Mazingatio kutoka katika uislamu sehemu ya kwanza

Page 1

Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

MAZINGATIO KUTOKA KATIKA UISLAMU (LESSONS FROM ISLAM) Sehemu ya Kwanza Kimeandikwa na: S. M. Suhufi

Kimetarjumiwa na: Azizi Hamza Njozi Na Dr. Mohamed S. Kanju

7/15/2011

12:43 PM

Page A


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Š Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 - 512 - 64 - 5 Kimeandikwa na: Na: S. M. Suhufi Kimetarjumiwa na: Azizi Hamza Njozi na Dr. M. S. Kanju Kimehaririwa na: Ramadhani Kanju Kupangwa katika Kompyuta na: Ukhti Pili Rajab. Toleo la kwanza: Februari, 2010 Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info

7/15/2011

12:43 PM

Page B


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/15/2011

YALIYOMO Ukurarsa Dibaji ..........................................................................................................2 Kazi na Jitihada...........................................................................................7 Amali Njema...............................................................................................8 Kazi ni Ibada................................................................................................8 Kampeni Dhidi ya Ukosefu wa Ajira..........................................................9 Mwenendo wa Viongozi wa Uislamu.......................................................12 Jitihada katika kambi Mbili.......................................................................15 Kazi, Lakini si kila kazi.............................................................................17 Nyanja mbalimbali za Amali Njema..........................................................19 Nukuu........................................................................................................21 ELIMU (MAARIFA) Kueleweka vibaya.................................................................................... 24 Fadhila za Wanazuoni................................................................................34 Kapeni Dhidi ya Elimu..............................................................................35 Nukuu........................................................................................................37 MAMA Ushawishi wa Mama kwa Mwanawe........................................................43 Upole na wema kwa Mama ni Fidia ya Dhambi za Mtu..........................49 Kutoridhika kwa Mama.............................................................................50 Mapendekezo ya Kumtendea Wema Mama..............................................51 Siku ya Mama............................................................................................53 Baada ya kifo cha Mama...........................................................................55 Nukuu........................................................................................................55

12:43 PM

Page C


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

WEMA Upole kwa Yatima..................................................................................... 60 Kuwapatia mahitaji wahitaji..................................................................... 65 Nukuu....................................................................................................... 72 POMBE Nukuu........................................................................................................74 Kamari.......................................................................................................90 Kampeni ya Msingi Dhidi ya Kamari......................................................104 Nukuu..................................................................................................... 108 UONGO Uongo huruhusiwa kwa Malengo yake...................................................125

UHUSIANO WA KIJAMII Kutengeneza Furaha................................................................................138 Kukidhi Mahitaji ya watu........................................................................139 Kusengenya........................................................................................... 139 Kuwaudhi na kuwachokoza watu........................................................... 140 Kutafuta Makosa.................................................................................... 141 Dhihaka.................................................................................................. 142 Nukuu..................................................................................................... 144 ADABU ZA KIJAMII Kuonyosha Heshima kwa Watu...............................................................148 Kuwatendea watu kwa Wema..................................................................154 Kuwa Mpole na Mnyenyekevu...............................................................158 Kutimiza Ahadi....................................................................................... 162 Nukuu..................................................................................................... 166

D

12:43 PM

Page D


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

HISIA ZA UDUGU NA UDUGU..........................................................166 URAFIKI Nukuu......................................................................................................196 Usafi........................................................................................................197 Nukuu..................................................................................................... 213 Kanuni za kujifunza............................................................................... 213

E

12:43 PM

Page E


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

NENO LA MCHAPISHAJI Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza kiitwacho, Lessons From Islam. Sisi tumekiita, Mazingatio Kutoka Katika Uislamu. Uislamu ni dini na mfumo wa maisha. Kwa hiyo, mafundisho ya Uislamu yanazingatia maendeleo ya kiroho na maendeleo ya kimwili - yaani maisha ya ulimwengu huu tulionao. Uislamu kimsingi uko dhidi ya kufuata kibubusa. Tofauti iliyopo baina ya Uislamu na dini nyinginezo ni kwamba Uislamu unamtaka mtu kwanza aelewe na awe na maarifa juu ya anayotaka kuamini kisha aamini, ambapo dini nyinginezo zinasema kwamba kwanza amini kisha utaelewa baadaye. Hivyo, ni muhimu mtu kuelewa mafundisho ya Uislamu kabla ya kuamini. Vivyo hivyo, ni muhimu kuelewa imani za wengine ili wasije wakakuyumbisha. Inawezekana kusemwa kwamba wale ambao hawaelewi kabisa mtazamo wa imani tofauti, hawaelewi kwa ukamilifu (mtazamo) wa kwao wenyewe. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili za watu. Kutokana na ukweli huo, taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili.

F

12:43 PM

Page F


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Tunamshukuru ndugu yetu, Dk. M. S. Kanju na Aziz Hamza Njozi kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation S. L. P. 19701 Dar-es-Salaam, Tanzania.

G

12:43 PM

Page G


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

MPENDWA MSOMAJI. Assalaam Alaykum Warahmatullah Wabarakatuh. Kitabu hiki ni chapisho la Al-Itrah Foundation. Machapisho yake yameandaliwa ili kukidhi mahitaji ya kiroho ya zama hizi kwa kuzingatia msisitizo maalum wa kusafisha akili na fikra ya Mwislamu. Al-Itrah Foundation imefanya jitihada kubwa kuwasilisha kile tu ambacho ni Sahihi na cha kuaminika kwa mujibu wa Uislamu. Tunakuomba ukisome kitabu hiki kwa dhamira iliyokusudiwa. Pia unaombwa ututumie maoni yako juu ya machapisho yetu, maoni ambayo sisi tutafurahi sana kuyapokea. Kueneza ujumbe wa Uislamu ni kazi inayotaka ushirikiano wa watu wote. Al-Itraha Foundation inawaalikeni kwenye kazi hii, ambayo ni mwitikio wa aya ya Qur’an isemayo:

“Sema: Siwapatieni isipokuwa nasaha moja, kwamba msimame kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kwa pamoja na mkiwa mmoja mmoja. (34:46). Mwenyezi Mungu Mtukufu awabariki! Ndugu zenu katika Uislamu Al-Itrah Foundation

H

12:43 PM

Page H


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

KUHUSU SISI WENYEWE Mtu makini leo hii anagundua mabadiliko katika maisha ya kiakili ya mwanadamu. Sayansi na teknolojia pamoja na mafanikio yake ya ajabu vinaonekana kufikia kilele chake. Mahitaji ya mali na vitu pamoja na uchu wa madaraka na utukufu vimemwelekeza mwanadamu kwenye upotevu wa dhahiri wa maadili yake yote. Katika hali hii ya kukatisha tamaa, mtu hulazimika kutulia na kutafakari hatari kubwa inayomkabili mwanadamu. Mwanadamu kwa mara nyingine tena ameelekeza macho yake kwa Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwingi wa Kurehemu kwani amebaini kuwa Suluhisho la matatizo yake na hatima ya uokovu wake unategemea kuyafuata maamrisho ya Mwenyezi Mungu. Mabadiliko haya kutoka katika fikra za kuwazia mali na utajiri (uyakinifu) kwenda katika fikra za kiroho yanaendana kabisa na malengo ya Islamic Seminary. Maadili ya kidini, sambamba na maendeleo ya zama zetu, hutoa lile kimbilio hasa linalohitajika kwa ajili ya akili inayosumbuka na yenye wasiwasi. Ni matokeo ya hili ongezeko la uelewa kwamba sasa inatambulika kuwa siri ya kuishi kiuchamungu katika dunia hii kunaongoza kwenye maisha yenye furaha ya milele huko Akhera. Huu ndio ujumbe wa Uislamu kwa watu wote. Seminari ya Kiislamu (Islamic Seminary) inataka kunyanyua kurunzi la mwongozo wa kidini na kusaidia kwa bidii zote katika kukuza urithi wa kiroho wa mwanaadamu. Inawasilisha mfumo wa maisha wa Qur’ani katika utukufu wake wa asili. Inawasilisha kile tu ambacho ni sahihi na cha kuaminika. Machapisho yake yameandaliwa ili kukidhi mahitaji ya kiroho ya zama zetu. Yatatumika kama chemchem isiyokauka kwa wale wenye kiu ya elimu na maarifa.

I

12:43 PM

Page I


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/15/2011

Seminari ya Kiislamu (Islamic Seminary) ni taasisi ya kilimwengu inayofanya jitihada za kujenga hisia za udugu wa Kiislamu. Inafaidika na michango ya watu wenye ujuzi mkubwa kabisa, pamoja na uungwaji mkono wa kimataifa katika kufikia malengo yake. Ina vituo ndani ya Bara Asia, Afrika, Ulaya, Canada na Mashariki ya Mbali.

J

12:43 PM

Page J


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/15/2011

12:43 PM

Page 1


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwingi wa Kurehemu DIBAJI Uislamu huyachukulia kwa mazingatio mahitaji yote ya mwanadamu. Mwongozo wake ni kwa ajili ya zama zote na sehemu zote. Mtu akiyasoma mafundisho ya Uislamu kwa undani itamdhihirikia waziwazi kabisa kuwa Uislamu ni dini bora kabisa na kwamba pale mtu anapopata elimu na umaizi hujinyenyekesha kwa Mwenyezi Mungu kwa kusilimu na kuifuata dini hii adhimu, dini ya Uislamu. Hivyo, mtu aliyeelimika akajaaliwa kuwa mwenye elimu na busara ana nafasi bora zaidi ya kuyaelewa mafundisho ya Uislamu. Uislamu ni dini yenye kujitosheleza. Ni chanzo cha riziki ambayo hutoa uhakikisho wa kujitosheleza na hutoa njia na mbinu za mafanikio na wokovu wa mwanadamu. Sheria na kanuni za Kiislamu sio matokeo ya akili ya mwanadamu, hivyo kwamba ufanisi wake uweze kubakia ndani ya muda maalumu au sehemu maalum tu. Kinyume chake, sheria na kanuni na miongozo ya Uislamu imeundwa na Mwenyezi Mungu Mwenye Nguvu zote ambaye kwa utashi Wake amemuumba mwanadamu. Mwenyezi Mungu ambaye anajua matatizo yote ya uhai wa mwanadamu. Hivyo ni Mwenyezi Mungu anayejua vizuri zaidi ni kitu gani kina manufaa kwa ustawi na furaha ya mwanadamu na ni mambo gani yanaweza kumletea mwanadamu misiba na maafa. Kuja kwa Uislamu kumethibitisha ukweli huu bila chembe yoyote ya shaka kwamba Mwenyezi Mungu akipenda anaweza kuwabadilisha watu wanyonge, wapumbavu na wadhaifu kuwa taifa lililostaarabika na kuelimika katika kipindi kifupi kwa kiasi kile cha kuweza kuchukua jukumu muhimu sana la kumuongoza mwanadamu katika kuwa jamii yenye uta2

12:43 PM

Page 2


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

maduni na vilevile kufikia kilele cha elimu na hekima. Mtu kama akiitazama historia huko nyuma na kufunua kurasa zake zinazotoa maelezo ya matukio kabla ya kuja kwa Uislamu, ataiona hali mbaya na ya kuhuzunisha waliyokuwa wakiishi nayo watu. Mtu akiitazama kwa makini historia ya kuibuka na kukua kwa Uislamu, ataona ni jinsi gani watu wale wale wa Zama za Giza walivyopiga hatua ya maendeleo na ustawi na kujenga jamii njema iliyojaa maarifa, busara na maadili, na jinsi misingi na mafundisho ya Uislamu yalivyoibadili jamii nzima na kuwa taifa lenye nidhamu. Lakini inasikitisha kusema kuwa maadui wa Uislamu walipanda mbegu ya utengano kati ya Sheria ya Mwenyezi Mungu na Waislamu, na wameugawanya umma wa Kiislamu, na wamepanda utengano na ufisadi kiasi cha Waislamu kupoteza utukufu na nguvu zao zilizopita. Mtukufu Mtume (s.a.w.) alilitangaza hili wakati wa uhai wake kwamba Qur’an na Ahlul-Bayt wake (wateule wa nyumba ya Mtume) havitatengana, na vyote viwili ni muhimu sana kwa uongofu, ustawi na uokovu wa Waislamu. Hivyo Mwislamu yeyote anayetaka kupata ustawi na wokovu lazima ayapate mafundisho ya Qur’an kutoka kwa warithi halisi wa Mtume, yaani; Imam Ali (a.s.) (a.s.) na Maimamu kumi na moja wanaotokana na kizazi chake ambao waliteuliwa na Mtume kwa amri ya Allah Azza wa Jala, kisha mtu huyo akayafuata kwa uaminifu mafundisho hayo. Jitihada zimefanyika kuyawasilisha mafundisho ya Uislamu katika kitabu hiki kwa lugha ya Qur’ani Tukufu, Mtukufu Mtume (s.a.w.), na kizazi chake kitukufu na kuyajadili mafundisho hayo katika nyanja mbalimbali za maisha katika njia nyepesi na fasaha ili kuyafanya mafundisho hayo yaeleweke vyema. Nukta muhimu inayopaswa kuzingatiwa ni kuwa wakati wa mjadala wetu katika mada mbalimbali, maoni ya wanazuoni mbalimbali yamenukuliwa 3

12:43 PM

Page 3


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

ili kuonyesha kwamba, baada ya miaka mingi ya jitihada hatimaye wamekiri ubora, uhai na manufaa ya mafundisho na misingi ya Uislamu aliyopewa mwanadamu kupitia kwa kiongozi wa Uislamu miaka zaidi ya 1400 iliyopita. Na pia wasomaji wanapaswa kujua kuwa Waislamu wana hazina kubwa sana katika miliki yao lakini hawana habari nayo. Tunamuomba Mwenyezi Mungu atujaalie tuirejee hazina hii ili milango ya hekima ifunguke na kutuonesha njia ya kutoka katika usingizi mzito na kuturejesha kwa Mwenyezi Mungu na mafundisho ya Mwenyezi Mungu ili madhambi yetu yaweze kufidiwa. Nukta nyingine muhimu ni kuwa katika zama hizi, kizazi kipya na wasomi wanaonyesha shauku kubwa ya kutaka kujua na kuelewa ujumbe halisi wa Uislamu, shauku ambayo mfano wake haukuwahi kutokea kabla. Ni vitabu vile na tasnifu, vilivyoandikwa juu ya dini kwa mtazamo wa kimantiki na havihitaji tafsiri zisizo za lazima ndivyo vinavyohitajika zaidi siku hizi kuliko vitabu vingine. Wasomi wanataka kuyaelewa mafundishio ya kidini kwa mtazamo wa elimu na busara na Uislamu unakubali na kuuthibitisha mtindo huu wa kutaka kuielewa dini na kwa kusema kweli misingi na mafundisho yake yamejengwa juu ya utaratibu huu (wa kutumia mantiki elimu na busara katika kuelewa mambo). Mara zote na katika kila jambo, Uislamu umekuwa ukiwahimiza wafuasi wake na watu wengine wote kutumia hoja na akili zao. Kamwe Uislamu hauwashauri watu kufuata mafundisho yake kibubusa na bila hoja. Katika Uislamu hakuna kitu ambacho hakina hoja za kiakili au kinachopingana na hoja za kiakili. Hii ndiyo sababu Uislamu umefanikiwa kwenda sambamba na maendeleo ya kisayansi, na hivyo umeweza kuhifadhi na kudumisha utukufu na heshima yake.

4

12:43 PM

Page 4


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Kizazi cha zama hizi kinaelewa vema mitazamo ya madhehebu mbalimbali inayotokana na vyanzo vya Mashariki ya Kati na Magharibi (Ulaya na Marekani), na pia wanaelewa dhana na fikra mbalimbali za kifalsafa. Hivyo mwanadamu anatamani kwamba kutokana na elimu kubwa ambayo ameipata, basi imani yake pia lazima iwe katika muundo wa hali ya juu kwa mtazamo wa maadili ya kiroho. Lakini dini ambayo haiwezi kukidhi mahitaji ya wakati itapoteza mvuto wake mbele ya ushawishi wa sayansi na hoja. Wakati Mwanafalsafa wa Kiingereza, Bertrand Russell anapoibua Swali kwamba kwa nini yeye sio Mkristo na anajitenga na dini yake, sababu kubwa nyuma yake ni kwamba katika hali halisi Ukristo hautoi suluhisho lolote la kinahisho lake na wokovu. Licha ya hayo anasema kuwa, anashindwa kuuelewa kule kuwepo haswa kwa Mwenyezi Mungu ambaye Ukristo unamuelezea kwa sababu si dhana ya Mungu yenyewe wala ya dini yenyewe inayofikia kwenye kiwango cha elimu na mantiki. Hata baadhi ya wanazuoni na wanafalsafa wakubwa wa kikristo pia wana maoni kama haya juu ya Ukristo kwa sababu wanauona Ukristo kuwa si dini iliyojengwa juu ya msingi ya kiakili na hoja za kimantiki. Mawazo na mitazamo yao juu ya dini yao wenyewe yanachapishwa kila mara na pia kuna baadhi ya makundi ya watu ambao wana elimu ya juu juu tu kuhusu dini yao kwa sababu elimu hiyo wanaipata kutoka katika mamlaka ya Kanisa na kwa sababu hiyo wamejenga dhana yenye mashaka na uadui na hata bila ya kujaribu kufanya uchunguzi na utafiti, wanaweka uadui na chuki dhidi ya Uislamu vilevile, na wanaziona dini zote hizi (Ukristo na Uislamu) kuwa si za kuaminika na za kukubalika. Hivyo wale wote wanaovisoma vitabu hivyo wanapaswa kujua kwamba kwa sababu watunzi wa vitabu hivyo ni Wakristo, wanauchukulia na kuuandika Uislamu kwa kinyongo na chuki na kwa maoni ya Ukristo, vitabu hivyo si chochote zaidi ya kuwa ni kifurushi cha mawazo ya kizushi na upuuzi. Maoni ya waandishi hao wa vitabu yanaweza kuwa sawa kwa Ukristo lakini sio juu ya Uislamu. 5

12:43 PM

Page 5


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Mwanazuoni yeyote wa Kikristo ambaye amezichunguza dini nyingine kwa kina, na akauelewa ubora wa uzuri wa mafundisho ya Uislamu, bila kusita atakiri umaarufu wa dini hii tukufu ya Uislamu na kukubali athari zake kwa kuutukuza kwa sifa nyingi. Katika zama zetu, kizazi chetu kipya kilichoelimika na wanazuoni wana imani isiyoyumba juu ya kanuni za kudumu za Uislamu kwa sababu mara nyingi imeonekana kuwa vijana wetu walioelimika wanafanya utafiti wa kina ili kupata elimu juu ya mafundisho ya dini yao ili kwa kutumia akili na hoja wanaweza kupata amani, ustawi na uokovu. Islamic Seminary ambayo ipo karibu na matabaka mbalimbali ya watu ndani na nje ya nchi na hususani kizazi kipya na ambayo hupokea mamia ya barua kila siku zinazoulizia juu ya habari za kidini, inaelewa vizuri upendo wa Waislamu juu ya dini yao. Vitabu vyenye mwelekeo wa kitafiti na machapisho mengine sahihi yaliyoandikwa na wanazuoni wakubwa maprofesa na watu wengine mashuhuri juu ya mafundisho ya kidini, elimu na ujuzi, ni ushahidi thabiti juu ya ukweli kwamba waandishi hawa waongofu wana mapenzi makubwa juu ya dini hii tukufu ya Uislamu na inatia moyo kuona kwamba jambo hili linazidi kupanuka siku hadi siku. Islamic Seminary ina matumaini kuwa kitabu ulichonacho mikononi kitazitia nuru akili za vijana wetu makini, na kitakuwa kama utangulizi kwenye utafiti mpana zaidi juu ya Uislamu. Kitawashawishi kuutambua Uislamu kuwa ni dini adhimu na bunifu, itawasaidia katika kutengeneza maisha yao na kuwaandaa kwa mihanga mikubwa. Bila shaka kabisa kitawasukuma vijana kuunda na kujenga jamii bora zaidi, yenye afya zaidi na yenye furaha zaidi.

Wachapishaji.

6

12:43 PM

Page 6


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

KAZI NA JUHUDI Katika Uislamu, umuhimu mkubwa umewekwa juu ya kazi na juhudi, na hili huhesabiwa kuwa ni moja ya vipengele vikubwa vya Ustawi wa mwanadamu katika dunia hii na kesho Akhera. Katika aya zaidi ya themanini, Qur’ani Tukufu imeielezea imani na amali (matendo) njema kuwa ni shuruti za msingi kwa ustawi na hali njema ya mwanadamu na kustahiki kwake pepo. Wanazuoni wametoa tafsiri mbalimbali juu ya kazi, hata hivyo, katika msemo wa kawaida “Kazi maana yake ni kutenga muda na kuutumia kwa kumenyeka ili kulifikia lengo fulani.” Kwa hiyo, kitendo chochote anachokifanya mwanadamu ili kufikia lengo fulani kwa kawaida huitwa ‘kazi.’ Fundi umeme anayemenyeka kutengeneza mota ya umeme, kwa hakika anafanya kazi. Mhandishi anayechora mistari kwenye karatasi ili kuandaa plani ya ujenzi wa jengo, pia anafanya kazi. Mpaka rangi anayepaka rangi mandhari ya asili katika ubao kwa kutumia muda wake na kuumiza ubongo wake pia anafanya kazi. Mlinzi anayesimama katika njia mkabala na jengo akiliangalia na kulilinda pia huwa yupo kazini. Jamii haiwachukulii watu hao kuwa hawana kazi na inayachukulia matendo yote haya kuwa ni kazi. Lakini jamii humhesabu mtu anayetembea katika njia au kuchora mistari katika karatasi bila malengo yoyote kuwa hana kazi na kutembea huko na kuchora mistari kwenye karatasi kwa kujifurahisha tu hakuwezi kukaitwa kazi. Kwa kuzingatia mifano hio hapo juu tutakuwa tumebaini kuwa jamii haiichukulii kazi kuwa ni matendo yanayofanywa kwa nguvu za mwili peke yake pamoja na jitihada zake, kwa mfano kama mtu aliyepo katika 7

12:43 PM

Page 7


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

mahakama ya Sheria ataukiri ukweli unaokwenda kinyume na maslahi yake, lakini kukiri ambako kutamuwezesha mtu mwingine kupata haki yake stahiki, jamii humhesabu kuwa amefanya kazi kubwa. Mwalimu anayefundisha wanafunzi au mzungumzaji au mhubiri anayetoa hotuba kwa ajili ya uongofu wa watu huwa anaongea tu lakini jamii haimhesabu kuwa hafanyi kazi. Lakini badala yake jamii inakuhesabu kufundishia na kuhutubia kwake kuwa ni kazi yenye thamani.

AMALI NJEMA Kifungu hiki cha maneno “amali njema” kilichotumika katika Qur’ani Tukufu kinabeba maana ya jumla ya kazi ya heshima, inafanywa kwa nia njema na kulifikia lengo lenye manufaa. Kwa mfano mama anayeamka usiku kumnyonyesha na kumlisha mwanawe anafanya kazi ya heshima, lakini kubakia macho usiku huku mtu akinywa pombe na kusababisha bugudha, sio kazi ya heshima. Kufanya juhudi ili kuchuma riziki ya halali ni amali njema na ni kazi ya heshima, lakini kuwa kupe na kuwaomba wengine ni kazi isiyo ya heshima. Katika Uislamu, kazi zenye manufaa kwa mtu na jamii na zina manufaa kwa watu duniani na akhera zinachukuliwa kuwa ni amali njema.

KAZI NI IBADA Juhudi na shughuli za halali ambazo mtu huwa anazifanya ili kuweza kumpatia mahitaji yote zinachukuliwa na Uislamu kuwa ni ibada. Mtu aliyejengeka vizuri, mwenye miraba minne, aliyekuwa na mikono na misuli yenye nguvu na mwili wenye afya alipita mbele ya Mtume (s.a.w.w.) na masahaba zake. Masahaba wa Mtume walimtazama mtu yule kwa kupendezewa na wakaambizana kuwa “Ingekuwa ni heri kubwa kiasi 8

12:43 PM

Page 8


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

gani kama mtu huyu angetumia nguvu zake nyingi katika njia ya Mwenyezi Mungu na kutafuta radhi Zake.” Mtume akawaambia: “Ikiwa mtu huyu atafanya kazi ili kuwapatia riziki wazazi wake au atafanya kazi ili kuwapatia mahitaji binti zake wadogo au atafanya kazi ili kumtimizia mahitaji mkewe kwa njia za halali au atafanya kazi ili kujichumia riziki yeye mwenyewe ili asiwaombe watu wengine, basi atakuwa anafanya kazi katika njia ya Mwenyezi Mungu.” Kwa mujibu wa hadithi nyingine, Mtume (s.a.w.w.) anasema: “Mtu akichukua kamba na kwenda milimani, akakusanya kuni na kuzibeba mabegani mwake na kujipatia riziki yake kwa njia hii, basi jambo hili ni bora kuliko kuomba. (Sahihi Bukhari).

KAZI NI JIHADI Katika maneno ya viongozi watukufu wa Uislamu, wamesema kuwa kazi na juhudi vimehimizwa mno kiasi cha kuwa haiwezekani kuhimizwa tena kwa namna kubwa kuliko hivyo. Imam Ridha (a.s.), Imam wa nane, anaichukulia kazi kuwa ni bora kuliko jihadi (vita vitakatifu) katika njia ya Mwenyezi Mungu, na anasema: “Malipo na thawabu za mtu anayemenyeka katika kujipatia riziki yake na ya familia yake na anatafuta riziki yake kwa rehma za Mwenyezi Mungu kwa kutumia kazi na jitihada zake ni makubwa kuliko malipo ya mtu anayepigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu” (Wasa’ilush-Shi’ah).

KAMPENI DHIDI YA UKOSEFU WA AJIRA Uislamu umepiga kampeni ya dhati dhidi ya kukaa bila kazi na ukosefu wa ajira, na unachukulia mtu kukaa bila kazi kuwa chanzo cha matatizo na bahati mbaya. 9

12:43 PM

Page 9


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Imam Sadiq (a.s), Imam wa sita, aliuliza juu ya hali ya Umar bin Muslim, akajulishwa kuwa Umar alikuwa ameamua kujishughulisha na ibada. Alikuwa ameacha kazi na biashara yake na alikuwa akishughulishwa na ibada muda wote. Imam hakuridhika alipolisikia jambo hili naye akasema: “Namhurumia! Hajui kuwa maombi ya mtu asiyefanya kazi hayajibiwi na Mwenyezi Mungu?” Kisha akaendelea kusema: “Masahaba wa Mtukufu Mtume waliposikia aya hii: ‘Na anayemuogopa Mwenyezi Mungu na kumtii, (Mwenyezi Mungu) humtengenezea njia ya kuokoka, na humpatia riziki kwa mahali asipopatarajia’ (Suratul Talaq 65:2-3), waliacha kazi na jitihada zao, walifunga milango yao na wakabaki wakifanya ibada tu na wakadhani kuwa hapakuwa na haja tena ya wao kufanya kazi au biashara. Mtukufu Mtume alipobaini shughuli zao, aliwaita na kuuliza “Kwa nini mmeacha kazi na mmeridhika na kufanya ibada peke yake?” Walijibu: ‘Mwenyezi Mungu Mtukufu ametuhakikishia riziki zetu. Hivyo tumeacha kazi na tumeamua kufanya ibada tu’. Mtume aliwakemea na kusema: ‘Maombi ya mtu anayefuata mwenendo huu na kuacha kazi, hayawezi kukubaliwa. Ni muhimu kwenu kufanya kazi na kujichumia riziki huku mkitaka msaada wa Mwenyezi Mungu.’” Mtukufu Mtume amesema: “Chakula bora na kisafi zaidi mtu anachokula ni kile alichokipata kwa kufanya kazi ngumu kwa bidii.” Ingawa Uislamu unachukulia kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kusali kuwa matendo ya wajibu lakini unapinga vikali mtu kutumia muda wake wote kwa ajili ya Sala bila kufanya kazi yoyote. Ata bin Ziyad Harthi, mmoja wa masahaba matajiri wa Imam Ali (a.s.) aliwahi kuugua. Siku moja Imam Ali (a.s.) alikwenda kumjulia hali. Nyumba yake ilikuwa nzuri sana na yenye nafasi, Imam Ali (a.s.) akamuambia: “Ingekuwa uzuri ulioje kama ungekuwa na nyumba kama hii huko akhera ambayo ungekaa humo daima milele. Hata sasa, ukiwa utawaalika masiki10

12:43 PM

Page 10


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

ni na watu wasio na msaada katika nyumba hii kama wageni wako, na ukawapokea na kuwakirimu ndugu zako, na ukawapa haki zao wanaozistahiki; haki zilizo wajibishwa na Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu atakupa nyumba kama hii huko Akhera.” Licha ya kweli kwamba Ata bin Ziyad wakati ambapo yeye mwenyewe ananyenyekea kiutiifu kwa mtukufu Imamu alisema: “Ewe Amiri wa Walioamini! Nina malalamiko dhidi ya ndugu yangu Asim.” Imam akauliza: “Amefanya nini?” Ata akajibu: “Amevaa nguo zilizochanika, ameacha kazi na mambo yote ya maisha na amebaki akifanya ibada peke yake.” Imam Ali (a.s.) akasema: “Kamlete hapa.” Asim bin Ziyad alikuja, Imam Ali (a.s.) akamwambia: “Ewe adui wa nafsi yako! Shetani amekutumbukiza katika mashaka na huzuni. Kwa nini hukuwa na huruma kwa mkeo na watoto wako na kwa nini umetwaa mwenendo huu potofu? Unafikiri kuwa Mwenyezi Mungu alipozihalalisha fadhila zake juu yako, Yeye hakutaka uzitumie?” Asim alisema: “Ewe Amiri wa Waumini! Nimekufuata wewe katika kuvaa nguo zisizo nzuri na kula chakula kilicho duni.” Mtukufu Imam akasema: “Nakuhurumia! Mimi sio kama wewe, na wajibu wako sio sawa na wangu. Mwenyezi Mungu amefanya kuwa ni wajibu kwa viongozi wa kweli wa kidini na Maimamu kuishi maisha wanayoishi maskini na wanyonge ili ufukara wa watu maskini usiwahuzunishe na kujiona hawana lao.” Tunapotazama kulizingatia tukio hilo, inatudhihirikia kuwa hakuna Mwislamu yeyote, katika hali yoyote, hata awe amejitosheleza kiasi gani, anayeruhusiwa kuacha kazi na kutotoa mchango wowote katika jamii.

11

12:43 PM

Page 11


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

MWENENDO WA VIONGOZI WA UISLAMU Namna na mwendo wa viongozi watukufu wa Uislamu na ushiriki wao katika shughuli zenye manufaa ni ushahidi wa wazi wa ukweli kuwa Uislamu ni dini ya kimaendeleo na yenye usaidizi, ambayo kwamba mbali na kuziimarisha na kuziboresha roho na kutoa uhakikisho wa furaha ya mielele huko akhera (kwa waja wema), pia inawahimiza wafuasi wake kufanya jitihada katika fani mbalimbali za shughuli ili wawe ni taifa lenye ustawi na linalojishughulisha na la kupigiwa mfano. Ukristo unafundisha na kuwaita watu katika kujitenga na dunia na kuishi maisha ya utawa na unawataka watu kuikataa na kuipuuzia dunia, Ukristo pia unasema: “Ulimwengu ni kama daraja, vuka juu yake lakini usikae juu yake.” Lakini Uislamu ni dini inayoishi ambayo inatoa nguvu na uhai mpya. Uislamu unajali mwili, roho na ustawi wa watu duniani na akhera. Mtume wa Uislamu aliendelea kufanya kazi ya kuchunga mifugo na biashara kwa miaka mingi. Imam Ali (a.s.) alikuwa akilima na kupanda miti, viongozi wengine wa Uislamu walikuwa wakifanya kazi na kufurahia kufanya shughuli nyingine zenye manufaa. Muhammad bin Munkadir, aliyekuwa mmoja wa waliokuwa wakijiita “Wasufi” waliojitenga na dunia, anasema: “Siku moja nilikwenda kwenye moja ya vijiji vidogo pembezoni mwa Madina. Nilimuona Imam Muhammad Baqir akiwa ameegemea kwenye mabega ya watumishi wawili huku akitoka jasho na alikuwa akienda kuangalia masuala yanayohusiana na kulimwa kwa shamba lake. Nikasema ndani ya nafsi yangu: ‘Mwenyezi Mungu atukuzwe! Mmoja wa wazee wa kikureishi anakwenda kutafuta mapato ya kidunia katika jua kali namna hii. Lazima nikutane naye na nimnasihi.’ Nikiwa na wazo hili akilini nilikwenda karibu na Imam na baada ya salamu nilimwambia: Je, unatafuta mapato ya kidunia katika 12

12:43 PM

Page 12


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

jua kali kiasi hiki? Kifo kikikuta katika hali hii, vipi itakuwa nafasi yako? Imam Ali (a.s.) alisimama na kunijibu kwa ufasaha na maneno yenye uamuzi yaliyokuwa yanaonyesha utukufu na ubora wa mafundisho ya Uislamu: “Nikifa wakati huu, nitakuwa nimekufa kwenye wakati nikiwa hasa katika ibada ya Mwenyezi Mungu. Nimeshughulishwa na kufanya kazi ili nisiwategemee nyinyi na wengine kama ninyi ili niwapatie mahitaji yao watu wa familia yangu na endapo kifo kikinikuta katika hali hii, sina kitu cha kuogopa kwa sababu nipo ndani ya ibada ya Mwenyezi Mungu. Muhammad bin Munkadir aliaibika. Aliomba radhi kwa pingamizi lake la kitoto na lisilo na msingi na alisema: “Nilitaka nikushauri lakini kwa upande mwingine umenipa ushauri na umeniondoa katika upotofu mkubwa.” Imam Ali (a.s.) katika enzi za uhai wake mtukufu aliwafundisha watu somo la shughuli zenye manufaa kwa kufanya kazi yeye mwenyewe. Abu Nizar, mwangalizi wa shamba la Imam Ali (a.s.) anasema: “Siku moja Mtukufu Imam Ali (a.s.) alikuja kukagua hali ya shamba. Kwa vile ulikuwa ni wakati wa kifungua kinywa, aliniuliza kama nilikuwa na chochote cha kula. Nilisema: “Ninacho chakula lakini hakimfai Amir wa Waumini. Nimepika maboga baada ya kuyachuma kutoka katika Shamba hili hili.” Imam Ali (a.s.) akasema: “Nenda kayalete.” Kisha alisimama na kwenda kwenye ukingo wa mfereji mdogo wa maji ambako aliosha mikono yake. Kisha akala sehemu ya yale maboga, akaosha mikono yake na kusema, “Alaaniwe yule ambaye tumbo lake linamvutia katika moto wa Jahanamu.” Kisha alichukua Sururu, akaingia katika mfereji huo na akaanza kuuchimba. Alifanya kazi kwa saa moja, alichoka na jasho lilianza kutoka kwenye uso wake, kisha alitoka katika mfereji, alifuta jasho usoni kwake, akashika sururu tena na kuingia mferejini. Aliendelea kuchimba mpaka maji yakaanza kububujika. Alitoka nje ya mfereji haraka na kusema: “Ninamwomba Mwenyezi Mungu kushuhudia kuwa nimeamua kuutoa mfereji huu kama sadaka ili mapato yake yatumike kwa ajili ya man13

12:43 PM

Page 13


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

ufaa ya wenye shida.” Kisha akaniambia: “Niletee kalamu na karatasi.” Nikatekeleza kwa kumpelekea vitu hivyo. Kwa mkono wake aliandika ifuatavyo: “Kwa Jina la Mwenyezi Mungu. Mwingi wa Rehema, Mwingi wa Kurehemu. “Kwa mujibu wa hati hii Amiri wa Waumini Ali ameyatangaza mashamba mawili yaitwayo Qanat Abi Nizar na Baghibghab kuwa ni zaka kwa ajili ya mafukara na maskini wa Madina na wale wanaoishiwa na fedha wakiwa safarini. Nimefanya kitendo hiki ili nipate radhi za Mwenyezi Mungu na nibaki salama kutokana na mateso ya Siku ya Hukumu. “Mashamba haya mawili hayawezi kuuzwa au kutolewa kama zawadi lakini yatumiwe kwa manufaa ya masikini hadi Mwenyezi Mungu Mtukufu atakapoyarithi, naye ni Mbora wa Warithi.”

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Yule ambaye ni goigoi na legevu kuhusiana na mambo yake ya kidunia atakuwa goigoi zaidi kuhusiana na mambo yake ya Akhera.” Katika hadithi nyingine Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Mtu bora miongoni mwa Waislamu sio yule anayeitelekeza Akhera kwa ajili ya dunia wala yule anayeitelekeza Dunia kwa ajili ya Akhera, bali Mwislamu bora ni yule anayenufaika na dunia na halikadhalika na Akhera pia.” (Hayatul Haiwan). Qur’ani Tukufu katika kuhusiana na mapendekezo ya watu wenye busara wa wakati wake Qarun wanamuambia:

“Na utafute makazi ya Akhera, yale aliyokupa Mwenyezi Mungu wala usisahau sehemu yako ya dunia, na ufanye wema kama Mwenyezi 14

12:43 PM

Page 14


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Mungu alivyokufanyia hisani wewe .....� (Suratul Qasas, 28:77). Ni sifa bainifu ya Uislamu pekee ambao katika maamrisho yake umewataka watu wachanganye dunia na Akhera ili kupata furaha duniani na Akhera kwa kufanya amali njema na kufanya jitihada katika pande zote.

JITIHADA KATIKA MEDANI MBILI Watu wengi wanauliza swali kuwa kama kweli Uislamu unaunga mkono kufanya kazi na juhudi na umewahimiza wafuasi wake kujishughulisha na kuwa wachapa kazi sasa itawezekana vipi kuzitafsiri na kuziawili zile hadithi zinazoishutumu dunia? Jibu la swali ni kuwa dunia haikushutumiwa moja kwa moja kabisa katika hadithi za Kiislamu. Kwa upande mwingine, katika mlolongo wa hadithi imeshutumu ile dunia ambayo imechafuliwa na tamaa ya ubinafsi na lengo lake ni kulundikana kwa matamanio duni, maonevu kwa wengine na kufutilia mbali hisia na ukweli wa hali halisi. Katika baadhi ya hadithi, mapenzi ya dunia yameshutumiwa kwa sababu mapenzi ya dunia yakipenya kwenye moyo wa mtu, yatamfanya ayaelekee makosa, madhambi na kushutumiwa na hatimaye kuangukia kuwa mawindo ya balaa. Uislamu unawataka watu wautazame ulimwengu kwa namna halisi, watathmini thamani yake ya kweli, na wafanye jitihada kwa busara ili wanufaike nayo, wawe washughulikaji katika njia sahihi na halali, na wakati huo huo wasiyasahau maisha ya Akhera ili nako wakapate furaha na usitawi wa milele. Uchunguzi wa maisha ya nyumati ya zamani na za sasa unaonyesha wazi kwamba kundi la watu lilifanya uhalifu, lilimwaga damu, liliiba na kuwakandamiza wengine kwa sababu ya kuipenda kwao dunia na ikawa ni 15

12:43 PM

Page 15


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

aibu isiyofutika katika jina zuri la heshima ya mwanadamu. Uislamu unasema: “Msitumie njia zisizo za kibinadamu ili kupata mapato ya kidunia na msiivuke mipaka ya uchamungu na ubora.� Kwa hiyo, hakuna shaka juu ya ukweli kwamba Uislamu umeweka msisitizo mkubwa sana juu ya maisha katika ulimwengu huu na umeweka kanuni na taratibu kwa kinaganaga juu ya hili, kwani majadiliano yote juu ya biashara (uuzaji na ununuaji), yote ambayo yanahusiana na masuala ya kijamii na yanaambatana na maisha ya kidunia ya wanadamu, hushughulika na haki za kiraia za mwanadamu zilizo kubwa zaidi na muhimu zaidi. Na licha ya ukweli kwamba wanasheria wa kidunia wamefanya tafiti kubwa kuhusu haki za kiraia na kuzitekeleza kufikia kiwango cha juu, bado hawajafanikiwa kufikia kiwango cha haki ambazo Uislamu umeamrisha juu ya mwanadamu. Taratibu ambazo zina msimamo wa kisheria na ambazo hutekelezwa katika nchi za Kiislamu siku hizi hazifikii hata sehemu moja ya mia ya mahubiri yaliyofanywa na wanachuoni wa Kiislamu na wanasheria (fuqahaa) kuhusiana na suala hili. Inaweza kusemwa kwamba maandiko ambayo yalichukuliwa kutokana na sheria za Kiislamu ni madogo kuliko kitabu cha msingi cha mwaka wa kwanza kulinganishwa na silabasi ya chuo kikuu iliyosambazwa kwenye miaka kadhaa. Kama Uislamu ungekuwa haujaweka umuhimu mkubwa katika masuala ya kijamii na mambo mbalimbali ya kidunia yanayohusiana na watu, na kanuni zilizopo na kuyachukulia maisha kuwa ni kitu cha kubuniwa na upuuzi, usingeweka taratibu na sheria nyingi kiasi hiki. Na kama Uislamu ungekuwa kama Ukristo ambao unautazama ulimwengu kama mzoga ambao unapaswa kuchukiwa na kutupiliwa mbali, pasingekuwa na haja yoyote ya kuweka sheria katika Uislamu.

16

12:43 PM

Page 16


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Mbali na mijadala ya biashara, ambayo yote yanahusiana na masuala ya kidunia ya watu kuna mambo mengine mengi tu ya kidunia ambayo yamezingatiwa wakati wa kujadili matendo ya ibada. Mbali na ukweli kwamba watu wanapaswa kuzingatia na kumkumbuka Mwenyezi Mungu Mtukufu, kuna malengo mengine pia ya ibada, mengi ya hayo yanahusiana na maisha ya kidunia ya wanadamu. Hata katika Sala na Saumu, matendo ambayo huonekana na wengi kama ni matendo ya ibada tu na ni njia ya kuwasiliana na Mwenyezi Mungu, kuna fursa na manufaa mengi mno kwa ajili ya maisha ya kilimwengu ya wanadamu yaliyojificha humo kiasi kwamba tukiamua kuyajadili hapa, tutakuwa tunaikimbia mada yetu kuu. Kwa kuzingatia hayo tuliyoyasema hapo juu, tunaweza kuhitimisha kwa kusema kuwa Uislamu umeyapa umuhimu maalumu masuala ya watu ya kidunia na umeweka kanuni zote zinazofaa kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa mtu mmoja mmoja na jamii. Kwa kifupi, isisahaulike kuwa Uislamu huwataka watu wapambane katika medani zote mbili, na kwa kuzingatia mahitaji ya mwili na akili zao, wanapaswa kuilinda dhidi ya uchafuzi, na wawe na njia itakayowawezesha wanadamu kuishi maisha yenye ustawi na furaha duniani na Akhera. Uislamu unasema: “Fanya juhudi na uwe na ustawi na furaha katika dunia zote mbili (hapa na Akhera) kwa shughuli za busara na zenye maana.�

FANYA KAZI, LAKINI SI KILA KAZI Katika Uislamu, kuna kazi kadhaa ambazo zimetangazwa kuwa haramu kwa sababu ufisadi na uovu huchipuka kwa kuzifanya. Kwa mfano, utengenezaji wa vifaa vya kuchezea kamari ni kazi, lakini ni kazi ambayo mwisho wa safari italeta uovu mkubwa. Kutengeneza na kuuza pombe ni kazi, lakini ni kazi ambayo imetangazwa na Uislamu kuwa ni haramu kutokana na athari zake zenye madhara na 17

12:43 PM

Page 17


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

kuleta hasara. Qur’ani Tukufu inasema:

“Enyi mlioamini, hakika pombe, kamari, masanamu na ramli, vyote ni uchafu na kazi ya shetani, hivyo jitengeni navyo ili mpate kufanikiwa. Hakika Shetani anataka kujenga uadui na chuki miongoni mwenu kwa kutumia pombe na kamari, na ili awasahaulisheni kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kusali. Basi je ninyi mtaviacha? (SuratulMaidah, 5:90-91). Tofauti nyingi sana zinajitokeza baina ya marafiki wakati wa kucheza kamari na uadui usiosuluhishika unajengeka kwa sababu ya kamari. Kiasi kikubwa cha mali kinateleza kutoka mikononi mwa wamiliki wake na matajiri wengi wanafilisika kwa sababu ya kamari. Uhalifu mwingi unafanywa na watu kama matokeo ya kamari. Pombe na vileo vyote ni vitu vyeye maangamizi. Wanazuoni na watafiti wa kilimwengu wamefanya utafiti wa kina na wameandika makala nyingi sana ili kuujulisha umma juu ya athari zenye madhara za pombe katika mwili wa mwanadamu, uhalifu unaofanywa na walevi pamoja na hatari mbalimbali zinazoitishia jamii.

18

12:43 PM

Page 18


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Kwa kuzingatia athari mbaya za kamari na ulevi katika mwili wa mwanadamu, Uislamu umeviona vitu hivi viwili kuwa visivyofaa na umeharamisha utengenezaji wake, uuzaji na utumiaji wake. Kwa kuzingatia ukweli huo, tunahitimisha kwa kusema kuwa kazi na jitihada ni mambo yaliyosifiwa katika Uislamu na yanayostahili malipo ya kiroho kama tu yalivyo matendo ya ibada ili mradi tu kazi hiyo iwe halali na yenye manufaa kwa watu.

VIPENGELE MBALIMBALI VYA MATENDO MEMA Inafaa ikumbukwe kuwa maneno “matendo mema” yaliyotajwa huko nyuma yana maana nyingi: i)

Hutumika katika matendo mbalimbali ambayo watu huyafanya katika kuyaboresha maisha yao na kupata ujira kwa masaa waliyofanya kazi.

ii) Hutumika katika hatua mbalimbali ambazo watu hupaswa kuzichukua katika kuyaboresha mahusiano yao ya kijamii na ili kupata ustawi wa kiroho. iii) Upole na wema kwa watu, shughuli za kijamii, jitihada za kuhakikisha kuwa wanadamu wenzake wanakuwa na ustawi mzuri mafanikio nk., ni matendo bora na ya heshima zaidi. Qur’ani Tukufu inasema:

19

12:43 PM

Page 19


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

“Na kwa hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha uadilifu, hisani na kuwapa jamaa. Anakataza uchafu, uovu na uasi. Anawaonyeni ili mpate kuzingatia. (Suratul Nahl, 16:90). Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Mtu anayependwa zaidi na Mwenyezi Mungu ni yule mwenye manufaa zaidi kwa watu.” Ni kazi ipi inaweza kuwa nzuri kuliko mtu ambaye nafsi yake huwa ni chanzo cha wema na huduma kwa jamii na watu hunufaika kutokana naye! Katika kila jamii kuna watu wengi wenye umri mkubwa, wagonjwa na walio dhaifu, na katika kila taifa kuna watoto ambao ni yatima na hakuna mtu wa kuwaangalia. Ni kazi gani inaweza kuwa nzuri kuliko mtu kujiongezea muda wake wa kazi kwa saa moja ya ziada, na malipo ya hiyo saa moja akayatumia kwa ajili ya mahitaji ya mtoto ambaye hana mlezi, au kwa mtu mgonjwa au maskini. Matendo na huduma hizi za heshima huwa ni sababu ya mtu kupendwa na Mwenyezi Mungu na nafsi yake mtu huyu huridhika na kuwa na amani. Mwenyezi Mungu humlipa matendo yake katika dunia zote mbili. Imam Ja’far Sadiq (a.s) anasema: “Wafanyie wema wale wanaostahiki na wasiostahili. Kama wao hawastahili kufanyiwa wema huo, wewe unapaswa kustahiki wema huo.” Imam Baqir (a.s.) amesema: “Kama nikiwatazama jamaa wa familia za Waislamu na nikatoa kwa ajili ya chakula chao na nguo zao na kuwalindia 20

12:43 PM

Page 20


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

heshima yao katika jamii, huipenda kazi hiyo zaidi kuliko kufanya Hijja Sabini zilizopendekezwa.” (al-Kafi, Tara’iful-Hikam). Masaa ya mapumziko na kutokuwa na kazi ya kufanya humtokea kila mtu katika maisha, na watu huchagua njia mbalimbali za kuyatumia masaa haya, kwa bahati mbaya watu walio wengi huyapoteza masaa haya yenye thamani katika mambo yasiyo na maana ingawa wanaweza kutumia katika mambo yenye manufaa katika maeneo mbalimbali na kuutumia kikamilifu muda wao usio na kazi. Mahospitalini kuna mamia ya binadamu wenzetu ambao hawawezi kutoka vitandani kwa sababu miili yao inaumwa na ni dhaifu na nyoyo zinazohuzunika na zimekata tamaa. Wanahitaji kufarijiwa na kuhurumiwa. Baadhi yao wanahitaji msaada wa kifedha pia. Ikiwa, kama ishara ya shukrani kwa afya zetu njema, sisi tutawajulia hali wagonjwa wakati wa muda wetu wa ziada, tukiwasikiliza matatizo na huzuni zao, tukiwahurumia na kuwapa msaada uliopo ndani ya uwezo wetu, hiki kitakuwa ni chanzo cha mafanikio katika dunia zote mbili. NUKUU 1). Yeote mwenye kufanya jitihada anaifanyia nafsi yake. Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitegemea na hahitaji msaada wa wakazi wa ulimwengu (Qur’ani Tukufu). 2). Jitihada hufunga mlango wa umaskini. 3). Mwenyezi Mungu anamchukia mtu anayekaa bila kufanya kazi. 4). Yeyote yule ambaye ni mzigo kwa wengine amelaaniwa – (Mtukufu Mtume). 5). Jiepusheni na tamaa na uvivu kwa sababu ukiwa na tamaa hutaridhika na haki yoyote utakayopata na ukiwa mvivu hutaweza kutoa haki 21

12:43 PM

Page 21


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

yoyote kwa wanaozistahiki. (Imam Sadiq). 6). Ugoigoi katika kufanya kazi humfanya mtu ashindwe kufikia malengo yake. 7). Mtu mwenye busara hutegemea juhudi zake na mpumbavu hutegemea matumaini yake yasiyo na mafanikio. 8). Fanya juhudi ili uhakikishiwe kupata mafanikio – (Imam Ali (a.s.)). 9). Ikiwa huna uhakika kwamba ulichofanya ni chenye manufaa kwa jamii huwezi ukasema kuwa umefanya kitu cha heshima. (Tolstoy) 10). Lengo la maisha limeegemea katika vitu vitatu: dhamiri, kazi na mafanikio (Pasteur). 11). Furaha ni kwa yule ambaye hufanya kazi kwa ajili ya furaha ya wengine – (Ashtur Gatha). 12). Mwenye bahati njema ni yule ambaye hufanya matendo mema (Ciceron). 13). Asilimia tisini na tisa ya ‘kipaji’ ni jasho la paji la uso na kwa hiyo asilimia moja ni msukumo wa nafsi. – (Edison). 14). Kazi ndio mtaji wa ustawi - (Socrates). 15). Kazi ni rafiki bora kabisa wa mwili na nafsi ya mtu – (Falileo). 16). Watu watukufu huwa hawaegemei chochoe isipokuwa kazi zao na hawamuombi msaada yeyote – (Confucius). 17). Dunia ni mali ya wafanyao bidii bila kuchoka - (Methali ya Kijerumani). 22

12:43 PM

Page 22


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

18). Kazi na juhudi ni namna na njia iliyonyooka kwa ajili ya kufikia malengo – (Dr. Garlank). 19. Kazi na juhudi sio tu kwamba huyafanya maisha kuwa mazuri na rahisi kwetu, bali pia humfanya mtu awe na thamani na maarufu – (Schiller). 20). Tumeletwa duniani ili tuwe na manufaa kwa wengine – (Akambas). 21). Ushindi ni kwa wale wafanyao jitihada zaidi na bila kuchoka kuliko wengine – (Napeleon). 22). Siri ya mafaniko na maendeleo yangu imo ndani ya maneno mawili; kazi na imani – (Edison). 23). Kwa kadri mtu anavyofanya kazi zaidi ndivyo atakavyokuwa hodari zaidi wa kufanya kazi zaidi – (William James). 24). Moja ya vitu vizuri juu ya kazi ni kuwa huifanya siku kuwa fupi na maisha kuwa marefu – (Diedro). 25). Kwa kadri mtu anavyojibidiisha katika kazi ndivyo atakavyokuwa anaikaribia furaha – (Ciceron). 26). Kazi na shughuli za saa moja huuridhisha moyo na kuujaza mfuko fedha kuliko kuteta na kusengenya kwa mwezi mmoja – (Benjamin Franklin). 27). Nimelazimika kufanya kazi, kwani vinginevyo, maadili yangu yataharibika – (Tolstoy). 28). Wapumbavu wanaweza kufundishwa kwa kufanyishwa kazi nyingi na kumenyeka – (Buzar Jumhayr). 23

12:43 PM

Page 23


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

29). Kama wanaume wanavyopata haiba miongoni mwa watu na jamii, wanawake pia wanaweza kupata hadhi katika mazingira ya nyumbani kwa kuwalea watoto na kutekeleza majukumu yanayohusiana na wao – (Balzac). 30). Kama unatamani kwamba wengine watende kwa mujibu wa unavyosema, wewe mwenyewe unapaswa kutenda kwa mujibu wa unavyosema. – (Anashirwan).

*

*

*

*

ELIMU Moja ya mambo yaliyotiliwa mkazo mkubwa kabisa na Uislamu, na ambalo umelikokoteza sana ni elimu na busara. Kutafuta elimu kunahesabiwa kuwa ni moja ya wajibu za Kiislamu. Katika kitabu hiki hatukusudii kuuhubiri Uislamu chini ya kichwa cha habari “elimu na busara” na kunukuu kutoka katika Qur’ani na hadithi na historia na kusema Uislamu umeunga mkono suala la elimu kwa namna hii na ile na umewahimiza sana watu kuitafuta. Hapana. Hatudhani kwamba suala hili limefichika kwa yeyote na mengi sana yameandikwa na kusemwa juu ya jambo hili kiasi cha kuwa haionekani kwamba ni muhimu kulirudia tena. Aidha, kuandika na kuzungumza juu ya masuala haya hakusaidii kitu kwani baada ya karne za kuzungumza na kuandika juu ya jambo hili, hali ya Waislamu bado iko kama tunavyoiona leo. Marhum Sharfud-din Amili, aliyekuwa kiongozi mkubwa wa Shia wa Lebanon alimenyeka kwa miaka na akaandika na kuchapisha vitabu vyenye thamani na manufaa kwa faida ya wanachuoni wa Kiislamu. Hata 24

12:43 PM

Page 24


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

hivyo, baada ya kazi yote hiyo ngumu, alitupia jicho kwenye hali ya kusikitisha ya Shia wa Lebanon na kwa uchungu mkubwa alikuta wengi wao wakiwa katika hali ya chini kabisa. Alikuta kwamba walio maskini zaidi, wenye shida zaidi na watu walio nyuma zaidi katika matabaka mbalimbali nchini Lebanon walikuwa ni Shia. Kulikuwa hakuna madaktari, wahandisi, maprofesa au watu wowote wanaoheshimika miongoni mwao, na hata kama walikuwepo basi walikuwa ni wachache sana kiasi cha kutokuwa na athari yoyote. Shia walikuwa wakiendesha mabafu ya umma ya kulipia, saluni za kunyolea nywele na kufanya kazi nyingine za hali ya chini kama vile ukuli na kufagia barabara. Baada ya kutazama hali hii, mtu yule maarufu alianza kutafakari kuwa vitabu vyake vitakuwa na faida gani wakati Shia walikuwa wakiishi maisha duni na ya nyuma ya kuhuzunisha kabisa, na watu watakaosoma vitabu vyangu na kulinganisha na hali halisi ya Shia wataweza kuhoji kuwa kama kweli Shia ni madhehebu ya maana na ya kiukombozi basi Shia ambao ni wafuasi wa madhehebu haya wangekuwa na maisha bora na ya kuheshimika zaidi! Baada ya kutafakari hivi aliamua kukusanya nguvu zake ili kuboresha hali ya maisha ya Shia na kuleta mabadiliko muhimu na ya msingi. Alianzisha jumuia nyingi za kusaidia jamii pamoja na shule na alifanikiwa kwa kusaidiwa na wafuasi wake kuwaondoa Shia wa Lebanon kutoka katika ujinga na uduni. Kwa kusema kweli inashangaza sana kuona kwamba sisi Waislamu tumeridhika kwa maneno tu na tumebakia nyuma katika suala zima la kutafuta elimu na ujuzi. Katika wosia wake wa mwisho, Imam Ali (a.s.) aliwaonya Waislamu wa dunia kwamba waangalie wasiokuwa Waislamu wasije wakawazidi na kuongoza kwa sababu watakuwa wameamua kuyatekeleza mafundisho ya 25

12:43 PM

Page 25


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Qur’ani na Waislamu kubaki nyuma wakishangaa. (Nahjul–Balaghah). Mwandishi wa Kifaransa, Dr. Gustav Leabon anasema: “Katika kipindi ambacho utamaduni wa Kiislamu ulifikia kilele chake nchini Hispania, vituo vyetu vya elimu vilikuwa na makasri ambamo walikuwa wakiishi makabaila na mamwinyi waliokuwa wakiishi maisha ya nusu-ushenzi na walikuwa wakijivunia wenyewe kwa kutojua kwao kusoma na kuandika. Miongoni mwetu, sisi wakristo, waliokuwa wamesoma zaidi walikuwa ni makasisi wajinga ambao waliyatumia maisha yao yote kwa kuleta vitabu kutoka katika makanisa ya Ugiriki na Urumi, na walikuwa wakivifuta na kuandika juu yake maneno na visomo vya kidini visivyoeleweka kirahisi katika karatasi za ngozi” Will Durant anaandika: “Katika zama za kati, Waislamu walikuwa ni vinara katika fani ya Sayansi na maendeleo makubwa yalipatikana nchini Azarbaijan na Morocco katika fani ya Hisabati, jambo lililodhihirisha kwa mara nyigine tena ukomavu wa ustaarabu wa Kiislamu. Sayansi ya mimea ambayo ilikuwa imesahauliwa kabisa baada ya kufa kwa Theophrastus ilikuja kufufuliwa na Waislamu. Idrisi aliandika kitabu juu ya mimea na alielezea tabia za mimea ipatayo 360. Yeye hakuwa ameshughulishwa na nadawa peke yake; bali pia alishughulika na masomo ya sayansi pamoja na elimu ya mimea. Katika kipindi hiki pia, kama ilivyokuwa kwa vipindi vingine, madaktari wakubwa wa Asia, Afrika na Ulaya waliibuka kutoka miongoni mwa Waislamu. Uislamu ulikuwa unaongoza duniani kwa kuwa na hospitali bora. Hospitali iliyojengwa na Nuruddin mwaka 556 A.H. (1160 B.K.) ilitoa huduma za matibabu bure kwa wagonjwa kwa karne tatu na vilevile aliwapa dawa walizohitaji bure. Pia hospitali za wagonjwa wa akili zilikuwepo katika miji yote mikubwa ya Kiislamu kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wenye matatizo ya akili. (History of Civilization, Juz. 11, uk. 297301).

26

12:43 PM

Page 26


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Katika wakati ambapo Ulaya na Ukristo vilikuwa vikiteketea kwa ujinga, Waislamu walikuwa na ustaarabu wao, yaliyoelezwa hapo juu na wanahistoria ni sehemu tu ya ustaarabu huo. Bila shaka ustaarabu waliokuwa nao ulipatikana kutokana na mafundisho ya Uislamu kwa sababu hata hawa Waislamu, kabla ya kuja kwa Uislamu, walikuwa wamezama katika ujinga na upotofu kama tu yalivyokuwa mataifa mengine na historia inatueleza waziwazi juu ya hali mbaya ya maisha waliyokuwa wakiishi. Uislamu ulikuja na mfumo mpana na kwa mafundisho yenye uhai na ukombozi, taratibu Uislamu uliiongoza jamii iliyokuwa imechafuka na kupotoka kuelekea kwenye ustawi, Uliwabadilisha watu wale waliokuwa nyuma na kuwa taifa lenye elimu na lililoendelea. Uislamu haujaweka sharti lolote la kutafuta elimu na Uislamu umelifanya jambo la kutafuta elimu kuwa ni wajibu kwa Waislamu wote, katika hatua zote za maisha, katika kila sehemu na kwa kupitia mwalimu yeyote. Kauli hiyo inathibitishwa na maagizo manne yafuatayo yaliyotolewa na Mtukufu Mtume wa Uislamu: (i) Kutafuta elimu ni wajibu kwa kila Mwislamu, mwanamke na mwanaume. Katika kauli hii hakuna sharti wala kinzano lolote linaloweza kuonekena, kama ilivyo katika maamrisho yaliyo mengi ya Uislamu, na katika suala hili pia hapajatengwa jinsia yoyote kwa sababu neno Muislam linawahusu wote wanawake na wanaume. Katika hadithi hii Mtume amewaambia wanadamu kwamba kutafuta elimu ni wajibu na jukumu la jumla halikuwekewa mipaka kwenye jinsia au tabaka maalum.

