Kauli sahihi zaidi katika kufafanua hadithi

Page 1

KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI: “Nimemuona Mola Wangu Akiwa na Sura ya Kijana Mzuri”

‫القول األسد في بيان حال حديث‬ ”‫“رأيت ربي في صورة شاب أمرد‬

Mwandishi: Sayyid Abul Yasar Abdul Aziz bin al-Sadiiq al-Ghammari

Kimetarjumiwa na: Jopo la Wafasiri

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 1

10/20/2015 5:15:20 PM


‫ترجمة‬

‫القول األسد في بيان حال حديث‬ ‫“رأيت ربي في صورة شاب أمرد”‬

‫تأليف‬ ‫السيد المحدث الشريف أبو اليسر عبد العزيز ابن الصديق الغماري‬

‫من اللغة العربية إلى اللغة السواحلية‬

‫‪10/20/2015 5:15:20 PM‬‬

‫‪14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 2‬‬


© Haki ya kunakili imehifadhiwa na: Al-Itrah Foundation ISBN No: 978 - 9987 – 17 – 022 – 7 Mwandishi: Sayyid Abul Yasar Abdul Aziz bin al-Sadiiq al-Ghammari Kimetarjumiwa na: Jopo la Wafasiri Kimehaririwa na: Alhaj Hemedi Lubumba Selemani Na Alhaj Ramadhani S. K. Shemahimbo Kimepangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation Toleo la kwanza: Machi, 2016 Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. - 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: www.alitrah.info

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 3

10/20/2015 5:15:20 PM


Yaliyomo Dibaji ......................................................................................... vi Neno la Mchapishaji........................................................................ 1 Faslu ya Kwanza.............................................................................. 7 Sura ya Kwanza............................................................................... 9 Sura ya Pili..................................................................................... 17 Sura ya Tatu................................................................................... 18 Sura ya Nne.................................................................................... 19 Faslu ya Pili................................................................................... 34 Faslu ya Tatu.................................................................................. 35 Hadithi Nyingine............................................................................ 47 Ufahamisho wa Vizito Viwili Juu ya Uzushi wa Kiti cha Enzi kiko chini ya Miguu ya Mwenyezi Mungu.............. 51 Utangulizi....................................................................................... 51 Kuyahakiki maneno juu ya ngano ya “kursii ni mahali pa kuweka miguu ya Mungu.............................. 55 Mjadala juu ya sanad za “kiti (kursii) ni mahali pa kuweka miguu........................................................... 63

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 4

10/20/2015 5:15:20 PM


Kursii mahali pa kuweka miguu, ni riwaya ya Kiyahudi, yenye kumfanya ........................................................... 68 Mungu ana umbo na ni yenye kukataliwa..................................... 68 Mjadala wa mwana lugha Abu Mansur Al Azhariy....................... 70 Kuna kauli ya tatu inayofafanua Kusrii kwa maana ya uwezo. Amenukuu Qurtubiy na Ibn Taymiyya ameegemea huko, nayo ni hii:...................................... 72 Mwisho ........................................................................................ 74

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 5

10/20/2015 5:15:20 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

DIBAJI

K

itabu hiki ni toleo la Kiswahili la taasisi ya Al Itrah Foundation. Chapisho lake limelenga kukidhi mahitaji ya kiroho ya zama hizi pamoja na Ubongo na fikra zinazokuwa za Muislam. Jitihada kubwa zimefanywa na Taasisi kuweka chapisho hili la Kiswahili katika msingi wa haki na wenye kukubalika katika Uislam. Unaombwa kwa Taadhima ukisome kitabu hiki katika malengo yaliyokusudiwa. Pia Unaombwa kuwasilisha kwetu maoni yako huru juu ya chapisho letu hili, jambo ambalo tutashukuru sana. Kutangaza ujumbe wa Uislam ni kazi ambayo inahitaji ushirikiano wetu sote. Taasisi inakuomba kuungana na kushirikiana kama ilivyoagizwa katika aya ya Qur’an: (Surat Saba’ 34:46). Na rehma za Allah ziwe juu yako. Wako katika Uislam Al Itrah Foundation Barua Pepe: alitrah@yahoo.com SMS: +255 778 300 140

vi

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 6

10/20/2015 5:15:20 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

NENO LA MCHAPISHAJI

K

itabu ulichonacho mikononi mwako kinaaitwa, Kauli Sahihi Zaidi katika Kufafanua Hadithi: “Nimemuona Mola Wangu Akiwa na Sura ya Kijana Mzuri.” Huu ni utafiti uliofanywa na mwandishi juu ya hadithi: “Nimemuona Mola wangu akiwa na sura ya kijana mzuri.” Hii ni hadithi ambayo hupatikana katika vitabu vingi vya hadithi, lakini kwa mtazamo wa haraka utaona hadithi hii ina mapungufu mengi na haikubaliani na vipimo vilivyowekwa vya kupima usahihi wa hadithi husika. Katika kitabu hiki mwandishi amefanya utafiti wa kina juu ya hadithi hii kwa kutumia ushahidi uliopo kwenye Qur’ani, hadithi na matukio ya kihistoria, na kufikia hitimisho zuri la kumtakasa Mwenyezi Mungu kutokana na dhana hii ya kishirikina. Sisi kama wachapishaji, tunakiwasilisha kitabu hiki kama kilivyo kwa wasomaji wetu na kuwashauri wasome yaliyomo kwa makini, wayafanyie kazi na kuyazingatia, na kufaidika na hazina iliyoko ndani yake. Hii ni moja kati ya kazi kubwa zilizofanywa na Taasisi ya Al-Itrah katika kuwahudumia kielimu wasomaji wake wazungumzaji wa Kiswahili. Na kwa maana hiyo hiyo, imeona ikichapishe kitabu hiki chenye manufaa makubwa kwa lugha ya Kiswahili kwa lengo lake lile lile la kuwahudumia Waislamu, hususan wanaozungumza Kiswahili. Hivyo, ni matumaini yetu kwamba wasomaji wetu watanufaika vya kutosha kutokana na kitabu hiki, kwani 1

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 1

10/20/2015 5:15:20 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

tumekiona ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni vitu ambavyo havina nafasi tena katika akili za watu. Tunamshukuru mwandishi wa kitabu hiki, Sayyid Abul Yasar Abdul Aziz bin al-Sadiiq al-Ghammari kwa kazi kubwa aliyofanya kwa ajili ya Umma huu wa Waislamu. Allah Azza wa Jallah amlipe kila la kheri na amuingize Peponi kwa salama na amani insha’Allah. Halikadhalika tunalishukuru Jopo la Wafasiri wetu kwa kukifanyia tarjuma ya Kiswahili kitabu hiki, insha’Allah na wao Allah Azza wa Jallah awalipe kila kheri hapa duniani na Akhera pia, bila kuwasahau na wale wote waliochangia kwa namna mmoja au nyingine mpaka kufanikisha kuchapishwa kwake. Allah Mwenye kujazi awalipe wote malipo mema hapa duniani na Akhera pia. Mchapishaji Al-Itrah Foundation

2

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 2

10/20/2015 5:15:20 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬ KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU, MWENYE KUREHEMU, MWINGI WA REHEMA

S

hukrani zote ni za Mwenyezi Mungu aliyemtuma Mtume Wake kwa uongofu na dini ya haki ili aidhihirishe juu ya dini zote, japo atachukia muovu aliyehasirika. Rehema na amani zimwendee bwana wetu, Muhammad, bwana wa mwanzo na wa mwisho. Na ziwaendee Aali zake na Maswahaba wake wenye utukufu mkuu wenye fahari. Hiki kitabu ni juzuu ya kufafanua juu ya Hadithi: “Nimemuona Mola wangu akiwa na sura ya kijana mzuri.”1 Nimekiandika baada ya kufanya istikhara kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu juu ya kuibatilisha Hadithi hiyo, na hivyo ndivyo ijtihadi yangu ilivyonipeleka na macho yangu kunifikisha baada ya kufanya utafiti na marejeo. Pengine kwa mtazamo wa mtu mwingine mwenye ujuzi huu, hii ni Hadithi thabiti yenye kukubalika, kwa sababu mitazamo ya watu yatofautiana.2 Na hii yote yatokana na vile Mwenyezi Mungu alivyompa kila mmoja kipaji chake cha ufahamu na utambuzi. Kila mmoja huangalia kaida na misingi inayorejea kwenye natija ya kumkhalifu mwingine. Na kila mwenye ijtihad ni mwenye kupata 1 2

Katika nakala imeandikwa “…amevaa nguo nyekundu.”   Katika maneno haya kuna ishara ya kuwepo mwenye kukubali usahihi wake, kwetu sisi hauna thamani hata akiwa ni katika wanahadithi wa zamani, inasemekana kuwa Abu Zar’a alisema hivi juu ya Hadithi hii: “Ni Hadithi sahihi, hakuna anayeipinga ila ni Muutazilah.” 3

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 3

10/20/2015 5:15:20 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

malipo ya thawabu kama inavyojulikana kwa wataalamu wa Hadithi, Mungu awazidishie utukufu, nasi atujaalie tuwe ni wenye kufuata nyendo zao na kuwa chini ya bendera zao. Hakika mwenye maono anaweza kujua daraja ya Hadithi, usahihi wake, udhaifu wake, na je ni hasan, au ni ya uzushi na uwongo kabla hata hajachunguza mlolongo wa wapokezi wake, ambao kwa kawaida ndio ngazi ya kujulia sifa za hadithi hiyo. Na hiyo ni kwa kufanya utafiti wa kina wa muda mrefu katika elimu hii tukufu. Isitoshe maimamu wa elimu ya fani hii wamesema: “Asiyejua usahihi wa Hadithi na udhaifu wake kabla hajaangalia sanad yake huyo hatafuti Hadithi.”3 Kwa sababu hukumu ya hilo ni kuangalia zaidi fani na hivyo kufikia yale yanayotakiwa. Ama kung’ang’ania kwenye sanad tu ni kuonyesha kushindwa kufikia lengo la elimu hii, na pia ni kukosa umakini ule anaouhitajia mwenye elimu hii, mbali na elimu zingine.4 Kwa sababu kila zama watu waongo kutoka mila mbalimbali wanatunga Hadithi kulingana na matamanio na malengo yao, kuna wanaochomeka sanad sahihi na kuweka njia ya kubandika kutoka kwa wapokezi wanaotegemewa. Hivyo mjuzi wa Hadithi asipokuwa ni mwerevu mwenye kuona mbali, ambaye damu yake, roho yake na mwili wake umechanganyika na Hadithi, huenda zikamhadaa Hadithi hizo mwanzoni kutokana na sanad za uongo zilizowekwa na wazushi hao, na hawezi kujua ukweli wake ila baada ya kutafiti kwa makini sana, na mara nyingine ni vigumu kuongoka kupata ukweli wake.   Mahafidhi wengi wa Hadithi wamehukumu kuwa Hadith fulani ni batili na haisihi kabla hata ya kuangaliwa sanad yake mwanzo. Kuna mifano mingi, mmoja ni kauli ya Hafidh Ibn Hajar katika Talkhis (2:210) katika Hadithi: “Hapana talaka ila baada ya kupita nikahi,” na mlolongo wa wapokezi wake ni watu waaminifu, ameipokea Bin Adiyy kutoka kwa Ibn Swaid, amesema Ibn Swaid: “Sioni kama ina ila.” Nasema: Lakini Ibn Adiy ameitia ila. 4   Jambo lililotangulia na kuanza katika umma huu kuhusu usahihi wa Hadithi ni kupinga matini kabla ya kuichunguza sanad yake. Ni mara ngapi Bibi Aisha O amezikataa hadithi za Ibn Umar au Abu Huraira kama alivyofafanua hilo Al-Zarkashi katika kitabu Al-Ijabat fi Istidraki Sayyida Aisha Ala Swahabah, na huu ni mlango muhimu na maarufu. 3

4

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 4

10/20/2015 5:15:20 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

Kutokana na uzushi huu na uenezaji uongo wa kuwatia watu shakani, imekuwa ni lazima mwanahadithi afanye ijtihadi na aangalie kaida na hali za Hadithi mpaka afikie hali ya kutoa hukumu juu ya Hadithi bila ya kuangalia zaidi sanad, bali katika elimu hii anafikia daraja la mtu mwenye kupewa ilhamu ambaye anatoa habari za jambo bila dalili na wala hawezi kutoa dalili kama walivyosema mahafidhi wa Hadithi.5 Ndipo baadhi yao wakasema: Elimu ya Hadithi ni uchawi, hiyo ni kwa maana hii nilioitaja. Lakini elimu nyingine haziko hivyo. Lakini mimi naona hii ni tawfiki tu ya Mwenyezi Mungu kwa wataalamu wa Hadithi ili waingize katika sharia ya Kiislamu yanayofaa kuingia na kuyaepusha yasiyofaa na asiyokuja nayo Mtume Muhammad 8, kwa kuwa Sharia asili na matawi yake vimechukuliwa kutoka kwenye Hadithi za Mtume Muhammad 8, na Allah amechukua dhamana ya kuhifadhi Sharia Zake, ndipo akawapa ilhamu wataalamu wa Hadithi na kuwapa tawfiki mpaka ikawa elimu hii waliyonayo ni ya kulinda hadithi za Mtume 8. Utakapojua hili, tambua kwamba Hadithi hii sikuihukumu upande wa maana na matini yake,6 na pia maneno yake hayakunifanya niichukulie kuwa ni ya uwongo, inaweza kuwa maana yake iko sawa, na hasa iliposemwa katika Hadithi nyingine ambayo baadhi wamesema ni sahihi, kuwa Mtume 8 “Alimuona Mola Wake akiwa na sura nzuri,” tamko7 ambalo linathibitisha maana hii, kama   Angalia kitabu Tadribu Rawi (1:253) na Siyar Aalamin-Nubalai (13:254), na vinginevyo.   Pamoja na kuwa ni Hadithi batili ya uwongo, hata kama sanadi yake ni sahih, Mwenyezi Mungu ametakasika kuwa na sura au awe na umbile la kijana mzuri kama wasemavyo wapotevu. Utakatifu ni Wako, umetakasika mbali na yale wanayokuzushia ewe Mola Mwenye enzi! 7   Katika nakala nyingine: Imeandikwa ‘sahih”, badala ya “wamesema ni sahihi”, lakini maana ya maneno ya mtunzi kayafupisha mwisho katika risala yake kwa kusema kuwa “si sahih”, hivyo yale tuliyothibitisha yanakuwa ndio kweli, nayo ni tamko: “wamesema ni sahih.” 5

6

5

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 5

10/20/2015 5:15:20 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

ambavyo pia inachukuliwa kuwa kumuona huko kulikuwa ni kwa ndoto. Hivyo nimeihukumu kuwa ni batili kutokana na njia ya sanad ambayo ndio mlango wa kawaida wa kuingilia ili kufikia kwenye njia sahihi isiyo na kombo. Unapothibiti kwangu ubatili wa sanad yake basi kwa sababu hiyo bila shaka kunathibiti kutokufaa kwa matini yake, kwa hivyo basi anayeafiki maoni yangu hafai kuikubali maana yake na kuiamini usahihi wake kwa sababu haifai kutumia Hadithi ambayo sanadi na njia zake ni dhaifu. Na ukisema kuwa Hadithi ambayo wamesema ni sahihi “Nimemuona Mola Wangu yu katika sura ya kijana mwenye sura nzuri” inashuhudia usahihi na kuipa nguvu. Ninasema kuwa haishuhudii hilo katu, kwani ile waliyosema ni sahihi, hata tukikubali kuwa kweli ni sahihi, yenyewe haina ibara isemayo: “Akiwa katika sura ya kijana mzuri akiwa amevaa vazi jekundu”, kama ilivyo katika Hadithi hii. Ambapo Hadithi hiyo nayo pia ina mambo yake ya utata kama tutakavyoeleza baadaye kwa uwezo Wake Allah Mtukufu. Juzuu hii nimeiandika kwa haraka katika hali ya usongo wa moyo hivyo nimefupisha maneno na nimejaribu kueleza misingi ya masuala kwa muhtasari bila ya kurefusha. Inshaallah kitabu hiki kitawapa faida wasomi na nimekiita: Kauli sahihi zaidi katika kufafanua Hadithi: “Nimemuona Mola Wangu akiwa katika sura ya kijana mzuri.” Namuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu tawfiki ya kufuata njia iliyonyooka zaidi na anijaalie niwe katika watu walioko kwenye kundi la Mtume Wake mteule, shukrani ni Zake Allah, mwanzo na mwisho.

6

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 6

10/20/2015 5:15:20 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

FASLU YA KWANZA

A

mesema Al-Khatib katika kitabu, Tarikh Baghdad8: “Ametupa habari Al-Husein bin Shuja As-Sufi, ametupa habari Umar bin Jafar bin Muhammad bin Salim Al-Khatliy, ametuhadithia Abu Hafs Umar bin Fayruz, ametuhadithia Affan bin Swamad, yaani Bin Kisan, kutoka kwa Hamad bin Salamah, kutoka kwa Qatadah kutoka kwa Ikrimah, kutoka kwa Ibn Abbas kutoka kwa Mtume 8, amesema: “Nilimuona Mola Wangu akiwa katika sura ya kijana mzuri akiwa amevaa vazi jekundu.” Akasema Affan: “Na nikamsikia Hamad bin Salamah akiulizwa juu ya Hadithi hii, akasema: “Iacheni, amenihadithia Qatadah, na hakuwepo nyumbani kwangu mwingine zaidi yangu mimi na yeye.” Amesema Ibn Addiyy9: “Ametuhadithia Abdallah bin Al Hamid Al Wasiti, Ametuhadithia An-Nadhar bin Salama Shadhan, kutoka kwa Hamad bin Salama, kutoka kwa Qatadah kutoka kwa Ikrimah kutoka kwa Ibn Abbas kutoka kwa Mtume 8 amesema: “Amemuona Mola katika sura ya kijana mzuri, chini amevaa nguo ya lulu na miguuni amevaa viatu vya rangi ya kijani.” Na At-Tabrani katika ‘As-Sunna’ amesema: “Ametuhadithia Abdallah bin Ahmad bin Hanbal, ametuhadithia baba yangu, ametuhadithia Al-Aswad bin Amir na akatuhadithia Muhammad bin Uqbah Ashaybani Al-Kufi, ametuhadithia Al-Hasan bin Ali AlHalwani, ametuhadithia Affan, ametuhadithia Abdu Swamad bin Kisan, na akatuhadithia Muhammad bin Swalih bin Al-Walid AnNursy, ametuhadithia Isa bin Shadan, ametuhadithia Ibrahim bin Abi Siweid Ad-Dari, wamesema: “Ametuhadithia Hammad bin Salamah 8 9

Tarikh Baghdad (11:214)   Katika kitabu Al-Kamil Fi Dhuafaa (2 : 261) 7

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 7

10/20/2015 5:15:20 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

kutoka kwa Qatadah kutoka kwa Ibn Abbas amesema: “Mtume 8 amesema: “Amemuona Mola katika sura ya kijana mzuri akiwa na……..” At-Tabrani amesema: “Nimemsikia Abu Bakr bin Swadaqah akisema: ‘Hadithi ya Qatadah iliyopokewa kutoka kwa Ikrimah, kutoka kwa Ibn Abbas juu ya ndoto ni sahihi, hiyo ameipokea Shadhani, Abdu Swamad bin Kisan na Ibrahim bin Abu Suweid, hii haikanushwi na yeyote ila awe Muutazilah.”’ Nami nasema: La, Wallahi si sahihi, nami naikanusha na mimi si Muutazilah wala sina urafiki nao bali mimi ni Msunni kwa njia ya Maswahaba na waliowafuatia wao katika mambo mema. Lakini kauli hii ndio iliyonifanya nichunguze na kutafiti kwa jicho la kina katika hukumu ya Hadithi hii, na hilo nitalifafanua kupitia sura zifuatazo:

8

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 8

10/20/2015 5:15:20 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

SURA YA KWANZA:

U

fafanuzi wa udhaifu wa Hadithi hii ni kutoka kwa upokezi wa Hamad bin Salamah, nao uko kwa mambo yafuatayo:

Kwanza: Hamad bin Salamah alipozeeka uwezo wake wa kutunza kumbukumbu ulikuwa si mzuri, kama alivyosema AlBayhaqi, na hatujui ni wakati gani alipokea Hadithi hii, ni wakati ule akili yake ingali nzuri au ni alipozeeka na kumbukumbu yake kuwa mbaya, inapokuwa hali kama hii basi yapasa kusimamisha upokezi wake mpaka ijulikane hali yake. Kasoro hii pekee yatosha kuipinga Hadithi hii na kuifanya kuwa si sahihi kwa wenye elimu ya Hadithi. Pili: Bukhari aliiacha Hadithi ya Hamad bin Salamah ilipothibiti kwake kuwa mtu huyo alikuwa akikosea. Ama Muslim yeye alifanya ijtihad na akaiandika Hadithi yake kutoka kwa Thabit kadiri alivyosikia kutoka kwake, kabla ya kubadilika kwake, isipokuwa Hadithi zake kutoka kwa Thabit, hazifiki Hadithi kumi na mbili alizoziandika. Na Hamad bin Salamah imeonekana alikuwa na makosa katika Hadithi hii kama tutakavyoeleza zaidi. Tatu: Huyu Hamad alikuwa akitaja Hadithi ‘Munkar’, kama alivyosema Ibn Saad,10 na hadithi hii huenda ni miongoni mwa Hadithi munkar kama alivyosema Ad-Dhahaby katika Al-Mizan,11 yeye baada ya kutaja njia zake amesema: “Hii ni kati ya zile Hadithi Munkar zaidi alizozileta Hamad, na hii ni ndoto, ikiwa kweli basi ni ya usingizini.”   Katika Tabaqaatul-Kubra (7:282) na hii ni nafasi ya dhahabu aliyotupa Seyyid Abdul Aziz, Ad-Dhahabi na wengineo hawakutaja katika wasifu wa Hamada! 11   Al-Mizan (2:364), na hii ilikataliwa kwetu kwa sababu Mwenyezi Mungu haonekani usingizini au hata katika hali ya kuwa macho, sababu hana umbo, sura wala nuru, wala kiza “macho hayamuoni”. 10

9

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 9

10/20/2015 5:15:20 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

Nne: Yeye amekuwa wa pekee katika Hadithi upande wa matini na sanad, na hasa katika Hadithi zinazozungumzia sifa za Mungu, na Hadithi hii ni miongoni mwazo, Ibn Adiyy katika kitabu Al-Kamil, ametaja Hadithi nyingi ambazo ni yeye tu Hamadi peke yake kataja matini na sanadi husika, na katika hizo akaitaja Hadithi hii. Pia Nasai, amesema katika aliyoyataja Al-Baji12 katika kitabu Rijalul Bukhari, kwamba Nasai aliulizwa kuhusu mtu huyo, akasema, si mbaya, na kabla ya hapo alisema ni mwaminifu. Amesema Qasim, nikamzungumzia, akasema: “Nani athubutu kumsema?” Kisha Nasai akawa akieleza zile Hadithi ambazo ni yeye tu Hamad kazitaja, zile zinazohusu sifa za Mungu,13kama aliyekuwa akiogopa watu wasije kusema: Amefuata njia zake.14 Tano: Yeye anatuhumiwa kwa Hadithi zenye kuzungumzia sifa za Mungu, wamesema: “Hakika yameongezwa mambo katika vitabu vyake, pia yasemekana mlezi wake, Ibn Abul Awja aliyekuwa mzandiki, kama alivyosema Ibnu Jawziy katika kitabu Daf’u shabhu tashbiih, ndiye aliyeongeza mambo katika vitabu vyake. Amesema Dawlabiy: “Ametuhadithia Muhammad bin Shujaa At-Thalajiy, ametuhadithia Ibrahim bin Abdu Rahman bin Mahdi, akasema: “Alikuwa Hamad bin Salamah hakubali Hadithi hizi zenye kuzungumzia sifa za Mungu, mpaka wakati mmoja alipotoka kwenda Ibadan ndipo akaja hali anasimulia Hadithi hizo, mara nikamsikia Ubada bin Suhayb akisema: Hamada alikuwa hawezi kuhifadhi. Na walikuwa wakisema alikuwa akiongeza mambo katika vitabu vyake,   Kitabu At-Taadil wa Tajriih (2: 523), Chapa ya Daruliwaa, chapa ya kwanza mwaka 1406 A.H.Riyadh. 13   Katika Kitabu Al-Bahi limechapishwa neno tashbih badala ya sifaat. 14   Maneno haya huandikwa kwa wino wa dhahabu kwa sababu yametufunulia uhakika wa ilivyoandika nukuu katika kitabu cha Al-Baji: “kama kwamba aliogopa watu wasije kusema kuwa alimzungumzia Hamad kutokana na njia zake, kisha akasema watu wa Hadithi ni wajinga.” Na huku ni kukubali kwa Nasai ujinga wa watu wa Hadithi waliokubali Hadithi za sifa kukoka kwa Hamad. 12

