Mtazamo wa ibn taymiyyah juu ya imam ali (as)

Page 1

Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu Ya Imam Ali (a.s.)

ABU TALIB

Jabali Imara la Imani Kimeandikwa na: Kimeandikwa na: Sheikh Ja’far Subhani Faisal Hasan

Kimetarjumiwa na: ABDUL- KARIM J. NKUSUI

Kimetarjumiwa na: Muhammad A. Bahsan Kimehaririwa na: Alhaji Hemedi Lubumba (Abubatul)

Kimehaririwa na: Hemedi Lubumba Selemani

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 1

1

11/25/2014 3:00:31 PM


‫ﺗﺮﺟﻤﺔ‬

‫ﺁﺭﺍء ﺍﺑﻥ ﺗﻳﻣﻳﺔ ﻓﻲ ﺍﻹﻣﺎﻡ ﻋﻠﻲ )ﻉ(‬ ‫‪2‬‬

‫ﺗﺮﺟﻤﺔ‬

‫ﻋﻠﻲِﻜﺮﺍً) ﻭﻉﻣ(َﻨﻬﺠﺎً‬ ‫ﺗﻴﻤﻴﺔ ﻓ‬ ‫ﻓﻲﺍﺑﻦ‬ ‫ﻛﺘﺎﺏ‪:‬‬ ‫ﺍﻟﺜﺎﻟﺚ‬ ‫ﺍﻹﻣﺎﻡ‬ ‫ﺍﺑﻥﻣﻦﺗﻳﻣﻳﺔ‬ ‫ﺍﻟﻔﺼﻞﺁﺭﺍء‬ ‫ﺍﻟﻔﺼﻞ ﺍﻟﺜﺎﻟﺚ ﻣﻦ ﻛﺘﺎﺏ‪ :‬ﺍﺑﻦ ﺗﻴﻤﻴﺔ ﻓِﻜﺮﺍً ﻭﻣَﻨﻬﺠﺎً‬

‫ﺁﺭﺍء ﺍﺑﻥ ﺗﻳﻣﻳﺔ ﻓﻲ ﺍﻹﻣﺎﻡ ﻋﻠﻲ )ﻉ(‬ ‫ﺍﻟﻔﺼﻞ ﺍﻟﺜﺎﻟﺚ ﻣﻦ ﻛﺘﺎﺏ‪ :‬ﺍﺑﻦ ﺗﻴﻤﻴﺔ ﻓِﻜﺮﺍً ﻭﻣَﻨﻬﺠﺎً‬

‫ﺁﺭﺍء ﺍﺑﻥ ﺗﻳﻣﻳﺔ ﻓﻲ ﺍﻹﻣﺎﻡ ﻋﻠﻲ )ﻉ(‬ ‫ﺗﺄﻟﻳﻑ‬ ‫ﺗﺄﻟﻳﻑ‬ ‫ﺗﺄﻟﻳﻑ‬ ‫ﺍﻟﻔﺼﻞ ﺍﻟﺜﺎﻟﺚ ﻣﻦ ﻛﺘﺎﺏ‪ :‬ﺍﺑﻦ ﺗﻴﻤﻴﺔ ﻓِﻜﺮﺍً ﻭﻣَﻨﻬﺠﺎً‬ ‫ﺟﻌﻔﺭ ﺍﻟﺳﺑﺣﺎﻧﻲ‬ ‫ﺍﻟﺳﺑﺣﺎﻧﻲ‬ ‫ﺍﻟﺷﻳﺦﺟﻌﻔﺭ‬ ‫ﺍﻟﺷﻳﺦ‬

‫ﺍﻟﺷﻳﺦ ﺟﻌﻔﺭ ﺍﻟﺳﺑﺣﺎﻧﻲ‬

‫ﺗﺄﻟﻳﻑ‬ ‫ﺍﻟﺷﻳﺦ ﺟﻌﻔﺭ ﺍﻟﺳﺑﺣﺎﻧﻲ‬

‫ﻣﻥ ﺍﻟﻠﻐﺔ ﺍﻟﻌﺭﺑﻳﺔ ﺇﻟﻰ ﺍﻟﻠﻐﺔ ﺍﻟﺳﻭﺍﺣﻠﻳﺔ‬

‫ﻣﻥ ﺍﻟﻠﻐﺔ ﺍﻟﻌﺭﺑﻳﺔ ﺇﻟﻰ ﺍﻟﻠﻐﺔ ﺍﻟﺳﻭﺍﺣﻠﻳﺔ‬

‫‪11/25/2014 3:00:32 PM‬‬

‫‪01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 2‬‬


‫ﺁ‬ ©Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 - 17 - 003 - 6 Kimeandikwa na: Sheikh Ja’far Subhani Kimetarjumiwa na: Muhammad A. Bahsan Kimehaririwa na: Hemedi Lubumba Selemani Kimepangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation Toleo la kwanza: Septemba, 2013 Nakala: 2000 Toleo la pili: Aprili, 2015 Nakala: 2000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. - 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: www.alitrah.info

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 3

11/25/2014 3:00:32 PM


YALIYOMO Neno la Mchapishaji.............................................................................. 01 Dibaji..................................................................................................... 03 Utangulizi.............................................................................................. 04 Ibn Taymiya apinga fadhila za Imam ‘Ali (a.s.).................................... 07 1. Kumtuhumu Imam ‘Ali (a.s.) kwamba alikuwa akimuudhi Bibi Fatima (a.s.)............................................................................. 13

Utafiti wa Riwaya kwa Upande wa Sanadi:..................................... 20

Masuala Kadhaa Ndani ya Riwaya hii:............................................ 23

2. Madai ya Ibn Taymiya Kwamba Maswahaba Wengi Walikuwa Wakimchukia ‘Ali (A.S.)....................................... 32 3. Ibn Taymiya aipinga Hadithi ya Undugu....................................... 39 4. Ibn Taymiya apinga Hadithi ya Ndege........................................... 45

Kuathirika Kimadhehebu ndiko Kulikopelekea Kudhoofishwa Hadithi ya Ndege............................................................................ 53

Mpingaji hanufaiki na Hoja:........................................................... 61

5. Tuhuma zake dhidi ya Imam ‘Ali (a.s.) kwamba alipigana kwa ajili ya dunia na sio kwa ajili ya dini....................................... 64 6. Ibn Taymiya apinga kumuudhi Imam ‘Ali (a.s.) kuwa ni alama ya kuwatambua wanafiki..................................................... 73 iv

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 4

11/25/2014 3:00:32 PM


7. Upanga wa ‘Ali (a.s.) haukuwa na faida.......................................... 78 8. Madai yake kwamba watu wengi walikataa kumpa Imam ‘Ali (a.s.) kiapo cha Utiifu..................................................... 85 9. Matokeo ya Ukhalifa wa Imam ‘Ali (a.s.)........................................ 94 10. Ibn Taymiya na ushukaji wa Ayatul – Wilaya kwa Imam ‘Ali (a.s.)...............................................................................100 11. Mitazamo mingine ya Ibn Taymiya kwa Imam ‘Ali (a.s.) na Maswahaba wake......................................................................105 12. Ibn Taymiya na Hadithi: “Wewe ni Kiongozi wa kila Muumini baada yangu”................................................................. 120 13. Ibn Taymiya na Hadithi ya kufunga milango yote isipokuwa mlango wa ‘Ali (a.s.).................................................... 124 14. Ibn Taymiya apinga Hadithi ya Lango la Jiji la Elimu................. 130 15. Ibn Taymiya na kauli ya Mtume (s.a.w.w.): “Kadhi wenu ni ‘Ali (a.s.)”............................................................. 145 16. Ibn Taymiya na Hadithi ya kupambana dhidi ya wavunja viapo vya Utiifu, waasi na waovu................................................. 148 17. Ibn Taymiya na kauli ya Mtume (s.a.w.w.): “Mwenye kumpenda ‘Ali, amenipenda mimi”.............................. 153 18. Ibn Taymiya na kushuka Sura ‘Hal Ataa’ kwa Ahlul Bayt (a.s.)...................................................................................... 157 19. Mjadala wa Ibn Taymiya juu ya sifa za kipekee za Imam ‘Ali (a.s.)......................................................................... 163 20. Upofu wake juu ya Qur’an............................................................ 165 v

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 5

11/25/2014 3:00:32 PM


01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 6

11/25/2014 3:00:32 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Neno la Mchapishaji

K

itabu ulichonacho mikononi mwako kinaitwa, Ibn Taymiyyah Fikran wa Manhajaa kilichoandikwa kwa lugha ya Kiarabu na Sheikh Ja’far Subhani. Sisi tumekiita, Mtazamo wa Ibn Taymiyyah juu ya Imam Ali (a.s.). Kitabu hiki kinazungumzia sehemu tu ya historia ya Ibn Taymiyyah inayohusu itikadi yake potofu juu ya Mtume (s.a.w.w), Imam Ali (a.s) na kizazi cha Mtume (s.a.w.w). Ibn Taymiyyah kama inavyofahamika alikuwa mfuasi wa Imam Hanbal, lakini baadaye alibadilika na kwenda kinyume na Imamu wake na madhehebu yake ya Hanbali. Kama kawaida alipata wafuasi wengi, hivyo, akawa na kundi lake na mafundisho yake yakaenea sehemu nyingi. Alipata upinzani mkubwa sana kutoka kwa wanavyuoni wa wakati huo ambao waliaandika vitabu vingi kuwatahadharisha Waislamu juu ya fitna hiyo iliyokuwa ikienezwa na Ibn Taymiyyah na waliomfuata nyuma yake. Ibn Taymiyyah amewahi kuandika vitabu kadhaa katika matawi mbalimbali ya dini kwa mtazamo wake akipinga mambo mengi ya asili ya dini na akawapotosha watu wengi. Baada ya kufariki kwake, mtu aliyekuja kumfuata na kuhuisha mafundisho yake alikuwa ni Muhammad bin Abdul Wahhab, ambaye alitumia nguvu huku akisaidiwa na watawala kueneza mafundisho yake, na wafuasi wake wakajulikana kwa jina lake kama Wahabi. Mawahabi hawapendi kuitwa kwa jina la mwasisi wao. Wanatumia majina kadha wa kadha, kama vile, Answar Sunnah, Salafi, n.k. 1

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 1

11/25/2014 3:00:32 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa makubwa hususan wakati huu wa sayansi na teknolojia kubwa ambapo ngano, hadithi za kale na upotoshaji wa historia ni vitu ambavyo havina nafasi kwa watu wa sasa. Taasisi yetu ya Al-Itrah imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili. Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni chenye manufaa makubwa kwao. Tunawashukuru ndugu yetu Muhammad A. Bahsan kwa kukitarjumi kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili, pia na wale wote waliosaidia kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake na kuwa mikononi mwa wasomaji. Allah Mwenye kujazi awalipe wote malipo mema hapa duniani na huko Akhera. Amin! Mchapishaji Al-Itrah Foundation

2

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 2

11/25/2014 3:00:33 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

DIBAJI ‫بسم ﷲ الرحمن الرحيم‬ Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema Mwenye kurehemu.

N

dugu msomaji mpendwa, kitabu hiki kilicho mikononi mwako ni tafsiri ya sehemu tu ya kitabu ‘Ibn Taymiya Fikran Wamanhaja’ kilichotungwa na mwanachuoni mashuhuri Allama Sheikh Ja’far Subhaniy. Katika kitabu chake hicho ameeleza itikadi mbalimbali za Ibn Taymiya namna anavyomuitakidi Mtume (s.a.w.w.) pamoja na Ahlulbayt wake (a.s.) Kwenye kitabu hiki tumeamua kutaja sehemu moja ya itikadi yake, nayo ni kuhusiana na Imam Ali (a.s.) Kwa kweli Ibn Taymiya ameonesha chuki za wazi dhidi yake, kwa kukataa na kupinga kila jema linalomhusu yeye (a.s.), licha ya kwamba mema hayo ya Imam Ali (a.s.) pamoja na fadhila zake zimethibitishwa katika vitabu sahihi na kutoka katika kinywa kitakatifu cha Mtume (s.a.w.w.) na kukubaliwa na jopo la wanachuoni wa madhehebu yake, kama vile Imam Ahmad ibn Hanbal. Muhammad A. Bahsan

3

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 3

11/25/2014 3:00:33 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

UTANGULIZI MSIMAMO WA AHMAD IBN HANBAL JUU YA IMAM ALI (A.S.)

N

i kweli kwamba Ahmad ibn Taymiya ni mfuasi wa madhehebu ya Imam Ahmad ibn Hanbal ambaye alikuwa akidhihirisha utukufu wa Ahlulbayt (a.s.) hasa kwa wa mwanzo wao; Imam Ali (a.s.), na hayo utayashuhudia katika mlango unaoelezea fadhila za Maswahaba. Na hapa tutajaribu kutaja baadhi ya mambo yanayodhihirisha msimamo wa Imam Ahmad ibn Hanbal juu ya Imam Ali (a.s.) na pia msimamo wake kwa yule aliyemfanyia uhasimu (uadui) Imam Ali (a.s.), naye ni Muawiya ibn Abi Sufiyani: 1. Muhammad ibn Mansur at-Tusiy amesema: “Tulikuwa kwa Ahmad ibn Hanbal, mtu mmoja akamwambia: Ewe Abu Abdullah, unasemaje juu ya hadithi hii iliyopokewa kwamba Ali amesema: ‘Mimi ni mgawaji wa Moto.’ Imam Ahmad akasema: ‘Ni kipi kinachowafanya kuipinga hadithi hiyo? Je, hatujapokea ya kwamba Mtume (s.a.w.w.) alisema kumwambia Ali: Hakupendi wewe isipokuwa Muumini, na wala hakuchukii isipokuwa mnafiki?’ Tulisema: Ndiyo. Akasema: ‘Muumini anakwenda wapi?’ Tukasema: Anakwenda Peponi. Akasema: ‘Mnafiki anakwenda wapi?’ Tukasema: Anakwenda Motoni. Akasema: ‘Basi Ali ni mgawaji wa Moto.’’’1

2. Na akasema tena: “Nilimsikia Ahmad ibn Hanbal akisema: 1

Twabaqaatul- Hanabilah Juz. 1, Uk. 320. 4

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 4

11/25/2014 3:00:33 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

“Hakuna Swahaba wa Mtume (s.a.w.w.) aliye na fadhila bora zaidi kuliko Ali (r.a.)’’2 3. Ibn Jawziy amesimulia kwa njia ya Abdullah ibn Ahmad ibn Hanbal, amesema: “Nilimuuliza baba yangu: Unasemaje kuhusiana na Ali na Muawiya? Aliinamisha kichwa chake, kisha akasema: Niseme nini kuhusiana nao? Ali alikuwa na maadui wengi sana, maadui wake walijaribu kumtafutia sifa mbaya, lakini hawakuzipata, baadaye wakaenda kwa mtu aliyempiga vita (Muawiya) wakambambikizia sifa nzuri kwa sababu ya chuki zao kwake (kwa Imam Ali (a.s.).’’3 Ibn Hajar amesema baada ya kunakiliwa maneno haya: “Hii inaashiria juu ya yale waliyoyabuni kwa Muawiya, fadhila ambazo hazina mashiko yoyote, na kumepokewa hadithi nyingi zenye kueleza fadhila na ubora wa Muawiya, lakini si zenye kusihi katika upande wa sanadi, na haya yamehakikiwa vyema na Is-haq ibn Rahawayhi, An-Nasaiy na wengineo. 4. Fikra ya kuwepo Makhalifa wanne waongofu, ni jambo lililoasisiwa na Ahmad ibn Hanbal, na ilikuwa ni jambo zito kwa watu walioshikamana na hadithi (wafuasi wa Uthmani ibn Affan) kukubali Ukhalifa wa Imam Ali (a.s.), kama tunavyomuona Abi Ya’laa akipokea kwa sanadi yake kutoka kwa Duwayza al-Humsiy akisema: “Niliingia kwa Ahmad ibn Hanbal pale alipomfanya Ali r.a. kuwa ni Khalifa wa nne, nikasema: Ewe Abu Abdullah! Kufanya hivi ni kumdhalilisha Talha na Zubair. Akasema: Ni mabaya yalioje uliyoyasema, sisi tuna makosa gani kutokana na vita vya watu! Nikasema: Mwenyezi Mungu akutengenezee 2 3

Mustadrak Alaa Swahiyhayn Juz. 3, Uk. 107. Al-Maudhuatu libn Jawzi Juz. 2, Uk. 24. 5

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 5

11/25/2014 3:00:33 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

mambo yako, hayo nimeyasema kwa sababu ya kumfanya Ali kuwa ni Khalifa wanne na yale yanayopaswa kwa maimam kabla yake, aliniambia: Ni kitu gani kinachonizuia kufanya hivyo? Nikasema: Ni hadithi ya ibn Umar. Akaniambia: Umar ni bora kuliko mtoto wake, kwani Umar alimridhia Ali kuwa Khalifa kwa Waislamu, pale alipomteua kuwa katika mashauriano ya kumpata Khalifa, na Ali ibn Abi Talib amejiita mwenyewe kwamba ni Amirul-Muuminina. Nikasema: Waumini hawana Amiri! Basi nikaondoka kutoka kwake.’’4

4

Twabaqaatul- Hanabilah Juz. 1, Uk. 393. 6

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 6

11/25/2014 3:00:33 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Ibn Taymiya apinga fadhila za Imam Ali (a.s.)

T

umeuona msimamo wa Imam wa Mahambali ambaye ni Imam wa Ibn Taymiya juu ya Imam Ali (a.s.), Ibn Taymiya alipaswa kumfuata Imam wake, lakini amemkhalifu katika hilo na kukataa katakata juu ya Imam Ali (a.s.) kupata fadhila hizo na utukufu, amezikataa sifa nyingi za Imam Ali (a.s.) zilizonakiliwa na wapokezi mbalimbali wa hadithi, na kuzieleza kwa ibara ambazo uso unaona aibu na kalamu kuogopa kuziandika! Upingaji wake huo wa fadhila za Imam Ali (a.s.) umewashitua wanachuoni wa ki-Ahlu Sunna kiasi cha kuwafanya wazipinge rai zake kuhusiana na fadhila za Imam Ali (a.s.). Ibn Hajar anasema: “Nimeyapitia majibu yaliyotajwa (kitabu cha Ibn Taymiya kiitwacho ‘Minhaju Sunna’ ambacho ni majibu juu ya kitabu kiitwacho ‘Miftahul Karama’ cha Allamatul Hilliy), nimemgundua kuwa ni mwenye makosa mengi katika kujibu hadithi alizozinakili Ibn Mutahhar (Allamatul Hilliy), ijapokuwa nyingi kati ya hizo ni za kutungwa na zisizo na mashiko, lakini pia katika jibu lake amezikataa hadithi nyingi ambazo ni sahihi, hiyo ilitokana na kutegemea sana hadithi alizokuwa amezihifadhi, na wakati wa kutunga kitabu chake hicho hakuweza kuzikumbuka kutokana na kuhifadhi kwake hadithi nyingi, na mwanadamu ana tabia ya kusahau, na ni mara ngapi katika kuyadhoofisha kupita kiasi maneno ya Mashia imepelekea kupinga fadhila za Ali r.a., na maelezo haya hayahitaji ubainifu na kuelezewa kwa 7

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 7

11/25/2014 3:00:33 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

mifano, na Allamatul Hilliy alipopata vitabu vilivyotungwa na Ibn Taymiya alimuandikia kwa beti za mashairi.5 Na beti hizo za mashairi ambazo Allamatul Hilliy amezitunga kumuambia Ibn Taymiya ni kama zifuatazo: “Lau kama unaelewa kila wakielewacho wanadamu wote, basi ungekuwa rafiki wa kila ulimwengu. Lakini umekuwa mjinga kiasi cha kusema, wote wasiofuata rai yako si watambuzi.” Na jambo la ajabu ni kwa Sheikh Taqi Diin Assabakiy ambaye alimjibu Ibn Taymiya na kumtuhumu kwa kuzidisha mambo na ni kwamba huichanganya haki kwenye batili, amepongeza majibu ya Ibn Taymiya kwa Allamatul Hilliy, kama alivyosema katika kaswida yake: “Na ibn Mutwahhar, tabia zake hazijatoharika, analingania kwenye urafidhi (Ushia), akiwa ni mwenye chuki za kupindukia. Na Ibn Taymiya amemjibu kwa majibu mazuri yalio kamilika.” Ninasema: Mwenyezi Mungu ailaani chuki, Assabakiy anadiriki kusema maneno haya juu ya Allamah Ibn Mutwahhari, licha ya kwamba Ibn Hajar al-Asqalaniy amemsifu kwa kusema: “Ibn Mutwahhari alikuwa mtu mashuhuri na mwenye tabia nzuri.’’ Na pindi kilipomfikia kitabu cha Ibn Taymiya alisema: “Lau kama anafahamu niyasemayo ningemjibu.’’ Kutokana na beti hizo mbili za mashairi za Assabakiy, Sayyid Muhsin al-Amini amelazimika kuzisahihisha beti hizo kwa kusema: 5

Lisanul- Mizan Juz. 6, Uk. 319. 8

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 8

11/25/2014 3:00:33 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

‘’Na Ibn Mutwahhari, tabia zake zimekuwa nzuri, ni mlinganiaji wa haki, bila ya kuwa na chuki, na Ibnu Taymiya alimjibu, lakini hakufanya vyema katika kumjibu katika kila kipengele.’’ Baada ya hapo Sayyid aliongeza beti nyingine zifuatazo: “Yanamtosha Ibn Taymiya yale aliyokuwa akiyaamini yeye na wafuasi wake kutoka Misri au Damascus, matatizo yake yalidhihiri baada ya kukaa jela, alitoka na fikra ya kwamba Mwenyezi Mungu ana viungo, na Mola wetu Muumba ametakasika na sifa hiyo ya kuwa na viungo, ni kwamba siku moja alibainisha wazi katika mimbari yake huko Sham (Syria), hili linatosha kuwa ni miongoni mwa aibu zake, alisema Mwenyezi Mungu huteremka kutoka mbinguni kama mimi ninavyoteremka kutoka kwenye mimbari, kwa kweli hili ni miongoni mwa aibu zake.’’6 Kisha mfuasi wa madhehebu ya Ibn Taymiya wa zama hizi anayejulikana kwa jina la Sheikh al-Baniy ameisahihisha hadithi maarufu ijulikanayo kwa jina la hadidhi ya ‘Ghadir’ katika kitabu chake ‘Silsilatul- Ahaadithi Swahihah’ inayoelezea kauli ya Mtume (s.a.w.w.) isemayo: “Ambaye mimi ni kiongozi wake, basi Ali ni Kiongozi wake, Ewe Mola Wangu! Muunge mwenye kumuunga Ali na mfanyie uadui mwenye kumfanyia uadui Ali.’’ Baada ya uchambuzi wa hadithi hii, al-Baniy amesema yafuatayo: “Kilichonisukuma kuinakili hadithi na kubainisha usahihi wake ni kumuona Sheikhul-Islamu; Ibn Taymiya akidhoofisha sehemu ya kwanza ya hadithi, ama sehemu ya pili, amedai kwamba ni uzushi! Kwa uoni wangu ni kwamba amefanya hivyo kutokana na haraka yake ya kudhoofisha ha6

A’yanu Shia Juz. 5, Uk.398 9

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 9

11/25/2014 3:00:33 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

dithi kabla ya kukusanya njia zake na kuzipitia kwa makini, na Mwenyezi Mungu ndiye wa kuombwa msaada.’’7 Utetezi huu wa kumtetea Ibn Taymiya ya kwamba hufanya haraka katika kuzidhoofisha hadithi kabla ya kuzikusanya njia zake, ni jambo ambalo si la kweli, na ukweli kwa kila mwenye uelewa na uadilifu kuhusu namna Ibn Taymiya anavyoamiliana na hadithi, ataona si kwamba tu Ibn Taymiya anafanya haraka, bali ni hufanya makusudi kuzidhoofisha hadithi zinazoelezea fadhila na ubora wa Imam Ali (a.s.), hii ni kutokana na chuki alizonazo katika nafsi yake dhidi ya Imam Ali (a.s.) Inakumbukwa kwamba Ibn Taymiya amesema: “HadithulMuwaalaati (inayozungumzia Uongozi wa Ali (a.s.) aliyoipokea Tirmidhiy na Ahmad katika Musnad yake kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.), kwamba amesema: “Ambaye mimi ni kiongozi wake, basi Ali ni Kiongozi wake.’’ Ama ziada ambayo inasema: “Ewe Mola wangu! Muunge mwenye kumuunga Ali na mfanyie uadui mwenye kumfanyia uadui Ali.’’ Hakuna shaka kwamba sehemu hii ni ya uzushi.’’8 Hivi ndivyo Ibn Taymiya anavyodai ya kwamba sehemu ya pili ya hadithi imezushwa, licha ya kwamba sehemu hiyo imesimuliwa kwa mapokezi sahihi kutoka kwa Abi Tufail, kutoka kwa Ahmad katika Musnad yake, juzuu ya 4, ukurasa wa 370, An-Nasaiy katika kitabu chake kijulikanacho kwa ‘Khaswaiswu’ ukurasa wa 90, Ibn Habban katika sahihi yake, ukurasa 2205, Ibn Abi A’swim katika ‘Sunna’, ukurasa 1367, At-Tabraniy katika ‘Mu’jamul- Kabir,’ ukurasa 3968, Adhiyau katika Mukhtara, ukurasa 527. Al-Haythamiy amesema katika ‘Majmauz Zawaidi,’ juzuu ya 9, ukurasa wa 104: Ameipokea Ahmad, na wapokezi wake ni 7 8

Al-Ahaadithu Swahihah Juz. 4, Uk. 330. Minhaju Sunna Juz. 7, Uk.319. 10

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 10

11/25/2014 3:00:33 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

watu madhubuti (Sahihi), isipokuwa Fatr ibn Khalifa ambaye ni mtu thiqa (mkweli).’’ Na al-Baniy naye amesema: “Na sanadi yake ni sahihi kwa mujibu wa masharti ya Bukhari.’’ Pia ameitoa Abdullah ibn Ahmad katika Musnad yake, juzuu ya kwanza ukuraza 119 kwa njia ya Yazid ibn Abi Ziyad na Sammaak ibn Ubaid ibn Walid al-Absiy, kutoka kwa Abdu Rahman ibn Abi Layla, kutoka kwa Ali (a.s.) Al-Baniy amesema: “Ni sahihi kwa njia zote mbili kutoka kwake.” Na wameitoa kutoka kwa Zayd ibn Arqam, Ahmad, ibn Abi Aswim, Tabraniy, na al-Hakim, na amesema: “Ni sahihi kwa mujibu wa masharti ya Bukhari na Muslim.’’ Al-Baniy amesema: “Dhahabiy ameinyamazia, kama vile alivyosema: “Lau kama si Habibu kuwa mwenye kughushi (ingekuwa sahihi) kwa vile ina sanadi iliyoshikana.’’ Na pia ameitoa Tabraniy katika Mujamul- Awswat kutoka kwa Zayd ibn Arqam. Haythamiy katika Majmau Zawaidi amesema: “Wapokezi wake ni madhubuti.’’ Al-Baniy amesema: Majumuisho ya maneno kuhusiana na hadithi isemayo: “Ambaye mimi ni kiongozi wake, basi Ali ni Kiongozi wake, ewe Mola Wangu! Muunge mwenye kumuunga Ali na mfanyie uadui mwenye kumfanyia uadui Ali, ni hadithi iliyo sahihi katika sehemu zake zote mbili.’’9 Kwa kweli al-Baniy amepatia katika kuthibitisha ukweli juu ya usahihi wa hadithi hii, lakini amekosea katika maelezo yake, pale aliposema: “Ama kuhusiana na yale wanayoyasema Mashia kuhusiana na hadithi hii na nyinginezo ya kwamba Mtume (s.a.w.w.) alimwambia Ali (a.s.) ya kwamba “Yeye ni Khalifa wangu baada yangu,’’ ni maneno yasiyo 9

Silsilatul- Ahaadithi Swahihi Juz. 4, Uk. 343. 11

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 11

11/25/2014 3:00:33 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

sahihi kwa vyovyote vile, bali hayo ni miongoni mwa dalili juu ya uovu wao uliozidi, kama historia inavyowashuhudia juu ya uongo wao, kwani lau kama kweli Mtume (s.a.w.w.) angeyasema hayo, basi yangekuwa kama alivyosema, kwa sababu maneno yake ni Wahyi anaofunuliwa, na Mwenyezi Mungu Mtukufu hakhalifu ahadi yake.’’ Kwa masikitiko ni kwamba al-Baniy ameshindwa kutofautisha kati ya ibara inayotoa habari juu ya jambo lililofanyika na ile ya jambo linalotakiwa lifanyike, na hapa ibara inabainisha juu ya kutakiwa watu wafanye jambo (Kumfanya Ali (a.s.) Khalifa wao baada ya Mtume (s.a.w.w.)), na wala haielezei jambo lililotendwa. Na katika Qur’an na Hadithi kuna ibara mbalimbali zenye sura ya kuhabarisha lakini zimekusudiwa kutoa amri ya kufanyika jambo katika wakati ujao, kwa mfano aya isemayo: “Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walio pamoja naye ni wenye nyoyo thabiti mbele ya makafiri, na wenye kuhurumiana wao kwa wao…’’ (Qur’an 48:28). Je, Waislamu walikuwa kama aya inavyoeleza? Mimi sijui. Na msomaji mtukufu anajua vyema yale yaliyotokea kati ya Maswahaba miongoni mwa vita vikali! Na sasa tuangalie baadhi ya mifano inayobainisha mtazamo wake juu ya Imam Ali (a.s.)

12

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 12

11/25/2014 3:00:33 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

KUMTUHUMU IMAM ‘ALI (A.S.) KWAMBA ALIKUWA AKIMUUDHI BIBI FATIMA (A.S.)

K

atika kitabu chake ‘Minhaju Sunna’ kuna maneno yanayomaanisha ya kwamba Ibn Taymiya alikuwa na chuki kubwa dhidi ya Imam Ali (a.s.), na hili linaonekana kwa wingi katika kitabu chake hicho, na hapa tutataja kwa mukhtasari baadhi ya hayo: Amesema: “Lau itasemwa kwamba Abu Bakr alimuudhi Fatima, basi hakumuudhi kwa ajili ya kujinufaisha nafsi yake, bali kwa ajili ya kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na kwa ajili ya kufikisha haki kwa wale wanaostahiki, na lengo la Ali r.a. kumuoa Fatima lilikuwa ni kumuudhi, kinyume na Abu Bakr, imetambulika kwamba Abu Bakr yuko mbali sana na kumuudhi Fatima ikilinganishwa na Ali, kwa hakika alichokusudia Abu Bakr ni kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake…”10 Katika maelezo yake haya aliyoyataja, kuna mambo mawili: Abu Bakr amemuudhi Fatima (a.s.) katika kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake (s.a.w.w.) Ali (a.s.) alikusudia kumuoa Fatima (a.s.) ili amuudhi. Na sisi hapa tutazichambua nukta zote mbili: Ama nukta ya kwanza: Pale alipoeleza ya kwamba Abu Bakr hakumuudhi Fatima kwa ajili ya maslahi ya nafsi yake, bali kwa ajili ya kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, 10

Minhaju Sunna Juz.4, Uk. 255. 13

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 13

11/25/2014 3:00:33 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

maneno haya yanakwenda kinyume na maneno ya Abu Bakr aliyoyasema wakati wa mwisho wa umri wake, kwani alijutia kitendo cha kuikashifu nyumba ya Bibi Fatima (a.s.), na wengi miongoni mwa wanahistoria wamelieleza hilo, miongoni mwao ni kama wafuatao: 1. Abu Ubaid, mwenye kitabu ‘Al-Amuwalu,’ amemnukuu Abdur-Rahman ibn Awfi akisema: “Niliingia kwa Abu Bakr ili kumjulia hali kutokana na ugonjwa uliomsababishia kifo chake, nilimsalimia, kisha nikasema: Nakuona hujambo, Alhamdu lillahi, na wala usisikitike juu ya dunia, naapa kwa Mwenyezi Mungu! Sisi hatukujui isipokuwa ulikuwa mtu mwema mwenye kufanya mazuri, Abu Bakr akajibu kwa kusema: ‘Mimi sisikitiki juu ya kitu, isipokuwa mambo matatu niliyoyafanya, na ningependa lau kama nisingeyafanya, na mambo matatu ambayo sikuyafanya, ningependa lau ningeyafanya, na mambo matatu ambayo ningependa lau kama ningemuuliza Mtume kuhusiana na hayo. Ama yale niliyoyafanya na kupenda lau nisingeyafanya ni mambo kadhaa wakadhaa (aliacha kuyataja), Abu Ubaida alisema: Sitaki kuyataja. Na siku ya Saqifa Bani Sa’da (siku ya kuchaguliwa Khalifa) ningetamani kuuwacha Ukhalifa kwa mmoja kati ya watu wawili (Umar au Abu Ubaid) akawa ni amiri na mimi nikawa waziri…’”11 Mwandishi wa kitabu cha ‘Al-Amuwalu’ ameona vibaya kuyataja yale mambo ambayo Abu Bakr ameyafanya na hatimaye kuyajutia, si jingine alilohofia isipokuwa kule kuikashifu nyumba ya Bibi Fatima, kutokana na ushahidi wa wapokezi wengine waliolitaja hilo kwa uwazi. 11

al-Amuwalu Uk.193-194. 14

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 14

11/25/2014 3:00:34 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

2. Ibn Abil Hadid amekielezea kisa hicho kwa kusema: “Ahmad amepokea na Mubarrid amepokea katika kitabu cha ‘al-Kamil’ chimbuko la kisa hicho ikiwa ni kutoka kwa Abdur-Rahman ibn Awfi, amesema: ‘Ama mambo matatu niliyoyafanya na kutamani lau nisingeyafanya: Ningetamani lau kama sikuikashifu nyumba ya Fatima na kuicha, hata kama ungefungwa kwa ajili ya (kupanga) vita, na ningetamani siku ya Saqifa Bani Sa’da ningeliacha jambo la Ukhalifa kwa mmoja kati ya watu wawili: Umar au Abu Ubaida, akawa amiri na mimi nikawa waziri, na ningetamani pale nilipoletewa Faja-at nisingemchoma moto, na badala yake ningemuua kwa upanga au kumuacha huru.’’12 3. Masuudiy pia amekieleza kisa hiki kwa urefu katika kitabu chake ‘Muruji dhahabi’ ameandika yafuatayo: “Ama mambo matatu niliyoyafanya na kutamani lau nisingeyafanya: Ningetamani lau kama sikuikashifu nyumba ya Fatima, na ningetamani lau kama sikumchoma moto Faj-at…”13 4. Naye Abul-Qasim Sulayman ibn Ahmad At-Tabraniy amepokea kisa hiki, Abu Bakr alisema: “Ama ambayo ningetamani lau kama sikuyafanya: Ningetamani lau kama nisingeikashifu nyumba ya Fatima na kuiacha, hata kama ingefungwa kwa ajili ya vita.’’14 5. Naye Abdur Rabbihi amekinukuu kisa hiki, Abu Bakr alisema: “Ama ambayo ningetamani lau kama sikuyafanya: Ningetamani lau kama nisingeikashifu nyumba ya Fatima kwa chochote kile, hata kama ingefungwa kwa ajili ya vita.”15 Sharhu Nahjul Balaghah ibn al-Hadih, Juz. 2, Uk. 45-47. al-Kamil Juz.1, Uk.11. Muruju Dhahabiy Juz. 2, Uk. 301. 14 Mu’jamul- Kabir Juz.1, Uk. 62. 15 Al-Aqdul- Farid Juz.4, Uk.93. 12 13

15

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 15

11/25/2014 3:00:34 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

6. Naye Ibn Asakir amenakili katika kitabu ‘Mukhtasar Tarikh Dimishq’ kisa hiki, akasema Abu Bakr: “Ama yale ambayo ningetamani lau kama ningeyaacha…ningetamani lau kama nisingeikashifu nyumba ya Fatima kwa chochote kile, licha ya kwamba waliifunga kwa ajili ya vita.’’16 7. Ibn Abil-Hadid naye amenukuu kutoka kwa Ahmad ibn Abdul-Aziz al-Jawhariy ambaye ni mtunzi wa kitabu ‘AsSaqifa’ ameeleza maneno yake (Abu Bakr): “Mimi sisikitiki isipokuwa kwa mambo matatu…, kisha akasema: Laiti nisingekuwa ni mwenye kuikashifu nyumba ya Fatima na kuicha licha ya kwamba ilifungwa kwa ajili ya vita.”17 8. Na pia Dhahabiy amepokea kisa hiki na kueleza maneno aliyoyasema Abu Bakr kama yalivyo katika kitabu kilichotangulia.18 9. Na pia Haythamiy amekipokea kwa maneno yaliyotangulia.19 10. Na pia Ibn Hajar al-Askalaniy amekipokea kwa maneno yaliyotangulia.20 11. Na pia al-Muttaqiy al-Hindiy amekipokea kwa maneno yaliyotangulia.21 Mpaka hapa majibu yanayohusiana na nukta ya kwanza yamekamilika. Ama nukta ya Pili: Maneno ya Ibn Taymiya ya kwamba Imam (a.s.) alimuudhi Bibi Fatima. Chimbuko la kauMukhtasar Tarikh Dimish-q Juz.13, Uk.122 Sharhu Mahjul Balagha Juz. 2, Uk. 46-47. 18 Tarikhul-Islam Juz. 3, uk. 188-199. 19 Majma’u Zawaidi Juz. 5, uk. 202-203. 20 Lisanul-Mizan Juz. 4, uk. 188-189. 21 Kanzul-Ummal Juz. 5, uk. 631, Hadithi Na.14113. 16 17

16

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 16

11/25/2014 3:00:34 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

li yake hii ni kutokana na kisa kinachodaiwa ya kwamba Imam Ali (a.s.) alimposa binti wa Abu Jahli. Katika kisa hiki cha kutungwa kuna majibu yetu yafuatayo: Katika kitabu chetu ‘al-Ahadithin-Nabawiy bayna Riwayati wa Dirayati’ tumethibitisha kwa uwazi kwamba kisa hiki ni kisa kilichotengenezwa na watu wenye chuki na bughudha ambao wametapakaa matope ya uovu na batili, kwa lengo la kujitafutia utukufu, na hapa tunakunukulia yale tuliyoyatafiti ili ewe ndugu yangu msomaji ikubainikie ya kwamba maadui wa Imam Ali (a.s.) humsingizia mambo ambayo yako mbali sana na yeye. Tirmidhiy amepokea kutoka kwa Abi Malika, kutoka Abdullah ibn Zubair, ni kwamba Ali alimtaja binti wa Abu Jahli, habari hiyo ikamfikia Mtume (s.a.w.w.), akasema: “Hakika Fatima ni sehemu yangu mimi, yananiudhi mimi yale yanayomuudhi…”22 Lakini Bukhari ameipokea kwa namna tofauti kutoka kwa Mis-war ibn Makhrama katika milango mbalimbali, nayo ni kama ifuatavyo: 1. Amepokea kwa mujibu wa sanadi yake kutoka kwa Walid ibn Kathir, kutoka kwa Muhammad ibn Amru ibn Halhalt Addualiy, kutoka kwa Ibn Shihab, ni kwamba Ali ibn Husein alimsimulia: Pale walipowasili Madina kutoka kwa Yazid ibn Muawiya ambaye ni muuwaji wa Husein ibn Ali (a.s.), alikutana na Mis-war ibn Makhrama, akamwambia: Je, unashida ya jambo, ili uniamrishe nikutekelezee? Nikasema: “Hapana.” Akamwambia: “Je, uko tayari kuutoa upanga wa Mtume (s.a.w.w.)? Kwani nahofia watu wakakushinda 22