27

12:43 PM

Page 27


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

(ii) Tafuteni elimu toka mkiwa wachanga hadi mnaingia kaburini. Katika hadithi hii, sharti la wakati na umri limeondolewa na imeelezwa kwamba hakuna wakati maalum au zama fulani ambapo elimu na ujuzi vinapaswa kutafutwa bali mchakato huu unapaswa kuanza tangu mtu anapozaliwa na kuendelea hadi anapokufa. (iii) Ujuzi ni Mali ya Muumini iliyompotea. Ujuzi unajumuisha maneno imara, ya kimatiki na sahihi. Katika hadithi hii Waislamu wameshauriwa wasishughulishwe sana na chanzo ambako elimu na ujuzi vinapatikana, wameshauriwa kuichukua hata kama ni kutoka kwa washirikina na wanafiki. Ni lazima tukumbuke kuwa katika hadithi hii neno hikmat limetumika. Ina maana kuwa maneno ya kweli ya kimantiki yanapaswa kukubaliwa kutoka kwa yeyote yule awaye. Hata hivyo kuna sharti la msingi kwamba maneno hayo yasiwe na shaka yoyote juu ya usahihi wake. Hivyo watu ambao hawawezi kuhukumu na kutofautisha kati ya maneno ya kweli na ya uongo hawapaswi kulichukulia kuwa ni kweli kila neno wanalolisikia kutoka kwa yeyote awaye, na wasishawashike na propaganda za wapotoshaji. (iv) Tafuteni elimu, japo iwe China. Katika hadithi hii sharti la sehemu limeondolewa na imeelezwa waziwazi kuwa elimu itafutwe hata kama itakuwa ni sehemu ya mbali kabisa na upatikanaji wake unaweza kuhusisha shida na matumizi ya fedha. Kiini cha maelekezo manne yaliyotajwa hapa juu ni kuwa ni muhimu kwa Waislamu wote katika hatua zote za maisha yao kupata elimu na hikma kutoka sehemu yoyote ile na kwa yeyote yule itakapoweza kupatikana na huu ni wajibu wa kidini.

28

12:43 PM

Page 28


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Kilichotajwa hapo juu ni sampuli tu ya mapendekezo ya Uislamu juu ya utafutaji wa elimu na hikma na kama tulivyoeleza hapa awali, sio lengo letu kutaja yote yalioagizwa na Uislamu juu ya suala hilo. Waislamu wa siku za mwanzo za Uislamu waliyatekeleza mafundisho haya matukufu ya Uislamu kwa karne kadhaa na hivyo wakafanikiwa kuwa taifa lenye kutukuka duniani. Kama ilivyodokezwa huko nyuma, wanakemia mashuhuri, wanajiografia na wanajimu walitukuka na wanachuoni waliobobea katika fani mbalimbali za Sayansi na teknolojia na viwanda waliibuka kutoka miongoni mwa Waislamu. Wasomaji wanaotaka kupata habari zaidi za kina juu ya hili, wanashauriwa kusoma kitabu kiitwacho “History of Civilization” cha Jurji Zaidan, History of Civilization cha Will Durant, Civilization of Islam and the Arabs kilichoandikwa na Gustav Leo Bon na Fehrist Ibn Nadim. Kwa kuzingatia hayo yaliyoelezwa hapo juu, je hili sio suala la majuto makubwa kwamba licha ya kumiliki mafundisho mazuri kiasi hiki, na mafanikio yanayong’aa kiasi hiki tuliyoyapata huko nyuma pamoja na watu wenye elimu kubwa, bado Waislamu walale usingizi mzito, na bila ya kuzungumzia kumiliki kwao shahada mbalimbali za elimu, wengi wao hawajui kusoma na kuandika na mara zote wananyoosha mikono yao kuomba msaada kwa maadui wa Uislamu? Sababu ya msingi ya masaibu na mikosi yote hii ni uzembe wa Waislamu katika kipindi cha Zama za Kati pamoja na hujuma za wakoloni wa kikristo. Will Durant anasema: “Minara mirefu ya makanisa ya kikristo na minara ya kengele za kanisa inawiwa na minara ya misikiti. Kufufuka kwa usanii wa ufinyanzi wa vyungu nchini Italia na Ufaransa ulikuwa ni matunda ya kuhamia kwa mafundi stadi wa Kiislamu kwenye nchi mbili hizi ambao uliotokea katika karne ya 12 na vilevile ilikuwa ni matokeo ya safari za wapagazi hawa wa kitaliano kwenda Hispania ya Kiislamu. Wahunzi wa 29

12:43 PM

Page 29


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

vyuma, watengenezaji wa vyombo vya kioo na watengenezaji wa vitabu wa Italia na watengenezaji wa dereya na ngao za chuma wa Hispania wote hawa walijifunza ujuzi huu kutoka kwa mafundi wa Kiislamu. Karibu katika maeneo yote ya Ulaya, wafumaji wa nguo walikuwa wakienda katika mataifa ya Kiislamu kujifunza ujuzi huo kiasi kwamba hata mabustani yalitengenezwa huko ulaya kwa kufuata staili ya Kiiran. Upenyaji huu wa Uislamu na Waislamu katika nchi za Ulaya kulifanyika kwa kutumia biashara, vita, kutafsiri maelefu ya vitabu kutoka katika Kiarabu kwenda katika Kilatini na safari za wanachuoni kama vile Gerbert, Michelscot na Adelaid Bath katika nchi ya Hispania ya Kiislamu na pia vijana wa Kikristo ambao walipelekwa na baba zao wa Kihispania kwenye mabaraza ya wana wa wafalme wa Kiislamu kwenda kujifunza na kufundishwa upandaji wa farasi kwa sababu baadhi ya waungwana wa Kiislamu walikuwa wanaonekana kuwa mahiri zaidi katika upandaji wa farasi na walioadilishwa vyema. Wakristo na Waislamu katika nchi za Syria, Misri, Sicilia na Hispania walikuwa na maingiliano ya kudumu. Wakati pale wakristo walipopata maendeleo katika maeneo ya Hispania ya Kiislamu, zile athari za fani za fasihi, sayansi, falsafa na sanaa waliyojifunza kutoka kwa Waislamu zilibebwa katika mkondo wake kwenda kwenye ardhi nyingine za Kikristo. Kama kwa mfano, tunaweza kusema utawala wa Kikristo katika Talitala mnamo mwaka 478 A.H. (1080 A.D.) ulisaidia sana kuongeza kukuza kiwango cha elimu ya Wakristo katika fani ya unajimu na kuthibitisha imani yao juu ya uduara wa dunia. Hata hivyo, manufaa haya waliyoyaazima kutoka kwa Waislamu hayakuuzima moto wa chuki. Hii ilitokana na ukweli kwamba, baada ya chakula, hakuna kinachopendwa zaidi na mwanadamu kuliko imani yake ya kidini. Mwanadamu hawezi kuishi kwa chakula tu na ili aishi anahitaji dini pia ili 30

12:43 PM

Page 30


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

iweze kumpatia matumaini katika maisha yake. Kwa sababu hii mwanadamu hulipuka kwa kitu chochote kitakachohatarisha chakula au dini yake. Kwa karne tatu nzima Wakristo walishudia uvamizi wa Waislamu ukizinyakua ardhi za Wakristo moja baada ya nyingine mfululiza na kwa mfuatano wakawapeleka wakristo kwenye zile nchi ambazo walikuwa wamekwisha kuziteka. Mikono ya Waislamu yenye nguvu iliziteka biashara za Wakristo na ilisikika kila mahali kuwa Waislamu waliowachukulia Wakristo kuwa ni makafiri. Hatimaye mgongano uliokuwa ukitarajiwa ulitokea, na kambi mbili hizi za ustaarabu zikapambana katika vita vya msalaba ambapo sehemu kubwa ya watu kutoka pande zote mbili, Mashariki na Magharibi waliuliwa. Uadui huu wa kubadilishana ulikuwa ni jambo lenye uathiri katika historia ya Zama za Kati. Dini ya tatu, yaani Uyahudi pia ilijikuta ukishambuliwa na pande zote zinazogombana. Nchi za Magharibi zilishindwa katika vita vya msalaba lakini ziliibuka washindi katika mabishano bishano ya kidini. Wakristo wote waliokuwa wanapenda na kuchochea vita waliondolewa katika ardhi takatifu lakini Waislamu ambao ushindi wao uliochelewa ulikuwa umenyonya damu zao na ambao nchi zao zilikuwa zimeharibiwa vibaya na Wamongolia, walikabiliwa na zile Zama za giza, na ujinga na umaskini vikatawala juu yao. Kwa upande mwingine nchi za Magharibi zilizokuwa zimeshindwa na ambazo zilikuwa zimepata uzoefu kutokana na jitihada za mfululizo zilisahau kule kushindwa kwao, wakakata kiu yao ya elimu na kupenda maendeleo kutoka kwa audi zao, wakajenga makanisa ya kifahari na wakaanza kupita katika njia ya elimu kwa bidii zote. Kwa kusema kweli, msomaji wa kawaida anaweza kushangaa juu ya maelezo haya marefu juu ya Ustaarabu wa Kiislamu ambapo mwanachuoni mtafiti anasikitikia ufupi wake usiofaa. Ni katika vipindi vya ustawi bora vya historia ambapo katika kipindi kifupi, jamii iliweza 31

12:43 PM

Page 31


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

kutoa watu mahiri katika fani za siasa, elimu, fasihi, jiografia, historia, hisabati, unajimu, kemia, falsafa, na utabibu ambao walionekana katika karne nne za Kiislamu kuanzia wakati wa Harun Rashid hadi wakati wa Ibn Rushd.” (Taz. Will Durant, History of Civilization, Juz. 11, uk. 320 – 322). Hii ni hisoria ya huko nyuma ya Waislamu na huu ndio ustaarabu wao. Huku ndio kuporomoka na kuanguka kwa Waislamu na pia hizi ndio sababu na vipengele vyake. Hapa inafaa ieleweke kwamba kuandika tu na kusema:

“Mwenyezi Mungu atawainua waumini na wale wenye elimu katika madaraja” (Suratul-Mujadillah, 58:11): na kusoma:

“Je wale wanaojua wanaweza kuwa sawa na wale wasiojua?” (Suratuz-Zumar, 39:9) na hadithi zinazozugumzia suala hili hakutatui tatizo hili na kaulimbiu hizi takatifu lazima ziletwe kwenye matumizi na harakati za kivitendo lazima zifanye kazi na kutumika ili mabadiliko ya kivitendo yaweze kutokeza miongoni mwa umma wa Kiislamu kwa ajili ya utafutaji wa elimu na ukamilifu. Ni lazima kuwa kama mataifa yaliyostaarabika yalivyopata heshima na mafanikio kutokana na jitihada za bila kuchoka za wanachuoni wao. Edison mara zote aliendelea na shughuli zake za Kisayansi pamoja na majaribio ya Kisayansi kwa ustahamilivu wa ajabu na wakati mwingine alikuwa akifanya kazi kwa masaa ishirini kwa siku. Mara nyingi alikuwa akisema: “Nina kazi nyingi za kufanya na maisha ni mafupi. Hivyo lazima nifanye haraka.” Alipokuwa akifanya majaribio alikuwa akipata majeraha. 32

12:43 PM

Page 32


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Wakati fulani tindikali ya betri ilimmwagikia na kuinguza nguo yake mpya na kubambua ngozi yake. Mara nyingi tu alikuwa akiumia kwa mishtuko ya umeme. Alikuwa akifanya kazi kwa bidii sana nyakati za mchana na usiku alikuwa akilala masaa machache sana tena juu ya mabenchi ya kiwanda. Maisha yote ya Edison yaliyochukua kama nusu karne yalipita namna hii. Hakuacha kazi na uchunguzi mpaka siku ya mwisho ya uhai wake.

Uelewa mbaya Baadhi ya watu wanafikiri kuwa kwa neno ‘elimu’ Uislamu unamaanisha ni elimu ya teolojia tu – Ufufuo, majukumu ya mtu mmoja mmoja na ya kijamii, kanuni za ibada na vitu vingine kama hivi, ingawa mara nyingine neno elimu limetumika kwa maana ya jumla na bila ya kuwa na sharti lolote juu yake. Pia kwa kuzingatia lengo ambalo Uislamu unalo juu ya Umma wa Kiislamu tutona kuwa elimu inayozungumziwa hapa sio ya fani moja tu. Uislamu unataka Waislamu waheshimike, wawe huru na wanaojitegemea. Uislamu unataka Waislamu wawe na uhuru wa kiuchumi na kijamii. Uislamu hautaki Waislamu wanyooshe mikono yao kuwaomba wengine. Uislamu unataka Waislamu wawe mbele kuliko mataifa mengine yote katika fani zote, kimaada na kiroho. Ili kuyafikia malengo haya, Waislamu wanapaswa kuwa na wanavyuoni wakubwa na waliobobea katika fani mbalimbali za sayansi na sanaa pamoja na wataalamu na mabingwa watakaofanya kazi katika fani mbalimbali. Kama hatuna wataalamu katika fani za uchumi, kilimo, utatibu, viwanda na sanaa na sayansi nyingine za kisasa, bila shaka tutaendelea kuwategemea wengine na hili la kuwategemea wengine linapingana moja kwa moja na malengo ya Uislamu.

33

12:43 PM

Page 33


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Hivyo wajibu wetu wa kidini unatutaka kila mmoja wetu, kwa vyovyote vile nafasi na hadhi yake itakavyokuwa, anapaswa atoe mchango wake katika kuendeleza na kukuza elimu na ujuzi. Anapaswa awafundishe wengine yale anayoyajua yeye mwenyewe. Atoe elimu yake kwa wengine kwa kuandika makala na vitabu na kuandaa mikutano na makongamano. Atafsiri kwenda katika lugha yake, vile vitabu vyote vyenye manufaa vilivyoandikwa katika lugha nyingine. Anapaswa awahimize vijana kutafuta elimu na ubora na awashawishi waendelee na masomo yao na kupata shahada mbalimbali za maendeleo. Awazuie vijana wasipoteze muda wao na kwa nia ya kuyafikia malengo haya aanzishe maktaba na vituo vya kujifunzia na kusomea. Anunue vitabu vyenye manufaa na kuwapatia wanafunzi na wale wote wanaotafuta elimu. Wajibu huu – kukuza na kupanua elimu – linapaswa lijumuishwe na kuunganishwa na wajibu mtukufu zaidi wa kuimarisha imani na utekelezaji wa adabu njema na nidhamu katika jamii. Ni muhimu kwamba kwa kadri maendeleo ya Kisayansi yanavyokua, kanuni za kiroho na kimaadili zinapaswa pia kuimarishwa ili matokeo yatakayopatikana yawe bora na yenye manufaa na elimu ihakikishe ustawi wa jamii. Vinginevyo, elimu bila imani ya kiroho inaweza kuwa kitu cha hatari sana.

FADHILA ZA WANACHUONI Makundi mawili ya Waislamu yalikuwa yamekaa katika kona mbili za msikiti wa Madina. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliingia na kuyatazama makundi yote mawili na kuuliza: “Hawa wanafanya nini?” Alijulishwa kuwa kundi moja lilikuwa likijishughulisha na visomo pamoja na dua wakati kundi jingine lilikuwa likijadili mambo ya kielimu. Mtukufu Mtume alisema: “Makundi yote yanafuta njia ya wema. Lakini nitajiunga na kundi linalojadili masuala ya kielimu kwa sababu nimeteuli34

12:43 PM

Page 34


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

wa katika kazi ya utume kuwaongoza watu kwenye elimu na ukamilifu.” Kisha akajiunga na kukaa katika kundi hilo.” (Munyatul Murid). Katika mkutano ambao ulihudhuriwa na masahaba zake wakuu na wale wenye umri mkubwa, Imam Ja’far Sadiq alimpa cheo Hisham bin Hakam, aliyekuwa na umri mdogo kuliko wote (Biharul-Anwar, Juz. IV). Kwa kuwa Hisham alikuwa ni mwanachuoni, khatibu (mhutubiaji) mwenye mvuto na mtumishi mkweli na mwaminifu wa Uislamu, Imam Ja’far alikinyanyua cheo chake. Kuwaheshimu na kuwatukuza wanachuoni na watafutaji wa elimu ni moja ya njia bora za kuwavutia wengine katika kutafuta elimu na ujuzi na njia hii imekuwa ikitumika mara zote na viongozi watukufu wa Uislamu.

KAMPENI DHIDI YA ELIMU Wakoloni wa Kikristo, kwa kupitia maajenti wao na wale wanaowaunga mkono, wameanza kueneza propaganda miongoni mwa wasomi vijana wa Kiislamu kwamba sababu ya kurudi nyuma kwa nchi za Kiislamu ni dini yao. Hivyo, kama wanataka kuondokana na uduni wao wanapaswa kuachana na dini ili waweze kupata maendeleo waliyoyapata mataifa yaliyostaarabika, kama vile walivyofanya Wakristo wenyewe kujinasua kutokana na minyororo ya Ukristo na hivyo hatimae wakafanikiwa kupata maendeleo haya ya ajabu. Wameijenga dhana hii potofu na mkanganyiko kwa makusudi ili kwa kuwapotosha vijana wa Kiislamu waweze kuzinyonya nchi za Kiislamu kwa kiasi kikubwa zaidi na waendelee kuwaacha Waislamu nyuma. Ni kweli kwamba Wakristo walipiga hatua na kushika njia ya maendeleo kwa kujinasua kutokana na minyororo ya Kanisa na kutupilia mbali hizi zilizokuwa zikidaiwa kuwa ni kanuni za kidini zilizowekwa na mapadri na 35

12:43 PM

Page 35


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

viongozi wengine wa kanisa. Lakini kuzifananisha imani za kishirikina za kanisa kwa upande mmoja na sheria za milele za Uislamu itakuwa ni kuchafua jina la Uislamu na dhulma kubwa kabisa isiyo ya kibinadamu. Kwa kutumia hizo sheria za kitoto zilizobuniwa na wachungaji wa kikristo, kanisa lilizuia mkondo wa maendeleo ya kisayansi na viwanda na kanisa likawaua na kuwatesa wasomi na watafiti wengi. Kanisa lilikuwa limeweka baadhi ya iliyoitwa mitazamo na rai za kisayansi juu ya jamii ya watu wa Ulaya na kuipa mitazamo hiyo majina ya “Sheria Takatifu za Mwenyezi Mungu” na wakati sayansi ilipothibitisha kuwa fikra za kanisa hazikuwa sahihi na ni upuuzi mtupu, basi watu hawakuwa na namna isipokuwa kulipuuza kanisa na kanuni zake, na wakajinasua kutoka katika minyororo ya mapadri na kuamua kuiamini elimu na ujuzi. Wakati huo huo kitu kilichosaidia zaidi kulipindua kanisa na Ukristo wake kilikuwa ni kung’ang’ania kwa viongozi wa kanisa waliokuwa wanataka kurejesha heshima na utukufu wao uliopotea. Ung’ang’anizi na kutobadilika huko kulifikia hatua kwamba, ili kulazimisha hizo imani za kanisa, kanisa liliamua kutumia udikteta na mabavu na liliwabana watu katika nyanja zote za maisha kama jinamizi na likawanyang’anya watu amani na utulivu wao. Kwa amri ya viongozi wa kanisa, taasisi ya hatari na kutisha iitwayo “Inquisition” (Yaani taasisi iliyowekwa na kanisa na Roma - Mahakama ya Pope - katika karne ya 15-16 ). Taasisi hii iliwatesa vikali kwa mateso ya kila aina watu wote waliokuwa wakipingana na mawazo ya kanisa. Kanisa pia liliwatesa wasomi na wanavyuoni wengi. Liliwachoma moto wasomi kwenye matanuri kwa kosa tu kwamba waliamini kuwa dunia inazunguka na ina umbo la mvirigo na kwamba ilikuwa hivyo daima, hivyo wakawa wameufichua ukweli.

36

12:43 PM

Page 36


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Mateso haya yalifikia hatua kubwa kiasi kwamba kila mtu msomi aliona kuwa ni wajibu wake kushirikiana na wengine ili kuuondoa uovu huu kabisa na kuuzima kwa nguvu zote ili kanisa liondolewe katika nyanja zote za maisha milele kabisa na mamlaka yake yakomeshwe. Huu ndio ulikuwa mwelekeo wa kanisa juu ya wasomi, watafiti, wanachuoni na watu wengine wote! wenye upeo mpana na wa kimaendeleo. Ni wazi kwamba siri ya mafanikio na maendeleo ya Ulaya inatokana na uamuzi wa wazungu wa kuiondoa taasisi kama hiyo ambayo ilikuwa inakwamisha maendeleo na kukua kwa sayansi, kwa kutumia jina la dini na Sheria za Mwenyezi Mungu. Lakini matukio kama haya ya kutisha hayakuwahi kuonekana miongoni mwa Waislamu hata kwa mfano kidogo, na kama tulivyoona huko nyuma, Uislamu sio tu kwamba unakubaliana na elimu na ujuzi bali pia ni muungaji mkono mkubwa sana wa watafutaji wa elimu. Hivyo mawazo ya kwamba dini inakwamisha maendeleo ya umma ni kweli kwa upande wa ukristo lakini sio kweli kwa uande wa Uislamu. Ni adui yetu anayetutaka tuamini hivyo ili tuzubaike tuipuuzie elimu ili wao waweze kuyafikia malengo yao ya kikoloni. Kwa mazingiri haya, ni jukumu la Waislamu kwa ujumla wao kuipiga vita propaganda hii na kuueneza mwanga wa ukweli wa Uislamu katika jamii ambao utanawirisha mwelekeo wa ubinadamu, na kufikia ubora na maendeleo na hivyo kutekeleza wajibu wao kwa Uislamu na Waislamu.

NUKUU 1). Mwenyezi Mungu atawafanya waumini walio na elimu waheshimiwe na kutukuzwa kwa kuwainulia daraja zao (Qur’ani Tukufu). 2). Jitahidini kutafuta elimu toka mkiwa wachanga hadi mnaingia makaburini. 37

12:43 PM

Page 37


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

3). Wanazuoni ni warithi wa Mitume. 4). Elimu ni msaidizi mkubwa wa imani. 5). Mbora wa wanadamu ni yule mwenye elimu zaidi, na asiye na thamani kabisa ni yule asiye na elimu (mjinga) kuliko wote. – (Mtukufu Mtume Muhammad). 6). Wanazuoni wako hai hata kama watakuwa wamepumzika makaburini na wajinga wamekufa hata kama wapo hai. 7). Yule atakayenifundisha neno moja huwa amenifanya kuwa mtumwa wake – (Imam Ali (a.s.)). 8). Wafundishe wengine kile unachokijua ili msingi wa elimu yako uwe imara na tafuta elimu kwa wengine ili kiwango cha ufahamu wako kiweze kupanda – (Imam Hassan).

MAMA Mama neno zuri na tukufu lilioje. Ni neno ambalo mtu hupata harufu nzuri ya upendo, hisia za moyoni na huhisi vuguvugu na uaminifu. Nchi za Magharibi zimetambua thamani na umuhimu wa mama hivi majuzi tu wakati Waislamu walilitambua hili karne nyingi zilizopita kwa msaada wa mafundisho matukufu ya Uislamu. Uislamu umeweka umuhimu mkubwa sana kwa mama na umevuta mazingatio ya watu waitambue thamani na umuhimu wake kwa kauli mbalimbali. Uislamu unaiona radhi ya mama kuwa ni sharti muhimu kabisa la kufikia kiwango cha juu kabisa cha ukamilifu (Yaani Pepo), na unasema: “Pepo 38

12:43 PM

Page 38


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

ya mtu ipo chini ya nyayo ya mama yake.” Hadithi hii, ambayo imesimuliwa kutoka kwa Mtume ni medali ya heshima kwa mwanamke na ikiwa mijadala, maelezo, sentensi na maneno yote ya watu juu ya hadhi ya mama yakiwekwa kwenye upande mmoja wa mizani na sentensi “Pepo ya mtu ipo chini ya nyayo za mama” ikiwekwa upande wa pili wa mizani, upande wa mizani wenye kauli ya Mtukufu Mtume: “Pepo ya mtu ipo chini ya nyayo za mama” utakuwa mzito zaidi. Ili kumtukuza mama, Uislamu haukuridhika na mapendekezo na mlolongo wa maneno matupu, Bali kwa upande wa kuweka sheria umeamuru utii kwa mama katika amri zote chanya na hasi katika baadhi ya mambo kuwa ni wajibu isipokuwa katika madhambi. Kwa mfano ikiwa sheria ya Mwenyezi Mungu isiyo ya faradhi itagongana na amri ya mama, basi watoto wanapaswa kutii amri ya mama na kuacha amri ya Mungu ya sunna. Ikiwa mtoto, wa kiume au wa kike anataka kufunga sunna ili apate thawabu na ubora au kama anataka kusafiri safari ya sunna, na mama yake akimkataza basi ni wajibu wa mtoto kumtii mama yake. Akiiasi amri ya mama yake sio tu kwamba hatapata thawabu bali pia atapaswa kuadhibiwa. Mahali pengine ambapo amri ya mama inapewe kipaumbele juu ya amri ya Mwenyezi Mungu, ni pale ambapo amri ya wajibu inakabiliana na katazo la mama ilimradi tendo hilo sio katika yasiyoweza kufidiwa (kama vile Sala tano na funga ya mwezi Ramadhani) basi utii kwa mama ndiyo unaopaswa kuchukua kipaumbele juu ya amri hiyo. Kwa mfano ikibidi kutokea jihadi kwa wote ambao wanafaa vyema kushiriki katika vita dhidi ya adui, lakini ikiwa mama hatamruhusu (na kutoshiriki kwake hakutaleta madhara yoyote kwa Waislamu), basi mtu huyo, katika kukubaliana na amri ya mama yake, anaweza kujizuia kwenda vitani na akabakia na mama yake huyo. Mtu mmoja aliyebahatika kumtembelea Mtukufu Mtume alimwambia: “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Nina afya njema, uwezo na ninata39

12:43 PM

Page 39


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

mani kushriki katika jihadi kwa ajili ya maendeleo ya Uislamu. Lakini mama yangu hataki nitengane naye na kwenda vitani.” Mtukufu Mtume akasema: “Nenda ukae na mama yako. Ninaapa kwa Yule aliyeniteuwa kufanya kazi hii ya Utume, kwamba thawabu za kuutumia usiku mmoja kwa kumhudumia mama yako na kumfanya afurahi kukuona ni kubwa kuliko kupigana jihadi kwa mwaka mmoja – (Al-Kafi, Juz. 2). Uislamu unaona kuwa mtu kuwaheshimu wazazi wake na kuwapatia haki zao ni jukumu muhimu kabisa la watu mara tu baada ya kutekeleza haki za Mwenyezi Mungu. Juu ya hili Qur’ani Tukufu inasema: Nishukuruni Mimi na Wazazi wenu” – (Suratul Luqman, 31:14). Hapa mara tu baada ya kutaja haki Yake, Mwenyezi Mungu anatoa amri juu ya haki za wazazi. Mtu mmoja alikuja kwa Mtukufu Mtume na kusema: “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Niongoze juu ya nani nimfanyie wema ili niweze kupata thawabu kamili za wema wangu huo.” Mtukufu Mtume akajibu: “Mfanyie wema mama yako.” Yule mtu akauliza: “Baada yake?” Mtume akajibu. “Mfanyie wema mama yako.” Akauliza tena, “Nani nimfanyie wema baada yake?” Mtume akajibu, “Mfanyie wema mama yako.” Mara ya nne yule mtu akauliza, kisha nimfanyie nani wema? Mtume akasema, “Baba yako.” – (Biharul-Anwar, Juz. 74). Mtu mmoja alimuuliza Imam Ja’far Sadiq (a.s.): “Inamaanishwa nini kuwafanyia wema wazazi, kule ambako Mwenyezi Mungu amekuamrisha ndani ya Qur’ani Tukufu?” Imam Ali (a.s.)jibu kuwa “Wema” huo ni kutangamana nao kwa wema na heshima na adabu na uwatimizie mahitaji yao baada tu ya kuyatambua na wala usingoje wakuombe.” Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: “Hamtafikia wema mpaka mtoe vile mnavyovipenda” – (Suratul Aali Imran 3:92). Wazazi wako wakikuudhi, wewe usiwaudhi. Badala yake 40

12:43 PM

Page 40


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

unapaswa uwaombee dua njema, na uwatizame kwa upendo na upole na usiwapandishie sauti na usitembee mbele yao.” – (Al-Kafi, Juz. 2). Imam Sajjad (a.s.) amesema: “Haki ya mama yako ni kwamba lazima ujue kwamba alikulisha na kukubeba katika tumbo lake kwa miezi kadhaa na alikulisha kwa tunda la moyo wake na kinywaji cha roho yake. Alijitoa kikamilifu kwa nafsi yake yote kwa ajili ya kukulinda na kukulisha. Alikuwa hajali njaa yake wewe unapokuwa umeshiba wala kiu yake mradi wewe ukate kiu yako, wala kubaki kwake bila nguo wewe unapokuwa umevaa, wala yeye kuwa juani wewe unapokuwa kivulini. Aliacha usingizi wake mtamu kwa ajili yako na alistahamili shida ya kutokulala kwa ajili yako. Alistahamili shida zote hizi ili akumiliki wewe na uwe wake. Unapaswa kujua kuwa huna uwezo wa kutosheleza kumshukuru mama yako, isipokuwa kwamba Mwenyezi Mungu akusaidie na kukupa uwezo wa kumpatia haki zake.” – (Makarimul-Akhlaq). Haki ambazo zimeamurishwa juu ya mama katika Uislamu na mifano yake ambayo imenukuliwa hapo juu zimetokana na taabu nyingi anazostahamili katika kumlea na kumlisha mtoto wake na kumkabidhi katika jamii. Ni wazi kuwa mama anayestahiki haki hizi ni yule tu anayetekeleza majukumu ya mama kwa uhalisia wake, na kumkuza mtu mwenye uwezo na manufaa kwa kutumia jitihada zake zote. Mama anayekwepa kumhudumia mtoto wake kwa kujiendekeza au kwa kuhudhuria tafrija za usiku au maeneo mengine ya starehe na ufisadi na hivyo kumkabidhi mtoto wake kwenye vituo vya kulelea watoto wadogo kwa malipo, anamfanyia mwanawe uhalifu usiosameheka hastahili kupata hadhi na hizi haki za mama. Maisha ya watoto katika vituo vya kuelelea watoto yanavyooneka ni mazuri sana na yanayokubalika. Nguo zao ni safi na nadhifu, na nywele 41

12:43 PM

Page 41


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

zao zimesafishwa na kuchanwa vizuri, kituo cha kulelea watoto kina mazingira safi kabisa ya kiafya na vyumba vyake vimejengwa kwa maelekezo ya kiufundi na kitaalamu. Vitanda vimetandikwa vizuri kwa mashuka safi na chakula cha watoto kinaandaliwa vizuri. Watoto wanacheza kwa mujibu wa ratiba na wanalala katika muda muafaka. Kwa kifupi, sehemu muhmu ya mahitaji ya kimwili na kisaikolojia ya mtoto hukidhiwa. Hata hivyo, mtoto ana hisia nyingine na silika ambazo haziwezi kukidhiwa katika mazingira ya watoto wengi katika taasisi ya kulelea watoto. Mpapaso maalumu wa kimahaba ambao humpatia mtoto furaha na bashasha unaweza tu kupatikana katika mapaja ya mama na sio katika vituo vya kulelea watoto. Mtoto anayeishi na watoto mia moja na haishi maisha huru hawezi akaitambua haiba yake halisi na uhuru wake binafsi, vitu ambavyo ni sifa muhimu ya binadamu. Katika mazingira ya familia, shughuli zote za mtoto kama vile kucheza na kucheka ni kiini cha upendo mkubwa na vinapatikana kwa wazazi tu na mtoto hupata mazingatio kutoka kwenye uangalizi kama huo na hata kuufurahia. Hata hivyo, shughuli za mtoto miongoni mwa watoto wengine mia moja ni sawa na wimbi moja lisiloonekana na lililovunjika kati ya mamia mengine ya mawimbi tofauti. Elimu na mafunzo ya mtoto huhitaji uangalizi wa kudumu ambao hauwezi kutolewa na yeyote isipokuwa wazazi kwa sababu tangu mwanzo wa maisha ya mtoto ni wao tu, na hususan mama ambao huzitambua tabia zake za kimwili na kiakili na vitu anavyovipandelea, maendeleo ambayo yanapaswa kuwa kiini cha mafunzo na elimu yao. Upotofu mkubwa ambao jamii ya sasa inaupata ni kwamba imebadilishana, kutoka mwanzo kabisa wa maisha ya mtoto, kati ya vituo vya kuele42

12:43 PM

Page 42


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

lea watoto na familia na yale makumbatio ya mama. Akina mama wanaowakabidhi watoto wao katika vituo vya kulelea watoto ili waweze kufanya kazi za maofisini au ili wajiingize katika mambo ya tamaa na starehe au kazi za uandishi na za kisanii au kupoteza muda kwa kucheza karata au kutazama filamu, wanazifanya hali za nyumba na familia zao kuwa za kuchosha na zilizofifia. Ni katika mazingira ya familia ambapo watoto wanaweza kupata vitu vingi vizuri. Maendeleo ya watoto wanaoshi katika familia zao ni mazuri zaidi kuliko ya wale wanaoishi katika nyumba za mabweni. Mtoto upesi sana hujenga msingi wa akili, mwili na hisia zake za moyoni kwa mifano inayotolewa na mazingira yake na kwa sababu hii anajifunza kidogo sana ikilinganishwa na wale wa rika lake. Na wakati anapokawia nyuma shuleni kama mtu asiyeeleweka vizuri anakuwa kafanya maendeleo mazuri. Akina mama wanaowapeleka watoto wao katika vituo vya kulelea watoto sio tu kwamba wanayawekea kiwingu maisha ya baadaye ya watoto wao, bali pia wanatoa pigo kali kwa jamii na hata kwao wao wenyewe kwani huwa hawapati manufaa yoyote kutoka kwa watoto wao. Mtoto asipopata upendo na huruma kutoka kwa mama yake na ikiwa hajahisi upendo wa hisia za mama yake, hauwezi pia kutarajiwa upatikane kuoka kwake atakapokuwa mkubwa.

Athari ya Mama juu ya Mwanawe Watu mashuhuri na maarufu wa ulimwengu, wana madeni mno juu ya mafanikio yao kwa mama zao ambao waliyatekeleza majukumu yao mazito kwa ukamilifu na walifanya wajibu wao wa msingi katika kuzijenga haiba na tabia zao. Marhum Haj Sheikh Murtaza Ansari, mwanachuoni mkubwa wa Kiislamu, alilia kwa uchungu sana mama yake alipofariki. Alikaa pembeni mwa maiti 43

12:43 PM

Page 43


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

ya mama na akatokwa na machozi. Mmoja wa wanafunzi wake wa taaluma alimwambia kwa kumfariji kuwa, “Sio sawa kwamba bila kujali kuwa na nafasi kubwa kama mwanazuoni wewe uweze kutoa machozi na kuhisi uchungu mkubwa kiasi hicho kwa ajili ya kifo cha mwanamke mzee.” Mwanazuoni huyo mkubwa alinyanyua kichwa chake na kusema: “Inaelekea kwamba bado hujajua hadhi na daraja kubwa alilonalo mama. Mafunzo mazuri niliyopewa na mama yangu huyu na taabu mbalimbali ambazo mama yangu alistahamili kwa ajili yangu vilinipandisha mpaka katika nafasi yangu hii niliyo nayo na mafunzo ya awali aliyonipatia ndiyo yaliyonisafishia njia ya kupata maendeleo haya na kupata daraja hili kubwa katika ulimwengu wa elimu.” Huu ulikuwa ni mfano mmoja wa taathira ya mama kwa mwanawe na kuna wanazuoni wengi mashuhuri ambao chimbuko kubwa kabisa la maendeleo yao lilitokuwa ni juhudi na mafunzo ya mama zao. Alipokuwa kijana mdogo, Edison, sio tu kwamba hakuonyesha kipaji chochote bali pia alionekana kuwa na akili nzito. Kwa vile kichwa chake kilikuwa kikubwa sana wenzake walifikiri kuwa alikuwa taahira. Maoni yao haya yaliungwa mkono pia na maswali yaliyokuwa yanaonekana ya ajabu na alipewa jina la “zuzu” (Hakuhudhuria shule kwa zaidi ya miezi mitatu). Kwa sababu hii siku moja alirudi nyumbani akiwa analia na akamwambia mama yake juu ya jambo hilo. Mama yake alimshika mkono na kwenda naye shuleni. Alimwambia mwalimu, “Huelewi unachokisema. Mwanangu ana akili nyingi kuliko wewe na hiki ndio chanzo cha tatizo. Nakwenda naye nyumbani na nitamfundisha mimi mwenyewe, kisha nitakuonyesha ni kipaji gani kilichojificha kwake.” Huu ulikuwa ndio utabiri wa ajabu wa mama yake Edison. Kwa hiyo, baada ya hapo, kama alivyomwambia mwalimu wake, alianza kumfundisha yeye mwenyewe. Rafiki wa familia ya Edison anaandika kuhusiana na hili: “Wakati mara kwa mara ninapopita nyumba ya Edison nil44

12:43 PM

Page 44


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

imuona mama yake Edison amekaa mbele ya sebule akimfundisha mtoto wake. Sebule ile ilikuwa ndio darasa na Edison alikuwa ni mwanafunzi pekee. Mwenendo na tabia za mtoto huyu zilifanana na za mama yake. Alikuwa anampenda sana mama yake. Mama yake aliposema kitu, alikuwa msikivu sana. Inaweza ikasemwa kwamba mama yake alikuwa ni bahari ya elimu.” Kutokana na jitihada za mama yake Edison, alisoma vitabu vizito vya waandishi kama vile Gilbon, Hume, Plato na Shakespeare kabla hajafikisha umri wa miaka tisa. Mbali na haya, mama yake mwenye hekima na busara alimfundisha pia jiografia, historia, hisabati na maadili. Edison hakwenda shule kwa zaidi ya miezi mitatu na chochote kile alichokisoma akiwa mvulana mdogo ni hicho tu alichofundishwa na mama yake. Mama yake alikuwa ndio mwalimu wake katika hali zote kwa sababu hakumfundisha tu bali pia alitafuta vipaji vya asili vya mwanae na kuvikuza. Baadaye Edison alipofikia kilele cha umaarufu na mafanikio makubwa alisema: “Nilijua toka nikiwa mvulana mdogo uzuri na umuhimu wa mama. Mwalimu wangu aliponiita “zuzu” yeye alinitetea. Nilidhamiria kuthibitisha kuwa hakuwa ameunda wazo la uongo juu yangu” Pia alisema: “Kamwe sitasahau fikra za elimu na mafunzo nilizopewa na mama yangu. Kama asingenitia moyo, nisingweza kuwa mgunduzi. Mama yangu aliamini kuwa, kuhusu watu wengi wanakuwa hawana manufaa yoyote wanapofikia umri mkubwa wasingeweza kuwa watu wasio na faida katika jamii kama uangalizi zaidi ungetolewa kwenye elimu na mafunzo mazuri walipokuwa watoto. Uzoefu mwingi aliokuwa ameupata mama yangu kama mwalimu ulifichua siri nyingi za maumbile (asili) ya mwanadamu kwake. Mara zote nilikuwa mzembe. Kama mama yangu asingenijali, ningepotea kwenye upotofu. Lakini ustahamilivu na wema wake ulikuwa ni nguvu madhubuti zilizonizuia nisipotoke na kupotoshwa.” Smiles anasema: “Mfano na sampuli ndio kipengele muhimu sana katika ufundishaji wa maadili kwa mtoto. Kama mtu anatamani watoto wake 45

12:43 PM

Page 45


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

wawe na tabia na maadili mema lazima awapatie mifano bora kabisa. Na kiigizo na mfano wenye nguvu kabisa ambao hudumu milele mbele ya macho ya mtoto ni mama yake. Akina mama wenye akili na wapole hukubali kutaabika ili waweke msingi wa maisha yenye mafanikio ya watoto wao na kuwaandaa kwa ajili ya mustakbali wao, ambapo akina mama wapumbavu na wabinafsi husukumia watoto wao katika mikosi na balaa kwa matendo yao potovu. Wakati akijadili athari na ushawishi ambao wazazi hufanya kwa watoto wao, Will Durant anasema: “Nyumba bora, shule bora na bora ya kila kitu kingine ni kile ambacho ndani yake amri zake ni chache zaidi. Inaweza ikaonekana ni jinsi gani watoto wanaweza kufanywa wawe na tabia njema bila makaripio wala amri. Kama katika hali fulani tabia hii njema haitathubutu kuwa na nguvu, basi ni kwa sababu sisi wenyewe wazazi hatuyatekelezi yale tunayohubiri kwa watoto. Tunawashauri kutumia vitu kwa wastani lakini sisi tunafanya ufujaji (israfu) katika ulaji na unywaji. Tunawapendekezea kuwa wapole lakini sisi wenyewe tunagombana mbele za watu. Tunawaonya watoto dhidi ya kula pipi au kutazama picha za mapigano lakini sisi wenyewe tunavifanya ni ruhusa kwetu na siku moja mtoto anakuja kutambua vitendo tunavyofanya kuwa ni kinyume na tunavyohubiri. Tunafundisha kusamehe kwa kutumia ukali, na tabia njema kwa kutumia ufedhuli. Tunatarajia unyenyekevu kutoka kwa mtoto wakati sisi wenyewe tunaonyesha tabia na umungu mtu asiyeshindika. Hata hivyo, watoto huzingatia tabia zetu na sio maneno yetu. Na kutojua kwao wafanye lipi na waache lipi hutokana na ukweli kwamba wanaiga matendo yetu ya nyuma. Nionyeshe mtoto wako ili nikueleze wewe mwenyewe vile ulivyo na unavyostahili. Kama unataka mwanao awe mpole, kuwa mpole kwanza wewe na kama unataka mtoto wako awe mchamngungu, kuwa mchamungu kwanza wewe binafsi. Hakuna jingine ambalo ni muhimu 46

12:43 PM

Page 46


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

zaidi. Hata kama ukiwa mkali na kusema maneno makali wakati ukiwa na hasira kali, utaweka ukali ule na maneno yale makali yakiwa hai kwenye akili ya mtoto kwa njia ya kuiga. Tabia njema inaweza tu kufundishwa kwa njia ya kuweka mifano na hilo pia kwa kulisimamia kwa ustahimilivu endelevu. Hii ni kazi ngumu kiasi cha kutuwajibisha na sisi tujifunze tabia hizo upya. Kwa njia hii huwa tumefundishwa na watoto wetu.” Uislamu huona kuwepo kwa wazazi waliopotoka kama sababu kubwa ya upotofu wa watu. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amelieleza hili waziwazi: “Kila mtoto huja duniani akiwa na tabia safi na inayoweza kuamini juu ya upweke wa Mwenyezi Mungu na wakiwa na maadili mema. Ni wazazi ambao kwa mafundisho yao mabaya humfanya apotoke na kumfisadisha na wakati mwingine humpeleka kwenye ukafiri au ushirikina. (Safinatul Bihar, Juz. 2, uk. 373). Ni kutokana na ushawishi na taathira kubwa ya wazazi kwenye akili za watoto wao kwamba viongozi watukufu wa Uislamu (Mtume na Maimamu), walitoa mapendekezo mengi juu ya kuwapenda wazazi kama shukrani na kuweka thamini kubwa juu ya taabu walizozivumilia. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: “Waheshimu watoto wako na wafundishe tabia na adabu njema ili ubarikiwe na Mwenyezi Mungu.” Sehemu nyingine anasema: “Ni vizuri kuwalea watoto wako huku ukiwafundisha maadili na tabia njema kuliko kutumia sehemu ya mali yako katika njia ya Mwenyezi Mungu” – (Makarimul Akhlaq uk. 355). Katika hadithi nyingine, amenukuliwa akisema: “Mtu anapokufa, daftari lake la amali hufungwa na mafungamano yake na ulimwengu huu hukatika isipokuwa katika mambo matatu: (i) Amali njema alizozifanya wakti wa uhai wake na ambazo bado zinawanufaisha watu. 47

12:43 PM

Page 47


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

(ii) Elimu aliyoiacha duniani kwa manufaa ya watu. (iii) Mtoto mwema na ambaye ameachwa na mzazi wake na akawa anamuombea dua. Wazazi wanapokuwa wametekeleza jukumu lao kwa watoto wao katika suala la kuwapatia elimu na mafunzo mazuri, wataweza kupata haki zote za wazazi kwa ukamilifu wake pamoja na baraka za kuwa na watoto wachamungu na ni katika hatua hii ambapo Uislamu huongea na watoto na kuwapa mapendekezo kuhusiana na wazazi wao. Imam Ja’far Sadiq (a.s.) anasema: “Huruma kwa wazazi ni uthibitisho wa kumtambua Mwenyezi Mungu kwa sababu hakuna ibada ambayo humridhisha Allah kama mtu kuonyesha heshima kwa wazazi wake.” – (Misbahush-Shari’ah, uk. 48). Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Mtu anapomtazama baba yake au mama yake kwa upendo na huruma, kitendo hiki huhesabiwa kuwa ni ibada.” – (Kashaful Ghumma, uk. 243). Imam Riza (a.s.) anasema: “Kama unataka Mwenyezi Mungu akupe umri mrefu, wafurahishe wazazi wako.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: “Radhi za Mwenyezi Mungu ni radhi za wazazi wake mtu, na hasira Yake ni hasira yao.” Imam Baqir anasema: “Kuna mambo manne ambayo kama mtu yeyote atakuwa nayo basi Mwenyezi Mungu humpatia mtu huyo nyumba huko peponi: (i) Kuwalinda mayatima na kuwapatia hifadhi. (ii) Kuwahurumia wanyonge na wenye shida. (iii) Kuwa na huruma na mwenye tabia njema kwa wazazi wake mtu. 48

12:43 PM

Page 48


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

(iv) Mtu kuwastahi na kuwa mpole kwa watumishi wake na watu wa chini yake kwa cheo (Khisal Saduq).

HURUMA KWA MAMA NI FIDIA YA DHAMBI ZA MTU Uislamu huhesabu wema wa mtu kwa mama yake kama njia ya kafara ya dhambi zake na kuwa ni chanzo cha radhi na msamaha wa Mwenyezi Mungu. Mtu mmoja alikuja kwa Mtukufu Mtume na kusema: “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Nimefanya madhambi mengi sana katika maisha yangu. Je! mlango wa toba uko wazi kwangu? Na je Mwenyezi Mungu atakubali toba yangu?” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akauliza: “Je kuna mzazi wako yeyote ambaye bado yuko hai?” Yule mtu akajibu, “Ndiyo. Baba yangu yuko hai.” Mtume akamwambia “Nenda ukamfanyie wema” (Ili dhambi zako ziweze kusamehewa). Yule mtu alipoondoka, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Natamani laiti mama yake angekuwa hai!” – (Biharul Anwar). Kwa kauli hii alimaanisha kuwa kama mama yake angekuwa hai na akamtumikia dhambi zake zingesamehewa haraka zaidi. Imeelezwa katika hadithi nyingine kwamba mtu mmoja alimwambia Mtukufu Mtume kuwa: “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Mwenyezi Mungu alinijaalia mtoto wa kike na nilimlea mpaka akavunja ungo. Siku moja nilimpamba na kumvisha nguo nzuri. Kisha nilikwenda naye kwenye ukingo wa kisima kisha nikamsukumia ndani yake. Maneno ya mwisho niliyoyasikia kutoka kinywani mwa msichana huyo asiye na hatia kutoka ndani ya kisima yalikuwa ni: “Ewe baba yangu mpendwa!” Sasa ninajuta 49

12:44 PM

Page 49


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

kwa dhambi nililofanya. Ni nini fidia ya dhambi yangu na nifanye nini ili dhambi yangu isamehewe?” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliuliza: “Je mama yako yuko hai?” akajibu hapana. Mtume akauliza, Je Shangazi yako yupo hai?” Akajibu Ndiyo.” Mtume akasema: “Ana nafasi sawa na mama yako. Nenda ukamfanyie wema na kumfanyia wema kwako kutakuwa ni njia ya kusamehewa dhambi zako.” – (Safinatul Bihar, Juz. 2, uk. 687).

KUCHUKIA KWA MAMA Katika Uislamu hasira za mama na kuchukia kumehesabiwa kuwa ni sababu ya maangamizi na dhiki kwa mtoto. Katika baadhi ya hadithi imeelezwa kwamba mtu mwenye tabia mbaya na nidhamu mbaya kwa wazazi wake hatapata japo harufu ya pepo na hatauona uso wa neema. Mmoja wa masahaba wa Mtukufu Mtume aliugua na akawa mgonjwa wa kitandani. Mtukufu Mtume alikwenda kumjulia hali ya afya yake. Hali yake ilikuwa mbaya sana na alikuwa katika mlango wa kifo. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimwambia: “Kiri Upweke wa Allah kwa kusema: Hakuna apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah.” Yule Sahaba akawa anatamka kwa kigugumizi na akashindwa kutamka. Mtukufu Mtume akamuuliza mwanamke aliyekuwepo hapo: “Je mama wa mtu huyu yupo hai?” Akasema: “Ndiyo, mimi ndio mama yake.” Mtume akamuuliza: “Je una hasira naye?” Akajibu: “Ndiyo. Na ni miaka sita sasa siongei naye.” Mtume alimshauri kupuuza kosa lake na amsamehe mtoto wake. Akasema yule mama: “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Ninamsamehe kwa ajili yako na sasa niko radhi naye.” 50

12:44 PM

Page 50


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Kisha Mtukufu Mtume akamgeukia mtu yule na akasema: “Hakuna apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah.” Ulimi wake ukaanza kutamka na hivyo akatoa shahada kirahisi – (Amali at-Tusi, Juz. 1, uk. 62). Imam Ja’far amesema: “Mtu anayetaka maumivu ya kifo yasiwe makali basi awafanyie wema ndugu zake na aonyeshe tabia njema kwa wazazi wake. Kifo kitakuwa rahisi kwa mtu anayefuata mwenendo huu na hatapata umaskini na ufukara – (Amali Saduq, uk. 234). Mtu mmoja alimuuliza Mtukufu Mtume juu ya kuwafanyia wema wazazi. Mtukufu Mtume alimshauri kuwa amfanyie wema mama yake mara tatu na amfanyie wema baba yake mara moja. Pia alitoa kipaumbele kwenye ule ushauri alioufanya kwa ajili ya wema kwa mama kabla ya baba – (Al-Kafi, Juz. 2, uk. 162).

MAPENDEKEZO KWA UPENDELEO WA MAMA Zakariya bin Ibrahim anasimulia: “Nilikuwa Mkristo kisha nikasilimu na nilibahatika kufanya Hijja katika Nyumba ya Mwenyezi Mungu. Wakati wa safari nilipata heshima ya kukutana na Imam Ja’’far as-Sadiq. Nilimwambia kwamba awali nilikuwa mkristo na kwamba sasa nimesilimu na kuwa Mwislamu.” Imam Sadiq alimuuliza: “Ni sababu ipi iliyokufanya usilimu?” Nilijibu: “Ni aya hii ya Qur’ani aliyonifanya niukubali Uislamu:

51

12:44 PM

Page 51


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

“..... mlikuwa hamjajua kitabu ni nini wala imani ni nini, lakini Tumekifanya Kitabu hiki (Qur’ani) iwe nuru ambayo kwayo tunamuongoza Tumtakaye katika waja wetu ” – (Suratul Ash-Shura. 42:52). Imam Sadiq alisema: Mwenyezi Mungu amekuongoa katika Uislamu na ameungaza moyo wako kwa nuru yake.” Kisha aliniombea dua na akamuomba Mwenyezi Mungu anipe uongofu zaidi. Nikamwambia: “Wazazi na ndugu zangu bado ni Wakristo na mama yangu ni kipofu. Je inaruhusiwa mimi kuishi nao? Imam Sadiq aliuliza: “Je wanakula nguruwe?” Nikajibu hapana. Imam Sadiq alisema: “Haikatazwi kushirikiana nao na kuishi nao.” Kisha akaongezea kusema “Mwangalie mama yako. Kuwa mwema na mpole kwake, na atakapopumua pumzi yake ya mwisho, uchukue jukumu la mazishi yake. Nilipofika Kufa (moja ya miji ya Iraq) nikitokea Hijja nilionyesha huruma nyingi na upendo mkubwa kwa mama kama nilivyoamrishwa na Imam Sadiq. Mimi mwenyewe ndio nilikuwa ninamtengea chakula, nampangia nguo, namchana nywele na kumfanyia shughuli nyingine zote. Pale mama alipoona tofauti zote hizi katika tabia zangu alisema: “Mwanangu! Ulipokuwa unafuata dini yangu, haukuwa na tabia njema kiasi hiki. Ni sababu gani iliokufanya unipende kiasi hiki baada ya kuwa kwako Mwislamu?” Nilimjibu, mmoja wa vitukuu vya Mtume wa Uislamu ameniamrisha kwamba nikuonyesha huruma na tabia njema.” 52

12:44 PM

Page 52


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Akaniuliza, “Je huyo ni Mtume?” Nikajibu Hapana, hakuna atakayeteuliwa tena kuwa Mtume baada ya Mtume wetu. Yeye anatokana na kizazi cha Mtume wetu. Akasema: “Amri hizi ni amri za Mitume na dini yako ni nzuri zaidi kuliko yangu. Niongoze ili na mimi niwe mwislamu.” Nilimfundisha nguzo za Uislamu na akawa Mwislamu. Alisali sala ya adhuhiri, alasiri, magharibu na sala ya Isha kisa akawa mgonjwa wakati wa usiku wa manane. Nilikuwa pembeni ya kitanda chake na nilikuwa namuuguza. Aliniambia: “Mwanangu mpendwa! Nisomee tena imani za Kiislamu.” Nilirudia kuzisoma zote naye akazikiri zote. Usiku huo huo akafariki dunia. Asubuhi ikafika. Mazishi yake yalifanywa kwa mujibu wa taratibu za Kiislamu. Niliisalia maiti yake na kumzika kwa mikono yangu.” Matukio mengi ya aina hii yamenukuliwa katika hadithi zilizotoka kwa watu wa nyumba ya Mtukufu Mtume. Katika zote hizi, umuhimu wa nafasi ya mama umesisitizwa sana na watoto wamehimizwa na kushauriwa kujitahidi kuwapa mama zao haki zao.

SIKU YA MAMA Nukta, muhimu inayopaswa kutajwa hapa ni kuwa kila mwaka tarehe 10 Mei huwa ni siku ya mama duniani na sherehe hufanywa kuhusiana na hilo. Magazeti huchapisha makala yanayoendana na tukio hilo, washairi husoma mashairi yenye sifa na watu hutoa zawadi kwa mama zao. Bila shaka hili ni jambo zuri, lakini kufanya sherehe na kutoa zawadi tu haitoshi kwa kulipa haki za akina mama. Kwa upande mwingine jitihada zifanyike ili kuwafanya akina mama wajue majukumu yao muhimu na wapaswe kujua kuwa uendeshaji wa masuala ya familia na uleaji wa watoto ni moja ya majukumu makubwa na la thamani kabisa na kwamba haku53

12:44 PM

Page 53


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

na kazi muhimu na yenye utukufu kuliko kulea watoto wema. Napolean amesema: “Mama anabembeza kitanda cha mtoto mchanga kwa mkono mmoja na ulimwengu kwa mkono wa pili. Hivyo inawezekana kwamba kwa busara na jitihada zisizochoka, mama anaweza akalea mtoto ambaye anaweza kuleta mapinduzi katika ulimwengu wa mwanadamu. Akina mama wanapaswa wajitahidi kuikabidhi jamii watoto waliofunzwa na waaminifu na wahakikishe wanakuwa na imani thabiti katika dini kwa sababu uzoefu umeonyesha kuwa mtoto asiyekuwa na imani sio tu kwamba hana manufaa kwa wazazi bali pia wakati fulani huwa ni hatari vilevile. Mara nyingi tunaona na kusoma katika magazeti kuwa kijana amempiga mama yake au baba yake au hata kuitapakaza mikono yake kwa damu yao. Kwa nini inakuwa hivyo? Uzoefu unaonyesha kuwa sababu ya kufanyika kwa uhalifu huo si chochote bali kutokuwa na imani juu ya Mwenyezi Mungu na ukosefu wa msaada wa kiroho. Na kama wazazi wanataka kupata matokeo mazuri kutoka kwa watoto wao katika maisha haya na kesho akhera basi wanapaswa kuwekea mkazo katika suala la dini na imani zao kama tu wanavyoyaangalia masuala ya elimu na afya. Kadhalika watoto wanapaswa kujua wajibu walionao kwa wazazi wao na wanapaswa kujua kuwa ustawi mwema wa watoto umefungamana na radhi za wazazi wao. Ikiwa waandshi, wazungumzaji na washairi wataitumia siku ya mama katika njia hii na wakawajulisha akina mama na watoto juu ya wajibu wao wa msingi, tunaweza kusema kuwa wametoa mchango na kutimiza wajibu wao.

54

12:44 PM

Page 54


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

BAADA YA KIFO CHA MAMA Kifo cha mama yake mtu ni hasara isiyofidika, lakini kwa mujibu wa hekima ya Mwenyezi Mungu, mfumo wa maumbile umejengwa juu ya kanuni hizi kwamba siku moja kila kiumbe hai lazima kife. Mwanaadamu anapaswa kuikubali amri hii ya Mwenyezi Mungu, lakini baada ya kifo cha mama au baba, majukumu fulani huwaangukia watoto, ambayo uekelezaji wake ni moja ya njia za mafanikio yao. Kwa maneno mengine, haki za wazazi huwa haziishi baada ya vifo vyao na watoto wanapaswa kulipa haki zao hata baada ya kufa kwao. Imam Muhammad Baqir, anasema: “Inawezekana mtoto akawa mwenye huruma na mwema kwa wazazi wake wakati wa uhai wao, lakini baada ya vifo vyao anaweza asiwalipie madeni na anaweza asiwaombee msamaha (na anaweza akawasahau kamwe). Hivyo Mwenyezi Mungu humhesabu kama mtu aliyewakosea heshima wazazi wake.” – (al-Kafi, Juz. 2, uk. 130). Kwa hiyo huwa ni muhimu kwamba kama mtu wazazi wake wana madeni, ajitahidi kuwalipia na pia awaombee maghfira. Atoe sadaka kwa niaba yao na awalishe wahitaji au kuwasaidia na kuwalinda mayatima au kufanya vitendo vingine vyema kwa kuliwaza roho zao. Faida na thawabu za matendo haya huenda kwa wazazi wa mhusika na kwake mwenyewe pia na Mwenyezi Mungu humjaalia neema za ziada kwa wema wake – (alKafi, Juz. 2, uk. 127).

NUKUU 1). Tumemuusia mwanaadamu juu ya wazazi wake. Mama yake anambeba tumboni mwake kwa udhaifu juu ya tahadhari na kumnyonyesha kwa miaka miwili. Hivyo anishukuru Mimi na wazazi wake. Kwangu ndio marejeo ya vitu vyote. Wakijaribu kuwalazimisha kunishirikisha 55

12:44 PM

Page 55


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

na vile msivyokuwa na elimu navyo basi hapo msiwatii. Ishini nao kwa wema na adabu katika dunia hii. 2). Mola wako amekuamrisha kuwa usimuabudu yeyote asiyekuwa Yeye na uwafanyie wema wazazi wako – Qur’ani Tukufu). 3). Pepo iko chini ya nyayo za mama. 4). Kuwatazama wazazi wako kwa upendo na huruma ni ibada. 5). Radhi za Mwenyezi Mungu zinategemeana na radhi za wazazi na ghadhabu Zake zinategemea ghadhabu zao – (Mtukufu Mtume). 6). Kama unataka Mwenyezi Mungu akupe maisha marefu, basi wewe wafurahishe wazazi wako – (Imam Ja’far Sadiq).

* * * * * UKARIMU Maisha ya mwanaadamu huwa ni mazuri tu ikiwa yatakuwa na roho ya kibinadamu na ikiwa uhusiano wake na jamii umejengwa juu ya amali – (matendo) njema. Ni wale watu wanaostahili kupewa jina tukufu la mwanaadamu ndio ambao lengo lao la maisha ni ukarimu kwa wanaadamu na ambaye furaha yake hupatikana kwa kuwafanyia wema watu. Katika Uislamu, umuhimu maalumu umewekwa kwenye suala la amali na matendo mema na Waislamu wamehimizwa sana kwamba wawe wapole na wema.

