Imam husain ni kielelezo cha kujitoa muhanga na fidia

Page 1

IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

‫اإلمام الحسين رمز التضحية والفداء‬

Kimeandikwa na: Sheikh Hasan Musa as-Saffar

Kimetarjumiwa na: Abdul-Karim Juma Nkusui


‫ترجمة‬

‫اإلمام الحسين رمز التضحية والفداء‬

‫تأليف‬ ‫الشيخ حسن الصفار‬

‫من اللغة العربية إلى اللغة السواحلية‬


©Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION

ISBN: 978 - 9987 –17 – 081 - 4

Kimeandikwa na: Sheikh Hasan Musa as-Saffar

Kimetarjumiwa na: Abdul-Karim Juma Nkusui

Kimehaririwa na: Alhaji Hemedi Lubumba

Kimepitiwa na: Mbarak Ali Tila

Kimepangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation

Toleo la kwanza: Novemba, 2014 Nakala: 2000

Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. - 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: www.alitrah.info


Fidia

Imam Husein ni Kielelezo cha Kijitoa Muhanga na Fidia

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi waRehema Mwenye Kurehemu. Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi waRehema Mwenye Kurehemu. Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi waRehema Mwenye Kurehemu.

š⎥⎪Ï%©!$#tβθäóÏk=t7ãƒÏM≈n=≈y™Í‘«!$#…çμtΡöθt±øƒs†uρŸωuρtβöθt±øƒs†#´‰tnr&ωÎ)©!$#34’s∀x.uρ«!$$Î/$Y7ŠÅ¡ym∩⊂®∪

6

š⎥⎪Ï%©!$#tβθäóÏk=t7ãƒÏM≈n=≈y™Í‘«!$#…çμtΡöθt±øƒs†uρŸωuρtβöθt±øƒs†#´‰tnr&ωÎ)©!$#34’s∀x.uρ«!$$Î/$Y7ŠÅ¡ym∩⊂®∪

“Ambao walifikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu na kumwogopa Yeye, wala hawamwogopi yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu Ndiye anayetosha kuhisabu.” 6 Ahzab: 39). (Suratul-


Yaliyomo Neno la Mchapishaji........................................................................1 Utangulizi.........................................................................................3 Mwangaza Kutoka Katika Maisha ya Imam....................................6 Kuzaliwa kwake...............................................................................6 Kupewa kwake jina..........................................................................6 Familia yake.....................................................................................6 Katika Qur’ani Tukufu.....................................................................7 Manukato ya Mtume........................................................................9 Miongoni mwa Tabia yake Njema.................................................10 Maneno yake ya Kimapinduzi....................................................... 11 Maandiko Kutoka Katika Kitabu cha Mapinduzi .........................16 Mazingira ya Utawala wa Bani Umayya.......................................16 Yazid bin Muawiya awa Mtawala..................................................19 Husain Anapinga Kutoa Kiapo cha utii.........................................23

v


Husain Anaondoka Madina............................................................24 Mwitikio wa Kufah........................................................................25 Kwenda Irak...................................................................................27 Karbalaa ........................................................................................28 Ashura ........................................................................................29 Msafara wa Mateka wa Kike.........................................................31 Kujitoa Muhanga na Fidia.............................................................32


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

‫بسم اهلل الرحمن الرحيم‬ NENO LA MCHAPISHAJI

K

itabu ulichonacho mikononi mwako asili yake ni cha lugha ya Kiarabu kwa jina la, al-Imam Husayn Ramza ‘t-Tadhhiyati wa ‘l-Fidaa’, kilichoandikwa na Sheikh Hasan Musa as-Saffar. Sisi tumekiita, Imam Husain ni Kielelezo cha Kujitoa Muhanga na Fidia. Imam Husain (a.s.), mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w.) alikataa kula kiapo cha utii kwa mtawala dhalimu na badala yake akaamua kujitoa muhanga kwa ajili ya kuinusuru dini ya Allah kutokana na upotoshaji uliokuwa ukifanywa na mtawala dhalimu wa wakati huo - Yazid bin Muawiya bin Abu Sufyan. Imam Husain aliishi kwa malengo makubwa ya kuwasaidia na kuwakomboa wanyonge kutokana na ukandamizaji wa watawala madhalimu, na hususan kuurudishia Uislamu heshima yake. Kwa hakika hakuinusuru tu dini ya Allah, bali pia alijitoa muhanga kwa ajili ya wanyonge na wanaokandamizwa ulimwenguni pote. Hii ndio maana kila mwaka inapofika mwezi wa Muharram, Waislamu ulimwenguni kote hukusanyika si kwa ajili ya kuomboleza tu, bali pia kukumbushana yale ambayo Imam (a.s.) aliyatolea muhanga na kuhimizana kuyasimamia na kuyafanyia kazi. Mwandishi wa kitabu hiki anatumia kalamu yake kuelezea harakati za Imam Husain (a.s.) zilivyoinusuru dini ya Allah na kuwakomboa wanyonge na wanaokandamizwa ulimwenguni pote. Azma yake ni kuendeleza harakati hizo katika ulimwengu huu wa sasa ambao akina Yazid bado wapo na wanaendelea kujitokeza kila wakati. 1


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu ambapo watawala mabeberu na madhalimu wamezidisha mbio zao za kuwakandamiza wanyonge na kuyakandamiza na kuyaonea mataifa madogo ulimwenguni kwa kuanzisha vita baina yao na kupora rasilimail zao. Kutoka na ukweli huu, taasisi yetu ya Al-Itrah imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumini yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili. Tunamshukuru ndugu yetu Abdul-Karim Juma Nkusui kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kukitarjumi kitabu hiki kwa Kiswahili kutoka lugha ya asili ya Kiarabu. Aidha tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Allah awalipe wote malipo mema hapa duniani na kesho Akhera – Amin. Mchapishaji Al-Itrah Foundation

2


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

‫بسم اهلل الرحمن الرحيم‬ UTANGULIZI

M

wanzo wa kila mwaka mpya wa Hijiria huwa inatusubiri kumbukumbu ya Imamu Husain bin Ali bin Abi Twalib (as), na huwa tunaipokea kwa wigo wake na kwa malengo yake matukufu ya Kiislamu na kwa mafunzo yake mazuri ya kimapambano. Na kwa kuwa umma wetu wa Kiislam leo hii unaishi katika zama za mapambano ya jumla, hivyo ni wajibu kwako kusimama sana katika kituo cha kumbukumbu ya Imamu Husain (as) ili kutoka kwake ujiongezee nguvu ya imani na itikadi na uchukue uvumilivu na muhanga kutoka kwake. Kumbukumbu ya Imam Husain (as) inamaanisha nini? Hakika inamaanisha kujiamini na kujijengea uvumilivu bila kujali nguvu za adui na ukubwa wa jeshi lake. Karbala jeshi la Husain (as) lilikuwa na wapiganaji sabini wakati jeshi la maadui lilikuwa na maelfu ya wanajeshi, pamoja na hivyo jeshi la watu sabini liliingia katika mapambano ya kuinusuru haki kwa kujiamini na kwa ukakamavu, anasema Imam Shahid:

‫أال واني زاحف بهذه األسرة مع قلة العدد‬ ‫وخذالن الناصر‬ “Fahamuni hakika mimi naondoka pamoja na familia hii, licha ya uchache wa idadi na kusalitiwa na msaidizi.”1 1

Abdurazak al-Muqaram katika Maqtalul-Imam Husain Uk. 234 chapa ya tano Beirut 1979. 3


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

Nayo inamaanisha uzuri wa kujitoa muhanga, kutoa na kujitolea katika njia ya Mwenyezi Mungu bila ya mipaka. Katika Siku ya Ashura Husain (as) alitoa watoto wake wote, na watu wa familia yake na vipenzi katika masahaba wake na wafuasi wake, hadi wake zake na familia yake, na akajitoa muhanga yeye mwenyewe kwa kila kitu katika njia ya kutetea maadili ya Uislamu yenye kudumu na misingi yake adilifu. Na hakuwa ni mwenye kusikitika katika utoaji huu bali alikuwa na furaha anamuhimidi Mwenyezi Mungu kwa taufiki na kujitolea huku, na hivyo historia inatusimulia kwamba alipoanguka shahidi uso wake ulikuwa mkunjufu kwa furaha. Na katika sekunde za mwisho za uhai wake alikuwa anamuomba Mwenyezi Mungu hali amelala katika mchanga wa Karbalaa, hajali mapanga yenye kuchanachana mwili wake wala mikuki yenye kuchoma mwili wake mtukufu, akiwa katika hali hiyo, alisema katika maombi yake kwa Mwenyezi Mungu:

‫ يا غياث‬،‫صبراً على قضائك ال إله سواك‬ ،‫ وال معبود غيرك‬،‫ مالي رب سواك‬،‫المستغيثين‬ ‫ يا غياث من غياث له‬،‫صبراً على حكمك‬ “Huu ni uvumilivu juu ya hukumu yako, hakuna Mungu asiyekuwa Wewe, Ewe uliye msaada kwa mwenye kuomba msaada, mimi sina Mola isipokuwa Wewe, wala sina wa kumwabudu asiyekuwa Wewe. Huu ni uvumilivu juu ya hukumu yako, Ewe ambaye ni msaada kwa asiye na msaada.”2 2

aaqir Sharif al-Qarashiy katika Hayatul-Imam Husain, Juz. 3, Uk. 288, Chapa ya kwanza B 1396 Hijiria. 4


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

Na hiyo inamaanisha jukumu la kila mwislamu na wajibu wake katika kufanya kazi kwa ajili ya kutengeneza jamii na kupiga vita upotovu. Na katika mapinduzi ya Imam Husain (as) mwanamke alikuwa anapigana pembezoni mwa mwanaume na vijana walikuwa wanawatangulia watu wazima katika kupata shahada, na watumwa walikuwa wanashirikiana na waungwana katika utukufu wa kujitoa muhanga na hata watoto wadogo walikuwa na nafasi katika vita ya Karbalaa. Mwisho: Hakika ni juu ya kila mtu kuitumia vyema kumbukumbu hii katika kuifahamu shakhsiya ya Imam Husain (as) na wigo wa mapinduzi yake na malengo ya mapambano yake matukufu. Na kujaribu kuelewa mafunzo yake na kushikamana na misingi yake na kufuata njia ya Imam Husain (as) katika kushikamana na dini na kupigana jihadi kwa ajili ya kutetea maadili mema na kujenga uvumilivu katika sharia zake na mifumo yake. Husain (as) ni mtoto wa binti ya Mtume wa Waislamu wote, na yeye alijitoa muhanga kwa ajili ya Uislamu, dini ya Waislamu wote, na kwa hiyo yeye ni Imam wa Waislamu wote, hahusiani na madhehebu maalum, wala haijuzu kundi maalum kumfanya ni wa kwao peke yao. Kijitabu hiki kidogo kilichochapishwa zamani hivi sasa nakipeleka katika chapa mpya pamoja na nyongeza ndogo ili kuchangia katika kutukuza kumbukumbu ya Imam Husain (as) na kuelezea jukumu lake tukufu, na hakika Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kutia tawfiki.

5


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

‫بسم اهلل الرحمن الرحيم‬ MWANGAZA KUTOKA KATIKA MAISHA YA IMAM HUSAIN (AS) Kuzaliwa kwake:

T

arehe tano ya mwezi wa Shabani katika mwaka wa nne Hijiria ilichomoza nuru ya Husain (as) katika nyumba tukufu ya Ali (as).3

Kupewa kwake jina: Babu yake, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alimpa jina Husain (as) kama alivyompa jina kaka yake Hasan (as) ambaye alizaliwa kabla yake, na hayo ni majina mawili ambayo hayakuwa yakijulikana bali yalifunuliwa kwa Nabii (saww) kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Imepokewa kutoka kwa Imran bin Sulaiman kuwa alisema: “Hasan na Husain ni katika majina ya watu wa peponi hayakuwepo wakati wa ujahiliya.”4 Familia yake: Husain (as) anatokana na ukoo mtukufu na familia tukufu katika historia ya binadamu, babu yake kwa upande wa mama yake ni Mtukufu Mtume (saww) na baba yake ni Kiongozi wa Waumini Ali bin Abi Twalib (as), na mama yake ni Bibi mbora wa wanawake wote wa ulimwengu Fatma Zahra binti ya Mtukufu Mtume. I bnu al-Athiyr katika Usudul- Ghaba fiy ma’arifati swahaba Jz. 1 uk: 496 – Daarul fikri – Beirut 1989. 4 Rejea iliyotangulia 3

6


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

Katika Qur’ani Tukufu: Husain (as) ni mtu wa tano katika watu wa kishamiya ambao kwao iliteremka aya ya kuwatakasa:

َّ ‫ْت‬ ِّ ‫ُري ُد اللهَُّ لِي ُْذ ِه َب َع ْن ُك ُم‬ َ ‫الر ْج‬ ِ ‫س أَ ْه َل ْال َبي‬ ِ ‫إِن َما ي‬ َ ‫َوي‬ ‫يرا‬ ً ‫ِّر ُك ْم َت ْط ِه‬ َ ‫ُطه‬ “Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.”5

Na maelezo yafuatayo yamekuja katika tafsiri ya Ruhul-Maaniy ya al-Alusiy al-Baghidadiy kuhusu aya hii tukufu: “Amepokea Tirmidhiy na al-Hakim na wamesema ni riwaya sahihi, na Ibnu Jarir, Ibnu Mundhir, Ibnu Marduwayhi na Bayhaqiy katika Sunan yake kutoka katika njia ya Ummu Salama (r.a), amesema: ‘Katika nyumba yangu iliteremka ‘Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.’ Na ndani ya nyumba alikuwemo Fatma, Ali, Hasan na Husain, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) akawafunika kwa kishamiya kisha akasema: Hawa ni watu wa nyumba yangu basi waondolee uchafu na watakase kabisa kabisa.’” Na imepokewa kutoka kwa jamaa kutoka kwa Umar bin Abi Salama mtoto wa kulea wa Mtukufu Nabii (saww), amesema: Ummu Salama alisema: ‘Je na mimi niko pamoja nao?’ Akasema 5

Suratul-Ahzab: 33 7


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

(saww): ‘Wewe uko mahala pako, na hakika wewe uko katika kheri.’ Na habari za Mtume (saww) kumwingiza Ali, Fatma na watoto wao (r.a) ndani ya guo na kutomwingiza Ummu Salama ni nyingi na hazihesabiki, nazo ni zenye kuainisha ni akina nani watu wa nyumba ya Mtume (saww) kwa maana yoyote ile ya nyumba, na makusudio ni wale waliofunikwa kwa guo, na wala hawaingii humo wake zake.”6 Na Husain (as) ni katika jamaa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu ambao Mwenyezi Mungu amefaradhisha kwa Waislamu wajibu wa kuwapenda katika kauli yake (swt):

