Mazingatio kutoka katika uislamu sehemu ya pili

Page 1

Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

MAZINGATIO KUTOKA KATIKA UISLAMU (LESSONS FROM ISLAM)

Sehemu ya Pili

Kimeandikwa na: S. M. Suhufi

Kimetarjumiwa na: Azizi Hamza Njozi Na Dr. Mohamed S. Kanju

7/16/2011

11:26 AM

Page A


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Š Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 - 512 - 68 - 3 Kimeandikwa na: Na: S. M. Suhufi Kimetarjumiwa na: Azizi Hamza Njozi na Dr. M. S. Kanju Kimehaririwa na: Ramadhani Kanju Kupangwa katika Kompyuta na: Ukhti Pili Rajab. Toleo la kwanza: Februari, 2010 Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info

7/16/2011

11:26 AM

Page B


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

YALIYOMO Kuwafundisha watoto.................................................................................2

MKOPO MZURI......................................................................20 Riba imekatazwa....................................................................................... 23 Kumpa Zawadi mkopeshaji.......................................................................27 Nyumba ya mdaiwa haipaswi kunyang’anywa......................................... 32

KAMPENI DHIDI YA UFISADI........................................35 Kueneza Madhambi ya watu.................................................................... 45 Usimamizi wa kitaifa.................................................................................46 Adhabu ya Wenye dhambi huko Akhera..................................................48 Adhabu ya Wenye dhambi katika Dunia hii..............................................50

HAKI ZA WANANDOA........................................................51 Hadithi za Mwalimu..................................................................................66 Haki za Mwalimu......................................................................................71 Jukumu la Mwalimu..................................................................................77 Sisi wote tunapaswa kuwa Waalimu.........................................................79

KUREJESHA AMANA KATIKA UISLAMU................81 Kuvunja Amani..........................................................................................86 Kurejesha Amana ni wajibu wa kibinadamu.............................................89 Kutoaminika katika Amana ni Dalili ya kutokuwa na imani....................91 Aina za Amana...........................................................................................92

11:26 AM

Page C


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio

SHERIA YA MAADILI NA TABIA NJEMA................95 Nukta chache Muhimu............................................................................107

UHALISIA WA KISAYANSI KATIKA UISLAMU....108 Kufundisha Sayansi ya Tiba....................................................................110 Ardhi na Hewa sio Element Sahili..........................................................111 Oksijeni................................................................................................... 113 Kujizungusha kwa Dunia katika Mhimili wake......................................115 Mwanzo...................................................................................................118 Viungo vya Mwili wa Mwanaadamu.......................................................119 Oksijeni na Haidrojeni katika Maji..........................................................122 Uchafuzi wa Anga...................................................................................123 Kumlaza mtoto mchanga upande wa kushoto wa mama........................126 Mwanga, Njia ya kueneza maradhi.........................................................133

KUTEKELEZA AHADI......................................................142 Wastani (Njia ya Kati na Kati).................................................................157 Wastani katika Ibada................................................................................161 Wastani katika matunzo...........................................................................164 Wastani katika Ulaji.................................................................................165 Wastani katika Urafiki na Uadui..............................................................169 Wastani umehimizwa kwa mara nyingine tena.......................................171

WAJIBU WA MATAJIRI.................................................... 171 Matajiri ni Nguzo za Jamii......................................................................173 Onyo kwa Matajiri...................................................................................175 Ndugu Wawili katika Ncha mbili tofauti.................................................178 Haki ya Mali ...........................................................................................179 Kutoka katika Njia ya Mwenyezi Mungu ...............................................181 D

11:26 AM

Page D


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Kuwasaidia wahitaji................................................................................182 Athari Njema za Zaka .............................................................................184 Ulezi wa Mayatima .................................................................................185

USTAHIMILIVU...................................................................188 Ustahimilivu wa Mtukufu Mtume ........................................................ 195 Kudumu katika Tabia Njema .................................................................199 Ustahimilivu katika Uadui .....................................................................201 Hitimisho ................................................................................................209

E

11:26 AM

Page E


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio

NENO LA MCHAPISHAJI Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza kiitwacho, Lessons From Islam. Sisi tumekiita, Mazingatio Kutoka Katika Uislamu. Uislamu ni dini na mfumo wa maisha. Kwa hiyo, mafundisho ya Uislamu yanazingatia maendeleo ya kiroho na maendeleo ya kimwili - yaani maisha ya ulimwengu huu tulionao. Uislamu kimsingi uko dhidi ya kufuata kibubusa. Tofauti iliyopo baina ya Uislamu na dini nyinginezo ni kwamba Uislamu unamtaka mtu kwanza aelewe na awe na maarifa juu ya anayotaka kuamini kisha aamini, ambapo dini nyinginezo zinasema kwamba kwanza amini kisha utaelewa baadaye. Hivyo, ni muhimu mtu kuelewa mafundisho ya Uislamu kabla ya kuamini. Vivyo hivyo, ni muhimu kuelewa imani za wengine ili wasije wakakuyumbisha. Inawezekana kusemwa kwamba wale ambao hawaelewi kabisa mtazamo wa imani tofauti, hawaelewi kwa ukamilifu (mtazamo) wa kwao wenyewe. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili za watu. Kutokana na ukweli huo, taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili. F

11:26 AM

Page F


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Tunamshukuru ndugu yetu, Dk. M. S. Kanju na Aziz Hamza Njozi kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation S. L. P. 19701 Dar-es-Salaam, Tanzania.

G

11:26 AM

Page G


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio

MPENDWA MSOMAJI. Assalaam Alaykum Warahmatullah Wabarakatuh. Kitabu hiki ni chapisho la Al-Itrah Foundation. Machapisho yake yameandaliwa ili kukidhi mahitaji ya kiroho ya zama hizi kwa kuzingatia msisitizo maalum wa kusafisha akili na fikra ya Mwislamu. Al-Itrah Foundation imefanya jitihada kubwa kuwasilisha kile tu ambacho ni Sahihi na cha kuaminika kwa mujibu wa Uislamu. Tunakuomba ukisome kitabu hiki kwa dhamira iliyokusudiwa. Pia unaombwa ututumie maoni yako juu ya machapisho yetu, maoni ambayo sisi tutafurahi sana kuyapokea. Kueneza ujumbe wa Uislamu ni kazi inayotaka ushirikiano wa watu wote. Al-Itraha Foundation inawaalikeni kwenye kazi hii, ambayo ni mwitikio wa aya ya Qur’an isemayo:

“Sema: Siwapatieni isipokuwa nasaha moja, kwamba msimame kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kwa pamoja na mkiwa mmoja mmoja. (34:46). Mwenyezi Mungu Mtukufu awabariki! Ndugu zenu katika Uislamu Al-Itrah Foundation

H

11:26 AM

Page H


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio

KUHUSU SISI WENYEWE Mtu makini leo hii anagundua mabadiliko katika maisha ya kiakili ya mwanadamu. Sayansi na teknolojia pamoja na mafanikio yake ya ajabu vinaonekana kufikia kilele chake. Mahitaji ya mali na vitu pamoja na uchu wa madaraka na utukufu vimemwelekeza mwanadamu kwenye upotevu wa dhahiri wa maadili yake yote. Katika hali hii ya kukatisha tamaa, mtu hulazimika kutulia na kutafakari hatari kubwa inayomkabili mwanadamu. Mwanadamu kwa mara nyingine tena ameelekeza macho yake kwa Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwingi wa Kurehemu kwani amebaini kuwa Suluhisho la matatizo yake na hatima ya uokovu wake unategemea kuyafuata maamrisho ya Mwenyezi Mungu. Mabadiliko haya kutoka katika fikra za kuwazia mali na utajiri (uyakinifu) kwenda katika fikra za kiroho yanaendana kabisa na malengo ya Islamic Seminary. Maadili ya kidini, sambamba na maendeleo ya zama zetu, hutoa lile kimbilio hasa linalohitajika kwa ajili ya akili inayosumbuka na yenye wasiwasi. Ni matokeo ya hili ongezeko la uelewa kwamba sasa inatambulika kuwa siri ya kuishi kiuchamungu katika dunia hii kunaongoza kwenye maisha yenye furaha ya milele huko Akhera. Huu ndio ujumbe wa Uislamu kwa watu wote. Seminari ya Kiislamu (Islamic Seminary) inataka kunyanyua kurunzi la mwongozo wa kidini na kusaidia kwa bidii zote katika kukuza urithi wa kiroho wa mwanaadamu. Inawasilisha mfumo wa maisha wa Qur’ani katika utukufu wake wa asili. Inawasilisha kile tu ambacho ni sahihi na cha kuaminika. Machapisho yake yameandaliwa ili kukidhi mahitaji ya kiroho ya zama zetu. Yatatumika kama chemchem isiyokauka kwa wale wenye kiu ya elimu na maarifa.

I

11:26 AM

Page I


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Seminari ya Kiislamu (Islamic Seminary) ni taasisi ya kilimwengu inayofanya jitihada za kujenga hisia za udugu wa Kiislamu. Inafaidika na michango ya watu wenye ujuzi mkubwa kabisa, pamoja na uungwaji mkono wa kimataifa katika kufikia malengo yake. Ina vituo ndani ya Bara Asia, Afrika, Ulaya, Canada na Mashariki ya Mbali.

J

11:26 AM

Page J


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

11:26 AM

Page 1


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio

UFUNDISHAJI WA WATOTO Jamii inayoweza tu kuchukuliwa kama yenye bahati ni ile ambayo imeundwa watu wachaji, wema, wawajibikaji na waaminifu. Ili kutengeneza jamii kama hiyo na kupata watu kama hao, ni muhimu kufuata malezi sahihi na mafunzo ya watoto kwa ajili ya siku zijazo. Kwa kawaida watu huwaangalia watoto kijuujuu na hawawi makini katika mafunzo yao sahihi, ingawa ni kweli kwamba watu wazima wa leo ni watoto wa jana na watoto wa leo ni watu wazima wa kesho. Mtoto ambaye hapati mafunzo sahihi wakati wa umri wake mdogo, hawezi kutegemewa kukua kama mchamungu na hivyo kuweza kuwa mtu wa manufaa katika jamii. Umuhimu wa suala la kufundisha watoto umepata mazingatio katika ulimwengu wa kisasa na wanachuoni wameandika vitabu vingi juu ya somo hili. Kwa mujibu wa wataalamu katika nyanja ya kuwafundisha watoto, mafunzo ni lazima yaanze mapema baada ya kuzaliwa kwa mtoto na lazima yaendelee kidogo kidogo mpaka mtoto afikie kilele cha ukamilifu. Kwa mujibu wa Uislamu kipindi cha mafunzo huanzia wakati ambapo mwanamume na mwanamke wanapoingia katika ushirika wa ndoa, kama wazazi wa baadae lazima wenyewe wajione kuwa wawajibikaji kwa malezi ya watoto wao. Unaweza ukashangaa kwamba ni nini maana ya mwanzo wa mafundisho ya mtoto kabla hajazaliwa! Hata hivyo, baada ya tafakuri ndogo, umuhimu wa maelekezo haya huwa wazi.

2

11:26 AM

Page 2


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Kwa mujibu wa sheria ya mirathi ambayo inakubaliwa na wanachuoni, hali na sifa nyingi za kidunia na kiroho huhamishwa kutoka kwa wazazi kwenda kwa mtoto na kitu hiki haswa huandaa mazingira mazuri au mabaya kwa ajlili yake katika siku za baadae. “Hali zote za kimwili na kisaikolojia za mama zina athari juu ya mtoto, kwa sababu katika mfuko wa uzazi mtoto yuko kama kiungo cha mama. Kama ambavyo hali za kimwili za mama zilivyo na athari juu ya mtoto, katika njia hiyohiyo mawazo na tabia zake (mama) huathiri mwili wake na nafsi na wakati mwingine hutokea kwamba mtoto anaathirika zaidi kuliko mama mwenyewe. Kwa mfano, kama wakati wa ujauzito wake mama anapatwa na hofu, athari ambayo hali hii ya kisaikolojia anayokuwa nayo katika mwili wake ni kwamba uso wake unapauka, lakini mtoto aliyeko kwenye mfuko wa uzazi anapata madhara makubwa kwa tukio hili. “Kama wakati wa ujauzito mama anatishika kiasi hicho mpaka uso wake unapauka na anaanza kutetemeka, madoa huonekena mwilini mwa mtoto mchanga ambayo huitwa alama za kuzaliwa.” (Dr. Ghiyathuddin, I‘jaz-i Khorakihaa, uk. 172) Huzuni, wasiwasi, hasira, fadhaa, ushawishi mbaya, misukosuko, kukosa rajua, uhabithi na kwa ufupi sifa zote mbaya za mama na vivyo hivyo imani yake, uchaji, tabia nzuri, uaminifu, upendo, huruma, hisani, amani na utulivu wa akili, ujasiri na ushujaa na hatimaye sifa zote za kimaadili za mama zina athari mbaya au nzuri juu ya mtoto na kuweka msingi wa ufanisi wake au dhiki katika nyumba ya uzazi. Kama ilivyosemwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.): “Msingi wa ufanisi au dhiki za watu lazima vitafutwe kwenye matumbo ya uzazi ya kina mama.” (Biharul Anwar, Jz. 3, uk. 44) Wataalamu wa tiba ya magonjwa ya akili wamethibitisha kwamba 60% ya watoto ambao wanasumbuliwa na magonjwa ya akili wameyarithi magonjwa hayo kutoka kwa mama zao, na kama ni mwenye afya na hali 3

11:26 AM

Page 3


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio nzuri, mfumo wa neva wa mtoto wake vilevile utakuwa na afya nzuri. Mtukufu Mtume (s.a.w.) anasema: “Chagueni sehemu nzuri kwa ajili ya mbegu zenu.” Kuchagua hapa ina maana kuchagua mwenza mzuri baada ya kuchunguza idadi kubwa ya watu wanaofanana. Katika hadithi hii Mtukufu Mtume ameelezea kwamba tumbo la uzazi la kila mwanamke sio lenye kufaa kumzalia mtu watoto na mtu lazima achague mwanamke bora zaidi na mwenye kufaa kwa ajili ya madhumuni haya muhimu na nyeti. Katika hadith nyingine Mtukufu Mtume (s.a.w.) anasema: “Jiepusheni na majani ya chanikiwiti yanayoota kando kando ya marundo ya takataka”. Watu wakauliza: “Ewe Mtume wa Allah! Ni nini hiyo?” Mtukufu Mtume akajibu: “Ni mwanamke mrembo aliyelelewa katika familia fisadi.” Ili kuwazuia Waislamu kutokana na kuzaa kizazi fisadi, Uislamu umechukua tahadhari zote katika suala la ndoa na imeweka mazingatio kwenye vipengele vyote vya kisaikolojia, kimwili na maadili ya mume na mwanamke. Uislamu umewaonya watu dhidi ya kuoa watu punguani, mazezeta na walevi. Qur’ani Tukufu imewazungmzia mwanawake kuwa ni shamba kwa ajili ya mwanaume, na inasema: “Wake zenu ni mashamba yenu, basi yaendeeni mashamba yenu kwa nama mtakavyo...” (2:223). Bila shaka mtu anaweza kupata mazao ya kuridhisha kutoka kwenye shamba wakati akipandikiza mbegu katika ardhi nzuri na yenye kufaa, kwa sababu “ardhi ya chumvi chumvi haizalishi maua ya tunguu.” Karne nyingi kabla ya taaluma ya baiolojia kutokea katika ulimwengu kama sayansi inayojitegemea, Mtukufu Mtume alisema: “Jiepusheni kuoa wanawake mazezeta na wapumbavu kwa sababu kushirikiana nao ni huzuni na msiba, na kama wakizaa watoto watakuwa hawana faida.” (Mustadrak, Kitabun Nikah). 4

11:26 AM

Page 4


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Ama kuhusu athari za maziwa ambayo mtoto huyatumia wakati wa kuzaliwaza, Mtukufu Mtume anasema: “Msiruhusu watoto wenu kunyonya kutoka wanawake waovu na mafisadi na halikadhalika kutoka kwa wanawake wale ambao ni punguani, kwa sababu tabia, fikra na hali za mama ambaye humnyonyesha mtoto huhamishiwa kwa mtoto huyo.” (Makarimul Akhlaq, uk. 254) Inaweza kueleweka kutokana na maelekezo yaliyotolewa na Uislamu kama ilivyotajwa kabla kwamba jukumu la kufundisha watoto lazima lizingatiwe kabla ya kufunga ndoa ili kwamba watoto ambao wanafaa kufundishwa wapate kuzaliwa, na uangalifu mkubwa lazima vilevile uchukuliwe katika suala la kunyonyesha ili msingi upate kutayarishwa kwa ajili ya kunyanyuliwa kwao na maendeleo yao, na malekezo wanayopewa yawe yenye manufaa zaidi. Watoto ambao wanazaliwa na wazazi wenye afya nzuri na wachamungu wanafaa zaidi kupokea mafunzo na maelekezo. Kipindi cha utoto ni wakati mzuri wa kuchukua njia iliyonyooka ya maisha kwa sababu uwezo wa kuiga na kupata na hisia ya kukubali vitu ni mkubwa zaidi kwa watoto kuliko ilivyo kwa watu wazima, na mtoto anaweza kuhifadhi matendo yote, tabia na maneno ya mfundishaji maadili katika akili yake katika njia nzuri iwezekanayo. Imamu Ali (a.s.) alimuambia mtoto wake Imamu Hasan (a.s.): “Moyo wa mtoto mdogo ni kama ardhi ambayo haijalimwa ambayo inafaa kwa mbegu yoyote au mbogamboga. Hukabali kila mbegu yoyote inayopandwa kwayo na kuistawisha. Mwanangu mpenzi! Niliutumia utoto wako na nikakimbilia kwenye mafundisho yako kabla moyo wako ambao ulikuwa unafaa kupokea maelekezo haujakuwa mgumu na akili yako haijashughulishwa na masuala mengine.” (Nahjul Balaghah)

5

11:26 AM

Page 5


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Kama vile ambavyo wakufunzi wanavyojali afya ya mwili ya mtoto hivyo lazima waweke umuhimu kwenye maendeleo ya nafsi yake na hisia zake na afanye juhudi kwamba mwili na roho lazima viendelee kukua sambamba kwa pamoja. Kuanzia maisha ya mapema kabisa ya mtoto mkufunzi wake lazima amfundishe ukweli, upole, huruma, hisia za uwajibikaji na sifa nyingine nzuri na safi na lazima waweke mfano wa kimatendo mbele yao kwa mwendo wao mzuri. Wazazi wanaweza wakafanya ushawishi mkubwa katika masuala ya mafunzo ya watoto na wanaweza wakatekeleza wajibu muhimu katika kuweka msingi wa ufanisi wao. Hili linaweza kufanywa haswa na mama ambaye anawajibika katika eneo kubwa kwa ajili ya hali ya mwili, nafsi, hisia na maadili ya mtoto, na ni kwa sababu hii kabisa kwamba mapaja ya mama yanaitwa kiti cha kwanza cha kujifundishia kwa ajili ya elimu na mafunzo ya mtoto wake. Kama mtoto akipata mafunzo mazuri wakati wa utoto wake, inaweza kusemwa kwamba atakuwa na furaha mpaka mwisho wa maisha yake, na wenye bahati ni wale watoto ambo wanalelewa vizuri na mama zao wanaojiweza kuanzia mwanzo kabisa na ambao hupata sifa nzuri. Wakati wa utu uzima, watu kama hao hutumia walichojifundisha kutoka kwa mama zao bila ya kupata taabu ya kujenga tabia zao. Katika moja ya hutuba ambazo Imamu Husein (a.s.) alizozitoa katika siku ya mwisho ya uhai wake - siku ya Ashura, aligusia juu ya umuhimu wa mafunzo sahihi na athari yake ya ndani juu ya maisha ya mtu na akasema: “Enyi watu! Jueni kwamba Ubaydullah bin Ziyad, mwana wa haramu wa baba mwanaharamu anasisitiza juu ya vitu viwili: vita au fedheha (kwa kukubali kula kiapo cha utii kwa Yazid). Itakuwa ni jambo la kusikitisha kwamba nisalimu amri kwenye unyonge na udhalilishaji. Siruhusiwi kufanya hivyo imma na Allah au na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), au na yule 6

11:26 AM

Page 6


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio mama mchamungu ambaye amenilea au na fikra hasa ya baba yangu mchamungu na mwenye kuheshimika. Hakuna katika wao anayeniruhusu kwamba nipendelee udhalili kuliko kifo cha heshima.” Katika maneno haya machache mtukufu Imamu alichomaanisha haswa ni kusema kwamba kutokujisalimisha kwa watu duni ni matokeo ya mafunzo ya kufaa ya wafundishaji wake wa maadili. Aliendelea kusema: “Kwa vile nimenyonya kutoka kwenye matiti tohara na nimepata mafunzo kutoka kwa baba halisi, waliotukuka, na wenye kuheshimika na wafundishaji wa maadili, nimerithi heshima, hadhi na uhuru na siwezi kujinyongesha na kujidhalilisha ili niishi maisha ya fedheha.” Maneno haya ni somo la kimaelekezo ambalo Imamu Husein (a.s.) amelitoa kwenye mataifa mbalimbali, kwamba lazima watafute heshima yao, utukufu na ustawi kwa maelekezo sahihi. Watu ambao wamelelewa katika familia tukufu na zenye heshima hawajawahi kupatwa na udhalilishaji na hawako tayari kwa hali yoyote kupitiwa na unyonge na fedheha kwa ajili ya kuishi maisha ya kufedhehesha. Mafunzo yasiyo sahihi huuwa moyo wa heshima na uhuru katika watu na kuondosha vipaji vyao kwa ajili ya maendeleo na uongozi na kustawisha moyo wa unyonge, kujipendekeza na udhalili katika tabia zao na kuupitisha moyo huu kwenye vizazi vijavyo. Hii huonesha jinsi gani ulivyo mkubwa uwajibikaji wa wazazi na wafundishaji wa maadili! Kama uleaji wa watoto utashia tu kwenye chakula, nguo, usafi na elimu, utakuwa mwepesi mno na rahisi. Lakini maendeleo ya vipaji na ustadi wao na uimarishaji wa uwezo wa kiroho ni kitu cha kina sana na nyeti na huhitaji uangalizi maalumu na uangalifu. Imamu Ali (a.s.), ambaye ni mtu bora na mfano mkamilifu kwa ubinadamu, kwa usahihi anakumbuka mafunzo aliyopata wakati wa utoto 7

11:26 AM

Page 7


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio wake chini ya malezi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kuwa na fahari kuwa na mfundishaji maadili mwenye uwezo kama huyo. Anasema: “Mnajua sana undugu wangu na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na nafasi maalumu niliyofaidi katika heshima yake. Nilikuwa mtoto wa umri mdogo. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alizoea kuniweka kwenye mapaja yake. Alinikumbatia. Alinikandamiza kwenye kifua chake. Wakati mwingine alinifanya nilale katika kitanda chake. Alinipapasa pasa na kufanya ninukie manukato mazuri ya mwili wake. Kila uchao alinionesha mfano wa sifa za unyofu wake na kuniongoza kufuata mwenendo na maadili yake. (Nahjul Balagha) Kama ubinadamu umenyenyekea mbele ya Imamu Ali na kumuona yeye kuwa yu juu ya watu, na kama wafuasi wa dini nyingine mbali ya Uislamu vilevile humsifia huyu mfadhili mwema wa ubinadamu kwa hamasa na kudhihirisha mapenzi na kuvutiwa kwa ajili yake, moja ya siri nyingi za msingi juu ya hilo ni nukta yenyewe ambayo ilitegemewa na Imamu Ali mwenyewe. Mtu ambaye ana hazina bora za kiroho na kimwili kwa mtazamo wa urithi na amelelewa katika familia tukufu mno na chini ya uangalizi wa mfundishaji wa maadili mwenye kufaa sana [yaani, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)] wakati anapokua na kuwa mtu mzima anastahiki kuwa mtu mashuhuri na kiongozi bora. Uislamu umeweka umuhimu mkubwa sana kwenye uleaji sahihi wa watoto ambao huchukulia kuwa ni haki rasimishi ya mtoto juu ya baba yake. Imamu Zainul Abidin anasema: “Mtoto anakuwa na haki juu yako ambayo lazima uelewe kwamba kuwepo kwake ni sehemu ya kuwepo kwako na dhiki na faraja yake katika ulimwengu huu inahusiana na wewe. Lazima uelewe kwamba wewe ukiwa katika wadhifa wa mlezi wake, una wajibu wa kumlea kwa kumpa mafundisho sahihi na kumuongoza kwa Allah Mwenye nguvu zote na kumsaidia katika utiifu Kwake. Lazima uwe baba 8

11:26 AM

Page 8


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio ambaye anajua wajibu wake na majukumu. Lazima uwe baba ambaye anajua kwamba akifanya jema kwa mtoto wake atalipwa kwalo na kama akimfanyia madhara ataadhibiwa kwayo.� (Makarimul Akhlaq, uk. 486) Ni jukumu la wazazi kutengeneza na kudumisha mazingira ya ucha Mungu katika nyumba ambayo kwayo upendo, huruma, dhamiri, upole, uchaji, wema na sifa nyingine nzuri na tabia za kusifika lazima ziwepo na ambazo zitawafanya watoto kuwa waangalifu, makini na wapole. Mwanasaikolojia anasema: “Nyumba na familia ni mazingira ya kwanza ya kijamii ambayo kwayo mtoto analelewa chini ya usimamizi na malezi. Kwa hiyo, yana athari mno juu ya kukua na maendeleo kidogo kidogo ya mtu binafsi kuliko mazingira mengine yote ya kijamii, na kabla ya kuja chini ya ushawishi wa hali za kijamii za nje anaweza kubakia chini ya ushawishi wa familia yake. Tabia na mitazamo ya mtoto huanzia kwenye nyumba yake na ukitupa jicho juu ya tabia na mitazamo hii kutafanya umuhimu wa ushawishi wa familia kuwa dhahiri kabisa. Mtoto hujifundisha kutoka kwenye mazingira ya nyumba yake tabia zote, kama adabu katika kula chakula, kuzungumza, kutembea na njia ya kawaida ya kushughulika na watu halikadhalika na mtazamo kuhusu jinsia, mali na haki za wengine, uhusiano kati ya mwanaume na mwanamke, uhusiano kati ya wazazi na watoto na ulezi na nafasi na jukumu la mtu katika familia. Kwa ufupi, mara tu mtoto anapowasili katika ulimwengu huu na kujikuta mwenyewe katika susu, hupasika kwenye mazingara ambayo yana fikra, hisia, maoni, matumaini na matarajio ya jamaa wa familia. Nyumba ni sehemu ambayo watoto hujifunza mfumo wa maisha kwa ujumla na hususan utamaduni wa wazazi wao. Mtu wa kwanza wa familia ambaye kwamba mtoto ana mawasiliano naye ya moja kwa moja ni mama yake, na maisha yake huanza na uhusiano wa kibailojia kati yao wote katika maana ya kwamba mwanzoni uhusiano wa mtoto na mama yake ume9

11:26 AM

Page 9


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio tegemea juu ya uridhikaji na mahitaji ya kibaiolojia kama chakula na usingizi na humtambua mama yake tu kwa sababu ya lishe na vilevile humhitaji (mama) kwa hilo. Baadae, akiwa amekwishakua taratibu huigeuza hali ya mwili na uhusiano wa kibailojia kuwa muambatano wenye nguvu wa kiakili na kihisia. Baada ya hapo, huanzisha mawasiliano yake na baba yake, kaka zake, dada zake, jamaa zake na hatimaye na ulimwengu wa nje wa jamii yake, na hivyo ushawishi wa pili huja katika mapambano baadae. Kwa hiyo, inaweza kusemwa kwamba maisha ya mtoto huanza na kuambatana na mama na kunyimwa kuwepo kwa mama kwa hakika ni kunyimwa maisha yenyewe. Mtoto hujifanyia mfano kwa ajili yake mwenyewe na kufuatanisha tabia yake na kila tendo, imma zuri au baya, ambalo analiona na kila neno analosikia, imma la adabu au lisilo la adabu. Na uigaji huu usiofaa kwanza kabisa unafanywa na wazazi, kwa sababu katika familia mtoto anaathiriwa na wazazi wake zaidi kuliko mtu yeyote au kitu kingine chochote. Kwa sababu hii hasa, Uislamu katika mafundisho yake umevuta nadharia ya wazazi kwenye uwajibikaji mkubwa na jukumu gumu mno ambalo huwazunguka wao na imewapa maelekezo muhimu katika kila suala. Imamu Ja’far Sadiq (a.s.) anasema: “Wapendeni watoto. Kuweni na huruma kwao. Wakati ukifanya ahadi nao lazima uitimize kwa hali yoyote, kwa sababu watoto hukuchukulia wewe kama mlishaji wao.” (Wasailush Shi’ah, Jz. 5, uk. 126). Imamu Ali (a.s.) anasema: “Sio sahihi kwa mtu kuongopa kwa uzito hasa au kwa utani na sio sahihi kwa mtu kutoa ahadi kwa mtoto wake na kuivunja.” (Wasailush Shi’ah). Kwa uaminifu kamilifu mtoto anawachukulia wazazi wake kuwa watu maarufu na watukufu sana katika uso wa ardhi na hamkubali mwingine yeyote kuliko wao, huwaona kama mfano kwa ajili yake na kufuata nyayo 10

11:26 AM

Page 10


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio zao. Kama wazazi wakimuongopea na kutotekeleza ahadi zao walizofanya kwake, hisia zake zinavurugika vibaya sana na kwa kupata tabia hii mbaya hutenda kwa mujibu wa tabia hiyo maishani mwake mwote. Hebu fikiria kwamba wakati tusipofanikiwa kumridhisha mtoto kwa njia za kawaida, halafu tunakuwa tunamdanganya, tunampa ahadi za uwongo na kumwogopesha kupita kiasi. Kuna akina mama wengi ambao ili kumtuliza mtoto ambaye huwazuia wasitoke nyumbani, humuambia kwamba wanakwenda kumnunulia mwanaserere. Mtoto hungojea kwa hamu kubwa kurudi kwao, lakini hatimaye huona kwamba wamerudi nyumbani mikono mitupu. “Gari liko tayari. Baba anataka kuondoka kijijini kwenda mjini. Wakati uleule anataka kuingia ndani ya gari mtoto wake mdogo anakuja mbio anamkimbilia na kusema kwamba na yeye anataka kwenda mjini. Anasisitiza. Anasihi. Na kwa vile mtoto bado hajajifunza kwamba ‘hapana’ humaanisha kukataa kabisa anaendelea kusihi na baba anatambua kwamba sio kazi rahisi kumshawishi. Kwa hiyo, upesi sana anakimbilia kwenye kisingizio na kusema: ‘Mpenzi mwanangu! huwezi kwenda mjini katika hali hii. Nenda kabadilishe nguo zako ndio uje.’ Kwa ajili ya imani ambayo kwa kawaida mtoto anayo kwa baba yake anarudi mbio kubadilisha nguo zake. Hata hivyo, wakati wa kurudi haoni kitu chochote pale isipokuwa vumbi lililoachwa nyuma na gari. Kwa kuona vile mtoto akashindwa kuvumilia na akakasirika. Akapiga kelele: ‘Wewe umwongo! Umuwongo!’ Yuko sahihi. Baba yake ni mwongo na kuna uwezekano mkubwa kwamba mtoto yule pia kwa upande wake atakua akiwa muwongo.” (Maa wa Farzandaan-i Maa) Vitendo na tabia kama hizo za wazazi kwa kiasi fulani huacha fikra juu ya moyo usio na hatia wa mtoto, na ambazo baadhi yake hazifutiki mpaka mwisho wa maisha yake.

11

11:26 AM

Page 11


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Uislamu umekataza kwa nguvu sana vitendo visivyo sahihi ambavyo huharibu tabia za watoto na kujenga fikra mbaya. Ingawa Uislamu umefanya mapendekezo mengi katia suala la kumlea mtoto, haukuruhusu kwamba mtoto atendewe vibaya au kumtesa. Mtu moja alikuja kwa Imamu Ali (a.s.) na kulalamika juu ya mtoto wake. Mtukufu Imamu akasema: “Usimpige kwa gongo mtoto wako na kuvunja uhusiano naye ili kumrekebisha, na usirefushe muda wa hasira yako bali patana naye baada ya muda mfupi.” (Biharul Anwar, Jz. 13, uk. 114) Katika hadithi hii mtukufu Imamu amekataza adhabu ya kimwili na ameelekeza kwamba ili kumrekebisha mtoto hisia zake zinapasa kutiliwa maanani. Baba ndiye mhifadhi pekee tu kwa ajili ya mtoto na wakati anapopuuzwa na baba yake anaumia kiroho na kihisia na maumivi haya yanaweza kuwa na athari kubwa juu ya mtoto. Baada ya kutoa maelekezo haya mtukufu Imamu mara moja alipendekeza kwamba baba asibakie na hasira kwa muda mrefu, kwa sababu kama hasira ya baba ina athari kubwa juu ya hisia za mtoto kurefushwa kwake kutasababisha mtoto kuchanganyikiwa. Na kama hasira hii haina athari sana juu ya mtoto muda wake mrefu utashusha haiba ya baba katika macho yake na hatua hii ya kurekebisha baadae itakuwa haina athari zaidi. Siku moja Imamu Hasan (a.s.) alimuita mtoto wake na watoto wa ndugu zake na akawaambia: “Leo ninyi ni watoto wa jamii na inaweza kutumainiwa kwamba kesho mtakuwa watu mashuhuri katika jamii. Lazima mfanye bidii kupata elimu na hekima na wale ambao miongoni mwenu ambao hawana kumbukumbu nzuri na kuweza kuhifadhi mambo yenye maana lazima wayaandike na kuweka maandishi hayo nyumbani mwenu kwa ajili ya kutumika wakati wa kuhitajika”. (Biharul Anwar, Jz. 1, uk. 110) 12

11:26 AM

Page 12


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Katika hadithi hii Imamu Hasan (a.s.) amechukua njia ya kushawishi kwa ajili ya kuwafundisha watoto na hii pia ni njia ya kutumia hisia ya mtoto. Kwa asili kila mwanadamu ana silka ya kujipenda na kipi kinaweza kuwa bora kuliko hiki kwamba badala ya kutoa adhabu ya kimwili kwa watoto wanaweza kushawishiwa kutekeleza kazi zao kwa kuamsha silka zao na kuwashawishi kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo yao ya baadae halikadhalika kwa ajili ya maendeleo ya jamii. Katika ulimwengu wa kisasa ushawishi huchukuliwa kama moja ya njia bora na ya kufaa sana ya maelekezo na walimu ambao wana uwezo wa kutumia njia hii kwa ajili ya kuwafanya wanafunzi wapate elimu na kufanya matendo mema kwa kulinganisha watakuwa wamefanikiwa zaidi katika nyanja yao. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: “Wapeni heshima watoto wenu na kuweni na mwenendo wenye adabu njema”. (Biharul Anwar) Ukali unaofanyiwa watoto huwafanya watekeleze kazi zao kwa wakati fulani, lakini kamwe hauwezi kuwafanya kuwa watu mashuhuri na tabia imara. Kama ambavyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amewaelekeza wafuasi wake kuwa na tabia nzuri kwa watoto wao kwa heshima, yeye mwenyewe vilevile alifuata kanuni hii kwa mpango makini kabisa. Ummul Fazl, mke wa Abbas bin Abdul Muttalib, ambaye alipata heshima ya kufanya kazi kama yaya wa Imamu Husein, anasema: “Siku moja wakati Husein alipokuwa katika kipindi chake cha kunyonya, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimchukua kutoka mikononi mwangu na akamuweka mapajani mwake. Mtoto yule akalowesha (kwa mkojo) nguo za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Nilimchukuwa mtoto yule kwa ghafla kutoka kwenye mapaja ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na mtoto yule akaanza kulia. 13

11:26 AM

Page 13


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akaniambia: ‘Tulizana. Kwa nini umemfanya mtoto alie? Maji yanaweza kutohorisha nguo zangu, lakini je, kuna kitu ambacho kinaweza kuondoa huzuni na majonzi kutoka kwenye moyo wa Husein?’” (Hadyatul Ahbaab, Muhadithi Qummi). Mtoto mwenye kunyonya, licha ya udhaifu wake wote, huhisi huruma na ukali. Huruma humfanya kuwa na furaha na hucheka ambapo ukali humfanya ahuzunike na kulia. Na furaha na huzuni hii ina athari nzuri na mbaya mtawalia juu ya tabia yake. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alionesha tabia nzuri kwa heshima sio tu kwa watoto wake mwenyewe bali kwa watoto wote. Kama ilivyoandikwa na wanahadithi, upole kwa watoto ilikuwa ni moja ya tabia zake tukufu. Wakati pale Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliporudi kutoka safarini na akaona watoto wa watu njiani, anasimama na kuwaambia masahaba zake wawalete watoto kwake. Wanapofika huwakumbatia baadhi yao na kuwafanya wengine wakae mabegani mwake na vilevile huwashauri masahaba zake kuwakumbatia watoto. Watoto wakawa na furaha mno kwa ajili ya upole huu na upendo wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na wakauhifadhi kama kumbukumbu tamu baada ya kukua na kila mara walikumbuka tukio hili kama ukumbusho wa kupendeza wa maisha yao ya mwanzo na kuona fahari kwayo. (Muhajjatul Bayaza). Mtukufu aliwafundisha wafuasi wake kivitendo kuipa heshima haiba ya watoto ili kwamba na wao vilevile kwa zamu yao wapate kuwashughulikia watoto kwa heshima na hivyo msingi sahihi wa mafunzo ya watoto kupata kuwekwa. Nukta ambayo lazima itajwe hapa ni kwamba hatupaswi kwenda mno zaidi katika masuala ya upendo kwa watoto kwa sababu malezi sahihi ya kumlea mtoto ni kwamba aweze kutayarishwa kwa ajili ya kuishi maisha ya furaha na ustawi. 14

11:26 AM

Page 14


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Kupanda na kushuka, machungu na kushindwa na huzuni na kutokufanikiwa kunakuwepo, taka usitake, katika maisha ya kila mtu na mfundishaji wa maadili mwenye uwezo ni yule ambaye humfurahisha mtoto kukabiliana na kuyashinda matatizo ya maisha. Watoto ambao hufaidi mno upendo na ambao wazazi wao hukubali matamanio yao yote bila masharti na wakaipa sura ya hekima kwa mielekeo yao yote ya mema na mabaya, hukua wakiwa wakaidi na wabinafsi. Hutegemea na kutumaini kwamba watu wote lazima wawafanyie kama walivyofanyiwa na wazazi wao na kwamba watawatii na kama matumaini yao haya hayatekelezwi wanakuwa wenye hisia kali na kukosa rajua kuhusiana na kila mtu. Imamu Muhammad Baqir (a.s.) anasema: “Baba waovu ni wale ambao hudekeza na kuendekeza watoto wao zaidi mno kuliko ilivyo muhimu. Na watoto waovu ni wale ambao huwaudhi baba zao kwa sababu ya kukosa adabu na kushindwa katika kazi zao.” (Tarihk-i Yaqubi, Jz. 3 uk. 53). Welbertt Robin anasema: “Kuendekeza watoto kusiko na sababu husababisha kuwa na hali ya mhemuko mkali usio wa kawaida na tabia ya ujeri hatimaye mtoto huchukuwa madaraka mikononi mwake na huenda mbele kwa kasi kubwa. Na ingawa ana moyo wenye hisia kali hupata ubora kwa njia ya udanganyifu na ukali. Watoto walioharibiwa hukua kama wenye bahati mbaya, wanyonge na watu wasio na malengo. Kama huko nyuma watu walipomuambia mama asiyejali kwa utani: ‘Mtoto wako hakuharibika bali ameangamia.’ Watakuwa hawakuongeza chumvi bali walifanya utabiri wa kweli.’ “Wakati mwingine kushuhudia uzembe katika suala la uleaji wa watoto humfanya mtu agwaye kwa sababu kwa kusema kweli, tunaweza tukatabiri mauwaji ya kikatili ya watu wengi wasio na hatia ambayo yamkini yangeweza kuepukwa kwa hali yoyote ile.” (Tarbiyat-i Alfaal-i Dushwaar).

15

11:26 AM

Page 15


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Raymond Beech anasema: “Ni muhimu kwamba lazima tutaje baadhi ya makosa ambayo hufanywa wakati wa kipindi cha mwanzoni kabisa mwa maisha ya mtoto. Yaliyo ya kawaida zaidi katika makosa hayo ni ile tabia ambayo huharibu mtoto. Udekezaji usio na sababu na uendekezaji wakati wa mwanzo kabisa huharibu watoto. Kwa hakika wazazi hutamani ustawi na mafanikio ya mtoto wao na ndio maana hutoa mazingatio ya ziada kwenye udekezaji. Humpendeza mno na kumkinga na maumivu yote na matatizo hata yale ambayo ni madogo sana. Na wakati mtoto anapokua pole pole humpatia njia zote za burudani zinazolingana na umri wake. Hapana shaka hisia hizi kwa wazazi ni zenye kufaa sana, lakini kwa uhalisi ni za hatari mno sana. (Maa wa Farzandaan- i Maa). Nukta halisi, nyeti na za uangalifu kwa malezi ya watoto ni nyingi sana kiasi kwamba uchunguzi wake wa kina huhitaji kuandika vitabu vikubwa. Wanachuoni na wanasaikolojia wamefanya utafiti katika suala hili na wameweka matokeo yake mbele za watu. Jambo muhimu katika suala la malezi ya watoto ambalo linakubaliwa takriban kwa pamoja na wanachuoni wa nchi za Mashariki na Magharibi, ni kwamba kama wazazi wanapenda watoto wao wapate malezi sawa sawa, lazima watumie mafunzo ya dini na lazima wawazoeshe watoto wao na mafunzo hayo wakati wa mwanzo kabisa wa maisha yao. Raymond Beech anasema: “Hapana shaka familia ina wajibu zaidi wa kutoa maelekezo ya maadili na dini kwa mtoto kuliko kwa kitu kingine chochote kwa sababu kumfundisha mtoto bila kuzingatia maadili humfanya mtoto kuwa mhalifu mjanja. Kwa upande mwingine akili ya mwanadamu haielekei kwenye maadili bila dini na kama mtu anataka kujifunza kanuni za maadili bila dini ni kama kutengeneza mwili unaoishi ambao hauna roho. Wazo la kwanza ambalo hufanywa kuhusu Mungu kwenye akili ya mtoto chanzo chake ni kutokana na uhusiano na wazazi wake na halikadhalika 16

11:26 AM

Page 16


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio ufahamu wake wa kwanza na baba yake katika suala la utii, ukarimu na uaminifu unategemea juu ya tabia ya familia. Ni muhimu kwamba masuala yote haya yanakamilishwa katika kipindi cha mwanzo cha utoto, kwa sababu wakati wa kipindi hiki akili ya mtoto ni yenye kuhisi zaidi kuhifadhi kuliko atakachojifunza baadae katika sehemu ya maisha yake. “Sio tu kwamba wazazi wana muda na fursa ya kufanya mazingatio ya mtoto wao kwenye mwongozo wa kiroho na kielimu, bali ni wenye wajibu kuwazoesha watoto wao na Mungu pamoja na wema Wake wote na uwezo pamoja na makusudio Yake yote na ukubwa Wake. Kwa ajili ya madhumuni hayo wanaweza kutumia mafundisho ya dini na mambo ya kawaida. “Wazazi na wafundishaji maadili lazima wakumbuke kwamba ili kumlea mtoto, dini ndio ushawishi wao wa nguvu sana na uwezo. Imani ni kama mwenge ambao huangaza njia yenye giza nene kabisa. Huchochea na kuamsha dhamiri na wakati wowote kunapokuwa na mtu aliyepotoka, kwa urahisi kabisa imani humuongoza kwenye njia iliyonyooka”. (Maa wa Farzandaan-i Maa). Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: “Allah awaokoe watoto wa wakati wa baadae kutokana na tabia mbaya za baba zao.” Watu wakamuuliza “Ewe Mtume wa Allah! Kutokana na tabia za baba zao ambao ni washirikina?” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akajibu: “Hapana, bali kutokana na tabia mbaya za baba zao Waislamu ambao hawafundishi watoto wao majukumu ya dini na kama watoto wakielekea kwenye kujifundisha masuala ya dini huwakataza kufanya hivyo na huridhika nao kuhusiana na mambo ya kidunia yasiyokuwa na maana. Nachukizwa nao, vilevile nao wanachukizwa na mimi.” (Mustadrakul Wasa’il). Abu Abdir Rahmani Salmi, ambaye alikuwa akisoma Qur’ani Tukufu mjini Madina, aliwafundisha watoto wa Imamu Husein (a.s.) Sura alHamd, Sura ya kwanza ya Qur’ani Tukufu. Wakati mtoto aliposoma Sura ile mbele ya baba yake, Mtukufu Imam alimpa mwalimu tuzo na zawadi 17

11:26 AM

Page 17


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio zenye thamani. Baadhi ya watu walikosoa kitendo hicho cha Imamu cha kutoa zawadi kubwa kama ile kwa mwalimu wa mtoto wake kwa kumfundisha Sura moja tu ya Qur’ani Tukufu. Katika kujibu upinzani uliotolewa na watu, Mtukufu Imam alisema sentensi ambayo ilikuwa ni ghali zaidi kuliko zawadi zote zilizokwishatajwa. Alisema: “Kuna ulinganisho gani unaoweza kuwepo kati ya tuzo ambayo nimempa mwalimu wa watoto wangu dhidi ya ufundishaji wake wa Qur’ani - Zawadi ambayo amempa mtoto wangu?” Katika majibu yake Mtukufu Imam ameiita tunu aliyoitoa yeye ‘tuzo’ na sio ‘zawadi’, na kuhusiana na kitendo cha mwalimu ameipa jina la ‘zawadi ya ukarimu na aliongeza kwamba hakuwezi kuwa na ulinganisho kati ya vitu viwili hivyo. Kwa kutoa heshima nyingi kama hizo kwa mwalimu, Mtukufu Imam alitoa somo kwa watu kwamba Waislamu lazima washughulikie maelekezo ya dini ya watoto wao na kuwa na shauku kwayo na kulichukulia suala hili kuwa la muhumi ili kwamba watoto waweze kupata uzoefu wa majukumu ya dini yao kuanzia mwanzo kabisa wa utoto wao. Imamu Ja’far Sadiq (a.s.) anasema: “Wafanyeni watoto wenu wajifundishe hadithi za Kiislamu na amri za dini mapema iwezekanavyo kabla wapinzani hawajakutangulieni na kujaza mioyo ya watoto wenu maneno ya upotofu”. (al-Kafi) Wakati alipokuwa anafafanua juu ya aya tukufu: “Wabashirie waumini habari njema (Surah al-Baqarah, 2:97) Imamu Hasan Askari (a.s), Imamu wa kumi na moja, anasema: “Siku ya Hukumu Allah atatoa zawadi kubwa kwa wazazi wa mtoto. Watasema ‘Ewe Mola wetu! Ni kwa ajili ya nini baraka na neema hii inatolewa kwetu? Matendo yetu hayakustahili zawadi kama hii!’ Itasemwa katika kuwajibu: ‘Baraka zote hizi ni kwa 18

11:26 AM

Page 18


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio sababu kwamba mumemfundisha mtoto wenu Qur’ani Tukufu na kumuelemisha kwa amri za Uislamu na kumuogoza kwenye kuwa mapenzi juu ya Mtukufu Mtume wa Uislamu, Muhammad (s.a.w.w.) na mrithi wake Imamu Ali (a.s) na kumpa maelekezo kuhusu mafundisho yao yenye mwanga.’” (Mustadrakul Wasa’il, Jz. 1, uk. 290). Kilichoelezwa hapo juu ni mfano mfupi sana wa mafundisho ya Uislamu kuhusu malezi ya watoto, na historia inaonesha kwamba utekelezaji wa mafundisho haya katika karne ya kwanza na ya pili Hijiria, yalikuwa yenye kujenga sana katika kuzalisha miongoni mwa watoto wa Kiislamu, wanaume na wanawake ambao walikuwa watu mashuhuri na wakarimu, wasomi na wenye uwezo na mashujaa na watu wasafi ambao wamewapita wengine wote katika nemsi na ubora wa mwanadamu. Na wanawake ambao wana adabu nzuri na wasafi wa tabia. Katika mwanga wa mafundisho haya haswa na kwa kutekeleza maelekezo haya muhimu kabisa, jamii ya Kiislamu ikawa mbele sana, iliyostaarabika na kuendelea kati ya jamii zote za wanadamu na ikawa, kwa karne nyingi sana, mshika mwenge wa nuru ya elimu na ustaarabu ulimwenguni pote. Kuanzia siku mfumo wa Kiislamu ulipopatwa na rangi ya umagharibi, na tabia za ovyo na mbovu za wageni zikafanywa kama mtindo kwa ajili ya Waislamu wasio makini na wenye tabia mbaya, matatizo makubwa na shida zikaanza katika vipengele vyote vya maisha yao. Siku hizi Waislamu wengi hawayajui mafundisho yao muhimu na yenye maana ya dini ambayo ndio yenye kudhamini ustawi na ufanisi wao. Lengo la kuchapisha khutba hizi ni kwamba uhalisia wa Uislamu lazima uwekwe wazi kwenye akili za watu bila mapambo yoyote na hivyo hatua zaweza kuchukuliwa kwenye ufahamu wa maelekezo ya dini.

19

11:26 AM

Page 19


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Inategemewa kamba kwa kuzingatia na kutekeleza mafundisho ya Kiislamu, Waislamu watageuka kuelekea kwenye njia sahihi na kufanya marekebisho juu ya hali ya kurudi kwao nyuma na kuanguka hadhi yao.

MKOPO MZURI Uislamu huchukulia miliki ya mtu binafsi kuwa halali na humtambua kila mtu ambaye anamiliki mali kwa uhalali kuwa ni mwenye mali hiyo. Wakati huohuo imeweka sheria maalumu ili kuzuia ulimbikizaji wa mtaji mikononi mwa baadhi ya watu ili kwamba kwa kuzitekeleza hizo, umma wa Kiislamu katika wakati wowote usiweze kutumbukia na kuhusika katika maovu ya mtu binafsi au ya wengi yatokanayo na ulimbikizaji kama huo kama ilivyo kwenye mfumo wa kisasa wa kibepari. Mbali na majukumu ya halali na ya wajibu ambayo yamekabidhiwa Waislamu matajiri kuhusiana na ulipaji wa sehemu ya pato lao kwa ajili ya ustawi wa tabaka la masikini, vilevile wametakiwa kufanya idadi kadhaa ya majukumu ya pamoja na kutokana na mtazamo wa kimaadili na dhamiri wameahidiwa kama malipo mbadala kwayo, malipo katika ulimwengu huu na halikadhalika katika Akhera. Moja ya wajibu ulioelelekezwa kwa ajili ya watu matajiri ambao kwamba Uislamu umeweka msisitizo ni kutoa mkopo kwa wenye haja, ambao umepewa jina la ‘qarzul hasan’ (yaani, pesa inayotolewa bila riba na kulipwa kwa wasaa wa mkopaji). Katika suala la mikopo kama hiyo kwa kuchukua kitu chochote kwa njia ya faida zaidi na juu zaidi ya kiasi cha rasilimali hairuhusiwi na riba imetangazwa kuwa ni haramu. Aina hii ya mkopo ambao unaweza kupewa jina ‘Mkopo wa Kiislamu’ una mwelekeo wa huduma halisi ya jamii na ni katika wakati huohuo 20

11:26 AM

Page 20


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio huchukuliwa kama wajibu wa kidini - kiasi kwamba katika hadithi za Kiislamu mikopo kama hiyo imetangazwa kuwa aula kuliko utoaji wa sadaka. Hii ni kwa sababu inawezekana kwamba sadaka ikatolewa kwa mtu ambaye kwa hakika hana shida nayo, lakini mkopo kwa kawaida hutolewa kwa mtu ambaye kwa hakika huuhitaji, na mtu anayejihusisha katika mkopo ni yule tu ambaye huhitaji pesa kwa ajili ya madhumuni muhimu ya haraka. (Safinatul Bihar, Jz. 2, uk. 424). Sio hilo tu kwamba mkopo kama huu hauna madhara kwa jamii na hauharibu utaratibu mzuri wa familia kama ulaji riba, bali una msaada sana kwa kutatua matatizo ya kifedha ya watu na hutekeleza wajibu muhimu sana katika kuimarisha uhusiano wao na kutengeneza urafiki kati yao. Uislamu umeweka umuhimu mkubwa kwa ajili ya msaada wa aina hii ambao wakati ambapo unaboresha hali ya watu, ni tofauti kabisa na kusaidia omba omba. Umewahimiza Waislamu kuchukua hatua kama hizo na kwazo kuihudumia jamii na kusaidia waumini. Imamu Ja’far (a.s.) anasema: “Kila Mwislamu ambaye hutekeleza haja ya ndugu yake katika imani hutangazwa na Allah hivi: Malipo yako yapo kwangu Mimi na sitaki malipo kwa ajili yako wewe yaliyo madogo kuliko Pepo.” (Thawabul A‘mal) Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: "Allah ataondolea mbali wasiwasi na huzuni, katika dunia zote, kwa mtu ambaye kwamba hushughulikia matitizo ya ndugu yake Mwislamu mpaka yanatatuliwa." Ibn Abbas anasema: "Imamu Hasan alikuwa anafanya itikafu ndani ya Masjidul Haram na alikuwa akifanya tawaf ya Ka'bah tukufu. Wakati ule ule mu'umin mmoja alimfutata na akasema: 'Ewe mtoto wa Mtume wa Allah! Nadaiwa kiasi fulani cha pesa na fulani na fulani. Tafadhali kama inawezakana unilipie deni langu.' Mtukufu Imam akasema: 'Nasikitika kwa wakati huu sina kiasi hicho cha fedha'. Yule mtu akasema: 'Basi tafadhali muombe anipe muda kwani amenitishia kwamba atanitupa gerezani kama 21

11:26 AM

Page 21


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio nitashindwa kulipa mkopo huo.' Mtukufu Imam alikatiza tawaf yake na alifuatana na mtu yule kwa ajili ya kumuona yule mdai na akamuomba ampe mdaiwa muda. Ibn Abbas anasema: 'Nilisema: Ewe mtoto wa Mtume wa Allah! Umesahau kwamba umesema uliamua kufanya itikaf msikitini?' (kwa sababu mtu anayefanya itikaf hapaswi kutoka msikitini kabla ya muda uliolekezwa haujaisha). Imamu akasema: "Sijasahau kitu hicho. Hata hivyo, nilisikia kutoka kwa baba yangu kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: "Yoyote ambaye huitekeleza shida ya ndugu yake mu'umin ni kama mtu ambaye amemuabudu Allah na akabakia macho wakati wa usiku kwa miaka mingi." (Safinatul Bihar, Jz. 1) Imamu Muhammad Baqir (a.s.) anasema: "Kama mtu atamkopesha mtu muhitaji pesa na akampa muda (wa kulipa) mpaka hali yake kifedha itakapokuwa nzuri, mali yake hiyo itakuwa sawa na zaka na malaika humuombea na kumtakia baraka mpaka siku atakapolipwa deni hilo." (Man La Yahdhuhurul-Faqih, uk. 361) Imamu Ja'far Sadiq (a.s.) anasema: "Hili neno mashuhuri - ma'ruuf (matendo mema) ambayo hutokea kwenye aya tukufu ndani yake lina maana kutoa mkopo kwa watu. Allah anasema: "Hakuna kheri katika mengi ya wanayo shauriana kwa siri, isipokuwa kwa yule anayeamrisha kutoa sadaka, au kutenda mema, au kupatanisha baina ya watu. Na mwenye kufanya hayo kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu, basi tutakuja mpa ujira mkubwa". (an-Nisa; 4:114; Tazama katika Man La Yahdhuhurul Faqih, uk. 361.) Imamu Sadiq anaendelea kusema: "Wakati mtu anampa mtu mkopo na akaweka muda wa kulipa deni hilo lakini mkopaji akashindwa kulipa katika muda huo na kama muda wa kukawiza unaruhusiwa na mkopeshaji Allah atamfidia kwa malipo ya sadaka kwa kila siku iliyozidishwa." (Thawabul A'mal, uk. 76). 22

11:26 AM

Page 22


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: "Kama namkopesha ndugu yangu katika imani mara mbili dirham 1000 kutoka kwenye mali yangu hukiona kitendo hicho kuwa ni bora zaidi kuliko kutumia kiasi kama hicho kwenye tukio moja kwa ajili ya Allah." (Tahdhib, Jz. 2, uk. 61). Maelekezo haya yenye mkazo yametolewa pamoja na lengo hili katika kuzingatia kwamba Waislamu wangetatua matatizo ya ndugu zao katika imani kwa njia ya mali zao na kutoa njia za ustawi na ufanisi wa maisha yao bila ya kutamani pato la kidunia na bila ya kujihusisha na ulaji riba.

Ulaji Riba Umekatazwa: Mtu ambaye hustahiki mema haya ya Matukufu na malipo ni yule tu ambaye lengo lake la kutoa mkopo si kwa ajili ya kupata faida, bali anayefanya kazi hii kwa ajili ya ustawi wa jamii na kutaka radhi ya Allah. Kama faida inakadiriwa na kupatikana juu ya mkopo, unakoma kuwa mkopo mzuri na kuangukia chini ya sifa ya ulaji riba, ambao huchukuliwa na Uislamu kuwa moja ya madhambi makubwa bali haswa moja ya madhambi makubwa kupindukia. Kuhusiana na tafsiri ya aya za Sura al-Baqarah, Allama Tabatabai anasema: "Katika aya hizi Allah amekuwa mkali kuhusiana na riba kwa kiasi ambacho hajakuwa mkali kuhusiana na tawi lolote la imani, isipokuwa uhusiano na maadui wa Uislamu. Ingawa lugha iliyotumika kwenye dhambi kubwa nyingine kama zinaa, ulevi wa pombe, kamari na hata kuuwa zimetajwa ni za kuchukiza sana, bado sio za kuchikiza kama zile zinazohusiana na laana hizi mbili. Ukali huu umetokana na ukweli kwamba ambapo dhambi nyingine haziathiri zaidi ya mtu mmoja au watu wachache lakini uovu wa athari wa dhambi hizi mbili huangamiza misingi ya dini, huharibu taasisi za jamii na kuidhulumu asili ya mwanadamu.

