Mazungumzo ya wazi pamoja na sheikh qaradhawi

Page 1

MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI ‫حواضاث مفخوحت‬ ‫مع فضيلت الشير يوػف اللطرضاو‬ Kimeandikwa na: Sheikh Ja’far Subhani Kimetarjumiwa na: Amiri Mussa


‫حواضاث مفخوحت‬ ‫مع فضيلت الشير يوػف اللطرضاو‬

‫تأليف‬ ‫الشيخ جعفر السبحاني‬

‫من اللغة العربية إلى اللغة السواحلية‬


©Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 – 9987 – 17 – 006 – 7 Kimeandikwa na: Sheikh Ja‟far Subhani Kimetarjumiwa na: Ustadh Amiri Mussa Kimehaririwa na: Ustadh Al-Haji Hemedi Lubumba Kimesomwa prufu na: Al Haji Ramadhani S. K. Shemahimbo Kimepitiwa na: Al Haji Mujahid Rashid Kimepangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation Tole la kwanza: Novemba, 2017 Nakala: 2,000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Al-Itrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.alitrah.info Vitabu mtandaoni: www.alitrah.info/ebooks/ ILI KUSOMA QUR‟ANI MUBASHARA KWA NJIA YA MTANDAO, TEMBELEA www.somaquran.com


YALIYOMO Dibaji………………………………………….. Mchapishaji……………………………………. Utangulizi………………………………………

7 8 10

Faslu ya Kwanza

16

Imani ya Abu Talib kwa mwangaza wa Kitabu na Sunnah…………………………………..

16

Faslu ya Pili

27

Uchunguzi juu ya Muawiya …………………...

27

Faslu ya Tatu

38

Kumuoza Bikra na Usimamizi wa Baba ……… Mjadala wa kwanza……………………………. Mjadala wa pili………………………………… Mjadala wa tatu………………………………...

38 40 43 47

Faslu ya Nne

50

Kumwita Mtoto kwa Jina Abdu Masihi 'Mtumwa wa Masihi' ……………………………... 50 Faslu ya Tano

55

Usawa baina ya Diya ya Mwanamke na Diya ya Mwanaume ………………………………... Wanazuoni wamekubaliana juu ya nusu diya:...

55 57


Mafuriko ya Sunnah juu ya nusu Diya................ 60 Nusu diya katika diya ya viungo.……………… 62 Kuna maslahi gani katika kufanywa nusu diya:.. 63 Faslu ya Sita

65

Jibu la Utata unaochochewa kuhusiana na Shia na Itikadi zao..……………………………... 65 Mosi: Bidaa ya kinadharia……………………... 75 Madai ya wosia kwa Amirul-Muuminina … 75 Elimu ya Maimamu  kuhusu mambo ya ghaibu……………………………………… Umaasumu wa kizazi cha Mtume ………….. Kutukana Maswahaba: ………………………... Pili: Bidaa ya kivitendo ……………………….. 1. Kurudia maombolezo ya Husein  kila mwaka: ……………………………………. 2. Yale yanayofanywa sehemu za maziara ya

80 82 85 88 88

Ahlul-Bayt  ni miongoni mwa shirki:….. 90 Majibu mengine juu ya Mheshimiwa Sheikh Qardhawi……............................................... 96 Faslu ya Saba

102

Kuruhusu tendo la kupuna tupu za mbele (Punyeto)…………………………………...

102

Faslu ya Nane

108

Kutosheleza Bismillahi wakati wa Kula……….

108


Faslu ya Tisa

112

Madai ya Uharamu wa Ndoa ya Muta………… 1. Uchukuaji wa milele katika maana ya ndoa:... 2. Malengo ya ndoa:…………………………… 3. Madai yake kuhusu kuharamishwa milele ndoa ya Muta:……………………................

112 114 116

4. Je, Mtume  aliharamisha ndoa ya Muta?.... 5. Mharamishaji ni khalifa mwenyewe:…..........

117 121 124

Faslu ya Kumi

131

Nyimbo na Miziki katika kitabu na Sunnah…… Uharamu wa nyimbo katika Kitabu na Sunnah na kauli za wanazuoni:…………………….. Uharamu wa ala za muziki katika Sunnah:……. Dalili ya asemaye kuwa inaruhusiwa:…………. Angalizo juu ya hadithi:………………………..

131 135 140 143 148


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬

DIBAJI Kitabu hiki ni toleo la Kiswahili la taasisi ya Al Itrah Foundation. Chapisho lake limelenga kukidhi mahitaji ya kiroho ya zama hizi pamoja na Ubongo na fikra zinazokuwa za Muislam. Jitihada kubwa zimefanywa na Taasisi kuweka chapisho hili la Kiswahili katika msingi wa haki na wenye kukubalika katika Uislam. Unaombwa kwa Taadhima ukisome kitabu hiki katika malengo yaliyokusudiwa. Pia Unaombwa kuwasilisha kwetu maoni yako huru juu ya chapisho letu hili, jambo ambalo tutashukuru sana. Kutangaza ujumbe wa Uislam ni kazi ambayo inahitaji ushirikiano wetu sote. Taasisi inakuomba kuungana na kushirikiana kama ilivyoagizwa katika aya ya Qur‟an: (Surat Saba‟ 34:46). Na rehma za Allah ziwe juu yako. Wako katika Uislam Al Itrah Foundation Barua Pepe: alitrah@yahoo.com SMS: +255 778 300 140 7


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬ NENO LA MCHAPISHAJI Kitabu ulichonacho mikononi mwako kimetarjumiwa kutoka lugha ya Kiarabu kwa jina la, Hawarat Mahfutah ma’a Fadhilah ash-Shaykh Yusuf alQardhawi, kilichoandikwa na Allamah Mhakiki Sheikh Ja'far Subhani. Sisi tumekiita, Mazungumzo ya Wazi na Sheikh Yusuf al-Qardhawi.. Hiki ni kitabu kizuri na kinafaa sana kusomwa ili kujua ukweli wa mambo. Mazungumzo ya Wazi ni utafiti wa wazi wa kielimu uliofanywa na mwandishi wa kitabu hiki juu ya masuala mbalimbali yaliyozua utata juu ya Waislamu. Mfano suala la Uislamu au ukafiri wa kusingiziwa wa baba mzazi wa Imam Ali, yaani Abu Twalib, uhalali au uharamu wa ndoa ya muta, muziki na mengine kama hayo ambayo Sheikh anayatolea ufafanuzi wa kielimu. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni vitu ambavyo havina nafasi tena katika akili za watu. 8


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

Kutokana na ukweli huu, Taasisi yetu ya Al-Itrah imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumini yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu hususan wazungumzaji wa Kiswahili. Tunamshukuru ndugu yetu Alhaj Amiri Mussa kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Allah Mwenye kujazi awalipe wote malipo mema hapa duniani na kesho Akhera – Amin. Mchapishaji Al-Itrah Foundation

9


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬ UTANGULIZI Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu. Sifa zote njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu. Kisha rehema na amani ziwe juu ya mwisho wa Manabii na Mitume, Mtume wetu Muhammad na Aali zake watoharifu. Ama baada: Hakika Imam Ali  amesema: “Zigonganisheni rai mpaka ipatikane iliyo sahihi kati yake.”1 Na umekuja kuhusiana na hilo usemi maarufu usemao: “Uhakika ni zao la utafiti,” kama kwamba ukweli na ufichuaji wa mambo ni uhalisia na zao la kukabiliana kwa rai na fikra mbalimbali. Ni ukweli usiojificha kwamba hakika majadiliano ya kielimu ni chimbuko la uhakika ambao umesimama juu ya mwenendo wa elimu, na pindi unapouimarika nguzo zake basi mnara wake hurefuka juu zaidi. Na hakika wanazuoni wetu waliotangulia wameshikamana na mfumo huu, na wale waliowafuatia pia. 1

Ghurarul-Hikam na. 2567.

10


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

Walikuwa huru katika kufanya tafiti na mijadala mbalimbali, na tija iliyofikiwa ilikuwa ni jambo linalopendeza zaidi kwao kuliko kitu chochote kile. La msingi na muhimu zaidi kwao ni kuhusiana na jambo husika, basi wao – kutokana na yale aliyokuwa nayo kila mmoja wao miongoni mwa heshima, upendo, na utukuzaji – hawakusita wala kuchelewa katika ukosoaji wa rai na maoni, na uchanganuzi wa maneno, na utukuzaji wa uhakika na ukweli. Bali walikuwa wakipitia masuala ya hadithi, mjadala, ukosoaji na utoaji wa majibu mpaka meli ya maarifa ishushe nanga katika ufukwe wa haki, na mawingu ya ujinga yatawanyike na kusambaa huku na huko, na kustawi mbingu ya fikara na itikadi. Kuhusiana na ukweli wa jambo hili, Sheikh wetu mwanafikihi, Sheikh wa sharia wa Isfahani, akinukuu kutoka kwa baadhi ya wasomi katika mlango huu amesema kwa kauli yake: “Hakika kukosekana upendo baina ya wanazuoni wao kwa wao, ni matokeo mabaya na makubwa yanayoukumba umma huu, ambao Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameutukuza huo kwa neema. Kwa namna ambayo amewahifadhi hao kutokana na fedheha na aibu ya kuwapenda waandishi wa vitabu viwili wenye kusababisha upotoshaji wa yale yaliyomo katika hivyo viwili, na kuviingiza hivyo viwili kwa watu wa 11


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

dini mbili. Hawakumwachia msemaji aliyesema kauli iliyo na uduni isipokuwa waliubainisha. Na hawakumuacha mtendaji wa kitendo hicho cha upotoshaji ila walikisImamisha, mpaka zikaeleweka wazi rai husika, matamanio yakaisha, na sharia ikadumu wazi wazi na kujaa ukanda wa anga mwangaza wake, na kuponya nyoyo kwayo kutokana na kuitekeleza hiyo, ikahifadhika kutokana na upotoshaji, na ikalindwa kutokana na ukoseaji.”2 Hivyo ndivyo ulivyokuwa mwenendo wa wale waliofuatia katika michakato ya kufikia ukweli na uhakika, na kupatikana kwa haki. Ndiyo yanarandana na yale anayoyasema mshairi nguli aliyebobea katika ushairi, naye sio mwingine, bali ni Ustadh mwanautafiti Muhammad Abdul-Ghani Hasan, mwandishi wa kitabu kiitwacho Taaliif Munti’at, akiwasifu wanazuoni na tabia zao: “Inazidi sababu ya ugomvi wa maneno – lakini anakuwa laini wa maungo na maumbile. Na vivyo hivyo wanazuoni wetu katika tabia zao – wanajiweka mbali na mifarakano wanakutana haraka. Katika haki wanatofautiana isipokuwa hakika wao – hawazitafuti haki zilizopotea. 2

Ibanatul-Mukhtar: Utangulizi.

12


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

Hakika sisi inatukusanya itikadi na kuwa umma mmoja – na inatuweka pamoja dini ya uongofu kuifuata. Na Uislamu unaleta upendo baina ya nyoyo zetu – popote tutakapokwenda katika uongofu makundi kwa makundi.” Hakuna kitu kigeni, hakika usimamaji katika uhakika, na uondoaji sitara kutoka kwenye uso ni dhamana inayotegemea mjadala wa kielimu, na mazungumzo na midahalo. Hakika suala la ukutanaji fikra za wenye mitazamo mbalimbali ni kama vile mawimbi ya umeme yanavyopita: hasi na chanya ambazo huzalisha nuru. Vivyo hivyo nuru ya hakika inaenea mbele yetu kwa ubadilishanaji wa fikra mbili, na kupingana na hizo mbili kwa kukanusha na kukubali, kwani mara nyingi mwanadamu hujiona ni mwenye kupatia katika fikra yake. Ikiwa tutazifanyia hizo mbili utafiti na majadiliano na ukapatikana ukanushaji na uthibitishaji, huenda ukadhihirika uduni wake na udhaifu wake. Ndiyo, inamlazimu mfanya utafiti kuhusiana na uhakika asImamishe rai zake na fikra zake katika mazingira tulivu kwa ubongo uliyo huru, uliyoepukana na king‟ang‟anizi kwa ajili ya kundi lililopita. Au fikra ya sasa au rai iliyotangulia isiyo na dalili na ushahidi. Basi ni kwa njia hii pekee tutahifadhi alama za kudumu Uislamu na kubakia 13


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

kwake, na alama ya kuwa kwake ni mtazamo safi wa hali ya juu katika kila zama na kizazi. Na kutokana na mwelekeo huu, tumesimama kudurusu na kuyapitia baadhi ya yale aliyoyaeleza Dr. Sheikh Yusuf Qardhawi, katika nyanja za itikadi na sharia, katika kumjibu yeye na majibu yake kutokana na maswali ya wasomaji wa jarida la SHARIA la Jordan,3 au yale aliyoyaandika na kuyachunguza ndani ya kitabu chake Al-Halal wal Haram fil Islam. Akikusudia katika makala yake na hutba zake kubainisha yale ambayo ni halali na haramu katika sharia takatifu ya Kiislamu, anajaribu kuondoa shaka na utata kutokana na upande wa baadhi ya hukumu. Basi juhudi zake kwa upande huu ni muhimu mno. Lakini uonaji huu hautuzuii sisi kuchunguza yale ambayo yanapatikana katika baadhi ya rai na fatwa zake, kutokana na mapungufu na makosa yake. Na tutapitia na kusoma hapa kwa mwangaza wa Kitabu na Sunnah tukufu, tukitarajia kwavyo uchunguzaji wa kina. Ikiwa ataikuta hiyo ni haki basi atangaze na 3

Uongozi wa uhariri umesimamia jarida la “Sharia� la Jordan unaoheshimiwa kwa usambazaji wa baadhi ya mijadala yetu mbalimbali kuhusiana na mfutu maswala mbalimbali ya mheshimiwa sheikh Qardhawi juu ya kurasa za baadhi ya matoleo yake. Mwenyezi Mungu awalipe malipo mazuri, na tunatambua mchango muhimu wa kubainisha haki na kuhudumia uhakika.

14


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

arudi na aachane na rai yake ya kwanza. Na ikiwa atakuta ndani yake mapungufu au kasoro basi atukumbushe kwayo, na tutakubali ukosoaji wake kwa kumshukuru na kuupokea kwa mikono miwili. Na lengo letu katika kusambaza majibu haya si jingine isipokuwa ni ili wapendwa wasomaji ambao ni miongoni mwa watu wa umma wetu wa Kiislamu, wapate kujua upande mwingine wa kadhia na masuala mbalimbali yaliyoelezwa. Na wao wako huru baada ya hivyo katika kuchagua yale watakayoyaona kuwa ni haki. Na haki ni haki kufuatwa. Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu. Jaâ€&#x;far Subhani.

15


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬ FASLU YA KWANZA IMANI YA ABU TWALIB KWA MWANGAZA WA KITABU NA SUNNAH4 Mheshimiwa Ustadh Yusuf Qardhawi, Mwenyezi Mungu amhifadhi. Amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yenu. Tunamuomba Mwenyezi Mungu awape afya nzuri na uwezesho kwa ajili ya kuutumikia Uislamu na Waislamu. Ama baada: Hakika tumepitia moja ya majarida ya Kiislamu, katika makala ya maombolezo yenu kuhusiana na kufariki mwanafikra mkubwa wa Kiislamu, Sheikh Ghazali , makala husika ilikuwa na anwani: Nyota ichomozayo. Na hakika Sheikh Ghazali kweli alikuwa – kama mlivyomsifu yeye – ni akili erevu, na moyo msafi, na muongofu katika fikra na shujaa katika haki, na mwenye wivu juu ya dini. Hakika alitangaza yale ambayo aliona kuwa ni haki bila kuogopa upinzani 4

Uhariri wa jibu hili umetimia tarehe 15 mfunguo pili mwaka 1417H, kujibu mihadhara iliyotolewa na Sheikh Qardhawi katika nchi ya Qatar.

16


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

utakaojitokeza dhidi ya rai yake ya wazi kutokana na ukosoaji na upingaji, kwani yeye alikuwa – kama mlivyosema – ni mtu mwenye fikra na mawazo huru. Alikuwa huru wa maneno na utumiaji wa kalamu (maandiko), kwa sababu yeye alikataa kunyenyekea matamanio ya watu wa kawaida kama walivyofanya walinganiaji wa elimu, ambao watu wanawadhania kuwa ni walinganiaji!! Na hakika tumepitia wakati huo huo barua zenu nzuri kuelekea jumuiya ya pili ya ukurubishaji baina ya madhehebu ya Kiislamu huko Ribat (12 – 14 mfunguo saba 1417H) ambayo imetokana na roho iliyofunguka yenye kudhihirisha utukufu wa Waislamu na ufahamu wa kina zaidi na mantiki ya Qur‟ani na Sunnah. Kwa hakika umetustaajabisha ndani yake mtazamo wenu sahihi kuhusiana na yale yanayozuia upatikanaji wa umoja wa Kiislamu na ukaribishaji baina ya matapo ya Waislamu na makundi yao. Na kati ya mambo hayo ni kukosekana maumivu makubwa na matarajio makubwa katika nyoyo za Waislamu, na hatimaye kuendekeza kupambana na kushambuliana juu ya masuala madogo na yasiyo na msingi yanayotokana na matawi ya itikadi au fikihi. Na hakika imekuwa ni wajibu – kama mlivyosema – juu ya walinganiaji na wanafikra wa Kiislamu wajishughulishe na jamhuri ya Waislamu kwa majonzi makubwa ya umma wao na waelekeze macho yao, 17


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

nyoyo zao na akili zao hadi kwenye udharura wa kujikita na kutilia mkazo juu ya umoja pamoja na uamsho juu ya umoja huo. Na ni haki kama mlivyosema: mushkeli mkubwa wa Waislamu wa leo sio katika yule ambaye anayeawili aya za sifa na hadithi zake, bali ni yule anayekanusha dhati na sifa zote za Mungu na analingania katika njia ya usekyula na ulahidi. Na mushkeli na tatizo la Waislamu sio yule anayedhihirisha Bismillahi au anayeificha au asiyeisoma katika Swala, wala si yule anayeachia mikono yake katika swala au anayefunga mikono yake. Hakika mushkeli na tatizo ni yule asiyemuinamia Mwenyezi Mungu akiwa mwenye kurukuu wala asiyemsujudia wala haujui msikiti wala hamjui yeye…wala .. wala.. . hakika sio vinginevyo … Na ufuatao ni mushkeli na tatizo kweli, nao ni: Kuwa na itikadi katika nafsi na kuipa likizo sharia maishani, kuporomoka kwa maadili katika jamii, kuzipoteza haki, uzuiaji wa zaka, kufuata matamanio, kuenea maovu, kutapakaa kwa rushwa, kuharibika kwa dhamana, matumizi mabaya ya ofisi, kuacha faradhi za msingi, kutenda mambo ya haramu, na kuwatawalisha na kuwafanya vipenzi maadui wa Mwenyezi Mungu, Mtume Wake na waumini. Hakika mushkeli wa Waislamu – kama mlivyosema – unaonekana katika kuitupilia mbali akili na kutoipa nafasi ya kufikiria na kuua utashi, na kuua uhuru, na 18


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

kuangamiza haki mbalimbali, na kusahau wajibu, kuenea ubinafsi, na kuziacha Sunnah za Mwenyezi Mungu ulimwenguni na katika jamii. Hayo ndio matatizo hasa, na hasa hasa yale ambayo mliyoyataja katika nambari saba chini ya anuani; mambo saba ya msingi yaletayo majonzi. Na hakika yametushangaza maono yote hayo kijumla na kiufafanuzi, na tulitamani lau ungelikuwa mtazamo na maono kama haya yawe yameenea kati ya wanafikra wa Kiislamu na wanazuoni wake wa leo wa Kisunni na Kishia, kutoka katika makundi yote na madhehebu yote. Na kuwepo hali ya kusaidiana kwa kweli, kwa kina na kwa muunganiko katika utatuzi wa mishkeli, maadamu vikundi vyote hivi na madhehebu yote haya yameafikiana juu ya umoja wa Mwenyezi Mungu, na utume wa Nabii wa mwisho, Muhammad bin Abdillah , na nguzo za Uislamu wa kivitendo, na tabia njema, na mambo mengi mengine yasiyohesabika, ambayo ni vigumu kuyahesabu na kuyazingira. Na tulitamani lau wangelikuwa Waislamu wanajizuia – upande huo – na upitishaji mwepesi wa mishale ya tuhuma baina yao, na wanafungua vifungo vya kimakundi na mbinu zake za kijahilia. Na badala ya hayo kila mmoja anasimama na kufanya usomaji wa dondoo za tofauti kwa roho ya kidugu na mfumo wa kielimu, na njia nzuri. Na wawe wanatoa kwa wote 19


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

fursa ya uelezaji kuhusiana na madhehebu yake, na kujulisha kwa dalili zake na hoja zake kwenye anga lililojaa ustahamilivu wa kifua na kuenea fikra na usamehevu. Na waache kuchochea yale ambayo yanaziweka mbali nyoyo zao, na yanayosumbua na kuchafua usafi, na kuharibu upendo. Lakini ni kwamba imetufikia sisi habari kuwa, katika mhadhara wenu mlioutoa huko Qatar, Sheikh mmemzungumzia kwa ubaya mzee mnusuru wa Uislamu na aliyemhami Nabii wake , naye si mwingine ni Abu Twalib . Ambaye alimlea Mtume  na kumhifadhi yeye, aliyemhami yeye baada ya kutumwa rasmi na utume. Na akajitolea muhanga raha yake nafsi yake pamoja na watoto wake ambao ni hazina ya ini lake, katika njia ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) na katika ulinganio wake. Alikuwa ni mwenye kuficha imani yake, na mwenye kujikinga na watu wake ili abakie kwenye cheo chake, kwa ajili ya kutoa huduma katika kivuli cha Mtume na utume. Na alimkinga yeye na maudhi ya wale wenye kupinga hayo mawili. Aidha alikitegua kitimbi chao kama alivyofanya muumini wa ndugu wa karibu wa Firaun muda wote wa miaka arobaini, bila kukatika. Je, unaona ilikuwa ni haki kukanushwa fadhila yake, na kutotambulika huduma na mchango wake? Yeye ambaye amesema waziwazi usahihi wa utume wa Mtume Muhammad  na akausadikisha wito wake wa unabii wa mwisho katika kaswida yake na 20


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

mashairi yake yanayofasiri imani yake, kwa kusimama dhahiri – yeye na watoto wake wakiwa wa mwanzo – upande wa Mtume  ambapo anasema: “Mmekadhibisha naapa kwa nyumba ya Mwenyezi Mungu, mliposema tunamshinda Muhammad – na pindi mtu mwingine anapomponda, sisi tunamtetea. Na tunamsalimisha yeye mpaka tunapambana kumhami yeye pembezoni kwake – na tunasahau watoto wetu wa kuwazaa na watoto wa kufikia. Naapa kwa umri wangu, hakika nimemlea Muhammad na kuwa naye bega kwa bega - na ndugu zake wenye tabia ya upendo wenye kuendelea. Dunia itaendelea kuwa nzuri kwa watu wake – na pambo kwa yule aliyemtawalisha yeye Mola Mlezi wa mambo makubwa. Basi ni nani mfano wake katika watu, ambaye mwenye matumaini – ikiwa watawala watampima yeye katika ubora na fadhila. Mpole muongofu mwadilifu sio mzembe – anampenda Mungu na sio yeye mwenye kughafilika. Hakika wamejua kwamba watoto wetu sio wenye kudanganywa kwetu –wala haikusudiwi kauli ya batili. 21


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

Basi akawa kwetu sisi Ahmad ni kipaumbele cha juu kabisa – hakifikiwi na yeyote mwenye matamanio makubwa. Imepinda nafsi yangu haitomuacha katika kumhami yeye – na nitamkinga yeye na vipingamizi na vizuizi. Basi akamuunga mkono Mola Mlezi wa waja kwa kumnusuru yeye – na akaidhihirisha dini haki yake na sio batili.”5 Ibn Hisham amenukuu katika kitabu chake cha historia beti tisini na nne za kaswida hii, wakati Ibn Kathir Shaami katika kitabu chake cha historia ameeleza beti tisini na mbili. Na Abu Hifan Ibadi Jaamiu katika diwani "Abi Twalib” ameeleza beti mia na ishirini na moja, baadhi ya hizo zimo katika diwani hiyo. Na huenda hizo zikawa ni ukamilifu wa kaswida nzima, nayo ipo katika kiwango cha juu cha utamu na uzuri, na ipo katika kilele cha nguvu na uzuri. Pia inazidi katika pande hizi mashairi yote saba ambayo walikuwa Waarabu wa zama za ujinga wakijifaharisha kwayo na wakiyahesabu kuwa ndio bora zaidi kati ya mashairi yaliyosemwa. Na anayo nyuma ya beti hizo zinazoishia na Laam (L), kaswida nyingine ya kishazi cha Miim, basi yeye – amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake – 5

Siirat Nabawiyya, Juz. 1, uk. 272 – 280 cha Ibn Hisham.

22


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

anasema kinaga ubaga ndani yake kuhusiana na utume wa mtoto wa ndugu yake, na hakika yeye ni Nabii kama vile Musa na Isa , pale aliposema: “Ili watu wema wajue hakika Muhammad – ni Nabii kama vile Musa na Isa bin Maryam. Ametujia kwa uongofu mfano wa ule ambao waliokuja nao – basi kila amri ya Mwenyezi Mungu anaongoza na anakinga.”6 Na mfano wa hiyo ni kaswida yake inayoishia na B na ndani yake anasema: “Je, hamkujua hakika sisi tumemkuta Muhammad – ni Nabii kama vile Musa, imeandikwa katika vitabu vya mwanzo.”7 Je, baada ya ufafanuzi na uwazi huu inasihi binadamu mwenye upeo na utambuzi wa mambo amkufurishe bwana mwenye kujilaza chini ya mchanga au aweke shaka katika imani yake?! Na hata tukikubali kuwa hakuwa Mwislamu je, huu ni mushkeli uliopo katika umma wa Kiislamu wa leo, ilihali nyinyi mnajua zaidi mishkili na matatizo ya umma. Na je, kumsema vibaya mhami na mtetezi wa Mtume  ni kuuhudumia umma?! 6

7

Majmaul-Bayaan, Juz. 7, uk. 37, Al-Hujjat, uk. 56 na Mustadrakul-Hakim Juz. 2, uk. 623. Majmaul-Bayaan, Juz. 7, uk. 36. Na hakika amenukuu Ibn Hisham katika kitabu chake cha Historia Juz. 1, uk. 352 beti 15 kutokana na kasida hii.

