipizia kisasi yeye mwenyewe.” Subiri ewe Bilal! Unakwenda wapi? Hivi unamletea Nabii wako fimbo katika siku zake za mwisho?! Hivi unamlipa kipenzi chako kwa fimbo itakayomuumiza Mtume wa Mwenyezi Mungu 4?! Haitoshi wewe kupiga kichwa chako kwa mikono yako, au kuosha uso 40

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 40

4/23/2016 2:45:51 PM


HUYU NDIYE BILAL

wako kwa machozi yako. Urithi wa jihadi yako kwa ajili ya Mwenyezi Mungu hautoshi mbele ya nukta ya maumivu ya Muhammadi 4. Rudi Bilali. Dunia yote inanadi kwamba rudi. Ardhi na mbingu zinasema rudi. Usiwalize Malaika wa ulimwengu wala mawe ya ardhini. Ni moyo upi unaweza kuvumilia maumivu ya Muhammad 4? Na ni mkono upi unaweza kubeba fimbo ya kulipizia kisasi kwake?! Utamwambia au atakwambia nini Fatimah? Huzuni ya Fatimah ni ya zama zote. Basi mpunguzie huzuni yake. Mimi nimezama katika bahari ya utiifu na mapenzi, baina ya kumtii Muhammad 4 na kumtii Muhammad 4. Ni nani basi atakayeiongoza njia ya sawa safina yangu?! Bilali akagonga mlango wa Fatimah I na kumwambia: “Ewe Binti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu! Nipe fimbo ya Mtume.” Fatimah akamuuliza: “Ewe Bilal! Anataka kuifanyia nini baba yangu. Na leo si siku ya Hijja wala siku ya vita?” Akasema: “Ewe Fatimah! Baba yako Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 anawaaga watu, na anaachana na dunia na kutoa kisasi dhidi ya nafsi yake.” Fatimah I akasema: “Ni nani huyo ambaye nafsi yake imeridhika kulipiza kisasi kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4? Ewe Bilal! Waambie Hasan na Husein wasimame mbele ya mtu huyo alipize kisasi kwao, na wala wasimwache alipize kisasi kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4.” “Ndiyo, ni nani huyo ambaye nafsi yake imeridhika kulipiza kisasi kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4? Atakuja zama gani, na kutoka katika udongo wa mlima upi?! Waambie Hasani na Husein wawe fidia kwake 4. Na ole wako Bilali mtu huyo alipize kisasi kwa baba yangu. Mwili wa Hasan ambaye ini lake lilisambaratika kutokana na sumu anaweza kuvumilia kisasi! Mwili wa Husein aliyekatwakatwa kwa mapanga na kupondwapondwa na kwato za ngamia…” 41

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 41

4/23/2016 2:45:51 PM


HUYU NDIYE BILAL

Ewe Binti wa Muhammadi! Kwa nani unamfidia?! Unamfidia Muhammadi 4 kwa maua yake na roho yake! Ninyi nyote ni kutokana na asili na roho moja, na nafsi moja. Furaha yenu ni moja, na huzuni yenu ni moja, na maumivu yenu ni mamoja. Anakutosheni Mwenyezi Mungu. Bilal akaingia msikitini na kumkabidhi Mtukufu Mtume 4 fimbo, Mtume akamkabidhi Akashah fimbo. Wakasimama Hasan na Husein F wakasema: “Ewe Akashah! Si unajua kwamba sisi ni wajukuu wa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4, na kulipiza kisasi kwetu ni sawa na kulipiza kisasi kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4?” Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 akawaambia: “Kaeni enyi ambao ni burudisho la macho yangu. Mwenyezi Mungu asisahau sehemu hii kwa ajili yenu.” Kisha akasema: “Ewe Akashah! Piga ikiwa ni mwenye kupiga.” Akashah akasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Ulinipiga wakati nikiwa tumbo wazi bila nguo.” Mtume akafunua tumbo lake. Waislamu wakanyanyua sauti kwa kilio na kusema: “Hivi kweli Akasha anataka kumpiga Mtume wa Mwenyezi Mungu 4?” Akasha alipolitazama tumbo la Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 kama moja ya aina za nguo za katani hakujizuia kumkumbatia na kulibusu tumbo lake huku akisema: “Baba na mama yangu wawe fidia kwako. Ni nani nafsi yake itaridhika kulipiza kisasi kwako?” Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 akasema: “Ima upige, na ima usamehe.” Akasema: “Nimekusamehe ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nikitaraji Mwenyezi Mungu nami anisamehe Siku ya Kiyama.”74 Tunasema: Kwanza: Imam Sajjad B alihiji kwa kutumia ngamia wake miaka ishirini na tano, bila kumpiga hata mara moja ngamia wake, bali ali74

Kalimat Imam Husein, uk. 97. 42

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 42

4/23/2016 2:45:51 PM


HUYU NDIYE BILAL

kuwa anamtishia kwa mjeledi na kumwambia: ‘Ah, kama si kisasi.” Na anauzuia mkono wake usimfikie.75 Pili: Je mjeledi huo ulimpata kwa makusudi au kwa kutokukusudia? Katika sura ya kwanza: Ni lazima mtu huyo alitenda tendo analostahili pigo hilo, au kemeo kali. Na kama ulimpata bila kukusudia basi moja kwa moja alikuwa amesamehewa na hakuna kisasi hapo. Na mhusika yeye mwenyewe ametamka wazi kwamba hajui kama Mtume 4 alifanya makusudi katika kumpiga au la. Na Mtukufu Mtume 4 alimkinga kwa utukufu wa Mwenyezi Mungu kwamba hawezi kumpiga makusudi. Tatu: Hakika kisasi cha Hasan na Husein F ni cha ajabu sana. Hakuna kisasi kwa mtu asiye na hatia.. Sasa itakuwaje ikiwa huyu anayejitolea kuwa mbadala wa kisasi, ni mtoto mdogo ambaye umri wake haujavuka miaka sita au saba?! Anatangaza sharia na maamrisho ya Mtukufu Mtume 4: Kuna majukumu na huduma nyingi alizozitekeleza Bilal kwa ombi la Mtukufu Mtume 4, lakini ni wajibu tuzitazame zile zilizomtambulisha kama mfikishaji wa amri za Mtukufu Mtume 4 kwa Waislamu wote, katika mambo muhimu na nyeti, kuanzia kuwatangazia vita mpaka kufikisha vipengele vya sharia na mengineyo. Tunataja yaliyopokewa katika hilo: 1. 75

Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alimtuma Bilal akawatangazie watu kwamba: Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 amese-

Iilamul-Waraa, Juz. 1, uk. 490. Biharul-An’war, Juz. 61, uk. 216. Mustadrakul-Wasail, Juz. 18, uk. 289. Al-Wasail, Juz. 11, uk. 485. 43

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 43

4/23/2016 2:45:52 PM


HUYU NDIYE BILAL

ma kwamba msiswali isipokuwa mkaswalie kwa Bani Quraydhah.76 2.

Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alimwamuru Bilal atangaze kwamba: Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 ameharamisha samaki aina ya mkunga, mjusi na punda wa mjini.77

3.

Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alimwamuru Bilal awatangazie watu kwamba wamtafute adui yao.78 Na katika vita vya Hamraul-Asad Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alimwamuru Bilal atangaze kwamba: Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 anakuamrisheni kumtafuta adui yenu. Na wala asitoke pamoja nasi isipokuwa yule aliyehudhuria mapigano jana. 79

4.

Baada ya Mushrikina kuondoka katika vita vya Handaki, Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alimtuma Bilal akawatangazie watu kwamba: Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 anakuamrisheni kwamba msiswali isipokuwa mkaswalie kwa Bani Quraydhah.80

5.

Na katika kitabu Sunan Daramiy, imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas kwamba alisema: Bedui mmoja alikuja kwa Mtukufu Mtume 4 na kumwambia: “Mimi nimeona mwezi mwandamo.” Mtume akamwambia: “Unashahidilia kwamba hapana Mungu isipokuwa Allah, na kwamba hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu?” Akasema: “Ndiyo.” Mtume akasema: “Ewe Bilal! Watangazie watu, kwamba wafunge kesho.”81

Maghaziy cha al-Waqidiy, uk. 498.   Tahdhib, Juz. 2, uk. 284, Hadithi ya 35. 78   Al-Maghaziy, Juz. 1, uk. 326. 79   Al-Maghaziy, Juz. 1, uk. 334. 80   Al-Maghaziy, Juz. 2, uk. 497. 81   Sunan Daramiy, Juz. 2, uk. 5. Sunan Ibn Majah, Juz. 1, uk. 529. 76 77

44

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 44

4/23/2016 2:45:52 PM


HUYU NDIYE BILAL

6.

Na katika Sahih Bukhari, imepokewa kutoka kwa Zainab mke wa Abdullah, kwamba alimwambia Abdullah: “Muulize Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 je inatosheleza mimi kukupa sadaka wewe na mayatima waliyo chini ya uangalizi wangu?” Abdullah akasema: “Muulize wewe mwenyewe Mtume wa Mwenyezi Mungu 4.” Zainabu anasema: Basi nikaenda kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4, nikamkuta mwanamke mwingine wa Kianswari akiwa mlangoni, naye haja yake ni kama yangu. Mara akapita Bilal, tukamwambia: “Muulize Mtume wa Mwenyezi Mungu 4, je inatosheleza mimi kumpa sadaka mume wangu na mayatima waliyo chini ya uangalizi wangu?” Akaingia na kumuuliza, Mtume akasema: “Ni kina nani hao?” Akasema: “Ni Zainabu.” Mtume akasema: “Zainabu yupi?” Akasema: “Mke wa Abdullah.” Mtume akasema: “Ndiyo. Naye ana malipo mara mbili: malipo ya ukaraba. Na malipo ya sadaka.”82

7.

Zaidi ya hapo ni kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alikuwa akimwamuru anadi kwa ajili ya Swala ya jamaa.

8.

Wakati wa vita vya Khaybari, Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alimwamuru Bilal awatangazie watu kwamba: Hataingia peponi isipokuwa mtu muumini. Na hakika Mwenyezi Mungu ataipa nguvu dini hii hata kupitia mtu muovu.83

9.

Imepokewa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 kwamba alimwamuru Bilal awatangazie watu kwamba: Hakika pepo si halali kwa mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu.84

Katika yote hayo yaliyotangulia, tunapata heshima kubwa aliyoipata Bilal kwa neema ya Uislamu, baada ya kuwa ni mtumwa   Sahih Bukhar, Juz. 2, uk. 128. Sahih Muslim, Juz. 3, uk. 80.   Al-Muswannaf, Juz. 5, uk. 270. 84   Kitabus-Sunnah, uk. 49. 82 83

45

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 45

4/23/2016 2:45:52 PM


HUYU NDIYE BILAL

mwenye kuteswa katika changarawe za moto za Makkah. Hatimaye akawa mara anawakusanya Waislamu kwa ajili ya jihadi, na mara nyingine anawakusanya kwa ajili ya Swala. Na akawa anakabidhiwa majukumu mbalimbali na Mtume wa Mwenyezi Mungu 4. Uaminifu wa Bilal kwa mtazamo wa Maswahaba: 1.

Katika Sahih Bukhari: Amepokea Fadhlu bin Abbas, kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 hakuwahi kuswali ndani ya Kaaba. Na Bilal amesema kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 aliwahi kuswali ndani ya Kaaba. Chukua kauli ya Bilal.85

2.

Kutoka kwa Ibn Umar: Kwamba alikuwa anapoingia Kaaba, anakwenda moja kwa moja bila kupinda, kwa kuielekea Kaaba huku mgongo wake ukiwa usawa na mlango alioingilia. Anakwenda mpaka anapofika karibu na ukuta wa kibla yake kwa ukaribu wa dhiraa tatu. Hapo ndipo anaposwalia, anafuata sehemu aliyoelekezwa na Bilal.86

Alikuwa ni mmoja kati ya wateule wa Mtukufu Mtume 4: Katika maelezo yafuatayo kuna ushahidi ambao huenda ndio ushahidi muhimu zaidi wa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 juu ya haki ya Bilal. Nao unasisitiza kwamba Bilal hakuwa ni mtu tu mwenye kumhudumia Mtume wa Mwenyezi Mungu 4, au mwadhini tu, au mpiganaji tu miongoni mwa wapambanaji, na hatimaye yakamfikia mapenzi ya bwana wake na ya Waislamu. Hapana, si hivyo tu, kwani Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 hatamki kwa matamanio yake. Bali ni kwa wahyi anaofunuliwa. 85 86

  Sahih Bukhari, Juz. 2, uk. 133.   Sahih Bukhari, Juz. 2, uk. 133. 46

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 46

4/23/2016 2:45:52 PM


HUYU NDIYE BILAL

Ushahidi wake 4 juu ya haki ya Bilal si kueleza mapenzi yake na ukaribu wake kwake, bali ni ushahidi ambao unaeleza uhalisia na ukweli wa Bilal. Unaeleza imani yake, sifa zake, mwenendo wake na nafasi ya mchango wake. Ibn Asakir ametaja katika kitabu chake cha Historia, kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4, kwamba yeye 4 alipewa wateule kumi na nne, saba kati ya hao ni kutoka miongoni mwa Muhajirina, nao ni Abdullah bin Mas’udi, Salman, Abudhari, Hudhayfah, Ammar, Mikidadi na Bilal.87 Labayka: Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 anauliza: Yuko wapi Bilal? Na haraka sana Bilal anamjibu: Labayka ya Rasulallah.88 Nayo ni taabiri inayoonesha kiwango chake cha kujisalimisha na utiifu wake kwa Mtume, na kwamba ameiweka nafsi yake sehemu ya utii na kujibu. Kwa kadiri uitikiaji huu unavyoonesha maadili ya Bilal na tabia yake, ni kwa kadiri hiyo hiyo unaonesha kiwango cha mapenzi yake kwa Mtukufu Mtume 4 na alivyo tayari kuitikia wito wake na kuharakisha kujibu ombi lake. Bila shaka hayo yote yanatokana na maana za mapenzi alizonazo ndani ya nafsi yake, na inatokana na kiwango cha maarifa na uwelewa sahihi aliokuwa nao juu ya nafasi ya Mtukufu Mtume 4, na utukufu na ukaribu alionao Mtume mbele ya hadhara ya Mwenyezi Mungu. Labayka ni taabiri ya utii na kujisalimisha. Na mara nyingi alikuwa akirudia neno hilo kusisitiza jinsi alivyozama na kujisalimisha katika hadhara ya unabii. Ni kweli kiasi gani jibu lake! Pindi Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alipomwita katika vita vya Hunayni, alimjibu kwa kusema: “Labayka niko hapa kwa ajili yako. Na mimi ni fidia kwako.”89   Al-Ghadir, Juz. 10. uk. 19.   Mustadrakul-Wasail, Juz. 14, uk. 205. Al-Manaqib, uk. 348. 89   Baghiyyatul-Bahith, uk. 219. 87 88

47

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 47

4/23/2016 2:45:52 PM


HUYU NDIYE BILAL

Mwadhini wa Mtukufu Mtume 4: Alijulikana na kupata umashuhuri kwa jina hilo. Na kwa sifa hii yaliongezeka mapenzi ya Waislamu na heshima yao kwake. Kwa kweli ni heshima kubwa mtu kutofautishwa kwa sifa hii. Mtu kuwa mwadhini wa Mtukufu Mtume 4, hasa ukizingatia nafasi na heshima ya Swala, nayo ndio nguzo kuu ya dini na ibada tukufu kuliko zote. Na kitendo cha Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 kumkabidhi yeye jukumu hili na kumtanguliza katika hili kuliko Waislamu wengine, ambao walikuwa tayari kuweza kutekeleza tendo hili la kiibada, kitendo hicho kinakujulisha kiwango cha kuaminiwa kwake, alichokuwa nacho kwa Mtukufu Mtume 4. Nukuu za kihistoria zimetaja kwamba, alikuwa akimwadhinia Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 nyumbani na safarini.90 Na maadamu yupo Bilal ambaye alikuwa akijitahidi kuwepo, hakuwa akiadhini yeyote mwingine. Na ikitokea kwa nadra kuwa hayupo pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu 4, hapo ndipo alikuwa akiadhini mwingine. Saad aliadhini mara tatu katika uhai wa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4, na katika mara zote hizi tatu Bilal hakuwepo. Na hii inaashiria kwamba daima alikuwa anategemewa Bilal katika jukumu hili, bali pia lilikuwa linamuhusu yeye tu. Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alilibainisha hilo kwa Saad kwa kumwambia: “Usipomuona Bilal pamoja nami, adhini.”91 Nini maana ya yeye 4 kukataza yeyote asiadhini mbele ya hadhara ya Bilal, na kumtanguliza Bilal juu ya mwingine yeyote, na kusisitiza kwamba: “Hakika Bilal ndiye mwadhini wa Mtume, bali ndiye bwana wa waadhini wote.”? Imepokewa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 kwamba alisema: “Ni mwema mno Bilal, naye ndiye bwana wa waadhini wote.”92   Ikhtiyar Maarifatir-Rijal, uk. 189.   Al-Muswannaf, Juz. 1, Hamish ya 494. 92   Hilyatul-Awliyai, Juz. 1, uk. 147. 90 91

48

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 48

4/23/2016 2:45:52 PM


HUYU NDIYE BILAL

Na ilikuwa ni katika ada yake, kuadhini muda wowote Mtukufu Mtume 4 anapofika Kuba, ili awajulishe watu kwamba, Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 amekuja, ili waweze kukusanyika kwake. Na ilitokea siku moja kwamba, Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alifika Kuba bila kuwa pamoja na Bilal, waafrika wakajitazama wao kwa wao kwa namna yenye kuamsha shaka na wasiwasi, ndipo akajitokeza Mwislamu aliyekuwa akiitwa Saad, akapanda juu ya mtende na akaadhini. Alipomaliza kuadhini, Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 akamuuliza: “Ni kitu gani kilichokufanya uadhini ewe Saad?” Akasema: “Baba yangu na mama yangu wawe fidia kwako, nimekuona ukiwa katikati ya watu wachache, na sijamuona Bilal pamoja nawe. Na nimewaona waafrika hawa wanatazamana wao kwa wao na wakikuangalia wewe, nikaingiwa na hofu dhidi yao juu yako. Hivyo nikaamua kuadhini.” Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 akasema: “Umepatia ewe Saad. Usipomuona Bilal pamoja nami, adhini.”93 Bila shaka uchaguzi na uteuzi huu, bali msisitizo na mhimizo wa uteuzi huu kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4, una dalili na maana ya kina zaidi. Ukiachilia mbali imani ya Bilal, kujitolea kwake, jihadi yake na ukaribu wake na Mtume wa Mwenyezi Mungu 4, sifa ambazo zinazotosha kukujulisha nafasi yake, isipokuwa ni kwamba pia kuna ujumbe ambao Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 anataka kuuwelekeza katika jamii ambayo, ndio kwanza imebadilika kutoka katika jamii ya kijahiliya. Jamii ambayo bado inaishi na ada, dhana na matamanio mengi ya kijahiliya. Mtume anaona kwamba kumtanguliza mtumwa huyu Mhabeshi aliyekuja kutoka nchi ya mbali, na ambaye hafungamani na Makuraishi wala makabila mengine ya Kiarabu kwa nasaba wala cheo, hakika kumtanguliza juu ya mabwana na waheshimiwa, ni pigo imara linalolenga kuvuka 93

Majmauz-Zawaid, Juz. 1, uk. 336. 49

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 49

4/23/2016 2:45:52 PM


HUYU NDIYE BILAL

vizuizi, matakwa na ada za kijahiliya ambazo hazina nafasi kabisa katika Uislamu, na ni kuzitokomeza kabisa. Kupitia Bilal, Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 aliiambia jamii ya Kiislamu ya wakati huo, na jamii zilizofuatia baadaye, bali aliviambia vizazi vya wakati wote, kwamba Uislamu haukomei kwenye rangi, tabaka, ukoo, jografia na nafasi aliyonayo mtu kijamii na kimada. Bali kuamini na kushikamana na roho ya Uislamu na madhumuni yake ndiyo kigezo cha msingi, na ndiyo kituo cha heshima na uzingativu. Na Bilal alilipata hili, na kwa ajili hiyo kila alipokuwa akianza kuadhini moyo wake ulikuwa ukimdunda na hisia zake kubadilika, na akiona kwamba, anajadidi agano lake na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake katika adhana yake. Alikuwa anashikwa na woga, anapomuona Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 na makundi ya Waislamu, katika matabaka yao na nafasi zao mbalimbali, wanamsikiliza na wananyenyekea kwenye wito wa kujisalimisha na kutii, unaowafikia kupitia adhana yake. Ambapo wito huo unawazidishia hali ya kukiri zaidi na zaidi adhama ya dini hii na mafanikio yake. Ambapo na yeye alikuwa anafungua njia mbele ya wasio na kitu katika maisha, kwamba si tu wahisi uwepo wao, bali pia wajiandae kupata nafasi ya juu ambayo mabwana, wakuu, na wenye nguvu na uwezo wanaitamani lakini hawaifikii. Na pia tutaashiria hapa, sehemu ya nukuu kuhusu adhana yake wakati wa vita alipokuwa pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu 4. Kati ya nukuu hizo ni ile iliyopokewa katika kitabu al-Maghaziy kuhusu vita vya Hudaybiyyah, Nafiri, Umratul-Qadhai, Ukombozi wa Makkah na vita vya Handaki.94 Imepokewa katika kitabu al-Maghaziy kuhusu adhana yake huko Batni Arafah, ameeleza kwamba: Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 94

  al-Maghaziy, Juz. 1, uk. 216, 217, 248, 371. Na Juz. 2, uk. 464, 472, 473, 582, 737, 738. 50

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 50

4/23/2016 2:45:52 PM


HUYU NDIYE BILAL

alihutubia huko Batni Arafa juu ya ngamia wake al-Qas’wau baada ya jua kukengeuka. Alipokuwa anakaribia kumaliza, Bilali aliadhini na Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 akasitisha maneno yake. Baada ya Bilal kumaliza adhana yake Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 akaendelea na maneno na akashuka kutoka kwenye kipando chake. Bilal akakimu Swala na Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 akaswalisha Adhuhuri. Kisha akakimu tena Mtume 4 akaswalisha Alasari. Alikusanya pamoja Swala hizo mbili kwa adhana moja na Ikama mbili.95 Na kuna nukuu zimaonesha kwamba Bilal anapomaliza Adhana, na akitaka kumjulisha Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 kwamba ameshaadhini, alikuwa akisimama mlangoni na kusema: “Njooni kwenye Swala. Njooni kwenye mafaniko. Swala ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu.” Mtume 4 akitoka na kumuona Bilal moja kwa moja huanza kukimu.96 Na imepokewa kutoka kwa al-Waqidiy kwamba, Bilal alikuwa akisimama mlangoni kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 – yaani baada ya Adhana - na kusema: “Amani iwe juu yako ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu.” Na mara nyingine alikuwa akisema: “Amani iwe juu yako, baba yangu na mama yangu wawe fidia kwako ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Njooni kwenye Swala. Amani iwe juu yako.”97 Bilal, katika Hadithi za Mtukufu Mtume: Hakika mwenye kufuatilia Hadithi Tukufu zilizopokewa kuhusu haki ya Bilal, ataona jinsi Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alivyompa umuhimu Bilal. Hivyo tunamuona wakati mwingine akisisitiza kuhusu umuhimu wake, na akimshahidilia pepo. Na katika hilo kuna ubainifu wa wazi wa daraja yake ya juu katika imani, na nafasi yake   al-Maghaziy, Juz. 3, uk. 1102.   Aayanus-Shiah, Juz. 3, uk. 603. Tabaqatul-Kubra cha Ibn Saad, Juz. 3, uk. 234. AnsabulAshraf, Juz. 1, uk. 187. 97   Taratibul-Idariyyah, Juz. 1, uk. 75. 95 96

51

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 51

4/23/2016 2:45:52 PM


HUYU NDIYE BILAL

ya juu katika Uislamu. Na yeye ni miongoni mwa waliotangulia mwanzo kabisa kuitikia wito wa mbinguni (Uislamu), na ni miongoni mwa waliovumilia na kufanya subira dhidi ya maudhi, na kamwe hakuzembea katika kupambana na kujitoa muhanga katika njia ya kusimamisha nguzo na mihimili ya dini. Na yeye ni miongoni mwa wachache ambao Mtukufu Mtume 4 aliwateua na kuwatunuku heshima na sifa makhususi, jambo walilofanyiwa wale waaminifu wakweli wa kizazi cha kwanza (cha Uislamu). Ambao walisimama imara katika njia ya uongofu na wakaendelea kubaki katika mapenzi ya kumpenda Mtukufu Mtume 4 na watu wa nyumbani kwake F. Mwenyezi Mungu anasema:

‫إِ َّن الَّ ِذينَ قَالُوا َربُّنَا للاهَّ ُ ثُ َّم ا ْستَقَا ُموا تَتَنَ َّز ُل َعلَ ْي ِه ُم ْال َملاَ ئِ َكةُ أَ اَّل تَخَافُوا َو اَل‬ َ‫تَحْ َزنُوا َوأَب ِْشرُوا بِ ْال َجنَّ ِة الَّتِي ُك ْنتُ ْم تُو َع ُدون‬ “Hakika wale ambao wamesema: Mola Wetu ni Mwenyezi Mungu! Kisha wakawa na msimamo, huwateremkia Malaika (kuwaambia): Msiwe na hofu, wala msihuzunike; nanyi furahini kwa Pepo mliyokuwa mkiahidiwa.” (Sura Fussilat; 41:30).

Na hakika hizo Hadithi za Mtukufu Mtume 4 ni alama za utukufu na heshima, ambazo zitadumu muda wote na vizazi vyote kupitia ulimi wa Bwana wa Manabii na Mitume 4, nasi hapa tunataja baadhi ya Hadithi hizo: 1.

Kutoka kwa Anas bin Malik, amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alisema: “Pepo ina shauku na watu wanne: Ali, Salman, Bilal na Ammar.”98

Tahdhibu Taarikhu Damashqiy al-Kabir, Juz. 3, uk. 309. Al-Ghadir, Juz. 9, uk. 26. Siyaru Aalamin-Nubalai, Juz. 1, uk. 355.

98

52

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 52

4/23/2016 2:45:52 PM


HUYU NDIYE BILAL

2.

3.

4.

5.

Kutoka kwa Qasim bin Rabiah, kutoka kwa Zaydi bin Arqam, amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alisema: “Ni mwema mno Bilal, naye ndiye bwana wa waadhini wote.”99 Kutoka kwa Zayd bin Muslim, amesema kwamba, Bani Bakir walikuja kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4, nao ni kutoka katika Bani Kinanah, wakamwambia: “Muozeshe dada yetu kwa Fulani.” Mtume 4 akawaambia: “Kwa nini msimuozeshe Bilal?” Kisha wakaja mara ya pili na ya tatu, na mara zote wanamwambia Mtume wa Mwenyezi Mungu 4: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu 4! Muozeshe dada yetu kwa Fulani.” Na Mtukufu Mtume 4 anawaambia: “Kwa nini msimuozeshe Bilal. Kwa nini msimuozeshe kwa mtu miongoni mwa watu wa peponi?” Wakamuozesha kwa Bilal.100 Kutoka kwa Anas, amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alisema: “Mimi nitawatangulia Waarabu. Salman atawatangulia Waajemi. Suhaybu atawatangulia Warumi. Na Bilal atawatangulia Wahabeshi.”101 Na sisi tunaona kwamba Hadithi hii ni ya uwongo, kwani yeye Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 atawatangulia viumbe wote. Kama ambavyo Suhaybu alikuwa ni mtumwa muovu kama ilivyopokewa katika baadhi ya riwaya.102 Al-Hafidh na Tabaraniy wameandika kutoka kwa Ibn Abbas kwamba, Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alisema: “Wa-

Hilyatul-Awliyai, Juz. 1, uk. 147. Siyaru Aalamin-Nubalai, Juz. 1, uk. 355. MajmauzZawaid, Juz. 9, uk. 300. Tahdhibu Taarikhu Damashqiy al-Kabir, Juz. 3, uk. 313. 100   Ansabul-Ashraf, Juz. 1, uk. 190. Tahdhibu Taarikhu Damashqiy al-Kabir, Juz. 3, uk. 314. 101   Tahdhibu Taarikhu Damashqiy al-Kabir, Juz. 3, uk. 309. Tanqihul-Maqal, Juz. 1, uk. 183. Aayanus-Shiah, Juz. 3, uk. 603. Qamusir-Rijal, Juz. 2, uk. 238. 102   Al-Wasail, Juz. 20, uk. 148. Khulaswatul-Aqwal, uk. 83. Biharul-An’war, Juz. 22, uk. 142. 99

53

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 53

4/23/2016 2:45:52 PM


HUYU NDIYE BILAL

chukueni Wasudani, hakika watatu kutoka miongoni mwao ni mabwana wa peponi: Luqman mwenye hekima, Najashi na Bilal mwadhini.” Tabaraniy anasema: “Wasudani aliowakusudia ni Wahabeshi.”103 6.

Muhammad bin Hasan, kutoka kwa Muhammad bin Ali bin Mahbub, kutoka kwa Muawiya bin Hakim, kutoka kwa Sulayman bin Ja’far, kutoka kwa baba yake, amesema: Aliingia mtu mmoja miongoni mwa watu wa Sham kwa Abu Abdullah B, akamwambia: “Hakika wa kwanza aliyetangulia peponi ni Bilal.” Akasema: Kwa nini? Akasema: “Ni wa kwanza aliyetoa adhana.”104

7.

Kutoka kwa Ibn Abi Umayri, kutoka kwa Muawiya bin Hakim, kutoka kwa Abu Abdullah B, amesema: Abu Abdullah alisema: “Hakika wa kwanza aliyetangulia peponi ni Bilal.” Akasema: Kwa nini? Akasema: “Ni wa kwanza aliyetoa adhana.”105

8.

Kutoka kwa Sahli bin Saad, amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alisema: “Niliingia peponi, na mara nikahisi, kuangalia nikamkuta ni Bilal.”106 Na sisi tuna shaka na Hadithi hii, kwani hakuna yeyote atakayemtangulia Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 kuingia peponi, si Bilal wala si mwingine.

9.

Al-Hafidh ameandika kutoka kwa Sulayman bin Buraydah, amesema: Bilal aliingia kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 wakati akila chakula cha mchana. Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 akasema: “Tunakula riziki yetu, na ubora wa

Tahdhibu Taarikhu Damashqiy al-Kabir, Juz. 3, uk. 313.   Tahdhib, Juz. 2, uk. 284, Hadith ya 1133. Qamusir-Rijal, Juz. 2, uk. 396. 105   Tanqihul-Maqal, Juz. 1, uk. 182. Tahdhib, Juz. 2, uk. 284. 106   Majmauz-Zawaid, Juz. 9, uk. 299. Tahdhibu Taarikhu Damashqiy al-Kabir, Juz. 3, uk. 309. Siyaru Aalamin-Nubalai, Juz. 1, uk. 355. 103 104

54

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 54

4/23/2016 2:45:52 PM


HUYU NDIYE BILAL

riziki ya Bilal uko peponi. Unajua ewe Bilal kwamba, mwenye kufunga mifupa yake humsabihi Mungu, na Malaika humuombea maghufira?”107 10. Kutoka kwa Ibn Umar, amesema: Nilimbashiria Bilal, akaniambia: “Ewe Abdullah! Unanibashiria nini?” Nikasema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 akisema: “Bilal atakuja Siku ya Kiyama akiwa juu ya ngamia ambaye miguu yake ni kutokana na dhahabu, na hatamu yake ni kutokana na yakuti. Atakuwa na bendera ambayo itawaongoza waadhini. Atakuja nayo na kuwaingiza peponi, kiasi kwamba ataingia hata yule aliyeadhini siku arubaini tu kwa kutaka radhi za Mwenyezi Mungu.”108 11. Kutoka kwa Mtukufu Mtume 4 amesema: Bilal ataletewa ngamia miongoni mwa ngamia wa peponi, atampanda na kutoa adhana. Na hapo atamsadikisha kila aliyemsikia miongoni mwa Waumini, mpaka atakapoingia peponi. Na humo Bilal ataletewa nguo mbili miongoni mwa nguo za peponi na kuvishwa, hivyo wa kwanza atakayevishwa miongoni mwa waadhini ni Bilal, na waumini wema.109 12. Kutoka kwa Mtukufu Mtume 4 amesema: “Itakapofika Siku ya Kiyama, nitabebwa juu ya Buraq, na Fatimah atabebwa juu ya ngamia wangu al-Adhbau, na Bilal atabebwa juu ya ngamia miongoni mwa ngamia wa peponi, naye atakuwa akisema: ‘Allahu Akbar,” mpaka mwisho wa Adhana ambayo itasikiwa na viumbe wote.110   Majmauz-Zawaid, Juz. 9, uk. 300. Kanzul-Ummal, Juz. 11, uk. 654. Al-Muujam alAwsat, Juz. 4, uk. 375. 108   Tahdhibu Taarikhu Damashqiy al-Kabir, Juz. 3, uk. 313. 109  Tahdhibu Taarikhu Damashqiy al-Kabir, Juz. 3, uk. 313. 110   Tahdhibu Taarikhu Damashqiy al-Kabir, Juz. 3, uk. 313. Ansabul-Ashraf, Juz. 1, uk. 190. 107

55

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 55

4/23/2016 2:45:52 PM


HUYU NDIYE BILAL

13. Kutoka kwa Amru bin Aidh, kwamba Abu Sufiyan alikwenda kwa Salman, Suhaybu na Bilal wakati wakiwa katika kundi la watu. Wakasema: “Wallahi hazikuzuiliwa panga za Mwenyezi Mungu dhidi ya adui wa Mwenyezi Mungu kama zilivyozuiliwa dhidi yako.” Abubakri akasema: “Mnamwambia hili mzee wa kikuraishi na chifu wao?” Basi Abubakri akamfuata Mtukufu Mtume 4 na kumwambia habari hiyo, Mtume 4 akasema: “Ewe Abubakri! Huenda umewaudhi, na kama umewaudhi basi tambua kuwa umemuudhi Mola Wako.” Abubakri akawafuata, akasema: “Enyi ndugu zangu! Je nimekuudhini?” Wakasema: “Hapana. Mwenyezi Mungu akusamehe.”111 14. Kutoka kwa Ja’far, kutoka kwa baba yake, amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alisema: “Bilal atafufuliwa akiwa juu ya ngamia miongoni mwa ngamia wa peponi huku akiadhini: Nashahidilia kwamba hakuna Mungu isipokuwa Allah. Na hakika Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Akimaliza kuadhini atavishwa nguo miongoni mwa nguo za peponi.”112 Hadithi ya Mtukufu Mtume 4 kuhusu riziki ya Bilal: Kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 kwamba alisema kumwambia Bilal: “Chakula ewe Bilal.” Bilal akasema: “Mimi nimefunga.” Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 akasema: “Tunakula riziki yetu, na ubora wa riziki ya Bilal uko peponi. Unajua ewe Bilal kwamba, mwenye kufunga, mifupa yake humsabihi Mungu, na Malaika humuombea maghufira?”113   Sahih Muslim, Juz. 7, uk. 173. Al-Ghadir, Juz. 1, uk. 19. Taarikh Ibn Asakir, Juz. 5, uk. 21. 112   Al-Wasail, Juz. 4, uk. 617. 113   Sunan Ibn Majah, Juz. 1, uk. 556. Kanzul-Ummal, Juz. 9, uk. 247. Taarikh Madinat Damashqi, Juz. 1, uk. 464. 111

56

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 56

4/23/2016 2:45:52 PM


HUYU NDIYE BILAL

Hakika kuwepo tofauti kati ya kula kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 na kufunga kwa Bilal, kama inavyofahamika kutokana na riwaya iliyotangulia, huenda ni kwa sababu Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alikuwa ametoka safarini, au ni kwa sababu nyingine. Lakini lililo bayana ni kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alimbashiria Bilal ni wapi ulipo ubora wa riziki yake. Na akaendelea kuelezea kuhusu swaumu yake ili kuonesha ubora wa malipo ya mwenye kufunga. Na inaonekana Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alikuwa ana yakini na umakini wa Bilal katika kujua wakati, na ni kwa ajili hiyo Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 aliwaruhusu Waislamu waanze kujizuia katika swaumu wanaposikia adhana ya Bilal. Usia wa Mtukufu Mtume 4 kwa Bilal: Hapana shaka kwamba kitendo cha Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 kumpa Bilal usia makhususi, kinaashiria maana na mambo mengi yanayohusu jinsi alivyokuwa anamjali na kumpenda. Na hili ndilo alilokuwa analitamani kila swahaba wa Mtukufu Mtume 4, hata kama hilo linahusu hekima na utashi wa watu wenyewe. Na bila shaka ni kwamba kujipamba kwake na adabu za Uislamu, na kuyatumia kwake vizuri maarifa yake, kulichangia sana katika kujiongezea nafasi baina ya Waislamu. Kwa sababu upekee na umakhususi huu aliopewa na Mtukufu Mtume 4 unamuweka Bilal katika cheo kinachomfaa miongoni mwa Waislamu. Kwani unaonesha imani yake 4 kwake, kiasi cha kumuweka katika nafasi ya kufaidika na usia wa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 katika kujenga utu wake kiimani na kitabia. Miongoni mwa usia wake 4 kwa Bilal ni: 1.

Kutoka kwa Bilal, amesema kwamba, Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alimwambia: “Ewe Bilal! Kufa fakiri na wala 57

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 57

4/23/2016 2:45:52 PM


HUYU NDIYE BILAL

usife tajiri.” Nikamwambia: Nitawezaje kufanya hivyo ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: “Usiweke akiba unachoruzukiwa. Na usizuie unachoombwa.” Nikamwambia: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Nitakuwaje? Akasema: “Ni hivyo, au moto.”114 2.

Na imepokewa kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alimwambia Bilal: “Tambua, isikupite funga ya siku ya Jumatatu. Hakika mimi nilizaliwa siku ya Jumatatu, na nilifunuliwa wahyi siku ya Jumatatu. Nilihama siku ya Jumatatu na nitakufa siku ya Jumatatu.”115

3.

kwa Mtukufu Mtume 4 amesema: “Ewe Bilal! Hakuna amali bora kushinda jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu.”116

Ni mpokezi wa Hadithi za Mtukufu Mtume 4: Bilal alipata hadhi ya kupokea Hadithi za Mtukufu Mtume 4, hivyo kwa fadhila za ukaribu wake kwa Mtume 4, alipata hadhi ya kuchukua mafunzo yake na kujiongeza kwa Hadithi zake 4. Na jambo linalohitaji kutiliwa umuhimu ni lile tunalolipata katika vyanzo vya historia, kwamba Mtukufu Mtume 4 katika tukio zaidi ya moja, alikuwa akimgeukia Bilal kwa lengo la kumpa Hadithi au usia. Bila shaka jambo hili lina maana nyingi ambazo zilikuwa zinaongeza nafasi yake na ubora wake miongoni mwa Waislamu. Na hapa tunataja baadhi ya Hadithi zilizopokewa kutoka kwake: 1.

Kutoka kwa Bilal: Siku moja Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alitutokea ilihali ni mwenye tabasamu na kicheko, uso

Hilyatul-Awliyai, Juz. 1, uk. 150. Al-Ghadir, Juz. 8, uk. 375. Tahdhibu Taarikhu Damashqiy al-Kabir, Juz. 3, uk. 314. 115   Sirat Ibn Is’haq, uk. 130 – 131. 116   Tahdhibu Taarikhu Damashqiy al-Kabir, Juz. 3, uk. 315. 114

58

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 58

4/23/2016 2:45:52 PM


HUYU NDIYE BILAL

wake ukiwa umejaa furaha uking’aa kama mbalamwezi. Abdurahman bin Awfi akasimama na kusema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu! Hii nuru ni ya nini?” Mtume akasema: “Ni habari njema niliyoletewa na Mola Wangu kuhusu ndugu yangu na binamu yangu, kwamba Mwenyezi Mungu amemuozesha Fatimah kwa Ali..”117 2.

Kutoka kwa Bilal: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 akisema: “Waadhini ni waaminifu kwa Waumini juu ya Swala zao, nyama zao na damu zao. Hawamuombi Mwenyezi Mungu Mtukufu chochote isipokuwa huwapa. Na wala hawamuombei mtu katika jambo lolote isipokuwa hukubaliwa.”118

3.

Kutoka kwa Bilal: Kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alimwambia: “Usiadhini mpaka alfajiri itakapokupambanukia hivi.” Akanyoosha mkono wake kwa upana.119

4.

Kutoka kwa Bilal, amesema: Siku moja niliadhini wakati wa alfajiri yenye baridi kali, akaja Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 msikitini bila kumuona yeyote. Akasema: “Watu wako wapi?” Nikasema: Baridi imewazuia. Akasema: “Ewe Mungu Wangu! Waondolee baridi.”120

5.

Kutoka kwa Bilal: Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alisema: “Amkeni kwa ajili ya Swala ya Subhi, hakika ina malipo makubwa sana.”121

Usudul-Ghabah, Juz. 1, Uk. 206. Al-Ghadir, Juz. 2, Uk. 316. Qamusir-Rijal, Juz. 2, Uk. 237. Swawaiqul-Muhriqaha cha Ibn Hajar, Uk. 103. 118   Al-Amali cha Swaduq, Uk. 280. 119   Sunan Ibn Dawud, Juz. 1, Uk. 120. 120   Usudul-Ghabah, Juz. 1, Uk. 208. 121   Siyaru Aalamin-Nubalai, Juz. 1, Uk. 351. 117

59

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 59

4/23/2016 2:45:52 PM


HUYU NDIYE BILAL

6.

Kutoka kwa Bilal: Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alikuwa akilinganisha sawa mabega na nyayo zetu katika Swala.122

7.

Kutoka kwa Bilal: Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alisema: “Amkeni kwa ajili ya ibada za usiku, hakika huo ni mwenendo wa watu wema.”123

8.