23

11:26 AM

Page 23


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio "Mwenendo wa historia umethibitisha usahihi wa mtazamo wa Uislamu kuhusiana na hatari zitokanazo na laana hizi mbili, kwa sababu uhusiano na maadui wa Uislamu na kuwaelekea wao kuliwavuta Waislamu kwenye hatari kama hii ya mporomoko kwamba mema yote yaliondoka miongoni mwao na hali zao zikawa kama hivyo kiasi kwamba walikoma kuwa wamiliki wa mali zao wenyewe, maisha na heshima na wakaanza kufanya harakati kati ya maisha na kifo. Ulaji riba na ulanguzi mkubwa vilevile vikawa sababu ya ukiritimba wa mali na mgawanyiko wa watu katika makundi mawili, yaani matajiri na masikini. Hatimaye vita vya dunia vikatokea na machafuko yakawa matokeo ambayo yaliporomosha chini milima, yalitetemesha ardhi na yakatishia ubinadamu kwa maangamizo. Na hatimaye nini kilitokea kinajulikana vyema." (al-Mizan, J. 2). Uislamu umefanya juhudi ya kuanzisha moyo wa ushirikiano, kuaminiana, kusaidiana kwa wote na huruma kati ya Waislamu katika namna nzuri iwezekanayo. Riba ni aina ya biashara ya kubadilishana ambayo hudhoofisha mshikamano huu na hisia za upendo, hupanda mbegu za uadui mkubwa na chuki katika nyoyo na kuchafua hali ya jamii pamoja hisia za ulipizaji kisasi. Mfumo wa ulaji riba umetegemea juu ya kanuni hii kwamba katika hali zote, yaani iwapo mkopaji akipata faida au akipata hasara kwa kuufanyia kazi mkopo huo, mkopeshaji lazima apate faida kwa kiasi kikubwa. Kamwe hahusiki na hasara, kama itakuwepo yoyote ambayo mkopaji atakuwa ameipata. Hata kama mkopaji masikini akiishiwa au akifilisika lazima alipe faida yote bila msamaha, ingawa hali hii ya kusikitisha haina uwiano na kiwango cha usawa, haki na maadili. Haki huhitaji kwamba kama mlariba atachukuwa faida kutoka kwa mkopaji kwa faida anayoipata, lazima vilevile ashiriki katika hasara anayoipata mkopaji. Nafasi hii kwa dhahiri sio ya haki kwamba lazima wakati wote awe anatafuta faida na hana lolote la kufanya kwa hasara iliyopatikana kwa mshirika mwingine. Shughuli kama hiyo sio ya haki haisimami juu ya kitu 24

11:26 AM

Page 24


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio chochote zaidi ya mwelekeo wa asilimia ya pato binafsi. Mkopaji anajua kwamba mlariba amefanya pesa kuwa ni njia ya unyonyaji wa tabaka la watu masikini ambalo halimiliki mtaji wowote. Ingawa anakubali biashara hiyo chini ya ulazimishaji wa mazingira bado hasahau dhulma na asili ya unyama wa mlariba. Katika mfumo wa ulaji riba kwa kawaida hufikia hatua wakati wakopaji huhisi maumivu makali ya makucha ya mlariba kwenye makoo yao. Hali gani itaibuka wakati mkopaji akiwa hana uwezo wa kupata faida yoyote kutoka kwenye mkopo bali faida hujilimbikiza katika hali ambayo inakuwa mara nyingi kama kiasi kile cha msingi na uhai na maisha ya mkopaji masikini yenyewe yanakuwa hatarini? Katika hali kama hiyo nini kitategemewa kutoka kwa mkopaji isipokuwa kwamba lazima atamlaani mlariba yule na kuwa na kiu ya damu yake! Ni katika hali ngumu kama hizo kwamba idadi ya jinai za kusikitisha hufanyika. Mara kwa mara imeonekana kwamba wakopaji ambao wanakuwa hawajiwezi kabisa huwauwa wakopeshaji katika njia ya kikatili sana na kuacha familia zao katika hali ya huzuni mno na bila msaada. Wengi wao wanakuwa wamechoka mno na maisha yao kiasi kwamba hawaoni ufumbuzi mwingine isipokuwa kukatisha maisha yao na kujiua. Mahakama za sheria zimeona matukio mengi ya umwagaji damu wa kadhia hizi za kujinyonga na vilevile katika magazeti ya kila siku mtu ataona matukio mengi ya mauwaji na ya kujiua ambayo yanasababishwa na riba. Hebu natumuangalie mlariba katika mtazamo wa kiroho na uadilifu. Ni mtu ambaye ameupa kwaheri uadilifu. Anafikiria tu faida yake, na yuko tayari kwa ajili hii kutoa kila aina ya shinikizo kwa mkopaji. Hana hisia za ubinadamu. Ukatili wa aina maalumu huamka kwenye akili za watu hawa. Huangalia kila kitu kwa mtazamo wa pato la kidunia. Hali yao ya kiroho na haiba ya ubinadamu huweza kuelezewa kwa mukhtasari katika upataji wa faida. Mapenzi haya ya faida hayawaruhusu kuelewa matokeo ya hatari ya riba kwa kiasi ambavyo mkopaji anahusika. Uwezo wao wa ukadiriaji 25

11:26 AM

Page 25


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio wa maadili umetoweka. Hivyo Qur’ani Tukufu inafafanua hali ya wala riba:

"Wale wanaokula riba, hatasimama ila kama anavyosimama yule ambaye shetani humpoozesha kwa kumshika…" (2:275) Riba haiathiri uadilifu wa mla riba tu bali kwa upande mwingine inasababisha maovu mengi ya kijamii, maadili, uchumi na maovu mengine, na ni kwa sababu hii haswa kwamba Uislamu huichukulia kama uasi dhidi ya Allah. Qur’ani Tukufu inasema:

"Enyi mlioamini! Mcheni Allah na acheni yaliyobakia katika riba ikiwa ni wenye kuamini. Msipofanya (hivyo) basi fahamuni mtakuwa na vita kutoka kwa Allah na Mtume wake, na kama mkitubu, basi mtapata rasilimali zenu, msidhulumu wala msidhulumiwe. Na kama (mdeni) ni mkata, basi (mdai) angoje mpaka wakati wa uweza. Na mtakapotoa sadaka, ni heri yenu, ikiwa mnajua." (2:278-280) Qur’ani inaendelea kusema: “Enyi mlioamini! Msiliane mali zenu baina yenu kwa batili ila itakapokuwa ni (mali ya) biashara kwa kuridhiana kati yenu…"

26

11:26 AM

Page 26


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Imamu Muhammad Baqir (a.s.) anasema: "Kilichomaanishwa na neno batil (dhulma) katika aya hii ni riba, kamari, kumlaghai mnunuaji na kufanya dhulma." (Tafsir Majma 'ul Bayana). Qur’ani Tukufu imewalaani Mayahudi kwa kutenda dhambi, kuchukua faida juu ya pesa na kuvunja haki za watu wengine katika suala la mali. Inasema:

“Basi kwa dhulma ya mayahudi tuliwaharamishia vitu vizuri walivyohalalishiwa, na kwa sababu ya kuzuilia kwao (watu) njia ya Allah kwa wingi. Na kwa kuchukua kwao riba na hali wamekatazwa, na kula kwao mali ya watu kwa batili, na tumewaandalia makafiri katika wao adhabu iumizayo. (an-Nisa; 4:161) Wafasiri wanasema: "Mayahudi wakati walipokuwa wakikaimu kama majaji, walichukua rushwa na waliandika vitabu wenyewe na kuwaambia watu kwamba vimetoka kwa Allah na kukusanya pesa kwavyo kwa ajili hiyo."

Kutoa zawadi kwa mkopeshaji Ni muhimu kuweka wazi kwamba faida ambayo ni haramu ina kitu kile ambacho wakati ule wa kutoa mkopo mkopeshaji anaweza kuweka masharti kwamba mkopaji atalipa kitu juu na zaidi ya kiasi halisi cha mkopo. Hata hivyo, kama mkopeshaji atatoa pesa kama 'mkopo mzuri' bila ya masharti ya kulipa zaidi na mkapoji wakati wa kulipa, akatoa kitu zaidi ya kiasi halisi cha mkopo sio tu kwamba kitendo hicho sio haramu bali ni kitendo halali kinachopendekezwa.

27

11:26 AM

Page 27


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Imamu Ja'far Sadiq (a.s.) anasema: "Ulanguzi katika mkopo ni wa aina mbili, mmojawapo ni halali na mwingine ni haramu. Aina ambayo ni halali ni ile ambayo mtu anaweza kutoa pesa kama mkopo kwa matumaini kwamba atapata faida, lakini bila masharti au kuweka masharti. Kama katika hali hiyo, mkopaji anampa kitu (zaidi ya kiasi halisi cha mkopo) ni halali kwake lakini hastahiki kwenye malipo yoyote ya Mungu. Na faida iliyo haramu ni ile ambayo mkopeshaji anaweza kuweka masharti kwamba mkopaji atamlipa kitu zadi ya kiasi halisi cha mkopo. Kitendo hiki sio halali na ni haramu. Imamu Muhammad Baqir (a.s.) aliulizwa: "Mtu mmoja ametoa mkopo kwa mtu mwingine na mkopaji akapeleka zawadi kwa mkopeshaji. Je, inaruhusiwa au la?" Mtukufu Imam akajibu: "Inaruhusiwa na hakuna madhara katika kuichukua." (Mustadrak, Jz. 2, uk. 492) Hadithi za Kiislamu juu ya somo hili ni nyingi mno na zinasomwa na wote na kuchukuliwa pamoja kwamba inawezekana kuweka mfumo sahihi wa benki kwa mujibu ambao kwamba haki za wale ambao hutoa mitaji zinakuwa salama na wakopaji halikadhalika lazima wasilazimike kukabiliana na huzuni na shida kwa matokeo ya ulipaji wa faida kubwa kupita kiasi. Ni dhahiri kwamba mishahara na gharama za watumishi na uandaaji wa bili na hati nyingine zinazofanana na hizo zitakuwa hazihusiki na 'faida'. Kwa maelezo zaidi juu ya somo hili rejea vitabu cha Iqtisaaduna (Uchumi wetu) na al-Bank al-laa Rabawi Fil Islam (Banki Isiyo na Riba katika Uislam) vilivyoandikwa na Shahid, Sayyid Muhammad Baqir Sadr na halikadhalika vitabu vingine vilivyoandikwa na wanachuoni wa Kiislamu. Mbali na mapendekezo yaliyotolewa na Uislamu kuhusu utoaji wa 'mkopo mzuri' na kujiepusha na riba, wakopaji nao vilevile wameambiwa kujaribu kwa uwezo wao wote kulipa madeni yao. 28

11:26 AM

Page 28


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Kwa mujibu wa sheria za Kiislamu mkopo ni wa aina mbili: Aina ya kwanza ya mkopo ni ile ambayo kwa ajili ya kuulipa umewekewa muda. Katika hali hiyo mkopeshaji hana haki ya kudai kulipwa deni hilo kabla ya wakati uliowekwa kupita isipokuwa katika tukio la kifo cha mkopaji anakuwa na haki ya kudai na kulipwa kiasi cha mkopo huo kabla ya mirathi haijagawanywa. Aina ya pili ya mkopo ni ile ambayo kwa ajili ya kuulipa kwake hakuna muda uliowekwa. Katika hali hiyo ni wajibu juu ya mkopaji kulipa mkopo mara moja wakati mkopeshaji anapotaka hivyo, hata kama ni kuuza baadhi ya mali yake ambayo si muhimu kwa maisha na kama mzembe katika kulipa atakuwa na hatia ya dhambi. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: "Kama mtu ni mzembe katika kulipa madeni yake licha ya kuwa katika hali ya kuweza kulipa, dhambi mara kumi huandikwa kwenye kitabu chake cha matendo kwa kila siku moja ya muda wa kuchelewesha." (Wasa 'ilush Shi'ah, Sura juu ya madeni). Imamu Ja'far Sadiq (a.s.) anasema: "Mtu ambaye anachukua mkopo na hakusudii kulipa mkopo huo ni kama mwizi." (Furu'ul Kafi) Imamu Ja'far Sadiq (a.s.) anaendelea kusema: "Mtu ambaye humuendea mtu mwingine kwa ajili ya mkopo na akakusudia kutokulipa ni mwizi katili". (Man La Yahdhuruhul Faqih, Jz. 2, uk. 60) Imamu Muhammad Baqir (a.s.) anasema: "Shahidi katika njia ya Allah hurekebisha kila dhambi isipokuwa kwa madeni ya watu, ambayo hayawezi kufidiwa na chochote isipokuwa na mkopaji mwenyewe au kabidhi wasii au mlezi alilipe au mkopeshaji alisamehe". (Wasa'ilush Shi'ah, Jz. 8, uk. 83). Mu'awiya bin Wahab anasema: "Nilimuambia Imamu Ja'far Sadiq (a.s.): Nilisikia kwamba mtu mmoja kutoka miongoni mwa Ansar alifariki akiwa anadaiwa dinari mbili na mtu fulani. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikataa kumfanyia ibada za mazishi na akawaambiwa ndugu zake kumfanyia wao 29

11:26 AM

Page 29


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio wenyewe ibada za mazishi. Hata hivyo, walichukua jukumu la kulipa deni hilo na ilikuwa baada ya hilo ndipo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamfanyia ibada zake za mazishi." Imamu Ja'far akasema: "Hadithi hii ni sahihi na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alichukua hatua hii ili kwamba watu wapaswe kuheshimu haki za wengine na wasije wakachukulia madeni yao kuwa ni kitu chepesi bali lazima walipe madeni hayo." Imamu Muhammad Baqir (a.s.) anasema: "Tone moja la damu ya shahidi ambalo hudondoka ardhini ni utakaso kwa ajili ya dhambi zake, isipokuwa utakaso kwa ajili ya madeni yake ni kulipa madeni hayo na hakuna njia nyingine. (Wasa'ilush-Shi'ah, Jz. 8, uk. 85). Abu Thumama anaripoti kwamba alimuambia Imamu Muhammad Taqi: "Nimeamua kuweka makazi Madina na Makka. Hata hivyo, nadaiwa na watu fulani. Nini maoni yako katika suala hili? Mtukufu Imam akasema: 'Rudi kwenye mji wako wa nyumbani na ubakie hapo mpaka utakapolipa madeni na lazima ujaribu kujihakikishia kwamba hudaiwi na mtu yeyote katika siku utakayokutana na Mola wako (Siku ya Hukumu), kwa sababu mu’mini wa kweli hawezi kuwa mdanganyifu.'" ('Ilalush Sharaaya, uk. 178) Katika hadithi hii Imamu wa tisa amechukulia uzembe katika suala la ulipaji wa deni na kushindwa kulipa haki za watu kama udanganyifu, kama tu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alivyouita 'ukandamizaji.' Imamu Ali (a.s.) anasema: "Nilimsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema kwamba Mwislamu ambaye anaweza kulipa deni lake na akapuuza kufanya hivyo anatenda ukandamizaji juu ya Waislamu." (al-Kafi) Katika hadithi hizi mbili kushindwa kulipa haki za watu kumeelezewa kuwa ni udanganyifu na ukandamizaji juu ya Waislamu na huu ni ukweli 30

11:26 AM

Page 30


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio usiokanushika kwa sababu katika jamii hali ya uchumi ya watu ni ya kutegemeana na mwingine kama shanga za kidani cha shingo. Kama vile mtu mmoja anadaiwa na mtu mwingine inawezekana pia kwamba mkopeshaji anadaiwa na mtu mwingine wa tatu na yeye kwa upande wake inawezekana anadiwa na mtu mwingine. Kama mmoja wa watu hawa si mkweli na anashindwa kulipa deni lake, inawezekana kwamba mtu wa pili vilevile akawa hayuko katika hali ya kuweza kulipa deni kwa mtu wa tatu na kadhalika na kadhalika. Kwa hiyo, kwa sababu ya kutokuwa na uaminifu kwa mtu mmoja, kundi la Waislamu linakuwa katika shida. Aidha, jamii ya Kiislamu imeasisiwa katika kuaminiana na heshima kwa haki za wenyewe kwa wenyewe na kama mtu yeyote anaposaliti imani ya raia kwa kitendo cha woga, yaani kwa kupuuza haki za watu, ana hatia ya udanganyifu na dhulma iliyofanyiwa jamii ya Uislamu. Uislamu unachukulia uvunjaji wa haki za watu wengine kuwa ni dhulma na dhambi isiyo sameheka, na kukubaliwa toba kwa dhambi hii ni kulipa haki za watu. Imamu Muhammad Baqir (a.s.) anasema: "Haki ni ya aina tatu: (i) Dhulma ambayo haiwezi kusamehewa kwa sababu yoyote ile, na hiyo ni kumfanya mtu yeyote kuwa mshirika wa Allah. (ii) Dhulma ambayo inaweza kusamehewa inakuwa na dhambi ambazo mtu ametenda dhidi yake mwenyewe na suala hilo liko kati yake na Allah tu. (iii) Dhulma ambayo haiwezi kusamehewa na Allah inakuwa na haki za watu na madeni anayodaiwa na watu wanaohusika". (Khisal Saduq, Jz. 1, uk. 134) Ili kulinda haki za watu Uislamu unaeleza kwamba kama marehemu ana deni, madeni yatakuwa ya kwanza kulipwa kutoka kwenye mali yake baada ya kulipia gharama zinazohusiana na sanda yake na mazishi.

31

11:26 AM

Page 31


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: "Kama mtu anakufa, kwanza gharama za mazishi yake lazima zilipwe kutoka kwenye mali yake na kisha madeni yake lazima yalipwe. Baada ya hapo wosia wake, kama upo wowote lazima utekelezwe na kama kuna kitu chochote kilichobaki kitagawiwa miongoni mwa warithi wake." (Mustadrakul-Wasa'il, Jz. 2, uk. 491) Wanachuoni wa Shi'ah (Mujtahid) kwa pamoja wanakubaliana juu ya nukta hii kwamba kama mkopaji yuko katika hali ya kulipa deni lake na mkopeshaji naye akawa anahitaji alipwe, mkopaji hastahili kusali Sala zake wakati muda unatosha kufanya hivyo mpaka kwanza alipe deni lake kisha ndipo asali Sala zake. Kuhusiana na hili uwamuzi wa wanachuoni unatolewa hapa chini: "Kama mtu anasali Sala zake ndani ya wakati wa Sala na kisha mkopeshaji akataka alipwe deni, lazima alipe wakati huo wa Sala, kama anaweza kulipa katika hali hiyo. Hata hivyo, kama haiwezikani kulipa bila kuvunja Sala, basi atavunja Sala yake, atalipa deni kisha atasali Sala zake". (Tawzihul Masa 'il Muhashshi, makala - 1170) "Kama mkopaji yuko katika hali ya kuweza kulipa deni lake na mkopeshaji anataka alipwe, ni haramu kwa mkopaji kusali Sala wakati wa mwanzo wa Sala kabla ya kulipa deni hilo." (Shaykh Bha'i, Jami 'Abbasi, uk. 144) "Kama ulipaji wa deni uliotakiwa na mkopeshaji hutengemea juu ya kuvunja Sala, ni wajibu kwa mkopaji kuvunja Sala kipindi cha wakati wa Sala ili alipe deni." (Urwatul Wuthqa, uk. 252).

Nyumba ya Mdaiwa Haipaswi Kuchukuliwa Ingawa Uislamu umeweka mapendekezo makali kuhusiana na haki za watu na kulipa madeni, na umeuchukulia uzembe katika suala la kulipa madeni kuwa ni dhulma, usaliti na dhambi, wakati huohuo umewataka 32

11:26 AM

Page 32


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio wakopeshaji kuwapa muda wakopaji wa kulipa na wasiwafanye kuwa katika wakati mgumu na huzuni. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: "Kama ambavyo hairuhusiwi kwa mkopaji wako kupuuza kulipa deni wakati yuko katika hali ya kuweza kulipa deni hilo, katika hali hiyo hiyo hairuhusiwi kwako wewe (mkopeshaji) kumuwekea shinikizo wakati unajua kwamba yuko kwenye mazingira ya shida." (Wasa'il-Shi'ah, Sura 25, Madeni) Kwa mujibu wa sheria za Kiislamu hairuhusiwi kwa mdai kuchukua haua yake yeye mwenyewe au kuuza nyumba ya kuishi ya mdaiwa na halikadhalika vitu muhumu vya maisha kama nguo, mazulia, vyombo vya nyumbani nk. Ili kulipia deni lake. Imamu Ja'far Sadiq (a.s.) anasema: "Nyumba ya kuishi haiwezi kuuzwa kwa ajili ya kulipia deni, kwa sababu ni lazima kwa kila mtu kuwa na sehemu ya kuishi." (Furu'ul-Kafi, Jz. 1, uk. 35) Muhammad bin Abi Umayr alikuwa muuza nguo na mfuasi muaminifu wa Imamu Ja'far Sadiq (a.s.). Kwa matokeo ya ukandamizaji wa Makhalifa wa Bani Abbas hali yake ya kifedha ikawa dhaifu sana na akapoteza mtaji wake wote na akabakia nyumbani tu. Mmoja wa jamaa zake alikuwa anamdai dirham 10,000. Alipoona hali mbaya ya Muhammad bin Umayr, aliuza nyumba yake ya kuishi na akaleta pesa zile kwake. Muhammad akamuuliza mtu yule: "Pesa hizi ni za nini?" Akajibu: "Ni pesa ile unayonidai". Muhammad akamuuliza: "Je, umepata kitu chochote kutoka katika mirathi?" Akajibu: "La". Muhammad akamuuliza: "Je, yuko mtu aliyekupa pesa hii kama zawadi?" Akajibu: "Hapana". Muhammad akamuuliza: "Je, unamiliki mali yoyote isiyohamishika ambayo umeiuza?" Akajibu: "Hapana. Si katika vitu hivyo, bali nilipoona hali yako nimeuza nyumba yangu na nimeleta pesa za mauzo yake ili kulipa deni langu". Muhammad akasema: "Ingawa nahitaji kila 33

11:26 AM

Page 33


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio dirham ya pesa hizi, sitachukua hata dirham moja, kwa sababu kiongozi wangu Imamu Ja'far Sadiq (a.s.) amesema: 'Usimfukuze mtu kwenye nyumba yake ili kulipa deni lako'. Chukua pesa zako na karudishe nyumba yako." (Wasa'ilush-Shi'ah, Jz. 2 uk. 622) Kwa yale yaliyoelezwa hapo juu tunatoa mahitimisho yafuatayo: * Uislamu unapinga kwa nguvu ulaji wa riba, hususan ikiwa ni kati ka kuwadhuru watu. * Mkopo mzuri ni huduma kubwa ya kijamii na kitendo cha thamani cha kidini sawa na kumuabudu Allah. * Riba hairuhusiwi katika hali yoyote na chini ya anuani yoyote na ni sawa na kuasi dhidi ya Allah. * Waislamu wako chini ya wajibati za kuheshimu haki za wengine na wasiwe wenye kupuuza kulipa mikopo. * Kama wakopeshaji wakijua kwamba wadaiwa wako kwenye hali ngumu kifedha, lazima wawape muda ili kwamba mazingira yao yawe mazuri. * Hairuhusiwi kuchukua nyumba ya kukaa na mahitaji ya maisha ya mkopaji katika kulipa deni. Mwisho tunawalingania ndugu zetu Waislamu kusoma mfumo wa uchumi wa Uislamu uliondikwa kwa ukamilifu kabisa juu ya somo hili ili kwamba wawe na uelewa zaidi juu ya ukarimu wa Uislamu na taratibu zake za kudumu zenye kujitegemea. Na wakati huo huo pamoja na kusoma mfumo wa uchumi wa Uislamu vilevile lazima wayatekeleze kwa vitendo ili kwamba baraka ya Allah, huduma yenye thamani inaletwa kwa jamii na hatua kwenda mbele inachukulia kuelekea kwenye ustawi wa katika ulimwengu huu na wa kesho Akhera. 34

11:26 AM

Page 34


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio

KAMPENI DHIDI YA MAOVU Nguvu nyingi zisizoonekana zimewekwa hivyo katika mwili wa mwanadamu kiasi kwamba kila moja inatekeleza wajibu mkubwa katika maisha ya mtu. Ingawa nyingi ya nguvu hizi bado hazijatambuliwa kikamilifu lakini athari zao zimegunduliwa kwa kiasi fulani na wanasaikolojia. Moyo wa haki, uaminifu, uadilifu, ubinadamu, hisani, huruma, upendo kwa ajili ya wema nk, vyote hivi vinakuwepo katika tabia ya mtu. Halikadhalika silka kama uchoyo, ubinafsi, tamaa ya ukubwa, kulipiza kisasi, mapenzi juu ya raha nk., vilevile hupatikana ndani yake. Nguvu hizi zilizofichika humvuta mtu kwenye uchamungu au kwenye maovu. Kama mbegu za sifa nzuri ambazo wamepewa wanadamu wote zinaruhusiwa kustawi sawasawa chini ya mazingira mazuri, zingezaa matunda na ambayo kwamba mwanadamu hupata ukamilifu unaotakikana, na kama silka za uovu na tabia mbaya zikiwa na nguvu na kutawala mambo ya maisha matokeo si chochote bali maovu na uharibifu. Mtu kwa asili yake hasa anataka kufaidi bila ya vikwazo vyovyote starehe za maisha ya kidunia lakini hali yenyewe ni kwamba anajiingiza katika starehe zisizo za halali ambazo huharibu matarajio ya ustawi wake na kumuweka katika matatizo.

Matendo yasiyo ya halali ambayo huitwa 'dhambi' kaika istilahi za dini bila shaka huleta matukio mabaya na hasara isiyorekebishika katika tabaka mbalimbali za maisha. Kwa mujibu wa viongozi wa Uislamu shida zote za watu binafsi na za 35

11:26 AM

Page 35


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio kijamii na mateso mengi yanayowapata watu ni matokeo ya dhambi zao na maadili mabaya. Qur’ani tukufu huchukulia uharibifu na kutoweka kwa mataifa mengi ya nyuma ambayo yaliishi katika ulimwengu huu kwa wakati fulani na ambayo si chochote isipokuwa majina yao sasa ndio yaliyobakia katika historia kuwa ni matokeo ya matendo yao maovu na dhambi na hivyo inasema: "Ni kama hali ya watu wa Firauni na wale waliokuwa kabla yao, walizikadhibisha aya za Mola wao, kwa hiyo tukawaangamiza…" (8:54) Vivyo hivyo Qur’ani huchukulia dhambi kuwa sababu ya kupotea kwa neema, na inasema: "Hayo ni kwa sababu Allah habadilishi kabisa neema aliyowaneemesha watu mpaka wabadilishe yaliyomo ndani ya nafsi zao…" (8:53) Imamu Muhammad Baqir (a.s.) anasema: "Allah ametangaza kwa uwazi kabisa kwamba wakati Akiweka neema juu ya mtu Haiondoi kutoka kwake isipokuwa afanye dhambi kwa matokeo ambayo kwamba anastahili kwamba neema ile yaweza kundolewa kutoka kwake." (al-Kafi, Jz. 2, uk. 209) Imamu Ja'far Sadiq (a.s.) anasema: "Hakika dhambi huwa ni sababu ya mtu kunyimwa mgao wake wa kila siku na kuwa katika ufukara. (al-Kafi, Jz. 2, uk. 208) Dr. Alexis Carrel, mwanafiziolojia mashuhuri anasema: "Haitakuwa busara kama tunapenda kusahau kuwepo kwa dhambi kwa sababu kama suala la kanuni, dhambi ina madhara. Kama tujuavyo, maisha huwaharibikia mapema au baadae wale ambao hutenda dhambi." "Dhambi inakuwa pamoja na kukandamiza kanuni za maisha kwa makusudi au bila kukusudia, na kanuni za maisha pia hazibatiliki kama kanuni ya mchanganyiko wa gesi au kuanguka kwa miili. Hata hivyo, kwa vile 36

11:26 AM

Page 36


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio adhabu ya dhambi inakuja baadae mtu bado hajatambua ubaya wa matokeo ya dhambi. Kila dhambi ni sababu ya kuonekana kwa machafuko ya kiogani, kiakili na ya kijamii yasiyorekebishika. Kama ambavyo haiwezekani kuondoa maradhi ya kimwili ya mlevi sugu kwa kutubia kwake au kasoro zilizorithiwa na mtoto katika njia hiyo hiyo, haiwezekani kuondoa athari zenye madhara za wivu, kuteta, chuki, na kusengenya. Punde au baadae dhambi hufikia kilele katika kuangamiza na hatima ya kifo cha muovu au kizazi chake au taifa. Kwa hiyo, mtu lazima atofautishe kwa usahihi kati ya mtu mbaya na mtu mzuri na lazima aelewe mpaka usioonekana umewekwa kati ya mema na mabaya katika nyanja ya ukweli. (Rah wa Rasm-i Zindagi) Imamu Ali (a.s.) huchukulia utendaji wa kila dhambi mpya kama sababu ya msiba mpya, na anasema: "Wakati watu wakitenda dhambi mpya ambayo hawajawahi kuitenda kabla, Allah huwafanya wapasike kwenye msiba mpya ambao hawajawahi kuupata kabla." (Al-Kafi, Jz. 2, uk. 211) Imamu Ali (a.s.) anasema: "Wallahi! Haijatokea kwamba taifa lingeweza kuishi katika ustawi, starehe na neema na kwamba stsrehe na neema zile zikaweza kuondolewa kutoka kwenye taifa lile isipokuwa kwa sababu ya dhambi zake ilizozitenda. Hii ni kwa sababu Allah kamwe hawadhulumu waja Wake." (Nahjul Balaghah) Katika Qur’ani watu wametakiwa kusafiri katika ardhi na kuchunguza hali ya umma zilizopita na kugundua na kuelewa ukweli wa kuanguka na kutoweka kwao ambako kulikuwa kwa sababu ya dhambi zao. Qur’ani Tukufu inasema:

37

11:26 AM

Page 37


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio

"Sema: Safirini katika ardhi na muone jinsi ulivyokuwa mwisho wa wale waovu." (27:69) Vile vile inasema:

“Je, hawakusafiri katika ardhi wakaona jinsi ilivyokuwa mwisho wa wale waliokuwa kabla yao? Wao walikuwa wenye nguvu zaidi na athari kuliko hao, lakini Mwenyezi Mungu aliwaadhibu kwa sababu ya makosa yao, wala hapakuwa na kuwalinda na Mwenyezi Mungu." (40:21) Historia hutuambia jinsi dhambi ilivyowafanya watu kuwa katika shida na kuwafanya waendelee kwenda kwenye ulimwengu wa giza. Tukio lifuatalo limesimuliwa katika A'laamun Naas: "Waziri wa Khalifa wa Banu Abbas, Mu'tasim, ambaye alifaidi fursa zote za maisha, alijenga kasri kubwa yenye ghorofa nyingi. Alizoea kukaa juu ya sakafu ya juu ya kasri na kuchungulia kwenye nyumba za watu kupitia madirishani na kutizama wanawake na wasichana wao. Siku moja macho yake yaliangukia kwa msichana mrembo na akampenda vibaya msichana yule. Alifanya uchunguzi kujua msichana yule ni nani, hatimaye alijua kwamba msichana yule alikuwa ni binti wa mfanyabiashara mmoja mjini pale. 38

11:26 AM

Page 38


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Aliomba amuoe msichana yule lakini wazazi wake walikataa matakwa yake. Alifanya juhudi kubwa kwa ajili hii na akawafanya watu watukufu na mashuhuri kumuombea kwa niaba yake juu ya suala hili, lakini hakufanikiwa kufikia lengo lake. Alimueleza mmoja wa rafiki zake kuhusu suala hili na akamtaka ushauri wa kutatua tatizo hili. Akamjibu: 'Kama utatenga kwa ajili yangu dinari 1000 nitafanya mipango ya kufanikisha haja ya lengo lako'. Waziri akasema: 'Nimejitayarisha kutumia hata zaidi ya dinari 100,000 kwa ajili hii.' Hivyo basi alitoa zaidi ya dinari 1000 na kumpa mtu yule mara moja. Mtu yule akachukuwa dinari zile 1000 na akaenda kwa watu kumi mashuhuri ambao kwamba ushahidi wao ulikuwa unachukuliwa kama wa kuaminika kwa Jaji. Aliwaelezea suala hilo na akasema: 'Nataka mchukue kutoka kwangu dinari 100 kila mmoja na kuwasilisha mbele ya Jaji kwamba waziri amemuoa msichana huyu. Mtakuwa hamfanyi dhambi yoyote kwa kutoa ushahidi huu, kwa sababu, kwanza maisha ya mwanadamu yako hatarini na pili waziri atampa maelfu ya dinari msichana huyu kama mahari. Aidha, baba wa msichana huyu anataka kumzuia msichana huyu asiolewe na kwa kutoa ushahidi kama huo mtakuwa mnafanya kitu ambacho ni halali. Na hatimaye cheo chenu kitaongezeka mbele ya macho ya waziri na atakuwa mwenye shukurani kwenu maishani mwake mwote.' Kwa ajili ya pesa na ahadi walizoahidiwa kwao watu wale kumi walikubali kutoa ushahidi wa uwongo, ambao ni moja ya dhambi kubwa na sababu ya ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. Baada ya kukubaliana na watu wale kumi waziri alifungua kesi kwa Jaji na kusema: 'Nimemuoa bintiwa fulani ambaye ni mfanyabiashara na nimetoa kiasi kadhaa kwa ajili ya mahari kwa ajili yake. Suala hili linajulikana kwa watu kumi wenye kuaminika. Lakini baba mkwe wangu anamzuia nyum39

11:26 AM

Page 39


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio bani kwake na hataki kumtoa kwangu'. Baada ya kusikiliza ushahidi kutoka kwa mashahidi Jaji aliamuru kwamba msichana lazima ahamishiwe nyumbani kwa waziri kwa nguvu na usisikilizwe upinzani wowote kutoka kwa baba yake. Msichana yule alihamishiwa kwenye nyumba ya waziri, lakini baba yake vile vile hakukaa kimya na aliendelea na juhidi zake na kampeini yake. Hata hivyo, kwa bahati mbaya mtu ambaye angeweza kuingilia na kurudisha msichana yule kwake alikuwa ni Khalifa Mu'tasim na mfanyabiashara yule hana njia za kumuendea. Baada ya uchunguzi mzuri alikuja kufahamu kwamba Khalifa anajenga ikulu mpya na anakwenda kwenye eneo lile kila siku kwa muda wa saa moja au zaidi kuona maendeleo ya ujenzi yanavyoendelea. Mfanyabiashara akavaa nguo za kibarua aliyeajiriwa katika kazi ya ujenzi, akajiunga na kundi la vibarua wale na akaanza kufanya kazi. Wakati Khalifa alipowasili, mfanyabiashara yule akaanza kulia na kulalamika. Khalifa akamuuliza alikuwa na nini. Akamzungumzia tukio lote. Palepale Khalifa alimuita waziri sehemu ileile. Waziri akaja na kukiri kosa lake kwa matumaini kwamba Khalifa atamsamehe. Kisha mashahidi wale kumi waliitwa nao vilevile wakakiri kosa. Kisha Khalifa akaamuru wale mashahidi wote wanyonge kwenye kizingiti cha ikulu. Amma kuhusu yule waziri alifungwa kwenye mfuko akapigwa sana kwa kiboko cha chuma mpaka mwili wake ukabadilika kama nyama iliyotafunwa. Kisha Khalifa akamuambia yule mfanyabiashara kumchukua binti yake nyumbani kwake pamoja na mahari yote, kama ilivyotajwa na mashahidi." (A'laamun Naas, Atlidi, uk. 190) Tukio hili la kihistoria ni moja ya mifano ambayo inaweza kuonesha matokeo maovu ya dhambi, na kama tukiangalia kwenye historia ya 40

11:26 AM

Page 40


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio zamani na hata katika maisha ya wakati wetu huu tutakumbana na mifano mingi kama hiyo. Familia nyingi zimeharibikiwa kwa sababu ya kuchafuliwa na dhambi. Wanaume wengi na wanawake wengi wameanguka kwenye mporomoko mkali wa dhambi na heshima na hadhi zao zimeingia doa. Afya na ustawi wa vijana wengi wa kiume vimetolewa mhanga kwenye starehe sizizo za halali na starehe ya mpito. Ili kuhakikisha ustawi wa watu na kuwaokoa kutokana na misiba inayotokana na dhambi, Uislamu umeelezea matokeo mabaya ya dhambi na kuwashauri watu kujiepusha nayo. Kwa vile watu wengi hawaelewi matokeo ya dhambi zao na ni wenye kupupia kwenye matamanio maovu, Allaha swt. amewaonya dhidi ya tabia hii mbaya na Anasema: "‌Huenda mkachukia kitu nacho ni kheri kwenu, na huenda mkapenda kitu nacho ni shari yenu. Na Allah anajua na ninyi hamjui." (2:216) Lodi Iboury, mwandishi mashuhuri wa Kiingereza anaandika: "Hatari zinahusika kwenye maisha ya anasa ambayo kama yataangaliwa, hufanya kwetu kuwa ni ushauri kujiepusha na starehe za mpito ambazo hutugharimu kiasi kikubwa mno. Lazima siku zote tuiweke nukta hii kwenye mtazamo kwamba maisha yanaunganishwa na machungu na shida na kama wakati fulani tunavunja sheria hii iliyothibitika na kujisalimisha wenyewe kwenye starehe za kuvutia punde hivi tutaona matokeo ya ukaidi huu. "Starehe za kimwili, kwa kiasi chochote kiwacho cha uchangamfu na kukubalika kokote kutakako kuwa, ni za mpito na kwa kawaida mara nyingi tutapata shida zaidi kuliko manufaa halisi. Hivyo kwa nini tujiingize wenyewe katika hasara ya milele kwa ajili ya starehe ya muda? "Starehe za mpito ni hatari iwakayo ambayo huangaza katika giza la maisha na mng'aro wake hutunduaza macho ya mjinga. Hata hivyo, mara 41

11:26 AM

Page 41


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio tu moto wake huchoma mavuno ya himaya na bahati nzuri na kufanya baadhi ya watu wasio na matumaini kukaa juu ya marundo ya majivu kwa majuto na kukata tamaa. "Starehe za kiuovu ni kama mazigazi ambayo hudhihiri yenyewe katika eneo la mchanga la ulimwengu kutoka mbali na jinsi tunavyoyakaribia hatuoni kitu isipokuwa joto na mchanga unaochoma. Starehe hii ya udanganyifu ambayo huvutia vijana ni kama ukungu na umande ambao hufunika anga wakati wa asubuhi. Mtu mwenye busara haiwekei muhimu hali hiyo na anajua kwamba umande huu hivi punde tu utatoweka kutokana na joto la jua." Dr. Alexis Carrel anasema: "Mtu asiye na simile kamwe hayuko kama tai ambaye huruka kwenye sehemu zisizo na mpaka za angani. Kwa upande mwingine hufanana zaidi na mbwa ambaye amekimbia makazi yake na kwa hofu ya kukamatwa hukimbia akipita katika makelele makali ya magari." Watu wengi waovu wanajiingiza katika maovu kwa sababa ya uzembe na ujinga wa kutojua matokeo yake na bila ya shaka kama wangejua madhara yanayoletwa na maovu kwenye mwili na roho ya mtu na katika ulimwengu na katika Akhera wenyewe wangechukua tahadhari na wangejizuia kutokana na starehe zenye madhara ambazo zimefanywa haramu na Allah. Ni dhahiri kwamba watu wanaoweza kujizuia kutokana na maovu kwa ajili ya Allah ni wale tu ambao wana imani na itikadi za kidini. Amma kuhusu waovu wasio na imani hakuna litakalowazuia kutenda maovu isipokuwa nguvu. Kwa hiyo, katika mafundisho ya Uislamu, suala la imani limepewa kipaumbele kwenye kila kitu na juhudi kubwa imefanywa kwamba kwa kujifunza ukweli wa kidini, Waislamu lazima wapate imani yenye nguvu ili kwamba nguvu ya imani iweze kuwafanya wasitende maovu.

42

11:26 AM

Page 42


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Amri ya nguvu hii isiyoonekena, ambayo makao makuu yake ni kwenye kina cha nyoyo na roho za watu ni yenye kupenyeza na kufaa kiasi kwamba wakati wa kujitokeza kwa hatari ya maovu humuokoa mtu kutokana na ushukaji wa hadhi na upotokaji. Nguvu hii haswa chini ya msukumo wa Mungu huwafanya watu kukimbilia kwenye ukarimu, huruma ya kiuchaMungu, haki, huduma kwa umma na mema mengine ya ubinadamu. Uzoefu umeonesha kwamba kama mtu ana nguvu ya imani, kiasi chochote cha udhaifu utakavyokuwa, atajiokoa mwenyewe kutokana na kuangukia shimo la maovu kwa kitendo chake cha kumkumbuka Allah. Imeandikwa katika historia kwamba Fuzail bin Ayaz alikuwa mnyang'anyi mbaya. Alizoea kuishambulia misafara na kupora mali za watu. Misafara iliyokuwa inapitia eneo la Sarkhas ilichukua tahadhari zote muhimu ili wasije wakaangukia kwenye mitego ya Fuzail. Mhalifu huyu hatari alitokea kumpenda msichana mmoja na akaamua kwenda nyumba ya msichana yule usiku ili akutane naye. Wakati wa usiku wa manane alikwenda na akapanda ukuta wa nyumba ile. Hata hivyo, wakati akiwa hajaingia kwenye nyumba ile alisikia sauti nzuri ya kupendeza ya mtu kutoka nyumba iliyoungana na ile akisoma aya ya Qur’ani Tukufu:

"Je wakati haujafika kwa wale walioamini kwamba nyoyo zao zinyenyekee kwa kumkumbuka Allah?" (57:16) Kwa kusikia aya hii tukufu, Fuzail alihisi mabadiliko ya haraka na akasema: "Ee Mola wangu! Wakati kwa ajili ya hilo sasa umefika." Kisha alishuka kwenye ukuta ule haraka sana na akajizuia kufanya uovu alioukusudia kuufanya. Ukumbusho huu haswa ukawa ni sababu ya Fuzail kuachana na matendo yote uovu. Wakati wa usiku uleule ambao mabadiliko 43

11:27 AM

Page 43


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio yanayosemwa yalikuja kwa Fuzail alibahatika kupita karibu na hoteli ambako msafara ulikuwa umewasili na kushusha bidhaa zao. Fuzail akatambaa mpaka kwenye kona ya nyumba na akaanza kusikitikia uovu wake uliopita. Wakati uleule alisikia jamaa wa msafara ule wakiongea kuhusu saa ya kuondoka kwao. Mmoja wao akasema: "Enyi rafiki zangu! Msiondoke hapa na usiku huu na ngojeni hali iwe ni ya kuridhisha, kwa sababu, kwa mujibu wa taarifa tulizozipata, Fuzail yuko njiani na ni tishio kwa msafara." Mazungumzo haya ya wasiwasi wa watu hawa wa msafara yaliwasha moto ndani ya moyo wa Fuzail. Alihuzunishwa mno kuona kwamba uhalifu wake umewatia watu wasiwasi na kuwahuzunisha kwa kiasi kikubwa kama hicho. Mara moja alijitokeza kutoka sehemu ile na akasema: "Mabwana! Mnapaswa kujua kwamba mimi ni Fuzail bin Ayaz na lazima muwe na hakika kwamba Fuzail hatatenda kosa la wizi tena na sitaivizia misafara tena. Amerudi kwa Allah na ametubia dhambi zake." (Rawdhatul Jannat, Fuzail) Kitu kilichomzuia mtu huyu kutenda maovu na kubadilisha muelekeo wake ilikuwa ni ukumbusho. Bila shaka, alikuwa anazo itikadi na imani, ingawa dhaifu, hivyo kwamba ukumbusho ungeweza kuuvutia moyo wake na kuleta mapinduzi na mabadiliko ndani yake. Kwa hiyo, hatua ya kwanza kuelekea kwenye mapambano na maovu na dhulma ni kwamba watu lazima wawe na ufahamu wa ukweli wa dini na imani kwa Allah, Siku ya Hukumu, hesabu ya matendo mema au mabaya na malipo ya thawabu au adhabu nk., yaweza kustawi katika nyoyo zao na kuzaa matunda. Dr. Ki Niya anasema: "Washa moto wa imani katika nyoyo za watu, kwa sababu imani ni silaha yenye nguvu sana katika kupambana dhidi ya maovu yote ya kijamii na kimaadili. (Ulum-i Jina’i, Jz. 2)

44

11:27 AM

Page 44


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Hatua nyingine ambayo Uislamu imeichukua kwa ajili ya kupambana dhidi ya maovu ni kuweka mipaka kwanye zana na vipengele vya maovu. Kama tunavyojua kwamba, ili kuuangamiza ungonjwa, mashirika ya kiafya huzingira vipengele vyote vya sababu za ugonjwa na kufanya juhudi za kuviharibu kwa njia tofauti. Huwachanja watu, huweka karantini za lazima na huweka upatikanaji wa dawa muhimu kwa watu kwa kiasi cha kutosha ili kuwawezesha kuzuia ungonjwa huo. Halikadhalika, katika kuangamiza maovu, ni muhimu kwamba watu lazima wajiandae na silaha ya nguvu ya imani ili kuwawezesha kupambana dhidi ya maovu, na wakati huohuo mazingira lazima yasafishwe kuondoa uchafu wa maovu na chochote kinachokuwa sababu ya maovu lazima kizuiwe na kuwekewa mipaka. Uislamu umechukuwa hatua juu ya safu hizi kwa ajili ya kupambana dhidi ya pombe, kamari, wizi, zinaa, mauwaji, riba nk. Kwanza kabisa, kutumia imani na itikiadi za kidini ya Waislamu, Uislamu umetangaza matendo haya kuwa ni haramu na utendaji wake kuwa ni sababu ya ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na kwa upande mwingine kwa kuweka wajibu wa mtu binafsi na wa pamoja wa Waislamu, umezuia kuwepo kwa mazingira mazuri kwa ajili ya kujitokeza kwa maovu. Qur’ani Tukufu inatoa pendekezo lifuatalo kwa Waislamu: “…Na saidianeni katika wema na taqwa wala msisaidiane katika maovu na uadui…" (5:3)

Kutangaza maovu yake mtu Ili kuweka mazingira kuwa safi, Uislamu hauruhusu watu wadadisi kuhusu maovu ya watu wengine na umetoa amri za wazi kuhusiana na hili: “Enyi mlioamini jiepusheni sana na dhana kwani dhana ni dhambi wakati mwingine, wala msipeleleze, wala baadhi yenu wasiwatete wengine. Je, mmoja wenu atapenda kula nyama ya nduguye aliyekufa?..." (49:12) Kama wakati fulani mtu atapata kufahamu uovu wa mtu mwingine ulio45

11:27 AM

Page 45


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio fichika, haruhusiwi kuutangaza na kuutaja mbele ya watu wengine, kwa sababu kwa kufanya hivyo matokeo yake atafedheheka na kwa ajili hiyo atakuwa ni mwingi sana wa kufanya maovu. Kueneza habari kuhusu kupotoka, uhalifu na ukosefu wa watu kujizuia hufanya uovu kuwa kitu chepesi na cha kawaida katika macho ya jamii na kuwa sababu ya kuwepo kwa maovu. Qur’ani Tukufu imeonya kuhusu mateso makali kwa wale ambao wanasaidia katika utangazaji wa maovu kwa kueneza taarifa na inasema:

“Kwa hakika wale wanaopenda uenee uchafu kwa walioamini, watapata adhabu yenye kuumiza katika dunia na Akhera, na Allah anajua, na ninyi hamjui." (24:19) Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: "Dhambi ya yule ambaye hueneza habari za tendo baya miongoni mwa watu ni kama mtu yule ambaye haswa amekitenda kitendo kile." (Safinatul Bihar, Jz. 2, uk. 296)

Usimamizi wa kitaifa Moja ya njia ambazo Uislamu umeelekeza kwa ajili ya kampeni dhidi ya dhambi na aina mbalimbali za uovu, ni sheria ya usimamizi wa kijamii. Sheria hii huwaruhusu Waislamu wote bali pia huwafanya kuwa wenye kuwajibika, kwamba lazima wafanye usimamizi kwa ajili ya usimamishaji wa sheria za Mwenyezi Mungu, na kama wakimuona mtu yeyote akivunja sheria hawapaswi kukaa kimya bali lazima wajaribu kumrekebisha kwa njia sahihi na ya busara, kumzuia asifanye kitu chochote kisicho halali na hivyo kuzuia utendaji wa maovu.

46

11:27 AM

Page 46


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Qur’ani Tukufu inasema:

“Ninyi ni kundi bora mliotolewa kwa ajili ya watu, mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamwamini Allah…" (3:110) Viongozi wa Uislamu wamehimiza juu ya Waislamu kwamba kama wanataka kwamba madhara, dhulma, maovu, uonevu na maovu mengine yasiwepo katika jamii na kwamba jamii isipelekwe kwenye maangamizi na shida lazima wakumbuke sheria ya usimamizi wa jamii na lazima siku zote watende juu ya kanuni mbili muhimu; yaani kuamrisha mema na kukataza maovu. Wakati ikinukuu mapendekezo yaliyofanywa na Luqman kwa mtoto wake, Qur’ani Tukufu inasema:

“Ewe mwanangu! Simamisha sala na uamrishe mema, na kukataza mabaya na usubiri juu ya yale yanayokupata, hakika hayo ni katika mambo yanayoazimiwa". (31:17) Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: "Muda ambapo wafuasi wangu wanaamrisha mema na kukatazana maovu na kushirikiana wao kwa wao katika matendo mema watabakia kuwa wenye kuneemeshwa na kustawi. Na kama wakiacha wajibu huu watanyimwa rehma na baadhi zitaenea juu ya wengine na kwa matokeo ambayo kwamba watakuwa hawana sehemu ya kujihifadhia na bila msaada na hakuna atakayekuja kuwasaidia kutoka upande wowote". (Tahdhib, Jz. 2, uk. 58) Kama tukitafakari kidogo juu ya kanuni hizi mbili, yaani kuamrisha mema na kukataza maovu tunatambua kwamba kanuni hii ni moja ya miujiza 47

11:27 AM

Page 47


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio mikubwa ya Qur’ani, kwa sababu wakati wa zama hizi, baada ya kupita zaidi ya karne kumi na nne za ujio wa Uislamu, mataifa yaliyostaarabika yamesimamisha na kutekeleza sheria kama hizi na kuzichukulia kuwa msingi wa demokrasi na maendeleo yao wenyewe. Ibrahim Khwaja Nuri anaandika: "Hata hivyo, huu vilevile ni ukweli usiokanushika kwamba ili kuhakikisha haki ni ya muhimu, kwa mfano, kama taifa la Uswisi, kwamba kila mtu binafsi wa jamii yetu lazima awe mlinzi wa haki na, kama ilivyowekwa katika katiba yao kama aya tukufu za kimbinguni. 'Kwa upesi utakapoona dhulma ndogo sana ni wajibu juu ya jamaa wote wa jamii kutokukaa kimya mpaka dhulma hiyo imerekebishwa'. Kama unavyoweza kuona, huu ni wajibu uleule ambao umewekwa na Uislamu juu ya Waislamu wote. Hapana shaka kama zoezi hili linakuwa la kawaida na la kidesturi, haki itakuwa imehakikishika moja kwa moja na upinzani kwa hilo bila shaka utakuwa hauwezekani." (Taqiyya, Sura ya Kuamrisha mema) Imam Ali (a.s.) alisisitiza juu ya suala hili kubwa na muhimu katika wosia wake wa kihistoria alioufanya juu ya kitanda chake alichofia kishahidi. Alisema: "Msiache kuamrisha mema na kukataza maovu, kwa sababu kama mkiliacha hilo, watu waovu watawatawaleni na ninyi mtasali na kumuomba Allah ili aondoe fitna yao, lakini maombi yenu hayatakubaliwa." (Nahjul Balaghah)

Adhabu kwa ajili ya waovu kesho Akhera Katika Qur’ani Tukufu na katika hadithi za Kiislamu bahati mbaya na shida za waovu katika Akhera zimechambuliwa na kuelezwa kwa urefu na hii yenyewe ni mbinu ya kupambana dhidi ya uovu. Qur’ani Tukufu inasema:

48

11:27 AM

Page 48


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio

"Na ungeliwaona waovu wakiinamisha vichwa vyao mbele ya Mola wao (na kusema): Mola wetu! Tumekwishaona na tumekwisha sikia, basi turudishe, tutafanya vitendo vizuri, hakika (sasa) tumethibitisha. Na tungetaka, tungempa kila mtu mwongozo wake, lakini imehakiki kauli iliyotoka Kwangu. Kwa hakika nitaijaza Jahannam kwa wote hawa majini na watu. (wataambiwa): Basi onjeni (adhabu) kwa sababu ya kusahau mkutano wa Siku yenu hii, hakika Sisi tutakusahauni, na onjeni adhabu yenye kudumu kwa yale mliyokuwa mkiyatenda. (32:12-14) Katika Aya nyingine Qur’ani Tukufu inasema:

“Ingawa watafanywa waone, mwenye kosa atapenda ajikomboe katika adhabu ya siku hiyo kwa kulipa watoto wake. Na mke wake na ndugu yake. Na jamaa zake waliomzunguka. Na (kulipa) vyote vilivyomo katika ardhi, kisha aokoke. Sivyo, kwa hakika huo ni moto uwakao. Unaobabua ngozi ya mwili. Utamwita kila aliyegeuza mgongo na akageuka. (70:11-17) 49

11:27 AM

Page 49


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Aya hizi na nyingine kama hizi huvuta mandhari ya waovu kwenye wakati mgumu ujao ambao huwangojea ili kwamba kabla ya kupasishwa kwenye adhabu ya Mwenyezi Mungu lazima watafute tiba na kuchukua hatua kuelekea kwenye wokovu na wakati mzuri ujao kwa njia za kutubia na utakaso wa maovu yao.

Adhabu kwa ajili ya Waovu katika dunia hii Uislamu umeamuru adhabu kwa wale ambao wanapinga au kuvunja sheria, kwa utekelezeji wake ambao dhulma na uhalifu vinaweza kung'olewa kutoka katika jamii au kupunguzwa mpaka mwisho. Kama ambavyo sheria za adhabu za Kiislamu zimewekwa na Allah, adhabu hizo zimewekwa kwa mujibu haswa wa kiwango cha uhalifu, yaani sio nyepesi mno na kidogo kiasi kwamba mhalifu angeshawishika kutenda uhalifu, au kali mno na za ukatili kiasi kwamba haziwezi kuafikiana na akili. Sheria hizi zimejadiliwa katika vitabu juu ya sheria za Kiislamu chini ya anwani ya Huduud. Wale ambao wanataka kuwa na ufahamu kwa kina na ukubwa wa sheria hizi na taratibu zake, itawapasa kurejea kwenye vitabu vikubwa juu ya suala hili. Kilichoelezewa hapo juu ni mfano mkubwa wa kampeni za msingi za Uislamu dhidi ya uovu, dhulma na uhalifu. Ni matumaini yetu kwamba kwa kuzingatia kwenye sheria hizo tukufu za Uislamu na utekelezaji wake sahihi, Waislamu ulimwenguni watakuwa na uwezo wa kuweka jamii ya uchaji na yenye nguvu iliyo huru kutokana na dhulma na uovu, na itapata ustawi katika ulimwengu huu na halikadhalika katika ulimwengu wa kesho Akhera.

50

11:27 AM

Page 50


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio

HAKI ZA WANANDOA Mwanaume peke yake ni kiumbe pungufu na halikadhalika mwanamke peke yake vilevile ni kiumbe pungufu. Upungufu huu ndani yao uko juu ya sababu hii kwamba kwa ajili ya muendelezo wa jamii na kuwepo kwa maisha, wote kwa pamoja wanategemeana. Ndoa iliyoruhusiwa na ya halali huondoa upungufu wao na kufanya maisha yao kuwa ya mafanikio. Mbali na muendelezo wa jamii, utengenezaji wa familia ni muhimu kwa kila mwanaume na mwanamke kwa mtazamo wa siha ya mwili na roho na kufaidi kwa usahihi fursa za maisha. Wanawake na wanaume ambao huishi peke yao wanakabiliwa zaidi na tishio la wahaka au mfadhaiko na maradhi ya akili, kwa sababu kama wanazikandamiza silka zao za kijinsia husababisha kutokea kwa magonjwa ya kutisha, na kama wakiwa hawawezi kujizuia na kukidhi silka hii kiharamu hatari itakayowazunguka bado itakuwa ni mbaya zaidi. Ndoa na uundaji wa familia, pamoja na utekelezaji wake wa masharti muhimu ni amri ya asili na kanuni ya maumbile, na uvunjaji wake huhusisha adhabu kali. Mwanaume na mwanamke ambao hutekeleza jukumu hili muhimu kwa kufunga ndoa lazima vilevile waweke akilini majukumu na wajibati zilizoambatanishwa kwenye ushirika huu ili kuishi maisha ya furaha. Hawapaswi kuweka msingi wa ndoa juu ya hisia na ridhaa ya matamanio ya uovu, na vilevile hawapaswi kufunga ndoa kwa ajili ya utajiri na urembo, kwa sababu mafungamano kama hayo dhaifu na ndoa kama hizo hazina msingi imara. Lazima wakumbuke lengo kubwa ambalo lazima waliweke katika mtazamo wakati wanapochukua hatua hii, na lazima wachague wenza au washirika wa baadae kwa ajili ya maisha yao kutoka miongoni mwa waumini, wenye busara na watu wenye uwezo baada ya kila uchaguzi wa makini.