S unan Tirmidhiy Juz. 5, uk. 699, Hadidhi Na. 3869, na pia ameipokea Ahmad katika Musnad yake, Juz. 4, Uk. 5. 17

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 17

11/25/2014 3:00:34 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

nguvu na kukunyang’anya, naapa kwa Mwenyezi Mungu! Lau kama utanipa mimi huo upanga, katu hawatoupata isipokuwa pale itakapotolewa roho yangu. Hakika Ali ibn Abi Talib alimposa binti wa Abu Jahli ili awe mke mwenza wa Fatima (a.s.), nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akiwahutubia watu katika mimbari yake hii kuhusiana na posa hiyo, na mimi siku hizo nikiwa tayari nimekwisha baleghe, alisema: ‘Hakika Fatima anatokana na mimi, na mimi nachelea kuja kufitiniwa katika dini yake.’ Kisha alitaja ukwe wake kwa Bani Abdi Shamsi, huku akiusifu uhusiano huo wa ukwe. Akasema: Amenisimulia na kunisadiki na ameniahidi na akanitekelezea aliyoniahidi, na mimi siharamishi yaliyo halali na wala sihalalishi yaliyo haramu, lakini, naapa kwa Mwenyezi Mungu! Katu binti wa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hawezi kuwa mke mwenza na binti wa adui wa Mwenyezi Mungu.’’23 2. Na amepokea kwa sanadi yake kutoka kwa Zuhriy, amesema: “Ali ibn Husein amenisimulia: Hakima Mis-war ibn Makhzamat amesema: Kwa hakika Ali alimposa binti wa Abu Jahli, mara Fatima akasikia habari hiyo, akamuendea Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na kumwambia: Watu wako wanadhani ya kwamba wewe hukasiriki kwa ajili ya mabinti zako, na huyu Ali ni mwenye kutaka kumuoa binti wa Abu Jahli. Mtume (s.a.w.w.) alisimama, na baada ya kutoa shahada nikamsikia akisema: Ama baada ya hayo: Nimeoa kwa Abul-Aswi ibn Rabiy’i akanisimulia na kuniamini, na kwa hakika Fatima ni sehemu yangu mimi, na mimi nachukia Ali kumkasirisha, naapa kwa 23

Sahihul Bukhari Juz. 4, Uk. 84, Babu maa dhukira min Dar’I Nabiy (s.a.w.w.) 18

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 18

11/25/2014 3:00:34 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Mwenyezi Mungu! Katu binti wa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hawezi kuwa pamoja na binti wa adui wa Mwenyezi Mungu chini ya mume mmoja. Kutokana na maneno hayo, Ali akakatisha posa yake kwake.’’24 3. Na amepokea kwa sanadi yake kutoka ibn Abi Mulaykat, kutoka kwa Mis-war ibn Makhramat, amesema: Nilimsikia Mtume (s.a.w.w.) akisema wakati akiwa juu ya mimbari: Kwa hakika Bani Hisham ibn Mughira wametaka ruhusa ya kumuozesha binti yao kwa Ali ibn Abi Talib, basi mimi sikubali, kisha sikubali, na tena sikubali, isipokuwa mwenyewe ibn Abi Talib (Imam Ali) atakapomuacha binti yangu na kumuoa binti yao, kwani huyo binti yangu ni sehemu yangu mimi, yananitia wasiwasi yale yanayomtia yeye wasiwasi na yananiudhi yale yanayomuudhi yeye.’’25

24 25

Sahihul-Bukhar, babu dhikri Asw-hari Nabii (s.a.w.w.) Sahihul-Bukhari Juz. 7, Uk. 37. Babu dhabb Rajuli an ibnatihi fil-ghiytati walinswaf. 19

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 19

11/25/2014 3:00:34 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Utafiti wa Riwaya kwa Upande wa Sanadi

K

wa hakika kuwepo tofauti ya maneno katika riwaya hizi, kuwepo sura mbalimbali za kisa hiki, na kubainika maneno ya ziada katika kila sura, bila ya shaka ni mambo ambayo msomaji mahiri ameyaona hayo kwa jicho lake la haraka haraka, kabla ya kurundikana maswali mengi katika kichwa chake kutokana na ibara mbalimbali zilizozizunguka riwaya hizo. Jambo kubwa linalotia shaka juu ya usahihi wa riwaya hii ni yale madai ya kwamba asili yake ni Ibn Zubair na Mis-war, hiyo ni hata bila ya kuangalia sanadi za wapokezi ambao walikuwa ni watu waliokuwa na chuki dhidi ya Imam Ali (a.s.) pamoja na Ahlulbayti wake, hata kama wanachuoni wote wa elimu ya kuadilisha na kujeruhi wapokezi hawakueleza vibaya juu ya uaminifu wao, miongoni mwa wapokezi hao ni: 1. Ibn Abi Mulayka, jina lake ni Abdullah ibn Ubaidullah ibn Abi Mulayka ibn Abdullah ibn Jud’an al-Qurashiy al-Taymiy, alifariki mwaka 117A.H., alikuwa ni kadhi wa Abdullah ibn Zubair na mwadhini wake.26 2. Ibn Shihabu Az-Zuhriy, alifariki mwaka 124 A.H, alikuwa mtu wa karibu kwa watawala wa kibanu Ummaiyya, kama vile: Abdul Malik, Hisham, na Yazid ibn Abdul Malik, ambaye alimfanya kuwa kadhi pamoja na Habibu al-Muharibiy.27 Umar ibn Ruwaih alisema: “Nilikuwa pamoja na ibn Shihabu Az-Zuhriy tukitembea, Amru ibn Ubaid aliniona, akasema: ‘Una jambo gani na kihanchifu 26 27

Tahdhibul-Kamal Juz. 15, Uk. 256. Tarikh Dimish-qi Juz. 55, Uk. 357. 20

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 20

11/25/2014 3:00:34 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

cha watawala!’ Alikuwa akimkusudia Ibn Shihabu.’’28 Na Yahya ibn Ma’in amesema kuhusiana na Mansuur ibn al-Mu’tamir na Az-Zuhriy: Wawili hao ni sawasawa, na Mansuur ni bora zaidi kwangu, kwa sababu Az-Zuhriy alikuwa akijipendekeza kwa watawala.29 3. Al-Walid ibn Kathir al-Qurqshiy al-Makhzumiy, alifariki mwaka 151A.H. Sajiy amesema: al-Walid alikuwa ni muibaadhi, lakini alikuwa ni mkweli. Na ibn Daud anamuona kwamba ni mkweli, isipokuwa alikuwa ni muibaadhi. Na Ibn Sa’d amesema: Si lolote. Na al-Uqayliy amemtaja katika madhaifu.30 Wala kusudio letu katika kutaja mirengo wanayoifuata wapokezi hawa wakati wa kuthibitisha udhaifu wa riwaya hii, si kumtetea Ibn Zubair na Mis-war, hasa ikizingatiwa kuwa historia sahihi imethibitisha chuki na uadui aliokuwa nao Ibn Zubair dhidi ya Imam Ali pamoja na Ahlulbayti wake (a.s.) na Bani Hashim wengine. Ama kwa upande wa Mis-war, ili kujua mwelekeo wake na hawaa yake yatakutosha yale aliyoyataja Dhahbiy kuhusiana naye, amesema: - Alikwenda Syria akiwa tarishi kutoka kwa Uthman kwenda kumuomba msaada Muawiyah. - Alikuwa ni khawariji - Ibn Ur-watu amesema: Sijawahi kumsikia Mis-war akimtaja Muawiya, isipokuwa humtakia rehema - Hakika Ibn Zubair alikuwa haamui jambo huko Makka bila ya Mis-war.31 Kitabu kilichotangulia. Tahddhibul Kamal Juz. 26, Uk. 442. 30 Kitabu kilichotangulia Juz. 3, Uk. 73. 31 Siyar A’lam an-Nubalaa Juz. 3, Uk. 390 – 394. 28 29

21

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 21

11/25/2014 3:00:34 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Ndiyo kusudio letu katika kutaja hayo si kumtetea Ibn Zubair na Mis-war, bali ni kutaka kujua je riwaya imetoka kwa watu wawili hawa au la, hiyo ni kwa kuwa sababu zilizopelekea kueneza uwongo uliokuja katika riwaya, wenye kumchafua Imam Ali (a.s.) zilikuwepo tangu kabla, hivyo basi ni kwa nini riwaya hiyo isielezwe na kuenezwa katika zama za uhai wake? Na kwa nini maadui wa Imam Ali (a.s.) kama vile watu wa Jeshi la Ngamia (jeshi la bibi Aisha) na kundi ovu lililokuwa likiongozwa na Muawiya wasiitumie riwaya hiyo katika kumuaibisha na kumtia doa? Kwani hao ni watu ambao hawakuacha ovu lolote isipokuwa wamemtupia, licha ya kwamba historia imewashuhudia ya kwamba wao walikuwa ni mahodari wa kutengeneza tuhuma mbalimbali za uwongo dhidi yake! Na ni kwa nini madai haya hayakusimuliwa na Ibn Zubair pale Hijaz ilipokuwa mikononi mwake, mtu ambaye alionesha uadui wa wazi wazi juu ya Bani Hashim na kwa mtoto wa Imam Ali (a.s.) (Muhammad ibn Hanafiya?). Ni kwa nini Ibn Zubair akimbilie maamuzi ya kuacha kumswalia Mtume (s.a.w.w.) ili Banu Hashimu wasije wakajitukuza kwa kuwaswalia kwake, na ilhali alikuwa na silaha hii kali (riwaya ya kumuudhi Fatima)! Au si ingekuwa bora kwake kisiasa kumswalia Mtume (s.a.w.w.) pindi anapomtaja, kisha akaeleza ghadhabu ya Mtume (s.a.w.w.) juu ya kiongozi wa Bani Hashim zama hizo (Imam Ali (a.s.)), ili kuwafanya wainamishe vichwa vyao na kuyafumba macho yao! Haya yote yanabainisha wazi kwamba, riwaya hii ilitengenezwa baada ya zama kupita, hasa pale Banu Umayya waliposhika hatamu za kisiasa na Maswahaba wengi kuondoka duniani.

22

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 22

11/25/2014 3:00:34 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Masuala Kadhaa Ndani ya Riwaya hii

N

dugu mpendwa msomaji, ule wakati wa kujiuliza maswali mbalimbali yanayotokana na riwaya hii umewadia, maswali yaliyo muhimu kujiuliza ni haya yafuatayo:

Kwanza: Mis-war alizaliwa Makka ikiwa ni miaka miwili baada ya Hijra, na aliwasili Madina pamoja na baba yake mwishoni mwa mwezi wa Mfunguo tatu mwaka wa nane Hijriya, alikuwa ni mdogo zaidi kuliko Ibn Zubair kwa miezi minne, wakati Mtume (s.a.w.w.) alipofariki Mis-war alikuwa na umri wa miaka nane.32 Basi ni vipi ipokewe kutoka kwake katika sura ya kwanza kama ilivyo katika riwaya ya Bukhari, kwa kusema: “Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu akiwahutubia watu juu ya mimbari yake hii kuhusiana na hilo (posa ya Imam Ali (a.s.) kwa binti wa Abu Jahli), na mimi wakati huo nikiwa nimeshabaleghe! Ni wazi kwamba mtoto wa miaka nane haambiwi amebaleghe, wala kama aliye baleghe. Pili: Ni kwa nini habari ya posa hii haikupokewa na Maswahaba wengine isipokuwa Ibn Zubair na Mis-war, licha ya kwamba wakati Mtume (s.a.w.w.) anafariki walikuwa na umri wa miaka nane?! Na ikiwa jambo lenyewe lilikuwa na madhara makubwa kiasi cha kumfanya Mtume (s.a.w.w.) apande mimbari na kuhutubia waziwazi, ilikuwa ni jambo la kawaida habari hiyo ipokewe na idadi kubwa ya Maswahaba na hasa wale waliokuwa na umri mkubwa na uelewa mkubwa zaidi 32

Al-I’stiab Juz. 3, Uk. 1399. 23

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 23

11/25/2014 3:00:34 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

ikilinganishwa na hawa watoto wawili wadogo, basi ni kwa nini riwaya hii inaishia kwa hao wawili tu? Tatu: Mafungamano ya visa viwili (kisa cha upanga wa Mtume (s.a.w.w.) na posa ya Imam Ali (a.s.)) kati ya maneno ya Mis-war pamoja Imam Zaynul-Abidin ni mafungamano yaliyokatika, kutokana na hali hii, washehereshaji wamejaribu kuleta mashikano kati ya visa hivyo viwili, kwa mfano, Karmaniy ametaja namna tatu, lakini kutokana na udhaifu wa namna hizo, Ibn Hajar ametusaidia kwa kutaja namna moja tu ambayo ameielezea kama yenye kutegemewa, amesema hivi: “Kama vile ambavyo Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa akipenda kuinyanyua hadhi ya Fatima, basi na mimi pia napenda kuinyanyua hadhi yako kwa vile wewe ni mtoto wa mtoto wa Fatima, basi nipe upanga wako ili nikuhifadhie.’’33 Lakini Ibn Hajar baadaye ameikosoa kauli hii kwa kusema Bado nashangazwa na Mis-war, ni vipi amefikia kiwango cha mapenzi ya hali ya juu kwa Ali ibn Husain, mpaka anafikia kusema: Lau kama atauweka upanga wake kwake, hakuna yoyote atakayeweza kuuchukua mpaka hapo roho yake itakapotoka, kwa ajili ya kuchunga heshima ya mtoto wa mtoto wa Fatima kwa kutumia hoja ya hadithi ya mlango huu (hadithi ya posa ya Imam Ali kwa binti wa Abu Jahli), lakini bila ya kuangalia kwamba maneno yaliyopo katika hadithi iliyotajwa yanamdhalilisha Ali ibn Husein kutokana na kumdhalilisha babu yake ambaye ni Ali ibn Abi Talib (a.s.), kwa vile alipeleka posa ya kutaka kumuoa binti wa Abu Jahli wakati alipokuwa amemuoa Fatima, hali iliyompelekea Mtume kulipinga jambo hilo. Bali nashangazwa zaidi na Mis-war kwa kutaka kuuhifadhi upanga kwa lengo la kulinda 33

Fat-hul Bariy Juz. 6, uk. 214. 24

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 24

11/25/2014 3:00:34 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

heshima ya mtoto wa mtoto wa Fatima, na namna alivyotoa juhudi yake mbele ya mtoto wa Fatima (Husein ibn Ali) ambaye alifikwa na yaliyomfika kutoka kwa watawala madhalimu mpaka wakamuua, lakini inadhaniwa kwamba kujitetea kwake (kwa kutoshiriki vita pamoja na Imam Husein) ni kwamba pale Husain alipotoka kwenda Iraqi, Mis-war pamoja na watu wa Hijazi hawakudhania ya kwamba Husain ibn Ali atafikwa na yale yaliyomfika, na Mwenyezi Mungu ni mwenye kujua zaidi.�34 Utetezi huu juu ya Mis-war wa kutomnusuru Imam Husein (a.s.) hauna mashiko yoyote, tumetangulia kusema kwamba, mapenzi yake yalikuwa yako juu ya maadui wa Imam Ali (a.s.) na jamaa zake, basi ni vipi itarajiwe nusra ya kumnusuru mtoto wa Fatima kutoka kwake na hata kama anajua ya kwamba Imam Husein atafikwa na yaliyomfika.?! Nne: Ni vipi iwezekane kwa Imam Ali ibn Husein (a.s.) amnukulie Az-Zuhriy kisa hicho ambacho kinaishusha hadhi ya babu yake; Imam Ali ibn Abi Talib (a.s.), hasa ikizingatiwa wakati ule ambao aliishi kwa majonzi ya hali ya juu kutokana na kuuwawa kinyama kwa baba yake; Imam Husein (a.s.) pamoja na jamaa zake na wafuasi wake, na huku akisikia habari za uwongo na upotoshaji kutoka kwa vyombo vya habari vya Banu Umayya, habari ambazo zilikuwa na lengo la kuwashusha hadhi watu wa familia ya Mtume (s.a.w.w.)?! Kwa kweli jambo hili haliwezi kufanywa na mtu wa kawaida, basi ni vipi lifanywe na mtu ambaye alifikia kilele cha akili, elimu tabia njema na uchamungu, hata kama ni kweli alikisikia kisa hicho kutoka kwa Mis-war! 34

Fat-hul Bariy Juz. 9, jk. 327. 25

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 25

11/25/2014 3:00:34 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Tano: Ummah wa Kiislamu kwa umoja wao unakubaliana kwamba, lau kama Imam Ali (a.s.) angetaka kumuoa binti wa Abu Jahli ili awe mke mwenza wa bibi Fatima, ni kwamba jambo hilo linafaa, kwani ni jambo linaloingia katika sheria ya aya inayojuzisha mwanamme kuoa wake wanne, na huyo binti wa Abu Jahli anayetajwa katika kisa hicho, alikuwa ni Muislamu, kwa sababu kisa hicho kilitokea baada ya kukombolewa Makka, na watu wote wa Makka walisilimu kwa hiyari zao kwa kule kukosa budi, na wapokezi wa kisa hicho wanakubaliana juu ya hili, kama alivyobainisha ibn al-Hadidi.35 Basi ikiwa hiyo ndio sheria ya Mwenyezi Mungu, iweje mbora wa viumbe na mwenye kusifika kwa tabia njema, akasirike kwa sababu ya kutekelezwa sheria hii mbele ya mkusanyiko wa watu, tena mwenye kukasirikiwa akiwa ni mtoto wa ami yake ambaye pia ni mkwe wake na muhifadhi wa siri zake na baba wa watoto wake, kama Bukhari alivyosimulia juu ya kisa hicho, ikiwa ni kweli Imam Ali alifanya hivyo, basi inaingia akilini kwa mtu ambaye amepelekwa ili awe ni rehema kwa viumbe, na mpole kwa Waumini kuweza kuzungumza kwa lugha hiyo ilio kali mbele ya watu dhidi ya mtu ambaye ndiye mnusuru wake mkubwa na tegemezi lake katika jihadi na mtu wa mwanzo kumuamini yeye! Kwa mtu mwenye kuzingatia na kutambua utukufu wa Mtume (s.a.w.w.) hawezi kukubali kwamba Mtume (s.a.w.w.) alikasirika kwa kiwango hicho kutokana na jambo ambalo si haramu. Ama wale wenye kukitukuza kitabu cha Sahihi Bukhari na Sahihi Muslim kwa kudai kwamba kila riwaya iliyomo humo ni sahihi, wamejaribu kutoa sababu mbalimbali juu ya kisa hicho, Ibn Tiyn amesema: “Ukweli unaoweza kue35

Sharhu Nahjul-Balaghah Juz. 4, jk. 65. 26

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 26

11/25/2014 3:00:34 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

lezwa juu ya kisa hiki ni kwamba Mtume (s.a.w.w.) alimharamishia Ali kumuoa binti wa Abu Jahli na kuwa mke mwenza wa Fatima, kwa sababu jambo hilo linamuudhi, na kumuudhi ni jambo lililo haramu kwa mujibu wa makubaliano ya Waislamu, na maana ya tamko lake: “Si haramishi yaliyo halali.” Ni kwamba Ali kumuoa binti wa Abu Jahli ni halali kwake lau kama asingekuwa na Fatima, ama kuwa na wake hao wawili kwa pamoja, ni jambo ambalo linapelekea kuudhika kwa Mtume (s.a.w.w.) kutokana na kuudhika kwa Fatima, kwa hivyo ndoa hiyo si halali.’’ Ibn Hajar naye amesema: “Mwingine amedhani ya kwamba, dhahiri ya maneno inaonesha kwamba jambo hilo ni halali kwa Ali (kumuoa binti wa Abu Jahli), lakini Mtume (s.a.w.w.) alimzuia ili kulinda heshima ya Fatima, na yeye Ali alikubali kutekeleza amri ya Mtume (s.a.w.w.), na inavyonibainikia mimi ni kwamba jambo hili haliwezi kuwa mbali na yale mambo yanayomhusu Mtume (s.a.w.w.) peke yake, ya kwamba mabinti wake wasiolewe wake wenza, na huenda ikawa jambo hili linamhusu Fatima (a.s.) peke yake.’’36 Hivi ndivyo ambavyo dhana zinavyotofautiana na kila moja kushika njia yake, yote hayo ni kwa ajili ya kuitetea riwaya, na lau kama riwaya hiyo ingekuwa inamzungumzia Swahaba mwingine, na ingeonekana mitazamo na misimamo mingine. Pamoja na hayo, yale aliyoyasema Ibn Hajar yanatofautiana yale yaliyosemwa na Ibn al-Hadidi kwamba kuna makubaliano ya wanachuoni wa Kiislamu juu ya uhalali wa Ali kuoa mke mwenza wa Fatima. Wanachuoni hao wamesahau kwamba Imam Ali (a.s.) alikuwa kama Mtume (s.a.w.w.) katika kulinda heshima ya bibi 36

Fat-hul Bariy Juz. 9, uk. 328-329. 27

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 27

11/25/2014 3:00:34 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Fatima, na akiudhika pindi Bibi Fatima anapoudhika, basi ni vipi Imam Ali (a.s.) asihisi majonzi na huzuni ya Bibi Fatima ikiwa atamuolea mke mwenza, na kuachana na jambo hilo ili kuonesha mapenzi kwa mliwazaji wake na mwenza wake katika maisha, na ambaye ni kipenzi cha Mtume (s.a.w.w.), ni vipi afanye hivyo mpaka impelekee kwenda kupeleka mashitaka kwa baba yake?! Kisha pale Mtume (s.a.w.w.) alipoelekeza lawama zake kali dhahiri shahiri kwa Ali (a.s.) (kama wanavyodai) na kueleza mahusiano yake ya ukwe pamoja na Bani Abdi Shamsi, hata kama katika kufanya hivyo ni katika kumridhisha binti yake Fatima, je, jambo hilo halimuudhi Ali (a.s.) Mtume (s.a.w.w.) yuko mbali na kitendo cha kumpunguzia mtu murua wake kwa sababu ya kutenda jambo lililo halali, na pia yuko mbali na kitendo cha kwenda kinyume na yale aliyowatahadharisha watu dhidi ya kumuudhi Ali (a.s.) kama vile alivyotahadharisha hilo dhidi ya Bibi Fatima. Kwani Ibn Abdu Barri al-Malikiy amepokea kwa sanadi yake kutoka kwa Amru ibn Shasi, amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu aliniambia: Umeniudhi. Nikasema: Mimi sipendi kukuudhi. Akasema: Mwenye kumuudhi Ali ameniudhi mimi.”37 Na kama ilivyokuja katika riwaya ya Imran ibn Huswayn namna Mtume (s.a.w.w.) alivyowapinga Maswahaba wanne ambao walikwenda kwake kumueleza yale aliyoyafanya Imam Ali (a.s.), amesema: “Mtume (s.a.w.w.) aliwaelekea na huku ghadhabu ikiwa imetanda katika uso wake, akasema: Ni kitu gani mnakitaka kwa Ali? Ni kitu gani mnakitaka kwa Ali? Ni kitu gani mnakitaka kwa Ali? Kwa haki37

Al-Isti’ab Juz. 3, uk. 1183. 28

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 28

11/25/2014 3:00:35 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

ka Ali anatokana na mimi, na mimi natokana na yeye, na yeye ni kiongozi wa kila Muumini baada yangu.’’38 Kwa kumalizia, tunasema: Kile ambacho walichokifanya baadhi ya washereheshaji akiwemo Ibn Hajar ni katika kujali kutetea hasira za Mtume (s.a.w.w.) na posa ya Imam Ali kwa binti wa Abu Jahli, na kujaribu kuleta mafungamano kati ya kisa kinachohusiana na upanga wa Imam Zaynul-Abidina na kisa cha posa, visa hivyo vyote viko katika kundi moja la dhana na ni kujaribu kuoanisha matukio hayo kusiko rahisi. Wajibu wa wanachuoni hao ulikuwa ni kutoa juhudi zao katika kuzisahihisha riwaya hizo kwa kuyaangalia maisha ya Imam Ali (a.s.) na usuhuba wake wa dhati pamoja na Mtume (s.a.w.w.), kwani alikuwa akimfuata Mtume (s.a.w.w.) kama vile ndama anavyomuambata mama yake, na wakati wote alikuwa makini kwa yale yanayomridhisha Mtume (s.a.w.w.) na mwenye tahadhari kwa yale yanayomuudhi. Basi ni kweli inamkinika ampose binti wa Abu Jahli ambaye alikuwa adui mkubwa wa Uislamu ili awe mke mwenza wa binti wa Mtume (s.a.w.w.), bila ya kumshauri na kumtaka ruhusa Mtume (s.a.w.w.)?! Kwa kweli hatusemi kwamba kumposa binti wa Abu Jahli ambaye alikuwa Mwislamu ilikuwa ni jambo la haramu, lakini si kila jambo halali hutendwa. Na haya yanabainika kwa wazi kutokana na dalili za uhakika tulizozieleza, hasa ikizingatiwa kwamba waliokieleza kisa hiki wamekisimulia kwa maneno tofauti na kwa sura mbalimbali, yote hayo ni kwa lengo la kutaka kuishusha hadhi ya Imam Ali (a.s.) kwa Mtume (s.a.w.w.) na daraja aliyonayo kwake, 38

Sunan Tirmidhiy Juz. 5, uk. 296. 29

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 29

11/25/2014 3:00:35 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

huku wakisahau kwamba kitendo chao hicho kimemdhalilisha Mtume (s.a.w.w.) kwa kumfanya ni mwenye kufuata matakwa ya nafsi yake, hukasirika kwa jambo ambalo sheria ya Kiislamu imelihalalisha!! Na wamekieleza kisa hiki kwa jambo linalomhusu Bibi Fatima kwa lengo la kufikia makusudio yao na kujaribu kuficha ukweli, na pia kuwaghafilisha watu juu ya wale waliomkasirisha Fatima kikwelikweli, kutokana na nafasi yake kwa baba yake (s.a.w.w.) kama alivyosema: “Fatima ni sehemu ya mwili wangu, basi mwenye kumkasirisha atakuwa amenikasirisha mimi.”39 Na pia Bukhari amepokea ya kwamba bibi Fatima (a.s.) alimuomba Abu Bakri ampe mirathi yake baada ya kufariki Mtume (s.a.w.w.) katika vile ambavyo Mwenyezi Mungu alimpa. Abu Bakr alimwambia: “Hakika Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Sisi (Mitume) haturithiwi, vile tulivyoviacha ni sadaka.’’ Kutokana na kauli hiyo, Bibi Fatima alikasirika, basi alimsusa Abu Bakr, akawa katika hali hiyo ya kumsusa mpaka Bibi Fatima akafariki dunia.”40 Na amepokea tena Bukhari kwamba, Fatima Binti wa Mtume (s.a.w.w.) alikwenda kwa Abu Bakr kutaka sehemu ya mirathi yake katika yale ambayo Mwenyezi Mungu alimpa huko Madina, na Fadak (shamba) na katika yaliyobakia katika khumsi ya Khaybar…, ni kwamba Abu Bakr alikataa kumpa Fatima chochote katika hivyo, Fatima alimkasirikia Abu Bakr kwa hilo, na alimsusa, hakusema naye mpaka Bibi Fatima akafariki, na aliishi baada ya kufariki Mtume (s.a.w.w.) kwa muda wa miezi sita, na yeye alipo39 40

Sahihul-Bukhari Juz. 5, uk. 51. Sahihul-Bukhari Juz. 4, uk. 79. 30

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 30

11/25/2014 3:00:35 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

fariki alizikwa usiku na mume wake; Ali (a.s.), na wala hakumpa habari ya msiba huo Abu Bakr, na yeye (Ali) ndiye aliyemswalia.’’41

‫ان َل ُه َق ْلبٌ أَ ْو أَ ْل َقى ال َّس ْم َع َوھ َُو‬ َ ‫إِنَّ فِي ٰ َذل َِك َل ِذ ْك َر ٰى لِ َمنْ َك‬ ‫َش ِھي ٌد‬

“Kwa yakini katika jambo hili mna ukumbusho kwa mwenye moyo au kwa ategaye sikio, naye mwenyewe awe dhahiri.” (Qur’an, 50:37).

41

Sahihul-Bukhari Juz. 5, uk. 139. 31

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 31

11/25/2014 3:00:35 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

MADAI YA IBN TAYMIYA KWAMBA MASWAHABA WENGI WALIKUWA WAKIMCHUKIA ‘ALI (A.S.)

I

bn Taymiya amesema: “Hakika Mwenyezi Mungu ameeleza ya kwamba atawafanyia mapenzi wale walioamini na kutenda matendo mema, na ahadi yake ni ya kweli. Ni jambo linalotambulikana ya kwamba Mwenyezi Mungu amejaalia mapenzi kwa Maswahaba katika kila moyo wa Mwislamu, na hasa wale Makhalifa waongofu, na katika hao, hasa Abu Bakr na Umar, kwa hakika Maswahaba wote na Matabiina walikuwa wakiwapenda wawili hao, na hao Maswahaba walikuwa katika karne zilizobora. Na jambo hilo la kupendwa halikuwepo kwa Ali, kwani Maswahaba wengi pamoja na Matabiina walikuwa wakimchukia, kumtukana na kumpiga vita.’’42 Katika maneno yake haya, kuna maangalizo yafuatayo: Kwanza: Maneno yake haya yanamaanisha ya kwamba Imam Ali (a.s.) hakuwa ni miongoni mwa muradi wa Aya hii:

‫ت َس َيجْ َع ُل َل ُھ ُم الرَّ حْ ٰ َمنُ وُ ًّدا‬ ِ ‫ِين آ َم ُنوا َو َع ِملُوا الصَّال َِحا‬ َ ‫إِنَّ الَّذ‬ “Hakika wale walioamini na kutenda mema, Mwenyezi Mungu Mwenye Rehema huwafanyia mapenzi.” (Qur’an; 19:96).

Kwa mujibu wa Ibn Taymiya ni kwamba dalili ya mtu kuwa Muumini ni kupendwa na watu, na kwa vile Maswa42

Minhaju Sunna Juz. 7, uk.137. 32

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 32

11/25/2014 3:00:35 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

haba wengi pamoja na Matabiina walikuwa wakimchukia na kumtukana Ali, basi hii ni dalili ya kwamba yeye hakuwa Muumini na mwenye kutenda mema. Je, ni haki kwa Mwislamu kusema maneno haya, na kumtoa katika kundi la Waumini mtu wa kwanza kumuamini Mtume (s.a.w.w.)?! Hapana! Kwa jina la Mwenyezi Mungu, maneno yanayotoka vinywani mwao yamekuwa makubwa mno! Pili: Lau kama dalili juu ya imani ya mtu ni kupendwa na watu wote, basi katika ardhi hii kusingekuweko na Muumini, kwani hakuna yoyote anayependwa na watu wote, kwa mfano, Mayahudi wanamchukia Nabii Isa kama ambavyo wanamchukia Mtume (s.a.w.w.), na watu wanaoabudu vitu, wanawachukia watu wenye kumpwekesha na kumwabudu Mwenyezi Mungu. Kwa kweli ni wazi kwamba Ibn Taymiya hakufahamu makusudio ya Aya, na amefanya haraka katika kutoa hukumu. Tatu: Makusudio ya Aya ni kwamba, wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na kutenda matendo mema, hupendwa na baadhi ya watu, hii ni kutokana na kule kuwa na imani thabiti huwasukuma katika kutenda mambo mema yenye manufaa kwa watu, ikiwa haya ndio makusudio ya Aya, basi Imam Ali (a.s.) ndiye wa mwanzo wao. Nne: Lau kama aliyoyaeleza Ibn Taymiya ni sahihi, basi ingepelekea Maswahaba wengi pamoja na Matabiina kuwa wanafiki, kutokana na yale yaliyopokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) wakati aliposema kuhusiana na Imam Ali a.s: “Hakupendi isipokuwa Muumini, na wala hakuchukii isipokuwa mnafiki.’’43 43

Sahihi Muslim Juz.1, uk. 61. 33

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 33

11/25/2014 3:00:35 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Na pia imepokewa na wapokezi wengi wa hadithi, maneno ya Mtume (s.a.w.w.) yasemayo: “Mwenye kumtukana Ali atakuwa amenitukana mimi, na mwenye kunitukana mimi atakuwa amemtukana Mwenyezi Mungu.’’44 Na pia Bukhari amepokea maneno ya Mtume (s.a.w.w.) yasemayo: “Kesho nitampa bendera mtu ambaye Mwenyezi Mungu ataleta ushindi kwa kupitia mkono wake, anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na yeye anapendwa na Mwenyezi Mungu na Mtume wake.” Watu wakaingia katika usiku huku wakikesha kwa kufikiria ni nani ambaye atakayepewa hiyo bendera, ilipoingia asubuhi walikwenda kwa Mtume (s.a.w.w.) huku kila mmoja akitarajia kupewa bendera, Mtume (s.a.w.w.) akauliza: Yuko wapi Ali ibn Abi Talib? Akajibiwa: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni kwamba yeye anaumwa na macho. Akasema: Nileteeni. Basi akapelekwa, Mtume (s.a.w.w.) akamtemea mate katika macho yake na kumuombea dua, basi alipoa kama kwamba hakuwahi kuumwa, Mtume (s.a.w.w.) alimpa bendera. Ali (a.s.) akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Je, niwapige mpaka wawe kama sisi? Mtume (s.a.w.w.) akasema: Tekeleza ulichotumwa na ufike kwenye uwanja wao na uwalinganie kwenye Uislamu na uwaeleze yale yaliyo wajibu kwao miongoni mwa haki za Mwenyezi Mungu, naapa kwa Mwenyezi Mungu! Lau kama Mwenyezi Mungu atamuongoa mtu mmoja kwa kupitia kwako, basi ni bora kwako kuliko kuwa na ngamia mwekundu.’’45 Je, baada ya hadithi hii inayotupa taswira sahihi juu ya nafasi ya Imam Ali (a.s.) kwa Mwenyezi Mungu na Mtume 44 45

Mustadrakul Hakim Juz. 3, uk. 121. Sahihul Bukhari Hadithi Na. 421. 34

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 34

11/25/2014 3:00:35 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

wake, inatupasa tushikamane na madai batili ya Ibn Taymiya, eti kwamba Maswahaba wengi pamoja na Matabiina walikuwa wakimchukia Imam Ali (a.s.) na kumtukana? Kwa hakika madai yake haya yanawadhalilisha Maswahaba na Matabiina kutokana na kumchukia, kumtukana na kumpiga vita yule ambaye anapendwa na Mwenyezi Mungu na Mtume wake!! Tano: Madai yake kwamba, Ali hakuwa ni miongoni mwa makusudio ya Aya, ni madai yanayopingwa na yale yaliyopokewa na wanachuoni wa hadithi wa Kisunni, kwani imepokewa kutoka kwa Ibn Mardawayhi na Daylamiy kutoka kwa Barau ibn Azib kwamba amesema: Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kumuambia Ali, Karrama llahu wajhahu, sema: Ewe Mola Wangu nijaalie ahadi (malipo mema) kwako, na unijaalie mapenzi kwenye nyoyo za Waumini. Hapo Mwenyezi Mungu aliiteremsha Aya hii:’’ Hakika wale ambao wameamini na kutenda mema, Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema huwafanyia mapenzi.’’ Allamah al-Alusiy amesema: Shia Imamiya wamepokea kutoka kwa Ibn Abbas habari ya kuteremka Aya hii kwa Ali Karrama llahu wajhahu.’’46 Ni chuki ya aina gani inayomsukuma sheikhul-Islamu wa Kibanu Ummaiyya kwenye upotofu huu, na huku tukishuhudia tofauti ya wazi kati ya madai yake na yale yaliyomo katika riwaya?! Sita: Madai yake kwamba Maswahaba wengi pamoja na Matabiina walikuwa wakimchukia Ali (a.s.), kwa kweli ni madai ya uongo, ni madai yanayomfedhehesha kwa mujibu wa historia ya Maswahaba na Matabiina, kwani kuna ushahidi 46

Ruhul-Maaniy, al-Alusiy Juz.16, uk. 143. 35

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 35

11/25/2014 3:00:35 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

tosha unaobainisha namna ya Maswahaba mbalimbali kuwa pamoja na Imam Ali (a.s.) katika vita vikali alivyopigana, hii ni ishara ya wazi ya mapenzi waliyokuwa nayo juu yake. Ama kwa upande wa Matabiina nafasi yetu ni finyu kuweza kuelezea mafungamano yao ya dhati juu ya Imam Ali (a.s.) Na licha ya Abu Bakr kupewa kiapo cha utiifu katika ukumbi wa Saqifa bani Saida kwa namna vile ilivyokuwa, ni kwamba nyoyo za Maanswari wote zilikuwa na mapenzi naye, kama yalivyoelezwa hayo na mmoja wa wakuu wao, anayetambulika kwa jina la Nu’man ibn Ajlani Zurqiy pale aliposema katika kaswida yake: “Utashi wetu ulikuwa kwa Ali, kwa sababu yeye ndiye anayestahiki kuwa Khalifa katika hali ambayo tunajua na katika hali tusio ijua.”47 Na hili pia linatiliwa nguvu pale Umar na watu wengine walipompa kiapo cha utiifu Abu Bakr katika ukumbi wa Saqifa, Maanswari walisema, au baadhi yao: “Hatumpi kiapo cha utiifu isipokuwa Ali.’’48 Muhajirina wengi pamoja na Maanswari walioishi katika zama za ukhalifa wa Imam Ali (a.s.) walijiunga pamoja naye, na hoja hii inapata nguvu kwa pale ambapo Muawiya alipofanya uasi dhidi ya Imam Ali (a.s.) na kumuandikia barua ya vitisho, Imam Ali (a.s.) naye akamjibu kwa kumuandikia: “Na mimi naharakia kuelekea kwako nikiwa katika jeshi la miongoni mwa Muhajirina na Maanswari, na wanaowafuata kwa wema, wakiwa katika msongamano mkubwa…”49 Al-istia’b Juz. 4, uk.1505. Al-Kamil fi Tarikh Juz. 2, uk. 325. 49 Nahjul Balagha, barua ya Na. 28. 47 48

36

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 36

11/25/2014 3:00:35 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Na pia jeshi la Imam Ali (a.s.) lilipokwenda Sham (kupambana na Muawiya), Imam Ali (a.s.) alikuwa katikati ya wapiganaji wa mji wa Madina, na wengi wa hao watu wa Madina walikuwa ni Manswari, na pia mlikuwa na watu wa Madina kutoka ukoo wa Khuza’a, Kinana na wengineo.50 Kwa hakika wale waliomkubali Ali kuwa Kiongozi wao walikuwa ni miongoni mwa Muhajirina na Maanswari, na wale walioshiriki pamoja naye katika vita dhidi ya Muawiya na kundi ovu, majina yao ni katika majina mashuhuri katika utukufu, uchamungu na imani thabiti, watu hao ni wengi mno, miongoni mwao ni kama wafuatao: Hudhayfa ibn alYamaniy, Abu Dharr al-Ghaffariy, Ubayya ibn Ka’b, Miqdad ibn As-wad, Abbas, Fadhlu ibn Abbas, Abdullah ibn Abbas, Abu Haytham ibn Tayhani, Jabir al-Answariy, Abu Ayoub alAnswariy, Uthman ibn Hunaif, Sahlu ibn Hunaif, Hudhaima ibn Thabit al-Answariy, Ammar ibn Yasir, Qays ibn Sa’d ibn Ubada, Abdullah ibn Budayl al-Khuza’iy na wengineo. Basi Ibn Taymiya atutajie majina ya Maswahaba waliokuwa wakimchukia Ali na kumtukana na kumpiga vita, na pia aweke bayana historia yao na matendo yao, na yale waliokuwa wakiyaitakidi, na pia aeleze bayana wale waliokuwa pamoja na Muawiya katika vita vyao vya kidhalimu dhidi ya Imam Ali (a.s.) Bila ya shaka, licha ya uchache wao, ni kwamba watu hao walikuwa wamezama katika dunia yenye kudanganya na kuhadaa, na yenye kugeuka geuka na yenye unafiki. Na Mwenyezi Mungu amrehemu Abu Qaysi al-Awdiy kutokana na yale aliyoyasema: “Nimewadiriki watu wakiwa katika matabaka matatu: Watu wenye dini wakiwa ni wenye 50

Al-Kamil fi Tarikh Juz. 3, uk. 297. 37

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 37

11/25/2014 3:00:35 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

kumpenda Ali, na watu wa dunia wakimpenda Muawiya, na Makhawariji.’’51 Hongera kwa Ibn Taymiya, anawasifu watu wa dunia, na kujipanga nao safu moja!!