Kutoka kwa Swanabahiyyu, amesema: Nilimuuliza Bilal kuhusu Laylatul-Qadri, akasema: “Ni usiku wa mwezi ishirini na tatu.”124

Nafasi ya Bilal katika kisa cha kupumzika usiku safarini: Baadhi ya wapokezi na wanahistoria wanataja kisa cha Taaris, yaani kulala na kupumzika kwa msafiri usiku. Wanasema: Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alipomaliza vita ya Khaybar, alianza safari kurejea Madina, akatembea usiku mpaka alipopatwa na usingizi, hivyo akaamua kupumzika na kulala, akasema: “Je hakuna mtu mwema atakayeyahifadhi macho yake bila kulala, ili atuhifadhie Swala ya Subhi isitupite?” Bilal akasema: “Mimi ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu!” Basi Bilal akaswali (swala za usiku) kadiri alivyowezeshwa. Na Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 na Maswahaba zake wengine wakalala. Ilipokaribia alfajiri Bilal alimwegemea mnyama wake ilihali akiwa kaelekea upande inapochomozea alfajiri. Mara usingizi ukamshinda akalala ilihali kaegemea mnyama wake, si Bilal wala Swahaba mwingine yeyote aliyeweza kuamka, mpaka walipopigwa na jua, na Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 ndiye aliyekuwa wa kwanza wao kuamka. Bilal anaelezea hali iliyompata, anasema: “Nilijifunika joho langu na nikaelekea upande inapochomozea alfajiri. Sijui ni wakati   Hilyatul-Awliyai, Juz. 10, Uk. 25.   Sunanul-Kubra, Juz. 2, Uk. 502. 124   Al-Muswannaf cha Ibn Shaybah, Juz. 2, Uk. 395. 122 123

60

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 60

4/23/2016 2:45:53 PM


HUYU NDIYE BILAL

gani hasa nilishikwa na usingizi na kulala, isipokuwa ni kwamba sikuamka isipokuwa kwa joto la jua na sauti za kauli ya watu ‘Hakika sisi ni wa mwenyezi Mungu, na hakika kwake Yeye tutarejea.’ Na hapo watu wakaanza kunilaumu, na Abubakri ndiye aliyenilaumu kwa ukali zaidi.” Kisha wao waliwalisha wanyama wao kidogo, kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 akatawadha na akamwamuru Bilal atoe adhana ya kwanza. Watu walipokusanyika, Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 akasema: “Rukuuni rakaa mbili za Alfajiri.” Kisha alimwamuru Bilal akimu, akakimu Swala, Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 akawaswalisha watu. Alipotoa salamu akawageukia na kusema: “Nafsi zetu zilikuwa mikononi mwa Mwenyezi Mungu, na laiti angetaka angezichukua moja kwa moja, naye ndiye Mmiliki wake. Lakini alipozirudisha kwetu tulisimama na kuswali.” Kisha akamwelekea Bilal na kumwambia: “Usijali ewe Bilal.” Bilal akasema: “Baba yangu na mama yangu wawe fidia kwako. Hakika aliichukua nafsi yangu Yule aliyeichukua nafsi yako.” Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 akawa anatabasamu.125 Sisi binafsi hatuungi mkono usahihi wa kisa hiki, hiyo ni kutokana na sababu kadhaa, nasi hapa tutataja baadhi yake kama ifuatavyo: Sisi tumekuta riwaya hii imepokewa pia kwa namna nyingine, na kuna mgongano na mpingano baina ya riwaya za kisa hiki, jambo linalojulisha kuwa kuna mikono iliyochezea kisa hiki, kwani imekuja katika baadhi ya nukuu, kwamba tukio hilo lilitokea wakati wa safari ya kuelekea Hudaybiya. Na katika nukuu nyingine imetajwa kuwa lilitokea katika Vita vya Tabuk. Na katika nukuu ya tatu ni kuwa lilitokea wakati wa kurejea kutoka katika Vita vya Hunayni,126   Al-Maghaziy, Juz. 2, uk. 711. Taratibul-Idariyyah, Juz. 1, uk. 77. Sunan Ibn Majah, Juz. 1, uk. 227. 126   Majmauz-Zawaid, Juz. 1, uk. 318 na 323. Sunan Abi Dawud, Juz. 1, uk. 122. 125

61

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 61

4/23/2016 2:45:53 PM


HUYU NDIYE BILAL

wakati ambao maelezo yaliyotangulia yanaonesha kuwa lilitokea wakati wa kurejea kutoka Khaybar. Ama uwezekano wa kuwa lilitokea zaidi ya mara moja katika sehemu tatu au nne tofauti, ukiachilia mbali kwamba hakuna ushahidi wala kigezo kinachounga mkono uwezekano huo, pia ni jambo lililo mbali zaidi. Na kwa upande mwingine, hakika baadhi ya nukuu zinatamka bayana kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 ndiye aliyekuwa wa kwanza kuamka kutoka usingizini. Na riwaya nyingine zinataja kuwa yeye Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 hakuamka isipokuwa kwa sauti za maneno kutoka kwa Maswahaba zake.127 Na tofauti iliyopo inadhihirika vizuri katika maelezo yaliyokuja kuhusu nafasi ya Bilal katika hilo linalodaiwa kutokea. Kwa mfano tu, nukuu ya kwanza tulioitaja inadai kwamba Bilal aliamua kukesha lakini akapitiwa na usingizi akalala. Wakati ambapo nukuu nyingine inasema: Aliyeamua kukesha na akapitiwa na usingizi hadi akalala ni Abdullah bin Masudi.128 Nukuu ya tatu inasema ni Dhumukhbir, naye ni mhabeshi ambaye alikuwa akimhudumia Mtume 4. Nukuu ya nne inasema ni Anas. Na zaidi ya hayo yote, kuna nukuu ya tano ambayo inatamka bayana kwamba watu saba wote walikuwa wameamua kukesha lakini wote wakapitiwa na usingizi na kulala.129 Zaidi ya hapo ni kwamba, katika nukuu nyingine kadhaa, kuna dokezo la kwamba hakuna yeyote aliyechukua jukumu la kukesha, kama inavyosema riwaya ya Abu Qatadah, ambayo inaeleza kuwa: “Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alisimama na sisi tukasimama. Kila mmoja akafanya dhiraa ya mnyama wake kuwa mto wake, na hatukuamka hadi jua lilipochomoza.” Na riwaya nyinginezo.130   Sunan Abu Dawud, Juz. 1, uk. 118. Nasburayat, Juz. 1, uk. 282 na 283. Siratun-Nabawiyyah cha Ibn Hisham, Juz. 3, uk. 355. 128   Majmauz-Zawaid, Juz. 1, uk. 319 – 320. Nasburayat, Juz. 1, uk. 282. 129   Majmauz-Zawaid, Juz. 1, uk. 319 – 320. 130   Sunan Abu Dawud, Juz. 1, uk. 119. 127

62

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 62

4/23/2016 2:45:53 PM


HUYU NDIYE BILAL

Baada ya hayo yote yaliyopita, itawezekanaje sisi tuamini hayo yaliyonasibishwa na Bilal? Hebu turudi katika nukuu yetu ya awali ili tuangalie mambo mawili: Kwanza: Hata tukijaalia kuwa Bilal alijitolea kukesha kisha akalala, je hili linawajibisha kumlaumu na kumbebesha uwajibikaji wote, kutokana na wao kupitiwa na usingizi kiasi cha kutoidiriki Swala? Wakati tunajua kuwa kupitiwa na Swala kutokana na usingizi si maasi, na wala si uzembe, bali uzembe ni pale mtu awapo macho, kama ilivyopokewa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4. Aidha, yamekuja maelezo katika moja ya nukuu za kisa hiki cha kulala na kupumzika, kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alisema baada ya Swala: “Hakika sisi tunamhimidi Mwenyezi Mungu, kwamba hatukupitwa na Swala yetu kwa sababu ya kujishughulisha na jambo lolote la kidunia. Lakini roho zetu zilikuwa mikononi kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na akaziachia pale alipotaka…”131 Ni kana kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alitaka kulisahilisha jambo hili kwa wale waliokuwa pamoja naye, na kuondoa hali ya wao kuona wametenda jambo baya sana. Hasa baada ya wao kuwa wameamka kutoka usingizini wakiwa na wasiwasi na woga kwa sababu ya Swala yao. Na huenda yeye 4 aliashiria katika maana hiyo kwa kauli yake: ‘Polepole, taratibu.”132 Alipowaona wakiwa katika hali hiyo. Na katika nukuu nyingine ni kwamba walipomlalamikia hali iliyowapata aliwaambia: “Hakuna kosa wala haidhuru.”133 Kisha ni kwa nini Abubakri ndiye awe mkali zaidi katika hilo kuliko Mtukufu Mtume 4, ambaye kwa mujibu wa nukuu hii tunamuona amemtabasamia Bilal?!   Al-Muswannaf cha Abdurazaq, Juz. 1, uk. 589. Majmauz-Zawaid, Juz. 1, uk. 320. Sahih Bukhar, Juz. 1, uk. 212 na 213. Nasburayat, Juz. 1, uk. 281 – 283. 132   Rejea mwanzo wa riwaya. 133   SahihBukhar, Juz. 1, uk. 213. 131

63

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 63

4/23/2016 2:45:53 PM


HUYU NDIYE BILAL

Pili: Ijapokuwa sisi hatuko katika kuhakiki suala la Mtukufu Mtume 4 kupitiwa na usingizi hadi kushindwa kuidiriki Swala ya Subhi, ila ni kwamba ni lazima tuashirie kwamba, kama hilo ni sahihi basi tafsiri yake ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu Ndiye aliyemlaza kwa huruma Yake, ili kuwahurumia watu, kwani kitendo hicho kimekuwa ni kigezo kwa ummah. Na kama isingekuwa hivyo, basi kila anayepitiwa na Swala ya Subhi kutokana na usingizi angekuwa analaumiwa na kutiwa dosari, na angekuwa anatuhumiwa kuwa hajali Swala yake.134 Adhama Nyingine ya Adhana ya Bilal: Miongoni mwa taufiki za Mwenyezi Mungu kwa Bilal ilikuwa ni kule kupigana na kuadhini kwake mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 katika vita na misheni mbalimbali, baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kuwa amemkabidhi yeye jukumu la adhana.135 Hivyo alikuwa akiadhini kwa ajili ya Swala kwa kuzingatia hali ya wapiganaji na uwezo wao wa kutekeleza Swala. Wanapokuwa katika mazingira ya vita basi huzingatia mazingira hayo. Alikuwa akitumia fursa inayopatikana kwa kuanza Adhana yake na takbira, ambayo ndio mwanzo wa wito wenye kuita kwenye Swala, na ambayo ndio kauli ya wapiganaji wanapokuwa ndani ya vita. Hivyo alikuwa akichanga sauti yake kwa ute wa hamasa ya kivita pamoja na ute wa kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu, Ambaye hatuna uwezo wa kuzidhibiti sifa za uwezo Wake na nguvu Zake na elimu Yake. Na Yeye ni Mjuzi wa kila kitu. Kisha ananadi kwa kushahidilia Umoja na Upweke wa Mwenyezi Mungu, na Utume wa Muhammad 4, wakati ambapo Waislamu wanalithibitisha hilo kivitendo katika medani ya vita. Hali hiyo inawazidishia azma na ari ya kuitetea dini ya Mwenyezi Mungu, na uimara juu ya itikadi yao ya haki. Kisha anawaita katika Swala,   Al-Wasail, Juz. 5, uk. 350. Qamusir-Rijal, Juz. 11, uk. 20.   Al-Maghaziy, Juz. 1, uk. 248, 371, 216, 217. Na Juz. 2, uk. 464, 472, 473, 582.

134 135

64

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 64

4/23/2016 2:45:53 PM


HUYU NDIYE BILAL

wito wa kutoka mbinguni (kutoka kwa Mwenyezi Mungu) kwenda kwa watu wa ardhini, na hivyo shauku ya Waumini kuitikia wito wa Mola Wao inaongezeka, na hapo wao wanawasilisha mahitaji yao na kumuomba ushindi dhidi ya maadui zao. Ama Adhana yake katika siku za Hijja, ilikuwa na mvuto wa kipekee, hasa pale alipopanda juu ya paa la Kaaba mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu 4, na kuanza kuichungulia kwa chini milima ya Makkah yenye kushuhudia jihadi yake na subira yake. Hivyo alipoanza wito wake wa Adhana, milima na vilivyomzunguka navyo vilirudia wito wake, kana kwamba vimechanga sauti yao katika sauti yake katika dimbwi la ukombozi na ushindi. Na katika nukuu zilizopokewa kuhusu hilo ni kwamba, Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alipomaliza ibada na matendo ya Hijja, aliingia Nyumba Tukufu. Aliendelea kuwemo humo mpaka Bilal alipoadhini kwa ajili ya Swala ya Dhuhri, akiwa juu ya paa la Kaaba.136 Na Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alikuwa amemwamrisha kufanya hivyo. Ama kuhusu Adhana yake huko Arafa mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 na Mahujaji wengine, imekuja kwamba, Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alihutubia huko Batni Arafa juu ya ngamia wake al-Qas’wau baada ya jua kukengeuka. Alipokuwa anakaribia kumaliza hotuba yake Bilali aliadhini na Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 akasitisha maneno yake. Baada ya Bilal kumaliza adhana yake Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 akaendelea na maneno na akashuka kutoka kwenye kipando chake. Bilal akakimu Swala na Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 akaswalisha Dhuhri. Kisha akakimu tena, Mtume 4 akaswalisha Alasari. Hivyo akakusanya pamoja Swala hizo mbili kwa adhana moja na Ikama mbili.137   Al-Maghaziy, Juz. 2, uk. 737 - 738.   Al-Maghaziy, Juz. 3, uk. 1102.

136 137

65

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 65

4/23/2016 2:45:53 PM


HUYU NDIYE BILAL

Faslu ya Nne MWENENDO WA JIHADI YAKE Tutazungumzia: 1.

Bilal na safari ya jihadi.

2.

Mwenyezi Mungu anampa uwezo dhidi ya aliyekuwa akimtesa.

3.

Ushujaa wake na kujitolea kwake.

4.

Kuhamia kwake Madina.

5.

Kurudi kwake Makkah kwa kishindo.

6.

Adhana ya Bilal yafunga ukurasa wa masanamu.

7.

Mpiganaji katika Nchi ya Sham.

8.

Bilal anamdhibiti Khalid bin Walid kwa kilemba chake.

Bilal na safari ya jihadi: Bilal alihudhuria vita vya Badri, Uhud, Handaki na vita vyote vingine pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu 4.138 Kushiriki kwake katika vita mbalimbali walivyopigana Waislamu chini ya uongozi wa Mtukufu Mtume 4, haikuwa isipokuwa ni mwendelezo wa safari ndefu ya kijadi na kujitolea katika njia ya Mwenyezi Mungu. Nayo   Al-Maghaziy, Juz. 1, uk. 155, Ansabul-Ashraf, Juz. 1, uk. 193. Tahdhibu Taarikhu Damashqiy al-Kabir, Juz. 3, uk. 304. Darajatur-Rafiah, uk. 363. Tabaqatul-Kubra cha Ibn Saad, Juz. 7, uk. 386. Tanqihul-Maqal, Juz. 1, uk. 182. Rijalutusiy, uk. 8. ManhajulMaqal, uk. 68.

138

66

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 66

4/23/2016 2:45:53 PM


HUYU NDIYE BILAL

ndio safari iliyoanzwa tangu hatua za mwanzo za utume wa Mtukufu Mtume 4. Pale Mushrikina walipommwagia kila aina ya mateso na maudhi hadi akakaribia mauti. Alishiriki katika vita wakati ambao Waislamu walikuwa wachache kwa idadi na nguvu. Na alishiriki katika vita wakati Waislamu ni wengi kwa idadi na nguvu. Alihudhuria katika matatizo ya vita na akaingia katika maeneo ya hatari, kutoka vita moja hadi vita nyingine. Kutoka katika mapambano haya hadi mapambano yale. Katika yote akitafuta radhi za Mwenyezi Mungu na kuimarisha nguzo za dini Yake. Hivyo maisha yake yote yalikuwa ni safari ya jihadi iliyojaa maana za imani na roho ya uthubutu, ushujaa na subira, bila kufuata matamanio ya nafsi wala kuipenda dunia. Mwenyezi Mungu anampa uwezo dhidi ya aliyekuwa akimtesa: Nayo ni ahadi ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake, kwamba atawapa ushindi na uwezo. Umayyah bin Khalaf, ambaye alikuwa akimtesa Bilal na kumtesa mfululizo, sasa anaangukia mikononi mwa Bilal katika vita vya Badri, naye Bilal anamuuwa. Imepokewa kutoka kwa Abdurahman bin Awfi, kwamba alisema: “Umayyah bin Khalaf alikuwa ni rafiki yangu huko Makkah, na wakati huo jina langu lilikuwa ni Abdu Amru. Niliitwa Abdurahman wakati niliposilimu. Hivyo alipokuwa akikutana na mimi wakati tukiwa Makkah, alikuwa akisema; ‘Abdu Amru, hivi kweli umeacha jina alilokupa baba yako?’ Nami nilikuwa nikimwambia: Ndiyo. “Alikuwa akisema: ‘Mimi simjui Rahman, basi weka jina jingine baina yangu mimi na wewe niwe nakuita kwa jina hilo. Kwani wewe huniitikii ninapokuita kwa jina lako la awali, na mimi siwezi kukuita kwa jina nisilolijua.’ Hivyo nikawa simwitikii anaponiita: Abdu Amru. 67

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 67

4/23/2016 2:45:53 PM


HUYU NDIYE BILAL

“Nikamwambia: Weka jina lolote unalolitaka ewe Abu Ali. Akasema: ‘Basi wewe ni Abdu Ilahi (mja wa Mungu).’ Nikamwambia: Ndiyo. Hivyo basi, akawa akiniita Abdu Ilahu (mja wa Mungu) kila ninapopita kwake. Nami nikawa namwitikia na kuzungumza naye. Mpaka ilipotokea siku ya Badri, nikapita kwake akiwa amesimama pamoja na mwanawe Ali bin Umayyah, amemshika mkono wake. Nami nikiwa nimebeba deraya baada ya kuziokota. Aliponiona akasema: ‘Ewe Abdu Amru.’ Lakini sikumwitikia, akasema: ‘Ewe Abdu Ilahi (mja wa Mungu).’ Nikasema: Ndiyo. Akasema: ‘Je naweza nikawa mateka wako? Mimi ni bora kwako kuliko deraya hizi ulizonazo.’ Nikasema: Ndiyo, njoo basi. “Nikatupa deraya nilizokuwa nazo mikononi, nikakamata mkono wake na mkono wa mwanawe Ali, ilihali akisema: ‘Katu sijapata kuona siku kama hii. Hamna haja yoyote na maziwa?’139 Nikatoka natembea nao.140Mara Umayyah bin Khalaf akaniambia: ‘Ewe Abdu Ilahi, miongoni mwenu ni nani anayejulikana kwa huruma aliyonayo kifuani mwake?’ Nikasema: Hamza bin Abdul-Muttalib. Akasema: ‘Yule ndiye aliyetutendea haya aliyotutendea.’141 Wallahi niliendelea kwenda nao mpaka Bilal alipomuona akiwa pamoja nami. Na yeye Umayyah ndiye aliyekuwa akimtesa Bilal huko Makkah ili auache Uislamu. Alikuwa akimpeleka kwenye changarawe za Makkah pindi jua linapokuwa kali, anamlaza chali kisha anaamrisha liletwe jiwe kubwa na kuliweka juu ya kifua chake, kisha anasema: ‘Utaendelea kuwa hivyo mpaka uachane na dini ya Muhammad.’ Lakini Bilal aliendelea kusema: ‘Mungu Mmoja wa pekee, Mungu Mmoja wa Pekee.’   Ibn Hisham anasema: Makusudio ya maneno hayo ni kwamba: Yeyote atakayenichukua mateka nitampa fidia ya ngamia mwingi wa maziwa. 140   Tahdhibul-Asmai Walughat, Juz. 1, uk. 136. Tanqihul-Maqal, Juz. 1, uk. 182. DairatulMaarif al-Islamiyyah, Juz. 4, uk. 73. Siratun-Nabawiyyah cha Ibn Hisham, Juz. 2, uk. 70 – 71. Rijalutusiy, uk. 87. Sharhu Nahjul-Balaghah cha Ibn Abil-Hadid, Juz. 14, uk. 135. Usudul-Ghabah, Juz. 1, uk. 207. 141   Yaani ndiye aliyepelekea tukawa mateka kwa ushujaa wake katika vita hivi – Mtarjumi.. 139

68

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 68

4/23/2016 2:45:53 PM


HUYU NDIYE BILAL

“Hivyo Bilal alipomuona pamoja nami alisema: ‘Kiongozi wa Ukafiri ni Umayyah bin Khalaf, sintasalimika kama utaendelea kuwa salama.’ Nikamwambia: Ewe Bilal, unasema hayo kwa mateka wangu? Akasema: ‘Sintasalimika kama wataendelea kuwa salama.’ Nikasema: Na unaongea waziwazi ewe mwana wa mwanamke mweusi?! Akasema: ‘Sintasalimika kama wataendelea kuwa salama.’ Kisha akanadi kwa sauti ya juu: ‘Enyi watetezi wa Mwenyezi Mungu! ‘Kiongozi wa Ukafiri ni Umayyah bin Khalaf, sintasalimika kama wataendelea kuwa salama.’ Mara tukazungukwa, wakatuweka katikati huku mimi nikimhami. Mmoja akampiga upanga mwanawe na hatimaye akadondoka. Umayyah akapiga ukelele ambao kamwe nilikuwa sijawahi kuusikia mfano wake. Nikamwambia: Jiokoe mwenyewe, na wala hakuna uokovu. Wallahi sikufai chochote. Basi wakawakatakata kwa panga zao mpaka wakawamaliza. Hivyo Abdurahman (anajikusudia yeye mwenyewe) alikuwa akisema: Mwenyezi Mungu amrehemu Bilal. Deraya zangu zilikwenda na akaniumiza moyo kwa mateka wangu.”142 Imepokewa kwamba Abu Umayyah bin Khalaf, alisema huku akiwa juu ya ngamia wake siku ya Badri: “Je mnajua ni nani mnayepigana naye? Hivi hamkumbuki maziwa?” Bilal akasema: “Ewe Umayyah naapa kwa Mola wa Kaaba, sintasalimika kama utaendelea kuwa salama.” Akampigisha magoti ngamia wake, kisha akampiga pua yake, akaikata na hatimaye akafa. 143 Na Abu Muhammad Shaqratisiy amesema katika kaswida yake mashuhuri: “ Bilal alipata mateso kutoka kwa Umayyah, lakini subira aliyokuwanayo ilimfikisha mahali patukufu.   Taarikhul-Umam Wal-Muluk, Juz. 2, uk. 452. Siratun-Nabawiyyah cha Ibn Hisham, Juz. 2, uk. 632. Taarikhul-Islam cha Dhahbiy, uk. 39. 143   Ansabul-Ashraf, Juz. 1, uk. 191. 142

69

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 69

4/23/2016 2:45:53 PM


HUYU NDIYE BILAL

Walimtesa kwa matatizo ya utumwa, naye katika misukosuko ya shida alivumilia bila kuteleza. Walimlaza kwa kulalia uso wake, katika changarawe za moto, na wakaweka mawe mazito juu yake. Naye aliendelea kumpwekesha Allah kwa moyo mmoja. a mgongoni kwake kukadhihiri makovu makubwa N yasiyofichika. Yalidhihiri makovu kwa Walii wa Mwenyezi Mungu mgongoni kwake. aye akauchana moyo wa adui wa Mwenyezi Mungu kifuani N kwake.”144 Na kuhusu yeye alisema mshairi siku ya Badri: “Hongera. Mwingi wa huruma akuzidishie kheri. Bila shaka umeipata kheri yako ewe Bilal. Hukupata udhaifu wala uoga, hukuwa chakula cha mishale mikali.”145 a pia kuhusu yeye umekuja ubeti katika shairi la Ghulami N kuhusu watu wa Badri; “Kisha mwadhini wa Mtume Hashimaya, Bilal mwenye tabia na maadili matukufu.”146   Al-Istiaab, Juz. 1, uk. 144. Al-Iswabah, uk. 3.   Ansabul-Ashraf, Juz. 1, uk. 193. Darajatur-Rafiah, uk. 363. Tahdhibul-Asmai Walughat, Juz. 1, uk. 136. Zahrul-Adab, Juz. 1, uk. 72. 146   As’habul-Badri, uk. 106. 144 145

70

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 70

4/23/2016 2:45:53 PM


HUYU NDIYE BILAL

Ushujaa wake na kujitolea kwake: Bilal alikuwa na fungu kubwa la ushujaa na subira pembeni ya nguvu ya kiroho na kimwili. Bilal hakuitumia katika shari au batili zawadi hii aliyopewa na Mungu. Na wala hakuiacha iwe mateka wa matamanio yake, bali aliielekeza katika mwelekeo sahihi. Katika njia ya uongofu na kutekeleza ujumbe. Hivyo akafanya subira juu ya maudhi makali na maumivu machungu, mbele ya Makurayshi wenye kumchapa mijeledi. Na hatimaye akajitofautisha na wenzake na kuwakabili mpaka mwisho wale waliokuwa wanamtesa. Akawapa changamoto ndani ya majumba yao, akaamsha hasira na ghadhabu zao mpaka akawa ndani ya moyo wa kila mtesaji, na ndani ya roho ya kila Mwislamu. Wanavuna nguvu kutoka katika msimamo wake na wanajifunza kutoka katika subira yake somo la kufanya subira wakati wa mateso makali zaidi. Imepokewa kwamba, wachapaji mijeledi wa Kikurayshi walikuwa wakimwambia: “Dini yako ni Lata na Uzza.” Yeye anawaambia: “Mola Wangu ni Allah, Mmoja wa pekee, Mmoja wa pekee.” Kisha anasema: “Wallahi ningekuwa najua neno lenye kuwachukizeni zaidi ya hili ningelisema.”147 Hivyo japokuwa anatishwa kwa mauti, na hakuna wa kuweza kuzuia mijeledi iliyokuwa inakula mgongo wake, huku changarawe za moto zikimchoma, lakini bado unamuona anawapa changamoto, na anajitahidi kuwaghadhibisha kadiri awezavyo. Na kwa kweli hakupata neno zito zaidi juu ya Mushrikina, wala kitendo chenye kuwakera zaidi kushinda kauli yake: Mungu Mmoja wa pekee. Mungu Mmoja wa pekee. Maneno haya yalikuwa yakishuka katika nyoyo zao kama mijeledi, yakiwaumiza sana na kuwakera mno. Hivyo akaweza kuwafanya   Tahdhibu Taarikhu Damashqiy al-Kabir, Juz. 3, uk. 307.

147

71

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 71

4/23/2016 2:45:53 PM


HUYU NDIYE BILAL

mateka ilihali yeye ni mwenye kufungwa kamba. Kalazwa juu ya changarawe za moto, lakini anawaadhibu kwa kauli yake: Mungu Mmoja wa pekee. Mungu Mmoja wa pekee. Ili kwa hali hiyo achore sura ya kuvutia zaidi katika uvumilivu na subira. Na subira yake hii ni alama tosha ya ushujaa wake. Kiongozi wa Waumini Ali B anasema: “Subira ni ushujaa.”148 Ama ushujaa wake vitani, ulionekana na kudhihiri bayana katika vita vya Badri, navyo ni vita vikubwa walivyopigana Waislamu pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu. Alipigana bila hofu wala woga. Akaua aliowaua na akawageuza mateka wale aliowageuza. Na miongoni mwa aliowauwa ni Umayyah bin Khalaf ambaye alimtesa huko Makkah. Abu Bakri akamwambia: “Hongera. Mwingi wa huruma akuzidishie kheri. Bila shaka umeipata kheri yako ewe Bilal. Hukupata udhaifu wala uoga, hukuwa chakula cha mishale mikali. Wanapoogopa wanaume, wewe hubaki thabiti. Mpaka ushiriki wewe katika lile waliloogopa wanaume.”149 Ni kheri ya Mwenyezi Mungu ewe Bilal: Walitaka kubomoa Uislamu wako, mara wewe ukawa ndiye mtetezi wake. Na kauli “Mungu Mmoja wa pekee. Mungu Mmoja wa pekee”, ni muhtasari wa kila lugha ya uvumilivu wako na imani yako. Neno lako ni moja lakini liliwatikisa na kuwaangusha katika changamoto. Hawa hapa wanatumia kila aina ya silaha zao dhidi yako, la  Nahjul-Balaghah, Juz. 4, uk. 3, Hekima ya 4.   Ansabul-Ashraf, Juz. 1, uk. 193. Darajatur-Rafiah, uk. 363. Zahrul-Adab, Juz. 1, uk. 72.

148 149

72

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 72

4/23/2016 2:45:53 PM


HUYU NDIYE BILAL

kini wewe unatumia neno: “Mungu Mmoja wa pekee. Mungu Mmoja wa pekee.” Na ndiyo silaha zako zote. Walitaka uendelee kuwa mtumwa duni bila uhai, lakini ukabadilika na kuwa wimbo mzuri na mnara wenye nuru. Uliwatia hasira mpaka ukafikisha kisu chako katika mfupa. Na ulifanya subira katika dini yako mpaka wakatambua kwamba, imani uliyonayo na dini unayobeba, haidhibitiwi kwa mijeledi na changarawe za moto, na wala kwa hikdi za wachapaji mijeledi. Umayyah hakukutesa ewe Bilal, licha ya kukumiminia mijeledi yake, lakini kilichokutesa hasa ni shirki, muhtasari wa shirki, ujahiliya, hikdi na unyama. Na wala mkono wako haukummaliza, hata kama ulimpiga kwa upanga wako, lakini kilichommaliza hasa ni Uislamu, roho ya imani, uadilifu na huruma. Uislamu uliobebwa na mafakiri na wale wenye kuteswa ndani ya nyoyo zao, unaandika somo jipya kupitia mikono yako. Na sasa Bilal ndiye anayemuuwa Umayyah bin Khalaf, kwa malipo na si kwa bahati mbaya. Watumwa ambao walilazwa chini ya mijeledi, ndio ambao sasa wanawauwa wale waliokuwa wakiwachapa mijeledi. Wenye kuteswa ambao walikandamizwa chini ya nyayo za ukandamizaji, ndio ambao leo hii wanawaadhibu wale waliokuwa wakiwatesa. Kuhamia kwake Madina: Baada ya mateso na ukandamizaji wa muda mrefu, na baada ya ujeuri wa mabwana wa Kikurayshi, na kuongezeka ugumu wa mazingira kwa Waislamu, Mtukufu Mtume 4 aliwaamuru Waislamu kuhamia Yathrib. Na Bilal alihama pamoja na Ammar bin Yasir, Saad bin Abu Waqas na Abdullah bin Mas’ud, kabla ya kuhama kwa Mtukufu Mtume 4.150   Taarikhus-Swaghir, Juz. 1, uk. 52.

150

73

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 73

4/23/2016 2:45:53 PM


HUYU NDIYE BILAL

Alipofika Madina, alifikia kwa Saad bin Khaythamah,151 na akapata hadhi ya kulindwa na kufanyiwa umuhimu kama wahajiri wengine. Na haukupita muda mrefu akaungana tena na Mtukufu Mtume 4 baada ya yeye 4 kuhama Makkah, ili akaukusanye ummah na kuupa nguvu ujumbe na kuunda Dola ya Kiislamu huko Madina. Bilal aliishi katika vipindi vyote hivi ambavyo vilishuhudia nguzo za dini zikiimarishwa, undugu wa Muhajirina na Ansari ukipatikana, daawa ikienezwa, sharia zikifundishwa, na nguvu zikikusanywa ili kuingia katika mapambano na kufika Makkah. Kurudi kwake Makkah kwa kishindo: Baada ya miaka nane ya kuhama, Waislamu waliongezeka na wakaungana watu kutoka kila pembe ya karibu na mbali. Walisukumwa na hisia zao na matarajio yao, wakaunda jeshi la maelefu ya askari. Jeshi kamili lililo tayari kwa kila kitu. Na kwa ishara kutoka katika vidole vya Mtume wake, ujumbe uliwakusanya ikiwa ni pamoja na mateso na machungu, utiifu na wajibu waliokuwa nao. Mtume 4 akatangaza safari ya kuelekea Makkah, na mara vinywa vikafumbuka, macho yakang’aa na huzuni ikafunguka. Wapiganaji wakachukua nafasi zao na Bilal akawa pembeni ya Mtume wa Mwenyezi Mungu 4, akitafakari kwa kina je macho yake hayaongopi kwa kile yanachokiona?! Ile ndio Makkah, kwa Nyumba yake Tukufu na nyumba zake. Sasa kumbukumbu inafunguka mbele ya macho yake, lakini hofu yake kwa Mungu na matumaini vinamtuliza. Siku zote za nyuma zinapita katika kumbukumbu yake na haraka sana zinatoweka katika kumbukumbu yake. Kwa nini Bilal asisadiki wakati Mwenyezi Mungu ameahidi kumnusuru yule atakayemnusuru Yeye?! Hakika sasa yuko pembezoni mwa Makkah, anarudi Makkah, amevaa silaha kwa maandalizi   Ansabul-Ashraf, Juz. 1, uk. 187. Tabaqatul-Kubra cha Ibn Saad, Juz. 3, uk. 233.

151

74

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 74

4/23/2016 2:45:53 PM


HUYU NDIYE BILAL

kamili, kifua mbele, wakati ambapo alitoka akiwa mwenye hofu na mwenye kukandamizwa. Leo yuko pamoja na nani? Yuko pamoja na Muhammad, kiumbe bora kuliko wote ardhini. Naye yuko pembeni yake na mikononi mwake, na wala si safu ya mbali wala sehemu za nyuma, ambako anatoa juhudi zake zote ili macho yake yamuone kiongozi. Bali hakika yeye yuko kwake, pamoja naye na macho yao wote wawili kwa pamoja yanaitazama Makkah. Kuna tofauti kubwa kati ya jana na leo. Ni mtukufu mno muumbaji wa uhai, ambaye ameshikilia funguo za nyakati na mwendo wake. Ambaye anaandaa sababu za kumpa mtu nguvu na ushindi. Bilal anatazama lile kundi dogo lililohangaika katika kutafuta hifadhi huku na kule, analiona ni kundi kubwa imara linalong’ara kwa roho ya ari na imani. Ni nani mwenye uhuru zaidi, hamasa na saada leo hii, kumshinda Bilal?! Hakika ni Bilal mpya aliyepo katika milima ya Makkah. Si Bilal yule aliyemwamini Muhammad 4 kwa akili yake na maumbile yake, na akatangaza mapenzi yake kwake mwanzo kabisa. Si Bilal yule hata kama bado ni mwenye kulinda maumbile yake haya na hajaachana na akili yake. Bilal anayeingia Makkah leo ni mtu ambaye maisha yamemkomaza na tajriba imemuimarisha. Matatizo na misukosuko vimemfanya imara zaidi, mpaka kwamba undani wake unaonekana kwa nje. Bilal wa leo ni mzoefu na ni mjuzi wa mambo yanavyokwenda. Amekusanya uwelewa kwenye uimara wake, na elimu kwenye kujitolea kwake, hivyo zimekamilika pande hizo kwake, mpaka amekuwa ni mtu mwenye kutegemewa. Na leo hii wote wanaiona nafasi yake na ukaribu wake kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4. Saa za jeshi kusonga mbele zinakaribia, tena katika mwezi wa utiifu na jihadi, na Bilal anazidi kupatwa na shauku na anatikiswa 75

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 75

4/23/2016 2:45:53 PM


HUYU NDIYE BILAL

na ari ya kutaka kufika mahala alipokulia. Vikosi vilivyoizunguka Makkah vinajiandaa na mara vinaanza kusonga mbele. Jeshi lote ni askari mmoja, linatamka neno moja, nalo ndio mishipa ya damu ya Uislamu na roho yake na lengo lake: “Lailaha Ilallah.” Na mara Makkah inaamka kwa neno hili ambalo wakati wowote watu wa Makkah wanapolisikia humpiga mawe mwenye kulitamka. Humwadhibu, humtesa na kumfukuzia mbali. Lakini leo hii wanajua kwa yakini kabisa kwamba “Lailaha Ilallah” na Mungu wa Muhammad Ndiye aliyeshinda. Na kwamba miungu yao ya uwongo walioitengeneza kwa mikono yao imeshateketea zamani. Hakika ni wakati wa ukombozi, lakini ni ukombozi bila silaha, bila hata kutikiswa au upanga kuchomolewa, au mikuki kurushwa. Ni “Lailaha Ilallah” tu ndio silaha yenye uwezo kushinda silaha zote. Na sasa Makkah inarudi mikononi mwa Uislamu. Ni wakati wa ushindi uliojengwa juu ya msingi wa imani. Hivyo utaendelea kuwepo mpaka Siku ya Kiyama. Sasa Muhammad yumo ndani ya Makkah, na yuko pamoja na jeshi la wale watembea peku ambao waligandamizwa kwa kila aina ya ugandamizaji. Wamekuja kusaidia kutengeneza muujiza. Toa takbira ewe Bilal….. Toa takbira ewe Bilal. Panga ziko tayari kwa lolote lile, lakini makali yake yametengenezwa kwa huruma iliyoletwa na Uislamu, kwa mikono ya Muhammad 4. Leo ni siku ya huruma. Leo ni siku ya uhuru. Toa takbira ewe Bilal. Muhammad 4 anatangulia mbele na jeshi linazidi kutisha kwa mkusanyiko wake. Na Bilal yuko kwa kipenzi chake anamfungulia njia katikati ya makundi yaliyokusanyika, nayo yamenyanyua shingo kwa hamu ya kutaka kumuona anayekuja. Na ndimi zao zinazungumzia upande atakaoelekea na kuishia safari yake. Mtukufu Mtume 4 anakatiza katikati ya makundi kutokea sehemu ya juu ya Makkah. Anaelekea Nyumba ya kale na mashukio ya Manabii na 76

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 76

4/23/2016 2:45:54 PM


HUYU NDIYE BILAL

Malaika. Anaingia katika Nyumba hiyo na watu wachache miongoni mwa Maswahaba zake, kwa ajili ya Swala. Na Bilal alikuwa ni mmoja kati ya walioingia, na Bilal ndiye aliyefunga mlango.152 Mtukufu Mtume 4 anakaa ndani ya Nyumba hiyo muda mrefu. Na mara Mtume wa rehema anasimama kwenye mlango wa Kaaba na kusema: “Hapana mungu isipokuwa Allah peke Yake. Amesadikisha ahadi. Amemnusuru mja Wake na ameyashinda makundi peke Yake.” Ushindi wa Mungu unakamilika na hatimaye masanamu yanavunjwavunjwa. Na sauti ya Abu Jahli na za vigogo wote wa shirki zinanyamaa. Na nafsi zote, nyumba na mitaa yote, zinanyenyekea kwenye sauti ya Bilal, mwenye kuadhini Allahu Akbaru… Allahu Akbaru. Adhana ya Bilal yafunga ukurasa wa masanamu: Ukaingia wakati wa Dhuhri ilihali watu wamejaa kwa kuizunguka Kaaba. Mtukufu Mtume 4 akamwamuru Bilal apande kwenye paa la Kaaba na kutoa Adhana.153 Ili Adhana hiyo ya Mungu ipae kwa mara ya kwanza katika pande zote za Makkah. Bilal ndiye mwadhini pekee aliyepata hadhi hii, na aliyepata heshima hii na kuhodhi utukufu huu. Inamaanisha nini Adhana kutolewa toka juu ya paa la Kaaba kwa mara ya kwanza? Hakika ni tukio la kipekee la kihistoria. Linatangaza ushindi wote, linatoa taarifa ya kuanza zama nyingine na kipindi kipya kilichotokomeza kila kitu, ikiwa ni pamoja na asili kutoka kwenye itikadi za ujahiliya na ada zake za kuabudu masanamu. Na hivyo kwa Adhana ya Bilal yalianguka masanamu ya Makkah, moja baada ya jingine.154   Sahih Bukhari, Juz. 4, uk. 15; Musnad Ahmad, Juz. 2, uk. 3; Sahih Muslim, Juz. 4, uk. 96. 153   Al-Maghaziy, Juz. 2, uk. 846; Dairul-Maarif, Juz. 4, uk. 73; Majmaul-Bayan, Juz. 5, uk. 136; Tahdhibu Taarikhu Damashqiy al-Kabir, Juz. 3, uk. 314. 154   Safinatul-Bihar, Juz. 1, uk. 104. 152

77

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 77

4/23/2016 2:45:54 PM


HUYU NDIYE BILAL

Hakika ni siku kati ya siku za Mwenyezi Mungu. Ameyashinda masanamu na dini Yake mpya imechukua nafasi yake ili iweze kufika katika kona zote za ardhi. Kitendo cha Bilal kuadhini siku ya ukombozi, mbele ya masikio na macho ya masanamu ya kibinadamu yenye kutembea, ambayo yalitambua ukubwa wa ushindi huu juu yao na juu ya washirika wao, madhalimu na mabeberu wao, ni ujumbe mzito wenye kubeba maana ya kina. Nyuso za watu wa Makkah zilishuhudia mtumwa wa Bani Jamhi,155 Bilal Mhabeshi, ambaye hakuwahi kuwa na nafasi wala umuhimu wowote katika fikra zao. Na wala hawakumtazama isipokuwa kama mtumwa na bidhaa isiyo na thamani, wao na wale waliopo katika mgongo wa ardhi tukufu zaidi, leo hii wamemshuhudia akitangaza nyakati za kushindwa kwao na kuanguka kwao. Wakaungua kwa ghadhabu kutokana na tukio hili la kutisha, ambalo liliwapa mshtuko mkubwa. Tukio la mtumwa kutangaza kuporomoka kwa mabwana. Inakuwaje hawa watumwa ambao hawamiliki jaha wala dhahabu wala nafasi za ubwana, wanaweza kuwashinda mabwana wenye nafasi na nasaba za ubwana. Wenye kuzungukwa na mali, silaha na mamlaka?! Hivi wamefahamu kweli hawa, kwamba leo hii neno ni la Mwenyezi Mungu na waja Wake wenye ikhlasi, na si silaha, mali na uwezo? Hakika tukio lile lilikuwa ni sawa ni tetemeko kubwa lililoitikisa jamii ile ya kijahiliya tangia kwenye asili. Na yanayowasilishwa na riwaya zinazozungumzia tukio lile yanaonesha kiwango cha hasira na ghadhabu zilizochukua nafasi katika nafsi za Makuraishi. Khalid bin Said bin al-Aswi alisema: “Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu aliyemtukuza baba yangu kwa kutokuwepo katika siku hii.”   Al-Maghaziy, Juz. 2, uk. 846.

