IMAM MAHDI َعلَ ْي ِه السَّالم NA HABARI ZA UGHAIBU اإلمام المهدي و أخبار الغيب Mfululizo wa Mihadhara ya Sayyid Hasan Nasrullah
سلسلة محاضرات لسماحة السيِّد ح َسن نصْ ر هللا Kimeandaliwa na: Kituo cha NUN, (Kinachojishughulisha na utunzi na kutarjumi vitabu)
Kimetarjumiwa na: Alhaji Hemedi Lubumba
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 1
3/5/2016 3:11:05 PM
سلسلة محاضرات لسماحة السيِّد ح َسن نصْ ر هللا
اإلمام المهدي و أخبار الغيب
إعداد
مركز نون للتأليف والترجمة
نشر جمعية المعارف اإلسالمية الثقافية دار المودة للترجمة والتحقيق والنشر
من اللغة العربية إلى اللغة السواحلية
3/5/2016 3:11:05 PM
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 2
©Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 –17 – 019 – 7 Kimeandikwa na: Sayyid Hassan Nasrullah Kimetarjumiwa na: Alhaji Hemedi Lubumba Kimehaririwa na: Al-Haj Ramadhani S. K. Shemahimbo Kimepitiwa na: Mujahid Rashid Kimepangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation Toleo la kwanza: Juni, 2016 Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. - 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: www.alitrah.info
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 3
3/5/2016 3:11:05 PM
Yaliyomo Dibaji ......................................................................................... vi Neno la Mchapishaji........................................................................ 1 Utangulizi......................................................................................... 3 Faslu ya Kwanza.............................................................................. 4 Uchunguzi juu ya Njia za Kuijua Ghaibu........................................ 4 Ghaibu na Mustakabali ni jambo lenye kuzusha mjadala................ 5 Na kutiliwa umuhimu...................................................................... 5 Ghaibu ni Nini?................................................................................ 7 Kuamini Ghaibu ni Sehemu ya Itikadi Yetu.................................... 8 Ghaibu na Dhahiri ni mambo ya kunasibisha.................................. 8 Elimu ya Ghaibu.............................................................................. 9 Njia zenye kuaminika katika kuitambua Ghaibu........................... 10 Njia mbalimbali za kuijua Ghaibu................................................. 11 Ndoto na Uhusiano Wake na Mustakabali..................................... 15 Je Ndoto ni Hoja?........................................................................... 17 Kwanini Allah Amefunga Mlango wa Ghaibu?............................. 17 Tutawezaje Kujua Habari za Mustakabali?................................... 19 Faslu ya Pili......................................................................... 20 Mtazamo wa Uislamu juu ya Habari za Ghaibu na Mustakabali.................................................................. 20 Quran Tukufu Inavyozungumzia Mustakabali:............................. 21 Mustakabali ni wa Waja Wema:..................................................... 24 Uongozi wa Kiungu na Mustakabali wa Waja Wema:................... 26 Habari za Mustakabali Katika Riwaya:......................................... 26
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 4
3/5/2016 3:11:05 PM
Vigawanyo vya Riwaya Zinazohusu Mustakabali:........................ 27 Faida ya kujua habari za mustakabali:........................................... 31 Faida ya Kiitikadi:.......................................................................... 31 Kuwasadikisha Manabii:................................................................ 32 Faida ya Kisaikolojia:.................................................................... 33 Faida ya mwanzo ya kujua mustakabali:....................................... 34 Kulisogeza tumaini karibu:............................................................ 36 Alama na viashiria:........................................................................ 37 Faslu ya Tatu....................................................................... 38 Vigezo vya kufuata wakati wa kusoma na kutabikisha alama za kudhihiri Imam Mahdi................................. 38 Mfumo unaofuatwa katika kuzifanyia kazi nususi za Sunna Tukufu:........................................................................... 38 Mfumo unaokubalika kiakili katika kupokea habari:.................... 40 Hadithi za uwongo:........................................................................ 40 Suala la Imam Mahdi na hatari yake wakati wa kutabikisha:........ 41 Mahdi wa uwongo:........................................................................ 43 Hatari zilizopo wakati wa kutabikisha alama za kudhihiri kwa Mahdi ď …:.............................................................. 45 Mifano ya hatari zitokanazo na kuoanisha anuani hizi katika zama zetu:..................................................................... 49 Mwenendo wa kufuatwa katika Hizbullah:................................... 51 Sifa za alama makhususi:............................................................... 52 Kuainisha wakati atakaodhihiri:.................................................... 53 Ungojeaji salama:........................................................................... 55 Ahadi ya Allah hutimia kwa utashi wa Allah:............................... 56 Matumaini na kungojea:................................................................ 57
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 5
3/5/2016 3:11:05 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
DIBAJI
K
itabu hiki ni toleo la Kiswahili la taasisi ya Al Itrah Foundation. Chapisho lake limelenga kukidhi mahitaji ya kiroho ya zama hizi pamoja na Ubongo na fikra zinazokuwa za Muislam. Jitihada kubwa zimefanywa na Taasisi kuweka chapisho hili la Kiswahili katika msingi wa haki na wenye kukubalika katika Uislam. Unaombwa kwa Taadhima ukisome kitabu hiki katika malengo yaliyokusudiwa. Pia Unaombwa kuwasilisha kwetu maoni yako huru juu ya chapisho letu hili, jambo ambalo tutashukuru sana. Kutangaza ujumbe wa Uislam ni kazi ambayo inahitaji ushirikiano wetu sote. Taasisi inakuomba kuungana na kushirikiana kama ilivyoagizwa katika aya ya Qur’an: (Surat Saba’ 34:46). Na rehma za Allah ziwe juu yako. Wako katika Uislam Al Itrah Foundation Barua Pepe: alitrah@yahoo.com SMS: +255 778 300 140
vi
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 6
3/5/2016 3:11:05 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
NENO LA MCHAPISHAJI
K
itabu ulichonacho mikononi mwake ni tarjuma ya Kiarabu ya kitabu kiitwacho, al-Imam al-Mahdi wa Akharu ‘l-Ghayb ambacho ni mfululizo wa mihadhara muhimu ya kifikra ya Sayyid Hasan Nasrullah, kiongozi wa Hizbullah nchini Lebanon. Sisi tumekiita, Imam Mahdi na Habari za Ughaibu. Moja ya nguzo za imani ambazo Qur’ani hudai na kuthibitisha ni nguzo ya imani katika Imam Mahdi na sifa zake. Qur’ani Tukufu inasema: “…Hatukupuuza Kitabuni kitu chochote…” (6:38); na katika sehemu nyingine, Kitabu cha Allah kinaeleza: “… na tumekuteremshia Kitabu hiki kubainisha kila kitu…” (16:89). Ili kuelezea msimamo wa Qur’ani kuhusiana na imani ya Umahdia, hadithi nyingi zimesherehesha aya hizi kupitia nyororo za wasimulizi wa Kishia na halikadhalika wa Kisunni. Hadithi hizi kwa uwazi husema kwamba aya hizi huelezea kuhusu Imam Mahdi E Qur’ani ina vipengele mbalimbali vya kujitokeza tena, ughaibu na pia sifa za Imam Mahdi . Vyote hivi vikiwa vinakubaliwa na wote, wanachuoni wa Shia na halikadhalika wanachuoni wa Sunni ambao ni wenye mamlaka zaidi na wakuaminika. Aya za Qur’ani kuhusu kujitokeza tena na mapinduzi ya Imam Mahdi - imani ya kawaida kwa Ahli Sunna pia - hutaja sifa nne na malengo ya utawala wa ulimwengu wa Imam Mahdi :
• • • •
Kusimamisha utawala mmoja wa ulimwengu. Madaraka kamili kwa dini ya Uislamu. Mazingira ya usalama kamili na amani. Uangamizaji wa ushirikina (shirk). 1
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 1
3/5/2016 3:11:05 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
Atajitokeza tena na kusimama wakati wa kipindi cha mwisho na ataujaza ulimwengu kwa uadilifu na usawa kama ambavyo utakuwa umejaa dhulma na ukandamizaji. (Kifayatu ‘l- Athar, uk. 12) Atasafisha uso wa ardhi kutokana na aina zote za dhulma na udikiteta na kuitakasa kutokana na aina zote za maovu. Hii ni moja kati ya kazi kubwa zinazofanywa na Taasisi ya AlItrah katika kuwahudumia kielimu wasomaji wake wazungumzaji wa Kiswahili. Na kwa maana hiyohiyo imeamua kukichapisha kitabu hiki chenye hazina kubwa kwa lugha ya Kiswahili kwa lengo lake lilelile la kuwahudumia Waislamu hususan wanaozungumza Kiswahili. Hivyo, ni matumaini yetu kwamba wasomaji wetu watanufaika vya kutosha kutokana na kitabu hiki, kwani tumekiona ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni vitu ambavyo havina nafasi tena katika akili za watu. Tunakishukuru Kituo cha NUN kinachojishughulisha na utunzi na kutarjumi vitabu kwa kazi kubwa wanayoifanya kwa ajili ya Umma huu wa Waislamu, Allah Azza wa Jallah awalipe kila kheri na waendelee na kazi hii adhimu. Halikadhalika tunamshukuru Ustadh Alhaji Hemedi Lubumba kwa kukitarjumi kwa Kiswahili kitabu hiki, insha’Allah na yeye Allah Azza wa Jallah amlipe kila kheri hapa duniani na Akhera pia, bila kuwasahau wale wote waliochangia kwa namna mmoja au nyingine mpaka kufanikisha kuchapishwa kwake., Allah Mwingi wa baraka awalipe wote malipo mema hapa duniani na huko Akhera. Mchapishaji Al-Itrah Foundation
2
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 2
3/5/2016 3:11:05 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
UTANGULIZI
K
ila sifa njema ni ya Mwenyezi Mungu Mola mlezi wa walimwengu. Swala za Mwenyezi Mungu zimwendee Bwana wetu Muhammad, yeye na Aali zake watoharifu. Kijitabu hiki kimekusanya mfululizo wa baadhi ya mihadhara muhimu ya kifikra, iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Hizbullah, Mheshimiwa Allamah Sayyid Hasan Nasrullah, Mungu amhifadhi, katika mikesha ya Ashura mnamo mwaka 1436 A.H.1 katika mhadhara hiyo ilizungumziwa kwa kina suala la Imam Mahdi na habari za ghaibu, kwa njia nyepesi na bayana. Kutokana na umuhimu wa maudhui hizi, na kuhitajiwa kwake zaidi na watu, tumeamua kuiweka mihadhara hiyo katika maandishi na kuiwasilisha katika somo hili ili iwe na faida zaidi. Mchapishaji wa Chapa ya Kiarabu.
1
Mwanzo wa Muharam 1436 A.H. ulisadifiana na 26 Oktoba 2014, hivyo mihadhara hii itakuwa iliwasilishwa na Sayyid mwaka 2014 A.D.- Mtarjumi. 3
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 3
3/5/2016 3:11:05 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
FASLU YA KWANZA
FASLU YA KWANZA UCHUNGUZI JUU YA NJIA ZA KUIJUA GHAIBU
2
Utangulizi:
UCHUNGUZI JUU YA NJIA ZA KUIJUA Hakika miongoni mwa mambo yaliyotiliwa umuhimu na wa GHAIBU2 katika zama zote, sasa na zamani, ni kutaka kujua habari
mustakabali na yatakayotokea katika siku na miaka ijayo, kati miongo na karne zijazo, mpaka siku ya kusimama Kiyam Maudhui hii imeshughulisha sehemu kubwa ya uzingativu w akika miongoni mwa mambo yaliyotiliwa umuhimu na watu watu, na hasa katika zama za matatizo na wakati wa misukosuk katika zama zote, na zamani, kutaka kujua habari za wa kujikwam kwasasa sababu wakati wanishida watu hutafuta mlango mustakabali na yatakayotokea katika siku na miaka ijayo, katika na matatizo na misukosuko, hivyo huenda kwenye matarajio miongo na karne zijazo, mpaka siku yanakusimama Kiyama. Maudmambo ya utabiri, haya ndio huitwa mambo ya ghaibu.
Utangulizi:
H
hui hii imeshughulisha sehemu kubwa ya uzingativu wa watu, na Bali hata tunapopekua kurasa zakwa historia hasa katika zama za matatizo na wakati wa misukosuko, sababutunakuta kwam watawala na wafalme na wakuu wa majeshi walikuwa wakifan wakati wa shida watu hutafuta mlango wa kujikwamua na matatizo hivyo. Na ilikuwa maarufu kwamba, Bani Israil na Mayahudi kw na misukosuko, hivyoujumla huendawalikuwa kwenye matarajio na mambo ya utawana hazina kubwa ya habari za ghaibu biri, na haya ndio huitwa mambo ya ghaibu. mustakabali, kwa sababu wao wana idadi kubwa ya Manabii,
hivyokurasa kama za kilahistoria Nabii atazungumzia kisa watakimoja tu au viwili, Bali hata tunapopekua tunakuta kwamba lazima watakusanya habari nyingi. Na daima wakati wa matati wala na wafalme na wakuu wa majeshi walikuwa wakifanya hivyo. yao walikuwa wakikimbilia kwa Manabii kwenda kuwauliza jin Na ilikuwa maarufu kwamba, na Mayahudi kwanaujumla ya kupata Bani faraja,Israil wepesi na suluhisho, wao Manabii walikuw walikuwa wana hazina kubwa ya habari za ghaibu na mustakabali, wakiwaeleza baadhi ya mambo. kwa sababu wao wana idadi kubwa ya Manabii, na hivyo kama kila Nabii atazungumzia kisa kimoja tu au viwili, ni lazima watakusanya 2
Ghaibu naMustakabali ni Jambo Lenye Kuzusha na Kutiliwa Umuhimu: Nasrullah, Mungu Mjadala amhifadhi, huko Beirut, Lebanon,
otuba hii aliitoa Sayyid Hasan H usiku wa mwezi tano Muharam, 1436 A.H. sawa na 29 – 10- 2014 A.D. Ilikuwa ni katika kikao cha maombolezo ya Ashura. Na katika zama za mwisho, alitambulika mtabiri
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 4
au mnajim anayejulikana kwa jina laNostradamus.Yeye ana mashairi kuhu 4 habari za ghaibu na Vita Vikuu vya Dunia. Makundi yen kuzozana yalifaidika na mashairi yake na utabiri wake, hiv mashairi yake yakaenea miongonimwa watu kwa tafsiri yake maelezo yake, bali ni kwamba yalitumiwa pia katika Vita Vik 3/5/2016 3:11:06 PM vya Dunia.
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
habari nyingi. Na daima wakati wa matatizo yao walikuwa wakikimbilia kwa Manabii kwenda kuwauliza jinsi ya kupata faraja, wepesi na suluhisho, na wao Manabii walikuwa wakiwaeleza baadhi ya mambo. Ghaibu na Mustakabali ni Jambo Lenye Kuzusha Mjadala na Kutiliwa Umuhimu: Na katika zama za mwisho, alitambulika mtabiri au mnajimu anayejulikana kwa jina la Nostradamus. Yeye ana mashairi kuhusu habari za ghaibu na Vita Vikuu vya Dunia. Makundi yenye kuzozana yalifaidika na mashairi yake na utabiri wake, hivyo mashairi yake yakaenea miongoni mwa watu kwa tafsiri yake na maelezo yake, bali ni kwamba yalitumiwa pia katika Vita Vikuu vya Dunia. Ama hivi sasa, baada ya maendeleo ya habari na mawasiliano, maudhui hii imekuwa maarufu zaidi, hasa ukizingatia uwepo wa matukio na maendeleo makubwa na nyeti yanayoshuhudiwa na ulimwengu, na yanashuhudiwa na ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu pia, ambapo katika baadhi ya maeneo maudhui hii imekuwa ikitumika kwa namna mbalimbali, na kwa mfano tu: Baadhi ya watu hukimbilia kwenye habari za mustakabali na zinazohusu zama za mwisho, ili waweze kuthibitisha kwamba njia yao ndio njia ya haki, ili wasisitize kwamba maamuzi yao na chaguo lao ni sahihi. Na wengine, ili waweze kuzungumzia ushindi na kushindwa, hutumia habari hizi, na wala si sharti kwamba wawe wanazungumzia riwaya makhususi zinazonasibishwa kwa Swahaba na Mtukufu Mtume ndio waitwe kuwa ni watabiri na wanajimu, bali huzitumia habari hizo katika vita vya kisaikolojia. George Bush na Regan walikuwa ni katika fungu hili. Walijenga taswira kuwa Marais wa Marekani au kwa uchache baadhi yao, walikuwa wakikimbilia kwenye habari hizi, na wakijenga miradi mikubwa kwa kutegemea 5
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 5
3/5/2016 3:11:06 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
utabiri huu. Zaidi ya hapo ni kwamba maudhui hii, kwa sasa imekuwa ni maudhui muhimu katika habari na mradi unaotumiwa kwa faida. Vyovyote iwavyo ni kwamba, jambo hili limekuwa ni maudhui ya kawaida, na wala hatuwezi kuwaambia watu kuwa msifuatilie habari za mustakabali na tunakokwenda, hapana haiwezekani. Bali ni kinyume, kwani hata Qur’ani imetoa habari zinazohusu mustakabali, na Waislamu wanamiliki utajiri mkubwa wa riwaya kutoka kwa Mtukufu Mtume , na habari zilizopo katika vitabu vya Waislamu zinazoeleza kuwa mwisho wa zama kutakuwa na mambo kadha wa kadha. Hivyo katika mipaka ya Uislamu, ni maudhui iliyotiliwa umuhimu na mkazo, hususani jambo linapofika katika mas’ala muhimu sana kama mas’ala ya Mahdi Mwenye kungojewa , sawa tuseme kwamba ameshazaliwa, kama wasemavyo Shia na baadhi ya maulamaa wakubwa wa Kisunni, au kama wasemavyo wengi katika ndugu zetu Masunni, kwamba bado hajazaliwa, na kwamba atakapofikisha miaka arubaini ndipo zitapotimia habari hizi zilizopatikana katika Hadithi. Na hata ukiachana na Hadithi zinazomhusu Mahdi na nyinginezo, bado jambo hili lina uhusiano na mustakabali, na kwa kuwa jambo hili ni miongoni mwa maudhui zinazowagusa watu, ni maudhui inayozusha maswali na kuvutia, nimependelea katika usiku huu kuzungumzia maudhui hii. Maudhui ambayo inawashughulisha watu wengi, nayo si maudhui ya kinadharia, bali ni maudhui iliyopo katika vyombo vya habari na vitabu. Tunataka kujua ni upi mwongozo wa Uislamu katika jambo hili. Leo nitazungumzia sehemu tu ya maudhui, na nitaikamilisha katika mikesha mingine. 6
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 6
3/5/2016 3:11:06 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
Ghaibu ni Nini? Mustakabali ni wakati ujao, wakati uliyopita upo nyuma yetu, na sisi tupo katika wakati uliopo, na ghaibu ni jambo lililo mbali na sisi, na sisi hatujaushuhudia mustakabali, bali tunaungojea. Na yeyote anayetaka kutoa habari za mustakabali ni wajibu awe ni mjuzi wa ghaibu, kwa sababu mustakabali ni sehemu ya ghaibu. Kuna ulimwengu wa ghaibu na ulimwengu wa dhahiri. Dhahiri ni yale tunayoyashuhudia na ambayo tunaweza kuyadhibiti kwa milango yetu ya fahamu. Ama ghaibu ni yale yaliyo mbali na milango ya fahamu, yale yaliyofichika, yale ya batini. Na yale yasiyofikiwa kwa milango ya fahamu huhesabiwa kuwa ni ghaibu, hivyo ulimwengu wa dhahiri ni ulimwengu wa yale yenye kuonekanana, yenye kufikiwa kwa milango ya fahamu. Na ulimwengu wa ghaibu ni ulimwengu wa yale yaliyo nje ya milango ya fahamu, hivyo kila kinachohusu Muumba Mtukufu, wahayi aliyouleta Allah, na kila kinachohusu Malaika, mauti na yaliyo baada ya mauti, ikiwemo kaburi, Barzakh, misukosuko ya Siku ya Kiyama na hali zake, thawabu na adhabu, Pepo na Moto, yote haya ni sehemu ya ghaibu. Kwa mfano, mwanzo wa uumbaji, licha ya maendeleo makubwa ya kielimu, lakini kuna nadharia tu mbalimbali kuhusu suala hilo, bila kuwepo uhakika yakinifu wenye kuonekana kuhusu namna Mwenyezi Mungu alivyoumba mbingu, mwanadamu, mnyama, Adam, Hawa, Pepo na Moto, haya yote ni sehemu ya ghaibu. Hivyo basi, kuna ghaibu yenye uhusiano na wakati uliopita, na ipo ile yenye uhusiano na mustakabali, na hii ndio tunayoiita ‘Hali za ghaibu zitakazoupata ulimwengu.’ Ulimwengu na uhai kwa ujumla utapatwa na nini? Mwanadamu atapatwa na nini? Utakuwaje mwisho wa uwepo wa mwanadamu? Maswali yote haya yana uhusiano na mustakabali, na habari zinazohusu mustakabali zinafungamana na ghaibu.
