Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:22 PM Page i
Maadili ya Ashura Mwandishi: Sayyid Jawad Naqvi
Mtarjuma: Dkt. M. S. Kanju
Mhariri: Al-Haj Ramadhani K.S. Shemahimbo
Kimepitiwa na: Mubarak A. Tila
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:22 PM Page ii
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:22 PM Page iii
©Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 – 17 – 045 – 6
Mwandishi: Sayyid Jawad Naqvi
Mtarjuma: Dkt. M. S. Kanju
Kimepangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation
Toleo la kwanza: Machi, 2014 Nakala: 1000
Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. - 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: w.w.w.alitrah.info
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:22 PM Page iv
Yeye ndiye Aliyempeleka Mtume kwa watu wasiojua kusoma, aliyetokana na wao, awasomee Aya zake, na awatakase, Na awafunze Kitabu na hikima, japokuwa hapo kabla walikuwa katika upotofu ulio dhahiri (Qur’ani 62:2)
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:22 PM Page v
YALIYOMO Neno la Mchapishaji. Madhumuni ya kuasi kwa Imamu Husein (a.s) 1. Madhumuni ya kuasi…………………………….…..…............................…...01 2. Kuamrisha mema na Kukataaza mabaya…………………................…….…..02 3. Maana ya Kuamrisha mema na Kukataza mabaya……….....................……...06 4. Kigezo katika Kuamrisha mema na Kukataza mabaya……………………….07 5. Jamii zinazoishi na zilizokufa…………………………...………………….…08 6. Tofauti kati ya vita vya maadili na vita vya madaraka…………………….….11 7. Jukumu la wanawake katika vita vya maadili………………………………...13 8. Imamu Husein (a.s) – mfasiri wa kimatendo wa kazi ya Kuamrisha mema na Kukataza mabaya………………….………….………..………..…16 9. Uhusein na Uyazid……………………………………….………….………...21 Maadili ya kwanza – Agano na uwajibikaji 1.Agano na Uwajibikaji……...……………………………………………..…....24 2.Kusujudu kwa Shabbir (a.s) – Ni usalama kwa ajili ya uhai wa Dini na Ubinadamu……................………………….........................................24 3. Hakuna wakati maalumu au uliowekwa kwa ajili ya kusoma Du’a.….............25 4. Shukurani kwa ajili ya kuzaliwa katika nchi ya Waabudu Mungu Mmoja (Tawhid).……….................................................26 5. Maadili ya Husein (as) yanaweza tu kumfanya mtu kuwa Huseiniat (mfuasi wa Husein)...........................................................................27 6. Je, tukio la Karbala lilikuwa ni majibu ya madai ya kiapo cha utii?................28 7. Ushahidi wa jibu sahihi...…………...................................................................29 8. Uimamu ni Agano la Allah (s)...........................................................................31 9. Mazingira ya Madina wakati wa kuasi kwa Imamu Husein (as)......................32 10. Mantiki na namna ya fikira ya Imamu Husein (as).........................................33 11. Majukumu yaliyoaminishwa juu ya watu wa Allah (s)...................................38 12. Mwisho wa watu wazembe..............................................................................39 13. Mwana wa Mina katika baraza ya Yazid.........................................................44 Maadili ya pili: Kutouvumilia Ukatili 1. Ukandamizaji – Uovu Mkubwa mno.................................................................48 2. Kutouvumilia Ukatili – Maadili ya Ashura........................................................49 3. Kutouvumilia Ukatili – Somo kutoka Karbala..................................................50 4. Imam Huseiin (a.s) – Mrithi wa Mtume (s.a.w.w)............................................50
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:22 PM Page vi
5. Ukristo Uliopotoshwa – Uvumilivu wa Ukatili.................................................53 6. Mitume (a.s) ni Washuhuda na Watabiri............................................................54 7. Athari za kufundisha Ukristo uliopotoshwa kwa Waislamu..............................55 8. Uvumilivu kwenye Ukatili – Dhambi Kubwa...................................................56 9. Sababu za Ukandamizaji....................................................................................57 10. Sababu za Ndani na Nje za Ukandamizaji.......................................................63 11. Tofauti kati ya Mustadha’af (Mkandamizwaji) na Mustadha’if (Mkandamizaji)........................................................................65 12. Karbala – Njia ya kutovumilia kwenye Ukandamizaji...................................66 Maadili ya tatu: Utukufu (Izzat) 1. Mhuishaji wa Heshima (Utukufu)......................................................................69 2. Tofauti kati ya heshima ya kweli na ya uwongo................................................70 3. Chanzo cha Heshima..........................................................................................72 4. Mtu anayemvutia kila mtu haheshimiwi............................................................74 5. Husein (a.s) – Kiongozi wa Heshima na Utukufua...........................................75 6. Maana ya Heshima.............................................................................................76 7. Familia yenye kuheshimika zaidi.......................................................................78 8. Karbala – Njia ya Heshima................................................................................79 9. Kuzitoa Muhanga Heshima katika njia ya Allah (s.w.t)....................................81 10. Walinzi wa Heshima za Uwongo.....................................................................83 Maadili ya nne: Kutoa katika njia ya Allah. 1. Kutoa katika njia ya Allah– chanzo cha mema yote..........................................86 2. Kutoa katika njia ya Allah katika Qur’ani.........................................................87 3. Kutoa katika njia ya Allah – Maadili ya Ashura................................................88 4. Msingi wa mahusiano........................................................................................88 5. Aina ya uhusiano wa kidini................................................................................89 6.Imamu Ali (a.s) – Kigezo (Us-wa) cha Kutoa katika njia ya Allah....................95 7. Bibi Zahra (a.s) – Mfano wa Kutoa katika njia ya Allah..................................97 8. Mjadala kuhusu wasio maasum.......................................................................102 9. Upana wa mipaka ya Kutoa katika njia ya Allah.............................................107 10.Imamu Husein (a.s) – Ufafanuzi wa kimatendo wa Kutoa katika njia ya Allah..........................................................................................109 Maadili ya tano: Ukombozi (Uhuru) 1. Imamu Husein (a.s) – Kiongozi wa watu huru................................................112 2. Aina za utumwa................................................................................................113 3. Mtu huru kwa mtazamo wa Ali (a.s)................................................................114 4. Imam Khomeini (r.a) – Mfano bora wa mtu huru...........................................115 5. Ulimwengu kwa mtazamo wa Ali (a.s)...........................................................116
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:22 PM Page vii
6.Ali (a.s) – Mtu aliyeufedhehi ulimwengu huu..................................................117 7. Utendaji wa ulimwengu kwa mateka wake......................................................118 8. Utendaji wa Shetani kwa mateka wake...........................................................119 9. Ni lini tutasherehekea uhuru?..........................................................................120 10. Waliochukua masomo ya uhuru kutoka kwa Imamu Husein (a.s)................120 11.Imamu Husein (a.s) – Kigezo cha Ukombozi (Uhuru)...................................121 12. Mateka wa Damascus na Uhuruu..................................................................123 13. Hurr (a.s) na Ukombozi (Uhuru)...................................................................125 Maadili ya sita: Subira (Sabr) 1.Subira – Maadili ya Ashura...............................................................................129 2. Cheo cha subira kuwepo katika Quran Tukufu................................................129 3. Subira katika simulizi za Maasumin (as).........................................................130 4. Subira – Daraja la Mawalii wa Allah (s).........................................................132 5. Maana halisi ya Subira....................................................................................132 6. Ujana – Muda mzuri kwa ajili ya kujizoesha Subira......................................134 7. Upotoshaji katika maana ya Subira..................................................................135 8. Maana ya Subira...............................................................................................136 9. Mazingira kwa ajili ya Subira..........................................................................138 10. Allah yuko pamoja na wenye kusubiri (Sabiriyn).........................................143 11. Imam Husein (a.s) – Kigezo cha tabia ya Subira..........................................143 Maadili ya saba: Ghera na Heshima (Ghairat). 1. Ghera na Heshima (Ghairat) – Maadili ya Ashura..........................................147 2. Maana ya Ghera na Heshima...........................................................................148 3. Tofauti kati ya “Kupendelea katika Ujinga” na Heshima................................153 4. Ni Mtu gani mwenye kujiheshimu zaidi?........................................................154 5. Ghera kwa ajili ya Dini– Msingi kwa Ghera nyingine na Heshima................157 6. Vilele vya Ukosefu wa Aibu- Mifano..............................................................157 7. Imamu Husein (a.s) – Kigezo cha Wajibu cha Ghera na Heshima.................159 8. Abbas (a.s) – Kilele cha Utii na Ghera na Heshima (Ghairat)........................160 Maadili ya nane: Utukufu wa Mambo. 1. Mwenendo wa Imamu Husein (a.s) na vita vya maadili.................................163 2. Maana ya Utakatifu (Taqaddus).......................................................................163 3. Kukanyagwa kwa Utakatifu.............................................................................164 4. Aina tofauti za Utakatifu..................................................................................166 5. Utakatifu wa Msikiti........................................................................................167 6. Utakatifu wa mikusanyiko ya Maadhimisho (Majalis)....................................167 7. Utakatifu wa Mimbar.......................................................................................168 8. Mfano wa kilele cha kufuru kwa utakatifu wa Mimbar..................................170
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:22 PM Page viii
9. Kufuru kwa Utakatifu wa Ali (as) ni kufuru kwa vitu vyote vitakatifu..........171 10. Kufuru ya njia na madhumuni.......................................................................173 11. Imamu Husein (a.s) – Mto wa utukufu wa utakatifu.....................................174 12. Karbala – Njia ya Mbinu Takatifu.................................................................175 13. Maadili ambayo yalihuika kutokana na mkutano wa Imamu Husain (a.s) na Juhfi.........................................................................177 14. Hitimisho........................................................................................................181 Maadili ya tisa: Uadui katika njia ya Allah 1. Kutengeneza Maadui ni Maadili ya ki-Huseini...............................................183 2. Uhusiano wa Misiba na Maadili......................................................................184 3. Tawalla na Tabbarra.........................................................................................184 4. Mwenendo wa Nabii Musa (as) na Tabarra.....................................................185 5. Mrithi wa Musa (as) katika kuutokemeza U-Yaziid (Yazidiat).......................186 6. Tabarra (Kujitenga) katika Mwenendo wa Imamu Ali (a.s)............................187 7. Wale ambao huokoa ngozi zao kutokana na misiba........................................188 8. Athari za Maadili..............................................................................................189 9. Jaribio chafu la kuondoa Maadili kutoka kwenye nafasi zao..........................190 10. Maadili na Misiba ya Bibi Zahra (as)............................................................192 11. Shukurani juu ya Misiba................................................................................193 12. Imam Husein (a.s) - Kigezo cha wajibu cha Maadili na Misiba...................194 13. Kila siku ni Ashura na Kila ardhi ni Karbala................................................195 14. Ashura ni Siku ya Allah................................................................................196 Maadili ya kumi: Dhabihu (Isaar) 1. Dhabihu – Maadili ya Ashura..........................................................................199 2. Maana ya Dhabihu...........................................................................................200 3. Dhabihu katika mtazamo wa Qur’ani..............................................................201 4. Dhabihu miongoni mwa Maasumin (a.s).........................................................202 5. Mashahidi wa Uhud – Kujitokeza kwa Dhabihu.............................................203 6. Ahlul-Bayt (a.s) – vigezo bora vya Dhabihu...................................................203 7. Imamu Sajjad (a.s) – Kigezo cha Wajibu cha Dhabihu...................................207 8. Imamu Sadiq (a.s) – Mtangaza imani ya Dhabihu..........................................210 9. Karbala – Miraji ya Dhabihu............................................................................211
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:22 PM Page ix
NENO LA MCHAPISHAJI Kitabu ulichonacho mikononi mwako ni tarjuma ya Kiswahili ya kitabu cha Kiingereza kiitwacho, Values of Ashura. Sisi tumekiita, Maadili ya Ashura. Kitabu hiki huelezea kwa mukhtasari masaibu ya Karbala ambayo kwayo Imam Husain (a.s.) alitoa muhanga si maisha yake tu bali na vyote alivyokuwa navyo. Hii ilkuwa ni vita ya Jihadi ya kuuokoa Uislamu kutoka katika mikono ya watu waliodhamiria kuuangamiza. Siku ya Ashura (yaani tarehe 10 mwezi wa Muharram, mwaka 61 Hijria) ndiyo siku ambayo Imam Husain (a.s.) aliuliwa kikatili na majeshi ya Yazid (l.a.). Kama alivyosema Imam Husain mwenyewe kwamba hatoki kwa ajili ya kupata maslahi ya kidunia bali anatoka kwenda kupigana kwa ajili ya Uislamu na kuurudisha katika maadili yake ya awali kama yalivyowekwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Mwandishi wa kitabu hiki, anatuelelezea hatua kwa hatua kuanzia Imam Husain (a.s.) alivyotoka Madina mpaka Makka, na hatimaye Karbala ambako alikutana na masaibu haya. Hivi vilikuwa ni vita vya ukombozi si kwa ajili ya Uislamu tu bali halikadhalika kwa wanadamu wote wanaokandamizwa na madhalimu ulimwenguni humu. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu ambapo nchi za Kiislamu zimevamiwa na majeshi ya tawala dhalimu za Magharibi kwa kisingizio cha demokrasia ilhali wanachofanya ni kupora utajiri wa nchi hizo na kufisha juhudi za Uislamu za kuamrisha mema na kukataza maovu na kuleta amani katika ulimwengu. Ukweli ni kwamba nchi hizi (za Magharibi) hazitaki kuona Waislamu wanakuwa kitu kimoja, kwa hiyo hulete chokochoko na kuwachonganisha Waislamu wapigane wenyewe kwa wenyewe ili wawasambaratishe na kuwapotezea lengo lao la kuamrisha mema na kukataza maovu. Na lengo kubwa la madhalimu hawa ni kuuza silaha zao zilizojaa kwenye maghala yao na kisha kupora utajiri uliopo katika nchi hizi. Mwandishi wa kitabu hiki anawataka Waislamu wazindukane na wamsome Imam Husain (a.s.) jinsi alivyofanya pale Karbala na hatimaye yeye mwenyewe kujitoa
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:22 PM Page x
muhanga siku ile ya Ashura. Kwa kuzingatia hili, tunaweza kushinda vita hivi vya kidhalimu dhidi ya Uislamu na Waislamu. Kutokana na ukweli huu, taasisi yetu ya Al-Itrah imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumini yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu hususan wazungumzaji wa Kiswahili. Tunamshukuru ndugu yetu Dkt. M. S. Kanju kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kukitarjumi kitabu hiki kutoka lugha ya Kiingereza, pia na wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Allah awalipe wote malipo mema hapa duniani na kesho huko Akhera – Amin. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation S. L. P. 19701 Dar-es-Salaam.
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:22 PM Page xi
Madhumuni ya kuasi kwa Imamu Husein (a.s) 1. Madhumuni ya kuasi…………………………….…..…............................…...01 2. Kuamrisha mema na Kukataaza mabaya…………………................…….…..02 3. Maana ya Kuamrisha mema na Kukataza mabaya……….....................……...06 4. Kigezo katika Kuamrisha mema na Kukataza mabaya……………………….07 5. Jamii zinazoishi na zilizokufa…………………………...………………….…08 6. Tofauti kati ya vita vya maadili na vita vya madaraka…………………….….11 7. Jukumu la wanawake katika vita vya maadili………………………………...13 8. Imamu Husein (a.s) – mfasiri wa kimatendo wa kazi ya Kuamrisha mema na Kukataza mabaya………………….………….………..………..…16 9. Uhusein na Uyazid……………………………………….………….………...21
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:22 PM Page 1
Maadili Ya Ashura
1.Madhumuni ya kuasi
Maadili ambayo yamerejea kwenye uhai kwa matokeo ya kuasi kwa Imamu Husein (a.s) hutajwa kama ifuatavyo: Maadili ya Ashura na Maadili ya Husein (a.s). Kabla ya kujadili maadili haya ni muhimu kwanza kuelewa madhumuni ya mihanga hii mikubwa ilikuwa ni nini. Tukio hili la msiba limekuwa kwenye ndimi zetu tangu karne nyingi na mengi yamesemwa na kuandikwa kuhusiana nalo. Ni vizuri kumuuliza mtangulizi, kiongozi mwenyewe wa mashahidi, kuhusu madhumuni ya kadhia hii kuliko kuyaendea maoni na maandishi ya wachambuzi mbalimbali, waandishi, watafiti mahatibu, wanachuoni na wasomi, ambao wameelezea mitazamo yao juu ya kadhia hii. Lazima tutafakari juu ya maneno ya Imamu Husein (a.s) ili kuona kile alichosema kuhusiana na madhumuni ya kuasi kwake. Wakati wa kuondoka Madina, kwa mikono yake mitukufu, Imamu Husein (a.s) aliandika wosia wa urithi kwa ajili ya ndugu yake Muhammad bin Hanafia (a.s) na akamkabidhi.
1
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:22 PM Page 2
Maadili Ya Ashura Katika wosia huu wa urithi anaelezea madhumuni ya kuasi kwake:
“Siondoki (kutoka Madina) kama muasi, mkandamizaji na dhalimu, bali madhumuni yangu ni kuutengeneza Umma wa babu yangu. Njia pekee ya kufanya mageuzi haya ni Amr Bil Ma’ruf (kuamrisha mema, kwenye Maadili yajulikanayo) na Nahi Anal Munkar (kukataza maovu), yaani, nataka kuutengeneza Umma kwa njia ya Amr Bil Ma’ruf na Nahi Anal Munkar. Sio kwamba mimi ni mtu wa kwanza ambaye ninafuata njia hii ili kuutengeneza Umma, kabla yangu mimi babu yangu na baba yangu wote walifuata njia hii tu. Nami pia nataka kufuata mwenendo wao) wa kufanya Amr Bil Ma’ruf na Nahi Anal Munkar kwa ajili ya kuutengeneza Umma”. (Mawassai Kalimatul Imam Hussain – uk. 290-291)
2. Kuamrisha mema na Kukataza maovu A. Katika Qur’ani Tukufu. Qur’ani Tukufu imelifanya hili kama wajibu kwa Umma wote (wa Waislamu)
“Na liwepo miongoni mwenu kundi lenye kulingania kwenye heri, na kuamrisha mema na kukataza maovu (Amr Bil Ma’ruf na Nahi Anal Munkar ). Na hao ndio wenye kufaulu.” (3:104) Katika sehemu nyingine, Umma ambao unatekeleza wajibu huu wametajwa kama Umma bora:
“Mmekuwa ni umma bora mliotolewa kwa watu, mnaamrisha mema na kukataza maovu …” (3:110) 2
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:22 PM Page 3
Maadili Ya Ashura Katika mfano mwingine Allah (s.w.t) anasema:
“Wanafiki wanaume na wanafiki wanawake ni hali moja. Wanaamrisha maovu na kukataza mema na wanafumba mikono yao. Wamemsahau Mwenyezi Mwenyezi Mungu na yeye amewasahau. Hakika wanafiki ndio mafasiki.” (9:67) Kwa upande mwingine (wa pili) wa wanafiki kuna waumini ambao ni marafiki wao kwa wao, kama Qur’ani inavyosema:
“Na waumini wanaume na waumini wanawake ni mawalii wao kwa wao. Huamrishana mema na kukatazana maovu. Na husimamisha swala. Na hutoa zaka. Na humtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hao Mwenyezi Mungu atawarehemu. Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye nguvu mwenye hekima.” (9:71) B. Kuamrisha mema na Kukataza maovu katika hadith 1. Abu Saeed Az Zahri anasimulia kutoka kwa Imamu as-Sadiq (a.s) na Imamu Baqir (a.s): “Ole juu ya Umma ule ambao hauwi wa kidini kwa kuamrisha mema na kukataza maovu.” (Wasaelus Shia, J. 16, Sura 1, ya Amr Bil Ma’ruf na Nahi Anal Munkar, uk. 117)
2. Imam al-Baqir (a.s) anasema:
3
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:22 PM Page 4
Maadili Ya Ashura “Umma mbaya zaidi ni ule ambao huchukulia kuamrisha mema na kukataza maovu, kama utaratibu usiofaa” (Wasaelus Shia, J. 16, Sura 1, ya Amr Bil Ma’ruf na Nahi Anal Munkar, uk. 117)
3. Imam Ridha (a.s) anasema:
“Amrisheni mema na katazeni maovu., vinginevyo dhulma, ufisadi na watu waovu watakutawaleni, kisha hata maombi ya watu wema hayatakubaliwa.” (Wasaelus Shia, J. 16, Sura 1, ya Amr Bil Ma’ruf na Nahi Anal Munkar, uk. 117,119,121)
4. Mjumbe wa Allah (s.a.w) alisema:
“Wakati Umma wangu utakapoacha jukumu la kuamrisha mema na kukataza maovu., basi wasubiri Ghadhabu ya Allah” (Wasaelus Shia, J. 16, Sura 1, ya Amr Bil Ma’ruf na Nahi Anal Munkar, uk. 117,119,121)
5. Imam al-Baqir (a.s) anasimulia:
“Kuamrisha mema na Kukataza maovu ni wajibu wenye heshima, na ni kwa ajili ya matendo haya tu utendaji wa wajibat nyinginezo hufanya iwezekane. Hasira na ghadhabu za Allah hushuka kama wajibu unaachwa, na kisha adhabu ya Allah huwashukia wote. Watu wema katika jamii pia hutoweka kwa ajili ya watu waovu, kwa sababu Kuamrisha mema na Kukataza maovu ni mwendo wa Mtukufu Mtume (s.a.w) na watu wema. Huu ni wajibu mkubwa ambao hufanya utekelezaji wa wajibat nyingine kuwezekana. Ni kwa ajili ya utekelezaji wa wajibu huu kwamba amani inathibiti, biashara inakuwa halali, majanga yanaweza kuzuiwa, nchi 4
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:22 PM Page 5
Maadili Ya Ashura inaweza kustawi pamoja na watu, haki inaweza kufanyika pamoja na maadui na mambo yote yanaweza kukamilishwa kwa ajili ya hili.” (Wasaelus Shia, J. 16, Sura 1, ya Amr Bil Ma’ruf na Nahi Anal Munkar, uk. 117,119,121)
6. Imam as-Sadiq (a.s) anasimulia: Mtu mmoja alikuja kwa Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) na akauliza:
“Ewe Mjumbe wa Allah! Ni kipi kitu bora zaidi katika Uislamu? Yeye (s.a.w.w.) akajibu, kuwa na imani katika Allah (s). kisha mtu huyu akauliza, kitu kingine ni nini. Yeye (s.a.w) akasema, kuwa mpole na mwenye huruma kwa ndugu na jamaa. Mtu huyu akauliza tena ni kipi kingine? Yeye (s.a.w) akasema, Kuamrisha mema na kukataza maovu. Kisha mtu huyu akauliza, ni kipi kitu kiovu sana karibu na Allah? yeye (s.a.w) akajibu, kumshirikisha Allah (Shirk Billah). Mtu huyu akauliza tena nini kingine? Yeye (s.a.w.w.) kukata uhusiano na ndugu. Akauliza tena nini kingine? Yeye (s.a.w.w.) akajibu, kuamrisha maovu na kuzuiya kufanya mema.” (Wasaelus Shia, J. 16, Sura 1, ya Amr Bil Ma’ruf na Nahi Anal Munkar, uk. 121)
7. Imam Sadiq (a.s) Anasimulia kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w) kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w) alisema:
“Hali yenu itakuaje wakati wanawake wenu watakapokuwa waovu na vijana wenu kugeukia kwenye ufisadi kwa sababu mtakuwa mmeacha Kuamrisha mema na Kukataza maovu? Mtu mmoja akasema, Ewe Mjumbe wa Allah! Hili pia litatokea? Yeye (s.a.w.w) akajibu, hata baya zaidi ya hili litatokea. Hali yenu itakuaje wakati 5
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:22 PM Page 6
Maadili Ya Ashura mtapokuwa mnaamrisha maovu na kukataza mema? Mtu mwingine tena akauliza, Ewe Mjumbe wa Allah! Hili pia litatokea? Yeye (s.a.w.w) akajibu, hata baya zidi ya hili litatokea. Hali yenu itakuaje wakati ambapo mema yatageuzwa kuwa maovu katika macho yenu na maovu kuwa mema?” (Wasaelus Shia, J. l 16, Sura 1, ya Amr Bil Ma’ruf and Nahi Anal Munkar, uk. 117,119,122)
3. Maana ya Kuamrisha mema na Kukataza maovu Imamu Hussain (a.s) alitangaza wajibu huu mkubwa wa kimungu wa Kuamrisha mema na Kukataza maovu kama madhumuni ya kuasi kwake. Kiongozi wa mashahidi alijibu maswali yote na upinzani wote uliojitokeza mpaka Siku ya Hukumu katika wosia wake wa urithi. Mtu anaweza kushangaa, ni kwanini Imamu Husein (a.s) alitoa muhanga huu mkubwa, ufungwa, mashahidi wote hawa na mauaji ya watoto hawa wadogo? Majibu kwa maswali yote haya ni rahisi; Imamu Husein (a.s) alitaka kutekeleza kazi ya Kuamrisha mema na Kukataza maovu. Sifa za Kuamrisha mema hazijumuishi bila ya haki kuingilia maisha ya mtu, kuwanyoshea watu kidole na kuwa chanzo cha matatizo kwa mtu. Wakati mwengine, katika jina la wema, uovu husambaa na kwa ajili ya uovu, watu huzuiwa kufanya mema. Hii hutokea kwa sababu watu hawana utambuzi sahihi wa Maadili mema wala Maovu. Shahid mkubwa wa Shia, Murtadha Muttahheri (r.a) anaeleza kwamba hesabu ya maovu ambayo yanasambaa kwa jina la Kuamrisha mema ni kubwa zaidi kuliko maovu yanayoenezwa katika muktadha mwingine wowote. (Majmua Aasaar, J. 17, Ustadh Shaheed Muttahari (r.a) , uk. 576)
Kwa ujumla, Ma’ruf hutafsirwa kumaanisha mema au wema, ambapo Munkar hutafsriwa kumaanisha uovu. Katika vitabu visivyo vya fasihi maana ya Ma’ruf imeelezwa kama wema na Munkar kutafsiriwa kama uovu. Kwa mujibu wa fasihi, neno Ma’ruf linahusiana na Maarifat na Irfan. Maneno Maarifat, Irfan, Arif na Ma’ruf yanatokana na familia moja. Kama mtu akipata Maarifat (utambuzi) ya mtu fulani atachukuliwa kama Arif, je, hii pia ina maana kwamba ni mtu mwema? Ingawa haiwezi kukataliwa kwamba mtu ambaye ana Maarifat pia huambiwa kwamba ni mtu mwema na mwanachuo, maana ya neno Arif halitafsiri moja kwa moja kwenye maana ya ‘mtu mwema’. Katika vitabu vya fasihi, Maarifat maana yake kuwa na utambuzi, kutambua na kujua kitu fulani. Na Arif ni mtu ambaye hujua na ametambua kitu, kwa hiyo, Maarifat huja kumaanisha kitu ambacho tayari kinajulikana, kimetambuliwa na ujuzi wa kuhusu kitu hiki upo. Halikadhalika, Munkar hutafsiriwa kumaanisha vitu ambavyo hukataliwa, tupa, havikubaliwi, au 6
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:22 PM Page 7
Maadili Ya Ashura kitu ambacho hakiwezi kutambuliwa kwa kupitia kidesturi vyanzo vijulikanavyo vya utambulisho; kama ambavyo hatuitambui Israil kupitia utambulisho wake wa kidesturi na hivyo hatukubali kuwepo kwake. Munkar ni vitu vile ambavyo hubakia bila kutambuliwa daima na siku zote vitakataliwa. Hivyo, Amr Bil Ma’ruf maana yake kulingania kwenye vitu vile vizuri vilivyo tambuliwa na kukubaliwa, na Nahi Anal Munkar maana yake kuzuiya watu kutokana na vitu vilivyo kanushwa na kukataliwa.
4. Kigezo kwa ajili ya Ma’ruf na Munkar Ma’ruf maana yake vitu vile ambavyo hutambuliwa na kukubaliwa, ambapo Munkar maana yake vitu vile ambavyo hukataliwa. Kuna vyanzo viwili vya kutambua Ma’ruf na kukataa Munkar. Kazi ya vyanzo hivi viwili ni amma kutambua kukubalika kwa kitu mahususi au kukataa uhalali wa kitu mahususi na hivyo kukitupilia mbali. Chanzo cha kwanza kwa ajili ya wanadamu kutambua Ma’ruf na kukataa Munkar ni “Ufunuo” (Wahyi). Vitu vile ambavyo hukataliwa na Allah ni maovu (Munkarat), ambapo vile ambavyo vimetambuliwa na kufanywa sehemu ya sheria za mwanadamu ni maadili mazuri yajulikanayo (Ma’ruf). Chanzo cha pili kwa ajili ya Ma’ruf na Munkar ni “Akili” (Aql). Vitu vile ambavyo hufaa kutambuliwa na akili na ambavyo akili ya mwanadamu kwa kawaida imevikubali na kuvitambua hujulikana kama Ma’ruf. Munkar ni kinyume cha hivi. Sasa, kama tunatayarisha orodha ya vitu vyote vile ambavyo hukubaliwa na kutambuliwa kwa ufunuo, dini, na akili, orodha ndefu hujitokeza pamoja na mifano kama vile uanzishaji wa maadili, kufanya upendeleo na matendo mazuri, kusaidia watu wanao kandamizwa, kuwasaidia wasio na uwezo, kusimamisha sala, kufunga, nk. Matendo yote mazuri na sifa yatakuwa sehemu ya orodha hii. Shahidi Murtadha Muttahheri (r.a) anasema kwamba Ma’ruf hukusudia kushughulikia malengo yote bayana yaliyowekwa na Uislamu, ambapo Munkar humaanisha yale yote ambayo ni hasi. Kwa hiyo, Ma’ruf na Munkar imekuwa ikielezewa katika namna ya ainasafu (jenasi). Licha ya ukweli kwamba aina ya Ulinganiaji na Ukatazaji iliyoshughulikiwa chini ya Ma’ruf na Munkar ni mahususi sana, imethibitishwa kwenye hadithi, sheria na historia kwamba ulinganiaji na ukatazaji uliotajwa hapa huenea njia yoyote na zote za halali ziwezekanazo ambazo zitakuwa zenye faida kufikia malengo (yaliyo wekwa na Uislamu). (Majmua Aasaar, J. 17, uk. 575)
7
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:22 PM Page 8
Maadili Ya Ashura Orodha ya Munkar (maovu) itakuwa na vitu kama ukandamizaji, ubahili, kutosimamisha sala, unywaji wa pombe na matendo yote mengine na tabia. Imamu Husein (a.s) kwa maana anasema, ‘Naondoka ili kwenda Kuamrisha mema na Kukataza maovu. Nimekuja kuwalingania kwenye vitu vile ambavyo vimekubaliwa na Allah (s) na akili zenu kama vitu vizuri, na ninaondoka Madina ili kuwakatazeni vitu vile ambavyo vimekataliwa na Allah (s) na akili,’ vitu hivyo ni mwanadamu, Qur;an na maadili ya Kiislamu. Kwa madhumuni ya kuyarudisha tena maadili haya kwenye uhai, kuyatangaza, na kuyawasilisha kwa wanadamu, Mitume (a.s) walitumwa mmoja baada ya mmoja na wakasukumwa kimoyo ili kuwaongoza wanadamu kwenye maadili haya mazuri na kuwalinda kutokana na ambayo ni hasi, yaliyokataliwa, na sifa za uovu. Hivyo, Ma’ruf na Munkar kiuhalisia ni majina ya aina mbili za maadili. Ma’ruf ni jina la wanadamu wote na maadili ya kimungu, ambapo Munkar humaanisha maadili hasi, sifa zisizo za mwanadamu na matendo yote maovu. Kutoka hapa tunakuja kutambua maadili yana sehemu mbili, sehemu moja ni yale maadili ambayo yamekuwa kidesturi yametambuliwa na kukubaliwa kupitia ufunuo na akili, ambapo Munkar ni sehemu ile ambayo imekanushwa na kukataliwa, na si Muumba wala akili huyakubali haya. Lakini, wakati mwingine mfumo wa maadili haya hubadilika na watu huenda mbali ambako huanza kuichukulia Ma’ruf kama Munkar na Munkar kama Ma’ruf; kama ambavyo imekuja kwenye hadithi kutoka kwa Mjumbe wa Alla (s.a.w). “...... Hali yenu itakuaje wakati Mema yatakapoonekana Maovu na Maovu kuonekana Mema?” Kuamrisha mema na Kukataza maovu imetangazwa kama jukumu la Umma wote katika Qur’ani Tukufu, hivyo jukumu hili vilevile huhusika kwa Kiongozi wa Umma (Imam-e-Ummat). Wakati Kiongozi anaposhuhudia kwamba mfumo wa maadili umebadilika na Umma unayatazama mabadiliko haya kama watazamaji walio kimya, basi Kiongozi mwenyewe huchukua hatua zinazohitajika zote mwenyewe, sawa na kile Imamu Husein (a.s) alichosema wakati alipotangaza “Nataka kutekeleza kazi ya Kuamrisha mema na Kukataza maovu.”
5. Jamii zilizo hai na zilizokufa Ubinadamu na hususan Jamii ya Mwanadamu wako hai kwa sababu ya maadili. Ipo katika hadithi kwamba kuna aina tatu za vifo kwa wanadamu. Kwanza ni kifo cha 8
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:22 PM Page 9
Maadili Ya Ashura mwili, pili ni kifo cha nafsi na moyo. Na tatu ni kifo cha Umma na jamii za mwanadamu. Kifo cha mwili ni utenganisho wa mwili na roho, kifo cha moyo ni wakati ule kukiwa hakuna ukumbusho wa Allah (s) ndani yake; mioyo iliyokufa haina ukumbusho wa Allah (s), na kifo cha Umma na jamii ni wakati jamii zinapokuwepo bila maadili ya kibinadamu. Mwili unakuwa umetokwa na utwahara wake wakati roho ikitoka mwilini. Kama mtu akigusa mwili huu basi ni lazima kukoga josho la kisheria la kugusa maiti (Ghusl e Mase Mayyat). Amri ya dini kwa mwili wenyewe ni kwamba lazima ukoshwe josho la kisheria, kuvikwa sanda, kuwekwa kafuri na kisha baada ya kuswaliwa kaburi lazima lichimbwe katika eneo la makaburi na mwili lazima uzikwe kwa sababu sasa umekufa. Hakuna faida kwa maiti kuwa miongoni mwa viumbe hai, wala hakuna faida kwa vimbe hai kuwa pamoja maiti. Hii ni kwa sababu huu ni mwili uliokufa na kama haukuzikwa basi utaoza na utaanza kutoa harufu. Harufu hii inayotoka kwenye mwili mfu kwanza kabisa ni chukizo la mwili wenyewe na pia kuna hatari ya kusababisha magonjwa ya milipuko. Wakati mwanadamu anapopatwa na kifo cha mwili sheria za kidini kwa mwili huu ni kama zilivyotajwa hapo juu, lakini kama kifo cha nafsi kikitokea, ambacho ni wakati moyo unapokuwa wenye kupuuza utajo wa Mungu na ukajishughulisha na mchezo na burudani za ulimwengu, basi amri kama hii pia hutumika kwa aina hii ya kifo. Moyo kama huu uliokufa kwanza lazima upelekwe kwa daktari wa kiroho kwa matumaini kwamba nafsi itapona na kuhuika. Kama baada ya matibabu haya nafsi ikapona, basi hakuna matatizo kwa nafsi hii kuishi miongoni mwa viumbe wengine wanaoishi. Hata hivyo, hata baada ya matibabu nafsi inaweza isihuike kwa sababu imepenyezwa maradhi fulani ambayo hayaponyeki. Nafsi hii imejiingiza kwenye upuuzaji, mchezo na burudani kwa kiasi kwamba imefikia hatua ya Ukafiri (Irtad). Mtu huyu sasa amekuwa kafiri (Murtad) na atakuwa amemkana Muumba au Dini, na hapa pia hukumu kama hiyo hiyo hutumika na kufanya lazima kumtenga mtu huyo kutoka kwenye jamii ya wanadamu. Sasa ni nafsi iliyokufa ambayo haitakuwa na faida kwa viumbe wanaoishi na wala haitaweza kuwa na faida kwao kama itaachwa kuishi miongoni mwao. Nafsi hii sasa itasambaza maradhi ambayo yatakuwa hatari kwa nafsi nyingine zinazoishi. Harufu na maradhi ambayo yanaweza kusambazwa na nafsi iliyokufa ni Ukafiri, Ushirikina na uchupaji mipaka (Ilhad). Kwa hiyo, sheria takatifu za Uislamu huamrisha kuuawa kwa Kafiri (Murtad) ili kuisafisha jamii ya wanadamu kutokana nao, kwa sababu ukafiri (Irtad) ni mardhi yasiyo ponyeka. 1 1Katika Uislamu hukumu kwa ajili ya kafiri/Murtadi ni kuuawa. Lakini makafiri/Murtadi wako aina mbili, moja ni kafiri/Murtadi kwa asili ya kuzaliwa (Murtad Fitri) na nyingine ni kafiri/ Murtadi Mili. Murtadi, wa asili ya kuzaliwa ni mtu yule ambaye anakuwa kafiri licha ya kuwa
9
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:22 PM Page 10
Maadili Ya Ashura Mwislamu kwa kuzaliwa. Muhammad bin Muslim anasimulia kutoka kwa Imamu as-Sadiq (as) kwamba wakati Imamu as-Sadiq (as) alipoulizwa kuhusu kafir/Murtadi, alisema: Imamu alisema kwamba kafiri/Murtadi (Fitri) ni mtu yule ambaye licha ya kuzaliwa Mwislamu, huonesha wasiwasi kutoka kwenye Uislamu, hukanusha yale yote aliyoteremshiwa Muhammad (s.a.w.w.). Mtu kama huyo anabeba adhabu ya kifo cha wajib (Wajib Qatl). Mke wake anatenganishwa naye, mali yake inagawaywa kwa watoto wake na hata kama akitubia toba yake haikubaliwi. (Wasaelus Shia, Jz. 28, uk. 324, Sura 1, Sura ya “Haddul Murtad”, Hadithi ya 1) Kafiri/Murtadi (Mili) ni mtu yule ambaye hakuzaliwa Mwislamu, lakini badala yake alikuwa kafiri kabla, kisha akawa Mwislamu, na tena akawa kafiri. Hukumu ya kidini kwa ajili ya mtu kama huyo kwanza ni kumpa muda wa nyongeza wa siku tatu za kutubia na kuwa Mwislamu tena vinginevyo atauawa. Ali bin Jafar anasimulia kutoka kwa kaka yake Imamu Ridha (as) kwamba nilimuuliza: Je, mtu baada ya kuukubali Uislamu na tena akawa Mkiristo “Murtadi” nini hukumu yake? Yeye (as) akasema: Kwanza mpeni muda wa nyongeza ili kurudi na kama hafanyi hivyo muuweni. (Wasaelus Shia, J. 28, uk. 327, Sura 3, Sura ya “Haddul Murtad”, Hadithi ya 1)
Katika njia kama hiyo hiyo, kifo cha Umma vilevile hutokea. Umma wakati mwingine hufariki, ingawa mili na nafsi zao hubakia hai, mioyo yao huendelea kupiga, mili yao huendelea kuwa katika harakati, mapigo yao ya mishipa bado ni imara, ukumbusho wao wa Mungu utakuwepo, matendo ya ibada yataendelea kufanywa, lakini bado jamii na umma zaweza kuchukuliwa kama zilizokufa. Kifo cha umma hutokea wakati wajibu wa Kuamrisha mema na Kukataza maovu unapoachwa, wakati mfumo wa maadili unapokuwa umegeuzwa, wakati maadili miongoni mwao yamekufa, na watu wakaacha Kuamrisha mema na Kukataza maovu. Sio lazima kwamba kama mwili uko hai, basi pia nafsi na moyo viko hai. Watu wataendelea kufanya matendo ya ibada, lakini bado Ummah huchukuliwa kwamba umekufa; mapigo ya moyo wa Umma yamekufa, na hii ni kwa sababu jukumu la wajibu la Kuamrisha mema na Kukataza maovu limekufa miongoni mwa watu. Hii ndiyo sababu Kiongozi wa Mashahidi alisema kwamba naondoka kwa ajili ya kuutengeneza Umma wa babu yangu. Ingawa mlevi, mchupa mipaka na mtu dhalimu kama Yazid alikuwa katika mamlaka ya utawala, Imamu Husein (as) hakusema kwamba naanzisha uasi huu kwa ajili ya kuwarekebisha watawala. Kuanzia hapa tunatambua kwamba Umma ulikuwa 10
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:22 PM Page 11
Maadili Ya Ashura umekufa ; kulikuwa na ufisadi ndani ya Umma ingawa walikuwa wanafanya ibada za wajibu za kidini. Bado Yazid, fisadi, mlevi, mchupa mipaka na mkanushaji wa sheria za dini alikuwa anatawala juu yao. Uthibitisho mkubwa wa utiifu wa Umma kwenye matendo ya ibada za dini ni kwamba wakati Imamu Husein (as) anaondoka kuelekea Iraq kutoka Makka, Umma wote ulikuwa tayari wakiwa wamevaa Ihram zao kuelekea Mina. Walikuwa wanatekeleza ibada tukufu ya Hijja. Hivyo, Umma kwa hakika ulikuwa watu wa dini, walikuwa wameshikamana sana na sheria za dini, lakini bado hawakumuitikia Imamu Husein (as). Imamu Husein alivua Ihram yake na akawakumbusha watu kwamba huu sio wakati wa kufanya Hijja; bali ni wakati wa kuilinda Hijja. Wakati huu wajibu wetu wa dini sio wa kufanya Hijja bali kitu kingine, hivyo fuataneni na mimi. Lakini Umma ambao ulikuwa mfuasi wa Shariah, ambao mwili na nafsi yake ilikuwa hai bado haukuitikia mwito wa Kiongozi wa Umma (Imam-e-Ummat). Umma wa watu wa dini walishindwa kumsaidia Kiongozi wa Umma kwa sababu Umma na Jamii ilikuwa imekufa. Kiongozi wa Umma aliendelea kuita, lakini waliendelea kukataa kumsaidia kwa kutoa sababu za kidini na sababu za kufanya Hijja. Ufisadi katika Umma kwa dhahiri ulikuwa wazi kwa sababu mtawala dhalimu alikuwa anakubaliwa na Umma. Kama Umma ungelikuwa hai, basi ufisadi na watawala walevi wasingelikuwa na moyo wa kuja kwenye madaraka na kuanza kutawala juu ya Umma. Hivyo, maradhi halisi yalikuwa ufisadi huu ulioko ndani ya Umma, ambao Imamu Husein (as) kwa usahihi kabisa aliutambaua. Hili ni jukumu la Viongozi na Walinzi kutambua maradhi ndani ya Umma. Yule ambaye hawezi kutambua maradhi ya Umma hawezi kamwe kuchukuliwa kama kiongozi. Kiongozi ni yule tu mtu ambaye anaweza kutambua maradhi ya Umma, anajua wakati wa kuongea, dhidi ya yule anayetaka kumtolea kauli, sehemu ulipo ufisadi, na dhidi ya yule ambaye anataka kumtolea sauti yake. Hivyo, Kiongozi wa Mashahidi alisema kwamba “Naanzisha uasi huu kwa ajili ya kuutengeneza Umma� ingawa Yazid amefikia hatua ya Ukafiri (Irtad), alikuwa fisadi mchupa mipaka, na ana moyo uliokufa. Wakati huohuo, Umma vilevile ulikuwa umekufa na umetekwa na ufisadi; hali ambayo inalazimu marekebisho.
6. Tofauti kati ya Vita vya Maadili na Vita vya Madaraka Wakati watawala wanapopingwa, na uasi na mapambano yanaanzishwa dhidi ya watu wanaotawala, basi aina hii ya vita ni vita vya madaraka. Katika mapambano ya madaraka, mtu mmoja mwenye nguvu anashikilia hatamu za mamlaka ya utawala katika mikono yake na kuna mtu mwingine anataka kuinyakuwa nafasi kutoka kwake, kuchukuwa mamlaka ya utawala wake, na kwa kumuangamiza yeye 11
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:22 PM Page 12
Maadili Ya Ashura mwenyewe anataka kukalia kiti chake cha utawala. Vita hivi vinapiganwa kwa mpango wake mwenyewe wa kanuni, na katika serekali kila zama kuna silaha zinazotumiwa katika mapambano ya madaraka. Majeshi ni ya aina tofauti, michezo ya vita ni tofauti na mapambano vilevile huendelea kubadilika. Pia kuna aina fulani ya vita ambavyo sio dhidi ya mtu aliyeko katika madaraka, bali badala yake ni dhidi ya maadui wa maadili, na vita kama hivyo huitwa “vita vya Maadili�. Hii maana yake upande mmoja kuna watu wenye maadili makubwa ya binadamu na katika upande mwingine kuna watu mafisadi na maadili maovu ambao wanalenga kuyavunja yale maadili makubwa ya binadamu. Watu walio na maadili ya binadamu ya kimungu hujaribu kulinda maadili ya binadamu ya kimungu na kuyavunja maadili machafu na ya kiovu; hivyo hapo huanza vita vya miongoni mwao ambavyo hujulikana kama Vita vya Maadili. Aina hii ya vita pia ina taratibu na sera zake ambazo ni tofauti kabisa na vita vya madaraka. Vigezo vya kushinda na kushindwa vya vita hivi pia ni tofauti kwa kulinganisha na vita vya madaraka. Ili kushinda vita vya madaraka tunahitaji wanajeshi na wapiganaji wenye nguvu. Katika vita vya madaraka, mtu ambaye ana nguvu zaidi, jeshi kubwa, na rasilimali kubwa anaweza kushinda vita. Kama wanajeshi wa upande mmoja wakifa kwa wingi au kutoroka kutoka kwenye uwanja wa mapambano na mpinzani akateka uwanja, basi mtu ambaye amepoteza wanajeshi wake ameshindwa vita. Kanuni za vita vya maadili ni tofauti kabisa na vita vya madaraka. Vita vya maadili, wakati mwingine, hushinda wale ambao wamekufa na kushindwa wale ambao wametoka kwenye vita wakiwa hai. Kwa vita vya maadili sio lazima kuwa na mashujaa, watu mashuhuri, na askari wenye nguvu ili kushinda vita. Vita vya maadili vyinaweza kuwa vya ushindi kwa mzee mnyonge wa miaka tisini na tisa au kwa mtoto wa miezi sita. Ili kupigana vita vya madaraka, kundi la watu walioteuliwa ndani ya Umma wamepewa majukumu mahususi; hii ndio sababu wanawake hawatakiwi kujishughulisha katika aina hii ya vita. Hata hivyo, wakati ikija kwenye vita vya maadili jukumu la wanawake kwa njia yoyote sio dogo kama kushinda lile la wanaume. Silaha zinazotumika katika aina hii ya vita vilevile ni tofauti na zile zinazotumika katika vita vya madaraka. Ukweli ni kwmba mikono mitupu na hata mikono iliyofungwa kwa kamba inaweza kushinda vita vya maadili. Kutoka hapa tunatambua kwamba vita vya Karbala vilikuwa vita vya maadili; ambayo ni nani alikuwa mshindi na nani walioshindwa?
12
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:22 PM Page 13
Maadili Ya Ashura Ili kushinda vita hivi vya maadili huhitaji kuwa na silaha za utaalamu wa hali ya juu kama vile vifaru au mabomu bali unachohitaji ni maendeleo ya maadili hayo matukufu ndani ya nafsi zetu wenyewe. Wakati sifa zilizohusishwa pamoja na maadili haya zikiendelezwa, basi hata wazee, vijana, wanawake au watoto wanaweza kushinda vita hivi. Katika vita vya maadili hatuhitaji tu watu kama Habib ibn Mazahir na maaskari kama Abbas (as) na Ali Akbar (as) bali hata mtoto askari wa miezi sita kama Ali Asghar (as) pia ni wenye manufaa. Pambano la Ali Asghar lina umuhimu wa sawasawa na ule wa Ali Akbar (as). Athari ya kufa kwao wote mashahidi kuna fanana. Kwa kweli athari ya kifo cha shahidi cha Ali Asghar (as) ilikuwa ni zaidi. Wakati Ali Akbar (as) alipoingia kwenye uwanja wa mapambano, maadui bila ya shaka waliingiwa na hofu na woga, lakini wakati Ali Asghar (as) alipoingia kwenye uwanja wa mapambano, jeshi la Umar ibn Sa’ad llikuwa karibu kushindwa. Hivyo, mtu huyu maluun alisema “Muueni huyu mpiganaji mdogo upesi, kama akibakia katika uwanja wa mapambano kama hivi kwa muda mchache zaidi basi jeshi langu litaasi na tutashindwa.” Hii ni kwa sababu mpiganaji wa maadili na tabia njema amekuja kwenye uwanja wa mapambano.
7. Jukumu la Wanawake katika Vita vya Maadili Wakati Imamu Husein alipoanzisha vita vya maadili, vilevile alichukuwa wanawake pamoja naye, ingawa alishauriwa asiwachukuwe mabibi wale watukufu kama vile mabinti wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), mabinti wa Ali (as) na Fatima (as) katika safari hii. Sayyid ibn Taus anasimulia katika ‘Alharaf‘ kwamba asubuhi wakati Imamu Husein (as) alipokuwa anakaribia kuondoka Makka kuelekea Iraq, usiku ule ule ndugu yake Muhammad ibn Hanafiya alikuja kukutana naye na akasema “Ewe kaka yangu! Unatambua vizuri sana kuhusu uovu na ulaghai ambao watu wa Kufa walioufanya dhidi ya baba na kaka yako. Nina wasiwasi watakufanyia hivyohivyo, kwa njia ileile waliyoifanya kabla, hivyo kwa maoni yangu usije ukaondoka Makka,” Yeye (as) akajibu: “Ndugu yangu! Kuna uwezekano kwamba Yazid bin Mu’awiyya anaweza kuniuwa ndani ya Haram (Mji mtukufu wa Makka) yenyewe, na katika hali hii itakuwa ni karaha kwa utukufu wa Nyumba ya Allah”. Kwa hili Muhammad ibn Hanafiya akasema: “Kama hii ndio hali yenyewe basi nenda Yemen au sehemu nyingine yoyote, na kwa kweli watu wa Yemen ni wazuri kwa ulinzi na usalama.”
13
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:22 PM Page 14
Maadili Ya Ashura Yeye (as) alisema: “Nitafikiri kuhusu yote uliyosema”. Lakini punde tu ilipokuwa asubuhi, alianza safari yake kutoka Makka kuelekea Iraq. Muhammad ibn Hanafiya akaja mbio na akakamata hatamu za ngamia wake ambayo Yeye (as) alikuwa amempanda. Akasema: “Jana si uliniahidi kwamba utafikiri?” Imamu Husein (as) akasema: “Ndiyo, niliahidi”. Muhammad ibn Hanafiya akasema: “Sasa kwanini umeamua kuondoka mapema hivi?” Yeye (as) alisema: “Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) alinijia baada ya wewe kuondoka (jana usiku). Alikuwa ananiambia kwamba ‘Ewe Husein, ondoka sehemu hii. Ni utashi wa Allah (s) kwamba unauliwa Shahidi”. Muhammed bin Hanafiya akasema: “ Inna Lillahi wa Inna Ilaihi Raajeoon, kama hali ni hii, basi kwanini unawachukuwa wanawake pamoja na wewe? Yeye (a.s) akajibu: “Utashi na kusudio la Allah ni kwamba ili wawe mateka” (Mawassae Kalematul Imam Hussain uk. 328, 329)
Kwa vile Imamu Husein (as) alikuwa akipigana vita vya maadili, vilevile alichukuwa wanawake wake pamoja naye, hii ilikuwa ni kwa sababu hii sio aina ya vita ambavyo ni vinakatazwa kwa wanawake; bali hivi ni vita ambavyo vinajuzu kwa wanawake. Sasa swali ni vipi wanawake wa Karbala walivyoshinda vita hivi?
A. Sifa za Zainab (as) Bibi Zainab (as) alitikisa nguzo za batili kwa kutoa khutba kali katika sehemu ya soko na baraza. Ibn Ziad na Yazid wote walimuuliza maswali (Bibi huyu). “Je, umeonaje jinsi alivyokufanyia Allah? (Lahoof uk. 49)
Watu wote hawa walimdhihaki Bibi Zainab. Walifikiri kwamba ni mwanamke kwenye huzuni ambaye kaka, watoto na takriban watu wote wa karibu yake wote wameuawa kishahidi. Akiwa na moyo uliovunjika na ulioumia, mikono iliyofungwa nyuma ya shingo yake, kichwa wazi bila mtandio amesimama katika baraza; 14
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:22 PM Page 15
Maadili Ya Ashura hivyo tunaweza kumchoma na kuhuisha majiraha yake kwa kwa kumuuliza maswali. Bibi Zainab (as) alijibu:
“Tumeyaona matendo ya Allah (s) mazuri mno na ya kupendeza, na hatukuona kitu kingine chochote kama uzuri kutoka kwa Allah (s)”. Bibi huyu hapa anawasilisha maadili; kwamba sisi kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kamwe hatulalamiki kwa Allah, sisi ni wenye kupendezewa na wenye shukurani nyingi kwa Allah kwa kukubali mihanga yetu. Sisi ni mfano wa maadili mazuri (Ma’ruf) ambapo ninyi ni mfano wa uovu (Munkar), na katika vita vya maadili mazuri (Ma’ruf) dhidi ya uovu, ushindi siku zote uko pamoja na mazuri.
B. Bibi Fatima Zahra (s.a) na vita vya maadili Bibi Fatima (as) alikuwa mshindi katika vita vya maadili. Baada ya kufariki kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), hali ilibadilika. Watu wanafikiri kwamba hali ya wakati ule ilikuwa ni ya kupigania madaraka, lakini ukweli ni kwamba madaraka kamwe hayakuwa ndio suala. Hii ni dhahiri kutokana na ukweli kwamba suala la yupi atachukuwa madaraka lilipokuja, Ali (a.s) aliruhusu lichukuliwe na watu wengine na kwa muda wa miaka ishirini na tano alikaa kimya nyumbani kwake. Suala haswa lilikuwa ni lile la maadili baada ya kifo cha Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.), hivyo Ali (a.s) alimudu gharama ya kunyimwa madaraka lakini sio kutokana na maadili. Bibi Zahra (a.s) aliona kwamba maadili yalikuwa yanakanyagwa ambayo hujumuisha maadili muhimu sana ya kuunga mkono na kulinda Wilayat. Kulikuwa hakuna mtetezi wa Wilayat na Walii wa Allah ameachwa peke yake. Tangazo la Wilayat lilitolewa mwezi 18 Dhilhajj katika mkusanyiko wa mahujaji 120000 ambao walitoa kiapo chao cha utii kwa Wilayat ya Ali (as), hata hivyo, baada tu ya miezi miwili na siku kumi, wakati Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) alipofariki, Walii wa Allah (s) alitengwa. Hivyo, Bibi Fatima (as) alitoka nje kuitetea Wilayat ya Ali (as), yeye mwenyewe peke yake. Alivumilia aina tofauti za misiba ili kupata ushindi katika vita hivi vya maadili, alisema:
“Ewe baba yangu! Misiba ambayo imetupata juu yetu, kama (misiba) hii ingetokea katika siku zenye mwanga, (siku hizo) zingebadilika kuwa zenye giza.” (Manakibe Aale Abi Talib, Ibne Shaher Aashob, Jz. 1, uk. 208)
15
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:22 PM Page 16
Maadili Ya Ashura Bibi Fatima (s.a) aliendelea kuonesha huzuni zake kwa kiasi kwamba watu wa Madina walilalamika kwa Ali (as) mabibi zao wanasumbuka na watoto wao hawawezi kulala kwa sababu ya kuendelea kuomboleza kwa mke wake. Hivyo Ali (as) aliandaa Nyumba ya Huzuni (Baitul Huzun) na akamuambia Bibi Fatima (as): “Ewe bibi yangu! Njoo hapa na uomboleze, watu wa Madina wanasumbuliwa na maombolezi yako”. Maombolezi haya hayakuwa maombolezi tu ya hisia bali yalikuwa ni maombolezi kwa ajili ya maadili ambayo yalikuwa yanapotea. Sababu ambayo iliwafanya watu wa Madina wasiweze kuvumilia maombolezi haya ilikuwa ni kwa sababu maombolezi haya yalikuwa kwa ajili ya madhumuni makubwa na yamebeba ujumbe ndani yake.
8. Imamu Husein (a.s) – Mfasiri wa matendo wa kazi ya Kuamrisha mema na Kukataza maovu Imamu Husein (a.s) alitangaza kazi ya Kuamrisha mema na Kukataza maovu kama madhumuni ya harakati zake ambazo zilikuwa shuhuda kwa urithi wake. Wajibu huu mtukufu uko dhahiri kwenye sehemu mbalimbali katika simulizi na khutba zake. Wakati alipokuwa anaaga kwenye kaburi la babu yake, alisema:
“Ewe Allah! Hili ni kaburi la Mtume wako (s.a.w.w.) na mimi mjukuu wa Mtume wako Muhammad (s.a.w.w.). Nakabiliana na jambo ambalo unalijua vizuri zaidi kuliko mimi. Ewe Allah! Nayapenda maadili mema na nayachukia maovu.” (Mawassae Kalematul Imam Hussain, uk. 278)
Baadhi ya wanachuo vilevile wameisimulia hii kama sehemu ya Khutba ya Mina, katika hii Yeye (as) alionesha kwenye jukumu lake kubwa. Anasema:
“Mbona watawa wao na maulamaa wao hawawakatazi maneno yao ya dhambi na uadui na ulaji wao wa haramu? Hakika ni mabaya waliyokuwa wakiyafanya.” 16
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:22 PM Page 17
Maadili Ya Ashura
“Walilaaniwa wale waliokufuru miongoni mwa wana wa Israil kwa ulimi wa Daud na wa Isa mwana wa Maryam. Hayo Ni Kwa sababu waliasi, nao walikuwa wakiruka mipaka.
Walikuwa hawakatazani mambo mabaya waliyokuwa wakiyafanya. Hakika ni maovu waliyokuwa wakiyafanya.” (Surah Maida, Ayah 63, 78, 79)
“Hakika tuliteremsha Taurat yenye uongozi na nuru, ambayo kwayo Manabii waliojisalimisha na watawa na wanazuoni, waliwahukumu mayahudi; kwani walitakiwa kukihifadhi Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Nao walikuwa mashahidi juu yake. Basi msiwaogope watu bali niogopeni mimi. Wala msiuze Aya zangu kwa thamani chache. Na wasiohukumu kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio Makafiri.” (Surah Maida, Ayah 44 and Surah Tauba 71)
“Na waumini wanaume na waumini wanawake ni mawalii wao kwa wao. Huamrishana mema na kukatazana maovu. Na husimamisha swala. Na hutoa zaka. Na humtii Mwenyezi Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hao Mwenyezi Mwenyezi Mungu atawarehemu. Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye nguvu mwenye hekima.” (Mawassae Kalematul Imam Hussain, uk. 274, 275)
17
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:22 PM Page 18
Maadili Ya Ashura “Enyi watu! Jifundisheni kutokana na laana ambayo Allah (s) ameiweka juu ya wanachuoni. Wakati Allah (s) aliposema: Mbona watawa wao na maulama wao (Mayahudi) hawawakatazi maneno yao ya dhambi? Allah (s) anasema kwamba wale ambao wanatokana na Bani Israil ambao wamekuwa makafiri wamelaaniwa. Wamelaaniwa kwa kiasi kwamba chochote wafanyacho (wanachuoni wa Bani Israil) yalikuwa ni matendo maovu mno. Allah (s) amewalaani kwa sababu wanachuoni hawa wamezoea kuwaangalia wakandamizaji wakipituka mipaka na kueneza ufisadi mbele yao lakini bado hawawakatazi. Walikuwa wamevutiwa na manufaa waliyokuwa wakiyapata kutoka kwa wakandamizaji hawa na walikuwa wanaogopa kupata hasara na adhabu, ingawa Allah amewaambia watu kumuogopa Yeye tu na sio watu wengine. Allah (s) vilevile amesema kwamba: “Na waumini wanaume na waumini wanawake ni mawalii wao kwa wao. Huamrishana mema na kukatazana maovu.” Katika muktadha wa khutba hii Imamu Husein (a.s) anasema:
“Allah (s) ameamrisha wajibu wa Kuamrisha mema na Kukataza maovu kwa sababu kama wajibu huu utafikishwa na kutekelezwa basi wajibat nyingine ngumu na nyepesi vilevile zitatekelezwa. Sababu yake Ni kwamba Kuamrisha mema na Kukataza maovu ni wito kwenye Uislamu, kurudisha haki zilizoporwa, upinzani kwa wakandamizaji, uadilifu wa kugawa ngawira na kodi, na njia za kukusanya sadaka kutoka kwenye sehemu sahihi na kuzigawa kwa watu wanaostahiki.” (Mawassae Kalematul Imam Husain (a.s), uk. 274, 275)
Kusisitiza juu ya Kuamrisha mema ni sifa ya Imamu Husein (a.s). Wakati ambapo anatangaza kanuni za tendo hili ambalo ni thabiti mpaka Siku ya Hukumu, anasema:
“Nataka Kuamrisha mema na Kukataza maovu.” Imam Husein (a.s) ametuonesha maelekezo ya kimatendo ya aya hii kwa damu yake takatifu. 18
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:22 PM Page 19
Maadili Ya Ashura
“Na liwepo miongoni mwenu kundi lenye kulingania kwenye heri, na kuamrisha mema na kukataza maovu. Na hao ndio wenye kufaulu.” (Surah Aale Imran, Ayah 104)
Kuna wengine wengi ambao wameelezea Aya hii. Wafasiri wengi wakubwa wameelezea maoni yao kuhusiana na Aya hii katika vitabu vyao vya tafsiri lakini wamefanya hivyo kwa kukaa maktaba, wakichambua baadhi ya vitabu, kuowanisha baadhi ya Aya nyingine na hadithi, na kisha baada ya uchambuzi wa kielimu waliwasilisha maelezo ya Aya hii. Imamu Husein (a.s) ametafsiri juu ya suala hili katika njia tofauti kabisa. Alisimama katika kivuli cha panga katika joto kali linalounguza, akiumwa kiu na njaa, na kupigana na maadui katika uwanja wa mapambano, aliwasilisha tafsiri ya kimatendo ya Aya hii kwa matendo yake. Ujumbe ambao Imamu Husein (as) aliufikisha kwa watu ulikuwa kwamba kama wanataka kuielewa Qur’ani Tukufu na kuhitaji tafsiri ya Aya hii, basi kile ambacho Imamu Husein (as) alichokuwa akifanya siku hiyo ilikuwa ndio tafsiri yake. Wakati unapowaona kwamba watu wanafanya matendo maovu, wanayavunja maadili mema na hawatendi mema, ni wajibu juu yako kuweka kando mafunzo ya kielemu ya maadili na badala yake tenda juu ya mwenendo wake, tangaza ujumbe na kaulimbiu hii. Kazi ya Kuamrisha mema na Kukataza maovu haifanywi kwa kutoa hutuba katika mimbari. Huwezi kumuamrisha au kumuachisha mtu kwa kutoa amri katika mimbari. Sana utakachofanya katika mimbari ni kutoa hutuba ambazo hufafanua masuala na kutoa mwongozo. Unaweza kusoma baadhi ya Aya, hadithi au kisa fulani cha kihistoria katika mimbari. Hata hili linaweza kufanywa tu kutoka kwenye mimbari zile zenye kuendeshwa na watu wenye elimu. Kuna baadhi ya mimbari ambako mahatibu hueneza ujinga na udhalilishaji miongoni mwa watu. Zile mimbari ambazo zina adabu nzuri angalau hutoa hutuba ambazo huneza elimu na kujadili masuala ya kimaadili. Hata hivyo, kutoa darasa na hutuba, kuelemisha watu kufundisha maadili yote haya ni tofauti na utekelezaji halisi wa kazi ya Kuamrisha mema na Kukataza maovu. Hebu ngoja nielezee hili zaidi kwa mfano. Kama sheria za trafiki katika nchi zinavunjwa na unaamua kutenda dhidi ya makosa haya, kamwe huwezi kutokomeza makosa haya kwa kukaa ndani ya msikiti na kutoa hutuba kutoka 19
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 20
Maadili Ya Ashura kwenye mimbari kwa sababu kama kwa kweli unataka kuzuiya makosa haya basi lazima utoke nje kwenye njiapanda mtaani. Hapa ndio ambapo unaweza kuja na kusimama kwenye sehemu ya uvunjaji wa sheria, kwa kuashiria na kutoa ishara za mkono kwa trafiki, unaweza kurekebisha makosa haya ya uvunjaji wa sheria. Lazima usimame kwenye njiapanda na kusimamisha magari upande mmoja huku ukiyaruhusu magari kutoka upande mwingine na halikadhalika. Kama mtu yule ambaye yuko nje kwenye njiapanda akisema kwamba napigana dhidi ya uvunjaji wa sheria za trafiki, basi madai yake ni sahihi na kweli kwa sababu matendo yake yanaunga mkono madai yake. Hivyo kuzuiya uvunjaji wa sheria za trafiki haiwezikani kwa kuandika tu dhidi yake katika vitabu au kuongea kutoka juu ya mimbari. Halikadhalika kazi ya Kuamrisha mema na Kukataza maovu haitekelezwi tu kwa kuandika kwenye vitabu, darasa na kutoa khutba, kwa hili lazima ujiunge kwenye mapambano kati ya mema na maovu. Mema (Ma’ruf) na maovu (Munkar) yote yapo kwenye jamii. Unaweza tu kuzuiya uovu (Mukar) kwa kuwepo kwenye sehemu ambako maovu (Munkar) hufanyika na kusambazwa zaidi. Wakati watu walipomuendea Imamu (as), baadhi walimshauri asiondoke Makka, afanye mahubiri kwa kuhadhiri, kukaa juu ya mimbari na kufanya kazi ya Kuamrisha mema na Kukataza maovu, ili kwamba aondokewe na waji wake wakuanzisha jihadi. Imamu Husein (as) alisema kwamba yeye kamwe hatafanya hili, badala yake Yeye (as) atakwenda Iraq na kufanya kazi ya Kuamrisha mema na Kukataza maovu. Yeye (as) atapambana na maovu kwenye chanzo ambako yanasambazwa. Alisema:
“Je hamuoni kwamba watu hawafanyi uadilifu na batili haizuiliwi? Chini ya mazingira haya muumini lazima awe imara asitetereke hata kutoa uhai na kuwa tayari kukutana na Mola wake (Liqaallah).” (Mawassae Kalematul Husain – uk. 356)
Wakati ikiwa hakuna matendo mema na hakuna mtu yeyote anayekataza batili; basi haja ya Kuamrisha mema hujitokeza. Kisha lazima uvae mavazi ya kijeshi ya maadili, chukua upanga wa unyoofu na kuwa imara katika uwanja wa mapambano wa maadili. Kuwapinga wachupa mipaka ya maadili ni Kuamrisha mema na Kukataza maovu. 20
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 21
Maadili Ya Ashura
9. Wafuasi wa Husein na wafuasi wa Yazid Wakati Imamu Husein (as) alipoingia kwenye uwanja wa mapambano ya maadili na kuanzisha vita vya maadili, Yeye (as) alitangaza kwamba naanzisha uasi huu kwa madhumuni ya Kuamrisha mema na Kukataza maovu. Imamu Husein (as) alilinda misingi ya kimaadili na kuipa maisha ya milele wakati alipopigana na kushinda dhidi ya maadili hasi. Vita hivi vya maadili vilikuwa vinaendelea tangu zamani, wapiganaji kutoka sehemu zote waliendelea kupigana lakini alikuwa ni Imamu Husein (as) ambaye hatimaye alishinda mapambano haya kati ya mema na maovu. Ni maadili gani haya ambayo Imamu Husein (as) ameyahuisha, kuyapa uhai na kuyafanya kuwa imara, yakudumu na kweli kama siku nyeupe, mpaka Siku ya Hukumu. Sasa, hakuna Yazid kamwe atakaye thubutu kusogea dhidi ya maadili haya, kwa sababu mizizi ya maadili haya sasa ina damu ya Imamu Husein (as). Maadili haya yamekuwa yakirutubishwa kwa damu ya watoto na masahaba wa Imamu Husein (as), na yametegemezwa juu ya harakati za wanawake wa familia ya Imamu Husein (as) Haya ni maadili ya Ashura, maadili ya Karbala na Husein (as) ambayo hujulikana kwa jina la “Hussainiyat” ulimwenguni pote. Hussainiyat ni jina la maadili haya matukufu ambayo yanapingwa na baadhi ya maadili ya Yazid ambayo yamejitokeza kwa jina la Yazidiat. Ilikuwa ni maadili hayahaya ya kiuovu, kishetani na ya kinyama ambayo Imamu Husein (as) aliyatokomeza (katika zama zake). Sasa katika zama zetu, lazima tuyahudumie maadili ya Hussainiyat na Huseini na kupigana dhidi ya maadili ya Yazidiat na Yazidi; hii ndio sababu Imamu Husein (as) akasema: “Mtu kama mimi hawezi kamwe kula kiapo cha utii kwa mtu kama Yazid.” Wakati alipokuwa anazungumza na Walid bin Utba alisema:
Ewe Amiri sisi ni watu wa nyumba ya utume na makazi ya ujumbe, na mahali ambapo Malaika wana pishana, na ni mahali pa rehema. Kupitia kwetu Mwenyezi Mungu ameanzia na kumalizia. Na Yazid ni mtu muovu, mlevi, muuwaji na mwenye kutenda maovu wazi wazi, kwakweli mtu mfano wangu hawezi kutoa 21
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 22
Maadili Ya Ashura kiapo cha utii kwa mtu mfano wake. Lakini acha tuamke nanyi muamke, tungojee nanyi mngojee, tuone ni yupi mwenye haki ya kuwa Khalifa na kupewa kiapo cha utii.” (Mawassae Kalematul Imam Husain, uk. 383)
Hakusema kwamba hatakula kiapo cha utii kwa Yazid, bali badala yake alisema kwamba watakuwepo watu kama mimi na watu kama Yazid. Hii ina maana kwamba watu wa aina hiyo wataendelea kupigana dhidi yao, vita vya maadili vitaendelea kujirudia tena na tena. Na wakati huo mtu kama mimi atajitokeza na kufanya kazi ya Kuamrisha mema. Atapigana vita hivi vya maadili na atawazuiya wale kama Yazid kusambaza maovu. Atashinda juhudi zao za kushusha unyofu na maadili ya kidini. Hivyo, mtu yeyote akijitokeza kama Imamu Husein (as), akapigana dhidi ya Yazidiat kwa kufuata maadili ya Husein (as) ni Huseiniat na mtu anayepambana naye ni Yazid, Huseini anataka maadili ya Huseini kutawala (jamii) wakati ambapo Yazidi anataka utawala wa maadili na maovu ya Yazidi. Vita hivi siku zote vitakuwepo; vita vya maadili vitaendelea kutokea. “Mapambano yameendelea kutoka siku ya uumbaji mpaka siku kati ya Taa Mustafa (Mtume) na Maovu ya Abu Lahab” (Kulliyate Iqbal, Urd Bange Dara, uk. 343)
Ili kuyalinda maadili ya Ashura, ni muhimu kuyatambua maadili haya ili kwamba kwa kuyafuata tunaweza kuwa Huseini. Kwa nyongeza, vievile ni muhimu kuyatambua maadili ya Yazid ili kwamba tuweze kupigana dhidi yao. Katika kitabu hiki tutaelezea maadili kumi ya Ashura yaliyochaguliwa. Vilevile tutajadili mbinu kumi ambazo Kiongozi wa Mashahidi alizifuata ili kuyalinda maadili haya, kuyapa maana yao ya kweli na jinsi alivyoyashinda maadili ya kinyama, hivyo kuyafanya maadili ya Ashura ya kudumu na ukweli daima. Tunamuonba Allah (s) atupe fursa ili tukamilishe suala hili na pia kuchukua jukumu la kuwasilisha maadili mengine yaliyobakia ya Ashura. Kwa baraka za Allah, mjadala huu utaendelea katika machapisho yafuatayo (Insha Allah). 2
2 Tanbihi: Kwa wasomaji wanaohitaji maelezo zaidi juu ya nukta hii ya Madhumuni ya Uasi wa wa Imamu Husein (as) anaweza kurejea kwenye chapisho letu mahususi “The Philosophy of Qayam-eHussain (a.s)”
22
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 23
Maadili Ya Ashura
Maadili ya Kwanza Agano na uwajibikaji 1. Agano na Uwajibikaji……...……………………………………………..…....24 2. Kusujudu kwa Shabbir (a.s) – Ni usalama kwa ajili ya uhai wa Dini na Ubinadamu……................………………….........................................24 3. Hakuna wakati maalumu au uliowekwa kwa ajili ya kusoma Du’a.….............25 4. Shukurani kwa ajili ya kuzaliwa katika nchi ya Waabudu Mungu Mmoja (Tawhid).……….................................................26 5. Maadili ya Husein (as) yanaweza tu kumfanya mtu kuwa Huseiniat (mfuasi wa Husein)...........................................................................27 6. Je, tukio la Karbala lilikuwa ni majibu ya madai ya kiapo cha utii?................28 7. Ushahidi wa jibu sahihi...…………...................................................................29 8. Uimamu ni Agano la Allah (s)...........................................................................31 9. Mazingira ya Madina wakati wa kuasi kwa Imamu Husein (as)......................32 10. Mantiki na namna ya fikira ya Imamu Husein (as).........................................33 11. Majukumu yaliyoaminishwa juu ya watu wa Allah (s)...................................38 12. Mwisho wa watu wazembe..............................................................................39 13. Mwana wa Mina katika baraza ya Yazid.........................................................44
23
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 24
Maadili Ya Ashura
1. Agano na uwajibikaji Imamu Husein (a.s) alitangaza Kuamrisha mema na Kukataza maovu kama lengo la kuasi kwake, ambalo lilimaanisha uhuishaji wa maadili, marekebisho ya mfumo wa maadili, kuwaanzishia tena wanadamu maadili yale ambayo yaliharamishwa na kuwasilisha maadili hayo kama sifa za wanadamu. Maadili haya ambayo yalihuika tena pamoja na damu ya Imamu Husein (as) na ambayo yatakuwepo mpaka Siku ya Hukumu hujulikana kama maadili ya Husein (as) na maadili ya Ashura. Miongoni mwa maadili haya, maadili ya kwanza ni Agano na Uwajibikaji. Imamu Husein (as) alianzisha uasi wakati ambapo watu walikuwa wanafuata dini kwa kiasi fulani, Umma wa Uislamu walikuwa wakitekeleza majukumu yao ya kidini lakini watawala walikuwa wakichupa mipaka na ni wahalifu. Hata hivyo, aina ya ufisadi, upitukaji mipaka na maovu kama unywaji wa pombe na uzinifu ambao tunauona leo, ilikuwa si kitu cha kawaida miongoni mwa Umma wa Uislamu. Imamu Husein (a.s) alisema kwamba alikuwa anaanzisha uasi kwa ajili ya kuurekebisha Umma, kwa sababu wakati mtawala muovu na mwenye kuchupa mipaka anapokaa juu ya Umma, vilevile mfumo wa utawala utaharibika. Kuishi katika mfumo huo ulioharibika (wa ufisadi) ni suala lingine lakini kuukataa mfumo huu wa kifisadi na kuamsha sauti dhidi yake bado inabakia ni wajibu
2. Kusujudu kwa Shabbir (a.s) – Ni usalama kwa ajili ya uhai wa Dini na Ubinadamu Maombi mawili au sajida mbili za Imamu Husein (as) zinastahiki umuhimu wa hali ya juu, ingawa sajida zake zote, matendo ya ibada, ibada za kidini na matendo yake yote yana umuhimu wake wenyewe. Sajida mbili za Kiongozi wa Mashahidi (as) ni za muhimu na maana kihistoria; kwa kweli ziko hai na daima mpaka Siku ya Hukumu. Kama mwanadamu anaweza kuelewa maana ya sajida hizi mbili basi anaweza kwa urahisi kutambua kwamba ni kwa sababu ya sajida hizi mbili kwamba dini leo hii iko hai. kwa kweli, ni kwa sababu ya sajida hizi mbili kwamba ubinadamu uko hai. Leo, kama kuna kitu kinachojulikana kama ubinadamu basi ni kwa sababu ya baraka ya sajida hizi mbili. Alifanya sajida moja katika ardhi ya Karbala na nyingine aliifanya katika uwanda wa Arafa. Dua ambayo aliifanya kabla au baada au pengine 24
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 25
Maadili Ya Ashura wakati wa kusujudu katika Arafa leo hujulikana kwa jina la “Dua-e-Arafah”. Kama tunaweza kuelewa “Dua-e-Arafah” na kutambua maana yake, basi tunaweza kutambua madhumuni ya Karbala. Hii ni kwa sababu sajida hizi ni aina mbili za mfululizo huo huo, ni za aina mbili za mfumo huo huo na sajida zote zilifanywa kwa madhumuni hayo hayo. “Dua-eArafah” yote ni yenye kuelemisha na tukufu sana, ni utambulisho kamili (Maarifat), ni u-irfani kamili, sajida yote imejaa ilmu, lakini mwanadamu huhitaji mshauri ili kuelewa hata sentensi moja ya dua hii. Madhumuni ya dua hii hayafikiwi kwa kusoma tu na kurudia maneno yake kwa ndimi zetu. Dua hii huhitaji somo kutoka kwa mwalimu, yote na kila sentensi huhitaji uelewaji na uchambuzi.