23


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

Pamoja na misImamo hiyo mitukufu, na pamoja na yale ambayo yanayotoa athari ya wazi na kufichua imani yake kwa utume wa Nabii Muhammad , Je, Abu Twalib anakuwa ni mshirikina?! Na Abu Sufyan ambaye amewasha moto wa vita na akasimama kwa kufanya njama mbalimbali kwa muda wa miaka ishirini, yeye na wanawe ambao walikuwa ndiyo msingi wa matatizo na mwanzo wa upotokaji katika mwelekeo wa Uislamu, je wao wanakuwa ni Waislamu wenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu (s.w.t) wanastahiki kila heshima na kuutambua mchango wake kutoka kwetu sisi?! Na je, unaona kama angelikuwa Abu Twalib ni mzazi wa mtu mwingine asiyekuwa Ali bin Abi Twalib  angeliona matokeo haya kutoka kwa Waislamu?! Kwa nini ewe mheshimiwa mwalimu – kutokana na kiwango cha juu mlichonacho katika maono na utambuzi – usifuate njia ya rafiki yenu aliyefariki Sheikh Ghazali , ya kukiri haki, na kutonyenyekea kwenye riwaya batili? Sisi – hakika tumefanikiwa kupata sehemu ya yale mliyoyaandika yenye thamani kubwa kwa fikra zenye kung‟aa – hivyo tulikuwa na bado tunaendelea kutaraji kuwa mtafanya insafu na uungwana katika haki, bila kuangukia katika yale waliyoangukia wale wa awali kuhusiana na chuki zao na kutoyajua 24


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

makosa ya jinai yao. Na muwe marejeo ya kuaminika kwa vijana wa zama hizi katika kuisahihisha historia, kuisafisha hiyo kutokana na ngano za kale, na kuondoa majeraha na dhuluma dhidi ya wale waliodhulumiwa. Na Mwenyezi Mungu (s.w.t) amrehemu Ibn Abi Hadid aliposema: “Na kama si Abu Twalib  na wanawe – wala dini isingelifananishwa na watu wawili waliosimama imara. Basi huyu hapa Makkah amempa hifadhi na akamhami – na kule Yathriba yakamfika mauti.” Yote hayo ni kama habari iliyotufikia sisi kutokana na mihadhara yenu kuwa ni ya kweli. Na tunataraji isiwe hivyo. Hapa na tunatuma kwenu yale tuliyoyapata kutokana na somo la mapitio ya imani ya Abu Twalib  kwa mwangaza wa Kitabu, Sunnah na historia. Na hakika yamechapishwa ndani ya masomo yetu yanayozungumzia uhai na historia ya Bwana Mtume . Kisha hakika sisi kutokana na udharura wa kujituma na kuongeza ziada ya ufahamu na kuleta ukaribu tunawatumia nyinyi kitabu kinachoitwa: Al-I’tiswaam bil-Kitab wa Sunnah, Hukmul-Arjuli fil-Udhuui na Asmaau-Thalathat, na matarajio yetu ni kwamba 25


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

vitabu hivi vitakuwa ni hatua kuelekea katika njia ya kuleta ukaribu baina ya Fikhi mbili. Na mwisho tunasema: Hakika nyinyi katika barua yenu ya kongamano mliipa nguvu kauli ya Imam Ahmad katika suala la uumbwaji wa Qur‟ani, na haikuwa kauli yake isipokuwa ni Umwanzo wa Qur‟ani. Na vipi iwe kauli hii, ni kauli yenye nguvu zaidi ilihali umwanzo ni wa Mwenyezi Mungu (s.w.t)? Basi inakuwa Qur‟ani wakati huo ni Mungu wa pili, na hilo linapingana na msingi wa Tawhid?! Na kama makusudio ya umwanzo wa Qur‟ani ni kutangulia elimu yake (s.w.t) basi jambo hili halina uficho juu yake wala utata. Na la msingi ni kwamba Imam Ahmad angechukua itikadi kutoka katika Qur‟ani na Sunnah, na asizame katika suala hili kwa hoja ya kwamba, Kitabu na Sunnah havikutaja chochote kuhusiana na umwanzo wa Mwenyezi Mungu (s.w.t) na kuzuka kwake. Na kubalini katika kuhitimisha heshima zetu kwenu, na matumaini yetu bora zaidi, ni Mwenyezi Mungu (s.w.t) awafikishe na awawezeshe kwa elimu nzuri na amali njema, na amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yenu.

26


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

FASLU YA PILI UCHUNGUZI JUU YA MUAWIYA8 Ustadh mheshimiwa Sheikh Yusuf Qardhawi. Amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yenu. Tunathamini juhudi zenu za kielimu na yale ambayo mliyoyatanguliza kwa ajili ya umma wa Kiislamu kuhusiana na kupendana na athari muhimu katika nyanja mbalimbali. Tunamuomba Mwenyezi Mungu (s.w.t) aushike mkono wenu hadi kwenye yale anayoyapenda na anayoyaridhia. Pia akuwezesheni kwa amali njema. Pia tunathamini na kutambua mchango wenu mzuri katika suala la kuleta ukaribu na umoja baina ya madhehebu ya Kiislamu. Lakini hilo halituzuii sisi kuashiria sehemu ya maneno ambayo yametoka kwenu katika baadhi ya minasaba mbalimbali. 1. Hakika mmeeleza kuhusu imani ya bwana Abi Twalib ď ‹ na mmesema hakika yeye amekufa kafiri, licha ya kwamba vitendo vyake na amali zake kwa muda wa miaka kumi Makkah tukufu, na kaswida yake ya kujifaharisha, vinashuhudia kwamba yeye amekufa muumini. Na aliishi kama maisha ya muumini wa ndugu wa karibu wa Firaun. Na hakika 8

Barua hii imetumwa tarehe 10 mfunguo nane mwaka 1424H.

27


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

tumekutumia barua inayohusu maudhui hii hapo kabla. Na tulitilia mkazo kwamba, suala hilo sio miongoni mwa mambo ya dhurura hadi lisemwe juu ya mimbari mbalimbali. 2. Tumesoma katika moja ya magazeti kuhusu kumtetea kwenu Muawiya bin Abi Sufyan katika hotuba ya Swala ya Ijumaa. Na sisi tunajiuliza: Ni faida ipi inayopatikana kuhusiana na kumtetea Muawiya katika siku hizi ambazo umma wa Kiislamu unakabiliana na changamoto kubwa na hujuma mbalimbali?! Na tuna haja zaidi ya kuwasilisha ufahamu sahihi wa Uislamu, na kutoa picha ya wazi ya dhana zake na fikra zake, na msimamo uliyosalimika na sahihi kuelekea katika kadhia mbalimbali, aidha watu wake na shakhsia zake. Tufuate haki katika yote hayo, na tushikamane na sharia na tabia, na tuwe mbali zaidi na upendeleo binafsi na wa hisia binafsi, na ukataji tamaa ambao huenda umeanza kutokana na msingi wa dhana za makosa na taaluma potofu. Je, historia yetu ya Kiislamu imekosa watu walioujenga Uislamu kwa kaulimbiu, lengo na mfumo na silka, kwa roho na damu zilizomwagika katika njia yake..?! Je, watu hawa wamekosekana hata ategemewe mtu mfano wa Muawiya ili mchanganyiko huu wa makosa utumiwe kwa ajili ya utengenezaji na ungâ€&#x;arishaji wa uso wake usiopendeza?! 28


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

“Basi huyu hapa Ali  aliyetukuka kwa jina lake – Anapasua anga na ni mwenye kuangusha. Basi ninyi mleteni Muawiya. Mleteni mtoto wa Hindu ikiwa mtamkuta amesagika – na kama si hivyo mtamkuta mwenye kudhalilika.”9 Sijui ni kitu gani kinakipata kizazi chetu ambacho Ustadh Qardhawi anajituma katika kukitengeneza, kutoka kwa Muawiya ambaye ni mpingaji wa haki, mpambanaji dhidi ya uongofu, mmwagaji damu za watu wema, aliyeeneza matusi na laana, na akawafanya duni wale wenye nafasi na wenye manufaa. Na kinara wa watu wenye nyoyo zenye ugonjwa ambao wameathirika na maisha ya dunia kuliko kile ambacho ni bora na chenye kubakia?! Je, kwa kupambwa picha ya Muawiya na kufuatwa athari zake, inatarajiwa kutoka kwa kizazi hiki, kwamba matarajio yake yatatimia na hali ya kuvunja moyo itabadilika na kuwa ushindi. Na je kizazi kitahama kutoka katika ubabaishaji hadi katika elimu, na kutoka katika kugombana hadi katika kusaidiana, kama alivyoeleza Dr. Qardhawi?! Hakika Muawiya hakuondoka katika dunia yake yenye giza kwa fitina, chuki, vitimbi na udikteta 9

Allama mshairi Sheikh Abdul-Hamiid Samawi .

29


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

mpaka akahitimisha hayo kwa jinai kubwa isiyosameheka katika utendaji wa shari na kutii matamanio potofu. Akaeleza kwa ibara ya kauli yake: “Lau sio mapenzi yangu kwa Yazid ningeliiona njia yangu.” Na sisi tunamuuliza mlinganiaji mkubwa na mtu mwenye roho nyepesi Ustadh Qardhawi: Je, ni haki kuondoa sitara juu ya yule anayetenda makosa ya jinai mabaya kama haya, ambayo hayana mfano wake na kumkabidhi madaraka ya Waislamu Yazid mtu muovu na mnywaji pombe?! Na utendaji wake wa maasi hayo ambayo yanapita zaidi ya unyama kwa kuua mtoto wa binti wa Mtume na watu wa nyumbani kwake na masahaba wake. Na kumwaga damu za Waislamu katika tukio la uhalalishaji wa mambo machafu, kubaka wanawake na kuwanyanyasa pamoja na kuondoa heshima zao?! Na tunapenda tukumbushe hapa baadhi ya yale ambayo yamepokewa katika haki ya kiongozi wa kundi ovu Muawiya: Dhahabi amesema: “Na aliuawa Ammar akiwa upande wa Ali, na ikabainika na kudhihirika kwa watu kauli ya Mtume  aliyosema: „Ammar atauliwa na kundi ovu.”‟10 10

Siyar A’laam Nubalaai, Juz. 3, uk. 142, Tarjumat Muawiya na. 25.

30


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

Amesema mhakiki wa kitabu kilichotajwa: “Nayo ni hadithi sahihi mashuhuri bali mutawatiri. Na pindi Muawiya aliposhindwa kuikanusha, alisema: „Hakika wamemuua wale waliomleta vitani.‟ Basi Ali  akajibu: „Kwa hivyo hakika Mtume  amemuua Hamza pindi alipotoka naye kwenda vitani.‟ Na hili likamfanya akose jibu, na hoja kwa upinzani wake juu ya hayo.‟” Imepokewa na Muslim katika Sahihi yake kutoka kwa Aamir bin Sa‟d bin Abi Waqas, kutoka kwa baba yake amesema: Muawiya bin Abi Sufyan alimwamrisha Sa‟ad akasema: Kitu gani kinakuzuia kumtukana baba wa mchanga? Akasema: Ama nikikumbuka mambo matatu ambayo bwana Mtume  alimweleza yeye, siwezi kumtukana. Kwani nikiwa nalo mimi moja kati ya hayo inanipendeza mimi kuliko ngamia wekundu. Nimemsikia Mtume akimwambia pale alipomwacha katika baadhi ya vita vyake, akasema: Ewe Mtume! Unaniacha mimi pamoja na wanawake na watoto? Mtume  akamwambia: “Je, huridhii kuwa wewe kwangu mimi ni kama vile alivyokuwa Haruna kwa Musa, isipokuwa hakuna Nabii baada yangu.” Na nikamsikia akisema katika vita vya Khaybar: “Nitampa bendera mtu ambaye anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na ambaye anapendwa na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake.” Akasema: Basi ukapita muda kwetu akasema: “Nileteeni Ali, basi 31


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

akaitiwa, alikuwa anaumwa ugonjwa wa macho. Hapo Mtume  akamtemea mate machoni mwake na akamkabidhi bendera, basi Mwenyezi Mungu (s.w.t) akaikomboa ng‟ome ya Khaybar kupitia yeye. Na pindi ilipoteremka aya hii:

ُ َ ُ َ َ َ َ ُ َ َ​َ َ َ ُ َ َ َ ُ َ ‫ؼضءلم َاأهف َؼىض‬ ‫… فلل حعضلوا هسع أبىضءهض اأبىضءلم ا ِوؼضءهض ا ِو‬..” ُ ُ َ “….. ‫َاأهف َؼنم‬ „…..Basi waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake wetu na wanawake wenu na nafsi zetu na nafsi zenu...‟11 Mtume  aliwaita Ali, Fatuma, Hasan na Husein, akasema: Ewe Mwenyezi Mungu! Hawa ni watu wa karibu wa nyumbani kwangu.”12 Amesema: Ibn Abi Najiih amesema: Pindi alipohiji Muawiya alitufu Kaaba akiwa pamoja na Sa‟ad, na alipomaliza akaenda kwenye sehemu ya mikutano na akamkalisha juu ya kitanda chake, basi Muawiya akamuona Ali na akaanza kumtukana. Sa‟ad akajisogeza kisha akasema: Umenikalisha pamoja nawe juu ya kitanda chako kisha umeanza kumtukana Ali! Naapa kwa Mwenyezi Mungu mimi nikiwa na jambo moja miongoni mwa mambo ambayo anayo 11 12

Sura 3 aya 61. Sahihi Muslim: 1198, kitabu Fadhila za masahaba, mlango miongoni mwa fadhila za Ali bin Abi Twalib 1614, Daarul-Fikri Beirut mwaka 1424H.

32

, hadithi


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

Ali ni bora kwangu kuliko chochote ambacho kimechomokezewa jua. Hadi mwisho wa hadithi, na ndani yake ipo kauli ya Sa‟ad: “Naapa kwa Mwenyezi Mungu sintaingia nyumbani kwako siku zangu zilizobakia.” Na akainuka.13 Hakika Muawiya alibadilisha ukhalifa mwema hadi kuwa ufalme wa kimabavu, na akachukua baia kwa ajili ya mwanawe Yazid kwa karaha kutoka kwa watu wa Hulli na Aqud chini ya vitisho na kuwatamanisha watu kupenda anasa, starehe na matamanio. Na hakika alihiji katika mwaka wa 50 A.H. na akafanya Umra katika mwezi wa Rajabu mwaka 56 A.H, na lengo la safari lilikuwa ni kuchukua baia kutoka kwa Muhajirina na Answari kwa ajili ya mwanawe Yazid. Na hakika yalikuwa maneno baina yake na watu watukufu na wenye fadhila kutoka katika vizazi viwili, maneno atakayoyafahamu yule atakayesoma historia. Wala hatutaji chochote kutokana na hayo, kwani hayo ni katika yanayohusiana na jamii, na hakika anayatambua hayo kiziwi, bubu mpaka watu wa Magharibi!! Sayyid Muhammad Rashid Ridha katika kitabu chake Al-Manaar amesema: Alisema mmoja wa wakubwa 13

Muruuj Dhahab, Juz. 3, uk. 24 na Bidaayat wa Nihayat Juz. 8, uk. 83 matukio ya mwaka 55H.

33


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

miongoni mwa wanazuoni wa Ujerumani, katika baadhi ya miji ya Waislamu, na mbele yake wakiwepo viongozi wa Makkah: “Hakika inatupasa sisi kuweka sanamu la dhahabu la Muawiya bin Abi Sufyan katika uwanja huu katika mji wetu mkuu (Berlin).” Ikaulizwa: Kwa nini? Akasema: “Kwa sababu yeye ni yule ambaye amebadilisha nidhamu ya hukumu ya Kiislamu kutoka katika kanuni yake ya kidemokrasia hadi kuwa utawala wa mabavu. Na kama isingekuwa hivyo basi Uislamu ungeenea ulimwengu mzima, na sisi Wajerumani na wananchi wengine wa Ulaya, tungekuwa Waarabu Waislamu.”14 Je, yeye si ndio yule aliyewaua watu wasiokuwa na hatia miongoni mwa Maswahaba wa Mtume  na wengineo mfano wa Hujr bin Uday na masahaba wake, Amru bin Al-Humq Khuzai, Sharik bin Shidad Hadhrami na wengineo. Na hakika masahaba wake walikuwa: “wenye nyoyo imara mbele ya makafiri na wenye kuhurumiana wao kwa wao.”15 Na wao hawakuwa na dhambi yoyote ile isipokuwa hakika wao walikuwa ni miongoni mwa masahaba wa Ali  na wale wampendaye. Na katika lengo hilo akaandika barua Imam mtoharifu, mkataaji na muonewa, Imam Husein bin Ali Bwana wa mashahidi hadi kwa Muawiya, akasema: 14 15

Tafsir Manaar, Juz. 11, uk. 260. Sura 48 aya 29.

34


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

“Je, wewe si ndiye muuaji wa Hujru na masahaba wake wafanya ibada wenye kukereka, ambao walikuwa wanachukizwa na bidaa, wakiamrisha mema na wakikataza maovu?! Basi ukawaua kwa dhuluma na uadui baada ya kuwapa wao ahadi nzito zenye kutilia mkazo. Na huo ni ujasiri dhidi ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) na kuidharua ahadi Yake. “Au si wewe ndiye uliyemuua Amru bin Humqi ambaye uso wake ulikwisha kwa ibada, basi ukamuua baada ya kumpatia ahadi kemkemu ambazo lau ungelifahamu kuziheshimu basi ungeteremka kutoka vilele vya milima? “Au si wewe ndiye uliyemuua Hadhrami ambaye Ziyad alikuandikia kumhusu yeye: „Hakika yeye yuko katika dini ya Ali, Mwenyezi Mungu ameutukuza uso wake.‟ Na dini ya Ali nayo ni dini ya mtoto wa baba yake mdogo , ambaye amekufanya umekaa hapo ulipokaa. Na kama si yeye basi utukufu wako na utukufu wa baba zako ungekuwa ni tu kuvamia misafara miwili: Msafara wa vuli na kiangazi. Basi akawaondolea hayo Mwenyezi Mungu kupitia kwetu sisi, fadhila yake juu yenu.”16 Ndiyo amesimama zaidi ya mmoja miongoni mwa wale walioghafilika, wakahalalisha matendo yake 16

Imamat wa Siyasat, Juz. 1, uk. 160 na Jamhurat khutwab Arab, Juz. 2, uk. 255, na. 246.

35


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

kwa kutumia Ijitihadi, mpaka wakathibitisha kwake malipo, wenye kutegemea kauli maarufu isemayo: Yule anayepatia kufanya ijitihadi ana malipo mara mbili. Na yule anayekosea ana ujira mara moja. Na hakika limempita yeye hili kwamba lau itasihi basi ni ile ijitihadi inayochegemezewa juu ya Kitabu na Sunnah, ambayo ni alama ya kubakia dini na siri ya kudumu kwake, na sio ijitihadi katika kupingana na dalili za kisheria. Ni ajabu iliyoje, aandikiwe malipo yule anayeanzisha utaratibu wa kumtukana Ali  kipenzi cha Mtume , na ndugu yake ambaye alikuwa sanjari naye tangu udogoni mwake hadi Bwana Mtume  alipofariki?! Na mshairi mbunifu, Ustadh Muhammad Majdhuub, amesema katika kaswida yake: “Ziko wapi ikulu za baba wa Yazid na starehe zake – na majingambo yake, kujiona na utukufu. Ziko wapi rai nzuri, zimechinja utukufu wake – lawama za dunia zisizokwisha usiku wa manane. Imemng’oa yeye dunia basi umefaulu kwa kuipata – kisha ikakunjuka kama vile upole sehemu hiyo. 36


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

Huku ni kusema kwako kwa wazi lau ungeliona taabu yake – basi yangelichuruzika machozi yako kwa mafikio mabaya. Mkusanyiko kutokana na mchanga usio thamani wenye kuharibika – ulevi na nzi kwawo akawa anafanya ghasia na fujo. Hadi sehemu ya kuswalia yenye giza kama kwamba yeye – tangu alivyokuwa hakuruka mipaka kwa makusudi. Hayakuwa madhara yako lau ungeliepukana na malengo yake na ukapita njia ya haki ya mwenye kuipita. Na ukajilazimisha kuwa katika kivuli cha baba wa mchanga, naye ni yule – katika kivuli chake unatarajiwa mwelekeo wa sawa ambao ndiyo unaotakiwa.” Na huenda katika maneno haya mafupi ambayo ni sehemu ndogo kutokana na sehemu kubwa, na ni uchache kutokana na wingi, kutakuwa na ukumbusho kwa Ustadhi. Na mwendelee kuwa wenye kuwezeshwa.

37


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

FASLU YA TATU KUMUOZA BIKRA NA USIMAMIZI WA BABA17 Tumesoma katika jarida la Shariah18 lipendezalo, toleo la 474, mfunguo saba mwaka 1426 A.H. jibu la mwanachuoni wa fikihi wa zama hizi Yusuf Qardhawi, kuhusiana na swali lifuatalo: Je, ni sahihi kwamba Imam Shafii amejaalia miongoni mwa haki za baba ni amuoze binti yake baleghe bila ya ridhaa yake? Na ikiwa hivyo ni sahihi je, hili linaafikiana na mfumo wa Kiislamu wa jumla katika kushurutisha makubaliano ya msichana aliyefikia umri wa kuolewa? Na lililopatikana katika yale aliyoyajibu mheshimiwa ni: Mosi: Hakika hapa ipo kanuni ya msingi ambayo hawatofautiani kwayo wawili, nayo ni kwamba kila mfanya ijitihadi anapatia na anakosea. Na kila mmoja maneno yake huchukuliwa na huachwa, isipokuwa 17

Makala hayo yaliandikwa tarehe 2 mfunguo nane mwaka 1426A.H. 18 Jarida la (Sharia) linalotolewa Jordan, mwasisi wake ni marhum Taysiir Dhabyan na mhariri wake mkuu ni Bisaam Dhabyan.

38


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

maasumu, na Imam Shafi ni kiumbe ambaye sio maasumu. Pili: Miongoni mwa insafu na uungwana kwa wafanya ijitihadi ni tuweke rai zao katika upande wa historia, kwani hakika mfanya ijitihadi anajua zaidi mazingira yake na zama zake. Wala haiwezekani kughafilika na kiungo cha dhati ya mfanya ijitihadi. Na hakika Imam Shaafii aliishi katika zama ambazo, ilikuwa ni nadra sana msichana kujua lolote kuhusu yule anayejitokeza kumchumbia, isipokuwa yale wanayoyajua familia yake. Kwa hivyo alipewa mzazi wake wa kiume haki mahsusi ya kumuoza yeye na hata kama sio kwa kuomba ruhusu na idhini kutoka kwake.” Kisha akasema: “Na ni nani anajua, huenda Imam Shafii lau angeliishi mpaka zama hizi na akaona kiwango alichofikia msichana katika maarifa na elimu, na kwamba hakika yeye amekuwa ni mwenye uwezo wa kuchanganua baina ya wanaume ambao wanajitokeza kumchumbia yeye, basi huenda angelibadilisha rai yake.” Kulingana na kauli iliyo mashuhuri: “Uhakika ni zao la utafiti” sisi tunao mjadala kuhusiana na jibu hilo. Tunaliweka hilo juu ya meza ya utafiti, na huenda Ustadh akawa na jibu kuhusiana na hilo. 39


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

MJADALA WA KWANZA: Hakika ujumbe wa Uislamu ni ujumbe wa kudumu, na Kitabu chake Qur‟ani tukufu ni kitabu cha mwisho, hapana budi sharia hii iwe inaafikiana na maumbile ya binadamu na kuambatana na tamaduni zote katika zama tofauti. Na hakika maneno ya wanazuoni wa fikihi yametofautiana katika ulazima wa kuomba ruhusu na idhini, na kutokuomba. Malik, Shaafii na Ibn Abi Layla wamesema: “Ni baba tu ndiye anayemlazimisha yeye kuolewa.” Abu Hanifa, Thawri, Awzaai, Abu Thawri na wengineo wamesema: “Hapana budi kuizingatia ridhaa yake.” Na amewafikiana nao Malik kuhusiana na bikira, katika moja kati ya kauli mbili zilizotoka kwake.19 Hapana budi kuchanganua rai aliyopatia, yule atakayepima suala juu ya Kitabu na Sunnah, basi Sunnah iliyopokewa inaunga mkono rai ya pili. Na hakika Ustadh ameashiria hadithi hizi katikati ya jibu lake. Imepokewa kutoka kwa Abu Huraira kwamba, hakika Mtume  alisema: “Haozwi kijakazi mpaka ajulishwe, na haozwi bikira mpaka aombwe idhini.” 19

Bidayatul-Mujtahid, Juz. 2, uk. 5 kitabu Nikah.

40


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

Wakasema: Ewe Mtume : Ipi idhini yake? Akasema: “Akinyamaza.” Na amepokea Abu Daud na Ibn Majah kutoka kwa Ibn Abbas, amesema: “Hakika kijakazi bikira alikuja kwa Mtume  akasema kwamba baba yake amemuoza naye anachukia. Basi Mtume  akampa hiari yeye.”20 Na hadithi zilizopokewa kutoka kwa Maimamu wa Ahlul-Bayt  zinaunga mkono kauli ya pili. Amepokea Mansur bin Hazim kutoka kwa Imam Swadiq  kwamba alisema: “Bikira na asiyekuwa bikra huulizwa, wala haozwi isipokuwa kwa ridhaa yake.”21 Na hadithi zinginezo zisizokuwa hizo zilizopokewa kutoka kwa Maimamu wa Ahlul-Bayt  ambazo zinatilia mkazo sharti la kupata idhini ya mwanamke katika kuolewa kwake. Ninaongezea katika hilo: Hakika ndoa ni suala la kwanza la kuanzisha jamii kubwa, je, inafaa katika mantiki na akili tImamu baba awe na haki ya 20

Angalia kitabu Khilafu cha Tuusi, kitabu Nikah, suala la 10, Bidayat Mujtahid, Juz. 2, uk. 5, mlango Nikah na Al-Mughni Juz. 6, uk. 516 cha Ibn Quddamat. 21 Wasaail-Shi’ah, Juz. 14 mlango 9 miongoni mwa milango ya ufungaji wa ndoa, hadithi na. 1.

41


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

kumuoza binti yake bila ya idhini yake? Tukiliangalia hilo kwa jicho la mazingatio, hakika ndoa sio jambo la muda mfupi, bali huenda ikadumu hadi miaka hamsini au zaidi. Basi iwezekane vipi kufikiria kumlazimisha yeye katika maisha haya bila yeye mwenyewe kujua, kufikiria au kupata idhini yake?! Hakika uuzaji ni moja ya kuanzisha mahusiano baina ya vitu viwili; bidhaa na mali, na ndoa ni uanzishaji wa mahusiano baina ya nafsi mbili. Naapa kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) inashurutishwa ridhaa katika kusihi biashara, Mwenyezei Mungu (s.w.t) anasema:

َ ّ ٰ َ ُ ُ َٰ َ ُ َ ‫مولنم َب َيىنم ِبضلبـ ِط ِل ِإال أن َجنون‬ ‫… ال جأملوا أ‬..” ُ َ َ ًَٰ “….. ‫طاض ِمىنم‬ ٍ ‫ِججـطة عً ج‬ “…..Msiliane mali zenu baina yenu kwa batili ila itakapokuwa ni biashara kwa kuridhiana baina yenu..”22 Je, inafaa katika mantiki ya akili kusihi biashara kwa kuwepo maridhiano na kuacha suala la ndoa?! Na je, kuuza na biashara ni jambo kubwa na nyeti zaidi kuliko suala la ndoa ambayo juu yake inasimama jamii? Yote hayo yanajulisha juu ya kutosihi yale aliyoyasema mshairi na akayakubali Malik. 22

Suratin-Nisa; 4:29.

42


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

Huo ni upande wa kifikihi, wala hatutaki kurefusha mada. Hakika tumefafanua na kusema kwa marefu na mapana katika kitabu chetu kinachoitwa “Nidhamu ya ndoa katika sharia ya Kiislamu tukufu”.23 MJADALA WA PILI: Lau tutajaalia hakika hukumu ya Kiislamu katika haki ya msichana ni kufaa kumuoza bila idhini yake, na inafaa baba kumlazimisha yeye kuolewa, hata kama hayuko radhi, kama ilivyo fatwa ya Imam Shafiy na Imam Malik katika moja ya kauli zake mbili. Na kama itakuwa sharia imefanywa katika hali hii, basi vipi iwezekane kuibadilisha hukumu yake kwa kubadilika mazingira, pamoja na kuwa halali ya Muhammad ni halali hadi Siku ya Kiyama, na haramu yake ni haramu hadi Siku ya Kiyama? Na lile ambalo Ustadh amelinya kuwa ni udhuru, kwamba wasichana wa zama hizi ni wenye maarifa na elimu pana kinyume na msichana aliyeishi katika zama za Imam Shaafi, hilo halikubaliki, kwani hiyo itamaanisha kwamba, hakika utungaji sharia ya Kiislamu ni maudhui kwa ajili ya wale wanawake wasiokuwa na maarifa na wasiojua, wala haiwahusu wale wenye maarifa na walioelimika. 23

Angalia: Nidhamu Nikah fi sharia’t Islamiya Gharrai, Juz. 1, uk. 172-193.