155

78

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 78

4/23/2016 2:45:54 PM


HUYU NDIYE BILAL

Harith bin Hisham alisema: “Ooh mama yangu. Natamani ningekufa kabla ya siku hii, kabla sijamsikia Bilal akipaza sauti ya kunguru juu ya Kaaba.” Hakam bin Abul-Aswi alisema: “Wallahi hili tukio adhimu, kwamba mtumwa wa Bani Jamhi sasa anapaza sauti juu ya nyumba yake.”156 Wengine walisema: “Kwa nini mtumwa huyu mweusi anaadhini juu ya paa la Kaaba?”157 Na katika riwaya nyingine, ni kwamba baadhi yao walisema hapo: “Kuingia chini ya ardhi ni bora kuliko kumsikia huyu.”158 Mpiganaji katika Nchi ya Sham: Umri ulisonga mbele, na akawa hawezi kubaki Madina baada ya kifo cha kipenzi chake Muhammad 4, na baada ya kujitokeza mambo ambayo hakuwa na uwezo wa kukabiliana na matokeo yake wala kuvumilia athari zake. Hivyo ilikuwa ni wajibu kwake kuchafua uwanja atakaokwenda kumalizia umri wake uliobakia. Alikuwa hajasahau wosia wa Mtukufu Mtume 4: “Ewe Bilal! Hakuna amali bora kuliko jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu.”159 Maamuzi ni ya mtu mwenyewe, na hatima ya umri wa mtu huichagua mwenyewe kwa utashi wake. Ni mtu mwenyewe husema: Nataka kupambana katika njia ya Mwenyezi Mungu mpaka nife.160   Al-Maghaziy, Juz. 2, uk. 846; Darajatur-Rafiah, uk. 365; Siyaru Aalamin-Nubalai, Juz. 1, uk. 356. 157   Tahdhibu Taarikhu Damashqiy al-Kabir, Juz. 3, uk. 314. 158   Safinatul-Bihar, Juz. 1, uk. 104; Majmaul-Bayan, Juz. 5, uk. 136. 159   Tahdhibu Taarikhu Damashqiy al-Kabir, Juz. 3, uk. 315. 160   Tahdhibu Taarikhu Damashqiy al-Kabir, Juz. 3, Uk. 316. Usudul-Ghabah, Juz. 1, Uk. 207. 156

79

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 79

4/23/2016 2:45:54 PM


HUYU NDIYE BILAL

Alishuhudia ukombozi wa Sham,161 na aliishi humo kama mpambanaji.162 Licha ya kwamba alikuwa na umri mkubwa lakini alikuwa anaungua kwa shauku ya kutaka kuitetea dini ya Mwenyezi Mungu kwa upanga na neno. Hivyo alisimama miongoni mwa Waislamu akiwahutubia na kuwaita na kuwasisitiza kubeba silaha na kupigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu. Ushahidi juu ya hilo ni ile nukuu iliyopokewa kutoka kwa Amru bin Mirdas, ambaye alisema: Nilifika Sham katika moja ya safari zangu, mara nikamuona mtu mwenye midomo na pua ngumu, mbele yake kukiwa na silaha, huku akisema: “Enyi watu! Chukueni silaha hii na muiandae. Na piganeni katika njia ya Mwenyezi Mungu. Hivyo ndivyo alivyosema Mtume wa Mwenyezi Mungu 4.” Nikasema: Huyu ni nani? Wakasema: “Ni Bilal.”163 Bilal anamdhibiti Khalid bin Walid kwa kilemba chake: Watu wengine wanaweza kuthibitisha ujasiri wa Bilal kwa msimamo wake aliouchukua dhidi ya Khalid bin Walid, pindi alipomrukia akampokonya kilemba chake akakikunjua na kumdhibiti kwacho Khalid. Kama si ujasiri, anawezaje Bilal kumvua Khalid kilemba? Na anawezaje kumfunga mikono yake miwili wakati Khalid anajulikana kwa nguvu na ubabe wake. Naye ni mwenye kuheshimika kwa watu wake na mwenye nafasi kwa Waislamu?! Inawezekana wengine wakawa wanatafakari kuhusu usahihi wa kisa hiki hata kiwe ni ushahidi juu ya ujasiri huo. Lakini sisi hatutaki kuzama katika maeneo ya tafakari hiyo, na tunatosheka na kutaja yaliyotokea kama alivyoyataja Ibn Asakir ndani ya kitabu chake cha historia, Tarikh Ibn Asakir:   Dairul-Maarif, Juz. 4, uk. 73.   Tahdhibul-Asmai Walughat, Juz. 1, uk. 136; Tabaqatul-Kubra cha Ibn Saad, Juz. 3, uk. 234; Al-Iswabah, Juz. 1, uk. 165. 163   Musnad Ahmad, Juz. 3, uk. 16. 161 162

80

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 80

4/23/2016 2:45:54 PM


HUYU NDIYE BILAL

Ash’ath alimuomba zawadi Khalid kiasi cha (dinari au dirham) ishirini, naye akamruhusu kuchukua elfu kumi. Na hakuna kilichokuwa kinafichikana kwa Umar katika matendo ya Khalid. Alikuwa (Umar) anaandikiwa barua kuelezwa ni nani aliyetoka Irak, na ni nani aliyepewa zawadi huko Sham. Hivyo alimwita tarishi wake na akampa barua kwenda kwa Abu Ubaydah, kwamba amsimamishe Khalid, amfunge mikono kwa kilemba chake na amnyang’anye kofia yake, mpaka awaeleze ni kutoka katika mali ipi amemruhusu Ash’ath kuchukua zawadi. Je ni kutoka kwenye mali ya Mwenyezi Mungu au mali yake binafsi? Au ni kutoka katika ngawira aliyoipata? Kama atakiri na kusema kuwa ni kutoka katika ngawira, basi atakuwa amekiri kufanya khiyana. Na kama atadai kuwa ni kutoka kwenye mali yake binafsi, basi atakuwa amefanya ubadhirifu, na hivyo muuzulu katika hali yoyote ile, na ongeza majukumu yake kwenye majukumu yako. Abu Ubaydah akamwandikia ujumbe Khalid. Alipofika kwake, aliwakusanya watu na akaketi juu ya mimbari. Tarishi akasimama na kusema: “Ewe Khalid, je ni kutoka katika mali yako binafsi umeruhusu elfu kumi, au ni kutoka katika ngawira?” Khalid hakumjibu licha ya kurudia mara kadhaa swali hilo. Wakati huo Abu Ubaydah alikuwa kanyamaza kimya hasemi kitu. Ndipo Akasimama Bilal mbele yake na kusema: “Hakika Kiongozi wa Waumini ameamuru ufanywe hivi na vile.” Kisha akamnyang’anya kilemba chake, akakikunjua, bila kuzuiliwa na usikivu na utiifu. Kisha akamvua kofia yake akamsimamisha na kumfunga mikono kwa kilemba chake. Kisha akamwambia: “Unasemaje? Ni kutoka kwenye mali yako binafsi au kutoka kwenye ngawira?” Akasema: “Si kutoka kwenye mali yangu.”164   Tahdhibu Taarikhu Damashqiy al-Kabir, Juz. 5, Uk. 111. Al-Kamil Fii Taarikh, Juz. 2, Uk. 375.

164

81

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 81

4/23/2016 2:45:54 PM


HUYU NDIYE BILAL

Faslu ya Tano UTU WA BILAL Tutazungumzia: 1.

Sin ya Bilal.

2.

Bilal ni kama nyuki.

3.

Bustani ya elimu katika hadithi ya Bilal.

4.

Tunachojifunza kutoka katika Hadithi hii.

5.

Hebu tuzungumzie roho yake yenye hisia za kweli.

6.

Beti zinazonasibishwa na Bilal.

7.

Mtu mweusi hataingia peponi.

8.

Ni nani aliyeshinda?

9.

Ni miongoni mwa waliomsadiki.

10. Kupata kwake medali ya ukweli. 11. Kuoa kwake. 12. Mtukufu Mtume anamwozesha Bilal. 13. Ubaguzi warudi upya. Sin ya Bilal: Ni mashuhuri kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 kwamba alisema: “Sin ya Bilal ni Shin mbele ya Mwenyezi Mungu.� 82

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 82

4/23/2016 2:45:54 PM


HUYU NDIYE BILAL

Kutokana na riwaya mbalimbali inaonekana kwamba Bilal alikuwa akibadili Shin katika tashahudi yake kwa kuitamka kwa Sin. Badala ya kusema Ash’hadu alikuwa akisema As’hadu. Na baadhi ya watu walikuwa wakimdhihaki kwa hilo na wakizingatia kuwa ni upungufu na kasoro, na wanajaribu kushusha hadhi yake. Hiyo ni kwa sababu watu ambao ni madhaifu wa imani na nafsi wao jambo wanalolijali na kulitilia umuhimu ni muonekano wa nje na si zaidi. Hicho ndicho kigezo na kipimo cha maamuzi yao na ndio msingi wa mitazamo yao juu ya vitu. Ama Uislamu wenyewe unazingatia uchamungu kuwa ndio kipimo na kigezo. Na ni kwa msingi wa uchamungu ndio unapatikana ubora baina ya watu, na si kwa msingi wa ndimi zao au mavazi yao au rangi ya ngozi zao na mfano wa hayo. Kwani mambo hayo hayaakisi sura ya nafsi na moyo kama hayakuambatana na tabia ya matendo na vitendo. Hakika hayo ni sawa na maganda ya tunda ambalo linaweza kuwa tamu au chungu. Imam as-Sadiq B anasema: “Utamkuta mtu asiyekosea Lam wala Waw, ambaye ni hatibu hodari na bingwa, moyo wake una giza zito kushinda hata giza la usiku mnene. Na utamkuta mtu ambaye hawezi kueleza hata yale yaliyomo ndani ya nafsi yake, anang’aa kwa nuru kama inavyong’aa asubuhi.”165 Hakika wengi miongoni mwa watu hao walikuwa wanatokea kwenye misingi ya makosa. Wanadhani ni dosari kile kisichokuwa dosari, na ni kasoro kile kisichokuwa kasoro. Hiyo ni kwa sababu nafsi zao zilikuwa zimechafuliwa na uchafu wa jahiliya. Katika maneno ya Imam B tuliyoyataja hivi punde, kuna ubainifu wa jambo muhimu katika kusoma maadili ya kibinadamu na kuwatambua watu. Hakika Mwenyezi Mungu anaweza kuwaficha mawalii wake na hatimaye ikawa vigumu kuwatambua isipokuwa kupitia vigezo vya kiungu, kama ilivyokuja katika hadithi Qudsi: “Mawalii   Al-Kafiy, Juz. 2, uk. 422; Majmuat Waram, Juz. 2. uk. 161 na 210.

165

83

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 83

4/23/2016 2:45:54 PM


HUYU NDIYE BILAL

Wangu wako chini ya kuba Langu, hawatambui mwingine asiyekuwa Mimi.” Navyo ni vigezo vya kweli hata kama watu hawavijui. Na ni kwa msingi wa vigezo hivyo mtu anastahiki kusifiwa au kulaumiwa. Utamkaji vizuri wa maneno si alama ya uzuri wala ubaya wa mtu, kwani unaweza kumkuta mtu ni hodari katika uongeaji wa mbinu mbalimbali, lakini moyo wake una rangi moja tu, nayo ni weusi utokanao na ubaya wa matendo yake na amali yake. Mkabala na mtu huyo, unaweza kumkuta yule asiyeweza kutamka vizuri, lakini moyo wake unatoa nuru ya maarifa na imani, na nuru hiyo inaongezeka kwa kila amali njema mpya. Hivyo basi, kigezo ni amali njema ambazo hutokana na utashi mwema, ambao hutoka ndani ya moyo ulioangaziwa na nuru ya maarifa. Kuna mifano mingi katika wakati wetu huu, mifano ya wale wenye maneno mengi lakini wachache wa vitendo. Wanawawaidhi watu bila wao wenyewe kuwaidhika. Wanasema kwa vinywa vyao yale wasiyoyatenda, kisha utakuta wana vyeo vikuu katika jamii, na wanazungukwa na aina mbalimbali za heshima na sifa. Alikuja mtu mmoja kwa Kiongozi wa Waumini Ali B akasema: “Ewe Kiongozi wa Waumini! Hakika leo Bilal alikuwa anajadiliana na Fulani lakini akawa anakosea katika maneno yake, na Fulani akiongea kwa kiarabu fasaha huku akimcheka Bilal.” Kiongozi wa Waumini Ali B akasema: “Ewe Abu Abdullah! Kunyoosha matendo na kuyatakasa ndio lengo la kupatikana ufasaha wa maneno na upangiliaji wake. Hautamfaa chochote Fulani ufasaha wake na upangiliaji wake wa maneno iwapo matendo yake ni mabaya zaidi. Na wala hakutamdhuru Bilal chochote kukosea kwake katika maneno iwapo matendo yake yamenyooka safi, na yametakasika vizuri.”166   Darajatur-Rafiah, uk. 363. Safinatul-Bihar, Juz. 1, uk. 105.

166

84

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 84

4/23/2016 2:45:54 PM


HUYU NDIYE BILAL

Hivyo lengo la ufasaha wa maneno ni ili ufasaha huo uwe njia ya kunyoosha matendo na kuyatakasa. Ufasaha si lengo wala kigezo katika thamani ya mtu, wala si sifa yenye kuakisi uhalisia wa nafsi yake. Hivyo basi, wale ambao wamenyoosha matendo yao na kuyatakasa hawahitaji ufasaha wa maneno. Mwache Bilal akosee katika maneno yake, kwani matendo yake yana balagha na bayana zaidi, kama ambavyo kitendo ni zaidi ya neno na fikra. Na kitendo kinaweza kufikisha kwa wengine ujumbe unaotarajiwa, kwa kuathiri mara elfu zaidi kuliko maneno anayoweza kuyafikisha mwenye nayo. Kwa nini basi tupoteze kiini kwa kung’ang’ania ganda. Hakika Bilal ni sawa na nuru juu ya mnara, na jua katikati ya mchana. Kukosea kwake katika utamkaji hakumpunguzii chochote, wala ufasaha wake haunyooshi matendo yake. Na je huyo Fulani anamjua Bilal hata amdhihaki na kumcheka kwa kasoro za matamshi yake? Huyo ni kipofu hata kama ana macho, na ni duni ambaye ufasaha wake hauwezi kumkweza. Hakika yeye ni jahili, hajui yaliyomo katika mbavu za Bilal wala yaliyomo katika roho yake. Bilal ni kama nyuki: Imepokewa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 kwamba alisema: “Mfano wa Bilal ni sawa na mfano wa nyuki, hutoka asubuhi kwenda kula vitamu na vichungu, kisha yeye huwa utamu wote.”167 Ni tuzo nzuri ya kipekee aliyoipata Bilal kwa utamu wake. Na ni nadra sana kumkuta Mtume wa Mwenyezi Mungu amemfananisha mtu kwa tashibihi hii, inayobeba mapenzi, usafi na upekee. Nayo bila shaka ni tashibihi nyeti ambayo chanzo chake ni maarifa kamili aliyonayo juu ya hali za Bilal na sifa zake mbalimbali. Bilal alikwenda maeneo mbalimbali, na alisikia Hadithi nyingi, na aliingia katika tajriba nyingi, lakini muhtasari wa yale aliyovu  Majmauz-Zawaid, Juz. 9, uk. 300. Tahdhib Taarikh Daamashqil-Kabir, Juz. 3, uk. 314.

167

85

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 85

4/23/2016 2:45:54 PM


HUYU NDIYE BILAL

na kutokana na utamu na uchungu, katika yale aliyosikia, kuyashuhudia na kuyaingia, yamekuwa ni utamu mtupu usio na shaka. Kwa maana kwamba, mabadiliko ya siku hayajaweza kubadili na kuchafua usafi wa Bilal, au kubadili mwenendo wake na safari yake. Bali yalichangia katika kuzidisha utamu wake, na hatimaye akawa asili kwa ladha, thamani na faida. Na hivyo yaliyokuwa yakitoka kwake yalikuwa yakipendwa na kuridhiwa, na yakizidisha kumuweka karibu na nafsi za watu. Na hivyo wakawa wakiona kheri kutoka kwake na wakingojea kheri kutoka kwake. Na kwa nini isiwe hivyo, wakati yeye ni mwanafunzi wa mikono ya Mtume wa Mwenyezi Mungu 4. Bustani ya elimu katika hadithi ya Bilal: Imepokewa kutoka kwa Abdullah bin Ali, kwamba alisema: Nilibeba bidhaa yangu kutoka Basra kuipeleka Misri, nikaiacha hapo. Wakati nikiwa njiani mara nikakutana na mzee mrefu mng’aavu, mwenye kichwa na ndevu nyeupe, akiwa kavaa joho mbili kuukuu. Nikauliza huyu ni nani? Wakasema: “Huyu ni Bilal, huria wa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4.” Nikachukua mbao za kuandikia nikamfuata. Nikamsalimu kwa kumwambia: Asalam Alayka ewe mzee. Akanijibu: Waalayka salam. Nikamwambia: Mwenyezi Mungu akurehemu. Nisimulie uliyoyasikia kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4. Akasema: “Unajua mimi ni nani?” Nikasema: Wewe ni Bilal, mwadhini wa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4. Akalia nami nikalia, mpaka watu wakatukusanyikia nasi tukiendelea kulia. Kisha akasema: “Ewe Kijana! Unatoka mji gani?” Nikasema: Ni mtu wa Irak. Akasema: “Hongera sana.” Kisha akanyamaza kwa muda, kisha akasema: “Ewe ndugu yangu Mwiraki, andika haya: Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kure86

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 86

4/23/2016 2:45:54 PM


HUYU NDIYE BILAL

hemu. Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 akisema: ‘ Waadhini ni……”168 Nikasema: Mwenyezi Mungu akurehemu, niongeze. Akasema: “Andika haya: Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu. Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 akisema: ‘Yeyote atakayeadhini muda wa mwaka mzima, Mwenyezi Mungu atamfufua ilihali ameshamsamehe madhambi yake yote hata yakiwa kwa wingi wa namna gani, hata kama yana uzito sawa na mlima wa Uhud.’” Nikasema: Mwenyezi Mungu akurehemu, niongeze. Akasema: “Ndiyo, hifadhi na andika haya: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 akisema: ‘Yeyote atakayeadhini katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya Swala moja, kwa imani, na kwa kutaraji malipo na kwa kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu atamsamehe madhambi yake yaliyotangulia na atampa kinga ya kutotenda mengine katika umri wake uliobakia. Na atamkusanya yeye pamoja na mashahidi katika pepo Yake.”’ Nikasema: Mwenyezi Mungu akurehemu, niongeze. Nisimulie lililo zuri zaidi katika yale uliyoyasikia kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4. Akasema: “Ooh kijana, umekata mishipa ya moyo wangu.” Akalia, nami nikalia mpaka Wallahi nikamuonea huruma. Kisha akasema: “Andika haya: Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu. Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 akisema: ‘Itakapofika Siku ya Kiyama, baada ya Mwenyezi Mungu kuwakusanya watu katika udongo mmoja, Mwenyezi Mungu atawapelekea waadhini Malaika watokanao na nuru. Watakuwa na bendera zitokanazo na nuru, watakuwa wanawaongoza wanyama ambao hatamu zao zinatokana na zumaridi ya kijani, na makapu yao yana harufu nzuri ya miski. Waadhini wa  Biharul-An’war, Juz. 84. uk. 128.

168

87

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 87

4/23/2016 2:45:54 PM


HUYU NDIYE BILAL

tawapanda wanyama hao, watasimama juu ya wanyama hao ilihali Malaika wakiwaongoza, na wao wakitoa Adhana kwa sauti yao ya juu kabisa.’” Kisha alilia sana mpaka nami nikalia. Aliponyamaza nikasema: Ni kipi kilichokuliza? Akasema: “Ooh, umenikumbusha mambo ambayo nilimsikia kipenzi changu 4 akisema: ‘Naapa kwa yule aliyenileta kwa haki kuwa Nabii, hakika wao watapita mbele ya viumbe ilihali wamesimama juu ya ngamia wema. Watasema: Allahu Akbaru. Allahu Akbaru. Watakaposema hivyo utasikika ukelele kutoka katika ummah wangu.’ Usama bin Zaydi akamuuliza kuhusu ukelele huo, ni upi? Akasema: ‘Ni ukelele wa tasbihi, tahmidi na tahlili. Watakaposema: Nashahidilia kwamba hapana mungu isipokuwa Allah. Ummah wangu utasema: Ndiyo, Yeye pekee ndiye tuliyekuwa tukimwabudu duniani. Hapo wataambiwa: Mmesema kweli. Watakaposema: Nashahidilia kwamba hakika Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. ummah wangu utasema: Huyu ndiye aliyetuletea ujumbe wa Mola Wetu. Na tukamwamini hata bila kumuona. Hapo wataambiwa: Mmesema kweli. Huyu ndiye aliyekuleteeni ujumbe kutoka kwa Mola Wenu na mlikuwa mkimwamini. Ni haki juu ya Mwenyezi Mungu kuwakusanya pamoja ninyi na Mtume wenu. Na hapo watapelekwa katika makazi yao, humo kuna yale ambayo jicho halijawahi kuona, wala sikio halijawahi kusikia, wala moyo wa mwanadamu haujawahi kuwaza.”’ Kisha alinitazama na kusema: “Kama unaweza kuhakikisha kwamba haufi isipokuwa ilihali na wewe ni mwadhini, fanya hivyo. Na naomba uniache, kwani umenilazimisha kuvuka kiwango.” Nikasema: Sintakuacha mpaka unifikishie yale uliyoyasikia kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4. Akasema: Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu. Ama mlango wa subira wenyewe ni mdogo, una komeo moja tu litokanalo na yakuti 88

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 88

4/23/2016 2:45:54 PM


HUYU NDIYE BILAL

nyekundu. Ama mlango wa shukurani wenyewe unatokana na yakuti nyeupe na una komeo mbili, urefu uliyopo kati ya komeo mbili ni sawa na mwendo wa miaka mia tano. Hauna kelele wala manung’uniko, unasema: Ewe Mungu Wangu! Niletee watu wangu.’” Nikamwambia: Je mlango unazungumza? Akasema: “Ndiyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu atautamkisha. Na ama mlango wa balaa.” Nikamwambia: Je mlango wa balaa si ndio huo huo mlango wa subira? Akasema: “Hapana.” Nikamwambia: Balaa ni nini? Akasema: “Ni misiba, magonjwa, maradhi na ukoma. Nao ni mlango unaotokana na yakuti ya njano, una komeo moja. Ni wachache mno watakaoingia mlango huu.” Nikasema: Mwenyezi Mungu akurehemu, niongeze. Na nipe kwani mimi ni mhitaji. Akasema: “Ewe kijana! Umenilazimisha kuvuka kiwango. Ama mlango mkubwa zaidi huo wataingia waja wema. Nao ni wale watu wenye kujinyima, wenye kujizuia na haramu na wenye shauku ya kukutana na Mwenyezi Mungu na wanaliwazwa Naye.” Nikasema: Mwenyezi Mungu akurehemu, watakapoingia peponi watafanya nini? Akasema: “Watatembea juu ya mito miwili katika maji safi, katika safina za yakuti, ambazo kasia zake zinatokana na lulu, ndani yake kutakuwa na Malaika wa nuru, wamevaa nguo za kijani zenye kijani ya kung’aa.” Nikasema: Mwenyezi Mungu akurehemu, je nuru inaweza kuwa ya kijani? Akasema: Hakika nguo ndio za kijani, lakini zitakuwa na nuru miongoni mwa nuru ya Mola wa viumbe wote ili waweze (Malaika) kutembea kwenye kingo mbili za mto huo.” Nikasema: Ni lipi jina la mto huo? Akasema: “Ni Pepo ya Maawa.” Nikasema: Je katikati yake kuna nyingine? Akasema: “Ndiyo. Kuna Pepo ya Aden. Nayo ipo katikati ya bustani. Ama Pepo ya Aden yenyewe uzio wake ni wa yakuti nyekundu.” Nikasema: Je humo kuna nyingine? Akasema: “Ndiyo. Pepo ya Firdawsi.” Nikasema: Vipi kuhusu uzio 89

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 89

4/23/2016 2:45:54 PM


HUYU NDIYE BILAL

wake? Akasema: “Ooh, niache, kwa kweli umeujeruhi moyo wangu.” Nikasema: Bali wewe ndiye uliyenijeruhi. Sintakuacha mpaka ukamilishe maelezo na unieleze kuhusu uzio wake. Akasema: “Uzio wake ni nuru.” Nikasema: Vipi kuhusu vyumba vilivyomo humo? Akasema: “Ni kutokana na nuru ya Mola wa walimwengu.” Nikasema: Mwenyezi Mungu akurehemu, niongeze. Akasema: “Ooh, hapa ndipo alipoishia Mtume wa Mwenyezi Mungu 4. Hongera kwako kama utafikia katika eneo lenye sifa hizi. Na ni hongera kwa mwenye kuamini haya.” Nikasema: Mwenyezi Mungu akurehemu. Wallahi mimi ni miongoni mwa wenye kuamini haya. Akasema: “Ooh, hakika mwenye kuamini haya na kuisadikisha haki hii na njia hii, hatatamani dunia wala mapambo yake na itaizuia nafsi yake peke yake.” Nikasema: Mimi naamini haya. Akasema: “Nimekusimulia. Lakini wewe fanya kwa wastani bila kuzembea. Na tenda wala usifurutu. Taraji, ogopa na jihadhari.” Kisha alilia na kushikwa na kwikwi ya kilio mara tatu. Hadi tukadhani kwamba amekufa. Kisha akasema: “Baba yangu na mama yangu wawe fidia kwenu. Kama Muhammad 4 angelikuoneni basi yangetulia macho yake wakati mlipokuwa mnauliza kuhusu sifa hizi.” Kisha akasema: “Jiokoeni haraka. Fanyeni haraka kuondoka. Tendeni sana na jiepusheni kufurutu.” Kisha akasema: “Ooh, nisameheni kwa yale niliyoshindwa kuwaeleza. Mwenyezi Mungu akulipe pepo kama ulivyotekeleza na kutenda yale yaliyo wajibu kwako.” Kisha aliniaga na kusema: “Mche Mwenyezi Mungu na ufikishie ummah wa Muhammad 4 haya niliyokufikishia.” Nikamwambia: Nitafanya hivyo inshaallah. Akasema: “Naiweka dini yako katika uangalizi wa Mwenyezi Mungu. Na namuomba akuzidishie uchamungu na akusaidie katika kumtii Yeye kwa utashi Wake.”169   Al-Aamal cha Saduq, uk. 283; Biharul-An’war, Juz. 81, uk. 127; Man LayahdhuruhulFaqihi, Juz. 1, uk. 297; Darajatur-Rafiah, uk. 368 – 371.

169

90

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 90

4/23/2016 2:45:54 PM


HUYU NDIYE BILAL

Tunachojifunza kutoka katika Hadithi hii: 1.

Hakika Bilal alikuwa na nafasi katika jamii ya Waislamu, kiasi kwamba walikuwa wanafaidika na elimu yake na wakiandika Hadithi za Mtume 4 kutoka kwake. Hivyo basi, pamoja na yote haya pia alikuwa anapendwa na Waislamu, na walikuwa wana shauku kubwa ya kutaka kumuona na kusikia sauti yake.

2.

Bilal alikuwa anajali na kutilia umuhimu suala la kuandika Hadithi na kuzisambaza, kama inavyoonekana katika msisitizo wake aliomsisitiza mpokezi wa riwaya hiyo, kwamba aandike Hadithi ya Mtukufu Mtume 4, na akirudia mara kwa mara kutamka wazi kuwa aliisikia kutoka kwa Mtume 4. Na inaonekana na kudhihiri bayana hali yake ya kujali na kutilia umuhimu suala la kusambaza Hadithi za Mtume 4, katika maelezo ya usia aliomuusia mpokezi wakati akimwaga, alipomwambia; “Mche Mwenyezi Mungu na ufikishie ummah wa Muhammad 4 haya niliyokufikishia.� Na hilo si chochote isipokuwa ni kuhisi kwake majukumu na wajibu alionao mbele ya siasa iliyojitokeza ya kuzuia kueneza na kusambaza Hadithi. Na hazifichikani kwa yeyote athari mbaya zilizotokana na siasa hii, athari zilizokuwa zikitishia mustakabali wa utume na kuuweka katika mazingira mbalimbali ya aina za kutoweka na kupotoshwa. Na kuacha uwanja wazi kwa waongo na wazushi kuizulia dini uongo. Na mbele ya hali kama hii ni lazima kwa kila mwenye kuupenda na kuujali Uislamu kufanya awezalo katika kupambana na siasa hii. Na kusimama kidete dhidi ya waongo na wazushi ambao wanaufanyia vitimbi Uislamu, na wala hawaogopi wala kujizuia hata kidogo, kumnasibisha Mtukufu Mtume 4 na kila kitakachowaridhisha watawala, na kila kinachowaingizia kipato na kuimarisha maslahi yao binafsi na 91

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 91

4/23/2016 2:45:55 PM


HUYU NDIYE BILAL

kuifanyia uadui dini ya haki. Na kwa kweli mengi yaliyoupata Uislamu kama ujumbe, na matatizo tunayokutana nayo sasa kama ummah wa Kiislamu, ni matokeo ya hali halisi ya siasa hii.170 3.

Hakika Bilal alikuwa ananasibishwa na Mtukufu Mtume upande wa uhuru wake, kama inavyodhihiri kutoka katika jibu la watu waliomjibu Abdullah bin Ali, alipowauliza kuhusu yeye, naye hakuwa anamjua. Wakamwambia: “Huyu ni Bilal, huria wa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4.”

4.

Katika Hadithi hii kuna moja ya ushahidi kati ya ushahidi mwingi unaothibitisha kuwa, Bilal alikuwa akisifika kwa sifa njema, ambazo ni Maswahaba wachache waliokuwa nazo. Nayo ni sifa ya kuwa na uaminifu na uhusiano wa hisia za kina na Mtume wa Mwenyezi Mungu, kiasi kwamba unamuona analia na kupiga kelele kwa kilio kila anaposikia jina lake 4 au anaposikia ukitajwa usuhuba wake kwake.

5.

Bilal alipenda sana kuanza Hadithi kwa Bismillahi Rahman Rahim.

6.

Hakika kutoa Adhana ni amali ya sunnah. Sharia imesisitiza na kuraghibisha amali hiyo. Na riwaya kuhusu hilo ni nyingi, na huenda aliyoyapokea Bilal yanatosha kutoa sura halisi ya yale aliyowaandalia Mwenyezi Mungu waadhini, miongoni mwa thawabu na cheo adhimu. Na ni fahari tosha kwao kwamba Mwenyezi Mungu atawapa makazi pamoja na Ibrahim Khalil katika daraja yake, kama ilivyopokewa katika riwaya ya Bilal.

Rejea katika kitabu Swahih Min Siyratin-Nabiy, Juz. 1, uk. 26 – 30. Na katika kitabu al-Hayat Siyasiyyah Lil-Imam Husein, uk. 78 – 85. Vyote viwili ni vya Alammah Sayyid Ja’far Murtaza Amiliy.

170

92

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 92

4/23/2016 2:45:55 PM


HUYU NDIYE BILAL

Na ni heshima tosha kwao, yale yaliyopokewa, kwamba Mwenyezi Mungu huwapa wanayoomba na atawakubalia uombezi wao kwa watakaowaombea. Haya ndiyo malipo ya waadhini wakweli wenye moyo mmoja, ambao Mwenyezi Mungu anapotazama nyoyo zao wakati wanapokuwa wanalingania ukweli, huzikuta zimejaa yakini na zimejengeka kwa mapenzi na zinang’aa kwa mionzi ya nuru Yake na tauhidi Yake. Nazo Siku ya Kiyama zitakuwa kama pambo la mbingu. Unaona kuna siri gani katika hilo? Na la karibu kabisa tunaloweza kusema katika upande huu ni kwamba, kutangaza kwao tauhidi na utume na vipengele vingine vya Adhana, ambavyo hatujui undani wake na siri za ghaibu zilizomo humo, ndio kulikoleta athari yote hii, na ndio kumezifanya nyoyo zao ziwe mahali pa nuru kutokana na uongofu wa Mungu. Na siku ya Kiyama watadhihiri wanyama wenye hatamu za zamaradi ya kijani, wenye harufu ya miski. Watawapanda na kuanza kutoa Adhana. Na baada ya yote haya, jambo bora zaidi la kusemwa hapa ni kukumbusha yale aliyousia Bilal. Alimtazama Abdullah bin Ali kisha akamwambia: “Kama unaweza kuhakikisha kwamba haufi isipokuwa ilihali na wewe ni mwadhini, basi fanya hivyo.” 7.

Hakika Bilal aliilea nafsi yake na kuiadabisha, mpaka hamu ya kuitaka Akhera yake ikamtawala kushinda hamu zote. Na ghamu itokanayo na hofu ya kutotimiza amali, ikamtawala na kumsahaulisha ghamu zote. Hivyo tunamuona anasisitiza suala la kuidhibiti nafsi na kutofurutu. Na anausia suala la kuwa na matarajio, hofu na tahadhari. Kisha analia na kuwaliza wengine. Kisha anakariri “Jiokoeni haraka. Fanyeni haraka kuondoka. Tendeni sana na jiepusheni kufurutu.” 93

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 93

4/23/2016 2:45:55 PM


HUYU NDIYE BILAL

Hebu tuzungumzie hisia zake za kweli za kishairi: Miongoni mwa sifa za Bilal ilikuwa ni ushairi wake na fasihi yake, licha ya kwamba alikuwa ni Mhabeshi na amekulia katika mazingira magumu na ya kikatili sana. Katika kivuli cha utumwa, ugandamizwaji na ufakiri, lakini roho yake imara iliasi na kutoka nje ya mazingira haya na ikaishi katika mazingira ya fasihi. Hakika Bilal hata kama hakuwa miongoni mwa washairi bingwa waliotambuliwa na historia ya ushairi wa Kiarabu, isipokuwa ni kwamba hilo halipunguzi thamani ya mashairi yake, kwa kuwa yanatokana na roho ya ushairi hodari wenye hisia za kweli. Na kwa kuchunguza mashairi yake yaliyotufikia, tunakuta mashairi hayo yametokana na hali za kina zilizokuwa zimedhibiti hisia zake mbele ya mtu fulani au tukio fulani, ambalo alikuwa ameliona au amekabiliana nalo. Hivyo akawa ameamiliana nalo kwa hisia za ndani kabisa mpaka yakapita katika ulimi wake maneno yaliyojaa hisia za kweli. Hivyo ushairi wake hautokani na mawazo hewa, bali anatufikishia uhalisia wa hali yake na hisia zake kwa maneno bayana, yasiyo na uficho wala mafumbo. Na alipenda kueleza hisia zake kwa Mtukufu Mtume 4 na jinsi alivyoathiriwa na maneno yake ya kimaadili na kiroho, basi akasoma beti hizi kwa lugha yake ya kihabeshi: “Arahe Barahe Kankarahe. Karakiy Mundareh.” Mtume 4 akamwambia Hasan bin Thabit: “Ziweke katika Kiarabu.” Hasan akazisoma kwa Kiarabu: “Ikiwa tabia njema zitatajwa katika upeo wetu. Bila shaka ni wewe ndiye wakupigiwa mfano kwetu.”171 Na kulikuwa na mlipuko wa maradhi ya homa wakati Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alipofika yeye na Maswahaba zake Madina. Kutokana na mazingira hayo baadhi ya Maswahaba zake walipat  Darajatur-Rafiah, uk. 363; Safinatul-Bihar, Juz. 1, uk. 105.

171

94

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 94

4/23/2016 2:45:55 PM


HUYU NDIYE BILAL

wa na maradhi. Na kati yao alikuwa ni Bilal. Hivyo alikuwa akilala mbele ya nyumba yake pindi homa inapomuacha, kisha ananyanyua sauti yake kwa kusema: “Natamani nijue kama ipo siku nitalala tena usiku huko Fukhi,172 nikiwa nimezungukwa na maua yenye harufu nzuri. Na kama ipo siku nitakunywa tena maji ya Mijnah?173 Na kama ipo siku watanionesha tena Shama na Tufaylu.”174 Na imekuja kwamba, baada ya maneno hayo alikuwa akisema: “Ewe Mungu Wangu! Mlaani Ut’bah bin Abu Rabiah, na Umayyah bin Khalaf, kama walivyotutoa katika ardhi yetu.” Na hapo Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 akasema: “Ewe Mungu Wangu! Tufanye tuupende mji wa Madina kama tunavyoupenda mji wa Makkah, au zaidi yake.” Na wala sishangazwi na mapenzi ya dhati aliyokuwa nayo Bilal juu ya mji wa Makkah, kwani mji huo kwake una maana nyingi sana. Unafungamana naye kwa mafungamano ya itikadi na heshima. Na ni katika mji huo ndimo alimokulia. Ni katika mji huo alipata uhuru wake kwa Uislamu wake. Roho yake ilipata uhuru hata kama mbavu zake zilioza kwa mijeledi. Ni katika mji huo macho yake yalifunguka kwa kumuona kipenzi chake Muhammad 4, na hatimaye akatua mizigo ya moyo wake katika bustani ya imani, hata kama kifua chake kilichomwa na moto wa jangwa, na mawe yaliyopashwa moto yalitesa mwili wake.   Hili ni jina la bonde lililokuwepo huko Makkah.   Hili ni jina la eneo lililokuwa soko la Waarabu katika zama za ujahiliyyah. 174   Hii ni milima iliyokuwepo karibu na Makkah. REJEA: Siratun-Nabawiyyah cha Ibn Hisham, Juz. 2, uk. 589; Ansabul-Ashraf, uk. 193; Darajatur-Rafiah, uk. 363; Siyaru Aalamun-Nubalai, Juz. 1, uk. 354; Tahdhib Taarikh Daamashqil-Kabir, Juz. 3, uk. 309; Sahih Bukhari, Juz. 2, uk. 225; Muujamul-Buldan, Juz. 3, uk. 315. 172 173

95

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 95

4/23/2016 2:45:55 PM


HUYU NDIYE BILAL

Ni katika mji wa Makkah Bilal aliitambua nafsi yake, na mwili wake ukachanua na kukua kwa hewa yake. Na kwa wito wenye dawa, wa Muhammad 4: “Mwarabu si mbora kuliko asiyekuwa mwarabu. Wala asiye mwarabu si mbora kuliko mwarabu, isipokuwa kwa uchamungu,” Bilal alikua. Utashi wake ulikua na kuongezeka na mtumwa yule aliyekuwa akidhalilishwa na asiye na thamani mbele ya mwanadamu wa zama za ujahiliya, sasa ametambua utu wake na nafasi ya uwepo wake makhususi. Lakini leo hii ameuacha mji huo na kuwa mbali nao. Kwa nini asiumie, na asipatwe na ghadhabu?! Na kwa nini isiamke hali ya kuukumbuka mji wake, ambao ni sehemu ya kila mwanadamu. Sehemu ambayo hutembea ndani ya kifua chake hata awapo ndani ya mji wake. Vipi ikiwa amefukuzwa, amehamishwa na kukandamizwa?! Na kwa nini asimlaani Ut’bah na Umayyah, ambao wao ndio waliotengeneza mazingira ya misukosuko kwa Bilal, pia mateso na adhabu kwake?! Hakika Bilal anaeleza maumivu na mateso aliyoyapata kutoka kwa watu hao. Na huenda aliugusa moyo wa Mtume wake 4 na huzuni zake, akaamsha maumivu yake na uchungu wa moyo wake. Hivyo akasimama na kuomba dua kutoka katika moyo ulioungua kwa uchungu, wenye utulivu na huzuni, wenye kushiriki maumivu ya vipenzi vyake na wafuasi wake, wenye kuwafariji wakati wa upweke wao, akasema: “Ewe Mungu Wangu! Tufanye tuupende mji wa Madina kama tunavyoupenda mji wa Makkah, au zaidi yake.” Na kwa kuwa yeye 4 alikuwa anajua kwamba, jukumu analotakiwa kulitekeleza akiwa Madina, ni la muda mrefu na la miaka mingi. Na kwamba suala la kurudi Makkah lina vizuizi na changamoto. Na ili aziweke nafsi za Maswahaba zake katika subira na uvumilivu, alimuomba Mwenyezi Mungu awawafikishe na awafanye waupende mji wa Madina, kwa sababu wao bado ni wahajiri wapya 96

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 96

4/23/2016 2:45:55 PM


HUYU NDIYE BILAL

katika mji huo. Kwani hakika bila wao kukubali na kuridhia kubaki na kuishi katika mji wa Madina, ikiwa ni pamoja na kuingiliana na kuelewana na wenyeji wa mji huo, haiwezekani kuandaa nguvu na mazingira yanayotakiwa na yatakayowawezesha kurudi Makkah, na kusimamisha Dola ya Kiislamu. Ni mji huo ambao ulikuwa na kumbukumbu nyingi kwake. Na ni katika mji huo kilitokea kisa cha jihadi yake, na ilianzia safari ya mateso yake. Beti zinazonasibishwa na Bilal: Kuna beti kali zinanasibishwa na Bilal, sisi hatukupenda kuzileta katika kitabu hiki, lakini ili kutunza uaminifu wa kielimu kwamba tumewajibika kufuata masharti yake na utashi wake. Beti zenyewe ni hizi: “Wallahi sikuokoka kwa msaada wa Abubakri. Na kama si Mwenyezi Mungu, basi fisi wangelala juu ya mifupa yangu. Mwenyezi Mungu aliniandalia na kunikirimu kheri. Na hakika kheri hufuatwa kwa Mwenyezi Mungu. Sidhibitiwi na ufuasi wa kumfuata kila mzushi. Na mimi si mwenye kufuata mfano wa yale waliyozusha.”175 Mwenye kuchunguza beti hizi ataona kwamba, msemaji wake anazungumza kwa msukumo na kwa njia ya hamasa kubwa. Na inadhihiri kwamba yeye yuko tayari kuiingiza nafsi yake katika hatari kubwa ili tu kuihami na kuilinda dini yake. Na pia inaonekana kwamba, msemaji wa beti hizi ananasibisha uhuru wake kwa Mwenyezi Mungu. Lakini Mtume wa Mwenyezi Mungu ndiye aliyefan  Tanqihul-Maqal, Juz. 1, uk. 183; Qamus Rijal, Juz. 2, uk. 399; Darajatur-Rafiah, uk. 367.