56

12:44 PM

Page 56


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Qur’ani Tukufu inasema:

“Kwa hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha uadilifu na hisani na kuwapa jamaa. Anakataza uchafuna uovu na uasi. Mwenyezi Mungu anawausieni ili mpate kuzingatia.” – (Surat an-Nahl; 16:90). Katika aya hii Mwenyezi Mungu Mtukufu amehimiza juu ya kufanya uadilifu na huruma kwa pamoja kwa sababu jamii inahitaji vitu vyote viwili haki na huruma. Kama jamii ikikosa haki msingi wake hutikisika na ikikosa huruma itakuwa ni jamii kavu na isiyo na mwelekeo. Huruma na wema ambao hutokana na hisia za kibinadamu huipa jamii uhai na huyapatia fukuto mahusiano mazuri ya watu. Ni urafiki na usahibu, upendo na uchangamfu, uaminifu na huruma, kuwatembelea wagonjwa, huruma na bashasha kwa wanaokandamizwa na wenye shida, pendo na kujali kwa mayatima, pamoja na tabia nyingine njema za kibinadamu ambazo hujenga ukarimu na nguvu katika maisha ya mwanadamu na huondoa michosho na kukinai kwa maisha. Mwanadamu sio mashine na wanajamii sio magurudumu ya mashine yasiyo na uhai kiasi kwamba yanaweza kuzunguka bila maelewano mazuri baina yao na bila kumjali mwingine na hivyo kila moja kuishi maisha kipekee. Mwenyezi Mungu Mtukufu amemjaalia mwanadamu silika fulani ambazo zinahesabika kuwa ni rasilimali kubwa na zenye thamani kama ilivyo kwa mali asili nyingine ambazo kama zikiendelezwa katika mazingira na hali nzuri humpatia mwanaadamu msaada mkubwa katika maendeleo na ustawi wake. 57

12:44 PM

Page 57


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Katika mafundisho adhimu ya Uislamu, amri hizi zimepewa utekelezaji ambao unabeba thamani ya silika na ambayo hutoa matokeo yenye matunda mazuri katika maisha ya mwanadamu na amri zote hizi zinategemea juu ya amali za kiuchamungu. Kuna aya katika Qur’ani tukufu na kauli katika hadithi zilizosimuliwa na Maimamu wa Ahlul-Bayt, ambazo zinahimiza na kuwalingania watu katika kufanya amali njema. Baadhi yake zimetajwa hapa chini: Qur’ani tukufu inasema:

“Afanyaye amali njema moja, atalipwa mfano wake mara kumi, na afanyaye kitendo kibaya hatalipwa ila sawa na kitendo chenyewe na hakuna atakayedhulumiwa – (Suratul al-An’aam, 6:160). Katika aya nyingine Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

“Kama mkifanya wema, utakuwa ni kwa faida ya nafsi zenu, na mkifanya ubaya, mtajifanyia wenyewe .....” – (Surat Bani Isra’il; 17:7). Imam Ali (a.s.) amesema: “Fanyeni amali njema na msiione amali njema kuwa ni ndogo kwa sababu amali njema ni tukufu hata iwe ndogo kiasi gani.” – (Nahjul-Balaghah). Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Usinyooshe mkono wako isipokuwa katika kufanya amali njema na usiseme jambo lolote isipokuwa jema.”

58

12:44 PM

Page 58


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Imam Ali (a.s.) (a.s.) amesema: “Yeyote ambaye Mwenyezi Mungu atampatia mali ana wajibu kwamba kwa mali yake hiyo awasaidie ndugu zake, kuwaalika watu wenye njaa na kula nao, afanye mipango ya kuwaachia huru wafungwa na mateka, kuwasaidia kifedha maskini na fukara, kuwalipia madeni wale wenye kudaiwa na ajishughulishe na kulipa haki za watu wengine na kufanya amali njema ili aweze kupata thawabu, kwa sababu mtu anayekuza tabia kama hizo na akatumia mali yake katika njia hii hupata utukufu na heshima katika dunia hii na hupata mafanikio katika akhera.” – (Nahjul-Balaghah, Juz. 1). Imam Baqir (a.s.) amesema: “Kufanya amali njema humkinga mchamungu kutokana na kuhusika kwenye upotofu, na watu wanaofanya amali njema katika dunia hii watapata ustawi huko Akhera.” – (Amali Saduq, uk. 153). Imam Riza (a.s.) anasema: “Wafanyie wema watu wote, wawe wanaustahili (wema huo) au wawe hawaustahili. Hata wakiwa hawastahili wema huo, wewe unapaswa ustahili kuafanya wema huo.” (Uyunul-Akhbar, Juz. 2, uk. 35). Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: “Kitendo maarufu zaidi baada ya kuikubali dini ni kuwafanyia wanadamu upendo na huruma na kuwatendea wema watu wote.” (Uyunul-Akhbar, Juz. 2). Katika hadithi nyingine Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Amali bora kabisa katika dunia hii na akhera ni kwamba umsamehe yule aliyekuonea; kujenga mahusiano na mtu aliyejitenga na wewe; kumfanyia wema mtu aliyekudhuru; na kumpa zawadi mtu ambaye yeye alikunyima haki zako.” – (al-Kafi). Tulichonukuu hapa juu, kutoka katika Qur’ani Tukufu na hadithi za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Maimamu wa Ahlul-Bayt (a.s.) kinahusiana na kanuni ya wema na huhimiza na kuwaongoza watu katika kufanya amali njema. 59

12:44 PM

Page 59


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Tukivuka kutoka katika mada hii ya jumla tunakuta kwamba Uislamu umeamrisha utendaji wa matendo yote, yawe madogo au makubwa ambayo yanaangukia kwenye kundi la matendo matukufu na pia Uislamu umeahidi malipo si duniani tu bali na akhera pia. Nukta muhimu ambayo haipaswi kusahauliwa ni kuwa kwa kumakinika kidogo juu ya mafundisho ya Kiislamu itabainika kuwa amali njema zilizoamrishwa na Uislamu hayafanywi kwa ajili ya thawabu za akhera tu. Bali kwa upande mwingine, pamoja na kuhakikisha malipo kama hayo, pia matendo haya yanaathari za kimiujiza katika furaha na ustawi wa mhusika hapa duniani. Hapa chini tunatoa mifano michache ili kuiweka nukta hii wazi.

WEMA KWA MAYATIMA Uislamu umetoa mapendekezo mengi juu ya mayatima ambamo umesisitiza kwamba mali zao zilindwe, walelewe na kufarijiwa na waonyeshwe huruma. Qur’ani Tukufu inasema:

“Wala msikaribie mali za yatima isipokuwa kwa njia bora, mpaka atakapofikia baleghe” – Surat al-An’aam, 6:152). Katika aya nyingine, Qur’ani inasema:

“Hakika wale wanaokula mali za yatima kwa dhulma, bila shaka wanakula Moto watumboni mwao, na kwahakika wataingia Motoni.” 60

12:44 PM

Page 60


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

– Suratun-Nisa’a, 4:10). Aya nyingine zinazotokea katika Surat al-Baqarah, An-Nisaa, Bani Israil, Fajar na Ma’un ambazo ziliteremshwa kwa ajili ya mayatima zinafafanua juu ya umuhimu wa suala la mayatima. Imam Ja’far Sadiq anasema: “Yeote ambaye anataka Mwenyezi Mungu ampendelee kwa neema Zake na amwingize peponi anapaswa kuyatakasa maadili yake, atendee watu uadilifu, awahurumie mayatima, awasaidie wanyonge na wasio na msaada na awe mnyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu aliyemuumba.” – (Amali Saduq, uk. 234, Amali Tusi, uk. 46). Mtukufu Mtume anasema: “Yeyote atakayekuwa mlezi wa yatima na akamtimizia mahitaji yake, atakuwa nami Peponi.” (Qurbul Asnad, uk. 45). Imam Ali (a.s.) alisema yafuatayo katika wosia wake alipokuwa akipendekeza baadhi ya mambo muhimu kwa wanawe na wafuasi wake: “Mkumbukeni Mwenyezi Mungu juu ya mayatima wasije wakabaki na njaa hata siku moja na muwaangalie wasije wakakua kama watu waovu na wasiofaa; (yaani wafundishe tabia njema. –Nahjul-Balaghah). Sasa kwa vile tumeyaelewa baadhi ya mapendekezo ya Uislamu juu ya mayatima, sasa tungependa kulitizama suala hili kwa mtazamo wa kisaikolojia ili falsafa ya mapendekezo yote haya iweze kuwa wazi kwa kiasi kikubwa. “Uyatima, ama uwe umetokana na kifo cha baba au mama wa mtoto, huwa na matokeo mabaya sana kwa mhusika na jamii kwa ujumla. “Kwa kawaida, wakati ukifanywa uchunguzi juu ya suala hili, wanasaikolojia na wataalamu wa masuala ya elimu wamekuwa wakikuta kwamba uzururaji, maendeleo mabaya shuleni na katika jamii na vitendo vya 61

12:44 PM

Page 61


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

uzembe, uhalifu mkubwa na uhalifu wa aina nyingine, vyote hivi vilikuwa na mafungamano na mayatima. “Mmoja wa wanasaikolojia wa Kijerumani ambaye amefanya uchunguzi juu ya masomo ya watoto alibaini kuwa 44% ya watoto wote waliofeli ni wale ambao wamewapoteza baba zao na 33% ni wale ambao wamepoteza mama zao, hii ina maana 77% ya watoto waliofeli walikuwa ni yatima. “Kuhusiana na utafiti mwingine uliofanyika nchini Marekani kuhusiana na matatizo ya elimu katika moja ya shule katika Jiji la New York, ulionyesha kwamba 25% ya wale waliokuwa na matatizo ya kieleimu walikuwa ni mayatima. “Hali kadhalika katika utafiti mwingine ulioendeshwa nchini Ujerumani juu ya watoto na vijana waliokuwa na hatia ya makosa madogo ilionekana kati ya vijana 2704 waliokuwa wamefanya uhalifu mkubwa ni 1171, ambao ni sawa na 43% walikuwa ni mayatima. “Utafiti mwingine kama huu uliofanyika nchini Marekani juu ya wafungwa, umeonyesha kwamba kwa wastani 60% ya wafungwa waliofanyiwa utafiti walitokana na familia zilizoteseka kwa sababu ama hawana mama au baba tokea utotoni mwao. “Msomi mwingine wa Kijerumani aliyekamilisha utafiti juu ya sababu za uzururaji na tabia za kihalifu za watoto na vijana ambao hawajafikisha umri wa miaka 18 kisheria, amefikia uamuzi kama matokeo ya uchunguzi wake kuwa zaidi ya 38% ya wasichana waliojiingiza katika vitendo vya wizi, na 40% ya wale waliokuwa na hatia ya kuanzisha mahusiano haramu ya kingono au kufanya vitendo vya uchokozi, walikuwa ni mayatima. Na hatimaye tunaona kwamba kutokana na uchunguzi wa kijamii na kisaikolojia ulioendeshwa nchini Marekani, kwamba 70% ya wasichana wanaoshi katika hifadhi ya wasichana wahalifu, ama walikuwa wamepoteza ama mmoja wa wazazi wao au wazazi wote wawili. 62

12:44 PM

Page 62


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

“Mbali na kuwa mkosi binafsi, uyatima ni tatizo kubwa kwa jamii pia. Idadi kubwa ya uadui, uzururaji, mapungufu, maendeleo duni, mauaji, kujinyonga, vitendo vichafu na dosari za kisaikolojia, vyote vinatokana na hali ya kuwa yatima.” – (Dk. Sahibuz Zaman, Ruh-i Bashar). Ili mayatima wasiwe viungo vilivyopooza au kuoza vya jamii, na ili wasitumbukie katika uzururaji, uhalifu na ufisadi na ili wasiihatarishe jamii na ili tuweze kupata watu wenye staha na uwezo kutoka miongoni mwa yatima hawahawa, Uislamu umetoa amri zinazosisitiza sana juu ya kuwatazama mayatima pamoja na muongozo mzuri ambao kama utafafuatwa tutaweza kuondoa hatari zote hizi na kuzuia matatizo ya kiakili. Inawezekana kwamba hatua zinachukuliwa katika nchi zilizoendelea kwa ajili ya ustawi wa mayatima. Lakini hatua hizi zinaweza kuwa zimeshughulika na mahitaji ya kimwili peke yake ya yatima hao na upande wao wa kiroho ukawa umesahauliwa kabisa. Inawezekana kuna vituo vya kulelea mayatima vyenye virahisishi vyote vya maisha ya kisasa ikiwa ni pamoja na wauguzi stadi, nguo maridadi na safi, chakula bora kinachotosheleza, mazoezi ya viungo, elimu n.k. Lakini nyenzo na huduma zote hizi haziwezi kuwa ni mbadala toshelevu kwa hisia na upendo wa mtoto ambaye hujikuta kuwa ni yatima na asiye na baba na hujihisi hali ya udhalili na kutojiamini ikilinganishwa na watoto wengine. Huu ni msiba mkubwa. Hapa ndipo hatari inapoanzia na kilicho muhimu ni kuwa suluhisho la msingi la mkosi huu lazima litafutwe. Ili kuondoa tatizo hili, Mwenyezi Mungu, Muumba wa mwanaadamu, na ambaye anafahamu matatizo yote aliyonayo, mbali na kuhakikisha upatikanaji wa mahitaji ya kimwili, pia amezingatia hisia zao za kiakili na za upendo, hivyo ameweka sheria zinazogusa vipengele vyote hivi ipasavyo.

63

12:44 PM

Page 63


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Mbali na ukweli kwamba katika Uislamu, Waislamu wametakiwa kuwatazama mayatima na kuwapatia mahitaji yao, pia washauriwa kwa msisitizo kuonyesha upendo kwa mayatima. Uislamu unasema: “Yeyote atakayeweka mkono wake juu ya kichwa cha yatima kwa upendo atalipwa na Mwenyezi Mungu thawabu sawa na idadi ya nywele zilizo katika kichwa cha yatima huyo na yeyote atakayekula chakula na yatima atakuwa ameutakasa moyo wake dhidi ya uovu na atakuwa mtukufu.” (Safinatul-Bihar, Juz. 2). Tabia za viongozi watukufu wa Uislamu kwa mayatima ni fundisho bora ambalo linapaswa kuigwa na Waislamu wote kwa jumla. Wakati wa uhai wake, Imam Ali (a.s.) mara zote alikuwa mpole na mwema kwa mayatima. Alikuwa akienda nao nyumbani kwake, akiwapa uhuru wa kucheza nyumbani kwake kama watoto wake na kula chochote kilchokuwemo ndani ya nyumba. Watu walikuwa wakimwita ‘baba wa mayatima.’ Upendo huu na huruma kwa mayatima, ambao ni sehemu ya mpango angavu wa Uislamu, ni wa umuhimu mkubwa sana kwa ustawi wa jamii na huzuia uovu na ufisadi ambao unazikabili jamii zisizo za Kiislamu. Nukta muhimu ambayo lazima itajwe mwishoni mwa mjadala huu ni kwamba kilichoelezwa hapo juu kisiwanyong’onyeshe mayatima na kuwa sababu ya huzuni kwa sababu wanakuja kuhusika na matatizo ya uyatima wakati jamii haiwatendei kwa mujibu wa maamrisho ya Uislamu. Lakini ikiwa watalelewa kwa mujibu wa maelekezo ya Uislamu inawezekana wakafundishwa na kuwa watu wenye uwezo mkubwa kabisa katika wakati wao. Isitoshe Uislamu hauutazami uyatima kuwa ni upungufu au kasoro kwa sababu kama Qur’ani tukufu inavyoeleza wazi wazi kuwa Mtukufu Mtume wa Uislamu pia alikuwa yatima na mbali na yeye viongozi wengine mashuhuri wa Uislamu pia wamepata kuwa mayatima.

64

12:44 PM

Page 64


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

KUKIDHI MAHITAJI YA WENGINE Kufanya jitihada ili kukidhi mahitaji ya waja wa Mwenyezi Mungu ni moja ya zile amali njema ambazo zimesisitizwa sana katika amri za Uislamu. Imam Ja’far Sadiq amenukuliwa kuwa amesema: Mwenyezi Mungu alimteremshia wahyi Nabii Daud na akamwambia: “Pindi mmoja wa waja wangu akifanya amali njema, ninamtunuku pepo.” Nabii Daudi akauliza: “Ewe Mola! Ni amali gani hiyo njema?” Wahyi ukaja: “Ni kumfurahisha mja wangu muumini japo kwa kokwa moja ya tende.” Nabii Daud akasema: “Ewe Mola! Yeyote ambaye amekutambua na kuuelewa ukubwa wa wema na ukarimu Wako hapaswi kukata tamaa juu ya neema zako.” Imam Muhammad Baqir anasema: “Amali bora mbele ya macho ya Mwenyezi Mungu ni kuwafurahisha waja Wake, ama iwe kwa kumlisha chakula au kumlipia deni lake kama anadaiwa.” Imam Musa Kadhim anasema: “Mwenyezi Mungu anao baadhi ya waja Wake ambao hujibidiisha kukidhi mahitaji ya watu. Watu hao watasalimika dhidi ya misukosuko ya Siku ya Kiyama. Na kama mtu akimfurahisha muumini, Mwenyezi Mungu ataujaza moyo wake kwa bashasha Siku ya Kiyama.” – (al-Kafi, Juz. 2 uk.2). Imam Ja’far Sadiq amenukuliwa kuwa amesema kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: “Watu wote hula chembechembe za mabaki ya chakula kwenye kitambaa cha meza ya huruma Zangu na ninayempenda zaidi miongoni mwao ni yule ambaye ana huruma zaidi kwa waja wangu ambaye hujitahidi zaidi kukidhi mahitaji yao.” (al-Kafi, Juz. 2). 65

12:44 PM

Page 65


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Mtu aitwaye Sadqa-i Halwani anasema: “Mmoja wa rafiki zangu aliniomba katika Masjidul-Haraam kuwa nimkopeshe dinari mbili. Nilimwambia kwamba ningempatia baada ya kutufu Kaaba (tawaaf). Kabla sijamaliza kutufu, Imam Ja’far Sadiq pia aliwasili kwa ajili ya tawaaf. Aliuweka mkono wake juu ya bega langu na sisi wote tukaanza kutufu. Nilimaliza tawafu yangu lakini niliendelea kutufu ili kumsindikiza Imam. Rafiki yangu yule alikuwa amekaa kwenye kona. Hakumjua Imam na aliingiwa na fikra kwamba nimelipuzia ombi lake. Kila nilipopita pale alipokaa kwa hiyo, alikuwa akinionesha ishara ya kunikumbusha juu ya jambo lile. Imam akaniuliza “Kwa nini mtu huyu anakufanyia ishara?” Nikamjibu: “Naniwe fidia yako! Ananisubiri ili nikimaliza tawaf nimpatie mkopo. Hata hivyo, kwa kuwa umeniwekea mkono wako kwenye bega langu sikutaka kukuacha.” Imam aliondoa mkono wake kutoka kwenye bega langu mara moja na akasema: “Niache. Nenda kamtimizie haja yake.” Nilikwenda na nikampatia mkopo kama nilivyomuahidi mtu yule. Siku inayofuata nilikwenda kwa Imam. Alikuwa anazungumza na masahaba zake. Aliponiona aliacha kuongea nao na akasema: “Kama nikifanya jitihada kukidhi mahitaji ya ndugu yangu katika imani, hilo ni bora zaidi kwangu kuliko kuwaachia huru wafungwa elfu moja na kuwapatia vifaa vya kupigania wapiganji elfu moja wanaopigana katika njia ya Mwenyezi Mungu.” – Safinatul Bihar, Juz. 1). Imam Ja’far Sadiq anasema: “Wakati mtu anaponiomba nimtimizie haja yake hufanya haraka kumtimizia ili isije ikawa kitu alichokiomba kikamfikia kikiwa kimechelewa mno kiasi cha kutokuwa na manufaa tena kwake.” – (Uyunul Akhbar).

66

12:44 PM

Page 66


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Imam Muhammad Baqir anasema: “Mtu akitabasamu kwa upendo juu ya ndugu yake katika imani (na ikiwa tabasamu hili ni ishara ya upendo wa dhati) basi kitendo chake hiki kitahesabiwa kuwa ni amali njema.” – (alKafi, Juz. 2). Imam Jafar Sadiq amesema: “Ikiwa mtu ataombwa msaada na ndugu yake katika imani, na licha ya kuwa na uwezo wa kumsaidia akaacha kumsaidia, Siku ya Kiyama Mwenyezi Mungu atamfufua mtu huyo akiwa amefungwa mikono – (Biharul-Anwar). Imam Sajjad amesema: “Jitahidini kupata daraja la juu Peponi na kumbukeni kwamba mtu atakayepewa daraja la juu zaidi na sehemu tukufu zaidi ni yule mwenye manufaa zaidi kwa ndugu zake katika imani na mwenye msaada zaidi kwa wenye kuhitaji. Na wakati mwingine kutamka sentensi moja tu inaweza kuwa ni sababu ya mtu kuwa karibu na Mwenyezi Mungu na kupata wokovu wake. Kamwe usione wema kwa ndugu yako katika imani kuwa ni mdogo kwa sababu haya matendo mema yatakuwa na manufaa kwako siku ambayo vitu vingine vyote havitakuwa na manufaa yoyote kwako.” – (Biharul Anwar, Tafsir-i Imam). Katika maamrisho haya ambayo yamenukuliwa kama mifano tu kutoka katika maelfu ya mafundisho ya kidini, jitihada imefanywa ili kuzifanya amali mbalimbali zilizo njema kuwa za kawaida miongoni mwa Waislamu na ili jamii ya Kiislamu iweze kuwa jamii ya kibinadamu katika nyanja zote. Marhum Profesa Shaltut, aliyekuwa mkuu wa Chuo Kikuu cha Azhar cha mjini Cairo ameandika Sura moja juu ya amali njema katika Uislamu katika kitabu chake kiitwacho Min Tawjihatil Islam, ambayo sehemu ya maelezo hayo yanatolewa hapa: “Mtukufu Mtume wa Uislamu alikuwa mpole na mwenye huruma sana kwa waumini. Alidumisha mawasiliano na ndugu zake wa karibu, alibeba mzingo wa matatizo ya wengine juu ya mabega yake na aliwasaidia wanyonge. Wema wake usio na miaka haukuishia kwa 67

12:44 PM

Page 67


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

wanaadamu tu bali pia alionyesha huruma sana kwa wanyama. Alikuwa na huruma mno kiasi kwamba alikuwa akijaza maji kwenye chombo na kuyaweka mbele ya paka ili akate kiu yake kila anapohisi kiu.” Mtukufu Mtume amesimuliwa kuwahi kusema kuwa: “Mwenyezi Mungu alimuadhibu mwanamke mmoja katika moto wa Jahanam kwa sababu alimtesa paka na alimfungia kwa muda mrefu bila kumpa chakula wala maji mpaka paka huyo akafa.” Siku moja Mtukufu Mtume alisimulia hadithi ifuatayo kwa masahaba wake: “Mtu mmoja alipatwa na kiu kali akiwa katika jangwa lenye joto kali na alikata kiu yake kwa kunywa maji ya kisima. Alipotoka ndani ya kisima alimuona mbwa akisugua pua yake kwenye udongo kutokana na kiu kali kupita kiasi. Yule mtu aliwaza kwamba yule mbwa atakuwa anahangaika sana kama alivyokuwa yeye kutokana na kiu kali. Hivyo aliteremka kwenye kisima tena na akajaza maji kwenye viatu vyake na akaviweka mbele ya mbwa yule. Mwenyezi Mungu Mtukufu alimsamehe mtu yule madhambi yake kutokana na kitendo hiki kizuri.” Masahaba wakamuuliza Mtukufu Mtume: “Je tunapata thawabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa kuwa na huruma kwa wanyama pia?” Mtukufu Mtume alijibu: “Ndiyo, mtalipwa thawabu kwa kumhudumia mnyama yeyote mwenye kuteseka.” Siku moja mtu mmoja alimjia Mtukufu Mtume na kusema kwamba alikuwa na njaa sana. Mtukufu Mtume alimtuma mtu mmoja nyumbmani kwake mara moja akamletee chakula mtu yule. Hata hivyo, mke wake alisikitika sana kwamba hapakuwa na chakula chochote ndani mwake. Aliposikia hivi, Mtukufu Mtume aliwageukia masahaba zake na kusema: “Je kuna yeyote ambaye yuko tayari kumpokea mtu huyu kama mgeni wake?”

68

12:44 PM

Page 68


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Mmoja wa masahaba alijitolea kumhudumia mtu yule. Hata hivyo alipofika nyumbani kwake na mgeni wake hakukuta chakula chochote isipokuwa chakula kidogo kwa ajili ya watoto. Chakula kilipotengwa, alizima taa kwa visingizio fulani. Mgeni alikuwa anakula chakula gizani na alikuwa anafikiri kuwa mwenyeji wake naye alikuwa anakula kumbe mwenyeji wake alikuwa ananyoosha mkono wake tu na kumgusa yule mgeni bila kuchukua chakula.� Ni watu wangapi unawajua katika jamii zetu za kisasa ambao wanaweza kuwa na sifa hizi tukufu za kibinadamu? Baadhi ya watu wanapumzika kwenye vitanda laini na wakiwa na nyoyo zenye utulivu na kuziona neema za Mwenyezi Mungu zikiwazunguka pande zote. Nyuso za watoto na wake wao zimejaa furaha na bashasha kutokana na raha za maisha. Ewe ndugu yangu Mwislamu! Ikiwa na wewe una maisha kama haya, basi nayawe yenye kukuletea afya! Hata hivyo, usisahau kwamba miongoni mwa wanaadamu wenzako ambao wanaoishi katika lindi la umasikini na dhiki, wamefanya ardhi kuwa ndio godoro lao na waifanya anga kuwa ni paa/mfarishi wao. Unapowatazama watoto wako watanashati na wenye raha, hupaswi kusahau kuwa kuna wazazi ambao wameupitisha usiku wao gizani pembeni mwa watoto wao, huku watoto wao wakiwa na nyuso zilizofadhaika na matumbo matupu yenye njaa. Unacheza na kucheka na watoto wako kwa furaha lakini pia lazima ukumbuke kuwa kuna watoto ambao waliwahi kuishi chini ya ulinzi wa wazazi wao lakini sasa vumbi la uyatima limetua juu ya vichwani na nyusoni mwao na wanalia bila ya msaada wowote kwa ukosefu wa chakula na nguo. Hakuna wa kuwafariji na kuwafuta machozi yanayotiririka kutoka machoni mwao na kuwakidhia njaa yao. Unapaswa kuiogopa siku ambayo gurudumu la wakati lenye nguvu linaweza likawashughulikia watoto wako nao wakapatwa na hali kama hiyo.

69

12:44 PM

Page 69


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Ewe mwanamke mwenye furaha na bahati, ambaye unafurahia hifadhi ya mume wako mpole! Usisahau kwamba kuna wakati ambapo dada yako au mwanamke wa nchini mwako, ambaye sasa ni mjane, alikuwa pia na furaha na mafanikio kama wewe. Lakini ghafla mume wake alitafunwa na kifo na akabaki na huzuni na sononeko la moyo. Enyi watu mliojitosheleza na mlio na furaha tele! Mshukuruni Mwenyezi Mungu kwa baraka Zake, kwani Yeye amesema:

“Kumbukeni Mola wenu alipotangaza: kama mtashukuru bila shaka nitawazidishieni fadhila zaidi.� (Surat Ibrahim, 14:7). Hata hivyo, kuwa na shukrani hakumaanishi kutoa maneno machache ya shukrani au kuonyesha huruma ya kujisingizia tu kwa wanyonge wasio na msaada. Kutoa maneno ya shukrani au kuonyesha huruma tupu kunatatua matatizo gani? Je haya yanaweza kuwasaidia wenye njaa na maskini? Kuonyesha kujuta na huruma kunapaswa kuambatana na mwelekeo chanya. Unapaswa kufanya kitu fulani kitakachofufua moyo wa ukarimu, usamehevu, ujasiri, na uadiifu katika tabia yako. Unapaswa kuwasaidia wazazi wako, watoto wako na wanafamilia wengine. Je unafanya hivyo? Kuna watu wanaokaa katika meza za duara zilizopakwa rangi na kupoteza mali zao kwa kucheza kamari. Kuna wengine ambao wamezama katika michezo ya sataranji, porojo za ovyo na mamia ya mambo mengine yanayopoteza wakati kimadhambi. Watu wajinga wamejiingiza katika michezo na anasa. Jamii inatishiwa na ufukara, magonjwa, vifo, mashaka na maelfu ya balaa nyingine, nyumba zenye misongamano ya watu zinabakia kuwa magofu, nyoyo za wachamungu zinaelekea kujiingiza katika ukafiri, familia zinavunja 70

12:44 PM

Page 70


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

mafungamano ya udugu na umoja, na wasio na makazi wanakaa katika vipembe na kona za barabara, ambapo wewe unaishi katika raha na anasa na umejiingiza katika sherehe ambazo zinapingana na hadhi na daraja la mwanaadamu. Sasa nini wajibu wa wale ambao hawana sehemu ya kuishi na hawawezi kuwapatia makazi wapendwa wao na watu wao wa karibu? Hivyo, fanya haraka na ziache nyumba hizi za dhambi. Fanya haraka na wasaidie wenye shida hata kama ni kwa muda mfupi tu. Ufurahishe moyo mmoja, mpatie furaha mnyonge na mfariji yatima japo mara moja. Na ukifanya mambo yote haya utaonja ladha halisi ya Imani na utapata utulivu wa akili na maisha matamu. Kwa njia hiyo, utakuwa umemridhisha Mwenyezi Mungu, utakuwa umeiokoa jamii dhidi ya maangamizi na utakuwa umetekeleza wajibu wako wa kibinadamu. Siwalinganieni kufanya wema, kuwa wasamehevu na warehemevu kwa wahitaji kwa ajili ya dini na ubinadamu tu, bali kwa sababu ustawi wa taifa na maslahi yenu vinategemea mambo haya. Kwa kufanya amali njema, kuwasaidia wahitaji na kuandaa mipango ya ustawi wa jamii, inawezekana kuunda jeshi lenye kutoka miongoni mwa wazururaji hawa na kuzitumia nguvu zote hizi kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa nchi na hivyo kuzuia ufisadi unaoitishia jamii. Inawezekana kuiondoa kutu ya chuki kutoka mioyoni kwa njia ya amali njema na kupata dhamira njema, kujiamini na upendo kwa wengine na hatimae kujenga ushirikiano na hali ya kuaminiana miongoni mwa wanajamii. Wakati na pale unapomfanyia wema mtu mwenye kuteseka, huyo uliyemsaidia hujiona kuwa ni mtumwa wako na huonyesha bashasha na unyenyekevu mbele yako. Mara nyingi inawezekana kwamba kwa kujitolea muhanga kidogo tu mtu 71

12:44 PM

Page 71


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

anaweza kupata kiasi kizuri cha mali, na amali njema za mtu zinaweza kumuokoa mhusika kutokana na maangamizi. Jitokeze na uwe mfadhili halisi wa wanyonge kwa kufufua tabia njema za kibanadamu na kuchukua hatua muafaka kuimarisha malengo ya dini na jamii. Tokeza na uwahurumie wakazi wa ardhi ili kwamba Mola wa mbingu na ardhi aweze kuwa na huruma juu yako. Tulichokinukuu mpaka hapa kuhusiana na amali njema ni mfano mdogo tu wa mafundisho ya Uislamu. Nukta muhimu katika jambo hili ni kwamba Uislamu umefanya jitihada kubwa kukazia moyo wa wema na ukarimu kwa watu toka wakiwa wadogo ili watakapokua, waweze kutenda amali njema kwa uaminifu kabisa. Pia wafanye amali hizi njema kwa furaha, bila kinyongo na waone kwamba muda wanaoutumia kuwatumikia wengine kuwa ni muda wa furaha sana katika maisha yao. Maisha ya viongozi mashuhuri wa Uislamu, na watu waliowafundisha ni ushahidi bora kabisa wa madai haya, Waislamu wanapaswa kujifunza haya ili waelewe maadili yao mema na kuyatekeleza ili kupatikane amani, maendeleo na ustawi. NUKUU 1). Fanya wema. Mwenyezi Mungu anawapenda wafanyao wema. 2).

Kwa kila amali moja njema, mtu atalipwa mara kumi yake.

3). Ukifanya wema, itakuwa ni kwa faida yako, lakini ukifanya uovu itakuwa ni kwa hasara yako mwenyewe – (Qur’ani Tukufu). 4). Watu bora kabisa ni wale wanaowafanyia wema watu wengine bila kujali kuwa hao wanaofanyiwa wema ni watu wema au waovu – (Mtukufu Mtume). 5). Mwanaadamu ni mtumwa wa wema na huruma – (Imam Ali (a.s.)). 72

12:44 PM

Page 72


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

6).

Matokeo ya sadaka na amali njema ni mazuri zaidi kuliko mwanzo wenyewe – (Imam Hasan Mujtaba). 7). Kitendo kizuri, ambacho kipo jirani zaidi na thawabu kuliko vitendo vingine ni uadilifu na haki – (Imam Baqir). 8). Mtu akifuatwa na ndugu yake muumini kuombwa msaada, hiyo huwa neema ya Mwenyezi Mungu iliyotumwa kwake – Imam Musa Kadhim). 9). Mwenyezi Mungu anao waja wake ambao hufanya jitihada kukidhi shida za watu wengine. Hao watakuwa salama Siku ya Kiyama – (Imam Ali (a.s.) Riza). 10). Yeyote anayekuwa mwema hupata daraja la mfalme halisi wa watu na hutawala katika ufalme wa nyoyo. (George Herbert). 11). Yeyote afanyaye jitihada ya kuwatafutia mafanikio na ustawi watu wengine, hatimaye hupata ustawi yeye mwenyewe – (Plato). 12). Malipo yenu hutegmea kutenda kwenu wema – (Ciceron). 13). Tusipozivuta nyoyo za watu wazembe na wasiojali kwa wema na upole je ni njia gani nyingine tunayoweza kuitumia kuvutia nyoyo? – (Behraam Ghor). 14). Kuna mambo mawili mazuri ambayo matokeo yake mara zote huwa ni mazri na mtendaji kamwe huwa haandamani na majuto. Mojawapo ni kuwafanyia watu wema na jingine ni mtu kutekeleza wajibu wake. (Jean Jaques Rousseau). 15). Wema huvishinda vitu vyote, lakini kamwe wema huwa haushindwi na kitu chochote – (Tolstoy). 16). Mtu afanyaye wema kwa wengine hulipwa na Mwenyezi Mungu 73

12:44 PM

Page 73


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

duniani na akhera – (Sheikh Sa’di). 17.

Kwa vile wema huthubutu kuwa na manufaa kila sehemu, fanya wema na ona aibu kufanya uovu – (Firadosi).

POMBE Ingawa kuna idadi kubwa ya vitabu ambavyo tayari vimeshachapishwa juu ya pombe na suala hili la pombe tayari limeshatafitiwa na kuchambuliwa kutoka katika kila pembe lakini bado kutokana na umuhimu wa mada hii na hatari zinazotokana na matumizi ya pombe, tumeona kuwa ni muhimu kufanya uchunguzi kwa kifupi lakini wakati huohuo kwa upeo mpana juu ya hili. Inatarajiwa kuwa kwa kufanya hivi, tutakuwa tumetoa mchango wa huduma kwa jamii na kwamba watu hawatashawishika kutumia kinywaji hiki cha hatari. Ni jambo zuri na la kuvutia kwamba hakuna tofauti ya maoni ya wanazuoni juu ya suala la pombe na madhara yake na tunazo hoja za kutosha kuthibitisha madai yetu juu ya ubaya wa pombe. Inawezekana kwamba mpaka miaka michche iliyopita baadhi ya watu wasiojua walikuwa wanadhani kwamba pombe ikitumiwa kidogo, sio tu kwamba haina madhara bali pia ina manufaa kiafya. Hata hivyo, kutokana na utafiti uliofanywa na baadhi ya wasomi na madaktari wa Ulaya na Kimarekani, dhana hii isiyo na msingi ilitupitiwa mbali na imethibitishwa kwamba pombe hata inywewe kidogo kiasi gani bado ina madhara sawa kwa kiwango kile kile. Hapa tunaelekeza mazingatio yetu kwenye ripoti ifuatayo iliyopatikana kutoka katika vyanzo rasmi: Miaka kadhaa huko nyuma madaktari bingwa kutoka pande zote za dunia walipokutana katika Jiji la Washington kushiriki katika kongamano la 74

12:44 PM

Page 74


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

dunia la kampeni dhidi ya pombe, kwa mara nyingine tena walitoa ishara ya onyo kuwa: “Pombe ni adui namba moja wa ubongo.” Dk. Melvin Kingsley ambaye ametumia miaka mingi katika utafiti juu ya pombe, katika mkutano wa kwanza wa kongamano hilo, alisema: “Hata kama pombe ikiwa kidogo kiasi gani, huwa na madhara makubwa kwa ubongo. Mtu anapoona starehe na furaha kwa kunywa kiasi kidogo cha pombe, huwa hajui kwamba amesaidia kuangamiza chembehai za ubongo wake.” Dk. Kingsley ambaye ni Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Chuo cha Madaktari cha South Carolina ana maoni kwamba unywaji pombe wa kupita kiasi husababisha mabadiliko katika damu na mishipa kwa kiasi kwamba chembehai za ubongo hukumbwa na tatizo la upungufu wa oksijeni na hivyo huangamizwa au hujeruhiwa sana kiasi kwamba mtu anayehusika huvurugikiwa na akili. Wakati mwingine athari za pombe katika damu huathiri kwa kiasi kikubwa mzunguko wa damu na kati ka matukio mengine imeonekana kuwa ikisababisha kuganda na damu huwa mabonge bonge. Dk. Kingsley alisema mwanzoni kabisa mwa kongamano hili kuwa: “Kwa bahati mbaya jitihada zetu za kampeni dhidi ya pombe ambayo huathiri watu wengi kila kukicha hazijazaa matunda na idadi ya wanywaji wa pombe inazidi kuongezeka. Kwa mujibu wa takwimu tulizonazo sasa hivi ni kuwa duniani hivi sasa kuna mamilioni ya watu ni walevi wa kutupa na imewaathiri kiasi kwamba hawawezi kuacha tena. Nukta muhimu inayojadiliwa hapa ni kwamba kwa bahati mbaya watu wote wanafikiri kwamba kunywa pombe kidogo sio tu kwamba haina madhara, bali pia inaonekana kuwa ni jambo muhimu. Baadhi ya watu wana maoni kwamba kama wakinywa pombe kidogo kwenye tafrija hawatatawaliwa na ulevi au kwamba pombe hiyo kidogo haitaathiri mabongo yao, ingawa utafiti wa kina uliofanyika kuhusiana na hili 75

12:44 PM

Page 75


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

unaonyesha kuwa pombe hata kama itanywewa kidogo tu huleta mvurugiko katika mfumo wa chembehai katika ubongo.” Dk. Raymond Penignon ambaye aliwasilisha ripoti ya kurasa nne katika kongamano hilo, pia anaamini kuwa bila shaka pombe ni moja ya maadui wa hatari kabisa wa mwanaadamu yeyote, na hata wale ambao kwa mujibu wa fikra zao, wanaokunywa pombe kidogo na mara moja moja nao pia wapo katika hatari kwa sababu ya adui huyu. Kwa mujibu wa Dk. Penignon, athari ya kwanza ya kuathirika na pombe ni kuwa msahaulifu na mtu kupoteza ajira yake. Anasema: “Kwa mujibu wa utafiti nilioanya, nimekuja kubaini kuwa watu waliothiriwa na pombe huwa na tatizo la usahaulifu baada ya muda na hushindwa kufanya maendeleo yoyote. Hupoteza hamu ya kufanya kazi zao na hatimaye hupoteza kazi zao na kwa sababu hiyo hiyo huamua kukimbilia kwenye kulewa zaidi.” Daktari huyu pia anasema kuwa: “Ni jambo la kusikitisha sana kwamba vijana wengi wamezama katika unywaji wa pombe na wanafanya unywaji pombe ni njia ya kukwepa majukumu yao ya maisha. Kwa mujibu wa utafiti tuliofanya tulifikia hitimisho kwamba 70% ya vijana wanaonyesha kupenda pombe, na 20% hadi 30% yao wameshaathiriwa na pombe. Ongezeko la uhalifu ni moja ya dalili na ongezeko la kila siku la matumizi ya pombe na kumbukumbu zilizopo katika mashirika ya usalama zinaoyesha kuwa wengi wa wanaofanya uhalifu wa jumla ni wale walioathiriwa na pombe.” Dk. Herbert Miskoff, daktari mwingine aliyeshiriki katika kongamano hilo, anasema: “Pombe hudhoofisha seli za ubongo na huharibu uwezo wa mtu wa kuelewa mambo. Hata hivyo tatizo muhimu zaidi ni athari za urithi. Mtoto wa mtu mlevi sugu huwa mdhaifu, mvivu na mpumbavu. Huwa hana uwezo wa kupata elimu na mara zote huwa na wasiwasi. Licha ya hivyo imegundulika kuwa wakati mwingine watoto wa walevi sugu 76

12:44 PM

Page 76


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

huzaliwa wakiwa na mapungufu. “Matokeo ambayo yanaweza kupatikana katika kongamano hili na utafiti wa wataalamu bingwa yanaweza kuwa nguvu kwa watu wachache tu bali ni wazi kwamba hili haliwezi kusaidia kumaliza tatizo la pombe. Pombe imeeneza mizizi yake katika maisha ya mwanaadamu na ikiwa kampeni kabambe haitafanyika dhidi ya pombe ni wazi kwamba mizizi ya pombe itazidi kuimarika na itawanasa wengi katika mtego wake.� Ni uchunguzi wa utafiti huu wa kisayansi ambao hutulazimisha kuinamisha vichwa vyetu kiuficho kwa heshima juu ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake ambao walitangaza kuwa kunywa pombe haramu karne kumi na nne zilizopita kabla ya kupatikana maabara na kujengwa vyuo na vyuo vikuu na wakakataza matumizi ya japo tone lake. Wakati wa uhai wa mwanamagezi mkubwa wa Kishia. Marhum Ayatullah Burujardi, Dk. Arshah Tong, Katibu Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Kampeni dhidi ya pombe, alitembelea Iran. Wakati wa ziara yake aliomba aruhusiwe kuonana na kiongozi mkubwa katika ulimwengu wa Kishia ili amuulize baadhi ya maswali. Mkutano huu uliandaliwa kwa kupitia mmoja wa maprofesa wa chuo kikuu cha Tehran na Katibu wa Chama cha Kampeni dhidi ya madawa ya kulevya na pombe. Nukta muhimu za mazungumzo yao tumezinukuu hapa katika maneno ya Profesa huyo na katibu wa Chama hicho (cha kampeni dhidi ya pombe na madawa ya kulevya). Katika muda uliopangwa mapema, sisi tuliambatana na Dk. Arshah Tong kwenda kuonana na mtukufu Ayatullah Burujardi. Tulipofika tulivua viatu nje ya chumba na tukaenda pamoja kuibusu mikono ya Ayatullah. Tabia na haiba yake rahisi na ya dhati ilikuwa inavutia ajabu sana. Kwa furaha na bashasha Ayatullah aliielezea furaha yake ya kukutana nasi na alitaka kujua juu ya afya zetu. Baada ya kumshukuru Ayatullah kwa kukubali kukutana 77

12:44 PM

Page 77


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

nasi, mimi nilimwambia (Ayatullah). “Dk. Arshah Tong anatoka Switzerland na ni Katibu Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Kampeni dhidi ya Pombe. Baada ya kutembelea Indonesia na Tehran kwa ajili ya kuendeleza lengo lake hili (kampeni dhidi ya pombe), alipatwa na shauku kubwa ya kukutana na wewe na sasa anakuomba umpe majibu ya baadhi ya maswali yake.” Ayatullah alimruhusu aulize maswali hayo. Hapo ndipo Dk. Arshah Tong akauliza: “Ewe mtukufu! Kwa nini matumizi ya pombe na vileo (vitu inavyolevya) vimeharamishwa katika Uislamu?” Ayatullah alijibu: “Mwanaadamu ametambuliwa kuwa ni mbora wa viumbe kutokana na kuwa kwake na akili na lengo la kuumbwa kwake ni kusafiri katika njia ya kuelekea ukamilifu katika kumtambua Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu Mtukufu, alipokuwa anatupatia zawadi ya thamani kubwa, ya akili na hekima, pia alitoa amri ya kuilinda zawadi hiyo. Ni kwa sababu hii kwamba Mtukufu Mtume alikataza utumiaji wa vitu vyote vinavyolevya ambavyo husababisha ugoigoi na kuvurugika kwa akili na uwezo wa kufikiri na umuhimu wa kuharamisha vitu hivi upo wazi hata kwa mtu mwenye akili za kawaida.” Dr. Arshah Tong aliuliza tena: “Ikiwa matumizi ya pombe yakifikia hatua ya kumlevya mnywaji, huvuruga akili na uwezo wa kufikiri. Sasa wewe unasemaje ikiwa itanywewa kidogo na hivyo kutovuruga akili?” Ayatullah alijibu kwamba: “Inapokuwa imefahamika kuwa ubora wa mwanaadamu dhidi ya wanyama ni kwa sababu ya akili na uwezo wa kufikiri na inapokuwa imethibitika kuwa mwanaadamu anao wajibu wa kuilinda zawadi tukufu ya akili, hekima na uelewa, ambavyo vyote ni zawadi ya bure kutoka kwa Mwenyezi Mungu basi kitu chochote kitakachovidhoofisha vitu hivi hakitaruhusiwa na ni ukweli uliothibitika kuwa pombe hata iwe kidogo kiasi gani, huathiri hisia. Mbali na hayo kuna nukta nyingine ambayo ni muhimu nayo ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu 78

12:44 PM

Page 78


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

anaelewa vizuri hali ya mwanaadamu na anajua kwamba kwa asili mwanaadamu hutaka kingi zaidi ya kile anachopata sasa. Hivyo kama angekuwa ameruhusu watu wanywe pombe kidogo, ingeleta ugumu sana kuamua kuwa hiyo kidogo ni kiasi gani. Hivyo ili mwanaadamu aweze kubaki salama dhidi ya ulevi, ambao unamlazimisha kufanya mambo kinyume na maumbile yake, Mwenyezi Mungu Mtukufu amepiga marufuku kabisa unywaji wa pombe.” Aliposikia jibu la pili la Ayatullah, Dk. Arshah Tong alisema: “Ni zaidi ya miaka kumi sasa tangu niwe Mkuu wa Shirika la Kampeni dhidi ya pombe na katika kipindi hiki nimekuwa na majadiliano ya kina na viongozi wakubwa wa kidini, wa kisiasa na wa kijamii wa nchi mbalimbali. Hata hivyo, ninakiri kwamba hakuna aliyetoa maoni mapana na ya kushawishi kama yako ewe mtukufu. Maelezo yako yatakuwa ni mamlaka halali na madhubuti kwetu katika mapambano yetu dhidi ya unywaji wa pombe duniani na kwa kusema kweli njia bora ya kufanikisha malengo yetu itakuwa ni kufuata maamrisho ya viongozi watukufu wa Uislamu. Ninakushukuru bwana mtukufu kwa niaba yangu na kwa niaba ya Shirika la Kimataifa la Kampeni dhidi ya Pombe na ninataraji kwamba kwa muongozo wako huu tutashinda vita hivi vitakatifu.” – (Taz. Symposium on liquor in Medical College, Isfahan). Mwanafalsafa wa Kiingereza, Bentham anasema: “Moja ya mafundisho bora kabisa ya dini ya Muhammad (Uislamu) ni kwamba umeviharamisha vitu vyote vinavyolevya.” Mwandishi na mashuhuri wa Kifaransa na mwenye kusafiri mno, Pierre Loti amesema: Hakuna kitu kilichobaki kinachoweza kunifanya nisijione kuwaw ni Mwislamu kwa sababu kamwe sijawahi kugusa pombe wala kitu chochote kinacholevya.”

79

12:44 PM

Page 79


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Kundi la watu katika kabila la Qur’aysh walikuwa wamekaa katika Masjidul-Haram. Wakati huo mara akawasili Imam Baqir. Mmoja wa watu wale alimnyooshea kidole Mtukufu Imam na kuwaambia wengine: “Huyo ni kiongozi wa watu wa Iraq.” Kisha waliamua kumtuma mmoja wao ili akamuulize juu ya mas’ala fulani ya kidini. Huyo mtu alisimama na kumwendea Imam Baqir. Alimuuliza: “Ni lipi kati ya madhambi makubwa ni dhambi kubwa zaidi?” Imam alijibu kunywa pombe.” Mtu yule alirudi kwa wenzake na kuwaeleza alivyojibiwa. Hata hivyo, walimwambia yule mtu arudi na akaulize tena swali lile. Imam kwa bashasha alijibu kwamba, “Nimeshakujibu kuwa dhambi kubwa zaidi ni kuywa pombe.” Yule mtu alirudi kwa rafiki zake na kuwaeleza alivyojibiwa. Lakini walihimiza kwamba arudi akaulize swali lile kwa mara ya tatu. Alifanya hivyo kwa mara ya tatu Imam alimjibu kuwa, “Kunywa pombe ndio dhambi kubwa zaidi kwa sababu ulevi humpelekea mtu kwenye zinaa, wizi, mauaji na kumshirikisha Mwenyezi Mungu na madhambi ambayo yanatokana na ulevi ndio madhambi makubwa zaidi – (Wasailush Shi’ah, Juz. 17, Furu’al Kafi, Juz. 6). Mtu mmoja alikwenda kwa Imam Ja’fa Sadiq (a.s.) na akamuuliza: “Kwa nini Mwenyezi Mngu ameharamisha pombe wakati ni kitu kinacholeta hisia za furaha kuliko vitu vingine vyote?” Mtukufu Imam alisema: “Mwenyezi Mungu aliharamisha pombe kwa sababu pombe ni mama wa maovu yote. Mlevu hupoteza fahamu zake, huwa hamtambui Mwenyezi Mungu, hufanya kila uhalifu, huharibu heshima ya watu wengine, huvunja mahusiano na hujiingiza katika uchafu na ufisadi. Mlevi hudhibitiwa na Shetani. Kama Shetani akiamuru asujudie sanamu humtii na huenda kokote kule shetani anakomuamuru – (Wasailush Shi’ah). Kabla ya kuja kwa Uislamu na hata katika siku za awali za Mtukufu Mtume, uandaaji na uuzaji wa pombe ulichukuliwa kuwa ndio biashara 80

12:44 PM

Page 80


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

muhimu kabisa ya Waarabu kiasi kwamba neno “Tijarat” (biashara) lilikuwa likitumika kipekee katika biashara iliyofungamana na pombe na mtu ambaye ujuzi wake ulikuwa katika kushughulika na pombe alikuwa akiitwa “Tajir” (mfanya biashara). Jua la Uislamu lilipochomoza na mafundisho yake adhimu yalipowafikia watu, utengenezaji wa pombe uliokuwa ukisababisha balaa na hasara kubwa ulipigwa marufuku. Katazo la pombe katika Uislamu lilikuwa la nguvu mno na la uamuzi kiasi kwamba laana yake iliondolewa kutoka katika jamii ya Kiislamu ndani ya muda mfupi. Uislamu haukukataza kunywa pombe tu bali pia umetamka kwamba utengenezaji na shughuli zote zinazohusiana na pombe ni haramu. Mtukufu Mtume amewalaani watu wafuatao ambao wanahusiana na biashara ya pombe: (i) Anayelima zabibu kwa ajili ya kutengenezea pombe (yaani mazao yote ya kutenenezea pombe) (ii) Yule anayetengeneza pombe (iii) Yule anayeuza pombe (iv) Yule anayenunua pombe (v) Yule anayekunywa pombe (vi) Yule anayepitisha, glasi ya pombe kwa mnywaji mwingine (vii) Yule anayenufaika kwa namna yoyote kutokana na biashara ya pombe – Wasa’ilish Shi’ah, Juz. 17; Khasa’il, Iqabul A’mal) Imam Ja’far amesema: “Msishirikiane na walevi kwa sababu balaa itakapowashukia, itawazingira washirika wao pia” – (Wasa’ilush Shi’ah, Juz. 17). Mwenyezi Mungu, ambaye anajua madhara yote ya pombe kwa watu na watoto wao na jamii, sio tu kwamba amekataza unywaji, utengenezaji, 81

12:44 PM

Page 81


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

usambazaji, ununuaji na uuzaji wa pombe bali pia amekataza kufunga ndoa na mlevi kwa sababu pombe huathiri pia mbegu zao za uzazi na hupelekea kuzaliwa kwa watoto wasiofaa, mafisadi na wenye maumbile yasiyo ya kawaida. Imam Sadiq amesema: “Yeyote atakayemuozesha binti yake kwa mlevi atakuwa amevunja uhusiano na binti huyo. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: “Kama mtu akinywa pombe baada ya kuwa Mwenyezi Mungu ameshaiharamisha kupitia kwangu, basi asiozwe msichana hata kama atatoa posa ya kumchumbia na mtu yeyote akimtetea basi utetezi huo usisikilizwe na akinukuu habari yoyote asiaminiwe na mtu yeyote asimwamini mlevi na asiaminiwe kwa amana. Na mtu akiweka amana yake kwa mtu anayefahamu kuwa ni mlevi, Mweyezi Mungu huwa hawajibiki juu ya amana hiyo na ikiwa amana hiyo itapotea haitofidiwa wala kulipwa thawabu na Mwenyezi Mungu.” – (Li’ali’ul Akhbar). Kuna hadithi nyingi kuhusu hili zilizotufikia kutoka kwa Mtukufu Mtume na Maimamu na umuhimu mkubwa umewekwa kwenye mimba inayoingia kutokana na ushawishi wa pombe kwa sababu hili ni jambo la hatari sana. Imam Ja’far Sadiq amesema: “Mwanamke anayekubali kufanya mapenzi na mumewe ambaye yupo katika hali ya ulevi huwa anafanya makosa na madhambi yaliyo sawa na nyota za mbinguni na mtoto atakayezaliwa kutokana na mwanaume huyu atakuwa haramu na mchafu. Mwenyezi Mungu hakubali toba au fidia yoyote kutoka kwake (mwanamke huyo) isipokuwa Mume wake atakapokufa au ajiondoe kutoka katika kifungo cha ndoa hiyo – Li’ali’ul Akhbar, uk. 267). Wanachuoni wa sasa hawana shaka yoyote juu athari mbaya za pombe katika manii na utafiti wa kisayansi umethibitisha ukweli wa madai haya, kwa sababu watoto wanaozaliwa katika hali hizi, kwa kawaida huwa wanaugua magonjwa ya akili. 82

12:44 PM

Page 82


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Mbali na utafiti wa kisayansi uliofanywa na wanazuoni wa nchi za Mashariki na Magharibi, uzoefu pia umehibitisha kwamba watoto wa mtu aliyeathiriwa na pombe kali huwa ni wadhaifu na wenye maendeleo duni ikilinganishwa na watoto wengine. Hakuna shaka yoyote juu ya ukweli kwamba maradhi ya akili (ukichaa), upumbavu na kuvia na ulevi vina madhara makubwa katika maendeleo na kukua kwa watoto na watoto wanaozaliwa na wazazi wenye mapungufu haya huwa na dosari na ni wa kuhurumiwa. Kwa sababu hii Uislamu umetoa mapendekezo makali sana kwa wafuasi wake kuepuka ulevi na pia umewaonya dhidi ya mafungaano ya kindoa mabaya na machafu. Wanachuoni wa zama hizi pia wamelizingatia suala hili na wanapendekeza sana kuepuka ushirikiano wa ndoa za namna hiyo kiasi kwamba katika baadhi ya nchi za Amerika, sheria maalumu zimepitishwa kwa ajili ziweze kupata kizazi kisafi. Kwa mujibu wa sheria hizi, wavulana na wasichana ambao ni walevi wa kupindukia wanasafishwa kuondolewa uwezo wa kuzaa na hivyo kuzuiwa kupata watoto. Athari nyingine mbaya ya pombe kali inayoleta kwa watu ni kwamba Seli za ubongo na mishipa ya neva za fahamu huathiriwa na kujeruhiwa sana kiasi cha kusababisha maradhi ya akili. Mmoja wa maprofesa wa Chuo Kikuu cha Tehran amesema: Pombe ni moja ya visababishi vya hali ya ganzi na kupoteza hisia na hivyo huleta mkandamizo wa mfumo wa neva na matokeo ya kuharibiwa kwa seli za ubongo na hivyo kusababisha mvurugiko wa akili na uawendawazimu.” Alipokuwa akisheresha aya ya Qur’ani: “(Ewe Mtume) Wanakuuliza juu ya pombe.....” (Suratul Baqarah, 2:219), mfasiri wa Kimisri, katika kitabu chake Tafsiri al-Manar, anamnukuu daktari wa Kijerumani akiiambia Serikali yake kuwa, “Mnapaswa kufunga nusu ya baa na vilabu vya pombe ili hospitali za vichaa na za kawaida na jela za nchi zipungue kwa 83

12:44 PM

Page 83


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

nusu nzima ya idadi yake.” Katika hadithi za Mtume na Maimamu, imeelezwa kwa kifupi juu ya madhara yanayosababishwa na pombe katika akili na nafsi ya mwanaadamu chini ya mlango wa makatazo (haraam). Imam Riza amesema: “Mwenyezi Mugu ameharamisha pombe kutokana na maovu yake na kwa sababu huondoa uwezo wa kufikiri na uwezo wa ufanyaji kazi wa akili na huondoa stara.” – (Mustadrak, Juz. 3). Imam Sajjad amesema: “Dhambi ambayo huondoa uwezo wa kujizuia na madhambi mengine, yaani ile ambayo inalemaza hisia na ambayo huvunja nguvu ya maadili ya ulinzi ya mtu ni kunywa pombe na kucheza kamari – (Biharul-Anwar, Juz. 16). Mwanasaikolojia mmoja amesema: “Pombe huondoa stara, huchana vazi la usafi wa maadili na humuondoa mwanadamu kwenye majukumu yote ya kijamii, ya kidini na kimaadili, huikandamiza akili na humbadili malaika kuwa shetani. Kwa kawaida, hatua ya kwanza ambayo humuondoa mtu kutoka katika njia ya usafi wa kimaadili ni ile inayochukuliwa katika hali ya ulevi, kwa sababu ulevi ukiingia, busara na uwezo wa kufikiri huondoka na usafi wa kimaadili huwa hauna maana yoyote panapokuwa hakuna hekima na fikra. Wavulana, wasichana na wanawake waliopotoka ni wale watu waliokengeushwa kutoka katika njia iliyonyooka kwanza kabisa na yule binti wa zabibu (pombe). Kwa sababu hii wametangatanga katika jangwa la hatari la maisha na hatimaye kuzama katika dimbwi la upotovu na balaa.” Tolstoy amesema: “Watu wanayaelewa vizuri madhara ya pombe kwamba hukandamiza uamuzi wa akili, na ni kwa sababu hii kwamba pombe inaendelea kunywewa.”

