Mikingamo iliyomzunguka imamu ali

Page 1

Mikingamo Iliyomzunguka Imamu Ali (a.s.)

Kimeandikwa na: Shahid Ustadh Murtadha Mutahhari

Kimetarjumiwa na: Ramadhani Kanju Shemahimbo

1


©Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION

ISBN: 9987-665-28-4

Kimeandikwa na: Shahid Ustadh Murtadha Mutahhari

Mtarjumi: Al-Hajj Ramadhani Kanju Shemahimbo

Toleo la kwanza: Desemba 2003 Nakala: 1000

Kimetolewa na kuchapishwa na: Al-Itrah Foundation S. L. P. – 19701, Dar-es-Salaam. Tanzania. Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv.com Katika mtandao: www.alitrah.info

2


NENO LA MCHAPISHAJI ‫بسم اهلل الرّحمن الرّحيم‬ Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza, kwa jina la “Polarization Around The Character of `Ali Ibn Abi Talib” ambacho jina lake la asili ni, “Jādhibah wa dāfi’ah-e’Ali [a.s] kilichoandikwa na Mwanachuoni mkubwa Shahid as-Sheikh Allamah Murtadha Mutahhari. Kitabu hiki kwa ufupi huelezea matatizo, misuko suko na mafanikio yaliyo ambatana na maisha ya Imamu Ali [a.s]. Tumeona tukitoe kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili ili kizidishe mwanga wa elimu kwa Waislamu wazungumzaji wa Kiswahili, na hili likiwa ndilo lengo kubwa la Taasisi yetu ya ‘Al`Itrah Foundation’ katika kuwahudumia Waislamu hususan wazungumzaji wa Kiswahili. Tunamshukuru Ndugu yetu al-Akhy Ramadhani Kanju Shemahimbo kwa kukubali jukumu hili la kukifanyia tarjuma kitabu hiki. Vile vile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki. Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni mwanga kwa wasomaji wetu na kuzidisha upeo wao wa elimu katika dini. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation

3


YALIYOMO Utangulizi………..........................................................................5 Dibaji……………………………………………….……………8 Sehemu ya kwanza: Nguvu ya Mvuto ndani ya ‘Ali’………………………………...13  Mivuto yenye nguvu …………………………...14  Ushi’ah; madhehebu ya upendo,…………...….. 17  Kioevu cha upendo…………………………......20  Kuvunja vizuizi…………………………………24  Je ni wenye kujenga au kubomoa……………. ..26  Upendo na utii kwa wale walioko karibu na Mwenyezi Mungu………………………………31  Nguvu ya upendo katika jamii …………………37  Ni njia bora za kuitakasia nafsi …………..........39  Mifano kutoka kwenye historia ya Uislamu…....47  Mapenzi juu ya Ali ndani ya Qur’an na Sunnah .57  Siri ya nguvu ya mvuto wa ‘Ali’………………...62 Seheumu ya Pili: Nguvu ya Kingamizo ndani ya ‘Ali’ …………………………. ..66  Jinsi `Ali alivyopata maadui……………………..67  Nakithun, Qasitun na Mariqun…………………..70  Jinsi Khawarij walivyotokea kuwepo…………....72  Msingi wa maoni ya Khawarij………………… 80  Walichoamini kuhusu Ukhalifa…………………..81  Walichoamini kuhusu Makhalifa………………...82  Kuanguka kwa Khawarij…………………………83  Je, Ni kaulimbiu tu?................................................83  Busara ya demokrasia ya `Ali………………….....90  Maasi na upinzani wa Khawarij………………......92  Sifa bainifu za Khawarij………………………..... 94  Siasa ya “kutumia” Qur’an………………………115 4


 

Umuhimu wa kupiga vita unafiki…………………119 `Ali, Imamu na kiongozi wa haki………………...121

5


UTANGULIZI -1Kitabu hiki, ambacho jina lake la asili ni JADHIBAH WA DAFI’AH E- `Ali ‘ALAYHI ‘S-SALAM [“Mvuto na Kingamizo la `Ali (a.s.)”, au “Nguvu ya mvuto na nguvu ya Kingamizo la `Ali (a.s.)”], ni moja ya kazi maarufu za Marhum, mwanazuoni mkubwa, ash–Sheikh Murtadha Mutahhari, yule mwandishi wa Ki-Irani, Mwenyezi Mungu amrehemu. Mwandishi huyu, mwenyewe ametoa maelezo ya kichwa hiki cha habari katika utangulizi wake na katika sehemu mbalimbali ndani ya kitabu hicho, kwa hiyo hapana haja ya sisi kuielezea zaidi. Tusije, hata hivyo, tukakosa kutilia maanani ukweli kwamba nguvu ya mtu ya mvuto kwa wale wanaompenda na kumsaidia, hata wale wanaojitoa kwa ajili yake, na kwa upande mwingine; nguvu yake ya kingamizo inayomsababishia mtu huyo wapinzani, maadui na hata watu wanaotaka kumuua (tunatumia maneno mvuto na kingamizo kama vile tu mtunzi alivyotumia), ndio tabia za msingi katika mtu huyo, lakini ni semi mbili ambazo zinajumlisha tabia nyingi na athari zinazojitokeza zenyewe ndani ya mtu huyo. Seti moja ya tabia hizi ni ile ya “msingi” au “ndani” ambayo inapatikana kwa mtu huyo na ambayo inasababisha kuwafanya watu wampende na kumsaidia, au kumpinga na kumchukia. Wakati huohuo kuna tabia za msingi ambazo ziko kwa wasaidizi au maadui wenyewe, ambazo zinafanya kazi pamoja na ile seti ya kwanza ya tabia kuleta mapenzi hayo au uadui. Kuna pia tabia za nje zinazotia nguvu zile athari hizi za “msingi”, au kuanzisha vikwazo vya ukamilishaji wake. Sasa, kama tutamfikiria mtu anayejadiliwa kuwa huru kutokana na mazingira ya wakati wake, bali kama mtu wa zama na nyakati zote, tutalazimika kuona baadhi ya tabia kwa nyongeza ya zile zinazohusika na wakati wake mwenyewe, ambazo zitakuwa zimeungana na historia ya kuweko kwake katika maana kamili ya kibinaadamu. Ama hizi tabia za nyongeza zitazidisha zile za asili, au vinginevyo zitadhoofisha. Ya 6


muhimu sana katika hizi tabia za kihisroria ni ile orodha ya wale ambao wamempenda, na wamejitolea wenyewe, kwa ajili yake, na nafsi zao, na orodha ya wapinzani na maadui, na nafsi zao; na orodha hizi zinaendelea kuongezeka jinsi muda unavyoendelea na jinsi karne na vizazi vinavyopokezana kimoja baada ya kingine Hii inakuwa muhimu zaidi hasa pale tunapofikiria mtu wa msimamo kama ‘Amirul ‘l-Muminin (a.s), ambapo tunaona katika utu wake halisi sifa tukufu sana za kibinadamu zilizochanganyika na kipawa kikubwa mno kitokanacho na Mungu, na katika Mashia wake na maadui zake imani yenye, nguvu zaidi katika Ujumbe wa Mungu uliochanganyika na imani katika watu, na ujumbe wake mkubwa kabisa, kwa upande mmoja na, kwa upande mwingine, uadui kwa Ujumbe wa Mungu uliochanganyika na ukosefu wa imani ndani ya watu na uasi dhidi yao. Kama tutazingatia hizo nukta za hapo juu, tunaweza kupata wazi la kiasi kikubwa cha nguvu kinachohitajika kutumika, cha utafiti wa kina cha mafunzo ambacho lazima kichukuliwe kuwezekana kwa mtu kufanya haki kwenye suala hilo, ili matokeo ya maana yaweze kupatikana kutokana kwenye mbalimbali vya uchunguzi wake wa awali.

wazo la kiwango kabla ya kwamba vipengele

-2Kitabu hiki, kama alivyo mwandishi; mwanazuoni huyu, (Mwenyezi Mungu amuwie radhi), anajionyesha mwenyewe, kuendelezwa kutokana na mihadhara mine iliyotolewa mwanzoni kuhusiana na ukumbusho wa kuuawa kishahidi kwa al-‘Imam Amiru’l-Muminin (a.s). Ilikusanywa pamoja na kuchapishwa katika namna ya kitabu. Mtunzi huyu, Mwenyezi Mungu amuwie radhi, alikuwa akijifanyia mwenyewe uadilifu na kwenye kazi yake alipokiri, katika utangulizi wake, kwamba kitabu chake ni kielelezo tu kutoka kwenye somo lake kubwa ambalo vipimo vyake ni vipana na vyenye vipengele vingi. Ni bahati yetu mbaya kwamba mtunzi alijikuta hana uwezo wa kuelezea kinaganaga zaidi juu ya somo hili kuu kuliko zaidi ya mihadhara hii mine, ambayo imewekewa mipaka ndani ya mfumo wa matukio 7


maalum, yenye mpaka wa wakati, na yenye kujieleza ambamo alijikuta mwenyewe, mbali na viwango ambavyo mashinikizo ya wajibu wake yalimruhusu kuzipitia hizo taarifa kwa ajili ya uchapishaji. -3Shukrani zimwendee Allah swt Ambaye amemuwezesha mtunzi huyu, Mwenyezi Mungu amwie radhi, kufanikiwa kwa kiasi ambacho alifanya katika kuendelea na mjadala wake, unaohusika na nguvu ya mvuto na kingamizo la Amiru ‘l-Muminin (a.s). Amebahatika kuweza katika kazi yake hii kufikia kiwango kilekile cha juu alichopata katika maandishi yake mengine. Wakati tulipoziona fikra kubwa za Kiislam, uwasilishaji wa wazi wa kihistoria, uasili wake na ufafanuzi mpya uliomo ndani ya kitabu hiki na ambavyo kwamba idadi kubwa ya wasomoaji wanakubaliana nasi, na ambavyo vipo licha ya mipaka aliyowekewa juu yake, sisi tunaamua kukifanya kitabu hiki kitarjumiwe kwa Kiingereza. Tulikitoa kwa mtarjuma bingwa, ambaye, tunamshukuru Allah swt, ameweza kukitafsiri kwa Kiingereza kwa uasili wake na ujuzi uleule kwa kile ambacho mwanazuoni huyu, Mutahhari aliuonyesha katika maandishi ya asili. Tunamshukuru Allah swt kwamba, tumefanikiwa katika kukichapisha kitabu hiki katika toleo la Kiingereza. Tunamuomba Allah swt na kwa kumnyenyekea, kwamba aiwezeshe kazi yetu iwe tu, kwa ajili ya ibada halisi Kwake, na kwamba atuwezeshe sisi kufaulu katika jambo jema ambamo anawawezesha waja wake kufaulu. Kwani Yeye ndio Kiongozi na Msanii bora. WORLD ORGANIZATION FOR ISLAMIC SERVICES (Shirikisho La Dunia La Huduma za Kiislamu) BOARD OF WRITING, TRANSLATION AND PUBLICATION. (Bodi ya Uandishi, Tarjuma na Uchapaji). 15/8/1401. 18/6/1981. TEHRAN - IRAN. 8


Dibaji Hulka adhimu, yenye kutanuka ya Amirul-Muminin `Ali (a.s) - ni pana sana na yenye sura nyingi zaidi kuliko kitu kingine chochote ambacho mtu anaweza kukiingia katika nyanja na sehemu zake zote, au kuifanya akili yake isiyotulia, kuweza kutafakari. Kwa mtu mmoja binafsi, kiasi kinachowezekana ni kwamba achague moja au baadhi ya maeneo maalum machache kwa ajili ya kujifunza na kutafiti, na ajitoshelezee mwenyewe kwa hayo. Moja ya vipengele na maeneo ya utu wa mtu huyu mashuhuri ni ile athari aliyokuwa nayo juu ya watu, ama bayana au hasi, au, kwa maneno mengine, uwezo wake wa “mvuto na kingamizo,” ambao mpaka sasa unaonyesha athari zake zenye nguvu; na ni pamoja na hili ambalo tutashughulika nalo katika kitabu hiki. Maneno ya watu binafsi yote hayako sawa katika hisia wanazotoa katika nafsi na nyoyo. jinsi hulka ilivyo dhaifu, ndivyo itakavyoshulisha akili za wachache, kusisimua nyoyo chache na kuhamasisha. Jinsi ilivyo kubwa, na yenye nguvu au uwezo zaidi, ndivyo inavyosisimua zaidi na kuchochea hisia katika mawazo, ingawa hisia hizo zinaweza kuwa bayana au hasi. Yale maneno ambayo husisimua mawazo na kuchochea hisia, na ambayo husimuliwa kila mahali, ndio mada za midahalo na mabishano, yanakuwa ndio insha za ushairi uchoraji na sanaa nyingine, Na visa vya mashujaa na maandishi mengine. Haya ndio mambo yote ambayo ni halisi kwa kiwango kikubwa katika hali ya `Ali (a.s)* na kwa hili hana mpinzani, au takriban wapinzani wachache sana. Inasemekana kwamba Muhammad Ibn Shahrashub al-Mazandarani, aliyekuwa mmoja wa wanazuoni wakubwa wa ki-Shia wa karne ya saba *

(a.s.): ni kifupi cha usemi wa Kiarabu ‘alay-hi/ha/himu’s-s yake/yao)

9

(amani iwe juu


– Hijiria (karne ya 13 Miladia), alikuwa na vitabu elfu moja vyenye kichwa cha habari “Manaqib” (maadili mema), katika maktaba yake, vyote vimeandikwa kuhusu `Ali (a.s), katika wakati alipoandika “Manaqib”1 yake mwenyewe maarufu. Hii ni dalili moja ya kiasi gani hulka tukufu ya bwana huyu imeshughulisha akili za watu katika historia yote. Sifa kuu ya `Ali (a.s), na watu wengine ambao wanang’ara kwa mionzi ya Haki ni kwamba pamoja na kushughulisha akili za watu na kutawala mawazo yao, zinatoa mwanga, ukunjufu, upendo, imani na nguvu kwenye mioyo yao. Wana-falsafa kama Socrates, Plato, Aristotle, Ibn Sina au Descartes pia ni mashujaa wa kutawala fikra na matumizi ya akili. Viongozi wa mapinduzi ya kijamii, hasa katika karne mbili zilizopita, wamebuni, kwa kiasi kikubwa, namna ya kuheshimiwa miongoni mwa wafuasi wao. Mashekhe wa Kisuffi, mara kwa mara, huwafikisha wafuasi wao mbali sana katika hatua ya “ibada” kiasi kwamba kama “mtunza klabu ya pombe” atatoa kidokezo, watalowesha misala yao ya kusalia kwa mvinyo.2 Lakini sio katika yoyote kati ya masuala haya tunamoona ari na hamasa vilivyochanganyika na upole, wema, unyoofu na huruma, kama historia ilivyoonyesha miongoni mwa wafuasi wa `Ali. Kama Wa-Safavid waliwafanya madaruweshi kuwa kama jeshi la wapiganaji wenye ujuzi, walifanya hivyo kwa jina la `Ali, sio kwa majina yao wenyewe. Wema wa kiroho na ubora, ambavyo huletwa na upendo na unyoofu, ni kitu kimoja; ukubwa, neema, na kilicho na fursa katika maisha, ambacho ndicho kiongozi wa jamii anachoshughulikia, au akili na falsafa, ambayo ndio mwana-falsafa anayoshughulikia, au kuanzisha 1

Juz 3., Najaf, 1376/1956

2

Acha mvinyo umwagike kwenye mkeka wa kusalia, Na kama mlinda klabu anakuambia hivyo; Ni ada ya nani ipo kwenye barabara hii kuenda Njia zake na tabia njema zinajua.

10


“utawala” na mamlaka” ambayo ndio mlahidi anayoshughulikia; ni kitu kingine. Kuna hadithi mashuhuri sana kwamba, mmoja wa wanafunzi wa Ibn Sina alimuambia mwalimu wake kwamba kama, pamoja na ujuzi wake wa ajabu na maarifa, angekuwa atoe madai ya utume, watu wangekusanyika kumzunguka; lakini Ibn Sina hakusema chochote, mpaka wakati mmoja, walipokuwa kwenye safari pamoja wakati wa kipupwe, Ibn Sina aliamka usingizini asubuhi moja wakati wa alfajiri, akamuamsha mwanafunzi wake na kumwambia ana kiu na aende kumchotea maji. Yule mwanafunzi alisitasita na kutoa visingizio: kwa kila namna Ibn Sina alivyomchagiza, yule mwanafunzi hakuwa tayari kuacha kitanda chake chenye joto katika hali ya kipupwe chenye baridi. Muda huohuo sauti ya muadhini ilisikika kutoka kwenye mnara; “Allahu Akbar, Allahu Akbar…” Ibn Sina akaona kwamba huu ndio muda muafaka wa kutoa jibu kwa mwanafunzi wake, hivyo akasema: “Wewe ambaye ulithibitisha kwamba kama ningedai utume watu wangeniamini, tazama sasa, uone amri niliyotoa hivi punde tu kwako, wewe uliyekuwa mwanafunzi wangu kwa miaka na umefaidika kutokana na mafunzo yangu, haikuweza kuwa na athari ya kutosha kukufanya wewe ukiache kitanda chako chenye joto kuniletea mimi maji. Lakini huyu muadhini ameitii ile amri yenye miaka mia nne ya Mtume (s.a.w.w.), akaamka kutoka kwenye kitanda chake chenye joto, akapanda mpaka kwenye kilele hiki na kushuhudia upweke wa Mungu na wa Mtume wake. Angalia uone ni ukubwa gani tofauti hii ilivyo!” Wana-falsafa wanatoa wanafunzi, sio wafuasi; viongozi wa kijamii wanajifanyia wafuasi lakini sio watu kamili, wahutubu na masheikh wa Kisuffi wanakuwa “mabwana wa ibada” sio wapiganaji hai kwa ajili ya Uislamu. Kwa `Ali (a.s) tunapata sifa mapinduzi, sifa za Sheikh wa kitengo chake ni kitengo cha kitengo cha unyenyekevu na upeo wa utii na harakati.

za mwana-falsafa, sifa za kiongozi wa Ki-Suffi na baadhi ya sifa za Mitume. maarifa na fikra, kitengo cha mapinduzi, nidhamu, na kitengo cha wema, ubora,

11


Kabla hajawa kiongozi muadilifu (Imam) wa wengine, na kuwa na tabia ya uadilifu mbele yao, `Ali (a.s) alikuwa binafsi anakubalika, mtu aliyekamilishwa, alikuwa amekusanya pamoja ukamilifu wa ubinadamu. Alikuwa na akili ya kina na yenye kufika mbali, na upendo wenye huruma usio na kifani; alikuwa na ukamilifu wa mwili na roho, kwa pamoja; wakati wa usiku, katika ibada, alijitenga na kila kitu kinginecho, na wakati wa mchana alikuwa akishughulika miongoni mwa watu. Wakati wa mchana, watu waliziona huruma na uungwana, na walisikiliza ushauri wake, nasaha na maneno yake ya hekima; wakati wa usiku, nyota zilitazama chini kwenye machozi ya ibada zake na mbingu zilisikia sala zake za upendo. Alikuwa mtu mwenye elimu na hekima, mwenye nguvu za kiroho na kiongozi wa kijamii pia, mtu aliyejinyima nafsi yake na mpiganaji, hakimu na mfanyakazi, mzungumzaji na mwandishi. Kwa jumla, kwa namna zote alikuwa ni mtu mkamilifu pamoja na vivutio vyake vyote. *

*

*

Kitabu hiki ni mkusanyiko wa khutba nne ambazo zilitolewa kati ya tarehe 18 na 21 za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani 1388 A.H. (1969 Miladia) ndani ya Husayniyah-e-Irshad mjini Tehran. Kitabu hiki kimejumuisha Utangulizi na Sehemu Mbili. Katika utangulizi, ule ujumla wa mvuto na kingamizo katika maana zake pana, na “Mvuto” na “Kingamizo” la watu hasahasa, vimejadiliwa. Katika sehemu ya kwanza, uwezo wa mvuto wa `Ali (a.s) ambao umevuta na daima utavuta mioyo ya watu upande wake, falsafa ya mvuto huo, mafanikio na matokeo, ni mada ya majadiliano, na, katika sehemu ya pili, athari za kufukuza zenye nguvu sana, na jinsi alivyokwepa kwa uhodari na alivyoyaswaga makundi fulani, kumechunguzwa na kuelezewa. Imeonyeshwa kwamba `Ali (a.s) alikuwa mtu mwenye nguvu hizi pacha, na kwamba kila mtu anayetaka kufundishwa katika namna yake lazima awe na nguvu hizi pacha. Haitoshi tu kule kuelekeza kwenye nguvu hizi mbili za njia hii ili kuzifanya zijulikane. Katika kitabu hiki tumejaribu kuonyesha, kiasi 12


inavyowezekana, ni aina gani ya watu walivutiwa na nguvu zake za mvuto, na aina gani ya mtu alifukuzwa na nguvu yake ya kingamizo. Ni mara ngapi, sisi ambao tunadai kufuata njia ya `Ali, tumewasukumizia mbali watu walewale ambao `Ali (a.s) aliwavuta, na tukawavuta wale ambao walikingamizwa naye? Katika upande wa nguvu ya kingamizo la `Ali, tumejitosheleza na mjadala wa Khawaraj, lakini kwa vile kuna vikundi vingine ambavyo vilikuwa na uelekeo wa nguvu yake hii, pengine safari nyingine, au, angalau katika uandishi wa baadae wa kitabu hiki, mapungufu mengine ya kitabu hiki yatarekebishwa. Usumbufu wa kukisahihisha na kuzikamilisha khutba hizi, umebebwa na ‘Aalim Bwana Fathullah Umidi. Nusu ya kitabu hiki, kuweko kwake kunatokana na kalamu yake ya kimtindo, kwani, baada ya kuitoa kwenye kanda zilizorekodiwa, aliiandika tena, mara kwa mara akiisahihisha na kuiboresha. Nusu yake nyingine ni uandishi wa mwanazuoni huyu mwenyewe, au wakati mwingine, baada ya masahihisho yake yanayostahili, zile nyongeza za baadhi ya nukta nilizofanya mimi mwenyewe. Ninaamini kwamba kwa ujumla kitakuwa chenye msaada na chenye kuelekeza. Tunamuomba Allah (swt) Aliyetukuka atufanye sisi kuwa wafuasi halisi wa `Ali (a.s). Murtadha Mutahhari 11th Isfand, 1349 Sh. 4th Muharram, 1391 A.H. 2ND March, 1971 A.D. Tehran – IRAN.

13


Kanuni ya mvuto na kingamizo: Kanuni ya “mvuto na msukumo� ni kanuni ambayo inatawala kotekote katika utaratibu mzima wa maumbile. Kutokana na mtazamo wa mafundisho ya kisayansi ya sasa, mwanadamu ana uhakika kabisa kwamba hakuna hata chembe moja katika ulimwengu wa uhai iliyoko nje ya utawala wa mvuto wa kawaida, na hakuna inayoweza kuukwepa. Kutoka kwenye maumbo na mikusanyiko mikubwa ya dunia hadi kwenye chembe chembe zake ndogo kabisa, vyote vinayo hii nguvu ya muujiza inayoitwa nguvu ya mvuto, na vyote kwa njia moja au nyingine, vinaathiriwa nayo. Mwanadamu wa zamani alikuwa hakugundua kanuni hii ya kawaida ya mvuto iliyoenea, lakini yeye aligundua mvuto katika baadhi ya maumbo, na walifahamu baadhi ya vitu kama ishara ya nguvu hii, kama vile sumaku na ambari. Hata hivyo, hakujua juu ya uhusiano wa mvuto kati ya vitu hivi na vitu vingine vyote, kwani alikuwa amezoeana tu na uhusiano pekee: ule wa sumaku na chuma, au ambari na bua. Kila moja ya chembe katika chembe zilizopo kati ya dunia hii na mbinguni ipo, kwa namna yake pekee, kama bua na ambari.1 Mbali na hili, kulikuwa hakuna mazungumzo ya nguvu ya mvutano pamoja na vitu visivyokuwa na uhai; kuhusu dunia tu iliulizwa kwa nini ilikuwa imewekwa katikati ya mbingu. Iliaminika kwamba dunia ilikuwa imening’inizwa katikati ya anga na ilikuwa ikivutwa kila upande, na kwamba kwa vile uvutaji huo ulitoka pande zote, bila shaka ilikaa katikati na haikulemea kwenye upande wowote. Watu wengine waliamini kwamba mbingu hazikuivuta dunia, bali hasa kwamba ziliisukuma, na kwamba, kwa vile nguvu inayoiathiri dunia ilikuwa sawa kwa pande zote, matokeo yalikuwa kwamba dunia ilewekwa kwenye sehemu maalum na kamwe haikubadili nafasi yake. 1

Rumi, Mathnawi, kitabu cha 6.

14


Ilikuwepo pia imani ya kawaida katika welekevu juu ya mvuto na msukumo kwa upande wa mimea na wanyama, kwa maana kwamba ilitambulikana kuwa hizi zilikuwa na welekevu namna tatu wa msingi: welekevu rutubishi, welekevu wa ukuaji na welekevu wa uzazi. Kwa uelekevu rutubishi, waliamini kulikuwa na vielekevu saidizi: cha kuvutia, cha mfukuzo, cha kumeng’enya na yenye kushikilia. Inasemekana kwamba katika tumbo kulikuwa na nguvu ya mvutano ambayo ilivuta chakula kwake, au, mara chache, lilipokuwa halikukikubali chakula, lilikitoa kama taka au lilikisukuma2 ; na vivyohivyo ilisemekana kwamba kulikuwa na nguvu ya mvutano katika ini ambayo ililivutia maji lenyewe. Tumbo linajivutia chakula kwenda kwenye sehemu yake ya mapumziko, Moyo wa ini unaingiza ndani maji.3 Mvutano na msukumo katika ulimwengu wa mwanadamu Maana ya mvutano na msukumo hapa sio ule mvuto na msukumo unaohusiana na jinsia, ingawa hizi nazo pia ni aina maalum ya mvutano na msukumo, kwani hazihusiani chochote na mjadala wetu na zinaunda jambo la pekee la uchunguzi. Maana hapa hasa ni ule mvutano na msukumo ambao upo miongoni wanadamu mmoja mmoja uwanja wa maisha ya kijamii. Katika jamii ya wanadamu zipo pia aina za ushirikiano ambazo zimeegemea katika mgawanyo wa faida, lakini hizi pia kwa kweli, haziko katika nafasi ya mjadala wetu. Uwiano mkubwa wa urafiki na upendo, au uadui na chuki vyote ni ishara ya mvuto na msukumo. Mivuto na misukumo hii imeegemea kwenye kufanana na kulingana kwa kawaida, au upinzani na

2

Siku hizi, hata hivyo, utaratibu wa mwili unafikiriwa kuwa kufanana sana na mashine, na kitendo cha kutoa takamwili kinafananishwa na pampu. 3 RĹ­mi, Mathnawi, ibid.

15


kuchukiana kukubwa kwa pande mbili.4 Kwa kweli, sababu ya msingi ya mvuto na msukumo ni lazima itavutwe kwenye kufanana na kukinzana kwa kawaida (tadādd), kama vile tu katika mjadala wa metafizikia imethibitishwa kwamba kufanana kwa kawaida ndio sdababu ya muungano. Wakati mwingine binadamu wawili wanavutiana, na mioyo yao inawataka wawe marafiki na mwandani wa kila mmoja wao. Kuna siri katika hili, na siri hiyo si chochote zaidi ya kufanana kwa kawaida. Isipokuwa kuwepo na kufanana kati ya watu wawili hawa, hawawezi kuvutiana na kusogelea kwenye urafiki na kila mmoja wao. Kwa ujumla ule ukaribu wa wote wawili ni ushahidi wa aina ya kulingana na kufanana kwa kawaida kati yao. Katika kitabu cha pili cha Rŭmi cha Mathnawi kuna hadithi nzuri sana inayolielezea hili kwa mfano. Mtu mwenye busara alimuona ndege mkubwa jamii ya kunguru ambaye aliunda upendo juu ya korongo. Walitulia pamoja na kuruka pamoja! Ndege wawili wa aina mbili tofauti : huyu wa jamii ya kunguru hakuwa na kulingana kokote ama katika umbo au katika rangi na yule korongo. Yule mtu mwenye busara alishangazwa kwamba walikuwa pamoja. Alisogea karibu kwenda kuwachunguzana akagundua kwamba wote walikuwa na mguu mmoja kila mmoja. Yule mtu mwenye busara akasema: “Niliona umwandani Kati ya ndege jamii ya kunguru na korongo. Nilishangaa, na nikachunguza hali zao Ili kuona kuna dalili gani ya upamoja ningeweza kuipata. Hivyo nikanyemelea, na, lo na tazama! Niliona kwamba wote walikuwa wamelemaa.” Huku kuwa na mguu mmoja kulileta ushirika kwa aina mbili za wanyama ambao walikuwa marafiki kwa kila mmoja. Wanadamu, pia, kamwe hawatakuwa marafiki na mwandani wa kila mmoja bila ya 4

Kinyume na kinachosemwa kwenye mikondo wa umeme, ambapo ncha mbili zinazofanana zinasukumana, ambapo mbili zinazotofautiana zinavutana.

16


sababu fulani, kama ambavyo hawatakuwa maadui kamwe bila ya sababu. Kwa mujibu wa baadhi, mzizi wa mivuto na misukumo hii ni haja, na uondoshaji wa haja. Wanasema kwamba mwanadamu ni kiumbe mwenye kuhitaji, na kwamba ameumbwa kimsingi katika kuhitaji. Anajitahidi kwa bidii yake isiyotulia ili kujaza tumbo lake na kukimu mahitaji yake, lakini hili haliwezekani ila mpaka aungane na rafiki na kuvunja uhusiano wake unaomuunganisha na jamii, ili aweze kuchukua fursa kutoka kwa rafiki yake kwa njia hii na ajilinde mwenyewe kutokana na uharibifu kutoka kwenye kikundi kingine chochote. Na hatutapata uelekeo au chuki kubwa ndani ya mwanadamu isipokuwa inachipukia kutoka kwenye hisia zake za kuchukua fursa. Kutokana na nadharia hii, uzoefu wa maisha na muundo wa asili wa ukiumbe wake vimemlea mwanadamu awe wa kuvutiwa na kusukumwa, ili kwamba awe mwenye shauku kubwa kuhusu kile anachokiona ni kizuri katika maisha, na anakiweka mbali naye kile kisichokubaliana na malengo yake, bali anakuwa havutiki anapokabiliwa na kile ambacho si katika hivi, ni kile ambacho hakileti mafanikio yoyote kwake wala hakina madhara. Kwa kweli, mvuto na msukumo ni nguzo mbili za msingi wa maisha ya mwanadamu, na kwa kiwango chochote kile hivi vitakavyoshushwam vurugu inachukua nafasi ya utulivu katika maisha yake. Mwishoni yule ambaye hana uwezo wa kuziba mapengo yake anavuta wengine upande wake, na yule ambaye sio tu hazibi mapengo yake haya bali hasa anayaongeza mapengo anawafukuza watu mbali na yeye, na vivyo hivyo kwa wale ambao hawafanyi yote. Tofauti kati ya watu kwa mintaarafu ya mvuto na msukumo: Kwa kigezo cha mvuto na msukumo kuhusiana na watu wengine, sio watu wote wako sawa; kwa hakika wanaweza kugawanywa katika matabaka mbali mbali: 1. Watu ambao hawavuti na hawasukumi: Hakuna mtu anayewapenda wao, wala hakuna aliye adui wao; hawashawishi 17


mapenzi ya mtu yoyote, urafiki au upendo, wala uadui, wivu, kinyongo au chuki ya mtu yoyote; wanatembea miongoni mwa watu bila kujali, kama ambavyo ubamba wa jiwe ungekuwa miongoni mwao. Kiumbe kama huyo ni kama si chochote, hatoi athari yoyote, mtu ambaye ndani yake hamna kitu chochote cha uhakika kinachopatikana ama kwa kigezo cha wema au kwa kigezo cha uovu (maana ya “uhakika” halihusiki na wema tu – inahusika na uovu pia). Yeye ni mnyama, anakula, analala na anatembea mongoni mwa watu. Yeye ni kama kondoo ambaye sio rafiki wa yeyote na sio adui wa yeyote, na kama anachungwa. La,a amapewa maji yake na majani, ni kwa sababu nyama yake italiwa baada ya muda. Haanzishi wimbi lolote la kuafiki, wala wimbi la kutoafiki. Watu kama hao wanaunda kundi la viumbe wasio na thamani, wanadamu watupu na wasio na akili, kwani mwanadamu anahitaji kupenda na kupendwa, na tunaweza kusema pia kwamba anahitaji kuchukia na kuchukiwa. 2. Watu wanaovutia lakini hawasukumi: Wanaelewana vizuri na kila mtu, wanaanzisha uhusiano mchangamfu na watu wote, wanawafanya watu wa daraja zote kuwa wapendwa wao. Maishani, kila mtu anawapenda, na hakuna mtu anayewakataa wao, na pindi wanapokufa, Waislam wanawaosha kwa maji kutoka kwenye kisima cha Zamzam huko Makkah na kuwazika, ambapo Wahindu wanachoma maiti zao. Hivyo jizoeshe mwenyewe kwa mazuri na mabaya, Ili baada ya kufa kwako Waislam watakuosha katika maji ya Zamzam, Na Mahindu watakuchoma wewe.‡ Kwa mujibu wa ushauri wa shairi hili, katika jamii ambayo nusu yake ni Waislam na wanauheshimu mwili wa mtu aliyekufa, wakaupatia ghusl (josho la maiti), na pengine wakaupa ghusl hiyo kwa maji ‡

‘Urfi alikuwa ni mshairi wa Kiirani (963/1555 – 999/1590) aliyesafiri kwenda India na akalizoea Baraza la Mfalme Akbar.

18


matakatifu kutoka Zamzam kama matokeo ya heshima kubwa zaidi, na nusu ni Mahindu ambao wanachoma wafu na wakatupa majivu yake kwenye upepo, mtu unapaswa uishi katika hali ambayo Waislam wanakukubali wewe kama mmoja waona wanataka kukuosha baada ya kifo katika maji kutoka Zamzam, na Mahindu pia wanakukubali wewe kama mmoja wao na wanataka wakuchome baada ya kufa. Inadhaniwa mara nyingi kwamba ubora wa tabia, upole katika uhusiano na jamii, au, kwa lugha ya kisasa “kuwa mwenye kujumuika na watu�, kunakuwa nalo hili hasa, kuwafanya watu wote kuwa marafiki zako. Hata hivyo, hili haliwezekani kwa mtu ambaye ana lengo, ambaye anafuata njia, ambaye, miongoni mwa watu, anashikilia njia maalum ya fikra au ya maadili, na haangalii manufaa yake mwenyewe; mtu kama huyo, taka usitake, ana sura moja tu, ana uamuzi na ni muwazi katika tabia yake, isipokuwa, kwa kweli, kama ni mzandiki na mnafiki. Kwani watu wote hawafikiri kwa namna moja, au kuhisi kwa namna moja, na mapendeleo ya kila mtu sio ya namna moja; miongoni mwa watu wapo wale ambao ni waadilifu na wale ambao sio waadilifu, yupo mzuri na yupo mbaya. Jamii inao watu wake wa haki, na watu wake madhalimu; wapo watu waadilifu, wapo watu waovu. Watu hawa hawawezi wote wakampenda mtu mmoja, mwanadamu mmoja, ambaye kwa dhati kabisa anashikilia lengo moja na hivyo kugongana na baadhi ya maslahi yao. Mtu pekee atakaefanikiwa katika kuvuta urafiki wa matabaka yote mbalimbali na maadili mbali mbali ni yule ambaye anaficha hisia zake na kudanganya, na anayesema na kuonyesha kwa kila mtu kile ambacho kinakubaliana na matakwa ya mtu yule. Lakini kama mtu huyo ni mwaminifu na anafuata njia, kundi moja lenyewe litakuwa marafiki zake na jingine vivyo hivyo litakuwa maadui zake. Kundi lolote ambalo linafuata njia ile ile kama yeye litavutika kumuelekea yeye, na kundi lolote ambalo linafuata njia tofauti litamtenga yeye na litagombana naye. Baadhi ya Wakristo, wanaojionyesha wao wenyewe na dini yao kama watumishi wa amani, wanaamini kwamba mtu mkamilifu hana 19


chochote bali upendo, hivyo hana kitu ila nguvu ya mvuto, na huenda baadhi ya Wahindu pia wanaamini vivyo hivyo. Moja ya vitu kinachovutia sana katika falsafa ya Uhindu na Ukristo ni upendo. Wanasema kwamba mtu lazima ailee tabia ya mapenzi kwa vitu vyote na adhihirishe upendo wake, na tunapokuja kumpenda kila mtu ni kipi kinachoweza kumzuia yeyote yule kutupenda sisi – waovu pia watatupenda sisi, kwa vile wakakuwa wameuona upendo wetu. Lakini waungwana hawa waelewe kwamba haitoshi tu kuwa mtu wa upendo, mtu lazima pia awe mtu wa njia, kama vile tu Gandhi alivyosema: “Hii ndio dini yangu.” Upendo lazima ulingane na ukweli na, kama utalingana na ukweli utakuwa na njia fulani ambayo unaifuata, na kufuata njia kunafanya maadui, kama tukipenda au tusipende. Kwa kweli, ni ile nguvu ya mvuto ambayo inachochea kundi moja kujitahidi na linalitenga kundi jingine. Uislam pia ni sheria ya upendo. Qur’ani Tukufu inamuonyesha Mtukufu Mtume (S.a.w.w.) kama rehma kwa Viumbe wote: (rahmatan li’l-'ālamin) ‫ال رَحْ َم ًة لِلْعَالَمِين‬ ّ ِ‫ك ا‬ َ ‫وَمَاَاَرْسَلْنَا‬ Nasi hatukukutuma ila uwe ni rehma kwa walimwengu wote (Anbiyā’ 21:107) Hii ina maana kwamba wewe (yaani, Mtukufu Mtume) utakuwa ni rehma hata kwa adui wa hatari zaidi, na utawapenda hata wao.6 6

Inaonyesha, zaidi ya hayo, kwamba alipenda vitu vyote, hata wany ama na vitu visivyokuwa na uhai. Hivyo tunaweza kuona katika historia ya maisha yake kwamba vitu vyote alivyokuwa akivitumia vilikuwa na majina maalum. Farasi zake, panga zake na vilemba vyake vyote vilikuwa na majina maalum, na sababu pekee ya hili ilikuwa ni kwamba vitu vyote vilivyokuwepo vilikuwa ni vielelezo vya udhihirisho wa mapenzi na upendo wake; ni kana kwamba alikiona kila kitu kuwa na upekee. Historia haina kumbukumbu ya mwanadamu yeyote mwenye mwenendo kama huu mbali na yeye, na mwenendo huu kwa kweli unaonyesha kwamba alikuwa ni kielelezo cha upendo wa mwanadamu. Alipokuwa anapita karibu na mlima wa Uhud, aliutazama

20


Hata hivyo upendo ambao Qur’ani inauamrisha haina maana kwamba tufanye nbele ya kila mtu kwa kuafikiana na kile anachotaka na kinachomridhisha yeye, kwamba tutende mbele yake kwa namna ambayo inamfanya yeye kufurahi na kuvutika kuelekea kwetu kwa lazima. Upendo hauna maana kwamba tumuache kila mtu huru kufuata matakwa yao, au zaidi kwamba tunapaswa turidhie matakwa y ao; huu sio upendo, bali hasa ni uzandiki na unafiki. Upendo ni ule unaolingana na ukweli, unamsababisha mtu kufikia kwenye manufaa, na wakati mwingine yale mambo yanayotufikisha kwenye manufaa yanachukua hali ambayo haivutii mapenzi na upendo wa mtu mwingine. Kuna watu wangapi ambao mtu anawapenda kwa namna hii na ambao, pale wanapotambua kwamba upendo huu unapingana na matakwa yao wenyewe, wanakuwa wenye uadui badala ya kuwa wenye kufurahia. Aidha, upendo wenye uwiano na wa kiakili ni ule ambao ndani yake mna manufaa na maslahi ya wanadamu wote, sio manufaa ya mtu mmoja au kundi maalum. Kuna mambo mengi yanayoweza kufanywa kuleta manufaa kwa watu mmoja mmoja na kuonyesha upendo kwa ajili yao ambayo ni hayo hayo yanayoleta maovu kwa jamii kwa jumla na wanaweza (watu hao) kuwa maadui wake (jamii hiyo). Tunaweza kuwapata wanamageuzi wengi katika historia ambao walijaribu kutengeneza hali ya jamii na kuondoa shida zao, lakini ni nani, kinyume chake, hakupata shukurani bali uhasama na mateso kutoka kwa watu. Kwa hiyo sio jambo la kwamba kila mahali upendo unavutia; kwa hakika upendo wakati mwingine unajitokeza wenyewe kama msukumo mkubwa sana ambao unaikusanya jamii yote dhidi ya mtu mmoja. Abdur Rahman ibn Muljim alikuwa mmoja wa maadui wakaidi sana wa Ali, na yeye Ali alijua fika kwamba mtu huyu alikuwa ni mpinzani hatari sana. Wakati mwingine, hata watu wengine waliweza kwa upole kwa macho yake maangavu na kwa mtazamo uliojaa upendo, na akasema: jabal yuhibbunā wa nahibbuh – “Ni mlima ambao unatupenda sisi nasi tunaupenda.” Alikuwa ni mtu ambaye katika upendo wake milima na majabali yalishiriki pia.

