Kusheherekea maulidi ya mtume

Page 1

al-Ihtifalu Bi-Dhikrii Maulidi ‘n-Nabiyy

KUSHEHEREKEA MAULIDI YA MTUME (Sallallahu ‘Alayhi Wa-aalihi Wa-sallam)

Kimeandikwa na: Seyyid Abdur Rahim Al-Musawi

Kimetarjumiwa na: Ustadh Abdallah Muhammad


Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 - 427 - 51 - 9 Kimeandikwa na: Seyyid Abdul Rahim Al-Musawi Kimetarjumiwa na: Ustadh Abdallah Muhammad Kimehaririwa na: Sheikh Pingili Kupangwa katika Kompyuta na: Ukhti Pili Rajab. Toleo la kwanza: Februari, 2008 Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation P.O. Box 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu:+255 22 2110640 Simu/Fax: +255 22 2127555

Email: alitrah@raha.com Website: www.alitrah.org Online: www.alitrah.info


YALIYOMO Kusheherekea Maulidi.......................................................................2 Je kusherehekea Maulidi ya Mtume (s.a.w.w.) ni Bidaa au ni katika mambo ya dini...............................................................................4 Kupaswa kumtukuza Mtume (s.a.w.w.) akiwa hai au amekufa.........6 Siku aliyozaliwa Mtume ni katika siku za Mwenyeezi Mungu.......9 Tukio la kihistoria kwa siku ya mazazi ya Mtume (s.a.w.w)..........12 Kusherehekewa Maulidi ya Mtume (s.a.w.w) mbele ya viongozi na wanasiasa.........................................................................................13 Hukmu za Maulidi na mambo yake Mahsusi..................................14 Ibn Taymiyya na kaswida kwenye Maulidi.....................................15 Mjadala wanaosema kuwa kushereheka Maulidi ni haramu..........16


NENO LA MCHAPIZHAJI Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kiitwacho: kilichoandikwa na: sisi tumekiita: “Ksherehekea Maulid” Kuna hitilafu ya maoni miongi mwa baadi ya Waislamu kuhusu kuswihi kusomwa maulidi au kushherekea siku ya kuzaliwa Mtukufu Mtume (saw). Baadhi wanasema haiswihi kusomwa maulid na baadhi wanasema inaswihi na ni jambo zuri sana. Mwandishi wa kitabu hiki anatoa mwanga juu ya suala hili kwa kutumia Qur’an Tukufu, Sunna, hoja, elimu na mantiki: Kufanya hafla ya kusherehekea maulidi ya Mtume (S.a.w.w..) ni jambo lililozoeleka mingoni mwa waislamu kwa karne nyingi sana, na kumbukumbu hii bado ingalipo nyoyoni mwa waislamu wote ambapo hafla hizo hufanywa misikitini na majumbani katika miji mbalimbali ya kiislamu ili kuitukuza siku hii tukufu, wao katika kufanya hilo ni kama watu wengine wanaoheshimu mambo yao matukufu, siku na kumbukumbu zao adhimu. Vilevile kinachokusudiwa katika hafla hizi, pamoja na kuwa ni furaha na kumshukuru Mwenyezi Mungu, lakini vilevile ni kuleta mwamko na kumbukumbu, Kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote. Kutokana na ukweli huu, Taasisi yetu ya 'Al-Itrah Foundation' imeona ikitoe kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili, kwa madhumuni yake yale yale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili, ili kuongeza ujuzi wao katika masu-


ala ya dini na ya kijamii. Tunamshukuru ndugu yetu, Hemedi Lubumba Selemani (Lipumba) kwa kukubali jukumu hili la kukifanyia tarjuma kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki.

Mchapishaji: Al-Itrah Foundation S. L. P. 19701 Dar-es-Salaam, Tanzania.


F



Kusherehekea Maulidi ya Mtume s.a.w.w.

KUSHEREHEKEA MAULIDI Kufanya hafla ya kusherehekea maulidi ya Mtume (S.A.W.) ni jambo lililozoeleka miongoni mwa waislamu kwa karne nyingi sana, na kumbukumbu hii bado ingalipo nyoyoni mwa waislamu wote ambapo hafla hizo hufanywa misikitini na majumbani katika miji mbalimbali ya kiislamu ili kuidumisha siku hii tukufu mfano wao katika kufanya hilo ni kama wa watu wengine wanaoheshimu mambo yao matukufu, na wanazitukuza siku zake kubwa na kumbukumbu zao adhimu. Vilevile kinachokusudiwa katika hafla hizi, pamoja na kuwa ni furaha na kumshukuru Mwenyezi Mungu, lakini vilevile ni kuleta mwamko na wa kumbukumbu. Licha ya kudhihiri kufaa kwa kusherehekea Maulidi,ya Nabii, lakini kuna baadhi ya watu wanaotafuta mamabo yanayohalalisha kuzuia kuifanyia hafla siku hii wakitegemeza kauli zao kwenye fahamu iliyokosewa ya maana ya bidaa, fahamu hii imefanya yaharamishwe mengi yaliyo halali, kufanywa wakitoa sababu kwamba mamabo haya hayakutajwa na nassi mahsusi za kisharia. Hapa tutayaangalia mas’ala ya kusherehekea Maulidi, na tuone kwa umbali gani uhalali wake, kisha tutajadili juu ya maoni yanayodai kuwa ni haramu ndani ya mambo kadhaa: Tukio tukufu linaufanya wakati uwe mtukufu. Je zile siku na saa zilizotokea mamabno matukufu ya Mwenyezi Mungu ni tukufu; tukio humo laipa siku thamani, hivo zama hupata utakatifu wake kutokana na tukio. Kama ambavyo kheri na baraka ambayo Laylatul Qadri imepata, na siku za Ramadhani na usiku wake, au Idi ya Fitri na Adh-ha, 2