175

97

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 97

4/23/2016 2:45:55 PM


HUYU NDIYE BILAL

ikisha hilo kivitendo. Naye hakika alikuwa anatekeleza utashi wa Mwenyezi Mungu. Hivyo kunasibisha hilo kwa Mwenyezi Mungu hakupingani na kulinasibisha hilo kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4, kwani yeye ndiye aliyetekeleza kivitendo utashi wa Mwenyezi Mungu katika ulimwengu wa matendo. Mtu mweusi hatoingia peponi: Ndiyo, mtu mweusi hatoingia peponi. Bali hatoingia peponi hata kikongwe na ajuza. Ni maneno aliyoyasema Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 kumwambia Bilal, baada ya yeye kutaka kujua maana ya kauli ya Mtume 4: “Hakika maajuza hawataingia peponi.” Kauli ambayo Mtume 4 alimwambia ajuza ambaye alishuhudiwa na Bilal akilia juu ya hatima yake. Jibu la Mtume 4 kwa Bilal likateremka kama kimondo kwake na hatimaye naye akajikunyata pembeni mwa ajuza na kulia pia juu ya hatima yake. Abbas akawakuta wakilia, na wakati huo alikuwa ni mzee sana, akataka kujua sababu inayowapelekea wao kulia, nao wakamweleza. Alipopeleka jambo hilo kwa Mtume 4 naye akitaka ufafanuzi, Mtume 4 alimjibu: “Kadhalika kikongwe hataingia peponi.” Hivyo wakaenda wote huku wakilia. Ni utani alioukusudia Mtukufu Mtume 4 ili uwe njia ya kufafanua ukweli. Na hata kama utani huo umemliza kidogo Bilal, ajuza na kikongwe, isipokuwa ni kwamba ufafanuzi uliingiza furaha kubwa isiyosahaulika na ambayo haitatoweka ndani ya nafsi za watu hawa. Ni ukweli upi huo? Imepokewa kwamba, yeye 4 alimwambia ajuza wa Bani Ash’jai: “Ewe Muash’jaiyyah, ajuza hataingia peponi.” Bilal akamuona ajuza huyo akilia, akaenda kumwambia hilo Mtume 4. Mtume 4 akamwambia Bilal: “Kadhalika na mtu mweusi.” Wakakaa wao wawili 98

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 98

4/23/2016 2:45:55 PM


HUYU NDIYE BILAL

wakilia. Abbas akawaona, akamweleza Mtume 4, naye akamwambia: “Kadhalika na kikongwe.” Wakakaa wote wakilia. Mtume 4 akawaita na kutuliza nyoyo zao, akawaambia: “Mwenyezi Mungu atawafufua katika umbo zuri kushinda walilonalo.” Na akawaambia kwamba wataingia peponi wakiwa vijana wenye kung’aa kwa nuru.176 Hivyo ndivyo walivyosema wapokezi na wanahistoria. Lakini sisi hatusadiki kwamba Mtume 4 alikuwa sababu na chanzo cha hawa watu kulia, isipokuwa kama anataka kuwapa somo la namna ya kuamiliana na tamko la kiimani na kila tamko. Na kwamba ni juu yao kuwa na uwelewa mkubwa juu ya ukweli wanaofikishiwa, na kuwa na muono wa kina katika madhumuni ya maneno. Ili aweze kuwalinda na kuwakinga dhidi ya kutumbukia katika mitego inayoweza kuwa hatari juu ya mwenendo au itikidi, kiasi cha kuweza kuwafikisha katika hatari kubwa zaidi na hasara kubwa. Ni nani aliyeshinda? Bilal aliambiwa: Ni nani aliyeshinda? Akasema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu 4.” Pakasemwa: “Tumekuuliza kuhusu ngamia.” Akasema: “Na mimi nimewajibu kuhusu kheri.”177 Bilal hakuwa amejichanganya pindi alipojibu kwa jibu hilo alilojibu, na wala hakukusudia mzaha, yeye alikuwa anajua vizuri alichoulizwa, na alikuwa na uwelewa kamili wa alichojibu. Anamwambia muulizaji: Hakika ushindani unatakiwa ukomee katika mambo ya kheri. Na kwamba kila kisichokuwa kheri hakina thamani ya kumfanya mtu avutike nacho. Hakika jibu lake lilikuwa ni moja ya namna ya kuelekeza jambo ambalo, ni wajibu kwa Mwislamu mwenye imani kulielekea. Na ambalo ni wajibu kwake kuelekeza vitendo vyake na juhudi zake.   Darajatur-Rafiah, uk. 365.   Rabiul-Abrar, Juz. 1, uk. 681.

176 177

99

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 99

4/23/2016 2:45:55 PM


HUYU NDIYE BILAL

Kuna faida gani ya kujua ngamia aliyeshinda katika mashindano ya ngamia, ukilinganisha na mashindano makubwa na matukufu aliyoyakusudia Mwenyezi Mungu, mashindano ya kushindana katika kutoa na kutenda kheri.?! Kwa kufuata kanuni isemayo: ‘Na shindaneni katika mambo ya kheri.’ Watazame wenye kushindana katika medani na madhumuni haya, fuata nyayo zao. Haya ndiyo asemayo Bilal. Hakika mimi sidhani kama Bilal hakuona malengo mengine yasiyokuwa haya, hivyo jibu lote kwa swali lilikuwa mahala pake, kwa sababu kingine kisichokuwa kheri hakistahiki kutiliwa umuhimu wala kujibiwa. Ukweli wake: Bilal alimwandama Mtukufu Mtume 4 na kumfuata, na alijifunza na kufaidika na tabia zake na adabu zake. Hivyo akajipamba na kusifika kwa sifa njema na kwa maadili na tabia njema. Asingepata hadhi hiyo kama si ukweli wake katika kauli na juhudi zake katika matendo. Bilal alijulikana kwa ukweli wa Hadithi na usahihi wa matendo. Na jambo hilo likawa maarafu miongoni mwa Waislamu kutoka kwake. Na kila mmoja mwenye kumpenda hadi mwenye kumchukia akamtolea ushahidi juu ya hilo, kwa sababu alikuwa akitanguliza ukweli hata kama utamdhuru, na akiacha uongo hata kama utamnufaisha.178 Na tunajifunza kutoka katika vyanzo mbalimbali kwamba, ukweli wake ulimfikisha katika kiwango ambacho, kauli yake ikawa ndiyo ya mwisho katika maamuzi, hiyo ni pindi Waislamu wanapokuwa katika wasiwasi na shaka kuhusu nyakati za Swala na Swaumu. Pindi panapokuwepo na kauli nyingi juu ya nyakati za kuzama jua na kuchomoza alfajiri. Hivyo anapoadhini Bilal, wasiwasi   Imam Ali  alisema: “Iman ni kutanguliza ukweli hata kama wakudhuru, na kuacha uwongo hata kama wakunufaisha.” Nahjul-Balaghah, Juz. 4, uk. 150, Hekima ya 458.

178

100

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 100

4/23/2016 2:45:55 PM


HUYU NDIYE BILAL

na shaka yote ilikuwa ikiondoka. Na kama akiwaambia kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 anakula chakula cha jioni au daku, huitegemea nukuu yake, na kauli yake huwa yakini. Na imekuja katika kitabu Tabaqatul-Kubra, kwamba ndugu yake alimchumbia mwanamke kutoka katika familia ya Kiarabu, wakasema: “Kama Bilal atahudhuria basi tutakuoza.” Bilal akahudhuria, akamtolea ushahidi na kusema: “Mimi ni Bilal mwana wa Rabah, na huyu ni ndugu yangu. Na yeye ni mtu muovu katika maadili na dini. Mkitaka kumuozesha muozesheni, na mkitaka kuacha acheni.” Wakasema: “Yeyote ambaye wewe ni ndugu yake tutamuoza.” Hivyo wakamuoza.179 Na katika riwaya nyingine, imekuja kwamba, alimposea ndugu yake mwanamke wa kikurayshi, akawaambia jamaa zake: “Sisi mnatujua, tulikuwa watumwa lakini Mwenyezi Mungu akatupa uhuru. Tulikuwa tumepotea lakini Mwenyezi Mungu akatuongoza. Na tulikuwa mafakiri, lakini Mwenyezi Mungu akatutajirisha. Na mimi naposa kwenu kwa ajili ya ndugu yangu Fulani. Kama mtatuozesha basi sifa zote njema anastahiki Mwenyezi Mungu. na kama mtatukatalia basi Mwenyezi Mungu pekee ndiye Mkuu.” Wakamuoza ndugu yake. Walipoondoka, ndugu yake akamwambia: “Mwenyezi Mungu akusamehe. Haikupasa wewe kutaja historia yetu na uhusiano wetu na Mtume wa Mwenyezi Mungu 4.” Bilal akamwambia: “Ewe ndugu yangu, nimesema kweli, na hatimaye ukweli umekuoza mke.”180 Ni kauli iliyojaa ukweli. Hakuna nafasi tena ya kuuliza na kuchunguza. Matokeo ya ukweli husifiwa bila kujali ni wapi yanatoka. Nao ndio njia fupi na yenye kusifiwa, ya kufika katika lengo. Bilal   Tabaqatul-Kubra cha Ibn Saad, Juz. 3, uk. 237; Aayanus-Shiah, Juz. 3, uk. 602; Ansabul-Ashraf, Juz. 1, uk. 189. 180   Al-Aqdu al-Faridu, Juz. 6, uk. 91; Darajatur-Rafiah, uk. 371. 179

101

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 101

4/23/2016 2:45:55 PM


HUYU NDIYE BILAL

anasema: Tulikuwa ni watumwa madhalili, hatuna nasaba wala familia yenye kuheshimika. Hatuna ubwana wala jaha, isipokuwa ni kwamba, Mwenyezi Mungu alituneemesha kwa kutupa uhuru, nasi tukawa mabwana wa maamuzi yetu. Na tulikuwa tumepotea katika giza la upotovu, tunaabudu masanamu na ujinga, isipokuwa ni kwamba Mwenyezi Mungu alituongoza kwa Uislamu. Na tulikuwa mafakiri hatumiliki chochote, Mwenyezi Mungu akatuzawadia neema ya imani, hivyo basi, kama mtatuozesha tutamuhimidi Mwenyezi Mungu kwa zawadi Yake, kwani Yeye ndiye Mpaji. Na kama mtakataa basi Mwenyezi Mungu ndiye Mkuu na anayestahiki kutukuzwa kwa kutuongoza, kutuelekeza na kutupangilia mambo yetu. Hakika ni somo analoliwasilisha Bilal, na ndugu yake alihofia kwamba huenda atajaza athari za ushujaa na jihadi waliofanya pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu 4, ili ziwe shinikizo la wao kujibiwa na kivutio kitakachopelekea wao kukubaliwa. Hivyo akamlaumu kwa kutotaja hayo. Lakini somo la Bilal lilikuwa na ujumbe mzito, kwani hakika kwa kutegemea ukweli na kutafuta ridhaa umepata mke. “Hakika ukweli umekuoza mke.� Haiwezekani kwa Bilal ambaye alipata medali ya ukweli kutoka kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, awadanganye watu. Ageuze ukweli na aweke uzuri sehemu ya ubaya, au ubaya sehemu ya uzuri, hata kama suala linamhusu mtu wa karibu sana na yeye, na hata kama ni jambo zito la muhimu. Bilal alitamka haki, na alitoa hoja na akazungumzia uhalisia wa sifa za ndugu yake. Hivyo ukweli wake ulioambatana na kitendo cha kufichua mwenendo wa ndugu yake, ukatosha kabisa kumwozesha mke. Na ukawa ni dhamana ya mustakbali wa ndugu yake katika maisha na mke wake. Na alifanya vizuri mno pale alipodhihirisha mazuri na mabaya, hivyo kama watamkatalia, Mwenyezi Mungu atamuongoza njia yake. Na kama watamkubalia, basi hawatashtushwa na mwenendo wa kaka 102

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 102

4/23/2016 2:45:55 PM


HUYU NDIYE BILAL

yake, na wala Bilal hatakuwa amewaficha ukweli. Bali aliwasilisha utangulizi wa lazima mbele ya mke wa kaka yake, ili afanye kazi ya kumnyoosha, au kumwelewa au kumvumilia. Hakika mapenzi yake kwa ndugu yake na raghba yake ya kutaka apate mke, havikumsukuma kusema uwongo na kuzipamba tabia za ndugu yake, au kumnasibisha na sifa asizokuwa nazo. Au kutaja fahari za Uislamu na mapambano yao pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na hili ndilo lililomkera ndugu yake ambaye alimlaumu kwa kutotaja matendo yao na kushiriki kwao pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 katika mapambano. Wakati ambapo Bilal alikomea kusema: “Ewe ndugu yangu, nimesema kweli, na hatimaye ukweli umekuoza mke.” Kupata kwake medali ya ukweli: Mke wa Bilal alikuwa ananeemeka na maisha mazuri ya utulivu pamoja na mume wake, maisha yaliyojaa mahaba na mawada. Na je unangojea nini kutoka kwa Bilal, zaidi ya kuwa mume mwema mwenye tabia njema kwa familia yake?! Ilitokea siku moja alimsimulia Hadithi kutoka kwa Mtukufu Mtume 4, mke akashangazwa sana na analosimuliwa na akawa na shaka na nukuu yake, Basi suala hilo likamgusa Bilal na hivyo alikwenda kwa Mtukufu Mtume na kumshitaki mke wake, huku alama za ghadhabu zikionekana juu ya uso wake. Mtume 4 alitaka kuondoa shaka ya mke wake na kuondoa huzuni katika moyo wa Bilal, hivyo alikwenda nyumbani kwa Bilal, na akamwelekezea mke wake swali, akasema: “Kuna kosa lolote katenda Bilal?” Mke akasema: “Hapana.” Mtume akasema: “Huenda umemkasirikia Bilal.” Mke akasema: “Hapana. Yeye mara nyingi hunijia na kuniambia Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema. Mtume wa Mwenyezi Mungu ame103

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 103

4/23/2016 2:45:55 PM


HUYU NDIYE BILAL

sema.” Mtume akamwambia: “Lolote analokusimulia Bilal kutoka kwangu huwa amesema ukweli. Bilal haongopi. Usimghadhibishe Bilal. Haitakubaliwa amali kutoka kwako maadamu umemghadhibisha Bilal.”181 Ni fahari tosha kwa Bilal, Mtume wa Mwenyezi Mungu kuthibitisha ukweli wa nukuu zake na wa kauli zake. Hongera kwake, kwa hadhi aliyoipata ya kuaminiwa na Mtukufu Mtume 4. Kuoa kwake: Inadhihiri kutokana na waliyoyanukuu wanahistoria, kwamba Bilal alioa zaidi ya mara moja na kutoka katika miji tofauti. Imepokewa kwamba alimuoa Hindu wa kabila la Khawlani,182 kutoka mji wa Khawlani ya Yemen, si Khawlani ya Sham. Alimuoa kabla ya kwenda zake Sham. Na katika kitabu Tabaqatul-Kubra imepokewa kutoka kwa Qatadah, kwamba Bilal alioa mwanamke wa Kiarabu kutoka katika ukoo wa Bani Zahra.183 Na katika vyanzo vingine imetajwa kwamba, alioa huko Daraya katika mji wa Khawlan ya Sham. Hiyo ni wakati walipotua hapo na Abu Ruwayha. Walichumbia na wakaoa katika mji huo. Khawlani ni jina la miji miwili, mmoja uko Sham, na wa pili uko Yemen.184 Na katika vyanzo vingine imetajwa kwamba, Bani Bakir walimuoza dada yao kwa maombi kutoka kwa Mtukufu Mtume 4. Baa  Tahdhibu Taarikh Damashqul-Kabir, Juz. 3, uk. 313; Al-Iswabah, Juz. 4, uk. 428.   Tahdhibul-Kamal, Juz. 4, uk. 290. Kitabut-Thuqat, Juz. 3, uk. 28. Tahdhibu Taarikh Damashqul-Kabir, Juz. 3, uk. 304. Al-Iswabah, Juz. 4, uk. 428. 183   Tabaqatul-Kubra cha Ibn Saad, Juz. 3, uk. 238. Aayanus-Shiah, Juz. 3, uk. 602. Ansabul-Ashraf, Juz. 1, uk. 189. 184   Na Kwa mujibu wa baadhi ya Enklopedia, ni kwamba jina hilo linatumika pia kwa kabila ambalo ndio wenyeji wa mji wa Khawlan ya Yemen – Mtarjumi. 181 182

104

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 104

4/23/2016 2:45:55 PM


HUYU NDIYE BILAL

daye tutazungumzia kisa hicho.185 Na huenda alioa wanawake wengine ambao habari zao hazijatufikia.186 Vyovyote iwavyo, ni kwamba kuoa kwake mke zaidi ya mmoja lilikuwa ni jambo maarufu na lililoenea katika zama hizo. Na huenda Bilal alifuata njia hii na alikusanya pamoja wake zaidi ya mmoja wakati mmoja, isipokuwa ni kwamba kuthibitisha hilo kwa uhakika ni vigumu, na kuoa kwake mke zaidi ya mmoja hakumaanishi kwamba aliwakusanya ndani ya wakati mmoja. Na tunataja baadhi ya nukuu zilizopokewa kuhusu kuoa kwake, ile iliyokuja katika kitabu at-Tabaqat kwa sanadi yake kutoka kwa Shaabiy, kwamba yeye na kaka yake walichumbia katika nyumba moja ya huko Yemen, akasema: “Mimi ni Bilal, na huyu ni ndugu yangu. Tulikuwa watumwa kutoka Uhabeshi. Tulikuwa tumepotea lakini Mwenyezi Mungu akatuongoza. Na tulikuwa watumwa Mwenyezi Mungu akatupa uhuru. Hivyo kama mtatuozesha basi sifa zote njema anastahiki Mwenyezi Mungu. Na kama mtatukatalia basi Mwenyezi Mungu pekee Ndiye Mkuu.”187 Imepokewa kwamba Bilal na Abu Ruwayha walikwenda kuchumbia Daraya katika kijiji cha Khawlani, Bilal akawaambia: “Tumekuja kuchumbia. Tulikuwa makafiri, lakini Mwenyezi Mungu akatuongoza. Tulikuwa watumwa, lakini Mwenyezi Mungu akatupa uhuru. Na tulikuwa mafakiri, lakini Mwenyezi Mungu akatutajirisha. Hivyo kama mtatuozesha basi sifa zote njema anastahiki Mwenyezi Mungu. Na kama mtatukatalia basi hakuna uwezo wala nguvu isipokuwa kwa msaada wa Mwenyezi Mungu.” Wakawaoza.188 Na   Usudul-Ghabah Juz. 1, uk. 208. Siyaru Aalamun-Nubalai, Juz. 1, uk. 358. AayanusShiah, Juz. 3, uk. 602. 186   Aayanus-Shiah, Juz. 3, uk. 602; Tahdhibu Taarikh Damashqul-Kabir, Juz. 3, uk. 314; Tabaqatul-Kubra cha Ibn Saad, Juz. 3, uk. 237. Ansabul-Ashraf, Juz. 1, uk. 190. 187   Tabaqatul-Kubra cha Ibn Saad, Juz. 3, uk. 237. Aayanus-Shiah, Juz. 3, uk. 602. 188   Usudul-Ghabah, Juz. 1, uk. 208; Siyaru Aalamun-Nubalai, Juz. 1, uk. 358. AayanusShiah, Juz. 3, uk. 602. 185

105

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 105

4/23/2016 2:45:55 PM


HUYU NDIYE BILAL

huenda kisa hiki ni kimoja, ikiwa makusudio ya udugu wa Bilal ni udugu wa imani. Katika nukuu zote mbili, kuna maneno kutoka katika nafsi moja. Kutoka katika moyo wenye kung’ara kwa imani, ambao umeumbwa katika maumbile ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kumtumikia Yeye. Na huenda maneno yake haya hayakuwa yakijulikana katika namna nzima ya kuposa wanawake. Ada iliyokuwa imezoeleka kwao ni mchumbiaji au mwakilishi wake kutaja utajiri wake, nafasi yake kijamii, nasaba yake, ushujaa wake na mfano wa hayo, ili kuwavutia wahusika wamuoze kwake binti yao. Isipokuwa ni kwamba wanatauhidi wana lugha makhususi, wao wako huru mbali na vifungo vya dunia. Roho zao zimefungamana na Mwenyezi Mungu Mmoja Mwenye nguvu kushinda kila kitu. Hivyo hawakuona mwenye uwezo wa kuwafanikishia mahitaji yao isipokuwa Yeye, na hivyo wakawa wanazungumza kwa lugha ya kumpwekesha na wanatanguliza ukweli katika kila tukio na msimamo. Ni wachache wenye kufahamu, kuielewa na kuihimili mantiki hii, kwa sababu mtu ambaye kamsahau Mwenyezi Mungu na amejiweka mbali na medani ya tauhidi Yake, hukosa kionjo chenye kumsukuma kwenye kushikamana na ukweli na kujiepusha na uwongo. Na hii ni tofauti na mtu ambaye moyo wake umeungana na nuru ya tauhidi, anayemuona Mwenyezi Mungu katika kila kitu, na anaziona alama za tauhidi katika viumbe vyote. Mtu huyu hajui kingine isipokuwa ukweli katika kauli na matendo. Na Bilal ni miongoni mwa hao wenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa moyo mmoja. Mwenyezi Mungu ameweka nuru katika moyo wake, hivyo ulimi wake ukawa ni ukweli mtupu na kauli yake ni sahihi. Anaishi na ghaibu katika matukio, na imani yake inaonekana katika vitendo na matendo yake, na hata katika maneno yake. 106

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 106

4/23/2016 2:45:55 PM


HUYU NDIYE BILAL

Hivyo maneno yake yaliyotangulia yalitoka ndani ya moyo uliofurika bahari ya upwekeshaji wake kwa Mwenyezi Mungu. Yanapenya ndani ya vina vya nyoyo na yanakuna maumbile ya mwenye kusikia, na yanamrudisha hadi kwenye ukweli kama ulivyo. Na yanamchukua hadi kwenye ulimwengu uliojaa hali ya kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Na yeye anazingatia kwamba, kuongoka kwake baada ya kupotea, na uhuru wake baada ya utumwa, na utajiri wake baada ya ufakiri, ni zawadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ambaye ndio chanzo cha kheri zote. Na ambaye ni Mjuzi wa kila kitu na Mwenye kujua siri zote na yaliyomo ndani ya dhamira. Hivyo unamuona anaishi kwa utulivu bila mashaka, wakimuoza basi atamhimidi Mwenyezi Mungu kwa neema hii, na kama watamkatalia basi Mwenyezi Mungu ndiye Mtukufu kuliko kila sifa na himidi. Ni Mkuu kushinda uwezo, nguvu na mamlaka tunayoweza kuyataja, kwani yeye ni Muweza wa kutenda atakalo, na wala hakuna mwingine zaidi Yake anayeweza kufanya hivyo. Mtukufu Mtume anamwozesha Bilal: Imekuja katika vitabu vya historia kwamba, Bani Bakir walikuja kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4, nao wanatokana na Bani Kinanah, wakamwambia Mtume: “Muoze dada yetu kwa Fulani.” Akawaambia: “Kwa nini msimuoze Bilal?” Kisha walikuja mara ya pili na ya tatu, wakasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! muoze dada yetu kwa Fulani.” Akawaambia: “Kwa nini msimuoze Bilal. Kwa nini msimuoze kwa mtu wa peponi?” Wakamuoza kwake.189 Msimamo huu wa Mtukufu Mtume 4 si chochote isipokuwa ni moja ya misimamo yake ya kujali na kutilia muhimu mambo ya Bilal. Na inafichua raghba kubwa aliyokuwa nayo katika kutaka ku  Ansabul-Ashraf, Juz. 1, Uk. 190. Tabaqatul-Kubra cha Ibn Saad, Juz. 3, Uk. 602. Tahdhibu Taarikh Damashqul-Kabir, Juz. 3, Uk. 314 Aayanus-Shiah, Juz. 3, Uk. 602.

189

107

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 107

4/23/2016 2:45:55 PM


HUYU NDIYE BILAL

muoza. Na aliona kwake imani, uchamungu na tabia njema, kwa kiwango ambacho kilifanya pepo iwe ndio malipo na mafikio yake. Pamoja na raghba aliyoidhihirisha Mtukufu Mtume 4 katika jambo la Bilal, isipokuwa ni kwamba mwanzo Bani Bakir hawakuitikia ombi la raghaba yake 4, na wakapuuza kumuoza kutokana na misingi ya ujahiliya iliyokuwa imeimarika kwao. Hakuna kilichowazuia zaidi ya utumwa wake na ufukara wake, au wao waliona kwamba hafanani nao kwa rangi yake au nasaba yake. Hivyo Mtukufu Mtume 4 akawa akikariri masikioni mwao ni kwa nini msimuoze Bilal?! Walipokuja mara ya tatu ilihali hawajaamini kile alichowaelekeza, Mtume 4 akawaambia: “Kwa nini msimuoze kwa mtu wa peponi?� Hakika dhana za ujahiliya zilikuwa zimestawi katika jamii ya Peninsula ya Bara Arabu hadi mipaka ya mbali. Ilikuwa ni vigumu kuzitokomeza dhana hizo kwa kiasi ambacho haiwezekani kukabiliana nazo kwa sura itakayozaa matuna na kuleta tija, isipokuwa kwa mbinu imara ya muda mrefu, ambayo itajumuisha pande zote za jamii na vipengele vyake. Na inajulikana pia kwamba, masharti ya ndoa hayakuwa nje ya dhana za kijahiliya. Bali yalikuwa chini ya mwonekeno na sifa mbaya zaidi za ubaguzi wa kimatabaka na kirangi. Uislamu ulitilia umhimu tatizo hili, kwa umuhimu unaolingana na hatari zake na ugumu wa utatuzi wake. Hivyo ukazingatia kwamba ubora unatokana na msingi wa uchamungu na imani na kujiweka karibu na Mwenyezi Mungu, na si kwa msingi wa familia, nasaba, mali wala uzuri. Ni kwa njia hiyo Uislamu ulimnyanyua yule aliyekuwa chini katika zama za ujahiliya. Na ndivyo ulivyompa heshima yule aliyekuwa dhalili katika zama za ujahiliya. Hivyo muumini wa kiume akawa anafaa kwa muuimni wa kike, na Mwislamu mwanaume akawa anafaa kwa Mwislamu mwanamke, hata kama ni mtumwa wa kutoka Uhabeshi, au Uajemi au Urumi. 108

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 108

4/23/2016 2:45:55 PM


HUYU NDIYE BILAL

Muda wote Mtukufu Mtume 4 alikuwa akisisitiza mafunzo haya na kuhangaika kwa ajili yake. Daima yalikuwa mbele ya macho yake, bila kupoteza fursa inayofaa kufikisha mafunzo haya katika uhalisia na utekelezaji wa kivitendo, ili kuweza kuyaimarisha ndani ya jamii na kuisafisha dhidi ya kila aina ya ada na mila za ujahiliya. Na hapa yanadhihirika baadhi ya malengo aliyoyakusudia Mtukufu Mtume 4, na aliyotaka yatimie kupitia hatua yake hii ya kumuoza Bilal ambaye alikuwa mtumwa fakiri na si mwarabu. Hivyo ni wajibu kwa Mwislamu kufanyia kazi mafunzo ya Uislamu na amuoze muumini kwa sababu ya kufaa kwake, afanye hivyo bila khofu wala kusita. Hatua hii ya Mtukufu Mtume 4 imekuja kutekeleza kivitendo mafunzo haya. Hivyo Bilal hata kama alikuwa dhalili katika zama za ujahiliya, isipokuwa ni kwamba amepata heshima kwa fadhila za Uislamu. Na amekuwa na hadhi baada ya kuwa duni. Hivyo kama Bani Bakiri wanataka kumuoza dada yao basi ni kwa nini wasimuoze kwa mtu mwenye heshima na hadhi. Muumini ambaye amali zake zimemfikisha katika kiwango ambacho kimemfanya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wampende na hatimaye akawa ni miongoni mwa watu wa peponi?! Mtukufu Mtume 4 alifichua mbele ya masikio ya Bani Bakiri ukweli huu na nafasi aliyonayo Bilal kwa Mwenyezi Mungu, pale walipomjia kwa mara ya tatu ilihali bado hawajatekeleza lile alilowaelekeza. Na baada ya yale waliyoyasikia kuhusu ubora wa Bilal walimuozesha dada yao, katika hilo wakionesha na kusisitiza kushikamana kwao na mafunzo ya Uislamu na kukana kwao batili na mabaya ya ujahiliya. Ubaguzi warudi upya: Mtukufu Mtume 4 kwa juhudi kubwa na nzito alizofanya muda wote wa mapambano yake dhidi ya aina mbalimbali za ujahiliya, 109

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 109

4/23/2016 2:45:55 PM


HUYU NDIYE BILAL

aliweza kuleta mabadiliko ya kihistoria katika maisha ya vizazi vya Penasula ya Bara Arabu. Vizazi ambavyo vilipanda hadi katika kiwango cha ubinadamu na maisha mazuri, baada ya kuwa vimezama ndani ya giza la ujahili na ubaguzi. Jambo ambalo liliwadhuru wenye tamaa na wenye uchu wa utawala na uongozi. Na watu hao hawakuwa na njia nyingine isipokuwa kungojea kipindi cha baada ya kifo cha Mtume 4, huenda wakati huo watapata fursa itakayowaruhusu kufika katika malengo yao mabaya. Na hili ndilo lililotokea, kwani vifuniko vilifunuka na mafisadi wenye madhara wakajitokeza baada ya kifo cha Mtukufu Mtume 4. Hivyo harakati za kisiasa zikashuhudia majaribio mabaya ya kuchafua sura ya Uislamu na kuirejesha jamii kwenye ujahiliya. Hivyo roho ikazama katika dhana za ujahiliya ambao ulipata njia kuingia katika jamii baada ya hapo kabla kuwa umeteketea katika shimo. Na katika hali ya kawaida jambo la kwanza kushambuliwa na siasa hii lilikuwa ni mwenendo wa Mtukufu Mtume 4 katika ndoa, uliozingatia kwamba muumini wa kiume anamfaa muumini wa kike, jambo ambalo halikubaliki na linachukiwa katika dhana za ujahiliya. Na kuna maana kubwa Mtukufu Mtume 4 kumchagua Bilal, mtumwa fakiri, asiye na nafasi yoyote kijamii isipokuwa yeye ni mwadhini tu, kisha kumuoza mmoja kati ya mabinti wa kabila maarufu, na pia kuibadili Sin yake kuwa ni Shin kwa Mwenyezi Mungu. Kitendo hiki chenyewe ni ujumbe tosha wenye nguvu wenye kufanya kazi ya kusahihisha na kufuta misingi na vigezo ambavyo vilikuwa vimeenea katika zama hizo, na ambavyo ni muhtasari wa matatizo ya muda mrefu. Na ni kujenga na kuimarisha misingi mingine ya kijamii na kifikra, ambayo kikawaida ina uwezo wa kuleta mafungamano ya kibinadamu na kuyaimarisha juu ya misingi yake, ambayo ni maadili mapya yatokanayo na roho ya dini mpya. 110

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 110

4/23/2016 2:45:55 PM


HUYU NDIYE BILAL

Historia inatunukulia mateso waliyoyapata huria wakati wa kutekelezwa siasa hii ya ubaguzi iliyofuatwa zama hizo. Imekuja kwamba, huria walimfuata Kiongozi wa Waumini B wakamwambia: “Tunawashtaki kwako hawa Waarabu. Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alikuwa anatugawiya posho sawasawa na wao. Na alimuoza Salman, Bilal na Suhaybu. Lakini hawa (Waarabu) wametukatalia, na wamesema hawatafanya.” Kiongozi wa Waumini B akawafuata na kuongea nao. Waarabu wakapiga kelele kwamba: “Tumelikataa hilo kabisa ewe Abul-Hasan.” Basi akatoka ilihali kaghadhibika akiburuza joho lake na akisema: “Enyi kundi la huria! Hakika hawa wamekuwekeni sawa na Mayahudi na Wakristo, wanaoa kwenu wala hawawaozesheni na wala hawakupeni mfano wa yale wanayochukua. Fanyeni biashara, inshaallah Mwenyezi Mungu atawabariki. Hakika mimi nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 akisema: “Riziki ni mafungu kumi. Na mafungu tisa yako katika biashara… na moja katika mambo mengine.”190 Kwa nini Kiongozi wa Waumini B asighadhibike? Wakati anawaona Waarabu wanavunja ahadi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu 4, na wanaifanyia khiyana amana waliyokabidhiwa, na wanatenda yale waliyokatazwa. Hakika ni mabaya mno yale waliyotenda baada ya Mtume wao. Kwa kuchunguza hoja waliyoitia huria ya mwenendo wa Mtukufu Mtume 4 katika kuoza na kutoa posho, tunaweza kujua kwa namna iliyo bayana zaidi siri ya Mtukufu Mtume kuwaozesha Bilal na Salman. Na pia hekima ya yeye kuwang’ang’aniza Bani Bakir kumuoza dada yao kwa Bilal. Na kutokana na maneno ya Kiongozi wa Waumini B tunapata jambo jingine la kuongezwa kwenye ubaguzi wa kikabila, nao ni ubaguzi wa kijamii, ambao unafuta vigezo vya msingi alivyoweka Mtukufu Mtume 4.   Biharul-An’war, Juz. 42, uk. 160; al-Kafiy, Juz. 5, uk. 318 – 319; Nafsurahman, uk. 165.

190

111

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 111

4/23/2016 2:45:55 PM


HUYU NDIYE BILAL

Na hapa ndipo palipofichika sababu iliyopelekea Kiongozi wa Waumini B kuwataka huria wajishughulishe na biashara, ambapo inadhihiri kwamba Waarabu walikuwa wanawadharau huria kwa sababu ya ufukara wao na kutokuwa kwao na kitu. Hivyo wito wa Imam Ali B unadhihiri hapa kama radiamali ya utatuzi inayolenga kuchangia katika kuondoa tofauti zilizopo, baada ya Waarabu kumjibu kwa kusisitiza kwamba: ‘Tumekataa hilo ewe Abul-Hasan.” Na baada ya yeye kukata tamaa ya kuweza kuwakinaisha. Na ilikuwa ni lazima Kiongozi wa Waumini aghadhibike kwa ajili ya kulinda dini yake mbele ya hawa watu ambao, ni haraka sana wamegeuka na kurudi katika ujahiliya wao. Sasa wanatenda mienendo ya kijahiliya ambayo Mtukufu Mtume 4 aliipiga vita, na wameghafilika na maadili matukufu ambayo ndiyo roho ya Uislamu na nguzo zake za msingi. Umar bin Khattab anaashiria siasa hii ambayo ilienea baada ya Mtukufu Mtume 4, anasema mwishoni mwa miaka yake: “Kama nitaendelea kuishi katika mwaka huu, basi nitarudisha usawa baina ya watu. Sintamfadhilisha mwekundu juu ya mweusi wala mwarabu juu ya asiyekuwa mwarabu.”191 Hakika kitendo cha Umar kuashiria nia yake ya kutaka kutenda kwa usawa baina ya watu, kinaonesha ukubwa wa tatizo lililoletwa na ubaguzi uliokuwepo baina ya watu wa dini moja, na ambao ulivunja misingi iliyoletwa na Uislamu. Kama ambavyo pia, kutangaza kwake nia ya kutaka kuacha kutofautisha baina ya mwekundu na mweusi, mwarabu na asiyekuwa mwarabu, kunaonesha kwamba siasa ya ubaguzi wa kabila na kijamii haikuwa na wala haikutekelezwa na kundi maalumu tu miongoni mwa watu, bali ilikuwa ni siasa ya tabaka la kwanza miongoni mwa watawala, na kwamba wao waliitekeleza kwa wigo mpana. Nalo ni jambo linaloleta mshi  Taarikh Yaaqubiy, Juz. 2, uk. 154.

191

112

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 112

4/23/2016 2:45:56 PM


HUYU NDIYE BILAL

tuko na mshangao na masikitiko, na kuzua alama za maswali juu ya utekelezaji huo, ambao bila shaka uliacha athari mbaya katika dhana na mtazamo wa Waislamu katika suala hili, kadiri muda na zama zilivyosonga mbele. Na hapa inathibitika kwamba ujeuri wa Waarabu na kumkatalia kwao Kiongozi wa Waumini, ikiwa ni pamoja na kung’ang’ania msimamo wao, halikuwa ni jambo la ghafla. Bali jambo hilo lilikuwa ni mwenendo na sera inayofuatwa, bali inawezekana limekuzwa na kuenezwa katika kona zote za jamii ya Kiislamu ya wakati huo. Na ni kutokana na mtazamo huu tunaweza kufasiri na kujua, kwa nini Waarabu hawakusita kukataa ombi la Khalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu na Kiongozi wa Waumini B.

113

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 113

4/23/2016 2:45:56 PM


HUYU NDIYE BILAL

Faslu ya Sita BILAL NA AHLUL-BAYT F Tutazungumzia: 1.

Mapenzi yake kwa Ahlul-Bayt.

2.

Bilal alizuru kaburi la Mtukufu Mtume 4 na akutana na Husein B.

3.

Bilal atoa Adhana kwa ajili ya Fatimah na Husein H

4.

Bilal ajitolea kumhudumia Fatimah I.

5.

Bilal ashiriki katika kuandaa walima wa ndoa ya Fatimah na Ali H

6.

Bilal aenda kumnunulia manukato Fatimah I.

7.

Bilal asikia Hadithi ya Mtukufu Mtume 4 kuhusu nafasi ya Fatimah I.

8.

Bilal ahudhuria mbele ya Mtukufu Mtume 4 wakati wa maradhi yake. Na awaleta Hasan na Husein F.

9.

Ufuasi wa Bilal kwa Ali B.

10. Huzuni ya Bilal kutokana na kifo cha Fatimah I. 11. Habari njema kwa wenye kumlilia Mtukufu Mtume 4. 12. Bilal anapokea habari njema za wenye kuwapenda AhlulBayt F 114

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 114

4/23/2016 2:45:56 PM


HUYU NDIYE BILAL

13. Mtukufu Mtume 4 anamtetea Bilal. 14. Imam Ali B anamtetea Bilal. 15. Imam as-Sadiq B anamtetea Bilal. Mapenzi ya Bilal kwa Ahlul-Bayt: Imepokewa kutoka kwa Imam Ja’far as-Sadiq B kwamba alisema kuhusu Bilal: “Mwenyezi Mungu amrehemu Bilal. Hakika yeye alikuwa akitupenda Ahlul-Bayt.”192 Huu ni ushahidi wa Imam Ja’far bin Muhammad, ambaye ni mkweli kutoka nyumba ya Mtume F. Na neno hili lina umuhimu ulio bayana: 1.

Ameombewa rehema na mmoja kati ya watu wa Nyumba ya Mtume 4, baada ya kifo chake, wakati ambapo alikuwa anapata hadhi hiyo zama za uhai wake, kupitia ulimi wa kipenzi chake 4, alipokuwa akisema: “Mwenyezi Mungu amrehemu Bilal.”193

2.