43


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

Tukubali kwamba hakika Ustadh amefanikiwa katika kuifanya fatwa yake iwe na mashiko, basi vipi anafasiri rai nyingine ya Imam Shafii kuhusiana na kumgusa mwanamke ajinabi, ambapo amelihesabu hilo kuwa ni miongoni mwa vitenguzi vya wudhuu? Ni juu yako kuisoma mwenyewe fatwa husika. Shafii amesema: “Pindi akimgusa mwanaume mwenye wudhuu, mwanamke ajinabi bila ya kuwepo kizuizi, basi wudhuu wake unatenguka.” Na kwa ibara nyingine: Kugusana kwa ngozi na wanawake pasi na kizuizi wakiwa si mahramu kunaharibu wudhuu ikiwa kwa matamanio au bila matamanio, kwa mkono au kwa mguu. Au visivyokuwa hivyo viwili miongoni mwa viungo vya mwili, akiwa mwenye kukusudia au mwenye kusahau.24 Na linalojulikana ni kwamba rai hii ni ngeni kwa mitazamo miwili: Haina msingi wowote ule katika Kitabu na Sunnah, basi kauli yake (s.w.t) katika aya ya wudhuu inayosema: “Au mkiwagusa wanawake”25 ni kinaya ya kufanya tendo la ndoa, kama ilivyo hali katika aya za talaka. Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema: 24

Al-Ummu, Juz. 1, uk. 15, Mabsuut Juz. 1, uk. 67, AhkamulQur’ani, Juz. 2, uk. 369 cha Jaswas, na rejea zingine. 25 Sura 5 aya 6.

44


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

َ َ

ُ َ​َ

ّ

ُ ‫ؼضء مض لم ج َم ّؼ‬ َ ‫… إن طللخ ُم الي‬..” “….. ًَ ‫وه‬ ِ ِ “Kama mkiwapa talaka ambao hamjawagusa…..”26 Na akasema:

َ َ

ُ َ​َ

َ

ُ ‫موه ًَ مً بل أن ج َم ّؼ‬ ُ ‫” َاإن طللخ‬ “…..ًَ ‫وه‬ ِ ِ ِ “Na kama mkiwapa talaka kabla ya kuwagusa …..”27 1. Hakika fatwa hizi haziendani na utukufu wa mwanamke na daraja lake katika sharia ya Kiislamu, namna ambayo hakika aya za Mwenyezi Mungu (s.w.t) zimesifu na kueleza kuwa mwanamke ni mwenza wa mume na kwamba yeye anapata utulivu kwake. Mwenyezi Mungu (s.w.t) amesema:

َ

ُ َ

َ ُ

ُ َ

َُ َ َ​َ

ٰ ‫… دلق لنم مً أهفؼنم أ‬..” “….. ‫ظا ًجض ِلدؼنىوا ِإليهض‬ ِ ِ “…..Ni kuwaumbia wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao…..”28 Hakika sharia ya Kiislamu inategemewa katika misingi yake ya kijumla juu ya maumbile ya mwanadamu 26 27 28

Sura 2 aya 236. Sura 2 aya 237. Sura 30 aya 21.

45


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

wala haibadiliki hukmu yake kwa kubadilika zama na sehemu. Basi maadamu mwanadamu yupo juu ya ardhi hii, basi hukumu ya kisharia inarandana na maumbile yake wala haitoki katika hukumu hiyo hata kwa ukubwa wa unywele mmoja. Kwa hivyo hapana budi iwe ni yenye kuendelea daima na milele. Ndiyo, hakika imethibiti katika mahali pake hakika moja ya viungo vya kufutu masâ€&#x;ala ni zama na sehemu, ambacho kinahusiana katika kufutu masâ€&#x;ala na kufanya ijitihadi. Lakini hilo halimaanishi kufutwa hukumu na kuzitoa kutoka katika uwanja wake, na kuhalalisha hukumu nyingine mahali pake kwa ajili ya viungo hivyo viwili. Bali kwa maana ya ustaarabu na maendeleo huenda vikaathiri katika maudhui ya utoaji wake kutoka katika maudhui ya hukumu na kuingiza hiyo chini ya anuani katika maudhui ya hukumu nyingine, pamoja na kuhifadhi juu ya hukumu zote mbili katika sehemu zake. Na hebu acha tulete mifano: Hakika uuzaji wa damu ni haramu katika fikihi ya Kiislamu kwa kukosekana manufaa kwayo katika jambo la halali, na kama yapo manufaa huenda yakawa yamehusika tu katika ulaji. Lakini maendeleo ya elimu yamemwezesha daktari kunufaika na damu kwa njia ya halali, na hiyo ni katika mchakato wa uhamishaji wa damu kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine mhitaji hospitalini. 46


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

MJADALA WA TATU: Hakika kauli ya Ustadh kwamba Imam Shafii lau angeliishi mpaka zama hizi na akaona kiwango alichofikia msichana katika maarifa na elimu na maendeleo, huenda yeye angelibadilisha rai yake, hakika hili linasukuma katika kusallmu amri na kukubali dharura ya kurejea kwa mujtahidi aliye hai katika masuala yote. Na hiyo ni kwa sababu ya nukta ile ile aliyoitaja Ustadh, kwani wanazuoni wa sharia ya Kiislamu pamoja na kukiri kwao kwamba wao ni bendera za uongofu, hakuna tofauti baina ya yule aliyefariki miongoni mwao na yule aliye hai ambaye bado anaruzukiwa. Lakini mujtahidi hai ni mjuzi zaidi wa mazingira husika na hali za kijamii, na ni sawa na kauli ya msemaji: “Shuhuda huona yale ambayo hayaoni asiyekuwapo.� Basi yeye anajua muktadha wa zama na mahali, katika hali ambayo mwanachuoni wa sharia aliyefariki akirudi na kuwa hai hivi sasa, huenda akabadilisha rai yake na kufutu kinyume na alivyofutu hapo kabla. Na hili ndilo linawasukuma wanazuoni wa sharia kukokoteza kumfuata mujtahidi hai au kamati ya wanazuoni wa sharia ambayo inatengenezwa na walio hai na kuacha kuwafuata wasiokuwa hai. Ndiyo, maoni haya huenda yakawa ni mzigo mzito kwa yule aliyezoea kumfuata asiyekuwa hai. Lakini 47


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

hiyo inaambatana na maumbile ya binadamu ambayo yamejengewa juu yake, imesimama dini ya Kiislamu juu yake, na sio jambo la mbali kuhusiana na uhai wa wanadamu. Hakika jamii katika haja zake hurejea kwa madaktari na wahandisi walio hai, hakika wao wanajua zaidi haja za zama hizi kwa ugonjwa na dawa. Zaidi ya hapa ni kwamba, hakuna dalili iliyojulisha kwamba madhehebu za kifikihi zinakomea katika madhehebu nne tu. Na Waislamu walikuwa wakiitendea kazi sharia kabla hata hajazaliwa Imam yeyote yule miongoni mwa Maimamu wanne. Na wala haikuthibiti kwamba wao ni wasomi zaidi na wa bora zaidi kuliko yule aliyekuja baada yao au aliyekuwa katika zama zao miongoni mwa wanazuoni wakubwa wa sharia ď “, hata kama pia haijathibiti kinyume na hivyo. Hakika vipawa vya Mola Manani (s.w.t) ni vipana ambavyo havihusiani na kizazi kimoja na wakati fulani. Hakika fikihi imekamilika kwa mkono wa wale wapenzi wa fikihi katika kila zama, mpaka huenda ikawa wale waliokuja zama zilizokuja baadaye ni wenye kuona mbali zaidi na wako makini zaidi kuliko wale waliotangulia. Hakuna shaka kwamba hakika kufutu masâ€&#x;ala kwa jamaa au kikundi kuna uaminifu na ukweli zaidi 48


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

kuliko kufutu kwa mtu mmoja peke yake. Na mimi ninashauri juu ya wanazuoni wa sharia wa madhehebu mbalimbali katika kila nchi, watengeneze jumuiya ya wanazuoni wa sharia huru itakayojumuisha ndani yake wanazuoni wakubwa kutoka katika miji mbalimbali. Basi kamati hiyo inakuwa ndiyo rejea katika masuala yenye ikhtilafu, yawe ya kale au ya sasa. Na kwa maelezo mengine: Wapitie upya masuala yote yenye ikhtilafu, na watakapotoa fatwa wote, yaani wengi wao, basi hiyo inawajumuisha watu wote, sawa inaafikiana na madhehebu moja kati ya hizo nne au hapana. Hakika mgando juu ya fatwa ya Imam mahsusi, huenda ikawaingiza watoa hoja kwenye matatizo makubwa. Hakika baadhi ya madhehebu: Yanafaradhisha kutupa mawe Minaa siku ya kumi kuanzia wakati wa kuchomoza kwa jua hadi linapopinduka, wala haifai baada ya adhuhuri. Tofauti na siku mbili zitakazofuata, katika siku hizo haifai na hairuhusiwi asubuhi, bali inafaradhishwa utupaji uwe baada ya adhuhuri. Hakika ubanaji huu katika wakati wa utupaji mawe unasababisha uzito mkubwa juu ya mahujaji, na unapelekea kuuawa makumi kadhaa miongoni mwao, kwa kitendo cha kusongamana. Pamoja na hivyo katika baadhi ya madhehebu ipo ruhusa pana zaidi 49


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

ambapo inafaa kurusha mawe kuanzia kuchomoza kwa jua hadi kuzama kwake. Haya ni maoni, lakini vipingamizi huenda vikabadilisha kati ya mtu na mawazo yake. Sio kila kitu mtu anachokitamani anakipata….. Na amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yenu. FASLU YA NNE KUMWITA MTOTO KWA JINA ABDU MASIHI „MTUMWA WA MASIHI‟29 Tumesoma katika sehemu ya fatwa katika toleo la 479 kutoka katika jarida la Sharia la Jordan, maswali mbalimbali ambayo ameyajibu Sheikh na walimu mbalimbali (Mwenyezi Mungu aliyetukuka awahifadhi). Na miongoni mwa maswali hayo lipo swali linalofungamana na kufaa kumwita mtoto kwa jina Abdu Masihi “Mtumwa wa Masihi,” na hakika Sheikh Yusuf Qardhawi amejibu akisema: “Uitaji huu ni haramu, haramu, haramu. Ninamaanisha: Hakika uharamu wake umeongezeka mara tatu: Ya kwanza: Hakika kila jina lenye kumfanya mtu mja wa asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni haramu kujiita kwalo kwa ijimai ya Waislamu. 29

Makala haya yametolewa tarehe 16 mfunguo tatu mwaka 1426H.

50


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

Ninasema: Sisi tuna maelezo kuhusu sehemu ya kwanza ya jibu hili; maelezo ya kutanabaisha ili kuweza kuondoa utata unaochochewa kuhusu kufaa kutumia majina yaliyoenea baina ya Waislamu, kama vile Abdu Nabii au Abdu Rasuul na yasiyokuwa hayo. Na lau Sheikh angeliweka wazi maana ya Abdu katika mfano wa majina haya basi ijimai isingelidai juu ya uharamu wake, kwa sababu Abdu inakusudiwa kwa maana mbalimbali inayotofautiana hukumu yake kulingana na tofauti ya sehemu, na huu hapa ubainifu wake: 1. Abdu kwa maana ya Utumwa wa kimaumbile (uja), nao kwa maana hii unatokana na kumilikiwa kimaumbile ambako kunajumuisha mambo yote ya waja. Na chanzo cha umiliki ni kwa kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) ni muumbaji, na binadamu ni muumbwa. Basi utumwa ukiwa ni alama ya umilikiwa unaotokana na uumbwaji, basi huo hauongezwi ila kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) kama asemavyo Mola Manani:

َ ٰ َ ّ َ ‫الؼمٰـ ٰوث‬ َ ‫ُ ُّل‬ ًِ ‫الطحمـ‬ ‫ضض ِإال ءا ِحى‬ ‫ألا‬ ‫ا‬ ِ َ ِ ً‫ِإن مل م‬ ِ ً ‫َع‬ . ‫بسا‬

51


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

“Hakuna yeyote aliyemo mbinguni na ardhini ila atafika kwa Mwingi wa rehema kuwa ni mtumwa.”30 Anasema (s.w.t) akielezea maneno ya Masihi:

ٰ َ ُ َ ّ َ َ َ ٰ ‫النخـ َب َا َج َعلنى ه ِب ًيض‬ ِ ‫ضى ِإوى عبس الل ِـه ءاجى ِن َى‬ “Akasema: Hakika mimi ni mja wa Mwenyezi Mungu, amenipa Kitabu na amenifanya ni Nabii.”31 2. Abdu kwa maana ya Utumwa uliyowekwa, unaotokana na binadamu kumshinda mtu katika vita. Na hakika aliupitisha Mwenyezi Mungu mweka sharia, chini ya masharti maalum yaliyotajwa katika Fikihi. Basi akawaamrisha mateka – ambao wanaangukia mikononi mwa Waislamu – wakipelekwa kwa hakimu wa sharia, yeye atakuwa na hiari kati ya kuwaacha huru au kuwafanya watumwa. Ikiwa atalichagua jambo la tatu basi mateka atakuwa mtumwa wa Mwislamu, na kwa hivyo unaona hakika wanazuoni wa sharia wameweka mlango wenye jina la “Mtumwa na kijakazi.” Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema: 30 31

Sura 19 aya 93. Sura 19 aya 30.

52


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

َ ُ َ ّٰ َ ُ ٰ ٰ َ ‫بضزلم‬ ‫َاأ ِهن ُحوا ألايـ‬ ِ ‫مى ِمىنم االصـ ِلحين ِمً ِع‬ َ ُ َ َُ ُ ُ َ َُ َ ‫ضل ِه‬ ِ ‫ا ِإمض ِئنم ِإن ينوهوا فلطاء ي ِغن ِهم اللـه ِمً ف‬ َ َ ‫الل ُـه ٰاػ ٌعع َع ٌع‬ ‫ليم‬ ‫ا‬ ِ “Na waozeni wajane miongoni mwenu na wema katika watumwa wenu na wajakazi wenu. Wakiwa mafukara Mwenyezi Mungu atawatosheleza katika fadhila Zake, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa, Mwenye kujua.”32 Unakuta hakika (s.w.t) ananasibisha utumwa na ujakazi kwa wale ambao wanaowamiliki hao, anasema: “Watumwa wenu na wajakazi wenu” basi anaongeza utumwa kwa lisilokuwa jina Lake Tukufu. 3. Abdu kwa maana ya Utumwa wenye maana ya utiifu, na ni kwa maana hiyo watu wa vitabu vya lugha wamelitafsiri neno hilo.33 Na maana ya tatu, ndio inayokusudiwa na majina hayo, basi wanawaita watoto wao kwa jina la Abdul-Rasuul yaani mtiifu kwa Mtume, Abdul-Husein yaani mtiifu kwa Husein. Na kila Mwislamu ni mwenye kumtii Mtume  na Maimamu  baada yake. Hakuna shaka kwamba 32 33

Sura 24 aya 32. Lisanul-Arab: Mada ya Abdu (mtumwa), vivyo hivyo katika kamusi Muhiit katika mada hiyo hiyo.

53


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

inalazimu kumtii Mtume  na wale wenye mamlaka baada yake. Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema:

َ َ ‫”يٰـ َأ ُّلّي َهض َال‬ ُ ‫الل َـه َا َأ‬ ُ ‫ءامىوا َأ‬ َ ً‫صي‬ َ ‫طيعوا‬ ‫الطػو َى‬ ‫طيعوا‬ َ َُ ُ “…..‫مط ِمىنم‬ ِ ‫اأا ِل ألا‬ “Enyi mlioamini! Mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume na wenye mamlaka katika nyinyi.”34 Basi Qur‟ani imemweleza Mtume  kwamba ni mwenye kutiiwa na Waislamu, hakika wao ni wenye kumtii yeye. Wala hagombezwi mtu anapoidhihirisha maana hii kutokana na kuwaita watoto wake na dhati ya ini lake kwa majina haya matakatifu. Ndio, anayeitwa kwa jina la mtumwa wa Mtume, naye ni mtumwa wa Mtume, na katika wakati huo huo ni mja wa Mwenyezi Mungu pia. Wala hakuna msigano baina ya minasaba hiyo miwili, kama ulivyojua kuwa hakika utumwa katika aina ya kwanza ni utumwa wa kimaumbile unaotokana na uumbwaji. Lakini katika aina ya pili na ya tatu unatokana na umefanywa sharia na Mwenyezi Mungu (s.w.t), ambapo amejaalia aliyeshinda kuwa ni bwana na mateka kuwa ni mtumwa. Kama alivyofanya Nabii kuwa mtiiwa na mwingine ni mtumwa yaani mwenye kutii. 34

Sura 4 aya 59.

54


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

Na hivyo ni vitu viwili tofauti kati ya maana ya pili na maana ya kwanza. Wala simpati Mwislamu juu ya mgongo wa ardhi anamwita mwanawe jina la mtumwa wa Mtume kwa kukusudia kuwa yeye ni mja wa kimaumbile kwa Mtume. Na hakika anakusudia maana ya tatu, nayo ni kuwa kwake mwenye kumtii Mtume. Na zaidi ya hilo inasemwa inakusudiwa utumwa wa kiutukufu na uteremshaji kutokana na majazi na ufananishaji kwa utumwa uliyopo baina ya mabwana wanaojulikana na watumwa wao. FASLU YA TANO USAWA BAINA YA DIYA YA MWANAMKE NA DIYA YA MWANAUME35 Tumepitia toleo la 495 la mwezi wa tatu la mwaka 2007 la jarida la Shariah lenye kupendeza, na tumekuta ndani yake fatwa ya Sheikh Dr. Yusuf Qardhawi, ambayo imebeba kauli ya kwamba, diya ya mwanamke ni sawa na diya ya mwanaume. Na kwamba hukumu ya kuwa diya ya mwanamke ni nusu ya diya ya mwanaume haichegemezewi kwenye andiko la wazi la Qurâ€&#x;ani tukufu wala la Sunnah takatifu, kama ambavyo haiungwi mkono na ijimai wala Qiyas wala maslahi yenye kutegemewa. Na hakika rai yake ya kuwepo usawa baina ya diya mbili 35

Limehaririwa na kuchapishwa tarehe 17 mfunguo saba mwaka 1428H.

55


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

inaungwa mkono na rai za wanazuoni waliotangulia, miongoni mwao ni mtunzi wa kitabu Al-Manar na Sheikh Mahmuud Shaltuut na Sheikh Abu Zahra na Sheikh Muhammad Ghazali. Kisha hakika alitoa udhuru wa kwenda kinyume na fatwa za wanazuoni wa karne ya saba waliosema diya ni nusu, akadai kwamba, ni kwa sababu katika zama zilizopita kumuua mwanamke kimakosa au kwa namna inayofanana na kukusudia, ilikuwa ni nadra. Hivyo basi hakukuonekana kuwa ni tatizo kuhusiana na maudhui hata ipelekee kufanyiwa ijitihadi mpya kutoka kwa wanazuoni. Ninasema: Sisi tunaweza kufanya ijitihadi huru iliyo nje ya mipaka ya madhehebu maalum. Hakika ijitihadi ni alama ya kudumu kwa Uislamu na kuendelea kwa Sharia. Lakini tunatilia mkazo juu ya ulazima wa kutegemea katika ijitihadi yetu huru, juu ya Kitabu na Sunnah toharifu na ijimai na vyanzo na misingi mingine yenye kutegemewa, na kutokutoka nje ya muktadha wake angalau kwa ukubwa wa unywele mmoja. Hakika kilichopelekea diya ya mwanamke Mwislamu aliye huru kuanza kuwa gumzo ni kwa sababu hali halisi ya zama za leo, ni hali ya upole na kuwahurumia wanawake, kwa kudhani kuwa hakika wao walikuwa wamenyimwa haki katika zama za kale. Hivyo taasisi na jumuiya mbalimbali zimesimama ili 56


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

kutetea haki zao, na kuwatoa wao kutoka katika utumwa wa wanaume, na kujikomboa na kuwa huru. Na huenda mtu akadhani kwamba kusema diya ya mwanamke ni nusu ya diya ya mwanaume ni kuvunja haki zake na ni unyanyasaji dhidi yake na ni kumtweza yeye. Pamoja na hayo yote, suala hili lina dalili yenye kukata shauri inayotokana na Sunnah toharifu na ijimai ya Waislamu, kwamba diya ya mwanamke ni nusu ya diya ya mwanamume. Wanazuoni wamekubaliana juu ya nusu diya: Ama ijimai hakika imeafiki maneno ya wanazuoni wa kisharia juu ya nusu diya katika kipindi chote cha karne kumi na nne, na hawakutofautiana nao isipokuwa watu wawili, kwa hivyo hauzingatiwi upingaji wao. Ibn Quddamat katika Sharhu yake amesema: “Ibn Mundhir na Ibn Abdul-Barri wamesema: Wamekusanyika watu wa elimu juu ya diya ya mwanamke kuwa ni nusu ya diya ya mwanaume. Na wameelezea wasiokuwa hao wawili, kutoka kwa Ibn Uliyyah na Aaswam kwamba hakika hao wawili wamesema: Diya yake (mwanamke) ni kama vile diya ya mwanaume kwa mujibu wa kauli ya Mtume  inayosema: „Katika nafsi ya muumini wa kike ni ngamia mia moja.‟ Na kauli hii ni ngeni (imetoka nje 57


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

ya kanuni), inatofautiana na ijimai ya Maswahaba na Sunnah ya Mtume , kwani imekuja katika kitabu cha Amru bin Hazim: „Diya ya mwanamke ni nusu ya diya ya mwanaume.‟ Nayo ni finyu zaidi kuliko ile walioitaja, na kauli zote mbili zipo katika kitabu kimoja. Basi inakuwa tuliyoyataja ni tafsiri ya yale waliyoyataja. Na diya ya wanawake kila watu wa dini ni nusu ya diya ya wanaume wao, kwa mujibu wa yale tuliyoyatanguliza katika sehemu yake.”36 Na Qurtubi (amekufa 595 A.H) amesema: “Wamekubaliana kwamba diya ya mwanamke ni nusu ya diya ya mwanaume na nafsi.”37 Na Shamsu-Dini Surkhusi (aliyekufa 495 A.H) amesema: “Imetufikia kutoka kwa Ali  kwamba yeye alisema: Diya ya mwanamke ni nusu ya diya ya mwanaume katika nafsi na kilicho chini ya nafsi. Yaani viungo na majeraha. Na ni kutoka kwake (Ali) tunachukua.”38 Na yule atakayerejea vitabu vya kifikihi atakuta mfano wa maneno hayo, wala hakuna haja ya kunakili maneno yao. Na ambalo tunaelekeza kwake, mtazamo wa Ustadh, ni kwamba hawajatofautiana na kauli hiyo katika zama zilizopita isipokuwa watu wawili: 36

Al-Mughni, Juz. 9, uk. 531-532. Bidayatul-Mujtahid, Juz. 2, uk. 426. 38 Al-Mabsuut, Juz. 26, uk. 79 kitabu Diyaat cha Shamsu Dini Surkhusi. 37

58


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

Mmoja wao: Ibn Uliyyah, naye ni Ismail bin Ibrahim Mansur (aliyezaliwa 110 A.H. na akafa 193A.H.) ambaye alikuwa akiishi katika mji wa Baghdad, na akapewa uongozi na madhalimu mwishoni mwa ukhalifa wa Rashid. Na inatosha katika kuanguka rai yake, kwamba hakika yeye alikuwa na tabia mbaya na mwenendo usiyofaa. Abdullah bin Mubarak aliandika beti za mashairi kwa ajili yake: “Ewe unayejifanya mwanadini, wakati ni mwewe – unayewinda mali za watu masikini.”39 Wa pili: Abu Bakri Aswamm Abdul-Rahman bin Kaysan Muutazili, mwandishi wa makala mbalimbali katika misingi ya sharia. Na Muutazila wanategemea juu ya akili zaidi kuliko yale ambayo wanayoyategemea katika nukuu na maandiko. Kwa hivyo hawaitwi hao kuwa ni Ahlus-Sunnah kwa mujibu wa istilahi ya watu wa hadithi na Ashairah. Na ni ijimai gani kubwa zaidi na yenye yakini zaidi kuliko maafikiano ya wanazuoni wa fikihi, juu ya hukumu iliyopita na kudumu kwa karne kadhaa bila yeyote miongoni mwa mafakihi kutamka kinyume chake, isipokuwa watu wawili. Na umeshajua hali za 39

Twabaqatul-Fuqahaai, Juz. 2, uk. 61.

59


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

hao wawili. Na la ajabu ni kwamba, hakika Dr. katika mwanzo wa maneno yake anasema: “Haiungwi mkono na ijimai wala Qiyasi wala maslahi yanayozingatiwa.” Tumesoma mwishoni mwa habari hiyo mchangiaji wa mada ameandika kwamba, hakika rai hii ya Dr. Qardhawi inatofautiana na rai za wanazuoni wa sharia na viongozi wa madhehebu manne mashuhuri: Madhehebu ya Dhahiriy, madhehebu ya Ja‟fariy na madhehebu ya Ibaadhi. Na huenda alijaribu kutaka kuupa umuhimu utafiti huu. Hili ndilo ambalo inawezekana kulitaja kuhusu ijimai, na ama kuhusu Sunnah ni kwamba: Mafuriko ya Sunnah juu ya nusu diya: 1. Ameeleza Bayhaqi kwa sanad mbili; moja ni dhaifu na nyingine si dhaifu, imepokewa kutoka kwa Maadhi bin Jabal kwamba amesema: Mtume  amesema: “Diya ya mwanamke ni nusu ya diya ya mwanaume.”40 2. Ameeleza Bayhaqi kwa sanad yake kutoka kwa Mak-hul na Atwai wamesema: Tuliwaona watu wakisema kwamba diya ya Mwislamu huru katika zama za Mtume  ilikuwa ni ngamia 100. Basi akaimarisha diya hiyo Umar bin Khatwab kwa watu wa kijijini kwa dinar 1000 au 12000 dirham. 40

Sunan Bayhaqi, Juz. 8, uk. 95.

60


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

Na diya ya Mwislamu mwanamke huru akiwa ni miongoni mwa watu wa kijijini ni dinar 500 au 6000 dirham. Basi akiwa aliyemtendea ni miongoni mwa mabedui basi diya yake ni ngamia 50. Na diya ya mwanamke bedui akitendewa na bedui mwenzake ni ngamia 50. Hakalifishwi mwanaume bedui kutoa dhahabu wala fedha ya makaratasi.41 3. Ameeleza Bayhaqi kutoka kwa Hammad kutoka kwa Ibrahim, kutoka kwa Ali bin Abi Twalib , hakika yeye amesema: Akili ya mwanamke ni nusu diya ya akili ya mwanaume katika nafsi na katika kilicho chini ya nafsi.42 Na makusudio ya Ibrahim ni Ibrahim Nakhai‟ (aliyekufa mwaka 93 A.H) naye hakumuona Ali bin Abi Twalib , na sanad yake ni yenye kukatika. 4. Ameeleza Nasaai na Daru Qutni, na akaisahihisha hiyo Ibn Khuzayma, kutoka kwa Nabii  kwamba amesema: “Akili ya mwanamke ni mfano wa akili ya mwanaume mpaka inafikia theluthi ya diya yake.”43 41 42

Sunan Bayhaqi, Juz. 8 Uk. 95. Sunan Bayhaqi, Juz. 8, uk. 95.