21


kumwambia yeye kwamba alikuwa ni mtu hatari, na kwamba angeondokana naye. Lakini Ali aliuliza katika kujibu, “Nitoe adhabu kabla ya kosa? Kama yeye ndiye muuaji wangu, siwezi kumuua muuaji wangu mwenyewe: yeye aniuwe mimi, sio mimi nimuue yeye.” Ilikuwa ni kuhusu mtu huyu ambapo Ali alisema: ‫اُرِيْ َد حَيَا َت ُه وَيُريْ ُد قَتْلِي‬ Mimi nataka yeye aishi; lakini yeye anataka kuniua mimi.7 (yaani, “mimi nana upendo juu yake, lakini yeye ni adui yanguna anakusudia nia mbaya dhidi yangu”.) Pili, upendo sio dawa pekee ya kuponyesha kwa wanadamu; ukatili pia ni muhimu kwa ajili ya vionjo fulani na mienendo, na migogoro, kusukuma na kufukuzapia ni muhimu. Uislam ni dini ya vyote, mvuto na upendo na ni dini ya msukumo na adhabu (niqmah). 8 7

Biharu’l-anwar, Juz. 42, uk.193 – 194 (Tehran, toleo jipya).

8

Labda tungesema kwamba adhabu pia ni udhihirisho wa hisia za mapenzi na upendo. Katika du’a (maombi kwa Allah swt) tunasoma: “yā man sabaqat rahmatuh ghadhabah” – “Ewe ambaye kwako rehma na upendo vimepewa umuhimu wa kwanza juu ya ghadhabu”, yaani, kwa sababu Wewe unataka kuwa mwenye rehma umeghadhibika, vinginevyo, kama ile rehma na upendo vingekuwa havipo, hata hiyo ghadhabu isingekuwepo. Ni kama baba anayemchukia mwanae kwa sababu anampenda na anajali mustakabali wake. Kama mwanae huyo atampinga, anashikwa na ghadhabu, na anaweza wakati mwingine akampiga, lakini licha ya kiasi chochote cha tabia mbaya anachoweza kukiona kwa vijana na watoto wa wengine, hakimshughulishi kamwe. Kwa upande wa kijana wake mwenyewe anakasirika, kwa sababu ana mapenzi juu yake; lakini kwa upande wa wengine, hakasiriki, kwa vile hana mapenzi. Kwa upande mwingine, mapenzi wakati mwingine hudanganya, ni kusema kwamba kuna hisia ambazo akili haiwezi kuzielewa sawasawa, kama inavyosema Qur’an

ِ‫ال تَاْخُذْكُم بِهِمَا رَاْ َف ُة فِي دِينِ اٌلَله‬ َ َ‫و‬ Wala msiwe na huruma juu yao (wahalifu) katika hukumu ya Allah (yaani, zile sheria tukufu) (an-Nuur, 24:2) Sababu ya hili ni kwamba Uislam, wakati unaonyesha kujali na upendo kwa watu, unajali pia juu y a jamii. Dhambi kubwa sana ni dhambi ambayo inaonekana ni ndogo kwenye macho ya mtu na inaelekea kutokuwa na muhimu. Amir al-M u’minin alisema:

22


3. Watu wanaosukuma lakini hawavutii: wanakuwa na maadui lakini hawawi na marafiki wowowte. Hawa pia ni watu wenye kasorokatika sifa halisi za kibinadamu, kwani kama wangechukua sifa za binadamu, wangekuwa na makundi, hata kama yangekuwa madogo kwa idadi, ambao wangekuwa wafuasi wao na wameambatana nao. Kwani siku zote wapo watu wema miongoni mwa wanadamu, hata kama idadi yao ingekuwa ndogo kwa kiasi gani. Hata kama watu wote wangekuwa ovyo na madhalimu, uhasama wao ungekuwa uthibitisho wa ukweli na haki, lakini sivyo ilivyo kwamwe kwamba watu wote ni wabaya, kama vile tu ambavyo hawawi kamwe wote ni wema. Bila shaka, ubaya ndani ya mtu ambaye uadui kwa kila mtu ni wa kuonekana ndani yake mwenyewe, kwani vinginevyo itawezekana vipi kuwepo wema katika hulka ya binadamu na kisha kwa mtu huyo kukosa marafiki. Hakuna pande dhahiri katika hulka za watu kama hawa; hata katika hali zao za kiovu kabisa hulka zao zinakuwa na kisirani wakati wote, na zinakuwa na kisirani kwa kila mtu. Hakuna chochote ndaini yao ambacho ni kitamu hata kama ingekuwa kwa wachache tu. Ali (a.s.) alisema: ‫ وَأَعْجَزُمِنْه‬،ِ‫ب آ إلْخْوَان‬ ِ ‫س مَنْ عَجَزَ عَنِ اْكْتِسَا‬ ِ ‫َأعْجَزُ اْلنَا‬ ْ‫ن ظَفِرَ ِب ِه مِنْهُم‬ ْ َ‫ح م‬ َ َ‫مَنْ ضَي‬ Mtu mnyonge sana ni yule ambaye hawezi kupata marafiki wowote, na mnyonge zaidi ya hawa ni yule anayepoteza marafiki na akabakia peke yake.9

ُ‫اَشَدُ اْلذُنُبِ مَااٌسْتَهَانَ بِهِ صَهِبُه‬ Dhambi mbaya sana ni ile dhambi ambayo yule mwenye kuitenda anaidhania kuwa ndogo na isiyo na maana. (Nahju’l-balagha, hadithi ya 340). Kuenea kwa dhambi ni kitu ambacho kinaficha ule ubaya wa dhambi kwenye uoni wa watu, na inaifanya ionekane si chochote mbele ya macho ya mtu. 9

Nahju’l-balagha, hadithi na. 11

23


4. Watu ambao wanavuta kisha wanasukuma: wao ni watu wanaotembea katika njia, ambao wanatenda katika njia ya imani na utaratibu wao; wanavuta makundi ya watu upande wao wenyewe, wanachukua nafasi kwenye nyoyo za watu kama mtu anayependwa na kutakiwa. Lakini pia wanasukuma makundi fulani toka kwao na kuyafukuza. Wanakuwa na marafiki na vilevile na maadui; wanatia moyo maafikiano, na kutokubaliana pia. Watu kama hawa pia ni wa aina kadhaa, kwani wakati mwingine nguvu zao za mvuto na za msukumo zote zinakuwa na nguvu, wakati mwingine zinakuwa dhaifu, na wakatimwingine inakuwepo tofauti kati yao. Kuna watu wengine wenye hulka kama hiyo ambao nguvu zao za mvuto na za msukumo zote zinakuwa na nguvu, na hii inahusika na jinsi viwango vyao vya kujenga na kukanusha ndani ya nafsi zao vina nguvu kiasi gani. Kwa kweli, nguvu pia zina viwango, kufikia mahali ambapo wale marafiki ambao wamevutwa watafidia roho zao na kujitoa wenyewe kabisa kwa ajili ya sababu hiyo; na maadui pia watakuwa na kichwa ngumu zaidi kiasi kwamba watatoa maisha yao katika kusudi lao wenyewe. Na vinaweza kuwa na nguvu sana kiasi kwamba hata karne na karne baada ya kifo cha mtu yule, nguvu zao za mvuto na msukumo zitakuwa bado zinafanya kazi katika vichwa vya watu na zitaleta athari pan asana. Mvuto na msukumo huu wa vipimo vya namna tatu ni miongoni mwa sifa maalum za awliyÄ â€™ (wale wapenzi wa Allah), kama vile tu mialiko ya vipimo namna tatu kwenye njia ya Allah swt. ilivyo ya kipekee kwa mlolongo wa mitume. Kwa kuzingatia hili, ni lazima ionekane ni aina gani za watu zinazovutwa na ni aina gani zinazosukumwa. Kwa mfano, wakati mwingine wale wenye elimu wanavutwa, na wale wajinga wanasukumwa, na wakati mwingine kinyume chake. Wakati mwingine watu waungwana na waliostaarabika wanavutwa n wale wabaya na waovu wanasukumwa, na wakati mwingine kinyume chake. Hivyo, marafiki na maadui, waliovutwa na waliosukumwa, kila mmoja ni ushahidi wa wazi wa hali ya mtu kama huyo. 24


Haitoshi tu kuwa na nguvu za mvuto na msukumo, au hata kwamba ziwe na nguvu, ili kwamba tabia ya mtu iweze kusifiwa, bali sababu ya hili ni ile tabia yenyewe, na tabia ya mtu yoyote yule sio ushahidi wa wema. Viongozi wote wa dunia nzima, hata wale wahalifu kama Changiz Khan, HajjÄ j na Mu'awiyah, walikuwa ni watu ambao walikuwa na nguvu zote, za kuvuta na za kusukuma.Haiwi mpaka mtu awe na hoja za kujenga katika nafsi yake, hawezi kamwe kuwafanya maelfu ya wapiganaji wawe watii kwake, na kutuliza hiari zao: haiwi mpaka mtu awe na uwezo wa utawala, anaweza kukusanya watu karibu yake kwa kiwango kama hicho. Mfalme wa Iran, NÄ dir Shah (alizaliwa 1100/1688, alitawala 1148/1736, alikufa 1160/1747) alikuwa mtu wa namna hiyo. Alikata vichwa vingi sana na akafanya macho mengi yatolewe kwenye mashimo yao, lakini umashuhuri wake ulikuwa na nguvu za kipekee. Kutoka kwenye Iran iliyoshindwa na kuporwa mwishoni mwa muhula wa Safavid aliunda jeshi kwa gharama kubwa, na, kama vile tu sumaku inavyovuta taka za chuma, wapiganaji walijikusanya karibu yake ambao sio tu waliiokoa Iran kutoka kwenye nguvu za kigeni, bali walikwenda kwenye sehema za mbali sana za India na wakaleta maeneo mapya chini ya utawala wa Iran. Hivyo kila mtu anavuta namna yake, na anafukuza namna yake wale wasio sawa nay eye. Mtu wa haki na muungwana anavuta kuelekea kwake mwenyewe watu wema wanaojitahidi kwa ajili ya haki, na hufukuzilia mbali kutoka kwake wenye tamaa, wapenda pesa, na wanafiki. Mtu mhalifu anavuta wahalifu karibu yake mwenyewe, na kuwasukuma wale ambao ni wema. Na, kama ilivyoonyeshwa, kuna tofauti nyingine katika uwezo wa nguvu ya mvuto. Kama vile inavyosemekana kuhusu kanuni ya graviti ya Newton, kwamba kiwango cha athari na mvutano kinakuwa kikubwa kwa uwiano na kipimo cha ukubwa wa kitu na katika uwiano wa kinyume kwa kipimo cha umbali unaoingilia kati, hivyo pia

25


miongoni mwa watu kuna tofauti katika nguvu ya mvutano na athari ambayo inatokana na mtu huyo mwenye mvuto huo. Ali – mtu mmoja mwenye nguvu mbili: Ali ni mmoja wa wale watu ambao wanazo nguvu zote, zile za kuvuta na zile nguvu za kusukuma, na mvuto na msukumo wake vina nguvu mno. Huenda hakuna mvuto na msukumo wenye nguvu kama wa Ali unaoweza kupatikana popote pale katika karne yoyote au mwanzo wa kipindi muhimu katika historia. Alikuwa amepata marafiki wa ajabu, watu wa kihistoria kweli, waliokuwa tayari kujitoa muhanga wao wenyewe, kustahimili, walioungua kwa mapenzi juu yake kama miali toka kwenye moto mkubwa, na uliojaa mwanga. Walichukulia kuwa kutoa maisha yao katika njia yake kuwa lengo lao na heshima yao, na walikuwa wasiotambua kitu chochote katika urafiki juu yake. Miaka, hata karne, zimepita tangu kifo cha Ali, lakini mvuto wake bado unatoa miali ile ile ya mwanga, na watu bado wanapumbazwa pale wanapougeukia. Katika maisha yake yote, watu waungwana na waliostaarabika, wachamungu, wenye kujitoa, watu wasio na ubinafsi, wavumilivu, wenye huruma na wa haki, waliokuwa tayari kuhudumia watu walizunguka katika mhimili wa maisha yake hivyo kwamba hadithi ya yeyote kati yao ni yenye kufundisha; na, baada ya kifo chake, wakati wa ukhalifa wa Mu’awiyah na Bani Umayyah, makundi makubwa ya watu yalikamatwa kwa kosa la urafiki juu yake na walipitia mateso makubwa mno, lakini hawakulegea katika urafiki wao na mapenzi kwa Ali na walisimama imara mpaka mwisho wa maisha yao. Kwa watu wengine, kila kitu kinakufa pale wanapofariki na wakawa wamefunikwa, miili yao chini ya ardhi; lakini ingawa watu wa haki wanakufa wao wenyewe, ufasi na mapenzi wanayochochea yanakuwa mang’aavu zaidi katika kupita kwa makarne. Tunasoma katika historia kwamba miaka na karne baada ya kifo cha Ali watu kwa ujasiri sana waliikubali mishale ya maadui zake. 26


Miongoni mwa wale wote waliokuwa wamevutwa, na kupumbazwa na Ali, tunaweza kumuona Maytham at-Tammār ambaye, miaka ishirini baada ya kuuawa kwa Ali, alizungumza kutoka kwenye kuteswa kwake juu ya Ali na uadilifu wake na sifa za kibinadamu. Katika siku hizo, wakati ummah wote wa Kiislam ulipokuwa unanyimwa pumzi, wakati uhuru wote ulipokuwa umetupiliwa mbali na nyoyo zikawa tumwa ndani ya vifua vyao vyenyewe, wakati kimya cha kutisha kilijionyesha kama ukungu wa kifo kwenye uso wa kila mtu, bwana huyu alikemea kutoka kwenye msalaba wake ili watu waje wasikilize kile atakachowaambia kuhusu Ali. Watu walijazana kutoka pande zote kusikiliza kile Maytham alichotaka kusema. Serikali yenye nguvu ya Bani Umayyah, ambayo iliyaona maslahi yake yenyewe yakiwa kwenye hatari, ilitoa amri ya kuwekwa kifumba kinywa mdomoni mwake, na, baada ya siku kadhaa, wakamkatisha uhai wake. Historia imebeba kumbukumbu nyingi za aina hii ya upendo juu ya Ali. Aina hizi za mvuto wenye nguvu sio mahususi kwa wakati wowote maalum; katika zama zote tunauona udhihirisho wao na matokeo yao yenye nguvu. Alikuwepo mtu mmoja aliyekuwa akiitwa Ibn as-Sikkit ambaye alikuwa mmoja wa wanazuoni wakubwa na watu mashuhuri katika fasihi ya Kiarabu, na jina lake limetajwa miongoni mwa mabingwa katika lugha ya Kiarabu kama as-Sibawayh na wengine. Aliishi katika wakati wa khalifa wa Bani Abbas aitwaye al-Mutawakkil, kiasi cha miaka mia mbili baada ya kuuawa kwa Ali. Katika utawala wa alMutawakkil alituhumiwa kuwa Shi’ah, lakini hata hivyo, kwa sababu alikuwa na elimu sana na maarufu mno, al-Mutawakkil alimteua kama mwalimu kwa ajili ya watoto wake mwenyewe. Siku moja, wakati watoto wa al-Mutawakkil walipomjia, na Ibn as-Sikkit alikuwa yupo na alikuwa siku ile inavyoonekana aliwapa mtihani ambamo walikuwa wamejizoesha vizuri sana, al-Mutawakkil alionyesha kuridhishwa kwake na Ibn as-Sikkit, lakini labda kwa sababu ya mashaka kutokana na kuwa amesikia kwamba alikuwa na elimu kuhsu Uislam wa Kishi’ah, akamuuliza Ibn as-Sikkit kama wale wawili mbele yake 27


(yaani, watoto wake wawili) walikuwa na thamani mno kwake yeye au Hasan na Husein, wale watoto wawli wa Ali. Ibn as-Sikkit alivurugwa sana na swali hili na ulinganisho ule na akawa na wasiwasi sana. Akajiuliza mwenyewe kama mtu huyu mwenye majivuno amefikia kiwango kama hicho kwamba ameanza kuwalinganisha watoto wake mwenyewe wawili na Hasan na Husein. Akajiambia mwenyewe kwamba lilikuwa ni kosa lake kwa kuwa na mafanikio sana katika elimu yao. Kwa kumjibu al-Mutawakkil alisema: “Wallahi, naapa, mtumwa wa Ali, Qanbar, kwa hakika ana thamani sana kwangu kuliko hawa wawili na baba yao.� Al-Mutawakkil akatoa amri kwa wale watu waliokusanyika pale kwamba ulimi wa Ibn as-Sikkit ukatwe kutoka kwenye koo lake. Historia inaweza kueleza juu ya watu wengi waliozongwa kabisa ambao bila kukusudia waliyatoa muhanga maisha yao kwa njia ya upendo juu ya Ali. Ni wapi mvuto kama huo unapoweza kupatikana? Mtu hawezi kufikiria kwamba katika dunia nzima kuna anayelingana naye. Kwa kiwango hicho hicho, Ali alikuwa na maadui wakaidi, maadui ambao waliwafanya watu watetemeke katika kutajwa majina yao. Ali si wa kuangaliwa kama mtu binafsi, bali hasa kama falsafa nzima. Na ni kwa sababu hii kwamba kundi moja livutika kwake, na moja linasukumwa. Kwa hakika, Ali alikuwa mtu wa nguvu mbili. *

*

*

28

*

*


SEHEMU YA KWANZA NGUVU YA MVUTO NDANI YA `ALI           

MIVUTO YENYE NGUVU USHI’AH, MADHEHEBU YA UPENDO KIOEVU CHA UPENDO KUVUNJA VIZUIZI JE, NI WENYE KUJENGA AU KUBOMOA? UPENDO NA UTII KWA WALE WALIOKO KARIBU NA MWENYEZI MUNGU NGUVU YA UPENDO KATIKA JAMII NI NJIA BORA ZA KUITAKASIA NAFSI MIFANO KUTOKA KWENYE HISTORIA YA UISLAMU MAPENZI JUU YA `ALI NDANI YA QUR’AN NA SUNNAH SIRI YA NGUVU YA MVUTO YA `ALI

29


MIVUTO YENYE NGUVU Katika utangulizi kwenye juzuu ya kwanza ya The Seal of the Prophets (Mwisho wa Mitume), imeandikwa kuhusu mada ya miito kwa wanadamu: “Ile ‘Miito’ ambayo imetokea miongoni mwa wanadamu haikuwa yote ni yenye kufanana, na mionzi ya athari zake haikuwa ya namna moja tu. “Baadhi ya miito na mifumo ya fikra ni ya inaendea upande mmoja; inapotokea, inaingiza mamilioni ya watu huwa wafuasi, lakini basi kufikia mwisho wanafunga mlango na wanabaki

kipimo kimoja tu, na kundi kubwa la watu, baada ya muda wao kusahaulika.

“Mingine ina vipimo namna mbili, mionzi yao inasambaa pande mbili. Wakati inaingiza kundi kubwa la watu, na pia inaendelea kwa kiasi cha muda, umbali wao haukufungwa kwenye kipimo cha masafa na pia inaongezeka kwenye kipimo cha wakati. “Na baadhi ya mingine inaendelea katika wingi wa vipimo. Sio tu tunaiona ikivutia kundi kubwa la watu toka kwenye jamii ya wanadamu na kuwashawishi wao na kutambua athari za ushawishi wao kwenye kila bara, bali pia tunaona kwamba inajumuisha kipimo cha wakati, hii ni kusema kwamba, haikufungwa katika wakati mmoja au enzi moja bali inatawala kwa nguvu zao zote, karne baada ya karne. Pia inatoa mizizi katika vina vya roho za binadamu, na kiini hasa cha mioyo ya watu kiko chini ya udhibiti wao wenye nguvu; inatawala katika undani wa nafsi na kushika hatamu za mihemuko mikononi mwao. Aina hii ya miito ya vipimo vitatu ndio ya pekee katika mnyororo wa Mitume. “Ni shule gani za kisomi au za fikra za kifalsafa zinazoweza kupatikana ambazo, kama dini kuu za dunia, zikatumia mamlaka yao juu ya mamia ya mamilioni ya watu kwa karne thelathini, au karne ishirini, au, kwa kiwango cha chini kabisa, karne kumi na nne, na kuzama kwa kina kwenye kiini chao cha ndani kabisa.”

30


Nguvu za mvuto ziko pia kama hivi: wakati mwingine za kipimo kimoja, wakati mwingine viwili, wakati mwingine vitatu. Nguvu ya mvuto ya `Ali ilikuwa ya aina hii ya mwisho. Sio tu imevuta sehemu kubwa ya jamii ya wanadamu, bali pia haikukomea kwenye karne moja au mbili; kwa hakika, imeendelea na kupanuka wakati wote. Ni ukweli kwamba inaangaza kurasa za karne na zama, imefikia kina cha ndani ya mioyo na nafsi, kwa namna ambayo, baada ya mamia ya miaka, wakati anapokumbukwa na ubora wa tabia zake unaposikika, machozi ya upendo humwagwa, na kumbukumbu za misiba yake zinaibuka kwa kiasi kwamba hata maadui wanaguswa (kihisia) na machozi yakawadondoka. Hii ndio nguvu ya mvuto yenye uwezo zaidi kuliko zote. Kutokea hapa inawezekana kueleweka kwamba kiungo kati ya mtu na dini sio cha kimaada (cha kuonekana kwa macho), bali hasa ni cha namna nyingine, mfano wa kiungo ambacho hakiunganishi kitu kingine chochote kwenye nafsi ya mwanadamu. Kama `Ali asingekuwa mwenye sifa tukufu na asingekuwa mtu wa Mungu, angeweza kusahaulika. Historia ya mwanadamu imejaa kumbukumbu za mabingwa wengi, mabingwa wa kuzungumza, mabingwa wa elimu au falsafa, mabingwa wa madaraka na mamlaka na mabingwa katika uwanja wa vita, lakini wote hao wamesahauliwa na watu, au vinginevyo hawajulikani kabisa. Lakini, sio tu kwamba `Ali hakufa kwa kuuawa kwake, bali alipata uhai zaidi. Alizungumza kweli aliposema : ‫ن م َا بَقِىَ الدَهْرُاَعْ َيا نُهُمْ مَفْقُودَ ُة وَمْ َثا لُهُمْ فِي‬ َ ‫ك خُ َز انُ أال مْ َوالِ وَهُمْ أحْيا ُء وَالْعُلَماَءُ باَقُو‬ َ َ‫هَل‬ ُ‫اَلْقُلُوبِ مَوْ جُودَة‬ Wale wanaolimbikiza mali wanakuwa wafu hata wanpokuwa wako hai, lakini wale wenye elimu watadumu kwa kiasi dunia itakavyodumu. Miili yao inaweza kuwa imetoweka, lakini taswira zao zinaendelea kudumu mioyoni.” (Nahju’l-balagha: semi Na: 47) 31


Alisema kuhusu tabia yake mwenyewe: ‫عنْ سَرَ اِئِرِي وَتَع ِر فُونَنِي بَعْ َد خُلُوَِّ َمكَا نِي وَقِيَا ِم غَيْرِي مَقَامِي‬ َ ‫ن أَيَامِي وَيُكَْ شَفُ لَكُم‬ َ ْ‫غَدَ​َا تَرَو‬ “Kesho mtaziona siku zangu hizi na sifa zangu zisizojulikana zitadhihirika kwenu, na baada ya nafasi yangu kuwa imeachwa wazi na mtu mwingine ameikalia, mtanifahamu mimi.” (Nahju’l-balaghah, khutba na : 149) Iqbal aliandika: “Zama zangu mwenyewe hazielewi maana zangu za kina, Yusufu wangu si kwa ajili ya soko hili Ninakata tamaa kwa mabingwa wangu wa zamani, Sinai yangu inaungua kwa ajili ya Musa ambaye anakuja. Bahari yao ishwari, kama umande, Lakini umande wangu una mawimbi, kama bahari. Wimbo wangu ni wa dunia nyingine kuliko yao: Kengele hii inawaita wasafiri wengine kuichukua barabara. Washairi wengi walizaliwa baada ya kifo chake, Alifungua macho yetu wakati yake mwenyewe yamefumbwa, Na alisafari mbele tena kutoka pasipokuwepo. Kama waridi linavyostawi kwenye ardhi ya kaburi lake. Hakuna mto utakaochukua Oman yangu: Mafuriko yangu yahitaji mabahari mazima kuyabeba. Radi zimelala ndani ya nafsi yangu, Ninapeperuka juu ya mlima na bonde. Chemchem ya maisha nimepewa mimi ninywe,

32


Nimefanywa kirekebishio cha kitendawili cha Maisha. Hakuna aliyeniambia hii siri ambayo nitaisema Au aliyetunga lulu ya mawazo kama yangu Mbinguni kumenifundisha maarifa ya mapokezi haya, Siwezi kuyaficha kwa marafiki zangu.1 Kwa kweli `Ali ni kama utaratibu wa mambo ya asili ambayo yanabaki hayabadilishwi na wakati. Yeye ni jicho la kisima cha ukarimu ambacho kamwe hakikauki, lakini ambacho hasa huongezeka siku hadi siku. Katika maneno ya Kahlil Gibran (Jubran Khalil Jubran [1300/1883-1349/1931]), alikuwa ni mmoja wa wale watu ambaye alizaliwa kabla ya wakati wake. * ** USHI’AH, NI MADHEHEBU YA UPENDO Moja ya alama kubwa za ubora wa Ushi’ah juu ya madhehebu nyinginezo ni kwamba msingi wake na kiini chake ni upendo. Kutoka hasa wakati wa Mtume (s.a.w.w.) aliyeweka msingi wa madhehebu hii kumekuwepo na minonong’ono ya upendo; pale tunaposikia kutoka kwenye kauli ya Mtume maneno haya: “ `Aliyyun wa Shi‘atuhu humu’l-fa’izun.”2 “`Ali na kundi lake (shi‘ah) ndio wenye kufuzu.” Tunaona kwamba kulikuwa na kikundi kilichomuandama `Ali na waliojitolea kwake, waliokuwa na upendo mwingi sana juu yake na waliovutwa sana kwa mapenzi juu yake. Kwa hiyo Ushi‘ah ni dini ya 1

Muhammad Iqbal: Kitabu - The secrets of the self, tafsiri ya R.A. Nicholson, juz. 2 nakala iliyosahihishwa, Lahore 1940. 2 Katika ad-Durru’l-manthur, kwenye aya ya saba ya surat al-bayyinah (90), Jalalu’ d-Din as-Suyuti anasimulia kutoka kwa Ibn ‘ Asakir kwamba Jabir ibn ‘ Abdillah al -Ansari alisema kwamba alikuwepo mbele ya Mtume wakati `Ali alipomjia pia. Mtukufu Mtume akasema: “ Naapa kwa Yule ambay e maisha yangu yamo mikononi Mwake kwamba bwana huyu na wafuasi wake (Shi’ ah) wataokolewaa Siku ya Qiyammah.” Al -Manawi analisimulia hili katika hadithi mbili ndani ya Kunuzu’l-haqa’iq na al-Haythami

katika Majma‘u’z–Zawaid na Ibn Hajar katika Sawa’iqu’l-muhriqah anasimulia maana hii hii muhimu kwa namna tofauti.

33


upendo na kujitolea: kumchukulia `Ali kama rafiki yake mtu ndio njia au namna ya upendo. Ule msingi wa asili ya upendo umeupenyeza kabisa Ushi‘ah, na historia ya Ushi’ah imeunganishwa kwa jina na msururu wa watu wasiojulikana kabisa, waliojitolea, waliojawa na mapenzi na uhanga wa nafsi. Ingawa `Ali alitekeleza adhabu za Shari’a kwa baadhi yao akiwaadhibu kwa mijeledi na wakati mwingine kukata mikono ya mtu kulingana na ilivyoainishwa na Sheria Tukufu, hawakumgeuka na upendo wao kwake haukupungua hata chembe. Yeye mwenyewe alisema: “Kama nitaikata pua ya mu’min kwa upanga wangu huu ili awe adui yangu, haitasababisha uhasama, na kama nitamwaga (utajiri wa) dunia yote kichwani mwa mnafiki ili anipende, kamwe hatanipenda; kwa sababu hii imeamriwa na kutamkwa kwa ulimi wa Mtume (s.a.w.w.) aliposema: ‘Ewe `Ali, mu’min kamwe hatakuwa adui yako na mnafiki kamwe hatokupenda wewe!’”3 `Ali (a.s.) ndio kipimo na kigezo cha kupimia hulka asilia na silka za wanadamu: yule mwenye hulka nzuri na silka safi kamwe hatamfanyia uadui `Ali, hata kama upanga wake utaangukia kwenye kichwa chake, ambapo yule mwenye hulka yenye maradhi hataonyesha kamwe kujiambatanisha kwake, hata kama yeye `Ali atamfanyia wema mkubwa, kwa `Ali si chochote ila ni mfano halisi wa ukweli. Alikuweko rafiki ya ‘Amir-ul-muminin, mtu mzuri na mu’min ambaye kwa bahati mbaya alifanya kosa, na ambaye alikuwa aadhibiwe. ‘Amirul-muminin alimkata vidole vyake vya mkono wa kulia. Mtu huyo akaushika ule mkono wake uliokatwa, kwa mkono wake wa kushoto, na huku damu ikidondoka toka kwenye mkono huo, na akaondoka zake. Ibn al–Kawwa’, mchochezi mmoja wa ki-Kharij, akataka kutumia fursa ya jinsi mambo haya yalivyokwenda kwa faida ya kundi lake dhidi ya 3

Nahju’l-balaghah, Semi namba: 42.

34


`Ali, hivyo alimjia yule mtu kwa hali ya huruma kabisa na kusema: “Ni nani aliyekukata mkono wako?” “Ni yule mkuu wa warithi wa Mtume”, akasema, “yule kiongozi wa wale wasio na dosari wakati wa kufufuliwa, mwenye haki zaidi miongoni mwa waumini, `Ali ibn Abi Talib, Imam wa uongofu wa haki, ndie aliyekata vidole vya mkono wangu wa kulia… yule wa kwanza kuingia kwenye bustani za furaha kuu (peponi), shujaa wa mashujaa mlipiza kisasi dhidi ya watetezi wa ujahilia, mtoa Zaka… Kiongozi katika njia ya haki na sahihi, msemaji wa kilichokuwa kweli na chenye manufaa, bingwa wa Makkah, mtekelezaji imara.”… “Masikini wee!” akasema Ibn al–Kawwa’, “Yeye ameukata mkono wako, na bado unamtukuza hivyo!” "Kwa nini nisimtukuze,” akasema “sasa hivi kwa vile urafiki wake umechanganyika na nyama na damu? Naapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba hakuukata mkono wangu ila kwa haki ambayo Mwenyezi Mungu ameisimamisha.”4 Mapenzi haya na upendo huu ambao tunauona kwa namna hii katika historia ya `Ali (a.s) na masahaba zake, yanatufanya tugeukie kwenye suala la upendo na matokeo yake.

*

*

4

*

Biharu ‘l-anwar, juz. 40, uk.281-2 (nakala mpya); na Fakhru’d-Din ar-Razi, atTafsiru’l-kabir, kwenye aya ya 9, surah al-Kahf [ “Au unadhani…….”).

35


KIOEVU CHA UPENDO Washairi wa Kiajemi waliuita upendo “kioevu” – iksir - (elixir). Waalkemia waliamini kwamba kulikuwepo na kitu humu duniani walichokiita “kioevu”5 au “jiwe la mwana-falsafa” (kimiya) ambacho kingeweza kubadili maada moja kuwa maada nyingine, na walikitafuta hiki kwa karne kadhaa. Washairi hawa walichukua matumizi ya istilahi hii na wakasema kwamba kioevu cha kweli chenye uwezo wa kugeuza kitu ni upendo, kwa sababu ni upendo unaoweza kugeuza kitu. Upendo, peke yake, ndio kioevu hicho na kina rasilimali za jiwe la mwanafalsafa, ambazo hugeuza jinsi moja kuwa nyingine, na wanadamu pia na jinsi tofauti. ِ‫ّضة‬ َ ِ‫س مَعاَدِنُ كَمَعَادِنِ آلذَهَبِ َو الْف‬ ُ ‫اَلنَا‬ Watu ni kama migodi, kama migodi ya dhahabu na migodi ya fedha. Ni upendo unaofanya moyo kuwa moyo, na kama hakuna upendo, hakuna moyo, ni udongo wa ufinyanzi tu na maji. Kila moyo ambao hauwaki sio moyo; Moyo ulioganda si lolote bali konzi ya udongo 5

Katika kamusi ya lugha ya Ki-ajemi “Burhan-e-qati” yafuatayo yameandikwa kuhusu “kioezi” (iksir): “Ni kitu kinachoyeyuka, kinachokusanya na kukamilisha; ni kusema kwamba inatengeneza dhahabu kutokana na shaba na inafaa kwenye madawa. Inaelekea kwamba “kukamilisha” vilevile kunaitwa “upendo” kimajazi’.” Inatokea hivyo kwamba katika upendo, sifa hizihizi tatu zinapatikana – “unayeyusha”, “unakusanya” na “unakamilisha” – lakini sifa inayofahamika sana ki-majazi ni hii ya tatu, nguvu yake ya kugeuza ukamilikaji. Hivyo washairi wakati mwingine wameuita upendo kwa jina la “daktari”, “dawa”, “Plato” au “Galen”. Katika utangulizi wa Mathnavi Rumi anaandika: Karibu, Ewe Upendo unayetuletea neema tena – Wewe ndio tabibu wa maradhi yetu yote, Ewe tiba ya fahari na majivuno yetu, Plato wetu na Galen wetu! (tafsir ya Nicholson, kitabu cha 1, 1.23)

36


Eh! Mola! Nipe kifua chenye kuwaka moto, Na katika kifua hicho, moyo, na moyo huo, uliomezwa na moto. 6 Moja ya athari za upendo ni nguvu; upendo ndio nguvu ya kujivunia, inamfanya muoga kuwa jasiri. Kuku ataweka mbawa zake zikiwa zimekunjwa mbavuni mwake mradi akiwa peke yake. Ataranda kwa utulivu kabisa, akitafuta minyoo midogo ameze. Ataanza kwa kelele ndogo kabisa na kutorudi nyuma hata mbele ya mtoto dhaifu kabisa. Lakini wakati kuku huyohuyo atakapokuwa na vifaranga, upendo unachukua nafasi yake katikati ya nafsi yake na tabia yake inabadilika kabisa. Zile mbawa zilizokuwa zimekunjwa mbavuni mwake sasa zimeteremshwa kwa ishara ya kujiandaa kiulinzi, anajiandaa kwa mkao wa mashambulizi, hata sauti ya mlio wake inakuwa ya nguvu zaidi na kakamavu. Kabla ya hapo, aliruka penye uwezekano wa hatari, lakini sasa atashambulia pale penye uwezekano huo wa hatari, na atashambulia kwa ujasiri. Huu ni upendo unamuonyesha yule kuku mwenye woga katika hali ya mnyama jasiri. Upendo huwafanya wale wazito na watepetevu kuwa wepesi na wajanja, na hata huwafanya waliozubaa kuwa werevu. Mvulana na msichana ambao hakuna mmoja wao, wakati walipokuwa peke yao, aliyejikuta anakifikiri juu ya kitu chochote ila kile ambacho moja kwa moja kinahusiana na nafsi zao wenyewe, wanaona kwamba wanahusika juu ya msiba wa mwingine kwa mara ya kwanza tu mara wanapoangukia kupendana na kujenga mazingira ya kifamilia. Kipenyo cha mahitaji yao kinapanuka; na wanapokuja kuwa wazazi, ari zao hubadilika kabisa. Yule mvulana baleghe, mzito na legelege sasa amekuwa mchacharikaji na mhangaikaji, na yule msichana ambaye alikuwa hatoki kwenye mashuka ya kitanda chake hata wakati wa mchana, anatembea kama radi anaposikia kilio cha mwanae kitandani kwake. Ni nguvu gani hii ambayo imeshtua ule ulegevu na uchovu ndani ya hawa vijana wawili? Si chochote ila ni upendo.