7
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 7
3/5/2016 3:11:06 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
Kuamini Ghaibu ni Sehemu ya Itikadi Yetu: Sisi tunaamini ghaibu, na hii ni sehemu ya itikadi ya Manabii wote , hivyo pindi tunaposema Muumba, Kiyama, Wahyi na Malaika, yote haya ni sehemu ya ghaibu, na sisi tunayaamini. Na jambo hili ni bayana katika Itikadi ya Kiislamu, Mwenyezi Mungu anasema: “Alif Lam Mim. Hiki ni kitabu kisicho na shaka ndani yake; ni mwongozo kwa wenye takua. Ambao wanaamini ghaibu.” Hivyo sifa ya kwanza ya wenye takua ni kuamini kwao ghaibu. “Na wanasimamisha Swala, na wanatoa katika yale tuliyowapa. Na ambao wanaamini yaliyoteremshwa kwako.” Hivyo na yaliyoteremshwa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu ni sehemu ya ghaibu. “Na yaliyoteremshwa kabla yako” pia ni sehemu ya ghabu.“Na Akhera wana yakini nayo.”3 Pia ni sehemu ya ghaibu. Ghaibu na Dhahiri ni Mambo ya Kunasibisha: Imebakia nukta moja ambayo ni wajibu kuitazama. Ndiyo, ghaibu na dhahiri ni sehemu mbili za jambo la kunasibisha, ni kitu gani kitatokea leo na kesho? Sisi hatujui, na hii ni sehemu ya ghaibu, lakini kama tutaendelea kuwa hai mpaka kesho, yale yatakayotokea kesho yatakuwa dhahiri na wala hayataendelea kuwa ghaibu. Kadhalika mauti na kutoka roho mwilini, na yanayoipata roho, yote haya ni ghaibu. Lakini pindi mtu anapofariki, mambo haya kwa upande wa maiti huwa ni dhahiri kwake.4 Na Kiyama na yatakayotokea huko ni sehemu ya ghaibu, mpaka pale watakapopelekwa peponi wale watakaopelekwa peponi miongoni mwetu, na kupelekwa motoni wale watakaopelekwa motoni, hapo mambo yote yatakuwa ni ulimwengu wa dhahiri. 3 4
Sura al-Baqarah: 4. Waswahili husema: Adhabu ya kaburi aijuaye maiti - Mtarjumu. 8
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 8
3/5/2016 3:11:06 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
Elimu ya Ghaibu: Na swali hapa ni kwamba: Ni nani anayejua ghaibu na mustakabali huu? Sawa iwe katika kiwango cha dunia na ulimwengu, au ghaibu ya baada ya dunia, au ghaibu ya wakati uliopita? Ni nani anayejua ghaibu? Kila maudhui ina mtaalamu wake. Mgonjwa huenda kwa tabibu, na tunapotaka kujenga tunakwenda kwa mhandisi, na kadhalika kwa seremala, lakini ni kwa nani twende tunapotaka kujua ghaibu? Na ni nani anayejua mustakabali ambao ni sehemu ya ghaibu? Kwa mujibu wa Uislamu, jawabu yakinifu na lisilo na shaka ni kwamba “Haijui ghaibu isipokuwa Allah Mtukufu,” na sisi Waislamu hatudai kinyume na hivyo, na wala hatudai kuwa kuna kiumbe yeyote mwenye kujua ghaibu. Ndiyo, Allah Mtukufu kwa hekima Yake, rehema Yake, na kwa maslahi ya waja, na kwa ajili ya kuwaongoza watu, anaweza kuwajulisha baadhi ya waja Wake baadhi ya ghaibu au baadhi ya elimu Yake, na si elimu Yake yote. Hivyo Allah hajamjulisha yeyote miongoni mwa viumbe, wala miongoni mwa wanadamu na Malaika, yote anayoyajua. Hivyo kuna elimu aliyonayo Allah tu, Yeye binafsi, na pia kuna ghaibu ambayo Allah hajamjulisha yeyote miongoni mwa viumbe wote. Lakini ni kundi gani analolijulisha miongoni mwa waja Wake? Ni Manabii kwa mfano, Mitume, au baadhi ya Malaika. Hawa ndio waja anaowajulisha Allah elimu Yake au baadhi ya ghaibu, hivyo wao hujua yale aliyowajulisha Allah, na ndani ya mipaka aliyowajulisha, si zaidi ya hapo. Na wao huwa hawadai zaidi ya hapo, na hii ni mipaka ya maudhui, Mwenyezi Mungu anasema:
ۚ ون بِ َش ْي ٍء ِم ْن ِع ْل ِم ِه إِ اَّل بِ َما َشا َء َ َُو اَل ي ُِحيط 9
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 9
3/5/2016 3:11:06 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
“…..Wala hawajui chochote katika vilivyo kwenye elimu Yake ila kwa alitakalo…..” (Sura al-Baqarah; 2:255).
Na kwa upande wa kadiri ya elimu na mipaka ya maarifa, Manabii hawalingani katika maarifa na utambuzi. Wao ni wenye kutofautiana katika hilo, hususan kuhusu yale yatakayotokea mpaka siku ya Kiyama. Kwa mfano, Allah Ndiye mwenye kumwainishia yule ampaye elimu, mipaka ya elimu na kiwango cha elimu, mipaka ya maarifa na njia ya kumpia, sawa iwe ni elimu ya ghaibu au elimu nyingine. Njia Zenye Kuaminika Katika Kuitambua Ghaibu: Kwa upande binafsi wa elimu ya ghaibu, na pia elimu ya mustakabali, hakuna njia ya kuijua isipokuwa njia ambayo chanzo chake na marejeo yake ni Allah Mtukufu. Kwa mfano, sisi tunaamini kwamba Qur’ani Tukufu ni Kitabu cha Allah Mtukufu, alikiteremsha katika moyo wa Nabii Wake wa mwisho, Muhammad . Na elimu hii ni kutoka kwa Allah, na katika Qur’ani kuna habari kuhusu mustakabali na ghaibu ijayo, hivyo njia hii inakuwa ni ya kuaminika. Ama kuhusu namna ya kuzifahamu Aya, huo ni utafiti mwingine. Au njia ya maelezo ya Manabii kutoka kwa Manabii, au yaliyosikiwa na kizazi cha kwanza kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu , au yaliyotufikia, sawa iwe kwa njia ya Ahlul-Bayt au yaliyosikiwa kutoka kwao . Hii ndio njia pekee iliyopo mbele ya mwanadamu, inayomwezesha kuujua mustakabali kwa elimu sahihi na yakinifu, na si kwa dhana na shaka. Na huu ndio upande muhimu zaidi ambao nimenuwia kuuzungumzia kwa undani, na tunataka kuainisha namna ya kupata maarifa na namna ya kujua, na kuainisha wajibu wetu, na ni kwa namna ipi tunawajibika kuamiliana na aina hii ya habari zinazohusu 10
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 10
3/5/2016 3:11:06 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
mustakabali, hususan zinazohusu zama za mwisho, habari za kudhihiri Mahdi na mfano wa hizo. Njia mbalimbali za kuijua ghaibu: Lakini kabla ya kutaja njia hizo, kuna njia kadhaa nyingine ambazo watu wamekuwa wakizitumia katika muda wote wa historia. Tangu zamani, watu wenye kutilia umuhimu suala la kujua mustakabali wamekuwa wakitegemea njia kadhaa katika kutaka kupata maarifa na habari, kati ya njia hizo ni: 1.
Unajimu: Wamekuwa wakitegemea elimu ya unajimu na elimu ya falaki. Na kuna wataalamu wengi wa elimu ya falaki, na inasemwa kuwa mtaalamu wa elimu ya falaki husoma mwendo wa sayari, nyota, mwezi, mzunguko wake na utembeaji wake, hivyo ikiwa hivi itakuwa hivi….na kwa kupitia kusoma mwendo wa nujumu husoma mustakabali, hivyo utakuta wakisema: ‘Fulani atafariki siku fulani. Na kutatokea vita au amani.’ Na husema kuwaambia wafalme: ‘Msipigane vita katika mwaka fulani. Au piganeni vita katika mwaka fulani.’ Na haya ndio tunayoyashuhudia katika habari.
2.
Kupiga ramli: Huenda kwa mtu mwenye kupiga ramli, na yeye husema kwa mfano ‘Utaruzukiwa watoto watano, siha yao itakuwa hivi na vile, na majina yao ni fulani na fulani.’ Au kuhusu biashara, fanya biashara fulani, au usiingie katika biashara fulani. Na mengineyo.
3.
Kutizamia: Nako kuna namna nyingi, kama vile kusoma kiganja na mistari yake, au kutazamia kwa baadhi ya wanawake kwa kupitia kikombe, na kwamba itakuwa hivi na vile.
4.
Elimu ya tarakimu, herufi na jumla: Huhesabu herufi, nazo zina namba, na kuhesabu jumla yake, na kutokana na hesa11
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 11
3/5/2016 3:11:06 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
bu hizo anatoka na hitimisho na matokeo kwamba itakuwa hivi na vile. 5. Kuhudhurisha na kutumikisha majini: Baadhi ya watu kwa mfano, huhudhurisha majini, kisha huyauliza, na yenyewe humjibu na kumweleza habari za mustakabali, na yeye huwaeleza watu. Na hapa kuna tatizo la msingi, na baadhi ya watu wanachanganya mambo, na wanadhani kuwa majini yanajua ghaibu. Kwa yakini kabisa bila shaka yoyote ni kwamba majini hawajui ghaibu, wao ni kama wanadamu. Sisi wanadamu kwa mfano, tunazungumza mambo ambayo baadhi yake huwa ni sahihi, kadhalika jini, linachambua mambo lakini halijui ghaibu. Allah Mtukufu katika Sura Sabai anawazungumzia majini, kwamba wao walikuwa wakimtii Sulayman D na wakifanya kazi ya kumtumikia. Na wakati wa kutolewa roho yake D alikufa ilihali amesimama kwa kuegamia fimbo yake, huku majini wakiendelea na shughuli zao, na hawakujua kwamba Sulayman amefariki, nalo ni jambo la wakati uliyopo, itakuwaje sasa kuhusu jambo la mustakabali. Mpaka pale wadudu walipokuja na kuanza kula fimbo yake kidogo kidogo, Mwenyezi Mungu anasema:
َ ض ْينَا َعلَ ْي ِه ْال َم ْو ت َما َدلَّهُ ْم َعلَ ٰى َم ْوتِ ِه إِ اَّل َ َفَلَ َّما ق ت ْال ِج ُّن ِ َض تَأْ ُك ُل ِم ْن َسأَتَهُ ۖ فَلَ َّما َخ َّر تَبَيَّن ِ َْدابَّةُ أْالَر ب َ أَ ْن لَ ْو َكانُوا يَ ْعلَ ُم َ ون ْال َغي ِ ْب َما لَبِثُوا فِي ْال َع َذا ين ِ ْال ُم ِه 12
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 12
3/5/2016 3:11:06 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
“Tulipomkidhia mauti, hapana aliyewajulisha mauti yake ila nyama wa ardhi aliyekula fimbo yake. Alipoanguka majini walim tambua lau kuwa wangelijua ya ghaibu wasingelikaa katika adhabu ya kufedhehesha.” (Sura Sabai; 34:14).
Hivyo kama wangekuwa wanajua ghaibu wangejua kuwa amekufa. Na hata majini wenyewe wanajua kuwa hawajui ghaibu, lakini somo hili lilikuwa ni kwa ajili ya wanadamu ili wapate kujua kwamba hakuna yeyote ajuaye ghaibu isipokuwa Allah na yule mja ambaye kajulishwa ghaibu hiyo na Allah. 6.
Kuhudhurisha roho za wafu: Miongoni mwa njia wanazokimbilia watu wengi, si Mashariki tu hata huko Magharibi, Ulaya, Marekani na maeneo mbalimbali, ni njia ya kuhudhurisha roho za watu. Njia hii ina mitindo mbalimbali, miongoni mwa mitindo yake – huu upo Lebanon – ni kwamba mtu anakuja na kipande cha ubao au kipande cha karatasi ngumu, anaandika juu yake Aya fulani au herufi za Abjadi. Analeta kikombe na kukiweka katikati, na baadhi yao huanza kusoma Aya za Qur’ani, na hatimaye huiita roho ya maiti fulani na kuitaka ije kutoka kwenye ulimwengu wa Barzakh, nayo hudhihirika kupitia kikombe. Kisha huanza kuielekezea maswali, na hapo kikombe hucheza kwa kutembea juu ya herufi na hatimaye hutengeneza maneno.