10

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 10

10/20/2015 5:15:20 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

na imesemekana Abul Awjaa, mlezi wake pia alikuwa akiongeza mambo vitabuni mwake. Amesema Ad-Dhahabiy katika Al-Mizan: ‘At-Thalajiy si wa kuaminiwa kuhusu Hamad na watu mfano wake, na alikuwa akituhumiwa. Amesema Al-Hafidh katika Tahdhib, Ubada pia si chochote.’15 Nasema: Hii ni kweli Muhammad bin Shujaa alikuwa muongo mkubwa.16Alikuwa mfuasi shupavu sana wa madhehebu ya Hanafi,   Tuchukulie kuwa Ibn Thaljiy hasadikiwi kimjadala na Ubad si chochote, pamoja ya kwamba kauli zenye kutegemewa kuhusu wawili hao haziko hivyo, bado ukweli unashuhudia kwamba Hamad bin Salama alizusha balaa katika itikadi na sifa. Hii ni kama tukisema kuwa watu wa Hadithi kama AnNasai na wengineo hawakuthibitisha hilo! Itakuwaje ikiwa wamethibitisha kama walivyothibitisha! Na kitendo cha AdDhahabi na Ibn Hajar kupinga uhakika huu wa Hamad bin Salama hakina thamani. Baadhi ya Hadithi zake zimekataliwa na Ibn Saad. Na Ad-Dhahabiy katika Siyaru Aalamin-Nubalai, (9:253) na pia Hafidh Ibn Hajar katika Tahdhiibut-Tahdhiib (7: 303), katika wasifu wa Ali wamesema kutoka kwa Asim, kwamba Ahmad bin Hanbal alisema: “Hamad bin Salama alikuwa akikosea. Na Ahmad akaonyesha kwa mkono wake makosa mengi, na hatukuona vibaya kupokea kutoka kwake.” Kwa sababu yeye alikuwa ni katika wao, katika imani ya kumshabihisha Mungu na viumbe na kumpa Mungu umbile. Na katika Tahdhiibut-Tahdhiib (3:12): “Alikuwa mgumu katika sunna.” Al-Hafidh Suyuti amesema katika. Al-Hawi Lilfatawi (2:2260): “Hamada alizungumzwa vibaya juu ya uhifadhi wake na katika Hadithi zake kumeingia hadithi zisizokubalika ambazo ni munkaar, wametaja kwamba mlezi wake alikuwa akiongeza vitu katika vitabu vyake.” 16   Yeye amethbiti kwetu kuwa ni mwaminifu, na ufuatiliaji wa Sheikh katika kumsifu kuwa ni mwongo si chochote! Hawategemewi kwa hilo, kwa sababu wao walimfanyia uadui kwa kuwa alikuwa ni wa madhehebu ya Hanafi na akisema kuwa Qur’ani imeumbwa. Ad-Dhahabi amemsifu katika Siyaru Aalamin-Nubalai (12: 379): “Muhammad bin Shujaa ni fakihi, gogo la elimu, mchamungu, mwenye kufanya tahajudi na kusoma Qur’ani, alifariki akiwa katika sijda. Ana kitabu cha manasiki zaidi ya juzuu sitini ila alikuwa akisimama kwenye masuala ya Qur’ani na akiyapata kutoka kwa wakubwa. Na hapa si sehemu ya kuchambua habari zake.” Makusudio ya wakubwa hapa yaweza kuwa ni Ahmad bin Hanbal na Hamad bin Salamah. Na makusudio ya: ‘Na hapa si sehemu ya kuchambua habari zake.’ Ni kwamba wala haoni ubaya wake kama alivyokuwa haoni kwenye Al-Mizan, aliposema humo: “Alikuwa mwenye ibada na alikufa kwenye Swala ya Asri atarehemewa inshaallaah.” Dkt. Bashar Awada amesema katika maelezo yake katika Tahdhibul Kamal: (25: 365): “Wamemuwekea maneno mazito kwa sababu ya itikadi.” Yaani wamemtuhumu kwa uwongo na uzushi na bidaa kwa sababu tu ya 15

11

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 11

10/20/2015 5:15:20 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

hali hiyo ikamfanya kuwaponda watu wa Hadithi kwa kila chafu.17 Na alikuwa akichomeka Hadithi mbaya juu ya sifa za Mwenyezi Mungu ili awachafue watu wa Hadithi.18 Miongoni mwa hadithi hizo ni Hadithi ya ‘Kuendesha farasi’ aliyoipokea kutoka kwa Habban bin Hilal, na Haban ni mkweli kama alivyosema Ad-Dhahabiy, kutoka kwa Hamad bin Salamah, kutoka kwa Abul Muhzam, kutoka kwa Abu Huraira, kwamba: “Mwenyezi Mungu aliumba farasi kisha akamwendesha, akavuja jasho kisha akajiumba nafsi yake kutokana na huyo farasi.19 Hadithi hii, kuisikia tu kwatosha kuwa ni dalili ya ufuska na imani ndogo na uchache wa kuwa na dini.20 Lakini ung’ang’aniaji kutofautiana kwake na wanahadithi katika mas’ala za kiitikadi.   Hivi ndivyo alivyochukuliwa Ibn Thaljiy na watu wa Hadithi, nao wamekosea hapo, wameng’anga’nia madhehebu yao mpaka kufikia daraja hiyo. 18   Hii ni kauli ya Ibn Adiyy, nayo imepingwa, na Nasai kama ilivyotangulia ameikubali. Na wajinga wa Hadithi hawahitaji kuwekewa na wapinzani wao Hadithi za kumshabihisha Mungu na viumbe, kwa kuwa wao wenyewe wameweka Hadithi za kupendekeza umbo kwa Mungu, na wameweka mabalaa katika vitabu vyao, na Hadithi ya kijana mzuri ni mojawapo, wala hakuwawekea Muhammad bin Shujaa Al-Thalajiy, bali wao wamejiangusha wenyewe bila ya kuangushwa na mtu yeyote, usisahau hili! 19   Mwanachuoni Muhadithi Al-Kawthariy amesema K katika As-Sayfi Swaqiil (Uk. 97): “Hadithi ya kuendesha farasi ilikuwa maarufu baina ya mashekhe wa riwaya, mpaka akalalamika kwa uchungu juu ya hilo Ibn Qutaybah, na huyu alikuwa wakati wa Ibn Shujaa. Pia ameiandika Abu Ali Al-Ahwaziy kwa sanad yake kutoka kwenye njia ya Hamada bin Salamah kutoka kwa Habban bin Hilal kutoka kwa Hamad bin Salamah. Na kauli ya al-Hakima kwamba: ‘Alitupa habari Ismail bin Muhammad Shaaraniy kwamba yeye alisema: Nilifikishiwa habari kutoka kwa Muhammad bin Shujaa, kutoka kwa Haban bin Hilal, kutoka kwa Hamad bin Salamah’ haiwezekani kuchukuliwa kuwa ni hoja, kwa kuwa imepokewa na Hamad bin Salamah kwa njia ya Shujaa peke yake! Kwa sababu kati ya Ibn Shujaa na Shaaraniy kuna kiasi cha miaka mia moja. Hivi ndivyo Allah anavyomfedhehesha mtu anayewafanyia kiburi maimamu. 20   Nilimwondolea dhima Muhammad Shujaa At-Thalajiy kama tulivyonukuu kutoka kwa Al-Kawthariy, na mwenye kuizua kama alivyotaja Seyyid Abdul Aziz ni yeye. Na watu wa Hadithi na baadhi ya wapokezi walizua hadithi kama hiyo au zilizo mbaya zaidi kuliko hiyo, na miongoni mwa walizozua ni Hadithi ya kijana mzuri tunayoizungumzia! Na vitabu wanavyoviita kuwa ni vya Sunna ambavyo vinazungumzia sifa za Mwenyezi Mungu vimejaa mabaya kama haya, kama kitabu Sunna cha Ibn Ahmad ambacho humo inatajwa kuwa Kursii ni mahali pakuweka miguu ya Mungu, na majanga mengine kama 17

12

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 12

10/20/2015 5:15:20 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

wa rai na kuwachukia Masunni kunawapeleka hao kwenye kufru bila kujijua.21 Ibn Adiyy amesema: “Muhammad bin Shujaa alikuwa akizua Hadithi ya kumshabihisha Mungu na viumbe kisha anainasibisha na watu wa Hadithi ili aweze kuwachafua.22 Amesema Ad-Dhahabiy katika kitabu Diwaan dhuafaa wal matruukina: “Amesema Ibn Adiyy: ‘Alikuwa akizua Hadithi ya kumshabihisha Mungu na viumbe kisha akiinasibisha na watu wa Hadithi ili kuwajaribu nayo.23 Hivyo kumtoa kasoro Hamad bin Salamah upande huu, ni kushikamana na mambo mabovu kabisa,24 hayo. Na watu mfano wa Muhammad bin Shujaa ni: Hamad bin Dalil Al-Madainiy, Abu Zaid Kadhi wa Madain, naye ni katika watu wa Abu Hanifa. Imenishangaza kauli ya Dkt. Bashar Awad katika maelezo ya kitabu Tahdhibul lkamal (7:238): “Yahya na Ibn Ammar na Abu Hatim, wamemzingatia kuwa ni mwaminifu, na hao wanakutosha. Ama kumpinga kwao kwa ajili ya rai, Mungu atulinde na hawaa na atupe afya!” 21   Haya maneno hayamsalimishi mhusika, bali kushadidia Sunna na kung’ang’ania bila uchunguzi na kutazama namna ya kumtakasa Mungu ndiko kunampeleleka mtu katika hilo. Na watu wa maoni wako mbali na hilo! Na Sayyid Abdul Aziz yuko pamoja nao na yuko pamoja na wenye akili miongoni mwa wanahadithi katika kupinga Hadithi ya kijana mzuri, na kwamba hii Hadithi ni ya uzushi na uwongo. 22   Hakuna dalili ya hilo, Sheikh huyu Al-Kawthariy alipinga kauli ya Ibn Adiyy katika maelezo ya kitabu As-Sayfi Swaqiil Fii Raddi Ala bin Zafiyl, Uk. 97 akasema: “Ibn Shujaa alikuwa akiwatahadharisha wapokezi kuchukua riwaya potofu zilizowekwa na kuzuliwa na wazuaji wa Hadithi kwa ndimi za baadhi ya mashekhe na wapokezi wa Hadithi. Anajibibiwa na Sheikh Uthman bin Said ad-Daramiy ambaye ni mwenye kuitakidi kuwa Mungu ana mwili, akisema: “Wenye kutunga Hadithi watapataje njia ya kuingia kwa masheikh wapokezi kwa kuchomeka riwaya?” na Ibn Adiyy naye analigeuza jambo na kufanya kuwa anayeingia kwao ni Ibn Shujaa bila ya kuwa na dalili yoyote na kuwa na sanad yoyote. 23   Maneno haya yamekataliwa kama tulivyobainisha katika maelezo yaliyopita, nayo ni kuiga tu kwa Ibn Adiyy kutoka kwa ad-Dhahabiy. 24   Bali ndio ya kushikilia zaidi, amesema Al-Kawthariy katika marejeo yaliyotangulia: “Bali yatosha kumjua Hamad bin Salamah kwa kuangalia vitabu kwenye maudhui nyepesi katika mlango wa tawhid, msomaji ataona habari potofu zimepokewa kwa njia nyingi, bali Hadithi mbovu zilizopokelewa kwa njia yake, alizozitaja Ibn Adiyy mwenyewe katika kitabu Al-Kamil katika wasifu wa Hamad zatosha kujua kuporomoka kwa mapokezi ya njia zake zinazozungumzia Hadithi za sifa za Mungu. 13

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 13

10/20/2015 5:15:20 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

kama inavyojulikana wazi na hasa ukizingatia kuwa Ubad bin Suhayb ni muongo pia. Lakini la ajabu kwa Sheikh Muhammad AlKawthary Al-Hanafy ambapo ameichukua kauli hii kuwa ni hoja yenye nguvu isiyopingika katika kuidunisha Hadithi ya Hamad bin Salamah katika sifa, na yenyewe ni katika uzushi wa mlezi wake Ibn Abul Awjaa aliyekuwa akiviharibu vitabu vya Hamada bin Salamah.25 Na Al-Kawthary haujifichi kwake ubatili huu katu, lakini ile taasubi aliyokuwa nayo ilimfanya yeye kuwa kiongozi na nguzo yake26 mpaka ikampelekea kupinga Hadithi sahihi kwa rai potofu isiyo na dalili wala kitabu chenye mwangaza, na kwa ajili hii ndipo Mtume 8 alikuwa akijilinda na hawaa inayopotosha akisema: ‘Hakuna kilicho chini ya kivuli cha mbingu (dunia) kinachoabudiwa zaidi kuliko hawaa inayofuatwa.’27 Zingatia haya na ikatae taasubi na hawaa na zunguka na haki pale izungukapo ili usiangukie kwenye maangamivu, Mungu apishe mbali!”   Bali Muhammad bin Shujaa ni katika mafakihi wa kihanafi naye ni mwaminifu. Ilipokuwa madhehebu yake hayaafikiani na madhehebu yao na kwamba alikuwa akifichua aibu zao na hizo Hadithi za sifa na kumshabihisha Mungu na viumbe, ndipo walipomtia ila na kumkataa kama ilivyotangulia kuelezwa. 26   Bwana wetu Muhaddith Abdallah bin Swadiq amesema katika risala yake mashuhuri Baynii Wabayna Sheikh al-Kabiir, Uk. 86: “Sisi, hata kama tutamuaibisha Al-Kawthariy kwa kung’ang’ania kwake madhehebu ya kihanafi lakini twaheshimu elimu yake na ubora wake na anazingatiwa kuwa ni wa kipekee katika zama zake kwa kusoma sana na elimu nyingi na kutetea akida. Yatosha kuwa yeye ni mujahid aliyekimbia nchi yake na kuacha cheo chake cha uwakala wa masheikh wa kiuthmaniyya na akaishi hali ya ufakiri, mwenye kuipa nyongo dunia. Alipewa vyeo akavikataa, mara ngapi amesaidia watu katika kuchapisha na kuvihakiki vitabu bure bila ya malipo, hakula kwa kutegemea elimu yake kabisa. Hii ni fadhila ambayo haikupatikana kwa ulamaa wa wakati wake.” Nami nasema huyu hakuwa mwenye taasub ila alimtetea sana Imam Abu Hanifa, ndio wakamnasibisha na taasub. 27  Tabaraniy amepokea katika Muujamul Kabiir, Uk. 8: 103, na pia Ibn Asim katika As-Sunna (1:8) kutoka kwenye Hadithi ya Abu Umamah na iko hivi: “Hakuna kilicho chini ya kivuli cha mbingu (dunia) kinachoabudiwa zaidi kuliko hawaa inayofuatwa.” Amesema Al-Hafidh Al-Haythamiy katika Majmaa: “Ameipokea At-Tabaraniy katika AlKabir na yumo Hasan bin Dinar.” 25

14

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 14

10/20/2015 5:15:21 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

Sita: Kwamba riwaya ya Hamad bin Salamah kutoka kwa watu wa Basra, ni dhaifu kwa sababu yeye hakushughulika na Hadithi zao, na Qatadah ni mtu wa Basra, pamoja na kuwa Muslim ametolea hoja baadhi ya Hadithi ambazo zilithibiti kwake lakini hakutoa chochote katika Hadithi zake alizozichukua kutoka wa watu wa Basra kutokana na wingi wa Hadithi gharib zinazopatikana kutoka kwao. Ibn Tahir amesema katika kitabu, Shurtul Aimmatul khamsa: “Kwa sababu hii ndipo Muslim anatoa udhuru wa kutoandika Hadithi za Hamad bin Salamah, kwani yeye hakuziandika ila zile riwaya kutoka kwa watu mashuhuri kama vile Al-Baniy na Ayyub As-Sakhtany, na hiyo ni kwa kuwa alikuwa karibu sana na Thabit, kiasi kwamba sahifa ya Thabit ilibaki katika kumbukumbu yake baada ya kuchanganyika kama ilivyokuwa kabla ya kuchanganyika. Ama Hadithi zake kutoka kwa mtu mmoja mmoja kati ya watu wa Basra, Muslim hakueleza chochote kutoka kwao, kwa sababu ya wingi wa gharaib katika riwaya zao, na hiyo ni kwa sababu ya kutojishughulisha sana na Hadithi zao.28 Na ile Hadithi ya ‘Mlango’ aliyoipokea Hamad bin Salamah kutoka kwa Qatadah ambaye ni mtu wa Basra, nayo ni katika zile Hadithi gharib kutoka kwao. Saba: Pamoja na ukubwa wa elimu wa Hamad bin Salamah, Ad-Dhahabiy amesema: “Alikuwa na makosa makosa. Ndio, hata kama mwanadamu hakosi kuwa na makosa, hakika makosa na kuchanganya ni mambo ambayo mwanadamu hawezi kuyaepuka, kila kiumbe lazima afanye makosa, hivyo haifai kumtia kasoro kwa mambo hayo.” 28

Hii inaonyesha namna Hamad bin Salamah alivyokuwa na hifdhi mbaya. 15

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 15

10/20/2015 5:15:21 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

Na kwa hili Ad-Dhahaby amesema katika Diwanud-dhuafaa: “Hamad bin Salamah ni imam mwenye kuaminiwa na anakosea kama wengine.” 29 Nami nasema: Ila kumetokea maafikiano kati ya watu wa fani hii kwamba watu wa kuhifadhi na kudhibiti hadithi wamejiepusha naye katika Hadithi zao ila kama itakuwepo dalili inayoonesha kuwa mhifadhi alichanganya Hadithi, na hapa hapa ndipo kumepatikana dalili ya kukosea kwa Hamad bin Salamah katika Hadithi hii, nayo ni riwaya yake kutoka kwa Thabit kutoka kwa Anas. Amesema Daru Qutniy katika kitabu Al-Ifrad: “Ametuhadithia Abu Bakr Ahmad bin Isa Al-Khawwas, ametuhadithia Sufian bin Ziyad bin Adam, ametuhadithia Abu Rabia Fahdi bin Awfi, ametuhadithia Hamad bin Salamah, kutoka kwa Thabit kutoka kwa Anas, kwamba Mtume 8 amesema: “Nilimuona Mola Wangu akiwa katika sura nzuri sana.” Hapa kaida mbili miongoni mwa kaida za Hadithi zinapingana. Na hivyo waliyopokea Hadithi hii kutoka kwa Hamad, kutoka kwa Qatadah kutoka kwa Ibn Abbas ni wengi kuliko walioipokea kutoka kwa Hamad, kutoka kwa Thabit kutoka kwa Anas, jambo ambalo linaifanya Hadithi moja kuwa ni yenye kuhifadhiwa na maarufu, huku Hadithi nyingine kuwa ni munkar tena ngeni, hivyo itakayofanyiwa kazi ni ile ya wale walio wengi. Na hii ni kaida kuu na maarufu katika istilahi za elimu ya Hadithi, imefanyiwa kazi na wanahadithi wa zamani hadi wa sasa. Lakini kaida hiyo inapingwa na kukinzana na kaida makhususi ambayo inalazimu kuitanguliza riwaya ya Hamad, kutoka kwa Thabit, kutoka kwa Anas. Hiyo ni kutokana na kile kilichothibiti kwamba mtu aaminikaye zaidi kwa Thabit ni Hamad, na kwamba Hadithi za Hamad kutoka kwa Thabit 29

Hii tunapata kuelewa kwamba hawa wapokezi waaminifu wanakosea kwa hivyo twaweza kukataa Hadithi zao zinazokwenda kinyume na utukufu na ithbati! 16

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 16

10/20/2015 5:15:21 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

ni sahihi. Lakini mgongano na ukinzani huo wa kanuni hizi mbili (kuu na makhususi) unaondoka na kuanguka kutokana na udhaifu wa Fahdi bin Awfi mpokezi kutoka kwa Hamad. Na Allah ndiye ajuaye zaidi. Nukta zote hizi zaonyesha udhaifu wa Hadithi kutoka kwa Hamad bin Salamah.

SURA YA PILI: Udhaifu wake kutoka upande wa Qatadah30 nao ni upande wa pili. Qatadah ni mzushi mashuhuri kwa kazi hiyo, ametajwa na Al-Hafidh katika kitabu Tabaqat thalitha min tabaqat tadliis.31 Na Shuuba amesema: “Nilikuwa nauangalia mdomo wa Qatadah anaposema: ‘Ametuhadithia’ naandika, na asiposema siandiki. Na hapa hajasema ‘Ametuhadithia,’ si katika njia hata moja miongoni mwa njia za Hadithi hii, na jambo hilo lafanya tujizuie kuichukua kutoka kwake mpaka idhihiri kutoka kwenye njia nyingine kwamba ameisikia kutoka kwa Ikrimah, kama ilivyo zoeleka katika upokezi wa mwenye kuzusha.

Tazama wasifu wake katika Tahdhiibul Kamala cha Al-Mazy (23:498-518), na katika Sualaatil-Ukhra kutoka kwa Abu Daud kwamba Qatadah amehadithiwa na watu thelathini na hakuwasikiliza. 31   Tazama kitabu Taarif Ahlu Taqdiis Bimaratibul Mawsuufina bi Tadriis cha Hafidh Ibn Hajar Uk. 102. Chapa ya Darul Kutubil-Ilmiyyah, mwaka 1405 (A.H.), naye ni katika wenye daraja kubwa na tabaka ya tatu ambao Ibn Hajar amewataja kuwa: “Ni katika waliozusha sana, maimamu hawakutolea hoja Hadithi zao, kuna waliozikataa kabisa, na kuna waliowakubali.” 30

17

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 17

10/20/2015 5:15:21 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

SURA YA TATU: Ikrimah: Huyu japokuwa alikuwa ni katika watu wa Bukhari lakini Ibn Umar alimkadhibisha32 na akamwambia Nafiu: “Usinisemee uwongo kama Ikrimah alivyomsemea uwongo Ibn Abbas.” Na Ali Ibn Abbas alimfunga kutokana na uongo wake juu ya baba yake. Muslim pia amejiepusha na Hadithi zake na hakumtaja ila kwa kumwambatanisha na mwingine, na maneno juu ya hili ni mengi. Al-Hafidh Ibn Hajar amefupisha yale waliyoyasema maimamu katika Muqaddimatul fat-hi na kuwajibu waliomtoa kasoro, na kubainisha usahihi wa Bukhari katika kutaja Hadithi yake. Lakini itakubaliwa vipi Hadithi yake na hali wamemkadhibisha katika riwaya ya Hadithi ya kwamba Mtume 8 alimuoa Maimuna hali akiwa ndani ya ihram. Na alizungumzwa sana kwa ajili ya Hadithi hii, hivyo inapasa kutozichukua Hadithi zake hasa Hadithi munkar33 kama hii. Na ametolewa kasoro pia kwa rai za Makhawarij, kwani kutoka kwake Makhawarij wamechukua bidaa zao kama inavyojulikana.