6

Kutoka kwa Vahshi

37


Ni upendo unaomgeuza bakhili kuwa mfadhili, na mtu asiye na subira na uvumilivu kuwa mtu mwenye ustahimilivu na uvumilivu. Ni upendo uliompa yule ndege mchoyo aliyelimbikiza nafaka akijifikiria yeye tu akilini mwake na akajijali mwenyewe tu, umbile la kiumbe mkarimu anayewaita vifaranga wake anapopata punje ya nafaka; au ambaye, kwa nguvu za ajabu, zinamfanya mama, ambaye hadi jana yake alikuwa ni mtoto aliyeharibika ambaye alikula na kulala tu na alikuwa mwenye harara na asiye na subira, kuwa mwenye kuvumilia na kustahimili anapokabiliwa na njaa, ukosefu wa usingizi na uchovu, ambao unampa mama huyo uvumlivu wa kustahimili magumu ya umama. Kule kupatikana kwa wepesi na kuondoa uzito na mikwaruzo toka kwenye nafsi, au, ukiweka kwa lugha nyingine, ule utakasaji wa hisia, na pia ule uunganishaji na upweke wa lengo na umakinikaji, na kutoweka kwa vurugu na mtawanyiko ndizo kudura na mwishowe, nguvu ambazo zinatokana na kuja pamoja kwa athari za matokeo ya upendo. Katika lugha ya kishairi na fasihi, unapoongelewa upendo, tunakabiliana na maana moja zaidi kuliko nyingine, nayo ni uwezo wa upendo kuleta mvuto, na uvujaji wake. Kurumbiza alijifunza wimbo wake kwa upendeleo wa waridi, vinginevyo pasingeweza kuwa na Chochote katika wimbo huu na muziki uliotengenezeka kutoka mdomoni mwake.7 Ingawa upendeleo wa waridi, kama tutashughulika na maneno hayo tu, ni jambo mbali na kuwepo kwa huyo kurumbiza, kwa kweli si lolote bali ni nguvu ya upendo wenyewe. Unadhani kwamba Majnun alikuwa mwendawazimu(majnuni) hivi mwenyewe tu?

7

Hafiz

38


Ilikuwa ni kutupiwa jicho na Layla kulikomsafirisha miongoni mwa nyota.8 Upendo unaamsha nguvu zilizolala, na kufungulia minyororo na pingu, kama vile kugawanyika kwa atomu na kuachiliwa kwa nguvu za atomiki. Unawaka kwa mvuto na kujenga mashujaa – ni washairi, wanafalsafa, na wasanii wangapi wamekuwepo, ambao wametengenezwa na upendo wenye nguvu na uwezo. Upendo hukamilisha roho na huleta uwezo wa ajabu ya kipawa. Kutokana na mtazamo wa uwezo wa utambuzi, unavuta, na kutokana na mtazamo wa hisia, unatia nguvu nia na dhamiri, na unapopanda kwenye kiwango chake cha juu unaleta miujiza na vituko visivyo vya kawaida. Unasafisha nafsi kutokana na tabia na hali za mwili, au, kwa maneno mengine, upendo ni aina ya haluli (dawa ya chumvichumvi), unatakasa tabia mbaya zinazotokana na ubinafsi, au kutoka kwenye ubaridi na ukosefu wa ukunjufu, kama vile husda, uchoyo, woga, ulegevu, kiburi na majivuno. Unaondoa mifundo na nia mbaya, ingawa inawezekana kwamba kunyimwa, na kuvunjwa moyo katika upendo kunaweza kuzaa kwa vipindi vyao vyenyewe, hali ngumu na karaha. Kwa upendo, uchungu huwa mtamu, Kwa upendo, vipande vya shaba huwa dhahabu 9 Katika roho, athari za upendo zimo katika namna ya maendeleo na ustawi wake; katika mwili, ni katika namna ya kuyeyuka na kuchanguka kwake. Athari za upendo katika mwili ni kinyume kabisa cha kile kilichomo kwenye roho. Katika mwili upendo ni chanzo cha uharibifu, na sababu ya udhaifu na unyonge wa mwili, ya kutojisikia vizuri na mvurugiko wa mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na neva. Pengine athari zote ulizonazo katika mwili ni za uharibifu; bali kwa kuunganishwa na roho haziwi hivyo – inategemea kusudi la upendo na jinsi mtu huyo anavyovutika kwenye kusudio hilo. Kuacha pembeni athari zake za kijamii, unakamilisha kwa kuathiri zaidi katika roho na 8 9

Allamah Taba’taba’i Rumi, Mathnavi

39


mtu mwenyewe, kwa sababu unatia nguvu, huruma, utulivu umakini katika lengo na dhamira; unaondoa kabisa unyonge, ukatili, kero, kutojikusuru na ugoigoi. Unaondoa zile ghasia ambazo zinaitwa dassa ndani ya Qur’ani (91:10), yenye maana ya mchanganyiko wa usafi na uchafu, unaangamiza udanganyifu na kumtakasa mdanganyifu. Njia ya kiroho huharibu mwili, Na, baada ya kuuharibu, huurudisha kwenye ustawi: Oh! Furahi ewe moyo ambaye, kwa upendo na upeo, Uliacha meko na nyumba, utajiri na mali, Uliiharibu nyumba kwa ajili ya hazina ya dhahabu, Na kwa hazina hiyohiyo ukaijenga upya vizuri; Ukayakata maji na kusafisha chini ya mto, Kisha ukayafanya maji ya kunywa kutiririka chini ya mto; Ukachana ngozi na kuchomoa ile ncha ya chuma – Kisha ngozi mpya ikaota juu yake. Wale wakamilifu ambao wanatambua siri ya ukweli Wako kwenye upeo wa furaha, wamechanganyikiwa wamelewa na wametiwa wazimu na upendo. Hawakuchanganyikiwa kwa namna kwamba mgongo wake umemuelekea yeye, Bali wachanganyikiwa kwamba (wako) wamezama na kulewa na yule Mpendwa.10 *

*

*

KUVUNJA VIZUIZI Upendo humtoa mtu kwenye ubinafsi na kujipenda, bila kujali ni aina gani ya upendo – wa kinyama na wa kijinsia, wa kinyama na kiuzazi, au wa kiutu – na bila kujali ni kwa sifa na ubora gani alionao mwenye kupendwa, awe ama ni jasiri na hodari, mstadi au mwenye hekima, ama pengine awe (mwanamke) ana murua mzuri, hana aibu mbele za watu au sifa nyinginezo maalum. Kujipenda mwenyewe ni udhaifu na kizuizi 10

Imetolewa kutoka kwenye tafsiri ya Nicholson ya Rumi, Mathnavi, kitabu cha 1.

40


cha kujihami; upendo huvunja kabisa hiki kizuizi cha kujilinda na kisichokuwa nafsi. Mwanadamu ni dhaifu mpaka awe ametoka nje ya nafsi yake, ni muoga, mlafi, mwenye tamaa ya mali za wengine, mwenye kujitenga na watu, mwepesi wa hasira, mchoyo na fedhuli; roho yake haitoi cheche yoyote ya mng’aro, haina uchangamfu au shauku, mara nyingi imepooza na kujitenga. Hata hivyo, mara tu anapochukua hatua nje ya “nafsi” yake na akavunja vizuizi vyake vya kujilindia, hizi tabia na sifa mbaya nazo pia zinaharibika. Nguo ya yeyote yule ambayo imechanwa na upendo Amesafishika kabisa na kutamani vya watu na dosari.11 Kujipenda, kwa maana ya kitu ambacho lazima kiondoshwe, sio kitu ambacho kwa kweli kipo. Tunachomaanisha ni kwamba sio kujipenda kwake kwa kweli kulikopo ambako mtu lazima aachane nako ili aweze kuwa amekombolewa kutokana na “kujipenda binafsi”. Haileti maana kwa mwanadamu kujaribu kutojipenda yeye mwenyewe; taadhima ya mtu binafsi ambayo tunaweza kuiita “kujistahi” haikuacha kutiliwa maanani kwa makosa ili tuitupe nje. Kurekebika na kukamilika kwa mtu hakuna maana kwamba, tuchukulie labda, mfuatano wa mambo yasiyofungamana na kuwepo kwake mtu yanafikiriwa na kisha kwamba mambo haya yasiofungamana na yenye madhara lazima yaachwe. Kwa maneno mengine kurekebika kwa mtu hakupo katika kumpunguza, kupo katika kumkamilisha na kumuongeza. Wajibu ambao maumbile yameweka kwenye dhamana ya mtu uko katika uelekeo wa kawaida wa maumbile, yaani, katika ukamilifu na ukuaji, sio katika upunguaji na kupunguzwa. Kushindana na kujipenda ni kushindana na mipaka ya nafsi. Nafsi hii lazima ikuzwe, huu muundo wa kujihami, uliowekwa kuizunguka nafsi na ambao unaona kila kitu kingine, mbali na kile kilichounganishwa nayo kama mtu au pekee, kama kigeni “sio mimi” na tofauti nacho, lazima uvunjwe kabisa. Nafsi lazima ikuzwe kumchukua kila mtu mwingine, kama sio ulimwengu wote wa kimaumbile. Hivyo 11

Rumi, Mathnavi, kitabu cha 1.

41


kushindana na kujipenda ni kushindana na mipaka ya nafsi, na kwa hiyo kujipenda sio chochote ila ni mpaka wa namna ya kuwaza na kufikiri. Upendo hugeuza huba ya mtu na kumsukuma kuelekea kwenye kile kilichoko nje ya nafsi yake, unakuza kuwepo kwake mtu na hubadili mtazamo wa hali yake. Kwa sababu hiyohiyo, upendo ni kipengele kikubwa cha maadili na chenye kufundisha, kwa masharti kwamba umeongozwa vizuri na kutumika kwa usahihi. * * * JE NI WENYE KUJENGA AU KUBOMOA? Wakati mapenzi juu ya mtu au kitu yanapofikia kiwango cha nguvu sana kwamba yanayashinda maisha ya mwanadamu na yanakuwa ndio mtawala pekee juu ya utu wake, yanaitwa upendo. Upendo ndio kikomo cha mapenzi na hisia. Lakini isidhaniwe kwamba kinachoitwa kwa jina hili ni cha namna moja tu; ni cha namna mbili tofauti kabisa. Yale mambo yanayoitwa athari zake nzuri, yanaunganika na namna yake mojawapo, lakini namna yake nyingine ina athari haribifu kabisa na za kinyume. Hisia za mtu ni za namna mbalimbali na viwango tofauti; baadhi yao ziko katika namna ya shauku, hususan ashiki, na ni zile tabia ambazo zinachangiwa na mwanadamu na wanyama wengine, kwa tofauti kwamba mwanadamu, kwa sababu maalum ambayo maelezo yake hayawezi kutolewa kwa ufasaha sasa, zinafikia kilele chake na kuchukua nguvu kali isiyoelezeka; na kwa sababu hii zinaitwa upendo. Kamwe haiwi hali kama hii miongoni mwa wanyama, lakini, kwa hali yoyote, katika uhakika na dhati yake, si lolote ila ni mbubujiko, nguvu ya mpasuko, na dhoruba ya hisia. Inatokana kwenye chanzo cha ashiki, na inafikia ukomo wake hapohapo pia. Kupanda na kushuka kwake, ni kwa kiwango kikubwa, kilichounganishwa na shughuli za kifiziologia za viungo vya uzazi na vya kawaida kwa miaka ya ujana; inapungua na hatimae hukoma kabisa pamoja na ongezeko katika umri, kwa upande mmoja, na kwa upande mwingine, pamoja na kukinaisha na kujitenga. 42


Kijana anayehisi mtetemeko anapoona sura inayopendeza au msokoto wa nywele, au anayehisi msisimko anapoguswa na mkono laini, sharti ajue kwamba hakuna chochote kinachotendeka hapa zaidi ya mwenendo yakinifu wa kinyama. Aina hii ya upendo huja haraka na kuondoka haraka. Haiwezi kutegemewa, wala kupendekezwa, ina hatari na inauwa wema. Ni kwa msaada tu, wa staha na uchamungu na sio kwa kutelekezwa kwake kwamba kunaweza kumfaa mwanadamu; ni kwamba, ikiwa yenyewe, ni nguvu isiyomwelekeza mtu kwenye wema wowote. Lakini inatia nguvu na ukamilifu kwenye nafsi, kama itapenyeza ndani ya mtu, inakutana na nguvu ya staha na uchamungu, na kama nafsi itavumilia shinikizo lake – ili mradi haishindwi kwayo. Wanadamu wanayo namna nyingine ya hisia ambazo, katika hali zao halisi na asili, zinatofautiana na raghba; ni vema kuziita hisia hizi za kiungwana, au katika lugha ya Qur’ani, “upendo na huruma” (muwaddah wa rahmah [rejea 30:21] ). Mradi mwanadamu yuko chini ya mamlaka ya hisia zake, hajatoka nje ya nafsi yake, anatafuta mtu au kitu ambacho kinamvutia kwa ajili yake, na anakitaka sana. Kama anafikiria juu ya kitu cha mapenzi, ni pamoja na mawazo ya vipi ataweza kufaidika kwa kuungana nacho, au sana sana ni vipi atapata starehe kutokana nacho. Ni wazi kwamba hali kama hiyo haiwezi kuwa mkamilishaji au muelimishaji wa nafsi ya mtu, au kuisafisha. Hata hivyo, mtu wakati mwingine huja kwenye athari za hisia za hali ya juu ya kibinadamu; mpenzi wake hupata heshima na umaarufu mbele yake, anaitafuta furaha ya mtu huyo. Anakuwa tayari kujitolea mhanga kwa ajili ya matakwa ya mtu huyo. Aina hii ya hisia huleta usafi, uaminifu wema, upole na uungwana, kinyume na ile aina ya kwanza ambayo inasababisha utovu wa nidhamu, ukatili na uhalifu. Upole na mapenzi ya mama kwa mwanae ni wa aina hii ya pili. Kujitolea, na mapenzi kwa wale watu wasafi na watu wa Mungu, kama pia uzalendo na mapenzi ya kanuni, kote kunatokana na aina hiyohiyo.

43


Ni aina hii ya hisia ambayo kutokana nayo, inapofikia kilele na ukamilikaji wake, athari zote nzuri zilizokwisha tajwa mwanzoni hutokea; na ni aina hii inayoifanya nafsi iwe na hadhi, ubora na umashuhuri, kinyume na ile aina ya kwanza ambayo inaleta uduni. Vivyo hivyo ni aina hii ya upendo ambayo inadumu, na ambayo inakuwa na nguvu sana na uchangamfu pamoja na muungano, kinyume na ile ya kwanza ambayo sio ya kudumu na ambayo muungano wake makaburini unahesabiwa kuwepo. Ndani ya Qur’ani, uhusiano kati ya mume na mke umeelezwa kama “upendo na upole”12 , na hii ni nukta muhimu sana. Ni ishara ya utu na hali ya ubora-kuliko- mnyama kwenye maisha ya ndoa. Ni ishara kwamba vile viwango vya hisia sio viungo pekee vya asili katika maisha ya ndoa. Kiungo cha msingi ni usafi, uaminifu na umoja wa nafsi mbili; au, kwa maneno mengine, kitu kinachowakusanyisha wawili waliooana mmoja na mwingine, na kuwaunganisha, ni upole, huruma, ukweli na uaminifu, sio zile tamaa, ambazo zipo pia kwa wanyama. Katika njia yake mwenyewe ya kistadi, Rumi anapambanua kati ya tamaa na mapenzi ya kweli; anaiita hii ya kwanza ya kinyama na hii nyingine ya kibinaadamu. Anasema: Ghadhaba na tamaa ni sifa za wanyama, Mapenzi na upole ni sifa za mwanadamu. Hivyo Upendo ni tabia ya Adamu, inayokosekana kwa wanyama, ni upungufu.

12

‫وَمِنْ ا‬

“Na katika dalili zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu katika jinsi yenu ili mpate utulivu kwao, naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu”. (ar-Rum, 30:21)

44


Wanafalsafa wanaothamini mali pia hawakuweza kuikataa hii hali ya kiroho ambayo, kutokana na mitazamo mbalimbali, ina sifa isiyokuwa ya ki-mali na ambayo haingeweza kukubaliana na mwanadamu na kile kilicho kinyume naye kuwa ni mali. Katika kitabu Marriage and Morals, Bertrand Russell anaandika hivi: Kazi ambayo dhamira yake ni ya kifedha peke yake haiwezi kuwa na thamani hii, bali kazi inayoshirikisha baadhi ya aina za upendo (nia mbalimbali), ama kwa watu, ama kwa vitu au kwa wazo tu. Na mapenzi yenyewe hayana faida yanapokuwa kimilikishi; ndipo hapo yanapokuwa kwenye kiwango kimoja na kazi ambayo ni ya kifedha hasa. Ili kuipata namna ya thamani tunayoizungumzia,mapenzi lazima yaguse nafsi ya yule mtu anayependwa kwa umuhimu kama nafsi yake mwenyewe, na lazima atambue hisia na matakwa ya mwingine kana kwamba yalikuwa yake mwenyewe.13 Jambo lingine ambalo halinabudi kutajwa hapa na kushughulikiwa kwa makini zaidi ni kwamba tulisema hata mapenzi ya hisia yanaweza kuwa yenye manufaa, na hilo linatokea pale yanapounganishwa na uchamungu na uungwana, maumivu na machungu, mashinikizo na matatizo ambayo kwayo nafsi ingehusika huzaa matokeo mazuri na yenye manufaa. Ni kwa uhusiano huu ambapo masuffi wanasema kwamba mapenzi ya kiistiari yanageuka kuwa mapenzi ya kweli, yaani, mapenzi ya ile Asili ya yule Mmoja; na pia ni kwa kuhusiana na hili ndipo riwaya ifuatayo inasimuliwa: Yule anayekuwa mpenzi, anayeficha (Upendo wake) ambaye ni safi (katika upendo wake) na akafa (katika hali hiyo) amekufa kama shahidi.

13

B.Russell: kitabu – Marriage and Morals, London, 1976, uk. 86.

45


Hata hivyo jambo hili lazima lisisahauliwe kwamba aina hii ya upendo, pamoja na manufaa yake yote yanayoweza kupatikana, chini ya hali maalum, sio ya kupendekezwa – ni bonde la hatari kuliingia. Ni kwa sababu hii kama vile mateso, ambayo, kama yanamsumbua mtu na anayapinga kwa nguvu zake zote za uvumilivu wake na hiari yake, anakuwa mkamilishaji na msafishaji wa moyo wake; unakipika kilicho ghafi na kuchuja kilicho na matope ndani yake. Lakini mtu hawezi kupendelea mateso. Hakuna anayeweza kujisababishia mateso mwenyewe ili afaidike na mambo haya ambayo yanaandaa na kufunza moyo; wala hawezi kumletea mateso mtu mwingine kwa kisingizio hiki. Hapa, pia, Russell ana kitu cha maana cha kusema: Mateso huwajaza watu nishati, kama uzito mwepesi usio na thamani. Mtu anayejidhania kuwa ameridhika kabisa hatajihangaisha zaidi kwa ajili ya furaha. Lakini sipendekezi kwamba hii ifanywe ni kisingizio cha kusababishia wengine maumivu ili waweze kutembea kwenye njia ya faida, kwa sababu mara nyingi hutoa matokeo ya kinyume na huharibu watu. Bali ni vyema katika suala hili kuziacha nafsi zetu zenyewe kujaribu matukio yanayotutokea.14 Kwa kadiri tujuavyo, athari na manufaa ya mateso na shida vimesisitizwa sana katika mafunzo ya Uislamu, na vinajulikana sana kama ishara za Mungu, lakini hili kwa hali yoyote halimruhusu mtu yoyote kujisababishia mateso au kwa wengine kwa kisingizio hiki. Aidha, kuna tofauti kati ya mapenzi na mateso; na kwamba hii ni kuwa mapenzi, zaidi ya jambo jingine lolote, yapo dhidi ya akili. Popote yanapoweka mguu, yanaitoa akili kutoka kwenye sehemu yake ya utawala. Hii ndio maana mapenzi na akili vinajulikana sana katika fasihi ya mafumbo kama maadui wawili. Chuki kati ya wanafalsafa na masufi inaanzia hapa, hawa wa kwanza wakitegemea, na kuamini katika 14

Ibid. iliyotafsiriwa kutoka kwenye Kiajemi, ile ya asili haipatikani.

46


nguvu ya akili, na hawa wengine, katika nguvu ya mapenzi. Katika fasihi ya Ki-Suffi, akili mara nyingi inashutumiwa na kushindwa katika uwanja huu wa mashindano. Sa’di anasema: Wanaonitakia kheri wananishauri: Ni upuuzi kutengeneza matofali baharini. Lakini nguvu ya tamaa imetawala juu ya uvumilivu: Madai ya akili juu ya mapenzi hayana maana. Mshairi mwingine amesema: Nilifanya ulinganisho wa ushauri wa akili katika njia ya mapenzi: Ni kama kunyesha kwa umande kujaribu kuweka mkondo juu ya bahari. Ni vipi nguvu yenye uwezo kama huu, inayonyakua udhibiti wa nia nje ya mikono yetu, na ambayo, kwa maneno ya Rumi “inampeperusha mtu hapa na pale kama kipande cha jani kwenye mikono ya upepo mkali”, na katika maneno ya Russell “ni kitu chenye tabia ya utawala huria”, iweze kupendekezwa. Kwa vyovyote vile, ni kitu kimoja kuweza kuwa na matokeo yenye manufaa, lakini ni kingine kuweza kushauriwa au kupendekezwa. Kutokana na hili itaonekana kwamba pingamizi na malalamiko ambayo baadhi ya wanasheria wa Kiislamu wameyatoa dhidi ya baadhi ya wanafalsafa wa Kiislamu15 ambao wameliweka wazi suala hili katika falsafa ya nadharia zao na wameelezea matokeo na manufaa yake, ni batili. Kwani kundi hili la kwanza lilidhania kwamba wazo la kundi la pili la wanafalsafa lilikuwa kwamba jambo hili linashaurika na kupendekezeka pia, ambapo walizingatia tu zile athari zenye manufaa za aina hii ya mapenzi inayotokea chini ya masharti ya uchamungu na 15

Ibn Sina katika kitabu chake Treatise on Love (Risal-‘ishq), na Sadru’d – Din ash Shirazi katika safari ya tatu ya Asfar al –arba yake.

47


utawa, bila kuipendekeza au kuishauri, kama vile tu ambavyo wangefanya kwa mateso na bahati mbaya. * * * UPENDO NA UTII KWA WALE WALIOKO KARIBU NA MWENYEZI MUNGU Tumesema kwamba upendo haukukomea tu kwenye aina ya upendo wa kinyama au wa kijinsia au wa kiuzazi. Bali kuna aina nyingine ya upendo na mvuto ambayo iliyopo kwenye hali finyu zaidi, na iko nje kabisa ya mipaka ya maada au kimaumbile. Inaanzia kwenye silka ya mbali zaidi kuliko ile ya uhifadhi wa vizazi na vizazi, na kwa kweli ni kitu kinachotenganisha ulimwengu wa mwanadamu na ule wa wanyama. Huu ni upendo wa kiroho au wa kiutu, kupenda kwa uzuri zaidi na wema, kuwa na mapenzi sana na uadilifu wa mtu na uzuri wa hali halisi. Yale mapenzi ambayao ni kwa ajili ya rangi Sio mapenzi: mwishowe yanakuwa fedheha; Kwa vile penzi la wafu halidumu, Kwa sababu aliyekufa kamwe harudi kwetu. (Lakini) penzi la aliye hai ni la wakati wowote Bichi kuliko chipukizi ndani ya nafsi na mandhari Chagua upendo wa Yule Aliyehai Ambaye ni wa milele, Anayekupa wewe kunywa katika mvinyo unaoongeza uhai. Chagua pendo la Yeye ambaye kutoka kwenye upendo Wake Mitume wote walipata mamlaka na utukufu. 16 Na ni mapenzi ambayo yametajwa katika aya nyingi za Qur’ani, hususan kwa neno “mahabbah”. Aya hizi zinaweza kuwekwa katika makundi mbalimbali:

16

Imetolewa kutoka kwenye tafsiri ya Nicholson ya Rumi, Mathnavi, kitabu cha 1.

48


1. Aya zinazo waelezea waumini, na zinazozungumzia utii mkubwa na mapenzi waliyonayo kwa Mwenyezi Mungu au kwa waumini wengine.         Lakini wale walioamini wamezidisha kumpenda Mwenyezi Mungu. (Al Baqarah, 2:165)                           Na (pia wapewe) walio na makazi (yao Madina) na kushika kabla ya hao, wanawapenda waliohamia kwao, wala hawapati dhiki mioyoni mwao kwa hayo waliyopewa, na wanawapendelea kuliko nafsi zao ingawa wenyewe wana hali ndogo. ( Al-Hashir, 59:9 ) 2 Aya zinazozungumzia mapenzi ya Mwenyezi Mungu kwa waumini:         Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanaotubia na wanaojitakasa. (Al-Baqarah, 2:222)

49


     Na Mwenyezi Mungu anawapenda wanaotenda mema. (Al-‘Imran, 3:148 na Al-Maida 5:13)

      Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wanaomuogopa. (At-Tawbah, 9: 4 na 7)     Na Mwenyezi Mungu anawapenda wanaojitakasa. (At-Tawbah, 9:108)      Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wanaohukumu kwa haki. (Al-Hujurat, 49:9 na al-Mumtahimah, 60:8) 3. Aya zinazokusanya njia-mbili pendo na kupendana: mapenzi ya Mwenyezi Mungu kwa waumini, mapenzi ya waumini kwa Mwenyezi Mungu; na mapenzi ya waumini wao kwa wao:

50


                Sema (ewe Mtume wetu Muhammad),kama ninyi mnampenda Mwenyezi Mungu, basi nifuateni mimi atakupendeni Mwenyezi Mungu, na atawasamehe madhambi yenu, na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa msamaha. (Al-Imran, 3:31)       Basi hivi karibuni Mwenyezi Mungu atawaleta watu (ambao) anawapenda nao wanampenda. (Al-Ma’idah, 5:54 )           

Hakika wale walioamini na kufanya matendo mema, Rahamani atawafanyia mapenzi. (Maryam, 19:96)      Naye amejaalia baina yenu mapenzi na huruma. ِ(Ar-Rum, 30:21 )

51


Na ni mapenzi ambayo Ibrahim aliyataka kwa ajili ya kizazi chake, 17 na ambayo Mtume wa mwisho pia aliyaomba kwa amri ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kizazi chake.18 Kutokana na yale tuliyoambiwa kutoka kwenye hadithi, moyo na uhai wa dini si chochote bali ni mapenzi. Burayd al-Ijli amesema: “Nilikuwa katika hadhara ya Imam al-Baqir (a.s), na alikuwepo msafiri kutoka Khurasan ambaye amevuka mwendo huo mrefu kwa miguu. Alipata heshima ya kukutana na Imam. Miguu yake, ambayo ilkuwa inaonekana ndani ya viatu vyake, ilikuwa imepasuka, na alikuwa amevua viatu vyake. Akasema: “Kwa jina la Allah swt, kitu pekee kilichonileta kutoka huko nitokako ni mapenzi juu yenu, Watu wa Nyumba (ya Mtume).” Imam akasema: “Kwa jina la Allah swt, kama jiwe lingetupenda sisi, Mwenyezi Mungu angelikutanisha nasi, na kuliunganisha nasi. Hivi dini ni kitu mbali na mapenzi?” 19 Mtu mmoja alimwambia Imam as-Sadiq (a.s): “Tumewaita watoto wetu kwa majina, lako na ya baba zako; je, kitendo hiki kitakuwa ni chenye manufaa kwetu?” Imam akasema: Ndio, kwa jina la Allah swt; kwani dini ni kitu kingine kuliko mapenzi?” Kisha akasoma aya hii - Kama mnampenda Allah, nifuateni, na Allah atawapendeni- kama ushahidi.20 Kimsingi, ni mapenzi yanayoleta utii: yule mwenye kupenda anakuwa hana uwezo wa kukataa matakwa ya yule anayempenda. Tumeliona hili kwa macho yetu wakati kijana aliyekuwa kwenye mapenzi anapoacha kila kitu anapokabilwa na yule anayempenda, mpenzi wake, na akakitoa muhanga kila kitu kwa ajili yake (msichana). Utii na ibada kwa Mwenyezi Mungu viko katika uwiano na mapenzi ambayo mwanadamu anayo kwa ajili ya Mola, kama Imam as-Sadiq 17

Surat Ibrahim, 14:37 ash-Shura, 42:23 19 Safinatu’l-bihar, juz. 1, uk. 102 (chini ya Hubb) 20 Ibid uk. 662 (chini ya Sama) 18

52


(a.s) alivyosema: “Muasi Mwenyezi Mungu na uonyeshe kwamba unampenda Yeye; kwa maisha yangu, hicho ni kitu cha kushangaza. Kama mapenzi yako yangekuwa ya kweli, ungemtii Yeye, kwani mwenye kupenda huwa mnyenyekevu mbele ya yule anayempenda” *

*

*

NGUVU YA UPENDO KATIKA JAMII. Nguvu ya upendo ni kani kubwa na yenye kufaa katika uhusiano na jamii; jamii bora ni zile zinazoongozwa na nguvu ya upendo: mapenzi yote, yale ya kiongozi na mtawala kwa watu, na upendo na utii wa watu kwa kiongozi na mtawala. Hisia na upendo wa mtawala ni jambo muhimu kwa uimara na maisha marefu ya serikali, na mpaka jambo hilo liwepo, mtawala hawezi, au inamuwia vigumu kuiongoza jamii, kuwafundisha watu kuwa wenye kufuata sheria, na hata kudumisha haki na usawa katika jamii hiyo. Lakini pindi atakapofanya hivyo, watu watakuwa wenye kuchunga sheria kiasi kwamba watauona upendo wa mtawala wao na ni upendo huu utakaowavuta kwenye utii na kujituma. Qur’an inaongea na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na inamwambia kwamba anao uwezo mkubwa mikononi mwake wa kushawishi watu na kuiongoza jamii:                          Basi kwa sababu ya rehema ya Mwenyezu Mungu umekuwa mpole kwao; na kama ungekuwa mkali na shupavu wa moyo, wangekukimbia. Basi wasameha na uwaombee msamaha na ushauriane nao katika mambo (Al-Imran, 3:159)

53


Hapa imewekwa wazi kwamba kinachosababisha watu kuja kwa Mtume (s.a.w.w.) ni uungwana na upendo aliouweka juu yao. Kisha inamuamuru kuwasamehe na kuwaombea msamaha na kushauriana nao. Haya yote ni miongoni mwa athari za upendo na urafiki, kama ambavyo uvumilivu, subira na ustahimilivu ni miongoni pia mwa viwango vya upendo na upole Kwa upanga wake wa huruma yeye (Ali) alikomboa shingo nyingi Za kundi kubwa kama hilo kutoka kwenye upanga. Upanga wa huruma ni mkali kuliko upanga wa chuma; Hapana, ni wenye kuleta ushindi zaidi kuliko majeshi mia moja21 Qur’an Tukufu pia inasema:                       Mambo mema na mabaya hayawi sawa. Zuia (ubaya) kwa yaliyo mema zaidi, na mara yule ambaye baina yako na yeye kuna uadui, atakuwa kama rafiki mkubwa. (Fusslat, 41:34 ) Samehe, ewe mwanangu, mtu yule anaweza kutega Kwa utii na kufanya vitendo vya kinyama na pingu, Funga mnyororo shingo ya adui kwa huruma, Kwa kitanzi ambacho hakuna bapa kali linaloweza kukata.

21

Rumi, kitabu cha 1

54


Katika amri yake kwa Malik al-Ashtar, alipomteua kama gavana wa Misri, Amir al-Muminin pia alimwelezea jinsi tabia yake kwa watu itakavyokuwa: ، ْ‫ف بِهِم‬ َ ْ‫ َو ا للُط‬، ْ‫ َو اٌلْمَحَ َبةَ لَهُم‬، ِ‫ك الرَحْمَةَ لِلرَعِيَة‬ َ َ‫َو أَشْعِ ْر قَلْب‬ ْ‫ب َو تَ ْرضَى أَن‬ ُ ِ‫ل الَذْى تُح‬ َ ْ‫ك مِث‬ َ ِ‫ فَأعْطِهِمْ مِنْ عَفْوِكَ وَصَفْح‬.... ِ‫حه‬ ِ ْ‫ك اٌلّلَهُ مِنْ عَفْوِ ِه َو صَف‬ َ َ‫يُعْطِي‬ Amsha moyoni mwako huruma kwa watu wako na mapenzi juu yao, na upole juu yao………. Hivyo wape msamaha wako na huruma zako, kama vile ambavyo ungependa Allah swt akupe msamaha na huruma zake.22 Moyo wa mtawala lazima uwe ndio kiini cha mapenzi na upendo kwa ummah; madaraka na nguvu havitoshi. Watu wanaweza kuswagwa kama kondoo kwa madaraka na nguvu, lakini nguvu zao za ndani haziwezi kuamshwa na kutumika. Sio tu kwamba madaraka na nguvu havitoshi; hata haki, kama inatekelezwa kinyonge, haitoshi. Bali mtawala lazima awapende watu kutoka moyoni mwake kama baba mpendwa, aonyeshe utu wake kwao na pia awe na tabia inayovutia yenye kuendeleza utii, ili aweze kutumia matakwa yao, tamaa za (malengo) yao na nguvu zao kuu za kibinaadamu katika kuendeleza lengo lake binafsi vizuri zaidi. *

*

*

NJIA BORA ZA KUITAKASIA NAFSI Mjadala uliopita juu ya suala la upendo na mapenzi ulikuwa utangulizi, na sasa tunataka kwa taratibu kufikia hitimisho. Sehemu muhimu sana ya mjadala wetu – ndio hasa msingi wa mjadala wetu – ni kama upendo na mapenzi kwa wale walio karibu na Mungu, na utii kwa watu wabora lenyewe ni lengo, au kama ni njia ya kutakasia nafsi, kurekebisha tabia za mtu, na kupata wema wa kibinadamu na ubora. 22

Nahju’l-balaghah, barua na: 53.

55


Katika mapenzi ya kinyama, shauku zote na jitihada za mwenye kupenda ni kuhusu umbo la ampendaye na muoano wa viungo vyake na rangi na uzuri wa ngozi yake, na hizi ni silka zinazomvutia na kumpendeza mtu. Hata hivyo, baada ya kuridhika kwa silka, mioto hii inakuwa haina mng’aro, inafifia, na hatimae huzimishwa. Lakini mapenzi ya kiutu, kama tulivyosema, ni maisha na uzima; yanasababisha utii na uaminifu. Haya ndio mapenzi yanayomfanya yule mwenye kupenda afanane na anayempenda, humfanya ajaribu kuwa udhihirisho wa anayempenda na kielelezo cha tabia ya yule ampendaye, kama vile asemavyo Khawajah Nasiru’d-Din at-Tusi katika sherehe yake ya Kitabu’l-isharat wa’t-Tanbihat (kitabu cha maagizo na maelezo) cha Ibn Sina: (Mapenzi ya) nafsi ni yale ambayo chanzo chake ni msingi wa kufanana kwa nafsi ya mwenye kupenda na moyo wa ampendaye. Kupendezwa kukubwa zaidi kwa mwenye kupenda kupo kwenye tabia za yule ampendaye zinazotokea moyoni mwa yule anayependwa…….. Huifanya nafsi kuwa laini, yenye kutamani na yenye furaha na huipa uangalifu wa hisia zinazoutenga na mihangaiko ya dunia.23 Mapenzi husukuma kuelekea kwenye kufanana na kushabihiana, na nguvu yake humfanya mwenye kupenda achukue umbo la mwenye kupendwa. Mapenzi ni kama waya wa umeme unaounganisha utu wa mwenye kupenda na wa yule anayempenda na kuhamishia tabia za ampendaye kwake; na ni hapa ambapo chaguo la mwenye kupendwa ni la umuhimu wa msingi. Hivyo Uislamu umetoa umuhimu mkubwa katika suala la kutafuta rafiki na kuchagua sahiba. Kuna aya nyingi (za Qur’an) na hadithi za Mtume na Maimam katika uwanja huu, kwa sababu urafiki unasababisha mfanano, hujenga uzuri na huleta mambo

23

Sharh Kitab al-isharat wa ’t-Tanbihat, Tehran, 1379 A.H., Juz.3, uk.383.

56


ya kijinga. Pale unapomulika mwanga wake unaziona dosari kama sanaa, na mwiba kama waridi na jasmini.24 24

Na kwa upendo, kuna dosari pia. Miongoni mwa hizi ni ule ukweli kwamba mwenye kupenda, kama matokeo ya mshughuliko wa wema na mpenzi wake, anakuwa hajali mapungufu yake. ُ‫حُبُ اٌ لشَىءِ يُعْمِى وَيُصِم‬ Mapenzi ya kitu chochote huleta upofu na ukiziwi. ُ‫وَمَنْ عَشَ قَ شَئًا أَعْشَى بَصَرَهُ وَاَمْرَضَ قَلْبَه‬ Yeyote anayependa kitu, kuona kwake kunakuwa na kasoro na moyo wake unakuwa na maradhi. ( Nahju’l-balaghah) Sa’di ameandika katika kitabu chake ‘Rose Garden’ {Gulistan} (Bustani ya Waridi): Kwa kila mtu ni vilevile, akili ya mtu inaelekea kuwa kamili na mwanae mtu huwa mzuri. Athari hii mbaya haikinzani na tulichokisema mapema, yaani, kwamba athari ya mapenzi ni uhisishaji wa akili na utambuzi; uhisishaji wa akili una maana kwamba unamtoa mtuubozi (uzito wa akili), na kukamilisha nguvu ya uwezo wake. Hatahivyo, ile athari mbaya ya mapenzi sio kwamba inadumaza akili ya mtu bali ni kwamba inamfanya mtu asijali, mzembe, na suala la akili ni tofauti na lile la uzembe. Mara nyingi, kama matokeo ya uhifadhi wa uwiano katika wepesi wa kuhisi, watu wenye akili finyu wanaelekea kabisa kwenye uzembe. Mapenzi hufanya uelewa kuwa makini zaidi, lakini mazingatio huwa ya upande mmoja na ya njia moja. Hivyo tulisema kabla kwamba milki ya mapenzi ilikuwa ya uchaguzi, na ni kama matokeo ya uchaguzi huu na ulengaji kwamba kasoro zinajitokeza, na mazingatio kwa vitu vingine yanatoweka. Zaidi ya hayo, sio kwamba mapenzi yanasababisha kasoro tu, bali yanazionyesha hizo kasoro kama ni kitu kizuri; kwa moja ya athari za mapenzi ni kwamba popote yanapomulika mwanga wake, unapafanya mahali hapo kuonekana pazuri, yanageuza alama moja ya wema kuwa jua. Yanafanya vilevile weusi kuonekana kama weupe na giza kuwa mwanga. Kama Vahshi alivyosema: Kama ungekaa kwenye mboni ya jicho langu, Chochote usingeona bali wema wa Layla.