Kuna watu wengi Lebanon wamepoteza muda wao kwa hili. Na huko Najaf Tukufu wakati nilipokuwa masomoni, kulikuwa na baadhi ya wanafunzi wenye kujishughulisha na visa hivi, nami baada ya muda mchache nitasema jibu la Shahid Swadri5 kuhusu wao. Wanaitakidi kwamba wanazivuta roho za wafu ili waziulize kuhusu makosa yao na uzoefu wao. Kwa mfano roho ya babu yetu 5
Huyu ni Shahid Sayyid Muhammad Baqir Swadri, Mungu awe radhi naye. 13
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 13
3/5/2016 3:11:06 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
ituoneshe ilipo hazina ya mali. Huu ni mtindo mmoja miongoni mwa mitindo mingi. Na kuna mtindo mwingine unaotegemewa sana huko Magharibi (Ulaya), huonesha kuwa wao wameivuta roho ya maiti na kuiingiza kwa mtu aliye hai, naye huongea kwa ulimi wa maiti. Na hii pia ni moja ya njia ya kujua habari za mustakabali na za ghaibu. Je kikombe kinatikisika na kutembea chenyewe bila kitu? Bali ni kitu ndicho kinachokitikisa. Siku moja tukiwa kundi, tulikwenda kwa Sayyid Swadri huko Najaf, na Shahid Swadri alizungumzia maudhui hii, kwamba anayetikisa kikombe si roho ya maiti. Akasema: ‘Kwa mfano, Sheikh Tusi, mmoja kati ya wanazuoni wetu wakubwa, ameutumia umri wake wote katika kutafuta elimu na ujuzi, na amehamia kwenye ulimwengu mwingine kupumzika. Mara eti wanakuja watu kuleta upuuzi wa kikombe na kuileta roho ya Sheikh Tusi ndani ya kikombe?! Kutikisika kwake kwa kutembea kunaweza kufanywa na majini. Ni nani kasema kuwa Allah ametoa uwezo wa namna hii mpaka wao waweze kuhudhurisha roho za wafu? Jambo hili haliingii akilini na halina hoja ya kisharia. Na hata kama tukijaalia kuwa hii ni roho ya maiti, je maiti wakati alipokuwa hai alikuwa anajua ghaibu? Sisi wenyewe (tulio hai) hatujui yeye yuko wapi? Na ni jambo lipi Allah amemruhusu kulijua? Roho ya maiti inaweza kujua mambo ya nyuma iliyoishi nayo na baadhi ya ghaibu, na hii si njia ya kujua ghaibu. Vyovyote iwavyo, na kabla ya kuhamia kwenye nukta inayofuata, ni kwamba nukta zote sita nilizozitaja ni dhana tu na mawazo hewa na wala hazijulishi ghaibu. Na dalili juu ya hilo ni kwamba nyingi kati ya habari za wanajimu, wanafalaki, watazamiaji, waita majini, wahudhurisha roho, na watu wa hesabu na tarakimu, nyingi kati ya habari zao huwa hazisihi. Sehemu ya habari zao huwa sahihi na sehemu nyingine huwa si sahihi, na ile sehemu inayokuwa sahihi haijulishi kuwa njia ya kujulia habari hiyo ni sahihi. Hapa tulipo sisi 14
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 14
3/5/2016 3:11:06 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
si wanajimu wala si wanafalaki, wala si, mpaka mwisho, lakini tunapokuja na kuanza kuchambua na kutathmini hali ya kisiasa, kuna mambo yatasihi katika uchambuzi wetu na kuna mambo hayatasihi. Na kutokusihi kwa baadhi ya uchambuzi na habari kunatosha kuwa dalili ya kwamba njia hii si sahihi, na kwamba kila kinachosemwa katika njia hii ni dhana tu. Na hivyo hivyo mjamzito kwa mfano, atazaa ima mtoto wa kiume au wa kike, na mwaka ujao tunaweza kuingia katika vita au tusiingie. Kadhalika wanaozungumza katika runinga kwa kutoa matarajio fulani, ikiwa matarajio yao hayo watadai kuwa ni kutokana na elimu ya ghaibu, kwa kweli hilo litakuwa ni tatizo kubwa, na ni jambo la haramu na halijuzu, na si sahihi. Ndiyo, yeye anaweza kusema: kutokana na muono wangu na uchambuzi wangu mimi nataraji hivi na vile. Hapo hapana tatizo, lakini zote hizo ni dhana, na kufanya hivyo si kutoa wala kuelezea habari za mustakabali. Ndoto na Uhusiano Wake na Mustakabali: Na kuna njia nyingine nataka kuielezea, nayo ni ya ndoto. Kwa mfano mtu kaona ndotoni kuwa kumetokea vita katika Nchi fulani, na kaona hivi na vile, hakika jambo hili lipo leo. Leo hii kuna runinga zinajishughulisha na kutafsiri ndoto, na wakati anajibu huyatoa maneno yake kwa sura ya yakini na uhakika wa kila jambo, na kwamba ndoto hiyo na tafsiri yake inayotolewa vina uhusiano na mustakabali. Na dalili yao ni kwamba fulani aliona hivi na vile ndotoni na jambo hilo hivi sasa lipo. Maudhui ya ndoto na njozi ni somo refu lenye kina kirefu. Lina uhusiano na maudhui ya tiba, utamaduni, dini na sayansi. Kuna elimu kubwa yenye kuzungumzia maudhui hii, hivyo hapa tutafupisha fikra kwa kutaja mambo matatu, nayo ni: 15
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 15
3/5/2016 3:11:06 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
Kwanza: Hapana shaka kwamba watu huona mambo ndotoni, na jambo hili halihitaji dalili. Pili: Ndoto hizi zinaweza kuwa ni ndoto zilizoparaganyika. Tatu: Kuna aina za ndoto ambazo ni ndoto za kweli, na mimi sizungumzii ndoto za Manabii, kwani ndoto zao ni sehemu ya Wahyi na mawasiliano ya Mwenyezi Mungu na Manabii Wake. Kwa mfano Nabii Yusuf, aliona jua na mwezi, huu ni Wahyi. Na ndoto ya Mtukufu Mtume ya kuukomboa Mji wa Makkah, huu pia ni Wahyi. Na ndoto ya kweli si sharti kwamba ni lazima aiote muumini au mchamungu na walii miongoni mwa Mawalii wa Mwenyezi Mungu, bali ni kwamba mtu yeyote yule anaweza kuota ndoto ya kweli. Mwenyezi Mungu ametusimulia kuhusu Mfalme wa Misri, aliposema:
ُ َِوقَا َل ْال َمل ان يَأْ ُكلُه َُّن َس ْب ٌع ٍ ك إِنِّي أَ َر ٰى َس ْب َع بَقَ َرا ٍ ت ِس َم ٌ ِع َج ۖت ٍ ت ُخضْ ٍر َوأُ َخ َر يَابِ َسا ٍ َاف َو َس ْب َع ُس ْنبُلا “Na akasema mfalme: Hakika mimi nimeota ng’ombe saba walionona wanaliwa na ng’ombe saba waliokonda; na mashuke saba mabichi na mengine makavu…..” (Surat Yusuf; 12:43)
Na pia:
احبَ ِي ال ِّسجْ ِن أَ َّما أَ َح ُد ُك َما فَيَ ْسقِي َربَّهُ َخ ْمرًا َ يَا ِ ص ۚ ۖ َوأَ َّما آْال َخ ُر فَيُصْ لَبُ فَتَأْ ُك ُل الطَّ ْي ُر ِم ْن َر ْأ ِس ِه ان ِ ُق ِ َض َي أْالَ ْم ُر الَّ ِذي فِي ِه تَ ْستَ ْفتِي 16
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 16
3/5/2016 3:11:06 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
“Enyi wafungwa wenzangu wawili! Ama mmoja wenu atamnywesha bwana wake mvinyo. Na ama mwingine atasulubiwa na ndege watamla kichwa chake. Imekwishakatwa hukumu ya hilo jambo mlilokuwa mkiuliza.” (Surat Yusuf: 12:41)
Hizi (mbili) ni ndoto za kweli. Ndiyo, kuna ndoto zilizoparaganyika, na ndoto za kweli, na jambo hili katika kiwango cha fikra halina ubishi. Lakini sisi hatuwezi kutegemea ndoto, sawa ziwe ndoto za kweli au ndoto zilizoparaganyika. Ama ndoto za Manabii, hilo ni jambo jingine. Na hata tukiweza kuainisha kuwa ndoto hii ni ya kweli, ni nani atakayeifasiri? Kwa mfano, ndoto ya Firauni ni nani aliyeifasiri? Ilihitaji Nabii. Pia ndoto ya wafungwa wawili. Ni nani atakayetoa hitimisho katika tafsiri? Hili linahitaji Nabii. Je Ndoto ni Hoja? Lililo wazi kwetu ni kwamba ndoto si hoja kwa upande wa kisharia, na wala hawezi yeyote kusema nitafanya hivi na vile kwa sababu niliota hivi na vile. Au nataka kuacha biashara au kumtaliki mke wangu, au kwamba mmoja wao yuko katika medani ya vita msitari wa mbele, na ana uwezo wa kombora fulani, na ameshambulia kwa makombora bila kurudi nyuma, kwa sababu tu ameona ndotoni kuwa kalazimishwa hivyo. Ndiyo, ndoto zina athari ya kisaikolojia. Huleta matumaini, mwisho ni kwamba zina baraka, lakini si suala la kimaudhui (si kila ndoto), na Allah hafanyi jambo kwa upuuzi, lakini je ndoto ni njia yakinifu ya uhakika ambayo tunaweza kuitegemea? Jibu ni kwamba hatuwezi kuitegemea wala kuifanya kigezo. Kwa nini Allah Amefunga Mlango wa Ghaibu? Allah kwa upole Wake na ukarimu Wake amemrahisishia mwanadamu milango mingi ya elimu na maarifa, ambapo leo hii katika ulim17
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 17
3/5/2016 3:11:06 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
wengu wa teknolojia na mawasiliano na tafiti za kiakili na kifalsafa, kuna mambo mengi. Lakini Allah amefunga mlango wa elimu ya ghaibu, kwa nini? Allah aliyetupa uwezo wote tulionao na akatufungulia milango mingi ya elimu na maarifa, amefunga mlango wa ghaibu kwa hekima, kwani tunajua kwa yakini kwamba Allah si bakhili. Atakuwaje bakhili ilihali Yeye ndiye Mkarimu kushinda wakarimu wote. Na ni kwa ajili hii, Allah Mtukufu, kwa ajili ya kutuhurumia, ameufunga mlango huu. Mfano: Ikiwa mmoja miogoni mwetu Allah atampa elimu ya ghaibu, na akafahamu kuwa baba yake atafariki siku fulani, na mama yake siku fulani, na kwa maradhi fulani, na mke wake pia na mtoto wake watafariki siku fulani kwa maradhi fulani, swali hapa ni kwamba: Itakuwaje hali ya mtu huyu baada ya kujua kwake? Kwa mfano Allah akimjulisha mtu elimu ya vifo, na akawa na jedwali la kila anaowajua, na kujua jinsi watakavyokufa na ni lini watakufa, je atapata raha ya maisha mtu huyu? Hivi sasa tunapojua kwamba mtu fulani karibu atakufa huko hospitali, siku tatu zijazo, kwa maradhi ya kansa, kwa kweli huwa hatuwezi kuvumilia kumuona pindi tunapomtazama. Sasa tutawezaje kuvumilia maarifa haya? Na hata Manabii , uwezo wao wa kuvumilia na kuweza ulikuwa unatofautiana. Na Allah kwa sababu ni mwingi wa huruma kwetu, na kwa kuwa alitaka tuwe na maisha mazuri, alitufungia mlango huu. Pia Allah alitaka tujitume na kujibidiisha na kujitahidi, tujifunze na kujifundisha, tufanye subira na tuvumilie, kwani dunia hii ni dunia ya mitihani, na ni sehemu ya kutengeneza ukamilifu na sifa kupitia mitihani na majaribu yake. Hivyo kama kila kitu kitakuwa bayana mbele yetu maisha yatasimama, nayo Allah ameyaweka kwa hekima. Hivyo baadhi ya ghaibu ambayo Allah aliwaeleza Manabii Wake ni kwa kadiri ya maslahi yanayohusu maisha ya watu, dini yao, mustakabali wao na raha yao 18
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 18
3/5/2016 3:11:06 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
ya dunia na Akhera. Kwa huruma hiyo na hekima hiyo Mwenyezi Mungu hajafungua mlango huu. Tutawezaje Kujua Habari za Mustakabali? Hivyo basi, muhtasari tunaokwenda nao kwenye muhadhara wa usiku ujao, ambao ni sehemu ya pili, ni kwamba tunapotaka kujua habari za mustakabali, njia pekee itakayotufikisha katika maarifa sahihi, salama na yenye kutia matumaini juu ya habari za mustakabali angalau kwa kiwango cha chini, ni ile ambayo msingi wake ni chanzo cha kiungu. Na itategemea pia jinsi tutakavyokifikia, na tutakapokifikia itategemea tena jinsi tutakavyoamiliana nacho. Na ni kutokea hapo nitaingia kwenye maudhui ya alama na zama za mwisho. Walhamdulilahi Mola wa walimwengu wote.
19
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 19
3/5/2016 3:11:06 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
FASLU YA PILI MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA HABARI ZA GHAIBU NA MUSTAKABALI6 Qur’ani na Sunna ndio Vyanzo Muhimu vya Ghaibu:
K
atika muhadhara uliotangulia tulisema kwamba watu wa sasa na wa zamani ni wenye kutilia umuhimu mkubwa habari za mustakabali. Tukasema kwamba, habari zake (mustakabali) ni sehemu ya ghaibu, na wala haijui isipokuwa Allah, na Allah Mtukufu amezuia maarifa haya dhidi ya watu wa kawaida. Ijapokuwa Yeye amewafungulia milango mingi ya maarifa lakini amezuia aina hii ya maarifa dhidi yao. Amefanya hivyo kwa kuwahurumia ili maisha yao yaendelee na kwenda katika namna ya kawaida. Lakini Allah huwajulisha ghaibu baadhi ya waja Wake, kwa hekima na lengo maalum. Na hekima tuliyoifikia ni kwamba njia pekee yenye kufikisha katika habari za ghaibu ni kuwa habari hiyo iwe inarejea kwa Mjuzi wa ghaibu, naye ni Allah Mtukufu, na tuipate habari kupitia njia hii, na iliyo muhimu zaidi ni wahyi. Na sisi Waislamu tuna vyanzo viwili muhimu sana katika upande huu. Chanzo cha kwanza ni Qur’ani Tukufu, na chanzo cha pili ni Hadithi Tukufu na riwaya tukufu zilizotufikia. 6
Hotuba hii aliitoa Sayyid Hasan Nasrullah, Mungu amhifadhi, huko Beirut, Lebanon, usiku wa mwezi tano Muharam, 1436 A.H. sawa na 31 – 10 - 2014 A.D. Ilikuwa ni katika kikao cha maombolezo ya Ashura. (Inaonekana ilikuwa ni usiku wa mwezi sita Muharam, na si usiku wa mwezi tano – Mtarjumi.) 20
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 20
3/5/2016 3:11:06 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
Ama kuhusu chanzo cha kwanza ambacho ni Qur’ani Tukufu, sisi Waislamu tumekongamana kwamba yaliyomo humo kwa yakini kabisa yamekuja kutoka kwa Allah, na kila kilichomo humo ni kutoka kwa Allah, na kwa ajili hiyo ndio maana husemwa katika istilahi yake: ‘Hakika yenyewe ni chanzo yakinifu’, yaani kwa yakini kabisa imetoka kwa Allah, haina shaka ndani yake wala mjadala. Na yote yaliyomo baina ya gamba mbili ni maneno ya Allah. Hivyo jambo muhimu linalobakia hapa ni sisi kufahamu maana za Aya za Qur’ani na makusudio yake. Ama Aya zenyewe ni kutoka kwa Allah Mtukufu, ni yakini isiyo na shaka kwamba imetoka Kwake. Quran Tukufu Inavyozungumzia Mustakabali: Katika Quran Tukufu kuna habari nyingi za ghaibu na mustakabali, bali sehemu kubwa ya Qur’ani inazungumzia upande huu ikiwa tutakwenda kwenye maana ya ghaibu kwa maana pana, kama nilivyofafanua huko nyuma. Ama maudhui ya mazungumzo yetu kuhusu mustakabali, habari za ardhi na matukio mbalimbali, mambo hayo Qur’ani imeyazungumzia katika maeneo mbalimbali, lakini habari za mustakabali zilizozungumziwa na Qur’ani hazikuwa na mahusiano na matukio ya mwisho wa zama tu, bali kwa hekima maalumu ziligusa hata matukio ya karibu na zama za Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu . Miongoni mwa mifano juu ya hilo ni Sura Rum, Mtukufu Mtume alikuwa Makkah. Waumini wakiwa wachache na Mushirikina wengi. Mara kukatokea mapigano na vita baina ya mamlaka mbili za wakati huo, Uajemi na Urumi. Hizi zilikuwa ni mamlaka mbili kubwa. Uajemi ilikuwa ni mamlaka ya Majusi, na Urumi ilikuwa mamlaka ya Wakristo, na hatimaye Uajemi ya Majusi ikaishinda Urumi ya Wakristo. Mushrikina wa Makkah wakafurahi, kwa sababu wao walizingatia kuwa Majusi Washirikina wamewashinda Waumini 21
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 21
3/5/2016 3:11:06 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
Wakristo. Hivyo wao wakalichukulia tukio hili upande wa kheri kwao, kwa maana ya kwamba na wao watamshinda Muhammad . Ndipo ikaja Sura maalum kuja kutoa habari:
ض َوهُ ْم ِم ْن بَ ْع ِد ِ َالم ُغلِب ِ ْت الرُّ و ُم فِي أَ ْدنَى أْالَر ين ۗ لِهَّلِ أْالَ ْم ُر ِم ْن قَ ْب ُل َ ُِون فِي بِضْ ِع ِسن َ َغلَبِ ِه ْم َسيَ ْغلِب ۚ ِ َّون بِنَصْ ِر للاه َ َُو ِم ْن بَ ْع ُد ۚ َويَ ْو َمئِ ٍذ يَ ْف َر ُح ْال ُم ْؤ ِمن َّحي ُم ُ يَ ْن ِ ص ُر َم ْن يَ َشا ُء ۖ َوهُ َو ْال َع ِزي ُز الر “Alif Lam Mim. Warumi wameshindwa. Katika nchi iliyo karibu. Nao baada ya kushindwa kwao watashinda. Katika miaka michache. Amri ni ya Mwenyezi Mungu kabla yake na baada yake. Na siku hiyo waumini watafurahi. Kwa nusra ya Mwenyezi Mungu. Humnusuru amtakaye; na Yeye ndiye Mwenye uwezo, Mwenye kurehemu.” (ar-Rum: 30:1-5)
Lengo la kutoa habari hii ni kueleza imani ya Mtume wa Mwenyezi Mungu juu ya yale anayoyasema kupitia wahyi unaoteremshwa kwake, na ni ili kuitia nguvu imani ya Waislamu. Yaani utoaji huu wa habari katika zama zile ulikuwa na malengo na hekima maalum. Na katika eneo lingine idadi ya Mushrikina ilikuwa ni kubwa na Waislamu wachache, na daima Mushrikina walikuwa wakiwaambia Waislamu ni lazima tutawashinda. Na kwa dhahiri kauli yao ilikuwa inaingia akilini, kwani kulikuwa hakuna ulingano wa nguvu za kimada baina ya makundi mawili, si kwa upande wa idadi wala upande wa vifaa, au upande mwingine. Lakini mapema kabisa huko Makkah Allah akasema, nazo ni miongoni mwa Aya zilizotoa changamoto: 22
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 22
3/5/2016 3:11:07 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
ص ٌر َسيُ ْه َز ُم ْال َج ْم ُع َ ُأَ ْم يَقُول ِ َون نَحْ ُن َج ِمي ٌع ُم ْنت ون ال ُّدبُ َر َ َُّويُ َول “Au ndio wanasema: Sisi ni wengi tutashinda? Wingi wao huu utashindwa, na watasukumwa nyuma.” (Sura al-Qamar: 44 – 45.)