43

Taajul-Jaamiu Lil Usuul, Juz. 3, uk. 11, BulughulMaraami, namba 1212. 61


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

Nusu diya katika diya ya viungo: Hayo yote yalikuwa ni mazungumzo kuhusu diya ya nafsi, na sasa maneno yanahamia katika diya ya viungo na majeraha. Hakika wameafikiana wanazuoni wa fikihi kuwa diya ya mwanamke inalingana na diya ya mwanaume katika diya ndogo zenye kukadiriwa zisizo na kiwango maalumu, mpaka pale zitakapofikia na kuwa na kiwango maalumu. Itakapofikia hapo diya ya mwanamke itakuwa ni nusu ya diya ya mwanamume. Na kigezo hiki ni jambo lenye kuafikiwa, isipokuwa ni kwamba tofauti ipo katika kiwango maalumu ambacho iwapo diya hiyo itakifikia, itatakiwa diya ya mwanamke iwe nusu ya diya ya mwanameme. Na kigezo chenyewe kinatilia mkazo kanuni ya jumla katika diya ya mwanamke, kuwa ni nusu ya diya ya mwanaume. Na ikhtilafu na tofauti ni kuhusu kiwango maalumu ambacho iwapo diya hiyo itakifikia, itatakiwa diya ya mwanamke iwe nusu ya diya ya mwanameme. Na kauli iliyo mashuhuri ni kwamba mwanamke analingana na mwanaume katika diya ya viungo na majeraha, hadi theluthi ya diya. Na ikiwa itazidi theluthi itarejea kwenye nusu. Imepokewa kutoka kwa Amru bin Shuaâ€&#x;b kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake, kwamba hakika Mtume  amesema: 62


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

“Mwanamke analingana na mwanaume katika theluthi ya diya yake.” Na Rabi‟a amesema: Nikasema kumwambia Said bin Musayab: Ni ngapi katika kidole kimoja cha mwanamke? Akasema: Kumi. Nikasema: Katika vidole viwili? Akasema: Ishirini. Nikasema: Katika vidole vitatu? Akasema: Thelathini. Nikasema: Katika vidole vinne? Akasema: Ishirini. Nikamwambia: Pindi yanayomsibu yanapokuwa makubwa hupungua kiwango chake? Akasema: Hiyo ndiyo Sunnah. Kauli yake: “Hiyo ndiyo Sunnah” imejulisha kuwa anakusudia Sunnah ya Mtume , ijimai ya masahaba na taabiina.44 Na hakika ameeleza Bayhaqi kwa sanad inayoungana hadi kwa Zayd bin Thabit kwamba alisema: Majeraha ya wanaume na wanawake ni sawa katika theluthi, na yale yaliyozidi basi ni nusu.45 Kuna maslahi gani katika kufanywa nusu diya: Anasema Sheikh Qardhawi nusu diya haiungwi mkono na maslahi. Na huenda yeye anakusudia kwamba, kutofautisha baina ya diya mbili ni utofautishaji usio na sababu 44

Khilaaf, Juz. 5, uk. 254 – 256, mas-ala ya 63. Sunan Bayhaqi, Juz. 8, uk. 97, na angalia hadithi zingine zilizobakia katika rejea hiyo hiyo. 45

63


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

wala maslahi. Lakini yapo maslahi, tunaashiria hayo, nayo ni: Hakika hakuna shaka kwamba mchango na nafasi ya mwanamke Mwislamu katika jamii, ni sawa na mchango na nafasi ya mwanaume Mwislamu. Na wala diya yake (mwanamke) kuwa nusu ya diya ya mwanamume si dalili ya upungufu katika utukufu wake. Na hakika diya imewekwa ili kufidia madhara ya mali yanayopatikana juu ya familia kwa sababu ya kuua nafsi. Na linalojulikana ni kwamba madhara ya mali na matatizo ya kiuchumi ambayo yanaisibu familia kwa kumkosa mwanaume ni makubwa zaidi kuliko pale inapomkosa mwanamke. Na kwa hivyo ikawa diya ya mwanamke ni nusu ya diya ya mwanaume. Yote hayo ni kulingana na kawaida ya jamii ya Kiislamu ambayo imembebesha mwanaume majukumu ya kuongoza familia na kuisImamia. Na kuna mambo tata mbalimbali na shaka nyingi zilizoibuliwa kuhusiana na nusu diya. Tumeyaacha hayo ili kufupisha. Na mwisho tunamgeukia Ustadh na kumsihi aangalie maneno haya. Naye ikiwa amepata dalili mbalimbali za kisheria ambazo hazijatufikia sisi, na zinajulisha kwamba diya ya mwanamke ni sawa na diya ya mwanamume, basi na alete dalili na ushahidi wake. 64


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

FASLU YA SITA JIBU LA UTATA UNAOCHOCHEWA KUHUSIANA NA SHIA NA ITIKADI ZAO46 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu. Mheshimwa Sheikh Yusuf Qardhawi, zidumu baraka zako, amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yako. Ninamuomba Mwenyezi Mungu (s.w.t) akuhifadhi katika uimara wa tawhiid na ukaribishaji baina ya Waislamu. Na aufanye madhubuti mpango wenu wa kueneza maarifa ya Kiislamu ya haki katikati ya umma wa Kiislamu. Nimesoma ubainifu uliotoka kwenu, wa tarehe 13 mwezi wa Ramadhani mwaka 1429 A.H, inayosadifiana na tarehe 13 mwezi wa tisa mwaka 2008. Ambamo humo unajibu ndani yake yale yaliyosemwa na Shirika la Habari la Irani la Mehr (Mehr News Agency), na juu ya wasomi wawili wakubwa: Sayyid Muhammad Husein Fadhlullah na Sheikh Muhammad Ali Taskhiri ď “. 46

Imehaririwa na kuchapichwa barua hii tarehe 24 mwezi wa Ramadhani Mtukufu, mwaka 1429 A.H, na kusambazwa katika vyombo vya habari mbalimbali, na kisha nakala moja akapelekewa Sheikh Qardhawi.

65


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

Hakuna shaka hakika ubainifu uliotajwa umejumuisha mambo ambayo yanastahiki kusifiwa na kutambuliwa thamani yake, ambapo mmetaja kwa njia ya utoaji wa dalili kwamba Shia wako mbali na kauli ya upotoshwaji wa Qurâ€&#x;ani. Na msimamo wenu wenye kuunga mkono haki ya Iran katika kumiliki vinu vya nyukilia kwa matumizi na malengo ya amani. Hakika tumezoea kuwaona wanazuoni wetu wakubwa wakiangalia mambo kwa roho iliyo wazi na kutangaza msimamo kwa ushujaa. Na hili ndilo ambalo tumelishuhudia kwenu hapa, mkiwa mbali zaidi na uelemeaji wa kikundi na kuangalia tofauti mbalimbali za matapo, ambavyo vinazuia uonaji wa haki na kufikisha kwenye ufinyu. Hakuna shaka kwamba, ninyi ni miongoni mwa wanaume wenye kuleta ukaribu na kujituma katika kuhifadhi umoja wa umma. Na katika lengo hili ninyi mna makala na mihadhara mingi, na hili ni jambo wanalolijua watu wote. Na wala haiwezekani kutegemea kitu kingine kutoka kwenye heshima yenu isipokuwa kumfuata Sheikh wenu mkubwa marhumu Muhammad Shaltut, jambo ambalo linapelekea kuimarisha kamba ya kuleta ukaribu baina ya madhehebu. Hakuna shaka kwamba ikhtilafu baina ya Waislamu bado mizizi yake inaendelea kuwepo tangu wakati alipofariki Bwana Mtume  hadi hivi leo. Na tofauti hizi zitaendelea kuwepo hadi Siku ya Kiyama, wala 66


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

haiwezekani kuyatibu makovu hayo kwa siku moja au siku mbili au mwaka mmoja au miaka miwili. Na hakika lile ambalo tunalitegemea kutoka kwa watu wakubwa na shakhsia inayohukumu ni kuendelea juu ya maeneo ya ushirikiano na kutoangalia masuala yenye ikhtilafu. Na kuyawasilisha hayo yenye ikhtilafu katika mikutano na makongamano ya kielimu, mbali zaidi na makelele ya kisiasa, ili tuweze kuyazungushia duara finyu na lenye mipaka. Na hapa tunapenda kuwakumbusha kwa heshima yenu baadhi ya mambo ambayo ninayaona ni ya dharura na ya msingi: 1. Unajua mheshimiwa Sheikh, kama wanavyojua wanafikra, hakika watu wa Magharibi na Mayahudi wa ulimwenguni – kwa ajili ya lengo la kuwaweka mbali Waislamu na fikra ya Uislamu - kwa muda mrefu wamepaza juu kaulimbiu tatu, nazo ni: i. Uogopeshaji na uhadharishaji kuhusiana na Uislamu. ii. Uogopeshaji na uhadharishaji kuhusiana na Iran. iii. Uogopeshaji na uhadharishaji kuhusiana na Ushia. Na hakika vyombo vya habari vimefanya kazi kubwa kwa aina zake mbalimbali, kwa kila wawezalo na kwa kutumia nguvu na mbinu wanayoiweza, ili kugandisha hayo katika akili za walimwengu wa 67


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

kimagharibi, bali katika nchi zilizoimarika na kustawi kiuchumi. Na ukawa Uislamu ni jini mbaya ambaye anahatarisha na kutoa vitisho kwa watu na kuhatarisha amani ya ulimwengu!! Katika mazingira nyeti kama haya hatuoni kile kinachohalalisha kile ulichokifanya ewe Sheikh, kukutana na gazeti la Misri la kila siku, na kuzungumzia Ushia na uhubiri wa Ushia– kulingana na maelezo yenu – katika miji yenye Masuni wengi, na ukatahadharisha hilo na kuonya!! Ni matokeo gani ambayo anayapata msomaji hata ingelikuwa ni tofauti na mnavyokusudia? Je, matokeo anayotoka nayo msomaji ni uungaji mkono msimamo wa wenye kiburi na Uzayuni na kuyapa uhalali na usahihi yale yanayoenezwa na kufikishwa na vyombo vya habari vyenye sumu?!! 2. Hakika mheshimiwa Sheikh mmetilia mkazo kwa upande mmoja, kuwa ushia umezushwa, na kwa upande mwingine mmetilia mkazo kwamba kundi lililofaulu ni Ahlu Sunnah, nawe ni mwenye kuegemeza hilo katika hadithi maarufu ya Bwana Mtume  inayosema: “Umma wangu utagawanyika makundi sabini na tatu...” Na hapa tunakuuliza: ni matokeo gani yanayopatikana anayoyapata kijana mwenye taasubi miongoni mwa vijana wa Ahlu Sunnah? Je, sio msimamo huo unamfanya afunge 68


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

mkaja na kujiandaa kujilipua, ulipuaji ambao utagharimu idadi kubwa ya vijana, watoto wachanga na wanawake miongoni mwa waumini katika miji ya Iraq na mingineyo katika miji ya Kiislamu. Na hayo yanafanywa na vijana wengi wa Jordan, Saudia, Afghanistani na Morocco, wakitegemea fatwa yenu hii ya ukufurishaji na misImamo ya baadhi ya watu wenye kutegemewa katika ulimwengu wa elimu na fatwa. Mpaka jambo limefikia katika hali ya mtu mmoja ambaye ni Mjordan, amejilipua katikati ya waumini katika mji wa Hulla nchini Iraq, katika sherehe ya harusi ambayo maharusi walikuwa wakipongezwa na kupewa hongera kulingana na mnasba huo!!! Mheshimiwa Sheikh, kama wahenga walivyosema “Kila mahali kuna maneno yake,” je, katika mazingira haya ambayo umma wetu wa Kiislamu unapitia, ambapo nguvu zote za mabeberu wa ulimwengu zinaushambuliaa ulimwengu wote wa Kiislamu, unaona ni sawa yatoke kwa msomi na mwanafikra wa Kiislamu yale maneno ambayo yanachochea hasira na kuwasha moto wa chuki na ugomvi baina ya Waislamu, jambo ambalo, Mwenyezi Mungu aepushie mbali, linaweza kusababisha mapigano ya ndani?!!! Na ikiwa ndugu zetu Sayyid Fadhlullah na Sheikh Taskhiri – ambao unawafungamanisha hao na nyinyi 69


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

uhusiano wa upendo, na wao kuwa na hisia za kiupendo na heshima – hawaridhii njia mliyoitumia katika kuwasilisha suala hili, hakika ni kutokana na lile tulilolitaja, kwamba hilo halilingani na hadhi yenu na sio jambo zuri kwa Waislamu abadani. 3. Mmezingatia kitendo cha baadhi ya vijana wa Kisunni kutoka katika baadhi ya miji ambayo idadi kubwa ya wakazi wake ni Ahlu Sunnah, kuhamia katika madhehebu ya Shia, ni kutokana na mahubiri ya Ushia na ni hatari anayostahiki mtu kusimama dhidi yake. Na ukatoa onyo kali na kwamba hakika kukosekana upingaji dhidi ya uhubiri huo ni kwenda kinyume na dini na ni kuhini amana ambayo ipo shingoni mwenu. Lakini wakati huo huo mmeinamisha macho na kufumbia macho yale ambayo yanajiri huko Saudia na Falme za Kiarabu na sehemu nyingineyo katika miji ya Kisunni, ambapo kunafanywa mashambulizi makali na mabaya dhidi ya wanafikra wa Kishia na fikra ya Ushia. Haipiti saa isipokuwa utakuta uchapishaji wa kitabu, makala au barua wenye kuwashambulia wao. Na linalosikitisha ni kwamba yale yanayotolewa sio isipokuwa ni kurudufu tuhuma potofu zisizo na dalili wala hoja. Je, sio jambo linalofaa kwa heshima yenu kupinga mfano wa uvamizi na mashambulio kama hayo yenye upepo wa moto ambayo yanaelekezwa dhidi ya kundi kubwa la Waislamu!! 70


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

Bali tunakuta baadhi wamefikia kiwango cha juu katika upotovu na uongo kwa namna ambayo, wameandika vitabu katika kuwatusi Shia na kuvinasibisha vitabu hivyo na shakhsia za Kishia, kwa mfano marhumu Allamah Sayyid Askariy. Na baadhi wamevinasibisha na mimi mwenyewe, wakiwaonesha watu kwamba mimi ni mlinganiaji wa madhehebu ya uwahabi na ni mwenye kuushambulia Ushia!! Na mwisho kimechapishwa kitabu katika nchi yenu tukufu ya Misri kikikosoa mtazamo wangu katika upande wa sharia kuhusu suala la “swala ni bora kuliko usingizi.” Kitabu hicho kimejaa matusi na maneno machafu na uzushi… nacho kimeandikwa na Alau Dini Baswiri. Kisha kimechapishwa kitabu hiki mara ya pili katika mfululizo wa makala ya “Uchunguzi juu ya wahakiki wa Kishia” na wasambazaji wakakipa jina la “Ja‟far Subhani… si mhakiki mkurubishaji.” Na la kushangaza ni kwamba kitabu hiki kimetolewa na mwalimu miongoni mwa walimu wa chuo kikuu cha Azhar, naye ni Dr. Muhammad bin Abdul-Munuim Bariy, ambaye ni nguzo tegemezi ya masomo ya Kiislamu katika chuo kikuu cha Azhar, na Rais wa baraza la wanazuoni wa Azhar (kimechapishwa Misri na kusambazwa mwaka 2007, katika kituo cha Tanwiir cha Misri); sijui je, tafiti za kifikihi zinastahiki ubebaji wote huu na uoneshaji sura isiyopendeza na uangushaji?!! 71


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

4. Katika ubainifu wenu mmetilia mkazo juu ya hadithi inayosema: “Umma wangu utagawanyika makundi sabini na tatu.� Na hapa ninapenda kukumbusha kwamba, hadithi hii wahakiki katika elimu ya hadithi wameikuta ni dhaifu. Na hata tukijaalia uwepo wa sanad inayozingatiwa ya hadithi hii, bado haisihi kuitegemea hadithi ya mpokezi mmoja katika kuthibitisha msingi kama huu, na kuzingatia makundi sabini na mbili miongoni mwa makundi ya Waislamu kuwa ni watu wa motoni, na kuwahusisha watu wa peponi kuwa ni kundi moja tu. Hakika madhumuni ya hadithi yanafichua kutokusihi kwake, na mimi hapa sizungumzii kuhusiana na makundi ya Mayahudi na Manaswara, bali ninajiuliza yako wapi makundi ya msingi ya Waislamu yaliyofikia idadi hii? Na ama makundi ya matawi yaliyotajwa katika vitabu vya Milal wa Nihal hakika idadi yake ni zaidi ya hiyo bila shaka?! Na je, tunaweza kupata idadi hiyo ndani ya vitabu vya Milal wa Nihal? Na je, inawezekana kuzingatia tofauti katika mas-ala moja kuwa ni kigezo cha kuliona kundi moja ni kundi lenye kujitegemea? Hakika makundi ya Waislamu ya msingi hayapiti idadi ya vidole vya mkono mmoja. Na ni kuanzia hapa tunawaona watunzi wa vitabu vya Milal wa Nihal wakijihusisha na mambo yasiyo na msingi ili kuthibitisha idadi iliyotajwa ili iwe ni dalili juu ya uhalisia wa hadithi. 72


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

Hakika undugu wa kweli ni wategemeze itikadi zao katika hadithi ambayo ameipokea Bukhari ambapo amesema: Mtume  alisema: “Umma wangu wote utaingia peponi isipokuwa yule atakayekataa.” Wakauliza: Ni yupi atakayekataa? Akasema: “Yule anayenitii ataingia peponi na yule atakayeniasi hakika amekataa.” Hakika hadithi imeweka mpaka wa kigezo cha kuingia peponi na motoni, kwamba ni kumtii Bwana Mtume  na kumuasi yeye. Na linalojulikana ni kwamba hakika kuasi na kupituka mipaka kunasadiki katika hali ya kuwa binadamu hamiliki hoja na dalili yenye kuingia akilini juu ya amali yake. Na sio lenye kujificha kwenu na juu ya wanafikra kwamba, hakika Shia hutegemea katika masuala yenye ikhtilafu, dalili na hoja yenye kutosha, hata ikiwa hoja hiyo sio timilifi katika mtazamo wenu. Au sio kigezo katika uingiaji wa binadamu katika wigo wa imani, ni yale yaliyokuja katika hadithi ya Mtume  pale aliposema: “Uislamu umejengeka juu ya mambo matano; kushuhudia hakuna mungu apasaye kuabudiwa kwa haki ila Allah, Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, kusImamisha swala, kutoa zaka, kuhiji na kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani.” Wamepokea masheikh wawili. Kwa hivyo ikiwa misingi ya dini ni kumwamini Mwenyezi Mungu, Mtume Wake, vitabu Vyake, Mitume Wake, malaika Wake na Siku ya Mwisho, na 73


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

yale ambayo ndani yake kuna hesabu na yasiyokuwa hayo, basi Waislamu wote wenye Kitabu na Sunnah wanaingia chini ya kigezo hiki, na hakuna aina yoyote ile ya kuficha utukufu juu ya kundi na kuyatoa makundi mengine?! Na miongoni mwa yale aliyotakiwa kuyatekeleza Sheikh ni kumfuata Imam wa Ahlu Sunnah, Sheikh Ashiariy, ambapo ametunga kitabu kuhusiana na vikundi vya Kiislamu na akayaingiza yote chini ya anuani ya kitabu chake alichokiita: “Makalaatu Islamiyyina wa Ikhtilafu muswallina” basi akayapatia makundi yote rangi ya Uislamu na akajaalia tofauti zao katika matawi tu kwa ushahidi wa maneno yake: “Na ikhtilafu ya wenye kuswali.” Ahmad bin Zahir Surkhusi Ashiariy anasema: ““Pindi alipokaribia kufariki Sheikh Abu Hasan Ash‟ariy Daary huko Baghdad, aliniamrisha mimi kuwakusanya masahaba wake. Basi mimi nikawakusanya hao kwake, akasema: „Shuhudieni juu yangu simkufurishi yeyote miongoni mwa Waislamu kwa kufanya dhambi, kwa sababu mimi nimewaona hao wote wakiashiria kuwepo mwabudiwa mmoja. Na Uislamu unawashamili hao na kuwajumuisha.‟”47 Hakika mmeashiria katika ubainifu wenu kwamba Mashia wana bidaa mbili: 47

Al-Yaquut wal-Jawahir, uk. 58 cha Shaa‟rani.

74


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

Ya kwanza: Bidaa ya kinadharia. Ya pili: Bidaa ya kivitendo. Na ninapenda hapa kugusia uchambuzi wa bidaa kulingana na rai yenu: Mosi: Bidaa ya kinadharia: 1. Madai ya wosia kwa Amirul-Muuminina : Hakuna shaka kwamba hakika msingi wa Ushia na nguzo zake zinasimama juu ya itikadi ya uwepo wa uongozi wa kisharia, uongozi wa kisiasa, kifikra na kimatendo baada ya kufariki Bwana Mtume , nao ni miongoni mwa mambo ya kizazi kitoharifu, wa kwanza wao ni Amirul-Muuminina Ali . Na hakika wosia umethibiti kwake kwa mujibu wa hadithi mutawatiri lukuki na hapa ninatolea ishara baadhi yake: i. Pindi ilipoteremka kauli ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) inayosema:

َ َ​َ َ َ َ ‫شييج َو ألا َط ين‬ ‫َاأ ِهصض ع‬ “Na uwaonye jamaa zako walio karibu.”48 Mtume  aliwaita watu arobaini miongoni mwa Bani Hashim, akawaambia: 48

Sura 26 aya 214.

75


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

“Enyi wana wa Abdul-Mutwalib! Hakika mimi naapa kwa Mwenyezi Mungu simjui kijana wa kiarabu aliyekuja kwa kaumu yake na jambo bora zaidi kuliko lile ambalo nimewaletea nyinyi. Hakika nimekuja na heri ya dunia na akhera. Na ameniamrisha Mwenyezi Mungu nikuiteni kwalo, basi yupi kati yenu atakayenisaidia juu ya jambo hili, ili awe ndugu yangu, wasii wangu na khalifa wangu kwenu.” Akarudia maneno hayo mara tatu, na katika kila mara Ali alikuwa akisimama na akisema: “Mimi ewe Nabii wa Mwenyezi Mungu nitakuwa msaidizi wako.” Na katika mara ya tatu Mtume  aliuinua mkono wake juu pamoja na mkono wa Ali na akasema kwa haki yake mbele ya kadamnasi wakishuhudia: “Huyu Ali ni ndugu yangu, wasii wangu na khalifa wangu kwenu.” Na lau si kuchelea kurefusha ningelitaja rejea nyingi ambazo zimetaja hadithi hiyo, lakini ninatosheka kwa kusema: Hakika hadi mtu mfano wa Muhammad Husein Haykal amenukuu hadithi hii katika chapa ya kwanza katika kitabu chake “Hayatu Muhammad” na imefutwa katika chapa zilizofuata. ii. Hadithi isemayo: “Wewe kwangu mimi ni kama vile Haruna kwa Musa isipokuwa hakuna utume baada yangu.” Na linalojulikana ni kwamba kuvuliwa utume tu kunajulisha kuthibiti vyeo vyote ambavyo 76


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

alivyokuwa navyo Nabii Harun , mfano wa ukhalifa na uwaziri. iii. Hadithi isemayo: “Mfano wa Ahlul-Bayt wangu ni kama vile jahazi la Nuhu, yule aliyelipanda aliokoka na yule aliyeliacha aliangamia.” iv. Hadithi isemayo: “Yule ambaye mimi ni mtawalia wa mambo yake basi Ali ni mtawalia wa mambo yake. Ewe Mwenyezi Mungu mtawalishe yule atakayemtawalisha yeye na mfanye adui yule atayemfanyia adui yeye.” Na inatosha katika tawaturi ya hadithi kwamba iwe imenukuliwa na masahaba 120 na taabina 90, kama walivyonukuu wanazuoni 360 wa Kisunni. Pamoja na dalili zote hizo wanazozitegemea Shia, linalotegemewa kutoka kwenu kwa ukadiriaji wa chini zaidi ni kukubali udhuru wao katika msimamo wao na itikadi zao, na sio kuwasifu kwa bidaa, hasa hasa tutakapoangalia kiundani lile lililobainishwa na wanazuoni watukufu wa kifikihi wa Ahlu Sunnah kwa kauli: “Na yule mpatiaji ana ujira mara mbili na mkoseaji ana ujira mara moja.” Na hapa hapana budi Shia wastahiki thawabu na ujira na sio kuwasingizia kwa bidaa. Mmesema katika ubainifu wenu kwamba, hakika tofauti katika matawi ya dini na masuala ya amali na 77


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

hukumu za kiibada na miamala, hakuna uzito juu yake, na misingi ya dini inawajumuisha wote hapa, na tofauti zilizopo hapa baina yetu na Shia si kubwa zaidi kushinda zile zilizopo baina ya madhehebu za Kisunni. Na hapa ninapenda nikuulize swali; je, suala la uImamu na ukhalifa kwa Ahlu Sunnah ni miongoni mwa matawi au misingi ya dini? Hakika wamesisitiza wanazuoni wa Ashairah mfano wa Adhudu Diin Iyjiy katika kitabu Mawaqifu na mfafanuzi wa kitabu hicho Al-Miir Sayyid Shariif Jarjanii, na Saâ€&#x;d Diin Taftazani katika kitabu SharhulMaqaswid na wengineo kwamba: Hakika uImamu na ukhalifa ni miongoni mwa matawi kama vile kuamrisha mema na kukataza mabaya, kwani inalazimu juu ya Waislamu kueneza mema na kukataza mabaya. Na hili halipatikani isipokuwa katika kivuli cha serikali na uwezo wa kutekeleza hukumu, na hakika kitovu cha uwezo na uongozi ni Imam na khalifa ambaye inalazimu awepo katikati ya Waislamu. Na hili ni miongoni mwa mambo ambayo wanakubaliana kwayo Shia na Sunni, isipokuwa hakika tofauti inakuwapo katika kuainisha na kuweka mipaka ya khalifa na Imam ambapo zimeelezwa nadharia mbili: 78


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

Mosi: Uainishaji wa uImam unatimia kwa njia ya mashauriano kati ya Muhajirina na Answari. Pili: Uainishaji unatimia kwa utangazaji na usimikaji kutoka kwa Mtume . Hatupo hapa kutilia uzito nadharia moja dhidi ya nyingine, lakini swali ambalo linaulizwa hapa; vipi imekuwa nadharia moja kati hizo mbili imekubalika na kuanishwa, na nyingine kuelezwa kuwa ni bidaa?!! Na hali ni kwamba hakika nadharia ya kwanza haisImami isipokuwa juu ya sira yenye mapungufu ya makhaifa na sio zaidi ya hilo. Na ama nadharia ya pili inategemezewa dalili mbalimbali na nguvu ya hoja. Hakika maneno ya uungwana yanapelekea kuifanya nadharia ya pili kuwa nzito, na ukadiriaji wa chini zaidi ni kuziangalia hizo kwa uangaliaji mmoja, na sio kuangalia watu wa nadharia ya kwanza wao ni Ahlu Sunnah na wafuasi wa nadharia ya pili ni wazushi “Huo tena ni mgawanyo mbaya.”!! Na kumekwenda wapi kusameheana na kuishi maisha ya ushirikiano katika matawi ya dini?! Na linalofaa kusemwa ni kwamba, uhalalishaji wenu kuwasifu Shia kwa bidaa kulikuwa katika kukabiliana na yule anayesema hakika hao ni makafiri. Lakini kwa njia hiyo tatizo haliwezi kutatuliwa kamwe, bali ilikuwa ni wajibu juu yenu kumnusuru mdhulumiwa 79


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

na kumkinga yeye na tuhuma ya ukafiri na kutoka katika dini, na msiibadilishe tuhuma kwa tuhuma nyingine. Na hapa tunapenda kumuuliza Sheikh; lau hakika mtu atawatuhumu nyinyi kwa tuhuma hatari je, mtamruhusu yule anayewatetea nyinyi na kuwaondolea tuhuma hiyo aibadilishe tuhuma hiyo kidogo zaidi kuliko ya kwanza?!! 2. Elimu ya Maimamu  ya mambo ya ghaibu: Miongoni mwa mambo ambayo mliyoyazingatia kuwa ni dalili juu ya uzushi wa Shia ni kadhia ya “elimu ya ghaibu.” Hapa ninapenda kuashiria kwamba elimu ya ghaibu ipo ya aina mbili: Ya kwanza: Elimu ya ghaibu ya dhati isiyo na mipaka, nayo ni miongoni mwa mambo ambayo yanamhusu tu Mwenyezi Mungu (s.w.t). Mwenyezi Mungu (s.w.t) katika Kitabu Chake anasema:

َ َ ٰ​ٰ َ ُ َ َ َ َ َ َُ َ ‫يب ِإال الل ُـه‬ ‫ضض الغ‬ ِ ‫ل ال يعلم م ًَ ِ الؼمـو ِث األا‬ َ َ ُ َ ّ َ ُ َ َ ‫بعثون‬ ‫امض يشعطان أيضن ي‬ “Sema: Hapana katika mbingu na ardhi ajuae ghaibu isipokuwa Mwenyezi Mungu; wala wao hawajui lini watafufuliwa.”49 49

Sura 27 aya 65.

