Majibu yetu kwa mufti wa al azhar

Page 1

MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR Katika Mihadhara yake ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

‫مع شيخ ألازهر في محاضراته الرمضانية‬

Kimeandikwa na: Sheikh Ja’far Subhani

Kimetarjumiwa na: Alhaji Hemedi Lubumba


‫ترجمة‬ ‫مع شيخ ألازهر في محاضراته الرمضانية‬

‫تأليف‬ ‫الشيخ جعفر السبحاني‬

‫من اللغة العربية إلى اللغة السواحلية‬


©Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 – 9987 – 17 – 003 – 6 Kimeandikwa na: Sheikh Ja’far Subhani Kimetarjumiwa na: Ustadh Al-Haji Hemedi Lubumba Kimehaririwa na: Al-Haji Ramadhani S. K. Shemahimbo Kimepitiwa na: Al Haji Mujahid Rashid Kimepangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation Tole la kwanza: Machi, 2018 Nakala: 2,000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Al-Itrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.alitrah.info Vitabu mtandaoni: www.alitrah.info/ebooks/ ILI KUSOMA QUR’ANI MUBASHARA KWA NJIA YA MTANDAO, TEMBELEA www.somaquran.com


YALIYOMO Dibaji………………………………………….. Neno la Mchapishaji………………………….. Utangulizi……………………………………... Mhadhara wa Kwanza: Lengo la Mfululuzi wa Mihadhara hii………………………………. Mhadhara wa Pili: Maana ya Swahaba na upanuzi wenye lengo la kulinda…................. Mhadhara wa Tatu: Chanzo cha Uadilifu wa Maswahaba…………………………………. Mhadhara wa Nne: Uhusiano wa Sunni na Shia, na nafasi ya uadilifu wa Maswahaba katika Uislamu……………………………… Mhadhara wa Tano: Uchunguzi juu ya Maswahaba…………………………………. Mhadhara wa Sita: Maswahaba wanajua zaidi hali yao kuliko wengine wasiokuwa wao………………………………………….. Mhadhara wa Saba: Qur‟ani na Hadithi inazungumziaje Uadilifu wa Maswahaba….. Mhadhara wa Nane: Maana ya Umaasumu…. Mhadhara wa Tisa: Tofauti iliyopo kati ya Umaasumu na Uadilifu…………………….. Mhadhara wa Kumi: Ijtihadi mbele ya tamko bayana na andiko la wazi…………………… Mhadhara wa Kumi na Moja: Umaasumu wa Umma………………………………………..

7 8 10 13 17 22

31 42

49 55 72 79 88 96


Mhadhara wa Kumi na Mbili: Ni kutukana au ni kusoma Maisha ya Swahaba?................... Mhadhara wa Kumi na Tatu: Kuzikurubisha pamoja Madhehebu za Kiislamu……………. Mhadhara wa Kumi na Nne: Kuwapenda Maswahaba………………………………….. Mhadhara wa Kumi na Tano: Kumvunjia heshima mke wa Mtume ………………… Mhadhara wa Kumi na Sita: Kuwakufurisha Shia na kuwaita Marawafidhi………………. Mhadhara wa Kumi na Nane: Nafasi ya Uimamu kwa Sunni na Shia………………… Mhadhara wa Kumi na Tisa: Uchambuzi wa matukio ya Saqifa…………………………… Mhadhara wa Ishirini: Umaasumu wa Maimamu Kumi na Wawili............................ Mhadhara wa Ishirini na Moja: Ni kwa Njia Ipi Unapatikana Uimamu?.................................. Mhadhara wa Ishirini na Tatu: Hotuba ya Abu Bakri.............................................................. Mhadhara wa Ishirini na Nne: Madhumuni ya Kauli ya Mtukufu Mtume : “Yeyote ambaye Mimi ni Mtawala Wake basi Huyu Ali ni Mtawala Wake.”......................... Mhadhara wa Ishirini na Tano: Ali aliwapa Makhalifa kiapo cha Utiifu............................ Mhadhara wa Ishirini na Sita: Mifano ya sauti Adilifukutoka upande wa Mashia.................. Mhadhara wa Ishirini na Saba: Uimamu wa kidini na Uimamu wa Kisiasa........................

101 108 113 118 122 125 131 150 158 174

187 205 222 230


Mhadhara wa Ishirini na Nane: Imam Ali hakutafuta Uimamu wa Kisiasa...................... Mhadhara wa Ishirini na Tisa: Azhar ndio Taasisi ya Kidini yenye shauku kubwa na Umoja wa Waislamu kuliko zote...................

234

239


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬

DIBAJI Kitabu hiki ni toleo la Kiswahili la taasisi ya Al Itrah Foundation. Chapisho lake limelenga kukidhi mahitaji ya kiroho ya zama hizi pamoja na Ubongo na fikra zinazokuwa za Muislam. Jitihada kubwa zimefanywa na Taasisi kuweka chapisho hili la Kiswahili katika msingi wa haki na wenye kukubalika katika Uislam. Unaombwa kwa Taadhima ukisome kitabu hiki katika malengo yaliyokusudiwa. Pia Unaombwa kuwasilisha kwetu maoni yako huru juu ya chapisho letu hili, jambo ambalo tutashukuru sana. Kutangaza ujumbe wa Uislam ni kazi ambayo inahitaji ushirikiano wetu sote. Taasisi inakuomba kuungana na kushirikiana kama ilivyoagizwa katika aya ya Qur‟an: (Surat Saba‟ 34:46). Na rehma za Allah ziwe juu yako. Wako katika Uislam Al Itrah Foundation Barua Pepe: alitrah@yahoo.com SMS: +255 778 300 140 7


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬ NENO LA MCHAPISHAJI Kitabu ulichonacho mikononi mwako kimetarjumiwa kutoka kitabu cha Kiarabu kwa jina la, Ma‟a Shaykh al-Azhar fi Muhadharatuhu ar-Ramadhaniyyah, kilichoandikwa na Allamah Mhakiki Sheikh Ja'far Subhani. Sisi tumekiita, Majibu Yetu kwa Mufti wa al-Azhar katika Mihadhara Yake ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.. Mwandishi wa kitabu hiki, Sheikh Ja‟far Subhani ameandika kitabu hiki ili kujaribu kuondoa utata uliojitokeza katika mihadhara ya Mheshimiwa Mufti wa al-Azhar aliyoitoa katika darasa zake ambazo huzitoa kila siku katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani kila mwaka, na hii ni mihadhara aliyoitoa mwaka 1436 A.H. Sheikh Subhani ameandika majibu haya kwa nia nzuri tu ili kujaribu kusahihisha baadhi ya mambo ili tuweze kwenda pamoja na kufikia lengo letu la umoja. Hivyo, tunawaomba wasomaji wetu wafuatilie mihadhara hii ambayo Sheikh wetu huyu ameiorodhesha mmoja baada ya mwingine pamoja na maoni yake.Wafanye vivyo hivyo na kusoma kwa nia hiyohiyo ya kulete umoja. Wala wasiyafanye majibu haya kama mdahalo wa malumbano, bali wayachu8


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

kulie kama mjibu yaliyotolewa na mtu mwenye nia njema kwa Waislamu na Uislamu. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia, vitu ambavyo havina nafasi tena katika akili za watu. Kutoka na ukweli huu, Taasisi yetu ya Al-Itrah imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili. Tunamshukuru ndugu yetu Alhaji Hemedi Lubumbakwa kazi kubwa aliyoifanya ya kukitarjumi kitabu hiki kutoka lugha yake ya asili ya Kiarabu kuja katika lugha ya Kiswahili. Vilevilena wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Allah Mwenye Kujazi awalipe wote malipo mema hapa duniani na kesho Akhera – Amin. Mchapishaji Al-Itrah Foundation

9


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬ UTANGULIZI Kila sifa njema ni ya Allah Mola Mlezi wa viumbe wote. Kila sifa njema ni ya Allah, ambaye ametutaka tushikamane na kamba ya umoja na ametukataza kufarakana na kutengana. Sala na salamu zimwendee Nabii wa Rehema, yeye na watu wa nyumbani kwake ambao Allah amewaondolea uchafu na amewatakasa kabisa. Baada ya hayo, ni kwamba ulimwengu wa Kiislamu kila siku unashuhudia jinai za fedheha, umwagaji damu, ubomolewaji wa miundombinu na mauaji ya watu wasio na hatia. Na mengineyo miongoni mwa jinai ambazo hutikisa Arshi ya Rahmani. Na la kusikitisha sana ni kwamba vitendo vyote hivi vya kinyama hufanywa na kutekelezwa kwa jina na anwani ya dini, kiasi kwamba imekuwa ni rahisi zaidi kwao kumchinja binadamu ambaye Allah amemtambulisha kwa kusema: “Hakika tumewatukuza wanaadamu…”1 kushinda hata wanavyomchinja ndege au kuuwa mdudu. Na wakati matukio haya machungu yakiendelea, Seminari Kuu ya Kielimu ya Qum iliitisha konga1

Sura Israi: 70. 10


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

mano la kimataifa chini ya anwani “Rai za Ulamaa wa Kiislamu Kuhusu Makundi Yenye Misimamo Mikali na Utakfiri.� Ilikuwa ni mwendelezo wa makumi ya makongamano na mikutano ambayo imewahi kufanyika katika nchi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ili kuimarisha umoja na kuunganisha safu mbele ya hatari inayoukabili ulimwengu wa Kiislamu. Alhamdulilahi katika kongamano hili walishiriki waheshimiwa maulamaa kutoka makundi yote mawili, na maulamaa wengine walituma makala kadhaa na ambazo ziliwasilishwa katika kongamano. Kongamano hili lilikuwa na sauti katika jamii ya kielimu na vyombo vya habari, na Dkt. Mufti Ahmad Twayyib, Mufti wa Azhar alikuwa ni mmoja miongoni mwa waalikwa licha ya kwamba hakuhudhuria. Na ilitarajiwa kwamba Mufti katika mihadhara yake ya Mwezi wa Ramadhan, aliyokuwa akiiwasilisha jioni ya mwezi waRamadhan, mnamo mwaka 1436 A.H. angewasilisha lile lililokuwa linawafikiana na malengo ya kongamano hili. Lakini bahati mbaya ni kwamba, licha ya Mheshimiwa, Mungu amhifadhi, kulingania ukuruba, lakini wakati huo huo aliangazia mambo ambayo hayahudumii ukuruba baina ya makundi mawili (Suni na Shia). Ni kwa ajili hiyo tumeamua kuandika ujumbe huu ambao ndani yake tutajadili yale aliyoyawasilisha Dkt. katika mfululizo wa mihadhara hiyo, na tutabainisha maeneo yenye mwafaka na yenye tofauti, 11


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

huenda ukakubaliwa na ukachangia katika kuondoa matatizo yanayochochewa. Ja’far Subhani Qum Tukufu, Mwezi 10 Shawal 1436 A.H.

12


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬ MHADHARA WA KWANZA Siku ya Kwanza ya Mwezi wa Ramadhan, Mwaka 1436 A.H. Dkt. Ahmad Twayyib Mufti wa Azhar Mungu amhifadhi, katika mazungumzo yake yaliyojulikana kama mazungumzo ya kila siku, yaliyokuwa yakirushwa na runinga ya Misri kabla ya kufturu, alisisitiza mambo mawili: 1. Kwamba atatenga baadhi ya mihadhara ya mwezi huu au yote, kwa ajili ya maudhui yenye umuhimu sana, nayo ni maudhui ya cheo cha Maswahaba watukufu, na atabainisha itikadi ya Suni kuhusu Maswahaba. Aliendelea kueleza mpaka aliposema: “Na sisi hatutaki kukuza tofauti zilizopo au kuanzisha fitna, kwani Chuo Kikuu cha Azhar katika muda wote wa historia yake kimeendelea kuwa kituo cha umoja wa Waislamu kwa makundi yao yote na madhehebu yao yote. 2. Aliashiria uwepo wa majaribio ya kutikisa uhuru wa Misri kupitia kampeni ya kuwataka vijana wake waache madhehebu ya Suni ambayo wamelelewa nayo, na kuwapeleka katika madhehebu mengine (Ushia), na kuwaingiza humo kupitia lango la kuwapenda Ahlulbayti, ambao sisi tunawapenda 13


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

zaidi - kwa mujibu wa kauli yake – kushinda jinsi wengine wanavyowapenda. Nasema: Ilitegemewa kutoka kwa Mufti ambaye anadai kwamba Azhar katika muda wote wa historia yake ni kituo cha umoja wa Waislamu, katika mhadhara wake wa kwanza, na katika siku ya kwanza ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, angesisitiza umoja wa Waislamu na ukuruba wa madhehebu, na angeashiria kwamba Qur‟ani inatuamrisha kushikamana na kamba ya umoja, inasema: “Na Shikamaneni na kamba ya Mwenyezi Mungu nyote wala msifarikiane…”.2 Kutokana na umuhimu lililonao jambo hili, Aya Tukufu imeliashiria kwa lugha ya kuvutia mno wakati wa kuliwasilisha, ambapo Allah ameamuru kushikamana na kamba ya Allah badala ya kusema shikamaneni na Uislamu au na Qur‟ani au na jambo jingine mfano wa hayo mawili. Hakika haikutumia ibara zote hizo baliimetutaka tushikamane na kamba ya Allah, ikiashiria kwamba umma umefarakana na kugawanyika katika makundi. Imekuwa sawa na aliyedumbukia kisimani, hana uokovu isipokuwa kushikamana na kamba imara itakayomsaidia kutoka humo. Hivyo katika janga hili ambalo kila siku damu za Waislamu zinamwagwa na wajinga wao kwa sababu yake, ni wajibu kwa umma wa Kiislamu kushikamana 2

Sura Imran: 103.

14


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

na maeneo ya ushirikiano, na kuacha yale yenye mzozo yashughulikiwe katika mikusanyiko ya kidini na makongamano ya kielimu, kwani yanayowakutanisha pamoja ni mengi zaidi kuliko yale yanayowagawa. Nasi tutakapofuatilia katika Kitabu kitukufu cha Allah tutakuta Yeye Mtukuka amefanya mfarakano baina ya umma ni moja ya mifano halisi ya adhabu iteremkayo kutoka mbinguni au kutoka chini ya nyayo, anasema: “Sema: Yeye ndiye awezaye kuwaletea adhabu kutoka juu yenu au kutoka chini ya miguu yenu; au awavuruge (muwe) makundi, na awaonjeshe baadhi yenu jeuri ya wenzao. Tazama jinsi tunavyozieleza Ishara kwa njia mbali mbali ili wapate kufahamu.”3 Na kiongozi wa ufasaha wa mazungumzo Ali  amesema: “Na kuweni pamoja na kundi kubwa la Waislamu kwani mkono wa Mwenyezi Mungu uko pamoja na wenye kushikamana na umoja. Jihadharini dhidi ya mfarakano, kwani ajitengaye miongoni mwa watu ni mfuasi wa Shetani, kama vile ambavyo mwendapweke miongoni mwa kondoo ni wa mbwa mwitu. Angalieni! Mwenye kuita watu kwa kaulimbiu hii muuweni japo awe chini ya kilemba changu hiki.”4 Hivyo ilikuwa ni bora zaidi kwa Mufti wa Azhar Tukufu kusisitiza umoja wa Waislamu na kuwaita Waislamu kwenye kushikamana na maeneo ya 3 4

Sura An‟aam: 65. Nahjul-Balaghah, Hotuba ya 127. 15


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

ushirikiano ambayo ni mengi. Wanashirikiana katika kuamini Mungu mmoja, Mtume mmoja, Kitabu kimoja, Sunna moja, Sharia moja, Kibla kimoja, lugha moja ya kidini na mengineyo. Alipasa kufanya hivyo kuliko kuanzia mazungumzo kwenye nukta zenye mzozo na kuashiria tofauti iliyopo baina ya Suni na Shia kuhusu Maswahaba, au kuhusu kuenea kwa Ushia katika nchi ya Misri. Ama kuhusu hilo jambo la kwanza yanakutosha yale yaliyo haki katika maudhui hii. Ama kuhusu jambo la pili, ni kwamba mheshimiwa alionesha kukerwa kwake na suala la kuenea kwa Ushia, ni kana kwamba kuna muasi anayeipora ardhi ya Misri. Nako ni kukerwa ambako hatuoni uhalali wake kwa upande wa maudhui, wala hali halisi haitoi usahihi wa madai haya. Na hata tukijaalia kuwa ni madai sahihi, ni kwanini basi mheshimiwa amepuuzia misafara ya wamisionari ya kuwaingiza katika ukristo watu wa nchi ya Misri au wa nchi nyingine za Kiislamu, ambazo kwa uchache zinaamini kuwa Chuo Kikuu cha Azhar ndio kitovu chao, misafara ambayo ipo miaka mingi na ambayo inavunja umoja wa Waislamu?! Na kwanini hajagusia uwahabi ambao ndio lango la ugaidi, ambao unahatarisha umoja wa Waislamu katika nchi ya Misri na katika nchi nyingine kutokana na mali inayotolewa na uwahabi katika kuwanunua watu, waandishi wa kuajiriwa, wanapropaganda na makhatibu wa wafalme?! 16


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Haya ndiyo tunayoyawasilisha kwa Mufti wa Azhar Tukufu, Ahmad Twayyib kwa muhtasari, tukitaraji kwamba mheshimiwa Mufti atafuatilia angalau kwa kupitia tu fahrasi, ile juhudi kubwa walioifanya maulamaa wakubwa wa Kishia, na ule utunzi wa thamani ulioandikwa na vidole vya Mamufti wao na wanafikra wao katika upande huu. Zaidi ya hapo ni zile juhudi kubwa walizozitoa katika kuunganisha nyoyo na kuzisogeza karibu nafsi kupitia makongamano ya kimataifa yaliyofanyika Tehran, Qum na Najaf. Nataraji tutakutana tena na Mufti katika mazungumzo yake ya siku ya pili ambayo yalirushwa na runinga katika siku ya Ijumaa, siku ya pili ya Mwezi wa Ramadhan. MHADHARA WA PILI Jioni ya Siku ya Pili ya Mwezi wa Ramadhan, Mwaka 1436 A.H. Katika mhadhara wake wa pili alioutoa jioni ya siku ya pili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, Mufti alizungumzia kuhusu maana ya Swahaba, akasema: “Swahaba ni yule ambaye zimetimia kwake nguzo tatu: Kwanza awe alikutana na Mtukufu Mtume  hata kama hakumuona kwa macho kama pale awapo kipofu. Pili: Awe alikutana naye ilihali akiwa mwislamu. Na kwa sababu hiyo kundi la makafiri na mushrikina halikujumuishwa, hata kama walisilimu baada ya kifo cha Mtukufu Mtume . Tatu: Awe 17


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

alikufa ilihali akiwa mwislamu. Hivyo aliyetimiza nguzo hizi tatu ndiye Swahaba. Kwa sharti la kwanza ameondolewa tabiina na watu wa matabaka yaliyofuatia. Na kwa sharti la tatu ameondolewa Abdullah bin Jahshi.5 Yeye alikwenda Uhabeshi na akaritadi kutoka kwenye Uislamu akiwa huko. Kama ambavyo kwa sharti hilo hilo la tatu anaondolewa yule aliyekutana na Mtume na akasilimu, kisha akaritadi na kisha baada ya hapo akarejea kwenye Uislamu katika zama za uhai wa Mtukufu Mtume , kisha akafa akiwa mwislamu, kama vile Abdullah bin Abu Sarha.” Nasema: Suala usuhuba mrefu alilosisitiza Dkt. ni moja kati ya kauli mbili katika maana ya Swahaba, na kuna kauli nyingine ambayo yenyewe haioni usuhuba mrefu kuwa ni sharti katika kuzingatiwa mtu kuwa ni Swahaba. Katika maelezo yafuatayo tunaashiria baadhi ya wale waliosema kauli hiyo: Ahmad bin Hanbal amesema: “Swahaba wa Mtume wa Allah  ni kila aliyeandamana naye mwezi mmoja au siku moja au saa moja au aliyemuona.” Bukhari amesema: “Yeyote miongoni mwa Waislamu aliyemwandama Mtume wa Allah  au kumuona basi yeye ni Swahaba.” 5

Aliyeritadi kwa kuingia katika ukristo huko Uhabeshi ni Ubaydullah bin Jahshi. Ama Abdullah bin Jahshi yeye alikufa kishahidi siku ya Uhudi.

18


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Na Kadhi Abu Bakri bin Muhammad bin Twayyib amesema: “Hakuna tofauti baina ya wanalugha kwamba neno Swahaba limechukuliwa kutoka kwenye neno usuhuba, sawa uwe wa muda mchache au mrefu.” Na mwandishi wa kitabu al-Ghawaliy amesema: “Jina la uswahaba haitwi ila yule aliyesuhubiana naye. Kisha kwa jinsi jina lilivyowekwa kilugha, unatosha usuhuba hata wa saa moja. Lakini jamii inalitumia hasa kwa yule ambaye umekithiri usuhuba wake.”6 Wakati wa kuzungumzia mhadhara wa tatu tutaeleza kwamba Mufti ametaja uwepo wa kauli mbili katika kutoa maana ya Swahaba, moja ni ya kambi ya wanahadithi na nyingine ni ya kambi ya wanzuoni wa misingi ya sharia. Kisha akaeleza kwamba, kupanua maana ya Swahaba kama ilivyokuja katika baadhi ya rai hizi ni jambo ambalo halina nguvu kilugha wala kijamii, kwani hakika Maswahaba wa mtu ni watu ambao wana maingiliano naye na wanaishi pamoja naye muda mrefu, hivyo neno Swahaba halikubaliki kwa mtu ambaye hajamuona ila mara moja kwa mbali, au aliyesikia maneno au kuzungumza naye kwa muda mchache, au aliyeishi Madina kwa kipindi kifupi. Na sisi tunamuunga mkono Mufti katika hili. 6

Usudul-Ghabah: 1/ 11 – 12.

19


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Baada ya mapitio haya ya haraka katika kutoa maana ya Swahaba, hebu sasa tuugeukie mtazamo wa Mufti katika mambo mawili: Kwanza: Kudai kwake Ijmai katika maudhui isiyo na uainisho: Mufti Mungu amhifadhi, amedai kwamba dhana ya uadilifu wa Maswahaba ni miongoni mwa mambo yenye msitari mwekundu, akasema: “Ni jambo lililoafikiwa baina ya Masuni.� Sasa tunamuuliza, itakuwaje dhana ya uadilifu wa Maswahaba iwe ni sehemu ya mambo yenye msitari mwekundu au jambo lililothibiti kwao ilihali kuna tofauti kubwa kuhusu jambo husika. Hakika uwepo wa mwafaka juu ya hukumu unategemea uwepo wa mwafaka juu ya maana ainishi yenye kuainisha maana ya Swahaba. Na tayari umeshajua rai zao zilivyotofautiana, kiasi kwamba hata Mufti mwenyewe ametamka bayana katika mhadhara wake wa tatu kwamba wanahadithi wamepanua zaidi maana ya Swahaba. Pili: Upanuzi wenye lengo la kulinda heshima ya baadhi ya Maswahaba: Hakika upanuzi katika maana ya Swahaba hadi kumjumuisha yule aliyemuona mara moja kisha akauacha mji wa Madina, na hakumuona tena baada 20


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

ya hapo, hakika upanuzi huo umekuja kwa lengo la kulinda heshima ya baadhi ya Maswahaba. Na hilo litajulikana baada ya kubainisha nukta mbili zijazo: a. Bukhari amepokea ndani ya Sahih yake kutoka kwa Abu Huraira kwamba alikuwa akisimulia kwamba, Mtume wa Allah  alisema: “Litaletwa kundi miongoni mwa Maswahaba wangu na hatimaye watazuiwa wasiifikie Hodhi, nitasema: „Ewe Mola! Hao ni Maswahaba wangu.‟ Atasema: „Wewe hujui waliyozua baada yako, hakika wao waliritadi kwa kurudi nyuma ya visigino vyao.”7 b. Baada ya kufariki Mtukufu Mtume  waliritadi wengi miongoni mwa wale waliosilimu na kumwamini yeye huko Yamama na maeneno mengine, kwa kuongozwa na Musaylama al-Kadhabu na wengineo. Na hawa walioritadi walikuwa walishamshuhudia Mtukufu Mtume na kusikia hadithi zake, kisha waliuahama mji wa Madina na wakahesabiwa kuwa ni miongoni mwa Maswahaba. Na kwakuwa kuritadi kulikuwa kunashusha heshima ya Maswahaba, walijaribu kuzielekeza kwa wale ambao hawakumwandama Mtukufu Mtume  isipokuwa muda mchache usio wa 7

Sahih Bukhari, Kitabu Riqaq, Mlango wa Hodhi, Hadithi ya 6586. Na angalia riwaya nyingine za mlango huo katika namba 6576 – 6593.

21


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

kawaida, zile riwaya zinazojulisha kuritadi, ili kwa kufanya hivyo walinde heshima ya Maswahaba wengine. Lakini ni jaribio lisilo na ufaulu, kwa sababu maelezo aliyopokea Bukhari –kwa mwenye kuchunguza kwa kina - yanawahusu wale wanaozingatiwa ni miongoni mwa kundi hilo kubwa, na hilo liko bayana kwa mwenye kuzisoma riwaya husika. MHADHARA WA TATU Jioni ya Siku ya Tatu ya Mwezi wa Ramadhan, Mwaka 1436 A.H. Dkt. Ahmad Twayyib Mufti wa Azhar Tukufu, katika mhadhara wake wa kila siku, katika siku ya tatu ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan mwaka 1436 A.H. alizungumzia kuhusu Swahaba na uadilifu wao, na muhtasari wa aliyoyasema upo katika mambo haya: Kwanza: Aliashiria kwamba kuna kambi mbili katika kuainisha maana ya Swahaba kukutana na Mtume, nazo ni kambi ya wanahadithi na kambi ya maulamaa wa misingi ya sharia. Wanahadithi wao wamepanua sana katika maana ya Swahaba kukutana na Mtukufu Mtume , wakasema: “Makusudio ya kukutana ni kukutana kwa namna yoyote ile, hata kama si kwa kikao cha muda mrefu, cha muda mfupi, sawa awe alipokea hadithi kutoka kwake au hakupokea, na sawa awe alishiriki vita pamoja naye au hakushiriki.” Ama 22


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

watu wa misingi ya sharia, wao wamechukua tahadhari sana katika kutoa maana ya Swahaba, wamesema: “Ni yule aliyesuhubiana naye kwa muda mrefu na akamfuata kwa muda unaotosha kusema „fulani alisuhubiana na fulani.‟” bila kuainisha muda huu. Na imesemekana ni miezi sita, na imesemekana ni mwaka au vita moja. Pili: Hakika uadilifu wa Swahaba hauji kutokana na wingi wa ibada wala Swaumu, wala Swala, wala Hija wala Zaka. Bali hakika unakuja kutokana na kujumuika kwake na Mtukufu Mtume pamoja na Uislamu wake mpaka kufa kwake. Tatu: Uadilifu wa Swahaba kwa maana ya kwamba akipokea hadithi haichunguzwi ni kama wasemavyo: “Amevuka vipimo”.Mwingine asiyekuwa Swahaba hadithi yake haikubaliwi isipokuwa baada ya kuchunguzwa katika tasnia ya uchunguzi wa dosari na uadilifu wa mpokezi. Kwa sababu Swahaba ni mwadilifu na mwadilifu habari yake inakubaliwa. Nne: Suni hawathibitishi umaasumu isipokuwa kwa Manabii, na kwamba Maswahaba wote ni waadilifu na wanaweza kukosea. Nasema: Anajibiwa katika jambo la kwanza kwamba: Ni kama ulivyojua, kwamba kupanua maana ya Swahaba ili iwajumuishe hadi wale waliomuona Mtume kwa saa tu, ilikuwa ni kwa lengo makhususi, 23


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

nalo ni kulinda heshima ya Maswahaba maarufu, na hiyo ni kwa kurejesha kwa wale wasio maarufu ambao hawakumwandama Mtukufu Mtume isipokuwa kwa siku moja au chini ya hapo, zile riwaya zinazojulisha kuritadi kwa baadhi yao. Lakini jaribio halijatimia kwa mwenye kusoma vizuri zile riwaya zinazojulisha kuritadi kwa kundi miongoni mwao baada ya kufariki kwa Mtukufu Mtume .8 Kuhusu Jambo la Pili, anajibiwa kuwa: Aliyoeleza ya kwamba uadilifu wa Swahaba unazalika kutokana na kule tu kukutana na Mtukufu Mtume tu, ni jambo lisilokubaliwa na akili salama, kwani kwa maana hiyo kule kukutana tu kutakuwa sawa na kemikali katika kutengeneza utu bora wa Swahaba. Ni kama kemikali ambayo hutumika katika kubadili mada moja kuwa mada nyingine, kama vile kubadili shaba kuwa dhahabu, ili huo usuhuba wa kizazi kikubwa chenye watu karibia laki moja utengeneze umma na taifa adilifu la kupigiwa mfano ambalo litakuwa kigezo na mfano wa kufuatwa na vizazi vijavyo?! Na miongoni mwa walioelekea kwenye maana hii ni Imam Ibn Waziri (aliyefariki mwaka 842 A.H.) ambapo aliwaengua kutoka miongoni mwa Maswahaba wale ambao ulidhihiri wazi uovu au dhulma yao, kwa sababu yeye anaona kwamba huyu dhalimu 8

Sahih Bukhari, Kitabu Riqaq, Mlango wa Hodhi, Hadithi ya 6589, 6582, 6583, 6584, 6585, 6586, 6587.

24


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

na muovu anaupa sifa mbaya uswahaba wa kumwandama Mtukufu Mtume , akasema: “Ameenguliwa kutoka miongoni mwa Swahaba yule aliyetajwa kwa uovu wa wazi kama vile Walid bin Uqbah.” – na kama uswahaba ungekuwa unaathiri moja kwa moja kwa njia ya muujiza basi hata Walid asingekuwa muovu – na anasema: “Na miongoni mwa umuhimu wa mlango huu ni kusema kuwa Maswahaba wote kwa dhahiri ni waadilifu, isipokuwa yule ambaye imethibiti dalili kuwa ni muovu kwa tamko la wazi. Na kwa madhehebu yote ni wajibu kufanya uenguaji huu, na hata wanahadithi wanaposema kuwa Maswahaba wote ni waadilifu, hakika wao humwengua yule mwenye sifa hii, na hakika hawajamtaja kutokana na unadra wake, kwani hakika wao wamebainisha hilo katika vitabu vya kuwajua Maswahaba. Na wameshafanya kama hili waliposema: “Hadithi mursalu hazikubaliki zote bila kubagua.” Licha ya kwamba wao wanakubali Hadithi mursali za Maswahaba.9 Daawa ya Mtukufu Mtume  haikuwa ya kimuujiza iliyo nje ya kanuni za kimaumbile, hivyo Mtukufu Mtume  hakuwalea watu na kuwafunza isipokuwa kwa msaada wa njia za kimalezi na vifaa vilivyokuwepo wakati huo. Na daawa yenye kutegemea msingi huu athari zake hutofautiana kulingana na 9

As-Suhbat Was-Swahabah cha Farhan Malikiy: 44, Chapa ya kwanza ya mwaka 1423 A.H.

25


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

maandalizi na uwezo. Hivyo kwa kuchunguza yale tuliyotaja tunatoka na hitimisho lifuatalo: Hakika misingi ya malezi inahukumu kwamba miongoni mwa Maswahaba yupo anayeweza kufikia daraja za juu kabisa katika nguvu ya imani na uimara wa itikadi. Na kama ambavyo yupo anayeweza kufikia katika daraja za kati katika ukamilifu na fadhila. Na yupo ambaye inawezekana asiathiriwe na uswahaba na sababu nyingine zenye kuathiri isipokuwa kidogo tu kiasi cha kutomfanya kuwa katika safu za waadilifu na kundi la watu wema. Na hili ndilo linalotufanya tuwagawe Maswahaba katika viwango tofauti kama walivyo Tabiina, kwani kinyume na hivyo italazimu kule tu wao kukutana na Mtume kuwe sababu ya kuwafanya Maswahaba wote elfu moja kuwa watu wa kuigwa na wa mfano. Kana kwamba wao ni aina nyingine ya viumbe wasiokuwa wanadamu. Ama kuegemeza hilo kwenye Qurâ€&#x;ani Tukufu tutatafsiri Aya zinazohusu hilo baadaye inshaallah. Naamini kwamba tatizo si uaminifu wa Swahaba na kukubali riwaya zake, si jambo hilo ndilo lililomfanya Dkt. Twayyib asisitize madai yake, bali tatizo ni kuhusu matendo yenye kupingana na sharia na ambayo hayaoani na maadili ya Uislamu. Kwa mfano tu, Dkt. Atakiweka wapi kisa cha Malik bin Nuwayra na kuuwawa kwake na kutendewa unyama mke 26


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

wake?10 Atauweka wapi msimamo wa Abu Dhari11 na Ammar?12 Ataweka wapi kitendo cha kuwamakinisha Bani Umayyah na kuwarejesha wale waliokuwa wamefukuzwa kama vile al-Hakam na mwanawe Maruwani?13 Na kutokana na tuliyoyataja unadhihiri utata juu ya Jambo la Tatu, namaanisha kwamba, yeye Mufti anaikubali hadithi ya Swahaba bila kuipima katika tasnia ya kupima na kuchunguza dosari na uadilifu wa Swahaba. Maana yake ni kwamba kule tu kukutana na Mtume hata kwa saa moja au siku moja au kusikia 10

Riwaya nyingi zimetaja kwamba, Khalid bin Walid baada ya kumuuwa Malik bin Nuwayra kwa kisingizio chake hewa, alimuoa mke wa marehemu. Aliporejea Madina na habari zake kuenea, Umar alimwambia: “Umemuuwa mwislamu kisha umemuoa mke wake, wallahi nitakupopoa mawe kwa mawe yako.” tazama Tarikh Tabari: 3/ 279, matukio ya mwaka 11 A.H. 11 Uthman alimfukuzia huko Rabadha, akafariki huko akiwa peke yake. Tazama Ansabul-Ashraf: 5 / 52. 12 Tazama aliyoyaeleza Baladhariy katika al-Ansabu: 6/ 161, kuhusu yale yaliyotokea baina ya Uthman na Ammar, ambapo Uthman aliwaamrisha wasaidizi wake wamkamate Ammar, akakamatwa na kuingizwa kwa Uthman, akampiga hadi akazimia. Kisha akatolewa na kupelekwa nyumbani kwa Ummu Salamah, hakusali Adhuhri, Laasir na Maghrib, alipozinduka ndipo akachukua udhu na kuswali. 13 Al-Hakam bin al-Aswi, ambaye Mtume wa Allah alimfukuzia Twaifu yeye na mwanawe, isipokuwa ni kwamba Khalifa Uthman alimrudisha Madina na jambo hilo likawanyong‟onyesha Waislamu. Tazama al-Ansabu: 3/ 27.

27


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

hadithi, kumewafanya watu laki moja miongoni mwa watu waliokutana na Mtume, kuwa watu wa mfano na kuigwa, kwa namna ambayo wamekuwa ni watu wenye nguvu inayowazuia wao kutenda madhambi makubwa au madogo au mambo ya halali yasiyovutia. Na kwamba uswahaba ni sehemu ya muujiza unamwathiri yule aliyemuona Mtume kama inavyoathiri miujiza. Na hili ni jambo la ajabu, na kwa ajili hii hakuna yeyote aliyehesabu uswahaba kuwa ni muujiza miongoni mwa miujiza iliyo nje ya mipaka ya kanuni za maumbile ya kawaida. Na anajibiwa kuhusu Jambo la Nne, nalo ni kudai kwake kwamba umaasumu kwa Masuni hauthibiti isipokuwa kwa Mtume tu. Hakika madai hayo ni jambo lisilosadikishwa na Qur‟ani Tukufu. Huu hapa utajo wenye hekima unamsifu Mariam kwa kusema: “Na Malaika waliposema: Ewe Maryam! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteua na akakutakasa na akakuteuwa juu ya wanawake wa ulimwenguni.”14 Hivyo kauli yake “Na akakutakasa” hakusudii kumtakasa na uchafu bali alikusudia kuitakasa roho yake na uchafu wa kimaanawiya na kumpamba na tabia njema. Na ushahidi juu ya hilo ni kwamba alikariri neno “Alikuteua” na akaweka baina ya ibara hizo mbili neno “Na akakutakasa”. Ama kutafsiri utakaso kwa maana ya kumsafisha na tuhuma waliyomtuhumu Mayahudi ya kupata mtoto nje ya 14

Sura Imran: 42.

28


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

ndoa, ni tafsiri iliyo mbali na mtiririko wa Aya.15 Kwasababu Aya inazungumzia hali yake kabla hajashika ujauzito uliomfanya Mayahudi wakamtuhumu. Na ushahidi juu ya hilo ni kwamba kisa cha ujauzito wake kimekuja baada ya Aya hiyo, ambapo ni baada yake ndipo imekuja kauli ya Allah: “Waliposema Malaika: Ewe Maryam! Hakika Mwenyezi Mungu anakubashiria (mwana) kwa neno litokalo kwake; jina lake ni Masih mwana wa Maryam; mwenye heshima duniani na akhera na ni miongoni mwa waliokurubishwa.”16 Yeyote atakayesoma Aya zinazomtambulisha Maryam na nafasi yake ataamini kwamba yeye alikuwa Maasumu aliyeepushwa na kila aibu, Allah anasema: “Na akamlea Zakariya. Kila mara Zakariya alipoingia Mihrab hukuta vyakula. Akasema: Ewe Maryam, unatoa wapi hivi. Akasema: Vinatoka kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila hesabu.”17 Heshima hii inathibitishwa naQur‟ani kwa Maryam na ilikuwa kabla hata hajashika ujauzito wa Masihi , kama mtiririko wa Aya unavyothibitisha hilo. Kama ambavyo Qur‟ani Tukufu inavyomzungumzia mja miongoni mwa waja wa Allah, ambaye Allah alimpa rehema kutoka Kwake na akamfundisha elimu na akawa mwalimu 15

Tafsiri al-Baydhawiy: 1/ 159. Sura Imran: 45. 17 Sura Imran: 37. 16

29


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

wa Musa , ambapo Musa  aliyesema na Allah alimwambia: “Je, nikufuate ili unifunze katika ule uongofu uliofunzwa?”18Na mtu huyo wa kuigwa na kupigiwa mfano hakuwa Nabii, lakini hata hivyo alikuwa mwalimu wa Musa. Je unafikiri kwamba mtu asiyekuwa maasumu, ambaye mara anakosea na wakati mwingine anatenda maasi kisha anatubu, anaweza kuwa mwalimu wa Nabii? Na hili linatusukuma kusema kuwa umaasumu hauna sharti la unabii, kila Nabii ni Maasumu lakini si kila maasumu ni nabii. Na katika mtiririko huu tunaweza kuashiria maneno ya Razi katika tafsiri ya kauli ya Allah: “Enyi mlioamini! Mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume na wenye mamlaka katika nyinyi..”19 ambapo amesema: “Tambua kwamba kauli yake ”Na wenye mamlaka katika nyinyi” inajulisha kwetu kwamba Ijmai ya umma ni hoja. Na dalili juu ya hilo ni kwamba Allah katika Aya hii ameamuru kuwatii moja kwa moja bila kusita wale wenye mamlaka. Na mtu ambaye Allah ameamuru atiiwe moja kwa moja bila kusita ni lazima awe ni maasumu asiyekosea, kwani kama akiwa si maasumu asiyekosea Allah atakuwa ameamuru kufuata makosa, kwa kule tu kuwepo uwezekano wa yeye kukosea.” Razi ameendelea mpaka aliposema: “Hivyo imethibiti kwamba Allah 18 19

Sura Kahfi: 66. Sura Nisaa: 59.

30


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

aliamuru kuwatii moja kwa moja bila kusita wale wenye mamlaka. Na imethibiti kwamba kila ambaye Allah ameamuru kumtii moja kwa moja bila kusita ni wajibu awe ni maasumu asiyekosea. Hivyo inathibiti kwa yakini kwamba wenye mamlaka waliotajwa katika Aya hii ni lazima wawe ni maasumu.� Kisha akakiri kwamba hao maasumu ndio wenye maamuzi.20 Hivyo maneno ya Razi ambaye ni mmoja miongoni mwa maulamaa wa Kisuni yanapingana na madai ya Mufti wa Azhar, ya kwamba Suni hawathibitishi umaasumu isipokuwa kwa Manabii tu. Tutosheke na misitari hii mifupi, kwani nataraji kuwa tutakutana katika mhadhara ujao. MHADHARA WA NNE Jioni ya Siku ya Nne ya Mwezi wa Ramadhan, Mwaka 1436 A.H. Dkt. Ahmad Twayyib Muftiwa Azhar Tukufu, katika mhadhara wake wa siku hii, alizungumzia mambo ambayo huu ndio muhtasari wake: „Hakika Sunni na Shia ni Waislamu na Waumini. Sisi ni umma mmoja na watoto wa dini moja, na tuko upande mmoja. Na jambo hili si wajibu kulikaribia. 20

Angalia Tafsir Razi: 10 / 144.

31


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Lakini sisi hivi sasa tunazungumzia mambo ya madhehebu ndani ya Uislamu. Miongoni mwa mambo ya kimadhehebu yenye kutofautisha baina ya Suni na Shia ni suala la uadilifu wa Maswahaba. Suni wanaitakidi kwamba Maswahaba ni waadilifu, na Shia kwa bahati mbaya wao wanafungua wazi mlango wa ukosoaji kwa Maswahaba wa Mtume .‟ Mufti akaongeza: „Na wakati mwingine ukosoaji huu huwapelekea Maghulati na wafurutuada miongoni mwao, kupata ujasiri wa kuwakufurisha Maswahaba wa Mtume . Na jambo hili ni miongoni mwa misiba mikubwa iliyowapata Waislamu. Mwislamu kuitakidi kwamba yeye anaweza kuwakufurisha Maswahaba wa Mtukufu Mtume .‟ Kisha akataja kwamba binti mmoja wa Kishia alimwambia: “Sisi huwalaani Maswahaba baada ya kila Swala.” Na hili halisihi kamwe. Kisha akaashiria kwamba wahubiri wa Ushia baina ya jamii ya Suni wanasema kwamba, Umar – Mungu apishie mbali, na huu ni uwongo – alimpiga Bibi Fatima . Na akahitimisha maneno yake kwa kusema kwamba Suni wote wanaitakidi kwamba Maswahaba wote ni waadilifu. Nasema: Namshukuru Mufti huyu mkubwa kwa mambo mawili: 32


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Kwanza: Yeye amewafanya Shia na Suni kuwa ni umma mmoja na watoto wa dini moja, na walio upande mmoja. Na aliyoyasema ndio maamuzi ya Kitabu na Sunna, haya ndio yaliyopokewa kutoka kwa Umar bin Khattab, kwamba Mtume Mtukufu  alimwita Ali bin Abutalib siku ya Khaybar na akamkabidhi bendera, akamwambia: “Nenda na wala usigeuke nyuma mpaka Allah akupe ushindi.” Umar anasema: Ali akatembea mbele kidogo kisha akasimama bila kugeuka nyuma, akaita: „Ewe Mtume wa Allah! Nipigane na watu juu ya nini?‟ Akasema : “Pigana nao mpaka washahidilie kwamba hapana Mungu isipokuwa Allah, na kwamba hakika Muhammad ni Mtume wa Allah. Wakifanya hivyo watakuwa wameizuia damu yao na mali yao dhidi yako, isipokuwa kwa haki yake (haki ya mali) na hesabu yao ni kwa Allah.”21 Na katika hadithi nyingine kutoka kwa Ibn Umar ni kwamba Mtume wa Allah  alisema: “Nimeamrishwa kupigana na watu mpaka washahidilie kwamba hakuna Mungu isipokuwa Allah na hakika Muhammad ni Mtume wa Allah, na wasimamishe Swala na watoe Zaka. Wakifanya hivyo watakuwa wamenikinga dhidi ya damu yao na mali yao 21

Sahih Muslim: 7/ 121. Kitabu cha fadhila za Ali.

33


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

isipokuwa kwa haki ya Uislamu, na hesabu yao ni kwa Allah.”22 Ikiwa hiki ndio kipimo cha Uislamu, basi kila anayetoa shahada mbili na kuamini siku ya malipo atakuwa ameingia chini ya hema la Uislamu bila kutofautisha baina ya mwislamu huyu na yule. Na kwa msingi huu, uadilifu wa Maswahaba si miongoni mwa mambo ya dini ambayo yanapima imani na Uislamu wa mtu, bali wenyewe ni miongoni mwa mambo ya kitheiolojia, na kwa mujibu wa ibara ya Mufti, ni miongoni mwa mambo ya kimadhehebu. Ni kwanini basi tunakuza tofauti hii? Ilihali yenyewe si lolote isipokuwa ni kama mas‟ala nyingine zenye tofauti baina ya Waislamu, katika misingi na matawi, nazo ni nyingi? Ilimpasa Mufti ambaye alhamdulilahi ameruzukiwa kifua cha uvumilivu, kutopanua ombwe hili. Na ilimpasa Mufti kuwanasibisha Shia na yale yaliyopokewa kutoka kwa Imam wao na Imam wa Waislamu wote kwa ujumla, Ali , yeye anawaelezea Maswahaba kwa kusema: “Kwa hakika nimewaona Maswahaba wa Muhammad )saww(, simuoni yoyote kati yenu anayeshabihiana nao, kwa kweli walikuwa wanaianza asubuhi wakiwa na 22

Sahih Bukhar: 26, namba 25.

34


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

nywele timtimu na wakiwa wamejaa vumbi kichwani (na mwilini). Wamepitisha usiku katika hali ya kusujudu na kusimama (wakiswali swala za usiku), wakibadili kati ya paji zao za uso na mashavu yao. Na walikuwa wanasimama mfano wa aliyesimama juu ya kaa la moto kwa ajili ya kukumbuka marejeo yao, kana kwamba kati ya macho yao kuna goti la mguu wa mbuzi kutokana na sijda zao ndefu. Atajwapo Mwenyezi Mungu macho yao hutiririsha machozi mpaka yakilowesha kosi (kola zao), walikuwa wanayumba kama uyumbavyo mti siku ya upepo mkali, wakiogopa adhabu, na wakiwa na matarajio ya thawabu.”23 Na ana neno jingine kuhusu Maswahaba wa Mtume  anasema: “Wako wapi wale waliolinganiwa Uislamu na kuukubali? Na kuisoma Qur‟ani nakuitii, na kutenda kwa mujibu wake, na kuhimizwa kupigana Jihadi wakakimbilia ukimbiliaji wa ngamia anayenyonyesha kuwakimbilia watoto wake, kuzichomoa panga kutoka katika ala zake, na kwenda sehemu mbalimbali za nchini (kwa ajili ya Jihadi), kwa makundi makundi na kwa safusafu. Baadhi waliangamia na baadhi waliokoka, hawafurahishwi na walio baki hai, na wala hawahuzunishwi na waliokufa. Wameharibika macho kwa kulia, matumbo yamesinyaa kwa kufunga Swaumu, midomo imekauka kwa dua, rangi ya miili yao imekuwa njano 23

Nahjul-Balaghah, Hotuba ya 97.

35


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

kwa kukesha. Nyuso zao zinavumbi (alama) la wanyenyekevu.Hao ndio ndugu zangu walioondoka. Ni haki yetu tuwe na kiu kwa ajili yao, na tujiume meno vidole kwa kufarikiana nao.”24 Na huyu hapa Imam Ali bin Husein Zainul-Abidin  anasema katika dua yake: “Ewe Mwenyezi Mungu!Warehemu khususan masahaba wa Muhammad waliokuwa wema katika usuhuba. Na wale waliofaulu majaribu katika kumsaidia na kumhami. Walimwitikia kwa haraka alipowasikilizisha hoja za ujumbe wake…”25 Na kwa msingi huu, kusema kuwa Shia wanakanusha uadilifu wa Maswahaba wote si jambo sahihi, linabatilishwa na maelezo yaliyopokewa kutoka kwa Maimamu hao wawili. Shia wanaitakidi kwamba Maswahaba wako katika tabaka na daraja tofauti za imani, uchamungu na uadilifu. Wapo miongoni mwao waliofikia mawinguni, na wapo ambao hawakuchupa mipaka katika imani yao, kauli zao na vitendo vyao, na wapo ambao wapo katika nafasi ya kati. Ama kuhusu uthubutu na ujasiri wa Maghulat na wafurutuada dhidi ya Maswahaba wa Mtume , katika kujibu hilo inatosha kwamba wale wafanyao hivyo ni Maghulati, na Maghulati kwa mujibu wa 24 25

Nahjul-Balaghah, Hotuba ya 97. Sahifatus-Sajjadiyyah: Dua ya Nne.