84

12:44 PM

Page 84


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Kuna watu wengi ambao katika hali ya kawaida hawako tayari kufanya kitu kiovu au kisichofaa au kuchukua hatua isiyokuwa ya kibinadamu lakini hawasiti kuyafanya yote haya wanapokuwa wamelewa. Dk. Alexis Carrel amesema: “Upungufu wa jumla wa akili na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi unatokana na athari za pombe na aina zote za matumizi ya kupita kiasi na hatimaye kupatikana kwa mabadiliko ya tabia. Hapana shaka yoyote kwamba kuna uhusiano wa kiasi cha pombe kinachonywewa na udhaifu wa kiakili wa jamii. Kutoka miongoni mwa nchi zote zinazojishughulisha na kazi za kisayansi, nchi inayotumia pombe zaidi ni Ufaransa na nchi hiyo inapata Tuzo za Nobel chache zaidi kuliko nchi nyingine.” Takwimu zifuatazo zinatupatia picha kwa kiasi kikubwa juu ya athari mbaya za pombe: Adnre Minu, Katibu wa Baraza la Bunge la Tatifa la Kampeni dhidi ya pombe alitangaza kwamba: “Maradhi ya 80% ya wendawazimu na 40% ya watu wanaoumwa magonjwa ya zinaa yametokana na matumizi ya pombe. Miongoni mwa watoto 60% ya watoto mazuzu na 40% ya wahalifu, walizaliwa katika familia za walevi wa kutupa.” Hasara zinazotokea katika jamii za wanaadamu kutokana na pombe ni kubwa kuliko hasara nyingine zozote na maafa yake yanazidi maafa yanayosababishwa na yale magonjwa ya hatari kabisa. Kwa mujibu wa kauli za wasomi mahiri, pombe husababisha kansa katika mfumo wa uyeyushaji wa chakula, ini na tumbo, kifua na mbavu na kifua kikuu, maradhi ya akili, kudhoofu kwa neva za fahamu, usahaulifu na kubwa kuliko yote vilema vya kuzaliwa navyo kwa watoto wachanga. Moja ya hasara nyingine kubwa za kijamii zinazosababishwa na pombe ni ajali za barabarani. Kwa mujibu wa utafiti wa kitabibu na uchunguzu mbalimbali umeonyesha kuwa kunywa pombe hubadili welekevu wa uendeshaji wa madereva wazoefu wa ulevi jambo ambalo husababisha ajali za barabarani. 85

12:44 PM

Page 85


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Kama ilivyothibitishwa na Baraza la Usalama, robo ya vifo vinavyotokea kama matokeo ya ajali za barabarani vinahusiana na ulevi wa madereva. Leograin anasema: “Kati ya watu 761 wanaozaliwa na wazazi walevi, 322 ni wapotovu, 155 ni vichaa na 131 wana hatari ya kupatwa na kiharusi.” Asilimia 30% hadi 40% za wagonjwa wa akili katika hospitali za wagonjwa wa akili ni wale ambao wamelemaa kwa ulevi wa kutupwa. Katika mwaka 1344 A.H, watu 1875 walikufa nchini Iran kwa sumu kwa sababu ya ulevi. Pombe ni chanzo kikuu cha uhalifu. Pombe imesbabisha 75% ya mauaji, 38% ya mashambulizi ya kinguvu na 82% ya vitendo vya uchomaji moto wa mali kwa makusudi. Kwa kuzingatia madhara yote haya na taabu zinazosababishwa na pombe, Uislamu umeng’oa kwa uangalifu kabisa ule mzizi wa uovu huu kwenye chipukizi la mmea wake. Uislamu unasema: “Msikae katika meza ambapo wengine wanakunywa pombe. Msishiriki tafrija ambazo ndani yake pananywewa pombe hata kama hamtakunywa. Msiambatane na walevi msije mkaingia katika dimbwi la maovu.” Mmoja wa maafisa wa jeshi wa Mansur, Khalifa wa ukoo wa Bani Abbas, aliandaa sherehe katika mji wa Hayra kufuatia kutahiriwa kwa mwanaye wa kiume na alialika baadhi ya wageni wa heshima na watu wenye vyeo vya juu. Imam Ja’far Sadiq, Imam wa sita alikuwa pia ni mmoja wa waalikwa. Wageni walipokuwa wanashughulika kuchukua chakula mmoja wao aliomba maji. Badala ya maji, mtumishi alileta glasi ya pombe. Pombe alipoletwa tu pale mezani, Imam Ja’far Sadiq aliondoka katika meza hiyo ya chakula. 86

12:44 PM

Page 86


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Mwenyeji wake alimkimbilia na kumuuliza sababu za yeye kuondoka kwenye tafrija ile. Imam alijibu: “Mtukufu Mtume amesema kuwa anayekaa katika meza ambapo pananywewa pombe amelaniwa.” – (Biharul Anwar, Juz.11). Mbali na hicho kilichoelezwa hapo juu, kutupia macho kwenye kurasa za historia kunaonyesha kuwa pombe imekuwa ni chanzo cha maangamizi ya taifa au kusambaratika kwa familia. Hisoria inasema: “Pamoja na utukufu wa mamlaka ya Wabamersidi walikufa kwa pombe. Kama Barmesid Ja’far asingelewa na kupoteza fahamu kutokana na pombe, suala la Abbasa, dada wa Harun Rashid lisingeibuka na Wabarmesidi wasingekuwa wameuliwa kwa kiasi kikubwa. Ingawa mkosi uliwapata Wabarmesidi kutokana na uhalifu wao mkubwa waliokuwa wanafanya huku moja ya uhalifu huo ukipelekea kuuliwa shahidi Imam Musa Kadhim lakini balaa lao bado lilianza kwa sababu ya kulewa kwa Ja’far. Historia inasema kwamba ufalme wa Sultan Jalaludin Khawarazm Shah ulianguka kutokana na tabia yake ya ulevi pamoja na kuendekeza maisha ya tamaa ya wanawake na hivyo alipoteza kichwa chake na kiti chake cha ufalme kwa ajili ya ulevi. mfalme huyo shupavu na mpenda vita ambaye alipigana na wanajeshi wakali wa Kimongolia kwa miaka mingi na akamfadhaisha Chenghizkhan na askari wake hatimaye aliangukia kuwa mawindo ya uovu wa kunywa pombe. Wakati wa usiku Sultan alipokuwa akishughulika katika anasa na kupoteza wakati katika hali ya ulevi, afisa wake aliyekuwa akiaminiwa sana, Nuruddin Zaydari alimsomea utenzi huu:

87

12:44 PM

Page 87


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Na nini yatakuwa matokeo ya ulevi huu wenye kutia kichaa? Mfalme amelewa, na nchi imetelekezwa na maadui wametuzunguka kila upande. Matokeo ya hali hii mambo itayoyasababisha yako wazi.� Lakini hata hivyo si mfalme wala wasaidizi wake waliojali maneno haya. Wote walikuwa wamelewa. Usiku wa manane, wa-Mongolia walifanya shambulizi la kushitukiza na walilizunguka jeshi la Sultan na hema lake. Mmoja wa wasaidizi wa Sultan ambaye alikuwa amepata habari juu ya shambulizi hilo alifika kitandani kwa Sultani na akajaribu kwa taabu sana kumwamsha katika usingizi wake mzito na akamjulisha juu ya hali ya mambo. Akiwa amelewa sana, Sultani hakuweza kupanda farasi. Alijimwagia maji kichwani ili kupunguza ulevi. Hata hivyo alikuwa amechelewa sana na hapakuwa na la kufanya zaidi ya yeye mwenyewe kukimbia. Alikimbia katika hali hiyo hiyo ya ulevi lakini akauawa na mtu mgeni katika vilima vya Kurdistan, ambaye alitaka kumpora farasi wake na vitu vingine alivyokuwa navyo. – (Tarikh Kamil-i Iran, uk. 316). Historia inasema kuwa utawala wa Safawid uliporomoka kutokana na Shah Tehmasib kuwa mlevi wa kupindukia. Yote yaliyosemwa hapa yanafungamana na hasara zinazotokana na pombe, na madhara yanayosababishwa katika mwili na roho, kwa mtu mmoja mmoja na kwa jamii, mbali na hasara za kiuchumi. Lakini, kwa sisi tunaoamini juu ya Tauhidi kwa dhati, mwanzo na ufufuo, pombe ina mwelekeo mwngine pia ambao ni athari mbaya za milele katika maisha ya akhera. Mwelekeo huu pia unapaswa kuangaliwa kwa kina kwa sababu inawezekana baadhi ya watu wakawa tayari kukabiliana na hasara zote na 88

12:44 PM

Page 88


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

kila dhara linalotokana na pombe lakini Mwislamu hawezi, kwa gharama yoyote ile kusamehe furaha ya milele ya akhera. Imam Baqir amesema: “Mlevi atatokea katika uwanja wa hukumu kama mwabudu masanamu.” – (Wasa’ilush Shi’ah Juz. 17). Imam Ja’far Sadiq amesema: “Mwenyezi Mungu Mtukufu amewaharamishia pepo watu wa aina tatu, kundi mojawao kati ya haya ni lile la walevi.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: “Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba anayepuuzia Sala na anayekunywa pombe hatanufaika na uombezi wangu Siku ya Kiyama – (al-Kafi, Juz. 2). Hakim Sina’i, mshairi maarufu wa Ki-Iran, ametaja uovu wa pombe katika beti za shairi zilizotafsiriwa hapa chini. “Mtu mwenye busara huwa hanywi pombe na huwa halewi. Mtu mwenye akili hawezi kujitweza kirahisi hivyo. Kwanini unadhani kitu ambacho kikinywewa hukuonyesha tete kuwa ni mkaratusi na mkaratusi kuwa ni tete? Ikiwa katika hali hiyo utampa mtu zawadi hudaiwa kuwa ni pombe na sio wewe uliyetoa, na ukisababisha vurugu hudaiwa kuwa ni wewe uliyesababisha vurugu hizo sio pombe.”

NUKUU 1). Muhammad, wanakuuliza juu ya pombe na kamari, waambie kuwa kuna dhambi kubwa katika hayo. Ingwa kuna faida kwa watu lakini madhambi yake ni makubwa sana kuliko faida. 2). Enyi mlioamini, pombe, kamari na kupiga ramli yote ni matendo 89

12:44 PM

Page 89


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

yanayochukiza na ni kazi za Shetani. Yaepukeni ili mpate kufuzu. 3). Shetani anataka kuchochea chuki na uadui baina yenu kwa kupitia pombe na kamari na kuwazuieni kumkumbuka Mwenyezi Mungu na Sala. Je sasa mtayaepuka mambo hayo? – (Qur’ani Tukufu).

* * * * *

KAMARI Kamari ni moja ya shughuli mbaya za brudani na ni kiburudisho cha hatari ambacho kimekuwepo miongoni mwa watu toka karne na karne na kimesababisha madhara makubwa. Katika ulimwengu wa leo pia, kamari ni chanzo cha burudani kwa watu kwa kiasi kikubwa na kwa kutumia njia za kisasa jamii za wanaadamu zimetaabika vikali kutokana na mchezo huu angamizi. Kwa nchi kadhaa kamari imekuwa ni shughuli muhimu kwa mtazamo wa kiuchumi. Uzalishaji na uuzaji wa vifaa vya kuchezea kamari na ukusanyaji wa kodi kubwa kutokana na biashara hii ni vyanzo vya mapato ya serikali. Na si hivyo tu, bali pia watu wengi hujipatia riziki zao kutokana na taasisi za kucheza kamari. Katika baadhi a nchi za Ulaya na Amerika, vimejengwa vituo vikubwa vya kamari ili kuvutia watu matajiri. Wamiliki wa vituo hivi hupata fedha nyingi sana na kiasi kingine kikubwa huingia kwenye hazina ya serikali kama kodi.

90

12:44 PM

Page 90


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Mwelekeo wa kiuchumi unaotokana na kamari ulizingatiwa na Mtunga sheria wa Uislamu karne kumi na nne zilizopita na Qur’ani imelieleza hilo kwa uwazi kabisa. Hata hivyo, kwa vile hasara zake ni kubwa kuliko faida, kamari imeharamishwa ili katika kupata manufaa ya kimaada,Waislamu wasilazimike kupata madhara makubwa zaidi ya kimaada na kiroho. Qur’ani tukufu inasema:

“(Ewe Muhammad!) wanakuuliza juu ya kamari na pombe. Waambie kuna madhambi makubwa ndani yake. Ingawa vitu hivi vina faida kwa watu, hasara zake ni kubwa sana kuliko faida.” – (Suratul Baqarah, 2:219). Ingawa nchi za dunia zinafahamu matatizo yanayotokana na kamari haziipigi marufuku kwa dhati kwa sababu ya faida za kifedha ambazo serikali za nchi hizo zinazipata kutokana na kamari. Kamari iliharamishwa nchini Uingereza mwaka 1853. Lakini hata hivyo baada ya kupitishwa kwa sheria inayohusika, vituo 18 vya kamari vilijengwa kwa ajili ya watu wa hadhi za juu na maarufu. Kamari iliharamishwa nchini Marekani mwaka 1855, nchini Prussia ilipigwa marufuku mwaka 1854 na nchini Ujerumani ilipigwa marufuku mwaka 1882 na Uislamu uliiharamisha karne nyingi kabla ya nchi hizi zilizostaarabika. Hivi sasa kuna vituo vingi vikubwa vya kucheza kamari katika nchi za Amerika na Ulaya. Maelfu ya wacheza kamari hukusanyika huko kila siku kutoka mbali na karibu wakiwa na masanduku yaliyojaa pauni za kiingereza na dola, na kujiingiza kiwendawazimu katika uchezaji wa kamari.

91

12:44 PM

Page 91


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Gazeti moja liliandika yafuatayo juu ya Jiji la Las Vagas, ambalo ni kituo cha uchezaji wa kamari nchini Marekani: “Idadi kamili ya wacheza kamari wanaocheza kamari hapo haijulikani, lakini inazidi watu 40,000 katika masaa ishirini na nne. Katika nyumba hii ya kamari, sio mtu mmoja bali ni mamia ambao hupoteza madau yao. Hotel Sahara, ambayo ni moja ya hoteli kubwa katika Jiji hili ni jumba maalumu la kuchezea kamari kwa ajili ya mamilionea na kwa kila masaa 24 zaidi ya dola millioni kumi huwekwa madau katika kituo hiki peke yake. Mamia ya watu husimama kandokando ya mashine za umeme ziitwazo Sloti. Kila mara hudumbukiza sarafu kwenye mashine hizo kwa matarajio ya kupata mamia au maelfu machache ya dola, huvuta kishikio cha mashine hizo kwa nguvu zote. Hata hivyo, kwa vile udumbukizaji wa dola huwa hauleti matokeo yoyote, kazi hii inaendelea na dola zinaendelea kumiminika kwenye mashine hizo.” – (Yearly Review, 1962). Ni dhahiri kwamba faida kubwa zinazoongezeka kwa wamiliki wa vituo hivi (vya kuchezeshea kamari) pamoja na Serikali ndio jambo linalozuia kufungwa kwa vituo hivi vya ufisadi. Sababu ya sisi kuviita vituo hivi kuwa ni “vituo vya ufisadi” ni kwamba maovu mbalimbali hufanywa katika vituo hivi na uhalifu mkubwa kabisa hutendeka katika vituo hivyo. Mashirika ya habari na magazeti hutuonyesha kidogo uhalifu unaotendeka katika majumba haya ya kuchezea kamari: “Katika Jiji la Monte Carlo nchini Italia, raia mmoja wa Argentina alipoteza kiasi cha dola milioni nne ndani ya masaa kumi na tisa. Na milango ya majumba haya ya kamari yalipofungwa alikwenda moja kwa moja porini, akapasua kichwa chake na hivyo kuyamaliza maisha yake.” (The Magazine, Roshan Fikr, 1962).

92

12:44 PM

Page 92


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

“Shirika la Takwimu liitwalo “Gallop” limetangaza wakati lilipokuwa linachapisha takwimu, kwamba idadi ya vifo vya kujiua kutokana na kamari inaongezeka. Takwimu za shirika hilo zilionyesha kwamba ikilinganishwa na miaka ya nyuma, vifo vingi vya kujiua vilifanywa na wacheza kamari katika mwaka 1961 – (Weekly Ittila’at, Issue No. 1060). Moja ya Shirika la Takwimu la Marekani limehitimisha kwamba, kamari inahusika na 30% ya uhalifu. Daktari wa Kimerakani, baada ya kufanya utafiti kwa muda mrefu alihitimisha kuwa nchini Marekani peke yake zaidi ya watu 2000 hufa kila mwaka kutokana na kamari. Daktari huyu amethibitisha kwamba wakati wa kucheza kamari mioyo ya wacheza kamari hupiga haraka zaidi na mioyo ya wacheza kamari wazoefu hupiga zaidi ya mara 100 kwa dakika. Kutokana na kudunda huku kwa moyo kusiko kwa kawaida, wacheza kamari ama hufa katika meza za kuchezea kamari kutokana na moyo kushindwa kufanya kazi au huonekana wazee zaidi kwa miaka kumi hadi kumi na tano kuliko muda wa kawaida na hatimaye hufa.” – (The Magazine, Zohsan Fikr 1964). Moja ya uovu mwingine mkubwa wa kamari ambao una umuhimu sana kwa mtazamo wa kijamii na kisaikolojia ni uadui ambao hujijenga baina ya wahusika. Kucheza kamari huibua hisia za kuona kila jambo ni baya na kutaka kulipiza kisasi katika akili za watu, huvunja urafiki, upendo na uaminifu na huandaa mazingira ya kisasi na huamsha silika ya ghadhabu. Mwenyezi Mungu amesema:

“Shetani anataka kuchochea uadui na chuki miongoni mwenu kwa kutumia pombe na kamari na kuwazuieni kumkumbuka Mwenyezi 93

12:44 PM

Page 93


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Mungu na Sala.” – (Suratul Maidah, 5:91). Mwanasaikolojia mashuhuri amesema: “Katika mchezo wa kamari ya poka, sio lazima kwamba zile nia za uharibifu zibadili mwelekeo bali poka yenyewe imejengeka kakika mapambano. Katika mchezo huu kila mchezaji hujitahidi kwa kadri ya kanuni zinavyoruhusu kuwamiliki wenzake. Inawezekana akamdanganya mtu wa upande wa pili, au, kama inavyosemekana kwa kawaida, kumdanganya mwenzie kwa sababu lengo la mchezo wenyewe ni ama kumghilibu yule mwingine juu ya nguvu zake halisi au kuzionyesha nguvu hizo. Aina ya mchezo wa kamari iitwayo Chess pia ni uonyesheshaji wa mwelekeo wa mtu kusafisha silika zake mbaya. Tofauti ni kwamba katika mchezo huu kuna aina ya mwelekeo wa vita kati ya nchi mbili. Alipokuwa akifanya utafiti wa kisaikolojia kuhusiana na kamari ya Chess, Ernest Johnson anasema: “Ni ukweli unaokubalika kuwa kichocheo cha wale wanaocheza mchezo huo sio sura ya changamoto ya mchezo wa chesi tu ambayo ndio shughuli maalum ya michezo yote inayohusisha mapambano bali pia wana sababu mbaya na chafu zaidi ambayo ndio mwelekeo hasa wa ‘uuaji baba’ wa mchezo huu, kwa sababu lengo la mchezo huu ni kumnasa na kumshinda mpinzani wako. John Hess alijutia kuwahi kucheza mchezo wa chess alipokuwa gerezani kwa sababu aliamini kuwa kwa kufanya hivyo amezifunua hisia zake mbaya.” Kilichoelezwa hapo na mwanasaikolojia huyo ni upande mmoja wa shilingi na nukta nyingine ni kuwa kamari husababisha matatizo na uadui kutokana na hasara ya mali wanayoipata wacheza kamari. Ni dhahiri kwamba mali na akiba ya moja ya pande mbili inapomiminwa katika mfuko wa upande wa pili na mshindi huondoka na mali ya mwen94

12:44 PM

Page 94


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

zake kwa tabasamu la ushindi, mbegu ya uadui hupandwa katika moyo wa yule aliyeshindwa na hatimaye auadui huu huonyesha dalili za kisirani wakati unaofaa na sahihi. Hili ni jambo la kawaida. Ni vipi mpinzani asijenge kinyongo katika moyo wake anapouona utajiri wake alioupata kwa taabu sana ukiwa mikononi mwa mtu mwingine? Hivyo huyu aliyepoteza hawezi kumhurumia hasimu wake kwa vyovyote. Mwelekeo mwingine wa jambo hili ambao ni muhimu zaidi kuliko mwingine ni suala la kushindwa. Kama matokeo ya kushindwa katika mchezo, mcheza kamari hukabiliwa na wasiwasi mkali wa kisaikolojia na ili kufidia kushindwa kwake, hutelekeza usingizi na mapumziko, huiacha kazi yake na biashara na huendelea kucheza, akitaraji kuwa hatimaye atamshinda hasimu wake na hivyo kutuliza wasiwasi wake wa akili. Gazeti moja lenye usambazaji mpana liliandika kuwa: “Katika moja ya miji mcheza kamari alimshambulia hasimu wake kwa kisu na kumuua. Alipokuwa anahojiwa alisema: “Marehemu alishinda kiasi kikubwa cha fedha kutoka kwangu na hakuwa tayari kuendelea kucheza tena. Licha ya kuhimiza sana kuwa tuendelee kucheza, alikataa kuendeleza mchezo huo na akakimbia. Na mimi pia nikamfuatilia na.............� Hata kama mchezo ungeendelea na yule mcheza kamari, ambaye tayari alikuwa ameshapoteza, akipoteza kwa mara nyingine tena hataacha kucheza, na akiwa na matumaini ya kushinda haiweka dau mali yake tu bali hata heshima yake binafsi pia. Kabla ya kuja kwa Uislamu, watu wa Zama za Giza la Ujinga pia walikuwa pia wakicheza michezo mbalimbali ya kamari. Mwanzoni wachezaji walikuwa wakiweka dau mali na akiba zao na baadaye nyumba zao na vitu vingine. Na mcheza kamari alipopoteza utajiri na mali yake yote, alimuweka dau mke wake pia na hata kama alimpoteza mke wake huyo alimkabidhi kwa hasimu wake kwa kumtelekeza kusiko na aibu. 95

12:44 PM

Page 95


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Imam Ja’far Sadiq anasema: “Waqureishi walikuwa wakiweka mali na wake zao madau na kuwachezea kamari. Mwenyezi Mungu alipiga marufuku mila hii ya kuchukiza na aliwaonya watu dhidi ya kamari.” – (Biharul Anwar, Juz. 11). Pengine watu wengi wanaweza kushangaa kwamba inawezekanaje mtu akawa dhalili kiasi cha kuichezea kamari heshima yake! Lakini tukitizama matukio yanayotokea katika ulimwengu wa sasa uliostaarabika kila uchao, tunaona kwamba inawezekana kwamba kama matokeo ya kubobea katika kamari mtu yeyote anaweza kukumbana na hali hiyo. Hapa tunaelekeza fikra za wasomaji wetu katika ripoti ifuatayo: “Ricardo Lamos, mmoja wa wanabendi wa Jazz Orchestra ya Televisheni ya Mexico, ambaye alikuwa ni mpenzi sana wa mchezo wa kamari ya ‘poker’ aliandaa tafrija ya kamari nyumbani kwake usiku wa jana. Baada ya kupoteza kila kitu aliamua kukiweka dau kitu kimoja tu alichokuwa amebaki nacho ili aweze kuendelea na mchezo. Kitu hicho kilikuwa ni mke wake. Kwa bahati mbaya alimpoteza mke wake pia. Yule mwanamke alikataa kwenda kwa huyo hasimu wa mumewe. Licha ya kusisitiza sana, yule mwanamke alikataa kujitoa kwa huyo mshindi. Mume alimpiga sana mkewe mpaka akazimia. Hivi sasa mwanamke huyo mwenye bahati mbaya amelazwa kitandani hospitalini na hakuna matumaini kwamba atapona.” – (Mexico, French News Agency, 25th November). Kitendo kinayomsukumiza mtu kwenye tabia mbaya kama hiyo na ambacho kinakuwa sababu ya maafa makubwa kiasi hiki bila shaka kitakatazwa kwa mtazamo wa hoja za kimatiki. Uislamu ambao ni dini iliyojengwa juu ya busara, hekima na mantiki, ulitangaza kwa kulingana na Qur’ani na hadithi za Mtume na Ahlul-Bayt (Kizazi kiteulie cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)), kuharamisha kwa waislamu michezo yote ya kamari miaka zaidi ya 1400 iliyopita na mbali na mchezo wenyewe Uislamu pia umeharamisha utengenezaji, uuzaji na 96

12:44 PM

Page 96


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

ununuaji wa zana za kuchezea kamari. Uislamu pia umetangaza kuwa ni haramu kutumia kipato kilichotokana na kamari na umewaonya Waislamu dhidi ya kutumia kipato kilichotokana na kamari. Imam Riza amesema: “Mwenyezi Mungu ameharamisha aina zote za kamari na amewaamrisha watu kujiepusha nayo. Mwenyezi Mungu ameiita kamari kuwa ni uchafu na kazi ya shetani na akawaonya watu dhidi ya kujihusisha nayo kama vile sataranji Backgammons na aina nyingine za kamari. Na mchezo wa Backgammons ni mbaya zaidi kuliko sataranji.” – (Mustadrakul-Wasa’il, Juz. 2). Imam Baqir amesema: “Wakati aya ya: Enyi mliomamini, ulevi kamari, na madhabahu za mawe na ramli za mishale (ambavyo wapagani wanavishirikisha na sifa fulani takatifu) ni matendo haramu yanayohusiana na matendo ya shetani ilipashushwa, watu walimuuliza Mtume: “Maisir ni kitu gani (ambacho Mwenyezi Mungu amekiita ni uchafu na kazi ya shetani)?” Mtume alijibu kuwa: “Ni chochote ambacho kwacho mtu anaweza kuchezea kamari, inajumuisha pia dadu za mifupa na walnuts.” – (Tafsirul-Mizan, Juz. 6, uk. 144). Mwanasaikolojia mashuhuri K. Platonev amesema: “Katika nyumba za mapumziko za Urusi uchezaji wa kamari na karata zinzazohusisha kupata na kupoteza hauruhusiwi kabisa...... uchezaji wa karata ulianzishwa nchini Urusi mwaka 1646 na kampeni dhidi ya mchezo huo ilianza mwaka huo huo.” Ulafi na mwelekeo wa mcheza kamari juu ya kushinda humshawishi kuendelea kucheza na hatimaye hudhoofisha akili na busara zake. Mifano ya shauku na wasiwasi kama huo unaweza kuonekana katika aina nyingine za kamari. Kwa mfano nchini Urusi kuna mchezo maalumu ambao huchezwa na watoto. Katika mchezo huu watoto hupiga kofi mkono wa mtoto mwingine kwa matokeo ya sehemu ya nyuma ya mikono kuuma na kuvimba kwa kupigwa huko na watoto hawa wanazama katika mchezo huo kiasi 97

12:44 PM

Page 97


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

cha kutobaini madhara wanayoyapata katika mchezo wa namna hii. Halikadhalika mcheza kamari ambaye huwa mwathirika wa matakwa na tamaa zake huwa hajali ni thamani gani ya utu wake na nguvu kiasi gani inapungua na ni kiasi gani amepoteza udhibiti wa neva na utulivu wake.” (K. Plotonev, Psychology, uk. 227). Imam Baqir amesema: “Uharamu wa kamari unajumuisha michezo ya sataranji na Back Gammons – (Tafsiri Majma’ul-Bayan, Juz. 3) Chini ya uhifadhi wa mafundisho matukufu ya Uislamu, jamii ya Kiislamu ilijiepusha na laana hii ya hatari. Lakini kwa bahati mbaya, wakoloni na maadui wa Uislamu waliianzisha tena kwa kiasi fulani miongoni mwa watu wajinga na uchezaji kamari umejipenyeza tena katika baadhi ya nyumba. Kamari ilikuja kuwepo hususan katika hii jamii inayojiita ya kisasa na watu wamejiingiza katika biashara hii inayochukiza na haramu kwa kuwaiga wazungu tu na ili waonekane na wenzao kuwa wamestaarabika na kuwa ni watu wa kisasa licha ya ukweli kwamba wanaziona hasara lukuki wanazozipata wacheza kamari wa Ulaya na Marekani, na uhalifu mkubwa, kujeruhiana, wizi, matukio ya kujiua na maovu mengine yanayotokana na kamari. Miaka kadhaa iliyopita kuna habari ilichapishwa kwenye magezeti ambayo inaweza kuwa ni fundisho kwa wale wacheza kamari sugu. Maelezo ya habari hizo ambayo yaliandikwa kwa kichwa cha habari: “Mfalme wa Wacheza kamari ajiua:” Milionea mashuhuri wa Ujerumani na mfalme wa wacheza kamari wa nchi hii alijiua ndani ya wiki hii baada ya kuingia deni la Mark milioni kumi (Mark ni fedha za Ujerumani) katika makasino. Milionea huyu ambaye jina lake lilikuwa Ralph Lodar aliwahi kusema miaka ya nyuma huko alipokuwa sio tajiri: “Kaeni mkijua. Kipato changu kikiwa chini ya Mark elfu kumi kwa mwezi nitajiua.” Hivi karibuni mambo yalimwendea vibaya na hivyo akajiua. 98

12:44 PM

Page 98


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Ralph Lodar hakuwa na utajiri wowote nchini Ujerumani mpaka baada ya Vita. Lakini baada ya vita aliingia katika biashara na alipata utajiri ndani ya muda mfupi na kutokana na ustadi wake katika biashara akatengeneza faida ya mpaka Mark Milioni kumi kwa mauzo ya mara moja. Aliwekeza fedha hizi katika soko la hisa na huko fedha zake zilizaa zaidi. Lodar alikuwa na wazimu wa kupenda kamari, hasa mchezo wa kamari uitwao ‘roulette’ na kila usiku alikuwa akienda kucheza kamari hiyo katika makasino maarufu ya dunia. Cha ajabu ni kwamba alikuwa akishinda katika kamari hiyo ya roulette na kwa mujibu wa mmoja wa watu wake wa karibu alipata sehemu kubwa ya utajiri wake kutokana na kamari, na hususan kutoka katika mchezo wa Roulette. Pia alikuwa akishinda viwango vikubwa ambavyo wakati wote vilizidi ya Mark laki moja. Kwa sababu hii hasa alipewa jina la “Mfalme wa Wacheza Kamari” katika makasino. Meza yoyote aliyokwenda katika makasino, mmiliki wa kasino alikuwa akihesabu vibao (chips) vyake kwani alikuwa akijua kwamba angepoteza kiasi kikubwa cha fedha. Hadi miaka mwili iliyopita alikuwa amepoteza michezo minne tu katika kipindi chake chote cha kucheza kamari na jumla ya kiasi chote alichopoteza hakikuzidi Mark milioni tano. Hata hivyo katika miaka miwili iliyopita bahati yake ilimgeuka vibaya na akaanza kupoteza mara kwa mara.

Loday alipata faida kubwa katika shughuli zake kwenye soko la hisa lakini usiku alikuwa akipoteza mara mbili au mara tatu ya kiasi alichopata, katika kamari. Alipodhani kuwa katika makasino ya Ujerumani mambo yamemgeukia aliamua kuhamia Monte Carlo. Lakini huko pia alipoteza takriban kiasi cha Mark milioni nane. Pole pole Lodar alipoteza furaha na nguvu zake na kwa kuwa hakuwa na furaha na mwenye wasiwasi kutokana na alichopoteza usiku, hakuweza 99

12:44 PM

Page 99


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

kufanya kazi vizuri vilevile katika soko la hisa wakati wa mchana. Kwa sababu hiyo kipato chake kilipungua na pole pole aliendelea kupoteza kidogo kidogo utajiri wake huo mkubwa. Hadi kufikia mwezi mmoja uliopita, alikuwa amebakiwa na nyumba chache tu za fahari katika utajiri wake. Hizi nyumba pia aliziuza na akawaambia rafiki zake, “Kwa fedha hizi nilizopata kutokana na kuuza nyumba, nitaweza kurejesha utajiri niliopoteza.” Kwanza Lodar alikwenda katika kasino maarufu iliyokuwa karibu na mji wa Hamburg na kisha akaenda Monte Carlo. Hata hivyo, alipoteza katika maeneo yote haya mawili na akabakia hana kitu alichobaki nacho. Mbali na kupoteza kila kitu, aliingia deni la Mark millioni kumi. Ni kutokana na mazingira haya kwamba wiki iliyopita alikwenda katika nyumba yake ndogo iliyopo Cologne na akanywa kifuko cha vidonge vya usingizi kwa lengo la kujiua. Mwili wake ulipatikana kutoka katika nyumba yake masaa ishirini na nne baada ya kifo chake – (Weekly Ittila’at, Toleo no. 1521, Bahman, 1349). Iliripotiwa katika gazeti moja la Iran: “Baada ya kupoteza Tuman 460,000 katika kasino. Kijana mmoja alijiua” – (Firdosi Magazine, Toleo no. 998, 5th Bahman, 1349). Hii ni mifano ya baadhi ya maafa wanayoyapata wacheza kamari ambao baada ya kumenyeka katika maisha yao yote na kupata utajiri kwa mamillioni hupoteza afya na utulivu wao wa akili na kuwa mafukara na kukanganyikiwa wasijue la kufanya ili kujinasua katika balaa walilojitakia na hivyo huamua kukatisha maisha yao kwa kujiua wenyewe. Inawezekana kwamba baadhi ya watu wanaweza kufikiri kwamba uhalifu unatokana na kamari upo nchi za Magharibi na kwa Mamilionea tu. Lakini magazeti yetu ambayo huripoti matukio ya kutisha yanayokana na kamari, yanatuambia kuwa popote pale kamari inapopata njia, hutembea na uadui 100

12:44 PM

Page 100


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

pia na yeyote anayecheza kamari ni lazima asubiri mwisho wake wa maafa. Taarifa ifuatayo ilichapishwa katika gazeti moja la huko Iran miaka kadhaa iliyopita: “Mtu aliyekuwa amemuua hasimu wake kwa kumpiga risasi kama matokeo ya kamari alihukumiwa kifungo cha maisha jela. Mahakama Kuu pia ilikataa ombi la mshitakiwa la kusikilizwa upya kwa kesi hiyo na ikaamua kuwa alistahili adhabu hiyo. Mtu aliyehukumiwa adhabu hii ana umri wa miaka 49 na alifanya uhalifu huo mwaka jana. “Alasiri ya siku hiyo ambapo mauaji haya yalifanyika mhalifu pamoja na watu wengine walikunywa pombe katika kilabu moja. Kisha waliondoka sehemu hiyo na kwenda kukaa sehemu fulani wakacheza kamari. Ilipofika saa tatu usiku walianza kuzozana walipokuwa wanacheza kamari. Muuaji alimpiga mwenzake risasi kifuani na kumuua. Kutokana na uchunguzi uliofanywa katika kesi hii, mahakama ilimpata na hatia ya mauaji na mwendesha mashitaka wa Serikali alitaka muuaji apewe adhabu ya kifo. Faili lilipelekwa kwenye Mahakama Kuu ya Sheria huko Tehran na majaji wakiipunguza adhabu hiyo kwa digrii moja, wakamhukumu muuaji kutumikia kifungo cha maisha gerezani – (Kayhan Daily News Paper, Toleo No. 8266). Litafakari kwa makini tukio hilo hapo juu. Familia mbili zilipoteza walezi wao. Mmoja aliuawa na mwingine alifungwa kifungo cha maisha. Na kwa nini yote haya yalitokea? Kwa sababu ya pombe na kamari! Je si jambo linalofaa zaidi kwetu kwamba tuinamishe vichwa vyetu kwa unyenyekevu mbele ya mtunga sheria kwa Uislamu ambaye karne kumi na nne zilizopita alisema:

101

12:44 PM

Page 101


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

“Shetani anataka kuchochea uadui na chuki baina yenu kwa kupitia pombe na kamari na (anataka) kuwazuieni kumkumbuka Mwenyezi Mungu na Sala.” – (Suratul Maidah, 5:91). Imam Riza amesema: Acheni kucheza kamari kwa ‘Khawatim’ na ‘Arba’h Ashar’ (zana za kuchezea kamari za wakati huo) na zana nyinginezo hata kucheza kamari na walnuts, lozi na dadu za mifupa ambazo watoto hucheza nazo michezo ya kubahatisha.” – (Mustadrakul Wasa’il, Juz. 2, uk. 59). Ni muhimu kwamba tueleze hapa hukumu za Uislamu juu ya aina mbalimbali za kamari katika namna rahisi kueleweka ili kusibaki utata. Qur’ani Tukufu imetamka uharamu wa kamari katika maelezo fasaha yanayoungwa mkono na uwazaji wa kimantiki. Qur’ani pia inagusia juu ya faida na maovu yanayotokana na kamari na ikielezea kuunga mkono uharmishaji wa kamari kwa kuelezea kwamba hasara zake ni kubwa kuliko faida. Kwa vile watu wengi wanajiingiza katika uchezaji wa kamari kama burudani na kujifurahisha au ili wapate fedha, Qur’ani tukufu inakumbushia juu ya kuwepo hizi faida ndogo ndogo lakini inatamka kwamba maovu yatokanayo na kamari ni makubwa zaidi. Mwishoni mwa maelezo hayo inatutaka tutumie akili zetu ili tuweze kutoa uamuzi juu ya jambo hili. Sio busara kabisa kwamba tufanye mambo yenye hatari ya hasara kubwa kwa faida ndogo za kutarajiwa. Na wale wanaocheza kamari kwa ajili ya manufaa lazima wakumbuke kwamba hasara za kifedha, kijamii, kiakili na kimaadili zinazofungamana na kamari ni kubwa na mbaya sana kuliko 102

12:44 PM

Page 102


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

faida ambazo zinaweza kupatikana. Katika baadhi ya aya za Qur’ani, kamari imetajwa kuwa ni kazi ya mikono ya shetani na ni njia ya upotofu na Waislamu wametakiwa kujiepusha nayo. Katika aya nyingine kamari imetajwa kuwa ni jambo linalosababisha chuki na uadui kati ya watu, huamsha hisia za kulipiza kisasi, huwahusisha katika upotevu wa maadili na huwazuia watu kupata ubora wa kiroho pamoja na kudumisha mawasiliano na Mwenyezi Mungu – (tazama Qur’ani, Suratul-Maidah, 5:90-91). Katika sheria za Kiislamu, kamari inamaanisha ile michezo yote ya bahati nasibu ambayo vifaa maalumu hutumika kwa lengo la kushinda au kupoteza katika namna hii ambayo hukubaliwa kuwa atakayepoteza atapataswa kulipa kiasi fulani cha fedha au kitu kingine kwa mshindi. Aina hii ya kamari imeharamishwa katika Uislamu na mafakihi wote wameutambua uharamu wake kwamba uwe ni sehemu muhimu ya imani za Kiislamu – (Misbahul Faqaha). Aina nyingine ya kamari ni ile ya mchezo wa kubahatisha unaochezwa kwa kutumia vifaa maalumu (kama vile karata au sataranji) kwa ajili ya burudani lakini bila ya kuwepo sharti la kulipa au kulipwa chochote mtu akishinda au kushindwa. Kwa mujibu wa fatwa za mafakihi wa Kishia kwa ujumla, aina hii ya kamari pia ni haramu – (Jami’ul Maqasid; Tadhkira-i Allama). Aina ya tau ya kamari ni ile ambayo hiyo inaweza ikachezwa bila vifaa maalumu lakini kwa kuwepo sharti la kulipa na kulipwa iwapo mmoja wao atashindwa au kushinda. Kwa mujibu wa fatwa mashuhuri za Kishia, michezo kama hii pia ni haramu. Nukta nyingine ambayo inapswa kuzingatiwa ni kuwa kamari imeharamishwa katika Uislamu kwa vigezo viwili. Kwanza kwa sababu kamari yenyewe ni haramu na dhambi katika Uislamu. Na pili kwa sababu fedha inayopatikana katika kamari ni haramu pia. Kwa maneno mengine ni 103

12:44 PM

Page 103


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

kuwa mchezaji aliyeshinda hawi mmiliki wa fedha hiyo kwa mujibu wa sheria za Kiislamu. Hivyo hana haki ya kuzimiliki na anapaswa kuzirejesha kwa mwenyewe.

KAMPENI KABAMBE NA YA MSINGI DHIDI YA KAMARI Ili kuling’oa kabisa balaa hili, Uislamu haukuridhika na uharamishaji wake tu bali pia umekataza utengenezaji, uuzaji na ununuaji wa vifaa vya kuchezea kamari. Baadhi ya watu wanaweza kuuliza kuwa kwanini sataranji na michezo mingine kama hiyo ambayo haina masharti ya kuweka hisa za fedha kwa mwenye kushinda au kushindwa iwe haramu, ambapo michezo hii siku hizi hucheza kama kiburudisho cha akili na imeenea sana mashuleni na vyuoni? Jibu la swali ni kuwa bado haijathibitika kuwa michezo hiyo haina madhara. Kwa upande mwingine maoni kutoka kwa wanasaikolojia yaliyonukuliwa kwenye kurasa zilizopita yanaoonyesha kuwa michezo ina athari mbaya. Bila shaka, kuendesha kampeni kabambe ya namna hii inahitajika ili kuing’oa kabisa uovu kama huu, kwa sababu welekevu na vyombo vya kamari vinatengenezwa na kununuliwa na kuuzwa kwa uhuru kabisa, na kuviweka na kuvitunza kunaruhusiwa, watu wataanza kwa namna ya burudani na starehe na kitendo hicho hicho kitakuja kuandaa misingi ya kuenea kwa maovu haya. Kwa njia hii Uislamu umeng’oa fitna na udhalimu kabisa kwa kuharamisha aina zote za kamari na vyombo vyake na wale watu wanaoamini Uislam kwa dhati hawajishughulishi katika kitendo hiki ambacho ni moja ya yale madhambi makubwa kabisa. 104

12:44 PM

Page 104


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Hapana shaka kwamba kampeni kabambe ya aina hii inahitajika ili kuung’oa uovu huu kwa sababu ikiwa vifaa vya kuchezea kamari vitatengenezwa kuuzwa, kununuliwa na kuhifadhiwa bila vizuizi basi ni wazi kwamba watu wataanza kuvitumia kama burudani tu lakini huu utakuwa ndio mwanzo wa mizizi ya uovu kwani baadaye malipo yanaweza. Kwa njia hii, Uislamu umeng’oa mizizi ya uharibifu na ufisadi kwa kuharamisha aina zote za kamari pamoja na vifaa vyake kwa watu wote wanaoamini kwa dhati juu ya Uislamu na Waislamu wa dhati kamwe hawajihusishi ni kitendo hiki kiovu ambacho ni moja ya madhambi makubwa. Imam Ja’far Sadiq anasema: “Ni dhambi kumsalimia mcheza kamari na anayekaa kwenye zulia la kamari kama mtazamaji, na anayemuangalia mcheza kamari usoni wana madhambi sawa na anayemkaribisha mcheza kamari, na mkusanyiko wa wacheza kamari ni mkusanyiko unaostahili ghadhabu na adhabu ya Mwenyezi Mungu na ambayo wanapaswa kuitarajia adhabu hiyo muda wowote.” – (Jawahir, Mlango wa Biashara). Imam Musa al-Kadhim alizungumza kwa ufasaha kabisa dhidi ya ucheza kamari na sataranji. Mtu mmoja wa Basra alimwambia Imam: Mimi huwa ninakaa sehemu wacheza kamari wanapochezea, hata hivyo mimi huwa sichezi, huwa ni mtazamaji tu.” Mtukufu Imam Ali (a.s.)mjibu: “Unakaa kufanya nini katika mkusanyiko ambao hauna baraka za Mwenyezi Mungu?” Imam Ja’far Sadiq anasema: “Ni haramu kuuza vifaa vya kuchezea sataranji na kutumia mapato yake ni ukosa imani, kuvihifadhi ni ushirikina, kuvichezea na kumsalimia mcheza kamari ni dhambi na kumfundisha mtu mwingine kucheza sataranji ni dhambi kubwa.” – (Wasa’ilush Shi’ah). Hadithi zilizonukuliwa hapo juu ni mfano mdogo tu wa hadithi nyingi 105

12:44 PM

Page 105


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

zinazohusiana na kamari zilizotufikia kupitia kwa kizazi kiteule cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Watu waliofanya utafiti na kulitathmini suala hili kwa usahihi wanafahamu vyema maovu mengine ya kamari na mikasa wanayopata wacheza kamari kutokana na kamari. Washairi wa lugha mbalimbali pia wamegusia kwenye uovu wa kamari katika vitabu vyao. Wakati fulani nuksi ya kuiga huwa ni sababu ya kutokea kwa maovu kama vile kamari na kama tunavyoona siku hizi baadhi ya watu wamenasa katika balaa hili kwa kuigiza tu magharibi ambapo watu wenye busara wa magharibi wanakerwa na hali iliyopo katika jamii yao. Watu hawa wasio na bahati wamejiingiza kwenye kucheza kamari ili tu wasiachwe nyuma ya msafara wa ustaraabu kwa kufuata nyayo za wacheza kamari wa nchi za Magharibi. Hawa ni watu ambao hawajajiandaa na hawako tayari kuwaiga watu wa nchi za Magharibi katika medani za sayansi na teknolojia na viwanda na hivyo hawachukui hatua yoyote katika welekeo wa ustawi, lakini wao wanataka waonekane kama wamagharibi kwa kuiga uovu wao kwa upofu tu! Huko nyuma ni wanaume tu waliokuwa wakiteseka na maradhi haya ya hatari (ya kamari) ambao walikuwa wakikesha usiku kucha wakicheza kamari wakiwa katika hali ya welewa na shauku na kurudi nyumbani asubuhi wakiwa wamechoka kabisa. Lakini kwa bahati mbaya maovu haya yameshawanasa pia hata wanawake waulimwengu wa leo waliostaarabika. Inaweza kusemwa kwamba huu pia ni udhihirisho wa maendeleo ya wanawake na ili kuthibitsha madai yao ya ubora na usawa na wanaume, wanataka kuwa sawa na wanaume hata katika meza za kamari lakini hapana shaka yeyote kwamba wapo katika njia potofu. Hapa tutataja kwa kifupi nuksi za kamari: 106

12:44 PM

Page 106


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

• Kamari ni sababu ya maradhi ya mfumo wa neva, matatizo ya uyeyushaji wa chakula na matatizo ya akili. • Kamari huwa sababu ya uhusiano wa kulazimisha na kuvunja urafiki na kuishia kwenye uadui • Kamari husababisha upotevu wa mali na hivyo husababisha umaskini na ufukura. • Kamari husababisha kuvunjika kwa familia na dhiki katika maisha binafsi ya watu. Huwazuia kushughulikia masuala yao binafsi, elimu na mafunzo ya watoto na mambo mengine yenye manufaa. • Kamari huwasukumia watu katika maangamizi na huwafanya wajiue. • Kamari huchafua heshima na hadhi ya watu na kuhatarisha nafasi yao ya kijamii. • Kamari huifanya miili ya wacheza kamari kuwa dhaifu na yenye maradhi. • Kamari huharibu imani na kujiamini kwa watu na hii huwa ni sababu ya kustahiki ghadhabu za Mwenyezi Mungu. Kwa kifupi kamari huharibu matarajio ya ulimwengu huu na kesho Akhera, mwili na roho, heshima na mali na kila kitu ambacho ni mali ya mhusika. Sasa ni jukumu la kila mtu kujizuia yeye na familia yake kutokana na nuksi hii na kukwepa kushirikiana na wacheza kamari, na kuhudhuria tafrija zinazochezwa kamari na kila kitu kinachoweza kuwa sababu ya kuhusika katika balaa la hii biashara chafu.

107

12:44 PM

Page 107


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Kwa kusema kweli shetani wa kamari anapaswa kuchukuliwa kama ugonjwa wa kuambukiza hivyo ianzishwe kampeni kabambe dhidi ya kamari ifanyike (ambayo inapaswa kwa kweli iwe ya maana na ya hikma). Magonjwa ya hatari (kama kipindupindu na ugonjwa wa tauni) unapoelekea kuenea katika nchi, mashirika ya afya, ili kupambana nao, huwajulisha watu wote juu ya hatari zake, hupendekeza hatua za kuzuia maradhi haya na husambaza vifaa kwa ajili ya chanjo. Ikilazimu huweka karantini na kutoa chanjo na kuwazuia watu kuchanganyika na watu wanaoumwa maradhi haya. Wakati mwingine nguo za mgonjwa huchomwa moto. Wakati mwingine eneo lililoathirika huchomwa moto baada ya kuwahamisha wagonjwa. Wagonjwa hutengwa na familia zao. Hawaruhusiwi kukutana na watu (hususan watoto na vijana) na hupewa msaada wa bure wa vitu kadhaa kwa matumizi yao binafsi. Hivyo ni muhimu kwamba katika suala hili la kamari, hatua za msingi kama hizo pia zinapaswa kuchukuliwa. Watu wanapaswa kujulishwa juu ya nuksi na hatari za kamari na wanapaswa kufafanuliwa juu ya maovu yake. Vituo vya kuchezea kamari vinapaswa kufungwa. Wacheza kamari wanapaswa kuajiriwa katika kazi zenye manufaa. Vijana wanapaswa kupewa shughuli zenye manufaa katika muda wasiokuwa na kazi. Ushirikiano wa wacheza kamari na watu wengine (hasa vijana) unapaswa kupigwa marufuku na hatua madhubuti zinapaswa kuchukuliwa na madaktari wa magonjwa ya akili ili kuwabadilisha watu hawa ambao wameshakuwa walevi sugu wa kamari, na pia linaweza kufanywa na viongozi wa kidini ili kwa rehema za Mwenyezi Mungu, uovu huu wa hatari uondolewe katika jamii ya Waislamu.

NUKUU 1).

Shetani anataka kuchochea uadui na chuki baina yenu kwa kupitia pombe na kamari na kuwazuieni kumkumbuka Mwenyezi Mungu na Sala - (Qur’ani Tukufu).

108

12:44 PM

Page 108


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

2). Ni dhambi kumsalimia mcheza kamari na yule anayewaangalia wacheza kamari kama mtazamaji au yule anayemtakia kheri mcheza kamari, wote ni watenda madhambi sawasawa. Kwani mkusanyiko ulioundwa kwa lengo la kucheza kamari ni moja ya mikusanyiko inayostahili ghadhabu za Mwenyezi Mungu ambayo inaweza kutazamiwa muda wowote. – (Imam Ja’far Sadiq). 3). Mwenyezi Mungu ameharamisha aina zote za kamari na amewaamrisha watu kujiepusha nayo. Mwenyezi Mungu ameitangaza kamari kuwa ni uchafu na kazi ya shetani na akawaonya watu kutojihusisha nayo. – (Imam Ali (a.s.) Ridha).

UONGO Mwanaadamu amejaaliwa katika asili yake uaminifu na haki na Mwenyezi Mungu. Mwanaadamu akiihifadhi tabia yake ya asili yake na ushawishi wa nje, na mambo yasipompotosha kutoka kwenye njia ya maumbile, basi mwanaadamu mara zote ataelekea katika uchamungu na sifa bora na ataepukana na uovu na ufisadi. Kwa asili, mwanaadamu ni mkweli, mwaminifu, jasiri na mtukufu. Hata hivyo mambo mbalimbali kama vile mafunzo, mazingira n.k. huzuia kujitokeza kwa sifa hizi na hata kuzibadilisha na sifa chafu na duni. Moja ya wajibu muhimu wa Mitume ni kusaidia asili ya mwanaadamu dhidi ya mambo ya nje ili kwa kutumia mafundisho yao matukufu wazisaidia hisi za asili na kuziwekea mazingira ya kutwaa sifa bora za kibinadamu. Uongo unapingana na asili ya mwanaadamu na humsukuma mwanaadamu kutoka katika haki na uaminifu kwenda katika uovu na uharibufu na uongo pia husambaa kama ugonjwa wa kuambukiza kutoka kwa baba kwenda kwa mtoto, kutoka kwa mwalimu kwenda kwa mwanafunzi na kutoka kwa mteja kwenda kwa muuzaji na hili huifanya ile tabia yao ipotoke kutoka 109

12:44 PM

Page 109


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

kwenye maumbile yake ya asili. Pengine watu walio wengi wanauchukulia uongo kuwa sio jambo kubwa sana ingawa hasara zinazotokana na uongo ni kubwa sana ikilinganishwa na hasara zinazotokana na madhambi mengine na maangamizi yanayoikabili jamii kutokana na uongo ni makubwa kuliko tunavyoweza tukafikiri. Mara nyingi imetokea kwamba mtu mlaghai, ili ayafikie malengo yake maovu ametoa madai ya uongo ya utume na kwa uongo wake mmoja huo amewatoa maelfu watu kutoka katika njia iliyonyooka na kuwapeleka kwenye upotovu na maafa makubwa au tapeli mwingine amedai kuwa ‘Bab’ au ‘qutb’ n.k. na idadi kubwa ya watu imepotoshwa kutokana na madai yao ya Utukufu wa uongo. Ni kwa dhambi gani nyingine madhambi haya makubwa yanaweza kulinganishwa nayo, na kwa hasara za dhambi gani ambazo hasara zilizosbabishwa na uongo zinaweza kuamuliwa kwazo? Ni kwa sababu hii kwamba Uislamu umeuchukulia uongo kuwa ni tabia ya watu wasiokuwa na imani, na Qur’ani tukufu imelieleza hili bayana:

“Wale wasioamini katika miujiza ya Mwenyezi Mungu wanabuni uongo nao ni waongo.” – (Suratul Nahl, 16:105). Imam Ali (a.s.) ameuchukulia uongo kuwa ni laana mbaya kuliko zote na amesema: “Uongo ni kitendo cha aibu kuliko vyote.” – (Amali Saduq). Imam Muhammad Baqir ameuchukulia uongo kuwa ni mharibifu wa miziz ya imani na amesema: “Uongo ni chanzo cha maangamizi ya imani – (alKafi, Juz. 2).

110

12:44 PM

Page 110


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Imam Ali (a.s.) anachukulia kwamba kuuelewa uhalisia wa imani unahusiana na kuachana na aina mbalimbali za uongo. Amesema: “Si katika hali yoyote ile ambapo mtu anaweza kuuelewa uhalisia wa imani ikiwa mtu huyo hataacha kusema uongo, uwe ni uongo wa dhati au wa mzaha.” – (Mahaasin Barqi). Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliulizwa: “Je inawezekana muumini wa kweli akawa muoga?” Alijibu, “Ndiyo.” Kisha akaulizwa: “Je anaweza kuwa bahili?” Alijibu “Ndiyo” Kisha aliulizwa je, anaweza kuwa mwongo? Akajibu “Hapana” – (Wasa’ilush-Shi’ah). Katika hadithi nyingine Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesimuliwa kuwahi kusema: “Kauli mbaya zaidi na ya aibu zaidi ni kauli ya uongo. – (BiharulAnwar, Juz. 72, uk. 659). Imam Ali (a.s.) amesema: “Tabia ya kusema uongo ni chanzo cha ufukara na mashaka.” (Khisal Saduq). Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Ngojeni niwaambieni juu ya madhambi makubwa zaidi. Yanajumuisha pamoja na: Kumshirikisha Mwenyezi Mungu na yoyote yule, kuwaudhi na kuonyesha tabia mbaya kwa wazazi na kusema uongo.” – (Makaasib, Sheikh Ansani, uk. 50). Mwanasaikolojia mashuhuri anasema: “Kutoka miongoni mwa tabia mbovu na sifa zinazochukiza zaidi, uongo ndio kitu dhalili na kinachochukiza zaidi. Tabia hii chafu ama huchukua mizizi kwenye mmomonyoko wa maadili au ufisadi au ni matokeo ya maadili duni na woga. Inashangaza sana kwamba watu walio wengi wanautazama uongo kwa kutohusika na bila kujali na mara nyingi huwaelekeza watumishi na wakala wao kusema uongo. Bila shaka baadaye wakibaini kuwa wafanyakazi wao wanawaongopea hata wao wenyewe pia wasishangazwe na wasiudhike.” – (Morals, Samuel Smiles, uk. 281).

111

12:44 PM

Page 111


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Imam Hasan Askari ameuchukulia uongo kuwa ni ufunguo wa maovu yote na ufisadi. Amesema: “Maovu na madhambi yote yanapovamia nyumba sababu yake kuu ni uongo.” (Mustadrakul Wasa’il, Juz. 2). Hii ni kusema kwamba uongo huandaa mazingira ya uovu wote. Katika Uislamu, Waislamu mbali na kukatazwa kabisa kusema uongo pia wamekatazwa kuambatana na waongo. Imam Ali (a.s.) alimuusia mwanaye, Imam Hasan kuwa: “Mwanagu! Jiepushe kufanya urafiki na mtu mpumbavu kwa sababu hata akitaka kukufanyia wema, na bado kwa vile hawezi kutofautisha kati ya kitu kizuri na kibaya, hivyo atakudhuru. Jiepushe na bahili kwa sababu kutokana na ubahili wake atakunyima kitu utakachokuwa unakihitaji mno. Usifanye urafiki na fisadi na mtu fidhuli kwa sababu hatasita kukuuza kwa bei ndogo kabisa. Na jiepushe kufanya urafiki na muongo asiyeonyeka kwa sababu yeye ni kama magazigazi ambayo hukuonyesha vitu vilivyo mbali kuwa viko karibu na vilivyo karibu kuwa viko mbali. Kwa kauli zake za uongo huifanya kazi rahisi kuwa ngumu na kazi ngumu kuwa rahisi na hivyo hukuzuia kufikia malengo yako– (Nahjul-Balaghah). Kama ambavyo uongo humfanya mtu ajiingize katika madhambi, halikadhalika kujieusha na tabia ya kusema uongo au hisia za mtu kujutia na kutubu uongo aliosema huko nyuma kutamfanya ajiepushe na madhambi mengine mengi. Mtu mmoja alikwenda mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kusema: “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Mimi ninasali lakini pia huzini na kusema uongo. Sasa ninataka nitubu dhambi moja kati ya hizi na kuiacha kabisa. Sasa nishauri ni dhambi gani niiache kati ya hizi?” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimjibu: “Jiepushe kusema uongo.” Mtu yule aliukubali ushauri wa Mtukufu Mtume na aliamua kuacha kabisa kusema uongo katika hali yoyote. Aliacha kusema uongo tu na matokeo 112

12:44 PM

Page 112


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

yake ni kuwa alijikuta akiacha dhambi zote kwa sababu alipowaza kuzini aliwaza kichwani kuwa: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akiniuliza ikiwa nimezini toka siku ile nilipotubu dhambi ya kusema uongo, je nitamjibu nini? Kama nitakataa, nitakuwa nimesema uongo na nitakuwa nimekwenda kinyume na ahadi yangu. Na nikisema ukweli, nitakuwa ninakiri kuwa nimezini na nitaadhibiwa kwa hilo. Hali itakuwa hivyo hivyo kwa madhambi mengine.” Hivyo kuacha kwake kusema uongo kulimfanya asalimike na madhambi mengine yote.” – (Mustadrakul-Wasa’il, Juz. 2). Ni muhimu kugusia hapa nukta kwamba kwa vile uongo uchukua mizizi katika roho ni muhimu kuzifanyia mabadiliko nyoyo za waongo, sababu za tabia hii zinapaswa kugunduliwa na kisha hatua za marekebisho zinaweza kuchukuliwa kwa sababu kama chanzo hakikugundulika, hatua sahihi ya kuiondosha nuksi hii haiwezi kutwaliwa. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Mwongo huwa hasemi uongo isipokuwa pale anapojiona yu duni na mdogo nafsini mwake.” – (Mustadrakul-Wasa’il, Juz. 2). Kwa sababu hii hasa, kwa kuchunguza kidogo ile hali ya mtu mwongo, inakuja kufahamika mara moja kuwa sababu za yeye kusema uwongo ni udhaifu wa tabia, uoga, kutojiweza na kupoeza kujiamini au maradhi mengine ya kiakili yanayofanana na haya. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ameripotiwa kusema: “Mtu asiyekuwa na silka za kibinaadamu kabisa ni yule ambaye husema uongo.” – (Ikhtisas, uk. 232). Mtu mwenye ujasiri wa kimaadili kamwe hawezi akasema uongo. Anayesema uongo ni yule ambaye hujihisi udhaifu na udhalili ndani ya nafsi yake. Kwa kusema kweli inaweza kusemwa kwamba watu wasio na unyoofu, waoga na wadhaifu hukimbilia kusema uongo.