3. Hakuna wakati maalumu au uliowekwa kwa ajili ya kusoma Du’a Imekuwa ikisisitizwa kwamba dua maaluum lazima zisomwe wakati maalumu mahususi, kwa mfano ni tendo lililopendekezwa (Mustahab) kusoma “Dua-eArafah” ya Imamu Husein (a.s) mwezi 9 Dhilhajj. Hii haina maana kwamba lazima tusubiri mpaka siku hii ili kusoma dua hii. Halikadhalika, imesemwa pia kuhusu Dua-e-Kumail kwamba lazima isomwe siku ya alhamisi jioni, lakini hii haina maana kwamba hatuwezi kusoma dua hii siku nyingine yoyote au katika hafla yoyote. Baadhi ya waumini wanaweza wakafikiria kwamba kama wakisoma Dua-e-Kumail kwenye hafla yoyote isiyokuwa siku ya alhamisi jioni, wanaweza wakapatwa na hasara au itakuwa ni dhambi. Sio hivyo, dua hizi zinajuzu kusomwa kila siku kwa usiku na mchana. Unaweza kusoma dua hizi wakati wowote bila kufuata wakati wowote mahususi, ingawa muda ambao ni wenye manufaa sana umetajwa, lakini dua hizi zinaweza kusomwa mbali na nyakati hizi pia. Sio kwamba lazima ungojee mwezi 9 Dhihajj ili usome Dua-e-Arafah, kama unapenda, kila siku yako inaweza kuwa Siku ya Arafa. “Kila siku ni Ashura na kila sehemu ni Karbala” Hii ina maana, iko kwenye mamlaka yako, kama hutaki hata siku ya Ashura haitakuwa siku ya Ashura kwako, na ardhi ya Karbala pia haitakuwa Karbala kwako. Ardhi hii itakuwa Karbala kwa wale waliokunywa maana ya Karbala katika nafsi zao, siku hii itakuwa Ashura kwa wale ambao wana moyo wa Ashura ndani yao. Ashura huwa Ashura na nafsi yake, hivyo tunaweza kubadilisha siku yoyote tunayopenda kuwa Ashura. 25
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 26
Maadili Ya Ashura
4. Shukurani kwa kuzaliwa katikati ya Waabudu Mungu Mmoja Arafa ina vionjo vya hali ya juu. Tutajadili sentensi moja ya dua hii ambako Imamu Husein (as) wakati alipokuwa anatoa shukurani zake kwa ajili ya neema mbalimbali mbele ya Allah (s) alisema: “Ewe Mola wangu! Nakushukuru kwa neema zile ambazo umenibariki nazo kabla ya kuzaliwa kwangu na pia kwa neema zile ambazo nazipokea baada ya kuzaliwa kwangu.” Miongoni mwa neema nyingine nyingi, neema moja ambayo imekuwa msingi wa shukurani zake ambazo alizionesha katika Dua-e-Arafah kama “Ewe Mola wangu! Nakushukuru Wewe kwa kutoharisha sehemu ya kuzaliwa kutokana na ukafiri na ushirikina na hivyo kufanya maandalizi kwa ajili ya kuzaliwa kwangu.” Imamu (a.s) anasema katika dua hii:
“Ewe Allah! Ni kwa sababu ya huruma zako, neema na baraka juu yangu hukufanya mimi nizaliwe katika utawala wa viongozi wa ukafiri, wale ambao wamevunja agano lako na kuwakanusha Mitume wako. Umenifanya mimi nizaliwe katika zama zile za mwongozo. Kabala ya hili pia huruma zako na uswahiba wako ulikuwa pamoja na mimi wakati uliponiumba pamoja na uzuri na kunibarikia kwa neema zisizo na hesabu.” (Mafatihul Jinan, Page 475)
Ni nukta ya kuvutia kuona kwamba mtu asye na hawaa wala dosari yoyote kama Imamu Husein (as) anaelezea shukurani zake juu ya suala kama hilo. Imamu Husein (as) ni mtu adhimu sana kiasi kwamba hakukubali hata kuzaliwa katika sehemu ambako kuna utawala wa ukafiri na ushirikina. Imamu Husein (as) anashukuru kwamba kabla ya kuzaliwa kwake Allah (s) aliitoharisha ardhi ya Madina kutokana na ushirikina na ukafiri. Ni kitu gani Imamu Husein (as) anachosema hapa? Anatuambia kwamba usitamani hata kidogo kuzaliwa katika ardhi ya ushirikina, kama kweli unataka kuupata moyo wa Husein (as) ndani ya nafsi yako, kama unataka kuwa Huseiniat; basi kataa sehemu yako ya kuzaliwa kuwa ile ya ushirikina. Ingawa mazazi yako hayakuwa katika nchi yako lakini angalau mazazi ya watoto wako yako mikononi mwako. Kama kwa ajili ya hatima na majaliwa ya Allah (s) ulizaliwa katika ardhi ya ukafiri, ushirikina, uchupaji mipaka na uovu, basi kwa ajili ya watoto wako itoharishe nchi hiyo ili kwamba waweze kuzaliwa katika sehemu ambayo haina maovu haya. 26
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 27
Maadili Ya Ashura Imamu Husein (as) aliona kwamba ardhi ambayo Allah (s) aliisafisha kutokana na uchafu, ukafiri na ushirikina ilikuwa tena inachafuliwa na uchafu, uovu na ufisadi. Ingawa ilikuwa ni Damascus na sio Madina ambayo ilikuwa makao makuu ya serikali, na ambako kutoka huko ushirikina na ufisadi ulikuwa Madina. Sio Madina tu, ufisadi, uchafu na maovu kutoka Damascus ulikuwa unaenea ndani ya ulimwengu wote wa Kiiislamu. Chini ya mazingara haya, Imamu Husein (as) alianza uasi wake na alisema:
“Siondoki kama muasi, mchupa mipaka, fisadi na mkandamizaji, kwa kweli nataka kufanya marekebisho. Naanza safari yangu ili kuzuia ufisadi katika nchi za Kiislamu.” (Mawassae Kalemate Hussain (a.s), uk. 290, 291)
Maadili ambayo Imamu Husein (as) amewasilisha kwetu, ambayo hatimaye yakawa Maadili ya Ashura ni “Agano na Uwajibikaji.”
5. Maadili ya Husein (a.s) yanaweza kumfanya mtu kuwa Hussainiat (Mfuasi wa Husein) Kwa mijadala tu ya maneno kuhusu Karbala, mtu hawezi kuwa Mkarbala na kwa kujadili na kuzungumza kuhusu Ashura mtu hawezi kuwa Muashura, halikadhalika kwa mijadala tu na kusoma jina la Husein (as) mtu hawi Mhuseini. Ni mpaka hapo, iwapo maadili ya Husein (as) hayawi sehemu ya kuwepo kwetu na maadili ya Ashura hayafanyi sehemu ya maisha yetu, mtu hawezi kuwa Mhuseini. Wakati moyo wa Ashura unapokuwa sehemu yetu, hapo tu ndio tunaweza kuwa Waashura, Wakarbala na Wahusein. Kulikuwa na watu wengi waliokaa Karbala wakati Imamu Husein (as) alipowasili Karbala. Kulikuwepo na makabila mengi yaliyolowea kandokando ya Karbala. Wale ambao walikuwa wakikaa Karbala vilevile walikuwa wakiitwa Wakarbala, lakini watu ambao wanakuwa Wakarbala kwa sababu ya kukaa Karbala na watu ambao wanakuwa Wakarbala kwa kujifundisha kiini na makusudio yake ndani ya nafsi zao ni tofauti kabisa na wengine. Ili kutambua nafsi ya Ashura, Karbala na Imamu Husein (as), kwanza itatulazimu maadili yale ambayo Imamu Husein (as) ameyahuisha na kuyarejesha kwenye uhai siku ile ya Ashura pale Karbala. 27
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 28
Maadili Ya Ashura
6. Je, kadhia ya Karbala ilikuwa ni matokeo ya madai ya kiapo cha utii? Tunawasilisha hapa kwako swali, sio kwa madhumuni ya wewe kusoma au kwa ajili yetu ili wewe kutoa jibu, tunaleta swali hili pamoja na madhumuni kwamba lazima ufikiri kuhusu swali hilo sio sasa hivi, bali fikiri na kutafakari juu yake kila siku, kila saa mpaka mwisho wa pumzi yako, ili ufikie hitimisho zuri. Swali hili ambalo tunalileta ni “Je, Kadhia ya Karbala ilikuwa ni matokeo ya madai ya kiapo cha utii?� Hii ina maana kwamba kama mazingira haya dhahiri ya wakati ule ambao historia hutuambia hayakutokea, kwamba hata ingawa Yazid amepanda kwenye madaraka lakini kama hakudai kiapo cha utii basi kungelikuwa hakuna haja kwa Imamu Husein (as) kuondka Madina. Hivyo, pia kusingekuwa na haja ya kumpeleka mjumbe (Muslim bin Aqil) kwenda Kufa na watu wa Kufah pia wasingemsaliti na kumuacha Imamu (as) peke yake. Katika hali hii, nina swali kwa ajili ya Wahuseini ambao walikuwa wakiimba Husein, Husein kuanzia utoto wao, wale ambao wameona Shabih (vitu vya kufananisha) vya Husein (as) punde tu walipofungua macho yao wakati wa kuzaliwa, wale ambao walianza kusikia jina la Husein (as), wale ambao wametumia maisha yao yote wakisoma Husein, Husein, kama sasa mnao utambuzi na ufahamu kuhusu Husein (as), basi fikiri kama matukio yote haya yaliyotajwa mapema yalikuwa ni sharti kwa ajili ya kadhia hii ya Karbala, au kadhia ya Karbala ingelitokea hata bila masharti haya (au vigezo hivi)? Inawezekana kwamba mtu anaweza akafikiri kwamba hajui kama tukio la Karbala lingetokea au la? Anaweza akafikiri kwamba amesoma historia na ameelewa hali ambazo zilisababisha kadhia ya Karbala na hizi ni kwamba Yazid alidai kiapo cha utii, watu wa Kufa waliandika barua na kisha wakasaliti, na kwa matokeo ya yote haya tukio likatokea. Anaweza kwa kweli asielewe iwapo tukio la Karbala lingetokea bila matukio haya au la? Kama mtu ana rai hii kuhusu swali hili, basi ina maana kwamba hakumtambua Imamu Husein (as), yeye sio mfuasi wa kweli wa Husein (as), mtu ambaye ana moyo wa Ashura na Karbala ndani yake kamwe hawezi kusema kwamba sijui iwapo kadhia hii ingelitokea au la. Jibu lake lingekuwa kwamba kadhia hii ilikuwa itokee, lakini inawezekana kwamba ingeweza isitokee Karbala, ingeweza isitokee siku ya mwezi 10 Muharram, lakini ingeliweza kutokea mapema au baadae kwa vile ilikuwa imekadiriwa kutokea. Wakati Imamu Husein (as) alipokuwa anaondoka Madina watu walimshauri asiondoke. Imamu Husein (as) alisema kitu kama hicho hicho kwamba kadhia hii lazi28
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 29
Maadili Ya Ashura ma itatokea, kama sio leo basi ni kesho, kama sio kesho, basi ni keshokutwa, kama sio kwenye ardhi hii basi ni katika sehemu nyingine, lakini lazima itokee.
Alimuambia Ummu Salma: “Ewe mama yangu mpendwa! Naapa kwa jina la Allah (s) kwamba ninafahamu kwamba nitauliwa na sina changuo lingine mbali na hili.” (Mawassae Kalemate Imam Hussain, uk. 292) Ni kweli kwamba historia inasimulia kadhia hii kwamba Yazid alichukua hatua kwanza na Imamu Huseni (as) akajibu kwayo. Ni akili ya kawaida kwamba kama uasi huu uliofanywa na Imamu Husein (as) ulikuwa wa mjibizo na kama kungekuwa hakuna hatua yoyote, basi pia kusingekuwa na majibu. Hii ina maana kama Yazid asingechukuwa hatua na kudai kiapo cha utii basi Husein (a.s.) asingejibu kitu. Kama huu ndio uelewa wetu basi huonesha kwamba mpaka sasa hatujamuelewa Husein (as) na madhumuni yake. Kwa kweli alikuwa ni Husein (as) aliyechukua hatua kwanza na Yazid ndiye ambaye alijibu hatua za Husein (as). Wale ambao wanasema kwamba Imamu Husein (as) alizingirwa na akakimbilia Karbala kwa kujitenga, hao ni wale watu ambao wamesoma historia katika mtindo wa ngano; wanasema vitu kama hivyo bila ya kumuelewa Husein (as). Wale ambao wamemuelewa Husein (as), wanatambua kile ambacho kwa kweli kilitokea katika historia. Kwa juu huonekana kwamba walimzingira Imamu Husein (as) na kumpeleka Karbala, lakini kwa uhalisi alikuwa ni Imamu Husein (as) ambaye alizingira u-Yazidi wote na kuuleta Karbala. Alikuwa ni Imamu Huesin (as) ambaye alikuwa anasubiri kisababisho. Yeye (as) alikuwa akisubiri siku wakati Yazid atakapokuwa kashikwa katika mikono yake (as) ili kwamba aweze kuangamiza hekalu ya u-Yazidi, siku ambayo ataweza kuangamiza uovu, siku ambayo anaweza kuanzisha utawala wa maadili mema (Ma’ruf), siku ambayo anaweza kupata fursa kwa ajili ya mapambano ya maadili.
7. Ushahidi wa jibu sahihi Baba yake Yazid alikuwa mjanja na laghai. Ulaghai wake ulikuwa kwamba katika kila tukio aliweza kukwepa kukamatwa kwenye mikono ya Husein (as). Hii ina maana kwamba kila hatua yoyote ya uamuzi inapopangwa dhidi yake, alikuwa akikwepa kwa hila zake za ulaghai. Sio kwamba alikwepa majaribio ya Imamu Husein (as) tu, kabla aliweza kukwepa mashambulizi ya Imamu Hasan (as) na Imamu Ali (as) pia. Aliweza kuokoa ngozi yake kutokana na mapigo matatu ya 29
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 30
Maadili Ya Ashura Maimamu (as). Watu wawili wajanja walikuwepo katika historia; mmoja alikuwa baba yake Yazid na wa pili, mshauri wa baba yake, Amr ibn Aas. 3 Wakati mshauri wake alipomkabili Ali katika vita vya Siffin; jinsi alivyookoa maisha yake na kisha baada ya hapo, kauli ambayo aliitoa ilikuwa duni mno na ya kukirihisha kiasi kwamba hatuwezi kujileta wenyewe kuichapisha hapa. Alijulishwa jinsi alivyoukimbia upanga wa Ali (as). Matendo haya ya ujanja ujanja na hila yaliwapa usalama kila mara. Sio kwamba Imamu Hasan (as) alifanya mkataba na Mu’awiya ili kuokoa maisha yake, bali kwa matokeo ya mapatano haya maisha ya Mu’awiya yaliokolewa. Imamu Hasan (as) aliahidi kuumaliza kabisa mzozo huu wakati ulueule, Yeye (as) alitaka kuwaua kabisa na palepale watu hawa ambao walikuwa wakipanda mizozo na wasababishaji hawa wa matatizo, lakini adui mjanja siku zote hushinda mapambano, na kwa hila zake tu za kilaghai, huokoa maisha yake. Lakini Yazid hakuweza kutumia ujanja huu na hii ilikuwa fursa kamili ambayo kwayo Imamu Husein (as) alikuwa anaisubiri. Alikuwa anasubiri nafasi kwa ajili 3 Amirul-Mu’minin (as) anasema kuhusu Amr ibn Aas:
Wakati akiwa katika mapambano, pamoja na fahari kubwa hukemea na kuamrisha lakini ni mpaka tu panga zikija kwenye harakati. Wakati muda kama huo unapowadia hila yake kubwa ni kugeuka akiwa uchi mbele ya mpinzani wake. (Nahjul Balagha, Khutba 82, uk. 253) Mufti Ja’far Husein (ra) atoa ufafanuzi juu ya khutba hii kwamba mshindi wa Misr, Amr ibn Aas ameonesha ari yake kwa kugeuza uchi wake kuwa ni ngao. Tukio hili lilikuwa kwamba wakati wa vita vya Siffin, wakati alipopambana na Amirul-Mu’minin (as), ili kujikinga kutokana na pigo la upanga wa Ali (as) alikaa uchi. Wakati Amirul-Mu’minin (as) alipoona kitendo chake hiki cha kujidhalilisha aligeuza uso wake na kumhurumia maisha yake. Mshairi wa Kiarabu ameandika kuhusu yeye:
Hakuna sifa katika kuondoa matatizo kwa matendo ya udhalili, Njia ambayo Amr alikwepa matatizo siku ile ni kwa kujiweka uchi. Sio kwamba Amr ana akili ya uvumbuzi katika aina kama hizi duni, bali badala yake katika haya pia alikuwa mfuasi wa baadhi ya wengine. Hii ni kwa sababu mtu wa kwanza ambaye alifanya kitendo kama hicho alikuwa ni Talha bin Abi Talha, ambaye katika vita vya Uhud aliokoa maisha yake kwa kujiweka uchi mbele ya AmirulMu’minin (as) na kuonesha njia hii kwa wengine pia. Hata Basr ibn Abi Arthat alifanya kitu kama hicho wakati alipokuwa chini ya upanga wa Ali (as). Baada ya kufanya kitendo hiki alimuendea Mu’awiya katika hali hii ya uchi, ili kupoza hisia zake za udhalili Mu’awiya alimuwasilisha Amr ibn Aas kama rejea na akasema: “Ewe Basr, kwa nini uone uchungu na aibu kuhusu hili wakati tayari una mfano kama huo kwa Amr ibn Aas mbele yako.”
30
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 31
Maadili Ya Ashura ya kuangamiza mfumo mzima kabisa na kung’oa kila unywele wake. Imamu Husein (as) alipata fursa hii kwa sababu ya ujinga wa Yazid. Sio kwamba Yazid alifanya kitu na Imamu Husein (as) akajibu. Ilikuwa ni ujinga wake ambao uliishia kweye fursa iliyokuwa ikingojewa kwa hamu sana na Imamu Husein (as) ya kuuangamiza u-Yazid milele. Hivyo, sio kwamba kama matukio haya yaliyosimuliwa katika historia yasingetokea Imamu Husein (as) asingeanzisha harakati. Kama mtu anasema hivi basi kuwa na hakika kwamba hana uelewa juu ya Husein (as). Kwa nini? Hii ni kwa sababu kwa mujibu wa dhana hii, inaonekana kana kwamba Imamu Husein (as) alikuwa amekaa na kusubiri Yazid kutaka kiapo cha utii kutoka kwake, na kisha Imamu Husein (as) ilikuwa akatae hivyo ili kuruhusu mambo yatokee. Badala yake Imamu Husein (as) alikuwa akisubiri Yazid afanye ujinga ili kwamba Yeye (as) apate fursa ya kuuangamiza u-Yazid. Hii ni kwa sababu Imamu Husein (as) alikuwa mtu wa kuwajibika. Imamu na Uimamu wenyewe ndani yake ni jina la Agano (Ahad) na maana ya Agano ni Uwajibikaji.
8. Uimam ni Agano la Allah Qur’ani Tukufu imeelezea nafasi ya Uimamu (uongozi) katika maneno haya:
“Na Mola wake alipomjaribu Ibrahim kwa matamko, naye akayatimiza. Alimwambia: Hakika mimi nimekufanya Imam wa watu…” (Surah Baqarah, Ayah 124)
Wakati Allah (s) alipomuweka Nabii Ibrahim (as) katika mitihani mbalimbali na yeye kuishinda mitihani hiyo, kisha Allah (s) alimuambia Ibrahim (as) kwamba: Ninakufanya Imamu (Kiongozi) wa watu. Nabii Ibrahim (as) alimuomba Allah kwamba nafasi hii ya Uimamu iendelee katika kizazi chake pia.
“… (Ibrahim) akasema: Na katika Kizazi changu (pia) Akasema: Ahadi yangu haiwafikii madhalimu.” (Surah Baqrah, Ayah 124)
Allah alijibu na akasema: ‘Ewe Ibrahim, Uimamu ni agano langu na agano langu haliwezi kamwe kupewa kwa madhalimu na wakandamizaji.’ Kwa hili tunakuja kuelewa kwamba Uimamu ni agano la Allah (s) na maana ya agano ni uwajibikaji. 31
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 32
Maadili Ya Ashura Imamu ni mtu ambaye anachukuliwa na Allah (s) kama mwenye wajibu. Imamu maana yake mtu wa dini mwenye wajibu na mtu ambaye ana wajibu kwa mwongozo wa watu. Upinzani unaoneshwa tu na wale ambao hawahisi kulazimika kutenda kwa sababu ya akili yao ya kuzaliwa ya uwajibikaji, lakini matendo yao ni matokeo ya kile ambacho watu wengine huwafanyia wao. Watu wawajibikaji hawakai kimya wakingojea mtu fulani kutenda dhidi yao, hawakai tu kizembe na mikono iliyokunjwa na midomo iliyofungwa, macho yaliyoangushwa chini na ndege kutua juu ya vichwa vyao. Hawangojei muda kwa ajili ya mtu fulani kufanya kitu dhidi yao na kisha waoneshe upinzani wao. Mtu ambaye ana wajibu hatoi fursa kwa mtu fulani kutenda kwanza; yeye mwenyewe hutenda na hajiwekei mipaka kwenye ujibizo tu.
9. Mazingira ya Madina wakati wa upinzani wa Imamu Husein (as) Wakati Imamu Husein (as) alipoanzisha upinzani wake, mbali na yeye (as) Waislamu wengine wakubwa na mashuhuri walikuwa vilevile wakiondoka Madina. Sio kwamba ni Mashia tu ndio waliokuwepo Madina, kwa kweli Waislamu wakubwa walikuwepo kule. Masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wazee wenye miaka 80 mpaka 90 pia walikuwepo Mjini Madina, na baadhi ya masahaba wakati huo walikuwa wamevuka umri wa miaka mia moja. Hata miongoni mwa mashahidi wa Karbala, umri wa baadhi ya masahaba ulikuwa mkubwa zaidi ya miaka mia moja. Hii ina maana kwamba kuna watu ambao walishuhudia agano la Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.), agano la Amirul-Mu’minin (as), agano la Imamu Hasan (as) na sasa walikuwepo katika huduma ya Kiongozi wa Mashahidi (as). Wakati mwingine hutokea kwamba watu wote wakubwa hukusanyika sehemu moja, kama ilivyo leo Mashia wote wakubwa na mashuhuri wapo katika mji Mtukufu wa Qum nchini Iran. Halikadhalika masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), watoto wao na baadhi ya watu wenye kuheshimika na wanachuoni wakubwa walikuwepo mjini Madina. Mtu mashuhuri sana kama Abdullah ibn Abbas, ambaye alikuwa mwanachuoni mwanasheria, mfasiri na msimuliaji wa hadithi na mtu anayetambuliwa na wote Shia na Sunni alikuwepo Madina wakati huo. Mtu mwingine mkubwa alikuwa Abdullah ibn Zubair, ambaye dhidi yake Mua’wiya alimuonya mtoto wake (Yazid) katika wosia wake wa mwisho. Abdullah ibn Umar, mtoto wa Khalifa wa pili, Abdur Rahman bin Abu Bakr, mtoto wa Khalifa wa kwanza pia walikuwepo Madina. Katika hali kama hiyo, Yazid alipata taji la ufalme, na hapa ndio pale Imamu Husein (as) alipoanzisha maadili ya kwanza ambayo yalikuja kujulikana kama maadili ya Husein mpaka mwisho wa 32
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 33
Maadili Ya Ashura ulimwengu huu ambayo ni “Agano na Uwajibikaji.” Punde tu Yazid alipoingia kwenye madaraka, alitaka apewe kiapo cha utii na Husein (as) na wengineo, lakini kwa wengine, kwa namna fulani suala hili walilitatua. Abdullah ibn Umar alipiga kambi nje ya Madina na akawa anajishughulisha na ibada ili kwamba mtu yeyote asimsumbue na wala yeye asimsumbue mtu yeyote. Abdullah ibn Zubair pia kwa siri aliondoka Madina wakati wa usiku na kwa kupitia njia tofauti aliwasili Makka. Alichukua hifadhi ndani ya eneo takatifu la Kaaba Tukufu kwa vile ilikuwa sehemu takatifu hivyo kutakuwa hakuna hatari yoyote hapo. Abdullah Ibn Abbas alikuwa mwalimu, mwanachuoni – mwanasheria na mtu mkubwa. Aliendelea na mahubiri yake na darasa zake. Wanafunzi walikuwa wanahudhuria darasa zake na alikuwa amejishughulisha na hilo.
10. Mantiki na namna ya fikira ya Imamu Husein (as) Imamu Husein (as) hakuanzisha kambi kwa ajili ya kufanya ibada au kuendelea na mikutano yake ya mahubiri. Pia hakuenda kwenye Kaaba ili kupata kinga pale. Badala yake alikusanya familia yake yote, watoto, vijana na wanawake, alikusanya wasaidizi - wafuasi na masahaba wake na wakaondoka Madina. Watu wakamshauri kwamba kama alivyofanya Abdullah ibn Zubeir, na yeye pia lazima aiache njia ya kawaida na afuate njia isiyotumika sana ya jangwani ili kwamba mtu yeyote asiweze kumfikia, kumtambua na hivyo atakuwa salama kutokana na mashambulizi yoyote. Imamu Husein (as) alisema: Kamwe sitafanya hivi.4 Nitakwenda kwa kufuata njia ya kawaida inayotumiwa na wasafiri wote. Sitakwenda kwa siri kama wale wengine ambao kwa ajili ya kuokoa maisha yao waliacha njia sahihi na kusafiri katika giza, kupitia njia isiyojulikana ili kwamba asiwepo mtu yeyote wa kuwaona, badala yake mimi nitafuata njia ya kawaida ambayo kwamba kila mtu hutumia wakati wa kusafiri. 4 Wale waliompa ushauri Imamu Husein (as) 1. Muslim bin Aqeel alisema:
“Ewe Mtoto wa Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.), itakuwa bora kama tutaicha njia ya kawaida na kufuata njia nyingine, ninahofia kwamba watakuja kutuwinda.” Imamu Husein akasema: “Ewe ndugu yangu sitaiacha njia hii.” (Mawassae Kalemat Imam Hussain, uk. 299) 1. Masud bin Mukhtarema alituma barua kwenda kwa Imamu Husein (a.s)
33
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 34
Maadili Ya Ashura “Usidanganyike kwa barua za watu wa Iraq, Ibn Zubair ambaye anakuomba ili uungane naye ni msaidizi wako anayekuunga mkono. Kuwa ndani ya Nyumba Tukufu ya Allah na usiende popote. Kama watu wa Iraq wanakuhitaji basi watapanda ngamia wao na kuja mbio kwako, kisha unaweza kuanza upinzani wako pamoja na jeshi kubwa na madaraka.” Imamu Husein (a.s) Aliomba kwa ajili ya ustawi wa Masud bin Mukhtarema na akasema; “Nitaomba wema kutoka kwa Allah (s) katika suala hili” (Saabiq Sadr, Page 259) Hii ina maana kwamba Imamu Husein (as) alitaka kusema kwamba unafanya visingizio vya ibada na kutafuta hifadhi katika Kaaba Tukufu ili kukaa mbali na wajibu wako. Hii ni kwa sababu mtawala fisadi yuko kwenye madaraka na wakati ufisadi ukiwa kitu cha kawaida kila mahali basi ni lazima kwa watu wenye dhamiri kujitokeza na kuingia kwenye uwanja wa mapambano na sio kutafuta visingizio ili kuokoa maisha yao. Mohammad bin Hanafia alikuja kwa imamu (a.s) na akasema:
“Ewe ndugu yangu! Wewe ni mpendwa wangu na mtu unayeheshimiwa. Kamwe siweki ushauri wangu kwa ajili ya wengine kwa sababu hakuna mwingine ambaye anastahiki zaidi kuliko wewe. Una uhusiano wa damu na mimi; unahusiana na macho yangu, roho na nafsi yangu. Wewe ndiye ambaye kwako utii ni wajibu juu yangu (yaani, kukutii wewe) kwa sababu Allah (s) amekutunuku na hili (la kila mtu kukutii wewe). Na amekutangaza wewe kama kiongozi wa watu wa peponi… Nakushauri uende Makka, kama huridhiki na hilo basi nenda Yemen, kwa sababuwatu wa Yemen wamekuwa wasaidizi na wenye kumuunga mkono Babu yako (s.a.w.w.) na baba yako (as) na wana huruma na wakarimu sana, na pia mji wao ni mkubwa. Kama unaweza kukaa kule bila matatizo basi ni heri, vinginevyo ondoka Yemen na chukua hifadhi katika majangwa na mabonde, namna hii unaweza kuendelea kwenda kutoka mji mmoja kwenda mji mwingine na kusubiri mwisho wa watu hawa, ili kwamba Allah (s) Mwenyewe aweze kuamua kati yetu na jamii hii ya kiukandamizaji.” Imamu Husein (as) alisema:
“Ewe ndugu yangu naapa kwa jina la Allah (s) kwamba hata kama hakuna sehemu katika ardhi hii kwa ajili ya usalama wangu hata ikiwa hivyo sitakula kiapo cha utii kwa Yazid ibn Mu’awiya.” Muhammad bin Hanafiya alikatisha maneno yake akaanza kulia, Imamu (as) naye pia akalia kwa kitambo kidogo na kisha akasema:
34
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 35
Maadili Ya Ashura “Ewe ndugu yangu! Allah (s) akupe habari njema, umenitakia mema kwa ajili yangu na kutambua maajaliwa sahihi kwa ajili yangu mimi, kwa kweli nimekusudia kwenda Makka tu na nimefanya matayarisho kwa ajili ya hilo. Ndugu zangu, wapwa zangu na Mashia (wafuasi) wangu ambao wana mawazo kama yangu, ambao mambo yao ni mambo yangu ninaondoka nao. Lakini ndugu yangu! Wewe ubakie Madina na uwe muwakilishi wangu hapa na usinifiche mambo yao yoyote yahusianayo na mimi.”
Washauri walimuambia kwamba atangaze kwamba hatazungumza kitu chochote dhidi yao (wafuasi wa Yazid), kwamba yeye Imamu (as) hana chochote nao, wala hataingilia katika mambo yao na wala wao wasiingilie mambo yake. Kuna ambao walifanya kama hivyo na wakamshauri Imamu (as) ushauri uleule. Baadhi ya watu walimshauri aende Yemen wakati wa giza la usiku, hivyo hivyo baadhi ya watu walisema vingine na wengine vingine, Licha ya ushauri wa wengine wote, Imamu (as) alithibitisha ni mtu gani ambaye ana wajibu na mtu gani ambaye ni mzembe. Yeye (as) alithibitisha ni jinsi gani agano linavyosimamiwa na jinsi gani majukumu yanavyotekelezwa, alithibitisha Muashura ni nani. Si Muashura mtu yule ambaye anachokozwa na kwa kuvunjika moyo anafanya kitu fulani, anaonesha upinzani fulani; bali Muashura ni mtu yule ambaye husubiri fursa itokee, na punde anapoipata, anajitokeza nje kwenye uwanja wa mapambano. Hivyo, baada ya kusikiliza ushauri wote huu, Imamu (as) alisema:
“Mimi sitoki kwa lengo la kufanya uharibifu na ugandamizaji, lakini ninachotaka ni kuutengeneza umma wa babu yangu, hivyo nataka kutekeleza kazi ya Kuamrisha mema na Kukataza maovu.” (Mawassae Kalemate Imam Hussain, uk. 291) Imamu Husein (as alitaka kusema kwamba na mimi pia natambua kuhusu njia iendayo Makka, ninaweza kuchukua hifadhi katika Kaaba Tukufu, naweza pia kufanya sababu za kufanya ibada na kwa urahisi nikaachilia mbali wajibu wangu, lakini Allah (s) amenifanya mimi Imamu (Kiongozi) na Uimamu ni agano la Allah (s) ambalo maana yake ni wajibu uliotolewa na Allah (s). Wakati wajibu wa kuitetea dini uko juu yangu, basi vipi itawezekana kwamba mimi nimruhusu Yazid aendelee na utawala wake na mimi mwenyewe kujishghulisha na kufanya ibada. Hata kama asipofanya chochote dhidi yangu, nitahakikisha kwamba nachukua hatua dhidi yake, hivyo nitawezaje kufanya mapatano na kujitenga mbali na hali hii. Hii inaweza kuwa mantiki ya mtu mzembe na hii kamwe haiwezi kuwa mantiki ya Husein ibn Ali (as). 35
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 36
Maadili Ya Ashura Chini ya mazingira kama haya maadili ya kwanza ambayo Imamu Husein (as) ameyahuisha yalikuwa yale ya Agano na yana silka ya uwajibikaji. Kazi ya Kuamrisha mema na Kukataza maovu yenyewe ni jina la uwajibikaji ambao Allah (s) ameuweka juu ya mabega ya kila mtu mmoja binafsi wa Umma huu wa Waislamu: “Na liwepo miongoni mwenu kundi lenye kulingania kwenye heri, na kuamrisha mema na kukataza maovu… Mmekuwa ni umma bora mliotolewa kwa watu, mnaamrisha mema na kukataza maovu. (Surah Ale Imran Ayah 104, 110) Fanya kazi ya Kuamrisha mema na Kukataza maovu kwa watu. Hatukuambiwa kutoa tu hutuba na kupitisha tu maneno ya mahubiri. Hutuba na mahubiri yote yana umuhimu wake yenyewe, lazima utoe mihadhara, kuelimisha watu, kutoa hutuba, kuandika vitabu na yote haya ni mambo mazuri kwa usahihi wao wenyewe, lakini haya sio Kuamrisha mema. Kuamrisha mema ni kitu tofauti ambacho kimetolewa kama wajibu kwa kila mtu ili kwamba adili hii moja ipate kuendelezwa ndani ya wanadamu. Wanadamu wameambiwa kwamba iwapo hamuindelezi adili hii moja, hamtakuwa na uwezo wa kutekeleza madhumuni yenu katika maisha. Adili hii ni kwamba kila mmoja miongoni mwenu lazima ashikamane kwenye maagano na wajibat zake. Kila mwanadamu lazima awajibike. Kamwe isije ikatokea kwamba wakati ukiona kwamba dini ya Allah (s) na maadili ya dini yanakanyangwa chini, na mipaka iliyowekwa na Allah (s) inachupwa, wewe unakuwa mtazamaji tu aliye kimya na kusema kwamba huna la kufanya kwa hilo. Na wakati wewe mwenyewe unapotembea kwenye njia iliyopotoka na mtu fulani akakuzuia, na kisha unamjibu kwa kusema: huna la kufanya kwa hili. hii sentensi “Nifanye nini kwa hilo na utafanya nini kwa hili” ni mantiki za watu wazembe. Allah hataki watu kama hawa ambao wanaona dini inaposhambuliwa na kisha husema nina nini la kufanya kwa hili? Napaswa tu kujishughulisha na ibada yangu. Na wakati akinyooshewa kidole na mtu kwa kujiingiza katika mambo mabaya, anajibu kwamba haya ni mambo yangu binafsi una nini cha kufanya na hili. Allah (s) hataki sentensi kama hizi na watu kama hawa. Badala yake, wakati unaona dini inakabiliana na tatizo dogo sana basi chukua somo la uwajibikaji kutoka kwa Husein ibn Ali (as) na jinsi ambavyo Husein (as) alivyotekeleza wajibu wake, wewe pia unatembea njia hiyo hiyo. “Toka nje ya uwa wa Sufi na uhubiri utamaduni wa Shabbir. Kuwa na fahari kama Sufi katika uwa ni sawa tu na furaha kwenye moyo.” (Kulliyat e Iqbal, Aramgaan Hijaz, uk. 680) 36
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 37
Maadili Ya Ashura Je Imamu Husein (as) hakuwa na njia halali na sahihi za kuokoa maisha yake? Alijua njia zote ziwezekanazo lakini hapa lengo haikuwa kuokoa maisha yake. Ni kwa sababu majukumu ya mtu sio tu kuokoa maisha yake bali badala yake jukumu lake ni kutekeleza wajibu wake. Jukumu hili la Kuamrisha mema na Kukataza maovu limefanywa wajibu kwa kila mtu kwa sababu Allah (s) anataka sisi tuwe watu wenye kuwajibika. Ninawajibika kwa matendo yako na unawajibika kwa matedno yangu. Hii ina maana ni amri ya lazima kwa mimi Kuamrisha mema na Kukataza maovu (wito) kwa ajili yako na kwa wewe ni amri ya lazima kwako kufanya Kuamrisha mema na Kukataza maovu kwa ajili yangu. Kwa maneno mengine, mimi ni dhamana kwa ajili ya Mema yako na wewe ni dhamana kwa ajili ya Mema yangu. Lazima unizuie kufanya Maovu na lazima nikuzuie wewe kufanya Maovu. Kama tunalipuuza jukumu la wajibu huu, basi tutaulizwa (Siku ya Hukumu) ni kwa nini hatukushughulika juu ya amri hizi. Kuna hadithi kutoka kwa Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.):
“Kila mtu ni mchunga na kila mtu ataulizwa juu ya uchunga wake.” – (Kila mtu miongoni mwenu ana wajibu na ataulizwa juu ya wafuasi wake). (Biharul Anwar, Juz. 5, Mlango wa: Insaaf wa Adl, uk. 28) Kila mtu ni mwenye kuwajibika kwenye kuulizwa maswali, na ataulizwa kuhusiana na wafuasi na watu wake anaohusiana nao. Kwa kuweka wajibu huu wa Kuamrisha mema na Kukataza maovu, Allah (s) amemfanya kila mtu ni kamanda na gavana ambaye lazima azuie maovu. Kila mmoja lazima afanye kazi ya Kuamrisha mema na Kukataza maovu, lakini tunahitaji kukumbuka kwamba kufanya kazi ya Kuamrisha mema na Kukataza maovu ni tofauti na kutoa mihadhara na mikutano michache ya kuhubiri. Sio kwamba wale tu ambao wanafanya mambo mabaya ndio watakaoulizwa, wengine vilevile wataulizwa ni kwa nini hawakuwazuia? Je, hamkupewa maelekezo ya kufanya kazi ya Kuamrisha mema na Kukataza maovu? Je, hamkupewa mamlaka ya kuzuia? Hii ina maana kwamba kila mtu kutoka miongoni mwa Umma wa Waislamu amefanywa kuwa na wajibu na wataulizwa kuhusu mafanikio ya wajibu huu. Sasa kama mtu hatekelezi wajibu wake na hatekelezi wajibu wa mamlaka aliyopewa, anaweza kusema kwamba Moyo wa Husein unakaa ndani yake? Hii ni kwa sababu Husein (as) sio jina la kila mtu asiyejali ambaye ni mtazamaji 37
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 38
Maadili Ya Ashura aliye kimya juu ya mambo yanayotokea pembezoni mwake. Yeye (as) sio jina la kuinamisha kichwa na macho, badala yake wakati wote Umma unapokabiliwa na ufisadi na bila kujali ukweli iwapo mtu fulani anadai kiapo cha utii au la, Yeye (as) yuko nje kwenye uwanja wa mapambano. Husein (as) na Mhusein ni mtu ambaye hujiunga kwenye uwanja wa mapambano kwa utashi wake mwenyewe. Hii ndio mantiki ya Husein (as), na maadili ambayo kwamba Yeye (as) ameyawasilisha. Hivyo, kitu cha kwanza ambacho maadili ya Ashura yanatuonesha ni busara ya uwajibikaji. Yametufundisha kwamba kamwe tusiwe kama wale wanaotafuta visngizio katika sala zao, mihadhara, wake na watoto wao, ofisi na kazi zao kwa kutotekeleza wajibu wao. Mtu asiyejali kamwe hawezi kuwa mfuasi wa mtu anayewajibika na Imamu ni jina la uwajibikaji. Mtu mzembe hawezi kutembea na mtu anayewajibika.
11. Majukumu yaliyoaminishwa na Allah (s) juu ya watu Ni wajibat gani zilizoaminishwa na Allah (s) kwa watu? Lazima tuangalie kwenye Qur’ani Tukufu na kuona ni wajibat gani hizo ambazo zimewekwa na Allah (s) juu ya mabega yetu? Tunaweza kuchunguza mwenendo wa Maasumin (as) ili kuelewa wajibu wetu. Wajibu wetu sio wa kulisha tu watoto wetu, kuwapa nguo, kupitisha tu siku na masiku nk. wajibu wetu mkubwa ambao Qur’ani Tukufu imeutaja na ambao Imamu Husein (as) vilevile ameusisitiza ni kwamba ninakwenda kutekeleza wajibu na wajibu huo ni Kuamrisha mema na Kukataza maovu.
“Nataka Kuamrisha mema na Kukataza maovu.” Hii ndio sababu tunashuhudia hili katika visomo vya Ziyarat. “Tunashuhudia kwamba..... na umeamrisha mema na kukataza maovu.” (Mafatihul Jinan, Ziarat-e-Warisa) Hii maana yake ni kwamba umehuisha maadili mema katika jina la Ma’ruf na katika jina la Munkar umeyaangamiza maadili ya uovu, hivyo mpaka Siku ya Kiyama maadili ya Ashura yatabakia hai katika jina la Husein (as).
38
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 39
Maadili Ya Ashura
12. Mwisho wa watu wazembe Abdullah Bin Zubair Katika historia ya Uislamu, mtoto wa Zubair bin Awam, Abdullah bin Zubeir, alikuwa miongoni mwa watu mashuhuri na mwenye nguvu wa zama hizo na alikuwa na tabia ya ajabu na ngumu sana kueleweka. Zubeir bin Awam alikuwa mtoto wa Sofiya bint Abdul Muttalib shangazi yake Ali (as). Kuhusu Zubair, Ali (a.s) anasema: “Zubair siku zote aliishi na Ahlulbayt (a.s)”5 5 Maelezo: Wakati Abdullah alipofikia ujana wake alisababisha matatizo mengi kwa baba yake, kwa kiasi kwamba wakati Zubair alipotaka kujitoa kwenye vita vya Jamal, Abdullah alisema:
“Unajitoa kwa sababu ya kuogopa upanga wa Ali Ibn Abu Talib?” Zubair akasema:
“Ni kitu gani kimekutokea? Wewe ni mtoto wa kuchukiza na wa haramu.” Sentesi hii ilisemwa pia na Bibi Aisha:
“Ewe Abdullah! unakimbia kwa kuogopa upanga wa mwana wa Abu Talib? Naapa kwa Allah kwamba hizi panga ni kali sana na ziko tayari kuchuna ngozi, na hizi ziko kwenye mikono ya kundi shupavu sana na lenye ari. Kama unawakimbia kwa sababu ya kuwaogopa, basi hilo ni sawa kwa sababu kabla yahapa watu wengi wakubwa walikimbia kwa sababu ya hofu hii hii.” Zubair akajibu: “Katu sio kama hivyo bali ile sababu ya wazi ambayo nimekuambia ni ya ukweli.” (Ibn Abi Al Hadid, Sharh e Nahjul Balagha, J. 2, uk. 166-167, toleo la pili) Zubair bin Awam siku zote alikuwa akisaidiwa na Ali (as) mpaka mtoto wake Abdullah bin Zubair alipofikia ujana. Kuna ushahidi wa kihistoria juu ya hili: 1. Wakati watu walipotembelea nyumba ya Bibi Fatima (as) ili kuichoma moto na kumtaka Ali atoke nje, alikuwa ni Zubair peke yake aliyetoka na upanga uliofutwa ili kumlinda na kumtetea Ali (as), lakini alipigwa na kundi lile la magaidi. Historia ya ugaidi ni ya zamani sana, kuanzia toka ujio wa Uislamu. Magaidi walionesha ugaidi wao. Ilikuwa ni ugaidi kuchoma moto nyumba ya Bibi Fatima (as), kumlazimisha Amirul-Mu’minin (as) kutoka nje ya nyumba yake ilikuwa ni ugaidi, na ugaidi wa tatu ilikuwa ni maelekezo yaliyotolewa kumpiga Zubair bin Awam. Khalid bin Walid alichukua upanga wake na akaan-
39
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 40
Maadili Ya Ashura za kuupiga kwenye jiwe ili uwe butu. Kisha Zubair alipigwa mbele za watu. Hizi ni habari za kihistoria zilizothibitishwa ambazo zimo katika vitabu vya Ahlus-Sunnah. Muhammad bin Tabari anasimulia kutoka kwa Zaid bin Kalb kwamba mtu mmoja anayejulikana alifika nyumba ya Ali ibn Abi Talib. Wakati huo Talha, Zubair na wengineo kutoka Muhajirin pia walikuwepo. Walisema kwamba: “Tunaapa kwa jina la Allah kwamba ama mtoke ili mle kiapo cha utii kwa hiari wenyewe au sivyo tutaivamia nyumba yenu. Zubair akatoka nje na upanga uliofutwa, alianguka chini na upanga ukamponyoka, ambapo baada ya hapo wakamkamata. (Tarikh Tabari, Jz. 2, uk. 443) 2. Khalifa wa pili aliteuwa kamati ya ushauri ili kumteua mrithi wake. Kulikuwepo na baadhi ya majina yaliyopendekezwa kwa ajili ya Khalifa mwingine. Zubair pia alifanywa mjumbe wa kamati hiyo na Khalifa wa pili. Wakati kikao cha kamati hii ya ushauri ya watu sita kilipoanza, Zubair alikuwa mtu wa kwanza kuongea na akasema kwamba natoa mikono yangu kumuunga mkono Ali (as) na kura yangu ni kwa ajili ya Ali (as). Katika mkutano huo kura pekee ambayo ilikuwa upande wa Ali ilikuwa ile ya Zubair. 3. Ushahidi wa tatu kwa hili ni kwamba Zubair siku zote alimsaidia Ali (as) mpaka mtoto wake Abdullah alipokuwa kijana. Bibi Sayyida (as) siku zote alimsaidia Ali (as) kabla ya kifo chake. Wakati alipokaribia muda wa kifo chake Kitukufu, Bibi Sayyida (as) alimuambia Ali (as) kwamba nataka kusimulia wosia wangu, na lazima usikilize na utende kwa mujibu wa wosia wangu huu wa mwisho. Bibi Sayyida (as) alikuwa anatambua jinsi ambavyo Ali (as) asivyo na msaada, hivyo katika wosia wake huo pia alisema kwamba: “Ewe Ali kama kwa sababu yoyote inakuwahaiwezekani kwa wewe kutekeleza wosia wangu basi namteuwa Zubair bin Awam pia kama mrithi wangu.” Hivyo tunatambua kwamba Zubair alikuwa mtu ambaye Bibi Sayyida (as) alimteuwa kwa ajili ya wosia wake wa mwisho. Habari hizi za kihistoria ni uthibitisho kwamba Zubair alikuwa mtu aliyekuwa anatembea katika njia iliyonyooka na mtu ambaye alikuwa akijitoa muhanga katika njia sahihi. Lakini punde mtoto wake, Abdullah bin Zubair alipofikia ujana wake, alimpotosha baba yake kutoka katika njia iliyonyooka kwa kiasi kwamba baba yake, Zubair alitoka na upanga kumpinga Ali (as) katika vita vya Jamal.. Tunaweza kuona kwamba kuna watoto ambao wanaweza kuwapotosha baba zao kutoka kwenye njia iliyonyooka. Leo pia tunafanya kitu kama hicho. Tunawasomesha watoto wetu, huandaa malezi bora yawezekanayo, tunafanya kazi kwa bidii sana ili kumlea katika njia nzuri, wakati akiwa kijana, tunafanya juhudi tena, tunatumia mawasiliano yetu na watu, tunawasihi watu na kwa njia moja au nyingine tunafanikiwa kumpeleka Ulaya. Kisha, ni kitu gani mtoto anafanya? Badala ya kufuata utamaduni wetu, hupeleka Visa kwa ajili ya wazazi wake. Sasa mtu huyu wa dini mwenye ndevu ambaye alikuwa akihudhuria sala tano za kila siku msikitini anakwenda Ulaya. Baada ya kuenda kule, ananyoa ndevu zake na anaanza kumfuata mtoto wake. Kuna baadhi ya watoto ambao huwaleta wazazi wao kwenye njia iliyonyooka, wakati ambapo kuna wengine huwapotosha. Hiki sio kitu kipya, kama Ali (as) anavyosema kwamba tabu kama hii aliipata Zubair bin Awam, sahaba wa kuheshimiwa wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Imamu Ali (a.s) alimuita Zubair katika vita vya Jamal na akamuambia: “Unakumbuka hadithi ya Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) ambayo kwayo alisema: ‘Ewe Zubair utapigana na Ali na utakuwa Mkandamizaji,’” Zubair akasema: “Sisi ni wa Kwake na Kwake tutarejea, umenikumbusha kitu ambacho mimi nimekisahau kwa ajili ya athari za wakati.” Hatimaye Zubair akaondoka katika uwanja wa vita, na akiwa njiani kurejea Madina aliuawa na mtu anayeitwa Umruu bin Jarmuz. Upanga wake uliletwa kwa Ali (as) na Yeye (as) akasema: “Nimesikia kutoka kwa Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) kwamba Muuaji wa Zubair lazima apewe habari za Jahannam.” (Sharh Nahjul Balagha, Ibne Abi Al Hadid, Vol 1, Page 233-234) Abdullah bin Zubair alikuwa mtu mzembe na Allah (s) hamsamehe mtu mzembe hata kama atakuwa tayari kulipa fidia kubwa kwa ajili ya hili.
40
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 41
Maadili Ya Ashura Wakati tukio la Karbala lilipotokea alifurahi sana kwamba angalau hatua moja imekamilika. Alifikiri kwamba baada ya Imamu Husein (as) watu watageuza nadhari zao kwake. Baada ya tukio la Karbala alianza kuzungumza kuhusu Uimamu na Ukhalifa wake. Aliteuwa wawakilishi wake, akaanzisha kambi katika mji wa Makka na akaanza kujenga haiba yake kwa watu. Alianza mihadhara na midahalo, akaanza kutenda kama kiongozi na kwa kufanya vitu vingine mbalimbali akawa maarufu sana sehemu yote. Hujjaj bin Yusufu aliishambulia Makka ili amkamate. Alisimika makombeo (catapults) katika milima yote inayozunguka Makka na akaitupia mawe Nyumba ya Mwenyezi Mungu kutoka huko juu ya milima, hivyo akaitenga sehemu hiyo na vilevile akaibomoa Kaaba Tukufu. Abi Al-Hadid anasimulia kutoka kwa Jafar Muhammad ibn Jarir Tabari kwamba: Abu Jafar anasema kwamba Hajjaj alimzingira Abdullah kwa muda wa miezi nane. Isaak bin Yusuf anasema nimeona mimi mwenyewe makombeo ya watu wa Damascus ambayo kwamba yalikuwa yakimtupia mawe Abdullah. Wakati walipoanza kutupa mawe kutoka kwenye makombeo, walisikia mlio wa ngurumo kutoka angani na watu wa Damascus waliogopa na wakaliacha hili. Mwelekeo wa mtu mzembe siku zote ni wa kuwadanganya watu na Allah (s) : “Wanataka kumdanganya Mwenyezi Mungu na wale walioamini, lakini hawadanganyi ila nafsi zao nao hawatambu.� (Surah Baqarah, Ayah 9) Watu wazembe watafanya visingizio vya ibada zao, mafunzo yao na wakati mwingine kazi zao, hivyo wakijaribu kumdanganya Allah (s), lakini kiuhalisi wanajidanganya wenyewe. Abdullaha bin Zubeir anatokana na kundi hili. Wakati Imamu Husein alipokuwa anaondoka Madina, alimtaka kila mtu amuunge mkono ambao ni pamoja na Abdullah ibn Zubair, lakni hakutoa msaada wake kwa Imamu Husein (as). Alifuata njia tofauti na akachukua hifadhi katika Nyumba ya Allah (Kaaba) na kisha akakaa akisubiri nini kinatokea kwa Imamu Husein (as). Alitambua vizuri sana kwamba muda Imamu Husein (as) akiwa hai, yeye hatapewa umuhimu wowote lakini baada ya Imamu Husein kuuliwa kishahidi, atakuwa mtu mashuhuri anayeongoza katika ulimwengu wa Kiislamu.
41
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 42
Maadili Ya Ashura Hajjaj alivua joho lake na alienda ilipo kombeo, akaweka jiwe na akasema “Piga” … na wakaweka mawe wakatupa kwa kiasi kwamba Abdullah ibn Zubair alilazimika kukimbia. Watu wa Makka wakadai amani na usalama kutoka kwa Hajjaj, na baada ya hili alimuuwa Abdullah. (Ibn Abi Al Hadid, Sharhe Nahjul Balagha, Jz. 20, uk. 117-118) Vilevile ulikuwepo wakati Abraha alishambulia Nyumba ya Allah (s) ili aivunje, akiwa pamoja na jeshi la tembo. Allah alishinda na akaangamiza jeshi hili lote kwa kupitia jeshi la ndege jurawa (Ababil). Hata hivyo, wakati mtu mzembe kama Abdullah bin Zubair amechukua hifadhi katika Kaaba na Hajjaj bin Yusuf alikuwa akiiharibu Kaaba kwa kuitupia mawe, jeshi la jurawa (Ababil) halikuwasili kwenye tukio hili. Hii ni kwa sababu katika tukio kama hili huko nyuma, alikuwepo mtu muwajibikaji naye ni Abdul Muttalib (as) katika Kaaba lakini wakati huu kuna mtu mzembe katika Kaaba. Allah hajali hata kama Kaaba ikiharibiwa ili kumuangamiza mtu mzembe. Vinginevyo kuilinda Kaaba sio kazi ngumu kwa Allah (s). Uharibifu huu wa kihistoria wa Kaaba Tukufu ulikuwa ni matokeo ya uzembe wa mtu aliyekuwemo humo. Hata Masjd’ul-Haram sio pahala pa usalama kwa ajili ya wale ambao wanakimbia majukumu yao na kukaa katika eneo jirani na Kaaba, wakisali, wakiwa wamevaa Ihram, kwa njia hii wakifanya visingizio vya kufanya ibada na kutoa huduma kwa watu. Jambo la kuvutia ni kwamba hii ni sehemu ya usalama na hifadhi hata kwa wanyama, lakini kwa mtu mzembe sehemu hii haiwezi kuwa ya usalama kwake. Vinginevyo Allah (s) angepeleka jeshi la jurawa (Ababil) lakini uhalifu huu ulikuwa mkubwa sana kiasi kwamba Allah (s) alipendelea Kaaba iharibiwe ili kumuadhibu mtu mzembe (aliyejichimbia humo). Mtu kuwa mzembe ni dhambi na jinai kubwa ambayo Allah (s) kamwe hataisamehe.
B. Mughira bin Sheba Wale ambao hawashikamani na maagano yao baada ya kupata ujuzi kuhusu dini; basi ili kuhalalisha tabia yao ya uzembe na kuonesha uovu wao katika mwanga bainifu, wananukuu aya za Qur’ani na hadithi za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Hii ndio tofauti kati ya wanachuoni wenye ujuzi na wasio na ujuzi; wasio na ujuzi hawawezi kunukuu aya za Qur’ani na hadithi kuhalalisha makosa yao lakini wenye ujuzi wanajua namna ya kufanya hivyo.
42
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 43
Maadili Ya Ashura Mfano wa hili katika historia ya Uislamu ni Mughira bin Sheba. Alikuwa mtu mwenye elimu ya hali ya juu sana na alikuwa miongoni mwa washauri wa Makhalifa. Alifidiwa na kulipwa na serikali ya wakati huo kwa ajili ya ushauri wake. Wakati Ali (as) aliposhika madaraka kama Khalifa, Mughira alimshauri kwamba gavana wa Damascus (Mu’awiya) sio mtu mzuri, vilevile una uadui wa asili naye na tumetamani kwa muda mrefu kwamba lazima aondolewe kwenye nafasi hii ya ugavana. Alikuwa anamuomba Ali (as) kwamba kitu cha kwanza anachopaswa kufanya ni kumuondoa gavana wa Damascus. Imamu Ali (as) akasema kwamba hii ilikuwa ndio nia yangu kuanzia mwanzo bila kujali ushauri wako, lakini sikusudii kufanya hili kwa sababu uliyonayo katika akili yako, sababu niliyonayo akilini mwangu ni tofauti. Hivyo kwa kuwa kwake Khalifa, Amirul-Mu’minin (as) alitoa amri yake ya kwanza kumuondoa gavana wa Damascus katika nafasi hiyo. Yeye (as) alisema kwamba katika serikali yangu mtu mkandamizaji hawezi kubakia katika wadhifa wa serikali hata kwa siku moja. Baada ya muda kidogo mshauri huyu (Mughira) alikuja tena na kumpa ushauri mwingine. Alimuambia Ali (as) kwamba kwa mtazamo wa kisiasa hukufanya kitu sahihi. Hii ni kwa sababu nafasi yako kama Khalifa bado haijathibitika vizuri katika mji wa makao makuu ya serikali, hivi karibuni yalitokea mauaji ya Khalifa wa tatu na kuna mgogoro katika mji wa Madina – hali ya ghasia na machafuko kila sehemu. Chini ya mazingira haya, kwanza ungeimarisha makao makuu na kisha ndipo ukamkabili mtu mwingine, lakini bila kuzingatia hili umeanza mapambano na gavana, tena wa eneo kama Damascus. Hii sio hatua nzuri ya kisiasa. Ndani ya muda wa siku chache mshauri huyu wa serikali alitoa ushauri wa aina mbili tofauti, kabla ya gavana kuondolewa alishauri kwamba gavana huyu lazima aondolewe mara moja, lakini baada ya gavana kuondolewa mara moja aligeuza ushauri wake na akasema kwamba hatua hii haikupaswa kuchukuliwa. Siku moja mshauri huyu alizozana na Ammar (ra). Ammar (ra) aliingia kwenye mapambano naye wakati wanabishana juu ya suala fulani. Wakati Ali (as) alipata habari kwamba Ammar (ra) anabishana na Mughira, Yeye (as) alimuita Ammar na akasema “Ewe Ammar! Achana naye, usibishane naye, na usiwe na mazungumzo yoyote naye au kujadiliana naye.” Ammar (ra) akasema: Ewe Amirul-Mu’minin, anasoma hadithi za Mtume (s.a.w.w.) na kusimulia matendo ya Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.). Anawapotosha watu kwa kusoma aya za Qur’ani na hivyo ni wajibu kwangu mimi kuhojiana naye.” Ali (as) alisema: “Ammar achana naye. Anaelewa tafsiri ya aya za Qur’ani, ni mjuzi wa hadithi na matendo ya Mtume (s.a.w.w.), ni hafidhi wa Qur’ani, na anaelewa sheria za dini kwa ajili ya matendo ya ibada, laki43
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 44
Maadili Ya Ashura ni ametumia Qur’ani, hadithi, dini na sheria zake kama njia ya kuthibitisha na kuhalalisha makosa yake. Hii ndio njia anayotumia kuondokana na hatia, makosa na majukumu yake. “Wakati Imamu Ali (as) alipomsikia Ammar bin Yasir anabishana na Mughira, Yeye (as) alimuambia Ammar achana naye. Kwa sababu amechukuwa tu aina ile ya dini ambayo humleta karibu na dunia yake hii na kwa makusudi amejiingiza kwenye hali ya mashaka ili aweze kutumia shaka hizi kama njia ya kuhalalisha anasa zake.” (Nahjul Balagha, semi ya 405) Watu wazembe ni watu wenye tabia changamani sana na ya ajabu, lakini Allah kamwe hawasamehe watu wazembe.
13. Mtoto wa Mina katika baraza ya Yazid Imamu Husein (as) alikuwa hakabiliani tu na Umar bin Saad, kwa kweli alikuwa anakabiliana na wengine wengi kama Abdullah bin Zubair ambao wamevunja maagano yao. Tusiwaangalie tu wale ambao walimshambulia Imamu (as) kwa panga bali vilevile lazima tuwaangalie wale ambao waliiumiza nafsi ya Imamu (as). Kule Karbala kulikuwa na watu ambao waliujeruhi mwili wa Imamu (as), lakini kule Makka na Madina kuna watu ambao waliijeruhi nafsi ya Imamu (as). Kulikuwa na watu ambao walitumia panga zao katika nafsi ya Imamu (as) na wao vilevile wanajumuishwa katika kundi lilelile la wauaji. Wale ambao walishambulia mwili wake walimuuwa Husein (as), lakini wale walioshambulia nafsi yake waliuwa Hussainiyat na walijaribu kuyashinda madhumuni yenyewe ya Husein (as). Hawa walikuwa watu ambao badala ya kumsaidia Imamu Husein (as) walibadilisha mwelekeo wao na kuelekea Mina kwa kisingizio cha Hijja. Hii ni Mina ileile ambako kuna sehemu ya kumbukumbu kwa ajili ya dhabihu ya Nabii Ibrahim (as). Watu hawa wazembe, ambao walivunja maagano yao, walivaa Ihram zao na kujishughulisha katika kutoa dhabihu mbuzi na kondoo. Imamu Husein (as) aliondoka kwenye uwanda wa Arafa, akachukua njia ya kuelekea Iraq na akasema:
“Wale ambao wako tayari kutoa mihanga pamoja na sisi na wako tayari kukutana na Allah (s) nawafuatane nasi.” (Mawassae
44
Kalemat e Imam Hussain – Page 328)
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 45
Maadili Ya Ashura Hii ina maana kwamba ilikuwa si wakati wa kutekeleza ibada ya Hijja na kutoa dhabihu ya kondoo bali badala yake ni wakati wa kuilinda Hijja na kuiweka hai Mina. Kuna tofauti kubwa kati ya kutekeleza ibada ya Hijja na kuilinda Hijja. Mtu ambaye anatekeleza ibada ya Hijja hutoa dhabihu ya kondoo lakini wale ambao wanailinda Hijja wanahitaji kutoa muhanga watoto wao. Hivyo, wakati Imamu Zainul-Abidiin (as) alipojitambulisha mwenyewe katika baraza ya Yazid, utambulisho huu ulikuwa wa kipekee. Kila mmoja alijua kwamba anatokana na kizazi cha Mtume (s.a.w.w.), mjukuu wa Ali na Fatima (as), mtoto wa Husein (as), lakini bado alijitambulisha katika mtindo huu na akasema:
“Kwa wale ambao wanaonijua wananijua mimi, kwa wale ambao hawanijui mimi nitatambulisha vyanzo vyangu vya urithi, na nasaba yangu, ni kwamba mimi ni mtoto wa Makka na Mina na mtoto wa Zamzam na Safa� Wewe ni mrithi wa Mina, ni mtoto wa Mina kwa sababu mrithi wa Mina hawezi kuwa mtu yule ambaye anazuru Mina kutoa dhabihu ya kondoo, lakini mrithi wa Makka na Mina anaweza kuwa tu yule ambaye anatoa muhanga watoto wake, mtu ambaye hutoa muhanga ndugu zake, mtu anayeweza kumwaga damu na mtu ambaye huwatoa muhanga ndugu zake ili kuulinda utukufu wa Makka na Mina. Yeye (as) anasema kwamba hii Safa na Marwah, hii Makka na Mina sio yenu, hizi ni zangu. Vipi mtu anaweza kuwa mtoto wa Mina, mtoto wa sehemu ya dhabihu (muhanga) na mtoto wa Zamzam? Kutembelea tu Makka na kunywa maji ya Zamzam hakuwezi kumfanya mtu mtoto wa Zamzam. Ni yule tu ambaye anaweza kuokoa heshima na utukufu wa Zamzam na Mina ndiye anayeweza kuwa mtoto wake. Ni mtu ambaye hulinda utukufu na utakatifu wa Hijja. Picha ya Imamu Sajjad (as) ambayo makhatibu (Dhakirin) wameionesha iko mbali na uhalisia. Siku zote wanamuonesha kama mtu mgonjwa lakini hawajadili ari (raghba) na ushujaa wake. Ni muhimu hapa kutafakari kwamba Imamu Sajjad (as) huyu huyu wakati alipoingia baraza ya Yazid alikuwa na pingu nzito za chuma shingoni mwake, minyororo miguuni na alikuwa amefungwa pingu pamoja na shangazi zake na dada zake ambao wamesimama miguu mitupu bila viatu katika baraza hiyo (ya Yazid). Wakati Yazid alipoanza kuongea alisema, ni nani huyu na anataka nini? 45
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 46
Maadili Ya Ashura Imamu Sajjad (as) akasema: “Ewe Yazid! Unafikiria kwamba kwa kuweka pingu shingoni mwangu umefunga hadhi yangu na ulimi wangu pia. Naapa kwa jina la Allah (s) kwamba ni mikono na miguu yangu tu ndio imefungwa lakini ulimi wangu uko huru, midomo yangu iko wazi.� Baada ya maneno haya alitoa ile khutba ambayo ilimdhalilisha Yazid na Yazidiat (ufuasi wa Yazid) daima.
46
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 47
Maadili Ya Ashura
Maadili ya Pili
Kutouvumilia Ukatili 1. Ukandamizaji – Uovu Mkubwa mno.................................................................48 2. Kutouvumilia Ukatili – Maadili ya Ashura........................................................49 3. Kutouvumilia Ukatili – Somo kutoka Karbala..................................................50 4. Imam Huseiin (a.s) – Mrithi wa Mtume (s.a.w.w)............................................50 5. Ukristo Uliopotoshwa – Uvumilivu wa Ukatili.................................................53 6. Mitume (a.s) ni Washuhuda na Watabiri............................................................54 7. Athari za kufundisha Ukristo uliopotoshwa kwa Waislamu..............................55 8. Uvumilivu kwenye Ukatili – Dhambi Kubwa...................................................56 9. Sababu za Ukandamizaji....................................................................................57 10. Sababu za Ndani na Nje za Ukandamizaji.......................................................63 11. Tofauti kati ya Mustadha’af (Mkandamizwaji) na Mustadha’if (Mkandamizaji)........................................................................65 12. Karbala – Njia ya kutovumilia kwenye Ukandamizaji....................................66
47
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 48
Maadili Ya Ashura
1. Ukandamizaji – Uovu Mkubwa mno Ukandamizaji ni moja ya uovu mkubwa miongoni mwa maovu yote na kutokuwa mkandamizaji ni sifa muhimu sana ya mwanadamu. Wanachuoni wote wana rai ya wote pamoja kuhusu ukandamizaji kuwa ni kitendo cha kuchukiza, hata katika sheria za dini ukandamizaji unahesabiwa kama uovu mkubwa miongoni mwa maovu yote. Kila mtu anajua kwamba ukandamizaji ni kitu kibaya, hata kwa mtu ambaye anafanya ukandamizaji anatambua kuhusu uovu wake. Hii ndio sababu kwamba mkandamizaji hauiti ukandamizaji kwa jina lake na siku zote anajaribu kuupa ukandamizaji majina mengine na maneno mazuri, anajaribu kuficha ukandamizaji wake nyuma ya pazia la majina mazuri. Hivyo hakuna atakayekubaliana na ukandamizaji kuwa ni uovu na tendo la kuchukiza. Ni sanaa na sifa ya mwanadamu kwamba anahalalisha matendo yake maovu kwa majina mazuri na ya kupendeza. Mfano mkubwa wa hili unapatikana katika Afghnistan na Iraq leo. Wakati mwingine katika jina la demokrasia, wakati mwingine katika jina la uhuru na wakati mwingine katika jina la kupiga vita ugaidi. Watoto wengi na watu wasio na hatia wamekuwa waathirika wa ukandamizaji na ukatili wa Marekani. Allah anajua vizuri kuhusu hali ya watu wa Iraq wanayoishi. Mitaa ya Karbala, Kufa, Najaf na Baghdad imepakwa damu ya Waislamu wasio na hatia. Kila siku damu ya Waislamu inamwagwa na usafi wa wanawake Waislamu unaharibiwa. Ukandamizaji na dhulma waliyoionesha katika magereza ni aibu kubwa mno kiasi kwamba ni aibu kwa mtu mwenye adabu zake kuyasimulia wakati ambapo ukandamizaji huu ulishuhudiwa na ulimwengu wote. Katika jina la kupigana dhidi ya ugaidi, ukatili mkubwa ulifanywa juu ya Waislamu kwa kuwapa majina kama Wapiganaji wa Kiislamu. Tani nyingi za mabomu zilidondoshwa juu ya Waislamu wasio na hatia. Matendo yote haya ya ukandamizaji yamefichwa nyuma ya uzuri wa picha ya kinafiki ya uenezaji wa demokrasia, uhuru na uondoaji wa ugaidi. Ukweli ni tofauti kabisa, kama Marekani ilitaka kuupiga vita ugaidi, basi Sadam alikuwa gaidi tangu miaka ishirini iliyopita, sasa kwa nini wasimzuie tangu hapo? Badala yake walimpa Sadam silaha na siku zote walimhimiza kuendelea na matendo yake ya ukatili, kama vile walikuwa wanamuambia aendeleze dhulma yake na wao wataendelea kumsaidia. Hivyo lazima tuwe hadhiri na tusichanganywe na majina mazuri. Kwani kwa kuzipa tu sifa za uovu majina na maneno mazuri, haiwi matendo na sifa nzuri. Tendo 48
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 49
Maadili Ya Ashura ovu siku zote hubakia tendo ovu, kwa kubadilisha tu jina lake kwa kitu kizuri uhalisia wake haubadiliki. Ni sifa ya kushangaza ya ulaghai na ufundi wa mwanadamu kwamba huonesha maovu yake katika namna nzuri na ya kukubalika. Hata baadhi ya watu wenye ilimu ya dini, ilimu ya tafsiri, sayansi ya Qur’ani na masuala mbalimbali, wanakuwa waathirika wa sifa hii ya ulaghai na hivyo kuyapa matendo yao maovu majina mazuri, ambayo pia hudanganya wengine. Hivyo kama ukandamizaji na ukatili unapewa jina zuri, bado utabakia kuwa ukandamizaji, haifanyi tofauti juu yake kama jina linageuzwa. Kwa kuita uwoga kama kuona mbali, haiwi sifa nzuri, bado inabakia ni woga. Paka au mbweha kama akiitwa simba hazikui ndani yao nafsi na ujasiri wa simba, halikadhalika kwa kuiita autorickshaw kama “F16” haiwi “F16”. Kama jeshi la Anga la Pakistan linahitaji “F16” basi hawanunui autorickshaw kwa sababu wanajua ukweli na hawadanganyiki kwa majina haya ya bandia. Kwa hiyo, siku zote lazima tuwe na tahadhari. Kama ukatili ukija katika vazi la uadilifu, bado unabakia kuwa ni ukatili, jina la uadilifu haliubadilishi kuwa uadilifu. Katika mtindo kama huo, kwa kuupa ujinga majina ya Ujuzi na Utambuzi, haubadiliki kuwa ni kuelimika, ujinga hubakia kuwa ujinga. Hivyo mwanadamu anaweza kwa urahisi kutambua ukandamizaji. Hata kama ukandamizaji unalazimishwa juu ya wanadamu chini ya vazi lingine, bado ni dhidi ya asili ya kuzaliwa ya mwanadamu.
2. Kutouvumilia Ukatili – Maadili ya Ashura Katika vita vya Karbala, miongoni mwa maadili ambayo Imamu Husein (as) ameihuisha kati ya maadili ya Ashura, ya muhimu ni ‘Kutouvumilia Ukatili’ na kutokuukubali ukatili. Kinyume cha maadili haya ni Uvumilivu juu ya Ukatili ambao Yeye (as) ameufafanua wakati wote. Wakati mwingine, mwanadamu haelewi iwapo uvumilivu juu ya ukatili ni sifa hasi au bayana. Hii ni kwa sababu baadhi ya watu hufikiria kwamba kukandamizwa ni sifa nzuri kwa vile baadhi ya dini zimekuwa zikihubiri hili na baadhi ya watu na vitabu wamefundisha na kusisitiza juu ya hili. Katika vita vya maadili, wakati Imamu Husein (as) alidhihirisha maadili yote haya na tabia njema, ambavyo vilikuwa vyenye manufaa kwa hadhi ya hali ya juu ya wanadamu na vilikuwa vikiafikiana na nafsi ya ubinadamu, mkusanyiko wa 49
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 50
Maadili Ya Ashura maadili haya ulikuja kuitwa “Hussainiyat”. Kinyume chake, sifa na maadili hasi yalipewa jina la “Yazidiat”. Kuanzia hapa tutakuja kujua kwamba U-Yazid (Yazidiat) ulishindwa, na Hussaniyat ikapata ushindi. Kutouvumilia Ukatili ni Hussainiyat na kuridhia kwenye Ukatili na Ukandamizaji ni Yazidiat. 3. Kutouvumilia Ukatili – Somo kutoka Karbala Tunaleta kaulimbiu nzuri sana kwamba Karbala ni Chuo Kikuu chetu, lakini kwa bahati mbaya sana hili hubakia kwenye ukomo kwa kiasi cha kaulimbiu ya maneno tu na haitafsiriwi kwenye maana ya kimantiki. Sauti na kaulimbiu hupata umuhimu pale tu zinapotafsiriwa kwenye hatua za kimatendo. Hii maana yake ni kwamba Karbala kwa ukweli itakuwa Chuo Kikuu na Shule wakati watu wakijifundisha kitu kwa ukweli kutokana nayo (Karbala). Karbala ni jina la hatua za kimatendo na ni Chuo Kikuu kikubwa. Imamu Husain (as), masahaba wake, mashahidi wote na mateka wa Karbala ni walimu na maprofesa wa Chuo Kikuu hiki, ambapo Hussainiyat wote ni wanafunzi na wafuasi wa shule hii ya Karbala. Walimu wa Chuo Kikuu hiki cha Karbala wanatoa hutuba juu ya maadili ya Ashura. Wanayatambua na kuonesha kwa kuelekeza kwenye maovu yote. Kama Imamu Husein (as) anavyosema:
“Nataka kuamrisha mema na kukataza maovu” Tumekuja Kuamrisha mema. Tumekuja kuhuisha Ma’ruf na kuyashinda maovu (Munkarat). Chuo Kikuu hiki kikubwa vilevile hutupatia sisi somo hili kwamba Kutouvumilia Ukatili ni miongoni mwa maadili chanya na bayana ambapo kuvumilia ukatili huhesabiwa miongoni mwa sifa mbaya. Waalimu wa Karbala wamethibitisha kimatendo kwamba uvumilivu kwenye ukatili na ukandamizaji ni uovu zaidi kuliko hata kufanya ukandamizaji kwa sababu uvumilivu juu ya ukandamizaji ni moja ya sababu za ukandamizaji. Kama mkandamizwaji hakubali ukandamizaji, basi mkandamizaji anaweza kuzuiwa.