36


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

itikadi ya Shia ni Makafiri, hawazingatiwi kuwa ni Waislamu. Itawezekana vipi kuwakufurisha Maswahaba wa Mtukufu Mtume  ilihali kundi kubwa miongoni mwao ndio vinara wa Ushia, ambao walikuwa na mapenzi ya dhati na Ali  katika zama za Mtukufu Mtume  kwa kufuata usia wake. Na wakaendelea na wakabaki katika hali hiyo baada ya kufariki Mtukufu Mtume . Na vitabu vya historia vimetaja majina yao, watu mfano wa: Jundub bin Junadah (Abu Dhari), Ammar bin Yasir, Salman alFarisiy, Miqdad bin Amru bin Thaalabatul-Kindiy, Hudhayfa bin Alyamani mwenye siri ya Mtume, Khuzayma bin Thabit al-Answariy mwenye ushahidi wa watu wawili, Khubab bin Urtu Tamimiy, Saad bin Malik, Abu Said al-Khudriy, Abu Haytham bin Tayhani al-Answariy, Qaysu bin Saad bin Ubadah alAnswariy, Anas bin Harthi bin Munabihu mmoja kati ya wale waliokufa kishahidi huko Karbala, Abu Ayubu al-Answariy, Khalid bin Zaydi ambaye alimuomba Mtume awe mgeni wake wakati Mtume alipokuwa anaingia Madina, na wengine wengi ambao tumetaja majina yao katika kitabu chetu Aqidatul-Imamiyyah Fii Adalatus-Swahabah, uk. 144, rejea huko. Kisha ni kwamba ukweli wa kihistoria unathibitisha kwamba wengi miongoni mwa Maswahaba, bali wote 37


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

kutoka miongoni mwa Muhajirina na Answari, walikuwa pamoja na Kiongozi wa Waumini Ali  katika vita vyake vitatu. Zarqaniy katika kitabu Nahjul-Masalik amesema: “Katika jeshi la watu wa Iraki Ali alikuja na watu elfu sabini. Walikuwemo watu tisini walioshiriki vita vya Badri, na watu mia saba miongoni mwa wale waliotoa kiapo cha utiifu cha chini ya mti, na watu mia nne miongoni mwa Muhajirina na Answari wengine. Ama katika jeshi la watu wa Sham Muawiya alitoka na watu elfu thelathini na tano, kati ya hao hakukuwa na Answari isipokuwa Nuuman bin Bashir na Muslimat bin Mukhulad.”26 Na Masuudiy amesema katika kitabu MurujudDhahbi: “Na miongoni mwa walioshiriki vita vya Suffin wakiwa pamoja na Ali, walikuwa ni watu themanini na saba miongoni mwa wale walioshiriki vita vya Badri, walikuwemo Muhajirina kumi na saba na Answari sabini. Na katika vita hivyo walishiriki pamoja naye watu mia tisa miongoni mwa Maswahaba wa Mtume wa Allah  kutoka miongoni mwa Muhajirina na Answari ambao walitoa kiapo cha utiifu chini ya mti. Na wote walioshiriki pamoja naye miongoni mwa Maswahaba walikuwa ni watu elfu mbili na mia nane.”27 26 27

An-Naswaihul-Kafiyyah cha Alawi: 36. Murujud-Dhahbi: 2/ 352.

38


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Je inaingia akilini kwamba pamoja na uungaji mkono na msaada huu mkubwa walioutoa kwa Bwana wa Mawasii , Shia wasimame na kuwakufurisha Maswahaba wote na kuwatusi?! Na ni kuanzia hapa tunamuomba Mufti Twayyib atuletee ibara hata moja inayothibitisha kwamba maulamaa wa Shia na viongozi wao wamewadhoofisha Maswahaba wote na wamewakufurisha au wamejenga kanuni inayoashiria maana hiyo. Kisha mimi namshangaa Mufti vipi ameifanya kauli ya mwanamke mmoja wa kishia kuwa ni hoja kwa wote, na hatimaye ameitegemea?! Hiyo ni sawa na Shia kudai na kuwatuhumu Suni kuwa wanamtukana Ali  kwa hoja ya kumsikia mwanamke mmoja miongoni mwa Manawasib akimlaani Ali . Na aliyoyataja Mufti hapa yanapingana na aliyoyasema katika moja ya mihadhara yake, kwamba: “Mimi nimewasikia wakubwa kadhaa miongoni mwa maulamaa wa Shia wakipinga kauli hizi (za kuwalaani maswahaba) na wala hawaziridhii.” Ama kuhusu alilolikanusha, lile linalohusu yale yaliyompata Bibi Fatima , ni kwamba hatutaki kujeruhi hisia za watu, isipokuwa ni kwamba jambo husika ni miongoni mwa mambo yaliyothibiti na kukubalika katika historia kiasi kwamba mtu hawezi kukanusha. Nalo ni suala la kupekuliwa nyumba ya Fatima, ambapo maulamaa wengi wamelinukuu tukio hilo katika vitabu vyao. 39


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Huyu hapa Abdurahman bin Awfi anasema: “Niliingia kwa Abu Bakri kumtembelea wakati wa maradhi yake yaliyopelekea kifo chake. Nikamsalimu na kumwambia: Alhamdulilahi sioni tatizo kwako. Usiihuzunikie dunia, wallahi hatukujui isipokuwa kwamba wewe ni mwema mtengeneza mema. Akasema: „Mimi sihuzunishwi na chochote isipokuwa na mambo matatu niliyoyatenda, na natamani kwamba nisingeyatenda. Na ninahuzunishwa pia na mambo mengine matatu ambayo sikuyatenda, na natamani kwamba ningeyatenda. Na pia nahuzunishwa na mengine matatu ambayo natamani kwamba ningemuuliza Mtume wa Allah kuhusu mambo hayo. Ama yale niliyoyatenda na natamani kwamba nisingeyatenda, natamani kwamba nisingetenda kadha wakadha…‟” Abu Ubaydu anasema: sitaki kuyataja.28 Hakika mwandishi wa kitabu al-Amuwal licha ya kwamba amesitiri yale aliyotamani Khalifa kwamba asingeyafanya, isipokuwa ni kwamba wahakiki wengi wameyataja kwa ibara yake. Huyu hapa Mubaridu katika kitabu chake al-Kamil anasema: “Ama matatu ambayo niliyafanya na natamani kwamba nisingeyafanya, ni kwamba natamani kwamba nisingeipekua nyumba ya Fatima na ningeiacha hata kama ningelazimika kupigwa vita.”29 28 29

Al-Amuwal: 193 – 194, Maktabatul-Kuliyatil-Az‟hariyyah. Al-Kamil: 1 / 11.

40


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Na huyu hapa al-Masuudiy ananukuu kutoka kwa Khalifa, anasema: “Ama matatu ambayo niliyafanya na ninatamani kwamba ningeyaacha, natamani kwamba nisingeipekua nyumba ya Fatima.”30 Na kwakuwa kunukuu maneno ya wahakiki na watunzi kutarefusha maneno hapa, tunaashiria baadhi ya vyanzo hapa chini.31 Na yeyote anayetaka kuhakiki maudhui hii basi na aifanyie uchunguzi ili ajue ni nani aliyetoa amri ya kuvamiwa au kupekuliwa nyumba ya Fatima  na ni nani aliyetekeleza amri hii, na ni yapi matokeo yake. Ukweli utamdhihirikia kwa uwazi kabisa. Na haya ndio yanayotajwa na Shia kwa kutegemea vyanzo hivi. Hivyo tunatoka na hitimisho lifuatalo: Hakika Shia wanawaheshimu Maswahaba kwa kufuata mafunzo ya Maimamu wao na wala hawawakufurishi. Isipokuwa ni kwamba wao wanaona kuwa Maswahaba 30 31

Murujud-Dhahbi: 2 / 301. Tabaraniy katika al-Muujamul-Kabir: 1/ 62, namba 43. Ibn Abdirabih katikaal-Aqdu al-Faridu: 4 / 93. Ibn Asakir katika Mukhtasar Taarikh Damashqi: 13/ 122. Ibn Abil-Hadid katika Sharhu Nahjul-Balaghah: 2/ 46. Juwayniy katika FaraidusSamtwayni: 2/ 34. Dhahbi katika Taarikhul-Islam: 3/ 117. Nuruddin Haythamiy katika Majmauz-Zawaid: 5/ 102. Ibn Hajar Asqalaniy katika Lisanul-Mizan: 4/ 188. Al-Muttaqiy alHindiy katika Kanzul-Ummal: 5/ 631, namba 14113. AbdulWahhab Abdul-Maqsud katika Kitabul-Imam Ali: 4/ 74.

41


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

wana daraja tofauti katika imani, na viwango tofauti katika uchamungu na uadilifu. Ama kuhusu yale yanayonasibishwa kwa Ghulat na wafurutuada, ni kwamba Shia Imamiyyah wako mbali nayo. Na ama kuhusu suala la kupekuliwa kwa nyumba ya Bibi Fatima Zahra , ni kwamba hili ni jambo lililonukuliwa kwa wingi, lakini pamoja na hivyo tunalingania kwenye umoja badala ya mfarakano, tunasema: Hakika yanayotuunganisha ni mengi kuliko yale yanayotutofautisha. Hakika itikadi inatuunganisha pamoja umma mmoja. Unatukusanya pamoja ufuasi wa dini ya uongufu. Uislamu unaunganisha baina ya nyoyo zetu hata tukitofautiana mapenzi na makundi. Na kama Mufti asingegusia suala la Fatima  basi nasi tusingeligusia katika mhadhara huu, isipokuwa ni kwamba kwa ajili ya kuitetea haki na ukweli tumeona hakuna budi kuligusia. MHADHARA WA TANO Jioni ya Siku ya Tano ya Mwezi wa Ramadhan, Mwaka 1436 A.H. Dkt. Ahmad Twayyib Mufti wa Azhar Tukufu alisema: “Hakika Swahaba ambaye umethibiti uswahaba wake, uadilifu wake hauchunguzwi, wala hahitaji uthibitisho wa usafi wake, kwa sababu uswahaba huu wenyewe ndio unaompa bila hiyari uthibitisho huu.” Kisha Mufti Mungu amhifadhi aliendelea kutoa maana ya uadilifu mpaka aliposema: “Ikiwa Swahaba 42


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

atapokea hadithi au kutoa ushahidi juu ya tukio fulani basi riwaya yake inakubalika na pia ushahidi wake. Bila ya kusema: Yeye ni nani? Ni ipi historia ya maisha yake? Hii ndio maana ya uadilifu wa Swahaba, na kwa hili amejitofautisha na mwingine asiyekuwa Swahaba. Kwani asiyekuwa Swahaba kuanzia Tabiina, pindi anapopokea riwaya au kutoa ushahidi ni lazima uthibiti uadilifu wake kabla ya kukubali ushahidi wake au riwaya yake.â€? Mwishoni mwa maneno yake akamalizia kwa kusema kwamba, Swahaba fakiri ambaye huenda hamiliki hata kiatu cha kutembelea, kisha anajitolea nafsi yake na kila anachomiliki na yuko tayari kumwaga damu yake kwa ajili ya kumlinda Mtume wa Allah na dini, anastahiki kuteremshiwa Aya za Qurâ€&#x;ani Tukufu ili kuelezea uadilifu wake. Nasema: Katika maneno ya Mufti hakuna kitu kipya bali ni marudio ya yale aliyoyasema katika mihadhara iliyotangulia, lakini pamoja na hivyo tutamwasilishia Mufti nukta zifuatazo: Ya kwanza: Yale aliyoyasema Mufti Twayyib ni madai ambayo yanahitaji kuungwa mkono na dalili na hoja yakinifu ya kiakili au maandiko yaliyo katika kiwango cha hadithi na sunna. Hii ni kama haitanukuliwa kwamba dalili ya maandiko inatoa matokeo yaliyo kinyume na madai yake, kama itakavyokuja huko mbele. Kisha ni nani aliyesema 43


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

kuwa Swahaba anayejadiliwa ni yule mwenye sifa za juu na tukufu kama hizo alizozitoa Mufti Twayyib, ambaye anajitolea nafsi yake na kila anachomiliki na yuko tayari kumwaga damu yake kwa ajili ya kumlinda Mtume wa Allah na dini? Je Dkt. Alishawahi kumpata mtafiti mwadilifu au waadilifu miongoni mwa wanafunzi Mashia, anayemgusa kwa ubaya na shaka Swahaba mwenye sifa kama hizo? Wapi na wapi Swahaba kama huyo na yule aliyekunywa pombe na akatapika akiwa mihrabuni akiswali, na kabla ya hapo ilikuwa imeshateremka Aya ya Qur‟ani ikisisitiza uovu wake?32 Ya pili: Yeye amesisitiza kigezo cha uswahaba, na kwamba kilichowafanya kuwa waadilifu watu wote laki moja waliokuwa wamezama katika uabudu masanamu na tabia za kijahiliya, ni kule tu kumuona Mtukufu Mtume  na kusuhubiana naye kwa namna ambayo masharti yake ameyabainisha katika mihadhara iliyotangulia. Na kuanzia hapa tunasema: Hakika usuhuba wa Maswahaba wa Mtume wa Allah  haukuwa na nguvu wala imara wala mrefu kushinda usuhuba wa mke wa Nuhu na mke wa Luti. 32

Al-Kamilu Fii Taarikh: 2/ 246, matukio ya mwaka 30 A.H. Usudul-Ghabah: 5/ 452, namba 5468. Taarikhul-Khulafai: 144. Al-Istiaab: Sehemu ya Nne/ 1556, namba 2721. As-Siratul-Halabiyyah: 2/ 284. 44


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Wao wawili walisuhubiana na waume zao wema na wakaishi nao usiku na mchana, lakini hata hivyo usuhuba huu kwa bahati mbaya haukuwasaidia chochote kwa Allah, Allah Mtukuka anasema: “Mwenyezi Mungu amewapigia mfano waliokufuru mke wa Nuhu na mke wa Lut. Walikuwa chini ya waja Wetu wema wawili miongoni mwa waja Wetu. Lakini wakawafanyia hiyana, nao wasiwafae kitu. Na ikasemwa: Ingieni Motoni pamoja na wanaoingia!” (Sura Tahrim: 10). Ya tatu: Kitabu kitukufu kinawakemea baadhi ya wake za Mtukufu Mtume kwa sababu ya kufichua kwao siri yake, na kinawalaumu kuhusu hilo, Allah anasema: “Na Nabii alipomwambia mmoja wa wake zake jambo la siri. Basi alipolitangaza yule mke, na Mwenyezi Mungu akamdhihirishia Mtume, alimjulisha sehemu na akaacha sehemu nyingine. Alipomwambia hayo, huyo mke akasema: Nani aliyekwambia haya? Mtume akasema: Kaniambia Mjuzi Mwenye habari! Kama nyinyi wawili mtatubia kwa Mwenyezi Mungu, basi nyoyo zenu zimekwishaelekea kwenye haki. Na mkisaidiana dhidi yake Mtume, basi hakika Mwenyezi Mungu Ndiye kiongozi Wake, na Jibrili, na waumini wema, na zaidi ya hayo Malaika pia watasaidia. Akiwapa talaka, asaa Mola Wake akampa wake wengine badala yenu nyinyi, walio bora kuliko nyinyi, wanyenyekevu, 45


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

waumini, watiifu, walio tubu, wenye kushika ibada, wafanyao kheri, wajane na wanawali.” (Sura Tahrim: 3 – 5). Kuna kemeo lipi kali kushinda kauli ya Allah: “Kama nyinyi wawili mtatubia kwa Mwenyezi Mungu, basi nyoyo zenu zimekwishaelekea kwenye haki.”, yaani nyoyo zenu zilichepuka mbali na haki. Kama ambavyo kauli yake: “Na mkisaidiana dhidi yake Mtume,” inafichua uwepo wa mazingira ya wao kusaidiana dhidi ya Mtukufu Mtume  na kumkhalifu. Naye Allah Mtukuka ameelezea kutofaulu matamanio yao kwa sababu Allah, Jibril, aliye mwema kati ya waumini na Malaika ndio watakaomnusuru Mtukufu Mtume . Ya nne: Tafakuri ya kina katika Aya hizi inatubainishia nafasi ya wanawake hawa wawili, na kwamba Allah anawapa hiyari ya kuchagua moja kati ya mambo mawili: 1. Toba na kumrejea Allah. 2. Au kupigwa vita na Allah. Na kwamba Allah atakuwa msaidizi wa Mtume pamoja na Malaika na aliye mwema kati ya waumini. Na hili linajulisha kuwa jambo lililotoka kutoka kwao wao wawili ni dhambi na maasi, na kwa ajili hiyo walistahiki aina hii ya onyo na kemeo. Na laiti lingekuwa ni jambo jepesi na la kawaida basi 46


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

wasingestahiki kiwango hiki cha kemeo na onyo. Hakika Qur‟ani imeeleza kwa ufupi bila kufafanua, je wanawake hawa wawili walitubu au hawakutubu bali walibakia kama walivyokuwa wakimuudhi Mtume? Hakika Dkt. Ahmad Twayyib Mungu amzidishie umri mrefu, katika kuelezea kwake maana ya uadilifu aliashiria kwamba, nguvu ya uadilifu humzuia mtu kutenda madhambi makubwa, hivyo mtu hujizuia bila hiyari kusema uwongo, na pindi anapotaka kusema uwongo nafsi yake huwa haikubali. Nasema: Aliyoyasema ni sahihi, lakini hebu atafakari maelezo aliyoyapokea Bukhari kutoka kwa Aisha katika tafsiri ya Aya tatu zilizotangulia. Anasema: Alisema: Mtume wa Allah alikuwa anaramba asali kwa Zaynab binti Jahshi na anakaa kwake, nikapanga mimi na Hafsa kwamba akiingia kwa yeyote kati yetu basi amwambie: “Je umekula maghafira? Mimi nasikia reha ya maghafira kutoka kwako.” Alipoambiwa akasema hapana, lakini nilikuwa naramba asali kwa Zaynabu binti Jahshi, sintorudia tena, na nimeshaapa, usimwambie hilo yeyote.33 Hivi kumnasibisha Mtume na ulaji wa maghafira si uwongo? Na iko wapi hapa nguvu, wakati wanapanga dhidi ya Mtume wa Allah na wanaafikiana kusema 33

Sahih Bukhar: 3 / 3-8, Kitabu cha tafsiri (65), mlango kutoka Sura Tahrim, namba 4912.

47


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

uwongo katika jambo ambalo husuda au wivu ndio uliowasukuma kulitenda. Na yote haya yanajulisha kwamba suala hili la uadilifu wa Maswahaba ni suala lenye kukubalika lakini si kwa sura ya jumla inayomjumuisha kila Swahaba. Hakika Bibi Aisha anaheshimika kwetu, kwa sababu yeye ni mke wa Mtukufu Mtume , na tunasema kuhusu haki yake yale aliyoyasema Imam Ali  katika tukio la Jamal, aliposema: “Ama kuhusu fulani (Bibi Aisha) ameshikwa na rai ya kike, na kijicho kinatokota kifuani mwake kama jokofu (tanuri) la mfua chuma. Lau angeambiwa amfanyie kebehi mtu mwingine kwa kiwango alichonikebehi, asingefanya. Naye bado (kwangu mimi) anaheshima yake ya mwanzo, na hesabu (yake) ni kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.”34 Pamoja na hayo, hili halituzuii kuchunguza na kusoma yale aliyoyatenda katika vita vya Jamal, ikiwa ni pamoja na kukusanya majeshi na kuyapeleka Basra, na hapo akakiuka kauli ya Allah Mtukuka: “Na kaeni majumbani mwenu” na katika vita hivi wakauwawa maelfu miongoni mwa wanawe. Na Dkt. hajatutajia sababu iliyopelekea nguvu hii kutoweka na kumsemea uwongo Mtume wa Allah na kumweleza 34

Nahjul-Balaghah, Hotuba ya 156.

48


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

kinyume na ilivyo, kama ilivyokuwa katika kisa cha Walidi bin Uqbah na Bani Mustalaq, kisa kilichopelekea kuteremka Aya hii: “Enyi ambao mmeamini! Akiwajia fasiki na habari yoyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kutojua, na mkawa wenye kujuta kwa mliyoyatenda.”35 Pindi Walidi alipowasemea uwongo Bani Mustalaq kwa kusema yale ambayo hawakufanya, na ilikaribia kutokea fitina kubwa katika zama za Mtukufu Mtume  kama si Mungu kuingilia kati. Tutatosheka na uchunguzi huu mfupi, tunataraji kwamba tutakutana tena katika mhadhara ujao. MHADHARA WA SITA Jioni ya Siku ya Sita ya Mwezi wa Ramadhan, Mwaka 1436 A.H. Dkt. Ahmad Twayyib katika mhadhara wake alisema: “Hakika kanuni kuu ya madhehbu ya Suni inahukumu kwamba Maswahaba wote ni waadilifu, na umethibiti kwao uadilifu. Na sababu iliyopelekea kuwa na tofauti hii ya kipekee ni kule kusuhubiana kwao na Mtukufu Mtume , kwani uswahaba ndio unaopelekea uadilifu huu. Hakika watu wa Hadithi wanaona kwamba uswahaba unathibiti kwa kule tu kukutana na 35

Sura Hujurat: 6.

49


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Mtukufu Mtume , iwe ni kwa kipindi kifupi au kirefu. Na watu wa misingi ya sharia wameweka sharti la usuhuba mrefu.” Kisha akasema: “Tofauti iliyopo baina ya Suni na Shia katika nukta hii, ni kwamba Shia hawalioni hili. Ama Suni wao wanaitakidi kwamba Maswahaba wote ni waadilifu. Hivyo mpokezi asiyekuwa Swahaba huchunguzwa historia yake na maisha yake kupitia vitabu vya kutathmini dosari na uadilifu wa mpokezi, ili kwamba tufikie katika hitimisho kwamba mpokezi huyu ni mwadilifu ambaye riwaya zake zinakubalika, au si mwadilifu na hivyo riwaya zake hazikubaliki. Lakini kama mpokezi ni miongoni mwa Maswahaba, moja kwa moja uadilifu wake unakubalika na wala hayachunguzwi maisha yake wala historia yake, kwa sababu ule tu uswahaba unathibitisha uadilifu wake.” Nasema: Katika mhadhara wake wa siku hii ya sita ya mwezi wa Ramadhan, Mufti wa Azhar hajakuja na jambo jipya, bali amesisitiza aliyoyasema huko nyuma. Na ni kana kwamba anaitakidi kuwa uswahaba ni sawa na kemikali ambayo iliwabadili Maswahaba kutoka katika hali moja mbaya kwenda katika hali nyingine nzuri, kutoka katika uovu kwenda katika uadilifu, na mengineyo mengi yanayoweza kuwa ufafanuzi wa makusudio yake. Kama ambavyo pia anajenga picha kwamba huyu Swahaba kwa kule 50


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

tu kusuhubiana na Mtume amekuwa mtu mwadilifu aliyesafika mbali na kila dhambi. Lakini kwa bahati mbaya ni kwamba hata Swahaba mwenyewe hajioni kuwa ni mwenye cheo hicho. Maswahaba wanajua zaidi hali zao kuliko wengine wasiokuwa wao: Hakika yeyote atakayefuatilia historia ya Maswahaba baada ya kufariki kwa Mtume wa Allah  atakuta imejaa aina mbalimbali za mizozo na magomvi baina yao, imejaa mabadilishano na matupiano ya tuhuma na kashfa. Bali ni kwamba jambo lilikwenda zaidi ya hapo hadi katika kiwango cha kuuwana na kumwaga damu. Ni Maswahaba wangapi walioshiriki vita vya Badri na Uhudi lakini walivunjiwa heshima yao, wakateswa au damu yao kumwagwa na Swahaba mwingine. Na hili ni jambo lisilo na ikhtilafu baina ya watu wawili, isipokuwa ni kwamba jambo ambalo inapasa kulitambua ni kwamba, wote wawili wenye kupambana, kila mmoja alikuwa akiitakidi kwamba hasimu wake amechepuka kutoka katika njia sahihi, na kwamba anastahili adhabu au kuuwawa. Na itikadi hii hata kama inatokana na Ijtihadi lakini ni kwamba inafichua kwamba kila moja kati ya makundi mawili yaliyotofautiana halikuwa likiamini uadilifu wa kundi jingine. Ikiwa Swahaba anaitakidi kuwa hasimu wake amechepuka nje ya haki na amekwenda kinyume na 51


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

sharia ya Allah na Mtume wake, na kwa msingi huo akahalalisha kumchomolea upanga na kumuuwa, itakuwaje sisi tuwahukumu kuwa wote ni waadilifu na wasafi, na tuongeze juu yao nguo ya utakasifu kwao wote kwa kiwango kimoja?! Na tuwatakase na kila kila aina ya upotofu?! Je mtu mwenyewe si ndiye anayejua zaidi hali yake na nafasi yake? Je Maswahaba si ndio wanaojua zaidi misukumo ya nafsi zao na ya wale wa kizazi chao? Zaidi ya hapo ni kwamba, mazungumzo na mijadala iliyotokea baina yao inafichua itikadi waliyokuwa nayo Maswahaba wa kundi hili juu ya wale wa kundi lile. Kutuhumiana uwongo, unafiki, kashfa na matusi vilikuwa ni miongoni mwa mambo rahisi yaliyozoeleka baina yao. Huyu hapa Saad bin Ubadah chifu wa kabila la Khazraj, anamtuhumu Saad bin Muadh, ambaye alikuwa ni chifu wa kabila la Awsi, na anamnasibisha na uwongo. Hiyo ni kama alivyonukuu Bukhari katika Sahih yake kutoka kwa Aisha, kwamba alisema: “Akasimama Saad bin Ubadah aliyekuwa chifu wa Khazraji, akamwambia Saad bin Muadh: „Wallahi umesema uwongo….‟ Akasimama Usaydu bin Hudhayru naye alikuwa ni binamu wa Saad bin Muadh, akamwambia Saad bin Ubadah: „Umeongopa Wallahi tutamuuwa. Hakika wewe ni mnafiki unajadiliana kwa niaba ya wanafiki.‟ Basi yakazozana makundi mawili hadi wakakaribia kuuwana ilihali Mtume wa Allah kasimama juu ya 52


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

mimbari. Mtume aliendelea kuwatuliza mpaka waliponyamaza naye akanyamaza.”36 Je inawezekana kuyapa makundi yote mawili, kuanzia mtu wa kwanza wao hadi wa mwisho wao, sifa ya uadilifu na uaminifu, ilihali wao wako katika kiwango hiki cha ukosefu wa adabu na ukabila na kutokudhibiti nafsi mbele ya baraza la Mtume wa Allah?! Na mshangao unaongezeka pale unapojua kwamba sababu iliyopelekea jambo hili kutokea ni kauli ya Saad bin Muadh al-Answariy chifu wa Awsi, aliposema: “Ewe Mtume wa Allah! Mimi nitakupumzisha naye” – yaani mnafiki Abdullah bin Salul – ndipo akasimama Saad bin Ubadah chifu wa Khazraji na ni uzalendo wa kijinga ndio uliompelekea kumtetea Ibn Salul aliyekuwa mnafiki. Hivyo basi usafi waliozungushiwa Maswahaba ni jambo lililozuka ambalo lilitengenezwa na sababu mbalimbali, ikiwemo sababu ya kisiasa. Na miongoni mwa sababu ni ile waliyoiashiria wanazuoni wakubwa wa Kisuni katika tasnia ya kuchunguza dosari na uadilifu wa wapokezi, kama vile Sheikh Dhahbiy katika kitabu Maarifat Ruwat, ambapo amesema: “Na kama tutajifungulia mlango huu (wa kuchunguza dosari na uadilifu wa wapokezi) basi wataingia Maswahaba kadhaa na Tabiina na Maimamu. Kwani 36

Sahih Bukhari: 3/ 245, Kitabu cha tafsiri, Hadithi ya 4750.

53


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

baadhi ya Maswahaba waliwakufurisha Maswahaba wenzao kwa sababu ya tafsiri fulani.�37 Hili si jambo pekee katika mlango huu, kwani yapo mengine mfano wake yamepokewa katika Sahih na Musnad na ndani ya vitabu vya historia. Hivi hii si ajabu kubwa kwamba Swahaba mmoja anamsifu kwa unafiki Swahaba mwingine ambaye ni hasimu wake, na wote wawili ni miongoni mwa Answari na vigogo wao?! Lakini wale waliokuja baada yao wanawasifu kwa uadilifu, uchamungu, kujinyima na kujitenga na dunia. Je ulishawahi kusikia mfanyakazi aliye na huruma kwa mtoto kushinda mama yake?! Na wakati mchunguzi wa Kisuni anapokutana na vyanzo vingi vyenye kufichua makabati ya utendaji maasi na umwagaji damu zisizo na hatia, na kuvunja heshima, wakati anapokutana na ukweli huu huwa hana budi isipokuwa kurejea kwenye maelezo yanayopokewa kutoka kwa Umar bin Abdul-Aziz, na wakati mwingine kutoka kwa Imam Ahmad bin Hanbal, yanayolazimisha kunyamazia yale magomvi na ikhtilafu zilizotokea baina ya Maswahaba. Na mara nyingi husema kuhusu damu zilizomwagwa baina ya Maswahaba, ambapo waliuwana wao kwa wao, kwamba “Hizo ni damu ambazo Allah ameitakasa nazo mikono yetu, hivyo tusizichafue ndimi zetu 37

Maarifat Ruwat: 45.

54


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

kwazo.” Na kutokana na maneno haya inafahamika kwamba, damu zilizomwagwa katika vita vya Jamal, Suffin na Nahruwan, zilimwagwa kinyume cha haki, na hii ni chuki binafsi na hukmu iliyo batili, la sivyo ni dhamira gani huru inayohukumu kwamba kupigana na wavunja kiapo cha utiifu, waovu na waasi ni kupigana pasipo na haki?! Na sote tunajua kwamba Kiongozi wa Waumini  alikuwa na ubainifu kutoka kwa Mola Wake na ujuzi katika dini yake, haki inazunguka pamoja naye kwa kumfuata kokote aendapo, na yeye ndiye anayesema: “Wallahi hata kama nitapewa mbingu saba na vilivyo chini yake, ili kwamba nimuasi Allah kwa kumnyang‟anya mdudu chungu ganda la shairi, kamwe sintafanya.”38 Kwanini kunakuwepo na ukwepaji huu mbele ya ukweli uliyo wazi?! Hivi si ni kuhalalisha makosa, si ni kuukimbia ukweli na kuuchafua usafi, kule kujiepusha kuwakosoa Maswahaba?! MHADHARA WA SABA Jioni ya Siku ya Saba ya Mwezi wa Ramadhan, Mwaka 1436 A.H. Dkt. Ahmad Twayyib Muftiwa Azhar, mnamo siku ya saba ya mwezi wa Ramadhan aliendeleza mazungumzo yake kuhusu uadilifu wa Maswahaba, 38

Nahjul-Balaghah, Hotuba ya 224.

55


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

akasema: “Kauli hiyo ya uadilifu wa Maswahaba si uzushi kutoka kwa Suni bali ni kwamba imechukuliwa kutoka kwenye maandiko ya Qur‟ani Tukufu na Hadithi sahihi za Mtume. Ama Qur‟ani Tukufu, kauli hiyo inajulishwa na kauli ya Allah: “Na waliotangulia wa kwanza katika wahajiri na Ansari. Na wale waliowafuata kwa wema, Mwenyezi Mungu yuko radhi nao na wao wako radhi Naye; na amewaandalia Bustani ambazo hupita mito chini yake, watadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa.”39 Na akasisitiza kwamba Maswahaba wamepata ubora huu na uadilifu huu kwa kupewa na Allah na kwa sifa zake kwao. Kisha akatoa dalili ya sunna kupitia riwaya aliyoipokea Abu Said alKhudriy, alisema: “Mtume wa Allah  alisema: „Msiwatukane Maswahaba zangu, naapa kwa yule ambaye nafsi yangu imo mikononi mwake, kama mmoja wenu atatoa dhahabu mfano wa mlima wa Uhud kamwe hataweza kuwafikia wao (katika ubora) wala kufikia nusu yake.” Na nyinginezo miongoni mwa riwaya. Tafsiri ya Aya: Hakika Muftiwa Azhar aliishia kunakili tu Aya na wala hakutufafanulia ni kwa jinsi gani inajulisha uadilifu wa Maswahaba wote wa Mtukufu Mtume  kuanzia wa kwanza wao mpaka wa mwisho wao. Na huenda idadi yao ikafikia laki 39

Sura Tawba: 100. 56


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

moja, wakati ambapo Aya ni finyu kuliko madai anayodai Mufti, na hiyo ni kwa ufafanuzi ufuatao: Kauli ya Mtukuka: “Na waliotangulia..” inaashiria makundi matatu: 1. Waliotangulia wa kwanza katika wahajiri. 2. Na Ansari 3. Na wale waliowafuata kwa wema. Yaani waliowafuata kwa wema wale waliotangulia katika kuhama na kutoa nusra. Kisha ni kwamba Allah ametaja „utanguliaji na kuwa wa mwanzo‟ na wala hajataja viambata vya sifa hizo mbili, isipokuwa ni kwamba amewasifu wahusika kuwa wao ni Wahajiri na Ansari, jambo ambalo linaondoa ujumla kwenye Aya na kuonesha kwamba kigezo hasa ni kutangulia na kuwa wa mwanzo katika kuhama na kutoa nusra. Na ili tuweze kufafanua vizuri makusudio ni lazima kwanza tuchambue vifungu viwili vya kwanza kisha ndipo turejee kwenye kifungu cha tatu, tunasema: Hakika usifu wa Allah unawahusu tu waliotangulia katika matendo haya mawili; kuhama na kutoa nusra, na si kila aliyehama na kutoa nusra. Ushahidi juu ya hilo ni uwepo wa neno Min katika kauli ya Mtukuka ‘Minal-Muhajirina Waanswari‟, yaani katika Wahajiri na Ansari, hivyo yeyote atakayekuwa na sifa moja kati ya hizi mbili: kutangulia katika kuhama, au 57


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

kutangulia katika kutoa nusra, Allah anasema: „Allah yuko radhi nao na wao wako radhi Naye‟. Sasa maneno yanabakia kuhusu mifano halisi ya makundi haya mawili yenye sifa hizi, na bila shaka makusudio ni wale waliotangulia mwanzo kuhamia Uhabeshi au Madina Tukufu. Ama waliotangulia mwanzo kutoa nusra bila shaka ni wale waliompa Mtukufu Mtume kiapo cha utiifu cha kwanza na cha pili. Na idadi ya hao waliotoa kiapo cha utiifu cha kwanza miongoni mwa Ansari ilikuwa ni watu kumi na wawili. Na idadi yao katika kiapo cha pili ilikuwa ni takribani watu sabini. Hawa ndio waliotoa kiapo cha utiifukwa ajili ya kumnusuru na kumhami yeye  pindi atakapofika katika nchi yao, hawa ndio waliotangulia mwanzo kutoa nusra. Na wametajwa kwa upekee kwa sababu wao ndio waliovumilia aina nyingi za adhabu na mateso, na hivyo hakukuwa na namna nyingine ya kuepuka mateso hayo isipokuwa kuhamia Uhabeshi au Madina Tukufu. Au wale waliomnusuru Mtukufu Mtume na wakampa hifadhi yeye pamoja na wahajiri katika majumba yao wakati Uislamu ungali mchanga, hawa walikuwa katika kitisho kikubwa kutoka kwa maadui. Hivyo neno „waliotangulia‟ kutoka katika makundi yote mawili linawahusu wale waliohama kabla ya vita vya Badri, vita ambavyo vilikuwa ndio mwanzo wa kudhihiri Uislamu na nguvu zake. Au wale 58


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

waliomwamini Mtukufu Mtume miongoni mwa Answari na wakampa hifadhi yeye pamoja na kuwapa hifadhi wahajiri. Hivyo kifungu hiki cha tatu kinaelezea jinsi Allah alivyoliridhia kundi hilo, nalo ni lile la waliotangulia mwanzo katika kuhama na kutoa nusra kabla ya vita vya Badri. Hayo tuliyoyasema yanaungwa mkono na kauli ya Allah iliyopo katika Sura al-Anfal, aliposema: “Hakika wale walioamini na wakahajiri na wakapigania dini ya Allah kwa mali zao na nafsi zao; na wale waliokaribisha, hao ndio wanaosimamiana wao kwa wao...”40 Na kwa kuwa Sura al-Anfal iliteremka baada tu ya vita vya Badri hivyo basi inakuwa ni dalili ya kwamba wanaokusudiwa katika makundi hayo mawili ni wale wenye sifa ya kutangulia na kutoa nusra mpaka nusu ya mwaka wa pili wa hijriya. Mpaka hapa yametimia maneno kuhusu vifungu viwili vya mwanzo, ama kuhusu kifungu cha tatu, yaani kauli ya Mtukuka: “Na wale waliowafuata kwa wema.” Ni kwamba, ni wale walioyafuata makundi hayo mawili ya mwanzo katika kuhama na kutoa nusra. Hivyo hayo makundi mawili ya mwanzo ni viongozi wenye kufuatwa, na kundi la tatu ni wafuasi, nao ni wale waliohama baada ya Uislamu kupata nguvu na nguvu zake kuonekana, au waliomnusuru 40

Sura Anfal: 72. 59


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

katika hali hiyo. Na kwa sababu ya kuchelewa kwao kuhama na kutoa nusra wamekuwa wafuasi, hivyo kila aliyehama baada ya vita vya Badri au aliyeamini au kutoa nusra baada ya vita hivyo na kabla ya ukombozi wa Makka, huyo ndiye mwenye kukusudiwa katika kifungu cha tatu. Na kwa mujibu wa hayo tuliyoyasema ni kwamba, radhi ya Allah inayahusu makundi haya matatu tu, hivyo basi vipi Aya isihi kuwa dalili juu ya uadilifu wa Maswahaba wote kuanzia wa kwanza wao mpaka wa mwisho wao, mpaka wale waliosilimu katika mwaka wa tisa wa hijiriya, nao ndio mwaka wa wageni, mwaka ambao walisilimu wakazi wengi wa Bara Arabu, vipi Aya iwe ni dalili juu ya uadilifu wao?! Na hili ndilo tulilosema mwanzo kuwa, dalili ni finyu kuliko madai yanayodaiwa. Radhi imefungwa na sharti, haiko huru: Hakika Allah ameweka sharti la kupata radhi Yake kwa watu wa kundi la tatu, kwa kauli yake: “Waliowafuata kwa wema.� Yaani waliowafuata katika matendo mema, na sharti hili linafichua kwamba watu wa kundi la tatu wamegawanyika sehemu mbili: Wapo waliofuata kwa wema, na wapo waliofuata bila wema. Hivyo basi ikiwa mmoja kati ya watu wa kundi hili atashakiwa kuwa huenda hajatimiza sharti hili, Aya hii haiwezi kuwa dalili ya kuthibitisha uwepo wa sharti hilo kwa mhusika. Hiyo 60


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

ni sawa na iwapo msemaji atasema: „Mkirimu aalimu mwadilifu‟ kisha akawepo aalimu ambaye tuna shaka juu ya uadilifu wake, haiwezekani kutumia tena kauli „Mkirimu aalimu mwadilifu‟ kuwa ni dalili ya kuthibitisha uwepo wa sharti hili kwa muhusika. Mpaka hapa imedhihiri kwamba, Aya ni finyu zaidi kuliko madai, hiyo ni kwa sababu tatu: Ya kwanza: Kifungu cha kwanza kinawahusu wale tu waliopata sifa ya kuhama kabla ya vita vya Badri. Ya pili: Kifungu cha pili kinawahusu wale tu waliopata sifa ya kutoa nusra kabla ya vita vya Badri. Na wala haijumuishi wale walioamini, wakahama na kutoa nusra baada ya vita hivyo. Ya tatu: Hakika radhi katika fungu la tatu imefungwa kwa shari la kufuata kwa wema, hivyo kama iwapo tutakuwa na shaka juu ya uwepo wa sharti hili (wema), Aya hii haiwi tena dalili ya kuthibitisha uwepo wa sharti husika. Na kwa msingi huu, Aya imefichua kuwa radhi inalihusu kundi maalumu. Wapi na wapi hili mbele ya Maswahaba wote ambao idadi yao inafikia laki moja, na waliotajwa majina yao miongoni mwao ni karibuni elfu kumi na tano tu?! Na hapa mwenye kwamba watu wa

kuna nukta nyingine ameghafilika nayo kila kutumia Aya hii katika dalili, nayo ni Allah kueleza kuwa radhi Zake zinawahusu makundi haya matatu ni kwa sharti kwamba 61


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

waendelee kubakia kama walivyo katika imani, matendo mema na uadilifu, la sivyo kama dalili itajulisha na kuonesha kuwa kundi dogo au kubwa miongoi mwao walitoka nje ya kigezo basi Aya haitalihusu kundi hilo, na hiyo ni kwasababu mambo huzingatiwa kwa mwisho wake. Bukhari katika Sahih yake amepokea kutoka kwa Mtukufu Mtume  kwamba alisema: “Wakatimwingine mtu hutenda matendo ambayo watu wanamuona kuwa ni katika watu wa motoni ilihali kumbe yeye ni katika watu wa peponi. Hakika matendo huzingatiwa mwisho wake.”41 Hakika cheo cha Maswahaba wa mwanzo hadi wa mwisho si cha juu zaidi kushinda kile cha wale wanaozungumziwa na Qur‟ani Tukufu kwa kauli ya Allah: “Na wasomee habari za yule tuliyempa Ishara Zetu, kisha akajivua nazo, na shetani akamwandama akawa miongoni mwa waliopotea.”42 Na kwa mujibu huu radhi kukihusu kikundi fulani au mtu fulani katika kipindi maalumu si dalili ya radhi hizo kuendelea kumhusu hadi mwisho wa umri wao. Hivyo kama dalili itaonesha kukengeuka kwa watu 41

Sahih Bukhari: 7/ 177, Kitabu Riqaq, Mlango wa unaosema matendo huzingatiwa kwa mwisho wake. 42 Sura Aaraf: 175. 62


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

hawa kwa kwenda nje ya njia iliyonyooka, haitakuwa ni kinyume na Aya, kwa sababu kila moja lina wakati na muda makhususi. Kisha ni kwamba, Mufti Twayyib hakutubainishia dalili inayoonesha kuwa walibakia katika uadilifu na uaminifu bila kukengeuka, wakati walipotumbukia katika mambo yaliyo hatari zaidi kushinda hata uwongo wa maneno. Na hili ndilo alilokiri Barau bin Azib, ambapo Bukhari amepokea katika mlango wa vita vya Hudaybiyyah, kutoka kwa Alau bin Musayyab, kutoka kwa baba yake, kwamba alisema: “Nilikutana na Barau bin Azib, nikamwambia: „Hongera kwa kusuhubiana na Mtukufu Mtume na kumpa kiapo cha utiifu chini ya mti!‟ Akasema: „Ewe mwana wa ndugu yangu, hakika wewe hujui yale yaliyotutokea baada yake.”‟43 Bila shaka hakika mtu huyu alikuwa ni shuhuda wa hali halisi iliyotokea, na alikuwa na maarifa ya sababu zilizopelekea kuteremka Aya hizo takatifu. Na kwa ajili hiyo hakuzishikilia bali aliona kuwa zina sharti la kutokengeuka na kutotoka nje ya njia baada ya kifo cha Mtukufu Mtume , na ni lazima kuendelea na njia yake , na wala hakuzingatia uswahaba kama ulivyo bali hata kiapo cha utiifu kuwa mambo hayomawili yanatosha. 43

Sahih Bukhari: 5/ 66, Kitabu Maghazi, Mlango wa vita vya Hudaybiyyah.

63


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Mufti Twayyib atatufasiriaje kujilinda dhidi ya fitina kwa Ibn Abu Malikah, baada ya kunakili riwaya za hodhi? Bukhari amesema: “Ibn Abu Malikah alikuwa akisena: „Ewe Mungu Wangu! Hakika sisi tunajilinda kwako tusirejee kwenye visigino vyetu au kupewa majaribu ya kuwa mbali na dini yetu.”‟44 Ama kuhusu kutoa dalili kupitia katazo la Mtukufu Mtume , la kukataza kuwatukana Maswahaba zake, tunajibu hilo kwa kutazama mambo mawili: La kwanza: Hata kama hadithi itakuwa ni sahihi upande wa sanadi bado iko kinyume na makusudio yaliyolengwa kuthibitishwa, kwa sababu Mtukufu Mtume  anawahutubia Maswahaba na kuwaambia: Msiwatusi Maswahaba zangu. Na maana yake ni kwamba kulikuwepo na mwenye kutukana katika zama za Mtukufu Mtume  miongoni mwa Maswahaba wakiwatukana Maswahaba wenzao. Na inajulikana wazi kuwa kutukana ni uovu. Na imepokewa kutoka kwa Mtume wa Allah  kwamba alisema: Kumuuwa muumini ni ukafiri na kumtukana ni uovu.”45 Aidha inawezekana ikasemwa kuwa Mtume  alikuwa akiviambia vizazi vijavyo baada ya kizazi cha zama zake, lakini dai hilo ni kinyume na tamko la 44

Sahih Bukhari: 7/ 208, Kitabu Riqaq, Mlango wa Hodhi. Sunan Ibn Majah: 1/ 18, namba 46. Sunan Tirmidhiy: 4/ 131, namba 2771. 45

64


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

riwaya, ambapo yeye  anasema: “Msiwatusi.” Wanaoambiwa ni wale waliopo katika hadhira ya mzungumzaji, na laiti kama wanaoambiwa ni Waislamu wa vizazi vijavyo basi angebadili maneno yake na angesema: “Kuwatusi Maswahaba zangu ni haramu.” Kama alivyosema: “Kumtusi muumini ni uovu.” Na maana hii ndio ile ile aliyoifahamu Ibn Hajar, ambapo amesema: Makusudio ya kauli yake: “Maswahaba zangu” ni Maswahaba makhususi, kwani waliokuwa wakiambiwa ni Maswahaba.”46 Hapo hapo akafuatiliza maneno kuwajibu wale wenye kusema kuwa waliokuwa wakiambiwa si Maswahaba, kwa kuzingatia kwamba maneno hayo aliyasema kutokana na tukio la Khalid bin Walid kutukanana na Abdurahman bin Awfi.47 Kwa nyongeza ni kwamba, kutukana ni haramu, lakini hata hivyo kutaja sira ya maisha yao kwa kueleza mazuri yao na mabaya yao si kuwatusi. Na kwa ibara nyingine ni kwamba kumtusi mtu ni kumkashifu na kuvunja heshima yake, na hakuna shaka kwamba kumtusi muumini ni uovu. Ama kukosoa maisha ya Swahaba kwa kutaja mazuri yao na mabaya yao haihesabiki kuwa ni kuwatusi, bali ni 46 47

Fat’hul-Bariy: 7/ 34. Fat’hul-Bariy: 7/ 34.

