Mazungumzo katika dini, utamaduni na jamii

Page 1

Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii ‫أخاديث في الذين والثلافت وإلاجخماع‬

Kimeandikwa na: Sheikh Hasan Musa as-Saffar

Kimetarujumiwa na: Abdul Karim Juma Nkusui


‫جشجمت‬

‫أخاديث في الذين والثلافت وإلاجخماع‬

‫جأ ليف‬ ‫الشيخ خعن بن مىس ى الصفاس‬

‫من اللغت الػشبيت الى اللغت العىاخليت‬


©Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 – 9987 – 17 – 001 –2 Kimeandikwa na: Sheikh Hasan Musa as-Saffar Kimetarujumiwa na: Ustadh Abdul-Karim Juma Nkusui Kimehaririwa na: Ustadh Hemedi Lubumba Kimesomwa Prufu na: Al-Haji Ramadhani S. K. Shemahimbo Kimepitiwa na: Al Haji Mujahid Rashid Kimepangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation Tole la kwanza: Machi, 2018 Nakala: 2,000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Al-Itrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.alitrah.info Vitabu mtandaoni: www.alitrah.info/ebooks/ ILI KUSOMA QUR‟ANI MUBASHARA KWA NJIA YA MTANDAO, TEMBELEA www.somaquran.com


YALIYOMO Dibaji ………………………………………………………. Neno la Mchapishaji………………………………………... Utangulizi………………………………………………….. Sehemu ya Kwanza………………………………………… Mazungumzo ya Kwanza…………………………………...

12 13 15 20 20

Katika maisha ya Familia yenye Mafanikio

25

Kisimamo katika Hadithi ya Kisai:…………………………. Kuchunga haki ndani ya familia:…………………………… Mafanikio katika mahusiano ya kijamii:…………………… Mwanadamu baina ya mbinyo wa kimada na utukufu wa kiroho:……………………………………………………….. Kwanza: Baina ya matamanio na akili: …………………… Pili: Baina ya ubinafsi na utukufu:…………………………. Tatu: Baina ya ufinyu na maadili:………………………….

Mwezi wa Rajabu ni msimu wa kiroho: Kwanza: Saumu:……………………………………………. Pili: Umra:…………………………………………………… Tatu: Swala, dua na nyuradi:………………………………. Nne: Sadaka:…………………………………………………

Muamala wa Kibinadamu katika Sira ya Imamu Ali : Maji ni haki ya wote:………………………………………... Hata mhaini ana haki yake:………………………………… Kuzuia kutoa adhabu:………………………………………. Kumfanyia Wema Mkosaji:………………………………… Kusamehe kosa:……………………………………………..

28 30 34 41 42 43 43 44 45 46 48 49 50 51 53 55 56 57


Kukataza maovu ni Huruma na kufanya Marekebisho Kwanza: Kujali Maslahi ya Mwanadamu na Faida Zake:… Pili: Kuanza na Upendo wa Kweli kwa Mwanadamu:……… Tatu: Kuchunga Hali ya Jumla ya Mwanadamu:…………. Anawalingania waasi:………………………………………..

Ujumbe Wa Manabii Imani Na Utekelezaji Kwanza: Haja ya Kupata Maarifa:………………………… Pili: Haja ya Kijamii:………………………………………... Tatu: Haja ya Kitabia:………………………………………. Watu wa Mada na Utekelezaji wa Sharia:………………….

Upande wa Kijamii katika Maisha ya Imamu Husein  Upande wa Kijamii Katika Maisha ya Imamu: …………… Uhudhuriaji wa Kijamii:…………………………………….. Mfano wa Kitabia: ………………………………………….. Kuzingatia sehemu za madhaifu katika jamii:……………..

Imamu Mahdi Baina ya Akili na Nukuu Aina Mbili za Itikadi:………………………………………... Mandhari ya Muujiza: ……………………………………… Baridi na salama kwa Ibrahimu:……………………………. Amezaliwa Bila ya Baba: …………………………………… Israi na Miraji:……………………………………………….. Imamu Mahdi:………………………………………………. Hakuna kushabikia wala kukanusha:……………………….

Uchaguzi wa Mume baina ya Binti na Watu Wake Mwanamke thayibu (mtu mzima):…………………………. Binti bikra:…………………………………………………... Hekima ya idhini ya walii:………………………………….. Kutumia haki vibaya:……………………………………….

58 61 62 64 67 69 70 72 73 74 78 79 80 83 85 88 89 90 91 92 92 93 97 98 99 100 101 103


Mwezi wa Ramadhani na Ada za Kimakosa Hakuna nafasi ya uvivu na uzembe:………………………. Ni mwezi wa shughuli, harakati na kazi:…………………… Kuondoa matamanio ya chakula:…………………………. Kuenea kwa kisukari na maradhi ya moyo:………………..

Mwanachuoni wa Kidini na kuitakasa Nafsi Maana ya utakaso: ………………………………………… Mwanachuoni wa kidini:……………………………………. Kigezo chema:………………………………………………. Kutoka katika umateka wa tamaa: ……………………….. Usafi wa kuamiliana na watu:……………………………….

Mwezi wa Ramadhani na Kujichunguza Wito Kuhusu Kujichunguza: ……………………………….. Mwezi wa Kutafakari:………………………………………. Pande za Kutafakari: ………………………………………..

106 108 109 111 113 115 117 118 119 120 122 123 125 126 129

Upole wa Imamu Hasan  ni Njia ya Ukunjufu wa 132 Kijamii Maana ya Upole: ……………………………………………. Madhara ya ghadhabu na kukasirika: ……………………… Upole ni manhaji ya kijamii: ……………………………….. Namna gani tutaamiliana na hasira za makundi: ………… Mfumo wa Imamu Hasan: ………………………………….

Lailatul – Qadir: Maamuzi ya Mageuzi na Mabadiliko Falsafa ya Kuomba Maghufira: ……………………………. Maamuzi ya Mageuzi na Mabadiliko: …………………….. Nguvu ya dua: ………………………………………………. Ugumu wa Maamuzi: ……………………………………….

134 136 137 138 138 141 142 145 148 149


Ugomvi wa Kidini, Je una Kisingizio? Ni Iddi ya Upendo na Usafi, na si Iddi ya Kugombana:…… Mazingira ya Ugomvi: ……………………………………… Ugomvi Katika Dini: ………………………………………... Katika Duara la Uislamu: …………………………………… Mtazamo wa Kifikihi: ………………………………………. Iddi ya Upendo na Usafi: ……………………………………

Uswalihina na Kutafakari Kulazimiana baina ya uswalihina na akili: ………………… Uswalihina na kutafakari: ………………………………….. Kutafakari na kufuata uongozi wa kidini: …………………. Rejea ya akili: ……………………………………………….

Wenye Rai na Jukumu la Mjadala 1. Udhaifu wa kujali mambo ya jamii: ……………………… 2. Hisia za kutawala na kutisha: ……………………………. 3. Utengenezaji na hukumu zilizotangulia: …………………. 4. Kibano cha uchochezi kwa watu: ……………………… 5. Sehemu zenye nguvu: …………………………………….

Pengo la Kiroho: Huzuni na Mkanganyiko Mahitaji ya roho: ……………………………………………. Je, maendeleo ya kimaada yanatosha? ……………………. Albert Einstein ni mfano: …………………………………… Kuhusu hali ya jamii ya Kimarekani: ……………………… Somo na zingatio: …………………………………………...

Maendeleo ya Mtu Binafsi na Maendeleo ya Jamii Kuandaa fursa za maendeleo: ……………………………… Athari ya mazingira: ………………………………………... Matokeo na mwongezeko: …………………………………. Nafasi ya jamii: ……………………………………………...

150 150 150 152 155 157 159 161 161 163 165 168 170 173 174 174 177 179 179 182 184 185 186 188 189 190 191 191 192


Nafasi ya mtu binafsi katika maendeleo ya jamii: ………… 193 Namna gani mtu binafsi anachangia katika maendeleo ya jamii yake? ………………………………………………….. 194 Mazingatio ya kijamii: ……………………………………… 198

Jamii yenye Uelewa Uelewa katika mantiki ya Qur‟ani: ………………………… Uelewa wa kijamii: …………………………………………. 1. Uelewa na maarifa: ……………………………………… 2. Muamala mzuri: …………………………………………. 3. Kunufaika kutokana na uwezo………………………….

Mwanzo wa Kutengeneza Upya Mabadiliko ni sifa ya mwanadamu: ……………………….. 4. Ulimwengu ni uboreshaji wenye kuendelea: ……………. Malengo ya kutafakari na kudadisi katika ulimwengu:……. 5. Ushindani wa mabadiliko: ………………………………. 6. Kukabiliana na changamoto: ……………………………. 7. Uislamu: Ni Daawa ya Kujadidisha: …………………….

Roho ya Kujadidisha Alama na sifa za uvumbuzi: ………………………………… 1. Uelewa na matarajio: …………………………………….. 2. Kujiamini: ………………………………………………... 3. Mwanzo wa akili: ………………………………………… 4. Ushujaa na ujasiri: ……………………………………….

Uwezo wa Kuhiji na kupanga Vipaumbele Falsafa ya Hija: ……………………………………………... Sharti la kuweza: ……………………………………………. Kupanga vipaumbele: ………………………………………. Dharura ya maisha: …………………………………………. Haki za watu: ……………………………………………….. Haki za kisharia: …………………………………………….

198 200 202 204 206 208 209 210 212 215 215 216 216 218 221 221 223 225 226 228 229 232 233 234 235 236


Kanisa: Historia ya Dhuluma kwa Jina la Dini Msamaha wa Papa: …………………………………………. Ubabe wa ugomvi wa kimadhehebu:………………………... Ugaidi wa kifikra: …………………………………………... Ukandamizaji na ukoloni: ………………………………….. Somo na Mazingatio: ………………………………………..

Uimamu Baina ya Tamko na Shura Kwa nini kuwepo mazungumzo juu ya Uimamu? ………… Nabii na Mustakabala wa Daawa: ………………………… Shura: ……………………………………………………….. Tamko na kuteua: ……………………………………………

Ashura: Uelewa Na Upeo Utajiri wa kimaanawi: ………………………………………. Msimu wa Muharam: ………………………………………. 1. Kuimarisha Uchamungu: ………………………………… 2. Ustawishaji wa kijamii: …………………………………... 3. Mafunzo ya Ashura: ……………………………………… 4. Kujenga umoja wa kitaifa na Kiislamu:………………….

Semina Nafasi ya fikra ya Kishi‟ah katika majadiliano ya Kiislamu.. Kumbukumbu ya Sheikh Abdul-Hamid al-Aliyi ……………

Makala Fikra ya Kiislamu ina haja ya kujadidishwa katika kila zama. Majadiliano na ufuatiliaji: Ayaad Sharikh: ………………… Kujadidisha kadhia mbili: …………………………………... Majadliano pamoja na wengine: …………………………… Maslahi ya pamoja: …………………………………………. Kuanza na viongozi wa kifikra: ……………………………. Baina ya Qum na Najaf: …………………………………….

237 239 240 241 242 244 244 245 248 249 251 254 256 259 261 261 262 263 265 265 273 279 279 279 280 286 287 289 290


Hawza ya elimu katika Ghuba: …………………………….. Sababu za kielimu na kisiasa: ………………………………. Mwanamke na mwanaume wana nafasi sawa: …………… Mwanamke na siasa: ………………………………………... Kuhusu Muta: ……………………………………………….. Baina ya hazina ya Kisunni na Kishi‟ah: ………………….. Makosa kwa jina la Ashura: ………………………………… Ashura katika upande wa malezi: ………………………….. Vipaumbele vya kazi ya Kiislamu: …………………………

Mwezi Wa Mwenyezi Mungu Mwanzo wa makutano: ……………………………………... Mwezi mwandamo na mkanganyiko wenye kutatiza: ……. Kusimama katika vituo vya zama: ………………………… Ratiba ya Mwezi wa Mwenyezi Mungu: …………………… Vituo vya runinga: ………………………………………….. Kuboresha minasaba: ………………………………………. Safari ya kiroho: …………………………………………….. Saumu mbili katika mwezi wa Mwenyezi Mungu:…………. Kuongezaka mazingira ya kufuata katika minasaba: ……… Mabadiliko katika karne ya ishirini na moja: ……………….

Shi‟ah Na Ulimwengu Mbinyo wa kuiga: …………………………………………... Kiwango cha khatibu na lengo lake: ……………………….. Na jambo la mwisho: ………………………………………..

Maandiko Utangulizi wa kitabu (al-Kisau Fiy Ma‟arifil-UmmatilIslamiyah) …………………………………………………… Utangulizi wa kitabu (Swidiqatu Mariyamu al-Adharau: Muujizatul-Ajiyaali) ………………………………………… Utangulizi wa kitabu “Uqudatul-Haqaarati.”……………….. Utangulizi wa kitabu (Afghanistani: Tarikhuha Rijalaatuha) …………………………………………………

290 291 292 294 294 296 298 299 300 302 302 302 303 304 304 305 306 307 309 310 311 328 328 328 331 331 333 337 341


Kuheshimu Na Kutukuza

346

Utangulizi wa kitabu “Sharihu Shukuk”…………………….. 349 Utangulizi wa kitabu “Mu‟ujamu al-Mualafaati Shiati fiylJazirati al- Arabiyati.” ……………………………………… 351 Utangulizi wa kitabu “Taali ma‟iy linaqiraa”……………….. 357

Risala Kwa Misafara Ya Maombolezo Kuwatangaza Mawalii wa Mwenyezi Mungu………………. Je, tunahitaji propaganda na matangazo? …………………. Tangazo la kidini na msuguano wa ndani: …………………. Matangazo ya ratiba na misimamo: ………………………… Salaamu kwa jarida la al-Murshid………………………….. Maonyesho ya utamaduni hivi sasa katika Mamlaka ……. Upeo mwingine wa kazi ya kidini ………………………….. Jukumu lililozoeleka: ……………………………………….. Kazi zisizo muhimu: ………………………………………... Kazi za kijamii: ……………………………………………... Uzoefu wa ujumbe: …………………………………………. Majukumu muhimu: ………………………………………… Utangulizi wa kitabu “Maa yuriduhu shababu”: Ni ladha na badili………………………………………………………… Mihadarati: Hatari zake na njia za kujikinga nayo.………..

360 364 365 371 372 372 373 379 380 381 382 384 384 388 390


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬

DIBAJI Kitabu hiki ni toleo la Kiswahili la taasisi ya Al Itrah Foundation. Chapisho lake limelenga kukidhi mahitaji ya kiroho ya zama hizi pamoja na Ubongo na fikra zinazokuwa za Muislam. Jitihada kubwa zimefanywa na Taasisi kuweka chapisho hili la Kiswahili katika msingi wa haki na wenye kukubalika katika Uislam. Unaombwa kwa Taadhima ukisome kitabu hiki katika malengo yaliyokusudiwa. Pia Unaombwa kuwasilisha kwetu maoni yako huru juu ya chapisho letu hili, jambo ambalo tutashukuru sana. Kutangaza ujumbe wa Uislam ni kazi ambayo inahitaji ushirikiano wetu sote. Taasisi inakuomba kuungana na kushirikiana kama ilivyoagizwa katika aya ya Qur‟an: (Surat Saba‟ 34:46). Na rehma za Allah ziwe juu yako. Wako katika Uislam Al Itrah Foundation Barua Pepe: alitrah@yahoo.com SMS: +255 778 300 140

12


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬

NENO LA MCHAPISHAJI Kitabu ulichonacho mikononi mwako asili yake ni cha lugha ya Kiarabu kwa jina la, Ahadith fi„d-Din wa „th-Thiqafah wa „lIjtima‟, kilichoandikwa na Sheikh Hasan Musa as-Saffar. Sisi tumekiita kwa Kiswahili, Mazungumzo katika Dini, Utamaduni na Jamii. Kitabu hiki kimekusanya khutba na mihadhara iliyokuwa ikitolewa na Sheikh wetu huyu katika nyakati na sehemu mbalimbali Katika mfululizo wa vitabu vya mwandishi huyu, anahimiza waumini kuishi kwa kufuata mafundisho ya Uislamu ambayo yanagusa kila nyanja ya maisha na kiroho. Katika kitabu hiki anazungumzia juu ya mahusiano kuanzia katika familia, ndugu, jirani, jamii na utamaduni. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni vitu ambavyo havina nafasi tena katika akili za watu. Kutokana na ukweli huu, taasisi yetu ya Al-Itrah imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumini yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili. Tunamshukuru ndugu yetu Abdul Karim Juma Nkusui kwa kazi 13


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

kubwa aliyoifanya ya kukitarjumi kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili; pia na wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Allah awalipe wote malipo mema hapa duniani na kesho Akhera – Amin. Mchapishaji Al-Itrah Foundation

14


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬

UTANGULIZI Allammah, Dr. Sheikh Abdil Fadhil al-Haadiy al-Fadhiliy1 Kitabu hiki kimekusanya mihadhara mbalimbali ya utamaduni wa jumla aliyoitoa Allammah, Mhutubu, Sheikh Hasan Saffar katika siku za Ijumaa, katika msikiti ulioko al-Qatif, ambao yeye ndiye Imam wa swala ya jamaa humo. Na kabla ya kuzungumzia kitabu na mtunzi wake napenda kuashiria katika yale yanayozungumziwa na ambayo ndio anwani ya kitabu, nayo ni MAZUNGUMZO YA IJUMAA,2 huu ni mwonekano wa utamaduni wa Kiarabu uliokuwepo tangu mwanzo wa utunzi na uandishi wa Kiarabu, uliendelea kuchukua sura mbalimbali na kubadilika kadiri sababu na mazingira yalivyohitajia mabadiliko hayo. Kwa kweli hali yake ni sawa na hali za aina zingine za utunzi katika mazingira yetu ya utamaduni wa Kiarabu. Hali hii ndio iliyokuwa inajulikana kwetu kwa jina la IMLA huko mwanzoni mwa ustawi, na jina hili lilitokana na uhalisia wake wa kivitendo ndani ya utamaduni, ambapo mwalimu alikuwa – aghlabu – anaandika mada za imla zake katika karatasi, kisha anaziwasilisha kwa wanafunzi wake ambao wamemzunguka pembezoni mwake kandokando ya mimbari 1

Faqihi na mwanafikra wa Kiislamu kati ya wanachuoni wenye kuchomoza katika sehemu ya Mashariki katika mamlaka ya Saudi Arabia, kati ya waasisi wa harakati za Kiislamu Iraki amesoma katika kitivo cha fiqihi Najaf na chuo kikuu cha Maliki Abdul-Aziz, Jiddah na Chuo Kikuu cha Kiislamu London, na utunzi mwingi katika fiqihi na utamaduni wa Kiislamu baadhi ya vitabu vyake vimechaguliwa kuwa ni mataala wa masomo katika vyuo vingi vya kidini. 2 Anwani ya kitabu iliyopendekezwa kabla ya kutegemea anwani ya sasa.

15


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

yake, na wanafunzi nao wanaandika anayowasomea. Na wakati mwingine mwalimu alikuwa anawasomea kutoka katika maalumati yake, yaani bila ya kutumia karatasi. Na mada ya imla – mwanzoni – ilikuwa inaishia katika hadithi Tukufu, kisha wanachuoni wakaipanua ikawa inajumuisha elimu ya lugha ya Kiarabu, na fasihi yake, elimu ya sharia ya Kiislamu na hukumu zake, mawaidha na hekima, na aina mbalimbali zingine katika historia ya Kiislamu na mengineyo. Na zilizo mashuhuri zaidi katika imla, ni zile zilizopo katika maktaba zetu za Kiarabu: -

Imla za Abu Ali al-Qaaliy Imla za Sharifu al-Murtadhwa Imla za Ibnu al-Haajib na Nah‟wiyah Imla za Abi Saadati Ibnu Shajariy.

Na wakati huo huo, na kwa upande mwingine, hali hii ilikuwa inaitwa Majlisi (kikao), kwa sababu mwanachuoni anawasomea au anahutubia katika kikao cha wakati maalumu, kilichopangwa kwa muda maalumu na sehemu maalumu, na miongoni mwa Majalisi mashuhuri ni: -

Majalisul-Abrari wa Masalikul-Akhiyaar, cha Sheikh Ahmad Rumiy, nazo ni Majlisi mia moja katika kusherehesha hadithi mia moja.

-

Majalisu Thaalab an Nah‟wiy al- Baswariy

-

Majalisu Abi Sahli Naubakhatiy.

Na mada inayotolewa inaweza kupewa majina mawili pamoja, huitwa: Imla na huitwa: Majlisi. kama ilivyo katika yale aliyokuwa anayawasilisha Sheikh Suduqu, ambapo yamekuwa yakijulikana kwa jina la Aamaliy Suduqu (Imla za Sheikh 16


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Suduqu), na wakati huo huo yakijulikana kwa jina la Majalisu Suduqu (Vikao vya Sheikh Suduqu), ambapo ni majlisi mia moja. Na imla aghlabu hutolewa misikitini. Radio zilipoingia katika nchi za Kiarabu na kuanzishwa idhaa za Kiarabu, kulipatikana sambamba na majilisi hizo za misikitini ambazo bado zingalipo hadi leo, vipindi vya idhaa chini ya anwani MAZUNGUMZO. Nayo ni aina ya kuendeleza mwonekano huu wa kiutamaduni. Na walishiriki humo zaidi ya mmoja kati ya Maulamaa wa wakati huo, miongoni mwao ni: -

Dr. Twaha Husein, alikuwa anazungumza kila siku ya Jumatano kwa njia ya Idhaa ya Cairo katika fasihi ya Kiarabu, kisha yakakusanywa mazungumzo yake chini ya anwani MAZUNGUMZO YA JUMATANO, na yakasambazwa katika juzuu tatu, na zikawa ni katika rejea za fasihi ya Kiarabu.

-

Dr. Mahmud Mahdiy al-Baswiir, ambaye alikuwa anazungumza katika idhaa mara moja kwa wiki katika fasihi ya Iraki, katika karne ya kumi na tisa, kwa njia ya idhaa ya Baghdad, kisha mazungumzo yake yakakusanywa na yakaitwa Nahdwatul-Iraq al-Abadiyati Fil-Qarni Tasii Ashara, na yakasambazwa, na leo ni kati ya rejea muhimu ya fasihi ya Iraki katika karne ya kumi na tisa.

-

Na hivi sasa Sheikh Saffar anaongeza katika kazi yake nguvu katika kunyanyua kiwango cha watu wa jamii yake kiutamdani:

-

Majlisi zake za Siku ya Jumamosi katika nyumba yake huko Qatif, nayo ni mkusanyiko wa utamaduni.

-

Mazungumzo yake ya Siku ya Ijumaa, nayo ndiyo haya yaliyoko mbele ya msomaji mpendwa. 17


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Na lengo la kuwasilisha mazungumzo haya ya kila wiki ni kuelimisha na kufikisha ujumbe. Kwa sababu ni jukumu la kila mwenye kubeba fikra kunyanyua kiwango cha jamii kiutamaduni. Na hitimisho ni kwamba hotuba za Ijumaa na mazungumzo ya kila wiki - sawa yawe yale yanayotolewa Ijumaa au katika siku nyingine kati ya siku za wiki – yana nafasi kubwa katika kuinua kiwango cha uelewa kiutamaduni kwa wanajamii, na kuchangia katika kujenga utu wa mtu kiutamaduni na kuongeza hazina ya maarifa yake kiutamaduni. Ama tablighi – na nakusudia tablighi ya dini – ni wajibu muhimu sana kati ya wajibu wa mwanachuoni wa kidini na khatibu wa kidini, kwani kwa njia yake anashawishika Mwislamu kihisia juu ya dini yake, na kunyanyuka katika kiwango cha ujumbe wake katika maisha haya. Na umeshathibitisha uzoefu wa kuelimisha na kutangaza, kwamba mafanikio ya mwenye kufanya hayo yanategemea uwezo wake katika kufungamanisha fikra na uhalisia, na kiwango cha maarifa yake na nafsi za wasikilizaji wake na daraja za uelewa wao kiutamduni. Na haya ndio tunaweza kuyapata - kwa uwazi katika mazungumzo ya kitabu hiki ambacho kipo mbele yetu. Hakika Sheikh Saffar ni kati ya hao wachache ambao wamekusanya baina ya ujumbe wa msikitini na mimbari, kwani amehitimu katika Hawza ya elimu baada ya kukamilisha masomo yake ya elimu ya Kiislamu, na akashughulika na nafasi ya mwanachuoni wa dini katika mji wake wa Qatif. Naye ni kati ya wanaharakati watendaji katika nyanja hii, na 18


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

hususan wale wachache ambao wanakusanya baina ya asili na usasa, na amethibitisha hilo katika uwasilishaji wake mbalimbali. Hakika utayaona wazi haya katika utunzi wake na mihadhara yake. Na anahesabiwa kati ya wenye vipaji kwa hotuba zake, kwani yeye anamiliki ala za kuathiri za mimbari, na ana ala za kupenya kwenye akili za wasikilizaji kwa njia ya kuhutubia hisia zao. Hakika katika mazungumzo yake haya anaisukuma fikra kwa kasi ili kugusa uhalisia wa watu, na kufanya kazi ya kuwabadilisha kwenda kwenye yaliyo bora zaidi. Inafaa nisirefushe katika maelezo, niache mambo kwa msomaji mpendwa, ili aburudike na mazungumzo haya kwa kusoma, kufahamu na kisha kuelewa ili anufaike kwayo na kuwanufaisha wengine. Mwenyezi Mungu azibariki juhudi za ndugu yetu Saffar na ampe elimu zaidi katika huduma hii ya kheri. Hakika Yeye ni Mwenye kutoa taufiki na ndiye Mwenye kukusudiwa. Abdul-Haadiy al-Fadhwily.

19


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

SEHEMU YA KWANZA Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu

ٰ َ َ َ َ ‫ى‬ َ َ َ ّ ُ ‫احخ َعك ِ​ِتِ َوج ك ِذ ُلُ ِبكال ى ِى َكى‬ ‫ىغة ِكت‬ ‫ادع ِإ ٰلى َظ‬ ِ ‫احخىم ِكت واو‬ ِ ‫بيل َسِبكً ِب‬ ِ َ َ َ ُ َ َ َ َ ُ َ َ َ ُ َ ‫خع ُ ِ ى ى‬ َ ‫َأ‬ ِ َ ‫بيل ِ ِهِ َو ُه َى أغل ُ ِباوُخ‬ ‫ذين‬ ِ ‫ن ِإن َسبً هى أغل ِبمن ض ىل غن ظ‬ “Waite kwenye njia ya Mola Wako kwa hekima na mawaidha mazuri na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora. Hakika Mola Wako ndiye anayemjua zaidi aliyepotea njia yake na Yeye ndiye anayewajua zaidi walioongoka.” (Sura An-Nahl; 16:125). Sifa zote njema anastahiki Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu. Ewe Mwenyezi Mungu mteremshie rehema Muhammad hitimisho la Manabii na ukamilisho wa idadi ya Mitume, na Ahali zake wema watwaharifu na Masahaba wake wema.

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬ MAZUNGUMZO YA KWANZA Mazungumzo ya kidini yanabeba jukumu kubwa mbele ya mazingira ambayo jamii ya Kiislamu inaishi. Hiyo ni kwa sababu yana fursa kubwa katika kuathiri na kupenyeza, na yana nafasi kubwa na kiwango cha juu katika kukubalika na kuitikiwa. Ambapo watu wenye kushikamana na dini wanayasikiliza kwa usikivu na unyenyekevu, kama sehemu ya faradhi za ibada na 20


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

shughuli za kidini, kama hali ilivyo katika Swala ya Ijumaa ambayo inatanguliwa na hotuba mbili, na Swala ya Idd ambayo inafuatiwa na hotuba mbili. Ukiongezea na minasaba mingine ya kidini ambayo inakusanya humo waumini wenye kusikiliza kwa masikio yao na wenye kuhamasika kwa nyoyo zao na hisia zao, kwa yale yanayotolewa kwao miongoni mwa mawaidha na miongozo. Lakini angalizo ni kwamba harakati za kuathiri kwa mazungumzo ya kidini katika hali ya jamii ni ndogo kuliko inavyotarajiwa, ukilinganisha na nguvu ya kimaanawi inayomiliki na uwezekano uliopo wa kupenya katika nafsi, na kwa kuangalia hali ya hatari na mazingira nyeti unayoishi nayo umma. Umma unakabiliana na changamoto kubwa katika hali yake ya ndani, na katika upande wa nje, na inatakiwa mazungumzo ya kidini yaamshe nguvu za umma na kusheheni nguvu zake na uwezo wake ili kukabiliana na changamoto hizo za kimaisha. Wakati ambapo sehemu ya kubwa ya hotuba na mazungumzo haina uelewa wa changamoto hizi, na wala haioni kuwa inalengwa katika kukabiliana nazo, na badala ya kuwa ni mhamasishaji wa kuzinduka, aghlabu unafanya kazi ya kuimarisha hali ya kurejea nyuma, kwa kuweka mkazo katika masâ€&#x;ala binafsi ya kiibada, na kukuza vipengele na ufafanuzi katika nyanja za kiitikadi kwa kueneza ikhitilafu, na kushughulika na uchochezi na hamasa za kimadhehebu na makundi. Wakati ambapo mhutubu anasahau mazungumzo kuhusu jukumu la mwanadamu katika kujenga ulimwengu, na yanayomlazimu kati ya juhudi na harakati katika kujua mbinu za maisha na kanuni za mazingira, na anaghafilika kukumbuka nafasi ya umma katika kumshuhudia mwanachuoni, na kutoa mfano wa kisasa 21


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

ulio bora, na kusahau maadili ya msingi katika dini kama vile umoja, uhuru, uadilifu na haki za binadamu. Hii ni kwa upande wa malengo. Ama kuhusu kiwango cha muundo na mbinu za kueleza, aghlabu mazungumzo haya yanatumia njia ya mawaidha ya kuiga, na kutosheka na kusoma nususi za kurithi na ushahidi wa kihistoria bila ya kunufaika na ustawi wa elimu ya binadamu kama vile elimu ya nafsi na elimu ya jamii, na bila ya kutegemea lugha ya takwimu na taarifa za kitafiti, njia ya udadisi, ubainifu na utafiti wa kimedani jambo ambalo linaifanya lugha ya mazungumzo kuwa ni insha ya kukariri katika hali ya kaida na mifano. Na tunapoangalia kwa jicho la mazingatio yale mazungumzo yaliyo katika ushindani wenye nguvu na mkali, katika upande wa mazungumzo mengine ambayo yanamiliki nguvu zaidi, uwezo na uzoefu wa kielimu, teknolojia na fani, hakika hilo linaweka wazi kwetu sababu ya udhaifu na ufinyu wa kuathiri. Kwa hakika wasifu huu unalingana na sehemu kubwa ya mazungumzo ya kidini, lakini sasa hivi kuna mifano yenye kuchanua katika medani ya Kiislamu. Inatoa mazumgumzo yenye uelewa na yaliyofunguka, ambayo athari zake zinaonekana bayana na matokeo yake mazuri yanadhihiri katika kuanzisha harakati za kubadilisha medani ya Kiislamu tukufu, na katika uwepo wa kundi la ujumbe la kiimani kwa ajili ya kuhuisha maadili ya kimsingi na kulinda hali ya umma katika msingi wake. Hakika mabadiliko ya mazungumzo ya kidini ili yawe katika kiwango cha maadili ya kidini yenye kutukuka na ili yatatue changamoto za kileo zinazobana, na ili yaweze kuamsha umma, kuna haja ya kushirikiana na kuongeza juhudi kutoka kwa Marajii na viongozi wa kidini, na sehemu zenye uelewa wenye 22


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

kujali mustakabali wa dini na umma kwa ajili ya kuweka mbinu za miundo ya jumla. Na kila jamii inaweza kuhitaji mahitaji yake binafsi kutokana na baadhi ya hali zake na mazingira yake, na hivyo kuwataka wahusika wenye kujitolea humo kwa ajili ya mambo ya kidini kuboresha fikra zaidi, na kufikia mikakati iliyofanyiwa utafiti, ili kuelekeza mazungumzo katika mazingira yao, kwa kutoa kipaumbele chake na mbinu zake. Na ili yatimie matarajio haya hakika ni juu ya mwenye jukumu katika medani ya maelekezo ya kidini ajitahidi katika kuboresha kiwango cha utekelezaji wake, na aanzie katika sehemu ya kuhisi majukumu katika dini na jamii, na ajue kwa kina changamoto za kileo ili yainuke mazungumzo yake na yapande daraja hadi kwenye upeo unaotakiwa na unaofaa. Na mazungumzo haya ambayo yako mbele ya msomaji, hakika ni tajriba ndogo katika njia hii. Nilikuwa nazingatia kugusa matatizo ya jamii na mambo yake, na kujitahidi katika kutoa yale ambayo yanaweza kuchangia katika kutatua na kutibu, nikienda mbio kuboresha malengo ya mazungumzo na njia zake, kulingana na uwezo wangu na nguvu zangu ndogo. Niliyatoa mazungumzo haya kupitia mimbari ya Ijumaa katika msikiti wa al-Fatih Qatif, mwaka 1420 hijiria, na nilikuwa naandika kila mazungumzo baada ya kuyatoa ili wayapate ndugu zangu waumini, na huenda baadhi ya ndugu watukufu wamenisaidia kuandika baadhi yake kutoka kwenye kanda zilizorekodiwa. Na leo ninapotoa mkusanyiko huu katika kitabu hiki natarajia yapatikane humo ambayo yanamnufaisha msomaji na kuchangia katika kuboresha uzoefu baina ya wenye kuzingatia jambo la mazungumzo ya kidini. 23


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Kama ambavyo hainipiti kuwashukuru ndugu zangu watukufu ambao walishiriki pamoja nami katika kuzitoa juhudi hizi, na hususan ustadhi Dhakir Habil, Ustadhi Mirza al-Khuwailidiy, ambao mara nyingi nimesaidiana nao katika kuandaa mazungumzo na kuhakiki maalumati. Na vilevile Sheikh Husein Suwaileh ambaye amesimamia uchapishaji mazungumzo haya na kuyasambaza, na pia ndugu wengine, Mwenyezi Mungu awalipe wote malipo mema. Namuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu aikubali juhudi hii ndogo na ajaalie humo manufaa na faida na atupe taufiq sote ya kuitumikia dini na umma. Hakika Yeye ndiye mwenye kutoa taufiki, na sifa zote njema anastahiki Mola Mlezi wa walimwengu. Hasan Saffar 10/3/1422 Hijiria - 2/6/2001.

24


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬ KATIKA MAISHA YA FAMILIA YENYE MAFANIKIO Riwaya za kihistoria zinatofautiana kuhusu mwaka wa kuzaliwa Bibi Fatimah Zahra , ilikuwa ni kabla ya utume wa Nabii kwa miaka mitano kama wanavyopokea wengi wa Maulamaa wa Kisunni? Au ni baada ya utume kwa miaka mitano kama wanavyoona Maulamaa wa Kishia? Lakini takriban zinaafikiana katika siku na mwezi, ambapo riwaya nyingi zinasema kwamba kuzaliwa kwake ilikuwa ni tarehe 20 ya mwezi wa JumadulAkhir. Na sisi tunaweza kufikiria kiwango cha furaha ambayo ilijaa moyo wa Mtume wa Mwenyezi Mungu  kwa uzao wa binti yake Zahra . Kwanza: Kwa ukamilifu wa ubinadamu wake na kina cha hisia zake, ni lazima afurahie kwa kuzaliwa mtu mpya katika familia yake. Pili: Kwa yale ambayo Mwenyezi Mungu amemweleza kupitia wahyi miongoni mwa fadhila za mtoto huyu na nafasi yake kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwamba mwendelezo wa ukoo na kizazi chake kitukufu utapatikana kupitia kwake. Tatu: Kwa kuakisi ukarimu wake katika uhai wake na ujio wake mtukufu. Anasema Dr. Muhammad Abduh Yamaniy: Na Mtume  alifurahia kuzaliwa kwake na akamwambia mke wake Khadija: “Ewe Khadija hakika ni mtoto twahara aliyebarikiwa, na kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu atajaalia kizazi changu kwake.” Na kwa sababu hii alikuwa ni mahala pa 25


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

mazingatio ya baba yake na husasan kwamba alikuwa anafanana naye. Amepokea al-Hakim katika Mustadrak kwa sanadi yake kutoka kwa Anas bin Maliki kwamba alisema: “Alikuwa ni mtu anayefanana sana na Mtume wa Mwenyezi Mungu , mweupe anaelemea kwenye wekundu na ana nywele nyeusi.” Na kutoka kwa Ummul-Muuminin Ummu Salama  amesema: “Fatimah binti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu  alikuwa ni mtu anayefanana sana kwa uso na Mtume wa Mwenyezi Mungu .” Kutoka kwa Aisha Ummul-Muuminina  hakika amesema: “Sijaona yeyote katika viumbe vya Mwenyezi Mungu anayefanana sana kwa mazungumzo na maneno na Mtume wa Mwenyezi Mungu kama Fatimah.” Mwenyezi Mungu amridhie na amridhishe. Ilikuwa ni mbegu twahara, na mtoto mkarimu mwema. Bibi mtukufu anayefanana sana na Bwana wa viumbe, na alirithi utukufu kutoka kila pande na akapata utukufu.3 Katika kukumbuka uzao wake mtukufu tunataka kudondoa katika uongofu wa sira yake tukufu yale ambayo yanatuangazia njia ya maisha. Hiyo ni kwa sababu tutajaribu kudondoa sura yenye kuchanua katika upande wa maisha yake ya kifamilia ili tupate kutoka kwake somo na mazingatio, na ili tuendeshe maisha yetu ya kifamilia katika uongofu wake. Hakika familia ndio bembea la kwanza katika malezi ya binadamu, na inabakia kuwa ni ngao yake na kinga yake ambayo inamhami na ambayo anarejea kwayo anapokabiliwa na chamgamoto yoyote au tatizo lolote katika maisha yake. Na kila 3

Yaani: ni Muhammad Abduh, Innahaa Fatwimah Zaharaa, uk: 15 chapa ya kwanza 1996 Darul al- Manaar-Muasasatu uluml- Qur‟ani Dimishiq.

26


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

yanapokuwa mafungamano ya mwanadamu na familia yake ni yenye nguvu na imara ndivyo anavyoweza kuathari katika mazingira yake, na maadili yake yanakuwa ni yenye nguvu zaidi vile vile. Katika familia hii mtoto anajifunza lugha, anajifunza tabia na mwendo, nayo ndio inatengeneza njia ya ulinzi wa kwanza katika shakhsiya ya mwanadamu na matatizo yake, na Qur‟ani tukufu inatia mkazo mazingatio makubwa katika familia wakati muumini anapoomba kwa Mola Wake kumpa familia itakayokuwa ni kitulizo chake.

َ َ ‫َى‬ َ ‫ى‬ ُ َ َ ‫َ ُ ّ ّٰ ُ ى‬ َ ‫غحن َو‬ ٰ َ ‫اجػل ا ِل ُلمخلحن‬ ٍ ‫… سب ا هب ل ا ِمن أصو ِج ا ور ِسيك ِد ا كشة أ‬..” ً ‫إ‬ “‫ماما‬ ِ “…..Mola Wetu! Tupe katika wake zetu na wanetu yaburudishayo macho, na utujaalie tuwe waongozi kwa wenye takua.” (Sura al-Furqan; 25:74.)

Na kuomba kitu kunaakisi raghaba katika kupatikana kwake, na kwenda mbio kwa ajili ya kukipata pamoja na kuomba taufiki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa ajili ya hilo, na msaada Wake katika hilo katika kuondoa vizuizi na vikwazo. (Kiburudisho cha jicho) ama imechukuliwa kwenye neno: (qara) kwa maana ya baridi kwa sababu jicho katika hali ya sururi na furaha linatoka machozi ya baridi, na maana inakuwa: Tujaalie ni wenye sururi wenye kufurahia katika familia zetu hadi tupate humo machozi ya furaha ya baridi kutoka katika macho yetu. Hakika ni kinaya nzuri. Na ama imechukuliwa katika (qara) kwa maana amethibiti na ametulia. Hiyo ni kwa sababu mwanadamu anapotafuta mtu au kitu anageuka kulia na kushoto, na anapopata anachotaka linatulia jicho lake, yaani anaacha kugeuka na kutafuta kwa macho yake, na maana inakuwa: Jaalia nafsi zetu ziwe na utulivu zenye furaha katika hali yetu ya kifamilia ili tusitafute raha wala utulivu katika sehemu nyingine. 27


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Lakini ni mambo yapi yanayosaidia familia kuwa ni kitulizo cha jicho kwa mume na mke? Tukiangalia maisha ya kifamilia ya Bibi Fatimah Zahra tutakuta ni tajriba nzuri, njema kwa ajili ya kuiga na mfano. Yeye ni mfano kamili ambao Uislamu umeutoa kwetu ili tumfuate ili tufikie lengo hili tukufu. Namna gani yalikuwa maisha ya kifamilia ya Bibi Fatimah  na mume wake Imamu Amirul-Muuminina ? Kisimamo katika Hadithi ya Kisai: Inafaa sana tukitaka kupata sura ya familia hiyo tukufu tupate funzo katika tukio mashuhuri lililotokea katika nyumba ya Zahra na nyumba ya Amirul-Muuminina na limepokewa na vitabu vyote vya Waislamu, nalo ni kisa cha Hadithi ya Kisai, ambayo imepokewa katika rejea nyingi, isipokuwa ni kwamba rejea za Ahlulbayti  zimelipokea kwa kirefu kwa shauku yenye manufaa. Na Alhamdulilahi hivi karibuni imetoka fasili nzuri kwa kirefu ya Hadithi ya Kisai na imenyambua hukumu na adabu na makusudio ya ibara zake kwa utunzi wa Marjaa wa dini Imamu Sayyid Muhammad Shiraziy. Fasili hiyo ina kurasa 320 kwa anwani ya Min Fiqhi Zahra. Ukiachilia mbali kwamba hadithi hii inabainisha nafasi ya kizazi kitukufu, pia inawezekana ikawa moja ya sababu iliyopelekea Ahlulbayt  kuwahimiza wafuasi wao kusoma hadithi hiyo ya Kisai na kuisambaza ni kwa sababu hadithi hiyo inanukuu sura ya uhusiano na muamala ndani ya familia tukufu ya Nabii, ambapo tunasoma humo kwamba kila mwanafamilia anapoingia nyumbani anaanza kwa kuwasalimia watu wake. Mtukufu Mtume  anaingia kwa binti yake Zahra, anaanza kwa salamu, na Imam Hasan, naye ni mtoto mdogo anaingia nyumbani anamsalimia mama yake Zahra, na vilevile alifanya hivyo ndugu yake Imamu Husein mdogo kuliko wote alipoingia baada yake, 28


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

na vilevile baba yao alipoingia nyumbani anaanza kumsalimia mke wake Zahra . Kama ambavyo tunasoma katika Hadithi ya Kisai heshima baina ya wanafamilia ambapo Hasan anaomba ruhusa kwa baba yake Mtume wa Mwenyezi Mungu  ili aingie pamoja naye katika shuka, na vivyo hivyo alifanya ndugu yake Husein na baba yao Ali na mama yao Zahra . Katika Hadithi ya Kisai tunasoma kila mmoja katika wanafamilia kutangaza kwake upendo wake na shukrani zake kwa mwanafamilia mwingine, na kuthibitisha umahususi wake ambapo Bibi Fatimah  anawasemesha watoto wake wote kwa kauli yake: “Ewe mwanangu mpendwa na kiburudisho cha jicho langu na tunda la moyo wangu.” Na Husein  anamsemesha babu yake kwa kusema: “Amani iwe juu yako ewe babu yangu, ewe Mteule wa Mwenyezi Mungu.” Na Imamu Ali anamsalimia mke wake Zahra  kwa kusema: “Amani iwe juu yako ewe binti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu.” Naye anamjibu: “Amani iwe juu yako ewe baba Hasan na ewe Amirul-Muuminina.” na maneno mengine mengi yaliyopokewa katika Hadithi ya Kisai yanayoelezea upendo wa kila mmoja kwa mwingine na kuheshimu kwake shakhsiya yake. Na katika Hadithi ya Kisai tunaona thamani ya kukutana na vikao vya familia vya upendo, ambavyo vinajaza nyoyo za wanafamilia mahaba, upole, heshima na kutoa fursa kwao ya kubadilishana hisia na fikra na kuzidisha ushirikiano na mshikamano wa familia. Na imepokewa katika hadithi kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu  kwamba alisema: “Mtu kukaa na familia yake kunapendeza kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kuliko kukaa itikafu katika misikiti hii miwili.”4 4

Raishahary: al-Mahdiy, Mizanil-Hikimah, Juz. 4, uk: 287

29


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Wakati ambapo familia nyingi katika baadhi ya jamii zetu zinakosa mazingira ya huruma na upole, ambapo mwanaume yuko katika ulimwengu wake maalumu na mambo yake maalumu, na mke vilevile. Mwanamke na watoto wanamaliza wakati wao mwingi kwenye runinga na kompyuta au pamoja na marafiki zao nje ya familia. Hakika hali ya kutangamana na upendo katika familia inakuza katika nafsi ya mwanadamu kujiamini, utulivu, uadilifu na muamala mzuri pamoja na wengine, wakati ambapo mazingira ya familia yenye mkanganyiko yanazalisha mtikisiko katika shakhsiya ya mwanadamu na kupanda katika nafsi yake chuki mbalimbali. Kuchunga haki ndani ya familia: Na sura hii inayowasilishwa na Hadithi ya Kisai na inayonukuliwa na historia katika sira ya Ahlulbayt ď …, hakika ni utekelezaji wa kivitendo wa mafunzo ya Uislamu na adabu zake katika mazingira ya familia. Mwanadamu ndani ya familia yake mume au mke, au mtoto au mzazi, wote wana haki na adabu za kupokezana, hapati ridhaa ya Mola wake wala maisha yake hayawi mazuri ya kifamilia isipokuwa kwa kuzichunga na kushikamana nazo. Na cha ajabu ni kwamba baadhi ya watu wanaona nafsi zao zina haki kutoka kwa wengine kutoka nje ya familia yake, lakini yeye anadharau na anapuuza katika kuamiliana pamoja na familia yake na watu wake walio karibu naye. Haheshimu haki zao, bali anaruhusu katika nafsi yake kuwafanyia uadui, pamoja na kwamba Qurâ€&#x;ani tukufu inatia mkazo katika kujilazimisha sana katika kufanya uhusiano mzuri na familia, na inazingatia kuwa ni usadikishaji wa sharia ya Mwenyezi Mungu. Hilo limedokezwa katika sehemu kumi na tatu katika Qurâ€&#x;ani tukufu. Kumi kati yake katika nyanja ya mahusiano ya kifamilia, kama ilivyo katika 30


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Suratul-Baqarah, aya ya 230, na katika Surat Nisaa aya ya 13, na katika Surat al-Mujadala aya ya 4, na Surat Twalaqa aya ya 1. Na tunasoma katika hadithi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu  nususi nyingi ambazo zinatilia mkazo suala la kuheshimu na kuchunga haki za ndoa. Imepokewa kutoka kwake : “Mke mwenye kumuudhi mume wake, Mwenyezi Mungu hatokubali swala zake wala jema katika amali yake hadi amsaidie na amridhishe hata kama atafunga maisha. Na mwanamume naye ana mfano wa dhambi na adhabu hiyo, ikiwa atamuudhi na kumdhulumu mkewe.”5 Kana kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu  anataka kuwaambia watu kwamba hakika swala na saumu ni kuamiliana pamoja na muumba, lakini Mwenyezi Mungu hakubali muamala huu pamoja naye, maadamu muamala wako pamoja na viumbe hauko ndani ya mpaka na kanuni za kisharia zilizowekwa. Na miongoni mwa watu wa karibu zaidi kwa mke ni mume wake na vilevile kinyume chake. Na katika riwaya nyingine kutoka kwa Imamu al-Baqir  nayo ni muhimu katika nyanja hii, anasema Imamu : “Hakuna uombezi kwa mwanamke mwenye kufaulu kwa Mola Wake kuliko ridhaa ya mume wake.” Na alipofariki Fatimah  alisimama kwake Amirul-Muuminina  akasema: “Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi niko radhi na binti wa Nabii Wako.”6 Na tunanufaika na riwaya hii kwamba ikiwa Zahra  anahitajia ridhaa ya mume wake juu yake naye ni binti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu na Bibi wa wanawake wa watu wapeponi, hakika mwanamke mwingine yeyote anahijia zaidi hayo. Hakika 5

Al-Huru al-Amiliy: Muhammad bin al-Hasan, Wasailus-Shi‟ah Juz. 20, uk: 165 hadithi namba 25315 6 Al-Majiisiy: Muhammad Baaqir, katika Biharul- Anuwar, Juz. 100, uk: 256

31


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

sisi tuna haja ya kutilia mkazo juu ya haki za mke zaidi kuliko haki za mume, hiyo ni kwa sababu mume kwa tabia yake anahisi nguvu na kwamba yuko juu na ni mtawala kwa mke wake, ambapo ana haki za usimamizi… ama mke hayuko hivyo, hivyo Mtume  anasema: “Jibril hakuacha kuniusia juu ya mwanamke hadi nikadhani kwamba haipasi kumwacha.”7 Baadhi ya wanaume wanayapuuza maelekezo yote haya, na mtu anavunja haki za mke wake na anamkalifisha zaidi ya wajibu wake. Na anaamiliana pamoja naye kama mwajiriwa katika nyumba yake, na anaona kwamba yeye ni mwenye jukumu hata la kumhudumia yeye binafsi katika chakula chake, mavazi yake na makazi yake, na uhakika ni kwamba mke kumhudumia mume wake sio wajibu, bali ni jambo la mazoea tu na ni mustahabu kisharia na sio zaidi ya hapo. Na mwanamke akimhudumia mume wake hakika hilo ni jambo jema (hapana njia ya kuwalaumu wanaofanya wema), hivyo haijuzu kumkemea au kumpiga au kumdhalilisha anapoacha kufanya hivyo, kwa sababu sio wajibu juu yake aslani. Hakika mafunzo ya Kiislamu yanashajiisha mume kumhudumia mke wake, hivyo kuhudumiana iwe ni kwa kubadilishana kama hali ilivyo katika kusaidiana. Katika riwaya kutoka kwa Nabii  amesema: “Mume akimnywesha mke wake maji anapata malipo.”8 Na katika hadithi nyingine: “Hakika mwanaume analipwa anapomlisha mke wake tonge.”9 Na kuna riwaya nyingi na hadithi ambazo zinashajiisha mume kumhudumia mke wake hususan, na familia yake kwa ujumla. Na kwa hiyo anasema Mtukufu Mtume : “Mbora wenu ni 7

Al-Majilisiy: Muhammad Baaqir katika Biharul- Anuwar, Juz. 100, uk: 253 Al-Hindiy: Ali al- Mutaqiy, katika Kanzul-Umaal, Juz. 6, uk: 275, hadithi namba 444435 9 Al-Kaashaaniy: al- Maula Muhsin, katika al-Mahajatul-baidhaa, Juz. 3, uk: 70 8

32


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

yule aliye mwema zaidi kwa ahali yake, na mimi ni mwema kwa ahali zangu.” Na alipoulizwa Ummul-Muuminina Aisha mke wa Mtume  kuhusu tabia ya muamala wa Mtume  pamoja ahali yake, alisema: “Alikuwa anashona kiatu chake, anashona nguo yake na anafanya kazi katika nyumba anayoifanya mmoja wenu katika nyumba yake. Alikuwa anawatumikia ahali zake, unapowadia wakati wa swala anasimama kwenda kuswali.”10 Anasema Amirul-Muuminina : “Mke wako asiwe ni kiumbe muovu zaidi kwako.”11 Baadhi ya watu wanajitolea kuwatumikia wengine katika hafla za watu wengine, lakini hayuko tayari kumtumikia mke wake, anawatumikia wageni katika nyumba yake lakini anakataa kuihudumia familia yake. Maisha ya Ali na Zahra  ni kielelezo dhahiri na kinachoonekana katika mafunzo, na ni maelekezo hayo ambayo yanafanya maisha ya kifamilia kuwa ni maisha yenye mafanikio bila ya kikomo. Naye kiongozi wa waumini  anafafanua heshima yake na uchungaji wake katika haki za mke wake Zahra  katika maneno yake yafuatayo: “Wallahi sijamkasirisha wala sijamchukiza katika jambo hadi Mwenyezi Mungu Mtukufu alipochukua roho yake. Wala hajanikasirisha wala hajaniasi kwa jambo. Nilikuwa ninapomwangalia zinaondoka taabu na huzuni.”12 Imamu Ali  hakuvuka mpaka wala Bibi Fatimah  hakuzembea. Na kwa upande mwingine Bibi Fatimah  yeye pia amesisitiza hayo katika wasia wake maarufu kabla ya kufariki kwake ambapo amesema: “Ewe mtoto wa Ami yangu, hujanikuta ni 10

Tirimidhiy katika Auswafu Nabiyi, chapa ya Daru al-Jiiyl Beirut, na taaliq na Samihu Abbasi uk: 276 11 Al-Musawiy: Saharifu Ridhaa katika Nahjul-Balaghah, barua ya 31 12 Al-Qazuwiniy: Muhammad Kaadhim, katika Fatimatuz-Zaharaa minalMahdiy ilaa al-Laha chapa ya kwanza 1991 Musasatu Nur lilimatubuat – Beirut uk: 142.

33


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

muongo wala mwenye hiyana wala sijakukhalifu tangu umeishi na mimi.” Na Ali  anamjibu papo hapo “Najilinda kwa Mwenyezi Mungu, wewe unamjua mno Mwenyezi Mungu, wewe ni mwema na mchamungu, ni mkarimu na unamuogopa sana Mwenyezi Mungu, huwezi kunikhalifu.”13 Na katika mnasaba huu mtukufu nao ni kukumbuka uzao wa Zahra  inapasa kwetu kusoma maisha ya familia hiyo ambayo iliishi katika nyumba ya Bibi Fatimah  na kuzitaka nafsi zetu kubeba majukumu yake kikamilifu katika hayo, na kila upande usitupie majukumu kwa mwingine, na uiepushe nafsi yake na uzembe. Ni wajibu wetu tufanye kwa maelekezo ya Uislamu katika uhusiano wetu wa kifamilia na kuwaiga Ahlulbayt ili Mwenyezi Mungu atujibu dua zetu tunaposema: “Mola Wetu, tupe katika wake zetu na wenetu kiburudisho cha jicho.” Mafanikio katika mahusiano ya kijamii: Mwanadamu katika mahusiano yake na muamala wake pamoja na watu anakabiliwa na mtihani wa daima. Yeye kwa upande mmoja anakabiliwa na mawimbi mbalimbali na hali tofauti tofauti, na katika upande mwingine anahitajia muamala wa kubadilishana na kupeana pamoja nao, na ili awe ni mtu mwenye kufaulu katika muamala huu inapasa amiliki kifua kipana na nafsi yenye usamehevu. Kanuni za kuamiliana na mwanadamu zinatofautina na zile za kuamiliana na mazingira, ambapo kanuni za mazingira ni thabiti, wakati ambapo binadamu wana hali mbalimbali, na akili zenye kutofautiana, na maslahi mbalimbali. Na zaidi ya haya hakika tabia ya mtu mmoja sio thabiti daima bali inabadilika kwa kubadilika hali na mazingira ambayo yanamzunguka, jambo 13

Rejea iliyotangulia uk: 425

34


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

ambalo linaongeza ugumu mwingine juu ya ugumu uliopo. Unaweza kukutana na mtu siku moja na humo anakuwa ni mwenye furaha, sururi na bashasha, kisha unakutana naye siku nyingine, unakuta yuko kinyume kabisa. Na sio sahihi mwanadamu kutupia lawama katika matatizo ya kuamiliana na wengine, na kuizingatia kuwa nafsi yake haina hatia katika kila kasoro, au kuona kasoro na aibu za wengine tu. Sio sahihi kusema hakika watu hawamwelewi wala hawamheshimu, na kwamba wao hawafai kuheshimiwa na kutukuzwa. Na hakika wao kama wangekuwa hivyo muamala wake pamoja nao ungekuwa bora zaidi, na kama wangekuwa kama fulani na fulani, ningefaulu pamoja nao. Na ukweli ni kwamba watu hawawezi kuwa kama anavyotamani na anavyotaka kila mtu. Je, anadhani kwamba Mwenyezi Mungu anaumba kiumbe kulingana na matakwa yake na raghaba yake yeye? Je, watu ni vazi unalikunjua kulingana na utashi wako ili ulivae, au ni chombo unataka kukitumia na kutoa kipimo chake kwa fundi anapokutengenezea? Hakika watu hao ni watu, katika kila sehemu utakapowaendea watabakia hivyo. Mwenyezi Mungu hajamuumba yeyote katika viumbe Vyake hata Manabii Wake na Mitume Wake, kumuumbia watu wenye sifa maalumu ili afaulu katika muamala wake pamoja nao. Namna gani mwanadamu atafaulu katika muamala wake pamoja na watu pamoja na kutofautiana nafsi zao? Haya ndiyo ambayo aya ya 63 katika Suratu Furaqan imeyajibu ambapo anasema (swt):

َ ‫الشخم ك ك ٰكن ىال ك ك‬ ُ ‫َوغب ك ك‬ ُ ُ َ َ ‫كزين َيمش ك ككى َن َغ َه ك ككى َس َهى ً ك ككا َوإرا ك ككا‬ ‫كاد ى‬ ِ ِ ِ ِ ً‫احجٰكُلى َن كالىا َظلٰكما‬ ِ “Waja wa Mwingi wa rehema ni wale wanaotembea ardhini kwa unyenyekevu. Na wajinga 35


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

wakiwasemesha, husema: „Salama.‟” (Surat AlFurqan; 25:63). Ambapo aya inatia mkazo kwamba (waja wa Mwenyezi Mungu) ni wale ambao wananyenyekea katika amri Zake na makatazo Yake. Wanasifika kwa sifa muhimu zinazosaidia katika kufanikisha uhusiano pamoja na wengine na kuwaathiri juu yake. Na sifa hii ni kwamba wao (wanatembea katika ardhi kwa unyenyekevu) na wala hawatembei kwa kiburi na ubabe, na kwamba wao hawaangalii nafsi zao kwa kujitofautisha na wengine, wala hawahisi kwamba wao ni wa daraja la juu kuliko watu wengine. Na nafsi hii yenye kiburi haiwezi ikafaulu katika muamala pamoja na mtu mwingine, kwa sababu msingi muhimu wa kufaulu ni mwanadamu awe anaweza kunyanyuka katika daraja la kivitendo, na mwenye kuweza kudhibiti nafsi mbele ya athari za mchemko. Na atawezaje mwenye kiburi kufikia katika kiwango hiki? Hapana, hawezi. Kisha aya tukufu inasema: “Na wajinga wakiwasemesha, husema Salama.” Na wajinga sio lazima wawe katika tabaka la wasiosoma au wasioelimika, bali wanaweza kuwa ni watu waliosoma na wanachuoni waliobobea, isipokuwa wao ni wajinga katika namna ya kuamiliana pamoja na wengine, na wao sio lazima wawe wadogo kwa umri bali wanaweza kuwa ni wakubwa kwa umri ila miamala yao ni ya kitoto. Wale ambao ni katika waja wa Mwenyezi Mungu wenye uelewa hawakubali uchochezi wa wajinga bali majibu yao yanakuwa kama inavyotia mkazo aya (amani). Na amani hapa inamaanisha heri, yaani huu ni wakati wa kuagana baina yetu, yaani hakika sisi hatutowakubalia kusimama katika kila kitendo cha kijahili mnachokifanya, bali tunaendelea nayo na kupita kwa amani, kama inavyoashiria aya nyingine ambapo anasema (swt):

‫ى‬

ً ‫… َوإرا َم ّشوا باللغى َم ّشوا هش‬..” “‫اما‬ ِ ِ ِ ِ 36


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

“…..Na wanapopita kwenye upuuzi hupita kwa heshima zao” (Surat Al-Furqan; 25:72) Na katika aya nyingine:

‫ى‬ ُ ُٰ َ ُ َ ُٰ َ َ َ ‫اللغك َكى َأ‬ ‫غشضككىا َغ ك ُكه َوكككالىا ل ككا أغم كل ا َولى ك أغم كلى‬ ‫َو ِإرا َظك ِكم ُػىا‬ ُ َ ٰ َ َ َ ٰ . ‫لحن‬ ِ ُِ ‫َظلك ٌ َغليى ال بخ ِغى احجك‬ “Na wanaposikia upuuzi hujitenga nao na husema: Sisi tuna vitendo vyetu na nyinyi mna vitendo vyenu: Salaamun alaykum! Hatuwataki wajinga.” (Surat Al-Qasas; 28:55.) Haifai kwao kujibu kila jambo la kijahili, bali wao wako juu na wametukuka, na wao wanaondoka kwenda kwenye majukumu yao na kazi zao nzuri za msingi. Hawashughulishwi na uongo na ugomvi wa pembezoni. Na hizi ndio sifa ambazo zinasifika nazo shakhsiya zilizofaulu katika muamala pamoja na wengine. Na Imamu Ali bin Husein  anatupa mfano wa shakhsiya hizo: Ilitokea kwamba mwovu alimfanyia uovu akamtukana lakini yeye  hakukunja uso wake mbele yake. Muovu akakasirika na akawa anasema: “Nakukusudia wewe.” Imamu akasema haraka: “Nami nakupuuza.” Imamu akamwacha na akaondoka.14 Na siku moja alitoka msikitini na mara mtu akamtukana. Watu wakafanya haraka kutaka kumpiga, lakini yeye akawakataza hayo, na akamwelekea kwa kusema: “Aliyoyasitiri Mwenyezi Mungu kwako ni mengi je, una shida tukusaidie?” Mtu yule akaona aibu na akatamani ardhi immeze. Imamu alipomwangalia akamhurumia akamtupia nguo iliyokuwa juu yake na akaamuru apewe dirhamu elfu moja.15 14

Al-Qarashiy: Baaqir, katika al-Imamu Zainul-Abidin juzuu 1 uk: 77, chapa ya kwanza 1988 Darul- Adhuwaai Beirut 15 Rejea iliyotangulia

37


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Haya ndio matendo ya shakhsiya tukufu. Wakati unakuta baadhi ya watu wanakasirika hata kwa maneno ambayo yananukuliwa kwao kutoka kwa watu wengine pamoja na kwamba kunukuu kunaweza kusiwe sahihi. Inanukuliwa kutoka kwa Sheikh Akhundiy Muhammad Kadhim al-Khurasaniy  kwamba alikuwa ni kilele katika muamala wake na maadui zake na alikuwa anazingatia hususan kurejesha ubaya kwa wema. Siku moja aliingia kwake mmoja wa makhatibu maarufu kati ya waliokuwa wanampinga Sheikh Akhundiy kwa kuongoza kwake harakati yenye masharti, ambayo ilimtaka Mfalme al-Qajaariy wa Iran kutunga katiba ya nchi na kuanzisha bunge, na khatibu huyo alikuwa amejiunga na kundi lingine lililokuwa linaitwa alMustabiddah, linataka hali ibaki kama ilivyo, kwa kuogopa kuingia kanuni zisizokuwa za Kiislamu katika katiba, au kupenya watu kutoka nje ya mazingira ya kidini katika bunge. Na kwa kuwepo hali hii ya ikhitilafu, mara nyingi khatibu huyo alimzungumza Sheikh al-Akhundiy juu ya mimbari kwa kumkosoa na kushutumu msimamo wake. Na kudra ya Mwenyezi Mungu ikataka khatibu huyu auze nyumba yake ili alipe deni lake, mnunuzi akamwambia: “Kama al-Akhundiy atatia saini katika mkataba wa nyumba yako nitainunua, vinginevyo hapana.” Akaja Najaf akakutana na Sheikh al-Akhundiy, na Sheikh akamheshimu sana na akamkalisha mbele ya majilisi na akaelezea furaha yake kwa kukutana naye. Khatibu akamwambia: “Naomba usaini mkataba huu ili niweze kuuza nyumba yangu.” Sheikh akachukua mkataba kisha baada ya muda Sheikh akatoa katika hazina yake mifuko kadhaa ya pesa na akampa Khatibu na akasema: “Wewe ni katika watu wenye elimu na mimi siridhii kamwe watu wenye elimu kukabiliwa na shida. Chukua kiasi hiki, lipa deni lako, na usiuze nyumba yako na kuitaabisha 38


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

familia yako.� Khatibu akaona aibu kwa kitendo cha Sheikh, na baada ya hapo akawa ni kati ya wafuasi wa Sheikh na wapenzi wake.16 Jamaa wa karibu wa kwanza: Vyovyote itakavyokuwa, kuna haja ya kutumia tabia hii, wakati wa kuamiliana na watu ni muhimu sana, ila hakika kuamilina nayo pamoja na mazingira ya watu wa karibu kati ya watu ni muhimu zaidi na kubwa zaidi. Msamaha na huruma una thamani kubwa unapofanywa na mtu wa mbali, lakini thamani yake inaongezeka zaidi unapofanywa ndani ya familia kwa kuwafanyia jamaa na watu wa karibu na mtu, wazazi wawili wazee, mke na watoto, mafakiri na wanyonge na wasiokuwa na uwezo kabisa. Hiyo ni kwa sababu mwanadamu mwenye nguvu, nguvu yake inaweza kumsukuma kumsamehe kwa msukumo wa hofu, haiba na kujiepusha na matatizo. Ama mnyonge ambaye hamiliki uwezo wala nguvu, hakika kusamehe kwake hakusukumwi na hofu bali ni kutaka thawabu na malipo kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kutokana na uzuri wa moyo na utu. Ama baadhi ya watu, na sisi mara nyingi tunasikia visa hivi, wanapokosea katika haki yao baadhi ya ndugu zao, hakika wao wanakunjua makucha yao na wanalipiza kisasi kwa ubaya na kwa ukali zaidi. Na watu wengine wanapowakosea watu wageni kwao au wenye nguvu katika vituo vyao hakika wao wananyenyekea na wanarukuu na wanainamisha vichwa vyao chini, kisha hawakawii watakariri kwako neno la subira na kuvumilia (usijali dogo hilo, sio vibaya kuvumilia, shida na litaondoka), na kwa hiyo wanakuwa ni wasadikishaji wa kauli ya mshairi: 16

Mukhutaariy: Sheikh Ridhaa katika Simaai Swalihina, tarjama ya Sheikh Husein al-Kuraaniy - Darul- Balagha – Beirut 1992 uk: 278

39


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

“Ni simba kwangu na katika vita ni mbuni, muoga anaogopa kwa unyayo, Je usingejitokeza kuwinda asubuhi, bali kabla yako alikuwa katika mabawa ya ndege.” Natamani, yalikuwa wapi maneno haya alipokosea katika haki yako ndugu yako katika nasaba au imani? Na kwa nini umezingatia ghadhabu yako? Huko ni kurejesha utukufu wako na heshima yao ambayo ulidhani kwamba imevunjwa na imedharauliwa, ama hapa unageuka mwenye kusubiri anayengojea malipo? Ulikuwa wapi wewe na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

ُ َ​َ ُ ّ َ َ ُ ‫الى ّفاس ُ َخ‬ “….. ُ ‫ماء َبين‬ ‫… أ ِشذاء غهى‬..” ‫ِس‬ “…wana nguvu mbele ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao…” (Surat Al-Fath; 48:29) Hakika njia ya mtu ya kufikia mafanikio katika kuvuka changamoto za uhusiano wake pamoja na wengine, bila shaka inapita katika utangulizi huu, na maadamu mwanadamu si mwenye uwezo katika kudhibiti hasira za vitendo vyake mbele ya vitendo vya mwingine, hakika hatokuwa ni mwenye kufaulu katika muamala wake. Na tunayo katika sira ya Nabii  na Ahlul-Bayt wake kigezo na mfano bora, na hebu tufaidike na sira ya watukufu ambao walifikia vyeo vya juu lakini wao walishinda hisia za kulipiza kisasi. Huyu ni Yusuf mkweli  anawaambia ndugu zake walipoingia kwake Misri, naye akiwa ni mfalme, baada ya ndugu zake kumfanyia ubaya katika haki yake. Walimuonea husuda wakamtupia kwenye kisima kisha akauzwa kama mtumwa Misri. Akafungwa na akatuhumiwa, lakini alikuwa ni mtukufu na mkubwa kuliko kulipiza kisasi na chuki, bali aliwaambia:

َ ّٰ ُ َ َ َ ُ َ ُ َ ُ ‫َ َ َ َ َ ُ ُ َ َ َ ُ ى‬ ِ‫الش ِخمحن‬ ‫غفش اللكه لى وهى أسخ‬ ِ ‫كاٌ ال جثريب غليى الي‬ ِ ‫ىمِي‬ 40


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

“Akasema hakuna lawama kwenu leo Mwenyezi Mungu atawasamehe Naye ni Mwingi wa kurehemu kuliko wote” (Surat Yusuf; 12:92). Hakika usamehevu ni sifa ya lazima katika kufaulu katika maisha ya kijamii, na kuvuka matatizo, kushirikiana na kuamiliana pamoja na wengine katika jamaa wa karibu na wa mbali, nayo inafanya nafsi ya mwanadamu ipumzike na kukasirikia mabaya ya wengine, kama ambavyo inaipatia mishipa ya mwanadamu na hisia zake hali ya mkanganyiko na shinikizo linalotokana na kulipiza kisasi katika vitendo vya uadui. Mwanadamu baina ya mbinyo wa kimada na utukufu wa kiroho: Mwenyezi Mungu amemuumba mwanadamu akiwa ni mchanganyiko wa vitu viwili, kimoja wapo ni cha kimada na kingine ni cha kiroho. Tapo linalotokana na udongo na nuru inayotokana na roho, anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

ٰ ّ َ ٰ َ َ ُ َ ‫إر ك ك‬ ‫﴾فك ِكئرا َظك ىكىيخ ُه‬٧٧﴿ ‫كحن‬ ِ ٍ ‫كاٌ َسبك َكً ِل َلمل ك ِنى ِت ِإقككش ك ك ِل ٌم َ شك ًكشا ِمككن ك‬ ِ ٰ َ َ َ َ​َ​َ ُ ُ َ ﴾٧٧﴿ ‫ذين‬ ِ ‫فيه ِمن سوحى فلػىا له ظك ِج‬ ِ ‫و فخذ‬ “Mola wako alipowaambia Malaika: Hakika Mimi nitaumba mtu kutokana na udongo. Na nitakapomkamilisha na nikampulizia roho Yangu, mwangukieni kwa kusujudu.” (Surat Swad; 38:71-72). Mchanganyiko huu katika kuumbwa mwanadamu baina ya vitu viwili vya kimada na kiroho, ndio sababu ya hali ya mvutano ndani ya mwanadamu baina ya pande mbili za uwiano huu, udongo na roho. Sehemu ya udongo inavutia kwenye ardhi na kumteremsha kwenye mazingatio ya kimada, wakati ambapo sehemu ya roho inamsukuma kwenda juu na inapaa naye katika 41


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

anga la maadili mema. Na katika mvutano huu unatokea mtihani kwa mwanadamu, inakuwa ni changamoto kubwa, na katika matokeo ya mvutano huu inapangwa hatima ya mwanadamu na kinapevuka kiwango chake; ama katika unyoofu ambapo ataishi katika hali ya uwiano na anafanya mazingatio yake ya kimada katika kivuli cha maadili na chini ya dari la misingi, na ama anakuwa chini kuliko walio chini, ambapo atakapoyafanya matamanio yake kuwa ndio mungu wake, na akatawaliwa na matamanio yake na raghaba zake. Na tunaweza kupanga mikakati ya vitendo vyetu na nukta za mgongano baina ya mielekeo miwili katika maisha ya mwanadamu katika nyanja tatu zifuatazo: Kwanza: Baina ya matamanio na akili: Kutokana na sehemu ya udongo umepatikana kwa mwanadamu utashi na matamanio, nayo yanambana ili ayashibishe na kuyatimizia mahitaji yake ya kimwili na raghaba zake za chakula, vinywaji, mambo ya kijinsia na raha. Na yanayofungamana nayo miongoni mwa mali, cheo na jaha. Lakini kukubali moja kwa moja mwelekeo huu kunambadilisha mwanadamu kwenda kwenye kiwango cha wanyama, mifugo ambayo haina lengo isipokuwa raghaba zake tu, na haina mazingatio isipokuwa hayo tu. Wao wanakula kila sehemu; kwenye jalala au kwenye malisho, na wanakunywa maji yoyote safi au machafu, na wanafanya jimai katika hali yoyote kwa sababu wanaendeshwa na matamanio tu. Lakini hali ya akili kwa mwanadamu ambayo inatokana na sehemu ya roho, ndio inayomwekea mpaka na masharti katika kufanya vitendo vya matamanio yake na raghaba zake, anakula, kunywa, anaoa, anamiliki na anatawala, lakini yote hayo ndani ya maelekezo ya akili na uongofu wake. Na kuyakubalia kwa wingi matamanio, inamaanisha kuporomoka 42


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

zaidi kwenda kwenye kina cha hali ya udongo ya kimaada, wakati ambapo kutumia akili na udhibiti mzuri wa raghaba na matamanio, inamaanisha kutukuka zaidi katika upeo wa maarifa ya kiroho na kimaanawiya. Pili: Baina ya ubinafsi na utukufu: Upande wa udongo unaimarisha kwa mwanadamu hali ya ubinafsi, na inamaanisha kujali dhati yake tu, na maslahi binafsi kushinda kila kitu, ambapo mada kama mada yenyewe haina nguvu katika mwelekeo wa nje, kwani inaishi kwa ajili ya dhati yake tu. Wakati ambapo upande wa kiroho unamwelekeza mwanadamu kwenye upeo mpana zaidi, nje ya dhati yake. Anajua ridhaa ya Mola Wake na Muumba Wake, na kuzingatia hali za wengine pembezoni mwake. Na anafikiria katika maslahi ya jamii. Hakika ubinafsi unaotokana na udongo ndio ambao unamsukuma mwanadamu katika kuzifanyia uadui haki za wengine kwa ajili ya kupata yeye, nao unamzuia kutoa na kujitolea ili alimbikize kiasi kikubwa cha uwezo kwa ajili ya nafsi yake. Lakini dhamira ya mwanadamu na uwepo wake unaotokana na upulizo wa roho ya Mwenyezi Mungu, ndio ambao unamkanya juu ya dhulma na uadui na unamshajiisha kunufaisha wengine na kuwasaidia wao bali na kuwapendelea kabla ya dhati ya nafsi yake. Mwanadamu kuzingatia dhati yake zaidi ni mporomoko wa kimaada, na kuelekea kwake kwa wengine na kujali maslahi ya jamii ni utukufu wa kiroho. Tatu: Baina ya ufinyu na maadili: Udongo ni mada inayochukua sehemu ndogo ya muda na sehemu, nayo inamdhibiti mwanadamu kwa mpaka wa ufinyu wake mdogo na kumshughulisha na matakwa yake na mahitaji 43


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

yake ya muda na ya haraka. Wakati ambapo roho inafungamana na nguvu kuu isiyo na mpaka wala kikomo. Hakika ni upulizo kutoka kwa Mwenyezi Mungu “na nikapuliza humo roho Yangu” na nyongeza hapa ni ya utukufu, vinginevyo Mwenyezi Mungu hana mwili wala roho kwa maana iliyoenea kwetu. Na roho inamfungulia mwanadamu ulimwengu wa maadili na ubora, nao ni ulimwengu mpana uliotanuka na mpana, mwanadamu anapoujua anakuwa juu ya mada finyu na anaiandaa nafsi yake kutumikia maadili ya Mwenyezi Mungu ya milele. Anakuwa ni mlinganiaji wa kheri, na kiongozi wa uadilifu na mtendaji kwa ajili ya haki. Hapa hakika mwenye kuimarisha maisha yake kwa ajili ya mada anakuwa ni mwenye kuelemea kwenye udongo katika kuumbwa kwake, wakati ambapo mwenye kuiwekea nafsi yake nadhiri kwa ajili ya maadili na misingi anakuwa anaelea katika ulimwengu wa roho, mwenye kudumu katika neema za ridhaa ya Mwenyezi Mungu. Mwezi wa Rajabu ni msimu wa kiroho: Mwezi mtukufu wa Rajabu ni mwanzo wa miezi ya msimu wa kiroho katika umma wa Kiislamu, unafuatiwa na mwezi wa Shabani kisha mwezi mtukufu wa Ramadhani. Msimu huu wa kiroho unapasa kuimarisha katika nafsi zetu uelewa wa kiroho, na kuimarisha matakwa yetu kwa ajili ya kunusurika mja kiroho katika nafsi zetu, na kutusaidia katika kudhibiti mvutano wa udongo na raghaba za kimaada katika maisha yetu. Na zimepokewa katika utukufu wa mwezi wa Rajabu riwaya nyingi miongoni mwazo ni: Yaliyopokewa kutoka kwa Said al-Khudiriy kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu  kwamba amesema: “Fahamuni hakika Rajabu ni mwezi wa Mwenyezi Mungu Mtukufu nao ni mwezi 44


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

mtukufu.”17 Na ambayo yamepokewa kutoka kwa Imamu Musa bin Ja‟far  hakika amesema: “Rajabu ni mwezi mtukufu, Mwenyezi Mungu anaongeza humo mema na anafuta humo maovu.”18 Na kutoka kwa Imamu Ja‟far Swadiq  amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu : “Rajabu ni mwezi wa maghufira kwa umma wangu basi zidisheni humo kuomba maghufira. Hakika Yeye ni Mwingi wa maghufira na Msamehevu. Na unaitwa Rajabu al-Aswabu kwa sababu rehema katika umma wangu zinamiminwa humo kwa wingi, basi zidisheni kusema: Astaghafirullahi Waas‟aluhu tauba.”19 Na kuna riwaya na hadithi kutoka kwa Maimamu wa Ahlulbayti  zinazotoa picha mbele yetu ya baadhi ya ratiba za kiroho, kwa ajili ya kunufaika na mwezi huu mtukufu na kunufaika na kheri zake kimaanawiya, na miongoni mwa ratiba hizo muhimu na mustahabu ni: Kwanza: Saumu: Na saumu ni kumwaandaa na kumzoeza mwanadamu katika kudhibiti, kutawala raghaba zake na matamanio, ambapo mwanadamu anajizuia kwa matakwa yake na hiari yake na vitenguzi vya saumu, ambavyo ni kati ya raghaba zinazoonekana kama vile kula, kunywa na jimai. Na ikiwa saumu ni wajibu katika mwezi wa Ramadhani tu, hiyo ni kwa sababu hicho ndio kiasi cha chini anachokihitaji mwana17

Al-Huru al-A‟miliy: Muhammad bin al-Hasan, Tahswil wasaail ash-Shi‟ati ilaa tahaswli masaail shariati, Juz. 10, uk: 475 chapa ya kwanza 1411 Hijiria, Muasasatu aali al-baiti liihiyai Turathi – Qum - Iran. 18 Rejea iliyotangulia uk: 473 19 Al-Qummiy: Sheikh Abbasi katika Mafatihul Jinan uk: 185 chapa ya kwanza 1983 Daru al-Adhuwai - Beirut

45


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

damu katika maandalizi na mazoezi kwa mwaka, lakini wenye malengo na uelewa wa kupanda daraja kiroho na kuendelea kimaanawi hawatosheki na funga ya wajibu ya mwezi wa Ramadhan, hivyo Uislamu umeweka ratiba ya funga ya ziada kwa njia ya mustahabu ili kutoa fursa kwa hawa wenye matarajio na wenye uelewa. Na funga katika mwezi wa Rajabu ni kati ya ratiba hizo zinazoonekana. Mwenye kuweza kufunga mwezi mzima wa Rajabu basi amepata fungu kubwa, vinginevyo afunge nusu yake au theluthi yake au robo yake, na haipasi mwanadamu kupitwa na saumu ya mwezi wa Rajabu angalau siku moja. Imepokewa kutoka kwa Imamu Musa al-Kadhim : Rajabu ni mto wa peponi, mweupe kuliko maziwa na mtamu kuliko asali, mwenye kufunga siku moja ya Rajabu Mwenyezi Mungu atamnywesha katika mto huo.”20 Na kutoka kwa Ali bin Salim kutoka kwa baba yake amesema: Niliingia kwa Imamu Swadiq Ja‟far bin Muhammad  katika mwezi wa Rajabu, na zilikuwa zimebakia siku chache kutoweka, aliponiona akaniangalia akasema: „Ewe Salim je, umefunga chochote katika mwezi huu?‟ Nikasema: Hapana ewe Mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu. Akaniambia: „Umepitwa na thawabu asiyojua idadi yake isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Hakika mwezi huu Mwenyezi Mungu ameutukuza na akatukuza utukufu wake na akawajibisha kwa mfungaji humo ukarimu wake.‟”21 Pili: Umra: Mwanadamu kuzuru nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu, na 20

Al-Huru al-Amiliy: Muhammad bin al- Hasan katika Tafswilu wasaail Shaiati, Juz. 10, uk: 475 21 Rejea iliyitangulia uk: 475

46


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

kutekeleza ibada ya tawafu, swala na sa‟ayi na yanayomlazimu katika taklifu na kinachofuatia katika hukumu na wajibu. Ziara hii inatia mkazo katika nafsi ya mwanadamu ya kuwa mnyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu na kutekeleza amri Zake katika mambo yake yote, kama inavyomwelekeza kwamba Mola ndio kitovu cha maisha yake na harakati zake, na ajitahidi katika kwenda mbio kufikia radhi Zake. Na kila ibada na mafunzo ya haram tukufu, yanatengeneza kielelezo na mwangaza kwa mwanadamu katika maisha ya kiroho na upeo wake wa kimaanawi. Na ikiwa ni wajibu kwa mwanadamu kuizuru nyumba tukufu na kutekeleza Hija na Umra mara moja katika umri, hakika kurudia ziara katika nyumba tukufu, na kutekeleza ibada inamaanisha kuongeza kupata faida ya kiroho, na mwangaza wa Mwenyezi Mungu katika moyo wa mwanadamu na hatima yake. Na katika suna za mwezi mtukufu wa Ramadhani ni kutekeleza ibada ya Umra. Na ikiwa baadhi ya maulamaa wa Waislamu hawaoni sifa maalumu ya Umra katika mwezi wa Rajabu, hakika wafuasi wa Ahlulbayti  wanachukua kauli za Maimamu wao waongofu, ambazo zinatia mkazo mustahabu wa Umra katika mwezi huu na ubora wake humo kuliko miezi iliyobakia, na kauli za Maimamu ni hoja ya kisharia juu yetu. Aliulizwa Imamu Ja‟far Swadiq : Ni Umra ipi iliyo bora zaidi, Umra katika mwezi wa Rajabu au Umra katika mwezi wa Ramadhani? Akasema: Hapana, bali Umra katika mwezi wa Rajabu ni bora zaidi.22 Na kutoka kwake , amesema: “Mwenye kufanya Umra hufanya Umra katika mwezi anaotaka ndani ya mwaka anaotaka, 22

Rejea iliyotangulia, Juz. 14, uk: 301

47


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

na Umra bora zaidi ni Umra ya mwezi wa Rajabu.�23 Na alhamdulillahi fursa iko mbele yetu, sisi tunaishi karibu na misikiti miwili mitukufu na miundombinu imeandaliwa kwa ajili ya kufanya ibada ya Umra, hata kwa masaa machache, miundombinu inapatikana kwetu hivi sasa. Kuna misafara iliyoandaliwa kwa ajili ya Umra ndani ya mapumziko ya wiki siku ya Alhamisi na siku ya Ijumaa, pongezi kwa waliojitolea kwa ajili ya Umra katika mwezi huu mtukufu, kama ambavyo mpango mpya ambao umepitishwa na baraza la mawaziri na ambao unatoa fursa na kuwajibisha kufanya Umra kwa Mwislamu yeyote ndani ya miezi tisa katika mwaka, maamuzi haya yanaleta furaha na sururi katika nafsi za Waislamu wa ulimwengu, na yanawawezesha wenye uwezo miongoni mwao kutembelea haram mbili tukufu wakati wowote. Alhamdulillahi na una matokeo mazuri katika hali ya uchumi wa nchi ya Saudi Arabia, Mwenyezi Mungu awape taufiki viongozi katika kuitumikia dini na nchi. Tatu: Swala, dua na nyuradi: Swala ni ngazi ya muumini, ambapo anaondoka kwa roho yake, moyo wake na fikra yake kwenda katika anga za utukufu wa Mwenyezi kwa kuvuka mipaka ya mazingatio ya kimaada, kwa kwenda na kuelea katika anga la dhikiri ya Mwenyezi Mungu, akineemeka kwa utamu wa kuhudhuria katika hadhara ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na katika mwezi mtukufu wa Rajabu inapasa kudumu katika kutekeleza suna za kila siku na hususan swala za usiku. Vilevile kuna swala kwa namna maalumu ambazo ni mustahabu kuziswali katika mchana na mikesha ya mwezi huu mtukufu. Na kuna dua maalumu, zinazomkumbusha mwanadamu utukufu wa Mola 23

Rejea iliyotangulia uk: 303

48


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Wake na majina Yake matukufu, na kumwelekeza mwanadamu kwenye ukweli wa ulimwengu, na kwenye tabia njema, na mwenendo mzuri na sifa nzuri. Imepokewa mustahabu wa kuzisoma kwake na kudumu nazo katika mwezi huu mtukufu. Nazo zimetajwa katika vitabu maarufu vya dua kama vile Mafatihul-Jinan cha Sheikh al-Qummiy na Dua na ziyara cha Imamu Shiraziy. Nne: Sadaka: Hakika kuwasaidia mafakiri na wenye haja inaonyesha ukweli wa uchamungu wa mwanadamu. Na huenda kwa sababu hiyo imeitwa sadaka kutokana na ukweli, wakati ambapo kusahau hali za wasionacho ni alama ya uongo na kudai uchamungu. Haithibiti dini kwa mwanadamu na imani awapo ni mwenye kupuuza haja za wanyonge na mafakiri, anasema (swt):

‫َ َ ى‬ ّ َ َ ‫﴾ َفك ٰكزل ًَ ىالككزي َيك ُكذع‬٧﴿ ‫ين‬ ‫﴾ َوال‬٧﴿ َِ ‫اليدككي‬ ِ ِ ‫أ َس َءيككذ الككزي ُيىك ِكز ُل ِبالك ّكذ‬ ِ َ ٰ َ ﴾٣﴿ ‫عىحن‬ ِ ِ ‫ػام ا ِو‬ ‫َي ُدض غهى‬ ِ “Je, umemuona ambaye anakadhibisha dini? Huyo ni ambaye humsukuma yatima. Wala hahimizi kumlisha masikini.” (Surat al-Ma‟un; 107:1-3) Na ikiwa sadaka inatakiwa wakati wote, na ina matokeo makubwa katika maisha ya mwanadamu kabla ya akhera, ambapo imepokewa katika hadithi kwamba inaondoa balaa, kuongeza riziki na kurefusha umri, isipokuwa katika mwezi huu mtukufu ina thawabu nyingi zaidi na baraka nyingi zaidi. Na katika hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu , alikuwa anazungumza humo kuhusu fadhila za mwezi wa Rajabu na funga kisha akasema: “Anatoa sadaka ya mkate kila siku kwa masikini, naapa kwa ambaye nafsi yangu ipo 49


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

mikononi Mwake, hakika anapotoa sadaka hii kila siku anapata yaliyoelezwa na zaidi. Hakika kama viumbe wote watakusanyika ili wakadirie kiasi cha thawabu zake wasingefikia moja ya kumi ya yale atakayopata peponi katika fadhila na daraja.”24

MUAMALA WA KIBINADAMU KATIKA SIRA YA IMAMU ALI : Imejitofautisha sira ya Amirul-Muuminina Ali , kwa mambo mengi, na lililokuwa wazi zaidi ni muamala wake wa kibinadamu wakati wa kuamiliana na wengine, uliojengeka katika msingi wa kumheshimu binadamu kama binadamu, kwa kufumbia macho kitu kingine chochote, na kuhifadhi haki zake na shakhsiya yake kimaada na kimaanawi katika nafasi yoyote na sehemu yoyote, na vyovyote litakavyokuwa umbo lake na kiwango chake. Na umuhimu wa mwelekeo huu katika nyanja hii katika sira ya Amirul-Muuminina  unatokana na nafasi yake katika kuathiri maisha ya mwanadamu. Ni shakhsiya ya kijamii na ni njia ya kuelekea katika ridhaa ya Mola Mtukufu. Mimi na wewe tunaamiliana na binadamu, sawa wawe wanaafikiana na sisi katika dini na mwelekeo au hawaafikiani nasi. Na jambo muhimu hapa ni kujua namna gani tutaamiliana pamoja nao kwa muamala mzuri wa kinadamu, ambao utaakisi usafi wa Uislamu, na kumheshimu mwanadamu kama mwanadamu kabla ya kupata sifa yeyote nyingine itakayoongeza kwake mazingatio mengine. Na sira ya Amirul-Muuminina  imejaa mifano mingi katika muamala wa kibinadamu wakati wa kuamiliana na wengine, katika hali na mazingira mbali mbali. Naye kwa haki – baada ya 24

Al-Huru Al-Amiliy: Muhammad bin al- Hasan katika Tafswil wa Sailu Shiati, Juz. 10, uk: 483

50


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Mtume wa Mwenyezi Mungu  – ni mfano bora wa kuigwa, hususan katika wakati huu ambao tunajiandaa kukumbuka uzao wake mtukufu. Hakika kuwepo upeo huu katika maisha yake, ndiko kulikofanya shakhsiya yake iwe ni shakhsiya ya kibinadamu yenye kudumu katika kiwango chote cha ubinadamu, na sio katika historia ya Waislamu peke yao. Na kabla ya siku kadhaa zilizopita imetoka diwani mpya ya ushairi huko Beirut, ya Mkristo Maruniy naye ni Joseph al-Hashim, kuhusu Imamu Ali, chini ya anwani „Matukufu ya Ali.‟ Ama kitabu Sauti Ya Uadilifu Wa Ubinadamu cha mwanafasihi wa Kikristo Geoge Jordak ni Enklopedia nzuri mno, imechukua nafasi yake katika maktaba ya utamaduni na fasihi ya Kiarabu. Na vilevile rejea kubwa ya Idul-Ghadir, kitabu cha Paulo Salamah ambaye naye ni Mkristo, na visivyokuwa hivyo katika kazi ya fasihi na historia na fikra, ambavyo vinaelezea nafasi ya Imamu katika kiwango cha ubinadamu. Maji ni haki ya wote: Miongoni mwa ushahidi wa muamala wa kibinadamu wa Imam Ali , ni yaliyotokea katika vita vya Sifiin. Jeshi la Muawiya lilipolitangulia jeshi la Imamu kufika katika sehemu ya mapigano na kudhibiti ufukwe wa Mto Furati, na wakazuia jeshi la Imamu kwenda kuchota maji. Wafuasi wa Imamu wakapiga kelele kwa hilo, akasimama kwao akiwahutubia na akasema neno lake mashuhuri: “Wamekuandalieni vita basi kubalini udhalili na kuchelewa kuyafikia maji. Au zinywesheni panga damu ndipo mtakunywa maji. Mauti yapo katika maisha yenu mkishindwa, na uhai upo katika mauti yenu mkishinda.”25 Kwa maneno hayo Imamu alihamasisha jeshi lake kwenda kwenye ufukwe na haya ndio yaliyotokea kwa hakika, ambapo waliweza kuliondoa jeshi ufukweni na wao kuchukua udhibiti 25

Al-Musawiy: Sharifu Ridhaa katika Nahjul- Balaghah, khutuba ya 51

51


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

wake. Ilipotokea hali hiyo askari wake walipiga kelele kwa kumwambia: “Tuwazuie maji kama walivyotuzuia, na tuwapige vita kwa upanga wa kiu.” Lakini yeye alikataa hilo na akasema: “Chukueni mahitaji yenu na rejeeni kwenye kambi yenu na acheni njia baina yenu na maji. Hakika mimi sifanyi waliyoyafanya wajinga.”26 Na hivi ndivyo anatupigia mfano wa kuigwa katika kupinga kutumia vikwazo na kibano kuzuia mahitaji ya lazima ya maisha kwa adui. Ambaye anapigana naye katika vita kali hata kama adui atakimbilia kwenye njia hii. Kwa kweli hii ni tabia ya Kiislamu katika upeo wake mkubwa wa kibinadamu. Na unapotafuta mtazamo huu katika hali ya kiulimwengu wa kimadola, utakuta haupo katika kamusi ya siasa ya kimadola leo. Wewe utaona dola kubwa na yenye utawala, inatumia vikwazo dhidi ya wananchi dhaifu kwa hoja ya kusawazisha ikhitilafu zake na baadhi ya mifumo na watawala, pamoja na kwamba wao wanajua kwamba muhanga wa vikwazo hivi ni wananchi wenyewe. Wakati Marekani na nchi za Magharibi zinapoweka vikwazo kwa wananchi wa Iraki, wao wanajua kwa yakini kwamba vikwazo havitabadilisha chochote katika hali ya ubabe wa serikali ya Iraki, na hivyo havitaleta mabadiliko ya kisiasa humo, bali kinyume chake vitazidisha udhaifu katika msimamo wa wananchi dhidi ya utawala, kwa sababu watu mazingatio yao makubwa yatakuwa ni tonge la kuishi na kujilinda. Ama utawala utafaidika kutokana na hali hii katika kuweka kanuni ya udhibiti wa mamlaka yake kwa maslahi yake, kwa sababu serikali hii inapata katika vikwazo vilivyowekwa propaganda katika kutengeneza adui wa nje, na katika kubakisha hali ya hatari isiyotangazwa na kisha kukandamiza kila upinzani. 26

Al-Qazuwiniy: Sayid Kaadhim katika Aliyu minal – mahadi ilaa llahad, uk: 334 chapa ya al-Adabu Najaf al-Ashraf, 1967.

52


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Je, atadhurika kiongozi wa Iraki kwa vikwazo? Na je, watoto ambao wanakufa kwa sababu ya upungufu wa dawa na chakula ni katika watoto wa Raisi au Mawaziri au wanajeshi wa ngazi za juu? Hakika wamagharibi wanajua kwamba watoto ambao wanakufa kwa matokeo ya vikwazo wao ni watoto wa watu mafakiri na wasio na kitu, ama watoto wa wakubwa wao hawazaliwi isipokuwa na vinywani mwao kuna kijiko cha dhahabu kama inavyosemwa. Na wamagharibi wamelazimisha vikwazo Libya miaka mingi kwa ugomvi wao na serikali, na tumeona wakifanya zaidi ya hayo na Sudani, hadi mambo yakafikia kupiga mabomu na kuangamiza viwanda vya dawa katika nchi fakiri inayokabiliwa na upungufu mkubwa katika nyanja hii, na baadhi ya wanachi wake wanakufa kwa sababu ya upungufu mkubwa wa dawa na utapia mlo. Uko wapi ubinadamu katika haya yote… je, hiyo sio dalili ya kutoweka upeo wa ubinadamu katika fikra ya ustaarabu wa kimagharibi na mtazamo wake katika maisha? Na kinyume cha hayo tunaona ustaarabu wa Kiislamu na viongozi wake. Hata mhaini ana haki yake: Na miongoni mwa ushahidi katika sira Ali  katika nyanja hii ni kisa muhimu: Mwanaume katika wafuasi wa Imamu Ali  jina lake ni Ubaidullahi bin al-Hur al-Ja‟afi, alimfanyia Imamu hiyana na akajiunga na jeshi la Muawiya wakati wa usiku, na hiyo ni wakati vita vya Sufini vikiwa vimepamba moto. Na katika kanuni za vita huadhibiwa huyu mhaini kwa kuuliwa. Ubaidullahi aliweza kutoa msaada mkubwa kwa Muawiya. Ama mke wake 53


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

alikuwa Kufah na akasikia habari za kufariki Ubaidullahi katika vita, akakaa eda ya kufiwa na baada ya hapo akaolewa na mwanaume kati ya watu wa Kufah. Wakati ambapo Ubaidullahi alikuwa hai huko Shamu, na alipopewa habari ya kuolewa mke wake, akatoka Sham usiku na akakata masafa marefu na akawasili Kufah na akaingia usiku. Akaelekea haraka kwenye nyumba ya mke wake, na mke wake akatoka kwenda kwake akiwa amevaa gubigubi, na baada ya majadiliano mafupi akampa habari ya kuolewa kwake na mwanaume mwingine. Ubaidullahi akaona milango ya kurejea kwa mke wake imefungwa mbele yake, na akaona njia bora ya kutatua ni kwenda kumuona Maulana Amirul-Muuminina  na kumweleza kisa chake, na Amirul-Muuminina ni mtu mwadilifu na mshika haki, na haachi haki hata kama mwenye haki ni mhaini. Ubaidullahi alikutana na Amirul-Muuminina  hali yakuwa amevunjika moyo mwenye aibu, kwa kujua kwake kwamba yeye ni mhaini. Akamsalimia Imamu , Imamu akaitikia na akamuuliza kwa kumkanusha: “Je, wewe ni Ubaidullahi? Eee wewe mnafiki ambaye ulimfanyia hiyana Imamu wako na dini yako na ukajiunga na safu ya ukafiri na unafiki na hiyo ni katika hali ya vita. Je, wewe ni huyu mwanaume?” Ubaidullahi anajua kwamba Ali ni mtu wa haki na uadilifu, akatumia fursa na akasema: “Je, hiyana yangu inakuzuia kufanya uadilifu ewe AmirulMuuminina?” Imamu akamjibu: “Vipi?” Akaomba kwake asimulie kisa chake na akamtaka Imamu amsaidie katika jambo lake. Na Imamu akaamuru aletwe mke na mume wake wa pili na akasema: “Ni wajibu mke ajitenge na mume wake wa pili na aanze eda kuanzia 54


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

sasa, na baada ya kumalizika eda yake arejee kwa mume wake wa kwanza kama si mjamzito, na ikiwa ni mjamzito harejei kwa mume wa kwanza hadi ajifungue, na mtoto ni halali ni twahara na anamfuata baba yake, mume wa pili. Na baada ya hapo mwanamke atarejea kwa mume wake wa kwanza.” Na inafaa kutaja hapa kwamba mke ambaye mume wake ametoweka kama akienda katika mahakama ya Kiislamu ya kisharia na hakimu wa kisharia akampa talaka, kisha mume wa kwanza akarejea, hawezi kurejea kwake, wala haivunjiki ndoa ya pili, nayo ni sahihi. Ama mke wa Ubaidullahi hakuenda kwenye mahakama ya Kiislamu, bali yeye mwenyewe alikaa eda na kuolewa, na kwa hiyo imevunjika ndoa ya pili baada ya kurejea mume wa kwanza moja kwa moja na bila ya talaka.27 Hakika uadilifu ni sharia madhubuti haivunjiki hata katika kuamiliana na adui. Anasema Mwenyezi Mungu:

ُ َ َّ ٰ َ َ ُ َٔ َ ُ ‫َ َ َ ى‬ َ ‫اغذلىا ُه َى َأ‬ ‫كش ُل‬ ِ ِ‫ػذلىا‬ ِ ‫ىم غهى أال ح‬ ٍ ‫جشم ى ش كان ك‬ ِ ‫…وال ي‬..” ‫ى‬ “ …‫ي‬ ِ ٰ ‫ِللخلى‬ “Na wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu ndiko kunakokurubisha kwenye takua…..” (Surat AlMaida; 5:8). Kuzuia kutoa adhabu: Sira ya Imamu Ali imejaa ushahidi wa visa ambavyo vinatia mkazo kuheshimu kwake ubinadamu wa mwanadamu na kuhifadhi kwake utukufu wake, Imamu  alijiwa na mwanamke 27

Shiraziy: Sayid Muhammad Shiraziy katika al-Hukumatu al-Islamiyatu fiy ahdi Amirul-Muuminin, uk: 69 Muasasatu al-Fikri al-Islamiy lilithaqati walIlaami – chapa ya kwanza.

55


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

akasema: “Hakika mume wangu amemwingilia kijakazi wangu bila ya ruhusa yangu (yaani amembaka).” Akamwambia mwanamume: “Unasemaje?” Akasema: “Sikumwingilia ila kwa ruhusa yake.” Akasema kwa kumwelekea mwanamke: “Kama wewe ni mkweli basi nitampiga mawe na kama wewe ni muongo tutakupiga viboko.” Swala ikakimiwa na Imamu Ali  akasimama ili kuswalisha. Mwanamke akafikiria katika nafsi yake hakuona njia ya kutokea katika kupigwa mawe mume wake wala yeye kupigwa viboko, akatoka na hakurejea, na Imamu Ali  hakumuulizia tena. Wakati ambapo Imamu  alikuwa anaweza kuamuru akamatwe na kuletwa mume wake na kuadhibiwa mmoja wao, lakini yeye  alikuwa hapendi kuadhibu. Alihifadhi haki na nidhamu na hakuwa anabeba katika maamuzi ya nafsi yake chuki ya kuadhibu watu, na alikuwa anasamehe kadri anavyoweza.28 Kumfanyia Wema Mkosaji: Ama hali nzuri zaidi ya kibinadamu katika maisha ya Imam Ali  ilionekana wazi katika wakati wa mwisho wa maisha yake matukufu, wakati wa kuamiliana na mtu ambaye alimpiga upanga naye yuko kwenye mihirabu ya swala yake. Abdurahmani bin Muljim alikimbia kutoka msikitini akitaka kutoroka ila makelele ambayo yalienea katika anga la Kufah yaliwatoa wengi katika nyumba zao kwa kumtafuta muuwaji wa Amirul-Muumina katika vichochoro vya Kufah, na njia za Kufah zikaziba mbele ya Ibnu Muljim, hadi akakamatwa na baadhi ya wafuasi wa Ali  na wakamleta kwake. Wakati huo Imam 28

Shiraziy: Sayyid Muhammad Shiraziy katika al-Hukumatu al-Islamiyatu fiy ahdi Amirul-Muuminin, uk, 23 Muasasatu al-Fikri al-Islamiy lilithaqati wal-Ilaami – chapa ya kwanza.