ٰ‫ُق ْل لاَ أَ ْسأَلُ ُك ْم َعلَ ْي ِه أَ ْج ًرا إِلاَّ ْال َم َو َّد َة ِفي ْال ُق ْر َبى‬ “Sema: kwa haya siwaombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi katika ndugu.”7

al-Hafidh as-Suyutiy as-Shafi’iy amesema: “Amepokea Ibnu Mundhir, Ibnu Abi Haatim na Ibnu Marduwayhi katika tafsiri zao, na Tabaraniy katika Muujamul-Kabiyr kutoka kwa Ibnu Abbas kuwa amesema: ‘Iliposhuka aya hii “Sema: kwa haya siwaombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi katika ndugu.” Walisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu ni nani ndugu zako hawa ambao imekuwa ni wajibu kwetu kuwapenda? Akasema (saww): Ni Ali, Fatma na watoto wao.’”8 Sayyid Mahamud al- Alusiyal- Baghidadiy katika Ruhul-Maaniy Jz. 22 uk: 14 Daaru Ihiyaai turaathil- arabiy Beirut 7 Suratu Shuraa: 23 8 Jalalu Diyn Suyutiy katika Ihiyaail- mayiti bifadhail Ahlul-bait uk: 30 chapa ya kwanza - Tehran 1988 6

8


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

Manukato ya Mtume (saww): Imepokewa kwa tawatur kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) hadith nyingi zinazoeleza wajibu wa kumpenda sana mjukuu wake Husain (as) na ndugu yake Hasan (as), na humo anabainisha nafasi yao na fadhila zao katika masikio ya masahaba wake kama vile kauli yake (saww):

‫هما ريحانتاي من الدنيا‬ “Wao ni manukato yangu katika dunia.”9

Na kutoka kwa Ya’aliy bin Murrah amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww):

‫حسين مني وأنا من حسين أحب اهلل من أحب‬ ‫ حسين سبط من األسباط‬،‫حسينا‬ “Husain anatokana na mimi na mimi ninatokana na Husain, Mwenyezi Mungu anampenda mwenye kumpenda Husain, Husain ni mjukuu kati ya wajukuu.”10

Na katika Sunan Tirmidhiy kutoka kwa Abi Said amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww):

‫الحسن والحسين سيدا شباب أهل الجنة‬ “Hasan na Husain ni mabwana wa vijana wa peponi.”11 Al-Bukhariy katika Sahihi Bukhariy Jz. 5 uk: 33 Daarul- Jaliyli - Beirut Ibnu al-Athiyr katika Usudul- Ghaba Jz. 1 uk: 497 11 Abu Turabi Dhaahiriy katika Risalatu fadhil ahlul- bait wa huquukihim cha Ibnu Taimiya uk: 83 chapa ya kwanza 1984 Daarul- Qiblq Saudia 9

10

9


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

Na katika Mustadrakul-Haakim kutoka kwa Abu Huraira amesema: Nilimuona Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) naye amembeba Husain bin Ali naye anasema:

‫اللهم إني أحبه فأحبه‬ “Eee Mwenyezi Mungu hakika mimi ninampenda nawe mpende.”12

Tabia Yake Njema: Imam Husain (as) katika maisha yake na nyendo zake alikuwa anafuata maadili ya Uislamu na tabia njema za Mtume (saww), na wanahistoria wengi wametaja misimamo yake na sehemu ambazo zinaakisi picha, sifa na tabia yake njema, hapa tunataja baadhi yake tu:

12

1.

Miongoni mwa unyenyekevu wake na ukarimu wake ni kwamba aliingia kwa maskini wakiwa wanakula wakamkaribisha kwenye chakula akateremka kwenye kipando chake na akala pamoja nao, kisha akawaambia, nimeshawaitikia basi na nyie niitikieni, wakaitika wito wake na wakaondoka pamoja naye hadi nyumbani kwake, akamwambia mke wake Rabab toa ulichokiweka, akatoa aliyokuwa nayo miongoni mwa mali basi akawapa.13

2.

Na miongoni mwa ukarimu wake ni kwamba alimtembelea Usama bin Zaid katika maradhi yaliyopelekea kifo chake, alipofika kwake Usama alisema: “Aaah huzuni yangu.” Husain akamuuliza: “Ni nini huzuni yako?” Akasema: “Deni langu ambalo ni elfu sitini (60,000/=)” Husain akasema:

Rejea iliyotangulia uk: 16 Al- Qarashiy katika Hayaatu Imamil- Husain juzuu 1 uk: 125 akinukuu kutoka katika Tarikh IBnu Asaakir juzuu 13 uk: 54

13

10


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

“Basi hilo ni juu yangu mimi.” Usama akasema: “Naogopa kufariki kabla halijalipwa.” Basi Husain (as) akampa matumaini kwa kusema: “Hutokufa hadi nililipe badala yako.” Imam akajitolea na akalilipa badala yake kabla ya kufariki.14 3.

Na alikuwa ni kigezo katika uchamungu na ni mwenye kudumu katika daraja za ibada, siku moja mmoja wa wafuasi wake alimwambia: “Ni ukubwa ulioje wa hofu yako kwa Mola Wako?” Akasema (as): “Hatosalimika Siku ya Kiyama isipokuwa mwenye kumuogopa Mwenyezi Mungu duniani.”15 Na wakati wake mwingi alikuwa anautumia kwa Swala na Saumu. Na alisema juu yake Ibnu Zubair: “Ama Wallahi wamemuuwa mtu ambaye ni mwingi wa Swala usiku, na mwingi wa Saumu mchana.”16

Na alihiji Hija ishirini na tano kwa kutembea kwa miguu na sadaka zake zilikuwa zinatangulizwa mbele yake. 17Na alikuwa ni mwingi wa wema na sadaka, na alirithi ardhi na vitu, akavitoa sadaka kabla ya kuvipokea, na alikuwa anabeba chakula katika giza la usiku kuwapelekea maskini wa Madina.18 Maneno Yake ya Kimapinduzi: Katika mwanzo wa mapambano yake matukufu hadi kupata kwake shahada tukufu, katika matukio mbalimbali, aliuelekeza umma kwa maneno na hotuba zinazozingatiwa kuwa ni hazina kubwa na chemchem inayowapa wanamapinduzi na waungwana misimamo yake, Rejea iliyotangulia uk: 128 Rejea iliyotangulia uk: 133 16 Twabariy katika Tarikh al-Umamu wal-Muluk Jz. 6, uk: 273 chapa ya kwanza chapisho la al-Hasiniya Misri 17 Al- Qarashiy katika Hayaatul-Imamil-HusainJz. 1, uk: 134 18 Rejea iliyotangulia uk: 135 14 15

11


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

na inayoshibisha matakwa yao katika mapambano na mapigano. Na maneno hayo, hotuba na barua vinabainisha sababu zilizomwajibisha Imam Husain (as) kufanya mapinduzi yake, na malengo ambayo aliyakusudia katika harakati zake. Miongoni mwa maneno yake ni yale yaliyokuja katika wasia wake kwa ndugu yake Muhammad bin al-Hanafiya wakati wa kutoka Madina:

‫ وال‬،ً‫ وال مفسدا‬،ً‫إني لم أخرج أشراً وال بطرا‬ ‫ظالماً وإنما خرجت لطلب اإلصالح في أمة‬ ‫ أريد أن آمر بالمعروف وأنهى عن‬،‫جدي‬ ‫ وأسير بسيرة جدي وأبي علي بن أبي‬،‫المنكر‬ ‫ فاهلل أولى بالحق‬،‫ فمن قبلني بقبول الحق‬،‫طالب‬ ‫ومن رد علي أصبر حتى يقضي اهلل بيني وبين‬ ‫القوم وهو خير الحاكمين‬ “Hakika mimi sijatoka kwa shari wala kwa kiburi wala kwa kutaka ufisadi wala si kwa udhalimu, hakika nimetoka kwa ajili ya kufanya marekebisho katika umma wa babu yangu, nataka kuamrisha mema na kukataza maovu, na kwenda kwa mwenendo wa babu yangu na baba yangu Ali bin Abi Twalib, hivyo atakayenikubali kwa kuikubali haki basi Mwenyezi Mungu ni bora zaidi kwa haki, na atakayenikataa basi nitasubiri hadi Mwenyezi Mungu ahukumu baina yangu na baina ya kaumu Naye ni mbora zaidi wa kuhukumu.”19 19

Al- Qarashiy katika Hayaatul- Imamil Husain juzuu 2 uk: 264 12


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

Na alisema katika hotuba yake mbele ya jeshi la Bani Ummaya chini ya uongozi wa Hurr bin Yazid ar-Rayaahiy:

ً‫ «من رأى سلطانا‬:‫أيها الناس إن رسول اهلل قال‬ ً ‫ مخالفا‬،‫ ناكثاً لعهد اهلل‬،‫مستحال لحرم اهلل‬ ،ً‫جائرا‬ ‫ يعمل في عباد اهلل باإلثم‬،‫لسنة رسول اهلل‬ ً‫ فلم يغير ما عليه بفعل وال قول كان حقا‬،‫والعدوان‬ ‫على اهلل أن يدخله مدخله أال إن هؤالء قد لزموا‬ ‫ وأظهروا‬،‫ وتركوا طاعة الرحمن‬،‫طاعة الشيطان‬ ‫ وأحلوا‬،‫ واستأثروا بالفيء‬،‫ وعطلوا الحدود‬،‫الفساد‬ ‫ وأنا أحق من غير‬،‫ وحرموا حالله‬،‫حرام اهلل‬ “Enyi watu hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) amesema: ‘Yeyote atakayeiona serikali ovu inayohalalisha haramu ya Mwenyezi Mungu, yenye kutengua ahadi ya Mwenyezi Mungu, yenye kukhalifu sunna ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, yenye kuwafanyia waja wa Mwenyezi Mungu madhambi na uadui, na wala asibadilishe yaliyopo kwa vitendo wala kwa kauli, basi ni haki ya Mwenyezi Mungu kumwingiza motoni. Eee hakika hawa wameshikamana na kitendo cha kumtii shetani na wameachana na kitendo cha kumtii Mwenyezi Mungu, na wanadhihirisha ufisadi na wanavuka mipaka na wanakula mali, wanahalalilsha haramu ya Mwenyezi Mungu na wanaharamisha halali ya Mwenyezi Mungu, na mimi nina haki zaidi ya kufanya mageuzi kuliko mtu mwingine yeyote.”20 20

Rejea iliyotangulia uk: 80 13


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

Na alisema kuwahutubia wafuasi wake wakati wa kushuka Karbalaa:

‫ وإلى الباطل ال‬،‫أال ترون إلى الحق اليعمل به‬ ‫ ليرغب المؤمن في‬،‫يتناهى عنه‬ ‫ فاني ال أرى الموت إال سعادة والحياة‬،‫لقاء اهلل‬ ‫مع الظالمين إال برما‬ “Hivi hamuoni kuwa haki haifanyiwi kazi na batili haikatazwi, basi muumini na apende kukutana na Mwenyezi Mungu, hakika mimi sioni mauti isipokuwa ni utukufu na kuishi pamoja na madhalimu isipokuwa ni fedheha.”21

Na miongoni mwa hotuba zake kwa jeshi la Bani Ummaya kabla ya kuanza vita ni:

‫أال وإن الدعي ابن الدعي قد ركز بين اثنتين‬ ‫بين السلة والذلة وهيهات منا الذلة يأبى اهلل‬ ‫ وحجور طابت‬،‫لنا ذلك ورسوله والمؤمنون‬ ‫ من‬،‫ ونفوس أبية‬،‫وطهرت وأنوف حمية‬ ،‫أن يؤثر طاعة اللئام على مصارع الكرام‬ 21

Rejea iliyotangulia uk: 98 14


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

،‫أال وإني زاحف بهذه األسرة على قلة العدد‬ ....‫وخذالن الناصر‬ “Eee, hakika mtoto wa haramu atokanaye na mtoto wa haramu ametia mkazo wa kunitaka nichague moja kati ya mambo mawili, baina ya vita na udhalili, na ni mwiko kwetu kuchagua udhalili, Mwenyezi Mungu, Mtume wake na waumini wanakataa sisi kuchagua udhalili, na vilevile vizazi vitwaharifu, na pua zenye heshima, na nafsi takatifu, vyote vinakataa kuchagua kuwatii waovu badala ya kifo chenye utukufu. Eeee hakika mimi ni mwenye kuondoka pamoja na familia hii licha ya uchache wa idadi na usaliti wa msaidizi.”22

22

Rejea iliyotangulia uk: 193 15


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

MANENO KUTOKA KATIKA KITABU CHA MAPINDUZI Mazingira ya Utawala wa Bani Ummaya:

K

atika mwezi wa Jumad al-Awwal mwaka wa 41 Hijiria na baada ya suluhu ya Imam Hasan (as) yalitimia kwa Muawiya aliyokuwa anayataka na kuyaendea mbio, hivyo akawa khalifa na mtawala wa umma wote wa Kiislam. Na umma ukaingia katika mkondo wa utawala wa Bani Ummayya, ambapo misingi ya Uislamu na mifumo yake ikawa sio tena ni rejea na kipimo bali matakwa ya mtawala yakawa ndio dira na rejea, anafanya atakavyo na atakalo, na wala haingiliwi na idara nyingine na wala hathubutu yeyote kumpinga. Alianza kutekeleza mkakati wake wa kufyeka shakhisiya huru na tukufu za Kiislam, hivyo miongoni mwa wahanga wa mkakati huo alikuwa ni: Imam Hasan bin Ali (as) ambaye alipewa sumu, Hujur bin Udai swahaba mtukufu wa Mtume, Abdurahman bin Hasaan alGhanziy, Waswifiy bin Fasiyl Shaybaniy, Qabidhatu na Shariyk bin Shadad al Hadharamiy, Kadaam bin Hayaan al-Anziy, Muhriz bin Shihaab Tamimiy, Waafiy bin Haswin, Juwairiya bin Musahar alAbadiy na Abdillahi bin al-Hadharamiy. 23 Na wengineo miongoni mwa shakhisiya tukufu za umma zenye moyo safi. Kama ambavyo mtawala wa Bani Umayya alifanya kazi ya kuandaa mazingira ya jumla dhidi ya Ahlulbayt (as) na kumtukana Imam Ali bin Abi Twalib juu ya mimbari na katika kila hotuba ya Ijumaa, na akalazimisha hilo kwa watumishi wake na magavana wake na ilikuwa anayekataa miongoni mwao anamuuzulu, na sunna 23

aaqir Sharif al-Qarashiy – katika Hayaatul-Imami Hasan Jz. 2 uk: 358 – 385, rejea B maelezo yaliyotajwa na namna ya kuuliwa kwao. 16