4. Imam Huseiin (a.s) – Mrithi wa Mtume (s.a.w.w.) Imesemwa katika Ziarat-e-Waritha kuhusu Imamu Husein (as) kwamba:
50
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 51
Maadili Ya Ashura “Ewe Mrithi wa Adam (as), Ewe Mrithi wa Ibrahim (as), rafiki wa Allah, Ewe Mrithi wa Nuh Nabii wa Allah Ewe Mrithi wa Musa, aliyeongea na Allah, Ewe Mrithi wa Isa, roho wa Allah! Salaam na amani ziwe juu yako. (Mafatihul
Jinan, uk. 815)
Ulikuwa ni urithi gani huo ambao Imamu Husein (as) ameupokea kutoka kwa Mitume hawa (as)? Mitume (as) walikuwa hawana utajiri, mali, rasilimali, mashamba na ardhi ambazo wangeacha kama urithi kwa ajili ya Imamu Husein (as). Urithi ambao Mitume hawa (as) wameacha kwa ajili ya Imamu Husein (as) ni maadili haya makubwa ambayo kwamba Mitume (as) wenyewe walitumwa kwa ajili ya kuyahuisha. Mitume hawa (as) waliwasilisha maadili makubwa miongoni mwa watu na wakakabiliana na aina zote za matatizo tofauti tofauti katika njia ya haki na uadilifu. Walijitahidi na kupigana dhidi ya maovu yale ambayo yalikuwa dhidi ya maadili haya makubwa, hivyo kutoa ukombozi kwenye jamii za wanadamu. Imamu Husein (as) vilevile alipigana dhidi ya maovu hayo hayo ili kuhuisha maadili hayo hayo makubwa ambayo aliyapokea katika urithi kutoka kwa Mitume (as) na hivyo yeye (as) ni Mrithi wa Mitume (as). Yeye (as) alipokea kitu mahususi kutoka kwa kila Mtume (as). Alipokea sifa mahususi kutoka kwa Nabii Ibrahim (as), kutoka kwa Nabii Musa (as) alipokea sifa nyingine mahususi na hivyo hivyo kutoka kwa Nabii Isa (as) alipokea sifa tofauti. Kutoka kwa Nabii Musa (as) alipokea urithi wa harakati dhidi ya ukatili na uvumilivu kwenye ukatili, ambapo kwa Nabii Isa (as) alipokea urithi wa marekebisho ya mfumo wa maadili. Wakati Bani Israil walipokuwa wanaswagwa chini ya ukatili na ukandamizaji wa Firauni, sio kwamba Allah (s) alimtuma Nabii Musa (as) kupigana tu dhidi ya Firaun, badala yake vilevile alipelekwa kupigana dhidi ya sifa (hasi) za Bani Israil. Katika kipindi hicho, makundi yote yalikuwepo – moja la mkandamizaji na lingine ambalo lilikuwa linakubali na kuvumilia ukatili na ukandamizaji. Yote kwa pamoja yalikuwa na sifa za uovu. Allah (s) alimuambia Musa (as) nenda kwa Firaun kwa vile amekuwa mwenye kuchupa mipaka. Madhumuni ya maelekezo haya hayakuwa kwenda kwa Firaun tu kwa vile alikuwa anafanya ukandamizaji, bali “Ewe Musa! Halikadhalika nenda kwa Bani Israil, kwani wao vilevile ni wahalifu na uhalifu wao ni kwamba wanauvumIlia ukatili na ukandamizaji huu.” Musa (as) alipigana dhidi ya Firaun na vilevile alipigana dhidi ya Bani Israil ili kuushinda ukandamizaji na uvumilivu wa ukandamizaji. Hivyo Musa (as) alikuja 51
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 52
Maadili Ya Ashura na kupigana vita ili kuendeleza maadili haya, hivyo kuwapa ukombozi Bani Israil. Kisha aliwafundisha wasiwe wenye kuuvumilia ukatili na ukandamizaji; ambayo ni sababu ya wao kutawaliwa na Firaun. Lakini katika muda mfupi baada ya Nabii Musa (as) mfumo wa maadili ndani ya Bani Israil ulibadilika. Waliharamisha neema za kawaida kwa ajili yao. Walianza kuvitangaza vitu halali vilivyoruhusiwa na Allah (s) kama ni haramu na walikwenda mbele zaidi kwa kuchukulia wajibati fulani kama matendo ya haramu na matendo fulani ya haramu yalifanywa kuwa ya wajibu. Hivi ndivyo tokea wakati mfumo wa maadili ulipobadilika, Ma’ruf (maadili mema) yakawa Munkar (maovu) na Munkar (maovu) yakawa Ma’ruf (maadili mema). Mjumbe wa Allah alisema:
“Mtafanya nini wakati ule ambapo Ma’ruf (mema) yatakuwa Munkar (maovu) na Munkar (maovu) kuwa Ma’ruf (mema)?” (Wasaelus Shia, Jz. 16, uk. 122, Hadithi ya 12, Mlango wa 1, Sura ya Amr Bil Ma’ruf na Nahi Anal Munkar) Kadhia hii itakuwa inaendelea kujirudia, lakini wakati wowote mfumo wa maadili unapobadilika Allah huleta mtu ulimwenguni ambaye atapigana vita hivi vya maadili na kuyaharibu yale maovu ambayo yanasambazwa katika jina la maadili. Halikadhalika wakati mfumo wa maadili ulipobadilika ndani ya Bani Israil, Allah alimtuma Nabii Isa (as). Yeye Nabii Isa (as) alipigana vita vya maadili kwa ajili ya kurekebisha mfumo na kuurudisha mfumo kwenye njia sahihi. Qur’ani Tukufu inataja marekebisho haya ya mfumo:
“Leo mmehalalishiwa vilivyo vizuri…” (5:5) …….
“Basi kwa dhuluma ya ambao ni Mayahudi tuliwaharamisha vitu vizuri walivyohalalishiwa, na kwa sababu ya kuzuilia kwao wengi na njia ya 52
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 53
Maadili Ya Ashura Mwenyezi Mungu. Na kuchukua kwao riba nao wamekatazwa, na kula kwao mali za watu kwa batili, na tumewaandalia makafiri adhabu yenye uchungu.” (4:160-161) Nabii Isa (as) akavifanya tena halali vitu vilivyoruhusiwa, na wale ambao walikuwa wanajiepusha na majukumu yao aliwafanya tena wafuate wajibu wao wakati wote. Hivyo Qur’ani Tukufu imetaja marekebisho ya maadili kama rasilimali na mtaji wa Nabii Isa (as). Tunachosema:
Amani iwe juu yako ewe Mrithi wa Musa, aliyeongea na Allah. Amani iwe juu yako ewe ewe Mrithi wa Isa, roho wa Allah! (Mafatihul Jinan, uk. 815) Sasa maana ya maneno haya lazima iwe wazi kwamba Imamu Husein (as) alirithi kutoka kwa Nabii Musa (as) harakati dhidi ya Firaun na akahubiri kwa Bani Israil kutokuuvumilia ukatili. Kutoka kwa Nabii Isa (as) alipokea kurudi kwa maadili yaliyobadilika kwenye hadhi yao sahihi. Hivyo, hakuna shaka kwamba Imamu Husein (as) ni Mrithi wa Mitume (as).
5. Ukristo uliopotoshwa – Uvumilinu wa Ukatili. Licha ya mafundisho ya kuelemisha ya Nabii Musa (as) na Nabii Isa (as), Ukirsto umekuwa muathirika wa upotofu. Watu walipotoshwa kutoka kwenye njia ya Nabii Isa (as) na mfumo wa maadili katika Ukristo ulibadilika kwa mara nyingine tena. Vile vitu safi vilivyoruhusiwa ambavyo Bani Israil mwanzoni walivitangaza kuwa ni haramu, Nabii Isa (as) akavitangaza tena kuwa ni safi na vinaruhusiwa. Lakini katika tafsiri iliyopotoshwa ya Ukristo ambayo imekuja kuwepo baada ya Nabii Isa (as), mafundisho ya Nabii Isa (as) yalichafuliwa kabisa. Mfano mmoja wa hili ni kwamba Ukristo ulianza kuhubiri kwamba uvumilivu wa ukatili na mateso ya ukandamizaji kwa ukimya ni sifa nzuri sana ya mwanadamu. Kwa kuyahusisha kwa uwongo (mahubiri hayo) kwenye mafundisho ya Nabii Isa (as), watu walifundishwa kwamba uvumilivu wa ukatili ni moja ya maadili makubwa, na iliwasilishwa kama Ma’ruf. Walielezwa kwamba kama mtu akikupiga shavu la kulia, unamgeuzia shavu lako la kushoto ili nalo alipige pia. Kama mtu akikutukana, jitayarishe kupata kofi vilevile. Kama mtu anafanya kitendo cha ukatili dhidi yako, jitayarishe kwa kitendo kingine cha ukatili. Lakini haya yalikuwa ni mafindisho ya Ukristo uliopotoshwa. 53
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 54
Maadili Ya Ashura Qur’ani Tukufu imeonesha sifa hii ya Ukristo na ikasema kwamba watu hawa wanapotosha kila kitu: “…hugeuza maneno kutoka mahali pake…” (Surah Nisa: 46)
6. Mitume (a.s) ni Washuhuda na Watabiri. Qur’ani Tukufu imepangilia itifaki (protokali), sheria na kanuni kwa ajili ya Mitume (as) kwamba wakati wowote Mtume anapokuja anafanya vitu viwili, kwanza ni kwamba atatabiri kuhusu Mtume anayekuja baada yake na pili, atathibitisha kuhusu Mtume aliyepita kabla yake.
“Na Isa bin Maryam aliposema: Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, ninayethibitisha yaliyokuwa kabla yangu katika Tawrat, na mwenye kubashiria Mtume atakayekuja baada yangu; jina lake ni Ahmad…” (Surah As-Saff – Ayah 6) Nabii Isa (as) vilevile alitabiri kuhusu Mtume anayekuja baada yake na vilevile alithibitisha kuhusu Mtume aliyepita kabla yake. Wakati utabiri unafanywa kuhusu Mtume anayekuja, basi vilevile hujumuisha mafundisho ya Mtume anayekuja. Halikadhalika, wakati Mtume aliyepita akithibitishwa, shughuli zote, matendo na mafundisho ya Mtume aliyepita pia huthibitishwa. Kwa hiyo, Nabii Isa (as) alitabiri mafundisho yote ya Qur’ani Tukufu. Kama mtu anataka kuuelewa Ukristo basi hapaswi kuwauliza Wakristo kuhusiana nao. Nabii Isa (as) ana sifa mbili; moja, alitoa habari za Mtume Muhammad (s.a.w.w.) na pili alithibitisha kuhusu Nabii Musa (as). Hivyo sasa kama tukiangalia mafundisho ya Mtume Muhammad (s.a.w.w.) na yale ya Nabii Musa (as), sisi wenyewe tutaelewa mafundisho ya huyu mtabiri na mthibitishaji (yaani Nabii Isa (as). Kama Nabii Musa (as) alipata kukabiliana na Firaun, basi mthibitishaji huyu wa Musa (as) pia atakuwa dhidi ya Firaun (Mafarao). Nabii Musa alipigana dhidi ya Uvumilivu wa Ukatili, hivyo mthibitishaji wa Musa (as), yaani Isa (as) naye vilevile atakuwa miongoni mwa wale wanaopigana dhidi ya uvumilivu wa ukatili. 54
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 55
Maadili Ya Ashura Halikadhalika Mtume Muhammad (s.a.w.w.) alipigana dhidi ya Abu Jahl, Abu Sufyan na wengine, hivyo mtabiri wa Mtume Muhammad (s.a.w.w.) lazima na yeye atakuwa amepigana dhidi ya watu kama Abu Jahl. Haiwezekani kwamba Isa (as) afanye utabiri halafu akane mwenendo na mafundisho ya Mtume Muhammad (s.a.w.w.). Vivyo hivyo, je, inawezekana kwamba anathibitisha kuhusu Nabii Musa (as) halafu awe yu dhidi ya mafundisho yake? Hii itakuwa ni shutuma dhidi ya Nabii Isa (as) Mungu aepushie mbali; Kamwe Nabii Isa (as) hakuwaambia watu wavumilie ukatili na ukandamizaji. Hii ni kwa sababu Nabii Isa (as) ni mtabiri na mthibitishaji wa Mitume. Mitume waliopita na wa baadae wote walipigana dhidi ya ukandamizaji na uvumilivu wa ukandamizaji, hivyo, mthibitishaji na mtabiri vilevile atakuwa ameanzisha jihadi ya namna hiyo. Uvumilivu wa ukatili ni dhidi ya moyo wa Ukristo kwa sababu ni dhidi ya moyo wa Qur’ani, pia huwa sawa na mafundisho ya Taurat na Bibilia.
7. Athari za kufundisha Ukristo uliopotoshwa kwa Waislamu Ukristo umewafundisha watu kuvumilia ukatili kwa ajili ya staha na ufanisi. Makasisi na watawa wa makanisa wamewafundisha watu kwamba kama akikupiga shavu moja mgeuzie lingine alipige. Mafundisho haya yalikuwa na kishindo kikubwa kwa Waislamu. Walisahau staha na ufanisi uliofundishwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na wakafuata udhalili na ustawi unaofundishwa na Ukristo. Ingawa kwa uhalisia wafuasi wenyewe wa Ukristo hawakufuata mafundisho haya (uvumilivu wa ukatili) kwa maana ya kimatendo. Kama leo mtu akiupiga Ukristo juu ya shavu mmoja, je, unamgeuzia la pili? Au badala yake huendelea kulipiza kisasi cha pigo hili kwa mamia ya miaka? Mfano wa hili ni lile tukio la Septemba 11. Wakati kadhia ya Septemba 11 ilipotokea, Raisi wa Amerika alisema kwamba ataanzisha vita vya msalaba, tutalipa kisasi kwa Waislamu, na akafanya kitu kile kile kabisa. Kwa kuvunja vioo vya madirisha machache (ya WTC), wao kwa ukatili mkubwa wamemwaga na wanaendelea kumwaga damu ya watu (Waislamu) wa Afghanistan na Iraq. Allah (s) anajua vizuri ni Waislamu wangapi wamepoteza maisha yao katika vita katika nchi hizi mbili za Kiislamu. Ugaidi hutokea kila mahali na uko kileleni katika nchi ya Pakistan. Wamarekani wamewafundisha magaidi hawa na kisha hutoa visingizio kwa ajili ya kumwaga damu ya Waislamu wasio na hatia kwa kushambulia mataifa haya mawili ya Kiislamu. Ukristo wa leo unaendelea kulipiza kisasi cha kofi moja kwa miaka kadhaa, lakini watazame Waislamu wa leo, ni makofi mangapi waliyoyapata kutoka kwa Wakristo 55
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 56
Maadili Ya Ashura lakini bado baada ya kila kofi huweka mbele shavu lao lingine. Kama Waislamu wasingefuata mwelekeo wa uvumilivu wa ukatili, Quds (Yerusalem) isingekuwa chini ya udhibiti wa Israil leo. Leo damu ya Waislamu isingemwagwa katika sehemu mbalimbali za ulimwengu wa Waislamu; leo matendo ya aibu yasingefanywa dhidi ya wanawake nchini Iraq. Yote haya hutokea kwa sababu Waislamu wameuchukua mwelekeo huu muovu wa Uvumilivu wa Ukatili na Ukandamizaji. Ukristo na Ujuda kwa pamoja wamekataa uvumilivu wa ukatili. Je mtu anaweza kufikiria kwamba wakati Hizbullah anatoa pigo moja kwa Israil, basi Israil angeweka mbele shavu lake lingine? Katika mchakato huu wa kutufundisha ufanisi, Wakristo wametufundisha uvumilivu wa ukatili. Mafundisho yao ni kwamba kama wewe unajali haki za binadamu, kama unataka kuwa jumuiya ya kistaarabu na kama unataka kuwa mwenye kuona mbali, basi lazima ujifundishe kuwa mvumilivu kwenye ukatili. Lakini katika mafundisho ya Qur’ani Tukufu, uvumilivu wa ukatili ni dhambi kubwa.
8. Uvumilivu kwenye Ukatili – Dhambi Kubwa Kama kufanya kitendo cha ukandamizaji ni dhambi kubwa basi kuuvumilia ukandamizaji vilevile ni dhambi kubwa. Njia ambayo Mitume wamepigana dhidi ya ukandamizaji, vilevile walipigana dhidi ya uvumilivu wa ukatili. Kama Nabii Musa (as) alimuambia Firaun aache ukandamizaji, basi vilevile aliwafundisha Bani Israil kuacha kuuvumilia ukandamizaji. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) vilevile aliwaambia mushrikina wa Makka, Abu Lahab, Abu Jahl na Abu Sufyan kuacha ukatili na ukandamizaji, lakini vilevile aliwaambia wakandamizwaji kuacha kuvumilia ukandamizaji wao. Hii ni kwa sababu yote ni dhambi kubwa; kuuvumilia ukandamizaji ni sawa na kufanya kitendo cha ukandamizaji. Imamu Husein (as) alitoa masomo ya Kutovumilia Ukatili kule Karbala na akaupa Umma ukombozi kutokana na uvumilivu wa Ukatili. Imamu Husein (as) alijua kwamba atauliwa kishahidi huko Karbala, lakini licha ya hili Imamu Husein (as) aliendelea na mapambano ya maadili. Alitoa muhanga maisha yake na akatoa mihanga ya masahaba na watoto wake kwa ajili ya mageuzi (marekebisho) ya Umma…
“Hakika nakwenda kuutengeneza umma wa babu yangu.” (Mawassae
56
Kalemate Imam Hussain, uk 291)
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 57
Maadili Ya Ashura Kulikuwa na haja ya marekebisho ya Umma kwa sababu Umma ulikuwa unajiingiza katika aina ya ufisadi. Wakati ambapo watawala walikuwa mafisadi na wakatili, Umma vilevile umekuwa mvumilivu wa ufisadi na ukatili wao. Ili kuuangamiza wote kwa pamoja Imamu Husein (as) alisema:
Sitaweka mikono yangu katika mikono yako kama mtu dhalili, na wala sitatamani kutoroka mtu kama wewe kama watumwa. (Manakibe Aale Abi Talib, J. 3, uk. 234) Hivyo kuvumilia ukandamizaji ni dhambi kubwa kuliko ukandamizaji wenyewe. Imamu Husein (as) alitufundisha kwamba hutakiwi kuwa mkandamizaji wala hutakiwi kuvumilia ukandamizaji. Hii ni kwa sababu uvumilivu wa ukatili ni msingi wa ukatili. Mtu anayeukubali ukatili kwa ukweli anakaribisha dikteta kufanya ukandamizaji na anashiriki sawa sawa katika ukandamizaji huu. Kama uvumilivu huu katika ukatili usingekuwepo, basi dikteta asingekuwa na moyo wa kufanya ukandamizaji.
9. Sababu za Ukandamizaji Kuna sababu za nje na za ndani katika kila kadhia. Katika muktadha huu, sasa tutajadili baadhi ya matukio ya ukatili yaliyofanywa na baadhi ya madikiteta. Matukio haya maovu yalikuwa yale ambayo sababu zake za ndani zilitambuliwa na Imamu Ali (as). Mojawapo miongoni mwa sababu za ndani ilikuwa ni uvumilivu kwenye ukandamizaji na kukaa kimya juu ya kila tendo la ufidhuli.
A. Shambulizi la Anbar Baada ya vita vya Siffin wapiga debe wa Mu’awiya kutoka Damscus waliendelea kueneza hofu katika miji na vijiji ambavyo vilikuwa chini ya Amirul-Mu’minin (as).
Makamanda wenye tabia mbovu kama Busr Ibn Abi Artaat na Sufyan Ibn Auf Ghamidi walishambulia miji mbalimbali, wakawatishia watu wasio na hatia na raia wasio na ulinzi, walivamia na kupora nyumba zao na hivyo kuendeleza hali ya hofu. Ili kuishambulia Madina, Anbar na Hayyat, (majina ya miji) Amir-e-Sham (Mu’awiya) alimtuma Sufyan Ibn Auf Ghamidi pamoja na jeshi la watu elfu sita. Kwanza alifika Hayyat lakini baada ya kuona mji umetelekezwa, alielekea Anbar, ambako kulikuwa na kundi la wanajeshi elfu tano la Amirul-Mu’minin (as) 57
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 58
Maadili Ya Ashura waliopelekwa huko kwa ajili ya ulinzi. Walipoona jeshi hili kubwa la Mu’awiya, hawakuweza kusimama imara. Ni askari mia moja tu waliobakia imara na wakapigana dhidi ya jeshi la Mu’awiya kwa kiwango cha kiasi kiwezekanacho. Jeshi la maadui lilianzisha mashambulizi makali na hawakuweza kulizuia kwa vile kiongozi wa jeshi, Hassab ibn Hassan Al-Bakr, aliuawa shahidi pamoja na watu thelathini. Baada ya kuukamata uwanja wa mapambano, maadui kwa starehe waliupora mji mzima na kuuteketeza. (Sharh e Nahjul Balagha, uk. 162, kuhusiana na khutba ya 37) Wakati Amirul-Mu’minin (as) alipapata taarifa hizi, alitoa khutba ambayo ilikuja ikawa mashuhuri kama Khutba ya Jihad. Alisema: “Tahadharini! Niliwalingania (wakati wote) kuwapiga watu hawa usiku na mchana, kwa siri na kwa dhahiri na nikawashauri kuwashambulia kabla hawajakushambulieni ninyi, kwa sababu kwa jina la Allah, hakuna watu walioshambuliwa katika mioyo ya nyumba zao bali walipatwa na fedheha; lakini mnayaacha kwa wengine na kuyaacha mpaka maangamizi yakupateni na miji yenu ikatekwa. Wapanda farasi wa Banu Ghamidi wamefika al-Anbar na wakamuuwa Hassan ibn Hassan al-Bakri. Wamewaondoa wapanda farasi wenu kutoka kwenye ngome. Nimekuja kutambua kwamba kila mmoja wao aliingia katika Uislamu na wanawake wengine (Mayahudi) chini ya ulinzi wa Uislamu na wakawapora mapambo yao kwenye miguu yao, mikono, shingo na masikio yao na hakuna mwanamke atakayeweza kulizuia hilo isipokuwa kutamka aya, “Sisi ni wa Allah na Kwake tutarejea.”). Kisha wanarudi wakiwa wamebeba utajiri mkubwa bila majeraha au kupoteza maisha. Kama Mwislamu yeyote anakufa kwa kihoro (huzuni) baada ya yote haya si wa kulaumiwa lakini bali kuna sababu nzuri kwa ajili yake mbele yangu. “ (Nahjul Balagha, Khutba 27) Gaidi alichukua bangili kutoka kwenye mguu wa mwanamke wa Kiyahudi; hakuwa Mwislamu, lakini anaishi katika sehemu ambayo iko chini ya utawala wa Amirul-Mu’minin (as). Katika muktadha wa kadhia hii, Ali (as) alisema kwamba kama Mwislamu anakufa kwa kihoro baada ya kusikiliza taarifa hizi basi hawezi kulaumiwa kwa kifo hiki. Katika zama za wafuasi wa Amirul-Mu’minin (as), je hata staha ya wanawake Waislamu imelindwa? Imamu Ali (as) alielekeza kwenye sababu nyuma ya kadhia zote hizi: 58
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 59
Maadili Ya Ashura “Ajabu iliyoje! Wallahi moyo wangu hunyong’onyea kwa kuona umoja wa watu hawa katika maovu na utengano wenu katika mwenendo wa haki, mkapatwa na huzuni na kukata tamaa. Mmekuwa walengwa ambao kwamba mishale hupigwa. Mnauliwa na ninyi hamuuwi. Mnashambuliwa lakini hamshambulii. Allah anaasiwa na ninyi mnalikubali hilo. Wakati ninapowataka mtoke dhidi yao katika kiangazi mnasema ni msimu wa joto, tuache mpaka joto lipungue. Wakati ninapowataka mtoke wakati wa kipupwe mnasema kuna baridi sana; tupe muda mpaka hali ya hewa itakapokuwa nzuri. Hivi ni visingizio tu (vya kukwepa joto na baridi) kwa sababu kama mnakimbia joto na baridi, basi vilevile Wallahi mtakimbia (kwa kiwango kikubwa) kutoka kwenye panga (za vita). “Enyi mlio mfano wa wanaume, na sio wanaume. Akili yenu ni ile ya watoto na utambuzi wenu ni ule wa wakazi wa kanopi zenye pazia (wanawake waliowekwa katika faragha na kutengwa na ulimwengu wa nje). Natamani nisingewaona wala kuwajueni. Kwa jina la Allah, uhusiano huu umeleta aibu na kuishia kwenye kutubia. Allah akupigeni vita! Mmeujaza moyo wangu kwa usaha na kujaza kifua changu kwa hasira. Mmenifanya nimeze mikupuo iliyojaa huzuni mmoja baada ya mwingine. Mmepuuza ushauri wangu kwa kuniasi na kuniacha mara nyingi kiasi kwamba Kuraishi walianza kusema kwamba mwana wa Abi Talib ni shujaa lakini hajui mbinu za vita. Allah na awabariki wao! Je, kuna yeyote ambaye ni mkali zaidi katika vita na mzoefu zaidi kwayo kuliko mimi? Nilianza nikiwa bado katika umri wa miaka ya ishirini na hapa nilipo nimepita zaidi ya miaka sitini, lakini mtu ambaye hatiiwi hawezi kuwa na maoni.” (Nahjul Balagha, Sermon 27) Mwanachuoni mheshimika Mufti Ja’far (ra) kuhusiana na muktadha huu anasema kwamba wakati Amirul-Mu’minin (as) alipopata taarifa kuhusu shambulio hili, Yeye (as) alikwenda kwenye mimbari na kuwaamsha watu dhidi ya harakati za maadui na akawalingania kwa ajili ya Jihad. Lakini hakuna aliyesema “Labbayk” kwenye wito wake, kisha Yeye (as) akiwa katika hali ya ghadhabu na hasira, yeye mwenyewe alishuka kwenye mimbari na kuelekea walikokuwa maadui. Wakati watu walipoona hivyo, kujiheshimu kwao kuliamshwa na wao pia walianza kumfuata. Wakati Ali (as) alipopiga kambi katika bonde la Nakhila, wafuasi wake walimzunguka, wakamsihi arudi nyumbani, kwani wao wenyewe wanatosha kukabiliana na jeshi la adui. Wakati kusihi kwa watu kulipozidi zaidi, alikubali kurudi nyumbani na kisha Said bin Qais alielekea walikokuwa maadui pamoja na jeshi la watu elfu nane. Wakati Said alipowasili kwenye uwanja wa mapambano, jeshi la 59
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 60
Maadili Ya Ashura Sufyan bin Auf limekwisha ondoka na Said akarudi bila kupigana. Wakati Said alipowasili Kufa, kwa mujibu wa simulizi ya Ibn Abil Hadid, Ali (as) akiwa katika hali ya huzuni na masikitiko alikuja na kukaa juu ya Baab-e-Sidda (moja ya milango ya Kufa) na kwa sababu ya siha mbovu, aliandika khutba hii na kuikabidhi kwa mtumwa wake Saad ili aisome kwa watu. Kwa mujibu wa simulizi ya Mubarrad kutoka kwa Ibn Aisha, Ali (as) alitoa khutba hii mwenyewe kwa kusimama juu ya mlima katika bonde la Nakhila, na Ibn Misam pia alithibitisha hili. Katika khutba hii, ili kuwashawishi wafuasi wake kwa ajili ya vita hivi, alijadili mazingira ya zama za Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.). Yeye (as) aliwakumbusha kujitoa kwao mihanga masahaba wake (s.a.w.w.), Muhajiriin na Answar. Hao walikuwa wapenzi sana wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), walikuwa wachache kwa idadi wakati ambapo watu wa Iraq ni wengi zaidi kwa idadi lakini bado ni wazembe na wanyonge… Mtu mmoja mrefu alisimama na kusema: “Ewe Amirul Mumini! Wewe sio Muhammad (s.a.w.w.) wala sisi sio Answar!” Amirul-Mu’minin (as) akajibu: “Sikiliza kwa makini kabla ya kusema. Mama zako wakulilie, unaongeza kwenye huzuni na masikitiko yangu, ni lini nilisema kwamba mimi ni Muhammad (s.a.w.w.) na ninyi ni Answar? Nimetoa tu mfano kwamba wao ni vigezo wa jukumu lenu.” Sababu kubwa kwa mateso hayo ilikuwa ni huu uvumilivu wa ukandamizaji. Mtu fulani anakuwa muathirika wa mishale ya wengine kwa sababu tu alikuwa hayuko tayari kutoka na kupinga maadui kwa sababu ya uzembe na unyonge. Haya ndio matendo na hii ndio misimamo ambayo iliwapa nguvu maadui. Kama jumuiya inaamua kutokufuata uvumilivu wa ukandamizaji, wenyewe wasiwe walengwa wa mishale ya maadui, basi hakuna gaidi atakayethubutu kuja na kufanya ugaidi na ushenzi.
B. Shambulio la Yemen Busr ibn Abi Artaat alishambulia Yemen na kabla ya hili alishambulia Madina pia. Alikaa juu ya mimbari ya Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) na akawatusi masahaba wake, akachoma nyumba, kisha alitoka Madina na akaendelea kushambulia sehemu nyingine. Katika hali hii alifika Yemen. Ubaidullah bin Abbas alikuwa gavana wa Ali (as) katika Yemen wakati huo. Busr alifanya ukandamizaji na ushenzi wa hali ya juu katika Yemen, kwa kiasi kwamba aliwauwa watoto wawili wadogo wa Ubaidullah ibn Abbas mbele ya mama yao. Ubaidullah alikwenda Kufa pamoja na 60
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 61
Maadili Ya Ashura taarifa za kuuliwa watoto wake wawili ili aweze kumjulisha Ali (as) kuhusu ukatili na mateso ya Busr. Moja ya mifano ya ukatili huu ilikuwa ni vifo vya watoto wake wawili ambao waliuliwa katika hali ya kutisha mno. Ubaidullah alikuwa anatarajia kwamba Ali (as) atamliwaza na kumpa mkono wa rambirambi kwa ajili ya watoto wake na kusoma Surah Fatiha. Lakini punde tu Amirul-Mu’minin (as) alipopata taarifa hizi, Yeye (as) alikusanya watu katika Msikiti wa Kufa na kutoa khutba hii: Wakati Amirul-Mu’minin (as) alipopata taarifa za kufuatana kwamba watu wa Mu’awiya walikuwa wamevamia miji na maofisa wake katika Yemen kwa jina Ubaidullah ibn Abbas na Sa’id ibn Nimran ambao walikuja kwake baada ya kujitoa kwa kushindwa kwenye mikono ya Busr ibn Artaat, alihuzunika sana kwa ukosefu wa utashi wa watu wake mwenyewe katika kupigana Jihad na tofauti yao ya maoni pamoja na yeye. Alipanda juu ya mimbari na kusema: “Hakuna kilichobakia kwangu mimi ila Kufa ambayo naweza kuishikilia na kuipanua (ambayo iko kwenye mikono yangu na kucheza nayo). (Ewe Kufa) kama hii ndio hali yako kwamba vimbunga vinaendelea kuvuma juu yako basi Allah atakuangamiza.” Kisha alionesha hili kwa ubeti wa mshairi: “Ewe Amr! Kwa uzuri wa maisha ya baba yako, nimepata kiasi kidogo tu cha mafuta kutoka kwenye chungu hiki (mafuta ambayo yaligandia kwacho baada kumwagwa na kufanywa kitupu).” Kisha aliendelea: “Nimejulishwa kwamba Busr ameishinda Yemen. Kwa jina la Allah, nimeanza kufikiri kuhusu watu hawa kwamba kwa muda mfupi ujao wataweza kuishinda nchi nzima kwa umoja wao katika maovu yao na utengano wenu (kwenye haki yenu wenyewe), mgawanyiko, kutokumtii kwenu Imamu wenu katika masuala ambayo ni ya haki na utii kwa kiongozi wao katika masuala ya uovu, kutimiza kwao amana ya bwana wao na usaliti wenu, kazi nzuri katika miji yao na madhila yenu. Hata kama nikiwapeni ulinzi wa bakuli la mti nina wasiwasi mtakimbia nalo pamoja na mkono wake.” (Nahjul Balagha, Khutba 35) Kutokana na muktadha wa khutba hii, Mufti Ja’far (ra) anasema kwamba wakati Mu’awiya alipojiimarisha baada ya usuluhisho (kati ya Amr bin Aas na Ashari), 61
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 62
Maadili Ya Ashura alianza kupanga kuikamata miji iliyo chini ya udhibiti wa Amirul-Mu’minin (as) ili kupanua eneo chini ya udhibiti wake. Alituma majeshi yake katika miji tofauti ili kupata kiapo cha utii kwa ajili yake kwa kutumia nguvu na hofu. Ili kufanikisha hili alimtuma Busr bin Abi Artaat kuelekea Hijaz, ambaye alimwaga damu ya maelfu ya watu wasio na hatia kutoka Madina mpaka Yemen, aliwachoma moto wakiwa hai makabila mengi na kuwauwa watoto wadogo. Ukatili wake ulizidi kwa kiasi cha kuwauwa watoto wadogo wawili (Qasam na Abdur Rahman) wa Ubaidullah ambaye alikuwa gavana wa Yemen, mbele ya mama yao, Hurriya bint Khalid. Wakati Amirul-Mu’minin (as) alipopata habari kuhusu ukatili wao na umwagaji wa damu alitaka kupeleka jeshi kupambana nao, lakini kutokana na wakati mgumu wa vita unaoendelea, watu hawakutaka vita na badala ya kuhamasika, wamekuwa na chuki dhidi ya vita. Wakati Amirul-Mu’minin (as) alipoona kipengele hiki kwamba wafuasi wake walikuwa wanakimbia kutoka kwenye vita, alitoa khutba hii. Katika khutba hii Yeye (as) aliamsha kujiheshimu kwao na akawahamasisha kwa ajili ya Jihad kwa kutaja matendo maovu ya maadui na kwa kinyume chake, ule unyonge uliooneshwa na watu wake mwenyewe. Hatimaye Zaariya ibn Qaddama alisema “Labbaik” kuitikia wito wake (as) na akatoka kuelekea waliko maadui pamoja na jeshi la watu elfu mbili. Alipigana na maadui na akafanikiwa kuwaondoa katika maeneo yanayomilikiwa na Amirul-Mu’minin (as). Amirul-Mu’minin (as) hakumchukulia mshambuliaji huyu muovu (Busr ibn Abi Artaat) kama mtu ambaye alikuwa anahusika na yote haya, baala yake katika khutba hii aliwachukulia masahaba wake kuwa chanzo cha kuingiwa na moyo kwa mvamizi kuja kutoka kote huko Damascus na kuvamia miji mpaka Yemen. Yeye (as) aliwakemea wote wawili Ubaidullah ibn Abbas na Said ibn Namran kwamba wao vilevile walikuwa na jeshi, basi kwa nini waliruhusu watoto wao wauawe? Kwa nini wasipigane na Busr? Yeye (as) alisema: “Kwa jina la Allah! Sasa nina hakika kwamba washambuliaji hawa waovu watachukuwa utawala kutoka kwenu, kama mtaendelea kuonesha uzembe wenu na udhaifu wenu kamwe hawataacha vitendo hivi vya ukandamizaji. ”Kuna sababu nne za ukandamizaji dhidi yenu: 1. Hamna umoja. 2. Hamumtii Imamu wenu wa haki na mmemuasi Allah (s). 3. Hamuaminiki. 4. Hamuongezi idadi yenu na kukuza umma wenu. Wavamizi waovu nao pia wana sifa nne ambazo ziko kinyume kabisa na zile za kwenu: 62
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 63
Maadili Ya Ashura 1. Wameungana katika upotofu wao. 2. Ni waaminifu. 3. Ni watiifu kwa kiongozi wao laghai. 4. Wanaongeza idadi ya watu na kukuza miji yao. Imamu Ali (as) alionesha sababu za ndani nyuma ya ukatili huu, ingawa angeweza kwa urahisi kutaja sababu za nje, lakini alichosema yeye (as) kilikuwa ni: “Wavamizi jukumu lao ni kufanya mashambulizi na ukandamizaji, lakini ninyi mmewapa fursa washambuliaji hawa kutenda ukatili huu. Mmewaruhusu kuwakandamiza kwa sababu utengano wenu umekuwa msingi wa ruhusa hii. Wakati mnapokuwa sio waaminifu wa kutekeleza majukumu yenu, basi jihakikishieni kwamba mnatoa mwaliko kwa washambuliaji kutekeleza ukandamizaji. Kama hamuongezi idadi ya watu katika vituo vyenu, Misikiti yenu, Husainiya zenu, na kama hizi zikiwa tupu basi vipengele hivi (vilivyotajwa) siku zote vitakuwa ni mwaliko kwa wavamizi hawa.� Hivyo, Imamu Ali (as) hakusema kwamba chochote kile kilichokuwa kinatokea huko Yemen kilikuwa ni kwa sababu ya ukandamizaji wa watawala hawa madhalimu, bali badala yake yeye (as) alisema kwamba yote haya ni kwa ajili ya uvumilivu wenu wa ukandamizaji.
10. Sababu za Ndani na Nje za Ukandamizaji Nyuma ya kila kadhia kuna aina mbili za sababu, baadhi ni za ndani na baadhi ni za nje, na ni kwa ajili ya sababu hizi kwamba kadhia hizi hutokea. Kwa mfano kadhia ya Karbala kulikuwa na sababu fulani za ndani na sababu fulani za nje. Katika nchi yetu (Pakistan) pia zipo sababu zote hizi za ndani na za nje juu ya matukio yote haya ya ugaidi na mauwaji. Kila mtu anaweza kuona sababu za nje, wakati wowote tukio fulani linapotokea kati ya India na Pakistan, hata kama kosa ni la ndani, makosa hufichwa na lawama za tukio hutupiwa juu ya sababu za nje tu. Hiki ni kiwango cha sera za mataifa yote kwamba wakati wowote hali ya ndani inapokuwa mbaya, upesi sana wanatupia lawama zote juu ya sababu za nje na maadui wa nje, badala ya makosa yao wenyewe na kushindwa kwao, wanalaumu watu wa nje. Mwanadamu pia yuko hivi katika maisha yake binafsi, adui mkubwa wa mwanadamu yupo kwenye nafsi yake, kama ilivyosemwa katika hadithi:
Adui yako mkubwa ni nafsi yako ambayo iko karibu na wewe. (Uddatud Daee, Ibne Fahad Hilli, uk. 314) 63
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 64
Maadili Ya Ashura
Lakini mwanadamu anapofanya kosa, huwa anasema kwamba shetani amemsababishia kufanya hivyo. Hii ni tabia ya mwanadamu ya maumbile kwamba siku zote hutoa lawama ya makosa yake juu ya wengine, ingawa mambo yasiyofaa hufanywa na watu wao wenyewe.
“…hakika nafsi ndiyo iamrishayo mno uovu…” (Surah Yusuf, Ayah 53) “Shetani ananong’oneza tu na kuwasilisha vitu viovu katika hali safi na ya kupendeza zaidi kwa mwanadamu.”
Wallahi! Tulituma kwa umma zilizokuwa kabla yako, lakini shetani aliwapambia vitendo vyao…” (Surah Nahal, Ayah 63) Wanadamu hawazingatii sababu za ndani; badala yake wanazifumbia macho sababu hizi za ndani, ingawa sababu za ndani zina nguvu zaidi kuliko za sababu za nje. Kama ukandamizaji upo zaidi sehemu fulani basi miongoni mwa sababu za ndani yenye nguvu sana ni Uvumilivu wa Ukandamizaji. Kama watu wasingekuwa wavumilivu na wenyewe wasingekuwa wanyonge na waoga, basi kwa hakika ukandamizaji usingetokea. Qur’ani Tukufu imejadili kuhusu tabaka fulani za wakazi wa Motoni. Kutakuwepo na aina mbili za wakazi wa Motoni; moja itakuwa ile ya wale ambao walikuwa wavumilivu wa ukandamizaji na unyonge, ambapo nyingine itakuwa ya wale ambao waliokandamizwa na watawala madhalimu. Wakati hili tabaka la unyonge na uvumilivu litakapoulizwa ni kwa nini wamekuja motoni: “Atasema: Ingieni motoni pamoja na umma zilizopita kabla yenu za majini na watu. Kila utakapoingia umma utalaani ndugu zake. Mpaka watakapokusanyika wote humo, wa mwisho wao watawasema wa mwanzo wao: Mola wetu! Hawa ndio waliotupoteza basi uwape adhabu ya moto maradufu. Hawa ndio waliopoteza. Atasema: Itakuwa maradufu kwenu nyote, lakini hamjui. Na wa mwanzo wao watawaambia wa mwisho wao; basi nyinyi pia hamkuwa na ubora kuliko sisi. Basi onjeni adhabu kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyachuma.” (Surah Araf, Ayah 38 – 39) 64
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 65
Maadili Ya Ashura Hii ina maana kwamba tutapelekwa motoni kwa ajili ya wakandamizaji hawa, wamebakia kuwa mabwana zetu, viongozi na wakubwa wa jumuiya zetu. Ndio waliotusababishia sisi kufanya ukandamizaji; uhalifu na kisha ndio waliotufanya pia tupatwe na adhabu. Siku zote waliendeleza ukandamizaji na dhulma dhidi yetu. Wakandamizaji, wenye kiburi na watawala madhalimu watazungumza na watasema kwamba watu hawa wanadanganya, ukatili wowote tuliowafanyia sisi wakandamizaji ilikuwa ni kwa sababu ya wao wenyewe. Walikuwa wanyonge mno na dhaifu kiasi kwamba tulipenda kuwakandamiza. Kama wasingekuwa wavumilivu hivyo wa ukandamizaji, tusingeweza kuwakandamiza. Kama wapokeaji wa ukatili na wenye tabia ya kukubali ukandamizaji wasingekuwepo, sisi pia tusingeweza kufanya vitendo hivi vya ukandamizaji na sasa makazi yetu yasingekuwa motoni. Jibu litakuja kwamba ninyi wote ni wahalifu, ukandamizaji ni uhalifu pia na kuwa mkandamizwaji pia ni uhalifu. Imefunuliwa katika Surah Ahzab: “Siku ambayo nyuso zao zitapinduliwa pinduliwa katika Moto. Watasema: Laiti tungelimtii Mwenyezi Mungu na tungelimtii Mtume! Na watasema: Mola wetu! Hakika sisi tuliwatii mabwana zetu na wakubwa wetu, wakatupoteza njia.” (Surah Ahzab, Ayah 66 - 67)
11. Tofauti kati ya Mustadha’af (Mkandamizwaji) na Mustadha’if (Mnyonge) Mustadha’af ni mtu ambaye ukandamizaji na ukatili wa wengine humfanya kuwa dhaifu na muoga. Wakati ambapo Mustadha’if (Dhaifu) ni mtu ambaye yeye mwenyewe hujifanya kuwa dhaifu, mtu ambaye yeye mwenyewe hujijengea udhaifu na woga. Ana nguvu lakini bado anaonesha udhaifu kwa kukaa mvumilivu wa ukandamizaji. Qur’ani Tukufu imeahidi ukombozi kwa Mustadha’afin (sio Mustadha’ifin). “Na tunataka kuwafadhili waliodhoofishwa katika ardhi na kuwafanya wawe ni viongozi na kuwafanya ni warithi.” (Surah Qasas, Ayah 5) Hii ina maana Allah (s) atatoa ukombozi kwa Mustadha’afin. Mkombozi mmoja wa ubinadamu, Mahdi (a.t.f.s) wa zama za mwisho atatumwa na Allah (s) kutoa ukombozi kwa Mustadha’afin, wale ambao ukandamizaji wa wengine umewafanya kuwa dhaifu, kwa wale ambao ukandamizaji unatokea, kwa ajili ya ukombozi wao Imamu Mahdi (a.t.f.s) atakuja. Wale ambao ni Mustadha’ifin, wale ambao wameji65
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 66
Maadili Ya Ashura fanya wenyewe walengwa wa mishale ya wengine, wale ambao wamekuwa wazoefu wa kuvumilia ukandamizaji na udhalimu wa watawala, hakuna atakaye kuja kwa ajili ya ukombozi wao, bali badala yake wataangamia kwenye mikono ya wakandamizaji. Hii ni kwa sababu ni kanuni ya asili kwamba udhaifu na woga huleta umwagaji damu. Unaweza kwenda msituni na kuona kwamba ni asili ya sungura ambayo huruhusu wanyama (wala nyama) kuja na kumla. Kila mnyama dhaifu kwa udhaifu huu na woga hutoa ruhusa kwa wanyama wenye nguvu kuja na kuwala, njoo na uniangamize kutokana na kurasa za uumbaji. Mshairi amefanya uwasilishaji bora zaidi wa kanuni hii ya asili. “Hakimu wa hatima ana hukumuye kuanzia mwanzo Adhabu kwa ajiliye kuwa dhaifu ni kifo” (Kulliyaat Iqbal (Urdu), Bange Jibrael, uk. 157)
Katika mtizamo wa Qur’ani, aina hii ya udhaifu ni jinai kubwa ambayo haina namna ya wokovu. Kwa kweli mkandamizaji na wale ambao wameukubali ukandamizaji huu wote watakwenda motoni kama ilivyojadiliwa pamoja na rejea ya Qur’ani.
12. Karbala – Njia ya kutovumilia Ukandamizaji Watu wamekubali uvumilivu kwenye ukandamizaji kama sifa nzuri na maadili mema, kama ambavyo muundo uliopotoshwa wa Ukristo ulivyoanzisha hili kama maadili ya heshima na kulihubiri hili katika mielekeo hii. Lakini somo ambalo Imamu Husein (as) amelitoa juu ya kutovumilia ukandamizaji litabakia kuwa hai mpaka mwisho wa ulimwengu huu, na kwa ubora wa hili Yeye (as) ameonesha njia ya Kutovumilia Ukandamizaji daima. Umma ulikuwa mvumilivu wa ukandamizaji katika zama hizo na umekuwa na tabia ya kuzoea ukatili wa Bani Umayyah. Imamu Husein (as) alisema: “Napenda kuamrisha mema na kukataza maovu.” Nimekuja kuhuisha maadili na kutokomeza maovu. Uvumilivu kwenye Ukandamizaji ambao ni miongoni mwa maovu umekuwa suala la sifa kwa watu katika wakati huo. Yeye (as) aliurekebisha Umma usiwe na uvumilivu kwenye ukatili. Yazid ni mkandamizaji lakini kamwe msiwe taifa la Yazid, hivyo mfuasi wa Husein (as) ni mtu ambaye si mkandamizaji na wala havumilii ukandamizaji. Katika siku ya Ashura wakati mtu mmoja kutoka jeshi la Umar ibn Saad alisema: “Kwa nini huli kiapo cha utii (kwa Yazid)? Kwa nini hunyenyekei kwenye utawala wa Bani Umayyah, kama utanyenyekea na kuwakubali kama watawala suala hili 66
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 67
Maadili Ya Ashura litakuwa limekwisha.” Yeye (as) akajibu:
“Kamwe sitatoa mikono yangu katika mikono yenu kwa udhalilifu na wala sitakimbia kama watumwa.” (Manakibe Ale Abi Talib, Jz. 4, uk. 18) Hapana shaka kwamba kulikuwa na ukandamizaji katika Karbala na watu wa Karbala walikandamizwa, lakini hatuoni uvumilivu kwenye ukandamizaji. Uthibitisho muhimu kwa hili ni wale mashahidi na mateka, mtu yeyote ambaye hakubali ukandamizaji anapata kifo cha kishahidi. Kifo chake cha kishahidi (as) na kuuawa kishahidi kwa watoto wake na masahaba wake kumethibitisha kwamba njia ya Imamu Husein (as) ni kupigana dhidi ya ukandamizaji. Njia hii ni kuwa imara dhidi ya wakandamizaji na kukataa ukandamizaji wao na ukatili wao. Wale watu wakubwa walikuwepo wakati huo ambao hawakuuawa na hata upepo wenye joto wa Karbala haukuwagusa, hakuna aliyekwaruzana nao, kwa kweli walikuwa wanafurahia ibada yao na kutoa darasa zao, hii ni kwa sababu walikuwa wavumilivu wa ukandamizaji. Wakati mwingine washairi wetu husoma baadhi ya beti, ingawa beti hizi hazihubiri ukandamizaji lakini zina masomo ya uvumilivu kwenye ukandamizaji. Beti hizi lazima ziandikwe na kusomeka kama ambazo hazitoi masomo ya ukandamizaji wala kukubali uvumilivu wa ukandamizaji. Beti ambazo hutoa masomo ya ushujaa, katika moyo na uadilifu lazima ziandikwe.
67
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 68
Maadili Ya Ashura
Maadili ya Tatu Utukufu (Izzat) 1. Mhuishaji wa Heshima (Utukufu)......................................................................69 2. Tofauti kati ya heshima ya kweli na ya uwongo................................................70 3. Chanzo cha Heshima..........................................................................................72 4. Mtu anayemvutia kila mtu haheshimiwi............................................................74 5. Husein (a.s) – Kiongozi wa Heshima na Utukufua...........................................75 6. Maana ya Heshima.............................................................................................76 7. Familia yenye kuheshimika zaidi.......................................................................78 8. Karbala – Njia ya Heshima................................................................................79 9. Kuzitoa Muhanga Heshima katika njia ya Allah (s.w.t)....................................81 10. Walinzi wa Heshima za Uwongo.....................................................................83
68
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 69
Maadili Ya Ashura
1. Mhuishaji wa Heshima (Utukufu) Maadili muhimu ya Ashura, ambayo Imamu Husein (as) ameyashinda katika jihadi hii na mara nyingine akayahuisha, yalikuwa ni kuvunjika kwa uwepo wa “Heshima na Hadhi ya Wanadamu.” Kama tukitafakari juu ya kauli za Imamu Husein (as) wakati wa safari yake kutoka Madina kwenda Karbala, tutaona katika sehemu nyingi kauli zake (as) zinahusiana na Heshima, upatikanaji wa Hadhi na umbali kutoka kwenye udhalilishaji. Somo la Karbala ni lile la heshima, hadhi na utukufu wa wanadamu. Hebu natujitokeze na kujifunza kutoka Karbala ni nini haswa kinamaanishwa na heshima, ni nani mwenye kutukuzwa na kutoka wapi tunapata hadhi na heshima? Kama nafsi ya heshima inaondolewa kwayo, kinachobakia nyuma ni umbile lisilo na mwili la heshima. Hata wakati heshima ikibakia kama mwili usio na uhai, bado watu wanahisi busara ya heshima, lakini katika uhalisia haiheshimiwi. Wale ambao walikuwa na wazo la kwamba walikuwa wakitukuzwa kwa hali ya juu na kuheshimiwa, Mkuu wa Mashahidi (as) aliwajulisha kwamba kiuhalisia walikuwa wanajitumbukiza tu katika udhalilishaji, na wameupa udhalilishaji huu jina la heshima. Kama kwa kweli mnataka kujua kuhusu heshima na jinsi ya kuelewa cheo cha heshima, basi njooni, nitawaeleza heshima inamaanisha nini. Kwa vile watu hao walikuwa na furaha (katika zama) kwamba walikuwa sio wakandamizaji, lakini Imamu Husein (as) alisema kwamba ingawa ninyi sio wakandamizaji, bado muwavumilivu wa ukandamizaji, kwa vile ukandamizaji na kuwa mkandamizaji vyote ni uhalifu. Imamu Husein (a.s) alisema:
“Hamuoni kwamba haki haitekelezwi na hakuna mtu wa kukataza maovu, basi katika hali kama hiyo muumini lazima ajitayarishe kukutana na Mola wake. Nakiona kifo kama heshima na kuishi pamoja na wakandamizaji kama udhalilishaji .” (Mawassae Kalemat Imam Hussain (a.s), uk. 356) Usiwe mkandamizaji katika maisha yako wala usiwe tayari kuukubali ukandamiza69
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 70
Maadili Ya Ashura ji. Kwa kweli kwa kuishi na wakandamizaji, kupitisha hata siku moja ya maisha yako chini ya ulinzi na utawala wao ni jambo la udhalilishaji kwako. Ni bora kupata siku moja ya kifo pamoja na heshima hii na hadhi uliyopewa na Allah kuliko kuishi maisha yote ya udhalilishaji chini ya utawala wa wakandamizaji. Kama unataka heshima na kufuata njia yake, njoo na ujifunze kutoka kwa Imamu Husein (as) maana halisi ya heshima. Katika mazungumzo yake na Hurr bin Yazid Riyahi, yeye (as) alisema:
“Kuwa muoga wa kifo hakulingani na cheo changu. Kifo katika kutafuta heshima na kuiweka haki hai ni raha sana. Kifo katika njia ya heshima, ni jina la maisha ya milele, wakati ambapo maisha ya udhalilishaji si chochote bali ni kifo cha kudumu. Unanitishia mimi na kifo? Mishale yako imekosea shabaha na mashaka yako ni uovu, unafikiri mimi naogopa kifo. Nafsi yangu ni yenye ukunjufu wa hali ya juu na ari yangu ni ya juu zaidi kuweza kutanguliza kuukubali ukandamizaji kwa fidia ya woga wa kifo. Huwezi kufanya madhara yoyote kwangu mbali na kuniuwa. Tunasema karibu kifo katika njia ya Allah (s) lakini huwezi kuharibu utukufu, heshiima na hadhi yangu kwa kifo tu. Elewa kwamba sijali hata kidogo kuhusu kuuawa.� (Mawassae Kalemat Imam Hussain (a.s), uk. 360)
2. Tofauti kati ya heshima ya kweli na ya uwongo Mtu huyu mwenye hamu sana ya heshima na hadhi, ana kiu na njaa kwa ajili ya heshima na anapenda heshima zaidi kuliko maisha yake. Ili kuepusha kishindo kwenye heshima yake, mara kadhaa huyaacha hata majukumu yake, ibada zake na kuachilia mbali utekelezaji wake wa haki na wajibat. Jamii ambayo kwayo mwenendo wa maadili umepotea na imekuwa mfu, kadhia na mandhari kama hizo huonekana kwa wingi. Kila mmoja wetu atapambana na 70
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 71
Maadili Ya Ashura mambo kama hayo katika kila mtaa na uchochoro. Kama mtu anaambiwa kujitokeza na kutekeleza majukumu yake ya kidini na ya kiutawala, jibu kwa hilo ni: “Tunaheshimiwa sana na tunayo hadhi ya hali ya juu sana katika jamii na halikadhalika miongoni mwa jamaa zetu, watu wa nje, marafiki na maadui na tumekisimamisha cheo hiki cha heshima kwa shida kubwa. Imenichukua mimi miaka thelethini mpaka arubaini kufikia kwenye cheo hiki cha heshima.” Je, kushiriki katika mikusanyiko au mikutano ya upinzani ili kutekeleza majukumu yako, huangamiza heshima yako iliyopatikana kwa miaka thelethini mpaka arubaini? Allah (s) anasema:
“Na anapoambiwa: Mche Mwenyezi Mungu, hukumbuka heshima yake aliyoipata kwa kufanya dhambi.” (Surah Baqarah, Ayah 206) Hujitumbukiza kwenye heshima yake ya dhambi. Allah (s) anasema:
Basi enzi yote ni ya Mwenyezi Mungu (Surah Faatir, Ayah 10) Hadhi na heshima sio kile ambacho kinapatikana kwa dhambi, lakini kama unataka kupata heshima, lazima utie akilini kwamba hadhi na heshima yote iko kwa Allah (s). Heshima haiwezi kupatikana mitaani na vichochoroni, haiwezi kuja kutoka kwa marafiki na maadui, lakini kama uko katika kuitafuta heshima, basi kila sifa ya utukufu na heshima yaweza kupatikana katika hadhara ya Allah (s). Mwanadamu anatoa muhanga kila kitu, utajiri wake alioupata katika maisha yake, rasilimali yake, vyote, kwa ajili ya maisha yake. Hata kama ni kwa kukiachia cheo na kazi yake kwa ajili ya kuokoa maisha yake hufanya hivyo na husema kwamba sivitaki vyote hivi, nataka tu kuokoa maisha yangu. Lakini kuna kitu kimoja ambacho kina thamani zaidi kuliko maisha, na kitu hicho ni heshima ya mwanadamu. Ni vigumu kuafikiana juu ya heshima kuliko kutoa maisha, hivyo ili kuilinda heshima yake, mwanadamu hutoa hata maisha yake. 71
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 72
Maadili Ya Ashura Kama utawaangalia watu wa ulimwengu huu, katika hali ambako heshima yao na wanawake wao inapokuwa hatarini, hucheza na maisha yao, hata ikiwa wakati mwingine ni kuyapoteza, lakini kwao wao ni mafanikio ya kuweza kuokoa heshima na hadhi zao. Wakati vita vinapoanza kati ya nchi mbili tofauti, basi heshima ya taifa, nchi na jumuiya hujitokeza katika kuiokoa heshima ya jamii hata kama maisha ya watu wengi yatalazimika kutolewa muhanga kwa madhumuni haya. Kutoa maisha kwa ajili ya heshima ni njia ya kawaida kwa ajili ya mtu. Wale ambao huokoa maisha yao hawachukuliwi kama watu mashuhuri na wenye nguvu, bali wale ambao hutoa maisha yao katika njia ya heshima huchukuliwa kama watu mashuhuri. Hivyo, tunajua kwamba heshima ni rasilimali ya thamani zaidi, yenye kupendelewa na kitu cha kupendeza kwa ajili ya wanadamu. Heshima na hadhi ni maadili, madhumuni na lengo la maisha ya wanadamu wote, lakini bado hawaelewi maana ya heshima, ni wapi inaweza kutolewa na jinsi ya kuilinda. Ili kuelewa mambo haya ni muhimu kujifunza na kuchambua mafundisho ya Kiongozi wa Mashahidi.
3. Chanzo cha Heshima Miongoni mwa majina mazuri ya Allah (s), kuna jina la “Aziz” na miongoni mwa sifa Zake ni sifa ya utukufu (heshima). Haya yamejitokeza mara kwa mara katika Qur’ani Tukufu, Maombi na sala ya kunong’ona (Munajat). Mara nyingine jina hili na sifa hii ya Heshima (Utukufu) imejitokeza kiwenyewe na wakati mwingine pamoja na sifa nyingine. Katika njia hii hii sifa hii imetumika kwa Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) na pia kwa ajili ya waumini. “Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye utukufu - Yeye, na Mtume wake, na Waumini.” (Surah Munafiqun, Ayah 8) Hii ina maana kwamba Allah anatukuzwa, Mjumbe wake na hata waumini wanatukuzwa. Ni heshima ya aina gani hii ambayo imeainishwa kwa ajili ya Allah, Mjumbe Wake na waumini? Heshima (Utukufu) wa Allah hauna maana kwamba Allah anatukuzwa au kuheshimiwa na watu katika eneo lake, na marafiki, maadui na wageni. Heshima hii sio matokeo ya heshima iliyotolewa kwa Allah (s) na watu wengine. Vilevile sio kwa sababu kila kiumbe amenyenyekea Kwake. Heshima ya Allah (s) ni ya 72
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 73
Maadili Ya Ashura kujitegemea kwa ajili ya utii wa na uasi wa viumbe Wake. Anatukuzwa mbele ya wote waumini na halikadhalika wanafiki na wachupa mipaka. Utukufu wa Allah (s) wala hata hauangukii pamoja na ukanaji au unafiki au uasi wa yeyote kati ya viumbe Wake. Halikadhalika, wakati ikija kwenye wanadamu, Heshima sio kitu kilichotolewa na watu wengine. Chanzo cha heshima sio watu wale wa eneo ambao huonesha heshima kwetu. Watu hufikiri kwamba wanaheshimiwa sana katika jamii na kwa hiyo wana heshima. Kwa kweli, heshima ni ile mtu anayopewa na Allah (s). Chanzo cha heshima ni Allah (s):
“Na enzi yote ni ya Mwenyezi Mungu” (Surah Faatir, Ayah 10) Wakati mwingine tunafikiri kwamba kwa kutekeleza wajibu wetu, kwa kuwa wadilifu na kuongea ukweli dhidi ya mtu fulani, huenda tukapoteza heshima yetu katika jumuiya na watu wataacha kutuheshimu na kutupatia itifaki. Hili ndilo linalotajwa kama heshima kwa uasi (wa kumuasi Allah): “Na anapoambiwa: Mche Mwenyezi Mungu, hupandwa na mori wa kufanya dhambi...” (Surah Baqarah, Ayah 206) Wakati wanapolinganiwa kwenye mema, wanakumbuka heshima zao za uwongo na za dhambi. Ili kulinda hadhi yao ya uasi, wanajizuia kuwa mashahidi kwenye ukweli na hivyo kuficha ukweli na haki. Mkuu wa Mashahidi (as) aliona kwamba wengi wa wale watu wanaotukuzwa walikuwa wamekaa mjini Madina, lakini kwa ajili tu ya kulinda heshima zao, walikuwa hawanyanyui sauti zao kwenye haki. Na katika Makka pia, kwa ajili tu ya kulinda heshima zao hakuna hata mmoja wao aliyemsaidia Mkuu wa Mashahidi (as). Halikadhalika na watu wa Kufa pia, watu maarufu walikuwepo, lakini hata hivyo hakuna aliyemsaidia Imamu (as). Hii ni kwa sababu Ubaidullah ibn Ziad alikuwa mtu asiyekuwa na aibu na hakujali heshima za watu hawa; hivyo, kwa ajili ya kulinda heshima na hadhi yao ya kijamii, walimuacha mtoto wa Fatima (a.s.) akiwa ametengwa. Kwa uhalisia hii haikua heshima, badala yake walichokipata kutokana 73
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 74
Maadili Ya Ashura na matendo yao haya ilikuwa udhalilikaji tu. Hii ni kwa sababu heshima yaweza kutolewa na yule ambaye ametukuka. Mtu ambaye anamilki kitu fulani ndiye awezaye tu kutoa kitu hicho. Hivyo, mtu ambaye mwenyewe amedhalilishwa anaweza tu kuwapa watu wengine udhalilishaji. Wakati Allah (s) alipogawanya Heshima na udhalilishaji alisema: “Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye utukufu –Yeye, na Mtume wake, na Waumini.” (Surah Munafiqun, Ayah 8) Hivyo, heshima na utukufu iko kwa Allah, Mjumbe Wake tu na waumini. Wale ambao hawamsaidii Mjumbe wa Allah (saww) hawatokani na waumini, wao ni chanzo cha udhalilishaji. Chanzo cha heshima haswa na halisi ni Allah (s) Pekee. Utukufu na heshima yote anayo Allah (s) na heshima na utukufu alioupata Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) vilevile unatokana na chanzo kilekile. Kwa hiyo, chanzo cha heshima sio tofauti hizi tatu, badala yake zote ni moja. Kama waumini na Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) wanatukuzwa basi heshima hii wamepewa na Allah (s).
4. Mtu anayevutiwa na kila mtu haheshimiwi Baadhi ya watu wanafurahi sana na kujifaharisha kwamba wanatukuzwa kwa hali ya juu sana kwa sababu kila mtu huwaheshimu na kuvutiwa nao katika maeneo yao, katika maofisi yao, na kuwafanya waamini kwamba wameiendeleza heshima yao. Kwa vile Waislamu, wasio Waislamu, wafagiaji, walioathiriwa na madawa ya kulevya, walevi wa pombe, wahuni, wahalifu na watu kutoka kila kundi wanatuheshimu sisi, hivyo tunatukuzwa na tunaliona hili kama neema tuliyopewa na Allah (s). Wao wenyewe wanadhani kwamba hiyo ni neema waliyopewa na Allah (s). Mfano mmoja wa hili ni kwamba watu wanapata pesa kwa njia za haramu na hongo, kisha wanajenga nyumba kwa pato hili, na baada ya hapo anaweka kibao juu ya mlango kinachosomeka Hii inatokana na fadhila za Allah”
Suala linalojitokeza katika muktadha huu ni; iwapo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa anaheshimiwa na kila mtu? Je, alikuwa na uwezo wa kupata heshima kutoka kwa makafiri na wanafiki? Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) kamwe hajapokea aina kama hiyo ya utukufu na heshima. Kwa kweli, Yeye (s.a.w.w.) alikuwa akitukanwa, akilaaniwa, akiitwa kama mwenda wazimu na sio kila mtu pale alimsalimu. 74
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 75
Maadili Ya Ashura Kwa kweli kulikuwa na matukio ambamo watu walimtupia uchafu na kinyesi cha wanyama na kuweka miba kwenye njia yake. Kama maana ya heshima ni kwamba watu wote lazima watutazame kwa heshima, basi kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) haikuwa kweli. Lakini anachosema Allah (s) ni:
“Hakika utukufu ni wa Allah na mtume wake na waumini.” Mtume (s.a.w.w.) huyu huyu ambaye walikuwa wakimlaumu, wakimtukana, wakimtupia taka juu yake na kumpa maumivu ya aina yote hayo, alikuwa Mjumbe mpenzi mno wa Allah (s). Kama kila mtu angalikuwa anamheshimu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kusingekuwa na haja yoyote kwake yeye kuhama kutoka Makka. Ukweli ni kwamba watu wa Makka hawakujali heshima ya Mtume (s.a.w.w.). Lau watu kama Abu Jahl na Abu Lahb wangeanza kumheshimu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), isingelikuwa heshima, bali ni udhalilishaji na fedheha. Kwamba Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) ambaye anatukuzwa na Allah (s) na vilevile anaheshimiwa na maadui wa Allah (s) kamwe haiwezi kuchukuliwa kama aliye tukuzwa. Kama hili likitokea basi kuna kosa katika moyo wake, kwa sababu amewaweka waumini halikadhalika na makafiri kuwa na furaha juu yake yeye. Hii ina maana moyo wake una unafiki.
5. Husein (a.s) – Kiongozi wa Heshima na Utukufu Baadhi ya watu huona fahari kuhusu ukweli kwamba hata walevi na wachupa mipaka wanamheshimu. Wanayo dhana hii kwamba katika hali fulani kama kuna haja ya kusafiri, basi angalau lazima wawe na uhusiano fulani mzuri pamoja na wachupa mipaka hawa ili kwamba wawaangalizie nyumba na familia zao. Vilevile hawatadhuru usafi wa wanawake wao waliowaacha nyuma. Lakini swali ni kwamba, je, hawa wachupa mipaka, walevi walijali kuhusu heshima ya Husein ibn Ali (as)? Je, haikuwezekana kwa Husein ibn Ali (as) kupata heshima kutoka kwao? Je, wale waliochoma mahema ya Husein ibn Ali (as) wakati wa “Jioni ya Uhitaji” (Shaame Garibaan) hawakujua kwamba hawa walikuwa ni watoto wa Mtume (s.a.w.w.)? Kwamba hawa walikuwa ni Ahlul-Bayt (kizazi) cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)? Kwamba walikuwa mabinti wa Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.)? Kwamba walikuwa mabinti wa Fatima (as) na Ali (as) na kwamba ilikuwa lazima wawaheshimu? Je, yawezekana kwamba Husein ibn Ali (as) hakuweza kufanya angalau uhusiano fulani na watu hawa, ili kwamba baada ya kifo chake cha kishahidi wasiwasumbue familia yake? Lakini Husein ibn Ali hakutaka heshima yoyote ya uwongo kutoka kwa watu hawa kwa sababu watu hawamiliki heshima na utukufu, bali heshima na utukufu viko kwa Allah (s). 75
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 76
Maadili Ya Ashura Imamu Husein (as) alijua kwamba atauawa shahidi, na hawa wanyama wa jangwani wataupondaponda mwili wake na watachoma mahema yake, lakini hata hivyo Imamu Husein (as) hakuwaambia kwamba lazima waheshimu mwili wake au wanawake waliokuwepo kwenye mahema. Hii ilikuwa ni kwa sababu Imamu Husein (as) alikuwa anafahamu njia ya kwenda kwenye heshima. Yeye (as) alisema kwamba nimechagua njia ya Allah na ni Allah Mwenye Utukufu ambaye nimeona kwamba atanipatia mimi heshima na familia yangu. Nitatumainiaje kwa wale ambao hawana heshima ya wao wenyewe kuiheshimu familia yangu baada ya kuondoka? Hii ndio heshima ambayo Imamu Husein ibn Ali (as) ametufundisha. Wenye heshima ni wale ambao wakati wakikabiliana na udhalilishaji, wanadamu waliodhalilishwa hawawavumilii, bali wakati wakija kwenye uwanja wa heshima, wanakuwa viongozi wa heshima.
6. Maana ya Heshima Ni nini maana ya Heshima, ambayo hupendwa sana na kwa kuthaminiwa kiasi hicho kwamba mwanadamu yuko tayari kutoa muhanga maisha yake kwa ajili hiyo? Lazima tuelewe maana yake kwa sababu maana hiyo hiyo iko kwenye heshima na utukufu wa Allah (s), Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) na waumini, kama ilivyosemwa awali Allah ni Mwenye Utukufu na heshima, Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) ni mwenye heshima na utukufu na halikadhalika waumini pia. Kama Heshima maana yake ni kupata heshima kutoka kwa watu wa eneo, basi Allah (s) hana eneo, Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) alikuwa haheshimiwi na eneo lake, wanafiki, washirikina na makafiri walikuwa hawamheshimu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Wachupa mipaka hawakumheshimu Imamu Husein (as), basi ni aina gani hii ya heshima ambayo iko kwa waumini ambayo imethibitishwa kwa ajili ya Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) na iliyopatikana kutoka kwa Allah (s). Heshima katika fasihi ya Kiarabu humaanisha kitu kilicho na ugumu, ukakamaavu na mango, uwepo wa vitu hivyo ambao hauruhusu kitu kingine chochote kupenyeza, kupasua au kuingilia. Kwa mfano, kama unataka kupigilia msumari kwenye mbao, baada ya pigo moja au mawili ya nyundo na msukumo kidogo msumari utapenyeza kwenye mbao. Lakini kama ukijaribu kupenyeza msumari huo huo kwenye ukuta wa saruji, itachukuwa juhudi zaidi kwa sababu ukuta wa saruji ni mgumu ukilinganishwa na mbao. Msumari huu huu ambao unaweza 76
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 77
Maadili Ya Ashura kupenyeza kwenye ukuta wa saruji kamwe hautaweza kupenyeza kwenye mwamba. Hii maana yake ni kwamba mwamba au jiwe ni gumu, imara na kitu chenye uwezo kiasi kwamba hakiruhusu msumari kupenyeza ndani yake, licha ya idadi ya mapigo ya nyundo kwenye msumari. Inawezekana jiwe likavunjika lakini hata hivyo msumari hauwezi kupenyeza ndani yake. Nafsi ambayo ndani yake ina heshima ni sawasawa na hii. Kama aina yoyote ya kasoro, maovu, unyonge, lawama na shutuma zinatupiwa kwayo, hata pamoja na maelfu ya ushahidi, nafsi hii imara haitaruhusu vitu hivi kujipenyeza ndani au kushirikiana navyo. Nafsi kama hiyo huchukuliwa kama nafsi yenye heshima. Lakini kama aina yoyote ya lawama, shutuma na maovu yanahusishwa na nafsi, kwa urahisi hushirikiana nayo na kuthibitishwa. Nafsi kama hiyo huchukuliwa kama nafsi iliyodhalilishwa. Dhati ya Allah (s) ni Dhati ambayo ni ngumu kiasi kwamba hata kama walimwengu wote wakiungana ili kutafuta kasoro ndani ya Allah (s) hawatafanikiwa. Dhati ya Allah (s) haina kasoro au mapungufu na kwa hiyo hakuna kasoro na unyonge unaoweza kushirikishwa na Allah (s). Katika njia hiyo hiyo, nafsi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) vilevile ni maasum, hakuna kasoro, dhambi au makosa yanayoweza kuthibitishwa dhidi yake. Lawama na shutuma zozote dhidi yake zitarudi kwa mwenye kushutumu, haiwezi kupenyeza nafsi hii toharifu. Lakini kama kasoro yoyote inahusishwa na nafsi au shutuma zinafanywa dhidi yake, na kama kishindo hiki chepesi kikapenyeza ndani ya nafsi, basi nafsi hii ni nafsi iliyodhalilishwa. Udhalili katika Kiarabu maana yake ni; ulaini ambao kuwepo kwake huruhusu kukubali kila kitu kinachokuja kutoka nje. Kama inavyosemwa farasi mpole humruhusu kila mtu kumpanda kwa urahisi. Hivyo tunajua kwamba Heshima haina maana kwamba kila mtu lazima anyenyekee na kusalimu amri, kwa kweli, Heshima humaanisha kwamba aina na idadi yoyote iwayo ya shutuma zinazofanywa, hakuna itakayofikia nafsi hiyo. Kwa mfano, ujinga ni kasoro na ni uovu miongoni mwa maovu yote. Sasa kama inasemwa kuhusu mtu fulani kwamba ni mjinga, kama kweli mtu huyu ni mjinga, basi sifa hii hii ujinga itajipenyeza ndani mwake. Aidha kama dalili hizi za ujinga vilevile huonekana juu yake, basi kwa matokeo ya ujinga mtu huyu hana heshima na msumari wa ujinga utapenyeza kwa urahisi ndani yake. Kama hayo yanasemwa kwa mwenye akili, msomi, mwanachuo au mwanasheria kwamba ni mjinga, hata kabla akili zetu hazijamzingatia mshutumiwa tutamgeukia mshutumu kwa sababu kila mtu ana uhakika kabisa kwamba mshutumiwa ni 77
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 78
Maadili Ya Ashura mwanachuomi na mtu mwenye elimu. Hapa huu msumari wa ujinga hautapenyeza kwake na watu kwa kweli watamgeukia mshutumu. Watu walimtupia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) shutuma mbali mbali, kwa kiasi kwamba walimuita Mtukufu Mtume (sw) mshairi, mchawi na hata kumuita chizi mwendawazimu. Halikadhalika lawama na shutuma zilifanywa kwa AmirulMu’minin (as). Lakini hata leo baada ya karne kumi na nne, nafsi hizi ni safi (tohara) kama zilivyokuwa kabla na lawama na shutuma zote hizi zimegeukia kwa wenyewe wenye kushutumu. Sasa tunahitaji kuona, iwapo na sisi pia tuna heshima. Kama kuna kasoro zinazohusishwa na sisi, je, zinalingana na sisi au la? Kama ujinga, upumbavu, upuuzi, uzembe na kutokujali huhusishwa na sisi, lakini hauonekani ndani yetu, basi tuna heshima, vinginevyo hatuna. Mtu mwenye heshima ni mtu ambaye ndani yake hamna unyonge, mapungufu na kasoro zinazoonekana bila kujali iwapo watu wanamheshimu au la. Hivyo tunaelewa kwamba kwanza heshima ni kwa ajili ya Allah (s), kisha kwa Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) na kisha kwa waumini.
7. Familia yenye kuheshimika zaidi Allah (s) alifanya familia kuwa safi mno kiasi kwamba hata kama walimwengu wote wauhusishe uchafu na kasoro dhidi yao hawatafanikiwa. Familia kama hiyo iliyotakaswa ambayo imewekwa mbali na kila aina ya uchafu, maovu na kasoro ambayo kwamba Qur’ani inasema:
“Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.” (Surah Al-Ahzab, Ayah 33) Hii ni famila iliyo na heshima na uaminifu, ambayo hata shetani hawezi kuisogelea, ingawa shetani ameahidi kupoteza watoto wa Adamu (as). Wakati Allah (s) alipomuumba Mtume Adamu (as) na akampamba kwa mapambo ya majina Yake mazuri:
“Na akamfundisha Adam majina ya vitu vyote.” (Surah Baqarah, Ayah 31) 78
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 79
Maadili Ya Ashura
Allah (s) akathibitisha umuhimu wa cheo chake na fadhila juu Malaika, Majini na Shetani, na akasema:
“Na tulipowaambia Malaika: Msujudieni Adam,…..” (Surah Baqarah, Ayah 34) Shetani hakulipenda hili na hivyo alijaribu kunyakua utukufu na maadili ambayo alipewa Adamu (as) na akasema:
“Akasema: Naapa kwa utukufu wako, bila ya shaka nitawapoteza wote, isipokuwa wale waja wako miongoni mwao waliosafishwa.” (Surah Saad, Ayah 82, 83) Shetani anatoa changamoto hapa kwamba mwanadamu ambaye kwake mimi nimepoteza heshima yangu, na nimekuja hapa kama msaliti kutokana na uwepo wa dhati Yako, nitayaondoa maadili yaleyale kutoka kwa watoto wake ambayo kwa ajili ya maadili hayo wamepata upendeleo zaidi yangu mimi. Upotofu ni hatia na kasoro kubwa. Kama upotofu unahusishwa na mtu fulani na kwa ukweli kama ni mtu aliyepotoka anayeonesha dalilli za upotofu, basi adui huyu (shetani) anayeahidi amenyakuwa heshima yake. Hii ni kwa sababu upotofu umejipenyeza kwenye nafsi yake. Kama mwanadamu anajilinda mwenyewe kutokana na upotofu na akafuata njia ya Ahlul-Bayt (as) na akahesabiwa miongoni mwa watumwa waaminifu wa Allah (s), anakuwa mwenye heshima, ambapo shetani anapatwa na wasiwasi kwa kutokufanikwa kumpotosha. Ahlul-Bayt (as) ni watumwa waaminifu wa Allah (s) waliotakaswa na haiwezekani kwa shetani kuwasogelea watumwa waaminifu, hivyo Ahlul-Bayt (as) wametakaswa kutokana na aina zote za uchafu, kasoro na dhambi. Hivyo, ni viumbe wenye kuheshimika zaidi. 8. Karbala – Njia ya Heshima Karbala ni njia ya heshima na kwa kupita juu ya njia hii tu, tunaweza kuelewa na halikadhalika kujifundisha maana ya kweli ya Heshima. Imamu Husein (as) alisema:
79
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 80
Maadili Ya Ashura
Mzinifu huyu mtoto wa zinaa amenileta kwenye njia panda kati ya udhalili na panga kali zinazoshambulia. Na nasema hapana kwa udhalili. Allah (s) na Mjumbe Wake (s.a.w.w.) wametukataza sisi kufuata njia hii ya udhalili. Halikadhalika kinamama watakatifu, kizazi kitakatifu, watu wenye kujiheshimu na wakataaji wa ukandamizaji wametuombea sisi ili tupigane kwa ushujaa kuliko kufuata njia ya kukimbia. (Mawassae Kalemat Imam Hussain, uk. 423) Njia ya heshima ni ile ya kushambulia panga zilizofutwa ambapo njia ya udhalili ni ile ya kutulia kwa raha, ya anasa na kupata heshima kutoka kwa watu. Imamu Husein (as) anasema kwamba: “Udhalili kamwe hauwezi kuja karibu yetu. Allah (s) ametutakasa kwa kiasi kwamba udhalili hauwezi hata kutugusa.” Imamu Husein (as) ametupa somo la heshima. Kama unataka kujifundisha heshima basi njoo ujifundishe kutoka kwa profesa huyu wa heshima, sio heshima ile ambayo inayotazamiwa kutoka kwa watu, bali heshima ile ambayo inapatikana chini ya kivuli cha panga. Imamu Husein (as) amevaa heshima kwa vazi kama hili na amepuliza nafsi kama hiyo ndani yake, kwamba mpaka mwisho wa ulimwengu huu, kama mtu anataka kuheshimiwa basi lazima atembee juu ya njia ya Husein ibn Ali (as). Hii ni maadili iliyokufa ambayo kwamba mrithi huyu wa Nabii Isa (as) ameirudisha tena kwenye uhai wake kama mwokozi. Wakati Nabii Isa (as) alipokuja mbele za watu, alisema kwamba; “Mimi ni walii wa Allah, nimenyanyuliwa na Allah (s) na nimekuja kwenu kwa ajili ya mwongozo.” Wakati Nabii Isa (as) alipoona miili iliyokufa na magonjwa yasiyoponyeka, alisema: ‘Amkeni kwa idhini ya Allah.’ Ujio wa Nabii Isa (as) ulikuwa umekomea kwenye kuhuisha wafu. Lakini wakati mrithi wa Nabii Isa (as) alipoona wagonjwa na maiti za maadili, au akiona Ummah unaoumwa, alitenda kama mkombozi na kupulizia tena roho kwenye maadili hayo yanayoonja mavumbi na mara moja yanahuika. Alihuisha maadili yale yaliyokufa katika njia ambayo kwamba mpaka mwisho wa ulimwengu maadili haya yatabakia kuwa hai.