80


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

Ya pili: Elimu ya ghaibu ya kuchuma. Na aina hii ni yenye mipaka, kwa idhini ya Mungu mwabudiwa. Aina hii ya elimu ya ghaibu anaipata asiyekuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t). Hakika umekuja katika sura ya 12 uelezaji wa mambo ya ghaibu kwa ulimi wa Nabii Yakub na Yusuf ; na vivyo hivyo imekuja katika Qur‟ani tukufu hadithi kutokana na yule aliyeongozana na Musa  kwa kauli yake (s.w.t):

ً َ ُٰ َ ً َ َ َ​َ ‫ىسهض‬ ِ ‫فوجسا عبسا ِمً ِع‬ ِ ‫بضزهض ءاجيىـه َضحمت ِمً ِع‬ ٰ َ ّ َ ‫َا َعلمىـ ُه ِمً ل ُسهض ِع ًلمض‬ “Basi wakamkuta mja miongoni mwa waja Wetu, tuliyempa rehema kutoka Kwetu na tukamfunza elimu kutoka Kwetu.”50 Imepokewa kutoka kwa Amirul-Muuminina Ali  kwamba yeye alieleza baadhi ya mambo ya ghaibu. Mtu mmoja akamwambia: Ewe Amirul-Muuminina umepewa elimu ya ghaibu! Akasema: “Sio elimu ya ghaibu, hakika tumefundishwa na yule mwenye elimu.” Na kwa kuwa aina hii ya elimu ni yenye kikomo haiwi kwa maana ya kiistilahi elimu ya ghaibu, kwa 50

Surat al-Kahf; 18:65.

81


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

sababu makasudio hasa ya ghaibu ni kwamba hiyo haina mipaka na kikomo, nayo ni miongoni mwa yale mambo ambayo ni mahsusi tu ya Mwenyezi Mungu (s.w.t). Mpaka hapa ikiwa Maimamu wa Ahlul-Bayt ď ‡ wanajua mambo ya ghaibu na kueleza mambo ya ghaibu, basi hii ni aina ya pili ambayo inapatikana kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (s.w.t). Na hii inapatikana hata kwa watu wema na wenye maarifa ya kweli ya Mwenyezi Mungu (s.w.t), ambao wamejituma na kufanya juhudi na jitihada kubwa katika umri wao mrefu, katika kumtii Mwenyezi Mungu (s.w.t) na kupita njia kulingana na sharia takatifu ya Kiislamu. 3. Umaasumu wa kizazi cha Mtume : Miongoni mwa mambo ambayo mmeyazingatia kuwa ni bidaa ni kauli ya kusema Maimamu ni maasumu; hapa tunasema: Umaasumu haumaanishi isipokuwa ni hali ya juu zaidi anayoipata mwanadamu ambayo inamzuia kutenda yale ambayo hayaridhii Mwenyezi Mungu (s.w.t), na kinakuwa mbele yake kitu kinachomkinga yeye kutenda madhambi. Je, ni ajabu binadamu kufikia daraja la ukamilifu wa kiroho mpaka kufikia 82


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

kiwango cha kumkinga yeye na madhambi, na kwamba anafikia daraja lingine kwa namna ambayo hafanyi kosa? Hakika Mariam mtakatifu  hakuwa Nabii lakini alikuwa maasumu na mwenye kujizuia na dhambi. Hakika Qur‟ani tukufu imeashiria hilo kwa kauli yake (s.w.t):

ٰ ُ َ َٰ َ َ َ َ​َ ٰ ‫اصط‬ ‫فى ِو َاط َّه َط ِك‬ ‫َا ِإش ضل ِذ امللـ ِئنت يـ َم َطي ُم ِإ َن اللـه‬ َ َٰ َ ٰ َ َ ‫ؼضء العـلمين‬ ِ ‫ااصطفى ِو ع ٰ ِو‬ “Na (Kumbukeni) Malaika waliposema: Ewe Mariam! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteua na akakutakasa, na akakuteua juu ya wanawake wa ulimwenguni.”51 Ni jambo lililokubalika kwamba makusudio ya utoharifu ni kumtoharisha Mariam kutokana na dhambi na sifa mbaya. Na hapa tunauliza swali; kwa nini haiwi kauli ya umaasumu wa Mariam ni bidaa na kusema umaasumu wa Amirul-Muuminina  ambaye ni mwenza wa Qur‟ani kwa mujibu wa hadithi ya vizito viwili – ni bidaa?! Hakika hadithi ya vizito viwili ni miongoni mwa hadithi mutawatiri ambayo Mtume  kwayo ame51

Surat al-Imraan; 3:42.

83


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

linganisha kizazi chake kuwa ni sawa na Qur‟ani. Na hakika hivyo viwili havitatengana kamwe kama alivyosema: “Hakika mimi ninakuachieni vizito viwili; Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu, ikiwa mtashikama navyo hamtapotea kamwe.” Ni wazi kwamba hakika muktadha wa kizazi kuwa sawa na Qur‟ani tukufu ni kuwa kwake maasuma kama vile ulivyo umaasumu wa Qur‟ani tukufu. Wala haiwezekani kuzuka kutoka kwa hivyo viwili kitu hata kidogo cha kuleta mfarakano au kupingana. Ikiwa kauli ya kwamba Maimamu ni maasumu ni kufurutu ada katika kupenda, basi ni kwa nini kusema kwamba, Sahihi Bukhari ni kitabu sahihi zaidi baada ya Qur‟ani, haiwi nako ni kufurutu ada katika kupenda?! Je, ni sahihi uelezaji huu juu ya kitabu hiki ambacho ndani yake yamo yasiyofaa na yenye kutofautiana na akili iliyosalimika?! Je utambuaji wa madhehebu manne pekee na kutupilia mbali madhehebu mengine katika nyanja za amali na kuhukumu, si upitukaji na ufurutu ada katika kupenda?! Wakati umma wa Kiislamu uliishi salama hata kabla ya kuzaliwa yeyote miongoni mwa wenye madhehebu haya?! Na lau sio kuhifadhi usafi wa maji ya upendo tungelipanua zaidi maneno katika mambo hayo ambayo mmeyachukua na kuwahukumu kwayo Shia. Lakini 84


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

tumefupisha kwa hayo ili aangalie Sheikh mtukufu yote kwa jicho moja na fikra mahsusi. 4. Kutukana Maswahaba: Jambo ambalo linapelekea katika kizungumkuti, tahayuri na kushangaza, ni maneno haya kutoka kwa msomi mfano wenu. Hakika inafaa zaidi maneno hayo yatoke kwa watu wa kawaida wasio na elimu wala maarifa. Je, inawezekana kundi kubwa likawa linampenda Mtume  lakini linawachukia Maswahaba wake na kuwatukana?!! Hakika idadi ya Maswahaba wa Mtume inavuka elfu moja, na hakika wale ambao maisha yao yametajwa na watunzi wa vitabu vya elimu ya wapokezi wa hadithi wamefikia Masahaba elfu kumi na tano. Baadhi ya Maswahaba walikufa shahidi katika vita mbali mbali ambavyo Mtume  alishiriki, kwa mfano vita vya Badri, Uhudi, Khandaki, Khaybar na nyinginezo. Je, inafaa kwa Mwislamu anayemwamini Mwenyezi Mungu (s.w.t) na Siku ya Mwisho awafanyie watukufu hawa hayo?! Kisha hakika sehemu kubwa ya watu hao, miongoni mwa masahaba hatujui hali zao wala hatujui kutoka kwao chochote. Je, inaruhusiwa kwa mtu kupunguza au kugusa jambo la mtu mwingine asiyejua hali yake? Mpaka hapa tunasema: Hakika suala la kutukana Maswahaba kwa maana ambayo imeenea na kuzagaa 85


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

kwa watu wote, si chochote isipokuwa ni kisingizio ambacho baadhi wanajaribu kushikamana nacho. Kwani hakika maneno ya Shia ni maneno ya Imam wao Amirul-Muuminina  ambayo unayakuta katika hotuba ya 97, kutoka katika kitabu cha NahjulBalaghah. Amesema: “Hakika nimewaona Masahaba wa Muhammad  na simuoni yeyote miongoni mwenu anafanana nao. Walikuwa wakiamka wakiwa na nyoyo safi na wakipitisha usiku wakiwa wamesujudu na wamesimama. Na wakisimama juu ya mfano wa makaa ya moto kutokana na utajo wa mwisho wa maisha yao. Kati ya macho yao kumekuwa ni mgongo wa mbuzi kwa urefu wa sajda yao. Akitajwa Mwenyezi Mungu macho yao hububujika machozi mpaka vinaloa vifua vyao. Na wanainama kama vile miti inavyoinama siku ya kimbunga na upepo mkali kuhofia adhabu na kutaraji thawabu.” Hakika wafuasi wa Imam Amirul-Muuminina  wanachukua maneno ya Imam wao, ambapo pale aliposikia baadhi ya masahaba wake wakiwatukana watu wa Shamu – siku za vita vya Suffini – aliwahutubia akisema: “Hakika mimi ninachukia kuwa nyinyi watukanaji. Lakini nyinyi lau mngeliwasifu kwa 86


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

amali zao, na mngelitaja hali zao, ingekuwa ni vizuri na mngelipatia katika maneno, na kufikisha zaidi kwa kuomba samahani. Na sehemu ya kutukanwa kwenu mngelisema: Ewe Mwenyezi Mungu! Zuia damu zetu na damu zao, na utengeneze baina yetu na wao. Na uwaongoze hao baada ya upotofu wao, mpaka haki ijulikane kutokana na kutojulikana kwake. Na kutoweka upotovu na uadui pamoja na yule aliyetamka huo.”52 Basi ikiwa hii ndiyo itikadi ya Imam wa Shia kuhusiana na haki ya Maswahaba, vipi isiwe itikadi ya mfuasi wake ni kama vile itikadi yake?! Hakika kutukana ni kitendo cha wajinga ambao hawazuii ndimi zao kutokana na yale ambayo wasiyoyapenda. Kwa hivyo ninakuomba kwa heshima yenu, msiliseme jambo hili kwa aina hii. Ndio, hakika lile ambalo analoliitakidi Shia ni kwamba, hakika baadhi ya Maswahaba wa Mtume  ambao hawavuki idadi ya vidole vya mkono waliamiliana na Ahlul-Bayt wa Mtume baada ya kufariki kwake kwa muamala mbaya. Na kuanzia hapo Shia kwa sababu hii wakajitenga nao. Na hili sio jambo geni, huyu hapa Mtukufu Mtume  anajitenga na kitendo cha Khalid bin Walid na anasema: “Ewe Mwenyezi 52

Nahjul-Balaghah, maneno mafupi na. 206.

87


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

Mungu! Hakika mimi ninajitenga kwako kwa yale ambayo aliyoyafanya Khalid.” Lakini geuzeni mtazamo wenu wa juu hadi katika hadithi za kuritadi maarufu kwa jina la hadithi za Haudhi, ambazo zimekuja katika sahihi mbili Bukhari na Muslim,53 vipi mnafasiri hadithi hizi zitokazo kwa Mtume Mtukufu ?!! Pili: Bidaa ya kivitendo: 1. Kurudia maombolezo ya Husein  kila mwaka: Mmeashiria kwa heshima zenu baada ya kutaja bidaa ya nadharia, bidaa ya kivitendo na mkazingatia kwamba, kati ya bidaa hizo za kivitendo ni “Kurudia maombolezo ya Imam Husein  kila mwaka.” Wala sijui ni vipi yamekuwa maandamano ya milioni ya watu ambayo hufanywa ili kuhuisha kumbukumbu ya Bwana wa Mashahidi na mjukuuu wa Mtume , na kudhihirisha dhulma aliyotendewa, kuwa ni bidaa ambayo inastahiki lawama na kukemewa!! Lau mheshimiwa Sheikh ungelijua falsafa ya mapinduzi ya Imam Husein na ungelifikiri kwa maono ya mbali zaidi mapinduzi hayo matukufu, ungelifanya 53

Angalia: Sahihi Bukhari, Juz. 4, uk. 67 na Juz. 5, uk. 107, kitabu Maghazi.

88


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

kama anavyofanya Shia katika kuhuisha tukio hilo kubwa. Hakika kuandamana kwa ajili ya kukabiliana na dhulma na kukataa mfumo mbaya, na kusimama imara mbele ya serikali za kidhalimu, hapana budi ni mambo ambayo ni lazima yabakie hai katika umma wa Kiislamu. Na hili ndilo lengo la mapinduzi ya Imam Husein  ambayo yanaleta uhuru ulimwenguni, mfano wa harakati za Hamasi na Jihadi Islamiyyah huko Palestina dhidi ya Mayahudi walowezi waporaji. Kutoka hapa inakuwa wazi sababu ya kutilia umuhimu mapinduzi ya Husein zaidi kuliko kutilia umuhimu minasaba mingine ya Maimamu, kama vile kufa shahidi kwa Amirul-Muuminina Ali . Na hata kama yanafanywa maadhimisho ya minasaba hiyo pia isipokuwa maadhimisho hayo hayachukui muda mrefu na sehemu kama vile mnasaba wa kuadhimisha mapinduzi ya Imam Husein. Hakika mapinduzi ya Imam Husein  yanabeba ujumbe wa kuwachochea na kukifikia kila kizazi ambacho kinapatikana chini ya dhulma na ugandamizaji, ili kwayo zichemke damu za wenye wivu wa kutetea dini kama alivyofanya bwana wa vijana wa watu wa peponi katika kuitetea dini ya babu yake Mtume Muhammad . Vivyo hivyo vikao hivyo vya maombolezo vinakusudia kuamsha mori na kuleta hamasa ya kupambana 89


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

na ufisadi ambao ulipingwa na Ahlul-Bayt , uliowatia wao chini ya aina mbalimbali za mateso na ugandamizwaji. 2. Yale yanayofanywa sehemu za maziara ya Ahlul-Bayt  ni miongoni mwa shirki: Umetoa tuhuma katika maelezo yako kwamba, Shia wanafanya shirki katika sehemu za maziara ya makaburi ya Ahlul-Bayt . Lakini la msingi kwenu mlipasa kuashiria mifano halisi ya shirki hizo na si kuiacha kadhia ikiwa ni yenye kuelea hivi hivi. Je, asili ya kuzuru maziara ni shirki? Hakuna shaka kwamba jibu la swali hilo ni hapana. Na je, dua na kuomba uombezi kutoka kwa Mtume  na AhlulBayt wake  ni shirki? Hapana. Hakika ilifaa kwa heshima yenu kumfuata Imam mkubwa wa Mahanafi. Hakika amepokea mwandishi wa kitabu Fat’hulQadiir kwamba: Hakika Imam Abu Haniifa alisimama mbele ya kaburi la Mtume  na akasoma mashairi akisema: “Ewe mbora wa vizito viwili, ewe hazina ya uchamungu – nipe mimi kwa ukwasi wako na niridhie mimi kwa radhi zako. Mimi ninatamani katika ukwasi kutoka kwako – 90


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

na wala hakuwa Abu Haniifa katika wanadamu ni uchafu.”54 Kama kwamba Abu Haniifa amemfuata sahaba mtukufu Suwad bin Qarib ambaye alisoma beti kadhaa akisema: “Basi kuwa wewe kwangu mimi muombezi siku ambayo hakuna mwenye uombezi – kwa usaidizi asiokuwa nao Suwad bin Qarib. Hakika imekuja katika ubainifu wenu kwamba, kuwaomba Ahlul-Bayt  badala ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) huhesabiwa ni miongoni mwa shirki. Tunamuomba samahani mheshimiwa Sheikh, hakika maneno haya ni maneno ya kiwahabi ambao huyaegemeza wakati fulani katika kauli ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) inayosema:

َ َ ٰ َ َ َ َ َ ‫َاأ َن املؼـ ِج َس ِلل ِـه فال جسعوا َم َع الل ِـه أ َح ًسا‬ “Na hakika misikiti yote ni ya Mwenyezi Mungu, basi msimuombe yeyote pamoja na Mwenyezi Mungu.”55 Lakini inapaswa ieleweke makusudio ya neno “maombi” ni yapi hayo? Je, makasudio yake ni kumzungumzisha asiyekuwa Mwenyezi Mungu? Hakuna 54 55

Fat-hul-Qadiir, Juz. 2, uk. 336. Sura 72 aya 18.

91


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

shaka hakika hilo sio mradi wake, kwani inalazimu hilo ukufurishaji wa watu wote. Hakika binadamu katika uhai wake anawazungumzisha maelfu ya watu na akiomba msaada kwao. Ndio, makusudio ya maombi hapa ni ibada isiyokuwa ya Mwenyezi Mungu (s.w.t), kwa maana ya unyenyekevu na kujishusha mbele ya yule aliyekuwapo, kwa anuani ya kuwa kwake ni muumbaji na mpangaji wa mambo, basi inakuwa maana ya aya ni: “Na kwa hakika misikiti yote ni ya Mwenyezi Mungu msimwabudu yeyote pamoja na Mwenyezi Mungu.” Na kwa bahati nzuri upo ushahidi juu ya hilo, nayo ni kauli ya Mwenyezi Mungu (s.w.t):

َ َ َ ‫ػخجب َل ُنم إ َن َال‬ ُ ُ ‫َ َ َ ُّل‬ ً‫صي‬ ِ ‫ا ضى ض نم ازعووى أ‬ ِ ُ َ َ َ َ َ َ َ ‫سدلو َن َج َّه َى َم زاد‬ ً‫طي‬ ‫نكيان َعً ِعبضزحى ػي‬ ِ ِ ‫يؼخ‬ “Na Mola Wenu anasema: Niombeni nitawaitikia. Kwa hakika wale ambao wanajivuna kufanya ibada Yangu, wataingia Jahannamu wadhalilike.”56 Basi katika mwanzo wa aya limekuja neno “Niombeni” lakini mwishoni mwake limekuja neno “ibada yangu.” Na hili linaeleza kwamba hakika dua mahsusi kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) ni ile ambayo inabeba 56

Surat al-Mu‟min; 40:60.

92


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

sifa ya ibada, na sio aina yoyote ile ya dua na maombi. Na kama si hivyo basi asingelipatikana mwanatawhidi katika uso wa ardhi abadani. Mheshimiwa Dr. Qardhawi, hakika Qur‟ani tukufu imechora njia ya kumpambanua mpwekeshaji na mshirikina kwa kauli yake (s.w.t):

َ​َ ُ ٰ َ َ َُ َ ُ َ ‫حس ُه َل َف ُطجم َاإن ُي‬ ‫شطك ِب ِه‬ ‫ش ِلنم ِبأه ُه ِإشا ز ِع اللـه ا‬ ِ َ ُ ُ َ َ ّ َ ُ ‫بيي‬ ِ ‫ج‬ ِ ‫ؤمىوا فضاحنم ِلل ِـه الع ِ ِ الن‬ “Hayo ni kwa sababu alipoombwa Mwenyezi Mungu peke Yake mlikataa, na akishirikishwa mnaamini, basi hukumu ni ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mkubwa.”57 Je, ni kweli hakika Mashia wote na idadi kubwa ya Wamisri ambao wanakusanyika mahala panaposadikiwa ndipo kilipo kichwa cha Imam Husein , katika kisImamo cha Sayyida Nafisa na Bibi Zaynab , na wanafanya tawasuli kwao ili Mwenyezi Mungu (s.w.t) akidhi haja zao, je, watu hawa kwenu nyinyi ni washirikina?! Kwa maana hakika wao wamekengeuka na kuacha ibada ya Mwenyezi Mungu mmoja wa kipekee? Au inaongezeka imani yao kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) pindi ambapo wanapatikana katika sehemu hizo takatifu? Je, hayo sio maneno ya 57

Surat al-Mu‟min; 40:12.

93


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

wakufurishaji ambapo bado mnaendelea kulikosoa hilo na kuiona ni fikra potofu?! Mpaka hapa kalamu imesimama na haindelei kuandika. Tunatarajia kwa heshima yenu kuyajua yale yaliyowapita na ulinganio wa wote, ili kushikamana na kamba ya Mwenyezi Mungu imara na kuhimiza juu ya umoja wa umma. Basi tunataraji kwa heshima yenu, kuinua bango la uletaji karibu madhehebu na kujifunika kwa nguo yake katika kivuli cha misingi ambayo wameiweka watu wa ukaribishaji wa madhehebu, nayo ni: Imani ya Mwenyezi Mungu Mmoja na yale yanayolazimu hiyo kutokana na imani ya ghaibu, malaika, vitabu, manabii, na siku ya mwisho. Na yale aliyokuja nayo Mtume Muhammad , mwisho wa Manabii, katika Kitabu na Sunnah. Na yale ambayo Waislamu wamekubaliana katika misingi na matawi, hadi yasiyokuwa hayo miongoni mwa mambo yenye ushirikiano baina ya umma wa Kiislamu ambayo hawajatofautiana wawili. Kama ambavyo hakika matarajio ya wenye ashki ya kuleta ukaribu wa madhehebu ni kuingia katika uwanja wa mazungumzo kwa adabu na njia ya Qur‟ani:

َ ً ُ ٰ َ َ ُ ّ َ ّ َ ُ َٰ “‫بين‬ ٍ ‫… ا ِإهض أا ِإيضلم لع هس أا رلـ ٍل م‬..” 94


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

“Na hakika sisi au nyinyi bila shska tuko kwenye uongofu au upotovu ulio wazi.”58 Na yale tuliyoyasoma katika ubainifu yanapingana na maneno yenu kuhusiana na utandawazi, yale yaliyochapishwa katika jarida la Majmaul-Fiqh Islamiy, na haya ndio maandiko yake: “Na lakini ni juu ya umma kujua hakika uko katika hatari ikiwa hautajikusanya pamoja na kuwepo kati yake aina ya upendo na kusaidiana. Na kwa hivyo sisi tunawaita nyinyi enyi ndugu zetu katika maslahi ya pamoja, ambayo zinakusanyika hapo nguvu zote za umma katika hatua hii, hakuna sababu ya kugawanyika na kuwa makundi makundi. Huko kuna watu wanataka waufarikishe umma, nao ni maadui zetu. Wanataka hilo, ima wafarikishe kati yake ikiwa huko kuna wachache wasiokuwa Waislamu, basi wao huwachochea wachache hao. “Na ikiwa ni wachache kiasili, basi huonesha wako waarabu, wabarbar, mabedui na wakurdi. Ikiwa ni wachache kimadhehebu basi wanakuwa Sunni na Shia. Na ikiwa si huyu si yule, basi wanabakia wa kulia na wa kushoto, au wana mapinduzi na wahafidhina. Sisi tunataka tukusanye nguvu zote za umma na tunalingania uletaji suluhu hata kwa viongozi na wanazuoni, na baina ya watawala na jumuiya za 58

Surat as-Sabaa; 34: 24.

95


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

Kiislamu. Hakuna sababu sasa ya kutofautiana baina ya umma. Umma unawajibika kuwa mstari mmoja kama vile jengo imara linalokaza baadhi yake kwa baadhi nyingine wakati wa matatizo. Hakuna sababu ya kuikhtilafiana na kufarakana wala sababu ya mapambano ya kichinichini. Inapasa wote wasImame mstari mmoja.”59 Ninasema kauli yangu hii na ninamuomba Mwenyezi Mungu (s.w.t) msamaha na ninakuombeeni nyinyi. Na sifa zote njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu Mola mlezi wa walimwengu. “Ewe Mwenyezi Mungu! Hakika sisi tunaomba kwako serikali tukufu, ambayo kwayo utaupa nguvu Uislamu na watu wake, na kwayo utaudhalilisha unafiki na watu wake.” Na amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yenu. MAJIBU MENGINE JUU YA MHESHIMIWA SHEIKH QARDHAWI Baada ya kusambaza barua yetu hii tuliyoituma kwa Sheikh Qardhawi, tulipata idadi kubwa ya makala ambayo yamejibu yale aliyoyasema yeye, na tutaashiria hapa kwa ufupi katika mifano miwili, nayo ni: 59

Majallat Majmaul Fiqhul-Islamiy: Toleo 14 na. 14 Juz. 4, uk. 402.

96


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

1. Makala kwa kalamu ya Najib Zamil, kwa anuani “Je, alikuwa Sheikh wetu Qardhawi ni mwenye haki?” Miongoni mwa yale ambayo yaliyopatikana katika makala hiyo ni: Ninasema – na kutokana na mtazamo wa kihistoria na kimantiki katika maumbile ya dini mbalimbali: Hakika msimamo wa Sheikh Qardhawi katika suala la Iran kuhusu madhehebu ya Kishia na kuenea kwake, ninaufahamu kuliko Sheikh mtukufu Msunni mwenye kuyahami madhehebu yake. Na sisemi kwamba siafikiani naye katika msimamo wake, lakini mimi ninafahamu kwamba si wenye kusaidia. Nina yakini kwamba hakika dini zinatapakaa na kuenea kama vile yanavyopita maji chini ya ardhi kuilisha mizizi, daima maji hayo hufika. Na hata kama Iran itaafikiana na Sheikh Qardhawi na kukawepo makubaliano ya wazi mbele ya ulimwengu wote, kwamba madhehebu ya Ushia hayataingizwa katika nchi kubwa za Kisunni au ndogo. Na hata ikiheshimu makubaliano hayo, bado hakika madhehebu hayatosimama, kwa sababu kuenea kwa dini mbalimbali na madhehebu sio suala la nchi.”60 2. Makala kwa kalamu ya mwanafikra wa Kiislamu Jamal Banaa61 kwa anuani ya: “Majibu juu ya 60

Yamesambazwa makala juu ya kurasa za sehemu ya “uchumi wa Kuwait” tarehe 18/10/2008. 61 Naye ni ndugu wa mwasisi wa harakati za undugu wa Kiislamu shahidi (Hasan Banaa).

97


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

Qardhawi; kauli ya haki kuhusu muunganiko uliopo baina ya Shia na Sunni.”62 Kati ya yale yaliyomo humo ni: Ameona mheshimiwa Sheikh kwamba kuenea kwa Ushia katika sehemu ambazo hawakuwapo Mashia hapo kabla, ni mipango kazi, mikakati na ubunifu wa Irani. Na hili sio sahihi, na sahihi ni kwamba jamhuri ya watu walitaka kuwaadhibu watawala wao kwa kuunga mkono Ushia, kwa sababu adui wa adui wangu ni rafiki yangu. Mataifa ya Kiislamu hayana maadui isipokuwa Israeli na mtetezi wake Marekani, na hawa wawili ni maadui wa Iran.” Kisha akasema: “Na Sheikh Qardhawi amekosoa yale wanayoyaamini Shia kuhusiana na umaasumu wa Maimamu na kuwatukuza hao, lakini je, utukazaji huu haupatikani katika fikra ya Masunni wa kale? Je, hatusemi kuhusu Bukhari kwamba: Ni kitabu kilicho cha kweli zaidi baada ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Inakuwaje tunatosheka na madhehemu manne pekee, tunalazimika na maneno ya Maimamu wao, kana kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) amejaalia Uislamu kuwa umezingirwa katika madhehebu haya manne tu, wala hatufikirii madhehebu mengine? 62

Yamesambazwa makala juu ya kurasa za habari tarehe 19/10/2008.