Amethibitisha na kuyatolea ushahidi mapenzi yake kwa Ahlul-Bayt F. Na mapenzi haya ndiyo yaliyokuwa yakiuliwaza moyo wake daima. Nayo ni maneno machache lakini yanafichua maana nyingi. Na si kila Swahaba wa Mtukufu Mtume 4 alipata bahati hiyo, bali ni kwamba mapenzi yake ya kweli kwa Ahlul-Bayt F ndio yaliongeza utukufu wa daraja yake duniani na Akhera. Na hili si geni na wala si la kushangaza kwa Swahaba mwema kama Bilal (ra), hiyo ni kutokana na kutambua kwake nafasi ya Ahlul-Bayt na cheo chao chenye kusifika. Na yeye ni miongoni mwa wali-

Biharul-An’war, Juz. 22, Uk. 141. Al-Ikhtiswas cha Mufid, Uk. 73. Majmaul-Bahrayni, Uk. 640. Tahdhibul-Maqal cha Abtahiy, Juz. 5, uk. 312. Majmauz-Zawaid, Juz. 3, uk. 152. 193   Majmauz-Zawaid, uk. 102. Subulul-Huda Warishad, Juz. 8, uk. 418. 192

115

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 115

4/23/2016 2:45:56 PM


HUYU NDIYE BILAL

osikia maneno ya Mwenyezi Mungu na Mtume kuhusu haki yao na haki ya atakayewapenda wao na kuwatawalisha na kuwafuata. Mwenyezi Mungu anasema:

ْ ‫ت َويُطَهِّ َر ُك ْم ت‬ ‫َط ِهيرًا‬ َ ْ‫ب َع ْن ُك ُم ال ِّرج‬ َ ‫إِنَّ َما ي ُِري ُد للاهَّ ُ لِي ُْذ ِه‬ ِ ‫س أَ ْه َل ْالبَ ْي‬ “…..Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.” (al-Ahzab; 33:33)

Wao ni safina ya uokovu. Na wao ndio aliotoka nao Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 ili kwenda kuapizana na Wakristo wa Najran. Mwenyezi Mungu anasema:

ُ ‫ك ِمنَ ْال ِع ْل ِم فَقُلْ تَ َعالَوْ ا نَ ْد‬ ‫ع أَ ْبنَا َءنَا َوأَ ْبنَا َء ُك ْم‬ َ ‫ك فِي ِه ِم ْن بَ ْع ِد َما َجا َء‬ َ ‫فَ َم ْن َحا َّج‬ َ‫َونِ َسا َءنَا َونِ َسا َء ُك ْم َوأَ ْنفُ َسنَا َوأَ ْنفُ َس ُك ْم ثُ َّم نَ ْبتَ ِهلْ فَنَجْ َعلْ لَ ْعنَتَ للاهَّ ِ َعلَى ْال َكا ِذبِين‬ “Na watakaokuhoji baada kukufikia elimu hii, waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake zetu na wana wanawake wenu, na nafsi zetu na nafsi zenu, kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo.” (al-Imraan; 3:61).

Na wao ndio ambao Waislamu wamewajibishwa kuwapenda, na mapenzi yao yameota mizizi ndani ya nyoyo za Waumini. Na hili ndilo aliloashiria Ibn Abbas ilipoteremka Aya:

‫قُلْ اَل أَسْأَلُ ُك ْم َعلَ ْي ِه أَجْ رًا إِ اَّل ْال َم َو َّدةَ فِي ْالقُرْ بَ ٰى‬ “Sema: kwa haya siwaombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi katika ndugu.” (Shuraa; 42:23)

116

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 116

4/23/2016 2:45:56 PM


HUYU NDIYE BILAL

Akasema: Walisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! ni kina nani hao karaba wako ambao tumewajibishwa kuwapenda? Mtume 4 akasema: “Ni Ali, Fatimah na watoto wao.”194 Na katika riwaya nyingine ni kwamba walisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! ni kina nani hao karaba wako ambao tumewajibishwa kuwapenda? Mtume 4 akasema: “Ni Ali, Fatimah, Hasan na Husein.”195 Na imepokewa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 kwamba alisema: “Yeyote atakayenipenda na kuwapenda hawa wawili (Hasan na Husein) na baba yao na mama yao, atakuwa pamoja nami Siku ya Kiyama, katika daraja yangu.”196 Ni mazuri yaliyoje aliyoyasema Imam Shafii, aliposema: “Enyi watu wa Nyumba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, kukupendeni ni faradhi iliyotoka kwa Mwenyezi Mungu, aliyoiteremsha katika Qur’ani. Ni heshima kubwa kwenu ninyi, kwamba hakika yule asiyewaswalia nyinyi hana Swala.” Kama ambavyo tunaweza kujifunza kutokana na riwaya hiyo ya Imam Ja’far B kwamba, mapenzi ya Bilal kuwapenda Ahlul-Bayt F yaliendelea mpaka kufa kwake. Na iko wazi jinsi jambo hili lilivyo na heshima, kwani imepokewa kutoka kwa Mtukufu Mtume 4 kwamba alisema: “Yeyote atakayekufa ilihali ni mwenye kuwapenda Aali Muhammad, bila shaka amekufa shahidi.”197

Biharul-An’war, Juz. 23, uk. 232 – 251; Saadus-Suud, Juz. 1, uk. 140; ShawahidutTanzil, Juz. 2, uk. 189; Siratul-Mustaqim, Juz. 1, uk. 188; Al-Umdat, Juz. 1, uk. 47; Kashful-Ghummah, Juz. 1, uk. 106; Mutashabihul-Qur’an, Juz. 2, uk. 59. 195   Nahjul-Haq, uk. 175; Tafsirul-Kashif, Juz. 6, uk. 522. 196   Swawaiqul-Muhriqah, Uk. 187. 197   Tafsirul-Kashif, Juz. 3, uk. 1467; Jamiul-Akhbar, uk. 473. 194

117

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 117

4/23/2016 2:45:56 PM


HUYU NDIYE BILAL

Bilal alizuru kaburi la Mtukufu Mtume 4 na akutana na ­Husein B: Wakati akiwa anaishi Sham, siku moja Bilal aliamka kutoka usingizini ilihali ni mwenye huzuni na woga. Alimuona Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 usingizini akimlalamikia kwa kutomtembelea kwake. Na akamhimiza kumzuru baada ya kukaa muda mrefu bila kumzuru. Hivyo Bilal akapanda mnyama wake na kuelekea Madina Tukufu akikusudia kwenda kulizuru kaburi la Mtume 4.198 Tuna haki ya kufikiri jinsi alivyokuwa katika kaburi, pindi kumbukumbu zinapoamka katika nafsi yake, na yanapobubujika machozi yanayotokana na moto wa shauku. Na hatimaye uso wake unanawiri kwa udongo katika sura inayoakisi sura nzuri ya mapenzi, na inaelezea uchungu wa kutengana na hamu ya kukutana. Mara macho yake yanadondokea kwa Hasan na Husein F akiwa katika kaburi tukufu. Hasan ambaye ndiye anayefanana zaidi na Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 kuliko watu wote, kwa tabia na umbile. Na Husein ambaye yeye ni kutokana na Muhammad, na Muhammad amefanya kazi atakayofanya Husein.199 Bilal anajua vizuri kwa maarifa kamili cheo hiki, na anajua haki yao, ambapo Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 amesema: “Hasan na Husein ni wanangu. Yeyote atakayewapenda amenipenda. Na yeyote atakayenipenda amempenda Mwenyezi Mungu. na yeyote atakayempenda Mwenyezi Mungu atamwingiza peponi.”200 Basi Bilal akawakumbatia, akawabusu na kunusa harufu ya unabii na ufiadini kutoka kwao.

al-Ghadir, Juz. 5, uk. 146; Usudul-Ghabah, Juz. 1, uk. 208; Siratul-Halabiyyah, Juz. 2, uk. 100; Siyaru Aalamun-Nubalai, Juz. 1, uk. 358. 199   Fadhailul-Khamsah, Juz. 3, uk. 262 na 263. 200   Iilamul-Waraa, uk. 219. 198

118

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 118

4/23/2016 2:45:56 PM


HUYU NDIYE BILAL

Bilal atoa Adhana kwa ajili ya Fatimah na Husein H: Alipofariki Mtukufu Mtume 4 na yakatokea yaliyotokea baada yake, Bilal alijizuia kutoa Adhana, na akasema: “Sintamwadhinia yeyote baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu 4.”201 Lakini Fatimah I alisema siku moja: “Mimi nina hamu ya kusikia sauti ya mwadhini wa baba yangu, Bilal.” Zikamfikia habari hizo Bilal, basi akaanza kuadhini. Aliposema: “Allahu Akbar” Fatimah I akamkumbuka baba yake na siku zake, na hivyo hakuweza kujizuia kulia. Bilal alipofika: “Ash’hadu anna Muhammadan Rasulullah.” Fatimah alilia mpaka akaangukia uso wake na kuzimia. Watu wakamwambia Bilal: “Acha ewe Bilal. Hakika binti ya Mtume wa Mwenyezi Mungu ameaga dunia.” Kwani walidhani kuwa amefariki. Bilal akakata Adhana yake bila kuimalizia. Fatimah I alipozinduka alimuomba amalizie lakini hakufanya, bali alimwambia: “Ewe Bibi mbora kushinda wanawake wote! Hakika nina khofu juu yako kutokana na hali inayokupata unaposikia sauti yangu ikiadhini.” Basi akamwacha.202 Hiyo ilikuwa ni kabla ya kuhamia kwake Sham, kwani Fatimah hakuishi isipokuwa muda mchache baada ya kifo cha baba yake. Imepokewa katika vyanzo mbalimbali kwamba, baada ya kurudi kutoka Sham, Bilal alikwenda kwenye kaburi la Mtukufu Mtume 4, na mara walitokea Hasan na Husein F, akawakumbatia na kuwabusu. Wakamwambia: “Tunatamani uadhini usiku.” Basi alipanda juu ya paa la msikiti, aliposema: ‘Allahu Akbar. Allahu Akbar’ Madina yote ikalipuka kwa kilio. Na aliposema: “Ash’ hadu an laa ilaha ilallah.” Sauti za vilio zikaongezeka. Aliposema: “Ash’ hadu anna Muhammadan Rasulullah” wakatoka wanawake kutoka   Taarikhul-Khamis, Juz. 2, uk. 246; Darajatur-Rafiah, uk. 366; Tahdhibu Taarikh Damashqul-Kabir, uk. 316; Tabaqatul-Kubra cha Ibn Saad, Juz. 3, uk. 236; Ansabul-Ashraf, Juz. 1, uk. 192. 202   Man Layahdhuruhu al-Faqihu, Juz. 1, uk. 297 na 198; Swafuwatus-Swafuwa, Juz. 1, uk. 439; Darajatur-Rafiah, uk. 366. 201

119

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 119

4/23/2016 2:45:56 PM


HUYU NDIYE BILAL

katika majumba yao, na haikuonekana siku iliyowaliza watu wengi kama siku hiyo.203 Bilal ajitolea kumhudumia Fatimah I: Imepokewa kutoka kwa Mtukufu Mtume 4, kwamba alikuwa yeye na watu wengine msikitini wakimngojea Bilal aje kutoa Adhana. Lakini siku hiyo alichelewa kinyume na kawaida yake. Mtukufu Mtume 4 akamuuliza: “Ni kitu gani kilichokuzuia ewe Bilal?” Akasema: “Nilipitia kwa Fatimah I nikamkuta anatwanga chakula ilihali kamweka mwanawe kwenye jiwe la kutwangia, naye akilia. Nikamwambia: Ni kipi ukipendacho? Ukitaka nitakusaidia mwanao, na ukitaka nitakusaidi kutwanga? Akasema: ‘Mimi ndiye mwenye huruma zaidi kwa mwanangu.’ Basi nikachukua jiwe na kuanza kutwanga. Hilo ndilo lililonichelewesha.” Mtukufu Mtume 4 akasema: “Mwenyezi Mungu akuhurumie kama ulivyomhurumia.”204 Na hii ni taufiki na heshima ambayo hakuipata isipokuwa wachache miongoni mwa Maswahaba wema, kama vile Ammar, Abudhari na waliokuwa mfano wao. Na hiyo ni moja ya sifa iliyomfanya awe miongoni mwa watu waliowekwa karibu na Fatimah, baba yake, mume wake na wanawe. Alijitolea kumhudumia I ili apate huruma ya Mwenyezi Mungu kwa baraka ya dua ya Mtukufu Mtume 4 kwake. Bilal ashiriki katika kuandaa walima wa ndoa ya Fatimah na Ali H: Imepokewa kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alimwita Bilal, akasema: “Ewe Bilal! Nimemuoza binti yangu kwa binamu   Usudul-Ghabah, Juz. 1, uk. 208; Siyaru Aalamun-Nubalai, Juz. 1, uk. 358; Qamus Rijal, Juz. 2, uk. 239; Siratul-Halabiyyah, Juz. 2, uk. 100. 204   Darajatur-Rafiah, uk. 364; Safinatul-Bihar, Juz. 1, uk. 105. 203

120

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 120

4/23/2016 2:45:56 PM


HUYU NDIYE BILAL

yangu. Nami napenda iwe ni katika Sunnah ya ummah wangu kulisha chakula wakati wa ndoa. Kalete kondoo, na chukua mbuzi na pishi nne au tano. Niwekee katika beseni nitakaloweza kuwakusanya pamoja Muhajirina na Ansari. Ukimaliza kuandaaa niambie.” Akatoka na kwenda kutekeleza aliloamrishwa. Akaja na beseni akaliweka mbele yake 4. Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 akachomeka kidole juu ya chakula kile, kisha akasema: “Niingizie watu kundi mojamoja bila kurudia.” Basi watu wakaanza kuingia kwa makundi, kila lilipomaliza kundi moja liliingia jingine mpaka watu wote wakaisha.205 Bilal aenda kumnunulia manukato Fatimah I: Imepokewa kutoka kwa Abu Abdullah B kwamba alisema: “Wakati Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alipomuoza Fatimah kwa Ali B, Mtume aliingia kwa Fatimah na kumkuta akilia, akamwambia: ‘Ni kipi kinachokuliza? Wallahi kama kungekuwepo na aliye mbora kuliko yeye miongoni mwa watu wa nyumba yangu, basi ningekuoza kwake. Na wala si mimi niliyekuoza, lakini Mwenyezi Mungu ndiye hasa aliyekuoza na kutaja mahari yako kuwa ni dirhamu tano, maadamu mbingu na ardhi zingalipo.” Ali B anasema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 akasema: ‘Simama nenda kauze deraya.’ Nikasimama nikaenda kuuza na nikaja na thamani yake. Nikaingia kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 nikazimwaga dirhamu zote miguuni kwake. Hakuniuliza ni dirhamu ngapi na wala mimi sikumweleza. Kisha akachukua fungu katika dirhamu hizo na akamwita Bilal, akampa na kumwambia: ‘Kamtafutie manukato Fatimah.”’206 Na akawaamuru wamwandae, basi wakamtengenezea kitanda na mto kutokana na ngozi walioijaza vitambaa.   Al-Muswannaf cha Swanianiy, Juz. 5, uk. 487 na 488; Biharul-An’war, Juz. 1, uk. 222; Siratun-Nabawiyyah cha Dahlan, Juz. 1, uk. 22. 206   Al-Amaal cha Tusiy, uk. 40. Biharul-An’war, Juz. 43, uk. 94. 205

121

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 121

4/23/2016 2:45:56 PM


HUYU NDIYE BILAL

Bilal asikia Hadithi ya Mtukufu Mtume 4 kuhusu nafasi ya Fatimah I: Imepokewa kutoka kwa Abudhari (ra) kwamba alisema: “Nilimuona Salman na Bilal wakielekea kwa Mtukufu Mtume 4. Mara Salmani akaziangukia nyayo za Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 na kuanza kuzibusu. Mtukufu Mtume 4 akamkataza kufanya hivyo, kisha akasema: “Ewe Salman! Usinifanyie mimi mfano wa yale wanayoyafanya wasiokuwa Waarabu kuwafanyia wafalme wao. Mimi ni mja miongoni mwa waja wa Mwenyezi Mungu. Nakula wanayokula waja na ninaketi kama wanavyoketi waja.” Salmani akasema: “Ewe Bwana wangu! Nakuomba kwa haki ya Mwenyezi Mungu, niambie fadhila za Fatimah siku ya Kiyama.” Mtukufu Mtume 4 akamtazama kwa tabasamu na furaha, kisha akasema: “Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu imo mikononi mwake. Hakika yeye ni mwanamke atakayepita katika uwanja wa Kiyama juu ya ngamia ambaye kichwa chake ni kutokana na hofu ya kumhofu Mwenyezi Mungu.” Mtume 4 aliendelea kusema mpaka akasema: “Jibril atakuwa kuliani kwake na Mikail kushotoni kwake, Ali atakuwa mbele yake na Hasan na Husein nyuma yake. Na Mwenyezi Mungu akimlinda na kumhifadhi. Watapita katika uwanja wa Kiyama, na mara utasikika wito kutoka kwa Mwenyezi Mungu: ‘Enyi viumbe! Fumbeni macho yenu na inamisheni vichwa vyenu. Huyu ni Fatimah binti wa Muhammad 4 Mtume wenu, na mke wa Ali B Imam wenu. Mama wa Hasan na Husein F.’ Atavuka Sirat, atakapoingia peponi na kuona yale aliyoandaliwa na Mwenyezi Mungu, atasoma: “Na watasema: Alhamdulillah kwa ambaye ametuondoloea huzuni. Hakika Mola Wetu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye shukrani. Ambaye kwa fadhila Yake, ametuweka katika nyumba ya kukaa, humo haitugusi taabu wala humo hakutugusi kuchoka.”207 Mwenyezi Mungu at  Sura Fatir: 34 – 35.

207

122

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 122

4/23/2016 2:45:56 PM


HUYU NDIYE BILAL

ampa ufunuo kwamba: ‘Ewe Fatimah! Niombe nitakupa. Na tamani chochote toka Kwangu nitakuridhisha.’ Hapo atasema: ‘Mungu Wangu! Wewe ni zaidi ya matamanio yangu. Nakuomba usimwadhibu kwa moto yule anipendaye, na yule akipendaye kizazi changu.’ Hapo Mwenyezi Mungu atamfunulia kwamba; ‘Ewe Fatimah! Naapa kwa nguvu Zangu na utukufu Wangu na heshima ya nafasi Yangu. Nilichukua ahadi juu ya nafsi yangu, miaka elfu kabla hata sijaumba mbingu na ardhi, kwamba sintamwadhibu kwa moto yule akupendaye na akipendaye kizazi chako.’”208 Bilal ahudhuria mbele ya Mtukufu Mtume 4 wakati wa maradhi yake. Na awaleta Hasan na Husein F: Bilal alikuwepo kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu wakati wa maradhi yaliyomfisha.209 Imepokewa kutoka kwa Ali B kwamba alisema: “Mtukufu Mtume 4 alisema wakati wa maradhi yaliyomfisha: Ewe Ali! Wewe ni ndugu yangu duniani na Akhera. Na ni Wasii wangu na khalifa wangu kwa watu wangu.’ Kisha akasema; ‘Ewe Bilal! Niletee upanga wangu, deraya yangu, ngamia wangu, kitanda chake na hatamu yake na mikanda ninayoifungia deraya yangu.’ Bilal akaleta vitu hivi. Akasimama na ngamia mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu 4. Mtume 4 akasema: ‘Ewe Ali! Simama na umkamate.’ Nikasimama, na akasimama Abbas na kuketi sehemu yangu, nami nikamkamata ngamia. Akasema: ‘Mpeleke nyumbani kwako.’ Nikampeleka, kisha nikarudi. Nikasimama wima mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu 4. Akanitazama kisha akaitazama pete yake, akaivua na kunikabidhi. Akasema: ‘Chukua ewe Ali, hii ni yako duniani na Akhera.’ Wakati huo nyumba ilikuwa imejaa watu, Bani Hashim na   Mustadraku Safinatil-Bihar, Juz. 8, uk. 246; Biharul-An’war, Juz. 27, uk. 140; Taawilul-Ayat, Juz. 2, uk. 485; Baytul-Ahzan, uk. 43. 209   Kashful-Ghummah Fii Maarifatil-Aimmah, Juz. 2, uk. 35. 208

123

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 123

4/23/2016 2:45:56 PM


HUYU NDIYE BILAL

Waislamu wengine. Akasema: ‘Enyi Bani Hashim! Enyi Waislamu! Msimkhalifu Ali mkaja kupotea, na wala msimfanyie husuda mkaja kukufuru.’ Kisha akasema: ‘Ewe Bilal! Niletee wanangu Hasan na Husein.’ Nikadhani kwamba huenda wamemsababishia ghamu, nikaenda ili niwacheleweshe wasifike kwake haraka. Akasema: ‘Waache wanuse harufu yangu, nami ninuse harufu yao. Nijiongezee harufu nzuri nao wajiongezee harufu nzuri. Kwani baada yangu watakutana na misukosuko na mambo mazito. Mwenyezi Mungu awalaani wale watakaowatisha. Ewe Mungu Wangu! Mimi nawaacha amana kwako na kwa aliye mwema miongoni mwa waumini.’”210 Ufuasi wa Bilal kwa Ali B: Kuhusu mas’ala ya ukhalifa baada ya kifo cha Mtukufu Mtume (4saww), kuna nukuu ambazo zinaeleza kwamba Bilal alisimama upande wa Ali bin Abutalib B, akitoa hoja kwamba kiapo cha utii cha siku ya Ghadir bado kingali ni dhima shingoni mwetu mpaka Siku ya Kiyama.211 Na ilikuwa miongoni mwa matokeo ya kwenda kinyume katika jambo la ukhalifa ni mambo kuharibika, na hatimaye ikamlazimu Bilal kutokuendelea kuishi Madina na hatimaye akahamia Sham.212 Kwani baadhi ya nukuu zinaashiria kwamba, Khalifa Umar alimlaumu Bilal kwa kutoharakisha kwenda kumpa kiapo cha utii Abubakri. Isipokuwa ni kwamba sisi, hapa hatuko katika nafasi ya kuzama ndani katika suala hilo, bali tumeligusia tu kwa kadiri ya mahitaji ya maudhui na kwa kuheshimu uaminifu wa kielimu.   Kashful-Ghummah Fii Maarifatil-Aimmah, Juz. 2, uk. 35 – 36.   Darajatur-Rafiah, uk. 367. Aayanus-Shiah, Juz. 3, uk. 603; Safinatul-Bihar, Juz. 1, uk. 104; Qamus Rijal, Juz. 2, uk. 242. 212   Tahdhibu Taarikh Damashqul-Kabir, Juz. 3, uk. 316. 210 211

124

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 124

4/23/2016 2:45:56 PM


HUYU NDIYE BILAL

Bilal ni mja mwema, kwa nini? Riwaya zilizopokewa kutoka kwa Imam al-Baqir na Imam as-Sadiq F zimemwelezea Bilal kuwa alikuwa ni mja mwema. Na zimemwelezea Suhaybu kuwa alikuwa ni mja muovu. Na sababu katika hilo ni ule uadui dhidi ya Ahlul-Bayt F aliokuwa nao huyu wa pili, kama ilivyotamka wazi riwaya husika. Na kama ilivyotamka bayana kwamba Bilal alikuwa akiwapenda. Imepokewa kutoka kwa Abu Abdullah B kuwa alisema: “Mwenyezi Mungu amrehemu Bilal, alikuwa akitupenda sisi Ahlul-Bayt. Na Mwenyezi Mungu amlaani Suhaybu, hakika yeye alikuwa akitufanyia uadui.”213 Na imepokewa kutoka kwa Abu Abdullah B kuwa alisema: “Bilal alikuwa ni mja mwema K. Na Suhaybu alikuwa ni mja muovu.”214 Huzuni ya Bilal kutokana na kifo cha Fatimah I: Bilal alitoka Sham kuelekea Madina. Alipofika Madina watu walimpokea na habari za mauti ya Fatimah I, akalia na kusema: “Kipande cha nyama ya Mtukufu Mtume 4, ni haraka iliyoje kimekutana na Mtukufu Mtume 4.” Wakamwambia: “Panda utoe Adhana.” Akasema: “Sintafanya hivyo baada ya kuwa nimemwadhinia Muhammad 4. Lakini walipombembeleza sana alipanda. Wakakusanyika watu wa Madina, wanaume kwa wanawake, wadogo kwa wakubwa, wakasema: “Huyu hapa Bilal mwadhini wa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 anataka kutoa Adhana.” Aliposema: “Allahu Akbar. Allahu Akbar,” wote wakalipuka kwa kilio. Na aliposema: “Ash’hadu an laa ilaha ilallah”, wote wakalia. Aliposema: “Ash’hadu anna Muhammadan Rasulullah” hakubakia mtu mwenye roho Madina isipokuwa alilia na kupiga kelele. Na hata mabikira na vigoli walitoka   Man Layahdhuruhu al-Faqihu, uk. 503; al-Ikhtiswas, uk. 73.   Muujamu Rijalil-Hadith, Juz. 4, uk. 270; Biharul-An’war, Juz. 22, uk. 142.

213 214

125

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 125

4/23/2016 2:45:56 PM


HUYU NDIYE BILAL

kutoka katika majumba yao wakilia. Na ikawa kama siku aliyokufa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4. Ilikuwa hivyo mpaka alipomaliza Adhana yake. Akawaambia: “Nawapeni habari njema. Hakika moto hautaligusa jicho lililomlilia Mtukufu Mtume 4.” Kisha akarudi zake Sham.215 Habari njema kwa wenye kumlilia Mtukufu Mtume 4: Katika habari tuliotangulia kuitaja hivi punde, kuna maelezo kwamba Bilal alipomaliza Adhana yake, wakati watu wakiwa wanalia, alisema: “Nawapeni habari njema. Hakika moto hautaligusa jicho lililomlilia Mtukufu Mtume 4.”216 Nayo ni dhahiri kuwa ni habari njema kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 kwa ulimi wa Bilal. Itawezekana vipi moto uliguse jicho lililolia kutokana na mapenzi yake kwa kipenzi cha Mwenyezi Mungu? Na itawezekana vipi Mtume wa rehema 4 awaache katika adhabu wale wenye kumlilia? Hakika ulikuwa ni wito wa Bilal, unaowataka wayafanye machozi yao juu ya Mtume wa Mwenyezi Mungu 4, kuwa kinga ya adhabu, kupitia uombezi wake aliopewa na kuidhinishiwa na Mwenyezi Mungu. Na ulikuwa ni wito wa kutaka waamiliane na Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 baada ya kifo chake, kwa namna itakayojaa kumbukumbu ya kumkumbuka na kufuata njia yake. Bilal anapokea habari njema kuhusu wale wenye kuwapenda Ahlul-Bayt F: Imepokewa hadithi nzuri kutoka kwa Bilal, nayo ni hadithi yenye madhumuni ya juu na maana za kina, kuhusu haki ya Ali, Fatimah na wale wenye kuwapenda Ahlul-Bayt F. Imekuja katika nukuu ku  Taarikhul-Khamis, Juz. 2, uk. 246; Darajatur-Rafiah, uk. 367; Taratibul-Idariyyah, Juz. 1, uk. 75. 216   Darajatur-Rafiah, Uk. 367. 215

126

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 126

4/23/2016 2:45:56 PM


HUYU NDIYE BILAL

toka kwa Bilal bin Hamamah, kwamba alisema: “Siku moja Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alichomoza huku akitabasamu na kucheka, na uso wake ukiwa na furaha na uking’ara kama mbalamwezi. Abdurahman bin Awfi akasimama na kusema: ‘Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Nuru hii ya nini?’ Akasema: ‘Ni habari njema iliyonifikia kutoka kwa Mola Wangu kuhusu ndugu yangu na binamu yangu. Hakika Mwenyezi Mungu amemuoza Fatimah kwa Ali. Na amemwamuru Ridhiwan mlinzi wa pepo kuutikisa mti wa Tuba na hatimaye umepukutisha majani (yaani hati) sawa na idadi ya watu wenye kuwapenda Ahlul-Bayt. Na chini yake ameumba Malaika watokanao na nuru, na amempa kila Malaika hati. Itakapofika Siku ya Kiyama, Malaika atanadi mbele ya viumbe na hivyo hatabakia yeyote miongoni mwa wanaowapenda Ahlul-Bayt, isipokuwa atapewa hati yake ya kuepushwa na moto. Hivyo ndugu yangu na binamu yangu, na binti yangu, wamekuwa ni wakombozi wa wanaume na wanawake wa ummah wangu dhidi ya moto.’”217 Na mwenye kitabu al-Manaqib ametaja hadithi ya mpukutiko wa majani ya mti wa Tuba kutoka kwa Bilal, kwamba yeye alisema: “Siku moja Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alichomoza huku akitabasamu na kucheka, na uso wake ukiwa na furaha na uking’ara kama mbalamwezi. Abdurahman bin Awfi akasimama na kusema: ‘Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Nuru hii ya nini?’ Akasema 4: ‘Ni habari njema iliyonifikia kutoka kwa Mola Wangu kuhusu ndugu yangu na binamu yangu na binti yangu. Na kwamba hakika Mwenyezi Mungu amemuoza Fatimah kwa Ali. Na amemwamuru Ridhiwan mlinzi wa pepo kuutikisa mti wa Tuba na hatimaye ukapukutisha majani (yaani hati) sawa na idadi ya watu wenye kuwapenda   Usudul-Ghabah, Juz. 1, uk. 206; al-Ghadir, Juz. 2, uk. 316; Taarikhul-Khatib, Juz. 4, uk. 210; Al-Fusulul-Muhimmah cha Ibn Swabagh; al-Manaqib cha Khawarazmiy, na Swawaiqul-Muhriqah ya Ibn Hajar, uk. 103; al-Ghadir, Juz. 2, uk. 316; Qamus Rijal, Juz. 2, uk. 237.

217

127

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 127

4/23/2016 2:45:57 PM


HUYU NDIYE BILAL

Ahlul-Bayt wangu. Na chini yake ameumba Malaika watokanao na nuru, na amempa kila Malaika hati. Itakapofika Siku ya Kiyama, Malaika atanadi mbele ya watu na hivyo hatabakia yeyote miongoni mwa wanaowapenda Ahlul-Bayt, isipokuwa atapewa hati yake ya kuepushwa na moto. Hivyo ndugu yangu na binamu yangu, na binti yangu, wamekuwa ni wakombozi wa wanaume na wanawake wa ummah wangu dhidi ya moto.’”218 Hadithi ina maana kubwa, na wakati hautoshi kuchambua yale yanayoweza kusemwa upande wa sanadi yake na maana yake. Nasi tunatosheka na kutaja maana muhimu na cheo cha juu na kitukufu alichokipata Bilal, nacho ni yeye kuwa mtu aliyepokea Hadithi ya mpukutiko wa majani ya mti wa Tuba. Na kuwanukulia Waislamu habari njema iliyoutia furaha moyo wa Mtukufu Mtume 4, kwa Mwenyezi Mungu kumchagua Ali kuwa mume wa Fatimah I, na akawapa cheo cha kuuombea ummah wa Muhammad 4 Siku ya Kiyama. Zaidi ya hapo ni ile rehema aliyoiandaa Mwenyezi Mungu, kuwaandalia wale wenye kuwapenda Ahlul-Bayt F kwa kuwaepusha na moto. Mtukufu Mtume 4 anamtetea Bilal: Imekuja katika baadhi ya vyanzo kwamba Abu Dhari (Mungu amrehemu), alimwambia Bilal: “Ewe mtoto wa mwanamke mweusi.” Bilal aliposhitaki hilo kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4, alimwambia: “Umemtukana Bilal na kumdhalilisha kupitia weusi wa mama yake?” Akasema: “Ndiyo.” Mtume akasema: “Hivi unadhani kuna kiburi chochote cha ujahiliya usichokuwa nacho.” Basi Abudhari akalitupa shavu lake juu ya udongo kisha akasema: “Sintanyanyua shavu langu mpaka Bilal akanyage mashavu yangu kwa nyayo zake.”219 218   Kashful-Ghummah Fii Maarifatil-Aimmah, Juz. 1, uk. 351 na 352. 219  Tahdhibu Taarikh Damashqul-Kabir, uk. 314. al-Ghadir, Juz. 8, uk. 371.

128

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 128

4/23/2016 2:45:57 PM


HUYU NDIYE BILAL

Sisi tuna shaka na usahihi wa riwaya hii, kwani hakika Abu Dhari alikuwa ni mwenye kumcha Mwenyezi Mungu kiasi cha kutoweza kumwambia Bilal maneno hayo. Na jambo hili linatajwa kwa tofauti kidogo, katika kisa cha Ammar na baadhi ya Maswahaba wengine. Ni katika suala la ujenzi wa Msikiti wa Madina, ambapo Mtukufu Mtume 4 alimtetea Ammar. Sisi hatuko katika kuhakiki tukio hili, isipokuwa tunasema kwamba: Hakuna tofauti sawa tuikubali nukuu hii au ile, kwani hata tukikubali kwamba riwaya ya Abu Dhari na Bilal ni sahihi, bado ni kwamba tunachokipata katika riwaya hiyo ni mambo mawili: 1.

Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alimtetea Bilal, japo hatuwezi kuuzingatia utetezi huu, kuwa ni jambo linalowajibisha Swahaba mmoja kuwa mbora kuliko mwingine, kati ya hao wawili. Kwani iko bayana kwamba Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alimtetea Bilal kwa dhulma aliyotendewa. Na hakuna shaka kwamba jambo hili linaonesha jinsi Uislamu unavyochukia alama yoyote miongoni mwa alama za ujahiliya. Na jinsi unavyojitahidi kwenda hima kulea nafsi za binadamu na kuzitakasa. Hivyo Mtukufu Mtume 4 alielekeza komeo kali kwa Abu Dhari. Na pia linaonesha ukubwa wa maudhi yaliyompata.

2.

Ni ujumbe uliofikishwa na Abu Dhari kupitia kile alichofanya katika kuitakasa nafsi yake. Alikuwa anaweza kumuomba tu Bilal msamaha wa kawaida, au kujisogeza karibu naye kwa neno zuri na laini litakalomridhisha. Lakini hakufanya hivyo isipokuwa aliweka shavu lake juu ya udongo na akaazimia kutolinyanyua mpaka Bilal alikanyage, ili aweze kuhisi ukubwa wa tendo lake. Na aiadhibu adhabu kali nafsi yake iliyomhadaa. Abu Dhari alitaka kuiweka nafsi yake 129

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 129

4/23/2016 2:45:57 PM


HUYU NDIYE BILAL

katika mazingira ya kuitakasa na kuilea, na alifanikiwa katika hilo. Imam Ali B anamtetea Bilal: Mtu mmoja alikuja kwa Kiongozi wa Waumini B akasema: “Ewe Kiongozi wa Waumini! Hakika leo Bilal alikuwa anajadiliana na Fulani lakini akawa anakosea katika maneno yake, na Fulani akiongea kwa kiarabu fasaha huku akimcheka Bilal.” Kiongozi wa Waumini Ali B akasema: “Ewe Abu Abdullah! Kunyoosha matendo na kuyatakasa ndio lengo la kupatikana ufasaha wa maneno na upangiliaji wake. Hautamfaa chochote Fulani ufasaha wake na upangiliaji wake wa maneno iwapo matendo yake ni mabaya zaidi. Na wala hakutamdhuru Bilal chochote kukosea kwake katika maneno iwapo matendo yake yamenyooka safi, na yametakasika vizuri.”220 Bilal si mhanga wa kwanza wa tabia za jahiliya, na wala hakuwa wa mwisho. Ujahiliya hauna sehemu wala zama, wakati wowote na sehemu yoyote, panapokuwa na dhulma na ubabe basi pana ujahiliya, hata katika zama zetu hizi. Yale yaliyompata Bilal yanatokea sana katika jamii zetu sasa, ambazo zinadai kuwa zimestaarabika na kuendelea. Bali ni ustaarabu wa uwongo, ambao unaficha nyuma yake ujahiliya. Imam katika maneno yake amebainisha ukweli na kutoa jibu tosha kwa kila jahili mwenye kukomea katika ufasaha wa maneno, ili kwa ufasaha huo awanyanyue wengine na kuwatweza wengine. Nalo ni jibu linalowaweka hao wahafidhina mbele ya ukweli wa hali yao chafu, ambayo kwa makusudi kabisa wanaificha. Na hatimaye inawadondoka silaha iliyomo mikononi mwao, ambayo hawakushindwa kuinyanyua isipokuwa ni kwa sababu ya kushindwa kwao kuiweka mbele ya watu wenye imani.   Darajatur-Rafiah, uk. 363; Safinatul-Bihar, Juz. 1, uk. 105; Mustadrakul-Wasail, Juz. 4, uk. 279; Uddatud-Daiy cha Ibn Fahdi al-Hilliy, uk. 21.

220

130

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 130

4/23/2016 2:45:57 PM


HUYU NDIYE BILAL

Imam as-Sadiq B anamtetea Bilal: Bilal alitoa Adhana Madina miaka kadhaa, na Mtukufu Mtume 4 alikuwa akimtegemea katika kutangaza wakati wa Swala. Hivyo ilikuwa ni lazima Waislamu wamwamini na wamtegemee na kuegemeza kwake Swaumu zao na Swala zao. Na wamhesabu kuwa ni mjuzi wa nyakati.221 Isipokuwa ni kwamba imepokewa kutoka kwa Mtukufu Mtume 4 maelezo yaliyo kinyume na hivyo. Kama vile riwaya ya Ibn Umar kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 kwamba alisema: “Hakika Bilal hunadi usiku, hivyo basi kuleni na kunyweni mpaka atakaponadi Ibn Ummu Maktum.”222 Na lengo ni kama kutaka kumtuhumu Bilal kuwa hajui wakati wa Adhana, na pia kutaka kuishusha hadhi yake. Imam as-Sadiq B alipambana na yale yaliyonasibishwa na Bilal, akabainisha kuwa ni upotoshaji unaomgusa hata Mtukufu Mtume 4 kwa kumshushia hadhi yake. Na akasisitiza zaidi ya mara moja,223 kwamba Bilal hakuwa akiadhini usiku, bali alikuwa akiadhini inapochomoza alfajiri. Imekuja katika Hadithi sahihi ya Muawiya bin Wahbi, kutoka kwake B kwamba alisema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alikuwa na waadhini wawili, mmoja wao ni Bilal, na mwingine ni Ibn Ummu Maktum aliyekuwa kipofu. Yeye huyu alikuwa akiadhini kabla ya asubuhi, na Bilal alikuwa akiadhini baada ya asubuhi. Mtukufu Mtume 4 akasema: ‘Ibn Ummu Maktum anaadhini usiku, mtakaposikia Adhana yake kuleni na kunyweni mpaka mtakaposikia Adhana ya Bilal.’ Wafuasi wa watawala wakabadili Hadithi hii kwa kuitoa kwenye mwelekeo wake, wakasema: Hakika yeye 4 alisema: Hakika Bilal anaadhini usiku, mtakaposikia Adhana yake kuleni na kunyweni mpaka mtakaposikia Adhana ya Ibn Ummu Maktum.’”224   Safinatul-Bihar, Juz. 1, uk. 104.   Sahih Bukhar, Juz. 1, uk. 311, kitabu cha adabu, mlango wa 405, Hadithi ya 586. 223   Wasailus-Shiah, Juz. 4, uk. 625 na 626, mlango wa 8, Adhana, Hadithi ya 2 – 4. 224   Wasailus-Shiah, Juz. 4, uk. 625, mlango wa 8, Adhana, Hadithi ya 2. 221 222

131

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 131

4/23/2016 2:45:57 PM


HUYU NDIYE BILAL

Nukuu hii kutoka kwa Imam as-Sadiq B iko wazi, ikithibitisha upotoshaji wao wa kauli ya Mtukufu Mtume 4, na kwamba kauli yake imenukuliwa kwa kugeuzwa. Zaidi ya hapo ni kwamba imepokewa kwa sura sahihi Hadithi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 inayoafikiana na riwaya ya Imam as-Sadiq B, kwa sanadi mbalimbali kutoka katika njia za Ahlus-Sunnah. Ni riwaya kutoka kwa Aisha, na Anisah binti Khabib, na Zaydi bin Thabit, na Saad bin Ibrahim na wengineo.225 Na hakika Bilal aliashiria ule uwongo unaodaiwa dhidi yake, ambapo alisema: “Tulikuwa hatuadhini mpaka tuione alfajiri.”226

Musnad Ahmad, Juz. 2, uk. 185; Sunanul-Kubra cha Bayhaqiy, Juz.1, uk. 382; Nasburayat, Juz. 1, uk. 283; Fathul-Bariy, Juz. 2, uk. 85. AL-GHADIR 1 44 – 45; SunanulKubra cha Bayhaqiy, Juz. 1, uk. 382 – 383. 226   Nasburayat, Juz. 1, uk. 287. Muntakhabu Kanzul-Ummal, Juz. 3, uk. 276. 225

132

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 132

4/23/2016 2:45:57 PM


HUYU NDIYE BILAL

Faslu ya Saba KUANZA KWA ADHANA Tutazungumzia: 1.

Je Adhana ilianza baada ya Hijra kwa njia isiyokuwa wahyi?

2.

Adhana ilianza kwa njia ya wahyi.

3.

Maimamu wa Ahlul-Bayt wanautetea wahyi katika Adhana.

4.

Adhana ilianza lini?

5.

Wakati ilipoanzwa kutangazwa Adhana.

6.

Bukhari na Muslim wamezipuuza Hadithi za ndoto.

7.

Vipengele vya Adhana ya Bilal.

8.

Adabu za Adhana ya Bilal na sifa zake.

9.

Tupe raha ewe Bilal.