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

hiyo ikabakia na kuendelea hadi zama ya Umar bin Abdul-Aziz ambapo aliamuru kuiondoa alipotawala mwaka 99 Hijiria, yaani amri ya kumtukana Ali (as) iliendelea zaidi ya nusu karne kuanzia mwaka 41 Hijiria hadi mwaka 99 Hijiria. Na kibano cha ukandamizaji kutoka kwa utawala wa Bani Ummayya kiliendelea dhidi ya Ahlulbayt (as) na wafuasi wake, Muawiya alituma agizo kwa watumishi wake na magavana wake akisema: “Angalieni ambaye utathibiti ushahidi juu yake kwamba anampenda Ali na Ahlulbayt wake basi mfuteni katika daftari la orodha ya mgao, na muondoeni katika kumpa pato lake na riziki yake.” Kisha akaongeza katika nakala nyingine: “Na ambaye mtamtuhumu kwa kuwapenda watu hawa basi mwadhibuni na vunjeni nyumba yake.” na Imam al-Baqir (as) amezungumzia yale yaliyotokea dhidi ya Ahlulbayt na wafuasi wao miongoni mwa matendo ya kukandamizwa na adha walizofanyiwa katika zama za Muawiya, anasema: “Na wakauliwa wafuasi wetu kila mji na ikakatwa mikono na miguu kwa dhana, ilikuwa kila anayetajwa kwa kutupenda na kutufuata anafungwa jela au anaporwa mali yake au inabomolewa nyumba yake.”24 Zaidi ya hapo ulidhihiri ufisadi na kwenda kinyume na mafunzo ya dini kama vile kufuta hukumu, kufanya uovu na dhulma, Muawiya kumuunganisha Ziyad bin Abiihi (kwa Abi Sufian), kuwa na ujasiri wa dhahiri katika kukhalifu hukumu za kisharia hata katika ibada kama vile kuanzisha adhana katika Swala ya Idd, hotuba kabla ya Swala ya Iddi, kuchukua Zaka katika zawadi, kujipaka manukato katika ihram, kutumia vyombo vya dhahabu na fedha, na kuvaa vazi la hariri. Na hali ya watu kiuchumi ikawa mbaya kwa sababu Muawiya aliwawekea wao kodi mbalimbali na alikuwa anajipendelea yeye na 24

Rejea iliyotangulia uk: 356 17


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

wale walio pembezoni mwake katika mali ya Waislamu inayopatikana, na Muawiya alikuwa anajiona ana haki ya kufanya atakavyo katika mali ya umma wakati ambapo mafakiri na wanyonge wanateketea kwa njaa na ukosefu. Na inanukuliwa kutoka kwake: “Ardhi ni ya Mwenyezi Mungu na mimi ni Khalifa wa Mwenyezi Mungu basi nilichokichukua katika mali ya Mwenyezi Mungu ni changu na nilichokiacha kilikuwa kinajuzu kwangu.”25 Na Ibnu Hajar ametaja kwamba imekuja katika sanadi ya watu wake wakweli kwamba: “Hakika Muawiya alihutubia siku ya Ijumaa akasema: ‘Hakika mali na ngawira ni vyetu hivyo tunampa tumtakaye na tunamnyima tumtakaye.’”26 Na katika kitabu Rabiul-Abraar amesema: “Muawiya alihutubia akasema: ‘Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

َّ‫َوإ ْن ِم ْن َش ْي ٍء إلاَّ ِع ْن َد َنا َخ َزا ِئنُ ُه َو َما نُ َن ِّزلُ ُه إلا‬ ِ ِ ِ ُ َ ‫وم‬ ٍ ‫ِبق َد ٍر َمعْل‬

‘Hakuna chochote ila hazina yake iko kwetu na wala hatukiteremshi, isipokuwa kwa kipimo maalum’”27 (Suratul-Hijr: 21).

Hivyo kwa nini mnanilaumu mimi ninapozembea katika kuwapa.”28 Kama ambavyo Muawiya aliutawalisha umma magavana waovu wagumu wa mioyo walioeneza hofu na vitisho na wakawatawala watu kigaidi na kwa mabavu, watu mfano Samratu bin Jundub ambaye Ziyad alimtumia kama naibu wake huko Basra, basi akafanya uhammad bin Aqiyl katika Naswaaihu al- kaafiyatu liman yatwalaa muaawiya – uk: M 131 – 134 chapa ya ya 1981 – Daaru Zahraa Beirut. 26 Rejea iliyotangulia 27 Rejea iliyotangulia 28 Rejea iliyotangulia 25

18


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

israfu katika kuwauwa watu wasio na hatia na kuteketeza nafsi bila ya haki. Amesimulia Muhammad bin Saliym amesema: “Nilimuuliza Ibnu Siriyn: Je, Samra alimuuwa yeyote? Anasi akasema kwa kuchemka na ghadhabu, akaanza kwa kusema: ‘Je, wanahesabika aliowauwa Samra bin Jundub? Ziyad alimtawalisha Basra na yeye akaenda zake Kufah, aliporudi alikuta ameshauwa watu elfu themanini, Ziyad akamwambia: Je, unakhofia kuwa inawezekana kuna yeyote uliyemuuwa bila hatia? Samra akamjibu: Kama ningeuwa kwao mfano wa hao (wenye hatia) nisingeogopa.”’29 Na miongoni mwa magavana wa Muawiya madhalim ni: Basri bin Artwat ambaye alimpeleka Yemen na akafanya humo vitendo viovu ambavyo historia haijashuhudia mfano wake katika uovu na ubabe, na wapokezi wametaja kwamba Basri bin Artwat aliuwa Waislamu elfu thelathini ukiachilia mbali aliowachoma kwa moto.30 Na miongoni mwa magavana hatari wa Muawiya na mwingi wao wa dhulma na uovu ni Ziyad bin Abiihi, Muawiya alimtawalisha Basra, Kufah, Sajastaani, Fursi na India. Hivi ndivyo ulivyoishi umma wa Kiislamu katika utawala wa Bani Umayya na kwa kurejea vitabu vyepesi tu vya historia mtu anaona picha ya dhulma mbaya ya kutisha ambayo waliifanya Bani Umayya katika historia ya utawala wao muovu. Yazid bin Muawiya awa Mtawala: Na ili kukamilisha mkakati wa kuhakikisha umma unarejea kwenye ujahiliya, Muawiya bin Abu Sufian alihitimisha maisha yake kwa kumtawalisha mwanae Yazid juu ya Umma, ili kwa hilo uanze ufalme muovu na utawala wa kurithiana wa kifamilia, kinyume na 29 30

Baaqi Sharaf al-Qashar - rejea iliyotangulia uk: 194 Rejea iliyotangulia uk: 199 19


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

utaratibu uliowekwa na Uislamu na hata na ule waliouzoea Waislamu. Yazid hakuwa na hata chembe ya sifa za utawala na ukhalifa, kwani alikuwa ni mpuuzi mpenda kuwinda, alikuwa anawavalisha bangili za dhahabu na mavazi yaliyotengenezwa kutokana na dhahabu wale mbwa wa kuwindia, na anampa kila mbwa mtumishi anayemwangalia kama ambavyo alikuwa anacheza na manyani. Na alikuwa na nyani aliyekuwa anamuweka mbele yake aliyempa jina la Abi Qubais, alikuwa anamnywesha kinachobakia katika kinywaji chake,31 kama ambavyo alikuwa ni mlevi wa pombe kupindukia.32 Katika kutaja kwake madhambi makubwa ya Muawiya, Hasan al-Basriy anasema: “Na kumtawalisha kwake mwanae mlevi wa kupindukia baada yake, aliyekuwa akivaa hariri na akipiga zumari.”33 Na masahaba wakubwa walimpinga Muawiya alipotaka mwanae Yazid apewe kiapo cha utii ili awe mrithi wake, pale alipoitisha kikao katika mji mtukufu wa Madina kwa lengo la kukusanya jopo miongoni mwa masahaba watukufu ili kuwaeleza raghaba yake ya kutaka kumteua mwanae Yazid kuwa mrithi wake, Ja’far bin Abi Twalib mume wa Bibi Zainabu akamkemea kwa kusema baada ya kumshukuru Mwenyezi Mungu na kumtukuza:

‫أما بعد فإن الخالفة إن أخذ فيها بالقرآن فأولوا‬ ‫ وإن‬،‫األرحام بعضهم أولى بعض في كتاب اهلل‬ ‫ وإن‬،‫أخذ فيها بسنة رسول اهلل فآل رسول اهلل‬ Rejea iliyotangulia uk: 182 Rejea iliyotangulia uk: 183 33 Rejea iliyotangulia 31 32

20


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

‫أخذ فيها بسنة الشيخين أبي بكر وعمر فأي‬ ‫الناس أفضل وأكمل بهذا األمر من آل الرسول؟‬ ‫وأيم اهلل لو ولوه بعد نبيهم لوضعوا األمر‬ ‫وعصي‬،‫ وألطيع الرحمن‬،‫موضعه لحقه وصدقه‬ ‫ فاتق اهلل‬،‫ ومااختلف في األمة سيفان‬،‫الشيطان‬ ‫يامعاوية فإنك قد صرت راعياً ونحن رعية‬ ........ً‫فانظر لرعيتك فإنك مسؤول عنها غدا‬ “Ama baada, hakika ukhalifa kama utachukuliwa katika Qur’ani basi jamaa wa karibu na ndugu wao ndio wanaostahiki zaidi katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na kama ukichukuliwa katika Sunna ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, basi ni jamaa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, na ukichukuliwa katika sira ya masheikh wawili Abu Bakar na Umar basi ni watu gani ni bora zaidi na wakamilifu kushinda kizazi cha Mtume? Wallahi kama wangelishika jambo hili baada ya Nabii wao wangeweka mambo katika sehemu yake kwa haki yake na ukweli wake, na angetiiwa Mwenyezi Mungu na kuasiwa shetani, na wala panga mbili zisingetofautiana katika umma, muogope Mwenyezi Mungu ewe Muawiya hakika wewe umeshakuwa mchungaji na sisi ni raia basi tazama raia wako, hakika wewe ni mwenye kuulizwa juu yao kesho….”34

Na akajitokeza Abdillahi bin Umar akasema: Shukurani ni za Mwenyezi Mungu na akamswalia Nabii wake, akasema:

34

Rejea iliyotangulia uk: 205 21


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

،‫فإن هذه الخالفة ليست بهرقلية و القيصرية‬ ‫وال كسراوية يتوارثها األبناء عن األباء ولو كان‬ ‫ فواهلل ما أدخلني‬،‫كذلك كنت القائم بها بعد أبي‬ ‫ إال على أن‬،‫مع الستة من أصحاب الشورى‬ ‫الخالفة ليست شرطاً مشروطاً وإنما هي في‬ ً ‫قريش خاصة لمن كان لها‬ ‫أهال ممن ارتضاه‬ ...‫المسلمون ألنفسهم ممن كان أتقى وأرضى‬ “Ama baada: Hakika ukhalifa huu sio wa Harqali wala sio wa Kisra wanaourithi watoto kutoka kwa baba zao, na kama ingekuwa hivyo basi ningeuchukua mimi baada ya baba yangu, Wallahi hakuniingiza pamoja na watu sita katika watu wa Shura, isipokuwa ukhalifa sio sharti lililoshurutishwa bali ni mahususi kwa Makuraishi kwa ambaye anastahiki miongoni mwa aliyeridhiwa na Waislamu kwa ajili ya nafsi zao kati ya ambao ni wachamungu na wenye kuridhiwa…”35

Na kwa madhumuni hayo hayo alizungumza Abdillahi bin Abbasi na Abdillahi bin Zubair isipokuwa upinzani wa hawa maswahaba na wengineo miongoni mwa wakuu wa umma haukuathiri katika azma na dhamira ya Muawiya ya kumuweka mwanawe kuwa mtawala baada yake, bali alichomoa silaha ya kitisho mbele ya wapinzani na akasema msemaji wa Muawaiya mbele ya waliohudhuria, naye ni Yazid bin al-Muqani’i: “Kiongozi wa Waislamu ni huyu.” Akaashiria kwa Muawaiya. “Na kama akifa basi kiongozi ni huyu.” 35

Rejea iliyotangulia uk: 207 22


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

Akaashiria kwa Yazid. “Na atakayekataa basi ni huu.” Akaashiria kwenye upanga wake.36 Na Muawiya alikufa katika mwezi wa Rajabu mwaka wa 60 Hijiria na mtoto wake Yazid akawa Khalifa na mtawala wa Waislamu. Husain (as) anapinga Kiapo cha utii: Yazid akamwandikia gavana wa Bani Umayya katika mji wa Madina, Walid bin Utba bin Abi Sufian akimtaka kuchukua kiapo cha utii kwa nguvu kutoka kwa masahaba wakubwa na miongoni mwao ni Imam Husain (as). Usiku wa manane Husain (as) aliitwa kwenye kikao na Walid na akatakiwa kutoa kiapo cha utii kwa Yazid, Imam akajibu: “Hakika aliye mfano wangu hatoi kiapo cha utii kwa siri wala hakichukuliwi kutoka kwangu kwa siri, utakapotoka mbele ya watu na kuwataka watoe kiapo cha utii, basi hapo ndipo utakaponiita na mimi pamoja nao na jambo letu litakuwa moja.” Walid akakubali maneno ya Imam Husain (as) lakini Mar’wan bin al-Hakam aliyekuwa amekaa pembeni mwa Walid akakataa aliyoyasema Husain (as) na akamtaka Walid amlazimishe Husain (as) atoe kiapo cha utii haraka. Na ili kujibu kitisho hiki, Imam Husain (as) alitangaza msimamo wake wa kupinga kutoa kiapo cha utii kwa Yazid kwa kusema:

‫أيها األمير إنا أهل بيت النبوة ومعدن الرسالة‬ ‫ ومحل الرحمة بنا فتح اهلل‬،‫ومختلف المالئكة‬ ‫ قاتل‬،‫ ويزيد رجل فاسق شارب الخمر‬،‫وبنا ختم‬ 36

Rejea iliyotangulia uk: 203 23


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

‫ معلن بالفسق ومثلي اليبايع مثله‬،‫النفس المحرمة‬ ‫ولكن نصبح وتصبحون وننظر وتنظرون أينا‬ ‫أحق بالخالفة والبيعة‬ “Ewe kiongozi hakika sisi ni Ahlulbayt wa Nabii na chimbuko la ujumbe, mahala pa kushukia malaika, sehemu ya rehema, kupitia kwetu Mwenyezi Mungu amefungua na kupitia kwetu amehitimisha, na Yazid ni mtu fasiki mnywa pombe, muuaji wa nafsi isiyo na hatia, mwenye kutangaza ufasiki hadharani, na mtu mfano wangu hampi kiapo cha utii aliye mfano wake, lakini tutaamka na mtaamka na tutatazama ni nani kati yetu ana haki zaidi ya ukhalifa na kupewa kiapo cha utii.”37