113

12:44 PM

Page 113


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Imam Ali (a.s.) amesema: “Ikiwa tabia na sifa mbalimbali zitapangwa katika makundi kwa mujibu wa kufanana kwao, ukweli utakuwa pamoja ujasiri na uongo utakuwa pamoja na hofu na woga.” – (Ghurarul Hikam). Mwanasaikolojia mmoja amesema: “Uongo ni silaha bora ya watu wadhaifu na ni njia ya haraka zaidi ya kuepukana na hatari za muda. Kwa sababu hii tabia ya kusema uongo imekuwa ni tabia mashuhuri iliyopo miongoni mwa watu weusi ambao wamekuwa wakikabiliwa mfululizo na hisia za utumwa na mashinikizo makubwa chini ya kongwa za watu weupe na wanahisi yale mamlaka yanayoendeshwa na watu weupe juu yao. Katika baadhi ya mambo, uongo huwa si chochote bali ni uakisi wa hali ya unyonge. Tunapomwambia mtoto: “Je umegusa pipi hizi?” au “Umevunja gilasi hii?” Na mtoto anajua kuwa akikiri kuwa amefanya mambo haya ataadhibiwa, silika yake ya ulinzi humwambia ajibu: “Sijafanya hivyo.” – (Raymond Peach). Wakati mwingine tabia hii huonekana miongoni mwa watoto na isiporekebishwa vizuri kwa kutumia elimu na mafunzo sahihi tabia hii husababisha hatari kubwa, na wakati mwingine huwa ni tatizo lisilotibika. Jukumu la kwanza na muhimu zaidi kwa wazazi na walimu kwa ujumla ni kwamba wasiwaambie uongo watoto na wasiwapatie ahadi za uongo. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: “Mwenyezi Mungu ambariki baba ambaye humsidia mwanawe kufanya mema,” Msimuliaji alimuuliza (Mtume): “Je anawezaje kumsaidia mwanawe?” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimpa maelekezo manne yafuatayo kwa ajili ya hilo. (i). Anatakiwa apime nguvu na uwezo wa mwanae na aridhike na kazi anayoifanya mwanae kwa kulingana na uwezo wake. (ii). Asimlazimishe mtoto kutenda jambo lolote linalozidi uwezo wake. (iii). Asimlazimishe mtoto kutenda dhambi au uasi wa aina yoyote ili. 114

12:44 PM

Page 114


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

(iv) Asimdanganye mwanae na wala asifanye mambo ya kipumbavu mbele ya mwanaye – (al-Kafi). Moja ya sababu za watoto kusema uongo ni kuwapatia majukumu mazito mno na kuwatarajia kufanya mambo yaliyo nje ya uwezo wao. Ukali wa walezi wa watoto na kuwatarajia kufanya mambo yaliyo nje ya uwezo wao huwalazimisha watoto wakimbilie kusema uongo na kuwajengea tabia mbaya juu yao. Bertrand Russell anasema: “Uwezekano wa kusema uongo huwa haujitokezi katika akili ya mtoto mdogo tokea awali. Baadaye uwezekanao huu unadhihirishwa kwake kidogo kidogo – yaani huuona uwezekano huo wa kusema uongo kutoka kwa wakubwa zake. Woga pia humlazimisha asema uongo. Mtoto hugundua kwamba watu wakubwa humdanganya na kwamba akisema ukweli itakuwa ni hatari kwake. Kwa shinikizo na ushawishi wa hali hizi huanza kusema uongo. Ukijiepusha wewe mwenyewe kusema uongo, mtoto hatapata wazo la kusema uongo.” Reymond Peach anasema: “Ninamfahamu msichana mmoja ambaye hivi sasa ni mwongo mkubwa asiyerekebika. Alipokuwa na umri wa miaka saba alihudhuria katika darasa lenye wanafunzi 25. Mfanyakazi wao wa kike alikuwa akimpeleka shule na pia alikwenda kumchukua baada ya masomo kila siku. Mfanyakazi yule aliwajibika kumuangalia mtoto huyo, naye alitekeleza majukumu yake kwa ukamilifu kiasi cha yeye pia kujifunza masomo aliyokuwa anajifunza mtoto huyo. Kwa kifupi mwanamke huyu aliwajibika katika elimu ya mtoto huyu. “Kwa mujibu wa mfumo wa elimu wa siku hizo, ambao hivi sasa umeonekana kutokuwa na matunda na hivyo kuachwa, watoto walikuwa akitunukiwa madaraja kila siku kutokana na majaribio ya kuandika na walikuwa walitambulika wa kwanza, wa pili, wa tatu n.k. Kila siku, mtoto huyo alipotoka tu darasani na mkoba wake mkononi, yule mfanyakazi alikuwa akimuuliza kwa shauku, “Umeshika nafasi ya ngapi?” Na kama 115

12:44 PM

Page 115


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

angejibu kwamba alishika nafasi ya kwanza au ya pili, hapo mambo yalikuwa yanakuwa shwari. “Lakini ilipata kutokea kuwa katika siku tatu mfululizo, mtoto huyo alishika nafasi ya tatu na tunaweza kusema kwamba, kuwa mwanafunzi wa tatu kati ya wanafunzi ishiri na tano ni matokeo mazuri kabisa. Lakini mfanyakazi yule hakuwa miongoni mwa wale ambao walikuwa na uwezo wa kuuelewa uhalisia huo. Alimvumilia mtoto yule kuwa wa tatu mara mbili lakini hakuweza kuvumilia mara ya tatu na mtoto akiwa na uoga mwingi kutokana na mfadhaiko, mtumishi yule alipiga kelele: “Kwa hiyo hakuna mwisho wa wewe kushika nafasi ya tatu? Kesho lazima uwe wa kwanza. Umenisikia? Lazima uwe wa kwanza.” Msichana (mtoto) yule alizama kwenye mawazo sana juu ya amri hii kali na isiyo na mjadala kwa kutwa nzima na asubuhi ya siku iliyofuata pia alikuwa anaogopa juu ya jambo hili. Katika siku ile msichana yule alijitahidi kufanya jaribio lile vizuri kwa kadiri ya uwezo wake wote. Alipata maswali yote ya kutoa na kujumlisha. Alisoma vizuri sana masomo yake. Mpaka karibu na wakati wa mchana, mtihani wa imla ulipoanza, kazi yake yote ilikuwa inaridhisha. Hata hivyo kulikuwa makosa manne katika mtihani wake wa imla, na mwisho wa siku alishika nafasi ya tatu. Na safari hii pia, kuwa kwake wa tatu lilikuwa ni tatizo kubwa kwake. Kengele ya mwisho ilipogonga mfanyakazi yule alikuwa amesimama kwenye mlango wa darasa akimsubiri mtoto yule atoke. Alipomuona tu akamuuliza; ‘Kuna habari gani?’ Msichana yule alishindwa kupata ujasiri wa kusema ukweli na alijibu. ‘Nimekuwa wa kwanza.’ Na huu ulikuwa ni mwanzo wa tabia yake ya kusema uongo. Kuna wazazi wengi wenye tabia kama hiyo na kwa hiyo wanaubeba katika mabega yao mzigo wa madhambi na uwajibikaji wa uongo uliosemwa na watoto wao.

116

12:44 PM

Page 116


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Bertrand Russell anasema: Mtoto akianza kusema uongo, wazazi wanapaswa kuona kuwa wanawajibika kwa hilo. Wanapaswa kukiondoa chanzo na wamweleze kwa utulivu kwa kutoa hoja ya kwa nini ni vizuri zaidi kutosema uongo. Ili kusahihisha kosa la mtoto, wazazi hawapaswi kukimbilia kumpiga na kumuadhibu, kwa sababu kwa kufanya hivyo watakuwa wanamzidishia hofu ambayo ni moja ya vichocheo vya kusema uongo.” Kwa kusema kweli, ikiwa tunataka watoto wasiseme uongo, hakuna njia nyingine isipokuwa watu wazima lazima waonyeshe ukweli wakati wote mbele ya watoto. Wazazi wanapowafundisha watoto wao kutokusema uongo, lakini wakati huo huo watoto hao wanawaona wazazi wao wakisema uongo, ni wazi kuwa wazazi hao hupoteza mamlaka na ushawishi wa kimaadili kwa watoto wao. Aina nyingine ya uongo ambayo ina madhara sana kwa watoto ni kwamba wanatishiwa kuadhibiwa adhabu ambazo hazikusudiwi kutekelezwa. Dk. Ballard kwa maneno ya kusisitiza anasema: “Usitishie, lakini endapo ukitishia usiruhusu kitu chochote kikuzie kutekeleza tishio lako hilo kwa vitendo.” Ukakamavu wa wazazi na walimu unaweza kuwalinda watoto dhidi ya kuangukia kuwa mawindo ya laana ya kusema uongo. Mtoto asipodharauliwa na haiba yake isipovunjwa, kama watu wazima wasipowafanya wajifundishe kuongopa kwa wao wenyewe kusema uongo, ikiwa mambo yanayosababisha mtu kusema uongo (kama vile uoga, adhabu n.k.) yakiondolewa, ikiwa wazazi hawatakuwa wakali bila ulazima na wasipoonyesha utawala mzito na kwa kifupi wakitumia njia za busara na kwa upole, ni wazi kwamba mtoto huyu hatalazimika kujiingiza katika tabia mbaya ya kusema uongo.

117

12:44 PM

Page 117


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Wazazi huudhika sana watoto wao wanaposema uongo, na hususani pale uongo huo unaposhangaza na muongo mwenyewe anapokuwa hana uzoefu. Kwa nini mtoto anasema uongo? Wakati mwingine watoto husema uongo kwa sababu hawaruhusiwi kusema ukweli. Kama mtoto akimwambia mama yake kuwa anamchukia kaka yake, mama yake anaweza akamzaba kibao mara moja, lakini baadaye kidogo akisema kwa uongo kuwa sasa ameanza kumpenda kaka yake, inawezekana akambusu kwa furaha na pia akampa zawadi nzuri. Mtoto huwa anajifunza nini kutokana na tabia kama hii? Bila shaka ataamua kwamba kusema ukweli ndio mwanzo wa matatizo na kusema uongo huleta furaha na huishia katika kupata zawadi kutoka kwa mama. Hivyo kama tunataka kuwafundisha watoto kusema ukweli, basi tunapaswa kuusikiliza ukweli wao hata kama ukweli huo ni mchungu kama tu tunavyokuwa watulivu tunaposikiliza ukweli wao mtamu. Mtoto anapoadhibiwa kwa kusema ukweli, ni wazi kwamba atakimbilia kusema uongo katika kujilinda kwake. Wazazi hawapaswi kuwauliza watoto wao maswali ambayo yatawalazimisha kusema uongo. Watoto huwa hawapendi kuhojiwa na wazazi wao pasi na ulazima hususani ikiwa watajua kwamba majibu ya maswali yeyewe yanafahamika. Lengo letu pekee linapaswa kuwa ni kumfanya mtoto aelewe kwamba sio lazima kwake yeye kusema uongo. Nukta muhimu kabisa katika suala hili ni kuwakumbusha watoto juu ya wajibu wao wa kidini – kwamba ni dhambi kubwa kusema uongo na Mwenyezi Mungu hampendi na anachukizwa na mtu muongo.

118

12:44 PM

Page 118


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Kama watoto wakilelewa kwa mujibu wa misingi ya Uislamu na ikiwa maadili yao yanaendana na mafundisho ya Mwenyezi Mungu, basi hakuna dosari yoyote itakayojitokeza kwao kwa sababu hakuna kanuni inayotoa hakikisho la usimamiaji wa uekelezaji wa sheria kama imani juu ya Mwenyezi Mugu. Ni kanuni hii hasa ambayo huwazuia waumini kujihusisha na kusema uongo na kufanya madhambi mengine na kuwapatia kinga ya namna fulani ya kiroho. Al-Marhuum Allamah Naraaqi anasema: “Njia bora ya kuondoa tabia mbaya ya kusema uongo ni kuwa mtu azizingatie aya za Qur’ani na hadithi zinazolaani tabia ya kusema uongo ili ajue kwamba kusema uongo huleta maangamizi ya milele. Aidha, mtu anapaswa kujua kuwa, mbali na maangamizi haya huko Akhera, akiwa mwongo atapoteza hadhi na heshima mbele ya macho ya watu.” – (Jami’us Saadaat, Juz. 2, uk. 256). Dk. Alexis Carrel anasema: “Tabia zenye madhara zaidi katika upandishaji wa daraja la nafsi ya mtu ni kusema uongo, kuchonganisha, kusengenya, kuiba, kupora au kudhulumu mali ya wengine na mtu kutaka vitu vyote viwe kwa maslahi yake binafsi. Nafsi ya mwanaadamu kamwe haiwezi kustawi katika uchafu na uongo.” Imam Ali (a.s.) (a.s.) anasema: “Semeni ukweli, kwani Mwenyezi Mungu yupo pamoja na wakweli. Jitengeni na uongo kwani uongo huharibu imani. Mtu mkweli yupo katika njia ya ustawi na uokovu ambapo mwongo yupo katika ukingo wa fedheha na maangamizi.” – (Biharul-Anwar, Juz. 72, uk. 260). Mshairi mashuhiri wa ki-Farsi, Sheikh Sa’di anasema: “Mwanaadamu anapaswa kuwa mkweli hata kama matatizo yakimuangukia kama mvua ya mawe.

119

12:44 PM

Page 119


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Sema ukweli na usiogope, kwa sababu ukweli hauondoi riziki ya mtu wala huwa haumletei mtu kifo. Hasara mbalimbali zinazosababishwa na uongo huwa dhahiri wakati uchunguzi kidogo juu ya hali za waongo utakapofanyika.” Kwa mtazamo wa kijamii uongo huleta hasara zisizoweza kufidiwa kwa jamii. Hadhi ya muongo katika jamii huwa hatarini na siku zote huwa anatazamwa kwa dharau na aibu. Ni fedheha gani inayoweza kuwa kubwa kuliko hii kwamba uongo wake ufahamike kwa watu na heshima yake katika jamii kuharibika. Watu wenye busara wakati wote hutafuta kupata heshima katika jamii na wako tayari kutumia mali yao ili wapate heshima katika jamii. Rasilimali ya kujipatia heshima binafsi ni rasilimali yenye thamani kuliko zote. Lakini mtu muongo huipoteza rasilimali hii kwa mikono yake mwenyewe, kwa vitendo vyake visivyofaa. Mmoja wa viongozi wa madhehebu ya Shaykhiya, alikuwa akihutubu katika mimbari katika mji wa Tabriz. Katika hotuba yake alitaja majina ya wafalme wa majini na alitaja ni yupi alianza kutawala na ni nani alifuatia. Alisema kitu kama hiki, “Mfalme wa kwanza wa falme hii alikuwa Tehtamshah. Alifuatiwa na Qehqamshah kisha Jehjamshah na kdhalika.” Mzungumzaji aliendelea na hotuba yake mpaka alipofikia jina la mfalme wa kumi au kumi na moja, ambaye jina lake pia lilikuwa kama yale ya waliomtangulia. Alipofika hapo mtu mmoja mpenda maskhara aliyekuwa amekaa karibu na mimbari alisimama na kusema: “Bwana, je unaweza kurudia jina la mfalme wa tano?” Mzugumzaji hakuweza kujibu kwa sababu hakuwa anakumbuka jina alilokuwa amempa mfalme wa tano wa kubuni. Sasa wasomaji wapendwa wenye tafakuri wanaweza wakaelewa ni fedheha gani aliyoipata mzugumzaji huyu mpumbavu kwa kusema uongo huu 120

12:44 PM

Page 120


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

butu. George Herbert anasema: “Uongo hata ufichwe kwa namna gani, mwisho wa safari lazima utabainika tu.” Aidha, ule ukweli kwamba mwongo hupoteza heshima yake katika jamii, mwongo pia hupoeza imani ya watu juu yake, jambo ambalo ni msingi muhimu wa maisha ya mtu ya kijamii. Hakuna ambaye huyaamini maneno yake kiasi kwamba hata akisema ukweli watu huwa hawako tayari kumwamini. Aristole anasema: “Wale wanaosema uongo huadhibiwa katika namna ambayo hata wakisema ukweli huwa hawaaminiwi na yeyote.” Sa’di anasema: “Kama mtu ambaye ni mkweli, akifanya kosa, basi watu hulipuuza. Lakini kama anavuma kwa kusema uwongo, huwa haaminiki hata kama atatokea kusema ukweli.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: “Jiepusheni na kusema uongo kwani kusema uongo huletea fedheha kwa mtu mwongo.” Uongo pia una madhara sana kwa mtazamo wa kiuchumi, kwa sababu kupata mali kwa kawaida huhusisha kufanya biashara na watu na kama kwa kawaida tunavyoona, biashara hususani kubwa hufanyika kwa mkopo na msaada mkubwa katika biashara hiyo ni kuaminiana. Uongo huharibu uaminifu na hili huharibu biashara ya mtu mwongo na matokeo yake ni hasara. Hasara nyingine inayotokana na uongo ni kuleta wasiwasi katika akili jambo ambalo mara nyingi huwasababishia matatizo na maradhi makubwa ya kiakili. Mmoja wa waandishi mashuhuri wa vitabu, ameandika katika kitabu chake 121

12:44 PM

Page 121


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

kuwa: “Nilisema uongo mara moja kwa uzembe na matokeo yake ni kuwa nilipata maumivu ya akili kwa miaka thelathini kutokana na uongo huu. Tukio lenyewe lilikuwa hivi. Usiku mmoja nilikuwa na marafiki na washirika wangu katika tafrija. Mazungumzo yalianza juu ya safari za nje ya nchi. Wale waliokuwepo walizungumzia juu ya safari walizofanya katika nchi za Ulaya, Amerika, Mashariki ya kati na Mashariki ya Mbali. Ili nisionekane kubaki nyuma katika hili, mimi pia nilijiunga na mazungumzo na nikaelezea juu ya Safari niliyoifanya nchini Ufaransa licha ya ukweli kwamba mimi kamwe sikuwa nimewahi kufika au kufanya safari nchini Ufaransa. Lakini iliniijia kichwani kwamba mmoja wa watu waliokuwa katika tafrija ile ambaye amewahi kufika Ufaransa, angeweza kuniuliza swali juu ya nchi ya Ufaransa na ingekuwa ni jambo la fedheha kubwa kwangu. Nilibaki katika wasiwasi mkubwa mpaka hatimae tafrija ile ilipokwisha. Tokea usiku ule, nilikuwa nikimuona zimwi wa fedheha mbele ya macho yangu na wakati wote nilikuwa na mashaka kuwa isije kutokea siku moja akawepo mmoja wa watu waliokuwepo kwenye tafrija ile mahali fulani na kwa uzembe nikaja kusema kitu kinachopingana na madai niliyopata kutoa (yaani juu ya safari ya nchini Ufaransa) na hivyo nikajikuta nikifedheheka. “Maumivu haya ya kiakili yalinitesa sana kiasi cha kuamua kuondokana nayo kwa kuitembelea nchi ya Ufaransa. Kwa bahati mbaya sikuweza kupata namna za kutosheleza kufanyia safari hii na jitihada zangu hazikuzaa matunda mpaka baada ya miaka thelathini nilipofanikiwa kufanya safari hiyo na hivyo kuondokana na maumivu hayo ya kiakili. “Ilivyo ni kuwa nilisema uongo mara moja tu lakini niliteseka kwa miaka thelathini. Hata hivyo matokeo yalikuwa kwamba, nilidhamiria usiku uleule kuwa sitakuja kusema uongo tena maishani mwangu.” Wanahisoria wameandika kuwa: “Kulikuwa na maelewano mazuri kati ya Sultan Husayn Baiqara, Mfalme wa Khurasan na Zabulistan (Iran) na Sultani Ya’qub, mfalme wa Iraq na Azarbaijan walikuwa wakiwasiliana 122

12:44 PM

Page 122


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

mara kwa mara. Mfalme wa Iran aliamua kumtumia Sultan Ya’qub zawadi za thamani. Zawadi zilipokuwa zimeandaliwa tayari aliamuru kuwa nakala ya kitabu kiitwacho, “Kulliyaati-i Jaami” (Kazi za Jaami), kitabu kilichokuwa na thamani sana katika enzi hizo, kichukuliwe katika maktaba ya mfalme na kujumuishwe katika zawadi hizo. Mulla Abdul Karim, mkutubu mkuu, alikosea wakati wa kuchukua kitabu, badala ya kuchukua ‘Kulliyaat-i Jaami’, alichukua ‘Futuhat-i Makki’ na kukiongeza katika zawadi zile. Kosa hili lilitokana na ukweli kwamba hivi vitabu viwili vilikuwa vinafanana sana katika ukubwa na jalada. Amir Husayn Abiwardi, mtu aliyekuwa mashuhuri sana katika baraza ya mfalme, alipewa jukumu la kupeleka zawadi hizo ikiwa ni pamoja na ‘Kulliyaat-i Jaami’ kwenye baraza ya Sultani Ya’qub na akazikabidhi zawadi hizo kwake. Yeye pia alikichukua kitabu bila kukitazama ndani na akaondoka kwenda alikotumwa. Wakati Amir Husayn alipofika Tabriz na kupokewa na Sultan Ya’qub, Sultan alimkaribisha kwa furaha na akamwambia: “Lazima utakuwa umetaabika na kuchoka sana kutokana na safari hii ndefu.” Hata hivyo, kwa vile Amir Husayn alikuwa anafahamu jinsi Sultan alivyokuwa akikipenda kitabu cha Jaami, alisema kuwa: “Katika safari yangu, nilikuwa na rafiki yangu wa karibu, hivyo sikuhisi taabu zozote za safari.” Sultan aliuliza: “Ni nani aliyekuwa msafiri mwenzio?” Amir Husayn alijibu “Kazi za Jaami.” Sultan alifurahi sana kusikia hili na aliamuru kuwa akabidhiwe kitabu hicho. Amir Husayn alimtuma mtu na kitabu kikaletwa. Lakini kilipofunuliwa kikatokea kuwa Futuhat Makki na sio ‘Kulliyaat-i Jaami’.

123

12:44 PM

Page 123


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Amir Husayn hakuwa na la kusema juu ya uongo aliosema. Lakini kwa bahati mbaya maji yalikuwa yameshamwagika na kulikuwa hakuna marekebisho yanayoweza kufanyika juu ya tukio hilo. Hadhi ya mwanasiasa na mwanadiplomasia yule iliporomoka na heshima yake ikapotea, sio kati ya watawala hawa wawili tu bali pia kati ya nchi hizi mbili. Matukio mengi ya kihistoria yamerekodiwa katika vitabu vya historia juu ya hasara kubwa walizopata watu kutokana na kusema ongo. Tukiyatizama maisha ya watu tunaoishi nao leo hii, pia tunaweza kuona dhahiri uovu wa kusema uongo. Ni kwa sababu ya hasara hizi hizi kwamba Uislamu ulizindua kampeni kabambe dhidi ya uongo na ukauchukulia uongo kuwa ni laana za watu wasiokuwa na imani na wasiokuwa na maadili na unawahesabu waongo kuwa ni watu walilaaniwa na wakushutumiwa. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Malaika wanamlaani mtu anayesema uongo bila ya sababu za msingi. – (Jami’us Saadaat, Jz. 2) Imam Ja’far as-Sadiq (a.s) anasema: “Mtu muongo anakosa ushupavu.” (Khisal, Saduq, Juz. 1). Imam Riza anauchukulia ukweli na kurejesha amana kuwa ni kigezo cha imani na thamani ya watu, na anasema: “Wapime watu kwa mambo mawili: Mojawapo ni ukweli wakati wa kuzungumza na jingine ni kuwa mwaminifu katika kushika mali za watu anazokabidhiwa kama amana.” – (Gharurul Hikam).

124

12:44 PM

Page 124


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

UONGO UNAOHALALISHWA NA NIA Katika kurasa zilizopita tumeeleza kwamba uongo ni moja ya madhambi makubwa. Sasa tunataka kujadili juu ya uongo unaohalalishwa na nia na matlaba yake. Kimsingi, madhambi ambayo yamefanywa kuwa ni haramu na yasiyoruhusika katika Uislamu, ni ya aina mbili: (i) Yale madhambi ambayo tabia mbovu ni asili yake na ambayo moja kwa moja yanachukuliwa kuwa ni sehemu ya matendo maovu kwa mfano mauaji, ukandamizaji, kuvunja haki za wengine wizi n.k. (ii) Madhambi haya ambayo ni utangulizi wa ufisadi na huandaa mazingira ya uhalifu mwingine, kama ilivyoelezwa katika simulizi zilizopita, ndio ufunguo wa madhambi na maovu yote. Hivyo, kama mazingira yakitokea ambapo uongo ukawa ndio njia ya kuzuia dhambi au kuwa ni ufunguo wa kumnusuru mtu anayedhulumiwa, basi hapa kutokubalika kwake kunaondoka na huondolewa kimsingi katika kundi la dhambi. Hii ni kwa sababu uovu wao sio wa asili na uovu wake wa bahati mbaya huondoka kwa sababu ya malengo mazuri. Katika hali kama hizi uongo sio tu kwamba unakuwa halali basi pia huwa ni wajibu ikiwa utaleta usalama na heshima ya mwislamu. Imam Ja’far Sadiq anasema: “Ikiwa mwislamu ataulizwa kuelekeza aliko mwislamu mwingine na akasema ukweli na kwamba kwa matokeo ya kusema kwake ukweli, mwislamu mwingine akapata madhara, jina la Mwislamu huyo aliyesema kweli litarekodiwa katika orodha ya waongo. Na endapo Mwislam akiulizwa juu ya Waislamu wengine na akasema uongo, na kwa sababu ya uongo wake, Waislamu wengine wakinufaika 125

12:44 PM

Page 125


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

basi mwislam huyo atachukuliwa kuwa ni miongoni mwa watu wakweli mbele ya Mwenyezi Mungu. Sa’di, mshairi mashuhuri wa Iran anasema katika Gulistan: “Inasemekana kwamba mfalme aliamuru kuuliwa kwa mfungwa. Mfungwa huyo akiwa katika hali ya kukata tamaa alianza kumtukana mfalme. Kwani imesemekana kwamba mtu aliyepoteza matumaini ya maisha husema chochote kilicho katika moyo wake.” Mfalme aliuliza: “Anasemaje?” Waziri aliyekuwa na roho nzuri alisema: Mtukufu Mfalme! Amesema: “Mfalme amenihurumia na ameniondolea adhabu ya kifo.” Mfalme alimhurumia na akasitisha adhabu ya kifo. Waziri mwingine aliyepingana na waziri wa kwanza akasema: “Sisi watu hatupaswi kusema mbele ya mfalme isipokuwa ukweli. Mfungwa huyu amemtukana mfalme.” Mfalme aliudhika kusikia maneno haya na akasema: “Nimeupenda uongo wake zaidi kuliko ukweli wako kwa sababu uongo wake ulilenga katika heri na ukweli wako umelenga katika uovu, na watu wenye hikma wamesema: uongo unaolenga katika heri ni bora kuliko ukweli usababishao uharibifu.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: Uongo unaruhusuwa katika maeneo matatu: (i) kusema uongo wakati wa vita (ii) Ahadi ya mume kwa mkewe na (iii) Kusuluhisha baina ya watu.

MAELEZO (i)

Kuhusina na uongo wakati wa vita, wasomaji waliotaalimika wanapaswa kutambua kwamba katika Uislamu, vita kwa malengo ya kuteka ardhi haviruhusiwi. Vita vya kiislamu ni mapambano kati ya 126

12:44 PM

Page 126


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

ukweli na uongo, na udanganyifu katika vita kama hivyo unaruhusiwa kwa kuwa huwa ni njia ya kuuimarisha ukweli na kuudhoofisha uongo. (ii) Na kuhusiana na ahadi ya mume kwa mkewe, inaweza ikaelezwa kwamba Uislamu unajali sana ustawi na furaha ya wanandoa na unawataka waishi maisha yao ya ndoa kwa mapenzi na upendo mkubwa kabisa. Ni kwa sababu hii kwamba Uislamu umemruhusu mume kutoa ahadi ya uongo na lengo ni kuwa kama ataweza kutimiza ahadi na matakwa ya mkewe basi ni vizuri, lakini hata kama hataweza kutekeleza ombi lake au haoni haja ya lazima kulikubali, humwacha mkewe na furaha kwa kutoa ahadi kama hiyo na anakuwa ameepuka kuzibughudhi hisia zake (mkewe) za moyoni. (iii) Kuhusiana na kusuluhisha watu, inanaweza kusemwa kwamba Uislamu hutaka pawepo mahusiano mazuri ya kirafiki baina ya Waislamu na kama zikitokea tofauti baina ya watu wawili au hata makundi mawili, jitihada zinapaswa kuchukuliwa ili kuziondoa. Kuondolewa kwa tofauti baina ya Waislamu bila shaka kuna maslahi kwa pande zote mbili zinazohusika katika migogoro na jamii kwa ujumla na ni kwa sababu hii kwamba kusema uongo katika kuleta usuluhishi baina ya watu kumehesabiwa kuwa kunafaa. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: “Yule anayekusudia kuleta maelewano baina ya watu huwa hasemi uongo.” Imam Ja’far Sadiq anasema: “Kudanganya ni uovu na hakupendezi isipokuwa katika maeneo mawili: Kuzuia dhulma na ukamdamizaji na kuleta maelewano baina ya watu” – (al-Kafi). Kuzungumza kwa ujumla, pale wakati mtu anaposema uongo huku lengo lake likiwa ni kuwalinda Waisamu dhidi ya uharibifu au madhara au kuleta maelewano baina ya watu, uongo wake huwa ni mzuri na unaopendeza. 127

12:44 PM

Page 127


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Inakuwa hivi kwa sababu katika hali hii uongo huwa sio ufunguo wa dhambi tena, bali huwa ni ufunguo wa wema na huruma kwa watu. Kwa kweli uongo kama huo pia huruhusiwa wakati ambapo haiwezekani kusema ukweli na ni katika mazingira kama hayo tu ambapo uongo huruhusiwa au kuwa ni wajibu na kusema ukweli kunakatazwa na kutoruhusiwa. Mwisho inapaswa ifahamike kuwa uongo kwa nia njema na unaruhusiwa katika hali zile tu ambazo umekubaliwa na Uislamu, na katika hali ambapo uongo ukiachwa basi huwa ni chanzo cha hatari na hasara. Hata hivyo, uongo wenye lengo la kujipatia maslahi binafsi kama fedha na mali, hauingii katika kundi hili la ‘uongo wenye lengo zuri.’ Uongo wa aina hii ni haramu kabisa na huangukia katika vifungu vya sheria vya aya za Qur’ani na hadithi zinazokataza uongo na ni chanzo cha fedheha na dhiki katika dunia hii na kesho Akhera.

NUKUU 1). Wale wanaosema uongo sio waumini. (Qur’ani Tukufu) 2). Mtu muoga sana ni yule asemaye uongo (Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). 3).Tabia ya kusema uongo ni uovu mbaya kuliko uovu mwingine wowote. 4). Ni vizuri kwa mwislam kujiepusha kufanya urafiki na undugu na mtu mwongo. (Imam Ali (a.s.)). 5). Uongo huvunja msingi wa imani – (Imam Baqir). 6). Mtu mwenye busara huwa hasemi uongo, hata kama kwa kufanya hivyo kutamuwezesha kukidhi matamanio yake ya kimwili – (Imam Musa Kazim).

* * * * * 128

12:44 PM

Page 128


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

MAHUSIANO YA KIJAMII Hapana shaka yoyote juu ya ukweli kwamba kwa asili, mwanaadamu ni mchangamfu na anapaswa kuishi maisha changamfu na ya pamoja, kwa sababu mahitaji yake yanamlazimu kuyapata kwa kushirikiana na wanaadamu wengine. Kila mtu anapaswa kuwajibika kwa kazi fulani na kila kundi linapaswa kutatua tatizo fulani ili maisha yawe ya furaha na yenye neema kwa wote. Pia hakuna shaka juu ya ukweli kwamba kuishi pamoja kunaweza kuleta uhakika wa mafanikio na furaha tu ikiwa kila mmoja atatambua wajibu wake na kuheshimu haki za wengine. Pia mahusiano ya pamoja yanapaswa yajengwe juu ya uhusiano wa kibinaadamu uliochanganyika na hisia moyoni na tabia tukufu. Ikiwa huruma, wema kwa watu wa chini yako, subira, urahimu, upole, huduma kwa umma, ushirikiano n.k. havipo katika jamii, basi kamwe jamii kama hiyo haiwezi ikaitwa kuwa ni jamii iliyostaarabika na yenye ustawi. Uislamu, ambao ni dini ya Mwenyezi Mungu, umeweka umuhimu mkubwa katika mahusiano ya kijamii na umetoa amri na maelekezo kamilifu na yanayoeleweka vyema kwa ajili ya kuimarisha mafungamano ya undugu na urafiki wa mtu na watu wengine. Kama tunataka kusema kitu sahihi kabisa juu ya jambo hili tunapaswa kusema: “Uislamu umewaamrisha watu kufanya mambo yanayofaa na vyenye manufaa kwa ajili ya kuboresha na kuimarisha mahusiano ya kijamii na umewataka Waislamu kuepuka kufanya mambo yanayoleta madhara japo madogo kwenye mahusiano haya na yakawa sababu ya kuharibika uhusiano huo.

129

12:44 PM

Page 129


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Wale wanaoyafahamu vizuri mafundisho ya Uislamu hawahitaji hoja yoyote kuthibitisha ukweli wa hicho kilichosema hapo juu. Na kuhusu wengine, pia wanaweza wakaubaini ukweli huu usiopingika kama wataziangalia kanuni zilizopitishwa na mtunga sheria wa Uislamu (yaani Mwenyezi Mungu) kwa makusudio ya kuhifadhi, kuboresha na kuimarisha mahusiano ya kijamii. Inavutia kuona kuwa katika programu ya kijamii ya Uislamu, masuala haya yamezingatiwa ambayo watu wengi hawayajali na ambayo hawayapi umuhimu mkubwa, ambapo haya ni yale mambo madogo madogo hasa yasiyo na thamani lakini ambayo huzaa matokeo makubwa na muhimu. Kwa mfano mahusiano rahisi kabisa ya watu ni makabiliano na kukutana kwao mabarabarani, mitaani, katika mabasi, misikitini, mashulen n.k. Kukutana huku kunachukuliwa na watu walio wengi kuwa sio muhimu, ingawa kwa mtazamo wa Uislamu, kukutana huku kunapaswa kutokea katika namna maalum ambayo itakuza urafiki, upendo na wema. Uislamu unashauri kwamba kukutana huku kunapaswa kufanyike kwa moyo mkunjufu na kusalimiana, na ikiwezekana kwa kupeana mikono kwa bashasha. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: “Mtu bora kabisa mbele ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake ni yule ambaye huanza kuwasalimia wengine.” Imam Muhammad Baqir amesema: “Mwenyezi Mungu huwapenda waja wake ambao husalimiana kikamilifu na wazi wazi.” Imam Ali (a.s.) anasema: “Usiudhike wala usiwaudhi wengine. Salimianeni kwa uwazi na swalini Sala za usiku wa manane ili mpate Pepo na furaha ya milele.” – (al-Kafi, Juz. 4). Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: “Ninaapa kwa Mola Wangu ambaye mikononi mwake ipo roho yangu kwamba hamtoweza kuingia Peponi na 130

12:44 PM

Page 130


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

kupata furaha ya milele mpaka muwe waumini wa kweli na hamtokuwa waumini wa kweli mpaka kwanza mpendane.” Kisha aliwauliza watu: “Je niwaongozeni kwenye kitendo ambacho matokeo yake kitakuza upendo na urafiki?” Watu wakajibu ndiyo. Mtume hapo akasema: “Salimianeni kwa mioyo mikunjufu, furaha na bashasha.” (Huquuq-i Islami, uk. 341). Ingawa salamu inachukuliwa kuwa ni kitu kidogo na kisichokuwa muhimu, hutoa mchango mkubwa katika kujenga urafiki na upendo baina ya watu kwa kiwango kisichoweza kuelezeka. Dale Carnegie alifanya utafiti juu ya mtu mashuhuri aliyepata umaarufu sana miongoni mwa watu na akasema kuhusu yeye: “Moja ya sababu za umaarufu wake usio wa kawaida ni kuwa alikuwa akimsalimia kila mmoja.” (How to win friends and influence people, Dale Carnegie). Inawezekana kuwa watu wengi wameshapata kuona katika maisha yao kwamba urafiki wa kupigiwa mfano baina ya watu mbalimbali ulianza kwa salamu au salamu za mara kwa mara. Pia uadui baina ya watu mbalimbali umepata kuondoshwa kama matokeo ya salamu. Mbali na kupendekeza salamu na kuhimiza sana watu kusalimiana, ili desturi ya kusalimiana isije ikaachwa na watu, Uislamu umeamrisha kwamba endapo mtu akianza kuzungumza bila kusalimia kwanza, basi asijibiwe. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: “Usimjibu mtu anayeanza kuongea bila kusalimia kwanza.” (al-Kafi). Kadhalika Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kiongozi mkuu wa Uislamu amewaelezea watu wasio salimia kama watu mabahili kuliko wote. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: “Mtu bahili kuliko wote ni yule ambaye ni bahili katika suala la salamu.”

131

12:44 PM

Page 131


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Wajibu mwingine ambao Waislamu wanapaswa kufanya ni kuwa na uso wenye bashasha na tabasamu pindi wanapokutana. Imam Muhammad Baqir anasema: “Kitendo cha kutabasamu unapokutana na ndugu yako mwislam kinahesabiwa kama ni kitendo cha ukarimu na kitukufu.” – (Makarimul Akhlaq, uk. 314). Imam Ridha anasema:: “Mwenyezi Mungu atamlipa thawabu mtu ambaye hutabasamu anapokutana na ndugu yake katika imani.” – (Safinatul Bihar, Juz. 1 uk.. 613). Wanasaikolojia wa zama hizi wanaichukulia kanuni hii ya Kiislamu kuwa ni siri ya mafanikio ya mtu katika maisha. Albert Hubbard amesema: “Unapoondoka nyumbani kwako nyanyua kichwa chako na vuta pumzi kwa wingi na fyonza miale ya jua katika mwili wako na unapokutana na rafiki zako na wale unaofahamiana nao, kutana nao huku ukiwa na tabasamu usoni kwako, na unapopeana nao mikono, wapulizie roho yako.” Dale Carnegie amesema: “Matendo huzungumza kwa sauti zaidi kuliko maneno na tabasamu husema kuwa “Nakupenda. Unanifanya nifurahi. Nafurahi kukutana na wewe.” – (How to win friends and influence people). Methali ya kichina inasema: “Ambaye hana tabasamu katika uso wake hapaswi kufungua duka lake.” Jambo jingine ambalo limehimizwa sana na viongozi wa Uislamu katika suala la waislamu wanapokutana na Waislamu wengine ni kupeana mikono, na kuikandamiza kwa ukunjufu wa upendo. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: “Wakati wowote, pale yeyote miongoni mwenu anapokutana na ndugu yake mwislam, anapaswa kumsalimia 132

12:44 PM

Page 132


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

na kupeana naye mkono.” Aidha ameripotiwa kuwa amesema: “Salamu unapokutana na ndugu yako hukamilika tu pale inapoandamana na kupeana naye mkono.” – (Huquuq-i Islami). Hii ni hatua ya kwanza katika kujenga mahusiano mazuri katika jamii ya Kiislamu ili waweze kukutana katika mawasiliano yao ya kila siku katika halli ya uchangamfu, ili waweze kusimamisha uhusiano wao juu ya msingi wa uchangamfu na uaminifu. Baada ya kuifikia hatua hii, sasa tunayafikia mafundisho mengine ya nayotolewa na Uislamu yanayowataka Waislamu wawapende ndugu zao katika imani kwa upendo wa dhati kutoka kiini cha mioyo yao. Kuwapenda wengine ni moja ya matakwa bainifu ya mwanaadamu. Ni matakwa haya hasa ya kiroho ambayo humfanya mwanaadamu awajali wengine na huwafanya watu kuwa na huruma kwa kila mmoja wao na hujenga hisia za wajibu wa kushirikiana na wengine katika dhiki na faraja za kila mmoja wao. Kama ilivyo kwa matakwa mengine mazuri ya mwanaadamu, matakwa au mwelekeo wa upendo ni dhaifu na usio na uhai na huwa hauwi na nguvu bila mafunzo na mwongozo. Ikiwa wazazi na walimu watawajali watoto toka wakiwa katika umri mdogo na kutekeleza wajibu wao vizuri, pole pole wanaweza kuiendeleza sifa asili hii ya kibinadamu kwenye tabia zao na kuwakuza wakiwa ni watu wenye mapenzi juu ya binadamu na huruma. Ikiwa mapenzi binafsi yatasaidiwa na kuimarishwa yanakarahisha na kuvuka mipaka ya adabu. Hatimaye hubadilika na kuwa ubinafsi na kusababisha uovu mkubwa kabisa. Humuingiza mwanaadamu katika madhambi ya kimaadili na kupora haki za wengine na kumwelekeza katika vitendo visivyo vya kibinadamu.

133

12:44 PM

Page 133


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Ikiwa upendo kwa wengine utasaidiwa na kuimarishwa, basi huzishinda hisia za kiunyama, hudhoofisha silika za uharibifu, hukandamiza hisia za ukatili na ukali na humpatia mwanadamu moja ya sifa tukufu kabisa za kibinaadamu. Pia inafaa ielezwe kuwa tunaposema upendo kwa wengine tunamaanisha upendo na huruma kwa mtazamo wa maadili bora na sifa za kibinadamu. Haina maana kwamba lengo la upendo liwe kukidhi matamanio ya kiyakinifu na kimali. Mgonjwa huonyesha upendo kwa daktari anayemtibu na nesi anayemuuguza. Hata hivyo asili ya kisaikolojia ya upendo huu sio upendo kwa wengine na tabia njema za kibinaadamu. Huu ni upendo unaotokana na silika za mgonjwa za kujipenda na maisha yake. Mazingatio ya mgonjwa kwa daktari na nesi yanatokana na sababu kwamba wanamtibia na kurejesha afya yake hivyo wakiridhisha silika yake ya kujipenda. Upendo wa aina hii unapatikana hata kwa wanyama pia, haupatikani kwa binadamu peke yao. Mtu mwenye upendo wa dhati kwa wengine hasa ni yule anayewapenda wanaadamu kwa sababu tu ni wanaadamu na ambaye hamasa ya upendo wake imechochewa na hisia halisi za ubinadamu na usio na ubinafsi wala maslahi yeyote binafsi. Upendo wa aina hii ni ishara ya utukufu na usafi wa roho ya mtu na ni moja ya sifa za kipekee za kibinadamu. Upendo na mapenzi ya aina hii huyatofautisha maisha ya mwanaadamu na maisha ya wanyama, hudumisha uhusiano mzuri katika jamii za wanaadamu, huunganisha mioyo ya watu kwa mafungamano ya upendo wa kibinadamu na hufufua moyo wa udugu na ushirikiano. Upendo wa aina hii huwaweka watu mbali na tabia za kinyama na kikatili, huwapatia wanaadamu ulinzi na usalama, hujenga mazingira ya amani na uaminifu na huyafanya maisha kuwa matamu na ya kufurahisha.

134

12:44 PM

Page 134


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Katika dini takatifu ya Uilamu, suala la upendo kwa wanaadamu wengine limezingatiwa sana na viongozi wa kidini wanaiona tabia hii njema kuwa ni moja ya vipengele vya maendeleo na ustawi wa mwanaadamu na ni moja ya njia za kujipatia baraka za Mwenyezi Mungu. Imam Musa Kadhim anasema: “Madhali wakazi wa dunia wakiwa wanapendana, na wanarejesha amana na wakiwa na tabia zenye kuendana na ukweli na uaminifu basi watakuwa wanaendesha maisha yao chini ya neema na huruma.” – (Majmu’a Warram, Juz. 1). Imam Ali (a.s.) amesema: “Njia nzuri ya kupatia baraka za Mwenyezi Mungu ni kwamba uwe na moyo wa upole kwa wanaadamu wote.” – (Gharraul Hikam, uk. 212). Pia anaendelea kusema: “Mwenyezi Mungu anapenda kuona watu wakitakiana heri.” – (Ghurrarul Hikam, uk. 271). Mapenzi juu ya ubinadamu na ukarimu vilikuwa ni moja ya sifa muhimu kabisa ya Mitume wa Mwenyezi Mungu na viongozi wa kidini. Walikuwa wanapenda kuona ustawi na furaha za wanaadamu na walikuwa wakihuzunishwa na upotofu na ujinga wao. Nukta inayopaswa kudokezwa hapa ni kuwa wakati Uislamu unahimiza urahimu na wema kwa watu wote bila kujali rangi zao na nchi zao, pia Uislamu unaamini kuwa ili kujenga mafungamano imara na yenye kudumu zaidi ni muhimu pawepo msingi thabiti na imara ambao kamwe haupaswi kutingishika na unaopaswa kuwaunganisha na kuwakusanya wanaadamu wote pamoja. Uislamu haulichukulii wazo la kwamba lugha moja, nchi moja, rangi moja n.k. kama njia nzuri na ya kuaminika ya kuleta upendo na umoja kwa sababu ingawa vitu hivi vinaweza kuwa ni sababu ya mahusiano mazuri kwa kiasi fulani, lakini mambo mazito zaidi kama vile tofauti kubwa ya 135

12:44 PM

Page 135


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

vipato na migogoro, vikiibuka, mafungamano haya yatavunjika na nafasi yake kuchukuliwa uhasama na magomvi. Uislamu unaamini kuwa ikiwa wanaadamu wote watafuata sheria moja na dini moja, basi moyo wa undugu utashika mizizi yake na mahusiano yao yatakuwa ya kindugu na ya dhati hata kama wahusika watakuwa wanatoka katika nchi mbalimbali za wana rangi tofauti, na wanazungumza lugha tofauti. Katika hali hii, hakuna kitakachodhoofisha mahusiano yao au kuzifanya tabia zao kuwa za kiadui. Kutupia macho historia ya siku za mwanzo za Uislamu kunathibitisha mtazamo huu. Siku Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipoteuliwa kwa kazi ya utume akiwa na mafundisho adhimu ya Uislamu kwa ajili ya uokovu wa mwanaadamu, Peninsula ya Arabuni, licha ya ukweli kwamba wakazi wake walikuwa wakizungumza lugha moja, na walikuwa ni wa kabila moja na nchi moja, ilikuwa inaungua katika moto wa vita, uadui na udhalimu na kitu ambacho hakikuwa kinaweza kuonekana katika eneo hilo ni usalama, amani na uhusiano wa kibinaadamu baina ya watu. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alichukua jukumu la kuliongoza taifa hilo na ndani ya muda mfupi, watu wale wale walikuwa mahasimu kwa karne nyingi na waliokuwa wamejijengea tabia ya uhalifu na umwagaji wa damu, wakawa ndugu kwa kila mmoja wao chini ya msaada wa mafundisho ya Uislamu katika namna ambayo hapakubaki chembechembe zozote za roho mbaya, chuki, udhalimu na umwagaji wa damu na badala yake sifa za wema, utakasifu, upendo na huruma na tabia nyingine njema za kibinadamu zilichukua nafasi ya zile tabia za kijahili na zisizofaa. Qur’ani tukufu imeupa uhusiano huu jina la ‘kamba ya Mwenyezi Mungu’ na imesema:

136

12:44 PM

Page 136


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

“Na shikamaneni pamoja katika kamba ya Mwenyezi Mungu (kutafuta ulinzi Wake) wala msifarikiane; na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu, wakati mlipokuwa maadui na akaziunganisha nyoyo zenu, hivyo kwa neema Yake mkawa ndugu, na mlikuwa katika ukingo wa shimo la Moto, lakini Mwenyezi Mungu aliwanusuruni – (Suratul Aali Imran, 3:103). Uhusiano wa kidini na umoja una nguvu sana na mizizi mirefu kiasi kwamba kila Mwislam, awe wa rangi yoyote, awe wa eneo lolote la dunia, huwa hajioni kuwa yeye ametengana na ndugu zake katika imani. Hushiriki katika furaha zao na huzuni zao. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ameuelezea uhalisia huu katika maneno haya: Katika suala la upendo wao, urafiki wao, na hisia zao za moyoni, waumini ni kama mwili mmoja. Kiungo kimoja iwapo kikiumia, viungo vyote hushirikiana nacho katika hali ya maumivu – (Islam wa Huquuq-i Bashar). Qur’ani Tukufu inaona uhusiano huu halisi na usiovunjika kuwa ni uhusiano wa kidugu na imesema:

“Kwa hakika waumini ni ndugu. Rejesheni amani miongoni mwa ndugu zenu Muogepeni Mwenyezi Mungu ili mpate kurehemewa.” – (Suratul Hujurat, 49:10). 137

12:44 PM

Page 137


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Kuhusiana na fungamano hili, inakuwa ni muhimu kusimamisha uhusiano ulijengwa juu ya upendo wa dhati ili waislamu wapendane kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Imesimuliwa kutoka kwa Imam Ja’far Sadiq kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: “Mwenyezi Mungu anao waja wake ambao Siku ya Kiyama watapata nafasi chini ya kivuli cha Huruma na Neema Zake. Nyuso zao zitakuwa nyeupe sana na zinzaong’ara kama jua. Hao ni watu waliopendana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na walikuwa wakihurumiana.” – (Huquuq-i Islami, uk. 304). Ili mshikamano huu wa udugu usivunjike, Uislamu umetoa na kuhimiza miongozo ya kuuimarisha, na ukaelekeza kwa mkazo sana kuichunga , kama vile kusalimiana na kupeana mikono, kuwatembelea ndugu, marafiki na wagonjwa, kuonyesha huruma na upendo, vitendo vya ukarimu na kutoa misaada, kutoa huduma kwa umma, ukaribishaji na urahimu na kufanya jitihada katika kukidhi mahitaji ya wengine. Uislamu pia umekataza matendo yote yanayosababisha kuvunjika kwa moyo wa udugu na umewaonya Waislamu dhidi ya kuyafanya hayo, kwa mfano kutowajali watu, kusengenya, kutafuta makosa ya watu, kuwachokoza na kuwaudhi wengine, kuteta na kudodosa mambo ya wengine, dharau na kufoka, kutokuwa na ushirikiano, dhihaka n.k. Hapa tutataja kwa kifupi baadhi ya matendo yaliyohimizwa na yale yaliyokatazwa katika Uislamu ambayo yana uzito mkubwa katika mahusiano ya kijamii, pia tutanukuu mifano michache ya baadhi ya hadithi za viongozi watukufu wa Uislamu.

Kuleta Furaha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Anayemfurahisha Muumin huwa amenifarahisha mimi.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) pia amesema: “Kitendo kinachopendwa na Mwenyezi Mungu zaidi ni kumfurahisha Muumini.” – (Jami’us Sa’adat, Juz. 2). 138

12:44 PM

Page 138


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Kukidhi Mahitaji ya Watu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: “Thawabu anazopata mtu anayekidhi mahitaji ya ndugu yake muumini ni sawa na mtu aliyemwabudu Mwenyezi Mungu kwa amri wake wote.” – (Wasailush-Shi’ah). Imam Musa Kadhim amesema: “Mwenyezi Mungu ana waja katika huu uso wa ardhi ambao hufanya jitihada za kukidhi mahitaji ya watu. Hao watasalimika na ugumu na taabu za Siku ya Kiyama.” – (al-Kafi). Kutatua matatizo na kukidhi mahitaji ya wengine kuna athari kubwa katika kujenga upendo na kuimarisha uhusiano mzuri baina ya watu na mara nyingi tabia hizi huishia katika kujenga urafiki wa karibu.

Kusengenya Moja ya laana ambazo huleta madhara makubwa katika mahusiano ya kijamii na ambayo inalaaniwa vikali na Uislamu ni kusengenya. Qur’ani Tukufu imesema: “Msichunguzane wala kusengenyana – (Suratul Hujurat, 49:12). Katika moja ya hotuba zake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwakemea wasengenyaji na alisema: “Enyi watu mnaoielezea imani yenu katika ndimi zenu ilihali mioyo yenu ikiwa haiitambui imani hiyo! Msifungue midomo yenu kuwateta Waislamu na msitake kugundua makosa yao kwa sababu mtu anapododosa makosa ya Mwislam mwenzake, Mwenyezi Mungu huichana pazia yake (hayo msengenyaji) huyaanika makosa yake na humfedhehesha.” – (Jami’us-Sa’adat). Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: “Mkutano wowote ambao hunawiri na kushamirisha usengenyaji na utetaji utatelekezwa kwa mtazamo wa kidini. Enyi Waislamu! Yaepusheni masikio yenu na kusikiliza kwani yule anayesengenya na yule anayesikiliza wote ni washirika katika dhambi – (Ihya’ul Ulum, Juz. 3). 139

12:44 PM

Page 139


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Mchambuzi wa mambo ya kisaikolojia mmoja amesema: “Yule anayewasengenya wengine hatimaye hupatwa na fedheha na matatizo kwa sababu maneno yake huwafikia hao anaowasengenya na matokeo yake hupoteza marafiki. Yule anayemsikiliza huchoka kusikiliza ukosoaji wake na mazungumzo yake ya kiuovu. Inawezekana usengenyaji ukawa tabia kiasi kwamba mtu huanza kuwasengenya wengine bila kukusudia katika kila mkusanyiko wa watu. Kuwateta wengine huonyesha kuwa huyo msengenyaji anawaonea wivu wenzake na anajitahidi kujionyesha kuwa yeye ni bora kuliko wengine na kuwatambulisha wengine kuwa ni duni kwake. Na pia mtu anapokuwa hajiamini na ana mashaka juu ya thamani na nafasi yake hukimbilia kuanza kuzungumzia mabaya juu ya wengine.

Kuwakosea watu wengine Kuwakosea na kuwaudhi watu huharibu uhusiano baina ya mtu na mtu, huharibu upendo na maelewano, hujenga chuki na huwafanya watu kuwa na kinyongo na kutaka kulipiza kisasi. Katika kanuni za Kiislamu, Waislamu wamekatazwa kabisa kuwaudhi au kuumiza hisia za wengine. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: “Mwislam ni yule ambaye Waislamu wengine huwa wako salama na mikono yake na ulimi wake – (Huquuq-i Islami). Hii ni kusema kwamba Mwislam hapaswi kuwadhuru wengine kwa mikono yake na pia asiwaudhi watu kwa ulimi wake. Sehemu nyingine imeripotiwa kuwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: “Mwislam hapaswi kumtazama ndugu yake mwislam katika namna ambayo itamuudhi (huyo anayetazamwa) – (Jami’us-Sa’adat, Juz. 2). Hii ina maana kwamba Mwislam hapaswi kumuudhi na kumkasirisha Mwislam mwenzake kwa kumtazama kwa hasira, kejeli au dharau n.k.

140

12:44 PM

Page 140


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Pia amesimiliwa kuwahi kusema: “Ikiwa mtu atamuonyesha dharau muumini, Mwenyezi Mungu huendelea kumkasirikia mtu huyo mpaka atakaporekebisha kosa lake la utovu wa heshima.” – (Ihya’ul Uluum, Juz. 2).

Kutafuta Makosa ya Wengine: Kuna mwelekeo usiopendeza katika tabia ya baadhi ya watu ambayo huwafanya wadodose na kuchunguza mambo binafsi na siri za watu. Mwelekeo huu huleta matukio yasiyofaa ambayo kwanza kabisa huwaathiri wale walionao na huwasukumia kwenye mabalaa. Sababu ambayo humfanya mtu aanze kutafuta makosa ya wengine ni hali ya kutojiamini na hivyo mtu huamua kufichua dosari za wengine ili aweze kujijengea amani ndani ya nafsi yake. Hata hivyo huwa anasahau ukweli kwamba tabia hiyo huwafanya watu wamdharau na kumchukia. Hupoteza marafiki zake na kuharibu uhusiano wake na wenzake. Kama watu hawa wanapoteza nguvu nyingi kutafuta makosa ya wengine, kama wangetumia uwezo huo katika kuzitambua na kuzitibu dosari zao, wangeweza kupata matokeo mazuri sana. Ili kuhakikisha panakuwepo mahusiano mazuri ya kijamii, Uislamu umekataza tabia ya kutafuta dosari za watu kwa sababu hiki ni chanzo na utengano wa ugomvi na umewaonya Waislamu kujiepusha na tabia hii. Imam Muhammad Baqir amesema: “Ili kuthibitisha dosari za mtu hautoshelezi kuchunguza dosari za wengine na kuzisahau za kwake au kuwakemea wengine kwa kitendo ambacho yeye mwenyewe anashindwa kukiepuka au unawabughudhi rafiki zake kwa mambo yasiyomhusu.” – (al-Kafi, Juz. 2). Imam Ali (a.s.) amesema: “Yeyote ambaye ni mdadisi juu ya dosari za watu anatakiwa aanze kazi hiyo kwa kujidadisi yeye mwenyewe.” Imam Ali (a.s.) ana maoni kwamba mtu mwenye tabia ya kutafuta makosa ya 141

12:44 PM

Page 141


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

watu hafai kufanya naye urafiki na amewaonya watu kwa maneno haya: “Jiepusheni kutangamana na watu wenye tabia ya kuchunguza makosa ya wengine, kwa sababu hata rafiki zao huwa hawasalimiki na madhara yao.” – (Ghurarul Hikam).

Dhihaka: Dhihaka ni kutafuta dosari ambayo mwenye nayo hakuichagua na ambayo haiwezi kuondoka, kwa mfano tajiri humdhihaki maskini, mwenye sura nzuri humdhihaki mwenye sura mbaya, mwenye nguvu humdhihaki mtu dhaifu. Tabia hii chafu, yaani kudhihaki wengine inapandikiza mbegu ya uadui kwa sababu yule mtu anayedhihakiwa anashushwa hadhi mbele ya macho ya watu na hisia zake kuumizwa. Qur’ani Tukufu imesema:

“Enyi mlioamini, kundi moja (miongoni) mwenu lisilidhihaki jingine. Inawezekana hao mnaowadhihaki ni bora kuliko nyinyi.” – (Suratul Hujurat, 49:11). Hii ni kwa sababu, katika Uislamu kigezo cha ubora na wema sio mali, nguvu, uzuri n.k. isipokuwa hadhi na heshima (uchamungu) aliyonayo mtu mbele ya Mwenyezi Mungu. Uislamu, ambao ni dini inayopendelea heshima na hadhi kwa watu wote, hauruhusu kabisa hadhi na heshima ya mtu yeyote kuvunjwa na kuchafuliwa. Uislamu ambao unawachukulia waislamu wote kuwa ni ndugu, na unapenda kuona maendeleo ya uhusiano wao hivyo umefanya kampeni dhidi ya tabia hii isiyofaa na umewaonya wafuasi wake dhidi ya tabia hii. 142

12:44 PM

Page 142


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Kwa kawaida kuna aina mbili za watu wanaowadhihaki wengine: Kwanza, wale ambao ni wabinafsi, wanaojivuna na wenye wivu. Wanataka kujionyesha mbele za watu kuwa wao ni watu mashuhuri na wenye kuheshimika na wengine ni watu duni na wasio na thamani. Pili, ni wale ambao kazi yao ni kuwakebehi wengine na ambao lengo lao ni kuwafurahisha na kuwachekesha watu. Watu walio katika kundi hili ndio watu ovyo, wabaya kabisa kwa jamii. Imam Sajjad amewaita wachekeshaji na wafanya maskhara kuwa ni ‘mubtil’ (watu wasio na thamani). Siku moja mfanya maskhara mmoja alinyakua joho la Imam Sajjad kutoka mabegani kwake na akakimbia. Imam alibakia kimya. Sahaba wake (wa Imam) wakamkimbiza na kulirejesha joho kwa Imam. Imam aliuliza, “Alikuwa ni nani?” Alijulishwa kuwa ni mtu wa maskhara ambaye kazi yake ilikuwa ni kufurahisha watu. Hapo Imam akasema: “Mwambieni kuwa Mwenyezi Mungu ameweka siku maalumu (yaani Siku ya Kiyama) ili kupima amali njema na mbaya za watu na wale wanaojiingiza katika upuuzi kama huu, siku hiyo watakuwa ni wenye hasara.” – (Manaqib ibn Shehr Ashub. Juz. 2). Wale wanaowasikiliza wachekeshaji na kuwacheka wale wanaokejeliwa, wanapaswa kukumbuka kuwa wao pia ni washirika katika tabia hii ya uovu, kwa sababu wao wasipocheka, hao wachekeshaji biashara yao haiwezi kuchangamka kwa kuwadhuru watu. Kilichoelezwa hapa ni maelezo mafupi tu juu ya mafundisho ya Uislamu katika suala la ujenzi wa mahusiano mazuri katika jamii, jambo ambalo huwafanya watu waishi kwa salama na amani na jamii hupata mguso wa kibinadamu. Nukta ambayo inapaswa kudokezwa hapa mwisho ni kuwa Uislamu unawaita na kuwataka watu wawe na sifa njema kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na wema. Wanapaswa kuacha tabia chafu na badala yake wawe waaminifu, wakarimu na wapole kwa ajili ya ubinadamu na sio kwa ajili 143

12:44 PM

Page 143


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

ya kujipatia fedha na raha za dunia. Ni kwa sababu hii kwamba wale waliofundishwa chini ya mwongozo wa Uislamu, katika hali yoyote huwa hawapotoki katika mienendo yao ambayo huwa inaendana na mafundisho ya Uislamu na mabadiliko ya hali za maisha huwa hayawabadilishi chochote ambapo mwenendo wa wale waliofundishwa katika shule za kisekula hubadilika kwa kadri mambo yanavyobadilika kati ya matumaini na hofu katika maisha yao, kwa sababu mafunzo bila msaada wa kuyaimarisha huwa hayadumu. Ni muhimu kwa wale wanaopendelea masuala ya ustawi wa jamii wanapaswa kuwafundisha watu juu ya majukumu ambayo Uislamu umewapangia, ili kwa Rehema za Mwenyezi Mungu, jamii ya Kiislamu iweze kuwa jamii bora kuliko zote za wanaadamu. Qur’ani tukufu imesema: “Kwa hakika mtakuwa bora kuliko wote ikiwa mtakuwa waumini wa kweli. – ªSuratul Aali Imran, 3:139). NUKUU 1). Enyi mlioamini, kuweni na subira, saidianeni katika kusubiri na jengeni mahusiano mazuri baina yenu na Menyezi Mungu mpate mafanikio ya kudumu – (Qur’ani Tukufu). 2). Yule anayeianza siku bila kufanya jitihada katika masuala yenye maslahi na Waislamu, huyo sio mwislam. 3.

Mwislam ni yule ambaye Waislamu wenzake wamesalimika kutokana na mikono yake na ulimi wake.

4). Mtu anayependwa zaidi na Mwenyezi Mungu ni yule mwenye manufaa zaidi na watu – ªMtukufu Mtume (s.a.w.w.).

144

12:44 PM

Page 144


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

ADABU ZA KIJAMII Kitu chenye umuhimu mkubwa katika maisha ya kijamii ni kuwepo kwa mahusiano mazuri, uaminifu na utulivu baina ya watu. Tatizo kubwa kabisa la ulimwengu wa leo halipo katika chakula, mavazi na malazi bali katika mahusiano baina ya watu na jamii mbalimbali. Tatizo hili linazikumba pia nchi mbali mbali juu ya jinsi gani zidumishe uhusiano na nchi nyingine, na halikadhalia mtu mmoja mmoja juu ya ni jinsi gani avumiliane na wenzake. Kwa bahati mbaya maneno; “kuishi pamoja kwa amani� hayajatatua tatizo hili na hakuna dalili ya kupatikana ufumbuzi – isipokuwa katika mihadhara na makala ya baadhi ya watu. Kila siku moto wa vita huwashwa katika sehemu mbalimbali za dunia ambayo hutafuna idadi kubwa ya wanaadamu na kuziacha familia nyingi zikiwa hazina waangalizi na zikisononeka. Tofauti ndogo zinazotokea baina ya watu wa mji mmoja au eneo moja na wakati mwingine kati ya watu wa familia moja, zote hizi zinaashiria tatizo hili. Kwa kusema kweli, kama mahusiano ya wanaadamu hayakujengwa juu ya msingi wa imani na mafundisho ya kiroho, kiini cha tatizo kitaendelea kuwepo na haitawezekana kulitatua tatizo hili. Uislamu ambao ni dini tukufu na ya ki-Mungu, umezingatia umuhimu wa mafunzo na kuwabadilisha watu ili kutatua tatizo hili na pia umeweka msingi wa mafunzo haya katika imani juu ya Mwenyezi Mungu na kuimarisha moyo maadili na utu.