10. Adhana katika upande wake wa kisiasa na kiibada. 11. Adhana ya Bilal inawachukiza wanafiki na mushrikina. Je Adhana ilianza baada ya Hijra kwa njia isiyokuwa wahyi? Kuhusu namna Adhana ilivyoanza, kumepokewa riwaya mbalimbali ambazo madhumuni yake ni kubainisha kwamba, Adhana haikutokana na wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwenda kwa Mtume Wake 4. Bali ni ndoto aliyoiota mmoja kati ya Ansari, akamweleza 133

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 133

4/23/2016 2:45:57 PM


HUYU NDIYE BILAL

Mtukufu Mtume ndoto hiyo, naye akaamuru inadiwe kwa ajili ya Swala. Kati ya riwaya hizo ni ile iliyopokewa ndani ya kitabu Sunan Ibn Majah, kutoka kwa Abu Ubaydu, Muhammad bin Ubaydu bin Maimun, mwenyeji wa Madani. Kutoka kwa Muhammad bin Salmah mwenyeji wa Haran. Kutoka kwa Muhammad bin Is’haqa. Kutoka kwa Muhammad bin Ibrahim Taymiyyu. Kutoka kwa Muhammad bin Abdullah bin Zayd. Kutoka kwa baba yake, kwamba: “Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alikuwa amekusudia kuweka tarumbeta, na akawaamuru watu kutengeneza kengele na ikatengenezwa ya mbao. Ndipo akaoteshwa Abdullah bin Zayd usingizini, akasema: ‘Nimemuona mtu amevaa nguo za kijani huku kabeba kengele. Nikamwambia: Ewe mja wa Mwenyezi Mungu! Unauza kengele? Akasema; ‘Unataka kuifanyia nini?’ Nikasema: Kuitia watu kwenye Swala. Akasema: ‘Je nikujulishe lililo bora kuliko hilo?’ Nikasema: Ni lipi? Akasema: ‘Sema: Allahu Akbar. Allahu Akbar. Allahu Akbar.Allahu Akbar. Ash’hadu an laa ilaha ilallah. Ash’hadu an laa ilaha ilallah. Ash’hadu anna Muhammadan Rasulullah. Ash’hadu anna Muhammadan Rasulullah. Hayya Alas-Swalah. Hayya Alas-Swalah. Hayya Alal-Falah. Hayya Alal- Falah. Hayya Ala Khayril- Amali. Hayya Ala Khayril-Amali. Allahu Akbar. Allahu Akbar. Laa ilaha ilallah.’ Abdullah bin Zayd akaondoka mpaka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 akamweleza habari yote. Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 akasema: “Rafiki yenu huyu ameota ndoto. Nenda na Bilal msikitini 134

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 134

4/23/2016 2:45:57 PM


HUYU NDIYE BILAL

na umfunze hayo, hakika yeye ana sauti nzuri kuliko wewe.” Abdullah anasema: ‘Nikaenda na Bilal msikitini, nikamtamkisha huku naye akinadi maneno hayo. Mara Umar akasikia sauti. Akaenda kwa Mtume na kumwambia: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Wallahi hata mimi niliota mfano wa ndoto aliyoota.’”227 Habari ndio hiyo. Na riwaya zilizopokewa katika hekaya ya ndoto ya Abdullah ni nyingi, na zina mgongano na tofauti kiasi kikubwa. Ima katika matamshi yake au katika madhumuni yake. Lakini baadhi ya maulamaa wa baadhi ya madhehebu wamezing’ang’ania na kuthibitisha sharia ya Adhana kwa ndoto hii. Ukosoaji Muhimu: Hata tukifumbia macho mjadala unaohusu sanadi za riwaya hizo, bado tutasema: Sisi hatuwezi katu kuzisadiki riwaya hizi na kuzifuata, kutokana na baadhi ya nukta na kasoro zinazopatikana katika riwaya hizo. Hapa tunataja baadhi yake: Kwanza: Ni thabiti kwa namna isiyo na shaka kwamba Mtukufu Mtume 4 alikuwa anafungamana na Mwenyezi Mungu kwa njia ya wahyi. Na anapokea wahyi kutoka Kwake katika mambo mbalimbali, ambayo kati ya hayo ni uanzishaji wa sharia za Kiislamu: “Wala hatamki kwa matamanio. Hayakuwa haya ila ni wahyi uliotolewa.”228 “Sema, mimi si kioja miongoni mwa Mitume. Wala sijui nitakavyofanywa mimi wala nyinyi. Mimi nafuata niliyopewa Wahyi tu. Wala mimi si chochote ila ni mwonyaji, mwenye kubainisha.”229 Hivyo basi, hapa linajitokeza swali: Kuna siri gani   Sunan Ibnu Maajah Juz. 1, uk. 232 na 233; Al-Muswannaf cha Abdur-Razaq Juz. 1, uk. 455 – 456; As-Siratul Halabiyyah Juz. 2, uk. 94. Al-Muwatwau, Juz. 1, uk. 67; Nasburayat, Juz. 1, uk. 259; Sahih Tirmidhiy, Juz. 1, uk. 359; Al-Bidayat Wanihayat, Juz. 3, uk. 233. 228   Sura Najmi: 3 – 4. 229   Sura al-Ahqaf: 9. 227

135

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 135

4/23/2016 2:45:57 PM


HUYU NDIYE BILAL

iliyopelekea uanzishwaji wa Adhana uwe tofauti na sharia nyingine kwa namna makhususi? Je wahyi ulikuwa umemkatikia Mtume 4 kipindi hicho, mpaka akawa anangojea ndoto ya Abdullah bin Zayd ili atambue utashi wa Mwenyezi Mungu katika kuanzisha sharia ya Adhana? Baadhi ya maulamaa wa madhehebu za Kiislamu wameizungumzia maudhui hii, madhehebu zinazoona kwamba Adhana ilianzishwa kwa namna na mtindo huu. Wao wamebainisha baadhi ya sababu wanazoona kwamba zilipelekea Adhana kuanzishwa katika namna hii. Na tutakayotaja hapa ni kutoka kwenye jibu la Suhayliy, kwa sababu lenyewe limekusanya maelezo ambayo ndio muhimu zaidi yanayoweza kusemwa katika suala hilo. Katika kitabu Rawdhul-Anfi, imekuja kwamba: “Hakika hekima ya kiungu ndio iliyopelekea Adhana ianzishwe kupitia ulimi usiokuwa wa Mtukufu Mtume 4. Kwa kupitia ulimi wa mmoja miongoni mwa Waumini, ikiwa ni pamoja na Mwenyezi Mungu kumtukuza mja Wake na kuinua utajo wake. Basi Adhana hiyo ianzishwe kwa ulimi usiokuwa wake ili nimtukuze na kunyanyua hadhi yake. Hii ni maana iliyo bayana, kwani Mwenyezi Mungu anasema: ‘Na tukakunyanyulia utajo wako?’”230 Hakika maelezo haya hayafai kuwa jibu sahihi. Hiyo ni kwa sababu zifuatazo: 1.

Jibu hili si chochote isipokuwa ni dhana tu ambayo haiungwi mkono na dalili yoyote. Na hata katika riwaya za Adhana zilizotajwa hakuna maelezo yoyote yanayoashiria hilo, si kwa karibu wala kwa mbali.

2.

Ingekuwa ili Adhana imtukuze na kunyanyua utajo wake ni lazima ianzishwe kwa ulimi wa mtu mwingine, basi suala

Sura Inshirah: 4.

230

136

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 136

4/23/2016 2:45:57 PM


HUYU NDIYE BILAL

hilo lingekuwa ni wajibu pia katika uanzishwaji wa Swala, dua na nyuradi zenye kubeba utajo wa Mtukufu Mtume 4 na zenye kumtukuza na kunyanyua utajo wake. Wakati ambapo hayo mengine yote hayakuanzishwa kwa mtindo huo. 3.

Zaidi ya hapo ni kwamba, kuna Aya nyingi ambazo zimebeba utajo, sifa na utukuzo wa Mtume 4, na zote ziliteremka kwa njia ya wahyi, kama kauli ya Mwenyezi Mungu: “Hakika Mwenyezi Mungu na malaika Wake wanamswalia Nabii. Enyi ambao mmeamini! Mswalieni na mumsalimu kwa salamu.”231 Na kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na hakika wewe una tabia tukufu.”232 Na kauli ya Mwenyezi Mungu: “Hakika amewajia Mtume kutokana na nyinyi wenyewe. Yanamhuzunisha yanayowataabisha, anawahangaikia (nyinyi) sana, kwa waumini ni mpole, mwenye huruma.”233 Na kauli ya Mwenyezi Mungu: “Ewe Nabii! Hakika Sisi tumekutuma uwe shahidi na mbashiri na muonyaji. Na mlinganiaji kwa Mwenyezi Mungu kwa idhini Yake, na taa iangazayo.”234 Na lililo bayana zaidi ni kwamba, kwa nini halikuzingatiwa hilo katika shahada mbili, kama itasihi hekima hiyo inayodaiwa? Hakika katika shahada mbili kuna utukuzo wa kumtukuza Mtume 4 na kunyanyua utajo wake. Kwani kukiri na kuamini utume wake ni moja ya vitenganishi vinavyotenganisha kati ya imani na ukafiri, wakati ambapo Adhana haifiki katika kiwango hiki (cha kutenganisha).

4.

Hakika riwaya zilizotaja uanzishwaji wa Adhana kwa mtindo huu, zimebeba udhalilishaji na dharau dhidi ya Mtume

Sura Ahzab: 56.   Sura al-Qalam: 4. 233   Sura Tawba: 128. 234   Sura Ahzab: 45 – 46. 231 232

137

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 137

4/23/2016 2:45:57 PM


HUYU NDIYE BILAL

4, na si utukuzo na ukwezaji. Riwaya hizo zimetaja mambo yanayoshusha heshima na hadhi yake, kwa sababu zinamuonesha kuwa ni mwenye tahayari, hajui ni jinsi gani atawakusanya watu kwa ajili ya Swala. Na kwamba alikusudia kutumia tarumbeta, na akawaamuru watu watumie kengele, nalo ni jambo la Wakristo. Haya uko wapi hapa utukuzo na unyanyuaji wa jambo lake?! Pili: Hakika kundi hili la riwaya limenasibisha kwa Mtukufu Mtume 4 mambo na vitu ambavyo hawezi kuvisadikisha wala kuvidhania mtu aliyetambua cheo, adhama na ukamilifu wa tabia na sifa za Mtukufu Mtume 4. Kwani kutokana na riwaya hizo tunapata kwamba, alishikwa na ghamu na huzuni kwa kutokujua ni vipi atawakusanya Waislamu kwa ajili ya Swala, hivyo yeye na Maswahaba zake wakashauriana kuhusu jambo hili. Akaambiwa: Weka bendera pindi wakati wa Swala unapoingia, watu watakapoiona wataitana wao kwa wao. Lakini hilo halikumvutia. Na katika nukuu nyingine ni kwamba Mtukufu Mtume 4 alisema: Mpaka nikakusudia kuamuru watu watakaokuwa wanapita majumbani kuwajulisha watu kuingia kwa wakati wa Swala. Na mpaka nikakusudia kuamrisha watu watakaokuwa wanasimama katika ngome na kuwaita Waislamu. Na katika nukuu nyingine ni kwamba wao walimwambia: Ni bora tukanyanyua moto juu. Akasema: “Huo ni mtindo wa majusi.” Wakampa ushauri kwamba aweke tarumbeta la Mayahudi, lakini hakupendezwa na hilo. Na katika riwaya nyingine ni kwamba alikusudia kuweka tarumbeta kisha baadaye akaghairi kwa kuchukizwa nalo. Na wakamtajia kengele, lakini hakupendezwa nayo, akasema: “Huo ni mtindo wa Wakristo.” Kisha baadaye akajirudi na akaridhia kuwekwa kengele. Akaamuru hivyo, na hivyo ikatengenezwa ya 138

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 138

4/23/2016 2:45:57 PM


HUYU NDIYE BILAL

mbao ili iwe inapigwa kwa ajili ya Waislamu. Kisha akaachana na wazo hilo pale Abdullah bin Zayd alipomweleza ndoto yake. Je inafaa katika haki ya Nabii 4 awe katika upotevu hajui njia ya haki. Mara anakusudia kuweka tarumbeta kisha anaacha na kuhamia kwenye kengele? Wakati tunajua kwamba Mtukufu Mtume 4 anaongozwa na Mwenyezi Mungu, na tunajua kuwa hazushi sharia kwa utashi wake kiasi kwamba zikionekana ni mbovu ahame na kuziacha. Na wala haamrishi kitu bila amri hiyo kutoka kwa Mwenyezi Mungu:

‫ين ثُ َّم لَقَطَ ْعنَا ِم ْنهُ ْال َوتِينَ فَ َما‬ َ ‫َولَوْ تَقَ َّو َل َعلَ ْينَا بَع‬ ِ ‫او‬ ِ ‫يل أَلَخ َْذنَا ِم ْنهُ بِ ْاليَ ِم‬ ِ َ‫ْض أْالَق‬ َ‫اج ِزين‬ ِ ‫ِم ْن ُك ْم ِم ْن أَ َح ٍد َع ْنهُ َح‬ “Na lau kama angelituzulia baadhi ya maneno. Bila ya shaka tungelimshika kwa mkono wa kulia. Kisha kwa hakika tungelimkata mshipa mkubwa wa moyo! Na hapana yeyote katika nyinyi ambaye angeliweza kutuzuia naye.” (al-Haqqaq; 69:44-47).

Zaidi ya hapo ni kwamba, haijuzu kwa Mtukufu Mtume 4 kushauriana na watu katika suala la sharia inayotegemea uteremkaji wa wahyi. Mwenyezi Mungu anasema: “Sema: Hakika nafuata niliyopewa wahyi kutoka kwa Mola Wangu tu.”235 Na anasema tena: “Sema, mimi si kioja miongoni mwa Mitume. Wala sijui nitakavyofanywa mimi wala nyinyi. Mimi nafuata niliyopewa Wahyi tu, wala mimi si chochote ila ni mwonyaji, mwenye kubainisha.”236 Hivyo vipengele vya sharia vinavyoletwa na kutoka kwake si chochote isipokuwa ni wahyi wa Mwenyezi Mungu, alioufuata na kuwafikishia watu bila kugeuza wala kubadili chochote kwa utashi wake mwenyewe au kwa kushauriana na mtu. Mwenyezi Mungu anasema: “Sema: Haifai   Sura Aaraf: 203.   Sura al-Ahqaf: 9.

235 236

139

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 139

4/23/2016 2:45:57 PM


HUYU NDIYE BILAL

mimi kubadilisha kwa hiyari ya nafsi yangu; sifuati ila niliyopewa wahyi; hakika mimi naogopa, nikimwasi Mola Wangu, adhabu ya siku iliyo kuu.”237 Inaweza ikasemwa: Hakika Mtukufu Mtume 4 alichukua ushauri wa watu pale alipoungwa mkono na wahyi. Nasema: Hilo haliwezi kusaidia, kutokana na nukuu kuonesha kuwa aliamuru itumike kengele kutokana na ushauri wa watu, kabla hajahama na kubadili mawazo. Na hatimaye akachukua ndoto ya mwana wa Zaydi ambayo katika riwaya zinazotegemewa katika jambo hilo, hakuna ishara yoyote inayoonesha kuwa ndoto hiyo ina uhusiano wowote na wahyi. Tatu: Hakika mwenye kufuatilia historia ya Mtukufu Mtume 4 atakuta: Hakika yeye alikuwa na shauku katika ufikishaji wake wa ujumbe, ili kuthibitisha kuwa sharia anazoziweka ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na kuziepusha na kila aina ya shaka na dhana. Na hili ndilo tunaloliona katika kutoamuru kutumiwa moto au tarumbeta au kengele, akiogopa kuwa isije ikasemwa: Hakika hilo ni jambo la Majusi, au Mayahudi au Wakristo. Zaidi ya hapo ni kuwa, maadui wa ujumbe walikuwa wanasubiri fursa, ili waweze kupandikiza shaka kuhusu unabii wake, na wamtuhumu kuwa anachukua mafunzo yake kutoka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu: “Wao husema: Hakika wewe ni mzushi. Bali wengi wao hawajui.”238 Na katika Aya nyingine anasema: “Na hakika tunajua kwamba wao wanasema yuko mtu anayemfundisha.”239 Kutokana na hayo tunasema: Je kuchukua Adhana kutoka kwa Swahaba wake hakuwajibishi udhaifu katika msimamo wake, na udhaifu katika hoja yake, mbele ya shaka na tuhuma za maadui zake?   Sura Yunus: 15.   Sura Nahli: 101. 239   Sura Nahli: 103. 237 238

140

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 140

4/23/2016 2:45:57 PM


HUYU NDIYE BILAL

Nne: Ni tofauti na mgongano uliyopo katika riwaya. Hakika usomaji wa mwanzo tu unadhihirisha tofauti katika maeneo mengi, hapa tutataja baadhi: 1.

Hakika yeye aliota ndoto hiyo katika mikesha mitatu na si katika usiku mmoja, kama inavyojulikana kutoka katika ­riwaya nyingine.240

2.

Kuna tofauti katika idadi ya takbira alizoota mwana wa Zaydi. Imepokewa mara takbira nne nne, na mara takbira mbili mbili.241

3.

Kuna mgongano katika vipengele vya Iqama. Kuna riwaya inaonesha matamshi ya Iqama yalikuwa ni mara moja. Na kwamba takbira ya kwanza na ya mwisho nazo zilikuwa ni mara moja. Na riwaya nyingine inaonesha kuwa matamshi ya Iqama yalikuwa ni mara mbili mbili. Na takbira ya kwanza ilikuwa ni mara nne kama Adhana.

4.

Pia imekuja kwamba, Adhana iliyootwa matamshi yake yalikuwa ni mara mbili mbili, na Iqama ilikuwa pia matamshi yake ni mara mbili mbili.242

Tano: Ukiachana na yote hayo, Dawidiy amesimulia kutoka kwa Ibn Is’haqa kwamba: “Jibril alimletea Mtukufu Mtume 4 Adhana siku nane kabla Abdullah bin Zayd na Umar hawajamweleza ndoto yao.”243 Na kwa msingi huo itakuwaje Mtukufu Mtume 4   Al-Muswannaf cha Abdur Razaq, Juz. 1, uk. 461; Siratul-Halabiyyah, Juz. 2, uk. 95; Siratun-Nabawiyyah cha Ibn Hisham, Juz. 2, uk. 508; Al-Bidayat Wan-Nihayat, Juz. 3, uk. 231 – 233. 241   Majmauz-Zawaid, Juz. 1, uk. 329; Sunan Abu Dawud, Juz. 1, uk. 140; Al-Muswannaf cha Abdurazaq, Juz. 1, uk. 455; Siratul-Halabiyyah, Juz. 2, uk. 94; Siratun-Nabawiyyah cha Ibn Hisham, Juz. 2, uk. 508. 242   Siratul-Halabiyyah, Juz. 2, uk. 94 – 95. Sunan Abu Dawud, uk. 135. 243   Fat’hul-Bariy, Juz. 2, uk. 67; Al-Mawahibud-Daniyyah, Juz. 1, uk. 72. 240

141

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 141

4/23/2016 2:45:57 PM


HUYU NDIYE BILAL

awe ni mwenye kutahayari kuhusu namna ya kuwakusanya watu kwa ajili ya Swala? Jambo hili linahuzunisha kiasi kwamba awe hajui cha kufanya. Mara akusudie kutumia tarumbeta na mara nyingine akusudie kutumia kengele? Hasa baada ya kutazama yale yaliyopokewa, kwamba mwana wa Zayd alioteshwa ndoto hiyo katika usiku uleule, yaani baada ya Mtume 4 kushauriana na Maswahaba zake, na mwana wa Zayd akaguswa sana na huzuni ya Mtukufu Mtume 4. Na kwa kutazama zile riwaya zinazoonesha kwamba mwana wa Zayd hakuchelewa kumsimulia Mtukufu Mtume 4 ndoto yake.244 Adhana ilianza kwa njia ya wahyi: Katika baadhi ya nukuu yamekuja maelezo kwamba Mwenyezi Mungu alimfundisha Mtume Wake Adhana kabla hata hajahama Makkah. Jambo ambalo linapingana na madhumuni ya riwaya za ndoto, kwani inajulikana kuwa: Kisa cha ndoto kinajieleza kuwa ni cha mwaka mmoja baada ya hijra huko Madina. Hapa tunataja baadhi ya nukuu hizo: 1.

Kutoka kwa Ali bin Abutalib B kwamba alisema: “Mwenyezi Mungu alipotaka kumfundisha Mtume Wake Adhana, Jibril B alimjia na mnyama anayeitwa Buraq. Alipokwenda kumpanda akawa anagoma, Jibril akamwambia mnyama yule: ‘Tulia. Wallahi hajawahi kukupanda kiumbe mtukufu mbele ya Mwenyezi Mungu kushinda Muhammad 4.’ Basi akampanda mpaka katika pazia iliyo mbele ya Mwingi wa rehema. Wakati wakiwa hapo mara alitokea Malaika kutoka katika pazia hilo. Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 akasema: ‘Ewe Jibril ni nani huyu?’

Siratul-Halabiyyah, Juz. 2, uk. 95; Siratun-Nabawiyyah cha Ibn Hisham, Juz. 2, uk. 508.

244

142

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 142

4/23/2016 2:45:58 PM


HUYU NDIYE BILAL

Jibril B akasema: ‘Naapa kwa yule aliyekupeleka kwa haki kuwa Nabii, hakika mimi ni kiumbe niliye na nafasi ya karibu sana. Na hakika tangu kuumbwa kwangu, Malaika huyu sikuwahi kumuona kabla ya kumuona sasa.’ Malaika akasema: ‘Allahu Akbar. Allahu Akbar.’ Ikasikika ikisemwa kutoka nyuma ya pazia: ‘Amesema kweli mja Wangu. Mimi ndiye Mungu ambaye hapana mungu isipokuwa Mimi.’ Kisha Malaika akasema: ‘Ash’hadu an laa ilaha ilallah.’ Ikasikika ikisemwa kutoka nyuma ya pazia: ‘Amesema kweli mja Wangu. Mimi ndiye niliyemtuma Muhammad.’ Kisha Malaika akasema: ‘Hayya Alas-Swalah. Hayya AlalFalah.’ Kisha Malaika akasema: ‘Allahu Akbar. Allahu Akbar.’ Ikasikika ikisemwa kutoka nyuma ya pazia: ‘Amesema kweli mja Wangu. Mimi ndiye Mkuu. Mimi ndiye Mkuu.’ Kisha akasema: ‘Laa ilaha illallah.’ Ikasikika ikisemwa kutoka nyuma ya pazia: ‘Amesema kweli mja Wangu. Mimi ndiye Mungu ambaye hapana mungu isipokuwa Mimi.’ Kisha Malaika akamkamata mkono Muhammad 4 na kumtanguliza. Akawasalisha wakazi wa mbinguni akiwemo Adam na Nuhu B.”245 Nasi tuna maoni juu ya riwaya hii. Hakika inakaribia kumfanya Mwenyezi Mungu ana umbo, hivyo ni lazima tuiletee tafsiri nyingine au tuitupilie mbali.   Nasburayat, Juz. 1, uk. 260 – 261; Kashful-Astar, Juz. 1, uk. 178; Majmauz-Zawaid, Juz. 1, uk. 328; Rawdhul-Anfu, Juz. 2, uk. 285; Siratul-Halabiyyah, Juz. 1, uk. 373; Fat’hul-Bariy, Juz. 2, uk. 63.

245

143

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 143

4/23/2016 2:45:58 PM


HUYU NDIYE BILAL

2.

Kutoka kwa Ibn Umar, kutoka kwa baba yake, kwamba alisema: “Mtukufu Mtume 4 alipopelekwa mbinguni, Mwenyezi Mungu alimpa Adhana, akateremka nayo na akamfundisha Bilal.”246

3.

Kutoka kwa Zahriy, kutoka kwa Salim, kutoka kwa baba yake, kwamba Mtukufu Mtume 4 alipopelekwa mbinguni, Mwenyezi Mungu alimfunulia Adhana.”247

4.

Kutoka kwa Muhammad bin Hasan Tusiy, kutoka kwa Muhammad bin Ali bin Mahbub, kutoka kwa Ali bin Sandiy, kutoka kwa Ibn Abi Umayri, kutoka kwa Ibn Udhaynah, kutoka kwa Zurarah na Fadhlu bin Yasar, kutoka kwa Abu Ja’far B, amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alipopelekwa mbinguni na akafika Baytu Maamur, wakati wa Swala ulifika. Jibril Akaadhini na kukimu. Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 akatangulia mbele, Malaika na Manabii wakapanga mistari nyuma ya Mtume wa Mwenyezi Mungu 4.” Wanasema: Tukamuuliza aliadhini vipi? Akasema: “Allahu Akbar. Allahu Akbar. Ash’hadu an laa ilaha ilallah. ‘Ash’hadu an laa ilaha ilallah….’’248

5.

Kutoka kwa Husein bin Ali B, kwamba aliulizwa kuhusu Adhana na wanayosema watu. Akasema: “Ni wahyi ulioteremka kwa Mtume wenu. Ninyi mnadai kuwa alichukua Adhana kutoka kwa Abdullah bin Zaydi, lakini mimi nilimsikia baba yangu Ali bin Abutalib B akisema: ‘Mwenyezi Mungu alimteremsha Malaika wakati Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alipopaa mbinguni, akaadhini mara mbili mbili, na akakimu mara mbili mbili. Kisha Jibril akamwambia

Siratul-Halabiyyah, Juz. 2, uk. 93. Fat’hul-Bariy, Juz. 2, uk. 63.   Nasburayat, Juz. 1, uk. 262. 248   Tahdhib, Juz. 2, uk. 60, Hadithi ya 210; Al-Istibswar, Juz. 1, uk. 305; Biharul-An’war, Juz. 18, Uk. 307. 246 247

144

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 144

4/23/2016 2:45:58 PM


HUYU NDIYE BILAL

Mtume: Ewe Muhammad, hiyo ndio Adhana ya Swala.’”249 Hizi ni baadhi ya nukuu zilizopokewa zikionesha kuwa Mtukufu Mtume 4 alijifunza Adhana pindi alipopelekwa mbinguni. Na yeyote atakaye kupanua zaidi maarifa yake kuhusu hili, basi arejee vyanzo vilivyotajwa kwenye tanbihi.250 Kisha ni kwamba imepokewa kutoka kwa Anas, kwamba Jibril B alimwamuru Mtukufu Mtume kutoa Adhana wakati ilipofaradhishwa Swala.251 Nayo ni hadithi iliyo wazi na bayana mno, na wala haihitaji kuonesha jinsi inavyopingana na riwaya za ndoto zilizotangulia. Maimamu wa Ahlul-Bayt wanautetea wahyi katika Adhana:Baada ya yote hayo yaliyotangulia, Ahlul-Bayt walipambana na riwaya hizi, na wakazikadhibisha kwa njia na suhula mbalimbali. Wakabainisha haki iliyopo, nayo ni kwamba Adhana ni wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu ulioteremshwa na Jibril B kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4. Na habari katika hilo ni nyingi, hapa tunataja baadhi yake. 1.

Katika riwaya ya kitabu Daaimul-Islam, imepokewa kutoka kwa Ja’far bin Muhammad B, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake, kutoka kwa Husein bin Ali B, kwamba aliambiwa wanasema kuhusu Adhana kwamba, kulikuwa na ndoto aliyoiota Abdullah bin Zaydi, naye akamweleza ndoto hiyo Mtukufu Mtume 4, ndipo akaamuru iwe Adhana. Husein B akasema: “Ni wahyi ulioteremka kwa Mtume wenu. Ninyi mnadai kuwa alichukua Adhana kutoka kwa Abdullah bin Zaydi, ilihali Adhana ni dira ya

Al-Jaafariyat, uk. 42; Mustadrakul-Wasail, Juz. 4, uk. 17. Daaimul-Islam, Juz. 1, uk. 142. 250   Darajatur-Rafiah, Juz. 1, uk. 329; Nasburayat, Juz. 1, uk. 262; Tafsirul-Qummiy, Juz. 2, uk. 11; Mustadrakul-Wasail, Juz. 4, uk. 28; Biharul-An’war, Juz. 18, uk. 309; KanzulUmmal, Juz. 8, uk. 329; Nasburayat, Juz. 1, uk. 260 – 262. 251   Fat’hul-Bariy, Juz. 2, uk. 63; Al-Mawahibud-Daniyyah, Juz. 1, uk. 72. 249

145

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 145

4/23/2016 2:45:58 PM


HUYU NDIYE BILAL

dini yenu?” Husein B akaghadhibika na akasema: “Mimi nilimsikia baba yangu Ali bin Abutalib B akisema: ‘Mwenyezi Mungu alimteremsha Malaika wakati Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alipopaa mbinguni…” akasimulia Hadithi ya Miraji kwa urefu wake mpaka akasema: “Mwenyezi Mungu akamtuma Malaika ambaye hakuonekana mbinguni kabla na baada ya hapo, akaadhini mara mbili mbili, na akakimu mara mbili mbili.” Akataja Adhana ilivyo, kisha akasema: “Jibril B akamwambia Mtukufu Mtume 4: “Ewe Muhammad, adhini hivyo kwa ajili ya Swala.”252 Na katika kitabu al-Wasail imepokewa kutoka kwa Muhammad bin Mukiy Shahid, kutoka kwa Ibn Abu Aqil, kutoka kwa as-Sadiq B kwamba, aliwalaani watu ambao walidai kuwa Mtukufu Mtume 4 alichukua Adhana kutoka kwa Abdullah bin Zaydi. Akasema: “Wahyi unateremshwa kwa Mtume wenu, kisha ninyi mnadai eti alichukua Adhana kutoka kwa Abdullah bin Zaydi?!”253 2. Na katika Tafsiri Ayash imepokewa kutoka kwa Abduswamad bin Bashir, amesema: Ilitajwa mbele ya Abu Abdullah jinsi ilivyoanzishwa Adhana. Ikasemwa: Mtu mmoja miongoni mwa Ansari aliota ndoto usingizini, akasimulia ndoto yake kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4, ndipo Mtukufu Mtume 4 akamfunza Adhana Bilal. Abu Abdullah B akasema: “Wameongopa. Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alikuwa amelala ndani ya kivuli cha Kaaba, mara akajiwa na Jibril B akiwa na beseni lenye maji kutoka mbinguni. Akamwamsha na kumwamuru aoge maji hayo. Kisha akampandisha juu ya kipando chenye maelfu ya rangi zitokanazo na nuru. Akampandisha mpaka alipofika kwenye   Mustadrakul-Wasail, Juz. 4, uk. 17 -18; Daaimul-Islam, Juz. 1, uk. 142; Al-Jaafariyat, uk. 42, Hadithi ya 4061. 253   al-Wasail, Juz. 4, uk. 612. 252

146

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 146

4/23/2016 2:45:58 PM


HUYU NDIYE BILAL

milango ya mbingu…” Imam aliendelea kusimulia kwamba: “Mwenyezi Mungu akamwamuru Jibril, akasema: ‘Allahu Akbar. Allahu Akbar….’” Imam aliendelea kusimulia mpaka aliposema: “Kisha akamwamuru Jibri akakamilisha Adhana, akakimu Swala, na Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 akatangulia mbele akawaswalisha.” Kisha akasema Abu Abdullah: “Hivyo ndivyo ilivyoanzishwa Adhana.”254 Adhana ilianza lini? Na Bilal alijifunza Adhana lini? Kuhusu mwaka ambao Adhana ilianza, hata kama hatuko katika nafasi ya kuhakiki, isipokuwa ni kwamba, kuwa bayana kwa mas’ala hii, kutasaidia kuweka wazi hali ya riwaya zilizotangulia zinazohusu ndoto, na hasa katika maelezo yanayohusu wakati aliojifunza Bilal Adhana. Hivyo imekuwa ni lazima kwetu tuashirie angalau kwa ishara ya kupita. Tunasema: Si vigumu kusema kwamba Adhana ilianza huko Makkah kabla ya hijra. Na kwamba Mtukufu Mtume 4 yeye na wale waliomwamini huko Makkah, walikuwa wakiadhini kwa ajili ya Swala zao hata kabla hawajahamia Madinah. Lakini kwa namna ambayo ilikuwa inaoana na hali ya mazingira waliyokuwa wakiishi wakati huo. Hivyo walikuwa wakijiadhinia wao wenyewe bila kuitangaza na kuidhihirisha Adhana. Kwani imekuja katika Hadithi ya Anas kwamba, Jibril B alimwamuru Mtukufu Mtume 4 kuadhini pindi ilipofaradhishwa Swala.255 Na imekuja katika riwaya ya Miraji iliyotangulia, iliyomo katika kitabu Daaimul-Islam, kutoka kwa Husein bin Ali B kwamba, baada ya Jibril B kuadhini alimwambia Mtukufu Mtume 4: Ewe Muhammad hii ndio Adhana ya Swala.256   Tafsirul-Ayyash, Juz. 1, uk. 157 – 159, Hadithi ya 530.   Fat’hul-Bariy, Juz. 2, uk. 63; Al-Mawahibu ad-Daniyyah, Juz. 1, uk. 72. 256   Mustadrakul-Wasail, Juz. 4, uk. 17 -18; Daaimul-Islam, Juz. 1, uk. 142. 254 255

147

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 147

4/23/2016 2:45:58 PM


HUYU NDIYE BILAL

Hakuna lolote linalojulisha kuwa sharia hii ilikuwa makhususi kwa Mtukufu Mtume 4 tu. Sharia hii iliwahusu Waislamu wote kama zilivyokuwa sharia nyingine za Mwenyezi Mungu zilizomteremkia Mtukufu Mtume 4. Ndiyo, huenda Mtukufu Mtume 4 aliweka wakati na kipindi cha kuanza kuitangaza Adhana waziwazi kwa kungojea wakati utakaofaa. Imekuja katika riwaya ya Abdullah bin Umar kwamba alisema: “Mtukufu Mtume 4 alipopelekwa mbinguni, Mwenyezi Mungu alimpa Adhana, akateremka nayo na akamfundisha Bilal.”257 Hivyo katika nukuu hii kuna dalili kwamba Bilal alijifunza Adhana akiwa huko Makkah. Lakini hii haimaanishi kwamba aliamrishwa kuitangaza waziwazi, kwani kama ilivyo wazi ni kwamba maslahi ya kujifunza hayakomei katika kuitangaza. Na katika riwaya nyingine, ni kwamba imepokewa kutoka kwa Abu Ja’far kuwa alisema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alipopelekwa mbinguni na akafika Baytu Maamur, wakati wa Swala ulifika. Jibril Akaadhini na kukimu….” Riwaya imeendelea kueleza mpaka ikasema: “Tukamwambia: Aliadhiniaje?”Akataja B vipengele vya Adhana na Ikama na akasema: “Akamwamuru Bilal kuadhini hivyo, na aliendelea kuadhini hivyo mpaka Mwenyezi Mungu alipomfisha Mtume wake.’’258 Hapa imebaki kuashiria kwamba, Adhana ni jambo mustahabu katika Swala zote tano za faradhi, ya jamaa au mufrada. Hivyo hekima ya kuanzishwa Adhana haikomei na kufungika katika kuitangaza juu ya paa tu. Na jambo hili liko bayana na wazi halihitaji maelezo ya ziada. Lakini je kuna mtu yeyote aliyeitangaza waziwazi Adhana kabla ya hijra? Hili halijulikani kwa uhakika, hata kama imepokewa kwamba Bilal na wengine waliadhini huko Makkah.259   Fat’hul-Bariy, Juz. 2, uk. 63; Siratul-Halabiyyah, Juz. 2, uk. 93.   Tahdhib, Juz. 2, uk. 210; Al-Istibswar, Juz. 1, uk. 305. 259   Siratul-Halabiyyah, Juz. 2, uk. 93. 257 258

148

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 148

4/23/2016 2:45:58 PM


HUYU NDIYE BILAL

Wakati ilipoanza kutangazwa Adhana: Hakika mwenye kujua hali halisi ya mazingira ya kisiasa na kijamii yaliyokuwepo Makkah, anatambua kwamba Waislamu walibanwa kwa kuelekezewa mashambulizi makali ya kikatili kutoka pande zote. Wakati huo wao walikuwa kwanza ndio wako katika hatua za mwanzo kabisa za jengo lao, na walikuwa hawajajiandaa kwa maandalizi ya mapambano na makabiliano ya namna hiyo. Na hali hii mara nyingi ilikuwa inajiakisi kwa kuwanyang’anya Waumini uhuru wa kutekeleza ibada zao na matendo ya dini yao. Hivyo tunaloliona sisi ni kwamba Adhana ilidhibitiwa na hali hii, na hivyo maelezo yaliyopokewa kwamba Bilal au mwingine asiyekuwa yeye aliadhini huko Makkah, ni lazima awe aliadhini ndani ya mipaka maalumu. Kisha walipokwenda Madina na wakatofautiana namna ya kujikusanya kwa ajili ya Swala, ndipo Mtume 4 akamwamuru Bilal kuitangaza Adhana kwa kuiadhini waziwazi, baada ya kuwa tayari alishamfundisha Adhana hiyo tangu Makkah. Ushahidi juu ya hayo ni ile riwaya iliyokuja kutoka kwa Ibn Umar, kwamba alisema: “Waislamu walipofika Madina walikuwa wakijikusanya kwa kuvizia muda wa Swala, bila muda huo kutangazwa, ndipo siku moja wakamweleza Mtume kuhusu suala hilo. Baadhi wakawaambia wengine: ‘Tengenezeni kengele kama kengele ya Wakristo.’ Wengine wakasema: ‘Tarumbeta kama la Mayahudi.’ Umar akasema: ‘Kwa nini msichague mtu awe ananadi kwa ajili ya Swala?’ Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 akasema: ‘Ewe Bilal! Simama uadhini.’”260 Imepokewa kutoka kwa Anas bin Malik kwamba alisema: “Walitaja kwamba wanataka kujua wakati wa Swala kwa kuweka kitu kitakachowajulisha. Wakasema kwamba wanyanyue mnara wa   Al-Muswannaf cha Abdurazaq, Juz. 1, uk. 457.

260

149

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 149

4/23/2016 2:45:58 PM


HUYU NDIYE BILAL

moto, au wapige kengele. Ndipo akaamrishwa Bilal atoe Adhana kwa kutaja vipengele vyake mara mbili mbili, na akimu kwa kutaja vipengele vyake mara moja moja.”261 Kutokana na nukuu hizi mbili tunajifunza kwamba, Waislamu ndio waliotofautiana na kushughulishwa na jinsi gani watajikusanya kwa ajili ya Swala. Baadhi yao wakapendekeza jambo ambalo ni la Mayahudi, na wengine wakapendekeza ambalo ni la Wakristo. Ama Mtukufu Mtume 4 yeye hakuwa katika upotevu wala tahayari, hivyo alimwamuru Bilal kutoa Adhana baada ya kusikia aliyoyasikia kutoka kwa Maswahaba zake. Jambo ambalo linathibitisha kwamba Adhana ilikuwa imeshaanza na kufanywa sharia hata kabla ya wakati huo, na kwamba Bilal alikuwa anaijua Adhana kabla ya hapo. Bukhari na Muslim wamezipuuza Hadithi za ndoto: Hakika miongoni mwa mambo anayokutana nayo mtu mwenye kufanya uchunguzi, kuhusu riwaya zilizopokewa katika suala la kuanzishwa kwa Adhana, ni kitendo cha Bukhari na Muslim kuziacha Hadithi za ndoto. Wao katika vitabu vyao hawajaandika riwaya yoyote ile, inayoashiria kwamba kuna mtu yeyote miongoni mwa Waislamu aliota ndoto ya Adhana. Na wameungana wote wawili kwa kuiandika riwaya ya Ibn Umar262, ambayo haina ishara yoyote kuhusu ndoto ya Ibn Zayd au ya mwingine yeyote. Bali katika riwaya hiyo kuna maelezo yasemayo tu: Kwamba Waislamu walijadiliana kuhusu namna ya kujikusanya kwao kwa ajili ya Swala, wakatoa rai mbalimbali kuhusu hilo. Na ndipo Mtukufu Mtume 4 akamwamuru Bilal kunadi kwa ajili ya Swala. Kisha ni kwamba, hakika al-Hakim katika kitabu al-Mustadrak naye ameziacha riwaya hizi, licha ya kwamba yeye alijipa wajibu   Sahih Muslim, Juz. 2, uk. 2.   Sahih Bukhar. Sahih Muslim, Juz. 2, uk. 2.

261 262

150

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 150

4/23/2016 2:45:58 PM


HUYU NDIYE BILAL

katika kitabu chake hiki, wa kuandika Hadithi zote ambazo Bukhari na Muslim wameziacha, zile ambazo ni sunnah sahihi na alizoziona kuwa zimetimiza masharti ya hao wawili au ya mmoja wao. Jambo ambalo linajulisha kuwa hata yeye alizikuta si sahihi riwaya hizo za ndoto, kwa mujibu wa masharti ya Bukhari na Muslim. Asqalaniy ametamka bayana kwamba: Bukhari hakuiandika hadithi ya Ibn Zayd, kwa sababu ipo kinyume na masharti yake.263 Na al-Hakim ametaja ila na sababu iliyowafanya Bukhari na Muslim wazipuuze riwaya hizo za ndoto ya Adhana, anasema: “Hakika Masheikh wawili wameiacha Hadithi ya Abdullah bin Zaydi inayohusu ndoto ya Adhana aliyomsimulia Mtukufu Mtume 4, kwa sababu mauti ya Abdullah bin Zaydi yalitangulia kabla ya Adhana. Inasemekana alikufa kishahidi katika vita vya Uhudi. Na inasemekana ni muda mchache baada ya Uhud, na Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi.”264 Maneno haya ya al-Hakim yamejengeka katika dhana ya kwamba Adhana ilianza baada ya vita vya Uhudi, nalo ni jambo alilolichukua na kulipata Asqalaniy kutoka katika riwaya ya Ibn Abbas,265 ambapo imenukuliwa kutoka kwake kwamba alisema: “Hakika sharia ya Adhana iliteremka pamoja na Aya isemayo:

َّ ‫ي لِل‬ َ ‫يَا أَيُّهَا الَّ ِذينَ آ َمنُوا إِ َذا نُو ِد‬ ِ َّ‫صلاَ ِة ِم ْن يَوْ ِم ْال ُج ُم َع ِة فَا ْس َعوْ ا إِلَ ٰى ِذ ْك ِر للاه‬ َ‫َو َذرُوا ْالبَ ْي َع ۚ ٰ َذلِ ُك ْم َخ ْي ٌر لَ ُك ْم إِ ْن ُك ْنتُ ْم تَ ْعلَ ُمون‬ “Enyi mlioamini! Ikinadiwa Swala siku ya Ijumaa, nendeni upesi kwenye dhikri ya Mwenyezi Mungu, na wacheni biashara. Hayo ni bora kwenu, kama mnajua.’” (al-Jum’a; 62:9)   Fat’hul-Bariy, Juz. 2, uk. 63.   Mustadrakul-Hakim, Juz. 4, uk. 348. 265   Fat’hul-Bariy, Juz. 2, uk. 62. 263 264

151

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 151

4/23/2016 2:45:58 PM


HUYU NDIYE BILAL

Na inajulikana fika kwamba Sura al-Jum’ah iliteremka baada ya vita vya Uhud. Na kwa kuainisha muda ni mwaka wa saba wa hijiriya. Kwa kutegemea riwaya ya Bukhari kutoka kwa Abu Hurayra, ambapo amesema: “Tulikuwa tumeketi kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 ilipomteremkia Sura al-Jum’ah.” Na inajulikana bayana kwa Abu Huraira alisilimu mwaka wa saba wa hijiriya, hiyo ni kwa itifaki ya wanahadithi, kama alivyosema Imam Sharafudin, Mwenyezi Mungu amrehemu. Ama kuhusu suala la Abdullah bin Zayd kufariki katika vita vya Uhud, huenda yale maelezo yaliyokuja katika kitabu Hilyatul-Awliyai yakawa ni ushahidi juu ya hilo. Imepokewa kutoka kwa Ubaydullah bin Umar kwamba alisema: “Binti ya Abdullah bin Zayd aliingia kwa Umar bin Abdul-Aziz, akasema: ‘Ewe Kiongozi wa Waumini! Mimi ni binti wa Abdullah bin Zayd. Baba yangu alishiriki katika vita vya Badri na aliuwawa siku ya Uhud.’ Umar akasema: ‘Huo ni utukufu si birauli la maziwa yaliyokuwa kama maji, yakarudi baadaye yakiwa mkojo. Niombe utakalo.’ Akaomba, naye akampa atakalo.”266 Imam Sharafudin ametoa maelezo juu ya hilo akasema: Kama Abdullah bin Zayd angekuwa aliota ndoto hiyo kama wasemavyo, basi binti yake angelitaja hilo kama alivyotaja kushiriki kwake Badri na kufa kwake kishahidi katika Uhud, kama ilivyo dhahiri.267 Vipengele vya Adhana ya Bilal: Imepokewa kutoka kwa Zurarah na Fadhlu bin Yasar, kutoka kwa Abu Ja’far B kwamba alisema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alipopelekwa mbinguni na akafika Baytu Maamur, wakati wa Swala ulifika. Jibril Akaadhini na kukimu. Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 akatangulia mbele, Malaika na Manabii wakapanga mistari nyu  Hilyatul-Awliyai, Juz. 5, uk. 322; Al-Iswabah, Juz. 4, uk. 72.   An-Nassu wal-Ijtihad, uk. 233.