51

11:27 AM

Page 51


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Mwanaume na mwanamke hawafaidi nafasi yoyote juu ya mwingine kwa sabubu ya yeye kuwa mwanaume au mwanamke. Katika macho ya Muumba wote ni wanadamu na wanafaidi haki zote husika. Allah swt., anasema katika Qur’ani Tukufu:

“Enyi watu! kwa hakika tumekuumbeni kutokana na mwanaume na mwanamke, na tukakufanyeni mataifa na makabila ili mjuane, hakika aliye mbora zaidi kati yenu mbele ya Allah ni yule mchamungu zaidi‌ (49:13) Kama shirika lingine lolote lile, kuwepo kwa mlezi na mtu muajibikaji ni muhimu katika utaratibu wa nyumba, kwa sababu kampuni au shirika ambalo halina mamlaka yenye kuwajibika ni lazima litajiingiza katika mizozo na vurugu. Kwa kuzingatia maslahi ya shirika hili, hebu tuone ni nani anapaswa kupewa dhamana ya uwajibikaji. Je, ni lazima awe mwanaume au mwanamke au wote kwa pamoja? Hapana shaka utawala wa wote hautashindwa tu kutatua matatizo bali utaongeza matatizo, kwa sababu uzoefu umeonesha kwamba kuwepo kwa watawala wawili katika shirika moja ni hatari zaidi kuliko kutokuwa na mtawala kabisa, na nchi ambayo ina watawala wawili wanaojitegemea siku zote hukabiliwa na vurugu na machafuko. Kama kuna tofauti kati ya baba na mama kuhusu kusimamia mambo ya nyumba matokeo yake ni mzozo na vurugu. Mbali na hili, kwa mujibu wa wanasaikolojia, watoto wanaolelewa katika nyumba kama hiyo hukabiliwa 52

11:27 AM

Page 52


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio na kasoro ya kiroho na mchanganyiko wa mfadhaiko na matatizo ya akili. Kwa kuzingatia matatizo yaliyotajwa hapo juu hapana shaka kwamba uwajibikaji kwa ajili ya kusimamia mambo ya nyumba lazima udhaminiwe amma kwa mwanaume au kwa mwanamke, na vilevile ni hali isiyokanishika kwamba kwa mtazamo wa maumbile ya kimwili na ustadi wa kiakili mwanaume anafaa zaidi kubeba jukumu hili. Kwa mujibu wa maoni ya kitaalamu yanayoshikiliwa na wasomi na mabingwa, mwanamke hufaidi ubora juu ya mwanaume kadri ambavyo hisia na mihemuko huhusika wakati ambapo mwanaume ni bora kwa mwanamke katika suala la fikra na busara. Amma kwa utawala wa mambo kuna haja zaidi ya kutafakari na kufikia hukumu ya kimantiki na yenye kufaa, akili ya kuzaliwa huhitaji kwamba utawala na uangalizi wa familia ambao huhusisha uwajibikaji mkubwa, lazima uwekwe juu ya mwanaume na usimamizi na ulezi udhaminiwe kwake (mwanaume). Mtazamo huu wa Uislamu vilevile uko sawa kama wa kanuni ya asili. Hivyo, Allah anasema: “Wanaume ni wasimamizi wa wanawake kwa sababu Allah amewafadhili baadhi yao kuliko wengine na kwa sababu ya mali yao waliyotoa‌" (4:34) Ulinzi wa mwanaume kuhusiana na mke wake unakubaliwa katika nchi zote za ulimwengu na wanawake vilevile wana raha na mpangilio huu. Kwa mujibu wa kifungu cha 213 cha makala ya sheria mpya ya Ufaransa, ulinzi, udhibiti na usimamizi wa familia uko chini ya mwanaume na kwa mujibu wa sheria na taratibu za mataifa mengine vilevile hali ni hiyo hiyo. (Huquuq-i Zan, uk. 134) Allah ameudhamini mwongozo na usimamizi wa mambo ya familia kwa mwanamume. Hii ni kwa ajili ya kweli kwamba mwanaume ni mwenye nguvu zaidi kimwili na mwenye kufaa zaidi kufanya kazi ngumu na halikadhalika kulinda jamaa ya familia yake. 53

11:27 AM

Page 53


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Kutokana na kipengele cha nguvu za kimwili na kiroho, mwanamke ana usanifu maalumu na ana hisia za huruma na uwezo wa kuhisi. Aidha, wakati siku zake za mwezi na ujauzito na wakati wa miaka ya kunyonyesha mtoto, mwanamke sio tu kwamba hafai kwa kazi ngumu, bali anahitaji uangalizi mahususi na uzingativu vilevile. Mamlaka ambayo yatatekelezwa na mwanaume juu ya familia yake sio katika maana ya kwamba yeye ni bwana wa jamaa zake na wao ni watumwa wake, bali ina maana kwamba kama ilivyo dhidi ya usaidizi wa kipesa na hifadhi ya nguvu za kimwili na za akili anazotoa kwa jamaa ya familia yake, bila ya shaka atakuwa anatenda kama mtawala. Lakini ukomo wa mamlaka yake umeamriwa na Allah ili kwamba asije akavuka mipaka. Lazima vilevile iangaliwe kwamba wakati mwanaume anapewa nafasi ya ukuu wa familia, Uislamu haukupuuza matarajio ya mwanamke ya kupata furaha ya kiakili ya ubora na kuhusiana na hili amekabidhiwa wajibu wa kuendesha mambo ya nyumba. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: "Kila mtu yuko huru na ni mtawala. Mwanaume anafaidi uhuru na mamlaka katika mambo ya familia na mwanamke naye anafaidi hali hiyo hiyo katika mambo ya nyumbani." (Huquuq-i Zan, uk. 134) Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anaendelea kusema: "Nyote ninyi ni walinzi na wachunga kwa mujibu wa majukumu yenu na nyote ninyi ni wenye kuwajibika kwa kile ambacho umekichukulia jukumu. Mtawala na Imamu wanawajibika kwa ajili ya umma, mwanaume anawajibika kwa ajili ya familia, mwanamke anawajibika kwa ajili ya mambo ya nyumbani na watoto na kila mtu anawajibika kwenye upeo wa mamlaka aliyonayo na ana wajibu wa kutekeleza kazi zote zilizoaminishwa kwake na Allah." (Sahih Bukhari, Jz. 3, Sura juu ya Ndoa)

54

11:27 AM

Page 54


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Aidha, Allah swt., kwa uwazi amewakumbusha wanaume katika maneno haya: "Na kaeni nao kwa wema na kama mmewachukia, basi huenda mkachukia kitu na Allah ametia kheri nyingi ndani yake." (4:19) Sa'd bin Mu'az alikuwa mmoja wa masahaba waaminifu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye alipokea mazingatio mengi kutoka kwake. Wakati alipofariki, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe alihudhuria ibada zake za mazishi na akasema malaika vilevile wamesindikiza jeneza lake. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisali Sala yake jeneza na wakati mwili wa marehemu ulipokuwa unawekwa kaburini aliingia kaburini, akauweka sawa sawa akaziba mianya katikati ya matofali. Baada ya hapo akawaambia masahaba wake: "Ingawa najua kwamba kaburi hii itaharibika hivi punde, lakini Allah anapenda kwamba wakati waja wake wanapofanya kazi yoyote lazima waifanye kwa uimara na kwa uangalifu sana." Kaburi lilifunikwa kwa mchanga na likasawazishwa. Mama yake Sa'd ambaye alikuwepo pale wakati wote ule wa ibada ya mazishi na akaona uzingativu ule maalumu ukifanya na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), akasema kumuambia mwanawe bila kujitambua: "Ewe mwanangu! Pepo naikukaribishe." Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamuambia mama yake Sa'd: “Nyamaza! Unatarajia nini kutoka kwa Allah? Hivi punde kaburi limeporomoka na limembana Sa'd kwa nguvu". Akasema: "Ewe Mtume wa Allah! Kwanini?" Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akajibu: "Kwa sababu katika nyumba yake amemtendea vibaya mke wake." (Tabaqat Ibn Sa'd, Jz. 3) Imamu Ja'far (a.s.) anasema: "Allah ambariki mtu yule ambaye huweka msingi wa mahusiano na mke wake juu ya wema na huruma." (Man La Yahdhuruhul Faqih, Jz. 2, uk. 142) Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: "Mtu bora miongoni mwenu ni yule ambaye hukaa vizuri na watu wa familia yake, na mimi huwafanyia watu 55

11:27 AM

Page 55


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio wa familia yangu katika njia iliyo nzuri kuliko mtu yeyote yule." Vilevile alisema: "Mtu ambaye anavunja haki za watu wa familia yake anastahili kulaaniwa." (Wasa'ilush Shi'ah, Jz. 7, uk. 122) Kwa dhahiri, kama ilivyosisitizwa juu ya wanaume katika Uislamu kukaa vizuri na wake zao, wanawake vilevile wametakiwa kutekeleza kazi zao kwa heshima kwa waume zao na kuthibitisha wenyewe kuwa ni wenye uwezo na ni wake wenye manufaa. Imamu Musa Kadhim (a.s.) anasema: "Jihadi ya wanawake ni kwamba lazima wafanye majukumu yao ndoa sawa sawa." (Furu'ul Kafi, Jz. 2, uk. 60) Wakati wa mwanzo wa maisha yao ya ndoa Imamu Ali (a.s.) na mke wake mtukufu Bibi Fatima (a.s.) walimuendea Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ili kuainisha majukumu ya kila mmoja wao. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliaminisha kazi zote za nje ya nyumba kwa Imamu Ali na mambo yote ya nyumbani kwa binti yake, Fatima." (Qurbul Asnad, uk. 25) Kwa kuwa na busara na tabia sahihi, wanaume na wanawake wanaweza kuweka msingi wa maisha yaliyostawi na wanaweza kuepuka matendo kama yale ambayo yanayoweza kuharibu furaha yao. Wakati mwingine vitu vidogo visivyo na maana huwa vyanzo vya mapenzi na huruma na vivyo hivyo wakati mwingine mambo ya kipuuzi huwa sababu za ugomvi na utengano. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: "Ni vizuri kwamba mwanamke apaswe kuwasha taa ya nyumba na kutayarisha chakula na wakati wa mume wake anaporudi nyumbani lazima ampokee mlangoni na kumkaribisha na amletee maji na taulo ili kumsaidia kuosha mikono yake na asimkatalie ombi lolote lile bila sababu ya maana." Aliendelea kusema: "Mwanaume anayemuoa mwanamke lazima ajitahidi kumheshimu na kuwa na mapenzi naye sana." (Mustadrak, Sura 65, 68) Usitaje kasoro za mke wako mbele ya watoto wako, na hata kama wakilalamika kuhusu mama yao lazima uziweke akili zao katika amani kuhusiana na hili na kuthibitisha heshima kwa ajili ya mama yao katika akili 56

11:27 AM

Page 56


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio zao. Bila shaka, vilevile ni jukumu la mama kushawishi juu ya watoto wake kumheshimu baba yao". (A'in-i Kaamyaabi, uk. 116) Ni jukumu la mume na mke kujiweka wenyewe nadhifu, wasafi na wenye kuvutia mbele ya kila mmoja na kuepuka uchafu na kuwa katika hali ya kuchukiza. Hasan bin Jaham anasema: "Niliona kwamba Imamu Musa Kadhim (a.s.) ametia rangi nywele zake. Nilishangaa na nikamuuliza sababu ya kufanya hivyo. Akasema: 'Kama mwanaume akiremba uso na nywele zake na kuvaa nguo nadhifu na safi huzidisha usafi wa tabia ya mke wake (kwa sababu kama mwanamke anampenda mume wake hatawaangalia wanaume wengine). Wanawake wengi wamepotea kutoka kwenye njia ya usafi wa tabia kwa sababu ya uzembe na kutozingatia kwa waume zao'. Kisha akasema: 'Je, unataka kumuona mke wako katika hali ya kulaumika?' Nikajibu: hapana. Akasema: 'Yeye pia ni kama wewe na hataki kumuona mume wake akiwa mchafu na asiye nadhifu. Bila ya shaka, usafi, utumiaji wa manukato na mtu kuweka kichwa chake na sura yake katika umbo zuri ni katika mwenendo wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).'" Wakati wa mmoja wa makhalifa, mwanamke alilalamika kwa Khalifa dhidi ya mumewe na aliomba kwamba aitwe na atakiwe kumuacha. Khalifa akauliza sababu ya ombi hilo. Mwanamke akajibu: "Simpendi mume wangu na haivumiliki kwangu mimi kuishi naye." Khalifa alikuwa mdadisi na alimuuliza zaidi ili kujua sababu ya kuvunjika kwake moyo. Alimuambia: "Je, mume wako anapuuza kukutekelezea matumizi yako?" Akajibu: "Hapana". Akasema: "Je, anakupiga na kukutesa?" Akajibu: "Hapana". Khalifa akamuuliza: "Je, hakujali?" Akajibu: "Hapana. Hakuna katika vitu hivyo. Mume wangu ni mtu mzuri lakini simpendi."

57

11:27 AM

Page 57


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Khalifa akamuru mume wa mke yule aitwe. Baada ya muda maofisa walimleta mwanaume mbele ya Khalifa ambaye alikuwa mchafu sana na asiye nadhifu. Nywele zake zilikuwa timtimu, kucha zake zilikuwa ndefu na nguo zake zikuwa zimechanika na chakavu. Khalifa alimshambulia mwanaume yule kwa maswali ili ahakikishe sababu ya mwanamke yule kuvunjika moyo lakini hakupata dalili yoyote. Hata hivyo, ghafla ilitokea kwake kwamba inawezekana sababu ya kuvunjika moyo kwa mwanamke yule ni hali ya uchafu na uvaaji wa midabwada wa mumewe. Kwa hiyo akamuambia yule mwanamke: "Leo utakwenda na kesho utakuja pamoja na mume wako ili upatiwe talaka yako." Yule mwanamke akaenda zake. Baadae kwa ilivyoamrishwa na Khalifa, nywele za mume wake zilikatwa na alikogeshwa na kupewa nguo safi na nadhifu. Kisha Khalifa alimuamuru aondoke na kesho aje pamoja na mke wake. Kesho yake Khalifa alikaa kungojea lakini hakuna yeyote kati yao aliyetokea. Akatuma mtu kwenda kuwaleta. Walipowasili Khalifa alisema: "Sasa tuko tayari kuamuru talaka yako." Yule mwanamke akasema kwa wasi wasi mkubwa na woga : "Sitaki kabisa kumuacha mume wangu. Nampenda na nasikitika kwa kile nilichosema jana." Khalifa akatabasamu na akawahimiza kuishi maisha ya ndoa ya furaha. Khalifa alikuwa amekisia kwa usahihi. Hali ya kuchukiza ya mwanaume au mwanamke yaweza kuwa sababu ya kuvunjika moyo na ukosefu wa huruma na hata kuachana au kutengana. Imamu Muhammad Baqir (a.s.) anasema: "Mwanamke hapaswi kukaa bila kuwa na pambo lolote kwa ajili ya mume wake hata kama ikiwa ni mkufu tu wa shingoni." (al-Kafi).

58

11:27 AM

Page 58


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Kama mwanamke yuko makini kuhusu mambo haya haswa ambayo kwa dhahiri yanaonekana kuwa yasiyo na muhimu na ajirembeshe mwenyewe na kuiweka nyumba yake katika mpangilio mzuri anaweza kumfanya mume mwenye kichefu chefu na aliyevunjika moyo awe na hamu na yeye mwenyewe na nyumba, na anaweza kuifanya hali ya hewa ya nyumba kujaa uaminifu na upendo. Dale Carnegie anasema: "Kama nyumba imepambwa vizuri na vyumba viko katika mpangilio mzuri kiasi cha kuifanya nyumba ivutie na mwanamke akajisikia raha kwa kuwepo mumewe katika nyumba, badala ya mume kwenda hapa na pale pamoja na wanawake wengine, huja nyumbani kwake na polepole anakuwa ameambatana nayo. Hii ni kwa sababu kwanza kabisa mume hujihisi fahari ya hali yake na baadae anakuja kuvutiwa ndani ya nyumba. Muache mume awe huru ndani ya nyumba. Muache akae popote atakapo, ale chakula chochote atakacho, avute na asome magazeti na apate furaha kamili." (A'in-i Shauhar dari) Amani na furaha sio bidhaa ambazo mtu anaweza kuzinunua sokoni. Hupatikana tu katika uhusiano mzuri wa kindoa wa mume na mke. Imamu Sajjad (a.s.) anasema: "Maneno mazuri huongeza utajiri na riziki ya mtu, hurefusha maisha yake, huwa ni sababu ya yeye kupendwa na mke na watoto wake na kumuongoza kwenda Peponi." (al-Ziwaj Fil Islam, uk. 198). Wanachuoni wa Magharibi wameelezea maoni kuhusu majukumu ya mume na mke ambayo baadhi tutayadokeza hapa. Hata hivyo lazima ielezwe hapa kwamba kuna tofouti kati ya amri za Uislamu na maoni ya wanachuoni, yaani mafundisho ya Uislamu asili yake yanatokana na ufunuo wa Mwenyezi Mungu na yana kinga kutokana na makosa ya aina zote, ambapo maoni ya wanachuoni ambayo yanatokana na wao wenyewe juu ya msingi wa uzoefu na uchunguzi binafsi hayako huru kutokana na makosa. Kwa sababu hii haswa kuna tofauti nyingi kati ya maoni ya 59

11:27 AM

Page 59


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio wanachuoni juu ya matatizo mbali mbali. Aidha, maoni mengi ya wanachuoni waliopita huchukuliwa kama yasiyo sahihi na yanabadilishwa na maoni mapya. Hata hivyo, hata baada ya kupita karne kumi na nne kuanzia muda ambapo sheria za Uislamu ziliposimamishwa, zinaendelea kuwepo pamoja na nguvu kamili na sifa na zinathibitishwa na wanachuoni wa kisasa. Hapa kuna maelezo mafupi ya maoni ya wanachuoni wa Magharibi: Samuel Smiles anasema: "Ingawa sifa na heshima za mwanaume huunganishwa na akili yake na sifa njema ya mwanamke na maainisho ya mwanamke yanahusishwa pamoja na moyo wake, ni muhimu kwamba mwanaume lazima aufundishe moyo wake kuipenda akili yake na ni muhimu vilevile kwa mwanamke kwamba lazima aifundishe akili yake kuupenda moyo wake. Kama alivyo mwanamke mjinga na wa kawaida, mwanaume mwenye moyo mbaya na uliopotoka hana thamani au umuhimu katika jamii iliyostaarabika. Wanaume na wanawake wanaotaka kuwa na siha na tabia njema lazima wajitahidi kufundisha na kustawisha fikra zao na maadili kwa ujumla, kwa sababu mwanaume ni kiumbe dhaifu, asiye na thamani na mbinafsi na hana hisia ya uswahiba na kujali juu ya hali za wengine. Na mwanamke, kwa kiasi chochote cha urembo atakachokuwa nacho, bado ni mwanasesere aliyevalishwa nguo isipokuwa awe ana elimu na busara. Hakuna shaka kuhusu ukweli kwamba sifa na nemsi za upeo wa juu kabisa wa mwanamke hudhihirika wakati wa uhusiano na mawasiliano na wengine na kwa njia za hisia na upole wake. "Mwanamke ni mlezi aliyeteuliwa kwa ajili ya malezi ya mwanadamu na ni kwa sababu hii kwamba huwalea watoto wanyonge na wasiojiweza na kuwakuza kwenye mapaja ya upendo na huruma kutokana na silka zake za kurithi. "Mwanamke ni malaika ambaye huilinda nyumba, na kwa njia ya tabia zake nzuri na mwenendo mwema, huleta amani na utulivu katika familia ambao ni dawa ya kutia nguvu mwili (toniki) na lishe ya maadili na tabia 60

11:27 AM

Page 60


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio nzuri za hali ya juu. Kwa sababu ya tabia na umbile la mwili wake, mwanamke ni mpole, mwenye huruma, mvumilivu na mwenye kujitoa muhanga, na mwanga wa matarajio na matumaini huwaka kutoka kwenye macho yake yaliyojazwa na hisia za upole, ambazo hutoa matumaini kwa wasiojiweza na faraja kwa wenye huzuni na wenye mateso, popote itakapo angaza. "Ili jamii siku zote iweze kuwa na hali yenye hulka moja, ni muhimu kwamba lazima kuwe na usawa kati ya mafundisho ya mwanaume na mwanamke kwa sababu nemsi na usafi wa mwanamke na nemsi na uchamungu wa mwanaume huhusiana na kila moja na kanuni za maadili huweka usawa kwa wote pamoja. Kwa hiyo, kama jamii inataka kuwa halisi na safi na kuwa huru kutokana na kasoro za kimaadili ni muhimu kwamba wote, wanaume wake na wanawake zake lazima wawe wachamungu na waadilifu na kwa wote pamoja lazima wajiepushe na kila kitendo ambacho kinapingana na maamrisho ya dhamira na uadilifu. Wote lazima wakichukulie (kitendo hicho) kama sawa sawa na sumu yenye kuuwa kwa vile mara tu inapoingia mwilini haionndoki na athari ya uovu wake huharibu ufanisi na ustawi wa maisha ya baadae ya mtu. "Ili mwanaume aweze kuishi maisha ya kindoa ya furaha na ya usitawi ni muhimu kwamba lazima awe na uhusiano wa kiakili pamoja na mke wake. Hata hivyo, mwanamke hapaswi kabisa kuwa kibadala wa mwanaume na kamwe asimuigize katika kila kitu, kwa sababu kwa vile mwanamke hapendi kwamba mume wake awe kama mwanamke kwa njia hiyo hiyo mume hapendi kwamba mke wake awe na hali na tabia za mwanaume. "Ubora na sifa njema za mwanamke viko kwenye moyo wake na hisia zake na sio katika hoja na akili yake na mwanaume anatumia na kufaidi upole wake na sio hekima na elimu yake." Oliver Wendell Holmes anasema: "Siku zote tumeelekea zaidi kwa mwanamke ambaye ana moyo na hisia kuliko kwa mwanamke ambaye ana 61

11:27 AM

Page 61


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio mantiki na uwezo wa kiakili. "Wakati mwingine wanaume wanakuwa wenyewe wamejichoka sana kiasi kwamba wako tayari kusifia aina zote za sifa na tabia za mtu mwingine ambazo zaweza kuwa tofauti na za kwao." Anaendelea kusema: "Kama mtu ataniomba kueleza uthibitisho wa wema wa Mwenyezi Mungu nitasema katika kumjibu kwamba uthibitisho mzuri wa upole Wake kwetu ni wa tofauti ajabu ambao ameuweka katikati ya tabia ya mwanaume na mwanamke ili kwamba kwa njia hii waweze kuishi pamoja kwa amani na furaha." Henry Tubelov anasema: "Mwanamke mzuri lazima awe na sifa na tabia ambazo kwamba anaweza kuifanya nyumba kuwa sehemu ya utulivu na furaha kwa ajili ya mwanaume. Na kulifanikisha hili ni muhimu kwamba mwanamke lazima awe na uwezo wa kumuondolea mwanaume tatizo la kusimamia nyumba na hususan lazima amkinge kutokana na athari mbaya ya kukopa. Mwanamke lazima aonekane mwenye kupendeza na kukubalika mbele za macho ya mume wake na kwa mujibu wa vionjo vyake, kwa sababu vionjo vyake vinaafikiana na tabia yake na hakuna upendo unaoweza kupatikana bila hivyo. Kama katika maisha ambayo yamechanganyikana na mateso na shida nyumba sio mahali pa upendo na mapenzi. Kwa hakika haitakuwa sehemu ya utulivu na furaha, kwa sababu amani ya akili inaweza kupatikana tu chini ya hifadhi ya upendo na mapenzi. "Mwanaume hutegemea zaidi akili, busara, tabia ya kupendeza na moyo mkunjufu kutoka kwa mke wake kuliko ubembe (utamanishaji) na uigaji na hutamani zaidi upole wake wa moyo kuliko upendo wa kutia chumvi, hisia na hulka za ukaidi. "Kanuni ya maisha ya wanandoa ni 'uvumilivu na uimara'. Ndoa vilevile huhitajia sera maalumu kama serikali na wanandoa lazima watoe na kupokea, lazima wakubali na kukataa na lazima wawe na subira na uvu62

11:27 AM

Page 62


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio milivu. Sio muhimu kwamba mtu lazima awe kipofu dhidi ya hisia za wengine na kwamba hapaswi kuziona. Kitu pekee kinachohitajiwa ni kwamba lazima awe na nguvu za kutojali na lazima apuuze chochote kile anachokiona kwa huruma na upole. "Kutoka miongoni mwa sifa zote na tabia nzuri, uwastani ni wenye kufaa sana, muhimu zaidi na kudumu zaidi katika maisha ya ndoa, na kama tabia hii njema inaunganishwa na hali ya kujizuia, humfanya mtu kuwa mzoefu wa subira na uvumilivu na kumzoesha kukabiliana na shida na taabu kwa ustahimilivu, sio kutoa majibu kwa ajili ya maneno makali anayoweza kusikia, bali akae katika hali ya kutulia na katika hali ya ukimya mpaka hasira ya upande mwingine imeshuka. "Msemo kwamba 'maneno matamu huzima moto wa hasira' hutumika kwa kufaa zaidi kwenye maisha ya ndoa kuliko kwenye hali nyingine yoyote. Msemo mashuhuri wa Kiingereza unasema: 'Wasichana ni mahodari wa kufanya vishawishi, lakini masilahi yao yapo kwa kuwa wanapaswa kujua jinsi ya kutengeneza vitundu (mitego)'. "Kwa kawaida mwanaume anaweza kushawishika kwa urahisi sana kama ndege, lakini usalama wa malezi yao vilevile ni mgumu sana kama ule wa ndege. Kama mwanamke hawezi kuweka nyumba katika hali ya usafi katika hali ambayo mwanaume asingeweza kupata sehemu iliyo safi na ya kupendeza kuliko hiyo na kuweza kurudi humo kwa furaha baada ya kumenyeka siku nzima, masikini mwanaume huyo anastahili kuhurumiwa na kwa kweli anapaswa kuchukuliwa kwamba hana nyumba na ni mzururaji. Hakuna mwanaume mwenye busara anayeoa mwanamke kwa ajili tu ya urembo wake. Ni kweli kwamba hapo mwanzo urembo ni njia iliyofaa kumvutia na kumtamanisha mwanaume, lakini baadae ukakoma kuwa na athari yoyote katika maisha yake. Bila ya shaka, hatutaki kulaumu au kupuuza urembo au kuondoa thamani yake, kwa sababu urembo wa sura na mwili kwa kawaida ni dalili ya umbile lenye afya. Kwa upande mwingine tunachomaanisha ni kwamba kuoa mwanamke mrembo ambaye 63

11:27 AM

Page 63


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio hana maadili na nemsi za kiroho ni kosa kubwa ambalo kwamba hakuna marekebisho yaweyo kufanywa na hakuna fidia iwezekanayo. "Urembo wa nje hufifia na mara moja kuwa kitu cha kawaida wakati ambapo urembo wa kiroho na wema, katika muundo wowote utakaokuwa, siku zote ni mpya na wa kuvutia na pamoja na kupita kwa muda, badala ya kupungua mng'aro wake, siku zote huongezeka thamani na manufaa yake. Wakati muda takriban wa mwaka mmoja unapopita baada ya kufunga ndoa si mwanaume au mwanamke ambaye anakuwa makini sana kuhusu urembo wa sura ya mwingine. Kinyume chake wote kwa pamoja huangalia tabia na mwenendo wa kila mmoja wao." Duo Tow Copule anasema: "Wakati wa maisha yake mwanamume hawezi kupata msaada ulio mzuri kama mke mwema na mwenye tabia nzuri. Wakati wa maisha yangu nimeona watu wanyonge kiulinganishi ambao wameonesha nemsi kubwa na tabia nzuri katika masuala ya jamii, na sababu ya hili imekuwa kwamba wamekuwa na wake wenye tabia nzuri na wasafi ambao huwapatia msukumo kwa ajili ya kufanya kazi zao katika maisha ya ndoa na ambao huwaokoa kutokana na kuteleza na makosa." Kile kilichoelezewa kabla ni kielelezo cha Uislamu kuhusiana na haki za wanandoa. Sasa mwishowe tunakusudia kutaja haki za mwanaume na mwanamke moja moja. Amma kuhusu haki nyingine tungependa kuwashauri wasomaji kurejea kwenye vitabu juu ya somo linalohusika: (i) Ni wajibu kwa mwanaume kugharamia matumizi ya mke wake kama itakavyokuwa desturi. Matumizi haya yanajumuisha nguo, chakula, vyombo vya nyumbani, mtumishi na mahitaji mengine kulingana na hadhi ya mwanamke. (ii) Asimtie mwanamke kwenye shida na huzuni katika suala la matumizi ya maisha na lazima atoe njia za furaha kwake. (iii) Lazima amtukuze na kumheshimu mwanamke na asimkandamize na 64

11:27 AM

Page 64


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio kuumiza hisia zake. (iv) Asimlazimishe kufanya kazi ambazo hazifai kwa wanawake (kwa mfano, uchuuzi, kulima nk.) na hata majukumu ya nyumbani kama kufua nguo, kupika chakula na kuwaweka watoto katika hali ya usafi na nadhifu. Bila ya shaka, imependekezwa kwamba mwanamke anapaswa kufanya kazi za nyumbani na huduma zinazohusika kwa mume wake na watoto wake. (v) Asitilie maanani makosa na makosa ya kijinga ya mwanamke na amsamehe na iwapo wakati mwingine anakuwa mkorofi lazima avumilie na kuwa na subira na asiwe na wasiwasi usio wa lazima dhidi yake. (vi) Lazima awe makini katika kuweka mwili na nguo zake katika hali ya usafi. (vii) Lazima aseme mambo mazuri na kutoa majibu mazuri kwa maswali yake. (viii) Lazima amshawishi mwanamke kufanya mambo mazuri na lazima amzuie kufanya mambo maovu. (ix) Kama mwanamke akijifungua mtoto wa kike asimfanyie vibaya na lazima asiifikirie hiyo kama bahati mbaya. (x) Asitengane naye. (xi)

Ni wajibu juu ya mwanamke asimkorofishe mume wake na asiumize hisia zake kwa ukorofi wake, tamukali na lugha ya matusi.

(xii) Inapendekezwa kwa mwanamke kumsaidia mume wake katika kazi mbali mbali na hususan lazima achukue majukumu kusimamia 65

11:27 AM

Page 65


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio mambo ya nyumbani kama vile kupika chakula nk. (xiii) Lazima ampende sana mume wake na asishindwe kumpa sifa stahiki na heshima. (xiv) Ajipambe kwa ajili ya mumewe tu. (xv)

Asitumie mali ya mumewe bila ruhusa yake hata kwa njia ya sadaka na msaada.

(xvi) Lazima alinde heshima ya mumewe akiwa mbele yake na akiwa hayupo. Kutenda kwa mujibu wa maelekezo haya hufanya maisha ya wanandoa kuwa ya furaha na ustawi wa familia yao unakuwa wa hakika.

Uzoefu umeonesha kwamba takriban matatizo yote ya familia ni matokeo ya ujinga wa mume na mke kuhusu wajibu wao au kushindwa kwa upande wao kutekeleza majukumu yao. Wanaume na wanawake wenye imani ambao wanaamini wenyewe kuwa chini ya wajibu wa kutekeleza amri za Mwenyezi Mungu, hutenda kwa mujibu wa amri hizo bila kusita na mwishowe hujaaliwa baraka katika ulimwengu huu na halikadhalika kesho Akhera.

HADHI YA MWALIMU Kama ubora wa watu unakadiriwa juu ya msingi wa ubora wa kazi zao, hapana shaka walimu watapata moja ya vyeo vitukufu, kwa sababu watu wanaotokana na tabaka hili wanafanya moja ya jukumu muhimu na nyeti zaidi. Na matokeo ya kazi zao yanaweza kulinganishwa na yale machache 66

11:27 AM

Page 66


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio sana ya matabaka mengine. Daraja ya juu sana ni ya Mitume wa Mwenyezi Mungu, ambao wamechukua jukumu hili na waliaminishwa kazi ya kusomesha na kuelimisha watu.

Mwalimu wa Mitume ni Allah na ukweli huu umeelezewa kwa uwazi katika Qur’ani Tukufu kwa kurudiwa rudiwa mara kadhaa.

Wanafunzi na masahaba wa Nabii Isa (a.s) walimuita (Nabii Isa) 'mwalimu wa mema' na hapana shaka msemo huu umetumika kumtukuza yeye. Kwa wale ambao wana wajibu kwa njia moja au nyingine, kwa ajili ya masomo na mafunzo ya wengine ni heshima ya kutosha kwamba kazi yao inaangukia ndani ya masafa ya kazi za Mitume. Na kama siku moja wanadamu wanatabakishwa kutokana na mtazamo wa kazi zao, wataunda sehemu ya tabaka la wafadhili wakubwa wa wanadamu. Wakati Mitume wanapata shida na dhiki kubwa na hawategemei malipo yoyote kutoka kwa watu, wamejitahidi kuwavuta waja wa Allah kwenye matendo mazuri na nemsi na kuwashehenesha silaha za elimu na imani. Hawakuacha juhudi yoyote katika suala hili na hawana lengo lingine ila kuwaongoza watu. Nabii Isa mwana wa Mariamu (a.s.), aliwatendea wanafunzi wake kwa upole sana, aliwafanya wakae pamoja naye kama marafiki na kutoa maelekezo kwao. "Baada ya kumudu kile alichowafundisha aliwatuma kwenda maeneo mbali mbali ili kwamba wawafundishe wengine kile walichojifunza. Hakuna mwalimu anayefanya hivi, hata kama ana kazi ya kidini. Kwa 67

11:27 AM

Page 67


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio kawaida mwalimu hujaribu kufundisha watu yeye mwenyewe binafsi na kuwa na mawasiliano na wanafunzi wote katika darasa. Kwa mfano, wakati Socrates alipotaka kufundisha kitu fulani kwa mtu alifanya hivyo yeye mwenyewe. Bila ya shaka alikuwa na wanafunzi ambao wamefikia cheo cha ualimu lakini kamwe haikusikika kwamba aliwatuma kwenda sehemu mbali mbali kufundisha wengine". (Gilbert Height, The Art of Teaching, uk. 175). Nabii Isa (a.s.) mwana wa Mariamu aliwaambia wanafunzi wake: "Nina haja ya kitu fulani kutoka kwenu naomba mkifanye." Wote wakasema: "Tutafanya chochote utakachotuambia tufanye". Nabii Isa akasimama na kuosha miguu yao. Wakasema: "Ewe Mtume wa Allah! Ingekuwa vizuri kama sisi tungeosha miguu yako." Akajibu: "Mtu mjuzi ni mwenye kufaa zaidi kuliko yeyote yule katika kuwahudumia watu, na nimeonesha unyenyekevu huu na upole kwenu ili kwamba na nyie pia muweze kuonesha unyenyekevu kwa watu." (Wafi) Mitume wengine vilevile walifundisha na kuongoza kwa unyenyekevu na tabia njema na wakafanya wajifunze nemsi za ubinadamu na wema katika njia ya kimatendo. Mtukufu Mtume wa Uislamu (s.a.w.w.) ambaye alichanganya elimu na mafunzo alitumia kila nafasi kuwaongoza watu wakati wa mchana na usiku na ima akiwa safarini au akiwa amekaa mahali fulani. Aya za Qur’ani Tukufu na maneno ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ilikuwa ni masomo ambayo yalipenyezwa kwenye masikio ya watu na masomo haya yakaleta mapinduzi makubwa katika ulimwengu katika wakati ule muda wa chini ya robo karne ambao ulibadilisha mwelekeo wa umma, uliokoa watu kutokana na ibada ya masanamu, kuuwa watoto wa kike, mauaji, uhalifu na shida nyingine na kuwaongoza kwenye njia ya ustawi na ubinadamu.

68

11:27 AM

Page 68


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Imamu Ali (a.s.), mrithi wa kweli wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na yeye pia alichukuwa njia hiyo hiyo. Nahjul-Balaghah (tazama: Peak of Eloquence, ISP, 1984) ina sehemu za masomo ambazo aliwafundisha watu katika nyakati zinazohusika. Kila moja ya methali, maneno ya busara, barua, maagizo na hadithi nyingine ambazo zimekuja kutoka kwake ni hazina ya elimu na nemsi ambazo kwazo sio tu kwa wa rika lake bali wafuasi wake wote wamenufaika katika wakati wote mpaka sasa. Kwa maneno: 'Niulizeni chochote mnachotaka kabla sijatengana na ninyi', Imamu Ali (a.s.) aliwahimiza watu kuleta maswali yao na kumuuliza chochote walichotaka. Baada ya kuuliwa kishahidi kwa Imamu Ali (a.s.) utawala na mamlaka ya Bani Umayya ukawa ni kikomo cha shughuli za watukufu Maimamu, kukaa kwao nyumbani na kusimamishwa kwa mikutano yao ya kufundisha iliendelea mpaka wakati wa Imamu Baqir (a.s.). Hata hivyo, licha ya mashinikizo yote haya na mipaka, viongozi wakubwa wa Uislamu walitumia kila fursa kuwaelemisha watu. Wakati wa miaka ya mwisho ya maisha ya Imamu Muhammad Baqir (a.s.) Bani umayya walikuwa dhaifu na vilevile Bani Abbas walikuwa bado hawajapata madaraka. Nchi za Kiislamu zilikuwa zinawaka moto wa mapinduzi na katika muda huu haswa kati ya utawala wa Bani Umayya na Bani Abbas ilikuwa ni fursa iliyotumiwa na Imamu Baqir na Imamu Sadiq (a.s.) kuwaelemisha na kuwafundisha watu na kutangaza ukweli wa Uislamu na walianzisha mikutano yao ya kufundisha katika Msikiti wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) Madina. Katika shule ya Imamu Ja'far Sadiq (a.s.) zaidi ya wanachuo 20,000 walifundishwa, 4000 kati ya hao walianza masomo yao pamoja na katika wakati mmoja. Umuhimu wa shule ya Mtukufu Imam uko katika kuwafunza wanafunzi wake kwanza na kuwapa elimu baadae. Somo la kwanza alilofundisha lilikuwa kwamba ujuzi lazima upatikane kutenda juu yake na hekima lazi69

11:27 AM

Page 69


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio ma ipatikane ili kuhudumia dini na jamii na kunyanyua nafsi ya mtu. Takriban wasimuliaji wa hadithi 4000 wamesimulia hadithi kutoka kwa Imamu Ja'far. Walifanya kazi ya kukusanya na kuandika vitabu wakati wa uhai wake na kuandika vitabu 400 juu ya sheria (fiqh) ambavyo vinajulikana kama 'kanuni 400.' Vitabu vinne vyenye majina al-Kafi, Man La Ya Yahdhuhurul-Faqih, alTahdhib na al-Istibsar vimepatikana kutokana navyo. Jabir bin Hayyan, mmoja wa wanafunzi mashuhuri wa Imamu Ja'far Sadiq (.a.s.), alikuwa ni mkemia mashuhuri ambaye aliacha kitabu chenye kurasa 1000 zenye masomo ya Mtukufu Imam kama kumbukumbu yake. Muhammad bin Talha Shafi'i (amekufa 654 A.H.) anaandika hivi wakati alipokuwa anatoa maelezo ya maisha ya Imamu Ja'far Sadiq (a.s.): "Lulu za thamani mno zimekuwa zinapatikana kutoka kwenye bahari isiyo na mipaka ya ilmu ya Mtukufu Imam. Kumtazama humkumbusha mtu Akhera na kusikiliza khutba zake hufundisha mtu uchamungu na wema. Sifa na vipaji vyake vilikuwa havina idadi. Alikusanya pamoja ilmu na maadili bora na tabia yake hupatikana tu kwa Mitume na mawalii wa Allah." (Matalibus-Su'ul, uk. 81) Licha ya ukweli kwamba makhalifa wa Bani Abbas wamezuia kabisa shughuli zao, Maimamu wengine walijitahidi katika nyakati sahihi kuongoza na kuwafunza watu. Wakati ambapo mazingira yasiyofaa ya wakati hayakuruhusu watukufu Maimamu kuanzisha mikutano ya kielimu, walifundisha somo la wema na uchamungu kwa watu kwa tabia zao na elimu ya kimatendo ambayo kwa hakika ni yenye kufaa zaidi kuliko ya elimu ya maneno.

70

11:27 AM

Page 70


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Imamu Ali (a.s.) anasema: "Ni muhimu kwa mtu ambaye anajionesha mwenyewe kama kiongozi na mwongozaji wa watu, ajielimishe mwenyewe kabla ya kuelemisha wengine. Lazima awaongoze watu kwanza na tabia yake safi na baada ya hapo na kwa ulimi wake. Na mtu ambaye anachukua elimu yake, mafunzo na marekebisho, anastahiki heshima zaidi na sifa kuliko mwalimu ambaye hurekebisha watu". (Nahjul-Balaghah) Siri ya mafanikio ya Mitume ambao walikuwa walimu wa wanadamu ni kwamba, wao wenyewe walifanya yale waliyokuwa wakiwaamrisha watu kufanya na kujizuia na yale ambayo wanawakataza wengine kuyafanya. Walikuwa na imani kamili na matumaini katika yale waliyoyasema na chimbuko cha maneno yao kilikuwa ni kutoka kwenye nyoyo zao vilevile kilituama kwenye nyoyo za wengine. Bila ya shaka elimu na mafunzo yatolewayo na walimu na wafundishaji wa maadili ambao wenyewe wamejaaliwa na nemsi hufanya fikra nzuri sana isiyokoma juu ya wanafunzi.

Haki za Mwalimu Katika kaida za Kiislamu haki mbalimbali zimetajwa, baadhi ya hizo zimelezewa hapa chini: Imamu Sajjad (a.s.), Imamu wa nne anasema: "Haki iliyoamriwa na mwalimu wako juu yako ni kwamba siku zote lazima umtukuze na kumheshimu na chukulia kwamba ni penzi mno kujihusisha naye na kusikiliza maneno yake kwa makini na kukaa kumuelekea yeye na kujizuia kunyanyua sauti mbele yake. Kama mtu akiuliza swali wewe usitoe jibu kwalo umuache mwalimu ajibu yeye mwenyewe. Usizungumze na yeyote yule katika haddara yake. Usimtaje kwa ubaya mtu yeyote mbele yake na lazima umtetee kama watu wanamkashifu na kumzushia wakati akiwa hayupo. Lazima ufiche kasoro zake, mtukuze mbele za watu na jiepushe kushirikiana na maadui zake au kuwa adui kwa rafiki zake. Kama utatenda kwa mujibu wa 71

11:27 AM

Page 71


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio maelekezo haya malaika watashudia kwamba umetekeleza haki za mwalimu wako na umenufaika na ilmu yake kwa ajili ya kutafuta ridhaa ya Allah." (Biharul-Anwar, Jz. 2, uk. 42) Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: "Mtu ambaye anamfanya Mwislamu ajifundishe suala moja anakuwa bwana wake". Masahaba wakauliza: "Ewe Mtume wa Allah! Anaweza kumuuza?" Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akajibu: "Hapana. Lakini anaweza kumpa amri na anaweza kumzuia asifanye kitu chochote." (Biharul-Anwar Jz. 2) Imamu Ali (a.s.) anasema: "Haki ya mwalimu ni kwamba mwanafuzi hapaswi kumshambulia kwa maswali mengi na asitoe jibu mpaka mwalimu amuulize swali. Asimsisitizie juu yake katika suala lolote na asimlazimishe kuendelea na mjadala kama amechoka. Asimfanyie ishara kwa mkono au kwa jicho. Asimtaje yeyote kwa ubaya mbele yake na lazima amuheshimu akiwa mbele yake na halikadhalika akiwa hayupo. Kama akiwasili katika mkutano wake awaombee wote waliopo kwa ujumla na hususan mwalimu na lazima ampe heshima zake. Lazima akae mbele ya mwalimu kwa heshima sana na kama mwalimu anataka kitu fulani kifanyike lazima ajitahidi kutekeleza haja yake kabla ya wengine. Kama khutba ya mwalimu ikiwa ndefu asioneshe dalili za kuchoka. Hakika, mwalimu ni kama mti wa mtende na wanafunzi lazima wasubiri kunufaika kutoka kwake wakati muafaka utakapowadia." (Biharul-Anwar, Jz. 2) Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: "Wanyama wote watambaao wa aridhini, viumbe waishio wa angani na wakazi wa mbinguni na wa ardhini wanamuomba Allah kwa ajili ya ukombozi wa mwalimu ambaye huwaongoza waja wa Allah kwenye njia ya wema na ustawi." (Biharul-Anwar, Jz. 2, uk. 17) Mwanamke wa Kiislamu wa Madina alikuja mbele ya Bibi Fatima Zahra (a.s.) na akasema: "Mama yangu ambaye ni mzee sana na dhaifu, amekuwa na wasiwasi kuhusu baadhi ya masuala yanayohusiana na Sala na ameni72

11:27 AM

Page 72


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio tuma nije kwako ili nipate ufafanuzi wa hali hiyo." Bibi Fatima (a.s.) akasema: "Unakaribishwa kuuliza swali lolote." Mwanamke yule akamuuliza Bibi Fatima (a.s.) kuhusu tatizo fulani na akampa jibu. Kisha akauliza swali lingine na akapata jibu. Aliendelea kuuliza maswali mpaka akauliza maswali kumi na akapata majibu kwayo. Kisha yule mwanamke akasikia aibu na akasema: "Sitaki kukusumbua zaidi." Bibi Fatima (a.s.) akasema kwa upole: Unaweza kuuliza chochote unachotaka. Je, unafikiri kwamba kama mwanaume aliyeahidiwa malipo ya dinar 100,000 kwa kubeba mzigo mzito kuupandisha juu ya paa la nyumba atasikia kuchoka kwa kazi hiyo ukitilia maanani malipo mazuri aliyoahidiwa?" Mwanamke akajibu: “Hapana." Bibi Fatima (a.s.) akasema: "Ama kwa kila tatizo ambalo nalielezea kwako ninapata malipo kwayo mara elfu zaidi kuliko hivyo na inafaa kwamba nisisikie uchovu au kuchoka. Nimesikia kutoka kwa baba, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wa Allah, kwamba katika Siku ya Hukumu wanachuo wa Kiislamu watatokeza mbele ya Allah na kila mmoja wao atapewa malipo makubwa kwa kutilia maanani kiwango cha elimu na juhudi zilizofanywa na yeye kuwaongoza watu katika njia iliyonyooka". (Tafsir Imam Hasan Askari; Biharul-Anwar, Jz. 2, uk. 3) Imamu Ali (a.s.) anasema: "Kuna mambo matatu ambayo mtu hapaswi kuona aibu kwayo: kumkarimu mgeni, kusimama kama alama ya heshima kwa baba yake mtu au mwalimu wake na mtu kudai haki yake hata kama ingekuwa ni ndogo." (Ghurarul Hikam) Imamu Ja'far Sadiq (a.s.) anasema: "Kama mtu anafundisha tendo jema kwa mtu mwingine, mgao wa malipo ya kiroho kwa ajili ya tendo jema litakalofanywa na huyu aliyefundishwa mwisho vilevile yataolewa kwa 73

11:27 AM

Page 73


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio mwalimu." Msimuliaji alisema, alimuuliza Mtukufu Imam: "Je, mwalimu wa kwanza atapata mgao wa malipo ya kiroho kama mtu yule atafundisha elimu ile kwa mtu mwingine?" Mtukufu Imam akasema: "Hata kama akifundisha elimu hiyo kwa watu wote, mwalimu wa kwanza atapata mgao wa malipo ya kiroho pamoja na wote hao." Msimuliaji akauliza: Je, atapata mgao huo hata kama amefariki?" Imamu akajibu: "Ndio." (Basa'irud Darajat) Nukta muhimu ambayo kwayo walimu na wafundishaji wa maadili wanapaswa kuzingatia kwa ukamilifu ni kwamba ubongo wa mwanadamu, licha ya kipimo chake kidogo ni makazi ya akili na mantiki halikadhalika na kituo cha hisia za kugusa na mawazo. Kama tutatumia tu mantiki na akili na kujaribu kuimarisha na hatuzingatii mawazo, bila ya shaka yoyote ile tutakuwa tunatumia nusu tu ya ubongo na tutaipoozesha na kuiharibu nusu nyingine iliyobakia. Siku hizi katika nchi nyingi tatizo kubwa limejitokeza kwamba shule na vituo vya kielimu huchunga tu kipengele cha mantiki na akili cha watoto na vijana tu, vikijitahidi kumimina kwenye mbongo zao elimu ya kisayansi, historia na dhana na kanuni nyingine na vilevile wanafundisha mitazamo ya wanachuo kama mkanda wa kunasia sauti, lakini hakuna juhudi inayofanywa kutumia maoni na mawazo yao. Dr. Alexis Carrel, mwanafiziolojia mashuhuri Mfarasa anasema: "Umuhimu wa kwanza sio urutubishaji wa ustadi wa kiakili, bali ujenzi wa umbile asili la shauku ndani ya mtu ambalo litakuwa kama msaada kwa vipengele vyote vya ndani. Haja ya akili yenye uhuru wa kuchagua, hiari, kwa njia yoyote sio ndogo kuliko haja ya hisia za kusikia na kuona. Ni muhimu kwetu sisi kuendeleza tabia ya kutofautisha mema kutokana na maovu katika njia ile ile ambayo kwayo tunatofautisha mwanga na giza na sauti kutokana na ukimya na kisha tunapaswa kufanya kuwa wajibu wetu 74

11:27 AM

Page 74


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio kuepuka uovu na kutwaa wema. Hata hivyo, kuepuka vitendo viovu huhitaji akili nzuri na msingi wa kiroho. Ukuaji wa mwisho wa mwili na nafsi hauwezekeni bila ya kujitakasa. Wenye akili, wasomi na watu wenye busara hufuata kanuni za maisha mazuri. Wale ambao wanatafuta utukufu wa kiroho, kutokufuata kanuni hakuruhusiwi kwao. Kujiwekea nidhamu siku zote hupata malipo. Malipo ni uimara. Uimara huleta raha, ambayo haiwezi kuelezewa kwa ukamilifu na ambayo huwa upeo wa furaha ya maisha. Ingawa hali hii ya kifiziolojia na kisaikolojia yaweza kuwa ngeni kwa walimu wa kisasa na wanaelimu jamii wa Magharibi, bado inaunda elementi muhimu ya haiba ya mtu na ni kama uwanja wa ndege ambao kutoka hapo nafsi zaweza kuruka." Hazina ya elimu iliyokusanywa na mtu yaweza kuwa chanzo cha ustawi wake kama itaambatana na nemsi za uadilifu. Mtukufu Mtume wa Uislamu (s.a.w.w.), ambaye ni mfundishaji mkubwa wa maadili ya ubinadamu ameelezea kwa mukhtasari lengo la ujumbe wake katika sentensi moja. Alisema: "Nimeteuliwa kwenye kazi ya utume kwa ajili ya kukamilisha maadili mema." (Safinatul-Bihar, Jz. 1, uk. 411) Mitume ambao waliaminishwa jukumu la kuelemisha na urekebishaji wa ubinadamu waliweka msingi wa mafundisho yao juu ya kujitakasa na wakaweka umuhimu zaidi kwenye uadilifu na masuala ya hisi za moyoni kuliko kwenye kitu kingine chochote kile. Wakati ikielezea ujumbe wa Mtukufu Mtume wa Uislamu (s.a.w.w.), Qur’ani Tukufu inataja kwamba kujitakasa lazima kupatikane kabla ya elimu na inasema:

75

11:27 AM

Page 75


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio

“Yeye ndiye aliyeleta Mtume katika watu wasiojua kusoma, anayetokana nao, anawasomea aya Zake na kuwatakasa na kuwafunza Kitabu na hekima, na ingawa kabla (ya haya) kwa hakika walikuwa katika upotovu dhahiri". (62:2) Kabla ya umri wa miaka ishirini Abu Ali Sina alikuwa amekwisha jifundisha sayansi zote na sanaa zilizokuwepo katika wakati wake na alikuwa mtaalamu katika kila nyanja. Siku moja aliwasili katika duru ya masomo ya Abu Ali Maskuya, ambaye alikuwa msomi sana na msomi mashuhuri wa wakati wake na alikuwa hususan bingwa na muoni mzuri katika maadili na masuala ya kimaelekezo. Taharaatul A'raaq ni moja ya vitabu alivyoandika. Abu Ali Sina kwa jeuri alitupa lozi (kokwa) ambayo alikuwa ameishika mkononi mbele ya Maskuya na akamumbia akokotoe hesabu ya eneo lake. Abu Ali Maskuya alimpa Abu Sina sehemu ya kitabu cha Kitabul-Akhlaaq (Kitabu cha maadili) na akasema: "Ewe kijana! Umhitaji zaidi wa kurekebisha maadili yako. Nenda karekebishe maadili yako kwanza na kisha njoo tena kwangu ili nikukotolee eneo la sehemu ya lozi." Hakusahau ushauri huu maishani mwake na kwa kuuweka akilini na kutenda kwa mujibu wake kamwe hakutoka kwenye njia sahihi ya maisha. (Tarikh-i 'Ulum-i 'Aqli dar Islam). Mwanachuo wa Kifaransa H. Mossiear anasema: "Lazima ithibitishwe kwa wanafunzi kwamba kuna vitu vingine vya thamani vilevile mbali na ilmu na kuna njia nyingine za uainishaji vilevile kwa watu binafsi na mataifa, mbali na elimu."

76

11:27 AM

Page 76


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Kipaji kwa ajili ya kazi za kiufundi, upatikanaji wa utajiri na njia za ustawi wa umma, uwezo kwa ajili ya utawala au ugunduzi na vipengele vingi ambavyo vina athari kubwa ya kijamii. Mbali ya yote haya na vilevile juu ya ilmu kunakuwepo kipengele kingine ambacho kinajumuisha wema na uchaji." (Parvarish-i Zahn) Imamu Ali (a.s.) alimuambia mtoto wake, Imamu Hasan: "Hakika hekima inakuwa na uhuru mkubwa kutokana na kuhitaji, na ufukara mkubwa kabisa ni ujinga na upumbavu. Kitu cha kutisha sana ni majivuno ya mtu, na tabia yenye thamani sana ni yenye maadili mazuri." (Nahjul-Balaghah)

Wajibu wa Mwalimu Andre Maurois, mwandishi mkubwa wa Kifaransa, anaandika hivi kuhusu mwalimu wake, Emil Chartier: "Sifikirii kwamba ni mwenye deni kubwa kwa baba yangu kama kwa mwalimu huyu, kila ninachojua ni matokeo ya elimu niliyopata kutoka kwake". Ushuhuda uliofanywa na mwandishi huyu mkubwa na watu wengine mashuhuri kuhusu fikra kubwa iliyofanywa na mwalimu na matukio mengi ya kihistoria kwa ukamilifu hudhihirisha umuhimu wa wajibu unaofanywa na walimu. Mwalimu ambaye anatambua wajibu wake muhimu, na akatekeleza kazi yake kwa ungalifu anaweza kuacha fikra ya kudumu kwa watu kama kumbukumbu na ambayo itakuwa kama mwongozo, kama usemi maarufu wa Kiingereza unavyosema: "Kama Kristo alifufua watu mwalimu anaweza kuleta uhai kwa taifa." Historia inaonesha kwamba watawala ambao wamepata elimu sahihi na mafunzo mazuri wakati wa utoto na ujana wao kutoka kwa walimu hodari na waaminifu hufuata tabia nzuri wakati wa utawala wao.

77

11:27 AM

Page 77


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Umar bin Abdul Aziz, licha ya kuwa jamaa wa falme ya Bani Umayya, wakati wa ukhalifa wake alifuata sera tofauti mbali na zile za makhalifa wengine wa Banu Umayya, na kama alivyoshuhudia mwenyewe, ilikuwa ni kwa ajili ya mafundisho ya mkufunzi wake kwamba takribani alijiepusha na vitendo vya upotofu na makosa. Anasema: "Nilikuwa nimejishughulisha na masomo mjini Madina na nilikuwa nasoma kwa Ibn Mas'ud. Alisikia kwamba mimi pia namtukana Imam Ali kama wanavyofanya wanafamilia wengine wa Banu Umayya. "Siku moja nilimtembelea mkufunzi wangu. Nilikumta anaswali. Nilikaa chini na kusubiri mpaka alipomaliza kuswali. Kisha aligeuka na kuniambia: 'Ni lini ulijua kwamba baada ya Allah kuridhishwa na Waislamu ambao walipigana vita vya Badr na kula kiapo cha utii kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kule Hudaibiya, baadaye aliwakasirikia?' Nilijbu kwamba sijasikia kitu kama hicho. Akasema: 'Sasa ni vipi nasikia hivyo kuhusu wewe kuhusiana na Imamu Ali?' Nilimueleza kwamba naomba msamaha kutoka kwa Allah na halikadhalika kutoka kwake mwenyewe, na kuanzia siku hiyo na kuendelea niliacha kumtukana Imamu Ali." (Kamil ibn Athir, Jz. 5) Mazungumzo ambayo yalifanyika kati ya mwalimu na mwanafunzi yalikuwa mafupi sana na hakuna kati yao aliyefikiria kwamba maneno haya yatakuwa ni chanzo cha mapinduzi makubwa katika nchi za Kiislamu. Hata hivyo, maneno yaliyotolewa na mwalimu siku hiyo yalijichapisha ndani ya moyo wa mtoto na kumvutia sana. Miaka michache ilipita. Mtoto alikua na kupata nafasi miongoni mwa watu mashuhuri katika jamii. Mambo yasiyotegemewa na matukio mbali mbali yalileta mabadiliko makubwa katika nchi, yalimuweka mtoto wa wakati ule katika kiti cha Ukhalifa na kumpa utawala wa mambo ya mamilioni ya watu mkononi mwake. Maneno ya mwalimu yalikuwa mbegu ambayo ilipandwa ndani ya moyo wa mtoto siku ile. Wepesi uliotolewa na utawala na ufalme uliirutubisha 78

11:27 AM

Page 78


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio mbegu ile na hatimaye ikapata umbo la mavuno matukufu ambayo kwayo mamilioni ya watu walinufaika na wanaokolewa kutoka kwenye uasi wa kidini wa aibu wa kumtukana Imamu Ali." (Kudak, Jz. 2, uk. 32) Huu ulikuwa ni mfano mmoja wa athari kubwa ya maneno ya mwalimu na matukio mengi kama hayo yanaonekana katika historia.