65


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

kukosoa sira yao, kama ina kheri basi itaendelea kuwa kheri, na kama ina shari basi itaendelea kuwa shari. Na ushahidi juu ya hilo ni mazungumzo yaliyofanyika baina ya Muawiya bin Abu Sufiyan na Saad bin Abu Waqqas, ameyapokea Muslim katika Sahih yake, kutoka kwa Aamir bin Saad Ibn Abu Waqqas, kutoka kwa baba yake, amesema: “Muawiya bin Abu Sufiyan alimwamuru Saad, akamwambia: „Ni lipi linalokuzuia kumtukana Abu Turab (Ali)?‟ Akasema: „Ninapokumbuka mambo matatu aliyoyasema Mtume wa Allah kumhusu, kamwe siwezi kumtukana, kwani mimi kuwa na moja tu kati ya mambo hayo ni jambo nilipendalo zaidi kushinda hata ngamia mwekundu.”‟ Kisha aliashiria fadhila tatu za Imam Ali , nazo ni: 1. Kauli ya Mtume  kumwambia Ali : “Huridhii kwamba cheo chako kwangu mimi ni sawa na cheo cha Harun kwa Musa.” 2. Alimpa bendera siku ya Khaybar na alikuwa amesema: “Hakika kesho nitamkabidhi bendera mtu ambaye anampenda Allah na Mtume wake, na Allah na Mtume wake wanampenda.” 3. Ilipoteremka Aya: “Na watakaokuhoji baada kukufikia elimu hii, waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake zetu na wanawake wenu, na nafsi zetu na nafsi zenu, kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo.” Mtume wa Allah  66


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

alimwita Ali, Fatima, Hasan na Husein, akasema: “Ewe Mungu wangu hawa ndio watu wa nyumba yangu.”48 Hitimisho la maneno ni kwamba, jamaa wamechanganya baina ya kutukana na kukosoa, Shia hawatukani, wao wanaona kutukana ni uovu kwa mujibu wa kauli ya Mtukufu Mtume , nalo ni tendo la mtu dhaifu. Ama uchambuzi na ukosoaji, yaani kuchambua mwenendo wa Swahaba katika kipindi cha maisha yake kwa kutazama maeneo yenye nguvu na udhaifu, jambo hilo ni mwenendo wa Qur‟ani Tukufu ambayo imetaja mazuri ya Maswahaba na mabaya yao, amali zao njema na zisizo nzuri. Na wakati mwingine Qur‟ani Tukufu imetaja matendo yao mema kama ilivyotaja matendo yao mabaya, na hili liko wazi kwa yeyote atakayesoma Aya zifuatazo: 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7.

Sura al-Baqarah: 187. Sura Imran: 144. Sura Imran: 153. Sura Imran: 161. Sura Hijri: 6. Sura Ahzab: 22. Sura Jumu‟ah: 6.

Kisha ni kwamba, Mufti amewasifu Maswahaba kwa namna inayodhihirisha kwamba hakuwezi kukatokea 48

Sahih Muslim: 7/ 120.

67


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

watu mfano wao mpaka siku ya Kiyama. Wakati ambapo maneno yake haya ni kinyume na ilivyokuja ndani ya Qur‟ani Tukufu katika maeneo kadhaa: Eneo la kwanza: Qur‟ani Tukufu imeeleza uwezekano wa Maswahaba kuritadi baada ya kifo cha Mtume wa Allah , na hiyo ni pale baadhi ya Waislamu walipokimbia katika vita vya Uhud, na wengine wakauwawa. Ibn Kathir anasema: “Shetani alinadi kwamba Muhammad  ameuwawa, jambo hilo likakaa katika nyoyo za watu wengi na wakaitakidi kwamba Mtume wa Allah ameuwawa na wakaruhusu hilo (kwamba upo uwezekano wa yeye kuuwawa). Hivyo ukapatikana udhaifu na unyonge na hali ya kuchelewa kupigana. Ibn Najih amepokea kutoka kwa baba yake kwamba, mtu mmoja miongoni mwa Muhajirina alipita kwa mtu miongoni mwa Answari, ambaye alikuwa akigaagaa ndani ya damu yake, akamwambia: “Ewe Fulani hivi unajua kwamba Muhammad ameshauwawa?” Answari Yule akasema: “Ikiwa Muhammad ameuwawa bila shaka yeye ameshafikisha ujumbe. Hivyo basi ipiganieni dini yenu.” Ndipo Allah akateremsha: “Hakuwa Muhammad ila ni Mtume; wamekwisha pita Mitume kabla yake. Je, akifa au akiuliwa mtarudi nyuma? Na atakayerudi nyuma hatamdhuru kitu Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu atawalipa wenye kushukuru.”49 49

Sura Imran: 144. Tafsir Ibn Kathir: 1 / 409. 68


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Ibn Qayyim al-Jawziyyah amesema: “Vita vya Uhudi vilikuwa bayana mbele ya Muhammad , akawaeleza na kuwaonya juu ya kurudi kwao nyuma kama Mtume wa Allah atakufa au kuuwawa.”50 Eneo la pili: Qur‟ani Tukufu imeeleza kwamba, kama Maswahaba waliokuwepo Uhud au wengine, wataritadi: “Basi Mwenyezi Mungu atawaleta watu anaowapenda nao wanampenda, wanyenyekevu kwa waumini, wenye nguvu juu ya makafiri, wenye kufanya jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, wala hawaogopi lawama ya anayelaumu..”51 Na hii inajulisha kwamba, mustakbali si tasa kiasi cha kutoweza kuleta watu walio bora kushinda baadhi ya Maswahaba, na Allah ni neema isiyo na mipaka, na neema Yake haina mipaka. Eneo la tatu: Ni kauli ya Allah katika Sura Tawba: “Enyi mlioamini! Mna nini mnapoambiwa nendeni katika njia ya Mwenyezi Mungu mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na Akhera ni kidogo tu. Kama hamwendi atawaadhibu kwa adhabu iumizayo na atawaleta watu wengine badala yenu, na hamtam50 51

Zadul-Maad‟ 253. Sura Maidah: 54.

69


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

dhuru chochote; Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu.”52 Ibn Ashur katika tafsiri yake at-Tahrir Wat-Tan’wir amesema: “….Na tukifuata aliyowasilisha Ibn Atwiyyah kwa wahojaji, kwamba kauli ya Allah: „Enyi mlioamnini! Mna nini mnapoambiwa nendeni…‟ kuwa ndio Aya ya mwanzo iliyoteremka katika Sura Baraa, basi Aya hii itakuwa fokeo dhidi ya kujipa uvivu na kujitia uzito kulikodhihiri kwa baadhi ya watu. Hivyo neno Idhan (lililopo katika matini ya Kiarabu) litakuwa ni ala yenye kumaanisha mustakbali, kama ilivyo aghlabu. Na kauli yake: „Kama hamwendi atawaadhibu kwa adhabu iumizayo‟ itakuwa ni onyo la kuacha kutoka kwenda kwenye vita vya Tabuk.”53 Na Ibn Kathir amesema katika tafsiri yake: “Na atawaleta watu wengine badala yenu. Maana yake atawaleta kuja kumnusuru Nabii wake na kuisimamisha dini yake, kama alivyosema Allah Mtukuka: „Na mkigeuka atawaleta watu wengine badala yenu, nao hawatakuwa kama nyinyi.‟54 „Na hamtamdhuru chochote.‟ yaani hamtamdhuru Allah chochote kwa kukimbia kwenu jihadi, kujitia kwenu 52

Sura Tawba: 38 – 39. at-Tahrir Wat-Tan’wir: 10 / 94 – 95. 54 Sura Muhammad: 38. 53

70


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

uvivu na kwa kujitia kwenu uzito wa kwenda katika jihadi.”55 Tuhitimishe maneno hapa kwa neno alilolinukuu Dkt. Ahmad Amin katika kitabu Dhuhal-Islam, kutoka kwenye Risala ya mmoja kati ya Mazaydiyyah, amesema: “Hakika sisi tumeona Maswahaba wenyewe wakikosoana wao kwa wao, bali wakilaaniana wao kwa wao. Kama Maswahaba wao wenyewe wangekuwa ndani ya nafsi zao wana cheo ambacho haisihi kukosoa wala kulaani, basi wao wenyewe wangejua hilo ndani ya nafsi zao, kwa sababu wao ndio wajuao zaidi mahala pao kuliko watu wa kawaida wa zama zetu. Huyu hapa Twalha, Zubair, Aisha na wale waliokuwa pamoja nao na pembezoni mwao, hawakuona wajibu wa kujizuia dhidi ya Ali. Na huyu hapa Muawiya na Amru bin Aswi, hawakusita kumpiga wala kuwapiga wafuasi wake kwa upanga. Na ni kama ilivyopokewa kutoka kwa Umar kwamba aliituhumu riwaya ya Abu Huraira na alimshutumu Khalid bin Walid na akahukumu uovu wake. Na aliwaona ni mahaini Amru bin Aswi na Muawiya na akawanasibisha na wizi wa mali ya ngawira. Na ni mara chache kukuta katika Swahaba yule ambaye ulimi wake au mkono wake umesalimika. Na mengineyo mengi mfano wa hayo yaliyopokewa katika historia. 55

Tafsirul-Qur’ani al-Adhim: 4/ 135 – 136.

71


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Na Tabiina walikuwa wakiwapitisha Maswahaba katika njia hii, na wakisema kauli hii kuhusu wenye maasi miongoni mwao. Isipokuwa ni kwamba baada ya hapo ndipo Suni waliwafanya kuwa ni mabwana wakubwa, wakati ambapo Maswahaba ni kundi miongoni mwa watu, wana haki kama waliyonayo watu wengine na wana wajibu kama walionao watu wengine. Yule aliyetenda makosa miongoni mwao tutamlaumu, na yule aliyetenda mazuri tutamsifu. Na wao hawana ubora mkubwa zaidi kuliko walionao watu wengine isipokuwa kule tu kumshuhudia Mtukufu Mtume na kuishi katika zama zake, na wala si zaidi ya hilo. Bali huenda madhambi yao ni mabaya zaidi kushinda madhambi ya watu wengine, kwa sababu wao walishuhudia alama na miujiza, hivyo maasi yetu ni hafifu zaidi kwa sababu tuna udhuru zaidi.”56 MHADHARA WA NANE Siku ya Nane ya Mwezi wa Ramadhan, Mwaka 1436 A.H. Dkt. Ahmad Twayyib Muftiwa Azhar alisema: “Hakika umaasumu ni kutokuwa na uwezo wa kutumbukia katika dhambi. Na maasumu niyule ambaye atakapo kutumbukia katika dhambi Allah 56

Dhuhal-Islam: 3/ 75 – 76.

72


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

humzuia asiweze kutumbukia humo. Ama uadilifu, ni kwamba nguvu iliyojiimarisha ndani ya nafsi yake ndiyo inayomzuia mtu kudumbukia katika dhambi. Lakini katika umaasumu ni kwamba maasumu hatumbukii katika dhambi si kwa sababu ana tu nguvu hii, bali ni kwamba Allah Mtukuka amefanya kazi ya kumhifadhi asitumbukie katika madhambi ya dhahiri na ya batini.” Kisha alitoa mfano kupitia mfano wa Sayiduna Yusuf  kutoka kwenye kauli ya Allah: “Na hakika (mke) alimtamani naye angelimtamani.” Akasema: “Kutamani kwa Yusuf kulikuwa ni kutamani kwa mawazo na kujisemeza ndani ya nafsi, hivyo: “Kama asingeona dalili ya Mola Wake.” Kisha Mheshimiwa Dkt. Akaendeleza mazungumzo kwa kutaja tofauti iliyopo baina ya kutokea dhambi kutoka kwa Swahaba baadhi ya nyakati, na kutotokea kwa dhambi kutoka kwa Mtume maasumu, akasema: “Hakika vizuizi vinavyomzuia Swahaba ni vidhibiti vya ndani vya kibinadamu ambavyo inawezekana vikashindwa. Lakini vidhibiti vilivyopo kwa maasumu ni vidhibiti vya Mungu ambavyo humzuia maasumu wakati wote kutumbukia katika dhambi.” Na akasisitiza Mheshimiwa Dkt. kwamba ni kutokana na hali hii ndio maana imesihi Swahaba kutumbukia katika dhambi kinyume na Nabii. 73


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Kisha alihitimisha mazungumzo yake kwa kusema kwamba, hakika Shia wanaurefusha umaasumu mpaka kwa Maimamu kumi na wawili, kuanzia kwa Ali kupitia kwa Maimamu wawili Hasan na Husein, mpaka kufika kwa Imam wa kumi na mbili, ambaye wao wanasema kuwa yuko katika ghaibu. Na hili hawalisemi Suni. Sisi tuna nukta kadhaa juu ya maneno ya Mufti Mungu amhifadhi: Ya kwanza: Ni kuhusu alivyoutambulisha umaasumu: Dkt. Ameutambulisha umaasumu kuwa ni kutotumbukia katika dhambi, na akatoa sababu inayopelekea hali hiyo, kwamba ni uwepo wa vidhibiti kutoka kwa Mungu ambavyo humzuia maasumu asitumbukie katika dhambi wakati wote. Tunamwambia mheshimiwa Mufti: Hakika umaasumu ni fahari wanayopambika nayo Manabii na maasumu, hivyo kama kuwa nao huo umaasumu kungewafanya wasiwe na uwezo wa kutenda maasi na kukhalifu amri, basi umaasumu huo usingehesabika kuwa ni fahari kwao, kwa sababu ya kutokuwa na uwezo wa kutenda maasi pindi watakapotaka kuyatenda. Hivyo kama asiye na utupu atajifaharisha kwa kutozini, jambo hilo haliwezi kuhesabika kuwa ni fahari kwake, bali fahari ni kwa Yusuf ď ‚ ambaye alikuwa na nguvu zote lakini pamoja na hivyo akajizuia yeye mwenyewe. Na ni kwa ajili hiyo mke 74


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

wa mheshimiwa alikiri na akasema: “Hakika nilimtaka kinyume cha nafsi yake, lakini akajizuia.” Na kwa ibara nyingine ni kwamba, ikiwa kujizuia kutumbukia katika dhambi kunatimia kwa kizuizi cha nje anachowekewa mtu, nacho kinamzuia kutenda dhambi, basi kujizuia huko hakuna ubora wowote. Kwani jambo hilo ni sawa na kuwepo watu wawili, mmoja anatekeleza kitendo cha kuiba na mwingine hatekelezi kwa sababu wakati wote kaandamana na askari anayemfuatilia. Katika hali kama hii ni kwamba hata wa pili ni mwizi kama wa kwanza, lakini tofauti iliyopo kati yao ni kwamba wa kwanza anatekeleza kitendo cha kuiba kwa sababu hakuna askari anayemzuia, na wapili ni mwizi lakini askari ndiye anayemzuia kutekeleza kitendo cha kuiba.57 Na kwa mujibu huo ni kwamba, kutofautisha baina ya maasumu na mwadilifu kwa sababu eti wa kwanza hana uwezo wa kutenda maasi na wa pili ana uwezo wa kutenda, si sahihi.58 Uhalisia wa umaasumu: Sahihi ni kwamba umaasumu ni matokeo ya elimu yakinifu ya kujua 57 58

Al-Imamah cha Shahid Mutahariy: 203. Bali kwa nyongeza ni kuwa, kufanya hivyo ni kumpa ubora mwadilifu kuliko maasumu, kwani kwa upande mwingine mwaminifu si yule aliyekosa amana, bali mwaminifu ni aliyepewa amana kisha akaifikisha kama ilivyo. Mbora si aliyekosa changamoto, mbora ni aliyekutana na chamoto akazishinda – Mtarjumi.

75


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

matokeo ya maasi, ambapo elimu yakinifu ya kujua matokeo ya matendo ya hatari hutengeneza katika nafsi ya mtu kizuizi kizito kinachomzuia kutenda matendo hayo. Na katika maisha kuna mifano mingi kuhusu hilo, yeyote miongoni mwetu akijua kwa yakini kwamba nyaya hizi za umeme zina umeme ambao kikawaida humuuwa moja kwa moja yule mwenye kuugusa, katika hali hiyo yeye mwenyewe bila kuhisi atajizuia kugusa nyaya husika na hata kuzisogelea. Ni sawa na tabibu mwenye kujua vyema matokeo ya maradhi na madhara ya vijidudu, yeye anapokutana na maji ambayo humo kanawa mwenye ukoma na mbaranga, au chombo ambacho humo kanywea mwenye kikohozi, hatanawa wala kunywa maji hayo vyovyote itakavyokuwa anayahitajia. Hiyo ni kutokana na anavyojua matokeo ya kunywa au kunawa maji hayo. Tumia mifano hiyo kupima matokeo mengine ya hatari, ikiwemo heshima yako kuondoka mbele za watu, kiasi kwamba kwa kudondoka heshima yako maisha yako yanakosa raha. Ikiwa kuwa na elimu yakinifu juu ya matokeo ya kidunia ya baadhi ya vitendo kunaunda ndani ya nafsi ya mhusika, hicho kizuizi chenye kuzuia kutenda baadhi ya mambo, vipi atakapokuwa na elimu yakinifu juu ya matokeo ya Akhera ya maasi na matendo mabaya. Pale atakapokuwa na elimu isiyo na 76


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

shaka wala raiba, elimu inayoondoa vizuizi vyote kiasi kwamba mwenye nayo anaona kwa macho mawili matokeo hayo ya maasi na athari zake katika ulimwengu ujao. Ile elimu ambayo Allah ameizungumzia kwa kusema: “Si hivyo! Lau mngelijua kwa ujuzi wa yakini. Hakika mtauona Moto!”59 elimu mfano wa hii hutengeneza kwa mwenye nayo ubora na kizuizi ambacho humwezesha kutokumkhalifu Mola Wake hata kidogo. Wala katika maisha yake huwa havuki mipaka aliyochorewa hata kidogo. Na si tu husafika kwa kuwa mbali na maasi bali pia huwa hayafikirii wala kutafuta njia ya kuyatenda. Kutokana na tuliyoyataja inaonesha kwamba elimu ni hatua imara na nzito ambayo humwezesha mtu kuyashinda matamanio yake, na humzuia kutenda maasi na madhambi. Na tunapata maelezo haya katika maneno ya Jamaludin Fadhil Miqdad bin Abdullah Suyuriy al-Hiliy, katika kitabu chake cha thamani alLawamiu al-Ilahiyyah, anasema: “Umaasumu ni nguvu ya kinafsi inayomzuia aliyenayo kutenda maasi licha ya kwamba ana uwezo wa kutenda. Na nguvu hii inatokana na kuwa na elimu juu ya maangamizi ya maasi na ubora wa utiifu. Kwa sababu pindi inapopatikana staha ndani ya dhati ya nafsi na ikajiunga humo elimu kamilifu ya kujua mahangaiko yaliyomo katika maasi na saada iliyomo katika utiifu, 59

Sura Takathur: 5 – 6.

77


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

elimu hiyo hupelekea staha hiyo kujiimarisha katika nafsi na hatimaye huwa nguvu.”60 Haidaiwi kuwa kila elimu ya kujua matokeo ya matendo inamzuia mtu kutenda maasi, na kwamba elimu peke yake inasababisha umaasumu, hakika dai hilo ni batili bila shaka. Kwa sababu tunawaona wengi wenye elimu ya kujua madhara ya mihadarati na vilevi na matendo machafu, hawajizuii kutenda hayo. Hivyo ingekuwa kule kujua tu matokeo ya maasi kwa namna ya hisia za kawaida kama tunavyojua mambo kunatosha, basi hali hiyo ya kujizuia ingewafikia. Lakini aina ya elimu ambayo itamfanya mtu awe maasumu si miongoni mwa aina hizi za elimu za maarifa ya kawaida, bali ni elimu makhususi iliyo juu zaidi, ambayo huenda ikaitwa „elimu ya kushuhudia matokeo na kufichuka kikamilifu kiasi kwamba haibakii shaka kwa shuhuda‟. Ndiyo, yote tuliyoyaeleza yanarejea kwenye moja ya maana za umaasumu, nao ni umaasumu wa kujizuia kutenda maasi na kukiuka amri ya bwana. Ama umaasumu wa upande wa kupokea wahyi, kwanza. Kisha kuuhifadhi ulivyo, pili. Na kuufikisha kwa watu, tatu. Na umaasumu katika mambo binafsi na ya kijamii, umaasumu huo una sababu nyingine, tutauzungumzia katika tafiti zijazo inshaallah kwa idhini ya Allah. 60

al-Lawamiu al-Ilahiyyah: 170.

78


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Ya pili: Dkt, amesema: “Ni kutokana na hali hii ndio maana imesihi Swahaba kutumbukia katika dhambi kinyume na Nabii.” Nasema: Hakika Mufti amekuwa mtu pekee aliyekuja na rai hii, ambapo ametamka bayana dhahiri shahiri kwamba baadhi ya Maswahaba walitenda madhambi makubwa, isipokuwa ni kwamba maulamaa wengine wa Kisuni wasiokuwa yeye wanaamiliana na Maswahaba kama wanavyoamiliana na maasumu, ambapo wanajizuia kunasibisha dhambi kwao. Na kila inapoonekana kuwa Swahaba alitenda dhambi wao husema: „Alifanya ijtihadi, na mwenye kufanya ijtihadi hulipwa, kama amepatia hulipwa mara mbili, na kama amekosea hulipwa mara moja. Na kwa hivyo mwenye kutenda dhambi amekuwa na malipo.” Hili si lolote isipokuwa ni ufurutuada katika haki ya Maswahaba. MHADHARA WA TISA Siku ya Tisa ya Mwezi wa Ramadhan, Mwaka 1436 A.H. Dkt. Ahmad Twayyib alisema: “Hakika uadilifu kwa Suni ni uwezo wa kibinadamu unaomzuia mwadilifu kutumbukia katika maasi. Lakani hata hivyo vishawishi vinaweza kumzidia na hatimaye akatumbukia 79


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

katika dhambi. Ama umaasumu, unamaanisha kutowezekana kabisa kutumbukia katika dhambi kwa sababu ya ulinzi anaowapa Allah Mitume na Manabii ndani yao na nje yao ili wasiweze kutenda maasi.” Kisha mheshimiwa Mufti, Mungu amhifadhi, aliendelea na maneno yake kuhusu umaasumu wa Manabii kwa namna nzuri isiyo na tofauti. Kisha akasema: “Hakika maana ya uadilifu kwa Suni ni ule uadilifu ambao unaruhusu kutumbukia katika kosa, na maana hii inalingana na Maswahaba Allah awe radhi nao. Lakini Shia, wao walipopanua maana ya umaasumu walilazimika kufungua mlango wa wahyi kwa Maiamamu baada ya Manabii. Na sisi tunasema: Hakika umaasumu ni wa Manabii tu, na wahyi umeshakatika kwa kifo cha Mtukufu Mtume .” Nasema: Kuna nukta kadhaa za kuangazia katika maneno ya mheshimiwa Mufti Mungu amhifadhi: Ya kwanza: Hakika umeshajua kwamba umaasumu haulazimu kutowezekana kabisa kudumbukia katika dhambi, kwani ingekuwa ni hivyo basi usingekuwa ni moja ya fahari za Manabii, na bila shaka ufafanuzi wake umeshatangulia. Ya pili: Mara Mufti anasema: “Hakika uadilifu unaruhusu kuzidiwa na vishawishi na hatimaye 80


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

kudumbukia katika dhambi” lakini mara nyingine anasema: “Hakika uadilifu ni ule unaoruhusu kudumbukia katika kosa.” Na bila shaka ni wazi kabisa kwamba maana ya pili haina uhusiano wowote na uadilifu na wala hakuna mgongano baina ya kosa na uadilifu, ambapo ni kinyume na dhambi. Ya tatu: Hakika lile jambo alilolinasibisha na Shia, la kwamba wao walipopanua maana ya umaasumu walijikuta wanalazimika kufungua mlango wa wahyi kwa Maimamu baada ya Manabii, hakika ni kwamba, umma wa Kiislamu Suni na Shia wamesema kuwa mlango wa wahyi umefungwa baada ya kifo cha Mtukufu Mtume . Huyu hapa Imamu wa umma anasema wakati wa kumwandaa Mtukufu Mtume wa Allah  kwa maziko: “Baba yangu na mama yangu wawe fidia kwako ewe Mtume wa Allah! Kwa kifo chako yamekatika yale ambayo hayakuwahi kukatika kwa kifo cha yeyote mwingine asiyekuwa wewe, ikiwemo unabii na habari za mbinguni.”61 Hivyo basi itakuwaje Shia waseme kwamba Maimamu wanafunuliwa wahyi?! Isipokuwa ni kwamba Mufti katika hukumuyake hii, hajatofautisha baina ya kufunuliwa wahyi na kusemeshwa na Malaika. Hakika Maimamu wa Ahlulbayti  husemeshwana Malaika na wala huwa hawafunuliwi wahyi. Na Bukhari ametenga mlango mzima katika kitabu chake unaohusu 61

Nahjul-Balaghah, Hotuba ya 235.

81


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

kusemeshwa na Malaika, na inshaallah baada ya kutoa maana ya kusemeshwa na Malaika yatakufikia yale aliyoyaweka katika mlango huo. Anayesemeshwa (kwa maana ya kiistilahi) niyule anayesemeshwa na Malaika bila unabii wala kuona sura ya Malaika husika. Au anawekewa katika akili yake sehemu ya elimu kwa njia ya ilhamu kutoka chanzo cha juu, au anawekewa katika moyo wake ukweli ambao unafichikana kwa mwingine, au nyinginezo miongoni mwa maana ambazo zinaweza kukusudiwa. Kuwepo watu wenye sifa hii kutoka kwenye umma huu ni jambo lililoafikiwa na makundi yote ya Kiislamu, isipokuwa tofauti iliyopo ni kuhusu huyo msemeshwaji aliyesemeshwa na Malaika, ni nani hasa. Shia wao wanaona kuwa Ali Kiongozi wa Waumini na watoto wake Maimamu wa Ahlulbayti  ni miongoni mwa wasemeshwaji waliosemeshwa na Malaika. Na Suni wanaona kuwa miongoni mwa wasemeshwaji waliosemeshwa na Malaika ni Umar bin Khattab: 1. Bukhari ameandika katika Sahih yake, katika mlango wa fadhila za Umar bin Khattab, kutoka kwa Abu Huraira, amesema: Mtume wa Allah  alisema: “Katika watu waliopita kabla yenu miongoni mwa wana wa Israel walikuwemo waliosemeshwa na Malaika bila ya kuwa wao ni 82


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Manabii, na kama wapo watu wa namna hiyo katika umma wangu basi mmoja wao ni Umar.”62 2. Bukhari ameandika katika Sahih yake, kutoka kwa Abu Huraira, amesema: Mtume wa Allah  alisema: “Katika watu waliokuwepo kabla yenu katika umma zilizopita, walikuwemo waliosemeshwa na Malaika, na kama wapo watu wa namna hiyo katika umma wangu basi mmoja wao ni Umar.”63 3. Muslim ameandika katika Sahih yake, katika mlango wa fadhila za Umar, kutoka kwa Aisha, kutoka kwa Mtukufu Mtume  kwamba alisema: “Katika umma zilizopita kabla yenu walikuwemo waliosemeshwa na Malaika, na kama wapo watu wa namna hiyo katika umma wangu basi mmoja wao ni Umar.”64 Pia Ibn Hajar amesema: “Muhadathunani wingi wa Muhaddathu (aliyesemeshwa na Malaika), na wametofautiana kuhusu tafsiri yake, imesemekana ni Yule aliyepewa ilhamu, hiyo ndio kauli iliyosemwa na wengi. Wamesema: Muhaddathu (aliyesemeshwa na 62

Sahih Bukhari: 4/ 200, Mlango wa fadhila za Umar bin Khattab. 63 Sahih Bukhari: 4/ 200, Mlango wa fadhila za Umar bin Khattab. 64 Sahih Muslim, Sharhu ya Nawawi: 15, Hadithi ya 6154.

83


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Malaika) ni mtu mwenye dhana ya kweli, naye ni yule aliyewekewa kitu katika akili yake kutoka ufalme wa juu, hivyo anakuwa kama aliyeambiwa kitu hicho. Na hili ndilo aliloamini Abu Ahmad al-Askariy. Na inasemekana kwamba: Ni yule ambaye usahihi hupitia katika ulimi wake bila kukusudia. Na inasemekana: Ni yule anayesemeshwa na Malaika bila unabii, na hili limepokewa kutoka katika Hadithi isiyo na sanadi ya Abu Said al-Khudriy, tamko lake liko hivi: Pakasemwa: Ewe Mtume wa Allah anasemeshwaje? Akasema: “Malaika anaongea kupitia ulimi wake.” Imesimuliwa na Qabisiy na wengineo. Na hilo linaungwa mkono na yaliyothibiti katika riwaya isiyo na sanadi. Na inaweza ikarejeshwa kwenye maana ya mwanzo, yaani Malaika anamsemesha ndani ya nafsi yake licha ya kwamba hamuoni msemeshaji mwenyewe, hivyo inarejea kwenye ilhamu.”65 Na kuhusu mwenye kusemeshwa na Malaika na riwaya zilizopokewa kumhusu, wasomi wana maneno mengi ambayo yanafichua kwa uwazi uwepo wa tofauti baina ya mwenye kusemeshwa na Mailaika na Nabii, na kwamba si kila anayenong‟onezwa sikioni au kuwekewa kitu moyoni ni Nabii. Na tofauti iliyopo baina ya Suni na Shia kuhusu dhana hiyo ni upande wa mifano halisi ya wale waliosemeshwa na Malaika. 65

Fat’hul-Bariy: 7/ 50.

84


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Shia kwa upande wao, kama tulivyosema, wanaona kuwa Ali Kiongozi wa Waumini na watoto wake Maimamu wa Ahlulbayti ni miongoni mwa waliosemeshwa na Malaika. Wakati ambapo Suni kwa upande wao wanaona kwamba Umar bin Khattab ni miongoni mwa waliosemeshwa na Malaika. Kisha ni kwamba Mufti aliashiria katika mhadhara wake kwamba, kuna aina nyingine ya umaasumu kwa Masuni ambao ni lazima kuufafanua katika mnasaba huu. Nao ni umaasumu wa mjumuiko mzima wa umma na wala si wa mtu mmoja mmoja katika umma. Na kuna tofauti baina ya mjumuiko na mtu mmoja mmoja, hivyo kama maulamaa wa Waislamu watajumuika juu ya jambo na Waislamu wakalipokea kwa mapokezi mazuri, basi hakika jambo hili linakuwa ni haki. Kwani umma una umaasumu katika hukmu hizi, nazo ni wajibu kuzifuata, bali kongamano hilo ni hoja ya kisharia baada ya maandiko ya Qur‟ani Tukufu na Sunna ya Mtukufu Mtume. Kisha akasema: “Hakika Shia wanasema kwamba, kama katika kongamano la umma miongoni mwao atakuwemo Imam Maasumu kwa madai yao, basi kongamano hilo ni maasumu kwa umaasumu wa Imamu. Lakini kama miongoni mwao hayupo Imam maasumu basi kongamano la umma wakati huo si maasumu.” 85


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Anajibiwa kwa kusema: Miongoni mwa aina za tauhidi ni tauhidi katika sharia, kwa maana hakuna mweka sharia isipokuwa Allah, na wala yeyote yule mwingine hana haki ya kuweka sharia na kanuni: “Hapana hukumu isipokuwa ya Mwenyezi Mungu tu. Ameamrisha msimwabudu yoyote isipokuwa Yeye tu. Hiyo ndiyo dini iliyonyooka, lakini watu wengi hawajui.�66 Na kwa mujibu huu ni kwamba chanzo cha sharia ni Kitabu na Sunna tu. Ama kuhusu kutumia hoja ya akili, ni kwa sababu utambuzi wake hufichua hukmu ya kisharia, wala yenyewe haina haki ya kuweka sharia, bali yenyewe inafanya kazi ya kufichua tu yale ambayo ni hukmu kwa mweka sharia, kwa namna waliyoibainisha watu wa misingi ya sharia. Ama kuhusu kongamano la umma, hakuna dalili yoyote sahihi inayojulisha kwamba kukongamana kwao juu ya hukmu yenye dalili ya dhana, kunainyanyua hukmu hadi kiwango cha kuwa hukmu halisi isiyo na shaka, na inakuwa kama hukmu nyinginezo zilizothibiti kwa Kitabu na Sunna. Kwani hiyo itamaanisha kwamba Ijmai nayo ni miongoni mwa vyanzo vya sharia, wakati tayari umeshatambua kuwa kwa mujibu wa dhana ya tauhidi katika sharia, suala la kuweka sharia limefungika katika Kitabu na Sunna. Ama Shia wao hawaoni Ijmai kuwa ni 66

Sura Yusuf: 40.

86


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

miongoni mwa ala za sharia, bali wanaona yenyewe ni ala ya kufichua hukmu ya kisharia, hivyo kama Imam Maasumu atakuwa miongoni mwao basi Ijmai yao hiyo wakati huo itakuwa imefichua kile kitendo cha Imam kuafikiana nao, hivyo naye hapo anakuwa amefichua hukmu ya kisharia (kwa kuafikiana na umma). Ama katika sura isiyokuwa hii, Shia wanasema Ijmai ni hoja kwa njia mbalimbali zilizotajwa katika vitabu vya misingi ya sharia, na njia iliyo wazi zaidi ni pale inapofichua uwepo wa dalili ya kisharia baina ya wenye kukongamana, dalili hiyo imewafikia wao bila kutufikia sisi. Na kwa mujibu huo mzozo kuhusu uhalali wa hoja ya Ijmai unakuwa ni mzozo wa maneno tu usiyo na faida yoyote, kwani yenyewe ni hoja katika hali zote mbili. Sawa iwe Ijmai ni moja ya ala za sharia kama ilivyo rai ya Suni, au iwe ni ala ya kufichua kwa uyakinifu hukmu ya kisharia au dalili ya kisharia. Na sisi tunatoa maoni kwa Mufti wa Azhar, aruhusu fikihi ya Shia Imamiyyah isomeshwe katika Chuo Kikuu cha Azhar, ili ibainike kwamba tofauti zilizopo ni chache zaidi kuliko vile anavyodhani. Na kwamba hakuna masâ€&#x;ala yoyote ya kisharia isipokuwa yupo aliyeiafiki kutoka miongoni mwa mafakihi wa Kisuni wa zamani au wa sasa. Na katika hilo inatosha kusoma kitabu alKhilaf cha Sheikh Tusi Mungu amrehemu. Nami nilisikia kwa masikio yangu haya kutoka kwa fakihi wa zama za sasa, Dkt. Wahbatu Zuhayliy, alipokuwa mgeni wetu katika mji wa Qum Takatifu, alisema: 87


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

“Hakika mimi nashahidilia kwamba, tofauti zilizopo baina ya mafakihi wa Kisuni ni nyingi zaidi kuliko tofauti zilizopo baina ya Suni na Shia.” Allah anawirishe hoja yake. MHADHARA WA KUMI Siku ya Kumi ya Mwezi wa Ramadhan, Mwaka 1436 A.H. Dkt. Ahmad Twayyib katika mhadhara wake huu baada ya kubainisha tofauti iliyopo baina ya umaasumu wa Manabii na uadilifu wa Maswahaba, kwa muhtasari alisema haya: “Hakika uadilifu si umaasumu wa kutoka kwa Mungu, na kwa sababu hiyo uadilifu unaweza kudhoofika kwa Swahaba na hatimaye akazidiwa na vishawishi vya nafsi na kujikuta akitumbukia katika dhambi. Hata hivyo haraka sana hutubia kwa Allah. Lakini ni hali ya nadra, hivyo miongoni mwa Maswahaba yupo aliyetenda baadhi ya dhambi, na alikuwa akikiri dhambi yake na anakwenda kwa Mtukufu Mtume  kumuomba amsafishe kwa kumwadhibu. Na historia inatusimulia kwamba, baadhi ya Maswahaba waliingia katika lile linaloitwa Fitina Kubwa, nalo ni kule kuuwana kulikotokea na hatimaye akauwawa Sayiduna Uthman, na kule kulikotokea katika zama za Sayiduna Ali Allah awe 88


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

radhi nao, licha ya kwamba wao hawakuingia humo isipokuwa kwa kufanya ijtihadi na kuleta tafsiri zao. Kila mmoja alikuwa anaitakidi kwamba anapigana katika njia ya haki na kwa ajili ya maslahi ya Waislamu. Na inajulikana kwamba mwenye kufanya ijtihadi hulipwa mara mbili anapopatia, malipo ya kufanya ijtihadi na malipo ya kupatia haki. Na hulipwa mara moja anapokosea, nayo ni malipo ya kufanya ijtihadi. Hivyo basi mas‟ala hii haimtii dhambini Swahaba aliyekwenda na kuungana na jeshi lililokuwa likitafuta damu ya Uthman. Na wala haimtii dhambini Swahaba aliyejiunga na jeshi la Ali.” Nasema: Sisi tumeridhia kauli ya Dkt. kwamba Maswahaba walitokewa na dhambi kubwa, na alitaja mfano mmoja, nao ni wa yule aliyekwenda kwa Mtukufu Mtume  kumuomba amtakase kwa kumwadhibu. Lakini kiini cha tofauti kinachotufanya tutofautiane naye ni kuhusu wale waliompiga vita Khalifa wa halali kisharia, namaanisha Imam Ali , katika vita vitatu, Jamal, Suffin na Nahruwan. Ustadhi Mungu amhifadhi amewafanya kuwa ni wenye kufanya ijtihadi na akawathibitishia malipo. Kisha mwishoni mwa maneno yake akasema: “Si mwenye kufanya ijtihadi yule mwenye kunywa pombe kisha akadai kafanya ijtihadi, kwa sababu hakuna ijtihadi wala tafsiri iwapo kuna tamko bayana.” 89


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Na sisi tunasema: Hivi ni tamko lipi lililo wazi na bayana kushinda kauli ya Mtukufu Mtume  kuwaambia Fatima, Ali, Hasan na Husein: “Mimi ni mwenye kuwapiga vita wale wenye kukupigeni vita ninyi. Na ni mwenye kutoa amani kwa yule mwenye kuishi kwa amani na ninyi.”67 Na kauli yake: “Ewe Ali! Litakuuwa kundi ovu wakati wewe ukiwa katika haki. Yeyote ambaye hatakusaidia siku hiyo huyo si mfuasi wangu.”68 Na ni dalili ipi iliyo wazi kushinda kauli ya Mtume wa Allah  kumwambia Ammar: “Litakuuwa kundi ovu.” Na akasema tena: “Angalia Ammar! Litakuuwa kundi ovu, wakati huo utakuwa unaliita kwenda peponi, nalo linakuita kwenda motoni.”69 Na hakika jeshi la Muawiya ambalo Mtume wa Allah aliliita kuwani kundi ovu ndilo lililomuuwa. Hivi kitendo hiki cha kundi ovu si ni kufanya ijtihadi dhidi ya tamko la sharia. Sasa kuna tofauti gani baina ya kuhalalisha pombe wakati kuna tamko la riwaya lenye kuharamisha, na kumpiga vita Imam ambaye Mtukufu Mtume alitoa tamko kuwa mwenye kumpiga vita ni muovu na amevuka mizani 67

Majmauz-Zawaid: 9/ 169. Al-Muujam al-Awsat cha Tabaraniy: 3/ 179. Al-Mustadrak Alas-Sahihayni: 3/ 161, namba 4714. 68 Taarikh Damashqi cha Ibn Asakir: 12/ 370, namba 1220. Majmaul-Jawamiu cha Suyutiy: 6/ 155. Kanzul-Ummal: 11/ 613, namba 32970. 69 Al-Iswabah cha Ibn Hajar: 2/ 512, namba 5704. TahdhibutTahdhib: 7/ 409, namba 665. Al-Bidayat Wanihayat cha Ibn Kathir: 7/ 298, Matukio ya mwaka 37 A.H.

90


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

ya haki?! Au inasihi baada ya hilo kuwazingatia hawa kuwa ni waadilifu na kuhukumu kuwa wamefanya ijtihadi na hivyo watalipwa thawabu?! Kwa ibara nyingine ni kwamba, hali halisi ya mambo na hatari iliyotegemewa kutokana na vita hivyo vitatu inalazimu Mtukufu Mtume awe amekwishawatahadharisha wote dhidi ya vita hivyo, na awe ameshawachorea msimamo unaofaa ambao ni wajibu kwao kuuchukua wakati vitakapotokea vita hivyo. Kwa sababu yeye  aliwatahadharisha na vitu vyenye hatari ndogo kuliko vita hivyo, sasa itakuaje aache kuwatahadharisha na jambo lenye machafuko makubwa kama hayo, machafuko ambayo yalikaribia kuuteketeza ulimwengu wa Kiislamu?! Na hili ndilo linaloungwa mkono na riwaya zilizopokewa na Maswahaba wakubwa. Na maneno haya ya Maswahaba yamejaa ndani ya vitabu na enskolopedia, nayo yanaonesha kwamba Mtume wa Allah  alikuwa akiwahimiza Maswahaba zake kumsaidia na kumtetea Kiongozi wa Waumini Ali katika vita hivyo, na alikuwa akiwaita Maswahaba wapigane upande wake, na akiwaamrisha Maswahaba zake wawauwe wavunja ahadi, waovu na waasi. Na hapa tutaashiria mifano tu ya riwaya hizo zilizopokewa na Maswahaba wakubwa kama vile Kiongozi wa Waumini Ali bin Abutalib, Abu Ayubu al-Answariy, Ibn Masud, Abu Said al-Khudriy, Ammar bin Yasir na Ibn Abbas, jambo linaloonesha jinsi Mtume alivyotilia umuhimu suala hili. 91


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Al-Hakim ameandika katika Mustadrak70na Dhahbi katika at-Talkhis, kutoka kwa Abu Ayub al-Answariy, kwamba Mtume wa Allah  alimwamuru Ali bin Abutalib kuwapiga vita wavunja ahadi, waovu na waasi. Na pia kaipokea al-Kunjiy.71 Na al-Hakim kaandika tena72 kutoka kwa Abu Ayubu kwamba alisema: Nilimsikia Mtume wa Allah akimwambia Ali: “Utawapiga vita wavunja ahadi, waovu na waasi.” Na alipolaumiwa Abu Ayubu al-Answariy kwa kupigana vita na Waislamu wenzake alijibu kwa kusema ni agizo kutoka kwa Mtume wa Allah . Abu Swadiq amesema: Abu Ayubu alifika kwetu Iraq, kabila la Azdi likamwandalia zawadi ya nyama ya mbuzi, wakanituma nimpelekee, nikaingia kwake nikamtolea salamu, nikamwambia: “Ewe Abu Ayubu! Allah amekupa heshima ya kusuhubiana na Nabii Wake  na kwa yeye kufikia nyumbani kwako. Kwanini sasa nakuona unakabiliana na watu kwa upanga wako na kuwauwa, mara hawa na mara wale?” Akasema: “Hakika Mtume wa Allah  alituagiza tupigane upande wa Ali dhidi ya wavunja ahadi, na tayari tumeshapigana nao. Na alituagiza tupigane upande wake dhidi ya waovu – yaani 70

Al-Mustadrak Alas-Sahihayn: 3/ 139. Kifayatut-Twalib: 70. 72 Al-Mustadrak Alas-Sahihayn: 3/ 140. 71

92


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Muawiya na watu wake - na ndio hawa tumewaelekea wao. Na alituagiza tupigane upande wa Ali dhidi ya waasi, hao bado sijawaona.”73 Na Alqamah na Asuwad wamepokea kutoka kwa Abu Ayubu kwamba alisema: “Hakika mtafuta maji huwa hawadanganyi watu wake, na hakika Mtume wa Allah  alituamuru kupigana upande wa Ali dhidi ya makundi matatu: Kupigana dhidi ya wavunja ahadi, waovu na waasi.”74 Na Atabu bin Thaalabah amesema: “Abu Ayubu al-Answari alisema wakati wa ukhalifa wa Umar bin Khattab: „Mtume wa Allah  aliniamuru kupigana upande wa Ali dhidi ya wavunja ahadi, waovu na waasi.‟” Na Asbaghu bin Nabatah ameipokea hadithi hii kutoka kwake, isipokuwa katika upokezi wake kuna: “Alituamuru” badala ya “Aliniamuru.”75 Na imepokewa kutoka kwa Abu Said al-Khudriy kwamba alisema: “Mtume wa Allah  alituamuru kuwapiga vita wavunja ahadi, waovu na waasi. Tukamwambia: Ewe Mtume wa Allah! Umetuamuru 73

Sharhu Nahjul-Balaghah: 3/ 207. Taarikh Ibn Asakir: 42/ 472. Taarikh Ibn Kathir: 7/ 306, Matukio ya mwa006Ba 37 A.H. Kanzul-Ummal: 11/ 352, Hadithi ya 31720. Sharhu Nahjul-Balaghah ya Ibn Abil-Hadid: 3/ 207, Hotuba ya 48. 75 Taarikh Madinat Damashqi cha Ibn Asakir: 42/ 472. AlMustadrak cha al-Hakim: 3/ 139 – 140. Ibn Abdil-Barri katika al-Istiaab: 3/ 53, Sehemu ya Tatu/ 1117, namba 1855. 74

93


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

kuwapiga vita hawa, tutapigana pamoja na nani? Akasema: „Pamoja na Ali bin Abutalib.‟”76 Na imepokewa kutoka kwa Abu Yaqdhani, Ammar bin Yasir kwamba alisema: “Mtume wa Allah  aliniamuru kuwapiga vita wavunja ahadi, waovu na waasi.” Ameiandika Tabarani, na katika tamko lake jingine kutoka katika njia nyingine amesema: “Alituamuru.” Ameliandika Tabarani na Abu Yaala.77 Na amepokea kutoka kwa hao wawili Haythamiy. Na katika maneno ya Ammar bin Yasir aliyomwambia Abu Musa al-Ash‟ariy alisema: “Ama mimi, hakika nashahidilia kwamba Mtume wa Allah  alimwamuru Ali kuwapiga vita wavunja ahadi, na akanitajia majina ya baadhi yao. Na alimwamrisha pia kuwauwa waovu, na hata ukitaka nitakuletea mashahidi watakaoshahidilia kwamba hakika Mtume wa Allah  alikukataza kwa namna ya upekee na akakutahadharisha usiingie katika fitina.”78 Na jambo la kustaajabu ni kwamba Dkt. Analinganisha pande zote mbili na anaziona kuwa zote zilifanya ijtihadi. Hakika kuna tofauti kubwa baina ya miti miwili: Mti mzuri, mizizi yake ni imara na 76

Ameiandika al-Hakim katika Arbaunkama alivyoitaja Suyutiy. Na ameiandika Kunjiy katika al-Kifayah, uk. 72, nauk. 173, Mlango wa 38. Na Ibn Kathir katika Taarikh yake: 7/ 305. 77 Musnad Abi Yaala: 3/ 194, Hadithi ya 1623. MajmauzZawaid: 7/ 238. 78 Sharhu Nahjul-Balaghah: 14/ 15.