Husain anaondoka Madina: Imam Husain (as) aliondoka mji mtukufu wa Madina tarehe 28 Rajab mwaka 60 Hijiria kuelekea mji mtukufu wa Makka, hiyo ni baada ya kumwachia ndugu yake Muhammad bin al-Hanafiya wasia aliobainisha humo lengo la kutoka kwake na harakati zake, ambapo imekuja humo:

‫ وال‬،ً‫ وال مفسدا‬،ً‫إني لم أخرج أشراً وال بطرا‬ ‫ظالماً وإنما خرجت لطلب اإلصالح في أمة‬ ‫ أريد أن آمر بالمعروف وأنهى عن‬،‫جدي‬ 37

Rejea iliyotangulia uk: 255 24


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

‫ وأسير بسيرة جدي وأبي علي بن أبي‬،‫المنكر‬ ‫ فاهلل أولى بالحق‬،‫ فمن قبلني بقبول الحق‬،‫طالب‬ ‫ومن رد علي أصبر حتى يقضي اهلل بيني وبين‬ ‫القوم وهو خير الحاكمين‬ “Hakika mimi sijatoka kwa shari wala kwa kiburi wala kwa kutaka ufisadi wala si kwa udhalimu, hakika nimetoka kwa ajili ya kufanya marekebisho katika umma wa babu yangu, nataka kuamrisha mema na kukataza maovu, na kwenda kwa mwenendo wa babu yangu na baba yangu Ali bin Abi Twalib, hivyo atakayenikubali kwa kuikubali haki basi Mwenyezi Mungu ni bora zaidi kwa haki, na atakayenikataa basi nitasubiri hadi Mwenyezi Mungu ahukumu baina yangu na baina ya kaumu Naye ni Mbora zaidi wa kuhukumu.”38

Aliwasili Makka tarehe 3 Shaaban na akaanza kutangaza msimamo wake huko na kueleza rai yake kuhusu utawala wa Bani Umayya katika mkusanyiko wa Waislamu ambao waliwasili katika Nyumba tukufu kwa ajili ya Hija na Umra. Kama ambavyo Imam (as) pia alituma barua zake kwa wakuu wa Iraki huko Kufah na Basra akiwaeleza msimamo wake wa kupinga utawala wa Yazid na akiwataka wamuunge mkono na kumsaidia. Mwitikio wa Kufah: Mazingira ya mji wa Kufah yalikuwa yako tayari kwa mapinduzi dhidi ya utawala wa Bani Umayya, kwa hiyo watu wa Kufah walikubaliana na msimamo wa Imam Husain (as), na wakamtumia wa38

Rejea iliyotangulia uk: 264 25


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

jumbe na wakaandika maelfu ya barua wakitangaza kiapo chao cha utii kwake na utayari wao wa kumuunga mkono. Wanahistoria wanasema: Zilikusanyika kwake kwa nyakati tofauti barua elfu kumi na mbili na ikamfikia orodha ya majina 140,000 wakieleza dhamira na utayari wao katika kumsaidia na kumuunga mkono pindi atakapowasili Kufah, kama ambavyo zilipokewa kwake kwa siku moja barua mia sita.39 Ndipo Imam Husain (as) akamtuma kwao mtoto wa ami yake Muslim bin Aqiyl ili akaone uhalisia wa mazingira ya Kufah na achukue kiapo cha utii kutoka kwao kwa niaba ya Imam na aandae mambo kwa ajili ya ujio wa Imam. Muslim aliondoka Makka usiku wa nusu ya mwezi wa Ramadhan na alifika Kufah tarehe 5 ya mwezi wa Shawwal, ambapo alipokelewa na watu wake kwa furaha na bashasha, na watu wakajitokeza kumpa kiapo cha utii kama mwakilishi na balozi wa Imam Husain (as), akamwandikia Imam akimpa habari njema jinsi watu walivyomkubali na kumpa kiapo cha utii na akimhimiza kuharakisha kwenda Kufah. Lakini Mtawala wa Bani Umayya ambaye aliogopeshwa na uasi wa Kufah dhidi ya utawala wake aliharakisha kumuuzulu gavana wa Kufah Nu’uman bin Bishir kwa udhaifu wake katika kukabiliana na uasi, na Yazid bin Muawiya akamteua badala yake Ubaidullah bin Ziyad ambaye ni maarufu kwa ukatili wake na ubabe wake. Baada ya Ibn Ziyad kushika hatamu za ugavana wa Kufah akapanga kwa hila na ulaghai na akatumia mbinu kali za ukandamizaji na vitisho ili kumaliza uasi wa wafuasi wa Imam Husain (as), na matokeo yalikuwa ni kumkamata balozi wa Husain Muslim bin Aqiyl na kumnyonga mnamo tarehe 8 ya mwezi wa Dhulhija, yeye pamoja na wakuu wengine, na akalikamata na kulitia jela kundi kubwa la watu na wakuu wa Kufah na hatimaye kutangaza hali ya hatari. 39

Rejea iliyotangulia uk: 335 26


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

Kwenda Irak: Muslim bin Aqiyl alimwandikia barua Imam Husain (as) akimweleza kuhusu watu wa Kufah walivyokubali kuwa chini yake na kutoa kiapo chao cha utii kwake na shauku yao ya kuwasili kwake – hii ilikuwa ni kabla ya mabadiliko yaliyofuata baadae - Imam Husain (as) akaazimia kuondoka Makka kuelekea Irak, kwa sababu hakutaka Makka iwe ni uwanja wa mlipuko wa mapinduzi na mgongano dhidi ya utawala wa Bani Umayya, hiyo ni ili kuhifadhi utukufu wa Haram na amani yake, na kwa sababu watu wa Irak wamejiandaa zaidi kwa ajili ya mapinduzi kulingana na barua zao na mwitikio wao waliouonesha kwa balozi wa Husain (as). Aliondoka Makka siku ya Jumatatu ya mwezi wa Dhulhija mwaka 60 Hijiria, na wakati wa kuondoka ulikuwa na athari kwa mkusanyiko wa mahujaji na Waislamu ambao walikuwa wanajiandaa kwa ajili ya kutekeleza ibada ya Hija, kwa nini wanyimwe kuhiji pamoja na Imam? Imam katika safari yake alifuatana na idadi kubwa miongoni mwa watu wa nyumbani kwake wanaume na wanawake, na kundi kati ya wafuasi wake. Alipokuwa njiani katika moja ya sehemu zilimfikia Imam Husain (as) habari za mabadiliko hatari yaliyotokea katika mji wa Kufah na kwamba mji huo uko chini ya udhibiti wa Bani Umayya, na akapata pia habari za kuuliwa balozi wake Muslim bin Aqiyl. Ijapokuwa Imam (as) aliumizwa sana na yaliyotokea, isipokuwa aliazimia kuendelea na harakati zake na mwendo wake. Na utawala wa Bani Umayya ulipojua kwamba sasa Husain (as) anaelekea Irak, ulituma baadhi ya vikosi vya askari ili kumzuia Imam Husain (as) kuingia katika mji wa Kufah. Baada ya msafara wa Husain kuvuka sehemu inayoitwa Sharaf, walikutana na kikosi cha askari wa jeshi la Bani Umayya lenye 27


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

askari takriban elfu moja chini ya uongozi wa Hurr bin Rayahiy. Askari wa kikosi cha Hurr walikuwa wanakabiliwa na kiu kali sana kutokana na joto kali la jangwani, Imam akawaokoa kutokana na mauti yanayowakabili na akawapa wanayoyahitaji katika maji, kisha akaanza kuzungumza nao akiwaeleza sababu za kuja kwake Irak, lakini wao waling’ang’ania ajisalimishe kwao ili wampeleke kwa Ibn Ziyad gavana wa Bani Umayya huko Kufah, kama ambavyo hawakumruhusu kurejea alipotoka, wakaafikiana msafara wa Imam Husain (as) ufuate njia isiyomwingiza Kufah kama wanavyotaka wao wala isiyomrejesha Hijazi (Arabia) kama anavyotaka Imam. Karbalaa: Iliwasili kwa kiongozi wa kikosi cha Bani Umayya, Hurr bin Rayahiy barua kutoka kwa Ubaidullah bin Ziyad, inayomwamuru kumbakisha Imam Husain (as) katika jangwa na kutomlazimisha kuingia Kufah, amri iliyokuwa ni kinyume na uamuzi wake wa mwanzo, na huenda alifikiria kwamba kuingia kwa Husain Kufah kutasababisha mabadiliko yasiyotarajiwa na kupambana naye jangwani na mbali na watu ni bora zaidi. Na kutokana na amri hii mpya kikosi cha askari kikataka kuzuia msafara wa Imam (as) wakati ambapo Imam alikuwa anataka kuendelea na msafara, pamoja na kizuizi hicho na huku kukiwa na hali ya kuzozana walifika sehemu za pembezoni mwa mto Furati na ndipo Imam akauliza sehemu hiyo inaitwaje? Wakamwambia hakika sehemu hii ni Karbalaa, basi akaamuru watu wake wateremke hapo, kwani ni ardhi aliyoichagua Mwenyezi Mungu ili iwe uwanja na medani ya shahada yake na sehemu ya kaburi lake. Imam Husain (as) aliwasili Karbalaa siku ya pili ya Muharram mwaka 61 Hijiria.

28


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

Ashura: Jeshi la Bani Umayya lilisonga mbele kwa ajili ya kumzuia Husain (as) na wafuasi wake hapo Karbalaa, na wanahistoria wametofautiana kuhusu idadi ya jeshi lililokwenda Karbalaa, na huenda sahihi zaidi ni wapiganaji elfu 30,000.40 Wakati idadi ya wapiganaji wa Husain (as) haikuzidi watu themanini. Wakati ambapo utawala uliuzingira mji wa Kufah na ukatangaza hali ya hatari kwa watu wake, ili asipenye yeyote kwenda kujiunga na Imam Husain (as). Uongozi wa jeshi la Bani Umayya ulikuwa chini ya Umar bin Saad. Imam Husain alizungumza mara nyingi na jeshi la Bani Umayya lililokuja kumpiga vita ili kuwatambulisha nafsi yake na kuwaeleza sababu na malengo ya msimamo wake wa upinzani dhidi ya utawala wa Bani Umayya, na ili awaeleze ubaya wa hali ya maisha chini ya utawala wa Bani Umayya na jukumu la mapinduzi na kupinga dhulma yao na uovu wao. Lakini hotuba za Imam hazikuathiri isipokuwa idadi ndogo ya watu wachache kutoka katika jeshi kama vile Hurr bin Yazid Rayahiy, kiongozi wa kikosi cha askari ambao walikabiliana na Imam njiani, yeye aliathirika na msimamo wa Husain (as) na hotuba zake na akaasi jeshi lake na akajiunga na jeshi la Imam Husain (as). Na ili kutia kibano zaidi na kuongeza mbinyo wa kumzingira Imam Husain (as) na wafuasi wake, jeshi la Bani Umayya liliteka mto Furati na wakamzuia Husain (as), wafuasi wake na familia yake kufika kwenye maji, kuanzia siku ya saba ya Muharram. Ilipofika asubuhi ya siku ya kumi ya Muharram jeshi la Bani Umayya lilianza mashambulizi yake dhidi ya jeshi la Imam Husain (as), na hapo walijitokeza wafuasi wa Imam na wanaume katika familia yake ya Kihashimiya ili kumtetea Imam, familia yake na nafsi zao, na wakapigana kwa ushujaa mkubwa katika vita takatifu yenye 40

Rejea iliyotangulia uk: 122 29


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

kudumu, na wakajitoa muhanga kwa nia njema na safi, kwa namna ambayo historia haijaona mfano wake, na baada ya adhuhuri ya siku ya kumi ya Muharram wafuasi wote walikuwa wameshapata shahada na kusadikisha yale waliyomwahidi Mwenyezi Mungu, wakati ambapo Imam Husain (as) alibakia peke yake akipambana huku nyuma yake kukiwa kuna wake zake na watoto wake ambao wamebanwa na kiu, maumivu, huzuni na msiba, na wanasubiria mustakabali wa mateso baada ya kuwakosa mashujaa wao na walinzi wao. Imam alikabiliana na mapambano ya watu akawashambulia bila kujali wingi wa kundi lao, wala msiba na machungu havikudhoofisha azma yake na ushujaa wake hadi Mwenyezi Mungu aliporuhusu kukutana naye, hapo akaanguka akiwa shahidi katika jangwa la Karbalaa akiwa ametapakaa damu yake tukufu, huku akiwa ni shahidi wa jinsi umma ulivyopotosha ujumbe wa babu yake, lakini pia akawa amechora njia kwa ajili ya kizazi cha mapinduzi na mapambano kwa ajili ya kutetea msingi na utukufu. Jeshi dhalimu la Bani Umayya halikutosheka kwa kumuuwa Imam na wafuasi wake wote bali waliwauwa hata watoto wachanga kama vile kitoto kichanga Abdillahi bin Husain aliyekuwa chini ya umri wa mwaka mmoja, ambapo walimchinja akiwa katika kifua cha baba yake Husain (as), na hakusalimika katika jeshi la Imam Husain (as) isipokuwa mtoto wake Ali bin Husain Zainul-Abidin kwa sababu alikuwa ni mgonjwa mahututi. Maadui wakakusanya viwiliwili vitukufu vya Imam Husain (as) na wafuasi wake na wakakata vichwa vyao kisha wakakanyaga kanyaga mwili wa Imam Husain (as) kwa farasi wao na wakashambulia mahema ya wanawake wa Husain na watoto wake, wakayachoma kwa moto na wakapora vilivyokuwemo humo miongoni mwa vitu, na pia mapambo na mavazi waliyokuwa nayo wanawake na watoto. Jeshi ovu la Bani Umayya lilifanya kosa baya Karbalaa ambalo haisihi kulifanya hata kwa maadui makafiri 30