Hivyo Allah akawaahidi Waumini ushindi wa karibu, na akatoa habari juu ya ushindi huo. Ushahidi wa tatu na wa mwisho, ni ule uliopatikana katika Sura al-Fat’hu:
ِّ ق للاهَّ ُ َرسُولَهُ الرُّ ْؤيَا بِ ْال َح ق ۖ لَتَ ْد ُخلُ َّن َ ص َد َ لَقَ ْد ين َ ِين ُم َحلِّق َ ِْج َد ْال َح َرا َم إِ ْن َشا َء للاهَّ ُ آ ِمن ِ ْال َمس ون ۖ فَ َعلِ َم َما لَ ْم تَ ْعلَ ُموا َ ُين اَل تَ َخاف َ ُر ُءو َس ُك ْم َو ُمقَصِّ ِر ك فَ ْتحًا قَ ِريبًا َ ِون ٰ َذل ِ فَ َج َع َل ِم ْن ُد “Hakika Mwenyezi Mungu amemhakikishia Mtume Wake ruiya ya haki. Bila ya shaka mtauingia Msikiti Mtakatifu, Inshallah, kwa amani, na hali mmenyoa vichwa vyenu na mmepunguza. Hamtakuwa na hofu. Alijua msiyoyajua. Mbali na haya aliwapa ushindi ulio karibu.” (Sura al-Fat’hu; 48:27).
Na tukio hili lilitokea na kuthibiti, ambapo Mtukufu Mtume pamoja na Waislamu waliingia Makkah wakiwa wamenyoa vichwa vyao.
23
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 23
3/5/2016 3:11:07 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
Mustakabali ni wa Waja Wema: Ama upande wa habari za mustakabali huko kuna Aya mbalimbali, ama upande wa madhumuni ya maudhui yetu nitazungumzia Aya tatu: Aya ya Kwanza: Ni kauli ya Allah:
ض َ َونُ ِري ُد أَ ْن نَ ُم َّن َعلَى الَّ ِذ ِ ْين ا ْستُضْ ِعفُوا فِي أْالَر ين َ ِارث ِ َونَجْ َعلَهُ ْم أَئِ َّمةً َونَجْ َعلَهُ ُم ْال َو “Na tunataka kuwafadhili waliodhoofishwa katika ardhi na kuwafanya wawe ni viongozi na kuwafanya ni warithi.” (Sura al-Qasas; 28:5.)
Mwenyezi Mungu anasema kuwa ana utashi, na kwamba atawafadhili waliodhoofishwa katika ardhi na atawaneemesha kwa kuwafanya wao kuwa viongozi na watawala wa ardhi, na wao ndio watakaoirithi ardhi hiyo kutoka kwenye mikono ya mamlaka na watawala wote. Aya ya Pili: Ni kauli ya Allah:
ت َ َو َع َد للاهَّ ُ الَّ ِذ ِ ين آ َمنُوا ِم ْن ُك ْم َو َع ِملُوا الصَّالِ َحا ين َ ف الَّ ِذ َ َض َك َما ا ْستَ ْخل ِ ْلَيَ ْستَ ْخلِفَنَّهُ ْم فِي أْالَر ض ٰى لَهُ ْم َ َِم ْن قَ ْبلِ ِه ْم َولَيُ َم ِّكنَ َّن لَهُ ْم ِدينَهُ ُم الَّ ِذي ارْ ت َولَيُبَ ِّدلَنَّهُ ْم ِم ْن بَ ْع ِد َخ ْوفِ ِه ْم أَ ْمنًا ۚ يَ ْعبُ ُدونَنِي اَل 24
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 24
3/5/2016 3:11:07 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
ك هُ ُم َ ِك فَأُو ٰلَئ َ ِون بِي َش ْيئًا ۚ َو َم ْن َكفَ َر بَ ْع َد ٰ َذل َ يُ ْش ِر ُك ون َ ُاسق ِ َْالف “Mwenyezi Mungu amewaahidi wale ambao wameamini na wakatenda mema kuwa hakika atawafanya makhalifa katika ardhi, kama alivyowafanya waliokuwa kabla yao. Na kwa yakini atawaimarishia dini yao aliyowapendelea na hakika atawabadilishia amani baada ya hofu yao. Wawe wananiabudu, hawanishirikishi. Na mwenye kukufuru baada ya hayo, basi hao ndio mafasiki.” (Sura Nur; 24:55).
Inazungumzia ahadi ya Mwenyezi Mungu aliyowapa waja wema waumini, kwamba Allah atawafanya makhalifa katika ardhi, atawaimarisha na watatawala, na watapata amani, usalama na utulivu bila mashaka wala khofu. Aya ya Tatu: Ni kauli ya Allah:
ُ بَلْ قَالُوا أَضْ َغ اث أَحْ لاَ ٍم بَ ِل ا ْفتَ َراهُ بَلْ هُ َو َشا ِع ٌر ون َ ُفَ ْليَأْتِنَا بِآيَ ٍة َك َما أُرْ ِس َل أْالَ َّول “Na hakika tulikwishaandika katika Zaburi baada ya ukumbusho kuwa Ardhi watairithi waja wangu walio wema.” (Sura Anbiyaa; 21:5).
Imeandikwa katika Zaburi kwamba mustakabali wa ardhi ni mustakabali wa watu wema, na ni jamii na serikali ya watu wema. Nususi hizi za Qur’ani ziko wazi na maana zake nazo ziko bayana sana. Kwa muhtasari ni kwamba mustakabali wa wanadamu na mustakabali wa ardhi utakomea kwa Waislamu waliodhoofishwa, nayo 25
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 25
3/5/2016 3:11:07 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
ni serikali itakayotawala zama za mwisho na kabla ya kusimama Kiyama. Uongozi wa Kiungu na Mustakabali wa Waja Wema: Maana hii inajulishwa na Aya nyingi, Aya ya kwanza imetaja utashi wa Allah “tunataka”, na Aya ya pili imetaja ahadi, na Aya ya tatu imetaja ‘imeandikwa’, isipokuwa ni kwamba Qur’ani Tukufu haijaeleza kwa ufafanuzi ni nani atakayesimamisha serikali hii ya kimataifa zama za mwisho. Haijamgusia kabisa, bali Mtukufu Mtume ndiye aliyemtaja, na wafasiri wanapofika katika Aya hizi huja na riwaya mbalimbali ili zitupe sura bayana kwamba, ahadi hii itatimia mwisho wa zama mikononi mwa mtu adhimu, mikononi mwa Mahdi , “Ambaye kupitia yeye Allah ataijaza ardhi usawa na uadilifu baada ya kuwa imejaa dhulma na ukandamizaji.”7 Na yeye anatokana na kizazi cha Mtume wa Mwenyezi Mungu , kutokana na kizazi cha Fatima , na riwaya zenye madhumuni haya ni nyingi kwa Shia na Sunni. Kadhalika sisi Waislamu tunaitakidi kurudi kwa Masihi Isa ardhini, na ni kwa mabega ya Mahdi na Masihi utatimia katika ulimwengu huu urithi wa Waumini waliodhoofishwa, walio wema. Na itajengwa juu ya ardhi hii mamlaka ya amani, uadilifu na raha, na kila alichokuwa akikitamani mwanadamu tangu mwanzo wa ukhalifa wake kitatimia, inshaallah. Habari za Mustakabali Katika Riwaya: Ama chanzo cha pili, nacho ni Hadithi Tukufu, na waliyoyapokea Waislamu kutoka kwa Mtukufu Mtume , au yaliyopokewa ku7
Sheikh Saduq, Muhammad bin Ali bin Babawayhi al-Qummiy, Kamalud-Din Watamamun-Niimah. Kimehakikiwa na kusahihishwa na Ali Akbari al-Ghafariy. Kimechapishwa mwezi wa Muharram mwaka 1405 - 1363, Uk. 308. Kimechapishwa na kusambazwa na Muasasatun-Nashri al-Islamiy uliyo chini ya Jumuiya ya Walimu wa Mji wa Qum. 26
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 26
3/5/2016 3:11:07 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
toka kwa Ahlul-Bayt , katika upande huu kuna mamia ya riwaya na Hadithi zinazohusu habari za mustakabali, ghaibu na zama za mwisho. Bali baadhi ya maulamaa wamesema kuna maelfu ya riwaya zinazozungumzia mustakabali na zama za mwisho. Kadhalika katika anwani za baadhi ya vitabu kuna mlango unaoitwa ‘al-Malamihu Wal-Fitan’, na makusudio yake ni kueleza habari za mustakabali. Na katika zama za karibuni baadhi ya maulamaa walifanya kazi ya kukusanya kila riwaya ambazo kwa namna moja au nyingine zina uhusiano na Mahdi na wakaziweka katika enklopedia za riwaya bila kuzisanifu na kuzihakiki. Hivyo kuna idadi kubwa ya riwaya kutoka kwa Mtukufu Mtume zenye kutusimulia kuhusu mustakabali. Na makusudio ya mustakabali hapa ni kipindi cha baada ya Mtukufu Mtume . Na mtu anaweza kuzigawa riwaya hizi katika vigawanyo mbalimbali, lakini mimi nitategemea vigawanyo vitatu, kwa sababu hivyo ndivyo vyenye uhusiano na hitimisho la utafiti huu. Vigawanyo vya Riwaya Zinazohusu Mustakabali: Kigawanyo cha kwanza: Ni habari za mustakabali na ghaibu ambazo hazijafungamana moja kwa moja na Imam Mahdi na serikali ya zama za mwisho, bali zenyewe zimezungumzia kwamba kutatokea jambo fulani katika zama zijazo. Kwa mfano ni kauli yake: “Watu au ummah wangu utafikiwa na zama ambazo kutakuwa na hivi na vile.”8 Na nyingi katika hizo hazijafungamana na Imam Mahdi . Na mfano mwingine katika kigawanyo hiki ni yale aliyoyaeleza Mtukufu Mtume kuhusu awamu maalum itakayotokea baada ya kifo chake, kwamba utakuja wakati ambao Bani Umayyah wata8
Sheikh Kulayni, Muhammad bin Yaqub, al-Kafi. Kimehakikiwa na kusahihishwa na Ali Akbari al-Ghafariy. Kimechapishwa mwaka 1365, Chapa ya Nne, Juz. 2, uk. 91 na 296. Na Juz. 8, uk. 308. Kimesambazwa na Darul-Kutubi al-Islamiyyah, Tehran. 27
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 27
3/5/2016 3:11:07 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
tawala. Na haya yapo katika riwaya zinazozungumzia dhulma na utekelezaji wa watawala wa Kibani Umayyah, na riwaya zinazozungumzia kuanguka kwa utawala wa Bani Umayyah. Kisha zinazozungumzia kuanguka kwa Bani Abbasi, na hali za Bani Abbas na uvamizi wa Mangolia. Na hali za ulimwengu, vita, watawala, viongozi, maulamaa, wasomi, wanawake na wanaume, uhusiano wa kijamii na uhusiano wa mtoto na familia yake. Kisha ni zile zinazozungumzia matukio ya kimaumbile kama vile kuchomoza jua kutoka Magharibi, kupatwa na jua au mwezi, mvua na matetemeko ya ardhi. Riwaya zote zenye kuzungumzia aina hii ya habari ni habari za mustakabali. Katika juzuu ya pili ya kitabu al-Irshad cha Sheikh Mufid,9 mmekusanywa humo majumui ya riwaya hizi zenye kuzungumzia mapambo, vitabu, misikiti na misahafu, na humo mna ufafanuzi mkubwa sana uliomo ndani ya vitabu vya Shia na Sunni. Na nyingi kati ya habari hizi kama tukiangalia ulimwengu wa sasa na yanayoendelea, na yale yaliyotokea huko nyuma, tutakuta kwamba mengi yaliyotajwa na riwaya na hadithi hizi yametimia na kutokea. Kigawanyo cha pili: Ni habari zinazoelezea alama na matukio ambayo yanafungamana moja kwa moja na Imam Mahdi , au yana aina fulani ya mafungamano na yeye, isipokuwa ni kwamba habari hizi hazijasema kuwa kuna mafungamano ya wakati baina ya Mahdi na kutimia kwa habari hizo, bali zimeacha maudhui ikiwa huru upande wa wakati bila kuainisha umbali wa muda uliopo baina ya kutokea matukio hayo na kudhihiri kwake . Hivyo baadhi ya matukio yanaweza kutokea muda mrefu au karne nyingi kabla ya kudhihiri Mahdi , na Mwenyezi Mungu Ndiye ajuaye zaidi. 9
al-Mufid, Muhammad bin Muhammad, al-Irshad Fii Maarifat Hujajullah Alal-Ibad. Kimehakikiwa na kusahihishwa na Muasasat Aal-Bayti . Kimechapishwa mwaka 1413, Chapa ya Kwanza, Juz. 2, uk. 368. 28
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 28
3/5/2016 3:11:07 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
Kwa mfano riwaya inaposema: “Jambo hili halitatimia kabla ya kuwa hivi na vile.” Au “Hamtayaona myapendayo kabla ya kuwa hivi na vile.”10 Matukio haya na mambo haya yanafungamanishwa na Mahdi kwa maana ya kwamba yatatokea kabla ya kudhihiri kwake, lakini bila kuainisha umbali wa muda uliopo baina ya kutokea matukio hayo na kudhihiri kwake . Na wala haizuiliwi kutajwa pamoja baadhi ya habari za kigawanyo cha kwanza na cha pili, kama vile kutajwa Dola ya Bani Abbas na kuanguka kwao, habari ambazo zimetajwa katika kigawanyo cha kwanza, lakini umbali wa muda uliopo baina ya Dola ya Bani Abbas na kudhihiri Mahdi haujulikani. Ama kigawanyo cha tatu, ni habari zinazotaja matukio yanayofungamana na wakati. Katika riwaya hizo kuna maneno yaliyofungamana na wakati, na kwamba kuna matukio yatakayokutana na kudhihiri kwa Imam Mahdi , na kuna uainisho wa wakati, kwa mfano itakuwa katika Mwezi wa Ramadhan, au katika mwaka mmoja, yaani habari zimeainisha wakati. Aina hii ya alama, kwa sababu ina mafungamano ya wakati na Imam Mahdi tunaiita kuwa ni ‘Alama Makhususi’, na riwaya za namna hii zipo kwa Mashia na Masuni. Mfano wa riwaya hizo ni kama ile ya kujitokeza kwa Sufiyaniy,11 Khurasaniy12 na Yamaniy.13 Na alama hapa ni kujitoke Ibn Zaynab Nuumaniy, kitabu al-Ghaybah, kimehakikiwa na Faris Hasun Karim, Chapa ya Kwanza, mwaka 1422, uk. 33 – Qum, kimesambazwa na Anuwarul-Huda. 11 Huyu ni uzao wa kizazi cha Abu Sufiyani – Mtarjumi. 12 Huyu ni mzawa wa Mji wa Khurasani – Mtarjumi. 13 Huyu ni mzawa wa nchi ya Yemeni – Mtarjumi. Sheikh Saduq, Muhammad bin Ali bin Babawayhi al-Qummiy, kitabu al-Khiswal. Kimehakikiwa na kusahihishwa na Ali Akbari al-Ghafariy. Kimechapishwa mwaka 1403, Juz. 1, uk. 303. Kimechapishwa na kusambazwa na Muasasatun-Nashri al-Islamiy uliyo chini ya Jumuiya ya Walimu wa Mji wa Qum. Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq kwamba alisema: “Mambo matano yatatokea kabla ya kudhihiri mwakilishi (Mahdi): Kujitokeza kwa Yamaniy na Sufiyaniy, kujitokeza kwa mwenye kunadi atakayenadi kutokea mbinguni, ….. na kuuwawa kwa Nafsu Zakiyyah. 10
29
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 29
3/5/2016 3:11:07 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
za, na inawezekana mtu husika yupo, lakini maneno hapa ni kuhusu kujitokeza, na wala si kuhusu mtu husika na kuwepo kwake duniani. Na miongoni mwa matukio yenye mafungamano ya wakati na yatakayokutana na kudhihiri kwa Mahdi , ni kuuwawa kwa Nafsi Zakiyyah katika Kaaba, baina ya Rukni na Maqam. Baadhi ya riwaya zinasema kuwa, atakayeuwawa ni kijana wa kihashimiya, atokanaye na ukoo wa Hasan, naye atakuwa ni kijana mdogo. Na pia miongoni mwa matukio hayo ni wito utakaotoka mbinguni. Riwaya zinataja kwamba Jibril atanadi mbinguni na kumtambulisha Mahdi . Atatoa habari zake na kutaja jina lake na kuwataka watu waweze kumsaidia, na kwamba atawahutubia kila watu kwa lugha yao, na kwamba sauti hii ndani ya sekunde moja itaingia ndani ya masikio yote ulimwengu mzima. Na sauti hii itakuwa na aina fulani ya ukali. Na baadhi ya riwaya zinaashiria mshituko utakaowapata watu kutokana na kusikia sauti hiyo. Na baada ya siku kadhaa au wiki kadhaa tangu kutokea kwa sauti hiyo ndipo atakapodhihiri Imam. Na baadhi ya riwaya zinasema kuwa ni siku hiyo hiyo. Pia miongoni mwa matukio yenye mafungamano ya wakati na yatakayokutana na kudhihiri kwa Mahdi , ni kuangamizwa kwa eneo la Baydai, kwani Sufiyaniy atakapojitokeza atatuma jeshi moja kwenda Hijaz na jingine kwenda Iraq. Jeshi atakalolituma kwenda Hijaz litatenda maovu huko Madina kama walivyofanya jadi zake na wahenga wake (Yazid bin Muawiya). Jeshi hili litaangamizwa mwanzoni mwa njia eneo lililopo baina ya Madina na Makkah, na wala hatabakia katika jeshi hili isipokuwa watu wawili, na habari hizi zipo kwa Masuni na Mashia. Na aina hii ya matukio huitwa matukio yenye kuambatana katika wakati mmoja, na habari zake zinazungumzia kipindi cha wakati mfupi, kipindi cha mwaka mmoja au miezi au siku kadhaa. Baadhi ya riwaya zimeshabihisha jambo hili