Wote Tunapaswa Kuwa Walimu Heshima ambayo imepewa nafasi ya mwalimu katika maelezo ya viongozi wa Uislamu haishii kwa watu ambao wanashughulika na taaluma ya elimu. Kwa upande mwingine inahusu kila mtu ambaye humfanya mtu kujifundisha kitu fulani chenye manufaa. Ni dhahiri kwamba neno 'mwalimu' kwa uwazi linahusu wale ambao wanajishughulisha na utoaji wa elimu. Hata hivyo, kila mtu, katika hali yoyote atakayokuwa nayo mtu, anaweza na anapaswa kuwa mwalimu. Lazima awafundishe wengine kile anachojua, kuwaonesha njia ya ustawi na furaha na kujaribu kuwaongoza wenzake na ndugu zake katika imani ili kwamba aweze kubarikiwa na malipo ya Mwenyezi Mungu katika ulimwengu huu na halikadhalika katika wa kesho Akhera. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: "Kuna mambo manne ambayo ni muhimu kwa watu wenye busara miongoni mwa wafuasi wangu: (i) kusikiliza maneno yenye busara; (ii) kuyaweka kwenye kumbukumbu; (iii) kuyafanyia kazi na kutenda kwa mujibu wake; (iv) kuwafundisha wengine kile alichojifundisha". (Kanzul Fawa'id, Karachaki) Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) vilevile anasema: "Miongoni mwa sadaka ambazo mtu anatoa hakuna iliyo na thamani kama kutoa ilmu na hekima kwa wengine." Anaendelea kusema: "Hakuna zawadi iliyo na thamani kama ile ambayo mtu anapaswa kumuambia ndugu yake Mwislamu neno 79

11:27 AM

Page 79


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio la kweli kwa njia ambayo kwamba anaongozwa kwenye njia ya Allah na kuondokana na upotofu." Imamu Ali (a.s.) anasema: "Sadaka ya shukurani itolewayo na wanachuo wasomi kwa ajili ya neema ya ilmu ambayo Allah amewapa ni kwamba lazima watoe elimu yao hiyo kwa wale wanaostahiki." Imamu Ja'far Sadiq (a.s.) anasema: "Siku ya Hukumu Allah atawaita mbele Yake ulamaa na wanachuo na halikadhalika na wachamungu na waswalihina. Kisha wachamungu wataambiwa kwenda Peponi na wanachuoni wataamriwa kusubiri ili kuwaombea watu kwa ajili ya taabu walizopata katika njia ya mwongozo wao na marekebisho." (Biharul Anwar, Jz. 2, uk. 16) Sa'di, mshairi mashuhuri wa Kifarsi anasema: "Mchamungu mmoja alitoka kwenye nyumba ya utawa na akaja kwenye taasisi ya kidini, akaachana na fikra ya kujihusisha na zuhd (utawa). Nilimuuliza: 'kuna tofauti gani kati ya mwanachuo na zuhd kiasi kwamba umechagua njia hii kuwa ni bora kuliko hiyo?' Alijibu: 'Ni kwamba zuhd anataka kuvuta joho lake tu kwenye mawimbi ya bahari ambapo mwanachuo hujitahidi kuokoa watu wanaozama baharini.'" Kilichosemwa hapo juu ni maelezo mafupi na mukhtasari wa nafasi ya mwalimu na kazi yake ya uangalifu, na wajibu wenye manufaa katika jamii na halikadhalika na malipo yaliyowekwa na Allah Azza wa Jalla kwa ajili ya walimu wenye huruma na wakarimu. Tunataraji kwamba, kuweka katika mtazamo mambo yote haya, sisi wote tutafanya kazi zetu kwa mujibu wa mwongozo, elimu na mafunzo ya wenzetu hususan mwongozo wa watoto na vijana katika njia sahihi ili kwamba tuweze kufaidi neema za Mwenyezi Mungu katika ulimwengu huu na halikadhalika na kesho Akhera.

* * * * * 80

11:27 AM

Page 80


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio

UREJESHAJI WA AMANA KATIKA UISLAMU Uislamu haukuwa tu chanzo cha mabadiliko katika maisha ya mtu au msingi kwa ajili ya harakati za mwanadamu au sababu ya kurukia kwenye maendeleo na ukamilifu. Kwa upande mwingine umeupa maisha mapya na uhai mpya kwa ubinadamu, na kwa kweli kwa ujio wa Uislamu, mwanadamu alichukua msingi mpya wa maisha. Mwanadamu alikuwepo ulimwenguni hata kabla ya Uislamu. Hata hivyo, alikuwa kiumbe mbali na ustaarabu na alikuwa amemezwa katika maonevu mengi, uchafu mwingi, ushirikina na ibada ya sanamu, uhalifu na uuwaji wa ndugu na maelfu ya maovu ya kibinafsi na kijamii. Ulinganishi mfupi kati ya hali ya mwanadamu kabla ya Uislamu na hali yake baada ya ujio wa Uislamu hutujulisha jinsi alivyopata maisha mapya. Wakati wa kipindi cha chini kidogo ya robo karne, Uislamu uliwaleta watu ambao walikuja kuwa mfano wa hali ya juu sana wa ubinadamu na sababu ya fahari kwa ajili ya jamii ya binadamu. Moyo wa uchaji Mungu na wema ulipulizwa kwa watu. Uuwaji wa ndugu na umwagaji damu ukabadilika na mahala pake pakachukuliwa na huruma na uhisani. Ujamaa na undugu ukachukua sehemu ya maonevu na ubinafsi. Haki, uadilifu na heshima juu ya haki za wengine ikachukua nafasi ya udhulumaji na uchokozi. Mafunzo ya Kiislamu yakafundisha masomo bora zaidi kwa Waislamu na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akawaita watu kimatendo kwenye haki/uadilifu, urejeshaji wa amana na sifa nyingine nzuri.

81

11:27 AM

Page 81


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Urejeshaji wa amana kwa wenyewe ambalo ni somo tunalokusudia kujadili, ni moja ya masuala ambayo yana ushawishi usiokanushika juu ya maendeleo na ustawi wa jamii za wanadamu, na Uislamu umeweka umuhimu mkubwa kwenye hilo. Kitu kinachofanya urejeshaji wa amana kuwa suala la muhimu ni athari yake juu ya mtu binafsi na maisha ya kijamii. Wakati mmoja au mwingine katika kipindi cha uhai wake, kila mtu ima ameweka amana kitu fulani kwa mtu mwingine, au amepokea kitu kama amana kutoka kwa watu wengine, na mahitaji ya watu huhitaji kwamba mara chache lazima aweke amana za watu wengine katika ulinzi salama au kutoa vitu vyao wenyewe kuwapa watu wengine ili kuwekwa katika ulinzi wa salama. Kama watu wanakuwa makini kuhusu usalama na urejeshaji wa amana kwa wenyewe na imani ya wote pamoja inakuwepo katika jamii, ustawi wa watu utahakikishwa. Na kama uaminifu na ukweli unabadilishwa na kuwa khiyana na uovu imani ya watu wao kwa wao inaharibika na hatimaye matatizo mengi hutokea. Katika idadi ya aya zake, Qur’ani Tukufu imefanya kuwa wajibu kwa Waislamu kurudisha amana kwa wenyewe. Katika moja ya aya hizi inasema:

"Hakika Allah anawaamuruni kurudisha kile ambacho kimeaminishwa kwenu, kwa wenyewe wanaohusika.” (an-Nisa, 4:58) Qur’ani Tukufu inaendelea kusema: "Hakia wamefuzu wenye kuamini, ambao ni wanyenyekevu (kwa Allah) katika Sala zao… na wale ambao kwa amana zao na ahadi zao ni wenye kuzitekeleza (23:1, 2 na 8) 82

11:27 AM

Page 82


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Katika aya hizi Allah Azza wa Jalla anatangaza kwamba ni waumini tu ndio wanaostahiki kwenye ukombozi katika ulimwengu huu na wokovu katika Akhera na vilevile kufaidi bila ukomo neema za Peponi. Vilevile alizitaja tabia zao. Moja ya tabia za waumini wa kweli iliyotaja katika aya hizi ni kwamba wanakuwa waangalifu wa vitu walivyoaminiwa na kushikamana na maagano yao na kuyaheshimu. Mbali na aya mbili zilizotajwa hapo juu, kuna aya nyingine katika Qur’ani Tukufu ambazo kwazo uangalizi sahihi wa amana na urejeshaji wake umependekezwa. Urejeshaji wa amana vilevile umependekezwa katika khutba na simulizi nyingi za viongozi wa Uislamu. Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipomteuwa Mu'adh bin Jabal kama gavana wa moja ya majimbo ya Yemem, alimuelezea misingi ya kazi zake na akasema pamoja na mambo mengine: "Ewe Mu'adh! Napendekeza kwako kwamba uzingatie uchamungu na uaminifu katika khutba zako na kuheshimu ahadi zako, rejesha amana kwa wenyewe na achana na uovu." (Nasikhut Tawarikh, Jz. 5, uk. 267) Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesimuliwa akisema: "Yeyote yule ambaye ana hatia ya khiyana katika kutumia vibaya kitu alichoaminiwa katika amana si miongoni mwetu." (Wafi, Jz. 3) Katika hadithi nyingine Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anakosoa uzembe kuhusiana na amana na anasema: "Mtu ambaye anachukulia amana za watu kuwa ni kitu kidogo sio katika sisi, na mtu ambaye anatumia vibaya mali ya Mwislamu vilevile sio katika sisi." (Mustadrak, Jz. 2, uk. 505) Imam Muhammad Baqir (a.s.) anasema: "Ni wajibu juu yenu kuwa na mwendo safi na kujitahidi kufanya kazi zenu na kuwa muaminifu na kurejesha amana kwa mtu ambaye ameweka amana yake kwako, awe mtu mwema au mbaya. Kwa hakika kama muuwaji wa Imam Ali (a.s.) atawe83

11:27 AM

Page 83


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio ka amana kitu fulani kwangu, nitakirejesha kwake katika hali kamili." (Tuhaful Uquul) Abdur Rahman bin Siyaaba anasema: "Wakati baba yangu alipofariki mmoja wa rafiki zake alikuja nyumbani kwangu kutoa rambirambi za kifo chake na baada ya kuniliwaza aliuliza kuhusu hali yangu ya kifedha. Nikamuambia kwamba baba yangu hakuwa anamiliki kitu wakati wa kufariki kwake na mimi pia sina kitu. Alinipa dinari 1000 na akasema: 'Anzisha biashara na pesa hizi na tumia faida itakayopatikana kwa matumizi yako na ichunge sawasawa.' "Tabia yake ilinipendeza sana. Nilikwenda kwa mama na kumueleza jinsi Allah alivyotatua tatizo letu la kifedha. Wote tulilala kwa furaha sana usiku ule. "Siku iliyofuatia nilikwenda madukani na huko nikamkuta mtu ambaye alikuwa rafiki yake baba. Alinunua nguo kwa ajili yangu ambazo nilianza kuziuza pale pale pembeni. Niliendelea kuuza nguo na nikaanza kupata zaidi ya matumizi yangu ya nyumbani na biashara yangu ikastawi. "Msimu wa Hajji ukaja na nikaamua kwenda kuhiji kwenye Nyumba ya Allah kutekeleza ibada ya hijja. Kwa hiyo nilielezea nia yangu hiyo kwa mama. Mama yangu akasema: 'Bado unatakiwa kutekeleza jukumu muhimu zaidi nalo ni kwamba lazima urejeshe zile dinari 1000 kwa mtu yule ambazo aliziaminisha kwako na kuwa huru kutokana na deni.' "Nilitayarisha pesa zile na nikaenda kumkabidhi mwenyewe. Alisema: 'Ni nini kilichokufanya urudishe pesa hizi? Kama hazitoshi nitakupa zaidi'. Nikasema: Hapana. Ukweli ni kwamba nataka kwenda Makka kwa ajili ya hijja na nimeona ni bora nirejeshe pesa zako kabla ya kwenda hijja. Kisha nikafanya matayarisho muhimu na nikaenda Makka.

84

11:27 AM

Page 84


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Baada ya kutekeleza ibada ya hijja nilikwenda Madina. Kule nilipata nafasi ya mimi mwenyewe kuhudhuria mbele ya Imamu Ja'far Sadiq (a.s.). Kulikuwa na kikundi cha watu, na mimi nikiwa kijana nilikaa pembeni. Watu wakawa wanaeleza matatizo yao mbele ya Imamu mmoja baada mwingine na kuondoka baada ya kupatiwa majibu. Wakati wote walipoondoka Mtukufu Imam akaniuliza: 'Je, unalo la kufanya na mimi?' Nilijitambulisha mwenyewe kwake. Aliniuliza kuhusu baba yangu na nikamueleza kwamba amefariki. Akasema: 'Je, alicha mali yoyote kwako?' Nikasema: Hapana. Kisha akaniuliza: 'Umepata wapi pesa za kufanyia hijja? Nilimueleza kuhusu yule rafiki yake baba ambaye amenipa dinari 1000 ili kujishughulisha na biashara. Mtukufu Imam (a.s.) aliniuliza kwa wasiwasi mkubwa: 'Umefanya nini na pesa za mtu huyo?' nilijibu: Nimemrudishia mwenyewe. Akasema: 'Vizuri sana! Umefanya kitu kizuri sana'. Kisha akasema: 'Je, nikupe kitu ushauri kidogo?' Nikamuambia huo utakuwa ni ukarimu mkubwa kwake. Akasema: 'Lazima uwe mkweli kwa unayoyasema na lazima urejesha amana kwa wenyewe. Kama utashughulika na watu katika mwenendo huu utashiriki utajiri wao.'" (Wafi, Jz. 3, uk. 112) Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: "Mtu atendae kosa la amana na harejeshi mali ile aliyoaminishwa kwa mwenyewe atafanywa wakati wa kufa kwake kama ambaye hakuwa mfuasi wangu na atapasika na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu". (Man La Yahdhuhurul Faqih, Jz. 2, uk.198) Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: "Yeyote yule anunuaye mali ambayo imepatikana kwa njia za kuvunja amana anakuwa amehusika katika fedheha na dhambi ya mtu ambaye ametenda kosa hilo, na yeyote yule anunuaye mali akijua kwamba imeibiwa vilevile anakuwa amehusika katika fedheha na dhambi ya mwizi yule." (Iqaabul a’maal, uk. 47)

85

11:27 AM

Page 85


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Uvunjaji Wa Amana Katika hadithi nyingi yametajwa matokeo mabaya mno ya uvunjaji wa amana ili kwamba Mwislamu azingatie zaidi kwenye suala hili. AmirulMuminin Ali (a.s.) anasema: "Kama moja ya vitu vinne vikijitokeza katika nyumba huiharibu nyumba hiyo na kuikosesha ustawi wake na neema zake. (i) Uvunjaji wa amana (ii) wizi (iii) Unywaji pombe (iv) Uzinifu na mwenendo mchafu." (Khisal Shaykh Saduq, Jz. 1) Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: "Uwekaji salama na urejeshaji wa amana kwa mwenyewe anayehusika, humuongezea mtu utajiri, na kuifanyia (amana) mambo yasiyofaa huleta umasikini." (Qurbul Asnad, uk. 55) Watu wamekuwa na imani juu ya watu ambao ni wema na waaminifu na kwa matokeo ya imani hiyo wanaweza kwa urahisi kutatua matatizo ya maisha na biashara zao kustawi. Kwa upande mwingine hakuna anayetegemea juu ya watu wenye khiana na waovu. Wanatolewa katika jamii na kuhusika katika mateso na umasikini ambao ni matokeo ya khiana. Kurasa za historia vile vile zinaweza kutusaidia katika kuelewa kwa uwazi vipi khiana na uvunjaji wa amana ulivyotokea kwenye uharibifu: Katika wakati wa kipindi cha 'Azudud Dowla wa Daylami', kijana tajiri ambaye alitumia miaka yake mingi ya maisha yake katika maovu, ulevi na vifijo, alishikwa na maradhi na akabakia kitandani. Wakati alipopoteza matumaini yote ya kuishi aliahidi kwa Allah kwamba kama akipona ataacha maovu yote na kubadilika kuwa mchamungu. Allah akarejesha siha yake. Naye pia akatekeleza ahadi yake, akatupilia mbali zana za kamari na za burudani na pombe aliyokuwa nayo ndani ya nyumba yake na kuamua kwenda kutekeleza ibada ya Hija katika Nyumba ya Allah. 86

11:27 AM

Page 86


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Alikuwa na dinari 30,000 za dhahabu ambazo aliziaminisha kwa Jaji wa jijini pale, ambaye alikuwa na sifa njema kwa uaminifu wake, na akaenda zake Makka. Safari ilirefushwa. Alipatwa na ajali fulani njiani na akapata shida nyingi. Baada ya muda mrefu alirudi nyumbani kwake akiwa amechoka sana na kudhikika sana. Licha ya mateso yote haya alikuwa na furaha kwani alikuwa anazo dirham 30,000 taslimu za dhahabu na itawezekana kwake kuyatatua matatizo yote kwa njia ya pesa hizo. Hata hivyo, wakati alipomfuata yule Jaji kwa ajili ya kurejesha pesa zile yule Jaji akasema: 'Sikujui wewe na sikuchukua pesa yoyote kutoka kwako.' Kuomba na kusihi kote kwa mtu yule kulionekana kuwa ni bure. Hatimaye yule Jaji akamtishia kwamba kama atamsumbua zaidi atatoa ushuhuda kwamba alikuwa mwendawazimu na angempeleka kwenye hifadhi ya vichaa ambako atakaa huko mpaka mwisho wa uhai wake. Akiwa amekatishwa tamaa na kuchanganyikiwa mtu yule alikwenda kwa yule Jaji ambako alilia na kutokwa machozi kwa ajili ya bahati yake mbaya. Mmoja wa maafisa wa Azudud Dowla alikutana naye na akaelewa kuhusu tukio lile. Akalielezea tukio lile kwa Azudud Dowla. Azudud Dowla akamuambia mtu yule aende Isfahan akakae huko kwa muda wa siku kidogo. Kisha akamuita yule Jaji na akamuambia: ‘Kama unavyoona nimekuwa mzee na ulimwengu vilevile hauaminiki kabisa. Ninao watoto wadogo wa kiume na wa kike na nina wasiwasi kwamba kama nikifa ghafla na ufalme wangu ukiangukia kwa maadui zangu, watoto wangu watapata matatizo na mateso. Kwa hiyo, kwa hatua za tahadhari nimeamua kuweka akiba zaidi ya dinari milioni moja za dhahabu kwako 87

11:27 AM

Page 87


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio kwa vile wewe ni mtu mzuri na muaminifu, ili uje uwape watoto wangu baada ya kifo changu wasije wakapatwa na matatizo. Sasa nataka ujenge chumba cha chini ndani ya nyumba yako na usiku mmoja nihamishe pesa hizo kwa siri.' Yule Jaji akaonesha kukubali kwake kutekeleza jukumu hili na akamuacha mfalme. Alikuwa amefurahi sana na kuanzia wakati ule alianza kupanga mipango katika akili yake ya kujitwalia dinari milioni moja za dhahabu. Siku chache baada ya Jaji kumaliza kujenga chumba chini ya nyumba yake kwa ajili ya kuhamishia dhahabu zile, Azudud Dowla alimuita yule mtu aliyeonewa na akamuambia: 'Sasa nenda kwa yule Jaji na muambie akulipe pesa zako. Kama akikataa kufanya hivyo, mtishie kwa kumuambia kwamba utakwenda kumfungulia mashtaka kwangu'. Yule mtu akafanya kama alivyoelekezwa na mfalme. Wakati yule Jaji aliposikia vitisho vyake aliogopa kwamba kama habari hii itafikia masikio ya Azudud Dowla hataweka pesa zile kwangu. Kwa hiyo, akazungumza naye kwa ubashasha na akamrejeshea hesabu kamili ambayo imewekwa kwenye makasha mawili ya shaba. Yule mtu akapeleka pesa zile kwa Azudud Dowla na akamueleza kinachoendelea. Mfalme akawaamuru maofisa wake waende wakamlete yule Jaji, akiwa kichwa wazi miguu wazi mbele ya mfalme, wakamburuza katika hali ya fedheha. Kulikuwa hakuna muda wa kukanusha. Kila kitu kilikuwa wazi kabisa na bayana. Mfalme akesema: 'Laana ya Allah naiwe juu yako! Umekuwa mzee. Umefikia mwisho wa uhai wako. Uliteuliwa kwenye nafasi ya juu sana ya Jaji, lakini licha ya hivyo umefuja mali uliyoaminiwa kwako na Waislamu. Sasa nimetambua kwamba umekusanya mali na utajiri wote huu kwa njia ya rushwa na khiana na mali yote hiyo ni ya Waislamu.'

88

11:27 AM

Page 88


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Kisha, kama alivyoamuru mfalme, mali yake yote ilitaifishwa na akaondolewa katika kazi yake." (Siyasat Nama, Khawaja Nizamul Mulk, uk. 87) Mtu huyu alifikia mwisho mbaya na kupoteza mali yake yote, kazi yake, hadhi na kila kitu kingine kwa sababu ya kuvunja uaminifu aliopewa na kuhusiana na kiasi ambacho kiliwekwa amana kwake. Ni katika maana hii kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: "Kuheshimu amana humfanya mtu kuwa huru kutokana na mahitaji, na uvunjaji wa amana huleta umasikini na mateso."

Kurejesha Amana ni Wajibu wa Kibinadamu Inawezekana kwamba baadhi ya watu wanaweza wakafikiri kwamba urejeshaji wa amana ni lazima tu mwenyewe anapokuwa ni Mwislamu mchamungu na kama hali ni kinyume cha hivyo inafaa kuifuja. Hata hivyo, kama uzingativu mdogo utachukuliwa kwenye taratibu za Uislamu inakuwa dhahiri kwamba urejeshaji wa amana ni jukumu ambalo Waislamu lazima walitekeleze bila kujali utaifa, imani au kabila la mwenyewe. Kwa mujibu wa kanuni za kiislam kuna idadi ya wajibati ambazo Waislamu wanatakiwa kuzitekeleza juu yao wenyewe, na ambazo hazitekelezeki kwa watu wa itikadi tofauti. Vilevile idadi ya majukumu yameelekezwa kwa Waislamu kwa mafundisho ya Uislamu ambayo lazima wayatekeleze kwa kuzingatia watu wote, wawe wazuri au wabaya, na iwapo ni Waislamu au sio Waislamu, kwa mfano, urejeshaji wa amana na kuheshimu ahadi na maagano. Imamu Ja'far Sadiq (a.s.) anasema: "Kuna mambo matatu ambayo kwamba kuna mbadala na ambayo lazima yafanywe katika mazingira yote. Kwanza, ni kurejesha amana, iwe mwenyewe ni mtu mwema au mbaya. Pili, kutekeleza ahadi iwe mhusika ni mwema au mbaya. Na tatu, ni mtu 89

11:27 AM

Page 89


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio kuwatendea wema wazazi wake, wawe ni watu wema au watu wabaya." (Mustadrak, Jz. 2, uk. 505) Imamu Ali (a.s.) mrithi wa kwanza wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema hivyo wakati anatoa ushauri kwa Kumayl bin Ziyad: "Ewe Kumayl! Elewa na ujue kwamba haturuhusu mtu yeyote kuonesha uzembe katika suala la kurejesha amana kwa mwenyewe anayehusika na kama mtu yeyote ameninukuu kwamba nimetoa ruhusa hiyo atakuwa amesema uwongo na ataadhibiwa kwa Moto wa ghadhabu ya Mungu kwa uwongo wake huo. Naapa kwamba muda mfupi kabla ya kufa kwake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema mara tatu: 'Rejesheni amana kwa wenyewe wawe ni watu wema au watu wabaya na iwe kubwa au kidogo. Tekeleza wajibu wa kurejesha amana kwa mwenyewe hata kama ingekuwa isiyokuwa na maana kama sindano na uzi.'" (Mustadrakul Wasa 'il, Jz. 2) Mtu mmoja alimuambia Imamu Ja'far Sadiq (a.s.): "Mmoja wa sahaba zako anatokea kuwa na amana aliyowekewa na Banu Umayya na aliona ni halali kuifuja." Mtukufu Imam akasema: "Rejesha amana kwa wenyewe hata kama ikitokea kuwa ya Magi." (Wafi, Jz. 3, uk. 112) Mtu mmoja alimuuliza imamu Musa Kadhim (a.s.): "Mtu mmoja aliweka kitu chenye thamani kama amana kwa mmoja wa sahaba zako. Mwenye mali ile ni muovu, mpinga dini, katili na mchafu wa tabia. Mtu ambaye amechukua amana ile alikuwa kwenye nafasi ya kuizuia na haionekani kwamba atapatwa na madhara yoyote kwa kufanya hivyo. Je, anaweza kuizuia mali hiyo?" Mtukufu Imam akajibu: "Muambie arejeshe amana hiyo kwa mwenyewe, kwa sababu aliyempa amana hiyo alimchukulia kama mtu mwaminifu na hivyo akamuaminisha mali hiyo kwake kwa ajili ya uchaji wake." (Wafi, Jz. 2) 90

11:27 AM

Page 90


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Imamu Ja'far Sadiq (a.s.) anasema: "Kuwa mchamungu na ni muhimu kwako kurejesha amana kwa wenyewe. Hakika, kama muuwaji wa Amir'lMuuminin Ali angeaminisha kitu fulani kwangu kama amana kwa hakika ningeirudisha kwake." (Mustadrakul-Wasa 'il)

Ufujaji ni Dalili ya Ukosefu wa Imani Imenukuliwa kutoka kwa Imamu Musa Kadhim (a.s.) kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: "Mtu yeyote ambaye hayuko makini kuhusu urejeshaji wa amana atakuwa hana imani." (Mustadrakul-Wasa'il) Imamu Ja'far Sadiq (a.s.) anasema: "Mtu yeyote ambaye anazo sifa hizi tatu ni munafiki hata kama anasali na kufunga: (i) Mtu ambaye husema uwongo wakati wa mazungumzo. (ii) Mtu ambaye hutoa ahadi lakini hazitekelezi; na (iii) Mtu ambaye hufuja amana. (Tuhaful Uqul, uk. 316) Imamu Ali (a.s.): "Ufujaji wa amana ni chanzo cha unafiki.' Anaendelea kusema: "Jiepusheni kutokana na ufujaji wa amana kwa sababu ni dhambi mbaya mno na mtu anayeitenda atapasika kwenye mateso ya Moto wa Jahannam." (Ghurarul Hikam) Uislamu umekataza Waislamu kutenda hatia ya uvunjaji wa amana hata kama inahusiana na watu wale ambao wenyewe wana hatia ya dhambi hii na haukuruhusu kulipiza kisasi, kwa sababu khiyana na uvunjaji wa amana ni kitendo kichafu na haifai kwa Mwislamu kufanya mambo machafu. Imamu Ja'far Sadiq (a.s.) anasema: "Kama amekuchukulia wewe kuwa mtu muaminifu na akakuaminisha kitu fulani kwako, lazima urudishe amana yake katika hali nzuri na kama mtu ametenda kosa la uvunjaji wa amana kwako na akakusaliti, wewe usije ukamsaliti." (Wafi, Jz. 3, uk. 122)

91

11:27 AM

Page 91


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: "Usivunje amana na mtu ambaye amevunja amana na wewe, kwa sababu katika hali hiyo wewe pia utakuwa kama yeye." (Mustadrakul-Wasa 'il, Jz. 2, uk. 505) Aina Za Amana Amana haiishii kwenye pesa tu na hiyo ndio maana katika aya za Qur’ani neno hilo limetajwa katika wingi; Amanat. Allama Tabarsi anasema: "Amana ziko za aina mbili: (i) Amana ya Mwenyezi Mungu ambayo inajumuisha wajibu wa kidini kama Sala, Saumu nk., na (ii) Amana za watu kama akiba ya pesa, mikopo, shughuli za kibiashara, ushahidi nk. (Majmal'ul Bayan, Jz. 7, uk. 98) Kwa msingi huu tunapata kuzitambua safu za amana ambazo ni jukumu letu kuzilinda na kuzirejesha (kwa wenyewe). Qur’ani Tukufu ni amana ambayo Allah na Mtume Wake wameiweka kwa waislamu, ili kwamba kwa kutenda kwa mujibu wa amri zake, tutaweza kupata baraka katika ulimwengu huu na katika Akhera, na mbali ya kutenda kwa mujibu wa amri za Allah tunaweza kuwasilisha hayo kwa watu na kuwaelezea ubora sheria hii takatifu. Lazima tuwatukuze wanawake na watoto wetu kwa vile wao ni amana za Allah na lazima tuwaongoze kwenye njia iliyonyooka. Lazima tusipuuze kuwashauri ndugu zetu katika imani na kuwahurumia kwa vile tendo hili la kutoa ushauri kwa wengine vilevile ni amana ya Mwenyezi Mungu. Lazima tulinde kwa usalama siri za waja wa Mungu na tusihatarishe hadhi zao, kwa sababu siri za watu ni amana amabazo uvunjaji wake unahesabiwa kuwa ni dhambi. 92

11:27 AM

Page 92


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Imamu Ja'far Sadiq (a.s.) anasema: "Mtu hawezi kuchukuliwa kama mwaminifu mpaka ajaribiwe katika mambo matatu kama amana: (i) Mali (ii) Siri na (iii) Heshima. Kama anafaulu katika mambo mawili lakini akatenda kosa la kuvunja amana huyo si mwaminifu". Katika baadhi ya hadithi Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amechukulia mikutano ya marafiki kuwa ni amana na akasema: "Mikutano ni amana." (alKafi, Jz. uk. 49) Imamu Ja'far Sadiq (a.s.) anasema: "Mikutano ni amana na hakuna mtu mwenye haki ya kutoa siri ya suala lolote ambalo mtu anayehusika hataki siri hiyo itolewe, isipokuwa kama ikiwa kwa ruhusa yake au msikilizaji ni mtu mwaminifu au kinachosemwa ni katika kumsifia mtu huyo." (al-Kafi, Jz. 4, uk. 49) Wanafunzi ni amana katika mikono ya walimu wao na ni wajibu wa mwalimu katika nafasi hiyo kujitahidi kwa ajili ya mafunzo yao, elimu, uadilishaji wa maadili na kuzifanya imara imani zao kwa upole wa hali ya juu sana na shauku na kuwalea na kuwatoa kama wachamungu na watu wenye manufaa. Viwanda, tasnia, karakana ni amana katika usimamizi wa wakurugenzi, wahandisi na mameneja ambao lazima waweke katika fikra jukumu lao kama wadhamini, wasimamizi na kuziendeleza amana hizo na kunufaika kutokana nazo katika njia inayofaa. Utawala na kazi nyingine zote na vyeo ni amana na wale wanaoshikilia nafasi hizo lazima waweke katika fikra majukumu ambayo wanawiwa na Allah na Mtume Wake, kutekeleza wajibu wao kwa uaminifu mzuri na unyofu. Dereva ambaye anaendesha gari, mfanyakazi anayehusika na mashine za kilimo na za viwanda na fundi wa magari ambaye ameaminishwa jukumu 93

11:27 AM

Page 93


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio la kurekebisha mashine wote hawa ni wadhamini, ambao wanawajibika mbele ya Allah kwa kuhifadhi salama, kutunza na matengenezo sahihi ya amana zilizo kwenye malaka zao. Rasilimali za nchi za Kiislamu, ziwe za umma au za binafsi ni amana na yeyote anayezisimamia ana jukumu la kuziangalia na kuzirejesha kwa wenyewe wanaohusika. Mwisho tunarejelea kwenye kipengele cha sheria cha suala hili, kama ilivyoorodheshwa hapo chini: "Inapendekezwa kwamba amana inaweza kukubaliwa kutoka kwa watu, lakini wakati inapokubaliwa ni wajibu kwamba usimamizi sahihi kwayo lazima uchukuliwe." (Jaami’ Abbaasi, uk. 234) Anayestahiki kukubali amana ni yule mtu tu ambaye anaweza kuiweka kwenye ulinzi wa salama. Mtu ambaye anakubali amana atoe masharti ya kawaida na vifaa kwa ajili ya kuilinda kwake kwa usalama. Kama mwenye amana akitenga sehemu kwa ajili ya amana yake mdhamini haruhusiwi kuihamisha na kuipeleka sehemu nyingine. Kama amana imeharibika bila kosa lolote au uzembe kwa upande wa mdhamini, hawajibiki kwa hasara hiyo. Kama usalama wa amana kutoka kwa mwizi au kwa mdhulumaji unategemea juu ya kusema uwongo au kula kiapo, hilo linaruhusiwa, bali ni wajibu juu ya mdhamini kusema uwongo au kula kiapo cha uwongo na kama akishindwa kufanya hivyo mali iliyowekwa ikaharibika kwa matokeo hayo atawajibika kwayo. Wakati mwenye amana akitaka kurejeshewa amana yake, ni wajibu kwa mdhamini kuirejesha kwake, hata kama mwenye amana hiyo ni kafiri.

94

11:27 AM

Page 94


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Kama mdhamini akihofia kwamba amana hiyo wakati ambapo ikiwa mikononi mwake itaharibika lazima airudishe kwa mwenyewe au wakala wake." (Wasilatun Najaat, Sura ya Wadi'ah, Ayatullah Isfahani) Kilichosemwa hapo juu ni mfano wa maelekezo ya nguvu ya Kiislamu kuhusiana na umuhimu wa kuhifadhi na kurejesha amana (kwa wenyewe). Nukta ya kuvutia ambayo inahitaji kuzingatiwa katika suala hili ni kwamba wakati wa kupanga mjadala huu idadi ya vitabu juu ya maadili vilivyoandikwa na watunzi wa Magharibi vilitazamwa, lakini ilionekena kwamba licha ya umuhimu wa suala hili la urejeshaji wa amana, hakuna mahali popote imetajwa katika vitabu hivyo. Baada ya uchungzi zaidi tulifikia hitimisho kwamba kama ilivyo masuala mengine makubwa suala hili vilevile ni kipengele cha pekee cha Uislamu ambacho kimechunguzwa kwa undani kadiri zake zote pamoja na mvuto na maelezo elekezi na kuwaongoza Wislamu katika suala hili. Inatumainiwa kwamba kwa kuzingatia jukumu hili kubwa na kuitekeleza kiuwajibu, Waislamu kwa ujumla watatambuliwa kuwa wakutegemewa, waaminifu na umma wenye kuheshimiwa miongoni mwa mataifa ya ulimwengu na vilevile watajaaliwa na neema zake Allah Azza wa Jalla katika ulimwenu huu na Akhera.

KANUNI YA MAADILI MEMA Kama ambavyo mtu ana umbo la nje ambalo linaweza kuonekana kwa macho na linaitwa mwili wake, vilevile ana umbo la ndani ambalo linaitwa tabia zake. Na halikadhalika kama ambavyo inawezekana kwamba muonekano wa nje wa mtu kuwa wa kupendeza au wa kuchukiza, inawezekana pia kwamba tabia yake kuwa nzuri au mbaya.

95

11:27 AM

Page 95


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Umbo la nje la mtu limeundwa na viungo vyake kama kichwa, uso, mikono, miguu, macho, masikio nk., na umbo lake la ndani limeundwa na maadili yake, tabia na maumbile. Kama mtu ana viungo vyenye uwiano ambavyo vinapatana pamoja na uso na mwili, inasemwa kwamba ana umbo la kupendeza. Na kama viungo vyake sio vya kawaida na visivyo pendeza, umbo lake husemwa kuwa ni la kuchukiza. Halikadhalika, kama mtu ana tabia nzuri kama upendo na mapenzi, unyofu na uaminifu, uchaji na wema, uvumilivu na usahemevu, usikivu na unyenyekevu, husemwa kwamba ana tabia nzuri, na kama ni katili, mkorofi, ubinafisi, mwenye tamaa na mkaidi, husemwa kwamba tabia yake ni mbaya. Tabia zinazofaa kusifiwa huitwa 'mwenendo mzuri' au maadili mema' na tabia zisizo nzuri huitwa 'mwenendo mbaya' au 'maadili mabaya'. Hivyo 'mwenendo mzuri' ni pamoja na kuwa na sura ya wazi changamfu, hushughulika na watu kwa moyo mzuri na kuwa msikivu na muungwana katika ushirikiano na mazungumzo na watu wengine. Ingawa katika hali nyingi maadili mema na mabaya yana mwelekeo wa tamaa na ni zile tabia nzuri sana na tabia mbaya ambazo hujitokeza ndani ya mtu na polepole huchukua umbo la silka na tabia, anaweza kuzibadili kwa ungalifu mdogo na mazingatio na kuleta mabadiliko katika maadili yake. Akili ya kawaida na halikadhalika na dini hupendezewa na mtu mwenye maadili mema na kumlaumu mtu mwenye tabia mbaya, kwa sababu kila mmoja wao ana uwezo wa kubadilisha muundo wa tabia zake, na kama hali isingelikuwa hivyo, kusingekuwa na wakati wa ima kusifia au ukosoaji. Kwa kuzingatia ukweli huu wa kwamba kila mtu anaweza kuwa na maadili mema au mabaya kwa utashi wake mwenyewe, ni muhimu kwa kila mtu 96

11:27 AM

Page 96


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio kwamba lazima kwanza kabisa achukue hatua kurekebisha maadili yake na lazima aachane na tabia mbaya na afuate tabia nzuri kwa njia za juhudi za mfululizo na mazingatio. Moja ya mbinu ambazo hutusaidia sisi katika kurekebisha maadili yetu ni kuzingatia kwenye athari ya pekee ya maadili mema na halikadhalika kwenye hadhi za wale ambao wanayo na vivyo hivyo kwenye ubaya na uchafu wa maadili mabaya na mtu mwenye tabia hizo. Kanuni ya maadili ya viongozi wakubwa wa Uislamu ni mwongozo mzuri katika masuala haya. Hutukumbusha athari ya ndani ya maadili katika maisha yetu ya sasa na halikadhalika katika Akhera. Katika moja ya hadithi zake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ametaja umuhimu wa maadili mema katika maneno haya: "Lau watu wangejua tabia njema zina umuhimu gani na ni athari gani inaweka katika ufanisi wake wangejiona katika haja ya kuwa na maadili mema." (Biharul Anwar) Baadhi ya watu wanapuuza faida za maadili mema na hufikiri kwamba hazina maana kwao. Hususan wale watu ambao hujioana kuwa wao ni bora sana kuliko wengine katika suala la utajiri, elimu, hadhi nk., huyaona maadili mema kuwa ni kitu kilichopita kiasi na kisicho na maana, ingawa kwa kweli hakuna katika faida hizi inayoweza kuchukua nafasi ya maadili mema na mtu ambaye hana maadili mema anakosa thamani ya ubinadamu na sifa asilia. Kwa maneno mengine kama mtu akikosa utajiri, hadhi na elimu lakini akawa na maadili mema yeye ni bora zaidi kuliko watu ambao wana kila kitu isipokuwa maadili mema, kwa sababu maadili haya haswa hutuongoza na kutusadia kupata faida nyingine. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: "Hakika mtu mwenye maadili mema hupata ustawi katika ulimwengu huu na halikadhalika katika Akhera. 97

11:27 AM

Page 97


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio (Jami'us Sa'adat, Jz. 1, uk. 273) Furaha katika maisha ni moja ya neema ambazo zinaweza kupatikana kwa njia za mwenendo mzuri na watu wenye maadili mabaya wana jinyima wenyewe neema hii kubwa kwa mwenendo wao wenyewe. Imamu Ja'far Sadiq (a.s.) anasema: "Hakuna maisha ambayo yanakubalika na kupendeza zaidi kuliko yale yanayoendeshwa kwa tabia njema". (Ilalush Sharaaya) Vilevile alisema: "Yule ambaye maadili yake ni mabaya anajiingiza mwenyewe kwenye mashaka na mateso." (Jami'us Sa'adat, Jz. 1, uk. 271) Imamu Ali (a.s.) anasema: "Tabia njema ni rafiki mzuri wa mtu katika maisha (Biharul Anwar, Jz. 77, uk. 396) Watu hupenda kujihusisha na watu wenye maadili mema kwa vile tabia njema ina haiba ya kuvutia ambayo huwavuta watu kwake. Mtukufu Mtume wa Uislamu (s.a.w.w.) alikuwa ana maadili bora zaidi na Allah amesifia maadili yake katika Qur’ani Tukufu katika maneno fasaha zaidi na anasema: "Na hakika wewe una tabia tukufu". (68:4) Allah vilevile ameelezea katika aya nyingine sababu ya watu kuelekea kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na ameichukulia hiyo kuwa ni matokeo ya maadili yake mema mno, upole na tabia nzuri:

“Basi kwa rehema ya Allah umekuwa mpole kwao na kama ungekuwa mkali mshupavu wa moyo, wangekukimbia..." (3:159)

98

11:27 AM

Page 98


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Utendaji uliyofanywa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa watu, hata kwa waabudu masananmu na washirikina, ulikuwa umetegemea kabisa juu ya upole, tabia njema na maadili ya kibinadamu. Wasimuliaji wa hadithi wameandika hivyo kuhusu maadili yake: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alijihusisha na watu na hakumkimbia yeyote aliyekuwepo naye. Alitoa heshima kwa wakubwa wa kila taifa. Kama mtu akiomba kitu huitekeleza haja zake, na kama hiyo ilikuwa haiwezekani humridhisha mtu yule na upole mkubwa. Alikutana na kila mtu kwa uchangamfu. Alichukia kwa ajili ya mwenyezi Mungu lakini kamwe hakukasirika kwa sababu zake mwenyewe. Wakati wote alikuwa na tabasamu midomoni mwake. Hakuwa mwenye jazba na mkali. Kamwe hakutumia lugha chafu au ya matusi. Kamwe hakutafuta makosa ya yeyote. Anas bin Malik anasema: "Nilimtumikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa muda wa miaka kumi. Katika kipindi chote hiki kamwe hakuwa mkali kwangu. Kama nilishindwa kufanya kitu hakuniulizi ni kwa nini sikufanya kitu hicho. Wakati mwingi alikuwa akifungua saumu yake kwa maziwa kidogo tu au mkate ulioloweshwa kwenye maji. “Siku moja kwa bahati, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alichelewa kuja nyumbani. Kwa kufikiria kwamba huenda amekwenda kula chakula cha jioni sehemu nyingine, niliyanywa maziwa mimi mwenyewe. Aliwasili baada ya muda kidogo na niliwauliza masahaba zake iwapo amefuturu na wakajibu kwamba bado hajafuturu. Nilihuzunika mno na vilevile niliogopa isije akaniuliza chakula chake. Hata hivyo, hakusema chochote kuhusiana na hili mpaka adhana ya Sala ya al-Fajr na aliendelea na saumu yake siku iliyofuatia bila ya kula kitu chochote. “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikaa na masahaba zake kama marafiki wa karibu. Alikaa na kuongea nao katika hali ya kirafiki. Alikuwa mpole kwa watoto wao na aliwafanya wakae katika magoti yake. Aliulizia kuhusu hali za wagonjwa. Hakuamini katika ubaguzi wa aina yoyote kati yake na 99

11:27 AM

Page 99


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio watumwa wake na wajakazi katika suala la chakula na mavazi. “Kama alikuwa juu ya kipando hakutaka mtu yeyote kutembea pembeni pamoja naye. Amma alimfanya na yeye apande au alimuambia: "Unaweza kwenda na tutakutana sehemu fulani". Mmoja wa wenyeji wa Madina alimkaribisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na masahaba zake watano kwenye karamu ya chakula. Wakati walipokuwa wanakwenda nyumbani kwa mwenyeji yule walikutana na mtu njiani na yeye vilevile alifuatana nao. Walipokaribia karibu na nyumba ya mwenyeji Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamuambia yule mtu: Mwenyeji hakukukaribisha wewe. Utabakia hapa ili niweze kuongea naye kuhusu wewe na nipate ruhusa kutoka kwake kwa ajili ya wewe kushiriki katika karamu." Kama akipeana mkono na mtu hakuutoa mkono wake mpaka yule mtu mwingine ameutoa wa kwake, na kama mtu alikaa karibu yake hakuamka mpaka mtu yule mwingine ameamka pale alipokaa. Kamwe alikuwa hanyooshi miguu yake mbele ya mtu yeyote. Alimtakia mema kila mtu. Alimheshimu kila mtu aliyekuja kumuona na wakati mwingine hutandaza joho lake kwa ajili yake ili akalie juu yake. Aliwaita masahaba zake kwa majina yale wayapendayo wao. (Safinatul Bihar, Jz. 1, uk. 415) Idadi kubwa ya washirikina waliingia katika Uislamu kwa ajili ya kuvutiwa kwao na maadli ya hali ya juu na tabia za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Ili kuukwepa Uislamu Adiy bin Hatim Ta'i alikimbilia Syria na akakaa kule na wenzake wapinzani wa dini. Dada yake ambaye alikuwa mwanamke mwenye busara alimshauri kwenda Madina na kukutana na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Adiy anasema: "Wakati nilipowasili Madina nilikwenda Msikitini na nikajitambulisha mwenyewe mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Baada ya kunitambua alisimama kutoka sehemu aliyokaa na akanichukua mpaka 100

11:27 AM

Page 100


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio nyumbani kwake. Kwa bahati bibi kizee mnyonge alikuja mbele yake kule njiani. Kwa muda kiasi Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisimama kwa miguu yake na akamsikiliza mwanamke yule alichosema na akamjibu kwa maneno ya upole. Nikajisemea mwenyewe: 'Wallahi! Tabia ya mtu huyu sio ile ya mtawala mwenye tamaa'. Tulipofika nyumbani alikunjua tandiko lilotengenezwa kwa nyuzi za mtende na akaniambia nikae juu yake. Nilimuomba akae yeye mwenyewe, lakini hakukubali na akanifanya mimi nikae juu yake na yeye mwenyewe akakaa kwenye sakafu. Nikajisemea moyoni: 'Wallahi! Hawezi kuitwa mfalme.' Wakati tulipokaa alianza kuzungmza na kutaja siri fulani za maisha yangu ambazo hakuna mtu aliyekuwa anazijua. Nikiyachukulia mambo yote haya kwenye fikra, nilishawishika kuhusu kuwa kwake Mtume wa Allah na kuukubali Uislamu mikononi mwake." (Siirah Ibn Hisham, Jz. 4, uk. 580) "Bibi mzee na masikini alikuwa akifagia msikiti ambao kwawo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akisali Sala zake humo. Kwa kawaida alilala kando ya ua wa msikiti na chakula kwa ajili yake kilitayarishwa na watu waliokuja kusali msikitini pale. "Siku moja Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuja msikitini na hakumuona mwanamke yule. Kwa hiyo, aliuliza ni wapi alikokwenda. Watu wakajibu kwamba mwanamke yule amefariki usiku uliopita na amezikwa na ilidhaniwa kwamba hakuwa na umuhimu sana kwamba habari za kifo chake zingepelekwa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alichukia sana kusikia hivi na akawakaripia. Halafu akataka apelekwe kwenye kaburi la mwanamke yule. Aliongozwa kwenye sehemu ile na alikwenda pamoja na baadhi ya masahaba zake. Alisimama mbele ya kaburi pamoja na masahaba zake na akasali Sala za mazishi na du’a kwa ajili wokovu wake." (Daastaanhaa-i Az Zindagi-i Paygambar-i Maa, uk. 121)

101

11:27 AM

Page 101


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Katika maisha yake yote Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakuonekana kuwa mkali kwa mtu yeyote au kupata kutoa maneno yoyote ya dharau au jeuri. Bila ya shaka tabia kama hiyo huwavutia watu kwa mtu anayehusika, kwa sababu kwa kawaida mtu huelekea kwa wale ambao wana maadili mema na tabia njema. Luqman, mwenye busara, anasema: "Mtu mwenye tabia nzuri ni ndugu wa wageni, na mtu mwenye tabia mbaya ni mgeni kwa ndugu zake." (Amthaal wa Hikam, Dehkudaa, Jz. 2) Suala la maadili ni muhimu mno katika macho ya Uislamu kiasi kwamba Mwokozi Mkubwa wa ubinadamu - Mtukufu Mtume wa Uislamu (s.a.w.w.) ametangaza ukamilifu wa kanuni za maadili kuwa ndio lengo la kuteuliwa kwake kwenye kazi ya utume, na anasema: "Nimeteuliwa na Allah ili kukamilisha maadili mema." (Safinatul Bihar, uk. 41) Ili kufanya kazi hii ya kimbinguni ifanikiwe, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitumia njia ya kusema kwa mdomo na matendo, kurekebisha maadili ya jamii na kufanya kazi yake hiyo kwa juhudi zote bila kuchoka. Kabla ya kuteuliwa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwenye kazi ya kiutume maadili ya jamii yalikuwa yameporomoka kiasi kwamba watu walipoteza kabisa sura zao za ubinadamu na badala yake tabia za kinyama zikadhihiri miongoni mwa watu. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alifundisha masomo ya maadili kwa maneno yake na akatoa mifano kwa vitendo na tabia zake mwenyewe. Qur’ani Tukufu inasema: “Bila shaka mnao mfano mwema kwa Mtume wa Allah, kwa mwenye kumuogopa Allah na Siku ya Mwisho, na kumtaja Allah sana". (33:21) Kwa kulingana na uamuzi huu wa wazi wa Qur’ani Waislamu walikuwa chini ya wajibu wa kumfuata Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika mambo yao yote ya maisha na kufanya mwenendo wake mfano kwao wenyewe. Kwa 102

11:27 AM

Page 102


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio matokeo ya shule hii ya maadili ya Uislamu, pamoja na mwalimu maarufu kama huyu na wanafunzi waliofundika kama hawa, aliweza kuleta mapinduzi makubwa katika mfumo wa maadili ya watu. Katika hadith za Kiislamu, zenye maneno mbalimbali na maelezo, maadili mema yamehesabiwa kuwa ni njia za ustawi katika ulimwengu huu na Akhera na maadili mabaya yamefanywa kuwa ni sababu ya kupatwa na aina mbalimbali za mateso. Mtu mmoja alimuuliza Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): "Ewe Mtume wa Allah! Mwanamke fulani hufunga saumu wakati wa mchana na hukesha usiku katika ibada ya Allah na husali Sala za usiku wa manane, lakini ana tabia mbaya na huwaumiza jirani zake kwa ulimi wake (nini hukumu yake?)." Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akajibu: "Hana faida yoyote na ni mmoja wa wakazi wa motoni." (Biharul Anwar, Jz. 77) Katika hadithi hii Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amechukulia kufunga saumu na kusali wakati wa usiku kuwa ni bure kwa mtu ambaye ana tabia mbaya na ambaye huwadhuru watu kwa ulimi wake na amemtangazia mtu huyo kuwa ni mwenye kustahili Moto wa Jahannam. Imamu Ja'far Sadiq (a.s.) anasema: "Mtu ambaye hajitulizi wakati wa hasira na hana tabia nzuri kwa jamaa na rafiki zake, si mmoja katika sisi." (al-Imam Sadiq wal Madhaahibul Arba'ah, Jz. 2, uk. 350) Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: "Kuweni na tabia njema kwa sababu humpeleka mtu Peponi na jiepusheni kutokana na kuwa wagomvi kwa sababu kwa vyovyote humtupa mtu kwenye Jahannam." (Wasa'ilushShi'ah, Jz. 2, uk. 221) Imamu Ja'far Sadiq (a.s.) anasema: "Matendo mazuri na kuwa na uso wa tabasamu ni njia za kupokea upendo kutoka kwa wengine na kustahiki Pepo, uchoyo na tabia mbaya humsukuma mtu mbali na Allah na kumvu103

11:27 AM

Page 103


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio ta kuelekea Moto wa Jahannam." (Jami'us Sa'adat, Jz. 1, uk. 273) Washirikina wachache waliokuja Madina kwa nia ya kumuuwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na masahaba zake walikamatwa. Wakati hatia yao ilipothibitishwa, walikataa kutubia. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akaamuru kwamba mmoja wao aachiwe huru na wengine wauawe. Yule aliyeachiwa aliuliza kwa mshangao mkubwa: "Ewe Muhammad! Ni sababu ipi ya wewe kuniachia mimi peke yangu na kuamuru wengine wauawe?" Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akajibu: "Sasa hivi tu Malaika Mkuu Jibril ameleta taarifa kwangu kutoka kwa Allah kwamba wewe unazo sifa tano ambazo zinapendwa na Allah na Mtume Wake (i) uko makini sana kuhusiana na heshima na hadhi yako, (ii) wewe ni mkarimu sana, (iii) wewe ni mkweli (iv) wewe ni shujaa na (v) wewe una tabia mzuri. Mtu yule ambaye anajua zaidi kuhusu yeye mwenyewe kuliko mtu yeyote yule ajuavyo, alithibitisha aliyoyasema Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kisha alikiri utume wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), akajiunga na safu za Waislamu na akatoa mihanga mingi sana kwa ajili ya maendeleo ya Uislam." (A’amal Saduuq, uk.163) Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: "Mtu ambaye maadili yake ni mazuri na ambaye ni mnyenyekevu zaidi ana maana zaidi kwangu kuliko wengine wote na atakuwa karibu na mimi Siku ya Hukumu." (Qurbul Asnad) Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliendelea kusema: “Ushuhuda mkubwa ambao utavuta wafuasi wangu kwenda Peponi na upeo wa furaha ya milele, ni uchamungu na tabia njema." (al-Kafi, Jz. 2, uk. 100). Tabia njema ni rasilimali ya thamani na tunu ambayo ni ya hali ya juu kuliko vitu vingine vyote. Ni rasilimali ambayo vilevile huleta matokeo 104

11:27 AM

Page 104


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio mazuri katika maisha ya mtu ulimwenguni. Imamu Ali (a.s.) anasema: "Hazina za riziki zimefichwa katika tabia njema na uchangamfu." (Safinatul Bihar, Jz. 1) Imamu Ali (a.s.) anaendelea kusema: "Athari yenye nguvu ya kuridhika na ile faida isiyokoma ya tabia njema ni yenye kutosha sana kwa mtu." (Nahjul Balaghah, Jz. 2, uk. 195) Luqman, mwenye busara, alimshauri mtoto wake kuhifadhi hazina hii na akasema: "Mwanangu mpenzi! Hata kama ikitokea kupoteza mapato ya ulimwengu ambayo kwayo unaweza kufanya wema kwa ndungu zako na marafiki, usipoteze utajiri wa tabia njema na uchangamfu kwa sababu kama mtu ana sifa za tabia njema, watu wazuri watampenda na watu wabaya watamsaidia." (Safinatul Bihar, Jz. 1, uk. 410) Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: "Huna kabisa mtaji na utajiri ambao kwamba utakuwa na uwezo wa kuwasaidia watu masikini na mashinikizo ya maisha. Kwa hiyo, jitayarishe mwenyeye na utajiri wa maadili na punguza mizigo kutoka nyoyo za wengine kwa njia za tabia njema na uchangamfu." (Amali Saduq, uk. 9) Uislamu unachukulia tabia njema kuwa moja ya masharti ya imani na ibara ya ibada na husema kwamba mtu ambaye anazo sifa hizi atajaaliwa fidia ya thawabu. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: "Imani ya mtu, ambaye maadili yake ni mazuri, ni yenye manufaa zaidi." (Amali Saduq, uk. 126) Imamu Ja'far Sadiq (a.s.) anasema: "Imani ya mtu ambaye ana sifa nne iko kamili, ingawa anaweza kuzama katika dhambi. Ni: (i) Ukweli, (ii) urejeshaji wa amana kwa mwenyewe anayehusika (iii) adabu na (iv) tabia njema." (Al-Kafi, Jz. 2, uk. 99) 105

11:27 AM

Page 105


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Marehemu Allama Majlisi anasema hivyo katika maelezo ya hadithi hiyo hapo juu: "Maneno ya Imamu: 'Ingawa anaweza kuzama katika dhambi' humaanisha dhambi nyingi upande wa mtu anayehusika na inawezekana kwetu sisi kutafsiri kama 'madhambi madogo', kwa sababu mtu ambaye ana sifa maarufu zilizotaja hapo juu kwa hakika hatadumu katika kutenda madhambi makubwa na sifa hizi zenyewe humzuia mtu kutenda dhambi. Kwa mfano ukweli humzuia mtu kutenda uvunjaji wa amana kuhusiana na mali za watu na haki za Allah. Mtu kujisikia aibu mwenendo wake mbele za watu humzuia mtu kutenda dhambi, na kujisikia aibu mbele za Allah humzuia mtu kutenda dhambi kubwa kwa makusudi. Na tabia njema humzuia mtu kudhuru hisia za watu, humzuia kuwa na tabia mbaya kwa wazazi wake, humzuia kuvunja mahusiano na ndugu nk. Kwa ufipi kama mtu anazo sifa nne zilizotajwa hapo juu, moja kwa moja anakuwa na kinga kutokana na idadi ya madhambi, na kwa sababu ya sifa hizi Allah humpatia fursa ya kutubia na kufanya kafara kwa ajili ya dhambi zake na huishi maisha ya mafanikio na maisha mazuri ya baadae." (Biharul Anwar) Imam Ja’far Sadiq (a.s.) anasema: "Tabia njema humnyanyua mwenye kuwa nayo kwenye daraja la wale ambao hufunga wakati wa mchana na kusali wakati wa usiku, na vilevile humpatia malipo ya kiroho sawa na yao." (al-Kafi, Jz. 2, uk. 103) Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: "Wakati matendo ya watu yatakapokuja kutathminiwa Siku ya Hukumu hakuna kitakachokuwa bora kushinda tabia njema." (al-Kafi, Jz. 2, uk. 99) Kama ambavyo mapendekezo yamefanywa na viongozi watukufu wa Uislamu kuhusiana na tabia njema na athari zake katika ustawi wa watu katika ulimwengu huu na Akhera, vilevile wameshutumu mwenendo mbaya na uovu. Imamu Ali (a.s.) anasema: "Kuna toba kwa kila dhambi na kila mtu ambaye anatubia anaweza kutarajia kukubaliwa toba yake, isipokuwa mtu 106

11:27 AM

Page 106


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio mwenye maadili mabaya ambaye kabla ya kutubia kwa ajili ya dhambi, hujiingiza kwenye dhambi mbaya zaidi." (Safinatul Bihar, Jz. 1, uk. 424) Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: "Tabia mbaya huharibu vitendo vizuri vya mtu katika namna ileile siki inavyoharibu asali." (Majmu'a-i Warram, Jz. 1, uk. 90) Imamu Ali (a.s) aliulizwa: "Ni mtu gani ambaye hujiingiza zaidi katika wasiwasi na huzuni?" Akajibu: "Mtu ambaye maadili yake ni mabaya zaidi kuliko wengine." (Jami'ul Akhbar, uk. 107) Sa'id anasema: "Mtu mwenye tabia mbaya hukamatwa katika mikono ya adui kama huyo kiasi kwamba popote aendapo hawezi kujinasua nayo. Kama mtu mwenye tabia mbaya akitorokea angani kutokana na mateso atakuwa kwenye mateso hata huko kwa ajili ya tabia yake mbaya." Mtu ambaye alipata heshima ya kufika mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuomba ampe ushauri. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimshauri pamoja na mambo mengine: "Kukutana na watu kwa uchangamfu na heshima nzuri." (al-Kafi, Jz. 2, uk. 84) Imam Ja'far Sadiq (a.s.) anasema: "Huruma na tabia njema hufanya nchi istawi na kurefusha maisha ya watu." Aliulizwa: "Ni ipi mipaka ya tabia njema?" Alijibu: "Lazima ushughulike na watu kwa upole, sema mambo mazuri na kutana na watu kwa uso mchangamfu."