98


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

“Na inamaanisha nini – naapa kwa Mwenyezi Mungu – kutabikisha leo hii hukumu zilizowekwa na wale waliotangulia yapata miaka elfu moja sasa? Je hili halihesabiwi kuwa ni utukuzaji wa watu hawa waliotangulia, na kuona kwa macho yao, na kuhukumu kwa akili zao, kama kwamba sisi hatuna akili na maono? “Na Sheikh amejiweka mbali na wito wa Dr. Kamal Abu Majdi kwa kufunga faili hili. Na ninaona hakika huko ni kukimbia makabiliano na mapambano (na lakini kwa hekima na utulivu). Na uhalisia unasema hakika yeye hawezi kupambana katika uwanja huu kwa hekima na utulivu. Na hakika ametaja yeye mwenyewe yale ambayo inapasa kuyazuia, akasema: “Hakika jambo la kwanza analolifanya mlinganiaji wa madhehebu ya itikadi, ni kushambulia madhehebu mengine, na kubainisha kwamba ni upotofu na batili. Na kwamba madhehebu hayo yanamfikisha mhusika wake motoni. Na hakika hatookoka na moto isipokuwa kwa kushikamana na madhehebu mengine. Na hapa mwenye kushambuliwa anajikuta analazimika kujitetea, na njia nzuri ya kujitetea ni kushambulia. Basi anashambulia madhehebu ya mwenye kudai, na anaonesha ubatili wa misingi yake mmoja baada ya mwingine.” Na anasema Sheikh: “Na anaweza Msunni kutangaza kwa majigambo kwamba madhehebu yake ndio yenye 99


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

kuafikiana pamoja na yale wayatakayo watu wa zama hizi, kuhusuiana na uhuru na usawa bila ubaguzi. Familia ina haki ya hukumu yao bila kuingilia hiari yao, basi hakuna wosia kwao wa ulazima kutoka mbinguni, wala hakuna yeyote mwenye haki ya umaasumu asiyepingwa.” Na Sheikh ana haki kwa upande huu, lakini asikanushe kwamba, madhehebu ya Sunni yana mikondo mingi, sawa iwe katika fikihi au tafsiri au hadithi, nayo ni mambo yaliyojikita ambayo fikra ya Sunni imesimama juu yake, na ilikuwa ni nyenzo zilizochangia Waislamu kutoendea. Lakini hili ni jambo lingine ambalo linarefuka, na hapa sio mahali pake. Mheshimiwa Sheikh ni miongoni mwa wale wavumbuzi wa “fikihi ya mambo ya awali” na ninamuomba aizingatie fikihi hii katika kuweka mipakana misImamo. “Shia wanasema: Lailaha ilallah Muhammadun Rasulullah, wanaswali, wanafunga mwezi mtukufu wa Ramadhani, wanaelekea Kibla chetu, basi wao ni Waislamu, wana hifadhi ya Mwislamu na wana haki juu ya Waislamu waliobakia, kama vile walivyo na wajibu kuwaelekea wao. “Na anajua Sheikh na anatambua kwamba, hakika sisi tunaingia kwenye mapambano makali yasiyo na huruma, ambayo yanaongozwa na nguvu kubwa 100


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

ambayo inaungana na kuwa kitu kimoja katika kuufanyia uadui ulimwengu wa Kiislamu. Je, hili halituiti sisi katika umoja kuunganisha nguvu za Waislamu, ambao nao ni mwelekeo mmoja. Ikiwa itaanguka sehemu moja basi zitaanguka sehemu zinginezo, kama vile kikitoweka kimoja kitatoweka cha pili na cha tatu… n.k. Je, inaingia akilini tuwe kama vile watu wa Bizintwa ambao walijishughulisha na majadiliano yasiyo na maana hali ya kuwa adui anawazingira wao mpaka akawaangusha. Kwa hakika Sayyid Rashid ameweka shairi linalosema: “Tunasaidiana katika yale ambayo tunayokubaliana nayo. Na tunaombana msamaha kati yetu katika yale ambayo tunatofautiana kwayo.” Na akajengea Imam Hasan Banna shairi hili. Basi kwa nini hatuchukui kutoka kwake katika wakati huu wa msukosuko?! Hakika dhamana ni juu ya mafikio, yaani juu ya uhai au kifo cha eneo, je, huko yako yaliyo ya muhimu zaidi? Ninakuomba usiache fikra yenu ya kisalafi ikaishinda fikra yenu ya kisiasa. Kamwe lililopita halitatufaidisha wala uangaliaji wa nyuma, na hakika linatufaidisha la sasa na uangaliaji wa mbele. Hakika mtu mfano wa Sheikh Qardhawi katika uerevu wake na umashuhuri wake na daraja lake, na heshima aliyonayo ambayo inamfanya aachiwe matarajio, inafaa awe mbele ya suala la umoja na sio utengano, na kiongozi aliye mbele na si awe nyuma. 101


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

Na afanye kwa kusaidiana na sio kwa kugombana. Na aangalie mbele na aweke lengo la mustakabali, na asiangalie nyuma na kujisalimisha kwa yaliyopita (yaliyopita si ndwele tugange yajayo). Na yeye anafaa kwa hili na ni mahali pake, na hapo ndipo anapotakiwa, na Mwenyezi Mungu (s.w.t) amwafikishe yeye na amweke kwenye usawa na ayafikie matarajio yake. FASLU YA SABA KURUHUSU TENDO LA KUPUNA TUPU ZA MBELE (PUNYETO)63 Dr. Anasema katika mazungumzo yake kuhusiana na maudhui ya hukumu ya kupuna tupu za mbele: “Na hakika inachemsha damu ya ghariza (mhemko) kwa kijana, basi anautumia mkono wake na anafanya manii yatoke mwilini mwake ili aipe raha mishipa yake ya fahamu. Na anatulia kutokana na mapinduzi ya ghariza, nayo inajulikana katika zama hizi kwa jina la „kujichua misuli.‟ Kwa hakika wanazuoni wengi wameiharamisha, na Imam Malik ametoa dalili kwa kauli ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) inayosema: 63

Uhariri wa makala haya umetimia tarehe 10 mfunguo mosi mwaka 1429H.

102


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

ٰ َ ُ َ ‫َا َال‬ ٰ ‫﴾ إ ّال َع‬٥﴿ ‫طاج ِّهم حـ ِف ون‬ ‫صيً ُهم ِلف‬ ِ ِ َ َ َ ٰ َ َ​َ َ ‫أ ٰظا ِج ِّهم أا مض َملنذ أيمـ ُن ُهم ف ِئ َّن ُهم غ ُيي‬ َ َ َ ٰ َُ َ ٰ َ َ ٰ َ ‫ضاء ش ِلو فأالـ ِئو ُه ُم‬ ‫﴾ ف َم ًِ ابخغ ا‬٦﴿ ‫َملومين‬ َ ﴾٧﴿ ‫العضزان‬ “Na ambao wanazilinda tupu zao. Isipokuwa kwa wake zao au kwa iliyowamilikiwa mikono yao ya kuume. Kwani si wenye kulaumiwa. Lakini anayetaka kinyume cha hayo, basi hao ndio wapetukao mipaka.”64 Na yule anayejipuna tupu kwa mkono wake hakika ametafuta kwa ajili ya matamanio yake nyuma yake kitu kingine. Imepokewa kutoka kwa Imam Ahmad bin Hanbali kwamba, hakika yeye amesema kwamba manii ni uchafu wa mwili, kwa hivyo inafaa kuyatoa kama vile damu. Na hili amekwenda nalo yeye. Na amemuunga mkono katika hilo Ibn Hazmi, na wanazuoni wa Hanbali wakaweka masharti katika kufaa kwa jambo hilo kwa mambo mawili: La kwanza: Kuchelea kuangukia katika uzinifu. La pili: Kutokuwa na uwezo wa kuoa. 64

Surat al-Mu‟minun; 23:5-7.

103


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

Tunaweza tukachukua rai ya Imam Ahmad katika hali ya kufurika kwa ghariza na kuchelea kuangukia katika haramu, kama vile kijana anayesoma au anayefanya kazi nchi ya kigeni, na sababu za upotoshaji zipo nyingi mbele yake, na anaogopa uzinifu juu ya nafsi yake, hapo hakuna tatizo juu yake kutumia njia hii ya kuzima ghariza ambayo imezidi kiwango, kwa sharti la kutopitisha kiwango katika hilo na kulichukulia hilo kuwa ni jambo la kawaida. Na bora zaidi ya hilo ni lile aliloelekeza Bwana Mtume  kwamba kijana Mwislamu ambaye anashindwa kuoa, na afunge zaidi, saumu ambayo itapunguza matamanio, itafundisha subira na atatia nguvu uwezo wa takwa na kumtii Mwenyezi Mungu (s.w.t) katika nafsi ya Mwislamu, pale aliposema: „Enyi vijana! Yule atakayeweza kuoa basi aoe, hakika hilo linainamisha macho chini. Na yule ambaye hawezi basi ni juu yeke kufunga, kwani hilo ni zuio kwake.‟ kama alivyopokea Bukhari.”65 Ninasema: Hakika kauli ya uhalali wa kujitoa manii au kuchua misuli inatofautiana na maneno ya Mwenyezi Mungu (s.w.t), umashuhuri unaopatikana katika madhehebu ya kifikihi, na yale ambayo juu yake wamekwenda Maimamu Ahlul-Bayt  katika nyanja hii. 65

Halal wa Haram fil-Islami, uk. 164-165 chapa ya Qairo mwaka 1396H.

104


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

Ama kuhusu utajo wa Mwenyezi Mungu (s.w.t), hakika ameunukuu Sheikh katika maneno yake na hakuna haja ya kueleza, ambapo (s.w.t) ameamrisha kuhifadhi tupu katika kila hali isipokuwa kwa mke na yule mjakazi anayemmiliki. Na ikiwa ataruka mipaka ya hali hizi mbili na akafanya tendo la kujipuna tupu za mbele atakuwa miongoni mwa waliovuka mipaka na kuichupa, kwa kutoka katika yale aliyowahalalishia Mwenyezi Mungu na kutenda yale aliyowaharamishia. Na ama kuhusu umashuhuri wa wahakiki, ni kwamba hakika wamekwenda Maliki, Shaafii na Zaydiya katika kuharamisha hilo, kwa kuchukua yale ambayo yapo ndani ya Qur‟ani tukufu. Na dalili juu ya hilo imejikita katika mambo mawili: 1. Utengaji: “Isipokuwa kwa wake zao au wale waliomilikiwa na mikono yao ya kuume, basi hao hawalaumiwi.”66 2. Kauli yake (s.w.t): “Lakini anayetaka kinyume cha haya, basi hao ndiyo wapetukao mipaka.”67 Na ama kuhusu msimamo wa Maimamu wa AhlulBayt  ni kwamba, hakika imepokewa na Twalha bin Zayd, kutoka kwa Abi Abdillah  amesema: Hakika Amirul-Muuminina  aliletewa mtu aliye66 67

Surat al-Ma‟arij; 70:30. Surat al-Mu‟minun; 23:7.

105


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

fanya ukhabithi kwa kujipuna tupu za mbele, basi akampiga kwa mkono wake mpaka ukawa mwekundu, kisha akamuolea mke kwa mali za hazina ya Kiislamu.68 Imepokewa kutoka kwa Ammar bin Musa, kutoka kwa Imam Swadiq , aliulizwa kwamba mtu anamwingilia mnyama? Akasema : “Kila mwanaume anapoteremsha maji kwa namna hii au mfano wake basi ni zinaa.”69 Na hadithi zingine zenye kujulisha juu ya uharamu wa tendo hilo. Na ama yale aliyoyataja Dr. kuhusiana na tatizo la kutumia njia ya mkono kwa namna ambayo haina tatizo wala haichukulii hiyo kuwa ni kawaida yake, basi ni jambo la kushangaza mno. Hakika kujipuna tupu za mbele ni kitu chepesi zaidi cha kupata ladha ya kijinsi, basi vipi inawezekana kijana afanye hivyo wala isiwe ni kawaida?! Kwa kuongezea ni kwamba, hayo ni madhara ambayo madaktari wanayataja kwa yule aliyezoea kufanya tendo hilo. Na ama yale yaliyonukuliwa kutoka kwa Imam Ahmad bin Hanbali ambapo ameruhusu – kulingana 68

Wasaail Shia, Jz. 18 mlango 28 miongoni mwa milango ya ndoa za haramu, hadithi ya tatu. 69 Wasaail Shia, Juz. 18, mlango 26 miongoni mwa milango ya ndoa za haramu, hadithi ya kwanza.

106


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

na ulivyonukuu – kurudi katika njia hii ili kuzima kwayo kufura kwa ghariza pindi anapochelea kuangukia katika zinaa, hayo ni miongoni mwa yale ambayo haiwezekani kuyategemea. Na huenda chimbuko la maneno yake ni kanuni maarufu inayosema: “Dharura zinahalalisha vilivyokatazwa.” Na linalojulikana ni kwamba matumizi ya kanuni hii ni pale mtu anapopatwa na majaribu na mtihani bila ya hiari, basi muda huo inafaa kufanya maasi kwa uchache wa dhararu mbili, au kwa uchache zaidi ya haramu mbili. Kama ikiwa mfungaji atapata majaribu ya kiu hadi kufikia kutaka kuangamia, basi inafaa kwake kuondoa kiu kwa kunywa maji kwa kuhifadhi uhai wake. Au katika kwa kiwango cha kuweza kuokoka uhai wa binadamu kwa kutumia mali ya Mwislamu au kula mali ya mwingine. Katika mambo haya kanuni hii: “Dharura huhalalisha yaliyokatazwa” inafanya kazi. Lakini kwa sharti asiwe binadamu ni nyenzo yenye kuleta athari katika uletaji wa dharura. Na ama katika mada husika, ni wajibu kwake kuizuia nafsi na kujiepesha na yale ambayo Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameharamisha. Na kama ikiwa ufurikaji wa ghariza na kuchelea kuangukia katika haramu ni sababu ya kufanya zinaa kwa yule mwenye mume, je, inawezekana kufutu kujuzu kufanya lililo jepesi zaidi kuliko hilo? 107


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

Na njia iliyo bora zaidi ni ile aliyotuongoza kwayo Mtume  kama alivyonukuu hilo mtoa majibu, na akumbuke adhabu ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) juu ya maasi hayo. FASLU YA NANE KUTOSHELEZA BISMILLAHI WAKATI WA KULA70 Katika uchinjaji wa kisheria yanatakiwa yatimie masharti kadhaa, nayo ni: Litajwe jina la Mwenyezi Mungu (s.w.t) wakati wa kuchinja, Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema:

َ​َ َ ُ َ ُ ّ َُ َ ُ ٰ ‫ُ ُ ٔـ‬ ‫ؤمىين‬ ِ ‫فهلوا ِممض ش ِلط اػم الل ِـه عل ِيه ِإن لىخم ِبـضيـ ِخ ِه م‬ “Basi kuleni katika wale waliosomewa jina la Mwenyezi Mungu ikiwa nyinyi mnaziamini shara Zake.”71 Na anasema (s.w.t):

َ َُ

َ

َ

َ

َ

ُ َ

‫اػم اللـه َعليه َاإهه لف ٌع‬ ُ ‫” َاال جأملوا م ّمض لم ُيصلط‬ “…..‫ؼق‬ ِ ِ ِ ِ ِ ِ 70

Uhariri wa makala haya umekamilika tarehe 15 mfunguo mosi mwaka 1429H. 71 Surat al-Anam; 6:118.

108


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

"Wala msile wale wasiosomewa jina la Mwenyezi Mungu, kwani hilo ni ufasiki.�72 Wala hakuna utata katika sharti hili. Na juu ya hili hakiwi halali kile kinachochinjwa na watu wa kitabu, kwa dalili kwamba wao hawasemi jina la Mwenyezi Mungu wakati wa kuchinja, kuongezea kwamba miongoni mwa masharti ni mchinjaji awe ni Mwislamu. Na hakika imepatwa na majaribu miji ya Kiislamu kwa kuingizwa nyama kutoka katika miji isiyo ya Kiislamu, na ambayo tunajua fika wanapochinja hawataji jina la Mwenyezi Mungu (s.w.t). Na kwa hivyo wamesimama baadhi ya wale wanaojaribu kuufanya Uislamu kuwa ni mwepesi katika kizazi hiki cha sasa, basi wakafutu kwa kutosha kusema Bismillahi wakati wa kula, na inajulikana kwamba limeachwa kutajwa jina la Mwenyezi Mungu juu yake wakati wa kuchinja. Na hili ndilo alilolinukuu Sheikh Qardhawi na dhahiri ni kwamba ameliridhia, pale aliposema: “Na wanaona baadhi ya wanazuoni kwamba, hapana budi kusema Bismillaho, lakini sio lazima iwe hivyo wakati wa kuchinja, bali inatosha kutajwa wakati wa kula, kwani ikisemwa Bismillah 72

Surat al-Anam; 6:121.

109


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

wakati wa kula juu ya kile anachokila, hakiwi ni kula ambacho hakijatajwa jina la Mwenyezi Mungu juu yake.” Kisha akasema: “Na katika Sahihi Bukhari imepokewa kutoka kwa Aisha kwamba alisema: Hakika watu wa zama za ujinga walikuja kwa Mtume  wakamwambia Mtume : Hakika watu wanatuletea sisi nyama hatujui wametaja jina la Mwenyezi Mungu juu yake au hawakutaja! Je, tule hiyo au hapana? Mtume  akasema: „Litajeni jina la Mwenyezi Mungu na kuleni.‟”73 Anajibiwa kuwa: Hakika dhahiri ya kauli ya Mwenyezi Mungu (s.w.t): “Wala msile wale wasiosomewa jina Mwenyezi Mungu” ni uharamisho wa kula kile kilichochinjwa hali ya kuwa halikutajwa jina la Mwenyezi Mungu juu yake wakati wa kuchinjwa, sawa liwe limetajwa jina lake (s.w.t) wakati wa kula au hapana. Basi kauli ya kufaa kula kwa kutosheleza kutaja jina la Mwenyezi Mungu wakati wa kula inatofautiana kabisa na aya, bali inatofautiana na yale waliyokubaliana wanazuoni wa fikihi. Ama utoaji dalili kwa kutumia hadithi ya Aisha ni kwenda kinyume na maudhui kwa sura mbili, nazo ni: 73

Halalu wal haramu fil Islami, uk. 58.

110


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

1. Hakika mchinjaji alikuwa ni Mwislamu “Hadithi katika zama za Uislamu” kama tunavyoikuta katika kauli yake: „Hakika watu wa zama za ujinga walimwambia Mtume : Hakika watu wanatuletea nyama hatujui je, wametaja jina la Mwenyezi Mungu juu yake au hawakutaja.‟ Hakika jambo linalotujia kichwani ni kwamba watu hawa waliokuwa wanaleta nyama kwa watu wenye kumuuliza Mtume, walikuwa karibu na zama za ujinga na hivyo walikuwa ni Waislamu. Lakini nyama zinazoletwa kutoka nchi za ng‟ambo hivi sasa ni zile zilizochinjwa na watu wa kitabu au washirikina. 2. Hakika swali katika hadithi husika, ni shaka iliyopo katika usemaji wa jina la Mwenyezi Mungu, basi wakati huo inaliwa kwa kuwa tendo la Mwislamu ni sahihi. Na hili liko wapi mbele ya yale ambayo sisi tunayajua ya kutotajwa jina la Mwenyezi Mungu?! Na tija ya maneno ni kwamba: Hakika fikra ya ufanyaji wepesi Uislamu juu ya kizazi cha sasa ni fikra nzuri, lakini kwa sharti isivuke mipaka na misingi iliyowekwa. Basi ni juu ya wanazuoni wa Kiislamu na Waislamu wafanye moja ya mambo mawili: 1. Kuandaa sehemu ya ardhi ya kulima ili kuzalisha nyama katika miji yao mpaka wajitosheleze kutokana na uagizaji wa nyama kutoka nchi za kigeni. 111


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

2. Ikiwa lazima kuagiza basi hapana budi kutuma ujumbe wa watu waliobobea katika sharia ili kusimamia uchinjaji ili uambatane na masharti ya Kiislamu. FASLU YA TISA MADAI YA UHARAMU WA NDOA YA MUTA74 Sheikh Qardhawi amezungumza kuhusiana na suala la ndoa ya Muta akasema: “Hakika ndoa katika Uislamu ni fundo imara na ahadi kubwa. Inasimama juu ya nia ya maisha ya kudumu kutoka pande mbili, ili yapatikane matunda yake ambayo yametajwa na Qur‟ani, nayo ni utulivu wa nafsi, upendo na rehema. Na kilele chake ni kuendeleza kizazi na kubakia kwa binadamu. Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema:

َ ُ ُ َ َ َُ َُ ً‫” َاالل ُـه َج َع َل لنم ِمً أهف ِؼنم أ ٰظا ًجض َا َج َع َل لنم ِم‬ ُ ٰ َ ًَ َ َ “….. ‫ظا ِجنم َبىين َا َحفسة‬ ‫أ‬ “Na Mwenyezi Mungu amewafanyia wake kutokana ninyi wenyewe. Na amewafanyia kutoka kwa wake zenu wana na wajukuu…..”75 74

Uhariri wa makala haya umetimia tarehe 20 mfunguo mosi mwaka 1429H. 75 Surat an-Nahl; 16:72.

112


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

Ama ndoa ya Muta ni mafungamano baina ya mwanaume na mwanamke ya muda maalumu ambao wanakubaliana, wala haipatikani katika Muta maana hiyo tuliyoiashiria. Na hakika Mtume  aliruhusu hiyo kabla ya kutulia sharia ya Kiislamu, ameiruhusu hiyo katika safari na vita kisha akaikataza na akaiharamisha milele.” Kisha akaashiria Sheikh mazingira ambayo iliruhusiwa kisha ikaharamishwa, kwa kauli yake: “Ameeleza Muslim katika sahihi yake kutoka kwa Siirat Juhani kwamba, hakika yeye alipigana vita akiwa na Mtume  katika vita vya ukombozi wa Makkah, basi akawapa idhini wao kufunga ndoa ya Muta, na hakutoka hadi alipoiharamisha hiyo Mtume . Katika lafudhi ya hadithi yake amesema: „Hakika Mwenyezi Mungu ameiharamisha hiyo mpaka siku ya Kiyama.‟ “Lakini je, uharamisho huu umekuwa ni kama vile uharamu wa kumuoa mama na binti, au uharamisho ni mfano wa uharamu wa mzoga, damu na nyama ya nguruwe, basi inakuwa halali wakati wa dharura na kuhofia na tahayuri? Ambalo wameona masahaba wote ni kuwa ni uharamu wa moja kwa moja na wala hakuna ruhusa kwayo baada ya kufanywa kuwa sharia. “Na akatofautiana nao Ibn Abbas. Basi akaona hiyo inaruhusiwa wakati wa dharura, na pindi alipoona hakika watu wameipanua na hawakujihusisha nayo 113


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

katika sehemu ya dharura tu akajizuia na fatwa yake na akaiacha.”76 Nasema: Mwenyezi Mungu (s.w.t) amefanya sharia na kuihalalisha ndoa ya Muta kwa sura ambayo ni dawa na sio chakula, na ikabakia katika uhalali wake uliopita kwa lengo hilo. Na hili wamekubaliana madhehebu yote ya kifikihi. Na hakika wametofautiana katika uendeleaji wa uhalali wake na kuwa ni yenye kufutwa au hapana. Basi Shia Imamiyya na baadhi ya Maswahaba na Tabiina wanaamini kubakia uhalali wake, tofauti na madhehebu manne kwani hayo yanaiharamisha. Na sisi katika barua hii fupi hatuko katika kubainisha uhalali wake na ruhusa yake kutoka katika Kitabu na Sunnah, kisha kubakia uhalali wake hadi hivi leo. Hakika hilo litatufanya tupanue zaidi maelezo, na hakika tunayatolea maelezo yale yaliyokuja katika maneno ya Sheikh Qardhawi kama ifuatavyo: 1. Uchukuaji wa milele katika maana ya ndoa: Sheikh ameitolea maelekezo ndoa ya daima kwa kauli yake: “Hakika ndoa katika Uislamu ni fundo imara na ahadi kubwa. Inasimama juu ya nia ya maisha ya kudumu kutoka pande mbili.” 76

Halalu wal-haramu fil-Islam, uk. 180-181.

114


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

Anajibiwa kuwa: Mosi: Hakika yeye amechukua udaima katika maana ya ndoa, nayo ni maneno ya awali, hakika ndoa ya Muta (muda) ni katika vigawanyo vya ndoa. Nayo haitimii pia isipokuwa kwa mafungamano sahihi yenye kujulisha juu ya kukusudia ndoa kweli. Na kila ukaribu unaopatikana baina ya mwanaume na mwanamke bila ya akdi haiwi Muta, hata kama yatapatikana maridhiano na kupendana, na wakati ambao inapotimia ndoa inakuwa ni lazima kuitekeleza hiyo. Pili: Lau utakuwa udaima ni miongoni mwa yale ambayo yanasimamisha ndoa, basi muda huo inatoka ndoa ya Muta kwa maana yake, na inaingia katika zinaa. Hakuna hali ya katikati baina ya ndoa na zinaa iwapo mke ni huru. Basi italazimu hilo kwamba Mtume  aliruhusu zinaa kwa masahaba wake katika ardhi takatifu, tuna maanisha Makkah tukufu. Kama vile alivyosema kinaga ubaga Sheikh wakati wa kutoa majibu yake akinukuu kutokana na sira ya Juhani, kwamba yeye alipigana katika vita vya ukombozi wa Makkah akiwa pamoja na Mtume  basi akawapa idhini hao katika kustarehe na wanawake. Je, inafaa tumsingizie Mtume  kuwa aliruhusu uchafu na uovu, wakati ambapo Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema:

ً َ َُ ٰ ّ َُ َ َ َ ‫مضن فٰـح َش ًت َا‬ ‫ػضء َػبيال‬ ‫العوى ِإهه‬ ِ ِ ‫اال جلط وا‬ 115


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

“Wala msiikurubie zinaa. Hakika hiyo ni uchafu na njia mbaya.�77 2. Malengo ya ndoa: Sheikh ametaja miongoni mwa malengo ya ndoa kuwa ni kupata utulivu wa nafsi na upendo, na kuhurumiana. Na malengo haya yanapatikana katika ndoa zote mbili, hususan ikiwa muda ni mrefu. Hakika kuizuia nafsi na zinaa na kukinga uchanganyikaji wa nasaba ni jambo lenye kushirikiana kati ya ndoa hizi mbili. Kwani ni wajibu kwa mwanamke mwenye kufunga ndoa ya Muta kukaa eda ya hedhi mbili mpaka upone mfuko wa mzazi. Na akiwa ni mjamzito hadi atakaojifungua, na ikiwa hatakuwa hivyo basi ni hedhi mbili au tohara mbili. Na ama kuhusu yale aliyoyataja kwamba malengo ya juu kabisa ya ndoa ni kuendeleza kizazi na kubakia wanadamu, anajibiwa kuwa: Mosi: Hakika hilo linapatikana pia katika ndoa ya Muta hususan ukiwa muda ni mrefu. Pili: Hakika Dr. Amechanganya baina ya sababu ya kuwekwa sharia na hekima yake. Hakika kujenga familia na kupatikana kwa kizazi ni hekima ya sharia ambayo hukumu haikomei kwenye 77

Surat Bani Israil; 17: 32.