56


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

alikuwa bado ameathirika na pigo la upanga wenye sumu na damu zinatiririka kutoka katika utosi wa kichwa chake, na wafuasi wake wanapiga kelele huyu hapa adui wa Mwenyezi Mungu tumeshakuletea ewe Amirul-Muuminina. Imamu akamwangalia kwa mtazamo wa huruma na sio mtazamo wa kulipiza kisasi na kuadhibu na akamwambia: “Ewe Ibnu Muljim je, nilikuwa ni Imamu mbaya kwako?” Ibnu Muljim akawa analia na anasema: “Hapana, lakini je, wewe utamuokoa ambaye yuko motoni?” Na ukaendelea muamala wake mzuri wa kibinadamu pamoja naye hadi pumzi ya mwisho ya maisha yake. Matabibu walieleza kwamba maziwa ndio dawa na chakula cha Imamu , watu wakajitolea hadi mafakiri na wasio na kitu katika mji wa Kufah, kuleta wanayoweza katika maziwa kwenye nyumba ya Imamu. Imamu Hasan alibeba moja ya gilasi za maziwa kupeleka kwa Ali, alipokunywa kidogo alimpa mtoto wake kiasi kilichobakia na akasema: “Mpelekee mfungwa wenu, mlisheni katika mnavyokula na mnywesheni katika mnavyokunywa muangalieni mfungwa wenu.” Na sio ajabu – matokeo ya hayo – wanayoyaitakidi baadhi ya watu kwamba Imamu kama angeishi angemsamehe Ibnu Muljim. Na haya yanaafikiana na msamaha wa daima wa Imamu. Kusamehe kosa: Hakika kiwango hiki cha juu cha mwanadamu ambacho kilizunguka shakhsiya ya Ali, ndio ambacho kimemnyanyua Ali katika daraja za juu za utukufu na kudumu, ni mara chache kukuta mfano huu isipokuwa katika shakhsiya ya ustadhi wake na mwalimu wake, Mtume wa Mwenyezi Mungu . Imepokewa kwamba yeye  alikuwa amekaa na wafuasi wake, akapita kwao mwanamke. Mara watu wakamkodolea macho, 57


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

akasema : “Hakika macho haya ya mafahali yanatamaa na hakika hiyo ni sababu ya kuangamia kwake. Atakapoangalia mmoja wenu mwanamke anayemvuatia basi na amwendee mke wake, hakika yeye ni mwanamke kama alivyo mke wake.” Akasema mwanamume katika Makhhawariji: “Mwenyezi Mungu amlaani, ni kafiri anajua nini?” Watu wakamrukia ili wamuuwe. Akasema : “Taratibu tulieni – hakika ni tusi kwa tusi au kusamehe kosa.” 29 Na katika kumbukumbu ya Ali tunaweza kujifunza mengi na kushikamana na mengi katika mitazamo mitukufu na kudumu katika shakhsiya yake, isipokuwa uelewa wa upeo wa kibinadamu katika maisha yake yenye kudumu unabakia kuwa ndio upeo wenye mazingatio na umuhimu zaidi, ambapo mwanadamu anapata humo maendeleo ya kushangaza katika nyanja nyingi za maisha yake na anaweza kughafilika kwamba mafanikio yake hayatokamilika kama ukikosekana uwepo wa nyanja hii. KUKATAZA MAOVU NI HURUMA NA KUFANYA MAREKEBISHO Uislamu unaheshimu uhuru wa mwanadamu na kuupa umuhimu mkubwa katika sharia zake na mafunzo yake. Uhuru katika mtazamo wa Uislamu ni jambo tukufu haijuzu kuligusa wala haijuzu kwa mwanadamu mwenyewe kuvuka katika uhuru wake na kugeuka kuwa ni mtumwa wa mwingine: “Usiwe mtumwa wa mwingine wakati Mwenyezi Mungu ameshakufanya huru.”30 Na haijuzu kwa wengine kufanya uadui uhuru wa watu “Tangu lini mmewafanya watu watumwa wakati mama zao wamewazaa wakiwa huru.” 29

Al-Musawiy: Sharifu Ridhaa katika Nahjul- Balaghah, Qisqaaru al-hikam namba 420. 30 Al-Musawiy: Sharifu Ridhaa katika Nahjul-Balaghah, barua ya 31

58


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Na hakuna kugawanya katika uhuru wa mwanadamu bali umeenea nyanja zote za maisha yake, nazo zinalindwa katika kufuata kwake dini, itikadi na mwelekeo, nao unaagaliwa katika juhudi yake ya kiuchumi, kiasi kwamba mafakihi wamenufaika katika jumla ya hukumu za miamala, na kupata kanuni ya jumla, jina lake ni kanuni ya umiliki “watu ni wamiliki wa mali zao.” Vivyo hivyo katika kila jambo ambalo maamuzi yake yanahitajia matakwa ya mwanadamu mwenyewe. Pamoja na Uislamu kutambua uhuru huo kwa namna ambayo haijafika katika kiwango chake dini wala ustaarabu mwingine wowote, isipokuwa ni kwamba kuna baadhi ya wajibu wa kisharia ambao mwanadamu anaweza kudhani kwa mara ya kwanza kuwa unapingana na uhuru wa mwanadamu. Baadhi wanaweza kuuliza uko wapi wajibu wa kuamrisha mema na kukataza maovu sambamba na Uislamu kudhamini uhuru wa mwanadamu? Kuamrisha mema na kukataza maovu dhahiri ni kuingilia uhuru wa wengine kwa sababu unaamuru kitu walichokiacha wengine kwa uhuru wao na matakwa yao, na unawakataza kitu walichokifanya kwa matakwa yao na maamuzi yao, vinginevyo kama wangekuwa wamelazimishwa basi kusingekuwepo na haja ya kuamrisha mema na kukataza maovu. Hata daraja za chini kabisa za kuamrisha na kukataza zinadhamini katika uhalisia wake kupinga kitendo cha mwingine katika uhuru wake, hatua ya kwanza ya ulazima wa kuamrisha mema na kukataza maovu ni kupinga kwa moyo, ama hatua ya pili ni kubadilisha kwa ulimi na tatu ni kubadilisha kwa mkono, na hiyo ni kwa mujibu wa kauli ya Mtume wa Mwenyezi Mungu : “Mwenye kuona miongoni mwenu uovu basi na auondoe kwamkono wake, asipoweza basi kwa ulimi wake, na kama hatoweza basi achukie kwa moyo wake, na hiyo ni imani dhaifu kabisa.”31 31

Al-Qashiiriy, Muslimu bin al-Hajaji katika Sahihi Muslimi hadithi ya 78.

59


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Hatua hizi tatu ni kuingilia katika uhuru wa wengine na matakwa yao kwa dhahiri? Namna gani tunafahamu kuamrisha mema na kukataza maovu katika duara la ufahamu wetu juu ya uhuru wa mwanadamu? Na ulazima wa ufahamu huu ni kwa ajili ya kuondoa mkanganyiko na kutokuelewa ambako kumetokea kwa baadhi ya watu ambao wameacha wajibu huu kwa sababu ya kufahamu vibaya, kwamba hakika kunapingana na uhuru wa wengine. Unapowauliza baadhi ya watu: Kwa nini humuamrishi mema au hukatazi maovu? Jibu linakuwa: Tutafanyaje watu wanatumia uhuru wao. Hata wanaofanya maasi na maovu unapowaamuru au kuwakataza juu ya jambo jibu lao linakuwa: Wewe inakuhusu nini? Mimi niko huru nafanya nitakayo! Na baadhi yao wanakuambia kwa maneno makali: Hakika wewe hutaungua kwa moto wangu hivyo niache na mambo yangu. Na haya kwa pande zote mbili ni mkanganyiko na ni kosa kubwa … kwa nini? Kwa sababu uhuru wa mwanadamu hauna maana nje ya duara la hukumu na wajibu wa kisharia kwa wengine, kama unavyoamuru Uislamu kuheshimu uhuru wa mwanadamu, hakika vile vile unawaamrisha wenye kukalifishwa kutekeleza faradhi ya kuamrisha mema na kukataza maovu, kwani ni moja ya faradhi ambazo zina umuhimu na huenda unazidi faradhi zingine kama vile swala, saumu, hija na zaka. Na katika haya anasema Imamu Ali  katika neno muhimu na lenye mazingatio: “Na matendo yote mema na jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu mbele ya kuamrisha mema na kukataza maovu ni kama vile tone katika bahari kubwa.”32 32

Al-Musawiy: Sharifu Ridhaa katika Nahajul-Balaghah – Qiswaaru l-hikami 374

60


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Na katika hadithi yake nyingine : “Kuamrisha mema ni bora kuliko amali za viumbe.”33 Na katika hadithi nyingine kutoka kwa Imamu al-Baaqir : “Kuamrisha mema na kukataza maovu ni njia ya Manabii, na manhaji ya wema, ni faradhi kubwa, kwayo husimamishwa faradhi, yanasalimika madhehebu na huhalalishwa chumo, yanarejeshwa yaliyodhulumiwa, inastawishwa ardhi, wanafanyiwa uadilifu maadui na mambo yanayooka.”34 Je, kuamrisha mema na kukataza maovu kunapingana na uhuru wa mwanadamu au laa? Jawabu: Hakika hakuna mgongano wala kupingana. Hiyo ni kwa sababu Uislamu umeweka faradhi hiyo ndani ya mpaka na upeo, haupingi uhuru wa mwanadamu, bali ni kinyume cha hayo, kwani unaulinda na unadhamini mafanikio ya mwandamu, na mpaka huu na upeo huu ambao Uislamu unautarajia katika faradhi hii ni: Kwanza: Kujali Maslahi ya Mwanadamu na Faida Zake: Kuamrisha mema na kukataza maovu hakika kunalenga kwa uhakika kumwepusha mwanadamu na makosa na hatari zenye kuangamiza ambazo anaweza kutumbukia humo, kama hakuzinduka juu yake. Unapomwamrisha mwanadamu anayepita katika barabara ili atanabahi na shimo katika njia yake ili asitumbukie humo, jambo hilo ni kwa ajili ya maslahi yake yeye mwenyewe, ili asitumbukie na kuumia. Hivyo haingii akilini wakati huo kukujibu kwamba wewe huhusiki katika hilo. Na vivyo hivyo unapompa nasaha mtu kuepuka kula chakula chenye sumu, sio sahihi kukuambia kwamba mimi niko huru na kwamba wewe hupaswi kuingilia mambo yangu, kwa sababu wewe katika hilo 33 34

Al-Amadiy al Tamimiy: Abdul-Wahid katika Ghurarul-hikam namba 1198 Al-Huru al-Amiliy: Muhammad bin al-Hasan katika Wasailush-Shi‟ah, Juz. 16 uk: 119 hadithi ya 21132.

61


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

unatarajia maslahi yake, lakini ni haki yake apate tumaini la usahihi wa kuamrisha kwako au kukataza kwako, na sio kupinga kuamrisha na kukataza kwako. Kwa sababu Uislamu unataka watu kuishi katika hali ya kushirikiana na kujali maslahi ya wengine, na kuenea katika nyoyo za wanajamii upendo wao baina yao wao kwa wao, hivyo umeamuru mmoja wao kumwamuru mwingine yale ambayo humo kuna maslahi yake, au kumkataza mwenzake yale ambayo humo kuna madhara yake “Mpendelee ndugu yako unayoipendelea nafsi yako na chukia kwake unayoyachukia kwayo.” Na hiyo ndio njia ya kuwalingania wengine ambayo Mwenyezi Mungu ameuamuru umma wa Nabii Wake Muhammad  waipite

َ ٌ ُ ُ َُ َ َ ُ َ​َ َ َ َ ‫ػشون َو َين َ ككىن َغك ِكن‬ ‫َولككخىن ِمك ى أ ىمككت َيككذغىن ِإلككى احأحك ِكر ويككأمشون ِبككاو‬ ِ ٰ ُ َ ُ َ ُ ‫ن‬ ِ ‫او ى ِ​ِشِ َوأولك ِن ًَ ُه ُ او ِفلخى‬ “Na lipatekane miongoni mwenu kundi linalolingania katika kheri na linalokataza maovu na hao ndio wenye kufaulu.” (Surat Aali-Imran; 3:104) Pili: Kuanza na Upendo wa Kweli kwa Mwanadamu: Vipi unapasa kuwa mtazamo wetu kwa wenye madhambi na maasi ambao ni wajibu waamrishwe mema au wakatazwe maovu? Baadhi ya watu wanaangalia maasi na wenye maasi bila ya mazingatio wala kujali na wanaburudika na hali wanayoiona! Na kufanya hivyo hakika ni: Kwanza: Hakika ni aina ya ubinafsi kwa kutozingatia maslahi ya 62


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

wengine. Pili: Ni msimamo asiouridhia Mwenyezi Mungu, kwani wenyewe kwa dhati yake ni maasi, kukubali maasi na kuyanyamazia ni maasi kwa Mwenyezi Mungu. Kisha hakika maasi yote hayo ni madhara kwa maslahi ya jumla ya jamii, kwa sababu kubakia maasi bila ya kuyabadilisha inamaanisha hatari kwa wanajamii ya kupatwa na hali hiyo. Na wengine wanaweza kuchukua msimamo wa kinyume kwa wenye maasi, nao ni msimamo wa kisasi na kumalizana nao. Na msimamo huu ni kosa kubwa, hiyo ni kwa sababu Uislamu unataka kwetu tuwaangalie waasi kwa mtazamo wa huruma na upole. Huyu mwanadamu mwenye kutenda maasi si kingine ila ni mtu mgonjwa katika roho yake na nafsi yake, na sio katika mwili wake na kiwiliwili chake. Je inajuzu kwa yeyote anapomuona mgonjwa amchukie na ammalize? Je, Daktari anayetibu alipize kisasi au ni wajibu wake amhurumie kwa hali yake na kufikiria matibabu yake? Ilitokea wakati wa Nabii  kwamba alipelekewa mnywa pombe. Nabii akawaamuru Masahaba wake wamwadhibu, kisha wakasema: “Je, huoni haya kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu  kufanya haya?” Kisha akaachiwa. Alipoondoka watu wakawa wanamuombea laana na wanamtukana. Anasema msemaji: Ewe Mwenyezi Mungu mfedheheshe! Ewe Mwenyezi Mungu mlaani? Nabii  akasema: “Msiseme hivyo, msimlaani, msimsaidie shetani kwa ndugu yenu, lakini semeni: Ewe Mwenyezi Mungu msamehe. Ewe Mwenyezi Mungu muongoze.”35 Na makusudio ya nasaha, kuamrisha mema na kukataza maovu ni kutibu maradhi ya mwenye dhambi na mwenye kuasi. Ni lazima 35

Al-Kaandhalawiy: Muhammad Yusufu katika Hayatu Swahabati, Juz. 3 uk: 512, chapa ya Darul-fikri Beirut - Lenanon chapa ya kwanza 1974.

63


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

aanze matibabu kwa njia yenye madhara machache na muhimu kwa shakhsiya yake, na uadui shutuma, chuki na laana hazitotatua tatizo, bali inaweza kuongeza king‟ang‟anzi katika maasi. Ama kumuombea uongofu na mafanikio, na kufuata hekima na mawaidha mazuri katika mazungumzo pamoja naye yatakuwa na athari kubwa kwake katika kumili moyo wake na kubadilisha nyendo zake, na kwa hiyo inapasa kwa warekebishaji na watoa nasaha wafikirie katika mbinu na namna inayofaa kwa hilo, kama vile kuanza kwa mazungumzo pamoja naye kwa njia inayovutia, na kwa nukta iliyo mbali na maudhui ya maasi na dhambi yenyewe, ambapo mrekebishaji anaweza kupata upendo kwanza kisha anaelekeza kwake baada ya hayo angalizo au tanbihi inayohusiana na kosa na dhambi ambayo ameifanya, na hii ndio njia ya warekebishaji. Tatu: Kuchunga Hali ya Jumla ya Mwanadamu: Kiasi kwamba mrekebishaji anahifadhi kutomfedhehesha mwenye dhambi na kutangaza dhambi yake. Kuamrisha na kukataza ni wajibu na ni faradhi, isipokuwa kuvunja heshima ni haramu na mtendaji wake anaingia katika wale ambao Mwenyezi Mungu amewahesabu katika

َ ‫شيؼ الفٰكد َش ُت فى ىال‬ َ ‫”إ ىن ىال‬ َ ‫زين ُيد ّبى َن َأن َح‬ َ ‫زين‬ “…..‫ءام ىا‬ ِ ِ ِ ِ “Hakika wale ambao wanapenda kueneza uchafu kwa walioamini…..” (Surat An-Nur; 24:19)

Na maadamu mvunjaji hajatoa ushahidi wa kisharia juu ya usahihi wa madai yake na tuhuma yake kwa mwenye dhambi katika kutokea kwake, hakika inajuzu kwa mwenye kutuhumiwa kupeleka mashitaka ya kisharia kwa mtawala wa kisharia na kumwadhibu kwa kumzulia uongo na wala haijuzu kwa mtawala 64


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

wa kisharia mwenyewe kumtuhumu mtu kwa dhambi maadamu hana ushahidi. Ilitokea katika zama za khalifa Umar bin Khattab kwamba yeye alikuwa anatembea usiku mmoja, akamuona mwanaume na mwanamke wanafanya uchafu. Kulipokucha akawaambia watu: Je, mnaonaje kama kiongozi akiona mwanaume na mwanamke wanafanya uchafu na akawaadhibu mtafanyaje? Wakasema: Hakika wewe ni kiongozi. Akasema Ali bin Abi Twalib  hilo sio lako, hivyo utaadhibiwa, hakika Mwenyezi Mungu hakuamini jambo hili chini ya mashahidi wanne, kisha akawaachia aliyowaachia Mwenyezi Mungu, kisha akasema waulize watu. Wakasema mfano wa maneno yao ya kwanza na Ali akasema mfano wa maneno yake ya kwanza, na Umar akachukua kauli yake.36 Haya ni ikiwa mwenye dhambi na muasi anafanya maasi mbali na macho ya watu au bila ya kutaka kudhihirisha ufuska na maasi. Ama anayefanya maasi hadharani mbele ya watu basi amesha fedhehesha nafsi yake na wakati huo hakuna uharamu kwake kwa sababu hajavunja yeyote heshima yake bali yeye ndio ambaye amevunja heshima ya nafsi yake. Na tofauti ni kubwa baina ya mwenye kufanya dhambi kwa kuathirika pande kati ya pande za udhaifu wake, na baina ya anayeng‟ang‟ania maasi hata mbele ya watu. Huyu wa pili inajuzu kwake kuvunja heshima yake kwa sababu hajasitiri nafsi yake. Ama wa kwanza inapasa kumsaidia kuvuka hali ya udhaifu, na kusitiri dhambi yake ni kati ya hatua muhimu katika nyanja hii, ambapo kubakia utajo mzuri mbele ya watu itakuwa ni sababu yenye athari katika kumtoa kwake kwenye dhambi. Kana kwamba sisi tunampa fursa ya kuishi kwa utukufu baada ya utajo 36

Al-Amin: Abdul-Husein, Juz. 6, uk: 53, Muasasatu al-Alammiy lilimatubuaati Beirut „- Lebanon chapa ya kwanza 1994.

65


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

wake kukaribia kuharibika, amesema : “Mwenye kumstiri muumini katika ovu basi kana kwamba amempa uhai mtoto mchanga aliyeuliwa.”37 Na amesema Imamu Hasan  katika haki ya rafiki: “Hakika akiona kwako pengo analiziba au akiona kwako jema analihesabu.” Na katika upande mwingine hutokuta mtu yeyote aliyeepukana na kasoro au dhambi, mwenye kuona aibu za yeyote katika ndugu zake haijuzu kwake kufurahia, kwa sababu hajui nini kitatokea kwake miongoni mwa madhambi katika mustakbali wake. Anasema Imamu Ali : “Usifurahie kosa la mwingine, hakika wewe humiliki kupatia kamwe.”38 Na maadamu mwanadamu hamiliki kinga ya kutofanya maasi, hakika ni wajibu wake asimfedheheshe mwingine, vinginevyo Mwenyezi Mungu atamfedhehesha. Je mwanadamu anataka fedheha katika nafsi yake? Anasema Nabii : Usifuatilie aibu za waumini, hakika mwenye kufuatilia aibu za waumini Mwenyezi Mungu atafuatilia aibu zake, atamfedhehesha hata ndani ya nyumba yake.”39 Na imetokea kwa mtu mmoja kwamba alikuwa ni mwingi wa kufichua aibu za watu, na nasaha hazikumfaa kuacha hayo, hadi ikaja siku moja ambayo Mwenyezi Mungu alimfedhehesha mbele ya watu katika aibu zake na dhambi zake ambazo alikuwa anazifanya ndani ya nyumba yake. Na hiyo ni kwa ulimi wa mke wake ambaye alihitalifiana naye akawaambia watu aibu zake na maovu yake yote. Mtu mmoja alimuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu  akase37

Al-Hindiy: Ali al-Mutaqiy katika Kanuzl-Umaal, Juz. 2, uk: 249, hadithi namba 6388 38 Al-Amadiy Tamimiy: Abdul-Wahid katika Ghurarul-Hikam, fasil 85 hadithi namba 144 39 Al-Majlisiy: Muhammad Baaqir katika Biharul-Anuwar, Juz. 7, uk: 214

66


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

ma: Napenda Mwenyezi Mungu asitiri aibu zangu, nifanye nini? Akasema : “Sitiri aibu za ndugu zako Mwenyezi Mungu atasitiri aibu zako.”40 Bali hata katika Akhera Mwenyezi Mungu atasitiri aibu za wenye dhambi kwa fadhila za kusitiri kwao aibu za ndugu zao katika dunia, amesema : “Mwenye kumsitiri ndugu yake katika ovu aliloliona kwake Mwenyezi Mungu atamsitiri katika dunia na akhera.”41 Hakika kuamrisha mema na kukataza maovu sio tu ni chukio linalochemka analolitoa mwanadamu kwa mwenye madhambi, na sio tu ni wasila kati ya wasila wa kudhihirisha aibu bali ni raghaba ya kweli ndani ya mrekebishaji kwa ajili ya kubadilisha hali ya mwenye kuwa nayo kwenda kwenye hali nzuri zaidi. Hivyo na uwe wasila wake ni neno jema, njia inayopendeza na dua njema, maadamu ni wasila wenye kuathiri kwa watu na ni wenye kuhitajika kisheria. Anawalingania waasi: Na katika mazuri yanayonukuliwa katika kisa cha mwanachuoni mchamungu aliyejulikana kwa jina la Maarufu al-Karikhiy, ambaye ni kati ya wafuasi na wanafunzi wa Imamu Ridhaa , ametajwa na Ibnu al-Jauziy katika kitabu chake SwafuwatusSwafuwah ni kwamba: Maarufu alikuwa amekaa katika ufukwe wa mto Dijilah, wakapita vijana na mtumbwi, wanapiga makasia na wanakunywa. Ibrahim al-Atwirashi akamwambia na alikuwa pamoja naye: “Je, huoni hawa wanamwasi Mwenyezi Mungu, waombee.” Akanyanyua mikono yake mbinguni na akasema: “Ewe Mungu Wangu na Bwana Wangu! Nakuomba uwafurahishe peponi kama ulivyowafurahisha katika dunia.” Wakastaajabu 40 41

Al-Raishahariy: Muhammadi katika Mizanul-Hikimah, Juz. 7, uk: 145. Rejea iliyotangulia uk: 145

67


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

wafuasi wa Maarufu kwa dua hii, Maarufu akasema kwa kufafanua: “Kama Mwenyezi Mungu atawafurahisha katika akhera atawasamehe duniani, na wala hawatowadhuru ninyi kwa chochote.”42 Hivi ndivyo inavyopaswa uwe mtazamo wa muumini kwa wenye madhambi. Na hivi ndivyo alivyokuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu  hata pamoja na washirikina. Kila washirikina wanapozidi uasi na ukaidi hilo halikumzidishia ila subira na uvumilivu na kumnyenyekea Mwenyezi Mungu na kuwaombea awaongoze kwani wao hawafahamu! Na historia haijatutajia kwamba Nabii  aliwaombea maangamizi washirikina hata mara moja. Amesema swahaba Abdillahi bin Masuudi: “Kana kwamba mimi namtazama Nabii  anamzungumzia Nabii kati ya manabii, ambaye alipigwa na kaumu yake wakamtoa damu naye anapangusa damu usoni mwake na akasema: Mola Wangu wasamehe kaumu yangu hakika wao hawajui.” Na amesema Kadhi Ayaadh katika Shifaa: Hakika alipovunjwa meno yake ya mbele na akachanwa uso wake siku ya Uhudi, hilo likawa zito sana kwa masahaba wake wakasema: Walaani? Akasema: “Hakika mimi sijatumwa kuwa ni mwenye kulaani lakini mimi nimetumwa kuwa ni mlinganiaji na rehema. Ewe Mwenyezi Mungu waongoze kaumu yangu hakika wao hawajui.”43 Ama Imamu Husein  imenukuliwa kutoka kwake kwamba yeye alionekana analia Karbalaa, mmoja wa wafuasi wake akamuuliza. Ewe Mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu unalia kwa yaliyokufika? Akasema : “Hapana, nalia kwa ajili ya 42

Al-Answaariy Shaaraniy: Abdul-Wahaab bin Ahmad, katika Mukhitaswar Kitabu Swawafuti as Swafuwah, uk: 232 chapa ya nahadhwatu alHadioithah – Makkah 1967 43 Al-Qazuwiniy: Hasan Murtadhwa, katika Rasulul-Akram Madrasatul Akhilaaq, uk: 187 – 187, Darul bayaan al-arabiy chapa ya kwanza 1991.

68


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

hawa watu hakika wao wananiua na wataingia motoni kwa sababu yangu.� Ama wale ambao upeo wao ni mfinyu hakika wao wanaishi kwa uadui hata na watu waliokaribu sana nao, hawahisi kosa kwao ila wanawashambulia, wala hawagundui kwao dhambi ila wanaitangaza miongoni mwa watu. Hakika faradhi ya kuamrisha mema na kukataza maovu kama itatekelezwa katika mipaka yake na udhibiti wake haitapingana na uhuru wa mwanadamu. Bali hakika itanyanyua kiwango cha uelewa wa mwanadamu kwa uhuru wake, na itakuwa ni sababu ya kurekebisha mianya ya hali ya kijamii na kumnyanyua kwenda katika kiwango bora kinacholeta maslahi ya jumla, na kinachodhamini mafanikio ya wote. UJUMBE WA MANABII IMANI NA UTEKELEZAJI Mwanadamu anahitaji mwongozo wa Mwenyezi Mungu unaomwelekeza katika mambo mbalimbali ya maisha yake. Na mwanadamu alishapata uongofu huo katika mikono ya watu aliowachagua Mwenyezi Mungu ili kufikisha ujumbe Wake kwa watu, nao ni Manabii. Na baadhi wanaweza kudhani kwamba mwanadamu maadamu anamiliki akili basi hahitajii Manabii, kwa sababu akili inampa mwanadamu uwezo wa kupambanua kheri na shari, na kujua manufaa na madhara, jema na ovu. Na swali hili linaweza kuzunguka katika akili ya mwanadamu wa kileo, kama lilivyokuwa linaulizwa wakati uliopita, isipokuwa uelezaji wake leo unatimia kwa njia ya kina zaidi na yenye nguvu zaidi kuliko ilivyokuwa inaulizwa mwanzo. Hiyo ni kwa sababu mwanadamu ameweza kufikia kwa akili yake mafanikio makubwa, amezidi kuiamini akili yake kiasi anadhani kwamba amefikia kwenye kilele cha kujitegemea, na kwamba hahitaji upande mwingine wa nje. Na jawabu la swali hili na shaka hii, ni lile lile ambalo watu wa 69


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Mungu na wapwekeshaji waliwauliza wakanushaji, watu wa maada na wapinga utume. Swali halikubadilika bali limezidi kuulizwa, na jawabu pia halijabadilika bali limezidi kuwa wazi. Mwanadamu anahitaji kuwa na mawasiliano na mbinguni na mwongozo wa Mwenyezi Mungu katika nyanja tatu: Kwanza: Haja ya Kupata Maarifa: Akili pamoja na nguvu na uwezo inayoumiliki ila hakika haiwezi kujua kila jambo, na kupenya vizingiti vyote na vizuizi vyote, ambavyo vinasimama mbele ya njia ya kupata ziada ya majibu na maarifa anayoyatafuta. Na jambo muhimu ni kwamba mambo ambayo akili inashindwa kutoa majibu yenye kutosheleza ni mas‟ala muhimu na makubwa na nyeti sana, yanahusiana na msingi wa mwanadamu, kukua kwake na lengo la kuumbwa kwake na kutengenezwa kwake, samabamba na mpangilio huu wa kiulimwengu ambao unamzunguka, na mustakabali ambao unamsubiri hapo baadaye. Ni ipi hiyo nguvu ambayo imetuumba na ni ya namna gani? Na ni yapi mazingira ya mafungamano yetu Nayo na mafungamano Yake kwetu? Na mas‟ala haya akili haiwezi kuyajibu. Ndio, inaweza kuamua kwamba hakuna muumba na kwamba yeye hakuumbwa kutoka katika hali ya kutokuwepo, na kwamba hakuumba nafsi yake yeye mwenyewe

َ َ َ َ ٰ ُ َ ِ‫أم ِللىا ِمن غ ِ​ِحر ش ٍىء أم ُه ُ احأك ِللىن‬ “Au wao wameumbwa pasipo kutokana na chochote; au wao ndio waumbaji” (Surat At--Tur; 52:35) Isipokuwa hawezi kujibu zaidi ya haya, sio kwa sababu ya kasoro iliyopo katika dhati ya akili, bali ni kwa sababu Mwenyezi 70


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Mungu Mtukufu hakumpa zaidi ya uwezo huu. Na wahyi wa Mwenyezi Mungu ndio unaoweza kujibu mas‟ala haya, na bila ya hayo mwanadamu ataishi bila ya kujua sababu ya kuwepo kwake na lengo la kubakia kwake, na hilo litaathiri katika kufikia mafanikio yake, kwa sababu atabakia mwenye kukanganyikiwa, mwenye huzuni na mwenye mashaka. Na hata kama akifikia utatuzi wa matatizo yote ya kielimu na maarifa mengine na yakabakia mas‟ala haya ya msingi bila ya maarifa yanayokata kiu yake humo, hiyo itakuwa ni huzuni na sababu kati ya sababu ya uovu wake na ubaya wake. Na namna gani akili hii itafikia yenyewe ukweli huo? Kwani bado haijajua maalumaati yote ya kimaada yanayohusika ambayo anayahitajia, na wanakiri hilo wataalamu ambao walikuwa ni viongozi wa uvumbuzi wa kielimu. Huyu hapa Albert Einstein, anasema: “Hakika kiasi cha maalumati yangu katika nisiyoyajua ni kama kiwango cha ngazi hii ndogo katika maktaba yangu mbele ya maktaba pana na kubwa.” Yaani hakika asiyoyajua ni mengi zaidi na zaidi kuliko anayoyajua. Na siashirii katika ukweli huu kumteremsha mwanadamu upande wa kuongezeka elimu yake na maendeleo ya maalumati yake na fikra zake. Mwanadamu kila siku anavumbua elimu au kanuni ya elimu mpya, ambapo inamaanisha kwamba kuna vitu vingine atavivumbua katika mustakabali, na hivi sasa havijui. Na ukweli ni kwamba mwanadamu aghlabu anafikia kwenye hatua ya juu katika elimu kwenye maalumati muhimu zaidi kuliko maalumati ya zamani. Na ikiwa hajui ukweli wote wa kimaada, namna gani atajua ukweli wa ghaibu kuhusu mwanzo wake na mwisho wa hatima yake? Nayo ni maarifa ya lazima ambayo anayahitajia kabla ya maarifa yoyote mengine, namna gani atamjua ambaye amemuumba, na kwa nini amemuumba na nini hatima yake? - Hivyo ima mwanadamu abakie kuwa ni mwenye kupotea 71


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

kuhusu mas‟ala haya ya lazima na muhimu juu yake daima. - Na ima iingilie huruma ya Mwenyezi Mungu Mjuzi ili kuwaonyesha waja juu yake na kwa mitume Wake, kwa sababu (swt) ametakasika na kuwanyima waja Wake maarifa ya lazima kwao, na ametakasika vilevile kuwapa waja Wake hoja dhidi Yake wakawa na udhuru Kwake Siku ya Kiyama, kwamba wao hawakutii kwa sababu wao hawakuwa wanamjua, wala hawakuwa wanajua mas‟ala ya lazima kwa ajili ya uongofu wao katika ibada Yake na utii Kwake, akatuma (swt) Mitume ili iwe ni hoja ya wazi katika kuumbwa kwake. “Sema Mwenyezi Mungu ana hoja ya wazi.” (Suratul- An‟ am: 149), na amesema (swt):

‫َ ى‬ ّ َ َ َّ َ َ ٌ َُ َ ّ َُ ًُ ُ ‫اط َغهى الل ِكه ُح ىجت َ ػذ‬ ِ ‫”سظًل مب ِششين وم ِزسين ِلنًل يىىن ِلل‬ “….. ‫ل‬ ِ ِ ‫الش ُظ‬ “Mitume wabashiri na waonyaji ili isije ikawa watu wana hoja dhidi ya Mwenyezi Mungu baada ya Mitume.” (Surat An-Nisaa‟; 4:165). Hakika utume unaiongezea akili ukweli thabiti wa ulimwengu huu wa ghaibu, unaelekeza hisia za mwanadamu na unaijuza na kuielimisha juu ya ukweli na kuipatia njia ya kuwasiliana nayo. Pili: Haja ya Kijamii: Watu wanaishi kwa kujumuika baadhi yao na baadhi, hivyo ni lazima kuwepo na utaratibu wa kuendesha mambo yao na kuweka kanuni za uhusiano baina yao. Na kuweka nidhamu ya kijamii ya jumla, inalazimu kumjua kwa kina mwanadamu katika tabia zake, utashi wake na raghaba zake, kama ambavyo inalazimu kujua kwa umakini ulimwengu ambao unamzunguka mwanadamu, na maisha ambayo anaishi. Na namna gani 72


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

yatapatikana haya maarifa na kuyajua kama si kutoka kwa Mola wa mwanadamu na ulimwengu?

َ َ َ ُ َ​َ ُ ُ َ ُ َ َ​َ َ​َ​َ َ ُ ُ َ َ​َ َ ٰ ‫كش ُل ِإل ِيه‬ ‫ظىط ِب ِه فع ِهِ و دن أ‬ ِ ‫وللذ لل ا ِإلاقعكن وقػل ما جى‬ َ ‫من َخبل‬ ِ​ِ ‫الى‬ ‫سيذ‬ ِ ِ “Na hakika tumemuumba mtu, na tunayajua yana-yoitia wasiwasi nafsi yake. Na Sisi tuko karibu naye kuliko mshipa wa shingo.” (Surat Qaf; 50:16) Katika upande mwingine hakika kuweka sharia ya utaratibu wa kijamii wa jumla inahitajia usafi wa kimaudhui, kiasi kwamba mwenye kuweka sharia asifungamane na pande zote au asinyenyekee kwenye maslahi au asiathirike na raghaba au matamanio. Na mwanadamu anapotegemea nafsi yake katika kuweka utaratibu kama huu, hakika ataingia katika tajiriba yenye kufeli moja baada ya nyingine. Na historia ya leo inatuonyesha namna gani nusu ya jamii ya binadamu takriban imekabiliwa na tajiriba ya ujamaa wa kikomonisti hadi ikaporomoka, na nini kinamkabili mwanadamu hivi sasa katika utawala wa kibepari wa kimagharibi, ambao wanadai baadhi watazamaji wake kwamba ni mwisho wa historia kulingana na maneno ya Yoshihiro Francis Fukuyama. Kwa sababu hiyo wenye kuamini Mungu wanaitakidi kwamba binadamu anahitaji mwongozo wa Mwenyezi Mungu, ambao unampa uratibu wa kijamii unaotengeneza mambo yao na kuelekeza nyendo zao kuelekea kwenye mafanikio na ukamilifu. Tatu: Haja ya Kitabia: Mtazamo wa mwanadamu kwenye kanuni inayomhukumu hutofautiana kwa kuzingatia inatoka kwa nani. Inatoka kwa 73


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

wanadamu wenyewe au inatoka kwa Muumba wa binadamu. Inapokuwa ni kanuni ya kibinadamu wakati huo hakika mwanadamu huwa hahisi kulazimika kwa kina katika kushikamana nayo, na kujizuia kuikhalifu kwake, na kwa hiyo anaweza kufanya hila juu yake na kuiacha huku akidai kwamba anaitekeleza. Ama inapokuwa kanuni husika ni ya mbinguni na kwamba aliyeamrisha ni Muumba wa watu, hakika kanuni hii itamiliki, wakati huo – nguvu ya ndani katika nafsi ya kila mtu, inayomsukuma katika kuitekeleza, kwa kuitakidi kwamba, ambaye amemuumba anamwangalia katika vitendo vyake na shughuli zake zote na kwamba Yeye atamhisabu kwa kukhalifu kwake. Na huenda baadhi wakapinga na kusema kwamba, tabia hii wakati huo itakuwa ni mwenendo uliolazimishwa kwa mwanadamu, kwa kitendo cha nguvu kuu, naye ni Mwenyezi Mungu Mtukufu, wakati inapasa kitendo cha kitabia kiepukane na mbinyo na kulazimishwa. Isipokuwa ni kwamba upinzani huu sio madhubuti, kwa sababu kitendo kitatokana na matakwa ya mwanadamu huru. Ama kuhusu Mwenyezi Mungu Mtukufu, yeye analipa mema na anaadhibu katika uovu, hili ndio lengo la uadilifu na mwanadamu kuwa ni mwenye hiyari. Na inacholenga kanuni na sharia za mbinguni ni kumfanya mwanadamu katika nafsi yake awe ni mwenye kupewa tabia safi ya kimaumbile ambayo inaafikiana pamoja na imani na itikadi, na itikadi iwe ndio yenye kusukuma na kuendesha vitendo vya kheri, na uwe ni mwenendo mwema kwa kuakisi wema wa itikadi na usafi wa imani. Watu wa Mada na Utekelezaji wa Sharia: Mwanadamu kujiuliza juu ya haja ya kuwepo Manabii hilo ni swali la kawaida, ambalo linapelekea kuamini Manabii, kama atatumia akili yake na fikra yake kwa namna ya kimaudhui na ya 74


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

kimantiki. Ama Mwislamu na mwenye kumwamini Mtume na mwenye kukubali ujumbe wake, kuuliza juu ya haja ya kutekeleza sharia ambayo amekuja nayo Mtume kutoka kwa Mola Wake, swali hilo ni geni na la ajabu sana!! Kwa sababu maana ya kukubali na kumwamini Mtume, Mwislamu anaposema: “Nashuhudia kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu” ni kunyenyekea sharia yake na kutekeleza ujumbe wake:

ُ َ َ َ ُ ُ ‫الشظى ٌُ َف ُخ‬ ٰ ‫… َوما‬..” ‫ءاجى ُى ُ ى‬ “….. ‫زوه َوما ن ٰىى َغ ه فا ت ىا‬ “…Na anachowapa Mtume kichukueni na anachowakataza jiepusheni nacho.” (Surat AlHashr 59:7) Maadamu unaamini kwamba yeye ni Mtume, na kwamba aliyokuja nayo ni ujumbe kutoka kwa Mwenyezi Mungu kuja kwako, namna gani inajuzu kwako kuuliza au kushuku au kusitasita katika utekelezaji wake? Hakika inasikitisha sana kusikia baina ya wakati mmoja na mwingine kwamba, baadhi ya Waislamu katika nchi ya Kiislamu wanasita kutekeleza sharia. Kama ambavyo inasikitisha kwamba kudai tu kutekeleza sharia katika baadhi ya nchi za Kiislamu ni kosa ambalo dola inaadhibu juu yake. Na baadhi ya nchi za Kiislamu kuzuia baadhi ya mambo ya kidini kama vile hijabu na kusimamisha mambo ya Kiislamu. Na baadhi kuhesabu baadhi ya mambo haya au mengineyo ni kosa analotuhumiwa mwanadamu kwa sababu yake. Kama hali ilivyo Uturuki kwa mfano, nayo ni dola ya Kiislamu, bali ilikuwa kabla ya muda mfupi ni makao makuu ya ukhalifa wa Kiislamu, na wengi wa wananchi wake ni Waislamu, lakini kulingania kutekeleza Uislamu humo inazingatiwa kuwa ni kosa, na kuvaa hijabu katika taasisi rasmi ni kosa ambalo mtu anaadhibiwa kwalo kama ilivyotokea kwa mbuge Merve KAVAKÇI. 75


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Hakika baadhi ya watu kukataa kutekeleza sharia kunatokana na sababu kadhaa, miongoni mwazo ni: Sababu ya Kwanza: Sharia kutokuwa wazi na utaratibu wake kwa namna ya kutosha, na ni upi utaratibu wa Kiislamu tunaoutaka kuutekeleza? Na ni yapi mafunzo yake na vigezo vyake? Na ni ipi mipaka yake na miko yake? Waislamu wengi leo – kwa masikitiko – hawajui kwa ufafanuzi utaratibu wa kisiasa, kijamii, kiuchumi na wala hawaelewi ila baadhi ya hukumu na sharia za ibada, wakati ambapo upande huu hauwakilishi isipokuwa sehemu tu ya utaratibu kamili unaokidhi mahitaji yote ya binadamu, nao ni upande wa ibada. Na mara nyingine katika akili za watu fikra ya kutekeleza sharia hujifunga upande wa kutoa adhabu katika yale yaliyoharamishwa tu, na hilo ni jambo la kimakosa kwani adhabu ni sehemu ya utaratibu kamilifu. Na kama tukiweza kuuelezea na kuubainishia ulimwengu utaratibu wa Kiislamu kwa ukamilifu wake kwa njia inayofaa, yasingeulizwa maswali haya na sharia ingechukua nafsi yake katika jamii ya Kiislamu na ya kibinadamu. Sababu ya pili: Utekelezaji wa kupaka matope Uislamu katika zama za kihistoria zilizotangulia, ambapo Uislamu ulitumiwa kama pazia la vitendo vinavyopingana na haki za binadamu, na uadilifu wa kijamii. Bali baadhi ya utekelezaji wa kileo ambao unafanywa kwa jina la Uislamu kwa sura yake umeleta adha na uovu mkubwa, kama inavyotokea Afghanistan. Pamoja na kwamba kuna mifano yenye kuchanua na mizuri ya utekelezaji wa Uislamu katika wakati uliopita na hivi sasa, ila macho yanaelekezwa kwenye dhana mbaya zaidi na mifano inayojitokeza zaidi na iliyo mingi zaidi. Hivyo wengi wanaogopa utekelezaji wa Uislamu kuwa ni aina ya kurejea nyuma na kurejesha tajiriba mbaya katika historia au kuelekea hali mbaya katika wakati wa sasa. 76


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Sababu ya tatu: Kushindwa mbele ya fikra ya kimada ya kimagharibi: Fikra hiyo imesheheni elimu na teknolojia na maendeleo ya kijamii. Ama Waislamu wanaishi katika hali mbalimbali, wakati baadhi ya watu wanafikiri katika hali ya kutoendelea ambako wanaishi nayo Waislamu, wanafikiri kwa kudhani kwamba utatuzi ni kuacha dini na sharia!! Na matangazo ya kigeni, na utamaduni wa kimagharibi yana nafasi kubwa katika kueneza picha hii na kuiimarisha katika akili, hususani kalamu kutoka miongoni mwa Waislamu zinasambaza mahubiri ya fikra ya kimagharibi, sasa utatuzi uko wapi? Kwanza: Ni lazima kufungua mlango wa ijitihadi, kwa ajili ya kufichua na kuvumbua mifumo ya Kiislamu na ratiba zake, na kuvuka rundo hili katika picha iliyopakwa matope yenye makosa, na kuweka wazi mafuhumu ya Kislamu, na kubainisha mifumo na manhaji ya Kiislamu katika nyanja za maisha. Pili: Inapasa tusimamie tajiriba zetu za kihistoria na za sasa kwa kila ujasiri, ushujaa na upekee na tuweke wazi kwa ulimwengu na vizazi, pande zenye mwanga miongoni mwazo ambazo zinawakilisha Uislamu, na tutambue sehemu zenye giza humo ambazo ni kukhalifu Uislamu na hauziridhii. Na wala tusikubali kiukamilifu tajriba mbaya zilizotangulia na zinazonasibishwa na Uislamu. Tatu: Tujipambe na maanawiya yetu ya juu na wala tusishindwe mbele ya upakaji matope wake, na wala tusiache misingi yetu kwa mapambano na changamoto ndogo tu. Hakika ni wajibu wetu kuandaa nguvu zetu kubwa za kimaanawi na kufahamu kwamba sababu ya kurudi kwetu nyuma sio utekelezaji wa Uislamu, bali ni kinyume cha hayo. Hakika sababu ya kurudi 77


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

kwetu nyuma ni kuacha kuufanyia kazi Uislamu!! Vinginevyo hakika dini yetu ni dini ya haki nayo ni njia ya kumkomboa mwanadamu na kumuokoa kutokana na adhabu na mateso kama alivyosema mshairi: “Wanasema katika Uislamu kuna dhulma kwa sababu, unazuia watu wake njia ya maendeleo, ikiwa ni kweli vipi waliendelea, watangulizi wake katika zama yake ya mwanzo, ikiwa dhambi ya Mwislamu leo ni ujahili wake, Uislamu unahusikaje na ujahili wa Mwislamu?” Kisha hakika sisi katika mnasaba wa kumbukumbu ya utume wa Nabii ni lazima kila mmoja wetu afikiri yaliyo wajibu kwake kufanya katika kushikamana na ujumbe wa Nabii ) na sharia yake tukufu ambayo alikuja nayo. Vinginevyo sisi wakati huo tutakuwa kati ya wale wanaodai Uislamu nao hawautekelezi, na hivyo kuwa walengwa – Mwenyezi Mungu asijaalie hivyo – wa kemeo la aya:

َ َ َ َ َ َ ً َ ‫يٰك َأي َ ا ىال‬ َ ‫زين‬ ‫﴾ ه ُب َر َملخا ِغ َذ‬٧﴿ ‫ن‬ ِ ‫فػلى‬ ‫ءام ىا ِل َ جلىلىن ما ال ج‬ َ َ َ َ َ ‫ى‬ ﴾٣﴿ ‫ن‬ ِ ‫فػلى‬ ‫الل ِكه أن جلىلىا ما ال ج‬ “Enyi mlioamini! Kwa nini mnasema msiyoyatenda. Ni chukizo kubwa kwa Mwenyezi Mungu kusema msiyoyatenda.” (Surat As-Saf 61:2-3) UPANDE WA KIJAMII KATIKA MAISHA YA IMAMU HUSEIN  Hakika tunasherehekea kwa kuwakumbuka Maimamu watwaharifu  na tunaadhimisha minasaba ya Kiislamu ili tuungane 78


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

na historia kongwe, na tuchukue kutoka humo mafunzo na mazingatio katika yale yatakayotunufaisha kwa wakati wetu na kujenga mustakabala wetu. Na inapopita kwetu kumbukumbu ya uzao au kufa shahadi kwa Imamu kati ya Maimamu, hakika sisi tunazingatia ili tuangaziwe na sira ya Imamu huyo na tuongoke kwa maelekezo yake na mwongozo wake. Na kwa sababu sisi leo tupo katika kumbukumbu ya kuzaliwa bwana wa mashahidi Imamu Husein bin Ali , hakika sisi tutajaribu kuchukua dondoo katika maisha yake matukufu. Na ikiwa riwaya za kihistoria zimehitalifiana katika kuainisha tarehe ya kuzaliwa kwake je, ilikuwa ni katika mwaka wa tatu au wa nne hijiria? Je ilikuwa ni mwezi wa Shabani au ni mwisho wa mwezi wa Rabiul-Awwal, na je ni katika siku ya kwanza au ya tano ya mwezi wa Shabani, hakika ikhitilafu hii tunakabiliana nayo katika mengi ya matukio na historia, na maelezo ya watu wake, na hakuna tatizo katika kutegemea riwaya tunayoona ina nguvu zaidi katika kusherehekea mnasaba wowote muhimu, maadamu lengo ni kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kwa kuadhimisha alama Zake na kufaidika na uongofu wa mnasaba na utoaji wake. Upande wa Kijamii Katika Maisha ya Imamu: Na tutazungumzia – katika mnasaba huu – upande kati ya pande za maisha, upande tajiri wenye manufaa, nao ni upande wa kijamii katika sira yake tukufu. Na kwa kudokezea tu kwa haraka upande huu tunaufupisha kwa nukta tatu: 1. Uhudhuriaji wa kijamii 2. Mfano wa kitabia 3. Kuzingatia sehemu za udhaifu katika jamii. 79


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Uhudhuriaji wa Kijamii: Mwanadamu kubeba malengo makubwa au kumiliki kiwango cha juu cha elimu hakuathiri kitu katika harakati za uhalisia wa maisha, kama hakujaambatana na uhudhuriaji wa kijamii, unaoonyesha njia mbele ya malengo hayo makubwa, na kufasiri elimu kwa kitendo kinachoonekana. Na kwa hiyo Manabii na Maimamu walikuwa wanaishi ndani ya mazingira ya watu, na wanaamiliana pamoja nao na hawakuwa wanajitenga katika vilele vya milima au katika mapango na mabonde wala hawakuwa wanajinyanyua na kujikweza kwa watu katika maghorofa marefu. Na vyovyote kitakavyokuwa kiwango cha jamii katika kutoendelea na ujahili, au katika uovu wa mazingira ya ufisadi na upotovu, hakika hayo hayaleti kisingizio cha kukimbia na kujitenga na watu kwa warekeibishaji wa kimungu. Ni sahihi kwamba kuamiliana na watu ambao wanaishi katika hali ya ujahili na kutoendelea, au wanaonyenyekea katika mazingira ya ufisadi na upotovu, kunaweza kusababisha mengi miongoni mwa adha na taabu kwa watu wa Mungu, lakini hiyo ndio njia ya mabadiliko na marekebisho, kama ambavyo ni wasila wa kupata thawabu za Mwenyezi Mungu na radhi Zake. Imepokewa katika hadithi iliyopokewa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu  kwamba amesema: “Muumini ambaye anatengamana na watu na anasubiri katika adha zao ni bora kuliko muumini ambaye hatangamani na watu wala hasubiri juu ya adha zao.”44 Na katika hadithi nyingine ni kwamba  alimkosa mwanaume mmoja na akamuulizia akaja akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hakika mimi nilitaka kwenda kwenye mlima huu ili nijitenge humo na kufanya ibada. Mtume wa Mwenyezi Mungu  akasema: “Mmoja wenu kusubiria saa katika anayoyachukia katika baadhi ya nchi za Kiislamu, ni bora kuliko ibada ya kujitenga miaka arobaini.” Na katika ibara 44

Al-Hindiy: Ali al-Mutaqiy katika Kanzul-Umaali, hadithi namba 686

80


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

nyingine: “Miaka sitini.”45 Na Imamu Husein  amekuwa tangu mwanzo wa maisha yake ndani ya makuzi ya kijamii na ndani ya matukio, babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu  alikuwa ndio kitovu cha jamii na kiongozi wa juu, na baba yake  alikuwa ni waziri wa Mtume na msaidizi wake mkuu, bali alikuwa ni nafsi yake kama inavyosema Aya ya mubahala. Uwepo wake katika medani ni jambo la jumla na ni jambo la kawaida, kwa kuambatana kwake na babu yake Mtume  ambaye alikuwa anambeba mjukuu wake hata akiwa katika Swala, na anamchukua pamoja naye juu ya mimbari. Imepokewa kutoka kwa Abdillahi bin Buraidah kutoka kwa baba yake amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu  alikuwa anatuhutubia, mara akaja Hasan na Husein  huku wakiwa wamevaa kanzu mbili nyekundu wanaanguka na kusimama. Akateremka na akawachukua na akapanda nao kwenye mimbari.”46 Na katika msimamo ule nyeti baina ya Waislamu na manaswara Mtume  alipowaita katika mubahala, Husein alikuwa amebebwa katika mabega ya babu yake. Yeye na ndugu yake ndio watoto waliotajwa katika kauli yake (swt):

ُ َ ُ َ َ َ َ ُ َ َ​َ َ َ ُ َ َ َ ُ َ ‫عاءه َوأ ف َع ا‬ ‫…فلل حػالىا ذع أب اء ا وأب اءه و ِقعاء ا و ِق‬..” ُ ُ َ “….. ‫َوأ ف َعى‬ “…..Waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, wanawake zetu na wanawake zenu, na nafsi zeti na nafsi zenu…..” (Surat Aali-Imran; 3:61) 45 46

Rejea iliyotangulia hadithi namba 11354 Al-Sajastaniy: Abu Daud bin Suleiman bin al-Ash‟athi katika Sunan Abi Daudi, Juz. 1, uk: 358 hadithi namba 1109

81


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Na baada ya kufariki Mtume wa Mwenyezi Mungu  Husein aliikuta nafsi yake ndani ya machungu ya familia yake na mateso ya mama yake Zahraa , alikuwa anaandamana naye katika mizunguko yake katika nyumba za Muhajirina na Answari akitafuta haki yake.47 Na historia inanukuu msimamo wa Imamu Husein  katika mwanzo wa zama ya khalifa wa pili Umar bin Khattab, na Husein wakati huo alikuwa ndio kwanza anamaliza muongo wa kwanza katika umri wake: Anapokea Ibnu Hajar al-Asqalaaniy katika kitabu chake alIswabatu kutoka kwa Yahya bin Said al-Answariy kutoka kwa Ubaidullahi bin Hunain: “Amenisimulia Husein bin Ali akasema: Nilimwendea Umar naye anahutubia juu ya mimbari nikapanda kwake nikamwambia: „Shuka kwenye mimbari ya baba yangu, na nenda kwenye mimbari ya baba yako.‟ Umar akasema: “Baba yangu hakuwa na mimbari.” Na akanichukua akanikalisha pamoja naye nageuzageuza changarawe katika mikono yangu, alipoteremka akaenda nami katika nyumba yake akaniambia: Nani amekufundisha haya: Nikamwambia: Wallahi hakunifundisha yeyote. Akasema: Naapa kwa baba yangu natamani ungejaaliwa uwe unatutembelea mara kwa mara. Akasema: Siku moja nikamwendea, naye alikuwa amekaa faragha na Muawiya, na Ibnu Umar yuko mlangoni. Ibnu Umar akasimama bila kuingia ndani nami nikarejea. Baadaye akakutana nami akaniambia: Sijakuona. Nikasema: Ewe kiongozi mimi nilikuja, ulikuwa umekaa na Muawiya, basi nikarejea pamoja na Ibnu Umar. Akasema: Wewe una haki ya kuruhusiwa kuliko Ibnu Umar, hakika ameotesha unayoyaona katika vichwa vyetu Mwenyezi Mungu kisha nyinyi. Sanadi sahihi.48 47

Al-Qazuwiniy: Muhammad Kaadhim katika Fatimahtu Zahraa minal mahadi ilaa llahad uk: 407 chapa ya kwanza 1991 Muasasatu Nuur lilimatubuaati - Beirut. 48 Al-Asqalaaniy: Ibnu Hajar katika Iswabatu fiy tamyiizi swahabati Juz. 2, uk. 77 chapa ya kwanza 1992 Daru al-Jili - Beirut.

82


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Na katika kisa hiki kuna dalili za wazi zenye kuathiri, naye yuko katika umri mdogo anakwenda msikitini na anasema yaliyopo katika nafsi yake kwa khalifa, na anakiri kwamba kitendo hicho kimetokana na maamuzi yake mwenyewe, na hajaambiwa na yeyote, kisha anakwenda kumtembelea khalifa kwenye nyumba yake. Na tunamuona Imamu Husein katika zama za khalifa Uthman ameshajiunga na jeshi la Kiislamu kwa ajili ya ufunguzi wa Afrika, na jeshi lilikuwa chini ya uongozi wa Uqubatu bin Naafi‟i Abdi Shamsi, Abdillahi bin Nafii bin al-Harith, na humo kuna kundi la masahaba kama vile Abdillahi bin Abbasi, Ibnu Umar, Ibnu Ja‟far, Hasan na Husein. Kama ambavyo Husein alishiriki katika vita vya Waislamu pamoja na Waajemi huko Twabristaan na pande zake, na jeshi lilikuwa chini ya uongozi wa Said bin alAsi.49 Katika mkazo wa uwepo wake kijamii, majilisi yake ilikuwa katika msikiti wa Nabii, ambapo watu walikuwa wanamzunguka miongoni mwa wanaotafuta maarifa na watafuta elimu, na wenye shida, mtu alimuuliza Muawiya kwamba Husein anapatikana wapi? Akasema: Utakapoingia msikiti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu  ukiona mkusanyiko humo kuna watu wametulia kana kwamba juu ya vichwa vyao kuna ndege basi mkusanyiko huo ni wa Abu Abdillahi.50 Na ushahidi katika nyanja hii katika maisha ya Imamu ni mwingi hakuna nafasi ya kuelezea. Mfano wa Kitabia: Katika kuamiliana pamoja na jamii, anakuta mbele yake sehemu 49

Al-Husniy: Hashim maarufu katika Siratu al-Aimati al-Ithnaashara, Juz. 2, uk. 16 daaru taaruf lilimatubuaati – Beirut 1990. 50 Al-Qarashiy: Baaqir Saharif katika Maisha ya al-Imamu al-Husein, Juz. 1, uk: 137 chapa ya 1993 chapa ya Darul- Balagha – Beirut.

83


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

zinazotofautiana kiwango na tabia, na baadhi yao wanakabiliwa na chuki ya kinafsi, au upotovu wa kimwenendo, unaosukuma kwenye ubaya na uadui kati ya yanayosababisha mwanadamu kulipiza kisasi, na kujitetea dhati yake mbele ya sehemu hizi, na kukasirika kutokana na vitendo vyake. Lakini watu wa Mungu kwa mioyo yao mikubwa na nafsi zao za juu wanaelewa hali hizo na wanakabiliana nazo kwa upole, utulivu na wema. Na Imamu Husein  alikuwa ni kilele katika nyanja hii, alikuwa – katika ambayo wapokezi wamekusanya – haamiliani na muovu kwa ubaya wala na mwenye dhambi kwa dhambi yake, bali alikuwa anawahurumia kwa wema wake na ihsani yake. Jambo lake katika hilo ni jambo la babu yake Mtume  ambaye aliwaenea watu wote kwa tabia yake njema na fadhila zake na alijulikana kwa hali hii na ikaenea kwake, na baadhi ya watumwa wake walitumia fursa hii. Walikuwa wanakusudia kufanya ubaya kwake, ili waneemeke kwa uhusiano wake na wema wake. Wanasema wanahistoria: Hakika mmoja wa watumwa wake alifanya kosa kwake, kosa linalopelekea kutiwa adabu, akaamuru aadhibiwe, mtumwa akasema: Ewe kiongozi wangu, hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: “Na wenye kuzuia hasira.” Imamu akaamiliana naye kwa tabasamu la ukunjufu na akasema: “mwacheni, nimeshazuia hasira yangu…” Na mtumwa anafanya haraka “na wenye kuwasamehe watu.” Akasema: Nimeshakusamehe. Mtumwa akataka ziada ya wema kwa kusema: “Na Mwenyezi Mungu anawapenda wanaofanya wema.” Akasema: “Wewe uko huru kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.” Kisha akaamuru apewe zawadi nzuri inayomtosheleza kuomba na kuuliza watu.51 Na Marwan aliomba msaada wa uombezi kwake na kwa ndugu 51

Rejea iliyotangulia uk: 124

84


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

yake, naye ni kati ya maadui zao wakubwa baada ya kushindwa vita vya jamali na akaomba kwao uombezi kwa baba yao wakakaa faragha naye na wakamzungumzia kuhusu jambo lake na wakasema: “Atakupa baiya ewe Amirul-Muuminina.” Akasema: “Je hakunipa baiya baada ya kuuliwa Uthman, sina haja ya baiya yake, hakika ni mkono wa kiyahudi, kama atanipa baiya kwa mkono wake basi atafanya hiyana kwa kidole chake cha shahada.” Hawakuacha kumbembeleza hadi akamsamehe.52 Kuzingatia sehemu za madhaifu katika jamii: Unadhihirika ubinadamu wa mwanadamu na kusadikisha imani yake kwa kuwajali kwake wenye haja na mafakiri katika jamii vyovyote atakavyofikia mwanadamu katika elimu, au akijitahidi katika ibada. Hakika hautotimia ubinadamu wake wala hautasihi uswalihina wake atakapopuuza sehemu za udhaifu katika jamii. Je hajasema Mola Wetu:

َ َ َ​َ ّ ‫يذ ىالزي ُي َى ّز ُل ب‬ َ ‫﴾ َف ٰزل ًَ ىالزي َي ُذع‬٧﴿ ‫ين‬ ‫﴾ َوال‬٧﴿ َِ ‫اليدي‬ ِ ِ ‫الذ‬ ‫أس ء‬ ِ ِ ِ َ ٰ َ ﴾٣﴿ ‫عىحن‬ ِ ِ ‫ػام ا ِو‬ ‫َي ُدض غهى‬ ِ “Je, umemuona ambaye anakadhibisha dini? Huyo ni ambaye humsukuma yatima. Wala hahimizi kumlisha masikini.” (Surat Al-Ma‟un; 107:1-3) Mwenye kuwapuuza mayatima na asiyejali njaa ya mafakiri ni mwenye kukadhibisha dini, na si mkweli katika madai yake ya uswalihina, hata kama akijitahidi sana katika swala yake na ibada yake, bali anastahili maangamio na adhabu: 52

Rejea iliyotangulia uk: 126

85


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

َ َ َّ ُ ٌ َ​َ َ ‫﴾ ىال‬٥﴿ ‫ن‬ َ ُ َ ‫ى‬ َ ‫زين‬ ِ ‫ًلت ِ ظاهى‬ ِ ‫صل‬ ‫فىيل ِللم‬ ِ ‫﴾ الزين ِه غن ص‬٤﴿ ‫حن‬ َ َ َ َ​َ َ ﴾ ٧﴿ ‫ن‬ ِ ‫﴾ ويم ػىن اواغى‬٦﴿ ‫ن‬ ِ ‫ُه ُيشاءو‬ “Basi ole wao wanaoswali. Ambao wanasahau swala zao. Ambao wanafanya ria. Na wanazuia msaada.” (Surat Al-Ma‟un; 107:4 -7) Imamu Husein  ni kama Ahlul-Bayt , walikuwa wanaishi kwa ajili ya watu zaidi kuliko wanavyoishi kwa ajili yao:

ٌ

َ “…..‫صاص ِت‬

َ

ُ َ ٰ َ َ َ َ​َ َُ ِ ‫… ويؤ ِزشون غهى أ ف ِع ُِ ولى وان ِب‬..”

“…Na wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji.” (Surat Al-Hashr; 59:9) Na tangu mwanzo wa maisha yake, naye ni mtoto mdogo alishiriki na familia yake kufunga siku tatu na hawakuwa wanafuturu humo ila kwa maji tu, kwa sababu wakati wakufuturu walikuwa wanawaendea wenye kuhitaji na wanamwaachia chakula chao. Na kwao imeshuka kauli yake (swt):

َ ‫ى‬ َ َ ‫ى‬ َُ ً ‫هى ُخ ّب ِه معىي ً ا َو َي‬ ً ‫ديما َو َأ‬ ‫﴾ ِإ ما‬٨﴿ ‫ظحرا‬ ِ ِ ٰ ‫ويط ِػمىن الطػام غ‬ ‫ى‬ ُ ُ ‫اللكه ال‬ َ ُ ُ ُ ً ‫ضاء َوال ُش‬ ً ‫شيذ م ُى َج‬ ﴾٩﴿ ‫ىىسا‬ ِ ‫جه‬ ِ ‫ط ِػمى ِلى‬ ِ “Na huwalisha chakula, juu ya kukipenda kwake, masikini, na yatima na mateka. Hakika tunawalisha kwa wajihi wa Mwenyezi Mungu tu. Hatutaki kwenu malipo wala shukurani.” (Surat Al-Insan; 76:8–9) Na katika maisha yake yote alikuwa ni kimbilio la mafakiri na wasio nacho, na kimbilio la wenye shida, na alikuwa ni wazo la wageni wanaokwenda kwake kwa zawadi zake na utoaji wake. 86


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Anasema Kamalu Diyn bin Twalaha: “Ilikwishaenea kunukuliwa kwake kwamba alikuwa anamkirimu mgeni na anampa mwenye kuomba, anaunga udugu, anamsaidia mwenye kuomba, na anamvisha asiye na nguo, anamshibisha mwenye njaa, anampa mwenye kudaiwa, anamtia nguvu mnyonge, anamhurumia yatima na anamtosheleza mwenye haja na haikumfikia mali ila anaigawa.”53 Na wanasema wanahistoria kwamba hakika alikuwa anabeba katika giza la usiku mifuko iliyojaa chakula na fedha kwenda kwenye nyumba za wajane, mayatima na maskini, hadi hilo liliathiri mgongo wake, na alikuwa anapelekewa vitu vingi na hasimami hadi avigawe vyote.”54 Usama bin Zaid aliugua maradhi yake ambayo humo alifariki. Imamu aliingia kwake kwa ajili ya kumtembelea. Alipokaa na akatulia, Usama akasema: Eee huzuni yangu! -

Ni ipi huzuni yako ? Deni langu nalo ni elfu sitini Basi ni juu yangu Naogopa nitakufa kabla ya kulipwa? Hutokufa hadi nikulipie.

Imamu akajitolea kulilipa kabla ya kufariki kwake, na alimsamehe Usamah kwani hakumpa baba yake baiya, na hakumlipa kwa ubaya bali alimfanyia wema. Na siku moja alipitia kwa masikini wa Swaffah, aliwakuta wanakula. Wakamkaribisha chakula, akashuka kwenye kipando chake na akala pamoja nao, kisha akawaambia: Nimewaitikia basi nanyi niitikieni. Wakakubali maneno yake na wakaenda 53

Al-Qarashiy: Baaqir Saharif: Katika Hayatul-Imamu al-Hasan, uk: 127 chapa ya kwanza 1993 Darul al- Balaagha – Beirut 54 Rejea iliyotangulia uk: 128

87


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

naye kwenye nyumba yake akasema  kumwambia mke wake Rubab: Toa ulichokiweka. Akatoa aliyokuwa nayo katika fedha na akawapatia.55 Haya ni kidogo kati ya rundo na machache kati ya mengi na tone kati ya bahari katika maisha ya Imamu Husein , na tunaposherehekea uzao wake mtukufu hakika sisi tunalinganiwa kuiga uongofu wake na kufuata mwenendo wake, kwa kuzingatia hali za jamii yetu, na kukithirishe uhudhuriaji wetu katika medani ya jamii na tuvuke hali ya ubinafsi na kujitenga na kukaa kando, ili tuchangie katika kujenga nchi zetu na kuhudumia mambo ya umma wetu na kushirikiana katika wema na uchamungu. IMAMU MAHDI BAINA YA AKILI NA NUKUU Uislamu ni dini ya akili, na itikadi yake imesimama juu ya mtazamo wa kufikiria, na unapinga uongo na ukhorafi. Na unamkataza mwanadamu kuchukua kitu kabla ya kuwa na uhakika nacho (na wala usiyafuate usiyo na ujuzi nayo) au kuwaiga wengine na kuwafuata katika rai zao na fikra zao bila ya hoja na dalili. Na hapa wamesema wengi wa Maulamaa wa Kiislamu juu ya wajibu wa ijitihadi na kutazama katika mambo ya itikadi. Na wala haisihi humo kukalidi na kufuata, bali inasihi kukalidi katika mas‟ala ya kifikihi ya matawi kwa ambaye hajafikia daraja ya ijitihadi, na kuchambua hukumu. Ama katika itikadi hakuna takilidi humo. Na aya za Qur‟ani tukufu zinatia mkazo wa kurejea akili ya mwanadamu. Katika makumi ya aya imepokewa kauli Yake (swt): “Je, hawana akili” na “huenda watatafakari” na “Kwa watu wenye kufikiri” na aya zilizopokelewa humo na zinazon55

Rejea iliyotangulia, uk. 125.

88


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

yumbuliwa katika tamko hili zinafikia aya 50 takriban. Ama aya zinazozungumzia kuhusu kufikiria na zinazoamuru kufikiria na kuhimiza juu yake ni aya 18 takriban. Kama vile kauli yake (swt): “Huenda mtatafakari,” “Je, hamtafakari,” “kwa watu wenye kutafakari.” Kwa kuongezea ambayo yamepokewa katika aya tukufu kuhusu kuelimika, kutazama na elimu, na mengineyo, ambayo yanadhihirisha wazi kuirejelea akili na kitovu chake katika Uislamu. Na kwa hiyo hakuna nafasi ya ukhorafi na uongo katika itikadi ya Kiislamu, na Mwislamu hajengei jambo lolote kifikra ila baada ya kutafakari, hoja na dalili. Aina Mbili za Itikadi: Ya Kwanza: Itikadi zinazotegemea akili moja kwa moja, na hakuna nafasi ya kunukuu katika kupata imani kwazo, kama misingi ya itikadi, mfano kuamini kuwepo kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na Utume, ambapo maumbile yake safi yanamuongoza mwanadamu, na akili yake salama, na sio nususi, hadithi na aya. Ya Pili: Itikadi zinazotegemea nukuu lakini ndani ya rejea ya akili, na hiyo ni katika msingi na vidhibiti vifuatavyo: - Upande ambao inatoka huko nukuu uwe ni sehemu ya tegemeo la akili na matumaini yake, nao ni upande wa maasumu, ambaye akili haishuku katika ukweli wake na usafi wake, kama vile Qur‟ani tukufu, Nabii aliyetumwa na Imamu maasumu. - Nukuu ithibiti kutoka katika upande huo kwa njia ya kiakili kisharia. Na dalili humo iwe katika kusudio sahihi lenye kudhihiri kwa wenye akili. - Isiwe inakhalifu hukumu za kiakili zisizo na shaka, kama vile 89


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

kukusanyika pamoja vitu viwili kinzani au kuondoka vyote, uwepo wa sababu bila ya kisababishi, na kugawanyika kwa tatu kwa namba mbili sawasawa, na ubaya wa dhulma na uzuri wa uadilifu. Na katika mwanga wa yaliyotangulia hakika sisi kama Waislamu tunaamini baadhi ya itikadi ambazo zimepokelewa kutoka katika rejea ya kisharia inayotegemewa na kwa sanadi sahihi iliyothabiti, maadamu haikhalifu dharura ya kiakili, na kuiamini ndani ya vidhibiti hivi na sio nje ya duara la akili, bali ni katika kivuli cha rejea yake na muongozo wake. Mandhari ya Muujiza: Ndio, kuna baadhi ya mambo yaliyopokewa kidini, yanaonekana kwa mara ya kwanza kwamba kuyaamini kwake ni kukhalifu akili, na kwamba ni katika aina ya ukhorafi na uongo. Na hiyo ni kwa sababu hayajazoeleka kutokea na kupatikana na yanazingatiwa yanakiuka uwiano na kanuni za kawaida zinazojulikana. Isipokuwa sisi ni wajibu kudadisi na kutofautisha baina ya yanayokhalifu ada na yaliyozoeleka na ambayo yanapingana na akili na kugongana nayo. Hakika maendeleo mengi ya kielimu na teknolojia ya kisasa kama angesimuliwa mwanadamu wa karne zilizopita au zilizotangulia kati ya karne, angekataa kusadikisha, au kuamini uwepo wake, ikiwa atayaangalia kupitia mambo yake ya kawaida na mazoea yake. Ama akijaaliwa akayaangalia kupitia uwezekano wa kiakili na wa kimantinki hatokuta kizuizi katika kuyasadikisha. Na maendeleo ya kielimu katika maisha ya mwanadamu wa kisasa, yanatusaidia sana katika kufahamu mengi katika mandhari yenye kukiuka mazoea, ambayo dini inatusimulia. Na hivi sasa tunataja miongoni mwayo baadhi ya mifano ambayo 90


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

wanaamini kwayo Waislamu kwa kuthibiti kwake kidini, katika wakati ambao haugongani na hukumu ya akili. Baridi na salama kwa Ibrahimu: Kuhama joto kutoka kwenye mwili wenye joto jingi kwenda kwenye mwili wenye joto dogo, ili liwiane, ni kanuni ya kawaida inayofahamika. Hivyo hakika mwili wowote unaotupiwa katika moto unaungua kwa moto wake, lakini Nabii wa Mwenyezi Mungu Ibrahim al-Khalil  na mwili wake ni kama miili mingine ya binadamu, aliyetupiwa na kaumu yake katika moto huo uliowaka ambao waliuwasha kwa ajili ya kumchoma, na hakupatwa na adha yoyote, na akatoka humo akitabasamu; anasema (swt):

ٰ ُ َُ َ ٰ ُ ُ ُ َ ُ َِ ‫كالىا‬ ‫﴾ كل ا يك ُاس‬٦٨﴿ ‫لحن‬ ِ ‫ءال َُخى ِإن ه خ فك ِػ‬ ِ ‫خ ِّشكىه وا صشوا‬ ً ‫﴾ َو َأسادوا به َه‬٦٩﴿ َِ ‫هى إ ٰبشهي‬ ُ ُ​ُ ‫يذا َف َج َػل ٰك‬ ٰ َ ًٰ َ َ ً َ ِ​ِ ِ ‫هىقش بشدا وظلكما غ‬ َ ﴾٧٧﴿ ‫شين‬ ِ َ ‫َع‬ “Wakasema: Mchomeni na muinusuru miungu yenu, ikiwa nyinyi ni watendao jambo. Tukasema: Ewe moto! Kuwa baridi na salama kwa Ibrahimu! Na wakamtakia ubaya, lakini tukawafanya wao ndio wenye kupata hasara.” (Surat al-Anbiya; 21:68–70) Hakika Mwislamu anaamini bila ya shaka yoyote wala kusitasita maadamu kisa kimetajwa katika Qur‟ani, na kukabiliana na kuungua sio jambo linaloshindikana na lisilowezekana katika upande wa kiakili. Sisi tunaona hivi sasa namna gani zimebadilika njia za kuzuia mwili ndani ya masharti maalum kutokana na kuungua. 91


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Amezaliwa Bila ya Baba: Kanuni ya kawaida iliyozoeleka, kuzaliwa mwanadamu kunatimia kwa kukutana kwa mwanaume na mwanamke pamoja, na haijazoeleka kupatikana uzao kwa mmoja wao tu, lakini Qur‟ani tukufu inatuambia kuhusu uzao wa Nabii Isa bin Mariyam bila ya baba. Na hata mama yake Maryam alistaajabu alipopewa bishara na malaika kwa hilo, kwa sababu yeye hajaguswa na mwanaume na wala hajaolewa, namna gani anaweza kuzaa? Qur‟ani inasema:

َ ‫ى‬ ٰ َ َ ٌ َ َ َ ‫كالذ َس ّل َأ ّق ٰش َيىى ُن لى َو َل ٌذ َو َل َي‬ ‫كاٌ هز ِل ًِ الل ُكه‬ ِ‫مععنى ش ِش‬ ِ ُ ُ َ ُ َ ‫َ ٰ َ ً َ ى‬ ‫ن‬ ِ ‫مشا ف ِئ ما َيلى ٌُ ل ُه هن ف َيىى‬ ‫شاءِ ِإرا كض ى أ‬ ُِ ‫َيخل ُم ما َي‬ “Akasema: Mola Wangu! Nitakuwaje na mtoto na hali hajanigusa mtu yeyote? Akasema: Ndivyo hivyo, Mwenyezi Mungu huumba anavyotaka. Anapohukumu jambo huliambia „kuwa‟ likawa.” (Surat Aali-Imran; 3:47) Na maadamu Qur‟ani inatuambia haya, sisi tunaamini, nalo ni jambo lisilokuwa la kawaida katika mazoea, na halijazoeleka, lakini sio mustahili kiakili, na majaribio ya istinsaakh (nakala) ambayo yametokea katika miaka hii ya mwisho si kingine ila ni kutia mkazo uwezekano huu. Israi na Miraji: Waislamu wanaitakidi Israi na Miraji, ambapo Mwenyezi Mungu alimpeleka Israi Nabii Wake Muhammad  kutoka Makkah tukufu hadi msikiti wa mbali wa Palestina, kisha akampandisha hadi mbingu za juu, katika safari ya muujiza ndani ya anga na muda, na akarejea kwenye kitanda chake usiku ule ule karibu na mapambazuko ya alfajiri. 92


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Hakika kutokea hayo na hususan katika zama hiyo, ni jambo lenye kukanushwa. Linawajibisha kupingwa na kukadhibishwa, lakini ni habari ya kweli imekuja nayo Qur‟ani tunalazimika kukubali na kusadikisha. Anasema (swt):

‫ُ َٰ ى‬ َ َ َ َ ً َ َ َ ٰ َ ‫سج ِذ‬ ِ ‫ظبدكن الزي أظشي ِ ػ‬ ِ ‫شام ِإلى او‬ ِ ‫سج ِذ احخ‬ ِ ‫بذ ِه ليًل ِمن ٰاو‬ َ َ ‫َ َ ى‬ َ ‫ميؼ‬ ُ ‫الع‬ ‫ىل ُه ل ُجرَي ُه من ءايكد ا إ ى ُه ُه َى ى‬ َٰ ُِ ‫الب‬ ‫صحر‬ ِ ِ ِ ‫كصا الزي بكشه ا خ‬ ِ ِ

“Kutakata na mawi ni kwa ambaye alimpeleka mja Wake usiku kutoka Msikiti Mtakatifu (wa Makkah) mpaka msikiti wa mbali ambao tumevibariki vilivyo kandoni mwake ili tumuonyeshe baadhi ya ishara zetu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona.” (Surat Bani-Israil; 17:1) Ni sahihi kwamba ni jambo la ajabu na linalokhalifu ada na mazoea, lakini akili haihukumu kushindikana kwake na kuzuilika kwake, na maendeleo ya njia za mawasiliano ya anga na mwanadamu kwenda angani na kwenda kwenye sayari zingine yamefanya sura iwe wazi zaidi mbele ya mwanadamu wa leo. Imamu Mahdi: Na ndani ya mtiririko huu inakuja itikadi ya Imamu Mahdi anayesubiriwa  ambapo yamethibiti hayo kwa nukuu ambayo inakubaliwa na akili, ambapo Hadithi zimepokelewa kutoka kwa Nabii Muhammad . Na zimepokelewa kutoka kwa Maimamu wa Ahlul-Bayt  zimepita kiwango cha tawatur. Amesema Sheikh Ibnu Taimiyya: Hakika hadithi ambazo zinatolelewa hoja ya kutokea Mahdi ni hadithi sahihi amezipokea Abu Daud, Tirimidhiy, Ahmad na wengineo.56 56

Ibnu Taimiya al-Haraaniy: Sheikhul-Islami Ahmad katika Minhaaji Sunnah, Juz. 4, uk: 211 chapa ya kwanza al-Matbaatu al-kubra al- amiriya – Misri 1322H

93


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Na chini ya anwani: (khuruju al-Mahdiy haqiqatu indal-ulamaa) ametaja mwanahadithi wa kisalafi wa kileo Sheikh Muhammad Naswir Diyn al-Albaaniy majina kumi na sita ya wanachuoni kati ya maimamu wakubwa wa hadithi waliosema hadithi za kutokea Mahdi ni sahihi.57 Na jarida la al-Buhuthu al-Islamiya linalotolewa na al-Amaanatul-Amatu Lihaiati Kibaaril-Ulamaai Fiyl-Mamlakati alArabiyati as Suudiya, katika utafiti wa Sheikh Yusufu alBaraqaawiy chini ya kichwa cha habari Aqidatu al-Ummati FiylMahdiy al-Muntadhwar, ameandika: “Hakika maudhui ya Mahdi ni katika alama kubwa za Kiyama na masharti yake makuu ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu  alitoa habari kuyahusu. Masharti makuu ya Kiyama ni katika mambo ya ghaibu ambayo Mwenyezi Mungu amekalifisha waja Wake kuyasadikisha na kuamini kutokea kwake, na itikadi yetu inatuwajibisha kuamini hivyo.” Na imenukuliwa kutoka kwa al-Safariniy al-Hanbaliy kauli yake: “Kati ya masharti ya Kiyama ambayo habari zake zimepokewa kwa tawatur katika madhumuni yake, ya mwanzo wake ni kudhihiri Imamu Mahdi mwenye kufuatwa kwa kauli zake na vitendo vyake. Ni hitimisho la maimamu na hakuna Imamu baada yake, kama ambavyo Nabii  ni hitimisho la unabii na ujumbe hivyo hakuna nabii wala mtume baada yake.”58 57

Al-Baaniy: Muhammad Naswir Diyn, katika Silsilatu al-Hadithi as-Sahiha, Juz. 4, uk: 38 hadithi namba 1529 chapa ya kwanza: Daru salafiya - Kuwait al-maktabatu al-Islamiya - Jordan 1983. 58 Al-Barqaawiy: Yusufu bin Abdurahman katika Aqidatu al-Ummati fiylMahdiy al-Muntadhwar, majalatul- buhuthu al- Islamiya toleo la 49 uk: 304 – 305.

94


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Na Sheikh Lutufi llahi Swafiy amekusanya katika kitabu chake Muntakhabul-Athar Fiyl-Imami Thaniy Ashara hadithi zilizopokewa kuhusu Imamu Mahdi kutoka katika vitabu vya pande mbili, Sunni na Shia, zimefikia hadithi (6277).59 Hivyo kutokea Mahdi anayesubiriwa akhiri zamani ni mas‟ala yaliyothibiti kwa Waislamu pamoja na kutofautiana madhehebu yao isipokuwa wachache, kwa kupokewa habari yake katika njia inayoamini akili ukweli wake, na kwa sababu imekuja kwa njia sahihi zinazokubalika kisharia na kiakili. Kama ambavyo Waislamu wanaafikiana juu ya kwamba Mahdi ni katika kizazi cha Mtume  na katika kizazi cha Fatimah Zahra , lakini kuna ikhitilafu katika ufafanuzi wa itikadi hii, kama itikadi zingine za Kiislamu ambazo zinatofautiana madhehebu na makundi katika baadhi ya pande zake na ufafanuzi wake, kama vile tauhidi, utume na miadi. Na kila kundi linachukua yale ambayo yanasihi na kuthibiti kwake. Na Shia Imamiya wanaitakidi kwamba Imamu Mahdi ambaye Mtume wa Mwenyezi Mungu  amebashiri kutokea kwake alizaliwa tarehe 5 mwezi wa Shabani 255 Hijiria, na baba yake ni Imamu Hasan Askariy, katika kizazi cha Husein bin Ali na Fatimah , na kwamba bado angali hai anasubiria amri ya Mwenyezi Mungu kudhihiri kwa ajili ya kufanya jukumu lake la kiulimwengu, ili aijaze ardhi uadilifu na usawa kama ilivyojazwa dhulma na ujeuri. Kwa sababu tamko limeshathibiti kwao kutoka kwa Maasumina, wao wanalazimika kulikubali na kuliamini. Kuna hadithi sahihi thabiti kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu  anazungumza humo kuhusu Maimamu kumi na mbili au viongozi au Makhalifa wa dini hii na umma huu, na hayo yamepokewa katika 59

As-Swafiy: Lutuf llah katika Muntakhabu al- athari, chapa ya pili 1385 H, markaz al-kitab, Tehran – Iran.

95


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Sahihi Bukhari, na amepokea Tirimidhiy, Ibnu Hanbali, Abu Daud na amezitaja al-Albaniy katika silsila ya hadithi sahihi namba (1075).60 Na wala hawaafikiani na idadi hii ila maimamu kumi na mbili wa Ahlul-Bayt . Hadi hapa yanabakia mas‟ala ya uwezekano wa kuishi na uhai wa muda wote huu mrefu, namna gani jambo hili linaweza kuingia akilini? Hakika akili haioni kushindikana kwa jambo hilo, bali hakika elimu inajitahidi katika utafiti ili mwanadamu aweze kuvuka pingamizi za uzee na ukongwe, ili aneemeke na umri mrefu katika maisha haya. Na likithibiti tamko la kisharia juu ya kuwepo Imamu Mahdi hakika sisi tunalikubali kama hali ya muujiza, kama ambavyo tunakubali kutoungua Nabii Ibrahimu katika moto, na kuzaliwa Isa bin Mariya bila ya baba, Israi na Miraji na mfano wa hayo, mambo yote haya hayashindikani kiakili, bali yanakiuka ada na yanakhalifu yaliyozoeleka tu. Hakika Qur‟ani tukufu inatusimulia kuhusu kuishi Nabii Nuhu  muda mrefu, ambapo ulichukua unabii wake hadi wakati wa tufani miaka 950. Anasema (swt):

َ َ َ​َ َ ّ َ َ َ َ ً ‫ىم ِه فل ِبث في ِ ألف َظ ٍت ِإال معحن‬ ِ ‫ىخا ِإ ٰلى ك‬ َ ٰ ُ ّ ‫ن‬ ِ ‫الطىفان َو ُه ظك ِلمى‬

َ ‫َو َل َلذ َأ‬ ‫سظل ا‬ ُ ‫غاما َف َأ َ َز ُه‬ ً

“Na hakika tulimtuma Nuhu kwa kaumu yake, akakaa nao miaka elfu kasoro miaka hamisini. Basi tufani iliwachukua hali ya kuwa wao ni madhalimu.” (Surat An-„Ankabut 29:14) 60

Al-Abaniy: Muhammad Naswir Diyn katika silsila ya hadithi sahihi, Juz. 3, uk: 63, chapa ya tatu 1987 Maktabatu al-Maarifu – Riyaadh.

96


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Hii ni ukiacha maisha yake kabla ya utume na baada ya tufani. Sawa iwe hayo yalikuwa ni maalumu kwa Nabii Nuhu au umri wa binadamu katika wakati huo ulikuwa katika kiwango hiki, vyovyote iwavyo, inaonyesha juu ya uwezekano wa kuishi muda mrefu unaovuka ada na mazoea. Hakuna kushabikia wala kukanusha: Umma wetu wa Kiislamu umeishi katika vipindi kadhaa bila kuwa na maendeleo. Imetawala humo hali ya kasumba ya madhehebu na mizozo baina ya makundi na mifarakano, na umma haukuvuna kwa yote hayo ila mpasuko na kupotea na kuacha kujenga nguvu yake, na kukabiliana na changamoto za nje. Na ni thabiti kwamba maadui wa Uislamu wanashangilia kupigana kwa Waislamu na wanamwagia mafuta juu ya moto wa mfarakano na ugomvi. Na hivi sasa inatakiwa Waislamu kuvuka hali hiyo mbaya, pamoja na mabadiliko ya kiwango cha uelewa na nyezo za mawasilianao na kufunguka, na ikiwa kila kundi linaona kwamba haki na usahihi uko pamoja nao hakika linabeba jukumu la itikadi yake na rai yake mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na uwe utafiti juu ya ukweli ni lengo la wote, kupitia utafiti wa kimaudhui katika sehehmu za ikhitilafu, majadiliano yenye kujenga mbali na ushabiki na kushutumiana. Hakika Qur‟ani tukufu inakataza Waislamu kujadiliana pamoja na mayahudi na manaswara kwa njia isiyokuwa na adabu na inasema:

َ

‫ى‬

ّ

ٰ

َ

ٰ ُ

َ ‫هل الىخكب إال بال ى ى َى أ‬ َ ‫” َوال ججك ِذلىا أ‬ “….. ‫ن‬ ِ ُ ‫خع‬ ِ ِ ِ ِ ِ “Wala msijadiliane na watu wa kitabu isipokuwa kwa njia iliyo nzuri kabisa…..” (Surat Al„Ankabut; 29:46) Je, Qur‟ani inaridhia wanayoyafanya baadhi ya Waislamu dhidi 97


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

ya baadhi ya Waislam wenzao katika kushabikia na kushutumu na kucheza shere, kama inavyodhihiri wakati mwingine katika baadhi ya sehemu za medani za majadiliano katika tovuti au vipindi vya runinga? Je, njia hii inaonyesha isipokuwa tabia mbaya au udhaifu wa hoja au kutumikia maslahi ya maadui? UCHAGUZI WA MUME BAINA YA BINTI NA WATU WAKE Kila yanapokuwa maamuzi ambayo mwanadamu anataka kuyachukua yana athari kubwa zaidi katika maisha yake anahitajia utafiti zaidi na utulivu kabla ya kuchukua maamuzi, ili aepuke kuakisi hatari wa kosa katika maamuzi hayo. Ama ikiwa maamuzi yanahusiana na jambo jepesi, basi asiikalifishe nafsi yake taabu ya ziada katika kutafakari humo. Na huenda katika maamuzi muhimu zaidi ambayo mwanadamu anayachukua ni maamuzi ya kuchagua mshirika wa maisha, ili kuanzisha maisha yake ya kifamilia ya kijamii, kwa kuwa hayo yana athari pana yenye kuendelea katika mustakabali wake, na kwa kuwa maisha ya ndoa yana umuhimu na unyeti, yanagusa pande zote za shakhsiya ya mwanadamu. Ikiwa ameafikiwa kuchagua na Mwenyezi Mungu akamruzuku mke mwema, anaishi maisha mema. Ama akipata balaa ya kupata mke mbaya basi atakabiliwa na maisha mabaya na maisha machungu, na kwa sababu hiyo muumini anamwelekea Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa dua “Mola wetu tupe katika wake zetu na wanetu yaburudishayo macho.� (Suratul-Furqan: 74). Na wakati wa kufikiria katika uchaguzi wa mshirika mwanadamu anahitaji usalama na uwazi wa vipimo vya kuchagua, ni kwa msingi gani anachagua? Na ni sifa zipi zinapasa kutimia katika upande mwingine? Na mafunzo ya Uislamu yanamwelekeza mwanadamu kwenye vipimo sahihi ambavyo ni wajibu aviweke mbele ya macho yake 98


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

wakati wa kuchagua, na tunahitajia utafiti maalumu ili kuelezea na kuzungumzia juu yake. Na ambayo tunataka kuyatilia mkazo katika maudhui haya ni uamuzi wa binti katika kuchagua mshirika wa maisha yake. Mambo kwake ni muhimu sana kuliko mwanaume, hiyo ni kwa sababu fursa ya mwanaume katika kutatua kosa katika uamuzi huu ni kubwa zaidi kuliko fursa ya mwanamke, hamiliki haki hii ya kisharia ila katika hali finyu. Hapa binti anahitajia zaidi kutafakari wakati wa kuchagua, na tatizo wengi wa wasichana hakika wao wanatumbukia katika athari kwa sababu za matamanio ya kihisia kwa daraja kubwa zaidi, ambapo binti anaathirika aghlabu kwa anayoyasikia miongoni mwa maneno ya kutongoza na mapenzi na anahadaika na baadhi ya muonekano wa harakati za ujana, ambapo anaona nafsi yake inaishi duara la pembeni katika nyumba ya familia yake anavutika kwa fursa ya karibu zaidi ili kujenga maisha yake ya kijamii ya baadaye. Kwa kawaida haiwezekani kujumuisha. Kuna mabinti ambao wanamiliki upevu na uelewa na wanavuka athari hizi. Na ulinzi wa mustakabali wa binti, na kuongoza maamuzi ya uchaguzi wake, Uislamu umempa walii wa jambo lake nafasi ya maamuzi haya kwa mujibu wa rai ya jopo la mafakihi. Na hilo litabainika zaidi kupitia nukta zifuatazo: Mwanamke thayibu (mtu mzima): Ikiwa mwanamke alikwishaolewa na akaishi maisha ya ndoa, yaani alishaingiliwa na mume wake kisha akaachana naye, hakika wakati huo maadamu ni baleghe na mwelewa na ameshapitia tajiriba ya ndoa, maamuzi ya kuchagua mume mpya yanakuwa katika mamlaka yake na wala hamiliki yeyote haki ya kumpinga na kumzuia. Hii ni katika rai ya mafakihi wa Kishia na kihanafi. Yeye sio mgeni katika maisha ya ndoa, na inategemewa kwamba amenufaika na tajiriba iliyotangulia na maamuzi yake 99


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

yanatokana na ukomavu na ujuzi na sio msukumo wa kihisia na matamanio. Hakika haya hayamhusu ambaye amejitenga na mume wake au aliyefiwa na mume wake kabla ya kuingiliwa, kwa sababu ndoa tu haimfanyi awe thayibu (mtu mzima). Na ikiwa Uislamu umeafiki rai hii – haujampa yeyote katika familia yake haki ya kumzuia kuchukua maamuzi, hii haimaanishi kutohitajia ushauri wao, na kunufaika na rai yao, na hivyo mafakihi wamesema hakika inapasa kwa mwanamke ambaye anamiliki maamuzi yake, atake ruhusa kwa baba yake au babu yake, na kama hawapo basi kaka yake na kama wako wengi anachagua mkubwa zaidi.61 Binti bikra: Ama binti bikra ambaye hajawahi kuingia katika tajiriba ya maisha ya ndoa kuna rai mbili zilizo dhahiri: Rai ya kwanza: Kwamba yeye ana maamuzi kamili ya kuchagua, na wala hahitaji idhini ya kutoka kwa baba yake, babu yake au yeyote, na kwa rai hii limesema jopo la mafakihi wa Kishia waliotangulia, kama vile Sayidi al-Murtadhwa al-Iskaafiy, alHiliy, al-Mufidiy, al-Dailamiy, al-Muhaqiq, al-Fadhil na Mashahidi wawili.62 Na katika Mafakihi wa zama hizi ni Sayid Sabzawariy, Sheikh Muhammad Amin Zainul-Abidini, Sheikh Muhammad Jawad Mughuniya. Na wenye rai hii katika maimamu wa Kisunni ni Abu Hanifa na Abu Yusufu. Rai ya pili: Ni sharti kuwe na idhini ya walii wa binti nayo ni rai ya mafakihi wengi wa Kishia wa zama hii kwa fat‟wa au tahadhari ya wajibu. Na vilevile ni rai ya jamhuri ya Ahlul-Sunna. Walii wa binti ambaye inachukuliwa rai yake katika fikihi ya 61

Al-Yazidi: Sayid Muhammad Kaadhim Twabatwabaiy katika al-Uruwatu al-wuthiqah auliyaul Aqid – mas‟ala namba 14 62 Shiraziy: Sayid al-Huseiniy katika al-Fiqihi, Juz. 64, uk. 20

100


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Shia ni baba au babu wa upande wa baba tu, ambapo inatosha kuafiki mmoja wao na hakuna uwalii kwa wasiokuwa wao kwa binti aliyefikia umri wa uelewa. Wakati ambapo duara la uwalii katika nyanja hii kwa Ahlus-Sunna linawaenea pia jamaa wa mwanamke: baba kisha watoto kisha ndugu kisha baba wadogo katika ikhitilafu baina yao katika mpangilio wa mawalii. Hekima ya idhini ya walii: Imetangulia kuashiria kwamba sharia ya kuweka sharti la idhini ya walii katika kupitisha ndoa ya binti bikra, ni kwa ajili ya kuongoza maamuzi yake, ili uchaguzi usiwe unatokana na hali ya kihisia bila ya kuhakiki kufaa anayetaka kuwa mwenza wake. Na hususan katika jamii inayojilinda, hakika binti hayuko wazi katika jamii ya wanaume, ili kujua mwenendo wa anayemchumbia, kiwango chake na kiasi cha kufaa kwake, na baba yake au babu yake anatakiwa kuchunga maslahi yake na kupendelea kwao mafanikio yake, kwa hiyo rai yao inaingilia katika kupitisha ndoa yake. Ama wasiokuwa wao hawana haki ya kumzuia, kulingana na fikihi ya Shia. Ndio ni mustahabu kwa binti kumuomba ushauri anayemwamini katika jamaa zake lakini si haki kwa yeyote kumzuia. Na wanayoyafanya baadhi ya jamaa wa karibu katika kuingilia jambo la ndoa ya dada yake, binti wa kaka yake au binti wa dada yake au binti wa Ami yake au mfano wa hayo katika kuzuia na kukwaza, ni uingiliaji wa kitoto sharia haikubali. Anasema al-Faqihi Sayid Muhammad Said al-Hakim: “Hana yeyote katika jamaa pamoja na kutokuwepo baba au babu wa upande wa baba, haki ya usimamizi wa aliyebaleghe ambaye ni bikra ukiachilia wengine, bali anakuwa huru mwenyewe, na wanayoyafanya baadhi kwa mazoea ya jamaa kuingilia na kumzuia mwanamke anayoyataka au anayoyataka walii wake pamoja na kuwepo kwake ni dhulma iliyo wazi, na ni kutoka 101


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

katika vipimo vya kisharia na kuvunja mipaka ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na ni kupuuza hukumu Zake katika waja Wake. Nayo ni kati ya sababu za ufisadi mkubwa, ambao unaweza kusababisha kulipiza kisasi ambako hakuna mwisho mwema. Unabeba ufisadi na aibu yake duniani na akhera, na athari yake na majukumu yake katika akhera. „Siku ambayo rafiki hatomfaa rafiki yake kwa chochote wala wao hawatonusuriwa.‟”63 Hakika baadhi ya wasichana – kama nilivyoona – wanakasirika kwa vitendo vya walii wao kuchukua nafasi hii, na wanapatwa na hasira kali dhidi yao wakati walii anasimama dhidi ya raghaba zao katika kuchagua mume. Lakini kinachotakiwa kwa binti ni kufahamu hukumu hii ya kisharia, na kufahamu nafasi ya baba yake ambaye amemlea na amebeba jukumu la uangalizi wake, naye ni mwenye kujali mafanikio yake na mustakabali wake, naye ni mwingi wa tajiriba na ujuzi kuliko yeye na kujua hali ya jamii na watu wake, na anapomkataa mwenye kuchumbia anayekuja kumposa hakika ni kutokana na kutokuwa ni laiki yake na kutofaa kwake. Na inatokea katika baadhi ya hali kwamba binti anang‟ang‟ania katika raghaba yake katika kuolewa na mposaji maalum, pamoja na kukataa baba yake, na hapo baba analazimika kuacha rai yake, na kukubali matakwa yake, pamoja na kumbebesha jukumu la mustakabali wake, hutokea nini baada ya hapo? Mara nyingi inatokea binti mwenyewe anajikuta katika matatizo pamoja na mtu ambaye hana muamala mzuri pamoja naye, na wala hana sifa inayotakiwa na tabia inayofaa. Anatambua baada ya kupitwa na muda kwamba alikuwa ana makosa katika kuchagua, na analipa thamani kubwa. 63

Al-Hakim: Sayyid Muhammad Twabatwabaiy katika al-Ahkaami alFiqihiya aqidu Nikaahi wa auliyaai al-aqdi, uk: 356, mas‟ala namba 9 chapa ya tatu 1997 Darul-Swafuwatu - Beirut.

102


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Kutumia haki vibaya: Lakini baadhi ya baba wanaweza kutumia vibaya haki hii. Anapinga uchaguzi wa binti yake bila ya sababu, na anamzuia kuolewa pamoja na kwamba aliyekuja kwake ni laiki yake na anafaa, jambo ambalo linasababisha kuchelewa kwa muda mrefu na anaweza kuwa katika orodha ya wasiolewa. Na inaweza kuwa sababu ya msimamo huo wa baba ni baadhi ya vipimo vya kimaada na maslahi, ambayo anataka yatimie katika kuposwa binti yake, kama vile kuwa tajiri au kuwa katika kiwango cha kazi maalumu. Au kwa sababu baba anataka kumuozesha binti yake kwa mtu maalumu, katika jamaa zake au marafiki zake, au kwa sababu baina ya baba na mama wa binti kuna tatizo, kama vile kuwa ni mtalaka wake, au amemlea tu. Hivyo anamaliza tofauti yake pamoja naye kwa hisabu ya binti yake. Na imeonekana kwamba mmoja wa wazazi alikuwa na tamaa ya pato la binti yake anayefanya kazi na kwa hivyo anaweka vikwazo na kuchelewesha ndoa yake, kwa kutunga sababu na visingizio mbele ya waposaji. Hakika mfano wa hali hizi unaweza kutokea, lakini haipasi kuziangalia. Hakika Uislamu unapokonya haki ya walii ambaye anaitumia vibaya, hakika ni haki kwake kuzuia na kupinga ikiwa mposaji sio laiki yake na hafai. Ama akiwa ni laiki yake na anafaa, na pamoja na hivyo baba akapinga, hakika haki yake katika kupinga na uwalii wake kwa binti hapa unaporomoka. Wanasema mafakihi: “Walii akimzuia kuolewa na anayefaa ilihali ndiye raghaba yake, basi idhini yake inaporomoka.”64 “Maulamaa wameafikiana kwamba si ruhusa kwa walii kumzuia anayemsimamia, na kumdhulumu kwa kumzuia kuolewa, akitaka kuolewa na anayefaa kwa mahari ya mfano wake. Akimzuia katika hali hii ni haki kupeleka suala lake kwa kadhi ili 64

Al-Yazidiy: Sayyid Muhammad al-Kaadhim Twabatwabaiy katika alUruwatu al-Wuthiqah, auliyaul- aqid - mas‟ala namba 1

103


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

amuozeshe. Na wala uwalii hauhami katika hali hii kwenda kwa walii mwingine atayechukua nafasi ya walii huyu dhalimu, bali unahamia kwa kadhi moja kwa moja, kwa sababu kizuizi ni dhulma, na mamlaka ya kuondoa dhulma ipo kwa kadhi.”65 Na Qur‟ani tukufu inakataza kumzuia mwanamke, yaani kuzuia kuolewa kwake, anasema (swt):

ُ ‫َى‬ ُ ‫غن َأ َج َل ُ​ُ ىن َفًل َح‬ َ ‫لىه ىن َأن َي ى‬ ُ ‫ػض‬ َ ‫عاء َف َب َل‬ َ ‫لخ ُ ال ّن‬ ‫دن‬ ‫َو ِإرا ل‬ ِ ِ َ ُ َ َ ٰ ُ َ َ َ َ ‫يىغظ ِب ِه َمن وان ِم ى‬ ً‫ػشونِ ر ِل‬ ِ​ِ ‫أ ٰصو َج ُ​ُ ىن ِإرا ج ٰشضىا َب َين ُ ِباو‬ َ َُ ٰ َ ُ ٰ ٔ ‫ى‬ ُ َ َ َ َ ‫ُي ُ ى‬ ‫صوش لى َوأ َُ ُِشِ َوالل ُكه َيػل ُ َوأ خ‬ ‫ىم الكا ِ ِ​ِشِ ر ِلى أ‬ ِ ِ ‫ؤمن ِبالل ِكه والي‬ َ َ َ ‫ن‬ ِ ‫ال حػلمى‬ “Na mtakapowapa wanawake talaka na wakafikia muda wao, msiwazuie kuolewa na waume zao, ikiwa wamepatana kwa wema. Hayo anaonywa nayo yule miongoni mwenu, anayemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hayo ni mazuri mno kwenu na safi kabisa. Mwenyezi Mungu anajua, na ninyi hamjui” (Surat Al-Baqara; 2:232) Hakika Mwislamu yeyote anayeamini kwamba Mwenyezi Mungu ndio Muweka sharia na Msimamizi na Siku ya Kiyama ni ahadi ya hisabu na malipo, ni juu yake kuwaidhika kwa amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na wala hasababishi kuzuia ndoa ya binti yake bila ya sababu ya kisharia, kwa sababu hiyo ni dhulma kwake, na ni sababu ya kutumbukia katika ufisadi na matatizo katika jamii, na kwa sababu hiyo mwisho wa aya unasema: “Hayo ni mazuri mno kwenu na safi kabisa.” 65

Sabiq: Sayid katika Fiqihi Sunna, Juz. 2, uk: 136 chapa ya tatu 1977 DarulKitabu al-Arabiiy - Beirut

104


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Na zimepokewa riwaya na hadithi nyingi zinazohadharisha kuzuia kuwaozesha mabinti na kuwachelewasha kwake, kwa sababu hiyo inampotezea fursa inayofaa, kama inavyosababisha madhara ya kinafsi na kitabia katika jamii. Ali bin Asbaati alikuwa ni kati ya wafuasi wa Imamu Muhammad al-Jawad , na alikuwa na mabinti anaotaka kuwaozesha kwa maulamaa watukufu mfano wake, hiyo ikawa ni sababu ya kuchelewa kuwaoza, akaandika barua kwa Imamu al-Jawadi , Imamu akamjibu: “Nimefahamu uliyoyataja katika jambo la mabinti zako na kwamba wewe humpati yeyote aliye mfano wako, hivyo usisubiri katika hilo Mwenyezi Mungu akuhurumie, hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu  amesema: „Anapokujieni mnayeridhia tabia yake na dini yake basi muozesheni, kama msipofanya hivyo kutatokea fitina katika ardhi na ufisadi mkubwa.‟”66 Na katika hadithi nyingine: “Mwenye kuposa kwenu na mkaridhia dini yake na uaminifu wake basi muozesheni, msipofanya itatokea fitina katika ardhi na ufisadi mkubwa.”67 Na kutoka kwa Ali  amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu : “Anapokujieni mnayeridhia tabia yake na dini yake basi muozesheni.” Nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hata kama ni duni katika nasaba yake? Akasema: “Atakapokujieni mnayeridhia dini yake na tabia yake, basi muozesheni msipofanya hivyo itakuwa fitina katika ardhi na ufisadi mkubwa.”68 Na siku moja Mtume wa Mwenyezi Mungu alipanda mimbari akamshukuru Mwenyezi Mungu na akamhimidi kisha akasema: “Enyi watu hakika Jibril amenijia kutoka kwa Mpole na Mjuzi amesema: Hakika mabikira ni sawa na matunda juu ya mti, na 66

Al-Huru al-Amiliy: Muhammad bin al-Hasan katika Tafswil Wasailu Shi‟ah, Juz. 20, uk: 76 chapa ya kwanza 1993 Muasasatu Aali al-Bait liihiyai turathi – Beirut. 67 Rejea iliyotangulia uk: 77 68 Rejea iliyotangulia uk: 78

105


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

litakapoiva tunda lake na lisichumwe linaharibiwa na jua na litapeperushwa na upepo.” Akasimama mwanaume akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu: Nani tutamuoza? Akasema: “Wanaofaa.” Akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu na wanaofaa ni akina nani? Akasema: “Waumini baadhi yao ni laiki ya baadhi yao, waumini baadhi yao ni laiki ya baadhi yao.”69 Vipimo vya saizi na kufaa: ni dini na tabia njema, na zitakapotimia kwa mwenye kumposa binti hakuna sababu kwa walii wake kuchelewesha au kuzuia. Na inaonekana kukariri sana na tahadhari katika hadithi kwamba kuzuia ndoa kunasababisha fitina na ufisadi mkubwa katika jamii. MWEZI WA RAMADHANI NA ADA ZA KIMAKOSA Mwezi mtukufu wa Ramadhani ni wakati bora anaopitia mwanadamu katika mwaka, ambapo Mwenyezi Mungu Mtukufu ameufanya ni mahususi kwa kheri na fadhila, kati ya zama na wakati. Na amejaalia humo usiku wenye cheo, ambao ni bora kuliko miezi elfu moja, na akauchagua ili uwe ni uteremsho wa wahyi Wake na ujumbe Wake, ambapo humo imeshuka Qur‟ani na kabla ya hapo humo ilishuka Torati, Injili na Zaburi. Na inatosha katika fadhila za mwezi huu ambayo yamepokewa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu : “Bwana wa miezi ni mwezi wa Ramadhani.”70 Na kutoka kwake : “Enyi watu hakika umeshawajieni mwezi wa Mwenyezi Mungu kwa baraka, rehema, na maghufira, mwezi ambao kwa Mwenyezi Mungu ni mbora wa miezi, na siku zake ni bora ya siku, usiku wake ni mbora wa mikesha, na saa zake ni saa bora. Ni mwezi humo mmealikwa katika ugeni wa Mwenyezi 69 70

Rejea iliyotangulia uk: 61 Al-Hindiy: Ali al-Mutaqiy katika Kanzul-Umaal fiy suani al–Aquqaawaal wal-aqfu‟ali, Juz. 8 hadithi namba 23670 uk: 473 chapa ya tano 1985 Muasasatu risalati – Beirut.