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

ukiachilia mbali kukifanyia kizazi cha Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww). Na kwa hiyo Karbalaa imekuwa ikiwakilisha huzuni mbaya kabisa katika historia ya binadamu, na wakati ule ule ni vita vitukufu mno ambavyo vimesajili ushujaa, namna ya kujitoa fidia na kujijengea uvumilivu. Msafara wa Mateka wa Kike: Na katika siku ya kumi na moja ya Muharram jeshi la Bani Umayya lilizika maiti zao wakati ambapo waliacha mwili mtukufu wa Imam Husain (as) pamoja na maiti za wafuasi wake katika jangwa la Karbalaa zikipulizwa na upepo bila ya kuzikwa. Kisha wakawachukua wake wa Husain na watoto wake mateka hadi mji wa Kufah wakitanguliwa na kichwa cha Husain na vichwa vya wafuasi wake ambavyo vilikuwa vimetundikwa juu ya ncha za mikuki. Idadi ya mateka wa kike ilikuwa kumi na tisa, walipandishwa juu ya ngamia wasizokuwa na matandiko na wakaswagwa kwa ubabe na mateso. Mateka waliingizwa mji wa Kufah siku ya kumi na mbili katika hali ya mwonekano wa furaha na bashasha ya madhalimu hao kujiona kuwa wameshinda dhidi ya Ahlulbayt (as). Na baada ya mateka kubakia siku kadhaa hali yakuwa wanakabiliwa na udhalili na mateso waliswagwa hadi Sham pamoja na vichwa vya mashahidi, ulikuwa ni msafara wenye kuchosha kwa wanawake hao na watoto yatima. Huko Sham walipata aina mbalimbali za mateso na udhalili, hususan katika baraza la muovu Yazid bin Muawiya. Pamoja na kwamba Damascus ilikuwa ni makao makuu ya Bani Umayya na mazingira yake yalikuwa yamesheheni chuki dhidi ya Ahlulbayt (as) isipokuwa mateso ya mateka wa kike na habari za Karbalaa na mazungumzo ya Imam Zainul-Abidin, Bibi Zainab na Bibi Ummu Kulthum yote hayo yaliacha athari chanya kwa watu wa 31


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

Sham na kutengeneza kundi la watu waliosimama kukataa na kupinga siasa ya Yazid bin Muawiya, na kutokana na kuhofia kukua kwa kundi hilo Yazid aliamuru mateka warejeshwe Madina kulingana na matakwa yao. Hivi ndivyo ulivyorejea Madina msafara wa mateka kwenda kumshitakia Mtume wa Mwenyezi Mungu yale ambayo yamewasibu na kutendewa miongoni mwa dhulma na mateso yasiyo na mfano katika historia.41 Kujitoa Muhanga na Fidia: Usiku ulitanda kwa giza lake, na utulivu wake ukatawala katika maisha, na giza lake likafunika sehemu zote, na katika giza totoro la usiku na utulivu wake wa kina Imam Husain bin Ali (as) alikwenda katika msikiti wa babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) ili kutekeleza nyiradi zake na kuswali sunna yake ya usiku, na ili apate faragha ya kuwa na nafsi yake tu na kutafakari matukio ya kijamii ambayo yamejitokeza katika umma. Muawiya bin Abi Sufian ameshahiliki baada ya miaka ishirini ya utawala ambao umma uliteseka sana, na huyu ni mtoto wake Yazid bin Muawiya anarukia kiti cha ukhalifa ili afungue uwanja wa utawala wa kurithiana na uongozi wa ukabila. Yazid huyu anaanza utawala wake kwa kiburi cha udikteta na kumwandikia gavana wa Madina: “Chukua kiapo cha utii kwa watu wote wa Madina na hususan kwa Husain bin Ali, na kama akikataa mkate shingo yake na tuma kichwa chake kwangu!!� Lakini bado watu wa umma wanaishi katika hali ya mshangao na woga hawajui watafanya nini na wataamiliana naye kwa namna gani. Husain (as) alikaa akitafakari katika matukio haya na juu ya mazingira haya yenye kutia uchungu, huku akijua kwamba kadhia inayofuata si jambo jepesi bali ni jambo gumu na hatari ambalo linatishia hatima ya Umma na mustakabali wa ujumbe. Na baada ya 41

Hasan Safar katika al-Maraatu al-Adhiymah fiy hayaati sayidati Zainab 32


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

kutafakari kwa kina na kutaamali kwa makini kwa muda, Husain (as) alisimama wima na akaelekea kibla kisha akaanza kuswali swala yake ili apate hekima kutoka kwa Mwenyezi Mungu na maelekezo ya sawa, nguvu na uvumilivu, na huku ndio kuamiliana na swala kwa njia sahihi, kwani swala sio kwa ajili ya kumaliza muda wa faragha wala sio ibada ya wavivu, Mwenyezi Mungu amewalaumu watu wenye kuswali ambao wanatekeleza swala kwa njia ya uvivu, hawajali wala hawazingatii:

َ ‫ُرا ُء‬ ‫ون‬ ‫َوإِ َذا َقا ُموا إِلَى الص‬ َ ‫َّلاَ ِة َقا ُموا ُك َسالَىٰ ي‬ َّ‫ون ه‬ َ ‫اس َولاَ َي ْذ ُك ُر‬ ‫اللَ إِلاَّ َقلِيل‬ َ َّ‫الن‬ “Na wanapoinuka kwenda kuswali, huinuka kivivu. Wanajionyesha kwa watu. Wala hawamtaji Mwenyezi Mungu ila kidogo tu.” (Sura Nisaa: 142).

Bali swala ni kiunganishi baina ya mja na Mola Wake ili apate hekima katika vitendo vyake na unyoofu katika misimamo yake, na ili mja atumie swala hiyo kumwahidi Mola Wake kwa ikhilasi na msimamo. Husain (as) alimaliza swala yake na nyuradi zake kisha akamwelekea Mwenyezi kwa dua hali ya kunyenyekea na kuhofu, akasema:

‫اللهم إن هذا قبر نبيك محمد وأنا ابن بنت نبيك‬ ‫ اللهم‬.‫ وقد حضرني من األمر ما قد علمت‬. ‫ وأنا أسألك يا‬.‫إني أحب المعروف وأنكر المنكر‬ 33


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

‫ذا الجالل واإلكرام بحق هذا القبر ومن فيه اال‬ ‫اخترت لي ما هو لك رضى ولرسولك رضى‬ “Eee Mwenyezi Mungu hakika hili ni kaburi la Nabii wako Muhammad (saww) na mimi ni mtoto wa binti ya Nabii wako, na yamenijia mambo ambayo unayajua. Eee Mwenyezi Mungu hakika mimi napenda mema na nachukia maovu. Na mimi nakuomba Ewe Mwenye utukufu na enzi kwa haki ya kaburi hili na aliyemo ndani yake, nichagulie ambalo lina ridhaa Yako na ridhaa ya Mtume Wako.”42

Kisha akalia hapo katika kaburi hadi ilipokaribia asubuhi, akaweka kichwa chake juu ya kaburi na mara akapitiwa na usingizi, na ndipo akamuona Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) usingizini akimkumbatia katika kifua chake na akimbusu baina ya macho yake huku akisema: Kipenzi changu, ewe Husain si muda mrefu nitakuona jangwani ukiwa umetapakaa damu yako, umechinjwa na waovu zaidi katika umma wangu katika ardhi ya Karbalaa, na pamoja na hayo utakuwa na kiu kali na wala hutapewa maji, utahitajia maji na wala hutapewa maji, na wao pamoja na hayo wataendelea kutaraji uombezi wangu. Hapana Mwenyezi Mungu hatawapa uombezi wangu Siku ya Kiyama.

‫الى‬ ّ ‫حبيبي يا حسين إن اباك وامك واخاك قدموا‬ ‫ وأن لك في الجنة درجات لن‬.‫وهم مشتاقون إليك‬ ‫تنالها إال بالشهادة‬ 42

Al- Muqarram katika Maqtalul-Husain uk: 133 34


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

“Kipenzi changu ewe Husain hakika baba yako, mama yako na kaka yako wamekuja kwangu nao wana hamu ya kuwa pamoja na wewe, na hakika wewe una daraja peponi, ambazo hutozipata isipokuwa kwa shahada.�43

Hakika hadithi hii inatufunulia wazi siri ya ndani ambayo wengi wenye kushangazwa na shakhisiya ya Husain (as) yenye kudumu hujaribu kuitafuta siri hiyo. Pamoja na kupita miaka mingi, kupita karne nyingi na kupita vizazi vingi lakini bado shakhisiya ya Husain (as) inaendelea kudhihiri kila siku kana kwamba ni shakhisiya ya wakati huu na ya sasa, na kadhia yake inajitokeza kana kwamba ni tukio la sasa hivi. Kwa nini Mazingatio yote haya kwa Husain Misafara ya wenye kuzuru inakwenda katika kaburi lake na inapata utukufu wa kuzuru kaburi lake, na washairi na makhatibu vizazi kwa vizazi bado wangali wanakamua na kujitolea vipaji vyao katika kuzungumzia mapinduzi yake matukufu, na umma ungali unaadhimisha kumbukumbu ya mapinduzi yake na kufanya ni msimu wa kidini ambao humo wanapokea mafunzo ya uelewa na kutafiti misingi ya dini. Lakini cha kujiuliza kwa mara nyingine ni kwa nini kuwepo na mazingatio yote haya na umuhimu wote huu kwenye shakhsiya ya Imam Husain (as)? Je, ni kwa sababu ya sifa ya kimwili au ni kwa sababu ya nasaba yake? - Hapana!!

43

Al- Muqarram katika Hayatul-Imam Husain Jz. 2 uk: 260 35


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

Kwa nini Imam Husain amepata Mazingatio yote haya? Hakika mazungumzo yaliyotangulia yanatupa jibu la wazi juu ya swali hili pana ambalo linajitokeza kwetu lenyewe. Mtukufu Mtume (saww) anamwambia wazi:

‫الى‬ ّ ‫حبيبي يا حسين إن اباك وامك واخاك قدموا‬ ‫ وأن لك في الجنة درجات لن‬.‫وهم مشتاقون إليك‬ ‫تنالها إال بالشهادة‬ “Kipenzi changu ewe Husain hakika baba yako, mama yako na kaka yako wamekuja kwangu nao wana hamu ya kuwa pamoja na wewe, na hakika wewe una daraja peponi, ambazo hutozipata isipokuwa kwa shahada.”

Na Imam Husain alikufa shahidi na akapata daraja hizo na utukufu wake duniani ni moja kati ya daraja hizo, kama utafasiri utukufu wa Husain kuwa ni shahada yake na kujitolea kwake. Na hebu sasa acha tutilie mkazo mazungumzo yetu katika mistari hii upande huu wa maisha ya Husain (as) na ambayo ndio siri ya utukufu wake na cheo chake.

36


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

Upande wa Kujitoa Muhanga na Kutoa Katika njia ya Mwenyezi Mungu:

H

akika kujitoa muhanga katika njia ya Mwenyezi Mungu ni kitu kizuri na kitukufu ambacho hakikaribiwi na kitendo au amali yoyote, na heshima ya Mwenyezi Mungu Mtukufu anayoitoa kwa kitendo cha kujitoa muhanga na kwa wenye kujitoa muhanga hailinganishwi na heshima yoyote. Hii hapa Qur’ani tukufu inasema:

َّ‫إ َّن ه‬ ْ َ‫الل‬ َ ‫اش َت َرىٰ ِم َن ْال ُم ْؤ ِم ِن‬ ‫ين أَ ْن ُف َس ُه ْم َوأَ ْم َوالَ ُه ْم ِبأَ َّن‬ ِ ُ ُ ُ ْ َّ‫ه‬ ْ ْ َ َ ُ َ َ َ ‫ون َويُق َتل‬ َ ‫يل اللِ ف َيقتل‬ َ ‫ل ُه ُم ال َجنَّة يُقا ِتل‬ ‫ون‬ ِ ‫ون ِفي َس ِب‬ ُ ْ ِ ‫َو ْع ًدا َعلَ ْي ِه َح ًّقا ِفي التَّ ْو َرا ِة َوالإْ ْنج‬ ‫آن‬ ِ ِ ِ ‫يل َوالق ْر‬ َّ َّ‫َو َم ْن أَ ْو َفىٰ ب َع ْه ِد ِه ِم َن ه‬ ‫ْش ُروا ِب َب ْي ِع ُك ُم ال ِذي‬ ْ ‫اللِ َف‬ ِ ‫اس َتب‬ ِ ْ ْ َ ‫َبا َيعْتُ ْم ِب ِه َو َ ٰذلِك ُه َو ال َف ْو ُز ال َع ِظي ُم‬ “Hakika Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwamba wao wapate Pepo, wanapigana katika njia ya Mwenyezi Mungu, kwa hiyo wanaua na kuuawa. Ni ahadi aliyojilazimisha kwa haki katika Tawrat na Injil na Qur’ani. Na ni nani atekelezaye zaidi ahadi kuliko Mwenyezi Mungu? Basi furahini kwa biashara yenu mliofanya naye. Na huko ndiko kufuzu kukubwa.” (Sura Tawba: 111).

37


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

ْ ‫ون ِم َن ْالم‬ َ ‫ُؤ ِم ِن‬ َ ‫اع ُد‬ ‫ْر أُولِي‬ ُ ‫ين َغي‬ ِ ‫لاَ َي ْس َت ِوي ْال َق‬ َّ‫ون ِفي َسبيل ه‬ َّ َ ‫اه ُد‬ ‫اللِ ِبأَ ْم َوالِ ِه ْم‬ َ ‫الض َر ِر َو ْالم‬ ِ ‫ُج‬ ِ ِ َّ ‫َوأَ ْن ُف ِس ِه ْم َف‬ َ ‫اه ِد‬ ‫ين ِبأَ ْم َوالِ ِه ْم َوأَ ْن ُف ِس ِه ْم‬ َ ‫ض َل اللهَُّ ْالم‬ ِ ‫ُج‬ َّ ‫ين َد َر َج ًة َوكُلاًّ َو َع َد اللهَُّ ْال ُح ْس َنىٰ َو َف‬ َ ‫اع ِد‬ ‫ض َل‬ ِ ‫َعلَى ْال َق‬ َ ‫اع ِد‬ َ ‫اه ِد‬ ‫ات‬ ٍ ‫ين أَ ْج ًرا َع ِظيمًا َد َر َج‬ َ ‫اللهَُّ ْالم‬ ِ ‫ين َعلَى ْال َق‬ ِ ‫ُج‬ َ ‫ِم ْن ُه َو َم ْغ ِف َر ًة َو َر ْح َم ًة َو َك‬ ‫ورا َر ِحيمًا‬ ً ‫ان اللهَُّ َغ ُف‬ “Hawawi sawa waumini waliokaa wasiokuwa wenye madhara na wenye kupigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali zao na nafsi zao. Amewatukuza Mwenyezi Mungu katika cheo wale wapiganao katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali zao na nafsi zao kuliko waliokaa. Na wote Mwenyezi Mungu amewaahidi wema. Na amewatukuza Mwenyezi Mungu wenye kupigana Jihadi kwa malipo makubwa kuliko waliokaa. Ni vyeo kutoka Kwake na maghufira na rehema. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira Mwenye kurehemu.” (Sura Nisaa: 95 – 96).