Kusherehekea Maulidi ya Mtume s.a.w.w. au siku alipotumwa Mtume (S.A.W.)? Jibu ni kuwa, lau sisi tutaaangalia kwa makini kwenye riwaya zenye maana hii, itatuthibitikia kuwa matukio makuu na yenye baraka yanaeneza kitu cha ubora na utukufu wake juu ya nyakati nyingi. Kwa mfano imekuja Hadith juu ya fadhila za siku ya Ijumaa katika Sahih Muslim isemayo: “Mwenyezi Mungu alimuumba Adam siku ya Ijumaa na akamuingiza Peponi siku ya Ijumaa.”1 Na vile vile katika ubora wa mwezi wa Ramadhani, amesema Mwenyezi Mungu mtukufu: “Mwezi wa Ramadhani ndio mwezi ulioteremshiwa ndani yake Qur’an ukiwa ni uongofu kwa watu na ushahidi ulio wazi wa uongofu na ni kipambanuzi..”2 Pia baraka ya usiku wa Laylatul Qadri ambapo amesema Mwenyezi Mungu: “Hakika tumeiteremsha Qur’an katika usiku wa heshima. Ni nini kitakujulisha usiku wa heshima?..3 Kuendelea baraka katika siku hizi kumekuja ikiwa ni natija ya matukio muhimu ya Mwenyezi Mugu yaliyotokea kama kushuka Qur’an kwenye siku hizo. Ikiwa msingi wa kuzitukuza siku hizi watokana na matukio ya Mwenyezi Mungu yalyobarikiwa kwa nini isiwe siku aliyozaliwa Mtume (s.a.w.) ni siku iliyobarikiwa inayostahiki kutukuzwa nakusherehekewa kwa mtazamo huu? Hii inahthibitisha kuhusushwa mwa minasaba yenye nassi ambayo waislamu waliisherehekea waislamu katika enzi za kuletwa sharia, kama kusherehekea Idi za Fitri na Dhuha, au siku ya Ghadir auya Arafa,

1 Sahih Muslim Juz 3 Uk. 6 Kitabu Swalaa. Mlango: Ubora wa siku ya Ijumaa 2 Baqara: 185 3 Al Qadri: 1-3 3


Kusherehekea Maulidi ya Mtume s.a.w.w. Kuna vitendo vilivopetuka mpaka katika kutukuza minasaba hii na kukabiliwa na misimamo iliyojaribu kuondoa sherehe za minasaba yoyote inayofungamana na Mtume na Ahlu bayti wake, wakidai kwamba kwa kutukuza huko ni bidaa inayozushwa katika dini ambayo haifai kuinyamazia wakawa wanawaogofya waislamu kwa kuwatia tashwishi, wasisherehekee Maulidi na wakitoa wito wa tawhid ili chini ya bendera yake wafute kila kitu kinachofungamana na vipenzi vya Mtume na Ahlu bayt wake ambao wao ndio wenye uongofu ili waja wamjue Mola wao hasa.

Je kusherehekea Maulidi ya Mtume (S.A.W.) ni bidaa au ni katika mambo ya dini? Ili tujue kwanza ni wakati gani jambo linakuwa ni lenye kujuzu katika dini, tunasema hivi: Jambo huwa limejuzu au ni katika mambo ya dini pale inapokuja nassi juu ya jambo hilo, kama vile kusherehekea Idi za Fitri na Dhuha na kukusanyika siku ya Arafa haya hayana shaka. Wakati mwingine jambo huwa nikatika mambo ya dini au ni lenye kujuzu inapotokea maelezo ya kiujumla na hapo huachwa hiyari? ya kufuata njia ya kufanyaanavyotaka na na kwa jinsi gani, katika kulitekeleza, kwa sharti tu asiingie katika yaliyo haramu, mathalan: Kwanza: Sharia imeweka kuwaelimisha watoto ni lazima bila shaka hili kiujumla ni amri lakini njia zake zinabadilika kulingana na kuibadilika nyakati, kama vile zamani kuandika ilikuwa kalamu ya muanzi au nyoya la ndege vikitumika kuandikia lakini sasa mbinu za kuandikia na kusoma zimeendelea sana kiasi kwamba nyenzo za kisasa zinatumika kama vile tarakilishi (kompyuta) kanda za kaseti n.k. Kwa hivyo kwa mifano hii tunaona kwamba sharia imeamuru kusoma kiujumla, lakini njia na mbinu za kujifunzia ameachiwa mtu anayewajibika na hilo. Pili: Maswahaba, kama inavyosemekana, walikusanya Aya za Qur’a mbali mbali katikamsahafu mmoja, na hata mmoja wao hakusema kuwa hii ni 4


Kusherehekea Maulidi ya Mtume s.a.w.w. bidaa na hii ni kwa sababu kazi yao ilikuwa ni Mwenyezi Mungu (S.W.T.) aliposema:

ni kufuata nenola

“Hakika sisi ndio tulioiteremsha Qur’an na sisi ndio wenye kuihifadhi 15:9 Kwa hivyo kazi yao kwa hakika ilikuwa ni kuthibitisha kazi ya Qur’an na Sunna na kwa ajili hiyo ndipo waislamu wakawaitilia umuhimu sana Qur’an katika kuiandika na kuipanga, kuweka irabu maneno yake sentensi zake, kuzihesabu Aya zake na hatimaye kuichapisha na kuigawanya, pia kuwaheshimu walioihifadhi, kuwapa zawadi na kufanya hafla za Qur’an na mengineyo ambayo yote ni ya kuihifadhi. Tatu: Kuuhifadhi Uislamu dhidi ya maadui ambapo msingi thabiti uko kwenye Qur’an, kama alivyosema Mwenyezi Mungu (S.W.T.):

“Na waandalieni nguvu muwezavyo...8:60 Ama namna ya kujilinda, aina ya silaha, kujiunga na jeshi, hayo yote ni ufuatiliaji wa msingi huu, na uislamu unaangalia asili na unaacha aina kulingana na hali. Huu ndio msingi unaotofutisha kati ya bidaa, kufuatiza, kuvumbua na kufuata, hebu angalia baadhi ya maneno ya wanavyuoni juu ya maudhui ya utafiti: 1. Ibn Rajab amesema: “Pale Mtume aliposema: “Jiepusheni na uzushi (bidaa) wa mambo, kwani kila bidaa ni upotevu..” hii ilikuwa ni kuwatahadharisha umma juu ya kufuata mambo yaliyozushwa na akongeza kwa msisitizo kauli yake, “Kila bidaa ni upotevu..”Na makusudio ya bidaa ni kila jambo lililozushwa lisilo na misingi ya kisheria ya kulitambulisha, ama lile ambalo lina misingi hilo si bidaa, japokuwa kilugha ni bidaa. Na katika Sahih Muslim imepokewa kutoka kwa Jabir kuwa Mtume 5