80
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 81
Maadili Ya Ashura
9. Kuzitoa Muhanga Heshima katika njia ya Allah (s.w.t) Allah (s) ameanzisha kanuni ya kutoa muhanga moja ya vitu vyetu tunavyovipenda katika njia Yake. Kwa mujibu wa kanuni hii, Nabii Ibrahim (as) alitoa muhanga wake aupendao mno, alimtoa mwanawe Ismail (as) katika njia ya Allah (s). Allah (s) vilevile ameelekeza kuanzisha Infaq (kutumia) katika njia Yake. Kuna baadhi ambao wako tayari kutoa utajiri wao katika njia ya Allah (s) lakini hawako tayari kutoa maisha yao. Kuna baadhi ya wengine ambao wako tayari kutoa maisha yao katika njia ya Allah, lakini inapokuja kwenye heshima wanachukua njia ya kukimbia. Somo ambalo Imamu Husein ibn Ali (as) anatupatia sisi ni, kwamba kamwe tusisite kutoa maisha yetu katika njia ya Allah (s) kama ikihitajika kufanya hivyo na wakati inapokuja kwenye kutoa muhanga heshima katika njia ya Allah (s), hii vilevile lazima itolewe, kwa sababu Allah (s) Ndiye chanzo cha heshima zote. Kama tunatoa muhanga heshima katika njia ya Allah (s), Allah (s) atatupatia zaidi. Kadhalika kama tunawatoa muhanga watoto wetu katika njia ya Allah (s), basi mpaka mwisho wa ulimwengu huu Allah (s) atakiweka kizazi chetu hai. Husein ibn Ali (as) aliwatoa muhanga watoto wake pale Karbala na ni mtoto mmoja tu aliyebakia hai. Leo tunaweza kuona kizazi chake kila pembe ya ulimwengu. Kuna Masayyid (masharifu) kila sehemu ulimwenguni. Allah (s) alitoa neema kubwa kupitia kwa mtoto mmoja kiasi kwamba ulimwenguni pote sasa kuna watoto wa Husein (as). Inafaa kutaja kwamba kizazi chake kitakatifu lazima wawe makini na kuwa wenye kujali kuhusu wapi wanakotokana nako. Lazima wafuate mwenendo huo ambao kwa wenyewe huzungumza kwa sauti kubwa, kusema kwamba wanatokana na kizazi cha Husein (as). Imamu Husein (as) aliokoa mtoto mmoja tu wa kwake, hivyo mpaka Siku ya Hukumu, watu wanaweza kuona watoto wake na kutambua kizazi cha Imamu Zainul Abidin (as). Kwa upande mwingine wale ambao waliokoa watoto wao wote, Banu Umayyah na wasaidizi wao ambao walitoka wakiwa hai kwenye mapambano haya, hata kama tukijaribu kutafuta kizazi chao leo katika ulimwengu wote, hatuwezi kuwapata. Hata kama mtu atakuwa na habari ya kweli kwamba yeye ni kizazi cha Bani Umayyah, hatalifichua hili kwa yeyote. Allah (s) alitenganisha vizazi vyote vya maadui wa Husein (as). Kadhalika wale ambao wanahifadhi heshima na hawaitumii katika njia ya Allah (s), Allah (s) huzizika heshima za watu kama hao wenye kuhodhi kwenye mavumbi. Wale ambao hutoa heshima zao kwenye chombo cha uaminifu, Allah (s) huwaweka juu ya heshima mpaka Siku ya Hukumu. Hii ni kanuni ya kimungu. 81
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 82
Maadili Ya Ashura
“Na alipotangaza Mola wenu: Mkishukuru nitawazidishia na mkikufuru basi adhabu yangu ni kali.� (Surah Ibrahim, Ayah 7) Neema ambazo zimetolewa na Allah (s) lazima zitumike kwa sababu neema haipungui kwa kuitumia, kwa kweli huongezeka. Hii ndio tofauti kati ya chemchemu na kisima. Chochote kile ilichonacho chemchemu hukitumia ambapo kisima huhifadhi kilicho ndani yake. Jinsi kisima kinavyozidi kuhifadhi maji, ndivyo yanavyozidi kudorora na kuanza kunuka. Kama chemchemu vilevile nayo ikiamua kutomiminika na kuhifadhi maji, utaona kwamba magugu yataanza kuota ambapo viini vya maradhi na jemsi hukua ndani ya maji yaliyo dorora. Hata hivyo, kama ikiendelea kumiminika itabakia kuwa safi na Allah vilevile ataendelea kuizidishia. Mawingu na miti viko sawa na hili, kama ambavyo siku zote mawingu huleta mvua, lakini kamwe hayaishiwi na maji. Miti hutoa matunda na Allah hutoa zaidi. Hii sio kanuni tu kwa ajili ya vitu vya asili visivyo na uhai, bali vilevile ni kanuni kwa ajili ya wanadamu.
Mkishukuru nitawazidishia. Wale ambao hutoa watoto wao katika njia ya Allah, Allah huwazidishia kizazi chao, ambapo wale ambao huhifadhi watoto wao Allah huangamiza kizazi chao chote. Wale ambao wanahodhi heshima zao na hawazitumii katika njia ya Allah, wanakuwa dhalili daima. Wakati wa kipindi cha ukame baadhi ya watu walikusanya na kuhodhi vyakula, na wakati bei za vyakula zikipanda huviuza kwa bei ya juu. Aina hii ya kuhodhi ni dhambi kubwa sana. Wale ambao wanahodhi ngano, mchele na vyakula vingine na kuvihifadhi kwenye magunia, vilevile hawapendwi na Allah na atakuja kuwaadhibu pia. Lakini wahalifu wakubwa mno kuliko wote ni wale wenye kuhodhi heshima, wale ambao wanahifadhi heshima kwenye magunia ndani ya majumba yao wakifikiria kwamba kuna ukame kama huo wa heshima. Wale ambao walifanya vitu kama hivyo wakati uliopita, hata ukichukua majina yao huchukuliwa kama udhalili, ambapo wale ambao walifungua magunia yao ya heshima na kuyatoa kwenye masoko ya Kufa na Damascus, wamekuwa vyanzo vya heshima ambavyo vitabakia mpaka Siku ya Hukumu. 82
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 83
Maadili Ya Ashura
10. Walinzi wa Heshima za Uwongo Watu wa Kufa waliandika barua za kumkaribisha Imamu Husein (as), lakini wakati Ubaidullah ibn Ziad alipoingia Kufa, walitambua kwamba alikuwa ni mtu asiye na aibu na sasa sio maisha yao tu yaliyo hatarini bali vilevile hata heshima yao iko hatarini na kwamba walifanya usaliti (dhidi ya Muslim ibn Aqil). Kwa vile maadili yao yaliharibiwa na maana ya heshima walikuwa hawaijui, walilinda heshima yao ya bandia. Walijua kwamba Ibn Ziad ni mlevi, mzinifu na mtu muovu ambaye anaweza kufanya kitu chochote kinachowezekana. Kama watamsaidia Imamu Husein (as) atachoma nyumba zao, atawafanya watoto wao kuwa yatima na watapatwa na udhalili mkubwa; watu watasema nini kuhusu nyumba na familia zao. Kwa hiyo, wakaweka makufuli ya kutotii na heshima ya uwongo kwenye nyumba zao na wakakaa ndani ya nyumba zao katika hali ya woga. Haukupita hata muda mfupi; wakati Husein ibn Ali (as) alipoweka wazi juu yao kwamba makufuli haya yalikuwa ni udhalili uliowekwa kwenye nyumba zao. Imamu Husein (as) aliingiza moyo kwenye mwili wa Heshima iliyokufa na akaelimisha maana yake ya wazi Wale ambao walikaa ndani ya nyumba zao kwa ajili ya kuhifadhi heshima za mabinti wao na wake wa watoto wao, wakati walipoona mabinti na wake wa watoto wa Imamu Husein (as) wakiwa kama wafugwa mjini Kufa na Damascus, walitambua kile kilichomaanishwa na Heshima. Kisha watu wale wale waliunda jeshi la watu elfu nne; liliojulikana kwa jina la Tawwabin (Watubiaji) na kuziacha nyumba zao. Chini ya uongozi wa Suleiman ibn Sard Khazai walifika Karbala, wakakoga josho la kisheria katika mto Furati, wakatubia na hatimaye baada ya kupigana wote waliuawa kishahidi. Imesemwa kwamba miongoni mwa elfu nne hakuna hata wanne waliokoka, walipigana kwa ujasiri na ushujaa wakitoa mihanga maisha yao. Lakini sasa walikuwa wamechelewa sana. Hawakumsaidia Imamu Husein (as) kwa sababu ya kutokuelewa maana ya Heshima, lakini Imamu Husein (as) alipoonesha maana ya heshima katika Karbala, sasa itakuwa ni fedheha kwao kukaa ndani ya nyumba zao. Sasa hawakujali wanawake wao na walitambua kwamba maisha ambayo waliishi yalikuwa ya udhalili tu na kifo kilikuwa bora zaidi kuliko maisha kama hayo. Hii ni shule ya Karbala, somo la profesa wa Karbala na profesa wa maadili:
“Nataka kuamrisha mema na kukataza maovu.� 83
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 84
Maadili Ya Ashura Nataka kuhuisha Mema na kuyarudishia maadili uhai wake. Nataka kuwachukua watu mbali na maovu. Maisha ya udhalili ni maisha ya uovu; sio maisha ya kweli ya mwanadamu. Ingawa watu wanaweza kukuheshimu katika maisha ya udhalili, kazi yako itakuwa salama, nyumba yako itakuwa salama na kila kitu kitakuwa salama, lakini udhalili sio jina la maisha. “Kamwe sintachagua udhalili.” Kama udhalili na Husein (as) haviwezi kukutana katika sehemu moja, basi udhalili na wafuasi wa Husein (as) vilevile haviwezi kukutana katika sehemu moja. Maana hiyo hiyo ya Heshima, ambayo Imamu Husein (as) amefundisha, lazima iwe kwa wafuasi wa Imamu Husein (as). Namna ambayo Imamu Husein (as) alichagua njia ya Heshima, wafuasi wa Imamu Husein (as) vilevile lazima waipe kipaumbele hichohicho. Heshima haiundwi kwa kuhodhi; inaundwa kwa kutumia katika njia ya Allah, hivyo muhanga wa Heshima ni wenye heshima zaidi kuliko muhanga wa maisha. Imamu Husein (as) alikuwa muhanga wa maisha na halikadhalika muhanga wa heshima. Imamu Husein (as) alipata aina zote za muhanga, kwa heshima hiyo hiyo ambayo tumeihifadhi leo; Yeye (as) hakuihifadhi na kuihodhi. Bibi Ummi Salma alimshauri kwamba; “Ewe mwanangu kama unataka kwenda katika njia ya Allah (s), basi wachukue wanaume tu, usichukue wanawake. Nini matumizi ya wanawake katika njia hii?” Husein (as) akajibu:
“Ewe Mama yangu, Mwenyezi Mungu ameshataka kuniona nikiwa nimeuwawa, na ameshataka kuwaona wakiwa mateka.” Siendi kwa ajili ya mapambano ya madaraka, ninakwenda kwa ajili ya mapambano ya maadili na lazima nihubiri na kutoa masomo kuhusu Heshima na usafi pia. Nitatoa masomo kuhusu heshima na pamoja nami watoto wangu na masahaba wangu vilevile watatoa masomo kuhusu heshima. Nawachukua mabinti na dada zangu ili kwamba na wao pia watoe masomo ya kuhusu sheria kwa watu, kuwafundisha namna heshima na udhalili vinavyoundwa. Nani amefuata heshima na nani amefuata udhalili ni somo ambalo linahitaji kufundishwa, hivyo, Imamu Husein (as) alichukua dada na mabinti zake, akajitokeza kwenye uwanja wa mapambano wa maadili na akayashinda muovu. 84
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 85
Maadili Ya Ashura
Maadili ya Nne
Infaq Kutoa katika njia ya Allah 1. Kutoa katika njia ya Allah– chanzo cha mema yote..........................................86 2. Kutoa katika njia ya Allah katika Qur’ani.........................................................87 3. Kutoa katika njia ya Allah – Maadili ya Ashura................................................88 4. Msingi wa mahusiano........................................................................................88 5. Aina ya uhusiano wa kidini................................................................................89 6.Imamu Ali (a.s) – Kigezo (Us-wa) cha Kutoa katika njia ya Allah....................95 7. Bibi Zahra (a.s) – Mfano wa Kutoa katika njia ya Allah..................................97 8. Mjadala kuhusu wasio maasum.......................................................................102 9. Upana wa mipaka ya Kutoa katika njia ya Allah.............................................107 10.Imamu Husein (a.s) – Ufafanuzi wa kimatendo wa Kutoa katika njia ya Allah..........................................................................................109
85
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 86
Maadili Ya Ashura
1. Kutoa katika njia ya Allah – chanzo cha mema yote Miongoni mwa maadili ya Ashura ambayo Imamu (as) aliyakomboa katika mapambano ya maadili, ni maadili muhimu ya Kutoa katika njia ya Allah. Kutoa katika njia ya Allah maana yake ni kutumia katika njia ya Allah (s), ina maana kuacha kitu kando kwa ajili ya Allah (s). Qur’ani Tukufu imesisitiza juu ya hili takriban zaidi ya mara mia moja kwamba “Munfiqin” (wale wenye kutoa) wenye kuheshimiwa zaidi ni wale ambao hutoa utajiri wao na maisha yao katika njia ya Allah, ambapo kwa upande mwingine vilevile kuna wale ambao hawatoi chochote katika njia ya Allah. Qur’ani imelinganisha na kuwapima wote, ikisema kwamba wale ambao wanatoa katika njia ya Allah na wale ambao hawatoi katika njia ya Allah hawako sawa kwa ajili ya Allah. Kwa kweli mema yote ambayo Allah (s) ameyajadili, Kutoa katika njia ya Allah imeunda chanzo na msingi wao. Ni pale tu iwapo wema na sifa ya Kutoa katika njia ya Allah inapokuwepo kwa mwanadamu, ndipo sifa nyingine na maadili zinapoweza kuwa zenye manufaa kwa mtu huyo. Kama mtu hana sifa ya Kutoa katika njia ya Allah ndani yake basi maadili mengine yote yatakuwa hayana maana na yasio na faida. Allah (s) anasema:
“Hamtapata wema mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda…” (Surah Aali Imran, Ayah 92) Hivyo, Kutoa katika njia ya Allah ni chanzo cha mema mengine yote. Ilmu, uvumilivu, ujasiri, haki, kujiheshimu, heshima na tabia nyingine zote na sifa za mwanadamu zinakuwa zenye manufaa tu kama zinatumiwa katika njia ya Allah. Kwenda kinyume na sifa ya Kutoa katika njia ya Allah ni ubahili. Ubahili ni jina la kuhodhi. Ubahili ni jina la kutotumia katika njia ya Allah. Mapenzi ya utajiri hulingania wanadamu kwenye ubahili na uhodhi, katika hadithi tukufu inasemwa kwamba:
“Mapenzi ya ulimwengu huu ni chanzo cha sababu za maovu yote.” (Usool-e-Kaafi, Jz. 2, uk. 315)
86
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 87
Maadili Ya Ashura
2. Kutoa katika njia ya Allah katika Qur’ani Kama tulivyoandika kabla, kwamba kwa zaidi ya mara mia moja Kutoa katika njia ya Allah imejadiliwa kwa mapana katika Qur’ani Tukufu. Kwanza katika mwanzo wa Surah Baqarah wakati Allah (s) alipotaja sifa za wamumin na wanafiki; kwanza uamini katika visivyoonekana, kisha kusimamisha swala baada ya hapo ikasema:
“…na hutoa katika yale tuliyowapa (katika njia ya Allah).” (Surah Baqrah, Ayah 3)
Kama Qur’ani Tukufu inatafakariwa kwa makini na ikachambuliwa kuanzia mwanzo mpaka mwisho utapata kuelewa hadhi na cheo cha Kutoa katika njia ya Allah. “Mfano wa wale wanaotoa mali zao katika njia ya Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa punje moja iliyochipuza mashuke saba; katika kila shuke pana punje mia. Na Mwenyezi Mungu humzidishia amtakaye, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa, Mjuzi.” (Surah Baqarah, Ayah 261) “Na mfano wa wale wanaotoa mali zao kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu na uimara wa nafsi zao ni kama mfano wa bustani iliyo mahali pa juu, ikafikiwa na mvua kubwa ikatoa mazao yake maradufu; na isipofikiwa na mvua kubwa, basi manyunyu (huitoshea). Na Mwenyezi Mungu anayaona mnayotenda. (Surah Baqrah, Ayah 265) “Enyi mlioamini! Toeni katika vizuri mlivyovichuma na katika vile tulivyowatolea ardhini; wala msikusudie kutoa vilivyo vibaya, hali nyinyi wenyewe msingevipokea isipokuwa kwa kuvifumbia macho. Basi jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, Mwenye kusifiwa. Shetani anawatisha na ufukara na anawaamrisha ubakhili; na Mwenyezi Mungu anawaahidi msamaha utokao kwake na fadhila na Mwenyezi Mungu ni Mkunjufu, Mjuzi.” (Surah Baqarah, Ayah 267- 268) “…Na mali yoyote mnayoitoa ni kwa ajili ya nafsi zenu, wala hamtoi ila kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu. Na mali yoyote mnayoitoa mtalipwa kwa ukamilifu wala hamtadhulumiwa. Ni kwa ajili ya mafukara waliozuiliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu, wasioweza kwenda huku na huko katika ardhi. Asiyewajua hali zao anawadhania kuwa ni matajiri kwa sababu ya kujizuia. Utawafahamu kwa alama zao; hawaombi watu wakang’anga’nia. Na mali yoyote mnayoitoa, kwa hakika Mwenyezi Mungu anaijua. Wale watoao mali 87
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 88
Maadili Ya Ashura zao usiku na mchana kwa siri na dhahiri, wana ujira wao kwa Mola wao; wala haitakuwa hofu juu yao wala wao hawatahuzunika.” (Surah Baqarah, Ayah 272-274)
3. Kutoa katika njia ya Allah – Maadili ya Ashura Kutoa katika njia ya Allah na maadili mengine yalihuika kwa ajili ya Ashura; kwa hiyo hujulikana kama maadili ya Ashura. Kamwe isije ikaeleweka kwamba Maimamu wengine Maasumin (as) hawakuleta maadili haya au maadili haya hayakuwepo wakati wa uhai wa Maimamu wengine Maasumin (as) au kwamba uoni wao ulikuwa si wa kueneza maadili haya. Mitume wote wa Allah (as) na Maimamu (as), hata mawalii wa Allah (s) na wanachuoni wema ambao ni warithi wa Mitume wameelimisha maadili haya miongoni mwa watu, lakini njia ambayo Mkuu wa Mashahidi (as) alivyoelimisha maadili haya kwa watu na jinsi alivyoyahuisha maadili haya, hakuna mwingine aliyeyauhisha kwa njia hii, kwa hiyo, ni sahihi kuyaita maadili haya kama maadili ya Ashura au maadili ya Husein (as). Hii ni kwa sababu mizizi ya maadili haya ina damu ya Husein (as) na damu ya watoto wa Husein (as). Husein (as) alitoa heshima na usafi wake kwa ajili ya msingi wa maadili haya na akayachukua mpaka kwenye kilele chake. Kwa hiyo, kama watu wanajihusisha wenyewe na maadili haya, ni kwa ajili tu ya juhudi za Imamu Husein (as).
4. Msingi wa Mahusiano Watu wana uhusiano na dini, vilevile wanao uhusiano mahususi na Allah (s), halikadhalika watu walikuwa na uhusiano na Mitume na Maimamu (as), lakini swali ni iwapo mahusiano haya yalikuwa katika maadili mazuri yajulikanayo (Ma’ruf) au msingi wao ulikuwa umetegemezwa juu ya uovu na uwongo. Tunahitaji kuelewa ukweli huu wa kawaida kwamba tunao uhusiano miongoni mwa kila mmoja. Tunayaita mahusiano fulani kati ya wanadamu kama mazuri na baadhi kama ya uwongo au haramu. Wakati wa lawama na ukosoaji tunasema kwamba fulani na fulani wana uhusiano wa haramu. Hivyo, kunakuwepo nasaba na uhusiano, lakini tunachotaka kuona ni aina ya uhusiano ambao unafikiriwa vizuri. Kila uhusiano hauwezi kuwa mzuri na kila uhusiano hauwezi kuwa wa kupendelewa au kupendwa. Mahusiano mazuri ni yale ambayo yameanzishwa juu ya msingi wa maadili, ambapo mahusiano haramu ni yale ambayo siyo ya aina nzuri na msingi wake umetegemezwa juu ya maovu na uwongo. Hivyo, kama mahusiano yanaanzishwa kati ya wanadamu katika misingi ya matamanio, basi haya yat88
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 89
Maadili Ya Ashura achukuliwa kama mahusiano haramu, kadhalika kama uhusiano uko katika msingi wa ghadhabu basi utachukuliwa kama uhusiano wa uadui. Chuki na uovu pia ni aina ya uhusiano ambao umetegemezwa kwenye ghadhabu. Urafiki ni uhusiano mzuri kama haukutegemezwa juu ya matamanio, uroho na ulafi. Hali ya mahusiano kati ya wanadamu ni imma uhusiano huo ni mzuri na halali huku ukiwa umetegemezwa juu ya wema au uhusiano ambao ni haramu na umetegemezwa juu ya uovu.
5. Aina ya uhusiano wa kidini: Uhusiano wa mahitaji ya maisha Imamu Husein (as) ameeleza katika khutba zake muhimu, kwamba watu wapo pamoja na dini na kaulimbiu ya dini ipo midomoni mwao mpaka wakati dini itakapowatekelezea mahitaji yao maisha, lakini siku mahitaji yao yasipotekelezwa na dini, na hiyo dini haiwi msingi wa haiba ya utu wao, dini itakuwa ni ya mazungumzo na mashairi tu midomoni mwao. Dini itabakia tu kama msemo unaotolewa kutoka kwenye ndimi zao, mbali na hilo hakutakuwa na chochote katika jina la dini. Imamu Husein (as) anasema:
“Dini imekuwa ni msemo tu na onjo kwenye ndimi zao, hivyo wakati wanapopimwa, wachache sana watabakia na dini.” (Mawassae
Kalemat Hussain, uk. 356)
Khutba hizi za Imamu Husein (as) hazikuwa tu kwa ajili kuhubiri. Wakati alipoona kwamba katika vita vya maadili utawala wa maovu ulikuwa unaanzishwa, alianzisha mageuzi na akasema kwamba watu walikuwa na dini tu kwa ajili ya mahitaji yao ya maisha. Watu wanajihusisha katika kupata mahitaji yao ya maisha kutoka kwenye dini na wakati muda ukifika wa kutoa muhanga mahitaji haya ya maisha kwenye dini, utaona kwamba “wachache sana watabakia na dini.” Hii ni kauli ya Imamu Husein (as) na kilichotokea Karbala kilikuwa ni mwenendo wake, hivyo alikuwa anatuonesha, kwa maneno na mwenendo kwamba watu wa dini walikuwa wachache sana. Imamu Husein (as) aliona katika Madina jinsi wengi 89
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 90
Maadili Ya Ashura walivyokuwa watu wa dini wa kweli. Katika Masjid-e-Nabawi kulikuwa na safu ndefu za swala za jamaa. Hata leo kama utatembelea huko, pamoja na shukurani zote kwa Allah (s) utaona kwamba Masjid-e-Nabawi ni mfano bora wa uzuri wa kiusanifu. Kwa sifa njema wanaonesha picha (filimu) ulimwenguni kote kuhusu ujenzi mkubwa wa kisanifu wa msikiti huu. Wanataka kuthibitisha ukubwa wa Uislamu kwa jengo hili, na unapoona safu za swala ndani yake, ni pana na ndefu kwa kiasi kikubwa kwamba wakati mwingine msikiti wote hauwezi kuchukua idadi ya watu inayotakiwa kuswali humo. Lakini watu hawahawa wanaoswali katika safu ndefu walijaribiwa, walilinganiwa kwa ajili ya dini, mpaka wakati dini ilikuwa inatekeleza mahitaji yao ya maisha, Masjid-e-Nabawi ilibakia ikiwa imejaa na hai. Lakini wakati Imamu Husein (as) aliposema kwamba wamechukua vya kutosha kutoka kwenye dini na sasa ni wakati na wao kutoa chochote. Kwa vile muda wa mtihani umefika, safu hizi ndefu zenyewe zilipungua na Imamu Husein aliachwa na watu sabini na mbili. Halikadhalika katika Makka Imamu Husein (as) aliona kwamba watu wamevaa ”Ihram” (vazi la ibada) kwa ajili ya Hijja na kuvutiwa mno na dini kiasi kwamba walikuwa hawako tayari kuvua “Ihram” zao. Lakini dini ilipowaambia wavue “Ihram” na wavae sanda ya kifo “wachache sana walibakia na dini.” Wale ambao walisafiri na Kiongozi wa Mashahadi (as) kwa ajili ya kukusanya ngawira na kupata mahitaji yao ya maisha kupitia kwenye dini, wakati walipowasili njia panda ya Kufa, Imamu Husein (as) aliwaambia “kama mmefuatana na mimi mpaka hapa kwa tamaa kwamba katika jina la Husein mtapata chochote, basi jueni kwamba sasa sio wakati wa kuchukua kitu katika jina la Husein, badala yake ni wakati wa kutoa.” “Nani yuko tayari kutoa damu yake kwa ajili yetu?” (Mawassae
Kalemat Hussain, uk. 328)
Hivyo tunajua kwamba katika wakati wa majaribu na mitihani wachache sana hubakia na dini. B. Uhusiano wa mwongozo na utii Watu wengi wana uhusiano na dini kwa ajili tu ya kutekeleza mahitaji yao ya maisha, na kuna mifano mingi katika historia. Halikadhalika watu wamejaribu kuanzisha aina tofauti ya uhusiano na Mitume (as) 90
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 91
Maadili Ya Ashura na Maimamu Maasumin (as). Hii ni kwa sababu wakati watu wanaposogea mbali na muundo sahihi wa uhusiano basi hujaribu kuendeleza aina nyingine za uhusiano pamoja na watu haohaho. Hivyo wengi walikuwa wakijishughulisha na kufanya aina tofauti za mahusiano na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Leo vilevile mbinu hiyohiyo inafuatwa, kama watu wanataka kazi fulani ifanyike kutoka kwa mtu mwenye cheo, wanaanza kujenga uhusiano naye. Kama kuna gavana au mtu fulani aliyeko kwenye cheo au nafasi nzuri, watu siku zote hujaribu kuanzisha uhusiano mzuri naye ili kwamba aweze kuwa mwenye msaada wakati wa shida. Watu wanataka kuendelea na kufanikiwa kwa kutumia mahusiano; wanataka kutatua matatizo yao kwa mahusiano. Allah (s) alinyanyua Mitume na watu wakaanza kuendeleza mahusiano nao, mtu fulani akapata jina la mtoto, mtu fulani akawa baba mkwe, mtu fulani akawa mkwe mwana, na kadhalika, baadhi walikuwa wamevutiwa kuwatoa mabinti zao ambapo wengine walivutiwa kuchukua mabinti zake (s.a.w.w.) na yote haya ilikuwa ni kwa madhumuni tu ya kuanzisha uhusiano na Mtume (s.a.w.w.) na uhusiano huu utawasaidia katika nyakati za shida (hata baada ya hapo). Lakini wakati fursa ilipokuja uhusiano huu ulikuwa hauna maana. Kama mahusiano yanaanzishwa katika misingi kama hii basi mahusiano haya hayana maana. Wakati uhusiano utaanzishwa pamoja na mlinzi, hautakiwi uwe ule wa baba mkwe na mkwe mwana, uhusiano lazima uwe ule wa mwongozo na utii. Hivyo Allah (s) alisema kama unataka kuanzisha uhusiano na Kaaba Tukufu basi usiwe mtunza funguo na wale wanao toa maji kuwapa mahujaji, badala yake toa katika njia ya Allah (s) na uhusiano wako na Kaaba utathibitishwa. C. Uhusiano wa Maombi Allah amewapendelea wanadamu kwa neema kubwa na fursa, na neema hii ni Maombi. Maombi ni jina kwa ajili ya mawasiliano na Allah (s); ni njia bora ya kuendeleza uhusiano na Allah (s). Allah (s) anasema:
“Na waja Wangu watakapokuuliza habari Yangu, Mimi niko karibu. Naitikia maombi ya mwombaji anaponiomba. Basi nawaniitikie Mimi na waniamini Mimi ili wapate kuongoka.� (Surah Baqrah, Ayah 186) 91
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 92
Maadili Ya Ashura Ni nini maana ya maombi haya? Kwa kawaida msingi wa uhusiano wetu na mtu fulani ni kwa ajili ya kutatua matatizo yetu kwa msaada wa uhusiano huu. Ili kufafanua uwelewaji wa somo hili la Uhusiano hebu tuchukue mfano huu: utaona kwamba wakati watu wakimuona mtu wa dini, mjuzi, mwanasiasa na mtu mstaarabu, hupenda kuwa karibu na mtu huyo. Na kama ilivyo watu wakubwa vilevile hujaribu kuanzisha uhusiano na watu wengine wenye vyeo vya kiulimwengu; hususan kama wanaweza kujenga uhusiano na watu wa Magharibi, hufikiria kwamba hicho ni kitu kikubwa sana! Watu huona fahari ya kuanzisha uhusiano na hujivuna kwa kuwa na kiwango hicho cha uhusiano na fulani na fulani na kwamba wanatembelea nyumba yake na anakuja kwenye nyumba yao mara kwa mara. Tuna njia za kitamaduni za kuanzisha uhusiano kwa kutoa kadi la mwaliko kwa kila mtu tunayemtaka, kadi ambalo lina jina letu, cheo, email, fax, namba ya simu na anwani. Hii ina maana kwamba kama unataka kuwasiliana na mimi na unataka kuanzisha uhusiano na mimi unaweza kunipigia simu kwa namba hii. Nachukua kadi hili miaka mingi inapita, lakini sioni haja ya kuwasiliana naye kwa hiyo sifanyi mawasiliano yoyote, lakini basi siku moja nilinaswa katika shida fulani na sikuweza kupata njia ya kujinasua nayo. Punde tu nikakumbuka kwamba ninalo kadi la mwaliko la mtu ambaye kama nitawasiliana naye atakuwa na uwezo wa kutatua tatizo langu. Kwa hiyo nilimpigia simu na nikamueleza tatizo langu; ni mtu mzuri alitatua tatizo langu mara moja. Kisha tena kwa mara nyingine nilikuwa na shida, ilikuwa nimpatie kazi mtu fulani na kwa hiyo kwa ajili ya kumpatia kazi mtu fulani, niliwasiliana na mtu yule mwenye huruma tena na safari hii tena akalitatua tatizo langu. Halikadhalika wakati wowote ninapokuwa na shida ninawasiliana naye, kwa mfano kama ninataka viza ninawasiliana naye na hunipatia viza, wakati fulani nilipata shida ya kupata nyumba na akanisaidia kupata nyumba. Kwa ufupi yote haya ni kwamba, kwa chochote kile nilichohitaji niliwasiliana naye na alinipatia. Sasa ambacho lazima tutafakari hapa ni kwamba amenipa kadi kwa madhumuni ya kuanzisha uhusiano na yeye lakini nimeutumia uhusiano huu ili kutekeleza haja zangu na kukamilisha matamanio yangu. Hata hivyo, haja ya kuanzisha uhusiano na mtu yule ilikuwa kwa sababu na mimi vilevile ni mtu mashuhuri kama yeye, hivyo kulikuwa na ulazima wa kuwepo uhusiano kati ya watu wawili, hata hivyo niliutumia vibaya uhusiano huu na nikaufanya ni njia za kukamilisha matamanio yangu. Allah (s) alitufikiria sisi kuwa ni wenye kustahiki kuongea na Yeye na hivyo Allah (s) akatupa namba ya mawasiliano: “Ewe Mtume! Kama mtu akikuuliza kuhusu 92
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 93
Maadili Ya Ashura Mimi muambie niko karibu sana:” “Na waambie wakati wowote wanaponiita nitawasikiliza.” Lakini niligeuza uhusiano huu na Mola wangu kwa ajili ya kukamilsha matamanio yangu. Kwa vile Allah (s) ni mkarimu mno anatekeleza haja zangu. Hakuna hata siku moja wakati kwa maombi yangu nilimuomba Allah (s) kwa ukamilifu nikitafuta dhati Yake, bali kila nilipomuomba ni kwa ajili ya ukamilishaji wa matakwa yangu na utekelezaji wa haja zangu. Lakini baada ya Allah (s) kunipa namba ya mawasiliano, anatazamia kwamba siku moja mtumwa wangu ataniita kwa ajili Yangu tu na nitasema ndio. Mtumwa wangu atasema tu “Allah” na nitamuuliza iwapo aliniita ambapo yeye atasema: “nimekuita Wewe na Wewe tu.” Hatasema kwamba; nimekuita kwa sababu mateso yangu kutokana na maumivu fulani yaliyosababishwa na kiu na njaa au kwa sababu ya shida na umasikini. Badala yake atasema kwanba; nimekuita Wewe kwa sababu tu nilipenda kukuita Wewe na kwa ajli Yako tu. Anasubiri kwa ajili ya uhusiano kama huo. Hivyo, kama mja anataka kuanzisha uhusiano, basi hii ndio aina ya uhusiano ambao lazima uanzishwe. Huu ni uhusiano wa kweli, ingawa Allah (s) ni Muumba Mwenye nguvu na Mfalme, kama akiombwa kwa haja mahususi huitekeleza. Kama una uhusiano na mtu fulani mkubwa, ambaye vilevile huweza kutekeleza haja zako, basi Allah (s) ni Mola, Mtunga sheria, na kazi yake ni kutunga sheria, iwapo unamuomba au la Ubwana na utungaji sheria Wake utadhihirika. Imekuwa ni utamaduni katika nchi yetu kwamba kama wale ambao wameaminishwa kazi katika maofisi, hutoa huduma zao tu baada ya kupokea hongo. Hata kwa ajili ya sahihi ndogo tu, atafanya hivyo baada ya kupokea hongo; hii ni kwa sababu siku hizi huu umekuwa utamaduni. (Wala maofisa hao hawaoni aibu kuidai au kuipokea na mtoaji anaridhika kutoa bila maswali yoyote – huu ni msiba mkubwa!) Kwa hiyo tunafikiri kwamba bila hongo au rushwa hatuwezi kupatiwa huduma. Hata katika masuala ya dini tunafikiri kwamba mpaka niweke shilingi tano au mia tano… katika sanduku la sadaka msikitini na vituo vya dini, vinginevyo Allah (s) hataweka neema zake juu yangu. Hata kama ukiwa kafiri, mshirikina au mnafiki na ukaweka shilingi mia tano yako kwenye mfuko wako, basi hiyo pia haina athari yoyote kwenye utukufu wa Mola Wako. Amekupa kila kitu, amekupa macho bila kuombwa, amekupa miguu bila kuombwa, na bila ya kumuomba amekupa neema zote. Ataendelea kutoa utukufu Wake. Wakati ukiumwa na hata humuombi atakuponya, hii ni kwa sababu ni Muumba, ambapo maana yake ni kwamba ametufanya sisi kuwepo, ametuumba sisi. Hii ndio maana ya Ubwana, kwamba ametupa siha na kama ambavyo uumbaji wake hauna masharti, Ubwana wake ni kamili, hakuna masharti katika Sifa Zake, kwa kweli ni matendo yetu ndio yenye masharti.
93
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 94
Maadili Ya Ashura Allah (s) hakusema kwamba mpaka unipendeze vinginevyo sikupi chochote. Ingawa ametutaka tumuabudu, lakini kuna tofauti kati ya kupendezesha na kuabudu. Allah (s) wala hata hasemi kwamba kama huniabudu sitakupa kitu chochote, iwapo unamuabudu au la atakupa, faida za kuabudu ni zetu tu. Ndio, amesema kwa uhakika kuinama kwa kunyenyekea mbele Yake baada ya kupata Utambuzi (Maarifat) na kisha atasambaza neema Zake juu yetu na atamimina rehema Zake juu yetu. D. Uhusiano wa Kutoa katika njia ya Allah Uhusiano ambao unaasisiwa juu ya misingi ya kuvunjika wakati muda wa kutoa ukija, hivyo uhusiano ambao wanadamu wanapaswa kuanzisha na dini, lazima uwe ule wa Kutoa katika njia ya Allah. Hivyo, Allah (s) anasema, lazima utumie katika njia Yangu; ambapo humaanisha uhusiano wa kutoa, na sio kila siku kutegemea kupokea. Huu ndio msingi ambao kwamba Imamu Husein (as) alisema kwamba; watu wameanzisha uhusiano na dini kwa kupokea tu na kutekeleza mahitaji yao ya maisha. Wakati watu kama hao wakiona mahitaji yao ya maisha yako hatarini au kazi na ajira zao zinahatarishwa au ada zao kwa ajili ya kufundisha na kaulimbiu wanazopata kutoka kwa watu ziko kwenye hatari, wanaiacha dini nyuma. Watu wa dini ambao wamebakishwa wanaweza kuhesabiwa kwa vidole. Kama uhusiano unaanzishwa pamoja na Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) na kama uhusiano unafunganishwa na Maimamu Maasumin (as), basi msingi wake unahitaji kupimwa. Kama haya hayategei juu ya dini, bali yametegemezwa juu ya mahitaji ya maisha na vishawishi vya ulimwengu, basi uhusiano huu utavunjika mara moja. Hii ni kwa sababu mpaka wakati uhusiano huu umeendelea kukidhi madhumuni, kutekeleza haja na kukamilisha mahitaji ya maisha utabakia imara, lakini wakati wa kutoa ukija, mahusiano haya hayataendelea kama mwanzoni. Kama mwanadamu atatambua kwamba madhumuni yake yanaweza kutekelezwa mahali pengine, mara moja atabadilisha mwelekeo wake kuelekea kwenye chombo kingine pia. Leo aina ya uhusiano ambao upo ni sawa na uovu dhidi ya kile ambacho Imamu Husein (as) alianzisha mageuzi ili kupiga vita uovu na kuleta kwenye uhai maadili kama Kutoa katika njia ya Allah. Leo tunaweza kuona kwamba uovu unarudi tena. Tumeweka msingi wa uhusiano wetu pamoja na Maimamu Maasumin (as) kwa ajili 94
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 95
Maadili Ya Ashura ya kutekeleza matamanio na matakwa yetu. Tunaendesha tu biashara zetu kupitia wao, tunapata usalama wa maisha yetu na siha kutoka kwao, lakini siku wakituambia tumekupeni vya kutosha, sasa ni wakati wa kuchukua kutoka kwenu, hapo tutakuja kujua iwapo uhusiano wa aina hiyo hiyo unabakia nao au la, iwapo tumejitayarisha kwa ajili ya Kutoa katika njia ya Allah au la.
6. Imamu Ali (a.s) – Kigezo (Us-wa) cha Kutoa katika njia ya Allah Leo tunaishi katika zama za kunyimwa ambako tunanyimwa hata kuonana na Imamu wetu (a.t.f.s), Imamu (a.t.f.s) yuko nyuma ya pazia na anaishi maisha yake katika Ghaibat kubwa. Lakini kabla zama za ghaibat, watu walikuwa wakitoa heshima zao na kukutana na Maimamu Maasumin (as). Maimamu hawa Maasumin (as) walikuwepo miongoni mwa watu, na watu wenyewe walijitolea katika kuwahudumia Mitume (as) na Maimamu wa mwongozo (as). Ni uhusiano wa aina gani waliokuwa nao pamoja na Maimamu (as)? Ni mahusiano gani waliyokuwa nayo watu hawa pamoja na Imamu Ali (as)? Wakati wowote walipoomba msaada kutoka kwa Imamu Ali (as), hutaona hata mfano mmoja ambako Imamu (as) aliwarudisha mikono mitupu bila kutekeleza haja zao. Yeyote yule aliyeomba msaada kwa Ali (as), Ali (s) humtekelezea haja zake (za halali) na kumuondolea shida zake. Kuna mifano mingi ambayo ipo, lakini mmoja wao unajulikana na ni mashuhuri sana na tukio hilo ambalo halikanushiki halihitaji hata uthibitisho wa kihistoria kwa usahihi wake. Tukio hili lilikuwa wakati wa utawala wa Imamu Ali (as) na ukhalifa wake, wakati siku moja Ali (as) alipotoka nje ya nyumba yake na nje ya lango la mji, alimuona mjane mmoja akichota maji kutoka kwenye kisima ili ayapeleke nyumbani kwake, lakini alikuwa anapata shida kubeba kiriba kile cha maji, hivyo wakati mwingine alikuwa anakiweka chini, kisha akakibeba na kukiweka kichwani mwake. Wakati Imamu Ali (as) alipoona hali hii, alimuomba mwanamke yule iwapo atamruhusu ili amsaidie. Bibi yule akakataa na akasema kwamba ataweza mwenyewe; Imamu Ali (as) akasisitiza kwamba hataweza kubeba kiriba hicho na Imamu (as) akakichukua kiriba kile na akatembea na bibi yule. Njiani Imamu (as) alimuuliza ni kwa nini alikuja kuchota maji yeye mwenyewe; “Huna mwanaume katika nyumba yako? Huna mume?” Bibi yule alikuwa hajui anazungumza na nani, hivyo badala ya kujibu kwa upole kwamba mume wake aliuawa wakati akipigana upande wa Ali (as) dhidi ya gavana wa Damascus (Mu’awiya), alitumia maneno makali na akasema watoto wangu ni yatima, mume wangu aliuawa katika vita vya Siffin akifuatana na Ali (as). 95
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 96
Maadili Ya Ashura
Imamu Ali (as) alisikiliza majibu yake kwa makini na akafikisha maji yale nyumbani kwake na akasema, nisubiri kidogo nitarudi. Imamu Ali (as) akarudi nyumbani kwake, akachukua tende, unga na mahitaji mengine muhimu kisha akarudi nyumbani kwa bibi yule pamoja na mzigo ule wa chakula. Imamu Ali (as) akamwambia yule bibi, sasa kuna mambo mawili ya kufanya; moja ni kuwaangali watoto na la pili ni kutayarisha chakula kwa ajili yao. Kama ukiona ni sawa unaweza kuwaangalia watoto wako wakati ambapo mimi natatayarisha chakula au utayarishe chakula na mimi nitawaangalia watoto. Kisha akasema; kwa vile watoto wanahusiana na wewe huenda wakashangaa na wasipende kucheza na mimi, kwa hiyo, ni vizuri wewe uwaangalie watoto wakati mimi natayarisha chakula kwa ajili yenu wote. Imamu Ali (as) akawasha moto katika nyumba ile, ambapo kwa miezi mingi hakuna moshi ulioonekena humo, wanawake jirani zake waliona moshi wakasema, Allah (s) amewapa kitu cha kupika na kula. Mmoja wa wanawake wale akaja na akasema; leo moshi umeonekana kwenye nyumba yako pia, inaonekana leo umepata kitu cha kula. Yule mjane akasema, Allah ambariki mwanaume huyu, aliona hali yangu na akanisaidia kuchota maji, kisha alipata kitu na kutayarisha chakula, ni mtu mwenye msaada sana na tabia nzuri kiasi kwamba sasa anatayarisha chakula kwa ajili ya watoto wangu. Wakati wanawake wale walipomsogelea mtu yule kwa karibu walianza kupiga mapaji yao ya uso na kupiga kelele wakimuambia yule mjane Allah akuangamize, unajua mtu huyu ni nani? Ambaye umempa kazi kama hiyo? Yule mjane akajibu akasema sijui, nilijua tu kwamba ni mtu mwenye tabia nzuri. Mwanamke mwingine akamuambia kwamba, mtu huyu ni Amirul-Mu’minin (as); ni Khalifa Ali ibn Abi Talib (as) ambaye anakoka moto nyumbani mwako. Unajua ni kutoka kwa nani unapata huduma hii? Wakati yule mjane alipotambua kwamba anapata huduma hii kutoka kwa mtu maasum, alimuendea na akakunja mikono yake akasema huku akimuomba msamaha kwa maneno yake machafu na tabia mbaya. Akasema alikuwa mjinga; nilikuwa sijui wewe ni nani. Yeye (as) alisema sio hivyo, sio kwa sababu yako bali kwa sababu yangu mimi. Imehifadhiwa kwenye historia kwamba Ali (as) alisema: “Ilikuwa ni jukumu langu kwamba kwa kila askari yeyote aliyeuliwa katika jeshi langu, lazima mimi ningekuwa ndiye mwenye kuwaangalia watoto wake, lakini katika suala hili wewe umekuwa muangalizi wa watoto, kwa hiyo, unisamehe mimi kwamba sikuweza kuja kukupa msaada mapema.� (Biharul Anwar, Jz. 4, uk. 52, Sura 104, na Majmua e Aasaar, Jz. 18, uk. 347) 96
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 97
Maadili Ya Ashura Huu ni mfano mmoja wa sifa za Imamu Ali (as) za kutekeleza matakwa ya watu, yeyote yule anayeomba msaada kutoka kwa Imamu Ali (as), atamkuta yuko tayari kumsaidia kwa hali yeyote, kwa kweli, yuko tayari hata kupika chakula kwa ajili ya watoto wake na kuwaangalia. Yeye (as) ndiye anayetatua matatizo, yeye (as) ni njia ya kupata baraka ya Allah, yeye ni njia ya kupata riziki ya Allah na kwa hiyo, iwapo itaombwa kupitia kwake Allah hutoa riziki hiyo na kumpa huyo anayeomba. Lakini yeye (as) vilevile anasubiri wewe unapotambua cheo chao, na utawaomba kwa mujibu wa cheo chao na sio tu kwa ajili ya matakwa yako. Muombe Ali (as) kwa ajili yake, kwa ajili ya mapenzi na kwa kumtambua (maarifat) na sio kwa ajili ya kutekelezewa matakwa na haja zako. Tunahitaji kufikiria aina ya uhusiano tulio nao na Maimamu hawa watoharifu (as). Je Allah (s) ameniumba mimi ili kupokea tu kutoka watu hawa, je niendelee kuwaomba na waendelee kunipa? Wao vilevile wanaweza kuomba kitu kutoka kwetu, na katika njia hiyo hiyo kama walivyotusaidia kila wakati, lazima tujitokeze na kuwasidia wanapohitaji msaada wetu. Wakati wanapoita; “Njooni mtusaidie! Njooni na muwe tayari kujitoa muhanga, muwe tayari kutoa maisha yenu katika njia ya Allah kama sisi.” Lakini kama uhusiano wetu na wao unakomea tu kwenye kupokea, basi uhusiano huu huenda ukavunjika mapema sana, hata hivyo kama pamoja na kupokea tumejifunza vilevile kutoa, tutabakia imara na wenye maamuzi vilevile katika hatua ya kutoa. Familia ya Ahlul-Bayt (as) vilevile imetufundisha kutoa katika njia ya Allah. Tunawapenda Ahlul-Bayt (as), lakini kama mapenzi haya yanaanzishwa katika msingi wa kuchukua tu kutoka kwao, basi wakati wa kutoa ukija, inawezekana kwamba uhusiano huu huenda ukavunjika. Bali lazima tuangalie kutoka kwenye tabia zao na vilevile kujifunza kutoa. Kama haja ikijitokeza ambapo tunahitajika kutoa maisha yetu, lazima tuwe tayari kujitolea katika huduma yao, ni katika hali hii tu uhusiano hauwezi kuvunjika.
7. Bibi Zahra (s.a) – Mfano wa Kutoa katika njia ya Allah 1. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitoa zawadi shamba la Fadak kwa Bibi Zahra (as) na mapato ya shamba hili yalikuwa yakienda kwake, lakini baadae Bibi Zahra (as) alipokonywa shamba hili na wanyang’anyi. Siku moja Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimpeleka mgeni nyumbani kwa Bibi Zahra (as); ilikuwa ni nyumba ambayo ilikuwa ikipokea mapato kutoka kwenye shamba la Fadak. Mgeni aliingia ndani ya nyumba pamoja na Imamu Ali (as)
97
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 98
Maadili Ya Ashura Bibi Zahra (as) anamwambia Imamu Ali (as): “Ewe Abul Hasan jioni hatutakuwa na chakula chochote hata kwa watoto wetu, je itakuaje kwa mgeni?” Imamu Ali (as) alitoka nyumbani ili akachue mkate kwa mtu fulani. Kwa bahati njiani alikutana na Mikidadi (ra) na Imamu Ali akachukua dinari moja kutoka kwake kama mkopo ili akapate kumlisha mgeni ambaye yuko nyumbani kwake. Njiani akirudi kuelekea nyumbani akakutana na ombaomba ambaye alimuomba, “Ewe Ali! Leo hatuna chochote cha kula nyumbani kwetu.” Ali (as) alimpa ombaomba yule ile dinari moja aliyochukua kama mkopo na akarudi nyumbani mikono mitupu. Akamuambia Bibi Zahra (as): “Ewe Sayyida! Sasa hatuna chochote mbali na kufedheheka mbele za mgeni huyu, nilikuwa ninarudi na dinari moja niliyokopa, lakini njiani nilikutana na ombaomba na nikatoa ile dinari nikampa na nimerudi mikono mitupu.” Bibi Zahra (as) akasema: “Hiki chakula kilichopo humu ndani sasa hakikuletwa na wewe?” Amirul-Mu’minin akajibu: “Mimi sikuleta chakula hiki nilikwenda kuchukua mkopo, lakini nimerudi baada ya kuutoa mkopo huo vilevile kwa mtu mwingine.” Swali sasa ni kwamba hali katika nyumba ya Bibi ya Zahra (as) ilikuwa hivyo kiasi kwamba kulikuwa hakuna hata chakula kidogo kwa ajili ya mgeni, sasa yale mapato yote yanayotokana na shamba la Fadak yamekwenda wapi? Mapato yanayotokana na shamba la Fadak yalikuwa yakigawanywa miongoni mwa omba omba na masikini wote wa Madina. Mantiki ya Ahlul-Bayt (as) ilikuwa kwamba: “Hatukufuata dini kwa ajili ya kuchukua chochote, tumefuata dini kwa ajili ya kutoa. Hata mapato ya Fadak yakija tutayatumia katika njia ya Allah (s) na hata kama ni kutoa muhanga sehemu yetu tuipendayo mno ya uhai wetu tutaitoa katika njia ya Allah (s).” 2. Abu Said Khudri anasimulia kwamba Ali (as) baada ya mapumziko yake ya mchana (Kailula) alisema: “Ewe Fatima! Je, kuna kitu chochote cha kula?” Bibi Zahra (as) akajibu: “Naapa kwa dhati ile ambayo ilimuheshimu baba yangu kwa cheo cha Utume sina chochote ambacho naweza kukupa, kwa kweli kwa siku mbili hizi zilipita hatujakula kitu chochote.” Imamu Ali (as): “Kwanini hukunijulisha, ningepata kitu chochote kutoka mahali fulani.” Bibi Zahra (as) akasema: “Nimeona aibu kwamba Allah (s) angeniona mimi nadai kutoka kwako na kukuweka katika shida.” Imamu Ali (as) akiwa mwenye kumtegemea Allah (s) aliondoka nyumbani, akachukua dinar moja kama mkopo kutoka kwa mtu fulani, alitaka kununua kitu kwa ajili ya nyumbani kwake lakini ghafla akamuona Mikidadi (ra) ambaye rangi ya uso wake ilikuwa imebadilika kwa joto la kiangazi. Ali (as) akamuuliza: “Ni kitu 98
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 99
Maadili Ya Ashura gani kilichokusibu ewe Mikidadi? Kwa nini uko nje na joto lote hili kali?” Mikidadi akajibu: “Ewe Abul Hasan! Nipishe na usiniulize ni kwa nini nimetoka nyumbani.” Ali (as) akasema: “Ndugu yangu sio haki kwako wewe kuficha matakwa yako kwangu mimi.” Mikidadi (ra) akasema: Kwa vile ni lazima nikuambie, naapa kwa dhati ile ambayo imemtunuku Muhammad (s.a.w.w.) Utume, nimeiacha familia yangu wakiteseka kwa njaa, walikuwa wanalia na sikuweza kuvumilia hilo, kwa hiyo nimeondoka nyumbani katika hali hii ya joto kali.” Imamu Ali (as) alitiririkwa na machozi machoni mwake na ndevu zake zikalowa kwa machozi. Akasema: “Mimi pia naapia hivyo hivyo; mimi nimetoka nyumbani kwa sababu hiyo hiyo, hakuna kitu nyumbani kwangu, nimechukua mkopo dinar moja ambayo nakupa wewe sasa.” Ali (as) alimpa Mikidadi (ra) dinari ile na kisha akaenda kwa Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) na akaswali swala zake za mchana na baadae akaswali swala yake ya Magharibi na Isha. Wakati Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) alipomaliza swala yake na wakati anapita kwenye safu za jamaa, aliashiria kwa Ali (as) na akamuita. Ali (as) alisimama na akanza kutembea kuelekea kwa Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) kwenye mlango wa msikiti. Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) akasema: “Ewe Abul Hasan! Kuna nini cha kula kule leo jioni?” Ali (as) akabakia kimya, kwa hili Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Sema Hapana ili nisiende na wewe au sema Ndio ili niende na wewe nyumbani kwako.” Tayari ilikuwa umeshuka wahyi juu ya Mtume (s.a.w.w.), wa kula chakula cha jioni pamoja na Ali (as). Baada ya hili Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) alishika mikono ya Ali (as) na akaondoka naye kuelekea nyumbani kwake na wakaingia nyumba ya Bibi Zahra (as). Alikuwa amekaa kwenye mswala na nyuma yake kulikuwa chombo kikubwa cha kupikia (Chungu) kikiwa juu ya moto ambamo moshi ulikuwa unatoka humo. Wakati aliposikia sauti ya Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) mara moja alisimama na akamsalimia. Mtume (s.a.w.w.) naye pia akamsalimia. Kisha Mtume (s.a.w.w.) aliweka mkono wake kichwani mwa Bibi Zahra (as) na akasema: “Jioni ya leo ni mgeni wenu.” Bibi Zahra (as) alichukua kile chombo akakiweka mbele yake Mtume (s.a.w.w.). Wakati Ali (as) alipokiona kile chombo na kusikia harufu yake nzuri, aliendelea kumtazama bibi Zahra (as). Bibi Zahra (as) akamuuliza “Kwa nini umeniangalia hivyo? Je, nimefanya kosa lolote?” Ali (as) akasema: “Hapana, lakini leo hii ulisema kwamba siku mbili zilizopita hatukuwa na chakula cha kula hapa nyumbani, sasa hiki kimetoka wapi?” Bibi Zahra (as) akasema: Allah (s) anajua kwamba nilichokuwambia kilikuwa sahihi.” Ali akasema: “Basi hiki kimetoka wapi?” kisha Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) akaweka mikono yake kwenye mabega ya Ali (as) na akasema: “Ndugu yangu Ali, hii ni zawadi ya ile dinari ambayo kwamba ulifanya Kutoa katika njia ya Allah(s).” (Fatema Zahra (s.a), Bahjatul Qalbul Mustafa Min Mahedaha Ela Lahedeha) 99
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 100
Maadili Ya Ashura
“Hakika Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila ya hisabu” 3. Imesimuliwa kutoka kwa Kabul Ahrar kwamba siku moja Bibi Zahra (s.a) alikuwa anaumwa na wakati Ali (a.s) alipokuja nyumbani alimuuliza kama alikuwa anahitaji kitu chochote. Bibi Zahra akasema: “Tafadhali kama inawezekana nipatie komamanga.” Ali (as) kwa muda alishikwa na wasiwasi kwa sababu alikuwa hana pesa, lakini alisimama na kwenda sokoni. Alichukua dinar moja kama mkopo kutoka kwa mtu mmoja kisha akanunua komamanga. Wakati anarudi nyumbani akamuona mtu mmoja mgonjwa amekaa pembeni mwa njia, akamuuliza: “Moyo wako unatamani nini?” yule mtu mgonjwa akajibu: “Ewe Ali! Mimi naumwa siku ya tano leo, hakuna hata mtu mmoja aliyejali kuhusiana na mimi, nami naumwa ninajiona kama nakula komamanga.” Imamu Ali (a.s) alishikwa na wasiwasi kwamba amenunua komamanga moja tu, kama atalitoa na kumpa huyu mgonjwa basi kitu gani atampelekea Fatima (as), atakuwa amelikosa hili tunda. Lakini kama nisipompa tunda hili itakuwa ni kinyume na kauli ya Allah (s):
“Na ama mwenye kukuomba usimrudishe mikono mitupu!” (Surah ad-Dhuha, ayah 10) Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) vilevile amesema kwamba kamwe usikatae ombi la muombaji hata kama umepanda farasi. Ali (as) alimenya komamanga lile na kisha akampa yule omba omba. Muombaji yule pale pale akapona na kupata afya njema na Bibi Zahra (as) naye vilevile wakati uleule akapona. Wakati Ali (as) aliporudi nyumbani alikuwa anasikia aibu kumkabili Fatima (as). Wakati Bibi Zahra alipomuona, alisimama na kusema: “Kwanini unasikitika hivyo? Naapa kwa utukufu na uwezo wa Allah (s) kwamba punde tu ulipotoa komamanga lile na kumlisha yule omba omba, wakati uleule hamu yangu ya kula komamanga ilitoweka.” Ali (as) alifurahi sana na wakati uleule mtu alibisha hodi mlangoni. Ali (as) aliuliza: “Ni nani wewe?” Jibu lilikuwa: “Mimi ni Salman, tafadhali fungua mlango.” Wakati Ali (as) alipofungua mlango, alimuona Salman (as) akiwa na sinia mikononi mwake ambalo lilikuwa limefunikwa na nguo. Imamu Ali (as): “Ewe Salman! Umepata wapi hili?” Salman (as) akajibu: “Hili limekuja kutoka kwa Allah (s) kwa ajili ya Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) na Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) amekutumia wewe.” Wakati Imamu Ali (as) alipofunua sinia lile aliona katika sinia lile mlikuwa na makomamanga tisa. Ali (as) akamuambia Salman (ra): “Ewe Salman, kama (sinia) 100
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 101
Maadili Ya Ashura hili linatoka kwa Allah (s) kwa ajili yangu basi yangelikuwa kumi, kwa sababu Allah (s) amesema:
“Mwenye kufanya wema atalipwa mfano wake mara kumi…” (Surah Annam, Ayah 160) Salman (a.s) akacheka na akatoa komamanga moja mfukoni mwake na akasema: “Naapa kwa jina la Allah (s) yalikuwa kumi, lakini nilikuwa nakujaribu tu.” 4. Marehemu Tabari alisimulia hili kwa kulihusisha na Sahi kwamba alisema: “Mtu mmoja (mgeni) alikuja kwa Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) na akasema nina njaa. Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) alimuambia aende nyumbani kwa wake zake. Alipofika nyumbani kwa wake za Mtume (s.a.w.w.) walimrudisha, wakimuambia hawana kitu chochote cha kumpa isipokuwa maji tu. “Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) akasema: ‘Nani kati yenu atakayemchukua mgeni huyu jioni hii na kumpa chakula?’ Imamu Ali (as) akasema: ‘Mimi hapa, nitamchukua nyumbani kwangu.’ Ali (as) akamchukua mgeni yule mpaka nyumbani kwake, na akamuuliza Fatima (as): ‘Je, kuna chochote cha kula?’ “Bibi Fatima (as) akasema: ‘Kuna kiasi cha kutosha tu kwa ajili ya watoto, lakini tutakitoa hiki kwa mgeni wetu.’ Kwa hili Imamu Ali (as) alisema: ‘Walaze watoto, nitazima taa na kukaa pamoja na mgeni ili afikiri kwamba na mimi pia ninakula pamoja naye.’ Hivyo, Bibi Zahra (as) aliwalaza watoto kitandani na Ali (as) akaweka chakula mbele ya mgeni, kisha akazima taa na akawa anatikisatikisa mikono yake. Kwa njia hii mgeni yule alipata mlo kamili. Ilipoingia asubuhi, Ali (as) na Fatima (as) wote walikuja kwa Mjumbe wa Allah (s). Yeye (s.a.w.w.) alitabasamu na akasoma aya hii tukufu, ambayo ilishuka kwa ajili ya kuwasifia Ali (as) na Fatima (as)”:
101
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 102
Maadili Ya Ashura “…Na wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji. Na mwenye kuepushwa na uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufaulu.” (Surah Hashr, Ayah 9)
8. Mjadala kuhusu wasio maasumin Ni muhimu kabisa kujadili kuhusu watu wasio maasumin hapa kwa sababu wakati wowote tunapozungumza kuhusu tabia za Maasumin tunasikia minong’ono katika akili zetu kwamba wao walikuwa maasumin na sisi sio maasamin. Vipi tutajilinganisha na watu hawa, hadhi yao ni ya hali ya juu sana na yetu ni ya chini sana. Mpaka hapa ni kweli kwamba kuna tofauti kati ya hadhi yao na yetu na sio sahihi kabisa hata kuwa na shaka kwamba tunaweza kuwa maasumin. Wakati tunapozungumza kuhusu tabia za maasumin haina maana kwamba lazima tufanye vitu hivyo hivyo wanavyofanya ili kwamba nasi pia tuweze kuwa maasumin. Lakini kinachokusudiwa hapa ni kile ambacho Maasumin hawa watukufu wanachotaka kutoka kwetu, lazima tufuate kwa uaminifu. Maasumin (as) wanataka sisi tuwe wapenzi wao. Ili kujifunza hili, tutajadili tabia za wasio maasumin kama mifano. Bibi Khadija (as) ana uhusiano wa karibu sana na Umaasumin na hadhi yake sio ndogo kuliko ya maasum, lakini bado hayuko katika orodha ya maasumin kumi na nne. Cheo na hadhi waliyopewa maasumin kumi na nne haitumiki kwa Bibi Khadija (as). Ingawa jina lake hutajwa pamoja na wanawake wakubwa na watakatifu wa ulimwengu, kwa vile ni mama wa binti yule ambaye hutawala cheo kikubwa mno cha umaasum, hivyo hadhi ya mama juu ya msingi wa umaasum iko karibu na binti yake, lakini bado binti ni Maasum ambapo mama sio maasum. Bibi Khadija (as) sio maasum akilinganishwa na maasumin kumi na wanne, lakini kama asiye maasumin anaweza kupata hadhi kama hiyo basi hutupa matumaini kwamba njia hii inawezekana na kuamuliwa kwa kila mtu kwa kutegemea juu ya uwezo wa kila mtu mwenyewe. A. Bibi Khadija (s.a) - Bibi tajiri wa Makka Tumekuwa tukilisikia hili tangu utoto wetu kwamba Bibi Khadija (as) alikuwa ni Bibi tajiri wa Makka na taarifa kuhusu utajiri wake kwa kawaida ni maarufu kwetu. Ilikuwa ni utajiri huu huu ambao umekuwa njia ya uhusiano kati yake na Mtukufu Mtume wetu (s.a.w.w.). Yeye (s.a.w.w.) alichukuwa bidhaa za Bibi Khadija (as) kuzipeleka Damascus kuziuza na alikuwa maarufu kwa uaminifu wake; Yeye (s.a.w.w.) alihakikisha kwamba bidhaa hizo zinafika ziendako kwa dhamana kamili. 102
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 103
Maadili Ya Ashura Wakati Bibi Khadija (as) alipojua juu ya uaminifu wake (s.a.w.w.) alipendekeza posa kwa Mtume (s.a.w.w.). Mtume (s.a.w.w.) alikubali posa hiyo na wakaoana. Sasa mwanamke wa Makka mwenye rasilimali kubwa mno alikuwa kwenye uwanja wa ndoa wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Tumekuwa tukilisikia hili tangu zamani, lakini inasikitisha kwamba kamwe hatujakuwa na muda wa kutafakari juu ya kile tulichosikia. Tumetegemea tu juu ya kusikiliza, ingawa ni muhimu kutafakari juu ya kile tulichosikia ili kwamba tujue ukweli ni upi. Je, watu wengine ambao hawana mapenzi na utambuzi kwa watu hawa kama tulivyo sisi watakuwa na lipi la kusema kuhusu kile ambacho tumekisika? Watu wazembe na maadui wa Uislamu wanasema kwamba Uislamu hauna mantiki, mvuto na heshima ndani yake kwa sababu ambayo Uislamu ungeweza kuenea, badala yake Uislamu umeenea kwa sababu ya mambo mawili. Kwanza ilikuwa ni kwa sababu ya utajiri na rasilimali ya Bibi Khadija (as) na pili kwa sababu ya upanga wa Imamu Ali (as). Wanasema kwamba hizi zilikuwa njia mbili zilizotumika kueneza Uislamu, ikiwa na maana kwamba kwanza umeenea kwa fimbo na pili kwa pesa. Hii pia humaanisha kwamba Uislamu ni dini ya kutishia na uroho, na watu masikini kwa kurubuniwa na utajiri, kwa mara moja wakawa Waislamu. Hii ni sawa sawa na uingizaji wa watu kwenye Ukristo unaofanywa leo na wahubiri wa Kikristo katika Afrika. Wanaeneza Ukristo kwa watu masikini na walioathiriwa na ukame katika Afrika. Kwa kweli hili hufanyika pia katika nchi yetu, Baluchistan. Kuna takriban familia ishirini na tano katika Baluchistana ambazo zimeuacha Ushia na kuwa Wakristo. Wahubiri wa Kikirsto waliwaendea na wakasema: “Ninyi ni masikini, hamna nyumba, hamna kazi, lakini sisi tuko tayari kuwapeni kila kitu kwa sharti moja tu, kwamba mbadilike muwe Wakristo. Hivyo watu wale waliokuwa dhaifu wa imani wakafikiri kwamba dini hii waliyoifuata haikutupa sisi chochote mbali na umasikini na njaa, wakati ambapo Ukristo ambao unatupa sisi utajiri na mali ni bora zaidi. Maadui wamesema kitu kama hicho hicho kwa Uislamu kwamba katika Makka walikuwepo watu ambao walikuwa hawana kitu cha kula. Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) (Mungu aepushie mbali) alikuwa akiwarubuni kwa utajiri wa Khadija (as). Yeye (s.a.w.w.) alikuwa akisema kwamba niko tayari kuwapa chakula, nguo na hifadhi ilimradi tu muwe Waislamu. Masikini, watumwa na ombaomba wakaukubali Uislamu mara moja na wakati watu hawa walipofika Madina walichukua panga na kuwapiga matajiri wa Madina wakiwalazimisha kuingia kati103
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 104
Maadili Ya Ashura ka Uislamu. Kwa hiyo dini hii amma ni ya vitisho au ulafi. Wale tu ambao walitishiwa au walafi watakubali dini hii. Lakini wale ambao hawarubuniwi na ulafi wowote au wale ambao hawakubali kutishiwa kamwe hawatabadilika kuwa Waislamu. Hili ndilo ambalo maadui watasema, lakini wakati mwingine pia huwa tunawapa uthibitisho kwamba hili ni sahihi kwa kusema kwamba Uislamu umeenea kwa utajiri wa Bibi Khadija (as) na upanga wa Ali (as). (Majmua e Aasaar, Seerah e Nabawi, Jz. 16, uk.181, Martyr Muttahheri (r.a))
1. Uislamu umeenea kwa maadili yake mazuri Kama tukiifikiria habari hii kwamba Bibi Khadija (as), ambaye hapana shaka alikuwa tajiri mkubwa, na utajiri wake wote na rasilimali yake yote ilitumika kwa ajili ya Allah na kwa faida ya Uislamu tu. Lazima pia tutafakari juu ya ukweli kwamba Bibi Khadija (as) alikuwa tajiri wa Makka na sio yule wa Karachi. Kuna tofauti kubwa kati ya Bibi tajiri wa Makka wa wakati ule na bibi wa Karachi leo. Mawazo yetu mtu fulani kuwa tajiri leo ni tofauti sana na ufafanuzi wa mtu kuwa tajiri katika siku hizo. Kwa mtazamo wa kijamii, Makka ulikuwa ni mji mdogo na ulikuwa ni sawa na kijiji cha wakati wetu huu. Yalikuwepo makundi fulani miongoni mwa washirikina, mojawapo lilikuwa lile la wafanyabiashara, hivyo kulikuwa na idadi ndogo ya wafanyabiashara na hao walikuwa watu ambao walikuwa hawafanyi kazi kwa mtu yeyote kama vibarua. Watu hawa ambao walikuwa hawakuajiriwa na mtu yeyote na walikuwa na biashara zao binafsi walichukuliwa kama matajiri. Hivyo, Bibi Khadija (as) vilevile alikuwa bibi tajiri wa Makka kwa misingi hiyo hiyo, lakini dhana ya kuwa tajiri na utajiri ambayo tunayo leo kwa lugha ya mamilioni na mabilioni sio kweli kwa zama hizo. Kwa hiyo sio katika hali tunayofikiria na kuwaza, kwamba alikuwa milionea na kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amemuoa kwa ajili ya utajiri wake. Falsafa ya ndoa hii ilikuwa juu ya misingi ya maadili waliyokuwa nayo watu hawa wawili. Bibi Khadija (as) alishuhudia uaminifu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Yeye (s.a.w.w.) alishuhudia usafi na adabu yake, na hivyo ilikuwa ni ndoa kati ya uaminifu na usafi na sio ndoa kati ya uroho na utajiri.
2. Kutoa katika njia ya Allah kwa Bibi Khadija (s.a) Hapana shaka kwamba Bibi Khadija (as) alikuwa Bibi tajiri, lakini hakuwa bepari kama mawazo ambayo tunayo leo. Hii ni kwa sababu bepari hatajwi kama mtu tu ambaye ana utajiri, bali vilevile huashiria mtu ambaye anaweza kiuchumi kuiharibu jamii, mtu ambaye anakusanya utajiri na anafikiria tu kuhusu faida yake na hutumia njia zozote ziwezekazo kunyonya damu ya wengine. 104
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 105
Maadili Ya Ashura Kama Mwislamu akimtembelea Bibi Khadija (as) katika hali ya njaa, alikuwa akipata mlo mmoja, lakini nukta ya kutafakari hapa ni kwamba utajiri huu wa Bibi Khadija (as) haukudumu kwa muda mrefu. Wakati kila mtu aliyehusiana na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walipofukuzwa (na kuwa wakimbizi katika nchi yao) wakaishi uhamishoni katika bonde la “Shiibe Abu Talib”, Bibi Khadija (as) vilevile naye alipata shida ya njaa pamoja na hao watu wengine. “Shiibe Abu Talib”, ilikuwa bonde dogo kavu ndani ya Makka, lilikuwa na miti kidogo na vichaka ndani yake. Wakati watu hawa walipofanywa mateka hapo, walikuwa wakitumia kuchimba ardhi na kuishi kwa kula mizizi ya miti na kwa muda wote waliokaa hapo walikuwa wakiishi kwa kunyonya magome ya miti. Bibi huyu hakuwa na utajiri kiasi hicho cha kuweza kulimbikiza, bali alikuwa na kiasi tu cha kutosha kulisha matumbo ya watu masikini na yote hiyo ilitumika katika njia ya Allah (s). Utajiri ule haukuwa kiasi cha kutosha kukidhi haja katika “Shiibe Abu Talib”. Baada ya kuoana na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), hali ya nyumbani kwake ilikuwa sawa kama ile ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Infaq ilikuwa inafanywa kwa utajiri wote katika njia ya Uislamu. Kwa hiyo sio sahihi kusema kwamba Uislamu umeenea juu ya msingi wa utajiri na upanga, ingawa upanga umetetea na kuulinda Uislamu, dini hii ya Uislamu imeenea juu ya msingi wake wa maadili mema, kwa ilmu na mantiki sahihi uliyonayo. Bila ya shaka yoyote utajiri wote wa Bibi Khadija (as) ulitumika katika njia ya Allah (s), hiyo pia kwa kiasi kwamba na yeye mwenyewe alikuwa akiteseka kwa njaa katika Shiibe Abu Talib. Uhusiano kati ya Bibi Khadija (as) na Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) haukuwa juu ya msingi wa kupokea; ulianzishwa juu ya msingi wa kutoa. Hakuukubali Uislamu kwa ajili ya kuongezeka kwa utajiri wake au kupata cheo fulani. Hakuolewa na Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) na haiba yake kama msingi wa kujipatia manufaa binafsi kwa ajili yake na sio kwa ajili ya kujipatia heshima zaidi na cheo kwa kumtumia Mtume (s.a.w.w.) kuongeza mtaji wake. Alikubali Uislamu ili kutumia kitu katika njia ya Allah (s), hivyo kwa kukubali kufanya fungamano la ndoa pamoja na Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) alitoa muhanga utajiri wake wote juu ya Mtume (s.a.w.w.). Alitoa somo kwetu la kutumia katika njia ya Allah na Mjumbe Wake (s.a.w.w.).
B. Kutoa katika njia ya Allah kwa “Answar” (wasaidizi) Wakati wahamiaji (Muhajirun) kutoka Makka walipowasili Madina walikuwa mikono mitupu, hivyo Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) aliwaelekeza Answar (wasaidizi; wenyeji wa Madina) kwamba ni wajibu juu yao kutoa vyombo vyao 105
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 106
Maadili Ya Ashura vya nyumbani kuwapa wahamiaji (Muhajirun), ilikuwa watoe nusu ya rasilimali zao kwa wahamiaji (Muhajirun) na waiweke nusu nyingine kwa ajili ya matumizi yao. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakusema kwamba: “Enyi Answar! Kama mkikubali dini ya Allah (s) atawaongezeeni rasilimali yenu na utajiri, atakufanyeni ninyi kuwa watawala wa dola kubwa au atawapa udhibiti wa ulimwengu,” lakini alichosema Yeye (s.a.w.w.) ilikuwa kwamba; “kama mkikubali Uislamu basi kidogo chochote mnachomiliki vilevile kitatumika katika njia ya Allah (s). Hivyo Answar ambao punde tu wamekuwa Waislamu, nao pia walitoa vyombo vyao kuwapa wahamiaji (muhajirun). Hizi zilikuwa ni tabia za wasio maasumin, na hawa walikuwa ni wasio maasumin ambao uhusiano wao na Uislamu ulianzishwa juu ya msingi wa Kutoa katika njia ya Allah kuanzia siku ya kwanza yenyewe. Hawakukubali Uislamu kwa nia ya kuchukua kitu, ingawa walikuwepo baadhi ambao walikuwa na nia hii katika akili zao kwamba siku Uislamu ukienea, ukipata utawala na madaraka, tutaongeza mtaji na utajiri wetu kwa kupitia Uislamu. Walikuwepo baadhi ya watu ambao waliingia Uislamu katika hali ya umasikini, lakini wakati wa kufa kwao waliacha utajiri kwa kiasi kwamba wafanyakazi ilibidi wavunje matofali, na milundiko ya dhahabu ilipatikana katika nyumba zao. 6 Wakati Ali (as) alipochukua udhibiti wa utawala kulikuwa na nyumba kama hizo mjini Madina ambazo z-alitaka kutoa. Wale ambao walitaka na wamechukua kutoka kwenye Uislamu (utajiri wa kilimwengu) wamelaaniwa na Allah (s) milele, wakati ambapo wale ambao wametoa wamekuwa watukufu na watu waheshimiwa wa Allah (s) na Allah (s) akawafanya mtindo wa kuigwa na wengine. 6 Dkt. Ibrahim Ayati katika kitabu “A Probe into the History of Ashura” anasimulia kutoka kwa Masudi kwamba huyu Masudi katika kitabu chake “Muraweejuzhib” ameandika kwamba Zubair bin Awam mbali na kuwa na kasir mjini Basra vilevile ana nyumba nyingi zilizojengwa Basra, Kufa,Alexandria na Misri. Wakati Zubair alipofariki aliacha dinari 50,000 farasi elfu moja, vijakazi na watumwa elfu moja na malundo ya chakula katika miji tofauti. Vilevile aliandika kuhusu Talha ibn Abdullah kwamba pato lake la mwezi kutoka katika mali yake tu iliyoko Iraq peke yake ilikuwa dinari 1000. kwa mujibu wa hadithi nyingine, pato lake kutoka Damascus lilikuwa zaidi ya hili. Imeandikwa kuhusu Abdur Rahman bin Auf Zahri kwamba alikuwa na ngamia 1000 na kondoo 1000 katika zizi lake. Wakati alipofariki rasilimali yake iligawanywa miongoni mwa wake zake wanne na mtoto wake mmoja wa kiume. Kila mmoja katika wake zake alipata dinari 84,000 za dhahabu. Wakati Zaib bin Ibn Saabit alipofariki kiasi alichoacha cha dhahabu na fedha ilibidi zivunjwe kwa shoka kwa ajili kugawanywa, na mbali ya dhahabu na fedha, mali nyingine na akiba ya nafaka ilikuwa sawa na sarafu 100,000 za dhahabu. Dr Ibrahim Ayati, “A Probe into History of Ashura”
106
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 107
Maadili Ya Ashura
9. Upana wa mipaka ya Kutoa katika njia ya Allah Allah ameweka mipaka ya Kutoa katika njia ya Allah kwa ajili ya wanadamu. Infaq haina maana tu ya kutumia utajiri, dirham au dinar, kwa kweli Allah (s) amesema: “…na hutoa katika yale tuliyowapa.” (Surah Baqrah, Ayah 3) Chochote ambacho Allah ametupa sisi huchukuliwa kama riziki na Allah (s) amewaamuru wanadamu kufanya Infaq kutokana na riziki ambayo amewapa. Sasa tayarisha orodha ya kile ambacho Allah (s) amewapa wanadamu. Je, Allah (s) amewapa utajiri tu? Amewapa pesa tu na utajiri? Allah ametupa sisi uhai, ambao ni zaidi ya pesa na utajiri Allah (s) ametupatia sisi maisha, ametupa pumzi, ametupa afya na usalama. Allah (s) ametupatia sisi heshima na hadhi, ametupatia sisi haiba na cheo, Allah ametupatia sisi watoto. Na kwa muhutasari wa yote haya ni kwamba Allah (s) ametupatia neema zisizo na kikomo ambazo hazihesabiki.