116


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

mzunguko wake, na wala sio sababu yake. Na kwa hivyo tunaona uwepo wa ndoa sahihi pamoja na kutokuwepo hekima hii, hivyo ndoa huwa sahihi hata katika sura zifuatazo: i. Ndoa ya mwanaume asiyezaa na mwanamke anayezaa. ii. Ndoa ya mwanamke asiyezaa na mwanaume anayezaa. iii. Ndoa ya mwanamke aliyekoma kuzaa. iv. Ndoa ya msichana mdogo. v. Ndoa ya kijana wa kiume na kijana wa kike pamoja na azma ya kutozaa hadi mwisho wa umri wao. Je, inasihi ustadh kuizuia ndoa ya watu hawa kwa sababu ya kutoambatana na maana ambayo ameichagua yeye?! Na kwa hivyo imebainika kutosihi kauli yake: “Wala haipatikani katika ndoa ya Muta maana hiyo tuliyoiashiria.” 3. Madai yake kuhusu kuharamishwa milele ndoa ya Muta: Dr. ametaja kwamba hakika Mtume  aliiruhusu safarini na vitani, kisha akaikataza na kuiharamisha daima. Anajibiwa kuwa: Hakika kuruhusu na kuifanya haramu abadani kulingana na nukuu ya Dr. kulikuwa katika mwaka wa ukombozi wa Makkah. Na hakika ilikombolewa Makkah katika mwaka wa nane baada 117


‫‪MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI‬‬

‫‪ya kuhama kwake kuliko tukuka. Na kisha jambo la‬‬ ‫‪kuhalalishwa kwa wanawake lilitimia kabla ya miaka‬‬ ‫‪kadhaa, ambapo Mwenyezi Mungu (s.w.t) alianza‬‬ ‫‪kubainisha wanawake walio halali na wasiokuwa‬‬ ‫‪halali kwa kusema:‬‬

‫ُٰ ُ‬ ‫ُ​ُ َ َ ُ​ُ‬ ‫َ ُ ُ ُٰ ُ‬ ‫ُح ِّط َمذ َعلينم أ َمّهـخنم َا َ ىضجنم َاأد ٰوجنم َا َع ّمـخنم‬ ‫َ ٰ​ُٰ ُ َ​َ ُ َ َ​َ ُ ُ‬ ‫ُ ٰ ُ ُ ّٰ‬ ‫دذ َاأ َمّهـخن ُم الـتى‬ ‫ادـلـخنم ا ىضث ألا ِخ ا ىضث ألا ِ‬ ‫ُ‬ ‫َ َ َُ َ َ ُ​ُ‬ ‫َ َ ٰ ُ ٰ ُ‬ ‫الطرـ َع ِت َاأ َمّهـذ ِوؼض ِئنم‬ ‫أضرعىنم َاأد ٰوجنم ِمً‬ ‫ُ ّٰ‬ ‫َ َ ٰ ُ ُ ُ ّٰ‬ ‫ُ‬ ‫َ ُ‬ ‫ُ‬ ‫جوضلم ِمً ِوؼض ِئن ُم الـتى َزدلخم‬ ‫اض ـ ِئبنم الـتى ح ِ‬ ‫َ َ ُ َ َ ُ‬ ‫َ َ َ‬ ‫َ ُ‬ ‫ىضح َعلينم‬ ‫ِب ِه ًَ ف ِئن لم جنوهوا َزدلخم ِب ِهً فال ج‬ ‫َ‬ ‫َا َحلٰـئ ُل َأبىضئ ُن ُم َال َ‬ ‫صيً مً َأصلٰـب ُنم َا َأن َج َ‬ ‫جمعوا َبين‬ ‫ِ‬ ‫ِ‬ ‫ِ‬ ‫ِ‬ ‫ُ َ ّ‬ ‫َ َ​َ َ َ َ​َ َ‬ ‫مضن َغفوضاً‬ ‫ألادخ ِين ِإال مض س ػلف ِإن اللـه‬ ‫ّ‬ ‫َ ُ َ ٰ ُ َ ّ‬ ‫َ​َ​َ‬ ‫َض ً‬ ‫ؼضء ِإال مض ملنذ‬ ‫حيمض ﴿‪ ﴾٢٣‬ااملحصىـذ ِمً ال ِي ِ‬ ‫َ ُٰ ُ ٰ‬ ‫َ َ ٰ ُ‬ ‫َ َ ُ ُ َُ‬ ‫ضاء ش ِلنم‬ ‫أيمـىنم ِلخـ َب الل ِـه َعلينم َاأ ِح َل لنم مض ا‬ ‫ٰ َ َ‬ ‫َ َ‬ ‫َ َ َ‬ ‫َ ٰ ُ ُ‬ ‫حصىين غ َيي ُمؼـ ِفحين ف َمض‬ ‫أن جبخغوا ِبأمو ِلنم م ِ‬ ‫ُ َ َ ٔـ ُ َ ُ َ ُ َ َ َ ً‬ ‫َ َ ُ‬ ‫طيضت َاال‬ ‫اػخمخعخم ِب ِه ِمنهً فـضجوهً أجوضهً ف‬ ‫ُ َ َ​َ ُ‬ ‫َ‬ ‫َ َ ُ‬ ‫الف َ‬ ‫َ‬ ‫طيض ِت ِإ َن‬ ‫عس‬ ‫جىضح علينم فيمض ج ٰطريخم ِب ِه ِمً ب ِ‬ ‫َ‬ ‫ُ‬ ‫َ‬ ‫َ​َ َ‬ ‫ليمض َح ً‬ ‫مضن َع ً‬ ‫نيمض ﴿‪َ ﴾٢٤‬ا َمً لم َيؼخ ِطع ِمىنم‬ ‫اللـه‬ ‫َ ً َ َ َ ُ َ ٰ ُ ٰ َ‬ ‫َ​َ​َ‬ ‫ؤمىـ ِذ ف ِمً مض ملنذ‬ ‫طوال أن ي ِ‬ ‫ىنح املحصىـ ِذ امل ِ‬ ‫َ​َٰ ُ ُ ُ ٰ َ َُ َ َُ ٰ ُ‬ ‫َ ُٰ ُ‬ ‫ؤمىـ ِذ االلـه أعلم ِبئيمـ ِىنم‬ ‫أيمـىنم ِمً فخيـ ِخنم امل ِ‬ ‫َ‬ ‫َ‬ ‫َ ُ ُ‬ ‫ُ َ‬ ‫هل ِّه ًَ‬ ‫عضنم ِمً َب‬ ‫ب‬ ‫شن أ ِ‬ ‫عض ف ِ‬ ‫ضهنحوهً ِب ِئ ِ‬ ‫ٍ‬ ‫َا ُ‬ ‫جوض ُه ًَ بضملَعطاف ُم َ‬ ‫ءاجوه ًَ ُأ َ‬ ‫حصىٰـ ٍذ َغييَ‬ ‫ِ‬ ‫ُ ٰ ٰ َ ُ َ ِٰ َ‬ ‫َ ُ‬ ‫َ َ َ​َ َ‬ ‫حصً ف ِئن أجين‬ ‫دسان ف ِئشا أ ِ‬ ‫مؼـ ِفحـ ٍذ اال مخ ِذص ِث أ ٍ‬ ‫‪118‬‬


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

ٰ َ ُ َ​َ َ َ َ ٰ ُ ًَ ‫حصىـ ِذ ِم‬ ‫ِبفـ ِحش ٍت ف َعل ِيه ًَ ِهصف مض ع امل‬ َ َ​َ ُ َ َ​َ َ َ َ َ ٰ َ ‫صكياا‬ ِ ‫الع‬ ِ ‫صاب ش ِلو ِملً د ِش ى العىذ ِمىنم اأن ج‬ َ ُ ُ َ َ ُ َ ‫َ ٌع‬ َ ‫الل ُـه َغ ٌع‬ ‫فوض َض ٌع‬ ‫طيس الل ُـه ِل ُي َب ِّين‬ ‫﴾ ي‬٢٥﴿ ‫حيم‬ ‫ديي لنم ا‬ َ َ َ ُ ُ َ َ​َ ُ َ ُ َ​َ َ َ​َ ُ َ َ ‫لنم اّي ِهسينم ػنن الصيً ِمً ِبلنم ايخوب علينم‬ َ َ ‫ليم َح ٌع‬ ‫الل ُـه َع ٌع‬ ﴾٢٦﴿ ‫نيم‬ ‫ا‬ “Mmeharamishiwa mama zenu na binti zenu na dada zenu na shangazi zenu na khalati zenu na binti wa kaka na binti wa dada na mama zenu waliowanyonyesha na dada zenu wa kunyonya na mama za wake zenu na binti zenu wa kambo walio katika ulinzi wenu, waliozaliwa na wake zenu mliowaingilia – hapana vibaya juu yenu ikiwa hamkuwaingilia – na wake wa watoto wenu waliotoka katika migongo yenu, na kukusanya kati ya dada wawili (wakati mmoja) ila waliokwisha pita. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira, Mwenye kurehemu. Na (pia mmeharamishiwa) wanawake wenye waume; isipokuwa wale iliyowamiliki mikono yenu ya kuume. Ni sharia ya Mwenyezi Mungu kwenu. Na mmehalalishiwa wasiokuwa hao, 119


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

kwamba muwatafute kwa mali zenu kwa kuoa bila ya kufanya zinaa. Ambao mmestarehe nao katika wao, basi wapeni mahari yao yaliyolazimu. Wala si vibaya kwenu katika yale mliyoridhiana baada ya (kutoa) kile kilichowalazimu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye hekima. Na asiyeweza miongoni mwenu kupata mali ya kuoa wanawake waungwana waumini, basi (na aoe) katika wajakazi wenu waumini iliyowamiliki mikono yenu ya kuume; na Mwenyezi Mungu anajua sana imani yenu. Baadhi yenu mnatokana na baadhi; basi waoeni kwa idhini ya watu wao na muwape mahari yao kama ada, wawe ni wenye kujistahi si waasherati, wala wenye kujifanyia mahawara. Watakapoolewa kisha wakafanya uchafu, basi itakuwa adhabu juu yao ni nusu ya adhabu iliyowekwa kwa (wanawake) waungwana. Hayo ni kwa wenye kuchelea mashaka katika nyinyi. Na mkisubiri ni bora kwenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu. Mwenyezi Mungu anataka kuwabainishia na ku120


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

waongoza mwendo wa waliokuwa kabla yenu na awatakabalie toba. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye hekima.”78 Na hakika zimeteremka aya hizi miaka kadhaa kabla ya ukombozi wa Makkah. Na miongoni mwa yanayostaajabisha ni kwamba hakika Ustadhi hakuzama na kuielewa kwa undani aya inayojulisha uhalali wa ndoa ya Muta katika aya zilizotangulia. Ninamaanisha kauli ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) inayosema: “Na ambao mmestarehe nao katika wao, basi wapeni mahari yao yaliyolazimu.” Wafasiri wengi wamesema na kueleza kuwa, aya hiyo iliteremka kuhusiana na ndoa ya Muta, na ikiwa wanatofautiana ni katika ufutwaji wake au ubakiaji wa uhalali. Na sisi hatuko katika kubainisha jinsi aya ilivyo dalili juu ya uhalali wa hukumu ya ndoa ya Muta, kwani hakika hilo litatukokota sisi katika upanuaji wa maneno. 4. Je, Mtume  aliharamisha ndoa ya Muta? Dr. Qardhawi amedai kuwa hakika Bwana Mtume  ndiye aliyeiharamisha ndoa ya Muta ambapo amese78

Surat an-Nisa; 4:23-26.

121


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

ma: “Hadi alipoiharamisha hiyo Mtume . Katika lafudhi ya hadithi yake amesema: „Hakika Mwenyezi Mungu ameiharamisha hiyo mpaka Siku ya Kiyama.‟” Ninasema: Vipi linasibishwe hilo kwa Mtume  ilihali kundi la Masahaba watukufu limefutu uhalali wa ndoa ya Muta hadi Siku ya Kiyama. Tunataja miongoni mwao kama wafuatao: i) Abdullah bin Umar: Ameeleza Imam Ahmad kutoka katika hadithi ya Abdullah bin Umar, amesema Na hakika aliulizwa kuhusiana na ndoa ya Muta:Naapa kwa Mwenyezi Mungu hatukuwa katika zama za Mtume  tukizini wala tutifanya uchafu.” Kisha akasema: “Naapa kwa Mwenyezi Mungu hakika nilimsikia Mtume  akisema: „Atakuja kabla ya Kiyama Masihi Dajjal na waongo thelathini na zaidi.‟”79 ii) Abdullah bin Mas‟ud: Ameeleza Bukhari kutoka kwa Abdullah bin Mas‟ud, amesema: “Tulikuwa tunapigana vita tukiwa pamoja na Mtume  na hatukuwa sisi na chochote, basi tukasema: Je, tujihasi? Basi Mtume  akatukataza hilo, kisha akaturuhusu sisi tuoe mwanamke kwa nguo kwa wakati maalum, kisha akasoma aya hii: 79

Musnad Ahmad, Juz. 2, uk. 95.

122


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

َ ٰ َ َ ُ َ ‫يٰـ َأ ُّلّي َهض َال‬ َ ً‫صي‬ ‫ءامىوا ال ج َح ِّطموا ط ِّيبـ ِذ مض أ َح َل الل ُـه‬ َُ َ ُ ‫َ َ َ ُ ُّل‬ َ َ َ ‫عخ‬ ً‫سي‬ ‫لنم َاال حعخساا ِإن اللـه ال ي ِحب امل‬ Enye mlioamaini! Msiharamishe vizuri alivyowahalalishia Mwenyezi Mungu. Wala msipetuke mipaka. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wanaopetuka mipaka.”‟80 81 iii) Imran bin Haswiin: Ameeleza Bukhari katika Sahihi yake kutoka kwake, amesema: “Iliteremka aya ya Muta katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Basi tukaifanyia kazi pamoja na Mtume , na wala haikuteremka aya ya Qur‟ani inayoiharamisha hiyo na wala hakuikataza hiyo mpaka alipofariki. Akasema mtu kwa rai yake yale aliyoyapenda.”82 iv) Ameeleza Muslim kutoka kwa Ibn Jurayj, amesema: Amenisimulia Abu Zubeir amesema: Nilimsikia Jabir bin Abdillah akisema: “Tulikuwa tukifanya Muta kwa gau la tende na unga siku kadhaa katika zama za Mtume  na wakati wa Abu Bakri hadi 80 81

82

Surat al-Maidah; 5:87. Sahih Bukhari, Juz. 7, uk. 4, mlango wa yale yanayochukiza kuacha kuoa na kujihasi, kutoka katika kitabu cha ndoa. Sahih Bukhari, Juz. 6, uk. 27, tafsiri ya kauli ya Mola Manani (s.w.t) inayosema: “Basi atakaestarehe kwa kutoka katika umra mpaka kuhiji.” Sura 2 aya 196.

123


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

alipoikataza Umar katika jambo linalohusiana na Umar bin Harith.”83 v) Ameeleza Muslim katika Sahihi yake kutoka kwa Ubay Nadhrat, amesema: “Nilikuwa kwa Jabir bin Abdillah basi wakamjia Ibn Abbas na Ibn Zubeir wakatofautiana kuhusu Muta mbili, Jabir akasema: Waliifanya hiyo pamoja na Mtume  kisha akaikataza Umar wala hatukuirudia tena.”84 Hii ni mifano ya hadithi zilizopokewa kutoka katika tabaka la juu la Masahaba wa Mtume , ambao walikuwa wakifutu mas‟ala kwa kujuzu ndoa ya Mutaa, na lau Mtume  angelikuwa ni mwenye kuiharamisha lisingelifichika kwao hilo, na lau wangelijua wala wasingelimkhalifu wote. 5. Mharamishaji ni khalifa mwenyewe: Hakika Dr. hata kama ananasibisha uharamu wa ndoa ya Muta kwa Mtume  lakini yeye lau ataangalia kwa makini na kuchunguza undani wa hadithi na athari mbalimbali, atagundua kwamba mharamishaji ni khalifa wa pili Umar bin Khatwab, na sio mwingine. Hili ndilo ambalo tunalipata kutokana na 83

Sahihi Muslim, Juz. 4, uk. 131, mlango wa ndoa ya mutaa kutoka kitabu cha ndoa. 84 Sahihi Muslim, Juz. 4, uk. 131, mlango wa ndoa ya mutaa kutoka kitabu cha ndoa.

124


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

uangaliaji wa suala husika kwa mtazamo wa karibu, na hakika imepita kwako katika hadithi mbalimbali zilizotangulia kulingana na uharamishaji wake, na hii ni nyongeza: 1. Amesema Imam Ali Amirul-Muuminina  – kwa yale ambayo ameyaeleza Bukhari kwa isnadi yake: “Lau sio Umar kuikataza ndoa ya Muta asingelizini isipokuwa muovu.”85 Na huko zipo hadithi nyingi zilizopokewa kutoka kwa Khalifa mwenyewe, zinazoelezea kuwa uharamishaji ulitokana na rai yake, bila ya kuegemezea aya yoyote au hadithi. 2. Muslim ametoa kutoka kwa Ibn Jurayhj, amesema: Amenipa habari Abu Zubeir akasema: Nimemsikia Jabir bin Abdillah akisema: Tulikuwa tukifanya Muta kwa gau la tende na unga siku kadhaa katika zama za Mtume  na Abu Bakri mpaka alipoikataza Umar katika jambo la Amru bin Harith.86 3. Ameeleza Muslim katika Sahihi yake kutoka kwa Abi Nadhrat amesema: Nilikuwa kwa Jabir bin Abdillah, wakamjia Ibn Abbas na Ibn Zubeir wakatofautiana katika Muta mbili, akasema Jabir: 85

Tafsiri Twabari, Juz. 5, uk. 9. Sahihi Muslim, Juz. 4, uk. 131, mlango wa ndoa ya mutaa kutoka kitabu cha Nikah. 86

125


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

Tuliifanya hiyo katika zama za Mtume  kisha akatukataza hiyo Umar na hatukuirudia.87 4. Ameeleza Tarmidhi kwamba hakika mtu mmoja miongoni mwa watu wa Sham alimuuliza Ibn Umar kuhusiana na ndoa ya Muta, akasema: “Ni halali.” Akasema: Hakika baba yako ameikataza hiyo? Mtoto wa Umar akasema: “Je, umemuona ikiwa baba yangu ameikataza hiyo na hakika aliifanya Mtume  je, tuifuate amri ya baba yangu au amri ya Mtume ?”88 Na hadithi hizo zinaelezea maangalizo mbalimbali tunayajumuisha kwenye maangalizo mawili: Mosi: Hakika ndoa ya Muta uhalali wake ulikuwa unajulikana mpaka katika zama za khalifa wa pili Umar bin Khatwab. Na ulibakia uhalali wake katika siku zake mpaka alipoikataza na kuizuia. Pili: Hakika hiyo ni ijitihadi yake. Akasimama kwa kuharamisha yale yaliyohalalishwa na Kitabu na Sunnah. Na linalojulikana ni kwambba ijitihadi yake – lau ingelisihi kuita kwa jina la ijitihadi – ni hoja juu ya nafsi yake na sio kwa mwingine. Na miongoni mwa yale yanayojulisha kwa uwazi kwamba khalifa ndiye mharamishaji wake ni yale 87

Sahihi Muslim, Juz. 4 uk. 131, mlango wa ndoa ya mutaa kutoka kitabu chake na Nikah. 88 Sunan Tirmidhi, Juz. 3, uk. 186 na. 824.

126


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

aliyoyataja Ibn Qaym katika kitabu Zaad Maad, ambapo amesema: “Ikiwa itasemwa: Mnafanya nini katika yale aliyoyapokea Muslim katika Sahih yake kutoka kwa Jabir bin Abdillah, akasema: Tulikuwa tukifanya Muta kwa gau la tende na unga siku kadhaa katika zama za Mtume  na Abu Bakri mpaka alipoikataza Umar katika jambo linalohusiana na Amru bin Harith. Na kati ya yale yaliyothibiti kutoka kwa Umar kuwa amesema: Muta mbili zilikuwa katika zama za Mtume  mimi ninazikataza; Muta ya wanawake na Muta ya Hija? Itasemwa: Watu katika hili wamegawanyika katika makundi mawili: Kundi la kwanza linasema; hakika Umar yeye ndiye aliyeiharamisha na kuikataza hiyo na hakika Mtume  aliamrisha kufuata yale waliyoyaanzisha makhalifa waongofu. Na halijaona kundi hili usahihi wa hadithi ya Sabrat bin Ma‟bad katika uharamishaji wa ndoa ya Muta katika mwaka wa ukombozi wa Makkah. Hakika hilo linatokana na hadithi ya Abdul-Malik bin Rabii bin Sabrat kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake, na hakika Ibn Muiin amemtia kasoro na Bukhari hakupokea hadithi yake katika Sahih yake pamoja na kuwa na haja kubwa nayo na kuwa kwake ni msingi miongoni mwa misingi ya Uislamu. Na lau ingekuwa ni sahihi kwake basi asingesubiri wala kusita kuiandika na kuifanya hoja. 127


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

Wamesema: Hadithi hii ingekuwa ni sahihi basi asingeogopa Ibn Mas‟ud mpaka aseme kwamba wao waliifanya na atoe hoja kwa kutumia aya. Na pia ingekuwa ni sahihi basi Umar asingesema kwamba hakika hiyo ilikuwa katika zama za Mtume  na mimi ninaikataza na ninaadhibu juu yake. Bali alikuwa aseme: Hakika Mtume  ameiharamisha na ameikataza hiyo. Wamesema pia: Na kama ingekuwa ni sahihi basi isingefanywa katika zama za Abu Bakri Sadiq, nazo ndio zama za ukhalifa wa Mtume  kweli.”89 Hakika khalifa wa Bani Abbas, Maamun alikaribia kunadi katika siku za utawala wake, kuhalalisha ndoa ya Muta ila hakika yeye aliacha kuhofia fitina na kuleta mfarakano kwa Waislamu. Akasema Ibn Khalkan, akinukuu kutoka kwa Muhammad bin Mansur amesema: “Tulikuwa pamoja na Maamun tukiwa njiani kuelekea Sham basi akaamuru unadiwe uhalali wa ndoa ya Muta. Akaniambia Yahya bin Aktham na baba yangu Aynai: Amkeni kesho mapema kwake, mkiona kauli inamwelekeo basi semeni, na kama si hivyo nyamazeni mpaka niingie.” Anasema: “Basi tukaingia kwake naye akipiga mswaki akasema hali akiwa na ghadhabu: „Muta mbili 89

Zaadul-Maad, Juz. 1, Uk. 444, na mazungumzo yana muunganiko uliokuja katika yale ambayo uangaliaji wa kundi la pili basi chunguza hilo.

128


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

zilikuwa zama za Mtume  na katika zama za Abu Bakri na mimi ninazikataza, na wewe ni nani hadi unaharamisha lile alilolifanya Mtume  na Abu Bakri?‟ Basi akatoa ishara kwa macho yake Abu Aynai kwa Muhammad bin Mansur akasema: Mtu mmoja anasema kuhusiana na Umar bin Khatwab yale anayoyasema, na sisi tunasema naye? Basi tukanyamaza. Akaja Yahya bin Aktham akakaa, nasi tukakaa. Maamun akasema kumwambia Yahya: „Kwa nini ninakuona ni mwenye tahayuri?‟ Akasema: „Ewe Amirul-Muuminina ninayo huzuni kwa yale yaliyozuka katika Uislamu.‟ Akasema: „Ni kitu gani kilichozushwa?‟ Akasema: „Wito wa kuhalalisha zinaa.‟ Akasema: „Zinaa?‟ Akasema: „Ndiyo, Mutaa ni zinaa.‟ Akasema: „Na unalolisema unalitoa wapi?‟ Akasema: „Kutoka katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu (s.w.t) na hadithi ya Mtume . Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema:

َ ُ َ​َ َ َ ُ َ َ َ ‫الت ِهم‬ ِ ‫﴾ الصيً هم ص‬١﴿ ‫ؤمىون‬ ِ ‫س أفل امل‬ ٰ َ َ ُ َ َ َ َ َ ُ ‫اللغو‬ ‫ن‬ ﴾٣﴿ ‫عطرون‬ ‫م‬ ً ‫ع‬ ‫م‬ ‫ه‬ ً‫صي‬ ‫ال‬ ‫ا‬ ﴾ ٢ ﴿ ‫عو‬ ‫ش‬ ‫ـ‬ ‫د‬ ِ ِ ِ ِ َ َ َ َ َ ٰ ٰ َ ُ َ ُ َ ‫االصيً هم ِللعلو ِة فـ ِعلون‬ ‫﴾ االصيً هم‬٤﴿ َ َ ٰ َ ّ ٰ َ ُ ٰ ‫﴾ ِإال ع أظا ِج ِّهم أا مض‬٥﴿ ‫طاج ِّهم حـ ِف ون‬ ‫ِلف‬ ِ َ َ ٰ َ َ​َ َ َ َ ٰ ‫ابخغ‬ ًِ ‫﴾ ف َم‬٦﴿ ‫َملنذ أيمـ ُن ُهم ف ِئ َّن ُهم غ ُيي َملومين‬ ٰ َُ ٰ َ َ َ ﴾٧﴿ ‫ضاء ش ِل َو فأالـ ِئ َو ُه ُم العضزان‬ ‫ا‬ 129


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

„Hakika wamefaulu wenye kuamini, ambao ni wanyenyekevu katika swala zao, na ambao hujiepusha na mambo ya upuuzi, na ambao wanatoa zaka, na ambao wanazilinda tupu zao, isipokuwa kwa wake zao au kwa (wanawake) wale waliomilikiwa na mikono yao, basi hao si wenye kulaumiwa, lakini anayetaka kinyume cha haya, basi hao ndio warukao mipaka.‟90 Ewe Amirul-Muuminina mke wa ndoa ya Muta ni yule ambaye anayemilikiwa (kijakazi)?‟ Akasema: „Hapana, basi yeye ni mke ambaye mbele ya Mwenyezi Mungu anarithi na anarithiwa na mtoto anakuwa wake na ina masharti yake?‟ Akasema: „Hapana.‟ Akasema: „Hakika mwenye kuvuka haya ni mwenye kuruka mipaka.”‟91 Ninasema: Je, amesahau Ibn Aktham – na hakika alikuwa ni miongoni mwa wale maadui wa ndugu wa karibu wa Mtume  – kwamba hakika Muta imeingia ndani ya kauli ya Mola Manani (s.w.t): “Isipokuwa kwa wake zao”, na hakika kukosekana urithi ni kuifanyia umahususi hukumu, nako hakusigani na uthibiti wa ndoa. Na kuna mifano 90 91

Sura 23 aya 1-7. Wafayatul-A’yan Juz. 6 Uk. 149-150.

130


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

mingi katika hilo, kafiri hamrithi mume Mwislamu, na kinyume chake. Kama ambavyo muuaji hamrithi aliyemuua, vile vile kinyume chake. Na ama mtoto katika ndoa ya Mutaa hakika anaungana na anahusika kwa kukata shauri na wazazi wake, na uondoaji uhusika ima unatokana na kutojua hukumu yake au kujifanya mhusika hajui. Na yale ambayo yameharibu maneno yake namna ambayo ameifasiri ndoa ya mutaa kuwa ni zinaa, na hakika umma umekubali uhalali wake katika zama za Mtume  na khalifa wa kwanza, je, ibn Aktham anadhani Mtume  amehalalisha zinaa na lau kwa muda mfupi! FASLU YA KUMI NYIMBO NA MIZIKI KATIKA KITABU NA SUNNAH92 Miongoni mwa mambo ambayo Dr. Qardhawi amekwenda kinyume na lile lililo mashuhuri baina ya wanazuoni wa fikihi, ni suala la nyimbo na miziki ambapo amesema: “Na miongoni mwa upuuzi ambao nafsi zinastarehe na nyoyo kuvutika nao, na masikio kuneemeka nao, 92

Umetimia uhariri wa makala haya terehe 4 mfunguo pili mwaka 1429H.