Nukta Chache Zenye Manufaa (i) Kanuni za maadili ya Kiislamu, mifano ambayo kwayo imenukuliwa hapo juu, iliwasilishwa kwa watu karne kumi na nne zilizopita kupitia kwa Mtume wa Uislamu na warithi wake halisi yaani Amiru'l-Muminin Ali (a.s.) na watoto wake Ma’sumin kumi na moja (a.s.) walikuwa hawana chanzo kingine kuliko ufunuo wa Mwenyezi Mungu.

107

11:27 AM

Page 107


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Kama wakati wa zama hizi za kisasa waandishi wa Magharibi wamezingatia maadili na wamechapisha vitabu na makala kuhusiana na suala hili, vyanzo vyao kama ilivyo kwa sayansi nyingine nyingi, ni kutoka nchi za Mashariki na katika maandishi ya thamani ya Waislamu. (ii) Uislamu umeweka msingi wa maadili juu ya imani. Kwa hiyo, mabadiliko katika hali na mazingira ya Waislamu hayatoi nafasi ya kubadika katika maadili yake ambayo siku zote yako imara na yasiyobadilika. Katika jamii ambazo maadili yametegemezwa kwenye ulanguzi wa faida na mapato ya kilimwengu zina uwezakano wa kuporomoka na kubadilika wakati wowote na maadili kama hayo hayawezi kuwa ya kudumu. (iii) Moja ya sababu za kurudi nyuma kwa Waislamu ni ushukaji wa hadhi yao ya maadili na kujiingiza kwao katika mambo ya ovyo na duni, na matendo machafu. Sasa ni wajibu wa kila Mwislamu mwenye busara kuzingatia zaidi kwenye kanuni za maadili ya Kiislamu, na kufanya juhudi kwa njia zote zinazo wezekana kurekebisha maadili ya ndugu zao katika Uislamu, na hususan vijana, ili kwamba katika siku za usoni tuweze kuwa taifa bora na liliondelea la ulimwengu.

UHALISIA WA KISAYANSI KATIKA UISLAMU Kwa kadri maarifa ya mwanaadamu yanavyoongezeka na wanasayansi wanavyochukua hatua mpya kuelekea katika ugunduzi wa siri za maumbile, ndivyo thamani ya mafundisho ya Uislamu na utukufu wa viongozi wake unavyozidi kuwa dhahiri.

108

11:27 AM

Page 108


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Sheria, zilizopitishwa na Mwenyezi Mungu, Muumba Mwenye ujuzi wa yote, zinaendana na maumbile na kamwe haziwezi kuwa zilizopitwa na wakati. Watafiti wajuzi na wasio na upendeleo ambao wamefanya utafiti na uchunguzi juu ya sheria na kanuni za Uislamu wamesalimu amri kwa unyenyekevu mbele ya Uislamu na kuusifu. Baadhi yao wameifuata imani hii na wameona kuwa ni wajibu kwao kuifuata mpaka mwisho wa maisha yao. – (Taz. Why I Became a Muslim). Baadhi yao, kwa maono yao ya mbali, wameuona Uislamu kuwa ni dini ya dunia hii ya wakati ujao. George Bernard Shaw, mwandishi mashuhuri wa Kiingereza amesema: “Mara zote nimekuwa nikiitazama dini ya Muhammad kwa heshima kubwa kabisa kwa sababu ya nguvu tendaji yake ya ajabu. Ni dini pekee ambayo inaonekana kwangu kuwa na uwezo wa kustaarabisha na kudhibiti hali potovu na kubadilisha mazingira ya maisha na kuzikabili zama mbalimbali. Ninaweza nikabashiri – na ishara zake zipo dhahiri hata sasa – kwamba dini ya Muhammad itakubaliwa na Ulaya ya kesho. Kwa sababu ya ujinga wao au upendeleo viongozi wa kanisa wa Zama za Kati walionyesha picha ya rangi nyeusi (potovu) ya dini ya Muhammad. Kutokana na chuki yao na uadui wa kidini walimchukulia yeye kuwa ni mpinzani wa Yesu Kristo. Nimefanya utafiti juu ya mtu huyu – mtu huyu asiye wa kawaida – na nimefikia hitimisho kwamba sio tu kwamba hakuwa mpinzani wa Yesu kristo bali pia anapaswa kutambuliwa kuwa ni mkombozi wa mwanaadamu. Ikiwa mtu kama yeye atakuwa mtawala wa ulimwengu wa sasa atafanikiwa kuyatatua maswali na matatizo ya ulimwengu katika namna ambayo amani na ustawi unaohitajiwa na wanaadamu wote utahakikishika.” (Khuda Parasti wa Afkar-i Roz, uk. 21). Kazi za kumbukumbu ambazo zimedumu kutoka kwa Maimamu watukufu na viongozi watukufu wa Uislamu humshangaza kila mtafiti.

109

11:27 AM

Page 109


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Sisi ambao tunaamini kuwa viongozi wa Uislamu ni Maimamu walioteuliwa na Mwenyezi Mungu na kuchukulia kwamba elimu yao inatokana na elimu ya ki-Mungu hatushangai tunapokutana na utabiri wao wa kisayansi. Lakini watafiti wasiokuwa Waislamu wanaotaka kukisoma kila kitu kwa msingi wa kimaumbile na sayansi za kibinadamu wanashangaa sana, wanapokabiliana na tabiri hizi kiasi kwamba huwa hawawezi kuficha mshangao wao. Wakati fulani huko nyuma gazeti liitwalo “Khwandanihaa” lilitafsiri na kuchapisha kitabu kiitwacho “The Reflective Brain of the Shi’ah World.” Kitabu hiki kilikusanywa na kuchapishwa na kundi la wanachuoni na watafiti wa kituo ha Mafunzo ya Kiislamu cha Strasbourg, ambao wengi wao walikuwa ni wakristo - (Strasbourg ni moja ya miji ya Ufaransa na ni mji mkuu wa jimbo la Alsace, na upo katika ukingo wa mto Roun. Idadi ya watu katika mji huu ni 195,000 na una makanisa mazuri na ya fahari sana). Kitabu hiki ni cha wasifu (baigrafia) ya Imam Ja’far (a.s), Imam wa sita, na hekima zake zimetafitiwa na kuchambuliwa. Waandishi wanataaluma hawa wa kitabu hiki, ambao kila mmoja wao ni bingwa wa fani ya elimu moja au nyingine, wamelinganisha maelezo ya Imam Ja’far (a.s) na Sayansi na uguduzi wa zama hizi na wameshangazwa na kutatizwa na jinsi Mtukufu Imam alivyopata habari juu ya sayansi zote hizi! Hapa chini tumenukuu baadhi ya maelezo yaliyomo kwenye kitabu hiki kama mfano:

Kufundisha sayansi na utabibu “Kuna tafsiri mbili, moja inahakikisha na jingine inakataa, kuhusu kufundishwa kwa sayasi ya tiba katika kituo cha elimu cha Muhammad Baqir. Baadhi wanasema kuwa sayansi ya tiba ilifundishwa hapo ambapo wengine wanakana kwamba Muhammad Baqir aligawa maelekezo juu ya sayansi hii. Lakini hakuna shaka yoyote juu ya ukweli kwamba wakati Ja’far Sadiq mwenyewe alipotoa masomo juu ya sayansi ya tiba na kwam110

11:27 AM

Page 110


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio ba maoni yake ya kisayansi yaliathiri elimu hii ya tiba, na kwamba madaktari wa karne ya pili na ya tatu Hijiria walinufaika sana kutokana na maoni yake juu ya somo hili la utabibu. Tumesema kwamba hatujui kama Muhammad Baqir alifundisha utabibu au la na iwapo mtoto wake (Ja’far) alisoma sayansi hii (ya tiba) kwake au la. Lakini hatuna shaka yoyote kwamba Ja’far Sadiq mwenyewe alifundisha sayansi ya tiba na alianzisha mambo ndani yake ambayo hayakuanzishwa na daktari yeyote wa Mashariki hadi wakati huo. Na tunaposema Mashariki hatumaanishi Uarabuni, kwa sababu Uarabuni kulikuwa hakuna sayansi ya tiba na ilifika huko kutokea katika nchi nyingine baada ya kuja kwa Uislamu. Kama tutakiri kwamba Ja’far Sadiq alipata elimu hii kutoka wa baba yake itatubidi tukubali pia kuwa baba yake naye aliipata kutoka sehemu fulani na hatujui alikoitoa. Tunajua kwamba Ja’far Sadiq hakuwa kwenye taaluma ya tiba ambapo kwamba angeweza kupata ukamilifu katika fani hii ya elimu. Hivyo itaonekana kwamba alijifunza elimu hii kutoka kwa baba yake na ambapo swali jingine linaibuka pia kuhusu je, baba yake naye alijifunza kutoka wapi?

Ardhi na hewa sio Elementi Sahili Siku moja Ja’far Sadiq alipokuwa akisoma kwa baba yake, alifikia ile sehemu ya ‘Fizikia’ ya Aristotle ambapo (Aristotle) anasema kuwa kuna elementi nne tu duniani ambazo ni ardhi, maji, hewa na moto. Ja’far Sadiq alilipinga hili na kusema: “Ninashangaa ni vipi mtu kama Aristotle apuuzie ukweli kwamba ardhi sio elementi moja bali kuna elementi nyingi ndani yake na kila metali iliyomo katika ardhi inapaswa kuchukuliw akama ni elementi pekee inayojitegemea.” Kulikuwa kitambo cha miaka 1000 kati ya wakati wa Aristotle na ule wa Ja’far Sadiq na katika kipindi hiki kirefu hizi elementi nne kama zilivy111

11:27 AM

Page 111


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio oelezwa na Aristotle zilikuwa zinahesabiwa kuwa ni moja ya misingi ya fizikia na hapakuepo tu hata mmoja ambaye alitokea kutoamini wazo hili na hakutokea yeyote kulipinga. Ilikuwa ni baada ya miaka 1000 ambapo mvulana ambaye alikuwa hajafikisha umri wa miaka kumi na mbili bado alisema kwamba ardhi sio elementi moja bali umeundwa na elementi nyingi. Mvulana huyo alipoanza yeye mwenyewe kufundisha wengine, pia alilikataa wazo kwamba hewa ni elementi sahili na alisema: ‘Hewa sio elementi moja bali imeundwa na elementi kadhaa.’ Miaka elfu moja na mia moja kabla wanasayansi wa Kizungu wa karne ya 18 ya zama za ukristo hawajavigundua na kuvitenganisha viambata vya hewa, Ja’far Sadiq alisema kuwa hewa haikuwa elementi moja bali imekuwepo kwa muunganiko wa idadi kadhaa ya elementi nyinginezo. Hata kama baada ya kutafakari na kujenga hoja ilikubaliwa kwamba ardhi sio elementi moja bali imeundwa na elementi kadhaa, hakuna aliyetia shaka kuwa hewa ni elementi moja. Wanafizikia mashuhuri sana wa dunia baada ya Aristotle hawakujua kuwa hewa haikuwa na elementi sahili. Hata katika karne ya 18 A.D, ambayo ilikuwa ni moja ya karne zenye kung’aa katika mtazamo wa maendeleo katika Sayansi, wasomi wengi waliendelea kufikiri, hadi katika wakati wa Lavoisier* kuwa hewa ilikuwa ni elementi sahili na hawakudhania kwamba iliundika kwa elementi kadhaa. Na Lavoisier alipoitenganisha oksijeni kutoka katika gesi nyingine zilizopo kwenye hewa na alipoonyesha athari kubwa ya oksijeni katika upumuaji na uunguzaji, wanasayansi wote walikubali kuwa hewa sio elementi sahili bali imeundwa na gesi chache. Na siku moja mnamo mwaka 1794 A.D., kichwa cha Lavoisier kilikatwa kwa ncha ya bapa maalum la kukatia vichwa vya wahalifu, na baba wa kemia ya kisasa, ambaye angeweza kufanya ugunduzi zaidi kama angeendelea kuishi, akauawa na kupelekwa katika ulimwengu mwingine. 112

11:27 AM

Page 112


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Hivyo Ja’far Sadiq aliyetangaza kuwa hewa sio elementi rahisi aliutangulia wakati wake yeye kwa miaka 1100. Shi’ah wanasema kuwa Ja’far Sadiq alikusanya elimu hii na ukweli mwingine wa kisayansi kutokana na Elimu ya ki-Mungu, elimu aliyopewa kutokana na kuwa na nafasi ya cheo cha Imam. Siku hizi jambo hili linaonekana kuwa ni jambo la kawaida kwa sababu tunajua kuwa kuna elementi 102 ulimwenguni. Hata hivyo, katika karne ya 7 A.D. na karne ya kwanza Hijiria, lilikuwa ni wazo kubwa la kimapinduzi na akili ya mwanaadamu wakati huo isingeweza kukubali kuwa hewa sio elementi rahisi. Tunaweza kuongeza kuwa wakati huo, na katika zama zilizofuatia hadi katika karne ya 18 A.D. Ulaya haikuwa na uwezo wa kuwa na imani hii ya kisayansi na kimapinduzi na kuamini mambo mengine yaliyosemwa na Ja’far Sadiq ambayo yatatajwa katika sura zinazofuata:

OKSIJENI Alipokuwa akitoa hotuba yake, Imam Ja’far (a.s) alisema: “Hewa ina viambata kadhaa. Moja ya vimbata hivi hufyonzwa na baadhi ya vitu na huleta mabadiliko. Na katika hivi viambata vingi vya hewa kuna sehemu ambayo husaidia uunguaji. Kama sehemu hiyo isingekuwepo, vitu vingi viunguavyo visingeweza kuungua. Wazo hili lilifafanuliwa na Imam Ja’far (a.s) mwenyewe na alisema katika hotuba alizotoa baadaye: “Ikiwa kitu kilichomo ndani ya hewa ambacho husaidia uunguaji kitatenganishwa kutoka katika hewa na kupatikana katika hali yake halisi, kina ufanisi mkubwa sana katika uunguzaji kiasi kwamba kinaweza kuunguza hata chuma.” Hivyo mika 1000 kabla ya Priestley* na mapema kabla ya Lavoisier, Ja’far Sadiq aliielezea wazi wazi oksijeni na kwamba hakuipa tu jina la Oksijeni. Ingawa Priestley aliigundua oksijeni lakini hakujua kuwa inaweza kuunguza chuma. 113

11:27 AM

Page 113


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Lavoisier, licha ya ukweli kwamba alifafanua baadhi ya ‘tabia za oksijeni kwa kutumia majaribio, lakini hakuweza kubaini kuwa gesi hii inaweza kuunguza chuma, lakini Ja’far Sadiq alilibaini hili miaka 1000 kabla. Sasa tunajua kuwa ikiwa kipande cha chuma kitachomwa sana kiasi cha kuwa chekundu kisha kikatupiwa katika (gesi ya) oksijeni halisi, huwaka na kutoa miale yenye mwanga. Kama tu ilivyo kwa taa mafuta ya kawaida au ya mafuta ya taa za wakati uliopita, utambi uliwaka kwa mwanga unaon’gara, halikadhailika taa inaweza kuwashwa kwa kutumia utambi wa chuma uliochovywa kwenye oksijeni ya majimaji na utambi unachomwa kiasi cha kuwa mwekundu, utambi huu wa chuma utatoa mwanga mkali na kuubadili usiku kuwa mwanga wa mchana. Imesimuliwa kuwa siku moja, Muhammad Baqir, baba yake Ja’far Sadiq, alipokuwa akifundisha somo fulani alisema: “Kwa msaada wa Sayansi moto unaweza kuwashwa kwa kutumia maji ambayo kwa kawaida huzima moto.” Ikiwa maelezo haya hayakutafsiriwa kama kivutio cha kishairi, yalionekana kutokuwa na maana na kwa muda mrefu wale waliosikia maelezo haya walifikiri kuwa Muhammad Baqir alisema kitu cha kufurahisha tu. Lakini kuanzia karne ya 18 na kuendelea ilithibitika kuwa kwa msaada wa Sayansi, moto unaweza kuwashwa kutokana na maji na moto huo unaweza kuwa mkali kuliko moto utokanao na kuni au makaa ya mawe, kwa sababu joto litolewalo na haidrojeni (ambayo ni moja ya viambata vya maji) linapounguzwa kwa kutumia oksijeni hufikia nyuzijoto 6664. Mchakato wa kuunguza haidrojeni kwa kutumia oksijeni, unaitwa “uoksidishaji” na hutumika kwa kiasi kikubwa viwandani katika kufulia vyuma na kuchangamua vipande vya vyuma.

114

11:27 AM

Page 114


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio

MZUNGUKO WA DUNIA KATIKA MHIMILI WAKE Henry Poincare, mwanafalsafa maarufu wa Kifaransa aliyefariki mwaka 1912 A.D. akiwa na umri wa miaka 58, alikuwa ni mwanahisabati mkubwa kabisa wa zama zake, na tarehe ya kifo chake pia inaonyesha kuwa aliishi mpaka mwanzoni mwa karne ya 20. Lakini bado mwanasayansi huyu mkubwa alikuwa akisema: ‘Siamini kuwa dunia hujizungusha kwenye mhimili wake.’ Mwanasayansi kama Henry Poincare anapotia shaka mwanzoni mwa karne ya 20 juu ya iwapo kama dunia hujizungusha katika mhimili wake au hapana, ni dhahiri kwamba watu walioishi katika nusu ya mwisho ya karne ya kwanza na karne ya pili Hijiria (sawa na karne ya 7 na ya 8 A.D.) hawakuweza kukubali kabisa wazo kwamba dunia hujizungusha kwenye mhimili wake. Mzunguko wa dunia kwenye mhimili wake haukuweza kuthibitishwa kwa utambuzi mpaka mwanadamu alipotua juu ya mwezi na kuichunguza dunia kutokea hapo (juu ya mwezi). Hata katika miaka ya awali ya utafiti wa anga za juu, watafiti wa anga za juu hawakuweza kubaini mzunguko wa dunia kwa macho yao kwa sababu katika miaka hiyo hawakuwa na kituo tuli (kisichozunguka) na walikuwa ndani ya vyombo vya anga za juu tu na kila chombo katika hivi kilikuwa kikiizunguka dunia mara moja kila baada ya dakika tisini au zaidi kidogo. Na hivyo wakati wana anga wenyewe walipokuwa wakiizunguka dunia kwa kasi kubwa kiasi hicho hawakuweza kubaini mwendo wa dunia yenyewe.

115

11:27 AM

Page 115


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Hata hivyo, siku waliyotua juu ya mwezi na kuzifungua darubini (teleskopu) zao za kuchukulia filamu na kuzielekeza kwenye dunia waliona kwenye picha kwamba dunia ilikuwa inazunguka pole pole kwenye mhimili wake na siku hiyo mzunguko wa dunia kwenye mhimili wake ulithibitishwa kwa kuona dhahiri ......... kwa kuzingatia ule ukweli kwamba Galileo* alielewa vyema kwamba kama ilivyo kwa sayari nyingine zote za mfumo wa jua duniani hulizunguka jua, inawezekana kwamba alihisi (bila hakika) kwamba kama ilivyo kwa sayari nyingine, dunia pia hujizungusha kwenye mhimili wake. Lakini hata hivyo hatukuti bishara (utabiri) yoyote ya aina hii katika kazi zake alizoandika ........ Sio hili tu kwamba Galileo hakuzungumzia juu ya mzunguko wa dunia kwenye mhimili wake enzi za uhai wake, lakini hata baada ya kifo chake hakuna kilichokutwa katika kazi alizoandika zinazoonyesha alikuwa anaelewa juu ya mzunguko wa dunia kwenye mhimili wake. Katika karne ya kumi na sita ya kikristo, mnajimu mwingine aitwaye Tikhubraha aliyeishi Denmark, aliamini kuwa dunia hulizunguka jua. Kinyume na Capernicus* wa Poland, ambaye wakati fulani alikuwa akikaa bila ya kula chakula, Tikhubraha alitoka katika familia ya kimwinyi ya Denmark na aliishi maisha ya kifahari na alikuwa akiandaa sherehe kubwa katika kasri lake kubwa. Alikufa mwaka 1601 A.D. – yaani mwaka wa kwanza wa karne ya 17. Ni mtu ambaye utafiti wake wa masuala ya anga za juu ulimsaidia sana Kepler,** mwanasayansi wa Kijerumani, na bila Tikhubraha, isingewezekana kwa Kepler kugundua sheria zake tatu za kinajimu zinazohusiana na mwendo wa Sayari, ikiwa ni pamoja na mzunguko wa dunia kulizunguka jua. Licha ya hili Tikhubraha hakuweza kubaini mzunguko wa dunia kwenye mhimili wake na kama angekuwa analijua hilo, angeweza kulithibitisha wazi wazi kama (alivyofanya kwenye) mzunguko wa dunia kulizunguka jua...

116

11:27 AM

Page 116


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Kwa kugundua sheria tatu zinazohusiana na mzunguko wa sayari, Kepler, aliyefariki mwaka 1630 A.D. sio tu kwamba alipata sifa kutoka katika ulimwengu wa Kisayansi wa wakati huo, bali hata leo, yeyote anayezisoma sheria zake tatu, humsifu. Mwanasayansi huyu mkubwa ambaye alithibitisha uwezo wake usio wa kawaida kwa kugundua sheria tatu za unajimu, hakuweza kubaini mzunguko wa dunia kwenye mhimili wake. Lakini Ja’far Sadiq (a.s.) aligundua hili karne kumi na mbili nyuma kabla, kwamba dunia hujizungusha kwenye mhimili wake na kwamba sababu ya mfuatano wa kuwepo usiku na mchana sio matokeo ya jua kuizunguka dunia (nadharia aliyoiona kuwa isiyo na mantiki na isiyokubalika) bali ni mzunguko wa dunia kwenye mhimili wake ambapo nusu moja ya dunia hupata mwanga wa mchana na nyingine hubaki gizani. Watu wa kale ambao waliamini kuwa dunia ilikuwa mviringo walielewa kuwa mara zote kulikuwa na usiku katika nusu moja ya dunia na mchana katika nusu nyingine, lakini walichukulia kuwa mchana na usiku yalikuwa ni matokeo ya jua kuizunguka dunia. Ilikuwaje kwamba karne kumi na mbili hapo kabla, Ja’far Sadiq alibaini kwamba dunia hujizungusha kwenye mhimili wake na kwa sababu hii pakawepo usiku na mchana. Licha ya ukweli kwamba wanasayansi wa karne ya 15 na 17 ya kalenda ya Kikristo, ambao baadhi yao wametajwa majina hapa juu, waligundua baadhi ya sheria za kinajimu lakini hawakubaini kwamba dunia hujizungusha kwenye mhimili wake, sasa ni vipi Ja’far Sadiq, aliyekuwa akiishi eneo la la mbali kama Madina ambako kulikuwa ni mbali na vituo vya kujifunzia vya zama hizo abaini mzunguko wa dunia kwenye mhimili wake?

117

11:27 AM

Page 117


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio

MWANZO Ja’far Sadiq alisema yafuatayo juu ya uumbwaji wa ulimwengu: “Ulimwengu ulitokea kutokana na chembchembe moja na chembechembe hiyo ilikuwa na ncha mbili zilizo tofauti, na hizi ncha mbili tofauti zilikuwa ndio sababu ya kuzaliwa kwa atom na kisha maada ikatokea na maada ikabadilika na aina mbalimbali za maada hutokana na kupungua au kuzidi kwa atom zake.” Nadharia hii haina tofauti yeyote na nadharia ya kisasa ya atom juu ya kutokea kwa ulimwengu. Ncha mbili hizi ni chaji mbili – chanya na hasi – katika atom. Chaji hizi mbili zilikuwa ndio sababu ya kutokea kwa atom na atom zikaleta maada. Na tofauti inayoonekana katika maada (yaani elementi) inatokana na kupungua au kuzidi kwa vitu vilivyomo ndani ya atom za elementi. Shi’ah wanasema kwamba vitu vyote alivyosema Ja’far Sadiq (a.s.) juu ya kutokea kwa ulimwengu, unajimu, fizikia, elementi, kemia, hisabti na vitu vingine alivijua kutokana na elimu yake kama Imamu – yaani elimu aliyopewa na Mwenyezi Mungu Mtukufu. Tumeanza somo la elimu ya Ja’far Sadiq (a.s.) katika jiografia, unajimu, na fizikia chini ya somo kuu la uumbwaji wa ulimwengu na tutaendelea na mazungumzo juu ya elimu yake ya fizikia na kisha tutajadili masomo mengine. Na kuhusiana na hili tunasema kuwa Ja’far Sadiq (a.s.) alisema vitu juu ya fizikia ambavyo hakuna aliyevisema kabla yake na hakuna aliyekuwa na uwezo wa kuyasema hadi katikati ya karne ya 18 na karne za 19 na 20.

118

11:27 AM

Page 118


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio

VIUNGO VYA MWILI WA BINADAMU Ja’far Sadiq (a.s.) alikuwa akisema kama Waislamu wengine kwamba mwanaadamu ameumbwa kutokana na udongo. Tofauti yake na Waislamu wengine ni kuwa alisema vitu juu ya uumbaji ambavyo vilikuwa havifahamiki kwa Waislamu wa zama zile. Hata wakati wa zama zilizofuatia hakuna Mwislamu aliyekuwa na elimu juu ya maumbile ya mwili wa mwanaadamu ambayo ingeweza kulingana na ile ya Ja’far Sadiq (a.s.) na kama mtu yeyote alisema chochote kwa njia ya moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja (basi) kilikuwa ni kile alichokisikia kutoka kwa wanafunzi wa Ja’faf Sadiq (a.s.). Imam Ja’far (a.s) alisema: “Vitu vyote vilivyomo katika udongo pia vinapatikana katika mwili wa mwanaadamu. Lakini kiasi chake sio sawa. Baadhi ya hivyo vinapatikana katika kiasi kikubwa katika mwili wa mwanaadamu na vingine vipo katika kiasi kidogo.” Kiasi cha vitu ambavyo ni vingi zaidi katika mwili wa mwanaadamu pia hakiko sawa (baina ya madini hayo, ambayo ni mengi) na baadhi ya (vitu) hivyo ni vichache kuliko vingine. Alisema kuna vitu vinne katika mwili wa mwanaadamu ambavyo vipo katika kiasi kikubwa na kuna vitu vinane ambavyo vipo katika kiasi kidogo na kuna vitu vingine vinane ambavyo ni vichache zaidi. Maoni haya juu ya maumbile ya mwanadamu ambayo yameelezwa na Ja’far Sadiq (a.s.) na ni mahsusi kwamba wakati fulani mtu hufikiri iwapo kama Shi’ah wanavyoamini, (Ja’far Sadiq) alikuwa na elimu ya Uimamu na alipata wazo hili kutokana na elimu hiyo na siyo kutokana na sayansi ya kibinadamu. Hii ni hivyo kwa sabau uelewa wa mtu hauwezi kukubali msimamo kwamba mwanazuoni tu aliyekuwa na hisia za kibinadamu anaweza 119

11:27 AM

Page 119


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio kujua ukweli huu karne kumi na mbili na nusu zilizopita ..... Ja’far Sadiq (a.s.), bila kujali iwapo alikuwa na elimu ya Uimamu kama inavyoaminiwa na Shi’ah au kwa mujibu wa wale wanaoamini katika elimu ya ilhamu kwamba alitegemea ilhamu au kwa mujibu wa maoni ya Bergson* alinufaika kutokana na elimu yake isiyo ya kawaida alisema vitu juu ya maumbile ya mwili wa mwanaadamu ambavyo vinathibitisha kwamba kuhusiana na elimu ya mwili wa mwanaadamu, alikuwa ni mtu wa pekee miongoni mwa watu wa zama zake na zama zilizofuatia, kwa sababu baada ya karne kumi na mbili na nusu usahihi wa maoni yake umethibitishwa kisayansi na hapana shaka yoyote juu ya hilo. Na Ja’far Sadiq (a.s.) hakutaja majina ya elementi zilizomo katika mwili wa mwanaadamu. Tunaweza tukasema kwamba kama Ja’far Sadiq alivyosema kila kilichomo ardhini pia kimo katika mwili wa mwanadamu. Kila kilichomo ardhini kimetokana na elementi 102 na hizi elementi 102 pia zimo katika mwili wa mwanaadamu. Lakini kiasi cha baadhi ya elementi hizi ni kidogo mno kiasi cha kutowezekana kuzibaini barabara.... kama tulivyosema hapo juu, usahihi wa maoni haya (ya Ja’far Sadiq) umeshathibitishwa. Elementi nane katika mwili wa mwanaadamu ambazo kwa mujibu wa Ja’far Sadiq (a.s.) zipo katika kiasi kidogo sana ni kama zifuatazo: (i) Molybadenum (ii) Selenium (iii) Fluorini (iv) Kobalti (v) Manganizi (vi) Ayodini (vii) Shaba (viii) Zinki. Elementi nane zilizomo katika mwili wa mwanaadamu ambazo zipo kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na hizo zilizotajwa hapo juu ni kama zifuatazo: 120

11:27 AM

Page 120


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio (i) Magnesi (ii) Sodiam (iii) Potasiamu (iv) Kalisi (calcium) (v) Fosforasi (vi) Klorini (vii) Salfa (viii) Chuma. Elementi nne zilizomo katika mwili wa binadamu kwa kiasi kikubwa ni: (i) Oksijeni (ii) Kaboni (iii) Haidrojeni (iv) Naitrojeni. Elimu ya juu ya kuwepo kwa elementi hizi katika mwili wa mwanadamu haikupatikana kwa siku moja au mbili. Kazi hii ilianza katika karne ya 18 ya kalenda ya kikristo kwa kuupasua mwili wa mwanaadamu na katika anatomia (elimu ya mwili wa mwanaadamu), Mataifa mawili Ufaransa na Austrialia, ndiyo yalikuwa waanzilishi. Katika nchi nyingine anatomia (upasuaji wa miili ya watu waliokufa ili kujifunza) ilikuwa haifanywi na katika nchi za Ulaya makanisa ya Orthodox, Kikatoliki na Kiprotestanti yalikuwa yakipinga (jambo) hili. Hata hivyo nchini Australia na Ufaransa upasuaji huu ulikuwa ukifanyika lakini bila kuziasi amri za kanisa wazi wazi. Licha ya hili upasuaji (huu) haukupanuka nchini Ufaransa hadi katika wakati wa Marat* na bado ilibakia kuwa takribani siri. Pamoja na upasuaji Marat, akisaidiwa na baadhi ya wanasayansi wa Kifaransa akiwemo Lavoisier aliyekatwa kichwa mwaka 1794 A.D, alikuwa akichanganua tishu za mwili wa mwanaadamu ili kujua elemeni zinazounda mwili. Baada ya Marat, wanafunzi wake waliendeleza kazi yake na pamoja na upasuaji pia walikuwa wakichanganua tishu za mwili wa mwanaadamu na kazi hii iliendelea katika karne yote ya 19 na mwanzoni mwa karne ya 20 na ilipanuliwa. Upasuaji ambao mwanzoni mwa karne ya 18 ya kalenda ya Kikristo ulifanyika nchini Ufaransa na Austria tu, ulienea katika nchi nyingine za Ulaya na kisha katika nchi za mabara mengine na sasa unafanywa kila sehemu isipokuwa kaika nchi chache ambazo hazina vyuo vinavyoweza kutoa elimu ya utabibu na upasuaji, kila upasuaji wa miili unapofanywa, pia utafiti huwa unafanywa juu ya elementi zinazounda mwili wa mwanadamu. Wakati fulani matokeo ya utafiti wa vituo viwili hutofatiana 121

11:27 AM

Page 121


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio kidogo sana lakini hakuna tofauti kubwa kati yao na uwiano alioutaja Ja’far Sadiq (a.s.) ni kamili bila mapungufu katika nchi zote kuhusiana na watu wote wenye afya.

OKSIJENI NA HAIDROJENI NDANI YA MAJI Muujiza wa Ja’far Sadiq haukuwa kwamba alihamisha mlima bali muujiza wake ulikuwa kwamba alijua kuwepo kwa oksijeni karne kumi na mbili na nusu zilizopita na pia alijua kuwa ndani ya maji kuna kitu kinachounguza. Kwa sababu hii alisema kwamba maji yanaweza kubadilishwa kuwa umeme. Inasemekana kwamba sifa pambanuzi ya Mtume ni kauli yake kwani huwa hasemi kitu kisicho na msingi..... Ni kama tunaposikia leo kwamba katika nusu ya pili ya karne ya pili Hijiria kuwa Ja’far Sadiq (a.s.) aligundua kuwepo kwa oksijeni (ndai ya maji), tunakiri kuwa ulikuwa ni muujiza. Mtu hustaajabu kufikiri ni jinsi gani Ja’far Sadiq (a.s.) au baba yake, Muhammad Baqir alijua juu ya gesi ya haidrojeni ambapo haikuwepo katika maumbile katika sura yake halisi na pia haina rangi, harufu au ladha. Ja’far Sadiq au baba yake alielewa kuwepo kwa haidrojeni ndani ya maji lakini hawakuweza kuitenganisha bila kuyachanganua maji. Kuyachanganua maji kunahitaji matumizi ya mkondo wa umeme, kwa sababu maji hayawezi kuchanganuliwa bila mkondo wa umeme. Na pia haikubaliki kwamba yeyote kati yao (Ja’far Sadiq au baba yake) angekuwa ameweza kutumia umeme kuyachanganua maji. Katika wakati huu, mtu wa kwanza aliyefanikiwa kuitenganisha haidrojeni kutoka katika maji alikuwa ni mwanasayansi wa kiingereza Henry 122

11:27 AM

Page 122


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Cavendish (1731 – 1810). Alijitahidi kwa miaka kuchangaua maji na alipofanikiwa kuigundua haidrojeni aliipa jina la ‘gesi inayolipuka’ na ilipowashwa kwa mara ya kwanza alimanusura imuunguze yeye mwenyewe na nyumba yake..... Gesi ya Haidrojeni iligunduliwa wakati matumizi ya nguvu ya umeme yalikuwa yameendelea sana kiasi cha kuweza kuutumia katika kuyachanganua maji. Lakini wakati wa Ja’far Sadiq (a.s.), matumizi ya nguvu za umeme yaliishia kwenye matumizi ya mabua na kaharabu na hizi zilikuwa zikichukuliwa kuwa ni shughuli za kipuuzi. Kipande cha kaharabu kilikuwa kikisuguliwa kwenye nguo ya Sufu na kusogezwa karibu na bua na kilikuwa kikivuta mabapa ya mabua. Je, Ja’far Sadiq (a.s.) au baba yake, Muhammad Baqir (a.s.), walitumia nyenzo ambayo bado wanasayansi hawajaijua katika kuitenganisha haidrojeni kutoka kwenye maji? Na je waliweza kuitenganisha haidrojeni kutoka katika maji kwa kutumia njia isiyokuwa ya mkondo wa umeme? Kuanzia siku ambayo Cavendish alifanikiwa kwa mara ya kwanza kupata haidrojeni mpaka leo, njia pekee ya kutenganisha haidrojeni kutoka katika maji imekuwa ni mkondo wa umeme na wanasayansi hawajaweza kuitenganisha haidrojeni kutoka katika maji kwa njia nyingine yoyote.

UCHAFUZI WA ANGAHEWA Wakati wa Ja’far Sadiq (a.s.) viwanda havikuwepo isipokuwa vile vya ufundi wa kazi za mikono na hapakuwa na hata kiwanda kimoja kinachofanana na viwanda vya kisasa kilichokuwepo. Metali zilikuwa zikiyeyushwa katika matanuri madogo na kwa vile metali zote hata chuma, ziliyeyushwa kwa kuni, hazikuchafua angahewa. Lakini hata kama chuma kingeyeyushwa kwa mvuke wa makaa ya mawe, kiasi 123

11:27 AM

Page 123


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio cha mazao hakikuwa kikubwa sana kiasi cha kuweza kuchafua angahewa. Hata mwanzoni mwa karne ya 18 madini ya chuma na chuma cha pua yalipoanza kuzalishwa kwa kiasi kikubwa nchini Ujerumani, Ufaransa, Uingereza na nchi nyingine za Ulaya, angahewa haikuchafuliwa ingawa mitambo yote ya kuyeyushia vyuma nchini Ujerumani, Ufaransa na Uingereza ilikuwa ikiunguza makaa ya mawe na utoaji wa moshi katika dohani za viwanda haukusimama hata kwa muda mfupi tokea mwanzo wa mwaka mpaka mwisho. Licha ya hili, angahewa haikuchafuliwa kwa moshi wa makaa ya mawe, achilia mbali wakati wa Ja’far Sadiq ambapo hapakuwa na kiwanda hata kimoja kinachofanana na viwanda vya kisasa na hakuna aliyechoma makaa ya mawe. Hata hivyo Ja’far Sadiq (a.s.), kama mtu aliyeweza kuziona hali za zana hizi, alisema: “Mwanaadamu anapaswa aendeshe maisha yake katika namna ambayo haitachafua mazingira yake, kwa sababu akifanya hivyo itakuja siku ambapo atapata ugumu au atashindwa kuishi kutokana na uchafuzi wa mazingira. Tatizo la uchafuzi wa hali ya maisha halikuwepo hata katika kipindi cha miaka arobaini iliyopita. Tatizo hili lilianza tokea bomu la kwanza la atomiki lilipolipuliwa na kuchafua angahewa katika ukanda wa mlipuko wake. Kama mwanaadamu angetosheka na hii hii milipuko ya kwanza, anga lisingekuwa limechafuka. Lakini nchi zilizokuwa na silaha za atomiki ziliendelea kufanya majaribio ya silaha hizo na sambamba na majaribio haya viwanda vya kuzalisha umeme vilianza kutumia nishati ya atomiki na uchafuzi wa angahewa uliongezeka kutokana na malighafi ya unururishaji. Wakati huo huo viwanda, na hususani vya nchini Marekani na Ulaya, vilichafua angahewa na maji ya baadhi ya mito, kwa mfano mto Roun huko Ulaya Magharibi ulichafuliwa sana kiasi cha viumbe jamii ya samaki kufa. Halikadhalika viumbe jamii ya samaki takribani wamepotea kabisa katika maziwa makubwa ya Amerika ya Kaskazini, yenye maji malaini 124

11:27 AM

Page 124


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio (matamu). Na uchafuzi wa maji ya bahari ni wa hatari zaidi kuliko uchafuzi wa angahewa na ardhi, kwa sababu viumbe wadogo wasioonekana kwa macho, waitwao Plankitoni ambao huishi juu ya maji ya bahari ambao huzalisha 90% ya Oksijeni duniani, watakufa kutokana na uchafuzi wa bahari na wakifa na kutoweka, kiasi cha oksijeni katika anga kitapungua na kubaki 10% ya kiasi cha sasa. Kiasi hiki hakitoshi ama kwa upumuaji wa wanyama akiwemo mwanadamu au kwa upumuaji wa mimea. Matokeo yatakuwa kwamba jamii ya mimea na wanyama katika dunia itatoweka. Hii sio nadharia tu ambayo usahihi au upotofu wake unaweza kubishaniwa. Kwa upande mwingine, hii ni hesabu ya kisayansi na kwa kuzingatia namna ambavyo uchafuzi wa bahari unavyofanyika hivi sasa, idadi ya plankitoni juu ya maji ya bahari itapungua kwa 50% katika kipindi cha miaka 50 ijayo na kiwango cha uzalishaji wa Oksijeni kitapungua pia kwa uwiano huo huo. Mtoto aliyezaliwa leo, baada ya miaka 50 (akiishi mpaka muda huo), atapumua sawa na anavyopumua mpanda mlima anayekwea kilele cha Himalaya, mlima mrefu kuliko yote duniani, anayepumua bila ya kifaa cha kupumulia. Ikiwa uchafuzi wa maji ya bahari utaendelea katika kipindi cha miaka 50 ijayo, namna ya upumuaji wa watu wote na wanyama itakuwa sawa na ile ya watu wenye matatizo ya moyo kwenda mbio. Baada ya miaka 50, ikiwa mtu atawasha kiberiti chake ili awashe sigara au jiko la mafuta katika nyumba yake, njiti haitawaka kwa sababu hapatakuwa na oksijeni ya kutosha hewani kuweza kuwasha moto. Maelezo haya sio ngano bali ni ukweli wa Kisayansi..... Ili kuelewa ni vipi kwa kupuuza mapendekezo yaliyotolewa na Ja’far Sadiq (a.s.) (kwamba mwanadamu asichafue mazingra yake) kunavyoliingiza taifa tajiri katika matatizo (basi) tuchukue mfano wa Japan.

125

11:27 AM

Page 125


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Leo hii Japan ni nchi inayoongoza duniani baada ya Marekani, kwa utengenezaji wa Magari, kompyuta na nguo za utembo bandia na inahesabika kuwa ni taifa linaloongoza mpaka sasa juu ya utengenezaji wa meli, redio, kaseti, televisheni, kamera na pikipiki unavyohusika. Kama tukisimulia ni jinsi gani Japani ilivyopata nafasi ya juu kama hiyo katika viwanda na biashara, kwa kipindi kifupi kiasi hicho kutokea sifuri tutakuwa tunatoka kwenye mada iliyo chini ya mjadala - yaani uchafuzi wa mazingira ya maisha. Tunaweza tukasema kwa kifupi kuwa mambo makuu mawili hasa ndio yalikuwa sababu za Japani kupata nafasi hii katika kipindi kifupi: (i) Uongozi mzuri (ii) Uaminifu wa wafanyakazi wa Japan katika kazi zao. Lakini kwa vile taifa hili tajiri na fanisi lilishindwa kuyahifadhi mazingira yasichafuliwe, sasa hivi linakabiliwa na tatizo kubwa sana kiasi kwamba afya za watu wake ziko hatarini na kutokana na uchafuzi wa angahewa, magonjwa yasiyo na mfano katika historia ya Sayasi ya tiba yameibuka nchini Japani. Mwanaadamu amebaini hivi punde tu hatari za kuchafua mazingira, hasa ardhi, mito na bahari. Lakini hata hivyo, watu wa zamani wenye hikma, kama Ja’far Sadiq (a.s.) walishabaini miaka 1200 iliyopita kwamba mwanadamu anapaswa kuendesha maisha yake katika namna ambayo hatachafua mazingira yake ya angahewa.

KUMWEKA MTOTO MCHANGA UPANDE WA KUSHOTO WA MAMA Moja za ishara za kipaji cha hali ya juu cha kisayansi cha Ja’far Sadiq (a.s.) ni ushauri wake kwa akina mama kwamba wanapaswa kuwaweka watoto wao wanaonyonya upande wao wa kushoto. Kwa karne (kadhaa) pendekezo hili lilionekana kuwa na ovyo au lisilo na umuhimu. Sababu ya hali hii ni kuwa hakuna aliyejua faida ya pendekezo 126

11:27 AM

Page 126


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio hili na baadhi ya watu waliona kuwa ni hatari kulifanyia kazi. Walifikiri kwamba mtoto akilazwa upande wa kushoto kwa mama, wakati wa kujigeuza akiwa usingizini, mama angeweza kumkandamiza mtoto. Muhammad bin Idris Shafi’i aliyezaliwa Ghazah mwaka 150 Hijiria, miaka miwili baada ya kifo cha Ja’far Sadiq (a.s.), na kufia Cairo mwaka 199 Hijiria, aliulizwa iwapo mama anapaswa kumlaza mtoto wake mdogo anayenyonya upande wa kushoto kwake au kulia kwake. Alijibu: “Hakuna tofauti yeyote kati ya upande wa kulia na kushoto. Mtoto anapaswa kulazwa upande ulio mujarabu zaidi kwa mama.” Wakati mwingine baadhi ya watu walichukulia maoni ya Ja’fa Sadiq (a.s.) kuwa ni kinyume na hukumu sahihi, kwa sababu kwa mujibu wa maoni yao upande wa kulia umetukuka zaidi kuliko upande wa kushoto na waliona kuwa mama anapaswa kumtazama mtoto wake katika upande wake wa kulia ili anufaike na baraka za upande wa kulia. Hakuna aliyejali ushauri wa Ja’far Sadiq (a.s.), si Mashariki wala Magharibi kiasi kwamba hata wakati wa Uamsho (Renaissance) ambapo kila mada ya kisayansi ilichunguzwa kwa jicho la umakinifu, hakuna aliyetia umuhimu wowote katika maoni ya Ja’far wala hakuna mtu aliyefikiria kuchunguza ikiwa maoni hayo yalikuwa na thamani au manufaa yoyote ya kisayansi au la. Karne za 16, 17 na 18 AD. ambazo zilikuwa ni karne za kipindi cha Uamsho na karne ya 19 ikawasili. Katika nusu ya pili ya karne hiyo, chuo kikuu cha Camell kilianzishwa nchini Marekani na kikaanza kufanya kazi. Ezra Cornell, mwanzilishi wa Chuo Kikuu hiki, aliyepata matatizo makubwa alipokuwa mchanga na alipokuwa mvulana mdogo, aliamua kuanzisha taasisi Maalumu katika Chuo hiki kwa ajili ya utafiti juu ya watoto waliozaliwa na watoto wachanga.

127

11:27 AM

Page 127


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Taasisi hii ilianzishwa na Chuo Kikuu cha Cornell katika mwaka wake wa kwanza wa kitaaluma na ilikuwa inahusiana na Chuo cha Utabibu. Ni zaidi ya karne sasa tangu iwe inajihusisha na utafiti juu ya watoto wachanga na watoto wanaonyonya. Hakuna kitu kinachohusiana na masuala ya watoto wachanga na wanaonyonya ambacho hakijachunguzwa na taasisi hii na hakuna kituo cha kisayansi duniani kinacholingana na hiki katika suala la kuwa na taarifa kuhusiana na watoto wachanga na wanaonyonya. Haiwezekani kwamba kunaweza kuwa na mada inayohusiana na watoto wachanga na wanaonyonya ambayo taasisi hii inaweza kuwa haijaichunguza. Hata chati ambapo juu yake pamechorwa picha za watoto wachanga na wanaonyonya imekuwa ni somo la utafiti la Taasisi hii. Katika nusu ya kwanza ya karne ya ishirini, watafiti wa Taasisi hii walizitazama chati zinazohusiana na watoto wachanga katika majumba ya makumbusho ya dunia, na kati ya chati 466 walizoona katika majumba mashuhuri ya makumbusho ya dunia walikuta kwamba katika chati zilizo nyingi akina mama walikuwa wamewabeba watoto wao katika upande wa kushoto. Katika chati 373 akina mama walikuwa wamewabeba watoto wao upande wa kushoto na katika chati 93, walikuwa wamewabeba upande wa kulia. Hivyo 80% ya chati katika majumba mashuhuri ya makumbusho zilionyesha kuwa akina mama walikuwa wamewabeba watoto wao upande wa kushoto. Katika jiji la New York baadhi ya hospitali kwa ajili ya akina mama wajawazito zinahusiana na Taasisi hiyo ya utafiti ya watoto wachanga na wanaonyonya ya Chuo Kikuu cha Cornell na madaktari wanaofanya kazi katika hizo hospitali za akinamama wajawazito huwasilisha matokeo ya uchunguzi wao kwenye taasisi hiyo. 128

11:27 AM

Page 128


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Kutokana na ripoti hizi zilizopokelewa na Taasisi hii kutoka kwa madaktari hawa, ambazo zilikuwa ni ripoti zilizoandaliwa kutokana na uchunguzi wa muda mrefu, ilihitimishwa kwamba katika siku za awali baada ya kuzaliwa, mtoto huhisi raha zaidi anapolala upande wa kushoto wa mama yake na akilazwa upande wa kulia (wa mama yake) huamka kila baada ya muda mfupi na kuanza kulia. Wachuguzi wa kituo cha utafiti hawakuishia utafiti wao kwa wamarekani weupe, lakini walipanga kutafiti ili kuona kama matokeo yatakuwa hivyo hivyo kwa upande wa watu weusi na wekundu. Baada ya safari ndefu ya utafiti katika watu wa rangi nyingine ilionekana kwamba matokeo yalikuwa yanafanana katika mataifa yote na kila sehemu watoto wachanga walikuwa wakisikia raha zaidi, hasa katika siku zao za mwanzo toka wazaliwe, wakilala upande wa kushoto wa mama zao kuliko wakilala upande wa kulia na ni ukweli unaowahusu watu wote sio watu weupe tu. Kituo cha utafiti cha Chuo Kiku cha Cornell kiliendelea na uchunguzi juu ya mada hii. Kwa masaa madaktari waliuchunguza mfupa wa nyonga wa mwanamke mjamzito kwa kutumia X–ray ili kumuona mtoto katika tumbo la mama. Lakini, uchunguzi wa mtoto tumboni haukuongeza chochote katika taarifa zao, mpaka chombo kiitwacho holografu* kilipogunduliwa. Baada ya kugunduliwa ‘holography’ madaktari wa kituo cha utafiti walipanga kuchukua picha za mimba katika tumbo la mama X-ray itakapokuwa imetupia mwanga hapo juu yake. Wakati huo walibaini kwamba mawimbi ya suati ya mapigo ya moyo wa mtoto ambayo hutawanywa katika mwili wake wote (wa mama) huyafikia masikio ya mtoto aliyeko tumboni.

129

11:27 AM

Page 129


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Baada ya hatua hii, na ili wapate habari zaidi, ilikuwa ni muhimu kwao kujua ikiwa kutulia kwa mapigo ya moyo wa mama kutaleta mwitikio wowote kwa mtoto aliyeko tumboni. Kwa vile hawakuwa wanaweza kusimamisha moyo wa mama kwa vile hilo lingemsababishia kifo, waliendelea na majaribio yao kwa wanyama wa jamii ya mamalia na kila waliposimamisha ufanyaji wa kazi wa moyo mnyama aliyebeba mtoto tumboni, waliona athari ilitokea kwa mtoto. Majaribio yaliyorudiwa na kukaririwa kwa baadhi ya wanyama wa jamii ya mamalia yalithibitisha kwamba pindi mapigo ya moyo wa mama yanaposimama, athari hutokea kutoka kwa mtoto tumboni na baada ya kifo cha mama, mtoto pia hufa.

Baada ya kufanya majaribio mengi, wasomi wa kituo cha utafiti cha Chuo Kikuu cha Cornell walifikia hitimisho kuwa mtoto katika tumbo la mama yake sio tu kwamba huzoea kusikia mapigo ya moyo wa mama yake, bali pia mapigo hayo yanahusiana na maisha yake na pindi mapigo haya yakisimamishwa mtoto hufa kwa njaa tumboni mwa mama yake. Tabia ya kusikia mapigo ya moyo wa mama yake huzoeleka kwa mtoto kiasi kwamba hata baada ya kuzaliwa, hujisikia ugumu asiposikia mapigo ya mama yake na akili ya mtoto mchanga inawaza kuyaelewa mapigo haya vizuri kabisa. Ni kwa sababu hii kwamba mtoto mchanga anapolazwa upande wa kushoto husikia sauti ya mapigo ya moyo wa mama yake na hujisikia amani, lakini akilazwa upande wa kulia huwa hasikii sauti hiyo na hivyo hukosa amani. Kama mwanzilishi wa Chuo Kikuu cha Cornell asingeanzisha kituo cha utafiti kinachohusiana na watoto wachanga na wanaonyonya, na kituo hiki kisingefanya utafiti huu wa kina, falsafa ya Ja’fa Sadiq (a.s.) inayopendekeza akina mama wawalaze watoto wao upande wa kushoto isingejulikana. 130

11:27 AM

Page 130


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Siku hizi katika vituo vyote vya kulelea watoto vinavyohusiana na kituo cha utafiti cha Chuo kikuu cha Carnell, vina chombo katika kila chumba ambamo watoto wachanga wanalala ambacho hutoa sauti ya mapigo ya moyo wa mama na kuna chombo cha kupokelea sauti hiyo katika kitanda cha kila mtoto mchanga ambacho hupeleka mapigo bandia ya moyo wa mama yake katika masikio yake. Moyo wa mtu mzima, awe mwanaume au mwanamke kwa kawaida hupiga mara 72 kwa dakika. Katika vituo vya kulelea watoto ambavyo vinahusiana na kituo cha utafiti cha Chuo Kikuu cha Cornell, imeshajaribiwa kwamba idadi ya mapigo bandia ya moyo wa mama ikifikia 110 au 120 kwa dakika watoto wote huanza kulia. Hivyo idadi ya hayo mapigo bandia yanapaswa kuwa 72 kwa dakika ili watoto wasione taabu na wasilie. Katika vituo vya kulelea watoto vinavyohusiana na kituo cha utafiti, jaribio lifuatalo limeshafanywa mara kadhaa. Baadhi ya watoto wachanga waliwekwa ndani ya chumba ambamo sauti za bandia za mapigo ya moyo wa mama hazikuyafikia masikio yao na watoto wengine wachanga waliwekwa katika chumba ambacho waliweza kuisikia sauti hiyo. Kila jaribio hili lilipofanywa, ilikutikana kwamba uzito wa watoto katika chumba ambacho sauti ya mapigo bandia ya moyo wa mama ilikuwa inaweza kusikika uliongezeka haraka zaidi kuliko wengine ingawa watoto wa vyumba vyote viwili walipewa vyakula vya aina moja. Ukweli ni kwamba watoto katika chumba ambapo sauti ya mapigo bandia ya moyo wa mama inasikika huko, wanakula chakula chao kwa hamu zaidi kuliko wale wengine. Utafiti pia uliofanywa katika vituo vya kulelea watoto vinavyohusiana na Chuo Kikuu cha Cornell juu ya ukubwa wa sauti ya mapigo bandia ya 131

11:27 AM

Page 131


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio moyo wa mama na ilionekana kwamba sauti ikiwa kubwa kuliko sauti ya asili ya mapigo ya moyo wa mama watoto hujisikia taabu na kuanza kulia. Katika safari zake kwenye mabara mbalimbali ya dunia, mmoja wa madaktari wa kituo cha utafiti cha Chuo Kikuu cha Cornell alichunguza kwa makini jinsi akina mama katika nchi mbalimbali wanavyowabeba watoto wao barabarani. Daktari aitwaye Dk. Lee Salk ambaye kwa sasa anafanya kazi katika kituo hiki cha utafiti anasema: “Wanawake walio wengi katika mabara yote duniani huwabeba watoto wao katika upande wao wa kushoto wanapotembea barabarani. Wanawake wengi wanaowabeba watoto wao katika upande wa kulia ni wale ambao hufanya kazi kwa mikono yao ya kushoto. Wanawabeba watoto wao katika upande wao wa kulia hasa wanapokuwa wanalazimika kubeba kikapu au vyakula ili waweze kuvibeba kirahisi kwa mkono wao wa kushoto. Katika hospitali za akina mama wajawazito zinazohusiana na kituo cha utafiti, Dk. Lee Salk anawauliza swali hili wanawake wote baada ya kuzaa na kuondoka hospitali na kuwabeba watoto wao wachanga katika upande wa kushoto. “Je mnajua ni kwa nini mnambeba watoto wenu wachanga upande wa kushoto?” Lakini hakuna aliyemwambia Dk. Lee Salk kwamba wanafanya hivyo kwa sababu moyo upo upande wa kushoto wa kifua na (kwamba) ina manufaa kwa watoto wachanga kusikia sauti ya mapigo yake. Akina mama wanawabeba watoto wao katika upande wao wa kushoto bila kujua ni kwa nini wanaupendelea upande huo. Hata wanawake Waafrika wenye ngozi nyeusi huwabeba watoto wao katika upande wa kushoto wa vifua vyao wanapokuwa hawajawabeba migongoni mwao. Katika makabila yote ya Kiafrika yenye ngozi nyeusi, wanawake wanajua kuwa mtoto mchanga akiwekwa upande wa kushoto hunyonya vizuri zaidi na hamu ya kunyonya watoto wachanga ziwa la kushoto ni kubwa zaidi ikilinganishwa na ziwa la kulia. 132

11:27 AM

Page 132


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Dk. Lee Salk amesikia kutoka kwa akina mama kuwa mtoto anaposikia njaa usiku hulipata ziwa la kushoto la mama gizani kwa wepesi wa kushangaza, huweka mdomo wake na kunyonya maziwa. Wanashangaa ni vipi mtoto analiona ziwa la mama yake, bila mwanga wa taa na kuweka mdomo wake haraka. Dk. Lee Salk anawafafanulia akina mama kuwa mtoto huongozwa na mapigo ya moyo wa mama yake katika kulifikia ziwa gizani. Mara tu anaposikia sauti ya mapigo hulipata ziwa bila kusitasita na huweka mdomo wake.