“… Na mkihisabu neema za Mwenyezi Mwenyezi Mungu hamuwezi kuzidhibiti…” (Surah Ibrahim, Ayah 34) Chochote ambacho Allah ametupa kinahesabika kama ni riziki kutoka Kwake.
A. Aina za Riziki Riziki ya kimaada: Neema zote za kiulimwengu ni riziki za kimaada. Riziki ya Kiroho: Sifa zote nzuri, ubora na ukamilifu kama ilmu nk. ni riziki ya kiroho. Riziki zote hizi zinatoka kwa Allah na ametuamuru kufanya Infaq kutokana na riziki alizotupa. Sasa kama mtu akiweka akiba riziki ya Allah , atakuwa mwenye kulimbikiza. Ingawa Allah amesema:
“…Na wale walimbikizao dhahabu na fedha na hawazitumii katika njia ya Mwenyezi Mwenyezi Mungu, basi wabashirie adhabu iumizayo.” (Surah Tauba, Ayah 34) 107
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 108
Maadili Ya Ashura Hii ndio Aya ambayo Abu Dharr (ra) akiitumia kama kaulimbiu dhidi ya mabepari wa zama zake. Wakati alipokuwa anatembea mitaani au barabarani au misikitini, wakati anapomuona mmoja wa wale walimbikizaji huwa anasoma Aya hii. Alikuwa anataka kuelezea kwamba kuna adhabu iumizayo inayo wangojea. Lakini ulimbikizaji sio mahususi kwa dhahabu tu na fedha, yeyote yule ambaye hatoi kile ambacho Allah amempa na akavilimbikiza basi kuna adhabu iumizayo inayomngojea. Allah ametoa ilmu, heshima na watoto, na mtu ambaye hafanyi Infaq kutokana na hivi lazima ajitayarishe kwa adhabu kali. Kaulimbiu ya Abu Dharr (ra) ilikuwa dhidi ya aina zote za ulimbikizaji. Kuna uhusiano wa kina kati ya sifa za kuhifadhi (ghalani) na ile ya kuchukua kila siku, mtu ambaye ana tabia hiyo ya kila siku kuchukua, atakuwa mlimbikizaji, lakini mtu ambaye ameifanya kuwa kawaida ya kutoa kamwe hatalimbikiza chochote. Katika hali za kulimbikiza vilevile imesemwa kwamba wanadamu wanaweza kuanza kuhifadhi na kulimbikiza muda na umri halikadhalika, ingawa umri, wakati na kila muda wetu ni upendeleo wa Allah. Ubahili ulioje ni kwamba mwanadamu ambaye hayuko tayari kufanya Infaq ya wakati aliopewa na Allah, hiyo pia hakuna mtu aliyempa thamani ya wakati wake. Wakati tukiambiwa tutoe muda fulani katika jina la Allah (s), wanasema hatuna muda. Ni nani awezaye kuwa bahili mkubwa kama yule ambaye hayuko tayari kutumia dakika mbili katika njia ya Allah? Ubahili ulioje wa mtu ambaye huanza kulimbikiza kile ambacho amepewa bure na Allah (s). Ingawa umri ni kitu ambacho hata hakiwezi kulimbikizwa, hakuna awezaye kuhifadhi umri katika magunia, unatumika katika njia yake yenyewe. Umri utakuwa ni visaga (wadudu wanaokula nafaka zilizohifadhiwa katika magunia), ambao huharibu umri uliohifadhiwa katika magunia. Tundu katika gunia la umri litamimina umri wote na kisha katika umri mgumu wa miaka thamanini na tisini, tutaona kwamba takriban umri wetu umefikia mwisho. Basi hata kama tukiomba ziada ya muda kidogo malaika wa mauti hatakuwa tayari kutoa hata dakika mbili. Hii ni kwa sababu hata malaika hatakuwa na muda; katika muda wako wote wa maisha umekuwa ukihifadhi umri wako na ulizoea kusema kwamba huna muda, basi, imekwenda wapi ile hifadhi ya umri? Kisha utakuwa hisia na tamaa na hatia kwamba natamani ningetumia maisha haya katika njia ya Allah (s). Natamani ningetumia mtaji huu huru katika njia ya Allah (s). Walimbikizaji wa muda watakumbana na adhabu hiyohiyo kama ile ya walimbikizaji wa mali.
108
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 109
Maadili Ya Ashura
10. Imamu Husein (a.s) – Ufafanuzi wa kimatendo wa Kutoa katika njia ya Allah Imamu Husein (as) aliona kwamba watu wameicha njia iliyoonyeshwa kwao na Mtukufu Babu yake (s.a.w.w.) na wazazi wake, watu wameanza kujipatia tu na kuchukua kutoka kwenye dini na maadili haya ya kimungu, kiutu na ya ki-Qur’ani ya Infaq yalikuwa yanauawa na watu sawa tu kama maadili mengine. Watu wameondoa nafsi katika maadili haya ya Kutoa katika njia ya Allah na yamebadilishwa na uovu (Munkar). Haichukui muda mrefu kwa maadili kubadilika, kwa muda wa miaka hamsini na moja tangu kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), maadili yote yamebadilika. Uhusiano wa watu umebadilika kutoka kwenye kutoa na kuwa wa pato, na uhusiano huu wa kila siku kupata na kuchukua kutoka kwenye dini ulikuwa ukihesabiwa kama maadili. Kiongozi wa Mashahidi aliwasilisha ufafanuzi wa kimatendo wa Infaq katika Karbala. Imamu Husein (as) aliwasilisha ufafanuzi wa kimatendo wa aya hii ya Kutoa katika njia ya Allah katika hali ambayo alitumia aina zote za riziki alizokuwa nazo katika hadhara ya Allah (s), na alitoa riziki hizo katika hali ambayo hakubakiwa na kitu. Imamu Husein (as) aliwasilisha ujuzi wake katika njia ya Allah, alifanya kitendo cha Kutoa katika njia ya Allah kutokana na mwongozo wake, aliendelea kutoa khutba ili kuwafanya watu wale maaluni waelewe na kuwaleta kwenye njia iliyonyooka, kisha baada ya hili aliwasilisha mali yote aliyokuwa nayo katika njia ya Allah (s), mke wake, hadhi yake, watoto wake, masahaba zake, kila kitu kilitolewa muhanga kwa ajili ya Kutoa katika njia ya Allah (as). Ni lini utapata watu wakarimu kama hawa? Watu wanatoa mfano wa Hatim Tai kama mtu mkarimu sana, ingawa Hatim Tai mkarimu alikuwa na uwezo tu wa kulisha watu masikini kutoka kwenye utajiri wake. Lakini, ni Karbala iliyoonesha na kutuambia kuhusu watu wakarimu mno katika ulimwengu huu. Jina la mtu mkarimu mno katika ulimwengu huu ni Husein (as). Chochote alichokuwa nacho, alikiwasilisha kwa Allah kimoja baada ya kingine. Mtu huyu mashuhuri wa Infaq alipita katika hali fulani wakati alipokuwa ametumia riziki yote aliyokuwa nayo katika njia ya Allah, alirudi kambini na kwenye mahema yake kuona kama kuna riziki yoyote iliyobaki. Alikwenda kwenye mahema ya masahaba zake na akaona kwamba riziki ya masahaba zake yote ilikuwa imekwisha; kila kitu kilikuwa kimetumika katika njia ya Allah. Aliona kwamba hema la Abbas (as) lilikuwa tupu kwa vile riziki hii ya Ali (as) vilevile ilikuwa imetumika katika njia ya Allah. Aliingia ndani ya hema la Ali Akbar (as) na akaona kwamba riziki hii pia imetumika katika njia ya Allah. Wakati alipokuwa ameachwa peke yake kabisa, 109
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 110
Maadili Ya Ashura alirudi kwenye uwanja wa mapambano na kuanza kuwaita masahaba zake kwa sauti ya juu. Aliangalia kushoto na kulia, lakini hakuona sahaba yeyote; wote walikuwa wamepumzika kwenye ardhi ile inayochoma ya Karbala. Yeye (as) akawaita kwa sauti ya juu na akasema:
“ Ewe Muslim bin Aqil, Ewe Hani bin Urwah, Ewe Habib bin Mazahir, Ewe Zuhair bin Qain... Enyi watu waaminifu! Enyi watu wenye ari! Enyi watu mliojitayarisha kwenda kwa ajili ya mapambano! Ni nini kilichowatokea? Nawapigieni ukelele wa kuwaita, lakini hamjibu, je, mmekwenda kulala? Ninayo matumaini kwamba mtaamka, au ahadi yenu ya utii na Imamu wenu imekwisha na ndio maana hamnisaidii? Hawa ni mabinti wa Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.), Enyi mabwana wa upole! Nyanyukeni kutoka kwenye usingizi wenu mzito ili muwahifadhi Harem (wanawake) wa Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) kutokana na wachupa mipaka hawa waliolaaniwa.“ (Mawassae Kalemate Imam Hussain – uk. 484) Nyoyo zangu shujaa, simba zangu! Mko wapi? Askari wangu mashujaa! Mko wapi? Kwa nini hamuamki kutoka kwenye usingizi wenu mtamu, amkeni? Watupeni maaluni hawa mbali na Harem (wanawake) wa Mjumbe wa Allah (s), amkeni! Wakingeni Ahlul-Bayt (as). Wakati hakuna jibu linalokuja, yeye (as) alishawishika kwamba sasa hakuna punje hata moja ya riziki iliyobakia. Ghafla Husein ibn Ali (as) alikuja na kumuuliza Bibi Rubab (as) ampe riziki hii ya Allah (s), kwa vile alikuwa anataka kuiwakilisha kwa Allah. (s). Hivyo alimuwasilisha kijana huyu vilevile mwenye umri wa miezi sita Ali Asghar (as) katika njia ya Allah (s).
110
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 111
Maadili Ya Ashura
Maadili ya 5 Ukombozi (Uhuru) 1. Imamu Husein (a.s) – Kiongozi wa watu huru................................................112 2. Aina za utumwa................................................................................................113 3. Mtu huru kwa mtazamo wa Ali (a.s)................................................................114 4. Imam Khomeini (r.a) – Mfano bora wa mtu huru...........................................115 5. Ulimwengu kwa mtazamo wa Ali (a.s)...........................................................116 6.Ali (a.s) – Mtu aliyeufedhehi ulimwengu huu..................................................117 7. Utendaji wa ulimwengu kwa mateka wake......................................................118 8. Utendaji wa Shetani kwa mateka wake...........................................................119 9. Ni lini tutasherehekea uhuru?..........................................................................120 10. Waliochukua masomo ya uhuru kutoka kwa Imamu Husein (a.s)................120 11. Imamu Husein (a.s) – Kigezo cha Ukombozi (Uhuru)..................................121 12. Mateka wa Damascus na Uhuruu..................................................................123 13. Hurr (a.s) na Ukombozi (Uhuru)...................................................................125
111
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 112
Maadili Ya Ashura
1. Imamu Husein (a.s) – Kiongozi wa wanadamu Huru Katika mapambano ya Haki na Batili, moja ya maadili muhimu ya mwanadamu ambayo kwayo Imamu Husein (as) alipata ushindi, ilikuwa ni “Ukombozi na Uhuru.” Ama kwa Ukombozi, sifa hasi iliyo mbaya zaidi ni Utumwa. Yeye (as) alifanya juhudi dhidi ya utumwa na akaushinda kwa ushujaa, na hivyo kwa kunyanyua bendera ya uhuru na uwekaji huru watumwa, na kuiwasilisha kwenye ubinadamu. Mapambano ya maadili ni ya kipekee katika muundo wake, silaha zake pia ni za kipekee na mtindo wa vita vilevile ni wa kipekee. Mtindo ambao kwamba Imamu Husein (as) alishinda vita hivi vya Ukombozi na kushinda maadili haya ya Ukombozi ni wa kipekee sana. Pamoja na moyo uliovutwa na umateka na damu iliyojaa uhanga, alipulizia roho katika maadili haya makubwa. Yeye (as) mwenyewe aliuawa shahidi, lakini aliwasilisha Ukombozi na uhuru kwenye Ummah. Alitoa muhanga heshima ya wanawake,watoto wa kiume na wa kike chini ya ufungwa wa mateka, ili Umma upate wokovu kutokana na ufungwa wa dini na imani yao ya uwongo. Wakati mwingine hushinda vita vya ufungwa katika njia ambayo kwamba ili kumfungulia mfungwa mmoja mpiganaji mwenyewe hufungwa kamba za ufungwa, ili kwamba aweze kuleta uhuru kwenye dini, ambayo iko chini ya ufungwa wa kutisha mno. Wakati mwingi shingo za wanadamu ziko huru, lakini akili, mawazo na imani zao ziko chini ya utumwa. Vilevile inawezekana kwamba Umma wote wanaweza kuwa watumwa, na wakati Umma wote unapokuwa watumwa, athari za utumwa huu vilevile zitadhihirika. Kama mtu akiwa mtumwa wa mtu, athari za utumwa huu kwa uwazi zitadhihirika zenyewe katika mtu huyu, kukomea kwake mwenyewe, lakini wakati Umma wote na jamii wakiwa watumwa, athari ya utumwa huu itaonekena katika kiwango cha Umma na kijamii. Imamu Husein (as) alishuhudia kwamba ni wakati ambapo watu binafsi na halikadhalika Ummah mzima na jamii ulikuwa umefungwa na utumwa na hivyo huamua kuifungua minyororo hii ya ufungwa. Kama inavyoonekana kwa wengine Yeye (as) alilazimika kuweka minyororo, pingu na chuma kwenye shingo yake, kujifunga kamba katika mikono yake, lakini hata hivyo anafungua kamba na kuondoa kamba za utumwa daima ambazo zimeizunguka hadhi ya Ummah. Kwa kuuawa shahidi yeye (as) mwenyewe ameihuisha heshima ya Umma iliyokufa, na mpaka Siku ya Hukumu ameonesha njia ya Ukombozi kwa ubinadamu na kuwapa ukombozi kutokana na utumwa. Msisitizo wake wa kupata uhuru na Wokovu ulikuwa wa juu sana. Hivyo, kutokana na miongoni mwa majina yake mengi, vilevile hujulikana kama “Abu Ahrar”, baba wa Ukombozi na hili limekuja katika Ziyarat kama: 112
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 113
Maadili Ya Ashura
“Ewe kiongozi wa watu huru, Ewe baba na mlinzi wa wanadamu huru, salaam na amani iwe juu yako kutoka kwetu.�
2. Aina za utumwa Tabia mbaya mno ni ile ya utumwa na ni wa aina mbali mbali. Kila aina ya utumwa ina athari na kanuni zake, na amma dhidi ya kila aina ya utumwa ni aina uhuru na kila aina ya uhuru ina athari na sera zake yenyewe. Lakini aina yoyote ya utumwa iwayo, huchukuliwa kama mbaya na uovu. Aina fulani za utumwa ziko kwa kiasi kwamba mtu hawezi hata kuhisi iwapo yeye ni mtumwa au mtu huru, anafikiri kwamba nasali sala zangu na hakuna anayenizuia kufanya hivi, kwa hiyo, mimi ni mtu huru. Nasujudu mbele za Mola Wangu, nafanya Hijja yangu, nafanya ibada nyingine, kwa hiyo mimi ni mtu huru, lakini hatambui kwamba sala, Hijja hizi na ibada nyingine ni zile za utumwa, na ibada hizi za utumwa hazitakuwa na faida yoyote kwake bali badala yake zitaongeza ukubwa wa utumwa ndani yake, Allama Iqbal anasema: Mulla nchini India kwa vile ana ruhusa ya kusali Mpumbavu huyu anafikiri Uislamu una uhuru (wa kusali) Aina tofauti za utumwa zina utumwa wa fikra, akili, busara na ulimi. Wakati mwanadamu anapokuwa mtumwa basi kanuni za utumwa na ufungwa hutumika kwake, mtu ambaye amekuwa mtumwa kwake, huanzisha kanuni na sera kwa ajili yake. Lakini mtu huru kamwe hawi chini ya kanuni za yeyote, hadhi na busara zake hubakia huru na kamwe hasalimu amri kwenye sera zinazotawaliwa na mtu mwingine. Utumwa wa ulimi ni wakati mtu hawezi kutoa hata maneno machache ya ukweli. Hata kama shingo yake haikufungwa na minyororo, hawezi kuzungumza ukweli, ingawa Imamu Sajjad (as) alivishwa minyororo ya ufungwa shingoni mwake, kiuhalisia aliondoa minyororo ya utumwa kwenye shingo za ubinadamu, kwa njia hiyo akaupa ubinadamu somo la uhuru wa ulimi. Kiuhalisia minyororo ambayo Imamu Sajjad (as) alivaa ilikuwa minyororo ya uhuru. Mtu ambaye ana minyororo shingoni mwake anaweza kuwa huru, wakati ambapo wale ambao shingo zao ziko huru bado wanaweza kuwa watumwa. Ni mtu wa aina gani huyu ambaye ana minyororo shingoni mwake, pingu mikononi mwake na minyororo miguuni mwake, lakini wakati kitu kinazungumzwa dhidi ya katiba ya Mungu, ulimi wake huanza kutikisika kwa haraka kuliko upanga. Ingawa shingo nyingi zilikuwa hazina miny113
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 114
Maadili Ya Ashura ororo, ndimi zao zilikuwa zimenaswa chini ya utumwa, hivyo, hakuna hata neno moja lililotoka kwao. Wakati mwingine mwanadamu huwa mtumwa wa vitu vingi vidogo na wakati mwingine wa vitu vikubwa, lakini mara anapokuwa mfungwa basi maishani mwake ufungwa na utumwa wake wa vitu huendelea kuvutia. Mara anapokuwa mtumwa wa kitu fulani basi atakuwa mtumwa wa kila kitu. Wakati mwingine mwanadamu anakuwa mfungwa wa matamanio yake na mapenzi, na wakati mwingine huanza kumtii Shetani kwa kuwa mtumwa wake. Lakini aina mbaya zaidi ya utumwa ni utumwa wa ulimwengu. Mara mtu anapokuwa mtumwa wa ulimwengu, basi aina zote za uovu na vitu vichafu huambatanishwa kwake.
Kila kosa huchipuka kutokana na mapenzi ya ulimwengu huu Mtu huru ni mtu ambaye hawi mfungwa na mtumwa wa ulimwengu huu.
3. Mtu mwema na huru katika uoni wa Ali (a.s) Imam Ali (a.s) amtambulisha mtu huru katika Nahjul Balaghah kama:
“Ni nani yule mtu huru anaye hiari kuacha”Lumazat” (chakula kinachobakia katikati ya meno) kwa thamani yake (mtu ambaye anastahili kitu kama hicho)?” (Nahjul Balaghah, Msemo, Na. 456) Mifano ya kushangaza ambayo Amirul Mu’minin (as) ameitoa kwenye ulimwengu huu ni ya hali ambayo kwamba hakuna mtu ambaye anaweza kuwa hata na fikra kidogo au mawazo kuhusu vitu hivi. Miongoni mwa mifano hii, mmojawapo ni “Lumazat” (mabaki ya chakula). Amirul Mu’minin (as) anafananisha ulimwengu huu kama “Lumazat.” “Lumazat” humaanisha vile vyakula vilivyobakia na kunasa katikati ya meno na baadae huondolewa kwa kutumia vijiti vya meno na kutupwa. Wakati tunapokula chakula hususan nyama vipande vidogodogo vya nyama hubakia katikati ya meno, hivi huitwa “Lumazat”. Ali (as) anasema kuhusu watu hawa wenye kutamani ulimwengu kwamba wale ambao wana matamanio na ulimwengu huu kiuhalisia wamebeba vijiti vya kuchokolea meno katika mikono 114
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 115
Maadili Ya Ashura yao na kwa kufunua mdomo wa ulimwengu huu wanaondoa vipande vilivyobakia na kuviweka kwenye vinywa vyao. Ulimwengu huu ni kitu cha fedheha mno na hufanana na mabaki ya chakula yaliyonasa katikati ya meno. Kama mtu akitumia kijiti cha kuchokolea meno ili kuondoa mabaki ya chakula kutoka kwenye mdomo wa mtu mwingine na kuweka kwenye mdomo wake mwenyewe; je hii haitakuwa udhalilishaji na kitendo cha fedheha? Amirul Mu’minin (as) anasema kwamba mtu mwema na huru ni mtu ambaye huacha “Lumazat” kwa thamani yake iliyonayo na halizingatii hilo kabisa. Je, mtu yuko tayari kufunua mdomo wake na kutumia kijiti cha meno kuchokonoa katikati ya meno na kuondoa mabaki ya chakula ili ayale yeye mwenyewe? Je, yawezekana hata mtu kulifikiria hili? Lakini katika uoni wa Ali (as) watumwa wa ulimwengu ni wale ambao wanaondoa mabaki ya chakula kwenye meno ya wengine na kuyala wao wenyewe.
4. Imam Khomeini (r.a) – Mfano bora wa mtu huru Leo Umma wote wa Waislamu ambao hujifikiria wenyewe kama safi na wengine (makafiri) kama wachafu; serikali za Waislamu, wote wanakula “Lumazat” za wengine. Israil imefunua mdomo wake na watu hawa wanachukua vijiti vya meno na kuanza kula vipande vya nyama kutoka kwenye meno machafu ya Israil. Marekani imeonesha meno yake na watu wengi wa serikali za Waislamu wakaanza kufaidi mabaki ya chakula kutoka kwenye meno yake. Kama huu sio ufungwa, utumwa na udhalili, basi ni nini? Hii ndio inaitwa Ukombozi na uhuru ambapo mnaondoa mabaki ya chakula kutoka kwenye meno ya hawa wanaojiita taifa kubwa na kisha kujaza tumbo la Umma wenu kwayo? Viongozi wetu (wa Pakistani) na mawaziri wanasema kwamba tuna ufinyu wa bajeti, tuna madeni na kwa hiyo tumefanywa wafungwa katika mikono ya wengine. Tumekuwa wafungwa wa Benki ya Dunia na mashirika mengine ya fedha. Sio kwamba wametununua au tumeuzwa kwao, walikuwa wanafurahia chakula chao wenyewe, lakini basi baadhi ya mabaki ya chakula yalibakia kwenye meno yao. Baadhi ya viongozi wetu mashuhuri ambao walikuwa wenye kuutakia mema Ummah, ambao kwa ajili ya ustawi wa nchi, walikwenda kwao na kuwaomba wafunue midomo yao ili kwamba waweze kuondoa mabaki ya chakula na kuyaweka kwenye matumbo ya watu wao. Kama tukimuuliza Ali (as) kuhusu hali ya Waislamu, je, tuko huru na wema? Je, hali hii yaweza kuchukuliwa kama hali ya Ukombozi na uhuru? Ali (as) atatupa 115
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 116
Maadili Ya Ashura jibu hili hili: “Ni nani mtu yule huru anaye hiari kuacha “Lumazat” (mabaki ya chakula) kwa thamani yaliyonayo?” Imamu Khomein (ra) alisikia tanafasi na maombi ya Ali (as) na kwa maneno ya kimatendo alisema kwamba mimi ni mtu huru, mimi ni yule mtu huru ambaye si tu atazika hii “Lumazat” kwenye meno yenyewe, bali badala yake nitayavunja na meno yenyewe pia, ili mataifa mengine ya Waislamu yaondokane na kula hii “Lumazat.” Ufalme wa Iran ulikuwa na kila kitu cha kula lakini mfalme wake amekuwa na tabia ya kula mabaki haya ya chakula, alizoea kuondoa “Lumazat” kutoka midomo ya wengine na kuiweka kwenye midomo ya Waislamu. Mtoto wa Ali (as) aliingia kwenye uwanja wa mapambano na kwa kuizika “Lumazat” kwenye meno pia aliyavunja meno. Hili lilikuwa somo la uhuru ambalo Imamu Khomein (ra) alilichukua kutoka kwa Imamu Ali (as)
5. Ulimwengu katika uoni wa Ali (a.s) Mfano mbaya zaidi wa utumwa ni utumwa wa ulimwengu, ambao ni sababu kubwa ya msingi kwa aina nyingine za utumwa. Imamu Ali (as) anasema kuhusu ulimwengu huu kwamba, ulimwengu huu ambao unaupenda kwa moyo wako na kuvutiwa nao kwa hali ya juu, basi ngoja nikuonesheni hali ya ulimwengu huu:
“Kwa jina la Allah! Kwangu mimi ulimwengu huu wenu ni duni kuliko utumbo wa nguruwe mikononi mwa mkoma.” (Simulizi na. 336) Ni picha ya kushangaza ambayo yeye (as) ameichora kwa ajili ya ulimwengu huu. Ukoma ni ugonjwa mbaya, Allah amlinde kila mtu kutokana nao. Lakini kama mtu akiupata ugonjwa huu basi anakuwa hafai hata kumuangalia, anaondolewa kwenye jumuiya na hakuna mtu anayetaka kufanya shughuli yoyote ya huruma kwa mtu huyo. Sasa kama mtu huyu anayeumwa ukoma atasimama na utumbo wa nguruwe mikononi mwake, na upande mwingine kuna mtu ambaye amevaa vizuri nguo nadhifu na safi akijifikiria mwenyewe kuwa ni mtu mkubwa, anaangalia kwa hamu sana hali hii na anasubiri fursa ipatikane wakati huyu mkoma akifunga macho yake na aweze kuunyakuwa utumbo ule kutoka mikononi mwake. Kwa hakika, ulimwengu kama huu hautamvutia mtu mwingine yeyote, bali wafungwa na watumwa. Mtu huru kamwe hatasogea hata karibu ya ulimwengu 116
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 117
Maadili Ya Ashura huu, hivyo tunajua kwamba utumwa wa ulimwengu ni mbaya zaidi kuliko aina zote za utumwa.
6. Ali (a.s) – Mtu ambaye ameufedhehesha ulimwengu huu Picha ambayo Amirul Mu’minin (as) aliichora kwa ajili ya ulimwengu huu na namna alivyoonesha ulimwengu sura yake ya fedheha kubwa katika historia, hakuna mtu ambaye amewahi kufanya kwa njia hiyo. Ni muhimu kutaja hapa simulizi ya mheshimiwa mwalimu wangu, mfasiri wa Qur’ani, mtafiti bingwa, Arif mkamilifu, mtaalamu juu ya Nahjul Balaghah na Qur’ani, mtu mzoefu na mfuasi wa kimatendo wa mwenendo wa Imamu Ali (as), Ayatullah Jawwadi Amouli. Simulizi hii ya Ayatullah Jawwadi Amouli haiko karibu na ukweli bali ni ukweli kamili na kwa hiyo ni muhimu kuitaja hapa. Mwanachuoni huyu mheshimiwa anasema: “Kama ulimwengu huu ungeulizwa, ni nani aliye kutweza zaidi, nani aliyekufanya dhalili zaidi, nani aliyefanya heshima yako kuonja vumbi la ardhi? Ulimwengu bado na utaendelea kujibu kwamba ni Ali (as) ambaye amenifedhehesha zaidi.” Kama ulimwengu utatakiwa kuleta malalamiko yake, kuandika malalamiko yake, basi malalamiko yote ya ulimwengu yatakuwa dhidi ya Ali (as). Hakuna shaka au kutokuwa na uhakika kwamba Ali (as) ameukosoa kwa ukali ulimwengu huu na siku zote ameufanya dhalili. Wakati mwingine akiutaja ulimwengu alisema:
“Ewe ulimwengu muovu! Uwe na tahadhari kwangu, kwa nini umekuja kwangu namna hii? Unataka kunirubuni? Allah aepushie mbali, kwamba nirubuniwe na wewe na kushawishiwa na wewe na starehe zako. Haiwezekani. Nenda kajaribu urubuni wako kwa mtu mwingine. Sitamani kukumiliki na sitaki kukupata. Nimekuacha talaka tatu ambazo kwazo haiwezekani kuungana tena. Maisha ya starehe ambayo unatoa ni ya muda mfupi sana. Hakuna umuhimu wa kweli katika kila unachotoa, hamu ya kukushikilia wewe ni matusi na udhalilishaji. Huzuni ndio hatima ya wale ambao wanataka kukupata. Hawatoi kwa ajili ya Akhera. Watalazimika kupitia safari ndefu katika barabara ngumu kuelekea mashukio ya vituo vingi.” (Nahjul Balaghah, Semi ya 77 uk. 831.) 117
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 118
Maadili Ya Ashura Katika mahali pengine wakati akiandika wosia kwa mwanae Hasani (as), anasema:
“Uwe na tahadhari mwanangu, usije ukabebwa mbali na kurubuniwa na tamaa za watu wa kiulimwengu katika maisha ya uovu na starehe zake, na usivutiwe na kuonekana kwao kufanya juhudi kubwa ili kuupata na kuumiliki ulimwengu huu. Allah kwa huruma kubwa amekuelezea wewe kila kitu kuhusu ulimwengu huu. Sio tu Mola Mwenye Rehema bali hata vilevile ulimwengu umekuelezea kila kitu; umekuonesha kwamba ni wenye kufa; kwa uwazi (ulimwengu) umetangazia udhaifu wake, mapungufu yake na uovu wake. Kumbuka kwamba watu hawa wenye akili ya kiulimwengu ni kama mbwa wanao bweka, wanyama wakali wenye njaa. Baadhi yao wakati wote wanawabwakia wengine. Mabwana wakubwa (wa ulimwengu huu) wanaua na kuwaua kwa ukatili watu masikini na wanyonge.� (Nahjul Balaghah, Barua ya 31.)
7. Ushughulikaji wa ulimwengu kwa mateka wake. Wakati mwingine mwanadamu huwa mtumwa wa mtu fulani ambaye ni duni sana na aliye dhalili. Mtu ambaye kwamba mwanadamu anakuwa mfugwa wake atamfanyia mfungwa wake kulingana na hadhi na nafasi yake. Kama mtu huyo ni mtu mkubwa, mzee mwenye heshima na mtu mkarimu, basi atawafanyia wafungwa wake katika hali ileile na mwenendo mzuri, lakini kama yeye mwenyewe ni mtu duni na wa hali ya chini, basi atawafanyia wafungwa wake katika hali ileile ya chini na duni. Mfano wa hali zote upo katika historia. Mfano mmoja ni wakati binti wa Hatim Tai alipokuwa mfungwa wa jeshi la Uislamu na aliletwa mbele ya Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.), Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuweka bibi yule kwa heshima kubwa. Yeye (s.a.w.w.) alimshughulikia kwa wema, sio kwa sababu bibi huyu alikuwa anahusiana na familia yenye heshima na binti wa mtu mwenye ukarimu kama Hatim Tai, hii ni kwa sababu mtu ambaye amekuwa mfungwa kwake alikuwa mtu mkubwa mwenye kuheshimiwa. Mtu ambaye kwake amekuwa mfungwa alikuwa mwenye huruma zaidi sana; alipata huduma nzuri kwa sababu yeye (s.a.w.w.) alikuwa mpole na mtu mtukufu. Mifano mibaya mno wanayofanyiwa wafungwa inaoneshwa na majeshi ya Marekani juu ya wafungwa wa Kiislamu nchini Iraq. Matendo hayo mabaya yanay118
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 119
Maadili Ya Ashura ofanywa juu ya Waislamu wanaume na Waislamu wanawake katika Gereza la Abu Ghuraib na watu hawa duni na viumbe waliofedheheka ni aibu kubwa na mbaya mno kwa ubinadamu wote. Wafungwa walivuliwa nguo na usafi wa wanawake ulinajisiwa, na ilifikia kiasi kwamba wafungwa wale wasio na hatia waliona ni bora kujiua kuliko kuvumilia mateso haya. Aina ya uovu wanaofanyiwa, jinsi heshima yao ilivyovunjwa ni mno, kiasi kwamba hata kulijadili hili huwafanya wanadamu kuwa na aibu kubwa. Picha za matendo haya ya ukandamizaji na matendo machafu wanayofanyiwa wanawake zipo kwenye vyombo vya habari vya ulimwengu na mitandao ya intaneti, na haivumiliki hata kuziangalia. Picha hizi hufanya nyoyo za Waislamu kutokwa na damu; hayo ndiyo matendo yaliyofanywa kwa wafungwa hao. Hii ilikuwa ni kwa sababu wale waliowafanya wafungwa walikuwa watu duni sana, watu wa hali ya chini na ya udhalili, na hii ni kanuni ya sheria kwamba mtu duni siku zote hufanya matendo duni tu, wakati ambapo mtu mwenye heshima na mwenye hadhi siku zote atafanya matendo yenye heshima na adabu. Katika njia hiyo hiyo kama mtu anakuwa mfungwa wa ulimwengu, basi ulimwengu huu ni kitu duni sana kama Wamarekani. Neno “ulimwengu “ kwa Kiarabu maana yake ni “Dunya” ambayo maana yake ni “duni” na “iliyo dhalili. Neno Dunya limetokana na neno la msingi “Adna” ambalo humaanisha “duni”. Dunya ni neno la kike kwa “Dana”. Neno “Dunya” hutumika kama kinyume cha “Aali” (juu). Kama ilivyo kinyume na neno la ujumla la “Ulya” (vitu vya hali ya juu na maarufu). Kwa vitu duni na dhaifu neno “Dunya” hutumika. Hivyo, kama mtu akiwa mfungwa wa ulimwengu huu wenye fedheha basi ulimwengu hautamfanyia mfungwa wake kwa hadhi ya mfungwa huyo, bali utamfanyia kwa hadhi na nafasi yake (huo ulimwengu). Ulimwengu umedhalilika mno kiasi kwamba huwafanya wafungwa wake dhalili pia. Kwa hiyo, wafungwa wa ulimwengu huu wasitegemee kufanyiwa wema na ulimwengu huu. Hii ndiyo sababu kama unataka kuona viumbe waliodhalilishwa mno katika historia, utaona kwamba mtu aliyedhalilishwa zaidi ni mfungwa wa ulimwengu huu.
8. Utendaji wa Shetani kwa wafungwa wake. Baadhi ya watu wamekuwa wafungwa wa Shetani. Wakati mwanadamu anapokuwa mtumwa basi matendo anayotendewa ni yale ya watumwa tu. Kama mtu anakuwa mfungwa wa Shetani basi sio kwamba Shetani atampa sifa na heshima nyingi. Shetani ataweka minyororo kwenye shingo yake na kumchukua katika kila mtaa na kichochoro akimdhalilisha mbele ya kila mtu. Hili ndilo linalofanywa kwa wafungwa; wanapitishwa kwenye mitaa na vichochoro vyote wakiwa na minyororo na pingu shingoni mwao. Pia Shetani hufanya hivyo hivyo, huweka 119
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 120
Maadili Ya Ashura pingu na minyororo ya tamaa na matamanio katika shingo za watumwa wake na kuwaburuza katika kila mtaa na uchochoro. Ingawa pingu za Shetani hazionekani, kama unataka kuona wafungwa wa Shetani basi hakuna haja ya kutembelea Gereza lolote, ingawa inawezekana wakawepo huko ambao vilevile ni wafungwa wa shetani. Lakini watumwa na wafungwa wengi wa Shetani wanapatikana kwenye masoko, maofisi, misikitini na hata kwenye Hussainiya. Pia unaweza ukawaona watumwa wa Shetani ndani ya maeneo matakatifu ya Kaaba Tukufu. Mtu ambaye ana pingu za tamaa, mapenzi makali, na woga kwenye shingo yake ni mtumwa wa Shetani, wakati ambapo mtu ambaye yuko huru kutokana na mitego ya matamanio kwa hakika ni mtu huru.
9. Ni lini tutasherehekea uhuru? Kama tunataka kupima iwapo tunaishi maisha ya uhuru au ya utumwa, hatupaswi kujaribu kutafuta iwapo tuna pingu kwenye shingo zetu au la, kwa kweli lazima tuangalie kwenye hadhi, dini na maadili yetu. Lazima tuangalie kwenye maneno, fikra, imani, uchumi, siasa na jamii yetu ili tuone iwapo zina pingu za utumwa kwenye shingo zao au la. Kama tunaona pingu za utumwa na udhalili, basi je tumewekwa huru? Kwa namna hiyo tunasherehekea kila mwaka uhuru wa Pakistan, lakini ni uhuru wa aina gani huu? Ni aina gani za pingu zimeondoka kwenye shingo zetu kutufanya sisi tusherehekee siku ya Uhuru? Ni aina gani ya kamba zimefunguliwa, kwamba tusherehekee siku hii? Ni minyororo gani tumefunguliwa kutufanya sisi tusherehekee kiasi hicho? Kwa kweli, siku tuliyopata uhuru tulikuwa na pingu chache shingoni mwetu ukilinganisha na zile tulizonazo baada ya miaka hamsini ya uhuru. Ni mzaha tu na kufanya mchezo wa uhuru kwa kuusherehekea baada ya kufungwa tena kwa minyororo mingi ya utumwa kwenye shingo zetu. Hii kwa uhalisi ni sherehe ya utumwa katika jina la uhuru. Kama Husein ibn Ali (as) (Abul Ahrar), kiongozi wa wenye kupenda uhuru anasahauliwa, na watu wanaanza kufuata viongozi wa watumwa, basi kitu utakachopata ni uhuru tu ambao utakufunga tena kwa utumwa. Muda wa kusherehekea uhuru ni wakati tuko huru katika vipengele vyote, wakati maamuzi yetu na mamlaka zetu ziko huru, wakati akili na fikra zetu ziko huru, wakati vyama na taasisi zetu haziko chini ya maelekezo ya mtu mwingine na tuna utashi wetu wenyewe na tuko huru kupitisha maazimio yetu.
10. Waliochukua masomo ya uhuru kutoka kwa Imamu Husein (a.s) Kama watu wanataka kuelewa, basi kila hatua iliyochukuliwa kule Karbala itawasaidia kugundua maelfu ya maadili yaliyohuika hapa. Kama tunataka kuchukua 120
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 121
Maadili Ya Ashura masomo ya Ukombozi na uhuru, basi tuje kwa kiongozi wa wapenda uhuru. Kama tunataka kutembea kwenye njia ya ukombozi basi tujifundishe hili kutoka kwa kiongozi wa wakombozi. Kuna baadhi ya watu ambao wanazungumza kwa maneno tu kuhusu Karbala lakini kuna wengine vilevile wale ambao huichukulia Karbala kama taasisi na kuchukua masomo kutoka huko. Imamu Khomeini (r.a) anasema: “Chochote tulichonacho ni kutoka kwa Kiongozi wa Mashahidi (as).” Kama watu kama sisi wakisema hili basi swali litakuja kwamba ni kitu gani tulichonacho hata tuseme hivi? Lakini wakati maneno kama haya yanapotolewa na mtu ambaye ana kila kitu, mapinduzi, dini na Marjaiyat, uongozi na mwongozo, Qur’ani, heshima, hadhi na uwezo, uhuru na uamuzi na hata baada ya hili, kama akisema kwamba yote haya ni kwa ajili ya Husein (as), basi tunaweza kusema kwa kujiamini kwamba huyu ni mfuasi wa kweli wa Husein (as). Kama mtu sitamuuliza mtumwa kama mimi, kwamba ni kitu gani umechukua kutoka kwa Imamu Husein (as)? Jibu langu litakuwa kwamba nimechukua jina la Husein (as). Lakini mtu niliyemtaja mwanzo mbali na kuchukua jina la Husein (as) vilevile amekunywa maadili ya Imamu Husein (as).
11. Imamu Husein (a.s) – Kigezo cha Wajibu wa Ukombozi (Uhuru) Imamu Husein (as) aliuhuisha ukombozi. Maadili yoyote mazuri hayawezi kuhuishwa kwa hutuba tu za wahutubiaji juu ya mimbari, mashuleni na misikitini. Ili kuyahuisha maadili, lazima tuingie kwenye uwanja ambako maadili yanachinjwa; ni kwa kwenda tu huko (uwanjani) ambako tunaweza kuyanusuru. Ukombozi ulikuwa unadhihakiwa katika uwanja wa Karbala ambapo utumwa na ufungwa ulikuwa ukitangazwa kama ulioshinda. Chini ya vivuli vya panga, katika uwanja wa mauaji, Imamu Husein (as) alihuisha maadili makubwa na uhuru na akaushinda utumwa na ufungwa. Wakati Imamu Husein (as) alipokuwa ameachwa peke yake katika uwanja wa mapambano alianza kupigana peke yake. Hata katika hali yake ngumu ya kiu kali wakati maadui walipoona ushujaa wake wa ajabu (imesimuliwa katika hadithi pia kwamba yeye (as) alishambulia katika hali ambayo aliukaribia mto wa Furati (Euphrates); walitambua kwamba hawawezi kupigana na Husein (as). Hivyo, 121
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 122
Maadili Ya Ashura mlaaniwa moja akasema kwamba, njia iliyo bora ya kumshinda Husein (as) ni kumuachilia mbali yeye mwenyewe na kuelekea kwenye mahema yake. Haya tuelekeeni kwenye mahema ambako mabinti wa Husein (as) wako huko, haya natuwavue shungi zao kupora na kuyaharibu mahema yao. Wakati sauti hii ilipotolewa Kiongozi wa wapenzi wa uhuru, “Baba wa wakombozi” (Abul Ahrar) wakati anapanda kwenye kipando chake alisema “Enyi wafuasi wa Abu Sufyan, Enyi warithi wa maadili ya Abu Sufyan, Enyi warithi wa maadili ya Bani Ummayya!” Yeye (as) hakuwaita kama Umma wa Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) au kama Waislamu kwa sababu walikuwa hawana maadili ya Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.), hawana dalili ya maadili yoyote ya Kiislamu ndani yao, kwa hiyo, aliwaita kama wafuasi wa Abu Sufyan. “Kama hamna dini yoyote, kama hamna imani juu ya Siku ya Hukumu, kama nyoyo zenu hazina hofu juu ya Siku ya Hukumu, basi angalau ishini maisha ya uhuru katika ulimwengu huu. Kama akili zenu haziikubali dini, basi angalau kuweni wanadamu huru katika ulimwengu.” (Mawassae Kalemat Imam Hussain, uk. 504) Yeye (as) alitaka kusema kwamba katika muda huu ninyi ni watumwa, dini yenu haiko huru wala ulimwengu wenu. Angalau tafakarini juu ya wahenga wenu, mnatokana na kizazi cha Kiarabu na Waarabu wana maadili fulani na desturi, wanazo desturi za kikabila. Wakati Mwarabu anapopigana vita, kamwe hawakandamizi watoto, wala kuleta matatizo kwa wanawake. Kamwe hatawashambulia wale ambao hawawezi kujitetea wenyewe. Haya yalikuwa ni maadili ya Waarabu wajinga na washirikina na walizoea kushikana nayo kwa umakini. Hata kama Mwarabu mshirikina akipigana, hawi mtumwa wa matamanio yake kiasi hicho; hatakuwa mfungwa wa matamanio yake na wa Shetani kwa kiwango hicho. Ameruhusiwa uhuru wa kiasi hicho, ambamo anaweza kuacha mateso dhidi ya wanawake na watoto. Kama hufuati dini yoyote, angalau onesha kiasi hiki cha uhuru katika ulimwengu huu, angalau heshimu maadili ya Waarabu. Hapa ndipo tunapokuja kujua kwamba kizazi cha Abu Sufyan ni wale ambao dini yao halikadhalika na ulimwengu wao vyote ni vya utumwa, wakati ambapo kizazi cha Ali (as) na kizazi cha Mtume (s.a.w.w.) ni wale ambao dini yao halikadhalika na ulimwengu wao vyote viko huru. Hii ndio tofauti kati ya kizazi cha Mtume (s.a.w.w.) na kizazi cha Abu Sufyan. Njia ya utumwa kamwe sio njia ya kizazi cha Mtume (s.a.w.w.), kizazi cha Ali (as) na Husein (as). Njia ya Husein bin Ali (as) kamwe ni ya kutokuwa mfungwa wa yeyote na wala kunyenyekea kwa yeyote kutokana na udhaliishaji. Yeye (as) anasema:
122
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 123
Maadili Ya Ashura
“Nakiona kifo katika njia ya Allah (s) kama heshima; nachukulia kama ni aibu na fedheha kubwa kuishi maisha yangu pamoja na mkandamizaji.” (Mawassae Kalemate Imam Hussain, uk. 356) Wakati maadui walipoamua kushambulia kambi yake, yeye alisema:
“Enyi wafuasi wa Abu Sufyan! Kama hamna dini yoyote na hamuogopi Siku ya Hukumu, angalau ishini kama watu huru katika ulimwengu wenu huu, kama ninyi ni Waarabu na kwa vile mnajiona kama Waarabu basi angalau watazameni wahenga wenu.” Shimr maalun akasema: “Ewe mwana wa Fatima (as)!Unasema nini? (Mawassae Kalemate Imam Hussain, uk. 504) Imam Husein (a.s) alisema:
“Sisi wanaume tumepigana wenyewe kwa wenyewe, hawa wanawake hawana kosa lolote ndani yake, mpaka muda niko hai acheni uasi wenu, kuchupa mipaka na ujnga mbali na wanawake wa familia yangu.” (Mawassae Kalemate Imam Hussain, uk. 504)
12. Mateka wa Damascus na Uhuru A. Imam Sajjad (a.s) - Mateka wa Damascus na uhuru Husein ibn Ali (as) ametupa sisi masomo ya Ukombozi. Ameondoa pingu za utumwa kutoka kwenye shingo zetu; amefungua kamba za utumwa ambazo ziliufunga Umma katika makucha yake. Lakini ili kuziondoa pingu hizi na kuzifungua kamba hizi, wakati mwingine lazima uwe mfungwa na wewe mwenyewe ujifunge minyororo pia. Hivyo Imamu Sajjad (as) alilazimika kuweka pingu za chuma shingoni mwake, lakini lazima tukumbuke kwamba simba kamwe hafedheheki hata 123
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 124
Maadili Ya Ashura kama amefungwa minyororo. Hii ni kwa sababu wale ambao hawawezi kuvumilia na kukubali simba atembee kwa uhuru, watafikiria kumfunga na minyororo. Ni wale tu wenye woga na simba ndio watamfunga minyororo. Simba ambaye amefungwa kamba bado atabakia ni simba tu. Imamu Sajjad (as) mwana wa simba wa Allah alithibitisha kwamba wanaweza kuweka kamba shingoni mwake lakini hawakuweza kufunga ulimi na fikra zake. Imamu Sajjad (as) anasema:
“Mtu huru yuko huru katika hali zote na mazingira yote. Kama akipatwa na msiba huwa na subira, kama akijiwa na matatizo bado anabakia asiyeshindwa. Hata kama akifanywa mateka na mfungwa, akikandamizwa na kuteswa na kama hali yake ikibadilika kuwa ile ya upweke na ya shida, bado haitaathiri ukombozi wake. Uhuru wa mtu mwaminifu na mkweli kama Yusuf (as) haukuathiriwa hata kidogo ingawa alifanywa mtumwa na mfungwa, na alikuwa mwathirika wa mateso. Hata hofu kubwa ya ndani ya kisima haikuweza kuacha hata athari hasi katika ukombozi wa Yusuf (as)” (Usool-e-Kaafi, Jz. 2, uk. 18) Mtoto huru wa Kiongozi wa wapenzi wa uhuru aliwasilisha silika nzuri ya uhuru kwa kuweka pingu za chuma shingoni mwake. Alipigana dhidi ya utumwa na ufungwa akiwa na minyororo miguuni mwake. Hata katika hali hii ya ufungwa na ukombozi, alifanikisha uhuru wa dini. Alipata uhuru kwa ajili ya ubinadamu wote kutokana na makucha ya utewezo wa kizazi cha Abu Sufyan na hivyo kuonesha njia ya kuishi kwa uaminifu. Mtu huru yuko huru hata kama amevaa pingu na minyororo, lakini mtumwa ni mfungwa hata bila pingu na minyororo. Utumwa na ufungwa sio fahari kwa waumini kwa sababu Allah amewaumba bindamu kuwa huru. Imam Ali (a.s) anasema:
“Usiwe mtumwa wa wengine, Allah (s) amekuumba wewe kama mtu huru.” (Nahjul Balaghah, Wosia, Barua ya 31) 124
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 125
Maadili Ya Ashura
B. Mateka wa Damascus – Bibi Zainab (s.a) na uhuru Uhuru hauji kirahisi hivyo, ili kupata uhuru mabinti wa Ali (as) walilazimika kupita masokoni na kwenye mabaraza. Mabinti wa Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) walilazimika kufunga kamba juu ya mikono yao. Mabinti na dada zake Husein (as) walifungua pingu zilizofunga dini na ubinadamu na badala yake wakaweka mbele mabega yao wenyewe kwa ajili ya minyororo. Kama hadithi zilizotufikia maelezo mengi yalitolewa na familia ya Ali (as), kuna kauli moja yenye kuumiza moyo sana ya Bibi Zainab (a.s.) ambayo hububujisha machozi kwenye macho yetu. Wakati mikono yake ikiwa imefungwa nyuma ya shingo yake, Bibi Zainab (as) aliwasili kwenye baraza ya Kufa aliona kwamba Waislamu walikuwa wamekaa pale na miongoni mwao walikuwepo wanachuoni, wataalamu wa Qur’ani Tukufu na watu wa dini, lakini fikra zao, dini na ulimwengu wao ulikuwa wa utumwa. Bi Mkubwa huyu alijiangalia kwanza yeye mwenyewe na kisha akaangalia umati ule wa watu akatoa kauli ambayo inatikisa nyoyo zetu. Bibi Zainab (as) alisema: “Kuna Mwislamu yeyote katika mkusanyiko huu wote? Kuna binadamu yeyote katika mkusanyiko huu wote?” Binti wa Ali (as) alitaka kusema kwamba: “Je, kuna mtu huru katika mkusanyiko wote huu, au wote waliokaa hapa ni watumwa tu?
13. Hurr (a.s) na Ukombozi (Uhuru) Mandhari ambayo ilikuja kutokea katika Karbala ilikuwa ni wakati kamba na pingu za utumwa zilipotupiliwa mbali na kitanzi cha shingo ya Shahidi kikakaribishwa kwa njia ya unyenyekevu kabisa. Ingawa jina la Hurr Riyahi (ra) lilikuwa “Hurr” ikimaanisha aliyekombolewa au mtu huru, kwa hali halisi dini yake ilikuwa ya utumwa na vilevile ulimwengu wake ulikuwa wa utumwa. Alikuwa na pingu za woga shingoni mwake. Akiwa pamoja na jeshi la askari elfu moja aliposimamisha msafara wa Abul Ahrar (Baba wa watu huru), Imamu Husein (as) alimuuliza: “Wewe ni nani?” Alijibu kwamba mimi ni Hurr, Imamu Husein (as) akasema: “Kwa nini umekuja hapa” Hurr (ra) alisema: “Nimekuja kufunga njia yako.” Imamu Husein (as) akasema: “Mama yako akulilie, unataka kitu gani?” Hurr (ra) akiwa mtumwa, alitaka kufunga njia ya uhuru. Hurr (ra) akasema: “Kama mtu yeyote katika ulimwengu huu wa Bara Arabu angesema hivi kwangu ningejibu kwa njia hiyo hiyo (kwamba na wewe mama yako akulilie), lakini siwezi kufanya hili kwako kwa vile mama yako ni mama ambaye siwezi kuishi bila kulichukulia jina lake kwa heshima, siwezi hata kulileta jina hilo kwenye ulimi wangu, mimi sio mkorofi kiasi hicho.” Kutokana na hili tunafahamu kwamba mtu huyu ambaye jina 125
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 126
Maadili Ya Ashura lake ni Hurr (ra) hakuwa mfungwa wa kiasi hicho, kwa sababu wakati ilipokuwa ni zamu ya kulichukua jina Bibi Zahra (as) alionesha heshima na adabu. Ewe Hurr! Umekuwa na aibu na adabu kiasi hiki kwamba hukutaja jina la Bibi Zahra (as) kwa namna ya ukorofi na utovu wa adabu. Tunatamani! Ewe Hurr (ra), ungekuwepo Madina wakati watumwa na wafungwa wa ulimwengu huu walipochoma mlango wa nyumba ya Bibi Zahra (as). Ungeiona mandhari ile kwa ujirani wa karibu, wakati Bibi Zahra (as) akiendelea kuita: “Enyi watumwa! Enyi wafungwa! Msichome moto mahala hapa, kwani hii ni nyumba ambamo Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) alikuwa akisoma Ayatut-Tathir (aya ya utakaso), huu ni mlango ambao mbele yake Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) alikuwa na mazoea ya kutoa salaamu.” Tunatamani! Ungekuwepo Madina, hisia zako zingehisi hili na nyumba ya AhlulBayt (as) isingechomwa. Ewe Hurr! Kwa hakika wewe ni “Hurr,” mtu huru. Wakati Hurr (ra) alipowasili Karbala alitambua nafasi yake ya utumwa na akajisemea mwenyewe: “Mama yangu ameniita “Hurr” (mtu huru) lakini dini na ulimwengu wangu vyote ni utumwa mtupu. Kiongozi wa watu huru yuko mbele yangu na ni mgeni tu wa siku moja zaidi, kama sivui hii minyororo ya utumwa leo basi nitabakia mtumwa mpaka Siku ya Hukumu.” Hurr (ra) alifurahishwa sana na fursa ambayo ameipata na akaja kwa Kiongozi wa wapenzi wa uhuru. Huku akiwa amenyoosha mikono yake alisema: “Ewe Kiongozi wa watu huru! Je, kuna njia yoyote yakuniondolea minyororo hii? Je, toba yangu itakubaliwa? Je, Hurr anaweza kupata uhuru au la?” Imamu Husein (as) akasema: “Hurr! Wewe ni kipenzi changu, simama kutoka hapo chini, usijitie mavumbi, wewe ni mgeni wangu. Husein (a.s.) amekukubali, sasa umefunguliwa minyororo na siku zako za utumwa zimepita.” Hurr (ra) akasema: “Ewe Bwana wangu! Kama niko huru basi nataka kushuhudia dalili ya uhuru huu na hili linaweza kufanyika kwa kunipa ruhusu ya kuwa mbele kwenye uwanja wa mapambano (Jihad).” Imamu akampa ruhusa ya kupambana.” Hurr (ra) alionesha ukubwa wa wema kwa kumpeleka kwanza mtoto wake kijana kwenye uwanja wa mapambano, baada ya kwenda yeye kupigana kwanza. Wakati mtoto wake alipouawa kishahidi, alichukua maiti ya mtoto wake katika mikono yake na akaiweka chini ya miguu ya Imamu Husein (as) na akasema: “Ewe Kiongozi wa watu huru! Ewe unayetoa wokovu kutokana na utumwa! Tafadhali ukubali muhanga huu wa mtumwa wako.” Baada ya hili alikwenda kwenye uwanja wa mapambano na kupigana kishujaa, alikabiliana na shahada. Wakati alipokuwa anakaribia kuanguka kutoka kwenye farasi wake aliita: “Ewe Bwana wa watu huru! 126
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 127
Maadili Ya Ashura Njoo kwenye maiti ya mtumwa wako na unibariki kwa fursa ya mwisho ya kukuona.” Imamu Husein (as) alikuja kwenye mwili mtakatifu wa Hurr (ra), alinyanyua mkono wake na akauweka juu ya paja lake na kusema: “Kwa usahihi kabisa mama yako amekuita Hurr, uko huru, na umeondoa minyororo yote mbele ya kifo chako.”
“Naapa kwa jina la Allah mama yako hakufanya kosa kwa kuliweka jina lako kama Hurr. Naapa kwa jina Allah kwamba uko huru katika ulimwengu huu na uliyetukuka akhera.” (Mawassae Kalemate Imam Hussain)
127
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 128
Maadili Ya Ashura
Maadili ya Sita Subira (Sabr) 1. Subira – Maadili ya Ashura..............................................................................129 2. Cheo cha subira kuwepo katika Quran Tukufu................................................129 3. Subira katika simulizi za Maasumin (as).........................................................130 4. Subira – Daraja la Mawalii wa Allah (s).........................................................132 5. Maana halisi ya Subira....................................................................................132 6. Ujana – Muda mzuri kwa ajili ya kujizoesha Subira......................................134 7. Upotoshaji katika maana ya Subira..................................................................135 8. Maana ya Subira...............................................................................................136 9. Mazingira kwa ajili ya Subira..........................................................................138 10. Allah yuko pamoja na wenye kusubiri (Sabiriyn).........................................143 11. Imam Husein (a.s) – Kigezo cha tabia ya Subira..........................................143
128
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 129
Maadili Ya Ashura
1. Subira – Maadili ya Ashura Maadili muhimu ya Ashura, ambayo Kiongozi wa Mashahidi (as) aliyahuisha kwa kuyarudishia roho yake na kuyaokoa kutokana na kusongwa roho na hivyo kuyawakilisha kwa wanadamu, ni maadili ya Subira. Maadili muhimu kama Subira ambayo ilivunjwa kama ilivyo kwa masomo mengine ya Kiislamu, maana ya Qur’ani Tukufu na maadili mengine ya kiungu pamoja na roho yake kuondolewa; kwa mara nyingine tena yaliwasilishwa pamoja na maana yake sahihi na Imamu Husein (as), na yeye (as) aliwasilisha hili kama zawadi kwa ubinadamu wote. Hivyo tunaweza kusema kwamba Subira ni maadili ya Ashura ambayo yamekuzwa kwa (kunyweshelezewa) damu ya Imamu Husein (as) na masahaba wake watiifu. Katika mapambano ya maadili, Subira ilijitokeza kama mshindi na kung’ara. Imamu Husein (as) alitufundisha jinsi ya kuwa na Subira na kwa kuonesha maana ya kweli ya Subira. Yeye (as) aliyapa wokovu maadili haya makubwa.
2. Cheo cha subira kuwepo katika Quran Tukufu Kuna hali tofauti za upandaji (hadhi) kwa ajili ya wanadamu katika Qur’ani Tukufu, na Allah (s) alifurahia wanadamu kwa kupata hadhi hizi mbali mbali. Miongoni mwa hadhi na vyeo hivi, kuna cheo muhimu cha wale ambao wana Subira. Katika sehemu mbalimbali katika Qur’ani Tukufu mwanadamu amesifiwa kwa kuwa na Subira, na malipo na thawabu vilevile yametajwa. Cheo cha mwanadamu mwenye Subira kinaelezewa na Qur’ani Tukufu katika maneno haya:
“…Na wape habari njema wanaosubiri. Ambao ukiwapata msiba, husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na Kwake Yeye tutarejea.” (Surah Baqrah, Ayah 155, 156) Wakati wengine watakapoona cheo hiki cha wanadamu wenye Subira mbinguni watajisikia vibaya na kuzungumza miongoni mwao wenyewe na kusema: “Tunatamani tungekuwa miongoni mwa wale ambao walikuwa na Subira.” 129
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 130
Maadili Ya Ashura Wanadamu wenye Subira wakati wanapoingia peponi watasalimiwa kwa heshima kubwa. Pepo itakuwa inazingojea nyayo zao; malaika na hata bawabu wa Pepo (Ridhwan) watakuwa wanawangojea. Malaika watawajia na kuwakaribisha kwa maneno haya:
“Assalaam alaykum (amani iwe juu yenu) kwa sababu ya mlivyosubiri (katika ulimwengu)…” (Surah Ar-raad, Ayah 24) Hivyo tunafahamu kwamba Subira ni cheo chenye heshima kubwa kwa wanadamu kiasi kwamba imetajwa kama bishara (habari njema) ya kimungu katika ulimwengu huu. Na katika Akhera pia, hukuza uwajibikaji ndani ya mwanadamu kiasi kwamba wao kama wanadamu wenye Subira wakati wanaingia Peponi malaika watakuja kuwakaribisha na watawaslimia na kuwatakia amani juu yao. Kutokana na roho ya Qur’ani tunaweza kufahamu kwamba Subira ni maadili kubwa kwa wanadamu. Katika hadithi pia, tutaona kwamba Maasumin (as) walisisitiza juu ya maadili haya (ya Subira) zaidi kuliko walivyoweka msisitizo juu ya maadili nyingine zozote.
3. Subira katika simulizi za Maasumin (as) Simulizi zao zenye nguvu sana na hadithi zote zilikuwa kwa karibu zinahusiana na Subira. Ili kufafanua umuhimu wa Subira tunawasilisha badhi ya simulizi kutoka Nahjul Balaghah. Imamu Ali (a.s) aliulizwa kuhusu imani, katika kujibu alisema::
“Imani inasimamishwa na nguzo nne: Subira, Kusadikisha, Haki na Jihad. Subira au Ustahimilivu una matawi manne: Ari. Hofu, Kujitenga na ulimwengu, na matumaini. Yeyote yule ambaye ana shauku kwa ajili ya Pepo atapuuza vishawishi; yeyote yule ambaye ana hofu ya moto wa Jahannam, atajizuia na vitu haramu; yeyote yule ambaye anapata kujitenga na ulimwengu, kwa urahisi atavumilia shida za 130
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 131
Maadili Ya Ashura maisha haya na yeyote yule ambaye ana matumaini ya kifo ataharakisha kufanya matendo mema.” (Nahjul Balaghah, Simulizi ya 30)
“Mtu ambaye hufuata Subira kamwe hatanyimwa mafanikio ingawa itachukuwa muda mrefu kumfikia.” (Nahjul Balaghah, Simulizi ya 152) “Mtu ambaye Subira haimpi nafuu anakufa katika huzuni na shida.” (Nahjul Balaghah, Simulizi 188)
Nataka kuwafundisha mambo matano; ili kuyapata kama itakulazimu kupanda ngamia na kumpeleka mbio mno itapendeza. Yeyote kati yenu asiwe na matumaini juu ya yeyote yule kuliko Allah (s) na usiogope kitu chochote kile mbali na dhambi zako. Kama yeyote miongoni mwenu anaulizwa kitu ambacho hakijui, basi asione aibu kukiri ujinga wake. Jipatie subira na uvumilivu kwa sababu mahusiano na hali hizo na imani ya kweli ni yale ya kichwa na mwili, mwili hauna maana bila kichwa, hali kadhalika imani ya kweli inaweza kuwa haina maana bila sifa za subira na uvumilivu. (Nahjul Balaghah, Simulizi ya 82)
“Kamilisha neema kwa kuwa na subira juu ya masuala ya utii wa Allah (s) na kwa kulinda vitu vile ambavyo vinahitaji ulinzi wako katika Kitabu Kitukufu… Allah (s) amakinishe nyoyo zetu kwenye Haki; Yeye (s) atupe sisi na ninyi subira zote na fursa kwenye Taufiq. (Nahjul Balagha, Simulizi 171) 131
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 132
Maadili Ya Ashura
4. Subira – Daraja ya Mawalii wa Allah (s) Siku zote Subira imekuwa ikijadiliwa katika majadiliano yote yanayohusiana na kunyanyuliwa madaraja na vyeo vya Mitume. Ingawa inajulikana sana kwamba miongoni mwa Mitume, Mtume Ayub (as) alikuwa mwenye subira zaidi lakini kama tukichunguza visa vya Mitume wengine (as) na kuchambua mazingira ya Mitume (as) katika Qur’ani Tukufu, tunaweza kuona kwamba Qur’ani Tukufu imetaja daraja ya Subira kwa kila Mtume (as). Nabii Ibrahim (as) ametajwa kuwa mwenye Subira na wakati wa kujadili kuhusu Mtume Nuh (as), Nabii Musa (as), Nabii Isa (as), Subira imekumbukwa katika mijadala yote. Kama Mtume mmoja (as) alikuwa akijulikana kwa uvumilivu wake, haiwezi kuchukuliwa kwamba Mitume wengine (as) na Maimamu Maasumin (as) wana daraja ya chini ya uvumilivu. Kwa kweli katika tabia za Maasumin wote (as) elementi ya Subira au uvumilivu imedhihirishwa sana. Subira inachukuliwa kama daraja ya kiroho miongoni mwa madaraja tofauti ya Mawalii wa Allah (s) kama ilivyojadiliwa na Irfan Usufii (Gnostics). Hii huonesha kwamba Subira sio tu sifa kwa mwanadamu, badala yake ni hadhi na daraja ya kiroho kwa ajili ya mwanadamu, kwa kupata sifa hii mwanadamu hufikia ile daraja ya kiroho ya uvumilivu.
5. Maana halisi ya Subira Kuna maadili mbalimbali ambayo maana zake ni hakika, lakini tumezibadilisha kwenye maana ya hasi. Tumeziwasilisha maadili hizi katika maana ya hasi. Mfano wa hili ni Uchaji (Taqwa/Takua). Takua imewasilishwa kwetu kama mtu asiye na vitu fulani, mtu asiye na tabia fulani na sifa mahususi. Kwetu sisi kukosekana kwa vitu hivyo hujulikana kama Uchaji (Takua). Sasa chukua Qur’ani na uone, Qur’ani haisemi kwamba kama mtu anakosa vitu fulani ni Mchamungu (Muttaqi), badala yake katika visheni ya Qur’ani, takua maana yake ni kufanya na kumiliki kitu. Halikadhalika, Mvumilivu sio mtu ambaye ana tabia hasi mahususi au hamiliki vitu fulani. Uvumilivu una nafasi bayana, ni jina la kuwa nacho na kufanya kitu, na sio jina la kutokufanya kitu. Watu wamechukua maana ya uvumilivu katika maana hasi kama kutokufanya kitu (kukaa kimya na kunyamaza), hivyo wanaitoa roho ya uvumilivu nje na kuiponda ponda. Kiongozi wa Mashihidi (as) alihuisha Subira na akaonesha kwamba Subira au uvumilivu sio jina la kutokufanya kitu chochote, bali ni jina la kufanya kitu. Mwanadamu ameelewa maana ya vitu mbalimbali katika maana hasi. Mno sana kwa kiasi kwamba anazungumza kuhusu vitu hasi wakati anapojadili na kuelezea maneno muhimu kama Umaasum (Ismat) na Uadilifu (Adil). Kwa mfano wakati anaelezea Umaasum inasemekana kwamba Maasum ni mtu ambaye hatendi dham132
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 133
Maadili Ya Ashura bi, hafanyi kosa, mtu ambaye havisogelei vitu haramu na ambaye hapitwi na tendo la wajibu. Kwa maelezo haya, inaonekana kwamba kutokufanya kitu chochote ni Umaasum na hapa ndipo pale Mkuu wa Mashahidi (as) alipotujulisha kwamba Umaasum sio jina la kutokufanya kitu bali ni jina la kufanya kitu chochote. Mtoto anapozaliwa pia naye ni maasum kwa sababu ya kukosa uwezo wa kufanya kitu. Lakini kuna tofauti kubwa kati ya Umaasum wa mtoto na ule wa Imamu Maasum (as). Watu wamechukua maana ya maadili makubwa kama Umaasum, Uadilifu, Takua na Subira kama hasi na kama kutokufanya kitu chochote. Wanafikiri kwamba Uadilifu unaweza kupatikana kwa kutokufanya kitu chochote. Takua na Umaasum vilevile huchukuliwa hivyo hivyo. Kwa hiyo, tunafikiri kwamba tunaweza kuchukua tasbihi mkononi mwetu na kukaa juu ya mswala msikitini na kwa urahisi ukawa Mwadilifu, Mchamungu, Mvumilivu na hata Umaasum kwa kukaa tu na bila kufanya kitu chochote. Lakini Kiongozi wa Mashahidi (as) alitufundisha kwamba maadili haya hayapatikani kwa kutokufanya kitu chochote, yapatikakana kwa kufanya kitu. Mpaka na iwapo matendo yanayohitajika hayatekelezwi, mtu hawezi kuwa Mwadilifu, mpaka afanye baadhi ya matendo fulani vinginevyo hawezi kuwa mchamungu na mvumilivu. Kama akiwa Maasum kwa wema kwa kutokufanya kitu chochote, basi atawekwa katika madaraja ya watoto, sio katika madaraja ya Mawalii wa Allah (Awliya Allah). Umaasum wa mtoto ni rahisi sana kwa sababu huja kwa kutokufanya kitu chochote. Mwanadamu anapokua, hahitaji kuwa maasum kama mtoto lakini kama vile watoto ambao hawafanyi kitu chochote, hujiona kwamba na yeye pia anaweza kuwa mpenzi wa kila mtu kwa kutokufanya kitu chochote. Kuna tofauti kubwa kati ya watoto na wakubwa. Watoto hawana akili za kimatiki; hawana uwezo wa kufanya kitu chochote kwa sababu Allah (s) hakuwapa nguvu hiyo, mamlaka na akili. Allah (s) hakuweka kigezo kwa ajili ya kutokufanya kitu chochote, lakini kuna masharti na vigezo vilivyoelekezwa kwa ajili ya kufanya kitu na vigezo hivi ni akili, mamlaka na utu uzima. Wakati Allah (s) anapomjaalia mtu kwa akili na uwezo, basi hutegemea kitu kutoka kwake na mtu huyo lazima afanye kitu fulani kwa sababu amepewa uwezo wa kufanya kitu. Uwezo huu amepewa na Allah (s) ili afanye kitu fulani. Hivyo Umaasum hauji kwa kutofanya kitu chochote, Takua na Uadilifu havipatikani katika hali hii, na kadhalika Uvumilivu au Subira pia sio jina la kutokufanya kitu chochote (yaani, kukaa kimya).
133
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 134
Maadili Ya Ashura 6. Ujana – Muda mzuri kwa ajili ya kujizoesha Subira Zama za mwanadamu hupita kwenye hatua nyingi na Allah amegawanya maisha ya wanadamu katika vipindi vitatu tofauti. Kipindi cha kwanza ni uchanga na utoto ambako mwanadamu ni dhaifu na hana uwezo wa kufanya mambo. Kisha hatua kwa hatua nguvu zake huongezeka na wakati ambapo mwili wake unakua na kuwa na nguvu umri wake hufikia zama ile ambako anapata nguvu kamili. Hiki ni kile kipindi cha thamani cha mwanzo wa ujana wakati nguvu zote na uwezo wa mwanadamu uko kwenye kilele chake. Wakati wa kipindi hiki cha maisha, uwezo wa mwanadamu wa kufikiri uko kamili na uwezo wote hufikia kilele chake na huu ndio wakati anapata fursa ya kufanya mambo fulani. Baada ya hili, kipindi cha tatu huanza wakati polepole nguvu zake zinapoanza kuisha na hatimaye hali yake huwa kama ile ya mtoto mchanga. Amedhoofika na kwa mara nyingine anahitaji msaidizi wa kumuangalia. Hivyo, Allah (s) amegawanya umri wa maisha ya mwanadamu kwenye vipindi vitatu, na zama ya ujana ni ile ya kilele na nguvu. Mwanadamu lazima afikiri, kwamba punde ninapofikia umri wa miaka kumi na tano, mwili wangu hupata nguvu na wakati huo huo sheria za dini huwa wajibu kwangu. Tunapoyahusisha haya mawili, tunatambua kwamba kwa kupatiwa kipindi cha ujana, Allah anategemea utekelezaji wa wajibu na majukumu kutoka kwa wanadamu wote. Allah anataka kazi fulani kutoka kwake sasa, ama katika utoto, hakuna wajibu uliowekwa juu yake na Allah, kwa kweli matendo ya mtoto yako huru kutokana na kuandikwa katika kitabu cha matendo, kwa vile hana uwezo wa kufanya mambo. Halikadhalika wakati wa uzee, kutokakana na shida, utekelezaji wa wajibat unasamehewa. Sio wajibu kwake kufunga. Kuanzia mwanzo wa umri wa ujana wajibat zinazolingana huwekwa juu ya wanadamu. Wakati nilipokuwa sina nguvu katika mwili wangu, sina busara za akili, Allah hakunichukulia mimi mwenye uwezo wa kutosha ili kuweka ibada Zake za dini na wajibat juu yangu. Kama dini na sheria zake zilikuwa zinahusiana na kutokufanya kitu chochote basi kipindi hiki cha kungojea cha miaka kumi na tano kisingekuwepo, hivyo, dini na sheria zake hutuambia kufanya mambo na sio kukaa tu kimya, maadili ya kiungu hutuongoza kufanya mambo fulani. Sheikh Tusi katika kitabu chake “Aamali� anasimulia hadithi kutoka kwa Mjumbe wa Allah (s) alimwambia Abu Dharr (ra): 134
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 135
Maadili Ya Ashura
“Ewe Abu Dharr! Yatumie mambo matano kama neema mbele ya mambo matano, Ujana kabla ya uzee, Siha kabla ya maradhi, utajiri kabla ya umasikini, muda ulio huru kabla ya na shughuli na maisha kabla ya kifo.” (Amaali, Sheikh Tusi, uk. 526) Kutoka hapa tunakuja kufahamu kwamba kipindi kilicho bora kutekeleza Subira au Uvumilivu ni kipindi cha ujana kwa sababu uvumilivu (Subira) maana yake ni kufanya mambo fulani, kuwa imara katika mazingira ya misiba na majanga pamoja na kukabiliana na panga na mikuki (sasa risasi na mabomu). Ujana ndio umri bora wa kuonesha maajabu ya ushujaa na ujasiri. Katika kipindi hiki cha maisha yake mwanadamu anaweza kufanya mambo mengi na huu ndio umri ambapo mwanadamu anaweza kupata daraja ya Subira (Saabirin). Kama mtu katika umri wake wa Ujana akafanya uzembe na kupoteza muda huu wa maisha yake na hajifunzi kukabiliana na majanga na shida, baadaye atapoteza ari hata kwenye suala dogo sana na hatapata uwezo wa kuvumilia machungu.
7. Upotoshaji katika maana ya Subira Mwanadamu anatamani kuishi maisha ya unyonge licha ya kuwa na nguvu; anapenda kuwa kama mtoto mnyonge ili kwamba mtu mwingine amtunze. Wakati ikija kwenye mahitaji na riziki yake ya maisha anakuwa sio mzembe, kwa sababu kama akifuata mwelekeo wa utegemezi, anajua matokeo yake na kwa hiyo huchukulia mwelekeo huo usiokubalika. Lakini katika masuala ya maadili ya Kiislamu, hujitokeza mbele kupotosha maana ya maadili ili kuokoa masilahi yake binafsi. Hubadilisha hata maana ya Uislamu na kusema kwamba Uislamu hautaki mimi nifanye kitu chochote, hivyo maana ya Takua, Uadilifu na Subira vilibadilishwa kumaanisha kutokufanya kitu chochote. Hivi ndivyo ambavyo roho ya Subira ilivyoondolewa. Maana ya Subira ilibadilishwa ili kuikubali fedheha na kuuvumilia ukandamizaji. Subira ikawa kimya, uafikiano na mazingira, kutokuzungumza, kutokuwa na harakati yoyote, inamaanisha tu kwamba mtu lazima akae kwa raha na kupoteza muda wao; na hii ndio maana ya Subira inayotumika leo. Yote haya ni kwa kiasi ili watu kubakia wenyewe kwa wenyewe pamoja na ushauri juu ya upatikanaji wa Subira ya aina hiyo. Kama baadhi ya watu wafedhuli wakikunyang’anya haki yako na ukalalami135
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 136
Maadili Ya Ashura ka kwa mtu mwingine atasema; “Ndugu yangu lazima uwe na subira.” Unachukulia tu kuwa ni sawa alichosema, hushughuliki hata kuuliza maana ya subira hapa ni nini. Kwa kweli, inakuja pia akilini mwako kwamba anakuambia kukaa kimya na usifanye kitu chochote dhidi ya mkandamizaji huyu. Ingawa sauti ya kauli hii (Kuwa na Subira) ni bayana, lakini maana hasi hupatikana kwayo. Kama unaangalia kwa nje msamiati wa kauli hii “ Kuwa na Subira,” huonekana kama vile mtu anakuambia kufanya kitu fulani, anakuambia kuwa na uvumilivu, lakini katika dhamiri yake alikuwa anakuambia usifanye kitu chochote, na wote tunaelewa kwamba mnafiki ni mtu ambaye nafsi ya nje na ya ndani zinatofautiana. Mfano wa hili ni, kama mwanadamu anaanza kuwasilisha maadili ya kidini katika hali ya bayana kwa nje yake lakini katika dhamiri yake anaua nafsi yake basi pia itakuwa inaitwa unafiki. Mwanadamu ameanzisha hii tabia ya unafiki katika mafundisho ya dini pia, hii ina maana kwamba ametengeneza mafundisho ya nje ya dini katika hali tofauti kuliko maana yake ya ndani. Twaa kuwa na Subira! Maana ya kauli hii sio kutokufanya kitu. Hili litawezakanaje wakati Allah anakupa habari njema na anasema: Ewe Mtume! Wape habari njema wenye kusubiri. Je, bishara hii ya habari njema ilitolewa kwa ajili ya kutokufanya kitu chochote au hii ni kwa ajili ya kufanya kitu? Hii hutuambia kwamba kubadilisha maana ya maadili ya dini ni muundo wa unafiki, na wale ambao wanabadilisha na kupotosha maadili ya dini kwa hakika ni wanafiki.