30
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 30
3/5/2016 3:11:07 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
na uzi katika ushanga14ambapo punje moja huifuata punje nyingine. Na matukio haya ni yenye kuungana, moja linalifuata jingine, na alama hizi huitwa kuwa ni alama makhususi. Hivyo basi tumepata vigawanyo vitatu vya riwaya: Kigawanyo cha kwanza ni zile habari zinazozungumzia mustakabali kwa ujumla. Na kigawanyo cha pili ni zile habari zinazofungamana na Mahdi lakini bila kufangamana moja kwa moja na wakati na muda. Na kigawanyo cha tatu ni zile habari zenye kufungamana na Imam Mahdi huku zikiwa na uhusiano na wakati maalum. Ama leo hii, baadhi ya watu wanaamiliana na alama na habari hizi kwa namna sahihi, na wengine wanaamiliana nazo kwa namna ya makosa, kama ilivyo katika kila kitu. Kama ilivyo katika elimu, maji na silaha, vitu ambavyo mtu anaweza kuvitumia vibaya, na pia anaweza kuvitumia vizuri. Faida ya kujua habari za mustakabali: Kuna faida gani ya sisi kujua na kutambua habari hizi zinazozungumzia zama za mwisho, na pia kujua alama, sawa ziwe zina mafungamano na Imam Mahdi au hazina mafungamano naye? Baadhi wanasema kuwa hakuna faida yoyote, sawa tuzijue au tusizijue, kwani ikiwa ni habari sahihi ni lazima zitatimia, na zitakapotimia tutazijua. Fikra hii si sahihi, kwani kujua na kujifunza na kuelewa jambo hili kuna faida nyingi sana: Faida ya Kiitikadi: Hakika Allah anapotuelezea habari za mustakabali, je aliziweka katika Qur’ani pamoja na Aya nyingine kama nyongeza na ziada au 14
Ibn Abi Zaynab, Muhammad bin Ibrahim, kitabu al-Ghaybah. Kimehakikiwa na Ali Akbari al-Ghafariy. Kimechapishwa mwaka 1397, Chapa ya Kwanza, uk. 255, humo mna: “Kutakuwa katika mwaka mmoja, mwezi mmoja na siku moja kule kujitokeza kwa Sufiyaniy, Yamaniy na Khurasaniy, kwa mpangilio kama mpangilio wa ushanga. 31
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 31
3/5/2016 3:11:07 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
ni kwa hekima maalum? Hakika Mwenyezi Mungu ana hekima na huruma katika kila ghaibu aliyowaeleza Manabii Wake. Na Mtukufu Mtume alipoeleza ufafanuzi wote huu kupitia riwaya mbalimbali, je alikuwa anawapa habari Waislamu kuhusu matukio haya kwa hekima, huruma na lengo maalum au la? Hakika bila shaka ni kwa lengo na hekima, na Allah alimjulisha ghaibu Mtume Wake na Manabii Wake kwa maslahi haya, hivyo basi hakika bila shaka ni kwamba kuna hekima maalum, sawa sisi tuigundue au tusiigundue hekima au faida hiyo. Kuwasadikisha Manabii: Na katika kiwango cha itikadi, ni kwamba kufuatilia hadithi hizi na kuzithibitisha na kuhakiki usahihi wake, ni jambo lenye faida kubwa, na daima Manabii walipokuwa wanakwenda kwa watu wao, walikuwa wanaombwa dalili na watu wao, na dalili ni muujiza. Na Mtukufu Mtume alikuwa na muujiza au miujiza ili jambo lisiwachanganye watu, isije ikawa kila mtu anadai unabii, utume na kuwa na mawasilianao na ghaibu. Na miongoni mwa miujiza ya Manabii waliotangulia, kwa mfano Musa na Isa , ilikuwa ni kueleza na kutoa habari za mustakabali, na kwamba kutatokea hivi na vile. Imepokewa kwamba Nabii Isa alikuwa akiwaeleza watu habari za ghaibu na yaliyomo majumbani mwao. Na Mtume wetu imepokewa kutoka kwake – baada ya kuthibiti nukuu hizi – kiasi hiki kikubwa cha habari zinazohusu mustakabali. Kisha tunasoma hali ya zamani na ya sasa na hatimaye tunakuta kwamba mengi kati ya yale aliyoeleza Mtukufu Mtume yametimia na kutokea. Je hii si dalili ya ukweli wa Nabii huyu? Bali si dalili ya adhama ya Nabii huyu? Je hii si dalili ya upana wa elimu ya Nabii huyu, ya kujua yaliyotokea huko nyuma na yatakayotokea mpaka Siku ya Kiyama? Sisi tunaoamini unabii wa Mtukufu Mtume Mu32
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 32
3/5/2016 3:11:07 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
hammad jambo hili linatuzidishia imani juu ya unabii wa Nabii wetu, na heshima ya kumheshimu Nabii wetu, na hili lina faida iliyo wazi. Pindi anapokuja mtu na kutueleza kuhusu jambo fulani na hatimaye likasihi, kisha akatueleza kuhusu jambo jingine nalo likasihi, akatueleza karibuni mambo mia na yote yakasihi, hali hii hutuzidishia hali ya kuamini uwezo wake hata kama hajazungumza jambo la ghaibu. Vipi sasa ikiwa Nabii wetu anatueleza kupitia wahyi na kwamba kutatokea hivi na vile katika kipindi cha miaka mia moja mpaka Siku ya Kiyama. Na yeye anazungumzia mambo ya ghaibu, na mengi kati ya hayo yametimia na kutokea, na yatatokea mengine huko mbeleni. Bila shaka hii ni faida ya kiitikadi itokanayo na maarifa, wakati ambapo kama tungepuuza uchunguzi huu na tukauacha katika vitabu tusingefaidika nao kwa chochote. Faida ya Kisaikolojia: Na hili ni jambo muhimu, nayo ni matarajio ya mustakabali. Leo hii mgandamizo wa kinafsi ni mkubwa kuliko wakati wowote ule uliopita. Katika zama zilizopita, matukio yanayotokea Mashariki hawakuwa wanayajua watu wa Magharibi. Yaliyokuwa yanatokea Iran hawakuwa wanayajua watu wa Afrika, kwa sababu mawasiliano yalikuwa mazito sana, kila mmoja alikuwa anajua mambo ya mji wake tu. Ama leo hii, kupitia setelaiti na vyombo vya mawasiliano tunasikia kila kitu na tunakiona, tunaathirika nacho na kutupa mgandamizo wa kinafsi. Na matukio yote yana muungano wa yenyewe kwa yenyewe kwa namna kubwa sana. Na ni kama ambavyo hapo zamani hapakuwa na miradi mikubwa kama ya leo hii. Miradi ya kuweza kuiendesha dunia nzima. Ama leo hii hali imebadilika. Leo kuna mizozo ya kimataifa 33
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 33
3/5/2016 3:11:07 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
na kikanda, mabalaa, maradhi changamoto na….katika Nyanja ya kifikra, kijeshi, kimazingira, kitamaduni na…. na mamilioni haya ya hawa wanadamu wenye kuongezeka. Na mambo yote haya hupelekea katika kushindwa iwapo hakuna matumaini. Hivyo basi, uwepo wa matumainini, uwepo wa nguzo, na matumaini hapa ni matumaini ya kiungu, kwamba utakuja wakati ambao Waumini wenye kudhoofishwa na walio waadilifu watatawala na wataleta amani na raha katika ulimwengu wote, na watafungua milango ya elimu kwa kiwango ambacho hajafikia yeyote. Na mwanadamu atajielekeza na kuvutika katika tumaini hili. Hali hii inatengeneza azma, utashi, na uvumilivu wa kutenda ili kuandaa na kuhudhurisha tumaini hili. Faida ya mwanzo ya kujua mustakabali: Na hili ni muhimu sana kwa upande wa ufafanuzi wa ndani pia, kwa sababu tukio la kiulimwengu lenye ukubwa kama huu, nalo ni tukio la kutoweka matwaghuti na mabeberu, na hatimaye kusimama serikali ya watu wema waumini waliodhoofishwa katika ardhi, ni tukio la kihistoria na la kiulimwengu ambalo halijawahi kutokea na ambalo halitokei kwa sekunde wala kwa ghafla, bali linahitaji utangulizi ili kulifikia. Hata katika kiwango cha dhihinia na fikra, kwani hakika wanadamu wanahitaji maandalizi kwa ajili ya tukio la kiulimwengu lenye ukubwa kama huu. Ndoto za Manabii zitatimia zama za mwisho, na jambo hili halitokei mara moja kwa ghafla, na wala haliwezi kutokea bila viashiria, alama na dalili, na wala hatuwezi kuamka na kuwakuta matwaghuti wote wameanguka ama kutoweka, na serikali ya uadilifu imesimama. Hivyo basi mwisho wa yote ni kwamba wanadamu wenyewe ndio nyenzo zitakazopelekea kupatikana serikali ya uadilifu wa kiungu. 34
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 34
3/5/2016 3:11:07 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
Hili linahitaji alama. Na jukumu letu ni kujiandaa kisaikolojia, kimaarifa na kufanya maandalizi kamili. Kwa mfano Nabii Musa , unabii wake ulikuwa wangojewa. Wana wa Israil walikuwa wanamngojea, tangu takribani mamia ya miaka kabla ya kutumwa kwake. Na katika kipindi hicho waliteswa na kufanywa watumwa wa Mafirauni, lakini walikuwa na tumaini waliloelezwa na Manabii wengine wa Kibani Israil, kwamba atakuja Nabii adhimu atakayekuokoeni kutoka kwa Firauni na matendo yake na dhulma yake. Na kulikuwa na alama za wakati huo atakaodhihiri Musa , na alama hizi Wana wa Israil walikuwa wanazijua, na hata Firaun na wasaidizi wake walizijua. Hivyo wakawa wanawachinja watoto wa kiume waliozaliwa ndani ya mwaka huo, ili waweze kuzuia kuzaliwa kwa Musa . Na Musa huyu mwenye kungojewa – ikiwa itasihi kumwita hivyo – ambaye watu wake walikuwa wakimngojea, hawakuwa wakimngojea bila chochote, bali walikuwa na alama walizokuwa wanazifanyia kazi. Pia Sayyid Masihi , alingojewa na Mayahudi wote, na pindi alipozaliwa na Mariam walimtuhumu Mariam na kumtuhumu, kwamba kitendo chake hicho ni dhambi kubwa. Lakini tambua kwamba hata hivyo walikuwa wanamngojea Sayyid Masihi tangu mamia ya miaka, na Manabii waliokuja kabla yake walikuwa wakimbashiri na wakimzungumzia, na alama za wakati atakaodhihiri zilikuwa zimeenea. Na Nabii wetu yumo ndani ya vitabu vya Mayahudi, na wao wanajua. Na walikuwa wanavizia kuzaliwa kwake na wakiwaambia Waarabu kwamba atazaliwa hapa Nabii wa zama za mwisho. Na tumaini hili lilikuwa linajulikana kwa Wakristo pia, na lilikuwa ni maarufu hata Iran, hivyo Salman al-Farsiy alikuja toka Iran ili afike kwa Mtukufu Mtume . 35
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 35
3/5/2016 3:11:07 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
Tukio lenye ukubwa huu, yaani la mfano kama huu wa kudhihiri Mahdi na kurudi aridhini Sayyid Masihi , halitokei ghafla bila utangulizi na maandalizi ya mwanzo ya kisaikolojia, kiroho, kimaarifa na kifikra. Wala bila maandalizi ya medani na watu, na pia bila ungojeaji chanya wa kweli na wa hakika. Kwa sababu kinachotakiwa kwa Sayyid Masihi si kurejea duniani ili Mayahudi wamfanyie njama upya, na wala kinachotakiwa kwa Mahdi si adhihiri ili watu wamtelekeze kama walivyomtelekeza babu yake Abu Abdillah Husein . Sio ili Karbala irudi upya na hatimaye kuwepo na ufiadini upya. Bali kinachongojewa ni kuwepo wasaidizi na watumishi wa kweli waumini ambao watairithi ardhi. Wakati huo ndipo Allah atakapotoa idhini kwa Mawalii wake waanze harakati na kudhihiri. Hivyo jambo hili halikomei katika faida hizi tu, lakini wakati haunipi fursa ya kuongeza zaidi ya hapo. Kulisogeza tumaini karibu: Faida nyingine ni kwamba, tunaona katika nchi zilizo mbali zinazohitaji kukata masafa marefu kuzifikia, kama vile Iran, wakati ukiwa unaendelea na mwendo mara nyingi wanakuwekea alama njiani zenye kukuonesha ukaribu wa masafa na idadi ya kilometa zilizopo. Jambo hili linakupa matumaini ya kufika, na kusogeza tumaini karibu, hivyo mtu hujiandaa kufika. Na sisi leo hii, tangu mamia ya miaka, ikiwa hakuna alama na ishara yoyote, basi jambo hili litatupeleka katika kuvunjika moyo. Na hata Aya za Qur’ani baadhi yake zinaelezea alama za mustakabali, kwamba ni alama za siku ya Kiyama. Wakati tunapokuwa na alama, habari na matumaini ya yale yatakayotokea, pindi ninapoambiwa kuwa kuna mambo mia moja 36
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 36
3/5/2016 3:11:07 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
yatatokea, na kwa mfano ishirini kati ya hayo yakatokea, hali hiyo itanisogezea tumaini karibu. Hivyo kufungamana na mustakabali ni jambo la lazima ili kutengeneza utashi, azma na ari. Alama na viashiria: Lakini ni wajibu kwetu kungojea alama ilihali tukiendelea kuwa na tumaini, lakini si alama ndio zenye kutengeneza tukio. Allah Mtukufu kwa utashi wake ameweka matukio na mazingira yatakayowezesha kutimia ahadi hii ya kiungu, na sehemu kubwa ya mazingira haya ni wajibu na majukumu ya wanadamu, lakini alama hizi zinatuonesha kuwa muda si mrefu na karibu tutafika. Ama alama makhususi zenyewe ni kiashiria chenye kuonesha muda wa karibu, kiasi cha mwezi au wiki au hata siku. Hivyo basi, alama hizi zinatupa kiashiria, mtazamo na muono, na tunatembea nao tukiwa na uongofu na maarifa bayana. Na mustakabali wetu unakuwa wazi bayana mbele yetu, na hili ni sharti la msingi katika mafanikio na kufaulu. Sasa umebakia uchunguzi wa mwisho, nao ni namna gani tutaamiliana na alama hizi na hadithi na riwaya zenye kutaja alama husika? Uchunguzi huo tutauhitimisha katika usiku ujao inshaAllah.