57


Katika baadhi ya aya za Qur’an Tukufu na hadithi za Mtume (s.a.w.w.) na Maimamu (a.s) linatolewa onyo kuhusu kuwaendea mara kwa mara na kufanya urafiki na watu wabaya na waovu, na kwa baadhi yao unafanywa mwito wa urafiki wa moyo safi. Ibn ‘Abbas alisema: “Tulikuwa kwenye hadhara ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ilipoulizwa: ‘Ni nani sahaba bora?’ Mtume akajibu: ‘Ni yule mtu ambaye mnapomuona, mnakumbushwa juu ya Mwenyezi Mungu; na anapoongea, elimu yenu inaongezeka; na anapotenda, mnaanza kufikiri juu ya akhera na siku ya Qiyammah.’”25 Mwanadamu yuko kwenye haja kubwa sana ya kioevu cha mapenzi kwa ajili ya watu wema na wachamungu, ili upendo uweze kupaliliwa, na ili mapenzi kwa ajili ya watu hao yaweze kuleta kufanana na kushabihiana na wao katika ubinadamu. Njia mbalimbali zimependekezwa kwa ajili ya urekebishaji wa tabia ya mtu na kutakasa nafsi, na mbinu mbalimbali zimekuja kuwepo, mojawapo ikiwa ni ile mbinu ya Socrate. Kulingana na mbinu hii, mtu lazima ajirekebishe mwenyewe kwa njia ya akili yake na upangaji wake mwenyewe. Mtu kwanza kabisa hana budi apate imani kamili katika manufaa ya utakasaji, na madhara ya kuchanganyikiwa katika maadili, na kisha, moja baada ya nyingine, agundue sifa zinazostahili kulaumiwa kwa chombo cha akili yake – kama mtu anayetaka kutoa nywele kutoka Na pengine ni kwa sababu hii kwamba mapenzi sio sawa na elimu, ambayo ni adhimisho la kinachojulikana. Mwelekeo wa mapenzi wa ndani na kiakili ni mkubwa kuliko mwelekeo wake wa nje na wa kweli, hii ni kusema, utulivu wa mapenzi sio dhihirisho la vipimo vya uwezekano na kiini cha mwenye kupenda. Kwa kweli mwenye kupenda ana kiini, kitu, moto uliojificha u naotafuta kisingizio, lengo. Kila unapotokea kukabiliana na lengo na kukuta upatanivu – siri ya upatanivu huu bado haijulikani, na ndio maana inasemekana kwamba mapenzi ni muhali - uwezekano huu wa ndani unajidhihirisha wenyewe na kusababisha wema kuling ana na uwezo wake wenyewe, sio kulingana na kilichopo kwa mwenye kupendwa. Hiki ndicho kile ule mstari wa hapo juu unachorejelea unaposema mapenzi huona dosari za mwenye kupendwa kama sanaa na mwiba kama waridi na jasmini. 25

Biharu’l-anwar, juz. 15, kitabu cha 10, uk. 51 (nakala ya zamani)

58


ndani ya pua yake, moja baada ya nyingine, au kama mkulima ambaye, kwa mkono wake mwenyewe, anang’oa magugu kutoka kwenye mitaro ya ardhi yake, au mtu anayetaka kusafisha ngano yake kutokana na vijiwe vidogo na udongo kwa mkono wake – na kisha asafishe hizi sifa mbaya kutoka kwenye mavuno ya utu wake. Kulingana na mbinu hii, mtu lazima aondoe taratibu upotovu wa tabia kwa subira, kwa kujilinda, kufikiri kwa uangalifu na mawazo mahsusi, na kutakasa dhahabu ya mtu mwenyewe kutokana na sarafu bandia. Pengine ingesemwa kwamba haiwezekani kwa akili kujiondoa kwenye jukumu hili. Wanafalsafa wanataka kurekebisha tabia kwa mawazo na kufikiri. Kwa mfano, wanasema kwamba usafi na kujizuia na tamaa ndio chanzo cha heshima na tabia ya mtu machoni mwa watu, na choyo na ulafi ni matokeo ya ugumu na udhalili; au tuseme kwamba elimu ni matokeo ya nguvu na uwezo, elimu ni kama hivi na kama vile, elimu ndio “mhuri wa ufalme wa Sulayman”, elimu ni mwanga kwenye njia ya mtu unaoangazia hatari zisizoonekana katika njia yake; au wanasema kwamba wivu na husda ni maradhi ya kiroho, ambayo kwayo matokeo maovu yatatokea kiasi jamii inavyohusika; na kadhalika. Hakuna shaka kwamba njia hii ndio njia sahihi, na njia hii ni njia nzuri; lakini tunazungumzia juu ya uwiano wa sifa ya njia hii kulinganisha na njia nyingine yoyote. Kama vile gari ilivyo, kwa mfano, njia nzuri, lakini inapolinganishwa na ndege ni lazima tuangalie vizuri ukubwa wa sifa yake. Awali ya yote, hatuna hoja juu ya sifa ya njia ya akili kuhusu mwongozo, hii ni kusema kwa mtazamo wa kiasi gani ilivyo hii inayoitwa hoja ya kiakili inavyoonyesha ukweli katika suala la maadili, ina ukweli kiasi gani, na wenye kukubaliana na ukweli, na sio wenye kasoro au makosa. Tutasema kiasi hiki tu, kwamba kuna shule za kifalsafa zisizo na idadi za maadili na elimu, na tatizo hili bado halijavuka mipaka ya mijadala na mahojiano kwa kiasi utoaji hoja unavyohusika. Aidha tunajua kwamba masuffi wote wanakubaliana wanaposema:

59


Mguu wa mti ni dhaifu sana.26 Mguu wa watoa hoja ni wa mti; Kwa wakati huu, mjadala wetu hauhusu kipengele hiki, badala yake unahusu ni, umbali gani njia hii inaweza kufika. Masufi na watu wa safari ya kiroho wamependekeza njia ya upendo na urafiki mahala pa njia ya akili na hoja. Wanasema kwamba mtu sharti apate kiumbe kikamilifu na aning’inie kwenye kamba ya upendo na urafiki pamoja naye uuzunguuke moyo wa mtu, kwa vile hii yote haina hatari zaidi kuliko njia ya akili na hoja, na pia ni (njia ya) haraka. Kwa ulinganisho, njia hizi mbili ni kama ile njia ya mtindo wa kizamani wa kufanya kitu kwa mkono na njia ya kukifanya kwa mashine. Athari ya nguvu ya upendo na urafiki katika kuondokana maadili maovu kutoka moyoni inafanana na athari ya kemikali kwenye vyuma; kwa mfano, mchoraji juu ya madini kwa tindikali huondoa kisichotakikana kwenye kipande chake cha chuma kwa kutumia tindikali yenye nguvu, sio kwa kutumia msumari, au ncha ya kisu, au chochote kama hicho. Hata hivyo, athari ya akili katika kurekebisha tabia mbaya ni kama kazi ya mtu anayetaka kutenganganisha taka za chuma kutoka kwenye vumbi kwa mkono; ni ugumu ulioje wa kuifanya kazi hii! Kama angekuwa na sumaku yenye nguvu sana ya kushika, pengine angeweza kuvitenganisha kwa mkupuo mmoja. Nguvu ya upendo na urafiki inakusanya zile tabia mbovu kama sumaku na kuzitupilia mbali. Masufi wanaamini kwamba mapenzi na urafiki na watu waliotakaswa na kukamilishwa ni kama mashine yenye kujiendesha yenyewe ambayo hukusanya maovu pamoja yenyewe na kuyatupa. Kama hali ya kuvutika inapata kitu sahihi, ni moja ya hali bora, na hii ndio inayochuja na kuweka katika tabia bora zaidi. Kwa hakika wale ambao wamechukua njia hii wanataka kurekebisha tabia zao kwa nguvu ya upendo, na wametegemea juu ya uwezo wa mapenzi na urafiki. Uzoefu umewaonyesha kwamba usahiba na watu safi na urafiki na mapenzi juu yao vimeathiri nafsi zao kwa kiasi 26

Rumi, Mathnavi, kitabu cha 1

60


ambacho kusoma mamia ya majuzuu juu ya maadili hakukuweza (kuleta athari yoyote). Rumi amesimulia ujumbe wa upendo kwa manung’uniko ya tete; anasema: Ni nani yule ambaye aliyeiona sumu na kiuasumu kama tete? Nani yule ambaye amemuona mwenye kuliwaza na mpenzi mwenye Shauku kama tete? Yeyote ambaye nguo yake imechanwa na mapenzi Ameondoshewa kabisa tamaa au dosari. Njoo, ewe upendo, unayetuletea mema tena – Oh, daktari wa maradhi yetu yote.27 Wakati mwingine tunamuona mtu mkubwa ambaye wafuasi wake wanamuigiza yeye hata katika namna ya kutembea, kuvaa, kukutana na watu na namna ya kutoa ishara. Uigizaji huu sio wa hiari, hujitokeza wenyewe tu na kwa nguvu ya asili. Ni nguvu ya upendo na urafiki iliyovuta dalili zote za kuwepo kwa mpenzi na zimemfanya afanane na yule anayempenda katika kila moja ya hali zake. Hii ndio sababu kila mwanadamu lazima atafute mtu wa hali halisi na ukweli kwa ajili ya kujirekebisha kwake mwenyewe, na kujitiisha mwenyewe kwake ili kwamba aweze kujirekebisha mwenyewe kiuhakika. Kama kuna tamaa ya muungano kwenye kichwa chako, Ewe Hafiz, Lazima uwe kama udongo wa ufinyanzi katika mikono ya fundistadi. Wakati mtu ambaye, hata kwa kiasi gani mwanzoni ameamua kuwa mchamungu na kufanya matendo mema, halafu anaangukia kuwa mawindo ya udhaifu katika misingi ya kutamani kwake (wema huo), akigundua upendo na urafiki, udhaifu huo na uzito hatimae vitaondoka, na azimio lake litakuwa imara na lengo lake litakuwa na nguvu. 27

Ibid

61


Mapenzi ya watu wema kifedhuli yameutupa moyo na dini; Ile ngome katika sataranji haiwezi kuchukua kiasi kikubwa Kama uso mzuri unavyoweza kuvutia. Unadhani Majnuni aligeuka wazimu kwa kupenda kwake? Ilikuwa ni kule kuangaliwa na Layla kulikomsafirisha miongoni mwa nyota. Sikuipata njia yangu peke yangu ya kwenye chanzo cha jua. Nilikuwa chembe ya vumbi, na mapenzi juu yako yamenichimbua. Ulikuwa ni ule mchirizo wa nyusi zako, ulikuwa ni mkono wako wa mbinguni, Ambao umeizingira shangwe hii na kuufanya moyo wangu kuwa wenye wazimu.28 Historia inaelezea juu ya watu wakubwa ambao katika nafsi na mioyo yao, mapinduzi yalijengeka kwa upendo na urafiki na mtu mkamilifu – angalau kwa maoni ya wafuasi wao. Mawlana Rumi ni mmoja wa watu kama hao.Hakuwa tangu mwanzo amemezwa (na mapenzi) na mwenye kujawa na ghasia. Alikuwa mwanazuoni, na alikuwa kwa utulivu na ukimya akijishughulisha na kufundisha katika pembe ya mji wake. Lakini kutoka siku alipokutana na Shams-e Tabrizi na tamaa ya urafiki naye ulipokamata moyo na nafsi yake, tabia yake ilibadilika moja kwa moja na moto ukawaka ndani ya mwili wake. Ilikuwa kama fyuzi iliyoanguka kwenye ghala ya baruti na kulipuka moto. Alikuwa, inavyoonekana, mfuasi wa Ash’ariyyah, lakini kitabu chake cha Mathnawi hakuna shaka ni kimoja kati ya vitabu vikubwa duniani. Ushairi wote wa bwana huyu unabingirika, katika mwendo. Alitunga Diwan of Shams (kiti kisicho na egemeo cha Shams) kwa kumbukumbu ya hamu yake, mpendwa wake; na katika Mathnawi pia, anamtaja sana sana. Tunamuona Mawlana Rumi katika Mathnawi akitafuta kitu, lakini mara

28

Allamah Taba’taba’i.

62


tu anapomkumbuka Shams dhoruba kali inajikusanya kwenye nafsi yake, na mawimbi yanayonguruma yanatoka kwa nguvu ndani yake; anasema: Katika wakati huu nafsi yangu imeng’oa kirinda changu; Amekamata manukato ya fulana ya Joseph. (Akasema:) “Kwa ajili ya miaka yetu ya usahiba, Simulia moja ya ule upeo wa furaha tamu, Ili ardhi na mbingu ziweze kucheka, Kwamba akili na nafsi moyo na jicho viweze kuongeza Kwa mara mia Nikasema: “Yule ambaye yuko mbali na mpendwa wake Yu kama mgonjwa aliyeko mbali na daktari. Ni vipi nitaelezea (hakuna wangu mshipa ulio na hisia) Yule rafiki asiye na mwenzi. Maelezo ya kujitenga huku na hii damu ya moyo Je kwa sasa hivi unaondoka mpaka wakati mwingine. Usitafute matatizo na ghasia na umwagaji damu: Usiseme zaidi kuhusu Shams-e Tabrizi.29 Na hii ndio maana inayokubaliana na alichokisema Hafiz: Chiriku alijifunza wimbo wake kwa upendeleo wa waridi, vinginevyo pasingeweza kuwa na Chochote cha wimbo huu na muziki uliotengenezwa kutoka mdomoni mwake. Kutokana na hili tunaweza kuhitimisha kwamba jitihada na kuvutwa, au kitendo na mvuto lazima viende pamoja. Hakuna kinachoweza kukamilika kutokana na juhudi bila mvuto, kama vile kuvutwa pale ambapo hapana juhudi hakutafikia lengo lake.

29

Imechukuliwa kutoka kwenye tafsiri ya Nicholson ya Rumi, Mathnawi kitabu cha 1

63


* * * MIFANO KUTOKA KWENYE HISTORIA YA UISLAMU Katika historia ya Uislamu tunaona mifano yenye kubainisha na ya kigezo ya mapenzi makubwa na utii wa Waislamu kwa utu wa Mtume. Kwa kweli, tofauti moja kati ya ‘shule’ ya Mitume na ‘shule’ ya wanafalsafa ni hii tu, kwamba wanafunzi wa wanafalsafa ni wanafunzi tu, na wanafalsafa hawana mvuto mwingine zaidi ya ule wa mwalimu; lakini mvuto wa mitume ni kama athari ya mtu, mpendwa, aliyeingia kwenye vina vya nafsi ya mwenye kupenda, akamkamata katika mikono yake, na akawa na nguvu katika kila kipengele chake cha maisha yake. *

*

*

Mmoja wa wale ambao walimpenda sana Mtukufu Mtume alikuwa Abu Dharr al- Ghifari. Mtume alikuwa ametoa amri ya kwenda Tabuk (farsakh mia moja – kama maili mia nne – kaskazini ya Madina, karibu na mpaka na Syria). Baadhi yao walitoa visingizio, wanafiki wakajaribu kuvuruga mambo, lakini hatimae likatoka jeshi lenye nguvu. Hawakuwa na vifaa vya kijeshi, na walikuwa na matatizo na mahitaji kuhusu chakula pia, kiasi kwamba wakati mwingine baadhi yao waliridhika na tende moja; hata hivyo wote walikuwa na nguvu na furaha. Upendo ulisababisha nguvu zao na nguvu ya mvuto ya Mtume iliwapa uwezo. Abu Dharr pia alikuwa akitembea kuelekea Tabuk na jeshi hili. Humo njiani watu watatu, mmoja baada ya mwingine, walirudi nyuma, na Mtume alijulishwa kuhusu kila mmoja wao pale alipojiondoa. Kila wakati alisema: ‘Kama kuna wema wowote alionao, Allah swt. atamfanya arudi; na kama hana wema wowote, ni bora aende.’

64


Ngamia mwembamba na dhaifu wa Abu Dharr alirudi nyuma, na kisha Abu Dharr pia alionekena kuwa nyuma. “Ewe Mtume wa Allah! Abu Dharr amerudi nyuma pia!” Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akarudia maneno yale yale: ‘Kama kuna wema wowote alionao, Allah atamfanya arudi; na kama hana wema wowote, ni bora aende.’ Jeshi hilo kisha likaendelea na safari yake na Abu Dharr akabakia nyuma; lakini hakukuwa na lolote la kufanya – mnyama wake alibakia katika hali hiyohiyo. Hata angefanya nini, hakuweza kusogea, na sasa alikuwa amebakia maili kadhaa nyuma. Alimwacha huru ngamia huyo na akauchukua mzigo kwenye mabega yake mwenyewe, na katika hali ile ya joto alianza kwenda juu ya mchanga unaochoma. Alikuwa na kiu na ilikuwa inamuua. Alipita kwenye mawe fulani katika kivuli cha kilima na miongoni mwao yamejikusanya maji ya mvua, lakini alijiambia mwenyewe kwamba hangeweza kunywa mpaka rafiki yake, Mtume wa Allah swt awe amekunywa. Aliijaza kiriba chake cha maji, akakining’iniza nacho pia mgongoni kwake, na akaharakishia walikoelekea Waislamu. Kwa mbali waliona mtu: “Ewe Mtume wa Allah! Tumeona mtu kwa mbali akija kuelekea huku tuliko!” Akasema kwamba atakuwa ni Abu Dharr. Alifika karibu zaidi – ndio, alikuwa ni Abu Dharr, lakini uchovu na kiu vilimzoa miguu chini yake. Alihofia angeanguka. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema apewe maji haraka, lakini alisema kwa sauti dhaifu kwamba alikuwa anayo maji. Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Unayo maji, lakini unakaribia kufa kwa kiu!”

65


“Ndio, Ewe Mtume wa Allah! Nilipoyajaribu haya maji nilijizuia kunywa kiasi chochote kabla ya rafiki yangu, Mtume wa Allah swt.”30 Kwa ukweli wote, ni katika dini ipi ya dunia hii tunamoweza kupata hali ya mvuto kama hii, kukosa starehe na kutokuwa na choyo kama huku? * * ** Mwingine kati ya watu wanaopendeza na wasio na ubinafsi alikuwa ni Bilal al-Habashi. Maquraishi walikuwa wakimfanyia maudhi yasiyovumilika huko Makkah, na walikuwa wakimtesa chini ya jua kali kwa kumlaza kwenye mawe yanayochoma kwa joto. Walimtaka ayataje majina ya masanamu na atamke imani yake juu yao, na kwamba amkane, na aseme kwamba hatajihusisha nae Muhammad kwa lolote. Katika sehemu ya sita ya Mathnawi, Rumi amesimulia hadithi ya kusikitisha ya Bilal, na ameifanyia kazi nzuri sana kwa haki. Anasema: Abu Bakr alimshauri afiche imani yake, lakini hakuwa na ushupavu wa kugeuza kwani “upendo daima ulikuwa una vurugu na hatari” Bilal alikuwa anatiisha mwili wake kwenye miba: Bwana wake alikuwa anamtandika kwa kumsahihisha, (Akisema:) “Kwa nini unamtukuza Ahmad? Mtumwa muovu, wewe huamini katika dini yangu!” Alikuwa akimpiga katika jua kwa miba (Ambapo) alipiga kelele kwa kujigamba “Mmoja!” Mpaka Siddiq (Abu Bakr) alipokuwa anapita jirani yake, Zile kelele za “Mmoja” zilifikia masikio yake. Baadae alimuona kwa siri na kumuonya: “Ficha imani yako kwa Mayahudi. Yeye (Allah) anajua siri (zote): ifiche tamaa yako.” Yeye (Bilal) akasema: “Natubia mbele yako, ewe bwana.” Kulikuwa na kutubia kwingi kwa namna hii, 30

Biharu’l-anwar, juz.21, uk.215-216 ( chapa mpya)

66


(Mpaka) mwishowe aliacha kutubia, Na akatangaza na kuuachia mwili wake kwenye matata, Akilia: “Ewe Muhammad! Ewe adui wa viapo na toba! Oh ewe ambaye mwili wangu na mishipa yangu imejazwa nawe! Itawezekanaje kuwapo nafasi ndani yake ya toba? Kuanzia sasa nitaondoa toba kutoka kwenye moyo huu. Nitawezaje kutubia kwa maisha ya milele?” Upendo ndio Mshindi wa Yote, nami nimedhibitiwa na upendo: Kwa upofu wa mapenzi nimefanywa mwangavu kama jua. Ewe upepo mkali, mbele Yako mimi ni jani kavu: Ni vipi nitajua ni wapi nitaangukia? Kama mimi ni Bilal au ule mwezi mpya, Ninaendelea kukimbia nakufuata mwelekeo wa jua Lako. Mwezi unahusiana nini na unene au wembamba? Unakimbia (mwezi) kwenye visigino vya jua, kama kivuli. Wenye upendo wameangukia kwenye mbubujiko mkali: Wameiweka mioyo yao kwenye amri ya Upendo (Wako) kama jiwe la kusagia linalozunguka na kuzunguka Mchana na usiku na kulalamika mfululizo.31 * * * Wana-historia wa Kiislamu wametoa majina ya Uvamizi wa ar-Raji na Siku ya ar-Raji kwa mpangilio, kwa tukio maarufu la kihistoria, na, siku ambayo lilitukia, na kuna hadithi ya kupendeza na kuvutia iliyoambatana nayo. Kikundi kutoka makabila ya ‘Adal na al-Qarah ambao inavyoonekana wametokana na kundi la nasaba moja kama Maquraishi na waliokuwa wakikaa jirani na Makkah walikuja kwa Mtume wa Allah swt katika mwaka wa tatu wa Hijrah na wakasema: - “Baadhi ya watu kutoka 31

Imechukuliwa toka kwenye tafsiri ya Nicholson ya Rumi, Mathnavi, kitabu cha 1.

67


kwenye kabila letu wamechagua Uislamu, hivyo tutumie kikundi cha Waislamu huku kwetu ili waweze kutuelekeza katika maana ya dini hii, watufundishe Qur’ani na watujulishe kanuni na sheria za Kiislamu.” Mtume wa Allah swt akawatuma masahaba wake sita pamoja nao kwa ajili ya jambo hili, na aliweka uongozi wa kikundi hiki kwa mtu anayeitwa Marthadha ibn Abi Murtadha al-Ghanawi, au vinginevyo kwa mtu anayeitwa ‘Asim ibn Thabit ibn Abi’l-Aqlah. Wajumbe wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) waliondoka pamoja na ujumbe huu uliokuwa umekuja Madina, hadi walipofika mahali ambapo walipokuwa wanaishi kabila la Hadhil, na hapo walisimama.32 Wale marafiki wa Mtume (s.a.w.w.) walikuwa wamekwishajiandaa kwa kulala bila ya kuacha chochote kutoka popote, wakati mara kundi la kutoka kabila la Hadhil liliwavamia kama radi na panga zao zikiwa zimechomolewa. Ilijitokeza wazi kwamba ule ujumbe uliokuja toka Madina ama ulikuwa na nia ya kufanya hila tangu mwanzoni, au vinginevyo walikata tamaa walipofika sehemu hii na wakawa wamebadili msimamo. Kwa vyovyote, inajulikana kwamba watu hawa walikuwa upande mmoja na hili kabila la Hadhil kwa nia ya kuwakamata hawa wajumbe sita. Mara tu wale marafiki wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walipogundua kinachotokea, walikimbilia haraka silaha zao, na wakajiweka tayari kujihami; lakini wale Hudhayli wakaapia kwamba hawakukusudia kuwaua. Walitaka kuwatoa kwa Maquraishi huko Makkah na wapate chochote kwa ajili yao, na walikuwa tayari kufanya mapatano nao pale na wakati uleule kwamba hawatawaua. Watatu wao akiwemo ‘Asim ibn Thabit walisema hawataikubali aibu ya mapatano na washirikina, na wakapigana mpaka wakauawa. Lakini wale watu wengine watatu kwa majina ya Zayd ibn ad-Dathinnan ibn Mu ‘awiyah, Khubayb ibn ‘Adiy na ‘Abdullah ibn Tariq walionekana kubadilika sana na wakasalimu amri. Wale Hudhayli wakawafunga barabara hawa watatu kwa kamba na wakaondoka kuelekea Makkah. Karibu ya Makkah, ‘Abdullah ibn Tariq 32

Mahali panapoitwa ar-Raji..

68


alimudu kuuacha huru mkono wake toka kwenye zile kamba na kuufikia upanga wake, lakini adui hakumwacha aitumie fursa hiyo na akamuua kwa kumrushia mawe. Zayd na Khubayb walibebwa mpaka Makkah, na wakauzwa kwa kubadilishana na mateka wawili kutoka kwa Hudhayli waliokuwa wanashikiliwa hapo Makkah, na kisha wakaondoka zao. Safwan ibn Umayyah al-Qurashi alimnunua Zayd kutoka kwa mtu anayehusika ili amuue kulipiza damu ya baba yake aliyeuawa huko Uhud (au Badr). Ili kumuua alimtoa nje ya Makkah. Watu wa Quraishi walikusanyika ili waone nini kitatokea, na walimleta Zayd kwenye sehemu yake ya kuuliwa. Alitoka mbele kwa mwendo wake wa ujasiri na hakutetemeka hata kidogo katika kutembea kwake. Abu Sufyan alikuwa mmoja wa watazamaji na alidhani anaweza kuchukua fursa ya mazingira ya dakika za mwisho za maisha ya Zayd: pengine anaweza kupata maelezo ya majuto na kuonyesha kujuta na kukiri chuki juu ya Mtume kutoka kwake. Alitokeza mbele na kumwambia Zayd: “Nakuapisha kwa Mwenyezi Mungu, wewe Zayd, hivi hupendi wewe kwamba Muhammad angekuwa pamoja nasi mahala pako ili tuweze kumkata kichwa chake, na kwamba ungekuwa na familia yako?” “Wallahi” akasema Zayd, “Sipendelei kwamba Muhammad kwa sasa angekuwa kwenye sehemu aliyoikalia na kwamba mwiba uweze kumdhuru, na kwamba ningekuwa nimekaa na familia yangu.” Mdomo wa Abu Sufyan uliachama kwa mshangao. Aliwageukia Maquraishi wengine na akasema: “Wallahi, ninaapa kamwe sijaona mtu ambaye amependwa sana kama masahaba wa Muhammad wanavyompenda yeye.” Baada ya muda, zamu ya Khubayb ibn ‘Adiy ikafika, naye pia alitolewa nje ya Makkah kwa ajili ya kuuliwa. Pale aliiomba hadhara ile imruhusu kusali rak’ah mbili. Wakamkubalia, na aliisali sala hiyo kwa

69


unyenyekevu wote, heshma na hushui. Kisha akaongea na ule umati, na akasema: “Namuapia Mwenyezi Mungu kuwa isingekuwa kwamba mungelifikiri kwamba nimechelewa kwa ajili tu ya woga wa kufa, ningeirefusha zaidi sala yangu.” Walimuweka Khubayb kwenye ubao wa kunyongea; na ndipo ile sauti tamu ya Khubayb ibn ‘Adiy iliposikika, na ukamilifu wa kiroho uliomweka kila mmoja katika kustaajabu na ikawafanya wengine kujitupa chini ardhini kwa hofu, alipokuwa akimsihi Mwenyezi Mungu kwa maneno haya: ‫ اَللَّهُمَ أَحْصِهِمْ عَدَدًا وَاٌقْتُلْهُمْ بَدَدًا وَال‬. ‫ن قَدْ بَلَغْنَا رِسَاَل َة رَسُولِكَ فَبَلِ ْغهُ الغَداةَ مَا يُصْنَعُ بِنَا‬ َ ِ‫اَللَهُمَ ا‬ . ‫تُغاَدِرْمِنْهُمْ ْ أَحَدًا‬ ‘Ewe Mola! Tumefikisha ujumbe wa Mtume wako; hivyo mueleze kesho kile tulichofanyiwa sisi. Eh! Mola! Wahesabu kwa idadi na uwafishe mmoja mmoja, usimfanye hata mmoja wao kubakia.33 * *

*

Kama tunavyojua, tukio la Uhud liliisha kwa namna ya kusikitisha kwa Waislamu. Waislamu sabini waliuawa mashahidi, pamoja na Hamzah, ami yake Mtume. Waislamu mwanzoni walikuwa wakishinda, lakini baadae, kwa matokeo ya kukosa nidhamu ya kikundi ambacho kilikuwa kimewekwa juu ya kilima na Mtume (s.a.w.w.), Waislamu walipatwa na mashambulizi ya kushitukiza kutoka kwa maadui. Kikundi kimoja kiliuawa, kingine kikatawanywa, ambapo kile kikundi kidogo kilichokuwa kimemzunguka Mtume (s.a.w.w.) kilibakia. Kitu pekee ambacho hiki kikundi kidogo kingeweza kufanya ni kukusanya majeshi yao tena na kuwa kikwazo cha kusonga mbele zaidi kwa maadui, hasa pale tetesi ya kwamba Mtume (s.a.w.w.) ameuawa ilipokuwa sababu 33

Ibn Ishaq katika kitabu - The Life of Muhammad, tafsiri ya A. Guilaume, London, 1955, uk. 426-428.

70


zaidi ya kutawanyika kwa Waislamu. Lakini mara tu waliposikia kwamba Mtume alikuwa bado yu hai, ari yao iliwarudia tena. Idadi kubwa ya majeruhi ilikuwa imelala chini na hawakujua kabisa hatima yao itakuwa ni nini. Mmoja wa waliojeruhiwa alikuwa ni Sa‘d ibn ar-Rabi’, na alikuwa amepata majeraha makubwa kumi na mbili. Katikati ya matukio yote haya, mmoja wa wale Waislamu wanaotoroka alimkuta Sa‘d, alipokuwa amelala pale chini, na akamwambia kuwa amesikia kwamba Mtume (s.a.w.w.) ameuawa. Sa‘d akasema: ‘Hata kama Muhammad ameuawa, Mola wa Muhammad hajauawa; dini ya Muhammad bado ipo pia. Kwa nini usibaki na ukaitetea dini yako?’ Mbali na hili, baada ya Mtume (s.a.w.w.) kuwakusanya na kuwahakiki masahaba wake, aliwahesabu mmoja mmoja kuona ni nani ameuawa na nani alikuwa bado yuko hai. Hakumuona Sa‘d ibnar-Rabi’, hivyo aliwauliza kuwa ni nani angeweza kwenda kumchunguzia kile hasa kilichomsibu Sa‘d. Mmoja wa Ansari akasema yuko tayari. Wakati yule Ansari alipomgundua kwamba Sa‘d yuko kwenye pumzi zake za mwisho, alimwambia: “Ewe Sa‘d! Mtume amenituma kumchunguzia kama uko hai au umekufa.” “Nitolee salamu zangu kwa Mtume,” Sa’d alisema, “na mwambie kwamba Sa’d ni marehemu sasa, kwani hakuna zaidi ya pumzi chache zilizobakia za uhai wake. Mwambie Mtukufu Mtume kwamba Sa’d amesema: ‘Mola akulipe kwa ajili yetu sisi malipo bora zaidi kuliko alivyomlipa Mtume yeyote kwa ajili ya watu wake.’” Kisha akaongea na yule Ansari na akamwambia: “Fikisha ujumbe pia kwa ndugu zangu Ansari na masahaba wengine wa Mtume (s.a.w.w.). Waambie kwamba Sa’d amesema: ‘Hamna msamaha kwa Mola wenu kama chochote kitatokea kwa Mtume wenu wakati mnaweza kutingisha kope za macho.’”34 34

Sherehe ya Ibn abi’l-Hadid ya Nahju’l-Balagha, Beiruti, juz. 3, uk. 574; na ibid. (maelezo 33) uk. 387.

71


* *

*

Kurasa za historia ya zamani ya Kiislamu zimejaa matendo kama hayo ya utii, matendo ya upendo na matukio kwa matukio ya haiba. Katika historia yote ya mwanadamu, hakuna anayeweza kupatikana ambaye alipendwa kama alivyopendwa Mtume (s.a.w.w.), na madhumuni ya upendo kiasi hicho kutoka kwa rafiki zake, sahiba zake, wakeze na watoto, waliompenda sana hivyo na kwa uaminifu. Ibn Abi’l- Hadid ameandika katika sherehe yake ya Nahju’l-Balagha: “Hakuna aliyemsikia yeye (Mtume) akizungumza bila mapenzi juu yake kuchukua nafasi katika moyo wake, na bila kuwa amemuinamia. Hivyo Maquraishi waliwaita Waislamu waliokuwa Makkah “subat” – waliopumbazwa na wakasema ‘Hofu ni kama al-Walid ibn al-Mughirah akitoa moyo wake kwenye dini ya Muhammad; na kama Walid, ambaye ndie mahiri wa Quraishi akitoa moyo wake, Maquraishi wote wataweka mioyo yao rehani kwenye moyo wake.’ Walisema pia: ‘Hotuba yake ni uchawi, inalewesha kuliko mvinyo.’ Waliwakataza watoto wao wasiketi pamoja naye ili wasije wakavutiwa na kuzungumza kwake na mvuto wa sura yake. Kila wakati Mtume alipokaa chini kando ya Ka’abah karibu na Jiwe la Ismail na kusoma Qur’ani kwa sauti kubwa, au alipoangukia kumdhukuru Mungu, waliweka vidole vyao kwa nguvu masikioni mwao ili wasisikie na ili kwamba wasije wakaingia kwenye pumbazo la mazungumzo yake na wakawa “wamerogwa” na yeye. Walikusanya nguo zao vichwani mwao na kufunika nyuso zao ili kupendeza kwake kusije kukawauvutia. Hata hivyo, watu wengi waliuamini Uislamu kwa kumsikia mara moja au kwa kuuona uso wake na wajihi wake na kuonja utamu wa maneno yake.”35 Katika mambo yote ya historia ya Kiislamu ambayo yangesababisha mshangao wa kila mwana-anthropologia au mwana-elimujamii, msomaji au mtafiti, ni yale mapinduzi ambayo Uislamu umeyaleta 35

ibid, juz.2 uk.220.

72


miongoni mwa Waarabu wa kabla ya Uislamu. Kwa kukisia kokote kwa kawaida pamoja na mbinu za kawaida za elimu na mafunzo, mabadiliko ya jamii kama hiyo yangehitaji kupita kwa muda mwingi ili kwamba vile vizazi vya zamani vilivyozoea uovu viweze kuwa vimefutwa, na msingi wa kizazi kipya kujengwa upya; lakini athari za uwezo wa mvuto hazipaswi kupuuzwa, kwani tulisema kwamba, kama zilivyo ndimi za moto, hizi huchoma mizizi ya uovu. Wengi wa masahaba wa Mtume walipendezwa sana na mtu huyu mkubwa, na ilikuwa ni kwa kupanda juu ya kipando (farasi) kizuri cha upendo ambapo umbali mrefu kama huu ukatembewa kwa muda mdogo kama huo, na kwamba kwa muda mfupi jumuiya yake ikawa imebadilika kabisa. Mbawa za ndege wangu zikawa kitanzi cha mapenzi juu yake, Kikinikokota njia yote kwenda mlimani kwake. Nitawezaje kuwa na taa mbele yangu au nyuma Wakati nuru ya mpenzi wangu haiko mbele yangu au nyuma? Nuru yake inaangaza kulia, kushoto, juu na chini Iko juu ya kichwa changu na kuizunguka shingo yangu kama taji na nira36 MAPENZI JUU YA `ALI NDANI YA QUR’ANI NA SUNNAH Tulichokisema mpaka hapa kimetoa mwanga juu ya maana na athari za mapenzi, na kwa bahati imekuwa wazi kwamba mapenzi juu ya watu safi ni njia ya marekebisho na utakaso wa moyo, sio kwamba yenyewe ndio mwisho wa yote. Sasa lazima tuone kama Uislamu na Qur’ani vimemchagua mtu ambaye tunapaswa kumpenda au la. Wakati Qur’ani inaposimulia kile ambacho mitume waliopita wamekisema, inaonyesha kwamba wote walisema: “hatuombi ujira kutoka kwa watu, malipo yetu pekee yanatoka kwa Mungu.” Hatahivyo inamuambia Mtume wa Mwisho kuwa: 36

Rumi, Mathnavi, kitabu cha 1.

73


            Sema: Kwa haya siombi malipo yoyote kwenu ila mapenzi kwa jamaa zangu wa karibu. (Ash-Shura, 42:23) Hapa kuna haja ya kujiuliza ni kwa nini mitume wote waliobakia hawakutafuta ujira lakini Mtume bora kabisa aliomba kwa ajili ya ujumbe wake; kwa nini alitaka urafiki kwa ajili ya jamaa zake wa karibu kama malipo ya ujumbe wake? Qur’ani yenyewe inatoa jibu kwa swali hili:                     Sema: Malipo niliyokuombeni, basi hayo ni kwa ajili yenu, malipo yangu mimi yako kwa Mwenyezi Mungu tu, Naye ni shahidi juu ya kila kitu. (Sabaa’, 34:47) Hiyo ni kusema, kile ninachoomba kama ujira kinawanufaisha ninyi wenyewe, sio mimi; urafiki huu ni hatamu kwa ajili ya ukamilifu wenu wenyewe na uongofu, na unaitwa ujira. Vinginevyo kwa kweli ni wema mwingine ambao ninaupendekeza kwenu kwa maoni kwamba Watu wa Nyumba na ndugu wa Mtume ni watu ambao hawakusanyiki kwenye uchafu , na ambao maneno yao ni safi na ya kweli. Mapenzi na unyenyekevu kwa watu hawa havileti matokeo mengineyo mbali na utii kwenye haki na kushikamana kwenye maadili mema, na ni urafiki juu yao ambao hubadili na kukamilisha kama kile kioevu. Vyovyote maana ya “jamaa” itakavyokuwa, ni hakika kwamba mtu dhahiri kabisa ambaye itatumika kwake ni `Ali. Imam Fakhru’d-Din arRazi anasema: 74


“Zamakhshari anasimulia katika (sherehe ya Qur’an) al-Kash-shaf yake: ‘Wakati aya hii iliposhuka walisema: “Ewe Mtume wa Allah! Ni nani hao jamaa ambao kwao mapenzi yetu ni wajibu?” Akasema: “ni `Ali na Fatimah na watoto wao”’ “Kwa hiyo imethibitika kutokana na hadithi hii kwamba watu hawa wanne ni “jamaa” wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na kwamba wanapaswa wapate heshima na mapenzi ya watu, na suala hili linaweza kufikiriwa kimantiki katika njia nyingi: “1 - Aya hii: ila mapenzi kwa jamaa zangu. “2 - Hakuna shaka kwamba Mtume alimpenda sana Fatimah, na akasema:’Fatimah ni sehemu ya mwili wangu; kinachomdhuru yeye kinanidhuru mimi.’ Na alimpenda `Ali pia na Hasanayn (Hasan na Husain), kwani idadi kubwa ya hadithi mutawatir (zile zinazosimuliwa na wengi sana kiasi cha kufanya mashaka yasiwezekane) zimetufikia kuhusu suala hili. Hivyo urafiki juu yao ni wajibu juu ya jamii yote,37 kwa sababu Qur’ani inaamuru hivi:      Na mfuateni ili mpate kuongoka. (al-A’raf, 7:158 ) Inaamrisha pia:         

37

Mapenzi ya Mtume kwao hayakuwa na mwelekeo wa kibinafsi, yaani, haikuwa tu kwa sababu, kwa mfano, walikuwa watoto wake na wajukuu zake na kama mtu mwingine yeyote angekuwa kwenye nafasi yao angempenda. Mtume (s.a.w.w.) aliwapenda kwa sababu walikuwa watu wa mfano na Mwenyezi Mungu aliwapenda, kwani Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na watoto wengine ambao hakuwapenda kwa kiwango hiki na ambao kwao jamii haikuwa na wajibu kama huu.