8. Maana ya Subira Namna ambavyo Imamu Husein (as) alivyoondoa unafiki katika nyoyo za watu, katika namna hiyo hiyo, Yeye (as) vilevile aliuondoa katika mafundisho ya dini, ambapo aina hii ya unafiki imeingia katika dini kwa sababu ya upotoshaji ulio tengenezwa na watu. Aliifanya nje na ndani ya dini kuwa na maana iliyo sawa. Subira ambayo mpaka sasa, kwa nje ina maana, kutokufanya kitu, Imamu Husein (as) alibadilisha maana yake kote nje na halikadhalika ndani kuwa na maana ya kitu cha kufanya. Imamu Husein (as) alifanya hivi na kufikisha ujumbe kwa watu kushuhdia kwamba Subira ni jina la chochote ninachofanya. Wakati wa mapambano ya Karbala Imamu Husein (as) aliona masahaba wake watiifu na watu wa ukoo wake wa Bani Hashim, askari wapiganaji ambao walikuwa na kiu sana, Yeye (as) aliwakusanya pamoja na akawahutubia kwa kuanza kuwaambia: “Enyi watoto wa utukufu! Enyi mabwana wa utukufu! Katika hali hii ya kiu kali chukueni panga zenu na mikuki na kuweni imara, katika uwanja huu wa mapambano wenye joto na piganeni na maadui, hii ni subira yenu.” Yeye (as) 136
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 137
Maadili Ya Ashura hakusema kwamba, kwa vile mna kiu sana fuateni uvumilivu, ambayo ina maana msifanye kitu chochote na kaeni kwa starehe katika mahema yenu. Kama yeye (as) angewataka kutekeleza aina hii ya Subira basi angemuacha kila mtu mjini Madina. Kutokana na hili tunaelewa kwamba katika hali hii daraja la kuwa mvumilivu lilikuwa sio kubakia Madina, bali upatikanaji wa daraja hii ya Subira (Sabirin) ilikuwa katika vivuli vya panga katika ardhi ya Karbala. Hawa ni wenye subira ambao katika joto kali na katika hali ya kiu kali walionesha maajabu ya ushujaa wao, wakitembea katika dharuba za panga na mikuki. Hawa ndio ambao malaika watawapa makaribisho motomoto kwa kuwatolea salamu ambapo bishara za kiungu zitawekwa tu juu yao na Allah. Hivyo maana halisi ya Subira ni kushikamana, uvuilivu na uimara. Kama ilivyotajwa kabla kwamba kipindi bora cha kufuata Subira ni kipindi cha ujana. Katika umri wa ujana mwanadamu anaweza kuvumilia mambo magumu, ambayo yanaweza yasiwezekane kwake kuyafanya katika umri wa uzeeni. Ingawa kwa kuwaondoa wale ambao nyoyo zao ni vijana, ambao nia na utashi wao bado ni vijana bado wanaweza kuvumilia shida. Kwa hiyo, Subira maana yake ni kukabiliana na majanga na matatizo kwa panga, mikuki (risasi na mabomu) na juu ya yote matamanio maovu. Ni ukweli ulio wazi kwamba wakati wa mapambano lazima ufanye kitu fulani; huwezi ukakaa na kuwa mtazamaji wakati wa mapambano. Imamu Husein (a.s) anasema:
“Enyi watoto wa utukufu! Fuateni Subira, kifo ni cha muda tu ambacho kwacho utavuka shida zote na majanga, na utaelekea kwenye neema za kudumu milele na Pepo. Ni nani miongoni mwenu ambaye hataki kuondoka kutoka kwenye jela kwenda kwenye kasri? Na kifo kwa maadui wenu ni kama mtu aliyetolewa kwenye kasri na kupelekwa kwenye jela na ghadhabu. Mheshimiwa baba yangu alinisimulia hadith kutoka kwa Mjumbe wa Allah (s) kwamba ulimwengu huu kwa mu’mini ni jela na kwa kafiri ni kasri.” (Mawassae Kalemate Imam Husain, 417) 137
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 138
Maadili Ya Ashura Imamu Sadiq (a.s) alisimulia kwamba Imamu Husein (a.s) alisali Sala yake ya Alfajiri kisha akawahutubia masahaba wake kama hivi:
“Allah amekupa ruhusa ya kupigana na maadui na sasa lazima mfuate Subira.”
9. Mazingira kwa ajili ya Subira Imamu Ali (a.s) ana hadithi isemayo subira lazima ifuatwe katika hali mbili:
“Subira ni ya aina mbili: Subira juu ya kile usichokitaka na Subira juu ya kile unachokitaka.” (Nahjul Balaghah, Simulizi ya 55) Aina moja ya Subira ni wakati unalazimishwa vitu ambavyo huvitaki na aina ya pili ya Subira ni wakati unapokabiliana na kitu ambacho unakitaka au ulicho na hamu nacho. Hii ina maana lazima ufuate Subira katika hali zote mapenzi na chuki. katika hadithi nyingine Amirul Mu’minin (as) anasimulia:
“Subira inafanywa katika hali tatu; hii katika hali halisi maana yake Mapenzi na Chuki yana hali tatu: Kwanza: Subira katika shida Pili: Subira katika utii Tatu: Subira katika uasi” (Tuhfal Uquul, Ibne Sheba Harani, uk. 206) Hii ina maana wakati majanga na shida zinapokuja basi lazima ufuate Subira. Mapenzi na Chuki yana jukumu kubwa katika masuala ya utii na uasi. Kwa hiyo, hali zote tatu zinategemea juu ya Mapenzi na Chuki. Hivyo, ili kuwa na Subira katika hali hizi tatu ni sawa na kuwa na mshikamano, uvumilivu na uimara, ili kutaja tena hilo ni jina la kufanya kitu fulani na sio jina la kutokufanya kitu chochote.
A. Subira katika hali za shida Mwanadamu lazima awe na Subira katika hali za matatizo kwa sababu majanga hushuka kumuondoa mwanadamu kutoka kwenye njia yake ya haki. Ni wale tu 138
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 139
Maadili Ya Ashura ambao wamezungukwa na majanga tu ndio wanaofuata Subira. Wale ambao wanapita njia hii ni wale waliozungukwa na majanga; vinginevyo watu waliokaa ndani ya nyumba vilevile huichukulia anasa kama majanga. Siku zote majanga yanakabiliwa na watumwa wa Allah katika njia ya Allah; wanataka kuendelea juu ya njia hii ambako aina tofauti za shida na vikwazo hujitokeza. Wameelekezwa kuendelea juu ya njia hii, bila kuonesha uzembe kwa sababu ya majanga na vikwazo, kuwa imara juu ya njia, usichukue hatua moja nyuma, usitikise ulimi wako kwa kusihi na kuomba, usiiache njia na kurudi nyuma bali kwa kweli vumilia shida zote na kamilisha safari juu ya njia hii ili kwamba wengine pia waweze kufikiria kupita njia hii kwa urahisi. Imamu Ali (a.s) anasema:
“Subira inatolewa katika uwiyano kwa kiasi cha majanga. Mtu ambaye anaonesha hasira kwa kupiga mapaja yake kwa mikono yake wakati wa janga juhudi zake zimebatilishwa.” (Nahjul Balaghah, Simulizi ya 143) Kwa hiyo, wakati wa shida kuliko kuonesha hasira lazima uwe imara, ukionesha uvumilivu na kichwa juu ya njia.”
B. Subira katika hali ya Utii Subira lazima ifuatwe wakati wa utii, kwa sababu utii ni mgumu sana. Mtu mtiifu anaweza kuhisi jinsi ilivyo na ugumu kuwa mtiifu. Qur’ani Tukufu imerudiarudia kuwataka wanadamu kuzingatia masuala ya utii:
“…Mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume na wenye mamlaka katika nyinyi…” (Surah Nisa, Ayah 59) Msisitizo huu ulikuwa muhimu kwa sababu watu walikuwa wakipata shida katika masuala ya utii, hivyo inasemekana kwamba lazima ufuate Subira katika hali za utii au vinginevyo utashindwa katika utii kwa sababu utii ni jambo gumu sana. Huenda tukawa katika hali ya dhana hii kwamba tuna utii kwa Allah (s), lakini hatukuka139
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 140
Maadili Ya Ashura biliana na matatizo yoyote! Ukweli ni kwamba, mtu mkweli na mtiifu anajua tu jinsi gani ilivyo na ugumu kuwa mtiifu. Uasi, uhalifu, uvivu na watu wachovu hawawezi kuelewa jinsi utiifu ulivyo na ugumu na kiwango cha Subira ambacho kinahitajika kwa ajili ya utii. Kuna hadithi ya Maasumin (as): “Ewe Allah! Hatujatoa haki za utii wako.” Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) anasema: “Surah Hud imenifanya niwe mzee.” (Khisaal, Sheikh Suduuq, uk. 199). Imenifanya mzee na kugeuza nywele zangu kuwa za mvi. Ingawa kuna sura nyingi katika Qur’ani Tukufu zilizopo, basi kwa nini Yeye (s.a.w.w.) aseme hili kulingana na Surah Hud tu? Kwamba je, ufafanuzi huu umemfanya yeye (s.a.w.w.) kuwa mzee au ni usomaji tu na uhubiri? Uchambuzi uliofanywa na wafasiri tofauti unatofautiana juu ya kwa nini Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) alisema kwamba Surah hii imemfanya mzee. Baadhi ya wafasiri wamefichua siri hii kwamba kuna aya moja katika Surah hii mubaraka ya Hud ambayo haipo katika Qur’ani nzima. Ni kwa sababu ya aya hii kwamba Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) amesema kwamba Surah Hud imegeuza nywele zake kuwa za mvi.
“Basi simama sawa sawa kama ulivyoamrishwa wewe na yule anayeelekea…” (Uonesha uvumilivu kama ulivyoamrishwa) (Surah Hud, Ayah 112) Lazima uoneshe uvumilivu kama ulivyoamrishwa kufanya, lazima uwe mtiifu kama ulivyoambiwa kufanya na kamwe usipwelee hata kwa namna ndogo kiasi gani. Ni kwa sababu ya utekelezaji wa aya hii kwamba Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) anasema kwamba Surah Hud imevunja mgongo wangu. Aya hii inasema: Ewe Mjumbe wa Allah! Onesha utiifu wako kwa subira na kwa njia ambayo umeamrishwa. Hivyo kwa kuwa na subira wakati wote katika masuala ya utii hali yangu imekuwa kiasi kwamba mgongo wangu umevunjika. 140
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 141
Maadili Ya Ashura Kutoka hapa tunaweza kutambua kwamba ni jinsi gani utiifu ulivyo mgumu. Utiifu hauna maana kuswali tu, saumu, Hijja bali kwa ukweli humaanisha kufanya matendo, ambayo ni muafaka na ridhaa ya Allah (s) na kujizuia kutokana na kila tendo ambalo huchukiwa na dhati ya uungu. Kama unataka kuhisi machungu ya utiifu basi jaribu kuwa mtiifu kwa muda wa saa ishirini na nne tu. Utatambua filosofia ya nywele za Mtume (s.a.w.w.) kuwa za mvi. Kuwa tu mtiifu kwa muda wa saa ishirni na nne, maana yake kula, kunywa, kuzungumza, kusimama na kila kitu lazima kifanywe kwa ajili ya Allah, basi utatambua tu kwamba utii kwa kweli ni shughuli ngumu. Lakini ni kipi yale macho ya waasi yanaona kuhusu utiifu; ulimi uzungumzao daima kamwe hautatambua shida za utiifu, lakini kwa wale ambao Allah (s) anasema:
“ Wala hatamki kwa matamanio. Hayakuwa haya ila ni wahyi uliotolewa” (Surah Najm, Ayah 3, 4) Mtu ambaye huzungumza yeye mwenyewe, lakini ulimi wake hutikisika tu kwa maelekezo ya Allah, tunaweza kusema kwamba macho yake pia hutazama tu kile ambacho ameelekezwa na Allah, masikio yake husikiliza tu kile ambacho Allah anataka asikilize. Haiba hii (ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)) ambaye ulimi wake, macho na masikio yake ni matiifu kwa kiasi ambacho hata baada ya kuishi maisha yake yote yeye anasema kwamba Surah Hud imevunja mgongo wake. Tunakuwa wazee kwa sababu ya matatizo binafsi, shida zinazohusika na pesa, masuala ya kifamilia na mashaka mengine. Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) anasema: “Enyi watu njooni kama mnataka kuvunja migongo yenu, kupata daraja la kuwa mtiifu. Kama mgongo wako ni lazima uvunjike kwa amri ya Allah, basi uache uvunjike. Kama ukianza kufanya visingizio basi jina lako litaondolewa kutoka kwenye orodha ya wenye Subira (Saabirin). Wenye Subira hawaleti visingizio; licha ya maelfu ya matatizo wanabakia imara katika utiifu.
C. Subira katika masuala ya Uasi Subira lazima itekelezwe wakati wa majanga kwa sababu ili kujilinda na majanga, kiwango cha juu cha nguvu kinahitajika. Wakati mwanadamu anapokuwa mtumwa wa ulimwengu, anaweka pingu za matamanio katika shingo yake, hatamu zake ziko kwenye mikono ya matamanio na kisha matamanio haya na ulimwengu humchukua mwanadamu kwenye taya za fedheha. Mtu mwenye ghera ana tamaa ya 141
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 142
Maadili Ya Ashura kupita katika kila uchochoro, anataka kupata mgao katika kila utajiri, macho yake ya uroho siku zote yanatazama kwenye utajiri wa wengine, matamanio yake ni kutazama kwenye wanawake maharimu, na aina kama hiyo ya mtu amejiingiza kikamilifu katika kukidhi matamanio yake. Mfano wa aina ya mtu kama huyo ni kama ile ya mbwa. Watu anbao wana mbwa huweka mkanda kwenye shingo ya mbwa na kamba ya kuongozea ikiwa mkononi mwao. Sasa popote pale aendapo mmiliki na mbwa naye lazima aende huko pia, kama bwana anakwenda kwenye mitaro michafu ya taka mbwa vilevile atakwenda naye. Katika njia kama hiyo, kama wanadamu wanakuwa wafungwa wa ulimwengu huu na matamanio yao, basi kuna uwezekano wa kwenda mwelekeo huohuo ambako matamanio yao yanawataka kwenda. Unafahamu vizuri vichochoro vya matamanio, matamanio kamwe hayatampeleka mwanadamu kwenye maadili ya heshima; siku zote mwelekeo wao ni kwenye machafu na aibu, siku zote kuelekea kwenye vichochoro viovu na vichafu. Hii ni hali ya uasi ambamo mwanadamu lazima atekeleze Subira. Hii ina maana lazima awe imara na kamwe asitumbukie katika matamanio, kwa kweli kwa kutoa hatamu zake kwenye mikono ya Mola Mwenye Huruma lazima aendelee kukataa wito wa matamanio, lazima apigane kwa nguvu zake zote, kamwe asiruhusu uvumilivu kumponyoka mikononi mwake, kama akifanya hivi basi hii ni Subira katika masuala ya Uasi. Inapatikana katika hadithi kwamba mara tu mtu alipokuja kwenye hadhara ya Imamu Husein (as) na kusema: “Mimi ni mtu muasi, sina udhibiti na subira, hivyo nimeasi, tafadhali nipe baadhi ya habari njema.� Imamu Husein (as) akasema: Fanya mambo matano baada ya hapo tenda dhambi yoyote ile utakayo: 1. Usile riziki iliyotolewa na Allah (s), kisha tenda dhambi unayotaka kufanya. Toka kwenye ufalme na mamlaka ya Allah (s), kisha fanya dhambi yoyote unayotaka kufanya. 2. Tafuta sehemu ambako Allah (s) hawezi kukuona, kisha fanya dhambi yoyote unayotaka kufanya. 3. Wakati malaika wa mauti atakapokuja kuchukua roho yako, mfukuzilie mbali na wewe, kisha fanya dhambi yoyote unayotaka kufanya. 4. Wakati Allah (s) anapotaka kukutupa kwenye moto wa Jahannam, basi usiingie kwenye moto huo wa Jahannam, baada ya hili fanya dhambi yoyote unayotaka kufanya. (Mawassae Kalemate Imam Hussain, uk. 773) 142
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 143
Maadili Ya Ashura Yeyote yule atwaaye njia ya aina yoyote ya Subira, iwapo ni subira katika utiifu au Subira katika wakati wa Uasi au katika wakati wa majanga, bishara za uungu zinaoneshwa juu yake na Allah na anakuwa mwenye kustahiki ukaribisho wa malaika. Malaika watamkaribisha kwa salaam na amani. Wale ambao wanataka kuendelea juu ya njia ya haki kwa Subira na uvumilivu Allah vilevile huwasaidia.
10. Allah (s) yuko pamoja na wenye kusubiri (Sabiriyn) Kwa wale ambao wanaonesha uvumilivu na wana ari za hali ya juu, maamuzi na makusudio ya kupita kwenye njia iliyonyooka na kufikia mwisho wake, Allah anasema: kwa vile umeamua kutembea kwenye njia iliyonyooka mpaka mwisho, na kwa vile umeshaanza safari hii, hii ni bishara yangu, kwamba niko pamoja na wewe.
“…Na Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye subira.” (Surah Baqrah, Ayah 249) Wakati mwingine mtu anaanza safari yake juu ya njia na kuishia huku akikabiliana na matatizo na shida katika njia, basi unamliwaza kwa kumwambia ndugu yangu endelea na safari yako, tuko pamoja na wewe, fanya kwa Subira, tunakuja kukusaidia. Lakini kama mtu atahisi kushindwa katika kupita katika njia hii na kukimbia, je, utamuambia aendelee kukimbia na kwamba uko pamoja naye? Hii itamaanisha kwamba wewe pia ni mwoga kama yeye. Allah anasema niko pamoja na wenye subira (Saabirin), hii ina maana kwamba wenye subira ni wale ambao wanafanya kitu fulani, wale ambao hawataiacha njia, wale ambao wanataka kufanya kitu fulani, ni wale ambao wanategemea msaada kutoka kwa Allah kwa sababu bila msaada utokao kwa Allah haiwezekani kuendelea juu ya njia iliyonyooka. Allah anawapa imani kwamba kamwe wasipoteze ari, Niko pamoja na wewe.
11. Imam Husein (a.s) – Kigezo cha tabia ya Subira Imamu Husein (as) ni kifano cha Subira na ndiye ambaye huhuisha Subira na ametuonesha njia ya Subira. Yeye (as) amepulizia roho kwenye maadili ya subira na kuyahuisha, vinginevyo sisi vilevile tungekuwa sawa na wale waitwao wenye subira ambao wanakaa ndani ya nyumba zao katika hali ya woga. Husein ibn Ali (as) 143
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 144
Maadili Ya Ashura ametuonesha sisi njia ambayo kama unataka kupata subira basi subira hupatikana katika uwanja wa mapambano, kamwe huwezi kuwa mwenye subira (Saabirin) kwa kukaa ndani ya nyumba yako. Subira ni maadili ya uwanja wa mapambano; kwa kweli maadili yote ya mwanadamu ni maadili ya uwanja wa mapambano tu. Ingawa tumegawanya mambo yetu kwenye mambo ya nyumbani, mambo ya kijamii nk., lakini Allah hakufanya migawanyiko yoyote katika dini, dini yote imejaa matendo, maadili yote na sifa za dini yako katika uwanja mmoja. Kama unataka kuendeleza sifa hizi ndani yako basi lazima uje kwenye uwanja wa subira kama Husein ibn Ali (as). Kama mtu anataka kuwa mwenye subira nje ya uwanja wa subira kamwe hawezi kuwa. Mpaka awe mwenye subira vinginevyo hapaswi kupata salamu na maamkuzi ya Malaika. Lakini kusikiliza tu visa vya watu wenye busara, basi mwanadamu hawezi kuwa mwenye subira. Ili kupata subira mwanadamu lazima aje chini ya vivuli vya panga na mikuki (risasi na mabomu). Kwa kunyanyua sauti yake kwa ajili ya ukweli na haki, na kwa kupinga uwongo, mwanadamu anaweza kuwa mwenye subira (Saabirin). Subira ni jina la kutetea haki, kwa kujihatarisha kwa kutoa muhanga uhai wake katika njia ya Allah maisha mwanadamu anaweza kuwa mwenye subira. Hii ni subira tuliyofundishwa na Husein ibn Ali (as). Hii sio subira ambayo inaweza kupatikana katika makao ya watawa wa Kisufi, misikitini, kwenye mimbari, kumbi za Hussainiyah. Ili kuipata subira hii lazima utoke nje kwenye uwanja wa Jihad, lazima ucheze na kifo, lazima uwasilishe mihanga ya watoto wako, ni baada ya kubeba maiti zao ndipo mtu anaweza kuwa mwenye subira.
Watoto, mabanati na wapwa wa Imamu Husein (as) walionesha kwamba kiwango hiki cha subira, ambacho hakijaonekana kabla na wala hakitaonekana katika siku zijazo. Hivyo, wakati Qasim (as) alipomuuliza ami yake katika mkesha wa Ashura: “Mpenzi Ami yangu, je jina langu pia limo katika orodha ya mashahidi?” Imamu Husein akamuuliza Qasim (as):
“Mwanangu! Unakionaje kifo? Unasemaje kuhusu kifo?” Qasim (a.s) akajibu:
“Kifo katika macho yangu ni kitamu kuliko Asali.” (Mawassae Kalemat Imam Hussain, uk. 402) 144
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 145
Maadili Ya Ashura
Aina hii ya uimara, uvumilivu na ghera inaitwa Subira, ambayo huchukua kifo kwa kukiona kuwa ni kitamu kuliko asali. Hapana shaka kwamba katika uwanja wa subira Imamu Husein (as) ni sehemu ya kingezo, ni Kiongozi wa Subira, na akili za walimwengu zimeduwazwa na Subira yake.
145
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 146
Maadili Ya Ashura
Maadili ya saba Ghera na Heshima (Ghairat) 1. Ghera na Heshima (Ghairat) – Maadili ya Ashura..........................................147 2. Maana ya Ghera na Heshima ........................................................................148 Haram na Harim Adabu za Ardhi Tukufu ya Allah (s) Adabu za Msimu Mtukufu wa Allah (s) Mahram na Na-Maharam Adabu za Dhati Tukufu (Haram-e-Dhaati) za Allah (s) Mwanadamu – Udhihirisho wa kilele cha Utukufu wa Mungu Ghera na Heshima- Matokeo ya Wageni
148 149 150 150 151 152 153
3. Tofauti kati ya “Kupendelea katika Ujinga” na Heshima................................153 4. Ni Mtu gani mwenye kujiheshimu zaidi?........................................................154 5. Ghera kwa ajili ya Dini– Msingi kwa Ghera nyingine na Heshima................157 6. Vilele vya Ukosefu wa Aibu- Mifano..............................................................157 7. Imamu Husein (a.s) – Kigezo cha Wajibu cha Ghera na Heshima.................159 8. Abbas (a.s) – Kilele cha Utii na Ghera na Heshima (Ghairat)........................160
146
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 147
Maadili Ya Ashura
1. Ghera na Heshima (Ghairat) – Maadili ya Ashura Moja ya maadili muhimu ambayo Kiongozi wa Mashahidi (as) aliyatetea na kuyahuisha kwa damu yake sambamba na maadili mengine ni Ghera na Heshima. Wakati kila mmoja alipokuwa amejiingiza katika maovu ya kutokuwa na aibu, Yeye (as) aliwasha taa ya dini na Heshima ya uungu ndani ya giza hili la utovu wa aibu. Kama Ashura isingetokea, basi leo jina la maadili hii ya Ghera na Heshima lingepotea daima; hivyo bila shaka yoyote, Ghera na Heshima yaweza kuchukuliwa kama Maadili ya Ashura. Allah ametoa sifa hii kuipa silka ya asili ya mwanadamu na mfumo wa kiumbo kwamba kwa kuzaliwa, mwanadamu anazaliwa na Heshima. Katika Qur’ani Tukufu, miongoni mwa mafundisho ya dini na maadili ya uungu, yaliyohubiriwa na kuhuishwa na Mitume, Ghera na Heshima ni ya muhimu zaidi, lakini kama yalivyo maadili mengine ambayo yamekanyagwa na kupoteza maana zao, Ghera na Heshima vilevile haikuwa salama. Pia zimepoteza ari yao, zilikanyagwa na kuwa muathirika wa upotofu. Imamu Husein (as) alishuhudia kwamba Ghera na Heshima, vimepoteza ari yao miongoni mwa watu na katika jina la Heshima uovu ulikuwa ukitokea. Ghera na Heshima, ambayo ilikuwa maadili ya Qur’ani na sifa ya mbinguni, imegeuzwa kwenye uovu miongoni mwa maovu yaliyomo kwa wanadamu, na uovu huu ulijulikana kama “Upendeleo katika Ujinga”. Imeainishwa katika Qur’ani Tukufu, hadithi na katika mwenendo wa Maasumin (as) kwamba wakati mwingine watu wana hatia ya maovu katika jina la Heshima. Hivyo, watu waliweka jina la “Kupendelea Ujinga” kama Ghera na kujiona wenyewe wenye Heshima. Upendeleo, iwapo ni wa kiasi kidogo au kikubwa, upo sio tu kwenye jumuiya, bali kwa kila mwanadamu katika muundo mmoja au mwingine. Watu wanafuata upendeleo na uzalendo pofu wakiyafikiria haya kama Heshima, ingawa hayana sifa zozote za watu wenye Heshima na wala hakuna matendo yoyote yanayofanana na yale ya wenye Heshima. Wakati mwingine watu wanakuwa na baadhi ya sifa za uovu na kisha ili kuzihalalisha sifa hizi huzihusisha na jina la baadhi ya maadili mema, lakini kwa kuyapa jina hayawi maadili mema, hubakia kama sifa hasi na uovu tu. Kiongozi wa Mashahidi (as) alishuhudia kwamba watu walikuwa wakijishughulisha na upendeleo na uzalendo pofu badala ya Heshima na wameupa upendeleo na 147
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 148
Maadili Ya Ashura uzalendo pofu jina la Heshima. Wakati alipoona kwamba watu hawakujitenga tu wenyewe na Ghera na Heshima, bali vievile wamejitenga wenyewe na maadili yote yale ambayo yalikuwa ni matokeo ya Ghera na Heshima, aliirudisha Ghera na Heshima kwenye uhai kwa kampeni ya damu katika ardhi ya Karbala na akahuisha roho ya maadili haya yaliyovunjwa, na hivyo kuiwasilisha kwenye ubinadamu wote katka muundo sahihi. Yeye (as) alisema:
“Nataka kuamrisha mema na kukataza maovu” (Mawassae Kalamate Hussain, uk. 291) Hii maana yake ni, nataka Kuamrisha mema na Kukataza maovu. Na maadili iliyo muhimu zaidi ni Ghera na Heshima. Kwa hiyo, ili kuyahuisha maadili haya, yeye (as) alianzisha mageuzi dhidi ya uovu. Tunaweza kwa furaha kabisa kueleza kwamba miongoni mwa maadili na sifa za Ashura na Imamu Husein (as), Ghera na Heshima ni maadili muhimu.
2. Maana ya Ghera na Heshima (Ghairat) Neno “Ghairat” limetokana na neno “Ghair” ikiwa na maana ya mgeni au mtu wa nje. Siku zote Ghairat itatajwa kwenye muktadha pamoja na baadhi ya watu wa nje au jina na athari za watu wa nje kuwepo kwenye kitu fulani. Kama hakuna dokezo la watu wa nje katika muktadha wowote, basi suala la Ghera na Heshima (Ghairat) pia halimo humo. Ili kuelewa uhusiano kati ya “Ghair” (wa nje) na “Ghairat” (Ghera na Heshima) tunahitaji kupitia baadhi ya fafanuzi.
I. Haram na Harim Mwanadamu katika maisha yake ana vitu fulani, ambavyo kiupekee huhusika na mtu mwenyewe. Huhifadhi vitu hivyo kwa kiasi cha upekee kwa ajili yake mwenyewe kwamba hawezi kuvumilia aina yoyote ya uingiliaji kutoka kwa mtu yeyote yule na hayuko tayari kukubali mtu yeyote wa nje kudai haki juu ya vitu hivi. Allah vilevile ameanzisha vitu fulani kwa kila mwanadamu ambavyo ni vya pekee kwa ajili yake tu na mtu yeyote au mtu wa nje hana ruhusa ya kuingilia kwenye vitu hivyo. Allah ameweka maeneo kwa ajili ya vitu hivi mahususi, ambavyo vimefanywa vya kipekee kwa watu binafsi. Maeneo yaliwekwa na katika fasihi ya Kiarabu maeneo 148
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 149
Maadili Ya Ashura kama hayo ya kiupekee huitwa “Harim.” Katika lugha ya Kiarabu kuta nne za nyumba pia huitwa “Harim”. Tunajenga kuta nne za nyumba ili kuzuia nyendo za wageni na kuhakikisha kwamba watu wa nje hawaingii nyumbani bila ruhusa. Kuta hizi nne huzuia watu wa nje kuingia kwenye maeneo ya nyumba, na hizi kuta nne huitwa “Harim.” Kwa dhana hii ya “Harim”nchi inagawanyika katika sehemu mbili, moja ndani ya maeneo; yaani ndani ya “Harim” na nyingine nje ya “Harim.” Wageni wanaelekezwa kukaa nje ya “Harim” hii na hawaruhusiwi kuingia ndani ya kuta hizi nne (yaani, “Harim”) kwa sababu ndani ya “Harim” hii imewekwa kipekee na mahususi na Allah kwa ajili yangu. Hivyo eneo hili wamekatazwa wageni kuingia humo. Vitu hivyo ambavyo vinaangukia kwenye eneo linalozungukwa na “Harim” hii hujulikana kama “Haram” na vile vitu vinavyobakia nje yake huchukuliwa kuwa nje ya “Haram”. Wale watu ambao wamepewa ruhusa ya kuingia ndani ya “Harim” ni “Mahram” (wenye kufahamiana) na wale ambao hawaruhusiwi kuingia kwenye maeneo ni “Na-Mahram” ( wageni).
II. Adabu za Ardhi Tukufu (Haram e Makani) ya Allah (s) Baada ya mjadala juu ya ”Haram” na “Harim”sasa lazima uwe na uwezo wa kutambua kwamba wakati unasafiri kwenda Makka kwa ajili ya Hijja mara tu unapokuwa unatembea katika ardhi ya jangwa unasimamishwa na kuambiwa kuvua viatu na kubadilisha nguo na kuvaa vazi liitwalo “Ihram” (vazi maalumu kwa ajili ya Hijja). Baada ya hilo unapata ruhusa ya kuendelea. Unaweza ukashangaa na kuanza kuuliza, “Ewe Allah! Nilikuwa natembea siku zote katika ardhi hii ambayo nimeizoea, lakini kwa nini nilisimamishwa na kuambiwa nivue viatu na kubadilisha nguo zangu zote za dhambi, kila kitu nilichokuwa nimevaa kiliondolewa ili niweze kuwa huru kuvaa hii “Ihram” na kuendelea mbele?” Jibu kutoka kwa Allah linakuja: “Ingawa ardhi hii inaonekana ya jangwa yote hufanana. Na ardhi iliyoko mbele yako pia ni sehemu ya jangwa hili hili, lakini sasa ardhi iliyoko mbele ni ardhi ile ambako Allah ametengeneza “Haram” Yake, ametengeneza kuta nne zenye nguvu kuizunguka. Eneo ndani ya mpaka huu wa kuta nne zenye nguvu limeitwa “Haram” na ardhi nje yake inajulikana kama “Hill” (nje ya maeneo). Unaruhusiwa kufanya chochote unachotaka kufanya nje ya “Harim”, lakini mara unapoingia kwenye “Harim” unaweza kufanya tu kile tutakachokuruhusu kufanya, utavaa tu aina ya vazi ambalo tumekuruhusu, vaa viatu vile ambavyo tunakuambia kuvaa, na ni baada ya hapo ndipo unaweza kuja, lakini kwa nia ile tunayokutakia hivyo. Ardhi ndani ya “Harim” huwa “Haram” na mahususi kwa watu wanaofahamiana (Mahram) tu, wakati ambapo ardhi nje ya “Haram” inakuwa Isiyo-Haram na ni 149
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 150
Maadili Ya Ashura kwa ajili ya watu wageni (Na-Maharam) tu. Watu wageni wanaruhusiwa kuvaa chochote watakacho, lakini wanatakiwa kusimama nje ya maeneo (Haram) ambayo yameitwa kwa jina la “Na-Mahram” (watu wageni). Ardhi ya “Haram” humaanisha ile ardhi inayoizunguka ambayo kuna mipaka ili kwamba ardhi ya nje na ya ndani iweze kutenganishwa, hivyo, kanuni na sheria ni tofauti kwa ardhi ya nje na ya ndani ya “Haram.” Unaweza kufanya mambo fulani ndani ya “Haram” wakati ambapo unafanya mambo mengine nje yake. Ili kuingia ndani ya “Harim” lazima uvae mavazi mahususi yajulikanayo kama “Ihram.” Wale ambao wanapewa ruhusa ya kuingia ndani ya “Harim” ni “Mahram” (waliojizoesha nayo) na wale ambao wanazuiwa kuingia ndani ni “Na-Maharam” (wageni). Kuna vitu vingi ambavyo vinaruhusiwa kwa “Na-Maharam”, lakini kwa “Maharam” hata vitu vingi vilivyo halali vinakuwa haramu. Kwa “Mahram” vitu ishirini na nne vimezuiwa, wakati ambapo vitu hivyohivyo vinaruhusiwa kwa “NaMaharam”. Hapa ndipo tunatambua tofauti kati ya “Maharam” na “Na-Maharam”. “Maharam” ni mtu ambaye haendi karibu na vitu haramu kwa sababu kwake yeye vitu vingi halali pia vimefanywa haramu kwake, na “Na-Maharam” ni mtu ambaye si kwamba haviendei tu vitu halali, bali pia huchukua vitu haramu. Vivyo, ili kuingia maeneo ya “Harim” ya Allah vitu vingi halali pia lazima viepukwe na ni muhimu kufuata adabu za kuingia “Haram”
III. Adabu za Msimu Mtukufu wa Allah (s) Allah pia ameanzisha “Harim” kwa misimu (yaani misimu mahususi ya mwaka). Wakati wa misimu hii vitu mahususi tu vinakuwa halali na vingine mahususi huwa haramu. Kama ilivyo katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, vitu mahususi halali kama kula huwa haramu wakati wa mchana. Huu ni msimu Mtukufu (Haram e Zaman) ambako maeneo yametengenezwa kwenye vipindi vya saa na ni wale tu ambao wanaheshimu adabu za “Harim” hizi wanaruhusiwa kuingia humo.
IV. Mahram na Na-Maharam Mtu ambaye ana uwezo wa kuingia maeneo ya “Harim” na kuzoeana na siri za “Haram” anaitwa “Mahram” au mwenyeji wa “Haram.” Mtu anayeweza kuingia ndani ya maeneo ya Allah, amekuwa “Mahram” wa siri za Allah na sasa ana haki ya kumuomba Allah na wakati Allah anapomuita hujibu kwa “Labayk, Labayk” (Niko hapa, Niko hapa). Hii ni kwa sababu sasa amekuwa mtambuzi wa siri za Allah na Allah pia hukutana naye, husikiliza maombi yake, maneno yake na kukubali maombi yake. 150
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 151
Maadili Ya Ashura Lakini, mtu ambaye hana uwezo wa kuingia ndani ya “Harim” ni “Na-Maharam” ambaye yuko nje ya “Harim” na humita Allah, humsihi, humuomba, kwa vile yeye si “Mahram” wa siri za Allah, vilevile Allah hasikilizi wito wake na maombi yake. Hata kama akipasua koo lake na kuita, Allah (s) hatamjibu. Kutoka hapa tunajua kwamba Allah hukubali tu maombi ya wale ambao ni “Mahram” wa Allah na wale ambao hawakuingia maeneo ya Allah, maombi yao hayatakubaliwa.
V. Adabu za Dhati Tukufu ya Allah (s) Allah ametengeneza “Haram” katika ardhi na akaanzisha maeneo na mipaka yake; hivyo hivyo miongoni mwa nyakati Allah ametengeneza nyakati mahususi kama “Haram” na akatengeneza maeneo kwa ajili ya nyakati hizo pia, Allah vilevile alitengeneza “Harim” na “Haram” kwa ajili ya sifa Zake za uungu na utungaji wa sheria, ambako sio kila mtu anapewa ruhusa wa kuingia na ni wale tu ambao kwa kukamilisha adabu zake wanakuwa “Mahram” wa siri Zake na wanaruhusiwa kuingia ndani. Watumwa wazuri na watakatifu wa Allah wanao uwezo wa kuingia “Harim” hizi. Wale ambao sio tu wanajiepusha kutokana na vitu haramu; bali vilevile hawaendi karibu na vitu vingi vilivyo halali; wanakuwa “Mahram” wa siri na wanaweza kuingia ndani ya “Harim” hizi takatifu. Allah ameanzisha “Haram” kwa ajili ya Dhati Yake pia, ambako hakuna mtu anayeruhusiwa kuingia humo.
“…Na anawatahadharisha Mwenyezi Mungu na Yeye Mwenyewe…” (Surah Ale Imran, Ayah 30) Allah ameanzisha “Haram” kama hizi kwa ajili ya Dhati yake ili hata jina la mgeni au watu waliotengwa hawavumiliwi hapa. Hataki yeyote kuwepo katika Dhati Yake Tukufu (Haram-e-Dhaati). Kwa hiyo, Amesema kwamba wakati unapotaka kuniabudu Mimi basi niabudu Mimi tu. Kama ukija ndani ya maeneo ya Dhati Yangu na wakati unaponiabudu Mimi hata kama unafikiri kuhusu mtu mwingine, nitapitisha ibada zako hizi kwa mtu huyo mwingine ambaye umemhusisha na Mimi wakati wa ibada yako. Hii ni kwa sababu Mimi ni Mola Wako Mtukufu (Ghayyur) ambaye hamvumilii mgeni yeyote katika ibada zako. Fikiria tu kiwango cha Heshima (Ghairat) ambayo Dhati ya Allah inayo, ambapo haruhusu mtu yeyote kuingia kwayo, Dhati Yake imetengwa kabisa na washirika wowote. Maeneo ya 151
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 152
Maadili Ya Ashura Dhati takatifu ya Allah yako hivyo kwamba hakuna mtu awezaye kuyaingia, ingawa nafsi nzuri na takatifu zaweza kuingia ardhi takatifu na nyakati takatifu, lakini wakati inapokuja kwenye suala la “Harim” na “Haram” ya Dhati hakuna mtu mwenye ruhusa ya kuingia.
VI. Mwanadamu – Udhihirisho wa kilele cha Utukufu wa Mungu Mwanadamu ni mwakilishi wa Allah (s), mwakilishi wa majina Yake ya uungu na ni mfano na udhihirisho wa sifa za uungu katika ardhi. Moja ya majina mazuri ya Allah ni “Mwenye Kuheshimiwa”. Kwa vile Allah ni “Mwenye Kuheshimiwa” anategemea wanadamu nao pia kuwa “Wenye Kuheshimiwa.” Allah hakuwaruhusu watu wa nje kuja ndani ya “Harim” na “Haram” Yake, hivyo, anataka kutoka kwa wanadamu kufanya “Harim” na “Haram” kwa ajili yao wenyewe na kisha kuzuia watu wa nje na “Na-Maharam” kuingia ndani humo. Kwanza Allah alitengeneza “Harim” na “Haram” kwa ajili Yake Mwenyewe na kisha akawaongoza na kuwaelimisha wanadamu kuanzisha “Harim” na “Haram” kwa ajili yao wenyewe, hivyo anawaelimisha kuwa wenye kuheshimiwa (Ghayyur). Madhumuni ya kuwaita kwenye Hajji, ni kukufanya utambue maana ya “Harim” na “Haram”, na kujifundisha jinsi ya kuwa “Mahram.” Lazima ujifundishe kutengeneza “Haram” na kuwa “Mahram” ili kwamba wakati ukirudi upate kutengeneza “Harim” na “Haram” kwa ajili ya umri wako uliobakia. Lazima uwe na uwezo wa kutambua watu “Mahram” katika maisha yako na kisha kuwaruhusu tu wale “Mahram” kuingia ndani ya “Harim” yako, hivyo kutowaruhusu “Na-Maharam” kuingia kwenye maeneo ya “Haram” yako. Hijja ni somo la Ghera na Heshima, ambalo wanadamu hulipata kutoka kwa Muumba wao. Kama tukifikiria dhana ya “Mahram” na “Na-Mahram” ni kati tu ya wanaume na wanawake, kisha hili huwa ni kweli katika Sheria (Fiqh) ambako istilahi hizi zinakuwepo katika utekelezeji kwenye uhusiano kati ya wanaume na wanawake lakini kiuhalisia dhana hii hii ya “Mahram” na “Na-Mahram” hutumika miongoni mwa wanaume na miongoni mwa wanawake. Hii ina maana wanaume miongoni mwao wenyewe vilevile ni “Mahram” na “Na-Mahram” wenyewe kwa wenyewe na vivyo hivyo hutumika kwa wanawake pia. Kila mtu wa aina hiyo ambaye ana uwezo na sifa za kuingia “Harim na Haram” ya mtu mwingine na kuwa “Mahram” kwa mtu huyo, na mbali na yeye wanaume wengine wote na wanawake ni “Na-Maharam” kwake. Amri kama hizo zipo kwa ajili ya wanawake pia, yeyote awe ni mwanaume na mwanamke ambaye ana ruhusa 152
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 153
Maadili Ya Ashura ya kuingia ndani ya “Harim” na “Haram” ya mwanamke huyu anakuwa “Mahram” wake na wengine wote ni “Na-Maharam”.
VII. Ghera na Heshima (Ghairat) – Matokeo ya Wageni (Gair) Jinsi ambavyo Kujiheshimu hujitokeza kwa wageni ni watu kwanza kuanzisha “Haram” na “Harim” kwa ajili yao wenyewe, na kisha kwa hili, kuwatambua “Mahram” na “Na-Maharam.” Mtu mwenye heshima ni mtu ambaye haruhusu mgeni yeyote kuingia ndani ya “Haram” yake, na mwanamke mwenye heshima ni mwanamke ambaye hamruhusu “Na-Maharam” mwanaume kuingia kwenye maeneo ya (Harim) lake. Mtu “Mahram” anaruhusiwa kuingia ndani ya maeneo (Harim) yaliyowekwa, lakini kwa sharti tu kwamba hawi sababu ya kusumbua Heshima, lakini kama mtu “Na-Mahram” akijaribu kuingia maeneo hayo basi mtu mwenye ghera kamwe hatamruhusu kuingia, kwani maadili hii ya ghera na heshima kamwe haitatoa ruhusa ya kuingia humo. Kwa hiyo, Heshima na Ghera maana yake ni kutovumilia hata hali ya uwepo wa wageni katika “Haram” yako na “Harim”, na kwa hivyo kuwatoa nje ya mipaka ya “Haram” na “Harim” yako.
3. Tofauti kati ya “Kupendelea katika Ujinga” na Heshima. Kuna tofauti kubwa kati ya chuki binafsi, kupendelea katika ujinga na Heshima. Heshima ni maadili ya kiungu wakati ambapo uzalendo pofu na upendeleo ni yale maovu ambayo kwamba Imamu Husein (as) alianzisha jihadi yake na akasema:
“Nataka kuamrisha mema na kukataza maovu” Nimekuja kwa ajili ya kupigana na maovu, maana yake, nimekuja kupigana dhidi ya uzalendo pofu na upendeleo ambao ni maovu na kubadilisha na maadili yajulikanayo (Ma’ruf) hivyo kuhuisha maadili ya Ghera na Heshima (Ghairat). Uzalendo pofu, upendeleo katika ujinga na kuwa na chuki binafsi humaanisha kutetea na kupendelea wengine kwa kisingizio cha damu, lugha, ujima au mahusiano ya kijogorafia. Hii huonesha kwamba bila ya kutengeneza “Haram” takatifu na “Harim” kwa ajili yao wenyewe, wanadamu wanaanza kupendelea na kutetea 153
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 154
Maadili Ya Ashura “Mahram” na “Na-Maharam”, wachupa mipaka na waovu, waumini na wakanushaji, wenye uwezo na wasio na uwezo katika njia ya halali au ya haramu kwa misingi tu ya damu, lugha, ujima na mahusiano ya kijogrofia. Kwa uwazi anaelezea kwamba ni jamaa zangu, kutoka kwenye jumuiya yangu, kizazi changu, tunaishi katika mji mmoja wa nyumbani, tunazungumza lugha moja, watu wangu kwa hiyo siku zote nitawatetea na kuwapendelea. Huu ni uzalendo pofu na upendeleo katika ujinga, na sio heshima, na kwa kweli huu ni uovu. Maeneo ya “Harim” yaliyowekwa na maadili ya Heshima (Ghairat) ni matakatifu na sio kila mtu anaruhusiwa kuingia humo. Wale ambao wanaweza kukamilisha adabu za “Harim” na ni wazingatiaji kuhusu masharti yake, hawa wanaweza kuwa “Mahram” na wana ruhusa ya kuingia humo. “Na-Maharam” na wasio na uwezo watabakia nje, bila kujali kuwa wao ni ndugu, kutoka jumuiya moja, chama kimoja, na nchi moja. Wakati Imamu Husein (as) alipoona ukweli kwamba Bani Umayyah lilikuwa ni kundi lenye uzalendo pofu na upendeleo, na badala ya kuonesha Ghera na Heshima (Ghairat) walikuwa waathirika wa uzalendo pofu na kujitumbukiza sana katika upendeleo, yeye (as) aliuvunjilia mbali uzalendo pofu na kuhuisha Heshima (Ghairat). Wakati inapokuja kwenye Heshima (Ghairat) huchukulii kwenye fikra kwamba mtu fulani anatokana na jumuiya yako au anaongea lugha yako, ana uhusiano wa kiurithi na wewe, hukaa na kupitisha muda pamoja na wewe au hukusaidia na kukuunga mkono. Lakini, Ghera na Heshima hupenda kupima kwamba mtu yuko katika eneo moja kama la kwako, kwani mtu aliyeko nje ya “Harim” yako na hakamilishi adabu za “Harim” na ni “Na-Maharam” kwako, anawekwa mbali na hana haki ya kupokea upendeleo wako. Kwa kweli, hana hata haki ya kuingia kwenye “Harim” yangu takatifu kwa sababu lazima niheshimiwe (Ghayyur) na mwenye kuheshimiwa ni mtu ambaye haruhusu watu wasio na aibu (Bi-Ghairat) kuingia “Haram” yake.
4. Ni Mtu gani mwenye kujiheshimu zaidi? Mtu mwenye kujiheshimu hutengeneza “Haram” na “Harim” kwa ajili yake na “Harim” hutengenezwa tu pale ambapo utakatifu na heshima hupatikana. Neno “Haram” lenyewe humaanisha kitu chenye heshima, utukufu na utakatifu. Kwa vile ardhi hii (Kaaba) ni takatifu inaitwa “Haram”. Haturuhusu watu wasio na aibu (Bi-Ghairat) kuja kwenye maeneo matakatifu na matukufu, hivyo wasio Waislamu hawaruhusiwi kuja Makka kwa sababu yoyote kwa sababu ardhi hii ni takatifu. Sio 154
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 155
Maadili Ya Ashura hilo tu kwamba hatuwarusu wasio Waislamu kuja kwenye “Haram”, kwa kweli utukufu wa “Haram” wenyewe hauwezi kuvumilia kuwepo kwa Wasio Waislamu ndani yake; hivyo hata katika misikiti ya kawaida ambayo pia ni sehemu ya utakatifu wasio Waislamu huzuiwa kuingia humo. Kila “Haram” ina kanuni hii ya utakatifu ambayo wachupa mipaka hawaruhusiwi humo. Wakati mwanadamu anapoingia katika maisha ya ndoa vilevile nyumba yake huwa “Haram” ndogo kwa ajili yake, sasa lazima ailinde “Haram” hii na kutoruhusu mgeni yeyote kuingia ndani ya nyumba yake. Lakini kama atafungua milango yake kwa wageni wote na hamzuii mtu yeyote kuingia humo na hutoa uhuru kwa “Na-Maharam” kuingia ndani, basi kamwe hataitwa mtu mwenye heshima (Ghairatmand). Katika Hadith-e-Qudsi, miongoni mwa mafundisho ambayo Allah (s) amempa Nabii Musa (as) mojawapo ni “Ewe Musa! Mtu mwenye heshima kamwe hafanyi zinaa na kamwe hatamani kitendo kama hicho, lakini mtu mwenye uzalendo pofu na upendeleo kuna uwezekano kwake kuingia kwenye aina hiyo ya matendo (maovu).” Mtu mwenye heshima awe ni Mwislamu au asiye Mwislamu kamwe hataingia kwenye “Haram” ya mtu mwingine yeyote yule, kamwe hatapita kwenye eneo takatifu la “Haram” ya mtu mwingine yeyote yule. Kwa hiyo, mtu mwenye hashima haruhusu kuwepo na mwingilio wowote wa mgeni ndani ya nyumba yake, familia, “Haram” na “Harim” yake, lakini kama mtu atavumilia mwingilio huo basi inasemwa kwamba ni mtu asiye na aibu (Bi-Ghairat). Vivyo hivyo, kama mtu anataka kunyang’anya mali ya mtu, anataka kumuibia na mtu huyu hajaribu hata kuitetea na akaruhusu mtu huyu kunyakua mali yake na kumpora, basi pia yeye itasemwa kwamba sio mtu mwenye heshima. Hii ni kwa sababu utajiri na mali vilevile ni sehemu ya “Haram” ya mwanadamu, hivyo mtu anayeruhusu mwiingilio wa wageni ndani yake sio mtu mwenye heshima (Ghayyur). Mtu ambaye hulinda wanawake wake, utajiri, rasilimali, nyumba, familia, kila kitu katika “Harim” na havumilii mwiingilio wa wageni ndani yake huchukuliwa kama mwenye ghera kubwa na mtu mwenye heshima, kwa sababu amehifadhi utakatifu wa “Haram” yake. Dini ndiyo iliyofanya wanawake, mali, damu na undugu kuwa takatifu kwa ajili ya wanadamu. Dini hii imeanzisha utakatifu wa uhusiano wa mwanadamu na wengine wote anaohusiana nao. Mwanadamu huonesha vizuri sana ghera yake ndani ya “Haram” iliyoanzishwa na dini (yaani, ikija kwa ajili ya wanawake wa familia yake, huwalinda na kuonesha heshima yake), lakini wakati mgeni anapoingia kwenye “Haram” ya dini hii, basi kwa nini hii isiwe changamoto ya Ghera (Ghairat) ya mwanadamu huyu? 155
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 156
Maadili Ya Ashura Hapana shaka kwamba ni mtu mwenye ghera (Ghayyur), mtu ambaye kwa kuilinda “Haram” yake haruhusu mgeni yeyote kuingia ndani, havumilii kuwepo kwa mgeni yeyote ndani yake, lakini ni upi ukubwa mno wa “Haram” zote? “Haram” kubwa mno na takatifu zaidi sio wanawake wake, hivyo kama akilinda kuhifadhi usafi na utakatifu wa wanawake wake anastahiki kuwa mtu mwenye ghera kubwa mno na mwenye heshima. Kwa hakika ni mtu mwenye heshima lakini sio mkubwa mno kwa wote. Vivyo hivyo, nchi au mali sio “Haram” takatifu zaidi kiasi kwamba mtu anayezilinda anaweza kuchukuliwa kama mwenye ghera kubwa na mwenye kuheshimiwa. “Haram” takatifu zaidi na iliyo kubwa sana ni dini, ina kiwango hicho cha utakatifu ndani yake kwamba kwa ajili ya dini wanawake, mali, nchi na vitu vingine vyote kwa ajili ya mwanadamu vimepata utakatifu, kwa hiyo, mwenye ghera kubwa mno ni yule ambaye havumilii uwepo wa mgeni ndani ya “Haram” ya dini. Hachukuliwi kama mtu mwenye ghera kubwa sana na mwenye heshima yule anayemlinda mke na dada zake, bali mkubwa mno ni yule ambaye huilinda dini na kuzuia njia ya mtu yeyote anayeingilia dini. Mungu aepushie mbali, kama mwanamke wa mtu fulani kutoka kwenye familia (mke, mama au dada) ananyanyaswa kijinsia au anafanyiwa dhihaka sokoni na licha ya kuwepo pale, akaifumbia macho picha ile. Anaonesha sababu kwamba yuko peke yake, hana rafiki katika soko hili, kama akiongea inawezekana akapoteza kazi yake pia anaweza kupoteza maisha yake, kwa hili kila mmoja atasema kwamba amekosa haya. Watu wenye heshima watatoa hukumu za uchupaji mipaka na uovu dhidi yake na kumfukuza aondoke mjini pale. Watasema kwamba kuwepo kwa mtu asohaya kama huyo katika eneo hili kutaeneza uovu wa kutokuwa na aibu kwa watu wengine. Kila mtu humuita mtu asiye na aibu kama anavumilia na kukaa kimya wakati wanawake wa familia yake wanaponyanyaswa, kwa sababu mwanamke ni mtakatifu kwa ajili ya mwanaume. Lakini tumesahau kwamba utakatifu wa wanawake huja kutokana na dini. Dini inasema kwamba wanawake wenu ni watakatifu. Qur’ani Tukufu imesema kwamba wanawake ni watakatifu, hakupata hadhi hii ya utakatifu kwa yeye mwenyewe, imekuja kutokana na dini. Sasa, kama kwenye soko la wazi dini inadhihakiwa, sheria na kanuni za Qur’ani zinakufurishwa, utakatifu wote wa dini umevurugwa na katika hali kama hiyo kama mtu anafumba macho yake, akayavumilia haya na haoneshi ghera kwa ajili ya Dini (Ghairat-e-din), basi mtu kama huyo anastahiki kuitwa mwenye ghera na mwenye heshima (Ghairatmand)? Kamwe! Kwa kweli ni mtu pujufu zaidi ambaye hawezi kuzuia uingiliaji na dhihaka ambayo wageni wanaifanya katika “Haram” ya Dini. 156
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 157
Maadili Ya Ashura Sio pujufu zaidi mtu yule ambaye haoneshi ghera kwa ajili ya matusi juu ya usafi wa wanawake wake, badala yake pujufu (asiye na haya) zaidi ni mtu ambaye haoneshi ghera wakati usafi wa Dini yake unaingiliwa na kuruhusu wageni kuja ndani ya maeneo matakatifu ya dini yake. Hivyo tunajua kwamba mtu mwenye ghera zaidi na mwenye heshima ni mtu ambaye ana Ghera (Ghairat) kwa ajili ya kuilinda Dini na mtu pujufu zaidi ni mtu ambaye hajali heshima (Ghairat) ya Dini.
5. Ghera kwa ajili ya Dini – Msingi kwa Ghera nyingine na Heshima. Ni hakika kwamba mtu ambaye hana Ghera kwa ajili ya Dini hataonesha ghera hata wakati ikija kwa ajili ya wanawake zake. Mtu ambaye anaonesha ghera kwa ajili ya dini anaweza tu kuonesha maadili ya ghera kwa ajili ya wanawake zake; hii ni kwa sababu usafi wa wanawake unatokana na dini, na mtu ambaye hawezi kuilinda dini yake hawezi kuwalinda wanawake zake pia. Vivyo hivyo, taifa pia ni “Haram” na “Harim” kwa ajili ya wanadamu, lakini mtu ambaye hawezi kuilinda dini yake, je, anaweza kulilinda taifa lake? Mtu ambaye hana Ghera kwa dini yake kamwe hawezi kutegemewa kulinda taifa na jumuiya yake, mtu ambaye hawezi kuonesha ghera kwa ajili ya dini hawezi kuonesha heshima kwa chochote kile. Leo tunaona jinsi wageni walivyoingia kwenye maeneo ya “Harim” zetu, wakiharibu na kusababisha maovu kwenye maeneo yetu matakatifu, lakini tumekuwa wanyonge kiasi kwamba hatuna hata uwezo kulinda maeneo matakatifu ya jumuiya zetu; hii ni kwa sababu ghera ya dini imetoweka kwetu.
6. Vilele vya Ukosefu wa Aibu (upujufu) (Bi-Ghairati) - Mifano A. Mfano wa Kwanza Miaka michache iliyopita kulikuwa na kauli iliyotolewa na Amerika wakati wa majadiliano juu kukamatwa kwa Aimal Kansi. Wakati wale waliomkamata kule Baluchistan walipoulizwa jinsi walivyoweza kumkamata na kumleta Amerika, walijibu kwamba waliweza kufanya hilo kwa ushirikiano wa watu wa Pakistan. Tulimshika kwenye ardhi ya Pakistan, na tulifanikiwa kumkamata kwa kuwapa dola elfu ishirini kwa baadhi ya watu wa Pakistan ambao walitupa ushirikiano na kutupatia taarifa zote. Mmoja wa waulizaji maswali katika usaili huu alisema ni upuuzi kutumia dola ishirini elfu kwa ajili ya kukamata jasusi na vilevile ni hasara kwa hazina ya Amerika, sasa kwa nini mmetumia dola ishirini elfu? Pia alisema kwa uwazi kabisa katika mahojiano hayo kwamba jumuiya ya Pakistan ni ile 157
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 158
Maadili Ya Ashura ambayo kwa dola mia moja tu wanaweza kutoa hata wanawake wao, dola hamsini tu zilikuwa zinatosha na zaidi kuweza kupata taarifa za kijasusi kutoka kwao. Enyi ambao mna Ghera (Ghairat) kwa ajili ya taifa! Enyi ambao ni wadai wa Ghera kwa ajili ya jumuiya! Enyi ambao mnatoa kaulimbiu za ukomunisti na lugha! Enyi ambao mnatoa kaulimbiu za Pakistan! Mmeipotezea wapi heshima yenu (Ghairat)? Watu hawa wageni wameingia ndani zaidi ya maeneo (Harim) yenu kiasi kwamba wamewafedhehesha wanawake wenu, lakini hakuna hata neno la upinzani kwa hili, yote haya ni kwa sababu watu wamejitoa wenyewe kwenye Ghera na heshima ya Dini (Ghairat-e-Din). B. Mfano wa Pili Mhalifu zaidi wa ulimwengu huu aliyedhalilika na muuwaji mkubwa (Rais mstaafu wa Amerika, Bill Clinton), alikwenda ziara ya utalii katika baadhi ya nchi, ambazo ilijumuisha Bangladesh, India na halikadhalika Pakistan. Alikaa kwenye vituo vyenu vya TV na akawadhihaki. Alipinga Heshima yenu (Ghairat), juu ya vitu vile ambavyo mnaonesha kujiheshimu kwavyo, wakati ambapo anapinga vitu vile kutoka kwenye njia zenu, kutoka kwa wazungumzaji wenu na kutoka kwa watu wenu na hakuna hata aliyetoa kauli ya Ghera hapa. Enyi mlio na Ghera kwa ajili ya taifa! Lazima mtambue kwamba kama hamjali utakatifu wa nchi (Pakistan), ambayo ilifanywa takatifu na Dini, basi nchi hii pia haiwezi kuwa takatifu kwa ajili yenu.
Kiuhalisi mnajiingiza katika usaliti na nchi hii, pamoja na jumuiya hii na taifa hili. Yote haya ni kwa sababu ninyi ni wasaliti wa Dini, na kwa kuwa kwenu wasaliti wa dini maana yake ni usaliti kwa vitu vingine vyote. Tumewavumilia wageni hawa kwa kiasi kwamba wanakuja na kukaa kwenye vituo vyetu vya TV, kufedhehesha na kuidhihaki jumuiya na Dini yetu na hata baada ya hili tunajiita wenyewe wenye Ghera Heshima (Ghuyyur). Ole wenu juu ya Heshima kama hiyo, kama hii ni Heshima (Ghairat), basi upujufu ni upi? Kama mtu anaweza kujenga nyumba ambayo kwamba kila mtu anaweza kuingia humo na kufanya atakalo, na kisha mtu huyu anatoka nje na kutoa hutuba kwamba sisi ni watu wenye heshima (Ghayyur), tutayaondoa macho yale hata ya wale ambao wanathubutu kuangalia taifa letu, tutang’oa ndimi zile za ambao wanaongea dhidi ya taifa letu, kama tabia hii inajulikana kama ghera na heshima basi upujufu (Bi-Ghairti) ni upi? Kama kweli unataka kujifundisha na kuijua Ghera ni nini, basi njoo na ujifundishe kutoka kwa Husein (as). Usiwalaghai watu kwa jina la uzalendo pofu. Usilete 158
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 159
Maadili Ya Ashura Upendeleo katika ujinga (Haamiyat-e-Jaahilya) badala ya Heshima (Ghairat). Heshima huja tu wakati mtu ana “Harim” na “Haram” yake na kisha hamvumilii mgeni yeyote humo. Dini yetu imetuambia kwamba lazima uwe na “Haram” ambayo ina baadhi ya Mahram na baadhi ya Na-Maharam ya kutembelea humo. Usiwaruhusu Na-Mahram kuingia kwenye “Haram” yako, hivyo ni mpaka na iwapo una “Haram” kwa ajili ya Dini yako, “Harim” na “Haram” kwa ajili ya taifa haitakuwa salama, na wala “Haram” za familia na jumuiya hazitakuwa salama. C. Mfano wa Tatu Leo hata chakula chetu, familia na kuta nne za nyumba zetu haziko salama; wageni wameingia na wamefika mpaka kwenye meza ya chakula na hata mpaka kwenye chumba cha kulala. Leo wakati ukifunga milango ya chumba cha kulala, usifikiri kwamba umekifunga na kwamba hakuna mtu atakayeingia humo. Umefunga tu kuzuia vumbi na uchafu; wageni wameweka ibada zao, desturi zao, utamaduni wao wote, tabia mbaya, maovu, ukaaji uchi, dansi, nyimbo na kila kitu chao ndani ya chumba chako cha kulala. Sasa hata chumba chako cha kulala hakiko huru kutokana na mikono na uingiliaji wa wageni. Kuvumilia kuwepo kwa wageni usiku mzima (kweye TV), hii ni Heshima (Ghairat) au upujufu? Wakati wanaingia kwenye nyumba kiasi hicho kwa ndani sana hadi kufika kwenye chumba cha kulala, wakati baba, bint, mama, mke na dada wote wamekaa pamoja na kuangalia picha za aibu, hivyo watu hawa wana Heshima (Ghayyur)? Ukosefu huu wa aibu umetokea wapi? “Haram” inayoheshimiwa zaidi (Dini) ambayo imetufundisha sisi heshima (Ghairat) inapuuzwa na watu. Kuanzia siku tuliyovumilia kuwepo kwa wageni katika Dini yetu, tulifungua milango ya dini kwa ajili ya wageni, kuanzia siku ile na kuendelea mambo yote haya ya aibu yaliingia kwetu. Wakati wageni hawa walipoona kwamba hatuwezi kulinda “Haram” muhimu zaidi ya Dini, kwa urahisi kabisa walichukua udhibiti wa “Haram” nyingine ndogondogo pia. Hivyo mtu ambaye hawezi kulinda dini yake kutokana na wageni, “Haram” ya mke wake, mama yake. Dada yake na bint yake naye pia hatakuwa salama. Utakatifu wa nyumba yake na mke wake kamwe hauwezi kuwa salama kutokana na mikono ya wageni. Wageni hawa wamekuja na kusababisha kufuru kwenye utakatifu wa “Haram” zetu zote, waliingia ndani kwa jinsi watakavyo na kueneza utamaduni wao na desturi zao. Je, hii ni Heshima (Ghairat) au upujufu? 7. Imamu Husein (a.s) – Kigezo cha Wajibu (Uswa) cha Ghera na Heshima (Ghairat) Wakati Imamu Husein (as alipoona kwamba maadili ya Ghera na Heshima yame159
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 160
Maadili Ya Ashura toweka, alitambua kwamba kuna haja ya kuyahuisha. Hii ni kwa sababu ni mpaka Ghera na Heshima iwapo hazijihuishi zenyewe ndani ya mwanadamu, maadili mengine vilevile hayatakuwa na nafasi kwayo, kwa hiyo, Imamu Husein (as) alionesha Ghera na Heshima (Ghairat). Ingawa watu wengi wakati huo walikuwa wanafikiri kwamba utakatifu wa nyumba zao, misikiti yao na sala zao vyote vilikuwa salama na kwamba wao pia walikuwa salama na ibada zao pia zimelindwa. Katika mawazo haya hata “Harim” (wanawake) wa Imamu Husein (as) walikuwa salama. Nani mwenye moyo hata wa kuwaangalia mabinti wa Imamu Husein (as) mjini Madina? Ilikuwa ni watu hawa wa nyumba hii kwamba wakati vijana wa Bani Hashim kama Abbas (as) na Ali Akbar (as) walikuwepo, ambao walithubutu hata kuwaangalia “Harim” wa Imamu Husein (as). Dada na mabinti wa Imamu Husein (as) walikuwa salama kabisa, lakini basi nini kilichomfanya Imamu Husein (as) abadilishe hali hii ya usalama kuwa kwenye hali isiyo salama? Kwa nini aliitoa familia yake nje ya usalama wa Madina na kuipeleka kwenye uwanda wa Karbala na kuwaweka kule kwenye mahema? Imamu Husein (as) angejibu hivi: “Wanawake (Harim) wake hapana shaka walikuwa salama na kulindwa mjini Madina, lakini “Haram” ya Allah (s) haikuwa salama, wageni wameingia kwenye dini ya Allah, muda wageni hawa wamo ndani ya dini ya Allah (s), heshima (Ghairat) ya Husein haimruhusu kutodhihirisha Ghera kwa ajili ya Dini (Ghairat-e-Din), inawezekanaje nisifanye juhudi kuikoa “Haram” ya Dini? Sababu ya kwa nini nimeigeuza familia yangu iliyo katika hali ya salama na kuiweka katika hali isiyo salama katika uwanda wa Karbala, ni kwa ajili ya kuikoa “Haram” ya Dini.” Kwa hiyo, anasema kwamba usalama wa “Haram” yangu unawezekana tu wakati “Haram” ya Dini ya Allah (s) inapokuwa salama. Hii ni Ghera na Heshima (Ghairat) ambayo kwamba haivumilii mgeni yeyote wa nje kuingia katika dini, kutovumilia wageni kuja kwenye Uislamu na “Haram” ya Dini yetu. Hii ilikuwa Ghera na Heshima ambayo kwamba Imamu Husein (as) alionesha na alitoa somo la Ghera na Heshima, akafundisha Ghera na Heshima na kwa hiyo Imamu Husein (as) ni Kigezo cha Wajibu (Us-wa) na bora kwa ajili ya Ghera na Heshima (Ghairat), ni mwanadamu mwenye Heshima (Ghayyur) zaidi.
8. Abbas (a.s) – Kilele cha Utii na Ghera (Ghairat) Abbas (as) alikuwa mfano wa utii na Ghera na Heshima (Ghairat). Utii wake peke yake ulikuwa Ghera. Kwa vile Abbas alikwa mwenye heshima (Ghayyur) ya hali ya juu, alithibitisha pia kuwa ni mwenye utii sana na utii wake ulikuwa ni matokeo ya Heshima yake. Ghera yake ilikuwa haikukomea kwenye kweli kwamba hakuna mtu aliyeweza kumuangalia Zainab na Ummu Kulthum (as), hakuna awezaye 160
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 161
Maadili Ya Ashura kumuangalia Fatima (as) na Sakina (as), au kwa dada yeyote mwingine au binti wa familia yake, lakini kwa kweli Heshima yake ilikuwa kwenye kiwango kwamba hakuna mtu yeyote awezaye hata kutazama dini kwa macho maovu. Kwa vile Abbas (as) ni mwenye Ghera na Heshima ya hali ya juu, ni wale tu ambao wana maadili yanayofanana ya Ghera na Heshima kama yale ya Abbas (as) wanaoweza kuwa wafuasi wake wa kweli. Mtu ambaye moyo wake unaopiga kama ule wa Abbas (as), mtu ambaye ana aina ileile ya utii, ana haki ya kuhusisha jina la Abbas (as) na yeye mwenyewe. Imamu Husein (as) hakumchukua Abbas (as) kuwa naye kwa ajili tu ya kulinda “Harim� ya familia yake, bali alimchukua kwa ajili ya kulinda Dini ya Allah. Ali (as) alifanya maandalizi kwa ajili ya mazazi ya Abbas (as) na alimuomba ndugu yake Aqil kumtafutia mwanamke kutokana na kabila lenye ari zaidi la Kiarabu. Nataka azae mtoto mwenye ari ambaye atakuwa mwenye heshima na utii, na ambaye mara moja atayaondoa macho ya wale ambao huthubutu hata kuangalia kwa ubaya dini ya Allah. Nataka mtu wa umbo la Ghera na Heshima, na utii, na kwa hili Ummul Banin (as) alipatikana. Ummul Banin (as) alikuwa pekee aliyeweza na kupitia kwake Allah (s) alimpa Ali (as) mwili wa Ghera na Heshima (Ghairat). Hivyo ili kuhuisha Heshima ya Dini (Ghairat-e-Din), Imamu Husein (as) alitoa muhanga mtu mwenye ghera kama huyu kama Abbas (as). Kama watu wenye ghera kama Abbas (as) wasingetolewa muhanga maisha yao kwa ajili ya dini, kusingalikuwa na kitu kama Ghera na Heshima ya Dini (Ghairat-e-Din) leo, hata kwa ajili ya jina. Abbas (as) alikuwa udhihirisho wa kilele cha Ghera na Heshima. Kwa hakika kilichomuweka Abbas (as) mnyenyekevu na mtiifu kamili kwa Imamu Husein (as) mpaka mwisho ilikuwa ni Ghera ya Abbas (as). Ghera ya Abbas (as) haikuweza kuvumilia uingiaji wa wageni kwenye dini; hivyo kwa kutoa muhanga maisha yake alihuisha Heshima ya Dini, ya wanawake na vitu vingine vyote.
161
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 162
Maadili Ya Ashura
Maadili ya Nane Utakatifu wa Mambo. 1. Mwenendo wa Imamu Husein (a.s) na vita vya maadili.................................163 2. Maana ya Utakatifu (Taqaddus).......................................................................163 3. Kukanyagwa kwa Utakatifu.............................................................................164 4. Aina tofauti za Utakatifu..................................................................................166 5. Utakatifu wa Msikiti........................................................................................167 6. Utakatifu wa mikusanyiko ya Maadhimisho (Majalis)....................................167 7. Utakatifu wa Mimbar.......................................................................................168 8. Mfano wa kilele cha kufuru kwa utakatifu wa Mimbar..................................170 9. Kufuru kwa Utakatifu wa Ali (as) ni kufuru kwa vitu vyote vitakatifu..........171 10. Kufuru ya njia na madhumuni.......................................................................173 11. Imamu Husein (a.s) – Mto wa utukufu wa utakatifu.....................................174 12. Karbala – Njia ya Mbinu Takatifu.................................................................175 13. Maadili ambayo yalihuika kutokana na mkutano wa Imamu Husain (a.s) na Juhfi.........................................................................177 14. Hitimisho........................................................................................................181
162
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 163
Maadili Ya Ashura
1. Mwenendo wa Imamu Husein (a.s) na mapambano ya Maadili Imamu Husein (as) alisema: “Naanzisha mageuzi haya kwa ajili ya Amr Bil Ma’ruf na Nahi Anal Munkar”
“Nataka kuamrisha mema na kukataza maovu” (Mawassae Kalemat Imam Hussain (a.s), uk. 29) “Ma’ruf” ni maadili yale ambayo yameanzishwa na Qur’ani Tukufu kwa ajili ya wanadamu, na “Munkar” ni zile sifa duni, pujufu na sifa ambazo Allah (s) amezitangaza kama haramu kwa wanadamu. Imamu Husein (as) alihuisha maadili ya “Ma’ruf” na akavunjilia mbali maadili ya “Munkar.” Hii ndio maana maadili ya “Ma‘ruf” hujulikana kama “Maadili ya Ashura,” kwa sababu yaliwasilishwa na “Ashura”, “Ashura” ambayo ilipulizia roho ya uhai kwenye maiti ya maadili ya “Ma’ruf” na kuyashinda maadili ya “Munkar.” Historia ya maadili imejaa taarifa za kupanda na kushuka. Ili kushinda vita hivi vya maadili ni muhimu kufuata mwenendo wa Imamu Husein (as) hivyo kwamba wanadamu waweze kuyahuisha maadili ya “Ma’ruf” na kutokomeza maovu (Munkarat). Imamu Husein (as) alithibitisha kupitia mwenendo wake mtukufu jinsi ya kupigana vita vya maadili na pia jinsi ya kushinda. Yeye (as) aliona kwamba kwa muda tu wa nusu karne baada ya tangu kufariki Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), mfumo wa maadili umebadilika, watu wamesahau maadili ya “Ma’ruf” na pahala pake walikuwa wamejiingiza katika maovu (Munkarat). Kutoka miongoni mwa maadili haya moja ya maadili muhimu ambayo si tu imekanyagwa chini, bali kwa hakika imegeuzwa kuwa ya uovu ilikuwa “utakatifu wa mambo” (Taqaduss-e-Umuur). Njia za uovu na chafu zilitumiwa na watu kwa ajili kufanya mambo matakatifu, na leo pia hali kama hiyo ipo. Maadili haya yamepatwa na ufisadi ndani ya wanadamu kwa kiasi kwamba sio umuhimu wake tu bali hata maana yake pia imepotea. Jamii ya wanadamu imepatwa na ombwe la maadili kama haya na kwa hiyo Imamu Husein (as) alihuisha maadili haya na kwa kadhia ya Karbala, kutoka Madina mpaka jioni ya siku ya Ashura, utakatifu unaonekana kwenye kila hali.
2. Maana ya Utakatifu “Quddus” ambayo maana yake ni toharifu, tukufu zaidi au takatifu, ni moja ya 163
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 164
Maadili Ya Ashura majina mazuri ya Allah na limejumuishwa miongni mwa majina mengine mazuri katika. Maana halisi ya neno “Taqaddus” ni kutoharisha kitu, kuondoa, uchafu na kasoro kutoka kwenye kitu. Hii ni maana ya “Tasbih” pia, mbali na tofauti nzuri asili na maana ya maneno “Taqadddus” na Tasbih” ni sawa. Utakatifu (Taqaddus) umeanzishwa na Allah kama maadili ya wanadamu ili kwamba mtu pia aweze kuwa mtakatifu na kuheshimu Utukufu na Utakatifu wa dhati ya Allah (s). Lazima amtukuze Allah bila ya kufikiria uchafu wowote katika dhati Yake, kamwe asihusishe kasoro zozote pamoja naye. Mwanadamu lazima alete tu vitu vitukufu na vilivyotoharishwa mbele ya Allah, kama akiwasilisha vitu vilivyochafuliwa na vitu viovu basi utakatifu (Taqaddus) utakuwa umepotezwa. Sio kwamba mwanadamu huwasilisha tu matendo ya ibada kwa Allah, hata matendo ya ibada lazima yaheshimiwe kwa kuyatoharisha kutokana na aina zote za uchafu kabla ya kuwasilishwa kwa Allah. mbali na hili kila kitu chochote kingine ambacho anataka kuwasilisha kwa Allah lazima kiwe safi na bila uchafu, hivyo kwamba kinafaa kuwasilishwa kwenye Uwanja wa Allah. Kama mtu atawasilisha uovu, vitu visivyo tohara na vichafu kwa Allah basi amepuuza utakatifu wa Dhati ya Allah na hivyo atakuwa ameukimbia utakatifu wa mambo yaliyopo. Kwa hiyo, kwa ajili ya utakatifu wa dhati ya Allah, utakatifu wa vyote na kila kitu kilichoingizwa katika mambo yetu lazima kirekebishwe. Mhimili wa mafundisho ya Mitume (as) ni utakatifu (Taqaddus) na “Tasbih” kama hii hii. Mwanadamu lazima ahakikishe utakatifu na utohara wa kila kitu ambacho anakiwasilisha kwa Allah hivyo kwamba yeye mwenyewe aweze kuwa mtakatifu na mwenye utukufu.