94


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

matawi yake yako mbinguni. Na mti muovu uliong'olewa juu ya ardhi, hauna uimara. Kuna umbali mkubwa baina ya miti miwili: Baina ya mti uliobarikiwa, na ule mti uliolaaniwa katika Qur‟ani kwa tafsiri kutoka kwa Mtukufu Mtume , bila kuwepo tofauti kwamba wao (Muawiya na jamaa zake) ndio mti uliolaaniwa uliotajwa na Qur‟ani, kama alivyosema Tabari.79 Ustadhi Muhammad Rashid Ridha katika Tafsir yake amenukuu kwamba: Mmoja kati ya wanazuoni wakubwa wa Kijermani aliwaambia baadhi ya Waislamu huko Astana,80 akiwemo mmoja kati ya vigogo wa Makka, kwamba: “Hakika tunapasa kutengeneza sanamu la dhahabu la Muawiya bin Abu Sufiyan, katika eneo moja la mji wetu mkuu wa Berlin.” Akaulizwa kwa nini? Akasema: “Kwa sababu yeye ndiye aliyebadilisha mfumo wa serikali ya Kiislamu kutoka katika msingi wake wa demokrasia, kuwa ubinafsi wa kushinda. Na kama si hivyo, ulimwengu wote ungeenea Uislamu, na hata sisi Wajerumani na mataifa mengine ya Ulaya tungekuwa Waarabu Waislamu.”81 Mwishoni hatuna budi kusema kuwa, hakika Dkt, mwishoni mwa maneno yake aligusia yale yaliyo79

Taarikh Tabari: 11/ 365. Mji Mkuu waKazakhstan – Mtarjumi. 81 Tafsirul-Manar: 11/ 260. 80

95


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

semwa na wakala wa habari wa Faris, na yeye alijibu hilo lililosemwa, nasi hatutaingilia hilo. MHADHARA WA KUMI NA MOJA Siku ya Kumi naMoja ya Mwezi wa Ramadhan, Mwaka 1436 A.H. Dkt. Ahmad Twayyib katika mazungumzo yake ya siku hii alisisitiza umaasumu wa umma, akasema: “Hakika kutukuza hadhi ya umma licha ya kutokuwepo dalili ya kiakili, hali hiyo inatupeleka kwenye maoni ya kwamba, umma unaweza kukongamanika katika jambo la upotovu. Na umma nyingi zilikongamanika katika upotovu mwingi katika historia. Na umma wa Kiislamu kiakili ulikuwa unaweza kukongamanika katika jambo la upotovu, lakini sharia ilikuja na kuuondoa umma wa Waislamu usiweze kukongamanika katika jambo la upotovu. Imepokewa kutoka kwa Ibn Umar kwamba Mtume wa Allah  alisema: „Hakika Allah haukusanyi umma wangu katika jambo la upotovu, na mkono wa Allah uko pamoja na jamaa.‟ Na imepokewa kutoka kwa Anas bin Malik kwamba Mtukufu Mtume  alikuwa akisema: „Hakika Allah ameuepusha umma wangu kukongamanika katika jambo la upotovu.‟ Hivyo umma kukongamanika juu ya jambo inamaanisha kwamba wenyewe umelindwa na kutokukosea katika jambo husika.” 96


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Nasema: Hakika vyanzo vya sharia vimefungika katika Kitabu, Sunna, Akili na Ijmai. Na makusudio ya Ijmai ni itifaki ya Waislamu juu ya jambo la kisharia, ambapo jambo husika huhesabiwa kuwa ni miongoni mwa mambo wanayoafikiana Waislamu wote. Na liko wapi hili mbele ya ukhalifa wa Makhalifa ambao waliteuliwa na kundi tu dogo la Waislamu huku wengine wakiwapinga. Hivyo kwa mujibu huu ukhalifa wao si miongoni mwa mambo ambayo wameafikiana Waislamu wote. Itakuwaje iwepo itifaki wakati kundi miongoni mwa Maswahaba waliupinga, nao ndio vinara wa Ushia wakiwemo watu wote wa nyumba ya Mtume?!Ilipasa mheshimiwa Mufti asome historia ya Saqifa na mzozo uliotokea humo ikiwa ni pamoja na mgongano wa rai, ugomvi, vitisho na kuchomoleana mapanga. Na yule aliyechukua cheo cha ukhalifa alipata cheo hicho kupitia rai ya kundi maalumu miongoni mwa Answari, nao ni Awsi, licha ya kwamba Makhazraji wote walikataa.82 Ama kuhusu hadithi aliyoitumia mheshimiwa Muftikama dalili, hakika yenyewe ni dhaifu, na ufafanuzi wake kwa ujumla ni kama ifuatavyo: 1. Ibn Majah katika Sunan yake amepokea kutoka kwa Anas bin Malik kwamba alisema: Nilimsikia Mtume wa Allah  akisema: “Hakika umma 82

Taarikh Tabari: 2/ 443 na vyanzo vingine.

97


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

wangu haukongamaniki juu ya upotovu, hivyo mkiona tofauti yoyote shikamaneni na kundi kubwa.”83 Katika sanadi yake yumo Abu Khalfu al-Aaama, Dhahbi amesema: “Hupokea kutoka kwa Anas, Ibn Muin amemzingatia kuwa ni mwongo. Abu Hatim amesema: Hadithi yake hukataliwa.”84 2. Tirmidhi amepokea kutoka kwa Ibn Umar kutoka kwa Mtume wa Allah  kwamba alisema: “Hakika Allah haukusanyi umma wangu (au umma wa Muhammadi) juu ya upotovu, na mkono wa Allah uko pamoja na jamaa. Na atakayejitenga atakuwa amejipeleka motoni.”85 Katika sanadi yake yumo Sulayman bin Sufiyan, Dhahbi amemtambulisha kwa kusema: “Ibn Muin amesema: „Yeye si chochote.‟ Na mara nyingine akasema: „Si mwaminifu.‟ Abu Hatim na Daruqutuniy wamesema: „Ni dhaifu, katika vitabu vinavyojulikana kama Sunan na Musnad hana hadithi zaidi ya hizi mbili.‟”86 3. Abu Dawud amepokea kutoka kwa Abu Malik Ash‟ariy kwamba alisema: Mtume wa Allah  alisema: “Hakika Allah amekuepusheni na sifa tatu 83

Sunan Ibn Majah: 2/ 1303, namba 3950. Mizanul-Iitidal: 4/ 521, namba 10156. 85 Sunan Tirmidhiy: 4/ 466, namba 2167, Kitabul-Fitnah. 86 Mizanul-Iitidal: 2/ 209, namba 3469. 84

98


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

– aliendelea kusema hadi aliposema:- na kwamba hamkongamani juu ya jambo la upotovu.”87 Katika sanadi yake yumo Muhammad bin Awfi Twaiy, Dhahbi amemtaja na kusema kwamba haijulikani hali yake.88 4. Ahmad amepokea ndani ya Musnad yake kutoka kwa Abu Dhari, kutoka kwa Mtukufu Mtume  kwamba alisema: “Mbili ni bora kuliko moja – aliendelea mpaka aliposema-: Hakika Allah Mtukuka hajaukusanya umma wangu isipokuwa katika uongofu.”89 Katika sanadi yake yumo Ibn Iyash al-Humayriy, Dhahbi amesema kumhusu: “Hajulikani.”90 5. Al-Hakim an-Nisaburiy amepokea hadithi hii ndani ya Mustadrak yake, kaipokea kwa sanadi tofauti lakini zote zinakomea kwa Muutamar bin Sulayman. Dhahbi amemtaja kwa kusema: “Muutamar bin Sulayman al-Basriy ni mmoja kati ya waaminifu wasomi. Ibn Kharash amesema: „Ni mkweli lakini hukosea katika hifdhi yake. Na anaposimulia kutoka kwenye maandishi yake huwa ni mwaminifu.‟ Nasema: Yeye ni mwaminifu bila 87

Sunan Abi Daud: 4/ 98, namba 4253. Mizanul-Iitidal: 2/ 676, namba 8030. 89 Musnad Ahmad: 5/ 145. 90 Mizanul-Iitidal: 4/ 594, namba 10821. 88

99


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

mipaka. Na imepokewa kutoka kwa Ibn Muin kwamba si hoja.”91 Vyovyote iwavyo ni kwamba bado hadithi hii ina kasoro ni hadithi ya mpokezi mmoja haileti uyakinifu hata iwe hoja katika milango yote. Na kwa ajili hiyo Tajuddin Sabkiy (aliyefariki 771 A.H.) amesema: “Ama hadithi hii sina shaka kwamba si mutawatiri, bali ni kwamba haina njia iliyosihi kwa namna yenye kuwaridhisha mahafidhi wakubwa…” mpaka mwisho wa aliyoyasema.92 Na kwa haya, inadhihiri kwamba, haiwezekani kuthibitisha usahihi wa ukhalifa wa Makhalifa kwa kutumia Ijmai, na hiyo ni kwa sababu mbili: 1. Kutokuwepo Ijmai kutokana na kuwepo wapingaji wengi. 2. Hakika si sahihi kuegemeza uhalali wa hoja ya Ijmai kama hii kwenye hadithi iliyotajwa, kwa sababu hadithi ya mpokezi mmoja si hoja katika mambo ya itikadi na maarifa na katika mambo mfano wa ukhalifa, ambao unahesabika kuwa ni miongoni mwa mambo muhimu. Zaidi ya hapo ni lile ulilolijua, kwamba hakukuwa na Ijmai, kwani wapo wengi miongoni mwa Answari waliokataa kutoa kiapo cha utiifu, kama vile Makhazraji na 91 92

Mizanul-Iitidal: 4/ 143, namba 8648. Raf’ul-Hajib Ani Ibnl-Hajib, Waraka wa 176.

100


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Aali Hashim wakiongozwa na Imam Ali bin Abutalib na kundi lililokuwa pamoja naye.93 MHADHARA WA KUMI NA MBILI Siku ya Kumi naMbili ya Mwezi wa Ramadhan, Mwaka 1436 A.H. Dkt. Ahmad Twayyib alisema: “Hakika uadilifu wa Maswahaba si jambo lenye mjadala baina ya Masuni, ni jambo lililoafikiwa bila mjadala. Baada ya Allah kuwaadilisha na kuwasifu katika matamko bayana kutoka katika Qur‟ani Tukufu,94 baada ya hapo haisihi uadilishwaji wa mwingine yeyote. Na wala haisihi kuwakalia juu, na yeyote atakayewakalia juu hakika atakuwa anapoteza imani yake, Allah atulinde na hilo.” Kisha akasema katika tamko lake lililochapishwa gazetini: “Na kisha ni kwamba haisihi kuchunguza 93

Taarikh Khulafair-Rashidin cha Ibn Qutaybah: 12. Sahih Bukhar: 5/ 83, Kitabu kinachozungumzia vita, Vita vya Khaybar. 94 Anakusudia kauli ya Allah: “Na waliotangulia wa kwanza katika muhajiri na Ansari. Na wale waliowafuata kwa wema, Mwenyezi Mungu yuko radhi nao na wao wako radhi Naye; na amewaandalia Bustani ambazo hupita mito chini yake, watadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa.” (Sura Tawbah: 100).

101


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

hali zao kwa nia ya kutaka kujua je Swahaba huyu ni mwadilifu au la? Kwa sababu Qurâ€&#x;ani Tukufu imekwishawapa ithbati ya usafi, na mwenye kuwa na shaka na hili basi anatilia shaka ithbati hii iliyotolewa na Mungu. Na kwa ajili hiyo, ndio maana hakuna katika chanzo chochote kile miongoni mwa vyanzo vya kutathmini uadilifu wa wapokezi kwa Masuni, jina la Swahaba hata mmoja. Na hili halijazushwa ndani ya vitabu vya Masuni, balini kwa sababu ya kujua kwao kwamba wao wameshaadilishwa kutoka juu ya mbingu saba. Nasema: Katika maneno ya Muftiwa Azhar, sijakuta jambo jipya la kutafakari. Imeshatangulia katika mhadhara wa saba, kwamba Aya hii haioneshi isipokuwa radhi ya Allah aliyonayo kwa baadhi ya Maswahaba na si Maswahaba wote kuanzia wa kwanza wao hadi wa mwisho wao. Zaidi ya hapo ni kwamba, hakika uadilishwaji wowote ule na usifiwaji wowote ule unategemea na una sharti la kubakia katika hali yake ya mwanzo mpaka siku ya Kiyama, ile sababu iliyopelekea kuwepo uadilishwaji. Na imeshatangulia kwamba Mtukufu Mtume  alieleza kuwa mambo huzingatiwa kwa mwisho wake. Na kwa mujibu huu haiwezekani kuitumia Aya hii iliyotajwa kuwa dalali juu ya uadilifu wa Maswahaba wote, maadamu dalili imeonesha kutokea kwa dhambi kutoka kwa baadhi yao. Na hasa iwapo Swahaba husika ni mmoja kati ya waliyompiga vita Imam aliyeteuliwa kwa tamko la Mungu, au Imamu ambaye 102


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Muhajirina na Answari waliafikiana katika kumpa kiapo cha utiifu, kama hali ilivyo kwa Imam Ali . Yeye ni Imam aliyeteuliwa kwa tamko la Mungu – kama wanavyoamini Imamiyyah – au aliyepewa kiapo cha utiifu na Muhajirina na Answari na hakuna aliyegoma kumpa kiapo cha utiifu isipokuwa watu ambao idadi yao haivuki vidole vya mkono. Kisha ni kwamba, hakika mheshimiwa Mufti hatofautishi baina ya kutukana na kusoma maisha ya Swahaba. Ama kuhusu jambo la kwanza, ni kwamba imeshatangulia kuwa si jambo linaloruhusiwa, na Shia Imamiya hawafanyi wala kuruhusu jambo hilo, hawamtukani yeyote wa kawaida sembuse Swahaba?! Ama kuhusu jambo la pili, ni kwamba lenyewe halina uhusiano wowote na kutukana, na huenda jambo hili ndilo ambalo yeye Mufti anadhani ni kumtukana Swahaba. Huyu hapa Bibi Aisha Mama wa Waumini, yeye hata kama ana heshima ya juu kama alivyosema Imam Ali , lakini heshima hiyo haituzuii kutathmini na kusoma matendo aliyoyatenda, ambapo alitoka kwenda kumpiga vita Imam wa zama zake, akiwa miongoni mwa watu wa juu katika jeshi aliloliongoza Twalha na Zubair, watu wawili ambao walikuwa wakiwahimiza watu wasimame dhidi ya Uthman bin Affan, lakini ni hao hao walirudi nyuma kwa visigino vyao wakawa wanatafuta kulipiza kisasi cha damu yake ambayo ilimwagwa kwa sababu yao wao wawili. 103


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Na wao hao wawili walimtumia mke wa Mtume  katika kuwahimiza na kuwashawishi watu watoke dhidi ya Imam Ali , mke ambaye aliamrishwa na tamko la Qur‟ani atulie ndani ya nyumba yake. Tabari amepokea kwamba: Hakika Aisha alipofika Sarif wakati akiwa njiani kurejea Makka, alikutana na Abdu bin Ummu Kilab, naye ndiye Abdu bin Abu Salamah – hutajwa kwa nasaba ya umamani kwake Aisha akamwambia: “Habari za huko?” Akasema: “Wamemuuwa Uthman na wamemuacha siku nane (bila kumzika).” Akasema: “Kisha wamefanya nini?” Akasema: “Wameuchukua mwili wake watu wa Madina kwa kujumuika pamoja, na kwa kupitia wao mambo yakaenda vizuri. Wamekubaliana juu ya Ali bin Abutalib.” Aisha akasema: “Wallahi natamani mbingu ingeangukia ardhi, kama jambo limetimia kwa kupewa rafiki yako. Nirudisheni. Nirudisheni.” Akaenda Makka huku akisema: “Wallahi Uthman ameuwawa ilihali kadhulumiwa. Wallahi nitaitafuta damu yake (nitalipiza kisasi).” Ibn Ummu Kilab akamwambia: “Kwa nini? Wakati Wallahi mtu wa kwanza aliyepindisha herufi yake ni wewe, ulikuwa ukisema: Muuweni Naathal hakika amekufuru.” Aisha akasema: “Hakika wao walimtaka atubie kisha wakamuuwa. Mimi nilisema na kisha wao wakasema, na kauli yangu ya mwisho ndio bora kuliko kauli yangu ya mwanzo.” Ibn Ummu Kilab akamwambia (kishairi): “Uanzaji hutoka kwako na ubadilishwaji hutoka kwako. Upepo hutoka kwako na mvua hutoka 104


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

kwako. Ni wewe uliyeamuru Imam auwawe, na ukatuambia kwamba amekufuru. Mwisho tukakutii katika kumuuwa.Na kwetu sisi aliyemuuwa (Uthman) ni yule aliyeamuru (auwawe).” Akaenda Makka na kufikia kwenye mlango wa Msikiti, akaenda kuligusa jiwe, kisha akaweka pazia, watu wakamkusanyikia.”95 Hii ndio kazi yetu katika kusoma maisha ya Swahaba yeyote yule wa kiume au wa kike. Hatumzidishii chochote, hivyo basi ikiwa kufanya hivi ndio kuwatukana, basi mtu wa kwanza aliyewatukana wao Maswahaba ni waandishi wa Sira na historia ambao walikusanya maisha ya Maswahaba katika enklopidia zao zilizojaa historia yao. Na kwa ajili hiyo inadhihiri kwamba kutilia shaka uadilifu wa Swahaba fulani si kutilia shaka ithbati iliyotolewa na Mungu, yenyewe ni haki mahala pake na sehemu yake. Na kila ambacho watu mfano wa Mufti wa Azhar wanadai kuwa ni tusi si tusi, bali ni kauli za kusoma maisha yao na kuchambua matendo yao. Hivyo kama ni ya kheri yataendelea kuwa kheri, na kama ni ya shari yataendelea kuwa shari. Na si kuvunja heshima yao au ya familia zao na mfano wake. Na hapa kuna neno la thamani kutoka kwa Sheikh Muhammad Husein Kashif Ghatau, amesema: “Huenda msemaji akasema: „Hakika sababu ya uadui 95

Taarikh Tabari: 3/ 476, Matukio ya mwaka 36 A.H. Tazama al-Kamil Fiitaarikh cha Ibn Athir: 3/ 206 – 207.

105


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

uliyopo baina ya makundi mawili ni kwakuwa Shia wanaona kuwa inaruhusiwa kuwavunjia heshima Makhalifa au kuwashutumu. Na baadhi wanaweza kuvuka hadi kwenye kuwatukana na kuwakosoa, jambo ambalo linalichukiza kundi jingine na kuamsha hisia zao. Na hatimaye uadui na ugomvi uliongezeka.â€&#x; Jibu ni kwamba: Kama tutalitafakari hili kidogo na tukarejea kwenye hukmu ya akili bali pia kwenye sharia, tutalikuta si jambo lenye kupelekea uadui. Kwanza, jambo hili (la kuwavunjia heshima) si rai ya Mashia wote, bali ni rai ya mtu mmoja mmoja kutoka kwa baadhi yao, na huenda haliafikiwi na wengi wao. Vipi liafikiwe wakati katika hadithi za Maimamu wa Shia kuna katazo linalokataza hilo?! Hivyo haisihi kuwachukia Mashia wote kwa sababu ya utovu wa nidhamu wa baadhi ya wafurutuada kutoka miongoni mwao. Pili, hata kama tukijaalia kuwa hili lipo, bado haliwi ni sababu yenye kumfanya mtu awe kafiri na kutoka nje ya Uislamu. Bali jambo la juu kabisa linaloweza kusemwa ni kuwa ametenda maasi. Na kwakweli ni wengi wenye kutenda maasi kutoka kwenye makundi yote mawili. Na maasi ya Mwislamu hayawajibishi kumkatia kabisa uhusiano wa udugu wa Kiislamu. Tatu, Pia tendo hili linaweza lisiingie katika maasi na wala lisiwajibishe uovu, ikiwa limetokana na ijtihadi na itikadi, hata kama ni kosa. Kwani linalokubalika 106


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

kwa watu wote katika upande wa mlango wa ijtihadi ni kwamba, aliyekosea hulipwa mara moja, na aliyepatia hulipwa mara mbili. Na maulamaa wa Kisuni wameona ni sahihi vile vita vilivyotokea baina ya Maswahaba katika zama za mwanzo, kama vile vita vya Jamal, Suffin na vinginevyo, kwa sababu Twalha na Zubair na Muawiya walifanya ijtihadi licha ya kwamba walikosea katika ijtihadi yao, na jambo hilo halitii dosari uadilifu wao na heshima yao kubwa (kwa mujibu wa maulamaa hao wa kisuni). Na ikiwa ijtihadi inahalalisha na wala haioni vibaya kuuwa maelefu ya Waislamu na kumwaga damu yao, basi ni bora zaidi ikahalalisha pia bila kuona vibaya, kitendo cha baadhi ya wafurutuada cha kuwavunjia heshima waheshimiwa hao, maadamu ni kutokana na ijtihadi. Na lengo katika yote haya ni kwamba, vyovyote tutakavyozama katika uchunguzi na tukaenda kwa mujibu wa dalili, za kiakili au za kisharia, na tukajiepusha na matamanio, chuki na ushabiki, kamwe hatutapata sababu yoyote yenye kuhalalisha uadui na mfarakano baina ya makundi ya Waislamu, hata kama kutakuwa na tofauti kubwa kiasi gani kati yao katika masâ€&#x;ala mengi.96

96

Jarida la Risalatul-Islam, Toleo la Tatu la Mwaka wa Pili: 270. 107


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

MHADHARA WA KUMI NA TATU Siku ya Kumi naTatu ya Mwezi wa Ramadhan, Mwaka 1436 A.H. Dkt. Ahmad Twayyib, Mufti wa Azhar Tukufu alisema: “Hakika lengo letu ni kutafuta umoja wa umma wa Kiislamu na si kuufarakisha. Azhar hata siku moja haijawahi kuwa taasisi ya machafuko au ya kufarakisha baina ya Waislamu. Yenyewe ndio iliyotoa wito katika karne iliyopita wa kufahamiana baina ya Suni na Shia. Nayo ina shauku kubwa juu ya umoja huu, kwa sababu yaliyotupata na yanayotuchoma kwa moto wake hivi sasa, hayakutufika isipokuwa kwa njia ya kuwafarakisha watu wa madhehebu hizi mbili. Lazima hili lijulikane kwa wote.” Nasema: Kuzikurubisha pamoja madhehebu za Kiislamu ni shauku waliokuwa nayo watu waliojishughulisha na kazi hiyo ya kuzikurubisha pamoja Madhehebu za Kiislamu katika karne ya kumi na nne. Nao walikuwa ni maulamaa wenye ikhlasi wenye hamasa ya kutengeneza; “Hakika hao ni vijana waliomwamini Mola Wao na akawazidisha uongofu. Na tukazitia nguvu nyoyo zao….” Na ili kuweza kutimiza nia yao hii na shauku yao hii walifanya kazi ya kutoa jarida la Kiislamu la kimataifa kwa jina la Risalatul-Islam. Hakika jarida hili kwa njia yake 108


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

imara na umadhubuti wake kamilifu na kwa heshima yake ya kuheshimu pande zote na kujitenga na upendeleo na misimamo ya kisiasa, halikuzaa isipokuwa kheri na nasaha kwa Waislamu, na likapata hadhi ya kuaminiwa na maulamaa wa madhehebu zote. Hakika hawa walionyanyua bendera ya kuzikurubisha pamoja madhehebu za Kiislamu wameshahamia kwenye rehema za Allah Mtukuka, na miongoni mwa Shia walikuwemo maulamaa wenye kuheshimika mfano wa: 1. 2. 3. 4.

Mufti Muhammad Husein Aali Kashiful-Ghatau. Sayyid Hibatuddin Shahrastaniy. Sayyid Abdul-Husein Sharafuddin al-Amiliy. Mufti Muhammad Jawwad Mughniyyah.

Na walikuwemo pia Marajiu watukufu kama: 1. Ayatullah Burjurdi. 2. Ayatullah Swadruddin Swadri. 3. Ayatullah Sayyid Muhammad Taqiyyu Khuwansariy. Na miongoni mwa ulamaa wa Kisuni walikuwemo Mamufti wawili wakubwa wa Azhar: 1. Mufti Abdulmajid Salim. 2. Mufti Mahmud Shaltut. Na maulamaa wengine kutoka Azhar mfano wa: 3. Mufti Mahmud Abu Zahra. 109


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

4. Mufti Mahmud Muhammad al-Madaniy, aliyekuwa mhariri mkuu. 5. Ustadhi Abdul-Aziz Isa Amin, aliyekuwa Afisa Mtendaji Mkuu, na wengineo. Na miongoni mwa waandishi wakati huo alikuwa ni: 6. Ahmad Amin. 7. Abbas Mahmud Uqqad. 8. Muhammad Farid Wajadiy na mfano wao. Kundi hili la thamani ni mara chache kupatikana mfano wao kila zama. Hakika walibeba machungu ya Waislamu na wakatambua maeneo ya hatari yanayotishia usalama wa umma wa Kiislamu, hivyo wakaweka suluhisho. Natamani kwamba waliokuja baada yao wangefuata mwenendo wao na wakashikamana na maeneo ya ushirikiano ambayo kiuhalisia ni mengi, na wakayaacha maeneo ya tofauti kwenye vyuo na vituo vya elimu bila kuyasambaza katika jamii. Na yafuatayo ni maneno ya mmoja kati ya maulamaa waliokuwepo kwenye taasisi hiyo ya kuzikurubisha pamoja madhehebu za Kiisamu, alisema: “Ndiyo, huenda ikadhaniwa kuwa kuzikurubisha pamoja madhehebu za Kiislamu ni jambo lisilowezekana kutokana na kuwepo tofauti za kimsingi baina ya Shia na Suni. Shia wanaona kwamba Uimamu ni msingi miongoni mwa misingi ya dini, 110


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

nao ni sawa na Tauhidi na Unabii, na kwamba umetamkwa na maandiko kutoka kwa Allah na Mtume Wake. Na umma hauna mamlaka ya kuweka rai wala kuchagua chochote humo, kama usivyokuwa na uchaguzi katika unabii. Hali hii ni tofauti na ndugu zetu Suni, wao wamekubaliana kuwa wenyewe si miongoni mwa misingi ya dini. Na wametofautiana, yupo asemaye kwamba raia ndio wenye wajibu wa kumsimika Imamu na mfano wake, na wapo wasemao kwamba uimamu ni suala la kisiasa na dini haina uhusiano nalo, si katika upande wa misingi yake wala upande wa matawi yake. “Lakini pamoja na tofauti hii kubwa iliyopo baina ya makundi mawili katika suala hili, je umewahi kumkuta Shia yeyote anasema kuwa asiyeamini uimamu si Mwislamu (hapana na Allah atukinge na hilo), au umewahi kumkuta Suni yeyote akisema kwamba mwenye kuamini uimamau si Mwislamu (hapana na Allah atukinge na hilo). Hivyo basi, kuamini uimamu na kutouamini hakuna uhusiano wowote na ujamaa wa Kiislamu na hukumu zake ikiwemo uharamu wa kumwaga damu ya Mwislamu au kuvunja heshima yake au kupora mali yake. Na ikiwemo wajibu wa kutunza udugu wake, kutunza heshima yake na kutoruhusiwa kumteta, na mengineyo mengi mfano wa hayo miongoni mwa haki anazotakiwa Mwislamu kutekelezewa na ndugu yake Mwislamu. 111


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

“Kisha ni kwamba, lengo hasa la mwenye kulingania kwenye kuzikurubisha pamoja madhehebu za Kiislamu si kuondoa tofauti zilizopo baina ya Madhehebu za Kiislamu na kuzifanya madhehebu moja ya kisuni tu, au ya kishia tu, au ya kiwahabi tu.Litawezekanaje hilo wakati kutofautiana rai na mawazo ni katika tabia za asili ya kibinadamu?! Bali lengo hasa linalotafutwa katika hilo ni kuondoa hali ya tofauti hizi kuwa chanzo na sababu ya uadui na chuki. Lengo ni kubadili utengano na mashambuliano kuwa udugu na ukaribu. Hakika Waislamu wote vyovyote watakavyotofautiana katika misingi na matawi, lakini wote wameafikiana juu ya madhumuni ya Hadithi yakinifu zilizosihi kwao wao, kwamba yeyote atakayetamka shahada mbili na akaufanya Uislamu kuwa ndio dini yake, ni haramu kumwaga damu yake, kupora mali yake na kuvunja heshima yake. Na kwamba Mwislamu ni ndugu wa Mwislamu, na kwamba yeyote atakayeswali kwa kuelekea kibla chetu na akala kichinjwa chetu bila kufuata dini isiyokuwa yetu, basi huyo ni mmoja wetu, ana haki kama tulizonazo sisi, na ana wajibu kama tulionao sisi.�97

97

Makala ya Sheikh Muhammad Husein Kashiful Ghita, iliyochapishwa katika Jarida la Risalatul Islam

112


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

MHADHARA WA KUMI NA NNE Siku ya Kumi na Nne ya Mwezi wa Ramadhan, Mwaka 1436 A.H. Dkt. Ahmad Twayyib ametumia Aya: “Na waliokuja baada yao wanasema: Mola Wetu! Tughufirie sisi na ndugu zetu waliotutangulia kwa Imani, wala usijaalie ndani ya nyoyo zetu undani kwa walioamini. Mola Wetu! Hakika Wewe ni Mpole, Mwingi wa rehema”,98 kuthibitisha wajibu wa kuwapenda Maswahaba na wajibu wa kuwatendea wema. Akasema: “Aya hii ni dalili juu ya wajibu wa kuwafanyia ihsani na kuwaombea msamaha Maswahaba, kwa sababu Bwana Mtukuka amewawekea fungu katika ngawira wale watakaokuja baada yao maadamu tu watawapenda wao na kuwaombea msamaha. Na kwamba hakika yule atakayewatukana au kumtukana mmoja wao au kuitakidi shari yoyote kwao, hana haki ya kupata fungu hilo. Malik amesema: „Yeyote mwenye kumchukia Swahaba yeyote miongoni mwa Maswahaba wa Muhammad  au akawa na undani nao ndani ya nafsi yake, huyo hana haki katika ngawira ya Waislamu. Kisha alisoma Aya: Na waliokuja baada yao wanasema: Mola Wetu! Tughufirie sisi na ndugu zetu waliotutangulia kwa Imani, wala usijaalie ndani ya nyoyo zetu undani kwa walioamini. Mola Wetu! 98

Sura Hashri: 10.

113


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Hakika Wewe ni Mpole, Mwingi wa rehema.‟ Kwa Aya hii anathibitisha kwamba vizazi vijavyo vinavyofuatia baada ya Muhajirina na Answari wameamuriwa kuwafanyia wema na kuwaombea msamaha Maswahaba wa makundi yote mawili. Na hili linawajibisha uharamu wa kuwatukana wao, kuwalaani na kuwavunjia heshima.” Nasema: Hakika Allah katika Sura al-Hashri, katika Aya ya nane mpaka ya kumi, amewagawa Waislamu katika makundi matatu: 1. Aliloliashiria kwa kauli yake: “Wapewe mafukara wahajiri waliotolewa majumbani mwao na mali yao kwa ajili ya kutafuta fadhila kutoka kwa Mwenyezi Mungu na radhi Zake, na wanamsaidia Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Hao ndio wa kweli.” 2. Aliloliashiria kwa kauli yake: “Na waliofanya maskani na imani kabla yao, wanawapenda waliohamia kwao wala hawapati dhiki katika vifua vyao kwa walivyopewa, na wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji. Na mwenye kuepushwa na uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufaulu.”

114


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

3. Aliloliashiria kwa kauli yake: “Na waliokuja baada yao wanasema: Mola Wetu! Tughufirie sisi na ndugu zetu waliotutangulia kwa Imani...” yaani a. Wao wanajiombea na kujitakia msamaha wenyewe na kuwaombea na kuwatakia msamaha wale waliowatangulia katika imani. b. “Wala usijaalie ndani ya nyoyo zetu undani kwa walioamini.” Wao wanamuomba Allah aondoe hikdi na chuki na uadui toka ndani ya nyoyo zao, kwani imani haikai pamoja na chuki ya kumchukia muumini mwingine ndani ya moyo wa muumini. Kwa sababu kuwa na chuki na muumini ni kuwa na chuki na nafsi, nawaumini ni sawa na mwili mmoja. c. “Mola Wetu! Hakika Wewe ni Mpole, Mwingi wa rehema.” Yaani wanamuomba Yeye kwa sababu ndiye Mpole Mwingi wa rehema, ili awaondolee chuki na unafiki na azitakase nyoyo zao na sifa hizo. Maombi haya matatu yanatofautiana upande wa madhumuni, wao katika ombi lao la kwanza wanajitahidi kutengeneza nafsi zao. Na wanaomba msamaha na rehema kutoka kwa Allah kwa lengo hilo. Ama katika ombi la pili, ni kwamba wao wanawaombea msamaha na maghofira wale waliowatangulia katika imani. Na katika ombi la tatu 115


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

wanasisitiza hali ya kusafisha na kutakasa nyoyo zao na uchafu na chuki dhidi ya wale waliowatangulia katika imani. Katika dua hizi kuna vinu vya nuru kwa ajili ya Waislamu wote, na kila kizazi kinapasa kujiangazia kwa nuru hiyo katika mwenendo wao na muamala wao wanaoamiliana na ndugu zao, waamiliane nao kwa usafi na undugu. Kisha ni kwamba, kauli ya Allah: “Na waliokuja baada yao wanasema: Mola Wetu! Tughufirie sisi na ndugu zetu waliotutangulia kwa Imani...” ni dua ya Waumini wote kuviombea vizazi vilivyotangulia na wala si makhususi tu kwa Maswahaba bila kuwahusu wengine. Allah Mtukuka anawafundisha Waislamu wa kila kizazi kwamba wawaombee wenzao waliotangulia kabla ya kizazi chao. Dkt. alikuwa anadhani kwamba kifungu hiki kinawahusu wale ambao kwa mujibu wa istilahi ya watu wa Hadithi hutambulika kwa jina la Tabiina, nao ni wale ambao hawakumuona Mtume wa Allah  lakini walimuona aliyemuona Mtume. Na kwa hivyo umekuja msisitizo huo kuwataka wao wawaombee Maswahaba. Wakati ambapo ukweli ni kwamba kauli yake: “Na waliokuja baada yao” inawaamuru Waislamu kwa lugha ya habari, kwamba wawaombee Waislamu wote waliotangulia bila kuwa ni makhususi kwa Maswahaba tu. Na hata tukijaalia kwamba Aya inaonesha kuwa dua hiyo wanatakiwa waombewe Maswahaba tu, bado hiyo haioneshi uadilifu wao wote, na kwamba 116


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

mwenendo wa Maswahaba wote ulikuwa sahihi bila vumbi lolote. Bali inaonesha kwamba wao wanahitaji kuombewa msamaha na hilo halina uhusianao wowote na uadilifu. Hivyo tunapata hitimisho kwamba: Kwanza: Aya haiwahusu Maswahaba tu peke yao, bali madhumuni yake ni kuviombea dua vizazi vyote vilivyotangulia. Pili: Hakika kuwaombea msamaha watu wa vizazi vilivyotangulia au Maswahaba peke yao si dalili ya kwamba wao wote ni watu wema na waliofaulu. Jambo kubwa tunalolipata hapo ni kwamba wao wanahitajia msamaha wa Mola Muweza. Sasa imebakia kuzungumzia kifungu cha pili, yaani kauli ya Allah: “Wala usijaalie ndani ya nyoyo zetu undani kwa walioamini.� Hii nayo ni dua ya watu wote, si makhususi kwa ajili ya kizazi kimoja tu. Hivyo kuitumia Aya hii kama dalili katika maudhui ya Maswahaba ni kughafilika na madhumuni yake. Na mwishoni tunasema: Hakika hapa kuna mambo kadhaa ya kuzungumziwa: 1. Kuwatukana Maswahaba na kuwavunjia heshima yao na ya watoto wao na wake zao. 2. Kuwa na chuki na uadui na Swahaba kama Swahaba. 3. Kusoma hali za Maswahaba kuanzia mazuri yao hadi mabaya yao. 117


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Waislamu wote kwa ujumla wao na Mashia kwa umakhususia wao, hawaruhusu jambo la kwanza na la pili, na wanaona kufanya hayo mawili ni kwenda kinyume na ni upumbavu. Ama kuhusu jambo la tatu, hakika jambo hilo ni mwenendo wa wahakiki na werevu, ambao husoma maisha ya watu waliotangulia kwa mujibu wa Kitabu na Sunna na akili. Na kwa nyongeza ni kwamba, Aya za Sura al-Hashri zimeyafunga mazungumzo kwa Muhajirina waliotolewa majumbani mwao, na kwa Answari waliofanya maskani na imani na waliokuja baada yao. Hivyo hazina dalili yoyote ya kuwajumuisha chini ya Aya hii tukufu, wale waliosilimu katika mwaka wa Ukombozi wa Makka na baada yake. MHADHARA WA KUMI NA TANO Siku ya Kumi naTano ya Mwezi wa Ramadhan, Mwaka 1436 A.H. Dkt. Twayyib ametaja kwamba Shia humvunjia heshima mke wa Mtume  Mama wa Waumini Aisha, na baba yake Khalifa Abu Bakri. Na kuwatukana wao ni kumtukana na kumfanyia jeuri Mtume wa Mwenyezi Mungu . Nasema: Hakika Dkt. Mufti wa Azhar amekerwa na Shia kwa sababu wao humvunjia heshima mke wa Mtume , Mama wa Waumini Aisha, na baba yake. Sisi tunasema: Hakika Bibi Aisha ni mmoja miongoni 118


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

mwa wakeze wa Mtukufu Mtume  na ni mmoja kati ya Mama wa Waumini, na hakuna hata mmoja miongoni mwa Waislamu mwenye shaka na kutohusika kwake na tuhuma ya uzushi iliyotengenezwa na wanafiki na ikaenezwa na kusambazwa na nguzo ya wanafiki na kiongozi wao Abdullah bin Ubayya bin Salul, katika zama za Mtukufu Mtume , na Qur‟ani Tukufu ikazungumzia tuhuma hiyo katika Aya kadhaa, Allah anasema: “Hakika wale walioleta uzushi ni kundi miongoni mwenu. Msiufikirie ni shari kwenu, bali hiyo ni kheri kwenu. Kila mmoja katika wao atapata aliyoyachuma katika madhambi. Na yule aliyejitwika sehemu yake kubwa miongoni mwao atapata adhabu kubwa.”99 Kisha anasema: “Na mbona mliposikia msiseme: Haitufalii kuzungumza haya; utakatifu ni Wako! Huu ni uzushi mkubwa.”100 Ili kujua kwa undani kuhusu tuhuma hii na tafsiri ya Aya zilizoteremka kwa ajili ya tukio hili tunamrejesha msomaji kwenye tafsiri ya Aya hizo iliyopo ndani ya kitabu Majmaul-Bayan cha Tabrasiy.101 Lakini hili halituzuii kuchunguza na kusoma maisha yake aliyoishi baada ya kufariki Mtukufu Mtume  na hasa ushiriki wake katika fitna ya Jamal. Hili ni upande wake, ama kuhusu upande wa baba yake, ni 99

Sura Nur: 11. Sura Nur: 16. 101 Majmaul-Bayan: 4/ 130. 100

119


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

kwamba sisi hatukanushi kuwa kwake mmoja kati ya Maswahaba wa Mtukufu Mtume  na swahiba wake ndani ya pango, na kwamba yeye ni mmoja kati ya Muhajirina wa mwanzo. Lakini kukiri hili hakutuzuii kusoma na kuchunguza maisha yake, ukhalifa wake na misimamo yake. Na kwamba ni kwa namna ipi aliweza kupewa kiapo cha utiifu, na kilidumu vipi. Hayo yote yapo katika historia, kwani kuzuia kufanya utafiti na kusoma hali za Maswahaba kunawanyima wengine haki ya kujua yale yaliyotokea katika zama zao miongoni mwa matukio matamu na machungu. Na sisi tutakapochunguza kwa kina katika vyanzo vikuu vya hadithi na historia vilivyotungwa na maulamaa wakubwa wa Kisuni, tutawakuta hawaoni vibaya kuelezea uhalisia na kunukuu matukio ambayo siku hizi tumeanza kuogopa kuyagusia. Bukhari ameandika kwa njia yake kutoka kwa Ibn Abbas kwamba alisema: “Nilikuwa nawasomesha watu miongoni mwa Muhajirina akiwemo Abdurahman bin Awfi, wakati nikiwa nyumbani kwake huko Mina, na yeye akiwa kwa Umar bin Khattab, katika Hija ya mwisho aliyohiji, mara alirejea kwangu Abdurahman, kisha akaniambia: Natamani ungemuona mtu aliyekuja kwa Kiongozi wa Waumini leo na kumwambia: „Unalolote la kunena kuhusu fulani, yeye anasema: Bila shaka Umar akifa hakika nitampa kiapo cha utiifu fulani kwani wallahi japo kiapo cha utiifu alichopewa Abu Bakri kilikuwa kwa kushitukiza tu lakini kilitimia.‟” 120


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Na baada ya Bukhari kutaja sehemu iliyobaki ya riwaya alisema: Khalifa aliporejea Madina alisimama na akawahutubia watu, miongoni mwa aliyoyasema katika hotuba yake ni haya yafuatayo: "Kwa hakika nimepata habari kwamba kuna asemaye miongoni mwenu kuwa, Wallahi lau Umar atakufa nitampa kiapo cha utiifu fulani, basi na asijidanganye mmoja wenu kwa kusema kuwa kiapo cha utiifu alichopewa Abu Bakri kilikuwa cha kushitukiza lakini kilitimia. Ndiyo kilikuwa hivyo lakini Mwenyezi Mungu aliikinga shari yake.."102 Huyu hapa Bukhari na kabla yake ni Ibn Abbas na Abdurahman bin Awfi, wote hawakuzingatia kauli ya msemaji au kauli ya Khalifa kuwa ni tusi dhidi ya Abu Bakri na kwamba ni kumvunjia heshima, bali yeye Bukhari amelitaja kama tukio la kihistoria. Na pia Ibn Athir amesema katika kitabu an-Nihayah: “Makusudio ya neno Faltat (lililotumika katika maelezo)ni ghafla, na kiapo kama hiki chenyewe kilivyo kilipasa kuwa chanzo cha shari na machafuko, lakini Allah akazuia hilo na akakinga.” Kisha akasema: “Na Faltat ni kila kitendo kinachofanywa bila kutarajiwa, na hakika kiapo hicho kiliharakishwa kwa kukhofia kwamba jambo lisienee. Na inasemekana kuwa kwa neno hilo alikusudia ukwapuaji. 102

Sahih Bukhar: 2/ 1712, Hadithi ya 6830, Mango wa umpopoa mawe mjamzito iwapo atazini, Kitabu cha wanaostahiki kupigwa vita miongoni mwa makafiri.

121


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Kwa maana kwamba, nafsi ziliutamani uongozi katika siku ya Saqifa, na kwa ajili hiyo ulikithiri ugomvi kuuhusu, hivyo Abu Bakri hakuutwaa isipokuwa kwa kunyang‟anya na kuukwapua kutoka kwenye mikono ya wengine.”103 Haya ndio maneno ya Ibn Athir, nayo yako bayana katika kuashiria ugomvi na hamu ya kila kundi kuchukua ukhalifa na uongozi, miongoni mwa wale waliokusanyika Saqifa. Na wala Ibn Athir katika kuwasilisha kwake habari hii kwa kadiri ilivyo kama tukio la kihistoria, hajaona kuwa yupo katika hatari ya kuwatukana waliokusanyika katika ukumbi wa Saqifa. MHADHARA WA KUMI NA SITA Siku ya Kumi naSita ya Mwezi wa Ramadhan, Mwaka 1436 A.H. Mufti wa Azhar, Ahmad Twayyib, mnamo siku ya Ijumaa, mwezi kumi na sita Ramadhan, alikataa kuwaita Shia Marawafidhi. Na kwamba ni wachache miongoni mwa Suni wenye chuki binafsi ndio wanaowakufurisha Shia na kuwaita Marawafidhi. Akasema: “Itawezekana vipi kuungana ilihali Suni wanasikia uvunjaji huu wa heshima (dhidi ya Maswahaba) kutoka kwa wengi miongoni mwa wale 103

An-Nihayat Fii Gharibil-Hadith Wal-Athar: 3/ 467.

122


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

wanaojinasibisha na ushia.” Kisha akasema: “Sisi tunashuhudia baadhi ya matendo yasiyokuwa mazuri kutoka kwa watu wachache miongoni mwa Masuni wenye chuki binafsi, matendo ambayo yanawafanya Shia wajihisi unyonge, vitendo kama vile kuwakufurisha baadhi ya Shia na kung‟ang‟ania kuwaita Marawafidhi. Akasisitiza kwamba matendo haya hayafai. Nasema: Hakika kuwaita Shia Marawafidhi ni kutokujua maana yake, kwani neno Rafidhah ni msamiati wa kisiasa unaotumiwa kukiita kila kikundi kisichoikubali serekali iliyopo madarakani, sawa iwe ni ya haki au batili. Huyu hapa Muawiya bin Abu Sufiyan anawaita wafuasi wa Uthman – ambao hawakuikubali serikali na utawala wa Ali bin Abutalib – kuwa ni Marawafidhi. Na anaandika katika barua yake kwenda kwa Amru bin Aaswi huko Palestina, nayo inahusu kiapo cha utiifu, kwamba: “Ama baada ya hayo, hakika ni katika jambo la Ali, Twalha na Zubair yale yaliyokufikia. Na tayari Maruwani bin al-Hakam ameshawasili kwetu akiwa na kundi la Marawafidhi wa Basra. Na amefika Jarir bin Abdullah na kiapo cha utiifu kwa Ali, nami nimeizuia nafsi yangu dhidi yako hadi pale utakaponijia. Hivyo basi njoo nikukumbushe jambo.”104

104

Waqiat Suffin: 29.

123


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Bila shaka unaona jinsi Muawiya anavyowaita kuwa ni Marawafidhi wale waliokuja pamoja na Maruwan bin al-Hakam. Hawa walikuwa ni maadui wa Ali na wapinzani wake, na si kwa chochote isipokuwa ni kwakuwa kundi hili halikutii na kuikubali serikali iliyokuwepo madarakani wakati huo. Na kutokana na tuliyoyataja inadhihirika kwamba kila mwenye kuipinga serikali iliyopo madarakani ni Rafidhah, sawa awe ni Suni au Shia au mpagani. Na kwa maelezo hayo inajulikana kwamba yale maelezo aliyoyanukuu Ibn Mandhur katika Enklopedia yake kutoka kwa Aswimaiy si sahihi, ambapo amesema: “Walikuwa wamempa kiapo cha utiifu Zaydi bin Ali, kisha wakamwambia: „Wakane masheikh wawili (Abu Bakri na Umar) tupigane pamoja nawe.‟ Akakataa na akawaambia: „Hao wawili walikuwa wasaidizi wa babu yangu hivyo siwezi kuwakana.‟ Wakamkataa na wakamtenga mbali, na ndipo wakaitwa Marawafidhi.”105 Baada ya kuyatambua hayo sasa turejee katika kutathmini maneno aliyoyasema Dkt. Bila shaka aliyoyasema katika mhadhara huu ndio maneno mazuri zaidi na yenye manufaa zaidi kutoka katika maneno yake na mihadhara yake, na ndio matamu zaidi kuliko yote yaliyopatikana kutoka kwake katika mfululizo wa vipindi hivi. Kwani hakika kukurubiana 105

Lisanul-Arab: 7/ 157, neno Rafadha. 124


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

hakuwezi kupatikana bila kuheshimu adabu za Kiislamu alizoziashiria Allah kwa kauli yake: “Wala msiwatukane wale wanaoomba asiyekuwa Mwenyezi Mungu, wasije wakamtukana Mwenyezi Mungu kwa jeuri bila ya kujua. Kama hivyo tumewapambia kila umma vitendo vyao. Kisha marejeo yao yatakuwa kwa Mola Wao, Naye atawaambia yale waliyokuwa wakiyatenda.”106 Na sisi tunakaribisha wito wowote ule wenye nia ya kuwakurubisha pamoja Waislamu nakuleta umoja wao na kuwafanya safu moja mbele ya uzayuni na mabeberu ambao wanawafarakisha Waislamu ili wapate kuwatawala na kuwadhibiti, ambao kaulimbiu yao ni “Wafarakishe uwatawale.” Nasi tunazilaani na kuzipinga baadhi ya runinga ambazo zinavunja na kuudhuru umoja wa Waislamu kwa maelezo yake yaliyo mbali na adabu na mantiki za Uislamu. MHADHARA WA KUMI NA NANE Siku ya Kumi na Nane ya Mwezi wa Ramadhan, Mwaka 1436 A.H. Dkt. Ahmad Twayyib amesema: “Hakika suala la Uimamu kwa Suni si miongoni mwa misingi ya itikadi wala si miongoni mwa mambo yanayohusu imani au ukafiri, kwa sababu imani inajengwa juu ya 106

Sura An‟am: 108. 125


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

itikadi, ambapo ni jambo la moyoni, na si miongoni mwa mambo ya vitendo. Kinyume chake, Shia wao wanasema: Hakika Uimamu ni msingi miongoni mwa misingi ya dini, hivyo asiyeamini Uimamu imani yake ni pungufu na si Shia. Na misingi ya dini kwa Shia ni: Tauhidi, Uadilifu, Unabii, Uimamu na kuamini marejeo na ufufuo, yaani maisha baada ya kifo na pepo na moto. Shia na Suni wote wanaafikiana katika misingi yote hii isipokuwa katika jambo moja nalo ni uimamu. Wao Shia wanaitakidi kuwa ni miongoni mwa misingi ya dini, hivyo kama ambavyo ni wajibu kwa mwislamu kuamini unabii vivyo hivyo ni wajibu kwake kuamini uimamu. Nasema: Aliyoyataja Dkt. Katika kubainisha nadharia mbili yako wazi bayana. Na ili kubainisha ni ipi nafasi ya uimamu kwa Suni tunataja yale aliyoyataja Taftazaniy katika kitabu Sharhul-Maqaswid, ili ijulikane bayana kwamba jambo hilo ni moja ya matawi ya dini kwao wao.Taftazaniy anasema: “Hapana mzozo kwamba uchunguzi juu ya uimamu unaoana zaidi na elimu ya matawi ya dini, kwa sababu uimamu na kumsimika Imam mwenye kusifika kwa sifa makhususi ni miongoni mwa faradhi za kutosheleza, nazo ni mambo ya jumla yanayohusu maslahi ya kidini au ya kidunia, ambapo jambo hilo halitimii isipokuwa kwa kupatikana maslahi hayo. Na upatikanaji unaokusudiwa ni ule wa jumla bila kukusudiwa misingi yake kutoka kwa kila mmoja. Na wala haifichikani kwamba jambo hilo ni miongoni 126


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

mwa hukumu za kimatendo na si mambo ya kiitikadi.107 Sayyid Sharif katika kitabu Sharhul-Mawaqif anasema: “Uimamu si miongoni mwa misingi ya dini na itikadi, bali kwetu sisi wenyewe ni miongoni mwa matawi yanayohusu matendo ya mukalafina, kwani kwetu sisi kumsimika Imam ni wajibu juu ya umma. Na hakika tumelitaja hili katika theiolojia kwa kufuata tu wale waliokuwa kabla yetu, kwani imekuwa ni kawaida kwa wanatheiolojia kuutaja mwishoni mwa vitabu vyao kutokana na faida zilizotajwa mwanzoni mwa kitabu.”108 Nasema: Ikiwa mas‟ala ya uimamu ni miongoni mwa hukumu za matawi ya dini ambayo huenda ndani yake kukawa na tofauti nyingi, basi hakuna lawama kwa yule ambaye hataitakidi ukhalifa wa Makhalifa kwa kutegemea dalili yenye kumkinaisha, kama hali ilivyo kuhusu hukumu zote za kimatawi. Na wewe ukichunguza kitabu al-Mughniy cha Ibn Qudamah ambaye ni miongoni mwa wanazuoni wa mwanzo, au kama utasoma kitabu al-Fiqhi Alal-Madhahibil-Arbaa cha Jaziriy, ni mara chache utakuta mas‟ala kuu isiyokuwa na ikhtilafu. Na kama ilivyo kwamba amesamehewa kwa udhuru wake yule mwenye kutofautiana na mwingine katika mas‟ala hiyo, basi 107 108

Sharhul-Maqaswid: 5/ 232. Sharhul-Mawaqif: 8/ 344.