75


Bila shaka ninyi mnao mfano mwema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu )Al-Ahzab, 33:21) Sababu hizi zinathibitsha kwamba mapenzi kwa Familia ya Muhammad ambao ni `Ali, Fatimah, Hasan na Husayn – ni wajibu kwa Waislam wote.38 Vilevile kuna hadithi nyingi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) kuhusu mapenzi na urafiki juu ya `Ali: 1. Ibn al-Athir anasimulia kwamba Mtume (s.a.w.w.) alizungumza na `Ali na akasema: “Ewe `Ali, Mungu amekupamba na mambo, ambayo hakuna mapambo mazuri zaidi kuliko hayo, yanayopatikana kwa waja wake: kuipa nyongo dunia kumeteuliwa kwa ajili yako katika njia ambayo kwamba hunufaiki kutokana na dunia, wala dunia yenyewe kutokana na wewe. Juu yako yamewekwa mapenzi ya wanyonge; wanajivunia uongozi wako nawe pia unajivunia kukufuata kwao. Ameridhika yule anayekupenda, na ni rafiki yako wa kweli. Na ole wake yule anayeonyesha uadui kwako, na akasema uongo juu yako.”39 2. as-Suyuti anasimulia kwamba Mtukufu Mtume amesema kwamba: “Mapenzi juu ya `Ali ni imani, na uadui juu yake ni uasi.”40 3. Abu Na’im anasimulia kwamba Mtume aliwahutubia Ansari na akasema: “Je, niwaongoze kwenye kitu ambacho, kama mtakishikilia baada yangu, kamwe hamtapotea?” Wakasema: “Ndio, Ewe Mtume wa Allah swt!” Akasema: “Ni `Ali: mpendeni kwa mapenzi (mliyonayo) juu yangu, na mheshimuni

38 39 40

at-Tafsiru’l-Kabir, juz.27, uk.166 (chapa ya Misri) Usdu’l-ghabah, juz. 4, uk. 23. Kanzu’l-‘ummal. Katika Jam’u ‘l-jawami, ya as-Suyuti, juz. 6, uk. 156.

76


kwa heshima (mliyonayo) juu yangu. Kwani Mwenyezi Mungu Ameniamrisha kupitia kwa Jibril niwaambie haya.”41 Sunni pia wamesimulia hadithi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) ambayo ndani yake kuangalia uso wa `Ali na kuzungumzia juu ya sifa zake kunahesabiwa kama ni namna ya ibada: 1. Muhibb at-Tabari anasimulia kutoka kwa ‘A’ishah kwamba alisema: “Nilimuona baba yangu (Abu Bakr) akiuangalia mara kwa mara uso wa `Ali. Nikasema: ‘Ewe baba yangu! Ninakuona mara kwa mara ukiuangalia uso wa `Ali.’ Akasema: ‘Ewe binti yangu! Nilimsikia Mtume akisema: “Kuuangalia uso wa `Ali ni ibada.’” 42 2. Ibn Hajar anasimulia kutoka kwa ‘A’ishah kwamba Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Mbora wa ndugu zangu ni `Ali, mbora wa ami zangu ni Hamzah, na kumkumbuka `Ali na kuzungumza juu yake ni ibada.”43 `Ali alikuwa ndiye mtu anayependwa sana mbele ya Mwenyezi Mungu na Mtume, na hivyo bila shaka ni mbora wa wale wanaopendwa. Anas ibn Malik anasema: “Kila siku, mmoja wa watoto wa Ansari angefanya shughuli kwa ajili ya Mtume. Siku moja ikafika zamu yangu. Umm Ayman akaleta kuku wa chakula mbele ya Mtume na akasema; ‘Ewe Mtume wa Allah swt! Nimemkamata kuku huyu mwenyewe na nikampika kwa ajili yako.’ Mtume akasema: ‘Ewe Mola! Mlete mbora wa waja Wako ili ashirikiane nami katika kumla kuku huyu.’ Kwa 41

Hilyatu’l-awliya’, juz.1, uk.63. Kuna hadithi nyingi kuhusu suala hili, na tumezikuta zaidi ya tisini kwenye vitabu vya kuaminika vya Sunni, ambazo zote zinahusu mapenzi kwa Amir al-muminin. Zipo pia hadithi nyingi katika vitabu vya Shi’ah na yule mwanazuoni mashuhuri al-Majlis amezikusanya katika juz. 39 (ya chapa mpya) ya Biharu’l-anwar katika mlango wa mapenzi na chuki juu ya Amir al-muminin; amesimulia hadithi 123 katika mlango huu. 42 ar-Riyadhu’n-nadhirah, juz.2, uk.219; na nyingine kama hadithi ishirini, kwa kiasi tunavyoelewa, zimesimuliwa katika vitabu vya Sunni juu ya jambo hili. 43 as-Sawa’iqu’l-muhriqah, uk.74; na hadithi tano zaidi zimesimuliwa katika vitabu vya Sunni juu ya jambo hili.

77


muda uleule mtu akagonga mlangoni na Mtume (s.a.w.w.) akaniambia: ‘Anas! Fungua mlango.’ Nikasema: ‘Ewe Mola Wangu mfanye awe mtu wa Ansari!’ Lakini nilimkuta `Ali mbele ya mlango, na nikasema: ‘Mtume ana shughuli.’ Kisha nikarudi kusimama kwenye nafasi yangu. Mlango ukagongwa tena, na Mtume (s.a.w.w.) akasema: ‘Fungua mlango.’ Tena nikaomba awe mtu wa Ansari. Nikaufungua mlango na ikawa ni `Ali tena. Nikasema: ‘Mtume ana shughuli.’ Kisha nikarudi na kusimama kwenye nafasi yangu. Bado tena mlango ukawa unagongwa, na Mtume (s.a.w.w.) akasema: ‘Anas, nenda kafungue mlango, na umuingize ndani. Wewe sio mtu wa kwanza kuwapenda watu wako mwenyewe; huyo sio mmoja wa Ansari.’ Nilikwenda na nikamuingiza `Ali ndani na akala yule kuku pamoja na Mtume (s.a.w.w.).”44 SIRI YA NGUVU YA MVUTO YA `Ali Ni sababu gani ya urafiki na mapenzi juu ya `Ali katika mioyo ya watu? Bado hakuna mtu ambaye amegundua siri ya mapenzi haya, yaani, hakuna mtu aliyeweza kuieleza kwa usahihi na kueleweka, na kusema kwamba kama ingekuwa kama hivi basi ile ingefuata, au kama ingekuwa kama vile basi hii ingetokea. Vyovyote itakavyokuwa kwa hakika ina siri. Kuna kitu katika yale mapenzi kinachomzuzua yule anayependa na kumvuta kukielekea. Mvuto huu na mapenzi ndio viwango vikuu vya upendo; `Ali ndiye mtu ambaye nyoyo za watu zinamheshimu; ambaye wanadamu wanampenda. Kwa nini? Ajabu ya `Ali iko katika nini, kinachochochea mapenzi na kinachovuta nyoyo kukielekea, kwamba kinafanya ulingano wa maisha ya akhera na uhai daima? Kwa nini nyoyo zote zinajigundua zenyewe kupitia kwake, na hazimhisi yeye kama amekufa bali zinamuona anaishi? Bila shaka msingi wa mapenzi juu yake haumo kwenye mwili wake, kwa sababu mwili wake sasa haupo miongoni mwetu na hatukuuona kwa fahamu zetu. Mapenzi juu ya `Ali pia sio utukuzaji ushujaa, ambao 44

al-Mustadrak ala as-Sahihayn, juz.3, uk.131. Hadithi hii imesimuliwa kwa namna mbalimbali katika zaidi ya masimulizi themanini katika vitabu vya kutegemewa vya Sunni.

78


unapatikana katika kila taifa. Ni makosa pia, kusema kwamba mapenzi juu ya `Ali ni kwa namna ya kupenda ubora wa wema na utu, na kwamba mapenzi juu ya `Ali ni mapenzi ya kiutu. Ni kweli kwamba `Ali alikuwa ni udhihirisho wa mtu mkamilifu, na ni kweli kwamba mwanadamu anapenda watu mashuhuri wa ubinadamu; lakini kama `Ali angekuwa anazo zile sifa zote nzuri za ubora wa mwanadamu alizokuwa nazo – ile hekima na elimu, kule kujitolea na uungwana, ule unyenyekevu na staha, ule upole na huruma, ule ulinzi wa wanyonge, ule uadilifu, kule kutopendelea na kupenda uhuru, ile heshima ya ubinadamu, ule ukarimu, ule ujasiri, ule ukarimu mkubwa na huruma kwa maadui zake, na, katika maneno ya Rumi: Kwa ushujaa wewe ni Simba wa Mungu, Kwa ukarimu nani hasa anayekujua wewe ni nani? 45 Kwamba wingi wa ukarimu, wema na upaji – kama `Ali angekuwa anavyo vyote hivi, ambavyo alikuwa navyo, lakini hakuwa ana mguso wa kimungu ndani yake, ni wazi kabisa kwamba hakungekuwa na hisia ya huruma na muamsho wa mapenzi uliopo leo. `Ali anapendwa kwa maana ya kwamba alikuwa ana kiunganisho cha kimungu; mioyo yetu bila kufahamu imehusika sana na kuunganishwa kwenye Haki, ndani kabisa ya vina vyao, na kwa vile inamuona `Ali kama alama kuu ya Haki na udhihirisho wa sifa za Haki iko katika mapenzi na yeye. Kwa kweli, msingi wa mapenzi juu ya `Ali ni muunganiko wa nafsi zetu na Haki uliowekwa katika tabia zetu za asili, na kwa vile tabia zetu za asili ni za milele, mapenzi juu ya `Ali pia ni ya milele. Kuna sifa nyingi zinazojitokeza katika utu wa `Ali, lakini zilizompa nafasi ya fahari na ya kung’ara daima ni imani yake na uadilifu wake, na ndio hizo ambazo zimempa kipaji kitukufu.

45

Rumi, Mathnavi,kitabu cha 1. (kilichotafsiriwa na Nicholson).

79


Sawdah al-Hamdaniyah, mtu anayejitolea mhanga na mfuasi mtiifu wa`Ali, alimsifu `Ali mbele ya Mu‘awiyah na miongoni mwa mambo mengine akasoma shairi hili: Baraka za Mungu zithibiti kwake Ambaye kaburi lilimchukua na pamoja naye haki ilizikwa. Alikuwa na mapatano na Mungu kwamba asiweke mwingine badala yake, Hivyo aliunganishwa na Haki na Imani. Sa‘sa‘ah ibn Suhan al-‘Abdi alikuwa mtu mwingine katika wapenzi wa `Ali. Alikuwa ni mmoja wa wale walioshiriki usiku ule pamoja na wengine wachache katika mazishi ya `Ali. Walipokwisha kumzika `Ali na kufunika mwili wake na udongo, Sa‘sa‘ah aliweka mkono wake mmoja juu ya moyo wake, akatupa mchanga juu ya kichwa chake na akasema: “Kifo kiridhiane nawe, ambaye uzawa wako ulikuwa tohara, ambaye uvumilivu wako ulikuwa imara, ambaye jitihada zako tukufu zilikuwa mashuhuri! Ulifikia lengo lako na biashara yako ilizaa matunda. “Umeanguka chini mbele ya Muumba wako, na Yeye amekupokea kwa furaha na malaika Zake walitokea kukuzunguka. Uliwekwa karibu na Mtume, na Mungu akakupa nafasi karibu yake. Ulifikia kiwango cha ndugu yako, Mustafa, na ukanywa kutoka kwenye kikombe chake kilichojaa. Ninamuomba Mwenyezi Mungu ili niweze kukufuata na kwamba nifanye kulingana na njia zako; kwamba niweze kuwapenda wale wanaokupenda, na niwe adui wa wale ambao ni maadui zako, kwamba niweze kukusanywa kwenye banda la marafiki zako. “Ulikiona kile ambacho wengine hawakukiona, na kukifikia ambacho wengine hawakukifikia; uliiandama harakati tukufu kandoni mwa ndugu yako, Mtume (s.a.w.w.), na ulisimama kwa ajili ya dini ya Allah swt kama ilivyostahiki, mpaka tabia za kizamani zikaondolewa, ghasia 80


ikatawaliwa na Uislamu na imani vikaimarishwa. Rehma njema ziwe juu yako! “Kupitia kwako migongo ya waumini imefanywa thabiti, njia zikawekwa wazi na tabia zikavunjwa. Hakuna anayeweza kukusanya sifa zako na ubora wako kwake mwenyewe. Uliitikia mwito wa Mtume (s.a.w.w.); uliruka mbele ya wengine katika kumkubali yeye: ulikimbilia kumsaidia, na ukamlinda kwa maisha yako. Ulishambulia kwa upanga wako, Dhu’l-fiqar, kwenye sehemu za hofu na ukatili, na uliuvunja uti wa dhulma. Ulishusha chini miundo ya ushirikina na upotovu, na uliwaangusha chini wale waliopotea kwenye vumbi na damu. Hivyo unaweza kufurahi, Ewe Amir al-mu’minin! “Ulikuwa ndio mtu wa karibu sana kwa Mtume, ulikuwa ndio mtu wa kwanza kufuata Uislamu. Ulikuwa umejawa na uhakika, nguvu ya moyo na mwingi wa kujitolea kuliko yeyote, sehemu yako katika wema ilikuwa kubwa mno. Mola asitunyime sisi malipo kwa mateso yako, na tunamuomba Asitutweze sisi baada ya kuondoka kwako! “Wallah; Naapa kwamba maisha yako yalikuwa kama ufunguo wa wema, kufuli dhidi ya uhamisho; na kifo chako ni ufunguo kwa kila ovu na kufuli dhidi ya kila jema. Kama watu wangekukubali, baraka zingeshushwa juu yao kutoka mbinguni na ardhini; lakini walipendelea dunia hii kuliko ijayo.”46 Kwa hakika walipendelea dunia hii, na kama matokeo hawakuweza kuvumilia haki na kutokuyumba kwa `Ali. Mwishowe mkono wa ugumu na kudorora ukatoka kwenye mkono wa shati la watu na kumuua `Ali. `Ali – amani iwe juu yake – hana wa kulingana naye katika kuwa na marafiki waiso na ubinafsi kabisa na watu waliompenda, waliojitolea maisha yao katika njia ya urafiki na mapenzi juu yake. Wasifu zao nzuri sana, zenye kuteka na kutia bumbuazi zinatukuzisha kurasa za historia 46

Biharu’l-anwar, juz. 42, uk. 295-296 (chapa mpya).

81


ya Kiislamu. Mikono miovu ya watu washenzi kama Zayd ibn Abih na mwanae ‘Abdullah, kama Hajjaj ibn Yusuf na Mutawakkil, na juu yao wote Mu‘awiyah ibn Abi Sufyan, imetapakaa damu za haya maisha ya watu mpaka kwenye viwiko vyao.

82


SEHEMU YA PILI NGUVU YA KINGAMIZO NDANI YA `Ali              

Jinsi `Ali alivyopata maadui Nakithun, Qasitun na Mariqun Jinsi Khawarij walivyotokea kuwepo Msingi wa maoni ya Khawarij Walichoamini kuhusu Ukhalifa Walichoamini kuhusu Makhalifa Kuanguka kwa Khawarij Je, Ni kaulimbiu tu? Busara ya demokrasia ya `Ali Maasi na upinzani wa Khawarij Sifa bainifu za Khawarij Siasa ya “kutumia” Qur’an Umuhimu wa kupiga vita unafiki `Ali, Imamu na kiongozi wa haki

83


JINSI ‘Ali ALIVYOPATA MAADUI Tutaishilizia mjadala wetu kwenye kile kipindi chake tu cha ukhalifa, cha kama zaidi ya miaka minne. `Ali alikuwa wakati wote mtu wa nguvu-mbili; `Ali siku zote alikuwa na nguvu zote; ya mvuto na ya kingamizo. Kwa kweli, tunaona tangu mwanzo wa enzi ya Uislamu, kundi moja lililovutiwa zaidi karibu na `Ali, na kundi jingine ambalo halikuwa na uhusiano mzuri kama huo naye na ambalo mara chache lilikuwa likiudhiwa na kuwepo kwake. Lakini kipindi cha ukhalifa wa `Ali, na vilevile nyakati za baada ya kifo chake, hii ni kusema, kile kipindi cha kutokeza kwa “historia” ya `Ali, kilikuwa ni zama kuu ya kudhihirisha mvuto wake na kingamizo lake; kwa kiwango kama kilekile cha kabla ya ukhalifa mahusiano yake na jamii yalikuwa machache, na pia mvuto wake na kingamizo pungufu. `Ali alikuwa mtu aliyepata maadui na aliwapa watu kero, na hii pia, ni moja kati ya sifa zake kuu. Kila mtu muadilifu ambaye ana lengo na anafanya juhudi kulifikia, hasa yule mwana mapinduzi ambaye anashikilia utekelezaji wa malengo yake makuu na ambae anaelezwa kwa maneno ya Allah swt:          . Watapigania dini ya Mwenyezi Mungu, wala hawataogopa lawama za wenye kuwalaumu. (Al-Maidah 5:54.) Anapata maadui na kuwaacha watu wasioridhika. Hivyo kama maadui zake hawakuwa na idadi zaidi ya wale marafiki zake, hususan katika nyakati za uhai wake mwenyewe, hawakuwa wachache na wala sio wachache hata sasa.

84


Kama hadhi ya `Ali isingechafuliwa leo hii, bali ingekuwa kama vile tu ilivyo, wengi wa wale wanaojifanya kuwa ni marafiki zake wangechukua msimamo mmoja pamoja na maadui zake. Mtume (s.a.w.w.) alimtuma `Ali kama kamanda wa jeshi kwenda Yemen. Wakati wa kurudi kwake alielekea Makkah kwenda kukutana na Mtume, na, alipofika kwenye viunga vya Makkah, alimteua mmoja wa askari wake kushika nafasi yake na yeye mwenyewe akaharakisha kwenda kuwasilisha taarifa ya msafara wake kwa Mtukufu Mtume wa Allah swt. Yule mtu akazigawa zile nguo ambazo `Ali alikuja nazo pamoja na wao miongoni mwa wale askari, ili waingie Makkah wakiwa wamevaa nguo mpya. Wakati `Ali aliporudi alikipinga kitendo hiki, na alimlaumu yule mtu kwa kukosa nidhamu, kwa sababu hakuna uamuzi ambao ungechukuliwa kuhusu nguo zile kabla ya kupokelewa maelekezo kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) kuhusu nini kifanywe kuhusu nguo hizo. Machoni kwa `Ali, kitendo kama hiki kwa kweli kilikuwa ni kama kupora mali ya Waislamu(baytu’l- mali) bila ya kutoa taarifa, na kupata idhini kutoka kwa kiongozi wa Waislamu. Kwa sababu hii `Ali aliamuru kwamba wazivue nguo zile na kuziweka sehemu maalum, mpaka zifikishwe kwa Mtume na yeye mwenyewe ataweza kutoa uamuzi juu ya nguo hizo. Kwa sababu ya hili, askari wa `Ali hawakuridhika, na, mara tu walipokwenda kumuona Mtume, walilalamika kuhusu ukali wa `Ali juu ya nguo hizo. Mtume aliongea nao, na akasema: ‫ن فِى‬ ُ َ‫ال تَشْكُوا عَلِ ًي ا فَ َو اٌ لَل ِه اِ َنهُ الَْخْش‬ َ ‫س‬ ُ ‫ي َأ اَيُهَا ا لنَا‬ ‫ن اَنْ يُشْكَى‬ ْ ِ‫ذَاتِ اٌلَلهِ م‬ Enyi watu, msilalamike juu ya Ali. Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba yeye ni mkali sana katika njia ya Mwenyezi Mungu kuliko vile ambavyo mtu yeyote angelalamika kuhusu yeye.* *

Tazama kitabu The life of Muhammad cha Ibn Ishaq (Tafsiri ya A. Guillaume) uk 650.

85


`Ali hakuwa na shughuli na mtu yoyote katika njia ya Mwenyezi Mungu. Bali kama alionyesha shauku kwa mtu yeyote au alijishughulisha naye, ilikuwa ni kwa sababu ya Allah swt. Kwa kawaida, tabia kama hiyo husababisha maadui, na inaleta uovu kwenye nafsi zilizojaa uroho na tamaa na inawapa uchungu. Hakuna yeyote kati ya masahaba wa Mtume (s.a.w.w.) aliyekuwa na marafiki watiifu kama `Ali aliokuwa nao, kama ambavyo hakuna hata mmoja aliyekuwa na maadui wakakamavu na hatari kama aliokuwa nao yeye. Alikuwa ni mtu ambaye, hata baada ya kifo chake, maiti yake ingelishambuliwa na maadui. Mwenyewe alilitambua hili na aliyabashiri mapema mambo haya, na hivyo aliacha kama usia wake kwamba kaburi lake lije kufichwa na kutojulikana kwa wote ila kwa wanawe, mpaka baada ya karibu karne nzima na Bani Umayyah wakawa wamepinduliwa, na Khawariji wamepinduliwa pia, au wote wamefanywa dhaifu, na walipiza kisasi cha damu na cha kawaida wamekuwa wachache, na Imam as-Sadiq akaonyesha ardhi takatifu ya sehemu ya mapumziko yake (kaburi).

*

*

86

*


NAKITHUN, QASITUN NA MARIQUN. Katika kipindi cha ukhalifa wake, `Ali alifukuza vikundi vitatu kutoka karibu yake na akasimama kufanya vita navyo: watu wa (vita vya) Jamal, ambao yeye mwenyewe aliwaita Nakithun (wenye kuvunja kiapo chao); watu wa (vita vya) Siffin, ambao aliwaita Qasitun (wenye kupotoka); na watu wa (vita vya) Nahrawan, Khawariji, ambao aliwaita Mariqun (wanaokosa ukweli wa dini) 1 `Ali akasema: َ‫ط آخَرُون‬ َ َ‫أل مْرِنَكَثَتٌُ طَائِفَتٌ وَمَرَقَتْ أُخْرَى َو قَس‬ َ ْ‫ت بِا‬ ُ ْ‫َفلَمَأ نَهَّض‬ Nilipochukua madaraka ya serikali kundi moja likavunja kiapo chao cha utii (nakathah), jingine likakosa ukweli wa dini (maraqah), na jingine likapotoka (qasatah)2 Hawa Nakithun walikuwa wenye tabia ya kuabudu pesa, watu wenye tamaa na wenye kuonyesha chuki. Hotuba za `Ali juu ya haki na usawa zilikuwa hasa ni kwa mazingatio ya kundi hili. Hata hivyo mawazo ya hawa Qasitun yalikuwa ya kisiasa, udanganyifu na uchochezi wa maovu; waliuwa ili kuchukua madaraka ya serikali mikononi mwao wenyewe, na kuuangusha msingi wa serikali ya `Ali na ugavana wake. Baadhi ya watu walimshauri afanye muafaka nao na awape kwa kiasi fulani, kile wanachokitafuta, lakini hakukubali kwa sababu hakuwa mtu wa kufanya kitu cha namna hii. Alikuwa tayari kupinga dhulma, sio kuipasisha. Kwa upande mwingine, Mu’awiyah na genge lake walipinga msingi wa serikali ya `Ali, na kisha Qasitun walitaka kukalia kiti cha ukhalifa wa Uislamu wao wenyewe. Kwa 1

Mbele ya `Ali (a.s.), Mtume (s.a.w.w.) aliwaita watu hawa kwa majina haya alipomwambia “Baada yangu utakuja kupigana na nakithun, qasitun na mariqun,” Hadithi hii inasimuliwa na Ibn Abil-Hadid katika Sherehe yake ya Nahju’l’ balagha (juz. 1, uk .201). Pale anaposema kwamba ni mojawapo ya ushahidi wa Utume wa Muhamad kwani hadithi yenyewe iko wazi kabisa kuhusu wakati ujao na mambo ya

(ghaib) yasiyofaamika na hakuna aina yoyote ya tafsiri iliyojificha ni udondoshaji wa maneno ndani yake. 2 Nahju’l’ Balaghah- hotuba ya 3” ash-shaqshaqiah.”

87


kweli vita vya `Ali dhidi yao vilikuwa ni vita dhidi ya maasi na undumilakuwili. Kundi la tatu, ambalo lilikuwa la Mariqun, walikuwa na moyo wa ushupavu (ubishi) usiokubalika, unafiki na ujinga wa hatari. Katika kuhusiana na watu wote hawa, `Ali alikuwa ni kikwazo chenye nguvu na waliishi katika hali ya kotoelewana. Moja ya udhihirishaji wa utimilifu wa `Ali na kuwa kwake mtu mkamilifu ilikuwa kwamba, ilipolazimika, alikabiliana na vikundi mbalimbali na upotovu na alipigana dhidi yao wote. Wakati mwingine tunamuona katika uwanja, akipigana na wale waliokuwa na mapenzi kwenye pesa au kwenye dunia hii, na wakati mwingine pia kwenye uwanja akipigana na wanasiasa mabingwa wa aina ya kinafiki kabisa, na wakati mwingine na watu wajinga na wakengeukaji wenye uchaji bandia. Mjadala wetu umeelekezwa kwenye kundi hili la mwisho, Khawariji. Ingawa wamepinduliwa na hawapo tena, wanaonyesha historia ndogo yenye kufundisha na kuonya. Mawazo yao yameota mizizi miongoni mwa Waislamu, na hivyo ari yao daima imekuwepo, na bado ipo, katika sura ya watu wanafiki, wakati wote katika karne hizi kumi na nne, ingawa Khawarij wenyewe na hata jina lao wametoweka, na wanaweza kuhesabika kama kipingamizi kikubwa kwa maendeleo ya Uislamu na Waislamu.

*

*

88

*


JINSI KHAWARIJI WALIVYOTOKEA KUWEPO Hili neno “khawarij”, yaani, “waasi”, linatokana na neno “khuruj”3 lenye maana “maasi” na “upinzani”. Kundi hili lilitokea wakati ilipofanyika suluhu. Vita vya Siffin, katika siku yake ya mwisho ya mapigano, vilikuwa vikielekea kumfadhilisha `Ali; Mu’awiyah, kwa kushauriana na’Amr ibn al-‘as, walibuni hila mahiri sana. Alikuwa ameona kwamba mihangaiko yake yote haikuzaa matunda yoyote, na kwamba alikuwa hatua moja tu kuelekea kushindwa. Aliona kwamba hakuna njia yoyote ya kumuokoa ila kwa njia ya msaada wa kuanzisha fujo, hivyo aliamuru kwamba Qur’ani inyanyuliwe juu kwenye ncha za mikuki kuonyesha kwamba walikuwa watu wa sala na Qur’ani, na kwamba hicho Kitabu kitumike kwa kusuluhisha kati ya pande mbili hizo. Haikuwa mara ya kwanza hili kufanyika, kwani ni jambo hilo hilo ambalo `Ali alifanya kabla lakini ambalo halikukubaliwa. Hata sasa hawakulikubali; ilikuwa ni kisingizio chao cha kutafuta njia ya kujinusuru wao na kuwaokoa na kushindwa kwa dhahiri. `Ali akakemea: “Washambulieni! Wanazitumia kurasa na karatasi za Qur’ani kama ujanja, wanataka kujihami nyuma ya maneno na maandishi ya Qur’ani na baadae waendeleze ule mwenendo wao wa 3

Kama neno “khuruj” linatumika na shamirisho yaambiwa linalotokana na linakuwa na maana mbili zinazokaribiana. Moja ni kusimama kwenye nafasi kwa ajili ya kupigana au vita, na nyingine ni kuto tii, ukaidi na uasi. Kamusi la Kiarabu al-Munjid linasema kwamba “kharaja” pamoja na shamirisho yambiwa linalotokana na ‘alã lina maana ya kutoka mbele na kupigana na mtu, au linaweza kutumika kwa raia wanaoasi dhidi ya mfalme: upinzani dhidi ya utawala. Hili neno “khawãrij” kwa maana ya uasi, linatokana na “khuruj” katika maana ile ya pili. Kile kikundi kinachoshuhudia mamlaka ya Ali na kisha kikamuasi kinaitwa Khawarij. Kwa vile waliegemeza kutotii kwao juu ya namna ya imani na juu ya fikra ya kidini, wakawa madhehebu, na jina hilo likaja kutumika maalum kwa ajili yao; na hivyo halikutumika kwa watu wengine waliosimama baada yao na kuasi dhidi ya mtawala wa nyakati zao. Kama hawangekuwa na imani na dhana maalum, wangeweza kuwa kama waasi wengine wa nyakati zile za baada yao, lakini walikuwa na dhana na baadae dhana hii hii ikapata namna ya uhai huru. Ingawa hawakuweza kamwe kuunda serikali, waliweza kuanzisha madhehebu na vitabu vyao wenyewe. Walikuwepo watu binafsi ambao hawakufikia kamwe uasi kamili, ingawa waliuamini uasi huo, kama inavyosemekana juu ya ‘Amr ibn Ubayd na Mu’tazilah wengine. Ilisemekana juu ya baadhi ya Mu’tazilah waliokuwa na dhana zinazofanana na zile za Khawarij juu ya “kuamrisha mema na kukataza mabaya”, au juu ya suala la wale Waislam ambao wana hatia ya dhambi ya kimaadili bado wanapata sehemu katika pepo, kwamba “walifikiri kama wale Khawarij”. Hivyo kuna kiwango fulani cha ushirikiano kati ya maana ya kimsamiati ya neno lenyewe na matumizi yake maalum.

89


zamani wa kinyume na Qur’ani. Wakiwa wenye kupingana na haki, makaratasi na majalada ya Qur’ani hayana thamani na hayakustahiki heshima; ni mimi ambaye ndiye ukweli na udhihirisho wa kweli wa hiyo Qur’an. Wanayatumia makaratasi na maandishi ya Qur’an kama kisingizio cha kuuharibu ukweli na maana yake!” Kikundi cha watu wasio na busara, wasiojua na wenye unafiki, ambao waliunda sehemu kubwa ya kutosha, wanaashiriana wao kwa wao. Hivi `Ali ana maana gani? Wakakemea: “Hivi tupigane dhidi ya Qur’ani? Vita yetu ni ya kuanzisha tena Qur’an, na sasa wamejisalimisha kwenye Qur’an, hivyo tunapigana kwa ajili gani?” “Na mimi pia ninasema ninapigana kwa ajili ya Qur’an” `Ali akasema. “Lakini hawana uhusiano na Qur’an. Wamenyanyua juu maneno na maandishi ya Qur’an kama njia ya kuokoa nafsi zao.” Kuna swali katika sheria ya Kiislamu, katika kifungu cha jihad, kuhusu hali ya makafiri kujikinga nyuma ya Waislamu. Tatizo ni kwamba kama maadui wa Uislamu wakikiweka kikundi cha mateka wa kivita wa Kiislamu mbele ya safu zao kama ngao, na wao wenyewe wakawa wanajishughulisha na mambo yao, wakiendelea mbele nyuma ya ngome hii, ili kama majeshi ya Kiislamu yatajaribu kujihami, au kuwashambulia na kusimamisha maendeleo yao, hakuna njia nyingine tena ila pia ni kuwaua, kutokana na umuhimu, wale ndugu zao Waislamu waliokuwa ngao; yaani, kama hakuna uwezekano wa kupata njia ya kufika kwenye mapigano na kumshambulia adui mbali na ile ya kuwaua Waislamu, basi katika hali hii kule kumuua Muislamu, kwa umuhimu wa maslahi ya Uislamu, na ili kuokoa maisha ya Waislamu waliobakia, kunakuwa ruksa katika sheria ya Kiislamu… Kusema kweli, wao pia ni askari wa Uislamu na watakuwa wahanga (mashahidi) katika njia ya Mwenyezi Mungu. Hatahivyo, malipo ya kuua lazima yalipwe kwa ajili yao kutoka kwenye hazina ya Kiislamu kwa ndugu zao walio hai. Hii, kwa kweli, sio hali ya kipekee ya sheria ya Kiislamu tu, bali kuna sheria ya wazi kabisa miongini mwa kanuni na taratibu za kimataifa za vitendo vya vita na kijeshi kwamba kama adui anataka

90


kutumia vikosi vyako wewe mwenyewe, unaweza kuviua vikosi hivyo ili kuwafikia maadui na kuwarudisha nyuma.4 “Kama, wakati wanapokuwepo, Waislamu wa kweli, walio hai,” aliendelea `Ali, “na Uislamu unasema ‘Shambulia!’ ili kuhakikisha ushindi wa Waislam, basi hapawezi kuwa na pingamizi litakalofanywa kwenye karatasi na majalada ya vitabu. Taadhima juu ya kurasa na maandishi ni kwa sababu ya maana zao na yaliyomo. Leo kupigana ni kwa ajili ya maudhui ya Qur’an, lakini watu hawa wamenyanyua kurasa hizo kama njia ya kuharibia ile maana na maudhui ya Qur’an.” Hata hivyo, wajinga na wasiojua waliteremsha pazia jeusi mbele ya akili zao na kuuacha ukweli. “Kwa nyongeza ya ukweli kwamba hatutapigana na Qur’an,” walisema, “tunajua kwamba kupigana nayo kwenyewe ni dhambi, na ni lazima tuue ili kulizuia hili. Tutapigana na wale wanaopigana dhidi ya Qur’an.” Ni saa moja tu ilikuwa inahitajika kupata ushindi; Malik al-Ashtar, ambaye alikuwa afisa hodari, mtiifu na mwenye kujali wengine, alitoka hivyo kwenda kuvunja hema la Mu’awiyah la kuamrishia mapigano na kusafisha njia ya Waislam kutokana na vikwazo. Wakati huu huu, kikundi hiki kikamshinikiza `Ali kwa kusema watashambulia kwa nyuma. `Ali aliwasihi wasifanye hivyo, lakini walizidisha malalamiko yao, na, zaidi ya hayo, walionyesha kwamba wangekuwa wakaidi moja kwa moja. `Ali alituma ujumbe kwa Malik aache kupigana na aondoke kutoka sehemu yanapofanyika mapigano. Alituma jibu kwa `Ali kwamba angemruhusu kwa muda zaidi kidogo vita ingemalizika, na adui kuangamizwa. Lakini Khawariji walichomoa panga zao na kutishia kumkata `Ali vipande vipande labda amwuite arudi nyuma.

4

Kwa rejea zaidi, ile sehemu juu ya jihad katika tafsiri ya Kifaransa ya Sharã’I‘u’lIslam ya al-Muhaqqiq al-Hilli (kitabu cha Kiarabu juzuu nne, Najaf 1389/1969) inaweza kuangaliwa. Tazama Droit Musulman, Recueil des lois concernant les Musulmans Schyites tafsiri ya A.Querry (Paris 1871).

91


Kisha tena ujumbe ulitumwa kwake kwamba kama alitaka kumwona `Ali akiwa hai, asimamishe vita na arudi. Akarudi, na adui akawa na shangwe kwamba hila yao imeonyesha kufaa. Mapigano yakasimama ili waache usuluhishi kwenye Qur’an. Kamati ya usuluhishi ikaundwa, na wasuluhishi wakachaguliwa kutoka pande zote mbili kuamua kwa msingi wa kile kilichokubaliwa na pande zote mbili ndani ya Qur’an na sunnah na kumaliza uhasama; ama sivyo wataongezea tofauti nyingine kwenye tofauti zilizopo na kuifanya hali kuharibika. `Ali akasema kwamba wachague msuluhishi wao, na kisha yeye atatuma wake. Bila ya mabishano japo kidogo, walikubaliana kumchagua 'Amr ibn al-As, yule mzushi wa hila hiyo. `Ali alimpendekeza 'Abdullah ibn al-Abbas, ambaye alikuwa na ujuzi wa siasa, au Malik al-Ashtar, mtu mwenye kujitolea, mwenye uono safi na mtu wa imani, au vinginevyo mtu kama wao. Lakini wajinga wale walikuwa wanatafuta mtu wa namna kama yao wenyewe, na wakamchagua mtu wa namna ya Abu Musa al-Ash‘ari, mtu asiyekuwa na ukali wa maneno ambaye hakuwa na maelewano mazuri na `Ali. Kila vile `Ali na rafiki zake walivyotaka kuwaelimisha watu hawa kwamba Abu Musa hakuwa mtu wa kazi hii na kwamba uteuzi huo haumstahili yeye, walisema kwamba hawatamkubali mtu mwingine yoyote. Ndipo akasema kwamba madhali mambo yamefikia hatua hiyo, wafanye vyovyote wanavyotaka. Hivyo, mwishowe, wakamchagua huyu Abu Musa kama msuluhishi kutoka upande wa `Ali na masahaba zake. Baada ya miezi ya mashuariano, ‘Amr ibn al-As akamwambia Abu Musa kwamba ingekuwa vizuri kwa maslahi ya Waislamu kama si `Ali ama Mu‘awiyah angekuwa ndio khalifa, hivyo wangechagua mtu wa tatu, na kwamba hapakuwa na mtu mwingine yoyote wanayeweza kumchagua bali ni ‘Abdullah ibn ‘Umar, mkwe wake Abu Musa (aliyemuolea binti yake). Abu Musa akasema kwamba hiyo ni sawa na akauliza ni kitu gain wafanye. ‘Amr ibn al-As akasema: “Wewe umuondoe `Ali kwenye ukhalifa, na mimi nitafanya vivyo hivyo kwa 92


Mu‘awiyah. Kisha Waislamu watachagua mtu anayefaa ambaye kwa kweli atakuwa ni ‘Abdullah ibn ‘Umar. Hivyo mizizi ya uovu itang’olewa.” Walilikatisha suala hili na kutangaza kwamba watu wakusanyike pamoja wasikilize uamuzi wao. Watu wakakusanyika, Abu Musa akamgeukia ‘Amr ibn al-As asimame na kutangaza maoni yake. ‘Amr ibn al-As akasema: “Mimi? Wewe ndie mtu mwenye ndevu nyeupe unayeheshimiwa, sahaba wa Mtume. Kamwe sintathubutu kufanya kitu kama hicho cha kuongea kabla yako!” Abu Musa aliondoka kwenye sehemu yake ili kusimama aongee. Sasa kila mtu moyo ulikuwa unamwenda mbio, macho yote yalikuwa yanatazama, kila mtu alishika pumzi zake, wakingojea kuona matokeo yamekuwaje. Alianza kuongea: “Baada ya tahadhari inayostahili juu ya kile kilichoko kwenye maslahi ya ummah, tuliona kwamba sio `Ali wala Mu‘awiyah apasaye kuwa khalifa. Zaidi ya hili sio juu yetu sisi kusema, kwani Waislamu wenyewe wanajua ni nini wanachokitaka.” Kisha akachukua pete kutoka kwenye kidole cha mkono wake wa kulia na akasema: “Nimemuondoa `Ali kwenye ukhalifa, kama vile ninavyoondoa pete hii kutoka kwenye kidole changu.” Alipokwisha maliza akashuka chini. Ndipo ‘Amr ibn al-As akasimama na kusema: “Mmesikia nyote maelezo ya Abu Musa akisema kwamba amemuondoa `Ali kwenye ukhalifa. Na mimi pia ninamuondoa kwenye ukhalifa, kama alivyofanya Abu Musa.” Kisha akavua pete yake kutoka kwenye mkono wa kulia na akaivaa mkono wake wa kushoto, na akasema: “Ninamuweka Mu‘awiyah kwenye ukhalifa, kama vile ninavyovaa pete hii kwenye kidole changu.” Alipokwisha sema haya akashuka chini.