37
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 37
3/5/2016 3:11:07 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
FASLU YA TATU VIGEZO VYA KUFUATA WAKATI WA KUSOMA NA KUTABIKISHA ALAMA ZA KUDHIHIRI IMAM MAHDI15 Utangulizi: Tumefika katika nukta muhimu sana, na hitimisho tunalotaka kulifikia kuhusu riwaya zinazozungumzia habari za mustakabali, na yatakayotokea zama za mwisho, na hatimaye tufikie katika yale yenye mafungamano na suala la Imam Mahdi . Na nitajitahidi kumaliza uchunguzi huu ndani ya usiku huu. Mfumo unaofuatwa katika kuzifanyia kazi nususi za Sunna Tukufu: Pindi zinapokuja habari kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwamba alisema hivi na vile, ni wajibu tuchunguze ni nani aliyenukuu habari hizi kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu . Katika vitabu inapokewa kutoka kwa fulani, kutoka kwa fulani, kutoka kwa fulani, kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu , ni wajibu tuhakikishe kupitia kanuni na vipimo vya kielimu kwamba riwaya hizi zinakubalika na kwamba inaruhusiwa kuzitegemea. Na mimi hapa nataka kurahisisha maudhui na wala sitaki kutumia istilahi. Hakika Hadithi yoyote inayonukuliwa ina matini na sanadi, na mimi binafsi nimehifadhi hadithi kutoka kwa mmoja 15
Hotuba hii aliitoa Sayyid Hasan Nasrullah, Mungu amhifadhi, huko Beirut, Lebanon, usiku wa mwezi tisa Muharam, 1436 A.H. sawa na 02 – 11 – 2014 A.D. Ilikuwa ni katika kikao cha maombolezo ya Ashura. 38
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 38
3/5/2016 3:11:07 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
wa maulamaa wakubwa, na kutokana na uzuri wake na jamala yake imekaa kichwani mwangu, sanadi yake ni jamilu na matini yake ni nzuri. Ni kutoka kwa mmoja wa wapokezi, kutoka kwa Abu Hasan, kutoka kwa Abu Hasan, kutoka kwa Abu Hasan, kutoka kwa Hasan, kutoka kwa Hasan, kutoka kwa Hasan bin Ali , kwamba: “Hakika lililo zuri kushinda uzuri wote ni tabia njema.” Hapa tunaposema ‘kutoka kwa fulani, kutoka kwa fulani’ hii ndio sanadi. Na pindi tunaposema ‘Hakika lililo zuri kushinda uzuri wote ni tabia njema’ hii ndio matini. Maulamaa wa Kiislamu wamekubaliana na kukongamana kwamba si kila kinachopokewa kutoka kwa Ahlul-Bayt na kutoka kwa Mtukufu Mtume ni lazima moja kwa moja kiwe ni habari sahihi, na wala hawasemi kuwa si wajibu kwetu kufuatilia na kuchunguza. Hivyo kuna kongamano la Waislamu kwamba katika hadithi kuna zile zilizo sahihi, na zipo zisizokuwa sahihi, na kuna zinazokubaliwa na zinazozingatiwa. Na pia wamekongamana kwamba katika zama za uhai wa Mtukufu Mtume na baada ya uhai wake, kulikuwa na watu ambao waliweka hadithi za uwongo na wakazinasibisha na Mtukufu Mtume , na ni kwa ajili hiyo maulamaa wameweka tasinia ya ‘Elimu ya Uchunguzi wa Wapokezi’ na tasnia ya ‘Elimu ya Hadithi’, ili waweze kuchunguza na kuhakikisha. Kwa mfano fulani imepokewa kuwa alihifadhi Hadithi laki moja, hata hivyo ulamaa wetu hawakubali kwamba kila hadithi yake ni sahihi, na wala hakuna Mwislamu anayeamiliana na Hadithi zote hizi kwa itikadi kuwa ni sahihi na zinakubalika, na kwamba ni wajibu kuzitegemea. Hivyo basi, wao wanatilia umuhimu sana suala la kudurusu na kuchunguza sanadi, yaani fulani kutoka kwa fulani, je mtu huyu ni 39
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 39
3/5/2016 3:11:07 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
mkweli na maarufu kwa ukweli wake na kwamba je ni mwaminifu? Hivyo wanasoma Elimu ya Uchunguzi wa Wapokezi na Elimu ya Hadithi ili waweze kumhukumu, na hii ni kazi ya wabobezi. Mfumo unaokubalika kiakili katika kupokea habari: Lakini kama tukitaka kurahisisha mambo, kwa kupitia mwenendo wa kiakili wa watu wote, ni kwamba kwa mfano ikisemwa kaka yako amefariki, utakwenda kuwaita waombolezaji na wasindikizaji wa jeneza. Lakini je tutasadikisha habari hii kutoka kwa kila mtu? Na tukigundua kuwa mtoa habari ni mtu mwongo, kwa uchache kabisa tutachunguza maneno yake kabla ya kumsadikisha. Na hata mtu asiyejulikana akikupa habari kwamba kaka yako katokewa, na hili na lile, au katika nyumba yako kumetokea jambo fulani, ni wajibu kutoanza moja kwa moja kuzifanyia kazi taarifa hizo, bali ni wajibu kuthibitisha na kuchunguza usahihi wake. Hadithi za uwongo: Katika maisha ya kawaida mtu huwa hakubali mwanzoni isipokuwa kutoka kwa watu waaminifu. Kadhalika ndivyo ilivyo kuhusiana na Hadithi tukufu, hasa zile zinazohusu vipengele vya dini yetu na sharia yetu, jihadi yetu, mwenendo wetu, swaumu zetu na swala zetu. Na mtu kueleza kitu kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu haimaanishi kuwa jambo hilo ni lazima lisadikiwe, hasa tunapokutana na maudhui ya habari za mustakabali, katika upande huu tunahitaji kuhakiki zaidi, kwa sababu ni jambo linalokubalika baina ya maulamaa wa Kiislamu kwamba katika upande huu kuna Hadithi za uwongo zilizochomekwa. Na inasemwa na maulamaa waliobebea katika upande huu, kwamba hakika pande mbili zenye Hadithi nyingi zaidi za uwongo ni 40
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 40
3/5/2016 3:11:07 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
hizi: Upande wa habari za mustakabali, na upande wa habari zinazoelezea fadhila. Na baadhi ya makasisi wa Kiyahudi pia ni miongoni mwa walioingia katika Uislamu na hivyo wakanakili visa vya Kiyahudi na wakavinasibisha na Mtume wa Mwenyezi Mungu , au hawakuvinasibisha naye isipokuwa baadhi yao waliamiliana navyo kana kwamba visa hivyo ni habari na maelezo kutoka kwa Manabii . Na hili halikubaliki, kwani ili habari ikubalike ni wajibu inukuliwe kutoka kwa watu wanaojulikana kwa ukweli angalau kwa kiwango cha chini, ili tuweze kusema kwamba nukuu yao ni sahihi na inakubalika. Na hatimaye ndipo tuje kwenye ufahamu wa maana ya matini, madhumuni ya Hadithi na mfano wake. Hivyo basi, usia wa kwanza kwa ndugu zangu wote wa kiume na wa kike katika zama hizi, ni kwamba tusichukue kutoka kwenye kila kitabu kinachodondokea mikononi mwetu. Au kila riwaya tunayoiona inazungumzia zama za mwisho, hatupasi kuichukua na kuifanyia kazi kama inavyoeleza. Tambueni kwamba kuna Hadithi nyingi za uwongo au ambazo hazina vyanzo vinavyotambulika, au zimenukuliwa na watu wasiojulikana, na hizo hatuwezi kuzitegemea. Suala la Imam Mahdi na hatari yake wakati wa kutabikisha: Wakati wa kuamiliana na habari hizi, kwa mujibu wa matini na nususi, na maana iliyo wazi kutokana na baadhi ya riwaya mutawatiri au mustafidh, tunasema kwamba hakika asili ya maudhui ya Imam Mahdi ni jambo linalokubalika na wote na lisilo na shaka. Kwa upande wa Shia sisi tunaamini kwamba Muhammad bin Hasan ni kutokana na kizazi cha Husein , na ni kutokana na dhuriya wa Mtume wa Mwenyezi Mungu , na kwamba yeye ameshazaliwa. Na kwamba sifa zake hizi na zile zimo ndani ya riwaya mbalimbali, na ndivyo ilivyo kwa Waislamu wengi. Hivyo asili hii ya kwamba Mahdi ni kutokana na kizazi cha Fatimah inaonekana 41
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 41
3/5/2016 3:11:07 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
ni jambo linalokubalika lisilo na shaka, hivyo asili ya Mahdi haina utata. Maudhui ya Sufiyaniy:16 Kuna riwaya nyingi, na mtu anaweza kusema kwamba asili ya fikra ya Sufiyaniy kupitia wingi wa riwaya zilizopo katika vitabu vya Waislamu ni jambo lisilo na shaka. Ama kuhusu ufafanuzi na undani wa mtu huyo kuna riwaya mbalimbali dhaifu na zenye kutofautiana, na hilo linahitaji uhakiki. Asili ya Yamaniy: Katika riwaya hili ni jambo lililo wazi, au asili ya Khurasaniy, au asili ya bendera zitakazokuja kutokea Mashariki kuandaa jambo hili, - mimi hapa najikita katika alama tano au sita, kwa sababu kuna alama nyingi zenye ufafanuzi mwingi, na tukitaka kujikita katika kila alama tutakuta kuna makumi ya riwaya ambayo yanaelekeza alama hizo – Kwa mfano pia suala la ukelele. Ukelele au wito utakaotoka mbinguni, au mshituko utakaotoka mbinguni. Napia kuangamizwa kwa Jeshi la Sufiyaniy katika eneo la Baydai, litakalokuwa limetoka Madina likielekea Makkah. Hata riwaya zinazozungumzia Sayyid Hasaniy ambaye atadhihiri kabla ya Imam wa zama hizi . Hivyo basi, kuna watu walioelezwa na kusimuliwa katika riwaya hizi, lakini na hapa pia tahadhari ni wajibu. Mlango huu pia ni kama milango mingine, kama ambavyo Qur’ani Tukufu inavyofanywa biashara na silaha inayotumiwa katika kheri na shari, kadhalika elimu hii nayo pia inatumiwa kwa ajili ya mambo mabaya na madai ya uwongo.
16
al-Mufid, Muhammad bin Muhammad, al-Irshad Fii Maarifat Hujajullah Alal-Ibad. Kimehakikiwa na kusahihishwa na Muasasat Aal Bayti . Kimechapishwa mwaka 1413, Chapa ya Kwanza, Juz. 2, uk. 369. Na mna: “Na watadhihiri waongo sitini, na wote wakidai unabii. Na watadhihiri watu kumi na mbili kutoka katika ukoo wa Abutalib, na wote kila mmoja akijitangazia uimamu.” 42
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 42
3/5/2016 3:11:07 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
Mahdi wa uwongo: Tangu zama za Bani Abbas mpaka leo hii, kuna madai mengi ya watu kujitangaza kuwa wao ndio Mahdi,17 na hili si sahihi, kwa sababu Mahdi tuliyeahidiwa kwa mujibu wa riwaya ni Yule ambaye ‘ataijaza ardhi usawa na uadilifu, baada ya kuwa imejaa dhulma na ukandamizaji.’ Na haya ndio yaliyopatikana hata katika Aya tukufu zikizungumzia dola adilifu, wakati ambapo wote waliodhihiri na kujitangaza, dola adilifu haijatimia katika mikono yao. Na mimi binafsi nakumbuka kabla ya miaka kadhaa, ni mwaka 1979, tarehe 20 Novemba, miezi kadhaa baada ya Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. Ilikuwa ni sawa na mwezi mosi Muharam, mwaka 1400 Hijiriyyah, yaani siku ya kwanza ya mwaka wa kwanza wa Hijiriyyah, wa karne mpya ya Hijirriyah 1400. Kulitokea nini katika wakati huu? Kuna watu wawili waliwakusanya watu wenye silaha na wakakusanyika katika Msikiti Mtukufu wa Makkah katika Kaaba. Mmoja wao anaitwa Juhayman Utaybiy, na mwingine anaitwa Muhammad bin Abdullah Qahtwaniy, na Juhayman aliwataka wenye silaha wampe kiapo cha utii Muhammad bin Abdullah Qahtwaniy kwa anwani kwamba yeye ndiye Mahdi tuliyeahidiwa. Yakatokea mapigano na hatimaye Muhammad bin Abdullah Qahtwaniy akauwawa, na Juhayman akakamatwa na baadaye akanyongwa. Na hili ndilo lililoenea wakati ule kwamba Qahtwaniy amedai kuwa yeye ndiye Mahdi. Hili lilikuja baada ya Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislam ya Iran, hivyo kisa cha bendera za Mashariki kinaweza kutabikishwa na kuoanishwa, na kwamba Khurasaniy amejitokeza huko Iran, na Mahdi amedhihiri huko Makkah. Na jambo hili lina17
Sheikh Saduq, Muhammad bin Ali bin Babawayhi al-Qummiy, Kamalud-Din Watamamun-Niimah. Kimehakikiwa na kusahihishwa na Ali Akbari al-Ghafariy. Kimechapishwa mwezi wa Muharram mwaka 1405 - 1363, uk. 258. Kimechapishwa na kusambazwa na Muasasatun-Nashri al-Islamiy uliyo chini ya Jumuiya ya Walimu wa Mji wa Qum. 43
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 43
3/5/2016 3:11:07 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
vutia kwa upande wa zama, mazingira, tukio na wakati, mambo haya yapo na yataendelea kuwepo. Imepokewa katika riwaya mbalimbali kutoka kwa Mtukufu Mtume kwamba kuna watu watadai kuwa wao ndio Mahdi. Na wenye kuogopesha zaidi ni masharifu, kwa sababau ni sharti Mahdi awe anatokana na kizazi cha Fatimah na kutokana na kizazi cha Hasan na Husein. Hasa jina la mmoja wao kati ya hao wanaodai kuwa wao ni Mahdi linapokuwa ni Muhammad na baba yake ni Hasan, hivyo kuna watu kadhaa huko Iran waliodai kuwa wao ni Mahdi.18 Katika zama za Bani Abbas jambo hili lilitokea sana, kama ambavyo madai ya watu kudai wao ni Sufiyaniy ni machache, kwani bendera yake ni upotovu kwa ijimai ya Waislamu, hivyo jambo hili la wao kudai kuwa ni Sufiyaniy ni gumu. Lakini ni maumbile ya watu wote kwamba riwaya zinazozungumzia watu wazuri inawezekana kuzitumia kwa mtu kudai yeye ndiye mhusika mwenyewe. Inatosha kusema kwamba, kila aliyedai kwamba yeye ni Mahdi au yeye ni Khurasaniy, au Yamaniy au Hasaniy au Nafsi isiyo na hatia, hakuleta dalili yoyote. Ni ipi dalili yake? Na wala haiwezekani kumsadikisha bila dalili na yakini, kwa sababu hajawasilisha dalili yoyote inayojenga yakini. Na hili (la mtu kudai yeye ndiye Mahdi) kwa mujibu wa historia ni kwamba lilitokea ili kuteka hisia za watu na kuzitumia ili kupata wafuasi na waungaji mkono. Hivyo tunapokubali habari, alama na sifa za mtu, na kwamba tukio hili litatokea zama za mwisho, hakika jambo hili linahitaji tahadhari na uan18
Imepokewa kutoka kwa Abu Abdillah as-Sadiq , kwamba alisema: “Hatadhihiri Mwakilishi mpaka pale watakapodhihiri watu kumi na mbili kabla yake kutoka katika ukoo wa Bani Hashim. Na kila mmoja akidai kwamba yeye ndiye mwenyewe Mwakilishi.” Rejea al-Ghaybah cha Tusi, uk. 437 na 428. Iilamul-Wara, uk. 426. Na ameinukuu Allamah al-Majlisiy katika al-Bihar, Juz. 52, uk. 209 na 47. 44
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 44
3/5/2016 3:11:08 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
galifu, na huenda hii ni moja kati ya faida za kuelezeana kufahamu alama, na kufahamu habari za zama za mwisho. Hatari zilizopo wakati wa kutabikisha alama za kudhihiri kwa Mahdi : Miongoni mwa anwani hatari, ni tatizo la kutabikisha na kuoanisha alama husika, yaani kule kusema kwamba alama hii imetimia, au mtu huyu aliyetajwa katika riwaya ni fulani. Suala hili si madai ya kudai kwamba mimi ni Mahdi, kwani wenye kudai wao ni Mahdi tayari uwongo wao umeshathibiti tangu zamani, lakini wakati mwingine watu ndio wanaodai kuwa matukio na sifa hizi zinaoana na watu fulani wa zama zetu, na huenda watu hao wanaonasibishwa na sifa hizo hawajadai jambo hilo. Huko nyuma tulizungumzia vigawanyo, na kwamba kigawanyo cha kwanza ni habari za jumla ambazo Mtukufu Mtume alizungumzia zama za mwisho. Na pia kuhusu watawala, misikiti, ada, mila, wafalme, viongozi, wanawake, misahafu, mazingira ya ulimwengu, vita, maradhi na mengineyo, lakini yote hayo hakuyafungamanisha na kudhihiri kwa Imam Mahdi . Ndiyo, aina hii ya hadithi kwa kutazama zama tunazoishi, baadhi yake zimekwishatimia bila shaka yoyote, na hili hakuna anayebisha, kwamba baadhi yake zimekwishatokea. Na kwa mfano hadithi inayosema: “Hakika wanaume watavaa mavazi ya kike, na wanawake watavaa mavazi ya kiume.” Jambo hili lipo hivi sasa. Pia kutoweka kwa utawala wa Bani Umayyah, na utawala wa Bani Abbas, yote hayo yamekwishatimia, na wala hayana mjadala, kwa sababu lililotokea kwetu ni yakini na si shaka wala dhana. Hakika bila shaka kuna sehemu kubwa ya habari hizi imekwisha kutokea na kutimia. 45
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 45
3/5/2016 3:11:08 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
Na kigawanyo cha pili ni alama ambazo zinafungamana na kudhihiri kwa Mahdi , lakini haziainishi zama za kudhihiri. Na hizi ni alama za jumla, kwa mfano inawezekana kusema kwamba kutoweka kwa utawala wa Bani Abbas ni miongoni mwa alama za jumla, au kwa mfano, baadhi ya riwaya zilizopo zinazoeleza kuwa elimu itachimbuka katika mji wa Kufa na itastawi katika mji unaoitwa Qum.19 Lakini jambo hili litatokea lini? Hili halijulikani. Pia baadhi ya alama za jumla zimekwishatimia, na wala hakuna ishkali, na nyingine hazijatimia mpaka leo. Kigawanyo cha tatu, nacho ni kigawanyo cha alama makhususi. Yaani zile zilizotajwa katika riwaya kwamba zitakutana na kudhihiri kwa Imam Mahdi , na ambazo zipo katika namna makhususi, kwa mfano, Sufiyaniy, Yamaniy, Khurasaniy, wito kutoka mbinguni, na kuangamizwa kwa jeshi katika ardhi ya Baydai. Hapa pana muda, katika siku moja, katika mwezi mmoja.20 Wito kwa mfano, riwaya Rejea Biharul-An’war ya Muhammad Baqir bin Muhammad Taqiy, al-Majlisiy, Chapa ya Pili, mwaka 1403, Juz. 57, uk. 213, humo mna riwaya kutoka kwa Imam as-Sadiq : Kwamba ulitajwa mji wa Kufah, akasema : ‘Mji wa Kufah utabaki mtupu bila Waumini, na elimu itarudi nyuma kama anavyorudi nyuma nyoka katika shimo lake. Kisha itadhihiri elimu katika mji utakaoitwa Qum, nao utakuwa kitovu cha elimu na ubora, kiasi hatabakia katika ardhi aliye dhaifu katika dini, hadi watawa wa kike watakuwa. Na hiyo itakuwa ni karibu na kudhihiri kwa mwakilishi wetu. Hivyo Mwenyezi Mungu ataufanya mji wa Qum na watu wake kuwa makamu wa Hujja, na kama si hivyo basi ardhi na watu wake ingetoweka na isingebakia hoja yoyote ardhini. Kutokea hapo elimu itasambaa kwenda miji mingine Mashariki na Magharibi, na hatimaye hoja ya Mwenyezi Mungu juu ya viumbe wake itatimia, kiasi kwamba hatabakia yeyote katika ardhi ambaye dini na elimu haijamfikia. Kisha ndipo atadhihiri Mwakilishi na atakuwa sababu ya watu kufikiwa na adhabu ya Mwenyezi Mungu, na ghadhabu yake kuwashukia waja, kwa sababu Mwenyezi Mungu hawaadhibu waja isipokuwa baada ya wao kuikataa hoja. 20 Imepokewa kutoka kwa Abu Abdillah , kwamba alisema: “Kudhihiri kwa watu watatu: Sufiyaniy, Khurasaniy na Yaamaniy, kutakuwa katika mwaka mmoja, mwezi mmoja na siku moja. Na hakuna bendera yenye kuongoa zaidi kushinda bendera ya Yamaniy, kwa sababu yeye atakuwa analingania haki.” Tazama kitabu al-Ghaybah cha Nuumaniy, uk. 255. Pia al-Ghaybah cha Tusi, uk. 443 na 446. Iilamul-Wara, uk. 429. Na ameinukuu Allamah al-Majlisiy katika al-Bihar, Juz. 52, uk. 210. 19
46
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 46
3/5/2016 3:11:08 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
zinazungumzia kuwa ni katika mwezi Rajabu na mwezi wa Ramadhani, unaweza kuwa ni wito mmoja na unaweza kuwa ni wito wa kujirudia mara kadhaa. Kuangamizwa kwa jeshi katika ardhi ya Baydai, inajulikana kwamba jeshi hilo litatoka kutoka Madina kuelekea Makkah ili kwenda kumteka Imam Mahdi , na hapo ndipo litakapodidimizwa ardhini. Hapa kuna tatizo linalotokea wakati wa kutabikisha na kuoanisha: Ujinga wa kutokujua wakati wa kutokea alama: Sisi hatujui ni lini yatatokea matukio haya yenye kufuatana, ni nani anayejua? Hawezi yeyote kudai kuwa anajua, isipokuwa kama kuna watu makhususi wenye elimu kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu , ambayo haijatufikia sisi. Utabikishaji na uoanishaji huu haulazimu kudhihiri Imam Mahdi : Tatizo ni pale wanapokuja baadhi ya watu ili waweze kutabikisha na kuoanisha sifa za watu waliotajwa katika riwaya hizi juu ya watu waliopo sasa, kwa sababu alama hizo hazilazimu kudhihiri Mahdi na kusimama dola ya haki, na dola ya uadilifu wa kiungu itakayodhihiri miaka ijayo. Hivyo basi, hatari ninayopenda kuizungumzia katika kigawanyo hiki cha tatu ni muhimu zaidi: 1. Utabikishaji na uoanishaji bila elimu: Wakati ninapowaambia watu, kwa mfano, ‘hakika Fulani ndiye Sufiyaniy’, yaani nawaambia mngojeeni Mahdi baada ya miezi sita au miezi mitano, au miezi mitatu, kwa sababu hivi ndivyo ilivyo katika riwaya mbalimbali. Na nitakapowaambia watu: ‘Hakika Fulani ndiye Yamaniy au Khurasaniy, au ukelele tuliousikia jana usiku ndio wito wa kutoka mbinguni’, hii ni kama mimi nawaambia mngojeeni Mahdi baada ya wiki moja au wiki mbili. Na hapa 47
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 47
3/5/2016 3:11:08 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
ndipo unapodhihiri umuhimu wa maudhui hii, na tatizo linajitokeza wakati wa kutabikisha na kuoanisha, yaani kuoanisha baadhi ya anuani za sifa juu ya baadhi ya watu. Na hili ni kosa na makosa, kwa sababu ni kuoanisha bila elimu, na hii ni dhana, na dhana haisaidii haki chochote. Hivyo sisi hatujui kama kweli huyu ndiye Yamaniy au Khurasaniy au Sufiyaniy. 2.