51

Al-istia’b Juz. 3, uk.111 38

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 38

11/25/2014 3:00:35 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

IBN TAYMIYA AIPINGA HADITHI YA UNDUGU

A

llamatul-Hilliy ameitaja hadithi inayoelezea undugu kati ya Mtume (s.a.w.w.) pamoja na Imam Ali (a.s.), lakini Ibn Taymiya ameipinga hadithi hiyo kwa kusema: “Hadithi hii ni ya kupangwa kwa mujibu wa wanachuoni wa hadithi, na hakuna yeyote anayeshuku miongoni mwa wale wenye uelewa wa hadithi ya kwamba ni hadithi ya kupangwa iliyowekwa na mtu mjinga, amedanganya kwa uwazi kabisa, na yeyote mwenye maarifa madogo ya hadithi anajua kwamba amedanganya. “Kwa hakika hadithi inayoelezea undugu, yote ni ya kutungwa, na Mtume (s.a.w.w.) hakujifanyia undugu na yeyote, na wala hakuwafanya ndugu kati ya Muhajiri na Muhajiri, na wala kati ya Abu Bakr na Umar, na wala kati ya Maanswari na Maanswari, lakini alichokifanya ni kuwafanya ndugu kati ya Muhajirina na Maanswari mara baada ya kuwasili kwake katika mji wa Madina.”52 Katika maneno haya ya Ibn Taymiya, kuna mambo mawili 1. Kupinga kufanyika undugu kati ya Mujahirina. 2. Kupinga kufanyika undugu kati ya Mtume (s.a.w.w.) na Imam Ali (a.s.) kwa njia yoyote ile, na hili ndilo jambo muhimu mno kwa Ibn Taymiya. 52

Minhaju Sunna Juz. 7, uk. 360-361. 39

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 39

11/25/2014 3:00:35 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Na kabla hatujaanza kunukuu maneno ya wanachuoni wa hadithi na wapokezi kuhusiana na undugu kati ya Muhajirina, kwanza ninapenda ninukuu maneno ya Ibn Hajar al-Asqalaniy katika kumjibu Ibn Taymiyya, amesema: “Katika kumjibu Ibn Mutwahhar, Ibn Taymiya amepinga kufanyika undugu kati ya Muhajirina, na hasa undugu kati ya Mtume (s.a.w.w.) na Ali, amesema: Hiyo ni kwa sababu sheria ya undugu iliwekwa kwa lengo la kujenga urafiki na mafungamano wao kwa wao, na nyoyo kuzifanya ziungane, kwa hivyo hakuna maana ya kuwepo undugu kati ya Mtume na yeyote miongoni mwao. Na jawabu hili ni kwa mujibu wa kiasi (kukisia) na kughafilika kwake kutokana na hekima ya undugu, kwani baadhi ya Muhajirina walikuwa na uwezo wa kimali, kiukoo na nguvu ikilinganishwa na wengine, kwa hivyo Mtume (s.a.w.w.) akawaunganisha kati ya wale walio juu kwa wale walio chini, na kwa mantiki hii ndio akaunganisha undugu kati yake na Ali, kwani yeye ndiye aliyekuwa akimuangalia tangu akiwa mdogo kabla ya Utume na kuendelea baada ya Utume, na pia undugu kati ya Hamza na Zayd ibn Haritha, kwa vile Zayd alikuwa mtumwa wao hapo kale, imethibiti undugu kati yao licha ya kwamba wote wawili walikuwa ni Wahajirina, na yatakujia maneno ya Zayd ibn Haritha wakati wa UmratulQadhaa aliposema: “Kwa hakika binti wa Hamza ni binti wa ndugu yangu.’’53 Na sasa sikiliza baadhi ya maneno ya wanachuoni wa hadithi na wapokezi wake ambao wameeleza undugu kati ya Muhajirina, na pia wakaeleza undugu kati ya Mtume (s.a.w.w.) na Imam Ali (a.s): 53

Fat-hul Bariy Juz. 7, uk. 271. 40

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 40

11/25/2014 3:00:35 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Muhammad ibn Habibu al-Baghdadiy, anasema “Palifanyika undugu kati ya Mtume (s.a.w.w.) pamoja na Maswahaba wake Muhajirina kabla ya Hijra (kuhama Makka kwenda Madina), Mtume (s.a.w.w.) aliwaunganisha kiundugu kati yao kwa raha na majonzi huko Makka, na akaunga undugu kati yake na Ali ibn Abi Talib r.a., na akaunganisha undugu kati ya Hamza ibn Abdul-Muttalib na Zayd ibn Haritha aliyekuwa mtumwa wa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), na aliunganisha undugu kati ya Abu Bakr na Umar r.a., na kati ya Uthman ibn Affan na Abdu Rahman ibn Awfi…54 Baladhuriy amesema “Wamesema: Mtume (s.a.w.w.) aliunganisha undugu kati ya Hamza na Zayd ibn Haritha juu ya raha na majonzi, na kati ya Abu Bakr na Umar, na kati ya…, na akasema kumwambia Ali: Wewe ni ndugu yangu.’’55 Na amesema tena katika kueleza wasifu wa Zayd ibn Haritha: “Na Mtume (s.a.w.w.) alimuunganisha kiundugu kati yake na Hamza, na kwayo alimuusia Hamza siku ya vita vya Uhud pale alipotaka kupigana.’’56 Mpokezi na mkusanyaji wa hadithi; Ibn Abdu Barri amesema: “Mtume (s.a.w.w.) aliunganisha undugu kati ya Wahajirina huko Makka, kisha akaunganisha undugu kati ya Muhajirina na Maanswari huko Madina, na katika kila tukio kati ya hayo Al-Muhabbar Juz.70, uk. 71. Answbul-Ashraafu Juz. 1, uk. 270. 56 Kitabu kilichotangulia uk. 472. 54 55

41

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 41

11/25/2014 3:00:35 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

mawili alimwambia Ali: ‘Wewe ni ndugu yangu duniani na akhera.’ Mtume (s.a.w.w.) aliunganisha undugu kati yake na yeye, kwa hivyo ndio ikawa kauli hii na inayo shabihiyana na hii inatoka kwa Ali (a.s.)”57 Makusudio ya kauli hii na inayoshabihiyana nayo inatoka kwa Ali, ni kauli yake iliyopokewa kwa njia tofauti inayosema: “Mimi mja wa Mwenyezi Mungu, na ndugu wa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na hatoyasema haya yoyote asiyekuwa mimi ila mtu huyo ni mwongo.’’58 Amesema Jamalu-Diyn al-Mazziy katika kumuelezea Zayd ibn Haritha “Mtume (s.a.w.w.) alifanya undugu kati yake na Hamza ibn Abdul Muttalib.’’59 Pia wanahadithi mbalimbali wameinukuu hadithi inayoelezea undugu kati ya Mtume (s.a.w.w.) pamoja na Imam Ali (a.s.) katika vitabu vyao, na pia kauli yake aliyomwambia Imam Ali: ‘Wewe ni ndugu yangu’, na pia kauli ya Imam Ali (a.s.) pale aliposema: ‘Mimi ni ndugu wa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu.’ Miongoni mwa riwaya zao hizo ni kama zifuatazo: Amenakili Tirmidhiy kutoka kwa Ibn Umar, amesema: “Mtume (s.a.w.w.) aliunganisha udugu kati ya Maswahaba wake, Ali akamuendea huku macho yake yakibubujika machozi, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu umewafanyia undugu Maswahaba wako na mimi hujanifanyia ndugu mtu yeyote, Mtume (s.a.w.w.) akasema: Wewe ni ndugu yangu duniani na Akhera.” Al-Istiabu Juz. 3, uk. 1098 -1099. Kitabu kilichotangulia uk. 1098. 59 Tahdhibul Kamal Juz. 1, uk. 37. 57 58

42

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 42

11/25/2014 3:00:35 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Abu Issa (Tirmidhiy) amesema: Hadithi hii ni nzuri na ngeni.’’60 Imam Ahmad naye amepokea kwa sanadi yake kutoka kwa Ibn Abbas, amesema: “Wakati Mtume (s.a.w.w.) alipotoka Makka, Ali alitoka na binti ya Hamza, Ali, Ja’far na Zayd wakazozana juu ya binti huyo, mpaka mzozo wao huo wakaufikisha kwa Mtume (s.a.w.w)…, Zayd akasema: “Huyo ni binti ya ndugu yangu, wakati huo Zayd alikuwa ameunganishwa undugu na Mtume (s.a.w.w.) kati yake na Hamza, Mtume (s.a.w.w.) akasema: ‘Wewe ni mtu uliyekuwa mtumwa wangu na mtumwa wake (huyo binti)’, na akasema kumwambia Ali: ‘Wewe ni ndugu yangu na sahiba yangu.’ Na akasema kumwambia Ja’far: ‘Wewe unashabihiana na umbile langu na tabia yangu.’’’61 Na Hakim amepokea kwa sanadi yake kutoka kwa Ibn Abbas r.a. amesema: “Ali alikuwa akisema wakati wa uhai wa Mtume (s.a.w.w): Mwenyezi Mungu anasema: Je, akifa au akauwawa ndiyo mtageuka mrudi nyuma? (Qur’an; 3:144). Naapa kwa Mwenyezi Mungu! Hatutogeuka kurudi nyuma baada ya Mwenyezi Mungu kutuongoa, naapa kwa Mwenyezi Mungu! Ikiwa atafariki au atauwawa, basi nitapigania lile ambalo alilipigania mpaka nifariki, naapa kwa Mwenyezi Mungu! Kwa hakika mimi ni ndugu yake, rafiki yake, mtoto wa ammi yake na mrithi wa elimu yake, basi ni nani aliye na haki zaidi kuliko mimi.’’62 Baada ya Nuru-Diyn al-Haythamiy kuinakili hadithi iliyotangulia amesema: “Ameipokea Tabraniy, na wapokezi wake ni watu wanaokubalika.’’63 Sunan Tirmidhiy Juz. 5, uk. 595 . Musnad Ahmad Juz. 1, uk. 230. 62 Al-Mustadrak ala swahiyhayn Juz. 3, uk. 126. 63 Majma’u -Zawaid, Juz. 9. uk. 134. 60 61

43

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 43

11/25/2014 3:00:35 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Ndugu msomaji, umejionea namna sheikhul-Islami wa Kibanu Umayya anavyojipofusha mbele ya riwaya hizi za wazi kabisa, zilizopokewa na wapokezi bingwa na wakusanyaji mahiri wa hadithi wa Kiahlu Sunna, na anapinga bila ya haya na aibu undugu kati ya Muhajirina, na undugu kati ya Mtume (s.a.w.w.) pamoja na Imam Ali (a.s.)! Je, hivi si ndivyo mtu huyu anavyoonesha chuki kwa Imam Ali? Kwa hakika ni mwenye kuidhalilisha nafsi yake mwenyewe na kuingiza katika shimo la ujinga na upotofu. Mshairi amesema “Pindi mtu anapoidhalilisha nafsi yake, basi Mwenyezi Mungu hatomtukuza mwenye kumtukuza huyo mwenye kujidhalilisha.�

44

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 44

11/25/2014 3:00:36 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

IBN TAYMIYA APINGA HADITHI YA NDEGE

M

iongoni mwa hadithi mashuhuri zinazozungumzia fadhila za Imam Ali (a.s.) zilizopokewa na wapokezi wa Kiahlu-Sunna, ni hadithi ya ndege wa kuchoma, na Ibn Taymiya anadai kwamba hadithi hiyo ni miongoni mwa hadithi za uzushi. Kabla ya kuanza kutoa majibu juu ya Ibn Taymiya, ni vyema kwanza tuanze kuinakili hadithi hiyo kama ilivyopokewa kwa moja kati ya njia za upokezi za Hakim Nisaburiy katika Mustadrak yake: Hakimu amepokea kwa sanadi yake kutoka kwa Yahya ibn Said, kutoka kwa Anas r.a., amesema: “Nilikuwa nikimtumikia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), mara Mtume (s.a.w.w.) akaletewa ndege aliyechomwa, akasema: ‘Ewe Mola Wangu niletee kiumbe umpendaye zaidi ili ale pamoja nami ndege huyu.’ Nikasema: Ewe Mola Wangu, mjaalie awe mtu miongoni mwa Maanswari, mara akaja Ali r.a., nikamwambia: Mtume wa Mwenyezi Mungu ana shughuli, aliondoka, kisha akaja tena, nikamwambia: Mtume wa Mwenyezi Mungu ana shughuli, aliondoka, kisha akaja tena, Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema: ‘Fungua.’ Aliingia, na Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema: ‘Ni kipi kilicho kuzuia usije kwangu?’ Akasema: ‘Hii ni mara ya tatu nakuja, lakini Anas ananirudisha kwa madai kwamba una shughuli.’ Mtume (s.a.w.w.) akasema: ‘Ni kipi kilichokufanya ufanye hivyo?’ Akasema: ‘Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Nilisikia dua 45

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 45

11/25/2014 3:00:36 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

yako, kwa hivyo nikapenda aje mtu katika jamaa zangu.’ Mtume (s.a.w.w.) akasema: ‘Kwa hakika mtu huwapenda jamaa zake.’’’ Hakim amesema: Hadithi hii ni sahihi kwa mujibu wa masharti ya masheikh wawili (Bukhari na Muslim), lakini hawakuitoa. Na watu zaidi ya thalathini wameipokea kutoka kwa Anas, kisha riwaya hii imesihi kutoka kwa Ali, Abu Said al-Khudriy na Safina.’’64 Ibn Taymiya ameipinga hadithi hii, kama alivyofanya katika majibu yake ya kumjibu Allamatul-Hilliy. Na majibu yetu kwa Ibn Taymiya yatahusisha vipengele viwili alivyovitaja, navyo ni kama vifuatavyo: Kwanza: Kutafuta usahihi wa yale aliyoyasema Allamatul-Hilliy kwamba: “Wameipokea hadithi hii jamuhuri ya wapokezi wote.’’ Ibn Taymiya katika kuipinga kauli hii amesema: “Amewasingizia, kwani hadithi ya ndege haikupokewa na yeyote na wapokezi wenye vitabu Sahihi, na wala wanachuoni wa hadithi hawakusema kwamba ni sahihi, bali ni hadithi iliyopokewa na baadhi ya watu, kama vile zilivyopokewa hadithi nyingine zinazoeleza fadhila za wengine, na kuna hadithi nyingi zilizopokewa zinazoelezea fadhila za Muawiya na zimetungiwa vitabu vingi, na wanachuoni hawazikubali hadithi hizi (za Muawiya) wala zile (za Ali). Pili: Hadithi ya ndege ni katika hadithi za uwongo na uzushi kwa mujibu wa wataalamu wa elimu, kama maandiko yanavyothibitisha, Abu Musa al-Madaniy amesema: “Wapokezi walio wengi wameziorodhesha njia mbalimbali za hadithi ya ndege kwa ajili ya mazingatio na kutaka maarifa, kama 64

Al-Mustadrak ala Swahiyhayn Juz. 3, uk. 130-131. 46

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 46

11/25/2014 3:00:36 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Hakim Nisaburiy, Abu Nua’ym na Ibn Mardawayhi, na Hakimu aliulizwa kuhusu hadithi ya ndege, alijibu: ‘’Si yenye kusihi.” Na sasa ni zamu yetu kujadili maneno ya Ibn Taymiya kama ifuatavyo: Kwanza: Anakusudia nini katika ibara hii, “Wapokezi wenye vitabu sahihi’ pale aliposema: Hadithi ya ndege hakuipokea yoyote miongoni mwa wapokezi wenye vitabu sahihi.’’ Ikiwa anawakusudia Bukhari na Muslim na si wengineo, kauli yake itakuwa ni sahihi, lakini ikiwa anakusudia wapokezi wote wenye vitabu sahihi, kauli yake hiyo itakuwa si sahihi, kwa sababu hadithi ya ndege imepokewa na Abu Isa Tirmidhiy katika kitabu chake ‘Sunan Tirmidhiy,’65 kitabu ambacho ni moja kati ya vitabu sita vyenye kutegemewa na wafuasi wa madhehebu ya Ahlus-Sunna, bali hata baadhi ya wanachuoni wamediriki kusema kwamba ni kitabu kinachoshika nafasi ya tatu baada ya Sahihi Bukhari na Sahihi Muslim. Kisha wapokezi wenye vitabu sahihi kutopokea hadithi fulani, haimaanishi hadithi hiyo kukosa umaarufu na kutosambaa kati ya wanachuoni wa hadithi, bali pia haidhuru usahihi wake, ni hadithi ngapi zilizo sahihi ambazo zimeenea kwa wanahadithi ambazo hazikupokewa na watu wenye vitabu sahihi, na njia ya kuyajua hayo ni kurejea katika kitabu maarufu kijulikanacho kwa ‘Mustadrik alaa Swahiyhayn’ kilichoandikwa na Hakim Nisaburiy, amezikusanya hadithi zilizo sahihi kwa mujibu wa masharti ya Bukhari na Muslim, lakini hawakuziandika katika vitabu vyao, na Dhahabiy amewafikiana na Hakim Nisaburiy katika kuzikubali hadithi ny65

Sunan Tirmidhiy Juz. 5, uk. 636-637. 47

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 47

11/25/2014 3:00:36 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

ingi ikiwa ni kwa mujibu wa masharti ya wawili hao (Bukhari na Muslim) au mmoja kati ya wawili hao. Pili: Ibn Taymiya kuipinga hadithi ya ndege kwa madai kwamba ni hadithi iliyopokewa na baadhi ya watu, kwa hakika madai yake haya ni katika kuonesha dharau katika fani ya hadithi na wapokezi wake, kwa kweli dai lake halina msingi, ni dai ambalo linapingana na maneno ya wanachuoni wa hadithi wa Kiahlus-Sunna, kama wanavyosema: Hakimu Nisaburiy amesema: “Watu zaidi ya thalathini wameipokea kutoka kwa Anas…’’66 Dhahabiy amesema: “Ama hadithi ya ndege ina njia nyingi sana…’’67 Ibn Kathir amesema: “Hadithi ya ndege, watu wameiandika katika vitabu, na ni hadithi yenye njia nyingi…’’ Kisha akasema: “Watu wameiandika hadithi hii katika vitabu mbalimbali, miongoni mwao ni: Abu Bakr ibn Mardawayh, Abu Tahir Muhammad ibn Ahmad ibn Hamdan… na nimeona kitabu cha Abu Ja’far ibn Jariri At-Tabariy ambaye ni mfasiri na mwanahistoria kilichokusanya njia za hadithi hii na maneno yake…’’68 Sheikh Abdu Rahman ibn Yahya al-Muallimiy amesema: “Na hadithi ya ndege ni mashuhuri, imepokewa kwa njia nyingi…’’ Baada ya hayo, ni kwamba, ama Ibn Taymiya ni jahili wa njia hizi nyingi za hadithi na umashuhuri wake, kwa kutoa madai asiyo na ujuzi nayo. Sasa ni vipi ifikie hali ya kusifiwa Mustadrak alaa Swahiyhayn Juz. 3, uk. 131. Tadhkiratul Hufadh Juz. 3, uk. 104. 68 Al-Bidayah Wannihayah Juz. 7, uk.383, 387. 66 67

48

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 48

11/25/2014 3:00:36 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

na kutukuzwa kwa mambo asiyoendana nayo, kwa kuitwa Sheikhul-Islam?! Ama inawezekana kwa Ibn Taymiya kuwa ni mtambuzi wa njia hizo, lakini kwa makusudi amejaribu kuficha ukweli kutokana na chuki zake dhidi ya Imam Ali (a.s.). Tatu: Ibn Taymiya amenakili maneno ya Abu Musa alMadaniy aliyefariki mwaka 581A.H. ya kwamba: “Hakim aliyefariki mwaka 405A.H. aliulizwa kuhusiana na hadithi ya ndege, alijibu kwa kusema: Si sahihi.” Sasa ni vipi wakati Hakim yeye mwenyewe katika kitabu chake anaeleza bayana juu ya usahihi wa hadithi hii!! Ewe Sheikhul-Islamu wa Kibanu Umayya uko wapi uaminifu wa kielimu? Kutokana na Hakim Nisaburiy ambaye Dhahabiy amemueleza kwamba ni mkusanyaji mkubwa wa hadithi na ni Imam wa wanahadithi,69 kusema hadithi hii ni sahihi, kwa kweli hili ni pigo kubwa kwa Ibn Taymiya kutokana na madai yake kwamba wanachuoni wa elimu ya hadithi hawaikubali hadithi hii. Wala sio Hakim peke yake aliyesema hadithi hii ni sahihi na kuikubali, bali kuna njia nyingine ya usahihi kama ilivyo kwa Tabraniy na kukubaliwa na Haythamiy. Ameipokea Tabraniy kwa sanadi yake, kutoka kwa Abdu Rahman ibn Abu Naim, kutoka kwa Safina aliyekuwa mtumwa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) “Ni kwamba Mtume (s.a.w.w.) alipelekewa ndege, akasema: Ewe Mola Wangu niletee kiumbe umpendaye zaidi ili ale pamoja nami ndege huyu. Basi aliyekwenda alikuwa ni Ali r.a…”70 69 70

Tadh-kitatul Hufadh Juz. 3, uk.1039. Al-Mu’jamul Kabir Juz. 7, uk. 82. Hadith Na. 6437 49

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 49

11/25/2014 3:00:36 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Nuru-Diyn Haythamiy amesema: “Wapokezi wa Tabraniy ni sahihi (madhubuti), isipokuwa Fatr ibn Khalifa yeye ni Thiqa (mkweli).’’71 Na jambo la kushangaza zaidi, ni kwamba Dk. Muhammad Rashad Salim ambaye amekifanyia uhakiki kitabu ‘Minhaju Sunna.’ Amenukuu maneno ya Haythamiy yanayohusiana na hadithi hii, lakini amejighafilisha kutaja maneno yake haya: “Wapokezi wa Tabraniy ni sahihi (madhubuti), isipokuwa Fatr ibn Khalifa yeye ni Thiqa (mkweli).’’ Ni kwa sababu anaelewa fika kwamba maneno haya ya Haythamiy yanabatilisha madai ya Sheikh wake, kwa kutumia njia ya kutoyaorodhesha maneno ya wanachuoni yaliyosemwa katika kuthibitisha ubora na fadhila za Imam Ali (a.s.) na Ahlulbayt kwa ujumla! Nne: Ibn Taymiya anaidanganya nafsi yake na elimu yake kwa madai kwamba, hadithi ya ndege ni katika riwaya za uzushi na kupangwa kwa mujibu wa wanachuoni na wale wenye maarifa ya upokeaji wa hadithi. Hakuna yeyote kati ya watu wenye maarifa ya upokezi wa hadithi aliyethubutu kutoa madai haya, madai ambayo hayatolewi isipokuwa na yule aliyesibiwa na ujinga au mtu mkaidi na mwenye chuki binafsi. Ni kwamba wapokezi wengi miongoni mwa wapokezi wa Kiahlus-Sunna wamepokea hadithi hii na kuinakili katika vitabu vyao, na hata baadhi yao wametenga vitabu maalumu kwa lengo la kueleza njia ya tofauti zilizopokelewa hadithi hii, miongoni mwao ni: Abu Ja’far Tabariy, Hakim Nisaburiy, Abu Nu’aym Isfahaniy, Ibn Mardawayhi, na Shamsu-Diyn Dhahabiy, na hakuna yoyote kati ya hawa aliyesema ya kwamba hadithi hii ni ya uongo, na hata wale walioathiriwa na madhehebu yao hawakuthubutu kusema 71

Majma’u Zawaid Juz. 9, uk.126. 50

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 50

11/25/2014 3:00:36 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

hivyo katika kuikataa, bali walichosema ni kwamba hadithi hii ni dhaifu. Na ushahidi wa haya hebu tuangalie baadhi ya kauli zao: Baada ya Tirmidhiy kuipokea hadithi kwa njia ya Suddiy, amesema: “Hadithi hii hatuijui kwamba ni hadithi ya Suddiy isipokuwa katika njia hii, na hadithi hii imepokewa kwa njia tofauti kutoka kwa Anas…, na Suddiy jina lake ni Ismail ibn Abdu Rahman, na amemsikia Anas ibn Malik, na ameipokea Husain ibn Ali. Shu’ba amethibitisha ukweli wake, na Sufiyani Thauriy, na Zaida, na amethibitisha ukweli wake Yahya ibn Said al-Qattani.’’72 Abu Jafar Muhammad ibn Amru al-Uqayliy amesema: “Njia za hadithi hii zina ulaini (si madhubuti).’’73 Na Ibn Jawziy ambaye alifariki mwaka 597A.H. ameinakili hadithi hii katika kitabu chake kiitwacho ‘al-Ilalul-Mutanahiya’ kwa njia moja kutoka kwa Ibn Abbas na kwa njia kumi na sita kutoka kwa Anas,74 na wala hadithi hii hajaitaja katika kitabu chake ‘al-Maudhuat.’ Inaelezwa kwamba baadhi ya wahakiki na washereheshji wa vitabu vya hadithi, kama vile Allama Ali ibn Sultan Muhammad al-Qariy, amedai kwamba Ibn Jawziy amesema kwamba, hadithi ya ndege ni ya uwongo.75 Kwa kweli kauli hii si sahihi, na ukweli ni kwamba, amesema ni kuwepo hadithi nyingine ya uwongo, ambayo ni ile aliyoipokea alQasim ibn Jundub kutoka kwa Anas, amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w: “Ewe Anas, mtu wa mwanzo ataSunan Tirmithiy Juz. 5, uk. 636-637. Dhuafaul-Kabiir Juz. 4, uk. 189. 74 Al-ilalul- Mutanahiya Juz. 1, uk. 226-228. 75 Mirqatul- Mafatiih Juz. 9, uk. 393. 72 73

51

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 51

11/25/2014 3:00:36 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

kaye ingia kwa kupitia mlango huu ni kiongozi wa Waumini…, mara akaingia Ali r.a.’’76 Na Shamsu-Diyn Dhahabiy amesema: “Ama hadithi ya ndege ina njia nyingi sana, na nimeielezea kwenye kitabu, na kutokana na njia zake kuwa nyingi ni dalili kuwa ni hadithi yenye mashiko.’’77 Na amesema tena: “Hadithi ya ndege, licha ya udhaifu wake, ina njia njingi, na nimeielezea katika juzuu, na wala haikuthibiti, na wala mimi si mwenye kuitakidi ubatili wake.”78 Na Ibn Kathir amesema: “Watu wameikusanya hadithi hii katika vitabu mbalimbali na kuielezea…, kwa muhtasari, kwa yale yaliyomo moyoni mwangu (ninavyoamini) kuhusiana na usahihi wa hadithi hii, kunahitaji uchunguzi zaidi, licha ya kwamba njia zake ni nyingi.’’79 Ewe ndugu mpendwa msomaji, umejionea mwenyewe, kwamba wataalamu hawa wa fani ya hadithi wa Kiahlu Sunna, hawakusema kwamba hadithi ya ndege ni hadithi ya kutungwa na kuzuliwa, bali walichokisema ni kwamba hadithi hiyo ni dhaifu, na kwa kauli zao hizo, imebainika kwa wazi uwongo wa Ibn Taymiya kwa kule kudai kwake kwamba hadithi hii ni katika hadithi za uwongo na zilizobuniwa, haya ni kwa mujibu wa wataalamu wa elimu ya hadithi.

Al-Maudhuat libn Hawziy Juz. 1, uk. 376-377. Tadhkiratul- Kufadh Juz. 3, uk. 1042. 78 Syaru A’lamu Nubalai Juz. 13, uk. 233. 79 Al-Bidayah Wannihayah Juz. 7, uk. 387. 76 77

52

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 52

11/25/2014 3:00:36 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Kuathirika Kimadhehebu ndiko Kulikopelekea Kudhoofishwa Hadithi ya Ndege

U

kweli ni kwamba, lau kama wataalamu hawa wa fani ya hadithi, si kule kuathirika kwao juu ya imani ya kwamba Abu Bakr ndiye mbora wa Maswahaba, basi wasingethubutu kuidhoofisha hadithi hii, na haya yanashuhudiwa katika maneno yao yenye kugongana gongana, na haraka yao ya kuwahukumu wapokezi wa hadithi, ambayo imepokewa kwa njia njingi sana kwa mujibu wa maneno ya Dhahabiy kama tulivyoona, na pia kujaribu kwao kuleta tafsiri mbalimbali, pale walipokosa udhaifu wa wapokezi wake katika baadhi ya njia za hadithi hiyo. Ushahidi wa hayo ni kama ifuatavyo: 1. Kauli ya Dhahabiy, katika kuielezea riwaya ya Hakim, ambayo ameipokea kwa njia ya Muhammad ibn Ahmad ibn Iyadh ibn Abi Twayba, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Yahya ibn Hasan, kutoka kwa Sulayman ibn Bilal, kutoka kwa Yahya ibn Said, kutoka kwa Anas. Dhahabiy amesema: “Ibn Iyadh simjui.’’

Tunauliza: Je, huko kutomjua kwake Ibn Iyadh, kumemfanya aseme: “Zamani sana nilikuwa sidhani kwamba, Hakim asingethubutu kuiweka hadithi ya ndege katika kitabu chake (Mustadrakul Hakim)!!”80 Kwa nini Dhahabiy asidhanie kwamba Hakim alikuwa anaelewa yale asiyoyaelewa 80

Talkhis, fii dhayli al-Mustadrak ala Swahiyhayn Juz. 3, Uk.131. 53

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 53

11/25/2014 3:00:36 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

yeye, hasa ikizingatiwa kwamba Hakim alikuwa ametangulia kiumri kuliko yeye, na yeye mwenyewe amemuelezea kwamba ni Imam wa wanahadithi?! Bila ya shaka kwa mtu mwenye kufanya utafiti, itambainikia yale yaliyokuwa yamejificha katika nafsi ya Dhahabiy, inashangaza kueleza ya kwamba hamjui Muhammad ibn Ahmad ibn Iyadh, na ilhali katika tarjama yake amemuelezea kama ifuatavyo: Amepokea kutoka kwa Abi Ghassan Ahmad ibn Iyadh ibn Abi Twayyiba al-Masriy, kutoka kwa Yahya ibn Hasan, alitaja hadithi ya ndege, na Hakim akasema: Hadithi hii iko kwa mujibu wa sharti ya Bukhari na Muslim.’’ Dhahabiy akaongeza kusema: “Nilisema: Wote ni waaminifu, isipokuwa huyu ninamtuhumu, kisha ikanibainikia ya kwamba ni mkweli, Tabraniy amepokea kutoka kwake…, amefariki mwaka 261A.H. Ama baba yake mimi simjui.’’81 2. Kauli ya Sheikh Shihabud-Diyn Fadhlullahi Taurabashtiy, katika kusherehesha hadithi ya ndege kwa mujibu wa riwaya ya Tirmidhiy: “Licha ya kwamba sisi hatuzikatai fadhila za Ali r.a. na kutangulia kwake katika Uislamu, na uhusiano wake wa karibu kwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na kuwa na udugu naye katika Dini…, sisi hatuoni vyema kuzichambua mfano wa hadithi hizi, kwa yale yanayohofiwa miongoni mwa upotoshaji wa wenye kusifu kupita mpaka, na uchambuzi wa wajinga, na kwa hadithi hii mtu mzushi hurushia mshale wake, na kuunganisha ubawa wake, na 81

Mizanul-I’tidali Juz. 3, uk. 465. 54

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 54

11/25/2014 3:00:36 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

kuifanya kuwa ni sababu ya kuuponda ukhalifa wa Abu Bakr, ambao ni ukhalifa wa mwanzo waliokubaliana nao Waislamu katika ummah huu…, kwa kuwafikishwa na Mwenyezi Mungu. Tunasema Hadithi hii haiwezi kuzishinda zile ambazo zinawajibisha kutangulizwa Abu Bakr, na zinazoelezea ubora wake miongoni mwa hadithi sahihi pamoja na ijmai (makubaliano) ya Maswahaba juu ya ubora wake. Kutokana na sanadi yake (kuwa madhubuti), ndani yake kuna maelezo ya wapokezi, na wala haijuzu kuitafsiri mfano wa hadithi hii kwa yale yanayokwenda kinyume na ijmai, hasa ikizingatiwa kwamba katika sanadi yake yumo Swahaba Anas ambaye anaingia katika ijmai hii…, lau kama hadithi hii itathibiti usahihi wake, basi isitafsiriwe kwa tafsiri inayopingana na yale anayoyaitakidi (ubora wa Abu Bakr juu Maswahaba wote), wala kupingana na yale yaliyo sahihi zaidi katika matini na sanadi, basi maneno yake Mtume (s.a.w.w.) aliposema: “Kiumbe aliye bora zaidi kwako,” yatafsiriwe hivi: Niletee kiumbe aliye bora zaidi kwako ambaye ana wenzake katika ubora, nao ni wale walio na ubora kwa mujibu wa ijmai (Maswahaba), basi hadithi hii itafsiriwe kama hivi tulivyoeleza, au itafsiriwe hivi: Alikusudia kiumbe bora zaidi kwake miongoni mwa watoto wa ammi yake na jamaa zake, na ilikuwa ni kawaida ya Mtume (s.a.w.w.) kutamka maneno yanayojumuisha watu wote, lakini hukusudia watu maalumu, na pia kutamka maneno yenye kuhusisha watu maalumu…’’82 82

Sharhu Twaybiy ala mishkaatil- Aswbah Juz.11, uk. 270-271. 55

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 55

11/25/2014 3:00:36 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

3. Kauli ya Ibn Kathir kama ilivyotangulia: Kwa muhtasari, katika moyo kuna kitu katika kuikubali hadithi hii (hadithi ya ndege), licha ya kwamba njia zake ni nyingi. Bila ya shaka, wasiwasi wa kuikubali hadithi hii uko katika moyo, na sio katika sanadi yake na matini, na lau kama moyo ungeshikamana na haki na kusalimika na matamanio ya kinafsi, basi tatizo lisingekuwepo, na hadithi hii ingeandikwa katika vitabu sahihi vya hadithi. 4. Kupita kiasi kwa Ibn Jawziy katika kutumia lahaja kali za kuwadhoofisha wapokezi wa hadithi hii, pamoja na kufumbia macho lugha iliyotumiwa na wanahadithi wengine katika kuwaadilisha, kwa mfano: a. Hadithi aliyoipokea kwa njia ya Ubaydullah ibn Musa al-Absiy, kutoka kwa Isa ibn Umar al-Qariy, kutoka kwa Ismail ibn Abdur Rahman Suddiy, kutoka kwa Anas. Ibn Jawziy amesema: “Riwaya hii si sahihi, kwa sababu Ismail Suddiy amedhoofishwa na Abdur Rahman ibn Mahdiy na Yahya ibn Mai’n.”83 Hivi ndivyo Ibn Jawziy anavyosema, licha ya kwamba Suddiy aliyefariki mwaka 127A.H., Shu’ba amepokea kutoka kwake, na Sufiyani Thawriy, na Zaidatu ibn Qudama, wote hao wamesema kwamba ni mtu mwaminifu, na Muslim amepokea kutoka kwake kama ilivyo katika Sahihi yake (Sahihi Muslimu), na pia wamepokea kutoka kwake wanahadithi wanne (Tirmidhiy, Ibn Majah, An-Nasai na Abu Daud). Na Yahya ibn Said al-Qattan amesema kwamba ni mwaminifu, na pia Ahmad ibn Hanbal, al-A’jliyyi na ibn Habban. Na ibn Adiyy amesema: “Kwangu mimi ni mtu mnyooshaji wa hadithi, ni mkweli si mbaya katika hadithi.’’84 83 84

Al- Ilalu al-Mutanahiya Juz.1, uk. 230. Sunan Timidhiy Juz. 5, uk. 3721, Tahdhibul Kamal Juz. 3, uk. 132, Mizanul56