127


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

na asamehewe hivyo hivyo kwa udhuru wake yule mwenye kutofautiana na mwingine katika suala la ukhalifa wa Makhalifa. Na kutokana na tuliyoyataja inadhihirika kwamba tofauti iliyopo kuhusu uadilifu wa Maswahaba kuanzia wa kwanza wao hadi wa mwisho wao, si tofauti katika mas‟ala ya kimsingi ya kiitikadi bali ni kuhusu jambo la kihistoria ambalo upo uwezekano wa kuwepo tofauti na ikhtilafu kulihusu. Hivyo wenye kuafikiana na wenye kutofautiana wote wanajikinga chini ya hema la Uislamu, lakini wanatofautiana katika mambo ya kihistoria, na kila mmoja ana dalili yake na mashiko yake. Na mhakiki Saadudin Taftazaniy ana maneno kuhusu jambo hili, tunayataja hapa kama yalivyo: “Hakika yaliyotokea baina ya Maswahaba miongoni mwa vita na magomvi kama ilivyoandikwa katika vitabu vya historia, na ilivyoandikwa katika vitabu vya sunna vya watu waaminifu, kwa dhahiri yake yanaonesha kwamba baadhi yao walikengeuka na kuchepuka njia ya haki na wakafikia kiwango cha kutenda dhulma na uovu. Na kilichopelekea kufanya hivyo ni hikdi na kiburi, husuda na choyo, kutafuta ufalme na uongozi, na kuelemea kwenye matamanio na hawaa, kwani si kila Swahaba ni maasumu. Na wala si kila aliyekutana na Mtukufu Mtume  ana alama ya kheri. Isipokuwa ni kwamba, maulamaa kwa 128


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

sababu ya dhana yao njema waliyonayo kwa Maswahaba wa Mtume wa Allah wametaja tafsiri za matendo hayo zinazooana na matendo hayo. Na wakaona kwamba wao wamehifadhiwa dhidi ya yale yanayowajibisha mtu kuwa mpotevu na muovu, ili kulinda itikadi za Waislamu zisipotoke dhidi ya haki za Maswahaba wakubwa, na hasa Muhajirina na Answari na wale waliobashiriwa thawabu katika nyumba ya milele. Ama yale yaliyotokea baada yao ikiwemo dhulma waliyofanyiwa watu wa nyumba ya Mtume  ni mambo yaliyo dhahiri kiasi kwamba hayana nafasi ya kuficha, na ni mabaya kiasi kwamba hayana nafasi ya mgongano wa rai, kwani yanakaribia kuthibitishwa na kila kitu hata kisicho na akili na uhai. Na kwakweli yanaviliza vilivyomo ardhini na mbinguni. Yanatikisa milima na kupasua majabali. Na ubaya wake utaendelea kuwepo miezi na muda wote. Hivyo laana ya Allah imshukie aliyetenda moja kwa moja, au aliyeridhia, au aliyejituma kufanikisha hayo. Na adhabu ya Akhera ni kali zaidi na ni ya kudumu zaidi.”109 Ndiyo, nadharia ya Uimamu kwa Shia Imamiya imejengeka juu ya msingi wa kwamba wenyewe ni 109

Sharhul-Maqaswid: 5/ 310 – 311.

129


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

cheo cha kimungu na si cha kijamii,110 na dalili juu ya hilo zimetajwa katika vitabu vya theiolojia ikiwa ni pamoja na kubainisha vyanzo vyake. Na kwakuwa lengo ni kufupisha uchambuzi wa maneno ya Dkt. Ahmad Twayyib, tutatosheka na haya tuliyoyataja, na yeyote anayetaka ufafanuzi kwa undani basi arejee kwenye vitabu vikubwa vya theiolojia vya maulamaa wa Uislamu.111 Na mwishoni ni lazima tuliweke sawa jambo moja, nalo ni kwamba misingi ya dini kwa Shia Imamiya inakomea katika mambo matatu: Tauhidi, Unabii na kuamini marejeo. Yeyote atakayeitakidi hayo matatu ni mwislamu, na ni haramu damu yake na mali yake isipokuwa kwa sababu za kisharia. Ama kuitakidi uadilifu na uimamu kwenyewe ni miongoni mwa misingi ya madhehebu, kwa maana kwamba, mtu hawi Shia isipokuwa pale atakapoitakidi mambo hayo mawili, na kwamba Allah kiakili ni mwadilifu hadhulumu, na kwamba uongozi halali wa kisharia baada ya kufariki Mtukufu Mtume , aliuweka Mtume  kwa umakhususi mikononi mwa Ali na Mawasii wake. Asiyeitakidi hayo haitwi kuwa ni Shia, lakini ni mwislamu na hukumu za Uislamu 110

Yaani Uimamu unatolewa na Mungu na si jamii, hivyo Imam wa umma anasimikwa na kuteuliwa na Mungu na si jamii – Mtarjumi. 111 Buhuthu Fil-Milal Wanahli: 1/ 456. Muhadharat Fil-Ilahiyat: 325 – 336.

130


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

zinamhusu. Ukitaka ufafanuzi zaidi rejea mahala pake. MHADHARA WA KUMI NA TISA Siku ya Kumi na Tisa ya Mwezi wa Ramadhan, Mwaka 1436 A.H. Dkt. Ahmad Twayyib alisema: “Mkutano wa Saqifa ni mfano wa mwanzo kabisa wa demokrasia ya Waislamu.” Na akasema: “Hakika uimamu ni dhana ya kimungu kwa Shia Imamiya, wakati ambapo kwa Suni ni dhana iliyo chini ya hukumu za wanadamu. Kwa sababu Suni wanaona kwamba, Mtukufu Mtume  hakumteua yeyote baada yake, bali aliacha jambo hilo kwa Waislamu wawe huru kumteua yeyote. Kama ilivyotokea mkusanyiko wa Maswahaba huko Saqifa, ambapo walimchagua Abu Bakri kuwa Khalifa wa Waislamu kwa njia ya demokrasia. Na jambo hili liko kinyume na ilivyo kwa Shia ambao wanasema: „Hakika Mtukufu Mtume  aliainisha Imam baada yake, naye ni Imam Ali bin Abutalib .‟ Na kwamba mas‟ala hii haimo mikononi mwa umma wala katika utashi wa Waislamu.” Kisha akaendelea kusema kwamba, Khalifa kwa Suni si maasumu, lakini ni maasumu kwa Shia. Kisha akasema: “Hakika uimamu kwa Shia ni msingi miongoni mwa misingi ya dini, na si jambo131


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

lililoachwa kwenye mamlaka na hiyari ya watu. Na asiyeitakidi hivyo basi si Shia, bali hawi mwislamu kwao wao. Ama ukhalifa kwa Suni si miongoni mwa misingi ya dini, bali ni miongoni mwa mas‟ala ya kielimu, kwani kwakuwa kuna hukumu zinazohitaji Khalifa au mtawala ndio maana tumesema ni wajibu umma kumteua Khalifa atakayeusimamishia hukumu na kuuhifadhia sharia ya Uislamu.” Dkt. Amesisitiza kwamba uchaguzi wa Khalifa wa kwanza huko Saqifa Bani Saad unawasilisha demokrasia iliyokuwepo katika zama hizo. Sisi hapa tutataja mambo yaliyojiri katika Saqifa ili ijulikane je kweli ulikuwa ni uchaguzi sahihi na wa kiakili, na kama ilivyo istilahi ya Dkt. Je ulikuwa kweli wa demokrasia au ulikuwa wa kushitukiza? Na wala haiwezekani kuainisha moja kati ya pande mbili bila kusimulia kisa kama kilivyo katika vyanzo na rejea bila kubadili, kisha kuhukumu na kuchambua matukio kama yalivyotajwa. 1. Mtume wa Allah  alifariki wakati Abu Bakri akiwa Sun‟hu, lakini Umar alikuwepo, akasimama na kusema: “Hakika watu miongoni mwa wanafiki wanadai kwamba Mtume wa Allah amefariki. Wallahi hajakufa lakini amekwenda kwa Mola Wake kama alivyokwenda Musa bin Imran. Wallahi Mtume wa Allah atarejea na ataikata mikono na 132


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

miguu ya watu hawa wanaodai kuwa Mtume wa Allah amekufa.”112 2. Zilipomfikia habari Abu Bakri alikuja hadi kwenye mlango wa msikiti, wakati huo Umar alikuwa akiwasemesha watu, akaingia kwa Mtume wa Allah, wakati huo Mtume wa Allah alikuwa kalazwa pembezoni mwa nyumba, akaenda akaufunua uso wake akautazama na kuubusu, kisha akaufunika, akasema: „Ewe Umar kwakweli Mtume amekufa. Enyi watu yeyote aliyekuwa akimwabudu Muhammad basi atambue kwamba hakika Muhammad amekufa. Na yeyote aliyekuwa akimwabudu Allah basi atambue kwamba hakika Allaha angali hai hafi.” Kisha akasoma Aya hii: “Hakuwa Muhammad ila ni Mtume; wamekwisha pita Mitume kabla yake. Je, akifa au akiuliwa mtarudi nyuma? Na atakayerudi nyuma hatamdhuru kitu Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu atawalipa wenye kushukuru.”113 Ndipo Umar akasema: “Nimetambua kwamba hakika Mtume wa Allah amekufa.”114 3. Alipofariki Mtume wa Allah  kundi miongoni mwa Answari walijikusanya kwa Saad bin Ubadah huko Saqifa. Wakati huo Abu Bakri na Umar 112 113 114

Taarikh Tabar: 3/ 200. Sura Imran: 144. Taarikh Tabar: 3/ 200.

133


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

walikuwa nyumbani kwa Mtume  wakitafakari namna ya kumwandaa Mtukufu Mtume  kama walivyokuwa Muhajirina wengine. Na mara walifika watu wawili miongoni mwa Answari, nao ni Uwaybu bin Saidah na Muinu bin Udiy,115 wakasema: „Kundi miongoni mwa Answari wako pamoja na Saad bin Ubadah huko Saqifa Bani Saidah wamemzunguka, hivyo kama mna haja ya kuwa viongozi wa watu harakisheni kabla jambo halijakuwa kubwa.‟ Wakati huo Mtume wa Allah alikuwa nyumbani kwake bado hawajamaliza kumwandaa, ndugu zake wamefunga mlango. Umar anasema: Nikamwambia Abu Bakri: „Twende zetu kwa ndugu zetu hawa kutoka miongoni mwa Answari, ili tukajue wana jambo gani.‟116 4. Wao wawili wakaingia Saqifa wakiwa pamoja na Abu Ubaydah, wakamkuta Saad bin Ubadah akihutubia akisema: “Enyi kundi la Answari! Ninyi mna sifa na ubora asiyekuwanao yeyote miongoni mwa Warabu. Hakika Muhammad  alikaa katika jamii ya watu wake karibuni miaka kumi akiwalingania, hawakumwamini isipokuwa wachache. Hawakuwa na uwezo wa kumlinda wala wa kuipa dini yake nguvu wala wa kumuondolea madhara. Mpaka pale Allah alipotaka kuwapa 115 116

Taarikh Tabar: 2/ 335. As-Siratun-Nabawiyyah: 2/ 656.

134


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

ubora, aliwaletea ninyi heshima na akawaruzuku imani ya kumwamini Yeye na Mtume Wake, na kumlinda yeye na Maswahaba zake, na kumpa nguvu yeye na dini yake, na kupigana jihadi dhidi ya adui yake. Hivyo ninyi mkawa wakali mno kwa adui yake kuliko watu wote, mpaka Warabu wakafuata amri ya Allah kwa kupenda na kwa kutokupenda. Warabu wakasogea kwa Mtume wake kwa msaada wa panga zenu, na Allah amemfisha ilihali yuko radhi nanyi.„Lihodhini jambo hili mbali na watu wengine.‟” Wote walimjibu kuwa umefanya rai muwafaka na umesema kauli sahihi, hatukiuki rai yako, tutakutawalisha jambo hili, hakika wewe unafaa na unakubalika na Waumini.117 5. Kisha Abu Bakri alihutubia na kusema: “Ninyi enyi kundi la Maanswari ni watu ambao ubora wao katika dini haukanushwi wala utanguliaji wao katika Uislamu. Allah amewaridhia muwe watetezi wa dini Yake na Mtume Wake, hivyo akafanya kwenu kuwa ndio sehemu ya kuhamia kwake. Baada ya Muhajirina wa mwanzo hana yoyote daraja mliyonayo kwetu, kwa hiyo sisi ndio maamiri na ninyi ni mawaziri. Hamtaachwa katika ushauri wala hayatapitishwa mambo bila ninyi.”118 117 118

Al-Kamil Fii Taarikh: 2/ 327. Taarikh Tabari: 2/ 241 – 242. Al-Kamil Fii Taarikh: 2/ 329. Taarikh Tabari: 2/ 242.

135


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

6. Kisha akaongeza: “Kama jambo hili watalifikia Makhazraji basi Maausi hawatawaachia. Na kama watalifikia Maausi basi Makhazraji hawatawaachia (kati yao kulikuwa na mauaji yasiyosahaulika wala vidonda vyake kutibika). Na kama yeyote miongoni mwenu ataasi basi atambue kuwa atakuwa ameketi kati ya ndevu mbili za simba, atabanwa na Muhajirina na kujeruhiwa na Answari.”119 7. Hapo Hubab bin al-Mundhir alisimama baina ya kundi na akasema: „Enyi Answar shikilieni jambo lenu kwa kuwa watu wako kwenye kivuli chenu wala hatothubutu mwenye kuthubutu kwenda kinyume na ninyi, na wala hatafuata isipokuwa rai yenu. Ninyi mna nguvu, idadi kubwa, uwezo na pigo kali. Na hakika watu wanatazama mtafanya nini. Wala msitofautiane lisije likawaharibikia jambo lenu. Na endapo hawa watakataa isipokuwa kwa mliyoyasikia basi kwetu kutoke Amiri na kwaoAmiri.‟ Kisha akasema: „Mimi ndio kigogo cha kurejewa na shina la kuogopwa. Mimi ni simba dume katika kichaka cha simba.Wallahi mkipenda tutalirejesha upya kama lilivyokuwa!‟120 8. Umar akasimama na kusema: “„Hilo liko mbali sana! Panga mbili haziwezi kuwa katika ala moja. Wallahi Warabu hawatoridhia kukufanyeni muwe 119 120

Al-Bayan Watabyiin: 4/ 10. Al-Kamil Fii Taarikh: 2/ 329.

136


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

maamiri hali Nabii wao anatoka kwa asiyekuwa ninyi, lakini Warabu hawakatai kumtawalisha jambo lao mtu ambaye unabii upo katika wao.Na sisi tuna hoja na nguvu ya wazi kwa mwenye kuamini. Nani atagombania na sisi mamlaka ya Muhammad ilihali sisi ni wapenzi wake na jamaa zake!?” Umar akajibu vitisho vya Hubab pale aliposema: “Hivyo basi Mwenyezi Mungu atakuuwa.” Yeye akasema: “Bali atakuuwa wewe.”121 9. Mjadala ulipotimia baina ya makundi mawili, na hatimaye kimya kikatawala, hakuna aliyetamka isipokuwa Bashir bin Saad al-Khazrajiy, ambaye ni binamu wa Saad bin Ubadah, alipohisi kwamba Answari wanaelemea kwa Saad bin Ubadah, naye alikuwa na uadui na chuki naye na wala hakuwa akiridhia uongozi wake, akasema: “Enyi kundi la Answar! Hakika Muhammad anatokana na Makurayshi, na watu wake ndio wenye haki naye zaidi. Wallahi, Mwenyezi Mungu asinione nikishindana nao katika jambo hili kabisa, hivyo basi mcheni Mwenyezi Mungu wala msiwapinge wala kushindana nao.” 10. Katika hali hii Abu Bakri alitumia fursa na akasema: “Huyu hapa Umar, na huyu hapa Abu Ubaidah, mumtakaye kati ya hao wawili mpeni kiapo cha utiifu.” Wao wawili wakasema: 121

Al-Kamil Fii Taarikh: 2/ 330. Taarikh Tabari: 2/ 241 – 243.

137


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

“Wallahi hatuwezi kulitwaa jambo hili juu yako. nyoosha mkono wako tukupe kiapo cha utiifu.” Walipokwenda ili kumpa kiapo cha utiifu mara aliwatangulia Bashir bin Saad, akampa kiapo cha utiifu. Hapo Habab bin al-Mundhir akamwita kwa kumwambia: “Umemhusudu mtoto wa ammi yako asiupate uongozi.” 11. Watu wa kabila la Aus walipoona alilofanya Bashiru bin Saad na wanaloitia Makuraishi na wanalolitaka watu wa kabila la Khazraji, ambalo ni kumfanya Saad bin Ubadah awe Kiongozi wao, waliambiana wao kwa wao, akiwemo Usaid bin Hudhwayru, naye alikuwa ni mmoja wa machifu: “Wallahi endapo mtawatawalisha juu yenu kabila la Khazraj hata mara moja, hilo litabaki kuwa ni ubora wao juu yenu, na wala hawatowafanyieni na nyinyi muwe na hisa pamoja nao abadan.Hivyo basi simameni mumpe kiapo cha utiifu Abu Bakri.” Ndipo walimwendea Abu Bakri na wakampa kiapo cha utiifu. Saad bin Ubadah na Khazraji wakaharibikiwa na hatimaye kulikosa jambo walilokusanyikia.122 12. Basi watu (Awsi) kutoka pande zote wakaenda kumpa kiapo cha utiifu Abu Bakri, na walikaribia kumkanyaga Saad bin Ubadah. Watu miongoni 122

Taarikh Tabari: 2/ 241 – 243.

138


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

mwa wafuasi wa Saad wakasema: “Jihadharini msimkanyage Saad.” Umar akasema: “Muuweni! Mwenyezi Mungu amuuwe.” Halafu alimsimamia kichwani na akasema: “Nilikusudia nikukanyage mpaka mwili wako upondeke.” Qays bin Saad akazishika ndevu za Umar na akasema: “Wallahi lau ungemnyofoa hata unywele mmoja basi haungerejea na kitu kinywani mwako (ningekung‟oa meno yote).” Abu Bakri akasema: “Polepole, ewe Umar! Upole hapa wafaa mno.”Ndipo Umar akamwacha. Saad akasema: “Ama wallahi lau ningekuwa na nguvu ambazo kwazo ningeweza kuinuka, basi ungesikia kutoka kwangu katika nchi na vichochoro vyake, ngurumo ambayo ingekuzuia wewe na swahiba zako.Na wallahi ningekukutanisha na kaumu ambao wewe kwao ni mfuasi na si kiongozi. Nibebeni kunitoa mahali hapa.”Wakambeba na kumwingiza nyumbani mwake, akaachwa siku kadhaa kisha akapelekewa ujumbe aende, akasema: “Wallahi hata kama majini na watu wangekusanyika katika kukupeni ninyi kiapo cha utiifu, kamwe nisingekupeni kiapo cha utiifumpaka nifikishwe kwa Mola Wangu na nijue ni ipi hesabu yangu.” Umar akasema: “Msimuache mpaka atoe kiapo cha utiifu.” Bashir bin Saad akasema: “Hakika amegoma na kukataa, na wala hatawapeni ninyi kiapo 139


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

cha utiifu mpaka mumuuwe, na hatauwawa mpaka auwawe pamoja naye mwanawe, watu wa nyumbani kwake na jamaa zake.” Hivyo wakamuacha.123 13. Likaja kabila la Aslamu likatoa kiapo cha utiifu, na kupitia wao Abu Bakri akapata nguvu.124 Zahri anasema: “Alibaki Ali, Banu Hashim na Zubair miezi sita bila kumpa kiapo cha utiifu Abu Bakri, mpaka alipofariki Fatima radhi za Allah ziwe juu yake.125 Hii ndio sura fupi na muhtasari wa matukio ya Saqifa, nimeyanukuu kutoka kwenye vyanzo vyake bila kubadili hata kidogo. Hebu sasa turejee kwenye maneno ya Dkt. Je utoaji huu wa kiapo cha utiifu ulikuwa ni demokrasia au jambo la kushtukiza na la ghafla? Hebu turejee kwenye yale tuliyoandika, uchambuzi kuhusu matukio ya Saqifa. 1. Ilikuwaje Umar akashindwa kutambua jambo hili lililo bayana ilihali Mtukufu Mtume  amelazwa ndani ya nyumba yake?! Na ilikuwaje akadai kuwa ametoweka kama alivyotoweka Musa  na atarejea baadaye?! Na la ajabu kushinda yote hayo ni kwamba 123

Taarikh Tabari: 2/ 244. Al-Kamil Fii Taarikh: 2/ 331. 125 Al-Kamil Fii Taarikh: 2/ 331. 124

140


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

yeye alijirudi haraka aliposikia Aya aliyoisoma Abu Bakri, namaanisha kauli ya Allah: “Hakuwa Muhammad ila ni Mtume; wamekwishapita Mitume kabla yake. Je, akifa au akiuliwa mtarudi nyuma? Na atakayerudi nyuma hatamdhuru kitu Mwenyezi Mungu naMwenyezi Mungu atawalipa wenye kushukuru.”126 Na nidhanialo mimi, kama linavyojulishwa na ushahidi wa kimazingira, ni kwamba aliwasilisha fikra hii ili aweze kuwatoa watu kwenye lile walilokuwa wakifikiri, yaani ni nani atakayechukua nafasi ya Mtukufu Mtume . Alifanya hivyo ili azigeuzie fikra zao katika upande mwingine, ili usitokee utoaji kiapo cha utiifukwa yeyote kabla hajafika swahiba wake.Na hakukuwa na mtu ambaye fikra za watu zilikuwa zimemzunguka isipokuwa Ali, hiyo ni kutokana na maandiko yanayojulisha hilo kama tunavyoitakidi, au kwa sababu yeye ndiye aliye bora zaidi kuliko watu wote. Kiasi kwamba Muhajirina wote na Answari wengi walikuwa hawana shaka kwamba Ali ndiye mwenye jambo hili baada ya Mtume wa Allah.127 2. Ikiwa uchaguzi wa kumchagua Khalifa ni kwa njia ya mashauriano kwa kukusanyika watu wenye maamuzi, basi ni kwamba sharti hili halikutimia huko Saqifa Bani Saidah. Kama wangetaka kufanya 126

Sura Imran: 144. Sharhu Nahjul-Balaghah ya Ib Abil-Hadid: 6/ 21. Saqifa 85 – 86. 127

141


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

uchaguzi sahihi wa kumchagua Khalifa ilikuwa ni wajibu kwao kuwaeleza Muhajirina wote, na wa kwanza wao ni Banu Hashim, yale yanayoendea Saqifa Bani Saidah ili wakusanyike wote na washauriane siku kadhaa ili wamchague yule afaaye zaidi. Wakati ambapo tunaona kwamba Masheikh wawili (Abu Bakri na Umar) hawakumweleza yeyote miongoni mwa Muhajirina ila Abu Ubaydah au mtu wa nne. Na hili linajulisha kuwa msimamo wao huu ulikuwa ni wa kutumia fursa, kwani kama Banu Hashim akiwemo Ali bin Abutalib wangekuwepo kwenye baraza la mashauriano, basi jambo hili lisingetimia kwa haraka hii katika siku moja au saa moja au saa mbili kwa kumchagua Abu Bakri. 3. Hakika Khalifa katika sharia ya Uislamu ana masharti na vigezo, hivyo ilikuwa ni lazima watu hawa wachunguze uwepo wa sifa hizo kwa mtu yeyote miongoni mwa Muhajirina na Answari, ili waweze kumchagua yule aliye mjuzi zaidi wa Kitabu cha Allah na Sunna ya Mtume wake. Yule mwenye uwezo zaidi wa kuendesha mambo, na aliye na sifa nyingine miongoni mwa masharti hayo. Lakini sisi tunaona waliokusanyika Saqifa waliacha vigezo hivi na wakakimbilia kwenye vigezo vya kijahiliya na ukabila. Maanswari wao wakaegemea kwenye madai ya kwamba wao ndio waliomnusuru Mtukufu Mtume , wakawapa hifadhi Muhajirina na kupigana na Mushrikina. Na Masheikh wawili pamoja na Abu Ubaydah wao wakategemea dai la kwamba Mtukufu 142


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Mtume  ni kutoka miongoni mwao. Na vigezo vyote viwili haviwajibishi Khalifa kutoka miongoni mwao. Kwani kuinusuru kwao dini hakujulishi kwamba mgombea wao ana vigezo, kama ambavyo pia Mtukufu Mtume kutoka miongoni mwao hakulazimu hilo. 4. Makabila yote mawili, Awsi na Khazraji yalikuwa yakishindana na kuhasimiana tangu zamani. Na siku ya Buathu ilikuwa ndio siku mbaya zaidi kwa mapigano kati yao, lakini Mtukufu Mtume  aliwafanya ndugu na akawaamuru kusahau yaliyopita. Lakini la kusikitisha ni kwamba, unamuona Khalifa Umar akiashiria ule ushindani wa kishetani uliokuwepo baina yao, anasema: “Kama jambo hili watalifikia Makhazraji basi Maausi hawatawaachia. Na kama watalifikia Maausi basi Makhazraji hawatawaachia (kati yao kuliwa na mauaji yasiyosahaulika wala vidonda vyake kutibika). Na kama yeyote miongoni mwenu ataasi basi atambue kuwa atakuwa ameketi kati ya ndevu mbili za simba, atabanwa na Muhajirina na kujeruhiwa na Answari.”128 Kwa maneno yake haya yeye alifufua iktilafu na mizozo ya kijahiliya iliyokuwa imezikwa, maneno yake haya yakawa sababu ya kuondoka umoja baina ya Answari. Pamoja na kwamba Mtukufu Mtume  aliyafanya ndugu makabila haya 128

Al-Bayan Watibayan: 4/ 10.

143


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

mawili na akawaamuru kusahau tofauti walizokuwanazo huko nyuma, lakini mabaki ya ushindani na mvutano yalikuwepo. Na ushahidi juu ya hilo ni yale maelezo aliyoyapokea Bukhari kutoka kwa Bibi Aisha kuhusu uwongo aliozushiwa, anasema: “Siku hiyo hiyo Mtume wa Allah alisimama akaomba apumzishwe na Abdullah bin Ubayya akiwa juu ya mimbari, akasema: „Enyi kundi la Waislamu! Ni nani atakayenipumzisha na mtu huyu, yamenifikia kutoka kwake maudhi yake kuhusu mke wangu. Wallahi sijui lolote juu ya mke wangu isipokuwa kheri. Na wamemtaja mwanamume ambaye sijui lolote juu yake isipokuwa kheri, na wala huwa haingii nyumbani kwangu isipokuwa pamoja nami.‟ Akasimama Saad bin Muadh ndugu wa Bani Abdul-Ash‟hal, akasema: „Mimi hapa ewe Mtume wa Allah nitakupumzisha naye, ikiwa mtu huyo ni miongoni mwa Awsi basi nitaikata shingo yake. Na kama ni miongoni mwa ndugu zetu Khazraj utatuamrisha cha kufanya nasi tutatekeleza amri yako.‟ Akasimama Saad bin Ubadah chifu wa Khazraj, na kabla ya hapo alikuwa ni mtu mwema lakini aliyeelemewa na hasira za kijinga, akasema kumwambia Saad: „Wallahi umeongopa, hutamuuwa wala huna uwezo wa kumuuwa. Na kama angekuwa ni kutoka katika kabila lako usingependa auwawe.‟ Akasimama Asidu bin Hudhayru ambaye ni binamu wa Saad, akasema kumwambia Saad bin Ubadah: „Wallahi umeongopa nitamuuwa. Hakika wewe ni mnafiki unajadili kwa niaba ya wanafiki.” 144


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Ukazuka mzozo baina ya makabila mawili Awsi na Khazraji mpaka wakakaribia kupigana, wakati huo Mtume wa Allah alikuwa juu ya mimbari, Mtume wa Allah  aliendelea kuwatuliza mpaka wakanyamaza naye akanyamaza.129 5. Tunamuona Abu Bakri anawatanguliza watu wawili kwa ajili ya kupewa kiapo cha utiifu, anawaambia wote wawili Umar na Abu Ubydah: Nyoosha mkono wako nikupe kiapo cha utiifu. Na wao wanamrudishia jambo hilo yeye wanamwambia: Wewe ndiye unayefaa zaidi. Yote hayo yanajulisha uwepo wa itifaki na makubaliano baina ya watu watatu hawa ili hatimaye jambo liishie kwa Abu Bakri. 6. Je haikuwa ni lazima kwa Khalifa kumtafuta ndani ya Saqifa na nje yake, yule anayefaa zaidi kwa ajili ya ukhalifa, badala ya kuwapendekeza hawa wawili? 7. Hakika utoaji wa kiapo cha utiifu uliofanywa na Awsi haukuwa umejengeka juu ya msingi wa kwamba Abu Bakri ndiye mwenye vigezo vinavyotakiwa ili mtu awe Khalifa. Bali wao walimpa kiapo cha utiifu kwa asili kwamba, ukhalifa huo usilifikie kabila lenye upinzani na wao, jambo hilo likawa ni ubora wao juu yao. 129

Sahih Bukhar: 5/ 101.

145


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

8. Hakika baraza la mashauriano hutawaliwa na utulivu na kusikiliza hoja ya upande wa pili, kisha hatimaye rai huchukuliwa kwa uaminifu maalumu. Sharti hili hatulioni angalau kwa uchache wake katika baraza la Saqifa. Bali baraza hilo lilikuwa kama baraza la ubabe, ambapo Saad bin Ubadah anazikamata ndevu za Umar na anasema aliyoyasema. Naye Umar anamjibu kama ilivyotangulia. Mpaka ikafikia kumkanyaga Saad bin Ubadah, yule mzee ambaye aliuhudumia Uislamu kuanzia wakati alipoamini. Inakuwaje Dkt. Anausifu uchaguzi huu kuwa ni uchaguzi wa demokrasia, wakati aliyekuwa rafiki wa Khalifa tangu katika ujana wake mpaka uzeeni, anausifu uchaguzi huu kuwa ulikuwa wa kushtukiza na ghafla na kwamba Allah aliwakinga Waislamu na shari yake?! Bukhari amepokea ndani ya Sahih yake kutoka kwa Ibn Abbas, kutoka kwa Umar kwamba alisema: "Kwa hakika nimepata habari kwamba kuna asemaye miongoni mwenu kuwa, Wallahi lau Umar atakufa nitampa kiapo cha utiifu fulani, basi na asijidanganye mmoja wenu kwa kusema kuwa kiapo cha utiifu alichopewaAbu Bakri japo kilikuwa cha kushitukiza lakini kilitimia. Ndiyo kilikuwa hivyo lakini Mwenyezi Mungu aliikinga shari yake."130 130

Sahih Bukhar: 1712, namba 6830, Mlango unaozungumzia kumpopoa mawe mjamzito iwapo atazini.

146


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Na bila shaka alisadikisha kwamba: “Kiapo cha utiifu alichopewa Abu Bakri kilikuwa cha kushitukiza.” Kwani uchaguzi ulifanyika kwa haraka mno kiasi kwamba haikubaki nafasi ya mwenye kutafakari kuweza kutafakari maudhui husika, wala ya mpingaji kutoa hoja yake. Ulikuwa ni ghafla juu ya ghafla, huku hisia za uadui kwa Awsi zilizochochewa na upande wa Abu Bakri zilikuwa na mchango katika kumchagua Khalifa. Hivyo haiwezekani kwa mchunguzi kuifanya ni kigezo kwa ajili ya kizazi kijacho, aina hii ya uchaguzi. Kwani tukio lote kuanzia mwanzo wake hadi mwisho wake lilifanyika bila Ali kujua wala Bani Hashimu. Nafasi yao ilipuuzwa kana kwamba hawakuwa ni miongoni mwa Waislamu, au hawakuwa miongoni mwa waliokuwepo Madina isipokuwa baada ya kukamilika kila kitu.131 Je kulikuwa na kizuizi chochote cha kisharia au kiakili au kijamii kilichozuia kucheleweshwa zoezi la kutoa kiapo cha utiifu, mpaka pale watakapomaliza kumwandaa Mtume wa Allah?! Kwanini basi wasikabidhi mamlaka ya kulinda amani chini ya uongozi wa jeshi kwa muda, mpaka pale litakapotimia jambo la ukhalifa? Je kiwango hiki cha subirahakikuwa kinafaa zaidi kwa hawa waliofiwa?! Ambao wao ndio amana ya Mtukufu Mtume  iliyoachwa kwao na wawakilishi wake kwao. 131

Saqifa: 108.

147


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Hakika yaliyowapata watu wa nyumba ya Mtume  baada ya Khalifa kuchaguliwa, na yaliyompata binamu wa Mtume wa Allah na pande la nyama yake, hebu acha tuizuie kalamu isitaje matukio hayo machungu. Na kuhusu machungu yake inatutosha kauli ya mshari wa Mto Nile, Hafidh Ibrahim aliposema katika shairi lake: “Na kauli aliyoisema Umar kumwambia Ali, ni tukufu kwa aliyeisikia, lakini ni nzito kwa aliyeitoa: „Nitaichoma nyumba yako, sintakuachia kama hautatoa kiapo cha utiifu, hata kama binti wa Mustafa atakuwemo humo.‟ Hakuwa zaidi ya baba Hafsa aliyesema kauli hiyo, mbele ya Jemedari wa Adnani na muhami wake.” Kiapo cha utiifu kinachohitaji vitisho vya kuchoma nyumba na waliomo humo, je kinahesabiwa kuwa ni kiapo cha kisharia cha Kiislamu?! Kama hiki ndio kiapo cha utiifu cha kiislamu basi Uislamu umekwisha. Ni demokrasia gani hii ambayo wapinzani wanatishiwa kuuwawa, kupelekwa uhamishoni na kuwachoma moto wao na nyumba zao?! 9. Tunahitimisha jibu letu kwa maneno ya Imam Ali , pale zilipomfikia habari za Saqifa, baada ya kufariki kwa Mtume wa Allah , alisema : “Wamesema nini Maanswari (wenyeji wa Mji wa Madina)?” Wakasema: “Wamesema: „Sisi tuwe na 148


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

kiongozi wetu na nyinyi muwe na kiongozi wenu.‟ Akasema (a.s): “Je hamkuwatolea hoja kwamba Mtume  ameusia atendewe mema aliye mwema miongoni mwao na asamehewe muovu wao?” Wakasema: “Katika hili kuna hoja gani dhidi yao!”Akasema : “Lau Uimamu (uongozi) ungekuwa katika wao, wasingeusiwa.” Kisha akasema : “Makuraishi walisema nini?” Wakasema: “Wametoa hoja kuwa wao ni mti wa Mtume .” Akasema : “Wameutolea hoja mti na wamelipoteza tunda.”132 Na Imam Ali  ana maneno mengine kuhusu hilo, alisema : “Nawashangaa, Ukhalifa unapatikana kwa usuhuba, na wala haupatikani kwa usuhuba na ukaribu?!” Na limepokewa shairi lake likiwa katika maana hii: “Ikiwa ni kwa mashauriano umemiliki jambo lao, limetimiaje hili wakati watoa ushauri hawakuwepo? Na ikiwa ni kwa ukaribu umemtolea hoja hasimu kutoka kwao. Basi asiyekuwa wewe ndiye bora zaidi kwa Nabii na mwenye ukaribu zaidi naye.”133 Kutokana na tuliyoyataja msomaji mwerevu anaweza kufikia hitimisho kwamba, kitendo cha watu hawa wakati wa kumchagua Khalifa hakikutegemea kanuni 132 133

Nahjul-Balaghah: Hotuba ya 67. Nahjul-Balaghah: 502, Sehemu ya hekima, namba 190.

149


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

ya Uislamu, na wala hakikuwa isipokuwa ni maamuzi ya haraka yaliyoongozwa na hisia binafsi kuanzia mwanzo hadi mwisho. Na vigezo vilivyotegemewa katika kumchagua Khalifa vilikuwa ni vigezo vya kijahiliya, na kwa ajili hiyo vinaoana na kilichosemwa na kauli ya Allah Mtukuka: “Hakuwa Muhammad ila ni Mtume; wamekwishapita Mitume kabla yake. Je, akifa au akiuliwa mtarudi nyuma? Na atakayerudi nyuma hatamdhuru kitu Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu atawalipa wenye kushukuru.�134 MHADHARA WA ISHIRINI Siku ya Ishirini ya Mwezi wa Ramadhan, Mwaka 1436 A.H. Dkt. Ahmad Twayyib katika mazungumzo yake ya siku hii, ambayo yalikuwa yakirushwa katika runinga ya Misri kabla ya kuftari, alitaja kwamba: 1. Miongoni mwa tofauti kubwa inayowatofautisha Suni na Shia ni kwamba, kwa Suni Maimamu kumi na wawili ni wanadamu, wanakosea na kupatia. Wakati ambapo wao ni maasumu kwa Shia. 2. Kwa Shia Maimamu hao ni wabora kushinda hata Manabii na Mitume isipokuwa Mtukufu Mtume 134

Sura Imran: 144.

150


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

. Na hili ni kinyume na itikadi ya Suni ambao wao wanaitakidi kwamba Manabii na Mitume ni maasumu na ni wabora kushinda wanadamu wengine. Kwa sababu wao wanafunuliwa wahyi kutoka kwa Allah. Katika mhadhara huu Mufti wa Azhar alisisitiza mambo mawili: Kwanza: Umaasumu wa Maimamu kumi na wawili. Pili kwamba hao Maimamu ni wabora kushinda hata Manabii na Mitume . Ama kuhusu jambo la kwanza, katika kuthibiti kwa jambo hilo zinatosha zile hadithi sahihi zilizothibiti kutoka kwa Mtume wa Allah , miongoni mwazo ni: 1. Hadithi ya Vizito viwili: Mtukufu Mtume  alisema: “Enyi watu! Hakika si muda mrefu nitaitwa (na Mola Wangu) nami nitajibu.Hakika mimi nimeacha kati yenu vizito viwili, kimoja ni kikubwa zaidi kuliko kingine: Kitabu cha Allah na kizazi changu. Hivyo basi angalieni jinsi mtakavyoishi navyo baada yangu. Hakika hivyo viwili havitatengana mpaka vitakaponifikia kwenye hodhi.” Na hakika hadithi hii imethibiti kwa tawaturi katika vyanzo vya makundi yote mawili (Shia na Suni).135 Hakika Mtume wa Allah  katika hadithi hii ya vizito viwili ameeleza uwepo wa mshikamano baina 135

Al-Mustadrak Alas-Sahihayn: 3/ 109. Ameiandika al-Hakim kutoka kwa Zaydi bin Arqam.

151


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

ya kizazi chake watu wa nyumbani kwake na Kitabu Kitukufu. Na amewausia Waislamu kushikamana navyo vyote viwili pamoja, ili waepuke kutumbukia katika upotovu. Na kwa kauli yake “Hakika hivyo viwili havitatengana mpaka vitakaponifikia kwenye hodhi” akaashiria kwamba vyenyewe ni sawa na makhalifa wake wawili wasioachana. Na hili linapelekea Ahlulbayti  kuwa sawa na Kitabu katika upande wa uwepo na hoja.La sivyo, italazimu kiwepo kimoja bila kuwepo kingine kati ya vitu viwili visivyotengana. Na kwa ibara nyingine ni kwamba, hadithi hiyo inajulisha kuwa katika kila zama lazima kuwepo hoja maasumu mwenye kuaminika ambaye watu wana yakini na usahihi wa kauli yake. Na linalounga mkono maelezo tuliyoyataja ni kwamba, mwishoni mwa baadhi ya riwaya imetajwa kwamba baada ya Mtume  kutaja kwamba ameacha Kitabu cha Mola Wake na kizazi chake watu wa nyumbani kwake, aliukamata mkono wa Ali  akaunyanyua juu, akasema: “Huyu Ali yuko pamoja na Qur‟ani, na Qur‟ani iko pamoja na Ali, hawatatengana mpaka watakaponifikia katika hodhi.”136 Na suala la Qur‟ani kusalimika na makosa ni jambo lenye kukubalika halina shaka, hivyo ni lazima kusiwe na shaka pia juu ya umaasumu wa yule ambaye hatatengana kamwe na Qur‟ani. 136

As-Sawaiqul-Muhriqah: 124.

152


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Hadithi ya Safina:Kuna riwaya nyingi kutoka kwa Mtukufu Mtume  ambazo humo amewa-fananisha Ahlulbayti na safina ya Nuhu , akasema; "Bila shaka mfano wa watu wa nyumba yangu kwenu ninyi ni mfano wa Safina ya Nuh kwa watu wake, yeyote mwenye kuipanda ataokoka na mwenye kuipa mgongo atazama.137 Na hakika mfano wa watu wa nyumba yangu kwenu ninyi ni mfano wa mlango wa msamaha kwa Wana wa Israil, aliyeingia kupitia mlango huo alisamehewa."138 Sayyid Sharafuddin Aamiliy anasema: “Na wewe unajua kwamba makusudio ya kuwashabihisha wao na safina ya Nuhu , ni kwamba atakayerejea kwao katika dini na akachukua matawi yake na misingi yake kutoka kwa Maimamu wao wema, ataokoka na adhabu ya moto. Na atakayewapa mgongo atakuwa kama yule aliyekimbilia mlimani siku ya tufani ili mlima huo umlinde na amri ya Allah. Lakini mtu huyo alighariki ndani ya maji, na huyu ataingia motoni. Allah atuepushe na hilo.Na sababu ya kuwashabihisha wao na mlango wa msamaha, nikwa sababu Yeye Allah aliufanya mlango huo kuwa moja ya madhihirisho ya unyenyekevu mbele ya utukufu wake na utiifu mbele 137

Al-Mustadrak Alas-Sahihayn: 2/ 343. Majmauz-Zawaid: 9/ 168. Kanzul-Ummal: 2/ 435 na Juz. 12, uk. 98. 138

153


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

ya hukmu yake, na kwa ajili hii akaufanya sababu ya kupata msamaha. Na amefanya kitendo cha umma huu kuwafuata Ahlulabayti na Maimamu wao kuwa moja ya madhihirisho ya unyenyekevu mbele ya utukufu wake na utiifu mbele ya hukmu yake, na kwa ajili hii akawafanya sababu ya kupata msamaha. Hii ndio sababu ya kuwashabihisha.” Ibn Hajar katika maneno yake139 – baada ya kutaja Hadithi hii na nyinginezo mfano wa hizi – amesema: “Na lengo la kufananishwa kwao na Safina ya Nuhu ni kwamba, atakayewapenda na kuwatukuza kwa kushukuru neema ya aliyewatukuza, na akachukua uongofu wa wanachuoni wao, ataokoka kutokana na kiza cha khitilafu mbalimbali. Na atakayelipa mgongo jambo hilo atazama ndani ya bahari ya kukufuru neema, na ataangamia ndani ya jangwa la upotofu.” Aliendelea kueleza mpaka aliposema: “Na mlango wa msamaha – yaani lengo la kufananishwa kwao na mlango wa msamaha - ni kwamba, Allah alifanya kuingia ndani ya mlango huo, ambao ni mlango wa Ariha au kuingia Baytul-Muqaddas kwa unyenyekevu na kuomba msamaha, ndiyo sababu ya kuomba msamaha na kupata msamaha.Na akaufanyia umma huu mapenzi ya kuwapenda watu wa nyumba ya Mtume kuwa ni sababu ya kupata hilo."140 139 140

As-Sawaiqul-Muhriqah: 151. Al-Murajaat: 77 – 78, barua ya 8.

154


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Na ama kuhusu jambo la pili, namaanisha ubora wa Maimamu  juu ya Manabii wasiokuwa Mtukufu Mtume , ni kwamba dhahiri ya Kitabu inaonesha kuwa Ali  ni bora kushinda Manabii wengine, kwa sababu yeye amechukuliwa kuwa ni nafsi ya Mtukufu Mtume  katika Aya ya Maapizano (mubahalah), Aya iliyoteremka katika maapizano ya Mtukufu Mtume na Wakristo wa Najran, Allah anasema: “Na watakaokuhoji baada kukufikia elimu hii, waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake zetu na wana wanawake wenu, na nafsi zetu na nafsi zenu, kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo.”141 Nususi nyingi zimeeleza kwamba makusudio ya kauli ya Allah: “nafsi zetu” ni Ali bin Abutalib. Na kwamba makusudio ya kauli yake: “watoto wetu” ni Hasan na Husein. Na makusudio ya kauli yake: “wanawake zetu” ni Fatima .142 Hivyo kama Ali ni nafsi ya Mtukufu Mtume  na yeye Mtukufu Mtume ndiye bora kushinda Manabii wengine, basi na Ali ndivyo alivyo. Pamoja na hayo ni kwamba mas‟ala hii si kauli waliyoafikiana Shia wote, bali ni mas‟ala ya kitheiolojia. Huyu hapa Sheikh Mufid anasema: 141

Sura Imran: 61. Tazama tafsiri za riwaya kama vile Tabari, Durul-Manthur, al-Kashaf na Tafsir ya Razi. 142

155


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

“Kundi miongoni mwa Imamiyyah wamehukumu kwamba Maimamu kutoka nyumba ya Muhammad ni wabora kushinda Mitume na Manabii wengine isipokuwa Mtume wetu Muhammad . Na kundi lingine miongoni mwao limewajibisha ubora wao juu ya Manabii wote isipokuwa wale ambao ni UlulAzmi. Na kundi lingine miongoni mwao limezikataa kauli zote hizo mbili na wakahukumu kwa yakini kwamba Manabii wote ni wabora kushinda Maimamu , na akili hazina nafasi ya kukubali au kukataa katika mlango huu. Wala hakuna Ijmai ya pamoja juu ya kauli yoyote kati ya hizo tatu. Hata hivyo, katika hadithi kutoka kwa Mtukufu Mtume  kumhusu Amirul-Muuminina  na dhuriya wake miongoni mwa Maimamu, na pia katika hadithi kutoka kwa Maimamu wakweli baada yake, na katika Qur‟anipia, kuna maeneo yenye kutilia nguvu azma ya yale yaliyosemwa na kundi la kwanza katika maana hii. Na mimi nimezichunguza na ninajilinda kwa Allah na upotevu.”143 Bila shaka umeona, Mufti Mufid, Muftiwa Mashia, hajachukua msimamo mmoja. Na kuna maelezo mengine ya Allamah Sayyid Hibatuddin Shahrastaniy, aliulizwa na muulizaji kwamba; “Je Maimamu ni wabora kushinda Manabii, au jambo ni kinyume na 143

Awailul-Maqalat: 42 – 43.