Kuwapoteza watu: Miongoni mwa hatari za uoanishaji huu, ni kwamba unapelekea kuwapotosha na kuwapoteza watu, kwa sababu kama bendera ni nzuri itakuwa ni kana kwamba wewe unawaambia watu iteteeni. Na kama ni mbaya itakuwa ni kana kwamba wewe unawaambia watu ipigeni vita.
3.
Kuzusha shaka katika suala la Mahdi na alama zake: Nayo ni miongoni mwa hatari kubwa zaidi wakati wa kuoanisha hizi anuani za sifa juu ya watu hawa, kwani mtu huyu anapokufa jambo hili hupelekea kuzuka shaka dhidi ya alama, habari na riwaya zinazohusu Mahdi, bali ni kwamba linaweza kupelekea kuzuka shaka hata dhidi ya asili ya imani ya fikra ya Mahdi. Na hili ni kosa katika kuoanisha na kuharakia katika uoanishaji wa kimakosa, na hili ni miongoni mwa hatari kubwa.
Na hatari za kuoanisha zipo katika kila zama, ima kwa ajili ya kutaka kutumia mwanya huo kwa maslahi binafsi, au kwa ajili ya baadhi yao kutaka kuongeza uhalali juu ya wanayempenda, au kwa ajili ya kutaka kukifanya kitabu chake kiwe mashuhuri. Na hili ni lengo la kibiashara, lakini jambo hili lina hatari kubwa sana. Hivyo basi kuoanisha ni kosa na ni kutenda makosa makubwa, na kuna hatari kubwa sana. 48
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 48
3/5/2016 3:11:08 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
Mifano ya hatari zitokanazo na kuoanisha anuani hizi katika zama zetu: Kwa mfano, kuna wakati walisema: Hakika Sufiyaniy ndiye Sadam Husein, na kwamba amefanya hivi na vile. Sasa Sadam Husein amekufa, yaani Sufiyaniy ameondoka, tunafanya nini sasa? Na pia huko Iraki kwa mfano, wengi walisema: ‘Hakika Abu Masuab Zaraqawi ambaye alifanya kazi ya kukufurisha, kuuwa, kuchinja na kumwaga damu za wasiokuwa na hatia, kuwa ndiye Sufiyaniy.’ Na kwamba bendera ya Sufiyani imedhihiri, na jambo likazidi kuwa tata zaidi, kwa sababu Sufiyani atadhihiri kutokea eneo linaloitwa WadulYabis, nalo lipo katikati ya utatu wa Syria, Jodan na Palestina. Na wakati wanadai Zaraqawi ndiye Sufiyaniy yeye alikuwa huko, na sasa Zaraqawi amekufa. Tatizo ni kwamba wao wanauaminisha ulimwengu jambo hili. Na sasa Abu Bakri Baghdadiy (Kiongozi wa Daesh) ndiye Sufiyani kwa mujibu wa baadhi ya watu. Na yeye kwa mujibu wa baadhi ya riwaya ni kwamba siku mbili zilizopita ameuwa watu sabini kutoka ukoo wa Abu Namri. Na kwa mujibu wa baadhi ya riwaya ni kwamba ameuwa watu mia mbili. Na kwa mujibu wa riwaya nyingine ni kwamba ameuwa watu mia tatu, wapo aliowauwa na wapo aliowachinja miongoni mwa wanaume, wanawake na watoto. Na kuna wakati watu wengi waliathiriwa na bendera ya Iran, na kwamba Khomein ndiye Khurasaniy, kwa kuzingatia kwamba yeye ni sharifu, na kwamba Iran yote inahesabika kuwa ni Khurasan. Hivyo hata kijiji cha Khomen au mji wa Qum ni sehemu ya Khurasan, na kwamba Imam Khomein ndiye Khurasaniy na ndiye atakayemkabidhi Imam Mahdi bendera ya mapambano. Na Mwenyezi Mungu ameshamfisha Khomein. Na hata baadhi yao walipomuona Imam Khomeini mgonjwa amelazwa hospitali walidai kuwa Muntadhariy ndiye Khurasaniy, naye hivi sasa Mwenyezi Mungu ameshamfisha. 49
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 49
3/5/2016 3:11:08 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
Anaweza kuja mmoja wao hivi sasa na kusema: ‘Hakika Sayyid Khamenei ndiye Sayyid Khurasaniy,’ na mimi binafsi ninatamani sana uhalisia uwe hivyo, lakini kwa dalili ipi? Na kwa msingi upi? Na kwa kigezo kipi? Ndiyo, wakati mwingine tunaweza kuoanisha baadhi ya sifa juu ya baadhi ya watu, lakini huwa ni katika wigo wa dhana na si uhakika na yakini. Na tunapokuja kwa Yamaniy tunakuta huko kuna madai mengi zaidi. Kwa mfano huko Iraki, kuna watu wawili au watatu wanaodai kuwa wao ndio Yamaniy. Na hata Lebanon, baadhi ya wenye mapenzi na Hizbullah wamedai kwamba bendera ya Hizbullah ndio bendera ya Yamaniy, na kwamba fulani21 ndiye Yamaniy. Ndiyo, natamani ingekuwa hivyo, lakini ni kwa dalili ipi? Na sisi tunatakiwa tusizungumze tusiyokuwa na elimu nayo. Hivyo kukosea katika kuoanisha kunapelekea katika matokeo yasiyokuwa salama. Na kitendo cha makosa hayo kujirudia kinapelekea kuwa na shaka dhidi ya alama zote hizi, na hili ni jambo tunalowajibika kujiepusha nalo kwa nguvu zote. Na haitoshi tu niya kuwa nzuri. Hili ni kosa, na linapelekea katika haramu na linatia dosari vipimo. Kwa mfano, mtu anaweza kusema kwamba anaongeza aina fulani ya uhalali na heshima kwa Sayyid Khamenei. Lakini je Sayyid Khamenei anahitaji nyongeza hii ya uhalali?! Hakika uhalali wake ni jambo muhimu, kwa sababu umejengeka juu ya kanuni, mwenendo, matendo, uchamungu, hali ya kujinyima, hekima zake, ushujaa wake na uzoefu wake wa juu na wa kutukuka. Na uhalali huo ndiyo unaomwongezea mapenzi ya kupendwa na watu, na heshima kutoka kwa Waumini. 21
Hapa Sayyid anajikusudia mwenyewe, yaani baadhi ya wapenzi wa Hizbullah wamedai kwamba yeye Sayyid Nasrullah ndiye Yamaniy. 50
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 50
3/5/2016 3:11:08 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
Mwenendo wa kufuatwa katika Hizbullah: Kwa mfano, baadhi ya watu wanasema kwamba kupigana vita Syria ni kupigana dhidi ya Sufiyaniy. Sisi hatuhitaji maneno haya. Haya hayajulikani, na uhalali wa sisi kupigana vita unategemea misingi ya kifikihi, kisharia, kimatendo na kiuhalisia, na wala hatuhitaji aina hii ya maandalizi. Sisi tunapambana huko Syria kwa ajili ya kuihami Lebanon, Syria, Palestina, ukanda huu na raia wa ukanda huu. Tunawahami dhidi ya udhibiti na ukandamizaji wa Marekani, Israeli na wakufurishaji, ambao kama watashika hatamu za uongozi basi watatutendea sisi kama Abu Bakri Baghdadi anavyoutendea ukoo wa Abu Namri. Na inawezekana visa vyote (Kudhihiri kwa Khurasaniy, Yamaniy na Sufiyaniy) vikatokea baada ya miaka hamsini, na inawezekana wakati huo tukawa hatupo. Sisi hatuhitaji hili (kwamba kupigana vita huko Syria ni kupigana dhidi ya Sufiyaniy), sisi tuna akili, mantiki, kanuni na misingi, na tuna Qur’ani na Sunnah ya Nabii, mfumo wa uthibitishaji kwa dalili, mfumo wa ung’amuzi wa sharia na misingi ambayo juu yake ndimo zimejengeka harakati zetu, mienendo yetu, ufahamu wetu wa vipengele vya sharia na wajibu wetu wa kisharia. Na visa vyote hivi (kwamba kupigana vita Syria ni kupigana dhidi ya Sufiyaniy) vinategemea dhana na shaka, kama nilivyozungumza usiku uliopita. Vinategemea ramli, utazamiaji na unajimu, na sisi hatutaki hayo. Sisi tuna akili na maarifa, hivyo ni wajibu juu yetu kuwa wenye tahadhari na waangalifu katika ulimwengu huu. Ndiyo, tunabakiwa na uwezekano, na hili halina ubaya, kila kitu kinawezekana. Kwa mfano tunasema kwamba Fulani aliyetajwa katika riwaya mbalimbali ndiye fulani na ndio tukio fulani. Ndiyo kusema kama sehemu ya uwezekano, hakuna ubaya katika hilo. La51
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 51
3/5/2016 3:11:08 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
kini tatizo ni kwamba uwezekano huu unawasilishwa kwa watu kwa namna ya kwamba ni uhakika na yakini, na kwamba hivyo ndivyo. Na unahubiriwa katika Huseiniya na misikiti, na unawasilishwa kwa watu. Sifa za alama makhususi: Kuainisha na kufafanua yanayohusu alama makhususi (mtu anaweza kusema, Sayyid wewe umetuongezea ugumu). Alama makhususi kwa mujibu wa riwaya ambazo ni sahihi na zenye kukubalika, zipo ambazo maulamaa wametofautiana na wana rai tofauti kuzihusu. Ndiyo, kwamba katika mwaka atakaodhihiri Mahdi atadhihiri pia Yamaniy, Khurasaniy na Sufiyaniy, na kwamba utasikika wito kutoka mbinguni na kuangamizwa jeshi huko Baydai ni katika yasiyo na tofauti. Na tutakaposogea karibu na alama hizi hatutapotea, na inatutosha kuwa tu na maarifa na alama hizi, kwa sababu alama hizi zitaungana na matukio yatafuatana moja baada ya jingine, na mambo yatakuwa wazi zaidi. Alama zajithibitisha zenyewe: Na la muhimu lililomo katika baadhi ya riwaya, ni kwamba atakuja mtu fulani na wala hatutamtambua. Na hapa inakuja riwaya nyingine kusema kwa mfano, hakika Sufiyaniy halitapoteza jambo lake, yeye yuko wazi bayana. Lakini pamoja na hivyo riwaya inakamilisha kwamba, ninyi kama mtashindwa kujua jambo la Sufiyaniy hamtashindwa kujua jambo la wito utakaotoka mbinguni, litausikia wito huo kila sikio katika ulimwengu wote, na kila watu watausikia kwa lugha yao. Baadhi ya watu wanasema: Hakika wito wa kutoka mbinguni unaomaanishwa katika riwaya ni chaneli. Watu hawa inawezekana kuwajibu kwamba kuna baadhi ya miji haina dishi wala chaneli, wala vitafsiri sauti haviwezi kutafsiri lugha zote za ulimwenguni 52
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 52
3/5/2016 3:11:08 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
katika wakati mmoja. Hivyo basi, wito utakaotoka mbinguni una anuani na hali ya muujiza, nayo ni alama kubwa, hivyo tukishindwa kuitambua alama yoyote ile, utakuja wito ili uwe alama ya wazi ambayo haitampoteza mtu. Kuainisha wakati atakaodhihiri: Na anwani ya kabla ya mwisho katika mazungumzo yetu ni maudhui ya wakati atakaodhihiri, ambapo huja baadhi ya watu na kuainisha wakati atakaodhihiri, ni kana kwamba wanajua ghaibu. Kwa mfano atadhihiri baada ya miezi sita, au siku ya Ijumaa hii na ile, au katika mwezi ishirini na moja Safar. Huu wote ni uwongo, na mwenye kusema haya ni mwongo. Na bila kusita na kwa uwazi na wepesi kabisa nasema kuwa, Maimamu wetu wamekataza hili. Na limenukuliwa katazo dhidi ya jambo hilo kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu , katika riwaya iliyopokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq kwamba alisema: “Ewe Abu Muhammad! Hakika sisi Ahlul-Bayt hatuainishi wakati.”22 Na Mtukufu Mtume Muhammad alisema: “Wameongopa wenye kuainisha wakati.”23 Na huu ni msisitizo wa katazo la kukataza kuainisha wakati, na kuwapinga wenye kuainisha wakati, na wamesema uwongo wenye kuainisha wakati, na riwaya kuhusu hilo ni nyingi. Pia imepokewa katika riwaya kutoka kwa Imam as-Sadiq , riwaya ya Muhammad bin Muslim: “Ewe Muhammad! Atakayekupa habari kutoka kwetu kuwa tuliainisha wakati usiogope kumkadhibisha. Na hakika sisi hatumwainishii yeyote wakati.”24 Ibn Abi Zaynab, Muhammad bin Ibrahim, Kitabu al-Ghaybah. Kimehakikiwa na Faris Hasun Karim. Kimechapishwa mwaka 1422, Chapa ya Kwanza, uk. 289. 23 Sheikh Kulayni, Muhammad bin Yaqub, katika al-Kafi. Kimehakikiwa na kusahihishwa na Ali Akbari al-Ghafariy. Kimechapishwa mwaka 1407, Chapa ya Nne, Juz. 1, uk. 368. Kimesambazwa na Darul-Kutubi al-Islamiyyah, Tehran. 24 Ibn Abi Zaynab, Muhammad bin Ibrahim, al-Ghaybah. Kimehakikiwa na Faris Hasun Karim. Kimechapishwa mwaka 1422, Chapa ya Kwanza, uk. 289. 22
53
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 53
3/5/2016 3:11:08 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
Na miongoni mwa masuala ya hatari katika faili hili ni maudhui ya kuainisha wakati, yametokea wapi maudhui haya? Kwa mfano, fulani ameota ndoto, na tulisema kwamba ndoto sio hoja. Au kwa mfano aalimu fulani alisema hivi na vile, ametoa wapi hilo? Katika baadhi ya riwaya imekuja kwamba suala la kudhihiri ni analijua Mwenyezi Mungu tu na wala hamjulishi mwingine yeyote. Na kwamba hili ni miongoni mwa mambo ya kujua Kiyama, na baadhi ya watu wanathubutu hata katika kiwango hiki na wanaainisha wakati na wanatengeneza wakati wa kudhihiri. Hivyo, nukta ya kwanza kwa anwani ya mwisho ni kukataa moja kwa moja kuainisha wakati, na kutokukubali wakati, na kumkadhibisha mwenye kuainisha na kutaja wakati. Na hata kama mtu atakuja kwetu ili kutuainishia wakati tutapasa kumkataza kufanya hivyo, na hekima ya kukataza kuainisha wakati huenda ikawa ni kuzuia kuwapoteza watu, na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye. Kuwavunja watu matumaini (kurefusha muda): Na nukta ya pili katika anwani hii baada ya kukataza kuainisha wakati, ni ile inayofanywa na baadhi yao kwa kutumia kitendo cha kuainisha wakati au kinachofanana na kuainisha wakati, ili wawaambie watu kwamba, kwa mfano, kweli ninyi ni wenye kumngojea Mahdi na dola ya uadilifu? Hili ni jambo la muda mrefu na wala hakuna kitu hivi karibuni, bali ni jambo la mbali. Kufanya hivi nako ni kuainisha wakati na kuwavunja watu matumaini, na hili nalo ni kosa. Na nilitaja huko nyuma wakati wa kutaja faida za alama hizi, kwamba wakati Mtukufu Mtume alipoanza kutaja alama za baada ya kifo chake, kati ya faida za alama hizi ni kuwatia watu matumaini kwamba sisi tuko karibu tunakaribia kufika. Lakini pindi unaposema kumwambia mtu kwamba wakati wa kudhihiri kwake utakuwa ni baada ya miaka mia mbili kwa uchache, kisha anakuja mtu mwingine naye anasema kuwa atadhihiri kwa mfano wiki ijayo, hali zote mbili ni maneno ya54
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 54
3/5/2016 3:11:08 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
siyo na elimu, nalo ni kosa, na jambo hilo lina hatari za kifikra, kiitikadi na kisaikolojia. Hivyo ima lipelekee katika kuvunja matumaini na kuangusha, na ima lipelekee katika kukanusha na kukataa. Hivyo basi, ni upi muamala sahihi kwa mujibu wa maelekezo ya riwaya? Na hii ndio nukta ya mwisho. Ungojeaji salama: Sisi kwa mujibu wa yale yaliyotufikia kutoka kwenye Hadithi za Mtukufu Mtume , na yaliyokuja katika Qur’ani, tuna imani yakinifu na isiyo na shaka kwamba mustakabali wa ardhi, ni mustakabali wa ushindi wa tauhidi, na ushindi wa dini ya Mungu na waliodhoofishwa. Na kwamba mustakabali wa ardhi ndio mustakabali wa hekima, raha na starehe, na hatimaye kila walichokitolea juhudi, walichokipigania na kukivujia jasho na kuja nacho Manabii wa Mwenyezi Mungu muda wote wa historia. Kitatimia katika kiwango cha dunia kabla ya kiwango cha Akhera. Na yaliyotufikia kupitia Hadithi za Mtume wa Mwenyezi Mungu na yakathibiti kwetu kwamba ni sahihi na yanakubalika, na inawezekana kuyategemea, sisi hayo tunayangojea. Na wakati wa kungojea kwetu hatuainishi wakati wa kutokea kwake. Naam, namna bora ya kuamiliana na jambo ni kwa namna ifuatayo: Ni tulingojee jambo hili asubuhi na jioni na wala tusilifanye kuwa ni jambo la mbali, lenyewe linawezekana katika kila usiku na kila saa na kila siku. Na pia jambo liko chini ya utashi wa Allah Mtukufu. Hivyo Allah akitaka ahadi Yake itimie katika usiku huu, je uwezo wa Allah unashindwa? Hapana, hivyo ni katika saa, siku, wiki, miezi na miaka anaweza Mwenyezi Mungu kutaka liwe na litokee. Je sisi tunajua ghaibu? Je tunajua ayatakayo Allah? Hivyo ni wajibu tungojee jambo hili asubuhi na jioni, na tumuombe Allah Mtukufu alisogeze karibu na kuliharakisha. Na huu ndio ufahamu na hisia sahihi. 55
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 55
3/5/2016 3:11:08 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