MWANGA – NJIA YA KUENEZA UGONJWA .... Moja ya maoni ya Ja’fa Sadiq (a.s.) ambayo huthibitisha kipaji chake cha hali ya juu katika sayansi ni maoni yake kwamba ugonjwa unaweza kuenea kwa njia ya aina fulani za mwanga. Ja’far Sadiq (a.s.) alisema: “Kuna baadhi ya mianga ambayo ikitokea kwa mgonjwa na kwenda kwa mtu mwenye afya inaweza kumfanya mtu mwenye afya kuwa mgonjwa.” Inafaa ikumbukwe hapa kuwa kinachozungumziwa sio angahewa au ueneaji wa vimelea vya magonjwa ambayo watu walikuwa hawavijui kabisa katika nusu ya kwanza ya karne ya pili Hijiria bali ni juu ya mwanga. Na pia haisemwi kuwa mianga yote ina tabia ya kumuuguza mtu mwenye afya ikimfikia kutoka kwa mtu mgonjwa bali ni baadhi tu ya mianga ndio inayoweza kufanya hivyo. Wasomi wa bailojia na utabibu waliyaona maoni haya kama badhilifu kwa sababu waliamini kwamba vitu vinavyoeneza maradhi kutoka kwa 133

11:27 AM

Page 133


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio mgonjwa kwenda kwa mtu mzima ni vimelea vya maradhi au virusi, ikiwa njia za ueneaji wa ugonjwa zilikuwa ni wanyama wa ngeli ya reptilia, maji, hewa au kugusana kimwili kati ya mgonjwa na mtu mzima. Kabla ya kujulikana hivyo vimelea vya maradhi, harufu ilikuwa inachukuliwa kuwa ni njia ya uenezaji wa maradhi na hatua zote zilizochukuliwa zamani kuzuia ueneaji wa maradhi zilikuwa zimeegemea kwenye kuzuia harufu ili mtu mwenye afya asije akapata ugonjwa kwa uambukizwaji kutoka kwa mgonjwa. Hakuna aliyesema katika kipindi chochote kuwa ikiwa mwanga kutoka kwa mgonjwa utamfikia mtu mwenye afya utamfanya augue. Lakini ni Ja’far Sadiq aliyesema hili. Kama tulivyosema hapo juu kwamba wanasayansi wote waliliona wazo hili ni badhilifu hadi utafiti wa kisayansi ya kisasa ulipothibitisha kwamba huo ni ukweli na kwamba kuna baadhi ya mianga ambayo inawafanya watu wenye afya kuwa wagonjwa kama ikiwamulika. Ilikuwa ni Urusi iliyolitambua hili kwa mara ya kwanza. Katika jiji la Novo Sabirisk lililopo katika Muungano wa Urusi (Siberia) na ambalo ni moja ya vituo vikubwa kabisa vya utafiti katika utabibu, kemia na baiolojia, ilithibitika kisayansi na kwa ushahidi wa kutosha kabisa kwamba kwanza mionzi hutoka katika seli za mtu mgonjwa na pili kuna mionzi ambayo hutoka kwenye seli za mtu mgonjwa na kuzifanya seli za mtu mwenye afya ziugue zinapomfikia bila (hata) ya kugusana kwa seli za mgonjwa na za mwenye afya na bila kuenea na kusambaa kwa vimelea vya magonjwa na virusi kutoka kwenye seli za mgonjwa kwenda kwenye seli za mtu mwenye afya njema. Utaratibu uliotumiwa na wanasayansi waliokuwa wakishughulika katika utafiti huko Novo Sabirisk ulikuwa huu: Walichagua makundi mawili ya seli zenye umbile moja kutoka kwa mnyama na wakazitenganisha na wakaona aina fulani ya fotoni (kipimo cha nishati ya mwanga) zilikuwa zinatoka kutoka katika seli hizo. 134

11:27 AM

Page 134


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Baada ya kuchagua makundi mawili ya seli zinazofanana kutoka kwa mnyama na kuzigawanya katika sehemu mbili, walizipatia maradhi seli za kundi moja ili kuona kama mionzi ilikuwa inatoka katika seli hizo (hata) katika hali ya ugonjwa na walikuta kwamba fotoni zilikuwa zikitoka katika seli hata zilipokuwa zinaugua. Wanasayansi waliweka seli za kundi la pili ambazo zilikuwa na afya katika masanduku mawili. Moja ya masanduku haya lilikuwa limetengenezwa kwa kioo aina ya Silika (Quartz) na sanduku jingine lilikuwa limetengenezwa kwa kioo cha kawaida. Kioo aina ya silika kina tabia kwamba huwa hakiruhusu aina zote za mionzi kupita isipokuwa mionzi ya ‘Ultra Violet.’ Kioo cha kawaida kina tabia kwamba huruhusu aina zote za mionzi kupita isipokuwa ya urujuani ‘Ultra Violet.’ Baada ya masaa kadhaa seli zenye afya zilizowekwa kwenyue glasi za silika na glasi za kawaida zilipoachwa wazi kuonana na seli zinazougua, ilikutwa kwamba seli zenye afya kwenye glasi ya silika zilikuwa zimeugua ambapo zile zilizokuwa kwenye glasi ya kawaida hazikuugua. Jaribio hili lilirudiwa mara 5000 katika kipindi cha miaka 20 kwa kutumia magonjwa mbalimbali na seli zinazofanana na zisizafanana, kwa sababu wanasayansi hao hawakutaka pawepo na chembe yoyote ya shaka juu ya matokeoa yaliyofikiwa. Katika majaribio yote 5000 matokeo ya mwisho yalikuwa yanafanana – kwamba seli zinazougua hutoa aina fulani ya mionzi ikiwemo ya urujuani (ultra violet) isiyoonekana kwa jicho la mwanadamu. Pia, pindi seli zenye afya zikiwekwa kwenye mazingira yenye mionzi ya urujuani iliyotolewa na seli zinazougua (na sio mionzi mingine ya urujuani) huugua. Pia ugonjwa wake huwa ni sawa na ule wa seli zinazougua.

135

11:27 AM

Page 135


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Katika kipindi chote hiki cha majaribio kilichodumu kwa miaka 20, hapakuwepo na kugusana au kukaribiana kati ya seli zenye afya na zile zinazougua ambapo inaweza ikadhaniwa kuwa virusi au vimelea vya maradhi vya kundi moja viliambukiza kundi jingine kwa njia ya kugusana na wanasayansi walijua kwa hakika baada ya majaribio 5000 kwamba wakala wa kuonekana kwa ugonjwa katika seli zenye afya ni miozi ya ultra violet ambayo hutoka katika seli zinazougua na kuzifikia zile nzima. Kutokana na majaribio yaliyofanywa na wanasayansi wa Urusi, tunaweza tukahitimisha kuwa, kila seli ya miili yetu ni kama mtumaji na mpokeaji ambaye hutoa mionzi na pia huathirwa na mionzi hiyo na huihifadhi..... Ni dhahiri kwamba ukweli huu wa kisayansi ambao umethibitishwa kwa majaribio 5000 uliofanyika katika kipindi cha miaka 20 umefungua uwanja mpya kwa wanabailojia na madaktari kwa kutibu magonjwa mbalimbali. Utafiti umefanywa katika medani hii nchini Marekani pia na matokeo yaliyopatikana yanafanana na yale waliyoyapata wanasayansi wa Urusi na yameripotiwa katika Jarida la Kisayansi la Marekani. Mmoja wa watafiti wasomi aitwaye Dk. John Oat pia ameandika kitabu juu ya mada hii. Kutokana na hayo yaliyosemwa hapo juu, tunaweza kuhitimisha kwamba maoni ya Ja’far Sadiq (a.s.) katika nusu ya kwanza ya karne ya pilii Hijiria kwamba mianga husababisha maradhi (maoni ambayo awali yalichukuliwa kuwa ni uzushi) ni ukweli na tunajua sasa kwamba mionzi ya urujuani ikisafiri kutoka kwa wagonjwa kwenda kwa watu wazima, mionzi hiyo huwafanya hao wazima nao waugue ambapo mionzi mingine ya urujuani, na muhimu zaidi ya mionzi yote ya urujuani ya jua haisababishi maradhi yoyote inapoangukia viumbe hai. Ikiwa mwanga wa mionzi ya urujuani ya jua itaifikia miili ya viumbe hai bila ya kuwepo hewa kati yake na kukawa hakuna kizuizi kati ya mwili na mionzi hiyo, (basi) mionzi hiyo inaweza kuleta maafa kwa viumbe. Lakini mionzi hii hii ikifika duniani baada ya kupita kwenye hewa, haimuuguzi yeyote. 136

11:27 AM

Page 136


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Katika hali yoyote ugunduzi wa kisasa wa kibailojia na kitabibu umethibitisha usahihi wa maoni ya Ja’far Sadiq (a.s.) baada ya kupita miaka 1250.

ELIMU ZA DUNIA NYINGINE: Swali jingine ambalo Ja’far Sadiq (a.s.) aliulizwa lilikuwa hili: “Ni nani anaweza kuchukuliwa kuwa anajua kila kitu na ni katika hatua gani ambapo mwanaadamu anaweza kuhisi kwamba amejifunza kila kitu?” Ja’far Sadiq (a.s.) alimwambia muulizaji; “Unapaswa uligawe swali katika sehemu mbili na unapaswa uniulize kila swali tofauti toauti. Sehemu ya kwanza ambayo unaweza kuniuliza: “ni nani anaweza kuchukuliwa kuwa anajua kila kitu?” “Ninakujibu kuwa hakuna anayejua kila kitu isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na haiwezekani kwa mwanaadamu yeyote kujua kila kitu. Iko hivi kwa sababu elimu ni pana mno kiasi kwamba hakuna anayeweza kujua mambo yote yanayopasa kujua hata kama ataishi kwa maelfu ya miaka na akawa anashughulika sana katika kipindi chote hicho katika kutafuta elimu. Baada ya kuishi kwa maelefu ya miaka pengine anaweza kujua fani zote za elimu zinazohusiana na ulimwengu huu. Lakini, mbali na dunia hii kuna dunia nyingine na maarifa mengine katika dunia hizo. Hivyo mtu aliyesoma elimu zote za dunia hii atakuwa ni mjinga atakapowasili katika dunia nyingine na atapaswa kuanza masomo yake kuanzia sifuri ili aweze kujua maarifa ya dunia hizo. “Ni Mwenyezi Mungu Mtukufu tu ndiye anayejua kila kitu kwa sababu hakuna mwanaadamu anayeweza kupata elimu juu ya kila kitu.” Kisha wanafunzi wa Ja’far Sadiq (a.s.) wakauliza sehemu ya pili ya swali – kwamba ni wakati gani mwanaadamu anaweza kuhisi kuwa amejifunza 137

11:27 AM

Page 137


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio kila kitu. Ja’far Sadiq alijibu: “Jibu langu la kwanza linajibu na swali hili pia, kwa sababu nimewaambia kuwa hata kama mwanaadamu ataishi maelefu ya miaka na kusoma mfululizo, hawezi kujifunza vitu vyote vinavyoweza kujulikana. “Hivyo, kamwe muda hautakuja ambapo mwanaadamu atahisi kuwa hahitaji elimu zaidi. Ni watu wajinga tu ndio huhisi kuwa hawahitaji elimu zaidi na kila aliye mjinga huhisi kuwa hahitaji elimu.” Ja’far Sadiq (a.s.) aliulizwa kuwa ilimaanisha nini kusema: “Elimu za dunia nyingine? Alijibu: “Mbali na ulimwengu huu tunaoishi kuna dunia nyingine nyingi ambazo ni kubwa kuliko hii na katika dunia hizo kuna maarifa ambayo ni tofauti na maarifa ya dunia hii.” Ja’far Sadiq aliulizwa: “Ni ipi idadi ya hizo dunia nyingine?” Alijibu: “Hakuna anayejua idadi, ya dunia hizo mbali na Mwenyezi Mungu.” Aliulizwa: “Ni vipi kujifunza katika dunia nyingine kunavyotofautiana na kujifunza katika dunia hii? Je elimu haifunziki? Na inawezekana vipi kitu kinachofundishika kiwe tofauti na elimu za dunia hii?” Alijibu: “Katika dunia nyingine kuna aina mbili za elimu: Elimu za aina moja zinafanana na elimu za dunia hii na mtu yoyote akitoka katika dunia hii, na kwenda huko ataweza kuzipata. Lakini katika dunia nyingine hizo kuna elimu (nyingine) ambazo haiwezekani kwa watu wa dunia hii kuzielewa kwa sababu akili zao haziwezi kuzifahamu.” Maneno haya ya Ja’far Sadiq (a.s.) yalikuwa ni kitendawili kwa vizazi vilivyofuatia. Baadhi ya watu waliyachukulia (maneno haya) kuwa hayakubaliki na walisema (kuwa) alichosema hakina msingi. Mmoja wa watu waliotilia shaka kauli ya Ja’far Sadiq (a.s.) alikuwa ni Ibn Rawandi wa Isfahan. Alisema kuwa akili ya mwanaadamu inaweza kuele138

11:27 AM

Page 138


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio wa kitu chochote ambacho ni elimu – kiwe ni elimu ya dunia hii au dunia nyingine. Lakini, wanafunzi wa Ja’far Sadiq (a.s.) waliyakubali maneno ya mwalimu wao na waliamini kwamba katika dunia nyingine kuna elimu nyingine ambazo haziwezi zikasomwa na wanaadamu kwa sababu akili ya mwanaadamu haina uwezo wa kuzielewa. Lakini katika karne iliyopita. Nadharia ya Einstein ya uwiano ‘Relativity’ ilifungua sura mpya na isiyokuwa na mfano katika Fizikia na baadaye nadharia ya kiini (kisicho–mata) ilipita kutoka katika hatua ya nadharia na kufikia hatua ya Sayansi na wanasayansi wakaja kubaini kwa yakini kuwa kisicho – mata (anti-matter) kipo. Kutokana na maendeleo haya, maelezo ya Ja’far Sadiq (a.s.) kwamba dunia nyingine kuna elimu ambayo mwanaadamu hawezi kuielewa, sasa yanaeleweka, kwa sababu katika ulimwengu wa kisicho–mata, sheria za kiumbo zitakuwa tofauti na sheria za kiumbo za dunia yetu na mbali na hili pia kunaweza kuwa sheria za mantiki na hoja za kiakili katika dunia hizo ambazo zinaweza kuwa haziwezekani kwa akili zetu kuzitengeneza au kuzielewa. Ulimwengu wa kisicho-mata ni ulimwengu ambako chaji ya elektroni katika atom ni chanya ambapo chaji ya protoni (katika kiini cha atom) ni hasi, lakini katika ulimwengu wetu chaji ya electroni ni hasi na chaji ya protoni (katika kiini cha atom) ni chanya. Haiwezi kusemwa ni sheria gani za kiumbo zinazotawala ulimwengu ambamo chaji za elektroni za atomu ni chanya na chaji ya protoni ni hasi. Kwa mujibu wa mantiki yetu na hoja za kiakili: “Kizima” ni bora kuliko “Sehemu” lakini inawezekana kwamba katika ulimwengu huo neno “sehemu” linaweza kuwa bora kuliko “kizima” na akili yetu haiko katika nafasi ya kuelewa au kukubali wazo hili.

139

11:27 AM

Page 139


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Katika ulimwengu wetu tunapotupa kitu kizito ndani ya maji hupungua uzito kwa mujibu wa sheria iliyogunduliwa na Archimedes, lakini inawezekana kwamba katika ulimwengu huo kitu kinaweza kuwa kizito zaidi ndani ya maji au kimiminika kingine. Katika ulimwengu huu, kwa mujibu ya sheria iliyogunduliwa na Rascal,2 mgandamizo unapogandamizwa juu ya sehemu moja ya kimiminika katika chombo, mgandamizo huo husambaa katika sehemu zote za kimiminika hicho. Ni kwa kutumia sheria hii kwamba breki za hydroliki zimeandaliwa kwa ajili ya magari na hasa magari makubwa na mgandamizo wa mguu wa dereva juu ya pendeli za breki unapogandamizwa juu ya mafuta, husambaza kanieneo katika sehemu zote za mafuta na hivyo, mbinyo katika magurudumu ya gari huwa mara elfu moja zaidi ambao hulisimamisha gari mara moja. Lakini, inawezekana kwamba sheria hii ya kiumbo inaweza isitumike katika ulimwengu wa kisicho-mata na mgandamizo unaotoka katika sehemu moja ya kimininika inaweza isisambae katika sehemu nyingine. Ikiwa mtu anayeishi katika ulimwengu huu atawasili katika ulimwengu wa kisicho-mata inawezekana kwamba pole pole anaweza kuzoea sheria za kimaumbile za ulimwengu huo ambazo ni ngeni na zisizo za kawaida kwake kama tu wanaanga wanavyozoea hali ya kutokuwa na uzito. Lakini, vitu ambavyo mwaadamu hawezi kuvikubali katika ulimwengu wa kisicho-mata ni vile ambavyo havikubaliani na mantiki yake na hoja za kiakili. Ikiwa katika ulimwengu huo atakuta kuwa ‘sehemu’ ni bora kuliko ‘kizima’ au akikuta kwamba watu katika ulimwengu huo hawazingatii kanuni katika kujumlisha, kutoa, kuzidisha na kugawanya au akihisi kwamba katika ulimwengu huo joto hugandisha maji au baridi kuvukisha maji bila hata ya kuwepo ombwe hawezi akaelewa hali hizi zisizowiana. Huu ni wakati mujarabu ambapo maoni ya Ja’far Sadiq (a.s.) yanaonekana kukubalika kwamba katika baadhi ya dunia kuna maarifa ambayo hai140

11:27 AM

Page 140


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio wezekani kwa mwanaadamu kuyapata.. Hitimisho linaloweza kufikiwa kutokana na mjadala huo hapo juu ni kwamba kwanza Ja’far Sadiq (a.s.) aliichukulia elimu kuwa haina kikomo na pili aliamini kwamba kuna maarifa katika dunia nyingine ambayo mwanadamu hawezi kuyaelewa kwa kutumia akili na busara ambayo huitumkia kujifunzia vitu katika dunia hii na sasa, kama ilivyoelezwa tayari hapo juu, ambapo Nadharia ya Einstein ya uwiano - ‘relativity’ na wazo la kisicho-mata ambalo limevuka mipaka ya nadharia na zimefikia katika hatua ya ukweli wa kisayansi, tunaweza tukasema kuwa Ja’far Sadiq (a.s.) alikuwa ametoa wazo sahihi karne kumi na mbili na nusu zilizopita.” (Khwandaniha). Mifano hiyo hapo juu, ambayo inaonyesha tone tu kati ya bahari isiyo na mipaka ya elimu ambayo kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na viongozi wa Uislamu, huifanya nukta hii kuwa wazi kwamba walipata elimu yao kutoka katika chanzo ambacho wanaadamu wa kawaida hawawezi kufikia na pia haiwezekani kwa mtu kunufaika kutokana na chanzo hicho isipokuwa kwa kupitia kizazi cha watu wa nyumba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Mifano hii pia inashuhudia kuwa katika hali yoyote hatupaswi kupuuzia kuyatekeleza mafundisho ya Uislamu na kamwe tusizembee kuzitekeleza amri zake tukufu, kwa sababu kila amri ina falsafa nyuma yake na tukiziasi tunaweza kuingia katika matatizo ambayo wakati fulani hayatibiki na yanaweza kuuharibu msingi wa mafanikio yetu. Mwisho tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu awasaidie Waislamu kufuata amri za Uislamu kikamilifu chini ya muongozo wa kizazi kiteule cha nyumba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

141

11:27 AM

Page 141


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio

KUTEKELEZA AHADI Kutekeleza ahadi na kutimiza maagano ni moja ya sifa ambazo zinatambuliwa na tabia ya kila mwanaadamu. Thamani na umuhimu wa kutekeleza ahadi, na halikadhalika tabia mbaya ya kuvunja mikataba na kutotekeleza ahadi na maagano inatambulika na kila mtu, awe wa rangi au taifa lolote na awe wa madhehebu au wa dini yoyote, kiasi kwamba hata watoto, kufuatia kanuni za maumbile, wanaungalia mwenendo wa wazazi wao, ambao wanawapa ahadi na hawaziheshimu, kuwa ni tabia mbaya na isiyofaa, na kuishutumu kwa pingamizi za kitoto. Umuhimu wa kutimiza ahadi huwa dhahiri pale athari zake za kijamii zinapozingatiwa vema, na hatari zinazotokana na kuvunja ahadi na kukiuka maagano yanapofikiriwa. Kuheshimu mikataba na ahadi kuna athari za moja kwa moja na zisizokatalika katika nyanja zote za maisha ya kila mtu, jamii na taifa. Jamii inayoheshimu mikataba na maagano huishi maisha ya raha na kustahili heshima mbele ya macho ya jamii nyingine. Masuala ya kifedha na kiuchumi ni nguzo muhimu kabisa na za msingi za maisha ya kila jamii. Watu wakiheshimu ahadi zao katika masuala ya kifedha, gurudumu la uchumi wa jamii huzunguka vizuri na shughuli za kiuchumi huchukua sura nzuri. Mdaiwa hulipa deni lake katika tarehe iliyopangwa na mkopeshaji pia humpa bidhaa zake kwa uhakika na imani. Kwa njia hii kila mmoja anaweza kupanga mipango kwa ajili ya maisha yake ya baadaye na kufanya mapatano na wengine. Katika jamii hiyo, ahadi za mdomo zinaweza kukidhi haja ya maandishi madhubuti kabisa na kuaminiana hujenga utaratibu mzuri katika uchumi 142

11:27 AM

Page 142


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio wa jamii. Hivyo, kama umma ukipoteza maadili haya mashuhuri na thamani ya kibinadamu kimaadili, huingia katika mabalaa yasiyorekebika na matatizo yasiyovumilika. Maelefu ya watu hawana makazi na wanatafuta nyumba za kupanga na maelfu ya nyumba ziko wazi na wamiliki wake wanataka kuzipangisha. Lakini, kwa vile kuaminiana hakupo, wamiliki wa nyumba huhiari kuziacha nyumba zao wazi kuliko kuzipangisha kwa watu wasiolipa kodi kwa wakati na wasiotimiza ahadi zao. Kiasi kikubwa cha mitaji kimekaa bure na wamiliki wake wanatafuta mshirika ili waanzishe biashara ya pamoja. Pia kuna watu ambao wako tayari kufanya shughuli za biashara lakini hawana fedha. Wao pia wanatafuta washirika ambao wana mtaji kwa ajili ya kuwekeza. Lakini, kwa vile hakuna kuaminiana kwa pande zote mbili, wamiliki wa fedha huhiari kuziacha fedha zikae tu kuliko kuwa na mshirika asiye mwaminifu. Pale masuala haya yatakapofikiriwa thamani na umuhimu wa kuheshimu ahadi na mapatano huwa wazi kabisa. Lakini hata hivyo, rasililmali hii yenye thamani anaweza kuipata yule mtu tu aliyepata mafundisho ya kidini kwa sababu kitu pekee ambacho huwafanya watu waheshimu ahadi zao ni nguvu ya imani na mafundisho ya kidini. Qur’ani Tukufu na Hadithi za Kiislamu zimeweka umuhimu mkubwa sana katika kuheshimu ahadi kiasi kwamba mtu anaweza kubaini kiwango chake tu kwa kurejea kwenye maelezo na maoni ya viongozi watukufu wa Uislamu. Katika Uislamu kuheshimu ahadi kumetambuliwa kuwa ni moja ya wajibu wa msingi wa kila Mwislamu na ni moja ya alama bainifu na sifa bora ya watu waumini. Qur’ani Tukufu inasema: “Hakika wamefuzu wenye kuamini. Ambao ni wanyenyekevu katika Sala zao..... Na ambao kwa amana zao na ahadi 143

11:27 AM

Page 143


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio zao ni wenye kuzitekeleza.” – (Surat al-Mu’min. 23: 1,2 & 8). Pia Qur’ani tukufu imesema: “..... Na tekelezeni ahadi, kwani ahadi itaulizwa.” – (Surat Bani Isra’il, 17:34). Imam Musa Kadhim (a.s.) amemnukuu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuwa amesema: “Yule ambaye haheshimu ahadi zake hana imani.” (Nawaadiir-i Raawandi, uk.5). Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: “Ikiwa mtu anayemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Hukumu atawekeana ahadi na mtu yeyote anatakiwa atimize ahadi hiyo.” (Wafi, Juz. 1, uk. 157). Hata alipokuwa katika kilele cha ujana wake na kabla hajateuliwa kwa kazi ya utume, mara zote Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akiheshimu ahadi na makubaliano aliyokuwa akifanya pamoja na watu wengine. Mtu mmoja aliyeitwaye Ammar, aliyekuwa mchungaji katika mji wa Makka anasema: “Nilikuwa nikipeleka kondoo wangu katika msitu wa Makka kwa ajili ya malisho. Muhammad (s.a.w.w.) pia alileta kondoo wake. Siku moja nilimwambia: ‘Kuna bonde la kijani baina ya vile vilima viwili, ambalo ni zuri sana kwa malisho ya kondoo. Ukikubali sisi sote tutapeleka kondoo wetu katika sehemu hiyo kesho.’ Muhammad (s.a.w.w.) alielezea kuridhika kwake na kisha tukarudi nyumbani jioni. Asubuhi niliwapeleka kondoo wangu sehemu tuliyoagana na nilimuona Muhammad (s.a.w.w.) akiwa tayari ameshapeleka kondoo wake hapo lakini alikuwa hawaruhusu kula. Nilipomuuliza sababu ya kufanya hivi alisema: “Nilifanya ahadi na kwamba tutalisha kondoo katika sehemu hii pamoja. Hivyo sikutaka kuwaruhusu kondoo wangu (kula) kabla wewe hujafika – (Biharul-Anwar). Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: “Siku ya Hukumu watu watakaokuwa karibu zaidi na mimi watakuwa ni wale wanaosema ukweli, wanajitahidi 144

11:27 AM

Page 144


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio zaidi kurejesha amana kwa wenyewe, ambao ni waaminifu katika kuheshimu ahadi zao, wenye maadili mazuri na wale wanaodumisha mahusiano mazuri na watu.” (Amali Tusi, Juz 1). Viongozi wa Uislamu wamechukulia mtu kuheshimu ahadi zake kuwa ni kigezo cha msingi cha utukufu na uadilifu na wamesema kwamba yule anayeheshimu ahadi zake anastahili heshima, urafiki na udugu. Imam Ali Riza (a.s.) amemnukuu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuwa amesema: “Mtu asipofanya dhulma kwa watu katika maswala ya biashara na asiposema uongo na akiheshimu ahadi, (basi huyu) ni mtukufu, muadilifu na anafaa kwa urafiki na udugu na ni haramu kumteta – (Uyunul-Akhbar, Juz. 2, uk. 30). Mmoja wa watumwa walioachwa huru na Imam Sajad (a.s.) alipata mtaji kutokana na kufanyakazi kwa bidii. Wakati fulani Mtukufu Imam alipatwa na ugumu wa kifedha. Alimuomba mtumwa huyo aliyeachwa huru kumkopesha dirham 10,000 ambazo angezirejesha atakapopata. Huyu mtumwa alitaka kitu cha kuwekwa rehani. Imam alivuta uzi kutoka katika joho lake na kumpa akisema: “Hii ni rehani yangu ambayo inapaswa kubaki na wewe mpaka deni litakapolipwa. Ilikuwa ni vigumu kwa huyo mkopeshaji kukubali kitu hicho chenye thamani ndogo kama rehani. Lakini, kwa hicho chenye thamani ndogo kama rehani. Lakini, kwa kuzingatia haiba ya Mtukufu Imam na maelezo yake, alimkabidhi fedha na akachukua uzi wa joho na kuuweka katika mkebe mdogo. Kwa bahati hali ya kifedha ya Imam iliboreka baada ya muda mfupi. Hivyo alipeleka dirhamu 10,000 kwa mkopeshaji na akamwambia fedha zako ni hizi hapa. Lete rehani yangu. Akasema: “Nimepoteza uzi wa joho.” Mtukufu Imam akasema: “Kama ni hivyo usichukue kiasi cha fedha za deni kutoka kwangu. Haipaswi amana yangu ichukuliwe kuwa ni kitu kisicho cha muhimu.” Kwa hiyo huyo mtu alilazimika kuleta mkebe na akaona kwamba uzi wa joho ulikuwa kama alivyopewa. Alimpatia Mtukufu Imam ule uzi. (Imam) 145

11:27 AM

Page 145


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio alimpatia fedha akauchukua ule uzi kutoka kwake na akautupa.” (Biharul Anwar, Juz.11) Uzi wa joho hauna thamani yoyote wenyewe kama uzi, lakini uzi huo unapokuwa ni ishara ya dhamana na wajibu wa mtu mtukufu na mwema, (uzi huo) huwa na thamani kubwa kiasi kwamba kiasi unaweza kuwa ni rehani ya kiasi kikubwa cha fedha na mkopeshaji huikubali kwa imani kamili na hulipwa deni lake katika muda uliopangwa. Kuheshimu ahadi ni moja ya sifa za Mwenyezi Mungu Mtukufu. Anasema wazi wazi katika Qur’ani tukufu: “Hakika Mwenyezi Mungu havunji ahadi.” (Suratul Ra’d. 13:31). Mtu ambaye ni madhubuti katika kutekeleza ahadi zake (basi) amejaaliwa moja ya Sifa Tukufu na hii peke yake ni moja alama ya kiwango chake cha ukamilifu na wema. Baada ya vita vya Siffin, kundi la watu waitwao Khawarij liliibuka. Watu wenye papara waliokuwa hawajui nguzo za elimu na imani walijiunga na kundi hilo na walijihusisha na uhalifu mbaya kabisa kwa miaka mingi. Serikali za wakati huo pia zilipambana nao katika njia mbambali. Wakati wa Hajjaj bin Yusuf, baadhi ya watu walikamatwa kwa kosa la kujihusisha na kundi hili na waliletwa mbele yake ili waadhibiwe. Hajjaj alichunguza kila kesi ya mmoja wao na kupanga adhabu yake. Zamu ya mtu wa mwisho ilipofika, muadhini aliadhini. Hajjaj alisimama na akamkabidhi huyo mtuhumiwa kwa Anbasa na akamwambia: “Muweke chini ya ulinzi wako wakati wa usiku na mlete kwangu asubuhi ili nimpe adhabu. Anbasa alitii amri na akaondoka katika Nyumba ya Gavana akiambatana na mtu huyo. Njiani mtuhumiwa alimwambia: “Je wema wowote unaweza kutazamiwa kutoka kwako?” Akajibu: “Kama unataka kusema lolote, (sema) nikisikie. Inawezekana nikafuata njia ya ukarimu na wema.” Mtuhumiwa akasema: “Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu, mimi sio 146

11:27 AM

Page 146


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Khawarji. Sijamshambulia mwislamu yeyote wala sijaasi dhidi ya yeyote. Mimi sina hatia yoyote ya makosa ninayoshutumiwa kuyafanya. Ingawa nimekamatwa bila ya kuwa nimefanya kosa lolote. Ninaamini katika Rehema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na nina uhakika kuwa atakuwa mpole na siwezi kuadhibiwa bila kosa lolote. Ombi langu kwako ni kuwa unaweza kunihurumia kiasi cha kutosha kuweza kuniruhusu niende usiku kwa mke wangu na watoto ili nikawaage, nitoe wosia na kulipa haki za watu na kisha nirudi kwako kesho asubuhi na mapema.” Anbasa anasema: “Kusikia ombi hilo kutoka kwa mtuhumiwa aliyoko chini ya ulinzi kuliamsha kicheko changu na sikumpa jibu lolote. Alirudia ombi lake na maneno yake yaliniingia na kunigusa. Nilijisemea kuwa ingekuwa vizuri kumtegemea Mwenyezi Mungu na nikakubali ombi la mtu huyo. Hivyo nilichukua uamuzi na nikamwambia: “Unaweza kwenda lakini lazima uahidi kwamba utarudi kesho asubuhi.” Akajibu: “Ninaahidi kuwa kesho nitarudi mapema asubuhi na namuomba Mwenyezi Mungu ashuhudie ahadi hii.” Kisha aliondoka na kutoweka mbele ya macho yangu. Nilipojirudia (kuwaza) nilipata mashaka na wasiwasi sana kutokana na niliyoyafanya. Nikajisemea: ‘Ni jambo la kipumbavu kiasi gani nililofanya mimi! Kwa nini nimejiweka katika ghadhabu za Hajjaj bila ulazima?’ Nilikwenda nyumbani nikiwa nimechanganyikiwa na nikasimulia kisa hiki kwa wanafamilia yangu. Wao pia walinikemea. Sikulala usiku kucha na nilibakia nikijisikia vibaya kama mtu aliyeumwa na nyoka au mwanamke ambaye mwanae amefariki. Asubuhi ikafika. Yule mtu alitimiza ahadi yake na alirudi katika masaa ya mapema sana. Nilishangaa kurudi kwake na nikamuulizia: ‘Kwa nini umerudi?’ Yeye akajibu; ‘Yeyote aliyebarikiwa kupata elimu juu ya Mwenyezi Mungu na kumjua Yeye pamoja na Nguvu Zake zote na 147

11:27 AM

Page 147


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Ukamilifu Wake hutekeleza ahadi yake pale anapomuomba Mwenyezi Mungu kuishuhidia na haivunji ahadi hiyo.’” Anbasa alimpeleka katika Nyumba ya Gavana mbele ya Hajjaj katika muda uliopangwa na akamsimulia kisa chote cha usiku uliopita. Hajjaj alishangazwa na imani na uaminifu wa mtuhumiwa na akamwambia Anbasa: “Je ungependa nikupatie zawadi ya mtu huyu?” Anbasa akajibu: “Nitashukuru sana ukiwa mwema kiasi cha kufanya hivyo.” Hajjaj alimpatia Anbasa zawadi ya mtuhumiwa. Alimtoa nje ya nyumba ya Gavana na kwa upole sana akamwambia, “Uko huru na unaweza kwenda popote upendako. Yule mtu aliondoka bila kuonyesha shukrani yoyote kwa Anbasa. Anbasa alihuzunishwa kuona ubaridi ule na hali ya kutoshukuru ya mtu (yule). Alijisemea kuwa inawezekana ni kichaa. Lakini alikuja kumuona Anbasa siku inayofuata na akashukuru sana. Akasema: “Mwokozi wangu alikuwa ni Mwenyezi Mungu na wewe ulikuwa ni sababu ya jambo hilo. Kama ningekushukuru (jana) ningekuwa nimekushirikisha na Mwenyezi Mungu katika kujaalia baraka Zake ambalo lingekuwa jambo la haramu. Kwa hiyo niliamua kumshukuru Mwenyezi Mungu kwanza na sasa nimekuja kutoa shukurani zangu kwako.” Kisha akamshukuru Anbasa kwa dhati hasa kwa wema wake, alimuomba radhi kwa usumbufu alioupata na akaondoka zake.’” (Kuudak, Juz. 2, uk. 18). Katika Hadith za kiislam hakuna upungufu uliotajwa kwenye kuheshimu ahadi yake mtu. Ina maana kwamba Waislam wana wajibu wa kuheshimu ahadi walizozitoa kwa watu wengine, hata kwa wale ambao sio waumini. Imam Ja’far as-Sadiq (a.s.) anasema: “Kuna mambo matatu ambayo Mwenyezi Mungu hakumruhusu mtu yoyote kuyatelekeza (i) kuwafanyia wema wazazi wake, wawe ni wazuri au waovu, (ii) kutimiza ahadi yake hata kama huyo mwenzie ni mtu mwadilifu ama ni fisadi na (iii) kurejesha 148

11:27 AM

Page 148


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio amana kwa mmiliki halali hata kama anaweza kuwa ni mwema ama muovu.” (Khisaal, Saduq, Jz.1, uk. 63). Jambo ambalo linapaswa kuelezwa hapa ni kwamba mtu kuenzi ahadi yake ni suala la wajibu endapo kama haifanyi kuwa halali yale mambo ambayo yamefanywa haramu na Mwenyezi Mungu swt. na kinyume chake. Katika masuala kama hayo, wajibu wa mtu kutimiza ahadi yake unaondoka na hakuna yeyote mwenye haki ya kufanya tendo lolote kama hilo. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwafundisha Waislam kwa vitendo somo hili la kutimiza ahadi, na yeye mwenyewe alizitimiza ahadi zake zote, mikataba na makubaliano aliyoyafanya na watu wote ikiwa ni pamoja na makafiri na maadui zake. Hudhaifa alikuwa ni mmoja wa wale watu ambao hawakushiriki katika Vita vya Badr na aliikosa neema hii kubwa. Yeye mwenyewe anasimulia hadithi yake kukosa huku kwa maneno haya: “Mwenzangu Abdul Hashal na mimi tulikuja Madina kujiunga na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na wapiganaji wa kiislam ambao walikuwa mstari wa mbele wa vita. Kwa bahati tukakutana uso kwa uso na kikundi cha washirikina wa kikuraishi. Walituuliza iwapo tunakwenda kujiunga na Muhammad. Kwa kuwa na woga nao na ili kukwepa fitna yao, tulijibu kinyume chake, hapana, na tukaongezea kwamba tunakwenda Madina. Walichukua ahadi kutoka kwetu kwamba kama wakituacha huru hatutakwenda kumsaidia Muhammad na kwamba hatutapigana dhidi yao. Tuliikubali ahadi hiyo na tukawa huru. Kutokea hapo tulikwenda kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), tukamjulisha juu ya tukio hilo na tukaomba ruhusa ya kushiriki katika vita hivyo. Mtukufu Mtume akatujibu: “Hapana, mmeahidiana nao na hampaswi kuipuuza ahadi hiyo. Muishikilie ahadi yenu na mwende zenu. Sisi pia tunaomba msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu.” (Islam wa Sulh-i 149

11:27 AM

Page 149


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Jahanii, uk. 264) Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alifanya makubaliano na jamii nyingi na makabila, kwa mfano ule Mkataba wa Hudaybiyah ambao alikubaliana na makafiri wa Quraishi, au yale makubaliano ya kutochokozana ambao aliyafanya na Mayahudi wa Madina. Na haikuwahi kuonekana kamwe kama angeweza kupuuza au kuvunja makubaliano yoyote. Pale Mtume huyu mashuhuri alipofanya ahadi na watu alichukulia kuzitimiza kwake kuwa ni wajibu juu yake yeye na kama ni sawa na deni la kawaida. Imam Ali ar-Ridhaa (a.s.) anasema: “Sisi ni familia ambayo tunaamini katika kutimiza ahadi tulizoziweka kuwa ni sawa na deni, ambalo kulilipa kwake ni wajibu. Ni kama vile tu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alivyofanya. (Biharul-Anwaar, Jz. 75, uk. 97.) Imam Ali (a.s.) amesema kwamba alimsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema: “Ahadi ambayo muumini wa kweli anaifanya na mtu mwingine ni sawa na kiapo kwa tofauti hii tu kwamba kuna fidia kwa kuvunja kiapo lakini hakuna fidia kwa ajili ya kuvunja ahadi. (Kashful-Ghumma, Jz. 3, uk.92) Imam Ali (a.s.) katika ushauri wake kwa Malik Ashtar alisema: “Jiepushe na kuwakumbusha watu wako juu ya wema uliowafanyia, na kuufanya wema wako kuwa ni mkubwa sana, na kuvunja ahadi ulizoweka kwao, kwa sababu kuwakumbusha wengine juu ya wema uliowatendea kunalivunja lile tendo jema na kuchukulia tendo zuri kuwa ni kubwa kunazima nuru ya ukweli na kuvunja ahadi kunakaribisha ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na ghadhabu za watu vile vile.” (Nahjul-Balaghah) Mahali pengine katika wasia huohuo alitoa mapendekezo yafuatayo kwa Malik Ashtar: “Endapo utafunga mkataba na adui yako, au utampatia 150

11:28 AM

Page 150


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio ulinzi, ni lazima utimize ahadi yako na kuheshimu ile hifadhi uliyompatia, kwa sababu miongoni mwa mambo yaliyofanywa na Mwenyezi Mungu kuwa ni wajibu, hakuna kilicho muhimu na chenye kuheshimiwa sana na watu sawa na kutimiza ahadi, licha ya tofauti zote miongoni mwao katika imani zao na mawazo.” Katika kipindi cha ukhalifa wa Ma’mun, mkazi mmoja wa Damascus, ambaye alishutumiwa kuasi dhidi ya serikali alikamatwa na kupelekwa Baghdad. Khalifa alimwita Abbas, mkuu wa polisi, na akamkabidhi yule mtu aliyeshutumiwa kwake na akasema kwa msisitizo kabisa: “Kuwa na tahadhari sana juu yake isije ikawa akatoroka, kwa sababu yeye ni hatari sana.” Abbas anasema: “Nilimkabidhi kwa maafisa wangu na akapelekwa makao makuu. Wakati wa usiku hata hivyo, nilihisi wasiwasi kwamba wale maafisa wasije wakawa wazembe na yule mtuhumiwa akaja kutoroka. Kwa hiyo niliamuru kwamba aletwe akiwa amefungwa pingu hadi kwenye chumba changu maalum ili niweze kumuweka chini ya ulinzi wangu mwenyewe. Aliletwa kule chumbani kwangu na akakalishwa chini kwenye pembe ya chumba. Pale maafisa hao walipokuwa wameondoka na tukabakia wenyewe tu katika chumba niliamua kutaka kujua mengi zaidi kuhusu yeye, na kujua ni kosa gani alilokuwa ametenda. Mimi nikamuuliza: ‘Wewe unatokea wapi?’ Akajibu: ‘Mimi ni mtu wa Damascus.’ Mimi niliwahi kuwa mtumishi wa serikali huko Damascus kwa muda mrefu, na pia nilikuwa na kumbukumbu isiyosahaulika kuhusu siku zile. Kwa hiyo nikamuuliza: ‘Je, unamfahamu mtu fulani huyu?’ Akanijibu: ‘Ndio ninamfahamu, lakini wewe umemfahamu vipi?’ Mimi nikasema: ‘Kulikuwa na tukio ambalo lilituhusu sisi wote.’ Yeye akasema: ‘Tafadhali naomba nijue tukio hilo lilikuwa lipi na kisha nitakusimulia hicho kisa changu.’ Nikasema: ‘Miaka kadhaa iliyopita mimi nilikuwa nafanya kazi huko Damascus pamoja na Gavana. Watu wa Damascus wakaasi dhidi ya gavana na wakaizingira nyumba ya gavana. Huyo gavana aliruka kutoka 151

11:28 AM

Page 151


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio juu ya paa la kasri hadi mtaani kwa kutumia kamba na akakimbia. Na mimi pia nilitoroka kupitia upande mwingine. Watu wakanifukuza na ilikuwa kidogo nikamatwe katika moja ya mitaa, nilipomuona mtu amekaa nje ya nyumba yake. Nilikimbilia kwake na nikamuomba anifiche ndani ya nyumba yake.’ Alinichukua kuniingiza ndani ya nyumba yake na akaniweka kwenye chumba. Vile vile alimwelekeza mke wake kubakia katika chumba kile kile na kuhakikisha usalama wangu. Watu wakamiminika ndani ya nyumba hiyo na wakafanya upekuzi kwenye nyumba yote hadi walipofikia kwenye kile chumba nilichokuwa nimejificha. Miguu yangu ilitetemeka kutokana na hofu kubwa iliyonizidi na ilikuwa ni vigumu kwangu hata kuweza kukaa chini. Walipofika mbele ya chumba hicho, yule mwanamke akasimama mkabala na mlango na akawapigia makelele akiwaambia: ‘Hamuoni aibu kujaribu kuingia chumbani kwangu?’ Watu wale wakaona haya na aibu waliposikia maneno yake na wakaondoka zao. Wakati ilipokoma kuwepo, yule mtu na mke wake waliniliwaza na kusema: ‘Usiwe na wasiwasi. Baada ya hapa hakuna atakaye kuingilia tena.’ Waliweka chumba kimoja kwa ajili yangu na wakanionyesha upendo mwingi na huruma juu yangu.’ Siku moja nilimwambia mtu huyo: ‘Ningependa nitoke nje ya nyumba ili niende kupata habari kuhusu watumwa wangu.’ Yeye akaniruhusu kutoka nje lakini akataka nimuahidi kwamba ningerudi pale nyumbani baada ya kumaliza kazi yangu.’ Nilitoka nje ya nyumba hiyo na nikajaribu kuwapata watumwa wangu bila mafanikio. Kwa hiyo nilirudi nyumbani kwa yule bwana. Baada ya siku kadhaa niliamua kuondoka kuelekea Baghdad. Wakati nilipoitaja nia yangu kwa bwana yule, yeye alisema: ‘Nisingependa kwamba usafiri peke 152

11:28 AM

Page 152


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio yako. Msafara fulani una mwelekeo wa kuondoka Damascus kwenda Baghdad baada ya siku tatu. Unapaswa kukaa hapa hadi siku hiyo na uondoke kwenda huko Baghdad pamoja na msafara huo. Nilikubali na nikakaa pale kwa siku nyingine tatu. Katika kipindi hiki alinionyesha upendo sana na wakati wa kuondoka kwangu alinipa suti, jozi ya viatu, upanga, mkanda, farasi, nyumbu na mtumwa na vilevile akanipatia dirham 5000. Nikamshukuru na kumwahidi Mwenyezi Mungu kwamba kamwe sitasahau upendo wake na nitakuja kuufidia kwa namna yoyote ile itakayowezekana. Hata hivyo, haijawezekana kwangu kufikia sasa, kuweza kumpatia yeye huduma yoyote ile. Hadi wakati huo, yule mtuhumiwa alikuwa amekaa na kulemewa kwake na pingu zile na huku akinisikiliza. Niliponyamaza kuongea yeye akasema: ‘Hivi utaweza kumtambua mtu huyo kama ukimuona?’ Nilimjibu kwa kukubali, ndiyo. Yeye akasema: ‘Mtu huyo unayemtafuta amekaa mbele yako na ni mfungwa wako.’ Niliukodolea macho uso wake. Yeye pia alitaja ishara zingine na nikaridhika kwamba masikini mfungwa yule alikuwa ni yule mwenyeji wangu mwenye huruma na mwenye kujitolea binafsi. Nilinyanyuka kutoka pale mahali pangu na nikambusu kwa wingi sana. Kisha nikawaita wale maafisa ambao walimfungua zile pingu kutoka mikononi mwake na miguuni na baada ya hapo nikamuomba asimulie kisa chake. Aliniambia kila kitu kwa kina chake. Nilishawishika na kuridhika kwamba alikuwa hana hatia na kwamba aliangukia kuwa mawindo ya njama za maadui zake. Halafu akaniambia: “Kama unataka kutimiza ahadi yako na kuwa mwema kwangu, basi tuma mtu akaniletee mtumwa wangu ambaye yuko mahali 153

11:28 AM

Page 153


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio kadhaa wakadha ili nimpe wasia wangu, kwa sababu wakati nilipotiwa nguvuni sikuruhusiwa kuagana na mke na watoto wangu wala kufanya wasia.” Nilimtuma mtu mara moja ambaye alimleta mtumwa wake. Katika kumuona yule mtumwa, yeye alianza kulia kwanza halafu akaanza kutoa wasia wake. Nilimwita msaidizi wangu na nikamwagiza kwamba waandaliwe farasi wachache na watumwa pamoja na mahitaji mengine kwani safari ya bwana yule ingefanywa kuwa tayari na kuondoka kwake Baghdad wakati wa usiku kuandaliwe. Yule bwana akasema: “Usifanye hivyo, kwa sababu hatia yangu ni kubwa sana machoni mwa Khalifa na amekasirika sana juu yangu na atanihukumu kifo.’ Mimi nikasema: “Huna haja ya kusumbuka kuhusu khalifa. Maandalizi muhimu kwa ajili ya safari yako yamekwisha kufanywa na kwa hiyo, unapaswa kuondoka na kuokoa maisha yako.” Yule bwana akasema: “Hili haliwezekani, kwa sababu kama nikiondoka wewe utakabiliwa na hatari. Sasa kwa vile umechukua uamuzi huo, unapaswa kunipeleka mahali pa usalama ili kwamba kama kutokeza kwangu mbele ya khalifa kutakuwa lazima kesho uwe na uwezo wa kunitoa.” Nilimkubalia na nikamhamishia kwenye sehemu yenye usalama. Nilikuwa sijamaliza bado swala yangu ya al-Fajr katika siku iliyofuatia wakati wale maafisa waliotumwa na khalifa walipokuja na kuniambia kwamba khalifa anataka yule mfungwa apelekwe mbele yake. Mimi binafsi nilikwenda mbele ya Ma’mun. Alipoona kwamba nilikuwa ninakuja peke yangu akasema: “Kama utasema yule mfungwa ametoroka nitakuua wewe mahali pake yeye.” Mimi nilijibu: “Hapana. Yeye hajatoroka na bado yuko kwenye udhibiti wa Khalifa. Mimi, hata hivyo, ninaomba 154

11:28 AM

Page 154


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio ruhusa nisimulie kisa chake.” Ma’mun akatoa ruksa. Nilisimulia kwa kina yale matatizo yangu ya kule Damascus na pia yale yaliyotukia usiku uliopita na nikasema: “Sasa ninataka kutimiza ahadi yangu. Kama bwana wangu akitaka kuniweka kwenye umauti badala yake, mimi tayari nimekwishavaa sanda ndani ya nguo zangu na niko tayari kabisa kukutana na majaaliwa haya, na kama akinisamehe atakuwa amefanya wema mkubwa sana kwa mtumwa wake.” Pale Khalifa aliposikia kisa hicho alisema: “Mwenyezi Mungu asikurehemu wewe! Yeye alikuwa hakujui wewe na akafanya wema juu yako, na wewe unamjua na unataka kumfanyia wema. Kwa nini hukiniambia kuhusu hili mapema ili nikaweza kumlipa kumzawadia kwa wema wake?” Mimi nikasema: “Ewe Amir wa Waumini! Yuko humu mjini kwa wakati huu na ingawa nilimsisitizia kutoroka usiku wa jana lakini alikataa kufanya hivyo, na akasema kwa kiapo kwamba hataweza kuondoka Baghdad mpaka awe ameridhika kuhusu mustakabali wangu.” Khalifa akasema: “Huo bado ni wema mkubwa zaidi ambao ameufanya juu yako. Hebu mlete kwangu.” Haraka sana nikafika pale mahali alipokuwa anakaa. Nikamhakikishia kwamba khalifa amemsamehe na kwamba amenituma nimpeleke mbele yake. Katika kusikia habari njema hizi, yeye aliswali rakaa mbili, na akamshukuru Mwenyezi Mungu na kisha sote tukaenda kwa khalifa. Ma’mun alionyesha upendo na upole mwingi juu yake na bwana yule akala chakula cha mchana pamoja na khalifa. Wakati wa kuondoka kwake, khalifa alimpa ugavana wa Damascus, lakini yeye mwenyewe akatoa udhuru. Kisha Ma’mun akasema: “Kuanzia sasa na kuendelea uwe unabakia mjini Damascus na uwe unaniandikia kila mara kuhusu hali ya Syria.” Alilikubali pendekezo hili. Baada ya hapo, kama ilivyoamriwa na khalifa, idadi kadhaa ya farasi na watumwa na mifuko kadhaa ya fedha vilitolewa kwake. Khalifa pia aliandika barua ya kumsifia kwa gavana wa Syria na 155

11:28 AM

Page 155


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio akampeleka Damascus kwa heshima kubwa.” (Thamaraatul Awraaq, Hamawi). Ili kwamba Waislam wasiweze kupatwa na aibu ya kuvunja ahadi zao imeshauriwa katika mafundisho ya kiislam kwamba kila mtu anapaswa, kabla ya kuingia kwenye mkataba au makubalilano, atathmini uwezo wake kwanza, na endapo akawa hana uwezo wa kutimiza ahadi hiyo, basi aache kujifunga nayo pale mwanzoni kabisa. Imam Ali (a.s.) anasema: “Usiweke ahadi pale mwanzoni kabisa kama hutaweza kuitimiza na usijiandae mwanzoni kabisa kutaka kufanya kazi ambayo iko nje ya uwezo wako.” Anaendelea zaidi kusema: “Usiweke ahadi ambayo kwamba huna hakika iwapo itawezekana kwako kuitekeleza kikamilifu.” (Ghurarul-Hikam) Sasa kwa vile umuhimu na ulazima wa kuheshimu ahadi, kama unavyoangaliwa na viongozi wa Uislam, umekuwa dhahiri kwa kiwango fulani, kuna umuhimu juu ya uhuishaji wa tabia hii bainifu kwamba watoto wawe na ufahamu wa jambo hili wakati wa utoto wao wakati wanapoanza kuelewa maana ya neno ‘ahadi’ na wajifundishe somo la utimizaji wa ahadi kutokana na maneno na vitendo vya wazazi na walezi wao ili iweze kuwa ndio tabia-asili yao ya pili. Kama mazingira ya nyumba na familia, ambayo ndio shule ya kwanza na ya msingi, ni ya hali ya uchamungu na maadili, bila shaka yoyote watoto wanajifunza somo la uchamungu na maadili na kutwaa njia na tabia za maisha zinazofaa. Viongozi wa Uislam wametoa mazingatio makubwa kwenye jambo hili muhimu katika malinganio na hotuba zao na kuona kwamba ni wajibu wa Waislam kutimiza ahadi zao katika mazingira ya kifamilia. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: “Wapende watoto wako na kuwa na huruma kwao na unapotoa ahadi basi heshimu ahadi hiyo, kwa sababu 156

11:28 AM

Page 156


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio wanakuchukulia wewe kama mfadhili wao.” (Wasa’il) Imam Ali (a.s.) anasema: “Sio sawa kwamba mtu aseme uwongo ama kwa mzaha au kwa dhati hasa na vilevile sio sawasawa kwamba mtu atoe ahadi kwa mtoto na halafu asiitimize.” (Wasa’il, Jz. 3, uk. 232) Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: “Pale mtu yeyote kati yenu atakapotoa ahadi kwa mtoto wake mdogo ni lazima aiheshimu ahadi hiyo.” (Mustadrak) Msisitizo wote huu uliowekwa juu ya kuheshimu ahadi zilizotolewa kwa watoto ni kwa sababu kwamba vitendo wa watu wazima vinagandamizwa katika akili za watoto na vina athari mbaya isiyotakikana kwenye mustakabali wao. Endapo watoto wataona kwamba wazazi wao na watu wazima wanavunja ahadi wanazoziweka, wao pia watachukua tabia hiyohiyo pale watakapokua na watathubutu kuwa watu wasio waaminifu. Mwishoni tunaomba kwa Mwenyezi Mungu atuwezeshe kutimiza ahadi zetu na kuwafundisha watoto wetu kwa misingi ya mafundisho ya kiislam ambayo ndiyo chimbuko la ustawi na ukamilifu.

WASTANI Kufanya mambo kwa wastani ndio msingi wa mafundisho yote ya Uislam na kuvuka mipaka kumekatazwa katika amri na kanuni zote. Wastani umekokotezwa sana katika suala la ibada, kutafuta elimu, chakula, mavasi, urafiki, uhasama na katika mambo yote. Qur’ani tukufu inasema: “Hivyo tumekuchagueni kuwa umma wa wastani.” (Surat al-Baqarah; 2:143) Aya hiyo hapo juu ina maana kwamba katika Uislam hakuna kitu kama kupituka mipaka, na kinyume na waumini wa dini nyingine, Waislam 157

11:28 AM

Page 157


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio wanafuata zile sheria na kanuni ambazo zimeariwa na Mtoa-sheria ambaye anayo habari juu ya mahitaji yote ya kawaida ya mwanadamu na alikuwa amezingatia kila kipengele cha maisha ya ki-maada na kiroho ya mwanadamu. Idadi kubwa ya watu, ili wasilazimike kufuata dini yoyote au imani yoyote, wanaonyesha kujali miili yao tu. Juhudi zao zote zimeelekezwa kwenye kuimarisha tamaa zao za kimwili na hawajali kitu chochote mbali na maisha ya kidunia, kuishi kwa uhuru na kuandama starehe. Hawajali kabisa juu ya maadili mema na sifa tukufu za kibinadamu na hawaamini juu ya asili (Mabda’) na Ufufuo (Ma’ad), wanajiingiza kwenye aina zote na machafu ya kiroho. Maisha yao yanakuwa kama maisha ya wanyama. Kuna watu (kama wakristo) ambao wanafuata dini ambayo imewaonya dhidi ya kuzingatia kuangalia mwili na kufanya starehe za dunia hii, na imewalingania katika kuimarisha nafsi na kuachana na dunia na kuendesha maisha ya kitawa. Watu hawa, vilevile, kwa kutoupuuza mwili, wameshindwa kupata ustawi na ukamilifu ambao kwao mwanadamu ameumbwa kwa ajili yake na Mwenyezi Mungu Mtukufu. Hata hivyo, Uislam ni dini ya wastani na ipo katikati ya mipaka hii miwili. Haiwarushu wafuasi wake kuendesha maisha ya kitawa na kuitelekeza dunia, wala kuridhia na kukubali kuendesha kwao maisha ya kinyama. Uislam umependekeza ule wastani wa kufaa na njia ya kiasi kwa maana hii kwamba Mwislamu apaswe kuangalia kwa makini juu ya kuimarisha mwili wake na pia roho yake, kwa sababu mwanadamu sio mwili peke yake kama vile ambavyo hawi na roho peke yake, bali anakuwa ni muungano wa vyote viwili na ili kupata ustawi halisi, mtu lazima alinde na kuimarisha muungano huu.” (Allamah Tabataba’i, Tafsiir al-Mizaan, Jz.1, uk. 319). Uislam unawaagiza Waislam kwamba ili kupata nafasi ya hali ya juu ya 158

11:28 AM

Page 158


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio kibinadamu wanapaswa kupunguza matamanio na silika zao. Lazima waweke welekevu wao ndani ya mipaka inayofaa na wautumie baada ya makadirio ya kihekima. Uislam unapongeza ujasiri ambao upo kati ya hofu na pupa. Uislam unauchukulia ukarimu wenye kufaa kwa Mwislamu, kuwa ni ule ambao unasimama kati ya unyimi na ubadhilifu. Uislam unakokoteza usimamishaji wa uadilifu ambao ni baina ya ukali na kujinyima. Mwenyezi Mungu Mtukufu ameyatukuza maadili bora ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kuyazingatia kwamba ni adhimu. Na maadili yanayopendeza, ambayo watu wote wenye hekima na busara wa ulimwengu huu wanamsifia na kumtukuza yule aliyenayo, yanakuwa pamoja na ‘tabia njema.’ Tabia njema maana yake ni kwamba uwezo wote wa ndani na sifa zake mtu lazima ziwe ndani ya mipaka ya kadiri, wastani na zisiende kinyume cha hayo. (Safinatul-Bihar, Jz. 1, uk. 211) Kuna silika na mielekeo mbalimbali ndani ya kila mtu ambayo kila mmoja unapingana na mwingine. Kama silika hizi sio za wastani na kila moja yao kama isipotumika baada ya makadirio mazuri, basi ustawi wa mtu unakuwa hatarini. Na kuhusu ubongo wa binadamu, ambao ni umbile la ajabu na kushangaza, Imam Ali (a.s.) anasema: “Cha ajabu sana kuliko mwanadamu mwenyewe ni ile sehemu ya mwili wake ambayo imeunganishwa na pingiti lake kwa misuli. Hiyo ni ubongo (akili) wake. Tazama mielekeo mizuri na mibaya inayochomoza kutoka humo. Kwa upande mmoja unashikilia hazina za elimu na hikima na kwa upande mwingine unaonekana kubeba matamanio mabaya sana. Kama mtu anaona hata mwanga mdogo tu wa mafanikio, kisha uroho unamlazimisha kujiaibisha yeye mwenyewe. Kama akiruhusu mwanya kwenye ulafi, basi tamaa zisizo na mipaka zinamharibu, kama amesikitishwa, basi kukata tamaa karibu kumuue. Kama akitaharuki basi anakasirika na kughadhibika. Kama akifurahi basi anaachana na kuchukua 159

11:28 AM

Page 159


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio tahadhari. Hofu ya ghafla humduwaza na kuwa na wasiwasi, na anakuwa hana uwezo wa kufikiri na kupata njia ya kumtoa kwenye hali hiyo. Katika nyakati za amani na ustawi anakuwa mzembe na kutojali hali ya baadae. Endapo atapata mali, basi anageuka na kuwa na majivuno na majigambo. Kama akitumbukia kwenye dhiki, basi kukereka kwake, kukosa subira na kuwa na wasiwasi kunamhuzunisha. Kama akizidiwa na umasikini, halafu akajikuta kwenye hali ya kusikitisha sana, njaa inamfanya kuwa dhaifu, na shibe ya ziada huwa na madhara vilevile. Kwa ufupi kila aina ya mapato na hasara huifanya akili yake kutotulia sawa sawa. (Taz. Peace of Eloquence, hadith ya 107, uk. 686, ISP, 1984). Njia pekee inayoweza kuondoa ukinzano wa mielekeo na kuridhisha kila tamaa ya kawaida ya kibinadamu kwenye nafasi yake hasa kwa makadirio sahihi ni ukadiriaji mzuri wa matamanio na kudhibiti vile vishawishi vya ndani kabisa. Suala la kuepukana na majisifu na mtu kukadiria matamanio ya kibinadamu kwa wastani sio tu wajibu jenzi na hakika wa kiislam. Bali umuhimu wa kudhibiti mielekeo ya kitamaa ya ndani ni kanuni yenye msimamo na isiyovunjikika kutokana na mtazamo wa kimantiki, kisayansi, kielimu, kimaadili, kiafya na kijamii, na kwa kifupi kutokana na mtazamo wa haja ya maisha. Ili kuendesha maisha ya kiafya na utulivu mwanadamu anawajibika kupuuza matamanio yake yasiyo na lazima na kujiepusha na vitendo visivyo vya kibinadamu. “Mwanadamu hawezi kuyaacha huru matakwa yake, bila ya kuyawekea masharti na vigezo, katika maisha yake na yale ya kijamii na wakati huo huo akapata wokovu.” (Adabun-Nafs, Jz. 1, uk. 26). Imam Ali (a.s.) amesema: “Kama tukichukulia kwamba hakuna matumaini ya Pepo na hakuna hofu ya Jahannam, na pia kwamba hakuna malipo ya thawabu au adhabu zitakazotolewa Siku ya Kiyama, hata hivyo bado ni muhimu kwamba tutake maadili mema na sifa za kibinadamu juu yetu, 160

11:28 AM

Page 160


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio kwa sababu kuwa na sifa nzuri na kuzitumia kwa vitendo ni njia yenye kufaa sana ya wokovu na chanzo halisi cha ustawi na furaha katika maisha ya mwanadamu.” (Jawaan az Nazar-i ‘Aql wa Ahsasaat, Jz. 1, uk. 308).