106


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Mungu, na mkafanywa ni katika watu waliokirimiwa na Mwenyezi Mungu.”71 Na katika msisitizo maalumu wa tofauti katika mwezi huu mtukufu, Mwenyezi Mungu amefaradhisha saumu kwa watu, ili waishi humo katika mazingira na ratiba ya kipekee inayowasaidia katika kunyanyuka kwa utukufu wa mwezi huu na nafasi yake kubwa. Na saumu ina faida na manufaa makubwa. Katika upande wa kiafya saumu inaleta raha ya kimwili kwa viungo vya mwili, na katika kazi ya kumeng‟enya chakula, kama ambavyo unaleta fursa ya kutumika chakula kilicho hifadhiwa, na kutoa sumu iliyorundikana humo, na kuchangamsha kazi ya mabadiliko ya harakati, na kwa hiyo hivi sasa jopo la matabibu linazingatia kile wanachokiita “funga ya tiba”, na wanakipa istilahi ya kiafya, ambayo inatibu mkanganyiko wa mwili na baadhi ya maradhi yake ya kudumu. Na wametunga kuhusu hilo vitabu vya elimu vilivyoenea kama vile kitabu cha Atadaawiy biswaum, mtunzi wake ni H. M. Shelton, ambacho kimetarujumiwa katika lugha ya Kiarabu na kimesambazwa mwaka 1987 na Darul-Rashid – Damascus/Beirut. Na katika upande wa kinafsi hakika ina dauru kubwa ya mazoezi kwa ajili ya kumlea mwanadamu katika kudhibiti raghaba zake na matamanio yake, ambapo anajizuia kwa maamuzi binafsi dhidi ya chakula na vinywaji, na vifunguzi vingine pamoja na kuvipenda kwake au kuvihitajia kwake katika baadhi ya nyakati. Na kijamii: Mwanadamu anahisi ndani ya saumu njaa ya mafakiri na wasionacho, anahisi mateso yao na haja zao. Kiroho: Hakika kujizuia na raghaba, na kujishughulisha na hali tukufu ya mwezi mtukufu kunazalisha usafi wa kiroho na uchangamfu wa kimaanawi wa hali ya juu. Lakini faida na 71

Al-Majlisiy: Muhammad Baaqair katika Biharul-Anuwar, Juz. 93, uk: 356 chapa ya pili 1983 Daru Tirathi al-Arabiy - Beirut.

107


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

manufaa haya na mfano wake, hakika zinapatika pamoja na uelewa wake na kuleleka kwake, na kutoa fursa katika faradhi ya saumu tukufu na kwa mazingira ya Ramadhani tukufu, kuleta utendaji wake na kutoa athari zake bila ya vikwazo au hali kinzani na pinzani. Na ambayo yanasikitisha ni kustawi kwa baadhi ya ada za kimakosa na hali mbaya ambazo zinatengua athari za saumu na kupunguza kunufaika na baraka za mwezi mtukufu. Na katika mazungumzo haya tunaangazia hali hizi mbili mbaya zinazoenea aghlabu ndani ya wafungaji, na kusababisha kuwanyima manufaa yanayotakiwa, kutokana na faidia ya mwezi huu mtukufu. Hakuna nafasi ya uvivu na uzembe: Mwanadamu anapomiliki wakati ghali na muhimu, ni juu yake kuutumia katika vitendo na ratibu bora zaidi, na sio kuupoteza katika mambo ya kipuuzi na yasiyo na maana. Mwezi wa Ramadhani ni fursa bora zaidi na wakati ghali zaidi unaopita kwa mwanadamu katika mwaka, inapasa kuuchunga sana katika saa zake, sekunde kati ya sekunde zake, kama ilivyopokewa katika maneno ya Mtume wa Mwenyezi Mungu : “Siku zake ni siku bora kabisa, usiku wake ni usiku bora zaidi, na saa zake ni saa bora zaidi.” Na maana ya hayo ni kuja mwezi wa Ramadhani kwa ratiba bora zaidi na vitendo bora zaidi, na uzalishaji wa mwanadamu humo uwe ni mwingi zaidi na harakati zake ziwe ni nyingi zaidi. Na kwa hiyo tunaona mafunzo ya Kiislamu yanatoa ratiba kwa wingi ya amali za ibada katika mwezi wa Ramadhani: - Kuna nyuradi na swala nyingi za mustahabu - Dua mbalimbali katika masiku na nyusiku za mwezi huu. Anasema al-Imamu Ali : “Ni juu yenu katika mwezi wa 108


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Ramadhani kukithirisha istighifari na dua.” - Kusoma Qur‟ani ni mustahabu kuzidisha na kukithirisha, kama ilivyopokewa katika hadithi kutoka kwa al-Imamu al-Baaqir : “Kila kitu kina vuli yake na vuli ya Qur‟ani ni mwezi wa Ramadhani.” Na katika nyanja ya kijamii: Kuna maelekezo ya kidini ya kuzidisha harakati za kijamii katika mwezi wa Ramadhani, kama tunavyosoma katika khutuba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu  kuhusu mwezi huu mtukufu ambapo anasema: “Na toeni sadaka kwa mafakiri wenu na masikini wenu. Na waheshimuni wakubwa wenu na wahurumieini wadogo wenu. Ungeni udugu wa jamaaa zenu, wahurumieni mayatima na watu watahurumiwa mayatima wenu.” “Mwenye kumfuturisha mfungaji miongoni mwenu katika mwezi huu kwa hayo atapata kwa Mwenyezi Mungu malipo sawa na kumwacha mtu huru, na msamaha wa yaliyotangulia katika madhambi yake.” Na katika hadithi nyingine: “Mwenye kumfuturisha mfungaji anapata mfano wa malipo yake.” Riwaya hizi na mfano wake zinamaanisha kwamba mwanadamu awe na ratiba nyingi ndani ya mwezi wa Ramadhani katika upande wa ibada na nyanja za kijamii, na wakati wa mwanadamu humo unakuwa umesheheni shughuli na umejaa harakati. Ni mwezi wa shughuli, harakati na kazi: Lakini waliyoyazoea wengi katika jamii zetu ni kuufanya mwezi huu mtukufu ni msimu wa uzembe na uvivu, ambapo humo hushuka kiwango cha ufundishaji katika madrasa, utendaji kazi katika maofisi na taasisi, na sehemu kubwa ya watu humo hutumia mchana kwa kulala na kupumzika, kwa hoja ya kufunga, 109


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

kana kwamba funga inalingania uzembe, au ni badala ya kazi. Mwanadamu anasimamisha shughuli zake ili afunge, na inaonekana katika ripoti kupungua kiwango cha uzalishaji wa kiutendaji katika sehemu ya jamii za Kiislamu katika mwezi wa Ramadhani. Wakati ambapo tunakuta katika historia ya Kiislamu kwamba mwezi mtukufu wa Ramadhani kulitokea vita vingi vikubwa baina ya Waislamu na makafiri, na Waislamu walipata ushindi na nusra kubwa, vita vya Badri vilitokea katika mwanzo wa mwezi wa Ramadhani. Mwenyezi Mungua alifaradhisha saumu yake katika mwaka wa pili hijiria, na ufunguzi wa Makkah tukufu ulipatikana katika mwezi wa Ramadhani mwaka wa nane hijiria. Na katika mwezi wa Ramadhani Waislamu walifungua kisiwa cha (Roudis) mwaka wa 35 Hijiria, kama ambavyo walifungua mipaka ya Andalusi (Hispania) chini ya uongozi wa Musa bin Nasir mwaka 91 Hijiria. Humo walishindwa Wafaransa wa kinaswara ambao waliteka Syria na viunga vyake katika mikono ya wanajeshi wa Kiislamu mwaka 584 Hijiria. Na baba zetu na mababu zetu walikuwa wanafunga mwezi wa Ramadhani pamoja na kufanya kazi zao za kimaisha. Kazi hazikuwa zinasimama katika nchi zetu wakati wa funga. Namna gani imetokea hali hii mbaya kwa kutawala uzembe na uvivu kwa wengi katika mchana wa mwezi wa Ramadhani? Hakika kukesha usiku wa siku za mwezi wa Ramadhani kwa ibada na amali za kheri ni jambo jema, lakini wengi wanakesha usiku katika vikao vya kipuuzi au ndani ya vipindi visivyo na faida. Humo kunatakiwa kupitisha wakati tu, kisha wanatumia mchana wao mwingi kwa kulala badala ya kazi ya uzalishaji. Na katika upande wa kiafya: Hakika kulala wakati wa funga kunadhoofisha mwili kunufaika, na saumu zimetaja rejea za 110


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

kitabibu: Kwamba harakati za viungo katika muda wa baada ya kufyonza chakula – wakati wa funga – unachambua kazi zote za oxcid kwa kila kiungo kinachoupa mwili nguvu na kufanya kazi ya kuchanganua mafuta, kama ambavyo pia unafanyakazi ya kutengeneza glucose katika ini kutokana na mafuta yanayotokana na mchanganuo wa mafuta katika rojorojo ya mafuta, na kutokana na rojorojo inayozalishwa na oxcid ya glucose katika misuli. Na kitabu Swiyaamu Muujizatul- Ilimiyah cha Dr. Abdul-Jawadi Swaawiy kina utafiti mzuri kuhusu maudhui haya chini ya anwani: Je, kilicho bora katika saumu ni kujishughulisha au kujipumzisha?72 Ukiongozea katika hayo hakika kulala mchana kwa mfungaji kunatengeneza uporaji wa malengo mengi ya saumu. Kwani hatohisi njaa wala haimshughulishi raghaba ya matamanio. Namna gani itasadiki kwa mfaungaji aliyelala kwamba anaonja njaa na anahisi mateso ya wasionacho? Au vipi anakuwa juu ya matamanio yake na raghaba zake na kustawi kipaji cha uchamungu? Na ikiwa mwanadamu mwaka mzima anakula na anakunywa wakati wa mchana, na anajizuia na kula na kunywa wakati wa kulala kwake usiku na anajizuia na kula naye amelala wakati wa mchana sasa kuna tofauti gani? Kuondoa matamanio ya chakula: Miongoni mwa faida za saumu za dhahiri ni kumlea mwanadamu katika kudhibiti matamanio ya chakula, na hiyo ni kwamba kuna viwango viwili katika mwanadamu kula chakula. 72

Swaawiy: Dr. Abdul-Jawadi katika Swaiyamu muujizatu ilimiyah, uk: 114 – 123 chapa ya kwanza 1993 Darul-Qiblati – Jiddah.

111


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Kiwango cha kwanza: Haja ya mwili kwenye chakula, kwa sababu umetengenezwa kwa chembechembe za ardhi: Udongo, maji na hewa, na Mwenyezi Mungua ameshadhalilisha mimea na wanyama kama chakula cha mwanadamu. Mwili wake unabaki hai kwa vitu hivi na virutubisho vyake, ili maisha yake yaendelee na kustawi, na inatosha kutimiza lengo hili kwa kiasi kidogo cha chakula. “Inamtosheleza mwanadamu tonge chache kwa ajili ya kuimarisha mgongo wake,” kama ilivyopokewa kutoka kwa Nabii .73 Kiwango cha pili: Hali ya raghaba ya matamanio, ambapo mwanadamu anaburudika kwa vionjo vya chakula, na anavutiwa na aina zake mbalimbali. Anakula kwa kuitikia hizi raghaba zake, na kuvuka haja ya mwili wake, bali anakula ambayo yanadhuru mwili wake katika idadi na aina. Na hapa mwanadamu anatofautiana na wanyama, ambapo matamanio yao yanafungamana na haja ya miili yao na kwa hadhi ambayo imedhalilishwa kwake. Ama mwanadamu matamanio yake yana upeo mpana zaidi kuliko mahitaji yake, akiyaitikia na akayakubalia katika kula na kunywa, hakika hayo yanasababisha kwake maradhi na magonjwa mengi. Na hivyo tiba inahadharisha kuchupa mpaka katika kula, na kutokuwa na uwiano humo, kama ambavyo yanatia mkazo juu ya hayo mafunzo ya dini. Imepokewa kutoka kwake : “Jihadharini na ziada ya vyakula, hakika inatia sumu katika moyo kwa ziada.” Na anasema Imamu Ali : Mwenye kukithirisha mlo wake inadhoofika afya yake.”74 Na matatizo mengi ya mwanadamu ya kiafya yanatokana na 73

Al-Majilisiy: Muhammad Baaqir katika Biharul-Anuwar, Ju. 63, uk: 329 chapa ya tatu Daru Turathi al- Arabiy – Beirut. 74 Raishahariy: Muhammadiy katika Mizanu al-Hikimatiu, Juz. 1, uk: 117 – 118.

112


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

kuendekeza matamanio ya kula na kunywa, na hususan katika zama hizi ambazo humo kuna njia za matangazo na propaganda ya kuhamasisha hali ya kutumia vyakula. Viwanda na maduka ya vyakula yanakwenda mbio kuchochea raghaba za watu zaidi katika aina za uzalishaji wa vyakula, kama ambavyo mazingira ya maisha kwa wengi hayalazimu kutoa juhudi na harakati ili kutumia nguvu ambayo inaletwa na chakula katika mwili. Na inakuja fursa ya saumu ili mwanadamu azinduke katika dharura ya kudhibiti chakula chake na vinywaji vyake na kudhibiti raghaba yake na shauku yake, lakini yanayosikitisha sana ni yale ambayo yanatawala maisha ya jamii zetu nyingi, ambapo unaongezeka utumiaji wa vyakula katika mwezi wa Ramadhani. Kulingana na baadhi ya ripoti za kiuchumi, hakika utumiaji wa dola za Kiislamu wa vyakula unaongezeka katika mwezi wa Ramadhani. Mwezi mtukufu wa Ramadhani umekuwa ni msimu wa vyakula, na mwanzo wa matamanio ya chakula! Unapofika tu wakati wa kufuturu mwanadamu anakimbilia kwenye meza ya chakula kwa pupa na uroho kana kwamba analipiza kisasi kwa ajili ya tumbo lake kwa muda wa kufunga kwake!! Kuenea kwa kisukari na maradhi ya moyo: Na katika jamii zetu na ambapo kuna wasaa wa kiuchumi, na kuendekeza shauku na raghaba, tumekuwa tunakabiliwa na kuenea kwa baadhi ya maradhi hatari, ambayo aghlabu yanazalishwa na kutodhibiti ratiba ya vyakula. Imetangazwa katika mkutano wa kisukari wa ulimwengu ambao ulifanyika Cairo, kwamba Saudi Arabia inaongoza katika orodha ya dola ambazo yanaenea maradhi ya kisukri, baada ya kubainika 900,000 za hali za kisukari katika Saudi Arabia yaani asilimia 17 katika jumla ya wakazi wake. 113


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Kama ambavyo ulifanyika mkutano wa tiba Dhwaharan kwa anwani ya “Kisukari maafa ya mustakabali,â€? uliashiria utafiti wake kwenye ongezeko la matatizo ya kisukari hatari kama vile kufeli figo na shinikizo la moyo na kukata viungo. Katika mwaka mmoja kulifanywa operesheni ya kukata viungo katika Saudi Arabia kwa sababu ya kisukari, Riyadhi peke yake operesheni 36 za kukata viungo hufanyika kila siku!! Nayo ni idadi ya juu katika wastani wa kiulimwengu. Na ripoti ya kila mwaka ambayo inatolewa na chama cha afya cha ulimwengu inaashiria wastani wa ongezeko la kila mwaka la maradhi ya kisukari katika Saudi Arabia, kwa wastani wa asilimia 4, yaani watu 36 elfu wapya kwa kila mwaka wanapatwa na kisukari katika Saudi Arabia!! Na sehemu ya Mashariki inaweza kuwa ni ya kwanza katika ongezeko la kupatwa na maradhi haya.75 Na sambamba na maradhi ya kisukari kunaongezeka maradhi ya moyo ambayo aghlabu yanatokana na ongezeko la kiasi cha kolostrol na mafuta katika mwili wa mwanadamu. Hakika ni wajibu wetu tuangalie upya katika ratiba yetu na mazoea yetu ya vyakula pamoja na kubadilisha mtindo wa uhai wetu na maisha yetu, na wala haisihi abadani kuitikia raghaba na matamanio mukabala wa afya zetu na mustakabali wa maisha yetu. Ni wajibu wetu tuziulize nafsi zetu: Je, sisi tunaishi ili tule au tunakula ili tuishi, ikiwa chakula ni kwa ajili ya kuisihi basi tudhibiti kulingana na maslahi ya uhai. Na mwezi wa Ramadhani inapasa tufanye mazoezi humo kwa kudhibiti chakula, ili tunufaike na faradhi tukufu ya saumu. Ewe Mwenyezi Mungu ulete kwetu kwa amani na imani, salama, Uislamu na afya tele na riziki pana na kuondoa maradhi. Ewe Mwenyezi Mungu turuzuku funga yake na kusoma Qurâ€&#x;ani humo. Ewe Mwenyezi Mungu usalimishe kwetu na usalimishe 75

Sahariq: jarida la kila wiki tolea la 999 uk: 14

114


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

kwa ajili yetu na utasalimishe humo.76 MWANACHUONI WA KIDINI NA KUITAKASA NAFSI (SHEIKH MANSUR AL-BAYAATI NI MFANO) Jukumu kubwa na lengo la msingi la dini ni kuitakasa nafsi, na katika hadithi katika wadhifa wa Mtume , Qur‟ani tukufu inataja kutakasa kama kazi ya kwanza, anasema (swt):

َ​َ َ َ َ ‫ُ َ ى‬ ََُّ ٰ َ ُ ً َ َ ّۧ ّ ُ ِ ‫”هى الزي ٰػث ِفى ِميكن سظىال ِمن يخلىا غلي ِ ءايك ِخ ِه ويضهي‬ َ َ َ َ ُ ُ َّ َُ “….. ‫ىم ِت‬ ‫احخ‬ ِ ‫الىخكب و‬ ِ ُ​ُ ‫ويػ ِلم‬ “Yeye ndiye aliyempeleka Mtume kwenye watu wasiojua kusoma, aliyetokana na wao awasomee aya Zake, na awatakase. Na awafunze Kitabu na hekima…..” (Surat Al-Jumu‟a; 62:2) Na yanakaririwa mfano wa hayo katika sehemu tatu zingine. Na utakaso ni hekima ya vipengele vingi vya sharia ya Uislamu. Kuchukua zaka, sadaka ni kwa ajili ya kuleta utakaso katika nafsi za wenye kupewa mawaidha. Anasema (swt):

َ ُ ًَ َ َ َُّ ٰ ‫” ُ ز من َأ‬ “….. ‫صذكت جط ِ ُّ ُش ُه َوجضهي ِ ِب ا‬ ُِ ‫مى ِل‬ ِ “Chukua katika mali zao sadaka uwasafishe na uwatakase kwayo.” (Surat At-Tawba; 9:103). Na kuinamisha macho dhidi ya yale yaliyoharamishwa, na kudhibiti matamanio ya kijinsia ni njia ya kutakasa vilevile, anasema (swt):

ٰ َ َ َ​َ ّ ‫” ُكل ل ُلمؤم َحن َي ُغ‬ َ ‫دفةىا ُف‬ ٰ ‫شوج ُ​ُ ِ ٰر ِل ًَ َأ‬ ‫صوش‬ ‫ضىا ِمن أبصك ِش ِه وي‬ ِ ِ َ “….. ُ​ُ ‫ل‬ 76

Dua ya Mtume wa Mwenyezi Mungu 

115


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

“Na waambie waumini wanaume wainamishe katika macho yao na wazilinde tupu zao. Hayo ni usafi zaidi kwao…..” (Surat An-Nur; 24:30) Na utakaso ni njia ya kufaulu na kushinda: “Hakika amefaulu aliyeitakasa” (Surat Shamsi; 91:9), pamoja na angalizo kwamba aya hizi zimekuja zikiwa ni jawabu la viapo alivyoapa Mwenyezi Mungu katika mwanzo wa Surat Shamsi, anasema (swt):

َ َ ‫َ ى‬ ُ ‫الشمغ َو‬ ‫﴾ َو ى‬٧﴿ ‫الل َمش إرا َج ٰلىُا‬ ٰ ‫ض‬ ‫الن ِاس ِإرا‬ ‫﴾ و‬٧﴿ ‫خىُا‬ ‫و‬ ِ ِ ِ َ َ َّ ‫َ ى‬ َ َ َ َ ٰ ٰ ٰ ‫ى‬ ِ ‫﴾ والع‬٤﴿ ‫يل ِإرا يغشىُا‬ ِ ‫﴾ وال‬٣﴿‫جلىُا‬ ِ ‫﴾ و س‬٥﴿ ‫ماء وما ب َنىُا‬ َ ُ َ​َ َ ّ َ َ َ ٰ ٰ َ َ َ ‫﴾ فألُمُا فجىسها‬٧﴿ ‫فغ وما ظىًُا‬ ٍ ‫﴾ و‬٦﴿ ‫وما دىُا‬ ٰ ‫َو َج‬ ﴾٨﴿ ‫لىًُا‬ “Naapa kwa Jua na mwangaza wake. Na kwa mwezi unapolifuatia. Na kwa mchana unapolidhihirisha. Na kwa usiku unapolifunika. Na kwa mbingu na kuzijenga kwake. Na kwa ardhi na kuitandaza kwake. Na kwa nafsi na kuilinganisha kwake. Akaifahamisha uovu wake na takua yake.” (Surat Ash-Shams 91:1-8) Baada ya viapo hivi vingi kwa vitu muhimu katika ulimwengu linakuja jawabu la kiapo “Hakika amefaulu mwenye kuitakasa.” Jambo ambalo linaonyesha juu ya umuhimu wa ukweli huu na unyeti wake. Na katika aya nyingine anasema (swt): “Amefaulu aliyejitakasa” (Suratul-Alaaa: 14). Na Malaika alipombashiria Bibi Mariyam binti Imran kwa kumzaa Nabii Isa  alitosheka na kumwelezea kwamba ni mtoto mwema.

۠ َ ‫َ ى‬ َ ُٰ َ َ ‫كاٌ ِإ ما أ ا َسظى ٌُ َسِّب ًِ ِ​ِل َه َب ل ًِ غلك ًما ص ِه ًّيا‬ 116


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii “Akasema: Hakika mimi ni mjumbe wa Mola Wako ili nikupe mwana mtakatifu.” (Surat Maryam 19:19)

Maana ya utakaso: Utakaso ni lengo la ujumbe na ni jukumu la Manabii, na ni hekima ya sharia, ni njia ya kufaulu na kushinda. Una maana gani na nini makusudio yake? Tazikiya (utakaso) linatokana na zakau na zakaatu. Amesema katika Lisanul- Arab: Ni kwa maana ya kustawi. Imekuja katika maneno ya Imamu Ali : “Mali inapungua kwa kuitoa na elimu inaongezeka kwa kuitoa.” Na kila kitu kinachoongezeka na kumea basi kinastawi na kunawiri. Na Zakaatu pia inamaanisha: Utwahara. Na kauli yake (swt): Tuzakiihim Bihaa wamesema: unawatakasa kwayo. Kama ambavyo linamaanisha: wema. Amesema al-Farau: Zakatu ni wema, na vilevile kauli yake (swt): “Na tukampa huruma itokayo kwetu na utakaso.” Amesema wema. Lakini Mwenyezi Mungu anamtakasa amtakaye yaani anamfanya kuwa mwema. Na katika hadithi ya Imamu al-Baaqir  amesema: “Utakaso wa ardhi ni kukauka kwake” anakusudia utwahara wake kutokana na najisi kama vile haja ndogo na mfano wake kwa kukauka na kuondoka athari yake.77 Na imekuja katika Majimaul-Bahrain: Tazikiya: Ni kutakasika na tabia mbaya. Na katika al-Gharib: “Amefaulu mwenye kuitakasa” yaani amefaulu aliyetwaharisha nafsi yake kwa amali njema. Kauli yake (swt): “Je, umeuwa nafsi isiyo na hatia” yaani twahara. Na kauli yake (swt): “Kijana mwema” yaani ni mwenye kutwaharika kutokana na madhambi. Na umekaririwa utajo wa zaka katika Kitabu na Sunnah, nao ima unatokana na ustawi kwa 77

Ibnu Mundhir katika Lisanu al-Arab al-Muhit, Juz. 3, uk: 36- Daru Lisanu al-Arab – Beirut 1988

117


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

sababu italeta baraka katika mali na kuongezeka kwake. Na ima unatokana na utwahara kwa sababu mali inatwaharika kutokana na uchafu, na nafsi bakhili inatwaharika kutokana na ubakhili.78 Na kutokana na maana yake ya kilugha yanabainika makusudio yake, na kwamba ni kuitakasa nafsi na kuirekebisha na kustawi utashi na mielekeo ya kheri kwayo. Mwanachuoni wa kidini: Na ikiwa dini inalenga kuleta hali ya utakaso katika nafsi ya mwanadama, hakika mafanikio yake na utekelezaji wake hakika unatimia kwa kujua uongofu wa kidini na maelekezo yake, na kwa kuwa karibu na vyanzo vyake na mazingira yake. Na mwanachuoni wa kidini kwa kujua kwake juu ya mafunzo, na kwa kuwasiliana daima na mafuhumu na nususi za kidini, hakika ni mbora zaidi na anafaa zaidi kumiliki hali hii ya utakaso wa nafsi. Na vilevile kwa kuwa yeye yuko katika nafsi ya kigezo kwa wengine, na mlinganiaji na mwelekezaji wao, ni lazima yeye asifike na ajipambe na yale anayowalingania wengine. Na hapa nususi za kidini zinatia mkazo dharura ya kupatikana kwa mwanachuoni wa kidini utwahara wa nafsi na usafi wake, na asiwe amening‟inia katika matamanio na shahawati, au amejifungia kwenye hasira, anasema (swt): “Hakika wanaomuogopa Mwenyezi Mungu katika waja Wake ni wanachuoni.” (Suratu Fatwir: 28). Na imepokewa kutoka kwa Amirul-Muuminina  kwamba amesema: “Mwanachuoni hawi ni mwanachuoni hasa mpaka asimhusudu aliye juu yake, wala asimdharau aliye chini yake, wala asichukue chochote katika elimu yake miongoni mwa manufaa ya kidunia.”79 78 79

Twariyhy: Fakhar Diyn katika Majiumaul-Baharain, Juz. 1, uk: 203 - 205 Al-AmadiyTamiymiy: Abdul-Wahdi katika Ghurararul-Kalimi, Juz. 2, uk. 270, Muasasatu al-Ilimiy lilimatubuati - Beirut

118


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Na kutoka kwake vilevile : “Mwenye kuifanya nafsi yake ni kiongozi wa watu basi na aanze kuifunza nafsi yake kabla ya kumfundisha mwingine. Na awaadabishe kwa sira yake kabla ya kuwaadabisha kwa ulimi wake. Na awe mwalimu wa nafsi yake mwenyewe na mwadabishaji wake kabla ya kuwa mwalimu wa watu na mwenye kuwaadabisha wao.”80 Imepokewa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu  kwamba amesema: Katika usiku niliopelekwa Israi nilipita kwa watu wanaokatwa midomo yao kwa mikasi ya moto. Nikasema: Ni nani hawa ewe Jibrail? Akasema: “Hawa ni makhatibu wa umma wako ambao wanasema wasiyoyatenda.”81 Na katika hadithi kutoka kwa Imamu Ja‟far Sadiq : “Atasamehewa jahili dhambi sabini kabla ya kusamehewa mwanachuoni dhambi moja.”82 Kigezo chema: Katika siku hizi tumepata msiba mkubwa, msiba wa kumpoteza mwanachuoni mchamungu mwenye kujinyima, kilele cha kigezo chema na utakasifu wa nafsi, naye ni Allammah Sheikh Mansuri al-Bayaan (Mwenyezi Mungu amrehemu). Hakika kufariki kwake kumeambatana na mazingatio ya wananchi, ambapo mazishi yake alasiri ya siku ya Jumanne iliyopita 29 Shaaban, yalionesha mshikamano mzuri wa kidini na wa kiraia katika Qatif, kama ambavyo mkusanyiko mkubwa ambao unaadhimisha majilisi ya maombolezo uliokusanyika kwa ajili ya 80

Al-Musawiy: Sharifu Ridhaa katika Nahjul-Balaghah Qiswaril-hikam namba 73 81 Raishahariy: Muhammady katika Mizanul-Hikima, Juz. 6, uk. 514 82 Al-Majilisiy: Muhammad Baaqir katika Biharul-Anuwar, Juz. 2, uk. 27.

119


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

marehemu, na rambirambi ambazo zimekuja kutoka kwa viongozi wakuu na kutoka kwa Marajii wa kidini na watu mbalimbali, yote hayo yanatia mkazo athari ya sira njema katika nafsi za watu. Na hatutaki kuzungumzia kuhusu fadhila yake ya kielimu, kwani ushahidi wa wanachuoni na Marajii juu yake unabainisha nafasi yake tukufu, kama ambavyo hatutaki kuzungumzia kuhusu utunzi wake na vitabu vyake ambavyo vinafikia vitabu 35, pamoja na kwamba alikuwa ni mlemavu wa macho, mzee, anakabiliwa na maumivu, magonjwa na maradhi. Hakika nitaelekeza mazungumzo yangu kuhusiana na aliyokuwanayo katika usafi wa nafsi na utwahara wa moyo, ambapo aliakisi uhalisia katika jamii yetu wa sira ya mwanachuoni mchamungu, ambaye alitakasa nafsi yake. Basi mwendo wake ukawa mzuri na sira yake ikawa nzuri. Na tunaashiria mafunzo mawili yanayoonekana katika sira yake nzuri, ili yawe ni mahala pa kuigwa na kigezo. Kutoka katika umateka wa tamaa: Wengi wanastaajabu katika maisha ya uchamungu ambayo alikuwa anaishi Sheikh, naye anatokana na familia tajiri, na chini ya harakati zake kulikuwa na uwezo mkubwa, lakini yeye tangu mwanzo wa maisha yake alichagua njia ya elimu, na dini ikachanganyika na nafsi yake na hivyo maisha ya kujinyima na kujizuia yakadhahiri. Yeye anakaa nyumba ndogo ya zamani na samani chache sana, na anajiepusha na aina mbalimbali za vyakula na vinywaji, isipokuwa kinachomuwezesha kuishi, na kumbakisha katika uhai. Kama ambavyo alikuwa ni mzalendo, mnyenyekevu katika muamala wake pamoja na watu na mambo, haihusishi nafsi yake na kiburi chochote, na baada ya kukata masafa katika masomo yake 120


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

katika mji wake wa Qatif, alikuwa na nafasi, heshima na kuaminika, lakini aliamua kuacha mji wake na kuhamia Najaf tukufu mwaka 1380 hijiria. Wakati huo alikuwa ana miaka 55 katika umri wake Alikwenda huko ili kuendelea na masomo, nao ni uamuzi wenye ushujaa mkubwa kwa mtu mwenye umri kama wake na hali yake, kama vile kukosa macho, na hana mtoto anayemsaidia, ambapo alikuwa ameshapoteza mtoto wake wa pekee (Ahmad) ambaye alikuwa katika umri wa ujana wake, kama ambavyo katika uamuzi huo ni kuachana na hali ya jamii inayomzunguka. Hivi ndivyo alivyochukua uamuzi wake na akasafiri akiwa tayari kwa matatizo na ugeni bila ya kumzuia katika hayo tamaa au kuelemea kwenye raha. Na akarejea katika nchi yake baada ya miaka 25, hali na mambo yalipoharibika Iraki. Alikuwa ameshapata kiwango cha juu cha elimu, lakini yeye hakuwa anataka cheo chochote au nafasi yoyote, na haikubadilika hali yake ya kuamiliana na watu, bali alizidi unyenyekevu na uchamungu, na kujiweka kando na tamaa. Na mwanachuoni wa kidini hawezi kutekeleza jukumu lake kwa ukamilifu ila atakaposifika kwa uchamungu, na asili ya uchamungu ni kutonyenyekea tamaa na matamanio, ili awe ni mwenye kuwalingania watu kwa sira yake na tabia yake, na kuwa ni mfano na usadikishaji wa kushikamana na maadili na misingi. Na kisha mawaidha yake yanachukua nafasi yake katika nyoyo. Ama ikiwa mwanachuoni wa kidini anapupia tamaa na vyeo na matamanio, hakika atatengeneza hatari kubwa katika dini ya Mwenyezi Mungu. Imepokewa katika hadithi kutoka kwa Imamu Ja‟far Swadiq : “Mwenye kuzidi kumjua Mwenyezi Mungu, na akazidi kuipenda dunia, basi anazidi kuwa mbali zaidi na Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu anazidi kuwa na ghadhabu juu yake.”83 Na 83

Rejea iliyotangulia, Juz. 70, uk: 124

121


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

kutoka kwake : “Mtakapoona mwanachuoni anaipenda dunia basi mtuhumuni katika dini yenu, hakika kila mwenye kupenda anajongea kwa anayoyapenda.”84 Hakika muonekano wa kujinyima uwazi wake unatofautiana kati ya mwanadamu na mwingine, na kinachotakiwa sio kuiga neno kwa neno maisha ya mwanakujinyima kati ya wanakujinyima, lakini cha muhimu ni kupata uhalisia wa kujinyima na asili yake, nayo ni kujikomboa kutokana na tamaa na matamanio, kama inavyopokewa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu  kwamba amesema: “Kujinyima sio kuharamisha halali lakini ni kuyatumaini zaidi yaliyoko katika mamlaka ya Mwenyezi Mungu kuliko yaliyopo mikononi mwake mtu.”85 Na inapokewa kutoka kwa Imamu Ali : “Kujinyima sio kutomiliki kitu lakini kujinyima ni kutomilikiwa na kitu.” Usafi wa kuamiliana na watu: Sheikh aliyeondoka alikuwa amefunguka kwa watu, kwa makundi yao mbalimbali, na mirengo yao mbalimbali. Na hakuwa anabeba katika moyo wake husuda kwa yeyote, wala chuki kwa yeyote. Pamoja na kwamba alikuwa na fikra zake na rai zake maalum, lakini hakumfanyia uadui yeyote kwa kuhitalifiana kwake naye katika rai, na wala hajaingia katika vita wala mzozo kuhusu kadhia kati ya kadhia. Ameishi pamoja na ikhitilafu za Marajii, baina ya nyumba ya Marjaa huyu na Marjaa yule, na baina ya kundi la Marjaa huyu na la Marjaa yule, lakini hakuchukua msimamo dhidi ya yeyote katika msingi huu, wala hajalitenga mbali kundi kati ya makundi, au kupiga vita mrengo kati ya mirengo, bali alikuwa amejiepusha na mambo haya na kuchukua msimamo wa ubaba na upendo katika jamii. Na kwa sababu hiyo wote walimheshimu na waliwasiliana naye na 84 85

Rejea iliyotangulia, Juz. 2 uk: 107 Rejea iliyotangulia, Juz. 74, uk: 172

122


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

wamehisi hasara kwa kumkosa kwake. Hakuwa anamtaja mwanachuoni yeyote katika wanachuoni ila kwa kheri, na hakuwa anaridhia kusengenywa yeyote au kudharauliwa katika majilisi yake, bali aliwalea waliokuwa pembezoni mwake kuwaheshimu watu wote. Na hivi ndivyo inapasa kuwa mwanachuoni wa kidini. Aepukane na chuki, awe mbali na uadui na mizozo, anaeneza upendo wake na anazatiti hali ya umoja na uelewano katika jamii. Jamii yetu imeteseka sana na ikhitilafu na mizozo ndani ya mazingira ya kidini, ambapo kila upande unatia mkazo misimamo yake na kuushadidia upande mwingine, na mtu anaifanya nafsi yake ndio mwamrishaji na ndio mwenye kuwahisabu wengine, katika rai zao na misimamo yao na maelekezo yao. Dini na haki ni ambayo anaiona yeye tu, ama wengine anawahukumu kwa kupotea, ufasiki na upotovu. Hivi ndivyo imeparaganyika jamii, na ukapungua usadikishaji na uaminifu wa wanachuoni wa kidini katika nafsi za watu. Hakika sisi tuna haja sana ya kuvuka hali hizi, na kujikita katika changamoto hatari ambazo dini yetu na jamii yetu inakabiliana nazo, na kusaidiana katika mambo ya pamoja, nayo ni mengi zaidi na muhimu zaidi kuliko masâ€&#x;ala ya ikhitilafu ndogo ndogo na za pembezoni. Na tuikuze hazina hii ya kimaanawiya ya kijamii, ambayo ameianzisha Sheikh aliyeondoka. Na mkusanyiko huu mkubwa ambao wote wameshiriki humo, ni kwa ajili ya kuimarisha hali ya umoja na uelewano katika jamii. Na iwe tabia yake njema na sira yake nzuri ni kigezo kwa waumini, na hususani kwa wanajamii wa aina yake kati ya wanachuoni na wanaotafuta elimu ya dini. MWEZI WA RAMADHANI NA KUJICHUNGUZA Kama kila mwanadamu atajitafakari mwenyewe na kusoma maisha yake atazijua fikra alizonazo, sifa za kinafsi na utu 123


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

alionao, na tabia mahususi alizonazo, na atagundua kwamba anaishi ndani ya hali na muundo unaopamba maisha yake binafsi na ya kijamii. Na suala ambalo ni wajibu mwanadamu ajiulize mwenyewe katika nafsi yake ni: Je, yeye yuko radhi na hali ambayo anaishi nayo? Na je, anaihesabu nafsi yake iko katika hali nzuri na bora zaidi? Au anakabiliwa na nukta za udhaifu na mapungufu? Je, fikra alizonazo, sifa na matendo anayotenda ni jambo la lazima kwake na haiwezekani kulibadili au kuliacha? Au ni kwamba yeye ni mwanadamu ameumbwa na Mwenyezi Mungu akiwa huru, mwenye matakwa na hiyari? Hakika maswali haya yamejificha katika nafsi ya mwanadamu mwenyewe na yanatafuta fursa ya kudhihirishwa na kufikiriwa pindi mwanadamu atakapoipa nafsi yake fursa ya kufanya hivyo, pindi atakapojichunguza na kuzama katika kina chake na kupenya katika maficho yake na mikondo yake. Pamoja na kwamba mwanadamu ana haja kubwa ya kujidhihirisha huku, kujikagua na kujichunguza, isipokuwa watu wengi hawasimami pamoja na nafsi zao kisimamo cha kutafakari na kufunguka, hiyo ni kutokana na sababu mbalimbali, zilizo muhimu zaidi ni hizi zifuatazo: Kwanza: Kuzama katika shughuli za kimaisha za kivitendo, nazo mara nyingi hubainika kuwa hazina thamani na umuhimu, na hudhihirika kuwa ni za kipuuzi na zisizo na maana. Pili: Na hili ndio muhimu zaidi, ni kwamba kisimamo cha mwanadamu pamoja na nafsi yake kinahitaji kuchukua maamuzi ya kufanya mabadiliko kuhusiana na nafsi yake. Na hili ndilo jambo ambalo watu wengi wanalikimbia kama ambavyo baadhi wanakimbia kufanya uchunguzi wa afya ya miili yao kwa kuo124


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

gopa kugundua maradhi yatakayomlazimisha kujizuia na baadhi ya vyakula au kutumia tiba maalumu. Wito Kuhusu Kujichunguza: Katika mafunzo ya Kiislamu kuna wito juu ya kujichunguza na kujitathmini, na kutokuendekeza kuzama katika mambo ya kimada na shughuli za maisha ambazo haziishi. Na Imepokewa katika Hadithi kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu : "Zifanyieni tathmini nafsi zenu kabla hamjahisabiwa, na zipimeni kabla hamjapimwa." Na kutoka kwa Imam Ali : "Ni haki ilioje kwa mwanadamu kuwa na muda usiku na mchana wa kutoshughulishwa na chochote, isipokuwa kuitathmini nafsi yake na kutazama aliyoyachuma kwa ajili ya nafsi yake na dhidi ya nafsi yake." Hakika wakati wa kutafakari na kujichunguza unatoa fursa kwa mwanadamu kutambua makosa yake na nukta za udhaifu wake na kumsukuma kuiboresha nafsi yake kwa kuitoa kwenye hali duni kwenda kwenye hali bora zaidi. Anasema Imam Ali : “Matunda ya kujitathmini ni kuirekebisha nafsi." Na anasema : "Mwenye kuifanyia tathmini nafsi yake amefaidika, na mwenye kughafilika nayo amepata hasara." Na huwenda miongoni mwa malengo ya kusimama usiku kwa ajili ya ibada ambapo mwanadamu husimama kwa hali ya kuhofu mbele ya Mola Wake, katika giza na utulivu, ni kutoa fursa hii kwa mwanadamu. Vilevile ibada ya itikafu miongoni mwa hekima yake inaweza kuwa ni lengo hili, na itikafu ni kukaa msikitini kwa lengo la ibada kwa muda wa siku tatu au zaidi pamoja na kufunga, ambapo mhusika hatoki msikitini isipokuwa kwa haja ya kisharia. 125


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Mwezi wa Kutafakari: Haupatikani mwezi mwingine unaolingana na mwezi wa Ramadhani. Ni mwezi bora ambao humo mwanadamu anasimama pamoja na nafsi yake kwa kutadaburi na kutafakari, kwani humo "Malipo huongezeka na makosa hufutwa," kama ilivyopokelewa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu , na katika mwezi huu kuna fursa kubwa ya kupata msamaha wa Mwenyezi Mungu: "Hakika muovu ni yule aliyenyimwa msamaha wa Mwenyezi Mungu katika mwezi huu mtukufu" kama ilivyo katika Hadithi ya Mtume  Na katika riwaya nyingine: "Mwenye kuudiriki mwezi wa Ramdhani na wala asisamehewe basi huyo yuko mbali na Mwenyezi Mungu." Pia imepokewa kutoka kwake : "Mtu asiposamehewa katika mwezi wa Ramdhani basi ni katika mwezi gani atasamehewa?!" Na baadhi ya watu wanaweza kughafilika na kusahau kwamba kupatikana matokeo hayo kunahitajia bidii na juhudi, kwani mwezi huu unapasa kuwa ni mwezi wa kurejea, kutafakari na kuitathmini nafsi. Wakati mwanadamu anapojizuia katika mwezi huu mtukufu kula, kunywa na matamanio mengine yanayojitokeza kila siku, hakika anakuwa ameepukana na vikwazo hivyo, jambo ambalo linampa fursa ya kuzinduka na kuitazama dhati yake na nafsi yake. Na hatimaye inajitokeza hali ya kiroho ambayo imehimizwa na kukokotezwa na mafunzo ya Kiislamu ili kuboresha fursa ya kunufaika na mwezi huu Mtukufu. Swala ya usiku kwa mfano ni fursa halisi kwa ajili ya kujipwekesha na ibada pamoja na Mwenyezi Mungu, na wala haipasi kwa muumini kupitwa na wakati wa usiku kwa kulala au kwa mafungamano mengine ya kijamii na kuinyima nafsi yake nusu saa ya kuwa peke yake humo na Mola Wake, baada ya nusu ya usiku, nao ndio mwanzo wa wakati wa swala hii tukufu ya mustahabu. Na inampasa muumini kupanga wakati kwa ajili ya swala hii ili ilete matunda bora zaidi na matokeo yake. Na aitekeleze huku akiwa katika uchangamfu na nguvu, na sio tu 126


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

kwa kutimiza wajibu au mustahabu, bali lengo lake liwe kutekeleza malengo yake Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

َ ‫َوم َن ىاليل َف َخ َه ىجذ به اف َل ًت َل ًَ َغس ٰى َأن َي‬ ً ‫بػ َث ًَ َسب ًَ َم‬ ‫لاما‬ ِ ِ​ِ ِ ِ ً‫َمدمىدا‬ "Na katika usiku amka kwayo, ni ziada kwa ajili yako; asaa Mola Wako akakuinua cheo kinachosifika." (Surat Bani Israil; 17:79) Na amesema : “Hakika mja anapokuwa mpweke na Bwana Wake katika giza la usiku na akamuomba Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu huthibitisha nuru katika moyo wake, kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu husema kuwaambia Malaika Wake: Malaika Wangu tazameni mja wangu amejipwekesha kwa ajili Yangu katika giza la usiku na wabatilifu wamepuuza na wameghafilika wamelala. Shuhudieni hakika mimi nimemsamehe." Na kusoma Qur‟ani tukufu ni jambo ambalo limehimizwa sana katika mwezi huu mtukufu, kwani ni mwezi wa Qur‟ani; anasema (swt):

ٰ ّ َ َ​َ ُ َ ُ ُ ً ‫شءان ُه‬ َ ‫ضان ىالزي ُأ ض‬ ٌ ‫اط َو َب ِّي ك ٍذ ِم َن‬ ‫ل‬ ‫ل‬ ‫ي‬ ‫ذ‬ ‫الل‬ ‫فيه‬ ‫”شُش سم‬ ِ ِ ِ ِ ُ “….. ‫ذي‬ ِ ٰ ُ‫ال‬ “Ni mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa katika (mwezi) huo Qur‟ani, kuwa mwongozo kwa watu na upambanuzi.” (Surat al-Baqara; 2:185) Na katika Hadithi tukufu imekuja: "Kila kitu kina msimu wa kuchanua, na kuchanua kwa Qur‟ani ni katika mwezi wa Ramadhani," kama ilivyopokelewa kwamba "Mwenye kusoma 127


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

humo aya atakuwa na malipo mfano wa mtu aliyekhitimisha Qur‟ani katika miezi mingine." Kusoma huku hakika kunahudumia na kumwelekeza mwanadamu katika kuichunguza dhati yake, kuifichua na kugundua upungufu wake na makosa yake, lakini hiyo ni kwa sharti la kutafakari katika usomaji huo wa Qur‟ani na kuzingatia kwa kufahamu maana yake na kutazama katika upeo wa kushikamana na maamrisho ya Qur‟ani na kuacha makatazo yake. Imepokewa kutoka kwa Imam Ali  "Hakuna kheri katika kisomo kisichokuwa na tafakari. Tafakarini aya za Qur‟ani na zingatieni yaliyomo humo, hakika ni mazingatio makubwa." Hakika baadhi ya watu wamezoea kusoma na kukhitimisha Qur‟ani mara kadhaa katika mwezi wa Ramadhani, nayo ni ada nzuri, lakini inapasa lengo lisiwe ni kumaliza kurasa tu bila ya kunufaika au kutafakari. Mwanadamu anaposoma aya ya Qur‟ani anapasa asimame na ajiulize juu ya msimamo wake kwa yale inayoyasema aya hiyo, ili atoe fursa ya kuathirika katika moyo wake na kwa ajili ya mabadiliko katika moyo wake na nyendo zake. Imepokewa kutoka kwa Mtume : "Hakika nyoyo hizi zinapata kutu kama kinavyopata kutu chuma.” ikasemwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu tutawezaje kuitakasa? Akasema: “Kwa kusoma Qur‟ani." Na kwa hiyo mwanadamu anatibu maradhi ya nafsi yake na upungufu wa shakhsiya yake, kwani Qur‟ani ni ponyo kwa yaliyomo katika nyoyo. Na dua zilizopokelewa katika mwezi wa Ramadhani kama vile dua ya Iftitaahi, dua ya Sahri na dua za mchana na usiku wa mwezi wa Ramadhan zote ni hazina ya malezi ya kiroho, Zinamletea mwanadamu ushujaa katika kurekebisha dhati yake na kuichunguza nafsi yake, na zinanoa azma yake na matakwa 128


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

yake kwa ajili ya mabadiliko na mageuzi na kumhimiza kutubia madhambi na makosa. Kama ambavyo zinatia mkazo katika nafsi yake utukufu wa Muumba na umuhimu wa hatima yake, na kuiweka mbele ya ukweli na uwepo wake na uhalisia wake bila ya kuwa na pazia. Na mwanadamu anaposoma dua kama vile dua ya Sahri ambayo ameipokea Abu Hamza Thumaaliy ď “ kutoka kwa Imam ZainulAbidin ď „ hakika ni juu yake azingatie vipengele vya dua, kuwa vinaelezea yaliyo katika nafsi yake yeye mwenyewe, na sio asome kana kwamba ni maelezo ya mtu mwingine kwa Mola Wake. Pande za Kutafakari: Hakika kitendo cha mwanadamu kutafakari na kurejea kina umuhimu mkubwa katika pande tatu: Upande wa kwanza: Kurejea katika fikra: Mwanadamu arejee fikra zake na imani yake na ajiulize juu ya kiasi cha haki na usahihi wake. Na lau kama watu wote wangerejea fikra zao na ufuasi wao pengine wangeweza kubadili makosa na upotovu uliopo katika imani zao, isipokuwa uhalisia wa watu wengi ni "Hakika sisi tumekuta baba zetu katika desturi na sisi tunafuata nyayo zao." Na mwanadamu anapaswa awe huru na nafsi yake, mwenye nguvu katika dhati yake. Anapogundua kwamba yuko katika kosa fulani, basi asiogope au asisitesite kubadilika na kusahihisha. Upande wa pili: Kuirejea nafsi: Mwanadamu arejee sifa za nafsi yake ambazo humo imefichikana shakhsiya yake, je ni mwoga au ni shujaa? Ni jasiri au ni mwenye kusitasita? Ni shupavu au ni dhaifu? Mkweli au 129


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

muongo? Muwazi au msiri? Mvivu au mchapakazi? Mwanadamu aulize katika nafsi yake idadi ya maswali ambayo yanafichua upande huu, mfano: Nitafanya nini kama atanijia fakiri katika nyumba yangu? Nitafanya nini kama watoto wangu watachezea samani za nyumba? Nitafanya nini kama kutatokea mbele yangu ajali? Na jibu langu litakuwaje kama nitakosewa mbele ya watu? Na nitaamua nini kama maslahi yangu binafsi yatagongana na dini au maslahi ya umma na jamii? Na umuhimu wa kujirejea huku unajitokeza kwa sababu mwanadamu baada yake anapaswa arekebishe kila upungufu wa kinafsi uliopo kwake, na afanye kazi ya kuboresha nafsi yake na kuisogeza hatua zaidi mbele. Upande wa tatu: Kurejea katika jamii na tabia Mwanadamu arejee nyendo zake na vitendo vyake dhidi ya wengine, kwa kuanzia na mke wake, watoto wake na kumalizia na watumishi wake na wafanyakazi wake na kwa jamaa zake na marafiki zake na watu wengine kati ya anaoamiliana pamoja nao au anaofungamana nao. Na mwezi huu mtukufu ni mnasaba bora wa kupanda daraja kwa utekelezaji wa kijamii kwa muumini, na kuondoa ikhitilafu zote, kasoro za kijamii na mifundo binafsi baina ya mwanadamu na wengine. Riwaya nyingi zimehimiza juu ya hilo kiasi kwamba baadhi ya riwaya zinaeleza: Kwamba maghufira ya Mwenyezi Mungu na msamaha Wake kwa mwanadamu unabakia umeningâ€&#x;inia kwa muda mrefu hadi aondoe yaliyo baina yake na wengine miongoni mwa ikhitilafu na kuwa mbali, hata kama wao ndio wakosaji katika haki yake. Katika hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Imam Ridhaa ď „ amesema: "Katika usiku wa kwanza wa mwezi wa Ramadhani wanafungwa waasi miongoni mwa mashetani na wanasamehewa kwa kila usiku watu sabini 130


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

elfu. Na unapofika usiku wa Lailatul-Qadir Mwenyezi Mungu husamehe mfano wa aliyosamehe katika mwezi wa Rajab, Shaaban na mwezi wa Ramadhani hadi siku hiyo, isipokuwa mtu ambaye baina yake na ndugu yake kuna ugomvi, atasema (swt): Waacheni hawa hadi wasuluhishane." Hata kama mmoja wao ni dhalimu na mwingine ni mwenye kudhulumiwa hakika wao kwa pamoja wanabeba dhambi ya kuhamana na kutengana, ambapo mwenye kudhulumiwa kati yao anaweza kumwanza ndugu yake kwa kusamehe na kuondoa ikhitilafu. Katika hadithi kutoka kwa Imam al-Baqir  amesema: "Hakuna waumini wawili wanaotengana zaidi ya siku tatu isipokuwa watatengwa mbali (na Allah).” Akaambiwa: Ewe mjukuu wa Mtume wa Mwenyezi Mungu: Hii ni katika hali ya mwenye kudhulumu, lakini vipi mwenye kudhulumiwa? Akasema : “Na kwa nini mwenye kudhulumiwa haendi kwa dhalimu na kusema: Mimi ndio dhalimu ili wasuluhishane." Ni uwazi ulioje katika wito wa suluhu ya kijamii, na ni utukufu ulioje wa matokeo kama utatimia ndani ya mwezi huu mtukufu. Na ni ukubwa wa cheo ulioje wa nyoyo hizo ambazo zinaweza kumaliza ikhitilafu zake na kusuuluhishana katika mwezi wa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kupata msamaha wa Mwenyezi Mungu? Hapa hakika mwanadamu anahitaji moyo safi uliotakasika na nia ya kheri na ya kweli kama alivyosema : "Muulizeni Mola Wenu kwa nia za kweli na nyoyo safi." Pongezi kwa mwenye kunufaika na mazingira ya mwezi huu mtukufu kwa kufunguka na kuwa muwazi juu ya dhati yake, na kurekebisha makosa yake na aibu zake na kuziba mapungufu yake na dosari katika shakhsiya yake. Na kurejea fikira zake na rai zake na kuzidurusu kimaudhui. Na anatafakari sifa zake za kinafsi ili aone nukta za nguvu na udhaifu humo. Na kutafiti nyendo zake za kijamii kwa ajili ya kujenga uhusiano bora zaidi pamoja na wanaomzunguka. 131


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Na kwa kurejea huku na kuacha makosa unapatikana msamaha wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa mwanadamu katika mwezi wa Ramadhani. Ama mwanadamu akibakia na akiendelea na bumbuwazi katika mazingira yake na hali yake, hakika ataikosesha nafsi yake fursa hii kubwa, na utamalizika mwezi wa Ramadhani bila ya kuacha alama yenye kuathiri katika shakhsiya yake na tabia yake, na kisha atainyima nafsi yake msamaha wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na yatasadikika kwake aliyoyasema Mtume wa Mwenyezi Mungu : "Hakika muovu ni yule aliyenyimwa msamaha wa Mwenyezi Mungu katika mwezi huu mtukufu.” "Hakika asiyenufaika na fursa hii wala hafaidiki na mazingira haya mazuri atakuwa ni muovu.” UPOLE WA IMAMU HASAN  NI NJIA YA UKUNJUFU WA KIJAMII Miongoni mwa sifa zinazoonekana sana za Imamu Hasan  ambazo amejulikana kwazo ni safu ya upole. Ambapo amekuwa ni mashuhuri kuwa ni mpole wa Ahlul-Bayt. Amepokea alMadainiy kutoka kwa Juwairiya bin Asmai, amesema: Alipofariki Hasan, walitoa jeneza lake. Mar‟wan bin al-Hakam akabeba jeneza lake, Husein akamwambia: “Leo unabeba jeneza lake na jana ulikuwa unammezea hasaira?” Mar‟wan akasema: “Ndio, nilikuwa nafanya hayo kwa ambaye upole wake ni sawa na uzani wa milima.”86 Na sifa hii kwa hakika ni manhaji ya muamala wa kijamii. Imamu amefanya kazi ya kuimarisha katika maisha yake na ni juu ya wafuasi wake na wapenzi wake kumwiga katika manhaji hii. Hakika sisi ni wajibu kusoma upole wa Imamu Hasan  kama 86

Ibnu Abi al-Hadid: Abdul-Hamid katika Sharh ya Nahjul-Balaghah, Juz. 16 uk: 13 Darul-Jiyl – Beirut chapa ya kwanza 1978.

132


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

manhaji katika usamehevu wa kijamii na tufanye kazi ya kuiwezesha jamii sifa hii. Na ni lazima sisi tuashirie kwamba Ahlul-Bayt  wote wanasifika kwa upole ila mazingira ambayo aliishi Imamu Hasan  yalipelekea na yamesaidia kudhihirisha sifa hii katika shakhsiya yake kwa namna iliyo wazi zaidi. Imamu alikuwa anakabiliwa na uasi na maudhi ya pande mbili: Upande wa kwanza: Wa nje, na unawakilishwa na Muawiya bin Abi Sufian, na kambi ya Sham, ambapo aliwekeza jitihada na nguvu yake na uwezo wa utawala wake na serikali yake katika kupaka matope sifa nzuri za Imamu Hasan, ili kumtenga na raia. Akafanya kazi ya kusambaza propaganda na uzushi wa uongo na wa chuki dhidi ya Imamu Hasan , na baba yake AmirulMuuminina, na akaweza kutokana na hayo kutengeneza kundi huko Sham linalowachukia Ahlul-Bayt , hadi baadhi walisadiki kwamba Ali bin Abi Twalib alikuwa haswali!! Na Muawiya alikuwa anafanya makusudi sana kumsikilizisha Hasan mbele yake baadhi ya maudhi. Na baadhi ya wafuasi wake na watu wake wa karibu, kama Mar‟wan bin al- Hakam na Amru bin al-A‟si na Mughira bin Shubah wanafanya mfano wa jukumu hili. Upande wa pili: Wa ndani, ambapo uamuzi wa Imamu wa kufanya suluhu pamoja na Muawiya, ambao ulilazimishwa kwake na mazingira, na kwa kuchunga maslahi ya Umma, ulichochea hisia kwa baadhi ya wanaomzunguka Imamu, na wakaiangalia suluhu kwamba ni msimamo wa udhalili na unyonge na kujisalimisha. Wakawa wanamuelekezea lawama zao za ubabe na shutuma zao kali kwa maneno mabaya na yasiyofaa. Huyu hapa Hujur bin Adiy, Swahaba Mtukufu anamsemesha kwa kusema: “Ama wallahi siku hiyo nilitaka ufe natufe pamoja na wewe.” Na Adiy bin Hatim anasema: “Umetutoa katika uadilifu na kutupeleka kwenye dhulma.” Na Bashir al-Hamdaniy na 133


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Suleiman bin Swarid al-Khuza‟iy anaingia kila mmoja wao kwake wakisema: “Amani iwe juu yako ewe mwenye kuwadhalilisha waumini.” Na baadhi ya wafuasi wake walimsemesha kwa kusema: “Ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu umedhalilisha shingo zetu kwa kusalimisha kwako jambo kwa huyu muovu.”87 Na imekuja katika al-Iswabah: “Wafuasi wa Hasan walikuwa wanamwambia: “Ewe fedheha ya kiongozi wa waumni.” Na anasema: “Fedheha ni bora kuliko moto.”88 Na mfano wa maneno haya hakuna shaka kwamba yanamuudhi mwanadamu na kuamsha hasira yake, lakini Imamu Hasan alikabiliana nayo kwa upole na utulivu mkubwa, na akaweza kwa hayo kufyonza athari na matokeo mabaya, ambayo yanaweza kumkasirisha. Kambi ya Imamu Hasan ilikuwa inahitaji mshikamano na ushirikiano. kulikuwa na masharti kwa Muawiya ya kuyatekeleza, lakini yeye atakapoona kambi ya Imamu Hasan imesambaratika na imehitalifiana na nafasi ya Imamu imetetereka ndani ya jamaa zake, hakika hilo litamhamasisha zaidi kupuuza maafikiano hayo naye kimsingi hakuwa ameazimia kuyatekeleza. Maana ya Upole: Ni kudhibiti nafsi na kutulia wakati wa kuchemka ghadhabu, kama anavyosema Raghib.89 Imamu Hasan  aliambiwa upole ni nini? Akasema: “Ni 87

Al-Qarashiy: Baqir Sahri katika Hayatul-Imamu Hasan, Juz. 2, uk: 273 182 Darul-kutubi al-Ilimiya Qum 88 Al-Asqalaaniy: Ibnu Hajar katika al-Iswabah, Juz. 2, uk: 72 chapa ya kwanza 1992 Darul-Jiyl - Beirut 89 Majumuatu minal-Mukhtaswina: Mausuatu Nadhwaartu naim fiy makaarim akhilaq Rasul al-karim uk: 1735, juzuu ya tano chapa ya kwanza 1998 Darul Wasilati Jiddah

134


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

kudhibiti hasira na kuimiliki nafsi,”90 yaani mwanadamu kudhibiti nafsi yake wakati anapokabiliwa na mtu mwingine kwa kitendo kinachoudhi. Hiyo ni kwa sababu utashi wa ghadhabu unataharuki kwake na kumpelekea mchemko ili kukabiliana na maudhi yanayoelekezwa kwake. Lakini mpole ni ambaye anajidhibiti katika kuelekeza utashi huu, na wala hautumii isipokuwa katika wakati wake unaofaa, kwa sababu kutoa fursa kwa utashi huu ulipuke katika utendaji wa mwenye hasira unaweza kumdhuru mwanadamu badala ya kumnufaisha. Ni mara ngapi aliyedhulumiwa alitumia hasira na akageuka kwa sababu ya kitendo hicho kuwa ni dhalimu mwenye kutuhumiwa, akatoa fursa kwa adui yake. Anasema Imamu Ali : “Ghadhabu ni shari ukiiachia inabomoa.”91 Ghadhabu kwa hakika ni matokeo ya uchochezi wa nje anaopokea mwanadamu, na kumfanya alipize kisasi kwa hasira. Na katika kudhibiti utashi huu, na katika kuuelekeza mwelekeo unaofaa, maelekezo ya Kiislamu yanasihi kumkumbuka Mwenyezi Mungu Mtukufu. Katika Hadithi al-Qudusiy: “Ewe mwanadamu nikumbuke unapokasirika.”92 Na amesema : “Ewe Ali usikasirike, na unapokasirika basi kaa na utafakari kudra ya Mola kwa waja, na upole Wake juu yao. Na unapoambiwa Muogope Mwenyezi Mungu, basi puuza ghadhabu yako na rejea kwenye upole wako.”93 Na hakuna kilicho kizuri zaidi kuliko mwanadamu kutibu mchemko wa ghadhabu yake kwa kurejea kwenye ibada, kuswali rakaa mbili kwa ajili ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa ikhilasi na unyenyekevu, hakuna shaka kwamba itamhamisha mwanadamu na kuwasiliana na ulimwengu wa 90

Al-Majilisiy: Muhammad Baqir katika Biharul-Anuwar, Juz. 75, uk: 102 Al-Amaadiy Tamiymiy: Abdul-Wahid katika Ghurarul-Hikami wa durarilkalimi 92 Al-Kulainiy: Muhammad bin Yaaqub katika al-Kaafiy, Juz. 2, uk: 304 93 Ibnu Shubatu al-Haraniy: al-Hasan bin Ali katika Tuhful-Uqul, uk: 18 91

135


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

ukamilifu na wa kiroho, ambapo anapata kutoka kwa Muumba wake neema za huruma Yake na upole wa ukarimu Wake. Kama zinavyonasihi baadhi ya riwaya kutoka katika hali moja kwenda kwenye hali nyingine wakati wa ghadhabu: Kutoka kwa Abu Dhari , hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu  amesema: “Anapokasirika mmoja wenu naye amesimama basi akae, kama itaondoka hasira yake basi, vinginevyo alale.”94 Na lengo la hilo ni kuondoa athari za ghadhabu katika harakati na hakuna madhara humo. Na katika hadithi kutoka kwa Mtume  hakika yeye anasihi kutawadha, amesema : “Hakika ghadhabu inatokana na shetani na shetani ameumbwa kwa moto, na hakika moto unazimwa kwa maji. Anapokasirika mmoja wenu basi na atawadhe.”95 Madhara ya ghadhabu na kukasirika: Baadhi ya watu wanatawaliwa na hali ya ghadhabu na kukasirika haraka kwa sababu za kipuuzi sana, kama ambavyo hutoa fursa kwa wepesi wa ghadhabu yake kuchukua mwelekeo wake wa ubabe, na hali hii ni mbaya na ni yenye kudhuru. Na matokeo yake makubwa ni mambo mawili: Kwanza: Madhara ya kiafya, ambapo ripoti za kitabibu zinaashiria kwamba ghadhabu na kukasirika kunazingatiwa kuwa ni sababu ya maradhi ya kisukari, shinikizo la damu na maradhi ya moyo, na kwa hiyo hakika mambo ya muhimu wanayousia matabibu kwa wagonjwa hawa ni kuidhibiti nafsi na kutokasirika. Pili: Kuongeza hali ya mshikamano wa kijamii, ambapo watu wa 94

As Sajastaniy: Abu Daud Suleiman bin al-Ashi‟ath katika Sunnan Abi Daud, Juz. 2, uk: 664 hadithi namba 4782 95 Rejea iliyotangulia hadithi namba 4784

136


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

jamii wanashughulika na matatizo madogo madogo na ya pembezoni, ambayo yanachochewa na hali ya hasira. Na katika zogo hilo yanatoweka malengo na matarajio makubwa ambayo yalikuwa yanapasa kila mtu kushugulika nayo, na jamii inachelewa kufikia malengo na maslahi makuu kwa sababu ya kushughulika na ikhitilafu za pembezoni. Upole ni manhaji ya kijamii: Wakati mwingine mazungumzo juu ya upole hufanyika kwa kuzingatia kuwa ni sifa nzuri ya pekee, na wakati mwingine upole unatafitiwa kama harakati ya kijamii kwa ujumla, baina ya mtu mmoja mmoja kati ya wanajamii, na baina ya makundi na mikusanyiko. Ambapo ni wazi kwamba kila jamii ina migawanyiko mbalimbali ya kijamii, kisehemu na kimakazi au kiukoo na kikabila, au kifikra na kimadhehebu au ufuasi wa kisiasa na mfano wa hayo. Swali: Namna gani inapasa uwe uhusiano baina ya kila kundi na lingine? Hakika kuenea hali ya hasira na ghadhabu inaathiri katika uhusiano huu wa ufuasi na kila kundi kutengana na kundi lingine. Ama upole ukitawala na ukunjufu ukaenea baina ya mikusanyiko na mirengo, upole wakati huo unageuka na kuwa ni mfumo wa jumla wa kijami na kuleta matunda yake katika kuleta umoja wa jamii na mshikamano wake, na kuelekeza juhudi zake na nguvu zake kwenye malengo makuu na changamoto hatari. Na angalizo ni kwamba ikhitilafu na mizozo baina ya makundi, mara nyingi inatokea kwa sababu ya vitendo vya kibinafsi vya hasira, kwa upande huu au ule, na kuamiliana na upande mwingine kwa mtazamo wa jumla na kuchukua hasira kwa msingi huo. 137


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Namna gani tutaamiliana na hasira za makundi: Kwanza: Kutojumuisha ubaya, na kuadhibu kundi lote kwayo. Pili: Kueneza roho ya ukunjufu na kufumbia macho mabaya, ambayo yanaweza kutokea kwa huyu dhidi ya yule na kinyume chake, ambapo inapasa watu binafsi na vingozi wa makundi wajipambe kwa upole, kwa sababu ubaya huo unaweza kuwa ni matokeo ya ufahamu au mkanganyiko, au kwa sababu upande fulani unataka kutengeneza tatizo baina ya pande mbili. Tatu: Kutokuza hali ya ikhitilafu ya kifikra na kiutamaduni hadi kwenye kiwango cha ikhitilafu na mzozo. Na kueneza utamaduni wa wingi na kukubali rai ya mwingine. Hakika kukuza ikhitilafu kuhusu baadhi ya mambo ya pembezoni, kama vile kuthibiti mwandamo wa mwezi wa Ramadhani au Iddi au kuchagua marjii taqlid au kufuata fikra hii au ile. Na kuzingatia mfano wa mambo haya ya pembezoni ni mpaka wa utenganisho baina ya imani na ukafiri, uadilifu na ufuska, ni jambo la kimakosa linalotokana na ujahili ua tabia mbaya. Mfumo wa Imamu Hasan: Upole ulikuwa ni mfumo wa mwenendo, na mafunzo yenye kujitokeza katika maisha ya Imamu Hasan , na alikuwa anaamiliana nayo mukabala wa maudhi binafsi ya uadui, pamoja na wenye mielekeo yenye kumkhalifu, na inayotofautiana naye, na ushahidi wa aina ya kwanza. Inapokewa kwamba alikuwa  na kondoo, siku moja akakuta amevunjwa mguu wake. Akamuuliza kijana wake: Nani amemfanyia haya? Kijana akasema: Mimi. Imamu akasema: Kwa nini umefanya hivyo? Kijana akasema: Ili nikuudhi na nikutie huzuni. Akatabasamu  na akamwambia: Basi nitakufurahisha. Akamwacha huru, na akam138


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

pa zawadi nzuri.96 Na kwa aina ya pili, wanahistoria wananukuu: kwamba alipenya kwa Imam mtu kutoka kwa watu wa Shamu kati ya ambao Muawiya amewajaza chuki na ubaya dhidi ya Ahlul- Bayt, akawa anammiminia Imamu matusi na shutuma, na Imamu yuko kimya hakumjibu kwa chochote katika maneno yake, na baada ya kumaliza, Imamu akamgeukia akamsemesha kwa kauli ya upole na akakabiliana naye kwa hali ya ukarimu na bashasha kwa kusema: “Ewe mzee: Nadhani wewe ni mgeni? Kama ungetuomba tungekupa. Na kama ukitutaka muongozo tungekuongoza. Na kama utatulaumu tutakulaumu. Na kama una njaa tutakulisha. Na kama unahitajia basi tutakutosheleza. Na ikiwa umefukuzwa tutakupa makazi.” Na hakuacha  kumfanyia upole mtu wa Shamu kwa haya na mfano wake ili aondoe roho ya uadui na shari kutoka katika nafsi yake, hadi akashangaa na hakuweza kujibu maneno na akabakia ametahayari kwa aibu namna gani ataomba msamaha kwa Imamu, na namna gani atafuta dhambi kwake! Akatikisa kichwa kwa kusema: “Mwenyezi Mungu anajua ni mahala gani anaweka ujumbe wake.”97 Hakika kati ya yanayosaidia katika kuchukua msimamo wa upole ni kufahamu upande mwingine na kujua mazingira ya kinafsi na kifikra ambayo yanamzunguka. Ukijua kwamba yeye ni mpotoshaji au mchochezi, na kwamba yeye pia ni muhanga wa adui mmoja, utakuwa ni mwenye kuweza kudhibiti msimamo, na kuubadilisha kwa maslahi yake na sio kwa maslahi ya adui yake. Na kwa hiyo mwenye akili ndio ambaye anamiliki upole, anasema Imamu Ali : Kwa utimilifu wa akili unapatikana upole.”98 96

Al-Qarashiy: Baaqir katika Hayatu al-Imamu al-Hasan, Juz. 1, uk: 214 Rejea iliyotangulia uk: 314 - 315 98 Al-Amadiy Tamiymiy: Abdul-Wahid katika Ghurari-Hikami wa DurarilKalimi 97

139


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Na anasema: “Shikamana na upole hakika ni tunda la elimu.”99 Na anasema Mtukufu Mtume : “Naapa kwa ambaye nafsi yangu iko mikononi Mwake, hakijajumuishwa kitu kwenye kitu kilicho bora kuliko upole kujumuishwa na elimu.”100 Mwanachuoni ndio ambaye anapaswa kujipamba na upole, kwa sababu anafahamu mabaya ya majahili na sababu za makosa yao. Na wakati mwingine inatokea wanakuja katika jamii watu kutoka katika jamii zingine wanabeba maalumati na fikra zenye kupotosha kuhusu jamii, fikra zake na itikadi zake. Ikiwa mtu anayekabiliana nao ni mwelewa, anajua kwamba wao ni wapuuzi na ni wenye kupotosha. Hakika anajua kwanza mgongano ambao utaletwa na maneno yao, kisha anaanza kubadilisha hali hiyo mbaya na kuwapa wageni kwa tabia yake na mwenendo wake mfano hai dhidi ya kosa la mawazo yake ya awali. Ama ikiwa anayekabiliana naye ni shakhsiya yenye hasira, basi yatamuudhi maneno hayo na kumjibu kwa maneno makali zaidi na kwa tuhuma na kwa sifa za kinyume. Na njia hii aghlabu inapelekea kuimarisha hali ya makosa katika jamii. Na katika yanayoleta mshangao na majivuno wakati mwingine, ni kuzingatia hawa watu vitendo vyao hivyo vya hasira ni ushujaa na mafanikio yanayostahiki kutajwa na kupongezwa. Utaona baadhi yao wanakuhadithia juu yake kana kwamba amenusurika dhidi ya adui, naye anajua kwamba kwa hilo amethibitisha kushindwa kwake. Katika hadithi kutoka kwa Mtume : “Mshindi sio yule mwenye kwenda mbio zaidi, bali mshindi ni ambaye anamiliki nafsi yake wakati wa ghadhabu.”101 99

Rejea iliyotangulia Al-Majilisiy: Muhammad Baaqir katika Biharul-Nauwar juzuu 2 uk: 46 101 Raishahariy: Muhammadiy katika Mizanul-Hikima, Juz. 7, uk: 234 100

140


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Katika kumbukumbu ya kumkumbuka Imamu Hasan  ni haja ilioje sisi kusoma sira yake nzuri na kushikamana na njia yake ya kiujumbe na kuchukua mfumo wake katika ukunjufu wa kijamii, ili mazingira yetu yatawaliwe na upendo, uelewano na tuelekee kukabiliana na maadui na hatari kwa kushikamana kama jengo madhubuti. LAILATUL – QADIR: MAAMUZI YA MAGEUZI NA MABADILIKO Mwenyezi Mungu anasifia usiku wa Lailatul-Qadir kwamba ni bora kuliko miezi elfu moja, na kwamba ndani ya Lailatul-Qadir huhukumiwa kila jambo jema, ambapo yanapangwa matukio, makadirio na mambo ya hatima ambayo yanafungamana na mwanadamu na maisha katika usiku huu kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kutoka kwa Ibnu Abbasi: "Hakika Mwenyezi Mungu anakadiria yatakayokuwa katika mwaka huo miongoni mwa mvua, riziki, kuhuisha na kufisha, kuanzia usiku huo hadi mwaka ujao."102 Na kutoka kwa Imam Ali bin Musa Ridhaa : "Lailatul-Qadir, Mwenyezi Mungu Mtukufu anakadiria humo yatakayokuwa mwaka hadi mwaka (ujao) miongoni mwa kuhuisha au kufisha au kheri au shari au riziki."103 Hivyo Lailatul-Qadir ni usiku wenye cheo kwa Mwenyezi Mungu kwa kukadiria ambayo yatatokea kwa watu katika mwaka wao unaokuja, na ni usiku wa maamuzi makubwa ya Mwenyezi Mungu, hivyo basi usiku huu uwe ni usiku wa maamuzi muhimu 102

Al-Fakhar Raaziy katika Tafsir al-Kabiir, Juz. 32, Chapa ya kwanza 1418 A.H (Beirut Muasasatu Daril-Islami), Uk. 28 103 Abdu Ali bin Jumu'a al-Arusiy al-Jariry katika Tafsir Nuru Thaqalain, Juz. 5, Chapa ya kwanza 1422 A.H - Beirut Muasastu Tarikhil-Arabiy, Uk. 630.

141


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

kwa mwanadamu. Ni taufiki tukufu ilioje na yenye thamani kubwa, mwanadamu kupanga ratiba kwa ajili ya nafsi yake, kufanya maamuzi ya hatima yake ya kimsingi, katika usiku huo mtukufu ambao Mwenyezi Mungu Mtukufu ameujalia kuwa ni muhula na wakati wa makadirio yake kwa mwanadamu. Kisha yanakuja mazingira ya kiroho matukufu ambayo yanazunguka usiku huu, ili kuzidisha hadhi ya mwanadamu kufanya maamuzi ya kimaisha yenye msimamo sahihi. Na hakuna shaka kwamba duara la maamuzi ya mwanadamu katika usiku huu mtukufu linapasa lipanuke kiasi cha kujumuisha kila lenye dauru, mchango na athari katika msimamo wake na maslahi yake, na lijumuishe mategemeo ya mwanadamu ya kidunia na ya Akhera. Aiwekee nafsi yake mipango na ratiba ya kivitendo na kitabia na kuifuata katika mwaka wake unaokuja. Kisha amwahidi Mwenyezi Mungu katika usiku huo, bali na katika mikesha yote ya Lailatul-Qadiri kuwa ataendelea kutekeleza ratiba hiyo, na aombe nguvu na msaada kwa Mwenyezi Mungu na ajaalie hukumu Yake na makadirio Yake yaafiki matamanio yake na matarajio yake mema. Falsafa ya Kuomba Maghufira: Hakika moja ya amali muhimu sana katika usiku huu ni kuomba maghufira kwani imepokewa kuwa katika sunna za usiku huu ni mtu aombe maghufira kwa Mwenyezi Mungu mara sabini. Na kutoka kwa Amirul-Muuminina Ali  kwamba amesema: "Ni juu yenu katika mwezi wa Ramadhani kuzidisha kuomba maghufira na dua. Ama dua inazuia balaa kwenu, ama kuomba maghufira kunafuta dhambi zenu."104 Na Nabii Mtukufu  anamlaumu mwenye kuinyima nafsi yake kupata msamaha wa 104

Wasailu Shi‟ah, Juz. 10, uk. 304.

142


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Mwenyezi Mungu katika mwezi huu mtukufu kwa kauli yake : "Muovu ni yule mwenye kunyimwa msamaha wa Mwenyezi Mungu katika mwezi huu mtukufu." Na anasema: "Mwenye kuudiriki mwezi wa Ramadhani na asisamehewe basi Mwenyezi Mungu amuweke mbali." Na pia amesema : "Ambaye hajasamehewa katika mwezi wa Ramadhani basi ni katika mwezi upi atasamehewa?" Na Ramadhani sio tu ni madrasa ya kiroho bali pia ni semina ya malezi. Humo anahitimu mwanadamu kwa kujipamba na mambo mema na mafanikio ili ayatumie katika mwaka wake uliobakia. Hapa ndipo maelekezo ya Kiislamu yanaonesha dharura ya kuomba maghufira kwa wingi, na yanatia mkazo juu ya umuhimu huo katika maisha yote ya mwanadamu. Anasema Mtume : "Zidisheni kuomba maghufira, hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu hajakufundisheni kuomba maghufira isipokuwa naye anataka kuwasameheni."105 Na amesema Imam as-Sadiq : "Mtume wa Mwenyezi Mungu  alikuwa anatubia kwa Mwenyezi Mungu katika kila siku mara sabini bila ya kufanya dhambi."106 Hakika kuomba maghufira ya kweli sio kusema tu Astaghafirullahi na kutikisa ulimi kwa matamko haya bali matamko haya yanapaswa yawe ni alama dhahiri ya maamuzi ya msingi na ya kina katika nafsi ya mwenye kuomba maghufira. Hakika uhalisia wa kuomba maghufira kwa hakika unatakiwa upitie hatua mbili muhimu za kimsingi: Kwanza: Kugundua kosa, na kukiri uwepo wake, na kwamba ni kosa haijuzu kuendelea nalo. 105 106

Mizanul-Hikma, Juz. 7, uk. 247. Wasailu Shi‟ah, Juz. 16, uk. 85, Hadithi 21047.

143


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Pili: Kuazimia juu ya kuling'oa na kuepukana nalo. Unapojua kosa na kulianisha, kisha ukaazimia kuliepuka na kuling'oa, wakati huo ndio utangaze maamuzi yako hayo ya moyoni, kwa ulimi wako na kusema: "Astaghafirullahi Rabbiy waatubu ilaihi." Hakika kuomba maghufira kwa maana hii kunageuka kutoka kwenye dhikiri tu, na kuhama kiaina na kuelekea katika hali bora na sahihi, na inakuwa ni dawa ya maradhi ya mwanadamu na ugonjwa wake; anasema : "Je, niwaonyesheni ugonjwa wenu na dawa yenu? Fahamuni hakika ugonjwa wenu ni madhambi na dawa yenu ni kuomba maghufira."107 Na kama tukimuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu : "Ni aina gani hii ya kuomba maghufira ambayo unaielezea kwetu ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Atasema kama ilivyo katika hadithi iliyopokelewa kutoka kwake : "Aina bora ya kuomba maghufira kwa Mwenyezi Mungu ni kung‟oa (dhambi) na kujuta."108 Ama ikiwa kuomba maghufira ni kutikisa ulimi tu, wala hakufichui azma yoyote ya kung'oa dhambi, hakika – hali ikiwa ndio hii - inageuka kuwa dhambi anayoadhibiwa kwayo mwanadamu; na ni kauli nzuri ilioje ya Imam Ali  katika kuashiria ukweli huu aliposema: “Kuomba maghufira pamoja na kung'ang'ania madhambi ni kuyaongeza upya."109 Hiyo ni kwa sababu kuomba maghufira kwa namna hii ni sawa na ahadi ya kauli isiyo na shaka pamoja na kuazimia kwa ndani kutoitimiza. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anajua yaliyomo katika nafsi yako. Na anasema Imam Ali Ridhaa  katika neno zuri: "Mwenye 107

Mizanul-Hikma, Juz. 7, uk. 247. Rejea iliyotangulia Juz. 7, uk. 255. 109 Rejea iliyotangulia 108

144


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

kutaka maghufira kwa ulimi wake na wala hakujuta kwa moyo wake basi ameichezea shere nafsi yake."110 Na anasema  katika hadithi nyingine: "Mwenye kuomba maghufira katika dhambi anayoendelea kuifanya ni sawa na yule anayemchezea shere Mola Wake."111 Maamuzi ya Mageuzi na Mabadiliko: Hakika kila mwanadamu anakabiliwa na makosa na wala hanusuriki na shimo hilo isipokuwa aliyehifadhiwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu:

ّ ّ ٌ ّ َ َ َ ‫َوما ُأ َب ّش ُا َ فس ىِ إ ىن ال ى‬ ‫ىء ِإال ما َس ِخ َ َسّبش ِإ ىن َسّبش‬ ِ ‫فغ ِلم َاسة ِبالع‬ ِ ِ ٌ ‫َغ‬ ٌِ ‫فىس َسخي‬ "Nami sijitakasi nafsi yangu; hakika nafsi ndiyo iamrishayo mno uovu, isipokuwa ile ambayo Mola Wangu ameirehemu. Hakika Mola Wangu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu." (Surat Al-Yusuf; 12:53). Na taufiki ni mwanadamu kuzinduka kwa ajili ya nafsi yake kwamba anapita katika kosa fulani, na kwamba bado hajapata taufiki ya kufikia kwenye ukamilifu kati ya ukamilifu mtukufu. Na huu ndio mwanzo wa taufiki ya Mwenyezi Mungu ambapo ndio nukta ya mageuzi kuelekea kwenye uongofu, anasema : "Hakika kila binadamu ni mwenye kukosea na wakosaji bora ni wale wenye kutubia."112 Na hapa mwanadamu anahitaji kuwa muwazi sana pamoja na nafsi yake kwa ajili ya kusahihisha kosa, na ajiulize namna gani 110

Rejea iliyotangulia Rejea iliyotangulia 112 Mizanul-Hikma, Juz. 1, uk. 541. 111

145


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

nitaweza kung'oa dhambi zangu na namna gani ninaweza kubadilisha makosa yangu na mapungufu yangu? Na unazidi umuhimu wa kujigundua na ukubwa wa umuhimu wote kila kosa linapogeuka na kuwa ni mazoea, hiyo ni kwa sababu mazoea ni tabia nyingine, na mazoea kwa kila mwanadamu ni mtawala, na kwa hiyo mazoea yanageuka kuwa ni mgomvi mwenye kushinda kwa mwanadamu. Mazoea ni yenye kutenza nguvu kama ilivyo katika maelezo ya AmirulMuuminina Ali bin Abi Twalib .113 Na kuomba maghufira ni kuazimia kufanya mabadiliko kwa kuachana na tabia ya kimakosa hata kama itageuka na kuwa mazoea aliyoyazoea mwanadamu kwa muda mrefu. Na huwenda kuna ugumu katika jambo, lakini aliyompa Mwenyezi Mungu mwanadamu miongoni mwa matakwa, azma, akili na uwezo wa kuchagua, yote hayo yanampa mwanadamu ushindi dhidi ya mapungufu yake na makosa yake. Ni sahihi kwamba taufiki ya Mwenyezi Mungu ni lazima ipatikane ili mwanadamu aweze kubadilisha, lakini taufiki inafuata matakwa ya mwanadamu na hiari yake. Wale wanaochagua wema kwa matakwa yao kwanza, Mwenyezi Mungu anawapa taufiki ya mafanikio.

ٰ َ ‫َ ى‬ ُ َ​َ​َ َ ‫َ​َ َىُ ُ َُ َ ى ى‬ َ ِ‫دع حن‬ ِ ‫زين جك َُذوا في ا لن ِذين ظبل اِ و ِإن‬ ‫وال‬ ِ ‫اللكه وؼ او‬ "Na wale wanaofanya juhudi kwa ajili Yetu, hakika tutawaongoza kwenye njia Zetu. Na hakika Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wema." (Surat Al-Ankabut; 29:69). 113

Rejea iliyotangulia Juz. 7, uk. 122.

146


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

َ َ ‫َ ى‬ َ ‫اهخ َذوا‬ …‫صاد ُه ُه ًذي‬ ‫والزين‬ "Na ambao wameongoka anawazidishia uongofu." (Surat Muhammad; 47:17). Ama ambao hawajachagua uongofu hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi:

ٰ ‫َغ‬ ‫هى‬ َ ‫ػذ‬ ِ

َ ‫هى غل َو َ َخ‬ ٰ َ ُ ‫َ َ َ َ َ َ ى َ َ َٰ ُ َ ٰ ُ َ​َ َى ُ ى‬ ٍ ِ ‫أفشءيذ م ِن اجخز ِإلكُه هىًه وأضله اللكه غ‬ َ ً ٰ َ ‫هى َب‬ ٰ ‫َظم ِػ ِه َو َكلب ِه َو َج َػ َل َغ‬ ‫ذيه ِمن‬ ِ ِ ‫ص ِش ِه ِغشك َىة ف َمن َي‬ ِ َ ‫ى َ​َ َ​َى‬ ِ ‫الل ِ ِكه أفًل جزه‬ ‫شون‬

"Je, umemwona aliyefanya hawaa yake kuwa ndio mungu wake? Na Mwenyezi Mungu akampoteza akiwa na ilimu, na akapiga muhuri juu ya masikio yake, na moyo wake, na akaweka kizibo machoni mwake. Basi nani atamwongoza baada ya Mwenyezi Mungu? Hamkumbuki?" (Surat al-Jathiya; 45:23) Hakika uongofu wa Mwenyezi Mungu kwa mwanadamu unafuata uchanguzi wa mwanadamu, hivyo haisihi kwa mwanadamu kutoa hoja ya kudhibitiwa na ada zake kwa sababu anaweza kutumia silaha ya matakwa dhidi ya ada yake. Waislamu wa mwanzo walitumia matakwa yao na wakajinasua na shiriki na wakafuata Uislamu, pamoja na kwamba ada zao za shirki zilikuwa zimewadhibiti na zikawa sehemu isiyotengana na maisha yao. Na hawa ambao wanaingia katika Uislamu sasa hivi namna gani wanajinasua na ada zao zinazofanana? Jarida la Ash-Shariq alAusat limenukuu kabla ya siku kadhaa zilizopita ripoti juu ya fikra za baadhi ya Waislamu ambao walisilimu karibuni, na miongoni mwao alikuwa ni balozi wa zamani wa Ujerumani Dr. 147


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Murad Haufman, humo limetaja: "Kwamba katika ujana wake alikuwa ametopea katika kunywa pombe na alikuwa ni mjuzi wa aina zake mbalimbali, na alikuwa anadhani ni vigumu sana kwake kuacha pombe na kwamba hawezi kulala vizuri bila ya funda la pombe!! Lakini alipokinaika na Uislamu na akashikamana na maamrisho yake, akajipamba na silaha ya matakwa akashinda ada hiyo ya kimakosa iliyojikita katika maisha yake."114 Hakika kuna umuhimu wa kuhudhurisha maana hii kubwa ya kuomba maghufira katika mwezi wa Ramadhani hususan, na katika siku hizi za mwisho za mwezi wa Ramadhan, kwa sababu hivi sasa bado fursa ipo ya kupata baraka za Mwenyezi Mungu na kupata msaada Wake katika kutimiza madhumuni na malengo ya kweli kwa mwanadamu ndani ya mwezi huu mtukufu. Nguvu ya dua: Na dua ambazo anazisoma muumini katika mwezi huu mtukufu sio zenyewe kwa dhati yake – kama baadhi wanavyodhani – ndio sababu tosha ya kupata maghufira, bali ni wasila wa kumkumbusha mwanadamu na ukelele wa kumsukuma, na ni mazingira ya kiroho ya mageuzi na mabadiliko. Ikiwa kosa lolote linahitaji kubadilishwa basi maamuzi yako ya kubadilisha yawe ni sasa hivi. Kwa mfano: Namna gani unaamiliana na swala? Je, unaiswali kwa wakati wake au unaipuuza? Na je, unadumu katika swala ya jamaa au hapana? Na ikiwa unaweza kwenda kuhiji umefanya nini katika maamuzi yako ya kwenda kuhiji? Na vipi kuhusu kutekeleza haki za kisharia kama vile khumsi na zaka? Ikiwa hukuwa unaihesabu nafsi yako katika kutekeleza khumsi, basi 114

Ash-Shariqi al-Ausat la tarehe 16/12/1999.

148


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

chukua maamuzi katika siku hizi ili mali zako ziwe twahara na chakula chako na vinywaji vyako viwe halali, na nyumba yako ambayo unaswali humo na mavazi ya kuswalia yawe ya halali, kwani uhalali ni sharti la kusihi swala na hilo halitimii kama hujatekeleza haki za kisharia. Na katika upande wa kitabia ukoje muamala wako pamoja na familia yako? Je wewe unafanya wajibu wako kwa wazazi wako na mke wako? Ziko wapi sehemu za kasoro na mapungufu? Na katika uhusiano wa kijamii je, una uadui na yeyote? Na kwa nini unaendelea na uadui na watu wengine kati ya watu wa jamii yako? Na hata katika ada binafsi kama vile kuvuta sigara na mazoea yasiyofaa kiafya au kiuchumi, ni wajibu wako ujipambe kwa ushujaa katika kuchukua maamuzi ya mageuzi na mabadiliko kuhusiana nayo. Ugumu wa Maamuzi: Hakika kusoma Qurâ€&#x;ani na kusoma dua zilizopokelewa kutoka kwa Ahlul-Bayti ď … na kujua thamani ya muda mtukufu kama vile usiku wa Laitul-Qadir yote hayo yanashajiisha matakwa ya mwanadamu, na yanaamsha ushujaa wake na yanajenga hali ya kujiamini katika nafsi yake, ili achukue maamuzi magumu ambayo kwayo anabadilisha kosa la ada zake na vitendo vyake. Kama ambavyo mazingira yanayomzunguka mwanadamu ikiwa ni mazuri yana athari kubwa katika kumsaidia katika mabadiliko ya kheri na wema. Na kinyume chake, kama akiwa katika mazingira mabaya na maovu basi maamuzi yake ya mwanzo yawe ni kuyahama na kuepukana nayo. Tunaomba Mwenyezi Mungu awape wote taufiki ya kutumia 149


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

fursa ya siku hizi tukufu kwa kuchukua maamuzi ya mabadiliko na kwenda kwenye hali bora zaidi. Na kama kila mwanadamu miongoni mwetu akichukua hata uamuzi mmoja mwema, na akashikamana nao mwaka mzima basi tungepata kheri nyingi. Hakika baadhi wanaweza kuamua lakini wanadhoofika na wanarejea nyuma wakati wa utekelezaji, na baadhi wanashikamana na maamuzi yao kwa muda kisha wanapuuza maamuzi na yanayeyuka maamuzi yake, na hii inadhihirisha kwamba haheshimu nafsi yake na wala haithamini. Imamu as-Sadiq ď „ anasema: "Mwenye kufanya kitendo kati ya vitendo vya kheri, basi adumu nacho mwaka mzima na wala asikatishwe na kitu kingine."115 UGOMVI WA KIDINI, JE UNA KISINGIZIO? Ni Iddi ya Upendo na Usafi, na si Iddi ya Kugombana: Ugomvi unakwaza maisha mazuri kwa watu, na unahadaa mazingatio ya jamii, na unapotosha mwelekeo wake. Ambapo ugomvi unateketeza sehemu kubwa katika mazingatio ya mwanadamu. Na katika ugomvi na mzozo mwanadamu anatumia nguvu zake nyingi, fikra na mawazo, na anatumia juhudi na muda wake wa thamani kwa ajili ya kupata ushindi, nguvu ambazo ilipaswa kuzielekeza katika kujenga na kukuza na kuendelea kuelekea kwenye kheri. Na kila jamii inapojiepusha na ugomvi na matatizo ya mizozo inaweza kukita juhudi zake kwa ajili ya kupata maslahi mazuri ya kijamii na lengo kubwa na zuri. Mazingira ya Ugomvi: Ugomvi unaweza kuwa ndio sababu ya kuzifanyia haki uadui au dhana ya kutaka kufanya uadui. Ikiwa upande wowote utafanya 115

Mizanul-Hikma, Juz. 7, uk. 17.

150


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

uadui katika haki za wengine, hakika hilo linachochea kwao utashi wa kutetea nafsi kulipiza uadui, na Uislamu unatia mkazo kuheshimu haki za wengine za kimada na za kimaanawi, na unaharamisha sana uadui au dhuluma yoyote. Na ikiwa utatokea ubaya au uadui baina ya wanajamii hakika unashajiisha kusamehe na usamehevu:

‫ى‬

َ​َ

َ

َ َ

َ

ُ ‫… ف َمن َغفا َوأصل َح فأ‬..” “….. ‫جش ُه َغهى الل ِ ِكه‬ "Na mwenye kusamehe na kusuuluhisha basi huyo malipo yake yapo kwa Mwenyezi Mungu." (Surat Ash-Shura; 42:40).

َ

ُ

ُ‫ى‬

ّ

َ َ

َ َ

َ

ٰ

ُ َ ِ ‫”… َوالىكةمحن الغيظ َوالػافحن غن ال‬ "‫حن‬ ِ ‫دع‬ ِ ِ ‫اطِ واللكه ي ِدب او‬ ِ ِ "…..Na wazuiao ghadhabu na wenye kusamehe watu na Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao ihisani." (Surat Aali-Imran; 3:134). Na kutoka kwake : "Sameheaneni mtaondosha chuki baina yenu."116 Na wakati mwingine sababu ya ugomvi inakuwa ni dhana tu, kwamba upande mwingine umefanya uadui au kwamba pengine utafanya uadui katika siku zijazo, jambo ambalo linaingia chini ya anwani ya dhana mbaya kwa wengine, au kuhisi husuda katika nafasi yao, na kuwa na ghera katika dhati kati yao. Anasema Imam Ali : "Dhana mbaya inaharibu mambo na inaleta shari." "Mwenye kushindwa na dhana mbaya hatoacha baina yake na rafiki suluhu." Na inawezekana kuugawa ugomvi na uadui katika aina nyingi: 116

Mizanul-Hikma, Juz. 6, uk. 367.

151


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

-

Ugomvi wa kidini. Ugomvi wa kimaslahi katika kugombania mali au cheo au ladha.

Na nukuu za historia zimekusanya matukio ya umwagaji damu yaliyotokea kwa sababu ya ikhitilafu za kidini na kiitikadi, ingawa wakati mwingine inafichikana chini yake ikhitilafu za kimaslahi za kimaada, na dini itakuwa ni mwelekeo tu au anwani au silaha katika vita. Ugomvi Katika Dini: Je, katika dini kuna yanayopelekea na kutoa kisingizio cha ugomvi? Na kwa maneno mengine je, inajuzu kukhitalifiana kwa sababu za kidini na kiitikadi na kutatua ikhitilafu zao hizo kwa vita na mapigano? Kwa kweli, hakika sisi tunapofuatilia hukumu za kisharia tunakuta kwamba hakuna kisingizio cha ugomvi katika dini kabisa na hiyo ni kwamba: Kwanza: Hakika dini ni jambo la moyoni na wala hakuna uwezekano wa kuwalazimisha watu itikadi fulani maadamu hawajakinaika nayo. Na Mwenyezi Mungu ameshawaumba watu wakiwa huru na wala hakuwalazimisha wamwamini, na wala hakuruhusu hata kwa Manabii Wake kuwalazimisha watu kuamini.

َ

ُ

َ َ َ

ّ

َ ‫"ال إ‬ “….. ‫ين كذ ج َب ىحن الششذ ِم َن الغ ِ ِّى‬ ِ ِ ‫هشاه ِفى الذ‬ ِ "Hakuna kulazimisha katika dini; uongofu ume-kwisha pambanuka na upotovu." (Surat Al-Baqara 2:256)

َ​َ َ َ َّ ُ َ َ ‫َ​َّ ى‬ َ ُ ﴾٧٧﴿ ‫يط ٍِش‬ ِ ‫﴾ لعذ غلي ِ ِبمص‬٧٧﴿ ‫فز ِهش ِإ ما أ ذ مز ِه ٌ ِش‬ 152


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

"Kumbusha hakika wewe ni mkumbushaji tu. Wewe si mwenye kuwatawalia." (Surat AlGhashiya; 88:21–22).

ُ

َ

َ

َ

ُ

ُ

َ ‫" َوكل‬ َ ‫شاء ف ُليؤمن َو َمن‬ َ ‫احخم من َسّبى ِف َمن‬ “….. ‫شاء ف َليىفش‬ ِ ِ ِ ِ "Sema hii ni haki itokayo kwa Mola Wenu, basi atakaye aamini na atakaye akufuru." (Surat AlKahf; 18:29). Pili: Hakika njia pekee inayomruhusu mwanadamu kumkinaisha mwingine kwa yale anayoyaamini na kuona ndio sahihi ni majadiliano na mdahalo, ama uadui na ugomvi hakika sio tu unashindwa kukinaisha upande mwingine, bali unamfanya kuwa adui mkubwa na uwiano unapobadilika basi matokeo pia yanabadilika:

‫َ َ َ َ َ ى‬ ‫َ َ َ ُ َ​َ ى َ ُ َ ى‬ َ َ ‫خع ُن ف ِئرا الزي‬ ‫الع ِّينتِ ادفؼ ِبال ى ِىى أ‬ ‫َوال حعخ ِىي احخع ت وال‬ َ َ ‫ٌ َ َى‬ ٌِ ‫َبي ًَ َو َبي ُه َغ ٰذ َوة هأ ُه َو ِلىِ َخمي‬ "Mema na maovu hayawi sawa. Zuia uovu kwa lililo jema zaidi. Mara yule ambaye baina yako na yake pana uadui atakuwa kama rafiki mkubwa." (Surat Fussilat; 41:34) Na Qur‟ani tukufu inatia mkazo kwamba mjadala na mdahalo pamoja na Ahlulkitabu ima uwe kwa njia iliyo bora au usifanyike kabisa:

َ​َ َ ‫َ َ َ ُ ى ى‬ ‫ٰ ّ ى‬ َ ‫َوال ُججٰك ِذلىا َأ‬ ‫زين ظلمىا‬ ‫الىخك ِب ِإال ِبال ى ِىى أخعن ِإال ال‬ ِ ‫هل‬ ُ ُ ٰ َ ‫َّ ى‬ ُ ٰ ُ َ ‫ءام ا ِبالزي أ ِض ٌَ ِإلي ا َوأ ِض ٌَ ِإليى َو ِإلك ُ​ُ ا َو ِإلك ُ​ُى‬ ‫ِمن ُ ِ َوكىلىا‬ َ ُ ُ َ ُ َ​َ ٌ ٰ ‫ن‬ ِ ‫علمى‬ ِ ‫و ِخذ و دن له م‬ 153


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

"Wala usijadiliane na watu wa Kitabu isipokuwa kwa njia iliyo nzuri kabisa; isipokuwa wale waliodhulumu miongoni mwao. Na semeni: Tumeamini yaliyoteremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwenu. Na Mungu Wetu na Mungu Wenu ni Mmoja na sisi ni wenye kusilimu Kwake." (Surat Al-„Ankabut; 29:46). Na anasema (swt):

ٰ َ َ َ َ ‫ى‬ َ َ َ ّ ُ ‫احخ َع ِ​ِتِ َوجك ِذ ُلُ ِبال ى ِى َى‬ ‫ىغة ِت‬ ‫ادع ِإ ٰلى َظ‬ ِ ‫احخىم ِت واو‬ ِ ‫بيل َسِبً ِب‬ ِ َ َ َ ُ َ َ َ َ ُ َ َ َ ُ َ ‫خع ُ ِ ى ى‬ َ ‫َأ‬ ِ َ ‫بيل ِ ِه َو ُه َى أغل ُ ِباوُخ‬ ‫ذين‬ ِ ‫نِ ِإن َسبً هى أغل ِبمن ض ىل غن ظ‬ "Waite kwenye njia ya Mola Wako kwa hekima na mawaidha mazuri na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora. Hakika Mola Wako ndiye anayemjua zaidi aliyepotea njia yake na Yeye ndiye anayewajua zaidi walioongoka." (Surat An-Nahl; 16:125). Tatu: Ikiwa inajuzu kwako kuwafanyia watu uadui na kugombana nao kwa sababu wameshikamana na kukinai kwao kinyume na kukinai kwako, hakika hilo linamaanisha kwamba wao pia wana haki kuamiliana pamoja nawe kwa njia hiyo hiyo, na ilihali wewe hukubali hilo. Na unapenda watu wangeheshimu itikadi yako na kukinaika kwako, maadamu uko hivyo basi amiliana na watu kwa yale unayopenda waamiliane na wewe. Anasema Imam Ali : "Ifanye nafsi yako ndio kipimo kwa yaliyo baina yako na wengine, mpendelee mwingine unayoyapenda kwa ajili ya nafsi yako na chukia kwake unayoyachukia kwa ajili ya nafsi yako."117 117

Nahjul-Balaghah, barua ya 31, uk. 397.