131


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

ni suala la muziki… na hakika Uislamu umehalalisha ikiwa tu hauna mahusiano na uovu, maneno machafu, au lugha mbaya au kuchochea kutenda dhambi wala hakuna tatizo kusikiliza muziki usioleta msisimko. “Na inakuwa ni mustahabu katika sherehe za furaha katika kuongeza furaha, na kukonga nyoyo. Na hilo ni kama vile katika siku za Iddi, harusi na kurudi aliyekuwa ughaibuni, na wakati wa sherehe, ndoa, akika na mwanamke anapojifungua.”93 Na akasema katika chapa nyingine ya kitabu chake na haya ndio maandiko yake: “Na ambalo ninaloliona ni kwamba muziki kama ulivyo hauna tatizo, na unaingia katika mambo mazuri ambayo Uislamu umeyahalalisha. Na hakika dhambi ni pale ambapo yanajumuishwa au kuungana na vitu ambavyo visivyohusika ambavyo vinauhamisha na kuutoa katika uhalali mpaka katika uharamu, au kutoka katika makruhu hadi katika uharamu.” Na Dr. Qardhawi katika kitabu chake kingine akasema: “Inawajibika juu ya mwanafikihi ambaye anafanya utafiti katika suala fulani, achunge mambo haya yote. Wala asiukite mtazamo wake juu ya upande mmoja, na kundi moja, mwenye kusahau kwamba waafrika wote hawatosheki na muziki na vile vinavyoongozana nao. Na hakika Ulaya yote, bali 93

Halal wal Haramu fil-Islam, uk. 280.

132


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

nchi za kimagharibi zote zinazingatia muziki – hususan baadhi ya aina yake – kuwa ni njia ya kukua kiroho na kimwili.”94 Kisha anasema katika sehemu nyingine: “Sisi leo tunataka tuoneshe Uislamu ulimwenguni, na ulinganio wake uwafikie umma zote. Na kati ya umma kuna mataifa ambayo yanaona muziki, kucheza muziki na taarabu ni sehemu ya maisha yao, wala huwezi kuutenganisha na maisha yao, wala kuishi bila ya hayo. Wala maisha hayawi tulivu ikiwa utaharamishwa, basi vipi unawavutia hao katika Uislamu na sisi tunawaharamishia muziki na nyimbo, na tunawatishia hao kwa risasi ya adhabu ambayo inawasibu masikioni mwao Siku ya Kiyama. Na aina nyingine za adhabu ziumizazo, katika wakati ambao wao wanazingatia muziki ni chakula cha roho.”95 Na hakika Sheikh ametolea dalili juu ya fatwa zake kwa hadithi ambazo matini zake zote au nyingi kati ya hizo, zinashuhudia kuwa ni uongo aliozushiwa Mtume Mtukufu. na tutarejea katika kuzijadili hizo. Na maneno yamejikita sasa katika yale ambayo ameelekeza katika uhalalishaji wa nyimbo na muziki katika kitabu cha pili, ambapo amejaalia kuwavutia 94

95

Fiqhul-Ghinaai wal-Musiiqi fi dhwaui Qur’ani wa Sunnah, uk. 7 chapa ya Qairo mwaka 2004. Fiqhul-Ghinaai wal-Musiiqi fi dhwaui Qur’ani wa Sunnah, uk. 148 chapa ya Qairo mwaka 2004.

133


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

wasiokuwa Waislamu kuukubali Uislamu ni sababu ya uhalalishaji wa nyimbo na muziki, akasema: “Vipi tuwavutie hao katika Uislamu na sisi tunawaharamishia nyimbo na muziki?” Na lau ikiwa hii ndio sababu ya kufutu uhalali wa muziki basi iwe pia ni sababu katika uhalali wa pombe, uchezaji wa muziki wa aina zake, ambapo wao wanazingatia hayo kuwa ni mambo ya dharura katika maisha, mpaka kundi ambalo linalojiita Mababa wa Kiroho linaangalia pombe kwa mtazamo huu. Na hakika mimi pindi niliposoma fatwa hii ya Sheikh Qardhawi yalinijia kichwani kwangu yale aliyoyapokea Ibn Athiir katika wasifu wa Tamiim bin Jarashat ambapo amesema: Nilikwenda kwa Mtume  nikiwa katika kundi la watu. Basi tukamsalimia na tukamuomba atuandikie kitabu ambacho ndani yake yapo masharti, akasema: Andikeni yale yanayowajia vichwani mwenu kisha nipeni. Basi tukamuomba katika kitabu chake atuhalilishie sisi riba na zinaa, basi akakataa Ali kutuandikia. Basi tukamuomba Khalid bin Said bin Aswi, Ali akamwambia: Unajua unayoandika? Akasema: Ninaandika yale ambayo waliyoyasema, na Mtume  ni bora zaidi kwa jambo lake. Basi tukaenda na kitabu hadi kwa Mtume  akamwambia msomaji: “Soma” na pindi alipofika katika riba 134


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

akasema : “Weka mkono wangu juu yake.” Basi akaweka mkono wake akasema: “Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na acheni yaliyobakia katika riba ikiwa ni wenye kuamini.”96 Kisha akaifuta hiyo, nikasema kimoyo: Ni juu yetu kuwa na utulivu kwa yale tuliyomrejea. Na pindi alipofika kwenye neno zinaa akaweka mkono wake juu yake akasema: “Na wala msikaribie zinaa hakika huo ni uchafu na njia mbaya”97 kisha akaifuta na akaamrisha kitabu chetu kifutwe hilo.98 Uharamu wa nyimbo katika Kitabu na Sunnah na kauli za wanazuoni: Ninasema: Hakika kuimba ni miongoni mwa mambo ambayo wanazuoni wa Kiislamu wameafikiana juu ya uharamu wake, wakiwemo Maimamu wa Ahlul-Bayt . 1. Amepokea Ali bin Ja‟far, kutoka kwa kaka yake Imam Kadhim, Musa bin Ja‟far  amesema: Nilimuuliza yeye kuhusu mtu anayeimba muziki, je akae naye? Akasema: “Hapana.”99 96 97 98 99

Sura 2 aya 278. Sura 17 aya 32. Usudul-Ghabah, Juz. 1, uk. 216. Wasaail Shia, uk. 12, mlango wa 99 kutokana na mlango wa yale yanaochumwa kwayo, hadithi 32.

135


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

2. Na katika Muwathaqat ya Abdullah bin A‟yan, amesema: Nilimuuliza Abu Abdillah  kuhusiana na muziki na nyimbo nikasema: Hakika wao wanadhani hakika Mtume  aliruhusu iimbwe: tumekujieni, tumekujieni, tuhuisheni tuhuisheni tumekujieni. Akasema: “Wamesema uongo, hakika Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema:

َ َ َ َ َ َ​َ َ َ ٰ َ ‫ألا‬ ﴾١٦﴿ ‫ضض َامض َب َين ُهمض لـ ِعبين‬ ‫امض دللىض الؼمضء ا‬ ٰ َ َ َ ً َ َ َ​َ َ َ​َ َ َُّ ُّ ُ ‫لو أضزهض أن هخ ِذص لّهوا الجذصهـه ِمً لسهض ِإن لىض‬ ُ َ َ َ ٰ ُ‫سم ُغه‬ َ َ ‫ضاح ّق َع َ البٰـطل َف َي‬ ِ ‫﴾ بل ه‬١٧﴿ ‫فـ ِعلين‬ ِ ِ ِ ‫لصف ِب‬ َ َ َ ‫َفئشا ُه َو ظاه ٌعق َا َل ُن ُم‬ ُ ‫الو‬ ﴾١٨﴿ ‫يل ِم ّمض ج ِصفون‬ ِ ِ “Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyomo baina yao kwa mchezo. Kama tungelitaka kufanya mchezo tungelijifanyia Sisi Wenyewe, kama tungekuwa ni wenye wafanya mchezo. Bali tunaitupa haki juu ya batili ikaivunja na mara (batili) ikatoweka. Na ole wenu kwa ajili ya mnayoyasifia.”‟100 Kisha akasema: “Ole wake fulani! Kutokana na yale ambayo anayaeleza. Mtu ambaye hakuwepo katika kikao.”101 100 101

Surat Anbiyaa; 21:16-18. Wasail Shia, uk. 12. Mlango 99 kutokana na milango ya yale yanayochumwa kwayo, hadithi ya 15.

136


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

Na zisizokuwa hizo miongoni mwa hadithi ambazo amezinukuu mwandishi wa kitabu Wasail katika enklopedia yake ya kisasa, nazo zinafikia hadithi thelathini. Na ama hukumu yake mbele ya wanazuoni wa Ahlu Sunnah ni kwamba, hakika Abdullah bin Mas‟ud ameharamisha, na akafuatiwa katika hilo na jamhuri ya wanazuoni wa Iraq, miongoni mwao: Ibrahim Nakhai, Aamir Sha‟bi, Hamad bin Abi Suleiman, Sufyan Thawri, Hasan Baswari, Hanafiya na baadhi ya Mahanbali. Na Mashafii, Maliki na baadhi ya Mahanbali wameona kuwa ni makruhu. Na kama usikilizaji wake ni kutoka kwa mwanamke ajinabi basi ni karaha kubwa sana. Na Maliki wakatoa sababu ya umakuruhu wake kwamba, kusikia kwake kunaharibu murua. Na Mashafii wakatoa sababu kwa kauli zao; Kwa kuwepo upuuzi humo. Na Imam Ahmad akatoa sababu kwa kauli yake: Haunishangazi mimi muziki kwani unaotesha moyoni mbegu ya unafiki.102 Na huenda makruhu iliyopo katika maneno yao ni umakuruhu wa uharamu na sio wa kawaida. Haya ni baadhi ya maneno yanayohusiana na suala hili, na la umuhimu ni yale yaliyokuja katika sharia 102

Angalia Mausu’at Fiqhiyat Kuwaitiya, Juz. 4, uk. 91, mada: Usikilizaji, na hakika zimetajwa humo rejea kwa urefu.

137


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

takatifu miongoni mwa yaliyoelezwa na hadithi mbalimbali, na ifuatayo ni dalili ya uharamu wa kuimba muziki: 1. Hadithi ya Ibn Abi Amamat, Mtume  amesema: “Msiuze vyombo vya muziki wala msinunue wala msifundishe hayo. Wala hakuna heri katika biashara hiyo, na malipo yake ni haramu. Na katika mfano huu imeteremka aya hii:

ّ َ َ َ َ َ َ َ َ ‫الى‬ ً‫سيث ِل ُي ِض َل َع‬ ً‫ا ِم‬ ِ ‫ضغ مً يشتي لّهو ااح‬ ِ َ َ ٰ ُ ًُ ُ َ َ​َ​َ َ َ َ ُ ‫بيل الل ِـه ِبغ ِيي ِع ٍلم ايخ ِذصهض هعاا أالـ ِئو لّهم‬ ِ ‫ػ‬ ‫صاب ُم ٌع‬ ‫َع ٌع‬ ‫ّهين‬ “Na miongoni mwa watu wapo wanaonunua maneno ya upuuzi, ili wawapoteze watu na njia ya Mwenyezi Mungu pasipo kujua, na wanaichukulia ni mzaha. Hao watapata adhabu ya kufedhehesha.”103 Na wanahadithi wameieleza hiyo: Ahmad, Tirmidhi, Ibn Majah, Ibn Abi Shayba, Bayhaqi na wengineo.104 103 104

Surat Luqman; 31: 6. Angalia Musnad Ahmad, Juz. 5, uk. 252, Sunan Tirmidhi, Juz, 3, uk. 579 na. 1282, na Sunan Ibn Maajah, Juz. 2, uk. 733 na. 2168, Muswannaf ibn Abi Shaybah, Juz. 6, uk. 301 na. 1171 na Sunan Kubra, Juz. 6, uk. 14 cha Bayhaqi.

138


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

Na wameitaja idadi kubwa ya wafasiri kama vile Twabari, Shawkani na wengineo wakati wa kufasiri kwao aya hii.105 Na uelezaji wa hadithi usio na masharti unakusanya vigao vyote vya muziki na nyimbo, sawa uwe madhumuni yake yanachochea na kuamsha hisia kwa fitna au hapana. 2. Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema:

َ​َ َ َ َ َ َ َٰ ‫﴾ َا ج َحنون َا ال‬٥٩﴿ ‫سيث ح َجبون‬ ِ ‫أف ِمً هـصا ااح‬ َ ٰ ُ َ َ َ ﴾٦١﴿ ‫﴾ َا أهخم ػـ ِمسان‬٦٠﴿ ‫جبنون‬ “Je, mnaistaajabia maneno haya? Na mnacheka wala hamlii? Nanyi mmeghafilika?”106 Imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas kuwa amesema: Huo ni muziki kwa lugha ya Himyar, inasemwa: Sammid lana, yaani tuimbie sisi, na anaambiwa mwanamuziki: Tukonge nyoyo, yaani: Tuburudishe kwa nyimbo.107 3. Amepokea Ibn Abi Dunia na Ibn Mardawayhi: “Hakunyanyua yeyote sauti yake kwa muziki ila 105

Rejea tafsiri mbalimbali kuhusiana na aya hii. Surat an-Najm; 53 :59-61. 107 Jamiul-Bayaan, Juz. 2, uk. 82 cha Twabari, na Jaamiu li Ahkaam Qur’ani, Juz. 17, uk. 80 cha Qurtubi. 106

139


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

Mwenyezi Mungu atamfufua pamoja na mashetani wawili wakimkalia juu ya mabega yake mawili, wakipiga kwa migongo yao juu ya kifua chake mpaka anatulia.”108 Hayo ni baadhi ya yale yaliyopatikana kutoka kwa Mtume  kuhusiana na suala la uimbaji na muziki. Na lau tungelinukuu yote ambayo yamepokewa kutoka kwa Mtume  huenda ingelifikia idadi ya hadithi 17. Na tunaitakidi kwamba yale tuliyoyataja yanatosha kwa yule ambaye anayetegea sikio naye ni shahidi. Uharamu wa ala za muziki katika Sunnah: Yote haya ni kuhusiana na uimbaji na muziki, na ama kuhusu ala za muziki inatosha kama ifuatavyo: Mosi: Yale aliyopokea Bukhari katika Sahih yake kutoka kwa Abdul-Rahman bin Ghanm Ash‟ari, amesema: Amenisimulia Abu Aamir au Abu Malik Ash‟ari, naapa kwa Mwenyezi Mungu hajaniongopea mimi, nilimsikia Mtume  akisema: “Watakuwa watu katika umma wangu wakihalalisha zinaa, hariri, pombe na vyombo vya muziki, na watapeperusha bendera kwa kuwa na uwezo wa 108

Jaamiu li Ahkaam Qur’ani, Juz. 14, uk. 37, Irshaad Saari, Juz. 13, uk. 351, Durrul-Manthuur Juz. 6, uk. 506.

140


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

kipato. Atawajia wao mtu kwa haja, basi watasema rudi kwetu kesho. Basi Mwenyezi Mungu atawapitishia hao usiku, atashusha bendera na atawabadilisha wengine kuwa nyani na nguruwe mpaka Siku ya Kiyama.”109 Sidhani yupo yeyote anayeweka shaka katika dalili ya hadithi, nayo ipo wazi katika uharamishaji wa vyombo vya muziki, nazo ni ala za muziki. Na kuhusu hilo Mtume  ameeleza kwamba kutakuwa katika umma wangu yule anayehalalisha yale ambayo Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameharamisha kutokana na utupu – nayo ni kinaya ya zinaa – na Hariri, pombe na vyombo vya muziki, na cha mwisho ni zana za muziki kama vile dufu, fimbo, ngoma na zumari. Pili: Yale ambayo ameeleza Imam Ahmad katika Musnad wake kutoka kwa Ibn Abbas kutoka kwa Mtume  amesema: “Hakika Mwenyezi Mungu amekuharamishieni pombe, kamari na vyombo vya muziki” na akasema: “Kila kilevi ni haramu.”110 Ama sanad ya hadithi hakika ameikuta ni sahihi Sheikh Ahmad Shakir katika uwekaji wa maelezo yake juu ya kitabu Musnad Ahmad katika sehemu 109

Sahih Bukhari na. 5268, Fat hul-Bari, Juz. 10, uk. 55 na Majmuu’ Juz. 20, uk. 241 cha Nawawi. 110 Musnad Ahmad, Juz. 1, uk. 274 na 289 na 350 na Juz. 2, uk. 158, 165, 171 na Juz. 3, uk. 422.

141


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

mbili,111 na Sheikh Albaani katika kitabu chake kinachoitwa Tahriimu alaat Twarab.112 Na ama dalili ni: Basi neno kuubat lililotumika katika Hadithi husika ni ngoma. Hakika amenukuu hilo Ibn Mandhur katika kitabu Lisaanul-Arab kutoka kwa Ibn A‟rabi, na Ibn Durid ndani ya kitabu Jamharat FillLughah, na Jawhari katika kitabu as-Wihaha FillLughah, na Ibn Faris katika kitabu Maqayiis Lughah, na Ibn Sayyidat katika Mukhaswas Filughah.113 Tatu: Amepokea Twabarani kwa isnadi yake kutoka kwa Aamir bin Sa‟ad Bajali amesema: Niliingia kwa Abi Mas‟ud na Ubay bin Ka‟ab, Thabit bin Ziyad, nikakuta vijakazi wakipiga dufu na huku wakiimba, nikasema: Je, mnaridhia na kulipitisha hili, na nyinyi ni watu wa Muhammad ? Akasema: “Hakika imeruhusiwa kwetu katika harusi, na kumlilia maiti bila kulalama.”114 Na uelezaji wa ruhusa katika sehemu mbili ni ushahidi mzuri juu ya kwamba, asili ni uharamu katika hali zote na kwa watu wote, isipokuwa ni kwamba kimevuliwa kile kilichovuliwa. 111

Angalia: Musnad Ahmad, Juz. 4, uk. 58 na 218. Tahriim Aalat Twarab, uk. 56. 113 Rejea hilo kwenye Maajim lughawiyat, mada “Kuub” 114 Muujam Kabiir, Juz. 17, uk. 347. 112

142


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

Na huenda yale ambayo tuliyoyataja miongoni mwa dalili ni utoshelezaji kwa yule anayeitafuta haki ili aifuate. Dalili ya asemaye kuwa inaruhusiwa: Ametoa dalili msemaji mwenye kuruhusu muziki na kuimba kwa kutumia hadithi ambazo katika matini zake zina mishkeli na yasiyofaa, mishkeli ambayo inamfanya mwanafikihi asiwe na haja ya kutaka kujua usahihi wa sanad zake, na ifuatayo ni baadhi ya mifano ya hadithi hizo: 1. Ameeleza Tirmidhi katika Sunan yake kutoka kwa Aisha kwamba amesema: Alikuwa Mtume  amekaa, basi tukasikia kishindo na sauti ya watoto. Mtume  akasimama, ghafla akaona kumbe ni mwanamke wa kihabeshi alikuwa akicheza na watoto wakiwa pembezoni mwake, akasema: „Ewe Aisha! Njoo uangalie.‟ Basi nikaenda nikaweka taya langu juu ya mabega ya Mtume , basi nikawa ninamwangalia kati ya mabega na kichwa chake, akaniambia: „Je, hujashiba?‟ Nikawa ninasema hapana, ili niangalie daraja langu kwake. Ghafla akaja Umar akawakataza watu kumtazama (mwanamke wa kihabeshi aliyekuwa akicheza). Basi Mtume  akasema: „Hakika mimi ninaangalia mashetani ya kijini na 143


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

watu, na hakika yanamkimbia Umar.‟ Anasema (Aisha): Basi nikarudi.115 Ninasema: Hakika hadithi hii vyovyote itakavyokuwa, hata kama sanad yake itakuwa ni sahihi, lakini haisihi matini yake na madhumuni yake. Mtukufu Mtume  ametukuka na ameepukana na kuangalia mandhari hayo, na pia Bibi Aisha ameepukana na madai hayo. Na kuna maneno ya Allamah Amiini kuhusiana na hadithi hii, anasema: “Hakika yale ambayo wametumia katika kuthibitisha fadhila ya Khalifa wa pili yanapelekea fedheha kwa Mtume  – ambaye ametakasika nayo – basi ni Nabii gani huyu anaangalia wanenguaji, anasikiliza nyimbo za wanawake na anashuhudia ngoma. Wala hatosheki kwa hayo yote mpaka amuonesha Bibi Aisha, na watu wakawa wakiwaangalia hao wawili kwa karibu, naye akisema kwa kumuuliza: Je umetosheka? Umetosheka? Naye akijibu: Hapana, kwa kutaka kujua cheo chake mbele yake. Wala haoni haya kwa cheo cha utume asimame na watoto ili ashuhudie upuuzi. Hiyo ni tabia ya wahuni, watenda dhambi, wasio na hadhi na watu waovu na walio changanikiwa. Na hakika 115

Sunan Tirmidhi, Juz. 5, uk. 621, na. 3691, MaswabiihulSunnah, Juz. 4, uk. 159, na. 4737, Mushkaatul-Maswabihu, Juz. 3, uk. 343, na. 1049 na Riyadh Nudhurah, Juz. 2, uk. 255.

144


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

imekuja sharia tukufu kuharamisha yote hayo katika Kitabu na Sunnah tukufu.”116 2. Imepokewa kutoka kwa Buraydah: Mtume  alitoka katika baadhi ya vita alivyopigana, na pindi alipoondoka akaja kijakazi mweusi, akamwambia: „Ewe Mtume! Hakika mimi nilikuwa nimeweka nadhiri ikiwa Mwenyezi Mungu atakurudisha wewe salama basi nitakupigia dufu na nitakuimbia.‟ Mtume  akasema: „Ukiwa umeweka nadhiri basi piga na kama si hivyo hapana.‟ Basi akaanza kupiga na akaingia Abu Bakri naye akiendelea kupiga. Kisha akaingia Ali akaendelea kupiga, kisha akaingia Uthmani akaendelea kupiga, kisha akaingia Umar akaificha dufu yake chini ya makalio yake, kisha akaikalia juu yake. Mtume  akasema: „Hakika shetani anakuogopa ewe Umar, hakika mimi nilikuwa nimekaa naye akiwa anapiga, akaingia Abu Bakri akaendelea kupiga, kisha akaingia Ali akaendelea kupiga. Kisha akaingia Uthmani akaendelea kupiga, na pindi ulipoingia wewe Umar akaificha dufu yake!‟ Na katika lafudhi ya Ahmad: „Hakika shetani anakukimbia ewe Umar.‟117 Ninasema: Na hadithi haifai kutolewa hoja kwa sura zifuatazo: 116 117

Ghadir, Juz. 8, uk. 99. Musnad Ahmad, Juz. 6, uk. 485, na. 22480, Sunan Tirmidhi, Juz. 5, uk. 620 na. 3690 na vinginevyo.

145


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

Mosi: Hakika amenukuu Ahmad bin Hanbali katika Musnad wake kwa sura mbalimbali. Mara amenukuu dufu ya kijakazi juu ya kichwa cha Mtume  pekee, pasi na kutaja chochote kutokana na uingiaji wa Abu Bakri, Umar na Uthman kwake .118 Na mara nyingine dufu ya kijakazi pamoja na uingiaji wa Abu Bakri, kisha Umar bila ya kutaja uingiaji wa Ali na Uthmani.119 Pili: Wamekubaliana wanazuoni juu ya ulazima wa utekelezaji wa nadhiri kwa jambo la halali na sio la haramu wala makuruhu, basi haithibiti nadhiri, likiwa jambo linalowekewa nadhiri ni la makuruhu sembuse la haramu. Na upigaji wa dufu ima uwe makuruhu au haramu, basi vipi Mtume  aruhusu upigaji wa dufu mbele ya kichwa chake?! Na hakika ameeleza Ahmad kutoka kwa Abi Amamat, kutoka kwa Mtume  kwamba alisema: “Linalala kundi miongoni mwa umma wangu wakila na kunywa na wakifanya upuuzi na mchezo, kisha wanaamka wakiwa nyani na nguruwe. Basi wale walio hai watatumiwa kimbunga ambacho kitawaangamiza kama vile walivyoangamizwa wale waliokuwa kabla yao kwa kuhalalisha kwao pombe, upigaji wao wa dufu na uchukuaji wao wa waimbaji wa kike.”120 118

Musnad Ahmad, Juz. 5, uk. 356. Musnad Ahmad, Juz. 5, uk. 353. 120 Musnad Ahmad, Juz. 5, uk. 259, Sahihi Muslim, Juz. 7, uk. 185, mlango wa fadhila za masahaba, ameeleza hiyo kutoka kwa Abu Huraira. 119

146


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

Na kwa dhahiri hii ya hadithi ni kwamba, hakika upigaji wa dufu ulikuwa ni jambo baya, na kwa hivyo pindi alipoingia Umar akakutana na kijakazi akaficha dufu chini ya makalio yake kisha akaikalia juu yake kwa kumuogopa Umar, basi Mtume  ni bora zaidi kumkataza jambo hilo wala hawezi kumruhusu yeye apige dufu juu ya kichwa chake. Kisha hakika dhahiri ya hadithi ni kwamba Uthmani aliingia akaketi, na kijakazi akaendelea kupiga bila kuacha, nayo ni tofauti na yale ambayo aliyoyapokea Ibn Abi Awfa, aliposema: Abu Bakri aliomba idhini kuingia kwa Mtume  wakati kijakazi akiendelea kupiga dufu, akaingia. Kisha Umar akaomba idhini ya kuingia naye akaingia. Kisha Uthmani akaomba idhini alipoingia kijakazi akaacha kupiga, Mtume  akasema: “Hakika Uthmani ni mtu mwenye haya.”121 Na tatu: Hakika kauli ya Mtume : “Hakika shetani anakuogopa ewe Umar,” ipo wazi kabisa kwamba hicho ni kitendo cha shetani, na huko ni kumfadhilisha Umar juu ya Mtume  na yule aliyehudhuria kwake. 3. Amepokea Abu Nasri Tuusi katika kitabu Lumuu kwamba, hakika Mtume  aliingia nyumba ya Aisha basi akakuta wapo kwake vijakazi wawili wakiimba na wakipiga dufu, basi hakuwakataza hao hilo. Na 121

Musnad Ahmad, Juz. 4, uk. 353.

147


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

akasema Umar bin Khatwab pindi alipo ghadhibika: Je, kuna zumari la shetani ndani ya nyumba ya Mtume? Akasema: “Waache hao ewe Umar hakika kila kaumu wana Iddi.”122 Angalizo juu ya hadithi: Hakika dhahiri ya maneno ya Umar ni kwamba dufu ni miongoni mwa zumari ya shetani, basi inakuwa kulitumia hilo ni jambo la haramu. Pamoja na hilo iweje aridhie Mtume  kwa uwepo wake nyumbani kwake, kwa hoja ya kila watu wana siku yao ya Iddi, wakati Iddi ya Waislamu inajulikana na ina mipaka yake. Na kudhania kwamba siku hiyo ilikuwa ni siku ya Iddi ni jambo la mbali?! Na juu ya kila ukadiriaji na hata kama ni hukumu mahususi iliyovuliwa kutoka kwenye ujumla basi hakika ni katika Siku ya Iddi na sio katika hali zote. Na ninadhani hakika mpokezi wa hadithi alikuwa na lengo la ubainifu wa fadhila ya khalifa wa pili, akighafilika kuwa mfano wa hadithi hizi hazilingani na utukufu na cheo cha Mtume . Na aina hii ya hadithi ni mfano wa hadithi nyingi, baadhi ya hizo ni: Ameeleza Ahmad bin Hanbali katika Musnad wake kutokana na hadithi ya Abu Huraira, wakati vijakazi wahabeshi wakicheza ngoma mbele ya Mtume , 122

Lamuu, uk. 345 na. 153.

148


MAZUNGUMZO YA WAZI PAMOJA NA SHEIKH QARADHAWI

aliingia Umar basi akachukizwa na hilo na kutaka kuwashambulia kwa kitendo chao hicho, basi Mtume  akasema: “Waache ewe Umar.”123 Na huenda kutokana na yale tuliyoyasema kuhusiana na maudhui ya uimbaji na muziki mpaka hapa yanatosha kwa yule ambaye anayetafuta haki ili aifuate. Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu ambaye kwa neema Zake yanatimia mambo mema.

123

Musnad Ahmad, Juz. 2, uk. 594, na. 8019.

149


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.