93


Mkutano huo uliangukia kwenye ghasia. Watu wakaanza kumshambulia Abu Musa, na wengine wakampiga na viboko vyao. Alikimbilia Makkah, na ‘Amr ibn al-As akaenda Damascus. Hawa Khawariji, waliosababisha huu mfululizo wa matukio, waliiona kashfa ya suluhu hii kwa macho yao wenyewe, na wakatambua kosa lao. Lakini hawakuweza kuelewa ni wapi hasa lilipokuwa kosa lao. Hawakusema kwamba kosa lao lilikuwa kwenye kunasa kwenye njama ya Mu ‘awiyah na Amr ibn al-As na kufanya vita isimame; wala hawakusema kwamba baada ya kuandaa hiyo sulhu waliboronga katika kuchagua “refa” wao, kwa kumuweka Abu Musa kama mwenza wa ‘Amr ibn al-As. La hasha; badala yake wakasema kwamba katika kuweka binadamu wawili kusuluhisha na kuwa “marefa” katika mambo ya dini ya Mwenyezi Mungu wamekwenda kinyume na sheria tukufu na wamefanya kitendo cha kufru, kwani hakimu ni Mungu tu, sio mwanaadamu. Kisha wakamjia `Ali na wakasema: “Hatukuelewa. Tulichagua mwanadamu kama msuluhishi. Umekuwa kafiri, na vilevile hata sisi. Lakini tumetubia; nawe pia unapaswa utubie. Vinginevyo, msiba huu utarudiwa tena.” “Katika hali yoyote,” `Ali akasema, “kutubia ni kuzuri. Sisi siku zote tunatubia kwa ajili ya madhambi yetu.” Lakini wakasema hii haitoshi, na kwamba ni lazima akiri kwamba usuluhishi ulikuwa ni dhambi, na kwamba ametubia juu ya dhambi hiyo. Lakini alisema kwamba haikuwa ni yeye aliyelileta suala la sulhu, walikuwa ni wao, na kwamba wameyaona matokeo yake wao wenyewe. Zaidi ya hayo, yeye atatamkaje kama ni dhambi kitu ambacho Uislamu umekifanya halali, au kukiri dhambi ambayo hakushiriki. Kuanzia hapa na kuendelea, walipanga kufanya kazi kama madhehebu ya kidini. Mwanzoni walikuwa kikundi cha uasi na uhalifu, na ilikuwa ni kwa sababu hii ndipo wakaitwa “Khawarij”, lakini taratibu, wakajiwekea imani za msingi wao wenyewe na kuunda “chama” ambacho kilikuwa na mwelekeo wa kisiasa tu kwa kuanzia lakini 94


ambacho hatua kwa hatua kilichukua sura ya kikundi cha kidini, kikachukua mwelekeo wa kidini. Baadae hawa Khawarij waliingia kwenye shughuli kama kikundi cha propaganda chenye hamasa kubwa kama wafuasi wa madhehebu ya kidini. Hatimae walipata mawazo kwamba wamegundua mzizi wa upotofu wa kidunia, katika Uislamu, na walifikia uamuzi kwamba ‘Uthman, `Ali na Mu‘awiyah walikuwa wote katika makosa na dhambi. Waliamua kwamba lazima wafanye juhudi dhidi ya upotofu huu uliopatikana, na waliupa jina la “kuamrisha mema na kukataza maovu.” Hivyo madhehebu ya Khawarij yakapatikana chini ya bendera hii. Sasa, “kuamrisha mema na kukataza maovu” kunazo, kabla ya kitu chochote kingine, kanuni mbili za msingi; moja ni utambuzi wa kina na wa kielimu katika dini, na nyingine ni utambuzi wa kina wa katika namna ya kutenda. Kama hakuna elimu ya kina katika dini, kama tunavyojifunza katika hadithi, hasara tunayoipata katika kufanya hili itakuwa kubwa kuliko faida. Na utambuzi wa kina kwenye njia sahihi ya kutenda unategemea juu ya sharti mbili ambazo zinaitwa, katika sheria ya Kiislam, ihtimalu’t-ta’thir, yaani, uwezekano wa kitendo chenye athari, na ‘adamu tarattub-i’l-mafsadatin ‘alayh, yaani, kukosekana kwa sababu yoyote yenye kuleta uovu, na hii inaweza kupatikana tu kwa kutumia akili katika majukumu haya mawili. 5 T unachomaanisha hapa ni kwamba amr bi’l-ma‘ruf wa nahy ‘ani’l-munkar (kuamrisha mema na kukataza maovu) kama kusudio lake, inayo ile ma‘ruf (yale mema, yenye manufaa) yaenezwe na munkar (yale ambayo yenye karaha,na mabaya sana) yafutiliwe mbali. Hivyo lazima pawe na kuamrisha mema na kukataza maovu kwenye sehemu ambapo kuna uwezekano wa athari inayotakikana, kuweza kutokea. Kama tunajua kabisa kwamba hapatakuwa na athari, itaendeleaje kuwa ni wajibu? Zaidi ya hayo, kusudi la msingi wa kisheria (katika istilahi za Kiislam) la shughuli hii ni kwamba kile chenye heri, manufaa, kitekelezwe. Hivyo ni lazima itokee wazi katika hali ambapo hapatatokea madhara makubwa yoyote. Kinachohitajika katika shurti hizi mbili basi ni kuelewa kwa ufasaha juu y a namna ya utendaji wa sawa. Mtu ambaye ana upungufu katika elimu hii hawezi kutabiri kama matokeo yanayohitajika ya tendo hili yatafuatia au la. Hii ndio maana upotofu utokanao na ushauri usio wa kielimu kwenye kutenda mema utakuwa mkubwa zaidi kuliko man ufaa yake, kama vile tu ilivyosimuliwa kwenye hadithi. Katika mazingira ya wajibat zingine, haikuwekwa kama sharti kwamba lazima kuwepo na uwezekano wa kutoa matokeo mazuri, na kwamba kama upo uwezekano huo inakuwa ni faradhi, vinginevyo hapana. Ingawa kitu kizuri na chenye manufaa kinajionyesha katika kila wajibu, utambuzi wa manufaa hayo sio jukumu la watu. Haikusemwa juu ya sala, kwa mfano, kwamba kama unaiona ina faida basi Sali, na kama huoni, basi usisali. Wala kusemwa juu ya funga (saumu) kwamba kama ina uwezekano wa kuleta kitu chenye manufaa basi funga, na kama haina uwezekano huo basi usifunge (ni katika kufunga tu imeelezwa kwamba kama unaona kuna madhara ndani yake, basi usifunge), na vivyo hivyo katika hija au zaka au jihad hakuna masharti kama hayo. Lakini masharti kama hayo yanakuwepo katika suala la 5

95


Khawarij hawakuwa na elimu dini ya kina, wala utambuzi wa kina katika kitendo cha busara; walikuwa ni watu wa ujinga, waliokosa elimu ya kina. Kwa kweli walikataa aina yoyote ya elimu ya kina ya namna ya kutenda, kwa sababu walilielewa jukumu hili kuwa ni kama jambo la utii na walidai kwamba linapaswa kufanywa kibubusa.

*

*

*

kuamrisha mema na kukataza maovu, kwamba mtu lazima aangalie na kuona ni matokeo ya aina gani, na athari ya namna gani itakayopatikana, na ikiwa tendo lenyewe liko kwa maslahi ya Uislam na Waisla m au la. Hiyo ina maana kwamba utambuzi wa manufaa ni jukumu la watu hao hao wanaotekeleza wajibu huu. Kila mmoja anayo sehemu katika wajibu huu, lakini ni muhimu kwamba lazima aonyeshe sababu, akili na maarifa ya namna ya kutenda sawasawa na mazingatio k wenye manufaa yake, na haya mambo ya hapa mwishoni sio suala tu la wajubu wa kidini. Sharti hili, kwamba ni muhimu kutumia akili ya tendo lenye athari katika kuamrisha mema na kukataza maovu, linakubaliwa kwa pamoja na madhehebu zote za Kiislam isipokuwa Khawarij. Kwa sababu ya ugumu wao hasa, kutoshawishika na ushupavu wao, walisema kwanba kuamrisha mema na kukataza maovu ni wajibu kamili wa kidini; hauna sharti la uwezekano wa matokeo mazuri au kukosekana kwa athari zozote za upotofu; mtu lazima akae na kufikiria hilo. Ilikuwa ni kwa kutokana na imani hii kwamba walisimama na kuzitishia nchi wakijua kwamba watauawa na damu yao itapotea, na wakijua kwamba hakutapatikana matokeo mazuri kwenye uasi wao.

96


MSINGI WA MAONI YA KHAWARIJI

Msingi wa yafuatayo:

Ukhawariji umeundwa

kutokana

na

mambo

manne

a) Walimuona `Ali, ‘Uthman, Mu‘awiyah, wapiganaji katika vita vya Jamal na wale wote waliokubali sulhu, kama makafiri, isipokuwa wale waliopendekeza sulhu lakini baadae wakatubia. b) Waliwaona kama makafiri wale ambao hawakuamini uasi wa `Ali, ‘Uthman na wale wengine waliotajwa katika sehemu (a) hapo juu. c) Dini, kwao haikuwa ni imani nyoofu tu, bali kutekeleza kwa vitendo zile amri na kuepukana na makatazo ilikuwa pia ni sehemu ya imani. Dini ilikuwa ni kitu kipana kilichoundwa na imani na vitendo. d) Kulikuwa na umuhimu usiokuwa na masharti wa kumuasi gavana na kiongozi dhalimu. Waliamini kwamba “kuamrisha mema” na “kukataza maovu” hakuwi na masharti juu ya kitu chochote, na kwamba kwa hali yoyote hii amri ya Mungu lazima itekelezwe. Kulingana na maoni haya, watu hawa walianza kuwepo kwa kutokana na kutambua kwamba watu wote duniani walikuwa makafiri, ambao damu yao haikuwa na thamani na ambao wote walikuwa na hatia ya kwenda Motoni.

*

*

97

*


WALICHOAMINI KUHUSU UKHALIFA Wazo pekee la Khawariji ambalo linaweza kutafsiriwa vizuri na wanafikra wa kimamboleo wa siku hizi ni ile nadharia yao kuhusu ukhalifa. Walikuwa na kiasi fulani cha dhana ya demokrasia juu yake, na wakasema kwamba khalifa lazima achaguliwe kwa uchaguzi huru, na mtu mwenye kustahiki sana alikuwa ni yule aliyekuwa na sifa kama vile imani na uchamungu vinavyohusika. Anaweza kutoka kwa Maquraishi au la, kutoka kwenye kabila mashuhuri na maarufu, au kutoka kwenye kabila lisilo na umaarufu na la nyuma, la Kiarabu au lisilo la Kiarabu. Kama, baada ya kuchaguliwa kwake na baada ya kila mtu kutoa kiapo cha utii kwake, alichukua hatua kwenye mwelekeo ulio kinyume na maslahi ya ummah wa Kiislamu, aondolewe kwenye ukhalifa, na kama akikataa, wapigane naye mpaka auawe. Katika suala la ukhalifa walichukua nafasi kinyume na ile ya Shi‘ah, amabao wanasema kwamba ni cheo cha ki-mungu na kwamba khalifa anaweza tu kuwa mtu aliyeteuliwa na Mwenyezi Mungu. Walikuwa pia wanapingana na Sunni, ambao wanasema khalifa anatokana na Quraishi na ambao wanashikilia ile kanuni ya “innama’-a’immatu min quraishin” - “hakika viongozi wanatokana na Quraish” Ni dhahiri wazo lao kuhusu ukhalifa halikuwa kitu walicho kifikia pale walipoanza kutokea. Kwani, kwa mujibu wa wito wao maarufu wa “la hukma illa li llah” – “hakuna mamlaka ila ya Allah swt”unavyotuambia, na pia kulingana na tunavyookoteza kutoka kwenye Nahju’l-balaghah6 , waliamini, hapo mwanzoni, kwamba watu na jamii hawakuhitaji kiongozi au serikali, na kwamba watu watumie Kitabu cha Mwenyezi Mungu katika utekelezaji wao wenyewe.

6

Tazama semi na. 40, na pia sherehe ya Ibn Abi’l-Hadid, juz. 2, uk. 308.

98


Hata hivyo, baadae, waligeuka kwenye imani hii na kwa uimara sana wakala kiapo cha utii kwa ‘Abdullah Ibn al-Wahab7 WALICHOKIAMINI KUHUSU MAKHALIFA Waliutambua ule ukhalifa wa Abu Bakr na ‘Umar kuwa ni wa haki, kwa sababu waliamini kwamba watu hawa wawili walichaguliwa kihalali na kwamba hawakupotoka kutoka kwenye njia ya maslahi bora wala hawakutenda lolote dhidi ya maslahi haya mazuri. Pia walitambua uchaguzi wa ‘Uthman na `Ali kuwa ni halali; hata hivyo walisema kwamba mwishoni mwa mwaka wa sita wa ukhalifa wake, ‘Uthman alibadilisha mwelekeo na akapuuza maslahi bora ya Waislamu. Hivyo alipaswa aondolewe kwenye ukhalifa, lakini kwa vile aliendelea katika madaraka aliuawa kama kafiri na kuuliwa kwake kulikuwa ni wajibu wa kidini. Ama kuhusu `Ali, kwa vile alikubali sulhu na hatimae hakutubia, aliuawa kama kafiri, na kuuliwa kwake kulikuwa ni wajibu wa kidini. Hivyo waliukana ukhalifa wa Uthman baada ya mwaka wake wa saba, na ule wa `Ali baada ya sulhu.8 Waliwachukia pia makhalifa wote waliobakia, na walikuwa siku zote kwenye vita nao. *

*

*

KUANGUKA KWA KHAWARIJI Kundi hili lilitokea kuelekea mwishoni mwa mwongo wa nne wa karne ya kwanza Hijiria kama matokeo ya kipande hatari cha tafsiri mbaya, na kabla ya karne moja na nusu haijakwisha, kama matokeo ya mpagao wa ujasiri wa kutojali chochote na uzembe, walikuwa ni shabaha ya kuandamwa na makhalifa, ambayo iliishia kwa uangamizwaji na uteketezwaji wa madhehebu yao wenyewe, na mwanzoni mwa utawala wa Bani ‘Abbasi walikuwa wamekwisha toweka kabisa. Ilikuwa ni mantiki yao isiyokuwa na huruma na moyo, ukatili na ukali wa tabia 7 8

Tazama Ibn Kathir, al-Kamil fi’t-tarikh. Tazama ash-Shahrastani, al-Milal wa’n-nihal, Cairo, 1961.

99


zao, kutokupatana kwa mienendo yao na maisha halisi, na, mwishowe, haraka haraka zao (ambazo pia zilivunja taqiyah [kugeuza ionekane vingine]9 katika hali halisi na maana yake) iliyosababisha kuangamia na kuteketea kwao. Madhehebu ya Khawariji haikuwa ni yenye kuweza kudumu kwa hali yoyote ile, lakini athari itokanayo nayo imebakia; mawazo na imani za Khawarij zimekuwa na athari kwenye madhehebu nyingine za Kiislam. Hata leo, Nahrawan wanapatikana kwa wingi, na, kama vile katika zama na wakati wa `Ali, hawa ndio hatari sana katika maadui wa ndani wa Uislam. Kama ambavyo siku zote kumekuwa , na siku zote kutakuwa na akina Mu ‘wiyah na kina ‘Amr ibn as-As, ambao watatumia kuwepo kwa “Nahrawani” wakati utapofaa, hata kama watahesabiwa kama maadui zao. *

*

*

JE, NI KAULIMBIU TU? Kugeuza mjadala wa Ukhawariji na Khawariji kuwa mjadala juu ya madhehebu ya kidini hakuna maana na hakuna sababu, kwani hakuna madhehebu ya kidini kama hiyo hapa duniani sasa. Hata hivyo, mjadala kuhusu Khawariji na ukweli wa kile walichokifanya una maelekezo kwa vyovyote vile, kwetu sisi na kwa jamii, kwa sababu, ingawa madhehebu ya Khawariji imetoweka, mtazamo wao haukufa. Mtazamo wa Ukhawariji umepandikizwa katika kampeni za wengi wetu. Nitaanza na utangulizi. Inawezekana kwamba madhehebu nyingi zinaweza kufa kwa namna kaulimbiu yao inavyohusika, lakini hai katika mtazamo, kama vile kinyume chake kinavyoweza kutokea pia: itikadi inaweza kuwa hai kama kaulimbiu, lakini ikawa imekufa kabisa katika mwelekeo. Hivyo inawezekana kuwa mtu mmoja au watu kadhaa wanaweza kuhesabiwa kama wafuasi na waumini wa madhehebu fulani kwa jina, lakini wasiwe wafuasi wa madhehebu hiyo katika mioyo, na kinyume chake, yaani, baadhi ya watu wanaweza kufuata madhehebu 9

Juu ya kanuni hii, tazama kitabu Shi‘ite Islam cha ‘Allamah S.M.H.Tabataba’I (tahsir ya S.H.Nasr), uk.223-225.

100


fulani katika mwelekeo ingawa hawaikubali kaulimbiu na wito wa madhehebu ile. Kutoa mfano unaofahamika kwa wote, mwanzoni kabisa, baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.w.), Waislamu waligawanyika katika makundi mawili, Sunni na Shi‘ah; Sunni wanaamini kaulimbiu moja na mfumo mmoja wa imani, na Shi‘ah katika nyingine. Shi‘ah wanasema kwamba khalifa mara tu baada ya Mtume (s.a.w.w.) ni `Ali, na kwamba alimteua `Ali kwenye ukhalifa na kama mshikamakamu wake kwa amri ya Mwenyezi Mungu. Nafasi hii kwa hiyo ni ya `Ali kwa haki maalum baada ya Mtume (s.a.w.w.). Lakini Sunni wanasema kwamba kwa kadiri sheria ya Kiislam inavyohusika, haina masharti maalum katika jambo la ukhalifa au Uimamu, bali jambo la kuchagua kiongozi limeachwa juu ya watu wenyewe. Kinachoweza kusemwa sana sana ni kwamba nafasi hiyo lazima itolewe miongoni mwa Maquraishi. Mashi‘ah wanazo baadhi ya shutma za kutoa juu ya masahaba wengi wa Mtume (s.a.w.w.) ambao wanahesabiwa kama watu wakubwa, watu wa kusifika na maarufu, ambapo Sunni wanachukua msimamo unaopingana kabisa na ule wa Shi‘ah katika jambo hili; wanamuona kila mtu aliyeitwa “sabaha” na tofauti kubwa sana, na ya kustaajabisha mno. Wanasema kwamba masahaba wote wa Mtume (s.a.w.w.) walikuwa ni watu wakweli na waaminifu. Sababu ya kuweko kwa Uislamu wa Kishi‘ah ni kufanya kupitia ukosoaji, utafiti, kuleta upingamizi na usahihi,10 sababu ya kuweko kwa Uislamu wa Sunni ni kufanya kazi kupitia kupata ufumbuzi unaofaa sana, uhalalishaji baada ya tendo na kuamini majaaliwa.11 10

Cha asili kinasomeka: “kutafuta unywele ndani ya mtindi.” (tr.) Haya maandishi yanasomeka,kihalisi, “insha’Allah swt alikuwa ni paka”. Huu ni ukumbusho wa hadithi maarufu ya mulla mcha-mungu na msomi ambaye joho lake liliguswa na mbwa, hivyo kulifanya linajisike (au, kulingana na maelezo mengine, aliambiwa baada ya kuwa amekunywa kwenye bakuli lake kwamba lilikuwa limeguswa na mbwa – matokeo ni yaleyale), na ambaye papo hapo akasema: “insha’Allah swt huyo alikuwa ni paka” Maana ni kwamba huyo paka anachukuliwa kama sio mnyama najisi. 11

101


Katika siku na zama hizi tunamoishi, inatutosha sisi kumtambua mtu kuwa ni Shi‘ah yule anayesema: “`Ali ndiye khalifa mara tu baada ya Mtume”, bila ya kuhitaji kitu kingine chochote zaidi toka kwake? Bila ya kujali ni mtazamo gani au ni aina gani ya fikra anayoweza kuwa nayo? Hata hivyo, kama tutarudi mwanzo wa kufika kwa Uislamu, tutaikuta namna maalum ya fikra ambayo itakuwa ndio namna ya fikra ya Uislam wa Kishi’a, na itakuwa ni wale tu waliofikiri kwa namna hiyo ambao wangeweza kwa uwazi kabisa kuukubali ushikamakamu wa Mtume (s.a.w.w.) kwamba ulikuwa ni wa `Ali bila ya kuwepo sababu ya shaka au kusitasita. Uliopinga mtazamo huu na namna hii ya fikra ulikuwa ni mtazamo na namna nyingine ya fikra ambayo, kwa njia ya uhalalishaji, maelezo au tafsiri, walipuuza ushikamakamu wa Mtume wakati wakiwa na imani kamili juu yake. Kwa kweli, utengano huu wa Kiislamu uliibukia kutoka hapa, kwani kundi moja, ambalo walikuwa, kwa kweli, ndio wengi, waliangalia mwelekeo wa juujuu tu, wakiwa hawana macho-makali ya kutosha au kupenyeza kufikia kina cha ukweli wa kila hali halisi. Waliona kile kilichokuwa wazi zaidi na kupata ufumbuzi unaofaa zaidi. Walisema kwamba baadhi ya watu wakubwa, masahaba na wazee, wale ambao waliutumikia Uislamu kwa muda mrefu, walitumia njia fulani, na haiwezi kusemwa kwamba walikosea. Lakini kundi jingine, ambalo waliokuwa ndio wachache, lilisema wakati huohuo kwamba litamheshimu mtu yeyote anayeheshimu haki; hata hivyo, pale walipoona kwamba misingi ya Uislamu imevunjwa mikononi mwa watu hawa hawa ambao wameutumikia Uislamu kwa muda mrefu, hawakuweza tena kuwaheshimu zaidi. Walisema wao ni wafuasi wa kanuni za Uislamu, sio wafuasi wa watu mashuhuri wa Uislamu. Ushi‘ah ulipatikana kwa mtazamo huu. Wakati, katika historia ya Kiislamu, tunapofuata nyayo za Salman alFarisi, Abu Dharr al-Ghifari, al-Miqdad al-Kindi, Ammar ibn Yasir na watu kama hao na tukatazama ni nini kilichowashawishi kujikusanya 102


karibu na `Ali na kuwaacha walio wengi, tunaona kwamba wao walikuwa watu waadilifu, waliojua misingi –kwamba wote waliijua dini na kuitekeleza kivitendo. Walisema kwamba hawataachia kuona na kuelewa kwao kwenye mikono ya wengine, ili kwamba pale watu hawa watakapofanya makosa na wao wenyewe pia watakuwa wamefanya makosa. Kwa ukweli msimamo wa watu hawa ulikuwa ni msimamo ambao juu yake kanuni na haki zimetawala, sio ubinafsi na umashuhuri. Mmoja wa masahaba wa `Ali alishikwa na shaka kubwa wakati wa vita vya Jamal. Aliangalia mwenyewe huku na huku, na akaona upande mmoja `Ali na watu mashuhuri katika Uislamu waliojikusanya karibu naye wakishambulia kwa panga zao; na ule upande mwingine alimuona mke wa Mtume (s.a.w.w.), ‘A’ishah, ambaye juu yake Qur’an imesema: ‫جهُ اُمَهاتُهم‬ ُ ‫ واَزوَا‬-Na wake zake ni kama mama zao. Katika waliokusanyika kumzunguka ‘A’ishah alimuona Talhah, mmoja kati ya watu wa mwanzo kuingia katika Uislamu, mtu mwenye rekodi nzuri huko nyuma, mpiganaji hodari katika uwanja wa vita kwa ajili ya Uislamu, mtu ambaye amefanya kazi nzuri ya thamani kwa Uislamu; na akamuona az-Zubayr, pia, mtu mwenye rekodi nzuri zaidi huko nyuma kuliko Talhah, ambaye alikuwa pia miongoni mwa wale ambao walikusanyika nyumbani kwa `Ali ile siku ya Saqifa12 Bwana huyu maskini alikuwa katika hali ya utatanishi mkubwa. Ni nini kilikuwa kinatokea! Hivi `Ali, Talhah na az-Zubayr sio miongoni mwa watu wa mwanzo katika Uislamu, watu waliojitolea sana, ngome imara za Uislamu? Sasa wanapigana uso kwa uso. Ni yupi aliye karibu zaidi na haki? Ni nini kifanyike katika mgongano huu? Lakini angalia: mtu huyu kamwe asilaumiwa sana katika kukanganyikiwa kwake huku. Pengine kama tungejikuta kwenye hali kama hiyo hiyo ambayo amejikuta yeye, umaarufu wa Talhah na azZubayr ungeweza pia kuzuzua macho yetu.

12

Kwa taarifa juu ya watu hawa na matukio tazama: The Origins and Early Development of Shi’ah Islam, cha S.H.M. Jafri (London1979), hasa mlango wa 2&4. (tr.)

103


Sasa kwa kuwa tunamuona `Ali na ‘Ammar, Uways al-Qarani na wengineo uso kwa uso na ‘A’ishah na az-Zubayr na Talhah, hatuhisi kusita hata kidogo, kwani tunaliona hili kundi la pili kama watu wenye sura za wahalifu, yaani, athari za uovu na usaliti zinadhihirika kwenye nyuso zao; na tunapoziangalia nyuso na tabia zao tunakisia kwamba wao ni watu wa Motoni. Lakini kama tungeishi katika nyakati zile, na tukajua maisha yao yaliyopita kwa karibu sana, pengine tusingeweza kuwa na kinga ya wasiwasi. Leo, wakati tunajua kwamba hili kundi la kwanza lilikuwa kwa ajili ya haki na hili la pili kwa ajili ya upotofu, ni kwa sababu tumekuja kumjua `Ali na ‘Ammar, kwa upande mmoja, na az-Zubayr, Talhah na ‘A’ishah, kwa upande mwingine, kama matokeo ya kupita kwa historia na ufafanuzi wa mambo, na katika muktadha hauu tumeweza kuamua kwa usahihi. Au, katika kiwango cho chote, kama sisi sio watafiti au wanafunzi wa historia, tumefundwa dhana hii kwamba mambo yalikuwa hivyi, kutoka utotoni mwetu. Lakini katika siku hizo, hakuna lolote kati ya mambo haya lililokuwepo. Hata hivyo, mtu huyu aliweza kuja kwa Amir al-mu’minin na kusema: “Inawezekana kwamba Talhah na az-Zubayr na ‘A’ishah wamekusanyika pamoja kwa ajili ya upotofu? Ni vipi watu maarufu kama hawa masahaba wakubwa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu wakosee, na kufuata njia ya upotofu? Kitu kama hicho kinawezekana kweli?” Katika jibu lake, `Ali alisema kitu ambacho Taha Husayn, mwanazuoni na mwandishi wa Misri amesema kwamba hakuna kitu chenye nguvu zaidi au kikubwa zaidi ya hicho kimesemwa. Aliandika kwamba baada ya wahy (ufunuo) kukoma na ule wito kutoka mbinguni kufikia mwisho, maneno yenye umashuhuri kama maneno haya hayajasikika. 13

13

Katika `Ali wa banuh (`Ali na wanae), uk. 40. 104


`Ali alisema: “Ni wewe uliyedanganyika; haki imekuwa potofu kwako. Haki na upotofu havitajulikana kwa kipimo cha uwezo na umaarufu wa watu. Sio sahihi kwamba upime kwanza umaarufu wa watu, na kisha upime haki na upotufu kutokana na vipimo hivi: hii ni kweli kwa sababu inapafikiana na hili, na lile ni uongo kwa sababu haliafikiani na hili. Hapana, watu wasifanywe vigezo vya haki na upotofu. Ni haki na upotofu ndio viwe vipimo vya watu na umaarufu wao.” Hii ina maana kwamba mtu mwenye kujua haki na upotofu, asiwe mjuzi wa watu na umaarufu; mtu apime watu, wawe ni watu maarufu sana au kidogo, kulingana na haki – kama wanalingana nayo, basi kubali umaarufu wao, la sivyo, basi achana nao. Basi hakuna swali la kwamba Talhah, az-Zubayr na ‘A’ishah wako kwenye upotofu au laa. Hapa `Ali anaonyesha ukweli wenyewe kama kigezo cha haki, na mtazamo wa Uislamu wa Kishi’a si mwingine mbali na huu. Kwa kweli, madhehebu ya Shi‘ah yametokana na wepesi maalum wa kuelewa na kukata shauri na kutoa umuhimu kwenye kanuni, sio kutoka kwa watu na watu. Ni dhahiri kwamba Shi‘ah ndio waumini wa kwanza na wavunja-masanamu. Baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.w.),`Ali alikuwa na umri miaka thelathini na tatu na kikundi kidogo pungufu ya idadi ya vidole vya mikono ya mtu mmoja; waliompinga ni watu wazima wa miaka sitini wenye kundi kubwa la wingi wa watu. Mantiki ya wengi ilikuwa ni kwamba hii ndio iliyokuwa njia ya viongozi na masheikh, na hawafanyi makosa, hivyo njia yao ni lazima ifuatwe. Mantiki ya wengi ilikuwa ni kwamba kile kisichokosea ndio haki, wazee lazima wajilinganishe wenyewe na haki. Na kwa sababu hii inaweza kueleweka ni wengi kiasi gani ambao kaulimbiu yao ni ile kaulimbiu ya Uislamu wa Kishi’ah, lakini ambao mtazamo wao sio mtazamo wa Uislam wa Kishi’ah. Njia ya Ushi’ah ni kama mtazamo wake tu: utambuzi wa haki na kuitekeleza. Na moja ya athari zake kubwa ni mvuto na kingamizo. Sio 105


kila mvuto au kila kingamizo – tumesema kwamba mvuto wakati mwingine ni mvuto wa kwenye upotofu, uovu, na uhalifu, na kingamizo wakati mwingine ni kikwazo cha kwenye haki na maadili ya kiutu – bali mvuto na kingamizo la mfano ule mvuto na kingamizo la `Ali. Kwa sababu Shi’ah wa kweli ni nakala ya tabia ya `Ali; Shi’ah huyo lazima pia, awe kama `Ali, awe na zile pande mbili za tabia zake. Utambulisho huu ulikuwa ili kwamba tuweze kujua kwamba madhehebu ya dini inaweza kuwa imekufa, lakini mtazamo wake ukawa unaishi miongoni mwa watu wengine ambao inavyoonekana sio wafuasi wa madhehebu ile bali ambao wenyewe wanadhani ni wenye kuipinga. Madhehebu ya Khawariji imekufa, hii ni kusema kwamba leo hii, duniani humu, hakuna kikundi kinachoweza kuonekana chenye jina la Khawariji ambacho baadhi ya watu, kwa jina hilo wanakifuata; lakini je, huo mtazamo wa Khawariji umekufa pia? Mtazamo huu haukujipandikiza wenyewe, kwa mfano, (Mungu aepushilie mbali), miongoni mwetu, hususan miongoni mwa sisi ambao, kusema kweli, tunajifanya ni wacha-mungu? Hili ni jambo ambalo lazima lichunguzwe peke yake. Ikiwa tunaweza kwa kweli kutambua mtazamo wa Khawarij, tunaweza pengine kujibu swali hili. Hii, kwa hakika, ndio faida ya mjadala wetu kuhusu Khawariji. Lazima tujue ni kwa nini `Ali “aliwakingamiza”, hiyo ni kusema, kwa nini mvuto wake haukuwavuta, bali, kinyume chake, nguvu yake ya kingamizo iliwasukumia mbali. Ni hakika, kama tutakavyoona baadae, kwamba sio vipengele vyote vya kiroho vilivyokuwa na athari katika utu wa Khawariji na muundo wa namna yao ya fikra vilikuwa viwe kama ndio sababu ya shinikizo na utawala wa nguvu ya mvuto wa `Ali. Sifa nyingi nzuri za kung’ara na hoja zenye nguvu nazo pia zinapatikana katika namna yao ya kufikiri, ambazo, kama zisingekuwa pale pamoja na mlolongo wa madoa meusi, zingeweza kuwa sababu ya uwezo na athari za nguvu ya mvuto wa `Ali. Lakini ule upande mweusi wa mtazamo wao ulikuwa na nguvu kiasi kwamba walichukua nafasi yao katika safu za maadui wa `Ali. * * * 106


BUSARA YA DEMOKRASIA YA `Ali `Ali alishughulika na Khawariji kwa wema wa hali ya juu sana na demokrasia. Alikuwa ndiye khalifa na wao walikuwa raia zake; kila aina ya kitendo cha adhabu kilikuwa kwenye mamlaka yake, lakini hakuwaweka jela, wala hakuwachapa mijeledi; hakupunguza hata mgao wao kutoka kwenye hazina (baytu’l-mal). Aliwafanyia kama alivyowafanyia watu wengine. Jambo hili halibanduki katika historia ya maisha ya `Ali, lakini ni jambo ambalo kwamba kuna mifano michache katika dunia hii. Kila mahali wao walikuwa huru kutoa maoni yao, naye `Ali na masahaba wake waliwapinga kwa uhuru kabisa kwa maoni yao wenyewe na wakazungumza nao. Pande zote mbili ziliwasilisha mantiki zao, na kupambana na mantiki za wapinzani wao. Pengine kiwango kama hicho cha uhuru hakina mfano uliowahi kutokea hapa duniani, ambamo serikali inawatendea wapinzani wake kwa kiwango cha demokrasia kama hicho. Walikuja ndani ya Misikiti na kuvuruga mazungumzo na khutba za `Ali. Siku moja, `Ali alikuwa akihutubia kwenye mimbar alipokuja mtu mbele na kuuliza swali, na `Ali akatoa jibu la papo kwa papo. Khawariji mmoja aliyekuwa miongoni mwa watu hao akasema kwa sauti: “Mwenyezi Mungu amuue mtu huyu; jinsi gani alivyokuwa mtu mwenye elimu!” Wale wengine walitaka kumzuia, lakini `Ali aliwaamuru wamwachie, akisema: “Ni mimi tu aliyenitukana.” Khawariji walikuwa hawasali nyuma ya `Ali katika sala za jamaa kwa sababu walimuona kama mtu asiyeamini, lakini walikwenda Msikitini na wakakataa kumwacha `Ali mwenyewe, wakati mwingine wakimsumbua kwa makusudi. Siku moja, `Ali alikuwa amesimama ili apate kusali na watu walikuwa wamesimama nyuma yake, wakati mmoja wa Khawariji ambaye jina lake lilikuwa Ibn al-Kawwa’ alipopiga kelele, na akasoma aya ya Qur’ani kama dokezo kwa `Ali:

107


               Aya hii aliambiwa Mtume (s.a.w.w.): Na kwa yakini yamefunuliwa kwako na kwa waliokuwa kabla yako: Bila shaka ukimshirikisha Mwenyezi Mungu a’amali zako zitaanguka, na lazima utakuwa miongoni mwa wenye kukhasiri. (az-Zumar, 39:65) Ibn al-Kawwa’ alitaka kupiga kijembe kuhusu `Ali kwa kusoma aya hii kwamba: “Ndio, tunaijua historia yako iliyopita katika Uislamu! Kwanza ulikuwa mu’min, Mtume (s.a.w.w) akakuchagua kama ndugu yake, kujitolea kwako kuling’ara ule usiku wa Mtume (s.a.w.w.) alipotoroka kutoka Makkah (laylatu’l-mabit) ulipolala kwenye nafasi ya Mtume kitandani kwake, ulijitokeza mbele kama chambo cha panga. Kweli kazi yako kwa Uislamu haikataliki. Lakini Mola pia amemwambia Mtume Wake: ‘Kama utawashirikisha (wengine pamoja na Mungu) kazi yako itakuwa bure.’ Sasa kwa kuwa umekuwa usiyeamini umefuta kabisa matendo yako yaliyopita.” `Ali angefanya nini, akiwa amekabiliwa na hili, kwa sauti ya mtu huyu ikisoma Qur’ani kwa kukemea? Alinyamaza kimya mpaka mtu huyu alipofikia mwisho wa aya; na alipomaliza, `Ali akaendelea na sala ile. Kisha Ibn al-Kawwa’ akairudia tena ile aya, na wakati huo`Ali alinyamaza kimya tena. Alikaa kimya kwa sababu ni amri ya Qur’ani kwamba:         

108


Na isomwapo Qur’ani, isikilizeni na mnyamaze ili mpate kurehemiwa. (al-A ‘raf, 7:204) Na huu ndio ushahidi wa lile suala la kwamba wakati kiongozi wa sala anaposoma Qur’ani, waumini lazima wanyamaze kimya na kusikiliza. Baada ya kuwa amerudia aya hii mara nyingi, akitaka kuvuruga ile sala, `Ali akasoma aya hii ifuatayo:             Basi subiri. Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya haki. Wala wasikupaparishe hao wasiokuwa na yakini. (ar-Rum, 30:60) Kisha hakumsikiliza tena na akaendelea na sala yake.14

*

*

*

MAASI NA UPINZANI WA KHAWARIJI Mwanzoni, hawa Khawariji walikuwa wenye amani,na walitosheka wenyewe kwa kule tu kushutumu na kuongea waziwazi. Mwenendo wa `Ali juu yao ulikuwa kama tulivyoona kabla, yaani, kamwe hakuwasababishia matatizo, hata angalau kuwakata malipo yao kutoka hazina (baytu’l-mal). Hata hivyo, walivyoanza kukata tamaa kuhusu kutotubia kwa `Ali, juhudi zao zilianza kubadilika kidogo kidogo. Waliamua kuleta mapinduzi, hivyo walikusanyika ndani ya nyumba ya mmoja wa ndugu zao, aliyetoa hotuba yenye ushari na uchochezi ambayo ndani yake amewataka marafiki zake kuasi kwa jina la “kuamrisha mema na kukataza maovu.” Alisema (baada ya kumshukuru Mungu): 14

Sharh, Ibn Abi’l-Hadid, juz.6, uk.311.