3. Kukanyagwa kwa Utakatifu A. Nukta ya upinzani kwa Malaika Allah alimuumba Adam (as) na kwa muda kidogo akamtambulisha kwa Malaika, kitu cha kwanza kilichokuja kwenye akili za Malaika na kukitoa kama nukta ya upinzani ilikuwa kwamba mwanadamu ni mjinga wa utakatifu au kwa maneno mengine mwanadamu sio mtakatifu. “Ee Mola wetu! (mwanadamu) hatapuuza tu kuhusu utukufu wake mwenyewe, bali halikadhalika atauvunjilia mbali Utukufu wa dhati Yako.” Wakasema:
164
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 165
Maadili Ya Ashura
“…utaweka humo watakaofanya uharibifu humo na kumwaga damu, hali sisi tunakutakasa kwa sifa zako na kukutaja kwa utakatifu wako?...” (Surah Baqarah – Ayah 30) Hii ina maana kwamba walikuwa wanasema kwamba sisi (Malaika) ndio tunaondelea kukutukuza na tunajali kuhusu Utukufu na Utakatifu Wako. Hiki ndio kitu cha kwanza ambacho kilikuja kwenye akili za Malaika kwamba inawezekana kwamba mwanadamu huenda hataweza kuwa mlinzi wa maadili haya ya utakatifu na watayatoa muhanga maadili haya kwa ajili ya kitu kingine. Waliwasilisha udhaifu wa mwanadamu kwa Allah wakisema kwamba mwanadamu hatatekeleza haki za utakatifu wa uungu. B. Majibu ya Allah kwa Malaika Utakatifu wa wanadamu ni wa msingi kiasi hicho na kitu kinachoishi kwamba Allah (s) alimtetea mwanadamu na akawaambia Malaika:
“…Hakika mimi nayajua msiyoyajua ninyi.” (Surah Baqrah – Ayah 30) Hii ina maana Allah alikuwa anasema kwamba mmepinga kwamba (mwanadamu) ataeneza ufisadi na kumwaga damu na kwa njia hii atapoteza utakatifu wake na pia kuzuia utakatifu Wangu, basi kuna ukweli ambao hamuutambui ambao kwamba Mimi naujua. Ukweli huu ni kwamba kwa umwagaji damu huu wenyewe atauweka hai utakatifu wake na vilevile ule wa Mola Wake, atakuwa mlinzi wa Utukufu wa Malaika na atathibitisha vipengele vitukufu vya kila kitu kitakatifu. Allah (s) alitoa jibu hili fupi kwa Malaika ambalo walilikubali na wakasema:
“Wakasema: Utakatifu ni Wako, sisi hatuna elimu isipokuwa ile uliyotufundisha…” (Surah Baqarah – Ayah 32) Hatujui zaidi ya hili, tutasubiri na tuone jinsi anavyochunga utakatifu wake. Sasa Malaika wanasubiri kuona jinsi mwanadamu huyu anavyokuwa mwanadamu wa kweli na kuweza kuwa mlinzi wa utakatifu wa Dhati ya Allah. kisha ukaja wakati 165
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 166
Maadili Ya Ashura ambapo Kiongozi wa Mashahidi (as) akahuisha utakatifu wa vitu vyote vitukufu, akahuisha vitu vyote vitukufu vilivyokanyagwa na hivyo Allah akakamilisha uthabiti wa maneno Yake ambayo Alisema kuwaambia Malaika:
(Hakika mimi nayajua msiyoyajua). Hii pia ilikuwa umwagaji wa damu, lakini katika umwagaji damu huu kuna utakatifu wa Allah uliohifadhiwa na vilevile ule wa mwanadamu na Malaika. Utakatifu wa maadili ya mwanadamu vilevile umepata hadhi kama hiyo kwa umwagaji damu huu wa Imamu Husein (as). Hii pia huthibitisha kwamba utakatifu ni maadili iliyo muhimu kiasi hicho kwamba imekuwa suala kubwa mno kwa wote Malaika na wanadamu, bila kujali iwapo mwanadamu ataweza kuyalinda maadili haya au la.
4. Aina tofauti za Utakatifu Kila kitu kina utakatifu wake mahususi. Msikiti, mikutano ya kidini, Kaaba tukufu, Msikiti wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na maeneo walimozikwa Maasumin (as), yote haya yana utukufu mahususi na utakatifu. Nyumba yako, wewe mwenyewe, jirani yako, kila mtu ana utakatifu wake na utakatifu wa kila kitu una aina yake mahususi. Halikadhalika ufisadi wa kila kitu vilevile ni wa tofauti na wa aina mahususi. Maji yakiwa safi ni tofauti na maji yaliyochanganyika na yasio safi. Inawezekana kwamba ni safi na yanafaa kwa wudhu lakini maji hayohayo yanaweza yasiwe mazuri kwa kunywa, au kwa njia nyingine ambapo maji huenda yakawa mazuri kwa kunywa lakini sio mazuri kwa wudhu, kama maji yaliyochanganywa na kitu kingine (kama sharubati). Daktari ndani ya Maabara anaweza akatamka kwamba maji hayana jemsi lakini maji hayo bado yanaweza kuwa na uchafu fulani ambao huyafanya maji hayo yasiwe mazuri kwa ajili ya wudhu. Aina hiyo ya maji itachukuliwa kama safi kabisa au matakatifu ambayo siyo safi tu kutokana na jemsi lakini vilevile kutokana na aina zote nyingine za uchafu. Hata kama yatakuwa safi kutokana na uchafu lakini bado jemsi wakaonekana humo, basi vilevile maji haya hayawezi kuchukuliwa kama matakatifu. Halikadhalika, utakatifu na uchafu wa nguo ni wa aina tofauti. Nguo zinazofaa kwa ajili ya swala lazima ziwe safi kutokana na uchafu lakini vilevile zisiwe za kupora. Ni maadili ya muhimu sana kwa ajili ya mwanadamu kutoa utakatifu mahususi kwa kila kitu tofauti na kuwa mlinzi kwa ajili ya kuheshimu vitu vitakatifu. Lakini 166
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 167
Maadili Ya Ashura mwanadamu amesahau maadili hii, hakuheshimu utakatifu wake mwenyewe na vilevile akaanza kuukimbia ule wa Allah. Ameyafanyia yasiyo matakatifu na machafu mambo yake yote yaliwasilishwa kwa Allah na kwa kweli kupoteza utakatifu wa vitu vyote na mambo yote. Wasiwasi huo huo ambao pole pole Malaika walikuwa nao ulianza kuonekana ndani ya wanadamu. Hii ilikuwa nukta ya upinzani wa Malaika kwamba (mwanadamu) hataweza kufanya uadilifu pamoja na kuwa na hadhi hii ya kuwa mtakatifu. Ilikuwa inadhihirika kwa matendo ya wanadamu kwamba haki hii ya utakatifu ilikuwa haitolewi, hivyo kulikuwa na haja tena ya kumfanya mwanadamu kuwa hadhiri wa maadili hii. Lakini kabla ya kuingia katika mjadala huu kwanza ngoja tuangalie vipi na wapi maadili hii ilikopotea.
5. Utakatifu wa Msikiti Msikiti ni sehemu takatifu; vilevile ni nyumba ya Allah (s) iliyobarikiwa na neema nyingi. Kila kitu ambacho hakina hadhi ya msikiti lazima kikae mbali na msikiti, na ni hapo tu msikiti huwa safi na mtakatifu. Wakati ambapo kila harakati ambayo ina hadhi ya msikiti ikifanywa ndani ya msikiti huthibitisha utakatifu wa msikiti. Sio tu kwamba kama uchafu wa kimaumbile ukija ndani ya msikiti ni kufuru kwa utakatifu wa msikiti, bali kila tendo kama hilo ambalo halihusiani na Allah likifanywa ndani ya msikiti, basi utakatifu wa msikiti umepotea. Msikiti ni sehemu ya ukumbusho wa Allah, ni sehemu ambapo maadili ya uungu lazima yawasilishwe, sasa kama mtu anaswali ndani ya msikiti kwa ajili ya kujionesha tu basi anaukimbia utakatifu wa msikiti. Kama msikiti ukibakia tupu kutokana na waabudu kutokuja kuswali humo basi huko ni kuufedhehesha msikiti. Utakatifu wa msikiti sio tu kwamba watu wanakuja na kuswali rakaa mbili na kuondoka, kama msikiti unafungwa saa ishirini na nne basi hii ni kufuru kwa msikiti.
6. Utakatifu wa Mikusanyiko ya Maadhimisho (Majalis) Kuna adabu mahususi za mikusanyiko ya maombolezo ya Imamu Husein (as), kama kitu chochote kinafanywa ambacho sio kwa hadhi ya juu ya mkusanyiko huu mtukufu basi utukufu wa “Majalis Husein (as)� utakuwa umepotezwa. Hata kama watu wamekaa katika hali ya wudhu, bado utakatifu wa mkusanyiko huu kwa ajili ya Husein (s) utapotea kama kitendo, ibada au shughuli inafanywa ambayo hailingani na madhumuni ya mageuzi ya Imamu Husein (as) na iko mbali na malengo haswa ya msingi wa Ashura na maadili ya Ashura. Maimamu watukufu (as) wametaka yafanywe mahubiri mazuri kwa kuandika Nauha na wamewapa zawadi washairi ambao wameandika na kusoma Nauha kwa ajili ya Imamu Husein (as). 167
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 168
Maadili Ya Ashura Lakini Nauha hizi zilikuwa za aina gani ambazo zilizawadiwa na Maimamu (as)? Nauha hizi zilikuwa zile ambazo zikisomwa zitaleta mapinduzi katika nyoyo za watu, kubadilisha hali ya Umma na ambazo zitatikisa mabaraza ya Bani Umayyah. Ile aina ya Nauha ambazo humuonesha Imamu Husein (as) kama mtu tegemezi na mnyonge hazipaswi kusomwa, hizi ni kufuru kwa mikusanyiko hiyo. Badala yake zisomwe Nauha ambazo huonesha na kuthibitisha Umma kuwa ni mnyonge na kwamba Husein bin Ali (as) ndiye mlezi wa Umma huu. Utakatifu wa msikiti sio kwamba tunatakiwa kukaa tu kusikiliza na mtu mmoja azungumze, bali tunahitaji kupima kile ambacho mzungumzaji anazungumza na tunasikiliza kitu gani. Kama mzungumzaji hajali kuhusu utakatifu wa mkusanyiko basi wale ambao wanasikiliza vilevile ni sehemu ya kufuru hii. Kama Hussainiyah (ukumbi maalumu kwa ajili ya maombolezo) inabakia imefungwa mwaka mzima na maombolezo hufanywa humo katika zile siku kumi tu za Muharram, basi hii nayo ni fedheha kwa utakatifu wa sehenu hizi. Kama wataalamu wakija na kukaa juu ya mimbari, wakadanganya, wakalingania watu kwenye matendo maovu, wakasababisha utengano katika umoja wa waumini na Waislamu, basi huku ni kupotea kwa utakatifu wa “Majalis” hii. Kama ilivyotajwa kabla, huu ulikuwa wasiwasi wa Malaika ambapo walisema: “Ee Allah! Mwanadamu huyu sio mtakatifu, atapoteza utakatifu Wako, atakufuru utakatifu wa waja Wako watukufu, na hatadumisha utakatifu wa misikiti na mikusanyiko mitukufu.” Allah alisema kwamba najua kile ambacho hamkitambui, baadhi ya watu wataendelea kukimbia vitu vitakatifu, lakini nitatuma baadhi ya viumbe wangu watakatifu, nitatengeneza sehemu tukufu na takatifu na nitaanzisha misimu mitakatifu. Kisha baada ya hili nitanyanyua kiumbe mtakatifu kama Husein (as) ambaye atarudisha tena utakatifu wa vitu vitakatifu uliopotea, atavifanya vitu vitakatifu kuwa vitakatifu na atavilinda vitu vyote vitakatifu.
7. Utakatifu wa Mimbari Miongoni mwa vitu vyote kimojawapo ni Mimbari, ambayo Allah ameianzisha kama njia nzuri na adhim ya kuhubiria. Kwa kuanzia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akitoa hutuba na darasa kwa kuegemea kwenye nguzo ndani ya Masjid-eNabawi. Baadaye aliamriwa na Allah kuwa na sehemu imara badala ya kuegemea kwenye nguzo. Mimbari ya kwanza katika historia ilitengenezwa na Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) na kuiweka ndani ya Masjid-e-Nabawi. Hii ni mimbari takatifu sana ambayo Mtukufu Mtume wetu (s.a.w.w.) alikuwa akikaa wakati akihutubia na kulingania mafundisho ya Kiislamu. Kufuru ya mimbari hutokea kama mazungumzo yasiyo na hadhi na utakatifu wa mimbari yatafanywa. Utakatifu wa mimbari 168
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 169
Maadili Ya Ashura hauko katika kukaa juu yake na kuzungumza kuhusu visa tofauti, bali utakatifu uko katika kuzungumza vitu vile ambavyo ni vya hadhi ile na madhumuni ya mimbari. Kama tunazifungua kurasa za historia tunaona kwamba muda mfupi tu baada ya kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) utakatifu wa mimbari yake ukaanza kupotea. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisimulia adabu, sifa na vipingele vitakatifu vya mimbari sana kabla na kwa hili vilevile alisema kwamba punde hivi utakatifu wa mimbari utapotea. Kutakuwa na wakati punde hivi tumbili wataanza kucheza dansi juu ya mimbari, wanyama kama hao watakaa katika mimbari ambao watafanana na tumbili, ambao watawafanya watu wacheke, watalaghai watu, na watapotosha watu kwa kucheza na mihemuko na hisia zao. Kisha kwa muda mfupi sana ulimwengu wote umeshuhudia kwamba tumbili wamekuja juu ya mimbari ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na mimbari ya Husein (as) aliyoachiwa na Mtukufu Babu yake (s.a.w.w.) kupitia kwa baba (as) yake na kaka yake (as) na kucheza dansi kama inavyosimuliwa katika hadithi:
Katika kitabu cha “Mustadrak”, imesimuliwa na Abu Huraira kwamba Mtukufu Mtume alisema: “Nimeona katika ndoto zangu kwamba Bani Hakam Bin Abi Aasir wanacheza dansi katika mimbari kama wachezavyo tumbili”, Abu Huraira akaendelea kusema kwamba baada ya hapa kamwe sijamuona Mtume (s.a.w.w.) akicheka mpaka pumzi yake ya mwisho. (Biharul Anwar, Jz. 62, uk. 240) Imamu Sadiq (a.s) anasema:
“Mjumbe
wa Allah (s.a.w.w.) aliona katika ndoto kwamba baada yake Bani Umayyah wamekaa katika mimbari na kupotosha watu. Alikuwa mwenye huzuni sana baada ya ndoto hii, ambapo baada ya hapo anasema kwamba Jibril (as) alishuka na kumuuliza ni kwa nini anahuzunika hivyo, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Ewe Jibril, usiku wa leo niliwaona Bani Umayyah wamekaa juu ya mimbari yangu baada ya kifo changu na kuwapotosha watu.” Jibril (as) akasema: “Naapa kwa jina la Mola Wangu kwamba Allah (s) alikutuma wewe kama Mtume wa haki na nimetengwa mbali na habari hii (yaani, Allah (s) hajawahi kumjulisha habari hii). Baada ya hili alirudi mbinguni na akashuka tena na aya anayosema kwamba: Ndoto ambayo tumekuonesha ni njia ya mtihani kwa watu, sawa na kizazi kilicholaaniwa cha mti katika Qur’ani Tukufu. Na hivi ndivyo tunavyodumu katika 169
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 170
Maadili Ya Ashura kuwaonya watu, lakini bado upotofu wao unaendelea kuongezeka. “ (Biharul Anwar, Jz. 62, uk. 240) Imamu Husein (as) mbali na kuwa tu mdhamini na mrithi wa utukufu wa dini vilevile ni mdhamini wa vitu vyote vitukufu vinayokuja chini ya uwanja wa dini. Imamu Husein (as) hakuchukua tu utakatifu wa Kaaba, Haram, Mina na Arafah, bali vilevile alichukua utakatifu wa Misikiti, Qur’ani, Dini na Mimbari.
8. Mfano wa kilele cha kufuru ya utakatifu wa Mimbar Kuna vitu vichungu katika historia ambavyo kujiheshimu kwetu hakuruhusu sisi hata kusema au kuviandika, hatuko hata tayari kusikiliza vitu hivyo, lakini historia ni kwa ajili ya kupata masomo, ni kwa ajili ya madhumuni ya kutabiri yajayo. Shahidi Muttahhari anayo maelezo ya utafiti kuhusu historia ambayo kwayo tunaweza kuamua uhalisia na filosofia ya historia. Shahidi Muttahhari anasema: “Kama Historia inahusika tu kwenye mazingira ya wakati uliopita, kama mazingira ya wakati uliopita yanasimuliwa kwa ajili ya wakati uliopita tu, basi hiyo sio historia, hizo ni hekaya tu na visa. Kama mazingira na matukio ya wakati uliopita yanasomwa kwa madhumuni ya kutambua wakati ujao, kama wakati uliopita unatumiwa kuamua njia za mbele kwa ajili ya wakati ujao, basi hii ndiyo inayoitwa Historia.” (Majmua Aasaar, cha Shahidi Muttahheri, Falsafa ya Historia, Jz. 1, uk. 130, 131, 190, 191). Hapa hatujadili (hadithi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuhusu mimbari) wakati huu uliopita kwa ajili ya wakati uliopita, au kuwasilisha hili kama kisa au hekaya fulani, lakini badala yake tunawasilisha habari iliyothibitishwa ya wakati uliopita. Ukweli huu ni kwamba baada ya miaka thelethini ya kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aina fulani ya watu walikuja, ambao walikaa juu ya mimbari ya Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) na wakamlaani Ali (as). Itifaki rasmi ilitolewa kutoka Damascus kwa makhatibu wote, Imami-Juma na Imami-Jamaat kuanza khutba zao kwanza kwa Bismillah na kisha wamlaani Ali (as). Hii ni habari iliyothibitishwa ambayo waandishi wote waaminifu Waislamu wa Shiah, Sunni, na hata wasio Waislamu wameandika kama mfano mbaya mno wa kufuru ya mimbari. Kwa takriban miaka mia moja na hamsini kitendo hiki kiovu kiliendelea, wakati mwingine kilifanywa kwa uwazi na wakati fulani kilifanywa katika hali ya kuficha. Hii iliendelea mpaka zama za utawala wa Abdul-Aziz wa 170
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 171
Maadili Ya Ashura Bani Umayyah, kisha akaumaliza uovu na utamaduni huu mchafu, lakini uliendelea katika njia ya kuficha. Sio kwamba alikuja na kuwaambia wote waliache hili na likaachwa tu, alilazimika kutengeneza sheria kwamba kitendo hiki kimekatazwa. Sasa imekatazwa kisheria kulaani, kutukana na kufanya dhihaka juu ya Ali (as). Tumbiri hawa waliokaa juu ya mimbari ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na mbele ya Umma walimtusi kiongozi wa haki wa Umma (Imam-e-Ummat), waliendelea kumlaani na Ummah huo huo uliendelea kuswali nyuma yao na kuvumilia utamaduni wa kulaani unaofanywa juu ya Ali (as). Huu pia ulikuwa wasi wasi wa Malaika: Ee Allah! mwanadamu huyu vilevile ataupoteza utakatifu wa waja Wako watukufu. Na hii imethibiti kuwa kweli ambapo utakatifu wa watu watakatifu kama Ali (as) ulipotezwa kutoka juu ya mimbari ya Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.).
9. Kufuru ya Utakatifu wa Ali (as) ni kufuru ya vitu vyote vitakatifu Vitu vyote vitakatifu vilipatwa na kufuru kwa upoteaji wa utakatifu wa Ali (as). Hii ni kwa sababu Ali (as) lilikuwa si jina la mtu fulani tu; Ali (as) lilikuwa jina la mwana wa Abu Talib (as) lakini vilevile alikuwa mlezi (Wali) aliyeteuliwa na Allah (s), alikuwa kiongozi wa Umma, mwongozaji, mawla (bwana), alikuwa mlinzi wa ufalme, Ali (as) vilevile ni mlinzi wa Umma na dini. Kama kitu kibaya kinasemwa kuhusu kiongozi wa Umma basi hii ni kufuru ya Ummah wote, ni upoteaji wa utakatifu wa dini yote na ufalme kamili. Ali (as) ni Qur’ani yenye kuelemisha, makamu wa Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) na mrithi wa Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) na vilevle mrithi wa Mitume wote (as). Kama kitu kibaya kinasemwa dhidi ya Ali (as) basi hii ni kufuru kwa Qur’ani, kufuru kwa Allah (s), Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) na kwa kweli kwa Mitume wote (as). Kwa hiyo, kama utakatifu wa mimbari ya Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) unapotezwa basi hupotezwa utakatifu wa vitu vyote vitakatifu, kwa kweli ni kufuru na kupotea kwa maadili yote. Taifa, watu vilevile wamekuwa si watakatifu kwa sababu wale makhatibu ambao walikuwa wamelishwa na Bani Umayyah walipanda mimbari na wakamlaani kiongozi wa Ummah na Ummah umekuwa ukisikiliza haya kama watazamaji walio kimya. Usikilizaji huu pia ulikuwa ni kufuru kwa utakatifu. Kama utakatifu wa kiongozi wa Ummah unapotezwa mbele ya Ummah na kwamba Umma ule baada ya kusikiliza kwa masikio yao bado wanaendelea kuswali nyuma ya makhatibu kama hao basi Umma huu unahusishwa na kufuru juu ya utakatifu.
171
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 172
Maadili Ya Ashura Amirul-Mu’mini (a.s) aliwambia masahaba zake:
Baada yangu atawekwa mtu juu yenu mwenye kinywa kipana na tumbo kubwa. Atameza chochote anachopata na atatamani kile ambacho hakipati. Lazima mumuuwe, lakini (najua) hamtamuuwa. Atawaamuru ninyi munitukane na kunikana mimi. Ama kwa kutukana, nitukaneni kwa sababu hiyo itakuwa na maana ya kunitakasa na ukombozi kwa ajili yenu. Ama kuhusu ukanusho, hamtaweza kunikanusha kwa sababu nimezaliwa katika dini ya asili (Uislamu) na wa kwanza kabisa katika kuikubali dini, na halikadhalika katika Hijra (kuhama kutoka Makka kwenda Madina). (Nahjul Balaghah, Khutba 57) Kwa muktadha wa khutba hii, Mufti Jafar Husein (ra) anaandika kwa mtu ambaye kwamba Amirul-Mu’minin (as) amedokeza, wengi wanataja kwamba ni Ziad bin Abih, baadhi wanasema ni Hujjaj bin Yusuf na baadhi wanasema ni Mughira bin Shu’ba, lakini wengi wa wafasiri wanafikiri kwamba mtu huyu ni Muawiya. Hii ni kwa sababu sifa ambazo Ali (as) ameziainisha katika khutba hii kiukweli zinachukuana na Muawiya. Ibn Abil Hadid ameandika kuhusu kula kupita kiasi kwa Muawiya na anasema kwamba Mtume (s.a.w.w.) siku moja alimuita Muawiya na akatambua kwamba alikuwa anakula chakula. Alimuita kwa mara ya pili na mara ya tatu vilevile alimtuma mtu kumuita, taarifa ikaja ileile kwamba anakula chakula. Kutokana na hili Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimlaani kwa kusema: “Ewe Allah! kamwe usilijaze tumbo lake.” Laana hii imekuwa na athari kiasi kwamba amekuwa anachoka kula na aliwaambia watumishi wake kuondolea mbali chakula hicho kwa kusema: “Wallahi, nimechoka kula lakini tumbo bado halijajaa.” (Ibn Abil Hadid, Sharh Nahjul Balaghah, Jz. 4 , uk. 55) Kitendo hiki cha kumtusi na kumlaani Ali (as) na kutoa maelekezo kwa wanachuoni wake ni miongoni mwa habari za kihistoria ambazo hakuna nafasi ya kuzikana. Maneno kama hayo yalitolewa kutoka kwenye mimbari, (maneno) ambayo yalijumuisha kufuru kwa Allah (s) na Mtume Wake (s.a.w.w.), kwa hiyo, Ummul Muminin Ummu Salma alimwandikia Muawiya:
172
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 173
Maadili Ya Ashura
“Wewe ni laana ya Allah (s) na Mjumbe Wake (s.a.w.w.) kutoka kwenye mimbari zako, hii ni kwa sababu unamlaani Ali bin Abu Talib (as) na rafiki zake. Nashuhudia kwamba Ali (as) vilevile ni rafiki wa Allah (s) na Mjumbe Wake (s.a.w.w.).� (Aqdul Farid, Jz. 3, uk. 131, katika tarjuma ya Sharh e Nahjul Balagha, tarjuma ya Mufti Jafar Hussain, Khutba ya 57, uk. 177)
10. Kufuru kwa njia na madhumuni. Mwanadamu yuko mbele zaidi katika kufuru kwenye maadili haya (Utakatifu wa mambo) kiasi kwamba alianza kufisidi madhumuni, njia za kufikia madhumuni na vitu vingine vingi, ingawa Mtume (s.a.w.w.) amemfundisha mwanadamu kuwa mtakatifu na vilevile kuweka madhumuni na malengo yake katika hali ya utakatifu. Mwanadamu alianza kuipoteza maadili hii taratibu na kwa kutumia njia zisizo za utakatifu na uovu ili kufikia malengo na madhumuni yake (bila kujali wao kuwa watakatifu au la), alifikia kiasi ambacho kwamba kila kitu ambacho kilikuwa kinatoa somo la utakatifu kwa wanadamu kikawa sio kitakatifu. Leo vilevile tunaona hali ileile ambapo wengi wanafuata matendo ya wengine (ambao hawana habari na Uislamu) na kwa kuwaangalia sasa wana imani hii kwamba kama madhumuni ni matukufu na matakatifu, basi kufikia madhumuni hayo matukufu inaruhusiwa kutumia njia yoyote, takatifu au isiyo takatifu. Hii sasa ni itikadi ambayo kwa madhumuni matakatifu njia zote na mbinu zinaruhusiwa; hata kama mtu haoneshi imani yake kwa uwazi, bado watu wengi muhimu kimatendo wanaonekana kuikubali mantiki hii. Katika muktadha huu hukumu na maamuzi ya kidini yamehitajika. Mtu anayefanya kazi kwenye shirika fulani anakuja na kuuliza kwamba shirika ambako ninafanya kazi, hakuna njia nyingine zaidi kuliko ya kuchukua hongo, wakati ambapo natambua kwamba kuchukua hongo kumekatazwa, lakini chini ya mazingira haya naweza kuchukua hongo? Naweza kupokea pesa hii ya hongo na kuitumia kujenga misikiti na Husaniyah, kuandaa mikutano (Majalis) ya maombolezo? Kuna watu wengi ambao kwamba kwao hakuna hata haja ya ushauri na kuuliza, kwao wao suala hili limetatuliwa tayari kwamba wakati madhumuni na malengo yako ni mazuri, basi ili kufikia madhumuni haya unaweza kufuata njia zozote za halali au za haramu. Watu hawa pia huhalalisha imani hii pamoja na ufafanuzi kwamba nia yao ni safi na kama nia ni safi, basi pia njia zote zimetakaswa, matendo yote na vitu 173
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 174
Maadili Ya Ashura vyote vilivyoshirikishwa huwa safi na vitakatifu. Mantiki yao ni kwamba kwa ajili ya malengo matakatifu njia yoyote na rasilimali zilizotumika, zote huwa takatifu; hii kwa maneno mengine ni kwamba pamoja na usafi wa madhumuni njia nazo huwa takatifu. Hivyo baadhi ya watu hutumia baadhi ya pesa zilizotokana na mapato yao ya haramu katika baadhi ya shughuli tukufu na kisha huamini kwamba mali hii iliyopatikana kiharamu nayo pia imekuwa safi na takakatifu.
11. Imamu Husein (a.s) – Mto wa utukufu wa utakatifu Katika mazingira hayo wakati Husein bin Ali (as) alipoona kwamba maadili iliyo kubwa mno ilikuwa inavunjwa, maadili ambayo ilianzishwa na Allah (s) kwa ajili ya wanadamu: “Enyi wanadamu mimi ni safi na mtakatifu, jukumu lenu sasa ni kukubali utakatifu wangu huu na kuutukuza. Lakini kama mkiacha utukufu na utakatifu, basi huwezi kuja karibu Yangu, kwa sababu dhati Yangu ni safi na takatifu.”
Wakati Husein (as) alipoona kwamba mwanadamu ameacha njia ya utakatifu na ameanza kuvunja vitu vyote vitakatifu, aliamua kwamba wakati umefika kurudisha utakatifu wa misikiti, mikutano ya kidini (Majalis), mimbari, Nyumba ya Allah, Qur’ani, Imamu, Umma na dini. Umma sasa lazima uoneshe njia ya utakatifu na mbinu kwa ajili ya kuuweka safi na hai. Muhanga ambao Imamu Husein (as) aliutoa ulikuwa ni uthibitisho wa utakatifu; muhanga huu ulitolewa ili kuokoa utakatifu wa maadili ya uungu wakati maadili ya uungu yalipokufa ndani ya Ummah, utawala na jamii. Haichukui muda mwingi kwa maadili kufa, hufa kwa haraka sana, na kwa muda wa nusu karne tu baada ya kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) maadili yalikufa. Hivyo ili kuhuisha maadili haya yaliyokufa ilihitajika Karbala, hivyo ndani ya karne kumi na nne, nusu karne nyingi kama hiyo zimepita, na takriban mara kumi na nane yangelikufa maadili haya. Hivyo, leo hali ni kama hiyo, utakatifu wa misikiti, majalis, mimbari, madhumuni na njia huangamizwa. Utakatifu wa mimbari sio ule wa mtu kuanza hutuba yake kwa “Bismillah” na kisha hakuna wasi wasi wa chochote kitakachokuja mdomoni mwake, madhumuni ni kupata sifa kutoka kwa watu na kuwafanya watoe kaulimbiu za jazba. Hawatambui kwamba kwa kuikufuru mimbari wanaangamiza utakatifu wa Qur’ani, wa Mtume (s.a.w.w.), utakatifu wa Imamu na utakatifu wa dini. Hapa ndipo tunapohitaji wa-Karbala, wa-Ashura na wa-Huseini. Baadhi ya watu lazima wajitokeze mbele kama wa-Huseini na kwa kufuata mwenendo na tabia ya Husein bin Ali (as) lazima wahuishe maadili na kurudisha utakatifu wa kila kitu, ili kwamba wasipatikane kizazi cha Bani Umayyah na kupata moyo wa kukaa juu ya mim174
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 175
Maadili Ya Ashura bari ya Ali (as) aliyoachiwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kupoteza utakatifu wa urithi na umakamu wa Ali (as) (rejea matusi yanayofanywa siku hizi juu ya Walie-Faqih). Kamwe asipatikane mtu yeyote kuwa na moyo wa kukaa katika mimbari ya Husein (as) na badala ya kuwasilisha maadili ya Husein (as) anawasilisha maadili ya Bani Umayya, kwa sababu wakati huo pia makhatibu wa mimbari walikuwa wanatoa majukumu waliyoaminishwa kwao na Bani Umayya na kwa muda wa karne moja na nusu walimtusi Ali (as). Imamu Husein (as) aliona kwamba sambamba na kufuru juu ya utakatifu wa mimbari, utakatifu wa sheri za dini na ibada pia umepotezwa. Swala ya jamaa ya Ijumaa inaswaliwa jumatano. Kuswali swala ya Ijumaa siku ya Jumatano ni mzaha wa dini na kuyadhihaki maadili ya uungu. Kwa hiyo, Imamu Husein (as) pamoja na muhanga huu mkubwa aliurudisha utakatifu wa dini, mimbari na msikiti. Alihuisha utakatifu wa njia, rasilimali na madhumuni katika hali ambayo wakati wowote mchakato wa kufuru ya vitu vitakatifu unapoanza, wakati wowote wale ambao wanakusudia kupoteza vitu vitukufu wanapojitokeza, unaweza kupigana nao kwa kufuata mwenendo wa Imamu Husein (as), ingawa ni hakika, kupigana nao lazima tulete mwenendo wa Imamu Husein (as). Alisema kwamba mtu kama mimi kamwe hawezi kula kiapo cha utii kwa mtu kama Yazid, na katika njia nyingine vilevile alisema kwamba wakati wowote mtu kama mimi akiamua kuhuisha maadili, basi lazima atoe muhanga kama wa kwangu, akiweza kufuata mwenendo wangu anaweza kupigana nao. Ametuonesha mbinu za kuhuisha vitu vitakatifu, ametufundisha sanaa ya kusafisha utakatifu wa dini na ametupa somo la utakatifu ambalo litabakia mpaka mwisho wa ulimwengu huu.
12. Karbala – Njia ya Mbinu Takatifu Kuhakikisha mbinu takatifu na rasilimali kwa ajili ya kufikia malengo matakatifu ilikuwa ni maadili ambayo imebadilika na ilikuwa imekufa. Imamu Husein (as) alipulizia roho katika maadili haya yaliyokufa, na kutoka Madina mpaka Ashura kote tumepata masomo makubwa ya jinsi ya kutumia njia hizi takatifu. Yeye (as) kimatendo ameonesha kwetu kwamba ili kufikia madhumuni matukufu ni haramu kwetu kutumia njia zisizo takatifu na za uovu. Ni muhimu kuwasilisha mfano wa kihistoria, ambao una masomo kote kama uthibitisho kwa nukta hii ya mjadala. Wakati Imamu Husein (as) alipotoka Makka na kuelekea Iraq alikutana na mtu njiani jina lake Ubaidullah bin Hurr Al-Juhfi. Mtu huyu alikuwa mwenyeji wa Kufa. Kufa ulikuwa mji mkuu wakati wa Ukhalifa 175
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 176
Maadili Ya Ashura wa Amirul-Mu’minin (as) na mtu huyu alikuwa anapatikana kwa ajili ya huduma tukufu za Amirul-Mu’minin (as) na alikuwa mpenzi wa Ahlul-Bayt (as). Wakati alipoona kwamba watu wa Kufa wameandika barua kwenda kwa Imamu Husein (as) na punde hivi Imamu Husein (as) atakuja Kufa, lakini basi kabla ya kuwasili kwake (as) maalun Ubaidullah bin Ziad ameingia na kuuteka mji wa Kufa, hivyo akabadilisha mazingira ya mjini hapo na kusababisha watu wa Kufa kubadilisha nia zao. Mtu huyu akiwa na nia ya kutoroka macho ya Imamu Husein (as) aliondoka Kufa. Alichukua panga zake, mikuki na akafungasha mikoba yake akaenda sehemu karibu na Kufa na akapiga kambi pale. Nia yake ilikuwa si kumsaidia Imamu Husein (as) wala Ibn Ziad. Kwa maneno mengine mtu huyu alikuwa anataka kuokoa ulimwengu wake huu na wa Akhera. Alikuwa anatambua kwamba chini ya mazingira haya kama atamsaidia Imamu Husein (as) basi atalazimika kuupoteza ulimwengu huu na kama akimsaidia Ibn Ziad basi anaipoteza dini yake, hivyo alitangaza kutokuwa na dhima kwake. Kwa bahati Imamu Husein (as) alipitia sehemu ile na akapiga kambi yake karibu na kambi ya mtu yule. Kisha akamtuma mtu kwenda kuuliza kuhusu mtu huyu ambaye amepiga kambi pale. Mjumbe wa Imamu Husein (as) alirudi na taarifa kwamba ni mtu kwa jina anaitwa Ubaidullah bin Hurr Juhfi na ametangaza kutokuwajibika kwake na hataki kujihusisha na upande wowote katika hali iliyopo sasa. Imamu Husein (as) alimtuma tena mjumbe ili amuite wakutane wazungumze. Wakati mjumbe aliporudi na wito wa Imamu Husein (as), Ubaidullah alimuambia yule mjumbe wa Imamu Husein (as): “Nenda kamuambie Imamu Husein (as) kwamba kwa hakika nampenda, na kumheshimu, lakini ameniita katika wakati ambapo ninaomba radhi kwa kutokuja kwa sababu nimeweka ahadi kwamba sitakwenda kwa Imamu Husein (as) wala sitaungana na maadui zake yeye (as), vinginevyo ahadi yangu itavunjika.” Wakati Ubaidulla bin Hurr alipokataa kuja kukutana na Imamu Husein (as), yeye Imamu Husein (as) mwenyewe alisimama na akaenda kwenye hema lake. Mtu huyu aliyepotoshwa alikaa kwenye hema lake na kiongozi wa Ummah alikwenda kwake kumwongoza. Mtu huyu aliyepotoshwa alikuwa anafikiri kwamba Imamu Husein (as) alikuwa katika hali ya unyonge na amenaswa kwenye shida; hivyo alikuwa mhitaji wa mtu na amekuja kwangu kutafuta msaada. Lakini kiukweli Imamu (as) hakwenda kwa mtu huyu aliyepotoka kuchukua chochote, bali kwa kweli alikwenda pale kumpa kitu, alikwenda pale kumuondolea upotofu wake, kumpa ukombozi kutokana na kuzama katika bahari ya maovu. Miongoni mwa majina ya Imamu Husein (as), kuna jina moja ambalo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alilisimulia kama “Safinati Najaat” (Uyune Akbari Riza, J. 1, uk. 176
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 177
Maadili Ya Ashura 59). Imamu Husein (as) alitaka kumwambia kwamba kuna vurugu sasa katika bahari ya mauaji, kuna mawimbi katika ulimwengu wa maovu na umesimama kwenye fukwe ya maovu ambayo iko karibu kukazamisha hivi punde. Nimekuja kwako kama safina ya wokovu, njoo upande safina ya maadili na utapata wokovu. Lakini Ubaidullah bin Hurr akajibu: “Ewe Husein! Kwa wakati huu unataka farasi wangu zaidi ya mimi, mikuki yangu na panga zangu zitakidhi zaidi madhumuni yako kuliko mimi.” Akiwa kama Mwarabu mshairi, alianza kusoma mashairi kuhusu farasi wake, mikuki na panga zake, hata leo mashairi hayo yamehifadhiwa kati vitabu vya historia. Alisema, alipata ushindi katika vita vingi pamoja na farasi hawa, vifua vingi nimevipasua kwa mikuki hii na shingo nyingi nimezikata kwa upanga wangu huu. Kwa kusema yote haya alitaka kutoa rasilimali yake isiyo takatifu na chafu kumpa Imamu Husein (as). Lakini Imamu Husein (as) katika kujibu alisoma aya hii:
“…Wala sikuwafanya wapotezao kuwa wasidizi (wangu).” (Surah Kahf, Ayah 51) Nimekuja kukuondoa upotofu wako sio kuchukua msaada kutoka mtu mpotofu kama wewe; sikuja kuchukua farasi wako, mikuki na panga zako. Sikuja kuchukua silaha hizi kutoka kwako, kama huko tayari kuja pamoja na mimi, basi pia sina haja na silaha zako chafu na rasilimali ya ufisadi. Kama umpotofu basi vilevile hatutumii rasilimali chafu kwa ajili ya malengo yetu matukufu na matakatifu, Mola Wangu ameamuru kwamba: “Siwezi kuchukua msaada kutoka kwa watu waliopotea.” Tukio hili la kihistoria huhuisha maadili, kwamba katika mazingira ya aina yoyote njia na rasilimali chafu haziwezi kuwa halali kwa ajili ya madhumuni matukufu. (Tukio la kukutana na Juhfi, Mawassae Kalemate Imam Hussain, 365 – 369)
13. Maadili ambayo yalihuika kutokana na mkutano wa Imamu Husain (a.s) na Juhfi Katika kila hatua katika Karbala maadili yaliyokufa yanahuika, kutokana na kauli za Husein ibn Ali (as) maadili yaliyokufa yanahuika na maovu yanazikwa. Wallahi! 177
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 178
Maadili Ya Ashura huenda ikachukua karne kumi na nne zaidi lakini bado muonekano wa maadili ya Ashura huenda yasikome, huku sio kuzidisha chumvi lakini ni ukweli wa wazi uliodhihiri. Sasa hebu tuangalie kwenye tukio hili la kihistoria na tuone ni maadili gani yanahuika. Maadili matatu yanapata uhai kutoka kwenye mkutano huu mfupi (kati ya Imamu Husein (as) na Ubaidullah).
A. Kuwa mwenye kutokujali – Ni sifa ya uovu Ubaidullah bin Hurr Juhfi alitangaza kutokuwajibika kwake na kutokuhusika kwake katika hali hii. Sasa tutaona, iwapo kutokujali ni maadili nzuri au inatokana na maovu. Leo kama utawauliza wanadamu, Waislamu na pengine waulize tu wengi wa wafuasi wa Imamu Husein (as) kwamba ni aina gani ya sifa ambayo ni ya kutokujali? Utaona wengi wanaunga mkono hii visheni ya kutokujali. Watu wengi huchukulia hili kama maadili mazuri (Ma’ruf). Lakini Imamu Husein (as) alisimulia kwamba kuwa katika hali ya kutokujali sio tabia nzuri, ni upotofu. Kuwa mtu asiyejali au kutokupendelea upande wowote katika mapambano kati ya Haki na Batili ni vibaya zaidi kuwa mfuasi wa batili. Ni jukumu la wajibu kwa mwanadamu siku zote kuunga mkono haki na kutangaza chuki yake na maudhi yake kwenye batili, na kwa kubakia kutokupendelea upande wowote, batili hupata nguvu.
B. Mwongozaji katika kutafuta wanadamu waliopotea Leo kama wanachuoni na wanafunzi wa shule za dini wakiambiwa kwamba sehemu fulani kuna watu waliopotoka na wanapaswa kwenda huko kuwaongoa, mara moja tunaanza kujitafutia wenyewe methali kwamba wale wenye kiu siku zote huja karibu na kisima. Siku zote wanatumia mantiki hii kwamba sisi ni wanachuo tunakaa misikitini, mashuleni na nyumbani mwetu, kama watu wanatutaka basi wanapaswa kuja kwetu na kuuliza, tutawafundisha dini. Hii ni kwa sababu sisi ni visima vya maji na watu ni wenye kiu, na kama ilivyo kisima hakiendi kutafuta watu wenye kiu, bali siku zote watu wenye kiu huja karibu na kisima. Hulichukulia hili kama suala la heshima na umakini (katika ibada) kutokuwafuata watu waliopotoka huko waliko. Kwa kweli kujifikiria wewe mwenyewe kama kisima cha maji na kuwafanya wengine kuwa wenye kiu ni moja ya maovu makubwa. Kuna tofauti kati ya maji ya kisima na yale ya kijito. Maji yaliyoko kwenye kisima hubakia chini ya kina chake na watu wenye kiu huanza kuyatafuta. Kama baadhi ya watu wenye kiu wakija kuchota maji, kisima hutoa kiasi kidogo cha maji. Lakini kijito vilevile ni chan178
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 179
Maadili Ya Ashura zo cha maji ambayo yako katika kutafuta wenye kiu, hutembea kwa kiasi kikubwa kutafuta mtu mwenye kiu, ili kuzima kiu yake. Husein bin Ali (as) alisema kwamba mimi sio kisima; mimi ni mfano wa maji ya chemchemu. Kama mtu fulani mpotofu haji karibu yangu basi mimi mwenyewe nitakwenda karibu yake. Kwa nini tunafikiria kisima tu wakati inapokuja kwenye suala la mtu mwenye kiu? Kwa nini hatuangalii mto au kijito katika umuhimu wa mtu mwenye kiu? Mazao shambani (na mimea mingine) kamwe hayatembei kwenda kwenye kijito, siku zote ni maji ya kijito ambayo hutafuta njia yake kuelekea kwenye mazao ya shambani. Imetajwa kwenye Qur’ani Tukufu:
“Yeye ndiye Aliyempeleka Mtume kwenye watu wasiojua kusoma (wa Makka), aliyetokana na wao… Japokuwa hapo kabla walikuwa katika upotofu uliodhahiri.” (Surah Juma, Ayah 2) Tulimpeleka Mjumbe miongoni mwa watu waliopotoka na hatukuwapeleka watu waliopotea kwenda kwa Mjumbe. Husein ibn Ali (as) alitenda juu ya mwenendo wa Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) na akawasilisha tabia hii ya kwenda kwa watu waliopotoka kama maadili.
C. Mwongozaji badala ya kuchukua kitu anakwenda kutoa kitu Wakati Imamu Husein (as) alipomwendea mtu huyu aliyepotoka (Juhfi), ilikuja akilini mwa mtu huyu kwamba Imamu Husein (as) yuko katika haja kubwa ya kitu fulani, na yuko katika shida ambayo yaweza kutatuliwa na mimi, hivyo ngoja niangalie anaomba kitu gani kutoka kwangu. Leo pia watu husema hivyo hivyo, kama mwanachuo wa dini akienda kwa mtu fulani, mtu yule hufikiri kwamba mwanachuoni huyu ana haja ya kitu na ametumbukia kwenye matatizo fulani; anataka kitu hivyo amekuja kwangu. Inawezekana kwamba kuna baadhi ya watu ambao wanakwenda kwa watu wakiwa wamevaa kama wanachuoni ili kuwaibia kwa kutoa visingizio ili kunyonya pesa kutoka kwa watu, lakini wanachuoni wa kweli hutenda juu ya mwenendo wa Imamu Husein (as) na badala ya kutegemea kitu kutoka kwao huwaendea na kuwapa kitu. Huwatembelea watu kwa maadili ya Husein (as), huenda tu kule kwa watu ili kuwaondolea upotofu wao na kuwaongoza. Miongoni mwa maadili ya Husein (as) kuna maadili inayojulikana kama “Infaq” (kutoa katika njia ya Allah), ambayo ina maana kwamba yeye (as) ametufundisha njia ya kutoa na hakutufundisha njia 179
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 180
Maadili Ya Ashura ya kuchukua. Mrithi wa Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) ndiye ambaye kama yeye (s.a.w.w.) huwaendea watu ili kuwapa kitu. Hii ni kwa sababu watu waliopotea hawana kitu chochote cha kutoa, wanaweza tu kutoa upotofu. Hivyo kila siku Mitume wamekuja kuwapa watu kitu, hii ndio sababu Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) anasema:
“Siombi malipo yoyote toka kwenu ….” (Surah Ash-Shura, Ayah 23) Sikuja kuchukua mshahara wowote kutoka kwenu bali badala yake nimekuja kuwazawadia kwa mapenzi ya Ahlul-Bayt (as). Siwaambii kwamba nilipeni mshahara bali nasema kwamba chukueni hii Thaqalain (zawadi ya vizito viwili) kutoka kwangu na muwapende kwa sababu kuna faida kubwa katika mapenzi haya kwao, na faida hii ni kwamba hamtapotea.
D. Utambulisho wa Njia Chafu. Sio kwamba ni hongo tu, mali ya kuiba au kunyang’anya huchukuliwa kama mali chafu, lakini badala yake yote na kila njia iliyopo yenye uchafu na watu waliopotea ni wachafu. Mali yote iliyoko kwa watu watakatifu na watukufu ni takatifu. Kama njia chafu zinachukuliwa kutoka kwa watu wachafu na kutumiwa kwa ajili ya madhumuni matakatifu, basi kanuni ile ile ya usafi na uchafu hutumika ambako iwapo vitu safi vinachanganywa na vitu vichafu basi vitu vichafu havikubali vitu visafi, kwa kweli vitu vichafu huacha athari kwenye vitu visafi. Wakati vitu vichafu na vitu visafi vinapochanganywa pamoja basi vitu vichafu huvibadilisha vitu visafi pia kwenye uchafu, kwa hiyo, njia chafu zitabadilisha madhumuni matakatifu pia kuwa machafu (kanuni hii ya mantiki inawasilishwa hapa kama sharti). Dhati ya Allah (s) ni safi na haikubali vitu vichafu. Kama watu wanataka kujenga Msikiti, Hussainiyah au wanataka kuandaa mikutano ya kidini, basi lazima watumie pesa kutoka kwa watu watakatifu na safi.
E. Utakatifu wa Matendo ni sharti kwa ajili ya kukubaliwa Kama kitu ni cha kuwasilisha kwenye Dhati Tukufu na takatifu ya Allah (s), basi lazima kiwe ni matokeo ya njia takatifu tu, dhati hiyo ni safi, takatifu na haitakubali kitu chochote kichafu, hivyo wengi wametoa katika mamilioni, lakini kwa vile vilikuwa vichafu Allah hakuvikubali. 180
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 181
Maadili Ya Ashura Tukio la “Habil” na “Kabil” liko mbele yako, mmoja wao aliwasilisha zawadi ya dhabihu ya gharama na mwingine akawasilisha ya rahisi, lakini aliyewasilisha ya gharama ilikuwa chafu na Allah hakuikubali, ile ya yule iliyokuwa ya rahisi ilikubaliwa na Allah kwa vile ilikuwa takatifu.
“…Allah huwapokelea wamchao tu.” (Surah Maida, Ayah 27) Hii maana yake ni kwamba Allah (s) hukubali kutoka kwa wale ambao ni wachamungu, watakatifu na wasafi.
14. Hitimisho Maadili ambayo Husein bin Ali (s) aliyahuisha na kuyafanya kuwa maadili ya Ashura na ambayo siku zote yatakuwa yanahifadhiwa kama Maadili ya Husein (as) ni “Utakatifu wa Mambo”. Kwa hiyo, Imamu Husein (as) alihuisha utakatifu wa misikiti, mimbari, Nyumba ya Allah (s) na Ishara zingine za uungu, na juu ya yote alihuisha utakatifu wa Uongozi (Imamat) na Mwongozaji (Haadi) Hata leo hii kama kuna kufuru ya maeneo matakatifu inayofanyika basi njoo na ujifundishe kutoka kwa Husein (as) ili asiweze kutokea mtu akakufuru maeneo matakatifu. Siku zote ni watu wachafu na waovu ndio ambao wanaupoteza utakatifu wa vitu. Hii ni kwa sababu kwa watu waovu na wachafu hakuna kilicho kisafi kwao, hata damu ya watu fulani sio takatifu, kwa kiasi kwamba kumwaga damu safi na takatifu ya Husein (as) huchukuliwa kama wajibu kwao. Allah (s) amlaani yule mtu maalun ambaye alitoa hukumu ya kumwaga damu ya Imamu Husein (as). Jinai ya Imamu Husein (as) ilikuwa ni nini? Kosa lake tu lilikuwa kwamba alianza mageuzi matakatifu dhidi ya batili, alisimama dhidi ya viumbe wachafu na akaja kwenye uwanja wa mapambano kurudisha vitu vitakatifu na kwa kuvihuisha alithibisha jinsi ya kuokoa maadili.
181
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 182
Maadili Ya Ashura
Maadili ya Tisa Uadui katika njia ya Allah
1. Kutengeneza Maadui ni Maadili ya ki-Huseini...............................................183 2. Uhusiano wa Misiba na Maadili......................................................................184 3. Tawalla na Tabbarra.........................................................................................184 4. Mwenendo wa Nabii Musa (as) na Tabarra.....................................................185 5. Mrithi wa Musa (as) katika kuutokemeza U-Yaziid (Yazidiat).......................186 6. Tabarra (Kujitenga) katika Mwenendo wa Imamu Ali (a.s)............................187 7. Wale ambao huokoa ngozi zao kutokana na misiba........................................188 8. Athari za Maadili..............................................................................................189 9. Jaribio chafu la kuondoa Maadili kutoka kwenye nafasi zao..........................190 10. Maadili na Misiba ya Bibi Zahra (as)............................................................192 11. Shukurani juu ya Misiba................................................................................193 12. Imam Husein (a.s) - Kigezo cha wajibu cha Maadili na Misiba...................194 13. Kila siku ni Ashura na Kila ardhi ni Karbala................................................195 14. Ashura ni Siku ya Allah................................................................................196
182
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 183
Maadili Ya Ashura
1. Kutengeneza Maadui ni Maadili ya ki-Huseini Moja ya maadili muhimu miongoni mwa maadili ya Ashura na sifa za Imamu Husein (as), ambayo Kiongozi wa Mashahidi (as) aliyahuisha siku ya Ashura kwa kuyapulizia tena roho ndani yao na kuyawasilisha tena kwa wanadamu, ni dhana ya kukaribisha misiba, matatizo, hatari, na halikadhalika kutengeneza maadui. Imamu Husein (as) alithibitisha kwa mwenendo wake kwamba kupata shida, kujihatarisha na kuingia ndani ya kambi za maadui ni maadili ya ki-Mungu, ki-Qur’ani na ki-Huseini. Roho ya maadili haya tangu hapo imeondolewa, na hata leo baada ya Karbala inaonekana kwamba roho ya maadili haya bado haionekani. Mwanadamu wa leo amezoeshwa kwenye starehe, furaha na anasa za maisha. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Wakati utakuja ambapo maadili mema (Ma’ruf) yatakuwa maovu (Munkar), na maovu (Munkar) utakuwa maadili mema (Ma’ruf).” (Wasailus Shia, Sura ya Amr na Nahi, Jz. 16, uk. 122) Zama hii ilitokea katika wakati huo na leo imejitokeza tena. Kwa kawaida inaeleweka kwamba mtu ambaye hutengeneza maadui hachukuliwi kama mtu mzuri. Mtu ambaye huingia kwenye mapigano na kusababisha wengine kuwa na chuki kwake kwa kawaida hachukuliwi kama katika mwanga bayana. Hata hivyo, Kiongozi wa Mashahidi (as) amesema kwamba watu wazuri ni wale ambao huingia kwenye migogoro katika njia ya Allah pekee. Kuna watu ambao wanaweza kuonekana wakipigana mitaani kwa ajili ya matamanio yao ya kidunia, wakikunjana shingo wenyewe kwa wenyewe, kuuwa wanadamu na kuhimiza umwagaji damu kwa ajili ya matamanio yao maovu. Mapigano na migogoro hii sio haswa suala na makusudio ya mjadala huu. Tunajadili maadili yale ambayo Imamu Husein (as) ameyahuisha, ambapo alitamka kwamba kama utayeyusha matamanio na makusudio yako katika makusudio ya Mola Wako, na kama huko dhidi ya utashi wa Allah, basi kwa njia hiyo hiyo ambayo unatamani starehe na amani, lazima utamani shida na misiba wakati wowote kama ipo haja. Vilevile utatafuta matatizo na migogoro, katika njia ya Allah pekee. Itakulazimu pia kuwatokomeza maadui, katika njia ya Allah tu. Haya ni maadili ya ki-Husein ambayo Imamu Husein (as) aliyahuisha.
183
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 184
Maadili Ya Ashura
2. Uhusiano wa Misiba na Maadili Kama mtu akiwa na maadili ya ki-Husein, basi sifa na maadili haya ya Ashura ambayo Imamu Husein (as) aliyawasilisha katika muundo wa ufahamu yanaendelezwa ndani ya mtu huyo, na athari ya sifa hizi zitadhihirishwa katika muundo wa misiba mbali mbali. Hivyo, misiba ambayo imewapata Ahlul-Bayt (as) ilikuwa ni matokeo ya sifa walizonazo. Kama Ahlul-Bayt (as) wasingekuwa na sifa hizi ndani yao, basi hakuna msiba ambao ungetokea kwao. Kwa uhalisia, chanzo cha misiba ni sifa njema; na ilikuwa ni sifa hizi ambazo ziliwafanya Ahlul-Bayt (as) kupatwa na misiba hii. Sifa hizi zilipeleka misiba kwenye mapaja ya Ahlul-Bayt (as). Kwa hiyo, Imamu Husein (as) alianzisha sera ambayo itaendelea mpaka Siku ya Mwisho; sera ambayo hueleza kwamba mtu ambaye ana sifa njema kamwe hawezi kuikwepa misiba. Kama mtu katika ulimwengu huu hapati kuhusika kwenye misiba kuanzia kuzaliwa kwake mpaka wakati wa kifo chake, basi inaeleweka kwamba mtu huyo ana sifa kidogo tu. Hivyo, kama mtu ana maadili mema kama vile kujiheshimu, hadhi, ghera, utambuzi wa majukumu yake, na ukarimu (Infaq) ndani yake, basi hawezi kukaa kimya nyumbani kwake. Kamwe hatajaribu kuokoa ngozi yake kutokana na misiba. Isipokuwa, huwa mnunuzi wa misiba.
3. Tawalla na Tabbarra Allah ametaja aina ya biashara kwa ajili ya wanadamu pale aliposema:
“Na katika watu yuko auzaye nafsi yake kwa kutaka radhi ya Allah, na Allah ni Mpole kwa waja.� (Surah Baqarah, Ayah 207) Aya hii hutuambia kwamba kuna baadhi ya watu ambao hufanya biashara na Allah, ambapo huuza nafsi zao kawa ajili ya kununua radhi Yake. Hivyo, wale ambao wamenunua radhi ya Allah hujiwasilisha wenyewe kwake kwa uaminifu. Kama wana furaha, basi furaha yao ni kwa ajili ya radhi ya Allah; na kama wana huzuni, basi huzuni yao pia ni kwa ajili ya radhi ya Allah. imekuwa ikitajwa mara nyingi katika mafundisho ya dini na maadili ya Kiislamu kwamba mapenzi na chuki vyote lazima viwe ni kwa ajili ya Allah na Yeye peke Yake. 184
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 185
Maadili Ya Ashura Hii ni kwa sababu ya ukweli kwamba mara unapokuwa umeuza nafsi yako kwa ajili ya Allah, umeuza utashi wako, matamanio yako na makusudio vyote kwa ajili ya Allah. Kwa hiyo, kwa ajili ya radhi ya Allah humchukia mtu fulani, hupigana na kufanya Jihad ndogo na kubwa. Kwa ajili ya radhi ya Allah, hutengeneza maadui, hupambana na misiba na kupatwa na matatizo. Hawa ni watu ambao kuwepo kwao kote kumejazwa kikamilifu na maadili mema. Ni marafiki wa marafiki wa Allah na ni maadui wa maadui wa Allah. Tawalla na Tabbarra, Amr bil Ma’ruf na Nahi Anal Munkar, Mapenzi na Chuki, vyote hivyo ni njia tofauti za kuelezea kitu hicho hicho. Katika njia hiyohiyo ambayo Allah amedai mapenzi kutoka kwetu; Yeye (s) pia amedai chuki kutoka kwetu. Jinsi ambavyo imeamriwa kwetu kufanya Amr bil Ma’ruf, vilevile imeamriwa kufanya Nahi Anal Munkar. Halikadhalika kama Tawalla inadaiwa kutoka kwetu, basi Tabarra pia inadaiwa kutoka kwetu. Wakati hisia kali za mapenzi na chuki ndani ya mwanadamu zikiingia kwenye hali iliyo ya juu, moja kwa moja hugeuka kwenye Tawalla na Tabarra. Wakati Tawalla na Tabarra ikija kwenye matendo kwa ajili ya wanadamu, inakuwa Amr Bil Ma’ruf na Nahi Anal Munkar. Na wakati Amr Bil Ma’ruf na Nahi Anal Munkar ikija katika uwanja wa kimatendo, hujidhihirisha yenyewe kama Jihad dhidi ya maadui na ujumbe wa kufa kishahidi kwa marafiki. Tawalla na Tabarra iko kabisa ndani ya dini; kama ilivyoelezwa na Imamu Baqir (as) katika hadithi:
Je, dini ni kitu kingine chochote kuliko mapenzi? (Usuuli Kaafi, Jz. 8, uk. 79)
4. Mwenendo wa Nabii Musa (as) na Tabarra Qur’ani Tukufu imezungumza kuhusu mwenendo wa Nabii Musa (as). Nabii Musa (as) alikuwa ni Mtume ambaye alikuwa amezoea kutengeneza maadui katika njia ya Allah (s); alikuwa akipigana mara kwa mara, na kuasi katika njia ya Allah (s). Ingawa Nabii Musa (s) alikuwa na maisha mazuri baada ya kumuoa binti ya Nabii Shuaib (as), kwa vile mahitaji yote ya maisha yalikuwemo ndani ya nyumba ya Nabii Shuaib (as), lakini bado alipuuza huduma hizo na akamuambia Mola Wake: 185
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 186
Maadili Ya Ashura “Ee Mola Wangu! Baada ya kukaa muda mrefu najifikiria mwenyewe kuwa mwenye kustahiki kutengeneza maadui katika njia Yako, sasa naweza kuvumilia chuki katika njia Yako, sasa naweza kuvumilia misiba katika njia Yako, nioneshe adui ambaye kwamba naweza kupambana naye.” Amri ilikuja kutoka kwa Allah: “Ewe Musa! Sasa umekuwa na maadili ya sifa njema ndani ya nafsi yako kwa kiasi kwamba sasa unastahiki kununua uadui, kwa hiyo, nenda ukanunue uadui; nakuambia kwamba Firauni ni mkandamizaji na mchupa mipaka mkubwa ulimwenguni.” Nabii Musa (as) alileta uadui wa mchupa mipaka mkubwa kabisa (Taghut) ingawa alikuwa na njia nyingi za kuweza kuokoa ngozi yake. Mke wake alikuwa mjamzito na kukaribia kujifungua wakati wa safari hii. Nabii Musa (as) alikuwa na uhalali wote uliokamilika kwamba punde tu hivi amepata mtoto, anahitaji kufikiri kuhusu ustawi wa familia yake, alikuwa na haki pia za watu wengine waliomzunguka na pia alihitaji kuokoa maisha yake. Lakini wakati Nabii Musa (as) alipoamua kuingia katika mapambano na Firauni Allah alimuonesha miujiza Yake na Musa (as) aliogopa.
“…Ewe Musa! Usihofu! Bila shaka mbele Yangu Mimi hawagopi mitume.” (Surah Naml, Ayah 10) Wakati Nabii Musa alipokuwa imara vya kutosha kuja kwenye hadhara ya Allah ili kuonesha utashi wake wa kupambana na adui, basi Allah (s) alimuelekeza kwa adui mkubwa na hatari sana. Sasa Musa (as) akaondoka kwa ajili ya kumtokomeza adui, wakati ambapo kulikuwepo kipindi Firauni alikuwa akimtafuta Musa (as), kwa sababu alihisi kwamba mtu kama Musa (as) asingepaswa kuzaliwa kwa sababu atakuwa adui yangu. Sasa, wakati Musa (as) alipokuwa mbebaji wa maadili, hadhi na heshima yake ikakua na kuwa kubwa katika nafsi yake, wakati huo Musa (as) alikuwa akimtafuta Firauni.
5. Mrithi wa Musa (as) katika kuutokemeza U-Yaziid (Yazidiat) Imamu Husein (as) ni mrithi wa Mitume (as). Habari hii imetokea mara nyingi katika (visomo vya) shuhuda za Ziyarat:
186
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 187
Maadili Ya Ashura
Imamu Husein (as) alichukua sifa hii ya kufanya maadui katika kurithi kutoka kwa Mitume (as). Sio kwamba Yazid alimlazimisha Imamu Husein (as) na matokeo yake yeye (as) akalazimika kupatwa na misiba yote hiyo katika njia isiyotamanika. Kulikuwepo na maelfu ya njia zilizokuwepo tayari kwa ajili ya Imamu Husein (as) kuikimbia misiba hii na watu pia walimpa ushauri mbali mbali. Baadhi walimshauri kwa ajili kumhurumia, baadhi walimshauri kwa ajili ya kumlaghai na kwa manufaa ya ulimwengu, baadhi walimshauri kwa ajili ya kutaka kupata cheo na madaraka, baadhi walimshauri aende Yemen na halikadhalika wengi walijitokeza kumshauri kufanya kitu hiki au kile. Imamu Husein (as) alisikiliza ushauri wa kila mtu. Kiongozi wa Mashahidi (as) yeye mwenyewe alikuwa anatambua kwamba ili kuepuka misiba, kuuawa shahidi, ufungwa na matatizo kwa ajili ya wanawake kulikuwa na njia nyingi. Lakini Imamu Husein (as) hakuwa aina ya mtu ambaye angechukua hifadhi sehemu fulani ili kuepuka misiba. Badala yake Imamu Husein (as) alisema kwamba, sasa wakati umefika kwa ajili ya Husein kuwa mtoaji wa misiba na kununua uadui wa maadui wa Allah. Hivyo lengo halikuwa kuokoa ngozi yake kutokana na misiba, bali ilikuwa ni kununua misiba. Imamu Husein (as) alikuwa hataki hifadhi, amani, raha, usalama wa maisha na ustawi wa familia yake kutoka kwa Allah, badala yake yeye (as) alisema: “Ewe Mola Wangu! Kwa kuweka maadili haya ndani yangu umenifanya mimi mtu wa hali ya juu wa kuwajibika, umenifanya mbebaji wa Uongozi (Imamat), umenipa heshima, umenionesha njia ya kufanya Infaq, kwa hiyo, sasa nioneshe adui yako ili kwamba nianzishe mapambano naye.� Hivyo Imamu Husein (as) alitoka kwa ajili kwa kumtafuta Yazid wa zama yake. Historia inatuambia kwamba ilikuwa ni Yazid ambaye alikuwa akimtafuta Imamu Husein (as), lakini kama ukiangalia katika uhalisia alikuwa ni Imamu Husein (as) ndiye ambaye alikuwa akimtafuta Yazid. Yeye (as) aliuzunguka Uyazidi na akaupiga dharuba kubwa ambalo mpaka Siku ya Mwisho hautakuwa na mafanikio. Ilikuwa ni shambulio la maadili ya ki-Huseini, ambalo lilitokomeza Uyazidi daima. Hivyo mtu yeyote ambaye sifa na maadili ya Husein (as) yanakua ndani yake, mtu huyo kamwe hawakimbii maadui, bali badala yake hupigana na maadui ili kununua uadui wao.
6. Tabarra (Kujitenga) katika Mwenendo wa Imamu Ali (a.s) Kila mtu anafahamu kuhusu mwenendo wa Imamu Ali (as). Alitembeza upanga wake katika njia ya Allah (s) kwa kiasi kwamba alikuwa mtu ambaye aliendelea 187
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 188
Maadili Ya Ashura kutengeneza maadui. Hili limetajwa katika Dua-e-Nudba:
“Yeye (as) alikuwa akitembea kwenye nyayo za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Alipigana vita vya Jihad kwa maelekezo ya Qur’ani kwa fahari kubwa kiasi kwamba alikuwa hajali kuhusu ukosoaji wa mkosoaji yeyote. Katika njia hii yeye (as) aliwashinda wakuu wengi wa Kiarabu, akawauwa mashujaa wao wengi na akawashinda watu wao wakatili. Nyoyo zao zikakusanya uovu wa Badr, Khaibar, Hunain na vita vingine; hivyo wakafanya mkataba wa kupigana kwa kuungana dhidi yake (as). Yeye (as) aliwauwa wale waliovunja kiapo cha utii, wale ambao wana uadui na Uislamu na wale ambao wametoka nje ya dini.” (Mafatihul Jinan). Imamu Ali (as) amefanya biashara na Allah ambapo ameuza nafsi yake na kupata radhi ya Allah . Katika umri wake wa utoto, ujana, utu uzima, katika kila kipindi cha maisha yake alikuwa akipigana na maadui kwa Zulfiqar yake. Bila kujali iwapo adui alikuwa akimtafuta Ali (as) au la, bali yeye alikuwa siku zote katika kuwatafuta maadui. Kwa mwenendo wake alitangaza kwamba ni nani yuko tayari kuwa na uadui na mimi katika njia ya Allah, nani yuko tayari kupigana vita na mimi katika njia ya Allah. Swali linalokuja ni kwa nini Ali (as) alinunua maadui wengi kiasi hicho? Alikuwa hana njia au mbinu za kuepukana na hili? Hapana shaka zilikuwepo njia nyingi lakini ilikuwa ni maadili ya Ali (as) ambayo yalimuelekeza moja kwa moja kwa maadui. Ghera ya Ali (as), heshima yake, ukombozi, hadhi na agano lake kwenye wajibat vilimnyanyua ili kutengeneza maadui. Ali (as) alikuwa mmiliki wa maadili mema na hivyo yeye (as) akawa mmiliki wa misiba vilevile. Wakati ikija kwenye maadili kama kujiheshimu, njia ya kujiheshimu imejaa misiba. Watu wenye kujiheshimu na wenye ghera sio wale ambao wanatembea mitaani kwa raha. Wale ambao hutoa kwa ajili ya Allah sio wale ambao hujua tu kuchukua, kwa kweli ni wale ambao wanajua kuchukua kisha kutoa kile walichokipata.
7. Wale ambao wanaokoa ngozi zao kutokana na Misiba Imamu Husein (as) amefundisha kwamba mtaa wa misiba hupita kwenye barabara 188
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 189
Maadili Ya Ashura ya maadili. Maadili ya Imamu Husein (as) haikumruhusu kukaa ndani ya nyumba yake, maadili yake matukufu yalimfanya ahangaike. Misiba yote ambayo aliipata ilikuwa ni kwa sababu ya yeye kumiliki maadili kama Kujiheshimu, Ghera, Ukombozi, Agano na utambuzi wa majukumu. Wakati wa kipindi hicho na kwa kweli katika zama zote ilikuwa ni uzuri kukaa mbali kutokana na kujiingiza katika matatizo, misiba, hoja na migogoro. Ilikuwa ni kawaida kusemwa kwamba watu lazima waokoe ngozi zao kutokana na shida, matatizo, hatari na uadui. Lakini kuna njia moja tu ya kuokoa ngozi yako kutokana na misiba, na hiyo ni kutokuwepo na maadili yoyote ndani ya mwanadamu. Hapaswi kuwa na heshima binafsi, hadhi, ghera, Infaq na utambuzi wa majukumu, na hapo ndio tu atakuwa salama na kuhifadhika kutokana na misiba. Mtu yeyote ambaye hamiliki maadili haya atakuwa salama kutokana na misiba, atahifadhika kutokana na kutengeneza maadui. Kama mtu anatamani kutokufikiwa na misiba yoyote, basi njia rahisi sana ni kutoa kuwepo kwake kutoka kwenye maadili yote na wema. Iwapo hakuna maadili, kutakuwa pia hakuna misiba yoyote. Wale ambao wanataka kuondokana na misiba kiuhalisia ni wale ambao hawana maadili kwa sababu maadili na misiba yana uhusiano wa kina.
8. Athari za Maadili Maimamu wetu Maasumin (as) wametuelekeza kwamba wakati wowote tunapokumbuka na kuzungumza kuhusu Ahlul-Bayt (as) lazima tuzungumzie yote, maadili na misiba yao. Hii ni kwa sababu maadili ya Ahlul-Bayt (as) na misiba ya Ahlul-Bayt (as) vina uhusiano wa kina, na mtu anayeelewa uhusiano huu atakuwa mfuasi wa Husein (as). Kwa kusikiliza tu maadili na misiba katika faragha, hatuwezi kuelewa asili ya maadili wala ya misiba. Maadili haya sio visa na hekaya, kama tunataka kusikiliza maadili ya Husein ibn Ali (as) basi njoo na usikilize kwa maneno yake mwenyewe matakatifu. Kama tunataka kusikiliza maadili ya AmirulMu’minin (as) basi sikiliza maneno yake mwenyewe, kwa kweli maadili hayahitaji kuzungumziwa sana, yenyewe hudhihirishwa na mwenendo wa tabia. Ni kama miski na manukato ambazo zenyewe huonesha kuwepo. Hakuna haja ya muuzaji wa manukato kuelezea sifa za manukato, kunukia kwa manukato kwenyewe hujieleza. Hivyo, maadili hayahitaji hutuba kubwa ili kuyaelezea, kwa kweli maadili yenyewe huonesha athari. Kwa athari hizi tunaweza kuona kuwepo kwa maadili mahususi na kama hakuna athari zinazoonekana basi ni wazi kwamba hakuna uwepo wa maadili.
189
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 190
Maadili Ya Ashura
9. Jaribio chafu la kuondoa Maadili kutoka kwenye nafasi zao Jaribio chafu la upotoshaji wa maadili lilifanywa katika historia kwa kuyaporomosha chini. Wakizungumzia maadili ambayo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliyazungumzia, watu waliwaondoa Ali (as) na Ahlul-Bayt (as) na kuwaweka katika muktadha mwingine. Lakini kwa vile athari za sifa na maadili hujionesha zenyewe jaribio hili lilishindwa vibaya. Mwanahistoria maarufu wa Sunni anasema: “Niseme nini kuhusu Ali ibn Abu Talib (ra), ambaye maadili yake yamefichwa na maadui kwa ajili ya uadui na marafiki kwa ajili ya woga, lakini bado leo wakati wowote tunapotupa macho yetu, tunaona maadili ya Ali ibn Abu Talib.” Kulikuwepo na tasinia zilizowekwa ili kuhusisha maadili ya Ali (as) kwa mtu mwingine, na katika shughuli hii mali nyingi, juhudi na madaraka vilitumika, lakini bado majaribio yote haya yalishindwa kwa sababu maadili hayathibitishwi kwa maneno, kuandika vitabu, kutoa hutuba na kughushi hadithi, badala yake maadili hujionesha yenyewe. Popote palipo na maadili athari yake hujidhihirisha yenyewe. Na moja ya athari za maadili ni kuwepo kwa misiba na maadili mema. Wale ambao hawanunui misiba, hawashughulishwi na shida na hatari wanajulikana kwa kutokuwa na maadili. Ibn Abil Hadid Mutazalli anaadika:
“Tuseme nini kuhusu Ali (as), ambaye maadui wake wakali pia hawawezi kujizuia kuyakubali maadili yake; hata wao hawawezi kukataa maadili na cheo chake. Ingawa unajua kwamba Bani Umayyah walikuwa kwenye mamlaka juu ya ardhi ya Waislamu kuanzia magharibi mpaka mashariki na walifanya kila juhudi 190
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 191
Maadili Ya Ashura iwezekanayo kuzima taa ya Ali (as). Waliwachochea watu dhidi yake, wakabuni tabia za kiovu dhidi yake, walitangaza kumlaani juu ya mimbari zote kama wajibu, waliwatishia na hata kuwakamata na kuwauwa wale wote ambao waliimba sifa zake, Bani Umayya walizuia watu kusimulia hadithi zile ambazo zina maadili ya Ali (as) na zenye kunyanyua hadhi yake, na walienda mbali kwa kiasi kwamba hakuna mtu aliyeruhusiwa kutumia jina la Ali. Lakini licha ya juhudi zote hizi hadhi na cheo cha Ali (as) bado viko juu. Mfano wake (as) ni kama ule wa Miski, jinsi unavyozidi kuificha kunukia kwake kunazidi kusambaa. Mfano wake (as) ni kama ule wa jua, ambalo haliwezi kufichwa kwa kiganja chako cha mkono. Yeye (as) ni kama mchana wenye mwanga ambao macho mengi yanauona hata kama mapazia yatawekwa kwenye jicho moja.” (Sharh e Nahjul Balaghah, Ibn Abil Hadid) Fakhri Razi anataja katika Tafsir Kabir kuhusiana na mjadala kuhusu suala la “Bismillahir Rahmanir Rahim” iwapo lazima isomwe kwa sauti au kimyakimya wakati wa swala. Anaandika hivi:
“Ali (ra) siku zote alikuwa akisoma Bismillah kwa sauti wakati wa swala na akasisitiza juu ya usomaji huu wa sauti. Lakini baada ya Bani Umayya walipopata madaraka kwa nguvu kabisa wakawaelekeza watu wasisome Bismillah kwa sauti wakati wa swala, hii ni kwa sababu hawakutaka kuacha hata jaribio dogo ili kutokomeza dalili za Ali (ra)… uthibitisho wa kimantiki uko pamoja nasi na matendo ya Ali (ra) vilevile yako pamoja nasi. Yeyote anayemkubali Ali (ra) kama kiongozi wake katika dini, amekamata kwa uimara kamba ya Allah katika dini yake na nafsi yake.” Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) amesema kuhusiana na Ali (as) kwamba: “Mimi ni jiji la ilmu na Ali ni mlango wake.” Kisha wengine wakaja na wakasema kwamba maadili hii sio ya mahsusi kwa Ali (as) tu, ni kwa ajili ya wengine pia. Walisema mtu fulani mwingine ni paa, mwingine ni dirisha, mwingine ni dohani, nk, kama Ali (as) ni mlango wa jiji basi kuna wengine ambao nao vilevile ni sehemu ya mji huu. 191
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 192
Maadili Ya Ashura Wanaweza kutoa majina mbalimbali, kuweka mabango makubwa, kumuita mtu kama Allama au Ayatullah; yote hayo hayana maana kama ilmu yao haipati kudhihirika. Wakati fulani Mtume (s.a.w.w.) alisema “Mimi ni Jiji la ilmu na Ali ni Lango lake, basi ilmu hii sio tu jina la maadili kwa Ali (as), hii ilidhihirishwa kimatendo katika mwenendo wa Ali (as). Hivyo, njia au kigezo cha kukubali sifa ya mtu ni kwa udhihirisho tu wa athari za sifa au maadili hayo. Kama maadili hayawezi kuonesha athari zake basi hatuwezi kuyakubali maadili hayo. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisimulia maadili ya Ahlul-Bayt (as), na maadili haya vilevile yalidhihiri kwa wazi katika maisha yao. Miongoni mwa dalili za maadili ya Ahlul-Bayt (as) ni kwa ujio wa misiba. Kiwango cha misiba ambacho kilishuka juu ya kizazi cha Mtume (s.a.w.w.) hakikushuka kwa mtu yeyote katika ulimwengu wote.