154


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Na kutokana na ukweli huu, hakika Uislamu haujaruhusu jihadi na vita pamoja na makafiri isipokuwa katika hali ya kujitetea, kama watawafanyia Waislamu uadui au katika hali ya kuwazuia na kuwakwaza kueneza Uislamu na kulingania imani yao. Na katika yasiyokuwa hayo hakika Uislamu unalingania kwenye muamala mwema pamoja na mwingine, anasema (swt):

َ ُ ُ ٰ ُ َ َ ‫َ ُٰ ُ ىُ َ ى‬ ّ ‫لىه فى‬ ‫خشجىه ِمن‬ ِ​ِ ‫الذ ِين َول ُي‬ ‫ال ين ىى اللكه غ ِن الزين ل يلك ِخ‬ ِ َ ُ َُ ُ َ​َ َ ُ ٰ َ َ‫ى ى‬ ُ ِ ‫لع‬ ‫طحن‬ ِ ‫لعطىا ِإلي ِ ِ ِإن اللكه ي ِدب او‬ ِ ‫ِديك ِشه أن جب ّروه وج‬ "Mwenyezi Mungu hawakatazi kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakuwapiga vita, wala hawakuwatoa makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu. " (Surat Al-Mumtahana; 60:8). Katika Duara la Uislamu: Na ikiwa kugombana na watu wa dini zingine inakatazwa, basi suala hilo la kugombana na watu wa madhehebu mengine katika dini moja inafaa lipingwe kabisa, ambapo anwani ya Uislamu inawaenea wote na "Kila Mwislamu kwa Mwislamu mwingine ni haramu mali yake, damu yake na heshima yake."118 Bali kinachotakiwa kwa watu wa madhehebu zote wafunguke na kuwa wawazi kwa madhehebu mengine, na Maimamu wa AhlulBayt wamewafundisha adabu wanafunzi wao juu ya hilo. Kutoka kwa Muawiya bin Wahab amesema: Nilimwambia Imam Ja‟far as-Sadiq : Namna gani inatupasa tufanye kati yetu, na watu wengine miongoni mwa watu kati ya wale ambao hawako katika jambo letu? Akasema: “Mtawatazama Maimamu wenu 118

Muslimu bin al-Hajaj al-Qarashiy Anisaburiy katika Sahihi Muslim, Chapa ya kwanza 1998, Riyaadh (Darul-Mughuniy) Hadithi namba: 2564.

155


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

ambao mnawafuata na mtafanya wanayoyafanya. Wallahi hakika wao wanawatembelea wagonjwa wao na wanasindikiza jeneza zao na wanatoa ushahidi kwao na kwao wanatekeleza amana."119 Na duara finyu sana ndani ya duara la Uislamu ni duara la madhehebu, ambapo inaweza kukawa na makundi na mirengo mingi ndani ya madhehebu moja. Katika madhehebu ya Ja‟fari kwa mfano, kuna tofauti baina ya Akhbariyina na Usuuliyina katika mfumo wa kung‟amua hukumu za kisharia na kuna ikhitilafu baina ya Shaikhiya na wengineo katika baadhi ya rai zinazofungamana na nafasi ya Ahlul-Bayt , kisha kuna mafungamano ya kisiasa na kijamii na kuwepo Marjaa wengi wa kukalidiwa. Lakini ikhitilafu hii na tofauti hii haisihi abadani iwe ni kisingizio cha ugomvi na uadui baina ya watu wa madhehebu moja na dini moja. Hakika jamii inapokuwa inashikamana na adabu za Uislamu na inajua madhara ya ugomvi juu yake, na inapokuwa imepevuka katika muamala wake pamoja na taklifu zake za kisharia, hakika itabadilisha kila mas'ala yenye ikhitilafu ya kielimu juu yake na kuwa ni nukta yenye nguvu inayoongezwa katika hazina yake, na sio kiungo cha kulipua na matatizo. Na mbele yetu kuna mifano ya ikhitilafu katika kuthibiti mwezi, nayo ni mas'ala siku hizi yamekuwa ni mazingatio ya wananchi wote wa nchi za Kiislam, ambapo inawezekana sana baadhi ya dola za Kiislamu kutangaza Iddi katika siku hii na dola nyingine katika siku nyingine. Na hata ndani ya madhehebu moja inawezekana kutofautiana rai katika kuthibiti mwezi au kutothibiti kwake. Je, inasihi mfano wa ikhitilafu hii kuwa ni sababu ya ugomvi au mzozo ndani ya 119

Muhammad bin Yaaqub al-Kulainiy katika al-Kaafiy, Juz. 2, 1405 A.H (Beirut Darul Adhuwaai) uk. 136.

156


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

jamii? Mtazamo wa Kifikihi: Ili kutatua maudhui haya ni lazima tutaje utangulizi. Nayo ni kwamba mbele ya mukalafu kuna kauli dhahiri ya kufunga katika hali ya kutothibiti mwandamo wa mwezi wa Shawwali, na kufungua inapothibiti kuandama kwake. Na maadamu hayajapatikana matumaini ya kuthibiti mwezi mwandamo haijuzu kwake kufungua bali ni juu yake kukamilisha idadi ya siku thelathini. Na ama matumaini ya kuandama mwezi yanapatikana kwa moja ya njia za kisharia zilizotajwa katika vitabu vya kifiqihi, nazo ni mtu mwenyewe kuona mwezi au waadilifu wawili kushuhudia, au kuenea habari (ya kuandama mwezi) kwa tawatur. Na kwa kuwa hukumu inategemea kupatikana kwa matumaini kupitia moja ya njia zilizotajwa, hivyo kama yatapatikana kwa njia yoyote kati ya hizi inathibiti kwa mukalafu hali ya kuwajibika kwa kufuata athari yake. Na kwa kuwa mukalafu wengi aghlabu hawaoni mwezi, kama ambavyo sio rahisi kila mmoja kusikia ushahidi wa mashahidi wawili waadilifu wa kuonekana kwake, na inawezekana zisienee kwa walio wengi, kwa hiyo watu wamezoea kutegemea rai ya maulamaa wanaoshughulikia jambo hili, ambao wao ndio sehemu ya matumaini yao na uaminifu wao, na anapothibitisha mwanachuoni ambaye anatumainiwa, hakika watu wanaomwamini wanafuata kauli yake. Na hapa ni wajibu kutia mkazo juu ya mambo mawili muhimu sana: Kwanza: Kila mukalafu anapofuata athari ya kisharia inayotokana na matumaini yake au kutopata matumaini haijuzu katika 157


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

hali ya kukhitalifiana kumfanyia uadui huyu na yule au kinyume chake, kwa sababu pande zote mbili zimefanya kulingana na taklifu yake ya kisharia. Na kulazimiana na hukumu ya kisharia katika mas'ala, hivyo haijuzu kuwa ni sababu ya ugomvi. Kama mtu atamkaribisha msafiri katika nyumba yake na akaswali kwa kupunguza swala haijuzu kwa mwenye nyumba kumfanyia uadui kwa hilo. Na hata kama jamaa watakhitalifiana kuainisha upande wa kibla na kila mmoja miongoni mwao akaswali kwa kuelekea upande anaoitakidi au anaodhani ndio kibla haijuzu hilo kuwa ni sababu ya ugomvi. Ndio, inawezekana kila mmoja wao kubainisha sababu ya kushikamana kwake na rai hii bila ya ile, pamoja na kuchunga adabu ya mjadala kulingana na ikhitilafu. Pili: Hakika watu kutegemea rai ya maulamaa katika kuthibiti mwezi au kutothibiti kwake ni kwa sababu wao wanaweza kutekeleza vipimo vya kisharia, isipokuwa ni kwamba hilo halisihi kuwa ni sababu ya kugeuza kitendo cha kuthibiti mwezi mwandamo au kupinga kwake kuleta hali ya mgawanyiko. Kila kundi litachukua rai ya mwanachuoni ambaye wanaelemea kwake, pamoja na kufumbia macho mtazamo wa wanachuoni waliobaki. Na hii haiwezi kutimia isipokuwa ikiwa huyu mwanachuoni ndio pekee katika mtazamo wao ambaye rai yake inaweza kuleta matumaini, ama mwinginewe kati ya maulamaa hana thamani katika maneno yao. Hakika haisihi kugeuza mas'ala haya ya kisharia kuwa ni kadhia ya mgawanyiko, yanapopatikana matumaini kwa mukalafu ya mwandamo wa mwezi wa Shawwali kwa uthubitisho wa mwanachuoni yeyote mwaminifu kwake, ni wajibu juu yake kumfuata katika hilo. Na ikiwa hajapata matumaini ya kuthibiti kwake basi hatofuata na hata kama aliyemthibitishia ni Marjaa anayekalidiwa, hakuna mafungamano baina ya Marjaa anayekalidiwa na mukalafu katika kadhia hii ya kimaudhui. Mukalafu anaweza kupata matumaini kwa moja ya njia za kisharia na kufungua wakati ambapo Marjaa wake amefunga, na anaweza kuwa 158


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

kinyume cha hivyo. Na hata katika kujengea juu ya nguvu ya utawala wa kisharia kwa mwandamo wa mwezi, hakika hiyo inashurutishwa kwamba asijue mukalafu kosa la mtawala wa kisharia wala kosa la tegemeo lake katika hukumu yake ya mwandamo wa mwezi.120 Iddi ya Upendo na Usafi: Hakika inatakikana sote tufanye juhudi ili Iddi iwe ni mnasaba wa kusambaza hali ya upendo na usafi, na kuzatiti upendo na udugu baina ya waumini na Waislamu. Hivyo ni muhimu kujongea katika mambo yafuatayo: 1. Kuzingatia na kufuatilia mwandamo wa mwezi kwani ni Sunna kufanya hivyo, na inapasa kudumu katika hilo kwani kila inapozidi idadi ya wanaotazama mwezi basi fursa ya kuona mwezi mwandamo inakuwa kubwa zaidi katika usiku wa kuandama mwezi. 2. Mwenye kuona mwezi mwandamo kutoa ushahidi wake mbele ya wanachuoni wanaohusika katika nchi yake wala wasizembee na kwenda kwa baadhi yao bila ya kuwashirikisha wengine, ili wanachuoni wote wanaohusika wawe katika mazingira yanayokaribiana yanayosaidia katika msimamo mmoja. 3. Tuwasukume na tuwashajiishe kukutana maulamaa wanaoshughulika na kuthibitisha mwezi mwandamo pamoja na baadhi yao na washauriane baina yao ili kuchukua msimamo mmoja utakaowapa raha watu kutokana na taabu ya ikhitilafu. 4. Kila upande uheshimu rai ya upande mwingine wakati wa kuhitalifiana katika kuthibiti mwezi. Atakayefungua au kufunga hiyo ni taklifu yake ya kisharia baina yake na Mola Wake, na wala haisihi kutuhumu nia, wala kuwa na dhana mbaya, wala kufanya uadui juu ya haki za wengine na kupaka 120

Imamu Ruhullah al-Musawiy al-Khumainiy katika Taharir al-Wasilah, Juz. 1, 1424 A.H (Beirut Daru Taarifu Lilimatubuati), Uk. 265.

159


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

matope shakhsiya zao au uchochezi dhidi yao. 5. Kueneza utamaduni wa kusameheana, na mafunzo ya Uislamu katika maingiliano mazuri na kuamiliana pamoja na watu hata kama wametofautina katika dini zao na madhehebu yao na rai zao na mielekeo yao. Kuna hadithi nyingi zilizopokewa kutoka kwa Maimamu watoharifu  zinazokataza ugomvi katika dini, wala sijui ni kwa nini tunasahau hadithi hizi na wala hatuelezani pamoja na kuzihitajia sana. Imepokewa kutoka kwa Imam Ja‟far as-Sadiq : "Msigombane na watu kwa ajili ya dini yenu, hakika ugomvi unatia ugonjwa katika moyo."121 Na kutoka kwake : "Jihadharini na ugomvi katika dini, hakika unashughulisha moyo na kuzuia utajo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na unarithisha unafiki na unaleta chuki."122 Na kutoka kwa Ali bin al-Yaqitwin amesema: Amesema Abu Hasan Imam Musa bin Ja‟far : "Waamuru wafuasi wako wazuie ndimi zao na waache ugomvi katika dini na wajitahidi katika kumwabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu."123 Na katika riwaya hizi kuna ishara ya madhara ya ugomvi katika dini nayo ni: a. Unamuudhi mwanadamu kinafsi (unaleta maradhi katika moyo) b. Unasababisha chuki na uadui katika jamii (unaleta chuki). c. Unamzuia mwanadamu na mazingatio halisi (unashughulisha moyo na kuzuia utajo wa Mwenyzi Mungu). USWALIHINA NA KUTAFAKARI 121

Biharul-An‟war, Juz. 2, uk. 133. Rejea iliyotangulia, Uk. 128. 123 As Suduq Muhammad bin Ali bin Babawayhi al-Qummiy, katika Tauhid (Beirut Darul-Maarifah) uk. 460. 122

160


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Zinazunguka katika mazingira ya baadhi ya waswalihina, fikra zinazokhalifu akili na mantiki, nazo zinafanana na uongo na ukhorafi na baadhi miongoni mwao wanatazama maisha ya vitu na matukio mtazamo wa kipuuzi na usioendelea, kama ambavyo inatokea kwa baadhi ya pande za kidini vitendo na misimamo mibaya na miovu. Na kinachosikitisha sana katika jambo ni kwamba kuna fikra, mitazamo na misimamo inanasibishwa na dini, jambo ambalo limeleta mushkeli na maswali juu upeo wa kuafikiana na uhusiano baina ya dini na akili, je, inamaanisha uswalihina ni kuondoa akili? Na je, dini ni badala ya akili? Hakika baadhi ya hao waswalihina unapojadiliana nao kuhusu rai zao, fikra zao na vitendo vyao, katika mwangaza wa akili na mantiki, wanafunga mlango wa majadiliano na mjadala, kwa msingi kwamba mambo ya kidini ni ya ibada na kwamba dini ya Mwenyezi Mungu haifahamiki kwa akili. Sasa ni upi uhakika wa uhusiano baina ya dini na akili? Je, uswalihina unamaanisha kudumaza dauru ya akili na kuifuta? Kulazimiana baina ya uswalihina na akili: Akili ni neema kubwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amemtofautisha kwayo mwanadamu na viumbe vingine, na dini ni ujumbe na uongofu wa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu amemneemesha kwayo mwanadamu. Chanzo cha akili na dini ni kimoja naye ni Mwenyezi Mungu Mtukufu, navyo vinalazimiana na hakitengani kimoja wapo na kingine. Na tunapoona mparaganyiko na utengano baina ya dini na akili, ni wajibu tudadisi, ili tufichue nukta za kutofahamika na mkanganyiko katika ambayo tumeyazingatia kuwa ni dini au akili, kwani dini sahihi haigongani na akili salama. Na uhusiano baina ya dini na akili ni uhusiano wa kukamilishana na kusaidiana kwa 161


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

kubadilishana, ambapo akili inaongoza dini na dini inaielekeza akili. Kwa sababu imekaririwa katika Qur‟ani tukufu kauli yake (swt): “Ni ishara kwa watu wenye akili.” (Suratul-Baqarah; 2:164). Na wahyi wa Mwenyezi Mungu hakika unawahutubia wenye akili, na kuamsha akili zao: “Hakika tumeifanya Qur‟ani kwa lugha ya Kiarabu ili mfahamu” (Suratu Zukhuruf; 43:2) na anasema (swt):

ٰ َ َ​َ َ ‫ءاجي ا‬ َ ‫ظش‬ ٰ ‫ذي َو َأ َوسز ا َبنى إ‬ ٰ ُ‫ال‬ ُ ‫مىس ى‬ ‫﴾ ُه ًذي‬٥٣﴿ ‫ب‬ ِ َ ‫الىخك‬ ‫َوللذ‬ ِ ‫ءيل‬ ِ ٰ َ ُ ٰ ﴾٥٤﴿ ‫ب‬ ِ ِ ‫هشي ِ​ِلو ِلى لبك‬ ‫َو ِر‬ “Na kwa hakika tulimpa Musa uongofu, na tukawarithisha wana wa Israil Kitabu. Ni uongofu na ukumbusho kwa wenye akili.” (Surat Al-Mu‟min (Al-Ghafir) 40:53-54). Na kama tungesoma nususi za Sunnah za Nabii na Hadithi za Maimamu wa Ahlul-Bayt tungezikuta zinatia mkazo mshikamano mkubwa baina ya dini na akili. Kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu : “Dini ya mtu ni akili yake na asiye na akili hakuna dini kwake.”124 Na kutoka kwake : “Hakika inafikiwa kheri yote kwa akili na hakuna dini kwa ambaye hana akili.”125 Kutoka kwa Imamu Ali : “Akili ni mtume wa haki.” 126 “Asili ya mwanadamu ni akili yake na akili yake ndio dini 124

Al-Hindiy: Ali al-Mutaqiy katika Kanzul-Ummal, Juz. 3, uk. 379, namba 7033 chapa ya tano 1985 Muasastu Risalat – Beirut. 125 Al-Majilisiy: Muhammad Baaqir katika Biharul-Anuwar, Juz. 74, uk. 143 chapa ya tatu 1983 Daru Ihiyai Turathi al-Arabiy – Beirut 126 Al-Amadiy Tamimiy: Abdul-Wahdi katika Ghuraril-Hikami.

162


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

yake.”127 Kutoka kwa Imamu Musa al-Kadhim : “Hakika Mwenyezi Mungu ana hoja mbili kwa watu: Hoja ya dhahiri na hoja ya ndani. Ama hoja ya dhahiri ni Mitume, Manabii na Maimamu , na ama hoja ya ndani ni akili.”128 Uswalihina na kutafakari: Ikiwa uhusiano baina ya dini na akili ni uhusiano wa kulazimiana, hakuna kutengana humo wala kuachana, namna gani tunafasiri hali hizo mbaya katika maisha ya wenye dini? Kwa hakika baadhi ya wenye dini wanafahamu dini vibaya, na wanadumaza akili zao kwa ujahili wao na kwa ubaya wa fahamu zao. Kisha wanazifunga nafsi zao na harakati zao dhidi ya dini, na kwa hiyo wanadhuru nafsi zao, na wanaichafua dini. Na haya ndio ambayo hadithi na nususi za kidini zimehadharisha, ambazo zinatia mkazo umuhimu wa kutafakari katika maisha ya mwanadamu mswalihina. Vinginevyo mwenye kunasibiana na dini, anabeba nembo yake na anwani yake na kufanya ibada zake na amali zake, lakini yeye ikawa hatumii akili yake, wala hafaidiki na fikira yake hakika uswalihina wake utakuwa ni wenye kukatika na una upungufu, bali umepakwa matope na una giza. Kutoka kwa Anas bin Malik  amesema: Kaumu ilimsifu mtu mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu : Akasema : Vipi akili yake? Wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu tunakueleza kuhusu juhudi yake katika ibada na mambo ya kheri, na unatuuliza kuhsu akili yake? Akasema : Hakika mpumbavu anafanya kwa upumbavu wake makubwa zaidi kuliko uovu wa muovu. Hakika watanyanyuka waja kesho katika daraja na 127 128

Al-Majilisiy: Muhammadi Baaqir katika Biharul-Anuwar, Juz. 1, uk: 82 Rejea iliyotangulia uk. 137.

163


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

wanapata ukaribu kwa Mola Wao kwa kadiri ya akili zao.”129 Na hadithi tukufu inaeleza wazi vitendo vya baadhi ya waswalihina wapumbavu, ambao umekosekana kwao uelewa, na ikatoweka akili, vikawa vitendo vyao ni vibaya kuliko uovu wa muovu, kwa sababu unapaka matope sura ya dini na sifa ya waswalihina. Na yanayotokea hivi sasa Aljeria na Afghanistani na Pakstani kati ya mauji na uovu na mapigano yanayofanywa kwa jina la dini ni ushahidi juu ya hilo. Na katika hadithi nyingine anatuhadharisha Mtume wa Mwenyezi Mungu  kuhadaika na muonekano wa uswalihina kwa mtu yeyote ikiwa hatujawa na uhakika na fikira yake kwa sababu fikra ndio kipimo cha uswalihina wake, na ni kipimo cha unyoofu, anasema : “Inapowafikia kuhusu mtu uzuri wa hali yake tazameni katika uzuri wa akili yake, hakika mtu analipwa kutokana na akili yake.”130 Na kwa utekelezaji wa maelekezo haya ya Nabii  amesema Salman : Nilimwambia Abu Abdillahi Ja‟far Swadiq : Kwamba fulani katika ibada yake, dini yake na fadhila yake ni kadha na kadha. Akasema: Namna gani akili yake? Nikasema: Sijui. Akasema: Hakika thawabu ni kwa kadiri ya akili.131 Hakika tatizo la baadhi ya waswalihina hakika wao wanaiweka dini katika mpaka wa fahamu zao dhaifu, na uelewa wao duni, kisha wanazingatia yasiyokuwa hayo ni ukafiri na ufasiki, kama inavyonukuliwa kutoka kwa mmoja wa masheikh ambaye alikuwa anasherehesha kwa wanafunzi wake ibara ya fikihi, anasema: Akitumbukia panya katika samli na akatoka hai basi samli inabakia twahara na halali. Na maana ya ibara ni kwamba 129

Rejea iliyotangulia uk. 84 Rejea iliyotangulia, Juz. 1, uk. 106 131 Rejea iliyotangulia uk. 84 130

164


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

panya hajafia katika samli, bali kharajati hayan – yaani ametoka akiwa hai – lakini Sheikh akafasiri: al-Faaratu tukhriju hayatan, yaani panya atatoa nyoka. Mmoja wa wanafunzi wake akambishia: Namna gani panya atatumbukia katika samli kisha anatoka akiwa ni nyoka? Na badala ya Sheikh kuzinduka katika kosa lake, akang‟ang‟ania katika maneno yake na akamfukuza mwanafunzi katika somo, kwa kumtuhumu kwa ukafiri na kuwa na shaka katika uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Je, Mwenyezi Mungu si anaweza kumbadilisha panya na kuwa nyoka? Kutafakari na kufuata uongozi wa kidini: Baadhi ya uongozi wa kidini unafanya jukumu lake la kimsingi katika kuondoa hali ya kufikiri katika medani ya Kiislamu, na kuimarisha hali ya kijuu juu na kutokuwa na maendeleo katika kiwango cha dini. Na hiyo ni ama kwa ufinyu wa uelewa wake na fikra yake au kwa sababu ananufaika na hali ya kutoendelea, na kuiacha, na kuistawisha kwa msukumo wa maslahi. Na hapa uswalihina unahitaji kutafakari katika mas‟ala ya kufuata uongozi. Uongozi wa kidini na kijamii. Mwislamu hasamehewi katika kusalimisha uongozi wake na hatamu za mambo ya dini yake kwa yeyote maadamu hajajua uadilifu wake, na hata mwanachuoni mwadilifu haisihi kumfuata kwa kufumba macho na upofu, maadamu sio maasumu na anakabiliwa na kupotoka na kukosea. Ni lazima kufikiri na kutafakari katika kuchagua upande wa kidini ambao unaufuata. Ibnu Sakiti al-Kufiy  alimuuliza Imamu Ali bin Musa Ridhaa : Nini hoja ya viumbe leo? Imamu  akajibu: Akili, anamjua kwayo mkweli kwa Mwenyezi Mungu na hivyo kumsadikisha, na muongo kwa Mwenyezi Mungu na kumkadhibisha. Ibnu Sakiiti akasema: Wallahi hili 165


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

ndio jawabu.132 Na mwanachuoni wa kidini anahukumiwa kwa misingi ya kidini, na vidhibiti vya akili. Inapasa kupima rai zetu na misimamo yetu katika mwanga huo, na wala haisihi kumfuata na kumtii katika ambayo yanakhalifu dini, na yanapingana na akili. Imekuja katika Sahih al-Bukhariy kutoka kwa Abi Abdurahaman kutoka kwa Ali bin Abi Twalib  amesema: Nabii  alituma kikosi – kikundi kidogo cha jeshi - akampa uongozi mwanaume katika Answar na akawaamuru wamtii. Akakasirika akasema: Je, amewaamuru Nabii mnitii? Wakasema: Ni kweli. Akasema nikusanyieni kuni. Wakakusanya akasema: washeni moto, wakauwasha. Akasema: Ingieni. Wakaogopa ikawa baadhi yao wanawashika baadhi na wanasema: Tumekimbilia kwa Nabii kutokana na moto. Hawakuacha kuwa hivyo hadi moto ukazimika, basi hasira yake ikatulia, ikamfikia Nabii  akasema: Kama wangeingia wasingetoka humo hadi Siku ya Kiyama, utii ni katika mema.133 Hakika Qur‟ani tukufu inawalaumu manaswara kwa sababu wao wamewapa viongozi wao hatamu zao za dini kufuata kwa upofu, na wamewafuata wao kufuata kwa jumla, bila ya vidhibiti vyovyote kutoka katika dini au akili, kana kwamba wao kwa hayo wanawafanya ni waungu na wanawaabudu wao kinyume cha Mwenyezi Mungu. Anasema (swt):

‫ى‬ ً ‫خباس ُه َو ُسهبٰك َن ُ َأ‬ َ ‫” ىاج َخزوا َأ‬ “….. ‫سبابا ِمن دو ِن الل ِ ِكه‬ “Wamewafanya makuhani wao na watawa wao kuwa ni miungu badala ya Mwenyezi Mungu...” (Surat At-Tawba; 9:31). 132 133

Rejea iliyotangulia, Juz. 1, uk. 105 Al-Bukhariy: Muhammad bin Ismail, katika Sahih Bukhari, Juz. 5, uk. 322 kitabul-Maghaaziy namba 340 al-Maktabat Thaqafiyati - Beirut

166


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Amesema Udai bin Hatim: Nilimwambia Mtume wa Mwenyezi Mungu : Hakika sisi hatuwaabudu wao, akasema : Je, si wanaharamisha aliyoyahalilisha Mwenyezi Mungu na mnayaharamisha, na wanahalalisha ambayo ameyaharamisha Mwenyezi Mungu na mnayahalalisha? Akasema: Nikasema: Ndio. Akasema: Hiyo ndio kuwaabudu kwao.134 Na kutoka kwa Maimamu wawili, al-Baqir na as-Swadiq  hakika wao wamesema: Wallahi hawajafunga kwa ajili yao wala hawajaswali kwa ajili yao lakini waliwahalalishia haramu na wakawaharamishia halali. Wakawafuata na wakawaabudu bila ya kujua.135 Twalha na Zuberi walipoamua, na wao ni masahaba wawili maarufu kwa Waislamu, wakiwa pamoja na Ummul-Muuminina Aisha, mke wa Mtume wa Mwenyezi Mungu  kupambana na ukhalifa wa kisharia, ambao unawakilishwa na Amirul-Muuminina Ali , wakakanganyikiwa baadhi ya Waislamu. Harithi bin Hutwi akaja kwa Imamu Ali  akisema: Je, unadhani watu wa jamali wako katika upotovu? Imamu akamjibu: Ewe Harithi hakika wewe umeangalia chini yako na wala haujaangalia juu yako ukatahayari. Hakika wewe hukujua haki na hivyo kumjua aliyeileta, na hukujua batili na kujua nani aliyeileta.136 Hakika baadhi ya wenye dini wanashangazwa na shakhsiya ya mwanachuoni fulani, na wanapita mpaka katika kumtukuza na kuichukulia kauli yake ni katika mambo ya kawaida, bila ya uelewa au kutafakari. Na hii ni kinyume cha maelekezo ya kidini. Imepokewa kutoka kwa Ali : Chukua hekima kwa aliyeku134

Twabarisiy: al-Fadhil bin al-Hasan katika Majmaul-Bayaan, Jz. 5, uk. 43, chapa ya kwanza, 1995, Muasasatu al-Ilimiy lilimatubuaati – Beirut. 135 Rejea iliyotangulia 136 Al-Musawiy: Sharifu Ridhaa katika Nahjul-Balaghah - Qiswaar al-Hikami 262

167


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

letea, na tazama aliyosema na wala usiangalie aliyeisema.137 Na katika riwaya nzuri kutoka kwa Imamu Ja‟afar Swadiq : “Chukua haki kutoka kwa watu wa batili wala usichukue batili kwa watu wa haki. Kuwa mchambuzi wa maneno, ni mara ngapi upotovu umepambwa kwa aya za Kitabu cha Mwenyezi Mungu, kama dirihamu ya shaba ilivyopambwa kwa fedha ya udanyanyifu? Kuangalia katika hilo ni sawa sawa, na watazamaji wake ni wajuzi.”138 Ni maelekezo mazuri yalioje yanayoamsha akili kwa ajili ya kutekeleza dauru ya kukosoa na kunyoosha, katika rai na fikra (kuweni wachambuzi wa maneno). Na inahadharisha kwa mwanadamu kuingia kwake upotoshaji na udanganyifu (na mara ngapi upotovu unapambwa kwa aya) na ni juu ya mwanadamu kujipamba na uoni na uelewa, ili awe mjuzi mtambuzi baina ya sahihi na kosa katika mwanga wa misingi ya dini na akili. Rejea ya akili: 1. Katika itikadi za msingi katika dini, akili inakuwa ndio rejea. Na kupitia kuangalia na kufikiri mwanadamu anafikia katika kuamini misingi ya dini. Na wengi wa maulamaa watafiti wanaona ni wajibu wa kulazimiana itikadi na njia ya akili na sio na nukuu na kufuata, bali Allammah al-Hiliy amedai kongamano juu ya hilo: “Maulamaa wamekongamana juu ya wajibu wa kumjua Mwenyezi Mungu na sifa Zake za thubutiya na yanayosihi kwayo, na yanayo kataliwa kwayo, utume, Uimamu 137

138

Al-Amadiy Tamiymy: Abdul-Wahdi katika Ghurarul-Hikami, Juz.1, uk. 355 chapa ya kwanza 1987 Muasasatu al-A‟alamiy - Beirut Al-Majilisiy: Muhammad Baaqir katika Biharul-Anwaar, Juz. 2, uk. 96 namba 39; Al-Answaariy: Sheikh Murtadha katika Faraaid al-Usuul, Juz. 1, uk: 382, chapa ya kwanza 1991 – Muasastu al- A‟alamiy llilimatubuaati – Beirut.

168


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

na miadi kwa dalili na sio kwa kufuata.”139 2. Katika Sharia ya Kiislamu akili inajitegemea katika rejea sehemu ya matawi na hukumu, anasema Sayyid Muhammad Taqiy alHakim: “Hakika akili ni chanzo cha hoja na kwayo inamalizikia, nayo ndio rejea pekee katika misingi ya dini, na katika baadhi ya matawi ambayo haiwezekani sharia tukufu kutoa hukumu yake humo, kama vile amri za kutii. Na vilevile migawanyiko inayofuatia taklifu, mfano elimu na kutokujua kwayo, au kuzingatia kujikurubisha kwayo inapotakiwa kuzingatiwa kwa kujaalia moja ya masharti ya taklifu, kwa ulazima wa dauru au mfuatano humo. Kwa kawaida hakika kutii amri za kutii kwa mfano, ama urejee kwenye akili au mfuatano usiokuwa na mwisho, ambapo ingekuwa ni ya kisharia swali lingeelekezwa juu ya ulazima wa utii wake, ikiwa ni ya kisharia swali linaelekezwa juu ya ulazima wa kutii kwake, hivyo ni lazima ijaaliwe humo kuwa ni ya kiakili, na ambayo yamepokewa katika amri za kisharia kwa kutii, hakika ni muongozo na mkazo wa hukumu ya akili na sio kwamba ni amri za kuasisi.”140 3. Na kwa akili mwanadamu anafahamu amri zingine za kidini, na anazichambua katika nususi zake na rejea zake za kisharia. Nayo haijitegemei humo na sharia, kwa sababu Mweka sharia ni Mwenyezi Mungu Mtukufu na wahyi ndio rejea ya kuweka sharia, lakini kufahamu maneno ya wahyi na kujua maana yake na sehemu za utekelezaji wake na kuainisha sehemu zake, rejea humo inakuwa ni akili. Na hapa vidhibiti wamevichambua na kuvihakiki maulamaa katika manhaji ya uchambuzi wa hukumu za kisharia, zinaratibu kazi ya ijitihadi ili kupata hukumu ya kisharia. 139

Al-Answaariy: Sheikh Murtadhwa katika Faraid al-Usuul, Juz. 1, uk. 382 chapa ya kwanza 1991 Muasasatu al-A‟alamiy lilimatubauaati – Beirut. 140 Al-Hakim: Muhammad Taqiy katika Usulul-Amati lilifiqihi al-Muqaarana, uk. 299 – 300 chapa ya pili 1979 Daru al-Andalusi - Beirut

169


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Na Ustadh al-Mudarisiy anafupisha dauru ya rejea ya akili, na upeo kukamilika kwake pamoja na wahyi, katika utafiti wake mzuri juu ya sharia ya Kiislamu anasema: “Kazi ya akili ni kujua wahyi, kuufahamu kwake na kujua wabebaji wake na kujua namna ya utekelezaji wake katika uhalisia wa matawi.141 WENYE RAI NA JUKUMU LA MJADALA Ili wananchi wetu wavuke hali ya kukwepana iliyoenea katika uhusiano wa makundi yake na mkusanyiko wake pamoja na baadhi yake kwa baadhi, na kufikia kiwango cha kufunguka, kuwasiliana na kushirikiana, ni lazima kuanze na kazi ya majadiliano mazuri ya wazi, yanayolenga kujuana moja kwa moja kila upande kwa mwingine, badala ya kutegemea maalumati yasio makini, na mazoea na misimamo iliyopita. Na itarajiwe kuvumbua mambo ya ushirikiano, na kutia mkazo katika maslahi makuu, maslahi ya Umma, na kukabiliana na changamoto hatari katika jamii na nchi. Wakati utandawazi unalazimisha uwepo wake katika maisha, na ulimwengu kugeuka na kuwa kijiji kimoja kidogo, athari za mipaka ya kijiografia na kisiasa humo zinakuwa finyu, haisihi kwetu kuhifadhi vizuizi hivi na kuta zenye kuimarisha utengano, ili tutenganishe baina ya watu wa umma huu, chini ya anwani za utaifa au madhehebu au vyama au ukabila. Na angalizo ni kwamba njia za mawasiliano baina ya kila kundi miongoni mwetu na ulimwengu ziwe ni nyingi zaidi pamoja na watu wa mazingira yake na washirika wake katika dini na nchi. Na majadiliano baada ya hapo ni faradhi inayotulazimisha kwayo dini yetu, ambayo inatuamrisha kuthibiti katika hukumu zetu na rai zetu, na misimamo yetu mbele ya wingine. Haisihi kwetu 141

Al-Mudarisy: katika Tashiriul-Islamiy Manahijuhu wa Maqaaswiduhu, Juz. 1, uk. 10 chapa ya kwanza 1991 Daru Raid al-Arabiy – Beirut.

170


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

kutengeneza picha kwa wengine kwa njia ya dhana na mazoea:

ُ َ ُ َ ُ َ َ​َ َ َ َ ‫ٌ ى ى‬ َ َ َ َ ‫ؤاد ول‬ ‫يغ لً ِب ِه ِغل ِ​ِ ِإن العمؼ والبصش والف‬ ‫َوال جلف ما ل‬ ً ٔ َ َ ٰ ُ ِ ‫أولك ِنً وان َغ ُه َمعك‬ ‫ىال‬ “Wala usifuatilie ambalo huna ujuzi nalo. Hakika masikio, macho na moyo, hivyo vyote vitasailiwa.” (Surat Bani Israil; 17:36). Na wala tusichukue maalumati yetu kuhusu baadhi yetu kwa baadhi kutoka katika pande zisizoaminika, na kupanda baina yetu chuki na uadui.

َ ‫يٰك َأي َ ا ىال‬ َ ‫زين‬ ً ‫جاء ُه فاظ ٌم ب َن َبئ َف َخ َب ىي ىا َأن ُجصيبىا َك‬ َ ‫ءام ىا إن‬ ‫ىما‬ ٍ ِ ِٰ ِ ُ َ ٰ َ ُ َ َٰ َ َ ِ ‫هى ما ف َػلخ ك ِذ‬ ‫محن‬ ‫صبدىا غ‬ ِ ‫ِبجُكل ٍت فخ‬ “Enyi ambao mmeamini! Akiwajieni fasiki na habari yoyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kutojua, na mkawa wenye kujuta kwa mliyoyatenda.” (Surat al-Hujurat; 49:6). Mwislamu mwenye kuzingatia ni ambaye anataka kujua rai mbalimbali na anajitahidi kujua rai kwa kutafuta ukweli:

َ ‫َ ى‬ َ ّ َ َ َ َ َ ‫ى‬ ‫اللى ٌَ ف َيد ِبػىن‬ ‫عخ ِمػىن‬ ‫﴾ الزين ي‬٧٧﴿ ‫باد‬ ِ ِ ‫”…ف َب ِشش ِغ‬ ٰ َ ٰ ُ ‫ى‬ ُ ُ َ ‫خع َ ُِهِ ُأولٰكن ًَ ىال‬ َ ‫َأ‬ ٰ ‫زين َه‬ “﴾٧٨﴿ ‫ب‬ ِ ِ ‫ذً ُ​ُ ُ الل ُِكهِ َوأولك ِن ًَ ُه أولىا لبك‬ ِ “…..Basi wabashirie waja Wangu. Ambao husikiliza maneno, wakafuata mazuri yake zaidi. Hao ndio aliowaongoza Mwenyezi Mungu, na hao ndio wenye akili.” (Surat Az-Zumar; 39:17–18) Ni wazi kwamba kutumia tamko (wanasikiliza) katika aya tukufu 171


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

badala ya wanasikia, linaashiria kwenye aina ya umakini na kukusudia. Lakini, nani ataanza kazi ya majadiliano? Na kwa nani linaangukia jukumu la kujitolea na kulifanyia kazi? Inanibainikia kwamba wenye kutafakari na wenye rai kati ya raia ndio kundi ambalo linapasa kubeba jukumu hili, kwa sababu wao ndio watu wenye rai na fikra, inatakiwa wawe wenye ufahamu wa kina zaidi, changamoto ambayo Umma unaishi nayo. Na wanaweza zaidi kuendesha mjadala kimaudhui na kwa ikhilasi. Kama ambavyo nafasi yao inawapa uwezekano wa kuathiri ndani ya makundi ambayo wanahusiana nayo na kuongoza rai kuu. Kama baadhi ya wenye rai watajitolea kutoka kila upande kufunguka kwa watu wa mfano wao katika upande mwingine, na kujadili maudhui ya uhusiano wa ndani baina ya pande na makundi, na namna ya kuyaweka katika hali ya Uislamu na nchi, jamii yetu ingekata masafa makubwa katika njia ya umoja, mshikamano na ushirikiano, na tungeutosheleza umma wetu hasara ya kutengana, mizozo na kupigana vita. Na tunaowakusudia ni wale watu wenye uwezo wa kielimu na kifikra, miongoni mwa wanaotumia nafasi kuelekeza na kuathiri katika jamii, kama vile maulamaa wa dini, wanafikra wenye mafanikio, na viongozi wa kijamii. Hakika kuzembea wenye rai wenye ghera na maslahi ya dini na nchi kuhusu kujitolea kuzuri, na kunyanyua sauti juu kwa kulingania kwenye kufunguka na majadiliano, ndio ambako kunatoa nafasi na kuacha medani kuwa wazi, kwa sauti za wenye kulingania chuki na wenye kuchupa mipaka, kutoka katika pande mbalimbali. Na tunaulizana hapa: Kwa nini inakosekana katika medani – au inapungua – kujitolea wenye rai katika kufunguka kwa baadhi yao kwa baadhi, na kujadiliana kwa ajili ya kuondoa mpasuko, na kuzingatia maslahi makuu, na kuvuka misimamo yao ya kifikra 172


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

na kijamii? Na katika kujibu swali hili tunaweza kusema: Hakika kuna sababu nyingi zinazodhoofisha mwelekeo wa wenye rai, na kupunguza kujitolea kwao katika majadiliano na zinazoonekana zaidi ni hizi zifuatazo: 1. Udhaifu wa kujali mambo ya jamii: Mwenyezi Mungu akimpa mwanadamu taufiki ya kuwa na fungu la elimu na maarifa na uwezo wa uelewa na ujuzi, hakika hiyo peke yake ni daraja. Anakuwa ni mwenye jukumu la kutumia hayo katika kutumikia jamii na maslahi ya jumla, lakini baadhi ya wenye rai wanaishi na mambo yao maalumu, na wanajitahidi kulinda maslahi ya kibinafsi. Na ikiwa majadiliano na kufunguka kwa wengine hakuleti manufaa binafsi, basi haiwi katika duara la mazingatio yao wala haiwi ndani ya ngazi ya vipaumbele vyao. Nilipendekeza kwa mmoja wa maulamaa wa kidini maudhui ya uhusiano wake na mwanachuoni mwingine anayehitalifiana naye katika mtazamo na anafanya kazi katika medani ya kijamii, akanijibu kwa kusema: Sioni nafsi yangu kama ina haja ya uhusiano pamoja naye. Mambo yangu yametulizana na hali yangu imeratibika vizuri! Na haya ni maneno ya wengi wa maulamaa wa kidini na wanafikra katika jamii yetu. Hakika hahisi haja binafsi na wala hatarajii manufaa binafsi katika kufunguka kwa mwingine na majadiliano pamoja naye. Lakini vipi kuhusu maslahi ya jumla? Hakika wewe unaweza kuwa humhitajii mwingine katika kiwango chako binafsi na yeye anaweza kuwa hakuhitajii vilevile, lakini nchi na jamii inahitajia kuafikiana rai na kuunganisha juhudi na kuziba mianya ya fitina na mizozo, na kuimarisha umoja wa nchi na kijamii. 173


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

2. Hisia za kutawala na kutisha: Mwenye rai anapokuwa katika nafasi ya juu katika nguvu au vyeo au uwezo wa kimali na kijamii, hakika anaweza kutawaliwa na hisia za kujikweza na kuwa juu kwa walio mfano wake, miongoni mwa wenye rai ambao hawafikii kwenye kiwango cha uwezo wake na kudra yake, na hivyo anajitenga na kuacha kuwa wazi kwao, na anajiengua na majadiliano pamoja nao, kwa sababu hawaoni kuwa ni hadhi yake, na anaona kwamba ni juu yao kumnyenyekea, na kukiri juu ya haki yake na ubora wake. Na mwenye rai anaweza asiwe katika nafasi yenye nguvu, lakini uwepo wake katika kundi unakuwa katika nafasi ya nguvu, linatosha hilo kumpa hisia ya kujikweza. Na kinyume cha hivyo, inaweza kuwa hisia ya udhaifu na woga kutoka upande mwingine ni sababu ya kujitenga na uwazi na majadiliano. Ambaye hajiamini katika nafsi yake au katika elimu yake na rai yake, hakika anapata kigugumizi kuwasiliana na wengine kwa kuogopa kudhihirika udhaifu wake, au hofu yake kutekwa nao au kufungua mwanya wa kuathiriwa watu wake na ngome yake. 3. Utengenezaji na hukumu zilizotangulia: Katika mazingira ya kutukanana na ugomvi, yanapokuwa masâ€&#x;ala ya ikhitilafu, yanagawa watu baadhi yao kwa baadhi mfarakano mkali, na baadhi yao wanatoa hukumu kali kwa baadhi hali ya kutokuwepo, huyu ni kafiri, na huyu ni fasiki na huyu ni mwanabidaa, na huyu ni fasiki na huyu ni Rafidhi, na huyu ni mughalii na huyu ni kibaraka! Hata taklid ya Marjaa imegeuka kuwa ni sababu ya mfarakano, watu wanatazamwa kupitia hilo. Mfarakano huu mbaya na yanayotokana nao ni katika hukumu mbaya. Kufanya haraka kuwaweka watu ndani ya makundi na mirengo finyu, yote hayo yanawakilisha hali ya kutoendelea inayovunja uaminifu baina ya watu wa umma, kama 174


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

ambavyo haiafikiani na ukunjufu wa Uislamu, na wigo mpana wa tabia njema. Wako wapi hawa wanaofanya haraka kuwakufurisha watu, na kuwatuhumu katika dini yao, na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

َ َ َ​َ ‫ى‬ ُ َ​َ َ ‫”يٰك َأي َ ا ىال‬ َ َ ‫زين‬ ‫بيل الل ِكه فخ َب ىي ىا َوال جلىلىا ِون‬ ِ ‫ءام ىا ِإرا ضشبخ فى ظ‬ َ َ َٰ ‫َ ٰ َ ُ ُ ى‬ َ َ ‫عذ ُمؤم ً ا َج َبخغى َن َغ َش‬ ٰ ‫احخ‬ “… ‫يى ِة الذ يا‬ ‫أللش ِإليى العلك ل‬ ِ “Enyi mlioamini mtakaposafiri katika njia ya Mwenyezi Mungu, basi hakikisheni wala msimwambie mwenye kuwapa salamu: Wewe sio muumini. Mnataka mafao ya duniani…..” (Surat An-Nisaa‟; 4:94). Anasema Sheikh Muhammad Twahir bin Ashur katika Tafsiri yake katika Aya hii: “Na aya imeshaonyesha juu ya hekima kubwa katika kulinda mkusanyiko, nayo ni kueneza uaminifu na amana baina ya watu wa umma, na kutoa ambayo kazi yake ni kuingiza shaka, kwa sababu unapofunguliwa mlango huu ni vigumu kuufunga kwake. Na kama ambavyo anamtuhumu mwingine na mwingine pia anamtuhumu aliyemtuhumu, na kwa hiyo unaondoka uaminifu, na inakuwa rahisi wadhaifu wa imani na waovu, ambapo tuhuma imeshakuwa inamfunika mkweli na mnafiki. Angalia muamala wa Nabii  kwa wanafiki, aliamiliana nao kwa muamala wa Waislamu. Kwa kuwa dini hii ni nyepesi kusambaa katika nyoyo inatosha watu wake kuingia wenyewe bila mjadala, ambapo hawakawii kuwazoea, kutangamana furaha yake na nyoyo zao. Wao wanavamia kwa shaka na kusitasita na inakuwa ni imani madhubuti, na kati ya yanayosaidia katika hayo ni uaminifu wa waliotangulia humo kwa wanaojiunga nao.”142 142

Ibnu Asour: Muhammad Twahiri katika Tafsiri Tahariri wa Taniwir, Juz. 4, uk. 226

175


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Na ananukuu Ibu Abi Shaibah katika kitabu chake kwamba: Ali aliulizwa kuhusu watu wa Jamal – ambao walimuasi na akawapiga vita – Akasema: Ikasemwa: Je, wao ni washirikina? Akasema: Walikwishakimbia ushirikina. Ikasemwa: Je, wao ni wanafiki? Akasema: Hakika wanafiki hawamtaji Mwenyezi Mungu ila kwa uchache. Ikasemwa: Sasa wao ni nani? Akasema: Ni ndugu zetu wametufanyia uovu.”143 Imepokewa riwaya kutoka kwa Imamu Ja‟far Swadiq  ambayo inatia mkazo maana ya riwaya hii ambapo inapokewa kutoka kwa baba yake : Hakika Ali  hakuwa anamnasibisha yeyote kati ya watu vita vyake kwenye shiriki wala kwenye unafiki, lakini yeye alikuwa anasema: Wao ni ndugu zetu wametufanyia uovu.144 Na mtu anapomnasibishia mwingine uadui na kuwatuhumu tangu awali, hakika hatopata msukumo wa kufunguka kwao na kujadiliana pamoja nao. Lakini hata tukifumbia macho juu ya kosa la ubaguzi na hukumu iliyotangulia, hakika haisihi kupuuza kwamba mabadiliko yako wazi katika kiwango cha uelewa, na kujiamini, na uhuru wa kutoa rai. Imeshatokea katika medani ya kijamii, kwa matokeo ya mabadiliko ya kielimu na kijamii, na hii ina maanisha kwamba fikra ya kimadhehebu, na mirengo ya kifikra, haidhibiti tena mamlaka yake katika rai zote na misimamo kwa wafuasi wanaojinasibisha nayo, hivyo haisihi kumhukumu mtu au uchamungu wake kupitia anayoyafanya katika misimamo kuhusu mwelekeo au upande ambao ananasibiana nao, hivyo hukumu ya jumla na kujumuisha kwa ujumla sio makini na wala haipatii. 143

Ibnu Shaibah: al-Hafidh Abu Bakar katika kitabu al-Musnaf fiy alAhadiithi wal Athar, Juz. 15, uk. 256 khabar namba 19709 chapa ya kwanza 1983 Darul salafiyah, India 144 Al-Huru al-A‟Miliy: Muhammad bin Hasan katika Tafswil Wasaili Shi‟ah, Juz. 15, uk. chapa ya kwanza 1993 Muasasatu Aal al-Bait liihiyai turathi Beirut.

176


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Kisha hakika mwingine kunasibiana na mrengo huu au ule na vyovyote litakavyokuwa kundi lako, hakika haisihi kukuzuia kujenga daraja la uhusiano wa kibinadamu na kijamii pamoja naye, na hususan pamoja na kuwepo maslahi ya pamoja. Na Mtume wa Mwenyezi Mungu  alifanya mkataba na Mayahudi wa Madina na Manaswara wa Najrani, na makhalifa baada yake wameamiliana na wafuasi mbalimbali wa dini zingine. Na imefanyika mikutano na majadiliano baina ya wakuu wao na viongozi wa Kiislamu. Na inatutosheleza kauli yake (swt):

ُ ُ ٰ ُ َ َ ‫َ ُٰ ُ ىُ َ ى‬ ُ َ​َ ّ ‫خشجىه ِمن‬ ِ ‫ال ٰ ين ى َى اللكه غ ِن الزين ل يلك ِخلىه ِفى الذ ِين ول ي‬ َ ُ ُ َُ ُ َ​َ َ ُ َ‫ى ى‬ ِ ‫لع‬ ‫طحن‬ ِ ‫لعطىا ِإلي ِ ِ ِإن اللكه ي ِدب او‬ ِ ‫ِديك ِشه أن جب ّروه وج‬ “Mwenyezi Mungu hawakatazi kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakuwapiga vita katika dini, wala hawakuwatoa makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu.” (Surat al-Mumtahana; 60:8). 4. Kibano cha uchochezi kwa watu: Baadhi ya viongozi wa kidini au wakifikira wakati mwingine wanapita mpaka katika kuwachochea watu wake dhidi ya rai nyingine na upande mwingine, na kuwatupia tuhuma mbalimbali na dosari humo, na kutia shaka katika nia zao, asili yake na tawi lake. Na kutokana na hilo anahukumu uharamu na hatia ya aina yoyote ya kuwasiliana pamoja naye, au kushirikiana hata katika mpaka wa ubinadamu wa chini kabisa. Na inapatikana hata ndani ya madhehebu moja kwamba wafuasi wa Marjaa fulani kuchochea watu wao dhidi ya Marjaa mwingine, kiasi kwamba hawawasiliani wala baadhi yao hawaswali nyuma ya jamaa wala hawashirikiani katika shughuli za pamoja. Hakika mfano wa uchochezi huu unakuwa ni kikwazo na kizingiti katika harakati za uzalishaji na kutia ugumu wa sehemu 177


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

ya kujasiri kufunguka kwa upande mwingine, au kujadiliana pamoja nao, kwa sababu watu wake wameleleka katika mwelekeo wa upinzani. Na sijui nini kisingizio cha kisharia cha hawa katika kuwalea watu wao juu ya chuki na husuda, na tabia mbaya? Pamoja na kwamba Qur‟ani tukufu inawaamuru Waislamu kuamiliana na makafiri wa kishirikina muamala ulio bora zaidi ili kudhihirisha mtazamo wa Kiislamu wa kimaendeleo wa kibinadamu, anasema (swt):

‫َ َ َ َ َ ى‬ ‫َ َ َ ُ َ​َ ى َ ُ َ ى‬ َ َ ‫خع ُن ف ِئرا الزي‬ ‫الع ِّينتِ ادفؼ ِبال ى ِىى أ‬ ‫َوال حعخ ِىي احخع ت وال‬ َ َ َ ‫ٌ َ َى‬ ٌِ ‫َبي ً َو َبي ُه َغ ٰذ َوة هأ ُه َو ِلى َخمي‬ “Mema na maovu hayawi sawa. Zuia uovu kwa lililo jema zaidi. Mara yule ambaye baina yako na baina yake pana uadui atakuwa kama rafiki mkubwa.” (Surat Fussilat; 41:34). Hakika muamala mzuri pamoja na wengine unakusaidia kuwavutia wao na kuwaathiri wakati ambapo muamala mbaya na tabia mbaya vinawakimbiza wengine katika haki ambayo nafsi yako inazingatia kwamba inailingania!! Kama ambavyo Mwenyezi Mungu Mtukufu anaamuru waja Wake waumini wawapokee watu – wote – kwa muamala mzuri na maneno mazuri anasema (swt):

ً

ّ

َ “….. ‫اط ُخع ا‬ ِ ‫… وكىلىا ِلل‬..” “Na semeni na watu kwa uzuri.” (Surat Al-Baqara; 2:83)

Na katika tafsiri ya Aya tukufu, anasema mwanachuoni wa Najid Abdurahmani As-Saadiy: “Kisha akaamuru kufanya wema kwa watu wote, akasema: “Na semeni na watu kwa uzuri.” Na katika kauli njema ni kuwaamrisha mema na kuwakataza maovu, 178


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

kuwafundisha wao elimu, kutoa salamu, bashasha na mengineyo katika maneno mazuri. Na ilipokuwa mwanadamu hawezi kuwaamrisha watu kwa amali yake akaamrishwa kwa amri anayoiweza kumfanyia wema kila kiumbe, nayo ni wema katika kauli na ikawa miongoni mwa hilo ni kukataza maneno mabaya kwa watu hata kwa makafiri.‟”145 5. Sehemu zenye nguvu: Kuna sehemu zenye nguvu za nje na za ndani, hazifurahishwi na kutawala mazingira ya uelewano na mshikamano kwa wananchi na umma, wala hawajitolei katika umoja wa nchi katika nchi za Kiislamu, na kwa hiyo zinatumia kila njia na mbinu kubakisha hali ya mfarakano na mizozo, na kuzuia ukuruba wowote baina ya pande na mirengo mbalimbali. Hizo ndio sababu za dhahiri – kwa nionavyo mimi – ambazo zinazuia kuanza kujitolea kufunguka na majadiliano baina ya wenye rai katika maulamaa na wanafikra katika jamii hizi, lakini wenye kuelewa wenye ikhilasi wanaweza kuvuka vizingiti hivi kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Imekwishawadia kubeba jukumu wenye rai katika jamii zetu na hususan maulamaa wa kidini, majukumu yao katika kuvuka hali ya utengano baadhi yao kwa baadhi, na wajipambe na ujasiri na ushujaa katika kufunguka na majadiliano na kuokoa jamii kutokana na matatizo, mizozo na ugomvi, kwani changamoto na harakati ambazo zinazikabili mara nyingi ni za kisasa, ni kubwa kuliko mambo ya pembezoni ambayo yanatimia katika msingi wake kubagua na mfarakano. PENGO LA KIROHO: HUZUNI NA MKANGANYIKO Mwanadamu katika maisha haya ana haja na mahitaji, na wala 145

As-Saadiy: Sheikh Abdurahaman bin Naasir katika Tafsir al-Karim Rahman fiy tafsiri kalaami al- Manaani, uk. 66 Daru Dhakhair – Musasatu Rayaan – Beirut 1997.

179


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

hayatulii maisha yake ila anapopata mbele yake fursa ya kuyapata mahitaji hayo. Na tunaweza kugawa mahitaji yake katika mafungu matatu, kila fungu linafungamana na fungu lingine kwa pande kati ya pande za shakhsiya yake. Fungu la kwanza: Mahitaji ya kimaada, na tunafungamana na upande wa kimwili wa kimaada katika maisha ya mwanadamu, kama vile haja ya chakula, kuvaa, kuishi, matibabu na jinsi. Nayo ni mahitaji ya dharura, ambapo yasipopatikana yanaparaganyika maisha ya mtu na jamii. Na inajulikana kwamba mateso ya ufakiri na ukosefu walau katika sehemu ya jamii yanapokonya amani na utulivu katika jamii yote, kwa sababu unatengeneza mazingira ya uasi na uovu, na kwa sababu hiyo imepokewa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu  kwamba amesema: “Ufakiri unakaribia kuwa ni ukafiri.”146 Na inanukuliwa kutoka kwa Swahaba mtukufu Abu Dharr al-Ghifariy  kauli yake: “Nimeshangaa kwa asiyepata chakula katika nyumba yake namna gani hatoki kwa watu hali ya kuwa mwenye kuchomoa upanga wake.”147 Fungu la pili: Mahitaji ya kiakili. Akili ambayo Mwenyezi Mungu amempa mwanadamu inahitajia elimu na maarifa, na inahitajia mazingira ambayo yanaipa uhuru wa kufikiri na wasila na vifaa vinavyosaidia kustawisha elimu na fikra. Na katika sekunde ya mwanzo ambayo Mwenyezi Mungu alimuumba humo mwanadamu, alimpa fursa ya elimu na kujifunza, anasema (swt):

‫َ َى َ َ َ َ َ ُى‬ “….. ‫ظماء ولُا‬ ‫”وغل ءادم‬ “Na akamfundisha Adamu majina ya vitu 146

147

Al-Hindiy: Ali al-Mutaqiy katika Kanzul-Umaal, Juz. 6, uk. 492 namba 16682 chapa ya tano 1985 Muasasatu Risala – Beirut. Khalid: Khalid Muhammad katika Rijaalu Haula Rasul, uk. 100 Darul kutubi al-hadiythati – Qahira 1968.

180


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

vyote…” (Surat Al-Baqara; 2:31).

ٰ َ​َ َ َ ُ َ ‫َى‬ ﴾٤﴿‫يان‬ ِ ‫الب‬ ‫﴾ غلمه‬٣﴿ ‫ن‬ ِ َ ‫ل َم ِإلاقعك‬ “Amemuumba mtu. Akamfundisha ubainifu.” (Surat Ar-Rahman; 55:3-4). Na unapozuiliwa kwa mwanadamu uhuru wake wa kifikra na uhuru wake wa kielimu, na akapokonywa haki ya kujua, hakika anakosa sehemu muhimu katika ubinadamu wake na kisha hatohisi utukufu na raha. Na kwa hiyo Uislamu umewajibisha kutoa elimu na kutoa fursa ya maarifa na kujifunza. Imepokewa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu  kwamba amesema: “Mwenye kuficha elimu yenye manufaa Mwenyezi Mungu atampiga kwa kijinga cha moto Siku ya Kiyama.”148 Na katika tafsiri ya kauli yake (swt):

ٰ َ َ “‫ن‬ ِ ‫… َو ِم ّما َسصك ك ُ​ُ ُي ِفلى‬..” “Na wanatoa katika yale tuliyowapa.” (Surat Al-Baqara; 2:3). Anasema Imamu Ja‟far Swadiq : “Katika tuliyowafundisha wanayafundisha.”149 Fungu la tatu: Maarifa ya kiroho ya kimaanawi. Mwanadamu ni roho na mwili, na kama ambavyo mwili una haja zake na mahitaji yake, vilevile 148 149

Al-Majilisiy; Muhammad Baqir katika Biharul-Anuwar, Juz. 2, uk. 78 Al-Majilisiy: Muhammad Baqir katika Biharul-Anuwar, Juz. 70, uk. 267

181


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

roho ina mahitaji yake nayo ni yenye athari kamilifu katika mwendeo wa upande wa kimaada katika maisha ya mwanadamu, kama atapata mahitaji yote ya kimaada lakini akawa anaishi katika upweke na njaa ya kiroho hakika maisha yake hayawezi kutulia au kuwa na raha. Mahitaji ya roho: Na roho inahitaji utulivu na uaminifu, ridhaa, raha ya dhamiri na uwepo, na maada kwa ufinyu wake, na harati zake, upungufu wake na dhiki yake haimpatii mwanadamu mafanikio, utulivu na utulivu wa kiroho. Hivyo ni lazima roho ya mwanadamu iwasiliane na ambayo yako juu ya maada kwa nguvu kuu ambayo haina mpaka na ambayo kwayo ndio marejeo ya mambo. Ni sahihi kwamba mwanadamu anamiliki kiasi cha nguvu na kudra, hususan katika zama hizi, ambapo kuna maendeleo ya uwezo wa mwanadamu, na uwezo wao wa kielimu umeendelea na teknolojia. Lakini mwanadamu anajua hakika uhai wake na uwezo wake na nguvu zake sio za dhati. Yeye amekuja katika maisha bila ya maamuzi yake, na atatoka kwayo bila ya hiyari yake na wakati wowote ambapo hawezi kudhibiti wakati wake. Na mwanadamu anajua kwa fadhila za maendeleo yake ya kielimu hivi sasa, upeo wa ufinyu wake na uchache wake ukilinganisha na ulimwengu huu mpana ambao anaishi ndani yake, umbo la ardhi ambayo anaishi juu yake. Umri wake ni kuanzia kabla ya miaka bilioni na nusu, nayo pamoja na ukubwa wake ni sayari tu inazunguka pembezoni mwa jua, pamoja na sayari zingine tisa, zinazotengeneza mkusanyiko wa jua. Na jua hili ukubwa wake ni mara 1,300,000 kwa ukubwa wa ardhi, nalo ni nyota moja tu baina ya bilioni ya nyota zinazotengeneza mkusanyiko unaoitwa Milky Way (mkusanyiko wa nyota), na unakadiriwa umri wake unakaribia kati ya miaka 10 na 15, na mkusanyiko huu ni mmoja kati ya mikusanyiko ambayo 182


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

inaogelea katika anga la ulimwengu.150 Na kama anavyosema mmoja wa wataalamu: Kama tukitaka kufananisha ulimwengu tungesema: Hakika ni bahari kubwa na kila mkusanyiko kati ya mikusanyiko ni kisiwa katika bahari hiyo kubwa, na kila mkusanyiko wa jua katika kila mkusanyiko ni kipande cha ardhi katika kisiwa hicho, na kila mkusanyiko wa jua katika kila mkusanyiko unafanana na kipande cha ardhi katika kisiwa hicho, na ardhi yetu ambayo tunaishi juu yake ni kwa kiwango cha sisimizi katika kipande cha ardhi, ndani ya kisiwa kati ya mabilioni ya visiwa katika bahari hiyo kubwa!! Sasa nini ukubwa wa mwanadamu ukilinganisha na ulimwengu huu mkubwa? Hakika anahisi udhaifu wake na kushindwa kwake, pamoja na yote aliyoyafanikisha na kuyapata katika maendeleo ya kielimu, na mafanikio ya teknolojia. Na yanadhihirika hayo wazi wakati majanga ya kimazingira yanapotokea kama vile tetemeko, volcano, mafuriko na upepo‌ naye anakosa udhibiti hata wa mwili wake na hisia za nafsi yake. Wakati yeye yuko katika kilele cha afya njema na uchangamfu, anashambuliwa na magonjwa na maradhi, na anapatwa na uzee na ukongwe. Na anapokuwa katika kilele cha furaha na burhani anaweza kupatwa na balaa na huzuni, na vivyo hivyo anageuka geuka katika hali mbalimbali, hawezi kuilinda nafsi yake kwa hali fulani, wala hawezi kujilinda nayo pia. Hisia hii ya kina kwa ufinyu na udhaifu, na hisia kubwa katika udogo na kushindwa inamsukuma mwanadamu kutafuta chanzo cha nguvu na uwezo na kuhusu upande unaotawala katika ulimwengu na maisha, ili nafsi yake ipate matumaini na mafungamano nayo, na ili moyo wake utulie na zitulizane hisia zake kwa kujikurubisha kwayo. Hiyo ndio dini ambayo inampa 150

Al-Mausuatu al-Arabiyati, Juz. 14, uk. 246 chapa ya pili Riyaadhi.

183


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

mwanadamu jibu kuhusu maswali yake yenye kutatiza kuhusu uwepo wake na hatima yake, na kumfungulia njia ya mawasiliano na kuamiliana na Muumba wa ulimwengu na uhai. Uswalihina ni hali ya kimaumbile kwa mwanadamu, kwa muundo wake wenye upambanuzi, roho, akili na mwili, William James Durant anasema katika Qiswatul-Hadhwarah: “Hakika Kuhani hakutengeneza dini, lakini ameitumia kwa ajili ya maslahi yake tu, kama mwanasiasa yeyote anavyomtumia mwanadamu kutokana na msukumo wa kimaumbile na ada. Haikumea itikadi ya kidini kutokana na ujanja ujanja au michezo ya kidini, hakika imemea kutokana na maumbile ya mwanadamu kwa ambayo humo kuna maswali yasiyoisha, hofu, huzuni, matarajio na kuhisi kujitenga.�151 Lakini mwanadamu anaweza kupotea njia ya dini sahihi, asipopata taufiki ya uongofu wa Mwenyezi Mungu na ujumbe wa mbinguni. Je, maendeleo ya kimaada yanatosha? Baadhi wanaweza kufikiri kwamba jamii zetu zinahitaji maendeleo ya kielimu, na maendeleo ya teknolojia, mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi, ili kuungana na msafara wa ustaarabu na maendeleo. Ama pande za kiroho na za kidini, ni jambo la pembezoni la kukamilisha tu, halina dauru katika kutengeneza hali ya mabadiliko na maendeleo. Lakini pamoja na kukiri jamii zetu kuhitajia maendeleo ya kielimu kiteknolojia, kisiasa na kiuchumi, isipokuwa kushibisha upande wa kiroho kuna umuhimu wa kimsingi, haiwezekani kupuuza upande wake. Hakika jamii za kimagharibi zilizoendelea ambazo tunataka 151

Deoranet: Wool katika Qiswatual-Hadhwarah, Juz. 1, uk. 117 Darul-Fikiri 1988.

184


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

kukaribia kiwango cha maendeleo yake unaishi katika matatizo hatari ya kijamii. Yanakwaza utamu wa maendeleo kwa sababu ya yale wanayokabiliwa nayo miongoni mwa mwanya na pengo la kiroho. Ustawi wa kimaada na maendeleo ya kielimu, peke yake haumpi mwanadamu mafanikio na matumaini, na ikiwa hajajaza pengo la kiroho hakika maisha ya mwanadamu yatakuwa yanakabiliwa na adhabu na mkanganyiko. Albert Einstein ni mfano: Mtu ambaye ameweka nadharia ya nisibiya alikuwa ni mwenye kufeli katika maisha yake binafsi, bali Albert Einstein alikuwa ni mpenda wanawake, mkali, mwenye muamala mgumu pamoja na watoto wake, baba wa binti asiyekuwa wa kisharia. Hakumuona wala hakumkubali anayeitwa Lieserl, na nyaraka zinafichua kumbukumbu baina yake kuna barua binafsi – ndani ya familia – kwamba ndoa ya Einstein ya kwanza kwa Malaga Marek ilipelekea talaka kwa sababu ya uhusiano wa siri uliomfungamanisha na jamaa yake wa karibu, Elissa. Na barua zinaonyesha uovu wa Einstein wa kumfanyia hila mke wake Malaga wakati wa kufarakana kwao, jambo ambalo lilipelekea kupatwa na mdororo wa mishipa na hakupona kwawo hadi kufariki kwake. Na unaendelea uovu huo katika muamala wake na watoto wake Hans Albert Einstein mkubwa na alikuwa na miaka kumi na tano wakati mzazi wake alipohama nyumba ya familia, na Eduard Albert Einstein mdogo ambaye alipatwa na wazimu baada ya kutalikiana wazazi wake na akamaliza maisha yake kwa kulazwa katika hospitali ya wagonjwa wa akili, na mzazi wake hakumtembelea hata mara moja.152 Na mfano wa Einstein uliotokea kwa Neil Armstrong naye ndiye mtu wa kwanza nyayo zake kukanyaga juu ya mwezi. Ilikuwa 152

Al-Hayatu: Jarida la kila siku – London 14 Swafar 1414H.

185


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

tarehe 20 July 1969, isipokuwa alikuwa hana furaha na utulivu kwani alimtaliki mke wake na akahitalifiana na watoto wake na akamaliza maisha yake kwa mkanganyiko na huzuni. Kuhusu hali ya jamii ya Kimarekani: Jamii ya Kimarekani iko katika kilele cha maendeleo ya kimaada ya kileo, lakini pengo la kiroho katika jamii hiyo limezalisha ongezeko na mateso hatari katika maisha na tabia kwa Waamerika, ambapo kunaenea huzuni, na matukio ya kujinyonga yanaongezeka, na makosa ya ubabe yanaongezeka, hata katika kiwango cha wanafunzi wa shule za msingi kama vilivyozungumzia hayo vyombo vya habari, ukiachilia mbali kiwango cha ufisadi wa tabia ulioenea. Mwaka uliopita ilitoka orodha ya vitabu vinavyouzwa zaidi Marekani. Kulingana na gazeti la New York Times, kitabu Final Exit kilichotungwa na Mwingereza Derek Humphry kinachozungumzia mbinu za kujinyonga na njia zake mbalimbali, kilichoandikwa kwa lugha ya mwongozo na kuelekeza, ndicho kinachoongoza.153 Hali hii mbaya ilizindua macho ya wanafikra wa kimagharibi sehemu ya kasoro katika maendeleo ya kimaada, nayo ni pengo na mwanya wa kiroho, kama ambavyo ilisukuma makundi ya jamii ya Kiamerika na ya kimagharibi kutafuta juu ya chanzo cha ilhamu ya kiroho, inayoziba pengo hilo, na kujaza pengo hilo, jambo ambalo limetoa nafasi ya kustawi mielekeo ya uongo na ukhorafi. Na kuhusu hali hii anazungumza mtafiti wa Kimarekani Rostow katika kitabu chake Stages of Growth, anaona: Hakika dola zinapita katika hatua nyingi: Hatua ya jamii ya mwanzo, hatua ya 153

Safir; Jarida la kila siku – Beirut 30 Muharram 1412 H.

186


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

kujitayarisha kuanza, hatua ya kupevuka, hatua ya utumiaji wa jamhuri na baada yake. Na anatilia mkazo kwamba majimbo ya Amerika yaliyoungana ni jamii pekee ambayo imefikia kwenye hatua ya utumiaji wa jamhuri, na kwamba inahamia kwa yaliyo baada yake. Na katika muonekano wa hatua hii ni kwamba jamii inazalisha zaidi kuliko inavyotumia, na inapunguza tatizo lake la kiuchumi katika kutengeneza mahitaji, na sio kutimiza lengo. Na vinatawala humo vyombo vya habari na zana za propaganda, ambapo inageuka kuwa ushibishaji wa kimaada kwenda kwenye ambayo yanaweza kuitwa mwelekeo wa kiroho, na kisha unaenea ukhorafi na dhana, madhehebu, bidaa na udanganyifu, ni sawa sawa unaambatana na dini au nje na dini au dhidi yake. Kama inavyoashiria katika jamii ya Kiamerika yenye umahususi na sifa maalumu nayo ni utajiri, bali hakika Marekani ni dola tajiri ambapo pato la taifa kwa jumla linazidi dola trillion 5.5, wakati ambapo wastani wa pato la mtu binafsi linazidi dola 22 elfu, pamoja na kuinuka kiwango, utengenezaji, maendeleo na teknolojia, na umri unatarajiwa wakati wa kuzaliwa. Na mwenye kudadisi katika maisha ya kiamerika anaweza kushituka kwa mandhari mbalimbali kutoka kwenye mdororo wa kijamii hadi kwenye fujo ya ndani ambayo haina mafungamano nayo. Na katika mambo ambayo yanazungumzwa na runinga ya Marekani vilevile ni masâ€&#x;ala ya kufichua yaliyojificha, na kujua bahati, au kisomo cha msomaji, na kutafuta yaliyopotea hata kama ni mpenzi au rafiki au huenda ni mali na cheo. Katika hali hii ni juu yako kuwasiliana na namba iliyoandikwa katika runinga na kueleza unayokabiliwa nayo, au unayoyatafuta au pengine unayotaka kujiepusha nayo, na utapewa jawabu kuhusu unayoyataka: Je umepoteza mali ? Je, umepoteza karatasi na nyaraka muhimu? Ataoneka kwako mtu kivuli au tabibu anakuongoza kwa maelekezo ili kupata ulichokipoteza, na hatimaye atapata kutoka kwako haja yake nayo ni mali bila shaka.154 154

Al-Hayatu: Jarida la kila siku – London, 29 Shawwali 1415 Hijiria

187


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Somo na zingatio: Sio makusudio katika kueleza chanzo cha udhaifu na kasoro katika maendeleo ya kimaada, kueleza sura mbaya yenye giza au maendeleo haya, na wala sio kudhihirisha hali ya jamii hizo tu kwani ni maendeleo yanayolazimisha utawala wake katika hali ya maisha, kwa mafanikio yake ya kielimu na teknolojia. Na ni wajibu kuwa na matarajio ya jamii zetu ili kuungana na msafara wake wenye kuendelea, na ili tufahamu umuhimu wa upande wa kiroho. Hivyo tusiupuuze na kuuacha, katika sensa ya hali ya jamii zetu bali tuzingatie ratiba na mikakati ambayo inastawisha uelewa wa kiroho na inayashibisha. Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anamhadharisha mwanadamu kwa kusahau upande wa kiroho kwamba kunasababisha huzuni ya mtu binafsi na mkanganyiko wa kijamii, na kisha kusababisha maisha ya dhiki, na maisha mabaya. Anasema (swt):

ً َ ً َ َُ ‫َ ى‬ َ ‫” َو َمن َأ‬ “….. ‫غش َ َغن ِرهشي ف ِئن له َمػيشت ض يا‬ “Na atakayejiepusha na mawaidha Yangu, basi hakika atapata maisha yenye dhiki…..” (Surat-Twaha 20:124), wakati ambapo uwiano na ukamilifu katika kuitikia mahitaji ya mwanadamu katika maelekezo yake ya kimaada, kiakili na kiroho unadhamini kwa mwanadamu maisha mazuri na mafanikio:

ً َ ًٰ َ ُ ‫َ َ َ ُ ٰ َ ُ َ ُ ٌ َ​َُ َى‬ ً ٰ َ َ َ ِ‫يىة ِّي َبت‬ ‫ديي ه خ‬ ِ ‫”من غ ِمل صك ِلخا ِمن ره ٍش أو أ ثى وهى م‬ ِ ‫ؤمن فل‬

“…..

“Mwenye kutenda mema, mwanaume au mwanamke, naye akawa ni muumini, tutamhuisha maisha mema…..” (Surat An-Nahl; 16:97).

188


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

MAENDELEO YA MTU BINAFSI NA MAENDELEO YA JAMII Kila mwanadamu aliye sawa sawa ana matarajio ya kuiletea nafsi yake maendeleo na utukufu katika maisha yake, na kuilinda dhati yake kutokana na mabaya na matatizo, nayo ni matumaini sahihi ya kisharia. Lakini ni njia ipi ya kufikia maendeleo? Na namna gani mwanadamu anafikia malengo yake na maslahi yake katika maisha haya? Hakika njia ya kawaida ni mwanadamu kuibua uwezo wake na vipaji vyake, na kuitaabisha nafsi yake kwa ajili ya nafsi yake. Anajifunza, anatafakari na anafanya kazi. Anajituma na kujitahidi, na kila anapojitahidi zaidi ndivyo fursa ya kuendelea inakuwa kubwa zaidi. Lakini swali linalojitokeza ni juu ya upeo wa uhusiano baina ya maendeleo ya mtu binafsi na maendeleo ya jamii ambayo anahusiana nayo, je, hali ya jamii inaathiri katika kiwango cha mtu binafsi na hali yake? Au mtu binafsi anaweza kutengeneza hali yake kwa kujitenga, na kuiletea nafsi yake maendeleo kwa kufumbia macho hali ya jamii yake, sawa iwe na maendeleo au isiwe na maendeleo? Hakika watu wengi wamejikita katika shughuli zao binafsi na wanajitahidi kupata maslahi yao binafsi bila ya kuwepo mambo makuu ya kijamii katika fikra zao au kutiwa katika orodha ya mazingatio yao, na hali ya kila mmoja wao ni: Mimi nashughulishwa na nafsi yangu kwa kujenga mustakabali wangu na kupanga mambo ya maisha yangu. Na mtazamo wenye uelewa katika maisha, unafichua kwa mwanadamu kwamba kuna uhusiano imara baina ya hali yake na hali ya jamii. Vyovyote utakavyokuwa uwezo wake na vipaji vyake, na vyovyote atakavyopata maendeleo na mafanikio, atabakia ni mwenye kuathirika na hali ya jumla ya jamii. Kwa hiyo inapasa fikira 189


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

yake na mazingatio yake yawe ndani ya duara mbili za kimsingi: Kujijenga kwa ajili ya nafsi yake, na kuchangia jengo la jumla la jamii. Na kwa kuzidi kuweka wazi zaidi tunaashiria katika baadhi ya nukta na ukweli ambao unadhihirisha kina cha mafungamano baina ya maendeleo ya mtu binafsi na maendeleo ya jamii. Kuandaa fursa za maendeleo: Ni sahihi kwamba mwanadamu anaendelea kwa juhudi zake na jitihadi zake na kwa vipaji vyake na uwezo wake. Lakini kupatikana fursa na maandalizi ya mazingira, ndio ambayo yanamuwezesha kuibua nguvu zake, na kutumia uchangamfu wake. Na jamii iliyoandaliwa inaleta kwa watu wake fursa za maendeleo, wakati ambapo jamii isiyoendelea zinakosekana au zinapungua humo fursa hizo. Kwa mfano katika nyanja za kujifunza, wanafunzi wetu katika nchi za Kiarabu sio wachache wa uelewa na uerevu kuliko wenzao wa Marekani, Japani au Ulaya, na baadhi ya watoto wetu wako juu katika juhudi na jitihada, lakini upeo wa maendeleo ya kielimu, na kiwango cha mfumo wa mafunzo na mazingatio ya kiwango cha uelewa na uerevu, na kupatikana nyenzo za kujifunzia katika jamii, katika nyanja zote na ubobezi, ndio ambavyo vinatia nguvu fursa ya mwanafunzi zaidi. Na katika nyanja za kifikra na maarifa kunapatikana katika nchi za Kiislamu akili shujaa na akili zenye mwanga, lakini uchache wa vituo vya utafiti na majaribio, na udhaifu wa vyombo vya kutoa rai unafanya fursa za maendeleo ya kielimu kuwa chache. Kwa ushahidi katika hilo, hakika baadhi ya watoto wetu katika jamii zilizoendelea wamepata maendeleo makubwa katika nyanja za kielimu na teknolojia mbalimbali, na Mwarabu wa kwanza kupata tuzo ya Nobel katika nyanja ya elimu ni Dokta Ahmad Zuwail, Mmisri ambaye anaishi Marekani na alipata tuzo mwaka 190


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

1999 katika Kemia. Athari ya mazingira: Ni kawaida mwanadamu kuathirika kwa mazingira ambayo jamii yake inaishi, na ikiwa mazingira ni mazuri anajipamba kwa maadili mema na yanashajiisha kwenye harakati na maendeleo. Hakika yanatengeneza mazingira yanayosaidia kumsukuma mtu na maendeleo yake, na ikiwa mazingira ya jamii ni mabaya yanatawaliwa na kutokuendelea na yanatawaliwa na hali ya uvivu na visingizio, na yamechanganyika na ufisadi na fitina, hakika yataacha athari zake na alama zake katika nafsi ya mtu na nyendo zake katika hali ya jumla. Mtu binafsi haishi katika kisiwa kilichojitenga au jangwani, bali yeye ni sehemu ya mkusanyiko, anaamiliana na anashirikiana pamoja na hali iliyotawala kwa kawaida. Na hii iko wazi katika nyanja ya kiafya kwa mfano, ambapo kuchanganyika kwake na watu waliopatwa na baadhi ya maradhi anaweza kupatwa na magonjwa kwa wepesi. Na vivyo hivyo, hakika fikira nyingi na nyenendo mtu anazichukua na kujipamba nazo kutokana na kuingiliana kwake na jamii. Matokeo na mwongezeko: Jamii ikipatwa na tatizo au fitina hakika matokeo yake na muongezeko utawakumba wote, bila ya kubagua aliyeshiriki na asiyeshiriki. Kuwepo kwa hali ya ufakiri katika jamii, kunaweza kuleta athari za ujeuri kwa matajiri na kuenea kwa maasi na maovu, yanayohadharisha hatari hata kwa wachamungu wema. Na kwa sababu hiyo anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

ً

‫ى‬ “…..‫اص ِت‬

َ​َ َ ‫َ ً ُ َ ى ى‬ ُ ‫ى‬ ‫زين ظلمىا ِم ى‬ ‫” َواجلىا ِفخ ت ال جصيبن ال‬

“Na jikingeni na fitina ambayo haitawasibu wale waliodhulumu miongoni mwenu peke 191


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

yao.” (Surat Al-Anfal; 8:25). Na hapa Mwenyezi Mungu amewajibisha kuamrisha mema na kukataza maovu, na akambebesha mwanadamu sio jukumu la kutengeneza nafsi yake tu bali na kufanya juhudi kuwaongoa wengine na kuwarekebisha wao vilevile, ili kulinda jamii kutokana na uharibifu na ufisadi. Na Mtume wa Mwenyezi  anafananisha matokeo ya vitendo vya mafisadi katika jamii yote na mwenye kutoboa meli. Ataisababisha kuzama na wote waliomo humo, anasema : “Mfano wa mwenye kusimama katika mipaka ya Mwenyezi Mungu na mwenye kuanguka humo ni kama mfano wa watu waliopanda meli baadhi yao wako juu na baadhi yao wako chini. Wale waliopo chini wanapohitaji maji wanapita kwa walio juu yao wakasema: Lau tungetoboa katika sehemu yetu tundu na tusiwaudhi walio juu yetu, kama watawaachwa na waliyoyataka wataangamia wote, na wakiwazuia watanusurika na watanusurika wote.155 Na mfano unaonekana mbele yetu wanayokabiliwa nayo wananchi wa Iraki waliopata balaa ya utawala wa Sadamu na siasa yake mbaya, ambapo hakusalimika na mbinyo na matokeo ya ufisadi huu yeyote miongoni mwao hadi ambaye anaona yuko mbali, na hahusiani na jambo kati ya mambo, hakika hakuwa ni mwenye kunusurika kutokana na adha na mateso. Nafasi ya jamii: Ikiwa unanasibiana na umma wenye nguvu na unafungamana na jamii tukufu, hakika hilo linakupatia ulinzi na kinga, na linatoa kwako nafasi za fursa yenye manufaa. Ama ikiwa umma wako 155

Al-Bukhariy: Muhammad bin Ismail katika Sahihul-Bukhariy, kitabu sharikati Juz. 3 uk. 278, al- Maktabatu Thaqafiyah – Beirut.

192


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

hauna nguvu, au jamii yako ni dhaifu, imekandamizwa, hutopata bahati ya kuangaliwa kwa heshima na wengine, kwa kuchunga haki zako na kuheshimu kipaji chako. Na kisha nafasi yako ya kijamii na nafasi yako miongoni mwa jamii ina uhusiano katika kupanga nafasi yako na hali yako utake usitake. Hakika sisi sasa hivi tunaona wazi namna gani kila upande katika ulimwengu unapigia hesabu, mara elfu moja katika kuamiliana na myahudi yeyote au jambo kati ya mambo ya myahudi, kwa sababu wao wamekuwa katika nafasi inayowapa wao hayo. Kabla ya muda serikali ya Misri iliamua kupasua njia ya kuzunguka Cairo kwa urefu wa kilometa 95, ili kupunguza msongamano wa mwendo katika mji mkuu, msongamano wa barabarani kila siku wa watu milioni 15, lakini njia hii inapitia katika makaburi ya zamani ya Wayahudi katika eneo la Basatin. Makaburi hayo yana zaidi ya miaka 70, na eneo lina makaburi 350 takriban, na ardhi ya makaburi kwa asili sio miliki ya Wayahudi, bali ni zawadi kutoka katika serikali ya Misri. Na serikali ilitaka kuondoa kaburi kwa kiasi cha mita 30 tu, ila Wayahudi walizua zogo kubwa ulimwenguni na wakaunda tume kati ya viongozi wa makundi ya Kiyahudi katika ulimwengu ili kukutana na Raisi wa Misri na viongozi wake. Na wakafungua madai kwa anwani mbalimbali katika mahakama ya Misri ili kuzuia kuguswa kwa namna yoyote makaburi ya wafu, na matokea yake makaburi yalibakia na kujengwa na daraja juu yake. Nafasi ya mtu binafsi katika maendeleo ya jamii: Katika yote yaliyotangulia inabainika kwetu mafungamano yenye nguvu baina ya hali ya mtu binafsi na hali ya jamii, na kwamba anayefikiria katika kujenga mustakabali wake na kupata maendeleo kwa ajili yake ni juu yake alete fikra na kuzingatia hali ya jamii yake na afanye hayo ni sehemu ya msingi katika ratiba yake ya harakati zake na juhudi zake. 193


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Namna gani mtu binafsi anachangia katika maendeleo ya jamii yake? 1. Hakika mazingatio ya mtu binafsi katika kujenga dhati yake, na juhudi yake katika kupata maendeleo na mafanikio kwa ajili ya nafsi yake, kwa hakika ni mchango kutoka kwake katika maendeleo ya jamii. Hiyo ni kwa sababu maendeleo ya jamii yanapatikana kwa maendeleo ya watu binafsi, hivyo kila mtu anaongeza nguvu katika hazina ya jamii kwa sharti la kuhisi kwake kunasibiana na jamii, na kushirikiana kwake pamoja na harakati za jumla za jamii. 2. Mtu binafsi anaweza kuelekeza juhudi zake na harakati zake ndani ya juhudi zake binafsi ili zilenge katika njia ya kuhudumia jamii, na kufanikisha mkakakti wa maendeleo yake. Mwanafunzi anapochagua ubobezi wa kielimu katika masomo yake ya juu ni wajibu wake aangalie haja ya jamii yake. Na mfanyakazi anapofikiria katika kuzalisha ni wajibu wake aelekee kwenye miradi ambayo inainua harakati za uchumi wa jamii na kutatua baadhi ya matatizo yake. Na mwanafasihi na mwanafikra atumie kipaji chake cha fasihi na uvumbuzi wake wa kifikra katika kuamsha jamii na kuendeleza hali yake. 3. Kama jukumu la mtendaji analifanya mtu binafsi katika maendeleo ya jamii atenge sehemu katika uwezo wake wa kifikra, kielimu na kimaada ili aitumie katika huduma inayonufaisha watu wote, na hiyo ni kupitia kushiriki katika taasisi za kijamii na shughuli za kujitolea. Na vyovyote atakavyoshughulika mwanadamu na mambo yake maalumu, hakika anaweza kutumia kiasi cha wakati wake kila siku au kila wiki kwa ajili ya kuhudumia umma. Na baadhi wanadhani kwamba kubeba baadhi ya majukumu ya kijamii na kutoa baadhi ya wakati wao au juhudi zao au mali zao itakuwa ni kwa hesabu ya mambo yao na shughuli zao maalumu. Lakini dhana hii sio makini, kwani matokeo ya wanayoyatoa katika maslahi ya jumla yataakisi kwao 194


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

kwa yale yaliyotangulia ubainifu wake katika athari na matokeo ya maendeleo ya jamii katika hali ya mtu binafsi. Na kwa hiyo anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

ُ

ُ َ

ُ

َ ُ

َ

َ ‫خعنخ أ‬ َ ‫”إن أ‬ “….. ‫خعنخ ِ​ِل ف ِعى‬ ِ “Mkifanya uzuri mnajifanyia wenyewe” (Surat Bani-Israil; 17:7). Kama ambavyo tunayoyaitakidi katika rehema ya Mwenyezi Mungu na ukarimu yanatupa imani na matumaini ya kurejeshewa ambayo mtu ametoa katika njia ya Mwenyezi Mungu, na katika kuwasaidia waja Wake, kwa nyongeza maradufu zaidi ya aliyotoa. Anasema (swt):

َٰ َ َ َ َ ‫ى‬ َ َ َ ‫َم َث ُل ىال‬ ‫بيل الل ِكه ه َمث ِل َخ ىب ٍت أ َبدذ َظ َبؼ‬ ‫مىل ُ​ُ فى َظ‬ ‫زين ُي ِفلىن أ‬ ِ ‫َ َ ُ ّ ُ َُ َ۟ ُ َ ى َ ى ُ ُ ٰ ُ َ َ ُ ى‬ ‫شاءِ َوالل ُكه ٰو ِظ ٌؼ‬ ِ ‫ظ ِابل فى و ِل ظنبل ٍت ِمابت خب ٍِتِ واللكه يضك ِػف ِون ي‬ ٌِ ‫َغلي‬ “Mfano wa wale wanatoa mali zao katika njia ya Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa punje inayochipuza mashuke saba; katika kila shuke pana punje mia. Na Mwenyezi Mungu humzidishia amtakaye, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa, Mjuzi.” (Surat Al-Baqara; 2:261). Na imepokewa kutoka kwa al-Habib al-Mustafaa  kwamba amesema: “Mbora wa watu ni yule mwenye kunufaisha, basi kuwa ni mweye manufaa kwao.”156 Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anambariki mwanadamu katika wakati wake, anapotoa sehemu yake katika kutumikia jamii, na anaongeza katika riziki yake anapotoa kwayo katika mambo ya kheri na anampa nguvu 156

Al-Hindiy: Ali al-Mutaqiy katika Kanzul-Umaal, Juz. 16, uk. 128, hadithi namba 44154 chapa ya tano 1985 Muasasatu Rusalati – Beirut.

195


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

na uchangamfu katika kwenda kwake mbio katika haja za watu na mambo yao. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

َ ُ َ َ َ َ ّٰ ُ َ َ ُ َ ُ ُ ُ َ ُ َ “‫كحن‬ ِ ‫الش ِص‬ ‫خلف ِهِ وهى حر‬ ِ ‫… وما أ فلخ ِمن ش ٍىء فُى ي‬..” “Na chochote mtakachotoa Yeye atakilipa. Naye ni Mbora wa wanaoruzuku.” (Surat Saba‟ 34:39) Ni ahadi ya kweli kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kumrejeshea ambaye anatoa katika njia ya Mwenyezi Mungu. Anasema Imamu Ali : “Waamrishe watu wako waende kuchuma mema na waingie katika haja za aliyelala. Naapa kwa ambaye usikivu Wake unasikia sauti zote, hakuna yeyote atakayetia furaha katika moyo isipokuwa Mwenyezi Mungu anamuumbia kutokana na furaha hiyo huruma, atakaposhukiwa na la kumshukia (kifo) itamwendea mbio kama vile mafuriko katika mteremko hadi ikifukuze kama ngamia anavyofukuza mgeni.” 4. Kusaidia mwenendo wa maendeleo katika jamii, ni juu ya watu binafsi washajiishe kila juhudi za shughuli nzuri, inayotokana na ardhi ya jamii yao. Kushajiisha na kushughulika ni jambo la dharura ili kuhifadhi uzalishaji, na maendeleo yake katika nyanja mbalimbali. Mwanachuoni anapozungukwa na watu wa jamii yake, na khatibu anapoamiliana pamoja nao wasikilizaji, na mwanafikra anapoona upokezi wa fikra zake, na mwanafasihi anapohisi kukubalika utoaji wake na mtengenezaji inauzika bidhaa yake. Na mtangazaji watu wanaponunua uzalishaji wake yote hayo yanatengeneza nguvu ya maendeleo na mabadiliko katika harakati ya jamii. 5. Ama kudharau uzalishaji wa ndani, na nguvu ya uananchi, kwa maslahi ya uagizaji kutoka nje, na kujifunga na yaliyo nyuma ya 196


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

mipaka, hiyo ni hali ya kushindwa na ubinafsi, wanaweza kupatwa baadhi ya jamii hadi ikaenea kwa watu methali inayosema: njiwa wa shamba haimbi (Jogoo wa shamba hawiki mjini). Na baadhi wamekuwa wanajifakharisha kwamba ananunua kutoka nje ya nchi yake au anatumia bidhaa za nje ya nchi yake, na anaweza kutoa hoja kwa uzuri wake na umakini wake, lakini mambo wakati mwingine hayaepukani na kuvutiwa na nje, na kuathirika kwa propaganda. Na ili kinyanyuke kiwango cha ubora na maendeleo ya uzalishaji katika nchi, ni lazima kushajiisha na kuunga mkono, pamoja na kutoa angalizo la mabadiliko na ukosoaji wenye kujenga. Na mara nyingi tunalazimika kuleta ushahidi kutoka katika hali pinzani, nayo ni hali ya Kiyahudi, kwa ajili ya kupata zingatio na somo. Wayahudi kila sehemu wanazingatia kushajiisha baadhi yao kwa baadhi, na kuunga mkono uzalishji wao wa ndani. Na ulipoanza utalii, Waisiraili wanakuja Jordani, baada ya maafikiano ya amani baina ya Jordani na Israil. Yalishitushwa mazingira ya utalii Jordani – kama yalivyoeleza magazeti na vyombo vya matangazo – kwa siasa ya ubakhili ambao anasifika nao mtalii wa Israil. Wao wanabeba pamoja nao chakula maalumu kwao, chini ya madai kwamba wao wanahifadhi ibada ya kula chakula cha kiyahudi, ambayo inalazimisha kwao kula chakula cha kiyahudi kilicho halali au al-kosher, lakini si kingine isipokuwa ni kisingizio, ambapo wao hawaleti chakula chao kilicho halili tu, bali na chupa za maji je kuna maji halali na mengine ni haramu? Na alikwishazungumza Waziri Mkuu wa Jordani wa zamani Abdu Salaam al-Majaaliy pamoja na viongozi wa Israil kuhusu maudhui kwa kuashiria kwamba chupa za maji Jordan ni rahisi zaidi kuliko Israil, pamoja na hivyo watalii wa Kiisrail, na wao ni kati ya wenye uwezo na matajiri wanaleta chupa za maji.157

157

Al-Hayatu – Jarida la kila siku – London 18 March 1995 uk: 12

197


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Mazingatio ya kijamii: Na mwisho hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu hakubali tuishi kwa ubinafsi, tufikirie na twende mbio katika mpaka wa duara la ubinafsi. Hakika hayo hayaafikiani pamoja na uswalihina halisi wa kweli, ambapo Qur‟ani tukufu inatia mkazo kwamba kupuuza mambo ya jamii, na sehemu dhaifu humo, ni dalili na alama juu ya uongo wa madai ya kuwa na dini, anasema (swt):

َ َ َ​َ ّ ‫يذ ىالزي ُي َى ّز ُل ب‬ َ ‫﴾ َف ٰزل ًَ ىالزي َي ُذع‬٧﴿ ‫ين‬ ‫﴾ َوال‬٧﴿ َِ ‫اليدي‬ ِ ِ ‫الذ‬ ‫أس ء‬ ِ ِ ِ َ ٰ َ ﴾٣﴿ ‫عىحن‬ ِ ِ ‫ػام ا ِو‬ ‫َي ُدض غهى‬ ِ “Je umemuona ambaye anakadhibisha dini. Huyo ni ambaye humsukuma yatima. Wala hahimizi kumlisha masikini.” (Surat-Mau‟n 107:1-3) Hakika kupuuza tu mayatima na kuwaacha na kutohimiza juu ya kujali haja za mafakiri, inamaanisha kwamba uswalihina ni wa uongo na wa udanganyifu. Mtume Muhammad  anamzingatia asiyejali mambo ya umma yuko nje ya duara la Uislamu “Mwenye kuamka na asijali mambo ya Waislamu basi sio Mwislamu.”158

JAMII YENYE UELEWA Ili mwanadamu awe ni shakhsiya huru yenye kuweza kuchukua maamuzi na kufanya mikataba na wengine ni lazima afikie kwenye kiwango cha uelewa, kulingana na hukumu za fikihi ya Kiislamu. Hiyo ni kwa kuwa hukumu za mikataba kuhusiana na mwanadamu zinatofautiana kwa kutofautiana hatua za maisha yake kiasi kwamba ukamilifu wa uwezo na upungufu wake, yeye 158

Al-Kulainiy: Muhammad bin Yaaqub katika al-Usulu Minal Kaafiy, Juz.2 uk. 163, Darul-Adhuwai – Beirut.

198


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

katika hatua ya kwanza, kuanzia kuzaliwa hadi umri wa utambuzi anakuwa ni mpungufu, na kwa istilahi ya kifikihi (hana utambuzi) hivyo hausihi muamala wake kikanuni kwa sababu hana uwezo. Na katika hatua ya pili: Katika umri wa utambuzi hadi umri wa uelewa, ambapo anapambanua mambo na anatofautisha lenye manufa na lenye madhara, lakini yeye bado hajafika kwenye hatua ya ukomavu na uelewa, hapa vilevile wengi wa mafakihi wanaona kutokuwa huru kwake katika kufanya muamala na kuchukua maamuzi katika miamala, hata kama ni baleghe na ni mwenye akili. Kubaleghe na akili ni masharti mawili ya taklifu ya kisharia kwa maana kwamba analazimika kwa taklifu na maamrisho ya kidini, lakini kama hajafikia kiwango cha uelewa uwezo wake hauwi ni wenye kukamilika kupitisha maamuzi yake na kusahihisha miamala yake. Hatua ya tatu: Mwelewa au mwenye ufahamu, ambapo inasihi miamala yake na maamuzi yake yote. Na maana ya mwelewa ni utendaji mzuri, na kuweka mambo katika mahala pake, na balehe inaweza kuambatana nao, na inaweza kuchelewa kidogo au zaidi, na inaweza kutangulia, lakini hakuna mazingatio kwake kabla ya kubaleghe. Na kwa mwelewa hakuna umri maalumu kwa watu wa fikihi, bali jambo linaachwa kwa utayari wa mtu na malezi yake, na nususi za kisharia hazipangi hilo. Na aghlabu sheria za kimji za hali za watu katika dola zinamzingatia mwanadamu kamilifu muweza na mwenye utu huru katika umri wa miaka kumi na nane, na baadhi yake kama vile sheria ya Misri inaisogeza hadi umri wa miaka 21. Kama ambavyo kujua uelewa wa mwanadamu unarejea kwenye kuangalia vitendo vyake na muamala wake, anasema (swt):

َ َ ّ ُ َ​َ َ َ ُ َ ّ َ ٰ ‫ابخ ُلىا ال َيخٰك‬ ً ُ ُ ‫عخ من‬ ‫شذا‬ ‫ياح ف ِئن ءاق‬ ‫”و‬ ‫ِ س‬ ِ ‫مش خ ٰى ِإرا بلغىا ال‬ 199


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

َٰ َ َ َ َ “….. ُ​ُ ‫مىل‬ ‫فادفػىا ِإلي ِ أ‬ “Na wajaribuni mayatima mpaka wafikilie umri wa kuoa. Mkiwaona wana uwekevu, basi wapeni mali zao.” (Surat An-Nisaa‟; 4:6). Ambapo mali ya yatima mdogo inakuwa chini ya mamlaka ya walii wake, na anapobaleghe na ukaonekana kwake uelewa anapewa mali zake, ili yeye abebe jukumu la kuisimamia. Na baadhi ya mafakihi wanatofautisha baina ya uelewa katika nyanja za kimali, na uelewa katika nyanja ya kijamii. Mwanadamu anaweza kuwa ni mzuri katika usimamizi wa mambo ya kimali lakini hamiliki ukomavu wa kijamii katika kuendesha maisha ya familia. Hapa hawi huru katika maamuzi ya kufunga ndoa, bali ni lazima kupatikane idhini ya walii wake, hata kama vitendo vyake vya kimali vinapitishwa na ni sahihi. Kama alivyoashiria hilo Sayyid Muhammad Kaadhim al-Yazidi katika al- Ur‟watulWuthqah katika mas‟ala ya nane katika mas‟ala ya mawalii wa ndoa. Uelewa katika mantiki ya Qur‟ani: Mazungumzo kuhusu uelewa yamekuja katika Qur‟ani mara kumi na tisa, na katika baadhi yake yamekuja kwa kutia dhuma Rau na kutia sakna Shin )‫ ) ُرشْد‬kama vile kauli Yake (swt):

َ

ُ

َ َ َ

ّ

َ ‫”ال إ‬ “….. ‫ينِ كذ ج َب ىحن الششذ ِم َن الغ ِ ِّى‬ ِ ِ ‫هشاه ِفى الذ‬ ِ “Hakuna kulazimisha katika dini uongofu umekwisha pambanuka na upotofu.” (Surat Al-Baqara; 2:256). Na kauli yake: “Mkipata matumaini ya uongofu kutoka kwao.” Kama vile kauli yake (swt): “Na tuandalie sisi katika jambo letu uongofu.” (Surat An-Nisaa‟: 6). Na imekuja katika sehemu nyingine kwa kutia fatiha Rau (‫ ) َرشَدا‬kama vile kauli yake (swt): “Na utuandalie sisi uongofu katika jambo letu. “ (Surat al200


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Kahf: 10), nayo ni maneno yenye kufanana na inaonekana kwamba makusudio ya Rushd (uongofu) katika mantiki ya Qur‟ani, ni ambayo ni mukabala wa Ghayi (upotovu) nayo ni kwa maana ya uongofu katika mkabala wa upotovu na kupotoka. Nao ni mukabala ulio wazi katika kauli Yake (swt):

ً َ ُ ‫ى‬ َ ‫بيًل َِوإن َي َشوا َظ‬ َ ‫… َوإن َي َشوا َظ‬..” ‫بيل‬ ‫شذ ال َيخ ِخزوه ظ‬ ِ ‫بيل الش‬ ِ ِ َ ً ُ ‫الغ ّى َي ىخخ‬ “….. ‫بيًل‬ ِ ‫زوه َظ‬ ِ ِ “Na wakiona njia ya uongofu hawaishiki kuwa ndio njia; lakini wakiona njia ya upotovu wanaishika kuwa ndio njia…..” (Surat AlA‟araf; 7:146). Kama ilivyokuja kutumia neno Rushd mukabala wa safihi, na inakuwa kwa maana ya muamala mzuri na uendeshaji, katika mukabala wepesi wa rai na udhaifu wa uendeshaji, na haya ndio makusudio ya mukabala katika mazungumzo kuhusu kuchunga mambo ya mayatima katika kauli Yake (swt):

‫َ َ َ َٰ ُ ى‬ َُ ‫ى‬ ُ ُ ُ َ ًٰ ُ ‫اسص‬ ‫كىه‬ ‫مىلى ُ ال ى َج َػ َل الل ُكه لى ِكيكما و‬ ‫” َوال جؤجىا العفُاء أ‬ ً ً َ َ َ َ ُ َ ‫ابخ ُلىا‬ ٰ ‫اليخٰك‬ ‫مش َخ ّ ٰى‬ ‫﴾ و‬٥﴿ ‫اهعىه َوكىلىا ل ُ​ُ كىال َمػشوفا‬ ‫في ا َو‬ َ َٰ َ َ َ ً ُ ُ َ َ ّ ُ َ​َ ُ َ ُ​ُ ‫مىل‬ ‫شذا فادفػىا ِإلي ِ أ‬ ‫ياح ف ِئن ءاقعخ ِمن س‬ ِ ‫ِإرا بلغىا ال‬

“…..