109


Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba haina maana kwa kikundi ambacho kinamuamini Mola Mwenye Rehma na ambacho kinafuata amri za Qur’an, kwamba dunia ionekane ya thamani kwao kuliko “kuamrisha mema na kukataza maovu” na kusema kweli, ingawa (shughuli) hizi zinaweza kuleta hasara na kusababisha hatari; kwani kila mmoja anayepata hasara na hatari katika dunia hii atalipwa Siku ya Qiyamah kwa baraka za Mola na pepo ya milele. Enyi ndugu zangu! Natuondokeni kwenye mji huu ambamo dhulma ndimo inamokaa (na twende) kwenye sehemu za milimani au miji mingine ili tuweze kuchukua msimamo dhidi ya bid’a hizi za upotofu na kuziwekea kikomo kabisa. Kwa hotuba hii ya hamasa na kali, wakawa wakali zaidi na wakaondoka kwenye sehemu ile kujaribu kuleta uasi na mapinduzi.Walitishia usalama wa barabara kuu na wakaingia kwenye ujambazi na uchochezi wa maasi. Nia yao ilikuwa ni kuidhoofisha serikali kwa njia hii, na kuuangusha utawala uliokuwepo wakati huo. Sasa haukuwa tena wakati wa kuwaacha huru, kwani halikuwa suala la maelezo ya imani, bali ya hujuma dhidi ya usalama wa jamii na uasi wa kijeshi dhidi ya serikali halali. Hivyo `Ali aliwafuatilia na akakutana nao uso kwa uso kwenye kingo za mto Nahrawan. Alitoa hotuba ambayo kwayo aliwashauri na akawapa ushahidi usiopingika. Kisha akaiweka bendera ya imani ya haki mikononi mwa Abu Ayyub alAnsari kama ishara kwamba kila mmoja atakayekusanyika karibu nayo alikuwa mu’min wa kweli. Katika watu elfu kumi na mbili, elfu nane waligeuka kutoka kwenye Ukhawariji ambapo wale waliobakia walionyesha ukaidi wao.Walipigwa vibaya sana, na mbali na kijikundi kidogo (kilichosalia) hakuna aliyebakia.

*

*

110

*


SIFA BAINIFU ZA KHAWARIJI Msimamo wa Khawariji ulikuwa wa kipekee kabisa. Walikuwa mchanganyiko wa wabaya na wazuri, na, kwa jumla, walikuwa kiasi cha kuchukua nafasi yao mwishoni moingoni mwa maadui wa `Ali. Haiba ya `Ali “iliwakingamiza”, “haikuwavutia” wao. Tutataja vyote; vipengele bayana na vizuri na (vipengele) hasi na vipengele vibaya vya nafsi zao ambavyo, wakati vikichanganywa, viliwafanya watu hatari na wa kutisha pia. 1.

Walikuwa na msimamo wa juhudi na kujitoa mhanga, na walipambana kijasiri katika imani zao na mawazo yao. Katika historia ya Khawariji, tunawakuta watu ambao sio wabinafsi kabisa ambao wana watu wachache sana wa kulingana nao katika historia ya mwanadamu, na uungwana wao na kujitolea kwao kulikuwa ni maisha ya ushujaa wao na madaraka yao.

Ibn ‘Abdu Rabbih alisema juu yao: “Kati ya madhehebu zote, hakuna iliyoshawishika zaidi au iliyotumia juhudi kama Khawariji, na pia hakuna waliokuwa tayari kufa kuliko wao. Mmoja wao aliwahi kupigwa kwa mkuki na mkuki huo ukawa umetumbukia sana mwilini mwake. Pamoja na hayo, alikmbia kumuelekea muuaji wake akisema: ‘Ewe Mola! Ninaharakishia kuja kwako ili uweze kuridhika.’ Mu‘awiyah alituma mtu kumfuata mwanae ambaye alikuwa Khawariji ili amrudishe, lakini baba huyu hakuweza kumfanya mwanae abadili mawazo yake. Mwishowe, akasema: “Mwanangu, nitakwenda kumleta mwanao mchanga ili kumuona kwako pamoja na hisia zako za ubaba kunaweza kukurudisha kwenye fahamu zako na kukulazimisha kuliacha hili.” Yule mwana akajibu: “Namuapa Mwenyezi Mungu, ninayo shauku zaidi ya mapigo makali ya panga kuliko shauku na mwanangu!”

111


2. Walikuwa watu wa ibada na utii, walitumia nyakati zao za usiku katika sala na hawakuwa na matamanio na dunia hii na vivutio vyake. Wakati `Ali alipomtuma Ibn ‘Abbas kuwaonya watu wa vita vya Nahrawan, alirudi na kuwaelezea kama watu elfu kumi na mbili ambao vipaji vya nyuso zao vimekuwa sugu kwa ziada ya kusujudu, ambao mikono yao imekuwa migumu kama miguu ya ngamia kutokana na kuminywa sana kwenye ardhi kavu inayochoma na kutokana na kukanyaga udongo mbele ya Mola wao, ambao mashati yao yamechanika na kwisha mpaka kwenye ngozi zao, lakini ambao walikuwa hawayumbi na wamejizatiti. Hawa Khawariji walikuwa kwa kweli ni watiifu kwenye kanuni na matendo ya wazi ya Uislamu; walikuwa hawaweki mikono yao juu ya kitu walichokiona kama ni dhambi. Walikuwa na taratibu na kawaida zao wenyewe, na kamwe hawakuzichanganya hizi na taratibu zilizo kinyume na zao wenyewe; walionyesha kukerwa kwao na mtu yoyote aliyechafuliwa na dhambi. Ziyad ibn Abih aliuwa mmoja wao na akatuma aletewe mtumwa wa mtu yule na akaulizia kwake alikuwa ni mtu wa namna gani. Yule mtumwa akasema kwamba hajamletea kamwe chakula wakati wa mchana, wala kumtandikia kitanda chake wakati wa usiku; wakati wa mchana alifunga na alitumia nyakati za usiku katika sala. Kila walipoweka hatua zao, walirejea nyuma kwenye imani zao na walikuwa watiifu kwenye vitendo vyao vyote. Wangeweza kuuwa ili kuendeleza imani zao. `Ali (a.s.) alisema hivi juu yao: Msiuwe Khawariji yeyote baada yangu, kwa sababu mtu anayetafuta ukweli na akakosea hawi sawa na anayetafuta upotofu na akaupata15

15

Nahju’l-balaghah,hotuba no. 60.

112


Alikuwa na maana kwamba walikuwa tofauti na wale walio karibu na Mu’awiyah, kwani waliitaka haki, lakini wakaangukia kwenye makosa, ambapo wale karibu na Mu’awiyah walikuwa walaghai toka mwanzo ambao mwendo wao ulikuwa ule wa upotofu. Hivyo kama walikuwa wauwe baada ya `Ali kuondoka ingekuwa ni kwa faida ya Mu’awiyah aliyekuwa mbaya zaidi na hatari sana kuliko wao. Ni muhimu, kabla hatujaendelea kuelezea sifa nyinginezo za hawa Khawariji, kukumbuka jambo moja, kwa vile tunazungumzia kuhusu kujisingizia kwao kwenye ibada, uchamungu na kujinyima. Moja ya mambo ya kushangaza, la kipekee na lisilo la kawaida katika historia ya maisha ya `Ali, ambalo mfano wake hauwezi kupatikana, ni ujasiri wake na kusimama kishujaa anapopigana dhidi ya wachaji wasiokubali mambo mapya na wenye kiburi. Mbele ya watu walioshikilia, waliojipamba wenyewe, na ibada ya nje na ambao nyuso zao zinajisingizia haki, ambao nguo zao zimechanika na ambao walikuwa ni waabudiaji wenye weledi, `Ali alichomoa upanga wake na akawawajibisha wote kwenye ncha yake kali. Kwa hakika, kama tungekuwa kwenye nafasi ya masahaba zake na tukawa tumeona nyuso za watu hawa, hisia zetu zingeguswa, na tungemlalamikia `Ali kuhusu kuchomoa panga dhidi ya watu kama hao. Hii hadithi ya hawa Khawariji ni moja kati ya masomo yenye kuadilisha sana kwa historia ya Ushi‘a kipekee, na kwa ulimwengu wa Kiislamu kwa jumla. `Ali mwenyewe alikuwa ana habari juu ya umuhimu na upekee wa hali halisi ya hatua gani alizochukua katika mazingira haya, kama alivyoeleza aliposema: َ‫ وَاْشْتَ َد كَلَبَُها‬،‫غيْهَبُ َه ا‬ َ َ‫ن مَا ج‬ ْ َ‫غيْ ِري بَعْدَ أ‬ َ ًٌُ‫علَيْهاَ أحَد‬ َ ‫ َوَلمْ يَكُنْ لِيَجْتَرىَء‬،‫فَإنِى فَقَاْتُ عَيْنَ الْفتْنَة‬

113


Nimelikoboa jicho la fitna. Hakuna ambaye angeweza kujasiri kufanya hivyo isipokuwqa mimi wakati msiba wake ulipoikumba, na ghadhabu yake imekuwa kali (kama mbwa mwenye kichaa). 16 Amir al-mu’minin (a.s) hapa anatoa maelezo aina mbili ya kuvutia. Moja ni ile ya maelezo ya “huzuni”,/msiba ambayo inasababisha mashaka na wasiwasi. Tabia ya ule utakatifu wa nje na uchamungu wa hawa Khawariji ulikuwa wa namna kwamba kila mu’min mwenye imani nzito alikuwa tena na wasiwasi; na kwa maana hii hali ya giza na utata ilijengeka, nafasi iliyokuja kujazwa na mashaka na kusitasita Nyingine ni kwamba ameifananisha hali ya hawa wachaji na kalabi, yaani ugonjwa wa kichaa cha mbwa, kichaa kinachowapata mbwa kiasi kwamba wanamuuma mtu yoyote wanayekutana naye. Kwa vile mbwa kama huyo ni mwenezaji wa vijidudu vya ugonjwa wa kuambukiza, pale meno ya mbwa huyo yanapopenya kwenye mwili wa mtu au mnyama yoyote, na kitu kikaingia kwenye damu ya mtu au mnyama huyo kutoka kwenye mate yake, mtu au mbwa huyu baada ya muda mfupi anakuwa ameambukizwa ugonjwa huu; naye pia anakuwa kichaa na anauma na kuwafanya wengine kuwa vichaa. Hii ndio maana watu wenye busara watamuua mara moja mbwa mwenye kichaa; ili angalau waweze kuokoa wengine na hatari ya kichaa cha mbwa. `Ali alisema kwamba walikuwa na tabia kama za mbwa wenye vichaa; walikuwa hawatibiki; waliuma na kuambukiza na kwa kawaida waliongeza idadi ya wagonjwa wa kichaa cha mbwa. Lakini, kwa ajili ya hali ya ummah wa Kiislamu wa wakati huo. Kikundi cha kiuchamungu, walioandaliwa pamoja, wajinga na wasiojua kitu walikuwa wakitembea kwa mguu mmoja na kuangukia kwenye moyo huu au ule. Ni nguvu gani inaweza kusimama dhidi ya nyoka hawa wenye sumu? Ulikuwa wapi ule msimamo wenye nguvu na uwezo ambao usingeyumba mbele ya nyuso hizi zenye kujinyima na za 16

ibid. , hotuba na.92.

114


kiuchaji? Ulikuwa wapi mkono ulioweza kunyanyuka wenyewe na kushusha panga juu ya vichwa vyao bila kutetemeka? Hiki ndicho alichomaanisha `Ali pale aliposema kwamba, hakuna aliyekuwa na ujasiri wa kufanya hivyo ila yeye. Mbali na `Ali na imani yake yenye utambuzi na uthabiti, hakuna mtu kati ya Waislamu, aliyemwamini Mungu, na Mtume na Qiyammah waliothubutu kuchomoa panga zao dhidi yao. Ni mtu tu ambaye hakumuamini Mwenyezi Mungu na Uislamu ndiye ambaye angethubutu kuwaua watu wa namna hii, na sio mu’min wa kawaida. Ilikuwa ni hili ambalo `Ali alilitaja kama namna ya heshima kubwa kwa ajili yake yeye mwenyewe: Nilikuwa ni mimi, na mimi tu, niliyetambua hatari kubwa iliyokuwa ikijionyesha kutoka upande wa hawa wachangu kupindukia kuelekea kwenye Uislamu. Sio vipaji vya nyuso zao vyenye sugu, wala nguo zao za kujihini, wala ndimi zao zenye kumkumbuka Mola daima, wala hata imani zao zenye nguvu na imara, zingeweza kuwa kizuizi cha utambuzi wangu juu yao. Ilikuwa ni mimi niliyejua kwamba kama wangepata upenyo kila mmoja angedhurika kwa ugonjwa wao, kwamba ulimwengu wa Kiislamu ungekuwa mgumu, ukishikilia mwelekeo wa nje, wa kijuujuu na uliopitwa na wakati, kwamba mgongo wa Uislamu ungepinda. Hiki sio kile Mtume (s.a.w.w.) alichotaja: Makundi mawili yatavunja mgongo wangu – wale wanaojua kisha wakafanya uzembe, na wale ambao ni wajinga lakini wakatangaza uchamungu. `Ali alitaka kusema kwamba kama asingepigana dhidi ya mienendo ya Khawariji katika ulimwengu wa Kiislamu, hakuna mtu mwingine ambaye angejitokeza na kuthubutu kupigana dhidi yao. Mbali na yeye hapakuwa na mtu yoyote aliyeona kwamba wale ambao vipaji vya nyuso zao vimeota sugu kwa kusujudu sana walikuwa wachamungu na watu wa dini lakini walikuwa kizuizi katika njia ya Uislamu, watu ambao walijiona wao wenyewe kwamba walikuwa wakifanya kazi kwa manufaa ya Uislamu, lakini ambao kwa kweli walikuwa ndio maadui wa kweli wa Uislamu; hakuwepo mtu wa kupigana dhidi yao na kumwaga damu zao. Ni yeye tu aliyeweza kufanya hivyo.

115


Alichokifanya `Ali kililainisha njia kwa makhalifa na watawala wa baadae ili waweze kupigana dhidi ya Khawariji na kuwaua; ili askari wa Uislamu pia waweze kuwatii bila ya kwa nini yoyote au kwa sababu gani; kwani `Ali alikuwa amepigana nao. Kwa kweli, mwenendo wa `Ali pia ulifungua njia kwa ajili ya wengine ili waweze, bila ya woga, kupigana na kundi lolote lililojionyesha lenyewe kuwa machoni ni la wachamungu, kujifanya watakatifu na kuwa na dini, lakini ambao kwa kweli walikuwa wajinga. 3. Khawariji walikuwa ni wajinga na watu wasiojua, na kwa sababu ya ujinga wao na ukosefu wa elimu hawakuweza kutambua ukweli, na walitafsiri matukio kwa makosa kabisa. Polepole ufahamu huu wa mambo uliopotoka ukachukua sura ya dini au imani katika hatua za uanzilishi ambayo wenyewe waliutumia kwenye kujitolea mhanga kwao kukubwa. Mwanzoni, mafundisho ya Kiislamu ya kukataza maovu yaliwaunda kwenye namna ya kundi ambalo lengo lao kuu pekee ni kuhuisha desturi za Kiislamu. Hapa ni muhimu kutua kidogo na kutafakari kwa uangalifu zaidi juu ya jambo kutoka kwenye historia ya Kiislamu. Tunaporejea nyuma kwenye maisha ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), tunaona kwamba katika kipindi chote cha miaka kumi na tatu cha Makkah hakutoa kamwe ruhusa kwa ajili ya jihad au hata vita vya kujihami kwa mtu yoyote, kwa kiasi kwamba Waislamu kwa kweli walipata dhiki, na, kwa idhini ya Mtume (s.a.w.w.), kikundi kikahamia Abyssinia (Ethiopia). Hata hivyo wengine wote walibaki na kupata mateso; Ilikuwa ni katika mwaka wa pili tu huko Madina ambapo ruksa ilitolewa kwa ajili ya jihĂŁd. Katika kile kipindi cha Makkah Waislamu waliyaona mafundisho; wakaufahamu msimamo wa Uislamu. Mfumo wa maisha ya Kiislamu ukapenya ndani ya vina vya nafsi zao, kwa matokeo kwamba baada ya kuingia kwao Madina kila mmoja wao alikuwa balozi wa kweli wa Uislamu, na Mtume wa Uislamu aliyewatuma kwenye eneo zima, aliweza kuwatumia kwa manufaa. Pia, walipotumwa kwenda kupigana

116


jihãd, walijua ni nini walichokuwa wanapigania. Katika maneno ya Amir al-mu’minin (a.s): ْ‫حَمَلُوا بَص َا ئر َهُ ْم عَلَى أَ سْي َا فِهم‬ Waliunganisha ufahamu wao wa kina na panga zao. Panga zao kwa hiyo ziliimarishwa na watu wakaelekezwa vema kwamba wangeweza kutimiza kazi yao ndani ya mipaka iliyowekwa na Uislam. Tunapoisoma historia na kuona kile walichokisema watu hawa ambao, mpaka miaka michache ya hivi karibuni, hawakujua kingine bali upanga na ngamia, tunavutiwa na kushangazwa na mawazo yao ya hali ya juu na utekelezaji wao mkubwa wa Uislamu Katika wakati wa makhalifa, kwa masikitiko makubwa sana, juhudi kubwa ilielekezwa kwenye mapambano, wakipuuza ukweli kwamba, pamoja na kupanua milango ya Uislamu kwa wengine, na kuwaweka kwenye mwelekeo wa Uislamu, ambapo kwa vyovyote walivutiwa na imani ya Mungu Mmoja ya Kiislamu na haki na usawa wake kwa Waarabu na wasiokuwa Waarabu, ilikuwa ni muhimu kufundisha utamaduni wa Kiislamu na njia yake ya maisha na kuwafanya watu wautambue vyema mtazamo wa Kiislamu. Khawariji walikuwa wengi wao ni Waarabu, ingawa walikuwepo pia baadhi ya wasiokuwa Waarabu; lakini wote, Waarabu na wasiokuwa Waarabu, walikuwa hawazijui kanuni, na hawakuwa wameuzoea utamaduni huo, wa Uislamu. Walitaka kufidia mapungufu yao yote kwa mkazo katika kusujudu. `Ali (a.s) aliielezea hamasa yao kwa maneno haya: Watu ambao sio waadilifu, wasio na mawazo mapana au hisia za werevu; watu ambao ni dhaifu, kama watumwa, walaghai waliokusanyika kutoka kila pembe, wanakutana pamoja kutoka kila upande. Ni watu ambao kwanza kabisa wangeelekezwa, wangefundishwa mwenendo wa Kiislamu, na ambao wangepata ujuzi wa jinsi ya kuishi kama 117


Waislamu wa kweli. Mwangalizi sharti awatawale na kuwashika mkononi, wasiachwe huru, kushika panga mikononi mwao na kutoa maoni yao kuhusu Uislamu. Hawakuwa muhajir (kutoka Makkah) waliohama kutoka nyumbani kwao kwa ajili ya Uislamu, wala Ansari (wa Madina) waliowakaribisha muhajirina kuwa miongoni mwao. Kule kutokea kwa tabaka la wajinga katika ummah pamoja na imani iliyoathiriwa na uchamangu bandia, ambalo kwalo hawa Khawariji walikuwa ni sehemu yake, kulikuwa ni gharama kubwa sana kwa Uislamu. Tukiwasahau, kwa muda huu, hawa Khawariji, ambao, pamoja na kurudisha nyuma kwao kote, walijaliwa na sifa ya ujasiri na kujitolea muhanga binafsi, kikunndi kingine kilijitokeza kutoka kwenye mwelekeo huu wa kiuchamungu ambao hawakuwa na sifa hizi. Watu hawa waliuvuta Uislamu kuelekea kwenye utawa na kuiacha (kuipa nyongo) dunia, walihusika na kutokea kuenea kwa hila na usufi. Kwa vile hawakuwa na sifa hizo hapo juu ambazo kwazo wangeshika upanga wa chuma dhidi ya wale waliokuwa madarakani, walitumia upanga wa maneno dhidi ya wale ambao walikuwa na elimu. Waliifanya kuwa ni desturi yao kuwaita wale wenye elimu kama ni wasioamini, mafasiki na wasio na dini. Kwa vyovyote vile, moja ya sura yenye kuonekana dhahiri ya Khawariji ilikuwa ni ujinga wao na kukosa elimu, na moja ya udhihirishaji wa ujinga wao ni kule kutoweza kwao kutofautisha kati ya maana ya nje ya Qur’ani, yaani, maandishi yake na majalada, na maana yake, na hivyo ndivyo ilivyokuwa kwamba walinasa kwenye mtego wa ujanja mwepesi wa Mu‘awiyah na ‘Amr ibn al-‘As. Pamoja na watu hawa, ujinga na ibada vilikwenda pamoja. `Ali alitaka apigane dhidi ya ujinga wao, lakini ni vipi angeweza kuutenga upande wao unaojinyima, wa kiuchamungu na wenye utii kutoka kwenye mwelekeo wao wa ujinga, wakati utii wao ulikuwa wa sawasawa na ujinga wao? Kwa `Ali, ambaye uzoefu wake katika Uislamu ni wa kiwango cha juu, ibada pamoja na ujinga ilikuwa haina thamani kabisa. 118


Hivyo aliwaangamiza, na wao hawakuweza kutumia kujinyima kwao, uchamungu na utii wao kama ngao kati yao wenyewe na `Ali. Hatari ya ujinga wa watu wa namna hii, na zaidi hasa ya aina hii ya kundi, ni ile namna ambamo wanakuwa vyombo na zana mikononi mwa wajanja, na kizuizi kwenye njia ambayo iko kwenye maslahi ya hali ya juu ya Uislamu. Wanafiki wasio na dini wanaweza wakati wote kuwachochea wachamungu wa kawaida dhidi ya maslahi ya Uislamu; wanageuka kuwa panga katika mikono ya watu hawa na mishale katika pinde zao. `Ali aliielezea tabia yao hii kwa kwa namna ya hali ya juu na ustadi, aliposema: ِ‫ب ِبه‬ َ َ‫ وَضَر‬، ‫ن مَرَا مِ َي ُه‬ ُ َ‫ن رَمَى ِب ِه الشَيْطا‬ ْ َ‫ وَم‬،ِ‫ثُمَ أَنْ تُمْ شِرَا ُر النَاس‬ ُ‫تِي َهه‬ Hivyo ninyi ni wabaya katika watu; nyie ni mishale mikononi mwa Shetani anayoitumia kulengea shabaha yake, na kupitia kwenu ninyi anawaingiza watu kwenye mchanganyo na mashaka. Tumesema kwamba hapo mwanzoni kundi hili la Khawariji lilitokea kuja kuhuisha mila na desturi za Kiislam, lakini kwamba kule kukosa utambuzi na kutokujua kuliwaburuza mpaka mahali wakazitafsiri vibaya aya za Qur’ani. Ni kutokea hapa ambapo ndipo walianza kuchukua sura ya kidini na kuanza kujulikana kabisa kama madhehebu na kama njia. Kuna aya ndani ya Qur’ani inayosema:             Hapana hukumu ila kwa Mwenyezi Mungu, anaelezea yaliyo kweli, Naye ni Mbora wa kuhukumu. (Al-An’aam, 6:57)

119


Katika aya hii, hukm imeelezwa kama moja ya sifa maalum za dhati ya Mungu, lakini ni muhimu kuona maana ya hukm ni nini. Bila shaka, maana ya hukm (hukumu) hapa ni sheria na taratibu za maisha ya mwanadamu. Katika aya hii, haki ya kutunga sheria imezuiwa yeyote yule isipokuwa Allah (s.w.t.) na hii imetambuliwa kama moja ya daraja za dhati ya Mwenyezi Mungu (au ya mtu ambaye amepewa mamlaka na Mwenyezi Mungu). Lakini Khawarij wamelichukulia neno hukm kwa maana ya neno hukumah (serikali), ambamo pia inaingia ile dhana ya hakamiyah (sulhu), na wakaweka wito wao wenyewe: la hukma illa li llah – serikali na sulhu ni za Allah swt pekee. Nia yao ilikuwa kwamba serikali (hukumah), sulhu (hakamiyah) na uongozi pia, kama vile kupanga sheria, ilikuwa ni haki maalum ya Allah swt, na kwamba, Mbali na Mwenyezi Mungu, hakuna aliyekuwa na haki ya kusuluhisha miongoni mwa watu au kutawala, kama vile walivyokuwa hawana haki ya kuunda sheria. Wakati mmoja ‘Amir al-muminin alikuwa katika sala (au pengine akihutubia watu toka mimbarini) walipokemea na kumwambia: la hukma illa li’llah, la laka wa as-habik – Ewe `Ali, kutawala ni kwa Allah swt pekee. Sio juu yako au ya marafiki zako kuongoza na kusuluhisha! Katika kujibu, akasema: Maneno hayo ni sahihi lakini vile (wanavyodhani) kuwa ndio maana yake ni makosa. Ni kweli kwamba hukumu (hukm) ni ya Allah swt pekee, lakini watu hawa wanasema kwamba uongozi ni wa Mwenyezi Mungu peke yake. Ukweli ni kwamba mwanadamu anahitaji kiongozi, mtawala, ama awe mzuri au (pengine) mbaya. Chini ya (kivuli cha) utawala wake, mu’min anafanya matendo mema, ambapo yule asiyeamini ananufaika kutokana na maisha yake ya dunia; na Mwenyezi Mungu hukifikisha kila kitu kwenye mwisho wake. Kupitia kwa mtawala huyo, kodi zinakusanywa, maadui nao wanapigwa, barabara 120


zinawekwa katika hali ya usalama, na haki za wanyonge zinachukuliwa kutoka kwa wenye nguvu, kusudi kwamba watu wema wawe wanafurahia amani na wanapata ulinzi kutokana na waovu.17 Kwa kifupi, sheria haijiweki katika utekelezaji yenyewe tu, hivi hivi; lazima awepo mtu, au kikundi fulani kinachojaribu kuiweka kwenye utekelezaji. 4.

Walikuwa na akili-finyu na watu wasioona mbali, ambao mawazo yao yalifanya kazi chini ya upeo mdogo sana; waliufunga Uislamu na Waislamu ndani ya kuta nne za mawazo yao finyu. Kama watu wengine wote wenye akili finyu walidai kwamba kila mtu mwingine yeyote alielewa vibaya, au hakuelewa kabisa; wote wamechukua njia potofu na wameandaliwa kwenda Motoni. Kitu cha kwanza ambacho aina hii ya mtu mwenye akili finyu anachofanya ni kwamba anaupa ufinyu wake wa akili muundo wa imani ya kidini; anaziwekea mipaka rehma za Allah swt, humfanya Yeye kukaa daima kwenye kiti cha enzi cha ghadhabu, akingojea tu mja wake afanye kosa ili aweze kumtosa kwenye adhabu ya kudumu milele. Moja ya imani za msingi wa Khawariji ni kwamba mtendaji wa dhambi yoyote kubwa, kwa mfano kusema uongo, kusengenya au kunywa pombe, alikuwa ni kafiri na alikuwa nje ya mipaka ya Uislamu, aliyehukumiwa milele kwenda Motoni. Hivyo, mbali na idadi ndogo sana ya watu, kila mmoja alikuwa amehukumiwa kwenda Motoni. Ufinyu wa akili ya kidini ulikuwa ni sifa maalum ya Khawariji, lakini tunaiona hii kwa mara nyingine tena miongoni mwa Waislamu leo hii. Ni kwa sababu hii ndipo tukasema kwamba bendera ya Khawariji imekufa na kutoweka lakini mwelekeo wa dini yao bado uko hai, kwa kiwango kikubwa au kidogo, miongoni mwa watu na vikundi.

Tunaweza kupata baadhi ya watu wenye imani kali wanaowaona watu wote duniani, mbali na wao wenyewe na idadi ndogo sana ya watu 17

ibid, Hotuba na: 40. 121


kama wao, kama wasioamini na makafiri; wanadhani idadi ya wale waliojumlishwa katika Uislam na Waislam kuwa ni ndogo mno kabisa. Tumetaja, katika mlango uliopita, kwamba Khawariji walikuwa hawakuzoea mwelekeo wa desturi ya Kiislamu lakini kwamba walikuwa majasiri sana. Kwa vile walikuwa wajinga, basi walikuwa na akili finyu; na kwa vile walikuwa na akili finyu, basi walikuwa wepesi wa kuwahukumu watu kama makafiri na madhalimu kwa kiasi ambacho waliiwekea mipaka maana ya Uislamu na Waislamu, iwe ni kwa ajili yao tu na kuwatenga Waislamu wengine ambao hawakuunga mkono imani zao, kama makafiri. Kwa vile walikuwa majasiri, mara kwa mara waliwajia wale wenye mamlaka na kulingana na vile walivyofikiria, waliwashurutisha kwenye “kuamrisha mema na kukataza maovu”, lakini basi waliuawa wao wenyewe. Tulisema pia kwamba katika vipindi vya baadae vya historia ya Kiislamu, ugumu wao, ujinga, uchamungu na kujifanya masufi kulirithiwa na wengine, lakini bila ya ujasiri wao, ushujaa na kijitolea muhanga kwao. Wale Khawariji wasiokuwa mashujaa, yaani ni kusema, wale masufi wa woga kupindukia, waliweka panga zao upande mmoja, wakaachana na “kuamrisha mema na kukataza maovu” kwa kadiri wale walio madarakani walivyohusika, ambao walikuwa ni hatari kwao, na kisha wakawageukia wale waliosoma kwa upanga wa maneno. Walileta namna fulani ya shutuma dhidi ya kila mtu aliyesoma kiasi kwamba ni wasomi wachache tu katika historia ya Kiislam ambao hawakuwa walengwa wa shutuma za kundi hili. Watamwita mtu mkana Mungu, mwingine mkanusha Qiyammah; wa tatu watamwita mkataa ile safari ya kimwili (mi‘raj-e jismani) ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), wa nne daruweshi, wa tano kitu kingine chochote, na kuendelea. Kwa namna hii, kama maoni ya hawa mapunguani yangechukuliwa kama kigezo, hakuna mwanazuoni wa kweli ambaye angeweza kuwa Muislamu. Wakati `Ali alipotuhumiwa kuwa ni kafiri, nafasi au hali ya wengine iko wazi. Ibn Sina, Nasiru’d-Din at-Tusi, Mullah Sadra, Fayd alKashani, Sayyid Jamalu’d-Din al-Asadabadi (al-Afghani), na, wa hivi karibuni sana, Muhammad Iqbal ni wachache kati ya wale walioonja

122


mfyonzo mchungu wa kikombe hiki. Ibn Sina aliandika kuhusiana na jambo hili: Kuniita mimi kafiri sio ukuzaji (utia-chumvi) rahisi, Kwani hakuna imani yenye nguvu kuliko yangu. Kama wakati mmoja angekuwepo mmoja tu kama mimi naye akawa kafiri. Je, alikuwepo kamwe Muislamu katika kipindi chochote? Khwajah Nasiru’d-Din at-Tusi, ambaye alituhumiwa kuwa ni kafiri na mtu mmoja aliyeitwa kwa jina la Nizamu’l-‘Ulama’ (mwenye kuweka nidhamu miongoni mwa wanazuoni) alisema: Kama “mwandaaji” anayekosa nidhamu akiniita mimi kafiri, Ninaweza kujiliwaza mwenyewe kwamba taa ya udanganyifu Kamwe haitatoa mwanga Nitamwita yeye ni Muislamu, kwani hakuna jibu kwa uongo ila uongo. Kwa vyovyote vile, moja ya sifa maalum za Khawariji ilikuwa ni kuwa na akili-finyu, na ilikuwa ni kutoona mbali kwao kulikomwita kila mtu hana dini. Akipinga kutoona mbali huku, `Ali alibisha kwamba ilikuwa ni njia ya makosa sana ya fikira wanayoifuata. Alisema kuwa Mtume (s.a.w.w.) angemuadhibu mtu na kisha asali sala za mazishi juu ya maiti yake, wakati ambapo kama kutenda dhambi kubwa kulimfanya mtu kuwa kafiri, Mtume asingalifanya hivi; kwani hairuhusiwi kusoma du’a juu ya maiti ya kafiri, ikiwa ni kitu Qur’ani imekataza.18 Alimpiga viboko mnywaji wa pombe, alikata mkono wa mwizi, alimchapa mijeledi yule mzinifu ambaye hajaoa, na kisha akawapa nafasi wote katika mikusanyiko ya Kiislamu, na hakukata malipo yao kutoka hazina - (baytu’l-mal), na aliwaozesha kwa Waislamu wengine. Mtume (s.a.w.w.) alitoa adhabu za Kiislamu kama zilivyotakikana, lakini kamwe hakufuta majina ya wale walioadhibiwa kutoka kwenye orodha ya Waislamu. `Ali aliwataka hawa Khawariji kuchukulia kwamba yeye 18

Surah at-Tawbah, 9:84.

123


amekwenda kombo, na kwamba, kama matokeo ya hilo amekuwa kafiri. Lakini kwa nini basi waliushutumu ummah wa Kiislamu kama ni makafiri? Hivi ilimaanisha kwamba kwa sababu mtu mmoja amepotoka na wengine pia wamelazimika kupotoka na kuwa makosani na kwamba waitwe kujieleza? Aliwauliza wao ni kwa nini walibeba panga zao mabegani, na kuwatiisha wasio na dhambi na wenye dhambi wote sawasawa kwenye ncha za panga zao.19 Hapa ‘Amir al-mu’minin aliwapinga kwa maelezo namna mbili; “kuzuia” kwake kumewakingamiza katika pande mbili. Moja ilikuwa kwamba wameijumuisha dhambi kwa wale ambao walikuwa hawana hatia, na wamewataka wajieleze kwayo, na nyingine ilikuwa kwamba walimdhania yule mtenda dhambi kwamba ni lazima awe ni kafiri na yuko nje ya Uislamu, yaani, waliuwekea mipaka upeo wa Uislamu na wakasema kwamba yeyote yule atakayepitukia mipaka ya baadhi ya maagizo ya Uislamu atakuwa ametoka nje ya Uislamu. `Ali aliwashutumu wale wenye akili finyu na wasioona mbali, na kwa kweli, mapambano ya `Ali na Khawariji yalikuwa ni mapambano na namna hii ya fikra sio mapambano na watu binafsi. Kwani, kama hawa watu wasingefikiri kwa namna hii, `Ali asingewatendea kama alivyowatendea na alimwaga damu zao ili kwamba mawazo haya yaweze kufa pamoja nao, ili Qur’an iweze kueleweka sawasawa, na Waislamu waweze kuuelewa Uislamu na Qur’an kama vilivyo na kama Mtunga-Sheria Wao alivyotaka. Matokeo ya kutoona mbali huku na fikra zilizopindika yalikuwa kwamba walikumbwa na siasa ya kunyanyua Qur’an juu ya mikuki, na hapo wakazua kubwa zaidi kati ya hatari za Uislamu. Na `Ali ambaye alikuwa amekwenda ili kuuchimbua mzizi wa unafiki na kumuangamiza Mu’awiyah na mpango wake mwanzo na mwisho, ilimbidi arudi nyuma na kupambana nao. Ni tukio gani la kisirani hili, lililoutokea ummah wa Kiislamu wakati ule!20 19

Kwa maandishi ya hotuba hii tazama Nahju’l-balaghah, Hotuba na: 126. Kwa makadirio ya watu wengi, misiba mikubwa sana iliyoukumba ulimwengu wa Kiislam ilikuwa ni dhoruba za kiroho zilizowaangukia Waislamu. Qur’ani iliweka 20

124


msingi wa wito wa kwenye Uislamu juu ya ujuzi na fikra za uhakika, na yenyewe inapendekeza njia zakufuata baada ya kuelewa (Ijtihad) na utambuzi wa kisomi:                     ..Lakini kwa nini halitoki kundi katika kila taifa miongoni mwao kujielimisha vema katika dini? (at-Tawbah, 9:122.) “tafaqqaha” (kutafuta elimu) haikutumika kwa uelewa mwepesi, bali ni ujuzi hasa kwa kutumia juhudi na maarifa. ُ          Kama mkimcha Mwenyezi Mungu, atawapeni (nuru) inayopambanua . (alAnfal, 8:29)         Lakini kwa wale wanaojitahidi kwa ajili Yetu, lazima tutawaongoza kwenye njia Zetu .(al-‘Ankabut, 29:69) Hawa Khawariji walianzisha ugumu na kuvia ambako kulikuwa kinyume kabisa na namna hii ya mafundisho ya Qur’ani yaliyotaka elimu ya Kiislamu (fiqh) kubakia daima inakwenda na iko hai. Waliifikiria elimu ya Kiislamu kama kitu kinachofisha na kisichosogea na wakaburuza maumbo na miundo migumu kwenye Uislamu. Uislamu kamwe haujashughulika tu na maumbo, miundo na dalili za nje za maisha; mafundisho ya Kiislamu yote yameelekezwa kwenye mwelekeo na maana na njia ambayo mtu anaweza kufikia lengo hilo na maana hizi. Uislamu umechukua kama sehemu ya eneo la elimu yake, malengo haya na maana hizi na mwongozo kwenye njia ya kufikia malengo haya, ambapo unamuacha huru mwanadamu katika lile lisilokuwa hili, na hivyo unaepukana na mgongano wowote wa maendeleo ya ustaarabu na utamaduni wa kweli. Hakuna njia ya kitu yakinifu au umbo la nje linaloweza kutokea katika Uislamu lenye upande wa “utakatifu” ambao Waislamu wataona ni wajibu wao kuuhifadhi. Na huu uepukaji wa migongano na maumbo ya nje, ya maendeleo ya kisayansi au utamaduni ni sababu moja ya kwa nini ukubalianaji wa dini ya Kiislamu na mahitaji ya nyakati

125


umekuwa rahisi, na kikwazo chochote kikubwa kwenye kuendelea kwa uhai wake kimeondolewa. Ni mchanganyiko huu hasa wa weledi na udini ambao kwa upande mmoja, umechukuliwa kama msingi, na ambao, kwa upande mwingine, unatenganisha hili la baadae (udini) kutoka kwenye maumbo. Unatupa mazingatio ya fani zote, na fani hizi zinaweza kuchukua idadi ya ishara tofauti za nje bila ya mabadiliko ya ishara hizi kusababisha mabadiliko katika ukweli. Hata hivyo ule upatanishanishaji wa ukweli na ishara zake za nje na dalili sio jambo rahisi kiasi hicho kwamba mtu yeyote anaweza kulifanya, kwani linahitaji utambuzi wenye kupenya na ujuzi halali. Khawariji walikuwa ni watu walioganda kwenye fikra yao, mbali na walichokisikia, na kukosa uwezo wa kuelewa. Hivyo wakati ‘Amir almu’minin alipomtuma Ibn ‘Abbas kwenda kujadiliana nao, alimwambia: “Usihojiane nao kwa Qur’an, kwa sababu Qur’an ina pande nyingi kwayo: utaongea na wao wataongea. Lakini hojiana nao kwa sunnah, kwa sababu hawawezi kupata ukwepaji wa hilo.” (Nahju’l-balaghah, barua na: 78) Kwa hili alimaanisha kwamba Qur’an inashughulika na fani nyingi, na katika kubishana, upande mmoja utachukua kitu kama dalili yake na kujadiliana kwa mujibu wa hicho, ambapo upande mwingine utachukua kitu kingine na kukitumia hicho katika kuhojiana na kubishaniana; hili bila shaka halitatoa matokeo yoyote. Hawa Khawariji, alitaka kusema, hawakuwa na ujuzi wa kutosha kwamba wangeweza kutambua kitu cha kweli ndani ya Qur’an na wakakilinganisha na matumizi yake halisi. Hivyo alimshauri Ibn ‘Abbas kuongea nao kwa kufuata sunnah ambayo inajipambanua na imeelekeza na matumizi yake. `Ali hapa alibainisha ule ugumu na kushupaa kiakili katika dini ambako kulionyesha kushindwa kwao kuoanisha weledi na dini. Khawariji hawa walikuwa ni makuzi ya ujinga na kuvia. Hawakuwa na uwezo wa kuchunguza na kuchanganua, na walikuwa hawawezi kutofautisha kati ya fani na matumizi yake; walidhani kwamba kwa vile sulhu imekwenda kombo katika kadhia hii, basi msingi wake wote utakuwa batili na usiofaa, ingawaje ulikuwepo uwezekano kwamba ungeweza kuwa imara zaidi na madhubuti, matumizi yake katika kadhia hii tu yakiwa sio sahihi. Hivyo tunaziona hatua tatu katika hadithi ya sulhu hii: i.

ii.