10. Maadili na misiba ya Bibi Zahra (as) Cheo kitukufu cha Bibi Zahra (as) kinachoonekana katika hadithi huishia tu kwenye maneno yalioandikwa katika hadithi hizi. Licha ya kuwa binti wa Mtume (s.a.w.w.), mke wa Ali (as), mama wa Hasan na Husein (as), pamoja na kuwa na cheo hicho kitukufu na heshima, bado maadili yake yalimfanya awe mnunuzi wa misiba. Wakati kulipokuwepo na shambulio la Wilayat. Wakati watu walipokataa kuikubali Wilayat, maadili ya Bibi Zahra (as) yalijitokeza mbele. Alikuja peke yake kabisa kwenye uwanja wa mapambano na akanunua misiba. Ingawa walikuwepo watu wakubwa mjini Madina, watu wakubwa ambao kwamba kwao kuna hadithi kubwa, lakini wakati ulipokuja wa kununua misiba hakuna hata mmoja wao aliyeinunua. Wote walimuacha Ali (as) peke yake na watu wote hawa wenye sifa walirudi nyuma na alikuwa ni Bibi huyu tu ndiye aliyetoka na kuingia kwenye uwanja wa mapambano kuonesha cheo cha maadili. Ni nani watu halisi wa sifa na maadili? Wale ambao kwao wao maneno tu ya maadili yametajwa walifunga milango yao na kutia makomeo kwa ndani. Hali sio nzuri, sio yenye manufaa, kazi ziko hatarini, masuala ya watoto na wake, yote haya yalikuwa ndio visingizio walivyofanya ili kukaa majumbani mwao. Hivi havikuwa visingizio tu bali kwa kweli walitaka kuonesha kwa vitendo vyao kwamba maadili yote yaliyozungumzwa kuwahusu wao yote yalikuwa ya uwongo na ya kubuni. Hawana maadili yoyote na kama wangekuwa nayo wangekuwa nje kwenye uwanja wa pambano. Bibi Zahra (as) alithibitisha kwamba hakuwa mwanamke mwenye maadili kwa 192
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 193
Maadili Ya Ashura sababu tu ya simulizi na hadithi zilipo kuhusu maadili yake. “Maneno na simulizi hizi ni visa vya kweli vya maadili yangu, kama mnataka kushuhudia maadili yangu kwa macho yenu wenyewe, basi njooni hapa muone kwa maadili yangu nimekuja kwenye uwanja wa misiba.” Alinunua misiba mingi kiasi kwamba yeye mwenyewe alisema:
“Misiba ambayo imenifika ilikuwa kiasi kwamba kama ingeshuka kwenye mchana mweupe ungegeuka kuwa giza la usiku.” Ewe Bibi mkubwa! Kwa nini misiba kama hii ilikushukia? Hii ni kwa sababu Bibi Zahra (as) alikuwa Bibi mwenye maadili. Idadi kubwa ya misiba ilimpata kwa sababu alikuwa na maadili makubwa katika ulimwengu wote na hakuna Bibi aliyekuwa na maadili ambayo alikuwa nayo yeye. Ni Kiongozi wa wanawake wa ulimwengu.
11. Shukurani juu ya Misiba Imamu Husein (as) alionesha pamoja na mwenendo wake safi kwamba hawezi kuikimbia misiba. Kama tunaikimbia misiba basi halikadhalika tutayapoteza maadili yetu. Mtu ambaye hana maadili amedhalilika, yu duni, mwoga na mtu mzembe. Allah amekupa bidhaa ya maadili na mbadala wa maadili haya unategemewa kuweka juu yako mwenyewe misiba yote. Lazima ubebe na kuvumilia misiba yote kwa ajili ya maadili uliyopewa. Hivyo, hata wakati mmoja Imamu Husein (as) hajalalamika, kamwe hakusema: Ewe Allah! Misiba mikubwa kama hii inakuja kwangu; natamani misiba hii isingekuja kwangu. Badala yake alionesha shukurani zake mbele za Allah (s) juu ya misiba hii. Bibi Zahra (as) alionesha kiwango cha hali ya juu cha shukurani juu ya misiba hii; alisema:
“Ewe Mola Wetu! Ukubali muhanga huu kutoka kwetu.” Bibi Zahra (as) alionesha shukurani juu ya misiba kwa sababu alijua uhusiano kati ya misiba na maadili. Alijua kwamba walikuwa wameteuliwa kwa ajili ya misiba hii kwa sababu wana maadili makubwa katika ulimwengu wote na kwa hiyo misiba mikubwa lazima iwapate. Na vilevile alijua kwamba njia ya maadili haikuwa njia ya raha na amani. 193
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 194
Maadili Ya Ashura
12. Imamu Husein (a.s) - Kigezo cha wajibu cha Maadili na Misiba Imamu Husein (as) alisema katika hutuba yake ambayo aliitoa asubuhi ya siku ya Ashura kwamba Maisha yangu ni kigezo na mfano kwa ajili yenu. Mnatakiwa tu kuangalia kile ninachofanya na kufanya hivyo hivyo. Mwenendo safi uliotakasika wa Imamu Husein (as), na yeye kama mfano amejaa maadili ya Ashura. Kama unataka kumfanya Imamu Husein (as) kigezo chako cha wajibu basi sio kwamba kwa kuchukua tu jina lake atakuwa kigezo chetu cha wajibu. Ili kumfanya Imamu Husein (as) kigezo chetu tutalazimika kuchagua njia ya misiba, lazima tupite juu ya njia ya Husein (as), na hii ni njia ambayo hupita kwenye vichochoro vya misiba ili kufika kwenye mabonde ya maadili. Hii ni kwa sababu Imamu Husein (as) amesimama katika uwanja wa mapambano katika siku ya Ashura, katika siku ya misiba, katika ardhi ya misiba, na wakati alipojipanga miongoni mwa sahaba zake, Hurr bin Yazid Riyah anatoa hutuba ambapo anasema: “Kama unataka kumfanya mtu huyu ambaye amesimama katika uwanja wa misiba kama Kigezo chenu cha Wajibu, basi hakikisheni kwamba mtalazimika kuchagua matatizo mengi kama hayo na misiba. Mwisho wenu utakuwa kama sawa kama ule Husein bin Ali (as). Kabla ya kuingia katika ulimwengu wa misiba lazima wenyewe mjizoeshe na maadili, kwa sababu kama mtu anaondoka kwenye ulimwengu wa maadili na kuingia kwenye ulimwengu wa maovu na udhalili basi hakuna misiba itakayompata. Ili kufikia bonde la maadili itakubidi kununua misiba.”
“Mimi ni Husain mwana wa Ali na Fatima binti ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, nafsi yangu ipo pamoja na nafsi zenu, familia yangu ipo pamoja na familia zenu, mimi ni kigezo chema kwenu.” (Mawassae Kalemat Imam Hussain, uk. 369) Katika barua iliyopelekwa kwa Ashraf bin Sard Khazi’i wa Kufa, alitaja hivyo hivyo yaani kumfanya Kigezo cha wajibu. “Nafsi yangu ipo pamoja na nafsi zenu, familia yangu na wanangu ipo pamoja na familia zenu na watoto wetu, mimi ni kigezo chema kwenu.” (Mawassae Kalemat Imam Hussain, uk. 377) 194
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 195
Maadili Ya Ashura
13. Kila siku ni Ashura na Kila ardhi ni Karbala Imamu Husein (as) alisema kwamba maisha yake ni kigezo kwa ajili yetu na hii itatokea tu wakati tutakapoyaendeleza maadili haya ya Ashura, yaani, maadili haya ya Husein (as) katika tabia zetu. Wakati maadili na sifa hizi zikijengeka ndani ya mtu basi suala la Husein (as) kuwa kigezo chetu hupata mwanga.
“Kila ardhi ni Karbala na Kila siku ni Ashura.� Ardhi ya Karbala haiwi tu Karbala kwa jina lake. Siku ya Ashura vilevile haiji kwa kuitaja tu siku hiyo kama siku ya Ashura. Kwa kuomboleza tu siku ya Ashura, siku hii haiwi Ashura hivi hivi, ili kupata asili yake ya kweli lazima tuifanye siku hii kama siku ya Ashura. Tunahitaji kulipima hili kwa uangalifu kwamba kile tunachofanya katika jina la Ashura na Arobaini ni maombolezo tu ya kumbukumbu ya mwaka ya kihistoria ya siku hizi. Je tunaambiwa kufanya maombolezo tu katika siku hizi? Je tumeambiwa kuadhimisha tu programu za kumbukumbu za mwaka za Imamu Husein (as) kama tufanyavyo kwa watu wengine waliokufa wa familia zetu na marafiki? Je, ni kwa sababu tu ya kuhuisha kumbukumbu za haiba za marehemu (Imamu Husein (as)), kuwa na majadiliano fulani katika jina lake na kisha baada ya hapo kwa mwaka mzima huna habari naye na kuendelea na biashara zetu? Tumeambiwa kwamba kila siku ni siku ya Ashura, unaweza kufanya kila siku kama siku ya Ashura, unaweza kubadilisha kila ardhi kuwa Karbala, hivyo vipi kila siku itabadilishwa kuwa Ashura, na vipi kila ardhi itabadilishwa kuwa ardhi ya misiba? Kuna njia moja ya kufanya hivi, na njia hii ni kuhuisha maadili ya Husein (as) katika maisha yetu. Siku ambayo maadili haya yanahuika kwetu, siku hiyo itakuwa siku ya Ashura. Ardhi ambayo maadili haya yanahuishwa huwa ni ardhi ya Karbala. Kama unachukua tu jina la Husein (as), ukaandaa Majalis kwa ajili ya kuomboleza lakini huna maadili yake, basi siku hiyo inaweza kugeuzwa kama siku ya kumbukumbu (Barsi) na sio siku ya Ashura. Hii ni kwa sababu Ashura ni jina la uwanja wa misiba. Kama misiba haiwapati basi kuna upungufu wa maadili na sifa njema. Hivyo wale ambao hugeuza migongo yao kwenye misiba kamwe hawawezi kutenda juu ya maadili ya Imamu Husein (as). Kama kila siku ni lazima iwe Ashura 195
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 196
Maadili Ya Ashura basi Imamu Husein (as) ametoa njia kwa ajili hiyo kwa maandishi. Njia hii ni kwamba kamwe usingoje siku ya kumi ya mwezi wa Muharram; usiseme kwamba katika ulimwengu wote kuna kipande kimoja tu cha ardhi kwa jina la Karbala. Lakini kwa kweli siku unayopenda unaweza kuifanya Ashura. Kila mmoja anajua kwamba ardhi ya Karbala ilikuwepo kabla ya Imamu Husein (as) kuwasili na halikadhalika siku ya kumi ya mwezi wa Muharram ilikuwepo kwenye kalenda kabla ya kadhia ya Karbala kutokea. Lakini alikuwa ni Imamu Husein (as) ambaye kuwasili kwake kwenye ardhi hii kuligeuza jangwa hili kuwa Karbala na siku hii ya kumi ya Muharram kama Ashura kwa kuhuisha maadili ya uungu katika ardhi hii na siku hii. Kama pia tunaweza kuendeleza maadili ya Imamu Husein (as) na kama pia tunaweza kuhuisha maadili haya, basi katika ardhi yoyote tutakayokuwa itakuwa ardhi ya Karbala na siku ambayo maadili haya yatahuishwa itakuwa siku ya Ashura.
14. Ashura ni Siku ya Allah (s) Mayazidi wamejaribu kuihusisha siku ya Ashura na Yazid na kuifanya siku hii kama siku ya Bani Umayya. Kama rejea inafanywa katika historia tunaweza kuona kwamba zimetaja adabu nyingi za siku hii. Rejea hizo zimeelekeza mambo mengi kwa ajili ya siku ya Ashura, kama siku ya sherehe, kuvaa nguo mpya na kugawa tamtamu. Bani Umayya walijaribu kuifanya siku hii kama siku ya Idd. Walianzisha vitu fulani, kama vitendo vya kusherehekea kama mfano wa Idd. Walikuwa na fikra kwamba kama wakiifanya siku hii kama siku ya Idd kwa watu basi siku hii itakuwa siku ya Yazid na siku ya Bani Umayya. Imamu Husein (as) alitaka kuifanya siku hii kama siku ya Allah , hivyo, aliifanya siku hii kama siku ya Allah daima na kuiwasilisha siku hii kwa watu kama siku ya Ashura ya Husein (as). Aliifanya ardhi ya Karbala kama Karbala ya Husein (as) na hii ilikuwa ni kwa sababu yeye (as) alihuisha maadili ya uungu katika siku hii na hivyo kuifanya siku hii kama siku ya Allah (s). hata leo iwapo siku ya Ashura au jina la Karbala linapokuja kwenye akili zetu, jina la Imamu Husein (as) pia huja mara moja kwa sababu katika siku hii Imamu Husein (as) alikuwa muelemishaji wa maadili hayo ya uungu, ambayo daima aliyaweka maadili ya Ashura ya Husein (as) hai na Ashura daima itakuwa siku ya Allah (s) Ashura ni siku ya misiba na kwa vile misiba ni matokeo ya maadili, hivyo Ashura vilevile ni siku ya siku ya maadili. Kwa maneno mengine ni siku ya kuzaa maadili ya Husein (as) na maadili ya uungu katika nafsi zetu. Kama maadili yanazaliwa 196
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 197
Maadili Ya Ashura ndani yako basi misiba itakuja kwa ajili yako na kama misiba haiji maadili haya yatakufukuzia kwenda kwenye misiba na utaanza kutafuta misiba. Ni kwa ajili ya maadili kwamba wanadamu hujenga uwezo na nguvu ili kubeba misiba kwa uvumilivu (Istiqamat). Wale ambao hawana maadili, punde wanapokuwa na mapambano kidogo na misiba wanaanza kuomboleza juu yake, wanapoteza mwelekeo wao, na wao wenyewe na Mola wao. Misiba mikubwa ambayo ilishuka kwa Imamu Husein (as) siku ya Ashura ni visa vya maadili makubwa yanayomilikiwa na Imamu Husein (as). Alimsimulia Imamu Husein (as) na akasema:
“Ewe Aba Abdillah! Hakuna siku kama siku yako� (Mawassae Kalemate Imam Husain (a.s), uk. 217)
197
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 198
Maadili Ya Ashura
Maadili ya Kumi Dhabihu (Isaar) 1. Dhabihu – Maadili ya Ashura..........................................................................199 2. Maana ya Dhabihu...........................................................................................200 3. Dhabihu katika mtazamo wa Qur’ani..............................................................201 4. Dhabihu miongoni mwa Maasumin (a.s).........................................................202 5. Mashahidi wa Uhud – Kujitokeza kwa Dhabihu.............................................203 6. Ahlul-Bayt (a.s) – vigezo bora vya Dhabihu...................................................203 7. Imamu Sajjad (a.s) – Kigezo cha Wajibu cha Dhabihu...................................207 8. Imamu Sadiq (a.s) – Mtangaza imani ya Dhabihu..........................................210 9. Karbala – Miraji ya Dhabihu............................................................................211
198
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 199
Maadili Ya Ashura
1. Dhabihu – Maadili ya Ashura Siku ya Ashura, Imamu Husein (as) mara nyingine tena alihuisha maadili kubwa ya mwanadamu, akayahubiri kwa wanadamu, aliwafanya sahaba zake na wafuasi wake kuyatekeleza, yeye mwenyewe alitenda juu ya maadili hayo, alijenga mvuto wa maadili hayo kwa Bani Hashim na akatangaza katika kambi ya maadui kwamba kama wanataka kuona wafuasi wa mwenendo wa mwanadamu, maadili, sifa za uungu na mkusanyiko wa maadili ya Husein (as), basi haya yote yalikuwepo katika jeshi la Husein (as). Kwa idadi jeshi hili lilikuwa dogo sana, la kuweza kuhesabika kwa vidole, lakini kuhusu ubora na sifa jeshi hili lilimiliki mamilioni kwa sababu maadili na mwenendo ambao ulionekana kwao, vyote na kila sifa na ubora wao ulikuwa mzito juu ya wanadamu elfu moja. Hivyo vilevile matokeo yalikuwa sawa wakati mujahidina mzee sana aliyekonda kutoka jeshi la Husein (as) alipotoka na kuingia kwenye uwanja wa mapambano kumsaidia Imamu Husein (as), akaujaza uwanja kwa miili ya maadui kila upande. Habib ibn Mazahir alikuwa mzee wa miaka tisini, mpiganaji wa maadili, dhabihu bora, wakati alipopambana na maadui, walifuata njia za kumkimbia. Ingawa umri wake mkubwa haukumruhusu hata kunyanyua upanga, kupanda farasi, kubeba ngao, kupigana kwa mkuki, kuzuia au kutupa mishale, lakini bado ari yake kwa ajili ya Dhabihu na kutoa kila kitu imedhihirisha shauku, hadhi yake na uwezo wake katika hali ambayo kwamba kuwepo kwake tu pale ilikuwa ni kukali zaidi kuliko silaha yoyote ambayo ingeweza kuwakata maadui vipande vipande. Kiongozi wa Mashahidi (as) hakuwashawishi masahaba wake kwa ahadi za kuwafanya magavana wa baadhi ya majimbo kama Kufa na Rae. Kwa kweli kabla ya kuanza safari yake aliwalingania kwa wito kwamba kama wanataka fursa za ulimwengu huu na Akhera basi lazima washiriki katika msafara huu wa fursa, ambako watapoteza maisha yao, watakatwa vichwa, ambako watalazimika kuviacha vitu vingi vya ulimwengu huu, lakini sifa zote za uungu na maadili ya kidini vyote vitakuja chini ya ulinzi wao. Hivi ndivyo watakavyokuwa vigezo vya wajibu kwa wanadamu mpaka mwisho wa ulimwengu huu, na watu watawaangalia wao ili kujenga mwenendo wao wenyewe. Wakati ambapo jeshi la madhalimu lilikuwa limetegemea juu ya idadi kubwa, hii ni kwa sababu wana maadili hasi na sifa za kishetani. Jeshi hili litakuwa lenye kulaaniwa na wanadamu wote. Miongoni mwa maadili haya ya fursa, Dhabihu na kutoa kila kitu ilikuwa ni maadili ambayo yalikuwpo katika kila askari wa jeshi la Kiongozi wa Mashahidi 199
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 200
Maadili Ya Ashura (as). Hivyo mifano mizuri ya dhabihu ilioneshwa na mashahidi wa Karbala kwa damu zao. Kuanzia siku ya pili ya Muharram wakati jeshi hili lilipokanyaga juu ya uwanda wa Karbala mpaka siku ya Ashura wakati ambapo hata kamanda wao aliuawa shahidi, katika kila hatua mifano kama hii mitukufu ya dhahibu inaonekana ambayo haiwezi kuonekena popote pale. Hivyo ni ukweli ulio wazi kwamba “Dhabihu (Isaar)” ni maadili ya Ashura.
2. Maana ya Dhabihu. Dhabihu ni moja ya maadili kubwa ya mwanadamu ikiwa na cheo kitukufu na hadhi kubwa. Dhabihu ni hatua ya mwisho ya ukarimu na yenyewe ina madaraja mbali mbali na viwango, ambavyo kwamba kiwango cha heshima zaidi cha dhabihu ni kutoa maisha katika njia ya Allah. Hivyo maana ya Dhabihu ni kutekeleza haja za watu wengine licha ya wewe mwenyewe kuwa mhitaji. Ina maana kupuuza haja zetu na kutoa kipaumbele kwa wengine. Wakati wowote uzuri na manufaa vinapoonekana mwanadamu lazima achukuwe hatua moja nyuma kutoa kipaumbele kwa mtu mwingine kusaidia haya, lakini kuna shida, misiba, matatizo na hasara zitakazopatikana, mwanadamu lazima aweke wengine nyuma na yeye mwenyewe kwenda mbele. Hii ni asili ya Dhabihu. Kama ilivyosemwa: Ukarimu na ubahili vyote vina madaraja na viwango. Kiwango cha juu sana cha ukarimu ni dhabihu. Dhabihu maana yake licha ya haja na mahitaji yako mwenyewe, unatoa mali yako kwa wengine, wakati ambapo ukarimu wenyewe una maana kutoa kile ambacho ni ziada. Lakini kutoa kitu ambacho wewe mwenyewe una haja nacho na mahitaji ni mazito, basi Dhabihu ni kiwango cha juu cha kutoa katika njia ya Allah (s).
“Tambua hakika ukarimu na ubahili kila kimoja kinagawanyika katika daraja mbalimbali, na hakika daraja la juu zaidi la ukarimu ni kumpendelea mwenzako, nako ni kutoa mali ingawa unaihitajia. Ama ukarimu wenyewe ni kutoa mali kwa muhitaji au kwa asiyekuwa muhitaji, na kuitoa kwa muhitaji ni ukarimu zaidi.” (Majmua Viram, Jz. 1, uk. 172) 200
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 201
Maadili Ya Ashura Katika njia hiyo hiyo Abil Hadid Mu’tazilli anaandika:
“Ukarimu (Sakhawat) ni hatua ya kwanza ambapo baada yake huja Upaji (Utoaji) wa hali ya juu (Juud) na kisha huja Dhabihu (Isaar). Mtu ambaye hutoa kitu kwa wengine na kuweka kitu kwa ajili yake mwenyewe ni mkarimu, wakati ambapo mtu ambaye hutoa zaidi kwa wengine na kuweka kidogo kwa ajili yake ni mpaji (mtoaji) wa hali ya juu. Lakini mtu ambaye hutoa kipaumbele kwenye haja za wengine juu ya haja zake zote na kuwapa wengine hata kile ambacho kilikuwa muhimu kwake mwenyewe, ni mtu ambaye hutoa Dhabihu (Isaar). (Sharh Nahjul Balaghah, Jz, 11, uk. 233) Dhabihu ni maadili kubwa mno ambayo huanza na kitu kidogo sana. Mifano midogo ya dhabihu yaweza kuonekana usiku na mchana katika maisha yetu. Kama mwanadamu ataendeleza sifa hii ya ki-Huseini katika nafsi yake basi maelfu ya fursa ya Dhabihu huja katika maisha yake. Imamu Ali (as) anasema:
“Usiogope kutoa kidogo, kwa sababu kumrudisha mtu mikono mitupu ni kitendo duni sana..” Lakini ubahili wetu, ubinafsi na haja imefanya maadili hii ya Dhabihu kutekwa na hivyo hatuwezi kuona haja za wengine. Kuna watu wengi sana katika maeneo yetu, ndugu ambao wana haja ya msaada wetu; kuna wengi wana maradhi, njaa, watu masikini ambao mahitaji yao yanaweza kutekelezwa na sisi. Lakini tumeweka Dhabihu nyuma ya migongo yetu na tumesahau maadili hii ya Husein (as). Kama sifa hii ya Dhabihu ikijengeka katika nafsi zetu basi inaweza kubadilisha rangi ya jamii yetu, hakuna mwanadamu ambaye atakuwa na haja na hakuna ombaomba watakaoonekana.
3. Dhabihu (Isaar) katika uoni wa Qur’an Dhabihu ni maadili ya Ashura na Qur’ani Tukufu ambayo kwamba Qur’ani imependezewa mno nayo.
201
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 202
Maadili Ya Ashura Allah anasema katika Qur’ani Tukufu:
“Na waliofanya maskani na imani yao kabla yao, wanawapenda waliohamia kwao wala hawapati dhiki katika vifua vyao kwa walivyopewa, na wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji. Na mwenye kuepushwa na uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufaulu.” (Surah Hashr – Ayah 9)
“Wanatimiza nadhiri, na wanaiogopa siku ambayo shari yake inaenea. Na huwalisha chakula, juu ya kukipenda kwao, masikini, na yatima, na mateka. Hakika tunawalisha kwa wajihi wa Mwenyezi Mungu tu. Hatutaki kwenu malipo wala shukrani. “ (Surah Insaan – Ayah 7,8,9)
4. Dhabihu (Isaar) miongoni mwa Maasumin (a.s) Kuna hadithi nyingi zinazopatikana kutoka kwa Maimamu Maasumin (as) kuhusiana na Dhabihu. Maimamu Maasumin (as) waliitekeleza maadili hii na walikuwa wakiwalingania na kuwavutia wengine kwenye maadili hii kubwa. Tunaweza kupata mifano mingi mikubwa ya Dhabihu kama tunachambua mwenendo wa Maimamu Watukufu (as). Katika taarifa hii tunawasilisha hapa baadhi ya hadithi: Imamu Ali (a.s) anasema:
“Kutoa kipaumbele kwa wengine hudhihirisha thamani ya ukarimu wa watu wakarimu.” (Gararul Hikam, Burudul Kalam, uk. 396) 202
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 203
Maadili Ya Ashura
“Ewe Ali! Ukweli wa imani uko katika mambo matatu (1) Kutoa wakati ukiwa katika hali ya dhiki, (2) Kuwa mwadilifu kwa wengine kama nafsi yako mwenyewe (3) Kufundisha ilmu kwa waitafutao. (Wasaelus Shia, Jz. 9, uk. 430)
“Muhanga (Isaaar) ndio kubwa kati ya matendo yote na ndio kiwango cha haliya juu cha imani.” (Gararul
Hikam, Burudul Kalam, uk. 396).
5. Mashahidi wa Uhud – Kujitokeza kwa Dhabihu (Isaar) Katika ujio wa Uislamu, Waislamu walionesha mifano mikubwa ya Dhabihu. Answar (Wasaidizi) walitoa dhabihu kwa Muhajirin (Wahamiaji) na Muhajirin walitoa dhabihu kwa ajili ya Answar katika vita vya Uhud wakati majeruhi walipokuwa wana kiu, na mtu aliyejeruhiwa husikia kiu sana kwa sababu ya damu kutoka mwilini. Katika vita hivi majeruhi saba walikuwa wamelala chini katika hali ya kiu kali. mbebaji maji alikuja, lakini alikuwa na kiasi tu cha kumtosha mtu mmoja. Wakati alipokuja kwa majeruhi wa kwanza, majeruhi yule akamuashiria majeruhi mwingine huku akisema ana kiu zaidi kuliko mimi hivyo apewe yeye kwanza. Wakati mbebaji maji alipokwenda kwa majeruhi wa pili, alimuashiria kwa majeruhi wa tatu. Kwa njia hii alikuwa akienda kwa kila majeruhi na kila majeruhi humuambia aende akampe mwingine kwanza, na wakati alipofika kwa majeruhi wa mwisho majeruhi wa kwanza akafariki. Kwa njia hiyo majeruhi wote saba wakafariki lakini hakuna hata mmoja aliyekunywa maji yale. Hivyo walitoka katika ulimwengu huu wakiwa na majeraha na kiu lakini walionesha mfano mkubwa wa Dhabihu (Isaar). (Majmaul Bayan – Jz. 9, uk. 391)
6. Ahlul-Bayt (a.s) – Viwango vya Dhabihu (Isaar) 203
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 204
Maadili Ya Ashura
Ahlul-Bayt (as) ni mfano wa viwango vya Dhabihu kwamba hakuna yeyote awezaye kupatikana na kushindana nao. Vitabu vya matukio ya kihistoria vimejaa hadithi kuhusu dhabihu za Amirul-Mu’minin (as). Katika usiku wa kuhama kwa Mtume (s.a.w.w.) Amirul-Mu’minin (as) alitoa maisha yake mwenyewe kwa kulala kwenye kitanda cha Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.). Hivi ndivyo ilivyo daraja ya mwisho na ya juu ya dhabihu na hivyo Allah (s) alizungumza na Malaika kuhusu dhabihu hii Amirul-Mu’minin (as). Allah (s) alimsifia Amirul-Mu’minin (as) mbele za Malaika na kisha Malaika mwenye uaminifu mkubwa Jibril (a.s.) alishuka na Aya hii Tukufu kwa kumsifia Amirul-Mu’minin (as):
“Na katika watu yuko auzaye nafsi yake kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa waja.” (Surah Baqrah, Ayah 207). (Merajus Saada Ahmad Naraqi, uk. 377) Nani anaweza kuwa mfano wa dhabihu kubwa kama hii? Kitu gani kinaweza kuwa cha mfano mkubwa wa dhabihu kuliko huu? Qur’ani Tukufu imepiga muhuri wake kuridhia kwa dhabihu hizi za Ahlul-Bayt (as) kwenye sehemu nyingi. Katika mijadala iliyopita kuhusu maadili ya Kutoa katika njia ya Mwenyezi Mungu (Infaq) matukio ya Amirul-Mu’minin (as) na bibi Fatima Zahra (as) kuhusiana na Kutoa katika njia ya Mwenyezi Mungu (Infaq) vilevile hutumika katika muktadha ndani ya maadili ya dhabihu, hivyo kwa ajili ya ufupisho tunaachia hapa. Kama tukitafakari juu ya Sura Hal Ata, sura yote imeshuka kwa kuwasifia AhlulBayt (as). Wakati wanataja sifa za kushuka kwake, wafasiri wanasema kwamba wakati fulani Hasanain (as) (yaani, Hasan na Husein) walikuwa wagonjwa. Imamu Ali (as) na Bibi Fatima (as) waliweka nadhiri kwa ajili ya ustawi wao wakisema kwamba watafunga siku tatu wakati wakipona. Baada ya kupona kwao Ali (as), Fatima (as) na Fizza walifunga. Nyumbani mlikuwa hamna kitu cha kula hivyo Ali (as) alitoka na akarudi na unga wa shairi aliokopa kutoka kwa mtu fulani. Alimpa Bibi Fatima (as), ambaye kwa mikono yake mitukufu alitayarisha chapati na akaziweka tayari kwa ajili ya kuliwa baada ya Magharibi kama futari wakati Ali (as) atakaporudi nyumbani. Familia hii ilikuwa imeanza tu kukaa kwenye kitanga cha chakula mtu mmoja akagonga mlango. Fizza akaenda kuuliza, yule mtu akasema mimi ni muombaji 204
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 205
Maadili Ya Ashura ambaye nimekuja kwenye mlango wa Ahlul-Bayt (as), na nina njaa na watoto wangu wana njaa. Wakati Ali (as) aliposikia hivi alitoa sehemu yake akampa yule omba omba. Fatima (as) naye akatoa sehemu yake akampa yule omba omba. Fizza alipoona hivi, alisema kwamba mimi pia nimelelewa katika familia hii na vilevile nimejifundisha masomo ya dhabihu, hivyo na yeye akasimama akampa sehemu yake. Wakati Hasan na Husein (as) walipoona hivi, nao pia wakatoa mgao wao wa chakula wakampa yule muombaji. Hivyo baada ya kufunga siku nzima walifuturu maji kisha wakalala. Walifunga tena siku iliyofuatia; ilipofika jioni na mara tu chakula kilipowekwa kwa ajili ya kufuturu, tena mtu akagonga mlangoni. Wakauliza ni nani. Jibu lilikuwa kwamba mimi ni yatima, ni muhitaji na nina njaa. Ali (as) akatoa sehemu yake akampa yule yatima, akifuatiwa na Fatima (as), kisha Fizza na Hasanain (as) pia wakatoa sehemu zao wakampa yule yatima. Hivyo siku ya pili pia walikunywa maji wakalala baada ya saumu ya siku nzima. Kisha tena siku ya tatu wakafunga, wakati wa kufuturu mtu akagonga mlangoni. Walipouliza jibu lilikuwa kwamba mimi ni mfungwa na nina njaa na nahitaji chakula. Katika hali ile ile kama ilivyokuwa siku mbili zile zilizopita, wote familia ile ya Mtume (s.a.w.w.) na Fizza wakatoa chakula kile wakampa yule mfungwa. Tena wakanywa maji kisha wakalala baada ya siku tatu mfululizo za kufunga na hivyo wakakamilisha nadhiri yao ya kufunga siku tatu. Wakati Ali (as) alipokuja kwa Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) pamoja na Hasanain (as), Yeye (s.a.w.w) aliona dalili za njaa na udhoofu kwenye nyuso za Hasanain (as) na akaanza kulia. Wakati Allah alipomuona kipenzi chake katika hali ile ya huzuni, alimtuma Jibril na Sura hii ya Hal Ata au Insaan na kisomo chake kikawa ni kitendo cha ibada kwa Waislamu wote. (Majmaul Bayan Jz. 10, uk. 611-613) Sura hii kwa hakika ni Sura ya Insaan (maana yake Sura ya wanadamu), huu ni mfano na kigezo cha wanadamu, dhahibu ambayo mwanadamu ameionesha na kuwasilishwa katika sura hii haipatikani popote pale. Sura imetwa Surah Insaan (mwanadamu), kwa sababu sura hii iliteremshwa kwa kuafikiana na dhahibu za wanadamu hawa.
205
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 206
Maadili Ya Ashura
“Wanatimiza nadhiri, na wanaiogopa siku ambayo shari yake inaenea. Na huwalisha chakula, juu ya kukipenda kwake, masikini, na yatima, na mateka.Hakika tunawalisha kwa wajihi wa Mwenyezi Mungu tu. Hatutaki kwenu malipo wala shukrani.“ (Surah Insaan – 7, 8, 9) Wanachuoni wameandika katika muktadha pamoja na mijadala inayohusika na mapenzi ya Ali (as) kwamba licha ya kwamba wao wenyewe walikuwa na haja ya chakula, walikuwa na hamu ya kula, walikuwa na njaa na wamefunga lakini kwa kuonesha Dhabihu (Isaar) walitoa chakula chao kwa yatima, masikini na mfungwa. Ni wapi tunaweza kupata mfano mkubwa kuliko huu kwa ajili ya Dhabihu? Haya ni mafundisho ya Maimamu wetu (as), ambamo kwamba wanaweza kuvumilia njaa yao wenyewe lakini masikini anapogonga mlangoni mwao hawawezi kulivumilia hilo la kwamba abakie na njaa na wao wale washibe. Ibn Abil Hadidi anaandika hivi:
“Sijaijiwa na mgeni tangu siku saba zilizopita, nakhofia isiwe Mwenyezi Mungu amenikasirikia.” (Sharhe Nahjul Balaghah, Jz. 11, uk. 242) Siku moja mtu mmoja alimuona Amirul-Mu’minin (as) akiwa amehuzunika na akamuuliza sababu yake. Yeye (as) akasema: “Imefikia juma zima sasa na hakuna masikini aliyekuja kwangu, nahofia isije Allah akawa amenipuuza.” Huu ni mwenendo wa Maimamu wetu (as) ambapo kama hakuna masikini anayekuja kwao kwa muda wa siku saba wanalia kwa kumuogopa Allah. kama tunaangalia watu wa karibu yetu, katika maeneo yetu na miji yetu, tunaweza kuona wengi wakihitaji msaada wetu. Kama tuna chakula majumbani mwetu lakini watoto wa jirani yetu wanalala na njaa basi vipi tutastahiki kuitwa wafuasi wa Amirul-Mu’minin (as)? Kama tu miongoni mwa wafuasi wa Ali ibn Abi Talib (as), waumini wa Husein ibn Ali (as), basi ziwapi tabia zile za Husein (as), maadili yale ya Ashura na sifa za Ali (as)? Kama wafuasi wa Ali ibn Abu Talib (As) hawana maadili ya Dhabihu basi Dhabihu haiwezi kutegemewa kwa wengine. Imamu Ali (as) anasema kuhusiana na Dhabihu ya Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.):
206
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 207
Maadili Ya Ashura
“Huu ulikuwa mwenendo wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba wakati vita vilipokuwa vinafikia kilele chake na wapiganaji wakaanza kurudi nyuma, katika hali hii Mtume (s.a.w.w.) alipeleka watu wa familia yake mbele kama ngao kuwalinda masahaba kutokana na mishale na mikuki. Hivyo katika vita vya Badr, Ubaida ibn Haris (binamu wa Mtume (s.a.w.w.)), katika Uhud, Hamza (as) na katika vita vya Mu’ta, Ja’far (as) waliuawa shahidi.” Kisha Amirul-Mu’minin (as) anasimulia kuhusu yeye mwenyewe kuhusiana na hili:
“Kama nikitaka naweza kutaja jina la mtu mwingine vilevile ambaye alitamani kufa shahidi kama mashahidi hawa, lakini kwa wao maisha yao yalikoma mapema lakini kwa ajili ya mtu huyu kifo chake kilibakia nyuma. Nashangazwa katika nyakati hizi ngumu wakati jina langu linatajwa pamoja na wale ambao hawakuonesha ule ukali katika uwanja wa mapambano kama mimi mwenyewe na wala hawana huduma ndefu kwenye Uislamu kama niliyonayo mimi.” (Nahjul Balaghah, barua ya 9, uk. 660)
7. Imamu Sajjad (a.s) – Kigezo cha Wajibu wa Dhabihu (Isaar) Imamu Zainul Abidiin (as) ana jina la Sayyadus Sajidin (kiongozi wa wale ambao wanasujudu), na kwa sababu ya kufanya ibada na kusujudu sana, watu wamezoea kumuita Zainul Abidiin (fahari ya wenye kuabudu). Yeye (as) alizoea kufunga wakati wa mchana na kuomba mbele za Allah (s) kwa ibada zake za usiku. Lakini mbali ya ibada na uchaji, sifa iliyo wazi zaidi ya mwenendo wake ilikuwa ni Dhabihu na huduma kwa Muumba. Wakati yeye (as) alipofanyiwa josho la mwisho la kiibada baada kifo chake cha kishahidi, mtu aliyekuwa anamkosha akaona kovu kubwa kwenye mgongo wake, aliuliza kwa mshangao kuhusu chanzo cha makovu haya kwenye mgongo wake. Mtu mmoja akasema kwamba huenda ni makovu ya viboko, ambavyo alipigwa mgongoni mwake baada ya Karbala. Mtu mwingine akasema kwamba huenda ikawa ni makovu ya kamba na minyororo ambayo alifungwa baada ya Karbala. Mwingine akasema kitu kingine. Lakini wakati mtoto wake Imamu Baqir (as) 207
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 208
Maadili Ya Ashura alipoulizwa sababu ya makovu haya, alisema; hizi alama za magunia ya nafaka, wakati mheshimiwa baba yangu alipoamka kwa ajili ya sala za usiku, basi kabla ya sala alikuwa akibeba magunia ya nafaka na chakula mgongoni mwake na kuzitoa kwenye nyumba za watu masikini. “Imamu Baqir (as) anasema: “Baba yangu, Ali ibn Husein (as) alichukua wajibu wa gharama za familia masikini mia moja za mjini Madina. Alikuwa anajisikia raha sana kwa kupeleka chakula kwa yatima, mafukara, walemavu na masikini ambao hawana njia nyingine za kujipatia riziki. Alikuwa akiwapa chakula kwa mikono yake mwenyewe. Miongoni mwa familia hizo wako ambao walikuja kwake (as) na kuchukua chakula kwa ajili ya familia zao kutoka kwenye chakula chake (as). Yeye (as) alikuwa akitekeleza kutoa sadaka kabla ya kila mlo.� (Manakibe Aale Abi Talib, Jz. 3, uk. 293) Imesimuliwa katika hadithi nyingine kutoka kwa imamu Baqir (as): Ilikuwa ni tabia ya Ali ibn Husein (as) kutoa sadaka kwa kubeba magunia ya mikate juu ya mgongo wake. Masahaba wake; Abu Hamza Thumali na Sufyan Puri walisema kwamba Imamu (as) alisema kwamba kutoa sadaka kwa siri hutuliza ghadhabu ya Allah (s) (Manakibe Aale Abi Talib, Jz. 3, uk. 293) Imamu Sajjad (as) alikuwa akitembelea nyumba na kugonga milangoni mwao, na huku akiwa ameficha uso wake aliweka magunia yale na kurudi nyumbani. Je, sio kwamba Allah (s) atawauliza wale ambao wanaswali swala zao za usiku (Tahajjud) kuhusu hali ya majirani zao, kuhusu hali ya eneo lao? Majirani zako wanakufa kwa njaa na umekuja kunidanganya kwa swala zako za usiku? Umekuja kuswali rakaa mbili za swala za usiku? Umekuja kufanya dhabihu ya rakaa mbili za swala za usiku Kwangu? Kwanza nenda, fanya dhabihu, kwanza nenda na tekeleza haja za masikini na kisha njoo kwenye hadhara Yangu. hii ni kwa sababu hawa ni viumbe wa Allah (s) na Allah (s) anawapenda viumbe wake sana kiasi kwamba Imamu Ridha (as) anasema;
Mtu ambaye hana shukurani kwa viumbe vilevile hana shukurani kwa Muumba. (Uyuune Akbare Raza, Sheikh Sadook, J. 13, uk. 24)
208
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 209
Maadili Ya Ashura Kwa hiyo mtu ambaye hana maana kwa viumbe hawezi kuwa na maana yoyote kwa Muumba. Barabara inayokwenda kwa Muumba hupitia kwa viumbe. Wale ambao hujitenga na viumbe na kujaribu kumtafuta Muumba wao katika nyumba za watawa wa Kisufi, lazima watambue kwamba Muumba hatafutwi kwenye nyumba za watawa na kwenye faragha. Muumba hapatikani kwa kujitenga kutoka kwa viumbe, Muumba yupo miongoni mwa viumbe. Muumba anaweza kupatikana kwa kuanzisha huduma za kibinadamu na kuhudumia wanadamu. Kama Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) anaulizwa, Maimamu Watukufu wanaulizwa kuhusu ni wapi pa kumtafutia Muumba? Watasema tu hivi; kwa kujitenga na jamii hutampata Muumba, kwa kweli, kama unataka kumuona Muumba wako basi anaweza kuonekana katika huduma kwa viumbe. Imetajwa katika hadithi kwamba siku moja Mjumbe wa Allah (s.a.w.w.) aliuliza aliko sahaba fulani ambaye alikuwa haonekani kwa muda mrefu. Alijibiwa kwamba sahaba wake amekwenda milimani kumuabudu Allah (s). Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema kuhusu yeye:
“Kuonesha subira na uvumilivu katika kutatua matatizo na shida zinazohusiana na ardhi za Kiislamu ni bora kuliko miaka arubaini ya ibada katika faragha.” (Miizanul Hikmat, Jz. 3, uk. 2720) Kuna msisitizo wa hali ya juu kuhusu ibada kwa Muumba na kutekeleza haja za waumini uliotajwa katika hadithi. Katika moja ya hadithi imesemwa kiasi cha kwamba kutekeleza haja ya mumini ni sawa na mizunguko kumi (Tawaf) ya Kaaba Tukufu. Imamu Sadiq (as) alimwambia Isaak ibn Ammar: “Ewe Isaak! Allah huandika matendo mema elfu moja katika hesabu ya mtu ambaye hufanya tawaf ya Nyumba ya Allah na kuondoa dhambi elfu moja kutoka kwenye hesabu yake, Allah hunyanyua cheo chake kwa daraja elfu moja, hupanda miti elfu moja katika Pepo kwa ajili yake, huandika malipo ya kumwacha huru mtumwa mmoja na anapofika mwisho wa tawaf, Allah hufungua milango nane ya Pepo kwa ajili yake na kumuambia ingia katika mlango wowote unaotaka kuingia.” Isaak akasema: “Uhai wangu uwe dhabihu juu yako; je, yote haya ni kwa ajili ya 209
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 210
Maadili Ya Ashura tawaf moja?” imamu (as) akasema: “Ndio!” Isaak akaomba kufanya hivyo, Imamu (as) akasema:
“Na wema huo ni wakati wowote unapo tekeleza haja za ndugu yako muumini mmoja basi Allah huandika kwa ajili ya mwenye kufanya wema huo tawaf, tawaf, tawaf…” na Imamu (as) alihesabu mpaka kumi. (Sawaabul Aamal, Sheikh Saduk, uk. 106)
8. Imamu Sadiq (a.s) – Mtangaza imani ya Dhabihu (Isaar) Maimamu wetu Watukufu (as) walitumia maisha yao kwa ajili ya wengine; wamechukua maadili ya kiungu kwenye kilele na wamekuwa kila siku wakiwafundisha watu kuhusu maadili matukufu. Wakati wowote walipofanya jambo ilikuwa ni kufundisha na kuelemisha wengine. Wao wenyewe pia walikuwa na maadili makubwa na vievile walijaribu kuwapamba wengine kwa mapambo haya. Imamu Sadiq (as) ni Profesa wa shule ya Dhabihu (Isaar). Inasemekana kwamba wakati fulani kulikuwepo na ukame kule Madina, watu walikuwa hawana kitu cha kula na walikuwa wanakufa kwa njaa. Imamu Sadiq (as) alimuuliza mtunza ghala wake: “Tuna ngano kiasi gani?” mtunza ghala kwa jina Mut’ab akajibu: “Tuna ngano ambayo inaweza kumaliza miezi kadhaa.” Imamu (as) akasema: Chukua ngano yote ukaiuze sokoni.” Mut’ab akasema: “Sasa hivi kuna ukame hapa Madina na itakuwa vigumu sana kupata ngano baadae.” Imamu akasema: “Bila kujali sababu yoyote nenda kaiuze ngano hiyo.” Baada ya ngano yote kuuzwa Imamu (as) akamuambia: “Sasa, wewe vilevile utanunua ngano kila siku kulingana na mahitaji yetu kama wengine.” (Wasailus Shi’ah, Jz 17, uk. 436, Mlango wa 32) Unaona kwamba huu ni mfano mkubwa wa Dhabihu. Hata kama Imamu (as) asingegawa ngano iliyokuwepo katika ghala kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kwake isingekua kosa, lakini maadili ya Dhabihu na kutoa katika njia ya Allah hayakumruhusu Imamu Sadiq (as) kuhifadhi ngano katika nyumba yake wakati watu wengine wanateseka kwa ukame. Kwa jumla kuna swali linaloletwa iwapo dini inaweza kutekeleza mahitaji ya jamii ya zama zetu. Je dini inafaa na kutosha kwa zama hizi? Kusaidia swali hili sababu inayotolewa ni kwamba kwa sababu sisi ni Waislamu na watu wa dini, jamii yetu 210
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 211
Maadili Ya Ashura haina maadili ya mwanadamu. Hatuna upendo, huruma, dhabihu, ushirikiano na huduma kwa viumbe katika jamii yetu ya Kiislamu, lakini kama ukienda na kuona jamii za Kimagharibi, ingawa sio za Kiislamu unaweza kuona huruma ya ubinadamu, dhabihu za ubinadamu zikiwepo huko. Wanasidiana wenyewe kwa wenyewe, lakini hatuoni mambo kama hayo katika jamii yetu ya Kiislamu. Jibu kwa swala hili ni kwamba kama ndani ya jamii yetu ya Kiislamu watu hawashirikiani wenyewe kwa wenyewe, hawasaidii wengine wenye shida; jamii yetu haitoi dhabihu, basi hii yote ni kutokana na sisi kuwa mbali na dini au ni kwa sababu ya kuwa watu wa dini? Yote hii ni kwa sababu ya kuacha maadili ya Ashura au ni kufuata maadili ya Ashura? Kama watu hawana huruma na hawatoi kipaumbele kwa wengine, basi watu kama hao hawaitwi Waislamu. Hii ni kwa sababu dini inasema kwamba kama wewe ni Mwislamu lazima uhisi maumivu ya wengine katika moyo wako na kutoa kipaumbele kwenye haja za wengine kuliko zako mwenyewe. Kwa hiyo, maovu yoyote yanayoonekana, yanatokana na kujiweka mbali na dini. Wakati wowote tunapoona machafu, uovu na dhambi, haya ni matokeo ya sisi kutovutiwa kwenye dini. Kama sisi ni wafuasi wa Karbala na Ashura, kama sisi ni Waislamu basi kwa nini hatuna maadili ya Husein (as), kwa nini sifa na dalili za Husein (as) hazionekani kwetu? Inaonekana kama tuwajinga wa Shule ya Imamu Sadiq (as). Kama wafuasi wa shule hii ambayo husisitiza sana juu ya Dhabihu na kutekeleza haja za Waislamu wengine hawaoneshi dhabihu na hawana huruma kwa wengine haya ni matokeo ya kujiweka mbali na shule hii kubwa.
9. Karbala – Miraji ya Dhabihu (Isaar) Imamu Husein (as) ni mfadhili wa wanadamu. Manufaa ya Imamu Husein (as) hayaishii tu kwa Waislamu, Shia au Sunni’ kwa kweli manufaa yake yako kwa wanadamu wote. Hii ni kwa sababu kama Imamu Husein (as) asingetoa dhabihu hizi, basi kusingelikuwepo na dini, imani au Uislamu. Hivyo, kusingelikuwa na Sunni wala Shia, kila mtu angekuwa hana dini, na kusingelikuwa na kitu kilichobaki kama dini kwa sababu wanadamu waliolaaniwa wa zama hizo walikuwa hawapangi tu kuangamiza maadili ya Shia au Sunni, walikuwa wanataka kuangamiza maadili ya mwanadamu. Kama leo tukimuona mwanadamu mwenye ubinadamu mahali fulani basi hayo ni matokeo ya dhabihu hii kubwa ya Imamu Husein (as). Yote ni kwa sababu ya dhabihu ya masahaba wa Imamu Husein (as) na Bani Hashim. 211
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 212
Maadili Ya Ashura A. Masahaba wa Imamu (a.s) – Vilele vya Dhabihu (Isaar) Masahaba wa Imamu Husein (as) walionesha dhabihu ikifikia kilele chake. Wakati wowote kunapokuwepo na haja ya maji, masahaba walikuwa wakishindana wenyewe kwa wenyewe na kila mtu alitaka kuchukua kiriba cha maji kukimbilia mtoni kuchukua maji, kupigana na maadui na kuleta maji kwa ajili ya masahaba wengine, watoto na familia ya Imamu Husein (as). Kama Imamu Husein (as) akiwa na haja ya kitu chochote, basi kila miongoni mwa masahaba hujaribu kuwa wa mbele zaidi kutekeleza haja yake. Kama Imamu (as) alionekana kutaka kulindwa basi masahaba walikuwa wakishindana miongoni mwao wenyewe ili kuchukua jukumu hili. kama Imamu (as) alitaka mtu fulani kwenda kwenye uwanja wa mapambano kwa ajili ya kujipatia kifo cha shahidi, basi kila askari hutamani kuwa wa mbele kuliko wengine kwenda mbele ili kuipata fursa hii. Hivyo, mara tu Imamu Husein (as) alipoanza kunyanyua mdomo wake mtukufu, wafuasi wake walikuwa wakipanga foleni mara moja ili kutoa uthibitisho wao kwa ajili ya kuipata fursa hii ya kwenda kwenye uwanja wa mapambano. Hivyo wakati Imamu Husein (as) alipokuwa akipanga safu za askari wake dhidi ya maadui asubuhi ya siku ya Ashura, katika hali hii Habib ibn Mazahir (as) alithibitisha kipaumbele chake ili kwenda kwanza kwa msingi kwamba yeye alikuwa mtu mzima miongoni mwao wote. Kwa upande mwingine Wahab (as) alitoa hoja yake kwamba lazima aende yeye kwanza kwa vile yeye ni kijana zaidi kuliko wote. Hurr (as) alisema toba yangu imekubaliwa tu hivi punde, hivyo lazima nipewe kipaumbele, kabla sijatenda tendo lolote la uasi. Zuhair ibn Qain alisema kwamba kwa vile natokana na kabila la familia ya maadui, hivyo lazima nipelekwe mimi kwanza nikapigane nao. Kila sahaba alikuwa akitoa uthibitisho wake wa kipaumbele juu ya wengine, na hii ilikuwa kwa sababu Imamu Husein (as) alikuwa na alikuza katika uhai wao uwezo wa dhabihu na kutoa katika njia ya Allah kabla ya kuingia Karbala. Kwa hiyo, ikawa karibu haiwezekani kwao kuishi mbele za wengine wanaopata kifo cha kishahidi. Waliona kubakia nyuma kuwa ni udhalili na fedheha, ingawa usiku kabla ya Ashura Imamu Husein (as) aliwaaga mara nyingi na kuwaambia waondoke na wamuache. Imamu (as) alisimama katikati yao na akatoa hutuba hii akisema:
212
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 213
Maadili Ya Ashura
“Kile kitakachotushukia juu yetu kiko wazi kwenu. Mmefunguliwa viapo vyenu na shingo zenu haziko chini ya aina yoyote ya kiapo kwangu na wala hamna agano lolote na mimi. Usiku umejitokeza, hivyo kwa kuchukua fursa katika giza lake mnaweza mkaondoka sehemu hii. Jumuiya hii (maadui) wanahusika na mimi tu na kama wanaweza kuzuia mwendo wangu basi hawana haja na mtu yoyote yule. (Mawassae Kalimat Imam Husain (a.s), uk. 316, 317) Wakati masahaba waliposikia hili, kila mmoja kwa sauti moja walisema:
“Allah ayafanye maisha yetu yawe gizani baada ya wewe; hatutaki maisha yoyote baada yako.” (Mawassae Kalimat Imam Hussain (a.s), uk. 316, 317) Kisha sahaba mmoja akasimama na kujibu: Je inawezekana kwamba tukuache wewe peke yako? Na kama tukifanya hivyo ni sababu gani tutakayotoa mbele ya Allah (s) katika utoaji wa haki kwako. Wallahi! Kamwe sitajitenga na wewe, muda ninao upanga mikononi mwangu nitaendelea kupigana na kuchoma mkuki wangu kwenye vifua vyao. Na kama nitaachwa bila silaha basi vilevile nitakulinda wewe kwa kuwatupia mawe, na nitafanya hivi mpaka wakati wa kufa. (Mawassae Kalimat Imam Husain (a.s), uk. 316, 317) Halikadhalika Zuhar ibn Qain (as) Said bin Abdullah Juhfi (as) na masahaba wengine walisimama na kuthibitisha kwamba hawatajitenga naye (as) chini ya mazingira yoyote. Ni rahisi kufa mara moja, lakini hata kama tunauawa mara sabini mbele ya macho yako basi hili ni suala la heshima na utukufu kwetu. Wakati Imamu Husein (as) aliposikia maneno yao, aliwaombea na akasema:
“Allah awalipe malipo mema! Hakuna mtu yoyote aliyekuwa na masahaba bora kama masahaba wangu hawa watiifu.” (Mawassae Kalimat Imam Hussain (a.s), uk. 402) 213
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 214
Maadili Ya Ashura
Kuna tukio linalohusiana na sahaba mmoja ambaye Imamu Husein (as) binafsi alimshauri kuchukua fursa ya giza lile la usiku na kuondoka ili kuokoa maisha yake. Hilal ibn Nafi anasema kwamba niliona kwamba katika giza la usiku Imamu Husein (as) alitoka nje peke yake kutoka kwenye hema lake na akaanza kutembea kuelekea kwenye uwanja wa mapambano. Mimi vilevile nilisimama na kumfuata. Baada ya kutembea kwa muda Imamu Husein (as) akaniona na akauliza: “Ni nani wewe? Wewe ni Hilal?” nikasema: “Uhai wangu na uwe dhabihu kwa ajili yako, ndio ni mimi Hilal.” Imamu (as) akasema: “Kwa nini umeondoka kambini?” nikasema: “Maadui wameweka kituo karibu sana na nilikuwa na wasi wasi kwamba wanaweza wakakuumiza.” Akasema kwamba Imamu Husein (as) alikwenda sehemu ya mapigano, akafanya utafiti wa uwanja wa mapambano na akafanya ramani ya uwanja wa mapambano. Kisha Imamu Husein (as) akachukua mkono wangu katika mkono wake na tukarudi kuelekea kambini. Njiani, Imamu Husein (as) aliniambia: “Hilal! Hutaki kuokoa maisha yako kwa kuchukua fursa ya giza hili la usiku? Nenda kajifiche kwenye milima ile ili kwamba maisha yako yawe salama.” Wakati Hilal aliposikia haya alisema: “Mama yake Hilal amlilie Hilal. Inawezekana kweli kwamba niondoke na nikuache wewe?” Bibi Zainab (as) anasema kwamba niliona katika usiku kabla ya Ashura Habib ibn Mazahir aliwakusanya masahaba wote katika hema moja na alikuwa anawahutubia: “Askari wangu! Mapambano yataanza asubuhi. Lazima muwe wa kwanza kwenda kwenye uwanja wa mapambano. Hatuwezi kuona Bani Hashim yeyote analoa kwenye damu. Hatutaruhusu Bani Hashim yeyote kwenda kwenye uwanja wa mapambano muda tuko hai, vinginevyo watu hawa watasema tumewasukuma maSayyid mbele na na sisi kubakia nyuma.” Masahaba wakaondoa panga zao na kuahidi kwamba: “Ewe Habib! Tunakutii wewe, amri yoyote utakayotoa tutakutii wewe. Asubuhi utaona kwamba sisi tutakuwa wa kwanza kwenda kwenye uwanja wa mapambano.” (Mawassae Kalimat Imam Hussain, uk. 401) Masahaba watiifu wa Imamu Husein (as) walifanya kile walichokisema. Muda masahaba walikuwa hai hakuna yeyote kutoka kwa Bani Hashim aliyeuliwa shahidi. Hii ilikuwa ni njia ambayo masahaba walionesha dhabihu katika kilele chake.
214
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 215
Maadili Ya Ashura
B. Bani Hashim - Vigezo vya wajibu vya Dhabihu (Isaar) Katika siku ya Ashura baada ya masahaba wote kuuawa kishahidi na ikawa ni zamu ya Bani Hashim kupata shahada, katika hali hii maadili ya Dhabihu yalifikia kupaa (Miraji) kwake. Imamu Husein (as) alifanya Dhabihu akafanya Miiraj (upaaji) kupitia kwa Bani Hashim, ingawa katika usiku wa Ashura kama alivyofanya kwa masahaba vilevile alitoa ruhusa kwa Bani Hashim kuokoa maisha yao. Yeye (a.s.) aliwaambia watu wa familia yake:
“Nimewapeni uhuru wa kuniacha mimi. Adui ana haja na mimi tu, hivyo niacheni mimi na hao maadui, na kwa kuchukua fursa ya giza la usiku huu mnaweza kuondoka mahali hapa.” (Mawassae Kalemat Imam Hussain, uk. 397, 401) Abbas ibn Ali (a.s) alisimama kwanza na kusema:
“Kwa nini tufanye hivi? Je, tunataka kuishi baada yako? Kwa nini tufanye hivyo? Allah (s) asituoneshe siku ambayo tunaishi baada yako.” (Mawassae Kalemat Imam Husain, uk. 397, 401) Kisha akawahutubia watoto wa Aqiil:
“Enyi Bani Aqiil! Shahada ya Muslim (as) inatosha kama mchango kwa upande wenu, hivyo mnaweza mkaondoka. Nimekupeni ruhusa.” (Mawassae Kalimat Imam Hussain, uk. 397, 400) Bani Aqiil wakajibu: “Hatutaki maisha baada yako. Vipi itawezekana kwamba tunamuacha mwana wa Fatima (as) peke yake katika makucha ya maadui? Tunaapa wallahi kwamba tutapi215
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 216
Maadili Ya Ashura gana mpaka pumzi yetu ya mwisho.” (Mawassae Kalimat Imam Husain, uk. 397, 400) Wakati Imamu Husein (as) alipoona uvumilivu na subira kwa masahaba wake na Bani Hashim, alimjulisha kila mmoja wao kuhusu cheo na daraja yao katika Pepo. Wakati mazungumzo haya yanaendelea, Qasim (as) alihisi moyoni mwake kwamba isije ikawa kwamba ni wale tu ambao majina yao yanachukuliwa ndio watakaobahatika kupata shahada, na kwamba yatima huyu wa Hasan (as) ataikosa fursa hii. Alisimama na akauliza: “Ami yangu mpenzi! Jina langu nami limo au halimo katika orodha ya mashahidi?” Imamu (a.s) alisema: “Ewe kumbukumbu ya kaka yangu, niambie unavyokitambua kifo?” Qasim (a.s) akamjibu ami yake:
“Ewe ami yangu! Kifo ni kitamu kuliko asali.” (Mawassae Kalimat Imam Husain, uk. 402) Wakati Imamu Husein (as) aliposikia jibu hili la Qasim (as), alisema: “Ewe alama ya kaka yangu, ami yako na awe Dhabihu kwa ajili yako. Kesho wewe pia utaonesha maadili ya Dhabihu miongoni mwa wengine, na kwa kufanya hivyo wewe pia utakunywa kwenye kikombe cha Shahidi katika sehemu mahususi.” Uso wa Qasim ulichangamka baada ya kusikia hili. Katika siku ya Ashura wakati kila mtu anakwenda kwenye uwanja wa mapambano baada ya kuomba ruhusa kutoka kwa Imamu Husein (as), Qasim (as) vilevile alikuja kwa Imamu Husein (as) na akamsalimia ami yake akaomba ruhusa kwa ajili ya Jihad. Inasimuliwa kwamba Husein (as) hakusita kumpa ruhusa Qasim (as). Qasim (as) akaanza kubusu mikono na miguu ya ami yake. Alianguka chini ya miguu ya Imamu Husein (as) na akaendelea kubusu miguu yake. (Hamas-e-Hussain, Jz. 1, uk. 247).
216
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 217
Maadili Ya Ashura Imeandikwa kwamba Imamu Husein (as) hakutoa ruhusa ya wazi kwa maneno kwa Qasim (as). Alisema tu: “Ewe alama ya kaka yangu njoo karibu yangu, nataka kukukumbatia kwa ajili ya kukuaga.” Wote ami na mpwa waliendelea kwa muda kiasi huku wakiwa wamekumbatiana. Kwa njia hii Qasim (as) alipata ruhusa ya kwenda kwenye uwanja wa mapambano. Bibi Zainab (as) anasema kwamba katika siku ya mkesha wa Ashura nilikuwa nimesimama nje ya hema la Abbas (as) na nilisikia makelele mengi kutoka ndani ya hema. Nilimuona Abbas amekaa juu ya magoti yake kama simba miongoni mwa Bani Hashim. Alikuwa akitoa hutuba, na aina hii ya hutuba sijawahi kuisikia kabla ya hapa kutoka kwa yeyote mwingine mbali na Imamu Husein (as). Mwisho wa hutuba Abbas (as) akasema kuwaambia wote: “Mnafikiriaje kuhusu pambano kali ambalo litaanza kesho asubuhi?” Kila mmoja kwa pamoja wakasema kwa sauti moja kwamba wewe ni kamanda wa jeshi amri yoyote utakayoitoa tutatii. Abbas (as) akasema: “Hawa masahaba ni wageni wetu na kila siku inapendekezwa kwamba mizigo mizito lazima ibebwe na wenyeji na sio wageni. Ikifika asubuhi, lazima mtangulie kwenda kwenye uwanja wa mapambano na msiruhusu masahaba kwenda kabla yenu. Isije ikatokea kwamba baadae ikasemwa kwamba wenyewe tumekaa nyuma na kuwapeleka wengine mbele.” Bani Hashim wakajibu kwa kuthibitisha. Tunaweza kuona kwamba masahaba kwa upande mmoja wanajaribu ili wafike kwenye uwanja wa mapambano kwanza, wakati ambapo kwa upande mwingine Bani Hashim wanajaribu nao kufanya hivyo hivyo. Mwishowe ilikuwa ni masahaba ndio waliofanikiwa katika juhudi yao ya kwenda kwanza, lakini wakati zamu ya Bani Hashim ilipofika alikuwa ni Ali Akbar (as) ambaye alipata shahada kwanza. Imamu (as) hakumpeleka mpwawe kwanza, wala hakuwapeleka ndugu, binamu zake kwanza kwenda kwenye uwanja wa mapambano, badala yake aliteuwa mtoto wake mdogo sana kwenda kwanza. Baada ya masahaba kuuawa kishahidi, Imamu Husein (as) aligeuka kwa Bani Hashim na akasema kwamba sasa ni zamu ya Bani Hashim, nani yuko tayari kwenda kwanza miongoni mwa Bani Hashim? Ali Akbar (as) akajitokeza mbele haraka na akaanguka chini ya miguu ya baba yake mkubwa akiomba ruhusa. Ilikuwa ni jambo la kawaida kwa Imamu Husein (as) kwa ajili ya masahaba wote na Bani Hashim, kwamba yeyote akija kuomba ruhusa, Yeye (as) alikuwa akimzuia huku akimuambia kwamba utapoteza maisha yako na kama inawezekana unaweza kuokoa maisha yako. Lakini hii ilikuwa ni mara ya 217
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 218
Maadili Ya Ashura kwanza kwamba mujahidina kama huyu alijitokeza mbele ambaye Imamu Husein (as) hakumzuia kwenda kwenye Jihad. Yeye (as) alimpa silaha kwa mikono yake mwenyewe na kisha akasema Ali Akbar nenda kapigane na maadui katika uwanja wa mapambano. Uliyokuwa ukisikiliza kwa mahatibu (Dhakirin) sio kweli. Mahatibu hawa wanasema kwamba Imamu Husein (as) alimzuia Ali Akbar (as) kwenda kwenye uwanja wa mapambano kwa kusema wewe ni mtoto wangu, lazima uwe na subira na usiharakishe kwenda kwenye uwanja wa mapambano. Huu ni uwongo kabisa na tusi kwa Imamu Husein (as). Hizi ni sifa za Dhabihu ya Husein (as). Haya ni maadili ya Ashura ambayo kwamba kule Karbala kila mtu alikuwa anajaribu kutoa muhanga maisha yake katika jina la Husein (as). Wale wote wanaodai kufuata mwenendo wa Husein (as) na kujiita wenyewe wafuasi wa Husein (as), wale wote ambao ni wafuasi wa Ashura na Karbala lazima wawe na sifa hii ya Dhabihu ndani yao. Itawezekana vipi mtu kujiita mwenyewe mfuasi wa Husein (as), lakini maisha yake hayana dalili za dhabihu, hata pia wakati Imamu Husein (as) alipotoa upaaji (Miraj) kwenye maadili ya Dhabihu kule Karbala. Ni ukweli usio na shaka kwamba huu ni upaaji (Miraj) wa dhabihu. Machapisho Mengine ya Kiingereza *Philosophy of Religion *Role of Women in the System of Wilayat *The Tragedy of Qods *Philosophy of Qayam-e-Hussain (a.s) *System of Wilayat in the vision of Qur’an
218
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 219
Maadili Ya Ashura
ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24. 25. 26. 27. 28. 29. 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37.
Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thelathini Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudharr Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur'an na Hadithi Elimu ya Nafsi Yajue Madhehebu ya Shia Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu Al-Wahda Ponyo kutoka katika Qur'an Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii Mashukio ya Akhera Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyezi Mungu na sifa zake Kumswalia Mtume (s) Nafasi za Ahlul Bayt (a.s)
219
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 220
Maadili Ya Ashura 38. 39. 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52. 53. 54. 55. 56. 57. 58. 59. 60. 61. 62. 63. 64. 65. 66. 67. 68. 69. 70. 71. 72. 73. 74. 75. 76. 77. 78.
Adhana Upendo katika Ukristo na Uislamu Tiba ya Maradhi ya Kimaadili Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu Kupaka juu ya khofu Kukusanya swala mbili Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kusujudu juu ya udongo Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) Tarawehe Malumbano baina ya Sunni na Shia Kupunguza Swala safarini Kufungua safarini Umaasumu wa Manabii Qur’an inatoa changamoto as-Salaatu Khayrun Mina -'n Nawm Uadilifu wa Masahaba Dua e Kumayl Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mtume Muhammad (s) Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili Kuzuru Makaburi Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita Tujifunze Misingi Ya Dini Sala ni Nguzo ya Dini Mikesha Ya Peshawar Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliyonyooka Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake Liqaa-u-llaah Muhammad (s) Mtume wa Allah Amani na Jihadi Katika Uislamu
220
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 221
Maadili Ya Ashura 79. Uislamu Ulienea Vipi? 80. Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) 81. Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) 82. Urejeo (al-Raja’a ) 83. Mazingira 84. Utokezo (al - Badau) 85. Hukumu ya kujenga juu ya makaburi 86. Swala ya maiti na kumlilia maiti 87. Uislamu na Uwingi wa Dini 88. Mtoto mwema 89. Adabu za Sokoni 90. Johari za hekima kwa vijana 91. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza 92. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili 93. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu 94. Tawasali 95. Imam Mahdi katika Usunni na Ushia 96. Hukumu za Mgonjwa 97. Sadaka yenye kuendelea 98. Msahafu wa Imam Ali 99. Ngano ya kwamba Qur’ani imebadilishwa 100. Idil Ghadiri 101. Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu 102 Hukumu zinazomuhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi 103. Huduma ya Afya katika Uislamu 104. Sunan an-Nabii 105. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) 106. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) 107. Shahiid Mfiadini 108. Kumsalia Nabii (s.a.w) 109. Ujumbe -Sehemu ya Kwanza 110.Ujumbe - Sehemu ya Pili 111. Ujumbe - Sehemu ya Tatu 112. Ujumbe - Sehemu ya Nne 113. Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu 114. Hadithi ya Thaqalain 115. Ndoa ya Mutaa 116. Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza 117. Ukweli uliopotea sehemu ya Pili 118. Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu 119. Ukweli uliopotea sehemu ya Nne 120. Ukweli uliopotea sehemu ya Tano
221
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 222
Maadili Ya Ashura 121. Mkutano wa Maulamaa wa Baghdad 122. Safari ya kuifuata Nuru 123. Fatima al-Zahra 124. Myahudi wa Kimataifa 125. Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi 126. Visa vya kweli sehemu ya Kwanza 127. Visa vya kweli sehemu ya Pili 128. Elimu ya Ghaibu ya Maimamu 129. Mwanadamu na Mustakabali wake 130. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) 131. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) 132. Khairul Bariyyah 133. Uislamu na mafunzo ya kimalezi 134. Vijana ni Hazina ya Uislamu 135. Yafaayo kijamii 136. Tabaruku 137. Taqiyya 138. Vikao vya furaha 139. Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 140. Visa vya wachamungu 141. Falsafa ya Dini 142. Azadari-Kuhuzunika na Kuomboleza 143. Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah 144. Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu 145. Kuonekana kwa Allah 146. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) 147. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) 148. Ndugu na Jirani 149. Ushia ndani ya Usunni 150. Maswali na Majibu 151. Mafunzo ya hukmu za ibada 152. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1 153. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2 154. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 155. Abu Huraira 156. Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. 157. Mazingatio kutoka katika Qur’an - Sehemu ya Kwanza 158. Mazingatio kutoka kaitka Qur’an - Sehemu ya Pili 159. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza 160. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili
222
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 223
Maadili Ya Ashura 161. Qur’ani Tukufu – Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili 162. Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) 163. Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani 164. Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu 165. Uislamu Safi 166. Majlisi za Imam Husein Majumbani 167. Je, Kufunga Mikono 168. Uislam wa Shia 169. Amali za Makka 170. Amali za Madina 171. Asili ya Madhehebu katika Uislamu 172. Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi 173. Ukweli uliofichika katika neno la Allah 174. Uislamu na Mifumo ya Uchumi 175. Umoja wa Kiislamu na Furaha 176. Mas’ala ya Kifiqhi 177. Jifunze kusoma Qur’ani 178. As-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah 179. Hayya ‘Alaa Khayri’l-’Amal Katika Adhana 180. Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura 181. Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na Ramadhani) 182. Uadilifu katika Uislamu 183. Mahdi katika Sunna 184. Maswali Ya Uchunguzi Kuhusu Uislam 185. Kazi na Bidii ni njia ya maendeleo 186. Abu Talib – Jabali Imara la Imani 187. Ujenzi na Utakaso wa Nafsi 188. Vijana na Matarajio ya Baadaye 189. Usalafi – Historia yake, maana yake na lengo lake 190. Ushia – Hoja na Majibu 191. Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) 192. Maombolezo – Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) 193. Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu 194. Takwa 195. Mwonekano wa Upotoshaji katika Hazina ya Kiislamu 196. Amirul Muuminina (‘as) na Makhalifa 197. Uongozi na Utawala katika Mwenendo wa Imam ‘Ali (‘a) 198. Kuvunja hoja iliyotumika kutetea Uimamu wa AbuBakr 199. Adabu za vikao na mazungumzo 200. Hija ya Kuaga 201. Uwazi baina ya Maslahi na Vikwazo 202. Fadhila za watukufu watano katika Sahih Sita
223
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 224
Maadili Ya Ashura 203. Mdahalo baina ya Mwanachuoni wa Kisunni na Mwanachuoni wa Kishia (Al- Muraja’aat) 204. Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (as) 205. Imam Husain ni Mfumo wa Marekebisho na Mageuzi 206. Mtazamo kuhusu msuguano wa Kimadhehebu 207. Nchi na Uraia – Haki na wajibu kwa Taifa 208. Mtazamo wa Ibn Taymiyyah juu ya Imam Ali (as) 209. Uongozi wa Kidini – Maelekezo na Utekelezaji wa Kijamii 210. Maadili ya Ashura 211. Mshumaa – Shahidi na Kifo cha Kishahidi 212. Mizani ya Hekima – Hadithi za Ahlul Bait (as) – Sehemu ya Kwanza 213. Imam Ali na Mambo ya Umma 214. Imam Ali na Mfumo wa Usawa 215. Uimamu na Tamko la Kutawazwa 216. Mfumo wa Wilaya 217. Vipi Tutaishinda Hofu? 218. Kumswalia Mtume ni Ufunguo wa Utatuzi wa Matatizo 219. Maeneo ya Umma na Mali Zake 220. Nahjul-Balagha – Majmua ya Khutba, Amri, Barua, Risala, Mawaidha na Semi za Amirul-Muuminin Ali bin Abu Talib (a.s.) 221. Mukhtar – Shujaa aliyelipiza kisasi dhidi ya wauaji wa Imam Husein (as) hapo Karbala KOPI NNE ZIFUATAZO ZIMETAFSIRIWA KWA LUGHA KINYARWANDA 1. 2. 3. 4.
Amateka Na Aba'Khalifa Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya Shiya na Hadithi ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION KWA LUGHA YA KIFARANSA
1.
Livre Islamique
224
Maadili Ya Ashura 10.3.2014:Maadili Ya Ashura 2 A5.qxd 4/4/2014 12:23 PM Page 225
BA CK
CO V ER
Kitabu hiki ni safari ya kuingia ndani ya Karbala kwa mtazamo wa uwasilishaji kuhusu kadhia hii ambao haijawahi kutokea kabla. Mtunzi, Ustadh Sayyid Jawad Naqvi analiendea tukio la Karbala kwa mtazamo ambao ni wa kipekee kabisa lakini ulio muhimu sana kwa kuifanya Karbala kuwa ni ya ukweli wa kivitendo kwa ajili ya wanadamu katika zama zote. Kawaida hasa vitabu, mawasilisho na mchanganuo juu ya hii kadhia ya Karbala na msiba huu unafanywa katika njia ya mfuatano wa matukio yanayoongozea kuelekea Ashura. Utaratibu huu wa mchanganuo wa kihistoria hauwezi kukanushwa au kushutumiwa na juhudi zinazofanywa na wachambuzi hao zinakubaliwa kabisa katika hili, lakini njia ambayo mwandishi ameitumia katika kitabu hiki ni tofauti. Inaliwasilisha tukio la Karbala kutoka kwenye kiini chake kikiwa ndio lengo la mageuzi ya Imam Husain (a.s.) katika maneno matukufu yake yeye mwenyewe. Kisha akienda chini mbali zaidi kwenye hususia maalum za lengo hili la marekebisho ya Umma na ule utaratibu ambao Imam Husain (a.s.) alioutumia, anatuelekeza kwenye nukta ambapo Karbala na Ashura vinatuwekea mbele yetu sisi wanadamu maadili ambayo ni haja tena ya muhimu kwa zama zote. Maadili ya Ashura ni mkusanyiko wa zile tabia na sifa ambazo kwa kawaida zinapaswa kuwemo ndani ya wanadamu wote, kama sio hivyo. basi angalau ndani ya waumini wote, na kama sio hivyo pia, basi angalau ndani ya wafuasi wa Imam Husain bin Ali (a.s.). Mtunzi amechagua masomo maalumu kumi ya maadili ambayo Ashura imeyawasilisha kwa wanadamu. Mwandishi anayathibitisha maadili haya kwa mwanga wa Qur’ani, hadithi na kisha kupitia kwenye maneno na matukio yanayohusiana na kadhia hii ya Karbala. Maadili ya Ashura sio kipande cha maandishi tu basi, kila sehemu ya kitabu hiki ina ujumbe wenye mwamsho, utambuzi, elimu na inasababisha msukumo, mwendo na shauku kuanzisha harakati tendani za kijamii ndani ya mfuasi mmoja mmoja wa Imam Husain (a.s.). Kitabu hiki sio makala ya kusoma mara moja tu, bali kwa kweli ni marejeo, mwongozo halisi wa kweli wa ndani ya tukio la Karbala na unaweza kuchukuliwa kama orodha ya masomo – katalogi kwa wale ambao watatamani mageuzi kwa ajili ya kusimamisha haki na uadilifu. Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. - 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@ryahoo.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: w.w.w.alitrah.inf