Kama utavyoona hilo katika kitabu Tadhhiibul Kamal (20: 279), lakini haisihi kuwa imetoka kwa Ibn Umar, kwa kuwa ni katika riwaya za Abu Khalaf Al-Jazar kutoka kwa Yahya al-Bukau, na Yahya ameachwa, wamemtuhumu kwa kusema kuwa ni muongo, kwa sababu alikuwa akipinga siasa za dola ya Bani Umaiyyah, na ni kwa ajili hiyo alitangatanga katika miji mbalimbali. Katika Tahdhibul Kamal Uk. 290: “Mas’ab bin Abdallah Az-Zubayr amesema: “Alikuwa akifuata rai za Makhawarij, baadhi ya watawala wa Madina wakamtaka, akatoweka kwa Daud bin Haswin mpaka akafariki kwake.” Ikrimah alifariki mnamo mwaka 105 akiwa na umri wa miaka themanini. Na Khawariji wanayemtuhumu ana jambo zuri lakini hawatambui. Na wala yeye si kama Muawiya bin Abu Sufiyan. Na Ikrimah kwetu ni mwaminifu. 33   Yaani kama Hadithi hii ya kijana mzuri licha ya kuwa mimi naamini kuwa ila na kasoro yake si Ikrimah. 32

18

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 18

10/20/2015 5:15:21 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

SURA YA NNE: Nne: Hadithi hii katika sanadi yake kumetokea mikanganyo, imepokewa kutoka kwenye njia nyingine kutoka kwa Ikrimah kutoka kwa Muadh kutoka kwa Ghufraa kutoka kwa baba yake. At-Tabaraniy amesema: “Ametuhadithia Ali bin Said Al-Razy, ametuhadithia Muhamad bin Hatim, ametuhadithia Qasim bin Malik Al-Mazniy, ametuhadithia Sufyan bin Ziyad,34 kutoka kwa ami yake Salim bin Ziyad, amesema: “Nilikutana na Ikrimah wa Ibn Abbas akasema: ‘Usiondoke mpaka nikufanye shahidi juu ya mtu huyu, mtoto wa Muadh bin Ufraa. Akasema: Niambie alivyokuambia baba yako kutokana na kauli ya Mtume 8. Akasema: Ameniambia baba yangu kwamba Mtume 8 alimwambia kwamba yeye “Alimuona Mola wa viumbe vyote Mtukufu katika hadhira ya qudsi akiwa na sura ya kijana amevaa taji linalomeremeta kwenye macho.’”35 Amesema Sufiyan bin Ziyad: “Nilikutana na Ikrimah nikamuuliza juu ya Hadithi hiyo akasema: “Ndio, hivyo ndivyo alivyonihadithia lakini alimuona kwa moyo wake.” Hadithi hii hata kama imehifadhiwa lakini ni dhaif pia kwa sababu ya kutojulikana huyo Ibn Muadh, na ikiwa si hivyo basi ina mikanganyo kwenye sanad yake, hata kama wapokezi wataifanya iwe Hadithi Jayyid. Tano: Kama ilivyo na mikanganyo katika sanad yake, Hadithi hii pia ina shida katika matini yake, na Hadithi mfano wa hii haifai kupokewa kimaana, kiasi kwamba mpaka kumetokea mabadiliko kutoka kwa wapokezi. Kama ambavyo chimbuko lake ni moja, basi haiwezi kusemwa kuwa Mtume 8 alitamka matamshi hayo yenye tofauti yenye kuwa na chimbuko tofauti, bali chimbuko lake 34 35

Sijapata wasifu wake wala wa ami yake.   Hadithi hii ni ya uongo, ya uzushi, sikuiona kwa Tabaraniy labda katika kitabu chake as-Sunnah. Ameinukuu Seyyid Abdul Aziz kutoka kwenye kitabu cha Suyutiy al-Laaliy al-Masnuuah (1: 30). 19

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 19

10/20/2015 5:15:21 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

linakomea kwa Ikrimah, hivyo baada ya hivi haifai kuwe na ikhtilafu katika matamshi yake yaliyopokelewa. Katika baadhi ya matamshi: “Nimemuona Mola Wangu akiwa katika sura ya kijana akiwa na vazi.”36 Na katika nyingine ni kwamba alimuona Mola wa viumbe vyote mtukufu katika hadhira ya qudsi akiwa na sura ya kijana amevaa taji linalomeremeta kwenye macho.”37 Katika tamshi jingine: “Nimemuona Mola Wangu akiwa katika sura ya kijana mzuri chini yake ana vazi la lulu, miguuni ana viatu vya rangi ya kijani.”38 Katika tamshi jingine: “Nimemuona Mola Wangu akiwa katika sura ya kijana mzuri akiwa na vazi jekundu.”39 Katika tamshi jingine: “Nimemuona Mola Wangu akiwa na nywele zilizosokotana akiwa amevaa vazi la rangi ya kijani.”40 Katika tamshi jingine: “Nilipopelekwa Israi, nilimuona Mola Wangu akiwa na sura ya kijana mzuri mwenye nuru inayomeremeta.” Hii ni katika Hadithi fupi wala si ngumu kwa mpokezi wake kuihifadhi na kuiwasilisha kama alivyoisikia. Sita: Wao wamekosoa Qatadah kusikia kutoka kwa Ikrimah. Amesema Al-Maruzi: “Nilimwambia Ahmad, wao wanasema kuwa Qatadah hajasikia Hadithi kutoka kwa Ikrimah. Akakasirika Ahmad akanitolea kitabu cha kuonyesha kuwa amemsikia katika Hadithi sita. Ni kiasi kidogo alichokionyesha Ahmad, na hii ni kuonyesha  Amepokea Tabaraniy katika kitabu chake As-Sunnah kama ilivyo katika al-Laaliy alMasnuuah (1: 29) cha Suyutiy. 37   Ameipokea Tabaraniy kama inavyoonekana katika al-Laaliy al-Masnuuah (1:30) cha Suyutiy. 38   Katika al-Laaliy al-Masnuuah (1:31) ameiegemeza kwa Ibn Adiyy, amesema: “Na katika Mizan, amesema Ibn Adiyy. 39   Ameipokea Al-Khatib katika Tarikh yake (11:31) kwa njia ya Hamad bin Salamah kutoka kwa Qatadah. 40   Nimeona kwa mtazamo wangu kuna maandishi ya makosa kati ya rangi nyekundu kwani michoro inafanana, na katika chapa zingine imepokewa kwa tamko la rangi ya kijani. Taz. Kamil cha Ib Adiyy (2:261). 36

20

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 20

10/20/2015 5:15:21 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

kutofanyiwa kazi yale aliyoyasikia Qatadah kutoka kwa Ikrimah kama inavyoonekana. Hizi sura sita zinahukumu udhaifu wa Hadithi kutoka katika riwaya ya Hamad bin Salamah kutoka kwa Qatadah kutoka kwa Ikrimah na kushuhudia ubatilifu wa Hadithi hii. Ametaja Muslim katika kitabu chake At-tamyiiz, kwamba Hamad bin Salamah kwao anakosea sana katika Hadithi ya Qatadah.41 Wameeleza mahafidhi wa Hadithi kuwa Hadithi ya Qatadah inayopokewa na masheikh kama vile Hamad bin Salamah, Hamam, Abba, na Awzaai huangaliwa, kama Hadithi hiyo imehifadhiwa kutoka kwa isiyokuwa njia yao kutoka kwa Mtume 8, na kutoka kwa Anas kwa njia nyingine, huwa haikataliwi. Ama ikiwa haijulikani ni kutoka kwa nani, kutoka kwa Mtume, na wala si kutoka kwa Anas, ila ni kutoka kwenye riwaya za huyu niliyemtaja, basi huwa ni yenye kukanushwa. Na Hadithi ya Qatadah kaipokea kutoka kwake Hamad bin Salamah na wala haijakuja kwa njia nyingine inayoweza kuwa ushahidi wa usahihi wake. Na wanaposema ‘masheikh’ wanakusudia wale wasiokuwa waandamizi wa mpokezi husika wenye kuhifadhi hadithi zake, na hiyo ni kudhoofisha hadithi ya mpokezi makhususi anayepokea kutoka kwa mpokezi huyo, na si wapokezi wote.42 Angalia Sharhu Ilal ya Tirmidhy (Uk. 364). Maelezo haya yanatosha kufafanua hali ya sanad ya Hamad bin Salamah, kutoka kwa Qatadah kutoka kwa Ikrimah kutoka kwa Ibn Abbas, kutoka kwa Mtume 8. Abu   Kitabu Tamyiiz cha Muslim, mwandishi wa kitabu Sahih Muslim, Uk. 218: “Kwao Hamad bin Salamah anapohadithia kutoka kwa Thabit ni kama Hadithi yake kutoka kwa Qatadah, Ayyub, Yunus Daud, Ibn Abu Hind, Al-Jarir, Yahya bin Said, Umar bin Dinar na wengineo, yeye hukosea sana katika Hadithi zao. 42   Ieleweke kwamba kila mpokezi huwa ana wapokezi waliopokea kwake miongoni mwa waandamizi wake. 41

21

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 21

10/20/2015 5:15:21 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

Bakr bin Daud43 baada ya kupokea Hadithi hii kutoka katika njia ya Hamad bin Salamah, amesema: “Hii ni miongoni mwa Hadithi munkari zaidi alizozileta Hamad, na ndoto hii ikiwa kweli basi ni ndoto ya usingizini.”44 Imekuja Hadithi kwa njia nyingine kutoka kwa Ibn Abbas, amesema At-Tabarani katika kitabu chake, As-Sunnah: “Ametuhadithia Ali bin Said Ar-Razy.45 Ametuhadithia Ahmad bin Ibrahim Ad-Dawraqiy, ametuhadithia Hajjaj bin Muhammad, kutoka kwa Ibn Jurayji, kutoka kwa Dhahhak, kutoka kwa Ibn Abbas, amesema: “Muhammad alimuona Mola Wake Mtukufu akiwa na sura ya kijana.” Nami nasema: Hii pia haisihi tena ni batili kwa ufafanuzi wangu kama ifuatavyo: 1. Sheikh Tabaraniy, Ali bin Said Al-Razy, hata kama alikuwa ni mwenye kuhifadhi, Ibn Yunus amesema kumhusu: “Watu wamezungumzia sana kasoro zake.” Hamza bin Yusuf amesema: “Nilimuuliza Daru Qutniy kumhusu, akasema: “Hakuna katika Hadithi zake jambo hilo, yeye ametaja Hadithi na hazikufuatiliwa.” Kisha akasema: “Mimi sina imani naye, na wenzetu wamemsema kwa kosoro zake huko Misri.” Kisha akaashiria kwa mkono wake akasema: “Huyo ana kadha wa kadha,” na akaashiria akisema: “Huyo si mwaminifu.”46   Hapa maneno yake ni mazuri lakini baba yake alimkadhibisha, baba yake ni Abu Daud, mwandishi wa kitabu Sunan Abu Daud. 44   Sisi twaonelea haiwezekani kumuona Mola ukiwa macho au usingizini, kwa kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu hana sura wala umbo. 45   Daru Qutniy ametangulia kusema juu ya Razi kuwa hakuwa pweke katika mambo mengi kama ilivyo katika kitabu, Diwanudhuafaa (2: 448). 46   Angalia kitabu, Lisanul-Mizan cha Hafidh Ibn Hajar (4: 231). 43

22

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 22

10/20/2015 5:15:21 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

Nasema: Kuna wengine waliomuamimi, iwe itakavyokuwa alikuwa na mambo aliyokuwa nayo. 2. Ibn Juraij ni mlaghai. Amesema Daru Qutniy: “Jiepushe na udanganyifu wa Ibn Juraij, alikuwa mbaya sana kwa kuzusha, hazushi ila aliyoyasikia kutoka kwa wasiokuwa waaminifu kama Ibrahim bin Abi Yahya, Musa bin Ubaydah na wengineo. Na yeye ameweka orodha ya wapokezi wasiojulikana katika hadithi hii, hivyo ni yenye kukataliwa kama kanuni ilivyo. 3. Hajjaj bin Muhammad alijichanganya mwishoni mwa umri wake, na Muin alimuona akichanganya mambo akamwambia mwanawe: Asiingie yeyote kwake. Abdallah bin Ahmad amesema kutoka kwa baba yake: “Nilimuona Sunaid kwa Hajjaj bin Muhamad naye akisikiliza kutoka kwake kitabu Al-Jamii cha Ibn Juraij: “Nimeambiwa kutoka kwa Az-Zuhry, na nimeambiwa kutoka kwa Swafwan bin Sulaym” na isiyokuwa hiyo. Akawa Sunaid anamwambia Hajjaj: “Eee Abu Muhammad! Ibn Juraij kutoka kwa Az-Zuhry, na Ibn Juraij kutoka kwa Swafwan bin Sulaym?” akawa akimwambia hivyo.” Abdallah anasema: Wala baba yangu hakumsifu kwa aliyoyaona akimfanyia Hajjaj na akamtuhumu kwa kufanya hivyo, baba yangu alisema: “Na baadhi ya Hadithi alizokuwa akizitoa Ibn Juraij ni Hadithi za uwongo za kuzua.” Ibn Juraij alikuwa hajali anapokea kutoka kwa nani. Na Hilal pia amesema hivyo hivyo. Amejichanganya mwenyewe katika sanad ya Hadithi hii kwani ameipokea mara nyingine kutoka kwa Ibn Juraij kutoka kwa Swafwan bin Sulaym kutoka kwa Bi. Aisha O, amesema: “Mtume 8 alimuona Mola Wake akiwa katika sura ya kijana amekaa juu ya kiti (Kursy) miguu yake inang’ara rangi

23

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 23

10/20/2015 5:15:21 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

ya kijani.”47 Ameipokea Tabaraniy kwa sanad iliyopita, akaonyesha kuwa alihadithia Hadithi hii kwa mikanganyo kwa hivyo hakuidhibiti sanad yake. Na hii peke yake yatosha katika kuipinga Hadithi hii na kutoikubali. Hadithi nyingine: Al-Khatib amesema katika wasifu wa Nuaim bin Hamad katika Tarikh Baghdad: “Ametwambia Al-Hasan bin Abu Bakr na Uthman bin Muhammad bin Yusuf Al-Ulaf, wamesema: “Ametwambia Muhammad bin Abdallah bin Ibrahim Shafii, ametuhadithia Muhammad bin Ismail Tirmidhiy, ametuhadithia Nuaim bin Hammad, ametuhadithia Ibn Wahbi, ametuhadithia Amru bin Al-Harith, kutoka kwa Said bin Abu Hilal kutoka kwa Marwan bin Uthman, kutoka kwa Ummara bin Amir, kutoka kwa Ummu Tufayl mwanamke wa Ubayy kwamba amemsikia Mtume 8 akisema alimuona Mola Wake usingizini akiwa na sura nzuri ya kijana amevaa soksi miguuni na sandali za dhahabu….48 Na amepokea Ibnul Jawzy katika Maudhuuat: “Ametwambia Abu Mansur Abdurahman bin Muhammad Al-Qazzaz, ametuhadithia Abu Bakr bin Ahmad Ali Thabit…. Na akasema katika Al-ilal lmutannahiyah “Ametwambia Abu Bakr bin Ahmad bin Ali bin Thabit kuhusu Hadithi hii.”   Ameitaja Hadithi hii As-Suyutiy katika al-Laaliy al-Masnuuah katika kundi la hadiithi za uzushi na uwongo (1: 30) 48   Hadithi hii ni ya uwongo na uzushi tena munkar. Ameipokea Tabaraniy katika kitabu Al-Kabir, (25: 143), na Al-Bayhaqiy katika Al-Asmau Waswifaat (446-447). Na Ibnul Jawziy katika Al-Maudhuuat (1: 12). Na wameitia ila Hadithi hii Maimamu kama vile Bukhari katika Tarikh yake (6:500), na Ahmad bin Hanbali na Yahya bin Muin na Nasai kama ilivyo katika Tarikh Baghdad (3:113). Na Ibn Habban katika Thuqaat (5: 245), na Ibn Hajar katika Tahdhibut-Tahdhiib (10: 95), yeye amesema: “Ni matini isiyokubalika munkar.” Angalia maelezo katika Daf’u Shubuhaat, Uk. 152. 47

24

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 24

10/20/2015 5:15:21 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

Nasema: Na hadithi hii nayo pia ni ya uzushi, na Yahya bin Muin alimkataza Nuaim bin Hamad kusimulia Hadithi hii. Amesema Abdul Khaliq bin Mansur: “Nilimuona Yahya bin Muin kama kwamba anamshutumu Nuaim bin Hammad kwa Hadithi ya Ummu Tufayl, Hadithi ya ndoto akisema ilikuwa haimfalii kutaja Hadithi kama hii. Na Ibnul Jawzy katika kitabu Al-Maudhuuaat49 na Daf-u shubuhaat amegusia suala la Nuaim bin Hamad kuhusu Hadithi hii na akataja aliyoyasema Nasai juu ya Marwan bin Uthman. Ama katika kitabu Ilalul lmutanahiya alikomea kutaja maneno ya Nasai kuhusu Marwan bin Uthman na kauli ya Ahmad kumhusu: “Ni mtu asiyejulikana,” na hivyo hivyo kwa Ammara bin Amir. Ibnul Jawziy amejipinga yeye mwenyewe katika Hadithi hii50 alipoitaja katika kitabu Al-Maudhuuat kinachoorodhesha hadithi za uwongo, na katika al-Ilalul muntahiya, pamoja na kuwa ametaja katika kitabu hiki cha pili Hadithi hewa ambazo hazifikii daraja ya kuwa hadithi za uzushi, kama alivyotaja hilo katika khutuba ya kitabu chake hicho. Na kwakweli amekosea katika utofautishaji huu, kwa sababu zote hizo ni uwongo na uzushi, ni vigumu sana kutofautisha baina ya hadithi hewa na zile za uzushi, kwa sababu katika uchunguzi, utafiti na uhakiki zote ni kitu kimoja. Na ili kubainisha jambo la Hadithi hii mimi nasema hivi: 1.

Nuaim bin Hammad hana dhambi na wala hahusiki na uzushi wa kuzua riwaya hii, bali hakika Yahya bin Muiin alichukia kitendo cha Nuaim kusimulia riwaya hiyo si kwa jingine bali ni kwa ubaya wa riwaya yenyewe, na mpokezi hafidhi wa Ha-

Al-Maudhuaat (1: 125) na Daf’u Shubuhaat, Uk. 152, Chapa ya Darul-Imam an-Nawawiy. 50   Hii haichukuliwi kuwa ni mgongano, nionavyo ni kitu kimoja. 49

25

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 25

10/20/2015 5:15:21 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

dithi hapaswi kuzungumza kila anachokisikia.51 Kama alivyosema Ali bin Abi Talib A: “Mtakapotaka kusimulia kutoka kwa Mtume 8 basi angalieni lile lililo ongofu zaidi na safi zaidi.”52 Na Yahya bin Muiin hakumdhoofisha Nuaim kwa sababu ya Hadithi hii kama ilivyo katika kitabu Llaaliy cha Al-Hafidh Suyutiy bali alimkataza kusimulia Hadithi hiyo,53 na kufanya hivyo kama ijulikanavyo kwa wataalamu wa fani hii si kumuona kuwa si mwaminifu katika Hadithi.54 Walimkataza Anas bin Malik   Msimulizi wa Hadithi anaposimulia Hadithi kama hii yampasa abainishe kuwa Hadithi hii ni ya uzushi na uwongo. Na Nuaim kwetu ni katika wanaosema Mungu ana umbo, na ni muongo. Angalia wasifu wake katika Tahdhibul-Kamal (29: 466) utaona humo jinsi alivyozua visa na Hadithi za uwongo dhidi ya Imam Abu Hanifa, na yeye ndiye mpokezi wa ibara: “Mwenyezi Mungu hushuka kutoka kwenye Arshi Yake yeye mwenyewe hasa.” Al-Hafidh Ibn Abdul Barri amekanusha hili katika Tamhid (7:144), aliposema: “Nuaim amesema: ‘Mungu mwenyewe hushuka akiwa juu ya Arshi yake.’ Akasema Abu Umar: ‘Hii si Hadithi chochote kwa wenye ufahamu katika Ahlu Sunna.’” Na Imam Al-Kawthariy amesema katika Taanibul-Khatib Uk. 100 chapa mpya, na Uk. 73 chapa ya zamani: “Nuaim bin Hammad ni maarufu kwa kutunga uwongo dhidi ya Abu Hanifa na ametajwa na wengi katika wanavyuoni wakubwa wa elimu ya misingi ya Dini katika orodha ya wanaoamini kuwa Mungu ana mwili na umbo, bali yeye ni miongoni mwa wale wanaosema kuwa Mungu ana nyama na damu, na yeye alilelewa na Ibn Abu Maryam ambaye maneno ya wachunguzi wa ila na dosari kumhusu yeye ni maarufu. Pia alilelewa na Muqatil bin Salman, Sheikh wa watu wanaodai Mungu ana umbo. Na yeye ndiye aliyetunga na kuzua Hadithi ya Ummu Tufayli, ya kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu alimuona Mola Wake akiwa katika sura ya kijana mrembo huku mguu yake akiwa katia kijani.” Tazama Tahdhibul-Kamal, Juz. 29, Uk. 475. 52   Ameipokea Ahmad (1:122 na 130). Na Ibn Majah (20) nayo ina sanadi sahih kwake. 53   Nuaim bin Hamad kwetu ni katika wapotofu, na alilosema Suyutiy katika Al-Laaliy (1: 30) ni kwamba: “Ibn Mansur alisema: Nilimuona Muin ni kama anamkwepa Nuaim bin Hammad katika Hadithi ya Ummu Tufayl, Hadithi ya kumuona Mungu, alisema: ‘Haifai kwake kutoa Hadithi kama hii.’ Haya yametajwa na Al-Mazniy katika TahdhibulKamal (29: 475).” Akakamilisha Suyutiy kwa kusema: “Hii yaonyesha kuwa alimkuta na ila na dosari kwa kuihadithia Hadithi hii kwa watu wa kawaida kwa sababu akili zao hazikubali kubeba jambo kama hii. Na si kwamba alimtuhumu kuwa yeye ndiye aliyeitunga na kuizua.” 54   Bali ni kuifanya dhaifu kama ilivyotangulia kuwa As-Suyutiy alisema katika DhaylulMaudhuu: “Nuaim bin Hamad ametuchosha na haya majanga mengi anayotuletea.” 51

26

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 26

10/20/2015 5:15:21 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

kumsimulia Hajjaj dhalimu Hadithi ya Al-Uraniin, wala hakuna hata mmoja aliyesema kuwa kufanya hivyo ni kumzingatia Anas kuwa si mwaminifu katika Hadithi. Inavyojulikana ni kuwa Yahya bin Muin alimuamini Nuaim bin Hammad na hakumnasibisha na uongo bali alimtuhumu tu kwa baadhi ya mikanganyo.55 Na la ajabu ni kuwa Ibnul Jawziy anasema katika kitabu Dafu tashbiih na katika Almaudhuuat juu ya Nuaim bin Hammad kuwa: “Amesema Ibn Adiyy: “Huyu alikuwa akizua Hadithi za uwongo.” Nukuu hii kutoka kwa Ibn Adiyy si sahihi, bali Ibn Adiyy alipokea shutuma za aliyemtuhumu Nuaim kwa kuzua Hadithi za uwongo, akatoa sababu iliyofanya Nuaim atuhumiwe kiasi hicho, kuwa Nuaim alikuwa amezidi sana ukali dhidi ya watu wa rai, hivyo wao watu wa rai walimtukana na kumtuhumu kwa uzuaji wa Hadithi za uwongo ili kulipiza kisasi na si kwa jingine.56 Angalia wasifu wa Nuaim bin Hammad kutoka katika kitabu Tahdhibi Tahdhiib (10: 409). Na Al-Hafidh Ibn Hajar katika utangulizi wa kitabu Al-Fat’h katika mlango aliozungumzia wapokezi wa Hadithi zilizomo ndani ya Sahihi Bukhari, ambao wamesemwa kwa baadhi ya kasoro, amesema: “Abu Bashar Ad-Dawlabiy alimnasibisha na uzuaji wa Hadithi za uwongo, na Ibn Addiyy akafuatiliza maneno kwa kusema   Bali imepokewa kutoka kwa Yahya bin Muin kwamba alimtuhumu akasema: “Anapokea Hadithi kutoka kwa watu wasio waaminifu.” kama ilivyo katika Tahdhibul-Kamal (29: 469). Na humo kuna maelezo kwamba Yahya bin Muin alimpinga ana kwa ana kwa kuleta Hadithi na kisha Nuaim akakiri baada ya hapo kwamba alikosea. Pamoja na haya walikuwa wakimtetea kwa kuwa alikuwa mkali dhidi ya Ujahmiyya kama wasemavyo. Amesema Yahya bin Muaim pia juu ya Nuaim Uk. 475: “Katika Hadithi hamna kitu ila yeye alikuwa ni mtu wa Sunna.” Hapa mtajua kisa na mafumbo yake. 56   Bali yeye mwenyewe Yahya bin Muin kama ilivyopita hapo awali katika maelezo kuwa alisema: “Katika Hadithi hamna kitu.” 55