145

12:44 PM

Page 145


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Kanuni za Uislamu katika suala hili zina uwezo mkubwa wa uangalifu kiasi kwamba kama watu watazitekeleza muundo na hali ya maisha yao vitang’aa na ushirikiano na kutangamana kwao na watu kutachukua sifa za kibinadamu. Katika hatua ya mwanzo, Uislamu umejitahidi kuwafanya watu waelewe ukweli kwamba wao wote ni kizazi cha baba mmoja na mama mmoja na hakuna mwenye ubora wowote dhidi ya mwenzake. Utaifa wa Weupe, weusi, wa njano na wekundu na kama kanuni ya jumla, rangi ya ngozi ya mwili na uso haiwezi ikawa ni kigezo cha ubora wa taifa moja dhidi ya jingine. Tofauti ya lugha na lahaja haziwezi kulifanya taifa moja kuwa bora kuliko jingine. Lakini kwa mujibu wa Uislamu, imani, uchamungu, elimu, uaminifu na unyoofu wa tabia vinaweza kuwa ni chanzo cha ubora wa mtu au jamii. Qur’ani Tukufu imeeleza waziwazi:

“Enyi watu! tumewaumbeni wanaume na wanawake na kuwaweka katika mataifa na makabila mbalimbali ili mjueane. Anayeheshimiwa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu mchamungu zaidi. Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa yote, mwenye habari zote – (Suratul Hujurat, 49:13). Katika aya nyingine:

“Mwenyezi Mungu atawanyanyua madaraja wale walioamini na wale waliopewa elimu. Mwenyezi Mungu anayajua yote mnayoyafanya.” (Suratul Mujadilah, 58:11).

146

12:44 PM

Page 146


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Hakuna Mwarabu mwenye ubora dhidi ya asiyekuwa Mwarabu (na hakuna taifa lililo bora kuliko jingine) isipokuwa kwa sababu ya kigezo cha uchamungu.� Wanadamu wanapoutambua ukweli huu, hitilafu na tofauti nyingi zinazotokana na ubinafsi na kujipendelea kwa kipumbavu zitatoweka na uhusiano wao utachukua sura mpya. Maoni haya ni sahihi katika kiwango cha kitaifa na kimataifa na pia yataondoa uhusiano wa kiadui na madhara yake yanayoibuka katika masuala ya ndani ya nyumba. Kinachopaswa kuzingatiwa katika mjadala huu ni kuwa familia za Kiislamu na Waislamu wanaaswa kuelewa mafundisho ya kijamii ya Uislamu ili kwa kuyatekeleza waweze kupata faida kubwa na nzuri zaidi ili uhusiano mzuri baina yao uweze kuimarishwa. Kuna watu wengi ambao wanataka kutangamana na wengine lakini kwa sababu ya kutojua kwao wajibu wa kijamii, wanalazimika kujitenga na wengine na hivyo hukosa nafasi zao katika jamii. Lenyewe ni jambo muhimu sana kujua ni jinsi gani maelewano mazuri na ya kirafiki yanaweza kudumishwa baina ya watu katika nyanja zote za maisha. Tunajua baadhi ya watu katika jamii ambao ni maarufu sana na kila wanakokwenda watu huonyesha kuwapenda sana. Kwa upande wa pili tunaliona kundi la watu ambao hakuna anayewajali na hawapendwi na watu. Katika kujibu swali la kwamba kwa nini baadhi ya watu ni maarufu sana na wengine sio maarufu tunaweza kujiridhisha kwa kusema kuwa tabia na sifa binafsi za kila mtu ni tofauti na za wengine na hutegemeana na tabia ya asili ya mtu iwapo ni maarufu au vinginevyo. Hata hivyo, wanasaikolojia hawalioni jibu hili kuwa ni sahihi na wanaamini kwamba, hutegemeana na mwenendo wa watu mbalimbali kama ni maarufu au la. Ni watu wenyewe ambao wanapaswa kujenga tabia zao kwa mwenendo mzuri na 147

12:44 PM

Page 147


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

kutekeleza wajibu wao wanapotangamana na wengine ili wafurahie urafiki na upendo wa watu.

1. KUONYESHA HESHIMA KWA WATU Moja ya jambo muhimu kabisa katika mfumo wa kijamii ni heshima kwa utu wa watu ambayo imezingatiwa vilivyo katika taratibu za maadili ya Kiislamu, na viongozi watukufu wa Uislamu wameitiisha kwa bidii sana. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wa Uislamu alikuwa alizingatia hata mambo yanayoonekana na wengi kuwa ni madogo madogo na yasiyo na umuhimu katika kuonyesha heshima kwa watu na hakuacha kufanya wajibu hata mdogo kabisa katika kuonyesha heshima kwa watu. Alipokuwa akitembelewa na mtu, alikuwa akimpa heshima anayostahili na mara nyingi alikuwa akimtandikia mgeni huyo joho lake ardhini ili akalie na (Mtume) pia alikuwa akimpatia mto wake. – (Biharul Anwar). Siku moja Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa amekaa peke yake ndani ya msikiti. Mtu mmoja alimwendea. Mtume aliondoka pale alipokuwa amekaa ili kumpisha. Yule mtu alisema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Msikiti hauna watu na kuna nafasi nyingi. Kwa nini umesogea kuniachia nafasi?” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alijibu: “Mwislam ana haki juu ya mwislam mwingine kwamba anapotaka kukaa karibu yake, huyo aliyekutwa anapaswa kumpisha huyo aliyekuja kama namna ya kuonyesha heshima.” (Biharul Anwar, Juz. 6). Wakati watu fulani walipokuwa wamekaa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), yeye ili kuhakikisha heshima kwa wote, alikuwa akimtazama kila mmoja wao kwa uchangamfu na kwa usawa. (Rawdhatul Kafi). Kila Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa akifika katika mkusanyiko wa watu, alikuwa akikaa katika sehemu yoyote iliyokuwa wazi na hakujali 148

12:45 PM

Page 148


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

kutafuta sehemu ya umaarufu. Kila alipokuwa akikutana na sahaba zake, mpangilio wa ukaaji ulikuwa wa duara ili pasiwepo nafasi ya hadhi kwa ajili ya mtu yeyote. Mgeni alikuwa akija katika mkusanyiko aliokuwepo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), mgeni huyo alikuwa anashindwa kumtambua Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kati ya waliokaa pale kwa sababu hakuwa na tofauti na wale wengine pale. Hivyo mgeni huyo alilazimika kuuliza ni nani kati ya watu wale aliyekuwa ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Meza za duara zinazotumiwa katika mikutano ya wakubwa na maarufu wa dunia siku hizi ni mfano wa mikutano ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) isipokuwa kwa tofauti moja kwamba lengo la mikutano ya meza za duara leo hii ni kinyume kabisa na alichokuwa nacho mawazoni mwake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wakati alipokuwa akiandaa mikutano yake. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akifanya mikutano yake katika mduara, kwa sababu hakutaka yeye awe na nafasi ya kipekee dhidi ya wengine na ili asiwepo yeyote aliyekaa katika nafasi yenye hadhi ya chini kuliko yake. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alijitahidi kwa nguvu zake zote alizokuwa nazo kuondoa ubaguzi wa kikabila, ubaguzi wa rangi na ubaguzi wa vioja vinginevyo kama hivyo visivyokuwa vya kawaida. Alijaribu kwa uwezo wake wote kuondoa viwango vya bandia ambavyo watu walikuwa wamejibunia katika kujifanya bora kuliko mwingine na badala yake akaweka vigezo vya unyoofu wa moyo na maadili na tabia tukufu za kibinadamu kuwa ndiyo kigezo cha utukufu na ubora.

Heshima ambayo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alionyesha kwa wengine ilimvutia kila mmoja kumfuata. Matabaka yote yalipata upendo wake 149

12:45 PM

Page 149


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

mwingi wa dhati na hakuna aliyedharauliwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) au kupuuzwa. Yeye mwenyewe Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema waziwazi: “Nimetumwa na Mwenyezi Mungu ili kuja kuyaboresha na kuyapandisha maadili ya watu katika kilele chake.” Wakati wa utawala wake, Imam Ali (a.s.) aliwahi kusafiri na mtu asiyekuwa mwislam. Mtu huyo hakuwa akimjua Imam Ali (a.s.). Alimuuliza: “Unakwenda wapi?” Imam alijibu: “Ninakwenda katika mji wa Kufa (moja ya mji ya Iraq).” Walipofika njia panda yule mtu alishika njia yake lakini kinyume chake alishangaa kumuona Imam Ali (a.s.) akizidi kuambatana naye. Hivyo yule mtu akamuuliza: “Je hukusudii kwenda katika mji wa Kufa?” Imam Ali (a.s.) akajibu; “Ndiyo, ninakusudia hivyo.” Yule mtu akamwambia njia inayokwenda Kufa ni ile pale. Imam Ali (a.s.) akajibu: “Ninaijua.” Kisha yule mtu akauliza: “Kwa nini hufuati njia yako?” Imam Ali (a.s.) akasema: Ili kutangamana kwetu na kusafiri kwetu pamoja kuishe vizuri, ni muhimu mmoja wetu amsindikize mwezako umbali fulani na haya ndiyo maelekezo tuliyopewa na Mtume wetu Mtukufu.” Heshima hii ya kweli ilimridhisha sana yule mtu asiyekuwa muislam na akauliza: “Je Mtume wenu alielekeza hivyo?” Imam Ali (a.s.) akajibu, “Ndiyo.” Mtu huyo akasema: “Wale waliomfuata Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wamepambwa na mafundisho yake ya kimaadili na tabia ya upole.” Kisha aliacha njia yake na kuambatana na Imam Ali (a.s.) kuelekea Kufa. Alizungumza masuala kadhaa na Imam Ali (a.s.) juu ya Uislamu na hatimaye akasilimu.” – (al-Kafi, Juz. 2; Kurbul Asnad; Biharul Anwar, Juz. 74). Kuonyesha heshima kwa watu ni muhimu sana katika utaratibu wa kijamii wa Uislamu, kiasi cha Qur’ani tukufu kumwagiza Mtukufu Mtumke kuwa:

150

12:45 PM

Page 150


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

“Waambie waja wangu kuzungumza maneno yaliyokuwa mazuri, kwa hakika shetani anapanda mfarakano miongoni mwao. Kwa hakika yeye ni adui wa wanaadamu aliye dhahiri – (Surat Bani Israil, 17:53). Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: “Usimdharau na kumshusha Mwislam yeyote, kwa sababu mwislmu hata awe mdogo kiasi gani, ni mkubwa mbele ya Mwenyezi Mungu.” Imam Muhammad Baqir amesema: “Waheshimu rafiki zao na wachukulie kuwa ni watu wenye kuheshima na msizozane na yeyote katika namna isiyokuwa ya upole.” Baadhi ya watu hutangamana na rafiki zao katika namna inayodaiwa kuwa ni ya kirafiki lakini hupuuza wajibu wa kuheshimiana kwa kisingizio cha urafiki, licha ya ukweli kwamba tabia hii hudhoofisha msingi wa urafiki na hujenga utengano. Imam Ali (a.s.) amesema: “Ili kuuhifadhi urafiki uliopo baina yenu, kamwe mmoja wenu asivunje haki za rafiki yake sababu mtu ambaye umemvunjia haki zake, hawezi kubakia kuwa rafiki yako.” – (Biharul Anwar, Juz. 74). Baadhi ya watu wajinga hufikiri kwamba moja ya njia za kuimarisha urafiki kati ya watu wawili ni kutumia lugha chafu na za kihuni zaidi na kwamba hawapaswi kuacha kushutumiana vikali. Wanaichukulia njia hii kwamba ndio namna ya kudumisha mahusiano ya karibu ya urafiki, ingawa kuwakejili na kuwabeza marafiki sio jambo linalopendeza na matendo haya mawili yasiyofaa hayawezi kuchukuliwa kwa ushabiki au kuwa ni uthibitisho wa urafiki wa karibu.

151

12:45 PM

Page 151


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Aristotle anasema: “Ili kuhakikisha udumishaji wa urafiki ni muhimu kwa marafiki kuelewa uadilifu na thamani ya kila mmoja wao na wautazame kwa heshima. Ikiwa marafiki mawili kila mmoja wao hatabaini wema na mambo mazuri ya mwenzake na kuyaheshimu, ni vipi wanaweza kudai kuwa wana urafiki wa dhati na uaminifu? Upole haumpunguzii mtu chochote, lakini badala yake unabeba faida nyingi. Malengo ambayo hayawezi kufikiwa kwa kutumia mali, yanaweza kupatikana kwa kutumia upole. Mtu mmoja aliyekuwa akiitwa Zuhari alikwenda kwa Imam Sajjad, akiwa na uso mzito wenye ghadhabu na moyo uliovunjika. Imam alimuuliza juu ya sababu ya sononeko lake. Alijibu: “Ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu! Nimezingirwa na huzuni na sononeko. Watu wenye wivu wasiotaka kuniona nikiishi kwa raha wananisababishia huzuni kwa tabia zao. Maadui zangu na watu waovu ambao wananihuzunisha, na kuna watu niliwatumikia na niliotarajia kuwa na urafiki nao lakini wananidhihaki.” Mtukufu Imam alisema: “Ewe Zuhari! Uchunge ulimi wako na usizungumze kila kinachokuja kichwani mwako ili usije ukapoteza rafiki zako na kuwafanya kuwa adui zako.” Zuhari akasema: “Ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu! Ninawatumikia watu hao na ninafanya wema kwa kuzungumza nao maneno mazuri.” Imam akasema: “Sio hivyo, Uepuke kusema mambo ambayo akili za watu haziko tayari kuyakubali.” Kisha akasema: “Ewe Zuhari! Kila asie na hikma timilifu huangamizwa kwa sababu ya mambo madogo kabisa.” Kisha Imam alimpa Zuhari ushauri ambao kama angeutekeleza asingehuzunishwa na mambo anayofanyiwa na watu: “Ewe Zuhari! kuna ubaya gani kama utawachukulia Waislamu wote kuwa ni familia yako na ni 152

12:45 PM

Page 152


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

ndugu zako? Unapaswa kuwachukulia watu wenye umri mkubwa kuwa ni baba zako, na wadogo kuwa ni watoto wako na wale unaolingana nao kuwa ni ndugu zako. Utakapochukua uamuzi huo, ni nani kati ya hao utakayekuwa tayari kumlaani? Je ungependa yeyote kati ya hawa afedheheke? “Ewe Zuhari! Ikiwa utapata wazo kuwa wewe ni bora kuliko yule na yule, inafaa ujishauri kwamba: Kama huyo ni mkubwa kuliko wewe, basi jikumbushe kwamba, ‘Ana kipaumbele juu yangu katika Uislamu na imani na amefanya amali njema nyingi zaidi kuliko mimi.’ Na kama ni mdogo kuliko wewe, basi jikumbushe kwamba: ‘Amefanya madhambi machache kuliko mimi’. Na kama ni wa makamu yako jikumbushe kwamba: ‘Ninazijua dhambi zangu lakini sizijui dhambi alizotenda yeye.’ Ikiwa watu wakikustahi na kukuheshimu, sema: “Ni kutokana na hisani ya watu wenyewe tu.” Na kama ni wakatili na wakali kwako sema: “Hii kwa sababu ya makosa niliyoyafanya.” Ukifuata njia hii maisha yako yatakuwa mazuri na utapata marafiki wengi na idadi ya maadui itapungua. Pia unapaswa kukumbuka kuwa watu humheshimu zaidi mtu ambaye huwa anawafanyia wema zaidi na hataki chochote kutoka kwao.” – (Biharul Anwar, Juz. 74). Kutokana na hayo yaliyosemwa hapo juu, moja ya siri muhimu kabisa za mafanikio katika maisha ya kijamii, kwa mtazamo wa Uislamu, ni kuonesha heshima kwa watu na kuwa mpole kwa kila mmoja. Zimepokelewa hadithi nyingi juu ya hili, lakini tutakazozitaja hapa chini ni baadhi yake tu.

153

12:45 PM

Page 153


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

II: KUWASTAHI WATU KWA ADABU Moja ya mafundisho ya kijamii ya Uislamu ni kuwa mtu anapaswa kuishi na kutangamana na watu kwa uungwana, wema na upole. Qur’ani tukufu inazungumzia tabia ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa kusema:

“Basi kwa sababu ya Rehema ya Mwenyezi Mungu umekuwa laini kwao na kama ungekuwa mkali na mshupavu wa moyo, wangekukimbia wote – (Suratul Aali Imran, 3:159). Katika aya hii takatifu, imeelezwa kwamba moja ya sababu za watu kuvutika kwa Mtume wa Uislamu ilikuwa ni upole wake na bila shaka mioyo ya watu huvutiwa na mtu mwenye sifa hii. Watu huchukia watu wakali na wanaoghadhibika kirahisi na watu wa aina hii hulazimika kuishi maisha ya kutengwa. Kwa kawaida watu huboronga wanapokutana au kutangamana na wenzao au hufanya mambo yanayopingana na matakwa ya kibinaadamu. Ni katika mazingira kama haya kwamba msamaha na kujiachia huru vinapaswa kuingia kati na kuzuia ukali na ukatili. Imam Ja’far Sadiq aliwahi kuulizwa: “Ni masharti gani ya kuwa na tabia njema? Alijibu: “Kuwa mpole na rahimu, kuzungumza maneno mazuri na mtu kukutana na ndugu yake katika imani akiwa na uso uliokunjuka na wenye furaha.” Imam Ali (a.s.) alipokuwa akimpa ushauri mtoto wake, Imam Hassan, alisema: “Jiandae kwamba pindi marafiki zako wasio waaminifu wakivun154

12:45 PM

Page 154


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

ja uhusiano na wewe, unapaswa ubakie kuwaamini na unapaswa kuendelea na uhusiano wako kwao na wasipokuchangamkia, wakiwa wakali kwako au wakijitenga na wewe, unapaswa wewe kuwa msamehevu na kuonyesha urafiki na unapaswa kujikurubisha kwao, na wakikuonyesha ukali na ukatili, wewe unapaswa kuonyesha upole na uungwana na wakifanya makosa, wewe unapaswa kukubali kuomba msamaha kwao na unapaswa utangamane nao kwa namna ambayo kana kwamba wana haki juu yako. Hata hivyo, unapaswa kuwa mwangalifu unapotwaa sera hii kuhusiana na wewe na unapaswa uitekeleze kwa wale wanaostahili tu.” Kupoteza udhibiti wa hasira na kuwaumiza watu kutokana na hasira zake mtu huwa ni sababu ya mtu kushindwa kudumisha mahusiano mazuri na marafiki zake. Bali huwa ni kawaida kwamba kutokana na msukumo wa silika zake za kutaka kutawala, mwanaadamu huyu huwaadhibu wengine kwa sababu ya makosa yao lakini akili ya kawaida inaamuru kwamba utaratibu huu haufai kwa sababu adhabu huwa haitoi matakeo yanayohitajika. Haiwezekani kuwaadhibu na kuwabadilisha wengine kwa ukali na ikiwa kuna njia nyingine ya kuweza kufanikisha lengo hili, basi ni ile iliyoshauriwa na Qur’ani tukufu, na imehimizwa sana na viongozi wa Uislamu. Njia waliyoielekeza wao ni kutangamana na watu kwa upole na urahimu na kuwaongoza kwa kutumia maneno mazuri na kufanya vitendo vizuri. Qur’ani tukufu ikikumbushia maelekezo aliyopewa Nabii Musa na ndugu yake Harun walipotakiwa kwenda kumuongoza Firauni inasema:

“Nendeni kwa Firauni; bila shaka amepitukia mipaka. Na kamwambieni maneno laini, huenda akashika mawaidha au akaogopa.” – Suratut-Taha, 20:43 - 44). 155

12:45 PM

Page 155


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Dale Carnegie anasema: “Ikiwa hasira yako itapanda na ukatamka maneno ya hasira, utahisi nafuu kwa kuwa utakuwa umezitoa hisia zako za hasira. Lakini vipi kuhusu ule upande wa pili (huyo uliyemwambia hayo maneno)? Je yeye pia atapata furaha kama yako? Je maneno yako makali ya kulipiza kisasi na tabia yako ya kiadui yatafanya mambo kuwa rahisi kwake kiasi cha kuwa na uhusiano wa kirafiki na wewe? Woodrow Wilson anasema: “Ukinijia ukiwa umekunja ngumi, ninakuhakikishia kuwa mimi pia nitakunja ngumi mara moja. Lakini ukija na kusema: Njoo, hebu tukae chini pamoja na kujadili masuala haya, na kama tuna tofauti zozote basi hebu tuangalie hizi tofauti zimekujaje, na ni nini hasa asili ya tofuaiti hizi; punde tu tunabaini kuwa hatutofautiani sana, na mambo tunayotofautiana ni madogo sana yasiyo na maana na tutakuta tunakubaliana katika mambo mengi. Tunaweza na tunapaswa kukubaliana kwa subira, uaminifu na hisia za kutaka maelewano.” (How to win friends and influence people). Mtu mmoja alikwenda kwenye hadhara ya Imam Sajjad, pakiwa na watu wa matabaka mbalimbali. Kutokana na kinyongo alichokuwa nacho dhidi ya Imam, alianza kumkashifu Imam na kusema mambo yasiyo na kichwa wala miguu na kisha akaondoka. Muda mfupi baada ya mtu huyo kuondoka, Imam aliwageukia watu waliokuwepo na kusema: “Mmeaona jinsi mtu huyu alivyokuwa fidhuli dhidi yangu na mmesikia maneno aliyoyasema! Sasa nataka kwenda na nyinyi kwake ili nikampe jibu kwa aliyoyasema.” Watu wote walikubali. Mtukufu Imam na masahaba zake waliodoka kuelekea kwenye nyumba ya mtu huyo. Watu wote walifikiri kuwa Imam angemjibu kwa maneno makali sana. Lakini walimsikia akisoma aya ifuatao kwa sauti ya chini:

156

12:45 PM

Page 156


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

“Na wale wanaozuia hasira zao na kuwasamehe watu. Mwenyezi Mungu anawapenda watu waongofu.” – (Surat Aali Imran, 3:134). Waliposikia hivi walitambua kuwa Imam hakuwa na nia ya kulipiza kisasi. Baada ya kufika kwenye nyumba ya mtu huyo walimwita. Alipojua kuwa Imam alikuwa amekuja na kundi la masahaba, alipata yakini kwamba Mtukufu Imam alikuwa amekwenda kumuadhibu. Pia alijiandaa kwa lolote ambalo lingeweza kutokea na alitoka nje na nyumba yake. Hata hivyo, kinyume na matarajio yake, alikuta kwamba uso wa Mtukufu Imam ulikuwa umejaa upole na bashasha. Mtukufu Imam akasema: “Saa moja lililopita ulikuja kwangu na kunitamkia maneno yasiyofaa. Nimekuja kukuambia kwamba kama umesema ukweli na kama uovu uliyodai ninao ni kweli ninao basi ninamuomba Mwenyezi Mungu anisamehe, lakini kama umesema uongo na umenituhumu kufanya mambo ambayo sikuyafanya basi ninamuomba Mwenyezi Mungu akusamehe na apuuze dhambi zako.” Yule mtu alijikuta akiwa hana la kusema mbele ya tabia hii ya kikarimu na alimuomba radhi Imam na alisema: “Ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu! Hakuna hata kitu kimoja kiovu katika nilivyokutuhumu ambacho ni cha kweli. Kwa kusema kweli mimi ndiye ninayestahili kuwa na mambo hayo niliyokutuhumu.” Kwa njia hii Mtukufu Imam alimlazimisha adui yake kuwa rafiki yake na hivyo akawa ametoa mfano kwa wafuasi wake kuwa wanapaswa kuwa watulivu pindi wanapochokozwa na wapuuze vitimbi vya wachokozi – (Irshad-i Mufid, Juz. 2). Kwa kusema kweli, fundisho hili ni moja ya mbinu muhimu kabisa katika medani ya mwenendo wa kijamii na ambalo limezingatiwa sana katika mafundisho ya Uislamu. Wafuasi wa Qur’ani tukufu wanapaswa kuendeleza mwenendo wa tabia ya kupendeza ya namna hii ili wanufaike na faida zake. 157

12:45 PM

Page 157


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

III. KUWA MUUNGWANA N A MWENYE STAHA Moja ya mambo yanayoleta matokeo mazuri katika mwenendo wa kijamii na ambayo humfanya mtu kuwa mashuhuri miongoni mwa watu ni unyenyekevu na staha. Sio tu kwamba unyenyekevu huwa hauharibu hadhi ya mtu bali pia huwa sababu ya ubora zaidi. Kitu ambacho huwafanya watu wamchukie mtu ni kiburi chake (kujisikia) na majivuno kwa sababu vitu hivi humzuia mtu kuonyesha heshima kwa watu na hupanda mbegu za chuki na uadui. Katika kuwasifu wachamungu. Qur’ani tukufu inasema:

“Miongoni mwa waja wa Rahmani ni wale wanaotembea kwa unyenyekevu katika ardhi na wajinga wanaposema nao, wao husema amani.” – (Suratul Furqaam, 25:63). Inamaanisha kwamba waja wema na watukufu ni wale ambao wanaendesha maisha yao katika uso wa ardhi kwa heshima na staha na bila ubinafsi na urasimu na wanaposikia maneno yasiyo na maana kutoka kwa wenye kiburi, wao hawatoi majibu mabaya na hawaoyeshi tabia kama zile za watu wajinga. – (Tafsir Majam’ul Bayan, Juz. 4, uk. 178) Tabia ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Maimamu wa Ahlul-Bayt ilikuwa imejengwa juu ya kanuni hii hasa. Walikuwa wakitangamana na watu wa kutoka katika matabaka ya maskini na mafukara, walikaa pamoja nao kwa ajili ya kula chakula na waliwatendea kama ndugu. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipiga kampeni kabambe dhidi ya umimi na ubinafsi wa watu na kila hali iliporuhusu, aliwafundisha somo la staha na uungwana. Siku moja alipokuwa amekaa katika hadhara yake na masaha158

12:45 PM

Page 158


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

ba zake wakiwa wamekaa katika mduara, Mwislam aliyekuwa masikini na aliyekuwa amevaa nguo zilizochanika chanika aliwasili na kwa mujibu wa desturi ya Kiislamu ni kwamba mtu anapowasili katika mkusanyiko wa watu, bila kujali hadhi yake, alikuwa akipaswa kukaa sehemu yoyote yenye nafasi na hakupaswa kutafuta sehemu inayoendana na hadhi yake ya kijamii, yule mtu alitupa macho huku na kule na alioa nafasi ya wazi na kukaa. Kwa bahati ilitokea kwamba mtu yule alikuwa amekaa pembeni ya mtu tajiri. Yule tajiri alijisikia wasiwasi kukaa jirani na yule mtu maskini hivyo alizikusanya nguo zake pamoja na alijisogeza pembeni ili uwepo umbali fulani kati yake na yule masikini. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliyekuwa anatazama tabia ya huyu mtu tajiri; aligeuka kumtazama tajiri yule na akasema: “Je uliogopa kwamba kitu fulani kutoka katika umaskini wako kingetoka kwake na kukung’ang’ania wewe? Yule mtu akajibu. “Hapana, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu!” Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akauliza: “Je uliogopa kwamba kiasi fulani kutoka katika utajiri wako kingehamia kwake?” Yule tajiri akajibu “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Hapana.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamuuliza tena: “Je uliogopa kuwa nguo zako zingechafuka kwa kugusana na nguo zake?” Yule tajiri akajibu “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Hapana.” Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamuuliza, “Sasa kwanini ulijisogeza mbali na naye?” Yule tajiri akajibu, “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Ninakiri kuwa nimefanya makosa na sasa ili kurekebisha kosa hili na kufidia dhambi niliyofanya nipo tayari kumpa huyu ndugu yangu mwislam nusu ya utajiri wangu.” Yule maskini aliposikia maneno yake alisema, “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Sipo tayari kupokea ofa yake hii.” Wale walikuwepo waliuliza kwa mshangao, “Kwa nini?” Akajibu, “Ninaogopa na mimi isije kwa sababu ya ushawishi wa utajiri nikajiingiza katika kiburi na majivuno hivyo na mimi siku moja nikamfanyia ndugu yangu mwislam kama alivy159

12:45 PM

Page 159


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

onifanyia huyu bwana mkubwa leo.” (al-Kafi, Juz.22). Plato anasema, “Kitu bora katika kuleta urafiki ni staha na uungwana wa kiwango kinachofaa.” Wanazuoni wakubwa wa Uislamu wameeleza kwamba kiburi, majivuno na kujishauwa ni vitu vyenye madhara makubwa kabisa juu ya urafiki. Mtu mwenye kiburi na majivuno huwafanya rafiki zake wamkimbie na ni watu wachache sana ambao hutaka kuwa rafiki zake. Lakini kwa upande mwingine, watu waungwana na wenye staha huwavutia marafiki kwa tabia zao. Mtu mwenye majivuno hawezi kuwa rafiki wa yeyote kwa sababu watu hawawezi wakavumilia ufidhuli na majisifu. Muhaddith marhum Qummi amesema: Majivuno na kujisifu kwa watu hudhihirika katika hatua zifuatazo: Mtu majisifu na mwenye majivuno mara zote hujiona yeye kuwa ni mtu maarufu na huwatizama wengine kwa dharau. Huwa hapendi alingane na wengine katika jambo lolote. Hupenda yeye atangulie mbele na akae nafasi ya juu kuliko watu wengine katika mikusanyiko. Hutarajia watu wengine wamsalimie yeye. Mtu yeyote akimpa ushauri yeye, hukereka na yeye akimpa ushauri mtu yeyote humuudhi na kumkera. Ushauri wake usipokubaliwa yeye hukasirika. Kama akifundishwa, huwabeza, na kuwafedhehesha wanafunzi na kuwakumbusha juu ya fadhila alizowafanyia na huwachukulia kuwa ni watumishi wake.” – (Safinatul Bihar, Juz. 2, uk. 459). Sasa tafakari juu ya suala hili na uamue iwapo kama mtu mwenye tabia hii anaweza kuwa na urafiki na wengine katika jamii na kwamba watu wanaweza kumjali mtu kama huyo? Ni kwa sababu hii kwamba Uislamu umepiga kampeni dhidi ya majivuno na majigambo na Qur’ani tukufu imeeleza waziwazi: 160

12:45 PM

Page 160


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

“Je Moto wa Jahanamu sio makazi ya watu wenye majivuno?” – (Suratul Zumar, 39:60). Imam Sadiq amesema: “Huko Jahanamu kuna sehemu mbaya kabisa waliyoandaliwa watu wenye majivuno.” (al-Kafi). Qur’ani tukufu imeyanukuu maneno ya busara ya Luqman aliyomshauri mwanaye wa kiume kuwa:

“Wala usiwafanyie watu jeuri, wala usitembee katika nchi kwa maringo; hakika Mwenyezi Mungu hawapendi watu wenye majivuno na wanaojifakharisha.” (Suratul Luqman, 31:18). Imam Sadiq anakitizama chanzo cha kisaikolojia cha majivuno kuwa ni kutojiamini na amesema: “Huwa hapatwi na maradhi ya kiburi isipokuwa yule asiyejiamini ndani ya nafsi.” (al-Kafi, Juz. 3). Baada ya kufanya uchuguzi wa kina wa kisayansi na kuzitafiti hali za watu wenye majivuno, wanasaikolojia wa zama hizi wameuthibitisha mtazamo huu na wanachukulia hali ya kutojiamini kuwa ni chanzo cha kiburi. Mick Byrde anasema: “Mtu au taifa linalotafuta ubora na umaarufu lina maana ya kuwadhalilisha na kuwadumisha watu na mataifa mengine. Chanzo cha chuki, uadui na misuguano ya zama hizi mara nyingi ni kutokana na kutojiamini. Sababu ya msingi wa tatizo la fikra hii ni namna ya ufidiaji wa bandia na upotofu wa kutojiamini, kwani vinginevyo hakuna mtu mwenye akili yake na mwenye kujiheshimu anayeweza kufikiri 161

12:45 PM

Page 161


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

kuwa kuna ubora au tofauti yoyote kati yake na matabaka mengine au watu wa rangi yingine.” – (Research on Mental and Moral Problems). Kwa kuzingatia hayo yaliyosema, staha na uungwana ni mambo yanayowiana kwa karibu sana kwa manufaa ya jamii kama ilivyokwisha kuelezwa tayari. Imeelekezwa na kuhimizwa katika mafundisho ya Uislamu kwamba watu wanapaswa kujilinda sana dhidi ya aina zote za ubinafsi na badala yake waonyeshe staha na heshima ili waweze kupata mafanikio ya pamoja na umaarufu mbele ya macho ya Mwenyezi Mungu na watu.

IV. KUTEKELEZA AHADI Kwa asili wanaadamu huhisi kuwa anapaswa kuheshimu ahadi alizozitoa kwa watu na kwamba anapaswa kuzitekeleza. Na kwa sababu jambo hili linaihusu asili hasa ya mwanadamu, mwanadamu anatambua ulazima wa kutimiza ahadi, kwa dini yoyote atakayoifuata, na anachukulia kuwa kuvunja ahadi na mkataba ni jambo baya na linalochukiza. Katika maisha ya kijamii, kutekeleza ahadi kuna athari nzuri sana kwani huwahakikishia watu kuwa na imani na uaminifu kwa mtu huyo. Kwa maneno mengine tunaweza tukasema kwamba kutekeleza ahadi ni moja ya sababu muhimu za ustawi wa jamii ambao una athari katika nyanja zote za maisha. Makubaliano yote yanayofanywa baina ya watu wawili yanatoa wajibu wa kimaadili wa kutekelezwa ingawa yanawezekana yakawa hayana kanuni yoyote ya kisheria au ya rasmi, ama jambo lenyewe la makubaliano hayo likawa dogo lisilo na umuhimu mkubwa. Qur’ani tukufu inachukulia utekelezaji wa ahadi kuwa ni sehemu ya masharti ya imani na sifa za waumini na imesema: “Kwa hakika waliofuzu 162

12:45 PM

Page 162


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

ni waumini, ambao ni wanyenyekevu katika Sala zao, ambao hujiepusha na tabia zote chafu........ na wale ambao kwa amana zao na ahadi zao ni wenye kuzitekeleza.” – (Suratul Muumin, 23:8). Katika aya nyingine, Qur’ani imesema: “Watu wema ni ....... na wale ambao hutekeleza ahadi zao pindi wanapoahidi ....” (Suratul Baqarah, 2:177). Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wa Uislamu amesimuliwa kwamba amesema kuwa: “Mtu ambaye hafanyi dhulma anapohusiana na kushughulika na watu na ambaye hasemi uogo katika shughuli zake na hutekeleza ahadi zake na hushehimu na kutekeleza majukumu yake, huyo yuko katika kilele cha ubinadamu na uadilifu, na ni muhimu na inafaa kwa watu kuwa na uhusiano mzuri naye.” (Biharul Anwar, Juz. 75). Imam Muhammad Baqir anasema: “Kuna mambo matatu ambayo ni wajibu kwa mwislam na Mwenyezi Mungu hajamruhusu yeyote kuyakiuka hayo: (i) kurejesha amali kwa mwenyewe, iwe huyu mwenye mali ni mtu muongofu au ni muovu (ii) Kuheshimu ahadi na maagano iwe imewekwa na mtu mwamiifu au na mtu asiyekuwa mwamiifu (iii) Kuwafanyia wema wazazi bila kujali kuwa wazazi hao ni waongofu au vinginevyo.” (al-Kafi, Juz. 2). Kama vile tu ilivyo kwamba kutekeleza ahadi hujenga hali ya kujiamini katika jamii na kujenga nidhamu katika tabaka mbalimbali za maisha, halikadhalika kuvunja ahadi na maagano (mikataba) husababisha vurugu na machafuko. Kama mtu akipotoka kutoka katika njia ya uchamungu na uaminifu na akavunja ahadi zake kirahisi na kutozingatia mikataba na maagano aliyowekeana na watu, hujenga chuki na uadui katika mioyo ya wengine.

163

12:45 PM

Page 163


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Kuvunja ahadi ni moja ya sababu kuu za mparaganyiko katika jamii na likiwa ni jambo la kawaida la kila siku katika jamii, basi huleta balaa na maangamizi katika jamii. Kwa bahati mbaya kuna baadhi ya watu ambao sio tu kwamba hawatekelezi ahadi zao, bali pia huona kuwa kuvunja ahadi na kufanya udanganyifu kuwa ni ujanja na ni njia ya maendeleo na huona huo kuwa ni ustadi, ingawa kitendo chao hakiendani na kanuni yoyote ya kimaadili na kibinadamu na bila shaka hawa ni maadui na wasaliti wa watu na jamii. Haya yalikuwa ni maelezo mafupi juu ya mafundisho ya Uislamu juu ya ushirikiano baina ya Waislamu na bila shaka kila moja ya maelekezo haya lina athari kubwa muhimu katika ujenzi wa mahusiano mazuri na ya dhati baina ya watu. Sasa mwishoni mwa mjadala, tungependa kuvuta usikivu wa wasomaji wetu katika adabu za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ili kwa rehema ya Mwenyezi Mungu tuweze kuwa wafuasi wa kweli wa kiongozi huyu Mtukufu na mkombozi wa wanadamu. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akikubali mialiko ya watu wote, wawe waungwana au watumwa, matajiri au maskini. Kila mara muhitaji alipomwendea Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa shida fulani, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akijitahidi kukidhi mahitaji yake. Kama mtu alitoa udhuru fulani yeye alikuwa akiukubali. Hakulipiza uovu wa wengine, badala yake alikuwa akipuuza makosa yao. Kila aliyekutana naye, yeye Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ndiye aliyeanza kumsalimia. Alistahamili matendo yasiyokubalika ya maadui zake kwa subira. Alikuwa akikaa chini bila kujali. Ilipobidi alikuwa akishona viatu na nguo zake. Alikuwa akiwatembelea wagojwa hata kama nyumba zao ziko mbali. Alikuwa akiwakaribisha na kula na maskini na alikuwa mpole kwao.

164

12:45 PM

Page 164


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Alikuwa hana upendeleo binafsi katika masuala ya chakula na nguo. Alikuwa akipeana mikono na waislamu na akiikumbatia kwa bashasha na uchangamufu. Mtu aliyependwa zaidi na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni yule aliyewasaidia watu zaidi na aliyewahurumia. Vikao alivyokaa vilikuwa ni vikao vyenye uvumilivu, staha, subira na uaminifu. Alionyesha heshima kwa wakubwa na upole kwa wadogo. Wakati wote alikuwa na tabia njema na tabasamu lililochangamka usoni mwake. Hakuwa na misimamo mikali. Hakuwa akimuwekea kinyongo mtu yeyote moyoni mwake. Alikuwa hapigi kelele. Kamwe hakuwahi kusema kitu chochote kibaya na kisichofaa dhidi ya yeyote hata kwa makafiri na waabudu masanamu. Kamwe hakumteta yeyote. Kamwe hakumkatiza yeyote wakati wa mazungumzo. Ikiwa yeyote katika masahba zake hakuwepo, alikuwa akiulizia habari zake. Hakupata kunyoosha miguu yake (wakati wa kukaa) mbele ya mtu yeyote. Alikuwa mpole kwa waja wote wa Mwenyezi Mungu. Alidumisha uhusiano mzuri na ndugu na rafiki zake na alikuwa akiwapenda. Alikuwa mwangalifu sana katika kutekeleza ahadi kuliko mtu mwingine yeyote. Ilikuwa mtu fulani akiwa anaongea naye, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimsikiliza kwa makini na alikuwa haridhiki na kumsikiliza tu bali aliacha shughuli zote na kumsikiliza kwa makini. Hii ni mifano michache ya tabia na maadili ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambayo imenukuliwa na wanahistoria na wanahadithi (muhadithina). Inatarajiwa kuwa wafuasi wake watafanikiwa katika kufuata nyanyo zake na watakuwa ni wafuasi wa kupigiwa mfano katika kuwahubiria wanadamu ili kutwaa mwenendo wa kimaadili kwa manufaa ya wanaadamu wote.

165

12:45 PM

Page 165


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

NUKUU 1). Mtu ambaye sio dhalimu anapotangamana na kushughulika na watu na hasemi uongo anapozungumza na hutekeleza ahadi zake na kuheshimu mapatano yake, huyo yupo katika kilele cha ubinadamu na uadilifu na ni muhimu kwa watu kuwa na mahusiano naye mazuri. (Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). 2). Ishi na watu katika namna ambayo ukifa watakulilia na ukiwa hai watataka kuwa karibu na wewe – (Imam Ali (a.s.).

HISIA ZA USUHUBIANO NA UDUGU Moja ya mahusiano yeye nguvu sana na yenye mizizi ya kina miongoni mwa wanaadamu ni uhusiao wa kindugu. Ndugu hupendana, huhurumiana na hujiona kuwa ni washirika katika dhiki na faraja. Inawezekana wakati fulani tofauti ikaibuka kati ya ndugu na hivyo kusababisha wasiwasi. Lakini punde mashaka haya huondoka na zile nyakati za huzuni husahauliwa na kuacha nafasi ya upendo na uaminifu tena. Ili kuimarisha utengamano wa kijamii na kuboresha uhusiano wa wanaadamu, Uislamu umeutumia uhusiano huu imara na umewapatia waumini wote wa kweli hali halisi ya udugu kwa kila mmoja wao. Kama tu ilivyokuwa kwamba ndugu wawili wameunganishwa na kukutanishwa kwa damu kwa kuwa na baba mmoja, Uislamu unamchukulia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuwa ni baba wa Umma na kwamba Waislamu wote ni watoto wake na hivyo Waislamu wote ni ndugu. Hakuna mipaka au kikwazo chochote katika suala la udugu wa kiislam na Waislamu wote, bila kujali rangi, nchi wala lugha, Uislamu wote wanakingwa na kanuni hii wanatambuliwa na uislamu kuwa wote ni ndugu wa kila mmoja wao. 166

12:45 PM

Page 166


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Qur’ani tukufu imeeleza waziwazi juu ya udugu huu na imesema:

“Kwa hakika Waumini ni ndugu. Hivyo patanisheni baina ya ndugu zenu, na Mcheni Mwenyezi Munguili mpate kurehemiwa. – (Suratul Hajarat, 49:10). Historia imeshuhudia uadui mwingi, ugomvi mwingi, migawanyiko na tofauti zilizokuwepo kabla ya kuja kwa Uislamu. Lakini kwa njia ya mafundisho yenye ukombozi ya Uislamu, ule moyo wa udugu wa kweli wa Kiislamu ulijengwa miongoni mwa Waislamu. Qur’ani tukufu imesema:

“Shikamaneni na kamba ya Mwenyezi Mungu nyote kwa pamoja wala msifarikiane, tafuteni ulinzi wa Mwenyezi Mungu na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu juu yenu, mlipokuwa maadui na akawaunganisha nyoyo zenu, hivyo kwa neema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa katika ukingo wa shimo la moto, naye akawaokoeni nalo .....” (Suratul Aali Imran, 3:103). Katika mafundisho ya Uislamu, zimewekwa haki maalumu kwa ndugu katika imani na Waislamu wote wamefanywa kuwa na wajibu wa kuziheshimu na kuzifuata. Imam Sajjad mesema: “Haki ya ndugu yako katika imani ni kuwa mara zote unapaswa kuwatafutia mafanikio yao na uwe mpole kwao. Na kuhusiana na wale ambao ni wabaya miongoni mwao, unapaswa uwe na huruma na bashasha kwao na unapaswa ufanye jitihada juu ya kubadilika kwao. 167

12:45 PM

Page 167


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Na kwa wale ambao ni wema unapaswa uwe na shukrani kwao. Ni wajibu kwako kuwaombea dua ndugu zako katika imani na uwasaidie wote kwa umoja wao na misaada kwa mtu mmoja mmoja. Unapaswa kuwachukulia wakubwa kuliko wewe kama baba yako na wadogo kuwa ni watoto wako na wale unaolingana nao kuwa ni ndugu zako. Yeyote miongoni mwa ndugu zako katika imani anapokujia, unapaswa umpokee vizuri. Unapaswa umuonyeshe ndugu yako katika imani tabia ambayo huonyeshwa na mtu kwa ndugu yake wa damu. (Bihanul Anwar, Juz. 74, uk. 12). Imam Ja’far Sadiq anasema: “Mwislam ni ndugu wa mwislam mwingine. Ni kama jicho lake (kwa vile anamfanya azione sifa zake nzuri na mbaya) na kioo chake (ambacho humuonyesha uzuri wake na ubaya wake). Yeye ni kiongozi wake. Kamwe mwislam huwa hadhulumu mali ya ndugu yake mwislam. Kamwe hamkandamizi ndugu yake Mwislam. Hamdanganyi na hachukulii kuwa ni jambo linalofaa kumsengenya au kumteta ndugu yake mwislam. (al-Kafi, Juz. 2, uk. 166). Juu ya haki alizonazo mwislam kwa ndugu yake mwislamu, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: “Mwislamu anapaswa kupuuzia na kusamehe makosa ya ndugu yake Mwislamu. Anapaswa kumhurumia ndugu mwislamu anapokuwa katika shida, atunze siri za ndugu yake, apuuzie makosa yake, akubali kuomba msamaha kwake na amlinde dhidi ya watetaji na wasengenyaji. Mara zote anapaswa kumpa ushauri na kudumisha uhusiano wa kirafiki naye. Akiugua anapaswa kumtembelea na kumjulia hali na afya yake. Anapaswa kukubali mialiko na zawadi zake. Anapaswa alipe fadhila juu ya zawadi zake. Anapaswa aongee naye pole pole na amshukuru kwa upendo wake. Anapaswa kufanya wema kwa marafiki zake. Hapaswi kumuacha peke yake wakati wa kukabiliana na shida. Anapaswa kumpendelea ndugu yake kile anachokipenda yeye mwenyewe na asimtakie kile ambacho yeye mwenyewe hakipendi.” (Biharul Anwar). Imam Ja’far Sadi anasema: “Mpendelee ndugu yako Mwislamu kile unachojipendelea mwenyewe. Kama ukihitaji kitu fulani kiombe kutoka 168

12:45 PM

Page 168


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

kwake, na yeye akihitaji kitu usimnyime. Usijizuie au kuonyesha kutofarahi unapomtumikia na kumfanyia wema, na yeye pia hapaswi kujizuia kukufanyia wema. Kuwa msaididi wake kwani yeye pia ni msaidizi wako. Ihifadhi heshima yake yeye anapokuwa hayupo. Anaporudi kutoka safari, uende ukamuone. Mheshimu na mpende. Yeye ni wako na wewe ni wake. Akiwa mkali kwako usivunje uhusiano naye lakini muombe radhi. Kama akipata kitu fulani, mshukuru Mwenyezi Mungu, na akiwa katika shida fanya haraka kumsaidia. Endapo maadui zake wakimfanyia hila na wakitaka kumtumbukiza katika matatizo, msaidie na umkinge kuingia katika matatizo.” (al-Kafi, Juz.3). Kilichoelezwa hapo juu ni baadhi ya mifano ya haki alizonazo ndugu katika imani, ambazo kwamba maamrisho yametolewa katika mafundisho ya Uislamu. Mbali na maamrisho haya ya jumla, kuna majukumu mengine ya waislamu ambayo kila mojawapo limeelezewa kivyake tofauti na viongozi mashuhuri watukufu wa Uislamu.

UDUGU – (MUWASAT) Muwasat ina maana ya kuwasaidia ndugu katika imani na kuwapatia msaada wa kifedha. Katika Hadithi jambo hili limehimizwa sana ambalo ndio njia ya kuboresha maisha ya matabaka ya watu wanyonge na wasiojiweza na kujenga upendo baina ya Waislamu na limetambulishwa kama ni moja ya sifa za lazima za kila Mwislamu na Muumini na ni chanzo cha thawabu. Imam Jafar Sadiq anasema: “Jifanye kuwa kipenzi machoni pa Mwenyezi Mungu kwa kuwasaidia kifedha ndugu zako katika imani (Khisal Suduq, Juz. 1, uk. 8).

169

12:45 PM

Page 169


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuusia Imam Ali (a.s.) kwa kusema: “Kuna amali tatu bora kabisa, kwanza, unapaswa uwafanyie uadilifu watu wote; pili, uwasaidie ndugu zako katika imani msaada wa kifedha na tatu, katika hali zote unapaswa kumkumbuka Mwenyezi Mungu – (Biharul Anwar, Juz. 74, uk. 3920. Imam Ali (a.s.) (a.s) anasema: “Kuwasaidia ndugu zako katika imani na kuwapa msaada (wa kifedha) kwa ajili ya Mwenyezi Mungu humuongezea mtu njia ya riziki yake – (Khisal Saduq, Juz. 2, uk. 94). Waqidi, ambaye alikuwa mmoja wa wanavyuoni wakubwa kabisa enzi za utawala wa Khalifa Maamun, amesemulia kisa hiki kifuatacho: “Nilikuwa na marafiki wawili ambapo mmoja wao alikuwa anatoka katika ukoo wa Banu Hashim. Urafiki wetu sisi watatu ulikuwa wa dhati kiasi kwamba tulikuwa (kama) roho moja katika miili mitatu. Ilipata kutokea wakati fulani, katika kipindi cha Iddi kwamba mimi nilikuwa fukara sana sikuwa na kitu chochote kabisa. Mke wangu aliniambia: “Wewe na mimi tunaweza kuvumilia matatizo yote haya. Lakini nina huzuni sana kwa sababu ya watoto kwani watawaona wenzao wakiwa wamevaa nguo mpya na kujipamba kwa ajili ya sherehe za Iddi ambapo za kwao ni za zamani na zimechanika. Jitahidi kupata fedha ukiweza ili niwanunulie nguo mpya.” Nilitafakari kwa kina juu ya jambo hilo lakini sikuweza kupata suluhisho la tatizo. Mwisho nilimwandikia barua rafiki yangu wa ki-Bani Hashim na nikamuomba anisaidie kwa kadiri yeye atakavyoweza. Rafiki yangu huyo alinitumia mfuko uliofungwa na alinijulisha kuwa ndani kulikuwa dirham 1000. Kabla sijaufungua mfuko huo, mtu mmoja aliyekuwa ametumwa na rafiki yangu yule mwingine aliwasili. Alinijulisha juu ya shida yake na alitaka msaada. Sikuufungua mfuko ule na nikamtumia kisha nikaenda msikitini nikiwa na moyo mzito. Kwa vile niliona haya kuonana na mke wangu, nililala huko huko msikitini usiku ule. Lakini 170

12:45 PM

Page 170


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

kinyume na matarajio yangu, niliporudi nyumbani asubuhi, mke wangu alinipokea kwa uchangamfu na bashasha na akaelezea kuridhishwa kwake kwa wema niliomfanyia rafiki yangu na kwa kumpa kipaumbele zaidi kuliko mimi mwenyewe. Wakati huo huo rafiki yangu wa ki-Bani Hashim aliwasili pale nyumbani kwangu na ghafla akaniambia” “Niambie ukweli. Umeufanyia nini ule mfuko wa fedha niliokutumia jana?” Nilimweleza kisa kizima. Baada ya kunisikia aliinamisha kichwa chake chini kwa muda kisha akasema: “Jana uliponitumia ujumbe na kuniomba msaada sikuwa na fedha isipokuwa mfuko huu. Nilikutumia wewe (mfuko huu) na nikamwandikia barua yule rafiki yetu mwingine ili kumuomba msaada. Alitumia huo huo mfuko wangu, ukiwa bado umefungwa na sikuweza kuelewa jambo hili limekuwaje mpaka ulivyonielezea sasa.” Waqidi anasema: “Sote watatu tuligawana fedha hizi kati yetu na dirhamu mia kati ya hizi, alipewa mke wangu. Maamun alizipata habari za tukio hili la ajabu. Aliniita na akataka kujua juu ya ukweli wa jambo hili. Nilimsimulia kisa chote kizima. Maamun aliamuru kuwa kila mmoja kati yetu apewe dirham 2000 na mke wangu apewe dirham 1000 kama zawadi.” (Mas’udi, Murujudh-Dhahab). Tukio hili ulilolisoma hapa ni tukio la kihistoria lililotokea kuhusiana na Waislamu wachache ambao walifundishwa chini ya nuru ya mafudisho ya Qur’ani. Walipata maadili safi kama haya na sifa za ubinadamu chini ya mafundisho matukufu ya Uislamu kiasi kwamba moyo wa udugu ulikuwa umeyatawala maisha yao kwa kiasi hicho. Kama tukiitazama historia ya siku za awali za Uislamu tunaweza tukaona moyo huu wa udugu baina ya Waislamu.

171

12:45 PM

Page 171


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Katika vita vya uhudi, ambavyo vilikuwa ni moja ya vita vikali kabisa vya Kiislamu, Waislamu walijitoa mhanga wa hali ya juu. Idadi kubwa kati yao walibahatika kufa kishahidi walipokuwa wakipigana kishujaa na wengine wengi ambao walikuwa wamejeruhiwa na baadhi yao kuzirai walikuwa wamelala chini. Wapiganjai saba wa Kiislamu walikuwa wamelala chini kando ya kila mmoja wao. Walikuwa wamejeruhiwa na walikuwa katika hatua za mwisho mwisho za uhai wao. Wote walikuwa taabani na wenye kiu. Mtu aliyekuwa ameteuliwa kuwapatia maji wapiganaji aliwaendea. Hata hivyo maji aliyokuwa nayo yalikuwa yanatosha mtu mmoja tu. Alimwendea mmoja wao na akamkaribisha anywe maji. Lakini huyu mpiganaji alimuomba yule mpeleka maji ampatie maji yale mpiganaji aliyekuwa pembeni yake. Huyo mpeleka maji alimpelekea maji mpiganaji anayefuatia lakini naye hakuyanywa na alimtaka ampatie maji hayo mpiganaji aliye pembeni yake. Kwa utaratibu huu watu sita wa mwanzo walimtaka mpeleka maji ampelekee maji mpiganaji anayefuatia. Alipomfikia yule mpiganaji wa saba naye alimtaka huyo mpeleka maji amfanye yule mtu wa kwanza kunywa maji hayo kwani yeye ndiye aliyekuwa na kiu zaidi. Alimrudia mtu wa kwanza lakini alikuta amekufa. Halikadhalika wale sita wengine pia walifariki dunia, Kwa kifupi wale watu wote saba walikufa kwa kukosa maji na hivyo waliwafundisha wegine kwa vitendo somo la udugu kusaidiana na kujitolea.� (Majma’ul Bayan, Juz. 9, uk. 260). Huu ulikuwa ni mfano wa somo la mazingatio walilojifunza kutokana na mafundisho ya Mtukufu Mtume wa Uislamu (s.a.w.w.) na wakayatekeleza hayo katika nyaja zote za maisha yao. ni jambo la kuhuzunisha kwamba licha ya kuwa na hazina hii ya thamani ya mafundisho adhimu, tumeshafikia hatua ambayo ule moyo wa udugu na kusaidiana unatoweka pole pole, na hali ya ubakhili na kutojali ambao ni zawadi kutoka nchi za Magharibi inachukua nafasi mahali pake. Hata 172

12:45 PM

Page 172


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

hivyo, wakati wote inapaswa kuzingatiwa kuwa tabia hii haiendani na mafundisho ya Uislamu na mwislamu hawezi kupuuzia shida na taabu wanazozipata ndugu zake katika imani. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: “Mtu anayeianza siku bila kufanya jitihada za kuboresha hali za Waislamu sio mwislamu.” (al-Kafi, Juz. 2, uk. 164). Imam Ja’far Sadiq amesema: “Watu bora miongoni mwenu Waislamu ni wale ambao ni wakarimu na wasemehevu na watu wabaya kabisa ni wale ambao ni wabahili na wenye akili finyu. Na moja ya matendo ya kiuchamungu na yanayotakikana ni mtu kuwa mwema kwa ndugu zake katika imani na kufanya jitihada za kukidhi mahitaji yao. Kufanya hivyo kunamfanya Shetani kuwa duni na anayefanya kitendo hiki hubakia kuwa mbali na moto wa Jahanam na huikaribia Pepo na ustawi wa milele.” – (Majalis Mufid, uk. 179, Amali Tuli, Juz.1). Mtu mmoja alimwendea Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kulalamika kuwa ana njaa. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimtuma mtu fulani kwenda katika baadhi ya nyumba za ndugu zake (Mtume) ili akamletee chakula mtu yule, lakini kwa bahati mbaya, katika nyumba hizo pia hakukuwepo na chakula. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwageukia wale waliokuwepo na kusema: “Je ni nani miongoni mwenu yupo tayari kumkirimu mtu huyu usiku wa leo?” Imam Ali (a.s.) alijibu: ‘Ewe Mtume wa Mwenyezi Mugu! Nitachukua wajibu wa jukumu hili.” Kisha aliushika mkono wa mtu yule na kwenda naye nyumbani kwake. Alimuuliza mkewe, Bibi Fatimah Zahra, “Una chakula kiasi gani ndani ya nyumba?” Akajibu: Kuna kiasi kidogo tu cha chakula kinachowatosheleza watoto wetu.” Imam Ali (a.s.) akasema: “Lazima tumpendelee mgeni wetu kuliko nafsi zetu na watoto wetu.” Baada ya uamuzi huu kuchukuliwa Bibi Fatimah aliwafanya watoto walale. Imam Ali (a.s.) alibeba chakula kwa mgeni na akazima taa kwa 173

12:45 PM

Page 173


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

kisingizio kuwa anaitengeneza. Kutika giza lile Mtukufu Imam Ali (a.s.) alimkaribisha mgeni chakula. Yeye pia alikaa katika mkeka wa chakula, na bila kula chochote, lakini alimfanya mgeni aamini kuwa yeye Imam Ali (a.s.) pia alikuwa anakula. Katika usiku ule Imam Ali (a.s.), bibi Fatimah na watoto wao walimkirimu mgeni wao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na wao wakalala bila kula. Mwenyezi Mungu Mtukufu alikisifu kitendo hiki cha wema na kujitolea kwa kuteremsha aya hii: “... Wanawapendelea (wageni n.k.) kuliko nafsi zao wenyewe ingawa wao wenyewe wana hali ndogo – ( Suratul Hashr, 59:9, Taz. Tafsirus-Safi, Juz. 2, uk. 684). Ni dhahiri na wazi kwamba haiwezekani kwa kila mtu kufanya hivi lakini Imam Ali (a.s.), amiri wa waumini, anatakiwa kujitolea kuchukua jukumu kama hili. Uislamu pia haujawataka wafuasi wake kufanya hivi kama jambo la wajibu. Kwa upande mwingine, kilichotambuliwa kama wajibu wa mkato ni udugu na kusaidiana katika namna hii kwamba Mwislamu anapaswa kuwasaidia ndugu zake katika imani wanapokuwa katika shida na dhiki; anapaswa kutumia sehemu ya kipato chake kwa ajili ya ustawi wa mafukara; anapaswa kuwatembelea wagonjwa, kuwaonyesha upole na kuwahurumia; awatazame na kuwalinda mayatima na wasio na msaada kwa kiasi kitakachowezekana; na ashiriki katika kuanzisha ujenzi wa vituo vya huduma kwa jamii. Mgiriki mmoja alibakia na Imam Ali (a.s.) kwa muda mrefu na alifanya utafiti juu ya Uislamu. Alipomaliza utafiti wake, alishawishika juu ya ukweli wa Uislamu na akasilimu mikononi mwa Mtukufu Imam. Alipokuwa akimpa maelekezo muhimu juu ya wajibu wake wa baadae, Imam Ali (a.s.) alimwambia: “Ninakuwaidhi na kukushauri kwamba uchunge usuhuba na wale wanaomfuata Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na mimi na kuwasaidia kwa kutumia mali ambayo Mwenyezi Mungu amekupatia, ukidhi haja zao, utatue matatizo yao na utangamane nao kwa namna 174

12:45 PM

Page 174


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

njema.” (Ihtijaj Tabarsi, uk. 114). Juu ya haki za ndugu katika imani, Imam Ridha anasema: “Miongoni mwa haki ambazo Muumin anazo juu ya ndugu yake katika imani ni kuwa anapaswa ampende kwa dhati amsaidie kifedha na achunge udugu naye na amsaidie ikiwa mtu mwingine anamfanyia udhalimu. Kamwe muumini wa kweli huwa hamuonei ndugu yake katika imani wala hamdanganyi, wala asimfanyie hila wala asimsengenye, wala asimwambie uongo.” (Biharul Anwar). Ikiwa mtu atampatia zawadi ya nguo ndugu yake katika imani, Mwenyezi Mungu atampatia nguo Peponi badala ya hiyo na mtu akimpa mkopo ndugu yake katika imani ili kutaka radhi za Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu atamlipa thawabu za mtu aliyetoa Sadaka. Na mtu akimuondolea huzuni ndugu yake katika imani, Mwenyezi Mungu atamuondolea huzuni zake huko Akhera.” Safwan Jammaal amesema: “Nilikuwa nimekaa katika hadhara ya Imam Ja’far Sadiq (a.s.). Mara akawasili mkazi mmoja wa Makka na kusema kuwa alikuwa ameishiwa fedha na hakuwa na fedha za kutosha kumrudisha nyumbani Makka.” Mtukufu Imam aliniomba nichukue hatua zinazofaa kumsaidia ndugu yagu mwislamu. Nilisimama wima mara moja na kutatua tatizo lake. Mtukufu Imam aliniuliza: “Umechukua hatua gani kumsaidia ndugu yako?” Nilimuarifu kuwa kwa rehema ya Mwenyezi Mungu suala lake limeshatatuliwa katika namna njema inayostahili. Hapo Mtukufu Imam akasema: “Kumbuka kwamba ukimsaidia mmoja wa ndugu zako katika imani, kitendo chako hicho hunifurahisha zaidi kuliko kufanya tawaf ya sunan katika Nyumba ya Mwenyezi Mungu kwa wiki moja.”