Kusherehekea Maulidi ya Mtume s.a.w.w. (s.a.w.) alikuwa akisema: “Hakika bora ya maneno ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na bora ya uongofu ni wa Muhammad, na yaliyo maovu ni yale ya uzushi, na kila uzushi ni upotevu..”; na ama neno lake ‘kila bidaa ni opotofu..’ ni katika maneno ya kiujumla hakitolewi hapo chochote, nayo ni asli kubwa katika misingi ya dini ni kama vile alivyosema yeye (s.a.w.): “Mwenye kuzusha katika jambo letu hili lisilokuwamo basi litapingwa.” Kwa hivyo kila mwenye kuzusha jambo katika dini lisilo na msingi basi atarudishiwa nalo mwenyewe hilo ni upotevu na dini imeepukana nalo.”4 2. Na amesema Ibn Hajar katika sherhe yake: “Neno lake Mtume (s.a.w.) ‘hakika bora ya maneno ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu..’ na ‘yaliyozushwa’ makusudio ya yaliyozushwa ni yale yasiyo na misingi katika sharia na katika sharia huitwa ‘bidaa.’ Na lililokuwa na misingi katika sharia hilo si bidaa kwa hivyo kila jambo lililowekwa bila ya mfano huitwa bidaa liwe ni zuri au si zuri.”5 Lakini Tunaporejea kwenye Qur’an na Hadith tukufu tutapata kwamba kuna msingi muhimu katika dini tunapata kwamba kuna msingi muhimu uliokuja katika dini juu ya haki ya Mtume (s.a.w.), nao ni ulazima wa kumtukuza akiwa yu hai au amekufa, na msingi uu muislamu hawezi kuukanusha; ama jinsi ya kuufuata msingi huu hili ameachiwa muislamu bora tu asiingilie kwenye yaliyo haramu.

3) Kupaswa kumtukuza Mtume (s.a.w.) akiwa hai au amekufa Kuhimizwa juu ya kuitukuza shakhsiya ya Mtume na kumpenda kumetajwa ndani ya Qur’an tukufu katika Aya nyingi miongoni mwazo ni: 4 Jawaamiul-uluumi wal-hikam Uk. 223 5 Fat-hul Baari Juz 13 Uk. 353 Sherhe ya Hadith Na. 7277 6


Kusherehekea Maulidi ya Mtume s.a.w.w.

“…Basi wale waliomuamini yeye na kumtukuza na kumsaidia na wakaifuata nuru iliyoteremshwa pamoja naye, hao ndio weye kufaulu. 7:157 Wafasri wametaja kuwa makusudio ya kutukuza katika Aya hii sio tu kunusuru kwani limeambatanishwa neno wakamnusuru, kwa hivyo maana yake ni kutukuza na kuheshimu au kunusuru na kutukuza.6 Nyigine ni Aya:

“Enyi mlioamini! Msiinue sauti zenu kuliko sauti ya nabii, wala msiseme naye kwa sauti kubwa kama mnavyosemezana nyinyi kwa nyinyi, visije vitendo vyenu vikaharibika na hali hamtambui. Kwa hakika wale wanaoinamisha sauti zao mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu hao ndio Mwnyezi Mungu amezisafisha nyoyo zao kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu, watapata msamaha na malipo makubwa. 49: 2-3 Aya hizi Qur’an yaonyesha namna gani adadabu inayofaa kuichunga 6 Majmaul Bayan Juz. 4 Uk. 604 Tasirul Qur’anil adhim ya Ibn Kathir Juz 9 Uk. 265, Tafsir Al-Mizan Juz. 8 Uk. 296 7


Kusherehekea Maulidi ya Mtume s.a.w.w. wakati waislamu wanapoamiliana na Mtume (s.a.w.) akiwa ni Mtume wao na muongozi. 3.Kauli yake Mwenyezi Mungu:

“Msifanye kumwita Mtume baina yenu kama kuitana nyinyi kwa nyinyi.”24: 63 Katika Aya hii kumekatazwa kumwita Mtume kwa jina lake kama waitwavyo watu wengine. Aya nyingine ni:

“Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanamtakia rehma Mtume, Enyi mlioamni! Mtakieni rehma na muombeeni amani...33 : 56 Katika Aya hii waislamu wameamrishwa wamtaje Mtume kwa dua na kumtakia rehma kwa kuwa yeye ana daraja kuu mbele ya Mwenyezi Mungu. Pia kumehimizwa kumpa heshima na kumpenda katika Hadith nyingi, k.v: 1. Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.) amesema: “Hatoamini mmoja wenu mpaka niwe mimi ni kipenzi zaidi kwake kuliko mali yake, watu wake wa nyumbani na watu wote.”7 7 Sahih Muslim Juz. 3 Uk. 275 na Juz 3 Uk. 183, pia katika Musnad ya Ahmad Juz 4 Uk. 183. Sunan al-kubra ya Nasai Juz. 6 Uk. 534 na katika Bukhari Juz. 1 Uk. 9 8


Kusherehekea Maulidi ya Mtume s.a.w.w. Pia imepokewa kwamba Umar bin Khatab alisema: “Ee Mtume wa Mwenyezi Mungu! Wewe ni kipenzi changu kuliko kila kitu isipokuwa nafsi yangu tu.” Mtume (s.a.w.) akasema: “Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu i mikononi mwake! Mpaka mimi niwe ni kipenzi zaid kuliko nafsi yako.” Umar akasema: “Wewe sasa ni kipenzi zaidi kuliko nafsi yangu.” Mtume akasema: “Sasa ee Umar?”8 Imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas, kutoka kwa Mtume (s.a.w.) Mtume alisema: “…wakanipenda kwa ajili ya kumpenda Mwenyezi Mungu, na wakawapenda ahlu bayt wangu kwa ajili ya kunipenda.”9 Kwa hivyo imethibiti kwa dalili za Qur’an na Hadith juu ya kumtukuza na kumpenda Mtume (s.a.w.) lakini sharia imewaachia waislamu jinsi na namna ya kufanya hivyo kulingana na inavyoafiiana na ada zao mbalimbali na hisia zao za mapenzi juu ya Mtume (s.a.w.) kwa sharti tu wasitende mambo ya haramu katika kufanya hivyo au wasiende kinyume na adabu za kiislamu zilizomo katika Qur’an na Hadith.