“Na wala msiwape wapumbavu mali zenu ambazo Mwenyezi Mungu amewajaalia kuwaendeshea maisha. Na muwakimu katika mali hiyo na muwavishe, na muwaambie maneno mazuri. Na wajaribuni mayatima mpaka wafikilie umri wa kuoa. Na mkiwaona wana uwekevu basi wapeni mali zao…..” (Surat AnNisaa‟; 4:5-6). Kabla ya kumiliki uwekevu mwanadamu anakuwa ni dhaifu wa 201


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

rai, hana uwekevu, nayo ndio inayoitwa safhi (wasio na akili), akivuka hatua hii anaitwa Rashidi mwenye akili (uelewa). Uelewa wa kijamii: Tunaweza kuzungumza juu ya uelewa katika kiwango cha watu binafsi, na tunaona mtu binafsi ni mwelewa anapambanua maslahi yake na anafanya muamala mzuri na usimamizi katika mukabala wa mtu dhaifu wa rai, hachukui msimamo unaofaa katika yanayomkabili katika nyakati na mazingira. Na tunaweza kuzungumzia juu ya uelewa katika kiwango cha jamii na makundi, kuna jamii yenye uelelewa na jamii isiyo na uelewa na upevu, namna gani tutanyoosha jamii na makundi katika nyanja hii? Na nini alama za uelewa wa kijamii? Katika Qur‟ani tukufu yamekuja mazungumzo kuhusu jamii yenye uelewa ndani ya kauli Yake (swt):

ُ َ َ‫ٰ َ َ​َىَ ُ ُ ُ َ​َ ى‬ ُ َ َ ‫َٰ ى ىَ َى‬ ُ ‫يى‬ ُ ‫يى‬ ‫ص‬ ‫لىبى وهشه ِإل‬ ‫ك‬ ‫فى‬ ‫ه‬ ‫ي‬ ‫و‬ ‫ن‬ ‫ك‬ ‫م‬ ‫إلاي‬ ‫… ولك ِىن اللكه خبب إل‬..” ِ َ ٰ ُ َ ِ ُ َ ُ َ َ ُ َ َ ‫الى‬ ُ ّٰ “‫ن‬ ِ ‫صيانِأولك ِنً ه الش ِشذو‬ ِ ‫الػ‬ ِ ‫فش والفعىق و‬ “…..Lakini Mwenyezi Mungu amewapendezea Imani na akaipamba katika nyoyo zenu, na akauchukiza kwenu ukafiri na upotovu, na uasi. Hao ndio walioongoka.” (Surat Al-Hujurat; 49:7). Na aya tukufu inaashiria katika sifa muhimu katika jamii ongofu, nayo ni mshikamano wa kinafsi na kifikira na kimwenendo pamoja na misingi na kanuni za kisharia. Msingi ambao jamii inaamini wakati mwingine ni anwani tu na wakati mwingine msingi unachukuliwa kwa msingi wa kupokea kutoka kwa waliotangulia bila ya uelewa na kukinai. Na jamii inaweza kuamiliana pamoja na itikadi kwa kiwango cha roho na nafsi, lakini katika upande wa kiakili na kifikra kuna uangalizi na 202


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

matatizo na inaweza kutokea kinyume kwa uwepo wa kukinai kifikra ya nadharia bila ya kupatikana kushadidia kiroho na kinafsi, na inaweza kuwa itikadi na kanuni zake ni jambo limelazimishwa katika jamii ile na uwepo wake, wakati inaamini itikadi ya kurithi bila ya kukinai au inaamini itikadi na haijilazimishi kutekeleza mfumo wake na kanuni zake katika uhalisia wa maisha yake, au inanyenyekea katika sharia yake kwa nguvu na kulazimishwa. Ama jamii yenye uelewa ambayo aya inaiashiria kwa kauli “hao ndio walioongoka� inasifika kwa sifa zifuatazo: 1. Kupenda itikadi na imani (amependezesha kwenu imani) kwa linalobeba neno la upendo katika maana za kuvutia nafsi na mshikamano wa kiroho. 2. Kuelewa itikadi (na amepambia katika nafsi zenu) yaani mmejua kwa akili zenu usahihi wa manhaji yenu ya kiimani, kwamba ni bora zaidi ambayo mnastawisha kwayo maisha yenu. 3. Kemeo la dhati juu ya kukhalifu na upotovu (na akawafanya mchukie ukafiri na ufusuka na maasi) nayo inatokana na sifa mbili zilizotangulia. Ikiwa mwanadamu anapenda itikadi yake kutoka ndani ya nafsi yake na mwelewa wa dini yake katika fikra yake na akili yake, hakika yeye kwa dhati yake anachukia maasi na anakimbia kwa kutoka katika mipaka ya nidhamu na kanuni, na vivyo hivyo hakika hali ya jumla katika jamii ongofu nayo ni kushikamana na kujidhibiti kwa msukumo wa dhati, na kujiepusha kukhalifu. 4. Hakika wakati Muumba Mtukufu anaponasibisha katika nafsi yake kupenda na kuchukia (amependezesha kwenu) na (amefanya mchukie) hakika haimaanishi kulazimisha kimaumbile katika hilo, bali makusudio ni kuandaa wasila na mazingira yanayofaa, na taufiki katika kukubali na kuitikia. 203


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Na kupitia aya tukufu na katika mwanga wa waliopanga mafakihi maana ya uelewa ambao ni sharti kutimia ili kukiri kufaa kufanya mkataba na kufaa kitendo kwa mwanadamu, tunaweza kuashiria kwenye alama muhimu na sifa za jamii yenye uelewa. 1. Uelewa na maarifa: Ikiwa mafakihi wanazingatia uwezo wa kupambanua maslahi na kutaofautisha kati ya kinachonufaisha na kinachodhuru, ndio mwanzo wa viwango vya uelewa ambao kwamba kunapatikana athari ya kisharia na kikanuni katika upande wa kukubali uwezo wa mwanadamu na uhuru wa utu wake, tunaweza kuiga kutokana na hilo kupanga mwanzo wa viwango vya uelewa wa kijamii, nao ni uelewa wa jamii na kujua kwake mambo na shughuli ambazo zinafungamana na hali yake ili aweze kubainisha maslahi yake na kutofutisha baina ya yale ambayo yanainufaisha na yale yanayoidhuru kama jamii. Hakika wengi kati ya watu katika jamii wanazama katika huzuni zao binafsi, au wanashughulika na masâ€&#x;ala ya pembezoni na wala hawaangalii katika mambo ya jamii yao, wala hawasaidii mazingira na hali ambazo zinazunguka umma wao. Na Qurâ€&#x;ani inatusimulia kuhusu jamaa yenye uelewa katika zama za Uislamu wa mwanzo, siku walipokuwa wachache Makkah wako katika mazingira ya ushirikina wakati huo, namna gani walikuwa wanazingatia matokeo ya vita baina ya Urumi na Uajemi. Yanayotokea katika nchi ya karibu Urumi na mpaka wake wa karibu na Uajemi, pamoja na umbali huu wa kijiografia ila hakika waumini Makkah walikuwa wanafuatilia vita. Na Waajemi washirikina walipowashinda Ahlul-Kitabu wa Urumi, waumini waliathirika kwa kushindwa kwa Urumi, pamoja na kutokuwepo mawasiliano au muungano baina yao, jambo ambalo linaonyesha juu ya uelewa na ufahamu wa vita hivyo, na athari zake na uakisi wake. Na kwa hiyo Mwenyezi Mungu Mtukufu ameteremsha 204


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

sura kamili ya Qur‟ani kwa jina la Surat Rum inayozungumzia kuhusu vita hivyo, na kuhusu harakati za waumini pamoja na matokeo yake na kuwabashiria wao kwa kubadilisha uwiano ndani ya muda mfupi, ambapo Urumi itanusurika katika miaka michache ijayo. Anasema Mwenyazi Mungu Mtukufu:

َ َ​َ َ َ َ َُ ّ ‫﴾ ُغ ِل َب ِذ‬٧﴿ ‫ال‬ ُِ ‫الش‬ ِ ‫﴾ فى أدقش س ِ وه ِمن‬٧﴿ ‫وم‬ ِ ِ ‫ػذ غل‬ َ َ َ َ َ ‫ػذِ َو َي‬ ُ ‫مش من َك‬ ُ َ ‫حنِ ِل ىل ِكه‬ ‫ىم ِن ٍز‬ ُِ َ ‫بل َو ِمن‬ ِ ‫ضؼ ِظ‬ ِ ‫غلبى‬ ِ ‫ظي‬ ِ ِ ‫ َ﴾ فى ِب‬٣﴿ ‫ن‬ ُ َُ َ ﴾٤﴿ ‫ن‬ ِ ‫ؤم ى‬ ِ ‫يفشح او‬ “Alif Lam Mim. Warumi wameshindwa katika nchi iliyo karibu. Nao baada ya kushinndwa kwao watashinda. Katika miaka michache. Amri ni ya Mwenyezi Mungu kabla yake na baada yake. Na siku hiyo waumini watafurahi.” (Surat Ar-Rum; 30:1-4). Na tukichukua kwa jicho la mazingatio dauru ya ushahidi wa ulimwengu, ambao Mwenyezi Mungu amewapa waumini

ّ

َ

ُ

َ ً

ً ُ ُٰ

َ ٰ َ

َ َُ ‫” َوهزلً َج َػل كى أ ىمت َو َظطا لخىى ىا ش‬ “….. ‫اط‬ ِ ِ ‫ذاء َغهى ال‬ ِ ِ “Na kama hivyo tumewafanya kuwa umma wa wastani, ili muwe ni mashahidi juu ya watu wote…..” (Surat Al-Baqara; 2:143). Hakika hayo yanamaanisha dharura ya uelewa wa jamii ya kiimani kwa kiwango cha juu katika uelewa, wanaweza kwayo kufuatilia mabadiliko ya kiulimwengu, na uwiano wa kimadola ukiachilia mbali kuelewa kwake hali zake na mambo yake. Anasema Imamu Ali : “Ni lazima kwa mwenye akili mambo matatu: Kuangalia jambo lake, kuhifadhi ulimi wake, na kujua wakati wake.”159 159

Ibun Shuubatu al-Haraaniy: al-Hasan bin Ali katika Tuhful-Uqul, uk. 144, chapa ya tano 1974 Muasasatu al-A‟alamiy lilimatubuati – Beirut.

205


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

2. Muamala mzuri: Namna gani jamii inaamiliana katika mazingira, matatizo na shida? Je, inatawaliwa na hali ya kujisalimisha na kusubiria muujiza kutoka kwa asiyefahamika? Au inatawaliwa na hasira, hisia na kuendeshwa na hamasa zisizokuwa na mkakati sahihi? Au inakabiliwa na changamoto kwa kufikiria kimaudhui, na ratiba yenye hekima? Uelewa wa jamii na upevu wake unapimwa kwa yale inayochagua na kufuata katika machaguo haya. Kushindwa mbele ya matatizo kunafichua ukosefu wa matakwa na udhaifu wa kujiamini, wakati ambapo kutumbukia katika hali ya hisia na hasira, na kutoweka hekima na kutafakari, kunaweza kuongeza na kuimarisha matatizo. Na kinachohitajia uelewa ni muamala mzuri, na kuchukua msimamo unaofaa katika nyakati zinazofaa. Mazingira yanaweza kuhitajia ukali na nguvu, na yanaweza kuhitajia hamasa na jaziba, na yanaweza kuhitajia upole na uelewa. Na katika sira ya Mtume Muhammad  kuna mifano ya muamala mzuri katika nyakati mbalimbali. Waislamu wa mwanzo pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu  walikuwa kama alivyowasifia Mwenyezi Mungu Mtukufu “Ni wana nguvu mbela ya makafiri.” (Suratul-Fatih; 48:29). Na vita na mapigano ambayo walipigana yanafichua juu ya ushujaa wao na kujitolea kwao, lakini hawa wenye nguvu mbele ya makafiri, walikubali suluhu ya Hudaibiya katika mwaka wa sita hijiria, kwa yale ambayo yalidhamini itifaki ya suluhu kwa masharti yaliyoonekana kwa dhahiri yake, kuwa ni maslahi kwa washirikina na ni kushusha utukufu wa Waislamu, hadi baadhi ya masahaba walitawaliwa na hali ya jazba na hasira na kupinga yaliyotokea, kama anavyotaja Ibnu Hishamu na wanahistoria wengine: Kwamba Umar bin al-Khatab alimwendea Mtume wa Mwenyezi Mungu  akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu je, 206


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

wewe si Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: Ndio (mimi ni Mtume). Akasema Je, sisi si Waislamu? Akasema: Ndio (sisi ni Waislamu). Akasema: Je, wao si washirikina? Akasema: Ndio (wao ni washirikina). Akasema: Kwa nini tunakuwa dhalili katika dini yetu? Akasema: “Hakika mimi ni mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, sitokhalifu jambo lake, na hatonipoteza!” Mwandishi anasema: Umar alikuwa anasema: “Sikuacha kuwa ni mwenye kutoa sadaka na kufunga na kuswali na kuacha huru (watumwa) kwa kuhofia maneno yangu niliyozungumza siku hiyo, hadi nilipotarajia kuwa itakuwa kheri.”160 Suhail bin Amru, mzungumzaji wa makuraishi alikataa kuandikwa katika waraka wa suluhu: Bismillahi Rahmani Rahiym, na akang‟ang‟ania aandike badala yake: Bismika Allahuma. Mtume  akaafiki juu ya hilo. Kisha Suhail akapinga neno “Haya ndio aliyokubaliana Muhammad Mtume wa Mwenyezi Mungu” kwa kusema: Kama ningeshuhudia kwamba wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu nisingekupiga vita, lakini andika jina lako na jina la baba yako tu: Mtume akaafiki katika hilo vilevile. Na Suhail akatoa sharti: Kwamba atakayemwendea Muhammad kati ya makuraishi bila ya idhini ya walii wake atamrudisha kwao, na atakayewaendea Makurasihi kati ya ambao wako pamoja na Muhammad basi hawatomrudisha kwake. Pamoja na kwamba ni sharti baya lakini Mtume  aliliafiki. Na ikatokea alikuja mmoja wa Waislamu mnyonge Makkah anakokota pingu zake na minyororo akakimbilia kwenye kambi ya Waislamu naye ni Jandal bin Suhail bin Amru. Akasimama baba yake Suhail na akampiga uso wake na akataka kutoka kwa Mtume  amrejeshe kwa makurasihi, na akatae kukimbia kwake. Mtume akaafiki juu ya hilo, Abu Jundal akapiga kelele: “Enyi Waislamu Je, narudi kwa washirikina na wananifitinisha na dini yangu?” Jambo ambalo lilichochea jazba kwa Waislamu lakini Mtume  160

Ibnu Hishamu: Siratun-Nabawiya, Juz. 346 chapa ya kwanza 1415 Hijiria Daru Ihiyai Turathi al- Arabiy – Beirut.

207


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

akamwambia: Ewe Jandal subiri na hesabia hilo kwa Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu atajalia kwako na kwa walio pamoja nawe katika wanyonge kuwa ni faraja na ukombozi.161 Pamoja na yote hayo, Mwenyezi Mungu aliichukulia suluhu hii ni ushindi mkubwa “Hakika sisi tumekufungulia ushindi wa dhahiri� (Suratul-Fatih; 48:1). Kwa sababu matokeo yake yalikuwa ni kheri katika maslahi ya Uislamu, hivi ndivyo inavyohukumu akili katika msimamo na sio hisia tu. Na jamii yenye uelewa ndio ambayo inapambana na mazingira na kuchukua msimamo unaofaa mukabala wake kimaudhui na kutafakari. 3. Kunufaika kutokana na uwezo Kila jamii ina uwezo wake wa kimazingira na wa kibinadamu ambao unatofautiana na unapitana kutoka jamii hadi nyingine. Na kinachotofautisha jamii yenye uelewa na nyingine ni mazingatio ya kuibua vipaji na kufanya kazi ya kuviendeleza na kunufaika navyo, na kuvitumia katika maslahi ya maendeleo ya jamii. Hakika baadhi ya jamii zinapuuza sehemu zake za kimazingira na kusahau vipaji na uwezo wa watu wake, wakati ambapo jamii zenye uelewa zinakwenda mbio kukuza sehemu zake na kunufaika na uwezo wake wa kimazingira na kibinadamu kadri iwezekanavyo. Na hii Cyprus kisiwa kidogo karibu yetu kinatoa mfano wa kunufaika na vipaji vya mazingira nacho kipo kona ya kusini mashariki ya bahari nyeupe ya kati, na kipo umbali wa kilometa 64 kusini mwa Uturuki na kilometa 100 Magharibi mwa Syria na wakazi wake ni chini ya watu 700,000. Na wao wako katika kiwango cha juu kama watu wa ulaya, na kiwango cha watu 161

Rejea iliyotangulia, uk. 347.

208


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

waliosoma humo ni asilimia 90. Pamoja na kwamba hawana utajiri wa mafuta na madini lakini wao wameendeleza mazingira mazuri na wamebadilisha nchi yao kuwa ni sehemu ya utalii muhimu, utalii unatengeneza humo sehemu ya kiuchumi na kisiasa, ukiongezea uzalishaji wa kilimo uliopo. Na katika nyanja ya kuendeleza sehemu za kibinadamu, Japani inatoa mfano mzuri, ambapo nguvu yake ya kielimu na kiuchumi inatokana na kuendeleza kiwango cha utendaji wa kiteknolojia na kiviwanda kwa watu wake. Japani hivi sasa ni nguvu kuu ya kiuchumi katika ulimwengu pamoja na uchache wa sehemu zake za kimazingira, nayo inaagiza sana mali ghafi ambazo viwanda vyake vinazihitajia. Ni kiasi gani zinamiliki jamii za umma wetu wa Kiislamu miongoni mwa vipaji na uwezo mkubwa, lakini unachokihitaji ni maelekezo ya kuziendeleza na kuzistawisha na kuzitumia kwa ajili ya maendeleo na ustawi.

MWANZO WA KUTENGENEZA UPYA Inasifika historia ya mwanadamu kwamba imejaa mabadiliko na mageuzi wakati ambapo viumbe vingine hai, vinaendesha maisha yao kwa muundo mmoja tu, na njia moja muda wote wa historia. Hakika baadhi ya wanyama wanaweza kufanya kazi na kutekeleza jukumu linalomshangaza mwanadamu kwa uzuri wake na ufanisi wake, lakini wanafanya hayo ndani ya hali iliyopangwa na namna thabiti, hayatokei kwayo mabadiliko au mageuzi yoyote. Nyuki, kwa mfano, huyu mdudu mzuri mwenye manufaa ambaye anatuzalishia asali, na anazalisha nta ambayo tunaitumia katika uzalishaji mbalimbali kama vile gundi, mshumaa na vifaa vya urembo kama ambavyo anahamisha mbegu za kiume kutoka ua hadi lingine, na kusaidia mimea kuzaliana. 209


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Huyu nyuki anaishi ndani ya nyumba ya mfano katika mapori au masega ya nyuki, kwa muundo wa sanduku ambalo linamasega ya asali, nalo ni mrundikano wa vijimawe vyenye umbo la sudusi. Wanalitengeneza wafanya kazi wa nyuki kutokana na nta inayozalishwa na miili yao, na kila sentimita 10 ina chembe 50,000 – 60,000 za sudusi (1/6) na baadhi ya makundi yana nyuki 50,000 – 60,000. Miongoni mwao kuna malikia mmoja kazi yake pekee ni kutaga mayai kwa wastani wa mayai 2000 kwa siku wakati wa vuli, yaani yai moja kila baada ya sekunde 43, na kundi moja lina mamia ya madume katika kizazi cha malikia. Hayana kazi isipokuwa kumzalisha malikia tu. Lakini sio kwamba malikia ndiye aliyewazaa, kwa sababu kwa kawaida wanaoana na madume yaliyozalishwa katika kundi lingine. Na kuna maelfu ya nyuki watumishi, wanafanya kazi ya kusafisha njia za masega, kuwaletea nyuki asali kuzalisha nta, kutengeneza masega ya asali, kulinda nyumba ya nyuki, na kukusanya utomvu unaoletwa na nyuki (wengine). Wafanyakazi wa nyuki wanaweza kuruka kwa kasi ya kilometa 25 kwa saa na kukusanya katika maisha yao utomvu unaotosha kutengeneza jamu 45 za asali. Huu ni mpangilio mzuri na utaratibu makini katika maisha ya nyuki, nayo ni hali madhubuti, hadi sasa imekwishapita miaka 80 milioni takriban tangu kuwepo kwa nyuki kulingana na makisio ya maulamaa, hajaguswa na mabadiliko au mageuzi.162 Mabadiliko ni sifa ya mwanadamu: Mwanadamu peke yake anamiliki akili, na kwayo anaweza kubadilisha na kujadidisha katika maisha yake. Ama wanyama na viumbe vingine wanaendeshwa na utashi wao na mazingira yake ambayo Mwenyezi Mungu amewaumbia, wala hawana uwezo wa kufikiri na kubadilisha. Hivyo inabakia njia yao katika maisha ni 162

Al-Mausuatu al-Arabiya al-Alamiyati juzuu 25 uk: 268 – 278 chapa ya ya pili 1999 Riyaadh

210


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

thabiti na ya mazoea, wakati ambapo yanaendelea mabadiliko na mageuzi katika maisha ya mwanadamu. Mwanadamu kila anapotumia akili yake na kutumia fikira yake, akanyanyuka kwa elimu yake na maarifa yake zinaongezeka njia za uboreshaji na mabadiliko katika maisha yake. Na kwa hiyo ananyanyuka kwenda katika kiwango kinachompambanua kama mwanadamu. Na anaposahau uwezo wake wa kiakili na akadumaza fikira yake na asiendeleze elimu yake na maarifa yake, anaishi maisha ya kulala na kudumaa, na kusogea kwenye uduni wa ulimwengu wa wanyama usio na mabadiliko. Na waliosoma historia ya mabadiliko katika maisha ya mwanadamu, wanaona wigo wa uhusiano wake na kiwango cha fikra na kielimu kwa mwanadamu. Hivyo hakika kizazi chetu cha sasa kinaonekana kana kwamba kimeshazaliwa katikati ya historia, kwa sababu kilichotokea katika kizazi chetu tangu kuzaliwa kwake hadi sasa kinalingana takriban na yaliyotokea katika historia ya binadamu tangu kwa Adamu ď „ hadi wakati uliopo. Na kwa mfano katika hilo: Katika mwaka 600 kabla ya kuzaliwa Isa, chombo cha usafiri wa haraka kilichokuwepo kwa mwanadamu ni ngamia, kwa kiwango cha maili 8 kwa saa, na kiwango hiki kimebakia kwa muda wa miaka 1600 takriban kabla ya kuzaliwa Isa. Walipogundua mkokoteni wenye matairi, ukaongezeka wastani wa kasi kwa kiasi cha maili 20 kwa saa, na kiwango hiki kimebakia maelfu ya miaka, karne 80 zilizopita na kwa fadhila ya meli za moshi zilizoendelea mwanadamu ameweza kufikia kasi ya maili 100 kwa saa, lakini baada ya mika 58 ya kutumia meli za moshi, ameweza katika mwaka wa 1938 kuruka kwa haraka kwa kasi ya maili 400 kwa saa, mara nne zaidi ya kiwango kilichotangulia. Na baada ya miaka 20, katika miaka ya tisini katika karne hii kasi ya ndege ya roketi imefikia hadi maili 4000 kwa saa, na mwanadamu ameweza kuzunguka ardhi hii kwa vipando vya angani ambavyo vinakwenda kwa kasi ya maili 211


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

18,000 kwa saa.163 Hivyo mabadiliko na uboreshaji ni alama ya kunyanyuka kwa mwanadamu katika kiwango kinachompambanua na viumbe wengine, na ni kiashirio cha kuendeleza neema ya akili ambayo amepewa na Mweneyzi Mungu Mtukufu. 4. Ulimwengu ni uboreshaji wenye kuendelea: Ulimwengu huu ambao tunaishi humo, uko katika hali ya kuendelea daima, ni uborekaji wenye kuendelea. Kuna nyota mpya zinazaliwa katika anga kwa mwendelezo, na wanaanga wanakiri kwamba wao hawafahamu upeo wa upana wa ulimwengu, pengine unapanuka bila ya kuwa na mwisho. Na wanaanga wamegundua kwamba mkusanyiko mwingi unaogelea baadhi yake uko mbali na baadhi kwa kasi sana. Na kwa kuongezea katika hayo inaonekana kwamba mkusanyiko ulio mbali zaidi na ardhi ndio ambao wenye mwendo kasi zaidi, kwa hiyo hakika Maulamaa wengi wanaitakidi kwamba ulimwengu unapanuka kwa mwendelezo. Anga la ulimwengu ulioundwa na mabilioni ya mikusanyiko uko katika hali ya upanuzi wa haraka, na utafiti wa anga umeashiria uwepo wa dalili zinazoonesha kwamba kuna hali ya kutengenezeka mkusanyiko mpya ndani ya anga. Na ukweli huo Qur‟ani tukufu inaukubali. Anasema (swt):

َ ّ َ ۟ َ ٰ َ​َ َ ‫َ ى‬ َ ِ‫ىظػىن‬ ِ ‫والعماء ب ي كُا ِبأيي ٍذ و ِإ ا و‬ “Na mbingu tumezifanya kwa nguvu na uwezo na hakika Sisi bila ya shaka ndio wenye kutanua.” (Surat Adh-Dhariyat; 51:47). Na katika aya nyingine anasema (swt): 163

Qafilatul Zait, uk. 16 tolea la Muharram 1416 Hijiria.

212


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

َ َ ٰ​ٰ ‫ى‬ َ َ ‫ُ ى‬ َ ُ ُ َٔ َ ِ‫ىم ُه َى فى ش ٍأن‬ ٍ ‫يعكله من ِفى العمكى ِث و س ِ ِ ول ي‬ “Vinamuomba Yeye viliyyo katika mbingu na ardhi. Kila siku Yeye yumo katika jambo.” (Surat Ar-Rahman; 55:29). Hivyo hali ya kutanuka ulimwengu ni yenye kuendelea kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ni kila siku. Na makusudio ya siku hapa ni wakati, yaani kila wakati na kila sekunde, na sio wakati maalumu kuanzia alfajiri hadi usiku. Katika kila sekunde kuna jambo kubwa na tukio muhimu linatokea katika ulimwengu. Al-Alusi amesema: Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu bado angalia anaumba watu na kuwauwa wengine na kuleta hali na kuondoa hali, kulingana na yanavyotaka matakwa ya Mwenyezi Mungu yaliyojengewa katika umakini wa hali ya juu. Na alBukhari amepokea katika Tarikh yake, Ibnu Maajah, Ibnu Hiban na jamaa kutoka kwa Abu Dardai kutoka kwa Nabii  kwamba amesema katika aya hii: Kwa uwezo wake anasamehe dhambi na kumnusuru mwenye matatizo, anawanyanyua watu na anawateremsha wengine.”164 Na imekuja katika hotuba ya Imamu Ali : “Namshukuru Mwenyezi Mungu ambaye hafi wala hayamaliziki maajabu Yake kwa sababu kila siku yuko katika jambo kati ya matukio mazuri ambayo bado hayajawa.”165 Na miili yetu kama sehemu ya ulimwengu huu inaishi katika hali ya mabadiliko na kujijadidi daima. Mada ya kimiminika ambayo 164

165

Al-Alusiy al-Baghdadiy: Sayyid Mahamuud katika Ruhul-Maaniy katika Tafsiril-Qur‟ani, Juz. 27, uk. 110 chapa ya nne 1985 Daru Ihiyai turathi alArabiyi – Beirut. Al-Huwaiziy: Tafsir Nuru Thaqalain, Juz. ,5 uk. 193 chapa ya nne 1412 hijiria Muasasatu Ismailiyaan Qum.

213


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

inapatikana katika chembechembe za damu zetu inaharibika kisha inajitengeneza upya. Na mfano wake ni mfano wa chembechembe zote za mwili, zinakufa na kuja mahala pake chambechembe mpya. Na utafiti wa kielimu unasema kwamba damu ya mwanadamu inajitengeneza upya ndani ya muda wa miaka minne, na chembechembe zote za mwili zinabadilika ndani ya miaka michache, hivyo mwili ni kama mto unaotiririka. Kila dakika katika mwili wa mwanadamu zinakufa chembechembe bilioni tatu takriban, na katika muda uleule zinazaliwa chem.bechembe kwa idadi mpya mfano wa hizo kwa kugawanyika chembechembe, badala ya chembechembe zilizokufa. Na chembechembe za ngozi iliyokufa zinadondoka, wakati ambapo zinapita chembechembe zilizokufa katika chembechembe za viungo vya ndani kwenda nje ya mwili pamoja na uchafu. Na unatofautiana muda wa chembechembe. Chembechembe za damu nyeupe kwa mfano zinaishi kwa muda wa siku 13 wakati ambapo chembechembe za damu nyekundu zinaishi kwa muda wa siku 120. Na chembechembe za ini zinaishi miezi 18 takriban. Ama chembechembe za mishipa zinaishi miaka 100 takriban.166 Hivyo kuna harakati ya kujadidi ndani ya asili ya vitu na wanafalsafa walikuwa wanaitakidi kwamba harakati haiwezekani katika kitu chenye kiwiliwili kabisa, kwa sababu kila harakati inapasa kuwa na kiwiliwili chenye kutembea kilichothabiti, ila viungo vyake vinaweza kubadilika, vinginevyo hakika harakati hazitakuwa na maana inayofahamika. Lakini wanafalsafa waliokuja baadae walipinga nadharia hii na wakaamini harakati ya asili, na wakasema: Hakika msingi wa harakati ni dhati (asili) ambayo inadhihiri athari yake katika viungo. Na wa kwanza aliyebainisha nadharia hii kwa ufafanuzi wa dalili ni al-Maula Swadir Diyn Shiraziy ambapo alisema: Hakika kila chembe za viumbe na ulimwengu wa kimaada ni zenye harakati, au kwa maneno mengine, hakika mada ya viwiliwili vya uwepo ni kama 166

Al-Musuatu al-Arabiya, Juz. 10, uk. 147 chapa ya pili 1999 Riyaadh

214


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

maji yanayotiririka ambayo hali yake ni yenye kubadilika, kila sekunde yanakuwa na hali mpya inayotofautina na uwepo wa awali na kwa kuwa mabadiliko haya yanaungana na baadhi yake hakika yanahesabiwa kuwa ni kitu kimoja.167 Malengo ya kutafakari na kudadisi katika ulimwengu: Wakati Mwenyezi Mungu anapotuamuru kutafakari na kudadisi katika ulimwengu, na kutukumbusha hali ya kujadidi na uvumbuzi wa daima katika viumbe, ni kwa malengo yafuatayo: Kwanza: Kufahamu ukubwa wa Muumba Muweza (swt). Pili: Kuelewa mazingira ya kanuni zinazotawala katika uwepo ili tusipatwe na kukata tamaa. Tatu: Kufahamu dauru ya mabadiliko na kujadidisha katika harakati. Tunapata kutokana na hayo somo na mazingatio katika muamala wetu pamoja na hali za kijamii na nyenendo zetu za kimaisha. 5. Ushindani wa mabadiliko: Maisha ni medani ya ushindani, wanasongambele humo viongozi wa mabadiliko na kujadidisha. Jamii yenye kujadidisha kwa wingi na yenye kasi ya mabadiliko inapata maendeleo na inazatiti nguvu yake na utawala wake, wakati ambapo jamii iliyosimama, chache ya harakati inaharibika hali yake na inapatwa na uzee, na inarudi nyuma na inanyenyekea katika utawala wa wenye kuendelea. Na hususan katika zama hizi, ambapo yametoweka masafa na imeondoka mipaka na vikwazo, na hakuna tena nafasi ya kusimama na kudumaa. Ama uwe ni mzalishaji wa harakati ya 167

Shiraziy: Sheikh Naswir Makarim katika al-Amthali juzuu 17 uk: 347 chapa ya kwanza 1992 Muasasatu al-Biithah Beirut.

215


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

mabadiliko na kujadidisha au uwe tayari kuipokea na kuielewa kwa daraja la pili, ili usigongane na uthabiti wako na misingi yako, vinginevyo utakumbwa na harakati zake zenye kusomba, bila ya hiari yako, na kuwa ni mfuataji mwenye kutumia wanayoyazalisha wengine miongoni mwa bidhaa za fikra, ratiba na tabia. 6. Kukabiliana na changamoto: Katika mwenendo wa maisha jamii inakabiliwa na matatizo na changamoto, na inaweza kuhitajia kukabiliana nayo kwa aina ya kujadidisha katika fikra, na kubadilisha katika ratiba, na kuboresha katika njia na mbinu. Jamii ikidumaa katika harakati ya mabadiliko na ikashikamana na iliyoyazoea na desturi, basi changamoto zitaishinda, na matatizo na shida zitakwamisha harakati zake. Na tunaona namna gani changamoto za mazingira na matatizo ya maisha ndio ambayo yanamsukuma mwanadamu kugundua na kuvumbua. Kuvumbua mbinu na nyenzo katika nyanja mbalimbali, na kwa hiyo amevuka changamoto hizo na matatizo kwa kiasi kikubwa, na hali ni hiyo hiyo katika kiwango cha kijamii. Ni lazima kuvumbua na kubadilisha, ndipo jamii inaweza kupambana na hali mbaya iliyopo, na kushinda ushawishi wa hali na mazingira. 7. Uislamu: Ni Daawa ya Kujadidisha: Ujumbe wa mbinguni umekabiliwa na hali ya kudumaa katika jamii zake, na zikashikamana humo na waliyoyarithi kutoka kwa watangulizi wao na kuyazoea katika maisha yao. Hivyo ujumbe huo ukajikita katika kulingania jamii kwenye kujikomboa kutokana na utumwa uliopita na minyororo ya sasa na kushikamana na haki na usahihi. Lakini maneno ya wasioendelea mbele ya Manabii wao yalikuwa: “Hakika sisi tuliwakuta baba 216


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

zetu juu ya desturi na tunaongoza nyayo zao.” (Sura Zukhurufu: 22). Waliyoyafuata baba (zetu) na iliyoyazoea jamii, ni wajibu yabakie na yaendelee, na fikra yoyote mpya wanaikabili kwa tahadhari na upinzani chini ya nembo ya: “Hatujasikia haya kwa baba zetu waliotangulia.” (Suratul-Muuminina: 24). Na Uislamu kama hitimisho la ujumbe wa mbinguni unalingania binadamu kujinasua na pingu ambazo zinakwaza na kuzuia harakati zake kuelekea kwenye haki na maendeleo. Anasema (swt) kuhusu Nabii Wake Muhammad :

َ ‫َ ٰ ى‬ َ َ َ​َ َ ‫ض ُؼ َغن ُ إ‬ “….. ِ ‫صش ُه َو غلك َل ال ى وا ذ َغلي‬ ‫… وي‬..” ِ “Na kuwaondolea mizigo yao na minyororo ambayo iliyokuwa juu yao.” (Surat Al-A‟araf; 7:157). Na inamhamasisha mwanadamu kufungua rai na mbalimbali, ili avumbue zilizo bora kati ya fikra hizo,

fikra

َ ‫َن‬ َ َ ‫ى‬ ُ َ َ ‫اللى ٌَ َف َي ىدبػى َن َأ‬ “….. ‫خع ِه‬ ‫زين َيعخ ِمػى‬ ‫”ال‬ ِ “Ambao husikiliza maneno, wakafuata mazuri zaidi…” (Surat Az-Zumar; 39:18). Na inalaumu akili yenye kudumaa na hali ya kudumaa, kwa sababu inampelekea mwanadamu kurudi nyuma katika msafara wa maisha na kumuweka katika orodha ya wafu. Imepokewa katika riwaya kutoka kwa Imamu Ja‟far Swadiq : “Mwenye kulingana siku zake basi ana hasara, na ambaye siku yake ni shari zaidi kuliko jana yake basi ana mtihani. Na ambaye haoni upungufu katika nafsi yake utadumu upungufu wake, na mwenye kudumu upungufu wake basi mauti ni bora kwake.”168 Na kwa 168

Al-Majilisiy: Muhammad Baqir katika Biharul-Anuwar, Juz. 75, uk. 277

217


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

madhumuni hayo hayo kuna riwaya kutoka kwa Imamu Musa alKadhim ď „169 na nyingine kutoka kwa Imamu Ali ď „.170 Hivyo ndio vyanzo muhimu vya kuanzia harakati ya mabadiliko na kujadidisha katika maisha ya mwanadamu Mwislamu. Na kujadidisha kuna manhaji yake, na vidhibiti vyake, na nyanja zake, na zana zake ili kuwe katika maslahi ya mwanadamu na kwenda sambamba pamoja na misingi na maadili.

ROHO YA KUJADIDISHA Kwa nini ongezeko la hali ya kujadidisha na mabadiliko inakwenda haraka katika baadhi ya jamii, wakati ambapo inadorora na ni ya taratibu au inakosekana katika jamii nyingine? Baadhi wanaweza kusema: Hakika sababu katika hilo ni kupatikana uwezo hapa na kukosekana au kupungua kule. Jamii ambayo inamiliki uwezo na utajiri inaweza kupatikana humo hali ya maendeleo, ama jamii fakiri hali yake ni kuishi kwa kusimama na kudumaa. Na wengine wanaona kwamba masâ€&#x;ala yana uhusiano na mizizi ya jamii na historia yake/Ikiwa inatokana na historia yenye maendeleo na historia kongwe, hakika hilo litaisukuma katika mabadiliko na maendeleo, ama ikiwa ni jamii mpya au mwanzo wake ulikuwa ni uzembe hakika itakuwa na mwendelezo wa historia yake iliyotangulia. Na kundi la tatu linaweza kusema kuathirika hali ya jamii kwa uwezo wa harakati yake, ambapo uhuru wa jamii na uhuru wake au kuangukia chini ya utawala wa adui au nguvu pinzani kunadumaza matakwa yake na kuzuia maendeleo yake. Rai hizi na mfano wake ingawa zina kiasi fulani cha ukweli, na 169 170

Rejea iliyotangulia uk. 327 Rejea iliyotangulia, Juz. 74 uk. 377

218


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

zina akisi sehemu ya picha, lakini hazifichui kwetu siri ya tofauti na asili ya tatizo. Historia ya maendeleo na umma za leo zinatusimulia kuhusu jamii zenye utajiri mchache, zilizopata miujiza ya maendeleo kama vile Japan. Na jamii changa zimekuwa kileleni kama vile Wamarekani, na jamii iliyozingirwa na kushindwa, imeweza kuvuka hali yake na kujenga nguvu yake upya kama vile Ujerumani na Japan baada ya vita kuu ya pili ya dunia. Wakati ambapo umma zingine zinamiliki utajiri na ukongwe wa kihistoria, na mazingira ya nje yanayofaa lakini hakika zinaishi katika uduni, kutokuendelea na kudumaa. Anasema Pawel Kenedy katika kitabu chake al-Tahadhir Liliqarni al-Wahid wal-ishirini: Hakika Korea na Ghana zilikuwa zinaishi katika kiwango cha uchumi kinachokaribiana mwaka 1960, na pato la mtu katika nchi mbili hizi ni kwa kiwango cha dola 230 kwa mwaka, na baada ya miaka 30 (1990) liliongezeka pato la Mkorea mara kumi na mbili na kuwa dola 2760, wakati ambapo limebakia pato la Mghana katika hali yake dola 230!! Kama ambavyo Japani na Misri walianza harakati zao mpya mwaka mmoja, na Japani ilikuwa inaishi katika wakati mgumu na mbaya baada ya kushindwa kwake katika vita kuu ya pili ya dunia na kupigwa kwake na kombora la nyuklia, lakini ni tofauti ilioje hivi leo baina ya maendeleo ya Japani na Misri? Mwamko na kujadidisha ni roho na ni hali ya ndani, kabla ya kuwa hali na uwezo wa nje. Ikienea roho hii katika umma, inaleta humo harakati na uchangamfu, na inatoka kutafuta uwezo, na kutengeneza historia, na kukabiliana na changamoto. Na umma ukikosa roho hii, uhai wake unageuka na kuwa mauti, na unashambuliwa na maadui kutoka kila sehemu na kila upande. Na kwa hiyo Qurâ€&#x;ani tukufu inatia mkazo juu ya umuhimu wa kubadilisha nafsi na inazingatia ni sharti pekee la kubadilisha hali ya nje. Mabadiliko yanaanza ndani ya nafsi ya mwanadamu na 219


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

umma; anasema (swt);

َ ّ َ ُ َ َُّ ُ َ ‫ى ى‬ “….. ُِ ‫ىم َخ ٰى ُيغ ِّحروا ما ِبأ ف ِع‬ ٍ ‫… ِإن اللكه ال يغ ِحر ما ِبل‬..” “Hakika Mwenyezi Mungu habadilishi yaliyopo kwa watu mpaka wabadilishe yaliyo katika nafsi zao.” (Surat Ar-Ra‟d; 13:11). Na vyovyote jamii itakavyomiliki vipaji na uwezo, kupatikana uwezo na utajiri hakika bila ya roho ya mwamko na kujadididsha nafsi yake haitopata kitu, bali utapotea uwezo wake bure. Na utajiri wake utapotea bure, na kuishi katika hali ya kudumaa na inakuwa karibu na maisha ya wanyama, kama anavyosema (swt):

َ َ ُ ٌُ َ ُ​ُ ‫بصشون ِب ا َول‬ ِ ‫أغحن ال ي‬ َ ‫َبل ُه َأ‬ ُ ‫ضلِ​ِ ُأولٰكن ًَ ُه‬ ِ

َ َ َ ٌ ‫… َل ُ​ُ ُك‬..” ُ​ُ ‫لىل ال َيفلُىن ِب ا َول‬ ٰ َ َ َ ٰ ُ َ َ َ ٌ ِ ‫ءاران ال يعمػىن ِب اِ أولك ِنً واِلقػك‬ َ ٰ “‫ن‬ ِ ‫الغك ِفلى‬

“…..Wana nyoyo lakini hawafamu kwazo, wana macho, lakini hawaoni kwayo, na wana masikio, lakini hawasikii kwayo. Hao ni kama wanayama bali wao ni wapotea zaidi; hao ndio walioghafilika.” (Surat Al-A‟araf; 7:179). Hakika wao ni wenye kughafilika kwa ambayo amewapa Mwenyezi Mungu Mtukufu katika neema, na iliyo muhimu zaidi ni neema ya akili na kufikiri “wana nyoyo lakini hawafamu kwazo” na hata viungo vyao na hisia zao hawanufaiki nazo faida inayotakikana “na wana macho lakini hawaoni kwayo, na wana masikio lakini hawasikii kwayo,” na hivyo hayatabadilika maisha yao, bali yanakuwa kama ya mnyama aliyesimama amedumaa kwa kuondolewa kwao katika uongofu wa Mwenyezi Mungu “hao ni kama wanyama.” Na ikiwa wanyama wanasamehewa kwa sababu wana matamanio bila kuwa na akili, nini udhuru wa mwanadamu? Hivyo “bali wao wamepotea zaidi” na wana hali 220


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

mbaya zaidi kuliko wanyama. Na katika aya nyingine anatia mkazo Mwenyezi Mungu (swt) juu ya umuhimu wa undani wa mwanadamu, na ambayo yanauzunguka undani wa nafsi yake kwa kauli Yake (swt):

‫َ​َ ى‬ َ ‫ظم َػ ُ​ُ ِ َو َلى َأ‬ َ ‫َ ًحرا َ َِل‬ ‫ظم َػ ُ​ُ لخ َىلىا َو ُه‬

ُ ‫َ​َ َ َ ى‬ ِ ‫ولى غ ِل اللكه في‬ َ ُ ‫ن‬ ِ ‫ػشضى‬ ِ ‫م‬

“Na kama Mwenyezi Mungu angelijua wema wowote kwao, angeliwasikilizisha; na kama angeliwasikilizisha, wangeligeuka hali wakipuuza.” (Surat Al-Anfal; 8:23). Ikiwa nafsi hazizungukwi na kheri wala hazibebi raghaba wala matakwa ya maendeleo na mabadiliko, basi hazitanufaika na jaribio lolote au fursa ya nje. Alama na sifa za uvumbuzi: Hakika roho ya kujadidisha na mabadiliko, inamaanisha kumiliki sifa na alama. Inajaza maisha ya mwanadamu uchangamfu na kuisukuma kwenye uvumbuzi na mafanikio, na kumfanya kuvuka vikwazo na vizuizi na kutafiti alama hizo muhimu. 1. Uelewa na matarajio: Hali ambayo anaishi mwanadamu ikiwa ni mbaya isiyo na maendeleo, hakika haileti natija thabiti wala uwezo unaotakiwa, bali ni matokeo ya sababu na visababishi mukabala wa mabadiliko na mageuzi. Na katika mwanzo wake kuchuma nafsi yake, kwani anabeba kwa daraja la msingi jukumu la hali ambayo anaishi nayo. Anasema (swt):

ُ

َ

َ َ

َ

ُ ٰ َ

َ ‫” َوما أصك َبى من ُم‬ “….. ‫صيب ٍت ف ِبما ه َعبذ أيذيى‬ ِ 221


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

“Na misiba inayowasibu ni kwa sababu ya yaliyotendwa na mikono yenu.” (Surat Ash-Shura; 42:30). Na kwa hiyo fursa inayotolewa kwa mwanadamu ili aondokane na hali hiyo mbaya, anapokataa kujisalimisha kwayo na kutaka kuivuka hatofanikiwa. Na historia imejaa mabadiliko ya kijamii. Ni jamii ngapi dhaifu zimekuwa na nguvu, na ni jamii ngapi zimetawala kisha zikaporomoka, na matakwa ya Mwenyezi Mungu Mtukufu yako pamoja na kila jamii inayokwenda mbio ili kuamka

َ ً َ َ​َ َ​َ ُ ُ ُ ‫َو‬ َ ‫شيذ َأن َ ُم ىن َغ َهى ىال‬ ‫جػل ُ​ُ أ ِب ىمت‬ ‫زين اظخض ِػفىا ِفى س ِ و‬ َ ٰ ُ َُ​َ َ​َ ِ ‫الى ِس‬ ‫زحن‬ ُ‫و جػل‬ “Na tunataka kuwafadhili waliodhoofishwa katika ardhi na kuwafanya wawe ni viongozi na kuwafanya ni warithi.” (Surat Al-Qasas; 28:5). Na ikiwa hali ya maisha ni nzuri sana, hakika ni juu ya mwanadamu asizingatie hali yake kuwa ndio mwisho na kikomo, wala asipatwe na ghururi na majivuno, na kusimama kuacha maendeleo. Na ikiwa hataendelea hakika anarudi nyuma, anasema Imamu Ali : “Asiyejua anahadaika na nafsi yake, na siku yake inakuwa ni mbaya zaidi kuliko jana yake.” 171 Mwenye kuhadaika na hali yake unapungua ujanja wake,172 na majivuno yanazuia maendeleo.”173 Hakika kutarajia yaliyo bora zaidi, na kutarajia yaliyo mazuri zaidi, ndio kichocheo cha kwanza ambacho inachomoza kwacho harakati za kujadidisha na kubadilisha, wakati ambapo uzembe na kuridhia hali ya kujisalimisha 171

Al-Amadiy: Tamiymiy: Abdul-Wahdi katika Ghurar al-Hikami wa duraril-Kalami 172 Rejea iliyotangulia 173 Rejea iliyotangulia

222


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

kwake, au ghururi na majivuno kwa aliyoyapata, yanamfanya mwanadamu anabakia katika sehemu yake, wala hahifadhi juu yake, kisha anarudi nyuma. Hakika taasisi zenye kufaulu ni ambazo zinasimamia utekelezaji wake kwa mpangilio, na zinaweka mkakati kwa ajili ya kunyanyua kiwango na kuongeza juhudi na uzalishaji. Na mafunzo ya Kiislamu yanatuelekeza katika uelewa na matumaini ya daima, katika nyanja mbalimbali. Katika dua ya MakarimulAkhilaq ya Imamu Zainul-Abidiin Ali bin Husein ď „ kuna ukumbusho kwa mwanadamu kutafakari katika maendeleo, katika upande wa imani na maarifa na kazi, na yanakuja haya maelekezo katika muundo wa dua na maombi, anayoomba mwanadamu kutoka kwa Mola Wake, ili ajizatiti ndani ya nafsi yake. Anabadilika kwenye ratiba katika maisha yake, dua inasema: “Na ifikishe imani yangu katika ukamilifu wa imani, na jaalia yakini yangu iwe ni yakini bora zaidi, na ifikishe nia yangu kwenye nia nzuri zaidi, na amali yangu kwenye amali nzuri zaidi.â€? Na ibara za dua zinamaanisha kwamba kiwango chochote cha imani au yakini au nia nzuri na amali njema, hakimaanishi mwisho au kikomo. Unabakia upeo wa ukamilifu na maendeleo uko wazi mbele ya mwanadamu, ili kufikia yaliyo mazuri zaidi na yaliyo kamilifu zaidi na yaliyo bora zaidi. 2. Kujiamini: Mwanadamu anapoona mafanikio ya wengine na uvumbuzi wao, ni wajibu hilo limsukume kujiamini na kuelekea katika kuibua vipaji vyake na uwezo wake, kwani yeye ni mwanadamu mfano wao, anamiliki wanayoyamiliki miongoni mwa akili na matakwa kama walivyotumia akili zao. Na wametumia matakwa yao wakavumbua na wakafanikisha. Ni juu yake mfano wa hayo ili avumbue na azalishe. Hii ndio ratiba sahihi. Lakini baadhi ya watu ni kinyume cha hayo. Wanashangaa kwa mafanikio ya wengine hadi wanakosa kujiamini, na kudumaza akili zao na 223


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

vipaji vyao kiasi kwamba hawaoni kuwa nafsi zao zinaweza kuwa jirani na kufanana, ukiachilia mbali kuhusu kuwa juu na kuendelea. Na kwa haya zinasimama harakati na inashindikana kubadilisha na kujadidisha. Na mara nyingine kuvutiwa na waliotangulia, kama vile kizazi kilichotangulia, au shakhsiyati za kihistoria, kunaongeza kwake na hali ya kujitukuza na kujikuza, inakuwa ni uzio wa fikra baada yake na mpaka katika mafanikio haiwezekani kuipita na kuivuka. Na kutumia kusimama katika kiwango cha ufahamu wa waliotangulia, na njia ya maisha yao, au kutukuza shakhsiya iliyokuwa na utukufu, na dauru ya kihistoria yenye kusifika, hajasiri yeyote kuikosoa, au kukhalifu rai zake na nadharia zake. Hakika asiyekuwa maasumu, vyovyote utakavyokuwa uwezo wake na kipaji chake, yeye ni binadamu ana kikomo cha muda na wakati wake na mazingira yake, na juhudi zake hazizuii ijitihadi baada yake, na rai yake inatarajiwa humo kukosea na kupatia. Hakika watangulizi wa umma wema inapasa kuwaheshimu na kunufaika kutokana na rai zao na uzoefu wao, lakini haipasi kusimama kwenye mpaka wa fahamu zao. Mwenyezi Mungu amekwishatupa akili kama alivyowapa wao, na ametusemesha kwa wahyi Wake kama alivyowasema wao. Huenda baadhi ya rai zao au mbinu za muamala wao zilikuwa ni kutokana na mazingira yao, kama ambavyo mabadiliko ya maisha na mrundikano wa uzoefu, unaweza kutufungulia upeo au unafichulia mambo ambayo hayakuwa yanapatikana kwao. Na shakhsiya za uongozi katika nyanja za elimu na kazi, vyovyote kitakavyokuwa kiwango cha elimu yao au ukubwa wa elimu yao, hakika mmoja kati yao hamaanishi ni mwisho wa elimu, wala kikomo cha kazi, na “ni mangapi ameyaacha wa kwanza kwa mwengine� kama anavyosema mshairi wa Kiarabu. Na anasema mshairi mwingine: 224


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

“Hakika mimi hata kama ni wa mwisho katika zama zake, nitaleta ambayo hawakuyaweza waliotangulia.” Na yenye ukweli zaidi ni kauli Yake (swt):

َ

ُ َ َ

“ٌِ ‫… َوفىق و ِ ّل ري ِغل ٍ غلي‬..”

“Na juu ya kila mwenye elimu yupo ajuaye zaidi.” (Surat Yusuf; 12:76). Na kwa mfano katika dauru ya kutukuza shakhsiya na kushangazwa nayo kwa kiasi cha kusimama na kudumaa, tunaashiria katika waliyoyataja maulamaa katika maelezo ya Sheikhe Tusiy Muhammad bin Hasan, Mwenyezi Mungu amrehemu (aliyezaliwa mwaka 384H na kufariki mwaka 460 H), hakika kwa utukufu wa nafasi yake ya kielimu katika nafsi za wanafunzi wake na walio baada yake, ilishapita kwa mashia miaka mingi vizazi vingi na haikuwa rahisi kwa yeyote miongoni mwao kukosoa nadharia za Sheikh Tusiy katika fatwa, na walikuwa wanahesabu maneno yake ni msingi uliosalimika, na wanatosheka nao, na wanahesabu kukosoa utunzi wake na fatwa yake ni kujasiri mbele ya Sheikh na kumdharau. Na hali iliendelea hivyo hadi zama ya Sheikh Idrisa-Muhammad bin Ahmad bin Idrisa alHiliy aliyefariki mwaka 598 Hijiria – walikuwa wanamwita alMuqalidah, naye ni wa mwanzo kukhalifu baadhi ya fatwa zake na kufungua mlango wa kupinga nadharia zake.”174 Na kama si ushujaa wa Sheikh Ibnu Idrisi na kujiamini na kupinga hali ya kushangaza na kunyenyekea mbele ya Sheikh Tusiy, ilikaribia kufungwa mlango wa ijitihadi katika mazingira ya kidini na kielimu. 3. Mwanzo wa akili: Kuna uhusiano madhubuti baina ya harakati za mabadiliko na 174

Al-Amin: Sayid Muhsin katika A‟ayan Shaiati, Juz. 9, uk. 160 Daru Taaruf lilimatubuatai – Beirut 1986.

225


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

harakati za kufikiri. Ikiwa watu watakandamiza akili zao kwa hofu au raghaba, kutawaliwa na hali ya ukandamizaji na ugaidi wa kifikra, kiasi kwamba inamzuia mwanadamu katika akili yake kutoka nje ya yaliyozoeleka, au jamii kukataa rai mpya za mabadiliko, wala hauzipi fursa ya kuzitoa, kuzijadili na uzoefu, wakati huo utasimama mwenendo wa kujadidisha, wala hayatapatikana mabadiliko au mageuzi. Hakika uhuru wa kufikiri na rai ni haki ya msingi, ni kati ya haki muhimu sana za mwanadamu, kwayo anahisi mwanadamu utu wake na anaistawisha neema kubwa aliyopewa na Mwenyezi Mungu, na kupitia hiyo anaweza kuudhalilisha ulimwengu, na kujenga maisha ambapo Mwenyezi Mungu ametaka hayo kwake. Na Uislamu umezingatia kulinda uhuru huu na kuudhamini, na kuelekeza utekelezaji wake ili asitumbukie chini ya athari za hawaa na matamanio. Aya nyingi katika Qur‟ani tukufu zinamlingania mwanadamu kuhimiza kutumia akili yake na kutumia fikra yake katika nyanja na sekta mbalimbali, na katika mtiririko wa mazungumzo kuhusu ulimwengu na maisha katika mambo ya jamii na dini, na inajirudia kauli Yake (swt): “Je, hamtafakari” (Suratul-An‟am: 50). Na ikiwa dini inaamrisha kutafakari na kutumia akili, haiwezekani kamwe kuridhia kupokonywa uhuru wa kutoa rai au ugaidi wa kifikra. Ndio, kuna vidhibiti vya kuhami uhuru huu, kutokana na upuuzi wa wapuuzi na ufisadi wa waharibifu. 4. Ushujaa na ujasiri: Mwanadamu anaweza kufichua kosa la fikra kati ya fikra zake au nukta ya udhaifu katika baadhi ya nyenendo zake na vitendo vyake. Na anaweza kujua mfumo ulio bora zaidi, njia nzuri zaidi, katika jambo kati ya mambo ya maisha yake, lakini ushujaa na ujasiri unamfanyia hiyana na yanamteka mazoea aliyoyazoea, au inamchukua huzuni kwa dhambi - kulingana na maneno ya 226


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Qur‟ani tukufu – na hapa anapoteza kwa nafsi yake fursa ya mabadiliko na kujadidisha, na kuchagua kilicho sahihi zaidi na kilicho bora zaidi. Ni sahihi kwamba mazoea yana mbinyo wake na nguvu zake katika maisha ya mwanadamu, kama anavyosema Imamu Ali : “Mazoea ni mtawala kwa kila mwanadamu.”175 “Na siasa ngumu zaidi ni kuhamisha mazoea.”176 Lakini nguvu ya matakwa inaweza kukabiliana na mazoea, na mwanadamu mwelewa ni ambaye anatoa maamuzi yake kutoka katika mbinyo wa mazoea na nguvu zake. Anasema Imamu Ali : Zishindeni nafsi zenu kwa kuacha mazoea na pigeni vita matamanio yenu mtayamiliki”177 “Zidhalilisheni nafsi zenu kwa kuacha mazoea na ziongozeni kwenye utii ulio bora zaidi.”178 Na katika upande wa kijamii hakika baadhi ya jamii zinajipamba kwa upole unaotosha na zinamiliki ushujaa na ujasiri wa kubadilisha baadhi ya mazoea yao na ada zao, inapobainika kwao yaliyo bora kuliko hayo. Lakini jamii zingine zinajikanganya kwa ambayo zimeyazoea, hata kama hayo ni kwa hesabu ya misingi yake na maslahi yake. Na kwa mfano juu ya hilo baadhi ya mazoea yaliyoenea katika minasaba ya ndoa na maombolezo, ambayo yanatugharimu matumizi mengi na kusababisha taabu na uchovu, pamoja na kwamba watu wengi wanaona ni jukumu zito wanatamani kuondokana nalo, na kuna kukinahi nadharia kwa hiyo, lakini ushujaa na ujasiri haupatikani kwa kiasi kinachotakiwa kwa kubadilisha mazoea haya, na kuyabadilisha kwa kilicho bora na rahisi zaidi. Na vilevile baadhi ya jamii za ghuba zimekwishazoea muundo 175

Al-AmadiyTamiymiy: Abdul-Wahid katika Ghurarul-Hikami wa DuaraulKalimi 176 Rejea iliyotangulia 177 Rejea iliyotangulia 178 Rejea iliyotangulia

227


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

maalumu wa maisha ya utumiaji siku za neema ya kiuchumi – kama wanavyosema – pamoja na kwamba hali ya kiuchumi imeshabadilika na imekuwa inabana maisha ya wengi kati ya watu, isipokuwa mazoea ya muda uliopita bado yangali yanatawala mahala pake kwa ugumu wa kuyabadilisha na kuyavuka kwa namna ya jumla. Hizi ni alama nne: Uelewa, matarajio, kujiamini na kutumia akili, ushujaa na ujasiri ndio muonekano wa roho ya kujadidisha, ambapo zikienea katika maisha ya jamii zinaiongoza kwenye mabadiliko na mageuzi, na zikikosekana hakutofaa nembo na matamanio, wala mapendekezo na nadharia hazinufaishi. UWEZO WA KUHIJI NA KUPANGA VIPAUMBELE Hija ni anwani ya msimu wa kiroho na wa kijamii ambao wanaamiliana nao Waislamu wote, ambao idadi yao hivi sasa inakaribia watu bilioni moja katika sehemu mbalimbali za ulimwengu. Ni sahihi kwamba wanaoshiriki hasa katika ibada ya Hija ni watu milioni mbili, lakini wao wananasibiana na koo na makabila na jamii za Kiislamu, kama ambavyo mtazamo wa Waislamu wote katika msimu huu, unaelekezwa Makkah na sehemu takatifu. Na Hija ni anwani ya safari ya kimaada na kimaanawi, anaifanya mwanadamu Mwislamu, kwa roho yake, mwili wake, fikra zake na hisia zake, humo anakata masafa ya sehemu na wakati ili kwenda kuambatana na pazia la Kaaba, Nyumba ya kwanza iliyowekwa kwa ajili ya watu, na ili kugusa jiwe jeusi (yamini ya Mweneyzi Mungu katika ardhi), na ili aswali katika kisimamo cha Ibrahimu baba wa Manabii na ili afuate hatua za Mtume wa Uislamu Muhammad , ambapo amekulia ndani ya Makkah na amekuja na daawa yake kutoka katika pango la Hirai. Na ikiwa Hija maana yake ya kilugha: Ni kukusudia katika upande wa kutukuza. Na maana yake ya kisharia: ni kukusudia 228


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

nyumba ya Mwenyezi Mungu tukufu kwa ajili ya amali maalumu katika wakati maalumu. Kulingana na maelezo ya Abul-Baqai, hakika kimsingi ni katika mwonekano wa jumla wa kidini, na tangu zamani, inasema Mausuâ€&#x;atul-Arabiyatu al- Muyasarah: Hija imejulikana tangu zamani, na dini tatu za mbinguni zimelingania hivyo. Na vilevile imejulikana katika dini zingine kama vile dini ya kibaniani ambayo katika ibada zake za kidini ni kuhiji katika mto al-Ghanji (Ganges), ambao upo katika sehemu ya Kaskazini mwa India, unaotoka katika milima ya Himalaya, na kutirirka Kusini Mashariki na kumimina maji yake katika ghuba ya Bangali. Na kwa umashuhuri wa Hija kama hali ya kidini ndipo imejulikana taarifu yake katika rejea za kiutamaduni na maktaba za maarifa kwamba: Ni safari ya kwenda kwenye sehemu takatifu kwa lengo la kidini. Na kwa malengo ya kidini ambayo wanayakusudia wenye dini katika kufanya Hija yanatofautiana kwa kutofautiana itikadi.179 Falsafa ya Hija: 1. Amali za Hija na ibada zake zinamfunza mwanadamu juu ya kumnyenyekea Mwenyezi Mungu Mtukufu, katika anayoyaamuru na kukataza, na yanatia mkazo katika wakati huo huo utumwa na kutii amri zake tukufu, kwa aina zake na namna zake. Na vyovyote itakavyolazimu katika taabu na adha, na hata kama mwanadamu hakujua makusudio yake na malengo yake moja kwa moja. Kuanzia na kitendo cha kuvaa ihramu, ambapo mwenye kuhiji anavua aliyokuwa ameyazoea katika mavazi yake ili avae vipande viwili vya ihram, shuka la chini na la kujilinda, na kisha anaachana na makatazo ya ihramu, ambayo yanakaribia 25, kwa ikhitilafu katika baadhi yake na katika ufafanuzi wake mingoni mwa mafakihi wa Kiislamu, na kuanzia na tawafu ya wajibu, saâ€&#x;ayi, kupunguza au kunyoa, kutupa mawe, kuchinja au nahri, kusimama Arafah ndani ya muda maalumu, na vile vile Muzdalifa, kulala Mina na mengine miongoni mwa ibada za Hija 179

Al-Fadhiliy: Dr. Abdul-Hadiy katika Mabaadiu ilimil- fiqihi, Juz. 3, uk. 4

229


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

na vipengele vyake, ambazo zinatengeneza kwa ujumla wake semina ya mafunzo yanayomlea mwanadamu katika utiifu na unyenyekevu kwa Muumba Wake katika mas‟ala ya wakati na sehemu, na ambayo yanafungamana na mwili wake na harakati zake na shughuli zake na kazi zake zingine. Anasema Imamu Ali : “Amefaradhisha kwenu kuhiji katika nyumba Yake tukufu, ambayo ameifanya ni kibla cha wanadamu, na akaifanya (swt) ni alama ya unyenyekevu wao kwa ajili ya utukufu Wake na utii wao kwa ajili ya utukufu Wake.180 2. Na Hija ni mafungamano na kuungana na mwenendo wa kiimani katika upeo wa kiimani na sehemu, na vielelezo na uongozi wa kihistoria, na hivyo dini haiwi ni itikadi ya kinadharia tu, bali ni harakati yenye kuendelea kupitia historia. Anafungamana nayo Mwislamu, anaona nafasi ya kuanzia na anaishi pembozoni mwa mwanzo wa dini yake, na anatembelea sehemu ambazo zimeshuhudia matukio yake ya kihistoria, na kuvuka zama na kuungana na maisha ya Manabii, na sira ya Maimamu na Mawalii, na misimamo ya masahaba na salafi wema. Kuna kisimamo cha Ibrahim, Hajar Ismail, kuna sa‟ayi, sehemu aliyozaliwa Muhammad . Na katika pango hili – pango la Hirai – ulikuwa ni mwanzo wa kushuka wahyi na utume wa Nabii. Na kuna sehemu aliyojificha Mtume wa Mwenyezi Mungu, pango la Thaur – pamoja na sahaba wake Abu Bakri wakati wa kuhama kwake kwenda Madina. Na kuna sehemu ya ushujaa wa Ali bin Abi Twalib; Badri, Uhud, Khaibar na Khandaq. Na kuna kujitolea kwa masahaba mashahidi wa kwanza wa Kiislamu. Na anaashiria kwenye hekima hii Imamu Ja‟far Swadiq  katika hadithi yake juu ya Hija ambapo anasema: “Na ujue athari za Mtume wa Mwenyezi Mungu na ujue habari zake na ukumbuke na wala usisahau.”181 180 181

Al-Musawiy: Sharifu Ridhaa katika Nahjul-Balaghah, khutuba 1 Ibnu Babawaihi al-Qummiy: Sheikh Suduq, katika Ilalu Sharai, uk. 406, al-Maktabatu al-Haidraiya – Najafu 1963.

230


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

3. Na katika Hija inaonekana mbele ya Mwislamu ulimwengu wa Kiislamu, na anahisi kujinasibisha kwake katika umma mpana wa Kiislamu, ambapo anatekeleza ibada ya Hija ndani ya kundi kubwa la binadamu, kutoka katika koo mbalimbali na mataifa, wananchi, makabila, madhehebu na mitazamo mbalimbali ambapo wanakusanywa na uzio wa Uislamu, na wanaunganishwa na nembo zake na misingi yake na nguzo zake. Na Mwislamu anaweza kuishi katika nchi yake na miongoni mwa kaumu yake, hivyo hajui upana wa duara la Uislamu, wala aina ya jamii za Kiislamu katika uhusiano wake na madhehebu zake. Lakini katika Hija anaona aina hii na idadi hii chini ya bendera moja na katika bendera moja ya Kiislamu. Wote ni Waislamu wanatufu katika Kaaba moja na wanaielekea hiyo katika swala zao, na wanakariri wito wa kuitikia amri za Mwenyezi Mungu: Labaika Allahumma Labaika, na wanafanya ibada ya pamoja. Sisi ni sehemu ya umma mkubwa unaoishi katika aina mbalimbali ndani ya msingi mmoja, wala hauathiri uhusiano huo wa kijamii na kimadhehebu juu ya ukweli wa ummoja wa umma, na kukusanyika kwake katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah ya Nabii Wake . 4. Na Hija ina manufaa yake na chumo lake kubwa katika nyanja zote za maisha ya umma kisiasa, kiuchumi, na kijamii. Kwa hiyo anazungumza Muumba Mtukufu kuhusu manufaa ya Hija kwa namna ya wazi kabisa anasema:

ُ ُ ٰ َ َ ً َ َ ‫احد ّج َي‬ َ ‫” َو َأ ّرن فى ال ّ اط ب‬ ‫ضام ٍش َيأجحن ِمن و ِ ّل‬ ‫أجىن ِسجاال وغ‬ ِ ‫هى و ِ ّل‬ ِ ِ ِ ِ ِ َ َ ٰ َ َ َ َ ُ “….. ُ‫﴾ ِليشُذوا م ك ِفؼ ل‬٧٧﴿ ‫ميم‬ ِ ٍ ‫ف ٍ ّج َغ‬ “Na watangazie watu Hijja; watakujia kwa miguu na juu ya kila mnyama aliyekonda kutoka kila njia ya mbali. Ili washuhudie manufaa yao.” (Surat Al-Hajj; 22:27–28). 231


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Na nakra ya (manaafiu) ni kwa ajili ya kutukuza na makusudio yake ni wingi nayo ni maslahi ya kidini na kidunia.182 Na Rabiu al-Khaitham anamuuliza Imamu Ja‟far Swadiq  kuhusu kauli yake (swt): “Ili washuhudie manufaa yao,” manufaa ya kidunia au ni manufaa ya Akhera? Akasema: Yote. 183 Sharti la kuweza: Ikiwa ibada na faradhi zingine za Kiislamu anazitekeleza mwanadamu akiwa katika nchi yake na sehemu yake, hakika faradhi ya Hija inamlazimu kusafiri, kutembea na kusogea. Kwa hiyo Mwenyezi Mungu Mtukufu amefaradhisha mara moja katika umri, ambapo ni wajibu kwa kila Mwislamu mwenye taklifu kuitekeleza faradhi ya Hija hata kama anaishi mbali sana na Nyumba Tukufu. Lakini hayo ni kwa sharti la uwezo na kuweza, anasema (swt):

ً

َ َ

َ

ّ

َ

‫ى‬

َ َ َ “….. ‫بيًل‬ ِ ‫يذ َم ِن اظخطاع ِإل ِيه َظ‬ ِ ‫اط ِحج الب‬ ِ ‫… و ِلل ِكه غهى ال‬..” “…..Na ni haki ya Mwenyezi Mungu juu ya watu kuhiji Nyumba hiyo kwa mwenye kuweza njia ya kuiendea …..” (Surat Aali-Imran; 3:97). Na ikiwa uwezo kilugha unamaanisha kuweza kufanya kitu au kujizuia nacho, ila hakika hapa inakusudiwa uwezo mahsusi. Hiyo ni kwa kuwa uwezo unamaanisha kumiliki nguvu ya kufanya kitendo au kujizuia nacho. Na ikiwa hilo linalazimu ugumu na taabu, lakini kuweza ni uwezo ambao hauchanganyiki 182

Ibnu Ashuru: Muhammad Twahir katika Tafsir Tanuwir wa Tahariri, Juz. 17, uk. 178 183 Al-Kulainiy: Muhammad bin Yaaqub katika Furuu‟u al-Kaafiy, Juz. 4, uk. 422 Darul-Adhuwai - Beirut.

232


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

na ugumu wala taabu, kama alivyoashiria hilo Sharifu Murtadha kwa kauli yake: “Uwezo ni neno la kuashiria kurahisisha jambo na kuondoka taabu humo, na sio kwa neno la kuweza tu.â€?184 Na jopo la maulamaa linaona kwamba uwezo unapangwa na jamii, na ndio ambao unakadiria kwamba mukalaf ni mwenye kuweza au sio mwenye kuweza. Na hiyo ni kulingana na hali ya mtu na mazingira yake ya kijamii, makusudio ya kuweza ni ule wa maana ya jamii unaofahamika katika neno hili, na sharia haina maana maalumu, wala istilahi mpya, bali makusudio ni maana ya jamii ambayo inatumika katika sehemu zingine.185 Na uwezo unajumuisha upana wa wakati ili utoshe kwenda katika sehemu takatifu na kuwahi siku za Hija, afya ya mwili na uwezo wake, kupatikana amani na usalama na uwezo wa kimali. Kupanga vipaumbele: Kwa kutafakari katika masâ€&#x;ala ambayo wanayataja mafakihi kuhusu maudhui ya kuweza, kama sharti la wajibu wa Hija kwa mukalaf, inabainika kwetu kadhia muhimu, nayo ni ulazima wa kupanga vipaumbele katika maisha ya mwanadamu. Mbele ya mwanadamu kuna majukumu mengi, na haja na raghba mbalimbali. Na baadhi ya watu hawana vidhibiti vinavyopangwa kwa msingi wake vipaumbele vya mazingatio yake na mielekeo yake, bali inavutia raghba maalumu au inaendeshwa na mazingira yanayomzunguka, na hivyo anaelekea kwenye jukumu kulingana na lililo muhimu au katika jambo la pembezoni kulingana na mambo ya msingi, na linatokea hilo katika upande wa kutoa juhudi ya kifikra au kutoa mali au harakati ya kivitendo. Wakati ambapo sharia inatuelekeza kutanguliza la muhimu zaidi 184 185

Al-Fadhiliy: Abdul-Hadiy katika Mabaadiu ilimil-fiqih, Juz. 3, uk. 15 Shiraziy: Sayid Muhammad al-Huseiniy katika al-Fiqihi, Juz. 38, uk. 10 chapa ya pili 1988 Darul- Ulumi - Beirut

233


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

katika ya muhimu, nayo ni katika kanuni za kifiqihi ambazo wanazitegemea mafakihi na katika kipaumbele cha faradhi cha wajibu kwa Sunnah ya mustahabu. Anasema Imamu Ali : “Hakuna kujikurubisha katika Sunnah inapodhuru faradhi.”186 Sunnah zikidhuru faradhi basi zikataeni.”187 Na pengine tunayoyaona katika upande wa kiuchumi – kwa mfano – kwa baadhi ya watu katika kutoa katika ukamilisho na mambo ya starehe kulingana na mambo ya kimsingi, ni mfano uliowazi wa kughafilika juu ya ukweli huu. Dharura ya maisha: Katika daraja la kwanza ni wajibu mwanadamu azingatie kupatikana mahitaji ya maisha yake kimaisha; chakula, mavazi, malazi, kuoa, matibabu na mahitaji mengine ambayo yanaweza kutofautiana kwa kutofautiana jamii na kiwango cha watu na mambo yao. Na mwanadamu akishindwa kupata kitu katika dharura ya maisha yake hakika ni juu ya jamii kumsaidia katika hayo ili kutatua haja yake. Na kwa hiyo mafakihi wametoa fatwa kutopatikana uwezo na wajibu wa Hija ikiwa itakuwa kwa hesabu ya dharura ya kimaisha, anasema Sayid al- Yazidiy: “Inatolewa katika hayo anayoyahitajia katika dharura ya maisha yake, hivyo haiuzwi nyumba yake ya kuishi inayofaa kwa hadhi yake, wala mtumishi wake anayemhitajia, wala nguo zake za kujipamba zinazofaa kwa hadhi yake, ukiachilia mbali nguo za kazi yake. Wala samani ya nyumba yake; godoro, vyombo na mengineyo kati ya anayoyahitajia. Bali hata pambo la mwanamke pamoja na kulihitajia kwa kiwango kinachofaa kwake kulingana na hali yake, katika zama zake na sehemu yake. Wala zana za utengenezaji anazo186 187

Al-Musawiy: Shariff Ridhaa katika Nahjul-Balaghah, hikimati namba 39 Rejea iliyotangulia hikima namba 279.

234


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

zihitajia katika maisha yake, wala farasi anayempanda pamoja na kumhitajia, wala silaha yake wala vitu vingine anavyovithitajia, kwa kulazimu taklifu kwa kuvitumia kwake katika hija kwa dhiki na shida. Wala haizingatiwi humo haja ya kivitendo, ndio kama vitazidi vitu vilivyotajwa katika kiwango cha haja ni wajibu kuuza ziada katika matumizi ya Hija.”188 Na anasema katika mas‟ala mengine: Ikiwa ana kiasi kinachomtosheleza kuhiji na nafsi yake ikahitajia kuoa, iliyo na nguvu ni kutokuwa wajibu wake juu ya hija – na kuacha kuoa ni dhiki kwake au inasababisha kutokea maradhi au kutumbukia katika zinaa na mfano wake.”189 Na anasema Sayid al-Khuiy: “Kureja kwenye kutosheleza nako ni kuweza kwa kitendo au kwa nguvu katika kuishi nafsi yake na familia yake baada ya kurejea. Na kwa maneno yaliyo wazi zaidi inalazimu mukalafu awe katika hali isiyoogopesha pamoja na nafsi yake na familia yake kushindwa na ufakiri, kwa sababu ya kutumia aliyonayo miongoni mwa mali katika njia ya Hija.”190 Haki za watu: Na kwa daraja la pili inapasa kwa mwanadamu kutekeleza anayodaiwa na watu katika haki za kimali. Na msingi kubakia deni au haki katika dhima ya mwanadamu ni jambo baya linalokera. Hakimbilii katika deni ila kwa dharura ya kuhitajia, na ni juu yake kujitolea kuitekeleza kwa haraka kadri iwezekanavyo. Na imepokewa hadithi kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu : “Jihadharisheni na deni, hakika ni huzuni usiku na ni udha188

Al-Yazidiy: Sayid Muhammad Kaadhim katika al-Uruwatu al-Wuthiqah, mas‟ala ya 10 Minal- istitwaati 189 Rejea iliyotangulia, mas‟ala ya 14 190 Al-Khuiy: Sayyid Abul-Qasim katika Manaasik al-Haji, mas‟ala 22 chapa ya nane 1397

235


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

lili mchana.”191 “Mwenye deni amefungwa katika kaburi lake, hafunguliwi ila kwa kulipa deni lake.”192 Na kinachosikitisha ni kwamba watu wengi wanapuuza katika maudhui ya madeni na haki za wengine, wakati ambapo wanatumia mali nyingi katika mambo ya starehe na mambo ya kujipamba (pembezoni). Mafakihi wamezingatia deni ni kizuizi cha wajibu wa Hija, na kwamba kipaumbele ni kulipa deni. “Ikiwa mtu ana mali inayotosha kwa ajili ya Hija, lakini anadaiwa kiasi kwamba kama atalipa deni lake hatoweza kuhiji, na kama akihiji hatoweza kulipa deni lake, hakika sio wajibu kwake Hija. Ni sawa sawa kama mdai amemdai wakati huo au baadaye, kabla ya kupata hayo au baada ya kupata.193 Haki za kisharia: Haki za kisharia za kimali ambazo ni wajibu kwa mwanadamu, kama vile Zaka, Khumsi, Kafara, ni haki za Mwenyezi Mungu Mtukufu katika upande mmoja, kwa sababu amezifaradhisha. Na ni haki za watu katika upande mwingine, kwa sababu zinafungamana na haki za makundi dhaifu na yanayostahiki katika jamii. Na ikiwa mwanadamu atapuuzia katika kutekeleza haki za kisharia, hakika anakuwa amefanya uadui katika haki za Mwenyezi Mungu na haki za mafakiri na wenye kuhitaji. Kwa ajili hiyo mafakihi wametoa fat‟wa katika kipaumbele cha kutekeleza haki za kisharia kwanza kabla ya kutekeleza faradhi ya Hija, bali kama akihiji kwa mali ile ile isiyotolewa Khumsi au Zaka basi Hija yake haisihi na wala faradhi haitaondoka kwake, bali ni mwenye dhambi katika kutumia kwake haki za wengine. Hivi ndivyo zinavyotufundisha hukumu za kisharia kuchunga 191

Al-Hindiy: Ali al-Mutaqiy katika Kanzul-Umaal, Juz. 6, uk. 232 Rejea iliyotangulia 193 Shiraziy: Sayyid Muhammad al-Huseiniy katika Manaasik al-Haji, mas‟ala 43. 192

236


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

daraja za vipaumbele, na kutanguliza la muhimu zaidi kabla ya lile la muhimu, pamoja na utukufu wa Hija na nafasi yake, ambapo Mwenyezi Mungu amezingatia kuiacha kwake ni ukafiri: “Na mwenye kukufuru hakika Mwenyezi Mungu ni tajiri kwa walimwengu,” ila ni kwamba haifuti vipaumbele vingine, wala haiwi kwa hesabu yake. Ewe Mwenyezi Mungu tupe taufiki ya kuhiji katika Nyumba Yako tukufu, na wafanyie wepesi mahujaji kutekeleza ibada ya Hija, na wakubalie amali zao na warejeshe kwenye nyumba zao salama salimini, na utushirikishe katika dua zao njema. Ewe Mola wa walimwengu. KANISA: HISTORIA YA DHULUMA KWA JINA LA DINI Hakika sheria za mbinguni na dini za Mwenyezi Mungu zimekuja ili kuleta uadilifu katika maisha ya mwanadamu na kupambana na dhulma na ujueri:

ٰ َُ َ َ َ َ​َ َ ‫اوحزان ل َي‬ ُ َ َ َ َ​َ ٰ َّ ‫لىم‬ ‫الىخك َب َو‬ ِ ِ ُ​ُ ‫”للذ أسظل ا ُسظل ا ِبالب ِي ك ِذ وأ ضل ا مػ‬ ُ ّ ‫ال‬ “….. ‫عط‬ ِ ِ ‫الل‬ ِ ‫اط ِب‬ “Kwa hakika tuliwatuma Mitume Wetu kwa dalili waziwazi, na tukateremsha Kitabu pamoja nao na mizani, ili watu wasimamie uadilifu…” (Surat Al-Hadid; 57:25) Na hakuna kitu kibaya baada ya kumshirikisha Mwenyezi Mungu Mtukufu kuliko dhulma na kuzifanyia uadui haki za watu. Huo ndio msingi wa daawa za Manabii na Mitume. Lakini masikitiko ni kwamba baadhi ya wanaojidai kuwa ni wanadini, wanatumia fursa ya nafasi zao za uongozi na utashi wa matamanio yao ya utawala na shahawati zao za kimaslahi kwa hesabu ya heshima ya watu, uhuru wao na haki zao. Wanafanya 237


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

dhulma na uadui kwa jina la dini, chini ya bendera yake na nembo yake. Na hiyo ni kwa kisingizio cha ujeuri wao na kuwapotosha watu na kuwadhalilisha kwao. Na ikiwa dhulma ni mbaya kwa kila aina zake na sura zake, hakika iliyo mbaya zaidi na uovu zaidi ni inayokuwa kwa jina la dini, kwani changamoto inayokanganya katika jambo la Mwenyezi Mungu, mosi ni kumzulia uwongo Mwenyezi Mungu:

َ َ ُ ‫ى‬ َ​َ َ َ‫ى‬ ‫دشاءِ أجلىلىن َغهى الل ِكه ما ال‬ ِ​ِ ‫”كل ِإ ىن اللكه ال َي ُأم ُش ِبالف‬ َ َ َ ّ َ​َ ُ “….. ‫عط‬ ِ ِ ‫الل‬ ِ ‫حػلمى‬ ِ ‫﴾ كل أم َش َسبش ِب‬٧٨﴿ ‫ن‬ “…..Sema: Hakika Mwenyezi Mungu haamrishi machafu; je, mnasema juu ya Mwenyezi Mungu msiyoyajua? Sema Mola Wangu ameamrisha uadilifu…..” (Surat Al-A‟araf; 7:28–29). Na pili ni kufanya uovu kwa waja Wake. Na wanadamu wameteseka sana kwa aina hii ya dhulma, ambayo inafanywa kwa kivuli cha dini, jambo ambalo limezua kulipiza kisasi kwa baadhi ya jamii dhidi ya asili ya dini, na kutengeneza kundi la ulahidi linalotuhumu dini kwamba ni ulevi wa wananchi. Na hivi ndivyo inavyokuwa, kutumia dini ni kutayarisha mazingira ya ulahidi na ukafiri. Na kanisa katika historia yake ndefu linawakilisha mfano wazi katika kutumia dini na kufanya dhulma kwa jina lake na chini ya nembo zake, kwani linanasibishwa kwa Nabii mtukufu wa Mwenyezi Mungu Isa bin Mariyam  na kutawala sehemu kubwa na uwanja mpana wa kidini kwa binadamu. Kanisa hili kwa kuzingatia kwamba ni rejea ya dini ya Masihi, na taasisi ambayo inachunga mambo ya wafuasi wa dini, limetumia vibaya nafasi yake. Badala ya kueneza upendo na uadilifu na kutetea waliodhulumiwa na wanyonge, na kupiga vita ujeuri na dhulma, 238


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

kama ulivyo msingi wa ujumbe na dini za mbinguni, ikawa ni kinyume cha hivyo kabisa. Msamaha wa Papa: Kimeongezeka kiwango cha uelewa na maarifa kwa watu, na ukweli umeendelea kafahamika. Watu wa kanisa hawanyenyekei tena na kupotoshwa kama mwanzo, bali zimefululiza humo harakati za malalamiko na sauti zikapaa za ukosoaji na upinzani. Na katika upande mwingine hakika wananchi wengine na jamii zilijaa ukandamizaji, dhulma na ujeuri, na zilirejesha kujiamini, na kuanza kudai haki zake na kurejesha mazingatio ya historia yake. Yote hayo yalikuwa ni sababu iliyomsukuma Papa Paulo kukiri baadhi ya makosa na kuomba msamaha, na kuomba radhi na maghfira, kuhusu historia mbaya ya kanisa. Kujitolea huku kwa kanisa kumekuja kwa ajili ya kujibu mbinyo wa ndani na wa nje, ambapo kuliundwa kamati ya makasisi wanane waliofanya kazi kwa muda wa mwaka kamili, kuandaa utafiti wa kurejea makosa yaliyopita katika kanisa na kutoa ripoti kwa Papa yenye kurasa 46, na kuamua baada yake kufanya sherehe maalumu Jumapili iliyopita 12/3/2000 ambayo iliitwa siku ya kusameheana, kutangaza ripoti na kutangaza kuomba msamaha na udhuru kutoka kwa Papa. Ilifanyika hafla kubwa ya kidini (ibada) katika kanisa takatifu la Petro Vatikan, kwa kuhudhuria idadi kubwa ya viongozi wa Italia na wanadiplomasia na watu wengi zaidi ya elfu ishirini takriban ndani ya kanisa na katika uwanja rasmi wa Vatikani. Ripoti inakiri kwamba pamoja na uovu na ubaya uliotokea katika historia ya kanisa: “Haikuja katika historia ya kanisa wito wowote wa kutubia na kupinga makosa na kuomba msamaha, na kwamba jaribio bora katika nyanja hii, lilikuwa linaishia kuwasifu makasisi ambao kulifanywa katika zama zao baadhi ya makosa, kwamba wao walikuwa nje ya ibada na mafunzo ya 239


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

kanisa, na wakafungamanisha makosa haya kwa watu wake bila ya kanisa lenyewe.�194 Ubabe wa ugomvi wa kimadhehebu: Ripoti ilizungumzia juu ya ubabe wa ugomvi wa kimadhehebu, na ukali wa mfarakano ambao ulitokea baina ya wafuasi wa kanisa Katholiki: “Kulitokea ikhitilafu kubwa baina ya wakristo na hususan katika karne inayomalizika. Katika mwanzo wa karne iliyopita (1054) ilijitokeza ikhitilafu kali baina ya kanisa la Mashariki na kanisa la Magharibi, na ikaendelea kwa muda mrefu na likaparaganyika kwa uadui. Na wakatuhumiana, na kukakosekana kuaminiana. Na angalizo ni kwamba kati ya vikwazo ambavyo vinasimama dhidi ya umoja wa wakristo ni sababu za kiutamaduni na mambo ya kihistoria na kasumba ambazo zinasheheni ikhitilafu miongoni mwa wakristo.195 Hakika ni ishara ndogo tu katika ambayo walikabiliwa nayo wakristo kutoka kwa uongozi wa kanisa lao, ambapo kanisa liligawanyika lenyewe na madhehebu ya kikristo yakawa mengi: Wakatholiki, Othodox na Waprotestanti. Na viongozi wa kanisa na madhehebu wanachochea wafuasi wao dhidi ya makanisa mengine, na wafuasi wa madhehebu mengine. Mfalme wa Kiitaliano alipoingia katika ukristo katika mwanzo wa karne ya nne na akajiunga na rai za Paulo, ambaye alikuwa myahudi mwenye kasumba dhidi ya unaswara, na mshirika katika kuwapiga vita, lakini yeye aligeuka ghafla kwenda kwenye ukristo kwa kudai kwamba yeye amekutana na Masihi. Na amekuwa mlinganiaji wa ukristo anayejulikana kwa jina la Mtume Paulo, mwasisi wa ukristo mpya, unaosimama katika kumfanya Masihi kuwa mungu na utatu, na akakandamiza rai pinzani ndani ya Wakristo. 194 195

Bayaanati al-Fatikani: tovoti ya Vatican katika intaneti Rejea iliyotangulia

240


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Alipopinga Arius mwaka 336 kauli ya uungu wa Masihi, lilifanyika kongamano la kanisa la kwanza ambalo lilijulikana kwa jina la kongamano la Nikai mwaka 325, na kuamua kumtuhumu Arius na kuchoma kitabu chake, na kuharamisha kukinunua, na kuwavua wafuasi wake nyadhifa zao na kuwafukuza, na kuhukumiwa kunyongwa kila mwenye kuficha kitabu chake. Na yalidhihiri madhehebu ya Protestant katika Ukristo, kwa kupinga rai iliyoenea katika kanisa la Kikatoliki. Na maana ya Protestant kwa kilatini ni: Mpinzani. Kanisa liliwakabili kwa ubabe na ukandamizaji, na mauji yakawa mengi, na yaliyo muhimu zaidi ni mauaji ya Paris 24/8/1572, ambapo wakatoliki waliwachapa fimbo wageni wao wa Kiprotestant ambao waliitwa Paris kuleta ukuruba baina ya mitazamo, kisha wakauliwa kwa hiana na wao wakiwa wamelala, na damu zao zikatiririka katika barabara za Paris. Na pongezi zikamiminika kwa Charles IX wa Ufaransa kutoka kwa Papa, wafalme wa katoliki na wakuu wao kwa kitendo hiki kiovu!! Na cha ajabu ni kwamba waprotestant walipopata nguvu walifanya uovu ule ule uliofanywa na wakatoliki, na hawakuwa ni wachache wa uovu katika muamala na maadui zao. Na kanisa la katoliki lina wakristo wengi zaidi, nalo linabeba jukumu la msingi la kukandamiza madhehebu mengine yenye watu wachache, na kukandamzia rai pinzani katika kufasiri kwake dini. Ugaidi wa kifikra: Kanisa lilifuata katika zama za kati rai za Aristotle na Ptolemy myunani katika mazingira na anga. Na wakayaita Jiografia ya Kikristo, na wakafanya kazi ya kuilazimisha kwa watu kwa kuizingatia ni itikadi ya kidini, na kwamba kinachoikhalifu ni ukafiri na uasi katika dini. Na zikaanzishwa mahakama za 241


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

upekuzi mwaka 1183, kwa kuwauliza watu kuhusu rai zao katika mambo ya mazingira na ulimwengu, na kumwadhibu mwenye kukhalifu miongoni mwao. Na inakadiriwa idadi ya watu ambao waliaadhibiwa na mahakama hizi ni watu 300,000, kati yao 32,000 walichomwa moto wakiwa hai, miongoni mwao ni mtaalamu wa mazingira maarufu kwa jina la Giordano Bruno, ambaye alihukumiwa kuuliwa, na kwamba lisimwagike tone la damu yake juu ya ardhi, hivyo akachomwa akiwa hai mwaka 1600. Na vilevile alihukumiwa kuuliwa mtaalamu wa anga wa Kitaliano, Galileo Galilei mwaka 1642 kwa sababu alisema rai yake kuhusu kuzunguka kwa ardhi na kulizunguka kwake jua. Ukandamizaji na ukoloni: Ripoti ya kuomba msamaha iliashiria baadhi ya mateso ambayo yaliwapata wengi katika wananchi na jamii nyonge, miongoni mwa nguvu ya Ulaya na wamagharibi, ambayo ilikuwa inafanya uovu wake na utawala wake wa kikoloni chini ya mtazamo wa kanisa na uangalizi wake na kubariki kwake. Wahindi wekundu, nao ni wakazi wa asili wa Amerika, ambao walihamia kutoka Asia kabla ya zaidi ya miaka 20,000, kulingana na makadiro ya wataalamu, lakini wazungu weupe walipoigundua Amerika na utajiri wake walikuja kuikalia na wakaingia katika vita ya muda mrefu na kali na Wahindi wekundu, iliyomalizika mwaka 1900 kwa kuwaangamiza na kupora ardhi zao. Na kuwafukuza na kuwakandamiza waliobakia miongoni mwao. Idadi ya Wahindi wekundi Amerika ilikuwa ni zaidi ya watu milioni moja, na katika mwisho wa vita vya maangamizi idadi yao ilipungua hadi 237,000!! Na Waafrika walikuwa wanashambuliwa na meli za kijeshi na za kibiashara za wazungu na kuwakandamiza kama wanyama bila ya huruma au utu. Mtoto anaporwa katika mapaja ya mama yake na ndugu anaporwa mbele ya ndugu zake, na kuchukuliwa kama mateka hadi Ulaya. Wanauzwa na wananunuliwa, na wana242


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

watumikisha katika kuwahudumia wazungu weupe kwa unyonge na udhalili. Na kwa kuingia karne ya 19 wazungu walikuwa wameshapeleka Amerika watumwa milioni kumi wa Kiafrika!! Kama ambavyo kanisa lilifurahia ukandamizaji wa Wayahudi na kuteketezwa kwao na Wanazi, na kwa kuitikia mbinyo wa Kiyahudi kimataifa, mazungumzo kuhusu kadhia yao yamekuja wazi kuliko kadhia nyingine yoyote katika ripoti ya kuomba msamaha. Ama mateso ya wananchi wa Kiislamu kutokana na uovu wa wazungu katika vita vya msalaba, mateso yaliyobarikiwa na kanisa, hayakuja mazungumzo yake, pamoja na kwamba yalikuwa ni mateso mabaya na ya muda mrefu, ambapo wazungu walipanga mashambulizi manane makuu ya kijeshi. Na yakaendelea kwa zaidi ya miaka 200 kuanzia mwaka 1096 hadi 1270, kwa kuiteka Palestina na viunga vyake kati ya nchi za Kiislamu. Mfalme wa Italia Alexios I Komnenos, mwaka 1095 aliomba msaada kutoka kwa Papa Urban wa pili, Papa wa kanisa la katoliki, katika vita vyake dhidi ya Waturuki, na Papa akaafiki katika hilo. Papa alifanya mkutano wakati wa kipupwe wa viongozi wa kanisa huko Ufaransa. Alihimiza humo wazungu kusimamisha vita baina yao, na kuteka ardhi takatifu ya Palestina na akawaahidi malipo ya kiroho na kimaada mkabala wa vitendo vyao, na akachochea raghba katika kuipiga vita Ulaya Magharibi. Maelefu yakajiunga na jeshi la wavamizi. Na yalitokea kutokana na ukoloni wa nchi za kimagharibi katika nchi nyingi za Kiislamu baada ya kuanguka ukhalifa wa Uthmaniya. Na kilichotokea katika hayo miongoni mwa ujeuri, hayakuwa ni yenye kufichikana kwa kanisa wala hayakuwa mbali na baraka zake. Na kuishi Wazayuni waporaji ndani ya nchi za Kiarabu na za Kiislamu, kuhami kwake na kuunga kwake mkono katika uwepo wake na uadui wake, sio kingine ila ni muonekano kati ya muonekano wa njama na chuki ya kimagharibi dhidi ya Uislamu na Waislamu. 243


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Somo na Mazingatio: Qur‟ani tukufu imetufundisha kwamba mazungumzo kuhusu dhulma na ufisadi wa umma zingine, ni wajibu yawe ni chimbuko la kutafakari na mazingatio. Na kufaidika na mafunzo na uzoefu kutokana na mabadiliko ambayo yalikumba umma zingine, ili tujiepushe na yale ambayo walitumbukia humo miongoni mwa makosa. Na kwa hiyo Qur‟ani imezungumzia juu ya Ahlul-Kitabu kwa kushiriki kwao pamoja na Waislamu katika kujiunga na ujumbe wa mbinguni, na kumwamini Nabii aliyetumwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Imekuja katika mazungumzo kuhusu Ahlul-kitabi kwa jina hili, katika zaidi ya aya 32 katika Qur‟ani, kama ambavyo yamekuja mazungumzo kuhusu Wayahudi mara 18 takriban, na kuhusu Manaswara mara 15 takriban. Ili Qur‟ani kuhadharisha Waislamu waliyoyafanya Wayahudi na Manaswara katika dini yao, ambapo waliipotosha na kuichezea na wakatumia anwani ya dini na nembo zake vibaya. Na kiongozi wa kanisa anapokiri makosa yaliyopita kwa kifupi na kwa muhtasari, na kuomba msamaha na maghufira juu ya historia yenye giza, hakika hilo ni wajibu taasisi zetu zote na pande zake za kidini kuwa makini na kujihadhari kwa uelewa na kuwa macho, ili Uislamu usipakwe matope kutokana na vitendo vyake na harakati zake. Dhulma inapelekea kumghadhibisha Mola na kuwakasirisha watu, kwa namna yoyote itakavyotokea, na kwa upande itakaotokea. Na Uislamu ni dini ya uadilifu na haki, ni wajibu kurasa zake ziwe safi zenye kuangaza na kumeremeta.

UIMAMU BAINA YA TAMKO NA SHURA Waislamu Sunni na Shi‟ah wanaafikiana katika kumwamini Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwa ni Mungu mmoja na hana mshirika, na kuamini unabii wa Nabii Muhammad  na 244


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

kwamba yeye ni hitimisho la Manabii na Mitume, na kuamini ufufuo, miadi na siku ya Kiyama. Na wote wanaamini Qur‟ani moja iliyoteremshwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Ndio, huu msahafu mtukufu uliopo baina ya Waislamu, bila ziada wala upungufu. Na kwamba Qur‟ani na Sunnah ndio chimbuko la dini na sharia. Kama ambavyo wanaelekea kibla kimoja katika kutekeleza swala tano, na wanahiji huko, na wanatoa zaka na wanafunga mwezi wa Ramadhani, hivyo wao wanaafikiana katika misingi ya dini na nguzo zake. Na nukta kubwa ya ikhitilafu baina ya Sunni na Shi‟ah, inatokana na maudhui ya Uimamu na Ukhalifa, ambapo Ahlus-Sunna wanaona kwamba ni jambo lilioachwa kwa umma, wenyewe ndio unachagua Imamu na khalifa kwa shura na uchaguzi, wakati ambapo Shi‟ah wanaona kwamba Uimamu unakuwa kwa tamko na uteuzi kutoka kwa Mwenyezi Mungu kupitia kwa Mtume . Kwa nini kuwepo mazungumzo juu ya Uimamu? Kwanza: Mazungumzo juu ya Uimamu hayataathiri katika mapito ya historia, na katika yaliyotokea na kupatikana, hususan katika maisha ya Waislamu, kwani khalifa wa kwanza alikuwa ni Abubakri bin Abi Quhafah na baada yake khalifa alikuwa ni Umar bin al-Khattab, na baada yake ni Khalifa Uthman bin Afan na baada yake ni Imamu Ali bin Abi Twalib, na baada yake ni mtoto wake Hasan kwa miezi michache. Kisha alitawala Muawiya bin Abi Sufian na wakarithishana ukhalifa Bani Ummaya baada yake, hadi ilipotoweka dola yao, na ikaja dola ya Bani Abbasi. Na hivi ndivyo ulivyokuwa mlolongo wa historia ya Kiislamu kama inavyofahamika. Pili: Mazungumzo juu ya Uimamu hayapaswi yawe ndani ya mtirirko wa kuchochea ikhitilafu na chuki, wala kutumika kwa njia ya ugomvi na hasira, na kuwazuia Waislamu kujishughulisha 245


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

na mambo ya hali yao ya leo, wao wana haja sana ya umoja na uelewano. Tatu: Ni dharura sana Waislamu kujuana baadhi yao kwa baadhi, na kuwa wazi mtazamo wa kila upande, kwa namna ya kimaudhui tulivu, na sio kwa lengo la kuhubiri madhehebu na kumkinaisha Sunni mtazamo wa Shi‟ah au kinyume chake, bali ni kwa sababu maarifa na uwazi unaleta mazingira ya kufahamiana na kuziba njia ya wachochezi, ambao wanapaka matope sura ya kila upande mbele ya mwingine ili wagombane katika maji machafu. Hakika nchi zilizoendelea sasa hivi zinategemea manhaji ya kujuana kimaudhui hata na makundi yanayokuja katika nchi zao, kwa ajili ya kuwaingiza wao katika jamii, na kutengeneza mazingira ya kuwakubali na kuwashirikisha katika maisha ya jumla, na kusimama mbele ya mirengo ya ubaguzi yenye kuchupa mipaka dhidi ya wengine. Na serikali ya Israil yenye hasira hivi sasa imeingia katika vita na kanisa la Kiisrail, kwa sababu waziri wa elimu na malezi anataka kupitisha baadhi ya manhaji ambazo zinadhamini maandiko ya fasihi ya wanafasihi wa kipalestina katika msingi wa dharura ya kufahamiana Waisraili na Wapalestina walio jirani yao. Na dini yetu tukufu ya Kiislamu inatulea katika kusikiliza rai ya mwingine:

َ ‫َن‬ َ َ ‫ى‬ ُ َ َ ‫اللى ٌَ َف َي ىدبػى َن َأ‬ “….. ‫خع ِه‬ ‫زين َيعخ ِمػى‬ ‫”ال‬ ِ “Na ambao husikiliza maneno, wakafuata mazuri yake zaidi…” (Surat Az-Zumar; 39:18). Na inatuamrisha kuwa na uhakika na maalumati yetu juu ya wengine, na tusiwatuhumu kwa chochote kwa ujahili, kabla ya kuthibitisha na kubainisha 246


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

ُ َ ً ‫”… َف َخ َب ىي ىا َأن ُجصيبىا َك‬ ٰ ‫ىما ب َجُٰك َل ٍت َف ُخصبدىا َغ‬ ‫هى ما ف َػلخ‬ ِ ِ َ ٰ “‫محن‬ ِ ‫ك ِذ‬ “…..Na ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kutokujua, na mkawa wenye kujuta kwa mliyoyatenda.” (Surat Al-Hujurat; 49:6). Na kwa hali hii tunazungumzia juu ya maudhui ya Uimamu baina ya tamko ambayo Shi‟ah anaitakidi ulazima wake humo, na shura ambayo Sunni wanaiona unapatikana ukhalifa humo. Uimamu na ujumla wa Uislamu: Uislamu kama mfumo wa jumla katika nyanja zote za maisha, je unapuuza maudhui ya uongozi na Uimamu katika umma? Hakika ni maudhui yenye hatari zaidi na muhimu sana. Ni lazima Uislamu uwe na rai humo na manhaji. Na tunaona kwamba utawala wowote wa kijamii unatoa kipaumbele cha kupanga kadhia ya uongozi na kubadilishana uongozi hata katika kiwango cha taasisi ndogo au jumuiya ya kheri. Ni namna gani inawezekana Uislamu kupuuza maudhui ya Uimamu? Na wala usibainishe mtazamo wake kuhusiana na hilo? Wala njia ya kuachiana kwake katika jamii ya Kiislamu? Pamoja na kujua kwamba jamii hii ni mpya na imeundwa juu ya muongozo wa Kiislamu? Hakika mafakihi katika kuzungumzia kwao swala ya jamaa wanazungumzia maudhui ya uimamu katika swala. Wanataja mafunzo ya Uislamu katika kupanga anayestahiki zaidi au anayefaa kwa uimamu wa jamaa. Kulingana na hadithi zilizopokelewa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu  katika nyanja hii, kuna ambaye unasihi uimamu wake, na kuna anayestahiki na anayefaa zaidi, na kuna ambaye ni makuruhu uimamu wake. Na katika vitabu vya fikihi kuna maelezo ya ufafanuzi katika mas‟ala haya na ikhitilafu baina ya madhehebu, 247


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

na ikhitilafu katika baadhi ya maelezo yake. Ikiwa uimamu wa swala ya jamaa una sehemu katika pendekezo na kuainisha katika sharia ya Kiislamu, je, inawezekana kughafilika juu ya kadhia ya uimamu wa Umma na ukhalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu ? Na kwamba Uislamu haukupanga mafunzo yake na vidhibiti vyake? Nabii na Mustakabala wa Daawa: Kufariki Mtume wa Mwenyezi Mungu  na kuondoka kwake duniani halikuwa ni jambo la ghafla kwake, yeye anajua kwamba jambo lake ni kama jambo la watu wengine: “Hakika wewe utakufa na hakika wao pia watakufa.” (Surat Zumar: 30), bali alikuwa anaashiria kukaribia kifo chake katika wakati wa mwisho wa uhai wake. Je, alikuwa anafikiria mustakabali wa daawa ya umma baada ya kifo chake? Au alikuwa hajali wala hazingatii hilo? Hakika msimamo mbaya katika mustakabali wa daawa, ni jambo lililo mbali na Mtume wa Mwenyezi Mungu , naye anajali kulinda dini na maslahi ya umma. Kama ambavyo utulivu na kuamini mustakabali, na kwamba hakuna hatari juu ya dini na umma na pengo la uongozi, ambalo litatokea kwa sababu ya kufariki kwake , nalo pia ni jambo lingine linalokhalifu mazingira ya hali za binadamu, na hususan katika jamii mpya, na ngeni katika zama za Uislamu. Na baadhi ya watu wake wamehifadhi upotovu wa historia yao iliyotangulia kutokana na uhusiano wa kikabila, ikhitiilafu, na mizozo ya kimaslahi, pamoja na kuwepo hatari za nje zinazozunguka Uislamu, na watu wanafiki waliojiingiza katika jamii ya Kiislamu. Na kuna ushahidi mwingi unaoonyesha kwamba Nabii  alizungumza kuhusu baadhi ya fitina na matatizo ambayo yataupata umma wake, na akahadharisha kwayo. Hivyo yeye anajali mustakabali wa daawa, na anajua hatari na changamoto 248


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

ambazo zinaukabili, na anatarajia kutokea hali mbalimbali na matukio. Na vipi isiwe hivyo na Qur‟ani tukufu ilikwishasema katika yaliyotokea kuhusu vita vya Uhudi, na proganda mbaya zilizowapata Waislamu humo, na kudhihiri propaganda za kuuliwa Mtume wa Mwenyezi Mungu  kwamba umeshatingishika msimamo wa jamaa kwa sababu ya propaganda hizo: Anasema (swt):

َ​َ ُ ُ َ​َ َ َ ّ ُ َ َ ‫لِ أف ِئ ۟ين ماث أو ك ِخ َل‬ ِ ‫” َوما ُم َد ىم ٌذ ِإال َسظى ٌ​ٌ كذ لذ ِمن ك ِبل ِه الشظ‬ ُ ٰ َ ٰ َ ُ َ​َ “….. ‫هى أغلك ِبى‬ ‫ا للبخ غ‬ “Hakuwa Muhammad ila ni Mtume; na wamekwishapita Mitume kabla yake. Je, akifa au akiuliwa mtarudi nyuma kwa visigino vyenu?” (Surat Aali-Imran; 3:144). Mtume  kujali daawa na mazingatio yake katika mustakabali wa umma, inapelekea kutatua maudhui ya pengo la uongozi ambalo litatokea kwa kifo chake. Shura: Kuna dhana mbili katika maudhui ya Uimamu baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu . Ya kwanza ni kwamba Mtume  aliacha jambo ili liwe shura miongni mwa Waislamu, kwani kuna kizazi cha masahaba kimeleleka katika mikono ya Mtume , na wamechota katika mafunzo ya wahyi, na katika mabega yao kuna jukumu la kumchagua imamu na khalifa kwa msingi wa shura na uchaguzi wao. Na dhana nyingine ni kwamba yeye  amekwishatamka mtu maalumu ili awe Imamu na Khalifa baada yake. Lakini angalizo hapa: Hakika shura ikiwa inafanyiwa kazi kama manhaji na mpango, basi ina haja ya kupendekezwa na kutiwa mkazo ndani ya umma, na kubainisha mafunzo yake na vidhibiti vyake. Ni nani watu wa shura? Je, ni Waislamu wote? 249


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Au ni watu wa mji maalum? Ni nani watu wa hilu wal-uqudu? Ni nani hasa? Je, ni kwa kongamano au ni kwa walio wengi? Yote hayo hayako wazi katika hadithi za Mtume  au sira yake. Katika upande mwingine: Hakika Mtume  hakuandaa masahaba wake na hakuufundisha umma wake kutumia shura katika mas‟ala haya ya uongozi. Wakati alipokuwa anaondoka Madina alikuwa anamwacha Abdillahi bin Ummi Maktum kwa ajili ya uimamu wa swala na mengineyo katika mambo, na hakuwa anaacha jambo la watu wachague wenyewe imamu na kiongozi. Na hali ni hiyo hiyo, anapotuma kikosi au kikundi katika jeshi, anawateulia kiongozi kutoka kwake na wakati mwingine kama ilivyotokea katika vita vya Muuta aliteua viongozi watatu kwa kufuatana, Jaafar bin Abi Twalib, Zaid bin Harithi na Abdillahi bin Rawaah. Yote hayo hapakuwepo na fikra ya shura katika jambo la uongozi na ukhalifa na kujikita wala haikuwa wazi katika akili za masahaba. Na anayesoma mjadala ambao ulitokea katika Saqifah ya Bani Saidah kabla ya ukhalifa wa Abubakri na kulingana na picha aliyoinukuu khalifa wa pili Umar bin al-Khattab, inabainika kwake kwamba rai ya masahaba na misimamo yao wakati huo haikutokana na fikra hii, na hivyo mlango ulikuwa wazi wa dhana mbalimbali, na kufuatana na kauli ya khalifa Umar: Hakika baiya ya Abubakr ilikuwa ghafla ila hakika Mwenyezi Mungu aliepusha shari yake.196 Na Ali bin Abi Twalib na baadhi ya masahaba pamoja naye walikataa kukubali matokeo yaliyopatikana Saqifah kwa muda. Kisha khalifa Abubakri alitegemea njia ya kuchagua khalifa, ambapo alikabidhi ukhalifa kwa Umar bin al-Khattab. Na khalifa Umar aliweka kanuni maudhui ya Shura wakati wa kufariki 196

Ibnu Abdul-Wahabi: Sheikh Muhammad katika Mukhtasar Sirati Rasuli, uk. 180 Muasastu Darul- Kitab Sauudiy – Riyaadh.