175

12:45 PM

Page 175


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Kisha Imam Ja’far (a.s) alisema: “Mtu mmoja alimwendea Imam Hasan (a.s) na akamweleza matatizo yake na kumuomba msaada. Imam alivaa viatu vyake mara moja na akaondoka na mtu huyo. Wakiwa wamo njiani walifika sehemu ambapo Imam Husein (a.s) alikuwa akisali. Imam Hasan akamuuliza mtu huyo: “Kwa nini usingemwendea Husein akutatulie tatizo lako?” Yule mtu akajibu: “Ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu! Nilitaka kumuomba lakini nilijulishwa kuwa alikuwa katika itikafu (kujitenga kwa ajili ya Ibada). Hivyo sikuenda kumuomba.” Imam Hasan (a.s.) alisema: “Hata hivyo kama angeweza kukusaidia ingekuwa ni bora kuliko kukaa itikafu kwa mwezi mmoja.” – (al-Kafi, Juz. 2, uk. 158). Imam Ja’far Sadiq (a.s.) amesema: “Mwislamu anapokidhi mahitaji ya ndugu yake Mwislamu, Mwenyezi Mungu husema: “Ni wajibu wangu kukulipa kwa kitendo hiki na sioni malipo yoyote yanayotosheleza kwako isipokuwa Pepo.” (Qurbul Asnad, uk. 19). Mtu aitwaye Abdul A’la aliyekuwa Shi’ah mashuhuri alisafiri kutoka Kufa kwenda Madina. Wafuasi wa Imam Ja’far (a.s) waliorodhesha maswali yao na kumkabidhi karatasi Abdul A’la ili wapate majibu kutoka kwa Imam. Pia walimuomba akamuulize mtukufu Imam awaelezee haki alizonazo Mwislamu kutoka kwa ndugu yake katika imani. Abdul A’la anasema: “Nilipopata heshima ya kukutana na Mtukufu Imam, aliyajibu maswali yote lakini hakusema lolote juu ya haki za ndugu katika imani. Siku nyingi baadaye nilikwenda tena kwa Mtukufu Imam lakini pia hakugusia jambo hilo. Muda wangu wa kukaa Madina ulikwisha na nikaenda kumuaga Imam na nikasema: “Ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu! Swali nililouliza wakati ule bado halijajibiwa.” Mtukufu Imam akajibu: “Sikulijibu kwa makusudi.” Mimi nikauliza “Kwa nini?” 176

12:45 PM

Page 176


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Imam Sadiq alisema: “Naogopa nisije nikakueleza juu ya haki za Waislamu nawe ukashindwa kuyatekeleza yale nitakayoyasema na ukatoka nje ya mipaka ya dini.” Kisha akaendelea kusema: “Kwa hakika mambo haya matatu yanaonekana kuwa ni mambo magumu kabisa ambavyo Mwenyezi Mungu ameyawajibisha kwa waja wake. Kwanza, mtu anapaswa kutenda uadilifu kati yake na wengine kwa maana kwamba awatendee ndugu zake katika imani kwa namna ambayo yeye mwenyewe angependa atendewe. Pili, mtu anapaswa kuchunga usuhuba na ndugu zake katika imani na awapitie msaada wa kiuchumi. Na tatu, anapaswa kumkumbuka Mwenyezi Mungu katika hali zote. Na ninaposema mtu amkumbuke Allah wakati wote simaanishi kwamba mtu aseme ‘Subhannallah’ au ‘Alhamdulillah’ kwa kukariri muda wote. Bali kinyume chake ninachomaanisha ni kuwa anapokabiliwa na kitendo cha haramu amkumbuke Mwenyezi Mungu na kisha ajiepushe kufanya kitendo hicho.” (al-Kafi, Juz. 2, uk. 170). Mafundisho haya yaliathiri mielekeo ya wafuasi wa Uislamu kwa namna ambayo tumeiona kwenye mifano iliyonukuliwa hapo juu – na historia ya Uislamu imejaa mifano kama hiyo ya hisia za udugu na kusaidiana – mwenendo ambao hakuna taifa jingine linaloweza kujilinganisha na mwenendo wao. Hivi sasa kwa vile karne nyingi zimepita baada ya kuja kwa Uislamu, na wanaadamu kwa kusema kweli wamepata maendeleo ya ajabu katika fani za sanaa na Sayansi, sio kwamba maadili haya adhimu ya kibinadamu hayaonekani katika nchi zilizoendelea bali kinyume chake kabisa ni kwamba yanaonekana hasa. Juu ya mahusiano ya pamoja ya wazungu, mmoja wa waandishi amesema: “Mahusiano ya watu ni mabaya na yasiyo na hisia thabiti zenye mizizi ya kina. Tunaweza tukasema kwamba upendo wa moyoni, ambao ni fungamano la hisia na ambao huyaangazia maisha umeshapondwa pondwa na magurudumu ya mashine za viwandani. Kwa kawaida, moyo wa kujitolea, 177

12:45 PM

Page 177


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

msamaha na huruma ni mambo yasiyojulikana na inawezekana idadi ya marafiki wa mtu alionao haizidi idadi ya vidole vya mkono wake. Wakati fulani nilipokuwa nimelazwa hospitali, ingawa idadi ya wageni wangu (waliokuja kuitembelea) haikuwa kubwa lakini bado naweza kusema kuwa watu wengi zaidi walikuja kuniona mimi kuliko wale waliokuja kuwaona wagonjwa wa kijerumani katika wodi ile. Na jambo hili hasa lilikuwa linawashangaza wafanyakazi wa hospitali ile, kwa sababu ni mara chache sana tulimuona Mjerumani akiwa amekuja kumuona angalau mgonjwa wa familia yake.� Haitakuwa vibaya na hatutatoka nje ya mada kama tukinukuu tukio moja la kuvutia kama mfano ili uweze kuelewa kiwango cha upendo na hisia katika nchi zilizoendelea. Miaka michache iliyopita profesa mmoja wa Kijerumani alisilimu mikononi mwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kiislamu ya Hamburg. Baadaye kidogo, profesa huyu aliyesilimu aliugua na kulazwa hospitalini. Baada ya kupata habari hizi, Mwenyekiti huyo wa Jumuiya ya Kiislamu alikwenda hospitali kumuona. Lakini kinyume na matarajio yake, alimkuta profesa akiwa mwenye huzuni na sononeko kubwa la moyoni, hivyo akamuuliza juu ya sababu ya huzuni yake. Profesa huyo, ambaye alikuwa kimya hadi wakati ule na aliyekuwa amezama katika lindi la mawazo, alifungua midomo yake na kusimulia kisa chake cha kushangaza na kuhuzunisha kwa maneo haya: “Leo mke wangu na mwanangu wa kiume walikuja kuniona. Waliambiwa katika Idara inayohusika kuwa ninasumbuliwa na saratani. Walipokuwa wakiniaga na kuodoka hospitalini waliniambia: Kwa mujibu wa taarifa tulizonazo, wewe una saratani na haielekei kwamba utaishi siku yingi. Hivyo tunakuaga kwa mara ya mwisho na tunaondoka, na tungekuomba utuwie radhi kwamba hatutakuja kukuona tena.�

178

12:45 PM

Page 178


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Kisha profesa huyu mgonjwa aliendelea: “Masononeko yangu makubwa na mateso ya kiakili hayatokani na kwamba nimepoteza matumaini yote ya kuishi. Kilichoniudhi na kunisumbua sana ni tabia ya kidhalimu na isiyo ya kibinadamu ya mke wangu na mwanangu wa kiume.” Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kiislamu, ambaye aliguswa sana na hali yake ya kusikitisha, alisema: “Kwa vile kuwatembelea wagonjwa kumehimizwa kwa msisitizo sana katika Uislamu nitakuja kukutembelea kila ninapopata muda na hivyo nitakuwa nimetekeleza wajibu wangu wa kidini. Maneno haya yaliutia nuru uso wake wenye huzuni na kuupatia furaha. Pole pole hali yake aliendelea kuwa mbaya na akaiaga dunia siku chache baadaye. Baadhi ya Waislamu walikwenda hospitalini hapo na kuuchukua mwili wake na kuufanyia maandalizi na ibada zote muhimu za mazishi. Lakini hata hivyo mambo hayakwishia hapo. Karibu na muda wa mazishi, alikuja haraka haraka kijana mmoja, ambaye uso wake ulikuwa unaonyesha wasiwasi wa dhahiri, na akauliza; “Uko wapi mwili wa profesa?” Kwa kujibiwa akaulizwa: Je wewe una uhusiano na marehemu?” Akajibu: “Ndiyo, alikuwa ni baba yangu. Nimekuja kuukabidhi mwili wake kwenye mamlaka ya hospitali kwa ajili ya malengo ya uchunguzi kwani siku chache kabla ya kifo chake nilikuwa nimeuza mwili wa baba yangu kwa mamlaka ya hospitali kwa Mark thelathini (Mark ni fedha za Ujerumani).” Ingawa alisisitiza sana kwamba apewe mwili wa baba yake, lakini hatimaye aliachana na wazo hilo baada ya kukutana na upinzani mkali kutoka kwa wale waliokuwepo pale. Baadaye kijana huyu alipoulizwa kuhusu ujuzi wa kazi yake alijibu kwamba: “Asubuhi huwa ninafanya kazi kiwandani na wakati wa alasiri huwa ninafanya kazi ya kuwahudumia mbwa.” Tukio hili, ambalo ni la kuhuzunisha sana, linaonyesha ni kwa kiasi gani hisia za ubinadamu zinamong’onyolewa katika jamii iliyoendelea, ya 179

12:45 PM

Page 179


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

kisasa na ilivyostaarabika! Katika zama hizi kurudi nyuma kwa ubinadamu kwa mtazamo wa maadili na kulipuka kwa maovu ya kijamii ni mambo yasiyokatalika. Wakati wakikiri uhalisia huu mchungu, wanafikra wakubwa wanazugumzia juu ya kulitatua tatizo hili na wana uchungu sana kutokana na hili. Wameyatambua maradhi haya kikamilifu na wanaiona haja ya kuzindua kampeni dhidi ya ubinafsi na kutojizuia (kufunya maovu) na kujenga ulimwengu mpya juu ya msingi wa imani na maadili. Wale ambao wao wenyewe wamezama katika aina hii ya maisha wameshabaini kuwa maisha ya aina hii ni tupu, bure kabisa na hayawezi kutoa mchago wowote katika ustawi wa mwanadamu. Itakuwa vizuri zaidi kama utasikiliza ushuhuda huu wa kukiri, wa kuvutia na wa wazi kutoka kwa mmoja wa maraisi wa Marekani aliyeuotoa wakati alipokuwa akiapishwa kushika madaraka: “Tunajikuta wenyewe ni matajiri kwa upande wa mali lakini tuna maadili yasiyoridhisha. Tunaufikia mwezi kwa ufanisi wa hali ya juu lakini hapa duniani tunakabiliwa na utengano mkubwa. Tunajiingiza katika vita na huku tunataka amani. Utengano umetuvunjavunja na huku tunataka umoja. Tunaona nyuso tupu katika mazingira yetu na maisha yetu ni bure kabisa. Na kinyume na machafuko ya kiroho ambayo yametuzidi sisi, tunahitaji tiba ya kiroho, na kwa hilo tunapaswa kujitazama sisi wenyewe tu. Tukisikiliza wito wa dhamira zetu za ndani tutaona kwamba zinathamini vitu rahisi na vya msingi kama wema, staha, upendo na huruma.� Uhalisia huu ukizingatiwa, kila mtu muadilifu huinamisha kichwa chake mbele ya mafundisho matukufu ya Uislamu. Ni Mwenyezi Mungu, Muumbaji, ambaye kwa kuzingatia mahitaji yote ya muda na ya kiroho na silika za kibinadamu, amepitisha sheria mwafaka ambazo zinaendana na maumbile hasa ya mwanaadamu na ambayo hukid180

12:45 PM

Page 180


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

hi mahitaji yake yote. Hizi ni sheria ambazo zimekuwa zikitekelezwa kwa karne kadhaa na zimetoa matokeo yanayoridhisha. Hizi ndio sheria ambazo hazikuwa kwenye karatasi tu bali zilitekelezwa kwa ukamilifu wa maana zake na hazikuwa na ugumu wowote hata katika kipindi chake cha utekelezaji. Kwa kadiri tunavyotafakari juu ya kukiri kwa wanafikra wa Magharibi ndivyo tunavyoelewa zaidi juu ya kufilisika kwao kiroho na kimaadili na zaidi hasa ndivyo tunavyoiona thamani zaidi na kuitukuza dini adhimu ya Uislamu. Kitu kinachopaswa kuzingatiwa hapa mwisho ni kuwa ni jukumu la Waislamu wote kuyaeneza na kuyatekeleza mafundisho ya Uislamu bila kutia nakshi yoyote na hususani tunapaswa kuwazoesha vijana juu ya mafundisho haya ili moyo wa udugu na kujaliana ambao umekuwepo miongoni mwa Waislamu kwa karne kadhaa uwe na nguvu zaidi na tunapaswa kupiga hatua kuiendea amani, maendeleo na ustawi chini ya mwavuli wa udugu wa Kiislamu.

URAFIKI Wanaadamu wanahitaji urafiki na ushirikiano na wengine katika hatua zote za maisha yao toka wanapozaliwa hadi wanapokufa. Kutokana na asili yake ya maumbile, mwanadamu analazimika kuishi katika jamii pamoja na wanaadamu wenzake na kunufaika na msaada na ushirikiano wa rafiki zake. Wale wenye marafiki mwandani kamwe huwa hawawi wapeke au bila msaada hapa ulimwenguni, kwa sababu marafiki zao wenye upendo na huruma ndio washirika na wasaidizi wao katika kila dhiki na faraja. 181

12:45 PM

Page 181


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Kwa asili mwanaadamu huhisi furaha anapokuwa na marafiki zake na huwa na wasiwasi na huzuni anapokuwa mpweke na bila rafiki. Imam Ali (a.s.) anawachukulia marafiki wa kweli kuwa ni rasilimali kubwa katika ulimwengu huu na akhera na amesema: Jitafutieni marafiki kutoka miongoni mwa ndugu zenu katika imani kwa sababu wao ni rasilimali kubwa katika ulimwengu huu na kesho akhera.” – (Wasa’ilush-Shia’h). Katika kauli nyingine, Imam Ali (a.s.) amewachukulia marafiki wa kweli kuwa ni wazuri kama kiungo muhimu kabisa cha mwili wa mwanadamu na anasema: “Yule anayempoteza rafiki mwema ambaye alifanya naye huo urafiki kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ni kama yule aliyepoteza moja ya viungo muhimu vya mwili wake.” – (Ghurarul Hikam). Nukta ambayo mara zote imekuwa ndio kiini cha mazingatio cha viongozi wa Uislamu katika suala la urafiki, ni kuwa urafiki wenye thamani ni ule tu unaofanywa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na rafiki wa kuaminika ni yule tu ambaye urafiki wake umejengwa juu ya misingi na mazingatio ya kiroho. Urafiki unaoibuka kutokana na mali, cheo au uzuri hukoma mara tu vitu hivi vinapoondoka na hakuna ushawishi wa mali unaoweza kusaidia kudumu kwa urafiki. Jambo jingine ambalo limepewa umuhimu mkubwa na Uislamu ni suala la kuchagua rafiki. Kwa mtazamo wa Uislamu, urafiki hauwezi ukafaywa na mtu yeyote au kila mtu, kwa sababu kufanya urafiki na baadhi ya watu kuna madhara na ni hatari. Bila shaka kila rafiki huwa na athari katika masuala ya kimali na kiroho ya rafiki yake na kila mmoja wao hupenya kwa kukusudia au kwa kutokukusudia katika imani, fikra, maadili na mwenendo wa mwenzake. Uzoefu pia umeonyesha kwamba urafiki mwingi umebadili majaaliwa ya watu na umeathiri (vizuri au vibaya) mwenendo wa maisha ya mwingine.

182

12:45 PM

Page 182


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Marafiki huvutiana katika masuala ya mwenendo, fikra na imani. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: “Mwenendo wa kila mmoja utakuwa ni kwa mujibu wa imani na kanuni za rafiki yake.” – (Wasa’ilush Shi’ah, Juz. 4). Nabii Suleiman amesema: “Usimhukumu mtu kuwa ni mwema au mbaya mpaka uwaone marafiki zake, kwa sababu kila mtu hujulikana kwa kupitia watu anaotangamana nao na hivyo hutambuliwa kwa rafiki zake na washirika wake.” – (Mustadrakul Wasail, Juz. 2). Mwanafalsafa mmoja amesema: “Niambie ni mtu gani unayempenda ili nikwambie wewe mwenyewe unani, ukoje na kiwango cha akili yako, ladha yako na maadili yako yakoje.” Urafiki na ushirikiano na watu wenye staha ni moja ya sababu kuu za furaha na ustawi na kutangamana na watu mafisadi na waovu kunachukuliwa kuwa ni moja ya sababu za dhiki na balaa. Socrates amesama: “Watu wote wana thamani zao. Mwingine hupenda mali, mwingine hutaka uzuri na mwingine hugombea heshima. Lakini mimi ninaamini kuwa rafiki mzuri ni bora kuliko vitu vyote hivi.” Mwandishi mmoja mashuhuri wa Kiingereza amesema: “Mtu anapaswa kuwa mwangalifu sana anapochagua marafiki. Sehemu kubwa ya matatizo yetu ni matokeo ya kutangamana na watu wasiofaa. Mtu anapotoka katika uchanga wake na kuingia katika maisha halisi, hufahamiana na aina mbalimbali za watu na hivyo hutangamana na kundi moja au jingine. Mara nyingi hutokea kwamba, kama matokeo ya kutangamanana watu dhalili (kitabia), yeye pia hutumbukia katika dimbwi la udhalili. Inawezekana kwamba watu hawa duni (kitabia) hawana nia mbaya juu ya washirika wao zaidi lakini kutokana na maumbile yao yalivyo mara huwa wanawang’ata wengine kama nge na hupenyeza ushawishi wao wenye sumu katika roho zao.

183

12:45 PM

Page 183


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

“Baadhi ya watu wanajiamini sana na juu ya usafi wao wa kimaadili na wema wao kiasi kwamba huwa hawadhani kwamba kutangamana kwao na watu wabaya kunaweza kuwadhuru kwa lolote. Wanaziona tabia zao kuwa zipo juu ya hili kiasi kwamba maadili mabaya hayawezi kuziathiri na wanasahau ukweli kwamba pamba iliyo jirani ya moto lazima itashika moto. Kwa bahati mbaya ufisadi na uovu huiathiri roho ya mwanaadamu haraka mno kama rundo la baruti linavyoripuka linapoguswa na cheche na kuunguza vitu vyote vya jirani yake. “Yule anayejivunia maadili yake na hajiepushi kutangamana na watu wenye maadili duni ni sawa na mtu anayejenga nyumba yake katika njia ya mafuriko kwa matarajio kwamba nguvu ya mawimbi ya maji haitaudhoofisha msingi wa nyumba yake.” Methali ya kiarabu inasema: “Rafiki mbaya ni kama mhunzi. Hata asipokuunguza, moshi wa karakana yake utayadhuru macho yako.” Jaalia kwamba unajimudu vyema na ni mtu mkarimu kiasi kwamba kutangamana na watu wenye maadili duni hakuathiri tabia yako adhimu. Lakini je watu watakuwa na maoni gani juu yako? Je hawatakuweka katika kundi la watu wabaya kwa sababu ya kule kushirikiana nao? “Katika hali yoyote isisahaulike kuwa kushirikiana na watu wema ni suala la bahati njema kwa sababu kuna watu wengi ambao hutaabika kwa masaibu mbalimbali kutokana na kutokuwa waangalifu katika kuchagua marafiki zao.” – (The Secret of Happines). Hatari inayotokana na urafiki mbaya haiishii kwenye maisha ya mtu tu. Aina hii ya urafiki itakuwa ni sababu ya majuto katika Siku ya Hukumu pia. Ikizungumzia kundi la watu watakaoadhibiwa na Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama, Qur’ani tukufu inasema: 184

12:45 PM

Page 184


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

“Ni siku ambayo dhalimu watajiuma mikono yake (kwa kujuta) akisema, laiti ningeshika njia pamoja na Mtume. Ole wangu! Laiti nisingemfanya fulani kuwa rafiki. Kwa hakika yeye alinipotoza nikaacha mawaidha baada ya kunifikia .....” (Suratul Furqan; 27-29). Imam Ali (a.s.) amesema: “Mazuri ya dunia hii na Akhera yameungaishwa katika mambo mawili – yaani kutunza siri na kufanya urafiki na watu wema. Na ubaya wa dunia hii na Akhera umejumuishwa katika vitu viwili ambavyo ni kutoa siri zake mtu na kutangamana na watu waovu.” (Ikhtisas). Sa’di, mshairi mashuhuri na mtu mwema sana anasema: “Kama mtu anafuatana na watu wabaya atahesabiwa kama mmoja miongoni mwao hata kama hayuko hivyo. Halikadhalika kama mtu atakwenda kilabu ya pombe kuswali atachukuliwa kama mlevi. Umejithibitisha mwenyewe kama mtu mpumbavu kwa kumchagua mtu mpumbavu kama rafiki yako. Wakati ninapomuomba mtu mwenye busara kunipa kipande cha ushauri, alisema, usifanye urafiki na mtu mpumbavu.” Mtukufu Mtume (s.a.w.) anasema: “Mtu mwenye bahati zaidi ni yule ambaye hujishirikisha na watu watukufu na wakarimu.” (Amali Saduq, uk. 14) George Herbert anasema: “Jihusishe na watu wema ili kwamba na wewe uhesabiwa kama mmoja wao.” Mwanamke mwenye busara alizoea kuwashauri watoto wake: “Kama ambavyo miili yenu inavyopata nguvu kutokana na chakula tunachokula, 185

12:45 PM

Page 185


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

vivyo hivyo, nafsi (roho) zetu hupata wema na uchamungu au uovu na mabalaa kwa sababu ya kujihusisha na marafiki wema au wabaya.” Haiwezikani kwamba uhusiano wetu na urafiki na watu wanaotuzunguka hautaacha athari za ndani katika maadili yetu kwa sababu kwa asili mtu ana mwelekeo wa kuiga wengine, na kwa hiyo, kila mtu takriban huvutiwa na harakati, tabia na mitazamo ya rafiki na washirika wake. Mtu mwenye busara anasema: “Kuna usemi maarufu kabisa kwamba mtu hujulikana kwa uswahiba alionao. Bado mtu mwenye akili hajihusishi na mlevi, mwanachuoni na mjinga, mwenye heshima na asiye na heshima. Kujihusisha na watu duni na wenye tabia mbaya hujenga ndani ya mtu hisia duni zaidi na kama mahusiano hayo yatadumu kwa muda mrefu, atahusishwa moja kwa moja kama mmoja wa watu duni kama hao.” Mtu mwenye busara alisema: “Hata kuongea na watu kama hawa kuna madhara na ni hatari, kwa sababu hata ingawa mahusiano nao kunaweza kuwa na madhara kwa muda tu, lakini hata hivyo hupandikiza mbegu katika bogo zetu ambazo huchipua wakati fulani baadae na kuchukua mizizi yake.” Mahusiano na watu kama hao ni kama tu vile tauni inavyompata mtu mara moja. Kujihusisha na watu wenye tabia nzuri na wenye akili timamu ni kiburudisho bora cha nafsi ya mtu, na kinyume chake, kuhusiana na urafiki pamoja na mjinga na watu wabaya huwa ni sababu ya misiba na majanga. Usemi wa Kihispania unasema: “Kama ukienda kwenye mbwamwitu, utakachojifunza ni makelele yao.” Urafiki na watu duni na wabinafsi hubeba hatari kubwa katika mkondo wake kwa sababu tabia zao za kimaadili hushawishi na kuharibu fikra za 186

12:45 PM

Page 186


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

mtu na kuuwa moyo wa kiutu na maadili ya hali ya juu ndani mwake. Na kama urafiki ukiendelea mtu anakuwa baridi na mnyonge na akili ya kimaendeleo na heshima huondoka. Kinyume chake, urafiki na watu ambao wana busara, makini na wenye uzoefu zaidi ni rasilimali yenye thamani, kwa sababu urafiki nao hunywesha moyo mpya kwa mtu na hutufundisha njia na tabia za maisha ya kufuzu na kuimarisha imani na rai zetu ikilinganishwa na wengine na hutufanya tushiriki ujuzi, hekima na uzoefu wao. Kwa hiyo, hakuna kilicho na nguvu na manufaa zaidi kwa kujenga maadili yetu kama kuanzisha urafiki na watu wenye maana na busara, kwa sababu kujihusisha nao huongeza nguvu zetu za kiroho na kuongeza kwenye utashi wetu na kufanya malengo yetu katika dunia kuwa juu na matukufu na hutufundisha kutenda wajibu wa kibinafsi na halikadhalika wajibu wetu kijamii. Sheikh Sa’di anasema kuhusu athari ya mahusiano na urafiki: “Siku moja nikiwa kwenye hamamu kipande cha udongo chenye kunukia kilifika kwenye mkono wangu kutoka kwenye mkono wa mpenzi. Nilikiuliza: ‘Wewe ni miski au ambari, kwa sababu napatwa na ulevi kwa manukato yako yenye kunukia uzuri.’ Kikajibu: ‘Nilikuwa tu udongo usiokuwa na thamani, lakini kwa muda mrefu niliwekwa pamoja na waridi. Harufu nzuri ya swahiba wangu imeniathiri, vinginevyo mimi ni kipande kilekile cha udongo duni.’” Imamu Ja’far (a.s.) anasema: “Wakati wa mlolongo wa khutba zake, baba yangu aliniambia: ‘Mwanangu! Yeyote yule anayejihusisha na watu wabaya hawezi kuepuka madhara kutoka kwao na yeyote anayetembelea mara kwa mara sehemu mbaya hupata sifa mbaya na yeyote yule ambaye haulindi ulimi wake anapaswa kujuta na kutubia.’” (Khisal Saduq, Jz. 1, uk. 80) Imamu Sajjad (a.s.) anasema: “Usijihusishe na watu wa aina tano na vilevile usizungmze nao na usisuhubiane nao kwa hali yoyote: 187

12:45 PM

Page 187


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

(i) Epukana na waongo kwa sababu wako kama mazigazi. Kwa maneno yao duni huelezea mambo kinyume na yalivyo kiuhalisi. Kwa uwongo wao huonesha vitu vilivyoko mbali kuwa karibu na ambavyo viko karibu kuwa viko mbali na kukupotosha kutoka kwenye njia ya haki. (ii) Jiepushe na mafisadi/maesherati na watenda dhambi kwa sababu urafiki wao sio wa kutengemewa na watakuuza kwa tonge au chini ya hilo. (iii) Jiepushe na watu wachoyo kwa sababu wakati wa kuhitaji na wa matatizo watu hawa watakufanya udhalilike. (iv) Kaa mbali na watu wapumbavu kwa sababu wanaweza wawe wenye kutaka kukufanyia wewe mema lakini watakuingiza kwenye matatizo kwa ajili ya upumbavu na upuuzi wao. (v) Jiepushe na watu wale ambao wamejitenga na ndugu na jamaa zao na kuwafanyia mambo mabaya kwa sababu watu hawa wamelaaniwa na Allah katika Qur’an Tukufu.” (Biharul Anwar) Hivyo Imamu Ali (a.s.) katika kuhusiana na ushauri aliompa mwanawe Hasan (a.s.), alisema: “Epuka maeneo yenye heshima mbovu na kaa mbali na mikutano ambayo inahusika na dhana na kumbuka kwamba swahiba mbaya humdanganya rafiki yake na kumhimiza kufanya matendo maovu na hatimaye kumharibu. (Wasa’ilush Shi’ia, Jz. 3.) Imamu Ja’far Sadiq (a.s.) anasema: “Marafiki waaminifu ambao wameambatanishwa kwa mtu kama ndugu ni wa aina tatu: Kwanza, rafiki ambaye anahesabiwa kuwa mtu mmoja mwenye uhakika wa mahitaji muhimu ya lazima ya maisha kama chakula na ambaye mtu husimama mwenye kumhitajia katika hali zote. Mtu kama huyo ni rafiki mwenye busara.

188

12:45 PM

Page 188


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Pili, mtu ambaye kuwepo kwake ni kama maumivu na maradhi. Mtu kama huyo ni rafiki mpumbavu. Tatu, Rafiki ambaye kuwepo kwake ni kama dawa ya kuokoa maisha. Rafiki kama huyo ni mwenye akili na busara sana. (Tuhaful Uqul) Marafiki wenye busara wanaweza kuwaokoa watu kutoka kwenye hatari kubwa wakati wa hali ngumu sana, na wale ambao wana marafiki kama hawa wana rasilimali yenye thamani na neema kubwa. Imamu Ali amekataza kufanya urafiki na watu vigeugeu na anasema: “Hakuna kitu chochote kizuri katika urafiki na mtu mwenye mawazo ya kubadilika badilika na kigeugeu kwa sababu upande wowote upepo utakapoelekea kuvuma, wataelekea upande huo pamoja na upepo huo. Ni wakarimu mno wakati ukiwa hutaki utajiri wao lakini kama utasimama kuhitaji utajiri wao, wanakuwa mabahili. Bila shaka wakati rafiki wanapohesabiwa ni wengi kwa idadi, lakini rafiki anayekuja wakati wa dhiki na haja kubwa ni wachache sana.” (Diwan-i Imam Ali (a.s.)) Imamu Ja’far (a.s.) anasema: “Epuka urafiki na watu wa aina tatu: msaliti, dhalimu na mbea, kwa sababu siku moja atawadanganya wengine ili kukupata wewe na siku nyingine vilevile atakudanganya wewe, na mtu anayewaonea watu kwa ajili yako siku moja atakuonea wewe vilevile, na mtu anayesengenya wengine mbele yako punde tu atakusengenya wewe mbele za watu wengine.” (Tuhaful Uqul) Ili kuchagua rafiki mzuri ni muhimu kabisa kwamba mtu afanye utafiti. Mark Orwel anasema: “Kama unataka kufanya urafiki na mtu, kabla ya mambo yoye yale kwanza angalia kiwango chake cha akili kiko kiasi gani, nini maoni yake kuhusu wema na ubaya? Ni umuhimu gani anaweka kwenye heshima na ufedhuli? Nini kinafanyiza bahati nzuri na shida katika macho yake? Hili ni muhimu ili kwamba usije ukashangaa baadae juu 189

12:45 PM

Page 189


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

ya yale unayosikia kutoka kwake au kile anachokuambia kwa sababu vitendo vyake vyote vinachukuana na kile alichokisema na kwa mujibu wa njia yake ya kufikiria.” (Friend and Friendship). Watu wenye busara na wazoefu wako makini sana katika kuchagua marafiki na kama wana hamu kubwa ya kuanzisha urafiki wa kweli hutenda kwa mujibu wa hekima na mantiki na hawaruhusu haraka na hisia za zisizofaa kuingilia kati katika suala hili. Kwanza wanafahamiana na yule mtu mwingine ili kwamba wawe na habari juu ya namna yake ya kufikiria, maadili na mambo yake yaliyotangulia. Hivyo humweka kwenye majaribio katika nyakati na matukio tofauti na kumfanya rafiki kama ataonekena kuwa mzuri kwa urafiki katika vipengele vyote. Urafiki kama huo uko safi kutokana na matatizo yoyote na uko imara na tulivu. Imamu Ali (a.s.) anasema: “Kama mtu ataanzisha urafiki baada ya kuchunguza, utakuwa imara na mtulivu.” (Ghurarul Hikam). Wakati alipokuwa anatoa ushauri kwa Ibn Mas’ud, Mtukufu Mtume alisema: “Ni muhimu kwamba rafiki yako lazima awe mchamungu na mwema na lazima unyooshe mkono wa undugu na urafiki kwa wale watu tu ambao wanajinyima na wema, kwa sababu Mwenyezi Mungu amesema katika Qur’ani Tukufu kwamba katika Siku ya Hukumu marafiki wote watakuwa maadui wenyewe wao kwa wao isipokuwa watu wachamungu ambao urafiki wao utakuwa imara. (Makaramul Akhlaq). Vigezo vyote, mipaka na sifa za rafiki zimetajwa katika mafundisho ya Uislamu ambayo yanaweza kuwa kama mwongozo kwa ajili ya kuchagua na kujaribu marafiki. Imamu Ja’far (a.s) anasema: “Urafiki una mipaka na masharti maalum. Mtu ambaye hatimizi baadhi ya masharti haya, huyo hawezi kuitwa rafiki aslani:

190

12:45 PM

Page 190


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

(i) Nje kwake na ndani kwake lazima kuwe sawa na chochote anachoshuhudia kuhusu wewe kwa ulimi wake halikadhalika lazima kitoke moyoni mwake. (ii) Lazima achukulie mambo yako mazuri kuwa mambo yake mazuri na mambo yako mabaya kuwa mambo yake mabaya. Kadhalika lazima achukulie heshima yako kuwa heshima yake na fedheha yako kuwa ni fedheha yake. (iii) Kama hali yake ya kiuchumi inakuwa nzuri na akakusanya utajiri au akapata cheo kikubwa hatakiwi abadilishe tabia yake kwako. (iv) Hatakiwi ashindwe kukusaidia wewe kwa kadiri ya uwezo wake na uhodari wake. (v) Hapaswi kukuacha peke yako na kukutelekeza wakati umezingirwa katika shida.” (Amali Saduq, uk. 397). Imamu Ja’far (a.s) anasema: “Kama mmoja wa jamaa zako anapokukasirikia mara tatu lakini haseni kitu kibaya kuhusu wewe, unaweza kunyoosha mkono wa urafiki kwake na kuanzisha uswahiba naye.” (Safinatul-Bihar) Imamu Ali (a.s.) anasema: “Mtu hawezi kuitwa ‘rafiki wa kweli’ isipokuwa wakati anapolinda heshima ya rafiki yake katika shida na katika wakati akiwa hayupo na baada ya kufa kwake.” Wastani katika urafiki ni nukta nyingine muhimu sana ambayo wakati wote lazima uchungwe kwa sababu inawezekana kwamba kupita kiasi katika urafiki kunaweza kusababisha hasara zisizoweza kurekebishika na unaweza kumuweka mtu katika hali ya hatari.

191

12:45 PM

Page 191


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Wakati wa urafiki, uaminifu lazima uwekwe juu ya rafiki kwa kiasi kwamba kama utengano utatokea katika hatua ya baadae kwa ajili kutofautiana asiweze kufanya madhara yoyote. Imamu Ali (a.s.) anasema: “Kama ukiwa na mapenzi na mtu katika moyo wako, elezea urafiki wako kwake ndani ya mipaka ya uwasitani na manufaa kwa sababu inawezakana kwamba siku moja anaweza kugeuka dhidi yako. Na vivyo hivyo, kuwa mpole kwa mtu ambaye humtaki kwa sababu siku moja uhusiano wenu unaweza kuacha kuwa wa majaribu na anaweza kuwa rafiki yako.” (Tuhaful Uqul) Sa’di ambaye ametiwa msukumo sana katika beti zake za kishairi na maandishi yake kutokana na hadithi za Mtukufu Mtume (s.a.w.) na Maimamu watukufu (a.s) anasema: “Usije ukatoboa siri yoyote kwa rafiki yako kwa sababu inawezakana siku moja akawa adui yako na usimfanyie madhara yoyote adui yako kwa sababu inawezekana kwamba wakati mwingine baadae akawa rafiki yako.” (Gulistan) Mwandishi mmoja wa Kiingereza anasema: “Kuwa na mwenendo mzuri na marafiki zako katika namna ambayo hata kama watageuka kuwa maadui zako hutaweza kudhurika nao na wafanyie maadi zako katika namna ambayo kama wakiwa marafiki zako hutalazimika kuwa na aibu. Kuna watu wengi ambao hawachungi kanuni hii na hatimaye huwa wenye wasiwasi na kuchanganyikiwa. Huwaambia marafiki siri zao muhimu sana, na matokeo yake ni kwamba wakati urafiki wao utakapovunjika na kubadilishwa na uadui, watu walewale ambao walikuwa marafiki wapenzi mpaka jana husimama kumuangamiza kwa silaha ambazo tayari anazo mkononi. Ilikuwa ni kwa sababu hii hii kwamba wakati mmoja wa makamanda wakubwa alipokuwa anaelekea kwenye uwanja wa mapambano alimuambia Louis XIV: “Nilinde kutokana na fitna za maadui zangu. Siwaogopi hao maadui.” Imamu Ali (a.s.) anasema: “Toa uchangamfu wako wote na mapenzi kwa rafiki yako lakini usiweke kujiamini kwako kote kwake. Msaidie katika 192

12:45 PM

Page 192


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

mambo yote lakini usiibue siri zako kwake.” (Kanzul Fawa’id, Karachaki) Kwanza kabisa ni vigumu kupata rafiki wa kuaminika na bado ni vigumu zaidi kudumisha urafiki. Kama haki na wajibu havikuzingatiwa katika urafiki, mfungamano wake huvunjika mara moja. Imamu Ali (a.s.) anasema: “Mtu mnyonge mno miongoni mwa watu ni yule mtu ambaye hawezi kupata rafiki, na mnyonge kuliko yeye ni yule ambaye anapoteza marafiki.” (Nahjul Balagha) Shakespeare anasema: “Mjali rafiki yako kama unavyojali maisha yako mwenyewe.” Sina’i anasema: “Mchukulie mtu kuwa mbaya yule ambaye ana marafiki wachache na kuwa mbaya kuliko wote yule anayepoteza marafiki baada ya kuwapata.” Kuna mambo mengi yanayofarakisha marafiki na moja katika hayo ni kumuudhi na kumsumbua rafiki yake mtu. Amiru’l-Muminin Imamu Ali (a.s.) anasema: “Wakati mtu anapomuudhi na kumkosea rafiki yake anatengeneza njia ya kukosana na kutengana.” (Nahjul Balagha) Kipengele kingine ambacho kinaweza kutenganisha marafiki ni kusikiliza usengenyaji wa wambea. Hapana shaka kuna watu ambao hujisikia kuhuzunishwa juu ya uhusiano mkunjufu wa kirafiki wa watu wengine na siku zote hujitahidi kusababisha hitilafu kati yao. Huchukuwa maneno kutoka kwa rafiki huyu kuyapeleka kwa rafiki huyu na kusababisha kuvunja uhusiano wao mzuri wa kirafiki. Imamu Ali (a.s.) anasema: “Yeyote yule anayetega sikio lake kwenye maneno ya mbea atampoteza rafiki yake mpenzi.” (Nahjul Balaghah) 193

12:45 PM

Page 193


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Ni jukumu la watu kukataa na kupuuza kile ambacho wachonganishi wambea wanachosema ili wajiepushe na tabia hii chafu na hatimaye wasipoteze marafiki zao. Kutafuta makosa ya marafiki zake mtu na kuambatanisha umuhimu usio na maana kwenye vikosa vidogo vidogo na kuboronga kwao ni jambo jingine ambalo linaweza kuvunja urafiki. Ni ukweli unaojulikana kwamba kila mtu hufanya makosa na kuyumba katika maisha yake na ni wajibu wa Mwislamu kutojali vikosa vidogo dogo vya ndugu yake katika imani na katika marafiki zake wapenzi. Imamu Ali (a.s.) anasema: “Kubali msamaha wa rafiki yako (kwa kosa alilolifanya) na ikiwa hawezi kuomba samahani upesi kwa ajili ya kosa lake tunga samahani moja kwa ajili yake. (Nahjul Balaghah) Mmoja wa watu wenye busara anasema: “Mtu lazima akubali samahani iliyotolewa upesi na rafiki zake hata kama itakuwa hairidhishi kwa sababu lile jambo la kwamba mtu amejuta na kuomba radhi huonesha kwamba amenyoosha mkono wake kwa ajili ya maendeleo ya urafiki na ni jukumu la mtu kwamba wakati mkono wa mtu umenyooshwa kwake ni lazima aupokee.” Sa’di anasema: “Rafiki hapati kukosewa na rafiki kwa sababu ya makosa yoyote na kama akikosewa na bado akidai kuwa rafiki, madai yake hayo siyo sahihi.” Utani, masihara, kudhalilisha na kuwafanyia mzaha marafiki ni sababu nyingine za kuvunjika kwa uhusiano wa kirafiki. Siku moja Harith mtoto wa A’war ambaye alikuwa mmoja wa masahaba wa Imamu Ali alielezea uaminifu na mapenzi yake na akasema: “Ewe Amir’l-Muminin! Mimi ni rafiki yako.” Wakati alipokuwa anataja urafiki 194

12:45 PM

Page 194


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

mtukufu Imamu alielezea mambo machache ambayo marafiki hawatakiwi kuyafanya kwa kuhusiana wao wenyewe kwa wenyewe. Alisema kama unamfanya mtu kuwa rafiki yako: Usigombane naye na usiwe na uadui naye. Usimdhihaki. Usibishane naye. Usimtolee utani mchafu. Usimdharau au kumchukulia kuwa dhaifu. Usidai kuwa na umuhimu au ubora juu yake. Mambo haya sio mazuri kwa kudumisha urafiki.” (Khisal Saduq, Jz. 1, uk. 296) Mmoja wa watu wenye busara anasema: “Wengi wa watu hupendelea kupata hasara kuliko kusikia maneno ya dhihaka.” Msemo wa kilatini unasema: “Dhihaka huharibu urafiki.” Tunafikia hitimisho kutokana na yaliyosemwa hapo juu: (i) Marafiki hufanya ushawishi wa kina na kutekeleza wajibu muhimu katika ufanisi au katika shida za kila mmoja wao. (ii) Urafiki lazima utegemee juu ya imani na uchamungu na lazima utokane na hali ya kiroho. Aina nyingine za urafiki haziaminiki. (iii) Mtu lazima aepuke urafiki wa watu waovu na wapotofu, kwa sababu watamharibu. (iv) Urafiki una mipaka yake na ni muhimu kwamba kabla ya kuanzisha urafiki majaribio yanayohitajika lazima yafanyike ili kwamba mtu asije akajuta baadae. (v) Urafiki wa marafiki waaminifu lazima uthaminiwe na uangalizi mkubwa lazima uchukuliwe ili kuuhifadhi.

195

12:45 PM

Page 195


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Nukuu: 1. Usishirikiane na watu wa aina tano na vilevile usizungumze nao na usifuatane nao katika hali yoyote. Epukana na waongo kwa sababu wako kama mazigazi. Kwa maneno yao yasiyo na msingi huonesha mambo tofauti na vile yalivyo kihalisia. Kwa uwongo wao huonesha kitu cha mbali kuwa karibu na kitu ambacho kiko karibu kuwa mbali sana na hivyo kukupotosha kutoka kwenye njia iliyonyooka. Waepuke waesherati, mafisadi na waovu watenda dhambi kwa sababu urafiki wao hauaminiki na watakuuza kwa tonge au hata kwa kidogo zaidi ya hicho. Waepuke watu mabahili kwa sababu katika wakati wa shida na magumu watu hawa watakufanya udhalilike na kunyongeka. Kaa mbali na watu wapumbavu kwa sababu wanaweza wakawa wanapenda kukufanyia wewe mambo mazuri lakini watakuingiza katika shida kwa sababu ya ujinga na upumbavu wao. Jiepushe na watu ambao wamejitenga na ndugu na jamaa zao na kuwafanyia mabaya, kwa sababu watu hawa wamelaaniwa na Allah katika Qur’an Tukufu. (Imam Sajjad) 2. Urafiki! Siri ya unganisho la nafsi! Tamu ya maisha! lehemu ya jamii. (Robert Blair, The Grave) 3. Niambie marafiki ulionao, na nitakueleza wewe ni nani. (methali) 4. Miliki ya kupendeza haina maana bila rafiki. (Seneca) 5. Njia pekee ya kupata rafiki ni kuwa rafiki. (Ralph Waldo Emerson, Friendship)

196

12:45 PM

Page 196


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

USAFI Moja ya vipengele muhimu na vyenye kuvutia katika mafundisho ya Kiislamu ni kile kinachohusika na usafi. Hivi sasa pamoja na maendeleo ya majarabio ya kisayansi na upatikanaji wa nyenzo na uanzishaji wa maabara mbalimbali, umuhimu wa suala la usafi na athari yake ya moja kwa moja juu ya afya ya mwanadamu umekuwa wazi kabisa. Wakati wa zama hizi za sasa mwanadamu ametambua vijiumbe maradhi na virusi na amegundua magonjwa yanayosababishwa navyo. Matatizo mengi ambayo sasa huchukuliwa na wanadamu kuwa ni ya kawaida na ya mahali pake yalikuwa hayajulikani mpaka karne iliyopita na hakuna mtu aliyekuwa na ujuzi wowote kuhusiana nayo, na kama wanasayansi wa wakati huu wameelezea umuhimu wa usafi na wakaupendekeza kwa watu hakuna geni au cha ajabu kuhusu hilo. Wamechungza maadui wasionekana kwa msaada wa darubini na wamefanya majaribio mengi juu ya kila mmoja, na sasa wanawajulisha watu juu ya hatari zilizo karibu kuibuka kutokana na kuwepo kwao. Inavutia kuona kwamba mpaka karne ya 16 ya zama za Ukristo, Wazungu si tu hawakuyazoea mambo haya bali maisha yao yalikuwa hayana kabisa dhana yenyewe haswa ya usafi kiasi kwamba kila mtu anashangazwa kujua habari hii. Hamamu za umma zilikuwa hazijulikani katika miji ya Ulaya na watu walikuwa dhidi ya kuzijenga na isitoshe, Wachungaji wa Wakristo vilevile hawakutoa ruhusa yao kwa ajili ya kuzijenga. 197

12:45 PM

Page 197


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Kulikuwa hakuna vyoo katika nyumba, na watu walitupa uchafu wao mitaani na barabarani. Ukweli huu umesimuliwa na wanachuoni watafiti wakubwa ma Kiingereza. Will Durant, mwandishi mashuhuri Mkristo, anasema kuhusu hali iliyokuwepo wakati huo katika Ulaya: “Wakristo wa mwanzo walizichukulia hamamu za moto za Kiroma kuwa hazina heshima na vituo vyote kama hivyo kuwa ni mashimo ya upotofu na vurugu ya ngono. Aidha, kama ukristo kwa jumla ulivyozungmzia kuhusu mwili kuwa wa kuchukiza na kufaa kwa kutelekeza, kufuata kanuni za afya hakukuweza kufikiriwa.” Katika sehemu nyingine anaandika: “Katika karne ya kumi na tatu Waparisi (Wafaransa) bila kipingamizi walikuwa wakimwaga ndoo zao za mikojo kwenye barabara kutoka kwenye madirisha na njia pekee ya usalama aliyokuwa nayo masikini mpita njia, ilikuwa tahadhari inayotolewa na wakazi wa nyumba hizo ambao watasema kwa sauti kubwa “Garl ‘eau” (msije mkaloweshwa). Matokeo kama hayo yasiyotegemewa yakawa moja ya dhihaka maalum za tamthilia ambazo ziliendelea mpaka wakati wa Moliere. Vyoo vya umma ilikuwa bado ni anasa. Katika mwaka wa 1255 baadhi ya vyoo vya umma vilikuwepo katika San Gimignano, lakini vilikuwa bado havijaanzishwa katika Florence. Watu walikojoa kwenye maeneo ya wazi, na juu ya ngazi, kutoka kwenye vyumba vya juu na hata katika kasri ya Louvre. Baada ya mlipuko wa tauni katika mwaka wa 1531 amri maalumu ilitolewa ikiwataka watu wote wanaomiliki nyumba mjini Paris kujenga vyoo kwa kila nyumba, lakini watu wengi walishindwa kutekeleza amri hizi. (History of Civilization, Will Durant, vol.XIII, uk. 502-503). Vita vya msalaba ambavyo viliendelea kati ya Wazungu na Waislamu kwa muda mrefu viliwazoesha Wakristo na hamamu na kuwafundisha kuhusu umuhimu wa usafi. 198

12:45 PM

Page 198


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Will Durant anaandika: “Moja ya matokeo mazuri ya vita vya msalaba ilikuwa kwamba katika kuiga hamamu za maji ya moto za Waislamu, hamamu za maji ya moto za umma zikawa sasa zinapatikana katika nchi za Ulaya. Hata hivyo, kanisa halikufurahia hamamu za umma.” (History of Civilization, Will Durant, vol.XIII, uk. 502-503) Hata katika wakati huu katika vyoo vya nchi nyingi za Ulaya makaratasi hutumika badala ya kuosha kwa maji na harufu mbaya ya mwili inazimwa kwa njia ya eua-de-colongne na vitu vingine kama hivyo. Huu ulikuwa ni mfano wa hali za nchi za Ulaya kuanzia karne ya kumi na tano kuendelea hadi leo. Sasa tunakwenda nyuma kidogo na kujiweka wenyewe katika ulimwengu wa giza wa karne kumi na nne zilizopita. Ulikuwa ni wakati binadamu anapambana katika giza la ujinga na hakujua chochote kuhusu ustaarabu, elimu na hekima. Katika wakati huo viongozi wa Uislamu waliwasilisha kwa watu mafundisho ambayo yana asili ya ki-Mungu na ambayo yaliwasilishwa kupitia ufunuo wa Mungu. Walitengeneza kaulimbiu ‘Usafi ni sehemu ya imani’ ifikie masikio ya watu, na wakaanzisha ‘Allah huwapenda wanaotubia na wale ambao ni wasafi’ kama hatua ya kwanza kuelekea kwenye usafi wa mwili na roho. Imamu Ali (a.s.) aliwahimiza watu kuwa wasafi na akasema: “Hamamu ni mahala pazuri. Joto lake humkumbusha mtu Moto wa Ghadhabu ya Allah na vilevile huondoa uchafu wa mwili.” (Wasa’ilush-Shi’a) Katika taratibu za Kiislamu, hamamu ‘zilizopendekezwa’ zimefanywa kama sehemu ya tendo ‘lililopendekezwa’ katika siku za Ijumaa, sikukuu za Idd na siku nyingine za heri.

199

12:45 PM

Page 199


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Amri ya kwanza kutekelezwa kabla ya kuzuru Makuba matukufu na makaburi matakatifu ni ile ya kukoga. Amri hizi zilitolewa katika nchi ambazo wakazi wake hawafaidi nafasi ya kuridhisha katika suala la maji na hata sasa huchota maji kutoka kwenye visima kukidhi haja zao. Ni kutokana na mkazo wa maelekezo haya ya kidini kwamba hata wakati wa Zama za Kati wakati Wazungu walikuwa wakiendesha maisha yao katika hali ya uchafu kabisa, Waislamu walikuwa wanafaidi utakaso na usafi wa kupendeza. Katika kitabu ‘Muslim life in middle Ages’, mwandishi wa Kifaransa ameonesha hali za nchi za Kiislamu, katika karne ya kumi na tatu mpaka kumi na nne za zama za Kikristo, kwa urefu. Anasema: “Baada ya ujio wa Uislamu utumiaji wa hamamu za umma ukawa kawaida na muda mwingi haukupita Waislamu wakajenga hamamu kubwa. Katika miji mikubwa kulikuwa na hamamu moja au mbili katika kila mtaa na katika miji midogo na vijijini, hamamu zilijengwa karibu na Misikiti. Katika karne ya kumi na mbili kulikuwepo na takriban hamam 5000 mjini Baghdad na 1170 mjini Cairo.” Kwa sababu ya kufuata sheria ya za Uislamu,Waislamu wamekuwa taifa safi zaidi la ulimwengu. Uislamu unapendekeza kwamba wakati Waislamu wakienda msikitini kusali, lazima wavae nguo zao nzuri, wajitie manukato, na wajizuie kula vitunguu na vitunguu saumu na vitu vyenye harufu mbaya. Inapendekezwa kwamba kabla ya kuondoka nyumbani kwao lazima wawe wamevaa nguo nzuri, wachane nywele zao na kujiangalia katika kioo kujihakikishia wenyewe kuhusu hali ya mavazi yao na umbile. Katika mafundisho ya Uislamu umakini umewekwa kwenye masuala yenye umuhimu sana na maelekezo ya lazima yametolewa kwa kinagana200

12:45 PM

Page 200


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

ga ili kuyafuata. Wanahadithi wasema kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.) aliwaamuru wafuasi wake kuwa wasafi na tohara na akawahimiza sana katika hilo. (Kanzul Fawa’id, Karachaki) Moja ya hadith ya Mtukufu Mtume (s.a.w.) ambayo imekuja katika muundo wa kaulimbiu ya kudumu na ya kupendeza kwamba, “Usafi ni sehemu ya imani ya mtu na imani humuelekeza mtu Peponi.” (Mustadrakul Wasa’il, Jz. 1, uk. 100) Hapa hatuhusiki na majukumu ya kidini ambayo yanahusika moja kwa moja na tohara za wajibu za watu na ambazo Waislamu huzitekeleza kama vifungu vya ibada bila upuuzaji mdogo au uvivu. Kwa mfano, hapa hatuhusiki na suala la wudhu ambalo hufanywa mara kadhaa na kila Mwislamu wakati wa mchana na usiku kwa ajili ya kusali na ambalo huleta usafi kuazia kichwani hadi miguuni. Vilevile hapa hatuhusiki na majosho ya wajibu ambayo lazima yafanywe na Waislamu wanaume na wanawake kila mara kama wajibu wa kidini na mwili wote lazima ukoshwe wakati wa kuyatekeleza majosho hayo. Halikadhalika hapa hatujadili jukumu la mwislamu kujiepusha na uchafu (najasat) na kuweka miili yao na nguo zao katika hali ya usafi kutokana na uchafu ulioelekezwa kidini. Hapa tunakusudia kujadili maelekezo ambayo yana kipengele kimoja cha mwongozo na ambacho kwacho maelezo ya suala la usafi yameshughulikiwa. Uislamu kwa msisitizo umependekeza utohara wa mwili na nguo na umewataka watu kuviweka katika hali ya usafi. Mtukufu Mtume (s.a.w.) anasema: “Yeyote yule anayevaa nguo ni lazima 201

12:45 PM

Page 201


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

iwe safi na tohara.” (Makarimul Akhlaq, uk. 117) Katika nguo za mabakabaka, hususan zile zenye rangi nyeusi, uchafu na najisi havionekani na matokeo yake kuna uwezekano wa uchafu kutokuwa wazi katika nguo za mtu na anaweza awe halijui hilo. Mtukufu Mtume (s.a.w.) anasema: “Miongoni mwa nguo zenu hakuna zilizo bora kama nguo nyeupe. Lazima mchague nguo nyeupe kwa ajili ya mavazi yenu”. (Makarimul Akhlaq, uk. 117) Idadi ya hadithi zimekuja kutoka kwa Maimamu watukufu kuhusiana na kuosha na kutoharisha nguo. Imamu Ja’far Sadiq (a.s.) anasema: “Nguo safi na nadhifu humdhalilisha adui yake mtu na uoshaji wa nguo huondoa huzuni. (Da’aa’i-mul Islam) Ama kuhusu makazi, imependekezwa kwa msisitizo katika Uislamu kwamba Waislamu lazima wajitahidi kuyaweka safi na nadhifu. Mtukufu Mtume (s.a.w.) anasema: “Fagia sehemu iliyo mbele ya nyumba yako na ifanye kuwa safi na usiwe mchafu kama Wayahudi.” (Makarimul Akhlaq, uk. 145) Imamu Ali (a.s.) anasema: “Kuwaacha bubui wabakie chumbani huleta umasikini na kuweka uchafu ndani ya nyumba baada ya kufagia humburuza mtu kwenye ufukara”. (Mishkatul Anwar) Mtukufu Mtume (s.a.w.) anasema: “Baada ya kula chakula, kuacha vyombo bila kuoshwa; kuruhusu buibui kutanda ndani ya nyumba, na kuacha vyombo vya maji wazi bila kufunikwa huleta ufukara.” (Jami’ul Akhbar)

202

12:45 PM

Page 202


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Mtukufu Mtume (s.a.w.) vilevile anasema: “ Usiache uchafu uliofagiliwa na uchafu mwingine kubakia ndani ya nyumba yako wakati wa usiku, kwa sababu ni makazi ya shetani.” (Makarimul Akhlaq, uk. 490) Inawezekana ikaulizwa kwamba ni vipi uchafu waweza kuwa makazi ya shetani. Ili kueleza suala hili ni muhimu kwamba lazima kwanza tuelewe maana yake halisi na kisha tuangalie ni katika maana gani imetumika katika Qur’an Tukufu na katika simulizi za viongozi wa Uislamu. Kwa mujibu wa kamusi ya Kiarabu neno ‘Shytan’ lina maana nyingi, moja wapo ya hizo humaanisha, “Kila asi na mkaidi awe imma ni mwanadamu au jini na imma iwe ni kiumbe kidogo au kikubwa.” (al-Munjid) Vilevile katika Qur’ani Tukufu neno ‘Shaytan’ limetumika katika maana mbalimbali: Ya kwanza, kuhusu ‘Iblis’ ambaye ni mshawishi wa wanadamu (Surah Ibrahim, 14:22) Ya pili, kuhusu wanafiki ambao kwa dhahiri waliukubali Uislamu, lakini kwa ndani wanashirikiana na maadui wa imani. (Surah al-Baqarah, 2:12) Ya tatu, kwa wale ambao wamejiunga na majeshi pinzani ya Mitume watukufu. (Surah al-An’am, 6:112) Ya nne, watu ambao wamepotoka huchukuliwa kama watu wa kundi la shetani. (Surah al-Mujdilah, 58:19) Kwa hiyo kila kiumbe ambacho huwa sababu ya upotofu au shida kwa wanadamu na kuwavuta kwenye uharibifu na mateso ni Shaytan, imma iwe katika muundo wa mtu, nyoka, kiumbe kidogo sana au vijiumbe maradhi. Katika msingi huu kama katika baadhi ya masuala tunatumia neno ‘Shaytan’ kuhusiana na vijiumbe maradhi na virusi ambavyo husababisha maradhi, tutakuwa tunazungumzia kitu sahihi kabisa kwa mtazamo wa 203

12:45 PM

Page 203


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

maana yake ya msamiati. Sasa tukiziweka nukta hizi katika mtazamo, kama tukisema kwamba baadhi ya sehemu za mwili wa mwanadamu ni sehemu za ustawishaji wa shetani, tuna maana kwa sababu hiyo, sehemu ambako usengenyaji, njama na uharibifu huishia humo au kwenye sehemu fulani za mwili kama makwapa au madoa chini ya masharubu na kucha, tutakuwa hatusemi kitu cha kimakosa katika hali yoyote ya hizi. Hii ni hivyo kwa sababu mikusanyiko ambayo kwamba njama na uharibifu hutokea siku zote huwa na mashetani ambao hufanya mipango ya kuwadhuru wengine na katika masharubu na makwapa na chini ya kucha, mashetani wa aina nyingine; yaani vijiumbe maradhi hufanya makazi humo. Katika hadith za Ahlul Bayt - a.s. (kizazi kiteule cha Mtukufu Mtume s.a.w.) neno ‘Shaytan’ mara kwa mara lilikuwa likitumika kwa vijiumbe maradhi. Karne kumi na nne (na zaidi) zilizopita watu walikuwa hawana habari ya vijiumbe maradhi na akili zao, pia, hawakuweza kutambua masuala haya. Na kama ilivyokuwa muhimu kwa viongozi wa Uislamu lazima wazungumze na watu kwa lugha zao na kutegemeana na kiwango cha akili zao walimtambulisha kiumbe huyu mdogo na Shaytan, jina ambalo kwa ukamilifu limezoeleka kwao na kuchukulia kuwa adui wao hatari. Kwa hiyo, kama Mtukufu Mtume (s.a.w.) anasema kwamba takataka zilizofagiliwa na uchafu ambao unakusanywa kutoka penu na kona za nyumba lazima zitupwe nje mara moja na zisiruhusiwe kubakia ndani ya nyumba wakati wa usiku kwa sababu ni makazi ya shetani humaanisha kwamba vijiumbe maradhi vyenye madhara ambavyo ni sababu kubwa ya maradhi na mateso ya mwanadamu hufanya makazi na kuishi humo. Na kama Imamu Ali (a.s.) akisema kwamba buibui, takataka na uchafu huleta umasikini ndani ya nyumba ina maana kwamba vijiumbe maradhi hukaa kwenye sehemu hizi, huzaana na kumfanya mkazi wa nyumba ile kuwa mgonjwa. Vijiumbe maradhi hivyo ni moja ya vipengele vikubwa vya ufukara na afya mbaya ambavyo humfanya mtu kutokuwa na uwezo wa kufanya kazi na vilevile kumtwisha mzigo wa gharama za matibibu ya 204

12:45 PM

Page 204


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

uganga na kwa kawaida wakati mtu akiwa hana uwezo wa kufanya kazi na gharama zake vilevile kuongezeka huwa fukara. Imamu Ja’far Sadiq (a.s.) anasema: Njia ya wazi sana ambayo kwayo shetani hupata ubwana juu ya mtu ni kwamba hukaa kwenye chini ya kucha zake”. (Wasa’ilush Shi’ah, Jz. 1, uk. 433) Mtukufu Mtume (s.a.w.) anasema: “Katu usiruhusu nywele kwenye makwapa yako kukua, kwa sababu shetani hukaa humo na kuyafanya kama hifadhi yake. (Wasa’ilush Shi’ah, Jz. 1, uk. 436) Vijiumbe maradhi huzaana katika sehemu zenye unyevunyevu na giza chini ya joto linalofaa. Ili kuamua aina ya vijiumbe maradhi au kutafuta mbinu za kampeni dhidi yao huwekwa katika maabara katika vyombo maalumu ambamo chakula wanachokipenda vilevile huwekwa humo. Kisha vyombo vile huwekwa kwenye sehemu za unyevunyevu na zenye giza ambazo ni zenye kufaa kwa vijiumbe maradhi na hatimaye vinakuwa vikubwa kwa muda mfupi na kuzaana kwa wingi sana. Mbinu hii ni mpya na bado hata karne moja haijapita. Hata hivyo, Viongozi wa Uislamu walilifanya suala hili kuwa wazi karne kumi na nne zilizopita. Madoa chini ya kucha ni sehemu nzuri kwa ajili ya kukua kwa vijiumbe maradhi kwa sababu kwa ajili ya mikono kushika chakula na vitu vingine, kiwango cha kutosha cha chakula huja kupatikana kwao, na unyevunyevu wa mikono na joto aslia la mwili husaidia kukua kwao na kuzaana ambako humuweka mtu katika hatari. Makwapa vilevile hutoa hali muhimu kwa ajili ya kukua na kuzaana kwa vijiumbe maradhi kama nywele zinazoota humo zikiwa ndefu na kwa vile mwanga wa jua haupigi humo pia, na uoshaji wake hufanyika baada ya 205

12:45 PM

Page 205


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

vipindi virefu, hatari inaongezeka. Hadithi nyingine ya Imamu Ali (a.s.) imetufikia ambayo kwayo suala hili limedokezwa kwa wazi. Anasema: “Usiweke vitu vyenye kuteleza na vyombo vya kuchukulia nyama, hanjifu au aproni katika nyumba kwa sababu hivi ni makazi ya shetani. (Wasa’ilush Shi’ah) Katika giza na sehemu za ndani zenye unyevunyevu za mikunjo ya leso/hanjifu na mkoba mnene unaonata ambamo baadhi ya vyakula hunasa humo, vifaa vyote vya chakula, mabaki, unyevunyevu na giza hupatikana na sehemu kama hizo huchukuliwa kuwa zenye kufaa kwa ukuaji wa vijiumbe maradhi. Imamu Ja’far Sadiq (a.s.) anasema: “Mtu hapaswi kuzungumza na mtu mwenye maradhi ya ukoma, isipokuwa kama kuna umbali wa takriban mita moja na nusu kati yao.” (Tibb-i Kabir) Katika uganga wa kisasa, bakteriojisti (watalaamu wavijiumbe maradhi) wamethibitisha kwamba unaposafiri umbali wa mita moja na nusu kutoka kwa wagonjwa wa ukoma vijiumbe maradhi vya ukoma huwa dhaifu na vichache katika angahewa. (Tibb-i Kabir). Wakati ule Imamu Ja’far Sadiq (a.s.) alipokuwa anawakataza watu kuwakaribia wagonjwa wa ukoma hakuna aliyejua kwamba viumbe wadogo sana walikuwa ndio wakala wa maradhi haya na inawezekana kwamba vilevile unaweza kupatikana kwao kwa kugusana kimwili. Kabla ya ugunduzi wa darubini kulikuwa hakuna taarifa zilizopatikana kuhusu viumbehai hawa wadogo. Sababu za ugonjwa huu zilikuwa hazijagunduliwa na juhudi zilizokuwa zikifanywa kwa ajili ya matibabu ya maradhi haya zaidi zilikuwa za kimakosa.