Siku aliyozaliwa Mtume ni katika siku za Mwenyezi Mungu Moja katika dalili za kisharia katika kufaa kusherehekea maulidi ni kauli yake Mwenyezi Mungu:

“Hakika tumemtuma Musa pamoja na miujiza yetu, (tukamwambia) uwatoe kaumu zako kutoka gizani na kuwapeleka kwenye nuru na uwakumbushe siku za Mwenyezi Mungu, hakika katika hilo kuna dalili kwa kila mwenye subira mwenye kushukuru...14:5 8 Kitabu: Sairatu bulghatul hubb wa shi’ir cha Said Hawiyy I Uk. 15 9 Sunan Tirmidhi Juz. 5 Uk. 622 na 3789 9


Kusherehekea Maulidi ya Mtume s.a.w.w. Hapo Mwenyezi Mungu anamtaka nabii Musa (a.s.) awakumbushe watu wake kuhusu siku za Mwenyezi Mungu, maana yake ni kwamba kuzikumbuka siu za Mwenyezi Mungu ni jambo linalotakiwa na linalopendwa na Mwenyezi Mungu, na si kwa watu wa nabii Musa pekee. Na makusudio ya siku si kwa muda pekee bali makusudio ni kukumbuka matukio makuu yaliyopita na yakaitwa siku kwa sababu siku ndipo matukio haya yalipotokea aidha yawe ni ya neema au ya mitihani na majaribu kwa sababu siku zakusanya aina zote mbili za matukio. Nayo ni uthibitisho wa mwenendo wa Mwenyezi Mungu katika jamii ya mwanaadamu kwa hivyo kuzikumbuka ni katika mambo ya muhimu ya Mtume……? Na kukumbusha na mawaidha hapa hayakuwa kwa jinsi watu walivyoafikiana, bali yametakiwa katika siku maalum za matukio yake. Na maana ya Aya ni kuwa, ee Mtume, wa Mungu wape mawaidha watu juu ya kuwapa habari njema na kuwatahadharisha, habari njema ni kuwatajia aliyowaneemesha Mwenyezi Mungu, wao na walikuwa kabla yao walioamini mitume waliopita katika siku zilizokuwa na matukio makuu kama yaliyotukia kwa Aad na Thamud na wengineo. Na siku za Mwenyezi Mungu kwa haki ya nabii Musa (a.s.) mitihani na majaribu na kuna siu za neema na ushindi.

ni siku za

Qura’n imetaja kuwa sababu ya kuzikumbuka siku hizi ni kwa kuwa zina mafunzo na dalili kwa kila mwenye subira na mwenye kushukuru.10 Hiyo 10 Kashaf cha Zamakhshari Jz. 2 Uk. 54 Tafsir Shaalabu Ju. 3 Uk. 375. Durrul manthur Juz. 4 Uk 132. Tafsirul kabir ya Fakhru Razi Juz 19 Uk 84. Ayaashi Juz. 6 Uk. 59. Majmaul Bayan Juz. 6 Uk. 59. Al Mizan ya Tabatabai Juz. 11 Uk. 18. Jamiul kabir Juz. 9 Uk. 342 10


Kusherehekea Maulidi ya Mtume s.a.w.w. yenyewe ni natija ya kupatikana watu wenye subira na wenye kushukuru nayo inafanya umma ufaulu na kuwafanya wawashinde maadui zao na kufuata sharia ya Mwenyezi Mungu barabara. Umma wa kiislamu katika historia yake umepitia kwenye matukio makubwa yenye mawaidha na mazingatio katika hayo kuna siku za neema, kuna za majaribu; na siku aliyozaliwa Mtume (s.a.w.) inachukuliwa kuwa ni siku yenye tukio kuu kwa waislau ni siku ambayo Mwenyezi Mungu amewaneemesha wao tu kwayo. Kwa hivyo kusheherekea kwake siku hiyo ni kama kuthibitisha yale Mwenyezi Mungu aliyowaneemesha waislamu na kufuatilia madhumuni ya Aya isemayo,

...na wakumbushe siku za Mwenyezi Mungu……14:5 Na siku ya kuzaliwa, kwa Mtume, huchukuliwa kuwa ni siku muhimu sana na yenye baraka Mwenyezi Mungu alimtolea salaam nabii wake Yahya siku aliyozaliwa kwa kumwambia:

“Ni amani iko juu yake, siku aliyozaliwa, na siku atakayokufa na siku atakayofufuliwa.19:15 Nabii Isa (a.s.) pia alijitolea salaam siku aliyozaliwa kwa kusema:

“Salaam juu yangu siku niliyozaliwa, siku nitakayokufa na siku nitakayofufuliwa.19:33 Na Mtume wetu Muhammad (s.a.w.) ambaye ndiye bora wa mitume hapana budi siku aliyozaliwa iwe ndiyo siku tukufu zaidi kuliko mitume wengine, na kuikumbuka kuwe ni kwa kuitukuza zaidi kuliko za wengine, kwani hiyo ni siku ambayo Mwenyezi Mungu amewaneemesha watu kwa 11


Kusherehekea Maulidi ya Mtume s.a.w.w. kuwapa mwisho wa mitume wote kabisa.

5) Tukio la kihistoria kwa siku ya mazazi ya Mtume (s.a.w.) Wanahistoria wanasema: “Kutukuzwa zaidi kwa Mtume (s.a.w.) kulizidi katika wa wachamungu kukawa ndio sababu ya kuadhimishwa maulidi mnamo mwaka 300 (A.H.)11 Yaani kwa maana hayo, sherehe ilifanywa kabla ya tarehe hii, hpo katika kipindi hicho ndipo ikabadilika sura ya jinsi ya kusherehekea kutoka kwenye mtu mmoja mmoja hadi kwenye watu wengi kwa pamoja, na iliyosababisha hilo ni wale wachamungu kutilia umuhimu jambo hilo. Na kwa ajili hiyo, imepokewa kutoka kwa Al- Kurji (aliyefariki 343 (A.H.), huyu alikuwa ni miongoni mwa wapaji nyongo dunia, wachamungu, yeye alikuwa hafungui ila siku za sikukuu za Idi mbili, na siku ya Maulidi ya Mtume (s.a.w.).12 Qastalani amesema: Waislamu wanaendelea kusherehekea mwezi aliozaliwa Mtume (s.a.w.) na kuandaa karamu, kutoa sadaka mbali mbali katika mikesha yake, wanadhihirisha furaha, kuongeza mambo mema, wanatilia manani kusoma Maulidi yake tukufu na kwa baraka yake huwadhihirikia fadhila enevu, mpaka alisema: baraka maridhawa…mpaka aliposema, “Mungu amrehemu mtu aliyezifanya siku za mwezi aliozaliwa Mtume (s.a.w.) kuwa ni sikukuu na zenye baraka.13 Kisha Al-Qastalaniy anamsifu Ibnul Haj kwa msimamo wake akisema: “Ibnul Haj ameongeza kwa kuwakanya watu wanaozusha bidaa kwa na kuimba Maulidi kwa nyimbo na ala za haramu, Mungu atampa thawabu 11 Al-mawaasim wal-maraasim cha Jafar Murtaha Al-Amili Uk. 41 12 Al-hudharatul islaamiyya fil qarnir raabii’ al-hijri Juz. 2 Uk. 298 13 Al-Mawaahibul laduniyya Juz. 1 Uk. 27. Seeratun nabawiyya cha Dahlan Juz. 1 Uk. 24 na Sera ya Halabiyya Juz. 1 Uk 83-84 12