250


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

kwake, ambapo alichagua watu sita katika masahaba ili wakutane na wabadilishane rai, na kuchagua mmoja kati yao awe khalifa katika umma. Na watu kumng‟ang‟ania Ali bin Abi Twalib baada ya kuuliwa khalifa Uthman kuchukua ukhalifa. Na yaliyofuatia katika jambo la ukhalifa baadaye ambapo Bani Ummaya na Bani Abbasi walirithishana ukhalifa kwa nguvu na kushinda.Njia zote hizi zilizotumika katika kutatua maudhui ya uimamu na ukhalifa zinaonyesha mafunzo ya Shura kutokuwa wazi, kama manhaji inayotegemewa kutoka kwa Mtume  au katika akili ya Waislamu. Tamko na kuteua: Kwa hiyo Shi‟ah wanaona kwamba Uimamu unakuwa kwa tamko na uteuzi kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu  kwa kuzuia dhana, ikhitilafu na mzozo. Na kwa sababu uteuzi wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake ni sahihi na ni bora zaidi, na kwa kupokewa nususi zinazothibitisha usahihi wake kwa Shi‟ah na wasiokuwa wao, ambazo wanafahamu Shi‟ah hoja yake katika kuteua na tamko la uimamu wa Ali bin Abi Twalib. Na katika matamko hayo ni hadithi ya Ghadir-Khum, ambayo imepokewa katika rejea za hadithi zinazoaminiwa na zinazotegemewa kwa Sunni na Shi‟ah kwa njia sahihi. Na hapa tunataja aliyopokea kuhusu hadithi hii muhadithi wa kisalafi wa zama hizi Sheikh Muhammad Naswir al-Albaaniy katika kitabu chake Silasilati al-Ahadithi Sahihi, mjaladi wa nne, hadithi namba (1750), ambapo amethibitisha riwaya yake kutoka kwa masahaba kumi, kwa njia ishirini na tatu, na imechukua katika kuzitaja njia hizo kurasa kumi na nne kuanzia ukurasa 330 hadi 344. Na masahaba kumi ambao ametaja al-Albaaniy riwaya zao katika hadithi ya Ghadir ni: 251


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8.

Zaid bin Arqam na ana njia tano kutoka kwake. Saad bin Abi Waqaasi na anazo njia tatu kutoka kwake. Buraidah bin al-Haswib, na anazo njia tatu kwake. Ali bin Abi Twalib na ana njia tisa kutoka kwake. Abu Ayub al-Answaariy na ana njia moja kutoka kwake. Al- Baraau bin Azib na ana njia moja kutoka kwake. Abdillahi bin Abbasi, na ana njia moja kutoka kwake. 9 na 10 Anasi bin Maalik, Abu Said al-Khudiriy na Abu Huraira na ana njia moja kutoka kwao.

Na tamko la hadithi ya Ghadir kwa njia moja ya kwanza katika hadithi ya Zaid bin Arqam kama alivyopokea al-Albaaniy: “Kutoka kwa Abi Tufail kutoka kwake amesema: Alipotoka Nabii  kwenye Hija ya kuaga na kateremka Ghadir-Khum, aliamuru pasafishwe chini ya miti ya Dauh kisha tukasimama kisha akasema: „Kana kwamba mimi nimeitwa na nimeitika, na hakika mimi ni mwenye kuwaachia vizito viwili, kimoja wapo ni kikubwa kuliko kingine: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu, Ahlul-Bayt wangu, tazameni namna gani mtanifuata kwavyo. Hakika viwili hivyo havitofarakana hadi vitakaponijia katika haudhi.‟ Kisha akasema: „Hakika Mwenyezi Mungu ni Kiongozi Wangu na mimi ni kiongozi wa kila muumini.‟ Kisha akashika mkono wa Ali  akasema: “Ambaye mimi ni kiongozi wake basi huyu Ali ni kiongozi wake. Eee Mwenyezi Mungu mpende atakaye mtawalisha na mchukie atakaye mfanyia uadui.” Kisha anaongezea muhadith al-Albaniy: Na hadithi ina njia nyingine nyingi, wamekongamana kundi kubwa, miongoni mwao ni al-Haithamiy katika al-Majmau (9/103-108), na nimekwishataja na kutoa yaliyoniwia mepesi miongoni mwayo, katika ambayo yanamthibitishia asiyejua, baada ya kuhakiki maneno katika sanadi zake kwa usahihi wa hadithi yakini, vinginevyo ni nyingi sana. Na amezitaja Ibnu Uqudah katika kitabu pekee akasema al-Hafidh bin Hajar: Miongoni mwazo ni sahihi na 252


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

miongoni mwazo ni Hasan.197 Na katika maulamaa wa Ahlus-Sunna waliopokea hadithi na wakaithibitisha na wakatetea usahihi wake ni muhadith Ahmad bin Hajar al-Haithamiy al-Makiy (aliyefariki mwaka 978H) katika kitabu chake Swaiqul-Muhriqah. Ametaja kauli yake  siku ya Ghadir khum, sehemu ya Juhfah - wakati wa kurejea kwake kutoka hija ya kuaga, baada ya kukusanya masahaba wake na akakariri kwao: Je, mimi si mbora wenu kuliko nafsi zenu? Na wao wanajibu kwa kusadikisha na kukiri. Kisha akanyanyua mkono wa Ali na akasema: Ambaye mimi ni kiongozi wake basi Ali ni kiongozi wake: Ewe Mwenyezi Mungu mpende atakaye mtawalisha na mfanye adui atakayemfanyia uadui na mpende atakayempenda na mchukie atakayemchukia, mnusuru atakayemnusuru na mdhalilishe atakaye mdhalilisha na izungushe haki pamoja naye popote atakapozunguka.” Na akatia mkazo Ibnu Hajar kwamba: “Hakika ni hadithi sahihi hakuna shaka humo, na wamekwishaitoa kundi kama Tirimidhiy, AnNasaiy, Ahmad na njia zake ni nyingi sana. Na kisha wamezipokea masahaba kumi na sita, na katika riwaya ya Ahmad ni kwamba wamesikia kutoka kwa Nabii  masahaba 30, na wameshuhudia kwayo Ali, alipoenguliwa katika ukhalifa wake, kama ilivyotangulia na itakuja, nyingi za sanadi zake ni sahihi na hasan, wala hakuna kumjali aliyekosoa katika usahihi wake wala aliyeikataa.198 Na hadithi hii ya Ghadir ni moja kati ya Hadithi nyingi, ambazo Shi‟ah wanaona kwamba zinamaanisha tamko la uimamu wa Ali 197

Al-Albaaniy: Muhammad Naswir Diyn katika Silsilati Ahadith Sahihah, Juz. 4, uk. 343 chapa ya kwanza 1983 Daru Salafia – Kuwait, Maktabatu al-Islamiya – Jordan. 198 Al-Haithamiy: Ahmad bin Hajar katika Sawaiqul-Muhriqah, uk. 40 Maktabatu al-Qahirah 1375 Hijiria.

253


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

bin Abi Twalib, wala hakuna kizuizi wao kuhitalifiana na wengine, katika kufahamu nususi hizi na hoja zake. Lakini fursa ni wajibu itolewe kwa wote kutumia haki na kufanya ijitihadi na kutoa rai na kuiangalia katika msingi wa maudhui ya kuheshimiana pamoja na kuhifadhi mazingira ya udugu na umoja wa Kiislamu.

ASHURA: UELEWA NA UPEO Aya nyingi za Qur‟ani tukufu zinamkumbusha mwanadamu neema za Mwenyezi Mungu Mtukufu juu yake, na zinazungumza kuhusu aina za neema hizo mbalimbali, ambazo Mwenyezi Mungu amemneemesha mwanadamu.

َ ٰ ‫ى‬ ‫َ​َ َ َ ى‬ َُ ‫ى‬ َ​َ َ​َ ‫ظبغ‬ ‫العمك ٰى ِث َوما ِفى س ِ ِوأ‬ ‫”أل ج َشوا أ ىن الل َكه َسأ َش لى ما ِفى‬ ًَ ُ َ ً ٰ ُ “…..ِ‫َغليى ِق َػ َمه ظك ُِ َشة َوبا ِ ِت‬ “Je, hamjaona kwamba Mwenyezi Mungu amevifanya viwatumikie vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini na akawakamilishia neema Zake zilizo dhahiri na siri?.....” (Surat Luqman; 31:20)

َ ‫َ َ ى‬ ُ ُٰ َ ُ ُ َ ‫ػمذ الل ِكه ال جدصىها‬ ‫مىهِ َو ِإن ح ُػ ّذوا ِق‬ ُِ ‫ءاجىى ِمن و ِ ّل ما َظألخ‬ ‫”و‬

“…

“Na akawapa kila mlichomuomba. Na mkihesabu neema za Mwenyezi Mungu hamtuwezi kuzidhibiti…..” (Surat Ibrahim; 14:34) Kama ambavyo aya nyingi zinatia mkazo kuzihudhurisha neema za Mwenyezi Mungu Mtukufu na kuziweka mbele ya macho na fikra, na katika sehemu nane imekuja kauli Yake (swt) “Na kumbukeni neema za Mwenyezi Mungu juu yenu.” Na katika 254


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

sehemu tatu zingine imekuja kauli Yake (swt) “Kumbukeni neema yangu ambayo nimewaneemesha juu yenu.” Kwa kuongezea na makumi bali mamia ya aya tukufu, ambazo zinaeleza neema za Muumba Mtukufu na utoaji Wake usio na mpaka. Hakika ukumbusho huu kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa neema Zake na upaji Wake unalenga mambo mawili: Kwanza: Ili mwanadamu azingatie kutekeleza wajibu wa kumshukuru mneemeshaji, kwa kunyenyekea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kushikamana na amri Zake, na kujiepusha na makatazo Yake. Pili: mwanadamu aangalie katika neema zinazomzunguka, na afikirie katika kuziendeleza na kunufaika nazo, kwani zimeumbwa kwa ajili yake, na zimedhalilishwa kwa ajili ya kutumikia maslahi yake na kutimiza mafanikio yake. Na kwa kadri mwanadamu atakavyoelekea kwenye kheri za ulimwengu na utajiri wa maisha, na juhudi zake za kuzivumbua na kuziendeleza, anatengeneza kiwango cha maendeleo yake na kubadilisha maisha yake. Neema za Mwenyezi Mungu ni nyingi na pana, zinawazunguka wanadamu wote, na zinamwenea kila mtu, lakini kuna anayeangalia baadhi ya neema na kunufaika nazo, na kuna anayeghafilika nazo na wala hazizingatii, kwa uzembe au kutojua. Anasema (swt):

َ ٰ ‫ى‬ َ َ َ ‫َو َه َأ ّين من‬ ‫العمك ٰى ِث َو س ِ َي ُم ّشون َغلي ا َو ُه َغن ا‬ ‫ءاي ٍت ِفى‬ ِ ِ َ ُ ‫ن‬ ِ ‫ػشضى‬ ِ ‫م‬ “Na ni ishara ngapi katika mbingu na ardhi wanazipita na hali ya kuwa wanazipuuza.” (Surat Al-Yusuf; 12:105). 255


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Na jamii zilizoendelea, siri ya maendeleo yake na mabadaliko yake ni utambuzi wake na uendelezaji wake katika uwezo na utajiri uliopo, wakati ambapo unapatikana uwezo uleule katika jamii zingine na unabaki bila ya kufanyiwa kazi na umedumaa. Utajiri wa kimaanawi: Harakati za mwanadamu na juhudi zake katika maisha haya, zinategemea kwa daraja la kwanza juu ya nguvu zake na uwezo wake wa kiroho na kimaanawi, utashi mkubwa na matakwa yenye nguvu, na msimamo wa kinafsi, na upeo mpana, na uhuru wa kifikra, na mwamko wa uwepo na dhamira, subira na umadhubuti na vipaji. Na sifa zingine njema zote zinatengeneza chimbuko na nguvu ambayo inamuongezea mwanadamu nguvu ya kuendesha mambo ya maisha, na kukabiliana na changamoto zake. Na pande na sababu ambazo zinakuza sifa hizi katika nafsi ya mwanadamu zinazingatiwa kuwa ni chanzo cha utajiri wa kimaanawi na nguvu ya kiroho. Kila inapokuwa hazina ya jamii katika vyanzo hivi, na sababu hizi ni kubwa zaidi, uwezo wake unakuwa ni bora zaidi, na kisha atakuwa na harakati zaidi na mafanikio na ufaulu. Kwa hiyo, hakika maadili matukufu, na misingi ya haki, na manhaji salama ni kati ya neema kubwa ambazo zinatajirisha maisha ya mwanadamu na kumfurahisha. Na kama ambavyo Mwenyezi Mungu ananeemesha waja Wake kwa neema Zake za kimaada na anawakumbusha kwazo, vile vile anawaneemesha kwa neema za kimaanawi ambazo ndio bora zaidi kwao kupitia uongofu wake wa kiungu, na ujumbe wake wa mbinguni, na anawazindua kwazo na anawakumbusha kwazo. Anasema (swt):

ً َ ُ َ​َ ُ ‫َ​َ َ ى ى‬ ُ َ َ ‫ؤم حن ِإر َ َػث في ِ َسظىال ِمن أ ف ِع ُِ َيخلىا‬ ِ ‫للذ من اللكه غهى او‬ 256


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

َ ‫َغ َلي ءايٰكخه َو ُي َض ّهي َو ُي َػ ّل ُم ُ​ُ ُ الىخٰك َب َواحخ‬ ُ ‫ىم َت َوإن وا ىا من َك‬ ‫بل‬ ِ ِ ِ ِ​ِ ِ ِ ِ َٰ ِ َ ُ ِ ٍ ‫لفش ضلك ٍل م‬ ‫بحن‬ “Hakika Mwenyezi Mungu amewaneemesha waumini kwa kuwaletea Mtume miongoni mwao anayewasomea aya Zake na anayewatakasa na kuwafundisha Kitabu na hekima. Na hakika kabla ya hapo walikuwa katika upotofu wa dhahiri.” (Surat Aali-Imran; 3:164).

ٰ ُ َ​َ َ َ َ َ ُ َ​َ ‫َ َ ى‬ ُ َ َ ‫الىخك ِب‬ ِ ‫…وارهشوا ِقػمذ الل ِكه غليى وما أ ضٌ غليى ِمن‬..” َ ‫َواحخ‬ “….. ‫ىم ِ​ِت‬ ِ “…..Na kumbukeni neema za Mwenyezi Mungu juu yenu, na Kitabu alichowateremshia na hekima,…” (Surat Al-Baqara; 2:231).

ُ َ َ َ ‫ُ ُ َ ً َ​َى‬ ‫غذاء فألف َبحن‬ ‫َغليى ِإر ه خ أ‬ ً “….. ‫ٰى ا‬

‫َ َ ى‬ ُ ‫ػمذ الل ِكه‬ ‫… َوارهشوا ِق‬..” ُ َ َ​َ ُ ُ َ ‫دخ ب‬ ‫ػم ِخ ِه ِإ‬ ‫لىبى فأصب‬ ِ​ِ ِ ‫ك‬

“Na kumbukeni neema za Mwenyezi Mungu juu yenu mlipokuwa maadui, naye akaziunganisha nyoyo zenu; hivyo kwa neema Zake mkawa ndugu…..” (Surat Aali-Imran; 3:103). Hakika uwepo wa uongofu wa kiungu, na manhaji sahihi katika maisha, na mafunzo na maelekezo ambayo yanatatua matatizo ya kinafsi na kijamii, na kulea mwanadamu na kustawisha uwezo wake na nguvu zake, na kuelekeza katika njia sahihi, hakika hilo linazingatiwa kuwa ni neema kubwa, hakika ni neema ya uongofu:

‫َ ُ ى ى‬ َٰ َ َ َ َ َ َ ُّ َ ٰ ٰ َ ‫ذً ا‬ ‫مذ ِلل ِكه الزي هذً ا ِلُكزا وما ه ا ِلن خ ِذي لىال أن ه‬ ‫… احخ‬..” ُ‫ى‬ “….. ‫الل ِكه‬ 257


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

“Sifa njema zote zinamstahiki Mwenyezi Mungu ambaye ametuongoza kwenye haya; na hatukuwa ni wenye kuongoka kama asingetuongoza Mwenyezi Mungu.” (Surat Al-A‟araf; 7:43). Lakini kupatikana neema za kimaanawi ni kitu kimoja na kuzitambua na kuziendeleza na kunufaika nazo ni kitu kingine, sawa kabisa kama ilivyo hali katika neema za kimaada. Ni jamii ngapi zinaishi katika hali mbaya na kutoendelea, na wanateseka na upotovu na maradhi yenye kuangamiza – ya kinafsi na kijamii – na zinatawaliwa na hali ya ujahili na mpasuko, na nyuma yao kuna ujumbe wa Mwenyezi Mungu, na Vitabu Vyake vitukufu, na mafunzo yake ya kidini matukufu. Lakini vimehamwa, vimepuuzwa, havitumiki kama manhaji ya maisha au kama chanzo cha nuru na mwangaza? Na katika mfano mkubwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anafananisha jamii ya kiyahudi, ambayo Mwenyezi Mungu aliteremsha kwao Tawrati, na wakashikamana nayo kwa anwani na muundo tu, na wakaacha madhumuni yake na manhaji yake katika maisha yao, kwamba hakika wao ni kama punda ambaye anabeba vitabu muhimu vya elimu katika mgongo wake, lakini hakika hanufaiki navyo kwa chochote:

ُ ‫ى‬ َ ‫َم َث ُل ىال‬ َ ‫ىسً َت ُز ى َل َيدملىها َه َم َثل احخ‬ ٰ ‫الخ‬ ‫دم ُل‬ ‫زين ُخ ِّملىا‬ ِ ‫ماس ي‬ ِ ِ ِ ِ ٰ ٔ ‫ى‬ ‫ى‬ ‫ى َ َ ى‬ َ ُ َ​َ َ ً ‫َأ‬ ‫زين هزبىا ِبكايك ِذ الل ِ ِكهِ َوالل ُكه ال َي ِذي‬ ‫ىم ال‬ ‫الل‬ ‫ل‬ ‫ث‬ ‫م‬ ‫ئغ‬ ‫ب‬ ِ ‫ا‬ ‫ظفاس‬ ِ ِ َ ّٰ َ َ ِ ‫ىم الةك ِل‬ ‫محن‬ ‫الل‬ “Mfano wa waliobebeshwa Tawrati kisha wasiibebe, ni mfano wa punda anayebeba vitavu vikubwa. Mfano muovu mno wa watu waliokadhibisha Ishara za Mawenyezi Mungu, Mwen258


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

yezi Mungu hawaongoi watu madhalimu.” (Surat Al-Jumu‟a; 62:5) Na umma wa Kiislamu unamiliki ujumbe wa mwisho na ulio bora zaidi wa mbinguni na sharia kamilifu zaidi. Hakika ni Uislamu, kwa mfumo wake wenye kuenea nyanja zote za maisha na mafunzo yake na manhaji yake ya kiakhilaqi, ndio ambao unamuongoza mwanadamu katika yaliyosawa zaidi, na kumfungulia njia ya mafanikio na wema. Na Waislamu walipokuwa wanajua uwezo wa neema hii, na wanashikamamna nayo na wanatengeneza maisha yao katika mwangaza wake, walikuwa ni umma bora ulioletwa kwa watu. Kinachosikitisha sana ni hali unayoishi nayo umma wa Kiislamu sasa hivi katika kutoendelea, kunakotokana na unyonge na udhaifu katika uwezo wa kimaanawi, na uwezo wa kiroho, pamoja na kwamba unamiliki pato kubwa na hazina ya kimaanawi na kiroho. Hakika kila manhaji katika manhaji ya Kiislamu inamuwezesha kutengeneza chemchem ya kiroho tajiri inayoleta azma na nguvu, na kuleta harakati na uchangamfu, kwa sharti la kuitambua, na kushikamana nayo na kuitumia katika uhalisia wa maisha. Ama vitendo vya kijuu juu na utendaji wa kijuu juu kwa pamoja katika manhaji ya dini, hakika unadhoofisha utendaji wa manhaji hiyo na unadumaza kazi yake inayotakiwa. Msimu wa Muharam: Katika mwanzo wa kila mwaka wa Hijiria, Waislamu wanapokea kumbukumbu ya shahada ya Imamu al-Husein bin Ali, mjukuu wa Mtume wa Mwenyezi Mungu na manukato yake. Na jamii za Kishi‟ah za Kiislamu zimekwishazoea kuadhimisha kumbukumbu hii, kwa kuitikia maelekezo ya maimamu wa Ahlul-Bayt  ambapo waliwaamuru Mashi‟ah wao na wafuasi wao kuhuisha kumbukumbu hii na kuizingatia. Na limekuwa kumi la mwanzo katika mwezi wa Muharam katika kila mwaka ni msimu 259


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

wa Husein, unajaa ratiba nyingi na harakati za kijamii, ambazo wanashiriki humo wanajamii wanaume na wanawake, wadogo kwa wakubwa, na kuupa msimu huu hali ya kipekee na hali ya upambanuzi katika hali jamii ya Kishi‟ah katika sehemu mbalimbali ulimwenguni. Hakika kuadhimisha kumbukumbu ya Ashura kunatokana na msukumo wa kidini wa dhati kwa jamhuri ya Mashia, kwa kuwapenda Ahlul-Bayt  na kuimarisha mapenzi maalumu katika kushikamana nao, na zinatolewa juhudi kubwa katika ratiba hii ya kuadhimisha, na uwezo mkubwa, ndani ya shughuli za kijamii za kiwananchi, humo yanashiriki makundi yote na tabaka zote. Mazingira ya Ashura na maadhimisho yake kuleta fursa kubwa inawezekana kuzistawisha na kuzinufaisha jamii hizi, na kuimarisha hali ya kidini, na kutatua mengi ya matatizo ya kijamii. Hiyo ni kwa sababu hakika nafsi zinakuwa zimeandaliwa, na harakati za watu ni kubwa, na ambayo wanayasikia katika sira ya Imamu al-Husein  yanawafanya wewe na utayari zaidi katika kuitikia, kujitolea na kutoa. Lakini baadhi ya watu wanafanya ratiba hizi kama ibada ya kuiga na nembo za kurithi zilizozoeleka bila ya kuzingatia kuziendeleza na kuzitumia kwa ajili ya kuhudumia maslahi ya jumla katika jamii na nchi. Kwani ni utajiri mkubwa na mwingi, na kuna uwezekano wa kutoa mengi katika kheri na utoaji katika jamii, wapi utapata mfano wa mkusanyiko huu ambao unakuja wenyewe otomatiki bila ya kutangaza wala vivutio vya kimaada, na kwa muda wa siku kumi asubuhi na jioni? Wapi utakutana na harakati na uitikiaji wa kihisia mkubwa? Na lini utaona mfano wa utoaji wa ukarimu katika mali kutoka kwa mafakiri kabla ya matajiri? Yote hayo yanapatikana katika msimu wa muharam katika jamii za Kiislamu za Kishi‟ah katika kuadhimisha kumbukumbu ya alImamu al-Husein . Namna gani tunanufaika na utajiri huu? 260


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Na namna gani tunatumia ambayo yanapatikana katika fursa hii nzuri na kubwa? 1. Kuimarisha Uchamungu: Watu hawa ambao wanakusanyika kwa jina la al-Imamu alHusein, na wanatumia wakati na juhudi katika kuhuisha kumbukumbu yake, na wanawasikiliza makhatibu na waelekezaji katika majilisi za maombolezo, hakika wanatangaza ufuasi wake wa kidini, na mshikamano wake wa kimoyo na kihisia kwa Maimamu wa dini na uongozi wake, na uitikiaji wake pamoja na maadhimisho na mambo ya kidini. Na hii inatubebesha majukumu na kutuandalia fursa ya thamani kwa ajili ya kuelimisha hawa watu mambo ya dini yao, na kuimarisha hali ya uchamungu katika nafsi, na kutengeneza nyenendo, tabia na misimamo katika uongofu wa dini. Hakika ratiba ya Ashura inatoa fursa bora ya kuelimisha na kuelekeza, na watu wana haja sana na maarifa na mafuhumu ya dini ya kweli, na kuwaondolea vumbi la uongo, na mrundikano wa ufahamu wa kijuu juu na mwepesi. Pamoja na mwanadamu kuzama katika zama hizi katika mazingatio ya kimaada yenye kusomba, na kukabiliwa kwake daima na vyombo vya matangazo ambavyo vinahamasisha humo matamanio na hawaa, ili kumfanya awe ni mwanadamu wa kimaada wa kimatamanio, anatafuta ladha na ana abudu maslahi, ni kiasi gani huyu mwanadamu anahitajia mazingira ya kiroho ya uhamasishaji, yanayomkumbusha maadili na kumfungamanisha na misingi, na mwelekeo wake katika vigezo vyema miongoni mwa Manabii, Maimamu na Mawalii. 2. Ustawishaji wa kijamii: Kupitia ratiba ya Ashura watu wanakutana baadhi na baadhi yao, jambo ambalo linaimarisha umoja wao wa kijamii, na kuzatiti 261


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

kwao hisia ya wingi. Na katika jamii kuna mahitaji, nukta za udhaifu, na mianya ya kasoro, ni lazima kuzalisha tariba hizi ili kuwaelekeza watu katika kubabiliana nazo na kuzitatua. Katika kiwango cha mafunzo inapasa kuhamasisha wanafunzi wa kiume na wa kike katika juhudi na jitihada ili kupata alama za juu na kupata kiwango bora na wastani, na haisihi kufumbia macho kuteremka kiwango cha mafunzo kwa ambayo yanapatikana katika hayo miongoni mwa kuchelewa na kurudi nyuma. Na katika kiwango cha kivitendo na kikazi ni juu ya wanajamii kuimarisha nguvu zao na kuchangia katika kujenga nchi yao, na kupitia ikhlasi zao katika kazi, na kutafuta fursa mpaya na miradi ya uvumbuzi na kutayarisha vipaji na ujuzi katika nyanja za teknolojia za kisasa na kwamba wasiweke rehani mustakabala wao kwa kupata kazi zilizotayari na kuzizingatia kuwa ndio chaguo pekee katika kujenga maisha yao. Na kijamii kuna nukta za udhaifu katika jamii miongoni mwa mafakiri, mayatima na wagonjwa, na kuna haja, mahitaji na huduma za kijamii. Inapasa kukumbusha jukumu la kijamii, na kushajiisha taasisi za jumla kama vile jumuiya rasmi za kheri, na yale ambayo kamati zinashughulika nayo kati ya vitengo vya kuangalia mayatima na mifuko ya kuozesha ya kheri na hafla za ndoa za pamoja na nyinginezo. Ili kuamsha nafasi yake na majukumu yake katika nyanja hii. Hakika kuna uwezekano wa mazingira ya Muharam kuleta msukumo mkubwa wa kimaanawi kwa ajili ya maslahi ya kustawisha jamii na kutumikia malengo yake matukufu. 3. Mafunzo ya Ashura: Tunaweza kusoma Ashura kama kisa cha kihistoria, matukio yake yaliyotokea katika zama na sehemu maalum, na kutoka kwa 262


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

watu maalumu. Na tunaweza kuisoma kama mzozo baina ya makundi mawili juu ya malengo na mambo mbalimbali. Na tunaweza kuisoma kama mateso na kuamsha huruma zetu na hisia zetu. Lakini kinachotakiwa ni kuisoma kama msiba wa kidini na wa kibinadamu wenye kigezo, tuwe tunachukua kutoka humo mafunzo na mazingatio na tunachukua kwayo maadili na vigezo. Katika matukio ya Ashura inabainika kulazimiana kiukweli na dini, na kujitolea kwa ajili ya misingi yake na kuchora picha nzuri ya utekelezaji na misimamo ya kishujaa. Katika Karbalaa kulikuwa na kijana ambaye alizatiti ujana wake kwa ajili ya kuhudumia ujumbe na umma, na mwanamke ambaye alipambana kwa hijabu yake na heshima yake na maneno yake na uvumilivu wake sanjari na kunusuru haki, na mzee kikongwe katika umri ambaye haukumkalisha nje udhoofu wake na uzee wake katika kushiriki katika vita vya kujitoa muhanga, na ndugu mtekelezaji mwenye kumliwaza ndugu yake katika nyakati ngumu kabisa, na kundi la waumini ambalo halikuzembea kutekeleza swala katika wakati wake chini ya mpishano wa mishale na mikuki, na majeruhi waliojeruhiwa ambao huzuni na mateso hayakuathiri uimara wao na misimamo yao. Hakika ni picha nzuri na mafunzo makubwa, inatupasa tuyasome ili tupate kwayo maadili na mazingatio, kwa ambayo yanatufaa kwa ajili ya kutengeneza wakati wetu wa sasa na kujenga mustakabali wetu katika mwangaza wa misingi na maadili. 4. Kujenga umoja wa kitaifa na Kiislamu: Changamoto ambazo zinatukabili katika kiwango cha nchi na Kiislamu ni wajibu zitusukume sote katika kushikamana na kushirikiana. Pamoja na madhehebu yetu Sunni na Shiâ€&#x;ah, hiyo isiwe ni kisingizio cha kuwa mbali na kuhitalifiana, maadamu 263


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

sisi tunaafikiana katika misingi, ambayo inatukusanya nchi moja na maslahi ya ushirikiano. Na ratiba ya Ashura inawezekana kunufaika nayo katika kuimarisha umoja wa nchi na wa Kiislamu na lugha ya mazungumzo ya Kiislamu iepuke uchochezi na dharau ya kiubaguzi. Na ratiba ya Ashura itengeneze fursa nzuri ili kuwafahamisha Waislamu waliobaki rai na vitendo vya ndugu zao Shi‟ah, ambapo imeenea katika baadhi ya jamii propaganda na maelezo ya kupaka matope na ya kimakosa kuhusu ukweli wa itikadi ya Kishi‟ah na namna ya kuhuisha msimu wa Muharam. Alhamdulillhi! Huseiniya zimefunguliwa katika kila sehemu katika ulimwengu, na ratiba ziko wazi na hakuna kisingizio cha kukanganyikiwa na propaganda za ushawishi, maadamu kuna fursa ya kufahamiana moja kwa moja. Na kumbukumbu za Imamu Husein ni wajibu iwe ni mnasaba wa kuimarisha umoja wa umma. Husein ni kadhia ya Kiislamu kwa ujumla, na sio mradi wa madhehebu maalum. Naye hakika amefanya mapinduzi na amekufa shahidi kwa ajili ya kutengeneza umma na maslahi yake kama anavyosema : “Hakika mimi sikutoka kwa shari wala kwa kiburi wala kwa uharibifu wala kwa dhulma, bali nimetoka kwa ajili ya kutaka kutengeneza katika umma wa babu yangu. Nataka kuamrisha mema na kukataza maovu, na kwenda kwa mwendo wa babu yangu na baba yangu Ali bin Abi Twalib. Atakayenikubali kwa kuikubali haki basi Mwenyezi Mungu ni aula zaidi kwa haki, na atakaye nikataa nitasubiri hadi Mwenyezi Mungu ahukumu baina yangu na kaumu kwa haki. Naye ni Mbora wa kuhukumu.” Amani iwe kwa Husein siku aliyozaliwa, siku aliyokufa shahidi na siku ya kufufuliwa. 264


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

SEMINA Nafasi ya fikra ya Kishi‟ah katika majadiliano ya Kiislamu.199 Maktaba ya Rasulil-Adham  imekamilisha katika Banid alQaar sehemu ya pili ya semina ya “Je, mjadala wa Kiislamu ni Sunnah au ni faradhi?” Semina ambazo zinaandaliwa kwa anwani ya semina ya Imamu Ali , ya kila mwaka, na hii ni ya mwaka wa nne. Na alizungumza katika sehemu ya pili Sheikh Hasan Saffar kutoka katika Mamlakatu al-Arabiayati Saudiya, na Dr. Twariq Suweidan na Ali al-Baghaliy, na semina iliendeshwa na Dr. Abdul-Azaz Saffar. Sheikh: Hasan Saffar: Ahlul-Bayt  ni watu wa ujumbe, walijua umuhimu wa majadiliano katika usambazaji wake. Sheikh Hasan Saffar alizungumzia kuhusu maudhui ya “Nafasi ya fikra ya Kishi‟ah katika majadiliano ya Kiislamu” ambayo aliyagawa katika nyanja tatu. Nyanja ya kwanza ilizungumzia dharura ya majadiliano na umuhimu wake na nafasi ya fikra ya Ahlul-Bayt  katika nyanja hii. Na sehemu ya pili alizungumzia mafunzo ya mtazamo wa nadharia ya majadiliano kwa Ahlul-Bayt , na sehemu ya mwisho inahusiana na nukta tatu, nazo ni majadiliano pamoja na wenye dini na misingi mingine, na majadiliano ndani ya duara la Kiislamu pamoja na madrasa na madhehebu mbalimbali ya Kiislamu, na mwisho majadiliano katika nyanja ya kisiasa, yaani baina ya mtawala na mtawaliwa na baina ya mirengo ya kisiasa katika umma. 199

Naduwatu al-Imamu Ali Sanatu Rabi‟i 2-2 Maktabatu Rasuli al-A‟adham, imenukuliwa kutoka jarida la al-Watwan 20 Ramadhan 1417H sawa na 29 Januari 1997 toleo la 7530/1976 mwaka 35.

265


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Na katika upande wa nyanja ya kwanza alisema: Hakika umuhimu wa majadiliano na dharura yake unatokana na sehemu nyingi za kimsingi. Mosi: Majadiliano ni wasila wa kufikia ukweli. Ambapo mwanadamu anaweza kudhani kwamba yaliyopo kwake ndio haki kamili lakini hawezi kuwa na uhakika wa hayo ila atakapojua rai za wengine na kuzipima katika rejea zake. Na hapa hakika Qurâ€&#x;ani tukufu inakumbusha kwamba miongoni mwa sifa za waumini, wanasikiliza kauli na kufuata iliyo bora zaidi. Na anapojua rai za wengine, ama atagundua kwamba rai yake ni ya makosa, na kisha anapata rai sahihi, au anakuwa na uhakika na usahihi wa rai yake, hivyo majadiliano ndio ambayo yanabainisha nukta za udhaifu na nguvu katika fikra yake. Pili: Majadiliano ndio njia salama ya kuwakinahisha wengine. Fikra hazilazimishwi, na kukinai hakuwi kwa kulazimisha. Kupitia majadiliano unaweza kukinahisha wengine kwa rai na misimamo. Tatu: Majadiliano yanaandaa uelewano baina ya pande mbalimbali, na kwa njia yake kila mmoja anajuana na upande mwingine na kila mmoja anafahamu msimamo wa mwingine na ambapo wametengana na wako mbalimbali na hawaelewani. Na kisha kuibua majadiliano yaliyo baina ya pande mbalimbali na kwa njia yake kila mmoja wao anafahamu msimamo wa mwingine na kisha kumaliza shutuma na matatizo. Na sehemu ya pili: inayowakilishwa na nafasi ya majadiliano katika fikra ya Ahlul-Bayt ď …, hakika madrasa ya Ahlul-Bayt ď … ndio udhihirisho wa fikra ya Kiislamu ya asili, ambapo walikuwa ni wafuasi wa ujumbe na hawakuwa ni watu wa utawala na serikali, ambapo wa kundi la mwisho (la utawala na serikali) anaweza asiwe na haja sana na majadiliano; Kwa sababu yeye anatekeleza rai yake kwa nguvu yake na utawala wake. 266


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Lakini mwenye ujumbe anafahamu umuhimu wa majadiliano katika kutoa ujumbe wake na kuusambaza, na Ahlul-Bayt  kwa kuzingatia wao ni watu wa ujumbe, kwa hiyo walikuwa wanayapa majadiliano umuhimu mkubwa. Na katika sehemu ya mafunzo ya nadharia ya majadiliano kwa Ahlul-Bayt hakika wao walibainisha umuhimu wa majadiliano, nalo ni neno linalofanana na neno (al-jadal) mijadala ambalo Qur‟ani tukufu imelitumia katika zaidi ya sehemu 27, wakati ambapo tamko al-Hiwaar limepokewa katika sehemu tatu. Na riwaya zilizonukuliwa kutoka kwa Ahlul-Bayt ni nyingi, ambazo zinashajiisha majadiliano sana, na kisha zinashajiisha katika kufunguka kwa rai zingine na mirengo mingine mbalimbali. Na imenukuliwa kutoka kwa Imamu al-Hasan al-Askariy  kwamba amesema: Ilitajwa kwa Imamu Swadiq  majadiliano katika dini na kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu  na Maimamu wameshakatazwa juu yake, akasema Imamu Swadiq : Hakukataza katika hilo kabisa, lakini alikataza kuhusu majadiliano kwa njia isiyokuwa bora zaidi. Je hujasikia Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: “Na wala usiwajadili watu wa kitabu ila kwa ambayo ni bora zaidi? (Suratul Ankabuti: 46), na amesema (swt):

ٰ َ َ َ َ َ َ ‫ى‬ َ ّ َ ٰ ُ ” ‫احخ َع ِ​ِت َوجك ِذ ُلُ ِبال ى‬ ‫ىغة ِت‬ ِ ‫احخىم ِت واو‬ ِ ‫بيل َسِبً ِب‬ ِ ‫ادع ِإلى ظ‬ َ ‫ى َى َأ‬ “….. ‫ن‬ ِ ُ ‫خع‬ ِ “Waite kwenye njia ya Mola Wako kwa hekima na mawaidha mazuri na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora zaidi…..” (Surat An-Nahl; 16:125). Majadiliano kwa njia bora zaidi wameyaambatanisha maulamaa na dini, na majadiliano kwa njia isiyokuwa bora yameharamishwa, na ameyaharamisha Mwenyezi Mungu kwa Shi‟ah wetu. 267


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Kisha anasema Imamu Swadiq : Namna gani Mwenyezi Mungu ameharamisha majadiliano kabisa; Naye anasema:

َ ّ َ‫َى‬ ُ َ َ ٰ ٰ َ َ ً ً‫شيِ ِجل‬ ِ ‫احج ت ِإال َمن وان هىدا أو صك‬ ‫َوكالىا لن َيذ َل‬ َ ُ ُ َٰ َ ٰ ُ ُ ِ ‫أما ِ ي ُ ِ كل هاجىا ُبشهك ى ِإن ه خ صك ِذ‬ ‫كحن‬ “Na walisema: Hataingia Peponi ila aliye Yahudi au Naswara (Mkristo). Hayo ni matamanio yao tu. Sema leteni dalili zenu kama nyinyi ni wasema kweli.” (Surat Al-Baqara; 2:111). Akajaalia dalili ya ukweli na imani katika hoja, na je ataleta hoja isipokuwa kwa kujadiliana kwa yale ambayo ni mazuri zaidi? Na katika upande wa mafunzo ya kinadharia kuna adabu ya mijadala. Ili uwe ni wenye matunda na manufaa katika pande mbili na kwa jamii kwa ujumla, ni lazima kuwepo na adabu zinazoulinda ili usigeuke na kwenda katika shutuma, kasumba na ugomvi. Hiyo ni kwa sababu zimepokewa hadithi kutoka kwa Maimamu  zinazobainisha adabu ya majadiliano, na wao wenyewe ni mfano mkubwa na kigezo katika nyanja hii, ambapo aliulizwa Imamu Swadiq  kuhusu majadiliano kwa njia iliyo bora zaidi na kwa ambayo sio nzuri, akasema: “Ama majadiliano kwa njia isio nzuri ni kumjadili mbatilifu na kukujibu kwa batili hivyo ukaacha kutoa hoja aliyoiweka Mwenyezi Mungu. Lakini ukapinga kauli yake au ukapinga haki anayotaka kwayo mbatilifu kuunga mkono batili yake na hivyo ukapinga haki kwa kuogopa kwamba yeye atakuwa na hoja dhidi yako, kwa sababu wewe hujui namna gani utajinasua kwake, hiyo ni haramu kwa Mashi‟ah wetu. Na sehemu ya tatu ya nadharia hii ni kukataa kujishughulisha kwa yasiyo na faida na yasiyo muhimu, ambapo Maimamu walikuwa wanakataza wafuasi wao badala ya kutumia juhudi za 268


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

watu na nguvu za jamii katika kubishana, kujadiliana na mazungumzo katika mambo ya pembezoni ambapo hayo yatakuwa kwa hesabu ya mambo muhimu na ya msingi katika umma na jamii. Na anapokea Imamu Swadiq  hadithi kutoka kwa babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu  anasema humo: “Katika uzuri wa Uislamu wa mtu ni kuacha maneno yasiyomhusu.” Na anasema Imamu Ridhaa  kwa mmoja wa wanafunzi wake: “Ewe Abdul-Adhwim: Wafikishie wafuasi wangu salamu na waamuru kunyamaza na kuacha majadiliano katika yasiyowahusu.” Na kwa ushahidi juu ya hilo aliulizwa: “Je, shiriki ni kubwa zaidi au kufuru?” Imamu akamkabili muulizaji kwa kusema: Una nini wewe na hayo? Kwa nini unaanzisha vita kuhusu maudhui hayo nayo hayana umuhimu. Na iliposambaa fitina ya kuumbwa Qur‟ani Maimamu walijizuia kuingilia humo na wakawakataza wafuasi wao kushiriki humo. Yaani Imamu alikuwa anaulizwa humo hakuwa anajibu bali alikuwa anatosheka na kusema: “Qur‟ani ni maneno ya Mwenyezi Mungu.” Na ilipozidi fitina aliandika Imamu al-Haddiy  kwa baadhi ya wafuasi wake barua akasema humo. “Mwenyezi Mungu atukinge sisi na wewe kutokana na fitina, hakika kama atafanya basi imeshakuwa ni neema kubwa sana kwayo, na kama hakufanya basi ni maangamio.” Na akasema kwamba majadiliano juu ya Qur‟ani ni bidaa, ameshiriki humo muulizaji na mwenye kujibu, hivyo anajishughulisha muulizaji kwa ambayo si yake, na mwenye kujibu anajikalifisha kwa yasiyo wajibu wake. Na Muumbaji si mwingine isipokuwa ni Mwenyezi Mungu Mtukufu na kisichokuwa Yeye ni kiumbe na Qur‟ani ni maneno ya Mwenyezi Mungu. Na katika maadili ya majadiliano kwa Ahlul-Bayt ni kupuuza majadiliano na ugomvi. Na majadiliano yanaweza yasifikie 269


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

maafikiano. Na Maimamu wanakataza mtu asichukue msimamo wa ugomvi kwa sababu ya hayo kwa kuzingatia kwamba kila mwanadamu ana uhuru katika rai yake na fikira zake na misimamo yake. Na ikiwa unaitakidi kwamba uliyonayo ni haki na kwamba upande wa pili unabeba jukumu lake la kukhalifu haki, anasema Imamu Swadiq : “Na wala usigombane na watu kwa ajili ya dini yenu, hakika ugomvi unatia moyo ugonjwa.” Na Mwenyezi alikwisha mwambia Nabii Wake : “Hakika wewe humuongoi unayemtaka lakini Mwenyezi Mungu anamuongoa amtakaye.” Na amesema pia: “Je, wewe unawalazimisha watu hadi wawe waumini,” waache watu, hakika watu wamechukua kutoka kwa watu. Na hapa inabainika kwamba wenye kugombana na watu chini ya uzio wa dini, wao wamekosea sana, kwa sababu dini haitaki kwako kuwafanyia watu uadui na kugombana nao, hata kama hawajakubali dini yako au rai yako. Na katika upande wa tatu unahusiana na utekelezaji wa kivitendo katika majadiliano katika maisha ya Ahlul-Bayt . Na upande wa kwanza unawakilishwa na mjadala pamoja na watu wa dini na misingi isiyokuwa ya Kiislamu nayo ni mingi. Waliingia humo Maimamu katika majadiliano pamoja na viongozi na wanafikra wa dini zingine, kwa msingi kwamba dini haiwi ila kwa kukinai, ambapo hakuna kulazimisha katika dini. Na kwa msingi wa majadiliano kwa njia iliyo bora zaidi ndio wasila uliamriwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kati ya misimamo iliyo dhaihri zaidi ni iliyotokea katika zama za khalifa al- Abbasiy al-Maamun alipokusanya viongozi wa dini na misingi kama vile manaswara na wayahudi na Majusi, Zaradishitiya na wengineo. Na yakafanyika baina yao na Imamu Ali bin Musa Ridwa  majadiliano mazuri na ya kuvutia, nayo yamehifadhiwa na yameandikwa katika Biharul-Anwaar ya alMajilisiy, na aliyoyakusanya Marhumu Twabarsiy katika kitabu cha al-Ihitijaaji. 270


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Na katika duara la majadiliano ndani ya duara la Kiislamu hakika karne ya pili hijiria kwa njia mahususi ilishuhudia ijitihadi mbalimbali na madhehebu mbalimbali ya kifikra na kifiqihi. Pamoja na kukinai Ahlul-Bayt kwamba mafunzo yao yalikuwa ni mwendelezo wa mafunzo ya Mtume wa Mwenyezi Mungu , na kwamba rai yao ndio rai sahihi. Ila hakika hayo hayakuwazuia kujadiliana na kuzungumza pamoja na wanaowapinga katika rai za kiitikadi na kifikihi. Na miongoni mwa mifano ya majadiliano hayo ni yaliyokuwa yanatokea baina ya Imamu Swadiq na Imamu Abu Hanifa kuhusu qiyasi na baadhi ya mas‟ala ya kifikihi. Na vilevile rai za Ahlul-Bayt katika mas‟ala ya jabri (kulazimisha) na tafwidh (kutegemeza) na mengineyo katika mas‟ala ya kiitikadi. Na sehemu ya tatu inaonekana katika majadiliano ndani ya nyanja ya kisiasa. Na katika kila jamii kuna mtawala na mtawaliwa, na inaweza kuwa uhusiano baina yao ni uhusiano wa ridhaa, kwa kuridhia mtawaliwa na siasa ya mtawala na wa mwisho kuridhika kwa mwenendo wa mtawaliwa na msimamo wake mukabala wake. Lakini katika baadhi ya wakati inaweza kutokea ikhitilafu baina yao. Ambapo mtawaliwa anakataa baadhi ya vitendo vya mtawala au anapinga sharia yake au msimamo wake katika utawala, na anaweza mtawala asiridhike na baadhi ya vitendo na muamala katika hali hii? Kuna njia mbili, ama kuwepo na kufunguka na majadiliano baina ya mtawala na mtawaliwa, na kwa sura iliyowazi zaidi baina ya mtawala na wapinzani, na kisha majadiliano haya yanaweza kupelekea mabadiliko na marekebisho ya misimamo ya pande mbili mukabala wa hadhi yao. Na kunaweza kusiwe na kufunguka na majadiliano na kuanza hali ya kushutumiana na matatizo na kisha kukapelekea mlipuko. Na mapinduzi na maandamano ambayo yanatokea katika historia ya Kiislamu na ambayo yanatokea katika zama zetu za leo katika nchi nyingi, si kingine ila ni matokeo ya kukosekana majadiliano na utatuzi wa kisiasa, na kunapokuwa na kufunguka kisiasa baina ya mtawala 271


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

na mpinzani fursa ya kumaliza ikhitilafu na mzozo inakuwa ni kubwa zaidi, na Ahlul-Bayt wana mtazamo wao na manhaji yao kamilifu katika mwelekeo huu. Kwanza wao wanatilia mkazo umuhimu wa kufunguka mtawala kwa wananchi na kwamba haisihi kwake kuweka pazia kwa wananchi wake. Amirul-Muuminina  nyingi ya barua na risala zake alizielekeza kwa Magavana wake anawaamuru humo kufunguka kwa watu; na miongoni mwa kauli zake: “Mtawala akijifungia na raia wake Mwenyezi Mungu atamzuia Siku ya Kiyama.” Na anasema katika zama za Maliki al-Ashtar: “Hakika magavana kujizuia na raia ni hali ya ufinyu na uchache wa elimu katika mambo. Na kujitenga nao kunakata kwao elimu ya ambayo wamejizuia dhidi yake na hivyo mkubwa anadharaulika kwao, na mdogo anatukuzwa. Zuri linakuwa baya na baya linakuwa zuri. Haki inachanganywa na batili, na hakika mtawala ni mwanadamu, hajui waliyoficha watu dhidi yake miongoni mwa mambo, pamoja na kwamba mahitaji mengi ya watu yapo kwake katika ambayo hakuna msaada humo juu yake miongoni mwa malalamiko ya kudhulumiwa au kuomba ziada katika muamala.” Na aliingia Imamu al-Baqir  kwa khalifa Umar bin Abdul-Aziz na akamwambia: Ewe Umar fungua milango na punguza walinzi, na mnusuru aliyedhulumiwa na zuia dhulma.” Na alitumia Imamu Ali  alipokuwa katika hatamu za utawala kiasi kikubwa katika kufunguka kwa wapinzani, ni sawa sawa kwa watu wa Jamal au jamaa wa Suffin na tukio la tahkim au pamoja na Khawariji. Na katika yanayofungamana na kufunguka kwa wapinzani, na watawaliwa kwa mtawala, Ahlul-Bayt  walikuwa na manhaji kamilifu katika hayo. Upinzani hausihi kuwa ndio shughuli, bali uwe ni upinzani kwa ajili ya kilicho bora na kwa ajili ya maslahi ya umma na jamii. Na haya yanahitajia upinzani kufunguka kwa mtawala maadamu kuna fursa, na kuzungumza naye kuhusu rai zake na mielekeo yake na ukosoaji wake. Na Ahlul-Bayt walikuwa wanafanya jukumu hili, 272


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

na waliwanasihi wafuasi wao kufanya hivyo. Katika hadithi kutoka kwa Imamu Kadhim  amesema: “Mwenye kumfikishia mtawala haja ya ambaye hawezi kuifikishia, Mwenyezi Mungu atathibitisha nyayo zake katika Sirat.” Na hii inamaanisha kuwepo watu katika jamii ambao ni sawa na madaraja (viunganishi) baina ya mtawala na watu. Na katika mfano wa hayo ni kwamba Imamu Ali  alikuwa anaona nafsi yake anafaa zaidi kwa ukhalifa baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu , ila yeye hakukimbilia kwenye mzozo na ugomvi pamoja na makhalifa ambao walichukua ukhalifa kabla yake, na wala hakuwatenga bali alifunguka kwao na alishirikiana nao na kuamiliana pamoja nao. Na Sheikh Swaffar alimalizia mazungumzo yake kwa kusifu tajriba ya Kuwait na akasema kwamba inatoa picha nzuri na ya kuvutia katika nyanja ya kufunguka na majadiliano baina ya upinzani na serikali, wakati ambapo dola zingine zinafunga milango ya majadiliano na zinashughulika na lugha ya ubabe na risasi. Ametilia mkazo kwamba utatuzi wa matatizo haya ni majadiliano na kufunguka baina ya mtawala na wapinzani. Kumbukumbu ya Sheikh Abdul-Hamid al-Aliyi 200 Amani iwe juu yenu nyote, rehema Zake na baraka Zake pia. Najikinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shetani aliyefukuzwa katika rehema ya Mwenyezi Mungu. Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu. Sifa zote njema anastahiki Mola Mlezi wa walimwengu, sala na salamu zimwendee mtukufu wa Manabii na 200

Alifariki 2/1/1419A.H. Ilitolewa kama ya kumbukumbu ya arobaini yake na kusambazwa katika Muujamul-Khutwabai, kilichotungwa na Sayyid Dakhil Sayyid Hasan, Juzuu ya nane chapa ya kwanza 1420 Hijiria / 1999 Darul Swafuwati Beirut – Lebanon.

273


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Mitume, bwana wetu Muhammad  na kizazi chake kitukufu kilichotwaharishwa. Ikiwa tabia njema ni alama ya dharura kwa kila mwanadamu muumini na kila binadamu anayetaka mafanikio katika maisha yake, basi ni dharura zaidi na muhimu zaidi kwa mtu wa dini; katika shakhsiya ya mwanachuoni na khatibu ambaye anatoa waadhi kwa watu na kuwaongoza na kuwafundisha mafunzo ya dini. Hiyo ni kwa sababu: Kwanza: Maulamaa wa kidini wao wanafaa zaidi kushikamana na mafunzo ya Kiislamu. Pili: Kwa sababu wao katika mtazamo wa watu wanatengeneza mfano na usadikishaji wa Uislamu na dini. Wao wanapojipamba kwa tabia njema na kushikamana na mafunzo ya dini. Hakika kushikamana kwao kutakuwa ni daawa bora na propaganda ya dini, kama alivyosema Imamu Swadiq  katika yanayopokewa kwake: “Kuweni walinganiaji wetu bila ya ndimi zenu.” Tatu: Kwa sababu mtu wa dini anahitaji uaminifu wa watu, na anahitaji kukubaliwa na watu, wala haupatikani uaminifu wala hakupatikani kukubalika ambako kunamuwezesha kusimamia ujumbe wake ila inapopatikana tabia njema katika shakhsiya yake. Na hapa hakika sifa ya tabia njema ndio sifa muhimu ambayo ni wajibu tuitafute katika shakhsiya ya mtu dini. Na inapopatikana kwake sifa ya elimu au sifa ya khitwaba na ubainifu au sifa ya idara na mfano wake katika sifa zingine zinazotakiwa, lakini ikakosekana sifa ya tabia njema - Mwenyezi Mungu apishe mbali - hakika uwezo wake wa kutekeleza ujumbe wake unakuwa dhaifu bali utakosekana, na inaweza kuwa kuathiri kwake katika jamii ni kinyume. Badala ya kuwa mlinganiaji wa dini anakuwa ni mwenye kukimbiwa na anakuwa anaipaka matope dini na uongofu wake. 274


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Hapa hakika sifa nzuri ambazo zimepatikana katika shakhsiya ya marehemu wetu mtukufu miongoni mwake ni sifa ya tabia njema, wanaafikiana wote wanaomjua na aliyeishi naye hata kwa muda mchache katika maisha yake. Wote wanaafikia juu ya tabia yake njema, uzuri wa sifa zake za kinafsi na kimwenendo. Na nimekwishamjua na kuona rai yake tangu siku za mwanzo ambazo nilipata taufiki humo katika kuhamia kwangu Najaf tukufu. Na huko pamoja na umri wangu, nilikuwa mdogo na nilikuwa nasoma, nakwenda mbio kujifunza khitwaba ya Huseiniya, nakumbuka kwamba nilisoma katika moja ya nyumba za Maulamaa nayo ni nyumba ya Sheikh Ahmad Aal Saif ď “, na ilikuwa ni kawaida yake ya kila wiki, na Sheikh marhum ni kati ya waliohudhuria. Nakumbuka namna gani aliamiliana nami baada ya kusikiliza kwake majilisi hiyo. Alinipokea kwa uzuri na kunikaribisha na kunishajiisha, ambapo nilijua kupitia kwake ukweli na ikhilasi ya mtu na uzuri wa nafsi yake, kwa sababu alimzingatia sana mwanafunzi mdogo anaeinukia sasa hivi ambaye ameanza kufuata njia ya elimu, khitwaba na kusoma. Na maadili ni masâ€&#x;ala muhimu, na masâ€&#x;ala ya maadili ya mtu wa dini tunaweza kuigawa sehemu mbili: Sehemu ya kwanza: Katika muamala wake pamoja na watu kwa ujumla. Hapana shaka kwamba ni dharura mtu wa dini kujipamba na tabia njema katika muamala wake pamoja na watu kwani yeye ni mwalimu wao naye ni kiongozi na ni baba, na katika watu kuna majahili, na katika watu kuna wasiokuwa na adabu na kuna wasiokuwa na elimu, inahitajia kwa mwanachuoni kuwa na subira na tabia njema ili aweze kuamiliana na watu na tabia zao mbalimbali na mielekeo yao. Na sitaki kuzungumzia sana kuhusu nyanja hii na sehemu hii. Sehemu ya pili: Tabia njema ya mwanachuoni pamoja na watu wa aina yake na tabaka lake. Hakuna shaka kwamba katika jamii kati ya jamii na hususan sasa hivi, wal-hamdulillahi pamoja na 275


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

medani ya kidini ambayo umevuma upepo wake katika jamii zetu, tumekuwa na matabaka na makundi mapana na watu wa dini kati ya Maulamaa na makhatibu na wanafunzi wa elimu ya dini. Katika baadhi ya zama, kijiji kimoja au mji mmoja kulikuwa humo na mwanachuoni mmoja, kwa hiyo hapakuwa na kundi la wanafunzi wala maulamaa. Ama hivi sasa alhamdulillahi katika kila kijiji tuna kundi la wanafunzi, maulamaa na makhatibu, tunamuomba Mwenyezi Mungu awaongoze na awape taufiq na ainufaishe jamii kupitia kwao. Namna gani mtu wa dini anaamiliana pamoja na watu wa aina yake? Nimekwishaona katika maisha ya Sheikh almarhum sifa muhimu. Alikuwa anaheshimu watu wote katika aina yake, na alikuwa haridhii kutaja ubaya wa mtu miongoni mwao. Kuna mzozo na kuna ikhitilafu lakini Sheikh alikuwa anakataa kuingia katika ikhitilafu hizi na mzozo huu. Na sijasikia kutoka kwake kwamba ameshiriki katika ikhitilfu au mzozo au mazungmzo dhidi ya upande kati ya pande za kidini. Na anajaribu kubadilisha mazungumzo katika majilisi kwa namna yoyote ile, na huu ni upande muhimu. Inapokewa kutoka kwa Imamu wetu Amirul-Muuminina Ali bin Abi Twalib  kwamba amesema: “Mwanachuoni hawi mwanachuoni hadi asimhusudu aliye juu yake wala asimdharau aliye chini yake.” Mwanachuoni anaheshimu maulamaa wote, ni sawa sawa wawe na daraja na cheo cha juu zaidi kuliko yeye, au wanalingana naye au wako kiwango cha chini kielimu. Kwa nini? Kwa sababu macho ya watu na masikio yao yanaelekezwa kwenye nyenendo za kundi hili, kwenye nyendo za watu wa dini. Wanapoona watu wana nyendo hizi na wao baadhi wanalaumu baadhi yao, na wanatofautiana baina yao na baadhi wanakosea 276


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

baadhi ya wengine, katika hilo kuna matokeo yenye kudhuru na mabaya. Na uhalisia wa watu wa dini unazingira jamii. Uaminifu wa maulamaa kwa ujumla unadhoofisha jamii na unatoa kisingizio kwa wapinzani wa dini na maulamaa, ili kuwaweka watu mbali na maulamaa wa dini kwa kisingizio cha ikhitilafu na mizozo hii. Hakika kuna tofauti baina ya ikhitilafu mbaya ya rai na baina ya muamalaa na tabia mbaya. Ikhitilafu katika rai ni hali ya kawaida katika mazingira ya kielimu. Kwa Maulamaa katika hawza za elimu katika masomo ya juu, tunamuona mwanachuoni anatoa rai yake, na anateteta rai yake na anabainisha nukta za udhaifu wa rai nyingine. Ikhitilafu hii ya kielimu hakuna tatizo humo, bali inatakiwa ili kuboresha rai na kupevusha fikra na masâ€&#x;ala, na maadamu mlango wa ijitihadi uko wazi basi kuna nafasi ya kuhitalifiana rai na mtazamo. Hakuna kizuizi kutofautiana mwanachuoni na mwanachuoni mwingine katika rai yake au mtazamo wake, lakini haikubaliki kamwe ikhitilafu hii ya rai kugeuka kuwa ugomvi na kuwa ni uadui. Watu wanapowaona maulamaa hawachungi adabu ya Uislamu baina yao, na wakimuona mmoja wao anatafuta kasoro na mabaya ya mwingine, hakika wao watasema namna gani hawa wanakuwa ni walinganiaji katika dini na tabia njema na wao hawashikamani na dini na tabia njema baina yao? Hivyo ni dharura sana marhumu kuwa ni kigezo chema na mfano kwa makhatibu wote na maulamaa na wanafunzi wa elimu ya dini katika mazungumzo ya baina yao na katika muamala wao pamoja na watu. Mlango wa majadiliano na mlango wa mazungumzo uko wazi. Inawezekana kwa mtu yeyote kujadiliana na mwingine anapotofautiana naye katika rai, ama kuchochea nyuma yake, ama 277


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

kwenda mbio kuangusha shakhsiya yake! Hakika hilo linakatazwa kwa kila mwanadamu Mwislamu, sasa itakuwaje ikiwa mwanadamu huyu ni miongoni mwa walinganiaji na watoa mawaidha? Mwenyezi Mungu amrehemu Marhum na amwingize katika rehema Yake pana. Tabia yake katika nyanja hii ilikuwa ni mfano, haijasikika kutoka kwake kwamba amechochea dhidi ya yeyote, au ameshiriki katika kumsengenya yeyote katika watu wa jinsia yake au kwa ujumla. Hii inaonyesha juu ya kujinyima kwake na uchamungu wake, Mwenyezi Mungu amrehemu. Na hatuwezi kusahau huduma yake katika mimbari, huduma yake kwa ajili ya Ahlul-Bayt ď …. Huduma hii tukufu, na kubwa ambayo atapata malipo yake makubwa kwa Mwenyezi Mungu ziada ya malipo na maghufira na ridhaa kwa Mwenyezi Mungu na kutoka kwa Ahlul-Bayt wa Mtume wa Mwenyezi Mungu amani iwe juu yao wote. Tunamuomba Mwenyezi Mungu amghufirie na amridhie, na Mweneyzi Mungu awape wote taufiqi ili wapite katika njia Yake salama na sahihi ili wajipambe kwa tabia yake njema. Alhamdulillahi maulamaa wetu na masheikhe wetu na makhatibu wetu wanapigiwa mfano wa juu katika kushikamana kwao na tabia yao, na yanayosemwa ni katika aina ya ukumbusho na kutia mkazo. Na naomba radhi kama nimerefusha kidogo. Nawashukuru ndugu zangu ambao wamefanya hafla hii ya kutekeleza baadhi ya haki za Sheikh huyu ambaye ana haki kwetu sote. Asalam alaikum warahamatullahi wa batakatuhu. 278


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

MAKALA Fikra ya Kiislamu ina haja ya kujadidishwa katika kila zama.201 Sheikh Hasan Saffar: - Hakuna vita baridi baina ya Qum na Najaf - Neema ya kuanzisha hawza ya elimu Ghuba - Fikra potovu hukabiliwa na fikra na si kitu kingine. Majadiliano na ufuatiliaji: Ayaad Sharikh: Imejitokeza katika medani ya fikra ya Kishi‟ah tangu mwanzo wa miaka ya tisini kitu kinachoitwa fikra ya kuboresha, ambapo walinganiaji wake wanataka kurejesha mtazamo katika baadhi ya mafuhumu na maadili, na kurejea manhaji na mbinu za kutoa ujumbe wa kifikra wa Kishi‟ah. Walinganiaji wametaka kwa fikra hii kusawazisha na kupuuza makundi na kufungua mfereji wa majadiliano na ushirikiano na wengine. Na wametangaza vita juu ya baadhi ya mazoea ambayo yanafanywa kwa jina la Ushi‟ah nayo hayahusiani nao, kama ambavyo medani imeshuhudia katika fikra ya Kishi‟ah rai mpya zinazojaa mambo ya msingi katika madhehebu ya Kishi‟ah kama Uimamu kwa Tamko, na Umaasumu wa Maimamu, na Mahdi Anayengojewa, bali kuna baadhi ya sehemu za fikra za Kishi‟ah, kwa kurejea baadhi ya riwaya mashuhuri katika madhehebu, ambazo zinachangia katika kuimarisha mfarakano pamoja na Sunni, au kuimarisha mtazamo wa ubaya kwa viongozi wao na maimamu wao. Na medani ya kifikra ya Kishi‟ah inashughulika na majadiliano wakati mwingine zinachanganyika nyaraka za kielimu na kimajimbo humo. Kama ambavyo yanazidi majadiliano hivi sasa 201

Majadiliano yaliyofanywa na jarida la al-Watwan la Kuwait 4 / Jumadi alAkhir 1319H – 24 Septemba 1998 toleo la 8121/2567 mwaka wa 37

279


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

baina ya madrasa zenye mtazamo mkali na madrasa zenye msimamo wa wazi, hususan Rais wa Jamhuri ya Iran Khatamiy (katika enzi yake), anazingatiwa kuwa ni katika wafuasi wa madrasa ya uwazi na wastani. Yanazunguka majadiliano ya “Shi‟ah – kwa Shi‟ah” katika ujumla wake juu ya msingi muhimu, nao ni wigo wa kukubali majadiliano na kurejea baadhi ya mas‟ala ya kifikra na ya kimsingi na upeo wa uwezekano kufunguka juu ya rai nyingine, na mpaka wa hilo. Na yanaathirika majadiliano haya kwa yanayotokea kisiasa katika medani ya Kiirani, Lebanon na Iraki. Bali mwishoni yanayotokea Ghuba. Na inabainika kwa mfuatiliaji kwa mbali kwamba kuna vita iliyofichikana juu uongozi wa kifikra kama maneno haya yatakuwa sahihi kutoka (Qum) hadi (Najaf) kwa kupitia katika sehemu za kifikra Lebanon, bali hata ngome ya Kishi‟ah katika Ghuba inafanya kazi ili ipate hisa katika kupanga nyaraka za fikra ya Kishi‟ah. Na alWatwan ilikuwa na kikao hiki pamoja na Sheikh Hasan Saffar. Katika majadiliano yaliyotokea kuhusu fikra mpya katika duara la Kiislamu kwa ujumla na Kishi‟ah kwa namna maalum, na majadiliano hayakuacha katika uwazi wa ubainifu. Na tunamuomba msomaji wetu mtukufu kusoma ufafanuzi wa majadiliano kupitia nukta zake zenye kuvutia, hususan hakika Sheikh Hasan Saffar ni kati ya viongozi wa madrasa ya kuboresha na walinganiaji wa kufunguka. Kujadidisha kadhia mbili: Al-Watwan: Imejitokeza katika medani fikra ya Kishi‟ah katika miaka ya mwishoni, kitu kinachoitwa fikra ya kuboresha, ambayo inalingania wastani na kukaribiana pamoja na wengine. Sheikh Hasan Saffar yuko wapi katika upande huu? Saffar: Kuboresha katika fikra ya Kiislamu ni hali iliyojitokeza katika medani ya Kiislamu katika madhehebu yote. Uislamu 280


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

kama Uislamu haubadiliki, lakini fahamu ya Waislamu kwa Uislamu katika baadhi ya nyanja inatokea kuacha kufuatilia mwenendo wa uboreshaji kifikra na kijamii. Na kunarundikana juu yake rundo la fikra na dhana ambazo zinaelezea juu ya fahamu isiyoendelea kutoka kwa baadhi ya Waislamu, lakini wao wanazinasibisha kwenye Uislamu. Lakini fikra ya Kiislamu inahitaji bali mwanadamu kwa ujumla baina ya muda na muda aina ya mapinduzi au mtikisiko au kuondoa yaliyorundikana juu yake miongoni mwa vumbi, na kuliondoa ili kuendana na mabadiliko ambayo yanatokea katika maisha ya jamii na maisha ya binadamu. Na hali hii inapatikana katika madrasa mbalimbli za kifikra na katika medani ya Kiislamu, na madhehebu yote ya Kiislamu vilevile katika hali nzuri ya kuamiliana na mfano wa hali hii ni hali ya kuboresha. Na katika hazina yetu kuna baaadhi ya nususi zilizopokelewa zinazoashiria katika upande huu, kama vile hadithi iliyoenea: “Kwamba katika mwanzo wa kila karne au kila miaka mia moja Mwenyezi Mungu anatuma mboreshaji wa dini kwa watu.� Na inawezakana isiwe makusudio ya miaka mia ni muda wa zama maalumu, bali makusudio ni baina ya mwongo mmoja na mwingine, watu wanahitajia mboreshaji anayesukuma hali ili kuendana na mabadiliko, na kuondoa mrundikano ambao unajitokeza na vumbi ambalo linapatikana katika ufahamu wa watu juu ya Uislamu na dini. Kuhusiana na mimi kadhia hii inazingatiwa ni chanzo cha shughuli zangu na harakati zangu, Nimekulia katika mazingira ya kidini yasiyo na mabadiliko na nimeona katika rika langu miongoni mwa vijana wenye kupinga dini na hali ya kidini. Na kuna waliovutiwa na mirengo ya kimaada inayokuja wakajiunga na vyama vya mrengo wa kushoto, ujamaa, baath na Qaumiya mbalimbali vilivyokuwepo wakati huo. Na kuna walioishi maisha ya kutojali, hawajali upande wa kidini wala wa kijamii, wanaifanya dini kwa mazoea ya kawaida ya kuiga, wakati ambapo 281


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

baadhi wameachana kabisa na vitendo hivi, nao ni wengi. Na katika mazingira haya nilianza kufikiria kwamba haiwezekani kasoro iwe ndani ya dini, kama ambavyo haiwekani kuwatuhumu hawa vijana kwamba wao wana uovu au maradhi au upotovu wa dhati wa kimazingira. Tatizo halipo katika dini wala halipo kwa watu wenyewe na vijana wenyewe, bali tatizo lipo katika kuitangaza dini na katika njia ya kuitangaza dini. Kwa hiyo nilianza kuelekea kwenye uboreshaji katika kueleza dini, na kuboresha katika ufahamu wa watu katika dini. Na nilianza kwa nafsi yangu. Kwanza nilijaribu kuelewa uhalisia wa dini, je, dini ni ile iliyoenea kwa baba zetu na mama zetu na katika mazingira ambayo tunayaona mbele yetu? Au ni kitu chenye kina zaidi na ukweli na kilicho karibu na uhalisia wa dini? Bila shaka kulikuwa na maandishi ya maulamaa wa Waislamu ambao waboreshaji wao ndio wamepanda mbegu za medani ya Kiislamu mpya tukufu. Kwa kuzisoma na kuzikaribia, na kutafakari humo niliweza kufikia ukweli kwamba inapasa mimi niwe na jukumu katika kusukuma na kuunga mkono harakati za kuboresha dini katika jamii; Kwa ajili ya watu kujua uhalisia wa dini yao, na kwa ajili ya kuwarejesha hawa watu kwenye dini yao, na hawa ambao wameacha dini yao, na wao kwa uhakika hawakuacha dini bali wameacha ambayo yanaitwa dini, na ambayo yamejulikana kwamba ndio dini katika mazingira yao na katika jamii yao. Tulianza – namshukuru Mwenyezi Mungu – kutekeza jukumu letu katika nyanja hii kupitia maandishi, hotuba na kupitia mahojiano ya moja kwa moja. Na kwa taufiq ya Mwenyezi Mungu tumechangia katika medani na katika nyanja hii. Tunamuomba Mwenyezi Mungu qabul na taufiki. 282


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Al-Watwan: Acha tuzungumzie juu ya uhuru katika nyanja ya fikra ya Kishi‟ah, kuna tajriba za Kishi‟ah zimeandika ambayo zinazingatia kuwa ni uboreshaji wa fikra ya Kishi‟ah katika kurejea kwake vitabu vya hazina ya Kishi‟ah na mtazamo wake katika baadhi ya riwaya na misimamo kutoka katika baadhi ya mambo, kwa mfano aliyoyaandika al-Musawiy na Ahmad alKaatibu na anayakariri mwishoni Sheikh Fadhwilu llahi na radu fiili katika mazingira ya Kishi‟ah. Je, mnaitakidi kwamba yanayozunguka katika uzio huu yanaelezea majaribio haya kwamba hayafai na yanatia shaka watu wake na kunakuwa na mwelekeo wa kuyaondoa, kwa maana ya kudhibiti uhuru wa kifikra katika duara la Ushi‟ah? Saffar: Kwa hakika inapasa kutofautisha kati ya aina mbili katika hali hizi. Kuna hali ya fikra halisi, kwa maana ya mwanadamu kuwa na rai au fikra, na fikra haikabiliwi ila kwa fikra. Na ikiwa kuna makabiliano ya kimakosa kupitia njia zingine zisizokuwa za makabiliano ya kifikra, basi ni makosa, na wala haisihi kukalia fikra kwa kitu kingine. Na hali hii ambayo humo kunakuwa na fikra na rai maalumu kama tukipekua historia ya Kishi‟ah na historia ya Maimamu  tungeona kwamba Maimamu wanapokea rai zinazowakhalifu, wao au ambazo wanazizingatia kuwa ni potovu kwa majadiliano. Katika zama za Imamu Ja‟far Swadiq  kulikuwa na makundi yaliyojulikana kwa uzandiki, na hawa walikuwa wanaingia kwa Imam Swadiq  na wanatoa kwake shaka zao na mitazamo yao ya kiulahidi. Imamu hakuwakabili kwa ghadhabu wala kuudhika na wala kwa muamala mbaya, bali kinyume chake, alikuwa anawakunjulia moyo wake na kifua chake na anazungumza pamoja nao kwa uwazi. Na wao walikuwa wanajipamba na tabia hii kwa Imamu Swadiq, hadi mmoja wa wanafunzi wa Imamu jina lake ni al-Mufadhwal bin Amru, Imamu alimwandikia barua muhimu na tukufu juu ya tauhidi inayojulikana kwa Tauhid al- Mufadhwal, na sababu ya Imamu kumwandikia risala hii ni kwamba siku moja alikuwa amekaa katika msikiti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu  Madina, 283


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

wakamjia hawa wenye kutia shaka katika dini na katika misingi, na walikuwa wanajulikana kwa uzandiki na ulahidi mfano Abdul-Karim bin Abi al-Aujaai na mfano wake akawa anazungumza mazungumzo yake ya kutia shaka. Al-Mudadhwal akakasirika na akakabiliana naye kwa hasira na ghadhabu, akamgeukia na akamwambia: “Ikiwa wewe ni mtu wa mantinki basi tusemeshe, na ikiwa ni katika wanafunzi wa Ja‟afar bin Muhammad wallahi hakuwa anaamiliana nasi hivi, na hakika sisi tulikuwa tunarejea kwake na tunatoa kwake maneno yetu yote, na zaidi ya uliyosikia hakuwa anaonyesha haya unayoyafanya wewe.” Maimamu  manhaji yao katika kukabilina na fikra ambayo wanaiona ni potovu na ya kimakosa ni manhaji ya majadiliano nayo ni manhaji ya makabiliano ya kifikra. Na kutoa rai hata kama inakhalifu hali iliyoenea na hata kama inakhalifu mazoea ni jambo ambalo haiwezekani kulizuia na kusimama dhidi yake. Sisi hatuwezi kuzuia fikra ya mwingine anayepinga kwa tunayaona na kuyaitakidi, na Mwenyezi Mungu Mtukufu pia hajatupa ruhusa ya kukandamiza fikra na rai, Qur‟ani inasema:

َ

ُ

َ َ َ

ّ

َ ‫”ال إ‬ “….. ِ‫ينِ كذ ج َب ىحن الششذ ِم َن الغ ِ ِّى‬ ِ ِ ‫هشاه ِفى الذ‬ ِ “Hakuna kulazimisha katika dini; uongofu umekwisha pambanuka na upotofu…..” (Surat Al-Baqara; 2:256). Na vilevile anasema (swt):

َ ‫َن‬ َ َ ‫ى‬ ُ َ َ ‫اللى ٌَ َف َي ىدبػى َن َأ‬ “….. ‫خع ِه‬ ‫زين َيعخ ِمػى‬ ‫”ل‬ ِ “Ambao husikiliza maneno, wakafuata mazuri yake zaidi.” (Surat Az-Zumar; 39:18). Na anasema: 284


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

َٰ

َ

ً ُ

َ َ ُ

َ ّ

ٰ ‫… َوإ ا أو إ ّياه لػ‬..” “ ‫بحن‬ ِ ٍ ‫هى هذي أو فى ضلك ٍل ُم‬ ِ ِ “…..Na hakika sisi au nyinyi bila shaka tuko kwenye uongofu au kwenye upotofu ulio wazi.” (Surat Saba‟; 34:24). Utamaduni na uhusiano wa kibinadamu: Al-Watwan: Maadamu tunazungumza kuhusu dini na kuboresha, basi turejee katika majadiliano kuhusu Kiislamu kwa Kiislamu. Hapana shaka kwamba medani ya Kiislamu imeingia katika tajriba nyingi sana, na kupitia tajiriba hizi imekabiliana na vikwazo mbalimbali dhidi ya ambayo yalikuwa yanatolewa miongoni mwa fikra. Na zimekabiliana vilevile na mifumo ya kisiasa. Zimeamiliana pamoja nazo kwa namna maalumu kiasi kwamba imepelekea kuchelewa maendeleo yake kwa kiasi fulani. Kisha ukapatikana uwazi huu ambao tunauona sasa hivi katika ulimwengu wote wa Kiarabu. Majadiliano ya Uislamu kwa Uislamu, sio tu baina ya madhehebu mbalimbali bali hata katika madhehbu moja tunaona mikusanyiko katika kadhia ya majadiliano na uwezekano wake. Ni lipi chimbuko la kadhia hii? Saffar: Dhana yangu ni kwamba chanzo cha chimbuko ni mambo mawili: Jambo la kwanza linafungamana na uelewa wa kimaisha kwa waliowengi katika mazingira yetu na jamii zetu, humo kuna udhaifu mwingi. Hakika anayefahamu maisha na kuelewa tabia ya mwanadamu na tabia ya jamii, na kuelewa mabadiliko ambayo yanatokea, hakika uelewa wake unamsukuma kufuata manhaji ya kufunguka na majadiliano pamoja na wengine. Ama anapoishi ndani ya fikra zilizogeuzwa, na ndani ya vitu vilivyo tayari na anaviamini, hii ni dalili kwamba uelewa wake ni dhaifu. 285


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Kwa hiyo hafanyi juhudi kwa ajili ya kufunguka kwa wengine na kunufaika kwa walivyo navyo na kuwakinahisha kwa aliyonayo yeye, hivyo jambo la kwanza ni jambo la uelewa. Ama jambo la pili ni jambo la tabia ya jamii ambapo inaonyesha kwamba kutoendelea au kuendelea umma wowote ni kwa sababu mbili: Upande wa kifikra na maarifa, na upande wa muundo wa uhusiano uliotawala. Na jamii yetu inakabiliwa na mengi miongoni mwa kutoendelea katika nyanja hii na muundo wa uhusiano ulioenea baina yake, na kwa hiyo inakuwa ni vigumu kwetu kushirikiana, na inakuwa ni vigumu kwetu kuelewana, na inakuwa ni vigumu kwetu kuhudumia maslahi yetu ya pamoja. Na hii inatokana na kutoendelea, kwa udhaifu wa mambo mawili, uelewa kwa maana akhlaqi ya kuamiliana na kushirikina, haya yako nyuma ya ufinyu wa upeo, na nyuma ya kujizuia juu ya majadiliano na kufunguka. Majadiliano pamoja na wengine: Kwa hakika mwanadamu anapokuwa na fikra au anapokuwa na rai je, anataka kuidhalilisha nafsi yake na kukinahika na kuchukua fikra ya kimakosa? Hakika yeye ni kama mwanadamu mgonjwa ambaye anapatwa na maradhi, kwa nini atumie dawa? Je si kwa sababu ya afya, hivyo ni wajibu atafute dawa ambayo itamfikisha kwenye afya. Mimi nataka fikra inayonifikisha kwenye ukweli, hivyo ni juu yangu ni hakikishe kwamba fikra ambayo ninayo ndio njia sahihi kuelekea kwenye ukweli. Namna gani nitakuwa na uhakika wa hilo? Kati ya njia za msingi za kuwa na uhakika ni kujua fikra za wengine ili nipate uhakika kwamba fikra yangu ndio sahihi, au kuna fikra nyingine iliyo sahihi, au iliyo sahihi zaidi kuliko fikra yangu. Mwanadamu kwa ajili ya dhati yake yeye ni wajibu 286


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

afunguke juu ya fikra zingine. Hakika mtu miongoni mwetu anapokwenda kununua bidhaa, hakika anajaribu kujua hiyari mbalimbali na wala hakubali hiyari ya kwanza inayotolewa kwake, kwa sababu anataka kuwa na uhakika kwamba bidhaa ambayo anaichukua ndio bora zaidi. Huu ni mfano tu. Ama katika upande wa kifikra ni wajibu tuwe ni wenye kujali sana usahihi wa fikra zetu na usalama wake. Kwa hiyo kuna neno zuri linanukuliwa kutoka kwa Imamu Hasan bin Ali  anasema: “Nimemshangaa mwenye kufikiri katika chakula chake namna gani hafikirii katika akili yake na kuliepusha tumbo lake na ambayo yanaliudhi, na anaingiza katika akili yake yanayoliharibu.” Katika upande wa kifikra ninaposikia fikra ni wajibu niwe na uhakika nayo. Na katika manhaji ya kuwa na uhakika ni kujua fikra za wengine. Na kujua kwangu fikra nyingine ama kunanihakikishia usahihi wa fikra yangu au kunanifichulia juu ya usahihi wa fikra nyingine. Na popote nitakapoikuta haki ni wajibu niichukue hata kama iko kwa mwingine. Maslahi ya pamoja: Katika duara la Sunni na Shi‟ah tutaanzia wapi? Saffar: Kwa hakika kuna mjadala kuhusu wapi mjadala uanzie, ambapo baadhi wanaona kwamba mjadala ni wajibu uanzie katika upande wa kiitikadi kwa kuzingatia kwamba misimamo ya kila upande au kila madhehebu miongoni mwa madhehebu inategemea juu ya itikadi zake, hivyo tuanze mjadala katika upande wa kiitikadi. Na hapa Maulamaa wanaamini rai hii na pendekezo hili. Na kuna rai ya pili, inaona majadiliano yanapasa yawe katika misingi ya kifiqihi na sharia kwa kuzingatia kwamba itikadi na 287


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

fikra zinakuwa ni hali ya kinafsi na kiakili, wakati ambapo sharia ndio hali ya kimaisha baina ya watu, na haiwezekani kujadili kuhusu masâ€&#x;ala mbalimbali ya kifiqihi kwa sababu yanategemea misingi maalumu. Basi tujadili kuhusu misingi hii nayo ni misingi ya fikihi. Ama pendekezo la tatu ni majadiliano yaanze katika maslahi ya pamoja na uhalisia wa maisha ambao umma unaishi nayo, na mimi binafsi naona ni bora majadiliano yaanze katika nyanja hii na sio katika nyanja mbili zilizotangulia kwa mambo mawili muhimu: Kwanza: Kwa umuhimu wa hali ambayo inazunguka umma wetu wa Kiarabu na wa Kiislamu katika zama hizi, na changamoto na hatari ambazo zinatuzunguka, na haya yanawajibisha kwetu kujadiliana kwa ajili ya kulinda nafsi zetu, sote tumepanda ndege moja na meli moja tukipatwa na gharika au uharibifu basi tutaangamia sote, pamoja na kutofautiana itikadi zetu na madhehebu yetu na rai zetu. Hivyo kwanza tuhifadhi meli hii ambayo tumeipanda, tuanze majadiliano kuhusu maslahi yetu ya pamoja, na kuhusu mambo ya maisha ambayo yanatuzunguka kwa sababu ndio yenye hatari nyingi na yenye athari zaidi. Pili: Kwa sababu yanatuandaa kinafsi, kifikira na kijamii katika kujadili pande zingine. Na tunapojadili vizuri na kufahamiana kuhusu maslahi ya pamoja, haya yanafanya nafsi zetu kuwa tayari kwa ajili ya kujadiliana katika mambo ya misingi ya kifikihi, katika mambo ya kiitikadi na katika mambo yote. Tunapoanza na maslahi ya pamoja inakuwa rahisi kwetu baada ya kuhama katika majadiliano ya kiitikadi na katika misingi ya kifikihi katika rai binafsi ambapo tumeanza katika nyanja hizo. Hili litatushughulisha na hali yetu ambayo haivumilii kucheleweshwa katika kukabaliana nayo, na katika kutatua mambo yake. Na inaweza kusababisha baadhi ya msuguano kwa sababu nafsi bado hazijawa tayari. 288


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Kuanza na viongozi wa kifikra: Katika kuitakidi kwamba kujitolea kunaanzia na viongozi wa fikra au taasisi za fikra, ni nani ataanza majadiliano na kujitolea kuita pande zingine, je, ni sahihi zaidi kujitolea huku kuwe ni kwa kupitia viongozi wa wananchi kifikra au ni kupitia taasisi na vyanzo vya fikra? Saffar: Kwa hakika viongozi wa kifikra wanaathari kwa watu na kwa jamii, nao ndio ambao inawapasa kujitolea kwa majadiliano. Na haya yalikuwa ndio tumaini la mashujaa wa medani ya Kiislamu na harakati za Kiislamu. Medani ya Kiislamu haipo tu kwa Shiâ€&#x;ah bila ya Sunni wala kwa Sunni bila ya Shiâ€&#x;ah. Kisha medani ya Kiislamu na mashujaa wa Kiislamu katika medani ya Kiilsamu kwa ujumla wanahusika na majadiliano. Mashujaa wa Kiislamu wenye uelewa ambao wanaunda hali ya medani ya Kiislamu inapasa majadiliano yaanzie kwao. Kama ambavyo naitakidi kwamba taasisi rasmi maalumu katika sehemu ya ghuba na kisiwa cha Kiarabu zinalengwa na majadiliano vile vile, vyama na harakati kwetu zinajua hatari zinazozunguka sehemu hii, na zimekabiliwa na matatizo ya kisiasa, ya ndani na nje, katika hatua zilizopita. Na mimi natarajia kuwa vyama hivi viwe vinashajiisha hali ya majadiliano baina ya wafuasi wa madhehebu yaliyopo katika nchi; kwa sababu hii ndio inadhamini kushikamana kwa wananchi baadhi yao pamoja na baadhi na kupambana na hatari. Na kwa hiyo natamani kwamba kati ya mazingatio ya majilisi ya kusaidiana ya Ghuba na serikali katika dola za Ghuba kuwe na hali ya kushajiisha hali ya kufunguka baina ya madhehebu yaliyopo ndani ya jamii za Ghuba na wananchi wa Ghuba. Sisi tunajua kwamba kuna wanaofuata madhehebu ya Zaidiya, na madhehebu ya Ibaadhi, na kuna wanaofuata madhehebu ya Ithina Asharia, na wanaofuata madhehebu manne katika AhlusSunna, na wote wanaishi katika sehemu hii, na kuna nguvu za nje 289


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

zinanyemelea sehemu hii. Na kama hakuna ushirikiano na kufunguka, hakika ikhitilafu hizi za kimadhehebu zinaweza kuwa ni mwanya kwa nguvu zingine za nje kupenya kwao na kuchezea amani ya sehemu yetu na nchi yetu. Serikali ya nchi vilevile inapaswa kushajiisha na kusukuma kuelekea kwenye majadiliano na kufunguka kimadhehebu. Baina ya Qum na Najaf: Tunahama kidogo katika duara hili, na tuzungumzie kuhusu yanayotolewa katika medani ya fikra ya Kishi‟ah kwa yanayoitwa vita baridi baina ya “Qum” na “Najaf.” Ikiwa hali hii ipo je, kwa itikadi yenu ina sababu na chanzo cha kielimu au kuna sababu za kimaeneo kwa maana baina ya Madrasa ya Iran na Madrasa ya Iraki? Saffar: Mimi siitakidi kwamba katika hatua hii kuna vita baridi baina ya Najaf na Qum; kwa sababu Najaf nafasi yake sasa hivi imedumaa na imesimama katika utawala wa Iraki, na hawza ya elimu Qum ndio hawza inayojitokeza na ambayo hivi sasa inalea Madrasa za kidini za Kishi‟ah na inalea maulamaa na Marajii. Ni sahihi kwamba katika Najaf tukufu kuna marajii na kuna kundi la wanafunzi lakini wao hawaamini hata katika nafsi zao, kama tulivyojua kupitia meizi iliyopita, kwamba wengi wa wanachuoni waliuliwa na kuteketezwa, na Maulamaa waliopo sasa hivi Najaf na Maraajii wakubwa hawako salama katika nafsi zao na kwa hiyo wamejifungia katika nyumba zao na hawapokei wageni wala hawatoki katika nyumba zao. Katika hali kama hii hakuna kuzungumzia kuhusu vita baridi baina ya Najaf na Qum. Hawza ya elimu katika Ghuba: Maadamu tunazungumza kuhusu hawza ya elimu, nini rai yenu katika yanayotolewa kuhusu kuanzisha au dharura ya kuwepo hawza ya elimu katika Ghuba? 290


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Saffar: Mimi naitakidi dharura ya jambo hili, na naitakidi dharura ya kuwepo hawza za kidini za Kishi‟ah kila sehemu katika nchi zao. Na hiyo ni kwa sababu wanaokwenda katika hawza za elimu aghlabu ni katika umri mdogo. Na kijana huyu ambaye anakuwa na hamasa ya kidini ikiwa hatapata masomo ya dini katika nchi yake na katika mazingira ya nchi yake, na kutoka kwenda nchi zingine, hatujui namna gani itakuwa hali yake, na ni mazingira gani ambayo ataishi humo katika nchi hizo? Na anabakia muda mrefu huko kisha anarejea haendani na mazingira yanayobadilika na kugeuka katika jamii yake. Ni bora kuwepo na hawza za elimu za Kishi‟ah katika sehemu zao katika Ghuba na kisiwa cha Kiarabu, wanafunzi wa elimu wasome masomo yao ya awali katika hawza hizi, na wakihitajia masomo ya juu, mwanafunzi anakuwa amekwishakua kiasi fulani na shakhsiya yake imepevuka, na amekwishavuka umri wa ujana na ubarobaro na mchemko. Na baada ya hapo hakuna tatizo kusafiri kwenda nchi nyingine kuendelea na masomo yake ya juu. Lakini kwa sababu ya kutokuwepo hawza za elimu za kidini za Kishi‟ah katika ghuba na kisiwa cha Kiarabu, hakika mtu yeyote anayetaka kusoma dini katika umri mdogo ni juu yake kuhama nchi yake na kwenda sehemu nyingine, naye yuko katika umri huu, na kuishi katika mazingira mengine yanayotofautina na mazingira ya nchi yake na hali ya nchi yake kisiasa, kijamii na kifikra. Na inaweza kutokea kwamba ameishi katika hali ya mkanganyiko au hali ya kutopevuka katika kuchukua ambayo ni wajibu ayachukue au kuyaacha, hivyo ni bora kuwepo na hawza katika sehemu za Kishi‟ah. Sababu za kielimu na kisiasa: Ni zipi sababu za kutokuwepo hawza hizi, Je ni sababu za kisiasa au kielimu? Saffar: Katika baadhi ya nyakati ni sababu za kielimu, kwa 291


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

sababu kuwepo hawza kunahitaji kuwepo idadi ya maulamaa wanaojihusisha na kufundisha, na maulamaa ni wachache katika nchi. Na waliopo miongoni mwao wanashughulika na majukumu ya kijamii. Na katika baadhi ya nyakati sababu inakuwa ni kutokuwa wazi umuhimu wa kuwepo hawza mbele ya pande zinazotawala na mbele ya mifumo na serikali, jambo ambalo linawafanya wao wawe hawashajiishi mfano wa mambo haya. Je, kuna fikra makini ya kuleta mfano wa hawza hizi katika Ghuba katika mustakabali? Saffar: Kuna mwanzo mzuri sasa hivi, lakini inahitaji kushajiisha na wakati ili kustawi kwa namna bora. Kwa mfano Kuwait tangu mwaka 1971 kulikuwa na tajriba ya kuleta hawza ya kidini, wakati alipokuwepo huko Imamu Sayyid Muhammad Shiraziy, alianzisha madrasa ya kidini na niliishi huko miaka mingi na lilikuwa ni jaribio elekezi na zuri. Sasa hivi kunapatikana jaribio katika sehemu mbalimbali za dola za ghuba na kisiwa cha Kiarabu kwa mwelekeo huu. Lakini linahitaji msaada sana kutoka kwa watu na kushajiisha kutoka kwa serikali katika sehemu hii. Mwanamke na mwanaume wana nafasi sawa: Sasa hivi tunahamia kwa mwanamke na nafasi yake katika fikra ya Kishiâ€&#x;ah, kuhusiana na kadhia ya mwanamke kuna hali isiyofahamika na utetezi unaohusiana na kadhia ya muta? Saffar: Ni vema kusema kwamba mwanamke katika Uislamu ana nafasi ileile aliyonayo mwanaume na hakuna tofauti baina ya thamani ya mwanaume na dauru yake au thamani na dauru ya mwanamke. Na katika nususi za Kiislaamu kupitia Qurâ€&#x;ani na kupitia hadithi na riwaya, na kupitia sira ya Waislamu wa mwanzo hakuna tofauti baina ya mwanaume na mwanamke Na tofauti hii ambayo tunaiona kivitendo katika maisha ya Waislamu 292


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

baina ya mwanaume na mwanamke sio ya Kiislamu bali ni kutokana na ufahamu wa mila, kuiga na kutokuendelea kwa ujumla ambako jamii zinaishi lakini imenasibishwa katika Uislamu, na hali hii sio ya Kiislamu na iko mbali nayo. Na mwanamke katika nyanja mbalimbali ni sawa sawa katika nyanja ya kisiasa au katika nyanja ya kijamii au katika nyanja ya kielimu, jambo lake ni kama jambo la mwanaume kabisa, ila yale yanayotolewa nayo ni machache sana. Na kwa hiyo unakuta kuna mapendekezo mapya na makini ya kuvuka hali hii ya kuunda baina ya nafasi ya mwanaume na nafsi ya mwanamke katika jamii ya Kiislamu. Mnajua kwamba sasa hivi Iran kuna uchaguzi wa baraza la Maulamaa nalo ni baraza ambalo linachagua uongozi. Na sasa hivi kuna mazungumzo muhimu katika medani ya Kiiran kwamba inapasa mwanamke kuchagua na awe na haki ya kuchagua baraza la Maulamaa. Na katika katiba ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hakuna kinachomzuia mwanamke kuchagua katika baraza hili, nalo ni chombo cha juu cha kuchagua uongozi Iran na kusimamia mwenendo wa uongozi. Na katika upande wa kifiqihi kuna mjadala baina ya maulamaa wetu kuhusu je, inajuzu kumqalid mwanamke au hapana? Na sisi tuna kitu kinachoitwa Marjaa, naye ndio anayefuatwa. Na mafakihi wote wako katika nafasi ya uhuru na majadiliano, wanasema hakuna kizuizi katika upande wa kisharia katika kumqalid mwanamke kwa sababu ya ujumla uliopokewa “Waulezeni wanaojua ikiwa nyinyi hamjui.” (Surat Nahli: 43). Hakuna humo kikwazo katika sharti kwamba wenye kujua ni katika wanaume, na riwaya na nususi zilizopokewa kwa kurejea kwa Maulamaa na kuwaheshimu maulamaa na elimu vilevile sio mahususi kwa wanaume bila ya wanawake, Qur‟ani tukufu inasema: “Sema je, wanalingana wanaojua na wasiojua.” (Surat 293


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Zumar: 9), na Qur‟ani inamtofautisha mwenye kujua na asiyejua, sawa sawa awe mwanaume au mwanamke. Na katika historia yetu mwanamke alikuwa na dauru ya uongozi, kisiasa, kielimu na kidini vilevile. Na sisi tunapozungumza kuhusu kadhia ya Karbalaa na Ashura tunataja kwamba Imamu Husein  alimuusia dada yake bibi Zainabu na alikuwa baada ya Imamu Husein kufa shahidi ndio marji‟i wa Kishi‟ah; kwa sababu Imamu Zainul-Abidin Ali bin Husein alikuwa mgonjwa, hivyo Shi‟ah walikuwa wanarejea kwa Bibi Zainabu. Na tunayo mambo mengi vile vile katika historia ya Maimamu wetu. Walikuwa wanaamuru kurejea kwa wanawake katika baadhi ya mas‟ala, jambo linaloonyesha juu ya mwanamke kuchukua nafasi ya kuwa Marjaa taqlid au rejea ya fatwa ya kisharia, na hakuna kizuizi humo. Mwanamke na siasa: Dauru ya siasa iko wazi tangu zama za mwanzo za Kiislamu katika msimamo wa Bibi Fatimah Zahraa  ambaye alikuwa mwenye rai ya kisiasa baada ya kufariki Mtume wa Mwenyezi Mungu . Na Bibi Aisha , vilevile ana rai ya kisasa inayokhalifu rai ya Imamu Ali  na kumalizikia na matukio mengi ambayo mwanamke humo alikuwa na rai na mchango katika siasa. Hivyo hali iliyopo ya tofauti baina ya nafasi ya mwanaume na mwanamke kiasi ambapo mwanamke anazingirwa kwa kazi za nyumbani tu, hali hii haitokani na Uislamu, bali inatokana na mila na kuiga katika jamii mpya. Na kwa munasaba huu mimi nina kitabu kilichochapishwa katika nyanja hii chini ya anwani Masuuliyatul-Mar‟atu humo kuna mjadala kuhusu nyanja hizi. Kuhusu Muta: Ama katika yanayohusiana na maudhui ya mut‟a mimi binafsi naona kinyaa kukariri sana kueleza maudhui haya na kuyatetea 294