Katika ushahidi wa kihistoria, `Ali hakufurahia kuwa na sulhu; alijua pendekezo la wafuasi wa Mu‘awiyah litakuwa ni hadaa na ulaghai. Alisisitiza sana juu ya jambo hili na akakataa kubadilishwa mawazo. Alisema, mara itakapokuwa imeamuliwa kuundwa kwa baraza la usuluhishi, kwamba Abu Musa alikuwa ni mtu ambaye hana uwezo wa kuona mbali na hakuwa na uhodari na kazi hiy o; alibidi

126


iii.

achaguliwe mtu hodari, na yeye mwenyewe akampendekeza Ibn ‘Abbas au Malik al-Ashtar. Msingi wa sulhu ni sahihi na hauna hatari. `Ali pia alisisitiza juu ya suala hili. Katika al-Kamil fi’l-adab, mtunzi, Abu’l-‘Abbas al-Mubarrad anaandika (chapa ya Misri, juz.2, uk.134):

“ `Ali binafsi aliwasihi Khawarij, na aliwaambia: ‘Wallah, hivi alikuwepo mtu kati yenu, aliyeipinga sulhu, kama mimi?’ “ ‘Wallah,’ walijibu, ‘wewe ni shahidi kwamba hata mmoja kati yetu hakuwepo!’ “ ‘hamkunihimiza mimi nikubali?’ aliuliza. “ ‘Wallah,’ wakajibu, ‘wewe ni shahidi kwamba tulikuhimiza’ “ ‘Sasa kwa nini,’ aliendelea, ‘munanipinga hivi sasa, na kwa nini mumejitenga nami?’ “ ‘Tumetenda dhambi kubwa,’ waliendelea, ‘na ni lazima tutubie. Sisi tumetubia, na wewe lazima utubie.’ “Hapo, `Ali akasema: astaghfiru’llah min kulli dhanbin – Ewe Allah, ninakuomba msamaha kwa kila kosa.’ Ndipo watu hawa, ambao walikuwa karibu elfu sita, waliporudi na kusema kwamba `Ali ametubia na kwamba wako tayari kwa amri yake ya kutoka kuelekea Damascus. al-Ash‘ath ibn Qays al-Kindi alimjia `Ali na kusema: ‘Watu wanasema kwamba wewe unatambua kwamba sulhu ni kosa, na kuikubali kwamba ni kufru katika Uislamu’ “ `Ali akapanda juu ya minbar na akatoa hotuba ambayo ndani yake alisema: ‘Yeyote anayedhani kwamba nimerudi nyuma juu ya sulhu anadhania kwa makosa, na yeyote anayefikiri kwamba sulhu ni kosa yeye mwenyewe yuko kwenye kosa kubwa mno.’ “Ndipo Khawariji wakatoka hapo msikitini na kwa mara nyingine tena wakamuasi `Ali.” `Ali alisema kwamba katika suala hili palikuwepo na kosa, kwa maana ya kwamba Mu‘awiyah na wafuasi wake walitaka kutumia ulaghai, na kwa maana kwamba Abu Musa alikuwa mzembe ingawa hata hivyo `Ali tangu mwanzo alikwishasema kwamba asichagaliwe. Lakini hiyo haikuwa ichukuliwe kumaanisha kwamba msingi wa sulhu haufai.

*

*

127

*


Na kwa tofauti yoyote kati sheria ya Qur’an na sheria ya watu binafsi, hakuna utofautishaji uliofanywa. Kukubalika kwa sheria au uongozi wa Qur’an kuna maana kwamba katika matukio yote kila kile ambacho Qur’ani inatuhimiza kufanya hapana budi kifanywe, ambapo sheria au uongozi wa watu una maana kufuata maamuzi na maoni ya watu hawa. Sasa, kwa vile Qur’ani haiwezi kuongea, ukweli wake lazima upatikane kwa utekelezaji wa baadhi ya matumizi, na hiyo itakuwa haiwezekani bila ya watu fulani. Juu ya jambo hili `Ali alisema: “Hatukutaja watu kuwa wasuluhishi, bali tuliitaja Qur’an kama msuluhishi. Qur’ani n kitabu, kilichojaladiwa kati ya majalada mawili, na hakiongei. Kwa hiyo kinahitaji mkalimani. Ni watu tu wanaoweza kuwa wakalimani hao. Wakati watu hawa walipotukaribisha kuitaja Qur’an kama msuluhishi kati yetu, hatukuweza ku jifanya sisi wenyewe kuwa lile kundi lililogeuka kutoka kwenye Kitabu cha Allah swt, kwani Alisema:            Na kama mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume… (an-Nisa’, 4:59.) “Kulirusha kwa Allah swt kuna maana kwamba tuamue kwa mujibu wa Qur’an, ambapo kurejea kwa Mtume kuna maana tufuate sunnah zake. Sasa, kama sulhu ingetekelezwa kwa haki kupitia Qur’ani, tungekuwa sisi ndio watu wenye kustahiki zaidi katika watu kuupokea (ukhalifa); na kama sulhu ni kupitia sunnah ya Mtume wa Allah swt, tungekuwa wa kwanza wao kuupokea.” (Nahju’l-balaghah,hotuba na:124) Kuna tatizo hapa kuhusu kuoanisha imani za Shi ‘ah na nafsi ya Amir al-muminin (tazama mwisho wa hotuba na: 2 katika Nahju’l-balaghah). Utawala na Uimamu katika Uislamu ni kwa uteuzi wa kimungu na kwa mujibu wa misingi ya maandishi (nass), hivyo kwa nini `Ali alikubali uamuzi wa sulhu na baadae autetee kwa dhati? Tunaweza kulielewa vizuri sana jibu la pingamizi hili kutoka kwenye maneno yaliyotangulia ya Imam, kwani, kama alivyosema, kama majadiliano na hukumu vingefanywa sawasawa kupitia Qur’an, hakuna uamuzi ambao ungefikiwa mbali na haki yake yeye kwenye ukhalifa na Uimamu, na sunnah ya Mtume (s.a.w.w.) inatoa uamuzi huo huo. Athari za Madhehebu za Kiislamu juu ya Kila Moja Yao: Uchunguzi wa maisha ya Khawariji una faida kwetu kadiri tunavyoweza kuelewa ni kwa kiasi gani walikuwa na athari katika historia ya Kiislamu, kutoka kwenye

128


mwelekeo wa kisiasa, kutoka kwenye ule wa imani na silika, na kutoka kwenye ule mwelekeo wa kisheria au kimaagizo. Kwa vyovyote vile madhehebu mbalimbali na vikundi vitavyoweza kutofautiana kila kimoja katika miito na taratibu zao, inaweza wakati mwingine kutokea kwamba mwelekeo wa madhehebu moja utapenya kwenye nyingine, na hii nyingine, ingawa inaweza kuwa pinzani kwa hii ya kwanza itanyonya mwelekeo na sifa -mwafaka zake. Asili ya mwanadamu ni mwizi; wakati mwingine mtu anaweza akaona watu ambao, kwa mfano, wanaweza kuwa ni Sunni, lakini ambao, katika mwelekeo na hisia, ni Shi‘ah, na wakati mwingine kinyume chake. Wakati mwingine mtu anakuwa mng’ng’anizi, mwenye kushikilia sheria na dhahiri, lakini kimwelekeo ni Suffi, na kinyume chake. Hali kadhalika inawezekana kwamba baadhi ya watu ni Shi‘ah kwa kuigiza na kwa mazungumzo yao, lakini kinafsi na kimatendo ni Khawariji. Hili ni sahihi kote, kwa watu mmoja mmoja, na kwa jumuiya na mataifa. Wakati vikundi vya kijamii vinapohusishwa kimoja na kingine, ingawa kila kimoja kitajaribu kulinda imani zao, hizi zitaenea kutoka kwa kimoja kwenda kwa kingine, kama vile, kwa mfano, “qam-e zani” [kupiga kichwa kwa upanga ili kujitia majeraha, mazoea miongoni mwa watu wa kawaida, kama hawa wawili wafuatao, waliohusishwa na maandamano wakati wa taratibu za maombolezo katika mwezi wa Muharam] na upigaji wa ngoma na upulizaji wa pembe, vilivyoingia Iran kutoka kwa Wakristo wa kanisa la Ordothox la Caucasia [wakati fulani ilikuwa sehemu ya Iran], na kwa vile mwelekeo wa watu ulikuwa tayari kupokea mila hizi, zilienea kama moto wa porini. Kwa sababu hii, mwelekeo wa kila madhehebu lazima ufunuliwe. Wakati mwingine madhehebu zinazaliwa kutokana na utayari wa kuona uzuri katika matukio au watu fulani “angalia tendo la ndugu yako katika mwanga bora”; kwa mfano, Sunni, ambao walizaliwa kwa maelekezo juu ya upendeleo kwa watu fulani. Na madhehebu mengine yanaweza kuzaliwa kutokana na namna ya mtazamo maalum na mkazo juu ya kanuni za Kiislamu, sio kutokana na mtu au watu. Na kwa mara moja moja watakuwa watu wakosoaji, kama wale Mashi‘ah wa mwanzoni. Madhehebu inaweza kuzaliwa kutokana na mkazo juu ya mwelekeo wa ndani na tafsiri juu ya undani huu, kama Masuffi, na madhehebu inaweza kuzaliwa juu ya mkazo wa imani kali na ugumu, kama Khawariji. Tunapokuja kuelewa mtazamo wa madhehebu na mazingira yake ya kwanza ya kihistoria, tunakuwa kwenye nafasi nzuri ya kuamua ni mawazo gani yamepita kutoka madhehebu hii kwenda nyingine katika karne zilizofuatia, na ni nani aliyeidhinisha mwelekeo wao na vilevile miito na mifumo ya vifungu vya maneno ya kawaida. Kwa hali hii, imani na fikra ni kama maneno wakati ambapo, bila kuwepo na nia yoyote, yanaingia kutoka kwenye lugha ya watu wamoja kwenda kwenye lugha ya wengine.

129


Kwa mfano, baada ya Waislamu kuiteka Iran, maneno ya Kiarabu yakaingia kwenye lugha ya Kiajemi, na kuelekea upande wa pili, maelfu ya maneno ya Kiajemi yakaingia kwenye lugha ya Kiarabu. Kuna athari kama hiyo hiyo ya Kituruki juu ya lugha za Kiarabu na Kiajemi; kama kwa mfano wa Kituruki cha wakati wa Khalifa alMutawakkil na Kituruki cha Seljuqs na Wa-Mongoli; na ni vivyo hivyo kwa lugha zote za ulimwengu zilizobakia. Mifano kama hiyo ingeweza kupanuka kwenye mitindo vionjo. Namna ya fikra na mwelekeo wa mawazo ya Khawariji – ugumu wa akili zao na kutenganika kwa ujuzi na udini katika itikadi yao – vimevujia katika ummah wa Kiislam toka zamani kwenye historia ya Uislam katika sura mbalimbali. Kwa kiasi chochote kile ambacho madhehebu nyingine zingejiona zenyewe ni wapinzani wao, tunaweza bado kuona mwelekeo wa Khawariji katika namna ya fikra zao; na sababu pekee ya hili ni matokeo ya kile tulichokisema: asili ya mwanadamu ni mwizi, na ni rahisi sana kuwa pamoja na mwizi huyu. Idadi kadhaa ya Khawariji wamekuwa siku zote wakiamini kwamba miito yao ingepambana na kitu chochote kipya. Wanatoa vilevile dalili ya utukufu inayoashiria wema kwenye njia ya maisha ambayo tuliizungumzia pale tuliposema kwamba hakuna njia ya kimaada au umbile la nje lililotakaswa katika Uislam, na wanachukulia matumizi ya kila njia mpya kama ni kufru katika Uislam na ukanaji Mungu. Miongoni mwa madhehebu za Kiislam za imani na elimu, na katika sheria pia, tunayaona yale yaliozaliwa kutoka kwenye mwelekeo wa kutenganishwa kwa weledi kutoka kwenye dini, na madhehebu kama hayo ni mifano sahihi ya fikra za Khawariji. Wanakataa kabisa matumizi ya akili katika kugundua ukweli na katika kupata sheria wakilishi; na wanaita huko kufuta akili kama ni bida’a na uovu, ingawa hata hivyo katika aya nyingi, Qur’ani inamwita mwanadamu katika mwelekeo wa a kili yake na inaweka utambuzi wa mwanadamu na ufahamu kama jiwe la pembeni la wito wa Mbinguni. Mu’tazilah, waliokuja kuwepo mwanzoni mwa karne ya pili Hijiria, walichukua asili baada ya majadiliano ya, na uchunguzi kwenye, tafsiri ya imani na kufuru, kama ikiwa tendo la dhambi kubwa humsababisha mtendaji wa dhambi kuwa kafiri au la, na bila shaka kuwepo kwao kulihusika na Khawariji. Mu’tazilah walikuwa watu waliohitaji kiwango fulani cha fikra huru, na kujenga maisha ya kisomi. Ingawa hawakunufaika kutokana na aina yoyote ya msingi au asili ya kisayansi, waliweza kuchunguza na kufikiria juu ya matatizo ya Kiislam, kwa kiwango fulani, kwa uhuru kabisa. Walizitathmini ahadith kwa makini sana kwa kiwango fulani, na walifuata tu yale mawazo na maoni ambayo yalitafitiwa kwa mujibu wa imani zao wenyewe.

130


Tokea mwanzo, hawa Mu’tazilah walichukua msimamo dhidi ya migogoro na upinzani kutoka kwa wale ambao walitegemeza kila kitu juu ya ahadith, na kutoka kwa wenye kufuata yanayofahamika kwa wote – (exoterists). Hawa wa mwishoni, ambao wanatambua maana ya nje tu ya ahadith kama ushahidi, na ambao wasingekuwa na lolote la kufanya kuhusu mwelekeo na maana ya ndani ya Qur’ani na ahadithi, hawakuamini kwamba hukmu yoyote ya wazi ingeweza kufuata kutokana na elimu. Kwa kiasi chochote hawa Mu’tazilah walivyothamini fikra za kielimu, watu hawa walidhani kwamba thamani inaweza kuambatanishwa tu na maana za nje. Katika muda wa karne moja na nusu uliopita katika uhai wa hii madhehebu ya mfarakano, majaliwa ya kushangaza yaliwatukia, mpaka, mwishowe, Ash’ari wakatokea, na mara nyingine tena thamani ya mawazo ya kielimu tu na mifano na mazingatio ya metafizikia halisi yalikataliwa. Hawa Ash’ari walidai kwamba ilikuwa ni muhimu kwa Waislam kuamini katika maana za hadithi za kawaida zinazofahamika kwa wote na sio kufikiri au kufakari juu ya maana zao za kina; kila aina ya swali na jibu, au kwa nini na kwa sababu gani, ilikuwa ni uzushi kwao. Imam Ahmad Hanbal, ambaye alikuwa mmoja wa Maimamu wanne wa Sunni, alikuwa akipinga kwa n guvu sana ile njia ya fikra ya hawa Mu’tazilah, kwa kiasi kwamba alikwenda jela kwa ajili ya maoni yake na akateswa, lakini bado aliimarisha upinzani wake. Mwishowe, hawa Ash’ari walikuwa ndio washindi, na madhehebu ya fikra za kielimu ikafungwa; na ushindi huu ulikuwa pigo kubwa kwa uhai wa usomi wa elimu za Kiislam. Hawa Ash’ari waliwafikiria hawa Mu’tazilah kuwa ni wazushi, na mshairi mmoja wa ki-Ash’ari aliandika hivi, baada ya ushindi wao: Utawala wa watu wa uzushi (bida’a) umefikia mwisho. Kisa chao kimekuwa kigumu na kimevunjika; Kundi ambalo shetani aliliunda kutokana nao Wametambiana wao kwa wao mpaka wamegawanyika. Enyi wamoja katika fikra! Hivi walikuwa naye mwanasheria Au Imam wa kuwaongoza katika uzushi (bida’a) wao? Madhehebu ya Akhbari pia ilikuwa ni namna ya utenganisho wa elimu na dini. Walikuwa ni madhehebu ya fiqihi ya Kishi’ah, na walifikia kilele cha uwezo wao katika karne ya kumi na moja na kumi na mbili Hijiria (karne ya 18 Miladia). Walifanana katika mambo mengi na ile madhehebu ya wanaofuata yanayofahamika kwa wote – (exoteric school) na muhadithiina miongoni mwa Sunni. Katika njia zao za kupatia sheria, madhehebu zote hizi zilifuata mfumo mmoja, tofauti yao pekee ikiwa ni katika ahadith gani wamechagua kuzifuata.

131


Hawa Akhbari walifunga kabisa kazi ya elimu, na walikataa manufaa yoyote au uwezo wa ushahidi wa utambuzi wa elimu katika kupata hukmu za Uislam kutoka kwenye maandiko yao. Walichukulia kwamba kufuata elimu kumekatazwa kabisa, na katika maandishi yao waliendesha kampeni dhidi ya Usũlỉs, waliokuwa wafuasi wa madhehebu nyingine ya fiqih ya Ki-Shi’ah. Walisema kwamba chimbuko pekee la ushahidi lilikuwa ni Qur’ani na Sunnah. Kwa kweli, walisema pia kwamba nguvu ya ushahidi wa Qur’ani nikupitia ufafanuzi uliotolewa na Sunnah na ahadith; hivyo, kwa kweli, waliipuuza kabisa Qur’ani kama ndio chanzo cha ushahidi na walitambua tu maana ya nje ya ahadith kuwa ndio ya kutegemewa. Sasa hivi hatuna mpango wa kuingia kwenye majadiliano ya njia ambazo mikondo mbalimbali ya fikra za Kiislam inavyotofautiana, na kuangalia kwa undani zaidi zile madhehebu ambazo zimetwaa ule utengano kati ya elimu na dini, ambao ndio tuliouita mwelekeo wa Khawariji. Huu ungeweza kuwa mjadala mrefu sana. Lengo letu pekee lilikuwa ni kuonyesha ni athari gani za madhehebu hizi zimekuwepo juu ya kila moja, na kwamba madhehebu ya Khawariji, ingawa huikudumu kwa muda mrefu, imeendelea kuonyesha mwelekeo wake katika kila karne na zama za Kiislam hadi sasa ambapo idadi ya waandishi wa kisasa na “wasomi” wa ulimwengu wa Kiislam wamebuni njia yao ya fikra katika muundo wa kisasa na wa wakati huu kwa kuiunganisha na falsafa ya kiutawala.

132


Kwa matokeo ya kutoona mbali kwao, hawa Khawariji walikataa katakata kuwatambua Waislamu wengine kuwa ni Waislamu, walikataa kuwatambua wanyama waliowachinja kama ni chakula halali, wakatambua umwagaji wa damu yao kama ni halali na kuoleana nao ni haramu.

*

*

*

SIASA YA “KUTUMIA” QUR’ANI Ni karne kumi na tatu sasa ambapo ile siasa ya “kunyanyua Qur’an kwenye mikuki” takriban imeenea miongoni mwa Waislamu. Inakuwa hasa imetapakaa miongoni mwa wale wanaotaka kufaidika nayo kila pale usuffi na kufahamika kwa watu kunapoongezeka na inakuwa yenye kupendelewa kwa mtu kuonyeshea uchamungu wake na utawa. Kuna masomo mawili ya kujifunza kutokana na hili. Kwanza: Wakati wowote mjinga, asiye na elimu na asiyejua anapoonyesha utakatifu na uchamungu, na watu wakayachukulia kama ni ishara ya Mwislamu wa vitendo, zana madhubuti inapatikana kwa wala njama wasio waadilifu. Wala njama kama hao siku zote huwageuza watu hawa kuwa ni chombo kwa faida zao, na kufanya kuwepo kwao kuwa kikwazo kikubwa kwenye maoni ya wanamageuzi wa kweli. Ni jambo la kawaida kabisa kuona watu wapingao Uislamu wakiitumia wazi wazi njia hii, hiyo ni kusema, ni kuifanya nguvu ya

133


Uislamu wenyewe ifanye kazi dhidi ya Uislamu. Ukoloni wa Magharibi ulikuwa umepata uzoefu sana katika matumizi ya njia hii, na kwa matokeo yake umenufaika na mwamsho wa kidanganyifu wa hisia za Waislamu, hasa katika nyanja ya kusababisha mifarakano kati yao. Aibu iliyoje, wakati, kwa mfano, Waislamu waliodhurika wanapopanga kuondosha athari za kigeni, na kisha ukawaona watu wale wale waliotaka kuwaokoa wanageuka kuwa kikwazo katika njia yao kwa jina, na chini ya bendera ya dini. Kwa hakika, kama wengi wa watu ni wajinga na wasioelewa, wanafiki watatumia ngome ya Uislamu wenyewe. Huko Iran, ambako watu wana fursa ya kukipenda na kukifuata kizazi cha Mtume (Ahlu’l-bayt), wanafiki wanajenga ngome dhidi ya Qur’an, Uislamu na kizazi cha Mtume (s.a.w.w.) kuwasaidia wanyang’anyi wa Kiyahudi, walioko nje ya ngome tukufu ya mapenzi ya Ahlu’l-bayt, na jina lao tukufu, na hii ndio sehemu yenye kuchukiza sana ya dhulma dhidi ya Uislamu, Qur’an, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Kizazi chake. Mtume (s.a.w.w.) amesema: ِ‫ف عَلَيَهِمْ سُ َؤ آلتَدْبِير‬ ُ ‫ف عَلَى أُمَتِى آلفَقْرَ وَلَكِنْ اَخَا‬ ُ ‫اِنِى مَا اَخَا‬ Mimi sihofii kuhusu kuvamia kwa umasikini miongoni mwa ummah wangu; bali kile ninachokihofia juu yao ni fikra potofu. Kile ambacho umasikini wa mawazo utakileta kwenye ummah wangu ni kibaya zaidi kuliko kile ambacho umasikini wa uchumi utachowaletea. Pili: Ni lazima tujaribu kuufanya utaratibu wetu wa kupata maana kutoka kwenye Qur’an kuwa wa kweli. Qur’ani ni kiongozi na mwelekezaji inapotegemewa kwenye kumbukumbu za kweli, inapotafsiriwa kwa hekima, wakati mwongozo unapochukuliwa kutoka kwa watu ambao kwa hakika wanaijua Qur’ani, ambao wameimarishwa vema katika elimu za Qur’an. Maadamu utaratibu wetu sio wa kweli, na maadamu hatujifunzi jinsi ya kunufaika kutokana na Qur’an, hatutapata faida yoyote kutokana nayo. Walanguzi au watu wajinga wakati mwingine huisoma Qur’an, na kisha hufuata uwezekano usio sahihi. Kama ambavyo inawezekana kuwa umesikia katika maneno ya Nahju’l-balaghah, “wanalisema neno “kweli” na kisha wanaweka akili 134


zao kwenye uongo!” Huku sio kuitumia Qur’ani au kuihuisha, huku ni kuiua. Qur’ani inawekwa kwenye matumizi pale inapoeleweka kwa ufahamu sahihi. Qur’an siku zote inawasilisha mpango wake katika muundo wa jumla na wa msingi, lakini utoaji na ulinganishi wa maalum kwa wote unategemea kule kuelewa kwetu kwa usahihi na uingiaji akilini. Kwa mfano, hatuoni kilichoondikwa katika Qur’an kwamba katika vita iliyotokea siku fulani kati ya `Ali na Mu’awiyah, `Ali alikuwa kwenye haki; yote tunayopata ndani ya Qur’ani ni kwamba:                       Na ikiwa makundi mawili kati ya waumini yanapingana, basi fanyeni sulhu kati yao, na ikiwa moja la hayo linamdhulimu mwenziwe, basi lipigeni lile linaloonea mpaka lirudi katika amri ya Mwenyezi Mungu. (AlHujarat, 49:9) Hii ndio Qur’an na namna yake ya maelezo; lakini haisemi katika ile vita kadha wa kadha fulani wa falani alikuwa kwenye haki na yule mwingine alikuwa kwenye batili. Qur’an haitaji majina; haisemi: baada ya miaka arobaini, zaidi au kidogo, mtu anayeitwa Mu’awiyah atatokea ambaye atapigana na`Ali, na mje kupigana katika vita hiyo upande wa`Ali. Na wala kamwe haingii katika kutoa habari kwa urefu. Kazi ya Qur’an sio ya kutayarisha orodha ya masuala na kuelekeza lipi liko sawa na lipi sio sawa; kitu kama hicho kingekuwa hakiwezekani. Qur’an imekuja kudumu daima, hivyo ni lazima ifanye mambo ya msingi na ya wakati wote yaeleweke vizuri, ili kwamba uongo uchukue nafasi yake ana kwa ana na ukweli katika kila zama, na watu waweze kutenda kwa mujibu 135


wa kigezo cha haya mambo ya wakati wote. Ni wajibu wa watu, kwa hiyo, kufungua macho kwenye ushauri wa msingi: “Kama pande mbili za waumini zikigombana . . . ”, na kutofautisha kati ya ule upande unaotishia na ule unaofanyiwa vitisho; na kukubali kama ule upande wenye ukaidi unakoma kuwa mkaidi. Lakini kama wataacha, na wakajaribu kuwa wajanja ili tu kujiepusha na kushindwa, na wakajiandaa kwa mashambulizi mapya, na wakawa wakaidi tena, na, katika maneno ya Qur’an, “kama mmoja wao atafanya ufidhuli dhidi ya mwingine”, kuweni imara, na msitoe mwanya kwenye hila zao. Ni juu ya watu wenyewe kutofautisha katika mambo yote haya. Qur’an inataka kwamba Waislamu waweze kuwa kielimu na kijamii wamekomaa, na matokeo muhimu ya ukomaaji wa kielimu kama huo ni uwezo wa kutofautisha kati ya mtu muadilifu na mtu dhalimu. Qur’ani haikuja kuwa kwa watu daima kama mlezi juu ya mtoto, kutekeleza mambo maalum ya maisha yao kama mhifadhi binafsi, na kutaja bayana kila jambo maalum kwa dalili yakinifu na kiashirio. Kwa kweli, kuwajua watu, kiwango cha uwezo wao, mipaka ya kuwa tayari kwao, na uhusiano wao, kwenye Uislamu na hali za uhakika wa Kiislamu kwenyewe ni wajibu, na mara kwa mara tunaupuuza wajibu huu. `Ali, amani iwe juu yake, alisema: ُ‫أَنَكُمْ لَنْ تَعْرِفُوا الرُ شْدَ حَتَى تَعْرِفُوا الَذِي تَرَ َكه‬ Kamwe hutaijua haki na kufuata njia sahihi mpaka umjue yule mtu ambaye ameitelekeza.21 Kujua kanuni na maneno ya kawaida peke yake hakutoshi mpaka ulinganifu na marejeo kwenye maelezo, viwe vimepatikana. Kwani inawezekana kwamba, kupitia kosa moja la hukmu juu ya wahusika na 21

Nahju’l-balaghah, hotuba na: 146.

136


watu binafsi au kwa kutokujua mazingira yake, mtu atatenda kwa jina la haki na Uislamu na chini ya bendera ya Uislamu, dhidi ya Uislamu na haki, na kwa ajili ya uongo. Dhulma na madhalimu, haki na waadilifu vimetajwa ndani ya Qur’ani, lakini utekelezaji wake lazima utafutwe. Tusichanganye dhulma na haki kuwa ni haki, na kisha tukate kichwa cha haki na ukweli kwa jina la kile tunachodhania kuwa ni kanuni ya wakati wote na hukmu ya Qur’ani.

UMUHIMU WA KUPIGA VITA UNAFIKI Mapambano magumu zaidi ni yale dhidi ya unafiki, kwani ni mapambano dhidi ya wajanja wanaowatumia wapumbavu kama silaha zao. Pambano hili ni gumu kwa kiwango cha juu zaidi kidogo kuliko vita na ukafiri, kwa sababu, katika vita na ukafiri mapambano ni dhidi ya mkondo wa wazi, wa dhahiri na usiojificha, ambapo kupambana dhidi ya unafiki kwa kweli ni kupambana dhidi ya ukafiri uliojificha. Unafiki una sura mbili: moja ni ile sura ya nje – Uislamu na Muislamu; na nyingine ni ya ndani – kutoamini (ukafiri) na uovu. Ni vigumu kwa watu wa kawaida kutambua hii sura ya pili, na wakati mwingine haiwezekani; na kwa hiyo mapambano na unafiki yanaishia katika kushindwa kwa sababu idadi kubwa ya watu hawana upeo mpana wa kutosha kujipenyeza kwenye vina vya ndani vya tabia za vitu. ‘Amir al-mu’minin (a.s) aliandika Muhammad ibn Abu Bakr, hivi:

katika

barua

aliyomtumia

Mtume wa Mwenyezi Mungu aliniambia: “Siuhofii ummah wangu kutokana na mu’min au kafiri. Kwani kwa mu’min, Allah swt atamlinda kwa sababu ya imani yake, na, kwa kafiri, Allah swt atamdhalilisha kutokana na ukafiri wake. Lakini nahofia juu ya kila mmoja wenu ambaye ni mnafiki moyoni

137


mwake na mjuzi wa kuongea. Anaongea unayoweza kuyakubali, lakini anafanya usiyothubutu kuyaafiki.”22 Mtume (s.a.w.w.) hapa anaonyesha hatari iliyoko kwenye unafiki na kwa mnafiki, kwa sababu wengi wa watu hawajui na hawaelewi, na wanadanganywa na mwonekano wa nje.23 22

ibid, barua na: 27. Hivyo tunaona katika mabadiliko anapotokea kwa maslahi ya madhalimu na walanguzi mara tu hujigeuza 23

historia yote ya Kiislam kwamba kila wakati mleta niaba ya watu kurekebis ha hali ya jamii yao na dini na walanguzi yanapokuwa hatarini, hawa madhaalim na na huuvaa usuffi na kuonyesha uchamungu wao na dini.

Wakati al- Ma’mun ar-Rashid, yule khalifa wa Bani Abbas maarufu katika historia ya watawala kwa upenda anasa na ubadhilifu wake, alipoona kwamba Alawi wako kwenye mamlaka, alibadili nguo na akajitokeza hadharani katika mwanga mpya. Ndipo Abu Hanifah al-Iskafi, ambaye, hakuchukua hata senti kutoka kwake, wala kupata manufaa kutoka kwake, akamsifu yeye juu ya hili na akatunga ushairi huu wa wasifu: Ewe Ma’mun, ambaye mfano wako miongoni mwa watawala wa Dola ya Kiislam Haujawahi kuonekana, kwa Mwarabu au kwa mkulima wa kawaida, Aliyevaa koti la ngozi kwa muda mrefu Mpaka likazeeka, likachakaa na kufundikana. Marafiki wa karibu walishangazwa na kupindukia huku Na wakamuulizia juu sababu ya hili. Akasema: “Hadithi huachwa nyuma na wafalme Miongoni mwa Waarabu na wasio Waarabu, sio kwa pamba laini au kitani!” Na kadhalika, kila mmoja kwa namna yake akizidisha katika siasa iliyojaribiwa vizuri na ya uonevu ya “kunyanyua Qur’ani juu ya mikuki”, na kushinda juhudi zote, na kujitoa mhanga, akizuia maendeleo yaliyofufuka tena. Hiki si chochote bali ni ule ujinga na kutokujua kwa watu, ambao haujui kutofautisha kati wito na hali halisi, hivyo hufunga njia ya kuinukia na kujibadili kwao wao wenyewe, na kisha wakaelewa kwamba kazi yote ya maandalizi imefutwa na kwamba ni lazima waan ze mwanzoni tena. Katika mambo yote makuu tunayojifunza kutoka kwenye maisha ya `Ali, tunaona kwamba aina hii ya mapambano haikuzuiliwa kwenye kundi lolote maalum, bali kwamba kila mahali ambapo kikundi cha Waislam, au wale walioandaliwa katika hali ya dini, wanakuwa ni chombo kwa ajili ya ongezeko la wasiokuwa Waislam na

138


Tahadhari ni lazima ichukuliwe katika ukweli kwamba kwa kila kidogo ambacho upumbavu unakiongeza, njia inafunguka zaidi kwa unafiki. Kupambana na wapumbavu na upumbavu ni kupambana na unafiki vilevile, kwani wapumbavu ni zana mikononi mwa wanafiki. Bila shaka, kupambano na wajinga na ujinga ni kuwanyang’anya silaha wanafiki, na kuuondoa upanga mikononi mwao.

*

*

*

ALI - IMAM NA KIONGOZI WA HAKI Katika hali zote za uhai wa`Ali, za historia na wasifu wake, silika na tabia zake, sifa na mwenendo wake, maneno na mazungumzo yake, kuna maelekezo, mifano ya kufuatwa, mafunzo na uongozi. Kama vile “nguvu ya mvuto” wa `Ali ilivyotufundisha na kutuelekeza, vivyo hivyo pia na “nguvu zake za kingamizo”. Kwa kawaida katika ziyarat 24 kwa `Ali na wale Watoharifu wengine, tunadai sisi ni “rafiki wa rafiki yako na adui wa adui yako”. Njia nyingine ya kuliweka hili itakuwa ni kusema: “Tutaliendea lile jambo ambalo liko kwenye kuendelea kwa ukoloni, na wakoloni hawa, kwa ajili ya ulinzi wa maslahi yao binafsi, huwapa kinga na kisha wakawatumia kama ngao yao, kiasi kwamba inakuwa vigumu kuwapiga bila kuziua kwanza ngao zao, kisha ni muhimu kuanza kwa kupigana na hizi ngao zao na kuzianagamiza ili kuondoa kikwazo njiani na kuwa na uwezo wa kushambulia katika kitovu cha adui. Huenda njama za Mu’awiyah zilikuwa na kuhusika kwa namna fulani na hujuma za Khawariji, na kwa hiyo hata katika siku ile Mu’awiyah, au angalau watu kama al-Ash’ath ibn al-Qays, na wakorofi wengine katika hujuma na ghasia hizo, walitoa kinga kwa Khawariji. Historia ya Khawariji inatufundisha ule ukweli kwamba katika kila muibuko (wa kivita), ngao ndio ziondoshwe kwanza na wajinga wapigwe, kama vile `Ali, baada ya matukio ya sulhu, kwanza kabisa aliwashambulia Khawariji na kisha akadhamiria kufuatilia nyendo za Mu’awiyah. 24

Aina ya maombi anayoombwa kupitia kwa mmoja au ma‘sum (wasio na dhambi) wote kumi na wanne – Mtume, binti yake Fatimah, na Maimam kumi na wawili. (tr.)

139


mwelekeo wa nguvu ya mvuto kwako na ambalo unavutia kwalo, na tutaamua kuwa mbali na lile jambo ambalo unalikanya.” Tulichokisema katika kitabu hiki ni tangazo la wazi la nguvu za Ali za “mvuto na kingamizo,” na uchache wa maneno yetu uko wazi kabisa, hususan katika suala hili la “kingamizo” lake. Hata hivyo, ni wazi kutokana na tuliyosema kwamba `Ali, aliyakanya kabisa makundi mawili – wanafiki wajanja, na watawa wajinga. Masomo haya mawili yanatosha kwa wale wanaodai kuwa ni wa “kundi” lake – Shi’ah – kufungua macho yao na sio kufanywa mazuzu na wanafiki, kuweka maono yao kuwa makali na kutupilia mbali ile hali ya muonekano wa nje wa mambo, mambo mawili ambayo kwayo jumuiyah ya Ki-Shia kwa sasa wanateseka nayo sana. * * * * *

140


Back cover

MIKINGAMO ILIYOMZUNGUUKA IMAMU ALI (AS) Kitabu hiki, “Mikingamo iliyomzunguuka Imamu ‘Ali (as)” kinazungumzia matatizo yaliyompata Imamu ‘Ali (as) na mafanikio kwa ujumla. Wanachuoni wa ki-Islamu wa Madhehebu mbali mbali na wasiokuwa Waislamu, wameandika vitabu, risala na makala nyingi zenye kumuelezea Imamu ‘Ali juu ya maisha yake, matatizo yaliyompata katika kuungoza Ummah huu wa ki-Islamu na mafanikio yaliyopatikana kutokana na juhudi zake. Marhum as-Sheikh Allamah Murtadha Mutahhari, Mwanachuoni mahiri, mwadnishi wa kitabu hiki, yeye ameelezea katika kitabu hiki mikingamo aliyowekewa Imamu ‘Ali katika kutekeleza majukumu yake kama Imamu na jinsi alivyoweza kuyatatua matatizo hayo na mikingamo aliyokuwa anafanyiwa. Ndani ya kitabu hiki utasoma kuhusu:  Nguvu ya mvuto ndani ya ‘Ali  Upendo  Siri ya nguvu ya mvuto wa ‘Ali’  Nguvu ya upendo katika jamii  Busara ya demokrasia ya `Ali  Mapenzi juu ya Ali ndani ya Qur’an 141


   

Jinsi `Ali alivyopata maadui Umuhimu wa kupiga vita unafiki Khawarij ni nani? `Ali, Imamu na kiongozi wa haki

Ufafanuzi wa haya na mengine zaidi tafadhali ungana na mwandishi ndani ya kitabu hiki. Kimetolewa na Kuchapishwa na: Al-Itrah Foundation S.L.P. 19701, Daressalaam. Tanzania. Simu: +255 22 2127555 / 2110640 Barua pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv.com Katika mtandao: www.alitrah.info

142


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.