Kusherehekea Maulidi ya Mtume s.a.w.w. kwa kusudio lake hilo jema.”14 Sakhawi amenena: “Waislamu katika miji mbalimbali wanaendelea kusoma Maulidi na usiku wake kutoa sadaka za kila aina na kudhihiri kwao baraka tele.”15 Ibn Ubbad amesema katika kitabu chake Risaalatul Kubra: “Ama kuhusu Maulidi, mimi naona kuwa Maulidi ni miongoni mwa sikukuu za waislamu na yote yafanywayo katika Maulidi ni ya uraha kwa kuwasha mishumaa na kujipamba mavazi mazuri, yote hayo ni mambo ya halali na hayakukatazwa na yeyote.” 16 Na Ibn Hajar amenena: “Ama yanayofanywa kwenye Maulidi lazima ieleweke kwamba kuna kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kusoma Qur’an, kutoa sadaka, kuandaa karamu, kumsifu Mtume (s.a.w.). Ama mengine yanayofuatia kama vile kusikia nyimbo ni halali kama hayapunguzi furha ya siku hiyo, ama yatayokuwa ya haramu au makruh basi hayo yanakatazwa.”17 Kusherehekewa Maulidi ya Mtume (s.a.w.) mbele ya viongozi na wanasiasa Imetajwa kwamba kiongozi wa kwanza kusherehekea Maulidi ni Amiri Abu Said Mudhaffar diin Al-Arbali (aliyefariki mwaka 639 A.H.). Huyu alikuwa akipokea wageni mbali mbali kutoka Baghdad, Mosul, Jazira, Sinjar nasiibin na Iran wakiwamo wanavyuoni, masufi, makhatibu, wasomaji Qur’an na washairi. 14 Al-Mawaahibul Laduniyya Juz. 1 Uk. 27, Seratun Nabawiyya ya Dahlan Juz. 1 Uk. 24 15 Sera ya Halabiyya Juz 1 Uk. 83-84, Seratun nabawiyya ya Dahlan Juz. 1 Uk 24 na Tarikhul Khamis Juz. 1 Uk. 223 16 Al-qawlul fasl fii hukmil ihtifaali bimawlidi kahyrir rusuli Uk. 175 17 Talkhiis min risaalat Hasan Al –Maqsad cha Suyuti, Uk. 90 13


Kusherehekea Maulidi ya Mtume s.a.w.w. Na walikuwa wakikaa hapo Arbala kuanzia mwezi wa Muharram hadi mwanzoni mwa Rabiiul’awal. Na alikuwa akiweka majukwaa makubwa ya mbao barabarani yaliyopambwa na hapo huka waimbaji na waigizaji wakionyesha watu.18 Sayyid Rashid Ridha anasema: “Mtu wa kwanza kuanzisha mkusanyiko wa kusoma Maulidi ni ni mmoja kati ya wafalme wa Sharakisa, nchini Misri. Na kuna vitabu vingi vilivyotungwa juu ya utafiti wa kuanzishwa kwa usomaji wa Maulidi na maadhimisho mengine, miongoni mwavyo ni: 1. At-Tanwiir fii mawlid siraajil muniir cha Ibn Dahiyya ambacho alikitunga kwa ajili ya Amiri Mudhaffarud diin ambapo Amir alimpa dinar elfu moja mbali na gharama za kukaa kwake katika muda huo.19 2. Risala ya Suyuti iitwayo Husnul maqsad. 3. Maulid cha Ibn Rabii. 4. An-Niimatul kubra alal aalam fii mawlidi sayyid walad Adam cha Shihabud Dini Ahmad bin Hajar Al-Haytham As-Shafii mwenye kitabu Sawaai’qul Muhriqah.20

Hukmu zaMaulid na mambo yake mahsus Katika siku ya Maulidi kuna hukmu za kisharia hasa kwayo pia kuna bara18 Wafiyatul Aa’yan Juz. 1 Uk. 436-437 Shadharatu dahab Juz. 5 Uk. 136-140 Seeratun Nabawiyya cha Dahlan Juz. 1 Uk. 24-25 Bidaaytu wan nihaaya Juz. 23 Uk. 137 19 Wafiyatul Aa’yan Juz 1 Uk. 138 na 437 Risalatu hausnil maqsad cha Suyuti Uk. 75 na 77 Bidayatu wan nihaaya Juz. 13 Uk. 137 Seertul halabiyya Juz. 1 Uk. 83-84 20 Rejea kwenye kitabu Al-Mawaasim wal-Maraasim cha Jafar Murtadha AlAmili 14


Kusherehekea Maulidi ya Mtume s.a.w.w. ka na vipawa Mwenyezi Mungu anavyowapa waja: Kama ilivyofahamika katika kauli za wanavyuoni kwamba siku ya Maulidi inazingatiwa kuwa ni sikukuu kama sikuu nyingine, mafano Sheikh Qastalani, Ibnul H aj Ibn Abbad na Ibn Hajar.21 Amesema Ibnul Jawzi: “Miongoni mwa yaliyo mahsus ni kuwapo amani mwaka huo na bishara njema kwa kupata makusudio.22 Kupendekezwa kusimama na kuswaliya (kumtakia rehmaMtume). Wamesema kuwa Waislamu husimama kwa ajili ya kumheshimu Mtume, na wamezungumzia juu ya hukmu hii. Amesema Safuri Shafii: “Kuhusu kusimama wakati anapotajwa muda wa kuzaliwa Mtume, hili ni jambo halikanushwi kuwa ni katika bidaa nzuri, wanavyuoni wengi wametoa fatwa kuwa yafaa pindi kunapotajwa kuzaliwa kwa Mtume watu wasimame, wengine wakasema yapasa atolewe salaam na hiyo ni miongoni mwa kumpa heshima na kumtukuza (s.a.w).23