Wastani katika Ibada Kama ilivyo wajibu kwa mtu kuchunga wastani kuhusiana na hisia za ndani na matakwa yake na hatimae kupata kuwa na maadili mema na sifa za kibinadamu, yuko chini ya wajibu kwa namna hiyo hiyo, asiache kufanya wastani katika mambo mengine ya maisha. Uthaman bin Maz’un alikuwa mmojawapo wa wale maswahaba mashuhuri wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na mwislamu mtiifu. Siku moja mke wake alikuja mbele ya Mtukufu Mtume na akasema: “Kwa muda mrefu sasa, mume wangu Uthman ameyatelekeza mambo ya kidunia na amejifunga mwenyewe kwenye ibada ya Mwenyezi Mungu. Anafunga saumu kila siku na anapitisha usiku wa kila leo katika kuswali na kumuabudu Mwenyezi Mungu.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye wakati wote akilingania wastani wa mambo na kufanya kampeni dhidi ya aina zote za vitendo vilivyozidi kiasi alikasirika sana katika kuyasikia haya na akaenda mara moja kwenye ile sehemu ambayo imeteuliwa na Uthman kwa ajili ya ibada zake. Uthman alikuwa anaswali. Alipomwona Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimalizia swala yake haraka haraka na akatoa heshima zake kwa Mtume. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamwambia: “Ewe Uthman! Mwenyezi Mungu hakuamuru maisha ya utawa na kuiacha dunia katika dini yangu. Kwa upande mwingine Yeye amenichagua mimi kwenye kazi ya utume pamoja na dini safi, rahisi na yenye uhuru. Mimi, ambaye ni Mtume wako, vilevile ninafunga na kuswali na kuwaangalia wake zangu na mambo ya maisha. Yeyote anayeipenda dini yangu anapaswa kufuata mwenendo wangu wa maisha na moja ya mwendo wangu ni ndoa na utengenezaji wa 161

11:28 AM

Page 161


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio familia na mtu kumjali mke wake na mambo ya maisha yake mtu.” (Safinatul-Bihar, Jz. 2, uk. 574) Uislam unawachukulia wale ambao wanaokwepa kumwabudu Mwenyezi Mungu kuwa wenye kustahili adhabu na umewaahidi hivyo, na wakati huo huo umewaonya dhidi ya kuitelekeza dunia na kuwa na maisha ya utawa. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Uislam ni dini nzuri na imara. Chukueni hatua madhubuti katika kutekeleza amri zake, na msiifanye ibada ya Mwenyezi Mungu kuwa yenye kuchosha na kuchukiza kwa viumbe Wake (kama matokeo ya ubadhilifu). Kama mtu utafanya hivyo, utakuwa kama mpanda ngamia mwenye pupa ambaye hafiki kwenye kituo cha mwisho wa safari yake, na pia humfanya ngamia wake akose nguvu na kuanguka.” (Biharul-Anwar, Jz. 71, uk. 211) Katika Hadith, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amedokezea juu ya athari mbaya ambayo ziada katika ibada inaisababisha juu ya wengine. Uzidishaji kama huo una madhara kwa yule mtu anayeufanya na vile vile kwa wale wanaoangalia ule utendaji wa ibada hiyo. Una madhara kwa wale wanaoangalia kwa sababu unawazuia kuelekea kwenye dini na kujinyenyekeza wenyewe kwenye yale majukumu ya wajibu yaliyoamriwa nayo. Wanadhani kwamba, kama mtu akitaka kuwa mtumishi wa Mwenyezi Mungu na kutekeleza wajibati za kidini ni lazima ayape mkono mambo ya maisha yake na kujinyima aina zote za shughuli, starehe na maliwazo na hapo tu kwamba anaweza kuwa Mwislamu muwajibikaji. Lakini basi, kama watu wataona kwamba Waislam pia wanaangalia mambo yao ya maisha, na pia wanamwabudu Mwenyezi Mungu na kutekeleza wajibati zao za kidini, bila shaka watapendezewa kuuelekea Uislam na kupata ustawi na furaha ya dunia hii na ya Akhera kadhalika. Imam as-Sadiq (a.s.) anasema: “Usijifanye mwenye kusitasita katika suala la ibada ya Mwenyezi Mungu, yaani, usijikalifishe na uzito wa kanuni ya ibada zilizopendekezwa na hivyo ukajichosha mwenyewe kwa sababu kwa matokeo ya hilo utakuwa mzito mwenye kusita katika suala la ibada.” (al162

11:28 AM

Page 162


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Kafi, Jz. 2, uk. 86) Imam Ali (a.s.), kuhusiana na maagizo yake kwa mwanawe wakati wa kifo chake alisema: “Mwanangu! kuwa mwenye wastani katika mambo ya maisha na pia fanya wastani katika suala la ibada ya Mwenyezi Mungu kwa namna ambayo kwamba utaweza siku zote kuwa na uwezo wa kuiendeleza.” (Amali Tuusi, Jz. 2, uk. 67) Imam Muhammad al-Baqir (a.s.), Imam wa tano, alimwambia mwanawe: “Ewe mwanangu! wakati wote chagua njia inayofaa ambayo ipo katikati ya njia mbili mbaya na zisizopendeza.” Mwanawe akauliza: “Ni ipi hiyo njia inayofaa?” Imam Baqir akajibu akasema: “Tunasoma katika Qur’ani tukufu kwamba ubadhilifu katika matumizi na ubahili zote ni njia mbaya na baina ya mbili hizi ndio kuna ile njia inayofaa ambayo ni ya kadiri na wastani unaofaa. Ni muhimu juu yako kuzingatia wastani.” (Tafsiir ‘Ayaashi, Jz. 2, uk. 319) Viongozi Watukufu wa Uislam wamechukulia kuvuka mipaka ya uwastani kuwa ni matokeo ya ujinga. Imam Ali (a.s.) anasema: “Inaonekana kwamba watu wajinga ama ni wabadhilifu au ni wachovu katika masuala yote na wastani kamwe hauwezi kuonekana kabisa kwao.” (Taz. Peak of Eloquence, ISP, 1984) Haihitaji maelezo kwamba katika suala la ibada, wale watu ambao ni wabadhilifu, ambao, bila kutekeleza kanuni za ibada za wajibu, wanajishughulisha katika ibada zilizopendekezwa kwa kiasi ambacho kwamba maisha yao yanalemaa na wanashindwa kutekeleza wajibati zao mbalimbali nyinginezo. Kuna watu wachache sana kama hao ndani ya jamii ya kisasa na kwa bahati mbaya wengi wa watu hao wanarudi nyuma katika suala la ibada na hawafanyi hata zile ibada za faradhi.

163

11:28 AM

Page 163


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio

Wastani Katika Matumizi Kufanya makadirio muhimu na kufanya wastani katika matumizi ni moja ya wajibu usiokwepeka wa kila Mwislamu. Wastani huu hauna chochote cha kuhusiana na uhaba na wingi wa kipato. Kwa hakika wale watu ambao kipato chao ni kichache huhisi umuhimu wa kufanya wastani kwa wingi zaidi. Hata hivyo, Uislam unapendekeza kwa wafuasi wake kuchunga wastani kwenye matumizi katika hali yoyote ile iwayo. Imam Muhammad Baqir (a.s.) anasema: “Mambo matatu humhakikishia mtu wokovu wake: (i) Kumwogopa Mwenyezi Mungu kwa siri na kwa dhahiri. (ii) Wastani katika matumizi wakati wa utajiri na pia wakati wa ufukara. (iii) Kusema maneno ya kweli wakati wa furaha na wakati wa hasira.� (Safinatul-Bihar, Jz. 2, uk. 431) Inawezekana kwamba matumizi ya kupita kiasi yasiwe ya kutaabisha kwa matajiri na baadhi yao pengine wataona suala la kufanya wastani kuwa ni jambo la makosa. Hata hivyo, jambo hili lazima lizingatiwe akilini kwamba hakuna aliye na uhakika kwamba walio matajiri leo watabakia kuwa matajiri mpaka mwisho wa maisha yao, kwa sababu mabadiliko ya wakati huwashusha wengi wa matajiri kwenye ufukara na kama wakiwa na tabia ya matumizi ya kupindukia, israaf, wakati wanapokuwa matajiri, wanapata matatizo sana wakati wa umasikini na ufukara. Zaidi ya hayo, matajiri pia wanapaswa kuzingatia hali ya baadae ya watoto wao, kwa sababu hakuna uthibitisho kwamba watoto wa matajiri pia wataendelea kuishi katika maisha ya kitajiri vile vile. Imeshuhudiwa mara kwa mara kwamba watoto wa tabaka hili la maisha wanakumbwa na hali ya dhiki. Endapo matajiri watapandikiza tabia ya wastani kwa watoto wao, dhiki inayoweza kupatikana haitawafanya wasijiweze. Matumizi badhilifu huwa yanaandaa uwanja wa dhiki na shida na bahati mbaya kwa watu ambapo wastani na makadirio yanayofaa huwahakikishia 164

11:28 AM

Page 164


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio mustakabali wao mzuri. Imam Ali (a.s.) anasema: “Utajiri wa mtu anayefanya wastani utadumu daima na ile sera ya wastani unaofaa itafanya marekebisho juu ya matatizo na dhiki za maisha yake.” “Mtu anayefanya wastani, wakati wa kuwa nacho na wa ufukara, anajiandaa mwenyewe na mabadiliko ya nyakati.” “Maangamizi na shida havipatikani katika matumizi ya wastani, yaani, yeyote anayechagua njia ya kati na kati baina ya mipaka miwili hiyo na akajiepusha na ubadhilifu usiofaa haingii kwenye mkumbo wa dhiki.” (Ghurarul-Hikam).

Wastani katika Chakula Kula na kunywa vile vile ni moja ya yale mambo ambayo kuhusu hayo watu huvuka mipaka, na kwa kweli, zaidi hasa katika upande wa ubadhilifu. Hakuna shaka kwamba mwanadamu anahitaji chakula ili kuishi na ni muhimu kwamba chakula lazima kizifikie chembehai za mwili ili ziweze kuendeleza uhai wao. Hata hivyo, swali muhimu ni, kwa kiasi gani chakula kinahitajiwa na mwili wa binadamu na iwapo chakula cha ziada ni bora kwake ama kina madhara kwake. Imam ar-Ridhaa (a.s.) anasema: “Lazima utambue kwamba mwili wa binadamu ni kama ardhi yenye rutuba. Kama wastani utatumika katika suala la kuiendeleza, yaani, kama kiasi muhimu cha maji kinamwagwa juu yake, ambacho wala hakitakuwa kingi zaidi kiasi kwamba ardhi ikazama majini na kuibadili kuwa kinamasi au topetope, wala kuwa machache zaidi kiasi kwamba ardhi ibakie kuwa na kiu, ardhi kama hiyo huendelea na kutoa mazao mengi zaidi. Hata hivyo, kama ardhi hiyo itakuwa haitunzwi 165

11:28 AM

Page 165


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio sawasawa inakuwa gumba isiyofaa kitu.” (Risaalatuz-Zahabiya). Mwili wa mwanadamu vile vile ni kama hivi. Wakati malezi yanayofaa yanapotekelezwa katika masuala ya vyakula na vinywaji, na makadirio sahihi yakifanywa, mwili unabakia wenye afya na imara. Wakati wa kipindi cha ukhalifa wa Harun Rashid, alitokea daktari mmoja maarufu wa Kikristo, ambaye aliishi katika mji wa Baghdad, akafanya mazungumzo na mwanazuoni mmoja wa wakati wake aliyeitwa Waqidi na walikuwa na mjadala ufuatao juu ya mada ya madawa. Yeye alimuuliza Waqidi: “Je, kuna chochote kuhusu madawa katika Qur’ani yenu?” Waqidi akamjibu: “Ndiyo. Ipo aya fupi tu ‘Kuleni na kunyweni wala msipite kiasi …..” (Surat al-A’raf, 7:31) ambamo Mwenyezi Mungu amewaagiza Waislam kutumia vyakula na vinywaji lakini wasijiingize katika matumizi ya kupita kiasi.’” Daktari huyo akauliza: “Je Mtume wenu amesema chochote kuhusu madawa?” Waqidi akajibu: “Ndiyo. Mtume wetu Mtukufu (s.a.w.w.) amesema: “Tumbo ndio makao ya maradhi yote na kujizuia mtu na akala kiasi kidogo ndio bora ya madawa yote.” (Biharul-Anwar, Jz. 14). Yule mganga wa kikristo akasema: “Imam na Mtume wa Uislam hawakuacha kitu chochote kwa ajili ya Galen kusema juu ya jambo la madawa na wameeleza kwa maneno machache sana kanuni za msingi kwa ajili ya kinga na tiba ya magonjwa.” (Barnaama-i Zindagi) Mwanachuoni mashuhuri, Victor Dean anasema: “Tunakula sana na kwa matokeo ya ulafi tunapoteza nguvu muhimu ambazo zingefanya kazi ya kuondoa uchafu. Hatimae tunakabiliwa na kuvimba kwa matumbo na ini na udhaifu wa kibofu. Tindikali ya mkojo (uric acid) inasambaa kwenye mwili na kutufanya sisi tuugue baridi yabisi (rheumatism) na kuvimba kwa viungo. Mafuta yanakusanyika kwenye moyo. Mtiririko wa damu unarudi 166

11:28 AM

Page 166


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio nyuma. Njia ya kumeng’enya chakula inadhaifika kutokana na kuzidi kwa mshughuliko na mtu anapatwa na ugonjwa wa kushindwa kumeng’enya chakula tumboni (dyspepsia). Daktari maarufu na mwenye kuamini kwamba kuna Mungu, Dr. Alexis Carell anasema: “Ulafi, licha ya kusababisha mvurugiko mkubwa wa utaratibu katika umbile la mwili wa mtu, unadhoofisha neva, hususan neva za ubongo, na huleta namna ya mchafuko wa kineva na kiakili ambao athari zake hujitokeza katika sura ya kutojisikia vizuri, sononeko, uvivu, kutojali, hali ya mfadhaiko na usingizi, huzuni, kutawaliwa kwa fikira, ndoto za kutisha na hofu zisizo na msingi.” (Tibb wa Bahdaasht, uk. 47) Imam Ali (a.s.) anasema: “Usinyooshe mkono wako kwenye chakula isipokuwa kama una njaa ya kweli kweli na uache kula kabla hujashiba kabisa. Tafuna chakula vizuri kabisa na ukilainishe kinywani mwako na chini ya meno yako, na usafishe matumbo yako (haja kubwa) kabla ya kwenda kulala. Kama ukifuata kanuni hizi nne basi hutahitaji huduma za daktari.” (Khisaal Saduuq) Baadhi ya madaktari wanasema: “Theluthi moja ya kile unachokula ina manufaa kwako, na zilizobakia mbili zinafanya maandalizi kwa ajili ya riziki ya daktari. Magonjwa yote yanatokea kutokana na mchafuko wa damu. Hivyo kuna tiba moja kwa ajili ya yote hayo, yaani, kutafuta chanzo cha mchafuko huu na kuuondoa kwa njia ya kujiwekea mipaka mwenyewe na kula chakula kinachofaa kwa kiasi kidogo.” (Tibb wa Bahdaasht, uk. 142) “Kila kiungo ambacho hakipumziki huchoka na kuwa dhaifu polepole na uchofu huu hupunguza umri wa kiungo hicho, yaani, unabatilisha utendeji wake wa kawaida na mabadiliko yake ya kiogani hukisababishia magonjwa mengi. Tumbo vile vile haliepukani na kanuni hii. Wale wanaokula kitu hiki au kile katika masaa ishirini na nne ni wasiotambua juu ya ukweli kwamba tumbo ambalo limejaa wakati wote linakuwa 167

11:28 AM

Page 167


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio linafanya kazi, na kazi ya ziada ya kila siku hulidhoofisha. Juhudi zinapaswa kufanyika, kwa hiyo, kwanza kabisa tumbo halijazwi sana wakati wowote, na mtu aache kula kabla hajamega tonge la kumshibisha zaidi, na pili tumbo lazima liruhusiwe kupumzika baada ya kula ili liweze kuwa tayari kwa mlo unaofuatia. Hisia za mtu juu ya njaa ndio kiongozi mzuri kwa ajili ya kula chakula, na juhudi lazima ifanyike kwanmba milo haichukuliwi isipokuwa pale mtu anapohisi kuwa na njaa. (Sad Dars-i Salaamati). Imam Ali (a.s.) anasema: “Inatokea kwa nadra kwamba mtu anaweza kula na kushiba na asiweze kuugua. Kuwa wakati wote na shibe kunazalisha magonjwa mengi mbalimbali.” (Ghurarul-Hikam) Ili kutambua kwamba tumbo la mwanadamu lina mpaka maalum na uwezo na kwamba haliwezi kupokea vyakula kupita uwezo huo na hiyo ndio hali halisi ya afya na jambo la hekima sana. “Ni kawaida kwamba wale wasioifuata kanuni hii na wakawa wanakula kupita kiasi na wala hawachungi utaratibu wowote kuhusiana na jambo hili wanaangukia kwenye kuathirika na kuvimba tumbo na kuwaka moto kwa tumbo. Wakati vinywaji vinaponywewa kwa wingi zaidi ya kiasi kinachohitajika havisababishi kushindwa kumeng’enya chakula tu bali pia vinaongezea kuwakwa na tumbo na kuna uwezekano wa kusababisha magonjwa ya utumbo. Na ili kurekebisha ulafi huu na uzidishaji wa kipimo, mtu anapaswa kujizuia katika suala la kula na kunywa na kujiweka kwenye mpango wa chakula maalum (special diet) kwa kipindi cha muda mrefu hasa.” (Dastuuraat-i Pizishki Baraa-i Hamaa, uk. 396) Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: “Msiiue mioyo yenu kwa kutokuwa na simile katika suala la kula na kunywa, kwa sababu moyo wa mwanadamu ni kama shamba lililopandwa ambalo huoza na kufa endapo litanyweshwa kupita kiasi.”

168

11:28 AM

Page 168


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Luqmaan Hikam alimwambia mwanawe: “Ewe mwanangu! wakati tumbo la mwanadamu linapokuwa limejaa, uwezo wake wa kufikiri unalala na ulimi wake wa hikma unakuwa bubu na viungo vyake hushindwa kumuabudu Mwenyezi Mungu.” (Jami’us-Sa’adaat, Jz. 2, uk. 3-4) Kuna Hadith nyingi na simulizi ambamo ziada ya kupindukia katika suala la kula na kunywa imeshutumiwa, baadhi yake ambazo zimetajwa hapo juu kama mfano. Nukta ambayo inastahili kuzingatiwa na kwamba zile Hadith zinazoshutumu ulafi au kusifia njaa hazina maana kwamba ziada katika kula kiasi kidogo kunafaa kusifiwa, kwa sababu, kama ilivyoelezwa mapema, Uislam haukubali ziada yoyote au kurudi nyuma na zile Hadith ambamo kushiba kumeshutumiwa na njaa kusifiwa zinaendana na sera maalum ambayo inajulikana kwa wale wenye utambuzi wa Hadith za Ahlul-Bayt. Uislam unashutumu kila kitu ambacho tabia ya mwanadamu inakipenda kupita kiasi. Katika hali kama hizo, wale ambao wanayaangalia mambo juujuu wanadhani kwamba Uislam unapenda ule mpaka mwingine (kinyume na ziada) lakini watu wenye elimu wanatambua kwamba kinachotakiwa na Uislam ni ule ‘wastani unaofaa.’ Kwa mfano, wakati tabia ya mwanadamu inapopendelea ulafi endelevu na shibe, Hadith zinapaswa kupendekeza njaa endelevu ili kwamba kile kinachotakiwa na tabia kikabiliane uso kwa uso na kile kinachokatazwa na sheria ya kidini na itaweza kubaki ndani ya mipaka inayofaa. Au pale tabia ya inapotamani sana utajiri na cheo, Hadith zinapaswa kushutumu kwa wingi sana kupenda dunia na tamaa ya mali ili kwamba mvuto kwa upande mmoja na katazo kwa upande mwingine viweze kwa pamoja kusababisha hali ya wastani ndani ya watu.

Wastani Katika Urafiki na Uadui: Ingawa Uislam unaunga mkono fungamano la urafiki ambalo lipo baina ya Waislam na kuuona urafiki huu kuwa ni rasilimali yenye thamani sana, 169

11:28 AM

Page 169


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio unakataza ziada hata katika kuhusiana na hili. Imam Ali (a.s.) anasema katika moja ya hotuba zake: “Usuhuba wako na rafiki yako sharti uwe ndani ya mipaka ya wastani, kwa sababu inawezekana kwamba rafiki yako huyo siku moja akaja kuwa adui yako.” (Taz. Peace of Eloquence, ISP. 1984) Kupitisha kiwango katika urafiki kunakuwa ni chanzo cha mtu kumwambia rafiki yake kuhusu siri zake za maisha. Kwa tukio kama hilo, endapo yule rafiki atabadili mwelekeo wake na akawa ni adui anaweza akazitumia siri zile zile dhidi yetu ambazo ni sisi wenyewe tuliomwambia. Iwapo, hata hivyo, urafiki umeanzishwa kwa misingi ya wastani, mtu humwambia rafiki yake zile siri ambazo hazina hatari yoyote kwake hata kama zitawekwa wazi. Zaidi ya hayo, urafiki wa namna hiyo unakuwa wa kudumu, ambapo uzoefu umeonyesha kwamba baadhi ya marafiki wanaovuka mipaka ya urafiki, baada ya urafiki wa pamoja kwa muda fulani, wametwaa njia ya uadui uliozidi kiasi na wamesimama kupigana wenyewe kwa wenyewe, ingawa uadui mkali na wa kupita kiasi pia ni wenye kudharauliwa mbele ya macho ya Uislam. Baada ya kupendekeza wastani katika suala la urafiki, Imam Ali (a.s.) anaendelea kusema: “Ni lazima pia uwe na wastani katika uhasama wako na adui yako na usije ukapita kiasi, kwa sababu inawezekana kwamba adui yako akabadilisha mwelekeo wake na siku moja akawa rafiki yako.” (Tuhfatul-Uquul) Endapo mtu hakuvuka mipaka katika suala la uhasama na adui yake, huwa haoni aibu iwapo siku moja wataamua kusimamisha uhusiano wao katika misingi ya urafiki. Kinyume chake, ikiwa amepitiliza mipaka katika suala la uhasama na akatumia nguvu zake zote dhidi ya adui yake, ataona aibu watakapoamua kuwa marafiki.

170

11:28 AM

Page 170


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Wastani Unapendekezwa kwa Mara Nyingine: Kama tulivyoeleza mwanzoni mwa mlango huu kwamba Uislam unapendekeza wastani katika mambo yote na kazi zote, na inapendeza kuona kwamba haukusahau hata yale mambo madogo kabisa ili kwamba Waislam waweze kuzingatia wastani katika kila jambo la kila siku na vile vile katika yale yaliyo muhimu na ya lazima kabisa. Luqmaan Hikam anamwambia mwanawe: “Na ushike mwendo wa kati na kati (usitembee polepole na kwa ulegevu, wala usiende mbio na kwa pupa), na uteremshe sauti yako (bali iwe wastani, iweze kuwafikia watu kwa kipimo)…..” (Luqmaan; 31:20) Kilichosimuliwa hapo juu kipo pamoja na mifano mifupi ya mafundisho ya Uislam katika suala la wastani na tukizichunguza sheria nyingine tunaona kwamba kanuni hii imezingatiwa katika masuala yote na njia ya kuvuka mipaka haikutwaliwa katika yoyote katika hayo. Inatarajiwa kwamba kuzingatia jambo hili muhimu kutatupasha habari juu ya wajibu wetu wa kihekima kuhusiana na kutii bila masharti maagizo ya Uislam na kufanya katika masuala yote ya maisha kwa mujibu wa muongozo unaotolewa na dini hii ya Mwenyezi Mungu na kutoa mazingatio maalum kwenye wastani katika kazi zote za maisha ili kwamba, kwa rehema zake Mwenyezi Mungu, tunaweza kukapata ustawi katika dunia hii na vile vile kesho Akhera; Amiin.

WAJIBAT ZA MATAJIRI Matajiri ni wadhamini wa watunza hazina wa Mwenyezi Mungu na rasilimali zao ni dhamana na hazina Zake Allah swt. Kama vile tu ambavyo Mwenyezi Mungu Muumba amekuwa mpole kwa 171

11:28 AM

Page 171


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio matajiri na amewapa heshima miongoni mwa viumbe Wake katika sura ya utajiri, amewalazimisha pia kwenye wajibat maalum na amewataka watekeleza baadhi ya majukumu. Kama vile tu matajiri wanavyoendesha maisha ya starehe kwa njia ya mali waliyopewa na Mwenyezi Mungu, wanaweza, na ni lazima pia wahakikishe ustawi katika Akhera kwa kutumia mali zao hizo. Kinyume na baadhi ya watu wajinga wanavyodhania, sio tu kwamba Uislam haupingi utajiri, bali unauona utajiri kama ndio njia ya udumu wa jamii (taz. Surat an-Nisaa; 4:5) ambayo bila huo haiwezi kuwa na nguvu. Kwa upande mwingine kanuni za kiuchumi za kiislam ambazo zinaonekana katika maneno ya Qur’ani tukufu na Hadith za viongozi watukufu wa Uislam, vinadokezea thamani na manufaa ambayo utajiri unafaidi katika macho ya Uislam. Na kama ingekuwa vinginevyo, yaani, kama mali na utajiri vingekuwa vinadharaulika machoni kwa Mwenyezi Mungu, asingezungumzia hata kidogo kabisa kuhusu utajiri na pia asingeweka mipaka na kanuni za kisheria kwa ajili yake. Endapo utajiri umeshutumiwa ndani ya baadhi ya aya za Qur’ani tukufu na baadhi ya Hadith, lengo lilikuwa ni kuwaonya watu dhidi ya hatari ambayo kwayo ustawi wao unaweza ukatawaliwa kwa sababu ya mali. Inawezekana, bila shaka kwamba mali inaweza ikamfanya mtu kuugua kutokana na maradhi ya majivuno, majigambo, ubinafsi, ubahili, choyo, unyonyaji, dhulma na kadhalika, na matokeo yake ustawi wao na pia ule wa jamii unaweza kuhatarika. Katika Hadith za viongozi wa Uislam suala la mali limechambuliwa kwa vipimo vyote, athari na maainisho na katika kila suala mapendekezo muhimu yamefanywa. Uislam unasema: Mali ni njia tu na sio mwisho na watu wanapaswa kupata ustawi wa dunia hii na ile ya kesho Akhera kwa njia ya mali. 172

11:28 AM

Page 172


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Katika jamii mali ni kama damu katika mwili wa mwanadamu. Kama vile damu ni lazima izunguke kwenye mwili wote na ipaswe kutiririka kwenye mishipa yote na mirija yote ya damu ili kila kiungo, sehemu na chembe hai za mwili ziweze kuitumia kulingana na mahitaji yake, mali pia inapaswa kuzunguka katika matabaka yote ya jamii ili watu wote waweze kuitumia na maisha yao yaweze kuwa salama. Kama damu ikiwa imechafuka au ikigoma katika sehemu moja ya mwili au ikisimama kwa kitambo kidogo kutembea kiungo kisichopata damu kinatishiwa na maradhi na kifo na kwa nadra sana hufikia katika kifo cha kawaida na kuangamia kwa mwili. Na kuhusu mali vile vile kama imepatikana kutokana na vyanzo haramu au ikilimbikizwa kwa watu wachache na watu wa hali ya chini wakawa hawanayo mali, inaleta hatari mbaya kwa jamii na kuiongozea kwenye kuoza na kuangamia. Kutokana na mtazamo wa kiuchumi, jamii yenye ustawi sana ni ile ambayo inatawaliwa na usawa wa kiuchumi na watu wote wanafaidi manufaa ya mali ya nchi kulingana na mafungu yao yanayohusika.

Matajiri ni Nguzo za Jamii Matajiri wanapaswa kutumia rasilimali zao kwa ajili ya ustawi na uboreshaji wa tabaka la wasionacho katika jamii na wawafanya mafukara kunufaika kutokana na mali zao. Imam Ali (a.s.) anawachukulia matajiri kuwa ni nguzo ya kasri la ustawi wa jamii alimradi wasipuuze kutekeleza wajibu ambao Mwenyezi Mungu ameagiza juu yao na hawadhuriki na maradhi ya uchoyo na ubahili. Alimwambia Jabir bin Abdullah Ansari: “Ewe Jabir! imani ya jamii inakuwepo kutokana na kuwepo kwa aina nne za watu:

173

11:28 AM

Page 173


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio (i) Mwanachuoni ambaye anaitumia elimu yake kwa vitendo na anaangaza njia kwa ajili ya watu kwa nuru ya elimu yake. (ii) Mtu mjinga ambaye anatambua ujinga wake na akawa hasiti kutafuta kupata elimu. (iii) Mtu mwenye huruma ambaye sio bahili katika kutumia mali yake kwa ajili ya ustawi wa jamii, utajiri ambao Mwenyezi Mungu Mtukufu amemjaalia nao. (iv) Masikini ambaye anastahimili dhiki za ufukara na hapotezi subira wala hauzi Akhera yake kwa ajili ya dunia hii. “Kama katika jamii wanachuoni wanaipoteza elimu yao na hawaitumii ipasavyo kwa manufaa, wale watu wajinga watageukia mbali utafutaji wa elimu na endapo matajiri hawatatumia utajiri wao kwa ajili ya ustawi wa jamii, masikini watapoteza subira, na kupuuza heshima zao binafsi na kuuza Akhera kwa dunia hii. “Ewe Jabir! Watu wanakuwa wenye kutegemea zaidi juu ya mtu ambaye amejaaliwa fungu kubwa la neema ya Mwenyezi Mungu. Na yule mtu tajiri anayetekeleza wajibu wake na akatenda kulingana na amri za Mwenyezi Mungu anahakikishia kudumu kwa utajiri wake na yule anayetumia utajiri wake vibaya na kwa ubadhilifu na akadhihirisha ubahili katika kutumia kwa ajili ya Allah na ustawi wa watu, huyo anauweka utajiri na ustawi wake hatarini.” (Nahjul-Balaghah, Fayz, uk. 1251) Mtu mmoja alikuja mbele ya Imam as-Sadiq (a.s.) na akaanza kuzungumza vibaya juu ya matajiri na akawaelekezea mashambulizi na shutuma. Imam as-Sadiq (a.s.) akamwambia: “Hebu nyamaza. Kama mtu tajiri akichunga uhusiano wake na akawasaidia ndugu zake kwa mali yake na akawafanyia wema ndugu zake katika imani, Mwenyezi Mungu humzawadia maradufu, kwa sababu Yeye anasema ndani ya Qur’ani tukufu: “Mali zenu wa wato174

11:28 AM

Page 174


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio to wenu sio njia ya kufikia kwa Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa yule mwenye imani na anayefanya matendo mema, watu kama hao watapata malipo maradufu na watasalimika na kila madhara katika makazi ya juu kabisa ya Peponi.” (Safinatul-Bihar, Jz. 2, uk. 327)

Onyo kwa Matajiri: Matajiri wanapaswa kuendeleza ustawi wa wanyonge kwa uwezo wa mali zao katika namna sahihi na iliyokokotolewa vyema na wachukue hatua za msingi kuwakidhia haja zao na kutatua matatizo ya maisha yao. Imam Ali (a.s.) anasema: “Mwenyezi Mungu Mtukufu huwapendelea baadhi ya viumbe Wake kwa neema ya mali na utajiri ili wengine waweze kunufaika kutokana na wao. Hata hivyo, anaweka utajiri huo mikononi mwao mpaka pale watakapoutumia kwa ajili ya ustawi wa watu. Endapo, kwa hiyo, wakati utafika ambapo watashindwa kutekeleza wajibu wao, Mwenyezi Mungu huuondoa utajiri huo kutoka kwao na kuuweka mikononi mwa watu wengine.” (Nahjul-Balaghah, Fayz, uk. 1275) Inawezekana kwamba baadhi ya watu matajiri walichukulie onyo hili la Imam Ali kizembe na waweze kudhania kwa kiburi kwamba utajiri wao hauwezi kuporomoka na ni wakudumu. Hata hivyo, historia ya wahenga inaonyesha kwamba hili ni jambo lisilopendeza kabisa na matajiri waliotumia utajiri waliopewa na Mungu kwa malengo maovu na ya dhambi au waliokimbilia kwenye ubadhilifu usiotakikana na ufujaji na wakawa hawakulipa haki ya Allah, na viumbe wake wakatumbukia kwenye ufukara, siku moja Mwenyezi Mungu alichukua mali hizo kutoka kwao na kuziweka mikononi mwa watu wengine. Qur’ani tukufu inasimulia kisa cha Karaun kama mfano kwa matajiri na inawaonya dhidi ya maangamizi yanayofanana kama hayo yake.

175

11:28 AM

Page 175


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Kaarun alikuwa wa kabila la Nabii Musa na alikuwa mmoja wa jamaa zake wa karibu. Mwanzoni alikuwa ni mtu mcha-Mungu. (Taz. Surat al-Qasas; 28:76). Hata hivyo, wakati kipindi cha kukaa na kutangatanga kwa Bani Isra’il huko Tiyah* kiliporefushwa, Kaarun aliwaacha watu wake na akajiingiza kwenye alkemia na kutengeneza dhahabu. Kwa njia ya kitendo hiki alilimbikiza mali nyingi na hazina ya dhahabu. Kikundi cha watu wachache wenye nguvu kilikuwa kikibeba funguo za hazina ya Kaarun. Mali na hazina vilimfanya Kaarun kuwa muasi na mwenye majivuno na vikamsukuma kwenye ombwe la maafa ya dhiki. Aliwaangalia waumini kwa dharau na kujiona yeye mwenyewe kuwa ni bora sana kwao kwa sababu ya mali yake. Pale watu wenye uoni mfupi walipoona ni maisha ya starehe kiasi gani Kaarun aliyokuwa akiyaendesha walimuonea gere na kujiambia wenyewe: “Lau kama na sisi pia kungekuwa na mali na fursa kama Kaarun, kwani yeye anafurahia maisha yake kikamilifu.” Watu wenye busara katika kabila lao wakawaambia: “Ole wenu! Msimuonee wivu Kaarun kwa maisha yake ya nje yanayovutia. Bila shaka malipo ya thawabu ni makubwa na yenye thamani bora zaidi kuliko haya.” Wakati baadhi ya watu wenye elimu wa Bani Isra’il walipouona ubadhilifu wa Kaarun walimuonya na kumwambia: “Ewe Kaarun! Usifurahi kwa sababu ya vitu hivi vya dunia vyenye kusisimua, kwa sababu Mwenyezi Mungu hawapendi watu wa namna hiyo. Kwa mali nyingi na neema zisizo na idadi alizokujaalia Mwenyezi Mungu, unapaswa kufanya maandalizi kwa ajili ya kesho Akhera na kuchukua hatua kwa ajili ya Allah. Nufaika na dunia na uwe na huruma kwa waja wake kwa namna ile ile ambayo kwamba Yeye amekuhurumia wewe. Usipite njia ya uovu na usifanye ufisadi kwa sababu Mwenyezi Mungu hawapendi wafisadi na wabadhilifu.” Kaarun akajibu: “Mimi nimelimbikiza mali hii kwa njia ya maarifa yangu ninayoyajua,” kana kwamba alikuwa hajui kwamba Allah swt. alikuwa ameteketeza umati mwingi kwa sababu ya dhambi zao, ambao walikuwa na nguvu zaidi na utajiri kuliko yeye na pia ni jambo rahisi sana 176

11:28 AM

Page 176


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio kwa Mwenyezi Mungu kumwangamiza yeye” (Qasasul-Qur’an, Jz. 1, uk. 148). Ukaidi na uasi wa Kaarun uliendelea na alikwenda kwa njia zake mwenyewe mpaka siku Mwenyezi Mungu alipoamua kumuangamiza na kama ilivyoelezwa wazi katika Qur’ani, yeye pamoja na mali yake walizikwa ardhini kama ilivyoamriwa na Mwenyezi Mungu. Qur’ani tukufu inasema wazi hivi:

“Wala wasidhani wale wanaofanya ubakhili katika fadhila zake kuwa ni bora kwao, bali ni vibaya kwao, watafungwa kongwa za yale waliyofanyia ubakhili Siku ya Kiyama. Na urithi wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa yale mnayoyafanya.” (Aali-Imraani; 3:180) Vile vile inasema tena:

“Hamtapata wema mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda, na chochote mnachokitoa basi hakika Mwenyezi Mungu anakijua.” (Aali Imraan; 3:92)

177

11:28 AM

Page 177


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Ndugu Wawili Katika Ncha Mbili Tofauti ‘Alaa bin Ziyaad Haarith alikuwa mmoja wa watu mashuhuri wa Iraqi na mtu tajiri. Alikuwa ni kamanda katika ngome moja katika jeshi la Imam Ali (a.s.). Pale afisa huyu jasiri alipolazwa kitandani kutokana na kuwa amejeruhiwa katika vita, Imam Ali (a.s.) alitoka siku moja, akiandamana na baadhi ya watu maarufu wa mji wa Kuufa, kwenda kumuona na kumjulia hali ya afya yake. Wakati alipoingia ndani ya nyumba yake aliiona kuwa ni kasri ya kifahari ambayo ilichukua eneo kubwa na ilikuwa pamoja na vyumba vizuri sana. Katika siku ile, Imam Ali, kiongozi mashuhuri wa Uislam, alimhutubia afisa wake huyu mgonjwa kwa maneno haya yafuatayo: “Utafanya nini na jumba lenye nafasi kubwa kama hili katika dunia hii? Kile unachohitaji hasa ni makazi yenye nafasi kubwa huko peponi ambako utakwenda kuishi milele. Kama kweli kabisa unapenda kumiliki kama hii huko, na kubwa kama hii, basi ifanye nyumba hii kuwa kituo chako cha ukarimu, wafanyie jamaa zako wema, kimbilia kuwasaidia; kuwa makini hususa katika kutekeleza wajibu wako na kutimiza majukumu yako, hapo ndipo utaweza kufikia lengo lako.” Baada ya kuyasikia haya, ‘Alaa alimuomba Imam amshauri na ndugu yake pia, ambaye jina lake lilikuwa Aasim bin Ziyad na ambaye kuhusu yeye Alaa alikuwa atoe malalamiko dhidi yake. Imam Ali aliuliza kama yeye alikuwa na matatizo gani na alikuwa na tabia ya namna gani. Yeye akasema: “Bwana! kwa kuvaa joho la sufi lililochakaa, ameukana ulimwengu huu na anaishi maisha ya mtawa.” Imam Ali (a.s.) akajibu: “Hebu mlete kwangu.” Wakati alipofika, Imam Ali (a.s.) alimwambia, “Ewe adui wa nafsi yako mwenyewe! Shetani amekupoteza wewe. Je, hujisikii huruma kwa ajili ya mke wako na watoto na watu wengine wa familia yako? Kwa nini huwaangalii? Kwa nini unadhani kwamba Mwenyezi Mungu atakuchukia kama utakuwa unakula, kwa kula na kutumia vile vitu vyote ambavyo Uislam umevihalalisha na ambavyo umevichuma kwa njia ya 178

11:28 AM

Page 178


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio uaminifu na uchamungu? Kwa nini uvikane vyote hivi? Unaishi chini kabisa ya kiwango chako; utakuja kuulizwa kuhusu kujihini huku.” Kwa maelezo haya ya Imam Ali (a.s.), yeye akajibu hivi: “Ewe AmirulMu’minin! Mimi ninafuata mfano wako. Hebu angalia mavazi yako, jinsi gani yalivyo duni yaliyochakaa na yasiyo na thamani kiasi kwamba hata yule mtu masikini kati yetu asingependa kuyavaa. Angalia chakula chako, ni mkate mkavu na uliochacha na usio na chumvi japo kidogo.” Imam Ali (a.s.) akasema: “Loh, rafiki yangu! Umekosea sana, wewe sio kama mimi. Mwenyezi Mungu amefanya kuwa ni wajibu juu ya Maimam wa kweli na waadilifu kujiweka wao wenyewe kwenye kiwango cha watu masikini kabisa na dhalili miongoni mwa watu, ili kwamba wale watu masikini na dhalili wasijisikie aibu na unyonge kwa sababu ya hali zao hizo, wasije wakafa moyo, wasije wakaruhusu kukata tamaa na huzuni na waweze kudumisha heshima zao binafsi.” (Taz. Peak of Eloquence, hotuba ya 214, ISP 1984)

Haki ya Mali na Utajiri Imam as-Sajjaad (a.s.) anasema hivi kuhusiana na haki alizonazo Mwislamu: “Haki ambayo iliyonayo mali juu yako ni kwamba usije ukaichuma kwa njia za haramu na uitumie kwa namna ya haki na halali tu. Utii amri za Mwenyezi Mungu katika suala la mali yako. Usijizuie kuitumia katika njia ya sawasawa, kwa sababu kama utafanya hivyo, utakabiliwa na majuto na adhabu ya Mwenyezi Mungu.” (Tabarsi, MakaarimulAkhlaq, mlango wa 12) Wakati akilinganisha utajiri na ufukara na kuashiria ni kipi bora kati ya hivyo kwa ajili ya ustawi wa mwanadamu, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: “Ufukara ni bora kuliko utajiri, isipokuwa kwa suala la mtu tajiri ambaye anawalipia madeni wale waliodhikika na wale wenye madeni kutoka mfukoni kwake mwenyewe na kuwaondolea mzigo wa madeni hayo na mkazo wa maisha au anayewasaidia Waislam masikini na wenye 179

11:28 AM

Page 179


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio shida kwa mali yake. Ufukara ni bora kuliko utajiri, kwa sababu Mwislamu masikini hadaiwi majukumu yoyote kwa wasio nacho na wenye haja, ambapo Mwislamu tajiri ana wajibu wa kutumia kutoka kwenye mali yake kwa manufaa ya jamii na kuitumia kwa ustawi na furaha ya ndugu zake katika imani.� (Biharul-Anwar, Jz. 72, uk.56). Imam Ali (a.s.) anasema: “Mwenyezi Mungu amefanya kuwa ni wajibu na kuainisha riziki ya masikini katika mali ya matajiri, na popote pale ambapo masikini ana njaa ni kutokana na ukweli kwamba mtu tajiri hakumpa haki yake. Hata hivyo, Mwenyezi Mungu atakuja kuwaita matajiri kujieleza katika suala hili.� (Nahjul-Balaghah, Fayz, uk. 1232). Thamani ya maneno ya Imam Ali (a.s.) inaweza kukadiriwa vizuri sana katika dunia ya kisasa ambapo mamilioni wanakabiliwa na njaa na umasikini na mali imerundikana na kukusanyika mikononi mwa kikundi kidogo cha watu. Kutokana na maoni ya wataalam na takwimu zilizopo, 85% ya utajiri wa dunia iko mikononi mwa 15% ya idadi yake ya watu na wanasosiolojia wanatabiri kwamba kama mabadiliko ya kimapinduzi katika hali za sasa hayatatokea na utajiri ukaendelea kukusanyika kwa wingi, uwiano wa hapo juu utabadilika baada ya miaka ishirini kufikia kiwango cha 90% kwa 10% kwa mtawalia. Jedwali ifuatayo inaonyesha jinsi mali ilivyolundikana katika sehemu fulani na kinyume na hivyo jinsi mamilioni na wanadamu masikini katika uso wa dunia walivyo kwenye kizingiti cha kifo na maangamizi: Idadi ya watu (%)

Mapato ya Dunia (%)

Nchi zilizoendelea Jumuiya ya Magharibi Ulaya ya kikomunisti Dunia ya Tatu

30.2 19.7 10.5 69.8 180

75.5 58.7 16.8 44.5

11:28 AM

Page 180


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Jedwali hilo hapo juu linaonyesha mgawanyo wa utajiri wa dunia katika miaka ya katikati ya 1960. Hakuna shaka kuhusu ukweli kwamba alimradi watu matajiri wa dunia hawatambui majukumu yao ya kibinadamu na hawajioni wenyewe kuwa wana wajibu mbele ya Mwenyezi Mungu na hawachukui hatua za msingi juu ya ugawaji wa haki wa mali, hali zitabakia kama zilivyo – bali zitazidi kuwa za kutisha zaidi.

Kutumia Katika Njia Ya Mwenyezi Mungu Matajiri wasiweke fedha zao zikiwa zimetulia bila kufanya kazi na wasijitengenezee hazina za pesa kwa njia ya amana za mabenki au kwa njia nyinginezo zile. Qur’ani tukufu inasema: “….. Na wale wakusanyao dhahabu na fedha wala wawazitoi katika njia ya Mwenyezi Mungu, basi wape habari za adhabu iumizayo.” (at-Tawba; 9:34) Imam Sadiq (a.s.) anasema: “Allah anamchukulia tajiri dhalimu na mzinifu mtu mzima na omba omba mwenye makuu kuwa ni maadui zake.” Kisha Imam akawauliza wale waliohudhuria pale: “Je, mnamjua omba omba mwenye makuu ni yupi.” Wao wakajibu: “Ni mtu fukara.” Imam akasema: “Hapana. Omba omba mwenye makuu ni tajiri ambaye hachukui hatua za kupata radhi za Mwenyezi Mungu na kuwa karibu Naye kwa kutumia mali yake katika njia Yake Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema katika Qur’ani tukufu: “Na wale wenye mali miongoni mwenu wasipuuze kuwapa jamaa zao na kwa wale wenye haja na kwa Muhajirina katika njia ya Allah. Waumini lazima wawe wakarimu na wasamehe na kuonyesha wema. Je, hampendi Mwenyezi Mungu awasamehe ninyi? Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa msamaha Mwingi wa neema.” (Khasaa’ilus-Saduq, Jz. 1, uk. 43) Ndani ya Nahjul-Balaghah Imam Ali (a.s.) ametaja baadhi ya majukumu ya matajiri. Yeye anasema: “Kama Mwenyezi Mungu anatoa mali na ustawi kwa mtu, huyo lazima aonyeshe huruma kwa ndugu na jamaa zake 181

11:28 AM

Page 181


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio wanaostahili, atoe msaada kwa masikini, na atoke kuwasaidia wale walipatwa na majanga, misiba na mashaka na awasaidie wale watu waaminifu kulipa madeni yao. Hivyo kwa kutenda majukumu yake ya wema kwa subira akistahimili matatizo kuwaondolea wengine mateso yao, atakuwa anajiwezesha mwenyewe kupata Malipo na Neema za Allah, kwa sababu ni sifa na tabia hizo tu zitakazomnyanyua kufikia kileleni mwa wema katika dunia hii, na kwenye kilele cha ubora katika Akhera.” (Taz. Peace of Eloquence, ISP, 1984)

Kutoa Msaada Kwa Wenye Shida Uislam umeendesha kampeni kubwa sana dhidi ya kuombaomba na hauwaruhusu wale watu wanaoweza kufanya kazi wawe wanaomba, na kama wakiomba, wanatenda uvunjaji wa sheria na pesa wanayoipata ni haram. Imam Ja’far as-Sadiq (a.s.) anasema: “Kama mtu ataomba bila ya kuwa na haja hasa, Mwenyezi Mungu atamfanya awe na dhiki na mwenye kutegemea katika kuomba na atamtengea mahali pake katika moto wa Jahannam.” (Furu’ul-Kafi, Jz. 4, uk.19) Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amewalaani wale ambao hawafanyi kazi licha ya kuwa kwao na nguvu za kutosha na wakawa wanawategemea wengine. Hata hivyo, haiwezi kukanushika kwamba katika kila jamii kuna watu ambao wameishiwa nguvu, wanyonge, wazee na watu waliostaafu ambao ambao hawana nguvu za kutosha kuweza kufanya kazi yoyote ile na vile vile hawana kipato cha kutosha kujikimu wao wenyewe. Matajiri wanao wajibu kuhusiana na watu kama hao kuboresha mapungufu yao kuhusiana na chakula, mavazi, makazi, matibabu na kadhalika.

182

11:28 AM

Page 182


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Imam as-Sadiq (a.s.) anasema: “Mashia wetu matajiri ni wadhamini wetu kuhusu Mashia wenye shida.” Kisha Mtukufu Imam anapendekeza kwa Mashia matajiri; “Hifadhini ile heshima inayotustahiki sisi kuhusiana na Mashia wetu wenye shida na haja ili kwamba Mwenyezi Mungu aweze kuwahifadhi ninyi.” (Safinatul-Bihar, Jz. 2, uk. 378) Mtukufu Mtume wa Uislam (s.a.w.w.) anasema: “Yeyote yule anayedumisha uhusiano wa kidugu na masikini na wenye shida, na akawafanya wachukue sehemu katika mali zao na akawa mwadilifu kwa watu, huyo ni muumini wa kweli.” (al-Kafi, Jz. 2, uk. 119) Imam Ali (a.s.) anasema: “Endapo mtu atatumia mali yake aliyopewa na Mwenyezi Mungu kwa malengo mazuri na katika njia ya Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu atamfidia katika ulimwengu huu kwa ajili ya matumizi aliyoyafanya na pia atampatia malipo ya ziada kesho Akhera.” (al-Kafi, Jz. 2, uk. 123) Wakati Imam ar-Ridha alipoketi karibu na kishamia cha chakula ili kupata mlo wake, alikuwa akitumia kuweka bakuli kubwa karibu na mkono wake na kuweka baadhi ya vile vyakula vizuri na vya aina mbalimbali ndani yake na akavipeleka vyakula hivyo kwa wenye haja. Kisha alikuwa akizoea kusoma aya hii: “Lakini hakupita ile njia nzito.” (al-Balad; 90:11), na alisema: “Mwenyezi Mungu alijua kwamba kila mtu hayuko katika hali ya kuweza kumuacha huru mtumwa. Yeye kwa hiyo aliwafungulia njia ya Peponi ili kwa kule kuwalisha wenye njaa na wenye shida, basi waweze kupata Pepo ya milele.” (Furu’ul-Kafi, Jz. 4, uk. 52) Ikiwa matajiri wanapenda kwamba mali zao na neema ziweze kudumu, na Mwenyezi Mungu asiwanyang’anye rehema na huruma Zake, basi wanapaswa kutumia katika njia ya Mwenyezi Mungu na wafanye utaratibu wa kudumu wa kuzisaidia familia zenye shida.

183

11:28 AM

Page 183


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Mtu mmoja alikuja mbele ya Imam Ja’far Sadiq na akasema: “Baadhi ya Waislam wana hali nzuri, na kipato chao kinazidi matumizi yao. Na kuna wengine ambao wamekwama na Zaka tu, pia inatosha kukidhi mahitaji yao. Je, inaruhusiwa katika hali ngumu kama hizi kwamba matajiri wabakie kutojali ndugu zao Waislam, ambapo wao wenyewe wanakula na kushiba na kuwaacha ndugu zao kubaki na njaa?” Imam alimjibu akasema: “Mwislamu ni ndugu wa Mwislamu. Hamuonei wala kumdhalilisha ndugu yake. Hamnyimi kutokana na utajiri wake. Inafaa kwamba Waislam watekeleze majukumu yao ya udugu kwa juhudi na uangalifu kabisa na waimarishe mafungamano yake na kusaidiana. Lazima wawe na huruma kwa wale wenye shida na waonyeshe silika za kibinadamu na wafuate vile walivyoamrishwa na Mwenyezi Mungu kwamba: Wao ni wapole wenyewe kwa wenyewe na ni wenye kuhurumiana wao kwa wao.” (Furu’ul-Kafi, Jz. 4, uk. 5.) Imam Muhammad al-Baqir (a.s.) anasema: “Kama nikiisaidia familia ya kiislam na kutoa chakula na nguo kwa ajili yao na nikailinda heshima yao katika jamii, ninalichukulia hilo kuwa ni bora kuliko kufanya hijja sabini zilizopendekezwa..” (Furu’ul-Kafi, Jz. 4, uk. 20) Athari za Sadaka: Kwa vile kuwasaidia wanyonge na kutoa sadaka kwa wenye shida ni njia mojawapo ya kupata radhi za Mwenyezi Mungu, kunaleta athari nzito na za ustawi ambazo baadhi yake zimehusishwa na Akhera na fungu lake kubwa linafungamana kwenye dunia hii yenyewe. Katika riwaya za viongozi watukufu wa Uislam athari hizi zimedokezewa, na baadhi yake zinatajwa hapa chini: Imam Ja’far as-Sadiq (a.s.) amesema: “Nilikuwa ninamiliki kipande cha ardhi pamoja na mnajimu mmoja aliyekuwa na uhodari wa unajimu na 184

11:28 AM

Page 184


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio tukaamua kukigawa ili sehemu ya kila mmoja wetu iweze kuainishwa. Mshirika wangu, yule mnajimu, hata hivyo alipoteza wakati na alikuwa wakati wote akijaribu kupata muda ambao utakuwa na heri kwake na wenye bahati mbaya kwangu mimi ili wakati huo wa kugawana aweze kupata sehemu yenye kupendeza zaidi. Mwishoni alipanga siku ambayo tuligawa ardhi hiyo. Hata hivyo, kinyume na matarajio yake na utabiri, mimi nilipata ile sehemu inayopendeza zaidi na yeye alipata isiyopendeza. Aliipopotoa mikono yake kwa hasira nyingi na kuchukia sana na akasema: “Sijawahi bado kuona siku mbaya kama hii yak leo.” Nikamuuliza: “Kuna tatizo gani?” Yeye akasema: “Kwa mujibu wa makadirio yangu hii ilikuwa ni saa ya kheri kwangu na ya bahati mbaya kwako, lakini sasa ninaona kwamba ile sehemu nzuri ya ardhi imeangukia kwenye fungu lako.” Mimi nikamwambia; “Ngoja nisimulie mbele yako hadithi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): Mtukufu Mtume amesema: “Yeyote anayetaka Mwenyezi Mungu aiweke mbali naye bahati mbaya ya siku atoe sadaka mapema asubuhi, na anayetaka Mwenyezi Mungu amwepushe na bahati mbaya ya usiku anapaswa auanze usiku huo kwa kutoa sadaka. “Kabla mimi sijakuja hapa kwa ajili ya ugawaji wa ardhi hii nilichukua hatua ya kwanza kwa kutoa sadaka. Kama na wewe pia ungefanya kwa mujibu wa amri ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ingekuwa na manufaa zaidi kwako kuliko kutegemea unajimu.” (Furu’ul-Kafi, Jz. 4) Imam Muhammad Baqir (a.s.) anasema: “Kufanya matendo mema na kutoa sadaka kunamlinda mtu kutokana na kuwa fukara, maisha yake yanarefushwa na anabakia amekingwa na kifo cha balaa.”