27

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 27

10/20/2015 5:15:21 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

kuwa Ad-Dawlaby alikuwa akimchukia kwa sababu ya kuwa kwake mkali dhidi ya watu wa rai, na hii ndio sawa.”57 Nami ninasema: Na ibara yake katika wasifu wake katika kitabu At-Tahdhiib ni: “Amesema Ibn Addiy: Na Ibn Hamad yaani AdDawlabiy ni mwenye kutuhumiwa kwa ayasemayo kuhusu Nuaim kwa kuwa alikuwa mkali dhidi ya watu wa rai.”58 Ama kauli ya Al-Azdiy, kuwa alikuwa akizua Hadithi za uwongo, huyu Al-Azdiy ajulikana kwa pupa yake na ukosefu wa umakini katika kuwatoa kasoro wapokezi wa Hadithi bila hoja yoyote, kama ilivyoonekana hivyo katika kitabu Buluughul-Aman min Maudhuaat Swaghaani, yeye mwenyewe si mwaminifu katika Hadithi, ni dhaifu aliyetuhumiwa kwa kuzua Hadithi za uwongo kama ijulikanavyo. Nuaim bin Hammad ni mmoja wa maimamu kama alivyosema Ad-Dhahabiy katika kitabu Al-Mizani (3:238).59 Ameaminiwa na maimamu, Ahmad na waliokuja baada yake, Bukhari pia alimsifu katika kitabu Khuluqul al-Af’aal (177), na akakanusha madai ya kwamba alikuwa ni mzushi mwenye kutenganisha watu. Nasema: Dhambi yake kubwa pekee kwa wanaomlaumu ni kuwa kwake mkali dhidi ya watu wa rai na kupokea kwake Hadithi zinazowashutumu na zinazopinga madhehebu yao na hasa Majahmiy.   Na kauli hii inakataliwa kwa aliyeisema, kama vile Ibn Adiyy na Ibn Hajar, kwa sababu Al-Hafidh mwenyewe ametaja huko kuwa Bukhari hakuandika Hadithi yake isipokuwa sehemu moja au mbili, na akamwekea maelezo. Na Muslim na pia Nasai hawajaandika Hadithi yake. Na hata Abu Daud, na hao ndio watu wa Hadithi si watu wa rai, ikiongezewa kauli ya Dawlabiy na mwingine na tukiziangalia riwaya hizo potofu alizozipokea Nuaim hapa maneno ya Ibn Addiy na Ibn Hajar yataporomoka na itabainika kuwa Nuaim alikuwa hana chochote! 58   Haya maneno yamepingwa kwa sababu watu wa Hadithi wameshuhudia kuwa Nuaim hana kitu katika Hadithi na Muslim hakupokea toka kwake na pia Bukhari alipokea Hadithi moja tu na ngano ya nyani, na maana yake ni kuwa yeye hakumtegemea na hali ni sheikh wake. 59   Alikubali Seyyid kwamba alikuwa Nuaim ana matatizo katika Hadithi na alibaki kuwa mmoja wa wajuzi lakini walio wapotofu wasio na thamani katika kuhakiki. 57

28

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 28

10/20/2015 5:15:21 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

Lakini la kustaajabisha na kunisikitisha sana ni kuwa inakuwaje kwa mtu anayejidai kwamba yeye anajua Hadithi, anaihudumia Sunna na ni mhakiki wa sanad, anakuja na sanad ambayo ndani yake yumo Marwan bin Uthman, ambaye Nasai na Abu Hatim wamesema kuwa huyu ni dhaifu. Na pia yumo Imara bin Amir ambaye Bukhari amemtaja kuwa hajulikani. Anawaacha hao wawili hawaangalii katika udhaifu wa sanadi zao na kasoro zao, lakini ananasibisha tuhuma ya Hadithi hii kwa Nuaim bin Hammad, Imam mwaminifu60 ambaye hajawahi kutajwa na yeyote kwa ubaya unaowajibisha kuachwa Hadithi yake. Jambo hili halifanywi ila na mwanafunzi mjinga asiyejua lolote katika ilimu ya Hadithi ambaye hatarajiwi kupasi katika kuijua.61 Kwa kuwa kaida ya elimu ya Hadithi ni kwamba watakapokutana katika sanad mwaminifu na dhaifu, ila na kasoro huambatanishwa na aliye dhaifu bila ya kumwangalia mwingine wala hauguswi upande wa aliye mwaminifu.62 Na hili ni maarufu halihitaji ufafanuzi. Mwangalie Nasai jinsi alivyoyapa mambo haki yake na akashikamana na kaida hii, hivyo yeye aliposikia Hadithi hiyo ya Ummu Tufayl, alisema, kama alivyoipokea kauli yake Al-Khatib katika kitabu Tarikh (31:1113) baada ya Hadithi hiyo: “Kutoka kwa Abu Bakr Muhammad bin Ahmad al-Haddad amesema: ‘Nimemsikia Abu Abdurahman Nasai akisema: ‘Na Marwan bin Uthman ni nani mpaka asadikishwe juu ya Mwenyezi Mungu.’”63   Vipi atakuwa mwaminifu mtu ambaye kwenye Hadithi yake kuna kombo? Na ambaye Ibn Muin amesema juu yake kuwa hajui kitu katika Hadithi? 61   Haturefushi maneno hapa katika kujadili mambo haya tumeshaeleza vya kutosha! 62   Ni kutoka wapi Nuaim atakuwa katika wakweli na hali maneno yao ni ya kumtuhumu yeye ni maarufu. 63   Angalia Sayaru Aalamun-Nubalaa (10: 602) na al-Mizan cha Dhahabiy (6: 400) na (7:43) Chapa mpya ya Darul Kutubil Alamiyya na Tahdhibut-Tahdhiib (10: 86 na IlalulMutanahiyah cha Ibnul Jawziy (1: 30). 60

29

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 29

10/20/2015 5:15:21 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

Nasai hakumwangalia Nuaim bin Hammad kabisa kwa kuwa tu yupo Marwan bin Uthman mdhaifu, na katika kuizingatia sanadi kuwa ni dhaifu huangaliwa yule dhaifu si yule mwaminifu.64 Na Marwan bin Uthman, Ad-Dhahabiy amemtaja katika kitabu chake al-Mizan (3:160) akasema hivi: “Abu Hatim amesema kuwa yeye ni dhaifu.” Na akasema Abu Bakr Muhammad bin Ahmad Al-Haddad: “Nimemsikia Nasai akisema; ‘Marwan bin Uthman ni nani mpaka asadikishwe juu ya Mwenyezi Mungu.” alisema hayo katika Hadithi ya Ummu Tufayl.” Ibnul Jawziy amesema katika kitabu Al-Ilalul-Mutanahiya (1:15): “Abu Bakr al-Khalal ametaja katika kitabu Al-Ilal akasema: “Muhammad bin Ali ameniambia akasema, nilimuuliza Abu Abdallah bin Hambal juu ya Hadithi hii, akageuza uso wake akasema: ‘Hii ni Hadithi isiyokubalika, munkar.” Na akasema: “Haijulikani na hajulikani huyu mtu”, yaani Marwan bin Uthman, akasema: “Hata Imara bin Amir pia hajulikani.” Al-Hafidh ameitaja Hadithi hii pia katika wasifu wa Ummu Tufayl kutoka kwenye kitabu Al-Iswabah65 akasema: ‘Marwan ni mtu aliyeachwa na watu.” Na wala hakumtia ila Nuaim bin Hammad kwa sababu ya hila tuliyoitaja. Ama kuhusu Imara bin Amir, Ad  Nuaim bin Hammad hakuwa mwaminifu katika upokezi wa Hadithi, na Seyyid amekubali kuwa huyu alikuwa kombo katika Hadithi na maneno ya watu wa Hadithi kwake ni maarufu. Nasai hakumtuhumu kwa sababu walikuwa wakiogopa kumtuhumu mtu kama huyu na Hamad bin Salamah! Nasai amesema hilo wazi juu ya Hammad bin Salama kama alivyonukuu Al-Bajiy katika kitabu chake, Rijalul-Bukhari, kwamba Nasai aliulizwa juu yake akasema: “si mbaya.” Na kabla ya hapo alisema: “Ni mwaminifu.” Amesema Qasim bin Mas’ada: “Nilimtaja kwake akasema: ‘Nani athubutu kumtaja.’ Kisha Nasai akawa akitaja Hadithi ambazo amezipokea yeye peke yake zinazozungumzia sifa, kama kwamba alikuwa akiogopa watu wasije kusema amemsema kwenye njia yake.” Kitabu Al-Baji kimechapiswhwa kwa jina la Taadilli Watajriih (2: 523). Kimechapishwa Riyadh na Daru Liwaa chapa ya kwana 2:523. 65   Al-Iswabah (8: 246). 64

30

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 30

10/20/2015 5:15:21 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

Dhahabiy amesema hajulikani,’ Bukhari amemtaja katika orodha ya madhaifu.66 Al-Hafidh katika kitabu Lisaan amesema: “Na katika kitabu cha waaminifu cha Ibn Haban yumo Imara bin Amir aliyepokea Hadithi kutoka kwa Ummu Tufayl.” Akataja Hadithi ya kumuona Mwenyezi Mungu, kisha akasema: “Haikubaliki ni munkar, wala Imara hakumsikia Ummu Tufayl, bali nimeitaja ili mtu mwenye kuiona asighulike nayo akaitolea hoja…”67 Nasema: Ibn Habban hakumtaja katika kitabu cha waaminifu isipokuwa kwa ajili ya kubainisha tu ubaya wa Hadithi hii, na si kwa kuwa yeye ni mwaminifu katika Hadithi, hata kama angemtaja kama mwaminifu kwake. Uaminifu wa mpokezi unaothibitishwa na Ibn Habban haukubaliwi kama asemavyo Ad-Dhahabiy katika Al-Mizan, na dalili kubwa ya hilo ni kule kuthibitisha kwake uaminifu wa Imara bin Amir asiyejulikana, ikiwa kweli amethibitisha uaminifu wake.68 Amesema Al-Haythamiy katika kitabu Al-Majma (7:179) alipotaja Hadithi kutoka kwenye riwaya ya Tabaraniy: “Ibn Habban amesema: ‘Hii ni Hadithi isiyokubalika, ni munkar kwa sababu Imara bin Amir bin Hazmi al-Answariy hajaisikia kutoka kwa Ummu Tufayl, ameitaja katika wasifu wa Imara katika kitabu cha waaminifu.’” Hivyo Hadithi hii ndani yake mna ila nyingi: Marwan bin Uthman, Imara bin Amir na kukatika, na Imara hakuisikia kutoka   Tarikhul Kabir cha Bukhari (6: 500)   Lisanul Mizan (4: 278) 68   Ibn Habban hakumzingatia kuwa ni mkweli katika AtThuqaat (5: 245) bali alisema: “Nimemtaja ili asighurike mwenye kumuangalia, asije kutoa hoja kupitia yeye. 66 67

31

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 31

10/20/2015 5:15:21 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

kwa Ummu Tufayl. Ama Nuaim bin Hammad, hahusiki nayo kabisa kama kutohusika kwa mbwa mwitu na damu ya Nabii Yusuf!69 Na dalili ya hilo ni kuwa ule ufuatiliwaji wa Hadithi hiyo kupitia kwa Ibn Wahbi ni mwingi zaidi kuliko ufuatiliwaji uliopitia kwake, jambo lisiloacha shaka kwamba hahusiki nayo. Kutoka kwa Ibn Wahbi ameipokea Yahya bin Bakir na Yahya bin Sulaiman al-Jaafiy na Ahmad bin Swalih, na wote ni waaminifu. Ufuatiliaji wa Yahya bin Sulaiman ameuweka Bukhari kwenye maelezo yake katika wasifu wa Imara bin Amir kwenye kitabu at-Tarikh (6:500). Na ameutaja Tabaraniy katika kitabu As Sunnah: 70“Ametuhadithia Ahmad bin Rushdin, ametuhadithia Yahya bin Sulaiman AlJaafiy. Ama ufuatiliaji wa Yahya bin Bakir na Ahmad bin Swalih, amesema Tabaraniy katika As Sunna: Ametuhadithia Ruh bin Faraj, ametuhadithia Yahya bin Bakir, ametuhadithia Ahamd bin Rashdiin, ametuhadithia Yahya bin Sulaiman bin Al-Jaafiy na Ahmad bin Swalih wamesema, ametuhadithia Abdallah bin Wahbi. Kisha akaitaja kwa sanad yake na matini yake sawasawa. Hadithi nyingine: Ibnul Jawziy ameitaja katika kitabu Daf’u Shubhi Tashbihi: 71 Kutoka kwenye Hadithi ya Anas, Mtume 8 amesema: ”Usiku niliopelekwa israa nilipaishwa mbinguni nikamuona Mola Wangu, nikaona kila kitu kutoka kwa Mola Wangu mpaka nikaona taji lililopambwa kwa lulu.”72 Ibnul Jawziy   Nuaim hasalimiki na dhima kwa sababu aliipokea na kuieneza kwa watu, na sanadi zote zina muongo, mzushi na dhaifu, na hao wote kama vile Hammad bin Salamah na Nuaim bin Hammad wameeneza Hadithi hii potofu, ilihali wanajua haiwezekani Mungu awe na sura ya mvulana mzuri! Hawamuonei haya Mola Wao? 70   Yaani je Tabarani anataka kuiteta itikadi ya kuwa Mungu ana sura kama wasemavyo mpaka aje na njia hizi licha ya kuwa Hadithi ni ya uwongo na uzushi? 71   Uk. 156, Chapa ya Darul-Imam an-Nawawiy. 72   Ameipokea Al-Khatib Al-Baghdadiy katika Tarikh yake (10:124) na Ibnul Jawziy katika Al-Maudhuuat (1: 115), nayo ni Hadithi ya uzushi ya uongo. 69

32

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 32

10/20/2015 5:15:21 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

amesenma: “Hii imepokewa na Abul Qasim Muhammad bin AlYasaa kutoka kwa Qasim bin Ibrahim. Nasema: Hivi ndivyo kilivyomtaja Muhammad bin Al-Yasaa kitabu Daf’u Shubhi Tashbihi73 na sijamuona katika vitabu vya ila za wapokezi nilivyonavyo, na nionavyo mimi ni kuwa yeye alichanganywa na Muhammad bin Hasan.74 Al-Hafidh ametaja katika Al-Lisaan (4:456) katika wasifu wa Qasim bin Ibrahim Al-Malatiy, kuwa miongoni mwa wapokezi wake ni Muhammad bin Hasan Al-Muqriy Al-Antakiy, Imam wa msikiti wa ijumaa wa Baytul Muqaddas. Dhana yangu kubwa ni kuwa aliyetajwa katika Daf’u Shubhi Tashbihi ni huyu, na Mola ndiye mjuzi zaidi. Na Hadithi hii nayo pia ni ya uzushi, Qasim bin Ibrahim Al-Malatiy, Daru Qutniy amesema kumhusu, kuwa ni mwongo mkubwa. Na Ad-Dhahabiy katika Al-Mizani amesema:75 “Huyu ameleta janga lisilowezekana.” Kisha akaitaja Hadithi hii. Na Al-Khatib amesema:76 “Amepokea maajabu miongoni mwa upotofu, kutoka kwa Al-Faryabiy kutoka kwa Abu Umayya Al-Mubarak bin Abdallah kutoka kwa Luin, kutoka kwa Malik. Na amesema Abdul Ghaniyy bin Said: “Hakuna katika Wamalati aliye mpokezi mwaminifu.”

Bali amesema Ibnul Jawziy katika Daf’u Shubhat: “Abdallah bin Muhammad Al-Yasaa wasifu wake umo katika vitabu vingi kama Lisanul Mizan (3:350) na asili yake, yaani al-Mizan. Na katika Tarikh Baghdad (10: 134) kuna Hadithi kwa sanad yake, lau Seyyid Sharif angerejea angeiona humo. Al-Azhari amesema juu yake kuwa: Si hoja.” 74   Imedhihirika kuwa yeye hayuko hivyo. 75   Al-Mizan (5: 446), Chapa ya Darul-Kutubil-ilmiyyah. 76   Kama ilivyo katikaTarikh Baghdad (12: 446) na Lisanul-Mizan (4: 456). 73

33

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 33

10/20/2015 5:15:21 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

FASLU YA PILI

H

aya ndiyo niliyoyapata katika maneno ya Hadithi hii na njia zake, na nimebainisha hali ya kila njia na nimefafanua kadri ya uwezo wangu na kadri ya wakati ulivyoniruhusu na pia nimetaja marejeo kuhusiana na Hadithi yenyewe na watu wa elimu ya Hadithi. Na katika hayo nimejua kuwa Hadithi hii ni ya uzushi ya uwongo na batili upande wa sanad na matini, wala haifai kuitaja na kuitegemea kama ilivyotokea kwa baadhi ya maulamaa. Miongoni mwao ni AlHafidh Suyutiy ambapo alimfuata Ibnul Jawziy katika Hadithi ya Ummu Tufayl kwa maneno yaliyo mbali na uthibitisho. Na akataja Hadithi ya Ibn Abbas kama ushahidi na kuipa nguvu sanad yake. Pia katika hilo akamfuata Ibn Arraq katika kitabu At-Tanziih Sharia al-Marfuua, na yote haya hayana asili. Na kama Suyuti angechunguza na kuangalia kwa makini na kuipa Hadithi haki yake kwa kuifanyia utafiti Hadithi ya Ibn Abbas na Ummu Tufayl, angeamua kwa yakini kabisa kuwa hadithi hiyo ni ya uzushi na ya uwongo, na angeihukumu kuwa ni batili, kama alivyoikataa AtTaju As-Sabakiy katika kitabu Tabaqaat (2:58). Na Ibn Arraq mara nyingi alikuwa akimfuata Al-Hafidh As-Suyutiy, hivyo amezidisha baadhi ya ziada juu yake, angalia ili ujue udhaifu wa maneno yake na ufuatiliaji wake.

34

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 34

10/20/2015 5:15:22 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

FASLU YA TATU

A

ma Hadithi tuliyoitaja katika utangulizi na tukasema kuwa wao wameiona kuwa ni sahihi na kuwa ina tamshi linalochukuliwa kuwa ni ushahidi japo kuna tofauti kati ya matamshi mawili, maneno kuhusu Hadithi hiyo ni marefu na yamepingwa sana na watu wa fani hii, lakini tutayafupisha kwa sababu lengo ni kujua yaliyosemwa juu ya Hadithi hiyo, na hilo litapatikana katika haya tutakayoyataja inshallah:

Tirmidhiy amesema katika Sunan yake:77“Ametuhadithia Muhammad bin Basshar, ametuhadithia Muadh bin Hani, Abu Hani Al-Yashkuriy, ametuhadithia Jahdham bin Abdullah, kutoka kwa Yahya bin Abi Kathir, kutoka kwa Zaid bin Salam, kutoka kwa Abu Salami, kutoka kwa Abdur-Rahman bin Ayish al-Hadhramiy, kwamba yeye ametuhadithia kutoka kwa Malik bin Yakhamir AsSaksakiy kutoka kwa Muadh bin Jabal K, amesema: “Mtume alizuilika kuja kwenye Swala ya alfajiri mpaka tukakaribia kuona kuchomoza kwa jua, mara akatoka haraka, Swala ikakimiwa kisha akaswali, akaacha baadhi ya vifungu visivyokuwa vya lazima katika Swala (akafupisha Swala), alipomaliza kutoa salam aliinua sauti yake akasema: “Bakini katika safu zenu kama mlivyo.” Kisha akasema: “Ama mimi nitawaambia kilichonifanya msinione asubuhi mapema. Nilisimama usiku, nikatawadha, nikaswali kiasi nilichoweza, nikasinzia katika Swala, nikashikwa na usingizi mzito, 77

Sunan Tirmidhiy (3235). Na ameipokeaTirmidhiy kutoka kwa Ibn Abbas (3233, 3234). Na katika Tahdhibut-Tahdhiib (5: 185) amesema: “Amesema Abu Zaraa Damishqiy: ‘Nilimwambia Ahmad, Ibn Jabir amepokea kutoka kwa Ibn Lajlaj kutoka kwa Abdurahman bin Aish Hadithi hii: Nilimuona Mola Wangu katika sura nzuri, na anaisimulia kutoka kwa Qatadah kutoka kwa Abu Qilabah kutoka kwa Khalid bin Lajlaj, kutoka kwa Ibn Abbas, akasema: “Huyu si chochote.” 35

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 35

10/20/2015 5:15:22 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

mara nikawa niko kwa Mola Wangu Mtukufu, nikamuona akiwa na sura nzuri, akasema: ‘Ewe Muhammad!’ nikamjibu, labayka ewe Mola. Akasema: ‘Malaika hugombania kitu gani?’ Nikasema sijui ewe Mola, akasema mara tatu. Nikamuona ameweka kiganja chake kati ya mabega yangu mawili mpaka nikahisi ubaridi wa vidole vyake katikati ya kifua changu.78 Kila kitu kikawa wazi kwangu, na nikatambua. Akasema: ‘Ewe Muhammad!’ Nikasema labayka Mola wangu. Akasema: ‘Malaika hugombania kitu gani?’ Nikasema: Kafara. Akasema: ‘Ni zipi hizo kafara?’ Nikasema: Ni kutembea kwa miguu kwenda kuswali jamaa, kukaa misikitini baada ya kuswali, na kutawadha wakati ambapo nafsi haipendi kuchukua udhu.’ “Akasema: ‘Na amali zipi nyingine?’ Nikamjibu: Kulisha chakula, maneno laini na kuswali usiku wakati watu wakiwa wamelala. Akasema: ‘Omba, sema: Ewe Mola, nakuomba nifanye mema na niache maovu, niwapende masikini, na nighufirie na nirehemu. Na kama utataka kuwatia watu majaribuni basi nifishe bila ya kutiwa majaribuni. Nakuomba penzi Lako na penzi la akupendaye na kupenda amali zitakazonikaribisha kwenye pendo Lako.” Kisha Mtume 8 akasema: “Hii ni kweli isomeni na muifundishe.”…79 Tirmidhiy amesema: Hadithi hii ni hasan, sahihi. Nilimuuliza Muhammad bin Ismail juu ya Hadithi hii, akasema: “Hii ni Hadithi hasan sahihi,80na akasema hii ni sahihi zaidi kuliko ile ya AlWalid bin Muslim kutoka kwa Abdurahman bin Yazid bin Jabir, ambayo amesema: “Ametuhadithia Khalid bin Lajlaj, ametuhadithia   Mungu aepushie mbali, huku ni kumpa Mola umbo, Mungu hana viungo wala sura wala umbile! 79   Hadithi ni ya uzushi, ya uongo, Ibn Hajar ameitaja katika an-Nukat Dharaf (4:382), Chapa ya Tuhfatul-Ashraf: “Amesema Muhammad bin Nasr Al-Maruzi katika kitabu Taadhimu Qadarus-Swalah: ‘Hadithi hii wametatizika wapokezi katika sanad yake, na haijathibiti kwa watu wa maarifa.’” 80   Haya maneno siitakidi kuwa yametoka kwa Bukhari, huu ni mkanganyo kutoka kwa Tirmidhiy au waliofuata Sunan Tirmidhiy na wapokezi wake. 78