َّ‫َيا أَُّي َها ال‬ ُ ‫ار ٍة تُ ْنج‬ َ‫ين آ َمنُوا َه ْل أَ ُدلُّ ُك ْم َعل‬ َ ‫يك ْم ِم ْن‬ ‫ج‬ ‫ت‬ ‫ى‬ ٰ ‫ذ‬ َ َ ِ ِ ِ َ‫َع َذاب أ‬ َّ‫ون ب ه‬ َ ‫اه ُد‬ ‫ون ِفي‬ ‫ل‬ ِ ِ ‫اللِ َو َر ُسولِ ِه َوتُ َج‬ ِ َ ُ‫يم تُ ْؤ ِمن‬ ٍ ٍ َّ‫َسبيل ه‬ ‫ْر لَ ُك ْم إِ ْن ُك ْنتُ ْم‬ ٌ ‫اللِ ِبأَ ْم َوالِ ُك ْم َوأَ ْن ُف ِس ُك ْم َذٰلِ ُك ْم َخي‬ ِ ِ َ ‫َتعْلَم‬ ‫ُون‬ 38


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

“Enyi mlioamini! Je, niwajulishe biashara itakayowaokoa na adhabu iliyo chungu? Mwaminini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na piganeni Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali zenu na nafsi zenu. Haya ni bora kwenu, ikiwa nyinyi mnajua.” (Sura Swaf: 10 – 11).

Na amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww):

‫بر بر حتى يقتل في سبيل اهلل فإذا‬ ٍ ‫فوق كل ذي‬ ‫قتل في سبيل اهلل فليس فوقه بر‬ “Juu ya kila mwema kuna mwema hadi auliwe katika njia ya Mwenyezi Mungu, basi hapo hakutakuwa tena na mwema juu yake.»44

Lakini je, kila mwanadamu anapata tawfiki ya kujitoa muhanga katika njia ya Mwenyezi Mungu? - Hapana!! Ni watu wangapi huwa wanatamani kujitoa muhanga na wanakodolea macho jambo hilo na huwa wana raghaba kubwa ya kufanya hivyo, lakini unapowadia wakati wake hawapati tawfiki ya kutimiza hilo. Je mmesikia kisa cha yule mwanaume ambaye alikuwa anakariri na kutaja kila wakati jina la Husain: “Tunatamani tungekuwa pamoja na nyinyi na sisi tukafaulu kufaulu kukubwa.” Usiku mmoja aliona usingizini kana kwamba amehudhuria katika uwanja wa Karbalaa na ni siku ya Ashura, Husain (as) akamtaka asonge mbele katika vita kutokana na raghaba yake ya kufa shahidi na shauku yake ya kujitoa muhanga kama alivyokuwa anakariri kwa ulimi wake. Lakini alitoa udhuru na alijaribu kujinasua na msimamo mgumu kwa sababu nafsi yake haikuwa tayari kwa ajili ya vita na kujitoa muhanga. Mwisho hau44

Al- Hurrul-A’amiliy katika Wasaailu Shi’a, Jz. 11 uk: 10 39


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

kumuokoa isipokuwa wito wa Bibi Zainab kwa ndugu yake Husain (as), na Husain alipogeuza uso wake upande wa dada yake Zainab akajinasua kwa kukimbia. Alipozinduka kutoka usingizini hali ni mwenye fazaa mwenye kulia na mwenye kuhuzunika, mke wake akamuuliza, akamsimulia kisa, akamwambia: Na kwa nini unahuzunika kwa jambo ulilokuwa unalitamani? Akajibu: Mshukuru Mwenyezi Mungu na mtaje Bibi Zainab kwa kheri nyingi, kama sio yeye tungetumbukia kwenye balaa sitini!! Na Qur’ani tukufu inatusimulia juu ya mifano ya aina hii, ya watu waliokuwa wanatamani shahada na kujitoa muhanga lakini wao hawakuandaa nafsi zao kwa ajili ya hilo na hatima yao ilikuwa ni kukimbia na kushindwa, na katika hilo kuna aibu katika dunia na adhabu kesho akhera. Anasema Mwenyezi Mungu (swt):

َ ‫أَلَ ْم َت َر إلَى ْال َم إَل ِم ْن َب ِني إ ْس َرا ِئ‬ ٰ ‫وس‬ ‫ى‬ َ ‫يل ِم ْن َب ْع ِد ُم‬ ِ ِ ِ َّ‫إ ْذ َقالُوا لَِنب ٍّي لَ ُه ُم ا ْب َع ْث لَ​َنا َملِ ًكا نُ َقا ِت ْل ِفي َسبيل اللِه‬ ِ ِ ِ ِ َ ُ ‫ْك ُم ْال ِق َت‬ ُ ‫ال َه ْل َع َسيْتُ ْم إ ْن ُك ِت َب َعلَي‬ َ ‫َق‬ ‫ال ألاَّ تُ َقا ِتلُوا‬ ِ َّ‫َقالُوا َو َما لَ​َنا أَلاَّ نُ َقا ِت َل ِفي َسبيل ه‬ ‫اللِ َو َق ْد أُ ْخ ِر ْج َنا‬ ِ ِ ُ ‫ِم ْن ِد َيار َنا َوأَ ْب َنا ِئ َنا َفلَ َّما ُك ِت َب َعلَيْه ُم ْال ِق َت‬ ‫ال َت َولَّ ْوا‬ ِ ِ َّ َُّ‫ه‬ َ ‫إِلاَّ َقلِيلاً ِم ْن ُه ْم َوالل َعلِي ٌم ِبالظالِ ِم‬ ‫ين‬ “Je, Hukuona wakubwa wa wana wa Israil baada ya Musa walipomwambia Nabii wao: Tuwekee mfalme ili tupigane katika njia ya Mwenyezi Mungu. (Mtume wao) akasema: Je, haielekei kuwa hamtapigana mtakapoandikiwa kupigana? Wakasema: Itakuwaje 40


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

tusipigane katika njia ya Mwenyezi Mungu na hali tumetolewa nje ya majumba yetu na watoto wetu? Walipoandikiwa kupigana, wakageuka isipokuwa wachache miongoni mwao. Na Mwenyezi Mungu anawajua madhalimu.” (Sura al-Baqarah: 246).

َ ‫ين ِق‬ َ ‫أَلَ ْم َت َر إِلَى الَّ ِذ‬ ‫يل لَ ُه ْم ُك ُّفوا أَ ْي ِد َي ُك ْم َوأَ ِقي ُموا‬ ُ ‫الز َكا َة َفلَ َّما ُك ِت َب َعلَيْه ُم ْال ِق َت‬ َّ ‫َّلاَ َة َوآتُوا‬ ‫ال إِ َذا‬ ‫الص‬ ِ َّ‫اس َك َخ ْش َي ِة ه‬ ٌ ‫َفر‬ ‫اللِ أَ ْو أَ َش َّد‬ َ َّ‫يق ِم ْن ُه ْم َي ْخ َش ْو َن الن‬ ِ َ ‫ْت َعلَ ْي َنا ْال ِق َت‬ َ‫ال لَ ْولا‬ َ ‫َخ ْش َي ًة َو َقالُوا َربَّ َنا لِ َم َك َتب‬ َ َ ٌ ِ‫الد ْن َيا َقل‬ ُّ ‫اع‬ ُ ‫يب ُق ْل َم َت‬ ‫يل‬ ٍ ‫أ َّخ ْر َت َنا إِلَىٰ أ َج ٍل َق ِر‬ ً‫ون َف ِتيلا‬ َ ‫ْر لِ َم ِن اتَّ َقىٰ َولاَ تُ ْظلَ ُم‬ ٌ ‫َو آْال ِخ َر ُة َخي‬ “Je, huwaoni wale ambao wameambiwa: Zuieni mikono yenu, na msimamishe Swala na mtoe Zaka. Walipolazimishwa kupigana, mara kundi moja katika wao wakawaogopa watu kama kumwogopa Mwenyezi Mungu au kwa hofu zaidi; na wakasema: Ewe Mola Wetu! Kwa nini ukatufaradhia vita? Laiti ungetuahirishia muda mchache! Waambie: Starehe ya duniani ni chache, na Akhera ni bora kwa wenye takua; wala hamtadhulumiwa hata uzi wa kokwa ya tende.» (Sura Nisaa: 77).

Sasa ni vipi mwanadamu muumini ataiandaa nafsi yake kwa ajili ya kujitoa mhanga katika njia ya Mwenyezi Mungu, ili matakwa yake yasimfanyie khiyana wakati inapohitajika kujitoa muhanga? Kutokana na maisha ya Imam Husain (as) na kwa kufaidika na mwanga wa kujitoa kwake muhanga mtukufu tunaweza kupanga 41


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

njia za kuiandaa nafsi na kuilea katika kujitoa muhanga na kujitoa fidia kwa kufuata mambo yafuatayo: 1. Kupambana daima na bila kusita, na matamanio ya kinafsi na ushawishi wa kimaada, kwa sababu kujitoa muhanga kunahitaji maamuzi ya uhakika ndani ya nafsi ya mwanadamu, na matamanio ya mwanadamu na raghaba zake huwa vinamwelekeza kwenye raha, starehe na matamanio, na hivyo wakati wa kujitoa muhanga hujitokeza mapambano makali na ya nguvu baina ya vishawishi vya matamanio na starehe, na baina ya raghaba ya kujitoa muhanaga, ikiwa mwanadamu hatakuwa amezoa kupambana na utashi wa raha na raghaba za kinafsi, kamwe hataweza wakati huo kuzishinda. Ili kuelezea ukweli huu Amirul-Muuminina Ali bin Abi Twalib (as) anasema:

‫ميدانكم األول أنفسكم إن قدرتم عليها كنتم على‬ ‫ وإن عجزتم عنها كنتم على غيرها‬،‫غيرها أقدر‬ ‫أعجز‬ “Medani yenu ya kwanza ni nafsi zenu; kama mtaziweza, na mengine mtayaweza zaidi na mkishindwa basi na mengine mtayashindwa kabisa.”

Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) anazingatia jihadi dhidi ya nafsi ni kazi ngumu zaidi kuliko jihadi ya kumpiga adui, kwa sababu jihadi dhidi ya nafsi ndio njia ya kwenda huko. Anasema Imam Ali (as), hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alituma kikosi, na kiliporejea akasema: “Karibuni, watu waliomaliza jihadi ndogo na imebakia kwao jihadi kubwa.” Ikasemwa: Ewe Mtume wa Mwe42


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

nyezi Mungu na ni ipi jihadi kubwa: Akasema: “Jihadi dhidi ya nafsi ni jihadi bora zaidi, jihadi ya yule mwenye kupigana dhidi ya nafsi yake ambayo iko baina yake.”45 Na kutokana na haya hakika Uislamu unatilia mkazo sehemu hii na unaona kwamba kupiga vita kasoro za nafsi na kusafisha mitazamo mbalimbali ndani ya mwanadamu na kupanda dhana ya jihadi na mapambano katika roho ya mtu, kitendo hiki ni jihadi kubwa nayo ndio inayomfanya mwanadamu kuwa katika maandalizi kamili ya kupigana jihadi na kujitoa muhanga na kujitoa fidia wakati wote na kila inapohitajia hivyo. Na kutokana na haya pia Imam Husain (as) alipigana na kupambana na ushawishi aliotangaziwa na Bani Umayya ili aachane na njia ya jihadi na kujitoa muhanga. Walimshawishi kwamba kama ataachana na msimamo wake wa kupigana jihadi kwa ajili ya dini watamtunuku mambo kadhaa. Walimshawishi kwa mali na cheo na wakampambia hali ya kujisalimisha kwao na kuwa laini mbele ya matwaghuti na madhalimu, lakini yeye alikataa kujisalimisha kwa ushawishi wa kimaada kwani walimwambia siku ya ashura: “Ewe Husain kuwa chini ya utawala wa watoto wa ami yako, hakika wao hawatakuonyesha isipokuwa unayoyapenda na hautakufikia ubaya kutoka kwao.” Akasema: “Hapana wallahi sitowapa mkono wangu kwa udhalili wala sintokimbia kama wanavyokimbia watumwa.”46 2.

45 46

Kuishibisha nafsi kwa utamaduni wa kidini na uelewa: Ambao unamwaandaa mwanadamu katika kujitoa muhanga na kujitolea, na kumpa shauku ya kujitoa muhanga na kujitoa fidia katika njia ya Mwenyezi Mungu, kama vile kuishibisha

Al- Hurrul-A’amiliy katika Wasailu Shi’a Jz. 11, uk: 124 Al- Muqarram katika Maqtalul- Husain uk: 229 43


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

aya za Qur’ani ambazo zinamuweka mwanadamu mbele ya majukumu yake ya kijamii na kumsukuma katika kubeba majukumu hayo kwa thamani yoyote ile itakayomgharimu, kama vile kauli yake (swt):

َ ‫َولاَ َت ِهنُوا ِفي ا ْب ِت َغا ِء ْال َق ْو ِم إِ ْن َت ُكونُوا َت ْألَ ُم‬ ‫ون‬ َّ‫ون ِم َن ه‬ َ‫اللِ َما لا‬ َ ‫ون َو َت ْر ُج‬ َ ‫ون َك َما َت ْألَ ُم‬ َ ‫َفإِنَّ ُه ْم َي ْألَ ُم‬ َ ‫ون َو َك‬ َ ‫َي ْر ُج‬ ‫ان اللهَُّ َعلِي ًما َح ِكي ًما‬ “Wala msilegee katika kuwafuatia hao watu. Ikiwa mnaumia basi na wao wanaumia kama mnavyoumia nyinyi. Na nyinyi mwataraji kwa Mwenyezi Mungu ambayo wao hawayataraji. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye hekima.” (Sura Nisaa: 104).