Ulezi wa Yatima: Ulezi kwa mayatima na kusimamia mambo yao ni moja ya majukumu yasiyotenguka ya matajiri. Watoto waliopoteza walezi wao wanastahiki upendo na huruma za watu wote hususan za matajiri. Ni muhimu kwamba waendeshe maisha yanayoheshimika na hivyo chakula, mavazi na makazi 185

11:28 AM

Page 185


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio lazima yatolewe kwao. Katika maagizo yake ya mwisho, yaliyolengwa kwa wanawe na wafuasi wake wote wakati alipokuwa kwenye kitanda cha umauti wake, na ambamo alielezea mambo muhimu ya Uislam, Imam Ali (a.s.) alizungumza hivi kuhusu mayatima: “Muogopeni Mwenyezi Mungu pale linapoibuka suala ya mayatima wasio na uwezo. Kamwe msije mkawaacha wafe njaa. Alimuradi ninyi mpo pale kuwakinga na kuwalinda, basi wasije wakaharibikiwa au kupotea. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wakati wote alishauri, alitahadharisha na kutukumbusha sisi juu ya wajibu huu, kwa kiasi kwamba mara nyingi tulidhani kwamba Mtume wa Allah (s.a.w.w.) angeweza, katika wasaa ujao, kuwapangia fungu kutoka kwenye mirathi yetu.” (Taz. Peace of Eloquence, Barua ya 47, uk. 617, ISP, 1984) Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: “Yeyote anayechukua jukumu la ulezi wa yatima mmoja na akakidhi matumizi yake atakuwa swahiba wangu ndani ya Pepo na atakaa kando yangu.” (Safinatul-Bihar, Jz. 2) Kutimiza mahitaji ya yatima ni ulazima wa jamii na kama matajiri watapuuza jambo hili muhimu, watoto kama hao wanakabiliwa na matatizo ya kisaikolojia na wanasababisha hatari isiyoponyeka kwa ajili ya jamii katika siku za baadae. Kutoa Heshima kwa Mafukara: Moja ya mambo ambayo matajiri wanapaswa kuliwekea mazingatio maalum ni kutoa heshima kwa matabaka ya wasio nacho na mafukara. Katika sheria ya Kiislam ifuatayo na Hadith za viongozi wa Uislam, jambo hili limesisitizwa sana na limekuwa ni lengo la mazingatio katika riwaya mbali mbali.

186

11:28 AM

Page 186


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: “Yeyote anayetoa heshima kwa Mwislamu fukara mmoja atakuja kutokea mbele ya Mwenyezi Mungu mnamo Siku ya Kiyama katika hali ambayo kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu atakuwa amemridhia.” (Safinatul-Bihar, Jz. 2, uk. 379) “Ifahamike kwenu kwamba endapo mtu atamdharau na kumdhalilisha Mwislamu fukara, anaichukulia haki ya Allah swt. kuwa haina thamani, na ili kumuadhibu kwa kitendo hiki kibaya, Mwenyezi Mungu atamtweza katika Siku ya Kiyama kwenye dharau na fedheha isipokuwa kwamba aonyesha majuto kwa kile alichokifanya na atubie mbele ya Mwenyezi Mungu.” (Amali Saduuq, uk. 257) Imam Ali (a.s.) anasema: “Ni jambo zuri na bora kiasi gani ambalo lazima litakuwa, kwamba ili kupata thawabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu, matajiri lazima wawe wanyenyekevu mbele ya masikini na kuwaheshimu.” (Nahjul-Balaghah) Mbali na mwelekeo wa kidini, kuonyesha dharau kwa mafukara ni kinyume na maadili mema na ubinadamu na kunasababisha matatizo mengi na uadui kati ya matajiri na masikini ambao wakati mwingine hufikia kwenye matukio yasiyopendeza. Kuonyesha matumizi makubwa katika anasa, ufujaji na ubadhilifu kunakofanywa na matajiri kunawasha moto wa uhasama na mfundo katika nyoyo za wenye shida. Wakati mwingine chakula kinachotayarishwa kwa ajili ya shereha kinazidi mahitaji na wakazi wa nyumba, bila kujali kwamba ni neema ya Mwenyezi Mungu, wanatupa hayo mabaki ya chakula kwenye mapipa ya takataka. Kwa upande mwingine wanaharibu neema ya ki-ungu na hivyo kutenda dhambi kubwa mno, na kwa upande mwingine, pale wapita njia walio masikini na wenye njaa wanapoiona hali hii ya mambo huwa wanakasirika na pengine kuwalaani hao wenye chakula hicho.

187

11:28 AM

Page 187


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Katika baadhi ya nyumba za matajiri, madirisha ya jikoni yanafungukia upande wa mitaani na ile riha ya kupendeza ya chakula hujaa kwenye angahewa la barabara na wapita njia ambao kwa hakika ni pamoja na masikini wanawake kwa wanaume na yatima wenye njaa wanapita kando kando ya nyumba hizo kwa majuto na bila shaka wanakuwa na hisia mbaya nyoyoni mwao juu ya wenye nyumba hizo. Wakati mwingine, pale watoto wa hao matajiri wanapotoka nje ya nyumba zao wanakuwa wamechukua pamoja nao matunda, lawalawa, matunda yaliyokaushwa na kadhalika, na wanaanza kuvila vitu hivyo mbele ya watoto wengine ambapo wale watoto masikini wanawakodolea macho saa zote kwa uchungu sana. Vitendo kama hivyo ni vya kulaumiwa kwa mtazamo wa kimaadili na ubinadamu, na kwa mujibu wa Uislam pia vitendo kama hivyo ni vibaya na vya aibu. Bila shaka kuna watu wengi wema na wawajibikaji miongoni mwa Waislam na athari za huduma zao za kijamii na kidini ziko dhahiri zinaonekana kila mahali. Matajiri kama hao wanapata heshima kutoka kwa watu na dua njema za watu kuwatakia heri ndio walinzi wa maisha yao na kwa mujibu wa ahadi ya Mwenyezi Mungu watapata ustawi katika Akhera.

* * * * * UIMARA Mafanikio katika kazi yoyote yanakwenda pamoja na uimara na hakuna anayeweza kufanikiwa katika jambo lolote bila hilo. Kama mtu anataka kuwa mwanazuoni, ni lazima astahamili taabu za kutafuta elimu na akae kwa adabu mbele ya mwalimu wake wakati wote 188

11:28 AM

Page 188


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio na kwa subira. Hapaswi kuyachoka masomo, anapaswa ajinufaishe na kila fursa ya kupata elimu na hapaswi kupoteza wakati wake. Ni katika njia hii kwamba pole pole anaweza kupata elimu na busara na kupata cheo cha mtu aliyesoma, mwanachuoni. Yule anayetaka kupata mali lazima afanye kazi kwa bidii na hapaswi kujiepusha na jitihada na bidii. Kama akikabiliana na kushindwa katika hatua ya awali na akipata hasara hapaswi kuvunjika moyo bali anapaswa kuendelea na jitihada ili pole pole akusanye mali. Mtu mgonjwa anayetaka kupona, lazima avumilie uchungu wa matibabu na mlo wenye masharti bora na wakati mwingine alipie ada ya upasuaji kwa ustahamilivu ili aweze kurejeshwa kwenye afya yake. Yule anayetaka kubadilika na kuwa na tabia njema badala ya zile mbaya anapaswa asimame imara dhidi ya vishawishi vya anasa na matamanio potofu na ajidhibiti dhidi ya tamaa zake na alifikie lengo lake kwa umadhubuti kabisa. Yule anayetaka kufanyakazi kama mwana mageuzi na kuiongoza jamii yake katika amani na ustawi hapaswi kuvunjika moyo kwa sababu tu ya harakati za wapinzani wake na asijitoe katika harakati zake. Bali ni sharti la msingi la kazi yake kwamba anapaswa kuvumilia shida zote na anapaswa kuwa na subira katika usumbufu wowote na anapaswa kuonyesha uvumilivu na umadhubuti. Mwislamu anayetaka kulinda imani yake ni lazima asimame imara dhidi ya kejeli na dharau za makafiri na anapaswa avumilie shida na mateso kwa subira. Anapaswa kuonyesha msimamo dhidi ya (vishawishi vya) kupenda mali, cheo na matamanio, avumilie shida, kunyimwa na ajipushe kujiingiza katika dhambi ili aweze kuilinda imani yake.

189

11:28 AM

Page 189


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Hali na shuruti zilizotajwa hapo juu ni mifano ya matatizo mbalimbali ya maisha ya kiyakinifu na kiroho ambamo mwanadamu anahisi haja ya umadhubuti na katika nyanja nyinginezo pia ni vigumu kupata mafanikio bila ya umadhubuti. Hivyo umadhubuti ndio sifa bainifu kabisa ya mwanadamu, kwa sababu kwa hili inakuwa ni rahisi kupata sifa zote za kibinadamu na maendeleo ya kiakili na kiroho. Kwa kupitia njia ya umadhubuti mtu asiyejua kitu anakuja kuwa mwanachuoni, bakhili anakuwa mkarimu, mtu wa majisifu anakuwa mchamungu na mtu masikini anakuwa tajiri. Mbali na hili mtu pia lazima awe mwenye kuvumilia kwa ajili ya kulinda ule msingi unaopatikana kwake, kwa sababu kama vile tu umadhubuli ulivyo muhimu kwa kufikia malengo ya mtu, ni muhimu vilevile kulinda malengo haya pale yanapokuwa yamepatikana. Imam Ali (a.s.) anasema: “Kama unatamani kuwa na wokovu na ustawi ni lazima uweke mbali uzembe, uache mambo ya kipumbavu na uchukulie kufanya kazi kwa bidii kuwa ndio wito wako.” Anaendelea kusema zaidi: “Ni muhimu juu yako kufuata njia ya umadhubuti kwa sababu njia hii hukupatia uongozi na umaarufu na kukuweka salama kutokana na lawama za watu.” (Ghurarul-Hikaam) Sakkaki alikuwa ni mmoja wa wanachuoni mashuhuri wa karne ya saba ya zama za Uislam. Wakati wa ujana wake alifanya kazi kama mfuachuma na alipata maendeleo makubwa katika taaluma hii. Wakati mmoja alitengeneza sanduku la chuma la kisanifu sana pamoja na kufuli na akaliwasilisha kwa khalifa. Ule uzuri, mtindo na wepesi wa sanduku hilo ulimvutia sana khalifa huyo na washauri wake. Walimsifu na kumtia moyo Sakkaki kwa usanii wake.

190

11:28 AM

Page 190


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Wakati huohuo akatokea mwanachuoni mmoja. Khalifa akasimama kama ishara ya heshima juu yake halafu akaketi mbele yake kwa magoti yake. Sakkaki akauliza kwamba mtu yule alikuwa ni nani aliyepewa heshima kubwa kiasi kile na khalifa na akajulishwa kwamba alikuwa ni mwanachuoni. Sakkaki akajisemea mwenyewe: ‘Mimi nimefanya kazi kwa bidii kwa muda mrefu katika kutengeneza sanduku hili maridadi na kitu pekee nilichokipata kilikuwa ni kusifiwa na kutiwa moyo. Kwa nini nisitafute elimu ili na mimi niweze kupata nafasi ile.’ Wakati alipotoka nje ya baraza la khalifa alikwenda moja kwa moja kwenye shule na akamuomba mwalimu wa hapo amfundishe. Wakati huo alikuwa na umri wa miaka thelathini. Katika siku ya kwanza mwalimu alimfundisha suala la fiqhi pamoja na maagizo ya kulirudia kesho yake. Lakini pale alipolirudia suala hilo alifanya hivyo katika namna potovu kabisa kiasi kwamba wanafunzi wengine wote wakaanza kucheka kwa nguvu sana. Mwalimu akawazuia wanafunzi kuendelea kucheka na akamfundisha Sakkaki somo jingine. Alifuatilia masomo yake kwa miaka kumi lakini juhudi zake zote hazikufaa kitu. Mwishowe, akiwa amechoka na kupoteza matumaini yote alikwenda msituni na kukaa chini ya mlima. Wakati akiwa amekaa hapo alianza kutafakari juu ya ile nafasi yake isiyotamanika. Wakati huo huo aliona kwamba matoni ya maji yalikuwa yanadondoka kutoka juu ya mlima huo na kutua juu ya jiwe, moja baada ya jingine, na yalikuwa yametengeneza shimo kwenye jiwe hilo. Alijiambia mwenyewe: ‘Moyo wangu sio mgumu kama hili jiwe.’ Kisha akaamka upesi sana, akarudi kule shuleni kwa dhamira mpya na akajishughulisha na masomo. Hatimaye, huyu mfuachuma mwenye umri wa miaka thelathini asiye na kipaji, kwa njia ya uthabiti na uvumilivu akawa mmoja wa wanachuoni mashuhuri na akajipatia cheo cha juu kabisa.” (Rawdhatul-Jannaat, uk. 747)

191

11:28 AM

Page 191


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Imam Ali (a.s.) anasema: “Yeyote atakayetumia nguvu zake na uwezo atafikia malengo yake.” Vile vile anasema pia kwamba: “Kama mtu ataendelea kupiga hodi mlangoni na akaonyesha umadhubuti katika kufanya hivyo, mlango huo utafunguka kwa ajili yake.” (Ghurarul Hikam) Jambo ambalo lazima lizingatiwe akilini ni kwamba umadhubuti ambao ni moja ya sifa kubwa sana ya mwanadamu, unakuwa na hili kwamba mwanadamu lazima afanye tafakari na uchunguzi bila kuingiliwa na silika potovu na hisia za chuki, na lazima ahakikishe usahihi wa lengo lake na aonyeshe uaminifu na umadhubuti kwa ajili ya ufanikishaji wa lengo hilo kwa ajili ya ulinzi wake. Hata hivyo, ikiwa mtu atachagiza kwa ajili ya kufanikisha lengo haramu, lisilo na msingi na potovu, haiwezi kuitwa ‘umadhubuti.’ Kwa upande mwingine huo ni ‘ukaidi’ ambao ni moja ya sifa mbaya na duni na chanzo cha upotovu na maangamizi. Jambo jingine ni kwamba umadhubuti ni wenye kufaa kwa ajili ya sababu zote zinazostahili na malengo halali na yenye mantiki, lakini sababu ambayo hasa inastahili umadhubuti na yenye taabu imo katika njia ya sababu ya Mwenyezi Mungu na ulinzi wa dini na kueneza mambo ya kiroho katika jamii. Hili liko hivyo kwa sababu matokeo pekee ya umadhubuti katika mambo ya kimaada ni kwamba mtu hupata vitu vya kimaada ambapo umadhubuti katika njia ya Mwenyezi Mungu ni mafanikio katika kupata ustawi katika dunia zote, hii na ya Akhera. Qur’ani Tukufu inaahidi starehe kuu ya milele kwa wale wanaotwaa umadhubuti kama huo. Inasema:

“Hakika wale waliosema: Mola wetu ni Mwenyezi Mungu, kisha wakadumu imara, hawatakuwa na hofu wala hawatahuzunika.” (alAhqaf; 46:13)

192

11:28 AM

Page 192


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Tabia ya Mtukufu Mtume wa Uislam (s.a.w.w.) ndio mfano bora kwa wafuasi wake katika suala hili. Qur’ani Tukufu inasema:

“Basi (Ewe Mtume) endelea kuwa imara kama ulivyoamriwa wewe na yule anayeelekea (kwa Mwenyezi Mungu) pamoja nawe, wala msiruke mipaka, kwani yeye anayaona mnayoyatenda.” (Suratul-Huud; 11:112) Kwa amri ya Mwenyezi Mungu, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alichukua uongozi na urekebishaji wa watu wakati alipokuwa hana nguvu yoyote ya dhahiri na msaada na nyenzo. Rasilimali yake kubwa katika njia hii ilikuwa ni imani juu ya Mwenyezi Mungu na umadhubuti mbele ya matatizo yote. Alikuwa na imani kamili kwa Mwenyezi Mungu na mwongozo Wake na wala hakujali kujitolea muhanga mali yake na maisha katika njia hii. Kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakujilegeza mwenyewe mbele ya hali ya vitisho au mashinikizo ya makafiri na alisimama imara kwa akili timamu iliyotulia. Yeye alifanikiwa vilevile katika kufundisha kikundi cha watu ambao hawakuogopa bahati mbaya na hatari na walikabiliana na dharura zote kwa bidii zote na nguvu. Ayyasg bin Abi Tabi’ah na mkewe Asma’ bint Salaamah walikuwa ni watu miongoni mwa wale waliokubali Uislamu katika miaka ile ya mwanzoni ya kazi ya utume ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na walipatishwa mateso makubwa sana na wale wasioamini (makafir) kwa sababu hiyo na wakakabiliana nayo kwa umadhubuti kamilifu kabisa. Ayyash alikuwa ndugu yake Abu Jahl na Harith kwa upande wa mama yake. Wakati aliposilimu alikuwa na umri wa takriban miaka thelathini na mke wake alikuwa na miaka ishirini. Watu wa familia ya Ayyash 193

11:28 AM

Page 193


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio walikasirika sana kwa sababu hii ya kusilimu kwake na kuwa Mwislamu na wakampa mateso makubwa sana ili kumfanya aitelekeze dini yake. Adhabu zao hata hivyo hazikuthubutu kuwa na athari kwake na akabakia madhubuti katika njia ya Uislamu. Ayyasha na mke wake walihamia Uhabeshi (Ethiopia ya sasa), wakiwa pamoja na baadhi ya Waislam, kwa ruksa ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Hata hivyo, wao walirejea Makka mapema sana kuliko wengine, na kwa mara nyingine tena wakapatwa na mateso kutoka kwa washirikina. Hali hii ya mambo iliendelea kuwepo mpaka pale wakati wa kuhajiri kwa Mtukufu Mtume wakati Waislam walipomfuata kwenda Madina na wakawa huru kutokana na mateso ya maadui. Wakati mama yake Ayyash alipokuja kujua kuhusu kuhama kwake, aliweka nadhiri kwamba, mpaka atakaporudi Makka, yeye hatapaka mafuta kwenye nywele zake wala hatakaa chini ya kivuli. Abu Jahl na Harith ndipo wakatembelea Madina, wakakutana na Ayyash na walipomwambia kuhusu nadhiri ya mama yake wakasema: “Kutoka miongoni mwa watoto wake wewe ndio kipenzi zaidi kwa mama yako na ni mfuasi wa dini ambayo inapendekeza wema kwa wazazi wake mtu. Unapaswa kwa hiyo kurudi Makka ambako utamuabudu Mola Wako kama unavyomuabudu Yeye hapa Madina.” Ayyash aliguswa sana kujua kuhusu hali ya mama yake na akakubali kuupokea ushauri uliotolewa na kaka zake. Alichukua ahadi kutoka kwao kwamba hawatamsaliti katika kurejea kwake Makka na kisha akaondoka Madina pamoja nao. Walipofika sehemu mbali kidogo na mji, adhabu na mateso vikaanza. Wale ndugu wakafunga mikono ya Ayyash nyuma ya mgongo wake na wakamfikisha Makka katika hali hiyo. Waliingia mjini Makka mchana kweupe na wakakemea kwa sauti kubwa: “Enyi watu wa Makka! Wafanyieni wajinga wenu ambao wameingia kwenye Uislam kwa namna ya kikatili kama 194

11:28 AM

Page 194


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio tulivyomfanyia mpumbavu wetu huyu.” Kisha wakamfungia kwenye chumba ambacho hakina paa na wakavunja ahadi zote walizoahidiana naye na wakampatia mateso makali sana kiasi ilivyowezekana. Ayyash alibakia ufungwani mjini Makka kwa miaka michache kadhaa na akavumilia mateso. Katika kipindi hiki hata hivyo, hakuna hata dalili ndogo kabisa za udhaifu au kuvunjika moyo kiroho kulikojitokeza kwake. Alifanya mawasiliano yake na Mwenyezi Mungu Mtukufu na akakabiliana na matatizo na usumbuvu wote kwa nguvu ya imani yake. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuombea mjini Madina kwa kurudia mara kwa mara na Waislam wote walikuwa na wasiwasi juu ya jambo hilo. Hatimaye mmoja wa Waislam aliwasili mjini Makka kwa siri na akapata kuachiwa huru kwa Ayyash kwa njia ya mpango uliopangwa kwa urahisi kabisa. Kisha wote wakarudi Madina pamoja.’” (Shabaab-i Quraysh, uk. 128; Jawaan, Jz. 2, uk.161). Watu wengine ambao walikuwa wamefunzwa katika shuli ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) – mwisho wa Mitume ya Mwenyezi Mungu, nao pia walijaaliwa na umadhubuti unaokubalika.

Uvumilivu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) Ule uvumilivu wa Mtukufu Mtume katika njia ya Mwenyezi Mungu ulikuwa ni somo la kivitendo kwa ajili ya wafuasi wake na walijifunza njia na mienendo ya umadhubuti na uvumilivu kutoka kwenye tabia yake. Waabudu masanamu wa Makka hawakubakisha njia yoyote ile katika kuizima nuru ya Uislam. Kwanza kabisa walitwaa njia ya majadiliano na ahadi za kuvutia sana. Walimwendea Abu Talib na wakamwambia, “Hebu zungumza na mpwa wako Muhammad na umuulize ni nini hasa lengo lake halisi katika mapambano yake dhidi ya masanamu na kuwalingania watu kwenye ibada ya Mungu asiyeonekana. Na endapo kama anataka pesa tuta195

11:28 AM

Page 195


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio muwekea kiasi kikubwa mno mikononi mwake. Na kama anataka mamlaka, sisi tuko tayari kumkubali yeye kama mtawala wetu.” Abi Talib aliwasilisha ujumbe huo wa waabudu masanamu kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Katika kulijibu hilo, Mtukufu Mtume akasema: “Mpendwa Ammi yangu! Waambie watu wa Makka kwamba mimi nimekabidhiwa wajibu na Mwenyezi Mungu Mtukufu ambao ni lazima kwangu kuutekeleza na lengo langu si lingine zaidi ya kutaka radhi za Mwenyezi Mungu na kutilia nguvu Amri Zake. Hata kama watu wa Makka wataliweka jua kwenye mkono wa kulia na mwezi kwenye mkono wa kushoto mimi sitaacha wito wangu.” Pale watu wa Makka walipokutana na kutoridhishwa walianzisha kampeni yao kwa ari na katika namna ya kiburi kabisa waligeukia kwenye mateso, lugha chafu, kashfa njama na hila na utendaji wa kikatili katika njia mbalimbali. Shinikizo na mateso vikachukua ukubwa kiasi kwamba Waislam walilazimika kuhamia Ethiopia na baadae Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) pia akahamia Madina. Hata baada ya hapo, mgogoro bado uliendelea katika muundo wa vita vya Badr, Uhud, Ahzaab na kadhalika. Hata hivyo, hakuna hata vita moja kati ya hivi vilivyoweza kuathiri ile dhamira imara ya Mtukufu Mtume na aliendele kubakia madhubuti mbele ya migogoro yote hii. Kwa matokeo ya hili, alifanikiwa katika kuieneza dini tukufu ya Uislam katika dunia ya wakati ule na kuwabadili wale nusu pori watu kuwa umma ulioendelea ambao ulipata sifa zote za kibinadamu. Jambo ambalo ni lazima litajwe hapa ni kwamba isije ikadhaniwa kwamba umadhubuti ni lazima uandamane na ukatili. Endapo kwa hiyo, mtu madhubuti anafananishwa na mlima ni kwa sababu ya mlima kuweza kuhimili dhoruba na mawimbi na sio kwa sababu ya ugumu wake. Na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye alikuwa ni kigezo kikamilifu na dhahiri cha umadhubuti alikuwa na tabia za kiungwana kabisa na moyo wa huru196

11:28 AM

Page 196


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio ma na upole huo huo ulikuwa ni moja ya vipengele vya mafanikio yake. Moja ya mambo muhimu na ya msingi yanayohusiana na haiba ya mtu na ubadilikaji kulingana na mazingira ni ule mnyumbuliko kulingana na mkusanyiko wa matukio. Watu wanaokabiliana na matukio kwa hekima na kujizuia na ukaidi na ubishi usio na haki wanaweza kuyashinda matatizo kirahisi kabisa na wanaweza kuonyesha haiba zao. Kwa upande mwingine wale watu ambao ni wakaidi na wasusuavu wa nyoyo wanakimbilia kwenye ubishi usio na lazima na hatimae kuvunja utu na haiba zao na mara kwa mara wanakabiliwa na matatizo yasiyovumilika pamoja na mateso. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: “Kwa kusimama dhidi ya dhoruba ya matukio, muumin ni sawa na kitita (cha zabibu) ambacho huinamia chini ardhini wakati upepo unapovuma na kurudia mahali pake wakati upepo unapotulia. Kwa kufanya hivyo kinajipatanisha chenyewe na mazingira na kinakuwa salama kutokana na ajali za bahati mbaya. Hata hivyo yule mpumbavu asiye muumini anasimama dhidi ya dhoruba ya matukio bila kujua na wala kuthibitika kama msonobari na hatimae unang’olewa.” (Tafsir-i Ruhul Bayaan, Jz. 4, uk. 356) Mtu mwenye afya nzuri ambaye ana mnyumbuliko na uwezo wa kurejea kwenye hali yake ya kawaida anaweza kustahimili kila analoshindwa. Husimama tena kwa miguu yake na kuanza juhudi zake upya. Na kwa vile anayo mishale mingi ndani ya pono lake (uwezo wa kufanya mambo mbalimbali), hufuata njia nyingine pale anapoona njia moja imefungwa na kisha anachagua shabaha mpya. Kwa upande mwingine, moyo dhaifu hauoni zaidi ya shabaha moja na unayo njia moja tu katika dunia, na endapo kutakuwa na kikwazo kwenye njia hiyo huwa anasikitishwa na kupoteza matumaini yote kabisa. Kiasi ambavyo mtu amejaaliwa zaidi na uwezo wa mnyumbuliko ndio anavyokosa woga zaidi wa kuvunjikiwa. Anaidhibiti nyanja ya mafanikio katika namna bora na kuifanya kuwa ni msingi mzuri wa shauku zake, vipawa na malengo yake. Na kama mtu hana uwezo huu, anaondoka kwenye nyanja ya mashindano upesi sana na kukubali kushind197

11:28 AM

Page 197


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio wa. Umadhubuti unapaswa wakati wote kuunganishwa na utulivu wa kujiamini na upole ili kwamba uweze kumuongozea mtu kwenye mafanikio na ushindi. Wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ilitokea mara kwa mara kwamba washirikina walimtendea mambo kwa ukatili. Na bila ya kujali kwamba alikuwa na nafasi ya kuweza kumuadhibu mtu yeyote kama huyo, yeye hakuruhusu huruma zake kumfanyia ukatili mtu huyo. Kinyume chake, yeye alizungumza naye kwa sura ya upole wa wazi na huruma isiyo ya kawaida kabisa hatimae alifanikiwa katika kumteka kwenye Uislam. Qur’ani tukufu inasema hivi:

“Basi kwa sababu ya rehema ya Mwenyezi Mungu umekuwa laini kwao na kama ungekuwa mkali, na mshupavu wa moyo, wangekukimbia. Basi wasamehe na uwaombee msamaha na ushauriane nao katika mambo, na unapoazimia basi mtegemee Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wenye kumtegemea. (Surat al-Imraan; 3:159) Ni muhimu kuelezea hapa kwamba katika aya hiyo hapo juu Mwenyezi Mungu amemwelekeza Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kushauriana na masahaba zake, na mashauriano yake yanahusu mambo ya kawaida tu kama vita, amani na kadhalika. Kuhusiana na Shari’ah za Kiislam na utekelezaji wake kwa maagizo yake, hata hivyo, haikuwa tu kwamba masahaba 198

11:28 AM

Page 198


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio hawakuweza kuziingilia kati bali hata Mtukufu Mtume alikuwa hana la kusema katika suala hilo. Sheria hizi zilitumwa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Mwenyezi Mungu naye akaziwasilisha kwa watu. Umadhubuti Katika Tabia Njema: Moja ya mambo ambayo kwayo umadhubuti ni muhimu sana kwa watu wote ni upatikanaji wa tabia nzuri na mienendo na kuachwa kwa tabia mbaya. Wakati wa kuzaliwa kwake, mwanadamu anakuwa hana cha sifa nzuri au mbaya. Pole pole anakuja kupata tabia na sifa, ama nzuri au mbaya, chini ya athari za wazazi wake na walimu na kutoka kwenye jamii. Tabia na sifa nzuri lazima zilindwe na umadhubuti na muhimu kwa ajili ya kuzihifadhi. Kama mtu hatafanya jitihada juu ya kuzilinda kwao anazipoteza haraka sana. Hivyo juhudi na umadhubuti ni muhimu vile vile kwa kuachana na tabia na mwenendo mbaya ili tabia na sifa nzuri na njema ziweze kupandikizwa mahala pake. Kama mtu yoyote anadhani kwamba tabia na sifa zisizopendeza haziwezi kubadilishwa amekosea vya kusikitisha sana. Uzoefu umeonyesha na wanasaikolojia pia wanakiri kwamba sifa zote za binadamu zinaweza kubadilishwa kwa dhamira na maamuzi. Hivyo endapo kwa sababu ya malezi yasiyofaa katika familia na mazingira mabaya ya kijamii mtu hakuweza kukua na kuwa mtu mwema na hawezi kuendana na jamii, basi asikate tamaa na asije akadhani kwamba atakuwa hana bahati ya kuwa mwenye kushindwa katika maisha. Kwa upande mwingine, anaweza kujibadilisha mwenyewe kwa dhamira imara na akapata shakshi ya heshima. Mtu kama huyo anao wajibu kwa mtazamo wa kidini na kielimu kufanya kampeni dhidi ya desturi mbaya na kufutilia mbali zile tabia mbaya ambazo ndio chanzo cha kukosa kwake na kupata njia ya mafanikio yake 199

11:28 AM

Page 199


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio kwa kujitwalia tabia nzuri za kiungwana. Imam Ali (a.s.) anasema: “Usiacha kufanya juhudi kujibadili mwenyewe, kwa sababu hakuna kitakachokusaidia wewe katika kazi hii isipokuwa ni juhudi na kupambana.” (Ghurarul Hikam) Yeye vile vile anaendelea kusema: “Enyi watu! Jichukulieni wajibu wa kujibadilisha nafsi zenu na mjiweke mbali na tabia mbaya.” (NahjulBalaghah) Imam Ja’far as-Sadiq (a.s.) anasema: “Jiepusheni wenyewe kutokana na yale yenye madhara kabla hamjavuta pumzi zenu za mwisho. Na fanyeni juhudi kuhakikisha uhuru wa nafsi zenu kama vile mnavyofanya juhudi katika kutafuta maisha, kwa sababu nafsi zenu zinaathiriwa na matendo yenu na haziwezi kuachwa huru bila ya juhudi zenu.” (Wasa’ilish-Shi’ah, Jz. 2, uk. 40) Tabia mbaya ambazo zimekuwa ni asili yetu ya pili katika mpito wa idadi kadhaa ya miaka hazikufutika mara moja. Kwa bahati nzuri hata hivyo, kama tukitenda kulingana na maamrisho ya hekima na mantiki pamoja na dhamiri thabiti na tukawa hatuchoki, kila tabia iliyoota mizizi mirefu kabisa inaweza kufutwa kwa muda mfupi zaidi kuliko ule ambao ilikuwa imepatikana. Ni lazima kwanza kabisa kwamba tunapaswa tuelewe zile kanuni za kawaida zinazotawala mwili wa mwanadamu. Baada ya hapo tujaribu kuelewa nafsi zetu wenyewe kwa kiasi kinachowezekana na tuone ni tabia na sifa gani zinazohitaji kubadilishwa, na ni zipi zinazohitaji kuendelezwa. Tunapaswa kujua hasa ni uwezo gani makhsusi tulionao sisi ambao unaweza kuwa chanzo cha mafanikio yetu. Tutakapokuwa tumefanikiwa katika kufanya uchambuzi huu, ni lazima tujivishe sifa za umadhubuti na subira na tulifanye ni lengo kwamba isipokuwa mpaka pale tutakapokuwa tumejibadilisha kwenye zile tabia tunazozitaka, hatuwezi tukaacha 200

11:28 AM

Page 200


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio mapambano na juhudi zetu. Ni dhahiri kwamba juhudi na dhamira ni mambo muhimu katika kufuta na kuondoa zile tabia na desturi ambazo zimeota mizizi ndani ya mwanadamu. Hata hivyo, ni ukweli unaokubalika kwamba, endapo mtu anaanza kazi kwa kudhamiria hasa na kuwa na subira katika hilo hana budi kufanikiwa.

UIMARA KATIKA SHIDA Kila mtu hukutana na matatizo na shida katika maisha ambazo haziwezi zikaondosheka bila subira na ustahamilivu. Hivyo kwa watu wenye sifa ya ustahamilivu, ni rahisi kwao kuyashinda matatizo na wanaweza kuvishinda vikwazo (wanavyokumbana navyo) katika njia yao. Qur’ani Tukufu inawashauri watu kwamba katika hali ngumu na za shida wanapaswa kutafuta msaada kwa subira, ustahamilivu na sala. Inasema:

“Enyi mlioamini, ombeni msaada kwa subira na Sala; hakika Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wenye subira.” – (Suratul Baqarah, 2:153). Ustahamilivu na kutafuta msaada ni mambo muhimu kwa sababu mwanaadamu hawezi akatatua matatizo ya maisha peke yake. Na kwa kuwa hakuna msaidizi halisi wa mwanaadamu isipokuwa Mwenyezi Mungu, msaada unapaswa kuombwa Kwake peke Yake na hupatikana kwa ustahamilivu, subira na kumkumbuka Mwenyezi Mungu ambako si chochote isipokuwa sala. Kwa kweli, hivi (vitu) viwili – subira na Sala ni njia bora kabisa za kuyashinda matatizo, kwa sababu subira na ustahamilivu 201

11:28 AM

Page 201


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio huyapunguza matatizo makubwa na kuyafanya kuwa madogo na mtu kuelekeza fikra zake kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kutafuta hifadhi Kwake huamsha nguvu za imani ndani ya mtu a humwambia kuwa wakati wa shida hayupo bila ulinzi na (kwamba) ana usaidizi imara – yaani usaidizi wa Mwenyezi Mungu Mtukufu.” (Allama Tabatabai, Tafsir alMizan, Juz. 1 uk. 152). Imam Ali (a.s.) amesema: “Vaa nguo ya subira na imani, kwani hili hulinda katika mafanikio na shida.” (Ghurarul Hikam). “Maisha ya mwanaadamu yana hali mbili. Wakati fulani kuna shida na taabu na wakati mwingine kuna amani na raha. Wakati fulani mwanaadamu amezama katika baraka na wakati mwingine huwa amezamishwa katika taabu. Ikiwa muda umekuwa katili kwa mtu muongofu na mwenye busara anaweza kuwa mstahamilivu na mwenye subira. Nikipatwa na taabu nitabakia kuwa imara na thabiti kama jabali.” (Imam Ali (a.s.). Kama historia inavyotuambia kuwa Imam Ali (a.s.) alilazimika kukabiliana na matatizo makubwa katika maisha yake yote, kwa sababu tangu alipokuwa na umri wa miaka kumi alipokusudia kuutumikia Uislamu na kumtumikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), hadi katika dakika ya mwisho ya maisha yake, alikabiliana na maelfu ya matatizo na hatari na alibakia imara na mstahamilivu katika kila tukio. Katika siku aliyolala katika kitanda cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) – Mtume alihama katika usiku ule kutoka Makka kwenda Madina. Katika siku aliyopewa jukumu la kuhakikisha usalama wa wanawake wa Kiislamu aliwasindikiza kwa usalama mpaka Madina. Katika siku aliyopigana na maadui wa kikuraishi katika vita vya Badr aliua wapiganaji wengi wa upande wa adui.

202

11:28 AM

Page 202


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Katika siku ambayo katika vita vya Uhud aliachwa peke yake amlinde Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na alipata majeraha yapatayo tisini kutokana na kupigana na adui – alipata sifa ya kipekee kuwa hakuna bingwa isipokuwa Ali na hakuna upanga isipokuwa Zulfaqar.” Katika siku ya vita vya Khandaq alipopigana dhidi ya Amr bin Abd Wadd – alinusuru Uislamu dhidi ya kuangamia katika kipindi hicho kigumu. Katika siku ya vita vya Khaybar aliingia uwanja wa vita baada ya Uislamu kuwa umeshindwa mfululizo (katika uwanja wa vita) kutokana na kutelekezwa na baadhi ya Waislamu wa uongo – aliteka ngome imara za Wayahudi. Siku alipokwenda Makka (kabla ya kutekwa kwa mji) kwa amri ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwenda kuwasomea Suratul Ba’rat (Tauba) – alitekeleza majukumu yake katika mazingira yaliyokuwa yamezugukwa na hatari kubwa kabisa. Na siku ilipopangwa njama katika ukumbi wa Saqifa Bani Sa’ida baada ya kufariki kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na Ukhalifa uliokuwa ni haki ya dhahiri ya Imam Ali (a.s.) uliporwa! Na siku Fadak, (shamba) lililokuwa linamilikiwa kihalali na mke wake, Bibi Fatima Zahara (a.s.), liliponyang’anywa kutoka kwake bila haki na sababu yoyote ya msingi. Na siku Aisha, alipoanzisha vita vya Ngamia kinyume na maelekezo ya Qur’ani dhidi ya Imam Ali (a.s.). Na siku Muawiya alipoanzisha vita vya Siffin dhidi ya Imam Ali (a.s.). Na siku suala la suluhu lilipoibuliwa dhidi ya ridhaa na ruhusa yake.

203

11:28 AM

Page 203


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Na siku Khawarij wa Nahrawar walipoasi dhidi yake na wakaanzisha maandalizi ya vita vya Nahrawan. Na katika matukio megine mengi amabpo Imam Ali (a.s.) alikumbana na matatizo na shida kubwa lakini alibakia kuwa madhubuti kama jabali na alitekeleza majukumu yake aliyopewa na Mwenyezi Mungu. Katika moja ya hotuba zake iitwayo Shishiqiyya (Taz. Nahjul-Balaghah – Hotuba ya 7, 15P 1984), Imam Ali (a.s.) anadokeza juu ya baadhi ya shida alizopata baada ya kufariki kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na anazugumzia juu ya subira na uvumilivu wake. Anasema: (Naapa) kwa Mwenyezi Mungu kwamba mtu yule aliupokonya ukhalifa kana kwamba ilikuwa nishani ambayo angewza kuivaa, ingawa alijua vizuri kuwa mimi ndiye nilikuwa khalifa mstahiki kama mhimili wa mashine/jiwe la kusagia (ambao uzungukaji wake huutegemea). Ubora wa nafasi yangu miongoni mwa watu wale ulikuwa kwamba nilikuwa kama chemchem aliyokuwa ikitirika hekima na hakuna ambaye angeweza kunifikia katika elimu yangu. Lakini nililazimika kustahamili upokonywaji huu na nikalipa kisogo balaa hili. Nilikuwa katika wakati mgumu. Nilikuwa na mambo mawili ya kuchagua mbele yangu; ama kupigania haki yangu bila msaada wa waungaji mkono, au kustahamili shida hii; kuvumilia kulikuwa kunaelekea kuwa muda mrefu na wa huzuni kiasi kwamba katika kipindi hiki vijana wangekuwa wazee, wazee wangepoteza nguvu zao na waumini wangemaliza siku zao bila mafanikio wakijaribu kuboresha hali zao. Baada ya kutafakari kwa kina, nilifikia hitimisho kwamba uamuzi wa busara zaidi kwangu ilikuwa ni kuikabili balaa kwa subira na ujasiri. Hivyo nilivumilia yote kwa subira, ingawa fikra ya kupokonywa haki yangu ya halali ilikuwa inaniuma na kunihuzunisha sana.

204

11:28 AM

Page 204


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Mwishowe Khalifa wa kwanza alikufa, lakini alipokuwa anakufa alimteua mtu mwingine kuwa Khalifa. (Hapa Imam Ali (a.s.) ananukuu ubeti wa mshairi, ambapo mshairi A’sha Hamdani analinganisha siku alizokuwa anaishi maisha mazuri, ya amani na ndugu yake, na tena pale ilipombidi akabiliane na matatizo peke yake. “Siku zangu sasa zimepita juu ya mgongo wa ngamia (katika shida) lakini kuna siku (za raha) ambapo nilifurahia kuwa na usuhuba na ndugu wa Jabir, Hayyan.” Haishangazi kwamba wakati wa uhai wake, Khalifa wa kwanza alikuwa akihitaji sana msaada wa wengine ili kufidia dosari na mapungufu na kuficha makosa na udhaifu wake, lakini wakati wa kifo chake alijifikiria kuwa mwenye hekima ya kutosha kuweka na kuteua mtu atakayeshika kazi zake ambazo yeye mwenyewe alikuwa ameshindwa kabisa. Kwa ufidhuli na ukosa maadili kabisa yeye na mrithi wake, katika zamu yake, walipora na kuteka nyara mali ya umma na kuiacha Dola katika hali ya kuumia vibaya sana kiasi kwamba kupita kwa wakati kulikuwa kunaongeza kukuza jeraha hilo. Ilikuwa takriban haiwezekani kuyaondoa madhara hayo. Na hatari ya kurudiwa tena na tena kwa unyonyaji huo wa kifidhuli ilikuwa dhahiri wazi kabisa. Lakini kuliendeshwa kwa sura bandia ya ‘sheria na taratibu’ na visingizio vingi visivyo na maana vikatolewa kuhalalisha majivuno yasiyo ya kidini na machafu na mengine mengi zaidi yalirudiwa baadae. Hivyo hali ilifikishwa kwenye kiwango cha juu kiasi kwamba kila aliyechukua hatamu za uongozi wa Dola au ukhalifa alikuwa katika hali ngumu ya kupanda ngamia jike mkaidi asiyefunzwa; kama alipotaka kumdhibiti mnyama huyo alizivuta hatamu zake kwa nguvu, angechana na kujeruhi pua zake, na kama alimruhusu kutembea kwa uhuru, mnyama huyo angekimbia pamoja na mpandaji wake na kujitosa kwenye maangamizi. 205

11:28 AM

Page 205


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio Naapa Wallahi kwamba watu walipotoshwa na wakakengeuka; waliikosa njia dini iliyonyooka. Lakini kwa kuyakubali yasiyoepukika bila kulaumu na kwa kukubali nilistahimili kile kipindi kirefu na chenye machungu cha uharibikaji wa haki za binadamu na dini, mpaka yule mtu wa pili naye akafariki; lakini kabla hajafa aliliacha suala la ukhalifa kwenye uamuzi wa kamati na alifikiria vile vile kuwa mimi naweza kuwa kwenye jopo la kamati hiyo (kwa sababu yeye mwenyewe alinichagua). Ewe Allah! Mimi nilikuwa na nini cha kufanya na kamati hii teule (sikuwa na chochote cha kufanana na mmojawapo yoyote wa wajumbe wake). Kwani sikuwa kamwe na wasiwasi juu ya ubora wangu uliotia fora pale unapolinganishwa na wa kwanza kwamba nikubali kuwa mmoja wa kundi la watu duni kwa umbali zaidi kwake yeye. Lakini kwa faida ya wanadamu na dini mimi nilijiunga na kamati hii teule. Ilinibidi kujishusha mwenyewe hadi kwenye kiwango chao, ili kudai haki zangu tu kutoka kwao kama nilivyokuwa nimefanya katika vipindi vya wale ambao walikuwa wabora kuliko wao. Mmoja wa wajumbe wa kamati hii aligeuka dhidi yangu kwa sababu ya chuki yake (kwa hili Imam alimaanisha ama Sa’ad au Talha), Mwingine (yaani Abdul Rahman bin Awf) alikuwa pia ameelekea ule upande mwingine kwa sababu ya dhahiri ya udugu, mbali na sababu nyingine chache ambazo dunia ilikuja kuzijua baadae (alikuwa shemejie khalifa Uthman). Hatimae wa tatu akachukua ukhalifa kana kwamba ulikuwa ni uwanja wa kibinafsi wa malisho ya mifugo, na kwa matumbo yaliyofura, yeye na watu wa ule ukoo wake (Bani Umayyah) wakaanza kupora mali ya ulimwengu wa Kiislam kwa njia ile ile ya kizembe na kilafi kama inayomuanisha ngamia pale anapokula nyasi za mavuno. Hata hivyo, mtu huyu alikutana na kifo asichokitarajia. Ulafi wa ukoo wake ulikuwa ndio chanzo na sababu ya mwisho wake mbaya. Baada ya kifo chake watu walinizonga mimi wakiniomba niuchukue huo ukhalifa. Walikusanyika kwa wingi sana na walikuwa na shauku ya 206

11:28 AM

Page 206


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio kuonyesha uaminifu wao kiasi kwamba wanangu wote Hasan na Husein karibu wakanyangwe na nguo yangu ilichanwa. Walikuwa wakiniangukia ili nikubali utawala na uongozi wao. Ningekataa ombi lao lakini nilihofia kwamba kwa kukataa kwangu wangekuja kuwa mbali kabisa na ukweli na dini. Nilipokubali uongozi wao na kuwafanya waifuate njia ya Mwenyezi Mungu - njia ile ile kama Mtume wa Allah (s.a.w.w.) aliyowafundisha kuifuata, wao waliasi. Kundi moja (Ummul-Mu’minin Aisha) likavunja kiapo cha utii; na kundi la pili (Khawariji) likawa lenye kuasi dini na kundi la tatu likatwaa njia potovu kabisa na likitamani mamlaka na mali ambavyo ni sehemu ya utawala kama huo, wakaanza kuwaonea na kuwagandamiza wenye shida Makundi yote matatu yalifanya kana kwamba hayajawahi kusikia kamwe Qur’ani ikisema, Pepo ni kwa ajili ya wale ambao hawafanyi ufisadi wala kuwaonea wanadamu: amani ya kudumu na furaha ni kwa ajili ya wale wanaoisha maisha ya kiuchamungu. Wallahi naapa kwamba wao walifanywa wayasikie maneno haya ya Mwenyezi Mungu kwa ukariri na maana yake ilielezwa kwao kwa uwazi kabisa. Lakini njia ovu za maisha ziliwapumbaza machoni na anasa zake, mbwembwe na shamrashamra zake, na pia mamlaka yake na mali viliwavutia mno. Naapa kwa Muumba wa ulimwengu huu kwamba hawakuwa wameapa kiapo kisicho na masharti kwangu; kama wasingeonyesha shukurani ya kina katika kukubali kwangu utawala wao; uwepo wa Ansari na wenye kuunga mkono usingefanya iwe lazima kwangu kuihami dini; na kama Mwenyezi Mungu asingechukua ahadi kwa wenye elimu kuzuia maisha ya anasa na uovu ya madhalimu na wakandamizaji na vile vile kujaribu kupunguza makali ya umasikini na njaa ya wale wanaodhulumiwa na kunyanyaswa; na kama asingefanya ni wajibu juu yao kuzirudisha haki za wanyonge kutoka kwa wenye nguvu na waonevu wenye uwezo mkubwa, ningekuwa hata sasa hivi nimeacha utawala wa Dola hii kama nilivyofanya 207

11:28 AM

Page 207


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio hapo kabla na ningeiacha itumbukie kwenye utawala huria na vurugu. Hapo mngeona kwamba machoni kwangu mimi, mvuto wa maisha ya kiovu ya dunia yenu hii ni sawa na chafya ya mbuzi.” Hii ndio mifano michache ya subira na uimara wa Amirul-Mu’minin, Imam Ali (a.s.), kama alivyozieleza yeye mwenyewe na ambamo hamna utiachumvi hata kidogo ndani yake. Uchunguzi wa historia ya maisha ya Imam Ali (a.s.) unamfundisha mtu somo la subira na umadhubuti ambao mfano wake ameuwekea msingi yeye mwenyewe. (Tazama kitabu: Sauti ya Uadilifu wa Mwanadamu - AU The Voice of Human Justice ISP 1982) Imam Ali (a.s.) amesema: “Mtu aliyejaaliwa na tabia ya subira na umadhubuti, huyo atafanikiwa.” (Ghurarul-Hikam) Maisha ya watu mashuhuri katika historia mara zote yamebarikiwa kwa subira na ustahamilivu katika shida na matatizo kiasi kwamba tunaweza tukasema kwamba subira na ustahamilivu vilikuwa ni vitu vya msingi katika maisha yao kwa maana kwamba hakuna hata mmoja aliyefanikiwa kupata ukubwa na utukufu bila kupata shida na matatizo. Anushirwan, Mfalme Jumhair na alimfunga mikono na miguu ya mrefu ulipita na mtu kubwa.

wa Sasania, alichukizwa na waziri wake Buzar katika chumba chenye giza. Pia aliamuru kwamba waziri ifungwe kwa minyororo ya chuma. Muda huyu mkubwa alibaki gerezani na akapata shida

Siku moja Anushirwan alituma mtu kwenda kuona hali yake na kuona ni athari gani juu ya hili ngumu ilikuwepo kwenye hamasa yake. Mtu huyo alikutana na Bazar Jumhair gerezani na kinyume na matarajio yake, alimkuta akiwa imara kiroho na akiwa na furaha kabisa na akiwa ameridhika moyoni. Kwa hiyo, alisema kwa mshangao: “Ewe Mtukufu! Licha ya 208

11:28 AM

Page 208


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio mazingira yasiyofaa na hali yenye majaribu unayoishi nayo nakuona una furaha kabisa, una amani na umeridhika. Ni nini sababu ya hili?” Buzar Jumhaira akasema: “Nimeandaa dawa inayoundwa na vitu sita: (i) Kumtegemea Mwenyezi Mungu Mtukufu (ii) Mtu hawezi kuwepa majaaliwa (ii) Subira na ustahamilivu (iv) Nisipochunga subira, ni kitu gani kingine nitafanya? Na siko tayari tuharakisha kuangamia kwangu kwa pupa na huzuni (v) Hali ngumu na zenye majaribu kuliko hali yangu ya sasa pia zipo na (vi) Mtu anaweza kutarajia nusura kwa kupita kwa wakati. Maneno ya busara ya Buzar Jumhair yalifikishwa kwa Anushirwan na pia alijulishwa juu ya hali yake. Kisha alimwachia kutoka gerezani na kumpa fadhila nyingi juu yake (Daastaanhaa-i Tarikhi, Safinatul Bihar, Taz. Sabr - subira).

HITIMISHO Tunatoa hitimisho lifuatalo kutokana na yaliyosemwa hapo juu. • Uimara na ustahamilivu ni siri ya mafanikio katika kila jambo: • Kusisitiza kudumu katika jitihada katika kufikia malengo maovu huu ni ukaidi na sio umadhubuti. • Uimara unaendana na upole na sio ukali. • Uimara wenye thamani zaidi ni ule ulio katika njia ya Mwenyezi Mungu na mafanikio ya kiroho. • Kuyasoma maisha ya viongozi wa Uislamu na kunufaika na semi zao ni njia bora zaidi ya kupata umadhubuti. 209

11:28 AM

Page 209


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio

Umadhubuti ni somo la mwisho la kitabu hiki kwa sababu kwa kusema kweli subira na ustahamilivu imekuwa ndio mtindo wa maisha ya Mitume na hii ni misingi ya maadili ya ubinadamu. Ni kwa kupitia sifa hizi kwamba mwanaadamu anaweza kulinda imani yake na kupata furaha na mafanikio katika dunia zote mbili: Lengo la kujadili kwetu nukta hii ni kwamba: • Tunapaswa kuimarisha imani zetu juu ya Allah na Mtukufu Mtume (s.a.w.w). • Tunapaswa kuukubali Uislamu, ambao umekuja kama neema ya Tukufu ya Mwenyezi Mungu kwa mwanadamu na ambayo hutoa hakikisho la maendeleo ya mwanaadamu na mafanikio, iko karibu zaidi na moyo wetu na kwa amali zetu tunapaswa kuthibitisha kuwa sisi ni wafuasi wake wa kweli na kuueneza kwa kauli na matendo yetu. • Tunapaswa tudhamirie kwa dhati kuwa tutaueneza Uislamu katika ulimwengu wote, na katika jamii yetu tunapaswa kuuimarisha katika muundo wake halisi kwa njia zote. • Tunapaswa tudhamirie kufanya kazi kwa ajili ya ukweli na uadilifu na kuziunga mkono kanuni za Uislamu kwa ajili ya umoja wa Waislamu bila upendeleo na ufinyu wa akili. • Tunapaswa tudhamirie kuwakomboa, wanyonge, wadhaifu na wanaokandamizwa sio katika jamii au nchi yetu tu bali katika dunia nzima na kwa lengo hili tungepigana na majeshi maovu na watawala madhalimu mpaka katika tone la mwisho la damu yetu. • Tunapaswa tudhamirie kwamba kamwe hatutawaruhusu makafiri, wanafiki na madikteta, ambao ni waislamu kwa majina tu au kundi lolote la watu hao, kutawala na kulinyonya taifa lolote la kiislamu au kuliingiza 210

11:28 AM

Page 210


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio katika utawala wao wa kikoloni. Kwa kifupi tunapaswa tudhamirie kwamba kwa baraka za Uislamu tutajitahidi kusimamisha uadilifu, haki, usawa na uhuru na kwamba hatutamsujudia yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba hatutavumilia utawala wowote wa kigeni. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: “Kwa hakika wale wanaosema: “Mola wetu ni Mwenyezi Mungu,”

kisha wakaendelea kwa kudumu wastahamilivu, watashukiwa na Malaika .....” – (Suratul Haa Mym Sajdah, 41:30). Tunamuomba Mwenyezi Mungu awe Msaidizi wetu.

211

11:28 AM

Page 211


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION: 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24. 25.

Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thalathini Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudharr Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur'an na Hadithi Elimu ya Nafsi Yajue Madhehebu ya Shia 212

11:28 AM

Page 212


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio 26. 27. 28. 29. 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52. 53. 54. 55. 56.

Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu Al-Wahda Ponyo kutoka katika Qur'an. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii Mashukio ya Akhera Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyeezi Mungu na sifa zake Amateka Na Aba'Khalifa Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana. Upendo katika Ukristo na Uislamu Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya Kupaka juu ya khofu Kukusanya swala mbili Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kusujudu juu ya udongo Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) Tarawehe Malumbano baina ya Sunni na Shia Kupunguza Swala safarini Kufungua safarini Umaasumu wa Manabii Qur’an inatoa changamoto as-Salaatu Khayrun Mina -'n Nawm Uadilifu wa Masahaba Dua e Kumayl 213

7/16/2011

11:28 AM

Page 213


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio 57. 58. 59. 60. 61. 62. 63. 64. 65. 66. 67. 68. 69. 70. 71. 72. 73. 74. 75. 76. 77. 78. 79. 80. 81. 82. 83. 84. 85.

Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mitume Muhammad (s) Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili Kuzuru Makaburi Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita Tujifunze Misingi Ya Dini Sala ni Nguzo ya Dini Mikesha Ya Peshawar Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliyonyooka Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake Liqaa-u-llaah Muhammad (s) Mtume wa Allah Amani na Jihadi Katika Uislamu Uislamu Ulienea Vipi? Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) Urejeo (al-Raja’a ) Mazingira Utokezo (al - Badau) Sadaka yenye kuendelea 214

11:28 AM

Page 214


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio 86. 87. 88. 89. 90. 91. 92. 93. 94. 95.

Msahafu wa Imam Ali Uislamu na dhana Mtoto mwema Adabu za Sokoni Johari za hekima kwa vijana Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu Tawasali Imam Mahdi katika Usunni na Ushia

96.

Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu

97.

Hukumu ya kujenga juu ya makaburi

98.

Swala ya maiti na kumlilia maiti

99.

Shiya na Hadithi (kinyarwanda)

100.

Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu

101.

Hadithi ya Thaqalain

102

Fatima al-Zahra

103.

Tabaruku

104.

Sunan an-Nabii

105.

Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza)

106.

Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili)

107.

Mahdi katika sunna

108.

Kusalia Nabii (s.a.w)

109.

Ujumbe -Sehemu ya Kwanza

110.

Ujumbe - Sehemu ya Pili

111.

Ujumbe - Sehemu ya Tatu

112.

Ujumbe - Sehemu ya Nne 215

7/16/2011

11:28 AM

Page 215


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio 113.

Ngano ya kwamba Qur’ani imebadilishwa

114.

Iduwa ya Kumayili

115.

Maarifa ya Kiislamu.

116.

Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza

117.

Ukweli uliopotea sehemu ya Pili

118.

Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu

119.

Ukweli uliopotea sehmu ya Nne

120.

Ukweli uliopotea sehmu ya Tano

121.

Johari zenye hekima kwa vijana

122.

Safari ya kuifuata Nuru

123.

Idil Ghadiri

124.

Myahudi wa Kimataifa

125.

Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi

126.

Visa vya kweli sehemu ya Kwanza

127.

Visa vya kweli sehemu ya Pili

128.

Muhadhara wa Maulamaa

129.

Mwanadamu na Mustakabali wake

130.

Imam Ali binamu ya Mtume Sehemu ya Kwanza

131.

Imam Ali binamu ya Mtume Sehemu ya Pili

132.

Khairul Bariyyah

133.

Uislamu na mafunzo ya kimalezi

134.

Vijana ni Hazina ya Uislamu.

135.

Yafaayo kijamii

136.

Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu

137.

Taqiyya

138.

Vikao vya furaha 216

7/16/2011

11:28 AM

Page 216


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

Uislamu na Mazingatio 139.

Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje?

140.

Uislamu na Mazingatio Sehemu ya Kwanza

141.

Uislamu na Mazingatio Sehemu ya Pili

142.

Azadari-Kuhuzunika na Kuomboleza

143.

Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah

144.

Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu

145.

Kuonekana kwa Allah

146.

Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza)

147.

Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili)

148.

Ndugu na Jirani

149.

Ushia ndani ya Usunni

150.

Maswali na Majibu

217

7/16/2011

11:28 AM

Page 217


Uislamu na mazingatio Sehemu ya Pili

M.Ramadhani & Lubumba Final.qxd

7/16/2011

Uislamu na Mazingatio

BACK COVER Uislamu huyachukulia kwa mazingatio mahitaji yote ya mwanadamu. Mwongozo wake ni kwa ajili ya zama zote na sehemu zote. Mtu akiyasoma mafundisho ya Uislamu kwa undani, itamdhihirikia waziwazi kabisa kuwa Uislamu ni dini bora kabisa na kwamba pale mtu anapopata elimu na umaizi hujinyenyekeza kwa Mwenyezi Mungu kwa kusilimu na kuifuata dini hii adhimu, dini ya Uislamu. Hivyo, mtu aliyeelimika akajaaliwa kuwa mwenye elimu na busara ana nafasi bora zaidi ya kuyaelewa mafundisho ya Uislamu. Uislamu ni dini yenye kujitosheleza. Ni chanzo cha riziki ambayo hutoa uhakikisho wa kujitosheleza na hutoa njia na mbinu za mafanikio na wokovu wa mwanadamu. Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info

218

11:28 AM

Page 218


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.