36

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 36

10/20/2015 5:15:22 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

Abdurahman bin Ayish Al-Hadhramiy, amesema: Nilimsikia Mtume 8 akisema… akaitaja Hadithi hii, na hii haikuhifadhiwa. Hivyo ndivyo alivyotaja Al-Walid katika Hadithi yake kutoka kwa Abdurahman bin Ayish amesema, nimemsikia Mtume 8. Naye Bishru bin Bakri amepokea kutoka kwa Abdurahman bin Yazid bin Jabir Hadithi hii kwa sanadi hii kutoka kwa Abdurahman bin Ayish kutoka kwa Mtume 8, na hii ni sahihi zaidi; kwani Abdurahman hakuisikia kutoka kwa Mtume 8. Ahmad amepokea katika Musnad yake: “Ametuhadithia Said mtumishi wa Bani Hashim, ametuhadithia Jahdham yaani AlYamani, ametuhadithia hadithi hiyo Yahya yaani Ibn Abu Kathir…81 Ameipokea Ibn Khuzaimah katika kitabu At-Tawhid, ametuhadithia Abu Musa, ametuhadithia Muadh bin Hany Hadithi hii. Isipokuwa katika sanad ya Ibn Khuzayma kutoka kwa Ibn Salam imetajwa kwamba yeye alihadithiwa na Abdurahman Al-Hadhramiy, na sahihi ni Zaid bin Salam kutoka kwa Abu Salam kutoka kwa Abdurahman bin Ayish kama ilivyo katika riwaya ya Ahmad na Tirmidhiy. Nami nasema: Hadithi ya Al-Walid bin Muslim ambayo ameitaja Bukhari kama ilivyo kwa Tirmidhiy, ameipokea Khuzayma katika kitabu At-Tawhid na Daramiy katika Sunan yake, na Ibn Sukan na Ibn Nuaim na Ibnul Jawziy katika Ilalul-Mutanahiyah kutoka kwenye njia zake, amesema: Amenihadithia Ibn Jabir kutoka kwa Khalid bin Lajlaj, kutoka kwa Abdurahman bin Aish al-Hadhramiy kwamba alimsikia Mtume akisema: “Nimemuona Mola wangu akiwa katika sura nzuri, akaniambia: ‘Ewe Muhammad! Malaika hugombania kitu gani?.........’ isipokuwa Ad-Daramiy hakuitaja Hadithi. 81

Musnad ya Ahmad (5:243). Angalia pia kwa njia nyingine (1:368) na (4:66) na (5:378), kwetu ni ya uzushi na uwongo. 37

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 37

10/20/2015 5:15:22 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

Amesema Ibn Khuzaymah katika At-Tawhid:82 “Hakika amepokea Al-Walid bin Muslim Hadithi ambayo wanafunzi wengi wa elimu ya Hadithi miongoni mwa wasiofahamu elimu hiyo, wanadhani kuwa ni Hadithi sahihi upande wa nukuu, lakini si hivyo kwa watu wa elimu ya Hadithi, nami nitabainisha ila na kasoro zake Mungu akiniwafikisha ili wanafunzi wasihadaike na Hadithi hii.” Kisha Ibn Khuzayma akasema:83 “Kauli yake katika Hadithi hii: ‘Nilimsikia Mtume 8’ ni mkanganyo, kwa sababu Abdurahman bin Aish hakusikia kutoka kwa Mtume kisa hiki, bali amekipokea kutoka kwa mtu miongoni mwa Maswahaba wa Mtume, wala sidhani kama pia amekisikia kutoka kwa Maswahaba kwa sababu Yahya bin Kathir amekipokea kutoka kwa Zaid bin Salam kutoka kwa Abdurahman Al-Hadhramiy kutoka kwa Malik bin Yakhamir, kutoka kwa Muadh, na amesema Yazid bin Jabir kutoka kwa Khalid bin Lajlaj kutoka kwa Abdurahman bin Aish kutoka kwa Swahaba mmoja wa Mtume 8. “Pia ametuhadithia Abu Musa Muhammad bin Al-Mathn, ametuhadithia Abu Amir bin Abdulmalik bin Amru, amesema: Ametuhadithia Zuhair naye ni Ibn Muhammad, kutoka kwa Yazid, amesema: Ametuhadithia Abu Musa naye ni Yazid, kutoka kwa Jabir kutoka kwa Khalid Lajlaj, kutoka kwa Abdurahman bin Ayish, kutoka kwa mtu kati ya Maswahaba wa Mtume 8, amesema: “Alikuja kwetu Mtume 8… na akaitaja Hadithi hii kwa urefu.”   Kitabu Tawhid Waithbat Swifat Rabbi (2:532), ambacho Raziy katika Tasfiri yake (14/17/151) amekiita kuwa ni kitabu cha shirki. Ibn Khuzayma alijuta kwa kukitunga kwake na akakiri makosa yake kama ilivyotajwa kutoka kwake kwa sanadi mbili katika kitabu Al-Asmau Waswifaat cha Al-Bayhaqiy, Uk. 267, kilichohakikiwa na Imam Kawthariy, na kitabu mfano wa At-Tawhid cha Ibn Khuzaymah ni kitabu as-Sunnah kilichonasibishwa na Ibn Ahmad, na vinginevyo vinavyotaja kuwa Mola ana umbo na mwili. 83   At-Tawhid (2: 537). 82

38

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 38

10/20/2015 5:15:22 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

Nasema: Wala si peke yake Al-Walid bin Muslim ndiye aliyesema wazi kuwa Abdurahman bin Ayish alisikia Hadithi hii kutoka kwa Mtume, bali alimfuata katika hilo Hammad bin Malik Al-Ashjai, Walid bin Mazid Al-Bayrutiy na Imara bin Bashar. Ufuataji wa Hamad bin Malik umeandikwa na Al Baghawiy, amesema: “Ametuhadithia Ibn Jabir, amesema: ‘Wakati tukiwa kwa Mak’huul, mara alipita Khalid bin Lajlaj akamwambia Mak’huul: Ewe Abu Aish, akasema, naam. Akasema: Nimesikia Abdurahman bin Aish akisema: Nimemsikia Mtume 8 …akaitaja Hadithi hii. Mwisho wake Mak’huul akasema: ‘Sijawahi kuona mtu anayeijua zaidi Hadithi hii zaidi ya mtu huyu.’ Na amesema katika Al-Mizan: Hamad bin Malik, inasemekana huyu ni mfuasi wa Maliki na walimtuhumu kwa uongo. Na akasema katika Al-Lisan: “Al Falas amemzingatia kuwa ni mwongo. Nasema: Sijawahi kuona katika vitabu nilivyonavyo isipokuwa wasifu huu tu na Mungu ndiye ajuaye, je ametajwa katika sanad au vinginevyo. Na ufuatiliaji wa Al-Walid bin Mazid, ameutaja Al-Bayhaqiy katika kitabu As-Sifaat:84 “Ametwambia Abu Abdallah Al-Hafidh na Abu Said Muhammad bin Musa, wamesema: Ametuhadithia Abul Abbas Muhmmad bin Yaqub, ametuhadithia Al-Abbas bin AlWalid bin Mazid Al-Bayrutiy, ameniambia baba yangu kwamba: Alitwambia Ibn Jabir… Akasema: Ametuhadithia pia Al-Awzai, ametuhadithia Khalid bin Lajlaj, amesema: Nilimsikia Abdurahman bin Aish AlHadhramiy akisema: Alituswalisha Mtume 8 alfajiri moja, mtu mmoja akamwambia: “Sikuona uso uliokuwa mwekundu kama wako asubuhi hii.” Akasema Mtume 8: “Mwenyezi Mungu 84

Al-Asmau Waswifaat cha Al Bayhaqiy (298-299). 39

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 39

10/20/2015 5:15:22 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

amenidhihirikia akiwa na sura nzuri, akasema Malaika hugombania kitu gani ewe Muhammad?... Nasema: Huku ni kufuatilia kukubwa kwa Al-Walid bin Muslim. Al-Walid bin Mazyad ni mwaminifu ambaye hakuna hata mtu mmoja aliyemsema kwa ubaya. Naye ni katika wapokezi wa Abu Daud na Nasai. Na mwanawe Abbas ni mwaminifu pia, amepokea kwake Abu Daud na Nasai, Na Al-Hafidh amesema katika AlIswabah: “Huu ni ufuatiliaji wenye nguvu.” Nasema: Na kauli yake kwa njia hii kutoka kwa Al-Awzai kutoka kwa Khalid, ni ufuatiaji mfupi kama ambavyo haifichiki kwa Walid bin Muslim. Lakini amesema Al-Hafidh katika kitabu Al-Iswabah: “Iliyohifadhiwa kutoka kwa Al-Awzai ni ile iliyopokewa na Isa bin Yunus na Muafi bin Imrani, wote wawili wamepokea kutoka kwa Al-Awzai kutoka kwa Jabir. Ameiandika Ibn Sukan kutoka kwenye riwaya ya Isa bin Yunus. Amesema katika mtiririko wake: “Nimemsikia Khalid bin Lajlaj kutoka kwa Abdurahman bin Aish, nimemsikia Mtume 8. Nasema: Inavyoonekana ni kuwa kila moja kati ya njia mbili ni yenye kuhifadhiwa, nayo ni zaidi katika sanad, huenda Al-Awzai alizungumza hivi na mara nyingine akazungumza vile. Hiyo ni kwa sababu Al-Walid bin Mazyad mara nyingi alikuwa akichukua kutoka kwa Al-Awzai na ndiye aliye sahihi zaidi kati ya wapokezi wa AlAwzai. Na anayekuwa hivi anakuwa mbali na makosa ya kukosea Hadithi ya Sheikh wake. Na ufuatiliaji wa Imara bin Bishru, ameutaja Daru Qutniy katika kitabu Ar-Ruuya kutoka kwenye njia yake. Ametuhadithia Abdurahman bin Jabir kutoka kwa Abu Salam kwamba yeye alimsikia Abdurahman bin Aish akisema juu ya Hadithi hii, kwamba yeye alimsikia Mtume, na akataja sehemu ya Hadithi hiyo. Na Imara 40

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 40

10/20/2015 5:15:22 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

bin Bishru amepokea kwake Nasai, na wala Al-Hafidh katika Tahdhib hakutaja maneno ya wachunguzi wa ila za wapokezi kumhusu yeye. Ad-Dhahabiy amesema katika Al-Mizan: “Sijaona mtu yeyote aliyemwamini bali hata kumzungumzia kwa ubaya. Nasai ameandika Hadithi yake, na Hadithi hii ameipokea Yazid bin Jabir ndugu yake Abdurahman bin Yazid, kutoka kwa Khalid akimpinga nduguye kwa sanadi yake, ambapo alimuweka swahaba kati ya Abdurahman bin Aish na Mtume 8. Ahmad amepokea kupitia njia yake kutoka kwa Ibnul Jawziy katika al-Ilalul-Mutanahiya, na Ibn Khuzayma katika at-Tawhid, kwa njia ya Zuhair bin Muhammad, kutoka kwa Yazid bin Jabir, kutoka kwa Khalid Lajlaj, kutoka kwa Abdurahman bin Aish, kutoka kwa swahaba mmoja amesema: “Mtume alikuja kwetu…….mpaka mwisho wa Hadithi. Al-Hafidh amesema katika Al-Iswabah (4:322: “Lakini riwaya ya Zuhair bin Muhammad kutoka kwa Washam ni dhaifu kama alivyosema Bukhari na wengineo. Abu Qilabah alimpinga Abdurahman bin Yazid na nduguye Yazid bin Yazid. Hivyo akaipokea kutoka kwa Khalid bin Lajlaj kutoka kwa Ibn Abbas. Ameipokea Tirmidhiy katika Sunan yake kwa njia ya Muadh bin Hashim kwamba: Ametuhadithia baba yangu kutoka kwa Qatadah, kutoka kwa Abu Qilabah, kutoka kwa Khalid bin Lajlaj kutoka kwa Ibn Abbas. Tirmidhiy amesema: Ni hasan, lakini ni ngeni kutoka upande huu. Nasema: Qatadah amekosea kama alivyosema zaidi ya mmoja akiwemo Ahmad. Amesema Abu Zar’ah Ad-Damishqiy: “Nilimwambia Ahmad bin Jabir asimulie Hadithi kutoka kwa Khalid, akamtaja. Na amsimulie Qatadah kutoka kwa Abu Qilabah, akamtaja tena. Akasema: Maneno hayo ndiyo aliyoyasema Ibn Jabir.”

41

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 41

10/20/2015 5:15:22 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

Ibn Abi Hatim amesema katika kitabu Al-Ilal:85 “Nilimuuliza baba yangu juu ya Hadithi aliyoipokea Muadh bin Hashim kutoka kwa baba yake kutoka kwa Qatadah kutoka kwa Abu Qilabah kutoka kwa Khalid bin Lajlaj kutoka kwa Ibn Abbas kutoka kwa Mtume 8: ‘Nilimuona Mola wangu mtukufu…..’ na akaitaja Hadithi hii katika kutawadha na kwingineko. Akasema baba yangu: ‘Hii ameipokea Al-Walid bin Muslim na kuisadikisha kutoka kwa Jabir, amesema: Tulikuwa na Mak’huul, mara akapita Khalid bin Lajlaj, Mak’huul akasema: Ewe baba wa Ibrahim. Akasema: Amenihadithia Ibn Aish Al-Hadhramiy kutoka kwa Mtume 8, na amesema baba yangu hii ndio inayofanana zaidi. Na inasemekana huyu Qatadah hajasikia kutoka kwa Abi Qilabah ila baadhi ya herufi tu kwani alipata kitabu miongoni mwa vitabu vya Abu Qilabah, hivyo hawakuweza kutofautisha kati ya Abdurahman bin Aish na Ibn Abbas’” Ibn Khuzayma amesema katika kitabu Tawhid: “Ile riwaya ya Yazid na Abdurahman in Yazid ina mshabaha wa ukweli kwa sababu wamesema wawili hao kutoka kwa Abdurahman bin Aish kutoka kwenye riwaya ya aliyesema imetoka kwa Abdallah Ibn Abbas. Nasema: Ayyub ameipoea kutoka kwa Abu Qilabah na wala hakumtaja Khalid bin Lajlaj. Na ameipokea Tirmidhiy katika Sunan na Ibn Khuzayma katika Tawhid, na Ahmad katika Musnad, na kwa njia yake Ibnul Jawziy katika kitabu Al-Ilal al-Mutanahiyah, kutoka kwenye njia ya Muammar kutoka kwa Ayyub kutoka wa Abu Qilabah kutoka kwa Ibn Abbas. Al-Hafidh amesema katika Al-Iswabah: “Hadithi hiyo ni mursal.” Nasema: Na kauli ya kuwa Abu Qilabah ameisikia kutoka kwa Ibn Abbas inathibitisha kuwa Hadithi hii si mursal. Pengine aliisikia kutoka kwake baada ya kuipokea kutoka kwake kwa wasita, hilo 85

Ilal Ibn Abu Hatim (1:20). 42

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 42

10/20/2015 5:15:22 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

halina kizuizi. Alifuatiwa na Bakr bin Abdallah Al-Mazniy ambaye aliipokea kutoka kwa Abu Qilabah, hivyo ndivyo alivyoipokea Daru Qutniy, na akaipokea Said bin Bashir kutoka kwa Qatadah kutoka kwa Abu Qilabah, lakini yeye akawakhalifu wote. Amesema kutoka kwa Abu Asma kutoka kwa Thawban. Na Said bin Bashir ni katika wale wapokezi wa vitabu vinne naye ni mwenye kujiamini ila alitajwa kwa kufanya makosa na kukanganya. Amesema Bin Numeir: “Huyu hupokea Hadithi zisizokubalika na munkar kutoka kwa Qatadah.” Na akasema Ibn Adiyy: “Saa nyingine hukosea na kukangaya.” As-Saji naye amesema: “Amesimulia kutoka kwa Qatadah Hadithi munkar.” Ibn Habban naye amesema: “Alikuwa na hifdhi mbaya hadithi zilizopokewa kwake ni zile zisizofuatwa.” Amesema Al-Hafidh: “Said amekosea kwenye Hadithi hii.” Nasema: Si yeye pekee aliyepokea Hadithi hii kutoka kwenye Hadithi ya Thawban. Amepokea Ibn Khuzayma katika At-Tawhid kutoka kwenye njia ya Muawiya bin Swalih kutoka kwa Abu Yahya. Amesema Ibn Khuzaymah: “Kwangu mimi ni kutoka kwa Sulayman au Salim bin Amir kutoka kwa Abu Yazid kutoka kwa Abu Salam Mhabeshi, kwamba amemsikia Thawban akisema kwamba Mtume 8 alichelewesha Swala mpaka asubuhi ikachomoza, akasema: Hakika nimechelewa kwenu, hakika Mola Wangu aliniambia: Ewe Muhammad! Je wajua ni kitu gani hugombania Malaika?... hadi mwisho wa Hadithi.” Amesema Ibn Khuzaymah: “Simjui Abu Yazid huyu kwa uadilifu au kwa ubaya.” Na ina njia nyingine ameipokea Al-Bazaar kutoka kwenye njia ya Abu Yahya, kutoka kwa Abu Asma Al-Rahbiy kutoka kwa Thawbani. Amesema Al-Haythamiy katika Majmaa: “Na Abu Yahya simjui lakini wapokezi wake waliobaki ni wakweli.” Yamehitilafiana 43

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 43

10/20/2015 5:15:22 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

maoni ya mahafidh katika njia za Hadithi hii. Ama Ibn Khuzayma ameibatilisha yote, hapa si mahali pa kunukuu maneno yake na aliwafuata katika jambo hili maimamu waliomtangulia. Ama Al-Bayhaqi alisema 86baada ya kuonyesha ikhtilafu iliyotokea katika njia zake: “Na imepokewa katika njia nyingine na zote ni dhaifu. Na njia iliyo bora zaidi kwake ni ya Jahdhamy bin Abdullah, kisha ni riwaya ya Musa bin Khalaf.” Na huu ndio msimamo wa Abu Hatim kama alivyounukuu mwanawe katika kitabu Al-Ilal, amesema: “Riwaya ya Jahdhamiy bin Abdallah AlYamamiy na Musa bin Khalaf Al-Ammiy inafanana sana na Hadithi ya Jabir.” Amesema Ibnul Jawziy katika Ilalul-Mutanahiya: “Asili ya Hadithi hii na njia zake ni zenye kuchanganya.” Daru Qutniy amesema: “Sanadi zake zote zina mikanganyo, si sahihi, amesema imepokewa kutoka kwa Anas, na imepokewa kutoka kwa Qatadah kutoka kwa Abu Qilabah kutoka kwa Khalid bin Lajlaj kutoka kwa Ibn Abbas, nayo ni makosa. Iliyohifadhiwa ni kuwa Khalid amepokea kutoka kwa Abdurahman bin Aish, na Abdurahman hakuisikia kutoka kwa Mtume 8 bali ameipokea kutoka kwa Malik bin Yakhazim kutoka kwa Muadh.” Na amesema katika kitabu Shab’hu tashbiih baada ya kuitaja Hadithi ya Abdurahman bin Aish: “Amesema Imam Ahmad Asili ya Hadithi hii na njia zake zinakanganya.” Lakini katika wasifu wa Musa bin Khalaf uliyomo katika Al-Mizan, amesema Ibn Addiyy: “Nilimuona Ahmad bin Hambal akiizingatia kuwa ni sahihi riwaya aliyoipokea Musa bin Khalaf.” Ama Al-Hafdih amesema katika Al-Isabah baada ya kuashiria kwenye baadhi ya njia zake: “Na inaonyesha katika mkusanyiko 86

Katika Asmau Waswifaat (300). 44

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 44

10/20/2015 5:15:22 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

wa niliyoyataja, kuna nguvu ya riwaya ya Abdurahman bin Yazid bin Jabir kwa ilivyo nzuri.87 na yeye hakujichanganya katika riwaya hiyo. Ama riwaya ya Abu Salam, yeye amejichanganya katika riwaya yake hiyo. Na amepokea Hamad bin Malik kama ilivyotangulia kama riwaya ya Abdurahman bin Yazid, na akampinga Zaid bin Salam, akaipokea kutoka kwa babu yake Abu Salam kutoka kwa Abdurahman bin Aish kutoka kwa Malik bin Amir kutoka kwa Muadh, ameitaja kwa kirefu na kisa kiko hivi hivi. Ameipokea Jahdhamiy bin Abdallah Al-Yamamiy kutoka kwa Yahya bin Abu Kathir kutoka kwa Zaid. Ameiandika Ahmad na Ibn Khuzaymah na Rawiyaniy na Tirmidhiy na Daru Qutniy na Ibn Adiyy na wengineo. Musa bin Khalaf akawakhalifu akasema: ‘Kutoka kwa Yahya bin Zaid kutoka kwa babu yake kutoka kwa Abu Abdurahman As-Saksakiy kutoka kwa Malik bin Amir kutoka kwa Muadh. Ameiandika Daru Qutniy na Ibn Khuzaymah na ameinukuu kutoka kwa Ahmad, amesema: ‘Njia hii ndio sahihi zaidi.’” Al-Hafidh amesema: “Ikiwa iko hivyo, basi Hadithi hii ameipokea kutoka kwa Malik bin Amir Abu Abdurahman As Saksakiy na si Abdurahman bin Aish, na Hadithi hii itakuwa na sanad mbili,88 ya Ibn Jabir kutoka kwa Abdurahman bin Aish, na ya Yahya bin Zaid kutoka kwa Abu Salam kutoka kwa Abu Abduraman kutoka kwa Malik kutoka kwa Muadh. Na jambo linalokuza ikhtilafu ni mtiririko wa maneno uliyopo baina ya riwaya mbili hizo.” Nasema: Imepokewa kutoka kwa Muadh kwa njia nyingine aliyoipokea Ibn Khuzaymah katika kitabu At-Tawhid kwa njia ya Said bin Suwaid Al-Qurashiy, kutoka kwa Abdurahman bin Is’haq   Amenukuu Al-Hafidh katika An-Nukat Dharaf (4:382) kama ilivyotangulia kutoka kwa Muhamad bin Nasr Al-Maruziy amesema: “Hadithi hii imekanganya wapokezi katika sanadi yake na haijathibiti kwa wajuzi. 88   Haya ni maneno dhaifu kutoka kwa Al-Hafidh, kwa maoni yangu hata yeye alichanganyikiwa na Hadithi hii, upande wa matini ni batili. 87

45

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 45

10/20/2015 5:15:22 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

kutoka kwa Abdurahman bin Layla, kutoka kwa Muadh bin Jabal, kisa hiki kwa kirefu kinafanana na habari ya Yahya bin Abu Kathir. Ibn Khuzaymah amesema: “Huyu Sheikh Said bin Suwaid simjui kwa uadilifu au kwa ubaya. Na Abdurahman bin Is’haq huyu ni baba yake Shibatul-Kufiy mwenye Hadithi dhaifu, na Abdurahman bin Abu Layla hajawahi kusikia kutoka kwa Muadh.”