266 267

152

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 152

4/23/2016 2:45:58 PM


HUYU NDIYE BILAL

ma ya Mtume wa Mwenyezi Mungu 4.” Wanasema: Tukamuuliza aliadhini vipi? Akasema: “Allahu Akbar. Allahu Akbar. Ash’hadu an laa ilaha ilallah. Ash’hadu an laa ilaha ilallah…. Ash’hadu anna Muhammadan Rasulullah. Ash’hadu anna Muhammadan Rasulullah. Hayya AlasSwalah. Hayya Alas-Swalah. Hayya Alal-Falah. Hayya Alal-Falah. Hayya Ala Khayril-Amali. Hayya Ala Khayril-Amali. Allahu Akbar. Allahu Akbar. Laa ilaha ilallah. Laa ilaha ilallah.’’’ Na Ikama ni kama Adhana, isipokuwa ina: ‘“Qad Qamat Swalah. Qad Qamat Swalah. Baina ya ‘Hayya Ala Khayril – Amali. Hayya Ala Khayril – Amali’ na ‘Allahu Akbar. Allahu Akbar.’” Hivyo Mtume wa Mwenyezi Mungu akamwamuru Bilal kuadhini hivyo. Aliendelea kuadhini hivyo mpaka alipofariki Mtume wa Mwenyezi Mungu 4.268 Na katika kitabu Muntakhabu Kanzul-Ummal imeandikwa: Bilal alikuwa akiadhini asubuhi, akisema: Hayya Ala Khayril-Amal.269 Adabu na sifa za Adhana ya Bilal: Kitendo cha Bilal kuhusika kwa namna ya pekee katika kuadhini mbele ya Mtukufu Mtume 4, na kuendelea kufanya hivyo mpaka alipofariki Mtukufu Mtume 4, kiliipa Adhana yake thamani na hadhi maalumu, mpaka zikawa sifa zote za Adhana yake ni jambo linalotiliwa umuhimu na kuthaminiwa na mafakihi na wachunguzi. Hivyo ni muhimu sasa tukawasilisha sura ya Adhana ya Bilal kupitia adabu na Sunnah mbalimbali. Na hili ndio tutakalojaribu kulibainisha kadiri tutakavyoweza, kupitia yale yaliyotajwa kuhusu Adhana yake:   Tahdhib, Juz. 2, uk. 60; Al-Istibswar, Juz. 1, uk. 305 na 306.   Muntakhab Kanzul-Ummal, Juz. 3, uk. 676; Majmauz-Zawaid, Juz. 1, uk. 330; KanzulUmmal, Juz. 8, uk. 432.

268 269

153

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 153

4/23/2016 2:45:58 PM


HUYU NDIYE BILAL

1.

Bilal alikuwa akipanda sehemu ya mwinuko iliyo juu, pindi anapotaka kuadhini. Na tendo hilo halikuwa ni utashi wake binafsi, bali ilikuwa ni kutekeleza amri ya Mtume wa Mwenyezi Mungu 4, kama ilivyopokewa katika baadhi ya riwaya. Imepokewa kutoka kwa Abu Abdullah B kwamba alisema: “Ukuta wa Msikiti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 ulikuwa mrefu. Mtume 4 alikuwa akimwambia Bilal: ‘Ewe Bilal! Panda juu ya ukuta na nyanyua sauti yako kwa Adhana. Hakika Mwenyezi Mungu ameiwekea Adhana upepo unaoisafirisha mpaka mbinguni. Malaika wanapoisikia husema: ‘Hii ni sauti ya ummah wa Muhammad 4 ukimpwekesha Mwenyezi Mungu.’ Hivyo huanza kuuombea ummah wa Muhammad msamaha mpaka wanapomaliza kuswali.’”270

Mwanamke mmoja kutoka ukoo wa Bani Najar ameilelezea Adhana ya Bilal wakati wa alfajiri kwa kusema: “Nyumba yangu ndio ilikuwa ndefu zaidi kushinda nyumba zote zilizokuwa zikiuzunguka msikiti. Bilal alikuwa akija na kuadhini kutokea juu ya nyumba yangu. Alikuwa akija usiku, anaketi juu ya nyumba akingojea alfajiri, akiiona alfajiri hujinyoosha kisha husema: ‘Ewe Mungu Wangu! Nakuhimidi na kukutaka uwasaidie Makurayshi waweze kuifuata dini Yako.’ Kisha huanza kuadhini. Wallahi sijui ni katika usiku upi aliacha kufanya hivyo.271 Na hapana shaka kwamba kutolea Adhana sehemu iliyo juu zaidi kunafikisha zaidi wito wa kuelekea kwenye Swala. Lakini kwa uhakika kabisa, hakuna yeyote anayeweza kudai kwamba, hiyo ndio sababu ya msingi iliyofanya sharia ipendekeze namna hii ya utoaji wa   Wasailus-Shiah, Juz. 4, uk. 640 na 641; Biharul-An’war, Juz. 84, uk. 148; SafinatulBihar, Juz. 1, uk. 16. 271   Sunan Abi Daud, Juz. 1, uk. 143, Hadith ya 519; Siratun-Nabawiyyah cha Ibn Hisham, Juz. 2, uk. 509; Nasburayat, Juz. 1, uk. 287 na 292 na 293. 270

154

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 154

4/23/2016 2:45:58 PM


HUYU NDIYE BILAL

Adhana. Hakika sharia ya Mwenyezi Mungu ina dhahiri na batini, na akili zetu hazina uwezo isipokuwa wa kutambua baadhi ya maslahi ya dhahiri. Na huenda yale yaliyopokewa kutoka kwa Mtukufu Mtume 4 katika hadithi iliyotangulia, ni ishara ya baadhi ya siri za hukumu ya Sunnah ya kutolea Adhana sehemu ya juu yenye mwinuko. 2.

Alikuwa akiweka vidole vyake masikioni wakati wa kutoa Adhana.272 Nacho ni kitendo cha Sunnah. Imepokewa kwamba Mtukufu Mtume 4 alimwamuru kufanya hivyo, alimwambia: “Hakika kitendo hicho kinanyanyua zaidi sauti yako.”273 na inajulikana kwamba, kunyanyua sauti ni jambo linalotakikana katika Adhana, kwa sababu kunaeneza tangazo na kunakamilisha lengo.

3.

Imepokewa kutoka kwa Mtukufu Mtume 4, kwamba alimuusia na kumfunza adabu nyingi zinazohusu Adhana, alimwambia: “Ewe Bilal! Vuta maneno wakati wa kuadhini, na harakisha wakati wa kukimu. Na acha muda baina ya Adhana yako na Ikama yako, kiasi cha mlaji kuweza kumaliza kula chakula, na mnywaji kunywa maji, na mwenye haja kumaliza kujisaidia.”274 Kutokana na usia uliotangulia tunaona jinsi Mtukufu Mtume 4 alivyojali na kutilia umuhimu Adhana ya Bilal katika upande wa sifa zake na vipengele vyake.

4. Bilal alikuwa na kawaida ya kumjulisha Mtukufu Mtume 4 kuwa tayari ameshaadhini. Alikuwa anapomaliza kutoa Adhana yake anakwenda kusimama mlangoni kwa Mtume 4 na kumwambia: ‘Hayyah Alas-Swalah! Hayya   Al-Muswannaf cha Abdurazaq, Juz. 1, uk. 468; Muntakhab Kanzul-Ummal, Juz. 3, uk. 276; Sahih Bukhar, Juz. 1, uk. 314. 273   Sunan Ibn Majah, Juz. 1, uk. 236, Hadith 710; Nasburayat, Juz. 1, uk. 274; Muntakhabu Kanzul-Ummal, Juz. 3, uk. 270; Majmauz-Zawaid, Juz. 1, uk. 334. 274   Muntakhabu Kanzul-Ummal, Juz. 3, uk. 271; Majmauz-Zawaid, Juz. 2, uk. 4; KanzulUmmal, Juz. 8, uk. 350, Hadith ya 23206. 272

155

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 155

4/23/2016 2:45:58 PM


HUYU NDIYE BILAL

Alal-Falah! Swala ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu.’ Mtume 4 akitoka, na Bilal akimuona, huanza kukimu.275 Na imenukuliwa kwamba, alikuwa akisema: “Asalam Alayka ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu!” Na wakati mwingine alikuwa akisema: “Asalam Alayka ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! baba yangu na mama yangu wawe ni fidia kwako ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Hayyah Alas-Swalah! Hayya Alal-Falah! Asalam Alayka ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu.” Na imenukuliwa kinyume hivyo.276 5.

Na miongoni mwa adabu alizokuwa akizifanya ni kuelekea kibla wakati anapotaka kutoa takbira katika Adhana.277 Na hapa tunapenda kuashiria kwamba, madhehebu ya AhlulBayt F yamesisitiza Sunnah ya kuelekea kibla wakati wa kusoma vipengele vyote vya Adhana.278

6.

Alikuwa haadhini nje ya wakati.279 Imepokewa kwamba, alikuwa anaadhini pindi jua linapokengeuka. Na anachelewesha kidogo ikama lakini hatoki nje ya wakati katika Adhana.280

7.

Na imepokewa kutoka kwa Bilal kwamba alisema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alituamuru tusiondoe nyayo zetu

Aayanus-Shiah, Juz. 3, uk. 603; Tabaqatul-Kubra cha Ibn Saad, Juz. 3, uk. 234; Ansabul-Ashraf, Juz. 1, uk. 187; Mustadrakul-Wasail, Juz. 4, uk. 77. 276   Taratibul-Idariyyah, Juz. 1, uk. 75; Muntakhabu Kanzul-Ummal, Juz. 3, uk. 28. KanzulUmmal, Juz. 8, uk. 366, Hadithi ya 23293. 277   Nasburayat, Juz. 1, uk. 275. 278   Miftahul-Karamah, Juz. 2, uk. 283. Jawahirul-Kalam, Juz. 9, uk. 92 na 93; RiyadhulMasail, Juz. 1, uk. 145; Masalikul-Af’ham, Juz. 1, uk. 27; Biharul-An’war, Juz. 84, uk. 114. 279   Sunan Ibn Majah, Juz. 1, uk. 236. 280   Tabaqatul-Kubra cha Ibn Saad, Juz. 3, uk. 235; Ansabul-Ashraf, Juz. 1, uk. 187 na 188. 275

156

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 156

4/23/2016 2:45:58 PM


HUYU NDIYE BILAL

kutoka mahala pake, wakati wa kuadhini na wakati wa kukimu.”281 8.

Imepokewa kwamba, alikuwa akiadhini kisha anasubiri, akimuona Mtukufu Mtume 4 ametoka ndipo anakimu Swala.282

9.

Na katika siku ya Ijumaa alikuwa akiadhini baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 kuketi juu ya mimbari kwa ajili ya Adhana. Na alikuwa akikimu baada ya kuteremka.283

10. Na kwa upande wa adhana ya alfajiri, imekuja kwamba, Mtukufu Mtume 4 alimwamuru asiadhini mpaka pale alfajiri itakapopambazuka.284 Haya ndio aliyoyatenda Bilal na akaendelea nayo mpaka inavyodhihiri kutoka kwenye kauli yake: “Tulikuwa hatuadhini kwa ajili ya Swala ya alfajiri, mpaka pale tunapoiona alfajiri.285 11. Na kuna nukuu zinazoeleza kwamba, alikuwa akiadhini huku akifuatisha midomo yake na akinema kwa kichwa chake kulia na kushoto.286 Zaidi ya hapo zimepokewa riwaya na hadithi nyingi kuhusu Adhana ya Bilal, sisi tumechagua baadhi yake, kati ya hizo ni: Swaduq katika kitabu al-Faqihu amepokea kutoka kwa Abu Baswiru, kutoka kwa mmoja wao (al-Baqir au as-Sadiq as), kwamba alisema: “Hakika Bilal alikuwa mja mwema, akasema siku moja: Sintomwadhinia yeyote baada ya Mtume wa Mwe  Nasburayat, Juz. 1, uk. 277.   Sunan Abi Daud, Juz. 1, uk. 113. 283   Al-Ghadir, Juz. 8, uk. 126; Tafsirul-Khazin, Juz. 4, uk. 260; Muntakhabu Kanzul-Ummal, Juz. 3, uk. 282. 284   Nasburayat, Juz. 1, uk. 283 na 287. 285   Nasburayat, Juz. 1, uk. 283 na 287. 286   Sahih Ibn Khuzaymah, Juz. 1, uk. 202 na 203. 281 282

157

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 157

4/23/2016 2:45:58 PM


HUYU NDIYE BILAL

nyezi Mungu 4. Na ndipo kilipoachwa kipengele: ‘Hayya Alaa Khayril-Amal.’” Na imepokewa kutoka kwa Zurarah, kutoka kwa Abu Abdullah B kwamba alisema: “Ibn Ummi Maktumi aliadhini kwa ajili ya Swala ya asubuhi, mtu mmoja akapita kwa Mtukufu Mtume 4 akamkuta anakula daku, Mtume 4 akamwita akala pamoja naye, mtu yule akasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Ameshaadhini mwadhini kwa ajili ya Swala ya alfajiri.” Mtume 4 akasema: “Huyu Ibn Ummi Maktum anaadhini usiku, Bilal akiadhini ndipo mjizuie.”287 Na katika riwaya hii kuna ushahidi mwingine kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alikuwa akimtegemea Bilal katika mambo muhimu, na yanayohitaji umakini na uangalifu, na yenye mafungamano na ibada muhimu kama Swala na Swaumu. Na inaonekana Mtukufu Mtume 4 alikuwa anaamini umakini wa Bilal, na alikuwa anataka msikilizaji awe hivyo, ili Adhana ya Bilal iwe kigezo kinachozingatiwa na kutegemewa na Waislamu. Tupe raha ewe Bilal: Tupe raha ewe Bilal.288 Ni ibara inayoonesha shauku aliyokuwa nayo Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 juu ya Swala, ambayo aliiona kuwa ndio kitulizo cha macho yake. Ambapo alikuwa akijiandaa kwa ajili ya Swala kwa kuchukua udhu, na kwa kujielekeza kwa Mwenyezi Mungu kwa furaha. Na katika kauli yake kwa Bilal: “Tupe raha.” Kuna dalili inayobainisha hali hiyo tukufu, na moto huo wa shauku aliyokuwa nayo, uliokuwa ukimuunguza ndani kwa ndani.   Al-Kafiy, Juz. 4, uk. 98; Muntaqal-Jaman, Juz. 2, uk. 509; Wasailus-Shiah, Juz. 10, uk. 120. 288   Al-Hadaiq an-Nadhirah, Juz. 6, uk. 334; At-Tafsir as-Swafiy, Juz. 1, uk. 126; Al-Hablu al-Matin, Uk. 154; Taarikh Baghdad, Juz. 1, uk. 444; Al-Aqdu al-Husayniy, uk. 42. 287

158

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 158

4/23/2016 2:45:58 PM


HUYU NDIYE BILAL

Tamko: ‘Tupe raha ewe Bilal’ linabeba ombi la kutaka msaada na auni, na linaonesha juhudi zake na uvumilivu wake katika kungojea kukutana na Mwenyezi Mungu. Hata kama yuko pamoja na Mwenyezi Mungu katika hali zake zote, lakini hali ya Swala, na hasa Swala ya wajibu, inatofautiana na hali nyingine. Tupe raha ewe Bilal. Kwa kukata kiu kwa utamu wa muungano. Simama na mpunguzie maumivu Mtume wako, hivi hauoni mahangaiko ya roho yake?! Moto wa mapenzi yake umemlainisha, na moyo mzito ndio chombo cha mapenzi yake. Basi uhurumie moyo wa kipenzi chako. Simama ewe Bilal. Mpe raha Mtume wako. Muondolee mashaka yake, kwani hakukuondolea mashaka yako?! Wewe ndiye unayemiliki njia ya kuelekea kwenye tulizo la macho yake. Wito mmoja kutoka kwako, unatuliza kiu yake. Ameshatawadha tangu zamani na yuko tayari. Simama na uadhini. Adhini hata kama muda wa kukutana hautapoza kiu ya aina hii. Kila kipenzi anapokutana na kipenzi chake, mapenzi huongezeka. Hakika mafuta huwasha miale ya taa, lakini nuru huzuia macho. Adhini ewe Bilal. Adhana katika upande wake wa kisiasa na kiibada: Wakati Waislamu wakiwa katika mapambano yao magumu na mazito, dhidi ya nguvu ya ukafiri na unafiki, Adhana ilidhihiri mpaka katika medani ya vita na mapambano ili iwe tendo la kiibada na kisiasa kwa wakati mmoja. Maadui wa Uislamu walitambua umuhimu wa Adhana katika kuwaunganisha Waislamu na kuwafungamanisha na dini yao na itikadi yao. Na waliliona hilo wakati wa vita vyao vya kijeshi au vya kifikra au vya kiuhubiri. Hivyo walifanya kazi ya kupambana na Adhana na wakati mwingine wakazuia isitolewe. 159

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 159

4/23/2016 2:45:58 PM


HUYU NDIYE BILAL

Na huenda haya yakabainisha hasira na chuki waliokuwa nayo dhidi ya Adhana: Kwamba walikuwa wanazuia Adhana pindi wanapoteka kijiji au mji wa Waislamu. Wakati mwingine walikuwa wakibomoa minara ya kutolea Adhana, na hili lilitokea sana katika maeneo mengi. Lakini Mwenyezi Mungu alitaka Adhana idumu na iendelee kuwa mwiba mkali wenye kujeruhi macho ya maadui, na iendelee kuwa wito wa ummah wote bila kujali makundi yao na madhehebu yao. Hivyo mpaka leo inanadiwa kila siku zaidi ya mara moja, ili igonge masikio ya nyoyo kwa kumtukuza Mwenyezi Mungu kwa takbira, kwa tauhidi Yake na kwa shahada ya utume Wake Muhammad 4. Kwa kweli ni zawadi ya Mwenyezi Mungu kwa ummah. Na kama tungekuwa tunayazingatia ayasemayo mwadhini na kuamiliana nayo, basi tungejiokoa kutoka kwenye matatizo mengi yanayotukabili. Na hapa ni lazima tuashirie kipengele cha kiibada na kimalezi kilichopo katika Adhana, ambapo katika kipengele hicho unatangazwa ukweli kuhusu Mungu, jambo ambalo linawataka Waislamu kuimarisha na kuonesha kivitendo itikadi yao kwa kuharakisha kwenda kutenda na kufanya ibada. Na inatutosha takbira inayotangazwa na mwadhini, kutuonesha Ufalme na Ukuu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Hakika kuitakidi ukuu huo kunamsukuma Mwislamu kujituma mbele ya mambo mbalimbali na katika maeneo tofauti, kwa kufuata mtazamo huu wa kiungu. Adhana ya Bilal inawachukiza wanafiki na mushrikina: Halikuwa ni jambo linalotarajiwa kutoka kwa Mushrikina wa Kikurayshi, kufurahia kusikia sauti ya Bilal akinadi shahada mbili na vipengele vingine vya Adhana, kutoka juu ya paa la Kaaba. Wao walimpiga vita Mtukufu Mtume 4 miaka kadhaa ili tu aache kulingania kwenye dini hii. Na Bilal ananyanyua sauti yake kutangaza maneno ya haki na ushindi. Hivyo maneno yake yalikuwa yanateremka juu 160

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 160

4/23/2016 2:45:58 PM


HUYU NDIYE BILAL

ya nyoyo zao kama mijeledi ya moto inayowasha ghadhabu na hasira zao, kiasi kwamba baadhi yao walitamani kwamba wangekufa kabla ya wakati huo. Na imekuja katika historia kwamba, Bilal alipofika: ‘Ash’hadu Anna Muhammad Rasulullah.’ Juwayriyyah binti wa Abu Jahli alisema: “Naapa, hakika amenyanyua utajo wako. Ama Swala tutaswali. Wallahi kamwe hatumpendi aliyewauwa vipenzi. Unabii alioletewa Muhammad aliletewa baba yangu kabla yake, lakini akaukataa, kwa sababu hakutaka kwenda kinyume na jamaa zake.”289 Tazama hasira na hasadi iliyompata pindi aliposikia shahada ya Utume. Hasadi ilitawala moyo wake mpaka ulimi wake ukatamka maneno haya. Alipokosa cha kutuliza hasira yake isipokuwa madai ya kwamba eti unabii ulipelekwa kwa baba yake lakini akaukataa, kwa sababu hakutaka kwenda kinyume na jamaa zake. Nayo ni madai ya dharau kweli. Na hali ya wanafiki walipokuwa wakiisikia Adhana haikuwa nzuri zaidi kuliko Mushrik wa Kikurayshi. Bali nao walikuwa hivyo, walikuwa hawawezi kuvumilia kusikia hilo. Na huenda kilichokuwa kinawaudhi zaidi ni kutangaza ushahidi wa Utume. Na hapa tunaashiria tukio lililotokea huko Madina, nalo ni: Bilal alipokuwa akisema: ‘Ash’hadu Anna Muhammad Rasulullah.’ Mnafiki mmoja alikuwa akisema: “Muongo achomwe.” Yaani Mtukufu Mtume 4. Hivyo siku moja mnafiki huyo alisimama usiku ili kutengeneza taa yake, mara moto ukaangukia katika kidole chake na hakuweza kuuzima mpaka ukaunguza kitanga chote cha mkono wake, kisha ukaendelea kuteketeza mkono wake mpaka ukamuunguza na kummaliza mwili wote.290   Sharhu Nahjul-Balaghah cha Ibn Abil-Hadid, Juz. 17, uk. 283, kutoka kwa al-Waqidiy.   Biharul-An’war, Juz. 18, uk. 68. Manaqib Aali Abitalib, Juz. 1, uk. 117.

289 290

161

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 161

4/23/2016 2:45:59 PM


HUYU NDIYE BILAL

Faslu ya Nane MAANDALIZI NA SAFARI Tutazungumzia: 1.

Aghani kwa kukumbuka mauti.

2.

Katika ardhi ya maandalizi.

3.

Maneno mengine kuhusu kuhamia kwake Sham.

4.

Hitimisho lisilo na mwisho.

5.

Kaburi lake ni kibla cha wenye kumzuru.

Aghani kwa kukumbuka mauti: Hakika miongoni mwa hali za wenye kujitambua na kumtambua Mola Wao, ni kule kujituma kwao kwa ajili ya kutaka kukutana na Mwenyezi Mungu, na kujinyima kwao dunia, kiasi kwamba kuwepo kwao katika dunia hii inakuwa ni jambo zito mno kwao. Hivyo si jambo la ajabu Bilal kujikumbusha mauti daima, na kuomba hilo kwa ukweli wote anapopanda juu kwa ajili ya Adhana, ambapo anakuwa karibu na haki. Alikuwa akisema: “Kwa nini Bilal asimlize mama yake, na paji la uso wake lisilowe kwa damu.”291 Hakika katika kauli yake hiyo kuna mwangwi wa lile linalotembea ndani ya nafsi yake, na ni alama ya maandalizi aliyonayo kwa ajili ya mauti. Na ya shauku aliyonayo ya kutaka kuitoa damu yake katika njia ya malengo ya Mwenyezi Mungu. Na hiyo ni taabiri   Tabaqatul-Kubra cha Ibn Saad, Juz. 3, uk. 235; Ansabul-Ashraf, Juz. 1, uk. 187.

291

162

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 162

4/23/2016 2:45:59 PM


HUYU NDIYE BILAL

kuu kabisa ya jinsi alivyojisalimisha kwa Mwenyezi Mungu, kiasi kwamba hata alipofikwa na mauti alisema: “Ooh ni furaha iliyoje…. kesho nakutana na vipenzi, Muhammad na kundi lake.”292 Hakika Bilal anatafuta shahada, ana haraka ya kuifikia na anaitaka kwa hamu. Kwa pigo la upanga utosini na juu ya paji la uso, na hatimaye maeneo hayo yanalowa damu. Akajiuguza mwenyewe kwa kuutazama mwili wake wenye kutoweka, kwa kuuzingatia ni udongo utakaosambaratika. Ni mpaka lini utaendelea kuwa mbali na vipenzi?! Mbona humlizi mama yako ili ukutane nao?! Bilal anatafuta pigo la Upanga ili ajiliwaze, hina yake ni damu yake inayofunika paji lake, na tamaa yake ni afunikwe na nguo ya shahada. Umejitolea imani yako ewe Bilal….shauku yako ya kutaka kukutana na Mwenyezi Mungu inakaribia kutikisa subira yako, na mapenzi yanautikisa utu wako. Unatangaza mbele za watu na kuwabainishia, kwamba mimi nimekufa kwa kumpenda Yeye, kwa mahaba yaliyojaa kuanzia juu ya kichwa changu hadi chini ya nyayo zangu. Kila kipande cha uwepo wangu kinanadi jina Lake. Na kila mshipa wa moyo wangu unamtamani Yeye, tangu nilipomjua Muhammad 4. Nilimtambua ipasavyo. Na ni kama mnavyoniona, uwepo umenishinda na safari imenichosha. Je kuna pigo lolote la upanga litakalotuliza kifua changu chenye kuungua kwa shauku?! Umejitolea imani yako ewe Bilal. Naapa hakika hayo ndio matamanio ya watu wa Mungu wenye kumtambua, matamanio ambayo husumbua vifua vyao mpaka hudhihiri katika midomo yao. Hakika shairi la Bilal limetoka kwenye chemchem safi na iliyojaa yakini. Limenadhimiwa na kupangiliwa na yale yanayozunguka katika nafsi yake. Herufi zake zimekusanywa kutoka katika uwanja wa miale ya   Taarikhu Damashqi cha Ibn Asakir, Juz. 3, uk. 317; Siyaru Aalamun-Nubalai, Juz. 1, uk. 359; Siratul-Halabiyyah, Juz. 1, uk. 298.

292

163

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 163

4/23/2016 2:45:59 PM


HUYU NDIYE BILAL

shauku iwakayo. Na ni vigumu kwa mshairi hata kama atatandikiwa mto, kufikia pale alipojifikisha Bilal. Maana ndio roho ya matamshi, na shairi kwa kiwango hiki linatoka katika kilele cha usafi, kwa ile roho liliyoiwakilisha na kuifikisha. Ili mshairi awakilishe maana kama hii ya imani aliyonayo, inahitaji awe na roho ya Bilal au mfano wa Bilal, watu ambao wamenawirishwa na nuru ya kipenzi, na wamechoshwa na umbali na mfarakano. Hivyo wakatambua uwongo wa dunia yao na wakakidharau kila kilichomo humo, na wakajiweka katika utiifu wa kumtii Mwenyezi Mungu kwa uwepo wao wote. Hivyo wakaonja utamu wake na uzuri wake, mpaka ikawa kuhangaika katika njia ya kumfikia kipenzi ni jambo walipendalo na tamu zaidi kwao kushinda asali. Na Bilal yuko katika daraja hii ambayo hawaifikii isipokuwa wale watu maalumu waliozishinda nafsi zao na wakazidhibiti kwa utashi wao. Katika ardhi ya maandalizi: Siku zilipita, na Muhammad 4 akaenda kwa kipenzi chake. Ardhi yote ikalizwa na kulia, na nyakati zote zikalizwa na kulia, kwa kufarakana naye. Bilal naye akarudi katika uyatima kama alivyokuwa hapo kabla. Alikuwa anamuona Muhammad 4 katika maisha kuanzia asubuhi mpaka jioni. Mchana wake ni Muhammad 4. Usiku wake ni Muhammad 4. Furaha yake ni Muhammad 4. Huzuni yake ni Muhammad 4. Tunangojea nini kutoka kwa Bilal, wakati ambapo tangia ile sekunde ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alianza kufunikwa na udongo, mpaka sekunde ya mwisho ya umri wa Bilal, yupo katika huzuni isiyoachana na moyo wake, na yuko katika hali ya ugonjwa ijapokuwa si mgonjwa? Ni kipindi kizito kiasi gani, na wakati mgumu kiasi gani kwa mtu mwenye kuona kwa macho yake safari ya kipenzi chake. Na 164

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 164

4/23/2016 2:45:59 PM


HUYU NDIYE BILAL

ni kipenzi gani huyu?! Uwepo wake wote ulikuwa ni Muhammad 4. Na sasa mauti yameandikwa na hakuna wa kupinga kauli aliyosema (Mwenyezi Mungu). Hivyo ni wajibu kwa Bilal kukusanya vitu vyake. Atakwenda wapi huyo aliyeelemewa na maumivu yake, ambaye alimeza imani na tauhidi hatua kwa hatua kutoka kwenye kinywa cha Mtume wake?! Ameshavuka kina kirefu cha umri, na hajabakiwa na kitu katika maisha isipokuwa ujazo wa birauli. Atainywea wapi na ni vipi atainywa? Maombolezo yake kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 ni apite njia yake, afuate hatua zake na aombe uombezi wake na atembee katika njia yenye kumridhisha. Je abaki Madina ambamo limo kaburi la Mtukufu Mtume 4, mji ambao jina lake limeungwa na cheo chake 4. Nalo ndio kumbukumbu yake? Au arudi Makkah, mji ambao ulivujisha jasho lake na kuutoa damu moyo wake. Mji aliokulia kwa mateso yake na hatimaye akaja kupanda juu ya Kaaba yake. Nao mara zote hutikisika kwa sauti ya Adhana yake, na huficha mateso na maumivu yake (Bilal) kati ya vichochoro vya majumba yake? Jambo hilo linakuwa gumu kwake kwa sababu zaidi ya moja. Hivyo uamuzi ukawa si kuishi katika mji huu wala ule, licha ya kwamba anaipenda miji hiyo. Na licha ya kwamba katika kifua cha mzee huyu kuna mizizi ya mafungamano yake na miji hiyo. Akaazimia kuingia katika mapambano. Sasa umefika wakati wa kuvunja kufuli la gereza hili, na kujitoa katikati ya kuta za gereza la dunia. Alitaka hatima ya maisha yake iwe ni miski. Akijiandaa kupambana katika njia ya Mwenyezi Mungu, mwenye kuwavizia maadui wa Mwenyezi Mungu katika moja ya mipaka ya jihadi. Hivyo akaandaa safari yake kuelekea Sham, kwani pepo iko chini ya nyayo za ngamia, na watu wake hawatalia Siku ya Kiyama, na hiyo ni biashara itakayowaokoa na adhabu kali ya moto. 165

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 165

4/23/2016 2:45:59 PM


HUYU NDIYE BILAL

Hakujali umri wake mkubwa, wala weupe wa nywele zake na ndevu zake. Hakika mwili ni makazi ya roho. Na ni mateso gani asiyonayo maadamu roho yake ingali katika mwili. Maneno mengine kuhusu kuhamia kwake Sham: Ama kuhusu sababu iliyompelekea kuhamia Sham, kuna nukuu zinazoonesha kwamba, sababu ya yeye kufanya hivyo, ilikuwa ni maneno yaliyotokea baina yake na Khalifa wa pili Umar. Ambapo Umar bin Khatwab alimlaumu Bilal kwa kutoharakisha kwenda kumpa kiapo cha utii Abubakri. Na Umar akatoa hoja ya kwamba Abubakri alichangia katika mchakato na hatua za kuachiwa kwake huru. Lakini hakumwitikia katika lile alilotaka. Na mwisho wa suala hilo ukawa ni kumtaka ahamie Sham.293 Na wanatoa ushahidi wa hilo kupitia beti kadhaa zinazonasibishwa na Bilal, zenye kubeba maana hii.294 Ama upande wetu, sisi hatuko katika nafasi ya kuhakiki hilo, isipokuwa tumegusia hilo ili kulinda tu uaminifu wa kielimu Hitimisho lisilo na mwisho: Umri wake uliobakia aliumalizia huko Sham295 kwenye mipaka ile. Katikati ya kijiji ambacho kilishambuliwa na maradhi ya tauni.296 Na ni hapo ndipo Bilal aliweka chini hatamu ya uwezo wake kwa kufariki katika ardhi ya vita. Ili kwamba kifunikwe kitabu cha mai  Darajatur-Rafiah, uk. 367; Qamus Rijal, Juz. 2, uk. 399.   Tanqihul-Maqal, Juz. 1, uk. 183; Qamus Rijal, Juz. 2, uk. 399; Aayanus-Shiah, Juz. 3, uk. 603. 295   Tahdhibul-Kamal, Juz. 4, uk. 290; Usudul-Ghabah, Juz. 1, uk. 165; Majmauz-Zawaid, Juz. 9, uk. 30; Tanqihul-Maqal, Juz. 1, uk. 182; Aayanus-Shiah, Juz. 3, uk. 601. 296   Katika kitabu Mustadrak Safinatil-Bihar cha Namaziy, Juz. 5, uk. 211, imeandikwa kwamba: Kulitokea ukame mkubwa na maradhi ya tauni huko Sham, mpaka wakafariki watu 25000, akiwemo Bilal mwadhini wa Mtume wa Mwenyezi Mungu . 293 294

166

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 166

4/23/2016 2:45:59 PM


HUYU NDIYE BILAL

sha yake na uwe mwisho wa maisha yake matukufu, na mwisho wa historia yake ndefu, kuanzia katika daawa na mateso, mpaka katika subira, jihadi na huzuni. Hivyo basi amefia katika ardhi ya vita. Ambapo kifo chake kilitokea mwaka wa ishirini Hijiriya, sawa na mwaka 641 A.D. Na kuna kauli nyingine tofauti na hiyo. Alifariki akiwa na umri wa miaka sitini na ushei, au sitini kamili.297 Ni huko ndiko Bilal alipofia akiwa mpweke. Ni huko ndiko Bilal alikopata uhuru wake mkubwa baada ya kujikomboa kutoka kwenye minyororo ya dunia, na akafuzu mtihani wake kwa kupata medani za fahari na ushindi. Na mkono uliomzika katika kipande hicho cha ardhi, ulikuwa unajua kwamba, kipande hicho cha jangwa – Babu Swaghir huko Damascus298 - kitakuja kuwa jiji la wenye mapenzi na ujumbe, kwani katika jiji hilo kumeenea makaburi ya vipenzi vya Muhammad 4 kutoka miongoni mwa wajukuu na watoto wa Ali B. Ambapo kuna makaburi kadhaa yenye kulizunguka kaburi la Bilal, kati ya hayo ni: Kaburi la Abdullah bin Ja’far Twayyar. Kaburi la Umma Kulthum binti ya Ali I. Kaburi la Maymuna binti ya Hasan I. Kaburi la Fizza mtumishi wa Zahrau I. Kaburi la Abdullah bin as-Sadiq B. Kaburi la Hasan bin Ja’far as-Sadiq B.   Tahdhibul-Kamal, Juz. 4, uk. 290. Swafuwatus-Swafuwa, Juz. 1, uk. 440; TahdhibutTahdhib, Juz. 1, uk. 411. Ansabul-Ashraf, Juz. 1, uk. 193; Aayanus-Shiah, Juz. 3, uk. 605. Tabaqatul-Kubra cha Ibn Saad, Juz. 3, uk. 238; Tahdhibul-Asmai Walughat, Juz. 1, uk. 137. 298   Tahdhibul-Asmai Walughat, Juz. 1, uk. 137; Siyaru Aalamun-Nubalai, Juz. 1, uk. 359; Tanqihul-Maqal, 1182; Qamus Rijal, Juz. 2, uk. 237. 297

167

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 167

4/23/2016 2:45:59 PM


HUYU NDIYE BILAL

Kaburi la Khadija binti ya Zainul-Abidin I. Kaburi la Abdullah bin Zainul-Abidin B. Na makaburi ya wengine wengi.299 Kaburi lake ni kibla cha wenye kumzuru: Kaburi la Bilal lipo katikati ya Jiji la Damascus, pembeni ya makaburi kadhaa ya dhuria wa Mtume 4. Unaingia eneo la kaburi lake kupitia njia ndogo iliyo kati ya kuta mbili. Na kumewekwa kuba ambalo limefunika kaburi lake na kaburi la Abdullah bin Ja’far. Na kaburi la Bilal linazingatiwa kuwa ni moja ya makusudio ya wenye kufanya ziara hapo, na wenye mapenzi ya dhati. Nyoyo hulielekea, na pia Waislamu hupishana hapo kutoka pande mbalimbali za ardhi. Na ukifika hapo utawashuhudia watu wa mataifa mbalimbali waliokuja kumzuru, ambao huswali karibu na kaburi lake, hutabaruku kupitia kwake, na hujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu katika dua zao kupitia kwake, ili kwamba maombi yao na mahitaji yao yatimie. Wanafanya hivyo wakiamini kwamba dua inayoombwa katika eneo hilo lenye baraka hujibiwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Watu hao hulizunguka kaburi na kumtaka Bilal Mhabeshi awe pamoja nao kwa utukufu wa imani yake, kwa sauti ya tauhidi yake, kwa mateso ya kinyama aliyofanyiwa juu ya changarawe za moto, kwa msimamo wake wa kihistoria dhidi ya vigogo wa kikurayshi, kwa jihadi yake, kwa ukaribu wake kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4, kwa uaminifu wake kwake na kwa sauti ya Adhana yake iliyosikika katika sehemu zote za ardhi ile tukufu aliyoishi na kuonesha Uislamu wake. Ibn Jabir katika kitabu chake Rihlat Ibn Jabir, amesema: “Hakika kichwani mwa kaburi tukufu kuna historia ya jina lake (ra). Na   Muujamul-Buldan, Juz. 2, uk. 468.

299

168

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 168

4/23/2016 2:45:59 PM


HUYU NDIYE BILAL

dua inayoombwa katika eneo hili tukufu hujibiwa. Na hilo limejaribiwa na mawalii wengi na watu wa kheri waliotabaruku kwa kumzuru yeye.�300 Mwenyezi Mungu amrehemu Bilal, kwa upole kamili uliotuliza kimbunga cha maisha yake na kufunika sitara ya umri wake. Hakuacha kuuthamini muda wake ili awepo katika zama za kila kizazi, na ili atengeneze ujumbe katika kila hatua. Leo hii baada ya miaka zaidi ya elfu bado yumo ndani ya moyo wa kila mtu aliye huru mwenye kupambana na dhulma, na ndani ya moyo wa kila mwenye kujituma na kujitahidi kuelekea upande wa haki na ukweli. Kweli adhana ya Bilal, Yule mtumwa fakiri ni kubwa kuliko zama zake, imevuka mipaka ya wakati wake. Na ni katika adhana ya Uislamu, kwamba umemgeuza Yule Mhabeshi kuwa taa inayowaangazia viongozi wakubwa, pamoja na watu wote. Tunataraji kuwa, kwa kurasa hizi chache tutakuwa tumewasilisha sehemu ya mwangaza kutoka katika kitabu cha Bilal, na sehemu ya nuru kutoka katika mwenendo wake. Na Mwenyezi Mungu ndio kusudio letu. Na sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa viumbe wote.

  Rihlat Ibn Jubayri, Uk. 229; al-Ghadir, Juz. 5, uk. 184.

300

169

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 169

4/23/2016 2:45:59 PM


HUYU NDIYE BILAL

KIAMBATISHO Tutazungumzia: 1.

Je Bilal alimrudisha Makkah Mtukufu Mtume 4?

2.