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

sana. Na naitakidi kwamba pande mbili zinashiriki; upande unaoeleza tatizo hili na kueneza maudhui haya na kuyazingatia kuwa ni kauli ya madhehebu ya Shi‟ah. Kuruhusu mut‟a kunapelekea kuenezwa na kuaibishwa Shi‟ah kwa sababu wao wanahalalisha Muta. Uenezaji huu unapelekea kuchochea ubaguzi. Na wote wanajua kwamba kadhia ya mut‟a sio mahususi kwa madhehebu ya Shi‟ah kwani imetajwa katika Qur‟ani tukufu, na imetajwa katika sahihi al-Bukhariy, na imetajwa katika sahihi Muslimu. Na asili ya sharia ya Muta wanaikubali wote, bali ikhitilafu ni kwamba imefutwa au haikufutwa. Na maadamu mas‟ala yapo katika Qur‟ani na katika hadithi sahihi zilizopokewa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu , anayesema hivyo hajazuia kitu chochote. Na sote tunakubali kwamba jambo hili lilikuwa la kisharia lakini je, limefutwa katika zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu , kama zinavyoonyesha riwaya zilizopokewa katika sahihi al- Bukhariy na sahihi Muslim au kufutwa ilikuwa ni katika zama za khalifa wa pili Umar bin al-Khatab kama ambavyo riwaya zingine zinaashiria? Na maadamu ni mas‟ala ya kifiqihi ambayo yanatafutwa katika kitabu cha fiqihi na Nikahi na yana asili katika sharia kwa nini linachukuliwa kama mada ya uchochezi na kuaibishana? Na katika upande mwingine, sisi Shi‟ah katika baadhi ya nyakati inatokea kusababisha uchochezi huu, na mimi ninapokuta kwamba kuna uchochezi najaribu kutetea nafsi yangi. Na vile vile rai yangu na msimamo wangu niko baina ya misimamo miwili, wa kwanza na wa pili kwamba yote imejaalia kuzingatia jambo hili kana kwamba ni kadhia kati ya kadhia na tatizo kati ya mataizo. Na katika upande rasmi, sasa hivi katika jamhuri ya Kiislamu ya Iran ndoa ya mut‟a hairuhusiwi na haifanywi. Na tunapokuja katika mazungumzo katika upande wa kijamii, je kuhalalisha huku kuna madhara au kuna manufaa; hili pia lina utafiti wa 295


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

kimaudhui. Ama kulichukulia kana kwamba ni anwani ya madhehebu ya Kishi‟ah, na Shi‟ah wanalichukulia kana kwamba ni vita ya kimsingi kwao, jambo hili halina sababu na linaleta kinyaa na kero. Baina ya hazina ya Kisunni na Kishi‟ah: Kuhusiana na Marjaa wa kifikihi na hazina ya Kishi‟ah kuna anayeitakidi kwamba kuna haja ya kurejea kwa matarajio ya kuzichambua baadhi ya riwaya zilizoandikwa ambazo zinazidisha ukubwa wa masafa baina ya madhehebu ya Shi‟ah na madhehebu meingine, na haya ni masafa marefu, je hamwitakidi kwamba kazi hii inahitajia mwenye kujitolea kwayo kwa juhudi? Saffar: Kwa hakika hazina yote ya Kiislamu ni sawa sawa iwe ni katika rejea za Kishi‟ah au za Kisunni zinahitaji kuchambuliwa na kukaguliwa na baadhi yake zinahitaji kuhakikiwa usahihi wake na kutokea kwake, na baadhi yake zinahitaji kutazamwa upya katika ufahamu wetu wa nasi (tamko) hata katika usahihi wa nasi (tamko) na vipi tunaifahamu. Hazina yote ni sawa sawa yaliyopo kwa Sunni na kwa yaliyopo kwa Shi‟ah yanahitaji utafiti, lakini kinachoshangaza, sisi tunakimbia kukosolewa na kila mmoja anaelekeza ukosoaji kwa mwingine na sio katika dhati yake. Shi‟ah anakosoa yaliyopo katika hazina ya Sunni lakini hana ushujaa wa kukosoa hazina yake. Na Sunni vilevile anakosoa yaliyopo katika hazina ya Shi‟ah na hana ushujaa wa kukosoa yaliyopo katika hazina yake vilevile na kutazama upya humo. Na kwa hakika hazina zetu zote, za Kisunni na za Kishi‟ah kuna haja ya kuzitazama upya. Na katika yanayosaidia kutazama upya katika hazina ya Kishi‟ah ni kwamba Shi‟ah hawana kitabu sahihi, na ikiwa Ahlus suna wana vitabu vitano sahihi au Sahihi Sita na ikiwa wana Sahihi Bukhari na Sahihi Muslmu, Shi‟ah hawana rejea ya hazina inayozingatiwa kuwa ni sahihi bali wanaona yote yaliyopo katika 296


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

rejea zao yanakubali kufanyiwa utafiti na kujadiliwa. Mfano vitabu vine kwetu sisi Shiâ€&#x;ah ambavyo tunavizingatia ni rejea: alKaafiy, Tahadhib, al-Istibswar na Man laa Yahudhuruhu alFaqih, vitabu hivi vinne kwetu tunavitegemea kama rejea na kila faqihi kati ya mafaqihi na kila marjiâ€&#x;i anapokuja ni lazima afanye ijitihadi katika kila riwaya katika rejea na wala haisihi kwake kutegemea kwamba riwaya hizi amezisahihisha Kulainiy, au Tuusiy, na kujengea katika hilo kitendo, bali ni wajibu atumie rai yake na ijitihadi yake humo. Na ametunga mmoja wa maulamaa wa kileo kitabu amekiita Sahihi al-Kaafiy, kimekusanya riwaya ambazo anaziona ni sahihi. Amekiita Sahihi al-Kafiy, lakini wakampinga Maulamaa; kwamba kwa sababu haya ni sahihi kwa mtazamo wake wewe na sio sahihi kwa mtazamo wa mujitahidi wengine, na wanaweza kutofautiana na wewe katika rai, hivyo hakuna ambayo yana uhakika na yamekubaliwa moja kwa moja katika vitabu vya hazina ila baada ya udadisi na utafiti katika baadhi ya riwaya, na ni sawa sawa katika usahihi wa sanadi na kuthibiti kupokewa kwake au katika ufahamu wao kwazo. Lakini ndugu zetu Ahlus-Sunna wanaweza kuwa na ugumu; kwa sababu baadhi ya sahihi na hususan Sahihi al-Bukhariy na Sahihi Muslim zimekuwa na nafasi katika nyoyo za watu na kuaminiwa kwa maulamaa kiasi kwamba inakuwa vigumu kukhalifu kitu kilichopokewa humo. Na kwa upande wa mtazamo wetu tunaona inatakiwa kuwepo na nafasi ya kurejea kutazama yote yaliyopokelewa. Na kisicho na shaka ni kitabu cha Mwenyezi Mungu ambacho hakipatwi na batili mbele yake wala nyuma yake, kisichokuwa hicho, kuna uwezekano, ama katika usahihi wa kupokea tamko au katika uelewa wetu wa tamko. 297


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Makosa kwa jina la Ashura: Ashuraa ni mnasaba wa kila mwaka, humo Shi‟ah wanazungumzia kwa njia ya kukariri matukio ya Karbalaa, na kunatimia kutengeneza humo kanuni ya kisharia ya kihisia na kimadhehebu kwa namna wanayoona baadhi haitumikii hata uhalisia wa fikra ya Kishi‟ah na yanayoambatana na mazingira ya mnasaba miongoni mwa kuvaa nguo nyeusi na mavazi ya watoto yanaandikwa juu yake: “Yaa lithaaril-Husein.” Matumizi haya ya kila mwaka wanapata nini Waislamu na umma wa Kiislamu? Je haiwezekani kubadilisha manufaa ya mnasaba huu kwa nembo ya ustawishaji na nzuri zinazokidhi haja ya Waislamu, na kuanzisha miradi ya kheri na kujadili matatizo ya umma na yanayoukabili miongoni mwa hatari? Saffar: Kwa hakika mazungumzo kuhusu Ashura kwa Shi‟ah yana pande mbili: Upande wa majaaliwa, na kuna upande wa uhalisia kivitendo ambao tunaishi nao. Kuhusiana na upande wa kivitendo wa kimuamala kwa hakika kuna mengi yanayohitaji mabadiliko na kuboresha, ni sawa sawa iwe ni katika upande wa hotuba ambazo zinatolewa juu ya mimbari katika muharam au katika mazingira ya jumla ambayo yanazunguka mnasaba. Na kuna ambayo yanahitajia kukosolewa na kuboresha, na haya yanapendekezwa hata ndani ya madhehebu na kutoka kwa maulamaa na wanafikra wa madhehebu. Lakini upande mwingine kuhusu msingi wa maudhui, asili ya mnsaba, kwa nini tunadhimisha mnasaba wa Ashura? Ashura ni mnasaba wa kila mwaka wa kujadidisha ufuasi wa Ahlul-Bayt wa Nabii , na haya kwa asili hakuna shaka humo, na kuna mnasaba mwingine katika mwezi wa Rabiul-Awwal kwa Waislamu wengi huhusu uzao wa Mtume wa Mwenyezi Mungu  na masahaba wake, na Waislamu katika sehemu mbalimbali wanaadhimisha mnasaba huu kwa sherehe na mapumziko rasmi katika nchi mbalimbali za Kiislam. Na kuna vituo vya muda Waislamu ndani yake wanataja mafunzo ya kihistoria na wanajadididsha ahadi katika shakhisya 298


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

ya dini yao na misingi yao. Na hii katika asili hakuna shaka humo, bali tatizo ni katika njia ya kuadhimisha na njia ya kivitendo. Na nukta ya pili kuhusiana na Ashura na yanayoambatana nayo katika hali ya kiroho na hisia ambayo inaizunguka, inawezekana kuitumia kwa matumizi bora zaidi na kunufaisha watu na kunufaisha nchi hizi, na kunufaisha wananchi hawa. Na mimi naitakidi kwamba kutekeleza mambo haya, hivi sasa tunayo makhatibu wenye uwezo ambao wanatoa khutuba nzuri zenye manufaa ya aina mbalimbali na wananufaisha jamii kupitia khutba hizi. Ashura katika upande wa malezi: Sisi tunaona kwamba kuna upande mwingine katika kuhuisha mnasaba huu, kwamba kunatusaidia sana katika kusimama dhidi ya mafuriko haya yenye kukokoteza miongoni mwa fikra za kimaada na za kimatamanio katika jamii zetu. Na tunaona sisi athari za mnasba huu; kwa sababu vijana wa kiume na wa kike katika siku hizi kumi wanaishi katika mazingira haya ya kidini na wanasikiliza khutuba na wanasikiliza mambo ya kidini, kihistoria na akhlaqi, nayo yana manufaa sana. Na tunaona sisi katika jamii zetu matokeo mazuri katika msimu huu kila mwaka, kiasi kwamba kama si msimu huu na uhamasishaji huu wa kidini na kiroho, hali katika jamii yetu katika upande wa tabia, kijamii na kidini ingekuwa mbaya sana, kuliko ilivyo hivi sasa. Lakini hii haimaanishi kukubali yote yanayotendeka, wala haisihi kutosheka na mbinu na njia zilizozoeleka kwa baba zetu na babu zetu pamoja na kubadilika wakati na zama Inapasa vilevile kubadilisha njia na mbinu, na haya sasa hivi yanapendekezwa, lakini kama mnavyojua watu wa kawaida na jamhuri wanapozoea ibada fulani, mabadiliko humo sio jambo rahisi, hususani na kuna nguvu za mazoea zinazokabiliana na jaribio lolote la kubadilisha na kuendeleza. Na sisi kwa mfano tumejaribu kupendekeza mkakati wa kujitolea damu katika siku za Muharam, na mkakati 299


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

huu umefaulu na waliojitokeza walikuwa wengi sana kiasi kwamba hatukuweza kutoa damu za wote waliojitolea katika mnasaba huu. Mfano katika mkakati huu unawakilisha upande kati ya pande za manufaa katika mnasaba huu, na mimi naunga mkono rai ambayo mmeitaja na nailingania na pia naipendekeza katika baadhi ya mihadhara yangu. Hakika sisi kila mwaka siku za Ashura inapasa kufikiria katika nembo kwa anwani inayolenga kuhusu khutuba na mapendekezo, na kuhamasisha katika mwelekeo wake. Wakati mwingine kuhusu umoja wa nchi, na umoja wa Kiislamu, na katika mwaka wa pili inakuwa kuhusu kunyanyua vipaji na wakati mwingine inakuwa kuhusu kukabiliana na hali ya uzembe na mambo ya ustawishaji. Sisi tunaona rai hii na tunaona vilevile kila mwaka tupendekeze mradi wa kijamii unaotokana na mnasaba huu, kama vile jamii kujenga nyumba za mayatima, na wakati mwingine kujenga vituo vya utafiti na kadhalika. Na fikra hizi tunazozipendekeza nazo zipo katika medani lakini hivi sasa zipo katika hatua ya awali ya kukabiliana na yaliyorithiwa, kuzoeleka na desturi. Vipaumbele vya kazi ya Kiislamu: Kazi ya Kiislam katika Ghuba au kwa kinachoitwa medani ya Kiislamu, inapungukiwa na nini, je, mahusiano baina ya makundi yake au kufunguka kwa watu katika kuingia katika miradi ya ustawishaji. Na medani hii ya Kiislamu yenye aina mbalimbali za madhehebu zake ni sawa sawa kifikra au kimadhehebu inapungukiwa na nini? Saffar: Kwa hakika kinachopungua katika medani hili kwa mtazamo wangu ni mambo mengi: Jambo la kwanza: Vipaumbele vya kijamii na kisehemu, kama 300


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

maneno yatasihi, makundi mengi ya Kiislamu na mirengo ya Kiislamu iliyopo katika ghuba katika asili ni madrasa za kifikra ambazo zimetoka katika sehemu zingine, na kisha tunaona kwamba zimehamisha mazingatio ya vipaumbele vya sehemu zingine kwenye sehemu zake, na havikuchukua uhalisia wa sehemu nyingi kwa jicho la mazingatio. Sisi tunahitaji kuzifahamu pande hizi za Kiislamu au makundi haya ya Kiislamu pamoja na mazingira yake na kuweka vipaumbele vyake, navyo ni vipaumbele vya sehemu na jamii zake, hii ni nukta ya kwanza. Nukta ya pili ni maudhui ya uhusiano na kufunguka pamoja na mirengo mbalimbali na pamoja na hali mbalimbali za kimadhehebu. Kwa ujumla ni wajibu kuwepo na kufunguka baina ya mirengo hii mbalimbali. Na maudhui ya tatu ni mliyoashiria kwayo, nayo ni masâ€&#x;ala ya ustawishaji na ushirikiano wake katika kustawisha jamii hizi, na katika kutatua changamoto ambazo jamii hizi zinaishi nazo. Na ninaongezea katika hayo kitu kingine cha nne, nacho ni uboreshaji wa kifikra. Jamii zetu katika ghuba ni jamii zilizojihifadhi, na fikra hiyo ya kujihifadhi imejikita katika medani yetu sana kuliko sehemu nyingine. Na harakati ya Kiislamu inapaswa kufanya kazi ya kuelimisha na kuboresha na kuwafahamisha watu harakati ya dini yao kwa ambayo yanaendana na zama hizi pamoja na yanayoendana na mabadiliko haya, na kubakia katika mafuhumu yaliyotangulia na istilahi zilizopita na kupendekeza mazingatio na vipaumbele vya zamani, na mengi inayokabiliwa nayo katika medani yake. Haya yanakuwa ni kikwazo cha kuboresha hali ya Kiislamu na medani ya Kislamu. Naitakidi kwamba mambo haya manne ndio ambayo hali ya Kislamu inayahitaji. 301


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

MWEZI WA MWENYEZI MUNGU202 Mwanzo wa makutano: Muadhamu al-Allamah al-Mujahidi Sheikh Hasan Saffar. Asalamu alaikum warahamatullahi wa barakatuhu. Karibu sana katika kikao hiki, na tunawapongeza kwa kuingia mwezi mtukufu wa Ramadhani, Mwenyezi Mungu aurejeshe kwetu na kwenu kwa neema, kwa maghufira na baraka. Mwezi mwandamo na mkanganyiko wenye kutatiza: Muadhamu Sheikh: Mara nyingi unatokea mkanganyiko wenye kutatiza katika medani ya Kiislamu kuhusu kadhia ya mwezi mwandamo, kiasi kwamba tunaona kuna anayefunga na asiyefunga, mwenye kufungua na asiyefungua. Je, hakuna sauti ya mwelekezaji ya kusimamisha mfarakano huu baina ya Waislamu? Kufunga na kufungua ni masâ€&#x;ala ya kisharia. Ni lazima humo kutegemea vidhibiti ambavyo vimewekwa na sharia ili kupanga taklifu humo. Kuna vidhibiti ambavyo ni wajibu kwa muktadha wake kufunga au kufungua kwa mukalifu na haisihi kuwa ni medani ya raghba, ufuasi na hisia. Ikiwa mukalafu ataona kwamba ni wajibu wake kufunga au kufuturu kulingana na vidhibiti vya kisharia ni juu yake kushikamana na taklifu yake, na wengine washikamane na taklifu zao ikitofautiana kuanisha kutimia vidhibiti hivyo, na kila mmoja amwache mwingine na hakuna sababu ya kuingia katika kadhia ya kuzozana na kutuhumiana wala kuwa ni sababu ya kugombana. 202

Majadiliano yaliyofanywa na jarida la Shahru llahi pamoja na Muadhamu Sheikh Hasan Saffaar katika toleo la sita, mwezi wa Ramadhani 1420 Hijiria / 1999.

302


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Hakika jamii zetu zina haja sana na uelewa na kuheshimu rai ya mwingine na kuikubali, na hususani katika nyanja ya kidini iliyosimama katika msingi wa kukinai na matumaini: “Hakuna kulazimishana katika dini.” (Surat Al-Baqara; 2:256). Na inadhihirika kwangu kwamba ikhitilafu katika maudhui ya mwezi mwandamo yataendelea maadamu mas‟ala yanategemea juu ya kuamini na kupata tumaini kwa kuonekana. Ndio, kama kadhia itatatuliwa ya kutegemea juu ya elimu na kauli makini ya wanaanga na vyombo vya anga, likitatuliwa katika upande wa kifiqihi na maraji‟i wakatoa fat‟wa kwa hilo, huo utakuwa ni utatuzi na ufumbuzi. Kusimama katika vituo vya zama: Ili tujue namna gani tutasimama katika vituo vya zama, ni namna gani tutapokea mwezi mtukufu wa Mwenyezi Mungu? Ni wajibu tupokee mwezi mtukufu wa Mwenyezi Mungu kwa maandalizi ya kuhesabu dhati. Kila taasisi ina muda wake wa kufanya hesabu zake na kurejea mambo yake, vile vile kila mwanadamu Mwislamu asimame katika kituo hiki cha wakati mtukufu ili kuihesabu nafsi yake. Na hadithi tukufu zinatuamuru kuhesbau nafsi zetu usiku na mchana, lakini mwezi wa Ramadhani kwa umahuhususia wake na baraka zake ni kituo bora zaidi cha kuhesabu na kurejea na takwimu ya kila mwaka. Mwanadamu naafichue siri za dhati yake na atafakari hali halisi ya nafsi yake, ili aone nukta za udhaifu wake na sehemu za nguvu yake, kisha aanze kupanga ili kuondoa nukta za udhaifu, na kustawisha sehemu za nguvu na kuziwekea ratiba kwa ajili ya mwaka unaokuja. Ni wajibu tupokee mwezi huu mtukufu kwa maandalizi ya kuhesabu, kurejea na takwimu, kuazimia juu ya kuboresha na kupangilia na ratiba. 303


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Ratiba ya Mwezi wa Mwenyezi Mungu: Mwezi wa Mwenyezi Mungu ni kituo cha wakati ambao Waislamu wanautumia ili kujiongezea nguvu ya kiroho na maarifa, utamadanni na mengineyo, ili kuelekea kwa Mwenyezi Mungu na akhera. Namna gani tutaasisi ratiba hii ya Ramadhani? Ratiba ya kiroho na ya maarifa katika mwezi mtukufu wa Ramadhani ni wajibu iwe chini ya utafiti na takwimu na kuboresha, na sio iwe ya mazoea na ya kuiga. Tunarithishana mbinu zake bila ya kuleta mapya na mahitaji kwa jicho la mazingatio, na hakuna shaka kwamba mapya yanatokea kwa wingi, na matatizo mengi yanapatikana katika jamii, na hali ya leo sio kama ya jana, na matatizo ya kizazi hiki sio ya kizazi kilichopita. Na sisi tunaona namna gani vyuo vikuu na shule za mafunzo zinarejea mitaala yake kila mwaka au baina ya mwaka na mwingine. Kwa nini sisi tunangâ€&#x;angâ€&#x;ania aina fulani ya mbinu na ratiba bila ya kubadilisha au kuboresha? Hakika madhumuni na malengo ni wajibu kuyahifadhi, ama mbinu na njia ni lazima zibadilishwe kulingana na mahitaji. Vituo vya runinga: Katika mwezi wa Ramadhani vyombo vya matangazo vinaleta mambo mbalimbali ya kiutamaduni na kisiasa na upotoshaji kimwenendo na mengineyo, katika vita ya kiutamaduni ya kubomoa. Je, haujawadia wakati wa kuleta vituo vya runinga vya Kishiâ€&#x;ah ili kutatua mambo yao ya mustakabali na mengineyo ya utamaduni wao kwa hazina ya utamaduni wa asili? Kuwa na vituo vya runinga imekuwa ni haja muhimu na tunachokitoa katika vipindi vyetu na Huseiniya zetu na katika 304


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

kila sehemu baadhi yake tu inatosha kuendesha mradi huu. Na ikiwa kunahitajia kujenga Misikiti na Huseiniya, hakika vituo vya runinga vinaweza kufanya kazi iliyo sawa na Misikiti na Huseiniya, bali hakika inaweza kuhami Misikiti na Huseiniya na kuhamasisha kuimarisha na kujongea karibu yake. Lakini mtazamo wa wafadhili wale ambao mikononi mwao kuna wakfu na haki za kisharia hawajui hadi hivi sasa kiwango cha umuhimu wa vyombo hivi vya kisasa. Hakika kila sehemu kati ya sehemu zetu zinaweza kusaidia kuanzisha kituo cha runinga kupitia waqfu na haki za kisharia na misaada ya waumini. Lakini sisi tunahitaji mwenye kubeba bendera ya kazi hii na anayemiliki kipaji kwa matakwa yake. Kama ambavyo inapasa kunufaika na fursa iliyopo katika baadhi ya vituo vya kukuza uelewa na kuelekeza kizazi kinachoinukia. Kuboresha minasaba: Namna gani tutaboresha uhusiano wetu na mazingira ya ibada, huzuni na furaha, misimamo na minasaba ya kihistoria na mingineyo katika mwezi wa Mwenyezi Mungu? Uhusiano wetu na mazingira ya kiroho na minasaba ya kidini inaboreka inapoendana na hali yetu ya kimaisha, na tunapofahamu lengo lake katika kufanikisha maisha yetu na kuboresha hali yetu ambayo tunaishi. Dini sio ratiba ya kutengeneza akhera tu, bali kabla ya hapo ni kutengeneza dunia, na kwa hiyo aya tukufu inasema:

ٔ ًَ ًَ “….. ‫… َسىب ا ءا ِج ا ِفى الذ يا َخ َع ت َو ِفى الكا ِ َش ِة َخ َع ِت‬..” “…..Mola wetu! Tupe mema duniani na (tupe) mema akhera…..” (Surat Al- Baqara; 2:201). 305


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Na katika hadithi tukufu: “Ambaye hana maisha hana marejeo.” Na katika hadithi nyingine: “Ambaye ni mwenye kushindwa katika dunia yake basi ni mwenye kushindwa zaidi katika akhera yake.” Hivyo ni juu yetu kuwa na uhusiano na mafungano ya nguvu baina ya ratiba ya kidini na uhalisia wa maisha ili tuone uakisi wa dunia yetu katika mambo ya dunia yetu. Na Mwenyezi Mungu amekwishatuahidi maisha yetu kuwa mazuri kama tutashikamana na dini yetu:

ً َ ًٰ َ ُ ‫َ َ َ ُ ٰ َ ُ َ ُ ٌ َ​َُ َى‬ ً ٰ َ َ َ ِ‫يىة ِّي َبت‬ ‫ديي ه خ‬ ِ ‫”من غ ِمل صك ِلخا ِمن ره ٍش أو أ ثى وهى م‬ ِ ‫ؤمن فل‬

“…..

“Mwenye kutenda mema, mwanaume au mwanamke, naye akawa ni muumini, tutamhuisha maisha mema…..” (Surat An-Nahl; 16:97). Safari ya kiroho: Namna gani tunaishi safari ya swala, saumu, dua na Qur‟ani katika mwezi wa Mwenyezi Mungu, na namna gani tunatengeneza mwanadamu mpya asiye na mafungamano na mwanadamu wa zamani? (Mwanadamu kabla ya Ramadhani): Kila mabadiliko katika maisha ya mwanadamu yanategemea matakwa yake na kufuata kwake njia sahihi ya mabadiliko. Katika mwezi mtukufu wa Ramadhani na kupitia mazingira ya swala, saumu, dua na kusoma Qur‟ani ni wajibu tuziamshe katika nafsi zetu nguvu ya matakwa, na tukomboe matakwa yetu kutokana na matamanio na hawaa. Na hili ni lengo la msingi la saumu: 306


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

ُ‫َ ُ َ ى‬ ُ َ​َ َ ُ َ ‫يام َهما ُهخ َب َغ َهى ىال‬ ّ ُ ‫الص‬ ُ ‫يى‬ ‫زين ِمن ك ِبلى ل َػلى‬ ‫”…ه ِخب غل‬ ِ ِ َ ‫َى‬ “‫ن‬ ِ ‫جخلى‬ “…..Mmeandikiwa kufunga kama walivyoandikiwa waliokuwa kabla yenu, ili mpate kuwa na takua.” (Surat Al-Baqara; 2:183). Na uchamungu (takua) ni kujikomboa kutokana na matamanio na hawaa. Mwanadamu anapokomboa matakwa yake na akaamua kuyatumia katika mwelekeo sahihi hiyo ndio njia ya mabadiliko na kujadidisha katika maisha yake na shakhsiya yake. Ama akidhoofika mbele ya matamanio na akanyenyekea mila na kuiga, na akaitikia sababu za uvivu na uzembe, hakika hatonufaika kutokana na baraka za mwezi huu mtukufu, hata kama atafunga, utakuwa ni usadikishaji wa hadithi tukufu: “Ni wafungaji wangapi ambao hawana katika saumu zao isipokuwa njaa na kiu?” Saumu mbili katika mwezi wa Mwenyezi Mungu: Kuna saumu mbili katika mwezi wa Ramadhani: Saumu ya mtu binafsi nayo ni safari ya kiroho ya kibinafsi pamoja na Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kuna saumu ya pamoja katika kiwango cha umma wa Kiislamu nayo ni safari ya jamaa kwenda kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Unadhani ni nini uhalisia wa saumu hizi mbili? Upande wa jamaa katika ibada ya Kiislamu una umuhimu mkubwa ambapo Mwenyezi Mungu hakuacha uhuru kwa mwanadamu kufunga muda fulani katika mwaka bali ameifanya saumu katika mwezi maalumu ili iwe ni faradhi ya saumu ya jamaa katika kiwango cha umma. Na vivyo hivyo, hakika hija ni katika siku maalumu ili iwe ni 307


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

msimu wa kukutana katika mazingira yake katika kiwango cha umma. Na swala ingawaje katika asili ni kuswaliwa furada lakini katika siku ya Ijumaa na Iddi mbili inaswaliwa jamaa (katika ufafanuzi wa kifikihi), na kwa ujumla ni bora iswaliwe jamaa. Hakika hayo yanaonyesha kwamba kutengeneza mtu binafsi haitoshi na wala haileti lengo linalotakiwa na ujumbe. Kinachotakiwa ni kuanzisha umma wenye imani, unaoasisi ustaarabu wa kiungu:

َ َ ً َ َ ً ‫َ​َ ٰ َ َ َ ُٰ ُى‬ ّ َ​َ َ َ ُ ‫اط َو َيىىن‬ ‫ال‬ ‫ى‬ ‫ه‬ ‫غ‬ ‫ذاء‬ ُ ‫ش‬ ‫ىا‬ ‫ىى‬ ‫خ‬ ‫”وهز ِلً جػل كى أمت وظطا ِل‬ ِ ً َ ُ َ ‫ى‬ “….. ‫الشظى ٌُ َغليى شُيذا‬ “Na kama hivyo tumewafanya kuwa umma wa wastani, ili muwe mashahidi juu ya watu wote, na Mtume awe shahidi juu yenu…..” (Surat AlBaqara; 2:143).

َ ٌ ُ ُ َُ َ َ ُ َ​َ َ َ َ ‫ػشون َو َين َ ىن َغ ِن‬ ‫” َولخىن ِم ى أ ىمت َيذغىن ِإلى احأ ِحر ويأمشون ِباو‬ ِ َ ُ “….. ِ‫او ى ِ​ِش‬ “Na liwepo miongoni mwenu kundi lenye kulingania kwenye kheri, na kuamrisha mema na kukataza maovu.” (Surat Aali-Imran 3:104). Hakika sisi tunapoishi na saumu katika kiwango cha umma, hiyo ni kwa sababu ni wajibu kuimarisha kwetu roho ya mshikamano wa umma huu na kubeba jukumu katika mukabala wake na tuishi mazingira ya saumu katika kiwango chake na sio katika kiwango cha mtu binafsi tu. 308


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Kuongezaka mazingira ya kufuata katika minasaba: Baadhi wanasema: Hakika ibada ya Ramadhani imebadilika katika akili ya wengi na kuwa ni mazingira ya mazoea na ibada mfu, kwa sababu inaendeshwa katika mazingira ya kuiga. Ni nini maelezo yenu juu ya kauli na fikra hii? Kauli hii ni sahihi kwa kiasi kikubwa. Kuamiliana na ibada kwa wengi miongoni mwa Waislamu kunatimia bila ya kuangalia lengo la ibada na madhumuni yake na roho yake. Waislamu wengi wanatekeleza swala lakini wao hawajui lengo la swala “hakika swala inakataza uchafu na maovu.” (Suratul-Ankabuti: 45). Na Qur‟ani tukufu inawatishia baadhi ya wenye kuswali kwa adhabu; Kwa sababu wao wanaghafilika na lengo la swala zao:

َ َ َّ ُ ٌ َ​َ َ َ ُ َ ‫ى‬ ﴾ ٥﴿ ‫ن‬ ِ ‫ًلت ِ ظاهى‬ ِ ‫صل‬ ‫فىيل ِللم‬ ِ ‫﴾ الزين ه غن ص‬٤﴿ ‫حن‬ “Basi ole wao wanaoswali. Ambao wanasahua Swala zao.” (Surat Al-Ma‟un; 107:4-5) Na saumu ni kwa ajili ya kuleta uchamungu katika nafsi:

َ

‫َ َى ُ َى‬

“‫ن‬ ِ ‫…لػلى جخلى‬..”

“Ili mpate kuwa na takua.” (Surat Al-Baqara; 2:21). Pamoja na kwamba Waislamu wengi wanafunga lakini wachamungu ni wachache, je, si hivyo? Na Hija imepokewa katika hadithi: “Ni wingi ulioje wa makelele na ni uchache ulioje wa wenye kuhiji.” Hakika yote hayo ni kwa sababu ya kujishughulisha na kutosheka na muonekano wa ibada bila ya kuelewa malengo yake na 309


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

madhumini yake. Anasema Amirul-Muuminina Ali : “Eee hakika Uislamu una malengo, basi fikieini kwenye lengo yake.” Mabadiliko katika karne ya ishirini na moja: Kwamba, wengi kati ya wasomi na wengineo wanazungumzia juu ya karne ya ishirini na moja na wanayoyaandaa watu wa magharibi miongoni mwa mapinduzi ya maalumati na mapinduzi ya teknolojia na mengineyo katika karne hii. Je, Wailsamu – wako katika kiwango cha ulimwengu – wako tayari kutoa mapya katika medani ya kiulimwengu yanayoendana na zama? Au wao watabakia katika hali yao ya uduni, kuchelewa na kutokuendelea kama wanavyosema baadhi? Matumaini kwa Mwenyezi Mungu ni makubwa, na katika medani tukufu ya Kiislamu, katika medani ya Kiislamu hivi sasa, viongozi wa kidini wenye uelewa, na mkusanyiko wa kiimani wenye ikhilasi, kuna ishara ya mwamko wa Kiislamu ulio tayari, lakini hivi sasa unakabiliwa na changamoto hatari na zilizo muhimu zaidi ni: Changamoto ya kuvumbua mafuhumu ya Kiislamu, mtazamo wake na manhaji zake baada ya kurundikana katika hazina ya Waislamu shaka nyingi kutoendelea, makosa ya kuiga na mbinyo wa kimaada. Changamoto ya teknolojia na ukandamizaji katika nchi nyingi za Kiislamu, ambazo haziruhusu kwa wanafikra watendaji kutangaza fikra zao na kutenda kulingana na jitihada zao. Changamoto ya kukabiliana na uadui na njama za nje, ambao hautaki umma kuendelea na kurudisha utukufu wake na heshima yake. Na kizazi cha Kiislamu chenye uelewa sasa hivi kinaingia katika changamoto hii na juu ya upeo wa chumo lake na kunusurika kwake na kupanga mustakabali wa Kiislamu na umma katika zama hizi. Je, unaendana na zama zake na kutoa mfano wake kwa 310


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

ulimwengu au utabakia wenye kuchelewa na kutoendelea?

SHI‟AH NA ULIMWENGU203 Ushi‟ah sio kundi la kiitikadi wala madrasa ya kifikihi ya kimadhehebu tu, bali ni mtazamo na msimamo mukabala na hali ambayo unaishi nayo umma wa Kiislamu. Sisi tuna haja ya mazingira huru na kufunguka kifikra na akili kufanya kazi na kuvumbua fikra. Umewadia wakati wa kufanya mijadala yenye kujenga na mikutano yenye malengo ili kusahihisha na kutafiti uhalisia wa hawza na maraji‟i. Tunahitaji vyuo maalumu kwa ajili ya khutuba za Huseiniya ndani ya hawza zetu za elimu. Swali: Mnaonaje hali ya uhusiano na muamala baina ya mitazamo na mikusanyiko mbalimbali ndani ya makundi ya Kishi‟ah? Ni lazima tuamue mwanzoni kwamba wingi na ikhitilafu katika jamii za kibinadmu ni hali ya kawaida na haki ya kisharia. Kama tukipembua hali za jamii za binadamu katika zama za historia, vyovyote zitakavyokuwa dini zao na madhehebu zao, tungeona hali ya ikhitilafu na makundi ipo na imesimama. Na baadhi wanaweza kuona kwamba jamii ya kidini haina nafasi humo ya kukhitilafiana na kuwa na makundi. Maadamu sote tunaamini dini moja, nini sababu ya ikhitilafu na kuwa na rai na mitazamo mingi? Lakini kwa kutafakari mwanadamu anavumbua kwa urahisi dhana hii. Kuna sababu na mambo mengi yanayolazimu kupatikana kutofautina na kutengana baina ya jamii ya kidini, na tunayo mafuhumu na mafunzo yanayoweka wazi sababu hizi na kutuelekeza namna ya kuamiliana pamoja nayo. 203

Majadiliano yaliyofanywa na Muadham Sheikh Hasan Saffar na Majalatu al-Muusimu fuswiliya muswawara linalojihusisha na athari na hazina linalotolewa kuhusu Darul-Muusimu liliilaam - Beirut toleo namba 11 mujaladi wa tatu 1990 / 1412 Hijiria.

311


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Kwanza: Kutofautiana katika kiwango cha imani na daraja zake, ambapo imepokewa katika nususi nyingi, amezitaja al-Allammah al-Majilisiy  katika rejea ya Biharul-Anwaar katika mlango maalum chini ya anwani: (Darajaatul-Imani wa Haqaiqihi) katika kitabu Imanu wal-kufur, Juz. 6, uk. 154 hadi 175. Na kwa hakika kutofautiana kiwango cha imani kunaweza kusababisha kutaofautiana katika rai, mwenendo na vitendo. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

َ َ َ ٌ َ ُ‫ُ َ​َ ٰ ٌ َ ى َ ى‬ ِ‫ػملىن‬ ‫ه دسجكذ ِغ ذ الل ِ ِكه واللكه بصحر ِبما ي‬ “Wao wana daraja mbele ya Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona yale wanayoyafanya.” (Surat Aali-Imran; 3:163). Na kutoka kwa Abdul-Aziz al-Qatwisiy amesema: Aliniambia Abi Abdillahi Swadiq : Ewe Abdul-Aziz; hakika imani ina daraja kumi kama ngazi, anapanda kwayo daraja baada ya daraja. Asiseme mtu wa daraja la pili kwa wa daraja ya kwanza: „Huna lolote,‟ bali hadi afikie daraja ya kumi. Usimdharau aliye chini yako asije akakuangukia aliye juu yako. Ukimuona aliye chini yako kwa daraja mnyanyue humo kwa upole na wala usimbebeshe asiyoyaweza na kumvunja. Hakika mwenye kumvunja muumini ni juu yake amfunge bandeji.”204 Na katika hadithi hii kuna ishara muhimu kwamba unapomtenga anayehitalifiana pamoja na wewe, hakika wengine watakutenga kwa kuhitalifaiana kwako pamoja nao, kama inavyoelekeza hadithi onyo kali kwa wanaoporomosha mazingatio ya ndugu zao waumini na wanasahau haki zao na shakhsiya zao, si kwa jingine ila kwa kuwa wao hawawaafiki katika kila wanayoyaitakidi au wanayoyafanya. 204

Al- Majilisiy: Muhammad Baaqir katika Biharul-Anuwar juzuu 66 uk: 165.

312


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Na katika riwaya nyingine kutoka kwa Imamu Swadiq  vilevile anaipokea Swabaah Abu Siyaabah kutoka kwake  kwamba amesema: “Mna nini nyinyi na chuki, baadhi yenu wanachukia baadhi? Hakika waumini baadhi yao ni bora kuliko baadhi, na baadhi yao ni wengi wa swala kuliko baadhi, na baadhi yao ni wenye uoni kuliko baadhi, nayo yana madaraja.”205 Pili: kutofautiana kiwango cha maarifa na uelewa: Sio kila ukweli anauvumbua kila mtu, na kwa daraja moja la uwazi. Na uelewa wa watu katika elimu sio mmoja. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

َ

ُ َ َ

َ

ٰ َ َ َ

“ ٌِ ‫شاءِ َوفىق و ِ ّل ري ِغل ٍ غلي‬ ُِ ‫… شف ُؼ د َسجك ٍذ َمن ق‬..”

“…..Tunawatukuza kwenye vyeo tuwatakao, na juu ya kila mwenye elimu yuko ajuaye zaidi.” (Surat Al-Yusuf; 12:76). Na kutofautina kiwango na maarifa kunasababisha kuhitalifiana katika rai na mtazamo. Ukweli unaweza kuwa wazi, baadhi yetu unawapelekea kukinai na kazi fulani, wakati ambapo wengine wanakataa kukinahi huko na kazi hiyo, kwa kutokujua kwao na kuweza kukinahi na ukweli huo kimsingi, na kwa hiyo anasema Imamu Ali : “Watu ni maadui wa wasiyoyajua.” Na anaweza kupata mmoja wetu maalumati yanayomsukuma kuchukua msimamo fulani, pamoja na kwamba asiye na maalumati hayo au asiyeyategemea hawezi kuchukua msimamo huo. Na haya yanawezekana sio tu miongoni mwa waumini bali hata kwa manabii na mawalii maasumina na muqarabina. Inapotaka hekima ya Mwenyezi Mungu kumfahamisha Nabii juu ya uhakika maalum, anauficha kwa Nabii mwingine. Matokeo yatakuwa ni aina ya tofauti na ikhitilafu katika rai baina ya 205

Rejea iliyotangulia 168

313


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

manabii hao wawili. Kama kinavyoonekana kisa cha Nabii Musa na al-Khidhir  ambacho Qur‟ani tukufu inakitaja katika Suratu Kahfi. Na vilevile hukumu ya Manabii wawili, Daud na Suleiman  walipohukumu katika shamba kama ilivyopokewa katika Suratul-Anbiyai. Na katika mazingira haya inatokea ikhitilafu baina ya mafaqihi na mujitahidina katika fat‟wa, ambapo kila mmoja anataoa juhudi yake ya elimu na anatumia uwezo wake wa ijitihadi ili kuvumbua hukumu ya Mwenyezi Mungu katika kila mas‟ala, lakini wao wanaweza kutofautiana katika fat‟wa zao hata katika madhehebu moja kama ilivyo mashuhuri kwetu. Na ikhitilafu yao ni muonekano katika uhalisia wa ikhitilafu katika maisha ya binadamu na Uislamu kukubali hali hii. Tatu: Ikhitilafu ya maslahi: Maasumu tu ndio anakuwa hana msukumo katika fikra zake na vitendo vyake, na misimamo yake inatokana na haki na inakusudia haki. Na umaasumu ni daraja tukufu, ni mahususi kwa malaika ambao:

َ َُ َ َ ُ ٌ َ َُ َ ‫مش ِه‬ ِ ‫ىشمى‬ ‫… َبل ِغباد م‬..” ِ ‫﴾ ال ي‬٧٦﴿ ‫ن‬ ِ ‫عبلى ه ِباللى ٌِ وه ِبأ‬ َ َ َ “﴾٧٧﴿ ‫ن‬ ِ ‫ػملى‬ ‫ي‬ “…..Bali hao ni waja waliotukuzwa. Hawamtangulii kwa neno nao wanafanya kwa amri Yake.” (Surat Al-Anbiya; 21:26–27). Na Manabii, Nabii ni maasumu (hatamki kwa matamanio. Ila ni wahyi unaofunuliwa, na Maimamu ambao Mwenyezi Mungu amewaondolea uchafu na akawatakasa kabisa. Ama watu wengine, na miongoni mwao ni waumini, vyovyote zitakavyokuwa juu daraja za imani zao, wao ni binadamu wana maslahi, na matamanio yanaingilia na kuathiri juu ya rai zao na 314


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

misimamo yao. Kila upande au kundi au jamaa inakwenda mbio kutetea maslahi yake na manufaa yake. Na katika msingi huo inachukuliwa misimamo na kujenga kukinahi kwake. Katika yote yaliyotangulia tunaamua kwamba hali ya kuhitalifiana na kutofautina ni hali ya kawaida kwa Shiâ€&#x;ah kama ilivyo kwa wasiokuwa wao. Lakini maneno kuhusu muamala pamoja na hali hii, ambapo ikhitilafu hii inakuwa na tofauti katika nyakati nyingi, ni sababu ya kuwa mbali na uadui na mizozo. Na haya ndio ambayo zinakabiliwa nayo baadhi ya jamii zetu, ambapo imekuwa ikhitilafu katika kumfuata Marjaa huyu au kumfuata Marjaa yule au ikhitilafu katika msimamo wa kisiasa na ufuasi wa chama au ikhitilafu hata katika baadhi ya rai na fikra. Katika baadhi ya wakati hata baina ya wenye Huseiniya na misafara ya maombolezo, ikhitilafu hizo zimekuwa ni sababu ya mzozo na ni kikwazo cha umoja na ushirikiano!!! Na kinachotakiwa kwetu sasa hivi ni kuingia katika hatua mpya, tuvuke humo kasoro za ikhitilafu, kwani ulimwengu pembezoni mwetu sasa hivi unaingia zama za wigo mpya, baada ya muda mrefu wa vita baridi baina ya kambi ya Magharibi na Mashariki. Na nchi zetu za mashariki ya kati zinaweza zikakaribia kuingia katika hali mpya, kama yanavyoashiria maneno ya wakuu wa siasa ulimwenguni. Na muongo uliopita ulijaa uzoefu na matukio, ni wajibu utupe uzoefu na upevu katika muamala wetu pamoja na baadhi yetu kwa baadhi ndani ya mpaka ufuatao: Kwanza: Kutambua hali ya vyama vingi na uhalali wake: Ama kila mmoja wetu akipinga uwepo wa mwingine, na akazingatia uwepo wake ndio sharia ya asili, na akataka kulazimisha amri zake juu ya wengine na waingie humo na wajiunge naye, hakika hilo litatufanya ni walengwa wa ugomvi na fitina. Na maslahi yetu yanakuwa kama madhehebu na kama kundi ni muhanga wa lengo hili lisilo na uhalisia. 315


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Pili: Kuweka kikomo cha mizozo na ugomvi, ili itawale tabia ya kuheshimiana. Tumekwishaona namna gani imerejea kwetu hali ya mzozo na propaganda na kutuhumiana. Imerejea kwetu sote kwa madhara, na pande za nje zimeitumia, na sehemu za uchochezi ndani mwetu. Hapa inakuja dauru ya watu, wakati wa kheri, walinganiaji na urekebishaji na miongoni mwa waelewa wenye ikhilasi, na ulamaa wa umma na mashujaa wake, kwamba wajitolee kwa ajili ya kutatua ikhitilafu inayotokea au sintofahamu inayotokea. Na kwa masikitiko makubwa, ni nadra aina hii katika misimamo, ambapo hakika wengi, ama wanakanganyikiwa katika mzozo na wanaingia katika moja ya pande zake au wanaacha kamba kwa watu wa Magharibi na wala hawaoni jukumu la nafsi zao katika jambo hili. Tatu: Utamaduni wa usamehevu na ushirikiano na kupiga vita fikra na uchochezi ambao unashajiisha kasumba na madhambi. Kutoka kwa Imamu Swadiq : “Mwenye kumtuhumu ndugu yake katika dini yake hakuna utukufu baina yao.” Na katika hadithi nyingine kutoka kwake : “Jihadharisheni na ugomvi katika dini, hakika unashughulisha nyoyo na utajo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na unaleta unafiki, na kuchuma chuki, na kuchochea uongo.” Na kitu kibaya zaidi ni kuongozea sifa ya kisharia katika ugomvi na mzozo ambapo baadhi wanaitakidi kwamba taklifu yao ya kisharia inakuwa katika kuangusha wengine wenye kuwakhalifu, na kwamba wana thawabu katika kusambaza maovu juu yao!! Nne: Kuweka tamko la ushirikiano baina ya pande mbalimbali katika kiwango cha jumla au katika pande za ndani, na hapa kuna bishara na matumaini makubwa katika kuanza hatua mpya inayotawaliwa na usafi na ushirikiano baina ya pande mbalimbali za makundi na katika kila kiwango chake inshaallah. Na nataraji jarida la msimu kufanya jukumu lake la uelekezi katika nyanja ya utangazaji na utamaduni kwa ajili ya kutumikia umoja na 316


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

ushirikiano ndani ya umma na kwa Waislamu wengine na kuwa ni mimbari iliyowazi kwa kila rai na pande zenye harakati. Swali: Je, kuna anayeona kwamba shughuli za kisiasa na kazi za ijitihadi ambazo wamezifanya baadhi ya harakati na pande za Kishi‟ah katika muongo uliopita zimeacha athari mbaya katika hali ya Kishi‟ah, kijamii na kisiasa, kama ambavyo umeondoa kisingizio cha kupaka matope sura yao katika kiwango cha kimadola, nini rai yenu? Inafahamika kwamba kuna mielekeo miwili katika kufahamu Uislamu, Ushi‟ah na uhusiano wake wa kijamii. Mwelekeo wa kwanza unatazama dini katika mpaka wa mas‟ala ya kiitikadi na kiibada na wa kimawaidha, bila ya kuzingatia na kuingilia katika mambo ya kisiasa na kijamii. Na kwa kujengea juu ya fahamu hii, harakati na shughuli za Kishi‟ah zinazingirwa katika kushikamana na fiqihi ya Ahlul-Bayt  na kuhuisha nembo zao, na kueneza fikra zao na fadhila zao. Na haipasi kuvuka hayo kwenda kwenye kazi ya jihadi na kisiasa, kwa sababu hayo yanapingana na mafuhumu ya taqiya (kulingana na mtazamo wao) na kwa namna ya kuwahi na kuharakisha dauru ya mabadiliko ya jumla ambayo atayafanya Swahibu Zaman . Na kwa wenye mtazamo huu wana rundo la fikra na harakati, wanatoa hoja kwazo kwa nususi mbalimbali za kidini na misimamo ya kihistoria, na sasa hivi hatuko katika sehemu ya kujadili maudhui haya lakini tunataka kuashiria kwamba swala linaloulizia undani huu, na kuanzia kwalo linapata matatizo haya. Ama mwelekeo mwingine unaona kwamba dini inahusika na pande zote za maisha ya mwandamu na jamii, na mambo ya kisiasa yana dauru yake ya kimsingi na athari kubwa katika nyanja zote za maisha. Haiwezekani kusahau umuhimu wake kwa mwanadamu muumini. Na Ushi‟ah sio kundi la kiitikadi wala sio madrasa ya kifikihi ya kimadhehebu tu, bali ni mtazamo wa msimamo mbele ya hali ambayo unaishi nayo umma, na 317


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

maelekezo ya Ahlul-Bayt , yanawasukuma wafuasi wake katika kubeba jukumu katika kutetea maslahi na mambo ya wanyonge. Amirul-Muuminina Ali , anasema: Mwenyezi Mungu hakuwafanya maulamaa “wakubali shibe ya dhalimu wala njaa ya mwenye kudhulumiwa.” Na Imamu al-Husein anapokea kutoka kwa babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu  kauli yake: “Mwenye kuona mtawala dhalimu anayehalalisha haramu ya Mwenyezi Mungu, mwenye kutengua ahadi ya Mwenyezi Mungu, mwenye kukhalifu Sunnah ya Mtume wa Mwenyezi Mungu anawafanyia waja wa Mwenyezi Mungu madhambi na uadui na wala hakubadilisha juu yake kwa kitendo wala kwa kauli, ni haki ya Mwenyezi Mungu kumwingiza motoni.” Na nyinginezo kati ya riwaya zilizopo katika madhumuni yake, na sambamba na mafunzo haya na maelekezo haya kuna maisha ya Maimamu wao wenyewe ambayo yalikuwa yamejaa misimamo na jihadi na mapinduzi na upinzani dhidi ya ufisadi na dhulma. Na matokeo ya hayo Ahlul-Bayt wamevumilia mateso ya misimamo ya kiujumbe, wametoa maisha yao thamani ya misimamo hiyo, na wameishi machungu, balaa na kufukuzwa na mateso. Na wafuasi wa Ahlul-Bayt na Mashi‟ah wao wamejulikana katika historia ya umma kwamba wao ni dhamira ya umma na walinzi wa ujumbe, na wanamapinduzi wa Alawiyina na Hashimiyina daima ni mfano katika hayo. Na harakati za kisiasa na harakati za jihadi katika harakati za Kishi‟ah leo hakika ni mwendelezo wa historia hiyo. Na ni chimbuko linalotokana na ufahamu huo katika dauru ya dini katika maisha na jukumu la muumini mbele ya uhalisia wa maisha, na kujengea juu ya fahamu hiyo na mwelekeo usio na lawama katika kuvumilia taabu na kusubiria juu ya msimamo wa kiimani wa kiujumbe na wenye mshikamano, kwa kuwaiga Ahlul-Bayt  ni kigezo kwao. Shakhsiya yao ilipakwa matope na baadhi wakashuku katika dini yao, kama hali ilivyo katika 318


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

makhawariji kumtuhumu Imamu Ali kwa shiriki, na propaganda ya Muawiya dhidi yake kwamba haswali wala haogi janaba. Kama ambavyo walimtuhumu Imamu al-Husein kwamba ametoka katika dini, wakatekwa wake zake na familia yake. Na inawezekana kusema kwamba maisha ya Ahlul-Bayt  ni mlolongo unaoendelea katika jihadi na kujitolea kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na wanyoge. Na katika upande mwingine, hakika zilichokifanya harakati za Kishi‟ah miongoni mwa jihadi na harakati, hakika yanakuja ndani ya medani ya mwamko wa Kiislamu. Ulivuma upepo wake kwa Waislamu wote, ambapo uliamsha jamhuri ya umma katika nafsi yake ili uone kwamba hali yake iko mbali na manhaji ya Mwenyezi Mungu na kwamba unaishi maisha ya kufuata na kutoendelea na unazungukwa na ukosefu na ujahili, na hatamu za mambo yake zipo katika mikono isiyo na uwezo na isiyo na ikhilasi. Ikatikisika ghera na hisia ya majukumu kwa wenye kuelewa na wenye ikhilasi, na wakatengeneza harakati na vyama, na yakatokea maandamano na mapinduzi katika nchi mbalimbali za Kiislamu. Na Shi‟ah wao ni sehemu isiyojitenga na Umma wa Kiislamu. Haikuwa inasihi kwao kurudi nyuma na msafara wa medani ya mwamko wa Kiislamu ambao unalenga kuitawalisha dini katika maisha na kunyanyua neno la Mwenyezi Mungu, na kurejesha utukufu wa Waislamu. Na yaliyotokea yalikuwa ndani ya mtiririko huu na ni katika jumla ya sababu ya kujifakharisha na utukufu, kama ambavyo ukali wa dhulma na ukandamizaji na mateso ambayo umma ulipata katika baadhi ya nchi unatengeneza sababu yenye kubinya na yenye kusukuma katika mwelekeo wa mapambano na kulipiza kisasi. Na ikiwa kuna machungu, mateso na kibano basi imetokea kwa umma wa Shi‟ah kwa sababu ya vitendo hivyo vya kisiasa na vya jihadi. Hakika haisihi kuzuia kwetu kuona mafanikio na faida ambayo imepatikana katika Uislamu na Waislamu kutokana na harakati hizo, ambapo lilipanuka duara la uelewa wa kidini na 319


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

ikaongezeka kujongea watu katika mambo ya Kiislamu, na wengi wakalazimika. Katika serikali nyingi zikajali Uislamu na kujidhihirisha kwa kushikamana nao, na Uislamu ukawa ni ukweli unaoafikiwa, unaotambulisha nafsi yake katika kiwango cha juu kiulimwengu, kisehemu na kijamii. Kwa hakika kuzungumzia uhalali wa harakati na sababu zake, shughuli zake za kisiasa na za jihadi haimaanishi kukubali vipengele na ufafanuzi wa vitendo vyote ambavyo vinapatikana kutokana na hayo. Na uwanja uko wazi na medani ni pana, kwa njia mbalimbali za kazi na namna zake mbalimbali, na inawezekana kujadili kuhusu baadhi ya vitendo, au kuelekeza ukosoaji kwa baadhi ya misimamo. Jitihada zimekwishakuwa nyingi, kumetokea mwingiliano na kupatikana makosa. Na haitupiti kuashiria kwamba pande za dola na utawala wa sehemu, na baadhi ya wapinzani wa kimakundi, wamefanya kazi sana ya kukuza baadhi ya dosari, uchochezi na tuhuma dhidi ya harakati za Kiislamu za jihadi kwa namna ya ujumla na hususani harakati za Kishiâ€&#x;ah miongoni mwazo. Na ni juu yetu tusiingie katika vita vya kinafsi, na kushindwa mbele ya upotoshaji wa matangazo. Matangazo yalikuwa na bado yangali ni silaha inayotumiwa na mabeberu na madhalimu dhidi ya harakati za wanyonge na wenye kudhulumiwa. Swali: Mukabala wa uchochezi wa fitina ya makundi na mfarakano wa kimadhehebu baina ya Sunni na Shiâ€&#x;ah kuna mapendekezo na harakati za kuleta ukuruba baina ya madhehebu ya Kiislamu na kuimarisha hali ya umoja baina ya Waislamu. Na kwa kuzingatia nyinyi ni kati ya wenye kuzingatia kupendekeza mambo haya katika maandiko yenu na khutuba zenu je, mnaona katika medani mapendekezo makini katika njia hii? Mizozo ya kimakundi katika umma na uchochezi wa mfarakano wa kimadhehebu kawaida nyuma yake kuna sababu mbili: 320


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Sababu ya kisiasa. Wakati pande za kigeni au serikali potofu zinapopanga kuwashughulisha Waislamu na mambo ya maendeleo au kusambaratisha umoja wao, na mara nyingi ilikuwa inatokea katika miongo iliyopita, kwa sababu ya jambo hili, uliogopa ubeberu wa kiulimwengu, na mifumo potovu ikahisi hatari kubwa ya kustawi harakati za Kiislamu, na harakati za Waislamu na kulingania kwao kwenye dini yao na kutaka kuitawalisha katika maisha. Na katika makabiliano haya ya mwamko wa Kiislamu maadui wametumia hatua nyingi na miongoni mwa hizo ilikuwa ni kufukua nyaraka za ikhitilafu za kimakundi na kimadhehebu. Na sababu ya pili ni hali ya kutoendelea ambayo zinaishi nayo sehemu kubwa za umma katika nyanja za utamaduni na akhlaqi. Na kutoendelea huku ambako kunadhihirika katika kutojuana Waislamu baadhi yao kwa baadhi, na katika kutokuwepo na kufunguka na majadiliano mazuri, na katika tabia za kasumba na ukali mbele ya rai nyingine, na muda wote wa historia kulikuwa na harakati mbili na aina mbili katika kuamiliana na ikhitilafu na wingi wa madhehebu, harakati za usamehevu na kuvuka sehemu za ikhitilafu kwenda kwenye wigo wa umoja wa Kiislamu na maslahi ya pamoja, na kundi la kasumba na ugaidi wa kifikra ambalo daima linachochea vipengele vya ikhitilafu na kuvikuza ili kusiwepo na fursa ya kukutana au kujadili na ushirikiano, na maelekezo ya jumla ya Maimamu wa Ahlul-Bayt  na wafuasi wao wenye uelewa, ni katika mapito ya harakati ya kwanza. Na sio katika upande wa maelekezo na muongozo tu, bali hata katika kiwango cha vitendo na utawala katika muda ambao utawala unakuwa katika mikono yao, kama anavyopokea Sheikh Tuusiy kwa mfano katika Tahadhib kuhusu msimamo wa Imamu Ali  alipochukua ukhalifa katika mas‟ala ya kifiqihi yanayokhalifu rai yake na wala haruhusu kutokea tatizo linaloharibu umoja au linalotumikia malengo ya wapinzani kwa ajili ya mas‟ala ya pembezoni. 321


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Imekuja katika Tahadhib kwamba: Alipowasili Amirul-Muuminina  mjini Kufah alimwamuru Hasan bin Ali awatangazie watu: Hakuna swala katika mwezi wa Ramadhani katika misikiti kwa jamaa – yaani swala ya tarawehe ambayo alitoa fat‟wa kwayo Umar bin al-Khatab katika zama zake – Hasan bin Ali akawatangazia watu yale aliyoamrishwa na Amirul-Muuminina, watu waliposikia maneno ya Hasan bin Ali wakapiga kelele: „Waa Umaraa …..‟ Hasan aliporejea kwa Ali akamuuliza sauti hii ni ya nini? Akasema: Ewe Amirul-Muuminina watu wanapiga kelele: Waa Umaraa waa Umaraa!! Amirul-Muuminina  akasema: Waambie waswali…206 Na hakika mimi nina matumaini sana katika hatua ya sasa kwamba kuna uelewa wa umoja umeanza kuenea katika safu za Waislamu, na kwamba tabia ya usamehevu, ukunjufu wa moyo na kuheshimu rai ya mwingine ndio kati ya alama ya zama hizi ambapo zinanyanyuka humo sauti za kulingania demokrasia na kuheshimu haki za binadamu. Huenda kati ya yanayotumikia umoja wa Kiislamu, ni kufunguka Waislamu baadhi yao kwa baadhi na kuenea maarifa ya kimadhehebu, kwa kutoa fursa mbele ya kila Mwislamu ili kujua kwa namna ya moja kwa moja rai za madhehebu mengine ya Kiislamu, ama ujahili na kujifungia ni maandalizi ya kukubali propaganda za upotovu wa wapinzani. Swali: Mazungumzo aliyoyaeleza Muadhamu al-Allammah Sayydi Muhammad Husein Fadhilullahi katika MajalatulMuusim katika toleo la nane yamechochea mijadala na maswali mengi na hususan katika yanayohusiana na maudhui ya umariji‟i wa kidini, nini rai yenu na maelezo yenu katika upande huu? Kwanza napenda kuheshimu na kujali dauru ambayo anaifanya 206

Tuusiy katika Tahadhib Juz. 3, uk. 70

322


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Muadhamu al-Allammah Fadhwilullahi katika kutajirisha utamaduni wa Kiislamu kwa mwelekeo wake wa kifikra ambao unabainika katika ufuatiliaji wake wa mahitaji ya medani na utatuzi wake wa matatizo na shida za kileo. Na vilevile ushujaa na ujasiri katika kupendekeza mambo na mas‟ala ambayo wengi wanaogopa kuyaeleza. Na katika yanayohusiana na mazungumzo ya Muadhamu kuhusu umarji‟i na hali wanayoishi nayo Mashi‟ah, napenda kuashiria katika nukta zifuatazo: Kwanza: Hakika sisi ni wajibu tuvuke hali ya hofu ya kukosolewa, na kuchukua misimamo mibaya na kupinga dhidi yake, maadamu sisi hatudai umaasumu kwa nafsi zetu, na tunatarajia kilichobora zaidi, na tunaamini dauru ya nasaha na kuusiana. Ni juu yetu kukubali kukosolewa na kusahihishwa katika hali zetu zote na mambo yetu yote, na ambao wanakataa kukosolewa kana kwamba wao wanadai umaasumu au hawatarajii kilichobora zaidi, na wanaona kwamba hakuna uwezekano wa kilichobora zaidi katika kazi zao, au wanajikweza na wanajinyanyua katika kukubali nasaha na wasia. Na Qur‟ani tukufu inapotaja maelekezo na Mwenyezi Mungu Mtukufu kumfunza adabu Nabii wake Muhammad  katika masikio ya vizazi, na anazungmza juu ya makosa na kasoro za jamii ya Kiislamu ya awali kwa kuwaelekeza katika kuyarekebisha na kuyasahihisha, hakika ni ili kuulea umma wa Kiislamu na binadamu kwa ujumla katika dharura ya kusahihisha, kurejea na kukosoa. Na kusawazisha sio msimamo wa kiuadui, wala haisihi kutazama ukosoaji wowote kwamba ni kujeruhi au kudhihirisha au kudharau. Na pengine baadhi wanadhani ndani ya dini kwamba ukosoaji unasababisha kufichua upungufu wetu na nukta za udhaifu wetu mbele ya wengine, na mbele ya jamhuri na 323


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

kupungua na kudhoofika uaminifu wake katika upande wa kidini. Lakini dhana hii inatokana na kutoelewa kuliko wazi, ambapo hali ya Mashi‟ah na hali ya umarji‟i sio tena ni jambo la kificho bali liko chini ya darubini na kuangaziwa. Na inajiri pembezoni mwake hali za utafiti upembuzi, na inaweza kuwa wanayoyajua wengine katika ufafanuzi wa hali zetu ni mengi zaidi kuliko wanayoyajua wengi wetu, na sababu ya kuenea uelewa na maarifa na kufunguka jamii yetu katika ulimwengu hakika maswali mengi na mzungumzo mapana yanazunguka ndani ya jamhuri ya Shi‟ah kuhusu taasisi zake za kidini na za kiongozi. Na ni juu yetu kuelekeza na kufafanua kadhia na mambo ili wasiyatumie maadui kwa kupotosha jamii zetu, na hayo ni kwa kuyajadili na kuyaeleza na kujadiliana kuhusiana nayo na sio kwa kificho na kuzuia. Pili: Hakika sisi tuna haja ya mazingira huru na kufunguka kifikra, ili akili zifanye kazi na kuvumbua fikra. Ama ukitawala ugaidi wa kifikra, na tukamtuhumu kila anayetoa fikra mpya, na tukashuku katika nia ya kila anayekosoa au anayepinga, hakika sisi kwa hayo tunaziharamishia nafsi zetu uvumbuzi wa kifikra, na tutadharau rai zenye kupatia na kudumaza akili na fikra. Tatu: Ikiwa maadili yetu na misingi yetu ni thabiti daima hakika ratiba, njia na mbinu zinakubali mabadiliko na kuboresha kila unapopita muda, kwenda kwenye uzuri zaidi na ubora zaidi. Na haya ni ambayo inayasisitiza dini yetu tukufu kama yalivyo madhumuni ya hadithi tukufu kutoka kwa Imamu Musa alKaadhim : “Ambaye siku zake zitafanana basi ni mwenye hasara, na ambaye mwisho wa siku zake mbili ni mbaya zaidi basi yuko katika upungufu, na ambaye yuko katika upungufu basi mauti ni bora kwake kuliko uhai.” Na iliyokaribu nayo ni hadithi ya Imamu Ali  na nyingine 324


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

kutoka kwa Imamu Swadiq  kama ilivyo katika BihrulAnuwar, Juz. 78, uk. 277, uk. 327 na Juz. 77, uk. 377, na katika dua ya siku ya Jumapili ya Imamu Zainul-Abidin  : “Na ijaalie kesho yangu na baada yake iwe ni bora kuliko saa yangu na siku yangu hii.” Na mwenendo wa maendeleo na mabadiliko katika maisha yetu ya leo yanakwenda mbio katika pande mbalimbali na teknolojia na njia za maarifa na matangazo na uendeshaji, na tukishikamana na mbinu zilezile na vifaa na manhaji za kurithi katika mazingira yetu ya kielimu na kidini, masafa ya kutenganisha baina yetu na msafara wa maendeleo ya kisasa yatakuwa ni makubwa na mapana. Na zimetoka ndani ya hawza za kidini na mazingira ya marji‟i sauti zenye ikhilasi na uelewa ambao zinalingania juu ya dharura ya mabadiliko na kuboresha katika manhaji za utafiti wa hawza na mbinu za kimalezi ya kielimu, na njia za kuelimisha na kuelekeza, na njia za jukumu la uongozi wa umarji‟i. Na maandiko ya Khomeni  na misimamo yake inazingatiwa kuwa ni madrasa kamili katika nyanja hii, kama ambavyo Marji‟i Shahidi Sayyid Swadir  katika rai na fikra za ukosoaji na mabadiliko katika hali ya hawza na nafasi ya maraji‟i, ameashiria kwenye baadhi yake katika utangulizi wa harakati zake katika elimu ya Usuul na katika mapendekezo yake kuhusu umarji‟i yenye manufaa na katika mhadhara wake wa mwisho ambao umechapishwa chini ya anwani “al- Mihnatu.” Na nchini Iran maudhui ya kuboresha hali ya umariji‟i ni mahali pa utafiti na mjadala kutoka kwa wengi katika maulamaa na wanafikra baada ya kufariki Sayid al-Burjurudiy . Na vilifanyika vikao ambamo alishiriki humo mfano wa Marhum Sayid al-Twalaqaaniy, Shahidi al-Mutwahariy, na mwanafikra Muhammad Taqiy Shariatiy na wengineo. Na kumechapishwa kutokana na hayo utafiti mwingi katika kitabu kwa anwani 325


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

“Marjiiyatu waruhaniyati” kwa lugha ya kifursi. Na umekwishatarijumiwa utafiti wa Sheikh Mutwahariy kwa lugha ya Kiarabu na umechapishwa kwa jina la “al-Ijitihadu fil-Islaam”. Na hatuwezi kusahau katika nyanja hii rai za ujasiri ambazo amezitoa al-Allammah al-Maruhum Sheikh Muhammad Jawadi Mughuniya ndani ya maandiko yake mbalimbali na mengi. Na umekwishawadia wakati maudhui ya maendeleo na utafiti wa hali ya hawza na umarjii yawe ni mahala pa utafiti na mjadala makani, ndani ya kamati zenye kujali au mikutano yenye malengo au majadiliano yenye kujenga kupitia mimbari za kiutamaduni na kimatangazo. Nne: Umarjaa wa kidini una nafasi yake muhimu katika umma na uhalisia wake unaathiri athari kubwa juu ya hali ya kundi la Kishi‟ah, na hivyo hauko mbali na kubeba jukumu la ambayo kundi linaishi nayo miongoni mwa hali na mazingira. Na ikiwa kuna vikwazo na vizingiti vinavyodhoofisha uwezo wa umarji‟i katika kukabiliana na uongozi, ni wajibu kundi lote kubeba jukumu la kuondoa vikwazo hivyo na kuondoa vizingiti. Na ikiwa changamoto kubwa za kileo zinalazimisha umma kuwa katika kiwango cha kukubali changamoto hizi, hakika umarji‟i ndio unahusika na hilo kwa daraja la kwanza. Kwa hiyo, ni haki ya wenye ikhilasi na wenye uelewa kupiga kengele ya hatari na kuonyesha hofu yao na huzuni yao juu ya mustakabali wa umaraji‟i wa kidini. Na matumaini yetu yapo kwa Maraaji‟i watukufu, na viongozi watukufu katika hawza za elimu, wasishughulishwe na mbinyo wa washabiki na wenye kuunga mkono katika kusikiliza sauti za wenye ikhilasi na wenye uelewa. Swali: Mimbari ya Husein na majilisi za Huseini zina nafasi kubwa na wazi katika hali ya jamii ya Kishi‟ah, na kwa kuzingatia kuwa nyinyi ni kati ya makhatibu wa mimbari hizo, 326


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

vipi mnatathimini jukumu la nafasi ya mimbari na hotuba za Huseiniya hivi sasa je, zinaendana na mazingira na mabadiliko ya kisiasa na kijamii? Kama ilivyo maarufu, mimbari ya Huseini imekuwa ni njia inayotoa nafasi ya kuelimisha umma kwa Mashi‟ah, na imefanya kazi kubwa katika kustawisha ufuasi wa Ahlul-Bayt , uimara wa kinafsi katika historia yao na kumbukumbu yao ndani ya jamii ya Kishi‟ah. Na kuna vitu na mambo ambayo ni nguvu kubwa inayopatikana katika mimbari na majilisi za Huseini miongoni mwazo ni: Hali ya uananchi ya watu katika muonekano huu, ambapo zinafanyika majilisi kwa kujitolea wananchi, hakuna shughuli wala nafasi ya utawala humo, na watu wanachagua makhatibu wao kulingana na raghba zao bila ya kuingiliwa na yeyote. Vile vile uitikiaji wa watu kuhusu majilisi za Huseiniya hususan katika siku za Muharramu na minasaba mingine ya kidini ni jambo linaloleta mvuto na mshangao. Kama ambavyo mazingira na huruma iliyojaa ambayo inatawala katika majilisi yanafanya nyoyo na nafsi kuwa tayari kuathirika na kuamiliana pamoja na anayoyaeleza khatibu. Na kwa hiyo majilisi za Huseiniya zimeweza kufanya mengi, na kuacha athari katika jamhuri ya Mashi‟ah, isipokuwa kuna baadhi ya vikwazo ambavyo vinadhoofisha dauru ya mimbari na uwezo wake katika kuleta athari kubwa kadiri inavyowezekana nazo ni: - Hali za kisiasa ambazo zinabana uhuru wa khatibu katika kutoa maudhui yanayoendana na mazingira na kujali mambo ya wakati. Maadamu uhuru wa kifikra na kisiasa haupatikani katika nchi nyingi, hakika mimbari inakuwa imebanwa na yanayoizunguka miongoni mwa mazingira. Na tunajua namna gani baadhi ya makhatibu ambao walitaka kufikisha ujumbe wao bila ya kujali mazingira yanayozunguka na 327


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

wametoa uhai wao kama thamani ya ushujaa wao. Na baadhi wamevumilia jela na mateso na kufukuzwa, kama ilivyotokea kwa makhatibu wa Kiirani wapigana jihadi katika zama ya Shah, na kama ilivyotokea Iraki. - Mbinyo wa kuiga: Ambapo baadhi ya jamii zinang‟ang‟ania khatibu kujilazimisha na muundo na njia ya kuiga na ya kurithi katika khutuba yake, na kukariri kwao waliyoyazoa miongoni mwa visa na mambo ya sira, bila ya kuzungumzia matatizo ya jamii na shida zake, kama ambavyo kipimo cha uzuri wa khatibu ndani ya uigaji huu unatokana na upeo wa uwezo wake wa kuamsha hisia na kiwango cha uzuri wa sauti katika kueleza masaibu ya Ahlul-Bayt . Kwa hakika ni lazima tuseme hakika mfano wa vibano hivi vimeanza kumalizika na kwisha kwa kuenea uelewa na ufahamu. - Kiwango cha khatibu na lengo lake: Pamoja na uzamani wa hotuba ya mimbari kwetu, na haja kubwa ya makhatibu, na kuenea majilisi za Huseiniya, isipokuwa maandalizi ya makhatibu inatimu kwa bahati mbaya na msukumo wa ratiba binafsi. Hatuna vyuo katika hawza zetu za elimu kwa ajili ya kuandaa makhatibu au kuboresha viwango vyao, na hakuna ratiba ya kusaidia kulea makhatibu na kuwaendeleza. Na kwa masikitiko hata kozi fupi ya kutengeneza hotuba katika kitabu cha mantiki cha Marhum Sheikh Mudhwafar, mara nyingi waalimu wanashughulika na wanafunzi na kulisomesha katika hawza za elimu, na yote hayo yamepelekea kuwa wengi wa makhatibu katika jamii yetu hawako katika kiwango kinachotakiwa katika kupevuka kwao kielimu na kiutamaduni. - Na jambo la mwisho: Kiwango cha lengo la ujumbe. Baadhi ya makhatibu, mimbari kwao imekuwa ni kazi na chanzo cha maisha, na baadhi ya wengine hotuba kwao imekuwa ni shughuli na kazi, na wala haipingiki kwamba tunalo – walhamdulillahi – kundi la makhatibu wenye lengo wanaharakati ambao wanai328


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

zingatia mimbari kuwa ni njia ya kuhudumia lengo tukufu, na wanaitumia mimbari katika kuelimisha watu na kuwaelekeza ili kubeba majukumu yao ya kidini na kijamii. Na kinachotakiwa katika hatua hii muhimu ni kuzingatia hali ya mimbari na majilisi za Huseiniya katika jumla ya makhatibu na pande zenye uelewa katika umma na inawezekana kutimia hilo kupitia mapendekezo yafuatayo: Kwanza: Marajiâ€&#x;i wa kidini waonyeshe mazingatio katika upande huu, kwa kuchunga mambo ya makhatibu na kuwajulia hali zao na kutoa maelekezo kwao. Kwa mfano anapotaka marijiâ€&#x;i wa dini kwa makhatibu kutia mkazo katika majilisi zao katika msimu huu (Muharamu au Ramadhani) katika maudhui maalumu anayoona umuhimu wake, hakika hilo litapokewa na kukubalika na makhatibu wengi. Na alikwishafanya hayo Marhum Imam al-Khumainiy ď ‘ ambapo alikuwa anapokea makhatibu wa Kiirani au makhatibu wa Tehran karibu na siku kumi za Ashura na kuwapa nasaha zake na rai yake na hiyo ilikuwa ni ishara nzuri pamoja na kuchukua tofauti kwa jicho la mazingatio. Pili: Kuweka ratiba ndani ya hawza ya elimu ili kulea makhatibu na kuwaendeleza. Tatu: Kufanya makongamano ya kiulimwengu baina ya makhatibu ili kubadilishana rai na uzoefu, na majadiliano katika kuchagua kwao maudhui na kuboresha malengo na mbinu za khitwaba. Hakika sisi tunashangazwa na habari za makongamano ambayo yanafanywa ulaya kuhusu mambo madogo na ya kipuuzi kama nilivyosoma mwishoni kuhusu kongamano la haki za wavutaji ambalo lilifanyika Helsink Finland mwishoni mwa mwezi wa kumi na moja mwaka 1990, na ambalo limesambazwa na jarida la wakala wa habari na kwamba liliendelea kwa siku mbili na lilihudhuriwa na wawakilishi 120 kutoka dola za ulaya, Marekani, Latini Amerika, Australia na Japani!! 329


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Wakati ambapo wito wa kongamano la makhatibu linakuwa ni jambo linaloleta mshangao na majadiliano katika mazingira yetu! Na baadhi wanaweza kutoa udhuru kwamba mazingira ya kisiasa hayatoi ushirikiano katika mfano wa haya, lakini hili halipo kila sehemu. Kuna nchi inawezekana kwa makhatibu wake kukutana au kubadilishana rai na uzoefu. Na katika kumbukumba ya huzuni katika nafsi yangu katika nyanja hii mwaka 1399H/1979 nilihamia katika sehemu ya Abadan, Khurasan na niliwaita makhatibu huko kutoka Abadan, na lengo ni ushirikiano wa kijamii na kuunda kundi la makhatibu, na walikuwa wanashiriki humo takriban makhatibu 40 kwa viwango vyao tofauti. Na tulikuwa tunakutana kila wiki, na kubadilishana faida, lakini kulitokea matatizo ya kisiasa huko kisha ikatokea vita ikabomoa umoja na mkusanyiko huo. Nne: Kutoa jarida maalumu ambalo linajishughulisha na khitwaba na mambo ya makhatibu. Na ulimwengu umejaa majarida maalumu katika nyanja mbalimbali za kifikra na za kijamii, na vilevile kuhusu umakenika na fani, na kuhusu mavazi, na kuhusu nyanja nyingi. Inafaa sana kutoa jarida linalojali habari za makhatibu na maelezo yao, waliopita na waliopo na habari za majilisi za Huseiniya na mambo ambayo yanajali makhatibu katika kiwango cha khutuba au mbinu zake. Tano: Wajitolee makhatibu wenye uwezo wenye kufaulu kwa kutoa uzoefu wao na fikra zao ili wanufaike makhatibu wengine, kama vile al-Allammah khatibu Muhammad Taqiy Falsafiy, Ustadh khatibu Dokta Sheikh Ahmad al-Wailiy na khatibu mahiri Sheikh Abdul-Hamid al-Muhajir. Hakika rai na uzoefu wa mfano wa hawa maustadhi viongozi utakuwa ni wenye manufaa na faida kwa makhatibu wapya na wanaoinukia. 330


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

MAANDIKO Utangulizi wa kitabu (al-Kisau Fiy Ma’arifil-Ummatil-Islamiyah)207 Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu peke Yake. Sala na salamu zimwendee ambaye hakuna nabii baada yake, Bwana wetu Muhammad na kizazi chake kitwaharifu maasumina. Ama baada: Kinanivutia kwa mtunzi wa kitabu mambo mawili: Kujali kwake utamaduni na maarifa, kwani yeye anakaa na maulamaa na anakithirisha kuwatembelea wanafasihi na makhatibu, na anawasiliana na jumuiya za kitamaduni za Kiislamu, na ananunua vitabu vya utamaduni kwa aina zake na miundo yake mbalimbali hadi amejitengenezea maktaba nzuri ambayo inatosheleza katika kona za faragha yake. Na inashibisha katika bustani yake kiu yake ya maarifa na fasihi. Na inapendeza kama kila mwanajamii wetu atamiliki mfano wa mazingatio haya hivyo ungetawala utamaduni na kuenea uelewa, na kumalizika pengo ambalo linasababisha upotovu na porojo. Na katika jamii zilizoendelea, maktaba inazingatiwa kuwa ni katika dharura ya nyumba, na ni sehemu muhimu katika samani za nyumba. Kama ambavyo mtu anatayarisha katika nyumba yake mashine ya kufulia, kiyoyozi na vile vile anaandaa maktaba na sehemu ya kusomea wanafamilia. Na sisi Waislamu – Wallahi – ndio aula zaidi kuliko umma zote 207

Al-Kisau fiy Maarifil-Ummatil-Islamiyah cha Haji Abdul-Qadir Ali Abu alMakaarim, Kuwait 1397 Hijiria.

331


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

katika kujali utamaduni na maarifa na kutayarisha njia zake. Qur‟ani yetu tukufu inasema: “Na sema Mola Wangu nizidishie elimu.” Suratul- Twaha: 114. Na Nabii wetu  anasema: “Tafuteni elimu kuanzia udogoni hadi wakati wa kufa.” Na kutoka kwa Imamu Amirul-Muuminina Ali bin Abi Twalib : “Jifunzeni elimu, hakika kujifunza kwake ni wema na kuifundisha kwake ni tasbihi na kuitafuta kwake ni jihadi na kumfundisha asiyeijua ni sadaka.” Na jambo la pili ni: Raghba yake katika kutoa huduma fulani, katika nyanja ya utamaduni wa kidini na maarifa ya Kiislamu. Kana kwamba mtu hakuridhia katika nafsi yake kuchukua tu, bali kuzalisha na kutoa, kwa kadri ya uwezo wake na kipaji chake, na hayo yanakuwa ni mchango katika kutangaza utamaduni wa Kiisalmu na maarifa yake, na kwa kuongezea kubakia jina lake na kudumu utajo wake na kuendelea thawabu zake kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na matumaini haya ni mazuri na yana manufaa kama yataenea kwa kila mtu kati ya watu wa jamii yetu na kila mmoja akaitaka nafsi yake isiishi muda wote wa maisha yake katika hali ya kuchukua, bali ni wajibu azalishe na kutoa utoaji wenye manufaa na wenye kudumu katika maisha. Nasema: Kama itapatikana hisia kisha ikatekelezwa kivitendo na kikazi kwa kila mtu, na kulingana na uwezo wake na kiwango chake mtu, harakati zetu za utamaduni zingekata masafa makubwa, na shughuli za kijamii zingekuwa katika kiwango kilichoendelea. Na kitabu hiki ambacho kipo mikononi mwako – ewe msomaji mtukufu – ni tunda la sifa hizi mbili. Zimepatikana kwa mtunzi mtukufu, kununua kwake vitabu na kudumu kwake katika 332


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

kusoma kumempatia rejea za maudhui na vipengele vyake. Na raghba yake katika kutoa imezalisha kitabu hiki kizuri. Na natamani kwa mtunzi awe ni kigezo kwa wengine katika nyanja hii. Ziada ya kujisomea na kutafiti. Ziada ya kuandika na kutunga – ewe Abu Adinan – Mwenyezi Mungu akupe taufiq na awakithirishe walio mfano wako. Hasan Musa Saffaar Qtif 16/7/1397H. Utangulizi wa kitabu (Swidiqatu Mariyamu al-Adharau: Muujizatul-Ajiyaali)208 Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu. Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu. Sala na salamu zimwendee Nabii wetu Muhammad na Kizazi chake kitwaharifu. Baada ya karne ishirini zilizopita katika maisha yetu, je, Bibi Mariyam binti Imran  anacho cha kutoa leo kwa wanadamu? Pamoja na maendeleo haya makubwa ambayo ameyapata mwanadamu kielimu, kiviwanda na kiteknolojia je, sisi tuna haja ya kusoma kurasa za waliopita ambao waliishi katika zama zilizopita zisizoendelea? Na mwanamke ambaye alisifika na akashika hatamu za utawa na akashika hatamu za nafasi ya uongozi katika dola muhimu za 208

Swidaiqatu Mariyamu al-Adharau: Muujizarul-Ajiyaal cha Sheikh Jaafar al-Amrad, Darul Bayaan al- Arabiy, Beirut chapa ya kwanza 1412 Hijiria.

333


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Ulimwengu katika karne hii, kama vile Mwingireza ambaye aliitawala (Magreti Sacher) muda unaozidi muongo wa zama, Mfaransa ambaye aliongoza baraza lake la mawaziri (Adiyat Kariyouf) na Mfilipino ambaye anaitawala (Kourazon Aqwinow) na India ambayo imenyenyekea katika utawala wa Indira Ghandiy muda wa miongo miwili, tukiachilia mbali Bengali na Pakistan. Mwanamke huyu wa kileo je, anapata katika maisha matukufu Mariyam ď Š ambayo yana umuhimu naye na yanatengeneza nyongeza yenye manufaa katika shakhsiya yake? Hakika maswali mengi sana ya aina hii yanakabili utafiti wowote au kusoma maisha ya mawalii na wema ambao walibebwa na zama iliyopita. Na tunaweza kupata jawabu la maswali haya kupitia kuashiria kwenye upande mwingine na muhimu zaidi katika maisha ya mwanadamu, nao ni upande wa kiroho, maadili na maanawiya. Mwanadamu sio mwili tu, wala sio kiumbe cha kimaada tu, hiyo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu alipomuumba kutokana na udongo, alipulizia humo roho Yake na akampa akili, matakwa na dhamira. Na hayatulizani maisha ya mwanadamu ila kwa kulingana pande mbili, za kiroho na kimwili, maada na maanawi. Ikiwa mwanadamu atapuuza mojawapo hakika maisha yake yatakuwa ovyo na hayana maana, kama yule anayekosa moja ya miguu yake au moja ya macho yake. Na yanayomkabili mwanadamu hivi sasa miongoni mwa mateso na machungu hakika ni matokeo ya kawaida ya ukosefu wa uwiano unaotakiwa, ambapo amepuuza upande wa kiroho wa kimaanawi, wakati ambapo ameendelea na amekuza mazingatio ya kimaada. Hakika mwanadamu leo ana haja sana na chemchem ya kiroho, na nguvu ya kimaanawi ili kuondoa uasi wa visababishi vya shari, ufisadi na uovu, ambao umekuwa unaungwa mkono na umesheheni uwezo na maedeleo makubwa ya kimaada. 334


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Na maisha ya mawalii ndio chanzo na chemchem ambayo inakata kiu ya mwanadamu katika maanawiya yake na maadili, nao ni upepo ambao unaipa uhai dhamira ya mwanadamu na uwepo wake na kumstawisha katika shakhsiya yake na mwelekeo wa kheri na wema. Na kitabu kilichopo mbele ya msomaji mtukufu ni jaribio zuri la kuandika sura nyepesi na ya wazi kuhusu maisha ya Bibi Swidiqah Mariyam binti Imran , naye ni kigezo na mfano wa kiungu na chemchem ya kheri kwa maadili na maanawiya. Pamoja na kupita karne ishirini tangu kufariki kwake ila hakika maisha yake na sira yake bado ingali ni tajiri na ni yenye kutoa. Inatia mkazo kwa binadamu kwa ujumla, na kwa wanawake hususan, dharura ya mafungamano na Mwenyezi Mungu Mtukufu na kunyenyekea katika sharia Yake, na umuhimu wa maadili matukufu ya kiroho na sifa za mwenendo na dauru yake katika mafanikio na kumwepusha kwake na hatari na shari. Bibi Mariyam  alikuwa ni mwanadamu mtukufu, hiyo ni kwa sababu uwanaume na uwanamke si kingine isipokuwa ni lengo tu la madhumuni ya uwanadamu. Na kwa kiasi ambacho yanatimia madhumuni na kunyanyuka daraja la malengo inakuwa ni thamani ya mwanadamu na utukufu wake bila ya mazingatio yoyote ya uwanaume au uwanamke. Mwenyezi Mungu alimchagua mwanamke huyu ili alete kupitia kwake muujiza wa kiungu wa nadra, na ili awe ni mama wa Nabii kati ya Manabii watukufu wa Mwenyezi Mungu na mmoja kati ya watu muhimu wa kubadilisha historia ya binadamu na wenye kuathiri humo, kuzaa Nabii wa Mwenyezi Mungu Isa , na umama wake kuwa ni namna ya kipekee isiyozoeleka ambapo hakuguswa na binadamu yaani bila ya mume, na makadiri haya ya Mwenyezi Mungu ni mtihani na balaa ngumu kwa bibi Mariyam  ambapo alilengwa na mishale ya wapinzani na 335


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

wazushi, lakini yeye alivumilia machungu na akasubiri mbele ya uchochezi na uzushi, na alikuwa kama alivyotaka Mwenyezi Mungu katika kiwango cha changamoto, na akafaulu katika mtihani mgumu. Huyo ndio mwanamke ambaye alitaabishwa na jamii ya maadui katika maisha yake. Hivi sasa amekuwa ni mwanamke wa kwanza miongoni mwa mabinti wa Hawaa katika utukufu na heshima. Zaidi ya nusu ya idadi ya binadamu wanamheshimu na kumtukuza. Wanamkubali na wanatabaruku kwa utajo wake, na wanatukuza kila chenye mafungamano naye. Nataraji kwamba mtunzi mtukufu amefanikiwa katika jaribio lake, na msomaji atapata katika kurasa za kitabu hiki ambayo yanampa nyongeza ya kumwamini Mola Wake na dhati Yake, na ambayo yanamsukuma kuangaziwa na nuru ya maisha ya huyu Swidaqah mtwaharifu na hususan katika jamii ya wanawake. Na natamani kitabu hiki kiwe ni utangulizi na mwanzo wa mwenendo wa kazi yenye malengo katika nyanja ya utunzi na uandishi kwa mtunzi mtukufu, ambaye ameweka nadhiri maisha yake katika kutumikia dini na jamii, na ameilea nafsi yake kwa tabia njema, Mwenyezi Mungu amhifadhi na anufaishe kwaye, na awakithirishe walio mfano wake katika jamii. Na amani daima iwe juu ya mkweli mtwaharifu Mariyam binti Imran na kwa mtoto wake Nabii mtukufu Isa na kwa Manabii wote na Mitume na Mawalii wa Mwenyezi Mungu na watu wema. Hasan Saffar 25/2/1412 A.H.

336


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Utangulizi wa kitabu “Uqudatul-Haqaarati.� 209 Sifa zote njema anastahiki Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu. Sala na salamu zimwendee Nabii wetu Muhammad na kizazi chake kitwaharifu. Hali ya jumla ambayo inaishi jamii ni natija na matokeo ya hali za watu binafsi na jamii. Zinaponyooka tabia za watu hali ya jumla ya jamii inakuwa ni salama. Na wanajamii wanapopatwa na upotovu na maradhi, hakika hali ya jumla ya jamii itakuwa mbaya na ovu. Katika mkusanyiko wa watu inaundwa jamii, na katika hali zao unatengenezeka uhalisia wa jumla. Na tunapoona hali ya jamii sio nzuri, ni lazima tusome hali ya wanajamii, ili tujue chanzo cha kosa na siri ya upotovu. Na aghlabu jamii zetu za Kiislamu leo zinaishi hali isiyoendana na mafunzo ya dini yetu tukufu, na wala hairidhiwi na akili, ambapo kutoendelea kumeenea, matatizo yenye kutia dhiki, maradhi yameenea, kunyenyekea dhulma, udhalili, mizozo na ugomvi. Na kwa ajili ya kurekebisha hali hii mbaya, ni lazima kuelekea katika kutafiti mzizi na sababu za kina. Chanzo chake ni nafsi za wanajamii, na hali ya kila mtu ni uakisi wa hali yake ya kinafsi, kama ambavyo hali ya jamii ni uakisi wa hali za watu. Tunapoona aghlabu ya wanajamii wanaishi bila ya kujali na kukimbia kubeba majukumu na kushindwa mbele ya changamoto, ni lazima tujue kwamba maradhi yanashambulia katika nafsi zao. Na bila ya kutibu maradhi hayo ya kinafsi na ya kiroho haiwezekani kurekebisha hali ya watu ambayo ndio njia ya kurekebisha hali ya jamii. 209

Uqudatul-Haqarati cha Ridhaa Aal Matwar, Darul-Bayaan al-Arabiy, chapa ya kwanza 1413 Hijiria.

337


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Na kwa sababu hii anasema Mola Wetu Mtukufu, Mjuzi wa yaliyofichikana na siri za viumbe Wake:

َ ّ َ ُ َ َُّ ُ َ ‫ى ى‬ “….. ُِ ‫ىم َخ ٰى ُيغ ِّحروا ما ِبأ ف ِع‬ ٍ ‫… ِإن اللكه ال يغ ِحر ما ِبل‬..” “Hakika Mwenyezi Mungu habadilishi yaliyoko kwa watu mpaka wabadilishe yaliyo katika nafsi zao.” (Surat Ar-R‟ad 13:11) Na kutokana na uhakika huu wa ukweli na thabiti, hakika anayefikria kurekebisha jamii ni lazima ajali kutibu maradhi ya kinafsi na kiroho katika wanajamii. Na hii ndio manhaji ya Manabii na Mitume na Maimamu, rehema na amani ziwe juu yao wote, ambapo wamezatiti juhudi zao katika kurekebisha nafsi na kuzitakasa:

َ​َ َ َ َ ‫ُ َ ى‬ ََُّ ٰ َ ُ ً َ َ ّۧ ّ ُ ِ ‫”هى الزي ٰػث ِفى ِميكن سظىال ِمن يخلىا غلي ِ ءايك ِخ ِه ويضهي‬ َ َ َ َ ُ ُ َّ َُ “…..‫ىم ِت‬ ‫احخ‬ ِ ‫الىخكب و‬ ِ ُ​ُ ‫ويػ ِلم‬ “Yeye Ndiye Alimpeleka Mtume kwenye watu wa siojua kusoma, aliyetokana na wao, awasomee Aya Zake, na awatakase na awafunze Kitabu na hekima…..” (Surat Al-Jumu‟a; 62:2). Na wenye kughafilika na ukweli huu wanaweza kuuliza kuhusu nafasi ya Manabii na Maimamu kwamba wao wamefanya nini kwa watu zaidi ya nasaha na mawaidha. Ndio, hakika muhimu zaidi wanayoyahitaji watu ni hizo nasaha na mawaidha, ambayo yanaangazia ndani ya nafsi ya mwanadamu, na hisia za moyo wake na kufichua sehemu za maradhi na hali za ugonjwa na kuiongoza katika matibabu sahihi. Na waelekezaji wa jamii sasa hivi kati ya maulamaa, makhatibu na waandishi ni juu yao kuendeleza kazi ya Manabii na Maima338


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

mu katika juhudi ya kutakasa nafsi za wanajamii kutokana na maradhi ya ubinafsi, kufeli na upotovu. Jamii yetu wakati uliopita ilikuwa inakabiliwa na kuenea maradhi ya kimwili, na kiwango cha vifo kiko juu. Na ulemavu ulienea, kwa kutokupatikana taasisi za kiafya kati ya hospitali na zahanati, na kwa kutokuwepo mkakati wa kinga ya maradhi kabla ya kutokea kwake, na katika kuyatibu baada ya kupatwa na maradhi, ilikuwa hata maradhi madogo mepesi yanaangamiza maisha ya wengi. Lakini kuendelea kiasi fulani katika nyanja ya afya kumepunguza wastani wa vifo na kuweka mpaka wa ulemavu na maradhi. Na wastani wenyewe na kwa nguvu unajipenyeza wenyewe katika upande wa kiroho na kinafsi, ambapo ni lazima kuwe na mkakati wa kujikinga kutokana na maradhi ya kinafsi na kiroho, na ni lazima kuwepo na ratiba ya tiba ya kutopatwa na maradhi. Na bila ya hayo hasara yetu itakuwa ni kubwa na mbaya, na iko wapi hasara ya maradhi ya kimwili katika hayo? Maradhi ya kinafsi hatari yake ni kubwa zaidi kuliko maradhi ya viwiliwili. Na taasisi za kidini, kiutamaduni na kijamii ni sawa na hospitali na zahanati za maradhi ya nafsi na roho. Na maulamaa, makhatibu na waelewa, wao ndio matabibu wanaoendewa kwa ajili ya kutibu maradhi hayo. Na maendeleo yoyote katika jamii katika kiwango cha taasissi za kidini, maulamaa na makhatibu inamaanisha ni dhamana zaidi na mazingatio makubwa zaidi katika kurekebisha hali ya jamii na kuibadilisha na kuwa bora zaidi. Imenifurahisha sana kusoma kitabu hiki kizuri, ambacho mtunzi wake ametoa juhudi zenye kushukuriwa katika utafiti wa kutibu maradhi hatari ya kinafsi na kiroho wanayokabiliwa nayo wengi kati ya wanajamii wetu. 339


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Hayo ni maradhi ya kukuosa ya kuamini (Uqudatul-haqarati) ambayo yanamfanya mtu kuwa mnyonge na dhalili, mwenye kujisalimisha katika kutokuendelea na kwenye dhulma, na ambayo yanamzuia mwanadamu kuibua nguvu zake na vipaji vyake, na yanaua kujiamini na kumnyima kufanya jukumu lolote lenye manufaa katika kutumikia jamii yake. Na wakati ule ule hakika maradhi ya kukosa ya kuamini (Uqudatul-haqarati) yanamsukuma mwanadamu kwenye tabia mbaya na mwenendo potofu na wakimakosa. Na mara ngapi tunaona katika jamii yetu watu wanakandamiza vipaji vyao na uwezo wao kwa udhaifu wa kutokujiamini. Na mara ngapi tunaona hali za udhalili na unyonge na kufeli mbele ya maadui dhaifu, waoga wasio na nguvu, isipokuwa kule kujisalimisha kwa wahanga wao na kutawaliwa kwao na hisia za kushindwa na udhaifu katika nafsi zao. Bila shaka, hakika sababu nyingi zimechangia katika kutengeneza maradhi haya na kuyasambaza katika nafsi za wanajamii. Ni zipi hizo sababu? Na namna gani tutakabiliana nazo? Haya ndio ambayo kurasa za kitabu hiki kizuri kinajaribu kuyajibu. Na hakika mimi nampongeza mtunzi kwa kitabu chake kizuri na namuomba naye ni kijana mwerevu mwenye ikhilasi, na ni khatibu mwanaharakati mwenye malengo, aendeleze juhudi zake katika utafiti wa maudhui haya kupitia uandishi na khitwaba. Kupitia juhudi zake na juhudi za wa mfano wake miongoni mwa waelewa wenye ikhilasi tunatarajia mabadiliko na mageuzi katika jamii yetu. Nataraji makhatibu na maulamaa wengine na watafuta elimu ya dini wataiga nyendo za kijana huyu mtukufu na kuijaza medani kwa khutuba zao na uandishi wao wenye malengo, utafiti ambao 340


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

unaelekeza mwanga katika mizizi ya kutokuendelea na kuwaelekeza kwenye njia ya kinga na utatuzi. Mwenyezi Mungu azibariki juhudi za mtunzi na apokee kazi yake na ampe taufiki ya kuzidi katika kuitumikia dini na jamii, na awakithirishe waumini walio mfano wake. Hasan Saffar 15/6/1414 Hijiria. Utangulizi wa kitabu (Afghanistani: Tarikhuha – Rijalaatuha)210 Kwa maneno ya al-khatibu wa mimbari al-Huseiniyah mahiri, na mwenye utunzi mzuri, mwanachuoni mtukufu na mwanafasihi mwenye kuheshimika, Samahatu al-Allammah al-Mujahidi Hujatul-Islami wal-Muslimina, Sheikh Hasan Saffaar (udumu umri wake katika kutumikia umma): Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu. Sifa zote njema anastahiki Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu. Sala na salamu zimwendee Nabii wetu Muhammad na kizazi chake kitwaharifu na masahaba wake wema. Hakika cha muhimu anachokihitaji mwanadamu katika kukabiliana na changamoto za maisha ni kujua nafsi yake na avumbue uwezo wake na vipaji vyake. Amiliki kujiamini na aibui vipaji vyake na kunyambua nukta za nguvu zake, na kumaliza sehemu za udhaifu na kasoro. 210

Afghanistan: Taarikhuha Rijalaatuha cha Sheikh Husein al-Fadhiliy, Darus-Swafuwati, Beirut – Lebanon, chapa ya kwanza 1414 Hijiria – 1993.

341


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Na kwa ajili hiyo nususi na riwaya za kidini zinatia mkazo juu ya nafasi ya kujua dhati; anasema Imamu Ali : Maarifa bora zaidi ni mwanadamu kuijua nafsi yake.” “Asiyeijua nafsi yake basi mwingine asiyekuwa yeye hatomjua kabisa.” “Na yatosha mtu kuwa mjinga kwa kutokuijua nafsi yake.” Na kibaya zaidi ambacho anakabiliwa nacho mwanadamu ni kutokuijua nafsi yake, na kutokuamini dhati yake. Na anakuwa ni mwenye kushindwa mbele ya changamoto ndogo kabisa; ni dhaifu mbele ya makabiliano madogo kabisa, mwenye kuwafuata wengine, na ni mzigo juu yao. Kama unavyoafikiana uwiano huu juu ya mtu binafsi na unaafikiana vilevile juu ya mwanadamu katika jamii, jamii yoyote ya mwanadamu vyovyote itakavyokuwa, thamani yake na nafasi yake kulingana na kujua kwake dhati yake, hakika anakabiliana na changamoto kwa matakwa imara, ama akikosa hayo anapata mtihani wa kuporomoka azima na udhaifu wa matakwa. Na inaoneka kwamba jamii zetu za Kiislamu zinakabiliawa na tatizo hili tangu kufunguka kwake katika maendeleo ya kimaada ya kileo, ambapo sababu zimeongezeka na visababishi vimeikosesha jamii yetu kujiamini na ikapatwa na maradhi ya kupoteza dhati. Kustaajabishwa na maendeleo ya kunusurika kumeleta hali ya kushindwa katika nafsi, ikawa haioni thamani yoyote ya historia yake, misingi yake na uhalisia wake au jambo lolote mbele ya maendeleo makubwa ya kimaada. Na vita vya kiutamaduni, vita vya kinafsi na propaganda za kimatangazo ambazo wamezisheheni maadui zilikuwa zinalenga kufuta dhati na kupinga hazina na kudhoofisha kujiamini katika 342


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

safu za wanajamii na yamekwishatimia kwao mengi kutokana na hayo. Na kisha sababu nyingine ya ndani ndio mbaya zaidi kuliko sababu ya nje, inawakilishwa na muamala mbaya baina ya pande na makundi ya umma, ambapo kila upande unakwenda mbio kuvunja upande mwingine na kufukia historia yake na athari zake, na matokeo ya mwisho ni kodhoofika jamii na kuchelewa kwake. Ni kawaida kuwa na mielekeo mingi ya kifikra, ufuasi wa kikabila, kiukoo na ufuasi wa kisiasa katika umma mkubwa wenye kupanuka. Lakini uhusiano baina na mielekeo hii na ufuasi huu ulikuwa ni wajibu uwe ni mzuri na wa kukamilishana, maadamu Uislamu ni uzio ambao unawajumuisha wote. Hayo ndio ambayo yalitakiwa, lakini yaliyotokea na yanayotokea ni kinyume cha hayo kabisa, ambapo kila upande unaona upande mwingine ni dhidi na ni adui. Unaimarisha uwepo wake, juhudi zake kwa ajili ya kumpiga vita hata kwa kuafikiana na kuungana na maadui wa nje wa kikweli kweli ambao wamenufaika na hali hii ya kutokuendelea katika umma, wakawa wanachochea upinzani baina ya pande za umma na wanawachochea baadhi yao kwa baadhi. Na vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Lebanon, vita vya Iraki na Irani, na vita vya Kuwait na mapigano ndani ya Afghanistani si kingine ila ni mifano ya hali hii chungu. Na umma hautovuka hali hii mbaya ila ukibadilika uwiano wa upinzani na ukaungana ndani ya umma na ikawa – adui ndio mpinzani hata kama akijidhihirisha kwa urafiki na upendo – na wa ndani ndio mwenza hata kama amehitalifiana pamoja naye kiukoo au kifikra au kisiasa. Na kuanzia na uwiano huu mpya unaotakiwa litakuwa jengo la nguvu ya dhati kwa kila upande katika umma, na kuhuisha 343


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

historia yake na athari zake, na kusonga mbele kiwango chake, na uhalisia wake unakuwa ni ile sehemu katika mkakati wa nguvu ya wote na maendeleo yao. Iraki haitoogopa kujenga nguvu ya Iran wala ghuba haitojihadhari na nguvu ya Iraki. Na vivyo hivyo baina ya nchi zingine za Kiislamu. Na hali ni hiyo hiyo baina ya madhehebu ya Kiislamu, hawatokasirika Ahlus-Sunna kwa maendeleo ya Mashiâ€&#x;ah, wala Shiâ€&#x;ah hawatachukia kustawi nguvu ya Sunni. Hakika sisi tunafanana na kaumu iliyoharibikiwa na meli baharini na wote wakakabiliwa na hatari ya mauti na kuzama. Watakapomuona mmoja wao anashikamana na chombo cha uokozi na kunusurika na kufika nacho ufukweni hakika hilo linaongeza manawiya yao na kuwashajiisha kufanya jaribio kama lake, na kuzatiti katika nafsi zao matakwa ya kuishi. Kunusurika kwake sio tu ni kwa ajili yao, na kunusurika kwake katika mawimbi ya bahari si tu kunusurika kwao bali ni kunusurika kutokana na hatari ambayo inawatishia wote. Na katika nchi kama Afghanistani, wameteseka watu wake Waislamu kwa karne kutokana na kutokuendelea, na miongo ya ukandamizaji wa uovu wa kisiasa. Na matokeo yake ni uvamizi wa Urusi wenye kuangamiza, ambao umebadilisha sehemu nyingi kuwa vilima, na umemaliza kheri za wananchi wake na wakafukuza na kuhamisha theluthi ya wakazi wake takriban. Nchi hizi, ni haja ilioje leo ya kuunganisha nguvu zao na kuongeza nguvu baina ya wananchi wake pamoja na kutoafautiana utaifa wao na madhehebu yao na vyama vyao, ili warejeshe kujenga nchi yao ilioharibiwa, na wawaamshe wananchi wao kuelekea kwenye maisha huru matukufu. Hayatatimia hayo kwa Afghanistani ikiwa akili za viongozi wake zitatawaliwa na uwiano wa upinzani wa ndani. Kiasi kwamba 344


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

kila upande umekuwa ukikwamisha maendeleo ya upande mwingine, na unazuia kushiriki na kutekeleza jukumu lake kamili katika kujenga nchi upya. Hakika historia ya Afghanistani na kuhuisha sehemu yoyote katika athari zake ni kutumikia Afghanistani yote na kila mwana Afughanistani. Na kisha ni kuhudumia maarifa yote na hazina yote ya Kiislamu na kibinadamu. Kwa mtazamo huu mzuri nimesoma sehemu za kitabu hiki kizuri ambacho kiko mbele ya mikono ya msomaji. Hakika kinaangazia juu ya sehemu iliyosahaulika katika historia ya Afghanistani ambapo kinazungumzia juu ya Shiâ€&#x;ah kwa kuzingatia kuwa wao ni sehemu isiyoweza kutenganishwa na hali ya mwananchi wa Afghanistani. Na ikiwa chuki na mizozo ya kitaifa katika wakati uliopita inazuia kuhuisha hazina ya makundi mbalimbali, hakika hali ya sasa ya Afghanistani ni wajibu itofautiane na yaliyopita. Wananchi wote na sehemu zote zimeshiriki katika kukabiliana na vita vya uadui wa Kirusi, na wote wametengeneza mshikamano wa muhanga wa kujitolea hadi wamewalazimisha wavamizi wenye kufanya uadui kuondoka. Hapana, sio hivyo tu bali wamechangia kwa juhudi zao kuanguka himaya ya kijamaa - Umoja wa Sovieti. Sasa hivi na baada ya kushinda Waafghanistani katika jihadi yao ndogo dhidi ya adui wa nje, ni wajibu wao wafaulu na washinde katika jihadi yao kubwa dhidi ya athari za kutokuendelea na kufeli kulikopita katika medani ya ndani. Je, watafanikiwa katika hilo? Hayo ndio anayoyatarajia kila Mwislamu mwelewa. Hakika jaribio hili zuri ambalo amelifanya mwandishi katika kitabu hiki, ili kuitambulisha jihadi ya kisharia na historia yake katika Afghanistani inazingatiwa kuwa ni mchango wenye kushukuriwa katika kujenga daraja la umoja na ushirikiano baina ya Waafghanistani. 345


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Na mwanzo wa kitabu hiki ni makala fupi aliyoiandika mtunzi na akanionyesha. Na kwa kujua kwangu umuhimu wa haja ya medani ya utamaduni, nilimuomba – Mwenyezi Mungu ampe taufiki – kupanua utafiti wake na kuukamilisha, na akakubali wazo hilo kwa uchangamfu mkubwa ambapo amefanikisha kutunga kitabu hiki kwa muda mfupi. Na mtunzi ni kijana mwenye mategemeo ya kuthubutu na kuendeleza utafiti wake katika hawza ya elimu. Na anahutubia vizuri kwa mafanikio, na kwa lugha ya Kiarabu, naye anatokana na kizazi cha familia tukufu. Mzazi wake ni Samahatu al-Allammah al-Hujah Sheikh Muhammad Ali al-Fadhwiliy, mwalimu wa Bahthul-kharijiy katika hawza ya Zainabiya. Na ni mtu mwenye tabia nzuri na unyenyekevu mkubwa. Na hakika mimi namtakia baraka mtunzi katika juhudi hizi nzuri na nataraji kutoka kwake aendeleze harakati zake za kifikra katika nyanja za uandishi na kutunga na vilevile katika utafiti wa khitwaba ili awe kwa taufiki ya Mwenyezi Mungu ni mmoja wa wajuzi wa dini na fikra katika medani ya Afghanistani ya Kiislamu. Mwenyezi Mungu atushike mikono sote katika ambayo humo kuna kheri na mafanikio. Na sifa zote njema anastahiki Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu. Hasan Saffar 20 Shawwal 1423 Hijiria

KUHESHIMU NA KUTUKUZA211 Kwa Samahatu al-Allammah al-Hujatul-Islamu, Sheikh Jaafar 211

Mafahimul-Qur‟an: Anatafiti shakhisiya ya Mtukufu Nabii  na maisha yake katika Qur‟ani Tukufu, ni utunzi wa Ja‟far Subhani, Juzuu ya saba chapa ya kwanza 1413 Hijiria / 1992, Darul-Adhuwai.