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 56

11/25/2014 3:00:36 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Kisha imepokewa kutoka kwa Abdur-Rahman ibn Mahdiy yale yanayopingana na kudhoofishwa kwa Siddiy, kutokana na Abdullah ibn Ahmad ibn Hanbal kusema: “Nilimsikia baba yangu akisema: Siku moja Yahya ibn Mai’n alisema mbele ya Abdur-Rahman ibn Mahdiy, na akaja Ibrahim ibn Muhajir na Suddiy, Yahya akasema: ‘Hao wawili ni madhaifu.’ Basi Abdur-Rahman alikasirika na kuchukizwa na yale aliyosema.’’85 b. Hivi ndivyo inavyodhihirika baada ya kuelewa maneno ya wanahadithi wakubwa wa Kiahlus-Sunna katika fani ya kujeruhi na kuadilisha wapokezi, juu ya Ismail Suddiy, ni kwamba wapokezi wa hadithi ya ndege ni watu madhubuti wenye kukubalika. Hadithi aliyoipokea kwa njia ya Hasan ibn Hammad Adhabiyy, kutoka kwa Mus-har ibn Abdul Malik, kutoka kwa Isa ibn Umar al- Qariy, kutoka kwa Ismail ibn Abdur-Rahman ibn Suddiy, kutoka kwa Anas. Kisha ibn Jawziy alimdhoofisha Suddiy na Mus-har, kutokana na kauli ya Bukhari: “Na kwa Mus-har kuna shaka.’’86 Ninasema: Ama Suddiy, imebainika ya kwamba wanachuoni wote wamethibitisha ukweli wake, na kuna wengine waliomdiriki katika maisha yake na kupokea kutoka kwake, nao ni watambuzi zaidi kuliko wale waliokuja baada yao, kama vile Yahya ibn Ma’in aliyefariki mwaka 233A.H. na wengineo. Ama Mus-hir, ni kwamba umethibitishwa ukweli wake na mwanafunzi wake; Hasan ibn Hammad Adhabiyy, ambaye I’tidali Juz. 1, uk. 236. Tahdhibul Kamal Juz. 3, uk. 135. 86 Al- Ilalu al-Mutanahiya Juz.1, Uk. 362. 85

57

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 57

11/25/2014 3:00:36 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

ni mwaminifu katika hadithi,87 na Abu Ya’ala al-Muswiliy, na Ibn Habban amemtaja katika kitabu chake cha ‘Athuqaat’ (wapokezi waaminifu), na akasema: ‘Hukosea na kubabaika.’ Na An-Nasaiy amesema: ‘Si madhubuti.’88 Na hadithi hii ameipokea An-Nasaiy kutoka kwa Zakaria ibn Yahya, kutoka kwa Hasan ibn Hammad, na ameipokea Abu Ya’ala al-Muswiliy aliyefariki mwaka 307A.H. kutoka kwa Hasan ibn Hammad, wote wawili wameipokea kwa sanad iliyotangulia. Kisha Ibn Jawziy ameipokea hadithi ya ndege kwa njia ya Ahmad ibn Farqad al-Juddiy kutoka kwa Abu Humma Muhammad ibn Yusuf al-Yamaniy kutoka kwa Abu Qurra ibn Musa ibn Tariq, kutoka kwa Musa ibn Uqba, kutoka kwa Abu Nadhar Salim, aliyekuwa mtumwa wa Umar ibn Ubaydullah kutoka kwa Anas ibn Malik, na wala hakuzungumza kuhusiana na wapokezi wake na wala kumjeruhi yeyote kati yao. Kwa hivyo, hadithi hii si yenye matatizo kwa upande wake, lakini wale waliokuja nyuma ya Ibn Jawziy, hawakuona ila kumtia aibu mmoja wa wapokezi wake bila ya kuwa na dalili yoyote ile, kwani Dhahabiy amesema wakati wa kumuelezea Ahmad ibn Said ibn Farqad Juddiy katika kitabu chake: “Amepokea kutoka kwa Abi Humma, na AtTabariy amepokea kutoka kwake, akaitaja hadithi kwa mujibu wa sanad ya Sahihi Bukhari na Sahih Muslim, basi huyo (Ahmad ibn Said) ni mwenye kutuhumiwa kwa utungaji wa hadithi.’’89 Tahdhibul Kamal Juz. 6, Uk. 133. Tahdhibul Kamal Juz. 27, uk. 577. Mizananul-Ii’tidal Juz. 4, uk. 113. 89 Mizananul-Ii’tidal Juz.1, uk.100. 87 88

58

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 58

11/25/2014 3:00:36 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Ibn Hajar al-Asqalaniy amesema baada ya maneno ya Dhahabiy: “Ameipokea Hakim kutoka kwa Muhammad ibn Salih al-Andalusiy kutoka kwa Ahmad huyu, kutoka kwa Abu Humma…, na Ahmad ibn Said ni maarufu kwamba ni katika masheikh wa Tabaraniy, na ninadhani kwamba ameingiza sanadi ndani ya sanadi!!90 Sayyid Muhsin al-Amin amesema: “Lau kama angekuwa ni miongoni mwa masheikh wa Tabaraniy, basi haiyumkiniki kwa Dhahabiy kumkubali, na vipi amkubali na wakati anapokea hadithi isemayo kwamba, Ali ni kiumbe bora kwa Mwenyezi Mungu na kwa Mjumbe wake (s.a.w.w.)! Kwa kweli hili ni jambo lisilowezekana.” Ama kule Ibn Hajar al-Asqalaniy kudhani kwamba ameingiza sanadi ndani ya sanadi, kwa hakika hiyo ni dhana ambayo haitengui haki, na hakuna upotofu kwa yoyote isipokuwa kauli yake iliyo mbali na njia ya sawa. Muhtasari wa uchambizi huu, tunasema ya kwamba: “Hadithi ya ndege ni hadithi iliyo mashuhuri kwa wafuasi wa madhehebu ya Ahlu Sunna, na ni sahihi kwa Hakim Nisaburiy na wengineo. Wengi miongoni mwa wanahadithi wameipokea kwa njia nyingi, na baadhi yao kwa mujibu wa masharti ya Bukhari na Muslim, na baadhi yao kwa sanadi ya wapokezi ambao wote kwa ujumla wao ni wapokezi wazuri na wakutegemewa, wote ni wa kweli isipokuwa mmoja, ambaye naye wanahadithi wamehitalifiana juu ya ukweli wake na udhaifu wake. Na kwa kiasi fulani tumethibitisha namna itikadi ya kimadhehebu ilivyoshika nafasi katika kuidhoofisha hadithi hii, kutokana 90

Lisanul- Mizan Juz. 1, uk. 177. 59

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 59

11/25/2014 3:00:36 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

na hili maneno makali yamepita mpaka yametumika katika kuwajeruhi wapokezi na kutuhumiwa kwa tuhuma nzito. Pamoja na yote hayo, hatujamkuta yeyote miongoni mwa wanachuoni wa hadithi aliyethubutu kusema ya kwamba hadithi hii ni ya uwongo na iliyobuniwa, kwa bali kauli zao ziko katika hali ya kusema ni hadithi iliyo sahihi au ni nzuri au ni dhaifu, na kuna ambao wamenyamaza kwenye baadhi ya njia zake, lakini Ibn Taymiya hajali ayasemayo, na wala hamuogopi Mwenyezi Mungu katika yale anayoyasena na kuyaandika, amedai kwamba hadithi hii ni katika hadithi za kutungwa na kuzuliwa, kama kwamba hakusoma kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo: “Na kila kidogo na kikubwa kimeandikwa.” (Qur’an,54:53).

60

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 60

11/25/2014 3:00:36 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Mpingaji hanufaiki na Hoja

S

heikh Zayn Diyn al-Munawiy al-Qahiriy, aliyefariki mwaka 1031A.H., amesema katika kumjibu Ibn Taymiya: “Na hadithi hizi, hata kama itaonekana kwamba zote ni dhaifu, lakini hadithi dhaifu haikataliwi, hii ni kwa sababu ya kupata uzito kutokana na wingi wa njia yake na kukithiri mapokezi yake, isipokuwa (hupingwa na) mtu mjinga asiye na ujuzi wa elimu ya hadithi, au mkaidi mwenye chuki, na ninadhani ya kwamba Ibn Taymiya anasifika na sifa hii ya pili.’’91

Na kwa kumalizia maudhui haya napenda niwatajie watafutaji wa haki sanadi nyingine ya hadithi ya ndege iliyonakiliwa na Ibn Kathir katika kitabu chake cha ‘al-Bidayah Wannihaya,’ na amekiri kwamba sanadi yake ni nzuri zaidi ikilinganishwa na sanadi ya Hakimu, kwani wapokezi wake wote ni wakweli, na hakuna yeyote mwenye maneno juu yao, basi sasa isome sanadi ya hadithi pamoja na maelezo ya wasahihishaji wa hadithi kuhusu wapokezi wake: Amesema Ibn Kathiri, huku akitaja njia nyingi za hadithi hii: “Na imepokelewa na Abi Hatim, kutoka kwa Ammar ibn Khalid al-Wasitiy, kutoka kwa Is-haqa al-Azraq, kutoka kwa Abdul Malik ibn Abi Sulayman, kutoka kwa Anas, kisha akaitaja hadithi.”92 Hii ndio sanadi ya hadithi, ama kuhusiana na maneno ya wasahihishaji ni kama yafuatavyo: 91 92

Faydhul-Qadiy, Sharhu Jami’u Swaghiyr Juz. 3, uk. 221. al-Bidayah Wannihaya Juz. 7, uk. 363. 61

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 61

11/25/2014 3:00:36 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Ibn Abi Hatim, jina lake ni Abdur Rahman ibn Muhammad ibn Idris al-Handhaliy Arraziy, alifariki mwaka 327A.H. Abu Ya’ala al-Khaliliy amesema: “Alikuwa bahari (amebobea) katika elimu na maarifa ya wapokezi.’’ Na Imam Abul Walid al-Bajiy, amesema: “Ni mkweli mwenye kunakili hadithi kwa usahihi.’’93 Ammar ibn Khalid al-Wasitiy. Abdur-Rahman ibn Abi Hatim amesema: “Alikuwa ni mtu madhubuti mkweli.’’ Na Ibn Habban amemtaja katika Thuqaat (Wapokezi wanaokubaliwa). Na Ibn Hajar amesema: “Ni mkweli.’’94 Is-haqa ibn Yusuf al-Azraq, aliyefariki mwaka 195A.H. Yahya ibn Ma’in amemthibitisha kwamba ni mkweli pamoja na al-A’jliy, naye ni katika wapokezi wa Sahihi mbili (Bukhari na Muslim), na wamepokea kutoka kwake watu wanne wenye vitabu vya Sunan (Ibn Majah, Tirmidhiy, An-Nasaiy na Abu Daud).’’95 Abdul Malik ibn Abi Sulayman Maysara al-Urzumiy, aliyefariki mwaka 145A.H., Ahmad ibn Hanbal amemkubali kwamba ni madhubuti, pia Yahya ibn Ma’in, al-A’jliy, AnNasaiy na wengineo, na kutoka kwa Sufiyani Thawriy alikuwa akisema kwamba Abdul Malik ibn Abi Sulayman ana daraja. Muslim amepokea kutoka kwake na watu wenye Sunan nne, na Bukhari ametoa ushahidi kupitia kwake katika Sahih yake, na amepokea kutoka kwake…96 Na mwenye kutaka kujua zaidi njia za hadithi hii, basi arejee katika kitabu ‘Abaqatul- Anwar’ cha Sayyid Hamid Siyar a’lami Annubalai Juz. 13, uk. 263. Tahdhibul Kamal Juz. 21, uk.187. 95 Tahdhibul Kamal Juz. 2, uk. 496. 96 Tahdhibul Kamal Juz. 18, uk. 322. 93 94

62

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 62

11/25/2014 3:00:36 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Husain al-Musawiy al-Kanturiy Allakhanuwiy, aliyefariki mwaka 1306A.H., na Sayyid Ali al-Milaniy amekifupisha na kukiita ‘Nafahatul-Azhari fii Khulaswatu Abaqatul-Anwar.’ Humo amefanya utafiti wa kina juu ya hadithi ya ndege kwenye juzuu mbili kamili, ambazo ni ya kumi na tatu na ya kumi na nne, ukipenda kazipitie.

63

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 63

11/25/2014 3:00:36 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

TUHUMA ZAKE DHIDI YA IMAM ALI (A.S.) KWAMBA ALIPIGANA KWA AJILI YA DUNIA NA SIO KWA AJILI YA DINI

K

wa hakika mwenye kukisoma kitabu ‘Minhaju Sunna,’ atagundua katika maudhui mengi namna mtungaji wake alivyo na chuki dhidi ya Imam Ali (a.s.) pamoja na watoto wake, na wakati mwingine hujaribu kuficha chuki zake hizo kwa kuwasifu, lakini ni haraka sana sifa hizo huzipinga na kuzikataa, kutokana na mwenendo wake huo, Ibn Hajar ameuelezea wasifu wa Ibn Taymiya kwa kusema: “Na miongoni mwao (Maulamaa) wako wanaomnasibisha na unafiki kutokana na maneno yake dhidi ya Ali kama ilivyotangulia. Na kutokana na kauli yake: ‘Alikuwa (Ali) ni mwenye kutengwa kila anapokwenda.’ Na ‘kwamba alijaribu kuutafuta ukhalifa mara nyingi, lakini hakuupata.’ Na ni kwamba ‘alikuwa akipigania uongozi na sio Dini.’ Na kutokana na kauli yake: ‘Alikuwa akipenda uongozi, na Uthman alikuwa akipenda mali.’ Na kutokana na kauli yake: ‘Abu Bakr alisilimu akiwa mtu mzima, akielewa aliyokuwa akiyasema, na Ali alisilimu akiwa mtoto, Uislamu wake hausihi kwa mujibu wa maneno (ya baadhi ya watu).’ Na maneno yake katika kisa cha kumposa binti wa Abu Jahal, na kuwa ‘alikufa bila ya kumsahau.’ Basi wanachuoni wakamnasibisha na unafiki, kutokana na kauli ya Mtume s.a.w.w: ‘Na hakubughudhi wewe isipokuwa Mnafiki.’”97 97

Addurul- Kamina Juz. 1, uk.155. 64

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 64

11/25/2014 3:00:36 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Maneno haya yanabainisha ni namna gani mtu huyu alivyo na chuki dhidi ya Imam Ali (a.s.) Na haya aliyoyataja Ibn Hajar ni machache tu kati ya mengi, na yeyote atakayejaribu kukipitia kitabu ‘Minhaju Sunna’ atakuta ibara nyingi zenye kushabihiana na hizi. Na Dkt. Mahmoud Sayyid Sabiih, amevipitia vitabu vya Ibn Taymiya kikiwemo ‘Minhaju Sunna’ na amekuta makosa dhidi ya Mtume (s.a.w.w.) pamoja na Ahlulbayt wake baada ya kusoma kurasa elfu arubaini, anasema: “Nimefuatilia kauli nyingi za wazushi wa zama hizi, nikagundua hutoa dalili kupitia maneno ya Ibn Taymiya, baada ya hapo nikafuatilia maneno ya Ibn Taymiya kwa kusoma takribani kurasa elfu arubaini au zaidi, nikagundua amekosea kuliko kukubwa dhidi ya heshima ya Mtume (s.a.w.w.) pamoja na Ahlulbayt wake na Maswahaba wake. Na wewe ndugu msomaji unaelewa kwamba Mtume (s.a.w.w.) na Ahlulbayt wake (a.s.) ni watu muhimu sana kwetu sisi sote kuliko Ibn Taymiya…’’98 Basi na sisi tunaangazia kitabu chake, ili tuyabainishe yale aliyoyaeleza, tena kwa kueleza mahala alipoyaandika, ili tuwe na yakini nayo. 1. Ibn Taymiya amesema: “Fatwa zake (Imam Ali) ni sawa na Fatwa za Umar na Uthman, si kwamba fatwa zake ni bora kuliko zao, na kauli zao zina uzito zaidi kuliko kauli zake, wala Mtume (s.a.w.w.) alikuwa hamridhii na kumsifu zaidi kuliko wao, bali msemaji amesema: ‘Haijulikani kwamba Mtume (s.a.w.w.) alimlaumu Uthman kwa jambo lolote lile, na amemlaumu Ali katika matukio mbalimbali, kwani pale alipotaka kumuoa binti wa Abu Jahli, Fatima alipeleka mashitaka kwa baba yake…’’’99 98 99

Akhtau ibn Taymiya uk. 6. Minhaju Sunna Juz. 4, uk. 241-242. 65

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 65

11/25/2014 3:00:37 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Mimi ninasema: Natija ya maneno yake ni kwamba, amemuweka Ali pamoja na Makhalifa wawili katika mizani moja katika utambuzi wa sheria za Kiisalmu. Inatosha kuwa maneno yake haya si sahihi kwa kule Umar kurejea kwa Ali katika matukio mengi, na kauli ya Umar imepata umashuhuri pale aliposema: “Lau kama si Ali, basi Umar angeangamia.”100 Na pia akikimbilia kwa Ali na kusema: “Mwenyezi Mungu asinibakishe (hai) baada ya Ibn Abi Talib (kufariki).”101 Inakuwaje Ibn Taymiya aseme maneno haya, wakati Umar alikuwa akisema mwenyewe: “Ali ndiye kadhi wetu.”102 Na katika kiburi chake amethubutu kumsingizia kipenzi cha Mwenyezi Mungu ya kwamba Mtume (s.a.w.w.) amemlaumu katika matukio mbalimbali. Ama madai yake ya kwamba alitaka kumuoa binti wa Abu Jahli, ni kwamba dai hilo tumeshalijibu katika maudhui yaliyotangulia, na huko tumethibitisha ya kwamba kisa hicho ni cha uongo kilichobuniwa na mahasimu wa Imam Ali (a.s.), kwa lengo la kumshusha hadhi yake na nafasi yake kwa Mtume (s.a.w.w.), na kuacha kuwaangalia wale walioghadhibikiwa na Fatmah na kuwasusa na kutosema nao mpaka akafariki akiwa katika hali hiyo. 2. Ibn Taymiya amesema: “Kauli ya Mtume s.a.w.w: ‘Nitampa bendera mtu anayempenda Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na yeye anapendwa na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake.’ Na kauli yake: ‘Kwa hakika ni ahadi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu kwangu mimi, ya kwamba hanipendi isipokuwa Muumini, na wala hanichukii isipokuwa mnafiki.’ l-Istiab Juz. 3, uk.1103. Ar-Riyadhun-Nadhra uk. 3, uk. 142. Manaqibu alA Khawarazmiy uk. 180. Al-Arbain lir-Razi, uk. 466. 101 Ar-Riyadhun-Nadhra uk. 3, uk.145. Tadhkiratul- Khawaswi, uk. 148. 102 Al-Istiab, Juz. 3, uk.1102. 100

66

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 66

11/25/2014 3:00:37 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Na kauli yake: ‘Je, huridhiki kuwa na daraja kwangu kama Harun alivyokuwa kwa Musa, isipokuwa hakuna Nabii baada yangu.’ Mambo haya si katika mambo yanayomhusu Ali peke yake, lakini ni miongoni mwa fadhila zake na sifa zake ambazo kwazo hujulikana ubora wake, na riwaya za aina hii zimekuwa mashuhuri kwa Ahlu Sunna, ili wazitumie katika kumtetea Ali kutokana na wale wenye kumdogesha, na kumuona kuwa ni kafiri miongoni mwa Makhawariji.’’103 Ninasema: Haina shaka kwamba mtu huyu ana lengo la kukataa mambo bora aliyonayo Imam Ali (a.s.) na kuyabadili kuwa ni katika fadhila zake, kisha kuonesha dharau kwa madai kwamba fadhila hizo wamezitaja ili kuwajibu Makhawariji ambao walikuwa wakimkufurisha Imam Ali (a.s.). Ni vipi yasiwe ni katika mambo yanayomhusu yeye tu, na wakati Mtume (s.a.w.w.) alimwambia pale alipokuwa akielekea katika vita vya Tabuki: “Je, huridhiki kuwa na daraja kwangu kama Haruna alivyokuwa kwa Musa, isipokuwa hakuna Nabii baada yangu.’’ Huku Mtume (s.a.w.w.) kutumia ibara isemayo: “Isipokuwa hakuna Nabii baada yangu,’’ ni dalili ya wazi kwamba madaraka yote ya kidini aliyonayo, pia yanathibiti kwa Imam Ali (a.s.) isipokuwa Unabii. Je, Mtume (s.a.w.w.) amemwambia Swahaba mwingine maneno haya zaidi ya Imam Ali (a.s.)? Na je, kuna yeyote aliyepambika na sifa hii asiye kuwa yeye Imam Ali (a.s.)? Na je, Mtume (s.a.w.w.) alimwambia Swahaba mwingine: “Hakupendi isipokuwa Muumini, na hakuchukii isipokuwa Mnafiki?” Bila ya shaka, maneno haya yaliyotoka katika kinywa kitakatifu cha Mtume (s.a.w.w.), ni dalili ya wazi juu ya heshima na nafasi ya juu aliyonayo Imam Ali (a.s.) 103

Minhaju Sunna Juz. 4, uk. 241-371. 67

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 67

11/25/2014 3:00:37 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Na mwanachuoni mkubwa wa hadithi anayeitwa Ibn Hajar katika kitabu chake ‘al-Iswaba’ ametaja kwa kina juu ya mambo yanayomhusu Imam Ali (a.s.) miongoni mwa fadhila, kwa hivyo ni vyema kwa mtafiti arejee kwenye kitabu hicho, ili aelewe yale aliyonayo Imam Ali katika sifa na fadhila ambazo hashiriakiani na mtu yoyote mwingine.104 3. Na amesema: “Inajulikana kwamba Waislamu wamekubaliana juu ya ukhalifa wa Makhalifa watatu, katika zama zao, upanga ulikuwa ukitumika dhidi ya makafiri, ukizuiliwa kutumiwa kwa Waislamu, ama Ali, Waislamu hawakukubaliana juu ya ukhalifa wake, bali katika ukhalifa wake kulitokea fitina (vita), na upanga ulitumika dhidi ya Waislamu na kutotumika kwa Makafiri.’’105 Ninasema: Kwanza: Upanga haukuwa ni wenye kuzuiliwa dhidi ya makafiri katika zama za ukhalifa wa Imam Ali (a.s.), bali ulikuwa ukitumika dhidi yao kwa lengo la kuimarisha Uislamu, kama ambavyo wanahistoria walivyoeleza, kwani maeneo mengi yaliingizwa katika dola ya Kiislamu. Ibn Athir amesema: “Katika mwaka 39A.H. Harith ibn Murra alielekea al-Abdiy alielekea kwenye mji wa Sandi kwa ajili ya mapambano kwa amri ya Amirul-Muuminina Ali (a.s.), akapata ngawira na watumwa wengi, na aliweza kugawa ndani ya siku moja vichwa elfu moja. Harith alibakia akiwa anapigana mpaka akauwawa katika ardhi ya al-Qayqani pamoja na askari wengi waliokuwa pamoja naye isipokuwa wachache ndio waliobakia mnamo mwaka 42A.H. wakati wa zama za Muawiya.’’106 Al-Iswabah Juz. 4, uk. 564-569. Minhaju Sunna Juz. 4, uk. 241-161. 106 Al-kamil fii Tarikh Juz. 3, uk. 381. 104 105

68

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 68

11/25/2014 3:00:37 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Pili: Tofauti zilizokuwepo pamoja na mapambano yaliyotokea wakati wa ukhalifa wa Imam Ali (a.s.), ilikuwa ni matokeo ya siasa za Makhalifa waliopita, hasa khalifa wa tatu (Uthman), ambaye alifuata siasa ya ukabila na matabaka badala ya uadilifu na vipimo vya Kiislamu, siasa ya Imam Ali (a.s.) ilikuwa ni kujaribu kuurudisha ummah wa Kiislamu katika usawa na uadilifu, na kufuata mwenendo wa Mtume (s.a.w.w.), lakini wale waliokuwa wakiipenda dunia walifanya uasi na kutayarisha jeshi kwa mali ambazo walizipora kutoka katika hazina kuu ya Waislamu kwa lengo la kumpiga vita Imam Ali (a.s.), naye (Imam Ali (a.s.)) alikabiliana nao kwa kuitikia wito wa Qur’ani na amri ya Mtume (s.a.w.w.), kama Abu Ayub al-Answariy alivyosema: “Mtume (s.a.w.w.) alimuamrisha Ali (a.s.) kupigana dhidi ya watakaovunja viapo vyao vya utiifu, waasi na waovu.’’107 Na Abu Said al-Khudriy amesema: “Mtume s.a.w.w ametuamrisha tupigane dhidi ya wenye kuvunja viapo vyao vya utiifu, waasi na waovu. Tukasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Umetuamrisha tupigane na watu hawa, ni pamoja na nani tupigane? Akasema: Pamoja na Ali ibn Abi Talib.”108 Kwa mujibu wa riwaya hizi, ni kwamba Imam Ali (a.s.) ametekeleza yale aliyoamrishwa na Mtume (s.a.w.w.), lakini Ibn Taymiya hajali kabisa maneno ya Mtume (s.a.w.w.) yanayohusiana na Imam Ali (a.s.), wala bishara zake ambazo zinaonesha ni namma gani anavyojishughulisha juu ya ummah wake, na mapenzi yake ya kutaka kufuata njia ya uongofu, na kuwa mbali na njia ya upotofu, kwa hivyo anawaelekeza kwenye njia salama, na kuwaongoza dalili 107 108

Al-Mustadrak Juz. 3, uk. 139. Tarikh ibn Kathir Juz. 7, uk. 305. 69

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 69

11/25/2014 3:00:37 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

zilizo wazi, kama alivyowaambia Maswahaba zake: “Hakika miongoni mwenu yumo atakayepigana juu ya ufafanuzi wa Qur’ani, kama mimi nilivyopigana juu ya kuteremka kwake.’’ Abu Said al-Khudriy akasema: “Watu walijitukuza kwa hilo (kila mmoja alihisi kwamba ni yeye), miongoni mwao alikuwemo Abu Bakr na Umar, Abu Bakr alisema: ‘Mtu huyo ni mimi’ Mtume (s.a.w.w.) akasema: ‘Hapana, sio wewe.’ Umar akasema: ‘Mtu huyo ni mimi’ Mtume (s.a.w.w.) akasema: ‘Hapana, sio wewe, lakini ni mshonaji viatu’, wakati huo Imam Ali (a.s.) alikuwa akishona viatu vya Mtume (s.a.w.w.), basi tulimuendea na kumbashiria kheri, wala hakunyanyua kichwa chake, kama kwamba tayari alikwishayasikia maneno hayo kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.)’’109 Kwa hivyo mapambano juu ya ufafanuzi wa Qur’ani ni katika mambo ya furaha, ndio sababu iliyompelekea Abu Bakr na Umar walipende jambo hilo, lakini utabiri huo haukusimama isipokuwa kwa mtu ambaye ni mwenza wa Qur’ani na shujaa wa Uislamu, ambaye katika muda wake wote alikuwa pamoja na Mtume (s.a.w.w.) katika mapambano juu ya uteremsho wa Qur’ani. Tunauliza: Je, hayo maneno ya Ibn Taymiya ya kumuaibisha mbebaji wa bendera ya utetezi wa Qur’ani, na kuihifadhi dhidi ya wafasiri waovu, hayazingatiwi kwamba ni katika kumbughudhi Mtume (s.a.w.w.), na kuitia doa furaha yake ya kubakia salama Qur’ani, ambayo imekuja kutengeneza kila kitu katika maisha ya mwanadamu, ikiwa imesalimika na uchafuzi baada ya kufariki kwake? Kisha upanga zama za Makhalifa watatu haukuwa ni we109

Al-Mustadrak Alaa Swahiyhayni Juz. 7, uk. 305. 70

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 70

11/25/2014 3:00:37 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

nye kutenganishwa na Waislamu, licha ya kuwa historia ya Kiislamu imeandikwa na wao, imeelezea kwa wingi namna Abu Bakr alivyopambana dhidi ya wenye kuritadi, lakini katika kurasa za vitabu hivyo utakuta kwamba kuna watu kati ya hao hawakuritadi, na wengine walikataa kutoa Zaka kutokana na sababu mbalimbali, na wala hawakupinga wajibu huo, na ushahidi wa hayo ni kauli ya Khafshish, ambaye alipinga utawala wa Abu Bakr, amesema: “Tulikuwa tukimtii Mjumbe wa Mwenyezi Mungu alipokuwa pamoja nasi, enyi waja wa Mwenyezi Mungu! Abu Bakr ana nini, je, Abu Bakr anatutawala baada ya yeye Mtume (s.a.w.w.) kufariki? Naapa kwa utukufu wa nyumba ya Mwenyezi Mungu, huko ni kuvunjika mgongo.’’110 Na pia dalili nyingine ni kisa cha Malik ibn Nuwayra, ambapo Khalid ibn Walid aliwauwa watu ambao wamethibitishwa Uislamu wao na Abu Qutada al-Harith ibn Rabiy alAnswariy, na alitoa ahadi ya kutoshiriki tena vita pamoja na Khalid ibn Walid baada ya vita hivyo. Abu Qutada amesimulia kwa kusema: “Baada ya giza kuingia, watu walichukua silaha, tukasema: ‘Sisi ni Waislamu.’ Na wao wakasema: ‘Na sisi ni Waislamu.’ Wakatuambia: ‘Basi hizo silaha ni za nini.’ Tukasema: ‘Ikiwa nyinyi ni kama mnavyosema, basi wekeni silaha zenu chini.’ Kisha tuliswali na wao wakaswali, Khalid alikuwa akitoa sababu za kumuua, kwa madai kwamba alisema: ‘Swahiba wenu hakuacha, isipokuwa alikuwa akisema kadha wa kadha.’ Akasema: ‘Je, wewe humhesabu kwamba ni swahiba wako?’ Kisha Khalid akamsogelea na kumkata shingo yake na shingo za wafuasi wake!!! 110

arikhul- Madinatul-Munawwara Libn Shubba uk. 547-548. Tarikh Tabarriy Juz. T 2, uk. 477. 71

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 71

11/25/2014 3:00:37 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Baada ya Umar ibn Khattab kupata habari za kuuwawa kwao, alizungumza maneno makali mbele ya Abu Bakr, akasema: ‘Ni adui wa Mwenyezi Mungu (Khalid), amemfanyia uadui mtu Mwislamu na kumuua, kisha akalala na mke wake…!’”111 Kisha ni kwamba Ali (a.s.) hakuingia vitani isipokuwa baada ya kutimiza hoja na kuwaelimisha jamaa lile lililo wajibu kwao, lakini baada ya kiburi chao na ujeuri wao hakuwa na budi isipokuwa kuwapiga vita mafisadi, wabadhirifu, na wenye uchu na madaraka wasiyostahiki. Hivyo mizozo na magomvi si kwa sababu ya serikali ya Ali (a.s.) bali ilikuwa ni matokeo ya malezi yasiyo ya Kiislamu ya tawala zilizomtangulia za wale walioikataa serikali ya uadilifu ya Mwenyezi Mungu na wakajituma katika kukidhi matamanio yao ya kidunia, ambapo Ali (a.s.) alisimama kidete kuwazuia kutimiza matakwa yao ya kishetani, jambo ambalo liliwapelekea wao kumfanyia hila na hatimaye kumpiga vita.

111

Tarikh Tabariy Juz. 2, uk. 503-504. 72

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 72

11/25/2014 3:00:37 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

IBN TAYMIYA APINGA KUWA KUMUUDHI IMAM ALI (A.S.) NI ALAMA YA KUWATAMBUA WANAFIKI

K

una riwaya mbalimbali zinazoelezea kwamba baadhi ya Maswahaba walikuwa wakiwajua wanafiki kwa kule kumuudhi kwao Imam Ali (a.s.), na hili ni katika fadhila zake, lakini Ibn Taymiya amelipinga hili pale aliposema: “Na mwenye kudhani kwamba amesikia kutoka kwa baadhi ya Maanswari jambo ambalo humpelekea kukasirika na hatimaye akakasirika, basi kwa kufanya hivyo atakuwa mpotofu mwenye kukosea, na wala hatokuwa mnafiki kwa jambo hilo. Na pia mwenye kuitakidi kwa Maswahaba baadhi ya mambo wasiokuwa nayo, kama vile kudhani kwamba ni makafiri au waovu, wakakasirika kwa hilo, basi atakuwa ni jahili mwenye kujidhulumu, na wala hawi mnafiki. Na hili linabainisha uongo uliopokewa kutoka kwa baadhi ya Maswahaba, kama vile Jabir, ya kwamba amesema: Katika zama za Mtume (s.a.w.w.) tulikuwa hatumjui mnafiki, isipokuwa kwa chuki zao dhidi ya Ali ibn Abi Talib. Kwa hakika huku kujulikana wanafiki kwa kumuudhi na kumchukia Ali ni uongo ulio wazi, uongo ambao unajulikana na watu wa kawaida, itakuwaje jambo hili lifichikane kwa mtu kama Jabir na mfano wake, kisha katika Suratu Tawba zimetajwa alama za mnafiki, na hakuna humo miongoni mwazo kumuudhi Ali.�112 Ibn Taymiya amejaribu kufanya kila awezalo, katika kupinga utukufu huu wa Imam Ali (a.s.) utukufu ambao unamhusu yeye tu, pasi na Maswahaba wengine, kwa hakika 112

Minhaju Sunna Juz. 7, uk.149. 73

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 73

11/25/2014 3:00:37 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

amedhihirisha chuki zake za kibanu Umayya dhidi ya Imam Ali (a.s.) kwa kutumia njia mbalimbali za upotofu ili kufikia lengo lake, jambo ambalo limemfanya kujipinga mwenyewe, lakini chuki imemfanya asilione hilo. Kwa kweli maneno ya Jabir, ya kwamba walikuwa wakiwajua wanafiki kwa kumuudhi Ali, ni maneno yanayonasibiana kabisa na maneno ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kumwambia Imam Ali (a.s.) kwa kusema: “Kwa hakika, hakupendi isipokuwa Muumini na hakuchukii isipokuwa mnafiki.’’113 Basi ni kwa nini Ibn Taymiya anatumia lugha hii nzito katika kupinga maneno ya Jabir, bali kuipinga hadithi tukufu ya Mtume (s.a.w.w.) Na jambo la kushangaza kwa Ibn Taymiya ni pale aliposema: “Qur’ani imetaja alama za wanafiki, na katika hizo hakuna kumbughudhi Ali.” Kisha yeye mwenyewe ananukuu kutoka kwa Bukhari na Muslim ya kwamba Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Alama za mnafiki ni tatu: Azungumzapo husema uongo, na anapoahidi hukhalifu, na anapoaminiwa hufanya khiyana.’’114 Alama hizi hazikutajwa katika Qur’ani Tukufu! Na pia amenukuu kutoka kwa Bukhari na Muslimu kwamba Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Alama ya imani ni kuwapenda Maanswari na alama ya unafiki ni kuwachukia Maanswari.’’115 Alama hizi pia nazo hazikutajwa katika Qur’ani Tukufu, na sababu iko wazi, nayo ni kwamba Aya zilizotaja alama za wanafiki hazikusema kwamba ni hizo tu, na hilo Ibn Taymiya analielewa, lakini chuki yake dhidi ya Imam Ali (a.s.) ndiyo iliyompelekea kuja na kauli hizi chungu. usnad Ahmad Juz. 1, uk.138. Sunan Tirmidhiy Juz. 5, uk. 343. Sahihi MusM lim Juz. 1, uk. 86. 114 Minhaju Sunna Juz. 7, uk.148. 115 Minhaju Sunna Juz. 7, uk.147. 113

74

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 74

11/25/2014 3:00:37 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Kisha ibn Taymiya ameyatafsiri maneno ya Jabir kwa mujibu wa rai yake, amesema: “Na makusudio yake hapa, ni kwamba haiwezekani kusemwa: Hakuna alama ya unafiki isipokuwa kumchukia Ali, na hakuna yeyote kati ya Maswahaba anayesema hivi.’’116 Tunamuuliza Ibn Taymiya: Ni nani aliyekwambia ya kwamba hivi ulivyoyatafsiri maneno ya Jabir, ndivyo ilivyokusudiwa?! Na baada ya kushindwa hoja, alirudia kwa kusema: “Lakini ambalo linaweza kusemwa, ni kwamba kumchukia Ali ni miongoni mwa alama za unafiki, kama ilivyo katika hadithi marfui: “Hanichukii isipokuwa mnafiki.” Hivi ndivyo ambavyo hadithi inaweza kufahamika, kwani mwenye kutambua namna Ali alivyomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na namna alivyopigana jihadi katika njia Yake, kisha akamchukia kwa hayo, basi huyo ni mnafiki.”117 Basi baada ya maneno yake haya, ni kipi kilichomfanya aingie katika mjadala huu na mzozo wenye kuchosha, na kwenda huku na kule kwa lengo la kujibu maneno ya Jabir?! Na sijui ni kipi kinachomfanya Ibn Taymiya aone kwamba kuwachukia Maanswari ndiko kunakomfanya kuwa mnafiki zaidi,118 kuliko kumchukia Ali, licha ya kwamba jambo hili linamhusu Ali peke yake, ambapo kwa Maanswari (ikiwa riwaya ni sahihi) ni mpaka pale watakapokuwa kundi (kuwachukia Maanswari wote), kwa kweli kuna tofauti kubwa kati ya kumchukia Ali akiwa mtu mmoja, na kule kulichukia kundi kubwa la Maanswari, hii inamaanisha ya kwamba, mwenye kuwachukia baadhi ya Maanswari haingii katika unafiki, Minhaju Sunna Juz. 7, uk.152. Kitabu kilichotangulia. 118 Kitabu kilichotangulia. 116 117

75

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 75

11/25/2014 3:00:37 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

katika wakati ambao kumchukia Ali peke yake kunamfanya mtu kuwa mnafiki, basi ni unafiki upi ulio dhahiri zaidi? Na la ajabu zaidi, ni kauli ya ibn Taymiya ya kwamba: Unafiki hupatikana na kudhihiri zaidi katika kumchukia Umar kuliko kumchukia Ali.’’119 Basi atuletee hadithi ya Mtume (s.a.w.w.) inayothibitisha madai yake hayo, ikiwa atashindwa, aelewe kwamba kuzungumza maneno yasiyo na dalili ni jambo ambalo wajinga hawashindwi kufanya hivyo. Isipokuwa Ibn Taymiya anadai kwamba yeye ni mtambuzi zaidi wa kumtambua Mtume (s.a.w.w.) kuliko Umar, na kauli yake (ibn Taymiya) ndiyo ya haki, na wala kauli ya Mtume (s.a.w.w.) haiwezi kuwa juu ya kauli yake!!! Baada ya hapo hatutokuwa na kauli pamoja naye, kwani inategemewa mtu mfano wa Ibn Taymiya kudai kwamba mtu huwa mnafiki zaidi katika kumchukia Yazid kuliko kumchukia Ali. Kwa kumalizia, ni kwamba waliosema kwamba unafiki hujulikana kwa kumchukia Imam Ali (a.s.) sio Jabir ibn Abdillah al-Answariy peke yake, bali kuna wengine, kama ambavyo Sheikh wetu alivyobainisha hayo katika kitabu chake kijulikanacho kwa jina la ‘Ghadir,’ miongoni mwao ni: 1. Abu Dharr al-Ghaffar, yeye amesema: “Tulikuwa hatuwajui wanafiki katika zama za Mtume (s.a.w.w.) isipokuwa kwa mambo matatu: Kwa kumpinga Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na kupuuza Swala, na kumchukia Ali ibn Abi Talib.” 2. Abu Said al-Khudriy, amesema: “Sisi Maanswari tulikuwa tukiwajua wanafiki kwa kumchukia Ali.” 119

Minhaju Sunna Juz. 7, uk.153. 76

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 76

11/25/2014 3:00:37 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

3. Abu Said Muhammad ibn Haytham, amesema: “Sisi Maanswari tulikuwa hatuwajui wanafiki isipokuwa kwa kumchukia Ali ibn Abi Talib.” 4. Abu Dardai, amesema: “Sisi Maanswari tulikuwa hatuwajui wanafiki isipokuwa kwa kumchukia Ali ibn Abi Talib.”