156


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

hivyo?” Mufti Mungu amrehemu akajibu kwa maelezo haya: “Ama kwa kuwalinganisha na Mtukufu Mtume , wao (Maimamu) wote hawamfikii katika fadhila, bali ni kwamba fadhila zao ni matone kutoka katika ubora wake, na elimu yao ni sehemu tu kutoka katika elimu yake, na utukufu wao ni tawi tu kutoka katika utukufu wake. Ama kwa kuwalinganisha na Manabii wengine waliotangulia, si muhali kundi miongoni mwa hawa (Maimamu) kuwa wabora na watukufu kushinda kundi miongoni mwao (Manabii), kwa sababu miongoni mwa hawa (Maimamu) yupo aliye na elimu zaidi, mtukufu zaidi, mwenye jihadi zaidi katika njia ya Allah, mwenye subira zaidi na mwenye manufaa zaidi kwa wanadamu, kielimu, kiadabu, kitabia na kijamii, na hivyo halibaki jambo lenye kuzuia mwendelezo katika njia ya ubora isipokuwa unabii. Na limepatikana hitimisho mahala pake kwamba, ukhalifa wa Mbora wa Manabii unaweza kuzingatiwa kuwa ni daraja adhimu zaidi kushinda baadhi ya Manabii. Na kwa ibara nyingine ni kwamba, haijathibiti kwamba ukhalifa wa Mungu wa nafasi ya Mbora wa Manabii ni wenye daraja la chini kuliko kila Nabii.”144 Haya ni maelezo kutoka kwa Masheikh wawili wa Kishia, mmoja ni wa zamani na mwingine ni miongoni mwa vigogo wao wa sasa. Maelezo haya yanaonesha bayana kwamba mas‟ala hii si eneo 144

Awailul-Maqalat: 43.

157


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

waliloafikiana Mashia wote hadi ihesabiwe kuwa ni miongoni mwa sifa zinazomtofautisha Shia na asiyekuwa Shia. Na namshangaa Dkt. Ni kwanini anawasilisha mas‟ala hii na mfano wake ili kutofautisha kati ya kundi moja na jingine kati ya makundi mawili (Shia na Suni)?! Na anayetaka ufafanuzi zaidi kuhusu mas‟ala hii basi arejee kitabu Mutashabahul-Qur’ani cha Sheikh mkubwa Muhammad Shahri Ashub Sarawi (488 – 588 A.H.), na kitabu Aslus-Shia Wausuliha cha Allamah mashuhuri, Sheikh Muhammad Husein KashfulGhatau(1294 – 1373).145 MHADHARA WA ISHIRINI NA MOJA Siku ya Ishirini na Moja ya Mwezi wa Ramadhan, Mwaka 1436 A.H. Mnamo siku ya ishirini na moja ya mwezi wa Ramadhan, mwaka 1436 A.H. Dkt. Ahmad Twayyib alisema: “Miongoni mwa mas‟ala zenye ikhtilafu baina ya Suni na Shia ni mas‟ala ya upatikanaji wa uimamu, yaani ni kwa njia ipi unapatikana uimamu? Kwa Suni kwao wao uimamu unapatikana kwa njia mbili na hakuna ya tatu. Ima kwa kusimikwa na Khalifa aliyetangulia, kama Abu Bakri alivyomteua Umar kuwa mrithi wake katika utawala. Au kwa 145

Mutashabihul-Qur’ani: 44 – 45. Aslus-Shiah Wausuliha: 64.

158


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

kupewa kiapo cha utiifu na kundi kutoka miongoni mwa maulamaa na watu wenye maamuzi, watakapomchagua mtu maalumu hapo kisharia mtu huyo huwa ni Khalifa au ndiye mtawala. Na hali hii inafanana kwa karibu na mazingira ya sasa lakini ni mazingira yaliyodogeshwa.” Akaongeza pia: “Ukhalifa mwema au ukhalifa wa unabii ndio uliotawala baada ya kifo cha Mtume wa Allah , nayo ni serikali inayotegemea baraza la mashauriano katika utaratibu wake. Na walishika madaraka ya kuendesha dola ya Kiislamu Makhalifa wanne miongoni mwa Maswahaba, na wote ni kutoka miongoni mwa watu kumi waliobashiriwa pepo, nao ni: Abu Bakri Swidiq, Umar bin Khattab, Uthman bin Affan, na Ali bin Abutalib. Haya ni kwamujibu wa itikadi ya Suni.” Akataja pia kwamba hadithi ya “Ukhalifa katika umma wangu ni miaka thelathini” ni muujiza wa Mtukufu Mtume , ambapo ukhalifa wa Makhalifa hawa wanne ulikuwa ni miaka thelathini. Nasema: Dkt. Mufti wa Azhar, katika mhadhara huu amesisitiza mambo mawili: Kwanza: Kwamba Ukhalifa unapatikana ima kwa kuteuliwa na Khalifa aliyepita, au kwa kuchaguliwa na watu wenye maamuzi. Pili: Hakika ukhalifa wa baada ya Mtukufu Mtume ni wa Maswahaba wanne wakubwa. Na kwamba hadithi “Ukhalifa katika umma wangu utadumu mika thelathini” ni muujiza wa Mtukufu 159


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Mtume .Ama kuhusu jambo la kwanza, ni kwamba al-Mawrudiy amesena: “Uimamu unatimia kwa njia mbili: Ya kwanza ni kwa uchaguzi wa watu wenye maamuzi. Na ya pili ni kwa kuteuliwa na Imam wa kabla yake.146 Nasema: Ingekuwa suala la uimamu linategemea uchaguzi wa watu wenye maamuzi basi Mtukufu Mtume asingepuuzia kutamka hilo na kuelekeza hilo. Itakuwaje apuuze hilo ilihali uimamu ni miongoni mwa mambo makubwa katika uhai wa umma, ambapo Imam ndiye atakayeuongoza umma wa Kiislamu baada ya kufariki Mtukufu Mtume . Ilikuwaje akanyamaza bila kubainisha hilo wakati ambapo tunamkuta yeye  alitaja hadi sunna za Wudhu, adabu za chakula na mengineyo miongoni mwa mambo ya sunna na mambo madogo madogo. Lakini pamoja na hivyo hajatamka wazi jambo hilo muhimu na nyeti ambalo hatima ya umma na mustakabali wake unalitegemea lenyewe?! Zaidi ya hapo ni kwamba, watu wenye maamuzi ni anwani isiyo bayana, ni akina nani hao watu wenye maamuzi? Na wanaamua nini? Mufti Abdul-Karim Khatib anasema: “Hao ni watu wenye elimu na wenye ushawishi ambao watu hurejea kwao katika mambo wanayoyapendekeza. Na je kuna daraja maalumu la 146

Al-Ahkam as-Sultaniyyah: 6 – 7.

160


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

maarifa na elimu ambalo iwapo mtu atalifikia anakuwa ni miongoni mwa watu wenye maamuzi? Ni daraja lipi hilo? Na hupimwa kwa kipimo kipi? Na ni nani mwenye mamlaka ya kutathmini daraja hiyo? Hakika neno „watu wenye maamuzi‟ lina utata zaidi kushinda hata neno „wenye kuwajibika.‟”147 Hakika kusema watu wenye maamuzi ni ibara nyingine yenye kumaanisha kwamba msingi wa utawala na chanzo chake ni baraza la mashauriano (Shura), ili wajumbe wa baraza la mashauriano washauriane kuhusu ukhalifa. Ingekuwa muundo wa serikali baada ya Mtukufu Mtume  ni wa baraza la mashauriano (Shura) basi ilikuwa ni wajibu kwa Mtukufu Mtume  kuujulisha na kuuelewesha umma suala hilo na kulitabikisha katika maisha yake, kwani kutengeneza serikali si jambo dogo, bali ni jambo nyeti na hasa katika jamii zenye makabila mchanganyiko, ambapo chifu wa kabila hili anashindana na chifu wa kabila jingine. Na hapa tunaleta muhtasari wa uhakiki wa Allamah Shahid Muhammad Baqir Sadri kuhusu suala hili: “Kama Mtukufu Mtume  angekuwa amechukua msimamo chanya kwa ajili ya mustakabali wa daawa baada yake, msimamo unaolenga kuuweka utaratibu wa baraza la mashauriano (Shura) katika nafasi ya 147

Al-Khilafa Wal-Imamah: 271.

161


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

utekelezaji moja kwa moja baada ya kifo chake, na kuegemeza uongozi wa daawa kwenye uongozi utokanao na utaratibu huu (Shura), basi jambo la kwanza kabisa ambalo msimamo huu chanya ungehitaji ni Mtume  kama kiongozi, kufanya kazi yakuuelimisha na kuuelewesha umma na walinganiaji utaratibu huu wa baraza la mashauriano (Shura), mipaka yake na vipengele vyake. Na kuipa hali halisi ya kidini iliyo safi, na kuiandaa jamii ya Kiislamu kwa maandalizi ya kifikra na kiroho ili kuweza kuukubali utaratibu huu. Nayo ni jamii iliyoanzia kutoka kwenye makabila mchanganyiko ambayo kabla ya Uislamu hayakuwa yamewahi kuishi katika mazingira ya kisiasa kwa msingi wa baraza la mashauriano (Shura), bali aghlabu yalikuwa yakiishi katika mazingira ya uongozi wa kikabila ambao sehemu kubwa ulikuwa unaoongozwa na sera za nguvu, utajiri na urithi. Na kwa urahisi kabisa tunaweza kutambua kwamba, Mtukufu Mtume  hakufanya zoezila kuelimisha na kuelewesha utaratibu wa baraza la mashauriano (Shura) na vipengele vyake vya kisharia au maana ya dhana zake. Kwa sababu kama zoezi hili lingekuwa limetekelezwa basi kikawaida lingejiakisi katika hadithi zilizopokewa kutoka kwa Mtukufu Mtume  na katika bongo za umma.Au kwa uchache katika bongo za kizazi cha kwanza chenye kuwajumuisha Muhajirina na Answari, kwa kuzingatia kwamba ndio 162


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

chenye kuwajibika kutekeleza utaratibu wa baraza la mashauriano. Wakati ambapo sisi hatukuti katika hadithi zilizopokewa kutoka kwa Mtukufu Mtume  sura yoyote ya kisharia yenye kuainisha utaratibu wa baraza la mashauriano (Shura). Na wala pia hatukuti alama yoyote au mwonekano wowote wa uelimishaji wa namna hiyo katika bongo za umma au za kizazi cha kwanza.”148 Na kwa ajili ya kutoeleweka nadharia yote ya baraza la mashauri (Shura), na kukosekana maandiko bayana kuhusu nadharia hiyo, Dkt. Twaha Husein anasema: “Na kama Waislamu wangekuwa na utaratibu huu ulioandikwa (utaratibu wa baraza la mashauriano) basi Waislamu wangejua katika siku za Uthman kile wanachotakiwa kukifanya na kile wanachotakiwa kukiacha, bila ya kuwepo mfarakano na ikhtilafu baina yao.”149 Nasema: Hakika kuna utata mwingine ukiacha huo uliotajwa, upande wa baraza la mashauriano kuwa ndio msingi wa utawala. Kwanza: Ni kina nani ambao ni wajibu kwao kushiriki katika baraza hili linalotajwa? Je ni maulamaa peke yao, au niwanasiasa peke yao, au ni wote pamoja maulamaa na wanasiasa? 148

Taarikhul-Imamah cha Dkt. Abdullah Fayadh, Sehemu ya utangulizi. 149 Al-Khilafat Wal-Imamat: 272.

163


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Pili: Ni kina nani wanaowachagua wajumbe wa baraza la mashauriano? Tatu: Ikiwa wajumbe wa baraza la mashauriano watatofautiana kuhusu mtu fulani, ni kigezo kipi kitatumika kumtanguliza mtu, je ni kigezo cha wingi wa kura au ni kwa kigezo cha uzito wa kura? Hakika mambo yote haya yana mahusiano na mas‟ala hii (Shura), hivyo inawezekanaje kuyaacha bila kuyafafanua na kuyabainisha? Na ilikuwaje Uislamu ukayanyamazia ikiwa kweli imefanya baraza la mashauriano (Shura) kuwa ndio njia ya kumuainisha kiongozi!? Kisha ni kwamba al-Marudiy mwenyewe, baada ya kuwasilisha njia mbili za kuufikia uimamu alijikuta katika mbabaiko ambao umewapata wanafikra wa Kisuni katika upande huu, ambapo alisema: “Ama kuhusu kupatikana kwake (Uimamu) kwa njia ya uchaguzi wa watu wenye maamuzi, ni kwamba maulamaa wametofautiana katika makundi tofauti kuhusu idadi inayotakiwa ili uimamu utimie: Kundi moja limesema:„Hautimii isipokuwa kwa kuwepo wote wenye maamuzi kutoka kila nchi ili awe ameridhiwa na wote na amekabidhiwa uimamu na wote.‟ Na wengine wamepinga, kwa kudai rai hiyo inapingwa na kiapo cha utiifu alichopewa Abu Bakri ili kuwa Khalifa, kwani alichaguliwa na waliohudhuria na wala haikungojewa ahudhurie yule ambaye hakuwepo. 164


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Na kuna kundi limesema: „Idadi ya chini kabisa ambayo kwayo uimamu unatimia ni watu watano, ambao watakubaliana kwa kumteua mtu au kumteua mmoja kati yao wao watano kwa kukubaliwa na wanne, na dalili katika hilo ni mambo mawili: Kwanza ni kwamba kiapo cha utiifu alichopewa Abu Bakri kilitimia kutokana na watu watano ambao walimteua yeye kisha ndipo watu wakawafuata katika kiapo hicho.‟ Na watu hao ni Umar bin Khattab, Abu Ubaydah bin Jarah, Asidu bin Hudhayru, Bashru bin Saad na Salimhuria wa Abu Hudhayfa. Pili, Umar aliunda baraza la mashauriano (Shura) la watu sita ili mmoja wao ateuliwe kwa kuridhiwa na watu watano. Na hii ndio kauli ya mafakihi na wanatheiolojia wengi wa kutoka Basra. Na wengine miongoni mwa maulamaa wa mji wa Kufa wamesema: „Unatimia kwa watu watatu ambao watamtawalisha uimamu huo mmoja wao kwa kuridhiwa na wawili, ili yeye awe mtawala na wao wawe mashahidi, kama inavyosihi kufunga ndoa kupitia walii na mashahidi wawili.‟ Na kundi jingine limesema: „Unatimia kwa mtu mmoja, kwa sababu Abbas alimwambia Ali: Nyoosha mkono wako nikupe kiapo cha utiifu, ili watu waseme: Ami yake Mtume wa Allah  amempa kiapo cha utiifu binamu yake, hivyo hawatatofautiana juu yako, na kwa sababu ni utawala, na utawala wa mtummoja hufanya kazi.”‟150 150

Al-Ahkam as-Sulataniyyah cha Mawurudiy: 6 – 7.

165


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Katika kuzungumzia kwake rai hizi, Ibn Hazmi hakughafilika na nukta ya ubovu wa rai hizi, ambapo baadhi yake zinahesabika kuwa ni kumkalifisha mtu jambo lisilowezekana, zaidi ya hapo ni kupoteza mambo ya Waislamu kabla sehemu ya mia moja haijakusanya sehemu ya waheshimiwa wa nchi hii, ilihali hata kama lingekuwa ni jambo linalowezekana lisingekuwa ni jambo la lazima, kwa sababu ni madai yasiyo na burhani. Ama kuhusu kauli ya mwenye kusema kwamba, uimamu hautimii isipokuwa kwa kuteuliwa na waheshimiwa na watu wenye hadhi ambao kwao wao ndiko kuna maamuzi ya kuchagua maimamu, ni kwamba watu wa Sham walidai hilo kiasi kwamba, jambo hilo likawapelekea kumpa kiapo cha utiifu Maruwani na mwanawe Abdul-Malik, na kwa kitendo hicho wakahalalisha damu za Waislamu. Nayo ni kauli mbovu,wenye nayo hawana hoja, na kila kauli katika dini isiyokuwa na hoja kutoka katika Qur‟ani au kutoka katika sunna ya Mtume wa Allah  au kutoka katika Ijmai ya umma wa wachamungu, ni batili kwa yakini. Allah Mtukuka anasema:„Sema: Leteni burhani yenu ikiwa kweli ninyi ni wakweli.‟ Ikasihi kwamba asiyekuwa na burhani juu ya usahihi wa kauli yake si mkweli katika kauli yake hiyo, na hivyo, kauli hii nayo pia imeanguka.151 Zaidi ya hapo ni kwamba, Dkt. Twayyib ameishia kutaja njia mbili tu zinazotumika kuainisha Khalifa, 151

Al-Faslu: 4/ 168.

166


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

ambazo ni uteuzi wa watu wenye maamuzi na kuteuliwa na Khalifa aliyetangulia. Ambapo ameacha njia ya tatu ambayo ni ushindi wa nguvu za kijeshi na silaha, Imam Ahmad amesema: “Na yeyote atakayewashinda kwa upanga mpaka akawa Khalifa na akaitwa kuwa ni Amirul-Muuminina, si halali kwa yeyote anayemwamini Allah na Siku ya Kiyama, kulala bila kumzingatia kuwa ni Imam, sawa Imam huyo awe mwema au muovu.”Na wakati anapokuwepo Imam mwenye kujitegemea, kisha akatokea mwingine kwa sababu ya kutaka ufalme akamvamia kijeshi na akamshinda, Imam Ahmad anasema: “Uimamu ni wa aliyeshinda." Katika hilo ametoa hoja kwamba Ibn Umar aliwaswalisha watu wa Madina wakati wa tukio la Hurrah na akasema: “Sisi tuko pamoja na atakayeshinda.”152 Jambo hili halikubaliki, kwani kama uimamu utathibiti kwa mtu kupitia ushindi wa nguvu za kijeshi, atakuja mwingine naye atamshinda na kutawala kwa nguvu za kijeshi, na hatimaye atamuondoa wa kwanza na yeye wa pili atakuwa ndiye Imam.153 Na kauli hii ni kama iliyotangulia, haitegemei hoja ya kisharia, bali ni kauli inayohalalisha tukio lililojitokeza kutokana na mazingira ya kisiasa, au msimamo waliouchukua baadhi ya watu kama vile Ibn Umar. 152 153

Al-Ahkam As-Sultaniyah Uk. 20-23. Maathirul-Inafah: 1/ 71.

167


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Haya yote ni kuhusu madai ya baraza la mashauriano (Shura) kuwa ndio msingi wa utawala. Ama kuhusu madai ya uimamu kutimia kwa kuteuliwa na Imam wa kabla yake, nayo hayana dalili yoyote isipokuwa kitendo cha Makhalifa, ambapo ukhalifa wa Umar ulitimia kwa kuteuliwa na Abu Bakri. Na ndivyo hali ilivyokuwa katika ukhalifa wa kizazi cha Umayyah na Abbas. Hivyo kama muundo wa serikali ya Kiislamu ulitegemea uteuzi wa Khalifa aliyetangulia basi sababu yake hasa ilikuwa ni udikteta unaopingana na roho ya Uislamu. Na ni kwa msingi huu usiokuwa wa halali kisharia ulihama ukhalifa baina ya vizazi vya Umayyah na vizazi vya Abbas, kutoka kwa mzazi kwenda kwa mtoto, bila wao kuwa na sifa za lazima zinazohitajika katika utawala.Na bila kuwa na uwezo wa kuendesha mambo, na bila kuwa na siasa yenye mafanikio wala ujuzi wa kutosha juu ya misingi ya Uislamu na sharia zake. Muhtasari wa maneno ni kwamba: Hakika Mufti wa Azhar na wale waliomtangulia miongoni mwa maulamaa wa Kisuni, wamefanya jambo lililotokea baada ya kufariki kwa Mtume  kuwa ndio dalili ya uhalali, bila kuchunguza na kuthibitisha usahihi wa jambo lenyewe kwa dalili kutoka ndani ya Kitabu, au Sunna tukufu ya Mtume. Kisha ni kwamba watu hawa wamepuuza yale maagizo yaliyopokewa kutoka kwa Mtume  kuhusu usia na ukhalifa, bila ya kutofautisha baina ya yale maagizo ya usia wa Imam 168


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

aliyoyatoa mwanzoni mwa utume, na yale aliyoyausia mwishoni mwa umri wake. Ama kuhusu usia alioutoa mwanzoni mwa utume ni kwamba ilipoteremka Aya: “Na waonye jamaa zako walio karibu.”154 Mtukufu Mtume aliwaita jamaa zake wa karibu na akawaambia: “Enyi watoto wa Abdul Muttalib, Wallahi hakika mimi simtambui kijana yeyote katika Waarabu ambaye amewaletea watu wake jambo bora kushinda nililowaleteeni nyinyi. Hakika nimekuleteeni kheri ya duniani na Akhera. Hakika Allah ameniamrisha nikuiteni katika hilo, hivyo basi ni nani kati yenu atakayenisaidia katika jambo langu hili,awe ndugu yangu, wasii wangu na khalifa wangu kwenu?” Ali anasema: “Watu wote wakanyamaza, nikasema wakati huo nikiwa ndiye mdogo kiumri kushinda wao wote, mwenye macho yenye kung‟aa, mwenye tumbo kubwa, na mfupi kuliko wao: „Mimi ewe Mtume wa Allah nitakuwa msaidizi wako.‟ Akaishika shingo yangu na kusema: „Hakika huyu ni ndugu yangu, wasii wangu na khalifa wangu kwenu, msikilizeni na mtiini.‟ Watu wakasimama huku wakicheka, wakimwambia Abu Talib: „Amekuamrisha umsikilize na kumtii mwanao.‟”155 154

Qur‟ani: 26:214. Taarikh Tabari: 2/ 216. Tafsirul-Khazin: 390. Musnad Ahmad: 1/ 159. Hayat Muhammad cha Haykal: 104. 155

169


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Ama kuhusu usia wa mwishoni mwa maisha yake, katika hilo yanatosha yale aliyoyafikisha kutoka kwa Allah Mtukuka kuhusu jambo la ukhalifa katika siku ya Ghadir, na kwa kuwa Hadithi husika ni maarufu kwa sanadi zake, tumetosheka na yale yaliyotangulia, na inshaallah utakufikia baadhi ya ufafanuzi wake katika mhadhara ujao. Dkt. Ahmad Twayyib Mungu amhifadhi, ametaja kwamba kauli ya Mtume wa Allah  kuwa ukhalifa katika umma wangu utakuwa ni miaka thelathini, kuwa kauli hiyo ni muujiza wa Mtukufu Mtume , ambapo ukhalifa wa Makhalifa wanne ulidumu miaka thelathini. Nasema: Dkt. Katika maneno yake haya ametegemea ile riwaya aliyoipokea Tirmidhiy katika Sunan yake kutoka kwa Ahmad bin Muniu, kutoka kwa Sarihu bin Nuuman, kutoka kwa Hashraj bin Nabatah, kutoka kwa Said bin Jamhan, amesema: Alinisimulia Safinah huria wa Mtume wa Allah, alisema: Mtume wa Allah  alisema: “Ukhalifa katika umma wangu utakuwa ni miaka thelathini, kisha baada ya hapo ni ufalme.”156 Nasema: Hadithi hii si hoja upande wa sanadi wala maana. Ama upande wa sanadi ni kwamba katika 156

Sunan Tirmidhiy: 3/ 341, Mlango unaozungumzia yale yaliyokuja kuhusu ukhalifa.

170


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

hadithi hii yupo Hashraj bin Nabatah. Abu Hatim amesema: “Hadithi yake huandikwa lakini haitumiwi kama hoja.” Na mara nyingine akasema: “Si imara (katika upokezi), Tirmidhiy ameandika hadithi yake moja tu kisha akasema: Hashraj ana hadithi nyingine ukiachilia mbali hii iliyotajwa, na hadithi zake ni hasan, za mpokezi mmoja mmoja na ngeni. Sajiy amesema: „Ni dhaifu.‟ Na Ibn Habban amesema: „Alikuwa mchache wa hadithi. Mwenye riwaya zisizokubalika. Haifai kutoa hoja kwa hadithi yake iwapo kaipokea yeye peke yake.‟”157Na katika sanadi yake yupo pia Said bin Jamhan mwenyeji wa Basra (aliyefariki mwaka 136 A.H.), Abu Hatim amesema: “Si hoja, na wengine wanamzingatia kuwa ni dhaifu, kwa Tirmidhiy hana hadithi zaidi ya hiyo.”158 Huu ni upande wa sanadi, ama kuhusu upande wa maana ni kwamba: Dhahiri ya Hadithi inaonesha kwamba Mtukufu Mtume  alikuwa anajua kwamba ukhalifa utadumu muda wa miaka thelathini. Ikiwa Mtukufu Mtume  alitamka wazi muda wa ukhalifa wao ni kwanini basi hakutaja na kutamka majina yao na utambulisho wao. Je kutaja muda wa ukhalifa ilikuwa ni jambo muhimu zaidi kuliko kutaja bayana utambulisho wao?! Kwa kuongezea ni kwamba, madhumuni ya Hadithi yana157 158

Tahdhibut-Tahdhib: 2/ 325. Tahdhibut-Tahdhib: 2/ 325.

171


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

pingana kabisa kiukamilifu na riwaya nyingi zilizopokewa kutoka kwa Mtukufu Mtume  zinazoeleza kuwa ukhalifa utadumu kwa kupitia watu kumi na wawili. Masheikh wawili (Bukhari na Muslim) wametenga mlango wa riwaya hizo na wamezitaja kwa sanadi mbalimbali, hapa tunataja sehemu ndogo tu ya riwaya hizo; a. Bukhari amepokea kutoka kwa Jabir bin Samrah, amesema: “Nilimsikia Nabii  akisema: „Kutakuwa na maamiri kumi na wawili.‟ Akasema neno ambalo sikulisikia, baba yangu akasema: Amesema kwamba wote watakuwa ni Makuraishi.”159 b. Muslim amepokea kutoka kwa Jabir bin Samrah, amesema: “Nilimsikia Nabii  akisema: „Dini haitaacha kuwa na nguvu hadi wapatikane Makhalifa kumi na mbili.‟ Akasema neno ambalo sikulifahamu, nikamuuliza baba yangu: Amesema nini? Akasema: Amesema kwamba wote watakuwa ni Makuraishi.” 160 c. Muslim amepokea kutoka kwa Jabir bin Samrah, amesema: Nilikwenda kwa Mtume wa Allah  nikiwa pamoja na baba yangu, nikamsikia akisema: „Dini hii itaendelea kuwa na nguvu na 159 160

Sahih Bukhari: 9/ 81, Mlango wa kuacha khalifa. Sahih Muslim: 6/ 3, Kitabu cha uongozi.

172


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

imara mpaka kuwe na Makhalifa kumi na wawili.‟ Akasema maneno ambayo sikuyasikia kutokana na kelele za watu, nikamuuliza baba yangu: Amesema nini? Akasema: Amesema kwamba wote watakuwa ni Makuraishi.”161 d. Ahmad bin Hanbal amepokea kwa sanadi yake kutoka kwa Masruq, amesema: Tulikuwa tumeketi kwa Abdullah bin Mas‟ud, mtu mmoja akamwambia: „Ewe Baba Abdurahman! Je mlimuuliza Mtume wa Allah  umma huu utamiliki Makhalifa wangapi?‟ Ibn Masuud akasema: „Ndiyo tulimuuliza Mtume wa Allah  akasema: Kumi na wawili sawa na idadi ya makabila ya wana wa Israil.”162 Na Ahmad amepokea pia kwa sanadi yake hadithi isemayo: “Makhalifa kumi na wawili” kutoka kwa Jabir bin Samrah, ameipokea kutoka katika njia thelathini na nne.163 e. Al-Hakim amepokea kwa sanadi yake katika alMustadrak kutoka kwa Awni binAbu Juhayfah, kutoka kwa baba yake, amesema: Mtume wa Allah  alisema: “Mambo ya umma wangu hayataacha kuendelea vizuri mpaka kupatikane Makhalifa 161

Sahih Muslim: 6/ 3, Kitabu cha uongozi. Musnad Ahmad: 1/ 391. 163 At-Tashayuu cha Abdullah Ghurayfiy: 150, amenukuu kutoka kwenye Musnad: 5/ 90. 162

173


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

kumi na wawili.....wote watakuwa ni Makuraishi.”164 Riwaya zote hizo zinajulisha kuwa ukhalifa utadumu zaidi ya miaka thelathini. Na kwakuwa sehemu ya pili ya riwaya imekuja kwa wingi basi ichukuliwe hiyo na iachwe ya kwanza. Namaanisha iachwe hiyo inayoonesha kuwa muda wa ukhalifa ni miaka thelathini. MHADHARA WA ISHIRINI NA TATU Siku ya Ishirini na Tatu ya Mwezi wa Ramadhan, Mwaka 1436 A.H. Dkt. Ahmad Twayyib amesema: “Hakuna umaasumu kwa Imam au Khalifa yeyote baada ya Mtukufu Mtume , kuanzia kwa Abu Bakri Swidiq mpaka siku ya kusimama Kiyama. Na haya ndio aliyosisitiza Sayiduna Abu Bakri katika hotuba yake aliyoitoa baada ya kusimikwa, alisema: "Enyi watu nimekuwa mtawala wenu ingawa mimi sio bora kuliko wengi miongoni mwenu. Nikitenda vyema nisaidieni. Nikipotoka nirekebisheni.” Anakiri kwamba Khalifa anaweza kukosea au kutopatia. Na kauli yake: “Nirekebisheni” yaani ni mnirudishe na kunirejesha kwenye usahihi. Hivyo hakuna yeyote mwenye umaasumu baada ya Mtukufu Mtume .” 164

Al-Mustadraku Alas-Swahihayn: 3/ 618.

174


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Kisha Dkt. Akafuatiliza mas‟ala ya kutokuwepo tamko juu ya uimamu wa Sayiduna Ali  akasema: “Hakika katika hadithi ambazo zimepokewa katika kuwasifu Makhalifa akiwemo Sayiduna Ali, hamna si kwa ukaribu wala kwa umbali, ishara yoyote inayoashiria uimamu wa Sayiduna Ali  baada ya Mtukufu Mtume . Na kama jambo lingekuwa kama wanavyoamini Shia basi angetamka hilo bayana waziwazi kwa kusema: “Enyi Waislamu! Ali ndiye Imam baada yangu.” Na jambo lingejulikana, lakini sisi tuko mbele ya tamko lisilo bayana, – kama alivyosema Sharif Murtadha ambaye ni miongoni mwa maulamaa wakubwa wa Shia - hivyo inawezekana likawa linajulisha (uimamu wake) au likawa halijulishi.” Nasema: Riwaya aliyoitegemea Mufti ya maneno yaliyopokewa kutoka kwa Abu Bakri yamepokewa katika namna mbii: Ya kwanza: "Enyi watu nimekuwa mtawala wenu ingawa mimi sio bora kuliko wengi miongoni mwenu. Nikitenda vyema nisaidieni. Nikipotoka nirekebisheni.”165 Ya pili: “Enyi watu tambueni kwamba mimi sijawekwa sehemu hii ili niwe mbora kuliko ninyi. Natamani kwamba mmoja wenu angekaa badala yangu. Kama mtanichukulia kwa namna ile ambayo Allah alikuwa akimrekebisha Mtume wakekwa wahyi hamtalikuta 165

Swawaiqul- Muhriqah cha Ibn Hajar: 11.

175


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

hilo kwangu. Mimi si lolote isipokuwa ni kama mmoja wenu. Mkiniona nimenyooka nifuateni, na mkiniona nimekengeuka nirekebisheni. Na tambueni kwamba hakika mimi ninaye shetani ambaye hunifikia mara kwa mara....."166 Ama kuhusu aina ya kwanza ya riwaya tunasema: Kama miongoni mwa Maswahaba yupo aliye mbora zaidi kuliko yeye ambaye ni mjuzi zaidi wa misingi na matawi ya dini, mjuzi zaidi wa uteremsho na tafsiri yake, ni kwanini hakumpendekeza huyo siku ya Saqifa ili watu wamchague na kumpa kiapo cha utiifu?! Huku si kuudhulumu umma! Aliye mbora kuchukua madaraka wakati yupo aliye mbora zaidi kuliko yeye, au asiye mbora kuchukua madaraka wakati yupo aliye mbora?! Ama kuhusu aina ya pili ya riwaya tunasema: Kukirikwake ni kwa ajabu na kwa hatari sana, kwani hakika suala la shetani kuingilia fikra zake wakati wa kubainisha hukmu na kutoa maamuzi ni jambo ambalo haliwezi kufumbiwa macho. Mtu kama huyu hana sifa ya kupendekezwa kwa ajili ya uongozi. Kisha ni kwamba lengo la kumpa mtu madaraka ni ili auendeshe umma kwa mujibu wa Kitabu na Sunna, na jambo hilo linahitaji Khalifa awe ni mjuzi wa yale ambayo umma unayahitajia katika utawala na siasa, 166

Taarikhul-Khulafai cha Ibn Qutaybah: 1/ 16.

176


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Ali  amesema: “Enyi watu! Kwa kweli mwenye kustahiki mno kwa jambo hili (Ukhalifa) ni yule mwenye uwezo nalo zaidi, mjuzi zaidi wa amri ya Mwenyezi Mungu humo. Endapo akifanya fitina mfanya fitina ataombwa kutubia, akikataa atapigwa vita.167" Na Imam Husein bin Ali  amesema: “Wallahi Imam si yeyote ila yule mwenye kusimamia uadilifu, mwenye kuhukumu kwa Kitabu na mwenye kujidhibiti mwenyewe upande wa Allah.”168 Na dhahiri ya maneno ya Khalifa ni kwamba katika jambo la uongozi yeye anahitajia watu wengine, na hivyo hitimisho linakuwa: Hakika hakuwa na vigezo na sifa za kuwa Khalifa. Kisha Dkt. Alikanusha uwepo wa tamko linalothibitisha uimamu wa Ali , na akanukuu kutoka kwa Sayyid Murtadha kwamba alisema: “Hivyo inawezekana tamko hili likawa linajulisha (uimamu wake) au likawa halijulishi.” Nasema: Dkt. Katika nukuu yake hii ametegemea yale aliyoyaandika Ahmad al-Katibu aliyeandika kuhusu maudhui hii, naye (al-Katibu) hakunukuu kwa usahihi. Hebu angalia maneno yake (Sayyid Murtadha) aliyoyagusia al-Katibu (Ahmad), amesema: “Jambo tunaloliamini ni kwamba Mtukufu Mtume  alitoa tamko la uimamu wa Imam Ali 167 168

Nahjul-Balaghah: Hotuba ya 172. Rawdhatul-Waidhina: 206.

177


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

baada yake, na akajulisha wajibu wa kumtii na kumfuata kwa kila mukalafu. Na tamko hilo katika asili linagawanyika sehemu mbilikwetu sisi: Moja inarejea kwenye kitendo na inajumuisha pia kauli. Na nyingine inarejea kwenye kauli bila kitendo.” Aliendelea hadi aliposema: “Tumeshaonesha kuthibiti kwa tamko juu ya uwalii wa Kiongozi wa Waumini  kupitia hadithi mbalimbali ambazo kuna kongamano na itifaki juu ya usahihi wake, ijapokuwa kumetokea ikhtilafu katika tafsiri yake. Na tumebainisha kwamba hadithi hizo zinajulisha kuwa ni tamko lenye kumthibitisha yeye  bila dhana wala tatizo, kama vile kauli yake : „Wewe kwangu mimi una cheo sawa na kile alichokuwanacho Harun kwa Musa.‟ Na „Yeyote ambaye mimi ni walii wake basi huyu Ali ndiye walii wake.‟ Na nyinginezo miongoni mwa zile tulizozionesha. Zaidi ya hapo ni kwamba Qur‟ani Tukufu inashahidilia hilo, kama kauli yake:

ُ َ​َ َُ ُ ُ​ُ َ َ َ َ َ َ ‫ءام ُنىا َال‬ َ ‫سىل ُه َو َال‬ َ ‫ذين‬ ‫ذين ُيقّيمىن‬ ‫ِإهما و ِلّيكم الّلـه ور‬ ‫الّص ّٰلىة‬ َ َ َ َ َُ ‫الل ٰىة َو ُ م ٰر ِ ىن‬ ‫و ؤىن‬ “Hakika walii wenu hasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wale walioamini ambao husimamisha Swala na hutoa Zaka wakiwa wamerukui.” (Al-Maida 5:55) 178


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Hivyo ni lazima tuitupilie mbali kila habari yenye kupingana na haya yaliyojulishwa na dalili hizi yakinifu, ikiwa habari hizo hazina uwezekano wa kutolewa tafsiri nyingine. Na tuzitolee tafsiri inayoafikiana nayo na kuoana nayo ikiwa inaruhusiwa kuzifanyia hilo.”169 Unaona yeye (Sayyid Murtadha Allah amrehemu) ameihesabu hadithi ya Ghadir kuwa ni miongoni mwa hadithi ambazo zinamthibitisha  bila dhana wala tatizo, na kwamba dalili yake ni yakinifu yenye kuwajibisha kuitupilia mbali kila habari yenye kupingana nayo. Na kwakweli nukuu isipofanywa kwa uaminifu huwa ni anwani ya hasara. Na ameihakiki maudhui hii Ustadh Haidar Muhammad Ali al-Baghdadiy at-Tahani katika kitabu chake Wahatul-Yaqin, na humo amefichua mashimo aliyodondokea mwandishi Ahmad al-Katibu katika kitabu chake kilichotajwa.170 Kisha Dkt. Alisema: Na kama jambo lingekuwa kama wanavyoamini Shia basi angetamka hilo bayana waziwazi kwa kusema: “Enyi Waislamu! Ali ndiye Imam baada yangu.” Nasema: Hakika Mtukufu Mtume alirudia kauli hiyo zaidi ya mara moja katika maisha yake, miongoni mwa maeneo aliyoitamka kauli hiyo ni: 169 170

Shafiy Fil-Imamah: 3/ 99. Wahatul-Yaqin: 418 – 428.

179


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Kwanza: Ni katika hadithi iliyotangulia kuhusu mwanzo wa daawa yake, na bila shaka tamko lake limeshatangulia huko nyuma. Pili: Ni katika hadithi ya uwalii, namaanisha kauli ya Mtukufu Mtume  kuhusu haki ya Ali  aliposema: “Ali ni sehemu yangu, na mimi ni sehemu ya Ali, naye ndiye walii wenu baada yangu.” Nayo ni miongoni mwa hadithi zilizokuja kwa njia nyingi, ambayo wameiandika maimamu zaidi ya mmoja miongoni mwa maimamu wa Sahih na Sunanna mahufadhi wa hadithi. Na sehemu kubwa ya maimamu wakubwa wa hadithi wameiandika katika vitabu vyao. Na kwa mujibu wa alivyoifuatilia mhakiki Sayyid Hamid Husein Lakuhanawi (aliyefariki mwaka 1306 A.H.), katika kitabu chake Aqabatul-An’war, idadi ya maimamu wakubwa wa hadithi waliyoiandika wanaweza kufikia 65, wakiwemo: I. Sulayman bin Dawud Twayalasiy (aliyefariki mwaka 204 A.H.). II. Abu Bakri Abdullah bin Muhammad bin Abu Shaybah (aliyefariki mwaka 239 A.H.). III. Ahmad bin Hanbal (aliyefariki mwaka 241 A.H.). IV. Muhammad bin Isa Tirmidhiy (aliyefariki mwaka 279 A.H.).

180


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

V. Ahmad bin Shuaib Nasaiy (aliyefariki mwaka 303 A.H.). Na wengineo miongoni mwa mahafidhi na wanahadithi wakubwa.171 Na hapa tunakuletea tamko la hadithi yenyewe: 1. Ameandika Nasaiy katika Sunan yake kwamba: Ametusimulia Waswil bin Abdul-Aala, kutoka kwa Ibn Fudhaylu, kutoka kwa Aaraj, kutoka kwa Abdullah bin Buraydah, kutoka kwa baba yake, amesema: “Mtume wa Allah alitutuma Yemen chini ya uongozi wa Khalid bin Walid, na akamtuma Ali  kuwa Amiri wa kikosi kingine, akasema: „Mtakapokutana Ali ndio atakuwa Amiri wa watu wote. Na mtakapoachana kila mmoja kati yenu ninyi wawili ataongoza kikosi chake.‟ Tukakutana na Bani Zayd katika watu wa Yemen tukapigana nao. Waislamu wakawashinda Mushirikina, tuliwauwa wengi na tukawachukua mateka dhuria wao. Ali  akajichagulia mwanamke mmoja kutoka katika mateka wale. Ndipo Khalid bin Walid akanipa barua nimpelekee Mtume wa Allah , ya kumpa habari juu ya tukio hilo na kumtoa dosari Ali. Nilipokwenda kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu  nilimkabidhi ile barua na kuanza kumtoa dosariAli, mara nikaona ghadhabu katika uso wa Mtume wa Allah , 171

Nafahatil-Azhar Fii Khilaswat Aqabatil-An’war: 15/ 51 – 54.

181


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

nikamwambia: Ewe Mtume wa Allah! hii ni sehemu ya mwenye kujilinda, ulinituma niwe pamoja na mtu ambaye umeniamrisha nimtii, nami nimefikisha nilichotumwa. Mtume wa Allah akaniambia: „Ewe Buraydah! Usimtuhumu Ali, hakika yeye ni sehemu yangu, na mimi ni sehemu yake, naye ni Walii wenu baada yangu.‟”172 2. Ahmad ameandika katika Musnad yake kutoka kwa Ibn Abbas, kutoka kwa Buraydah, kwamba alisema: “Tulikuwa vitani pamoja na Ali  huko Yemen. Mara nikaona kwake jambo lisilopendeza. Nilipofika kwa Mtume wa Allah  nikamtaja Ali  na kumshutumu. Mara nikauona uso wa Mtume wa Mwenyezi Mungu  umebadilika, akasema: „Ewe Buraydah, je mimi si ni mwenye mamlaka zaidi kwa waumini kuliko hata waliyonayo juu ya nafsi zao?‟ Nikasema ndiyo ewe Mtume wa Allah, akasema: „Yeyote ambaye mimi ni mtawala wake basi Ali ndiye mtawala wake.”173 Na ibara iliyokuja katika hadithi aliyoiandika Nasaiy kwamba Mtume alisema: “Ali ni sehemu yangu, na mimi ni sehemu ya Ali, naye ni Walii wenu baada 172 173

Khaswaisu Ali bin Abi Talib: 75. Musnad Ahmad bin Hanbal: 5/ 347.

182


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

yangu.‟ Haipingani na aliyoipokea Ahmad katika Musnad yake, na huenda Mtukufu Mtume alikusanya ibara zote mbili kwa kuzitamka, au mpokezi alipokea madhumuni na maana ya ibara, akasema: „Yeyote ambaye mimi ni mtawala wake basi Ali ndiye mtawala wake.‟ Vyovyote iwavyo ni kwamba hadithi mwishoni imemalizikia kwa maneno yanayojulisha uwalii wake baada ya kifo cha Mtukufu Mtume . Na jambo linalounga mkono hayo ni kwamba Imam Ahmad ameiandika hadithi hiyo kutoka kwa Imran Bin Huswin kwa namna ifuatayo: 3. Amesema: Mtume wa Allah  alituma jeshi, na akamteua Ali bin Abu Talib  kuwa kiongozi wa kikosi hicho. Alipokwenda Ali  alipata suria, lakini wengine hawakuridhika na jambo hilo, hivyo watu wanne miongoni mwa Maswahaba wa Mtume wa Allah  wakakubaliana kuwa: „Tutakapokutana na Mtume wa Mwenyezi Mungu  tutamueleza aliyofanya Ali .‟ Na ilikuwa ni kawaida Waislamu wanaporudi vitani, kwanza hupitia kwa Mtume wa Allah  na kumsalimu kisha ndipo huenda zao, hivyo kikosi kiliporudi kilikwenda kumsalimu Mtume, na ndipo akasimama mmoja kati ya wale wanne, akasema: „Ewe Mtume wa Allah! Ali alifanya haya na haya!‟ Lakini Mtume wa Allah  akampuuza. Kisha akasimama wa pili na akasema kama alivyosema 183


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

mwenzake, lakini Mtume wa Mwenyezi Mungu  akampuuza.” Akanukuu walivyosimama wengine watatu na jinsi Mtume alivyowapuuza, akaendelea kusimulia mpaka aliposema: “Mtume wa Allah akamwelekea wa nne wao huku hasira ikionekana usoni mwake, akamwambia: „Mwacheni Ali. Hakika Ali ni sehemu yangu, na mimi ni sehemu ya Ali, naye ndiye walii wa kila muumini baada yangu.‟”174 4. Tirmidhiy ameandika kutoka kwa Imran bin Huswin, na amenukuu hadithi kama alivyoinukuu Ahmad bin Hanbal, mpaka aliposema: “Kisha akasimama wa nne naye akasema kama walivyosema wenzake, hapo Mtume wa Allah  akawaelekea na kusema huku hasira ikionekana usoni mwake: „Mnataka nini kutoka kwa Ali? Mnataka nini kutoka kwa Ali? Mnataka nini kutoka kwa Ali? Hakika Ali ni sehemu yangu, na mimi ni sehemu ya Ali, naye ndiye walii wa kila muumini baada yangu.‟”175 Unaona jinsi riwaya inayozungumzia uwalii inajulisha kwamba yeye ndiye Imam baada ya kifo cha Mtukufu Mtume . Zaidi ya hapo ni kwamba, hakika hadithi ya Ghadir inajulisha uwalii wa Ali , 174 175

Musnad Ahmad: 4/ 438. Sunan Tirmidhiy: 5/ 632.