46

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 46

10/20/2015 5:15:22 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

HADITHI NYINGINE

A

l-Khatib amesema katika wasifu wa Hamad bin Dulayl Kadhi wa Madain katika kitabu chake Tarikh:89 Ametuambia Abul Hassan Ali bin Yahya bin Jaffar Imam wa Isfahan, ametuhadithia Sulaiman bin Ahmad At-Tabaraniy, ametuhadithia Hassan bin Ali Al-Muammariy90. Ametuhadithia Suleiman bin Muhammad AlMubarak, ametuhadithia Hamad bin Dulail kutoka kwa Sufian bin Said At-Thauriy, kutoka kwa Qaysi bin Muslim kutoka kwa Tariq bin Shihab au Abdurahman bin Sabit. Amesema Hamad bin Dulayl: Amenihadithia Al-Hassan bin Hayyi kutoka kwa Amru bin Murra, kutoka kwa Abdurahman bin Sabit kutoka kwa Abu Thaalabah Al-Khashaniy kutoka kwa Abu Ubaydah bin Al-Jarah kutoka kwa Mtume 8 amesema: “Nilipokuwa kwenye usiku ambao nilipelekwa Israi nilimuona Mola Wangu Mtukufu akiwa katika sura nzuri, akasema: Ewe Muhammad! Je wajua ni kitu gani hugombania Malaika?...,” akaitaja Hadithi hii. Tabaraniy amesema: “Hakuipokea Hadithi hii kutoka kwa Sufiani ila Hammad bin Dulayl.” 89 90

Tarikh Baghdad (8: 151).   Huyu Al-Muammariy ni muongo, imetajwa kwenye Al-Mizan (2:276) cha al Hafidh Ibn Hajar kwa kunukuu kutoka kwa Dhahabiy kwamba: “Anazo Hadithi gharaib…” Daru Qutniy naye amesema: “Hafidh amesema kweli.. Abdan naye amesema: Nimemsikia Razi na Jafar bin Junaydi wakisema: Al-Muammar ni muongo sana.” Ameongeza alHaffidh Ibn Hajar: “al-Khatib amesema: Alikuwa na ujuzi na ufahamu na akisifika kwa kuhifadhi, katika Hadithi zake kuna gharaib na mambo ya peke yake…. Na Abdullah bin Ahmad bin Hanbal amesema: Hasemi uwongo kwa kukusudia, isipokuwa ni kwamba alisuhubiana na watu wenye kupotosha Hadithi.” Na Musa bin Harun alimtuhumu kwa kupokea Hadithi za ajabu kutoka kwa masheikh waaminifu, na Ibn Addiy akasema: “Hasan bin Ali al-Muammariy alileta Hadithi zisizo na mnyororo wa wapokezi na akazidisha vingine katika matini za hadithi hizo, ambavyo havikuwemo, na alikuwa ni mwingi wa Hadithi.” Kisha Al-Hafidh amesema katika Al-Lisan: “Amesema Ibn Addiy: “al-Muammariy hasemi uongo kwa makusudi lakini alisuhubiana na baadhi ya watu wa Baghdad ambao wameongeza. Na hili liko sana kwa watu wa Baghdad katika Hadithi zao na katika Hadithi za waaminifu wao.” 47

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 47

10/20/2015 5:15:22 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

Na Al-Khatib pia amesema: Ametwambia hiyo Abdul Malik bin Muhammad bin Abdallah Al-Waidh: Ametwambia Abdul Baqi bin Qanii Al-Hafidh: Ametuhadithia Muhammad bin Ali Al-Madaniy: Ametuhadithia Abu Daud Al-Mubarakiy: Ametuhadithia Hammad bin Dalil: Ametuhadithia Sufian bin Said kutoka kwa Qaysi bin Muslim kutoka kwa Tariq bin Shihab. Na ametuhadithia Al-Hasan bin Imara kutoka kwa Amri bin Murrah, kutoka kwa Abdurahman bin Sabit, kutoka kwa Abu Thaalaba Al-Khashaniy kutoka kwa Abu Ubayda bin Al-Jarah kutoka kwa Mtume 8 amesema: “Nilimuona Mola Wangu Mtukufu akiwa katika sura nzuri, akasema: Ewe Muhammad! Je wajua ni kitu gani hugombania Malaika?...” akaitaja Hadithi hii. Ibnul Jawziy ameipokea katika kitabu Al-Ilal alMutanahiyah: “Ametwambia Abu Mansur Al-Qazaz: Ametuhadithia Abu Bakr bin Thabit: Ametuhadithia Abdul Malik bin Mahmud kuhusu Hadithi hii. Nasema: Kuhusu Hammad bin Dulayla, Ibn Muin amesema kuwa ni mkweli. Na Ibn Ammar pia amesema: Alikuwa ni katika watu wakweli. Abu Daud naye amesema: Alikuwa hana ubaya. Azdiy na wengineo wamesema alikuwa dhaifu.

48

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 48

10/20/2015 5:15:22 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

HADITHI NYINGINE

I

bn Habban katika kitabu Al-Majruhin (3:135) amesema: “Ametwambia Al-Hasan bin Sufian: Ametuhadithia Al-Hasan bin Muhammad Al-Sabbah: Ametuhadithia Yusuf bin Atiyyah, kutoka kwa Qatadah kutoka kwa Anas bin Malik, amesema: “Siku moja kulikucha asubuhi, Mtume akaja kwetu akasema: ‘Mola Wangu jana alinijia kwenye usingizi akiwa na sura nzuri mpaka akaweka mkono Wake kati ya mabega yangu nikahisi ubaridi wa mikono Yake kwenye kifua changu, na hapo nikajua kila kitu. Akaniambia: Ewe Muhammad! Nikamuitikia labayka Bwana Wangu, akasema: Ewe Muhammad! Je wajua ni kitu gani hugombania Malaika?...” Kisha akaitaja Hadithi hii.

Ibn Habban amesema: “Yusuf bin Atiyya alikuwa ni miongoni mwa watu waliokuwa wakigeuza sanad na kutia matini za kubandika kwenye sanad sahihi, na kisha huzisimulia Hadithi hizo alizozipotosha. Haifai kumtolea hoja kwa hali yoyote ile. Ad-Dhahabiy amesema katika Al-Mizan: “Ametajwa kwa ujumla juu ya udhaifu wake. Nasai pia akasema: “Huyo ameachwa.” AlFalas amesema: “Sikumjua kama alisema uongo lakini alikuwa akikanganya.” Yahya bin Muin amesema: “Hana kitu huyo.” Na akasema: Alikuwa na Hadithi munkar. Al-Hafidh amesema katika Al-Iswabah: “Riwaya hii ina makosa sana kushinda nyingine, ameiandika Abu Bakr Naisaburiy katika Az-Ziyaadat, na Daru Qutniy na Yusuf ikiwa imeachwa. Nasema: Hapana shaka kuwa Yusuf alikanganya katika Hadithi na kubadili sanad yake. Hii ni sehemu ya mwisho ambayo nimeimaliza siku ya Jumanne tarehe ishirini na moja, katika Mfungo wa Ramadhani mwaka 1370 49

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 49

10/20/2015 5:15:22 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

A.H. Kisha nikairudia tena nikaongeza mambo yanayohusiana na sanad za Hadithi hiyo, nilimaliza zoezi hilo siku ya jumatano, 26 Mfungo pili 1403 A.H. nyumbani kwangu Tangier.

50

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 50

10/20/2015 5:15:22 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬ Ufahamisho wa Vizito Viwili Juu ya Uzushi wa Kiti cha Enzi kiko chini ya Miguu ya Mwenyezi Mungu

MTUNZI: HASSAN BIN ALI AS-SAQAFF AL-QURASHI AL-HASHIMI ALHUSAYNI

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU; MWINGI WA REHEMA, MWENYE KUREHEMU

UTANGULIZI

S

hukrani zote ni za Mwenyzi Mungu asiye na mshirika na mfano. Rehema na amani ziende kwa bwana wetu Muhammad 8 bwana wa viumbe na waja, na Aali zake mabwana wakubwa, na radhi za Mwenyezi Mungu ziwaendee Maswahaba wacha Mungu. Miongoni mwa maneno mabaya na yenye ubatili kiakili na kisheria ni tafsiri ya Kursii katika kauli yake Mwenyezi Mungu: 51

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 51

10/20/2015 5:15:22 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

“Imeenea Kursii yake mbingu na ardhi.” Ya kwamba Kursii ni mahali anapoweka miguu yake Mola Mtukufu kama wanavyosema!! Hili katu halijathibitishwa kutoka kwa Mtume wetu 8, bali limepokewa kutoka kwa Abu Musa Al-Ash’ariy na Ibn Abbas, na pia haijathibitishwa kutoka kwao kihakika. Na hata tukijaalia kuwa hilo limethibiti kutoka kwa wawili hao au kwa mmoja wao, basi itakuwa wamelizungumza kutoka kwa watu wa Kitabu (Ahlulkitabi) kwa njia ya kulikanusha na kukataza na si kuliamini, na neno la Swahaba sio hoja ya usahihi kama inavyojulikana katika elimu ya Misingi ya Sharia. Ama kudai kuwa kauli ya Swahaba ambayo humo katoa rai yake haipaswi kukataliwa, hii ni katika nadharia zilizopingwa kama alivyosema Allama Ibn Hazm katika Usuulul Ahkam fi Ilmul Usul (2:72): “Ufafanuzi: Swahaba anaposema jambo la Sunna ni kadhaa, ilihali sisi tumeamrishwa kufanya kadhaa, hii haiwi sanadi, wala haiamuliwi kuwa imetoka kwa Mtume 8, wala hainasibishwi kwa yeyote kauli ambayo haijapokewa kuwa yeye ndiye aliyeisema, na ambayo hakuna hoja inayothibitisha kuwa yeye amesema. Imekuja kutoka kwa Jabir bin Abdillah kuwa amesema: ‘Tulikuwa tukiwauza mama za watoto wakati wa Mtume 8 mpaka Umar alipotukataza, tukaacha.’ “Wengine wamesema: ‘Sunna huwa ni hivyo.’ Yaani ile huwa ni sunna kwake kulingana na ijtihad yake. Katika hayo, Ametuhadithia Hammam: Ametuhadithia Al-Aswili: Ametuhadithia Abu Zaid Al-Maruzy: Ametuhadithia Bukhariy: Ametuhadithia Ahmad bin Muhammad: Ametuhadithia Abdallah: Ametwambia Yunus kutoka kwa Zahriy: Ametwambia Salim Abdallah akasema: Ibn Umar alikuwa akisema: ‘Haiwatoshi nyinyi Sunna ya Mtume wenu 8 kwamba akizuilika mmoja wenu kufanya Hija, basi atufu Al-Kaaba na Swafa na Marwa kisha kila kitu kitakuwa halali kwake mpaka 52

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 52

10/20/2015 5:15:22 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

ahiji mwaka unaofuata na hapo atatoa sadaka au afunge ikiwa hakupata sadaka.’” Abu Muhammad amesema: Hakuna tofauti kati ya watu wa umma wote, kwamba Mtume 8 alipozuilika kwenda kwenye AlKaaba, hakutufu, wala hakufanya Swafa na Marwa bali ilijitoa katika ihram pale alipokuwa, wakati huo alikuwa Hudaybiyya, na hakuna la zaidi alilofanya. Na haya aliyoyasema Ibn Umar hayakutokea kati kwa Mtume.”91 Nami nasema tena: Kama ilivyo dhahiri, kwamba Abdallah bin Zubayri ikiwa itathibiti kutoka kwake basi amekosea kama alivyothibitisha katika Hadithi nyingine kuwa alikosea. Imam Ahmad amepokea katika Musnad yake (4:4) kwa sanad sahihi akasema: “Ametuhadithia Yaqub bin Ibrahim: Ametuhadithia baba yangu kutoka kwa Ibn Is’haq amesema: Amenihadithia baba yangu Is’haq bin Yasar amesema: ‘Tulikuwa Makka mara akaja Abdullah bin Zubayr akakataza kufanya Umrat Tamatui, na akakanusha kuwa watu hawakulifanya hilo na Mtume 8, habari hiyo ikamfikia Ibn Abbas akasema: Amelijua wapi hili Ibn Zubayr hebu na arejee kwa mama yake Asmau bint Abu Bakri akamuulize. Habari hiyo ikamfikia Asmau akasema: Mwenyezi Mungu amsamehe Ibn Abbas, Wallahi Ibn Abbas amesema kweli, walihalalisha na tukahalalisha.” - Hapa kuna mazingatio ikiwa atazingatia. Na Hadithi ya turba iliyopokewa katika Sahih Muslim (2879) ambayo Bukhariy ameitaja katika Tarikhul Kabir (1:413-414) kwa usahihi zaidi hiyo ni riwaya ya Abu Hurayra kutoka kwa Kaabul 91

Kutokana na haya utajua kuwa elimu yake katika Misingi ya Sharia ni dhaifu, na katika hayo ni kauli yake katika kijitabu chake Al-As’ilatuin-Nafiah, Uk. 18, Chapa ya pili, mwaka 1400, Beirut: “Na hivyo imethibiti katika elimu ya Misingi ya Sharia kuwa kauli ya Tabiina kuwa, miongoni mwa Sunna ni kitu fulani, haipingiki, ambapo ni kinyume na endapo atasema hivyo swahaba, hapo itakuwa ni hukmu yenye kupingwa. 53

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 53

10/20/2015 5:15:22 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

Akhbar. Na kwakuwa imetamkwa wazi ndani ya Sahih Muslim kuwa ni riwaya isiyo na sanadi nzima basi kaida tuliyosema inathibiti.92 Ikiwa tutazipinga baadhi ya Hadithi zisizo na sanadi nzima zilizomo katika Sahih mbili, ambazo maelezo yamekuja wazi kuwa hazina sanadi kamili, na ambazo tunaamini wazi kwamba ni katika zilizopokewa na Maswahaba kutoka kwa Ahlul Kitab, itakuwaje juu ya Hadithi zenye fikra zilizokataliwa na kumpa Mungu umbo na kumshabihisha kwa uwazi?

92

  Amesema Ibn Kathir katika Tafsiir yake (1:99) chapa ya As-Shaab: “Hii Hadithi ni katika zile gharaib za Sahih Muslim, Ibnu al-Madaniy na Bukhari wameizungumzia na si mmoja katika Mahafidh wameizingatia kuwa ni maneno ya Kaabul Akhbar, Abu Hurayra alisikia maneno ya Kaabul Akhbar, baadhi ya wapokezi wameifanya ni marfuu. 54

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 54

10/20/2015 5:15:22 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

KUYAHAKIKI MANENO JUU YA NGANO YA “KURSII NI MAHALI PA KUWEKA MIGUU YA MUNGU”

I

bara hii imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas na Abu Musa AlAshary, lakini haikuthibiti kutoka kwao. Tutaonyesha juu ya sanad za riwaya hizo ambazo mimi naziona kuwa ni fikra za Kiyahudi zisizofaa. Amesema Ad-Dhahabiy katika kitabu Al-Uluwwu:93 Amesema Abdallah bin Imam Ahmad bin Hanbali katika kitabu As-Sunnah: Abbas bin Abdul Adhim aliniandikia kwa mkono wake mwenyewe: Ametuhadithia Ismail bin Abdul Karim: Ametuhadithia Abdu Swamad bin Muuqil: Nimemsikia Wahb bin Munabbih akisema: “Akataja utukufu wa Mwenyezi Mungu akasema: Hakika mbingu na bahari ziko kwenye tufe, na tufe liko ndani ya Kursii na miguu yake Mwenyezi Mungu iko juu ya Kursii na imekuwa ile Kursii ni kama kiatu kiko chini ya miguu yake.”94 Aliulizwa Wahb juu ya ardhi akasema, ni ardhi saba baina ya kila ardhi kumewekwa bahari na bahari yenye rangi ya kijani imezunguka na tufe liko nyuma ya bahari.95 Wahb alikuwa ni mwanachuoni 96 lakini elimu yake ni juu ya habari za umma za zamani, alikuwa na vitabu vingi vya visa vya fikra za Kiyahudi, na alikuwa akinukuu kutoka humo, na huenda   Kilichohakikiwa na Al Abdu Alfaqiir Uk. 385 nasu namba 323.   Hii kweli ni kauli ya mtu mwenye akili anayemuamini Mola asiye na mshabaha wala umbile?! 95   Hii imethibiti kutoka kwa Wahb, ameipokea Ibn Jarir katika tarikh yake (1: 41) na Abu Sheikh katika Al-Udhma Uk. 199 namba 572. Ibn Ahmad katika Sunna (2: 477) nayo ni katika ngano za Kiyahudi Mungu ameepukana na wasemayo! Mungu awe na sandal au miguu aiweka juu ya kitu, hii kwetu ni kufru kubwa! 96   Bali alikuwa mpotevu, mpotezaji aiacha Quran akawa anasoma vitabu vilivyopotoshwa na kueneza yaliyomo humo ya kufru kwa Waislamu ili kuiunga mkono dola ya Bani Umaiyyah, na nadhani yeye ni Myahudi, angalia tarjuma ya Siyarun Nubalai (4:544). 93 94

55

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 55

10/20/2015 5:15:22 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

yeye alikuwa na kapu kubwa kumshinda hata Kaab al-Akhbar, na hii aliyoitaja kuwa ni tufe na ardhi saba zimepambanuliwa na bahari na mengineyo, yahitaji uchunguzi, na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi. Hatuipingi97, wala hatuichukui kuwa ni dalili.” (Mwisho wa maneno ya Dhahabiy katika kitabu Al-Uluwwu). Inabainika katika maelezo haya ya Wahb bin Munabbih: “Miguu yake Mwenyezi Mungu iko juu ya Kursii na imekuwa ile Kursii ni kama kiatu kiko chini ya miguu yake.” Na kauli yake: “Tufe liko chini ya Kursii.” Yanatuthibitishia kuwa hizi ni fikra za Kiyahudi na ziko wazi juu ya kumshabihisha Mwenyezi Mungu na kumpa umbo. Na Mahanbali wamelitilia umuhimu sana hili na mengineyo kama vile Mungu kukaa juu ya Arshi, ambapo Mungu ameepukana na hayo wayasemayo. Huyu hapa Ibnu Taymiyya Al-Harrany naye ni katika wao anasema katika Majmuul-Fatawa (4:374): “Ikibainika hii basi wamehadithia wanavyuoni na mawalii kwamba Muhammad atakalishwa na Mwenyezi Mungu juu ya Arshi yake pamoja naye.” Mungu apishe mbali!! Hili ni jambo munkar lenye kukataliwa kwa kila mwenye akili! Hata Al-Albaniy ambaye huafikiana nao katika maswala mengi pia amelipinga. Al-Albaniy amesema katika kitabu chake Dhaiifa (2:255): “Katika mambo ya ajabu ambayo akili haikubali ni kule kueleza baadhi ya wanavyuoni waliotangulia juu ya Mungu kumkalisha Mtume kwenye Arshi pamoja Naye. Bali pia baadhi ya Muhadithina wamezidisha kupita kiasi wakasema: ‘Lau mwenye kuapa mara tatu akaapa kuwa Muhammad 8 atakaa na Mwenyezi Mungu kwenye Arshi basi ningemwambia umesema kweli.’ Dhahabiy amesema: 97

Bali yakupasa kuipinga na kujitenga na kufru hii, tumemuhadharisha Ad-Dhahabiy hatukumhukumu kwa ukafiri wake. 56

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 56

10/20/2015 5:15:23 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

‘Angalia utambue jinsi ufurutu ada ulivyomkokota huyu mwandishi wa Hadithi mpaka akawa tayari kupokea Hadithi munkar.’” Miongoni mwa wafuasi wa Mahanbali wenye kumpa Mwenyezi Mungu mwili ni Abu Muhammad Mahmud bin Qasim bin Badrani Dashty Al Hanbaliy, yeye ametunga kitabu “Ithbatul haddi llahi azza wajala waanna llaha qaaidun wajaalisun ala arshihi” (Kuthibitisha mipaka ya Mwenyezi Mungu, na kwamba Yeye Allah hukaa na huketi juu ya Arshi)98 Jina la kitabu tu lakuambia kiwango chake cha itikadi! Albaniy katika kitabu Silsilatul Hadithi dhaiif walmaudhuua, Juz. 2, ametaja baadhi ya Hadithi zinazoonyesha kuwa hao Mahanbali na baadhi ya Muhadithina wenye kumshabihisha Mungu wamepokea ngano zisizofaa za fikra za Kiyahudi juu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Katika hizo ni kauli ya Albaniy: 1.

Hadithi namba (866): “Hakika Kursii imeenea mbingu na ardhi na Yeye Mwenyezi Mungu huikalia kiasi cha vidole vinne na kwamba Kursii hiyo ina sauti kama sauti ya kipando kipya ambacho hutoa sauti kutokana na uzito wa mpandaji wake.” Kisha Al-Albany akaongeza kauli yake akasema: “Ni munkar, ameipokea Abul Alaa Al-Hasan bin Ahmad Al-Hamadani katika faslu ya sifa.” Huyu Hamadani ni Mhanbali mwenye kumpa mwili Mwenyezi Mungu, mwanafunzi wa Az-Zaghuny Mhanbali pia ambaye amepingwa na Ibnu Al-Jawziy katika kitabu Dafuu Shabhi Tashbiih, utapata maelezo yake katika Siyarul Aalam Nubalai (21:40). Kutokana na haya inakuwa rahisi kwa mwanafunzi kuchukua haraka na kwa ufupi fikra na itikadi za Mahanbali.

Kama uonavyo jina la kitabu kamili katika aliyoelezea muhakiki Al-Kawthar katika alKhatul Alhadh Bidhayli Tabaqatil Hufadh cha Hafidh Muhammad bin Fahd Al-Hashimy al-Makkiy Uk. 263, na akaashiria jina lake pia, lakini kwa kifupi Albaniy katika AdDhaifah (2:257) katika maelezo ya Hadithi namba 866.

98

57

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 57

10/20/2015 5:15:23 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

2.

Ametaja Albaniy katika Dhaifa pia Hadithi namba 876: “Mwenyezi Mungu atawaambia ulamaa siku ya Kiyama atakapokaa katika kiti chake ili kuwahukumu waja wake: “Mimi sikuiweka elimu yangu na hekima yangu kwenu ila na mimi nataka kuwasamehe….” Kisha akafuatisha Albaniy juu ya kauli hii maneno haya: “Ni maudhuu” kisha akasema katika ukurasa unaofuatia: “Kwa mukhtasari ni kuwa Hadithi hii ni maudhuu kwa mtiririko huu na pia kuna tamko la munkar nalo ni kule kukaa kwa Mwenyezi Mungu juu ya Kursii, wala sijui tamko kama hili katika Hadithi sahihi.” Hapa inaonesha Albaniy akimpinga Ibn Taymiyya katika imani ya Mungu kukaa juu ya Kursii pamoja na kuwa anaafikiana naye katika Mweyezi Mungu kukaa juu ya Arshi. Ni dhahiri kuwa watu hawa hawawezi kukubali kuwa Mwenyezi Mungu ametakasika na mahali au upande fulani, hivyo wao wanaafikiana katika baadhi ya mambo na kupingana katika mengine katika suala hilo hilo moja. Hapa inaonesha upeo wa kufananisha na kumpa Mungu mwili ulioko kwa Mahanbali na wanaodai kufuata njia ya Masalafi, nasi hatuwadhulumu tunapowaita kuwa wao ni watu wa kushabihisha na kumfanya Mungu ana mwili.