77

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 77

11/25/2014 3:00:37 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

UPANGA WA ALI (A.S.) HAUKUWA NA FAIDA

I

bn Taymiya amepinga nafasi kubwa na ya kipekee aliyokuwa nayo Imam Ali (a.s.) katika vita walivyopigana Waislamu pamoja na Mtume (s.a.w.w.), amesema: “Upanga wake ulikuwa ni sehemu ya panga nyingi…, na sehemu nyingi ambazo Uislamu ulishinda, upanga wake haukuwa na nafasi kubwa ya ushindi, kama vile katika vita vya Badr, huko upanga wake ulikuwa ni mmoja kati ya panga nyingi.’’120 Ninasema: tunapingana na kauli ya Ibn Taymiya kwa kuorodhesha majina ya washirikina waliouwawa kwa upanga wa Imam Ali (a.s.), kama ilivyo katika kitabu kijulikanacho kwa ‘As-Siratun-Nabawiyya’ cha Ibn Hisham: 1. Al-Aswi ibn Said ibn al-Aswi ibn Umayya. 2. Al-Walid ibn Utba ibn Rabiya. 3. Amir ibn Abdillah. 4. Twaima ibn Adiyy ibn Nawfal. 5. Nawfal ibn Khuwaylid ibn Asad. 6. Nadhru ibn Harith ibn Kalda. 7. Umeir ibn Uthman ibn Amru. 8. Harmala ibn Amru. 9. Abu Qaysi ibn al-Fakiha ibn Mughira. 120

Minhaju Sunna Juz. 7, uk. 98-90. 78

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 78

11/25/2014 3:00:37 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

10. Hajiz ibn Saib. 11. Muariya ibn Amir. 12. Ausi ibn Mi’yar. 13. Masud ibn Abi Umayya ibn Mughira. 14. Abdullah ibn Mundhir ibn Abi Rifaa. 15. Al-Aswi ibn Munabbih ibn Hajjaj. 16. Abul- Aswi ibn Qaysi ibn Adiyy. 17. Aqabatu ibn Abi Muitwi. Na ambao Ali (a.s.) ameshiriki katika kuuwawa kwao ni hawa wafuatao: 1. Hadhala ibn Abi Sufiyani, inasemekana kwamba: Watu watatu walishiriki katika kumuua, watu hao ni yeye Imam Ali, Hamza na Zayd ibn Haritha. 2. Utba ibn Rabiya ibn Abdi Shamsi, alishiriki yeye na Ubayda ibn Harith na Hamza. 3. Zama’at ibn As-wad ibn Muttalib, alishirikiana pamoja na Hamza na Thabit. 4. Aqil ibn As-wad ibn Muttalib, ameshirikiana pamoja na Hamza. 121 Hebu msikilize Imam Ali (a.s) wakati akimwambia Muawiya katika barua aliyomuandikia: “Kumbuka kwamba bado ninao upanga ambao niliwang’ata nao babu yako, mjomba wako na kaka yako mahali pamoja.” 121

As-Siyratun Nabawiya L ‘ibn Hisham Juz. 2, uk. 365-372. 79

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 79

11/25/2014 3:00:37 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Na alimhutubia katika barua nyingine: “Basi elewa kwamba, mimi ni Abul Hasan, muuaji wa babu yako na kaka yako na mjomba wako, kwa kuwakatakata, siku ya vita vya Badr.”122 Na Muslimu amepokea katika Sahih yake kwa sanadi yake kutoka kwa Qays ibn Ubadi, amesema: “Nilimsikia Abu Dharr akiapa kiapo kwamba, aya hii: “Hawa mahasimu wawili waliohasimiana kwa ajili ya Mola wao,” (Qur’an, 22:19), imeteremka kwa wale waliopambana siku ya vita vya Badr, nao ni Hamza, Ali, Ubayd ibn Harith, Utba na Shiyba watoto wa Rabiya, na Walid ibn Utba.’’123 Ama mafanikio ya Imam Ali (a.s.) katika vita vya Uhud ni jambo lililo mashuhuri sana, kiasi cha kuwafanya wanahistoria kunakili katika vitabu vyao vya historia, miongoni mwao ni Tabariy, amepokea kwa kusema: “Abu Kurayb ametusimulia, akasema: Ametusimulia Uthman ibn Said, amesema: Ametusimulia Habban ibn Ali kutoka kwa Muhammad ibn Ubaydullah ibn Abi Rafi’i, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake, amesema: Baada ya Ali ibn Abi Talib kuwauwa watu wa al-Alawiyat, Mtume (s.a.w.w.) aliona kundi la washirikina, basi alimwambia Ali: Pambana nao, basi alipambana nao na kuwatawanya, na kumuua Amru ibn Abdillah al-Juhmiy, kisha akaona kundi jingine, basi akamwambia Ali: Pambana nao, akapambana nao na kuwatawanya, na kufanikiwa kumua Shiyba ibn Malik, basi Jibril akasema: ‘Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Hakika jambo hili ni lenye kutia furaha,’ basi Mtume (s.a.w.w.) akasema: ‘Hakika yeye anatokana na mimi, na mimi ninatokana na yeye.’ Na Jibrili akasema: ‘Na mimi 122 123

Nahajul Balagh, Barua Na. 64 na 10. Sahihi Muslim Juz. 8, uk. 245. Tarikh Tabariy, Juz. 2, uk.198. 80

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 80

11/25/2014 3:00:37 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

natokana na nyinyi wawili.’ Anasema: Wakasikia sauti: ‘Hakuna upanga isipokuwa Dhul Fiqar, na hakuna kijana isipokuwa Ali.’’’124 Na ibn Abil Hadid amesema: “Idadi kamili ya washirikina waliouawa siku ya vita vya Uhud ni ishirini na nane, na Ali aliwauwa miongoni mwao kumi na mbili, na idadi hii ya waliouawa siku ya vita vya Uhud ni sawa na idadi ya washirikina aliowauwa siku ya vita vya Badr, ambao wanakaribia nusu yao.125 Na katika vita vya Ahzab (Handaki), je, Ibn Taymiya hajasikia kauli ya Mtume (s.a.w.w.) aliyoisema baada ya Ali kupambana na Amru ibn Abd Wuddi na kufanikiwa kumuua: “Imani yote imepambana na ushirikina wote.’’126 Fakhru Raziy amesema: Hakika Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Pigo la Ali siku ya vita vya Handaki, ni bora zaidi kuliko ibada za watu na majini.’’127 Na kutoka kwa Hakim: “Ni kwamba Yahya ibn Adam amesema: Sikuwa na shaka juu ya Ali kumuua Amr ila kwa kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo: “Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu waliwatimua, na Daudi akamuuwa Jaluti.” (Qur’an, 2:251).128 Je, Ibn Taymiya hajaisoma historia ya Kiislamu, na hajawahi kusikia vita vya Khaybari, na hajawahi kuyasoma yale yaliyomo katika Musnad Ahmad kwa njia nyingi, na SaTarikh Tabariy Juz. 2, uk.197. Sharhu Nahjul Balagh Juz.15, uk.54. 126 Kitabu kilichotangulia. 127 Nihayatul Fuswul fi Dirayatil Uswul uk.113. Tarikh Dimish-qi Juz. 1, uk. 55. Addurrul Mathur Juz. 5, uk.192. 128 Al-Mustadrak alaa Swahiyhayn Juz. 3, uk. 24. 124 125

81

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 81

11/25/2014 3:00:37 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

hihi Muslim na Sahihi Bukhari kwa njia mbalimbali, na kwa ujumla katika Sahih zote sita kutoka kwa Abdullah ibn Buraid aliposema: “Nilimsikia baba yangu akisema: Tuliizunguka Khaybar, na Abu Bakr akabeba bendera, akaondoka, lakini hakupata ushindi, kisha siku ya pili Umar akaibeba bendera, akarejea bila ya ushindi, na siku hiyo watu walisibiwa na matatizo, basi Mtume (s.a.w.w.) akasema: ‘Nitampa bendera hii mtu anayempenda Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na anayependwa na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, Mwenyezi Mungu ataleta ushindi kwa kupitia yeye.’ Watu wakalala wakijadiliana kati yao, ni nani atakayepewa hiyo bendera, baada ya kupambazuka, wote walikwenda kwa Mtume (s.a.w.w.) huku kila mmoja akitarajia kupewa, Mtume (s.a.w.w.) akasema: ‘Yuko wapi Ali ibn Abi Talib?’ Akajibiwa: Anaumwa na macho, akapelekwa kwake, alipofika kwake alimtemea mate katika macho yake na akamuombea, basi akapona ugonjwa wake, akampa bendera, Ali akaondoka, na hakurejea ila baada ya Mwenyezi Mungu alipoleta ushindi kupitia kwake. Umar ibn Khattab alisema: ‘Sikupenda uongozi isipokuwa siku hiyo, nilisubiri huku nikitarajia ya kwamba nitapewa bendera hiyo.’ Akasema: Mtume (s.a.w.w.) alimwita Ali ibn Abi Talib na kumpa bendera, na akamwambia: Nenda na wala usigeuke nyuma mpaka Mwenyezi Mungu alete ushindi kupitia kwako. Akasema: Ali alitembea bila ya kugeuka nyuma, akauliza: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Kwa ajili gani nipambane na watu? Akasema: ‘Pambana nao mpaka washuhudie ya kwamba hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na kwamba Muhammad ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, pindi wakifanya hivyo, basi damu yao na 82

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 82

11/25/2014 3:00:37 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

mali yao itakuwa imezuilika isipokuwa kwa haki, na malipo yao yako kwa Mwenyezi Mungu’ basi Mwenyezi Mungu alileta ushindi kwa kupitia kwake.?’’129 Na sasa tumsikilize Ibn Taymiya pamoja na wafuasi wake kuhusu kauli ya ibn Hisham iliyoko katika kitabu chake kijulikanacho kwa jina la ‘Siyratun Nabawiya’ kuhusiana na vita vya Hunayni, amesema: “Ibn Is-haq amesema: Na amenisimulia Aswim ibn Umar ibn Qutada, kutoka kwa Abdur Rahman ibn Jabir, kutoka kwa baba yake; Jabir ibn Abdillah, amesema: Kulikuwa na mtu kutoka Ahwazi akiwa juu ya ngamia wake akiwa na bendera, akifanya aliyokuwa akiyafanya (akiwauwa Waislamu), ikawa Ali ibn Abi Talib r.a. pamoja na mtu miongoni mwa Maanswari wakitaka ­kumuua, akasema: Ali ibn Abi Talib alimuendea nyuma yake, akaipiga miguu ya ngamia wake, akaangukia nyuma yake, na yule Answari akamdhibiti yule mtu, akampiga pigo lililoukata muundi wake, akaanguka kutoka kwenye ­mnyama wake, basi watu wakammaliza (wakamuua), naapa kwa Mwenyezi Mungu! Sikutarajia kwamba watu wangeshindwa mpaka pale nilipowaona mbele ya Mtume (s.a.w.w.) w ­ akiwa ni mateka waliofungwa kamba mikononi 130 mwao.’’ Mtu huyo alikuwa akijulikana kwa jina la Jarul, alikuwa akiwatesa Waislamu, na kutokana na kuuwawa kwake ushindi ulipatikana kwa Waislamu. Huu ndio mchango wa Imam Ali (a.s.) katika vita ambavyo ushindi wake ulisimamisha nguzo za Uislamu, lakini Ibn Taymiya huyafumbia macho, na kukataa kitu ambacho kiko wazi kuliko mwanga wa jua wakati wa mchana usio na S ahih Bukhar Juz. 4, uk.12 na 20. Sahih Muslim Juz. 5, uk.195. Sunan Tirmidhiy Juz. 5, uk. 302. Musnad Ahmad Juz. 2, uk. 384. 130 Siyratun Nabawiya Juz. 3, uk. 445. 129

83

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 83

11/25/2014 3:00:38 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

mawingu, na akaja na fikra ya kipekee kwa kusema: “Ushindi mwingi uliopatikana katika Uislamu, upanga wa Ali haukuwa na mchango!!’’ Na kitu kinachojulisha ya kwamba mtazamo huu alionao ibn Taymiya ni mtazamo wake peke yake, ni kauli ya mwanahadithi na mwanahistoria maarufu anayejulikana kwa jina la Ibn Abdu Barri al-Qurtubiy al-Malikiy, aliyefariki mwaka 463A.H. wakati anapoeleza wasifu wa Imam Ali (a.s.), amesema: “Wamekubaliana ya kwamba yeye Imam Ali (a.s.) ameswali akiwa ni mwenye kuelekea kibla mbili, na alihama Makka, na alishiriki vita vya Badr na Hudaybiya, na vita nyingine, naye alileta ushindi mkubwa katika vita vya Badr, Uhud, Khandak na Khaybar, na kuleta heshima kubwa.’’131 “Kwa hakika Ali – Karrama llahu wajhahu – alikuwa ni shujaa wa mwanzo wa Kiislamu, na ushujaa wake katika vita si sawa na watu kumi, bali makumi kwa makumi. Na kurasa ambazo zimesajili vita vya Mtume (s.a.w.w.), zinathibitisha ya kwamba Ali ibn Abi Talib alikuwa askari mkakamavu katika vita vyote kati ya Waislamu na washirikina. Na ukweli huu umethibitishwa na habari zilizoenea, katika tenzi na mashairi, kama ambavyo ni jambo lililoenea katika ndimi za watu na kupokelewa na kizazi kutoka kizazi kingine. Na ukweli ni kwamba, nafasi ya Ali ibn Abi Talib (a.s.) katika vita vya Jihadi na ushujaa wake, ni jambo lisilofichika nyuma ya moshi wa chuki na mjadala, na kufunikwa na maneno ya mahasimu.’’132

131 132

Al-Istiab Juz. 3, uk. 1096-1097. Ali ibn Abi Talib, Liabdil Karim al-Khatib al-Maswriy uk. 130, 145. 84

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 84

11/25/2014 3:00:38 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

MADAI YAKE KWAMBA WATU WENGI WALIKATAA KUMPA IMAM ALI (A.S.) KIAPO CHA UTIIFU

H

abari nyingi zimeenea ya kwamba Maswahaba wengi pamoja na Matabiina walimpa kiapo cha uaminifu Imam Ali (a.s.), na wachache tu miongoni mwao ndio ambao hawakutoa kiapo chao cha utiifu kwake (hawakuutambua ukhalifa wake). Na sasa sikiliza yale waliyoyasema wanahistoria. Ibn Wadhih al-Anbariy amesema: “Watu walimpa kiapo cha utiifu isipokuwa watu watatu miongoni mwa Makuraish: Marwan ibn Hakam, Said ibn al-Aswi na Walid ibn Uqba…, na watu miongoni mwa Maanswari walisimama na kuzungumza, na wa mwanzo kuzungumza alikuwa ni Qays ibn Shammas alAnswariy ambaye alikuwa ni khatibu wa Maanswari, alisema: ‘Naapa kwa Mwenyezi Mungu! Ewe kiongozi wa Waumini, ikiwa wamekutangulia katika uongozi (Makhalifa watatu waliotangulia), lakini hawakukutangulia katika Dini, na ikiwa walikutangulia jana, basi leo umekutana nao, kwa hakika wao walikuwa, na wewe ukawa si mwenye kufichika katika cheo chako, na nafasi yako ni yenye kutambulika, wanahojiana nawe kwa yale wasiyoyajua, na wewe hukuhojiana na yeyote pamoja na elimu yako.’ Kisha Khuzayma ibn Thabit al-Answariy alisimama, huyu ni yule mwenye shahada mbili, alisema: ‘Ewe kiongozi wa Waumini! Jambo letu hili hatutompa asiyekuwa wewe, na si lenye kuelekezwa isipokuwa kwako, na tunasadikisha katika 85

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 85

11/25/2014 3:00:38 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

nafsi zetu kwako, kwamba wewe ni mtu wa mwanzo kuamini, na mwenye kumtambua Mwenyezi Mungu zaidi, na Muumini bora zaidi kwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wewe unayo yale waliyonayo, na wala wao hawana yale uliyonayo.’ Na Swa’swa’at naye akasimama na kusema: ‘Naapa kwa Mwenyezi Mungu! Ewe kiongozi wa Waumini, kwa hakika umeupamba ukhalifa, na wala haukukupamba wewe ukhalifa, na umeunyanyua daraja na wala haukukunyanyua wewe, na huo ukhalifa una haja zaidi na wewe kuliko wewe kuwa na haja nao.’ Kisha Malik ibn Ashtariy alisimama na kusema: ‘Enyi watu, huyu ni wasii (aliyerithishwa Ukhalifa) miongoni mwa mawasii…ambaye utukufu umekamilika kwake, na wala Waislamu wa mwanzo na wale waliokuja baada yao hawakuwa na shaka juu ya kutangulia kwake katika Uislamu, wala juu ya elimu yake na utukufu wake.’ Kisha alisimama Uqba ibn Amru na kusema: ‘Ni nani ambaye ana siku (utukufu) kama siku ya Aqaba, na mwenye bai’a (kiapo cha utiifu) kama bai’a ya ridh-wani, na kiongozi muongofu zaidi ambaye hatarajiwi ukandamizaji, na mjuzi ambaye hatarajiwi kuonesha ujinga.’133 Na pia Imam Ali (a.s.) alisema kuielezea namna alivyopewa kiapo cha utiifu: “Mliukunjua mkono wangu, nami nikaurudisha, mliunyoosha nikaukunja. Halafu mlisongamana kwangu, msongamano wa ngamia wenye kiu wanapopelekwa kwenye madimbwi yao siku ya kwenda kwao (kunywa maji) hadi ndara zilikatika, na joho lilianguka, na mnyonge alikanyagwa, na furaha ya watu kunipa kwao mimi kiapo cha 133

Tarikh Tabariy Juz. 2, uk. 179. 86

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 86

11/25/2014 3:00:38 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

utiifu ilikuwa bayana kiasi kwamba, watoto waliifurahia, na wakubwa walijikokota kuielekea, mgonjwa alijivuta kuielekea, na nyuso wazi (baadhi ya wasio kuwa na nikabu) zilimiminika kuelekea huko.’’134 Na Ahmad ibn Hanbal amepokea kwa sanadi yake kutoka kwa Muhammad ibn Hanafiyya, amesema: “Nilikuwa pamoja na Ali wakati Uthman alipokuwa amezingirwa, mtu mmoja alimuendea na kusema: ‘Kiongozi wa Waumini (Uthman) ameuwawa.’ Ali alikwenda nyumbani kwake na akaingia ndani na akafunga mlango, mara watu wakamuendea na wakapiga hodi na kisha kuingia, kisha wakamwambia: ‘Mtu huyu (Uthman) amekwishauwawa, na hakuna budi kwa watu isipokuwa wawe na Khalifa, na hatujamuona yeyote anayestahiki zaidi kuliko wewe.’ Ali aliwaambia: ‘Hapana msinichague mimi, kwa kweli mimi kuwa waziri wenu ni bora zaidi kuliko kuwa amiri (Khalifa).’ Walisema: ‘Hapana, kwa jina la Mwenyezi Mungu! Hakuna yeyote anayestahiki zaidi kuliko wewe.’ Akasema: ‘Ikiwa mtanikatalia, basi viapo vyenu vya utiifu kwangu visiwe kwa siri, bali nitatoka niende msikitini, na atakeye kunipa kiapo cha utiifu atanipa.’ Basi alitoka na kwenda msikitini na watu wakampa viapo vyao vya utiifu.’’135 Riwaya hii inajulisha mambo yafuatayo 1. Imam Ali (a.s.) kutokuwa na tamaa ya kutaka uongozi kwa kujiweka nyumbani kwake, mpaka pale Maswahaba walipomuendea wakimtaka awe Khalifa wao. 134 135

Nahjul Balaghah, Khutba Na.229. Fadhailu Swahaba Juz. 2, uk. 573. Tarikh Tabariy Juz. 4, uk. 427. 87

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 87

11/25/2014 3:00:38 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

2. Maanswari na Muhajirina pamoja na watu wote kwa ujumla, ndio waliomuendea Imam Ali (a.s.) na kumtaka akubali kuchukua viapo vyao vya utiifu wa kuwa Khalifa wao, walimsisitiza sana mpaka akakubali. 3. Kwa mujibu wa mitazamo ya Maswahaba ni kwamba zama hizo mtu aliyestahiki zaidi kuwa Khalifa ni Imam Ali (a.s.), hii inatokana na msisitizo wao kwake ili akubali kuchukua viapo vya utiifu kutoka kwao, na pia kutokana na kauli yao kwamba: H ­ awamuoni yeyote anayestahiki zaidi kuwa Khalifa kuliko yeye. 4. Kupatikana makubaliano ya Muhajirina na Maanswari juu ya ukhalifa wa Imam Ali (a.s.), na ni watu wa Sham tu ndio ambao walimkataa, na jambo hili halidhuru baada ya makubaliano ya watu wa Madina.136 Na hiki kilichoelezwa na waandishi hawa wawili ni kwa misingi ya kwamba ukhalifa hupatikana kwa njia ya uchaguzi, na hili ndilo ambalo Imam Ali (a.s.) hakulipenda, kwa hivyo alisema: “Kwa hakika mimi kuwa waziri wenu ni bora kuliko kuwa amiri (Khalifa).” Ama kwa mujibu wa misingi iliyo sahihi, ni kwamba ukhalifa hupatikana kwa uteuzi kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na si juu ya Imam kuukataa, lakini kutokana na watu kulikataa hili, Imam Ali (a.s.) hakupenda kuutwaa ukhalifa kwa mujibu wa matakwa yao. Pamoja na ushahidi huu ulio wazi, na kwa mujibu wa misingi ya watu (kiongozi huchaguliwa), na riwaya ya Ahmad ibn Hanbal ni sahihi na wapokezi wake ni madhubuti, wapokezi 136

ai’atu Ali ibn Abi Talib fii Dhaw’I Riwayat Aswahiiha Liummi Malik al-Khalidiy B wa Hasan Farhaniy al-Malikiy uk. 104-105. 88

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 88

11/25/2014 3:00:38 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

waliopokea katika riwaya za Bukhari na Muslim, je kutakuwa na shaka yoyote juu bai’a ya Muhajirina na Maanswari kwa Imam Ali (a.s.)? Na je, ni haki kwa mtu mwadilifu kuyakubali maneno ya Ibn Taymiya pale aliposema: “Nusu ya watu – au chini ya hao au zaidi ya hao - hawakumba’i (hawakumpa Ali kiapo cha utiifu)?”137 Au pia kuamini yale aliyoyasema mahala pengine, akionesha chuki zake zaidi: “Katika Ukhalifa wake, Dini ya Kiislamu haikudhihiri (haikupata nguvu)!?”138 Na ili uwe na yakini zaidi, ewe ndugu msomaji mpendwa juu ya madai ya uongo wa Ibn Taymiya ya kwamba nusu ya watu au chini yake au zaidi yake hawakumba’i Imam Ali (a.s.), basi hapa tumekuandalia baadhi ya yale yaliyoelezwa na wanachuoni na wanahadithi namna watu walivyomiminika katika kutoa viapo vya utiifu kwa Imam Ali (a.s.) a. I bn Sa’d, ambaye alifariki mwaka 230A.H., yeye amesema: “Wamesema… na Ali r.a. alipewa bai’a huko Madina siku ya pili baada ya kuuwawa Uthman, waliompa bai’a walikuwa ni: Talha, Zubair, Sa’d ibn Abi Waqas, Said ibn Zayd ibn Amru ibn Nufeil, Ammar ibn Yasir, Usama ibn Zayd, Sahl ibn Huneyf, Abu Ayoub al-Answariy, Muhammad ibn Muslima, Zayd ibn Thabit na Khuzayma ibn Thabit, na wale wote waliokuwepo Madina miongoni mwa Maswahaba wa Mtume (s.a.w.w.) na wengineo.’’139 Minhaju Sunna Juz. 4, uk. 105. Kitabu kilichotangulia uk. 117. 139 Tabaqatul Kubra Juz. 3, uk.31. 137 138

89

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 89

11/25/2014 3:00:38 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

b. A bu Hanifa Daynuriy, amefariki mwaka 282A.H. amesema: “Baada ya kuuwawa Uthman, watu walibakia kwa muda wa siku tatu pasi na kuwa na kiongozi, na ambaye alikuwa akiwaswalisha watu alikuwa ni al-Ghafiqiy, kisha watu walimba’i Ali r.a., alisema: Enyi watu! Mmenipa viapo vyenu vya utiifu, kwa misingi ile ile ya wale waliopewa viapo vya utiifu kabla yangu, na kwa hakika maamuzi ni kabla ya kiapo cha utiifu kutimia, ama baada ya kutimia hakuna hiyari, na ni juu ya kiongozi kuwa mwadilifu, na ni juu ya raia kusalimu amri, na bai’a hii ni ya watu wote, basi atakayeivunja atakuwa ameukana Uislamu, na wala bai’a hii haikuwa ni ya kushitukiza (ya ghafla).” Kisha Daynuriy akasema: “Ali ibn Abi Talib alimuandikia Muawiya barua isemayo: Ama baada ya hayo, imekufikia habari juu ya yale yaliyomkuta Uthman, na watu kukusanyika kwangu na kunipa bai’a zao, basi ingia kwa usalama au tangaza vita.” Barua hiyo ilipelekwa na Hajjaj ibn Ghaziyya al-Answariy.140 c. Tabraniy amepokea kwa sanadi yake kutoka kwa Abi Bashir al-Abidiy, amesema: “Nilikuwa Madina wakati alipouwawa Uthman, na Muhajirina na Maanswari walikusanyika, miongoni mwao walikuwemo Talha na Zubair, walimuendea Ali, na wakamwambia: Ewe baba wa Hasan, njoo tukupe mkono wa utiifu. Akasema: Mimi sina haja na jambo lenu, mimi niko pamoja nanyi, yeyote mtakayemchagua nitaridhika naye, basi mchagueni. Walisema: Tunaapa kwa Mwenyezi Mungu! Hatutomchagua asiye kuwa wewe…”141 140 141

Al-Akhbariy Atwuwal uk.140 -141. Tarikh Tabariy Juz. 3, uk. 45. 90

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 90

11/25/2014 3:00:38 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

d. Hakim Nisaburiy amepokea kwa sanadi yake kutoka kwa As-was ibn Yazid Annakha’i, amesema: “Wakati Ali ibn Abi Talib alipopewa bai’a akiwa katika mimbari ya Mtume (s.a.w.w.), Khuzayma ibn Thabit alisema huku akiwa amesimama mbele ya mimbari: ‘Ikiwa sisi tutampa bai’a Ali, basi atatutosheleza kwa ile fitina tunayoichelea, kwani tumemkuta ni mtu aliye bora zaidi kwa watu, yeye ni mjuzi wa Makuraishi katika kukitambua Kitabu (Qur’ani) na Sunna, na ………’” Kisha Hakim amepinga yale yaliyodaiwa na baadhi ya watu kwamba watu walijizuia kutoa viapo vyao vya utiifu kwa Imam Ali (a.s.), na amewaeleza wale wanaodai madai haya kwamba ni watu wasiojua ile hali iliyotokea, ukweli ni kwamba watu hao walikataa kumnusuru katika vita, katika hili kuna habari mbalimbali, kisha Hakim alisema: “Kutokana na sababu hizi na zenye kufanana na hizi, ikawapelekea wengine kujizuia kushiriki vita pamoja na Ali r.a. au kupigana na wale waliompiga vita.”142 Na katika kuthibitisha kwamba baadhi ya Maswahaba walijizuia kushiriki pamoja naye katika vita, na sio kutompa bai’a’, ni kutokana na zile sababu walizomueleza, na kunakiliwa na Abu Hanifa Daynuriy, amesema: “Kisha Ali r.a. aliwataka watu wajiandae kwenda Iraq, mara Sa’ad ibn Abi Waqas, Abdullah ibn Umar ibn Khattab na Muhammad ibn Muslim walimuendea, aliwaambia: ‘Imenifikia habari ya kuchukizwa kwenu juu ya hilo (vita).’ Sa’d alisema: ‘Ni kweli ilikuwa kama ilivyokufikia, ama sasa nipe upanga ili nipigane pamoja nawe, mpaka ajulikane Mwislamu ni nani na kafiri ni nani.’ Na Abdullah ibn Umar alisema: ‘Nakukumbusha Mwenyezi Mungu, kwa kunichukua 142

Al-Mustadrak ala Swahiyhayn Juz. 3, uk. 114-115. 91

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 91

11/25/2014 3:00:38 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

kwenye jambo nisilolijua.’ Na Muhammad ibn Muslim naye akasema: ‘Hakika Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ameniamrisha nipigane kwa upanga wangu kwa ajili ya kile nilichowapigia mushirikina, ikiwa utapigiwa watu wa Swala (Waislamu) nilipige kwayo jabali la Uhudi mpaka utakapovunjika, na nilishauvunja tokea jana.” Kisha aliondoka kutoka kwake. Mwisho, Usama ibn Zayd aliingia na kusema: ‘Nisamehe dhidi ya kutoka pamoja nawe katika mtazamo huu, kwani mimi nimemuahidi Mwenyezi Mungu kwamba, sitopigana dhidi ya mwenye kushuhudia ya kwamba hapana mola anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu.”’143 Na pia kauli ya ibn Abil-Hadid inasisitiza hili, anasema: “Ama wenzetu (Mu’tazila) wanaeleza katika vitabu vyao kwamba, watu hawa walitoa sababu walizozitoa kutokana na kuwataka kuungana naye katika kupambana dhidi ya jeshi la ngamia (jeshi lililo ongozwa na Bibi Aisha), na kwa hakika hawakujizuia na utoaji wa bai’a, walichokifanya ni kujizuia kushiriki vita.” e. Imam Qurtubiy aliyefariki mwaka 671A.H. amesema: “Ukhalifa wake (wa Ali (a.s.)) ulitimu katika msikiti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), ambapo ni mashukio ya Wahyi wake, na makao ya Utume wake, na makao ya Ukhalifa, mbele ya Muhajirina wote na Maanswari, kwa matakwa yao na ridhaa zao…”144 Je Ibn Taymiya hayajui maneno haya na riwaya hizi zinazoeleza matukio? Sisi hatudhani hivyo, lakini ni chuki za kibanu Umayya ndizo zinazomfanya awe na misimamo ya aina hii. 143 144

Al-Akhbaru Twiwalu uk. 142-143. ai’atu Ali ibn Abi Talib fidihaw-i Riwayat Swahiyha uk.122, akiwa amenukuu B kutoka ‘Tadhkitatu lil-qurtubiy uk. 623. 92

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 92

11/25/2014 3:00:38 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Na kwa kumalizia, tunataja mfano mwingine wa wanachuoni waliokuja baada ya Ibn Taymiya kuhusiana na bai’a ya Imam Ali (a.s.) na watu wote kukubaliana juu ya hilo: f. H afidh ibn Hajar al-Asqalaniy aliyefariki mwaka 852A.H. amesema: “Bai’a ya Ali ya Ukhalifa ilikuwa baada ya kuuwawa Uthman, Muhajirina na Maanswari na wale waliohudhuria walimpa kiapo cha utiifu, na akawaandikia watu barua katika maeneo mbalimbali juu ya kutoa viapo vyao vya utiifu, walikubali kufanya hivyo, isipokuwa Muawiya aliyekuwa kiongozi wa watu wa Sham, kutokana na kukataa kwao, baadaye yakatokea yaliyotokea kati yao.”145 Na mwisho wa maudhui haya ni kwamba, mtungaji wa kitabu ‘Bai’atu Ali ibn Abi Talib fii dhaw-i Riwayat Swahiyha’ amefanya utafiti wa riwaya zinazodai kwamba Maswahaba walijizuia kutoa bai’a kwa Imam Ali (a.s.), na kuzijadili sanadi zake, utafiti wake umebaini kwamba riwaya hizo zote ni dhaifu au ni riwaya za uongo, na amenakili riwaya pamoja na maneno ya wanachuoni yanayothibitisha ya kwamba Muhajirina, Maanswari, Maswahaba walioshiriki vita vya Badr na Maswahaba wakubwa, wote kwa pamoja walimpa bai’a Imam Ali (a.s.), na mwisho utafiti wake alikuja na natija hii: “Riwaya zote zinazowatoa Maswahaba wakubwa, kama vile Sa’ad, Ibn Umar, Usama na wengineo, ni riwaya zilizo dhaifu tena ni za kupangwa, ni riwaya zinazopingana na riwaya sahihi, na mpaka sasa hatujapata riwaya sahihi inayothibitisha kukhalifu kutoa bai’a kwa Maswahaba hawa.”146 145 146

Fat-hul Barri Juz. 7, uk. 72. Bai’atu Ali ibn Abi Talib fii d haw- Riwayat Swahiyha Uk. 253-254. 93

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 93

11/25/2014 3:00:38 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

MATOKEO YA UKHALIFA WA IMAM ALI (A.S.)

I

bn Taymiya anasema: “Ali ibn Abi Talib hakumpendelea yeyote miongoni mwa jamaa zake katika mgao, lakini alianza kuwapiga vita wale ambao hawakuanza vita, mpaka wakauliwa miongoni mwao Waislamu elfu kwa maelfu, licha ya kwamba kitendo chake hicho huelezwa kwa maelezo yanayowafikiana na kundi la wanachuoni, walisema: Hawa walikuwa ni waovu, na Mwenyezi Mungu Mtukufu ameamrisha kupambana dhidi ya watu waovu kwa mujibu wa kauli yake: “Basi lipigeni lile linaloonea.” Lakini wanachuoni wengi wamempinga, kama wengi wao walivyompinga Uthman, na wakasema ni kwamba Mwenyezi Mungu amesema:

ْ‫ِين ا ْق َت َتلُوا َفأَصْ لِحُوا َب ْي َن ُھ َما ۖ َفإِن‬ َ ‫ان م َِن ْالم ُْؤ ِمن‬ ِ ‫َوإِنْ َطا ِئ َف َت‬ ْ ‫َب َغ‬ ‫ت إِحْ دَ ا ُھ َما َع َلى ْاأل ُ ْخ َر ٰى َف َقا ِتلُوا الَّتِي َت ْبغِي َح َّت ٰى َتفِي َء‬ ُ ِ‫ت َفأَصْ لِحُوا َب ْي َن ُھ َما ِب ْال َع ْد ِل َوأَ ْقس‬ ْ ‫ﷲ ۚ َفإِنْ َفا َء‬ ‫طوا‬ ِ َّ ‫إِ َل ٰى أَمْ ِر‬ ‫ين‬ َ ِ‫ﷲ ُيحِبُّ ْال ُم ْقسِ ط‬ َ َّ َّ‫ۖ إِن‬ “Na ikiwa makundi mawili katika Waislamu yanapigana, basi fanyeni suluhu baina yao, na ikiwa moja la hayo linamdhulumu mwenziwe, basi lipigeni lile linalolionea mpaka lirudi katika amri ya Mwenyezi Mungu, na kama likirudi, basi yapatanisheni baina yao kwa uadilifu.” (Qur’an, 49:9).