َ ‫ين آ َمنُوا َما لَ ُك ْم إ َذا ِق‬ َ ‫َيا أَُّي َها الَّ ِذ‬ ‫يل لَ ُك ُم ا ْن ِف ُروا ِفي‬ ِ ْ‫لأ‬ َ ‫اللِ اثَّ َاق ْلتُ ْم إلَى ا‬ َّ‫َسبيل ه‬ ‫ضيتُ ْم ِب ْال َح َيا ِة‬ ‫ر‬ ْ ِ ‫ض أَ َر‬ ِ ِ ِ ِ ْ‫آ‬ ْ‫آ‬ ْ ُّ ‫اع ال َح َيا ِة‬ ُّ ُ ‫الد ْن َيا ِم َن ال ِخ َر ِة َف َما َم َت‬ ‫الد ْن َيا ِفي ال ِخ َر ِة‬ ٌ ِ‫إلاَّ َقل‬ ُ ‫يل إلاَّ َت ْن ِف ُروا يُ َع ِّذب‬ ‫ْك ْم َع َذابًا أَلِي ًما َو َي ْس َت ْب ِد ْل‬ ِ ِ ِّ‫ض ُّرو ُه َشي ًْئا َواللهَُّ َعلَىٰ ُكل‬ ُ َ َ‫لا‬ ُ ‫ْرك ْم َو َت‬ َ ‫ق ْو ًما َغي‬ ‫ير‬ ٌ ‫َش ْي ٍء َق ِد‬ 44


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

“Enyi mlioamini! Mna nini mnapoambiwa nendeni katika njia ya Mwenyezi Mungu mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na Akhera ni kidogo tu. Kama hamwendi atawaadhibu kwa adhabu iumizayo na atawaleta watu wengine badala yenu, na hamtamdhuru chochote; Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu.” (Sura Tawba: 38 - 39).

‫اه ُدوا ِبأَ ْم َوالِ ُك ْم َوأَ ْن ُف ِس ُك ْم‬ ِ ‫ا ْن ِف ُروا ِخ َف ًافا َو ِث َقالاً َو َج‬ َّ‫ِفي َسبيل ه‬ َ ‫ْر لَ ُك ْم إِ ْن ُك ْنتُ ْم َتعْلَ ُم‬ ‫ون‬ ٌ ‫اللِ َ ٰذلِ ُك ْم َخي‬ ِ ِ “Nendeni mkiwa wepesi na wazito, na mpigane jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali zenu na nafsi zenu. Hilo ni kheri kwenu mkiwa mnajua.» (Sura Tawba: 41).

Hakika kuisoma Qur’ani na kutafakari katika aya zake kunampa mwanadamu moyo wa ikhlasi na msukumo kwa ajili ya jihadi na kujitoa muhanga, hivyo ni juu ya mwanadamu kuzidisha juhudi katika kuisoma Qur’ani na kujiongezea usafi na juhudi kutokana na aya zake tukufu, kwa kujiongezea nuru na uoni katika maisha na kuchukua kutoka ndani yake moyo wa imani na jihadi. Mfano kauli yake (swt):

َ ‫الَّ ِذ‬ ُ ‫ين َقالُوا لإِ​ِ ْخ َوا ِن ِه ْم َو َق َع ُدوا لَ ْو أَ َط‬ ‫اعو َنا َما‬ ‫ُق ِتلُوا ُق ْل َفا ْد َر ُءوا َع ْن أَ ْن ُف ِس ُك ُم ْال َم ْو َت إِ ْن ُك ْنتُ ْم‬ َّ‫ين ُق ِتلُوا ِفي َسبيل ه‬ َ ‫ين َولاَ َت ْح َس َب َّن الَّ ِذ‬ َ ‫صا ِد ِق‬ َ ِ‫الل‬ ِ ِ 45


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

َ ْ ً َ َ ‫ون َف ِر ِح‬ َ ‫ُر َز ُق‬ ‫ين‬ ْ ‫ِّه ْم ي‬ ِ ‫أ ْم َواتا َبل أ ْح َيا ٌء ِع ْن َد َرب‬ ْ ‫اه ُم اللهَُّ ِم ْن َف‬ ُ ‫ِب َما آ َت‬ َ ‫ون ِبالَّ ِذ‬ َ ‫ْش ُر‬ ‫ين لَ ْم‬ ِ ‫ضلِ ِه َو َي ْس َتب‬ َ‫ف َعل‬ ٌ ‫َي ْل َح ُقوا به ْم ِم ْن َخ ْل ِفه ْم أَلاَّ َخ ْو‬ ‫ْه ْم َولاَ ُه ْم‬ ‫ي‬ ِ ِ ِ​ِ َ َّ‫ه‬ ْ ‫ون ِب ِن ْع َم ٍة ِم َن اللِ َو َف‬ َ ‫ْش ُر‬ َ ُ‫َي ْح َزن‬ ‫ض ٍل َوأ َّن‬ ِ ‫ون َي ْس َتب‬ َّ‫ه‬ َ ‫ين الَّ ِذ‬ َ ‫يع أَ ْج َر ْال ُم ْؤ ِم ِن‬ ُ ‫ُض‬ ْ ‫ين‬ َِّ‫اس َت َجابُوا للِه‬ ِ ‫اللَ لاَ ي‬ َ ‫صا َب ُه ُم ْال َق ْر ُح لِلَّ ِذ‬ ‫ين أَ ْح َسنُوا‬ َّ ‫َو‬ َ َ‫ول ِم ْن َب ْع ِد َما أ‬ ِ ‫الر ُس‬ َ ‫ين َق‬ َ ‫ِم ْن ُه ْم َواتَّ َق ْوا أَ ْج ٌر َع ِظي ٌم الَّ ِذ‬ ‫اس إِ َّن‬ ُ َّ‫ال لَ ُه ُم الن‬ ْ ‫اس َق ْد َج َمعُوا لَ ُك ْم َف‬ ‫اخ َش ْو ُه ْم َف َزا َد ُه ْم إِي َما ًنا‬ َ َّ‫الن‬ ُ ‫َو َقالُوا َح ْسبُ َنا اللهَُّ َو ِن ْع َم ْال َو ِك‬ ‫يل َفا ْن َقلَبُوا ِب ِن ْع َم ٍة ِم َن‬ َّ‫ان ه‬ َّ‫ه‬ ْ ‫ض ٍل لَ ْم َي ْم َس ْس ُه ْم ُسو ٌء َواتَّ َبعُوا ِر‬ ْ ‫اللِ َو َف‬ َ ‫ض َو‬ ِ‫الل‬ ْ ‫َواللهَُّ ُذو َف‬ ‫يم‬ ‫ظ‬ ‫ع‬ ‫ل‬ ‫ض‬ َ ِ ٍ ٍ “Wale waliosema kuhusu ndugu zao na wao wakiwa wamebaki nyuma: Lau wangelitutii wasingeuawa. Sema, jizuilie na mauti (msife) ikiwa mnasema kweli. Na usiwadhanie kabisa wale waliouawa katika njia ya Mwenyezi Mungu kuwa wamekufa, bali wako hai mbele ya Mola wao wanaruzukiwa. Wanafurahia aliyowapa Mwenyezi Mungu katika fadhila zake, na wanawashangilia wale ambao hawajajiunga nao, walio nyuma yao, ya kwamba haitakuwa hofu juu yao wala hawatahuzunika. Wanashangilia neema na fadhila za Mwenyezi Mungu, na kwamba Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa waumini. Wale waliomwitikia Mwenyezi Mungu na Mtume baada ya majeraha yali46


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

yowapata; kwa waliofanya wema na takua wana ujira mkubwa. Wale ambao waliambiwa na watu: Hakika watu wamewakusanyikia kwa hivyo waogopeni. Lakini yakawazidishia imani, wakasema: Mwenyezi Mungu anatutosha na bora ya mwenye kutegemewa ni Yeye. Basi wakarudi na neema za Mwenyezi Mungu na fadhila, haukuwagusa ubaya na wakafuata radhi ya Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni mwenye fadhila kubwa.” (Sura Imran: 168 – 174).

Imam Husain bin Ali (as) alizijua na kuzielewa vizuri aya hizi tukufu na akazielewa kwa hisia yake ya kiimani amri hizi za Mwenyezi Mungu za kupigana jihadi na kujitoa muhanga, hivyo akaitika wito na akatekeleza amri za Mwenyezi Mungu katika kipindi hicho kigumu ambacho umma wa Kiislamu ulikuwa unakipitia. Amri hizo zinamtaka mwenye kuzisikia aya hizi na anayemfuata Mtume na kutii maneno yake aitike wito wa haki na asimame msimamo huu mtukufu, msimamo wa jihadi na kujitoa muhanga katika njia ya Mwenyezi Mungu. Kama ambavyo Imam Husain alielewa vyema maneno ya baba yake Ali (as) ambayo yanawalingania Waislamu kwenye jihadi na kujitoa muhanga katika njia ya kueneza uadilifu katika jamii na kutekeleza Uislamu katika maisha, na kwa mfano tu ni zile hotuba zilizopokewa katika Nahjul-Balaghah ikiwemo ile isemayo:

‫إن الجهاد باب من أبواب الجنة فتحه اهلل لخاصة‬ ‫ وهو لباس التقوى ودرع اهلل الحصينة‬،‫اوليائه‬ ‫وجنته الوثيقة فمن تركه رغبة عنه البسه‬ ‫ وديث بالصغار‬،‫اهلل ثوب الذل وشمله البالء‬ 47


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

‫ واديل‬،‫والقماءة وضرب على قلبه باالسهاب‬ ‫الحق منه بتضييع الجهاد وسيم الخسف ومنع‬ ‫النصف‬ “Hakika jihadi ni mlango miongoni mwa milango ya pepo, Mwenyezi Mungu ameufungua hususan kwa mawalii wake, nao ni vazi la uchamungu na ni ngao madhubuti ya Mwenyezi Mungu na kinga yake imara, na mwenye kuiacha kwa kuichukia Mwenyezi Mungu atamvisha vazi la udhalili na atapatwa na balaa, atadharaulika kwa udhalili na moyo wake utapatwa wazimu, na atazingirwa na haki kwa kupoteza jihadi na hatimaye ataonjeshwa udhalili na atanyimwa uadilifu.”47

Na Imam Husain alisikiliza wasia wa mzazi wake Imam Ali (as) na maneno yale yakabakia yakivuma katika masikio yake, na akaelewa maana ambayo Imam aliusia kwake na kwa ndugu yake Hasan wakati wa mwisho wa maisha yake akiwa katika kitanda cha mauti yake:

‫ وإن بغتكما‬،‫أوصيكما بتقوى اهلل وأن التبغيا الدنيا‬ ‫ وقوال‬،‫وال تأسفا على شيء منها زوي عنكما‬ ً‫ وكونا للظالم خصما‬-‫ لآلخرة‬-‫بالحق واعمال لألجر‬ ‫ اهلل اهلل في االيتام فال تغبوا افواههم‬.ً‫وللمظلوم عونا‬ ‫ اهلل اهلل في القرآن اليسبقكم‬. ‫وال يضيعوا بحضرتكم‬ 47

Nahjul-Balaghah, khutuba ya 27 48


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

‫ اهلل اهلل في الجهاد باموالكم‬.‫إلى العمل به غيركم‬ ‫ وال تتركوا األمر‬.‫وانفسكم والسنتكم في سبيل اهلل‬ ‫ فيولى عليكم شراركم‬،‫بالمعروف والنهي عن المنكر‬ ‫ثم تدعون فال يستجاب لكم‬ “Nawausieni kumcha Mwenyezi Mungu na wala msiitake dunia hata kama itawataka, na wala msisikitike kwa chochote kinachoenguliwa kwenu, na semeni haki na tendeni kwa ajili ya malipo ya akhera, na kuweni wagomvi kwa madhalimu na msaada kwa wanaodhulimiwa. Ala ala msiwanyime chakula mayatima, wala wasipotee mbele yenu. Ala ala msiache kufanya jihadi kwa mali zenu, nafsi zenu na ndimi zenu katika njia ya Mwenyezi Mungu, wala msiache kuamrisha mema na kukataza maovu na hatimaye walio waovu wakaja kutawalishwa, kwani hapo mtaomba na wala hamtajibiwa.”48

Wasia huu ukawa ni mpango wa kijamii na wa kijihadi kwa Imam Husain (as), na ukampa nguvu na ari katika nafsi kwa kumtia shauku ya kupenda kujitoa muhanga na kutoa katika njia ya Mwenyezi Mungu. Pia dua zina nafasi muhimu katika kuielekeza nafsi katika kujitoa muhanga na kujitoa fidia katika njia ya Mwenyezi Mungu, kwa mfano dua isemayo:

‫وتجعلني ممن تنتصر به لدينك وال تستبدل بي‬ .‫غيري‬ “Na unijaalie kuwa miongoni mwa wenye kuinusuru dini yako wala usinibadilishe na mwingine asiyekuwa mimi.” 48

Nahjul-Balaghah, barua namba 47 49


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

.................‫وقتال في سبيلك فوفق لنا‬ “Na utuwafikishe kupigana katika njia yako.”

Na tunakuta kwamba Imam Husain alikuwa anaomba dua hii juu ya kaburi la babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) kwa kunyenyekea kwa Mwenyezi Mungu:

‫اللهم إن هذا قبر نبيك محمد وانا ابن بنت نبيك‬ ‫ اللهم إني‬،‫وقد حضرني من األمر ما قد علمت‬ ‫ واسألك يا ذا‬،‫احب المعروف وأنكر المنكر‬ ‫الجالل واالكرام بحق هذا القبر ومن فيه اال‬ . ‫اخترت لي ماهو لك رضى ولرسولك رضى‬ “Eee Mwenyezi Mungu hakika hili ni kaburi la Nabii wako Muhammad (saww) na mimi ni mtoto wa binti ya Nabii wako na yameshanifikia mambo ambayo umeshayajua, Eee Mwenyezi Mungu hakika mimi napenda mema na nachukia maovu, na nakuomba ewe Mwenye utukufu na enzi kwa haki ya kaburi hili na aliyemo ndani, nichagulie lile ambalo lina ridahaa yako na ridhaa ya Mtume wako.”49

2. Kutekeleza kivitendo mazoezi ya kutoa na kujitoa muhanga: Kwa kiwango kinachowezekana na kulingana na uwezo uliopo kwa mtu binafsi, kama vile kutoa msaada kwa mafakiri na wanyonge na kushiriki katika shughuli za kidini na miradi ya kijamii. 49

Al- Muqarram katika maqtalulHusain uk: 133 50


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

Vinginevyo hakika mwanadamu ambaye anafanya ubakhili wa chochote katika mali yake na cheo chake au wakati wake, ambaye hataki kutoa chochote katika njia ya Mwenyezi Mungu, mwanadamu huyu hawezi kubadili nafsi yake kwa sekunde moja, hawezi kubadilika na kuwa mwenye kutoa, mwenye kujitoa muhanga, mwenye kufanya wema, mzuri wa nafsi na mwenye kutoa roho yake na kujitolea. Qur’an inatusimulia kuhusu watu waliotoa udhuru katika kutoa kidogo katika mali zao katika njia ya Mwenyezi Mungu, kwa kuahirisha hilo hadi wakati wa utajiri na pato, lakini ulipowajia utajiri nafsi zao hazikuwaruhusu kujitoa muhanga na kutoa, na hiyo ni katika kauli yake (swt):

َّ‫اه َد ه‬ ْ ‫اللَ لَِئ ْن آ َتا َنا ِم ْن َف‬ َ ‫َو ِم ْن ُه ْم َم ْن َع‬ ‫ص َّد َق َّن‬ َّ ‫ضلِ ِه لَ​َن‬ ْ ‫اه ْم ِم ْن َف‬ ُ ‫ين َفلَ َّما آ َت‬ َ ‫الصالِ ِح‬ ‫ضلِ ِه‬ َّ ‫َولَ​َن ُكو َن َّن ِم َن‬ َّ ُ ُ ‫ْر‬ َ ‫ض‬ ‫ون َفأَ ْع َق َب ُه ْم ِن َف ًاقا ِفي‬ ِ ‫َب ِخلوا ِب ِه َو َت َول ْوا َو ُه ْم ُمع‬ َّ‫ُقلُوبه ْم إلَىٰ َي ْوم َي ْل َق ْو َن ُه ب َما أَ ْخلَ ُفوا ه‬ ‫اللَ َما َو َع ُدو ُه‬ ِ ِ ِ​ِ ِ ْ َ ‫َو ِب َما َكانُوا َيك ِذب‬ ‫ُون‬ “Na miongoni mwao wako waliomwahidi Mwenyezi Mungu: Akitupa fadhila Zake hakika tutatoa sadaka na hakika tutakuwa miongoni mwa watendao wema. Lakini alipowapa katika fadhila Zake, walizifanyia ubakhili wakageuka na huku wakipuuza. Kwa hiyo ukawalipa unafiki katika nyoyo zao mpaka siku ya kukutana nao. Kwa sababu ya kumhalifu Mwenyezi Mungu yale waliyomwahidi na kwa sababu ya kusema kwao uwongo.” (Sura Tawba: 75 – 77).