Na hasa Ibn Taymiyya Al Haraniy Al Hanbaliy anadai kuwa tashbihi na kumfanya Mungu kuwa na mwili hakukutajwa kuwa ni makosa katika Qur’ani na Sunna na katika kauli za Maswahaba na Tabiina. Ibn Taymiyya katika kitabu chake Bayanutalbis ljahamiyya (1:101) amesema: “Si katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu wala Sunna ya Mtume Wake wala kauli ya Masalafi na Maimamu wa umma waliosema kuwa Mwenyezi Mungu hana mwili na kwamba sifa zake si miili”99 Pia amesema katika kitabu hicho hicho (1:109):   Baadhi ya wanafalsafa wamejaribu kukataa kama haya ni maneno ya Al-Harraniy na

99

58

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 58

10/20/2015 5:15:23 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

“Na ikiwa ni hivyo basi mwenye kushabihisha hajatajwa kwa vibaya katika Qur’ani wala Hadithi wala maneno ya Swahaba na Tabiina.”. Muhtasari wa maneno yake ni kuwa kumfananisha Mungu hakukukatazwa au kulaumiwa katika Qur’ani na Hadithi na Maswahaba na Tabiina! Bali lawama zimekuja baada ya Tabiina na Masalafi kama vile Ibn Mahdi, Ahmad, na Yazid bin Harun. Ama katika misingi ya Qur’ani na Sunna hakukutajwa kwa vibaya kulingana na maoni ya Sheikh Al-Harany. Hii ndio inathibitisha madai yetu juu ya maneno ya watu hao. Mungu atupe salama! Na katika balaa kubwa la maudhi haya yenye uharibifu wa itikadi ya tashbihi kwa Mola Mtukufu ni yale aliyoyataja Ibnu Qayyim Al-Jawziy katika kitabu Ijtimaa Juyuushil-Islamiyya (Uk. 109)100 aliposema: “Ametaja Abdurazak bin Muammar kutoka kwa Musayyib kutoka kwa Abu Hurayra, amesema: “Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu hushuka mpaka kwenye uwingi wa dunia Naye akiwa kwenye Kursii, anaposhuka kwenye mbingu ya duniani hukaa kwenye kiti chake kisha husema: Ni nani………………Inapofika asubuhi huinuka akakaa juu ya kiti chake!!.” Hebu angalieni sifa hii na kumfanya Mungu ana umbo na tashbihi. Ibnul Qayyim mwishowe asema: “Ameipokea Abdallah bin Munaddih, ameipokea kutoka kwa Said ni mursal. Amesema Shafii Mursal: Said kwetu sisi ni hasan.. Nasema: Hadithi hii ni ya uzushi na ni uongo, na imetangulia kauli ya Albaniy kwamba haijulikani na Shafii amesema kuwa ni hasan ya Mursal bin Musayyib lakini hakusema kuwa Hadithi kudai kuwa ni maneno ya watu wa ithbati, si kweli kwa sababu mbinu za uelezaji wa huyu Al-Harrany na muradi na itikadi zake vyajulikana, maneno haya ni yake na ni nguo ambayo ameivaa hawezi kuivua, hii ni kukiri na ni akida yake! 100   Hii ni chapa ya Ijtimaul Juyushil islamiyya iliyopitiwa na Dkt. Awwad, ama chapa ya Darul Kutubul Ilmiyya iko Uk. 55, rejea uhakikishe! 59

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 59

10/20/2015 5:15:23 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

hii ni hasan ambayo ni ya uongo. Kabla ya nasi hii Ibnul Qayyim katika Ijtimai Juyuushi ametoa dalili kwamba si munkar: “Na katika sanad ya Imam Ahmad, kutoka kwenye Hadithi ya Ibn Abbas kisa cha shafaa ni Hadithi ndefu imetajwa humo: “Nikamuendea Mola Wangu nikampata amekaa juu ya Kursii au juu ya kitanda chake.” Nasema: Neno ‘amekaa’ amelizidisha Ibnul Qayyim wala haliko katika Hadithi hiyo katika Musnad ya Imam Ahmad.101 (1:282-296) hii ni katika jumla ya uzushi wake na kuchomeka kwake maneno katika Hadithi. Kwa hivyo ni dhahiri kuwa wao ni wenye kumfanya Mungu kuwa na mwili japo wakijionyesha kwamba hulikataa hilo! Na wametaja kuwa Ibnu Taymiyya amesema kuwa ni Hadithi sahih, Hadithi ya kijana mzuri katika kitabu chake Bayan Talbiis Jahamiya, Juzuu ya 3, Uk. 241 anakusudia kuwapinga Jahamiyya na anathibitisha kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kutokana na wanayosema kuwa ana sura ya kijana nzuri, humo anasema hivi: “Inachukuliwa kuwa ni kuona kwa macho kama ilivyo katika Hadithi sahihi marfuu kutoka kwa Qatadah kutoka kwa Ikrima kutoka kwa Ibn Abbas ambaye amesema, amesema Mtume 8: “Nimemuona Mola Wangu katika sura nzuri akiwa na vazi katika rangi ya kijani.” Twajilinda na Mwenyezi Mungu na upotofu huu! Ikiwa huu si upotevu, basi upotevu ni upi tena kwenye imani ya kiislamu? Dhahabiy ametaja katika kitabu Siyaru Alaami Nubalai (10:505) kwa sanadi yake kutoka wa Abbas ad-Dawriy amesema: “Nimemsikia Abu Ubayd Al Qasim bin Salam, na akataja mlango ambao unataja kisa cha kuona na kiti kiko chini ya miguu miwili ya Mwenyezi   Amekubali AlbanIy katika Mukhtaswarul-Uluwwi Uk. 93 na mhakiki wa kitabu IjtimaulJuyush katika maelezo namba 1 uk. 108, na ilifaa Ibnu al-Qayyim akiite kitabu hicho Ijtimaul-Akaadhib! Na ni maudhuu za kupinga watu wa haki kwa ngano za Kiyahudi, na katika kitabu hiki Ibnu al-Qayyim ametaja Hadithi: “Mkirimuni ng’ombe” inayopelekea kwenye imani za kibaniani.

101

60

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 60

10/20/2015 5:15:23 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

Mungu,102 na akacheka Mola wetu, alikuwa wapi Mola wetu?103... ni Hadithi sahihi104…watu wa Hadithi na mafakihi wameikubali nasi hatuna shaka ndani yake, 105….lakini itakaposemwa anacheka vipi na vipi alivyoweka miguu yake, tutasema hili hatulifafanui wala hatujasikia mtu yeyote akilifafanua106…” Nasema hivi: Wamefafanua wanavyuoni maneno muhimu na yasiyokuwa muhimu na Aya za sifa na Hadithi zake hawakuweza kufafanua kabisa. Nayo ni ya muhimu kwa dini lau ingekuwa ufafanuzi wake ni wa lazima basi wangefanya haraka kufafanua jambo hilo na kujua kuwa yaliyoelezwa kwa haki hayana haja ya kuyafafanua.107 Wakajua kuwa kuyasoma na kuyapitia ni haki haya maelezo mengine zaidi ya hayo.108 Tunaamini hivyo na tunanyamaza kwa kuwafuata watu wema waliotutangulia waliokuwa wakiamini kuwa hizo ni katika sifa za Mwenyezi Mungu Mtukufu sifa hizo hazifanani na sifa za viumbe   Si Hadithi sahih bali ameihukumu Albany katika kitabu Dhaifah (2/306/906) kama ilivyotangulia kuwa ni dhaifu. 103   Isnad ni dhaifu na Hadithi ni ya uwongo na uzushi, Ahmad amepokea katika Musnad (4:11) na Tirmidhiy (5:288/3109) na Ibn Majah (1:64/182). Tabaraniy katika Al Kabir (19:207/468) na katika Sanad ya Wakii hakumsadikisha ila Ibn Habban, na hakupokea kwake ila Yaala bin Ataai, kisha Tirmidhiy amenukuu katika Sunan yake baada ya taawili ya Hadithi kutoka kwa Yazid bin Harun akasema: “Amesema Yazid bin Harun: “Ni kipofu, yaani hana kitu.” 104   Hadithi inapingana na zama zetu angalia Sunnan cha Ibn Qabi Asim Hadithi namba 216 na katika Dhaif cha Tirmidhiy Uk. 387 Hadithi namba 602, na katika Dhaif cha Ibn Majah namba 32, kama alivyosema katika Dhaif ya Tirmidhiy, na akasema katika Mukhtasaril Uluww uk. 186 maelezo namba 193, akasema: “Ameipokea Tirmidhiy na Ibn Majah na Sanad yake ni hasan! Hivi ndivyo alivyosema, nayo imekataliwa. 105   Watu wa Hadithi na mafakihi wameipinga, hii ni ngano tu ya kihambali! 106   Vitabu vya tafsiri vya kisalafi na vya sunna na hadithi vimejaa maelezo ya masalafi juu ya jambo hili! 107   Wamefanya haraka kwa alivyonakili Ibn Jarir na wengineo na vitabu vya tafsiri vimejaa hayo. 108   Hii inahukumu kwa kuangalia dhahiri ya maneno, nayo ni rai batili, kwani Ibn Abbas na masalafi hawakupitia tu bali walijitahidi kueleza na kubainisha maana zake. 102

61

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 61

10/20/2015 5:15:23 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

kama ilivyo dhati yake haifananishwi na za viumbe, Qur’ani na Sunna vimetaja na Mtume 8 na hakufafanua pamoja na kuwa Mwenyezi Mungu amesema: “Ili uwafafanulie watu waliyoteremshiwa.” Ni juu yetu kuamini na kuzikubali nassi. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kumuongoza amtakaye kwenye njia iliyonyooka. Mwisho wa maneno ya Dhahabiy kutoka kwenye kitabu chake Siyar. Nasema: Nami sijui vipi alighafilika Dhahabi kuwa Bukhari amenukuu katika Sahihi yake kutoka kwa Said bin Jubayr naye ni katika maimamu wa kisalafi maelezo ya Kursii kwa maana ya ilimu.!! Ambapo Bukhari amesema: “Amesema Ibn Jubayr: ‘Kursii ya Mwenyezi Mungu ni ilimu yake.’”109 Kama ambavyo Dhahabiy amesahau au kujisahaulisha kuwa katika sunan yake (3298) kuna hadithi: “Lau mtamteremsha mtu kwa kamba mpaka chini kwenye ardhi ya chini basi angemuangukia Mwenyezi Mungu.” Amesema yeye mwenyewe baada ya hadithi hii: “Baadhi ya ulamaa wamefafanua Hadithi hii wakasema na angeangukia kwenye elimu ya Mwenyezi Mungu na kwenye kudra Yake na ufalme Wake.” Sheikh wake Ibn Taymiyya Al Haraniy hakukubali maelezo haya katika kitabu Majmuul Fatawa (6:573) akasema huku akimpinga Tirmidhiy: “Tirmidhiy alipoipokea Hadithi hii na baadhi ya ulamaa wa Hadithi wakamfafanulia kuwa ni kuangukia kwenye ilimu ya Mwenyezi Mungu, na pia taawili yake kwa maana ya ilimu, ni wazi kuwa ni potofu kama zilivyo taawili za kijahamiyyah.” Hapa sasa Tirmidhy na baadhi ya watu wa Hadithi wamekuwa wanasema maneno ya kijahamiyya kwa sababu tu wameyapinga matamanio yao.   Katika kitabu Tafsiir (8:199) kutoka Fat-hul Bari kabla ya Hadithi namba 4535 katika mlango huo huo.

109

62

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 62

10/20/2015 5:15:23 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

MJADALA JUU YA SANAD ZA “KITI (KURSII) NI MAHALI PA KUWEKA MIGUU

H

ebu tuanze na ufafanuzi katika riwaya ya kutoka kwa Abu Musa Al Ash’ariy na Ibn Abbas juu ya kuwa Kursii ni mahali pa kuwekea miguu ya Mwenyezi Mungu, twasema hivi:

Ama kuhusu riwaya ya Abu Musa Al Ash’ariy juu ya hilo: Ibn Jurayri amepokea katika tafsiri yake (10:3-9), na Al Bayhaqiy katika Al Asmaa wa Sifaat Uk. 404 kutoka kwa njia ya Salama bin Kuhayli, kutoka kwa Umara bin Umayri, kutoka kwa Abu Musa Al Ash’ariy amesema: “Kursii ambapo ni mahali pa Mola kuweka miguu Yake miwili ina sauti kama sauti ya kipando. Amepokea kutoka kwa mtoto wake Ibrahim bin Abu Musa kama ilivyo katika maelezo yake katika Tahdhibul Kamal (21:256) na Tahdhibu Tahdhiib (7: 369) isnad imekatika. Na imekuja katika maelezo ya baadhi ya watoto wa Abu Musa Al Ash’ariy naye ni Abu Burda amepokea kutoka kwa Abdallah bin Salam Myahudi kama ilivyo katika Tahdhibul Kamal (33:66), na riwaya yake kutoka katika Bukhari ni (3814, 7342), kwangu mimi naona huyu ndiye aliyewasilisha kwa Ibn Umayr katika ngano za Kiyahudi kutoka kwa Abdallahs bin Salam kisha ikafanywa kuwa ni kauli ya Abu Musa! Na naongeza hapa kwamba ukoo wa Abu Musa una uhusiano mkubwa na wapokezi wa kiyahudi kama Abdallah bin Salam Myahudi na Kaabul Akhbar, na kuna uwezekano mkubwa wa wao kuzipokea Hadithi hizi kutoka kwao.

63

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 63

10/20/2015 5:15:23 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

Katika Siyarul Aalam Nubalai (5:6) “Amepokea Said bin Abu Burda kutoka kwa baba yake, amesema: “Abu Musa alinipeleka kwa Abdallah bin Salam ili nikasome kwake.” Angalia Muwataa Hadithi namba 243, uone uhusiano wa Kaabul Akhbar na Abdallah bin Salam, na kuendelea kwake Kaabul Akhbar kusoma Tawrati wakati wa Uislamu. Miongoni mwa jeuri ya Albaniy juu ya kuizingatia Hadithi kuwa ni sahihi au ni dhaifu ni kwamba amedai katika Mukhtasarul Uluwwi, Uk. 124 ……..kuwa sanadi ya Hadithi ya Abu Musa hii ya (Kursii ni mahali pa kuweka miguu ya Allah) ni sahih, akasema huko: “Nimesema kuwa sanadi yake ni sahihi.110 Hili ni kosa kubwa sana lisilo na mfano kwa sababu sanad hii imekatika. Ndugu zake pia wamempinga miongoni mwao ni mhakiki wa kitabu cha Kitabus Sunnah cha Ibn Ahmad, amesema huyo: “Katika sanadi ya Hadithi hii kuna kukatika kwa sababu Ummara hakukutana na Abu Musa.” Kisha Albaniy amemshutumu Allamah Al Kawthariy aliposema Hadithi hii ni dhaifu, na amesahau kwamba yeye aliangukia kwenye mkanganyo na mtelezo huku akijiona kuwa yeye ni mhakiki anayeweza kumpinga mwanachuoni Al Kawthariy. Ambapo Albaniy mwenyewe anajipinga katika Hadithi hii katika kitabu chake Dhaiifah (2:307), katika kuandika Hadithi namba 907. Na nilifafanua hilo katika kitabu Tanaqudhatil Aalbanil Waadhihah (2:291-289). Hebu rejea kitabu hicho. Kwa muhtasari ni kuwa Hadithi hii haikuthibiti kuwa imetoka kwa Abu Musa, na ni Hadithi Munkar na ni yenye kukatika sanad yake.   Hivi alikosea Al Hafidh Ibn Hajar aliposema katika kitabu Al Fat-hi (8:199) kwamba sanad ya Hadithi ya Abi Musa ni sahih, kwa kuwa isnad hii imekatika na si sahih!

110

64

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 64

10/20/2015 5:15:23 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

Ama riwaya ya Ibn Abbas: Ni maarufu kwa maulamaa kwamba imepokewa katika maelezo ya Aya isemayo: “Kursii yake Mwenyezi Mungu imeenea kwenye mbingu na ardhi.” Kutoka kwa Ibn Abbas kuna riwaya mbili: Ya kwanza ni inayoonyesha juu ya utakaso ambayo ni ile isemayo: “Kursii Yake ni elimu Yake” yaani elimu yake imeenea kwenye mbingu na ardhi yaani anayajua yaliyomo humo. Riwaya ya pili ni ile ionyeshayo juu ya kumfananisha (tashbiih) na kumfanya ana mwili (tajsiim) nayo ni hiyo ya “Kursii iko chini ya miguu miwili.” Ama riwaya ya kwanza Kursii Yake ni elimu Yake hii ni sahihi imethibiti: Ibn Hajar amesema katika Tafsiir yake (3:9): “Ametuhadithia Abu Kurayb na Salim bin Janada wamesema: “Wametuhadithia Ibn Idris kutoka kwa Mutarraf, kutoka kwa Jafar bin Abul Mughira kutoka kwa Said bin Jubayr kutoka kwa Ibn Abbas juu ya Aya ‘Kursii yake imeenea; akasema: “Yaani ni elimu Yake.” Mtiririko wa Aya waonyesha hivyo pia: “Wala hawajui chochote katika vilivyo kwenye elimu Yake ila kwa alitakalo. Elimu Yake imeenea mbingu na ardhi. …” Kwa sababu maneno katika Aya hii yapo katika maudhui moja. Na katika vitabu vya lugha kama Qamusil muhiit: Kursii ni kitanda na elimu. Bukhari ametaja katika Sahihi yake kutoka kwa Said bin Jubayr kwamba Kursii Yake, ni elimu Yake. Angalia kitabu: Fat-hul bary (8:119) kabla ya Hadithi namba 4535. Ibn Jarir Tabari amesema katika Tafsiri yake (3:11): “Ama inavyoonesha kuwa sahihi ni dhahiri ya Qur’ani, na kauli ya Ibn Abbas aliyoipokea Jafar bin Abul Mughira kutoka kwa Said bin Jubayr kutoka kwake walisema: Kursii, ni elimu ya Mwenyezi Mungu, na hiyo ni kwa dalili ya kauli yake Mwenyezi Mungu: “Wala hakumshindi kuzilinda.” 65

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 65

10/20/2015 5:15:23 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

Katika jambo la kushangaza ni amesema Ibn Mandah AlHanbaliy mwenye kumfanya Mungu ana umbo, kama alivyonukuu Dhahabiy katika Al Mizan (1:417) kwamba Ja’far bin Abul Mughira hakumfuatilia, na akasema pia: “Hakuwa na nguvu kwa Said bin Jubayr. Na Ibn Mandah hamjui Ibn Abul Mughira wala hajakutana naye na kuna kipindi cha muda mrefu kati ya maisha yao.” Hakika maneno yake haya nia yake ni kuifanya dhaifu tu riwaya hii inayoonesha kutakasa. Na amesahau huyu Ibn Mandah kwamba riwaya ya (Kursii ni mahali pa kuweka miguu miwili) haikufuatiliwa na yeyote katika kutaka kujua ni vipi Dahniy na Sheikh wake Muslim Al Batin waliipokea kutoka kwa Ibn Abbas, lakini ukinzani na kuwa mbali na kumtukuza Mungu kunapofusha na kutia uziwi!! Hadithi ya Jafar bin Abul Mughira ameifanya sahihi Ibn Habban katika Sahih (9:516), na Al Hakim katika Al Mustadrak, na Dhiyaa katika Al Mukhtara (10:99). Na Al Hafidh Ibn Hajar katika Al Fathi (10:235) amesema kuwa ni sahihi riwaya ya Ibn Abul Mughira kutoka kwa Said bin Jubayr. Amesema Abu Daud katika Sunan (1301): “Nimemsikia Muhammad bin Hamid akisema: Nimemsikia Yakub akisema: ‘Kila kitu nilichowahadithia kutoka kwa Jafar bin Mughira kutoka kwa Said bin Jubayr kutoka kwa Mtume 8 ni Musnad ya kutoka kwa Ibn Abbas kutoka kwa Mtume 8.’” Amesema Al Qurtubiy katika Tafsir (3:276): Amesema Ibn Abbas: “Kursii Yake ni elimu Yake.” Na Ibn Tabariy pia ameitilia nguvu akasema: “Miongoni mwayo ni kurasa pia zinazobeba elimu.” Ama riwaya ya pili kutoka kwa Ibn Abbas ambayo: Kursii ni mahali pa kuweka miguu ya Mwenyezi Mungu, hii haiswihi na ni batili, angalia ufafanuzi wake kama ifuatavyo: 66

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 66

10/20/2015 5:15:23 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

Riwaya hii iliyopokewa na Tabraniy katika Majmaul Kabir (12:39) kutoka kwa njia ya Sufian Thawriy kutoka kwa Ummara Duhniy kutoka kwa Said bin Jubayr kutoka kwa Ibn Abbas: ‘Kursii Yake imeenea mbingu na ardhi,’ akasema: “Mahali pa kuweka miguu Yake, hapawezi kukadiriwa kuwa Arshi Yake.” Nami nasema: Waarabu hawajui kuwa maana ya Kursii ni mahali pa kuweka miguu, bali wanajua kuwa Kursii ni kiti au elimu. Kwa isnad hii ametoa Al Hakim katika Al Mustadrak (2:282) na akaongeza “Kutoka kwa Duhniy kutoka kwa Muslim Al Batin, kutoka kwa Said bin Jubayr na pia alipokea kwa ithbati ya Muslim Al Batin: Abdallah bin Ahmad katika kitabu As Sunnah (1/103/586). Na Al Khatibul Baghdadiy katika Tarikh yake (9:251) na Ibnul Jawziy katika Al Ilalul Mutanahiyah. Na Muslim Al Batin hapa wamemuingiza katika sanad ili riwaya hii munkar iwe na nguvu, na dalili ya hilo ni Al Hafidh Mufasir Ibn Jarir hakuitaja kauli hii katika Tafsiir yake (3:10) kwa kuinasibisha na Ibn Abbas, bali ameinasibisha na kauli ya Muslim Al Batin. Humo Ibn Jarir amesema: “Ametuhadithia Ahmad bin Is’haq amesema: ametuhadithia Abu Ahmad Zubayri kutoka kwa Sufian kutoka kwa Ummar Dahniy kutoka kwa Muslim Al Batin amesema: “Kursii ni mahali pa kuweka miguu miwili.” Na hii inapinga riwaya ambayo ndani yake yumo Al Batin anaipokea kutoka kwa Ibn Jubayr kutoka kwa Ibn Abbas. Na inatuthibitikia kwetu kwamba baadhi ya wapokezi wameinasibisha na Ibn Jubayr na Ibn Abbas, nayo ni kauli ya Muslim Al Batin. Lau ingekuwa yajulikana kutoka kwa Ibn Abbas angeinukuu Tabariy kutoka kwa Ibn Abbas!! Na katika taasub za Dhahabiy ni kauli yake katika Al-Mizan (1:418) katika mwisho wa wasifu wa Jafar bin Abul Mughira: “Amepokea Abu Bakri Al Hadhliy111 na wengine kutoka kwa Said   Abu Bakri Al Hadhaliy, Bukhari amemtaja katika Tarikhul Kabir (4:198): “Si mwenye kuhifadhi kwao.” Pia ad Dahabiy amesema katika Diwanu Dhuafaa (1:276):

111

67

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 67

10/20/2015 5:15:23 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

bin Jubayr kauli yake: “Amesema, Kursii ni mahali pa kuweka miguu.” Na kitabu Al Mizan ni katika tungo zake za awali na baadaye akayakana mambo mengi yaliyomo humo, alikuwa amekitunga akiwa amefitinika na fikra na itikadi za Sheikh Al Harraniy!!. Aliyotaja Bukhari katika Sahih yake kutoka kwa Said bin Jubayr: “Kursii ni elimu yake”, hii ni maarufu, ni yenye kukubalika na sio ile riwaya ya munkar! ambapo ikiwa imetoka kwao basi wameieleza kwa njia ya kukanusha na kumpinga anayepinga itikadi zao. Ammar Duhniy au Muslim Al Batin wako peke yao katika riwaya hii munkar kutoka kwa Ibn Abbas ambayo hakuna aliyeifuata hata mmoja. Na riwaya ya Tabaraniy katika Muujamul Kabir kama ilivyotangulia ni katika riwaya za Ammar Duhniy kutoka kwa Said bin Jubayr moja kwa moja bila ya kuwa na Al Batin kati yao. Na Ammar Duhniy hajapokea kutoka kwa Said bin Jubayr kama alivyokubali yeye mwenyewe kama ilivyo katika Tahdhibul Kamal (21:210). Na katika Jamiu Tahswiil tarjuma namba 550, amesema Ahmad bin Hanbal: “Duhniy hakusikia chochote kutoka kwa Said bin Jubayr.” Hii yote inafanya Hadithi hii iwe na mikanganyo na kuwa ni dhaif kutoka kwa Ibn Abbas na haikuthibiti kwake! Na hasa imepingwa riwaya ya “Kursii mahali pa kuweka miguu” na wenye vitabu tisa: Bukhari, Muslim, Sunan Arbaa, Ahmad, Malik, na Daramiy. Lakini ameitaja Bukhari katika Sahihi yake kutoka kwa Said bin Jubayr: “Kwamba Kursii yake ni elimu yake.” (Angalia Fat-hul Bary (8:199) kabla ya Hadithi namba 4535. Kursii mahali pa kuweka miguu, ni riwaya ya Kiyahudi, yenye kumfanya Mungu ana umbo na ni yenye kukataliwa. Na kwa kuthibitisha riwaya hii kutoka kwa Ibn Abbas ni katika “Wameziacha Hadithi zake.” Pia akasema katika Diwanu Dhuafaa (2:773): “Mmoja kati ya walioachwa.” Hapa twajua riwaya ya Said bin Jubayr haina thamani. 68