346


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Subhaniy Mwenyezi Mungu amhifadhi: Salamu alaikum warahamatullahi wabarakatuhu na katika yaliyokuja humo ni: Kama ambavyo jeshi katika medani ya vita linahitaji kuungwa mkono na msaada wa chakula na zana, vilevile wanaolingania kwa Mwenyezi Mungu na viongozi wa harakati za Kiislamu, wao wana haja zaidi ya mwenye kuwapa fikra ya kina, na utafiti wa kielimu na utafiti wenye kulenga juu ya mambo mbalimbali na mafuhumu ya Kiislamu. Umma wa Kiislamu leo unaingia katika vita vya kimaendeleo na kifikra kali ambapo mabeberu wa kiulimwengu wanaogopa umma kurejesha kuiamini kwake dini yake na kujenga jengo la maendeleo ya Kiislamu upya kwa kutengua maendeleo ya kimaada ambayo mwanadamu ameonja adhabu yake na imebainika kwake ufisadi wake na upotovu wake. Hakika kuna uadui wa kijeshi na vita vilivyolazimishwa ambavyo vilielekezwa kwa Jamhuri ya Kiislamu na mashambulizi ya kigaidi, na ukandamizaji mbaya ambao unawakabili waumini wanaharakati katika kila sehemu, na weledi wa matangazo ya upotoshaji dhidi ya mapinduzi na harakati ya Kiislamu. Haya yote ni muonekano wa mbinu za vita vya kimsingi na mapigano ya kikweli kweli baina ya maendeleo ya Kiislamu yanayotarajiwa, na utamaduni wa kimaada wenye kupotoka. Na ikiwa uongozi wa kimedani, na matakwa ya kila siku katika mambo ya harakati na mapigano pamoja na maadui yanachukua muda na juhudi za maulamaa na wanafikra wa Kiislamu wenye uelewa, hakika hayo yataacha pengo hatari katika nyanja za utafiti wa kielimu wa kiitikadi na utoaji wa kifikra. Ni lazima kundi la maulamaa na wanafikra wenye kujua lielekee katika nyanja za mapambano ya kimaendeleo, na wenye kuelewa katika uelewa wa umma, ili wafanye jukumu la kusaidia na 347


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

kuunga mkono kifikra na kielimu, nyuma ya medani ya mapigano ya kiaskari, kisiasa na kimatangazo. Na fikra nyinyi ni miongoni mwa wanaotumainiwa na kutegemewa katika kujaza pengo hili na kukidhi haja hii muhimu. Hakika kujali kwenu kwa kutoa utafiti huu mzuri wa kiitikadi na kifikra kunatengeneza nguzo na msaada wa dharura kwa kila wanaharakati na wanajihadi katika kuinua neno la Mwenyezi Mungu na kuokoa ulimwengu na uduni wa kuporomoka kimaada. Nimekwishasoma nyingi kati ya juzuu zenu za (Tafsirul alMaudhui lil-Qurâ€&#x;ani) na utafiti wenu mzuri kuhusu (Tawhidi wa shirki), nikakuta humo nilichokuwa nakitafuta katika fikra ya kina, na upevu makini na maelezo yaliyotulizana kimaudhui Mwenyezi Mungu abariki juhudi zenu na adumishe taufiqi yenu na awanufaishe Waislamu kwa uzuri wa kazi yenu. Nataraji kuwa mtaendeleza uandishi wenu katika nyanja ya tafsiri ya maudhui katika Qurâ€&#x;ani kama ambavyo naona dharura ya kuharakisha katika tarjama ya utafiti huu katika lugha hai za kiulimwengu, na hususani lugha ya Kiingereza, kwani kuna wengi kati ya Waislamu ambao hawafahamu lugha ya Kiarabu wanahitaji kwa shauku kubwa mfano wa utafiti huu wa kielimu, kama ambavyo baadhi ya wanafikra wa kimagharibi na mashariki ni muhimu sana kwao kusoma mafuhumu ya Kiislamu katika nyanja ambayo imezunguka mapinduzi matukufu ya Kiislamu mtazamo wao kuhusu Uislamu. Namuomba Mwenyezi Mungu awape afya na uchangamfu na watendaji wote waumini awape taufiqi na mafanikio. Na amani iwe juu yenu na baraka zake na rehema zake. Hasan Saffar Qatif. 348


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Utangulizi wa kitabu “Sharihu Shukuk”212 Sifa zote njema anastahiki Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa viumbe, sala na salamu zimwendee Nabii wetu, kizazi chake na maswahaba wake wema. Hakika kati ya wajibu wa kwanza wa Mwislamu anapofikia umri wa taklifu ni kujifunza dini yake na kujifunza mas‟ala ya kisharia ambayo anakumbana nayo katika maisha yake. Na wengi wa waumini wana raghba ya kutekeleza wajibu huu wa kujifunza dini yao lakini wanaweza wasipate njia na zana na mazingira yanayosaidia kutimiza raghba hii. Na hususani vitabu vya fiqihi na hususan Risalatul- Amaliya mara nyingi haiko wazi wala haielezei ufafanuzi na mas‟ala yote ambayo anayahitajia mukalafu kama ambavyo kila risalatu al-Amaliya inatoa rai ya fat‟wa ya Marjii ambaye anaitoa. Na hapa kulikuwa na haja sana ya utunzi wa kifiqihi ambao unakusanya sifa mbili: Kwanza: Uwazi wa ibara na kueleza ufafanuzi mbalimbali. Pili: Kukusanya rai na fat‟wa mbalimbali za Maraji‟i, bila shaka inaweza kuwa ikhitilafu kidogo katika fat‟wa baina ya maraji‟i lakini ipo na ni muhimu kwa mukalafu kusoma rai ya marji‟i wake. Na zama hizi unasifika utamaduni wake na maarifa yake kwa uwazi na upana wa kuenea, kwa kufaidika na vyombo vya matangazo na zana za ufafanuzi, yote hayo yanamsukuma muumini mwelewa kujaza upungufu huu katika nyanja za maarifa ya kifiqihi. 212

Sharihu Shukuki, ambacho kinaungwa mkono na rai za Maulaa: Sayyid Muhammad Shiraziy, Sayyid Abul-Qasim al-Khuiy, Sheikh Husein alUsufuri, Sayyid Sistaniy, Sayyid Muhammad Ruhaniy, chenye rai za Shafiqi Muhammad al-Mughasilah chapa ya kwanza 1416 Hijiria.

349


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Na ndugu mtukufu mwelewa Shafiqi Muhammad al-Mughasilah ni kati ya ambao wamezinduka katika upungufu huu, akajitolea hali ya kushukuriwa katika kutatua tatizo hili, na kwa hiyo alichagua maudhui ya kifiqihi ambayo kwa kawaida inakithiri kukumbana nayo, nayo ni maudhui ya shaka katika swala. Na ameitaabisha nafsi yake katika kurejea kwake risala amaliya za kifiqihi mbalimbali kuhusu maudhui, kisha akaandika utafiti kwa ibara nyepesi na zilizowazi, akijaribu kueleza ufafanuzi na pande zote katika maudhui akieleza rai mbalimbali za mafaqihi na maraji‟i. Kwa hakika sikupata fusra ya kurejea vyanzo vya kifiqihi ili kulinganisha yaliyokusanywa na kitabu miongoni mwa fat‟wa, lakini mimi nina imani kwamba mtunzi Mwenyezi Mungu amhifadhi, ametoa juhudi kubwa na kamilifu katika kuhakiki mas‟ala yaliyonukuliwa katika fat‟wa za Maraaji‟i watukufu. Mwenyezi Mungu amlipe kheri katika juhudi nzuri na Mwenyezi Mungu amtakabalie amali yake na aifanye ni sehemu ya manufaa kwa waumini. Na mheshimu na walio mfano wake miongoni mwa vijana waumini wenye uelewa, kila mmoja abebe jukumu lake na achangie kwa anachokiweza katika kusambaza maarifa ya Kiislamu na utamaduni wa dini. Mwenyezi Mungu ampe mtunzi taufiqi ya ziada ya amali za kheri na abariki juhudi zake na awakithirishe walio mfano wake. Na sifa zote njema anasitahiki Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu. Hasan Saffar 13 Jamadi-Thani 1415 Hijiria. 350


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Utangulizi wa kitabu “Mu’ujamu al-Mualafaati Shiati fiylJazirati al-Arabiyati.” 213 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu. Sifa zote njema anastahiki Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu. Elimu na maarifa ni sifa ya Mwenyezi Mungu ambayo amempa mwanadamu:

‫َ َى َ َ َ َ َ ُى‬ “…..‫ظماء ولُا‬ ‫”وغل ءادم‬ “Na akamfundisha Adamu majina ya vitu vyote…..” (Surat Al-Baqara; 2:31)

ٰ َ َ ‫ى‬ ‫َغل َ ِإلاقعك َن ما ل َيػل‬ “Amemfundisha mtu (Surat Al-„Alaq; 96:5).

aliyokuwa

hayajui.”

Na kwa elimu mwanadamu anashika nafasi yake ya ukhalifa wa Mwenyezi Mungu katika ardhi

ً َ َ

“….. ‫ليف ِت‬

َ َ ‫” َوإر‬ ٌ ِ ‫كاٌ َسب ًَ ِل َلملٰك ِن َى ِت إ ّقش‬ ِ ِ ِ ‫جاغل ِفى س‬

“Na Mola wako alipowaambia Malaika: Mimi nitaweka khalifa katika ardhi…..” (Surat AlBaqara; 2:30).

213

Muujamu al-Mualafaati shaiati fiy al-Jazirati, taalifu Habib Aal Jami‟i Darul-Malaak lilitwibaati wanashir wa tauzi‟i - Beirut chapa ya kwanza 1417 Hijiria.

351


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

َ

َ ٰ َ

“….. ِ ِ ‫لك ِنف س‬

‫ى‬ َُ ‫” َو ُه َى الزي َج َػلى‬

“Naye ndiye aliyewafanya makhalifa ardhi…..” (Surat An-An‟am; 6:165).

wa

Na ana jukumu la kutumia uwezo na vipaji kwa ajili ya kujenga maisha:

ُ

َ

َ

َُ َ َ

َ ‫… ُه َى أقشأه م َن س َواظخ‬..” “…..‫ػم َشه في ا‬ ِ ِ “…Yeye ndiye aliyewaumba kutokana na ardhi na akaifanya iwe koloni lenu…..” (Surat Hud; 11:61) Na elimu na maarifa ni haki ya kisharia ya binadamu wote, haisihi kwa aliyepata kitu kwayo akilimbikize kwa ajili ya nafsi yake na kukizuia kwa watu. Na kila unapozidi umuhimu wa ambayo yapo kwa mwanadamu katika elimu na maarifu na anazidi kuihitajia, na jukumu linazidi kuwa kubwa na wajibu wake katika kutoa hiyo elimu na kuisambaza. Na hapa imepokewa katika Qur‟ani tukufu aya nyingi zinazohadharisha wenye elimu na maarifa na kuficha maarifa na ubakhili katika elimu Yake, na kuwabebasha jukumu, kusambaza elimu na kutoa maarifa kwa watu. Anasema (swt):

ُ َ ‫َٰ ى‬ ّ ُ ‫ٰ َ ََُُّى‬ ُ‫َ َ َ َ ى‬ ‫اط َوال‬ ِ ‫”و ِإر أ ز اللكه ميثكم الزين أوجىا‬ ِ ‫الىخكب لخب ِي ه ِلل‬ َُ ُ َ “…..‫جىخمى ِه‬ “Na Mwenyezi Mungu alipochukua ahadi na wale waliopewa Kitabu: lazima mtabainisha kwa watu wala hamtakificha…..” (Surat AaliImran; 3:187). 352


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

ّٰ ُ َ َ ‫ى ى‬ َ َ ‫ىخمى َن ما َأ َضل ا م َن‬ ٰ ُ‫ال‬ ُ ‫الب ّي ٰك ِذ َو‬ ‫ػذ ما َب ىي ك ُه‬ ‫ِإن الزين ي‬ ِ ‫ذي ِمن‬ ِ ِ َ ّٰ ُ ُ ُ َ َ َ ُ ‫ٰ ُ ٰ َ َ َ ُ ُ ُ ى‬ ّ ‫ن‬ ِ ‫بِ أولك ِنً يلػن اللكه ويلػن اللك ِػ ى‬ ِ ِ ‫الىخك‬ ِ ‫اط ِفى‬ ِ ‫ِلل‬ “Hakika wale wanaoficha tuliyoyateremsha, katika ubainifu na uongofu, baada ya Sisi kuyabainisha kwa watu Kitabuni, hao anawaaliani Mwenyezi Mungu na wanawalaani wenaolaani.” (Surat Al-Baqara; 2:159).

ٰ ً َ َ َ َ ‫الىخك ِب َو َيشترون ِب ِه ز َم ا‬ ِ ‫ِمن‬ ‫ى ّ َ َ َُّ ُ ُ ُ ى‬ َ ‫الل ُكه َي‬ ‫ىم‬ ُ‫ِإال ال اس وال يي ِلم‬

َ ‫ى‬ َ ُ َ ‫ى ى‬ ‫زين َيىخمىن ما أ َض ٌَ الل ُكه‬ ‫ِإن ال‬ ُ ٰ ً َ َ ُ َ َ ُ ِ ‫ك‬ ِ ‫ليًلِ أولك ِنً ما يأولىن فى ب‬ ِ ‫طىن‬ َ ٌ َ َُ​َ َُّ َ َٰ ٌِ ‫زال ألي‬ ‫الليكم ِت وال يضهي ِ ولُ غ‬ ِ

“Hakika wale wafichao aliyoyateresha Mwenyezi Mungu katika Kitabu na wakanunua kwacho athamani ndogo, hao hawali matumboni mwao isipokuwa Moto: wala Mwenyezi Mungu hatawasemesha Siku ya Kiyama na hatawatakasa; na wao wana adhabu chungu.” (Surat Al–Baqara; 2:174). Imepokewa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu  kwamba amesema: "Mtu yeyote aliyepewa elimu na Mwenyezi Mungu akaificha naye anajua atakutana na Mwenyezi Mungu Mtukufu Siku ya Kiyama hali ya kuwa anapigwa na vijinga vya moto.” “Mwenye kuficha elimu analaaniwa na kila kitu hadi samaki baharini na ndege angani.” Na katika kusambaza elimu na kuitawanya kuna mbinu na njia mbalimbali, lakini za kutunga na kuandika ndio zinazoonekana zaidi na ndio muhimu zaidi. 353


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Kwanza: Kwa sababu kuandika na kutunga ndio mbinu yenye umakini zaidi na yenye kuhifadhi haki za elimu. Elimu inapoandikwa inakuwa kwa kawaida inajikita zaidi kiakili, anapohutubia, au anapozungumza na fursa yake katika ufanisi na uhakika zaidi kama ilivyo dhahiri. Pili: Kwa sababu anawahutubia kizazi kijacho pia, wakati ambapo njia zingine aghlabu zinahutubia kizazi kinachoishi wakati huu na mwanachuoni. Hapa zimekuja nususi na hadithi za kidini zinashajiisha katika kudhibiti elimu kwa maandishi na kuihifadhi kwa ajili ya kizazi kijacho kupitia utunzi. Kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu  kwamba amesema: “Dhibitini elimu kwa maandishi.” Na kutoka kwake  amewaambia masahaba wake: “Idhibitini elimu, wakasema: Na nini udhibiti wake: Akasema: Kuiandika kwake.” Na kutoka kwake : “Muumini anapokufa na akaacha karatasi moja juu yake kuna elimu, karatasi hiyo Siku ya Kiyama inakuwa kizuizi baina yake na moto.” Na mwanachuoni ambaye anatunga kitabu katika nyanja ya elimu yake anakuwa ni msadikishaji wa kuitikia wito huu wa kiutume na ni mfano katika nyanja ya kutoa elimu na kusambaza maarifa. Wakati ambapo mwanachuoni ambaye hashughulishi kalamu yake kwa kuandika wala haikalifishi nafsi yake kwa taabu ya utunzi pamoja na uwezo wake juu yake, anaweza kuwa ni usadikishaji wa hali ya kuficha elimu na kuifanyia ubakhili. Hakika wanachuoni ambao wanatunga na kuandika wanafadhila kubwa katika kurithisha elimu na maarifa na katika kuhifadhi uzoefu wa kifikra na chumo la kielimu, kama ambavyo wao kwa 354


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

hilo wamekwishadumisha shakhsiya zao na majina yao na wameakisi kwa ajili ya vizazi vijavyo picha ya ambayo yalikuwa yanajiri katika zama zao miongoni mwa mazingira na hali na fikra. Na kwa masikitiko makubwa sana, baadhi ya maulamaa na wenye maarifa ya kifikra na fasihi wanazembea na wanajizuia kutunga na kuandika. Wanawanyima watu kujua waliyosheheni katika vifua vyao miongoni mwa maarifa, na fikra zinabakia zimefungwa katika akili zao hadi waache maisha haya bila ya kuacha athari ya kielimu wanatajwa kwayo na kuwarithisha wanaokuja baada yao. Na harakati za utunzi na uandishi katika kila jamii ndio kioo kinachoakisi kiwango cha elimu na kifikra katika jamii, bali na inafichua juu ya kiwango cha kinafsi kwa maulamaa wa jamii hiyo na wanafikra wake. Kila zinapokuwa nafsi zao ni zenye kutoa, na azma yao ni ya juu, na hisia yao kwa majukumu ni kubwa shughuli zao katika nyanja za uandishi na utunzi zinakuwa ni zenye kusonga mbele. Kwa hakika mazingira ya siasa na kijamii yana athari kubwa katika harakati za uandishi na utunzi. Kila yanapokuwa yametulia na kuwa mazuri yanatoa fursa zaidi kwa ajili ya kustawi harakati za elimu na utunzi, wakati ambapo mazingira magumu yanakwamisha harakati ya elimu na yanadhoofisha harakati ya uandishi na utunzi. Lakini maulamaa mashujaa walikuwa wanakabiliana na ugumu wa mazingira na ugumu wa hali za kisiasa na kijamii, na wanaendelea katika kubeba majukumu yao na wanatoa kwa vizazi vya kibinadamu hazina ya fikra zao, matunda ya akili zao vyovyote itakavyowakalifisha hivyo katika thamani na muhanga, hakika matunda ya kalamu hizo shujaa ni usadikishaji wa kauli ya Mtume wa Mwenyezi Mungu : “Wino wa Maulamaa ni 355


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

bora kuliko damu ya mashahidi.” Na katika sehemu hii iliyosahaulika, isiyofahamika katika ulimwengu (sehemu ya mashariki katika kisiwa cha Kiarabu) ilikuwa na bado ingali harakati za kielimu kifasihi zimezalisha watu wengi wa elimu na maarifa na fasihi, na wengi wamechangia miongoni mwa hawa wajuzi kwa kalamu zao katika kuitajirisha maktaba elimu na fasihi, lakini sababu mbalimbali zimefanya kalamu hizi ziwe zimefichikana na zisijulikane. Na Mwenyezi Mungu amempa taufiqi ndugu mtukufu Sheikhe Habib Aal Jami‟i ili afanye jukumu lake la kukusanya na kuwatambulisha watunzi kati ya watu wa sehemu hii kupitia kuandaa mu‟ujam nzuri, humo ameeleza majina yote ya watunzi na ameandika wajuzi wa sehemu hii kupitia karne za historia kama ambavyo ameandika anwani za vita vyao na utunzi wao kwa utunzi mzuri uliopangiliwa. Na nilikuwa nangojea mfano wa kujitolea huku kutoka kwa ndugu mtukufu kwa niliyojua katika uzingativu katika hazina ya sehemu hii na ufuatiliaji uzalishaji wake na utoaji wake. Tangu miaka kumi takriban nilifuatilia mwenendo wa Sheikh Habib katika Muasasatu al-Baqi‟i Liihiyai Turathi nikakuta ana shauku ya kina na ikhlasi kubwa na azma ya juu na uchangamfu wa kudumu daima katika kutumikia hazina ya sehemu hii, kwa hiyo amebeba jukumu la idara ya taasisi kwa muda wote huu, Mwenyezi Mungu amlipe malipo mema. Na imetangulia kwa mtunzi mtukufu kwamba amekwishaandika utafiti mwingi uliozungumzia wajuzi wa sehemu na amesambaza baadhi yake katika baadhi ya majarida. Na ninapokaribishwa leo katika kutoka utunzi wake mzuri mu‟ujamu mualifiy al-Mantwiqati nataraji Mwenyezi Mungu 356


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

atampa taufiqi ya ziada ya kuzalisha na kutoa, na huo uwe ni msukumo kwa kila mwenye ghera katika watu wa sehemu katika historia yao na hazina yao ili kusaidia juhudi hizi za kheri katika kuhuisha hazina na kwenda sambamba pamoja nao. Mwenyezi awape taufiqi wote katika kheri na mafanikio. Na sifa zote njema anastahiki Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa ulimwengu. Hasan Saffar Qatif 20 Dhulhijja 1415 Hijiria. - 20/5/1995. Utangulizi wa kitabu “Taali ma‟iy linaqiraa” 214 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu. Sifa zote njema anastahiki Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu, sala na salamu zimwendee Nabii wetu Muhammad na kizazi chake kitwaharifu na maswahaba wake wema. Tunapoona sura miongoni mwa sura za Qur‟ani tukufu ina anwani ya kalamu nayo ni Suratu al-Qalamu; Sura ya 98 katika utaratibu wa sura za Qur‟ani, na tunaona kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu anaapa katika mwanzo wa sura kwa kalamu na kwa matokeo ya kalamu (Nun, na naapa kwa kalamu na wanayoyaandika): Na tunapokuta kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu anazungumzia juu ya neema ya kumfundisha kwake mwanadamu kuandika kwa kalamu na katika mwanzo wa aya ambazo alizishusha kwa Nabii Muhammad  baada ya kuzungumzia juu ya neema ya kumuumba mwanadamu moja 214

Taali ma‟iy kilichotungwa na Abdul-Qadir Abu al-Maarim, DarulMakaarim liihiyai turath 1516 Hijiria.

357


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

kwa moja ambapo anasema (swt): “Soma kwa jina la Mola wake ambaye ameumba. Amemuumba mwanadamu kutokana na pande la damu. Soma na Mola wako ni mkarimu sana. Ambaye amefundisha kwa kalamu. Amemfundisha mwanadamu asiyoyajua: Hakika hilo linamaanisha kuzindua macho ya watu wa umma huu katika umuhimu wa kalamu na nafasi yake katika kuhifadhi maarifa ya mwanadamu na kuenea kwake na hazina yake kupitia karne na vizazi. Kwa kalamu inahifadhiwa elimu, unaandikwa uzoefu na yananukuliwa maalumati, na inabainika mipaka na haki. Na ilikuwa inatakiwa kwa watu wa umma huu ambao Kitabu chake cha kiungu kitukufu kimeipa kalamu thamani na nafasi hii, iwe kwa kila mmoja miongoni mwao uhusiano imara wa kalamu, sio katika nyanja ya kujifunza kuandika tu, bali katika kutumia kalamu katika nyanja ya kuandika elimu na maarifa. Hakika watu wengi ambao wanaandika vizuri na wanabeba kalamu katika mifuko yao wanakaribia kutumia kalamu zao ila katika namna maalumu na madhumuni ya maisha yao ya kikazi au ya kimaisha. Ama kuandika yanayojiri katika nafsi zao miongoni mwa rai na fikra, na wanayoyapita miongoni mwa matukio na uzoefu, na yanayopatikana kwao miongoni mwa ukweli na maalumati, hayo ni machache sana. Wakati ambapo tunaona watu wa jamii zilizoendelea namna gani wanahamasisha juu ya kuandika kumbukumbu zao, ukumbusho wao na fikra zao na maalumati yao kwa namna ya kuvutia mshangao. Na huenda wengi miongoni mwetu wameshuhudia utalii wa wageni wanapotembelea makumbusho ya kihistoria au sehemu yenye athari, ni namna gani wanajali kuandika na kupiga picha zake mukabala na kupita kwetu sisi katika athari hizo na 358


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

kumbukumbu hizo, tunapita tu (bila ya kujali)!! Hakika kudharau dhati au kupuuza ambayo yanapatikana kwa mtu katika maalumati, au uzembe au ambayo yanafanana na sifa mbaya, ndio ambazo zinafanya wengi miongoni mwetu wanahama maisha haya bila ya kuacha athari au kumbukumbu ya kielimu au kifasihi wanayochangia kwayo katika kunukuu uzoefu na kuboresha katika jamii zao. Hapa inakuja kuheshimu na kutukuza juhudi za ndugu mtukufu al-Haji Abdul-Qadir mtoto wa al-Hujah al-Marhumu Sheikh Ali Abu al-Makaarim, Mwenyezi Mungu amhifadhi. Kwani ni mfano mzuri na kigezo chema kwa wabeba kalamu ambapo ametoa juhudi zake za juu ili kutoa anachoweza katika kuhudumia dini yake na jamii yake kwa njia ya kuandika na utunzi. Na kitabu ambacho kiko mbele yako ni moja ya usadikishaji wa juhudi yake nzuri ambapo amejitahidi humo kuandika kiasi kikubwa kinachowezekana katika maalumati kutoka kwa ndugu zake na watu wa familia yake tukufu ya kielimu. Na kama akipata taufiqi mmoja katika kila familia miongoni mwa familia kubwa zinazojulikana katika jamii yetu tungepata sisi na vizazi vijavyo matokeo muhimu kati ya maalumati na maelezo kuhusu watu wa jamii na matukio yake ya kihistoria. Familia ya Aal Abi al-Makaarim ni uso mwangavu kati ya nyuso za historia ya sehemu hii na jamii hii. Amezaa kundi katika maulamaa watukufu, na wanafasihi watukufu na makhatibu wema, Mwenyezi Mungu awarehemu waliotangulia miongoni mwao na awahifadhi waliobakia, na adumishe katika familia hii tukufu utoaji wa kijamii na dauru yake kubwa ya kielimu. Na Mwenyezi Mungu amlipe malipo mema (Abu Adinan) katika kuunga kwake udugu wake, kutumikia kwake maarifa kwa 359


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

kutunga kitabu hiki kizuri, na Mwenyezi Mungu amzidishie taufiqi na unyoofu. Na sifa zote njema anastahiki Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu. Hasan Saffar Qatif 12 Safar 1416 Hijiria. - 11/6/1995.

RISALA KWA MISAFARA YA MAOMBOLEZO 215 Sifa zote njema anasitahiki Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa viumbe; sala na salamu zimwendee Nabii wetu Muhammad  na kizazi chake kitwaharifu na masahaba wake wema. Amani iwe juu yako ewe bwana wa Mashahidi, Imamu wa wanamapinduzi, na kigezo cha waliohuru, ewe mjukuu wa Mtume wa Mwenyezi Mungu na manukato yake, na bwana wa vijana wa watu wa peponi, ewe Abu Abdillah al-Husein. Amani iwe kwa wafuasi wako waliokufa shahidi mbele yako, na rehema za Mwenyezi Mungu na baraka Zake. Amani iwe juu ya vijana wa Huseini katika misafara ya maombolezo: Amani iwe juu ya nyuso tukufu kwa nuru ya Abi Abdillahi Amani iwe kwa vifua vilivyojaa mapenzi ya Abi Abdillahi Amani iwe juu ya viganja vyenye kupiga maatam katika msiba wa Abi Abdillahi. Pongezi zenu enyi vijana waumini. Mazingatio yenu ni kuhuisha kumbukumbu ya shahada ya Imamu al-Husein na kukumbuka mateso ya damu kupitia misafara ya maombolezo. Hakika nyinyi mnakesha usiku na mnabeba taabu na machungu na mnatoa juhudi na mnakabiliana na magumu kwa ajili ya kusimamisha 215

Neno lililotolewa la misafara ya maombolezo katika kumbukumbu ya Ashura tarehe 9/1/1417 Hijiria.

360


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

nembo za Huseiniya. Ninawaombea Mwenyezi Mungu awalipe malipo mema, na muwe kati ya wenye kupita katika njia ya Husein na wenye kushikamana na malengo yake matukufu ambayo ndio mafunzo ya Uislamu na hukumu zake. Hakika harakati ya Husein ni wajibu, ili udumu utajo wake muda wote wa zama ili iwe ni chemchem tamu na madrasa ya kiimani inayolea vizazi katika kushikamana na dini na kujitolea kwa ajili yake na kupambana na dhulma na ufisadi. Nyinyi mmechagua njia ya maombolezo katika kushiriki kwenu katika kuhuisha kumbukumbu hii na kuidumisha kwake. Na maombolezo ni aina kati ya aina za kudhihirisha ufuasi wa AhlulBayt , na sehemu katika nembo za Huseiniya ambazo wanazifanya waumini tangu zamani na katika sehemu na nchi mbalimbali. Na niruhusuni enye ndugu watukufu nilete kwenu; na nyinyi mko katika kilele cha harakati zenu na hamasa yenu ya Huseiniy, baadhi ya hisia na angalizo kwa ajili ya kuzalisha juhudi hizi kubwa ambazo mnazitoa katika kumpenda Abu Abdillahi  Nataraji kupata kwenu sikio lenye kusikia na moyo wenye kuelewa kwa baraka za siku hizi tukufu na maadhimisho matukufu ya Huseini. Kwanza: Hakika mapambano ya Husein na kufa shahidi kwa ajili yake, kama alivyosema mshairi katika ulimi wake: “Ikiwa dini ya Muhammad haiwezi kusimama, ila kwa kuuliwa kwangu; basi enyi mapanga njooni mnichukue.” Kusimamisha dini ni lengo la msingi la harakati ya Imamu Husein, na matarajio ya wenye kumuomboleza Huseini ni ili wawe ni wenye kujali kusimamisha dini na kushikamana nayo 361


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

katika nyanja mbalimbali za maisha yao. Hakika sisi tunafurahi kwa kuona mkusanyiko huu mkubwa miongoni mwa vijana wenye mapenzi katika msafara wa maombolezo na tunatamani kuwaona daima katika misikiti na katika mahudhurio ya swala ya jamaaa na Ijumaa, na mdumu katika kuhudhuria majilisi za maulamaa na kushiriki katika ratiba zingine za kidini na kijamii. Na inapendeza kama wakipatikana watu katika kila kamati ili kuwasiliana daima pamoja na wenye kuomboleza ili kuwashajiisha juu ya swala ya jamaa baina ya muda na muda mwingie, hakika ukumbusho unawafaa waumini. Pili: Vijana wenye kumfuata Imamu Huseini ni wajibu wawe ni kigezo katika mwenendo wake, tabia yake na akhlaqi yake, wawe ni wenye kudumu katika utafiti wao, wenye kufaulu katika kuvuka hatua zake. Hakika kushuka kiwango cha masomo, na kutohudhuria mara kwa mara mashuleni, na udhaifu wa kujali kujisomea na kurejea masomo ni hali mbaya isiyoridhisha dini wala haikubali Imamu al-Huseini, na inatishia mustakabali wa vijana kupotea. Na ambayo tunayatarajia kwa vijana ni kuwa kigezo katika nyanja hii na kuwashajiisha wengine juu ya hayo ili wawathibitishie watu kwamba ufuasi wao kwa Imamu Huseini na kuhuisha kwao kumbukumbu ya Imamu Husein katika maisha yao kwa ajili ya kumbukumbu yake unaakisi katika maisha yao kwa uzuri. Na maombolezo yanaleta hali nzuri na wanakuwa ni usadikishaji wa kauli ya Imamu Swadiq : “Kuweni ni pambo kwetu na wala msiwe ni fedheha kwetu.” Tatu: Hatari kubwa zaidi iliyovamia jamii zetu ni jaribio la kupenya muonekano wa ufisaddi na upotovu wa kiakhlaqi. Hakika vipindi vya wageni vinavyosambazwa, ambavyo vinanukuliwa na baadhi ya vituo vya runinga, au vinanaswa kupitia vyombo vya satelite, na uwepo wa hali ya pengo na udhaifu wa 362


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

kiwango cha uelewa wa kidini na uangalizi wa kifamilia, yote hayo yanasaidia jaribio la kusambaratisha jamii na kuiharibu kwake. Na unapoenea ufisadi na upotovu ni hatari kubwa kwa heshima yetu, misingi yetu, mustakabali wetu na amani ya jamii yetu. Vijana mikononi mwao wana jawabu kali juu ya hali hii ambapo wanaweza kushikamana na dini na uelewa wao wa kiinchi na shughuli za kijamii ili kuhami nafsi zao na jamii yao kutokana na maangamizi. Kama watakokotwa baadhi ya vijana – Mwenyezi Mungu apishilie mbali – na kundi hili, hakika wao watarudia kumuuwa tena Imamu Husein na kulenga mishale yao upya kwenye moyo wake mtwaharifu. Hakika Imamu al-Husein anawaamsha na bibi Zainabu anawapigia kelele ili kuhifadhi heshima zenu na kushikamana na manhaji tukufu na uchamungu. Je, kuna mwenye kuitika? Na iwe misafara ya maombolezo ni sawa na kujadidisha ahadi pamoja na Imamu al-Husein katika kushikamana na dini na kuhami utukufu na tabia njema. Nne: Tunataraji kwamba sauti zenu katika maombolezo ni kituo katika kuhuisha utajo wa Husein na kujadidisha maadili matukufu ambayo alijitoa muhanga kwa ajili yake, na katika kulingania umoja na uelewano na kushikamana na njia ya AhlulBayt . Na misafara iwe katika kiwango kinachotakiwa katika mpangilio na utaratibu na unyoofu wa safu katika utulivu na amani kama ilivyozoeleka kwenu ili mtoe kwa hilo picha tukufu angavu kuhusu jamii yenu na misingi yenu. Mwenyezi Mungu awalipe kheri na akubali amali zenu na awalipe katika juhudi zenu nzuri, na wala Mwenyezi Mungu 363


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

asijaalie iwe ni mwisho kwetu na kwenu kwa ajili ya kuhuisha utajo wa Abi Abdillah al-Husein ď „. Wasalaamu alaykum warahamatullahi wabarakaatuhu. Kuwatangaza Mawalii wa Mwenyezi Mungu 216 Haikuepukana zama kati ya zama, wala wakati kati ya nyakati na mazingatio ya kuwatangaza watu au fikra au mambo na matukio, lakini mbinu za matangazo na vipindi vyake vinatofautiana zama na zama nyingine, na jamii na jamii nyingine. Na matangazo katika zama hizi yanachukua daraja ya juu na viwango vya juu vya mazingatio. Zimeboreka mbinu zake na vipindi vyake, na imekuwa ni elimu inayofundishwa katika vyuo vikuu, na vyuo maalumu, na imegeuka kuwa ni kiwanda kinachotegemewa katika ujuzi, kipaji na uzoefu na inayo taasisi na vyuo vyake na zana zake za kisasa. Matangazo leo yanategemea mikakati na ratiba, na wananufaika na uzoefu na utafiti wa elimu ya nafsi na jamii, na kuratibu maalumati. Na maendeleo ya teknolojia na elimu yana nafasi kubwa katika kuimarisha nguzo za himaya ya matangazo katika kiwango cha kiulimwengu, hususani baada ya kutumia satellite na vituo vya kurushia matangazo ya moja kwa moja. Hakika matangazo leo ni sehemu ya msingi na kitu kinachoathiri katika nyanja mbalimbali za maisha ya mwanadamu, katika ulimwengu wa kisiasa, kiuchumi, kifikra na katika nyanja zote. Kwa hiyo hakika serikali yoyote au chama au shirika au kiwanda au shirika la kimaada au maanawiya ni lazima kutoa sehemu kubwa ya mazingatio yake na rasilimali yake na juhudi yake katika upande wa matangazo. Na ushindani huu ambao tunauona sasa wa 216

Ufunguzi wa jarida la al-Murshid, Dauri ya muswawaratu linalojihusisha na utamaduni na hazina na athari, toleo la 6 mwaka wa nne 1417 Hijiria – 1997 na mmiliki wake na mhariri wake mkuu ni Sheikh Husein Muhammad Ali al-Fadhiliy.

364


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

kuchukua nafasi katika tovuti kutoka katika pande za kisiasa na kidini, kifikra, kifani na kibiashara si kingine isipokuwa ni muonekano dhahiri wa kujua sote umuhimu wa matangazo na kuzingatia kunufaika nayo. Na hivi sasa hatuko katika kuzungumzia juu ya umuhimu wa matangazo na upeo wa kuathiri kwake, kwani ni jambo lililo wazi na linafahamika, kwanza kama ambavyo kuna rundo la vitabu, masomo na utafiti maalumu ambavyo vinafundisha nyanja zake mbalimbali. Pili, lakini tunachotaka kukizungumzia katika kurasa hizi chache ni kuamiliana na mazingira yetu ya kidini pamoja na masâ€&#x;ala ya matangazo. Je, tunahitaji propaganda na matangazo? Fikra iliyoenea katika mazingira mengi ya kidini ni kwamba mambo ya kidini hayana haja ya propaganda na matangazo na kutangaza, ambapo ni wajibu watu wakubali mambo ya kidini kwa kukinai na msukumo wa dhati, kama ambavyo dini inatia mkazo thamani ya ikhlasi kwa Mwenyezi Mungu na kujinyima katika cheo, kujitokeza na kudhihiri, na kuhadharisha kutokana na ria na kutaka kujulikana. Na mwanadamu muumini ni wajibu awe mnyenyekevu mwenye kuituhumu nafsi yake kwa upungu na kasoro, na wala haitakasi nafsi yake wala hajigambi kwa amali zake na wala hawi na kiburi. Wala hataki sifa na umashuhuri. Na yote hayo yanamsukuma mwanadamu muumini kuwa mbali na mwanga wa kukimbia matangazo. Na matokeo ya fikra hii iliyoenea hakika wengi kati ya watu wa dini na elimu wanaishi kwa kujificha na wala hawajui ulimwengu, bali hawajui umma wa Kiislamu na jamhuri yenye kuamini kitu chochote kuhusu maisha yao na nafasi yao ya kielimu na mafanikio yao ya kifikra na kivitendo. Na inatokea mara nyingi kwamba watu wanashtukizwa na mazungumzo kuhusu fadhila ya mwanachuoni na nafasi yake 365


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

ndani ya ratiba ya maombolezo yake (yaani baada ya kufariki kwake). Ama katika hali ya maisha yake hakuna yeyote anayejua chochote juu yake isipokuwa wachache waliokaribu naye. Hakika katika hawza zetu za elimu na katika mazingira ya kidini kuna wanachuoni wakubwa katika elimu na maarifa, na vipaji vikubwa katika fikra ya utamaduni, na mfano mzuri katika kushikamana na maadili, misingi, huduma na utoaji, lakini wamefichikana hawajulikani, jambo ambalo linaunyima umma na ulimwengu faida zake nyingi na manufaa yake. Na kuna juhudi kubwa tukufu katika nyanja mbalimbali za elimu na maarifa na ustaarabu lakini zinaishi katika giza nene na kificho. Hakika matangazo na propaganada katika shakhsiyati za kielimu na kidini na taasisi na shughuli ambazo anazifanya muumini ni jambo la dharura na muhimu na hiyo ni kwa visingizio vifuatavyo: Kwanza: Hakika shakhsiya za kielimu na harakati za kidini zinatekeleza maadili ya kheri na mema, na kuyatangaza na kudhihirisha inamaanisha kueneza na kuzatiti maadili ambayo unayawakilisha. Unapomsifu mwanachuoni na kumpamba, wewe kwa hakika unaipamba thamani ya elimu na kuiimarisha. Pili: Matangazo na kudhihirisha pande za kidini inamaanisha kutoa fursa ya watu wa umma ili kuzijua na kujongea karibu yake, na unanufaika nayo. Tabibu anayeishi sehemu iliyofichikana mbali na macho na bila ya kibao au ishara inayoelekeza kwake, wagonjwa hawatamwendea kwa sababu wao hawamjui pamoja na kumhitajia kwao. Tatu: Hakika matangazo ni silaha yenye nguvu katika mapambano ya maisha baina ya dini na misingi na maelekezo ya umma na jamii. Sisi kama watu wa dini na msingi haisihi kwetu kuacha medani yetu chini ya athari ya matangazo kwa watu, fikra na pande zingine. Bali ni lazima tuchomoe silaha ya matangazo ili kunyanyua maanawiyati ya watu wetu na kuwaelekeza katika 366


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

mbadala wa Uislamu ulioboara zaidi, na kwa kuimarisha kujiamini katika nafsi zao kwa dini yao na uongozi wao na shakhsiya zao na mashujaa wao. Bali hakika matangazo sahihi na yenye kuendelea yanatuwezesha kuathiri jamii na umma zingine, na kuwaelekeza kwenye maadili ya Kiislamu, misingi yake na utukufu wake. Nne: Katika upande wa kidini, hakika Uislamu unatulea katika kulingania na kutangaza Mawalii wa Mwenyezi Mungu na kuwadhihirisha na kuwaheshimu. Hakika Mwenyezi Mungu anamwamrisha Nabii Wake Muhammad  kudumisha utajo wa Manabii na Mawalii, kuzungumzia juu ya sifa zao tukufu. Anasema (swt):

ٰ ُ َ َ ً ‫ى‬ َ ‫الىخك ِب ِإ ٰبشهي َِ​ِ ِإ ُه وان ِص ّذيلا ِب ًّيا‬ ِ ‫وارهش ِفى‬ “Na mtaje Ibrahimu katika Kitabu, hakika alikuwa mkweli sana na Nabii.” (Surat Maryam 19:41).

ٰ َ ُ َ ُ‫ٰ ى‬ ُ َ َ ً َ ً ‫خل‬ ‫صا َووان َسظىال ِب ًّيا‬ ‫الىخك ِب مىس ِى ِإ ه وان م‬ ِ ‫وارهش ِفى‬ “Na mtaje Musa katika Kitabu, hakika yeye alikuwa na mwenye kutakaswa na alikuwa Mtume na Nabii.” (Surat Maryam; 19:51).

ٰ ُ َ َ ً َ َ ُ‫ٰ َ ى‬ َ َ ‫غذ َووان َسظىال ِب ًّيا‬ ِ ‫الىخك ِب ِإظمك‬ ِ ‫ػيلِ ِإ ه وان‬ ِ ‫صادق الى‬ ِ ‫وارهش ِفى‬ “Na mtaje katika Kitabu, Ismail. Hakika yeye alikuwa mkweli wa ahadi na alikuwa Mtume na Nabii.” (Surat Maryam; 19:54).

ٰ ُ َ َ ً ‫َ ى‬ َ ‫وان ِص ّذيلا ِب ًّيا‬ ِ ‫دسيغ ِإ ُه‬ ِ ‫الىخك ِب ِإ‬ ِ ‫وارهش ِفى‬ 367


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

“Na mtaje katika Kitabu, Idris. Hakika yeye alikuwa mkweli na alikuwa Nabii.” (Surat Maryam; 19:56). Na katika Qur‟ani tukufu kuna uwanja mpana wa visa vya Manabii na Mawalii kwa kuwasifia na kuwatanguliza kama kigezo na kuchukua mafunzo na mazingatio katika sira zao. Na Mtukufu Mtume  alikuwa anawasifu masahaba wake wema na anasifia fadhila zao na nafasi zao, kama vile kuwasifu kwake kwa wingi Ahlul-Bayt wake waongofu Ali, Fatimah, Hasan na Husein , na kuwasifu kwake masahaba wema kama vile Abu Dharr, Salman, Ammar bin Yaasir na mfano wao. Na vivyo hivyo walikuwa Maimamu maasumina wanawasifu wafuasi wao watukufu na wanatia umuhimu katika thamani yao na nafasi zao katika jamii. Bali hakika Nabii na Ahlul-Bayt wake  walikuwa wanashajiisha katika kusifu nafsi zao na kutukuza sifa zao tukufu na misimamo yao mizuri na mateso yao kutoka kwa madhalimu. Anasema Imamu Ja‟far Swadiq : “Hajasema kwetu msemaji ubeti wa shairi hadi anaungwa mkono na roho mtukufu”217 Na kutoka kwa Abu Twalib al-Qummiy amesema: “Nilimwandikia Abu Ja‟far  beti za shairi na nikamtaja humo baba yake, na nikamuomba aniruhusu niseme juu yake. Akakata shairi na akaliweka na akaandika katika sehemu iliyobakia ya karatasi: Umefanya vizuri, Mwenyezi Mungu akulipe kheri.”218 Na historia inanukuu kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu  kwa kuheshimu kwake washairi ambao walikuwa wanamsifia na wanataja sifa zake zote, kama vile kufurahika kwake kwa shairi la ami yake Abbas bin Abdul-Mutwalib aliposema: “Ewe 217 218

Al-Ghadir, Juz. 2, uk. 3 Al-Ghadir, Juz. 2, uk. 3

368


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Mtume wa Mwenyezi Mungu nataka nikusifie? Akasema : Sema, Mwenyezi Mungu asikifunge kinywa chako. Akasoma kaswida yake mwanzo wake ni: “Min qablihaa twibta wafiy dhilaali wafiy, mustauda‟i haithu yakhiswifu al- waraq”219 Na kama vile kufurahia kwake  shairi la Kaabi bin Zuhair alipomsomea katika msikiti wake mtukfu shairi lake la laam mwanzo wake ni: “Baanati su‟ad faqalbiy al-yaumi mutabal.” Nabii  akamvika shuka alilokuwa amelinunua Muawiya baada ya hapo kwa dirihamu elfu ishirini na makhalifa walikuwa wanalivaa katika iddi mbili. Na Kaabu aliposoma kaswida yake na akafikia kauli yake: “Inna Rasulallahi lanuur yastadhiu bihi, wa swaarimmin suyufi llahi masulul.” Akaashiria watu wakusanyike ili wasikilize kutoka kwake. Na alikuwa  anamuwekea Hasan mimbari katika msikiti wake mtukufu anasimama juu yake anajifakharisha kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu  na amesema : Hakika Mwenyezi Mungu anamuunga mkono Haasan kwa malaika Wake kwa aliyosifu au aliyojifakharisha kwa Mtume wake.” Na Kumaiti aliingia kwa Imamu Ja‟far  siku za mbalamwezi huko Mina akasema: Niwe fidia kwako je, nikusomee: Imamu  akasema: Hakika ni masiku matukufu. Kumaiti akasema: Hakika ni kwenu. Imamu aliposikia maneno yake akawaita jamaa zake wakawa219

Al-Ghadir, Juz. 2, uk. 4

369


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

sogeza kwake akasema: Haya soma shairi lako la laam kwa Hashimiyaati. Akapata bahati ya dua yake  na akaamuru apewe dinari elfu moja na akamvika nguo. 220 Mtume wa Mwenyezi Mungu na Ahlul-Bayt wake  hawahitajii sifa za wenye kusifia na sifa za washairi lakini wao walikuwa wanajua athari ya hayo katika jamii yao na nafasi yake katika vita vyao dhidi ya makafiri na mafisadi. Ni ukubwa ulioje wa daraja la ikhlasi na kujinyima kwa Mtukufu Mtume  na Ahlul-Bayt wake lakini wao walikuwa wanaridhia kusifiwa na kupongezwa na wanawashajiisha kwa yaliyomo humo katika kuhudumia hadhi yao ya kiungu na kwa malengo yao matukufu. Na pengine baadhi watauliza: Namna gani tunaoanisha ukweli huu, nayo ni dharura ya kutumia matangazo katika huduma ya kidini kupitia matangazo ya watu wa dini na taasisi za kidini na shughuli za Kiislamu na baina ya mafunzo ya kidini ambayo inatuhadharisha kutafuta umashuhuri na kujichafua kwa ria? Jawabu: Hakika hayo yanatokana na mazingira ya msukumo. Ikiwa matangazo ni kwa ajili ya umashuhuri na maslahi binafsi na ikiwa lengo la amali ya kidini ni kujidhihirisha nayo, hapa inakatazwa, nayo ni ambayo yanakatazwa na mafunzo ya kidini. Ama ikiwa amali ni kwa ajili ya radhi za Mwenyezi Mungu na yakatumika matangazo kwa ajili ya kuhudumia mwelekeo wa kidini, na makusudio ni kuimarisha dini kwa kudhihirishia watu wake na kuwashajiisha katika kheri kwa kutoa mfano, basi ni katika ambayo Uislamu unayapendelea na kuraghibisha humo. Na inaweza kusemwa: Namna gani tunaweza kuhukumu juu ya usahihi wa kitendo hiki kisharia au kinyume chake maadamu mas‟ala yanafungamana na msukumo na nia, na wala haijui isipokuwa Mwenyezi Mungu? Hakika kitendo cha kutangaza ni kama kazi zingine ambazo mwanadamu muumini anaziunga 220

Al-Ghadir, Juz. 2, uk. 20

370


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

mkono miongoni mwa swala, saumu, hija, kutoa na jihadi, na yote kunaingia dhana ya ikhlasi au ria. Na hatumaanishi kutafuta nia bali asili ya hukumu ni usahihi ili ibainike kinyume. Na ni juu yetu kukaribisha kitendo chochote cha matangazo kwa maslahi ya upande wa kidini, bila ya kutafiti au kujadili katika nia za wenye kufanya kitendo hicho cha matangazo kama tunavyoona katika swala ya Mwislamu yeyote au hija yake au kutoa kwake, je tunataka ushahidi wa kuthibitisha juu ya usahihi wa nia yake? Tangazo la kidini na msuguano wa ndani: Ni kawaida kuwepo kwa pande nyingi na mielekeo mingi katika medani ya kidini. Na kuna marajiâ€&#x;i wengi, na wengi kati ya maulamaa na mafaqihi, makhatibu na taasisi na shughuli za kidini. Inapasa wingi na idadi iwe ni chimbuko la furaha na kufurahika mwanadamu muumini, kwa sababu hayo yanatia nguvu upande wake mbele ya pande za upinzani, na yanaleta ushindani mzuri na kushindana katika kheri. Na ni haki ya kila upande, bali inakuwa ni wajibu kila upande uwe na mazingatio ya matangazo na kwenda mbio kudhihirisha alama zake na shakhsiya zake na kutangaza shughuli zake na kazi zake. Pamoja na kwamba inasikitisha sana kuangalia upande wa ubaya na upungufu wa matangazo ya upande mwingine, kana kwamba propaganda na matangazo ya upande mwingine yanatimia kwa hesabu yake. Au kwamba kumsifu marijii huyu na kudhihirisha kutangaza shakhsiya yake kunadhamini kumdharau marijii mwingine! Hakika ni mtazamo mbaya na finyu, kuthibitisha kitu hakupingi kisichokuwa hicho. Na unapoona juhudi za matangazo kwa maslahi ya mwanachuoni au taasisi sio juu yako kujua kwamba hayo yanalenga katika maslahi ya hali ya kidini na mwelekeo wa kidini kwa ujumla. Na hakuna ubaya kujitolea kudhihirisha mwanachuoni mwingine, na kutangaza shakhsiya yake, kwani medani iko wazi kwa wote, na watu wote wa umma wawajue Marajii, na ili ulimwengu usome tuliyonayo kati ya 371


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

vielelezo vya elimu na kifikra. Matangazo ya ratiba na misimamo: Hakuna shaka kwamba kudhihirisha shakhsiya za umma na kuelezea vipaji vya wanajamii wake ni jambo lenye faida kwa kunyanyua manawiya, na kutia mkazo kujiamini na kutekeleza kitu katika haki ya wajuzi wa watukufu. Na kinachounufaisha umma zaidi ni kutoa masomo na mazingatio kupitia sira na uzoefu wa wajuzi wa umma na shakhsiya zao. Na chenye umuhimu zaidi ni kubainisha ratiba na misimamo ya kila kiongozi wa kidini, na kiongozi wa kijamii katika umma. Umma unakabiliana na changamoto za maisha na unaleta mbele ya wanajamii wake maswali muhimu katika nyanja mbalimbali za maisha. Na ni muhimu sana kujua ratiba ya marajii wetu na viongozi wetu ili kuutoa umma kutoka katika matatizo haya na kukabiliana na changamoto kubwa, kujua rai zao na misimamo yao na majibu yao kuhusu maswali yao yaliyoulizwa. Salaamu kwa jarida la al-Murshid Nimemheshimu ndugu mtukufu Sheikh Husein al-Fadhiliy kwa juhudi yake ya hali ya juu na matarajio yake ya kiuongozi aliponiambia juu ya azma yake ya kutoa jarida la utamaduni la msimu na nikamshajiisha juu ya hilo. Lakini mimi nilimhurumia kutokana na jukumu la kazi hii ngumu kwa ninayoyajua miongoni mwa mazingira ya medani ya kidini ambayo aghlabu yanahitaji kushajiishwa na kuungwa mkono kwa kujitolea kuzuri na kupokea mkakati kwa kuuliza na kutia shaka, na kuwiwa na ugumu katika mimbari huru ambazo zinapokea mitazamo mbalimbali, na kuheshimu rai na rai nyingine. Na ninakumbuka mimi nilimsisitiza kiongozi wa uhariri dharura ya kutoka katika kibanda cha makundi na kuwa chini ya rejea 372


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

moja au mwelekeo mmoja au kundi moja, na jarida liwe ni mimbari ya medani ya Kiislamu pamoja na kutofautiana madrasa zake na rejea zake na vielelezo vyake na shakhsiya zake. Na ilinifurahisha, na mimi nafuatilia mwenendo wa jarida hili zuri – al-Murshid – kufunguka kwake kwa watu wote na nataraji jarida kuendelea na siasa hii nzuri ili liwe ni uwanja wa kujuana na msukumo wa kuleta ukuruba na mimbari katika mazingira ya kidini kiukamilifu. Naandika mistari hii na mimi nasoma sehemu mpya za toleo hili kutoka katika jarida (al-Murshid) ambalo linadhamini faili la mmoja wa marijii wakubwa naye ni Ayatullahi al-Udhmaa alMirzaa Ali al-Gharuwiy (Allah amhifadhi), ambaye leo anazingatiwa kuwa ni nguzo ya msingi katika Hawza ya elimu ya Najaf tukufu. Na wengi wanaweza kushitushwa na maalumati yaliyokuja katika jarida katika faili hili la maisha yake yaliyojaa kwa elimu, maarifa na akhlaqi tukufu, na uchangamfu wenye kuendelea katika kutumikia hawza ya kielimu, na kulea watu wake. Na hiyo inareja kwa ambayo yametangulia kutajwa kati ya sababu na visababishi vinavyowazuia waumini kudhihirisha shakhsiya zao na kuelekeza ushujaa wao. Mwenyezi Mungu auhifadhi umma kwa kielelezo hiki, Faqihi na Marijii na amzidishie taufiqi katika kutumikia dini na elimu. Na Mwenyezi Mungu awalipe waliojitolea kuandaa faili hili malipo mema, hali ya kulitakia jarida, maendeleo na mafanikio. Maonyesho ya utamaduni hivi sasa katika Mamlaka 221 Katika kiwango cha kutoa na uzalishaji wa utamaduni kuna angalizo katika mamlaka. Inastahiki kushukuriwa na kuheshimiwa ambapo tumekuwa na taasisi za kiutamdani nyingi na 221

Kushiriki katika faili lililoandaliwa na Jarida la al-Kalmatu, jarida la msimu linalotolewa Muntadaa al-Kalmati lilidirasaati wal abhaathi toleo la 17 mwaka wa nne, kipupwe 1997.

373


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

vitabu vya fasihi katika sehemu mbalimbali na nyanja za kifikra elekezi za kielimu. Lakini kiwango cha kujishughulisha mwananchi pamoja na harakati za utamaduni pamoja na mazingatio ya kifikra ya kimaarifa inahitaji utafiti na kutafakari. Tukiachilia kundi la wasomi na wenye kujali suala la fikra na fasihi, hakika wananchi wa kawaida hawatengi katika muda wao na juhudi zao na uwezo wao katika upande wa utamaduni ila kiasi kidogo sana na kifinyu. Na katika kiasi hiki kidogo cha wakati na juhudi ambayo anaitoa mwananchi hakika kuzungumzia kijuu juu na pembezoni, ndio hali ya walio wengi. Na inadhihirika kwamba mwanadamu katika zama hizi anazungukwa na mazingatio na vibano mbalimbali katika mambo ya maisha na kutayarisha mahitaji yake na katika vishawishi na raghba ambazo zinaungwa mkono na ratiba nyingi na zilizoendelea katika propaganda na matangazo. Lakini upande wa utamaduni hauna bahati ya chochote kinachofaa katika kutangaza, msukumo, na uhamasishaji mukabala wake. Hakika sisi tuna haja ya kutegemea njia za kimalezi na ratiba za maelekezo ili kulea watoto wetu juu ya kuzingatia utamaduni na maarifa, kama ambavyo tunahitaji ratiba ya kuangalia hali ya utamaduni katika jamii na kufuatilia viwango vyake na kutatua sababu za kuchelewa kwake na kuongeza mazingatio ya mwananchi kwayo. Kusifika na utamaduni na maarifa katika jamii ni jambo la kawaida. Mwenyezi Mungu amekwishampa kila mwanadamu akili anafikiri kwayo na anajua mambo. Na amejaalia akili ya mwanadamu na moyo wake ni sehemu huru hakuna njia kwa yeyote kuivamia kwa ubabe na nguvu, ambapo unaweza kulazimisha wengine kufanya jambo fulani, au kuwalazimisha juu ya kufanya kitendo fulani, lakini wewe huwezi kuwala374


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

zimisha wao kuamini fikra wasiyokinahika nayo hata kama watajidhihirisha kwa hilo mbele yako. Kama ambavyo viwango vya ufahamu wa watu vinavyotofautiana, na mazingira ya malezi na kijamii ambayo wanaishi nayo yanatofautiana na kwa hiyo imeathiri katika utamaduni wao na maarifa yao. Na kwa hiyo Qur‟ani tukufu inakubali kutofautiana kiwango cha maarifa baina ya watu, anasema (swt):

َ

ُ َ َ

ٰ َ َ َ

“ٌِ ‫… شف ُؼ د َسجك ٍذ َمن َوفىق و ِ ّل ري ِغل ٍ غلي‬..”

“…..Tunawatukuza kwenye vyeo tuwatakao. Na juu ya kila mwenye elimu yuko ajuaye zaidi.” (Surat Yusuf; 12:76). Bali hata katika kiwango cha Manabii  hakika Qur‟ani inaashiria kwenye tofauti katika kuzungumzia kadhia na hukumu humo, baina ya manabii wawili, nao ni Nabii Daud  na Nabii Suleiman :

ٰ َ ُ َ َ​َ َ َُ​َ َ ‫ىم‬ ‫” َوداو َۥد َو ُظليمك َن ِإر َيدى‬ ِ ‫مان ِفى احخ‬ ِ ‫شر ِإر فشذ‬ ِ ِ ‫فيه غ الل‬ ٰ ًّ ُ َ ٰ َ ُ ٰ ‫َ َ ى‬ َ ُ َُّ ً ‫ءاجي ا ُخ‬ ‫ىما‬ ‫نِ َوهًل‬ ِ ‫﴾ ففُم كُا ظليمك‬٧٨﴿ ‫ذين‬ ِ َ ُِ ‫ىم ُِ شك‬ ِ ‫وه ا ِحخ‬ ً ‫َو ِغ‬ “….. ‫لما‬ “Na Daud na Suleiman walipohukumu juu ya shamba, walipolisha humo mbuzi wa watu usiku. Na sisi tulikuwa Wenye kushuhudia hukumu yao. Tukamfahamisha Suleiman na kila mmoja wao tukampa hukumu na elimu….” (Surat Al-Anbiya; 21:78 – 79). Na kati ya Nabii Musa  na al-Khidhir  yamepokewa 375


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

mazungumzo kwa kirefu katika Suratul-Kahaf ambapo hakukubali na hakuelewa Nabii Musa  misimamo ya al-Khidhir na vitendo vyake mwanzo kwa kutokujua kwake juu ya undani wake, na Khidhir akamtaka udhuru katika hilo:

ُ ُ َ ٰ َ ُ َ َ َ​َ ‫هى ما ل ج ِدط ِب ِهِ ًبرا‬ ‫صبر غ‬ ِ ‫وهيف ج‬ “Na utawezaje kuvumilia yale usiyokuwa na habari nayo” (Surat Al-Kahf; 18:68). Hivyo hatuwezi kutaka kufanana rai na kuafikiana kwake katika mambo mbalimbali. Na kutokana na haya kunakuwa na rai nyingi za mafaqihi na mujitahidina katika mas‟ala moja na hukumu moja ya kisharia kwa msingi kwamba mujitahidi anapopatia anapata thawabu mbili na anapokosea anapata thawabu moja katika juhudi aliyotoa ijtihadi yake. Ndio, katika jamii ya Kiislamu kuna udhibiti wa kulazimiana na Kitabu na Sunnah pamoja na kutoa fursa katika aina na kutofautiana ufahamu katika nususi za Kitabu na Sunnah. Na Sheikh Ibnu Taimiyah ana kitabu kizuri kuhusu kutofautiana rai za Maimamu na madhehebu yao katika kufahamu mas‟ala ya dini, nacho ni kitabu „Raf‟ul-Malaam an Aimatil – a‟alaam‟ ambacho kimechapishwa na al-Jamiatul-Islamiyati al-Madinati al- Munawarah mwaka 1396A.H. Na Mamlaka ni sehemu ya Ulimwengu wa Kiislamu bali ni moyo wa ulimwengu wa Kiislamu, nayo ni nchi yenye sehemu pana na inaundwa na sehemu nyingi, na ni kawaida kuwepo humo na madhehebu ya kifikra na kifiqihi, na kila sehemu kuwa na aina ya tofauti katika utamaduni wake na fasihi yake. Lakini yote hayo katika uzio wa Kiislamu na kwa kushikamana na Kitabu na Sunnah. Na tofauti katika manhaji ya kufahamu na madrasa za tafsiri 376


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

katika hazina ya utamaduni na fasihi, maadamu ni ndani ya uzio wa Kiislamu, ni sehemu ya kutajirisha na kupevuka inapotumika katika kanuni ya kuheshimina na ndani ya adabu ya Kiislamu na tabia yake na kuelekea katika kutumikia maslahi ya jumla na kuhifadhi umoja wa jamii. Na naongeza hapa kwamba mamlaka kwa nafasi yake ya uongozi na uelekezi katika umma wa Kiislamu ni lazima kuelewa makundi mbalimbali na mielekeo, na madhehebu na madrasa za Kiislamu, bali na kufanya kazi ya kuhifadhi mshikamano na uelewano na kutengeneza daraja na mawasiliano baina ya wote kwa ambayo yanahudumia maslahi ya Uislamu na Waislamu. Na mamlaka inalea taasisi za Kiislamu za kiulimwengu kama vile Rabitatul-Alamil-Islamiy na Majimaul-fiqihi al-Islamiy, inaimarisha kwazo mwelekeo wa kufunguka kwa wote na kushirikiana na mirengo mbalimbali. Na sherehe za al-Janadiriya zimekuwa ni mfano ulio wazi wa kukutana mirengo mbalimbali na makundi kwa kuunga mkono msimamo mmoja wa Kiarabu na wa Kiislamu. Maelekezo ya kidini yanayotokana na khutuba za Ijumaa na vipindi vya masomo ya kidini na fatâ€&#x;wa katika masâ€&#x;ala ya kisharia yana nafasi ya msingi katika kutengeneza uelewa wa mwanadamu Mwislamu katika dini yake na kupanga msimamo wake wa kisharia na katika matukio na mambo. Na mwananchi wetu anashikamana na dini na anasikiliza rai na fatâ€&#x;wa za maulamaa wenye kuaminiwa na wenye kutegemewa. Na khutuba za Ijumaa zinafika kwa wote, ni sawa sawa kwa kuhudhuria na kusikiliza moja kwa moja kupitia kushiriki katika swala ya Ijumaa au kwa kuisikiliza kupitia vyombo vya matangazo na televisheni ambayo inahodhi nyanja pana ya vipindi vya kidini. 377


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Lakini ni kawaida khutuba na vipindi vya kidini visiwe katika kiwango kimoja, na kuna ambayo humo kunatimia sifa za ulekezaji mzuri na wa kisasa na kuna ambayo humo kunaonekana baadhi ya nukta za udhaifu. Pamoja na kubadilika hali za maisha na kusonga mbele kiwango cha elimu na kufunguka watu katika vipindi vya maarifa na kiutamaduni mbalimbali kupitia chaneli za televisheni na vituo vya kurusha moja kwa moja ni lazima zibadilike khutuba, na vipindi vya kidini visiwe vinaishia kwenye waadhi kutoa habari, amri na makemeo ya moja kwa moja, bali inapasa zizungumzie na kutoa fikra na mafuhumu ya kimalezi na maarifa ya kina na ziendane na mambo ya kisasa na matukio ya maisha, na ziwe zimesheni kwa namba na sensa na matokeo ya tafiti kimji katika yanayozungumzia mambo ya kijamii. Na ambapo medani ya Kiislamu imepata balaa ya baadhi ya changamoto za kuchupa mipaka ambazo zinapaka matope Uislamu kwa harakati zake na vitendo vyake vinavyopingana, hivyo ni lazima khutuba za Ijumaa na vipindi vya kidini vizingatie kutoa roho ya Kiislamu kunjufu na kutia mkazo katika manhaji ya kati na ya wastani na kupuuza kuchupa mipaka na kasumba, na kuwafundisha watu kuwakubali baadhi yao baadhi na kufunguka kwa baadhi yao na kuheshimiana, hata kama yatatofautiana madhehebu yao au madrasa zao au fikra zao. Ndio, kinachotakiwa ni majadiliano kwa njia iliyo bora na majadiliano yaliyosimama juu ya kutafuta ukweli na kutoa hoja:

ُ َٰ

ُ

“….. ‫… كل هاجىا ُبشهك ى‬..” “…Sema leteni dalili yenu…” (Surat Al-Anbiya; 21:24)

َ

َُ

َُ

َ

ُ

ُ ‫… كل هل غ ذه من غل فخخش‬..” “…..‫جىه ل ا‬ ِ ٍ ِ ِ ِ 378


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

“….Sema: Je, mnayo elimu mtutolee…” (Surat Al-An‟am; 6:148). Ama kuwakufurisha wengine na kuharakisha kutuhumu nia zao na kutia shaka katika dini yao hayo sio katika Uislamu kwa chochote. Upeo mwingine wa kazi ya kidini 222 Mwanadamu anapoelekea katika kusoma elimu ya sharia na kuungana na mwenendo wa maulamaa wa kidini, hii inamaanisha kwamba amekwishaweka nadhiri nafsi yake kuutumikia Uislamu, na amekuwa ni askari wa kujitolea kwa ajili ya kueneza itikadi na msingi. Hiyo ni kwa sababu maarifa ya dini na elimu katika hukumu zake, mwanadamu kubeba majukumu yake ya tablighi na kufundisha, kujua dini kumetangulia kuwaonya watu na kuwaelekeza, kama anavyosema (swt):

ّ ‫من ُ اب َف ٌت ل َي َخ َف ىلُىا فى‬ ‫الذ ِين‬ ِ ِ ِ ِ َ َ َ ُ‫َ َى‬ “‫سون‬ ِ ‫لػلُ يدز‬

َ ُ َ​َ َ​َ ‫…فلىال ف َش ِمن و ِ ّل ِفشك ٍت‬..” َ َ َ ُ َ َُ َ ِ ‫و ِلي ِزسوا كىمُ ِإرا سجػىا ِإلي‬

Kwa nini kisitoke kikundi miongoni mwao kujifunza dini na kuwaonya watu wao watakawarudia, ili wapate kujihadhari.” (Surat AtTawba; 9:122). Kwa kiasi anachojifunza mwanadamu katika dini ni juu yake kutoa elimu yake kwa wengine. Na kila linapokuwa fungu lake ni kubwa zaidi katika elimu, kwa kiasi hicho hicho yanaongezeka majukumu yake katika kueneza maarifa ya dini, na kubainisha hukumu zake na mafuhumu yake. 222

Katika munasaba wa arobaini ya marhum kipenzi Sheikh Husein Aal Sheikh 1385 – 1419 Hijiria, iliyosambawa katika kitabu cha (Afuidati wajaraah) kilichotungwa na Muhammad Amin Abul-Makaarim chapa ya kwanza 1421 Hijiria Darul-Makaarim liliihiyaai turathi.

379


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Na hususani katika mazingira magumu wakati unapotokea upotovu katika manhaji iliyo sahihi au kupotosha kiasi katika misingi ya ujumbe na malengo yake, au wakati akili zinaposhambuliwa na shubuhati za maadui na upotoshaji wa wapinzani, hakika kazi ya maulamaa na wajibu wao katika kubainisha ukweli na kutetea misingi inakuwa ni dharura na muhimu zaidi. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

ّٰ ُ َ َ ‫ى ى‬ َ َ ‫ىخمى َن ما َأ َضل ا م َن‬ ٰ ُ‫ال‬ ُ ‫الب ّي ٰك ِذ َو‬ ‫ػذ ما َب ىي ك ُه‬ ‫ِإن الزين ي‬ ِ ‫ذي ِمن‬ ِ ِ َ ّٰ ُ ُ ُ َ َ َ ُ ‫ٰ ُ ٰ َ َ َ ُ ُ ُ ى‬ ّ ‫ن‬ ِ ‫ب أولك ِنً يلػن اللكه ويلػن اللك ِػ ى‬ ِ ِ ‫الىخك‬ ِ ‫اط ِفى‬ ِ ‫ِلل‬ “Hakika wale wanaoficha tuliyoyateremsha, katika ubainifu na uongofu, baada ya Sisi kuyabainisha kwa watu Kitabuni, hao anawalaani Mwenyezi Mungu, na wanawalaani wanaolaani.” (Surat Al-Baqara; 2:159). Imepokewa katika hadithi kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu : “Inapodhihiri bidaa katika umma wangu, basi mwanachuoni naadhihirishe elimu yake, na asipofanya hivyo Mwenyezi Mungu anamlaani.” 223 Na ikiwa kazi ya mwanachuoni ni kubainisha ukweli wa dini, na kutetea misingi yake, hakika udhihirisho wa kufanya kazi hii na kujua jukumu hili unakuwa ni katika sura na namna mbalimbali na kupitia mbinu na njia mbalimbali, kulingana na kutoafautina hali na mazingira ya wakati, sehemu na jamii. Jukumu lililozoeleka: Lakini kinachoonekana ni kwamba majukumu yaliyozoeleka na kuigwa wanayafanya wengi wenye kujinasibisha kwenye nyendo za elimu ya kidini, katika hawza za elimu, aghlabu maulamaa 223

Biharul-Anuwar, Juz. 2, uk, 108 riwaya ya 35.

380


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

wengi na wanaojifunza elimu wanaelekea kwenye masomo na kufundisha, na utafiti katika elimu ya fiqih na usuuli na kazi ya umarijii na kutoa fat‟wa. Na katika jamii mara nyingi jukumu la mwanachuoni wa kidini linaishia katika mihrabu na mimbari, na yanayofuatia hayo miongoni mwa kufungisha ndoa, kupokea haki za kisharia, kujibu mas‟ala ya kifiqihi, na majukumu haya yanahitajika na ni muhimu, haiwezekani kuyapuuza wala kuyaacha. Lakini kinachopaswa kuangaliwa na kuzingatiwa ni kuishi jukumu katika mpaka huu wa majukumu haya yaliyozoeleka na yanayojulikana, pamoja na kuwepo pengo na haja kubwa katika nyanja na pande zilizobakia. Kwa mfano, katika upande wa elimu maulamaa wanatoa katika hawza za kidini juhudi kubwa katika wakati wao na fikira zao katika kutafiti masa‟ala ya kifiqihi na usuul, na wanakuwa na akili ya angavu, na kina cha kushangaza katika kuzienea hali zote na majaaliwa yote na mijadala yote kwa bidii na ufanisi. Na haya yanapelekea kujifakharisha na kujivunia kwa uhodari wao na ikhlasi yao ya kielimu. Kazi zisizo muhimu: Lakini maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja ya fiqihi na Usuul hayakuendana na maendeleo ya nyanja za elimu zingine za sharia, kama vile elimu ya tafsir, hadithi, na itikadi, historia, jamii na akhlaq. Ndio, kuna kujitolea kibinafsi katika baadhi ya nyanja hizi, kama vile mwelekeo wa al-Allammah Sayid Muhammad Husein Twabatwabaiy katika tafsiri ya Qur‟ani ambapo alifanikisha tafsiri yake nzuri (al-Mizani). Ametengeneza kwayo nyongeza yenye thamani ya juu katika nyanja ya tafsiri. Na vile vile mwelekeo wa al-Allammah Sheikh Abdul-Husein al-Aminiy 381


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

katika nyanja ya itikadi kupitia rejea yake muhimu (al-Ghadir), na mazingatio ya Sheikh Aghaa Barki Tehraniy katika kuangazia utunzi na tafiti za Maulamaa na wanafasihi wa Kishi‟ah, ambapo ametoa rejea yake ya Dhariatu. Na ni lazima kuashiria katika utafiti wa Shahidi Sayyid Muhammad Baqir Swadir ya uvumbuzi katika nyanja za falsafa, uchumi na mantiki katika vitabu vyake vitatu „Falsafatunaa,‟ „Iqtiswaadunaa,‟ na al-Ususu al-mantwiqiyatu liliistiqiraai.‟ Ilikuwa inawezekana kwa Sayyid Twabatwabaiy na Sheikh Aghaa Bazarak Tehraniy kuwa karibu na rika lao na wenzi wao katika maulamaa wa fiqihi katika kushughulika na tafiti za fiqihi na usuul, na katika kushughulika na nafsi ya kutoa fat‟wa na umarjii, lakini wao waliainisha haja na pengo katika nyanja zingine wakazielekea, na wakatumia maisha yao katika kuzitumikia. Mwenyezi Mungu awalipe kheri kwa ajili ya Uislamu na watu wake. Lakini mifano ya shakhsiya hizi ni michache, ina hesabiwa kwa vidole katika mukabala wa mwelekeo wa mamia ya maulamaa na wahakiki wajuzi katika nyanja zilizozoeleka na za kawaida katika hawza za elimu. Na ninarudia hapa, sikusudii kupuuza nafasi ya mwanachuoni yeyote aliyetumikia sharia katika nyanja yoyote kati ya nyanja za elimu, wala sikatai umuhimu wa elimu ya fiqihi na usuul, wala si dharau nafasi ya kutoa fat‟wa na kuchukua umarijii, lakini mimi naitakidi kwamba kuna dharura ya kujaza pengo la maarifa mengine vilevile, na kuboresha tafiti zake na kutatua matatizo ya mas‟ala yake, kwa daraja lile lile katika kina na mazingatio ambayo yanatolewa katika elimu ya fiqihi na usuuli. Hii ni katika upande wa hawza za elimu. Kazi za kijamii: Na ama katika upande wa kijamii, hakika kuna majukumu mengi 382


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

muhimu inawapasa kukabiliana nayo maulamaa na wanafunzi wa elimu ya kidini ambao wanafanya kazi ndani ya jamii, ukiacha jukumu la kuiga lililozoeleka katika mimbari na mihrabu kama ilivyotangulia. Jamii zetu zina haja ya taasisi na tafiti na vituo vya utafiti, kuchunga hali ya jamii, na kufuatilia uboreshaji wake na kubainisha mahitaji yake ya kifikra na kimalezi, kisha kuweka manhaji na ratiba ya kuelimisha na kufundisha na kurejea kutengeneza fikra na mafuhumu ya Kiislamu, kwa ambayo yanaendana na kulandana pamoja na changamoto za kisasa. Kama ambavyo haja inazidi katika zama hizi ya taasisi za matangazo ya Kiilsamu katika chaneli za televisheni, vituo vya tovuti, kutoa magazeti na majarida, na kuandika majarida ya fani kwa maslahi ya mambo ya Kiislamu na umma. Hakika nyanja hizi inapasa tabaka la dini zizielekee na kuzizingatia na kujitolea kujaza pengo humo. Lakini sehemu kubwa katika tatizo hili inatokana na kwamba jamii zetu hazitazami mfano wa nafasi hizi kwa mtazamo ule ule wa heshima ambayo anaipata mwenye kujitolea katika nafasi za kuiga na zilizozoeleka. Na kisha hazimpi msaada na kumshajiisha inavyotakiwa, ambapo imefanya wanajamii wengi kufuata mwenendo wa elimu ya kidini wasione nafsi zao wala wasihisi utekelezaji wa kazi yao na wajibu wao, isipokuwa ndani ya nafasi hizi zilizozoeleka. Na kwa kuongezea katika majukumu hayo ya kuiga yaliyozoeleka, yana mazoea yake na vidhibiti vyake vilivyo wazi. Na ambaye anajitolea kwa ajili yake anakuta mbele yake, mifano na uzoefu mwingi. Unampa matumaini na unampa ujuzi, kwani sio unaendea kazi isiyojulikana wala jukumu lisilofahamika. 383


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Wakati ambapo kuelekea nyanja zingine na kuchukua kazi mpya, inakuwa ni sawa na kujiingiza katika shida, na kunazungukwa na vikwazo, na kunahitaji juhudu kubwa kwa ajili ya kuanzisha, na kutayarisha fursa ya kufaulu. Hawayaendei hayo ila waelewa na walio tayari kwa kuvumilia taabu na majukumu katika njia ya kutumikia malengo matukufu ya kidini, na kwa ajili ya kurekebisha jamii zao na kuziendeleza. Uzoefu wa ujumbe: Na marehemu wetu mtukufu Sheikh Huseini Swalehe Aali Sheikh ď “ď€ ametoa kwetu uzoefu mzuri wa ujumbe katika nyanja hii. Hakika ni tawi bichi kutoka katika mti wa elimu wenye kustawi. Mizizi yake imejikita katika ardhi ya elimu na utukufu kwa karne nyingi. Naye ni matunda yaliyoiva kati ya matunda ya medani ya Kiislamu ambayo yameota katika jamii yetu katika mwanzo wa karne hii ya kumi na tano Hijiria. Alikata masafa katika masomo yake ya kielimu ya hawza, na ukapanuka ufahamu wake na upeo wake na kujua haja ya medani ya Kiislamu kwa ajili ya kazi ya utamaduni na matangazo, na pamoja na kuenea njia zote na mazingira kwake ili kutekeleza jukumu lililozoeleka kwa wanajamii katika mwenendo wa maulamaa wa kidini. Na pamoja na kumiliki kwake uwezo na kipaji katika kufaulu katika nyanja hii, ila ni kwa uelewa wake na ikhilasi yake kwamba aliamua kuelekea katika jukumu gumu katika ugumu wake na jukumu lake lililopuuzwa pamoja na hatari yake. Majukumu muhimu: Alibeba idara na uongozi wa kuhariri jarida la Baswair, nalo ni jarida la kifikra la Kiislamu linalolenga kina cha uelewa wa kidini na kueneza fikra ya kiujumbe, na kutatua mambo ya Waislamu ya kileo, na changamoto ambazo zinawakabili. 384


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Na aliye karibu na mazingira ya kazi ya matangazo ya kiutamaduni katika medani ya Kiislamu, anajua upeo wa ugumu wa jukumu na uzito ambao wanaubeba wenye kukabiliana nayo watendaji katika nyanja hii. Hakika wanachonga jiwe, ambapo mazingira hayawasaidii, wala uwezo hauwasaidii, wala hapati kushajiishwa inavyotakikana, katika uhariri. Na kuandaa mada inayofaa ni lazima kumkinahisha huyu na yule, kisha kukazana na kufuatilia ili kupata utafiti na makala yanayohitajika. Na wakati wa kuchapisha na kutoa, hawamiliki vyombo na taasisi ambazo zinawatosheleza kwa jukumu hili, na msaada hauna uhakika kwa wepesi, na baada ya hapo usambazaji na ugawaji unataka juhudi kubwa. Marehemu mtukufu alibeba jukumu hili hali ya kujua taabu yake na uzito wake, hali ya kuazimia kutoa na kujitolea katika juhudi zake na wakati wake binafsi kwa ajili ya kufanikisha kazi yake. Na utekelezaji wake katika njia nzuri na dalili kubwa katika kujitolea kwake ni kwamba mradi wa jarida la Baswair ulikwama baada ya kufariki kwake. Tunamuomba Mwenyezi Mungu alete badili yake atakayeendeleza mwenendo huu, na kuitajirisha medani ya utamaduni iliyo na kiu sana ya fikra safi. Na kisha jukumu lingine ndani ya upeo huu alilolielekea Sheikh ni kuzingatia hazina ya elimu na fasihi katika nchi, nayo ni hazina kubwa inayokabiliwa na kupotea na kupuuzwa, na inahitaji kuhakikiwa na kusambazwa. Na kwa uelewa wake wa kidini na hisia yake ya uananchi, Sheikh alijitolea katika kuchangia katika nyanja hii na akahakiki rundo la vitabu miongoni mwavyo ni: ◊ Mawadatul-Aali fiyl–adabi al-Arabiy, cha Sheikh Baqir Abu Khamsini. Alikihakiki na akasimamia uchapishaji wake katika Darul-Bayaan al- Arabiy – Beirut. ◊ al-Nnasu al-Jaliyu fiy Imamati Aliyi, cha Ayatullahi Sheikh 385


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Musa Abu Khamsini. Alikihakika na akasimamia uchapishaji wake katika Darul- Bayaan al-Arabiy – Beirut. ◊ al-Amini al-Hadiy wal-hudaatu min Aalihi, cha sheikh Baqir Abu Khamsini. Alikihakiki na alifariki na kiko mbioni kuchapishwa. ◊ Kashafatu al-Qanai fiy dhakati as-amaki, cha Imamu Sheikh Jaafar Abu al-Makaarim, alikihakiki na amefariki na kitabu kiko mbioni kuchapishwa vilevile. Kama ambavyo, Mwenyezi Mungu amrehemu, anashajiisha kuchapisha vitabu na kuvisambaza, na ametoa sehemu ya wakati wake na juhudi zake katika kuanzisha taasissi inayosimamia kazi ya uchapishaji na usambazaji; sisi – hususani katika zama hii – kuna haja sana ya nyumba za usambazaji kwa ajili ya kuchapisha vitabu vya utamaduni na kuvisambaza kwake. Mwanachuoni anapotunga kitabu na akakiacha kinafunikwa na vumbi, vipi kitabu hiki kitatekeleza jukumu lake la ujumbe? Kitabu katika sehemu nyingi katika mazingiraya elimu na kifikra kimekuwa ni mzigo wa mtunzi wake. Baada ya kuitaabisha nafsi yake katika kukiandaa na kukiandika, ni lazima ahangaikie uchapishaji wake na usambazaji wake. Jukumu hili – la uchapishaji na usambazaji – linafanywa na taasisi maalumu katika ulimwengu na sisi tuna haja ya mwenye kushughulika kwa umakini na jambo hili. Hazina ya Ahlul-Bayt ni kubwa, na hazina ya maulamaa wa madrasa ya Ahlul-Bayt ni hazina kubwa, ni utunzi mwingi ulioje? Na ni utunzi mwingi kiasi gani ungali bado unaandikwa? Ni kiasi gani cha utunzi uliopo katika maandishi ya mkono katika sehemu hii ambao unasubiria kuchapishwa na kusambazwa? Familia ya marehemu Aali Sheikh - ni utunzi mwingi ulioje wa 386


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

wajuzi wake uliopo katika maandishi ya mkono? Huenda kilichochapishwa katika vitabu vyao ni sehemu ndogo katika vitabu vyao ambavyo bado vingali vimehifadhiwa katika makabati! Havijachapishwa na havikusambazwa ili wanaufaike navyo watu. Hazina hii kubwa nani ataisambaza na kuitangza katika kiwango cha ulimwengu? Kusambaza ni muhimu zaidi kuliko kuchapisha, kwani hakuna faida ya kuchapisha kitabu na kukiweka ghalani. Nani atajitolea kushughulikia upungufu na kasoro hii katika utamaduni wetu na maarifa yetu, katika usambazaji na uenezaji? Kinachotakiwa ni kwamba baadhi ya maulamaa na wanafunzi wa elimu ya kidni wanaojua umuhimu wa maarifa ya kidini na umuhimu wa usambazaji wake waelekee katika jambo hili, kama alivyokuwa Sheikh marhumu anavyofanya. Hivi ndivyo alivyotoa kwetu Sheikh uzoefu wake wa kiujumbe mzuri pamoja na ugumu wake katika kubeba jukumu na kukabiliana na kazi ngumu na kuziendea sehemu zilizopuuzwa. Ni haja ilioje ya kunufaika na tajriba hii na kuiendeleza, hususan na imekwishapatikana katika jamii yetu idadi nzuri ya maulamaa na wanafunzi wa elimu ya kidini, ambao haipasi wote kuelekea katika kazi ya kuiga iliyozoeleka, na kuishia hapo, bali inapasa kundi miongoni mwao wajitolee katika kila nyanja kati ya nyanja katika kuihudumia dini na maarifa. Mweneyzi Mungu amrehemu Marehemu mtukufu kwa rehema Yake pana, na ampe thawabu katika aliyoyatoa na kujitolea katika kutumikia dini yake na jamii yake na aziimarishe nyoyo za jamaa zake, na hususan mzazi wake muumini mpole kwa subira na utulivu, na aipe badili njema jamii yetu. Hakika Yeye ni Msikivu na ni Mwenye kujibu. 387


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

Utangulizi wa kitabu “Maa yuriduhu shababu�: Ni ladha na badili 224 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu. Sifa zote njema anastahiki Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa viumbe, sala na salamu zimwendee Mtukufu wa Manabii na Mitume, Bwana wetu Muhammad na Ahlul-Bayt wake watwaharifu na masahaba wake wema. Vijana wetu wanakabiliwa katika zama hizi na changamoto hatari katika upande wa kutengeneza shakhsiya zao, kutengeneza fikra zao na nyendo zao. Wao hawajaachwa na fitra yao na akili zao ili wabainishe kupitia kwazo kizuri na kibaya. Na baba zao wanaishi katika mgongano wa mabadiliko na mageuzi makubwa ambayo yamekumba maisha yao. Yamewakosesha uwezo katika kuelewa mambo mapya ya zama sambamba na kuhifadhi maadili na misingi. Na pande za kidini hazimiliki vyombo vya kuathiri na mvuto, kama ambavyo havitokani na mpangilio uliosimama katika ratiba na mkakakti kwa aghlabu ya walio wengi. Ama mazingira yanayozunguka vijana hakika yamejaa mbinu za ushawishi na upotoshaji. Kuna chaneli huru zinazotawaliwa na matangazo ya matamanio na vivutio, na utamaduni wa kimaada kama vile mafuriko yenye kusomba yanataka kuwaangamiza wananchi wote katika msafara wa maendeleo ya kimagharibi chini ya nembo ya utandawazi. Na mazingira ya maisha ambayo yanazidi ukata na ugumu katika nyanja za elimu na kazi na mahitaji mengine ya kimaisha 224

Maa yuriduhu shababu: Twaâ€&#x;amu wal-badili, cha Abdul-Muhsin Ali Abu Abdillahi 1420 Hijiria.

388


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

yanawafanya vijana kuwa na hofu na mkanganyiko katika mustakabali na uwezekano wa kujenga maisha yao. Hakika wao wanamhitajia sana atakayesimama pamoja nao anayejua mazingira yao na anayejua ukubwa wa changamoto ambayo inawakabili. Na awape msaaada ili wavuke hatari za hatua hii nyeti na ngumu katika umri wao. Hakika baadhi ya vijana wanaporomoka mbele ya matatizo haya na baadhi yao wanaanguka katika njia ya changamoto. Na baadhi yao wanakanganyikiwa katika mwendo wake na anajikwaa katika kutembea kwake. Na matokeo ya hayo jamii ya vijana inatawaliwa na muonekano usio na raha. Na vinatoka kwa baadhi yao vitendo visivyo vizuri vinavyopelekea kuudhika wazazi na kukasirika kwa wanadini. Lakini kuudhika huku au ghadhabu hizi hazitatui tatizo bali zinaweza kuzidisha ugumu na kina cha kuporomoka baina ya vizazi na kuwakimbiza vijana katika dini. Na kinachotakiwa ni kujua kina cha hali ya vijana na matatizo yao na kisha kuwasaidia kuleta ufumbuzi na kugundua njia za ukombozi na kunusuru. Na ni wajibu wetu sote kuzingatia kujadili jambo hili na kufikiria humo na kutoa mapendekezo na kuweka ratiba. Na nimefurahi sana jaribio la ndugu mtukufu Ustadhi al-Haji Abdul- Muhsin Abu Abdillahi katika kuchangia katika jambo hili, ambapo amezungumzia baadhi ya matatizo ya vijana wa kileo na wanayokabiliwa nayo miongoni mwa hila za upotoshaji na upotovu, na kwenda mbio katika kutoa ambayo anayaona yanafaa katika mapendekezo na ratiba. Hakika mazingatio ya ndugu Ustadhi Abdul-Muhsin kwa mambo ya jamii yake ni ili kuvumbua juu ya uelewa wa jukumu lake la 389


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

kidini na kijamii kama unavyoonyesha utafiti wake mzuri katika ufuatiliaji wake wa kifikra na kiutamaduni. Na muomba Mwenyezi Mungu ampe taufiqi ya ziada ya kutoa katika kuhudumia dini na jamii. Na nataraji awe ni kigezo kwa ndugu wengine waumini wenye uelewa katika kubeba majukumu yao na washiriki katika kutatua mambo ya kidini na nchi kupitia neno zuri na elimu yenye manufaa. Mwenyezi Mungu awape taufiq wote kwa yale anayoyapenda na kuyaridhia. Hakika Yeye ndio Mwenye kuwafikisha. Hasan Saffar 9 Shaban 1420 Hijiria / 17 Novemba 1999.

Mihadarati: Hatari zake na njia za kujikinga nayo. 225 Amesema (swt):

َُ

َ

ُ

َ

ُ

‫… َوال جللىا بأيذيى إلى ى‬..” “….. ِ‫الت لى ِ​ِت‬ ِ ِ “…..Wala msijitie katika maangamivu kwa mikono yenu…..” (Surat Al- Baqara; 2:195). Mihadarati inazingatiwa kuwa ni kati ya hatari na maafa makubwa sana ambayo yanaikabili jamii yetu katika zama hizi nayo ni: Kwanza: Inaangamiza utu wa mwanadamu na kumkosesha matakwa na jitahada. Anakuwa ni mwenye kukimbilia mata225

Kalimatu iliyotolewa katika munasaba wa maonyesho juu ya hatari ya mihadarati iliyofanywa na Madrasa Saad bin Ubaadah, Qatif – sehemu ya mashariki.

390


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

manio na utashi mbali na kutafakari katika kujenga mustakali wake au kuhudumia umma wake na nchi yake. Pili: Mihadarati inabomoa afya ya mwanadamu kimwili na aghlabu inasababisha upungufu katika kinga ya mwili kwa maradhi, nayo ni katika sababu za maradhi hatari ya ukimwi, kama ambavyo inasababisha upungufu wa nguvu za kiume na mkanganyiko wa mishipa. Tatu: Hakika ni njia ya haraka ya kuyaendea mauti ambapo imekuwa ni hali ya vifo vya walevi ni yenye mahala pa mazingatio ya pande mahususi katika dola mbalimbali, na yanasambaza magazeti ya baadhi ya dola, sehemu juu ya hali ya vifo, na yanatangaza juu yake matokeo ya utumiaji mbaya wa mihadarati kama vile kutumia mafunda ya ziada au kutumia mchanganyiko wa mihadarati hatari au kutopata kilevi na kubadilisha kwa dawa au koloniya, yaani madawa mengine. Nne: Ni kupoteza mali na utajiri kwa watu wanaotumia na katika kiwango cha nchi, na kinachoonekana ni namna gani anaishi mlevi hali ya kufilisika daima na hususani pamoja na kupanda bei ya mihadarati kutokana na kukatazwa kwake na hatari ya kuenea kwake, na ni kiasi gani nyumba zimebomoka na kuvunjika familia kwa sababu hii. Tano: Hakika ni maandalizi ya uovu na kufanya ufisadi mbalimbali ambapo inamsukuma mlevi kutumia mbinu na njia za kupata aliyoyazoea. Na inaweza kuwa ni sababu ya kudharaulika ambapo baadhi ya waovu na makundi potovu kuwapa vilevi baadhi ya wavulana au wasichana kisha wanawalazimisha wanayoyataka katika masharti mkabala wa kuwapa ulevi mpya. Na imekwishaonekana kuwa kuna uhusiano madhubuti baina ya mihadarati na makosa mengi, kama vile ukahaba, liwati na wizi. Yote hayo ni wajibu kuzinduka kwa hatari ya maafa haya, na kazi kubwa ya kuweka kikomo cha kuenea kwake katika jamii 391


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

zetu za Kiislamu. Hakika kuna sababu nyingi zinazosaidia katika kuenea maradhi haya yenye kuangamiza na zilizo muhimu zaidi ni: ◊ Udhaifu wa roho ya kidini na udhaifu wa uelewa wa Kiislamu. ◊ Familia kushughulika na kutowajali watoto wao wa kiume na wa kike na kuwaacha kuwa ni wenye kupuuzwa bila ya uangalizi kamili na matunzo kamilifu. ◊ Kuwepo rataiba mbaya katika baadhi ya vyombo vya matangazo na hususani vya kigeni na kuenea vyombo vya kunasa vipindi hivyo. ◊ Wakati wa faragha ambapo kijana wa kiume au wakike hapati ratiba inayoshajiisha na yenye kufaa kwa ajili ya kuitumia humo. ◊ Kuwepo matatizo ya kinafsi na ya kijamii ambayo yanaweza kuwapelekea vijana kukimbia kwayo kuelekea kwenye mihadarati. ◊ Mamluki wanaokuja, na angalizo ni kwamba mengi ya majaribio ya kuingiza mihadarati yaliyogunduliwa yamepatikana katika mikono ya hawa, kama ambavyo baadhi wanawazingatia kuwa ni njia rahisi ya kutajirika na kupenya katika jamii. ◊ Na mwisho, hakika maadui wenye tamaa wanatumia silaha hii dhidi ya nchi yetu na umma wetu. Mwenyezi Mungu ameipendelea nchi yetu kwa kheri na baraka nyingi, na zilizo muhimu zaidi ni utajiri wa kiroho na hazina kubwa ya kimaanawi kuwa kwake ni sehemu ya Kiislamu na ardhi ya wahyi na utume. Na zinatukuka sehemu kwa ajili ya 392


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

sehemu mbili takatifu, na sambamba na neema hii kubwa Mwenyezi ameinemeesha nchi yetu utajiri wa kimaada unaowakilishwa na mafuta na madini na sehemu zingine. Shukrani na fadhila ni za Mwenyezi Mungu. Na ni jambo la kawaida nchi yetu kuwa ni shabaha ya wenye tamaa, kwani kila mwenye neema huhusudiwa. Na hakika njia harati zaidi ambazo wanazikimbilia maadui wenye tamaa ni kujitahidi kudhoofisha na kuangamiza utu na nafsi za kizazi kinachokua miongoni mwa vijana wa nchi hii. Na hiyo ni kwa kueneza mihadarati na vyombo vya ufisadi na upotovu ambavyo vinasababisha kupotea matakwa na kukosa juhudi na kusambaratisha shakhsiya. Hakika anayetumbukia katika mtego na nyavu hizi hatari, hatarajiwi kuwa ni katika wananchi wenye ikhlasi na wema wanayefanya kazi kwa kuitumikia dini yao na jamii yao, bali atakuwa ni mwenye shakhsiya ya ovyo, mwenye kwenda mbio nyuma ya matamanio na shahawati. Na atakuwa ni zana ya kubomoa na kuharibu katika kiini cha jamii. Na kusambaza mihadarati ni mchezo wa ukoloni. Zamani iliutumia Uingereza nchini India siku za kuitawala kwake, na China wakati walipoitawala, na vilevile wakati wa jeshi la Uingereza kuteka Misri ambapo jeshi hili lilitumia bangi kwa lengo la kuwatuliza wapiga kelele na kuondoa ghadhabu ya wasomi na kudhibiti utajiri dhidi yake. Na ripoti zilizopokelewa kutoka Misri katika miaka hii zinaonyesha kwamba Israil inawafundisha vibaraka na majasusi ili kuingiza mihadarati na kuisambaza Misri, na serikali ya Misri imekamata baadhi ya hawa. Hakika ni jambo la kawaida maadui kufuata kila njia ambayo inawawezesha kutudhoofisha na kuzuia maendeleo yetu, na kisha 393


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

inawapa wao fursa ya kuiba utajiri wetu na kututawala. Lakini sisi tunatakiwa tuwe macho na waelewa ili kutengua mbinu za maadui na kuzuia kupenya sumu yao na maafa yao katika jamii yetu. Na hiyo ni kwa kushikamana na kamba madhubuti ya dini ambayo inaharamisha kila aina ya ulevi na njia za ufisadi na upotovu, na sababu za kuangamiza na kuhilikisha. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Na msijitie katika maangamivu kwa mikono yenu.” (Suratul-Baqarah; 2:195). Na kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu : “Kila kilevi ni haramu na kila pombe ni haramu.” Na kutoka kwake : “Jihadharini na kila ulevi kwani kila ulevi ni haramu.” Na kwa kuwa wahanga wengi wa maafa haya ni katika kizazi kinachukua cha vijana, hivyo ni wajibu kuzingatia kuchunga kizazi hiki na kuandaa muongozo na maelekezo kwao na kujaza wakati wa faragha zao kwa ambayo yanakuza uwezo wao na vipaji vyao na kuwawezesha kuendelea katika mustakabali. Madrasa, kama ilivyo familia, ina dauru kubwa katika kuelemisha. Ni juu ya waalimu watukufu kutumia nafasi hii ya malezi mema kwa wanafunzi wao ili wawasaidie katika kushinda hatari ya wakati wa ujana wenye kutatiza. Na taasisi za kijamii zilizopo katika nchi, kama vile jumuiya, vilabu na vituo vya kheri, na kwa kushirikiana na wananchi na wanajamii zinaweza kutekeleza dauru zao za msingi katika kusimama dhidi ya hatari hizi. Hakika mustakabali wa nchi na mustakabali wa vijana wa nchi na watu wake unatishiwa na upotevu na kuangamia ikiwa mihadarati hii yenye kuhilikisha itasambaa. Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu aihifadhi nchi yetu na jamii yetu kutokana na kila baya, na awape taufiqi viongozi watendaji wenye juhudi 394


Mazungumzo Katika Dini, Utamaduni na Jamii

za kheri na kujitolea kuzuri kwa ajili ya maendeleo na mafanikio. Na ninatumia fursa hii inayofaa ili kutoa shukrani zangu kwa idara ya jumla ya mafunzo katika sehemu ya mashariki na idara ya shule ya msingi Qatif. Saâ€&#x;ad bin Ubaadah kwa ushirikiano wake mzuri katika kukabiliana na hatari yenye kuangamiza kwa kufanya maonyesho ya pili ya kuelimisha juu ya madhara ya mihadarati. Na tunatarajia juhudi hizi kufanya kazi yake inayotakiwa – Inshaallah. Sifa zote njema anastahiki Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa viumbe.

395


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.