184


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

kwani hakika Mtume wa Allah  alitaja katika hotuba yake tauhidi, utume na marejeo, akasema: “Si mnashahidia kwamba hapana Mungu isipokuwa Allah na kwamba Muhammad ni mja Wake na Mtume Wake, na kwamba pepo Yake ni haki, na kwamba moto Wake ni haki, na mnaamini Kitabu chote?” Wakasema: Ndiyo. Akasema: “Na mimi nashahidilia mliyoshahidilia na kunisadikisha. Hakika mimi nitatangulia nanyi mtanifuata, na nyinyi mtanikuta kwenye Hodhi, mtakaponikuta hapo nitawaulizeni kuhusu vizito vyangu viwili, mliishi navyo vipi?” Wakauliza: “Ni vipi hivyo vizito viwili?” Akasema: “Kikubwa kati ya hivyo viwili ni Kitabu cha Allah... Na kidogo ni kizazi changu....” kisha akaushika mkono wa Ali akaunyanyua juu na kusema: “Yeyote ambaye mimi ndiye mtawala wake basi Ali ndiye mtawala wake. Yeyote ambaye mimi ndiye walii wake basi Ali ndiye walii wake. Ewe Mungu Wangu mpende mwenye kumpenda na mfanyie uadui mwenye kumfanyia uadui.” Aliyasema hayo mara tatu, kisha Mtume wa Allah akamfunga Ali kilemba chake kwa mkono wake mtukufu, mbele ya mkusanyiko mkubwa wa waumini, akashusha ncha moja shingoni mwake. Na akawaamuru Muhajirina na Answari wamsalimu Ali kwa kuwa kiongozi wa Waumini. Huu ndio muhtasari wa yale yaliyotokea Ghadir, na katika hotuba yake yalihudhuria makundi mengi 185


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

kutoka kwenye maelfu ya watu, katika ardhi ya Ghadir Khum karibu na Juhfah. Hadithi ya Ghadir imepokelewa na takribani Maswahaba 119, na Tabiina takribani 90, na miongoni mwa maulamaa wa Kisuni walioipokea katika muda wa karne zote ni takaribani maulamaa 360. Na kwa kuwa risala hii ni finyu kiasi cha kutokutosha rejea zote basi ni juu ya Mufti kurejea kwenye Enskolopedia ya Ghadir ya Allamah Abdul-Husein Amini Najafiy. Yeye amekusanya wapokezi wa hadithi hii kutoka miongoni mwa Maswahaba na Tabiina na mahufadhi walioinukuu katika vitabu vyao. Al-Hakim amepokea katika kitabu al-Mustad-rak kwa sanadi inayokwenda kwa Abdullah bin As‟ad bin Zurarah, kutoka kwa baba yake, amesema: “Mtume wa Allah  alisema: “Nilifunuliwa mambo matatu kuhusu Ali: Kwamba yeye ni Bwana wa Waislamu, Imamu wa wachamungu na kiongozi wa watu mashuhuri.” Al-Hakim amesema: “Hadithi hii ni yenye sanadi sahihi lakini Masheikh wawili hawajaiandika.”176 Na Tabaraniy katika al-Muujam as-Swaghir amepokea hadithi mfano wa hiyo kutoka kwa Hakim Jahniy.177 Na Ibn Athir kaipokea katika Usudul-Ghabah,178 na Maghazaliy Shafiiy katika 176

Al-Mustadrak Alas-Sahihayni: 3/ 137 – 138. Al-Muujam as-Saghir: 2/ 360. 178 Usudul-Ghabah: 1/ 84. 177

186


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

kitabu al-Manaqib.179 Ukiona mchana unahitajia dalili basi tambua kuwa hakuna kitu kitakachokuwa sahihi akilini. MHADHARA WA ISHIRINI NA NNE Siku ya Ishirini na Nne ya Mwezi wa Ramadhan, Mwaka 1436 A.H. Mheshimiwa Dkt. Ahmad Twayyib Mufti wa Azhar alisema: “Hakika kauli ya Mtukufu Mtume : “Yeyote ambaye mimi ni mtawala wake basi huyu Ali ni mtawala wake.” Haisihi kuwa tamko bayana linalomlazimisha mwislamu kufahamu kuwa Ali ndiye Imam baada ya Mtume wa Allah , kwa sababu wote walifahamu kuwa hiyo ni heshima makhususi ya Sayiduna Ali.” Mheshimiwa Mufti katika maongezi yake ya siku hii akaendelea kusema: “Hakika matokeo ya lazima yatokanayo na kauli ya Shia ni kwamba Maswahaba walihaini ahadi ya Allah na ahadi ya Mtume wake na wakaridhia kupora ukhalifa kutoka kwa Sayiduna Ali, na maneno haya yahaingii akilini, kwani itakuwaje Maswahaba watukufu wahaini na kuvunja ahadi. Kisha ni kwamba Maswahaba hawa ndio waliyotufikishia Qur‟ani Tukufu na wakatufikishia dini hii 179

Manaqibul-Maghaziliy: 83.

187


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

tukufu, hivyo kama Maswahaba walikuwa wahainiinakuaje Shia wamechukua Qur‟anikutoka kwa Maswahaba kama Suni na wameifahamu kutoka kwao?!” Dkt. Katika mhadhara wake huu amesisitiza mambo haya: La Kwanza: Hadithi ya Ghadir haijafikia kiwango cha kuwa dalili ya kuthibitisha kuwa Ali ni Imam. La Pili: Ikiwa Ali ndiye Imam aliyetamkwa na nususi, maana yake ni kwamba Maswahaba walimhaini Ali. La Tatu: Kama Maswahaba walikuwa na sifa hii ilikuwaje Shia wakachukua Qur‟ani kutoka kwa watu wenye sifa hii? Hebu sasa kulichambue kila moja kati ya mambo haya matatu: Ama kuhusu jambo la kwanza: Hili tumeshalijibu katika mhadhara wa saba, na tulisema huko kwamba: Hakika hotuba ya Hadithi hii ya Ghadir ni dalili bora yenye kujulisha kwamba, hakika Mtukufu Mtume  alikuwa katika lengo la kubainisha msingi miongoni mwa misingi ya Uislamu, ambapo alichukua ushahidi kutoka kwa hadhirina juu ya misingi mitatu. Kisha aliunyanyua juu mkono wa Ali na akasema yale 188


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

aliyosema, na hivyo kama lengo lingekuwa ni kubainisha sifa fulani miongoni mwa sifa za Imam Ali basi asingehitajia kutaja misingi mitatu. Zaidi ya hapo ni kwamba, katika hotuba ya Mtukufu Mtume  kuna kauli yake: „„Je mimi si ni mwenye mamlaka zaidi kwenu kushinda hata mliyonayo juu ya nafsi zenu wenyewe?” Wakasema: “Ndiyo.” Akasema: “Basi yeyote ambaye mimi ni mtawala wake, Ali ndiye mtawala wake.” Na yanayojulisha kwamba Mtukufu Mtume  alikuwa katika lengo la kumweka Ali katika nafasi aliyonayo yeye  katika mamlaka aliyonayo juu ya watu wengine, na kwamba ndiye mwenye mamlaka zaidi juu ya nafsi na mali, yanalazimu mwenye sifa hizi kuwa kiongozi wa kimungu. Basi ni tamko gani lililo dhahiri kushinda hilo?! Zaidi ya hapo ni kwamba hadhara ilifahamu kutokana na hadithi hii kwamba, uongozi wa jamii umekabidhiwa kwa Ali . Hawa hapa Masheikh wawili (Abu Bakri na Umar), pindi Mtume alipowaamuru Waislamu kutoa heshima kwa Ali na kumpongeza kwa kuwa kwake kiongozi wa Waumini, walijitokeza na kumpongeza hadi Umar akasema: “Hongera, hongera ewe Ali, sasa umekuwa mtawala wa kila muumini mwanaume na kila muumini mwanamke.” Au kwa maneno yenyemaana inayokaribiana na hii.180 180

Tafsir Razi: 12/ 49. Al-Muswannaf cha Ibn Abi Shaybah: 12/ 78, namba 12167. Musnad Ahmad: 5/ 355.

189


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Na miongoni mwa waliokuwepo katika tukio hili la Ghadir ni Hassan bin Thabit, malenga wa zama za utume, alitengeneza hadithi ya Ghadir katika muundo wa kishairi akasema: “Siku ya Ghadir Mtume wao anawaita hapo Khum. Hebu sikiliza Mtume anatangaza. Akasema: Ni nani mtawala wenu na Nabii wenu? Wakasema bila kupepesa macho: Mungu Wako ndiye mtawala wetu na wewe ndiye Nabii wetu, na wala hautampata mwenye kuasi kuhusu uwalii miongoni mwetu. Akasema kumwambia: Nyanyuka ewe Ali, hakika mimi nimekuridhia kuwa Imam na kiongozi baada yangu. Hivyo yeyote ambaye mimi ni mtawala wake basi huyu ndiye walii wake, na kuweni wafuasi wa kweli kwake wenye kumtawalisha yeye. Hapo akaomba dua: Ewe Mungu Wangu mpende mwenye kumpenda na kuwa adui wa yule mwenye kumfanyia uadui Ali."181 Na kuna viashiria vingi katika matini ya hadithi, vinaweza kufikia kumi, amevifafanua zaidi mchambuzi na mtafiti mkubwa Allamah Amin katika Enskolopedia yake, na amethibitisha kwamba madhumuni ya hadithi hii ni kujulisha uwalii wa Ali ď ‚ aliopewa na Mungu. Na kama Mufti anataka 181

Al-Ghadir: 2/ 65. Amenukuu kutoka kwenye vyanzo kumi na mbili vya wanazuoni wa Kisuni, na kutoka vyanzo ishirini na sita vya wanazuoni wa kishia.

190


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

kujua zaidi kuhusu viashiria hivi basi arejee juzuu ya kwanza ya kitabu al-Ghadir. Haya yote ni kuhusu jambo la kwanza. Ama kuhusu jambo la pili, nalo ni kuwatuhumu Shia kwamba wanasema Maswahaba walifanya uhaini. Hakika kauli hii itokayo kwa Mufti inashangaza sana, na hiyo ni kwa sababu ya mambo yafuatayo: Jambo la kwanza: Hakika sehemu kubwa ya Maswahaba walibaki na kuendelea kuwa kama walivyokuwa katika zama za Mtukufu Mtume , hivyo wakasisitiza uimamu wa Ali na kwamba yeye ndiye aliyesimikwa kisharia kwa tamko la sharia. Na wao ndio vinara waUshia, na idadi yao inafikia mia mbili au zaidi. Nafasi hii haituruhusu kutaja majinayao, lakini Mufti Dkt. Ahmad Wailiy katika kitabu chake Hawiyyatut-Tashayyui alijivisha jukumu la kufanya kazi hiyo, hivyo ni juu ya Mufti Ahmad Twayyib kurejea kwenye kitabu hiki ili ajue kwamba sehemu kubwa ya Maswahaba hawakuafikiana na wenzao. Aidha Allamah Sayyid Ali Akhan Madaniy (aliyefariki mwaka 1120 A.H.) alimtangulia Dkt. Ahmad Wailiy katika kazi hiyo, katika kitabu chake ad-Darajatir-Rafiah Fii Twabaqatis-Shiah alImamiyyah, na akafuatiwa na wahakiki zaidi ya mmoja. Ama kuhusu suala la Maswahaba wengine kuacha uimamu wa Imam Ali na kuwafuata wengine, ni kwamba suala hili lilitokana na tafsiri binafsi na ijtihadi, ambapo wengi miongoni mwa Maswahaba 191


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

walikuwa wakitanguliza maslahi wanayoyaona wao juu ya tamko bayana. Na wala hili si eneo la kwanza ambalo chupa ilivunjika katika Uislamu, Maswahaba wana maeneo mengi ambamo waliacha tamko bayana wakafuata ijtihadi na rai binafsi. Hapa tutataja sehemu tu ya maeneo hayo: Eneo la Kwanza: Huzuni ya Siku ya Alhamisi: Bukhari ameandika kutoka kwa Ibn Abbas, amesema: "Mtume  alipozidiwa na maradhi yake, alisema: „Nileteeni karatasi ya kuandikia, niwaandikie maneno ambayo baada yake hamtapotea.‟ Lakini Umar akasema: „Hakika Mtume  amezidiwa na maradhi, na sisi tunacho Kitabu cha Allah. Kinatutosha.‟Hapo basi (maswahaba) wakakhitalifiana, na zogo likazidi, Mtume  akasema: „Niondokeeni! Haifai kuzozana mbele yangu.‟ Ibn Abbas akatoka huku anasema: „Msiba ulioje wa Mtume  kuzuiwa kuandika alichotaka kuandika.‟”182 Bila shaka umeona, Maswahaba waliokuwepo kwa Mtukufu Mtume  siku hiyo walikataa kutekeleza amri ya Mtukufu Mtume wakati akiwa hai, wakashikilia sababu na udhuru ambao kalamu inaona aibu kuuandika, ikiwa hali ni hivyo wakati wa uhai wake itakuwaje hali yao mbele ya maamrisho yake na maelekezo yake baada ya kifo chake?! 182

Sahih Bukhari: Kitabu cha elimu, namba 114.

192


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Eneo la Pili: Kupinga kwao Sulhu ya Hudaybiya: Ilipokamilika sulhu baina ya Mtukufu Mtume  na viongozi wa Mushirikina kwa kuzingatia maslahi yalivyotaka, Umar bin Khattab alikuja juu, alikuwa kashikwa na chuki, hakuweza kusubiri mpaka akaenda kwa Abu Bakri akiwa amezidiwa na hasira na ghadhabu, akasema: “Ewe Abu Bakri! Je, yeye si ni Mtume wa Allah?” Abu Bakri akasema: “Ndiyo, yeye ni Mtume wa Allah.” Akasema: “Je, sisi si ni Waislamu?” Abu Bakri akasema: “Ndiyo, sisi ni Waislamu.” Akasema: “Je, wao si ni Mushrikina?‟ Abu Bakri akasema: “Ndiyo, wao ni Mushrikina.” Akasema: “Basi ni kwa nini tuitie doa dini yetu?” Abu Bakri akamjibu: “Ewe mwanamume! Hakika yeye ni Mtume wa Allah, naye hamuasi Mola Wake.”183 Eneo la Tatu: Amri ya kujitoa katika ihramu: Ilipotimia sulhu ya Hudaybiya baina ya Waislamu na Mushrikina, waliafikiana kuwa Mtukufu Mtume  akomee hapo na arejee Madina, na arudi mwakani kufanya Umra katika wakati kama huo. Na miongoni mwa Waislamu alikuwemo aliyeambatana na mnyama wa kuchinja, hivyo Mtukufu Mtume akawaambia Maswahaba zake: “Nyanyukeni, mchinje na mnyoe.” Mpokezi anasema: “Wallahi hakusimama yeyote miongoni mwao, mpaka akasema 183

Sahih Bukhari, namba 2732. Sahih Muslim: 5/ 175.

193


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

hayo mara tatu. Na ilipokuwa hakusimama yeyote miongoni mwao, Mtume aliingia kwa Ummu Salamah na kumweleza ile hali aliyokutana nayo kutoka kwa watu, Ummu Salama akasema: „Ewe Mtume wa Allah umelipenda hilo? Toka kisha usimsemeshe yeyote miongoni mwao, mchinje ngamia wako na umwite kinyozi wako akunyoe.‟ Akatoka na hakumsemesha yeyote miongoni mwao na akafanya aliyofanya: Alimchinja ngamia wake na akamwita kinyozi wake akamnyoa. Walipoona hivyo ndipo wakasimama na wao wakachinja, na wakaanza kunyoana wao kwa wao, kiasi kwamba kwa hasira baadhi yao walikaribia kuwauwa wenzao wakati wa kunyoa.184 Hadithi hii na iliyotangulia zinajulisha kwamba, yale madai yaliyoshamiri baina ya watu kwamba Maswahaba walikuwa wakimtii Mtukufu Mtume  bila kusita kama kivuli kinavyomfuata mwenye nacho, ni madai yasiyo na msingi. Bali ukweli ni kwamba walikuwa wakiafikiana naye katika yale ambayo hayako kinyume na matamanio yao. Na ama maeneo ambayo wao walifanya ijtihadi baada ya kifo cha Mtukufu Mtume na kuzitolea tafsiri nususi, hayo ni mengi mno, na wala hatuna nafasi ya kuweza kuyaorodhesha yote bali tutaashiria maeneo machache tu kutoka katika hayo mengi. Tutataja maeneo 184

Sahih Bukhari, namba 2732.

194


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

mawili ili tu ujulikane msimamo wa Maswahaba wakubwa mbele ya nususi na kauli za Mtukufu Mtume . Eneo la Nne: Jeshi la Usamah: Mtume wa Allah  aliwaamuru Maswahaba zake wajiandae kutoa na kikosi ambacho alikiweka chini ya ukamanda wa Usamah bin Zaydi, na hiyo ilikuwa ni mwaka wa kumi na moja hijiriya, siku nne kabla ya kumalizika mwezi wa Swafar. Ilipofika siku ya pili, alimwita Usamah akamwambia: "Nenda kule alikouliwa baba yako. Mimi nimekuteua wewe kuwa kamanda wa jeshi hili.” Ilipofika tarehe 28 Swafar, Mtume  akaanza kushikwa na maradhi, alishikwa na homa kali na kichwa kumuuma.Kulipokucha tarehe 29 Swafar, na akaliona jeshi hilo bado halijaondoka, Mtume  alilitokea na kulihimiza liondoke mara moja. Ili kuwatia mori na kuwapa moyo, Mtume  yeye mwenyewe aliifunga bendera akampa Usamah kwa mkono wake mtukufu. Hata hivyo licha ya kusikia nususi zenye kubainisha wazi wazi wajibu wa wao kutoka haraka na jeshi hilo, hawakutoka na baadhi yao wakakosoa kitendo cha Usamah kupewa uongozi wa jeshi hilo. Yalipomfikia Mtukufu Mtume  maneno yao, alipanda mimbari, akasema: “Enyi watu! Ni kauli gani hizi zilizonifikia kutoka kwa baadhi yenu kuhusu kumpa ukamanda wa jeshi Usamah. Mkikosoa kumpa 195


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

kwangu ukamanda Usamah (hapana la ajabu), maana mlikwishanikosoa hapo kabla pale nilipompa ukamanda wa jeshi baba yake. Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu! Yeye alistahiki kuwa Kamanda. Na huyu (Usamah) anastahiki ukamanda huu baada yake.”Mtume  akawa anasema: “Jiungeni na jeshi la Usamah. Nendeni na jeshi la Usamah. Tokeni na jeshi la Usamah.” Aliendelea kuwahimiza kwa kuyarudia rudia maneno yake ingawa Maswahaba nao, kwa upande wao, waliendelea kutotii! Mwisho wake Usamah alitoka na wapiganaji elfu tatu, na hivyo baadhi ya watu ambao Mtume wa Allah aliwajumuisha katika jeshi la Usamah walikhalifu amri na hivyo hawakutoka naye, na hawakutii amri hiyo ya Mtukufu Mtume  mpaka Mtume anakutana na Mola Wake. Na haya hayakusababishwa na chochote isipokuwa ni kwa sababu wao walishikamana na nyudhuru mbovu, ya kwamba wao wana huruma zaidi na Mtukufu Mtume wakati alipokuwa amelala kwenye kitanda cha mauti, jambo hilo ndilo lililowazuia kuondoka. Wakati ambapo Mtukufu Mtume  alisema: “Jiungeni na jeshi la Usamah, Allah amlaani atakayejitenga nalo.”185 185

Taarikh Tabari, Juz. 1, Matukio ya mwaka 11 A.H. asSiratul-Halabiyyah: 3/209. As-Siratud-Dahlaniyyah: 2/240. Tabaqat Ibn Saad: 2/189 – 192. Al-Milal Wanahl cha Shahrastaniy: 1/23.

196


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Eneo la Tano: Kuondoa fungu la wenye kutiwa moyo: Allah alifanya wale wenye kutiwa moyo kuwa ni moja ya maeneo yenye kupata mgao wa Zaka, akasema: “Hakika sadaka ni ya (hawa) tu: Mafukara na masikini na wanaozitumikia na wanaotiwa nguvu nyoyo zao….”186, lakini Abu Bakri aliposhika madaraka walikuja hawa wenye kutiwa moyo, kuja kuchukua fungu lao hili, kama ilivyokuwa kawaida yao wakati wa Mtume wa Allah , Abu Bakri akawaandikia hati yenye kuwaruhusu kuchukua fungu lao, hivyo wakaenda na hati hiyo kwa Umar ili wakachukue fungu lao, yeye akaichanachana na akasema: “Hatuna haja na nyinyi, Allah amekwisha uimarisha Uislamu na hana haja nanyi, kwa hiyo mkisilimu mtasalimika vinginevyo upanga ndiyo utakaoamua baina yetu na ninyi.” Watu hawa walirudi kwa Abu Bakri wakamwambia: "Hivi wewe ndiye Khalifa au Umar? Umetupa fungu lakini Umar kachana hati.” Akasema: "Bali ni yeye Allah akipenda." Kisha akayapitisha aliyoyaamua Umar.187 Hatupo katika lengo la kuorodhesha maeneo yote ambayo watu hawa walikhalifu nususi na kauli za Mtukufu Mtume  na mafunzo yake, hakika maeneo hayo walimomkhalifu Mtume  yanaweza kufikia zaidi ya sabini, ni maeneo ambayo baadhi ya 186 187

Sura Tawba: 60. Ruhul-Maaniy cha Alusiy: 10/ 122.

197


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

maulamaa wameweza kuyaorodhesha. Sasa imebakia kuzungumzia maslahi waliyokuwa wakidai, ni maslahi yapi ambayo ndio hasa sababu ya wao kuacha maagizo na maamrisho ya Mtukufu Mtume ? Ibn Abil-Hadid Muutazaliy anasema: “Umar alisema: „Ewe Ibn Abbas! Hakika sahiba wako huyu ndiye mwenye kustahiki zaidi jambo hili (la ukhalifa) baada ya Mtume wa Allah, isipokuwa ni kwamba sisi tulimkhofia juu ya mambo mawili.” Aliendelea kueleza mpaka aliposema: “Ibn Abbas akasema: „Nikasema: Ni yapi hayo ewe Kiongozi wa Waumini? Akasema: Tulikhofia umri wake mdogo na kuwapenda kwake wana wa Abdul-Muttwalib.‟ Na katika sehemu nyingine ni kwamba alisema: „Tulichukia umri wake mdogo na kuwapenda kwake wana wa Abdul-Muttwalib.”‟188 Na Ibn Abil-Hadid amenukuu kutoka kwa Ahmad bin Abu Twahir, mwandishi wa kitabu Taarikh Baghdadiy kwamba amesema: “Niliingia kwa Umar mwanzoni mwa ukhalifa wake, nikamkuta kawekewa pishi la tende, akanikaribisha kula, nikala tende moja, naye akaanza kula mpaka akamaliza. Kisha akanywa kutoka kwenye jagi lililokuwa mbele yake, kisha akaegemea mto wake na akaanza kumuhimidi Allah kwa kurudia rudia, kisha akasema: „Umekuja kutokea wapi ewe Abdullah!‟ nikasema: Nimetokea msikitini. 188

Sharhu Nahjul-Balaghah: 6/ 51.

198


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Akasema: „Umemwachaje binamu yako?‟ nikadhani anamkusudia Abdullah bin Ja‟far, nikasema: Nimemwacha anacheza na vijana wa rika lake. Akasema: „Simkusudii huyo, namkusudia mkubwa wa nyumba yenu enyi watu wa nyumba ya Mtume.‟ Nikasema: Nimemwacha akimwagilia maji mitende ya fulani huku akisoma Qur‟ani. Akasema: „Ewe Abdullah, utawajibika kutoa fidia ya kuchinja mnyama kama utanificha, je kuna chochote kilichobakia katika nafsi yake kuhusu jambo la ukhalifa?‟ Nikasema: Ndiyo. Akasema: „Anadai kwamba Mtume wa Allah alimteua?‟ Nikasema: Ndiyo. Na nikuongezee kwamba, nilimuuliza baba yangu kuhusu madai yake, akasema ni kweli. Umar akasema: „Mtume wa Allah  alikuwa na kauli isiyothibitisha hoja wala kuondoa udhuru kuhusu jambo lake, na alikuwa akingojea wakati maalumukuliweka bayana jambo lake, hivyo wakati wa maradhi yake  alitaka kulitamka bayana jina lake, nikazuia hilo kwa sababu ya kuuonea huruma na kuulinda Uislamu. Naapa kwa Mola wa jengo hili, kamwe Makuraishi hawako tayari kujumuika kwake. Na laiti kama angemtawalisha basi kwa sababu yake wangesambaratika Waarabu kutoka pande zao zote. Mtume wa Allah alijua kuwa mimi nimejua kilichomo ndani ya nafsi yake hivyo akajizuia, na Allah hakutaka isipokuwa kupitisha aliyoyaamua.”‟189 189

Sharhu Nahjul-Balaghah: 12/ 20 – 21. Tazama pia uk. 53.

199


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Na Ibn Abdul-Hadid amenukuu sehemu nyingine mtazamo wa Khalifa kuhusu suala la unabii na ukhalifa kukusanyika katika nyumba moja, akamwambia Ibn Abbas kwa kusema: “Ewe Ibn Abbas! Hivi unajua kwanini watu walizuia Khalifa kutoka kwenu?” Akasema: “Hapana ewe Kiongozi wa Waumini.” Umar akasema: “Lakini mimi najua.” Akamwambia: “Ni kwa sababu ipi ewe Kiongozi wa Waumini?” Akasema: “Makuraishi hawakupenda kuona unabii na ukhalifa vinakusanyika pamoja kwenu ninyi, hivyo Makuraishi walijitazama wenyewe na hatimaye wakachagua, wakaafikiana na wakapatia.”190 Nususi hizi zinafichua sababu iliyopelekea Maswahaba kuacha tamko lililomteua Ali kuwa Khalifa. Hakika maelezo haya yanaonesha kwamba Khalifa hakuona kuwa ni jambo sahihi unabii na ukhalifa kukusanyika pamoja katika nyumba moja, wakati ambapo mkabala na mtazamo wake huu kuna utajo mtakatifu wa Allah unaoonesha kuwa unabii na uimamu ulikusanyika pamoja katika kizazi cha Ibrahim , Allah anasema: “Au wanawahusudu watu kwa alichowapa Mwenyezi Mungu katika fadhila yake? Basi tuliwapa watoto wa Ibrahim Kitabu na hekima na tukawapa ufalme mkubwa.”191 190 191

Sharhu Nahjul-Balaghah: 12/53. Sura Nisaa: 54.

200


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Hivyo ufalme mkubwa ni uimamu na ukhalifa uliotukuka ambao Allah aliwapa kizazi cha Ibrahim ikiwa ni pamoja na unabii, na akawatunuku usia. Tuliyoyataja ni matone kutoka katika mafuriko na ni machache kutoka katika mengi, miongoni mwa yale yanayoonesha kuwa kitendo cha watu kuipuuza hadithi ya Ghadir pamoja na nyinginezo mfano wake, zenye kujulisha uwalii na uongozi wa Ali , kilitokana na ijtihadi na tafsiri binafsi na maslahi yaliyofikiriwa. Kwani hakukuwa na shaka wala raiba yoyote katika nyoyo za waliohudhuria katika siku ya Ghadir, kwamba Mtukufu Mtume  alimfanya Ali Imamu wa watu na kiongozi baada yake. Hapa yamebakia mambo mawili: La Kwanza: Hakika Dkt. Ahmad Twayyib amedai kuwa hadithi ya Ghadir ni heshima makhususi aliyopewa Sayiduna Ali . Tunajibu kuwa: Ingekuwa madhumuni ya hadithi ya Ghadir ni kuonesha heshima makhususi kwa Ali, basi kusingekuwepo na dharura ya kuwakusanya watu wanaorudi kutoka Hijja, ambapo yeye  alipofika katika bonde la Khum karibu na Juhfah, eneo ambalo ndio mapandanjia ya njia za watu wa Madina, Sham na Irak, aliwaamuru watu kuteremka kutoka katika vipando vyao. Na yeye alikuwa miongoni mwa watu 201


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

waliokuwa karibu na Juhfah. Hivyo Mtume wa Allah  aliamuru kuwarejesha nyuma waliokuwa wametangulia mbele, na kuwangojea wale waliokuwa wamebakia nyuma, wote wakusanyike sehemu hiyo. Siku hiyo ilikuwa na joto kali kiasi kwamba mtu alikuwa akiweka joho lake juu ya kichwa chake au chini ya nyayo zake kutokana na kuchomwa na changarawe. Mtume  alitengenezewa kivuli kwa nguo iliyowekwa juu ya mti ili kumkinga na jua kali. Mtume  alipomaliza kuswali alisimama na kuanza kuwahutubia watu. Alisimama katikati ya watu juu ya vitanda vya ngamia na sauti yake iliwafikia watu wote waliokuwepo hapo. Alinyanyua sauti yake akamhimidi Allah na akahutubia mpaka mwisho wa hotuba yake. Hakika kutaja fadhila na heshima makhususi ya Ali hakuhitaji utangulizi wote huu na maandalizi yote haya. Nasi tunamuomba mheshimiwa Mufti, Mungu amhifadhi, arejee sababu ya kuteremka kauli ya Allah: “Ewe Mtume! Fikisha uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola Wako; na kama hutafanya, basi hukufikisha ujumbe Wake; na Allah atakulinda na watu. Hakika Allah hawaongozi watu makafiri.”192 Maulamaa zaidi ya mmoja miongoni mwa maulamaa wa Kisuni wametamka bayana kwamba, Aya hii iliteremka katika tukio la Ghadir. Na viashiria 192

Sura Maidah: 67.

202


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

vilivyopo katika Aya hii vinaunga mkono hilo, ambapo umuhimu wa maudhui ya kufikishwa ulifikia katika kiwango cha juu kabisa hadi ikasemwa kuuhusu: “Na kama hutafanya, basi hukufikisha ujumbe Wake;” Ni jambo gani hili ambalo kama hatalifikisha hatakuwa amefikisha ujumbe wa Mungu kwa ukamilifu? Wakati ambapo Mtukufu Mtume  ametumia miaka 23 ya umri wake mtukufu katika kufikisha ujumbe wa Mola Wake. Zaidi ya hapo ongezea kauli yake: “Na Allah atakulinda na watu”, kifungu hiki kinafichua unyeti wa jambo lenyewe, ambapo kutokana na unyeti wake limezungukwa na hatari na upinzani kutoka kwa wanafiki na kutoka kwa wale wenye nyoyo za maradhi. Mambo haya mawili yanaunga mkono kwamba Aya hii iliteremka katika jambo nyeti la kisiasa, ambalo kutolifikisha inahesabiwa kuwa ni kutofikisha ujumbe wote. Na kwamba katika kulifikisha kuna khofu juu ya nafsi na mali. Jambo hilo si lolote isipokuwa ni kutamka bayana uongozi wa juu wa jamii wa mtu kutoka katika nyumba ya Mtume wa Allah . Na miongoni mwa mambo yanayounga mkono kwamba hotuba ya Mtukufu Mtume  siku ya Ghadir haikuwa ni kwa ajili ya kuonesha heshima makhususi, ni riwaya walizozipokea maulamaa wakubwa wa Kisuni, akiwemo: 1. Ibn Asakir, katika wasifu wa Ali Bin Abutalib, amepokea kutoka kwa Abu Huraira kuwa alisema: 203


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

“Yeyote atakayefunga siku ya kumi na nane ya Dhulhija (mfungo tatu) ataandikiwa malipo ya funga ya miezi sitini, nayo ni siku ya Ghadir Khum, pale Mtume  aliposhika mkono wa Ali Bin Abutalib  na akasema: „Je mimi si ni mtawala wa Waumini?‟ Wakajibu: „Ndiyo ewe Mtume wa Allah.‟ Akasema: „Yeyote ambaye mimi ni mtawala wake basi Ali ni mtawala wake.‟ Umar bin Khattab akasema: „Hongera, hongera ewe mtoto wa Abutalib, sasa umekuwa mtawala wangu na mtawala wa kila Mwislamu.‟ Na ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha Aya.193 Al-Hakim al-Hasakaniy al-Hanafiy amepokea kwa sanadi yake kutoka kwa Abu Said al-Khudriy kwamba alisema: “Ilipoteremka Aya hii, Mtume wa Allah  alisema: „Allah ni mkuu kwa kuikamilisha dini, kwa kutimiza neema, kwa kuridhia Mola ujumbe wangu na kwa uwalii wa Ali. Ewe Mungu Wangu! Mpende mwenye kumpenda, kuwa adui wa yule mwenye kumfanyia uadui, msaidie mwenye kumsaidia na mtelekeze mwenye kumtelekeza.‟”194 La Pili: Dkt. Twayyib amesema: “Hakika Shia wamesema kuwa Maswahaba walihaini ahadi ya Allah na ahadi ya Mtume wake”.... aliendelea kusema hadi aliposema: “Kama Maswahaba walikuwa wahaini 193 194

Taarikh Damashaqi: 42/ 133. Shawahidut-Tanziil: 1/ 201, namba 211.

204


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

inakuaje Shia wamechukua Qur‟ani kutoka kwa Maswahaba kama Suni na wameifahamu kutoka kwao?!” Nasema: Sisi hatuwasifu kwa sifa hiyo aliyoitaja, kama ilivyotangulia. Bali sisi tunasema kwamba Qur‟ani Tukufu ndio Kitabu cha Allah ambacho Allah amechukua dhamana ya kukilinda dhidi ya kufikiwa na upotoshwaji na wala hakifikiwi na batili mbele yake wala nyuma yake, na Allah akasema: “Hakika ni juu Yetu kuikusanya na kuisoma.”195 Na hivyo hakuna mtoto wa mwanamke yeyote awezaye kutia upungufu wala kuzidisha chochote katika Qur‟ani Tukufu, bila kutofautisha baina ya Swahaba na asiyekuwa Swahaba. MHADHARA WA ISHIRINI NA TANO Siku ya Ishirini na Tano ya Mwezi wa Ramadhan, Mwaka 1436 A.H. Katika siku ya ishirini na tano ya Mwezi wa Ramadhan, mwaka 1436 A.H. Dkt. Ahmad Twayyib Mufti wa Azhar alisema: 1. Mimi sitaki kuanzisha fitina au farka baina ya Suni na Shia, hakuna kilichonisukuma kuendesha ratiba 195

Sura Qiyamah: 17.

205


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

hii isipokuwa ni kutaka tufahamiane kwa utulivu, kwa kuondoa sababu zinazopelekea mfarakano. Na kuzima njama za shetani mkubwa wa kimataifa zenye kuuelekea umma wa Kiislamu, kwa kuuongoza umma kwenye yale yenye kheri duniani na Akhera. 2. Hakika Ali aliwapa kiapo cha utiifu Abu Bakri na Umar na Uthman, na kama Mtukufu Mtume  angekuwa alimteua yeye kuwa Imamu basi asingeridhia kuwapa kiapo cha utiifu na angewapiga vita kama ilivyotokea baina yake na Muawiya baada ya miaka ishirini na tano. 3. Hakika uimamu wa kusimamia mambo ya serikali na wa kuteuliwa na Allah, hauingii akilini. Na kwa bahati mbaya sana ni kwamba nadharia hii ndio inayosababisha hivi sasa Suni kumuuwa Shia, na Shia kumuuwa Suni. 4. Hakika Shia wa mwanzo waliokuwa pembezoni mwa Ali hawakuutambua uimamu wa Imam Ali na uongozi wake baada ya Mtukufu Mtume , bali ni kwamba nadharia hii ilidhihiri katika karne ya pili ya hijriya. Tuliyoyataja ni muhtasari wa yale aliyosisitiza Mufti wa Azhar katika mazungumzo yake ya siku hii aliyokuwa akiyawasilisha katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, kwa njia ya runinga ya Misri. Nasi 206


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

tutalirejea na kulichambua kila moja kati ya mambo haya manne aliyosisitiza. Nasema: Ama kuhusu jambo la kwanza: Mheshimiwa Mufti ametaja kwamba lengo ni kungâ€&#x;oa na kuondoa vyanzo vya fitina na mfarakano, na kuuelekeza umma kwenye kufahamiana kwa utulivu. Hakika sisi tunalikaribisha lengo hili tukufu ambalo ndani yake kuna kuupa nguvu Uislamu na kulinda heshima yake. Lakini ilikuwa ni wajibu kwa Mufti, kabla ya kutoa muhadhara awakusanye maulamaa kutoka upande wa Suni na upande wa Shia kwenye meza ya mzunguko, ili wajadili mambo haya kielimu zaidi mbali na kelele za vyombo vya habari. Lakini ameacha njia hii sahihi kwa kutoa mhadhara kwenye runinga akibainisha tofauti zilizopo baina ya makundi mawili huku akiliunga mkono kundi moja na kulipinga lingine. Na kitendo hiki hakileti matokeo mazuri zaidi ya umwagaji mkubwa wa damu na kusambaratisha safu ya Waislamu, na hilo ni kinyume na anavyotarajia. Ama kuhusu jambo la pili, kwamba Ali aliwapa kiapo cha utiifu Makhalifa watatu, hakika katika historia halijapatikana jambo hilo, isipokuwa ni kwamba Ali alimpa kiapo cha utiifu Abu Bakri baada ya miezi sita, baada ya kifo cha binti wa Mtume wa Allah Fatimah Zahrau ď ‰. Imekuja katika Sahih Bukhari kwamba:......Abu Bakri hakumpatia chochote 207


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Bibi Fatimah  kutoka kile alichokuwa ameacha Mtume , na kwa sababu hiyo Bibi Fatimah  alimghadhabikia mno Abu Bakri,akamhama na kamwe hakuzungumza naye hadi kufariki kwake. Aliishi miezi sita tu tangu baba yake kufariki. Baada ya kifo chake, mume wake Imam Ali alimzika wakati wa usiku, na Abu Bakri hakuruhusiwa kushiriki katika mazishi, na alimswalia yeye mwenyewe Ali. Watu walikuwa wakimstahi Imam Ali wakati wa uhai wa Bibi Fatima  lakini baada ya kifo chake,watu walimgeuka Ali na kwa sababu hiyo akafanya sulhu na Abu Bakri na kumpa kiapo cha utiifu, na alikuwa hajampa kiapo cha utiifumiezi yote hiyo."196 Hivyo kama kiapo cha utiifu alichopewa Abu Bakri kingekuwa ni sahihi si fujo tupu, ni kwanini basi binti ya Mtume  naye ndiye Bibi Mbora kushinda wanawake wote wa ulinwenguni hakutoa kiapo cha utiifu mpaka kufa kwake, tena akiwa amemkasirikia Abu Bakri? Au Fatimah hakusikia kauli ya baba yake  aliposema: “Yeyote atakayekufa bila kutoa kiapo cha utiifu atakuwa amekufa kifo cha kijahiliya.”197 Je tunaweza kumtuhumu binti ya Mtume wa Allah  kwa hili lililopokewa ndani ya hadithi hii sahihi?! 196 197

Sahih Bukhari: 1036, namba 4241. Sahih Muslim: 56/ 22. As-Sunanu al-Kubra: 8/ 156.

208


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Na tunauliza tena, kwanini Ali  alichelewa kumpa Abu Bakri kiapo cha utiifu muda wote huu wa miezi sita?! Ndiyo, hakika Ali alipoona kuwa hawezi kufikia kiti cha ukhalifa, aliacha jambo hilo kwao kwa kuheshimu maslahi aliyoyaashiria katika baadhi ya hotuba zake, aliposema: “Sikufadhaishwa ila na kumiminika kwa watu kwa fulani, wakimpa kiapo cha utiifu. Niliuzuwia mkono wangu mpaka pale nilipoona kurejea kwa watu (kwenye ukafiri) wakiwa mbali na Uislamu, wakiwa wanalingania katika kuifuta Dini ya Muhammad , basi niliogopa ikiwa sintounusuru Uislamu na watu wake, kwa kuona dosari humo au mmong‟onyoko, itakuwa msiba mkubwa zaidi juu yangu kuliko kuukosa Ukhalifa wenu ambao ni starehe ya siku chache.Hutoweka kilicho kuwa kama yatowekavyo mazigazi, au kama yanavyotawanyika mawingu. Nikasimama katika matukio yale mpaka batili ilitoweka na kuyeyuka, na Dini kubaki katika amani na salama.”198 Ama kuhusu jambo la tatu, Dkt. Ameeleza kwamba uimamu wa kuteuliwa na Allah hauingii akilini na unazua ugomvi na mzozo baina ya Suni na Shia. Nasema: Nasikitika sana kwamba Dkt. Anaona kuwa uimamu ambao ni amri kutoka kwa Allah ni jambo lisiloingia akilini, wakati ambapo Mtukufu Mtume  198

Nahjul-Balaghah, Barua ya 62.

209


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

anaeleza usahihi wa uimamu wenye maana hii. Alieleza hilo pale alipojitambulisha kwa Bani Aamir ambao walikwenda Makka katika msimu wa Hijja. Alipowalingania kwenye Uislamu, mkubwa wao alisema kumwambia Mtume : “Tukikupa kiapo cha utiifu juu ya jambo lako, kisha Mungu akakupa ushindi juu ya wanaokupinga, je jambo hili litakuwa letu baada yako?” Mtukufu Mtume akasema: “Jambo limo mikononi mwa Allah, huliweka pale atakapo.”199 Na huyu hapa Ibn Sina (Avicena) anasema: “Na ukhalifa wa maandiko ndio sahihi zaidi, kwani huo haupelekei kwenye mfarakano, fujo na ikhtilafu.”200 Kisha la ajabu zaidi ni kitendo cha yeye Mufti kuona kuwa mapigano yanayotokea baina ya makundi mawili (Suni na Shia) yanatokana na itikadi ya kuamini kwamba, kiongozi wa juu lazima ateuliwe kwa maandiko kutoka kwa Mungu, wakati ambapo hakuna uhusiano wowote baina ya mambo hayo mawili. Ikiwa ukhalifa ni katika mambo ya matawi, na kuwepo ikhtilafu katika mambo ya matawi ni jambo la kawaida na lililoenea, ni ipi basi sababu ya Suni kumuuwa Shia? Bila shaka mapigano na mauwaji hayo ni matokeo ya kukuza tofauti na kuzinyanyua hadi kiwango cha imani na ukafiri, 199

Siratun-Nabawiyyah cha Ibn Hisham: 2/424 – 425. Shifaa: 452, Sehemu ya mambo yanayohusu Mungu, Makala ya kumi, Faslu ya tano. 200

210


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

ukuzaji unaofanywa na wafurutuada wenye misimamo ya kupindukia. Hakika damu zisizo na hatia ambazo zinamwagwa kila siku katika nchi za kingo mbili za mtoikiwemoYemen, zote ni matokeo ya fatwaza ukufurishaji zinazotolewa na asiye na elimu ya Kitabu wala Sunnah, na hautozuilika umwagaji huo mpaka kitendo hiki kibaya kidhibitiwe. Sayyid Amin amesema: “Hakika Sultani Salim aliuwa hukoAnatolia peke yake watu elfu arubaini, na inasemekana watu elfu sabini. Si kwa sababu yoyote isipokuwa ni kwakuwa tu wao ni Shia. Na katika kitabu al-Fusulul-Muhimmah imetajwa kwamba, Mufti Nuh al-Hanafiy alitoa fatwa ya kuwakufurisha Mashia na wajibu wa kuwauwa, hivyo katika kutekeleza fatwa hii waliuliwa maelfu ya Mashia kutoka katika mji wa Halab. Watawala wa Uthmaniyya walimuuwa Shahid Thaniy ambaye ni maarufu kwa uchaji Mungu wake. Na al-Jazzar aliyekuwa mtawala wa Acre huko Jabal Amil alifanya vitendo alivyovifanya al-Hajjaj huko Iraq. Al-Jazzar alinyangâ€&#x;anya mali za wakazi wa Jabal Amil na akachoma moto maktaba zao. Wakati maktaba hizo zinachomwa, katika maktaba ya Aali Khatun kulikuwa na enklopedia elfu tano, na mji wa Acre ukaendelea kuwaka moto kwa muda wa wiki nzima kutokana na vitabu vya wakazi wa Jabal Aamil, na 211


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

hakuna aliyesalimika na dhulma ya al-Jazzar isipokuwa yule aliyefanikiwa kukimbia.�201 Tunamuomba Mufti Twayyib arejee vizuri ukweli wa historia ya Waislamu ili tuweze kujua ni zipi sababu halisi za ugomvi uliojitokeza katika ulimwengu wa Kiislamu. Kwa mfano tu, tunaporejea kwenye vita vya Jamal na Suffin, uimamu kama ulivyo haukuwa na mchango wowote katika vita hivyo, bali vita vilisababishwa na kitendo cha baadhi ya watu kuuasi ukhalifa halali, kwa kisingizio cha kutafuta kulipiza kisasi cha damu ya Khalifa aliyeuwawa (Uthman). Ama vita vya Nahruwan, Makhawariji waliibuka kutokana na fikra ya kumkufuru Allah kwa sababu ya kuwapa watu mamlaka ya kuhukumu jambo la dini, kama walivyodai wao. Na ugomvi uliendelea na kukatokea ikhtilafu kubwa baina ya Waislamu katika zama za Bani Umayyah na Bani Abbas. Na baada ya kifo cha Harun Rashid kulitokea ugomvi mkubwa baina ya ndugu wawili, Amin na Maamun, na uimamu wa kuteuliwa na Mungu haukuwa na mchango wowote katika kuzua wala kuchochea ugomvi huo. Kisha ni kwamba imekuwaje Mheshimiwa Dkt, amepuuza hali ya kukufurishana na ugomvi uliotokea 201

Shiat Wal-Hakimuna cha Sheikh Mughniyyah: 195, amenukuu kutoka Aayanus-Shiah: 1/ 4.

212


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

baina ya Muutazilah na Ashairah. Huyu hapa Imam Ahmad – ikiwa ni kweli yale yaliyonukuliwa na Mahanbal – alisema: “Yeyote atakayedai kuwa Qur‟ani ni kiumbe basi huyo ni Jahmiyyah kafiri. Na yeyote atakayedai kuwa Qur‟ani ni maneno ya Allah na akanyamaza bila kusema kuwa si kiumbe, huyo ni khabithi zaidi kushinda wa kauli ya kwanza. Na yeyote atakayedai kuwa tuyatamkayo sisi na tuyasomayo sisi katika Qur‟anihayo yameumbwa, na Qur‟ani ni maneno ya Allah, basi huyo ni Jahmiy. Na yeyote asiyewakufurisha watu hawa na yeye ni mfano wao.”202 Je itikadi ya kuwa kuna maandiko yaliyomteua Imam atakayechukua ukhalifa baada ya Mtume  ina nafasi yoyote katika maneno yake?! Hiki hapa kitabu as-Sunnah cha Abdullah bin Ahmad, hajalisalimisha humo kundi lolote, humo imeandikwa: “Mur‟jiah203 202

Twabaqatul-Hanabilah cha Ibn Abi Yaala: 1/ 29. Murjiah ni moja ya makundi ya Kiislamu, wao wanaona kwamba kila mwenye kuamini upweke wa Allah hata kama atatenda dhambi kubwa kiasi gani haiwezekani kumhukumu kuwa ni kafiri, kwa sababu hukumu yake imo mikononi mwa Allah peke yake. Na itikadi ya kimsingi kwao wao ni kutokumkufurisha yeyote yule maadamu tu ni mwislamu aliyetamka shahada mbili, hata kama atatenda maasi kiasi gani. Hukumu yake wameiacha mikononi mwa Allah peke Yake, hivyo wao husema: “Maasi hayaidhuru imani chochote, na wala utiifu hausaidii chochote uwapo pamoja na ukafiri.” – Mtarjumi. 203

213


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

ni sawa na Msabai204 (uk. 616, na uk. 662), na Mur‟jiah ni Myahudi (uk. 662). Na kwamba hakuna watu wachafu kushinda Marafidha205 (hadithi 436) na kwamba wao wako mbali na Uislamu (1159).Na hakuna watu wenye kupingana zaidi na Uislamu kushinda Jahmiyyah na Qadiriyyah (Hadithi 2), na kwamba Jahmiyyah ni makafiri na pia Qadriyyah ni makafiri (Hadithi 1).” Je uimamu wa kuteuliwa na Mungu una nafasi yoyote katika ugomvi huu?! Na ni ipi nafasi ya uimamu wa kuteuliwa na Mungu katika suala la kuamini kuwa Mungu ana mwili, suala ambalo Ashairah waliwatuhumu nalo Mahanbali?! Na ni ipi nafasi yake katika suala la Taatwil, ambalo Mahanbal waliwatuhumu nalo Ashairah?! Na kutokana na masuala hayo zilimwagika damu nyingi. Bali ni kwamba chuki ilizidi bainaya wafuasi wa madhehebu manne ikafikia kiwango cha kukufu204

Hawa wametajwa na Allah katika Sura al-Baqarah, Aya 62. Usabai ni moja ya dini inayonasibishwa na Nabii Ibrahim  na kwamba iikuwa ni dini ya tauhidi. Na kwa mujibu wa mafunzo yake ni kwamba Uislamu ndio dini iliyo karibu nayo zaidi kuliko dini nyingine zote. Na wafuasi wake wanawafuata Adam, Shaythu, Idirisa, Nuhu, Sam mtoto wa Nuhu na Yahya bin Zakariya. Wafuasi wake walienea zaidi katika nchi za ukingo wa mto na Palestina. Na baadhi ya wafuasi wake bado wanapatikana katika nchi ya Iraq na Iran katika mkoa wa Ahwaz – Mtarjumi. 205 Hapa anawakusudia Mashia – Mtarjumi.