94

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 94

11/25/2014 3:00:38 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Walisema: Mwenyezi Mungu hakuamrisha kuanza kuwapiga watu waovu, bali pindi pakitokea vita kati ya Waislamu, ni kwamba Mwenyezi Mungu ameamrisha kusuluhishwa kati yao, na ikiwa kundi moja litawaonea kundi jingine, basi litastahiki kupigwa, na hali haikutokea kama hivyo.”147 Na akasema tena: “Na hapakutokea vita vyenye manufaa kwa dini wala kwa dunia, na wala hapakuuliwa kafiri katika ukhalifa wake na wala Mwislamu hakufurahi.”148 Ninasema: Yule anayesema: ‘Vita alivyopigana Ali (a.s.) dhidi ya watu wa ngamia (kati yake na jeshi la Bibi Aisha) na vita vya Siffin (dhidi ya Muawiya), havikutokana na amri ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), bali ilikuwa ni kutokana na rai yake,’ ama mtu huyo ni jahili wa hadithi zilizo wazi, ambapo Mtume (s.a.w.w.) alimuamrisha Imam Ali (a.s.) apambane dhidi ya watakaovunja viapo vyao vya utiifu, waasi na waovu. Na kwa ujumla, njia za hadithi hizi zinaonesha kwamba ni sahihi, na kwa kiwango cha chini ni kwamba hadithi hizo ni nzuri.149 Ibn Hajar amefafanua kwa kusema: “Wenye kuvunja viapo vyao vya utiifu ni watu wa jeshi la ngamia (jeshi lilikuwa likiongozwa na Bibi Aisha), na waasi ni watu wa Sham (jeshi la Muawiya), kwa sababu wao walipinga kumpa bai’a Imam Ali, na waovu ni watu wa Nahrawani (Makhawariji), kutokana na kuthibiti hadithi sahihi inayowaeleza: ‘Ni kwamba wao watatoka katika dini kama mshale unavyotoka katika upinde.”’150 Minhaju Sunna Juz. 8, uk. 231-232 Minhaju Sunna Juz. 7, uk. 454. 149 Bai’atu Ali ibn Abi Talib fii dhaw- Riwayat Swahiyha uk. 78. 150 Kitabu kilichopita, ikinakiliwa kutoka ‘Talkhisul- Khabar Juz. 4, uk. 51, cha ibn Hajar. 147 148

95

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 95

11/25/2014 3:00:38 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Bila ya shaka katika kutekeleza amri hii ya Mtume (s.a.w.w.) kuna manufaa makubwa mno ya Kidini, na heshima kwa Uislamu, na Imam Ali (a.s.) ambaye ametekeleza amri hii hana tatizo lolote, ikiwa Ibn Taymiya na wengineo mfano wake hawayajui manufaa hayo. Na ni vipi vita hivyo alivyopigana Imam Ali (a.s.) isiwe ni kutokana na amri ya Mtume (s.a.w.w.), na wakati imesihi kutoka kwake (s.a.w.w.) kwamba alimkataza Aisha kutoka dhidi ya Imam Ali (a.s.), Ahmad ibn Hanbal amepokea katika Musnad yake kwa sanadi yake kutoka kwa Qays ibn Abi Hazim, amesema: “Wakati alipotoka Aisha na kufika mahala penye maji ya Bani Amir wakati wa usiku, mbwa walibweka, Aisha akasema: ‘Haya ni maji gani?’ Wakasema: ‘Ni maji ya Haw-ab’, Aisha akasema: ‘Si mwenye kudhani, isipokuwa mimi ni mwenye kurudi.’ Baadhi ya watu waliokuwa pamoja naye walisema: ‘Bali ni vyema lau kama utakwenda ili Waislamu wakuone, huenda Mwenyezi Mungu akaleta suluhu kati yao.’ Aisha alisema: ‘Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema siku moja: Itakuwaje kwa mmoja wenu (kati ya wakeze Mtume (s.a.w.w.) atakapobwekewa na mbwa wa Haw-ab?’”151 Na katika riwaya ya Bazzar, amesema s.a.w.w: “Ninajua ni nani kati yenu atakayekuwa mpanda ngamia mwenye manyoya mengi, atatoka na atabwekewa na mbwa wa Haw-ab, watauwa watu wengi wa kuliani mwake na kushotoni mwake, kisha ataokoka baada ya kukaribia kuuawa.’’152 151 152

Musnad Ahmad Juz. 6, uk. 97. Haythamiy amesema katika ‘Majmau Zawaidiy Juz. 7, uk. 234.: Imepokewa na Bazzar na wapokezi wake ni wakutegemewa, pia amesema ibn Hajar katika Fat-hul Baariy Juz.13, uk. 55. 96

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 96

11/25/2014 3:00:38 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Na pia katika maudhui haya tunataja yale aliyoyapokea Hakim kutoka kwa Abi Said, amesema: “Tulikuwa tumekaa tukimsubiri Mtume (s.a.w.w.), alitujia akitokea katika moja ya nyumba za wake zake, tulisimama pamoja naye, mara kiatu chake kikakatika, akampa Ali ili akishone, Mtume (s.a.w.w.) akawa anatembea, nasi tukawa tunatembea pamoja naye, kisha akawa anamsubiri Ali, na tulisubiri pamoja naye, kisha akasema: ‘Hakika miongoni mwenu kuna yule ambaye atapambana katika kuieleza hii Qur’ani kama mimi nilivyopambana katika kushuka kwake.’ Tulijitukuza kwa kupata nafasi hiyo, na miongoni mwetu alikuwemo Abu Bakr na Umar, Mtume (s.a.w.w.) akasema: ‘Hapana, lakini (nafasi hiyo ni ya) mshona viatu.’ Tulimuendea Ali kwa ajili ya kumpa hongera, akasema: ‘Kama vile alikuwa amesikia.”’153 Ni kwamba Imam Ali (a.s.) hakuanza kumpiga vita yeyote, bali maadui zake ndio waliyoongoza jeshi dhidi yake, kwa mfano, jeshi la watu waliovunja ahadi zao (jeshi la Bibi Aisha), walikusanya mali nyingi sana kwa ajili ya vita na wakaingia Basra, Gavana wa Imam Ali wa zama hizo alikuwa Uthman ibn Hunayf, Uthman alimzuia Aisha na aliyekuwa pamoja naye kuingia, walisema: Sisi hatukuja kupigana, bali tumekuja kufanya suluhu. Basi wakaandikiana kati yao mkataba wa suluhu kwamba, pasifanyike lolote mpaka atakapowasili Imam Ali (a.s.), na kila kundi litakuwa katika hali ya usalama, kisha kila kundi likatawanyika, na Uthman ibn Hunayf akaweka silaha zake chini, askari wa Aisha walimnyofua ndevu zake na masharubu yake na kope zake na nyusi zake, na walikwenda kwenye nyumba ya hazina ya mali, na wakachukua kila kilichokuwemo humo…154 153 154

Mustadrakul Hakim Juz. 3, uk. 123. Tarikhul Ya’qoubiy Juz. 2, uk. 181, Tarikh Tabariy Juz. 3, uk. 485 na 486 97

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 97

11/25/2014 3:00:38 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Ikiwa hivi ndivyo watu walivyomtendea Gavana wa Imam Ali (a.s.), je, inafaa kwa Imam Ali (a.s.) awaache hivi hivi bila ya kuwachukulia hatua stahiki?! Vipi Imam Ali (a.s.) awaache, na ilhali wametoka Makka wakiwa na jeshi kubwa. Ibn Wadhih al-Akhbariy anasema: “Aisha alitoka akiwa pamoja na Talha na Zubair katika jeshi kubwa sana, na Ya’laa ibn Muniya alikuja kutoka Yemen akiwa na mali ya Yemen, inayokisiwa kufikia dinari laki nne, Talha na Zubair waliichukua mali hiyo na kuitumia katika maandalizi ya vita, na kisha wakaelekea Basra. Na dalili ya wazi kwamba Imam Ali (a.s.) hakuanza vita ni kauli yake kwa Maswahaba wake: “Msiwapige mpaka watakapoanza kuwapiga, kwani kwa baraka za Mwenyezi Mungu nyinyi muna hoja (dalili), na kuwaacha mpaka wakuanzeni kukupiga ni hoja yenu nyingine dhidi yao.” Kisha Imam Ali (a.s.) alichukua msahafu na kusema: “Na mwenye kuuchukua msahafu huu, na kuwalingania, basi malipo yake yatakuwa ni Pepo.” Kijana mmoja aliyekuwa akiitwa Muslim, alisimama na kuishika Qur’ani kwa mkono wake wa kulia na kuanza kuwalingania watu, mara watu wa jeshi la Aisha wakamkata mkono wake wa kulia, kisha akaishika kwa mkono wake wa kushoto, na kuwalingania, pia nao wakaukata, kisha wakampiga mapanga mpaka wakamuuwa.”155 Kisha majeshi ya Aisha yakawa yanawarushia mishale kwa mfululizo askari wa Imam Ali (a.s.), ambapo watu watatu waliuwawa au zaidi ya watatu, askari wake walinyanyua sauti zao na kusema: “Mishale yao imetuchoma, na hawa hapa watu waliouawa wako mbele yako,” baada ya hapo Imam Ali 155

Usudul Ghaba Juz. 3, uk. 308. Al-Aghaniy Juz. 10, uk. 203. 98

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 98

11/25/2014 3:00:38 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

(a.s.) alisema: “Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na hakika sisi tutarejea Kwake. Ewe Mola Wangu shuhudia.’’ Baada ya hapo akavaa nguo za kivita zilizokuwa za Mtume (s.a.w.w.) na akachukua upanga wake maarufu ujulikanao kwa ‘Dhulfiqar’ kisha akampa bendera nyeusi mtoto wake; Muhammad ibn Hanafiyya, na akawaambia Hasan na Husein: “Kwa hakika nimempa bendera mdogo wenu kuwaacha nyinyi kutokana na nafasi yenu kwa Mtume (s.a.w.w.)”156 Sasa ni vipi Ibn Taymiya anadai ya kwamba Imam Ali (a.s.) ndiye aliyeanza vita, na wala hakuleta suluhu kama ambavyo Mwenyezi Mungu aliamrisha?! Ni vipi anadai madai hayo, na wakati wapokezi wameeleza wazi kwamba Imam Ali (a.s.), kwa muda wa siku tatu alipeleka wajumbe wake kwa jeshi la Aisha, kwa lengo la kuwalingania na kuwataka warejee katika utiifu wao na kujiunga pamoja na Waislamu wenzao, lakini watu wale hawakuwa tayari kuitikia wito huo, hapo Imam Ali (a.s.) akalazimika kuwaendea na kupambana nao.157 Ewe Ibn Taymiya! Kwanza soma, kisha toa hukumu.

156 157

Sharhu Nahjul Balagha Juz. 9, uk. 111. Al-Akhbaru Twiwal uk.147. 99

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 99

11/25/2014 3:00:38 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

IBN TAYMIYA NA USHUKAJI WA AYATUL-WILAYAT KWA IMAM ALI (A.S.)

W

apokezi wa hadithi pamoja na wafasiri wa Qur’an wamepokea ya kwamba Ayatul-wilayat ilimteremkia Imam Ali (a.s.), Aya hiyo ni kauli yake Mwenyezi Mungu isemayo:

َّ ‫إِ َّن َما َولِ ُّي ُك ُم‬ ‫ُون الص َ​َّال َة‬ َ ‫ِين ُيقِيم‬ َ ‫ِين آ َم ُنوا الَّذ‬ َ ‫ﷲُ َو َرسُول ُ ُه َوالَّذ‬ َّ ‫ون‬ ‫ون‬ َ ‫الز َكا َة َو ُھ ْم َرا ِك ُع‬ َ ‫َوي ُْؤ ُت‬ “Hakika kiongozi wenu ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale walioamini, ambao husimamisha Swala na kutoa Zaka hali ya kuwa wamerukuu.” (Qur’an, 5:55).

Imepokewa kutoka kwa Anas ibn Malik ya kwamba muombaji alikwenda msikitini akisema: “Ni nani atakaye mkopesha masikini ambaye atarejesha deni?” Na Ali (a.s.) alikuwa amerukuu akizungumza kwa mkono wake wakati muombaji alipokuwa nyuma yake, akimwambia kwa mkono wake, vua pete kutoka mkononi kwangu.”158 Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Ewe Umar, imemstahikia.” Umar akasema: “Naapa kwa haki ya baba yangu na mama yangu, ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni nini kilichomstahikia?” Akasema: “Naapa kwa Mwenyezi Mungu! Imem158

Imam Ali (a.s.) alimuashiria kwamba avue pete iliyokuwa mkononi mwake. 100

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 100

11/25/2014 3:00:39 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

stahikia Pepo, kwani hakuivua kutoka mkononi mwake mpaka pale alipozing’oa dhambi zote na makosa yote.” Akasema: Hakutoka yeyote msikitini isipokuwa tayari Jibril aliteremsha kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo: “Hakika kiongozi wenu ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale walioamini, ambao husimamisha Swala na kutoa Zaka hali ya kuwa wamerukuu.” (Qur’ani; 5:55). Baada ya kuteremka Aya hii Hassan ibn Thabit akasema. “Ewe baba wa Hasan, nafsi yangu na roho yangu inajitoa muhanga kwa ajili yako ….Wewe ndiye ambaye uliyetoa wakati ulipokuwa umerukuu, nafsi za watu zimejitoa muhanga kwako, ewe mbora wa kurukuu, kwa pete yako yenye baraka ewe bwana mbora, na ewe mnunuzi bora na muuzaji bora. Mwenyezi Mungu akateremsha kwako uongozi ulio bora na kuubainisha katika hukumu madhubuti (Qur’ani).” Ikiwa umeshayajua haya, basi sasa na uyasome aliyoyasema Ibn Taymiya, na tuone namna alivyotoa hukumu ya wazi ya kupinga kwamba Aya hii haikuteremka juu ya Imam Ali (a.s.), na tutataja majina ya baadhi ya wafasiri na wanahadithi walionakili sababu ya kuteremka Aya hii juu ya Imam Ali (a.s.) Ibn Taymiya amesema: “Baadhi ya wazushi wameiweka hadithi ya uzushi ya kwamba Aya hii iliteremka kumuhusu Ali wakati alipotoa sadaka pete yake katika Swala, huu ni uongo kwa mujibu wa wanachuoni, na uongo wake ni wa wazi.”159 Kisha Ibn Taymiya alizijibu riwaya zinazoelezea kushuka Aya hii kwa Imam Ali (a.s.), lakini majibu yake ni sawa na kutanguliza matakwa binafsi mbele ya maandiko sahihi. 159

Minhaju Sunna Juz. 2, uk. 30. 101

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 101

11/25/2014 3:00:39 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Kwa sasa ewe msomaji mpendwa, kuwa pamoja nami ili nikuorodheshee baadhi ya majina ya wanachuoni ambao wamepokea riwaya zielezeazo kwamba Aya hii imeteremka kuhusiana na Ali (a.s.), wanachuoni wote hao ni wa madhehebu ya Kiahlu Sunna, na ni watu wanaotegemewa katika hadithi, tafsiri ya Qur’an na akida, na hawa ndio wazushi – Mwenyezi Mungu aepushe mbali - kwa mujibu wa mtazamo wa Ibn Taymiya! Wanachuoni hao ni: 1. Abdu ibn Humaid al-Kishiy, aliyefariki mwaka 249A.H., amepokea kwa sanadi yake kutoka kwa Ibn Abbas.160 2. Ibn Jariri At-Tabariy, aliyefariki mwaka 310A.H. kwa sanadi yake kutoka kwa Suddiy, Utba ibn Abi Hakim na Mujahid.161 3. Ibn Abi Hatim Ar-Raziy, aliyefariki mwaka 327A.H. katika tafsiri yake, kwa sanadi yake kutoka kwa Salama ibn Kuheyl na Utba ibn Abi Hakim.162 4. Abul Qasim At-Tabariy katika Mu’jamul-Awsat.163 5. Abu Bakr al-Jaswasw Ar-Raziy, aliyefariki mwaka 370A.H. katika kitabu chake ‘Ahkamul- Qur’an.’164 6. Abul Hasan al-Wahidiy Nisaburiy aliyefariki mwaka 468A.H.165 7. Abul- Qasim ibn Asakir Ad-Dimishqiy, aliyefariki mwaka 571A.H.166 Addulul Manthur Juz. 3, uk. 105. Jamiul Bayan (Tafsiru Twabariy) Juz. 4, uk. 372-273. 162 Tafsir ibn Abi Hatim Juz. 4, uk. 1162. 163 Al-Mu’jamul-Awsat Juz. 30, uk. 130 164 Ahkamul- Qur’an uk. 133. 165 Asbabun- Nuzul, uk. 133. 166 Tarikh Madinatu Dimishqi Juz. 12, uk. 305. 160 161

102

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 102

11/25/2014 3:00:39 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

8. Abul Faraj ibn Jawziy al-Hanbaliy aliyefariki mwaka 597A.H.167 9. Abu Sa’daat Mubarak ibn Athir Ashaybaniy al-Jazriy Ashafiy aliyefariki mwaka 606A.H.168 10. Al-Qadhiy Nasir Diyn al-Baydhawiy katika tasiri yake.169 Hawa ni wanachuoni kumi tuliowachagua kati ya wanachuoni wengi waliopokea ya kwamba Aya hii imeteremka kuhusiana na Ali (a.s.) kutoa sadaka ya pete yake wakati alipokuwa anaswali, wameyaeleza hayo kabla ya kuzaliwa Ibn Taymiya, na lau tungetaka tengewaorodhesha zaidi ya hao, na utafiti huu ungerefuka, lakini Sheikh wetu al-Amin ameeleza kwa wasaa, kiasi ambacho ametaja wanachuoni 66 wa hadithi, tafsiri na akida wanaosema ya kwamba Aya hii imeteremka juu ya Imam Ali (a.s.) Na baadhi ya watu wamejadili juu ya usahihi wa Aya hii kushukwa kwa Imam Ali (a.s.), kwa kudai kwamba Aya imetaja katika mfumo wa wingi (Plural Form), kwani tamko lake Mwenyezi Mungu aliposema: “Ambao” ni neno la wingi, kwa hivyo haiwezekani Ali akawa ndiye mlengwa peke yake wa Aya hii.170 Kwa hakika kuna wale waliotangulia kulijadili jambo hili, kama vile Ibn Kathir katika tafsiri yake.171 Wengi miongoni mwa wanachuoni wetu wameshalijibu hili, kwamba kutumika neno la wingi ni kwa ajili ya kuwatia motisha wengine kufanya kitendo hicho, na hii haipingani na kitendo hicho Arriyadhun-Nadhira Juz. 3, uk. 182. Jamiu’l-Usul, Juz. 9, uk. 478. 169 Anwari Tanzil Juz. 1, uk. 272. 170 Nathru Laaliy ala Nadhmil- Amaliy uk.167. 167 168

171

Tafsir ibn Kathir Juz. 2, uk.73. 103

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 103

11/25/2014 3:00:39 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

kutendwa na mmoja. Na pia katika Qur’an tukufu kuna maneno mbalimbali yaliyokuja katika mfumo wa wingi, lakini mlengwa ni mtu mmoja, miongoni mwayo ni Aya hizi:

ُ ‫ﷲ ِمنْ َبعْ ِد َما‬ ‫ظلِمُوا َل ُن َبوِّ َئ َّن ُھ ْم فِي‬ ِ َّ ‫اجرُوا فِي‬ َ ‫ِين َھ‬ َ ‫َوالَّذ‬ ۖ ‫ال ُّد ْن َيا َح َس َن ًة‬

“Na wale waliohama (makwao) kwa ajili ya Mwenyezi Mungu baada ya kudhulumiwa huko, bila ya shaka tutawakalisha katika dunia kwa wema…” (Qur’an, 16: 41). Aya hii ilishuka kwa Abu Jundul ibn Suheyl al-Amiriy.172

‫ﷲ َوأَ َقامُوا الص َ​َّال َة َوأَ ْن َفقُوا ِممَّا‬ ِ َّ ‫اب‬ َ ‫ون ِك َت‬ َ ُ‫ِين َي ْتل‬ َ ‫إِنَّ الَّذ‬ ‫َر َز ْق َنا ُھ ْم سِ ًّرا َو َع َال ِن َي ًة‬

“Kwa yakini wale wanaosoma Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na wakasimamisha Swala, na wakatoa katika yale tulioyowapa…” (Qur.an, 35:29). Aya hii iliteremka kwa Husayn ibn Harith ibn Muttalib ibn Abdi Manafi.

Ama kuhusiana na makusudio ya Aya, kwamba inazungumzia uongozi wa Imam Ali (a.s.), tumeeleza vya kutosha katika vitabu vyetu mbalimbali vya kiakida.

172

Tarikh Madinatu Dimishqiy Juz. 8, uk. 668. 104

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 104

11/25/2014 3:00:39 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

MITIZAMO MINGINE YA IBN TAYMIYA KWA IMAM ‘ALI (A.S.) NA MASWAHABA WAKE

T

umetangulia kueleza ya kwamba Ibn Hajar alipotaja wasifu wa Allamatul Hilliy alisema: “Na ni namna gani (ibn Taymiya) alivyochupa mipaka katika kuyadhoofisha maneno ya Hilliy, kiasi cha kupelekea baadhi ya wakati kuishusha hadhi ya Ali (a.s.)173

Na sio Ibn Hajar peke yake aliyezungumza hivi, bali wako waliomtangulia miongoni mwa wale waliovisoma vitabu vyake, kwa mfano, Allamatul al-Alawiy Ibn Tahir al-Haddad, amesema: “Na katika kitabu ‘Minhaju Sunna’ cha Ibn Taymiya kuna matusi na lawama mbalimbali zilizoelekezwa kwa Kiongozi wa Waumini; Ali ibn Abi Talib, Fatima Zahraa, Hasan, Husain na watoto wao, matusi ambayo yanazisisimisha ngozi na kutetemesha nyoyo, na wala hakuona haja ya kuwachambua maadui wa Uislamu na Makhawariji katika kitabu chake kwani yeye ni mwenye kushirikiana nao katika kupanda na kushuka katika vilima vyao na silka zao, basi chukua tahadhari dhidi yake na dhidi yao.174 Miongoni mwa tuhuma hizo ni kama zifuatazo: 173 174

Lisanul Mizan Juz. 6, uk. 319 Kaulil Faslu fimaa Libani Hashim Juz. 2, yamenakiliwa kutoka kitabu ‘Al- Maqalaatu Sanniya uk. 376. 105

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 105

11/25/2014 3:00:39 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

a. Shaka juu ya imani ya Imam Ali (a.s.) kabla ya kubaleghe: Ibn Taymiya ametoa hukumu ya kwamba Imam (a.s.) alikuwa kafiri kabla ya kufikia umri wa kubaleghe, amesema: “Imani ya mtoto mdogo si sawa na imani ya mtu aliyebaleghe, hao inathibiti kwao hukumu ya imani na ukafiri ikiwa wamefikia hali ya kubaleghe, na Ali naye inamthibitikia hukumu ya ukafiri na imani alipokuwa hajabaleghe, mtoto aliyezaliwa na wazazi wawili makafiri, kwa mujibu wa makubaliano ya Waislamu katika dunia huhukumiwa hukumu ya ukafiri, na pindi atakapoingia katika Uislamu kabla ya kubaleghe wanachuoni wana kauli mbili, ambapo ni kinyume na ambaye amebaleghe, kwani kwa mujibu wa makubaliano ya Waislamu yeye atahukumiwa kuwa ni Mwislamu. Kule kusilimu kwa watu watatu (baba, mama na mtoto) ndiko kunakowatoa katika ukafiri (akiwemo mtoto) kwa mujibu wa makubaliano ya Waislamu. Ama kusilimu kwa Ali, je, kunamtoa katika ukafiri, hapo kuna kauli mbili zilizo mashuhuri. Kwa mujibu wa madhehebu ya Shafii ni kwamba kusilimu kwa mtoto hakumtoi katika ukafiri.175 Kwa haki ya Mola Wako! Niambie, ni lini Ali (a.s.) alikuwa kafiri mpaka iambiwe kwamba alisilimu, wakati yeye alizaliwa katika nyumba ya Upwekesho (Al-Kaaba)?! Ni lini alikuwa kafiri na wakati yeye alilelewa na Mtume (s.a.w.w.) toka akiwa mdogo sana? Kabla ya Mtume (s.a.w.w.) kupewa Utume, alikuwa akimwabudu Mwenyezi Mungu kwa mujibu wa mafunzo ya dini ya Ibrahim (a.s.), na kujiweka mbali na ibada za masanamu, na kwenda katika Jabal Hira kwa ajili ya ibada akiwa pamoja na Ali (a.s.) kama mfuasi na mwanafunzi wake.176 175 176

Minhaju Sunna Juz. 8, uk. 285. Sharhu Nahjul Balagha Juz.13, Uk. 248. 106

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 106

11/25/2014 3:00:39 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Na mwenyewe Imam Ali (a.s.) anaeleza mafungamano yaliyokuwepo wakati huo kati yake na Mtume (s.a.w.w.) kwa kusema: “Na mnaijua fika nafasi yangu ya udugu wa karibu mno na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na daraja maalumu (niliokuwa nayo kwake). Alikuwa akiniweka mapajani mwake, nami nikiwa mtoto, ananikumbatia kifuani mwake, na kunilaza karibu naye kitandani mwake, na kunigusisha mwili wake, na kuninusisha harufu yake nzuri, alikuwa akitafuna kitu kisha ananilisha. Hajanikuta na uwongo katika kauli, wala kuteleza katika kutenda. Na Mwenyezi Mungu alimuambatanisha Mtume (s.a.w.w.) na Malaika Mtukufu mno miongoni mwa Malaika Wake tokea alipoacha ziwa. (Huyo Malaika) alikuwa akimpitisha kwenye njia bora, na tabia njema ya kilimwengu, usiku na mchana wake. Na nilikuwa namfuata ufuataji wa mtoto wa ngamia afuatavyo nyayo za mama yake. Alikuwa kila siku akininyanyulia bendera ya tabia zake na kuniamuru nizifuate. Kila mwaka alikuwa na mazoea ya kujitenga huko Jabal Hira, mimi nilikuwa namuona wala mtu mwingine hamuoni. Wala hapakuwa na nyumba moja siku hizo iliyo na Mwislamu ambaye si Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), Khadija na mimi ni watatu wao, nilikuwa naiona nuru ya wahyi na risala, na nikinusa harufu ya Unabii. Kwa hakika niliusikia ukelele wa shetani pindi wahyi ulipokuwa unamshukia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu huu ukelele ni wa nini? Akasema: Huyu ni Shetani amekata tamaa ya kuabudiwa. Kwa hakika wewe (Ali) unasikia niyasikiayo na unayaona niyaonayo, ila tu wewe si Nabii, lakini wewe ni waziri, na wewe uko katika kheri.’’177 177

Nahjul Balaghah Juz. 2, Khutba Na. 192 107

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 107

11/25/2014 3:00:39 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Ewe ndugu msomaji mpendwa! Niambie baada ya kumtanguliza Mola Wako, je, inayumkinika kunasibishwa na ukafiri mtu ambaye kila siku akifunzwa tabia njema na Mtume (s.a.w.w.) na kumuamrisha kuzifuata, na wakati wote huambatana naye katika Jabal Hira, na kushuhudia nuru ya Wahyi na kunusa harufu ya Utume? Kwa bahati mbaya ni kwamba, Ibn Taymia alikuwa hajali katika kupokea fikra chafu kutoka kwenye vitabu vya wale walimtangulia, fikra ambazo zilikuwa na lengo la kumshusha hadhi Imam Ali (a.s.), zaidi fikra hizi alizichukua kutoka kwa Jahidh. Kisha yeye akazipalilia zaidi, kiasi ambacho ilidhihirika chuki yake dhidi ya Imam Ali (a.s.) Miongoni mwa fikra za Jahidh ni pale alipoelezea ubora wa Uislamu wa Abu Bakr juu ya Uislamu wa Imam Ali (a.s.), baada ya kudai kwamba wawili hao walisilimu pamoja, na sababu ya msingi ya dai lake hili ni pale aliposema: “Hakika Ali alisilimu akiwa ni mtoto mdogo mwenye kulelewa, kwa hivyo Uislamu wake hauwezi kulinganishwa na Uislamu wa watu wazima.’’ Sheikh Abu Ja’far al-Iskafiy al-Mu’taziliy, aliyefariki mwaka 240 A.H. alimjibu Jahidh, na hapa tutanukuu baadhi ya majibu yake, ili pia iwe ni jibu kwa Ibn Taymiya. Amesema: “Tumebainisha kwamba yeye Imam Ali (a.s.) alisilimu akiwa ameshabaleghe, akiwa na umri wa miaka kumi na tano, au miaka kumi na nne, na ikiwa tutakubaliana na kauli ya mpinzani (Jahidh), na kusema kwa mujibu wa riwaya iliyo mashuhuri, ya kwamba alisilimu akiwa na miaka kumi na moja, hayalazimu yale aliyoyasema Jahidh, kwani mtoto wa miaka kumi huwa na akili timam kwa kutambua misingi mingi ya maarifa. Na lau kama aliposil108

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 108

11/25/2014 3:00:39 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

imu hakuwa mtambuzi wa mambo, basi Mtume (s.a.w.w.) asingemsifu kwa hilo, kwani alimwambia binti yake; “Fatima, nimekuozesha kwa aliye wa mwanzo katika Uislamu.” Na wala asingeongezea maneno yake: “Na mtambuzi wao zaidi na mbora wao wa akili.” Mambo haya mawili ni upeo wa utukufu, na lau kama aliposilimu hakuwa mtambuzi na mwenye kupambanua mambo, basi Mtume (s.a.w.w.) asingeusifu Uislamu wake kwa kuongezea sifa ya elimu na akili. Ni vipi Mtume (s.a.w.w.) amsifu kwa sifa ambayo haina malipo wala adhabu lau kama ataiacha? Lau kama hakuwa mtambuzi wakati aliposilimu, basi asingejifakharisha mbele za watu juu ya kutangulia kwake katika Uislamu, na wala asingehubiri juu ya mimbari, hasa katika zama ambazo alipambana dhidi ya jeshi la watu wa Basra, Sham na Nahrawani, na kushambuliwa na maadui na washairi kumtungia mashairi ya chuki, lau kama watu hawa wangepata jambo litakalomporomosha kwa yale anayojifakharisha nayo, miongoni mwa kutangulia kwake katika Uislamu, basi wangeanza na hilo, na kuacha yale yasio na maana. Kisha washairi walimsifu kwa kutangulia kwake katika Uislamu, basi ni kwa nini washairi wa maadui zake hawakuwajibu hao? Umar alizungumza kauli inayowahusu mama wa watoto, kauli iliyokuwa kinyume na sheria, watu waliizungumza kauli hiyo na kumtia aibu, basi ni vipi waliacha kumtia aibu Imam Ali (a.s.) kwa jambo analojifakharisha nalo, ambalo kwao si fakhari, na wakaweza kumuaibisha Umar kuhusiana na kauli ya mama watoto?

109

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 109

11/25/2014 3:00:39 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

b. Kuteremka Aya: “Msiikaribie Swala…’’ kwa ‘Ali Ibn Taymiya amemsingizia Imam Ali (a.s.) mambo ambayo yuko mbali nayo, kama alivyokuwa Nabii Yusuf kutokana na yale aliyosingiziwa, amesema: “Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ameteremsha Aya hii kwa Ali wakati alipokuwa anaswali, alisoma na kujichanganya:

‫ار ٰى‬ َ ‫ِين آ َم ُنوا َال َت ْق َربُوا الص َ​َّال َة َوأَ ْن ُت ْم ُس َك‬ َ ‫َيا أَ ُّي َھا الَّذ‬

“Enyi mlio amini! Msikaribie Swala, hali mmelewa, mpaka myajue mnayoyasema.” (Qur’an, 4:43).’’178

Wamepokea Tirmidhiy, Abu Daud, Tabariy na Ibn Abi Hatim kwa sanadi zao kutoka kwa Abdu Rahman Sulamiy ya kwamba, baadhi ya Maswahaba walialikwa katika moja ya nyumba ya mwenzao, aliwaandalia chakula, na kuwapa ulevi kabla ya ulevi haujaharamishwa, kisha walihudhuria katika Swala, mmoja kati yao aliwaongoza Swala, alichanganyikiwa katika Swala yake na akakosea kusoma Aya katika Qur’an. Riwaya zilizotajwa ijapokuwa zimepokewa kutoka kwa mtu mmoja lakini zimegongana kuhusu jina la mtu aliyetoa mwaliko, aliyeongoza Swala, na Aya iliyokosewa, hali ni kama ifuatavyo: 1. Katika riwaya aliyoipokea Tirmidhiy inasema: “Aliyetoa mwaliko ni Abdur Rahman ibn Awfi, na Ali ndiye aliyekuwa Imam.’’179 178 179

Minhaju Sunna Juz. 7, uk. 237. Sunan Tirmidhiy, Kitabu Tafsirul Qur’an, Babu ‘Wa min Suratun Nisai’ 110

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 110

11/25/2014 3:00:39 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

2. Riwaya ya Abu Daud inasema kwamba: “Mtu aliyetoa mwaliko ni mmoja kati ya Maanswari.”180 3. Na katika riwaya ya Tabariy na ibn Mundhir: Imam wa Swala ya jamaa alikuwa Abdur Rahman ibn Awfi.”181 4. Na katika riwaya ya Ibn Hatim: “Ni kwamba, wao walimtanguliza mtu182 (kwa ajili ya Swala).183 Ndugu msomaji! Umeona namna Ibn Taymiya alivyo na ugonjwa katika moyo wake kutokana na riwaya inayodai kwamba Imam Ali (a.s.) ndiye aliyekuwa Imam wa Swala ya jamaa, na huku akifumbia macho riwaya zinazowataja watu wengine, na bila ya kueleza tofauti zilizomo katika riwaya hizo, na alichokifanya ni kutoa hukumu ya kwamba Imam Ali (a.s.) ndiye mlengwa wa Aya hii. Kisha riwaya hii inapingana na riwaya iliyo sahihi, ambayo pia imepokewa kutoka kwa Abi Abdur Rahman Salamiy, kama ilivyokuja: “Hakim amepokea kwa sanadi yake, kutoka kwa Abi Abdur Rahman kutoka kwa Ali r.a. amesema: Mtu mmoja miongoni mwa Maanswari alitualika kabla ya kuharamishwa ulevi, mara ikaingia Swala ya Magharibi, mtu mmoja akatangulia kuongoza Swala, akasoma: “Sema: Enyi makafiri.” Akajichanganya, mara ikateremka Aya: “Enyi mlio amini! Msikaribie Swala, hali mmelewa, mpaka myajue mnayoyasema.”184 Sunan Abi Daud, Kitabul- Ashriba, Babu ‘Tahrimul Khamri.’ Jamiu’l Bayan Juz. 4, uk.128. 182 Tafsir ibn Abi Hatim Juz. 3, uk. 985. 183 Alai Rahman Juz. 2, uk. 413-422, Tafsirul Kashif Juz. 2. uk. 331- 332. 184 Al-Mustadrak ala Sahiyhayn Juz. 2, uk. 307, ameisahihisha Hakim, na Dhahabiy amewafikiana naye. 180 181

111

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 111

11/25/2014 3:00:39 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Kitu cha kuzingatia katika riwaya hii ni kwamba, haijaeleza kikao cha ulevi alichohudhuria Imam Ali (a.s.), bali aliyehudhuria ni mtu ambaye hakutajwa jina lake mtu ambaye aliongoza Swala ya jamaa na kukosea kuisoma kwa sababu ya kuwa mlevi. Ni wapi na wapi na madai aliyoyadai Ibn Taymiya ya kwamba Imam Ali (a.s.) ndiye aliyeswalisha na kuteremkiwa na Aya hii!? Yote ni kwamba Ibn Taymiya amekataa katakata kuichukua riwaya hii na mfano wa hii, na badala yake ameathiriwa na wale waliotoka katika dini ambao wamedai kwamba Aya hii imeteremka kwa Imam Ali (a.s.). Hakim amesema baada ya kuinakili riwaya hii “Na katika riwaya hii kuna faida nyingi, nazo ni: Makhawarzwa Waumini; Ali ibn Abi Talib (a.s.) kinyume na mwingine, na kwa hakika Mwenyezi Mungu amemtakasa na jambo hili, kwa kuwa yeye ni mpokezi wa hadithi hii.”185 Hongera kwa Ibn Taymiya kwa vile anafuata rai za Makhawariji, na hashikamani na wasiokuwa hao katika rai na kauli! Ni vizuri kama jambo hili la kugongana kwa riwaya lingekuwa liko kwenye riwaya zilizopokewa kutoka kwa Abi Abdur Rahman peke yake, lakini ni kwamba kuna tofauti kati ya riwaya zake na riwaya zilizopokelewa na wengine kuhusiana na sababu ya kuteremka Aya hii, kwa mfano, kutoka kwa Ibn Abbas amesema: “Aya hii iliteremka kwa baadhi ya Maswahaba waliokuwa wakinywa pombe kabla ya kuharamishwa, kisha wakashiriki Swala pamoja na Mtume (s.a.w.w.), Mwenyezi Mungu aliwakataza jambo hilo.”186 185 186

Kitabu kilichotangulia. Tafsirul Haddad Juz. 2, uk. 258. 112

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 112

11/25/2014 3:00:39 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Na kutoka kwa Muhammad ibn Ka’b al-Qurdhiy…, kisha iliteremshwa ile ambayo iko katika Suratun-Nisai, wakati Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa akiswali baadhi ya Swala, mara mlevi akawa anaimba nyuma yake, hapo Mwenyezi Mungu aliteremsha Aya isemayo: “Msiikaribie Swala wakati mmelewa.” Ikawa watu wanalewa na wengine wakaacha, kisha ikateremka Aya nyingine iliyoko katika Suratul Maida, Umar ibn Khatab alisema: “Ewe Mola Wetu, tumekoma kunywa.”187 Kwa kumalizia maudhui haya tunasema: Lau kama Ibn Taymiya angekuwa na uadilifu japo kidogo, basi angetaja riwaya zilizopokewa na wanahadithi wa madhehebu ya Kiahlu Sunna zinazoelezea sababu ya kushuka Aya hii, ili msomaji amuelewe kwa uwazi yule aliyekuwa akinywa ulevi na kuendelea kufanya hivyo mpaka pale Aya ziliposhuka na kubainisha kwa uwazi juu ya uharamu wake. Wamepokea Abu Daud, Tirmidhiy, An-Nasaiy, Tabariy, ibn Mundhir na ibn Abi Hatim kwa sanadi zao mpaka kufikia kwa Abu Maysara ibn Shurahbil, ni kwamba Umar ibn Khattab alisema: “Ewe Mola wetu! Tubainishie katika ulevi ubainisho wa wazi, basi ikateremka Aya iliyoko katika Suratul Baqara: ‘Wanakuuliza juu ya ulevi na kamari. Sema: Katika hivyo zipo dhambi kubwa na manufaa kwa watu, lakini dhambi zake ni kubwa zaidi kuliko manufaa yake.’ (Qur’an, 2:219). Umar aliitwa na kusomewa Aya hii, akasema: ‘Ewe Mola wetu! Tubainishie katika ulevi ubainisho wa wazi,’ basi ikateremka Aya ilioko katika Suratun Nisai: ‘Enyi mlio amini! Msikaribie Swala, hali mmelewa, mpaka myajue mnayoyasema.’ (Qur’an; 4:43). Umar aliitwa na kusomewa Aya hii, akasema: ‘Ewe Mola wetu! Tubainishie katika ulevi ubainisho wa wazi,’ basi ikateremka Aya iliyoko katika Suratul Maida: ‘Hakika Shetani anataka 187

Ad-Durul Manthur , Juz. 3, uk. 165. 113

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 113

11/25/2014 3:00:39 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

kutia uadui kati yenu na chuki kwa ulevi na kamari, na akuzuieni kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kuswali, basi je, mmeacha?’ (Qur’ani, 5:91). Umar aliitwa na kusomewa Aya hii, akasema: ‘Tumekoma kunywa.’”188 Sheikh Muhammad Jawad Mughniya amesema: “Kwa vyovyote vile, ikiwa imethibiti kwamba, baadhi ya Maswahaba walilewa na Imam wao akajichanganya katika kisomo, basi Maswahaba hao ni wale waliokuwa wakimshirikisha Mwenyezi Mungu na kuabudu masanamu, na kunywa ulevi na kula haramu katika zama za ujahiliya, na kuishi katika hali hiyo…, na Ali ibn Abi Talib hakuwa miongoni mwao, kwa sababu yeye amekulia na kulelewa katika mapaja ya Mtume (s.a.w.w.), na yeye ndiye aliyesimamia malezi yake tangu udogoni mwake na kumkuza kama vile alivyotaka yeye.”189 c. I bn Taymiya apinga fadhila za Maswahaba wa Imam Ali (a.s.) Kwa vile Ibn Taymiya alikuwa akimchukia Imam Ali (a.s.), kama alivyobainisha kwa wazi katika vitabu vyake, ni jambo la kawaida kwa mtu mwenye tabia hiyo kuwachukia Maswahaba wa Imam Ali (a.s.) na wafuasi wake, kwani rafiki wa adui yako, naye pia ni adui, uadui wake huo umedhihiri pale anapozikataa fadhila za hali ya juu za Swahaba Mtukufu Ammar ibn Yasir, kwani Waislamu wamewafikiana juu ya ubora wake kutokana na riwaya iliyopokewa kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akimwambia: “Pote ovu ndilo litakalokuuwa.” S unan Tirmidhiy, Hadith Na.3060. Sunan Abi Daud, Hadith Na. 3670. Jami’ul Bayan Juz. 5, uk. 44-45. 189 Tafsirul Kashif Juz. 2, uk. 232. 188