Ibn Taymiyya na kaswida kwenye Maulidi Ibn Taymiyya ameeleza wazi wazi kuwa sikukuu sio mahsusi kwa ibada, na sadaka, au mfano wa hayo, bali inayavuka hayo mpaka – kufikia – kucheza na kuonyesha furaha pia. Ameonelea Ibn Taymiyya kwamba hilo lina asili katika Sunna, yaani katika riwaya inayotaja kuwa kwa Mtume (s.a.w) kulikuwa na vijakazi wakighani. Abu Bakr akaingia na akalikataza hilo. Akasema: “Zumari ya 21. Al-Mawahibul Laduniyya Juz. Uk. 27 Seera Nabawiyya cha Dahlan Juz. 1 Uk. 24 Seeartuil halabiyya Juz. 1 Uk. 83-84 22.Al-Mawahibul Laduniyya Juz. 1Uk. 27 Tarikhul Khamis Juz 1 UK. 223 Jawahirul Bihar Juz. 3 Uk. 24 Seera Nabawiyya cha Dahlan Juz. 1 Uk. 24 23.Nuzhatul Majalis Juz. 2 Uk. 8 15


Kusherehekea Maulidi ya Mtume s.a.w.w. shetani yapigwa ndani ya nyumba ya Mtume?” Mtume akasema: “Kila watu wana sikukuu yao, na sisi sikukuu yetu ni siku hii ya leo.”24 Na akaongeza: “Yanayofanywa siku ya Idi kama vile kula, kunywa kuvaa kucheza na kustarehe yamo kwenye nafsi zote, ikiwa hakuna kizuizi na hasa katika nafsi za watoto na wanawake.”25 Jambo la sita: Mjadala na wanaosema kuwa kusherehekea Maulid ni haramu Ijapokuwa sharia iko wazi juu ya Maulidi ya Mtume s.a.w na kufungamana kwake na asili ya dini, lakini wale wanaojiita Masalafi bado wanang’ang’ania kuwa ni bidaa. Anasema Ibn Taymiyya: “Aidha wanayoyazua baadhi ya watu ama ni kama vile manaswara wanavyosherehekea kuzaliwa nabii Isa (Krismasi) ama kumpenda Mtume (s.a.w.) Mwenyezi Mungu huwapa thawabu kwa mapenzi haya na ijtihadi hii lakini si kwa bidaa ya kuyafafanya mazazi ya Mtume kuwa ni sikukuu pamoja na kuhitilafiana watu juu ya kuzaliwa kwake, hili halikufanywa na watu wema waliopita, lau lingelikuwa hili ni la kheri, basi wao ndio wangelikuwa na haki zaidi kulifanya kwani wao walimpenda zaidi Mtume na kumtukuza zaidi kuliko sisi…. Na akaongeza kusema: “Licha ya Ibnul Haj kuikubali siku ya Mauilidi kuwa ina fadhla, bado haafikiani na kuisherehekea kwa kuwa ndani yake mna mambo yaliyokatazwa, na kwamba Mtume alitaka kuwasahilishia umma wake na hakutaka jambo lolote lifanyike kwa ajili yake na likawa ni bidaa.”26 24Iqtidhau siratul mustaqiim Uk. 194-195na riwaya ipo katika SahihBukhari na Muslim. Bukhari Juz. 1 Uk. 111 Sahih Muslim Juz. 2 Uk. 22. Seeratul halabiyya Juz. 2 Uk. 61-62. Sherhe Muslim ya Nawawi 25 Iqtidhaus siraatl mustaqiim Uk. 195 26 Al-Madkhal cha Ibnul Haj 16


Kusherehekea Maulidi ya Mtume s.a.w.w. Kile tunachogundua katika maneno haya ni kuwa wale waliowakataza watu kusoma Maulidi na sherehe zingine za kiislamuna kuchukuliwa kuw ni haramu, wamejenga hoja zao juu ya ufahamu huu kuwa ni bidaa na wamesawirisha kuwa kukosekana jambo kufungamana na dini ni kutokuwapo msingi wa kuwekwa au kutokuwa na hoja hasa na maana ya kufungamana na dini ni kuwepo jambo hilo tangu wakati sharia zilipoletwa. Lakini kutokuwepo jambo wakati sharia zilipowekwa haisababishi kutofaa. Wengine wakajaribu kutoa dalili za kuharamisha Maulidi kwa kuwa sherehe hizi zina mamboyaliyoharamishwa k.v. muziki, nyimbo, kuchanganyika wanaume na wanawake namengineyo. Lakini sisi tunapokataa katakatakuwepo kwa hayo katika hafla zifanywazo na madhehebu ya Ahlu bayt pia tunasisitiza kuwa hilo halifuti asili ya kitendo na kusema kuwa ni haramu, kwani kusema hivyo ni kuwajibisha kubatilisha asili ya ibada zingine sahihi lau zitaambatana na alama za uharamu wake. Lau Swala ya wajib iambatanishwe na kumtazama mwanamke wa kando (ajnabiyyah) ambao hilo ni haramu, je hapo Swala ya wajib itasemwa kuwa ni bidaa haifai? (Mungu apishe mbali!). Lililo muhimu kwetu kulitaja hapa ni kuwa nassiza kisharia kwa sura ya jumla zimekuja mahali pa kutilia mkazo juu ya kuheshimu shakhsiyya ya Mtume (s.a.w.) akiwa hai au amekufa haifai mtu kukanusha au kushuku. Kutokea hao baadhi ya wanavyuoni wamepata dalili na kulichukulia jambo hili kuwa ni bidaa nzuri.

17


Kusherehekea Maulidi ya Mtume s.a.w.w. Amesema Ibn Hajar juu ya jambo hili: “Kusherehekea Maulidi ni bidaa ambayo haikunukuliwa kutoka kwa mabwana wema waliotangulia katika karne tatu za mwanzo, lakini imekusnya mazuri na mabaya yake; atakayefanya mazuri yake na kujiepusha na mabaya yake hapo yatakuwa ni bidaa nzuri, vinginenyo hapana.”27 Amesema Imam Abu Shama: “Miongoni mwa mazuri ya bidaa yafanywayo wakati wetu huu ni kusoma Maulidi kila mwaka miongoni mwayo humo ni kutolewasadaka, mapambo, na furaha, vilevileknafinyiwa mema mafukara kunkakoleyta mapenzi na taadhima kwa Mtume (s.a.w.) kwenye moyo wa wafanyao, na pia ni kumshukuru Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwa neema aliyowajaalia waja kwa kumtuma Mtume (s.a.w.) kuwa ni rehma kwao.28 Suyuti anasema katika Risala yake ‘Husnul Maqsad fii amalil mawlid’: “Nionavyo mimi ni kuwa msingi wa kusoma Maulidi ambapo watu hukusanyika na kusoma Qur’an, kutajwa kwa kisa cha Mtume (s.a.w.) alivyoanza ujumbe wake, na mihjiza iliyotokea ya kuzaliwa kwake; kisha watu wakala karamu bila ya kuzidisha jambo lolote na wakaondoka, hii ni bidaa nzuri ambapo aifanyaye hupata thawabu, kwani ndani yake hutukuzwa Mtume na kuonyesha shangwe ya mazazi yake matukufu.29 Na Ibn Taymiyya amenukuu kauli nyingi zinazotoa dalili ya uhalali wa kukusanyika na kusherehekea siku ya Maulidi ya Mtume mtukufu licha ya kuwa yeye ni katika wakinzani wa kubwa kwa anayefanya Maulidi kuwa ni sikukuu kama anavyodhania. Anasema: “Amesema Al-Maruzi: ‘Nilimuuliza Abu Abdillah juu ya watu wanaokesha, mmoja wao akasoma na wakaomba hadi kuche. Akamjibu: 27Jafar Murtadha Al-Amili Al-mawasim wal-Marasim Uk. 62 Risalatu maqsad iliyochapishwa na An-niimatul kubra Uk. 114 28 Siiratul Halabiyya Juz. 1 Uk. 83-84 29 Seratul Bulghatul hubb Uk 42 18