206

12:45 PM

Page 206


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Baada ya kugunduliwa kwa darubini, uchunguzi wa vijiumbe maradhi ambavyo vilikuwa haviwezi kuonekana kwa macho matupu, ikaja kuwezekana na katika mwaka wa 1683 kuwepo kwa bakteria kulitangazwa. Baada ya miaka 200 baadae, yaani 1869 Louis Pasteur, mwanasayansi mkubwa wa Ufaransa alithibitisha kwamba viumbe wadogo sana ndio wanaosababisha maradhi hayo na alikuwa mtu wa kwanza kuanzisha vita dhidi ya bakteria hawa. Pasteur, ambaye alikuwa amejiandaa na vyombo bora zaidi na kuwa na kipaji cha ajabu kwa masuala ya kisayansi alianza kuchunguza vijiumbe maradhi na maradhi yanayosababishwa navyo. Kama tunataka kuhukumu kwa haki lazima tukiri kwamba viongozi wa Uislamu wametiwa msukumo na ufunuo wa ki-Mungu na katika wakati huo mtu wa kawaida asingeweza kuelewa masuala haya. Imamu Ali (a.s.) anasema: “Kama unakunywa maji kwenye chombo (ambacho kimevunjika) usinywe kutoka sehemu iliyovunjika na pia usinywe kutoka upande wa mkono wake kwa sababu shetani hukaa katika sehemu hizi mbili. (Mahasin) Katika hadith hii vilevile uchafu na uwezekano wa kukua kwa vijiumbe maradhi kwenye sehemu zilizovunjika za chombo na sehemu ambako mikono inaunganishwa na chombo imedokezewa. Mapendekezo ya kimsisitizo yamefanywa katika hadith za ‘Ahlul Bayt’ (a.s.), kuhusu utohara na usafi wa mikono hususan wakati wa kula chakula. Mikono ni kiungo pekee ambacho kina mawasiliano na sisi na halikadhalika na maadui zetu, kwa maana kwamba hugusana na macho yetu na midomo na vilevile hugusana na vitu vichafu vya nje. Wakati fulani huweka tonge la chakula au tunda katika mdomo wetu na wakati mwingine 207

12:45 PM

Page 207


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

hugusana na usukani wa gari, meza, viti nk. Hali hii ya pekee ya mikono, huongeza uwezekano wa mikono hiyo kuchafuliwa na vilevile huongeza katika uwiano kama huohuo uwezekano wa kutuambukiza sisi. Imamu Ja’far Sdiq (a.s.) anasema; “Mtu ambaye huosha mikono yake kabla na baada ya kula ataishi maisha ya wepesi na atakuwa salama kutokana na maradhi.” (Wasa’ilush Shi’ah, Jz. XVI) Nukta nyingine ambayo inaonekana katika niaba hii ni kwamba wakati viongozi wa Uislamu waliosha mikono yao ili kula chakula chao hawakugusa kitu chochote baada ya hapo kwa mikono yao na hata hawakuikausha kwa taulo au leso, kwa sababu vilevile kuna kuwepo na uwezekano wa taulo kuchafuliwa. Mazarim anasema: “Aliona hivyo pale wakati Imamu Musa Kadhim (a.s.) alipoosha mikono yake kabla ya kula, hakuikausha na taulo, bali alitumia taulo baada ya kula na kuosha mikono yake.” (Wasa’ilush Shi’ah Jz. XVI, uk. 577). Wakati fulani Imamu Ja’far Sadiq (a.s.) alitokea kuhudhuria katika karamu. Wakati wa kula chakula aliosha mikono yake na mtumishi akamletea taulo. Hata hivyo, mtukufu Imamu hakulipokea taulo, na akasema: “Nimeosha mikono yangu kwa ajili haswa ya vitu hivi.” (Wasa’ilush Shi’ah Jz. XVI, uk. 572) yaani, uoshaji umefanyika kwa sababu mikono imegusa vitu vya nje, hivyo ni muhimu kwamba baada ya kuosha isiguswe tena na kitu chochote, hata taulo pia. Suala lingine ambalo huhitaji uzingatiaji ni usafi wa kinywa na meno. “Vijiumbe maradhi visivyo na idadi hupatikana katika kinywa, idadi ambayo kwayo hufikiriwa kuwa inazidi wingi wa watu katika jiji. 208

12:45 PM

Page 208


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Vijiumbe maradhi hivi huchukuwa fursa ya kuwepo kwa vidonda, takataka za mdomoni au hali ya udhaifu wa mwili kwa ujumla hufanya madhara makubwa kwenye kinywa na meno na kusababisha maradhi mbali mbali. Baadhi husababisha kuoza meno na vingine huleta kimenomeno (ufizi kutoa usaha ) pamoja na matokeo yake ya hatari. Bado vingine huzaliana kwenye fizi zilizovimba na kutoa damu na utando wa kinywani. Vijiumbe maradhi hivi huingia mdomoni kwa njia ya hewa na chakula au kutokana na ujirani wa mikono na vitu vingine na kupata hali nzuri kwa ajili ya kukua kwao na kuzaliana. Katika watu wenye afya, ulinganifu wa lazima kwa uzima huwepo na kinywa hujikinga chenyewe dhidi ya kushambuliwa na vijiumbe maradhi, vinginevyo ulinganifu huo wa uzima unavurugwa na maradhi hutokea.” (Marzha-i Danish, Dr. Mahmud Siyasi). Katika mafundisho ya Kiislamu, maelekezo yametolewa ambayo kwayo hatari hizi zinaweza kuondolewa vya kutosha na kuridhisha kabisa. Viongozi wa Uislamu wamependekeza kwamba baada ya kula chakula chembe chembe za chakula lazima ziondolewe katikati ya meno kwa kutumia kijiti cha meno. Mtukufu Mtume (s.a.w.) anasema: “Tumia kijiti cha meno baada ya kula chakula kwa sababu kitendo hiki huuweka mdomo katika hali ya afya na kuzuia meno kutokana na kuoza na kuharibika.” (Mustadrak, Jz. 3, uk. 100) Chembe chembe za chakula ambazo hutoka katikati ya meno kwa njia ya vijiti vya meno zisiliwe bali lazima zitupwe kwa uangalifu sana. Imamu Ja’far (a.s.) anasema: “Kamwe usile chembe chembe zinazotoka katikati ya meno kwa njia ya vijiti vya meno kwa sababu ni chanzo cha vidonda vya ndani.” (Furu’-i Kafi) Mtukufu Mtume (s.a.w.) anasema: “Yeyote yule ambaye anatumia kijiti 209

12:45 PM

Page 209


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

cha meno baada ya kula chakula asile kile kinachotoka nje kwa njia ya kijiti cha meno.” (Mustadrak, Jz. 3, uk. 277). Nafasi katikati ya meno husafishwa kwa njia ya kijiti cha meno na meno lazima yaoshwe kwa uangalifu na kutakaswa kwa njia ya mswaki. Imamu Ja’far Sadiq (a.s.) anasema: “kupiga mswaki ni moja ya tabia za Mtume (s.a.w.).” (Wasa’ilush Shi’a, Jz. 1, uk. 346) Mtukufu Mtume (s.a.w.) anasema: “Kama sikuhofia kwamba wafuasi wangu wangeweza kupatwa na shida na usumbufu, ningefanya kuwa wajibu kwao kupiga mswaki kabla ya kusali Sala za kila siku.” (Ilalush Shara’i, Jz. 1, uk.277). Amma kuhusu jinsi ya kutumia mswaki, Mtukufu Mtume (s.a.w.) ametoa maelekezo kama hayo hayo ambayo huchukuliwa kuwa njia nzuri za kupiga mswaki na madaktari wa meno wa nyakati hizi. Anasema: “Usipige mswaki kwa mpango wa msitari wa meno, bali piga kuanzia juu kwenda chini” (Mustadrak, Jz. 1, uk. 54) yaani nafasi katikati ya meno lazima zisafishwe na kisibaki kitu chochote katikati ya meno. Moja ya maelekezo ambayo yana athari kubwa katika suala la usafi ni kuhusu kusafisha pua na kinywa. Wakati vijiumbe maradhi vilipogunduliwa na kuwepo kwao kukatangazwa, watu walijitahidi kwa nguvu zote kuviona na wakaenda kwenye maabara. Kwa upande mmoja waliviona viumbe hivi hatari kwa msaada wa darubini na kwa upande mwingine waliona kwamba vijiumbe maradhi hivi vilikufa kwa joto na viliangamizwa kwa kuchemsha. Watu hawa wamepata maisha ya milele au angalau kubakia salama kutokana na madhara ya vijiumbe maradhi hivi. Waliweka chakula chao, nguo zao, mavazi ya kichwa na hata matandiko yao kwa kutumia dawa za kuulia wadudu. Baadaye walitambua kwamba vumbi huleta idadi kubwa ya vijiumbe maradhi kwa kugusana miili yao na vilevile ilikuwa vigumu 210

12:45 PM

Page 210


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

kutakasa hewa yao (kwa kutumia dawa). Na kwa upande mwingine kwa kuchemsha chakula ambacho matokeo yake ni kupotea kwa virutubisho muhimu kwa ajili ya uhai, idara ya takwimu ya vifo mara moja ilionesha idadi kubwa na kutangaza kwamba vifo vimeongezeka kwa sababu ya ukosefu wa vitamini. Ngoja tusitoke nje ya mada. Tunachomaanisha ni kwamba kuna vijiumbe maradhi vingi sana katika hewa na kwa vile mtu huvuta pumzi takriban mara kumi na sita kwa dakika moja baadhi ya hewa yenye vijiumbe maradhi hupita kwenye pua yake. Kwa hiyo, katika pua ya mtu, bali katika zile pua za kila mnyama anayevuta pumzi, idadi ya vijiumbe maradhi hupatikana humo. Imamu Ali Ridha (a.s.) alitaja suala hili karne kumi na tatu zilizopita katika maneno yafuatayo: “Shetani hupatikana katika pua ya kila mnyama ambaye hupumua.” (Biharul Anwar; Awwalin Danishghah, Jz. 1, uk. 55) Mtukufu Mtume (s.a.w.) anasema: “Kila mtu lazima afanye mazmaza ( kusukutua kwa maji safi) na istishaq (kuvuta maji puani) kwa sababu kitendo hiki hutakasa mdomo na kuondoa harufu mbaya (shetani). (Sawabul A’mal, uk. 11) Imamu Ali (a.s.) anasema: “Mazmaza na istishaq ni ibada ya kuvutia ya kidini ambayo hutakasa mdomo na pua.” (Khisal, Saduq, Jz. 2, uk. 156) Kile kilichoelezewa mpaka sasa kina maelezo mafupi sana ya mafundisho ya Uislamu kuhusu usafi na mafunzo zaidi ya kinaganaga ya suala hili huhitaji vitabu vikubwa vyenye juzuu nyingi. Kama tunavyojua sura ya kwanza ya vitabu vya fiqh (sheria) ambayo ina maelezo marefu zaidi ni kuhusu taharat (utakaso). Katika sura hii maelezo ya suala la usafi yamejadiliwa kwa uchache sana.

211

12:45 PM

Page 211


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Nukta ambayo ambayo ni lazima idokezwe mwishoni ni, kama ilivyo kwa masuala yote mengine, Uislamu umeweka uzingatiaji wake kwenye usafi wa mwili na halikadhalika usafi wa roho na huwalingania watu kudumisha usafi wa mwili sambamba na uchaji wa roho kwa pamoja. Qur’ani Tukufu inasema:

“Allah huwapenda wale ambao hutubia na wale ambao hujitoharisha.” (Surah al-Baqarah, 2:222) Kama tukienda ndani kwenye mafundisho ya Uislamu tunaona kwamba vitu vichafu vimegawanywa kwenye aina mbili na utakaso wao vilevile hufanyika katika njia mbili: Ya kwanza, kuna vitu fulani vichafu ambavyo vinaweza kuondolewa kwa maji, moto, mwanga wa jua na ‘istihaala’ (ugeuzaji wa muundo wake wa asili). Ya pili, uchafu wa kiroho ambao waweza kutoharishwa na kusafishwa kwa njia nyingine. Kwa mfano, mtu anayemsingizia Mwislamu na kuhatarisha cheo chake na heshima yake lazima aombe msamaha. Mtu ambaye huvuka mipaka ya mali za wengine na kuvunja haki yake au kuwa mmiliki wa mali za wengine kwa njia ya kamari lazima arudishe mali hiyo kwa wenyewe halisi. Na mtu ambaye humdanganya na kumpotosha mtu mwingine lazima amuelekeze kwenye njia iliyonyooka. Kila mtu wa aina hiyo lazima atubie kwa ajili ya matendo yake hayo na afanye uamuzi imara kwamba hatarudia matendo hayo katika siku zijazo. Katika aya tukufu: “Hakika Allah huwapenda wale ambao hutubia Kwake, na huwapenda wale ambao ni wachaji,” Qur’ani Tukufu imefanya rejea kwenye nukta hizi mbili ambazo ni usafi wa nje na wa kiroho na tunajifundisha katika aya hii kwamba wale ambao hufanya juhudi kuweka miili yao na nafsi zao katika hali ya usafi na kutekeleza wajibati 212

12:45 PM

Page 212


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

zao kwa usahihi ni marafiki wa Allah na vilevile Allah huwapenda. Mwisho tunaomba kwa Allah swt. kutupa sisi wote nguvu muhimu ili kutenda kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu ili kwamba tuweze kupata utohara na usafi halisi na kuwa wenye furaha katika ulimwengu huu na halikadhalika katika Akhera. Nukuu: 1. Usafi ni ishara ya imani, na waumini wataingia Peponi. (Mtukufu Mtume). 2. Usafi ni nusu ya Dini. (Imam Ali (a.s.) 3. Hakika, usafi ni karibu na uchamungu. Dress - Khutba juu ya mavazi).

(John Wesley, Sermom on

* * * * * KANUNI YA MAELEKEZO Ili kupata furaha ya kweli na ukamilifu wa mwanadamu ni muhimu kupata walimu wenye uzoefu na kutekeleza uangalifu mkubwa na tahadhari ili kwamba vipaji vya watu binafsi viweze kuendelea na mielekeo yao isiyo sahihi na yenye madhara iweze kukomeshwa. Bila elimu na mafunzo mtu hawezi kupata ukamilifu unaofaa kwa wanadamu na viwango sahihi vya mtu haviwezi kuchipua na kutoa matunda. Kama alivyo tofauti na wanyama wengine wote, ambao huendesha maisha yao kwa kutegemea msaada wa silka za kurithi na bila mwalimu au mwelimishaji, mtu huhitaji mwongozo, elimu na mafunzo. 213

12:45 PM

Page 213


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Asili ya maendeleo ya vipaji haiwezikani tu kwa kuzungumza, kusikia na kusoma, kwa sababu kuna watu wengi ambao hutambua wema lakini wao wenyewe sio wema na ambao huelewa ubaya lakini wao wenyewe bado ni wabaya. Mtunza bustani huangalia maua na miti kila mara. Hupanga na kuipa maumbo mazuri kwa njia zote alizonazo. Huondoa vichaka na matawi yaliyozidi. Wakati fulani hujengea vibanda vya kivuli kwa ajili ya miti michanga na kuvitumia vyombo vyote vilivyokuwepo kwa ajili ya maendeleo na ukuaji wao. Waelimishaji wenye uwezo lazima wachukue hatua za kiutendaji kuelemisha watu binafsi. Lazima wawaangalie katika kila hatua na kuwaongoza kwenye njia ya ufanisi na wema, kwa sababu kufundisha tu na kuelezea na kusifia vitendo vizuri hakutoshi kujenga watu binafsi bali mafunzo na vitendo vilevile ni muhimu. Wote tunajua kwamba ili kuendesha baiskeli ni muhimu kushikilia mikono yake kwa mikono miwili na kukaa juu ya kiti na kuzungusha mapedeli kwa miguu. Na ili kuelekea kulia au kushoto mikono lazima igeuzwe upande huo. Hata hivyo, kuujua tu utaratibu huu hakumuwezeshi mtu kuendesha baisikeli. Kwa upande mwingine vitendo vya kutosha ni muhimu kwa ajili ya kuweza kutumia gari hili rahisi linganishi la thamani ndogo. Katika mambo ya maisha vilevile mwongozo wa waelimishaji na halikadhalika vitendo vya kutosha ni muhimu ili kwamba watu binafsi waweze kufanya kazi zao kwa kujitengemea katika mazingira yote. Matatizo makubwa katika mfumo wetu wa elimu ni kwamba wazazi, walimu, wahubiri, wakufunzi nk. huweka elimu kwetu na huifanya ipatikane kwetu na kutueleza kuhusu majukumu yetu, lakini hakuna hata mwongozaji mmoja ambaye angetueleza wakati wa kitendo kwamba hivi na hivi ni wakati sahihi wa utekelezaji wa ujuzi ambao ametufahamisha kabla. 214

12:45 PM

Page 214


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Mbinu ambayo marehemu Ayatullah Haj Sheikh Ja’far Kashiful Ghita aliitumia kwa ajili ya maelekezo ya watu binafsi ilikuwa elekevu na yenye kufaa. Kwa mfano, alitaka mtoto wake aamke mapema na kusali sala za usiku katika hali ambayo angeendelea kuzisali kwa shauku ya moyo mkunjufu mpaka mwisho wa uhai wake. Siku moja alikwenda pembeni mwa kitanda cha mwanawe kabla ya adhana ya Sala ya Fajir, alimuamsha na akamuambia: Amka ili twende tukafanye ziara (ziarat) kwenye kaburi la Imam Ali (a.s.) (a.s.) Amir wa waumini.” Yule kijana alifikicha macho yake yenye usingizi na akasema: “Vizuri. Unaweza ukatangulia, na mimi nitakuja.” Hata hivyo baba yake akesema: “Hapana. Nitakusubiri hapa ili twende pamoja”. Kijana yule aliamka, akachukua wudhu na akaenda kwenye kaburi la Imamu pamoja na baba yake. Mbele ya viwanja vya kuba walimuona ombaomba amekaa huku amenyoosha mikono yake kwa watu. Baba akamuuliza mwanawe: “Kwa nini huyu mtu amekaa hapa?” Mtoto akajibu: “Ili kuomba na kutafuta msaada kutoka kwa watu.” Baba akauliza: “Unaweza kufikiria ni kiasi gani cha pesa anachoweza kupata kwa njia hii?” Mtoto akajibu: “Anaweza kupata kiasi kidogo cha dirham.” Baba akauliza: “Je, ni hakika kwamba anapata pesa hizi?” Mtoto akajibu: “Hakuna kinachoweza kusemwa kwa uhakika. Inawezekana kwamba akapata pesa kiasi na inawezekana kwamba asipate kitu.” Wakati baba alipoona kwamba uwanja umeshatayarishwa kwa kile ambacho alitaka kukisema, alisema: “Mwanagu! Unaweza kuona kwamba ombaomba huyu amekuja hapa wakati huu wa usiku na amenyoosha 215

12:45 PM

Page 215


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

mikono yake ili yamkini apate pato la kidunia ambalo hana hakika nalo. Kama kweli unaamini malipo ya kiroho yaliyowekwa na Allah kwa ajili ya mwenye kuamka usiku na kusali Sala za usiku na kuwa na imani na yale waliyosema Maimamu watukufu, kwa nini uwe unafanya uvivu kuhusiana na jambo hili?” Matokeo yalikuwa ni kwamba mtoto yule hakuacha kuamka mapema usiku, na kusali sala za usiku mpaka mwisho wa uhai wake. Matokeo haya yalikuwa ni kwa sababu ya ukweli kwamba mwelimishaji mwenye uwezo na baba mwanachuoni alijenga kwenye akili ya mtoto wake hisia isiyo na kikomo na ikawa kama kichangamsho katika kufanya kwake kitendo hicho kizuri. Wakufunzi lazima wajitahidi kuwafanya watu binafsi kurudia rudia matendo mazuri ili waweze kuendeleza tabia zao na hatimaye waweze kuyafanya bila kikwazo chochote. Imamu Ali (a.s.) anasema: “Tabia ni maumbile ya pili.” (Ghurarul Hikam) Wajibu wa tabia katika vipengele tofauti vya maisha haviwezi kupuuzwa, kwa sababu watu binafsi wanaweza kufanya kazi ngumu na za kuchosha kwa urahisi kwa ajili ya wao kupata kuziendeleza tabia hizo kwa mazoezi ya mara kwa mara. Kama waelimishaji na wafundishaji wa maadili wa jamii, kwa njia ya maelekezo sahihi na uangalifu, wataingiza kwa watu ile tabia ya kufanya matendo mema, kwa kawaida watu wataelekea kwenye kufanya mema na nemsi. Ni dhahiri kwamba waelimishaji watafanikiwa tu katika kutoa maelekezo sahihi kwa watu iwapo wao wenyewe watafanya kwa mujibu wa kile wanachosema na tabia zao kwa hakika ni mfano kwa wengine, kwa sababu kama wanawalingania watu kwenye maadili ya ubinadamu na matendo 216

12:45 PM

Page 216


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

mema kwa njia ya khutba tu na kuandika, matendo yao hayataafikiana nayo na matokeo yatakuwa kabisa kinyume na ilivyo kusudiwa. Qur’an Tukufu inasema: “Ni kosa kubwa mbele ya Allah kusema msiyoyatanda.” (Qur’ani 61:3) Imamu Ali (a.s.) amekosoa kwa nguvu sana tabia ya wafundishaji kama hawa wa maadili na amewalaumu. Kisha akasema: Laana ya Allah iwe juu ya watu wale ambao hulingania watu kwenye mema na vitendo vizuri lakini wao wenyewe hawavifanyi. Na laana ya Allah iwe juu ya watu wale ambao huwaonya wengine dhidi ya vitendo viovu lakini wao wenyewe huvifanya vitendo hivyo. (Nahjul Balagha). Kitu ambacho kinafaa sana kwa ajili ya uelimishaji wa watu ni kufuata kwao mifano kwa maana kwamba wakati vijana au watu wa tabaka jingine wakiangalia kwa macho yao wenyewe tabia njema za wafundshaji wao wa maadili na wakufunzi, bila ya hiari watakuwa ni wenye kuelekea kwenye mambo mazuri na kufuata tabia adhimu, mfano ambao kwamba wameuona wao wenyewe. Kwa hiyo, viongozi wa Uislamu wamependekeza kwamba Waislamu lazima kwa vitendo wawalinganie wengine kwenye uchaji na wema. Imamu Ja’far Sadiq (a.s.) anasema: “Hubiri na waongoze watu kwa vitendo na tabia yako na sio kwa khutba tu.” Ushauri ambao hupata njia kwenye moyo wa mwanadamu kupitia sikioni kwa hakika ni wenye nguvu sana, lakini nguvu yake ina kikomo na ya muda. Kwa hiyo kama kuhubiri na ushauri hakuambatani na mfano ambao kwamba watu wanaweza kuuona ushauri na mahubiri yanayofanywa kwa vitendo wanaweza kuufuata; kuhubiri tu hakutoshi. Mifano kama hiyo 217

12:45 PM

Page 217


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

huziweka nyoyo na nafsi za watu kusonga mbele na kuamsha akili zilizolala ambayo inaweza kuonwa na kuhisiwa na wao kwa macho yao wenyewe kabisa. Mifano yenye nguvu na yenye kufaa kama hiyo ina athari kubwa juu ya moyo wa mtu na huhesabiwa kuwa moja ya vichangamsho vikubwa vya maelekezo. kama ilivyoelezwa kwa dhahiri katika Qur’ani Tukufu, jukumu la kwanza na kubwa mno la Mtume mashuhuri wa Uislamu ilikuwa ni kufanya mageuzi na kuwafundisha watu wa ulimwengu. Qur’ani Tukufu inasema:

“Bila shaka Allah amewaneemesha waumini aliowapelekea Mtume miongoni mwao, akiwasomea aya Zake na akiwatakasa na akiwafunza Kitabu na hekima na ingawa zamani walikuwa katika upotofu ulio wazi. (3:164) Katika aya hii na nyingine kama hii Allah swt ameyapa mazoezi kipaumbele zaidi kuliko elimu na huonesha kwamba hatua ya kwanza kuelekea kwenye ufanisi ni ustarabishaji na ufundishaji wa watu binafsi kabla ya ueleweshaji na mafunzo. Ujuzi na hekima bila maelekezo ya kidini na uimarishaji wa vituo vya kiroho ni kitu cha hatari kama ambavyo uzoefu umethibitisha mtazamo huu. Siku hizi ule unaoitwa ulimwengu uliuostaarabika umesheheni zana na silaha za kisayansi na viwanda lakini hauna mafunzo ya kiroho. Kwa hiyo, matokeo yake ni migogoro, vita, makombora, uharibifu, majinai na maelfu ya misiba mingineyo. 218

12:45 PM

Page 218


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Kama wale watu ambao wana vyombo vya kisayansi na vya viwanda wangelikuwa na hisia na nguvu za imani na kiroho, wangefikiria ustawi wa mwanadamu badala ya uharibifu na misiba na wangeliweka gharama zote hizi kubwa mno katika kuwalisha wenye njaa na upigaji vita umasikini na shida za nchi zinazoendelea Ni hapa kwamba walimu wenye uwezo na wafundishaji maadili kabla ya kufanya chochote lazima waelekeze juhudi zao kwenye mazoezi ya watu binafsi na kuwasheheni nguvu ya imani na kiroho kabla ya kuwapa faida za kisayansi na viwanda. Kwa ajili ya jukumu hili zito la kiungu, Mtukufu Mtume alifuata njia sahihi na pana ya mambo mengi ya mazoezi kwa watu binafsi na akachunguza kila uwezekano katika suala hili. Aliwapa watu masomo ya kimaelekezo kwa njia ya tabia na mwenendo wake mwenyewe. Aliweka upole katika matendo, alizoea kuwasalimu watu wote na kupeana mikono na watu kwa uchangamfu. Alipokea watu kwa bashasha na uso wa tabasamu, alisikiliza maneno yao kwa usikivu mno, alitoa heshima kwa wageni wapya, alisimama mbele yao na kuwafanya wakae kwenye nafasi yake mwenyewe. Alizoea kushirikiana na wanyonge na watu mafukara na kushiriki huzuni za watu. Aliwahurumia watu katika shida zao na aliwapendelea wengine kuliko yeye mwenyewe. Imamu Ali (a.s.) ambaye alilelewa chini ya ulinzi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.) na ambaye yeye mwenyewe ni mfundishaji wa maadili wa ulimwengu wa ubinadamu, anasema: “Kamwe sijamlingania mtu kufanya tendo jema mpaka mimi mwenyewe kwanza nimelifanya�. Kama ukiongea kuhusu uadilifu, yeye mwenyewe kwanza kabisa alikuwa mtu mwadilifu na alifundisha somo la uadilifu kwa watu kwa mwenendo wake mwenyewe wa uadilifu. Aliwazuia kwa nguvu sana wakandamizaji na akatoa hifadhi kwa watu wenye shida kama baba mwenye huruma na mapenzi. 219

12:45 PM

Page 219


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Alidumisha usawa miongoni mwa Waislamu katika maana yake kamili na aliwafanya wanyonge wafaidi haki zao na aliwazuia waovu kwa nguvu zake zote. Aliwazuia watu kujiingiza katika anasa za kidunia na yeye mwenyewe vilevile alikuwa ni mfano wa uchamungu na kiroho. aliwahimiza watu kufanya kazi kwa bidii na yeye mwenyewe alifanya juhudi kubwa kujishughulisha katika kazi zenye manufaa. Alisamehe makosa ya mwenendo mbaya wa watu, na wafuasi wake walijifundisha masomo haya ya kimatendo kutoka kwa viongozi wao wakubwa na wafundishaji wa maadili na kutenda kwa mujibu huo. Malik Ashtar ambaye alikuwa mtu mwenye umbile lenye nguvu alipata maelekezo kutoka kwa Imamu Ali (a.s.). Siku moja alipokuwa anapita katika soko la mjini Kufa mchuuzi mwenye tabia mbaya ambaye hakumtambua Malik na alikuwa hajui nguvu zake na hadhi yake alimtupia takataka kwa njia ya mchezo na dhihaka. Jirani yake akamuuliza: “Unamjua huyu mtu ambaye umemtupia takataka?” Yule mtu akajibu: “Hapana. Alikuwa ni mtu fukara.” Yule jirani yake akamuambia: “Ole wako! Yeye ni Malik Ashtar kamanda wa majeshi ya Uislamu.” Yule mtu alianza kutetemeka aliposikia jina la Malik. Alichnganyikiwa mno akaanza sehemu zote kumfuata Malik ili kufanya marekebisho kwa ajili ya kitendo chake. Baada ya kuuliza uliza na kutafuta alimkuta katika Msikiti wa mjini Kufa. Alijutupa miguuni mwa Malik na kuomba radhi akisema: “Sikukutambua. Tafadhali nisamehe kwa kosa nililolifanya.” Malik alimuonesha huruma na akasema naye kwa ukarimu mkubwa: “Nimekusamehe na nimekuja msikitini hapa kusali Sala zangu na kukuombea msamaha wa Allah kwa ajili yako.”

220

12:45 PM

Page 220


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Kitendo hiki cha Malik kilikuwa ni mafunzo ya kimatendo na somo lisilosahaulika ambalo amelitoa kwa mtu yule na kumtahadharisha kabisa dhidi ya kuteleza kama huko tena. Mifano mingi ya masomo ya kimatendo kama haya inapatikana miongoni mwa wale waliojifunza katika shule ya Kiislamu na moja ya huduma tukufu sana iliyotolewa na mfundishaji mkubwa wa maadili na mwanamageuzi mkubwa na mwisho wa mitume, Muhammad (s.a.w.) kwa wakazi wa ulimwengu, ilikuwa ni kufungua shule tukufu kama hiyo na uwasilishaji wa mafundisho hayo. Kwa njia yake hii ya mwenendo mtukufu na mwongozo Mtukufu Mtume aliangamiza na kukomesha sifa mbaya katika watu ambao wamepata mafundisho kutoka kwake na akajenga kwao sifa nzuri na tabia za kibinadamu. Aliangamiza kiburi chao, ubinafsi, chuki, hasira, tabia mbaya, unyonge na udhalili na kuzibadilisha (tabia hizi) kwa upole, hisani, upendo, tabia njema, uchaji, kujiheshimu, uimara na ujasiri. Kabla ya ujio wa Uislamu watu wa Makka walishambuliwa na jeshi la waEthiopia (Wahabeshi) na licha ya ukweli kwamba jeshi la wa-Ethiopia halikustahiki kufikiriwa sana, watu wa Makka walikimbia na kuacha nyumba na meko zao. Hata hivyo, kwa mafundisho haya mapana Mtukufu Mtume wa Uislamu alitoa maisha mapya kwenye taifa hilo ambalo lilifanya wafalme wakubwa wa wakati huo kutetemeka. Kwa hiyo, Qur’ani Tukufu imetangaza mafundisho ya Uislamu kuwa chanzo cha maisha na uzima na imeshauri watu wa ulimwengu kuwa makini kwenye mafundisho haya na kutenda kwa mujibu wake kwa uangalifu sana ili kupata faida halisi ya maisha. Inasema: “Enyi mlioamini mwitikieni Allah na Mtume anapokuiteni kwa yale yatakayokupeni uzima...” (Surah al-Anfal; 8:24) 221

12:45 PM

Page 221


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Vilevile lazima ikumbukwe kwamba hakuna maelekezo yaliyo ya kina na ya kuaminika kama maelekezo ya kidini. Dr. Mahd, Ki Niya anasema: “Filosofa wa Kigiriki kwa usahihi amesema: ‘Hakuna sanaa iliyo ya Tukufu zaidi kuliko kutoa maelekezo’. Ni kwa sababu chini ya njia sahihi za maelekezo mtu anaweza kuendelea kwenye cheo cha juu zaidi cha maadili ya kibinadamu na anaweza kuwa huru kutokana na ufungwa wa ujinga, ufukura na utumwa”. (‘Ulum-i Jina’i) Georges Jacques Danton, msemaji fasaha na mtu mashuhuri wa Mapinduzi ya Ufaransa hakusema kimakosa: “Baada ya chakula na elimu, mazoezi ndio haja ya kwanza ya taifa. Jamii haiwezi kupata uzima bila mazoezi na mwongozo sahihi.” Hakuna maelekezo yatakayoiweka jamii katika usalama zaidi kutokana na misiba ya matendo maovu kama mafundisho ya dini. Mwanga wa dini, yaani imani ya kweli ambayo hukaa juu ya misingi ya busara na mazingatio kuelekea kwa Mungu huliongoza taifa kwenye njia iliyonyooka. Imani ya kweli ni tiba kwa ajili ya maradhi yote. Kama unataka kuuweka umma katika kinga kutokana na majanga ya maadili tepetepe lazima uanzishe imani imara katika mioyo yao. Imani huangaza moyo wa mtu pamoja na mwanga wa matumaini, na kiini cha msingi wa maisha ni matumaini. Mtu anaweza kushinda matatizo ya maisha chini ya mwanga wa imani na mwongozo wa akili na uamuzi imara. Henri Bergson, mwanafalsafa na mwandishi Mfaransa alisema: “Ufanisi wa mwanadamu uko chini ya yeye kurudi kwa Mungu”. Mtu ambaye nadhari yake siku zote imeelekezwa kwa Muumba wake hahitaji mvinyo kuvumilia shida. Na mtu ambaye siku zote ameleweshwa kwa 222

12:45 PM

Page 222


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

furaha ya imani hajikuti katika haja ya mvinyo bandia na furaha ya muda mfupi ya mvinyo. Kwa hiyo, hakuna sababu ya yeye kwenda kwenye klabu ya pombe na kupoteza hekima yake. Dale Carnegie, mwandishi wa wakati huu, ambaye maandiko yake kwa kiasi kikubwa yamewavutia watu, anasema: “Kama maelfu ya watu ambao wanakabiliana na misukosuko ya kiroho na ambao wanapiga kelele katika hospitali za vichaa wangenyoosha mikono yao kwa Muumba Mwenye nguvu zote kwa ajili ya msaada badala ya kupigana wenyewe vita vya maisha, ingewezekana kabisa wao kupata ukombozi�. Lau kama maelekezo kama hayo yangelipatikana mwanzoni kabisa na mwanga wa imani ungeangaza nyoyo zao, kusingekuwa na uwezekano wa mawazo ya kishirikina na mateso ya kiroho yasingejitokeza na kukita mizizi. Mtu hatakiwi kujitenga kutokana na tiba ya kiroho na wakati wowote mtu anapohitaji kushinda upungufu wa mwamko wake wa kiroho, lazima akimbilie kwenye ukumbusho wa Allah Mwenye nguvu zote, Mola Mlezi na Muumba. Hivyo, angazeni nuru ya imani ndani nyoyo zenu kwani ni imani ambayo huondoa maovu yote ya kijamii na maadili mabaya. Uislamu ulisimama ili kuvunja minyororo ya imani zisizo na msingi, ushirikina, dhulma, ujinga, ufukara na utumwa. Ulitangaza uhuru wa watu, ambao ulitegemea juu ya ufanisi, ukarimu, ujasiri, usafi wa maadili, uadilifu, upendo na mapenzi. Huu ulikuwa ni uhuru kwa maana kwamba mtu lazima awe huru kutokana na utawala wa ndani wa masanamu, matamanio maovu, ghadhabu, uchoyo na maovu yale yote ambayo humuweka mtu chini ya utumwa. Baadhi ya wasomi hufikiria kwamba maelekezo bila msaada wa dini yanaweza kumuokoa mtu kutokana na shida za kimaadili na kijamii na yanaweza kumhakikishia ustawi wa jamii, lakini uzoefu umeonesha 223

12:45 PM

Page 223


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

kinyume chake kabisa. Katika nchi za Magharibi zenye viwanda na zilizoendelea kanuni za maelekezo zinafundishwa kuanzia shule za chekechea mpaka kwenye kiwango cha chuo kikuu kupitia kwa walimu waliofundishwa na wazoefu, na licha ya hivi shida zao za pamoja na za binafsi na misiba huongezeka siku hadi siku na hali inakuwa kwamba hata serikali inashindwa kupata ufumbuzi. Mwaka wa 1962, John F. Kennedy alisema: “Hali ya baadae ya Amerika inatisha kwa sababu vijana wamezama mno katika maovu na hawawezi tena kutekeleza majukumu yao katika njia iliyo sahihi na kufanya kwa bidii majukumu yaliyoaminishwa kwao. Kwa mfano, katika watu saba ambao wanaandikishwa kwa ajili ya huduma ya jeshi sita huthibiti kuwa wasiojimudu na wasiofaa, na ni kwa sababu kupenda kwao mno anasa kumeondosha uwezo wao wa kimwili na kiroho.” Kama alivyosema Kennedy, Khrushchev vilevile katika mwaka wa 1962 alisema: “Hali ya baadae ya Urusi iko hatarini na vijana hawana kabisa matumaini ya baadae kwa sababu wamekuwa sio wawajibikaji na wametekwa na matamanio maovu.” Kwa mujibu wa taarifa ya polisi watu zaidi ya 10,000 wamejiuwa wenyewe nchini Ujerumani ya Magharibi katika mwaka wa 1967. Katika kipindi cha mwaka huo huo zaidi ya wanaume 6,000 na wanawake 7,000 nchini Ujerumani vilevile ambao walijaribu kujiua waliokolewa. Utumiaji wa narcotics (aina ya madawa ya kulevya) nchini Amerika umeenea miongoni mwa Waamerika katika hali ya kutisha. Hivi karibuni polisi wa New York waligundua miili ya watu 38 ambao umri wao ni kati ya miaka kumi na sita na thelathini na tano ambao wamekufa kwa matokeo ya utumiaji wa madawa kama hayo. Baadhi ya waathirika hawa wa laana hii hawakuwahi hata kuondoa mabomba ya sindano kutoka kwenye miili yao. 224

12:45 PM

Page 224


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Miongoni mwa wale ambao ni sugu kwa utumiaji wa narcotics, idadi ya wale ambao hutumia heroin ni kubwa mno. Katika wakati huu katika mji wa New York peke yake watu 100,000 ni sugu kwa utumiaji wa heroin kwa maana hii ni kwamba mtu mmoja kwa kila watu themanini hutumia morphine. Miongoni mwa tabaka la watu matajiri, wasanii (waingizaji wa kike na wa kiume, nk.) wanachukuwa nafasi ya kwanza. Mmoja wa waganga wa New York alisema: “Mmoja wa wasanii mashuhuri wa Marekani hujichoma sindano ya narcotic mwilini mwake mara kumi kila baada ya masaa ishirini na nne na bei ya kila sindano ni takriban dola sitini.” Akaongeza kusema: “Watu wengi mashuhuri ambao vifo vyao huchukuliwa rasmi kuwa vimetokea kwa ajili ya ugonjwa wa moyo, kwa hakika huwa wanakufa kwa ajili ya kutumia narcotics.” (Daily News Paper, Ittila ‘at, toleo no. 13015) Jamii yenye kupenda anasa bila kuwa na dhana ya Allah na dini imeyafanya maisha kuwa tasa na magumu kwa watu ambao wanamiliki vyombo vyote vya kimaisha na wamekuwa mashujaa wa ulimwengu kwa mtazamo wa utaalamu na viwanda. Maisha ya familia yamepoteza furaha na starehe yake na kiwango kinachozidi kuongezeka cha talaka kinavunja maisha ya familia. Hisia za ubinadamu zimetoweka hata miongoni mwa akina baba na watoto na uhalifu umeongezeka katika hali ya kutisha. Amani na utulivu wa akili ambao ndio kituo cha ufanisi wa mtu ni adimu sana katika ulimwengu wa kisasa, kwa sababu amani na utulivu huo unaweza kupatikana tu kwa njia ya imani na dini. Qur’ani Tukufu inasema: “...Hakika kwa kumkumbuka Allah, nyoyo hutulia.” (Surat ar-Ra‘d, 13:28).

225

12:45 PM

Page 225


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Maelekezo ya Kiislamu yametegemea juu ya kanuni ambazo kwamba nguvu za kila aina, na halikadhalika silika na hisia zote lazima zisafishwe na kupimwa na lazima zitumiwe sawasawa. Uislamu unadhibiti mielekeo ya tafakuri na silika za watu kwa njia tofauti ili kwamba isije ikashawishi akili za mwanadamu na yenyewe kuchukua mamlaka. Wakati huohuo huangalia kukubalika kwa ajili ya watu binafsi uwiano na mgao mzuri wa furaha ya silka zao. Uislamu haumuwekei mtu mpaka ndani ya kuta nne za vitu vya anasa na haumuangalii kwa mtazamo wa uchumi tu. Kwa upande mwingine umechukua na kuyaangalia mahitaji yake yote ya kimaumbile na umetegemeza mpango wa maelekezo yake juu ya kanuni za kiroho na kimaadili ambazo ni msingi kabisa wa maadili ya mwanadamu. Wakati huohuo haukupuuza masuala ya kidunia na uchumi na umewahimiza watu kufanya juhudi sahihi na kupata maendeleo ya maana. Hadithi imenukuliwa kutoka kwa Imamu Ali (a.s.) isemayo: “Wafundisheni watoto wenu njia na adabu nyingine kuliko zenu wenyewe, kwa sababu wameumbwa kwa ajili ya muda ambao ni tofauti na wenu.� Kama hadithi hiyo ipo; anachomaanisha Imamu hapa ni kwamba lazima uwalee watoto wako kwa elimu, hekima na adabu za zama zao ili kwamba waweze kuendelea mbele na zama yao. Baadhi ya watu wanaoitwa wasomi wamechukua fursa isiyofaa ya hadithi hii na kujifanya kusema kwamba Imamu Ali alimaanisha kwamba kama wakati ule utakuwa wa kucheza dansi, upunjufu na uovu, wewe pia lazima uwalee watoto wako kutokana na hali za wakati ule, ingawa kuhusisha maelezo kama hayo kwa mtukufu Imamu ni dhambi na ukafiri. Kwa maneno yake halikadhalika na vitendo vyake Mtukufu Mtume (s.a.w.) aliwahimiza na kuwashauri watu kufanya juhudi katika nyanja zote. Wakati huohuo alijitahidi kuwaeleza kwamba hawatakiwi kujiingiza 226

12:45 PM

Page 226


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

katika vitendo visivyo sahihi na vya uharibifu, isije ikawa mapenzi ya mali na cheo vikawashawishi au matamanio maovu na kupenda mno anasa vikapata mwanya katika maisha yao au lazima wajitoe mihanga kiroho na kimaadili kwa ajili ya mapato ya kidunia ya muda mfupi. Njia hii ya mazoezi ya kimatendo ilitekelezwa na viongozi wote wa Uislamu na kama ushahidi kwa historia athari zake za kuridhisha zilikuwa wazi kabisa katika jamii. Wakati Waislamu walipoona tabia za ubinadamu na za kimbinguni za viongozi wao kwa macho yao wenyewe walivutiwa na njia za mienendo yao bila kuwaza wala kufikiri. Wakati watu walipoona kwamba licha ya ukweli kwamba Imamu Ali alikuwa Khalifa na Mkuu wa Nchi na mamlaka yote yalikuwa yamewekwa kwake, hakuwa mkali au mkatili hata kwa muuwaji wake, na badala yake alitoa ushauri kwa watoto wake wamfanyie wema kimwili (yaani, wasimtese), kwa hakika walikuja kuelekea kwenye uadilifu na maadili ya ubinadamu, na hii ni njia tukufu sana ya maelekezo ambayo yanaweza tu kuonekana katika shule za mitume na wachaji watiifu kwa Allah. Katika mwaka wa sitini na tatu, mwaka wa Kiislamu, watu wa Madina waliasi dhidi ya Ukhalifa wa Yazid na tabia yake ya uonevu na wakaleta hali ya vurugu. Walimuondoa gavana wa Madina na wakawaweka jamaa wa Bani Umayya kwenye shinikizo kali. Marwan bin Hakam ambaye alikuwa mmoja wa viongozi wa Bani Umayya na ambaye ana kumbukumbu ndefu ya uadui mkubwa na familia ya Mtukufu Mtume alijikuta kwenye shinikizo kubwa la wanamapinduzi pamoja na wanafamilia wake. Hatari ilimzunguka kila upande. Alihofia mno na alikuwa akitafuta hifadhi ili kwamba aweze kuokoa maisha ya mke wake na watoto wake kutokana na wanamapinduzi hao. Alimfuata kila mtu aliyekuwa rafiki yake na kuwataka wampatie hifadhi kwa ajili ya familia na jamaa zake katika nyumba zao, lakini wote walimkatalia. Alikwenda kwa Abdallah bin Umar bin Khattab, 227

12:46 PM

Page 227


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

lakini na yeye pia hakuweza kumpatia hifadhi. Hatimaye alikwenda kwa Imam Zainul ‘Abidin, Imamu wa nne, na kwa kumbukumbu yake mbaya ya zamani na madhara aliyoyafanya kwa kizazi cha Mtukufu Mtume katika nyakati tofauti, hakuwa na matumaini ya majibu mazuri kutoka kwa mtukufu Imamu na ilikuwa ni ukataji tamaa mtupu tu uliomsukuma kwenda kwenye kizingiti cha Imamu. Hata hivyo, kinyume kabisa na matarajio yake, mtukufu Imamu alimpokea kwa uchangamfu na upendo mkubwa. Alitoa jibu linalofaa kwa ombi la Marwan na akawapeleka familia yake na yeye mwenyewe kwenye nyumba moja iliyoko Ta‘if, ambayo ilikuwa inamilikiwa na yeye (Imamu) na waliishi chini ya hifadhi ya Imamu mpaka mwisho wa mapinduzi ya Madina. (Kaamil ibn Athir). Hapana shaka masomo haya ya kimaelekezo yasio na mfano yalimvutia kila mwanadamu na kumtayarisha kufuata juu ya njia hiyohiyo. Viongozi wa Uislamu walitenda kwa uangalifu na kwa huruma katika masuala ya kimaelekezo ambayo yalivutia akili za watu katika vipengele vyote vya maisha na kuwavutia kuelekea kwenye sifa njema na nemsi. Hata katika maombi yao na Sala kwa Allah hawakuwa wazembeaji wa jukumu hili muhimu kwamba maombi yao lazima yawe ya kimaelekezo kwa ajili ya wanaosikiliza halikadhalika na kwa wasomaji (wa dua hizo). Katika moja ya (maombi) Du’a, Imamu Sajjad anasema: “Ewe Mola Wangu! Teremsha baraka zako kwenye nafsi ya Muhammad na kizazi chake teule na uwe swahiba wangu na unisaidie katika shida zangu. Nipe nguvu ili kwamba huu mzigo mzito usinilemee mabegani mwangu na usinizuie kutekeleza wajibu wangu. “Ewe Mola wangu! Wakati nitakaponyanyua kichwa changu kesho kutoka katika ardhi (yaani Siku ya Hukumu) nitakuwa mwenye kuwajibika kwa maneno na matendo yangu mbele ya mahakama Yako ya uadilifu. Ijaalie juu yangu mimi kwamba niweze kufikiri leo kuhusu kesho yangu na 228

12:46 PM

Page 228


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

niweze kutekeleza majukumu yangu katika namna inayopendwa na Wewe. “Jaalia kwamba maisha yangu yafikie mwisho katika utii Kwako na ibada Yako. Nifanye niwe huru kutokana na mali za wengine na nipe riziki ya kutosha. Niweke niwe salama kutokana na mabalaa na fanya hali yangu kuwa ya kuheshimiwa na utajiri ili kwamba nisije nikatamani mali za wengine. “Ewe Mola wangu! Jaalia kwamba mikono yangu iweze kufanya kazi kwa ajili ya uzuri na ustawi wa watu na halikadhalika weka mkono wangu wenye manufaa salama kutokana na kumkumbusha mtu msaada niliomfanyia na kutokana na kuwasumbua wengine na uweke ulimi wangu kuwa kimya kutokana na kujisifu na kujitukuza. “Ewe Mola wangu! Punguza cheo changu katika macho yangu mwenyewe kwa namna ile ile ambayo kwayo unakitukuza katika macho ya watu na nizoeshe na unyonge wangu uliojificha katika kipimo kile kile ambacho kwacho unaweka heshima juu yangu katika jamii ili kwamba nisisahau kabisa nafasi yangu nyenyekevu na nisije kuishi nje ya uwezo wangu (wa kipato). “Ewe Mola wangu! Rekebisha, kwa upole wako usio na kikomo, kila tabia mbaya ambayo unaiona kwangu ili kwamba iwe nzuri na ondosha kutoka kwangu kila kasoro ambayo hunihusisha na vitu viovu na niondolee kila upungufu ambao huzuia nafsi yangu kufikia ukamilifu. “Ewe Mola wangu! Jaalia kwamba niweze kuwapenda watu wote na niwe mwadilifu na mkarimu kwa wote. “Ewe Mola Wangu! Weka neema hizi kwangu na halikadhalika kwa Waislamu na waumini wote, wanaume na wanawake; waweke watoto wa watu chini ya hifadhi yako, huruma ya Ukarimu Wako na waneemeshe kama watoto wangu na wafanye kuwa wenye furaha na ufanisi katika ulimwengu huu na halikadhalika katika Akhera. 229

12:46 PM

Page 229


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

“Ewe Mola Wangu! Hivyo, itakabalie kwamba badala ya kujiingiza katika lugha chafu na za matusi na kutafuta makosa na kuridhia uwongo na kusema kitu kinyume na haki na kumsema kwa ubaya ndugu yangu kisogoni mwake na kwa uwongo kumshutumu mbele yake, moyo wangu uweze kuwa na shukurani tele Kwako na Kukutukuza Wewe na kukumbuka neema Zako na kulitaja Jina Lako Tukufu, ifanye iwe hivyo ili moyo wangu na ulimi wangu siku zote ubakie unang’ara kwa ukumbusho Wako. “Ewe Mola wangu! Tufanye tufurahie Huruma Yako katika ulimwengu huu na halikadhalika na katika Akhera na utukinge na mateso ya Jahannam na ukali wa ghadhabu Yako kuwa mbali na sisi.” Kutokana na yaliyosimuliwa katika maombi hayo hapo juu, tunahitimisha kama ifuatavyo: Bila ya kupata mafundisho sahihi, mwanadamu hawezi kupata ule ukamilifu ambao anaustahiki. Mbali na kutoa maelekezo kwa mdomo, wafundishaji wazuri wa maadili lazima wawe ni mfano wa hayo kivitendo. Ni maelekezo yale tu, yanayoweza kuchukuliwa kama ndio ya msingi na ya kuaminika, yale ambayo yameasisiwa juu ya dini na imani. Mfumo na mbinu za nchi za magharibi havikuweza kutatua matatizo ya jamii. Kwa mafunzo na mwenendo wao mtukufu wa kimbinguni, viongozi wa Uislamu walitoa masomo elekezi bora kwa watu na kuleta kuwepo kwa jamii zilizoendelea zaidi. Mwisho tunaomba kwamba Allah Mtukufu awabariki Waislamu wote kwa nguvu za kutosha ili waweze kufuata mafundisho ya Uislamu na kuwa taifa lilioendelea zaidi la ulimwengu.

* * * * * 230

12:46 PM

Page 230


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION: 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24. 25. 26. 27. 28.

Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thalathini Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudharr Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur'an na Hadithi Elimu ya Nafsi Yajue Madhehebu ya Shia Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu Al-Wahda Ponyo kutoka katika Qur'an. 231

12:46 PM

Page 231


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio 29. 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52. 53. 54. 55. 56. 57. 58. 59. 60.

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii Mashukio ya Akhera Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyeezi Mungu na sifa zake Amateka Na Aba'Khalifa Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana. Upendo katika Ukristo na Uislamu Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya Kupaka juu ya khofu Kukusanya swala mbili Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kusujudu juu ya udongo Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) Tarawehe Malumbano baina ya Sunni na Shia Kupunguza Swala safarini Kufungua safarini Umaasumu wa Manabii Qur’an inatoa changamoto as-Salaatu Khayrun Mina -'n Nawm Uadilifu wa Masahaba Dua e Kumayl Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mitume Muhammad (s) 232

12:46 PM

Page 232


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio 61. 62. 63. 64. 65. 66. 67. 68. 69. 70. 71. 72. 73. 74. 75. 76. 77. 78. 79. 80. 81. 82. 83. 84. 85. 86. 87. 88. 89. 90. 91. 92.

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili Kuzuru Makaburi Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita Tujifunze Misingi Ya Dini Sala ni Nguzo ya Dini Mikesha Ya Peshawar Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliyonyooka Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake Liqaa-u-llaah Muhammad (s) Mtume wa Allah Amani na Jihadi Katika Uislamu Uislamu Ulienea Vipi? Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) Urejeo (al-Raja’a ) Mazingira Utokezo (al - Badau) Sadaka yenye kuendelea Msahafu wa Imam Ali Uislamu na dhana Mtoto mwema Adabu za Sokoni Johari za hekima kwa vijana Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili 233

12:46 PM

Page 233


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio 93. 94. 95. 96. 97. 98. 99. 100. 101. 102 103. 104. 105. 106. 107. 108. 109. 110. 111. 112. 113. 114. 115. 116. 117. 118. 119. 120. 121. 122. 123. 124. 125.

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu Tawasali Imam Mahdi katika Usunni na Ushia Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu Hukumu ya kujenga juu ya makaburi Swala ya maiti na kumlilia maiti Shiya na Hadithi (kinyarwanda) Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu Hadithi ya Thaqalain Fatima al-Zahra Tabaruku. Sunan an-Nabii Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) Mahdi katika sunna Kusalia Nabii (s.a.w) Ujumbe -Sehemu ya Kwanza Ujumbe - Sehemu ya Pili Ujumbe - Sehemu ya Tatu Ujumbe - Sehemu ya Nne Ngano ya kwamba Qur’ani imebadilishwa Iduwa ya Kumayili Maarifa ya Kiislamu. Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza Ukweli uliopotea sehemu ya Pili Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu Ukweli uliopotea sehmu ya Nne Ukweli uliopotea sehmu ya Tano Johari zenye hekima kwa vijana Safari ya kuifuata Nuru Idil Ghadiri Myahudi wa Kimataifa Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi. 234

12:46 PM

Page 234


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio 126. 127. 128. 129. 130. 131. 132. 133. 134. 135. 136. 137. 138. 139. 140.

Sehemu ya Kwanza

147. 148. 149. 150. 151.

Visa vya kweli sehemu ya Kwanza Visa vya kweli sehemu ya Pili Muhadhara wa Maulamaa Mwanadamu na Mustakabali wake Imam Ali binamu ya Mtume Sehemu ya Kwanza Imam Ali binamu ya Mtume Sehemu ya Pili Khairul Bariyyah Uislamu na mafunzo ya kimalezi Vijana ni Hazina ya Uislamu. Yafaayo kijamii Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu Taqiyya Vikao vya furaha Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? Uislamu na Mazingatio Sehemu ya Kwanza Uislamu na Mazingatio Sehemu ya Pili Azadari-Kuhuzunika na Kuomboleza Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu Kuonekana kwa Allah Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) Ndugu na Jirani Ushia ndani ya Usunni Maswali na Majibu Elimu ya Ghaibu

152.

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.1

153.

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.2

154.

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3

155.

Uadilifu katika Uislamu

156.

Filosofia ya Dini

141. 142. 143. 144. 145. 146.

7/15/2011

235

12:46 PM

Page 235


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Kwanza

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio

7/15/2011

Sehemu ya Kwanza

BACK COVER Uislamu huyachukulia kwa mazingatio mahitaji yote ya mwanadamu. Mwongozo wake ni kwa ajili ya zama zote na sehemu zote. Mtu akiyasoma mafundisho ya Uislamu kwa undani, itamdhihirikia waziwazi kabisa kuwa Uislamu ni dini bora kabisa na kwamba pale mtu anapopata elimu na umaizi hujinyenyekeza kwa Mwenyezi Mungu kwa kusilimu na kuifuata dini hii adhimu, dini ya Uislamu. Hivyo, mtu aliyeelimika akajaaliwa kuwa mwenye elimu na busara ana nafasi bora zaidi ya kuyaelewa mafundisho ya Uislamu. Uislamu ni dini yenye kujitosheleza. Ni chanzo cha riziki ambayo hutoa uhakikisho wa kujitosheleza na hutoa njia na mbinu za mafanikio na wokovu wa mwanadamu. Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info

236

12:46 PM

Page 236


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.