114

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 114

11/25/2014 3:00:40 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Ibn Taymiya anasema: “Kuhusiana na riwaya hii kuna kauli nyingi za watu, wako wale ambao wanaidhoofisha hadithi ya Ammar, na miongoni mwao wako wanaoitolea tafsiri ya kwamba ‘Muovu’ maana yake ni mtafutaji, hii ni tafsiri iliyo dhaifu. Ama maulamaa waliopita (Masalafi) na maimamu walio wengi miongoni mwao kama vile Abu Hanifa, Malik, Ahmad na wengineo wanasema: Haikupatikana sharti ya kulipiga pote ovu, kwani Mwenyezi Mungu hakuamrisha kuanza kupigwa, bali aliloamrisha ni pale ambapo makundi mawili ya Waislamu yatapigana, basi yasuluhishwe kati yao, na ikiwa kundi moja litakataa na kufanya ujeuri, basi kundi hilo lipigwe, na watu hawa (kundi la Muawiya) walianzwa kupigwa kabla ya wao kuanza vita.’’190 Tumetangulia kueleza kwamba, mwenendo wa Ibn Taymiya katika kuamiliana na hadithi zinazoeleza fadhila za Imam Ali (a.s.) na jamaa zake pamoja na Maswahaba wake, hudai kwamba baadhi ya watu wamezidhoofisha, bila ya kuwataja watu hao. Jambo la ajabu zaidi kwa Ibn Taymiya ni kule kuidhoofisha hadithi iliyopokewa na Maswahaba wanaozidi ishirini, na mwanachuoni wa elimu ya Hadithi; Ibn Abdi Barri anasema: “Habari zimeenea kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) kwamba amesema: ‘Pote ovu litamuuwa Ammar.’ Hii ni miongoni mwa hadithi zilizo sahihi.”191 Ikiwa hadithi hii ni dhaifu, basi ni hadithi gani iliyo sahihi kwake?! Ibn Hajar ambaye ni mwanachuoni wa hadithi ana maelezo kuhusiana na hadithi hii, hapa tutayataja baadhi yake 190 191

Mihaju Sunna Juz. 4, 390 -391. Al-Isti’ab Juz. 3, uk. 1140. 115

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 115

11/25/2014 3:00:40 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

ili ijulikane kiwango cha chuki alichokifikia mtu huyu (Ibn Taymiya) dhidi ya Imam Ali (a.s.) amesema: “Faida: Hadithi hii: ‘Pote ovu litamuuwa Ammar.’ Imepokewa na kundi la Maswahaba kama vile: Qutada ibn Nu’man, Ummu Salama kama ilivyo kwa Muslim, Abu Huraira kama ilivyo kwa Tirmidhiy, Abdullah ibn Amru ibn Aswi kama ilivyo kwa An-Nasaiy, na Uthman ibn Affan, Hudhaifa, Abu Ayub, Abu Raafi, Khuzayma ibn Thabit, Muawiya, Amru ibn Aswi, Abul Yusri, na Ammar mwenyewe, wote hawa kama alivyopokea Tabraniy na wengineo, na njia zake nyingi ni sahihi au nzuri, na kuna wengine walioipokea, lakini nafasi ya kuwataja haitoshi. Katika hadithi hii kuna alama miongoni mwa alama za Utume na fadhila zilizo wazi za Ali na Ammar, na ni jawabu kwa wale wenye chuki wanaodai kwamba Ali hakuwa sahihi katika vita vyake.’’192 Inatosha hadithi hii kuwa sahihi kwa wafuasi wa madhehebu ya Ahlu Sunna, kwa vile ipo katika kitabu cha Bukhari na Muslim.193 Ama kauli ya Ibn Taymiya pale aliposema kwamba: “Wanachuoni wa zamani na maimamu, wengi wao wanasema kwamba, hapakuwepo sharti la kulipiga pote ovu…” Kwa kweli dai lake hili si la kweli, kwani yale yaliyopokewa kutoka kwa wanachuoni wakubwa kutoka kwa wanachuoni wa zamani yanapingana na dai lake, kwa mfano, Imam ibn Qudama al-Maqdisiy al-Hanbal, aliyefariki mwaka 620A.H., amesema: “Maswahaba r.a. wamekubaliana juu ya kuwapiga vita watu waovu, kwani Abu Bakr alipigana dhidi ya wale waliokataa kutoa Zaka, na Ali alipigana dhidi ya jeshi la Nga192 193

Fat-hul Baariy Juz.1, uk. 543. Angalia Sahih Bukhari Juz. 3, uk. 207, Sahih Muslim Juz. 8, uk.186. 116

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 116

11/25/2014 3:00:40 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

mia (jeshi la bibi Aisha), na Swiffin (jeshi la Muawiya) na watu wa Nahrawani (Makhawariji).”194 Na jambo linalothibitisha zaidi ni kwamba, wale waliotoa viapo vyao vya utiifu kwa Mtume (s.a.w.w.) chini ya mti na kuridhiwa na Mwenyezi Mungu, na watu walioshiriki vita vya Badr, wengi wao walikuwa pamoja na Imam Ali (a.s.) katika vita vya Siffin. Khalifa ibn Khayyat amepokea kutoka kwa Abi Ghassan kutoka kwa Abdu Salaam ibn Harb, kutoka kwa Yazid ibn Abdur Rahman, kutoka kwa Ja’far ibn Mughira, kutoka kwa Abdillah ibn Abdur Rahman ibn Abziy, kutoka kwa baba yake, amesema: “Walishiriki pamoja na Ali watu mia nane miongoni mwa wale waliotoa viapo vyao vya utiifu chini ya mti, alisema: Waliuawa miongoni mwao watu sitini na tatu, kati ya hao alikuwemo Ammar ibn Yasir.’’195 Sanadi hii ni sahihi, na wapokezi wake ni kati ya watu madhubuti na wale walio wakweli.196 Maswahaba hawa watukufu wana khofu kubwa kupigana na wale ambao halijathibiti kwao sharti la kuwa pote ovu, lakini Ibn Taymiya haipi uzito idadi hii kubwa ya Maswahaba kwa vile walikuwa upande wa Imam Ali (a.s.). Na miongoni mwa ushahidi wa yale yaliyotangulia, ni kwamba Abdullah ibn Umar ameliita kundi la Muawiya kuwa ni pote potevu, na alionesha majuto yake juu ya kutoshiriki kwake katika vita vya Siffin dhidi ya Muawiya. Umar ibn Shabbah, alifariki mwaka 262A.H., amepokea kutoka kwa Fadhli ibn Dukayn na Abu Ahmad Zubairiy, wamesema: Ametusimulia Abdullah ibn Habib ibn Abi Thabit, kutoka kwa Al-Mughniy Juz. 7, uk. 522. Tarikh Khalifa uk. 196. 196 Bai’atu Ali ibn Abi Talib Fii dhaw-I Riwayat Swahiha uk.196. 194 195

117

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 117

11/25/2014 3:00:40 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

baba yake, kutoka kwa Ibn Umar, ni kwamba amesema wakati alipofikiwa na mauti: “Sijakuta katika nafsi yangu jambo miongoni mwa mambo ya dunia, isipokuwa kule kutopigana pamoja na Ali ibn Abi Talib dhidi ya pote ovu.’’197 Hakim Nisaburiy amepokea kwa sanadi yake kutoka kwa Zuhriy, kutoka kwa Hamza ibn Abdillah ibn Umar, ni kwamba Abdullah ibn Umar alisema: “Sijakuta kitu katika nafsi yangu kuhusiana na Aya hii (Aya ya kuamrisha kupambana dhidi ya pote potovu), nililolikuta katika nafsi yangu ni kuwa mimi sikupigana dhidi ya pote hili ovu kama vile Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyoniamrisha.” Baada ya Hakim kupokea hadithi hii alisema: “Mlango huu ni mkubwa, kundi la wakubwa wa kitabiina wameipokea kutoka kwa Ibn Umar, na kwa hakika nimetanguliza hadithi ya Shuayb ibn Abi Hamza, kutoka kwa Zuhriy, na nikatosheka nayo kwa sababu ni sahihi kwa mujibu wa masharti ya Bukhari na Muslim.198 Tunauliza: Ni nani anayelitambua vyema kundi la Muawiya lililopambana dhidi Imam Ali huko Siffin, ni Ibn Taymiya au Ibn Umar ambaye aliishi katika zama za vita hivyo, na kuliita pote ovu kama alivyoliita Mtume (s.a.w.w.) hapo kabla, na kuonesha masikitiko yake ya kutoshiriki vita hivyo baada ya kupita miaka zaidi ya thelathini?! Mwisho tunasema: Hakika sisi tumezitaja dalili hizi kama jibu kwa Ibn Taymiya na wafuasi wake, ama kwa upande mwingine maneno haya ya Mtukufu Mtume s.a.w.w: “Pote ovu litakuuwa,” yanatosha kuthibitisha upotofu wa Muawiya na wafuasi wake, na iweje kwa Mtume alielezee kundi litakalomuuwa Ammar kwamba ni pote ovu kisha isithibitike kuwa na sifa za uovu 197 198

Al-Istiab Juz. 3, uk. 953. Al-Mustadrak ala Swahiyhayn Juz. 3, uk. 115-11 118

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 118

11/25/2014 3:00:40 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

na uadui?! Kwa hivyo kila anayedai kwamba kundi la Muawiya halikuwa kundi ovu atakuwa anapingana na kauli ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kuwa ni mwenye makosa kutokana na madai yake hayo. Mwenyezi Mungu awaepushe Waumini na usingizi wa akili na kuteleza kwenye uovu, na kula hasara.

119

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 119

11/25/2014 3:00:40 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

IBN TAYMIYA NA HADITHI “WEWE NI KIONGOZI WA KILA MUUMINI BAADA YANGU”

W

apokezi wa hadithi wamepokea kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimwambia Ali: “Wewe ni Kiongozi wa kila Muumini baada yangu.” Lakini maana ya hadithi hii haikumfurahisha Ibn Taymiya, hivyo ametoa hukumu ya udhaifu wake na kuzushwa kwake, amesema: “Na mfano wa kauli yake: ‘Wewe ni Kiongozi wa kila Muumini baada yangu.’ Kwa hakika hadithi hii ni ya uongo kwa mujibu wa makubaliano ya wanachuoni wa hadithi.”199 Na anasema tena sehemu nyingine: “Na pia kauli yake: ‘Yeye ni Kiongozi wa kila Muumini baada yangu.’ Ni uongo aliozushiwa Mtume wa Mwenyezi Mungu.”200

Ilikuwa ni juu ya Ibn Taymiya aseme: Hakika hadithi hii ni sahihi kwa mujibu wa wanachuoni wa hadithi. Lakini kama kawaida yake, alichokifanya ni kuidhoofisha kwa lengo la kukamilisha malengo yake. Je, mtu huyu anadhani ya kwamba wale waliyoinakili hadithi hii katika vitabu vyao si wataalamu wa elimu ya hadithi, akiwemo Imam wa madhehebu yake; Ahmad ibn Hanbal, ambaye ameieleza hadithi hii kwa sanadi iliyo sahihi? Amesema: “Ametusimulia Abdur Razzaq, ametusimulia Ja’far ibn Sulayman, amenisimulia Yazid ArRishki, kutoka kwa Mitraf ibn Abdillah, kutoka kwa Imran ibn Husain, amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipeleka kikosi cha wapiganaji, na akamfanya Ali kuwa kiongozi wao, 199 200

Minhaju Sunna Juz. 5, uk. 35-36. Kitabu kilichotangulia Juz. 7, uk. 391. 120

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 120

11/25/2014 3:00:40 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

katika safari yake Ali alifanya jambo fulani, watu wanne miongoni mwa Maswahaba wa Mtume (s.a.w.w.) waliazimia kulifikisha jambo hilo kwa Mtume (s.a.w.w.) Imran akasema: Ilikuwa pale tunaporudi kutoka katika safari, kwanza tukifikia kwa Mtume (s.a.w.w.), na kumsalimia. Akasema: Waliingia, na mtu mmoja miongoni mwao alisimama na kusema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Hakika Ali amefanya jambo hili na lile. Mtume (s.a.w.w.) aliwageuzia uso. Kisha akasimama mtu wa pili, naye akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Hakika Ali amefanya jambo hili na lile. Mtume (s.a.w.w.) aliwageuzi uso. Kisha alisimama mtu wa tatu, nae akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Hakika Ali amefanya jambo hili na lile. Kisha alisimama mtu wa nne, naye akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Hakika Ali amefanya jambo hili na lile. Akasema: Mtume (s.a.w.w.) alimuelekea mtu wa nne na huku uso wake ukiwa umebadilika rangi, akasema: Mwacheni Ali, mwacheni Ali, mwacheni Ali, kwani Ali anatokana na mimi, na mimi natokana na yeye, na yeye ni Kiongozi wa kila muumini baada yangu.” Na pia hadithi hii ameisimulia Abu Ya’laa al-Muswiliy, kutoka kwa Ubaydullah ibn Umar al-Qawaririy, kutoka kwa Ja’far ibn Sulayman, kwa sanadi iliyotangulia.201 Na Ibn Abi Shayba202 ameisimulia, na pia Habban katika Sahih yake203, Abu Nua’im al-Asfahaniy katika ‘Hilyatul-Awli-

Musnad Abi Ya’laa Juz. 1, uk. 203. Al-Muswanif Juz.12, uk.180. 203 Sahihi ibn Habban Juz. 5, uk. 374. 201

202

121

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 121

11/25/2014 3:00:40 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

yai’204 na Muhibbu Diyn Tabariy,205 Al-Baghwiy,206 Ibn Kathir katika kitabu chake cha historia,207 As-Suyutiy,208 na al-Muttaqiy.209 Na kuna wapokezi wengine wa hadithi waliopokea ya kwamba Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Mnataka nini kwa Ali? Mnataka nini kwa Ali? Mnataka nini kwa Ali? Hakika Ali anatokana na mimi na mimi natokana na Ali, na yeye ni Kiongozi wa kila Muumini baada yangu.” Walioipokea kwa maneno haya ni: Tirmidhiy, amesema: Hadithi hii ni nzuri iliyo ngeni,210 An-Nasaiy,211 Muhibbu Diyn,212 na Ibn Hajar, 213 wamesema: Sanadi yake ni yenye nguvu. Na pia kuna sanadi nyingine ya hadithi hii, nayo ni: Amesimulia Abu Daud Tayalasiy, kutoka kwa Abi Awana, kutoka kwa Abi Balji, kutoka kwa Amru ibn Maymun, kutoka kwa Ibn Abbas, kwamba Mtume (s.a.w.w.) amesema kumwambia Ali: “Wewe ni Kiongozi wa kila Muumini baada yangu.”214 Na sanadi yake ni sahihi na wapokezi wake wote ni madhubuti. Allamatul-Amin amesema baada ya kutoa maelezo ya kumrudi Ibn Taymiya katika hadithi hii na nyenginezo: Huu ni mfano mdogo tu wa chuki za Ibn Taymiya, na lau kama tungeeleza kila upotofu, uongo na uzushi uliomo katika ‘MinHilyatul- Awliyai Juz. 6, uk. 294. Riyadhun Nadhira Juz. 3, uk. 116. 206 Maswabihu Sunna Juz. 4, uk. 172. 207 Albidaya wannihaya Juz. 7, uk. 381. 208 Jamiul Hadith Juz. 4, uk. 352. 209 Kanzul-Ummal Juz. 11, uk. 608, Hadith Na. 32940, 23941. 210 Sunan Tirmidhiy Juz. 5, uk. 590. 211 Khaswaiswu Amiril Muuminina, uk. 92. 212 Riyadhun Nadhrah Juz. 3, uk. 115. 213 Al-iswabah Juz. 2, uk. 509. 214 Mustadrak Abi Daud Tayalasiy uk. 360, Hadithi Na. 2752. 204 205

122

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 122

11/25/2014 3:00:40 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

haji ya Bidaa yake’ yenye jumla ya juzuu nne, basi tungehitaji kuwa na juzuu kama hizo za majibu, na wala sina maelezo ya kumuelezea mtu huyu, isipokuwa nitatosheka na maneno ya Ibn Hajar yaliyomo katika kitabu chake kijulikanacho kwa jina la ‘Al-Fatawal Hadithiya’ aliposema: “Ibn Taymiya ni mtu aliyepuuzwa na Mwenyezi Mungu, na kumpotosha, na kumpofua na kumtia uziwi na kumdhalilisha, hii ni kwa sababu wanachuoni wameweka bayana ubaya wa hali yake na uongo wa maneno yake, na anayeyahitaji hayo, basi arejee maneno ya Imam Mujtahidi, ambaye wanachuoni wamewafikana juu ya uimam wake na utukufu wake, na kufikia daraja ya ijitihadi (uwezo wa kubainisha hukumu za kisheria), huyo ni Abul Hasan As-Sabakiy, na mtoto wake anayeitwa Taj na Sheikh Imam Izzu Ibn Jama’a, na watu walioishi katika zama zake na wengineo miongoni mwa wafuasi wa Imam Shafi, Malik na Abu Hanifa.’’215

215

Al-Ghadir: Jz. 307. 123

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 123

11/25/2014 3:00:40 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

IBN TAYMIYA NA HADITHI YA ­KUFUNGA MILANGO YOTE ISIPOKUWA MLANGO WA ‘ALI (A.S.)

I

bn Taymiya anajishungulisha mno kupinga kila fadhila miongoni mwa fadhila za Imam Ali (a.s.) zilizopokelewa na wapokezi madhubuti katika vitabu vyao, hiyo ni kutokana na fadhila hizo kutowafikiana na matakwa yake, ndio maana ikawa unamuona namna anavyokabiliana na riwaya zote na kuzieleza kwamba ni za uongo na zilizozuliwa, na hapa anasema wazi kuhusiana na hadithi maarufu inayozungumzia ufungaji milango kwamba ni hadithi iliyowekwa na Mashia kwa lengo la kukabiliana na hadithi kama hiyo (inayomhusu Abu Bakr).’’216

Katika kuthibitisha msimamo wake huu amesema yafuatayo: “Na ile ambayo ni sahihi ni hadithi iliyopokewa kutoka kwa Abi Said, kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.), ni kwamba alisema katika ugonjwa ambao ulikuwa ni sababu ya kifo chake: ‘Isibakie ‘Khawkhat’ katika msikiti isipokuwa ifungwe, ila ‘Khawkhat’ ya Abu Bakr.” Na pia ameipokea Ibn Abbas katika Sahih mbili (Bukhari na Muslim).’’217 Muulizaji atamuuliza Ibn Taymiya: “Ni wapi amejua kwamba Mashia wamezua hadithi kwa lengo la kukabiliana (na hadithi inayomhusu Abu Bakr)? Kwani kule tu Mashia kumpenda Ali (a.s.) si dalili ya kuwa wao wamezusha hadithi! Kisha je upinzani uliopo ndio dalili ya hadithi hii kuwa 216 217

Minhaju Sunna Juz. 5, uk. 35. Kitabu kilichotangulia. 124

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 124

11/25/2014 3:00:40 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

ya kuzuliwa? Na ni kwa nini isiwe kuwepo kwa upinzani ni dalili ya kuzushwa hadithi inayomuhusu Abu Bakr? Kwa hali yoyote ile, upinzani hauwezi kuwa ni dalili, ikiwa haiwezekani kukusanya hadithi mbili hizi, kwani kufungwa kwa mlango si kufungwa kwa ‘Khawkhat’ kwani maana ya ‘Khawkhat’ ni nishati fulani iliyokuwa ikitoka majumbani na kuingia msikitini, kwa hivyo hakuna kizuizi kwa Mtume (s.a.w.w.) kuamrishwa kufungwa kwa milango isipokuwa mlango wa Imam Ali (a.s.), na wakati huo huo kuamrishwa kufungwa kwa ‘Khawkhat’ isipokuwa ya Abu Bakr. Kutokana na haya, Allama al-Amin anasema katika kutoa angalizo la maneno ya Ibn Taymiya: “Sioni sababu yoyote iliyomfanya anasibishe uzushwaji wa hadithi hii na Mashia isipokuwa ni ile chuki na upingaji wake wa mambo halisi yenye ukweli kwa kupayuka, kwani hakika mbele ya macho ya mtu huyu (Ibn Taymiya) kuna vitabu vya Maimam wa Kiahlu Sunna, ikiwemo Musnadi wa Imam ya madhehebu yake (Musnad Ahmad), ambayo imesimulia hadithi hii kwa sanadi nyingi sahihi na nzuri, kutoka kwa Maswahaba mbalimbali, ambao kwa mujibu wa idadi yao, riwaya inafikia kiwango cha tawaturi (umashuhuri wa hali ya juu, ambao hauhitaji dalili).”218 Na sasa twende pamoja nami ili tuwasome wale walioinakili hadithi miongoni mwa wanachuoni wa hadithi, ili tuone ukweli wa maneno ya Ibn Taymiya. Miongoni mwa Maswahaba walioisimulia hadithi ni hawa wafuatao: Zayd ibn Arqam, Umar ibn Khattab, Al-Barau ibn Azib, Abdullah ibn Umar ibn Khattab, Abdullah ibn Abbas, Abu Said al-Khudriy, Said ibn Malik, Abu Hazim al-Ashjaiy, Jabir ibn Abdillah alAnswariy, Jabir ibn Samara, Sa’d ibn Abi Waqqas, na Anas ibn 218

Al-Ghadir Juz. 3, uk .285. 125

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 125

11/25/2014 3:00:40 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Malik. Zaidi ya hao, ni kwamba Imam Ali (a.s.) mwenyewe ameipokea hadithi hii, na ambaye atahitaji kujua matini ya hadithi na vitabu vilivyoinakili, basi arejee kwenye kitabu kijulikanacho kwa jina la ‘Al-Ghadir’.219 Na hapa tunataja baadhi ya riwaya za Maswahaba hao kama ifuatavyo: 1. Imam Ahmad amepokea (kwa sanadi sahihi) kutoka kwa Amru ibn Maymun, kutoka kwa Ibn Abbas, amesema: Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w: “Ifungeni milango inayoingilia msikitini isipokuwa mlango wa Ali.” Imepokewa na An-Nasaiy220 na Hakim, ameisahihisha, na Dhahabiy221 amewafikiana na Hakim juu ya usahihi wake. 2. Hakim amepokea kwa sanadi yake kutoka kwa Zayd ibn Arqam, amesema: Baadhi ya milango ya Maswahaba wa Mtume (s.a.w.w.) ilikuwa inaingilia msikitini, siku moja, Mtume alisema: “Ifungeni milango hii inayoingilia msikitini isipokuwa mlango wa Ali.” Kutokana na amri hiyo, watu walizungumza zungumza. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisimama na akaanza kumhimidi Mwenyezi Mungu na kumsifu, kisha akasema: “Ama baada ya hayo! Hakika mimi nimeamrishwa kuifunga milango hii isipokuwa mlango wa Ali, msemaji wenu akasema kuhusiana na amri hiyo, naapa kwa Mwenyezi Mungu! Mimi sijafunga kitu wala kukifungua, isipokuwa nimeamrishwa jambo nami nikalitekeleza.”222 Al-Ghadir Juz. 3, uk. 285 - 304. haswaiswu Amirul-Muuminina uk. 59. Hadithi Na. 42, na uk. 58, Hadithi Na. 41 K 221 Al-Mustadrak Alas Swahiyhayn Juz. 3, uk.132. 222 Kitabu kilichotangulia uk. 124. Hakim ameisahihisha, na Dhahabiy ameinyamazia. Musnad Ahmad: Juz. 4, uk. 372. 219

220

126

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 126

11/25/2014 3:00:40 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

3. Katika kutoa tanbihi, Ibn Hajar amesema: “Kuna hadithi zinazotofautiana juu ya kufungwa milango ya msikiti, kwani kuna hadithi isemayo: “Usibakie katika msikiti mlango wowote ila ufungwe, isipokuwa mlango wa Abu Bakr,” Miongoni mwa hadithi hizo ni hizi zifuatazo Hadithi ya Sa’d ibn Abi Waqqas, amesema: “Mtume (s.a.w.w.) alituamrisha kuifunga milango inayoingilia msikitini, na kuuwacha mlango wa Ali.” Imepokewa na Ahmad na An-Nasaiy, na sanadi yake ni yenye nguvu, na katika riwaya ya Tabaraniy katika kitabu chake kijulikanacho kwa jina la ‘Awsat’ wapokezi wake ni wenye kutegemewa, kukiwa na ziada ya maneno haya: Wakasema: “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Umeifunga milango yetu! Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Mimi sikuifunga, lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliyeifunga.” Na kutoka kwa Zayd ibn Arqam amesema: Baadhi ya milango ya Maswahaba wa Mtume (s.a.w.w.) ilikuwa inaingilia msikitini, siku moja alisema: “Ifungeni milango hii inayoingilia msikitini isipokuwa mlango wa Ali.” Kutokana na amri hiyo, watu walizungumza zungumza. Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Naapa kwa Mwenyezi Mungu! Kwa hakika mimi sijafunga kitu wala kukifungua, isipokuwa nimeamrishwa jambo nami nikalitekeleza.” Na kutoka kwa Ibn Abbas amesema: “Mtume (s.a.w.w.) aliamrisha kufungwa milango inayoingilia msikitini isipokuwa mlango wa Ali.” Na katika riwaya nyingine: “Aliamrisha kufungwa milango isipokuwa mlango wa Ali, akawa anaingia msikitini huku akiwa na janaba kwani alikuwa hana njia nyingine isipokuwa hiyo.” Wamezipokea Ahmad na An-Nasaiy, na wapokezi wake ni madhubuti. 127

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 127

11/25/2014 3:00:40 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Kutoka kwa Jabir ibn Samara, amesema: “Mtume (s.a.w.w.) aliamrisha kufungwa milango yote, isipokuwa mlango wa Ali, huwenda alikuwa akipita hapo, huku akiwa na janaba. Imepokewa na Tabraniy.” Kutoka kwa Ibn Umar, amesema: “Katika zama za Mtume (s.a.w.w.) tulikuwa tukisema: Mtume (s.a.w.w.) ni mbora wa watu, kisha Abu Bakr, kisha Umar, na kwa hakika Ali ibn Abi Talib alipewa mambo matatu, na lau nitakuwa na moja kati ya hayo, basi ni bora kwangu kuliko kuwa na ngamia wekundu: Mtume (s.a.w.w.) alimuozesha binti yake na akazaa naye, na alifunga milango inayoingila msikitini isipokuwa mlango wake, na alimpa bendera siku ya Khaybar.” Imepokewa na Ahmad, na sanadi yake ni nzuri. Na An-Nasaiy ameipokea kwa njia ya Alaa ibn Arar, amesema: “Nilimwambia Ibn Umar: Niambie kuhusiana na Ali na Uthman, basi aliitaja hadithi (hii). Na katika maneno yake: Ama Ali, usimuulize yeyote kuhusiana naye, au angalia daraja yake kwa Mtume (s.a.w.w.), kwani milango yetu iliyokuwa inaingilia msikitini ilifungwa, na kubakishwa mlango wake.” Wapokezi wake ni sahihi isipokuwa Alaa, lakini Yahya ibn Mu’in na wengineo wamethibitisha ukweli wake. Na hadithi hizi zinatiana nguvu zenyewe kwa zenyewe, na kila njia kati ya hizi zinafaa kutolea hoja seuze katika ujumla wake. Na Ibn Jawziy amezinakili hadithi hizi katika sehemu ya hadithi za uzushi, ameipokea miongoni mwa hadithi za Sa’d ibn Abi Waqqas, Zayd ibn Arqam na Ibn Umar katika hali ya kufupisha njia yake (hadithi) kutoka kwao, ameitia aibu kutokana na wale ambao walizungumza kuhusiana na wapokezi wake. 128

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 128

11/25/2014 3:00:40 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Lakini hilo si tatizo kutokana na yale niliyoyasema juu ya kuwepo njia nyingi. Na pia ameitia aibu kwa kudai kwamba hadithi hii inapingana na hadithi sahihi zinazoelezea kutokufungwa mlango wa Abu Bakr, na kudai kwamba ni katika hadithi zilizozuliwa na Mashia ili kukabiliana na hadithi ya Abu Bakr. Kwa hakika katika jambo hili amekosea kwa uwazi kabisa, kwani amezikataa hadithi zilizo sahihi kwa kudhania kwake tu kwamba kuna mgongano, licha ya kuwepo uwezekano wa kukusanywa (kukubalika) hadithi zote mbili.223

223

Fathul Bariy Juz. 7, uk. 14 -15. 129

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 129

11/25/2014 3:00:40 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

IBN TAYMIYA APINGA HADITHI YA “LANGO LA JIJI LA ELIMU”

I

bn Taymiya anasema hadithi: “Mimi ni Jiji la elimu na Ali ni lango lake.” Ni hadithi iliyo dhaifu mno, na kwa hivyo inahesabiwa kuwa ni katika hadithi zilizozushwa licha ya kupokewa na Tirmidhiy. Na Ibn Jawziy ameeleza ya kwamba njia zake zote ni zenye kuzushwa, na uongo wake unajulikana kwa hiyo matini yake.”224 Ninasema: Ni vipi anatoa hukumu ya kuzushwa hadithi hii ambayo wapokezi wameipokea kutoka kwa Maswahaba mashuhuri, hili ni la kwanza, pili, pia Matabiina walio wengi, na tatu wanachuoni mashuhuri karne kwa karne. Na dalili ya hayo ni yale aliyoyahakiki mwanachuoni aliyeishi katika zama zake ajulikanaye kwa jina la Sayyid Hamid Husain Allak-hanawiy, kiasi ambacho amebainisha sanadi yake katika juzuu maalumu katika kitabu chake kijulikanacho ‘AbaqatulAnwari’ na kunakikiliwa kwa lugha ya Kiarabu na Muhakiki Sayyid Ali al-Husainiy al-Milaniy katika kitabu chake ‘Nafahatul-Azhari’ na kuchapwa katika juzuu tatu. Ama Maswahaba waliyoipokea: 1. Imam Ali (a.s.), Imam Hasan (a.s.), Imam Husain (a.s.), Abdullah ibn Abbas, Jabir ibn Abdillah al-Answariy, Abdullah ibn Masud, Hudhayfa ibn al-Yama, Abdullah ibn Umar, Anas ibn Malik, na Amr ibn Aswi. 2. Ama matabiina waliyoipokea: 224

Minhaju Sunna Juz. 7, uk. 515. 130

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 130

11/25/2014 3:00:40 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Imam Zaynul Abidin (a.s.), Imam Muhammad Baqir (a.s.), al-Aswbagh ibn Nabata al-Handhaliy al-Kufiy, Jariri Adhabbiy, Harith ibn Abdullah al-Hamadaniy al-Kufiy, Sa’d ibn Tarif al-Hadhaliy al-Kufiy, Said ibn Jubair al-Asadiy, al-Kufiy, Salama ibn Kuhayl al-Hadharamiy al-Kufiy, Sulayman alMahramiy al-Kufiy, Aswim ibn Ghamra As-Saluliy al-Kufiy, Abdullah ibn Uthman ibn Khathyam al-Qariu al-Makkiy, Abdur-Rahman ibn Uthman At-Tamiymiy al-Madaniy, Abdur Rahman ibn Asila al-Muradiy na Mujahid ibn Jabr Abu Hajjaj al-Makhzumiy al-Makkiy. Ama wapokezi wa hadithi na wanahadithi, katika karne ya tatu wameipokea wapokezi nane, katika karne ya nne kumi na nne, katika karne ya tano kumi na mbili, karne ya sita wanane, karne ya saba kumi na mbili, karne ya nane na tisa, kumi, karne ya kumi, ishirini na mbili, karne ya kumi na moja, kumi na nne, karne ya kumi na mbili, kumi na tatu, karne ya kumi na tatu, kumi na tatu. Hivi ndivyo alivyoeleza mwenye kitabu cha ‘AbaqatulAnwari’ na katika karne ya kumi na nne waliinakili watu watano miongoni mwa watu waliobobea katika elimu ya hadithi.225 Majina haya na idadi hii ya wapokezi tuliyokutajia hapa kutoka kwa Allak-Hanawiy na al-Amin r.a. ni kutokana na juhudi za watu binafsi, lakini, lau kama kutakuwa na kamati maalumu ya watu wenye elimu na kubobea katika elimu ya hadithi na kufanya utafiti, basi idadi hii itazidi. Kisha ni vipi Ibn Taymiya anadai kwamba hadithi hii imezushwa licha ya kwamba Hakim Nisaburiy ameinakili kwa sanandi tatu, na hapa tutazitaja sanadi hizo: 225

Al-Ghadir Juz. 6, uk. 110-111. 131

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 131

11/25/2014 3:00:40 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Kwanza: Ametusimulia Abu Abbas Muhammad ibn Yaqub, ametusimulia Muhammad ibn Abdur Rahim al-Harawiy Biramla, ametusimulia Abu Swalt Abdus Salaam ibn Salih, ametusimulia Abu Muawiya, kutoka kwa al-A’ma, kutoka kwa Mujahid, kutoka kwa Ibn Abbas r.a., amesema: Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu: “Mimi ni Jiji la elimu na Ali ni lango lake, basi mwenye kulitaka Jiji, aliendee lango (lake).’’ Kisha baada ya hapo Hakim alisema: Sanadi ya hadithi hii ni sahihi, na Bukhari na Muslim hawakuipokea. Abu Swalt ni madhubuti na mwenye kuaminika, kwani nilimsikia Abu Abbas Muhammad ibn Yaqub katika historia akisema: Nilimsikia Abbas ibn Muhammad Ad-Duriy akisema: Nilimuuliza Yahya ibn Mu’in kuhusiana na Abu Swalt al-Harawiy, alisema: Ni madhubuti. Nikasema: Je yeye hakusimulia kutoka kwa Abu Muawiya kutoka kwa al-A’mash: “Mimi ni Jiji la elimu?” Alisema: Alisimuliwa na Muhammad ibn Ja’far al-Faydiy, ambaye ni madhubuti mwenye kuaminika, nilimsikia Abu Nasr Ahmad ibn Sahl al-Faqih al-Qabbaniy aliyekuwa Imam wa zama zake huko Bukharaa, anasema: Nilimsikia Salih ibn Muhammad ibn Habib al-Hafidh akisema: Na aliulizwa kuhusu Abu Swalt al-Harawiy? Alisema: Aliingia Yahya ibn Mu’in kwa Abu Swalt, nasi tukiwa pamoja naye (Yahya), alimsalimia, alipotoka nilimfuata na kumwambia: Hakika yeye anapokea hadithi kutoka kwa al-A’mash kutoka kwa Mujahid kutoka kwa Ibn Abbas kutoka kwa Mtume s.a.w.w: “Mimi ni Jiji la elimu na Ali ni lango lake, basi mwenye kulitaka Jiji, aliendee lango (lake).’’ Alisema: Kwa hakika ameipokea hadithi hii al-Faydiy kutoka kwa Abu Muawiya kutoka kwa al-A’mash kama alivyoipokea Abu Swalt.226 226

Al-Mustadrak Juz. 3, uk.126-127. 132

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 132

11/25/2014 3:00:40 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Ni jambo lililo maarufu kwa Dhahabiy, kwamba nafsi yake hunyongeka kutokana na hadithi zinazoelezea fadhila za Imam Ali (a.s.), ndio maana huonekana anazidisha katika kuzitia kasoro sanadi zake, na wakati mwingine huzipinga hadithi, licha ya kukubali usahihi wa sanadi zake.227 Ushahidi wa tabia yake hiyo ni pale alipotoa maelezo juu ya riwaya ya Hakim iliyotangulia, yeye amesema: “Abu Swalt: Abdur-Rahman, ametusimulia Abu Muawiya kutoka kwa al-A’mash kutoka kwa Mujahid kutoka kwa Ibn Abbas, ikiwa ni yenye kurufaishwa: “Mimi ni Jiji la elimu na Ali ni lango lake, basi mwenye kulitaka Jiji, aliendee lango (lake).’’ Ni kweli, (Nikasema): Bali ni yenye kuzushwa. Akasema: Na Abu Swalt ni madhubuti aliye mwaminifu. (Nikasema): Naapa kwa Mwenyezi Mungu! Si hivyo, si madhubuti wala yeye si mwenye kuaminiwa.”228 Ninasema: Dhahabiy ameihukumu hadithi kuwa ni yenye kuzushwa kwa sababu ya kuwepo Abu Swalt katika moja ya njia zake, na kama anavyosema kuhusu Abu Swalt hapa, kwamba si madhubuti wala si mwenye kuaminiwa, licha ya kwamba katika kueleza wasifu wake amemueleza kinyume na hapa, amesema: “Ni mtu mwema, isipokuwa ni Shia.” Kisha alimnakili Abbas Ad-Duriy akisema: “Nilimsikia Yahya akimthibitisha Abu Swalt.229 Pia Dhahabiy amehukumu juu ya kuzuliwa hadithi ambayo ameipokea Hakim kwa sanadi ya pili kwa njia ya Abdur-Razzaq Aswan-Aniy kwa sanadi yake iliyoishia kwa Jabir ngalia yale aliyoyaeleza mwishoni mwa hadithi ya Ibn Abbas: Mtume A (s.a.w.w.) alimuangalia Ali, akasema: “Wewe ni bwana katika dunia na Akhera…” Almustadrak ala Swahiyhayn, Juz. 3, uk. 128. 228 Al-Mustadrak Juz. 3, uk.126. Talkhiswu Dhahabiy, uk.126. 229 Mizanul-I’tidal Juz. 2, uk. 616. 227

133

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 133

11/25/2014 3:00:40 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

ibn Abdillah, kwa sababu ya kuwemo Ahmad ibn Abdillah ibn Yazid al-Harraniy katika sanadi yake, kwa kusema kuhusiana naye ni dajali aliye muongo.230 Kwa hakika hakuna sababu yoyote kwa Hurraniy kunasibishwa na uongo na udajali, isipokuwa ni kutokana na riwaya yake hii inayoelezea fadhila za Imam Ali (a.s.) Ushahidi wa hayo (ya kwamba kunakili fadhila za Imam Ali (a.s.) kunapelekea kutuhumiwa) ni pale Yahya ibn Mu’in alipomueleza Abu Swalt ya kwamba ni mtu mkweli, Salih ibn Muhammad alilipinga hilo kwa kusema: “Yeye amepokea hadithi isemayo: “Mimi ni Jiji la elimu na Ali ni lango lake, basi mwenye kulitaka Jiji, aliendee lango (lake).” (Ni vipi awe mkweli na wakati amepokea hadithi hii!). Ibn Mu’in alisema: Hii ameipokea al-Faydiy kutoka kwa Abu Muawiya, kutoka kwa al-A’mash kama alivyoipokea Abu Swalt.231 Hii inatubainikia ya kwamba, imani na madhehebu vina athari kubwa kwa wanaoadilisha na kujeruhi wapokezi, na msimamo wa wengi miongoni mwao, ni kuwajeruhi wale wanaosimulia hadithi zinazotaja fadhila za Imam Ali (a.s.) na Ahlulbayt wake. Ni juu ya mtafiti mwenye insafu na uadilifu ambaye anataka kujua uhakika wa mambo kuchunguza maneno yao kuhusiana na Muhammad ibn Ja’far (mpokezi wa hadithi tunayoichambua) ataona kwa uwazi namna maneno yao yanavyogongana, hali inayodhihirisha namna wanavyoamiliana na hadithi zinazokwenda kinyume na itikadi zao juu ya Makhalifa wao, ndio maana Ibn Taymiya na Dhahabiy kudiriki kusema kwamba, hadithi hiyo ni yenye kuzushwa, licha 230 231