214


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

rishana wao kwa wao, huyu hapa Muhammad Ibn Musa al-Hanafiy Kadhi wa Damascus (aliyefariki mwaka 506) anasema: “Ningekuwa nina mamlaka yoyote basi ningechukua kodi ya Jizya206 kutoka kwa Mashafi.” Na Mshafi mmoja mwenye chuki binafsi alipoulizwa kuhusu chakula kilichodondokewa na mvinyo wa zabibu, alisema: “Chakula hicho atapewa mbwa au mfuasi wa madhehebu ya Hanafi.”207 Na mengineyo miongoni mwa ikhtilafu ambazo uimamu wa kuteuliwa na Mungu hauna kabisa mchango wowote katika kutokea kwake. Ama kuhusu jambo la nne, Dkt, amedai kwamba Shia wa mwanzo hawakuutambua uimamu wa Imam Ali kwa maana ambayo ilidhihiri katika karne ya pili. Nasema: Hakika Shia wa mwanzo ni Waislamu kutoka miongoni mwa Muhajirina na Ansari na waliofuata wao kwa wema katika watu wa vizazi vilivyofuatia, wale waliobakia katika msimamo ule ule waliokuwa nao wakati wa Mtume  katika suala la uongozi. Hawakubadilisha wala hawakumuacha (Ali) na wala hawakuelemea kwa mwingine, na wala hawakuchukua maslahi yaliyofikiriwa kwa kuacha 206

Hii ni kodi wanayolipa wasiokuwa Waislamu wanapoishi katika miji iliyo chini ya mamlaka na serikali ya Kiislamu – Mtarjumi. 207 Imam Swadiq wal-Madhahibul-Arbaa cha Asad Haydar: 1/ 190.

215


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

maandiko yaliyothibiti. Na kwa hali hiyo hao wakawa mfano halisi wa kauli ya Allah: “Enyi ambao mmeamini! Msitangulie mbele ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mjuzi.”208 Katika misingi na matawi wakakimbilia kwa Ali na kizazi chake kitoharifu. Wakajitenga na kundi jingine miongoni mwa wale ambao hawakutii maandiko yanayohusu ukhalifa, uwalii na uongozi wa kizazi cha Mtume. Ambapo kundi hilo jingine liliacha maandiko likachukua maslahi waliyoyaona wao. Shia wa maana hii walikuwepo katika zama za Mtukufu Mtume  na baada ya kifo chake. Shia hawana historia zaidi ya historia ya Uislamu, na wala wao si zao la mijadala ya kisiasa wala ya kitheiolojia, bali Uislamu halisi na Ushia halisi ni sarafu moja yenye sura mbili (kichwa na mwenge), sura moja inawakilisha Uislamu na sura nyingine inawasilisha Ushia. Hakika riwaya zilizopokewa kuhusu haki ya wafuasi wa Imam Ali kupitia ulimi wa Mtukufu Mtume  zinaondoa nikabu na kufichua sura halisi, na zinaonesha jinsi baadhi ya Muhajirina na Answari walivyoweza kumzunguka Wasii, hivyo wakajulikana na kutambulika kuwa ni wafuasi wa Ali katika zama za utume. Na kwamba Mtukufu Mtume  aliwasifu 208

Sura Hujurat: 1.

216


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

katika maneno yake kwamba wao ndio watakaofuzu siku ya Kiyama. Na kama una shaka na hili basi hebu twende pamoja kwenye riwaya zilizopokewa kuhusu jambo hili: 1. Ibn Mardawayhi ameandika kutoka kwa Aisha kwamba alisema: “Nilisema: Ewe Mtume wa Allah! Ni nani aliye kiumbe bora zaidi kwa Allah? Akasema : Ewe Aisha! Hivi hausomi: „Hakika walioamini na wakatenda mema hao ndio viumbe bora.‟”209 2. Ibn Asakir ameandika kutoka kwa Jabir bin Abdullah, kwamba alisema: “Tulikuwa kwa Mtukufu Mtume  mara akatokeza Ali, Mtume akasema; „Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu imo mikononi mwake. Hakika huyu na wafuasi wake ndio watakaofuzu siku ya Kiyama.‟ Hapo ikateremka Aya: „Hakika walioamini na wakatenda mema hao ndio viumbe bora.‟ Maswahaba wa Mtume wakawa wanasema atokezapo Ali: Amekuja mbora wa viumbe.”210 3. Ibn Adiy na Ibn Asakir wameandika kutoka kwa Abu Said: “Ali ndiye mbora wa viumbe.”211 209

Ad-Durul-Manthur: 6/ 589, Aya ya saba ya Sura al-Bayyinah. Ad-Durul-Manthur: 6/ 589, Aya ya saba ya Sura al-Bayyinah. 211 Ad-Durul-Manthur: 6/ 589, Aya ya saba ya Sura al-Bayyinah. 210

217


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

4. Ibn Adiy ameandika kutoka kwa Ibn Abbas kwamba alisema: “Ilipoteremka Aya: „Hakika walioamini na wakatenda mema hao ndio viumbe bora.‟ Mtume wa Allah  alisema: „Ni wewe na wafuasi wako, siku ya Kiyama mtaridhiwa nanyi mtakuwa wenye furaha.‟”212 5. Ibn Mardawayhi ameandika kutoka kwa Ali kwamba alisema: “Mtume wa Allah  aliniambia: Hivi haujasikia kauli ya Allah: „Hakika walioamini na wakatenda mema hao ndio viumbe bora.‟ Ni wewe na wafuasi wako. Mimi na ninyi tutakutana kwenye hodhi pindi mataifa yatakapokuja kwa ajili ya hesabu, mtaitwa wenye vipaji vya nyuso zenye kung‟ara.”213 6. Ibn Hajar amepokea hadithi katika kitabu chake as-Swawaiq, kutoka kwa Ummu Salamah, alisema: “Ulikuwa ni usiku wangu, na Mtukufu Mtume  alikuwa kwangu, mara akaja Fatimah na akafuatiwa na Ali (Allah awe radhi nao), Mtukufu Mtume  akasema: „Ewe Ali! Wewe na wafuasi wako ni watu wa peponi. Wewe na wafuasi wako ni watu wa peponi.”214 212

Ad-Durul-Manthur: 6/ 589, Aya ya saba ya Sura al-Bayyinah. Ad-Durul-Manthur: 6/ 589, Aya ya saba ya Sura al-Bayyinah. 214 As-Swawaiqul-Muhriqah: 161. 213

218


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

7. Ibn Athir amepokea katika kitabu chake anNihayah, kwamba Mtukufu Mtume  alimwambia Ali: “Ewe Ali! Wewe na wafuasi wako mtakuja kwa Allah mkiwa ni wenye kuridhiwa na wenye furaha. Na ataletwa adui yako akiwa ameghadhibika mwenye kukabwa.” Kisha Mtume alikunja mkono wake shingoni mwake kuonesha jinsi watakavyokuwa wamekabwa.215 8. Zamakhshariy amepokea ndani ya kitabu chake arRabiu kwamba, Mtume wa Allah  alisema: “Ewe Ali! Itakapofika siku ya Kiyama nitakimbilia kwa Allah Mtukuka, na wewe utakimbilia kwangu, na wanako watakimbilia kwako, na wafuasi wao watakimbilia kwao. Unaona ni wapi tutakapopelekwa?”216 9. Ahmad alipokea katika al-Manaqib kwamba Mtume wa Allah  alimwambia Ali : “Hauridhii kwamba wewe utakuwa pamoja nami peponi, na Hasan na Husein na dhuriya wetu watakuwa nyuma yetu. Na wake zetu watakuwa nyuma ya dhuriya wetu, na wafuasi wetu watakuwa kuliani na kushotoni kwetu?”217 215

an-Nihayah: 4/ 106. Rabiul-Abrari: 1/ 808. 217 As-Swawaiqul-Muhriqah: 161. 216

219


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

10. Tabaraniy amepokea kwamba Mtukufu Mtume  alimwambia Ali : “Watu wanne wa mwanzo kuingia peponi ni: Mimi, wewe, Hasan na Husein. Dhuriya wetu watakuwa nyuma yetu, na wake zetu watakuwa nyuma ya dhuriya wetu, na wafuasi wetu watakuwa kuliani na kushotoni kwetu.”218 11. Daylamiy ameandika kutoka kwa Mtukufu Mtume  kwamba alisema: “Ewe Ali! Hakika Allah amekusamehe wewe na dhuriya wako, na kizazi chako na familia yako na wafuasi wako.”219 12. Daylamiy ameandika kutoka kwa Mtukufu Mtume  kwamba alisema kumwambia Ali : “Wewe na wafuasi wako mtaletwa kwenye hodhi ilihali mkiwa hamna kiu tena wenye kutosheka, na nyuso zenu ziking‟ara. Na hakika adui zako wataletwa kwenye hodhi ilihali ni wenye kiu kali wamekabwa.”220 13. Maghazaliy amepokea kwa sanadi yake kutoka kwa Anas bin Malik kwamba alisema: “Mtume wa Allah  alisema: „Kuna watu sabini elfu kutoka katika umma wangu wataingia peponi 218

As-Swawaiqul-Muhriqah: 161. As-Swawaiqul-Muhriqah: 161. 220 As-Swawaiqul-Muhriqah: 161. 219

220


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

bila hisabu.‟ Kisha alimwelekea Ali na akasema: „Hao ni wafuasi wako na wewe ndiye imamu wao......‟”221 14. Ibn Hajar amepokea kwamba, Ali alipita mbele ya kundi la watu, wakasimama haraka na kumwendea, akawauliza: “Ninyi ni akina nani?” wakasema: “Ni miongoni mwa wafuasi wako ewe Kiongozi wa Waumini.” Akawaambia: “Kheri basi.” Kisha akawaambia: “Enyi watu! Mbona sioni kwenu ninyi alama za wafuasi wetu na pambo la vipenzi vyetu?” wakanyamaza kwa kuona haya, akasema mtu mmoja aliyekuwa pamoja naye: “Tunakuomba kwa haki ya yule aliyekutukuzeni nyinyi watu wa nyumba ya Mtume, akawateua na kuwafadhilisha, tueleze ni zipi sifa za wafuasi wenu.” Akasema : “Wafuasi wetu ni wale wenye kumtambua Allah, wenye kutekeleza amri ya Allah.”222 15. Swaduq (306 – 381 A.H.) amepokea kwamba Ibn Abbas alisema: Nilimsikia Mtume wa Allah  akisema: “Itakapofika siku ya Kiyama na kafiri

221 222

Manaqibul-Maghazaliy: 293. As-Swawaiqul-Muhriqah: 154.

221


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

akaona thawabu na neema za kudumu alizowaandalia Allah wafuasi wa Ali......”223 Nususi hizi nyingi zisizohitaji uchunguzi juu ya sanadi zake zinaonesha kwamba Ali  alikuwa tofauti na Maswahaba wengine, ambapo yeye alikuwa na Shia na wafuasi, na wao walikuwa na sifa na alama zenye kuwatambulisha katika zama za uhai wa Mtukufu Mtume  na baada yake. Na yeye  alikuwa akiwasifu na akiwapa habari za kufuzu kwao, na wao bila shaka hawakukengeuka hata kidogo kutoka kwenye njia ya Mtukufu Mtume na Uislamu. Na jambo hili linasisitiza ukweli wa Ushia na chanzo chake ambacho si tofauti na kuanza kwa dini na kuendelea kwake. MHADHARA WA ISHIRINI NA SITA Siku ya Ishirini na sita ya Mwezi wa Ramadhan, Mwaka 1436 A.H. Dkt. Ahmad Twayyib katika mhadhara wake huu alisisitiza mambo yafuatayo: 1. Kizazi cha kwanza cha Shia hakikuwa kinaitambua nadharia ya uimamu wa kuteuliwa na Mungu, kwa 223

Ilalus-Sharaiu: 156.

222


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

dalili kwamba Sayiduna Umar aliwapa ugavana baadhi ya watu kutoka katika wafuasi wa Sayiduna Ali ď ‚, akiwemo Salman Farisiy, Malik Ashtar na Hujru bin Adiy. Hivyo imedhihiri kwamba nadharia ya uimamu haikuwepo katika zama hizo. 2. Ameashiria vitabu viwili: Kimoja ni cha Ahmad alKatibu kinachoitwa As-Sunnah Was-Shia Wahdatud-Din Khilafus-Siyasah Wataarikh. Na cha pili ni cha Sayyid Ali Amin kinaitwa as-Sunnah Was-Shiah Ummatun Wahidah. Wa kwanza ameeleza kwamba watu wa mwanzo waliokuwa wamemzunguka Ali walikuwa na msimamo chanya na safi kwa Makhalifa watatu. Na ilipoisha karne ya kwanza ya hijriya na Shia kukutana na ugandamizaji mkubwa wa kisiasa kutoka kwa Bani Umayyah, ndipo ilipozuka –kama radiamali dhidi ya ugandamizaji huu - katika kundi hili dogo nadharia ya uimamu wa kuteuliwa na Mungu. 3. Mheshimiwa Mufti alihitimisha mazungumzo yake ya siku hii kwa kusema kwamba, sisi tuna haja ya kupata sauti adilifu kama hii, ambayo inaweza kuchangia katika safari ya kufahamiana baina ya Suni na Shia kwa misingi iliyo wazi. Nasema: Ama kuhusu jambo la kwanza, madai yake ya kwamba kizazi cha kwanza cha Shia hakikuitambua nadharia ya uimamu wa kuteuliwa na 223


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Mungu, kwa ushahidi wa kwamba Sayiduna Umar aliwapa ugavana baadhi ya wafuasi wa Sayiduna Ali , wakawa magavana katika baadhi ya nchi, hakika ushahidi wake hauna hoja yoyote juu ya lile analotaka kulithibitisha. Hakika msimamo wa watu hawa si kinyume na msimamo aliokuwa nao Imam Ali  ambaye aliunusuru Uislamu na Waislamu katika zama za Makhalifa watatu, kwa sababu hali ya watu kuritadi ilikuwa imekaribia kuumaliza Uislamu kama alivyosema yeye mwenyewe : “Mpaka pale nilipoona kurejea kwa watu (kwenye ukafiri) wakiwa mbali na Uislamu, wakiwa wanalingania katika kuifuta Dini ya Muhammad , basi niliogopa ikiwa sintounusuru Uislamu na watu wake, kwa kuona dosari humo au mmong‟onyoko, itakuwa msiba mkubwa zaidi juu yangu kuliko kuukosa Ukhalifa wenu ambao ni starehe ya siku chache.”224 Tangu siku Ali  alipotenganishwa na uwalii wa haki aliona kwamba kunyanyua sauti ya mzozo na kusimama pamoja na wafuasi wake ili kupambana, ni jambo litakalosababisha kuufuta Uislamu. Na hasa ukizingatia kwamba wanafiki bado wangalipo ndani ya Madina wameenea kila kona wanasubiri tu fursa ili waweze kuumaliza Uislamu. Upinzani wa Warabu kwa upande mmoja, na njama za wanafiki kwa upande wa pili, mambo hayo yalimlazimisha Imam 224

Nahjul-Balaghah: Barua ya 62.

224


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

 na wafuasi wake kwenda na mambo yalivyohitaji, na ni kwa ajili hiyo Imam Ali  alisema: “Kwa kweli munajua kuwa mimi ni mwenye haki nao (ukhalifa) zaidi kuliko mwingine yoyote asiye kuwa mimi, na ninaapa kwa jina la Allah! Nitamwachia ukhalifa (Uthman) maadamu kumwachia yeye mambo ya Waislamu yatakuwa katika amani na dhulma haitokuwa isipokuwa kwangu tu, nikitaraji ujira wa hilo na fadhila zake, na kujiweka mbali na mnachoshindania na kujiweka kando na kuyafikia mapambo yake ambayo mnagombania.”225 Wafuasi wake walimfuata wakaamiliana na Makhalifa pindi maslahi yanapohitajia hilo. Ama kuhusu lile alilosema kwamba kizazi cha kwanza cha Shia hakikuwa kinautambua mfumo wa uimamu, bila shaka umeshagundua katika mhadhara uliopita kwamba ukweli ni kinyume chake. Na kwamba Mtukufu Mtume  ndiye aliyepanda mbegu ya kwanza ya ushia, na akalilea kundi liliokuwa likisifika kuwa wao ni wafuasi wa Ali  katika zama za Mtukufu Mtume . Nafasi haituruhusu kutaja majina ya watu hawa ambao walijitoa kwa dhati kwa moyo wao wote katika kumtawalisha Ali, na hawakuwa wakimtambua kiongozi isipokuwa yeye. Hapa yanakutosha yale maelezo aliyoeleza Kardu Ali katika kitabu chake Khutwatus-Sham, amesema: 225

Nahjul-Balaghah: Hotuba ya 74.

225


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

“Kundi miongoni mwa Maswahaba wakubwa walijulikana kwa kumtawalisha Ali katika zama za Mtume wa Allah , mfano wao ni Salman Farisiy aliyesema: „Tulimpa kiapo cha utiifu Mtume wa Allah kuwa tutawanasihi Waislamu na kumtawalisha Ali bin Abutalib na kumpenda.‟ Na mfano mwingine ni Abu Said al-Khudriy ambaye anasema: „Watu waliamrishwa mambo manne lakini wakatekeleza mambo manne na wakaacha jambo moja.‟ Alipo ulizwa ni yapi hayo mambo manne, alisema: „Ni Swala, Zaka, Swaumu ya Mwezi wa Ramadhan na Hijja.‟ Akaulizwa ni lipi hilo moja waliloliacha? Akasema: „Ni kumtawalisha Ali bin Abutalib.‟ Akaulizwa je jambo hilo lilifaradhishwa pamoja na hayo manne? Akasema: „Ndiyo, lilifaradhishwa pamoja na hayo manne.‟ Na mfano mwingine ni Abu Dhari al-Ghaffariy, Ammar bin Yasir, Hudhayfa bin Yamani, na yule ambaye ushahidi wake ni sawa na ushahidi wa mashahidi wawili Khuzayma bin Thabit, Abu Ayubu al-Answariy, Khalid Ibn Said na Qaysu bin Saad bin Ubadah.”226 Kisha ni kwamba Shia wa karne ya mwanzo, kama walikuwa hawatofautiani na ndugu zao Suni katika misingi na matawi na wanaitakidi ukhalifa wa Makhalifa, kuanzia kwa Abu Bakri mpaka kwa Ali, ni kwanini basi waligandamizwa kama hakukuwa na 226

Khutwatus-Sham: 5/ 251.

226


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

tofauti yoyote baina yao na Waislamu wengine? Mpaka wakimbilie kuanzisha nadharia ya uimamu wa Ali na wanawe katika karne ya pili? Kwani kule tu wao kumpenda Ali na watoto wake si kigezo chenye kuhalalisha ukandamizaji dhidi yao, kwa sababu Waislamu wote wanashirikiana katika kuwapenda watu wa nyumba ya Mtume . Ndiyo, Ahmad AlKatibu amesahau au amejisahaulisha sababu ya ukandamizaji huu waliofanyiwa. Hakika ni kwa sababu wao walikuwa wakinadi uwalii wa Ali baada ya Mtume , na walikuwa wanaona kuwa ukhalifa wa wengine si ukhalifa sahihi, na hatimaye si sahihi ukhalifa wa waliokuja baada ya Ali kama vile Muawiya na wanawe. Hivyo hiyo ikawa ndio sababu ya wao kukandamizwa, na kujitoa kwao kwa dhati katika kuwapenda Ahlulbayti na kuwafanya vigezo na viongozi katika maisha yao haikutokana isipokuwa na matamko sahihi waliyoyapokea kutoka kwa Mtukufu Mtume , na wala si radiamali ya ukandamizaji waliofanyiwa. Ama kuhusu lile aliloashiria mheshimiwa Mufti, la sauti adilifu, kwakweli huko si kuwasilisha sauti adilifu, bali huko ni kutaka kuuyeyusha ushia ndani ya usuni, na hili ni muhali. Ni kama ambavyo ni muhali kuuyeyusha usuni ndani ya ushia. Sauti adilifu ni kuchukua maeneo ya ushirikiano yaliyopo baina ya makundi mawili na kurejesha mada za kitheiolojia kwenye vyuo vya kielimu baina ya maulamaa. Na la ajabu ni kwamba mheshimiwa Mufti amesema 227


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

kumwambia Ahmad al-Katib na Sayyid Amin kuwa kuna dharura ya kuwepo sauti adilifu, akimuonesha shuhuda kwamba hiyo si hali ya nadra katika jamii ya Shia, na kwamba hali iliyoenea katika vyuo vya kishia ni ufurutuada na upindukiaji. Ni kana kwamba haijui ile sauti ya umoja iliyoweka mfano bora zaidi katika usawa katika muda wote wa historia. Hawa hapa maulamaa wa Kishia na Marjaa wao wanajitolea kufanya mapinduzi dhidi ya Uingereza katika Mapinduzi ya Ishirini, kisha wanaikabidhi serikali mikononi mwa ndugu zao Suni ndani ya sahani la dhahabu. Na kabla ya hapo walisimama upande wa kiongozi wa utawala wa Uthmaniyyah aliyekuwa Suni, licha ya kwamba yeye aliwanyima silaha na hakuweza kuwasaidia kwa chochote, bali baadhi ya watawala wa utawala huo walikula njama dhidi ya Mashia. Na pindi mashambulizi ya Marekani yalipozidi dhidi ya serikali ya Sadam, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilimnyima mvamizi Mmarekani kutumia sehemu yake ya anga, bahari na hata nchi kavu, licha ya maovu na jinai alizozitenda Sadam dhidi ya raia wa Iran. Na pindi Sadam alipoivamia Kuweit, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilisimama upande wa ndugu zao Wakuweiti, huku ikifahamu fika kwamba wao Wakuweiti waliisaidia serikali ya chama cha Baath (Serikali ya Sadam Husein) na waliipa kila ilichohitajia wakati wa vita vya uchokozi dhidi ya Iran. Na baada ya kuanguka kwa serikali ya Sadam 228


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

mwaka 2003 A.D. Shia walifungua na kuziacha wazi nyoyo zao kabla ya majumba yao na wakaomba kufungua ukurasa mpya, isipokuwa jibu walilojibiwa lilikuwa ni kali sana, na hivyo fungu lao likawa ni mabomu ya kujilipua yaliyokuwa yakilipuliwa, na katika hayo asilimia tisini na tano yalikuwa yakilipuliwa katika maeneo na miji ya Mashia na kuwauwa Mashia. Likiwemo lile lililobomoa kuba la Maimamu wawili . Na tukio la daraja la Maimamu huko Baghdad ambalo liliondoka na wahanga zaidi ya 1500 waliokufa kishahidi. Pamoja na yote hayo ofisi ya Marjaa wa Kishia inayoongozwa na Sayyid Sistaniy Mungu amhifadhi ilitamka wazi kwamba: “Msiseme ndugu zetu Masuni, bali semeni nafsi zetu Masuni.” Aidha tusisahau mchango wa Seminari kuu ya Qum na Marjaa wake wakubwa katika kuharamisha kuyavunjia heshima matukufu ya Suni, na kusimama upande wa Afghanistan na Hamas ambao wote ni Masuni, na kubeba jukumu kubwa katika kuwasaidia kwa mali na silaha na kusimama pamoja nao kisiasa. Ndiyo, ewe mheshimiwa Mufti, Shia walisimama na wataendelea kusimama upande wa ndugu zao Masuni, kwa sababu huo ni mwenendo waliourithi kutoka kwa Maimamu wa uongofu . Na ninatamani kwamba Dkt. Ahmad Twayyib angefuatilia uhusiano wa upendo ulioenea katika mitaa ya Iran baina ya Suni na Shia ili ajionee bila shaka udugu uliyopo baina ya 229


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

makundi mawili, na jinsi gani mwislamu Suni anaishi pembezoni mwa ndugu yake Shia, licha ya uwepo wa baadhi ya majaribio ya baadhi ya nchi za jirani ya kutaka kuchafua hali ya hewa kwa kuwachochea baadhi ya wasiojitambua na wapinzani. Ama kuhusu tathmini juu ya vitabu hivyo viwili alivyovigusia Mufti, hilo linahitajia kutunga kitabu kamili chenye kujitegemea. Ahmad al-Katibu amefanya upotoshaji mwingi katika makumi ya riwaya ili kuunga mkono fikra zake. Katika hilo kinatutosha kitabu alichoandika Ustadh Haydar Muhammad Ali al-Baghdadiy at-Twahan katika kitabu chake Wahatul-Yaqin. Ama kuhusu kitabu cha pili, maneno kukihusu yatakufikia katika uchambuzi wa nukuu alizonukuu katika mhadhara ufuatao. MHADHARA WA ISHIRINI NA SABA Siku ya Ishirini na Saba ya Mwezi wa Ramadhan, Mwaka 1436 A.H. Katika mazungumzo yake ya siku hii yaliyokuwa yakirushwa katika runinga ya Misri kabla ya kufuturu, Mufti wa Azhar aliendelea na mazungumzo kwa kusema: “Jambo jipya ambalo linaweza kusomwa kutoka katika kitabu cha Sayyid Ali Amin, ni kwamba anatofautisha baina ya uimamu wa kidini na 230


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

uimamu wa kisiasa. Uimamu wa kidini unamaanisha kuwepo mtu aalimu mchamungu ambaye atafuatwa na kurejelewa katika mambo ya dini na katika mambo mazito, na akusudie kuwaongoza watu kwa maneno yake. Ama uimamu wa kisiasa unamaanisha mtu ambaye atasimamia serikali na kuendesha mambo ya kijamii na kutekeleza sharia na adhabu na kumrudishia haki mdhulumiwa, akimaanisha mambo ya kidunia ya maisha ya kijamii. Hivyo kuna Imam wa maisha ya kidini na Imam wa maisha ya kijamii, na tofauti kati ya hayo mawili ni kubwa.” Mufti wa Azhar akaongeza kwamba: “Sayyid Ali Amin anaona kwamba kulitokea mkanganyiko kwa Mashia wengi baina ya mas‟ala ya uimamu wa kidini na mas‟ala ya uimamu wa kisiasa.” Nasema: Hakika sisi hatujakipata kitabu cha Sayyid Ali Amin, bali nahukumu nadharia yake kulingana na alivyoinukuu Mufti Twayyib. Kwani si jambo jipya bali ni nadhariya ya Kimagharibi ya kutenganisha baina ya dini na siasa, ameathiriwa na kauli mashuhuri: “Ya Kaisari mpe Kaisari, na ya Mungu mpe Mungu.” Itawezekanaje kukubali kutenganisha wakati Qur‟ani Tukufu inakusanya pamoja kwa kizazi cha Ibrahim vyeo vyote viwili, Allah anasema:

َ َ​َ ‫ۖ ق ءاؤينا‬

َ َ ّ ‫َ َ ُ َن‬ ٰ ‫اا َ ٰل ما‬ َ ‫الن‬ ‫ءاؤت ُ ُم الّل ُـه ِمن ِّل ِه‬ ‫ي ح و‬ ٰ ٰ َ ً َ َ ‫ءال إ ٰبز‬ َ ‫ّيم الكتـ َب َوالح‬ ً َ ‫كمت َوءاؤينـ ُ م ُمّلكا‬ َ .‫ظّيما‬ ِ ِ ِ 231


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

“Au wanawahusudu watu kwa alichowapa Mwenyezi Mungu katika fadhila yake? Basi tuliwapa watoto wa Ibrahim Kitabu na hekima na tukawapa ufalme mkubwa.”227 Kupewa kitabu na hekima ni alama ya unabii, na kupewa ufalme mkubwa ni serikali na ukuu. Mwandishi katika nadharia yake hii aliathiriwa na ile riwaya iliyopokewa kutoka kwa Umar bib Khattab, ambapo alimwambia Ibn Abbas: “Ewe Ibn Abbas! Hivi unajua kwanini watu walizuia Khalifa kutoka kwenu?” Akasema: “Hapana ewe Kiongozi wa Waumini.” Umar akasema: “Lakini mimi najua.” Akamwambia: “Ni kwa sababu ipi ewe Kiongozi wa Waumini?” Akasema: “Makuraishi hawakupenda kuona unabii na ukhalifa vinakusanyika pamoja kwenu ninyi, hivyo Makuraishi walijitazama wenyewe na hatimaye wakachagua, wakaafikiana na wakapatia.”228 Imepokewa kutoka kwa Imam Muhammad al-Baqir  kuhusu kauli ya Allah: “Au wanawahusudu watu kwa alichowapa Mwenyezi Mungu katika fadhila yake? Basi tuliwapa watoto wa 227 228

Sura Nisaa: 54. Sharhu Nahjul-Balaghah: 14/ 53.

232


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Ibrahim Kitabu na hekima na tukawapa ufalme mkubwa.”229 Kwamba alisema: “Aliweka Mitume na Manabii na Maimamu kutoka kwao. Inakuwaje wanakubali kuhusu kizazi cha Ibrahim lakini wanakataa kuhusu kizazi cha Muhammad .” Mpokezi anasema: “Nikasema: Vipi kuhusu „Na tukawapa ufalme mkubwa‟, akasema : „Ufalme mkubwa ni kwamba ameweka kwao Maimamu, na yeyote atakayewatii wao atakuwa amemtii Allah, na atakayewaasi wao atakuwa amemuasi Allah. Huo ndio ufalme mkubwa.‟”230 Hakika uimamu kwa maana ya maisha ya kidini halikuwa ni jambo makhususi kwa ajili ya Imam, bali baina ya Maswahaba alikuwepo aliyekuwa anafaa kuwa kigezo, miongoni mwa wale waliofikia katika kiwango cha juu cha imani na uchamungu. Ni kwanini basi Shia walishikamana na Ali  na wakamkataa mwingine asifikie cheo hiki kikubwa? Na hali hii inafichua kwamba uimamau wake ulikuwa ni jambo ambalo hawezi kulivaa isipokuwa yeye tu, nao si mwingine bali ni uongozi wa jumla katika dini na dunia. Kisha Dkt. Alinukuu kwamba Sayyid Amin alithibitisha nadharia yake hii kwa maneno ya Imam Ali  pindi watu walipomwendea ili kumpa kiapo cha 229 230

Sura Nisaa: 54. Al-Kafiy: 1/ 160.

233


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

utiifu baada ya kuuwawa Uthman bin Affan, ambapo alisema: “Niacheni na tafuteni mtu mwingine, kwa kuwa sisi twatazamia jambo lenye sura nyingi na rangi nyingi..." akasema baada ya kunukuu maneno ya Ali : “Yaani niacheni na mchagueni mwingine asiyekuwa mimi. Ni bora niwe mwenye kunasihi, mwenye kuamrisha mema na kukataza maovu miongoni mwenu, kuliko kuwa kiongozi wenu mwenye kusimamia uimamu na siasa.” Haya tutayajadii katika mhadhara ufuatao kwa taufiki ya Allah inshaallah. MHADHARA WA ISHIRINI NA NANE Siku ya Ishirini na Nane ya Mwezi wa Ramadhan, Mwaka 1436 A.H. Dkt. Twayyib alisema: “Hakika kauli ya Imam Ali : „Niacheni na tafuteni mtu mwingine.......Na mkiniacha (musiponipa kiapo chenu cha utiifu) mimi nitakuwa kama mmoja yeyote miongoni mwenu. Na huenda nitakuwa mwenye kumsikiliza na kumtii sana mtakayemtawalisha hili suala lenu, na mimi kuwa waziri kwenu ni bora kuliko kuwa amiri.‟ Inaonyesha kwamba yeye (r.a.) kamwe hakutaka uimamu wa kisiasa na wala haukuwemo kichwani mwake bali alikuwa anaukimbia. Na hii ilikuwa baada ya kuuwawa Uthman ambapo uwanja ulikuwa wazi mbele yake kuweza kuchukua uimamu wa Waislamu. 234


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Na hiyo ndio maana ya niacheni na tafuteni mtu mwingine. Nasema: Hakika Imam Ali  ana maneno mengi yenye madhumuni haya. Aliwahi kumwambia Ibn Abbas akiashiria viatu vyake: “Vina thamani gani viatu hivi?” Akasema: “Havina thamani yoyote.” Akasema : “Wallahi navipenda zaidi kuliko uongozi wenu huu.”231 Lakini kutumia maneno haya kama dalili inatokana na kutotambua ni wakati gani alitamka kauli hizi, na ni katika hali gani alikataa kiapo cha utiifu cha watu hawa na akasema: “Niacheni na tafuteni mwingine asiyekuwa mimi.” Na ni ukhalifa upi alioukataa na akasema kuuhusu yale aliyoyasema. Hakika wale waliotaka kumpa kiapo cha utiifu ndio hao hao waliowapa kiapo cha utiifu Makhalifa waliotangulia. Na Uthman alikuwa miongoni mwao, na alikuwa amejipendelea katika mali ya Waislamu, alipouwawa wakamwambia Ali: “Tunakupa kiapo cha utiifu kwa sharti utuongoze kwa sira ya Mtukufu Mtume.” Akawakatalia na akawaomba wamtafute mwingine asiyekuwa yeye. Kisha mwishoni mwa maneno yake akataja sababu ya kutokukubali kwake, akasema: “Niacheni na tafuteni mtu mwingine, kwa kuwa sisi twatazamia jambo lenye sura nyingi na rangi nyingi, nyoyo haziwezi 231

Nahjul-Balaghah: Hotuba ya 33.

235


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

kuvumilia wala akili haziwezi kulibeba. Kwa kweli mstari wa upeo wa macho umefunikwa na mawingu, na njia iliyonyooka haijulikani tena.”232 Akiashiria kwamba utata umezitawala akili na nyoyo, na watu wengi hawaijui njia ya haki. Katika mazingira kama haya mimi siwezi kuwaongoza kwa sira ya Mtukufu Mtume  aliyoitekeleza kwa Maswahaba zake kwa uhuru na ufanisi, kutokana na kuharibika kwa hali zenu na kutokutengemaa kwenu. Na haya aliyoyasema yalitimia, kwani Imam  alipochukua dola na kugawa mali baina yao kwa uadilifu, kuna kundi lilivunja kiapo, jingine likaasi na lingine likapetuka.233 Lile alilolikataa Imam ni ule ukhalifa wa kupewa kwa njia ya kiapo cha utiifu, ama ukhalifa wa kuteuliwa na Mungu ambao Allah alimvisha katika siku ya Ghadir na siku nyinginezo haukuwa ni pendekezo walilopewa watoaji wa kiapo cha utiifu wala Imam mwenyewe, ili aukatae au aukubali. Ama ule ukhalifa ambao watu wanautoa kwa njia ya kutoa kiapo cha utiifu, Imam na mwingine asiyekuwa yeye wote wako sawa mbele ya ukhalifa wa namna hiyo, na ni aina hiyo ya ukhalifa ndio aliyosema Imam: “Niacheni na tafuteni mwingine asiyekuwa mimi.” Ama ukhalifa wa kuteuliwa na Mungu wanaodai Shia kupitia nususi 232 233

Nahjul-Balaghah: Hotuba ya 92. Nahjul-Balaghah: Hotuba ya 3.

236


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

nyingi wenyewe hauhitaji kiapo cha utiifu isipokuwa kutii na kufuata. Na wala watu hawako sawa mbele ya uimamu huo, bali unamhusu yule aliyeteuliwa na Allah kwa ajili ya uimamu huo. Na yule aliyeteuliwa kwa ajili ya uimamu huo hana haki ya kuukataa wala kujiuzulu. Na uimamu kwa maana hii sio uliowasilishwa wakati wa mazungumzo hata Imam aukatae. Nawala haya si maneno ya mwanzo na mwisho ya Imam kuhusu kukataa kwake kiapo cha utiifu cha watu hawa, hata kama watamng‟ang‟aniza vipi, anasema: “Mliukunjua mkono wangu, nami nikaurudisha. Mliunyoosha nikaukunja. Halafu mlisongamana kwangu, msongamano wangamia wenye kiu wanapopelekwa kwenye madimbwi yao siku ya kwenda kwao (kunywa maji) hadi ndara zilikatika, na joho lilianguka, na mnyonge alikanyagwa. Na furaha ya watu kunipa kwao mimi kiapo cha utiifu ilikuwa bayana kiasi kwamba, watoto waliifurahia, na wakubwa walijikokota kuielekea, mgonjwa alijivuta kuielekea, na nyuso wazi (baadhi ya wasio kuwa na nikabu) zilimiminikia kuelekea huko.”234 Nasema: Hakika wale waliokuja ili kumpa kiapo cha utiifu Ali  miongoni mwa Maswahaba na Tabiina, walijaribu kutaka kumpa kiapo cha utiifu kama walivyowapa kiapo cha utiifu Makhalifa walio234

Nahjul-Balaghah: Hotuba ya 229.

237


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

tangulia, hivyo katika hali hii ni kwamba Khalifa anategemea uhalali wa ukhalifa wake kutoka kwenye kiapo cha utiifu cha watu. Na jambo hilo ndilo alilolikataa Imam na kwa kutambua kwamba, hawa wenye kumpa kiapo cha utiifu hawawezi kutaamali uadilifu wake na maamuzi yake. Wapi na wapi hilo mbele ya ukhalifa wa kuteuliwa na Mungu uliyothibiti kwa tamko la Mtukufu Mtume  alilolitoa katika maeneo zaidi ya moja?! Hakika wenye kutoa kipo cha utiifu katika mazingira hayo magumu hawakuwa na hamu yoyote isipokuwa kumsimika Khalifa, bila kutazama uimamu wa kuteuliwa na Mungu wa Ali , mpaka Imamu aukatae au aukubali. Na mwishoni tunapenda kuashiria nukta moja, nayo ni kwamba kiapo cha utiifu alichopewa Ali  kwa namna aliyoielezea Imam mwenyewe  kilikuwa ni tukio la kipekee, halikuwa na mfano wake kutoka kwa Makhalifa waliomtangulia. Pamoja na hayo tunaona kwamba dola ilipotua mikononi mwa Imam  ulidhihiri uasi ambao ulishughulisha akili yake, kuanzia alipochukua ukhalifa wa namna hiyo mpaka kufa kwake kishahidi. Kisha Imam mwishoni anabainisha sababu iliyompelekea kukubali kiapo cha utiifu cha watu hawa, licha ya kutokuutaka ukhalifa huo, anasema katika hotuba yake nyingine: “Angalia! Naapa kwa yule ambaye ameatua (ameiotesha) mbegu na kumuumba mwanadamu, lau si kufika kwa watu 238


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

na kulazimu hoja kwa kuwepo wasaidizi (askari wa kumnusuru) na ahadi iliyochukuliwa na Allah kwa wanachuoni, kuwa wasiridhike kimya kimya na ulafi wa madhalimu na kusagwa (kuvizwa) kwa haki ya mdhulumiwa, ningeitupa kamba ya Ukhalifa kwenye bega lake (ninge tupilia mbali suala la ukhalifa bila kujali) na ningemtendea wa mwisho kama wa kwanza. Na mngeona kwa maoni yangu ya kwamba, hii dunia yenu si bora kuliko chafya (kamasi) ya mbuzi.”235 MHADHARA WA ISHIRINI NA TISA Siku ya Ishirini na Tisa ya Mwezi wa Ramadhan, Mwaka 1436 A.H. Dkt. Ahmad Twayyib, Mufti wa Azhar, katika mhadhara huu ambao ndio mwisho wa mazungumzo, alisisitiza kwamba Azhar ndio taasisi ya kidini yenye shauku kubwa kuliko zote na umoja wa Waislamu, akasema: “Hakika mazungumzo yetu katika kipindi cha Mwezi mtukufu wa Ramadhan, hatukukusudia kwa mazungumzo hayo kuzua mfarakano au kuamsha chuki baina ya Suni na Shia.” Mheshimiwa akaendeleza mazungumzo yake kwa kusema: “Hakika Azhar hailazimishi kamwe rai yoyote, kwa sababu Allah Mtukuka anasema: „Sema hii ni kweli itokayo 235

Nahjul-Balaghah: Hotuba ya 3.

239


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

kwa Mola Wenu, basi atakaye aamini na atakaye akufuru.‟ Lakini tunasema: Njooni tukutane katika misingi iliyo bayana yenye kuzuia kutumbukia katika fitina. Njooni tusimamishe umwagikaji wa damu unaotokea baina ya Waislamu.” Mheshimiwa akaongeza kwamba: “Misri ni nchi ya Kisuni na wala hatutaki raia wake Waislamu wageuke na kuwa makundi mawili yenye kuuana kwa ajili ya madhehebu. Na hakika Misri hakuna Shia, na kwa ajili hiyo linalotafutwa sasa ni kuanzisha fitina humu kwa kuanzisha kundi la vijana lenye kufuata madhehebu ya Shia.” Kisha aliyaongezea nguvu maneno yake kwa utabiri wa Bernard Lewis kuhusu Mashariki ya Kati, anasema: “Hivi punde wala si muda mrefu historia itajirudia katika eneo hili (la Mashariki ya Kati) – anakusudia ugomvi baina ya Suni na Shia –kwa kudhihiri waziwazi. Uturuki ya Kiislamu na Iran ya Kiislamu zitagombania uongozi, na ushindani huo utakuwa kama ulivyokuwa tangu karne zilizopita baina ya madhehebu mawili: Suni na Shia.” Na mwishoni mwa maneno yake Mheshimiwa Mufti aliwaomba maulamaa wa Shia wakutane na wale wa Azhar ili kutoa fatwa ya pamoja, kutoka kwa Marjaa wa Kishia na kutoka kwa maulamaa wa Kisuni, itayoharamisha Shia kumuuwa Suni, na Suni kumuuwa Shia. 240


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Nasema: Hakika kuyakurubisha pamoja makundi ya Kiislamu ni miongoni mwa matumaini matukufu anayoyatamani kila Mwislamu mwerevu wa mambo, hasa katika mazingira nyeti na yaliyopo sasa kwa Waislamu, mazingira yaliyowazunguka katika pande zote za ulimwengu na katika miji yote. Na hakuna mwenye shaka na udharura huo isipokuwa watu wa namna mbili: Mjinga aliyejisahau na mpingaji mwenye kiburi. Kwani hakuna siku inayowapitia Waislamu isipokuwa kuna mauwaji makubwa yaliyowapata na vita vya kumwaga damu vilivyolazimishwa kwao na nguvu ya ukafiri. Nguvu ambayo inakhofia kuenea kwa Uislamu ulimwenguni, hivyo imekuwa ikikoleza na kuchochea moto wa vita baina ya muda huu na ule. Mara mwislamu anapigwa na mwislamu mwenzake, na mara anapigwa na kafiri, na hatimaye nguvu hiyo inatimiza malengo yake. Kutokana na hali hii, suala hilo la kukutana ni rai inayoafikiwa baina yetu na Dkt. Ahmad Twayyib Mungu amhifadhi. Na ushahidi juu ya hilo ni kwamba maulamaa wa Shia walikubaliana na Mufti wa Azhar wa wakati ule, Mufti Mahmud Shaltut, kuanzisha Jumuiya ya Kuzikurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu. Na walitumiana barua Mamufti wa Azhar na Marjaa wa Kishia kama vile Ayatullah Burjurdi na wengineo. Hivyo nukta hii ni jambo analolijua mwenye utambuzi na hali ya kuumiza iliyopo katika jamii zetu za Kiislamu. 241


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

Ndiyo, Mufti wa Azhari anakerwa na uwepo wa uhubiri wa kuhubiri ushia ndani ya nchi ya Misri, na kwamba ni nchi ya Kisuni si ya Kishia, lakini tunamuuliza Ustadhi ni kwanini hakerwi na uhubiri wa kuhubiri ukristo ndani ya Misri, uhubiri ambao una makumi ya miaka mpaka hata Wamisri wenyewe wamekuwa na mchango katika uhubiri huo?! Aidha mimi sidhani uwepo wa uhubiri wa madhehebu ya Shia ni kwa maana ya kumbadilisha Suni awe Shia, bali unalenga kuondoa vikwazo na vizuizi baina ya makundi mawili, na kuonesha kwamba baina ya makundi haya kuna maeneo mengi ya kushirikiana. Na miongoni mwa maajabu ya maneno ni mheshimiwa Dkt, kusema kuwa Suni ni asilimia tisini ya Waislamu wote wa ulimwenguni. Lakini taswira yake hii si sahihi, kwani Shia wanawakilisha robo ya Waislamu wote iwapo si zaidi ya hapo. Kisha ni kwamba miongoni mwao hao Mashia wamo maulamaa na wajuzi, waandishi na mahatibu, wasomi na walimu wa matabaka mbalimbali, nao wako huru kiasi kwamba Marjaa hawezi kuziba vinywa vyao kuwazuia wao kuongea kile wanachokiamini na kusambaza kile wakitakacho, hasa ikiwa ni kwa lengo la kuondoa dhana mbaya baina ya makundi mawili. Kama ambavyo maulamaa wa Azhar na wa Kisuni hawawezi kuwadhibiti wasomi wao wote na wajuzi wao wote na kuziba vinywa vyao wasiongee watakalo. Ndiyo, sisi tunapingana na kila uhubiri wa 242


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

kutoka katika kundi lolote lile, ambao unalenga kuwasha moto wa fitina na machafuko baina ya makundi mawili. Hakuna siku inayopita isipokuwa sisi tunaona kitabu au insha au makala yaliyosambazwa na mtu kutoka madhehebu ya Suni, akiwakufurisha Shia na kuwahimiza vijana wawauwe na kumwaga damu yao. Jambo hili si geni kwa mwenye kusoma angalau kidogo tu yale yanayoendelea huko Afghanistan, Pakistan, Iraq, Syria, Yemen na kwingineko katika nchi mbalimbali. Kisha ni kwamba, yale aliyoyanukuu kutoka kwa Bernard Lewis na akayaita kuwa ni utabiri si sahihi kabisa. Si utabiri ni mipango yao inayoandaliwa na kupangiliwa, kwani hakuna ushindani wowote wa kushindania uongozi baina ya Iran na Uturuki. Na aliyoyataja si chochote isipokuwa ni njama zinazopangwa na nchi kubwa za kibeberu ili kuweza kuzipiga nchi zote mbili kwa jina la utabiri. Na ninasema waziwazi kwamba: Hakika vita vinavyoendelea huko Iraq, Syria na Yemen ni vita vya kisiasa na wala si vita vya kimadhehebu. Na hakika mkono wa nchi kubwa uko nyuma ya vita hivi. Nchi hizi zinafaidika zaidi kwa kuwasha moto wa vita katika maeneo hayo, kwa sababu vita hivyo kwanza vinawadhoofisha Waislamu. Pili vinabomoa miundombinu yao ya kiuchumi. Tatu vinatoa fursa ya kuwauzia wapiganaji silaha. Nne vinaondoa kitisho na hatari kwa utawala haramu wa Izraeli na kuifanya 243


MAJIBU YETU KWA MUFTI WA AL-AZHAR

iishi kwa amani zaidi. Na mengineyo miongoni mwa athari mbaya dhidi ya Waislamu. Na la ajabu ni kwamba Azhar Tukufu imenyamazia umwagwaji huu wa damu unaoendelea huko Yemen, nchi ambayo inabomolewa kila siku kwa sababu za kipuuzi. Na haya ndio maneno yangu ya mwisho kwa Mheshimiwa Dakt, Ahmad Twayyib, Mufti wa Azhar, Mungu amhifadhi, nataraji atayafanyia kazi yale aliyoyaeleza ikiwa ni pamoja na kukutana pamoja na viongozi wa makundi yote mawili na kudurusu maudhui. Yaani umoja wa Waislamu na uokovu wao dhidi ya njama zinazowazunguka, ili kuweza kufika wote kwenye matumaini yao. Na sisi tuna imani na yakini kwamba kama kukutana huko kutafanywa kwa ajili ya Allah na kwa nia safi kwa ajili Yake, basi atawaongoza na kuwaafikishia jambo lao katika yale yenye manufaa na wema kwao. Allah anasema: “Wakitaka suluhu basi Mwenyezi Mungu atawawezesha, Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye habari.”236 Ujumbe huu umekamilika jioni ya siku ya Alhamisi, ya mwezi kumi na mbili ya Dhulqaadah, katika mji wa Qum Tukufu, kituo cha Aali Muhammad, sala za Allah ziwafikie wote. Ja’far Subhani. 236

Sura Nisaa: 35.

244


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.