51


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

Na tunakuta kwamba kutoa na kujitoa muhanga ilikuwa ni sehemu ya maisha ya Imam Husain (as) na ni sehemu ya mwenendo wake wa kila siku. Imekuja kuhusu ukarimu wa Husain (as) na kutoa kwake mali na kuwasaidia kwake mafakiri na wenye haja kwamba: Muombaji alikuwa akitembea katika mitaa ya Madina hadi akafika katika mlango wa nyumba ya Husain (as) akagonga mlango na akaanza kusema: “Hajapata hasara sasa hivi aliyekutarajia, na mwenye kusimama nyuma ya mlango wako, wewe ni mkarimu na wewe ni tegemeo, na baba yako alikuwa ni muuwaji wa mafasiki.” Husain alikuwa anaswali akafanya haraka katika swala yake na akatoka kwenda kwa bedui, na alipomtazama aliona kwake athari ya maradhi na ufakiri, hivyo akarejea na akamwita wakala wake, naye akaja haraka, akamwambia: “Kitu gani kimebakia kwako katika matumizi yetu?” Akasema: “Dirihamu mia mbili ulizoniamuru niwape familia yako.” Akasema: “Zilete, kwani amenijia mtu ambaye anastahiki zaidi hizo kuliko wao.” Akazipeleka kwa bedui huku akisema: “Zichukue hakika mimi naomba radhi kwako. Najua kwamba hakika mimi kwako ni mwenye huruma. Lau kama hali yetu ingeruhusu zaidi ya hayo, basi kheri zetu zingekumiminikia. Lakini hali yetu sio nzuri, pato letu ni dogo.” 50 Na amepokea Ibnu Asakir katika Taarikh yake kwamba alikuwa anapelekewa mali kutoka Basra na sehemu zingine, basi hasimami kutoka mahala pake hadi aigawe yote kwa mafakiri. Basi na tumuige Imam Husain (as) na tujizoeze kutoa na kujitolea yale tunayomiliki miongoni mwa mali, vyeo na uwezo ili nafsi zetu ziwe tayari kwa ajili ya kujitoa muhanga katika njia ya Mwenyezi Mungu. Na munasaba wa Ashura uwe ni fursa nzuri ya kuzirejea nafsi zetu na kuzilea kwa mambo matatu yaliyotajwa: 50

Al-Qarashiy katika Hayaatul-Imamil-Husain Jz. 1 uk: 132 52


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

1.

Kupambana na matamanio ya nafsi na ushawishi na udanganyifu wa maisha ya dunia.

2.

Kuishibisha nafsi utamaduni wa Kiislam na kuiongezea mafunzo ya imani, ikhlasi na jihadi kutoka katika aya za Qur’ani na Hadith, Sunna tukufu na dua zilizopokewa.

3.

Kutekeleza kivitendo mazoezi ya kutoa kadiri inavyowezekana.

Na amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yako ewe kielelezo cha kujitoa muhanga na fidia. Ewe Abu Abdillahi Husain, rehema zake na Baraka zake ziwe juu yako.

53


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1. i) Qur’ani Tukufu – Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili ii) Qur’an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thelathini 2. Uharamisho wa Riba 3. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza 4. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili 5. Hekaya za Bahlul 6. Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) 7. Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) 8. Hijab vazi Bora 9. Ukweli wa Shia Ithnaashari 10. Madhambi Makuu 11. Mbingu imenikirimu 12. Abdallah Ibn Saba 13. Khadijatul Kubra 14. Utumwa 15. Umakini katika Swala 16. Misingi ya Maarifa 17. Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia 18. Bilal wa Afrika 19. Abudhar 20. Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu 21. Salman Farsi 22. Ammar Yasir 23. Qur’an na Hadithi 24. Elimu ya Nafsi 25. Yajue Madhehebu ya Shia 26. Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur’an Tukufu 27. Al-Wahda 28. Ponyo kutoka katika Qur’an 29. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii 30. Mashukio ya Akhera 31. Al Amali 32. Dua kwa Mujibu wa Ahlulbayt (a.s) 33. Udhuu kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna 34. Haki za wanawake katika Uislamu 35. Mwenyezi Mungu na sifa zake 36. Kumswalia Mtume (s)

54


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

37. Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) 38. Adhana 39. Upendo katika Ukristo na Uislamu 40. Qur’ani na Kuhifadhiwa Kwake 41. Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu 42. Kupaka juu ya khofu 43. Kukusanya Sala Mbili 44. Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara 45. Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya 46. Kusujudu juu ya udongo 47. Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) 48. Tarawehe 49. Malumbano baina ya Sunni na Shia 50. Kupunguza Swala safarini 51. Kufungua safarini 52. Umaasumu wa Manabii 53. Qur’an Yatoa Changamoto 54. as-Salaatu Khayrun Mina -’n Nawm 55. Uadilifu wa Masahaba 56. Dua e Kumayl 57. Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu 58. Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake 59. Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata 60. Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mtume Muhammad (s) 61. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza 62. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili 63. Kuzuru Makaburi 64. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza 65. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili 66. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu 67. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne 68. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano 69. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita 70. Tujifunze Misingi Ya Dini 71. Sala ni Nguzo ya Dini 72. Mikesha Ya Peshawar 73. Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu 74. Ubora wa Imam ‘Ali na Ushia ndio njia iliyonyooka 75. Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake 76. Liqaa-u-llaah 77. Muhammad (s) Mtume wa Allah 78. Amani na Jihadi Katika Uislamu 55


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

79. Uislamu Ulienea Vipi? 80. Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) 81. Dhana ya Ndoa ya Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) 82. Urejeo (al-Raj’ah) 83. Mazingira 84. Utokezo (al - Badau) 85. Hukumu ya kujenga juu ya makaburi 86. Swala ya maiti na kumlilia maiti 87. Uislamu na Uwingi wa Dini 88. Mtoto mwema 89. Adabu za Sokoni Na Njiani 90. Johari za hekima kwa vijana 91. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza 92. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili 93. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu 94. Tawasali (AT- TAWASSUL) 95. Imam Mahdi katika Usunni na Ushia 96. Hukumu za Mgonjwa 97. Sadaka yenye kuendelea 98. Msahafu wa Imam Ali 99. Maimamu wa Ahlul Bait – Ujumbe na Jihadi 100. Idi Al-Ghadir 101. Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu 102. Hukumu zinazomuhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi 103. Huduma ya Afya katika Uislamu 104. Sunna za Nabii Muhammad (saww) 105. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) 106. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) 107. Shahiid Mfiadini 108. Mwanamke Na Sharia 109. Ujumbe -Sehemu ya Kwanza 110. Ujumbe - Sehemu ya Pili 111. Ujumbe - Sehemu ya Tatu 112. Ujumbe - Sehemu ya Nne 113. Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu 114. Hadithi ya Thaqalain 115. Ndoa ya Mutaa 116. Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza 117. Ukweli uliopotea sehemu ya Pili 118. Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu 119. Ukweli uliopotea sehemu ya Nne 120. Ukweli uliopotea sehemu ya Tano 56


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

121. Mkutano wa Maulamaa wa Baghdad 122. Safari ya kuifuata Nuru 123. Fatima al-Zahra 124. Myahudi wa Kimataifa 125. Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi 126. Visa vya kweli sehemu ya Kwanza 127. Visa vya kweli sehemu ya Pili 128. Elimu ya Ghaibu ya Maimamu 129. Mwanadamu na Mustakabali wake 130. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) 131. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) 132. Khairul l’Bariyyah 133. Uislamu na mafunzo ya kimalezi 134. Vijana ni Hazina ya Uislamu 135. Adhana ni Ndoto au ni Wahyi? 136. Tabaruku 137. Saada Kamili – Kitabu cha Kiada cha Maadili 138. Vikao vya furaha 139. Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 140. Visa vya wachamungu 141. Falsafa ya Dini 142. Kuhuzunika na Kuomboleza 143. Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah 144. Mjadala wa Kiitikadi 145. Kuonekana kwa Allah 146. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) 147. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) 148. Ndugu na Jirani 149. Ushia ndani ya Usunni 150. Maswali na Majibu 151. Mafunzo ya hukmu za ibada 152. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1 153. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2 154. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 155. Abu Huraira 156. Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. 157. Mazingatio kutoka katika Qur’an - Sehemu ya Kwanza 158. Mazingatio kutoka kaitka Qur’an - Sehemu ya Pili 159. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza 160. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili 161. Shia na Qur’ani – Majibu na Maelezo 162. Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) 57


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

163. Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani 164. Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu 165. Uislamu Safi 166. Majlisi za Imam Husein Majumbani 167. Je, Kufunga Mikono 168. Uislam wa Shia 169. Amali za Makka 170. Amali za Madina 171. Asili ya Madhehebu katika Uislamu 172. Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi 173. Ukweli uliofichika katika neno la Allah 174. Uislamu na Mifumo ya Uchumi 175. Umoja wa Kiislamu na Furaha 176. Mas’ala ya Kifiqhi 177. Jifunze kusoma Qur’ani 178. as-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah 179. Hayya ‘Alaa Khayri’l-’Amal Katika Adhana 180. Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura 181. Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na Ramadhani) 182. Uadilifu katika Uislamu 183. Mahdi katika Sunna 184. Maswali Ya Uchunguzi Kuhusu Uislam 185. Kazi na Bidii ni njia ya maendeleo 186. Abu Talib – Jabali Imara la Imani 187. Ujenzi na Utakaso wa Nafsi 188. Vijana na Matarajio ya Baadaye 189. Historia maana na lengo la Usalafi 190. Ushia – Hoja na Majibu 191. Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) 192. Maombolezo – Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) 193. Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu 194. Takwa 195. Upotoshaji Dhahiri katika (Turathi) Hazina ya Kiislamu 196. Amirul Muuminina (‘as) na Makhalifa 197. Tawheed Na Shirki 198. Kuvunja hoja iliyotumika kutetea Uimamu wa AbuBakr 199. Adabu za vikao na mazungumzo 200. Hija ya Kuaga 201. Uwazi baina ya Maslahi na Vikwazo 202. Fadhila za watukufu watano katika Sahih Sita 203. Mdahalo baina ya Mwanachuoni wa Kisunni na Kishia (Al- Muraja’aat) 204. Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (as) 58


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

205. Imam Husain ni Mfumo wa Marekebisho na Mageuzi 206. Mtazamo kuhusu msuguano wa Kimadhehebu 207. Nchi na Uraia – Haki na wajibu kwa Taifa 208. Mtazamo wa Ibn Taymiyyah juu ya Imam Ali (as) 209. Uongozi wa Kidini – Maelekezo na Utekelezaji wa Kijamii 210. Maadili ya Ashura 211. Mshumaa – Shahidi na Kifo cha Kishahidi 212. Mizani ya Hekima – Hadithi za Ahlul Bait (as) – Sehemu ya Kwanza 213. Imam Ali na Mambo ya Umma 214. Imam Ali na Mfumo wa Usawa 215. Uimamu na Tamko la Kutawazwa 216. Mfumo wa Wilaya 217. Vipi Tutaishinda Hofu? 218. Kumswalia Mtume ni Ufunguo wa Utatuzi wa Matatizo 219. Maeneo ya Umma na Mali Zake 220. Nahju ‘L-Balagha – Majmua ya Khutba, Amri, Barua, Risala, Mawaidha na Semi za Amirul-Muuminin Ali bin Abu Talib (a.s.) 221. Mukhtar – Shujaa aliyelipiza kisasi dhidi ya wauaji wa Imam Husein (as) hapo Karbala 222. Mazingatio Katika Swala 223. Imam Hasan na Mfumo wa Kujenga Jamii 224. Vyakula Na Vinywaji 225. Kuelewa Rehema ya Mwenyezi Mungu 226. Tiba ya Maradhi ya Kimaadili 227. Yafaayo kijamii 228. Shia Na Hadith- Majibu na Maelezo 229. Mkakati wa Kupambanana Ufakiri 230. Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu 231. Taqiyya Kwa Mujibu Wa Sheria Ya Kiislamu 232. Imam Mahdi Na Bishara Ya Matumaini 233. Jihadi 234. Majanga Na Jukumu La Jamii 235. Muhadhara wa Maulamaa 236. Mashairi ya Kijamii 237. Ngano ya kwamba Qur’ani imebadilishwa 238. Mwanamke Katika Harakati Za Mageuzi 239. Shia Na Sahaba- Majibu na Maelezo 240. Yusuf Mkweli 241. Hotuba Za Kiislamu Juu ya Haki Za Binadamu

59


IMAM HUSAIN NI KIELELEZO CHA KUJITOA MUHANGA NA FIDIA

KOPI NNE ZIFUATAZO ZIMETAFSIRIWA KWA LUGHA KINYARWANDA 1. Amateka Ya Muhammadi (s.a.w.w) Na Aba’ Khalifa 2. Nyuma yaho naje kuyoboka 3. Amavu n’amavuko by’ubushiya 4. Shiya na Hadithi

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION KWA LUGHA YA KIFARANSA 1. Livre Islamique

60


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.