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 68

10/20/2015 5:15:23 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

Hadithi mauquuf, nazo si za kutolea dalili, na kwetu sisi Ibn Abbas anapotaja mfano wa ngano hizi huwa anataja kwa njia ya kumponda Kaabul Akhbar kisha wapokezi baada yake wanadhani kuwa Ibn Abbas anaamini hivyo! Na dalili ya hilo ni kuwa Ibn Abbas amepokea kwa sanad sahih - kama ilivyotangulia - kwamba Kursii maana yake ni elimu ya Mwenyezi Mungu. Kisha nini maana ya Kursii ni mahali pa kuweka miguu na makusudio ya sifa hizi? Haina maana yoyote isipokuwa maana yake ni kuwa Mwenyezi Mungu ameweka miguu yake juu ya Kursii iliyoko mbele ya Arshi ambayo yeye ameikalia na huku ameweka miguu yake kwenye Kursii (kiti)!! Mwenyezi Mungu ametakasika na hayo kabisa na huu ni upotofu wa wazi kinyume na imani ya kiislamu ambayo inasema kuwa: “Mwenyezi Mungu hafanani na kitu chochote.” Na “Hakufanana na yeyote.” Na ikiwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ana miguu miwili na ameiweka kwenye kiti kama anavyoweka na kuinyoosha mwanadamu miguu Yake juu ya kiti basi atakuwa na umbile la kimwanadamu si kwa sifa pekee kama kusikia, kuona bali itakuwa ya kimaumbo. Na atakapokuwa na miguu miwili, uso, macho mawili, vidole kiganja na vinginevyo kama wanavyotaja basi huo utakuwa ni mwili. Vyovyote watakavyojaribu kufanya hivyo lakini Mwenyezi Mungu ameepukana na uzushi na uongo wao, ametakasika kabisa! Na la ajabu ni kuwa baadhi ya wanafalsafa wa kisasa pia wanasema hivyo kwa kuwa hawana akili, na wananukuu kutoka kwa wenye vitabu vinavyoitwa vya Sunnah. Wamepokea tamko hili ovu kina Daramiy katika Al Raddi alaBashar al mursy Uk: 71,73,74. Na Abdallah bin Ahmad katika kitabu chake Sunnah, na Ibn Abu Shaybah katika Kitabul arshi na Ibn Khuzaymah katika Tawhid, na Ibn Abu Hatim katika tafsiri yake na Al Harawiy katika Al Arbaiin na wengineo. 69

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 69

10/20/2015 5:15:23 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

Na jambo lenye hizaya zaidi ni waliyoyanukuu baadhi ya masalafi ambao walikuwa wakisema juu ya Hadithi hii munkar ambayo haina hoja kama ilivyotajwa katika Tarikh ya Ibn Muin, na riwaya ya Ad-Duwriy (3:520): “Nimemsikia Yahya akisema: “Nimeshuhudia Zakariyya bin Adiyy akimuuliza Wakii, akasema: “Ewe Abu Sufiyan, wasemaje juu ya Hadithi hizi?112 Yaani kama vile Hadithi za Kursii na mfano wake?” Wakii akasema: “Tuliwapata kina Ismail bin Abu Khalid na Sufiyan, na Musaar wakizitaja na wala hawakuzifafanua.”113 Yaani wanaeleza udhahiri wake tu ambao wanaueleza kuwa ukiisoma ndiyo umesoma maelezo yake.”!! Mjadala wa mwana lugha Abu Mansur Al Azhariy Mimi nionavyo ni kuwa Mansur Al Azhariy mwana lugha hutumia kipaji chake cha lugha kwa kubuni kaida za kilugha zisizo na misingi ili kuunga mkono madhehebu ya wenye kumfanya Mwenyezi Mungu ana umbo. Imekuja katika kitabu Lisanul Arab (6:194): “Amesema Abu Mansur: ‘Ni sahihi kutoka kwa Ibn Abbas katika Kursii, aliyopokea Ammar Duhniy kutoka kwa Muslim Al Batin kutoka kwa Said bin Jubayr kutoka kwa Ibn Abbas yeye amesema: Kursii ni mahali pa kuweka miguu miwili, ama Arshi haikadiriki.’ Akasema: “Na riwaya hii wameafikiana wanavyuoni juu ya usahihi wake.’ Akasema: ‘Na anayepokea kuwa Kursii maana yake ni elimu huyo amekosa.”’ Nami nasema: Hii ni kichekesho hasa! Watu wa lugha wajiingize katika maana za kisharia, hebu atuambie wapi katika maana ya   Angalia vipi wanavyozingatia hii kuwa ni katika jumla ya Hadithi.   Hii ikithibiti kwa Wakii au kwa mwengine ni yenye kukataliwa. Hii inaonyesha kwetu kuwa hawana akili, wamekosa utambuzi mpaka wanashindwa kutofautisha kati ya Hadithi na Athar batili, na kati ya inayokubaliwa katika akida na isiyokubaliwa. Maneno kama haya hayana thamani, bali kwetu sisi ni makosa yenye kukataliwa na hasa ni kuwa maneno yao sio hoja za kisheria.

112 113

70

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 70

10/20/2015 5:15:23 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

lugha inayosema Kursii maana yake ni mahali pa kuweka miguu? Hii ipo kwenye lugha? Jee hii iko kwa Waarabu? Kama wanavyuoni waliafikiana juu ya hilo waliafikiana wapi? Je waliafikiana kuwa Kursii ni mahali pa kuweka miguu Mola Mtukufu? Katika hili Abu Mansur na Ibn Mandhur wanapingwa. Na Ibn Jarir ni katika masalafi, amenukuu taawili ya Kursy kwa maana ya elimu kutoka kwa Ibn Abbas na akasema: “Dhahir ya Qur’ani yaonyesha hilo.” Na kuwa elimu ni moja katika maana za Kursii katika lugha ni wazi, licha ya Abu Mansur Al Azhariy na Ibn Mandhur wanaokosea na kubuni kaida kujifanya hawajui! Na anadai kuwa kutazama (nadhar) inapofuatiwa na (ilaa) maana yake ni kutazama kwa macho114na maneno ya lugha ya kiarabu yanakanusha hilo kama nilivyobainisha katika kitabu Ar-Ruuya.115 Na Azhariy alikuwa akiishi na Abu Ismail Al Harwiy, hao walikuwa katika zama moja. Alikuwa Abu Ismail pia akinukuu ngano hizo kutoka kwake! Al Azhariy pia alinukuu kutoka kwa Ibnul Arabiy kwamba kulingana si kutawala kama utakavyoona katika kitabu Al Uluwwu, nasu namba 454, pia angalia alivyonukuu Dhahabiy katika al-Uluwwu nasu namba 524 kutoka kwa Al Azhariy katika hilo. Tanbihi muhimu: Nilitaja katika kitabu Sahih Sharhul Aqida Twahawiyyah kwamba yapasa kutanabahi kwenye maswala nyeti yanayofungamana na maudhui ya kutoa maana ya neno kutoka kwenye kamusi za kilugha, nayo ni: Kwamba mara nyingi watunzi huingiza katika maana za kilugha maana za kisheria, au maoni ya watu binafsi yasiyo na uhusiano wowote na maudhui ya kilugha,   Kauli ya Abu Mansur katika kitabu al-Lisan (5:217) “Unaposema ..umeangalia haiwi ila kwa macho.” Haya ni maneno batili kama yale maneno ya Ibnul Arabi katika Aya ya istiwaa kwamba haijuzu kuifasiri kwa maana ya kutawala! Zote hizo zinakataliwa. 115   Angalia katika sherehe ya Diwanun-Nabighah chapa ya Daru Maktabul Hayaat, Beirut. Uk. 29. 114

71

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 71

10/20/2015 5:15:23 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

ndipo baadhi ya watu hudhani kuwa kwa kurejelea vitabu vya lugha kama Lisanul Arab au Tajul Aruus Sharhul Qaamuus, watapata maana ya maneno hayo yaliyothibiti kwa Waarabu, na hii si sahihi, kwani kutoa maana ya neno kutoka kwenye kamusi hizo za lugha kwahitajia mtafiti awe ni mwenye kulifahamu neno hilo na kuifahamu kadhia ndio asichanganye mambo. Mfano wa kuingiza hivyo ni: “Kwamba sirat ni daraja liko juu ya moto wa Jahannam nayo ni nyembamba kushinda unywele na ni mkali kushinda upanga.” Maana ya sirat kwa Zubaydiy - kwa mfano - alivyoeleza katika kitabu Tajul Aruus, pamoja na kuwa maana haya ni kwa mujibu wa baadhi ya Waislamu na si wote, nayo ni maana ya kisheria kwa baaadhi ya makundi ya Kiislamu ambapo si maarufu katika lugha ya kiarabu wala hakuna uhusiano nayo. Na hasa wakati wa kutafiti neno sirat katika kiarabu na wanakusudia nini wao Waarabu! Na la kuzinduka hapa ni kuwa hawa wenye itikadi ya kumfanya Mungu ana umbo wanawaweka mbali wanafuzi wasirejee vitabu kama vile Al Mufradaat cha Imam Al Isfahaniy ambacho ni kitabu kizuri sana cha lugha kinampa mtafiti upeo wa kulijua neno kwa maana zake nyingi zilizotajwa katika Qur’ani ili abainishe hakika yake ya maana ya kilugha. Na kudhihirisha ibara zake kwa uwazi zaidi baina ya maana za kilugha na istilahia za kisheria kwa watu fulani au kwa watu wote wa vikundi vya kiislamu, kitabu chake hicho kinachukuliwa kuwa ni miongoni mwa marejeo muhimu sana ya kilugha kwa ufafanuzi wake. Kuna kauli ya tatu inayofafanua Kusrii kwa maana ya uwezo. Amenukuu Qurtubiy na Ibn Taymiyya ameegemea huko, nayo ni hii:

72

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 72

10/20/2015 5:15:23 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

Amesema Qartubiy: katika Tafsiri yake (3:277): “Imesemwa kuwa Kursii ni kudra ya Mwenyezi Mungu inayoshikamana na mbingu na ardhi kama vile ukisema, hebu ufanyie ukuta huu uwe na kiti, yaani cha kutegemea na hii ni karibu na kauli ya Ibn Abbas katika kufasiri kauli yake Mwenyezi Mungu: “Kursii yake imeenea……..” Al Bayhaqiy amesema: “Tumepokea kutoka kwa Ibn Masud na Said bin Jubayr kutoka kwa Ibn Abbas katika kauli yake Mwenyezi Mungu: “Kursii yake imeenea..” Al Bayhaqiy amesema: “Tumepokea kutoka kwa Ibn Masud na Said bin Jubayr kutoka kwa Ibn Abbas katika kauli yake Mwenyezi Mungu: “Kursii yake imeenea..” akasema, ni elimu yake. Ameelekea kwenye maana hii Ibn Taymiyya Al Harraniy kwa kuitia shadda herufi ya raa katika Majmuul Fatawa (6:584) na akaitegemea116 ambapo alisema: “Imenukuliwa na baadhi yao kuwa Kursii, ni elimu ya Mwenyezi Mungu nayo ni kauli dhaifu kwani elimu ya Mwenyezi Mungu imeenea kila kitu kama alivyosema katika Qur’ani: “Ewe Mola Wetu, umeenea juu ya kila kitu kwa rehma na elimu…” na Mwenyezzi Mungu anajijua Yeye Mwenyewe na anajua yaliyokuwa na ambayo hayakuwa, lau itaambiwa kuwa elimu Yake imeenea mbingu na ardhi, maana hii haitalingana na hasa vile Mwenyezi Mungu amesema: “Wala haiwi uzito Kwake kuzihifadhi..” na hii inanasibiana na kudra Yake na si elimu. Yaani maana inayonasibiana katika maana ya Kursii ni kudra yake na si elimu yake.

Huenda alimpinga katika mahali pengine kwani yeye ni mwenye kujipinga katika rai na fikra zake, mara nyingine anathibitisha na mara nyingine anapinga!

116

73

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 73

10/20/2015 5:15:23 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

MWISHO

K

wa haya yote inatubainikia wazi kwamba riwaya ya KURSII kuwa ni mahali pa kuweka miguu kwa Mwenyezi Mungu si sahihi; na ile iliyothibiti kutoka kwa Ibn Abbas na Said bin Jubayr ya maana ya Kursii ni kwa maana ya elimu, na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kuwafiki. Kazi hii nimeimaliza mnamo usiku wa Jumamosi tarehe kumi na tatu mfungo Mosi mwaka 1425, sawia na 26/11/2004 Rehema na amani ziwaendee Bwana wetu Muhammad na Aali zake watoharifu kila wakati, Alhamdu Lilahi Rabbil Alamin.

74

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 74

10/20/2015 5:15:23 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

Orodha Ya Vitabu Vilivyo Chapishwa Na Al-Itrah Foundation 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24. 25. 26. 27. 28. 29. 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38.

Qur’an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu Ya Kwanza Mpaka Thelathini Uharamisho Wa Riba Uharamisho Wa Uwongo Juzuu Ya Kwanza Uharamisho Wa Uwongo Juzuu Ya Pili Hekaya Za Bahlul Muhanga Wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo Iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab Vazi Bora Ukweli Wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu Imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini Katika Swala Misingi Ya Maarifa Kanuni Za Ndoa Na Maadili Ya Familia Bilal Wa Afrika Abudharr Usahihi Wa Historia Ya Uislamu Na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur’an Na Hadithi Elimu Ya Nafsi Yajue Madhehebu Ya Shia Ukusanyaji Na Uhifadhi Wa Qur’an Tukufu Al-Wahda Ponyo Kutoka Katika Qur’an Uislamu Mfumo Kamili Wa Maisha Ya Kijamii Mashukio Ya Akhera Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu Kwa Mujibu Wa Kitabu Na Sunna. Haki Za Wanawake Katika Uislamu Mwenyezi Mungu Na Sifa Zake Kumswalia Mtume (S) Nafasi Za Ahlul Bayt (A.S) Adhana 75

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 75

10/20/2015 5:15:23 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

39. 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52. 53. 54. 55. 56. 57. 58. 59. 60. 61. 62. 63. 64. 65. 66. 67. 68. 69. 70. 71. 72. 73. 74. 75. 76. 77. 78. 79. 80.

Upendo Katika Ukristo Na Uislamu Tiba Ya Maradhi Ya Kimaadili Maana Ya Laana Na Kutukana Katika Qur’ani Tukufu Kupaka Juu Ya Khofu Kukusanya Swala Mbili Bismillah Ni Sehemu Ya Qur’ani Na Husomwa Kwa Jahara Kuwaongoza Vijana Wa Kizazi Kipya Kusujudu Juu Ya Udongo Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (S) Tarawehe Malumbano Baina Ya Sunni Na Shia Kupunguza Swala Safarini Kufungua Safarini Umaasumu Wa Manabii Qur’an Inatoa Changamoto As-Salaatu Khayrun Mina -’N Nawm Uadilifu Wa Masahaba Dua E Kumayl Sauti Ya Uadilifu Wa Binadamu Umaasumu Wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake Umaasumu Wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata Umaasumu Wa Mitume - Umaasumu Wa Mtume Muhammad (S) Nahju’l-Balaghah - Juzuu Ya Kwanza Nahju’l-Balaghah - Juzuu Ya Pili Kuzuru Makaburi Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu Ya Kwanza Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu Ya Pili Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu Ya Tatu Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu Ya Nne Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu Ya Tano Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu Ya Sita Tujifunze Misingi Ya Dini Sala Ni Nguzo Ya Dini Mikesha Ya Peshawar Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu Ubora Wa Imam ‘Ali Juu Ya Maswahaba Na Ushia Ndio Njia Iliyonyooka Hukumu Za Kifikihi Zinazowahusu Wanawake Liqaa-U-Llaah Muhammad (S) Mtume Wa Allah Amani Na Jihadi Katika Uislamu Uislamu Ulienea Vipi? Uadilifu, Amani Na Mtume Muhammad (S) 76

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 76

10/20/2015 5:15:24 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

81. Mitala Na Ndoa Za Mtume Muhammad (S) 82. Urejeo (Al-Raja’a ) 83. Mazingira 84. Utokezo (Al - Badau) 85. Hukumu Ya Kujenga Juu Ya Makaburi 86. Swala Ya Maiti Na Kumlilia Maiti 87. Uislamu Na Uwingi Wa Dini 88. Mtoto Mwema 89. Adabu Za Sokoni 90. Johari Za Hekima Kwa Vijana 91. Maalimul Madrasatain Sehemu Ya Kwanza 92. Maalimul Madrasatain Sehemu Ya Pili 93. Maalimul Madrasatain Sehemu Ya Tatu 94. Tawasali 95. Imam Mahdi Katika Usunni Na Ushia 96. Hukumu Za Mgonjwa 97. Sadaka Yenye Kuendelea 98. Msahafu Wa Imam Ali 99. Ngano Ya Kwamba Qur’ani Imebadilishwa 100. Idil Ghadiri 101. Kusoma Sura Zenye Sijda Ya Wajibu 102. Hukumu Zinazomuhusu Mkuu Wa Kazi Na Mfanyakazi 103. Huduma ya Afya katika Uislamu 104. Sunan an-Nabii 105. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) 106. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) 107. Shahiid Mfiadini 108. Kumsalia Nabii (s.a.w) 109. Ujumbe -Sehemu ya Kwanza 110. Ujumbe - Sehemu ya Pili 111. Ujumbe - Sehemu ya Tatu 112. Ujumbe - Sehemu ya Nne 113. Mariamu, yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu 114. Hadithi ya Thaqalain 115. Ndoa ya Mutaa 116. Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza 117. Ukweli uliopotea sehemu ya Pili 118. Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu 119. Ukweli uliopotea sehemu ya Nne 120. Ukweli uliopotea sehemu ya Tano 121. Mkutano wa Maulamaa wa Baghdad 122. Safari ya kuifuata Nuru 77

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 77

10/20/2015 5:15:24 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

123. Fatima al-Zahra 124. Myahudi wa Kimataifa 125. Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi 126. Visa vya kweli sehemu ya Kwanza 127. Visa vya kweli sehemu ya Pili 128. Elimu ya Ghaibu ya Maimamu 129. Mwanadamu na Mustakabali wake 130. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) 131. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) 132. Khairul Bariyyah 133. Uislamu na mafunzo ya kimalezi 134. Vijana ni Hazina ya Uislamu 135. yafaayo kijamii 136. Tabaruku 137. Taqiyya 138. Vikao vya furaha 139. Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 140. Visa vya wachamungu 141. Falsafa ya Dini 142. Azadari-Kuhuzunika na Kuomboleza 143. Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah 144. Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu 145. Kuonekana kwa Allah 146. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) 147. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) 148. Ndugu na Jirani 149. Ushia ndani ya Usunni 150. Maswali na Majibu 151. Mafunzo ya hukumu za ibada 152. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1 153. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2 154. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 155. Abu Huraira 156. Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. 157. Mazingatio kutoka katika Qur’an - Sehemu ya Kwanza 158. Mazingatio kutoka kaitka Qur’an - Sehemu ya Pili 159. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza 160. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili 161. Qur’ani Tukufu – Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili 162. Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) 163. Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani 164. Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu 78

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 78

10/20/2015 5:15:24 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

165. Uislamu Safi 166. Majlisi za Imam Husein Majumbani 167. Je, Kufunga Mikono 168. Uislam wa Shia 169. Amali za Makka 170. Amali za Madina 171. Asili ya Madhehebu katika Uislamu 172. Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi 173. Ukweli uliofichika katika neno la Allah 174. Uislamu na Mifumo ya Uchumi 175. Umoja wa Kiislamu na Furaha 176. Mas’ala ya Kifiqhi 177. Jifunze kusoma Qur’ani 178. As-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah 179. Hayya ‘Alaa Khayri’l-’Amal Katika Adhana 180. Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura 181. Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na Ramadhani) 182. Uadilifu katika Uislamu 183. Mahdi katika Sunna 184. Maswali ya Uchunguzi Kuhusu Uislam 185. Kazi na Bidii ni njia ya maendeleo 186. Abu Talib – Jabali Imara la Imani 187. Ujenzi na Utakaso wa Nafsi 188. Vijana na Matarajio ya Baadaye 189. Usalafi – Historia yake, maana yake na lengo lake 190. Ushia – Hoja na Majibu 191. Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) 192. Maombolezo – Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) 193. Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu 194. Takwa 195. Upotoshaji dhahiri katika Turathi (Hazina) ya Kiislamu 196. Amirul Muuminina (‘as) na Makhalifa 197. Uongozi na Utawala katika Mwenendo wa Imam ‘Ali (‘a) 198. Kuvunja hoja iliyotumika kutetea Uimamu wa AbuBakr 199. Adabu za vikao na mazungumzo 200. Hija ya Kuaga 201. Uwazi baina ya Maslahi na Vikwazo 202. Fadhila za watukufu watano katika Sahih Sita 203. Mdahalo baina ya Mwanachuoni wa Kisunni na Mwanachuoni wa Kishia (Al-Muraja’aat) 204. Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (as) 205. Mjadala wa Kiitikadi 79

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 79

10/20/2015 5:15:24 PM


KAULI SAHIHI ZAIDI KATIKA KUFAFANUA HADITHI

206. Mtazamo kuhusu msuguano wa Kimadhehebu 207. Nchi na Uraia – Haki na wajibu kwa Taifa 208. Mtazamo wa Ibn Taymiyyah juu ya Imam Ali (as) 209. Uongozi wa Kidini – Maelekezo na Utekelezaji wa Kijamii 210. Maadili ya Ashura 211. Mshumaa – Shahidi na Kifo cha Kishahidi 212. Mizani ya Hekima – Hadithi za Ahlul Bait (as) – Sehemu ya Kwanza 213. Imam Ali na Mambo ya Umma 214. Imam Ali na Mfumo wa Usawa 215. Mwanamke na Sharia 216. Mfumo wa Wilaya 217. Vipi Tutaishinda Hofu? 218. Kumswalia Mtume ni Ufunguo wa Utatuzi wa Matatizo 219. Mahali na Mali za Umma 220. Nahjul-Balagha – Majmua ya Khutba, Amri, Barua, Risala, Mawaidha na Semi za Amirul-Muuminin Ali bin Abu Talib (a.s.) 221. Mukhtar – Shujaa aliyelipiza kisasi dhidi ya wauaji wa Imam Husein (as) hapo Karbala 222. Uimamu na Tamko la Kutawazwa 223. Imam Husain ni Mfumo wa Marekebisho na Mageuzi 224. Saada Kamili – Kitabu cha Kiada cha Maadili 225. Maeneo ya Umma na Mali Zake 226. Imam Hasan na Mfumo wa Kujenga Jamii 227. Adhana ni Ndoto au ni Wahyi? Kopi Nne Zifuatazo Zimetafsiriwa Kwa Lugha ­Kinyarwanda 1. 2. 3. 4.

Amateka Na Aba’Khalifa Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya Shiya na Hadithi Orodha Ya Vitabu Vilivyo Chapishwa Na AL-Itrah ­Foundation Kwa Lugha Ya Kifaransa

1.

Livre Islamique

80

14_15_ Kauli Sahihi Zaidi Katika_20_Oct_2015.indd 80

10/20/2015 5:15:24 PM


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.