Kisimamo kifupi katika kisa cha Bilal na Jamanah

Je Bilal alimrudisha Makkah Mtukufu Mtume 4? Na miongoni mwa mambo ya ajabu yanayosemwa kuhusu yeye ni lile aliloliandika al-Hafidh Bin Haban, kutoka kwa Hasan bin Sufiyan, kutoka kwa Abubakri bin Abu Shaybah, kutoka kwa Qarad Abu Nuhu, kutoka kwa Yunus bin Abu Is’haqa, kutoka kwa Abubakri bin Abu Musa (al-Ash’ariy), kutoka kwa Abu Musa al-Ash’ariy, kwamba alisema: Abutalib alisafiri kwenda Sham, katika safari hiyo alisafiri pamoja na Mtukufu Mtume 4 na wazee wa kikurayshi. Walipofika karibu na kwa Kasisi walisimama na kutua mizigo yao, mara Kasisi aliwafuata, na kabla ya hapo walikuwa wakipita kwake lakini hawafuati wala kuwajali. Aliwafuata wakati wakiwa wanashusha mizigo yao, akawa anawachunguza mmoja mmoja mpaka alipofika kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 4, akamshika mkono wake na kusema: “Huyu ni Bwana wa viumbe wote. Huyu ni Mtume wa Mola Mlezi wa viumbe wote. Huyu atatumwa na Mwenyezi Mungu kuwa rehema kwa walimwengu wote.” Kisha akaenda akawatengenezea chakula. Wakati alipowaletea chakula hicho Mtukufu Mtume 4 alikuwa akichunga ngamia, Kasisi akasema: “Mwiteni.” Na mara akaja ilihali mawingu yamemfunika juu kwa kivuli chake. Kasisi akawaambia: “Hebu mtazameni, mawingu yamemfunika juu kwa kivuli chake.” Alipowasogelea watu 170

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 170

4/23/2016 2:45:59 PM


HUYU NDIYE BILAL

aliwakuta wamemtangulia katika kivuli cha mti, basi alipoketi mti ukaelemea kwake. Na mara Kasisi akanyanyuka huku akiwahimiza kwamba wasiende Sham, kwani kama Warumi watamuona na kumtambua watamuuwa. Na mara alipokuwa anarudi kwake akawaona watu saba waliokuja kutoka Urumi, akawapokea na kuwauliza: Kipi kilichokuleteni? Wakasema: “Tumekuja, hakika Nabii huyu (aliyetabiriwa) atasafiri katika mwezi huu. Hakuna njia isipokuwa kuna watu waliopelekwa katika njia hiyo kumtafuta. Sisi tumeelezwa na kupewa habari zake, hivyo sisi tukaamua kumtafuta katika njia yako hii.” Kasisi akawaambia: “Hivi mnadhani jambo ambalo Mwenyezi Mungu anataka kulitimiza, kuna yeyote katika watu anayeweza kulizuia?” Wakasema: “Hapana.” Wakamfuata na wakakaa naye. Kasisi akatoka na kuwafuata Makurayshi na kuwaambia: “Nawaulizeni, walii wake ni nani kati yenu?” Abutalib akasema: “Ni mimi.” Basi akaendelea kumhimiza mpaka Abutalib akamrudisha, na Abubakri akamtuma Bilal aende naye, na Kasisi akamuongezea mafuta na keki ya matunda.301 Kwa kweli hatuwezi kuitegemea riwaya hii. Ukiachana na uwepo wa watu dhaifu katika sanadi yake au wale wanaotuhumiwa kwa uwongo na uzushi,302 pia ina mambo kadhaa: 1.

Wahakiki wametamka kwamba: Miongoni mwa mambo ya ajabu ya kushangaza yaliyopo katika riwaya hii ni kwamba, ni miongoni mwa habari Mursal za Maswahaba.303 Jambo ambalo linaidhoofisha riwaya hii na kuishusha hadi katika

Kitabu Thuqat cha Ibn Haban, Juz. 1, uk. 42 – 44; al-Bidayat Wanihayat, Juz. 2, uk. 284; Siratul-Halabiyyah, Juz. 1, uk. 119; Taarikhul-Khamis, Juz. 1, uk. 258; TaarikhulIslam cha Dhahbiy, Juz. 2, uk. 26 na 27; Siratun-Nabawiyyah cha Dahlan, Juz. 1, uk. 49; Taarikhul-Umam Wal-Muluk, Juz. 2, uk. 279. Siratun-Nabawiyyah cha Ibn Kathir, Juz. 1, uk. 246; Dalailun-Nubuwwah cha Bayhaqiy, Juz. 2, uk. 25. 302   Tahdhibut-Tahdhib, Juz. 11, uk. 434; Mizanul-Iiitidal, Juz. 3, uk. 339. 303   al-Bidayat Wanihayat, Juz. 2, uk. 285; Siratun-Nabawiyyah cha Ibn Kathir, Juz. 1, uk. 248; Al-Iswabah, Juz. 2, uk. 360. 301

171

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 171

4/23/2016 2:45:59 PM


HUYU NDIYE BILAL

kiwango ambacho haiwezekani tena kuitegemea. Kwani Abu Musa al-Ash’ariy alikuwa hajazaliwa wakati huo, na wala hakushuhudia tukio hili.304 Alammah Amin, Mwenyezi Mungu amrehemu, anasema: “Abu Musa al-Ash’ariy alifariki mwaka 42/ 50/ 51/ 53/ akiwa na umri wa miaka 63 bila kuwepo tofauti yoyote. Na tukio hilo linalotajwa lilitokea miaka tisa baada ya mwaka wa tembo. Au miaka kumi na mbili kabla ya kuzaliwa kwa Abu Musa al-Ash’ariy 17/ 22/ 23/ 25. Ni nani aliyemsimulia tukio hili? Na je alisikia kutoka kwa mtu anayeamini nukuu yake? Na haijatuthibitikia kwamba alilisikia kutoka kwa Mtukufu Mtume 4, au kutoka kwa mtu anayeaminiwa katika nukuu zake. Hivyo huenda alilisikia kutoka kwa mtu anayetuhumiwa au kutoka kwa mkiristo ambaye alikuwa bado hajasilimu. Hivyo bado chanzo cha riwaya hii kinaendelea kuwa mahala pa shaka na utata. 2.

Kuna tofauti katika nukuu ya tukio hili. Jambo ambalo haliungi mkono kuchukua riwaya hii. Imekuja katika kitabu cha Sira cha Dahlan kwamba: Abutalibu alimrudisha pamoja na watumishi wake,305 na si pamoja na Bilal, kama inavyoonekana katika riwaya ya Abu Musa al-Ash’ariy. Na katika vyanzo vingine imeandikwa kwamba, aliyerudi naye ni ami yake Abutalib mwenyewe. Na imekuja katika baadhi ya riwaya, kama ile iliyomo katika kitabu cha Sira cha Dahlan, kwamba alirudi Makkah pamoja na Abubakri na Bilal. Lakini imesemekana kuwa nyongeza hii ina makosa. Na imesemekana kuwa ni sahihi.306 Zaidi ya yote hayo ni kwamba riwaya hiyo imeandikwa ndani ya kitabu al-Wafau

Al-Ghadir, Juz. 7, uk. 286.   Siratun-Nabawiyyah cha Ibn Kathir, Juz. 1, uk. 49; Siratul-Halabiyyah, Juz. 1, uk. 119. 306   Siratun-Nabawiyyah cha Dahlan, Juz. 1, uk. 49. 304 305

172

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 172

4/23/2016 2:45:59 PM


HUYU NDIYE BILAL

cha Ibn al-Jawziy, kutoka kwa Abubakri bin Abu Musa alAsh’ariy bila kumtaja Bilal.307 3.

Dhahbiy ametamka wazi kwamba: Hakika Bilal alikuwa bado hajazaliwa wakati huo.308 Na hakika maneno yake yako bayana na yanakubalika, kwani Bilal kama atakuwa alifariki mwaka wa 21 au 25 au 27 wa hijiriya, akiwa na umri wa miaka sitini na tatu, basi hakuwa ameshazaliwa wakati wa tukio hilo ambalo lilitokea miaka thelathini kabla ya Mtume kuanza jukumu la utume. Yaani kabla ya miaka arubaini na tatu ya Hijiriya.

Kisha ni kwamba hata tukijaalia kuwa alikuwa ameshazaliwa, bado hatuwezi kukubali kuwa alihudhuria pamoja na Mtukufu Mtume 4 katika tukio hilo, hiyo ni kutokana na sababu kadhaa: Kwanza: al-Hafidh Damyatwiy ametamka wazi kwamba: Abubakri na Bilal hawakuwa pamoja na Mtukufu Mtume 4 wakati wa tukio hilo.309 Na imekuja katika kitabu cha Sira cha Maghlatwiy kwamba Abubakri hakuwepo, wala hakuwa katika hali hiyo, wala hakuwa mmiliki wa Bilal isipokuwa baada ya miaka thelathini tangu kutokea tukio hilo.310 Pili: Ni yale waliyoyaeleza wanahistoria katika ufafanuzi wa yale yaliyompata 4 baada ya watu wake kufika kwa Kasisi, ambapo wamesema: Yeye 4 alijitenga mbali na jamaa wakati wa chakula cha Buhayra, aliketi chini ya mti. Na Buhayra alipowatazama jamaa bila kuona wingu juu ya yeyote miongoni mwao bali likiwa katika sura ile anayoiona kwa Mtume 4, na akaliona wingu hilo limejitenga na jamaa liko juu ya kichwa cha Mtukufu Mtume 4, alisema: “Enyi   Al-Wafau cha Ibn Jawziy, uk. 34.   Taarikhul-Islam cha Dhahbiy, Juz. 2, uk. 28. 309   Siratul-Halabiyyah, Juz. 1, uk. 120; Taarikhul-Khamis, Juz. 1, uk. 259. 310   Sirat Maghlatwiy, uk. 11. 307 308

173

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 173

4/23/2016 2:45:59 PM


HUYU NDIYE BILAL

kundi la Makurayshi! Yeyote miongoni mwenu asijitenge mbali na chakula changu.” Wakasema: “Ewe Buhayura! Hakuna yeyote aliyejitenga mbali na chakula chako miongoni mwa wanaopasa kuja kwako, isipokuwa kijana ambaye ndiye mdogo zaidi kiumri kuliko wote.” Akasema: “Msifanye hivyo, mwiteni.” Kisha akanyanyuka ami yake Harith bin Abdul-Mutalib akamkumbatia, akaja naye na akamkalisha pamoja na jamaa.311 Wakati Mtukufu Mtume 4 alipojitenga na chakula cha Buhayra, jamaa waliashiria kwamba yeye 4 ndiye mdogo zaidi kuliko jamaa wote waliokuwa katika msafara ule.312 Na inavyojulikana bayana, kama walivyotamka bayana hilo wanahistoria wengi, ni kwamba Abubakri alikuwa ni mdogo kuliko Mtume 4 kiumri, kwa tofauti ya miaka miwili au zaidi. Na Bilal alikuwa mdogo kiumri kuliko Abubakri, kwa tofauti ya miaka mitano au zaidi. Hivyo hao wawili hawakuwepo katika tukio hilo, na kama mmoja wao angekuwepo katika tukio hilo, basi Mtukufu Mtume 4 asingekuwa ndiye mdogo kiumri kuliko wote waliokuwepo katika msafara ule. Hivyo inabainika kwamba, kwa kuwa Mtukufu Mtume 4 ndiye aliyekuwa mdogo zaidi kuliko watu wote waliokuwepo katika msafara ule, hivyo basi hakuna nafasi ya kukubali maelezo ya riwaya ya Abu Musa al-Ash’ariy. Na ni kwa ajili hii Dahlan alisita kusema chochote katika kitabu chake cha Sira, kuhusu madai ya kwamba Abubakri ndiye aliyekwenda kumwita Mtukufu Mtume 4 na kwenda naye kwa jamaa zake. Na akaonesha kwamba aliyekwenda kumchukua ni Harith bin Abdul-Mutalib. Na maelezo haya yanaoana na   Siratun-Nabawiyyah cha Dahlan, uk. 92 na 93.   Taarikhul-Khamis, uk. 92. Siratul-Halabiyyah, Juz. 1, uk. 118; Siratun-Nabawiyyah cha Ibn Kathir, Juz. 1, uk. 244; Sirat Ibn Is’haq, uk. 74; al-Wafau cha Ibn Jawziy, uk. 132; Dalailun-Nubuwwah cha Bayhaqiy, Juz. 2, uk. 28; Siratun-Nabawiyyah cha Ibn Hisham, Juz. 1, uk. 181; Biharul-An’war, Juz. 15, uk. 409.

311

312

174

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 174

4/23/2016 2:45:59 PM


HUYU NDIYE BILAL

yale yaliyokuja katika vyanzo vingine, kama vile al-Wafau cha Ibn al-Jawziy na Siratul-Halabiyyah.313 Na la ajabu zaidi ni kwamba, yule asiyekubali uwepo wa Abubakri miongoni mwa watu wa msafara ule, wala kwenda kwake kumchukua Mtukufu Mtume 4 kumpeleka kwa jamaa zake, kwa sababu yeye Abubakri alikuwa ni mdogo zaidi kiumri kuliko Mtukufu Mtume 4, ni kwa nini haoni kuwa ni uwongo na batili tupu, yale yaliyonukuliwa na baadhi ya riwaya, kwamba: Mtukufu Mtume 4 alirejea Makkah akiwa pamoja na Abubakri na Bilal?314 Dhahbiy ametamka wazi, kwamba hakika Bilal alikuwa bado hajazaliwa wakati huo.315 Na hakika maneno yake yako bayana na yanakubalika, kwani Bilal kama atakuwa alifariki mwaka wa 21 au 25 au 27 wa hijiriya,316 akiwa na umri wa miaka sitini na tatu, basi hakuwa ameshazaliwa wakati wa tukio hilo ambalo lilitokea miaka thelathini kabla ya Mtume kuanza jukumu la utume. Yaani kabla ya miaka arubaini na tatu ya Hijiriya. Na hata tukijaalia kwamba Bilal na Abubakri walikuwa pamoja na Mtukufu Mtume 4, bado hatuwezi kukubali uwepo wa amri kutoka kwa Abubakri kwenda kwa Bilal, kama inavyoonekana katika riwaya hiyo. Hiyo ni kutokana na kwamba hakuna mwanahistoria yeyote aliyedai kuwa Abubakri alikuwa mmiliki wa Bilal wakati huo. Na wala si sahihi yale waliyoashiria baadhi kwamba, huenda mmiliki wa Bilal, ambaye ni Umayyah bin Khalaf ndiye aliyemtuma Abubakri katika jambo hilo (la kumwamuru Bilal), hivyo Abubakri akampa idhini Bilal arudi na Mtukufu Mtume 4 kwa kutegemea   Siratul-Halabiyyah, Juz. 1, uk. 119; Al-Wafau, uk. 132; Biharul-An’war, Juz. 15, uk. 410. 314   Siratun-Nabawiyyah cha Dahlan, uk. 94. 315   Taarikhul-Islam cha Dhahbiy, Juz. 2, uk. 28. 316   Sirat al-Halabiyyah, Juz. 1, uk. 120; Hayatul-Hayawan cha Dumayriy, Juz. 2, uk. 275. Taarikhul-Khamis, Juz. 1, uk. 259. 313

175

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 175

4/23/2016 2:45:59 PM


HUYU NDIYE BILAL

ridhaa ya bwana na mmiliki wake, ili awe mhudumu wake, amliwaze na amlinde. Kwani si lazima mtu awe mtumwa wako ndio umtume katika jambo.317 Zaidi ya hapo ni kwamba, mmiliki wa Bilal – sawa awe ni Umayyah bin Khalaf au Abdullah bin Jadhian318 - hawezi kumtuma mtoto mdogo katika safari ndefu bila uangalizi unaohitajika. Na wala hawezi kukabidhi hatima yake kwa mtoto mwenzake ambaye hajavuka umri wa miaka kumi, bila uangalizi wa wafanyabiashara wakubwa na viongozi wa makuraishi. Kisha ni kwamba mtoto huyu – yaani Abubakri – je alikuwa na mamlaka na uwezo wa kuamrisha na kukataza na kuainisha maslahi ya Bilal? Na Bilal, hata kama alikuwa ameshazaliwa, wakati huo umri wake ulikuwa haujvuka miaka miwili. Je yeye Bilal alikuwa na uwezo wa kuwa mtumishi, mhudumu na mtu wa kumliwaza Mtukufu Mtume 4 safarini, achilia mbali kumlinda? Vyovyote iwavyo, ni kwamba dhana hii haina dalili, bali dalili inathibitisha ubatili wake. Hapa imebakia tuashirie kwamba, Abutalib ni maarufu kwa akili yake na hekima yake, hivyo uko mbali sana uwezekano wa yeye kuchukua hatua kama hiyo. Hatua ya kumwacha mwana wa ndugu yake ambaye yuko katika mazingira ya hatari, aende na mtoto ambaye hawezi kumpa msaada wowote, na ambaye hana uwezo wa kubeba jukumu hili zito na kujiokoa yeye mwenyewe, achilia mbali kumwokoa mwenzake. Na kwa kuchunguza maelezo yaliyokuja katika vitabu vya historia, kwamba Mtukufu Mtume 4 alikamata hatamu ya ngamia wa ami yake, pindi alipomuona amejiandaa kutoka kuelekea Sham, akamwambia: “Ewe ami yangu! Unaniacha kwa nani? Sina baba wala mama.” Abutalib akamuonea huruma na akamwambia: “Wallahi   Sirat al-Halabiyyah, Juz. 1, uk. 121.   Sirat al-Halabiyyah, Juz. 1, uk. 297 na 298.

317 318

176

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 176

4/23/2016 2:45:59 PM


HUYU NDIYE BILAL

ataondoka pamoja nami na wala hatatengana nami, wala mimi sintatengana naye kamwe.”319 Inapata nguvu rai ya kwamba Abutalib hawezi kuchukua hatua kama hiyo ya kutengana naye, bali unathibiti ubatili wa kuwepo uwezekano wa hilo kutokea. Ukweli ni upi: Hakika tunaloweza kulichukua na kulikubali ni lile lililonukuliwa katika vyanzo kadhaa, kwamba aliyemrejesha Mtukufu Mtume 4 Makkah ni ami yake Abutalib. Imekuja katika kitabu cha Sira cha Ibn Hisham, kwamba ami yake Abutalib alitoka naye haraka sana mpaka akamfikisha Makkah.320 Na pia imekuja katika kitabu TaarikhulIslam cha Dhahbiy kwamba: Yunus bin Shihab amepokea hadithi ndefu ambayo ndani yake kuna maelezo kwamba: Alipofika umri wa kubalehe, Abutalib alisafiri naye katika biashara, wakafika Taymau, ndipo Kasisi wa Mayahudi wa Taymau akamuona, akamwambia Abutalib: “Huyu ni nani?” Akasema: “Ni mwana wa kaka yangu.” Akamwambia: “Wallahi kama utafika Sham hautarudi naye kwa jamaa zako kamwe, Mayahudi watamuua, kwani hakika yeye ni adui yao.” Abutalib akarudi naye kutoka hapo Taymau hadi Makkah.321 Na kwa kuchunguza yote yaliyotangulia, tunakuta maelezo haya ndiyo yenye kutuliza nafsi, na ndiyo tunayoweza kuyategemea. Na ndio yanayooana na shauku ya Abutalib ya kumjali mwana wa ndugu yake, hasa ukizingatia dhana ya uwepo wa mazingira ya hatari na uwezekano wa kuuwawa.   Dalailun-Nubuwwah, Juz. 2, uk. 27; Sirat Nabawiyyah cha Ibn Hisham, Juz. 1, uk. 180; Al-Kamil Fitarikh cha Ibn Athir, Juz. 2, uk. 23; As-Sirat al-Halabiyyah, Juz. 1, uk. 117; Siratun-Nabawiyyah cha Dahlan, Juz. 1, uk. 91; Biharul-An’war, Juz. 15, uk. 48. 320   Sirat Nabawiyyah cha Ibn Hisham, Juz. 1, uk. 183; Taarikhul-Umam Wal-Muluk, Juz. 2, uk. 272; Siratun-Nabawiyyah cha Ibn Kathir, Juz. 1, uk. 245; Sirat Ibn Is’haq,, uk. 45; Al-Bidayat Wan-Nihayat, Juz. 2, uk. 284; As-Sirat al-Halabiyyah, Juz. 1, uk. 119; Dalailun-Nubuwwah cha Bayhaqiy, Juz. 2, uk. 29. Biharul-An’war, Juz. 15, uk. 410. 321   Taarikhul-Islam cha Dhahbiy, Juz. 2, uk. 30. 319

177

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 177

4/23/2016 2:45:59 PM


HUYU NDIYE BILAL

Kisha ni kwamba, je Abutalib si ndio mwenye jukumu na wajibu wa kumtunza?! Ambaye alimlinda na kumsaidia na kumtetea mpaka mwisho wa uhai wake. Vipi sasa tukubali kuwa alijitenga naye katika mazingira hatarishi na nyeti yenye kuhatarisha uhai wake, wakati anajua hali halisi ilivyo? Na vipi tutakubali kuwa yeye Mtukufu Mtume 4 aliridhia hilo, ilihali kumng’ang’ania na kumwandama kwake ami yake kulifikia katika kiwango ambacho alikuwa hawezi kulala isipokuwa pembeni yake.322 Na anamwandama pindi anapomuona anajiandaa na safari hadi anasema: “Ewe ami yangu! Unaniacha kwa nani? Sina baba wala mama.” Katika hali hii ilikuwa ni lazima asitengane naye wala kumwacha kwa yeyote, bali alibaki pembeni yake na akarudi naye Makkah. Na huenda ni kutokana na hali hii Buhayra aliacha kuhimiza na kusisitiza. Asingeweza kuacha Mtukufu Mtume 4 aendelee na safari kwenda Sham, wala arejee Makkah kwa kusindikizwa na watoto, ilihali yeye anahisi hatari halisi juu ya uhai wake 4. Kisimamo kifupi katika kisa cha Bilal na Jamanah: Imepokewa kwamba Bilal alimchukua Jamanah binti ya Zahaf al-Ash’jaiy. Lakini walipokuwa katika bonde la Naam Jamanah alimshambulia Bilal na kumpiga sana. Kisha akakusanya kila alichokipenda miongoni mwa dhahabu na fedha, akapanda ngamia wa baba yake, na kutoroka kwa kujificha kwa kuondoka kutoka katika msafara wa jeshi, akaelekea kwa Shihab bin Mazin aliyekuwa akijulikana kwa jina la Kawkabu Duriyyu. Mwanaume huyo alikuwa amemchumbia mwanamke huyo kutoka kwa baba yake. Katika siku ya tukio hilo, Mtukufu Mtume 4 alipoona Bilal kachelewa kufika   Biharul-An’war, Juz. 18, uk. 7; Al-Wafau, uk. 131; Al-Bidayat Wanihayat, Juz. 2, uk. 286; Tabaqatul-Kubra cha Ibn Saad, Juz. 1, uk. 121; Siratun-Nabawiyyah cha Ibn Kathir, Juz. 1, uk. 249.

322

178

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 178

4/23/2016 2:45:59 PM


HUYU NDIYE BILAL

kinyume na kawaida yake, aliwatuma Salman na Suhaybu kumfuatilia ili kujua hali yake. Wakamkuta amelala juu ya ardhi akiwa maiti na damu zikimvuja. Wakarudi kwa Mtukufu Mtume 4 wakampa habari hiyo, naye akawaambia: “Msilie.” Kisha akaswali rakaa mbili na kuomba baadhi ya dua, kisha akachukua gao la maji akamnyunyuzia Bilal. Mara Bilal akaruka kwa kunyanyuka na akaanza kuzibusu nyayo za Mtukufu Mtume 4. Mtukufu Mtume 4 akamwambia: “Ni nani huyu aliyekutendea hili ewe Bilal?” Akasema: “Ni Jamanah binti ya Zahaf, nami nampenda.” Mtume 4 akasema: “Pokea habari njema ewe Bilal. Nitamtumia ujumbe na kumleta.” Kisha Mtukufu Mtume 4 akasema: “Ewe Abul-Hasan! Huyu hapa ndugu yangu Jibril, ananipa habari kutoka kwa Mola wa viumbe wote. Kwamba Jamanah alipomuuwa Bilal alikwenda kwa mwanaume anayeitwa Shihab bin Mazin. Yeye alikuwa amemchumbia kutoka kwa baba yake lakini hakufanikiwa kumuoa. Na tayari ameshamsimulia mkasa na hali yake, naye amekusanya kundi linalokusudia kutupiga vita, hivyo simama na mfuate na jeshi la Waislamu, Mwenyezi Mungu Mtukufu atakupa ushindi dhidi yake. Na mimi narudi Madina.” Imam Ali B akaondoka na Waislamu. Alikwenda kwa kasi mpaka akafika kwa Shihab, akampiga na Waislamu wakashinda. Shihab akasilimu, na pia Jamanah na askari wengine. Imam akawapeleka Madina na wakasilimu upya mikononi mwa Mtukufu Mtume 4. Mtume 4 akasema: “Unasemaje ewe Bilal?” Akasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! nilikuwa nampenda, lakini hivi sasa Shihab ndiye mwenye haki naye zaidi kuliko mimi.” Shihab akamzawadia Bilal suria wawili, farasi wawili na ngamia wawili.323   Al-Manaqib cha Shahri Ashub, Juz. 1, uk. 138 na 139; Safinatul-Bihar, Juz. 1, uk. 104; Al-Awail cha Isfahaniy, uk. 221 – 223; Simay Bilal Habashiy cha Kiajemi, uk. 196 - 199.

323

179

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 179

4/23/2016 2:45:59 PM


HUYU NDIYE BILAL

Uchambuzi wa riwaya hii upande wa madhumuni: Ukiachana na udhaifu uliyopo katika sanadi ya riwaya hii, tumepata pia baadhi ya nukta zenye utata katika madhumuni yake, hivyo imekuwa ni lazima kuashiria nukta hizo: Kwanza: Hakika riwaya haijaweka wazi uhusiano wa Bilal na Jamanah, haijabainisha pindi alipomchukua, alimchukua kama mke wake au mateka? Ijapokuwa kutokuwa kwake Mwislamu wakati alipomchukua, kunaipa nguvu dhana ya pili. Ndiyo, baadhi wamesema:324 Hakika Bilal alikuwa amemchumbia kutoka kwa baba yake, kisha baadaye akamuoa. Isipokuwa ni kwamba hakuna njia ya kuhakiki hilo na kupata ukweli wake. Na riwaya haijataja suala hili, kama ilivyo wazi katika maelezo yake. Na sijui waliwezaje wao kufahamu maana hiyo?! Pili: Hakika jambo muhimu tunalojifunza kutoka katika riwaya hii ni mauti ya Bilal yaliyompata kutokana na vipigo vya Jamanah. Na kwamba Mtukufu Mtume 4 alimhuisha baadaye. Kumhuisha maiti kwa nguvu ya Mwenyezi Mungu ni jambo thabiti, na halina mjadala juu yake. Na Mwenyezi Mungu ametupa habari kwamba lilitokea hilo mikononi mwa Isa B kwa kusema:

ِّ ‫ق ِمنَ ال‬ ُ ‫ين َكهَ ْيئَ ِة الطَّي ِْر بِإِ ْذنِي فَتَ ْنفُ ُخ فِيهَا فَتَ ُك‬ ُ ُ‫َوإِ ْذ ت َْخل‬ ‫ئ‬ ُ ‫ون طَ ْيرًا بِإِ ْذنِي ۖ َوتُب ِْر‬ ِ ‫ط‬ ۖ ‫ص بِإِ ْذنِي ۖ َوإِ ْذ تُ ْخ ِر ُج ْال َموْ ت َٰى بِإِ ْذنِي‬ َ ‫أْالَ ْك َمهَ َو أْالَ ْب َر‬ “Na ulipotengeneza kwa udongo kama umbo la ndege kwa idhini Yangu, kisha ukapuliza likawa ndege kwa idhini Yangu, na ulipowaponyesha vipofu na wenye mbalanga kwa idhini Yangu, na ulipowatoa wafu kwa idhini Yangu.” (Sura Maidah; 5:110).   Al-Awail cha Isfahaniy, uk. 221 na 222; Simay Bilal Habashiy cha Kiajemi, uk. 196 na 197.

324

180

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 180

4/23/2016 2:45:59 PM


HUYU NDIYE BILAL

Na amesema:

ِّ ‫ق لَ ُك ْم ِمنَ ال‬ ُ ُ‫أَنِّي قَ ْد ِج ْئتُ ُك ْم بِآيَ ٍة ِم ْن َربِّ ُك ْم ۖ أَنِّي أَ ْخل‬ ‫ين َكهَ ْيئَ ِة الطَّي ِْر فَأ َ ْنفُ ُخ فِي ِه‬ ِ ‫ط‬ ُ ‫فَيَ ُك‬ ۖ ِ َّ‫ص َوأُحْ يِي ْال َموْ ت َٰى بِإِ ْذ ِن للاه‬ ُ ‫ون طَ ْيرًا بِإِ ْذ ِن للاهَّ ِ ۖ َوأُب ِْر‬ َ ‫ئ أْالَ ْك َمهَ َو أْالَ ْب َر‬ “…..Mimi nimewajia na Ishara kutoka kwa Mola Wenu, hakika mimi nitawafanyia kama namna ya ndege katika udongo; kisha nimpulizie awe ndege kwa idhini ya Mwenyezi Mungu na niwaponye vipofu na wenye mbalanga. Niwafufue wafu kwa idhini ya Mwenyezi Mungu…..” (Sura Imran; 3:49).

Kama ambavyo hakuna mjadala juu ya uwezekano wa kutokea mfano wa hilo mikononi mwa Mtukufu Mtume 4. Imam ZainulAbidin B anasema: “Mwenyezi Mungu hakumpa Nabii yeyote kitu isipokuwa alimpa Muhammad kitu hicho, na alimpa kile ambacho hajawahi kuwapa hao wengine na wasichokuwa nacho.”325 Lakini hii haimaanishi kuwa tusadiki kumhuisha kwake Bilal, bila kuwepo ushahidi bayana unaothibitisha tukio hilo. Na riwaya tuliyonayo haijatimia upande wa sanadi, hivyo hatuwezi kuitegemea. Na wala hatuna njia nyingine ya kuthibitisha kutokea kwa jambo hili. Na ajabu zaidi ni kwamba vyanzo muhimu havijaeleza hadithi hii, licha ya kwamba ina umuhimu mkubwa. Kwani ni muujiza unaostahiki kupewa kipaumbele na umuhimu na wanahistoria. Na ajabu nyingine ni kwamba, muujiza wenye daraja kama hii uishi katika maficho bila kujulikana. Wakati ambapo ulipasa kujulikana baina ya Waislamu na unukuliwe na kusambaa kizazi hadi kizazi.

Biharul-An’war, Juz. 18, uk. 7.

325

181

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 181

4/23/2016 2:45:59 PM


HUYU NDIYE BILAL

Orodha Ya Vitabu Vilivyo ­Chapishwa Na Al-Itrah Foundation 1. i) Qur’ani Tukufu – Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili ii) Qur’an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thelathini 2. Uharamisho wa Riba 3. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza 4. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili 5. Hekaya za Bahlul 6. Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) 7. Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (a.s.) 8. Hijab vazi Bora 9. Ukweli wa Shia Ithnaashari 10. Madhambi Makuu 11. Mbingu imenikirimu 12. Abdallah Ibn Saba 13. Khadijatul Kubra 14. Utumwa 15. Umakini katika Swala 16. Misingi ya Maarifa 17. Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia 18. Bilal wa Afrika 19. Abudhar 20. Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu 21. Salman Farsi 22. Ammar Yasir 23. Qur’an na Hadithi 24. Elimu ya Nafsi 25. Yajue Madhehebu ya Shia

182

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 182

4/23/2016 2:46:00 PM


HUYU NDIYE BILAL

26. Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur’an Tukufu 27. Al-Wahda 28. Ponyo kutoka katika Qur’an 29. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii 30. Mashukio ya Akhera 31. Al Amali 32. Dua kwa Mujibu wa Ahlulbayt (a.s) 33. Udhuu kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna 34. Haki za wanawake katika Uislamu 35. Mwenyezi Mungu na sifa zake 36. Kumswalia Mtume (s) 37. Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) 38. Adhana 39. Upendo katika Ukristo na Uislamu 40. Qur’ani na Kuhifadhiwa Kwake 41. Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu 42. Kupaka juu ya khofu 43. Kukusanya Sala Mbili 44. Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara 45. Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya 46. Kusujudu juu ya udongo 47. Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) 48. Tarawehe 49. Malumbano baina ya Sunni na Shia 50. Kupunguza Swala safarini 51. Kufungua safarini 52. Umaasumu wa Manabii 53. Qur’an Yatoa Changamoto 54. as-Salaatu Khayrun Mina -’n Nawm 55. Uadilifu wa Masahaba 56. Dua e Kumayl 183

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 183

4/23/2016 2:46:00 PM


HUYU NDIYE BILAL

57. Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu 58. Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake 59. Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata 60. Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mtume Muhammad (s) 61. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza 62. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili 63. Kuzuru Makaburi 64. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza 65. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili 66. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu 67. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne 68. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano 69. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita 70. Tujifunze Misingi Ya Dini 71. Sala ni Nguzo ya Dini 72. Mikesha Ya Peshawar 73. Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu 74. Ubora wa Imam ‘Ali na Ushia ndio njia iliyonyooka 75. Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake 76. Liqaa-u-llaah 77. Muhammad (s) Mtume wa Allah 78. Amani na Jihadi Katika Uislamu 79. Uislamu Ulienea Vipi? 80. Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) 81. Dhana ya Ndoa ya Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) 82. Urejeo (al-Raj’ah) 83. Mazingira 84. Utokezo (al - Badau) 85. Hukumu ya kujenga juu ya makaburi 86. Swala ya maiti na kumlilia maiti 87. Uislamu na Uwingi wa Dini 184

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 184

4/23/2016 2:46:00 PM


HUYU NDIYE BILAL

88. 89. 90. 91. 92. 93. 94. 95. 96. 97. 98. 99. 100. 101. 102. 103. 104. 105. 106. 107. 108. 109. 110. 111. 112. 113. 114. 115. 116. 117. 118.

Mtoto mwema Adabu za Sokoni Na Njiani Johari za hekima kwa vijana Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu Tawasali (AT- TAWASSUL) Imam Mahdi katika Usunni na Ushia Hukumu za Mgonjwa Sadaka yenye kuendelea Msahafu wa Imam Ali Maimamu wa Ahlul Bait – Ujumbe na Jihadi Idi Al-Ghadir Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu Hukumu zinazomuhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi Huduma ya Afya katika Uislamu Sunna za Nabii Muhammad (saww) Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) Shahiid Mfiadini Mwanamke Na Sharia Ujumbe -Sehemu ya Kwanza Ujumbe - Sehemu ya Pili Ujumbe - Sehemu ya Tatu Ujumbe - Sehemu ya Nne Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu Hadithi ya Thaqalain Ndoa ya Mutaa Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza Ukweli uliopotea sehemu ya Pili Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu 185

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 185

4/23/2016 2:46:00 PM


HUYU NDIYE BILAL

119. Ukweli uliopotea sehemu ya Nne 120. Ukweli uliopotea sehemu ya Tano 121. Mkutano wa Maulamaa wa Baghdad 122. Safari ya kuifuata Nuru 123. Fatima al-Zahra 124. Myahudi wa Kimataifa 125. Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi 126. Visa vya kweli sehemu ya Kwanza 127. Visa vya kweli sehemu ya Pili 128. Elimu ya Ghaibu ya Maimamu 129. Mwanadamu na Mustakabali wake 130. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) 131. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) 132. Khairul l’Bariyyah 133. Uislamu na mafunzo ya kimalezi 134. Vijana ni Hazina ya Uislamu 135. Adhana ni Ndoto au ni Wahyi? 136. Tabaruku 137. Saada Kamili – Kitabu cha Kiada cha Maadili 138. Vikao vya furaha 139. Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 140. Visa vya wachamungu 141. Falsafa ya Dini 142. Kuhuzunika na Kuomboleza 143. Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah 144. Mjadala wa Kiitikadi 145. Kuonekana kwa Allah 146. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) 147. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) 148. Ndugu na Jirani 149. Ushia ndani ya Usunni 186

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 186

4/23/2016 2:46:00 PM


HUYU NDIYE BILAL

150. 151. 152. 153. 154. 155. 156. 157. 158. 159. 160. 161. 162. 163. 164. 165. 166. 167. 168. 169. 170. 171. 172. 173. 174. 175. 176. 177. 178. 179. 180.

Maswali na Majibu Mafunzo ya hukmu za ibada Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1 Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2 Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 Abu Huraira Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. Mazingatio kutoka katika Qur’an - Sehemu ya Kwanza Mazingatio kutoka kaitka Qur’an - Sehemu ya Pili Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili Shia na Qur’ani – Majibu na Maelezo Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu Uislamu Safi Majlisi za Imam Husein Majumbani Je, Kufunga Mikono Uislam wa Shia Amali za Makka Amali za Madina Asili ya Madhehebu katika Uislamu Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi Ukweli uliofichika katika neno la Allah Uislamu na Mifumo ya Uchumi Umoja wa Kiislamu na Furaha Mas’ala ya Kifiqhi Jifunze kusoma Qur’ani as-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah Hayya ‘Alaa Khayri’l-’Amal Katika Adhana Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura 187

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 187

4/23/2016 2:46:00 PM


HUYU NDIYE BILAL

181. Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na Ramadhani) 182. Uadilifu katika Uislamu 183. Mahdi katika Sunna 184. Maswali Ya Uchunguzi Kuhusu Uislam 185. Kazi na Bidii ni njia ya maendeleo 186. Abu Talib – Jabali Imara la Imani 187. Ujenzi na Utakaso wa Nafsi 188. Vijana na Matarajio ya Baadaye 189. Historia maana na lengo la Usalafi 190. Ushia – Hoja na Majibu 191. Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) 192. Maombolezo – Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) 193. Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu 194. Takwa 195. Upotoshaji Dhahiri katika (Turathi) Hazina ya Kiislamu 196. Amirul Muuminina (as) na Makhalifa 197. Tawheed Na Shirki 198. Kuvunja hoja iliyotumika kutetea Uimamu wa AbuBakr 199. Adabu za vikao na mazungumzo 200. Hija ya Kuaga 201. Uwazi baina ya Maslahi na Vikwazo 202. Fadhila za watukufu watano katika Sahih Sita 203. Mdahalo baina ya Mwanachuoni waKisunni na Kishia (Al- Muraja’aat) 204. Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (as) 205. Imam Husain ni Mfumo wa Marekebisho na Mageuzi 206. Mtazamo kuhusu msuguano wa Kimadhehebu 207. Nchi na Uraia – Haki na wajibu kwa Taifa 208. Mtazamo wa Ibn Taymiyyah juu ya Imam Ali (as) 209. Uongozi wa Kidini – Maelekezo na Utekelezaji wa Kijamii 210. Maadili ya Ashura 211. Mshumaa – Shahidi na Kifo cha Kishahidi 188

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 188

4/23/2016 2:46:00 PM


HUYU NDIYE BILAL

212. Mizani ya Hekima – Hadithi za Ahlul Bait (as) – Sehemu ya Kwanza 213. Imam Ali na Mambo ya Umma 214. Imam Ali na Mfumo wa Usawa 215. Uimamu na Tamko la Kutawazwa 216. Mfumo wa Wilaya 217. Vipi Tutaishinda Hofu? 218. Kumswalia Mtume ni Ufunguo wa Utatuzi wa Matatizo 219. Maeneo ya Umma na Mali Zake 220. Nahju ‘L-Balagha– Majmua ya Khutba, Amri, Barua, Risala, Mawaidha na Semi za Amirul-Muuminin Ali bin Abu Talib (a.s.) 221. Mukhtar – Shujaa aliyelipiza kisasi dhidi ya wauaji wa Imam Husein (as) hapo Karbala 222. Mazingatio Katika Swala 223. Imam Hasan na Mfumo wa Kujenga Jamii 224. Vyakula Na Vinywaji 225. Kuelewa Rehema ya Mwenyezi Mungu 226. Imam Mahdi na Bishara ya Matumaini 227. Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu 228. Shia Na Sahaba - Majibu na Maelezo 229. Majanga Na Jukumu la Jamii 230. Shia Na Hadith - Majibu na Maelezo 231. Upotofu Ndani ya Kitabu cha Mitaala kwa Shule za Sekondari 232. Ugaidi Wa Kifikra Katika Medani Ya Kidini 233. Yafaayo kijamii 234. Uswalihina Dhahiri Na Batini Yake 235. Mkakati wa Kupambana na Ufakiri 236. Mwanamke Katika Harakati Za Mageuzi 237. Jihadi 238. Hija Katika Maneno Na Ujumbe Wa Imam Khomeini (R.A) 239. Tiba Ya Maradhi Ya Kimaadili 240. Yusuf Mkweli

189

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 189

4/23/2016 2:46:00 PM


HUYU NDIYE BILAL

241. Taqiyya Kwa Mujibu Wa Sheria Ya KIISLAMU 242. Imam Mahdi (A.S) Imam Wa Zama Hizi Na Kiongozi Wa Dunia 243. Talaka Tatu 244. Safari Ya Kuelekea Kwa Mwenyezi Mungu 245. Hotuba Za Kiislamu Juu Ya Haki Za Binadamu 246. Mashairi Ya Kijamii 247. Ngano Ya Kwamba Qur’ani Imebadilishwa 248. Wito Kwa Waumini: “Enyi Mlioamini” 249. Imam Husain (a.s) ni Utu na Kadhia 250. Imam Husain ni Kielelezo cha Kujitoa Muhanga na Fidia 251. Imam Mahdi ni Tumaini la Mataifa 252. Kuchagua Mchumba 253. Mazungumzo ya Umoja – Ukosoaji na Usahihishaji 254. Utamaduni wa Mwamko wa Kijamii 255. Hekima za kina za Swala 256. Kanuni za Sharia za Kiislamu 257. Utamaduni kufuatana na Qur’ani na Utekelezaji wa Kivitendo (Sehemu ya Kwanza) 258. Kauli sahihi zaidi katika kufafanua Hadithi

190

10_16_Huyu Ndiye Bilal_23_April_2016.indd 190

4/23/2016 2:46:00 PM


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.