Kusherehekea Maulidi ya Mtume s.a.w.w. ‘Nataraji hapana makosa.’ Abu Sirri Al-Harbi amesema: “Amesema Abu Abdillahi: ‘Ni lipi ema zaidi ya watu kukusanyika wakaswali na kutaja alilowaneemesha Mwenyezi Mungu kamawalivysema maanswari? Akaongeza: ‘Na hii ni ishara ya aliyoyapokea Ahmad. Ametuhadithia Ismail, ametupa habari Ayyub, kutoka kwa Muhammad bin Sirin, amesema, “Nimepewa habari kuwa maanswari kabla ya kwenda Mtume Madina, walisema: “Ni vizuri kama tungelichagua siku tukawa twakusanyika katika siku hiyo tukawa twaikumbuka siku hii kuu aliyotuneemesha Mwenyezi Mungu. Wakasema; ‘Siku nzuri ni ya jumamosi, kisha wakasema la hatuwezi kukusanyika pamoja na siku ya mayahudi. Wakataja siku ya jumapili. Wakasema, la hatuwezi kukusanyika siku ya manaswara. Kisha wakaonelea iwe siku ya ijumaa; ndipo wakakusanyika siku ya ijumaa kwenye nyumba ya Abi Umama As’ad bin Zurarah. Kukachinjwa mbuzi. Wakala mpaka wakatosheka.30 Kwa hivyo mkusanyiko wa wa watu kwa kusherehekea na kuadhimisha mambo adhimu ya kidini, ni silika ya kibinaadamu inayokwenda sambamba na maumbile yake, kwa hvyo twaona ya kuwa waislamu hawakuweza kuiepuka silika hii ya kiutu katika minasaba yao mbali mbali ya kidini. Hili alilolinukuu Ibn Taymiyya kwa ajili yetu ni moja kati ya mengi yanayoadhihirisha tukio hili na kuakisi katika maisha ya waislamu, jambo linalonasibiana na na tabia ya itikadi zilikuwapo wakati huo, jambo linalooyesha kuwa kufanya hafla, na kukusanyika kwa ajili ya kuad30. Iktidhau sirat: Ibn Taymiyya Uk. 304 asili yake ni kutoka kwenye kitabu: Siratu Ibni Hisham Juz. 1 Uk. 707. Alamul wara cha Ali bin Ibrahim Al-Qummi. Majmaul Bayan cha Ibn Sirin 19


Kusherehekea Maulidi ya Mtume s.a.w.w. himisha kumbukumbu za mambo ya kiislamu ni jambo lililotokea kwenye zama za mwanzo wa kudhihiri mwito mtukufu wa kiislamu. Maoni ya Said Hawiyy ndio yaliyo huru zaidi kuliko yoyote yale juu ya suala hili pale alipounga mkono na kusema kwamba kujuzu kufanywa kumbukumbu za mabo ya kiislamu kuwa ni kwa sura ya ujumla, lakini za Maulidi ziwe ni mahsus, alitoa hoja mkataa na kuwashambulia wale wenye msimamo mkali wasioifahamu vyema maana ya kufanya bidaa. Licha ya kuwa yeye bado alikuwa akiamini kwamba bidaa imegawanyika marambili, nzuri na mbaya. Anasema: “Tunachosema ni kwamba, uchukuliwe mwezi wa Maulidi kuwa ni mnasaba wa waislamu kukumbuka sera ya Mtume (s.a.w.) hilo halina ubaya, na uchukuliwe mwezi huo kuwa ni wa mapenzi kwa Mtume, hilo pia halina ubaya, au ni mwezi wa kuelezwa kwa wingi sharia za alizokuja nazo Mtume pia ni sawa. Aidha vile ilivyotajwa na wengine kuwa kukusanyika kwa ajili ya mihdhara, au mashairi, au kaswida msikitini au ndani ya nyumba kwa mnasaba wa mwezi wa Maulidi hilo sioni kuwa lina ubaya pia lakini kwa sharti ya kuwa maana inayosemwa iwe sahihi. Asili ya kukusanyika kwa kutaja sera ya Mtume (s.a.w.) au kaswida ya kumsifu huko kunajuzu, na twataraji wanaofanya hilo watalipwa. Waonaje lau kutakuwa na madrasa yenye wanafunzi wahusike na aina moja ya somo kwa mwezi mzima je hilo ni dhambi? Anaongeza kusema: “Ustadh Hasan Al-Banna alikuwa kweli, anayeona mbali na ni kiogozi katika katka elimu, anaonelea kwamba minasaba ya kumbukumbu za kiislamu katika enzi za kukandamizwa ni muhimu kuihuisha. Miongoni mwa maneno yake: “La muhimu kuzihuisha siku zote zinazopasa waislamu kuzisherehekea, iwe kwa kusoma Qur’an tukufu, khutba, au mihadhara inayohusika.”