Ahadi ya Allah hutimia kwa utashi wa Allah: Baadhi ya maulamaa wanaweza kusema kwamba jambo hili halitatokea kabla ya Sufiyaniy, Khurasaniy, Yamaniy na wito na hivi na vile, na hata katika riwaya alama zimegawanyika katika sehemu mbili: Ambazo ni lazima zitatokea, na ambazo si lazima kutokea, kwa maana zinaweza kutokea au zisitokee. Lakini kila kitu kipo chini ya utashi wa Allah Mtukufu, kama ilivyo katika kauli yake: “Mwenyezi Mungu hufuta na huthibitisha ayatakayo”25, na wala hakuna uwezo ulio juu ya utashi Wake, elimu Yake, na hekima Yake Mtukufu. Na zile ambazo si za lazima ziko chini ya hili. Ama zile ambazo ni za lazima, baadhi ya maulamaa wanasema hata nazo ziko chini ya kanuni “Mwenyezi Mungu hufuta na huthibitisha ayatakayo”, yaani zinaweza kutokea au zisitokee. Kuna riwaya ambayo ndani yake Imam Jawad anaulizwa: Je Sufiyaniy ni miongoni mwa mambo ya lazima? Akasema: “Ndiyo, ni miongoni mwa mambo ya lazima.” Muulizaji akasema: “Je ananyenyekea chini ya kanuni ya kwamba Mwenyezi Mungu hufuta atakalo na huthibitisha?” Akasema: “Ndiyo.” Muulizaji akasema: “Je Mahdi atanyenyekea katika kanuni hii?” Akamwambia: “Hapana, Mahdi ni katika ahadi, na Allah hakhalifu ahadi.”26 Mpaka wapo baadhi wenye kuhoji kuhusu riwaya hii. Na hata tukisema kuwa zile ambazo ni za lazima, ni lazima zitatimia, bado sifa zake si katika mambo ya lazima. Hivyo inawezekana katika 25 26
Sura Raad: 39. Ibn Abi Zaynab, Muhammad bin Ibrahim, kitabu al-Ghaybah. Kimehakikiwa na Faris Hasun Karim. Kimechapishwa mwaka 1422, Chapa ya Kwanza, uk. 203, humo mna: “Alitusimulia Abu Hashim Daud bin Qasim al-Jaafariyyu, alisema: Tulikuwa kwa Abu Jaafar Muhammad bin Ali Ridha , ikatokea akatajwa Sufiyaniy na yaliyokuja katika riwaya kwamba jambo lake ni miongoni mwa mambo ya lazima. Nikamwambia Abu Jaafar : ‘Je hujitokeza mabadiliko kwa Allah katika jambo la lazima?’ Akasema: ‘Ndiyo.’ Tukamwambia tunakhofia yasije yakajitokeza mabadiliko kwa Allah kuhusiana na Mahdi. Akasema: ‘Hakika Mahdi ni miongoni mwa ahadi, na Allah hakhalifu ahadi.” 56
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 56
3/5/2016 3:11:08 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
usiku mmoja Mwenyezi Mungu akawadhihirisha Yamaniy, Sufiyaniy na Khurasaniy, na akadhihiri Jibril na wito kutoka mbinguni. Na Mwenyezi Mungu akamruhusu Walii Wake aliyemficha miongoni mwa viumbe Wake, adhihiri ili kutimiza ahadi Yake. Na inatosha ili jambo hili likubalike kwetu, ni kwamba kusiwepo tu kizuizi dhidi ya jambo hili. Na hii ndio maana ya sisi kusubiri na kungojea, na kuomba na kutaka adhihiri. Kwamba tuandae mazingira na kutaraji jambo hili asubuhi na jioni. Matumaini na kungojea: Na sasa tutatosheka na kadiri hii, na ninaitakidi kwamba fikra hii imekuwa wazi sana. Na faili hili ambalo liko katika daraja la juu ni miongoni mwa mambo yenye mvuto katika zama hizi, na nimtaji mkubwa sana unaotumiwa na wengi miongoni mwa wale wanaojaribu kulitumia vibaya faili hili kisiasa, kitamaduni na kibiashara. Nawaomba watu wema, wenye matarajio na matumaini na wenye kungojea, kwa mujibu wa yale niliyofafanua na kuwasilisha, tujitahidi kuamiliana kwetu na jambo hili kuwe ni kwa kutegemea vipimo bora na makini vya kielimu, kisharia na kiakili. Na wala tusielemee upande wa ulimwengu wa itikadi potovu wala ulimwengu wa ngano za uwongo. Wala katika kutumia kila njia ambayo haifikishi katika elimu, wala ambayo haiwi hoja baina yetu na Allah Mtukufu. Husein alifanya hivyo, na alielezwa na babu yake , na kisa hiki ni maarufu kutoka kwa Ummu Salamah. Hivyo Imam Husein alitekeleza wajibu wake. Baadhi ya watu kazi yao yote ni kudurusu na kusoma alama. Ndiyo, wabobezi ni vizuri wakasoma na kudurusu alama. Ama sisi tunao wajibu na jukumu la kisharia, na hili ni somo muhimu kati ya masomo ya Imam Husein kule Karbala.
57
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 57
3/5/2016 3:11:08 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
Orodha Ya Vitabu Vilivyo Chapishwa Na Al-Itrah Foundation 1. i) Qur’ani Tukufu – Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili ii) Qur’an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thelathini 2. Uharamisho wa Riba 3. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza 4. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili 5. Hekaya za Bahlul 6. Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) 7. Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (a.s.) 8. Hijab vazi Bora 9. Ukweli wa Shia Ithnaashari 10. Madhambi Makuu 11. Mbingu imenikirimu 12. Abdallah Ibn Saba 13. Khadijatul Kubra 14. Utumwa 15. Umakini katika Swala 16. Misingi ya Maarifa 17. Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia 18. Bilal wa Afrika 19. Abudhar 20. Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu 21. Salman Farsi 22. Ammar Yasir 23. Qur’an na Hadithi 24. Elimu ya Nafsi 25. Yajue Madhehebu ya Shia 26. Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur’an Tukufu 58
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 58
3/5/2016 3:11:08 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
27. Al-Wahda 28. Ponyo kutoka katika Qur’an 29. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii 30. Mashukio ya Akhera 31. Al Amali 32. Dua kwa Mujibu wa Ahlulbayt (a.s) 33. Udhuu kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna 34. Haki za wanawake katika Uislamu 35. Mwenyezi Mungu na sifa zake 36. Kumswalia Mtume (s) 37. Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) 38. Adhana 39. Upendo katika Ukristo na Uislamu 40. Qur’ani na Kuhifadhiwa Kwake 41. Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu 42. Kupaka juu ya khofu 43. Kukusanya Sala Mbili 44. Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara 45. Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya 46. Kusujudu juu ya udongo 47. Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) 48. Taraweheas 49. Malumbano baina ya Sunni na Shia 50. Kupunguza Swala safarini 51. Kufungua safarini 52. Umaasumu wa Manabii 53. Qur’an Yatoa Changamoto 54. as-Salaatu Khayrun Mina -’n Nawm 55. Uadilifu wa Masahaba 56. Dua e Kumayl 57. Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu 59
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 59
3/5/2016 3:11:08 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
58. Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake 59. Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata 60. Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mtume Muhammad (s) 61. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza 62. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili 63. Kuzuru Makaburi 64. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza 65. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili 66. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu 67. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne 68. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano 69. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita 70. Tujifunze Misingi Ya Dini 71. Sala ni Nguzo ya Dini 72. Mikesha Ya Peshawar 73. Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu 74. Ubora wa Imam ‘Ali na Ushia ndio njia iliyonyooka 75. Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake 76. Liqaa-u-llaah 77. Muhammad (s) Mtume wa Allah 78. Amani na Jihadi Katika Uislamu 79. Uislamu Ulienea Vipi? 80. Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) 81. Dhana ya Ndoa ya Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) 82. Urejeo (al-Raj’ah) 83. Mazingira 84. Utokezo (al - Badau) 85. Hukumu ya kujenga juu ya makaburi 86. Swala ya maiti na kumlilia maiti 87. Uislamu na Uwingi wa Dini 88. Mtoto mwema 60
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 60
3/5/2016 3:11:08 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
89. Adabu za Sokoni Na Njiani 90. Johari za hekima kwa vijana 91. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza 92. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili 93. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu 94. Tawasali (AT- TAWASSUL) 95. Imam Mahdi katika Usunni na Ushia 96. Hukumu za Mgonjwa 97. Sadaka yenye kuendelea 98. Msahafu wa Imam Ali 99. Maimamu wa Ahlul Bait – Ujumbe na Jihadi 100. Idi Al-Ghadir 101. Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu 102. Hukumu zinazomuhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi 103. Huduma ya Afya katika Uislamu 104. Sunna za Nabii Muhammad (saww) 105. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) 106. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) 107. Shahiid Mfiadini 108. Mwanamke Na Sharia 109. Ujumbe -Sehemu ya Kwanza 110. Ujumbe - Sehemu ya Pili 111. Ujumbe - Sehemu ya Tatu 112. Ujumbe - Sehemu ya Nne 113. Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu 114. Hadithi ya Thaqalain 115. Ndoa ya Mutaa 116. Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza 117. Ukweli uliopotea sehemu ya Pili 118. Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu 119. Ukweli uliopotea sehemu ya Nne 61
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 61
3/5/2016 3:11:09 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
120. Ukweli uliopotea sehemu ya Tano 121. Mkutano wa Maulamaa wa Baghdad 122. Safari ya kuifuata Nuru 123. Fatima al-Zahra 124. Myahudi wa Kimataifa 125. Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi 126. Visa vya kweli sehemu ya Kwanza 127. Visa vya kweli sehemu ya Pili 128. Elimu ya Ghaibu ya Maimamu 129. Mwanadamu na Mustakabali wake 130. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) 131. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) 132. Khairul l’Bariyyah 133. Uislamu na mafunzo ya kimalezi 134. Vijana ni Hazina ya Uislamu 135. Adhana ni Ndoto au ni Wahyi? 136. Tabaruku 137. Saada Kamili – Kitabu cha Kiada cha Maadili 138. Vikao vya furaha 139. Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 140. Visa vya wachamungu 141. Falsafa ya Dini 142. Kuhuzunika na Kuomboleza 143. Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah 144. Mjadala wa Kiitikadi 145. Kuonekana kwa Allah 146. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) 147. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) 148. Ndugu na Jirani
62
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 62
3/5/2016 3:11:09 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
149. Ushia ndani ya Usunni 150. Maswali na Majibu 151. Mafunzo ya hukmu za ibada 152. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1 153. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2 154. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 155. Abu Huraira 156. Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. 157. Mazingatio kutoka katika Qur’an - Sehemu ya Kwanza 158. Mazingatio kutoka kaitka Qur’an - Sehemu ya Pili 159. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza 160. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili 161. Shia na Qur’ani – Majibu na Maelezo 162. Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) 163. Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani 164. Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu 165. Uislamu Safi 166. Majlisi za Imam Husein Majumbani 167. Je, Kufunga Mikono 168. Uislam wa Shia 169. Amali za Makka 170. Amali za Madina 171. Asili ya Madhehebu katika Uislamu 172. Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi 173. Ukweli uliofichika katika neno la Allah 174. Uislamu na Mifumo ya Uchumi 175. Umoja wa Kiislamu na Furaha 176. Mas’ala ya Kifiqhi 177. Jifunze kusoma Qur’ani 178. as-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah 179. Hayya ‘Alaa Khayri’l-’Amal Katika Adhana 63
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 63
3/5/2016 3:11:09 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
180. Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura 181. Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na Ramadhani) 182. Uadilifu katika Uislamu 183. Mahdi katika Sunna 184. Maswali Ya Uchunguzi Kuhusu Uislam 185. Kazi na Bidii ni njia ya maendeleo 186. Abu Talib – Jabali Imara la Imani 187. Ujenzi na Utakaso wa Nafsi 188. Vijana na Matarajio ya Baadaye 189. Historia maana na lengo la Usalafi 190. Ushia – Hoja na Majibu 191. Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) 192. Maombolezo – Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) 193. Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu 194. Takwa 195. Upotoshaji Dhahiri katika (Turathi) Hazina ya Kiislamu 196. Amirul Muuminina (as) na Makhalifa 197. Tawheed Na Shirki 198. Kuvunja hoja iliyotumika kutetea Uimamu wa AbuBakr 199. Adabu za vikao na mazungumzo 200. Hija ya Kuaga 201. Uwazi baina ya Maslahi na Vikwazo 202. Fadhila za watukufu watano katika Sahih Sita 203. Mdahalo baina ya Mwanachuoni wa Kisunni na Kishia (Al- Muraja’aat) 204. Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (as) 205. Imam Husain ni Mfumo wa Marekebisho na Mageuzi 206. Mtazamo kuhusu msuguano wa Kimadhehebu 207. Nchi na Uraia – Haki na wajibu kwa Taifa 208. Mtazamo wa Ibn Taymiyyah juu ya Imam Ali (as) 209. Uongozi wa Kidini – Maelekezo na Utekelezaji wa Kijamii 210. Maadili ya Ashura 64
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 64
3/5/2016 3:11:09 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
211. Mshumaa – Shahidi na Kifo cha Kishahidi 212. Mizani ya Hekima – Hadithi za Ahlul Bait (as) – Sehemu ya Kwanza 213. Imam Ali na Mambo ya Umma 214. Imam Ali na Mfumo wa Usawa 215. Uimamu na Tamko la Kutawazwa 216. Mfumo wa Wilaya 217. Vipi Tutaishinda Hofu? 218. Kumswalia Mtume ni Ufunguo wa Utatuzi wa Matatizo 219. Maeneo ya Umma na Mali Zake 220. Nahju ‘L-Balagha – Majmua ya Khutba, Amri, Barua, Risala, Mawaidha na Semi za Amirul-Muuminin Ali bin Abu Talib (a.s.) 221. Mukhtar – Shujaa aliyelipiza kisasi dhidi ya wauaji wa Imam Husein (as) hapo Karbala 222. Mazingatio Katika Swala 223. Imam Hasan na Mfumo wa Kujenga Jamii 224. Vyakula Na Vinywaji 225. Kuelewa Rehema ya Mwenyezi Mungu 226. Imam Mahdi na Bishara ya Matumaini 227. Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu 228. Shia Na Sahaba - Majibu na Maelezo 229. Majanga Na Jukumu la Jamii 230. Shia Na Hadith - Majibu na Maelezo 231. Upotofu Ndani ya Kitabu cha Mitaala kwa Shule za Sekondari 232. Ugaidi Wa Kifikra Katika Medani Ya Kidini 233. Yafaayo kijamii 234. Uswalihina Dhahiri Na Batini Yake 235. Mkakati wa Kupambana na Ufakiri 236. Mwanamke Katika Harakati Za Mageuzi 237. Jihadi 238. Hija Katika Maneno Na Ujumbe Wa Imam Khomeini (R.A) 239. Tiba Ya Maradhi Ya Kimaadili
65
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 65
3/5/2016 3:11:09 PM
IMAM MAHDI علَ ْي ِه السَّالم َ NA HABARI ZA UGHAIBU
240. Yusuf Mkweli 241. Taqiyya Kwa Mujibu Wa Sheria Ya Kiislamu 242. Imam Mahdi (A.S) Imam Wa Zama Hizi Na Kiongozi Wa Dunia 243. Talaka Tatu 244. Safari Ya Kuelekea Kwa Mwenyezi Mungu 245. Hotuba Za Kisslamu Juu Ya Haki Za Binadamu 246. Mashairi Ya Kijamii 247. Ngano Ya Kwamba Qur’ani Imebadilishwa 248. Wito Kwa Waumini: “Enyi Mlioamini” 249. Imam Husain (a.s) ni Utu na Kadhia 250. Imam Husain ni Kielelezo cha Kujitoa Muhanga na Fidia
66
02_16_Imam Mahdi Nasrullah_5_March_2016.indd 66
3/5/2016 3:11:09 PM