20


Kusherehekea Maulidi ya Mtume s.a.w.w. Kisha anawashambulia wenye msimamo mkali asema: “Wenye msimamo mkali katika mambo kama haya msimamo wao mkali – hapa – si mahali pake, kwani asili katika vitu si uharamu bali asili katika vitu ni uhalali mpaka lije agizo la kuharamisha . Ama ile Hadith isemayo, ‘Kila lisilo katika mambo yetu ni lenye kupingwa.’ Wao wanaifahamu kimakosa.31 Kiuhakika ufafanuzi wa jamii juu ya hisia za kidini zilizo ndani ya nafsi za waislamu. Ilivyo hasa ni kuwa ufafanuzi juu ya hisia za kidini kwa jamii zilizomo ndani ya nafsi za waislamu ni jambo lililoachwa kwenye mazoea ya watu na njia zao mbalimbali na ada zao mahsusi za kijamii na mfano wa jambo hili ni vile zinavyofanya nchi zilizo nyingi au zote, jinsi zinavyosherehekea siku za uhuru, isipokuwa tu tofauti baina ya sherehe hizi na zile ni za hafla za Maulidi au sherehea za matukio mbalimbali mengine ya kiislamu, ni kuwa sherehe za kawaida zinafuata maagizo ya wanaoongoza bila ya kuwa na sharia kutoka kwengine. Lakini hafla za kumbukumbu za matukio ya kiislamu, na hasa Maulidi, zimekusanya amri za sharia za liislamu. Mwishowe hatuna budi kusema kuwa tunapoangaia aina ya njia wanazoshikamana nazo wafuasi wa madhehebu ya Ahlu bayti katika hafla mbalimbali za kiislamu ziwe ni za furaha au za huzuni na hasa katika kudumu na hafla za Maulidi, tutaona namna gani walivyo na hamu kubwa juu ya kubakisha mambo yahusuyo shakhsiyya ya Mtume (s.a.w.) mara kwa mara, na kujipamba na mafunzo ya risala ya kiislamu na kushikamana nayo; kwani atakayeziangalia ratiba za hafla hizo taona kwamba lengo lake la kwanza ni kuinua daraja ya Mtume (s.a.w.), kudhihirisha athari zake 31 Said Hawiyy Kay la tardhi Uk. 6, Seeratu bukghatul hubbi wa shiir Uk. 36-39 21


Kusherehekea Maulidi ya Mtume s.a.w.w. zeye kudumu ndani ya kaswida, maneno, khutba na makala ya kislamu yeye lengo bali hata wengine hupata nafasi ya kutoa masomo mbalimbali ya maisha yake matukufu na jihadi yake kubwa katika kuinua neno la Mwenyezi Mungu duniani na mengineyo yanayofungamana na Mtume (s.a.w.) na yanayowata nguvu waislamu juu ya sera yake , ni kipimo cha makosa.”32 Na kuwahimiza kumfuata na kufuata uongozi wake. Ili tuzidi kufafanua, hebu tuangalie maneno ya Seyyid Muhsin Al-Amini Al-Amili: “Ama kukumbuka mazazi ya manabii na mawalii-kama yanavyoitwa na mawahabi, sikukuu-ili kudhihirisha furaha na mapambo, mfano siku za kuzaliwa kwao ambazo zimekuwa ni neema za Mwneyezi Mungu kwa viumbe wake, na kusomwa visa vya mazazi yao, kama inavyojulkana yanavyosomwa maulidi ya Mtume (s.a.w.) na kuwatakia daraja, na kukariri kuwatakia rehma na amani manabii na watu wema; hayo hakuna ndani yake kizuwizi kiakili wala kisharia, maadam hayatakuwa na mabo ya haramu kama nyimbo na ufisadi, au kutumia ala za nymbo na mengineyo kama vile wafanyavyo watu wenye akili na mila katika siku walizozaliwa wakuu na manabii wao na kutukuza wafalme zao, hii yote ni namna ya utukuzo, ikiwa yule anayetukuzwa anafaa kufanyiwa hivyo, basi inakuwa twaa na ibada kwa Mwenyezi Mungu tu, lakini siyo kila aina ya kutukuza ni ibada kwa anayetukuzwa, hivo basi kuzilinganisha – taadhima kama hizo – na vitendo vya washirikiana kwa masanamu yao ni ulinganisho wa makosa.

32 Kashful Irtiyaab cha Seyyid Muhsin Al-Amini Al-Amili 22


Kusherehekea Maulidi ya Mtume s.a.w.w.

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION: 1.

2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24. 25. 26.

Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka kumi na sita Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo Juzuu ya kwanza Uharamisho wa uwongo Juzuu ya pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudhar Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur'an na Hadithi Elimu ya Nafsi Yajue Madhehebu ya Shia Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu 23


Kusherehekea Maulidi ya Mtume s.a.w.w. 27. 28. 29. 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49.

Al-Wahda Ponyo kutoka katika Qur’an. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii Mashukio ya Akhera Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyeezi Mungu na sifa zake Amateka Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana. Upendo katika Ukristo na Uislamu Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya Kupaka juu ya khofu Kukusanya swala mbili Bismillahi ni sehemu ya Qur’ani Sauti ya uadilifu wa Binadamu Kufungua Safarini. Kusujudu juu ya udongo. Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Malumbano baina ya Sunni na Shia

24


Kusherehekea Maulidi ya Mtume s.a.w.w.

BACK COVER MAULIDI Kufanya hafla ya kusherehekea maulidi ya Mtume (S.a.w.w..) ni jambo lililozoeleka mingoni mwa waislamu kwa karne nyingi sana, na kumbukumbu hii bado ingalipo nyoyoni mwa waislamu wote ambapo hafla hizo hufanywa misikitini na majumbani katika miji mbalimbali ya kiislamu ili kuitukuza siku hii tukufu, wao katika kufanya hilo ni kama watu wengine wanaoheshimu mambo yao matukufu, siku na kumbukumbu zao adhimu. Vilevile kinachokusudiwa katika hafla hizi, pamoja na kuwa ni furaha na kumshukuru Mwenyezi Mungu, lakini vilevile ni kuleta mwamko na kumbukumbu, Licha ya kudhihiri kufaa kwa kusherehekea Maulidi, lakini kuna baadhi ya watu wanaotafuta mambo yanayozuia kufanywa kwa Maulidi wakitegemeza kauli zao kwenye usemi kwamba hiyo ni bidaa, hili limefanya kuharamisha mambo mengi yaliyo halali kufanywa wakitoa sababu kwamba mambo haya hayakutajwa na nassi za kisharia.. Ili kuondoa dhana hizo potofu, mwandishi wa kitabu hiki anatoa mwanga juu ya suala hili kwa kutumia Qur’an Tukufu, Sunna, hoja, elimu na mantiki. Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation P.O. Box 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu:+255 22 2110640 Simu/Fax: +255 22 2127555 Email: alitrah@raha.com Website: www.alitrah.org Online: www.alitrah.info 25


Kusherehekea Maulidi ya Mtume s.a.w.w.

26


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.