Al-Mustadrak (Talkhis Dhahabiy) Juz. 3, uk.126. Kitabu kilichotangulia. 134

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 134

11/25/2014 3:00:41 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

ya kwamba inapatikana kwa njia mbili katika vitabu vyao, njia ya kwanza sanadi yake ni sahihi, na ya pili sanadi yake ni sahihi au ni nzuri. Na hili tutalithibitisha kwa dalili ya wazi, lakini baada ya kukunakilia maneno yao yanayopelekea mgongano na mchanganyiko. 1. Abul Walid Sulayman ibn Khalaf al-Bajiy, aliyefariki mwaka 474A.H., amesema: “Muhammad ibn Ja’far Abu Ja’far al-Kufiy alihamia Fayd, Bukhari amepokea kutoka kwake katika kitabu cha ‘Hayba’ kutoka kwa Muhammad ibn Fadhli, na sijamuona akitajwa pengine mbali ya kitabu hiki, anakaribia kuwa si mwenye kujulikana.”232 Ninasema: Wapokezi wengi wamemtaja al-Faydiy huyu, miongoni mwa wapokezi hao ni: Bukhari katika kitabu chake ‘Tarikhul Kabir,’233 Ibn Habban, aliyefariki mwaka 354A.H., amemtaja katika kitabu cha ‘Athuqat,’234 Ibn Adiy, aliyefariki mwaka 365A.H., Abul Qasim Hibatullah ibn Hasan Allalakaniy, aliyefariki mwaka 418A.H., Hakim Nisaburiy, aliyefariki mwaka 405A.H, katika kitabu ‘al-Mustadraka ala Swayhayn,’235 na al-Khatib Baghdad, aliyefariki mwaka 463A.H, katika kitabu chake ‘Tarikh Baghdad.’236 Ikiwa Abul Walid al-Bajiy alikuwa na sababu ya kusema: “Sijamkuta akitajwa pahala pengine isipokuwa katika kitabu hiki,” kwa sababu huenda vitabu hivi tulivyovitaja hakuvipata, au jicho lake halikuweza kuliona jina lake kwenye vitabu hivyo, basi hana sababu ya kusema: “Anakaribia kuwa si mwenye kujulikana.” Kwani kutofuatilia hali yake haiwi Tahdhibul Kamal Juz. 24, uk. 587. Tarikhul Kabir Juz. 1, uk. 57. 234 Athuqat Juz. 9, uk. 110. 235 Al-Mustadarak ala Swayhayn Juz. 3, uk. 127. 236 Tarikh Baghdad: Juz. 2, uk. 118. 232 233

135

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 135

11/25/2014 3:00:41 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

sababu ya kusema kauli kama hii…, kwani mpokezi huyo alikuwa maarufu, kwani wapokezi mashuhuri wamepokea kutoka kwake, kama vile Bukhari, Yaqub ibn Shayba As-Sudusiy na Muhammad ibn Abdillah al-Hadhramiy, ambaye ni mashuhuri kwa jina la Bimatwiyayn. 2. Ibn Hajar al-Askalaniy amesema: “Katika kitabu cha ‘al-Hiba’ kuna maneno haya: Ametusimulia Muhammad ibn Ja’far Abu Ja’far, na wala haikutajwa nasaba yake, na ambaye ninadhani ni al-Kuwaymisiy, kwani haina shaka kwamba jina la ubaba wake ni Abu Ja’far, kinyume na huyu, na alKuwaymisiy ni madhubuti mwenye kukusanya hadithi, kinyume na huyu, kwani ana hadithi zenye kukhitalifiana.237 Kwa hakika dhana hii si sahihi kabisa, ni rai iliyotanguliwa na hadithi: “Lango la Jiji la elimu.” Wakati al-Faydiy alipokea hadithi hii (ambayo kwayo amejeruhiwa kwa sababu inakwenda kinyume na itikadi zao), baadhi wamejaribu kumtoa katika wapokezi sahihi, au kumtaja kwa yale yasiyofaa. Kwa hakika al-Faydiy ni miongoni mwa masheikh wa Bukhari, na ni katika wapokezi wake walio sahihi, hayo yamebainishwa na wanachuoni, miongoni mwao ni: Ibn Addiy, Abul Qasim Allalakaniy, al-Khatib Baghdadiy, Abul Walid al-Bajiy, Assam-aniy, aliyefariki mwaka 562A.H.238 Ibn Asaki, aliyefariki mwaka 571A.H., Abdul Ghaniy al-Maqdisiy, aliyefariki mwaka 600A.H., Abul Hajjaj al-Mazziy, aliyefariki mwaka 742A.H.239 na Dhahabiy, aliyefariki mwaka 748A.H.240 basi jaribio la kuliondosha jina lake miongoni mwa wapokezi walio sahihi ni jaribio lililoshindwa. Tahdhibu At-Tahdhibi Juz. 9, uk. 96. Al-Ansab Juz. 4, uk. 416. 239 Tahdhibul Kamal Juz. 24, uk. 587. 240 Al-Kashif Juz. 3, uk. 28-29. 237 238

136

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 136

11/25/2014 3:00:41 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Kisha Abu Ja’far Muhammad ibn Ja’far amepokea hadithi katika kitabu ‘al-Hiba’ katika Sahihi Bukhari241 kutoka kwa Muhammad ibn Fudhayl ibn Ghazwan, na Ibn Fudhayl242 huyu, anazingatiwa kuwa ni miongoni mwa masheikh wa al-Faydiy, na wala hakuhesabiwa kuwa ni katika masheikh wa alQuwaymisiy, basi ni vipi Ibn Hajar anadhani kwamba makusudio ya Muhammad ibn Ja’far kuwa ni al-Quwaymisiy?! Ama kauli yake kwamba, hakuna ikhtilafu kwamba ubaba wa al-Quwaymisiy ni Abu Ja’far na si wa al-Faydiy, pia ni kauli isiyo sahihi, kwani Bukhari mwenyewe ameueleza ubaba wa al-Faydiy kwa Abu Ja’far, na kufupisha kwa ubaba huu, na pia al-Khatib Baghdadiy amefanya hivyo, na Abul Walid al-Bajiy na Assam’aniy.243 Hivi ndivyo inavyobainika kwa uwazi kabisa, ya kwamba al-Faydiy ni miongoni mwa masheikh wa Bukhari, na ni katika wapokezi wake walio sahihi, na hakuna sababu ya kuwa na shaka juu ya hilo, kwa hivyo hadithi ni sahihi kwa mujibu wa masharti ya Bukhari. 3. Dhahabiy amesema katika baadhi ya vitabu vyake kwamba hadithi “Lango la Jiji la elimu” ni hadithi iliyozushwa, lakini ameacha kufanya utafiti wa baadhi ya sanadi zake, amejilazimisha kukaa kimya na hakutoa maelezo yoyote kwenye riwaya ya Hakim Nisaburiy kutoka kwenye njia ya Muhammad ibn al-Faydiy, na wala hakueleza wasifu S ahihi Bukhari Juz. 2, uk.159, Kitabu al-Hiba, Babu Hadiyat maa Yukrahu Labsuha, (27), Na.2613. 242 Angalia wasifu wake katika: Tahdhibul Kamal Juz. 26, uk. 293, Na.5548, na angalia wasifu wa Muhammad ibn Ja’far al-Quwaymisiy katika kitabu hicho hicho Juz. 25, uk.13, Na.5122. 243 Angalia katika vitabu vilivyotangulia na namba hizo hizo za kurasa. 241

137

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 137

11/25/2014 3:00:41 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

wake katika kitabu chake ‘Mizanul-I’tidal’ ambacho ni makhsusi kwa wapokezi madhaifu, ili isemwe kwamba katika hadithi kuna yule ambaye ametajwa wasifu wake. Basi ni vipi amehukumu juu ya kuzushwa kwa hadithi?! Kisha Dhahabiy mwenyewe ameipokea hadithi kwa sanadi yake kutoka kwa Suwaid ibn Said, kutoka kwa Sharik, kutoka kwa Salama ibn Kuhayl, kutoka kwa Swunabahiy (AbdurRahman ibn Usayla), kutoka kwa Ali, kutoka kwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), amesema: “Mimi ni Jiji la elimu na Ali ni lango lake, basi mwenye kutaka kuingia katika Jiji, aliendee lango la Jiji.”244 Basi sasa angalia maneno ya wachambuzi wa hadithi kwenye sanadi ya wapokezi wake. — Suwaid ibn Said Muslim amepokea kutoka kwake katika Sahih yake, na Ahmad ibn Hanbal amesema: Natarajia kuwa ni mkweli. Au alisema: Hana tatizo. Ama ibn Mu’in amemzungumzia vibaya. Na Abu Hatim amesema: Ni mkweli, mwingi wa kughushi. Na Ajliy amesema: Ni madhubuti. Na Dhahabiy amesema: Alikuwa ni mwanahadithi na mkusanyaji…, huenda alinasibishiwa hadithi zisizo zake, yeye ni mkweli katika nafsi yake, mwenye kitabu sahihi.245 — Sharik ibn Abdillah Wengi wamesema kwamba ni madhubuti, kama vile, Yahya ibn Mu’in, Ajliy, ibn Habban na ibn Shahin, na zaidi ya 244 245

Mizanul- I’tidal Juz. 2, uk. 251. Mizanul-I’tidal Juz. 2, uk. 248, Wasifu Na. 3621, Tahdhibul Kamal Juz.12, uk. 247, Wasifu Na. 2643. 138

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 138

11/25/2014 3:00:41 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

mtu mmoja wamesema kwamba ni mkweli. Dhahabiy yeye amesema: Ni mkusanyaji wa hadithi, mkweli, mmoja wa maimam, alikuwa ni chombo cha elimu, wenye vitabu vya Sunan wamepokea kutoka kwake na pia Muslim, na Bukhari ametolea ushahidi kwake katika kitabu chake ‘Aljami’i’ na amepokea kutoka kwake mlango unaohusu kunyanyua mikono katika Swala na mengineyo.246 — Salama ibn Kuhayl Ni kweli kwa wanahadithi wote na wote wenye vitabu sita wamepokea kutoka kwake.247 — Swunabahiy Abdur-Rahman ibn Usayla Ni mkweli kwa wanahadithi wote, wote wenye vitabu sita wamepokea kutoka kwake.248 Kwa mujibu wa sanadi hii, ama hadithi hii ni sahihi au nzuri, kwa sababu wapokezi wake wako kati ya madhubuti na wakweli, basi ni vipi idaiwe kwamba ni hadithi iliyozushwa, je, hili si ndio kufuata utashi wa nafsi na kusema pasi na kuwa na elimu?! Na pia kuna mfano mwingine unaobainisha ya kwamba Dhahabiy ameamiliana na hadithi kwa mujibu wa madhehebu yake na si kwa mujibu wa mfumo wa kielimu: Amesema: Amesimulia Tirmidhiy kutoka kwa Ismail ibn Mussa, kutoka kwa Muhammad ibn Umar Ar-Rumiy, kutoka kwa Sharik, hadithi isemayo: “Mimi ni nyumba ya hekima na Ali ni mlango ahdhibul Kamal Juz.12, uk. 462, Wasifu Na. 2736, Mizanul-I’tidal Juz. 2, uk. T 270, Wasifu Na. 3697. 247 Tahdhibul Kamal Juz. 11, uk. 313, Wasifu Na. 2467. 248 Tahdhibul Kamal Juz. 17, uk. 282, Wasifu Na. 3905. 246

139

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 139

11/25/2014 3:00:41 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

wake.” Baada ya Dhahabiy kuinakili hadithi hii amesema: “Simtambui ni nani aliyeizua?” 249 Kwa hivyo yeye anawahukumu mmoja kati ya wapokezi wawili kwa kuizua hadithi hii, ima ni Ismail ibn Mussa, au Muhammad ibn Umar Ar-Rumiy. Basi na tuangalie maneno ya wanachuoni wa elimu ya kuadilisha na kujeruhi wapokezi, wanasema nini juu ya wapokezi hawa: — Muhammad ibn Umar ibn Abdillah Ar-Rumiy Bukhari amepokea kutoka kwake si katika Sahih Bukhari, na Abu Hatim Ar-Raziy, Yaqub ibn Sufiyan al-Farisiy na Abu Muslim Ibrahim ibn Abdillah al-Basiy al-Kajjiy. Mwanafunzi wake, Abu Hatim alisema: Yeye zamani alipokea hadithi isiokubalika250 kutoka kwa Sharik. Na pia kutoka kwake: Ana udhaifu. Abu Zar-at amesema: Ni sheikh ambaye ni mwepesi. Ibn Habban amemueleza kwenye kitabu cha ‘Athuqat’ (wapokezi mathubuti). Kasoro iliyozungumzwa juu ya mpokezi huyu ni kwamba ana ulaini au ni dhaifu, basi hiyo hukumu ya uzushi wa hadithi aliyonasibishwa nayo pamoja na mwanafunzi wake inatoka wapi? — Ismail ibn Mussa al-Fazariy, aliyefariki mwaka 245A.H Wapokezi wakubwa wa hadithi wamepokea kutoka kwake, kama vile Abu Daud, Tirmidhiy, ibn Majah na Bukhari katika 249 250

Mizanul-I’tidal Juz. 3, uk. 668, Wasifu Na. 8002. Kauli hii inabainisha kwamba tatizo liko kwenye matini ya hadithi na sio mpokeaji. 140

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 140

11/25/2014 3:00:41 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

kitabu (Af-al al-ibad), na Muhammad ibn Is-hak ibn Khuzayma na Muhammad ibn Abdillah ibn Sulayman al-Hadhramiy (Mutayyan). Mwanafunzi wake, Mutayyan amesema: Alikuwa mkweli. Abu Hatim amesema: Ni mkweli. An-Nasaiy amesema: Ana tatizo. Ibn Adiy amesema: Wamemkataa kwa sababu ya kubobea katika Ushia,251 ama katika riwaya, watu wamepokea kutoka kwake.252 Je, baada ya maneno haya, ni haki kuhukumiwa uzushi wa hadithi ya mmoja kati ya wapokezi hawa? Na jambo linaloshangaza ni kwa Dhahabiy kumsema vibaya al-Fazariy, licha ya kwamba amemueleza wasifu wake kwa kusema: Ni mkweli ambaye ni Mshia!253 Kisha sio al-Fazariy peke yake aliyepokea riwaya hii kutoka kwa Muhammad ibn Umar Ar-Rumiy, bali wako ambao nao pia walipokea kutoka kwake kama vile Abu Muslim alBasariy al-Kajjiy, na huyu al-Kajjiy amethibitishwa umadhubuti wake katika hadithi na Ad-Daru Qutniy na wengineo, na Dhahabiy amemueleza ya kwamba ni Imam, mwenye kukusanya hadithi na ni sheikh wa zama zake.254 Na kama ikiwa Dhahabiy ameamiliana na hadithi hii kwa mujibu wa madhehebu yake, kwa kuacha kuzichambua baadhi ya sanadi zake -kama ulivyoona - je ndiyo atarajiwe ibn Taymiya ambaye amejaa chuki dhidi ya Imam Ali (a.s.) kuliko yeye, afanye utafiti na uchambuzi wa kielimu wa hadithi hii? Kwa ipi amesema amebobea katika Ushia, kisha wapokezi hawa wakubwa wapoV kee kutoka kwake, akiwemo Bukhari na Ibn Khuzayma, na msimamo wao dhidi ya Mashia ni maarufu 252 Tahdhibul Kamal Juz. 3, uk. 210, Wasifu Na. 491, Mizaul- I’tidal Juz.1, uk. 251, Wasifu Na.958. 253 Al-Kashif Lidhahabiy Juz.1, uk. 129. Na.414. 254 Siyar-a’lamin–Nubalai Juz.13, uk. 423. 251

141

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 141

11/25/2014 3:00:41 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

kweli katu haitarajiwi kufanya hivyo, kwani haoni umuhimu wa kufanya utafiti katika sanadi zake, kwa vile hutosheka anapopitisha macho kwenye riwaya inayoelezea fadhila za Imam Ali (a.s.) kwa kutoa hukumu kwamba ni hadithi iliyozushwa!! Kutokana na msimamo wake huu ndio akamtegemea Ibn Jawziy katika kuzichambua njia kumi na saba za riwaya hizi miongoni mwa njia zake nyingi, amesema: “Ameitaja Ibn Jawziy, na amebainisha ya kwamba njia zake zote ni za kuzushwa na uongo unajulikana katika matini yake.”255 Kitu cha kuzingatia ni kwamba, Ibn Jawziy hakuzichambua njia zote za hadithi,256 hili ni la kwanza. Na la pili, ni kwamba amekwenda njia isiyo sawa katika kutoa hukumu katika baadhi ya njia zake, na amewanakili baadhi ya wanachuoni wa elimu ya upokezi wa hadithi kuwatuhumu baadhi ya wapokezi tuhuma ya kuiba hadithi, na wala hakutuwekea bayana majina ya wanachuoni hao! Na pia kuna wanahadithi wa madhehebu ya Ahlu Sunna wamewajibu Ibn Jawziy, Dhahabiy na wengineo miongoni mwa wale wanaodai kwamba hadithi hii imezuliwa, wanachuoni hao hawakuridhika na kauli yao hiyo ambayo inafunika ukweli, basi sikiliza baadhi ya majibu yao: Mkusanyaji wa hadithi Swalahud Diyn Khalil al-Alaiy Ad-Dimishqiy aliyefariki mwaka 671A.H. amesema: “Ibn Jawziy na wengineo wameihukumu hadithi hii kuwa ni yenye kuzuliwa, na mimi katika hilo kuna shaka…, na ukweli ulivyo ni kwamba njia yake inamalizikia katika daraja ya hadithi nzuri ambayo kwayo hutolewa hoja, na wala haiwi 255 256

Minhaju Sunna Juz. 7, uk. 515. Kwa mfano, iliyopokewa kwa njia ya Muhammad ibn Ja’far al-Faydiy (miongoni mwa wapokezi wa Bukhari), na njia ya Suwaid ibn Said (miongoni mwa wapokezi wa Muslim), na wengineo. 142

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 142

11/25/2014 3:00:41 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

dhaifu seuze kuwa ni yenye kuzushwa.”257 Hadithi hii ina njia nyingi katika Mustadrak al-Hakim, hali yake ya chini zaidi ni kwa hadithi kuwa na asili, basi haifai kusemwa kwamba ni yenye kuzushwa.”258 Na amesema tena katika fatwa ya hadithi hii: “Ni hadithi sahihi, na Ibn Jawziy amekhalifu na kuitaja katika hadithi zilizozushwa, na akasema: Ni ya uongo. Na ukweli ni ule unaopingana na kauli zake hizo mbili, kwani hadithi iko katika kundi la hadithi nzuri, na wala haipandi katika hadithi sahihi, na wala haiporomoki na kufikia katika hadithi za uongo, na maelezo ya bayana yanahitaji muda mrefu, lakini haya ndiyo ya kweli katika hili.”259 Na mwanachuoni al-Muttaqiy al-Hindiy aliyefariki mwaka 975A.H. amesema: “Nilikuwa nikijibu kwa jawabu hili (jawabu la Ibn Hajar) kwa muda mrefu, mpaka pale niliposimama kutokana na usahihishaji uliofanywa na Ibn Jariri wa hadithi ya Ali katika kitabu ‘Tahdhib al-Athar’ pamoja na usahihishaji wa Hakim kwa hadithi ya Ibn Abbas, basi nilifanya istikhara kwa Mwenyezi Mungu (nilimuomba anibainishie), basi nilibainikiwa ya kwamba hadithi imepanda kutoka daraja la uzuri hadi kufikia daraja la sahihi, na Mwenyezi Mungu anajua zaidi.”260 Ninasema: Kutokana na yaliyotangulia ni kwamba, hadithi ‘Lango la Jiji la elimu’ imesahihishwa na Yahya ibn Mu’in, Ibn Jariri, Hakim Nisaburiy, na al-Muttaqiy al-Hindiy. Ama walioiona kuwa ni nzuri ni Salahud Diyn al-Alai na Ibn Hajar. Na pia imebainika ya kwamba, wanaosema kuwa Annaktu albadi’iyat Lissuyutiy uk. 288-289. Lisanul Mizan Juz. 2, uk. 123. 259 Annukat al-Badiiat uk. 289, Kanzul Ummal Juz.13, uk. 148. 260 Kanzul Ummal Juz.13, uk. 149. 257 258

143

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 143

11/25/2014 3:00:41 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

hadithi hii ni batili, hawajaleta ila yoyote zaidi ya kudai tu kwamba ni hadithi ya kutungwa, kama alivyosisitiza hivyo Salahud Diny al-Alaiy Ad-Dimishqiy.261 Ninadhani kwamba kuichambua hadithi hii zaidi ya hivi, tutatoka nje ya utafiti huu, na ambaye anahitaji maelezo zaidi ya wanachuoni kuhusiana na hadithi hii anaweza kurejea vitabu vifuatavyo: ‘Aqabatul-Anwar,’ ‘Nafahatul-Azhar,’ na ‘alGhadir.’

261

Kanzul Ummal Juz.13, uk. 148. 144

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 144

11/25/2014 3:00:41 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

IBN TAYMIYA NA KAULI YA MTUME S.A.W.W “KADHI WENU NI ‘ALI”

I

bn Taymiya anasema: “Ama kauli ya al-Hilliy kwamba Mtume (s.a.w.w.) amesema: ‘Kadhi wenu ni Ali.’ Kwa hakika ukadhi unahitaji elimu na dini, kwa kweli hadithi hii haijathibiti na wala haina sanadi ambayo ina nguvu katika kutolea dalili.”262 Ni vipi anasema: Hadithi hii haijathibiti na wala haina sanadi ambayo ina nguvu katika kutolea dalili, na wakati Ahmad amepokea katika sanadi yake kutoka kwa Abu AbdurRahman: Nimeikuta hadithi hii katika kitabu cha baba yangu ikiwa imeandikwa kwa hati za mkono wake, alisema kumwambia binti yake; Fatima: “Je huridhiki ya kwamba mimi nimekuozesha kwa mtu aliyewatangulia wengine katika Uislamu, na mwenye elimu zaidi na mpole wao zaidi?”263 Na al-Baghwiy amepokea kutoka wa Anas, kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.), ni kwamba amesema: “Kadhi wa ummah wangu ni Ali.” Muhibbud Diyn Tabariy aliyefariki mwaka 694A.H. amesema: al-Baghwiy ameisimulia katika kitabu ‘alMaswabihi’ miongoni mwa hadithi nzuri, na akasema: Na kutoka kwa Umar amesema: “Kadhi wetu ni Ali.” Ameisimulia Assalafiy.’264 Minhaju Sunna Juz. 7, uk. 512-513. Musnad Ahmad Juz. 5, uk. 26. 264 Kitabu kilichotangulia Juz. 5, uk. 113. Mustarak al-Hakim Juz. 3, uk. 305. 262 263

145

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 145

11/25/2014 3:00:41 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Na Ibn Abdu Barri ameisimulia kwa sanadi yake kutoka kwa Abi Qarwa (Urwa ibn al-Harith al-Hamdaniy) amesema: “Nilimsikia Abdur-Rahman ibn Abi Layla, amesema: Umar amesema: ‘Ali ni Kadhi wetu.’” 265 Pia ibn Abdu Barri amepokea kwa sanadi yake kutoka kwa Al-Qama kutoka kwa Abdullah (ibn Masud), amesema: “Tulikuwa tukisimulia ya kwamba, hakika Kadhi wa watu wa Madina ni Ali ibn Abi Talib.”266 Na Ibn Hajar ameielezea katika ‘Fat-hul Bariy’ kauli ya Mtume (s.a.w.w.) isemayo: “Kadhi wa ummah wangu ni Ali.” Na pia alisema wakati alipokuwa akisherehesha kauli ya Umar ibn Khattab iliyopokelewa katika ‘Sahih Bukhar’: “Msomaji wetu (wa Qur’ani) ni Ubayya, na Kadhi wetu ni Ali.”267 Amesema: ameisimulia ikiwa sanadi yake imeishia kwa Swahaba. Na Tirmidhiy na wengineo wameisimulia kwa njia ya Abi Qulaba, kutoka kwa Anas ikiwa ni yenye kurufaishwa wakati wa kumtaja Ubayya. Kisha alisema maneno yafuatayo: “Ama kauli yake: “Na Kadhi wetu ni Ali” imepatikana pia katika hadithi iliyorufaishwa kwa Anas, amesema: “Kadhi wa ummah wangu ni Ali ibn Abi Talib.” Ameisimulia al-Baghwiy. Kutoka kwa Abdur-Razzaq, kutoka kwa Muammar, kutoka kwa Qutada, kutoka kwa Mtume s.a.w.w, amesema: “Mwenye huruma zaidi katika ummah wangu ni Abu Bakr na Kadhi wao ni Ali ibn Abi Talib.” Na pia tumeipokea katika kitaAl-Istiab Juz. 3, uk. 1102. Kitabu kilichotangulia, uk. 1103. 267 Sahihu Bukhar Juz. 5, uk. 149. 265 266

146

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 146

11/25/2014 3:00:41 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

bu ‘Fawaid’ cha Abu Bakr Muhammad ibn Abbas ibn Najih kutoka katika hadithi ya Abu Said al-Khydriy mfano wake. Na Bazzaz amepokea katika hadithi ya Ibn Masud, amesema: “Tulikuwa tukizungumza kwamba kadhi wa watu wa Madina ni Ali ibn Abi Talib r.a.”268

268

Fat-hul Bariy Juz. 8, uk. 167. 147

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 147

11/25/2014 3:00:41 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

IBN TAYMIYA NA HADITHI YA KUPAMBANA DHIDI YA WAVUNJA VIAPO VYA UTIIFU, WAASI NA WAOVU

N

a miongoni mwa mambo yanayobainisha chuki za Ibn Taymiya, ni kupinga riwaya inayoelezea kupambana na wavunja ahadi ya viapo vyao vya utiifu kwa Imam Ali (a.s.), riwaya ambayo imepokewa na wengi miongoni mwa Maswahaba, Matabiina, wapokezi, wanachuoni na waandishi, riwaya hiyo inaeleza hivi: Ni kwamba Imam Ali (a.s.) amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ameniamrisha kupigana dhidi ya watakaovunja viapo vyao vya utiifu, waasi na waovu.’’ Na katika matamshi mengine kutoka kwa mmoja kati ya Maswahaba, amesema: “Mtume (s.a.w.w.) alituamrisha kupigana dhidi ya watu wa aina tatu pamoja na Ali, kupigana dhidi ya watakaovunja viapo vyao vya utiifu, waasi na waovu.” Ama Ibn Taymiya anasema haya: “Ama hadithi iliyopokewa ya kwamba Ali ameamrishwa kupigana dhidi ya watakaovunja viapo vyao vya utiifu, waasi na waovu, kwa hakika hadithi hiyo ni ya kusingiziwa Mtume (s.a.w.w.)”269 Ninasema: “Mtume (s.a.w.w.) kumpa habari Imam Ali (a.s.) ya kwamba apigane na makundi haya matatu ya watu, ni habari ambayo imepokewa kwa sura tofauti, kiasi ambacho haimkiniki kwa mwanahadithi kudai kwamba hadithi hizi nyingi ni zenye kuzushwa au ni za uongo, ila tu ikiwa watu hao watakuwa ni wale ambao hukataa kila ambacho hakiendani na utashi wao. 269

Minhaju Sunna Juz. 6, Uk. 112. 148

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 148

11/25/2014 3:00:41 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Sura ya Kwanza Kauli ya Mtume (s.a.w.w.) kwa wake zake: “Hali itakuwaje, pale mmoja wenu atakapobwekewa na mbwa wa Haw-ab!?” Au kauli yake (s.a.w.w): “Ni nani kati yenu atakayebwekewa na mbwa wa Haw-ab?” Na kauli yake kwao: “Namjua ni nani kati yenu atabwekewa na mbwa wa Haw-ab, huku akiwa anaelekea upande wa Mashariki akiwa katika kikosi cha wanajeshi.” Na kauli yake (s.a.w.w): “Namjua ni ni nani kati yenu atakayekuwa mpanda ngamia mwenye manyoya mengi, na atabwekewa na mbwa wa Haw-ab.” Na kauli yake (s.a.w.w.) kumwambia Aisha: “Kwa hakika mmoja wenu atabwekewa na mbwa wa Haw-ab, na tahadhari usije ukawa ni wewe, ewe Humeyraa (Aisha).” Na kauli yake (s.a.w.w): “Ewe Humeyraa! Ni kama nakuona unabwekewa na mbwa wa Haw-ab, ukiwa unampiga vita Ali, na wewe ukiwa ni dhalimu.” Na kauli yake (s.a.w.w.) kwa Aisha: “Ewe Humayraa! Angalia usije ukawa ni wewe.” Kwa hakika hadithi hizi zimetajwa na wanahadithi pamoja na wanahistoria mahiri, kwa kutaka kujua vitabu vilivyoinakili, basi rejea katika kitabu ‘al-Ghadir,’270 na kwa kweli hatuna muda wa kutosha wa kutaja kitabu kimoja baada ya kingine kutokana na wingi wake. Na sasa tuone kidogo kile lilichopokelewa kuhusiana na jambo hili: Imam Ahmad amesimulia kwa sanadi yake kutoka kwa Qays ibn Abi Hazim, amesema: “Wakati Aisha alipotoka na kufika usiku sehemu yenye maji ya ukoo wa Aamir, mbwa 270

Al-Ghadir Juz. 3, Uk. 268-269. 149

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 149

11/25/2014 3:00:41 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

walimbwekea, akauliza: ‘Haya ni maji gani?’ Walimjibu: ‘Ni maji ya Haw-ab’ alisema: ‘Sitarajii isipokuwa mimi ni mwenye kurejea.’ Baadhi ya watu waliokuwa pamoja naye walimwambia: ‘Bali endelea na safari ili Waislamu wapate kukuona, ili Mwenyezi Mungu apate kuwapatanisha kati yao.’ Alisema: ‘Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema siku moja: Hali itakuwaje pale mmoja wenu atakapobwekewa na mbwa wa Haw-ab!’”271 Na pia Hakim amesema: “Ametusimulia Abu Abdillah Muhammad ibn Yaqub ambaye ni mkusanyaji wa hadithi, ametusimulia Muhammad ibn Abdul Wahhab al-Abdiy, ametusimulia Ya’laa ibn Ubaid, ametusimulia Isma’il ibn Abi Khalid kutoka kwa Qays ibn Abi Hazim, amesema: ‘Wakati Aisha alipofika katika nyumba za watu wa ukoo wa Aamir, mbwa walimbwekea, aliuliza: Ni maji gani haya? Walimjibu: Ni maji ya Haw-ab. Alisema: Sitarajii isipokuwa mimi ni mwenye kurejea. Zubair alisema: Hapana, bado hatujafika, bali endelea na safari ili watu wakuone, na Mwenyezi Mungu atawapatanisha kati yao. Aisha Akasema: Si tarajii ila ni mwenye kurejea, kwani nilimsikia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akisema: Hali itakuwaje, pale ambapo mmoja wenu atakapobwekewa na mbwa wa Haw-ab.”’272 Na tumetangulia kuonesha chini ya anwani “Natija ya Ukhalifa wa Ali’ jinsi Ibn Habban, Hakim, Dhahabiy, ibn Kathir na ibn Hajar, walivyoonesha kuwa hadithi hii ni sahihi, unaweza kurejea huko. 271 272

Musnad Ahmad Juz. 6, Uk. 52 na 97. Kitabu kilichotangulia Juz. 3, Uk. 120. 150

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 150

11/25/2014 3:00:41 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Sura ya Pili Na miongoni mwa yanayojulisha ya kwamba Mtume (s.a.w.w.) amemuamrisha Imam Ali (a.s.) kupigana dhidi ya watakaovunja viapo vyao vya utiifu, waasi na waovu, ni riwaya iliyopokelewa na Ibn Asakir kutoka kwa Abu Swadiq r.a., amesema: “Abu Ayub alifika Irak, al-Azdu alimzawadia ngamia, nikaingia kwake na nikamsalimia, kisha nikamwambia: “Hakika Mwenyezi Mungu amekukirimu kutokana na kusuhubiana na Mtume wake na yeye (Mtume) kuja kwako, basi ni kwa nini nakuona unakabiliana na watu kwa kuwapiga?! Mara unakabiliana na hawa na mara nyingine unakabiliana na hawa?” Alisema: “Hakika Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ametuamrisha tupigane pamoja na Ali, dhidi ya wale wenye kuvunja ahadi ya viapo vyao vya utiifu, kwa hakika tumeshawapiga, na ametuamrisha kupigana pamoja naye (Ali) dhidi ya waasi (Muawiya na jeshi lake), hawa tumeshakabiliana nao, na ametuamrisha kupigana pamoja naye dhidi ya waasi (makhawariji), hawa bado hawajajitokeza.”273 Hakim amepokea kutoka kwa Abi Ayub al-Answariy katika zama za ukhalifa wa Umar ibn Khattab, amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amemuamrisha Ali kupigana dhidi ya watakaovunja viapo vyao vya utiifu, waasi na waovu.’’274 Ibn Asakir amepokea kwa sanadi yake kutoka kwa Abdillah ibn Mas’ud, amesema: “Mtume (s.a.w.w.) alitoka na kufika nyumba ya Ummu Salama, mara akaja Ali, Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Ewe Ummu Salama! Naapa kwa Mwenyezi Mungu! Hakika huyu ni mwenye kupigana dhidi ya watakaovunja viapo vyao vya utiifu, waasi na waovu baada yangu.’’275 Tarikh Dimishqi L-ibn Asakir Juz. 16, uk. 54, Kanzul-Ummal Juz. 11, uk. 352. Mustadrak al-Hakim Juz. 3, uk. 139. 275 Tarikh Madinatu Dimishqi Juz. 42, uk. 470, Tarikh ibn Kathir Juz. 7, uk. 317, 273 274

151

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 151

11/25/2014 3:00:42 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Hadithi hii ina njia nyingi, na imetangulia katika anwani isemayo ‘Natija ya Ukhalifa wa Ali’, na kauli ya baadhi ya watafiti ni kwamba njia hizo zote zinamaanisha kwamba ni hadithi sahihi, au kwa kiwango cha chini kabisa ni hadithi nzuri. Sura ya Tatu Ahmad amesimulia katika Musnadi yake kutoka kwa Abi Rafi’i, ni kwamba Mtume (s.a.w.w.) alimwambia Ali (a.s.): “Kati yako na Aisha kutakuwa na jambo.” Ali akasema: “Je, nitakuwa mimi ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?” Akasema: “Ndio.” Akasema: “Nitakuwa mimi?” Akasema: “Ndio.” Akasema: “Je, mimi ndiye nitakayekuwa muovu wao? Akasema: “Hapana, lakini itakapokuwa hivyo, basi mrejeshe sehemu yake yenye amani.”276 Hii ndio sura halisi ya hadithi hizi mbalimbali zinavyobainisha ya kwamba, Imam Ali (a.s.) atakabiliana na makundi matatu ya watu baada ya Mtume (s.a.w.w.), makundi hayo yote yakiwa ni ya kidhalimu, yatakayotoka dhidi yake utokaji wa uasi dhidi ya Khalifa wao na Imam wao, kutokana na hali hiyo, ndio maana Imam Shafi akasema: “Lau kama si Ali kusingejulikana chochote miongoni mwa hukumu za kupambana na watu waovu.”277

Kanzul-Ummal Juz. 13, uk. 110. Musnad Ahmad Juz. 6, uk. 393, Majmauz Zawaid Juz. 7, uk. 234. 277 Sharhu Nahjul Balagha L-ibn Hadid Juz. 9, uk. 331. 276

152

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 152

11/25/2014 3:00:42 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

IBN TAYMIYA NA KAULI YA MTUME S.A.W.W “MWENYE KUMPENDA ALI, AMENIPENDA MIMI”

A

llamatul Hilliy amenakili hadithi mbalimbali zenye kueleza fadhila za Imam ali (a.s.), na miongoni mwa hizo ni: Mtu mmoja alimwambia Salman al-Farsiy: “Una mapenzi makubwa mno ya kumpenda Ali!” Akasema: “Nilimsikia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akisema: Mwenye kumpenda Ali atakuwa amenipenda mimi, na mwenye kumchukia Ali, atakuwa amenichukia mimi.” Baada ya hapo Ibn Taymiya alisema: “Kumi za mwanzo (miongoni mwa hadithi hizi zinazotaja fadhila za Imam Ali (a.s.) zote ni za uongo.”278 Ibn Taymiya aliyasema hayo aliyoyasema, bila ya kuleta dalili inayothibitisha juu uzushi wa hadithi hizo ikiwemo hadithi hii inayoelezea juu ya kumpenda Ali (a.s)! Basi ndugu msomaji, natuangalie baadhi ya vitabu vilivyoielezea hadithi hii: Hakim amesimulia kutoka kwa Abu Uthman An-Nahdiy, amesema: “Mtu mmoja alimwambia Salman al-Farsiy: “Una mapenzi makubwa mno ya kumpenda Ali!” Akasema: “Nilimsikia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akisema: Mwenye kumpenda Ali atakuwa amenipenda mimi, na mwenye kumchukia Ali, atakuwa amenichukia mimi.” Kisha Hakim akasema: “Hadithi hii ni sahihi kwa mujibu wa masharti ya 278

Minhaju Sunna Juz. 5, uk. 37-42. 153

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 153

11/25/2014 3:00:42 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

masheikh wawili, lakini hawakuisimulia.’’ Na Dhahabiy amelikubali hilo, kwani baada ya kuinakili hadithi hii ameweka herufi ya ‘Khau’ na ‘Miim’279 zikimaanisha ya kwamba hadithi ni sahihi kwa mujibu wa masharti ya Bukhari na Muslim, lakini hawakuisimulia.’’ Taraniy amesimulia kutoka kwa Ummu Salama, ni kwamba amesema: “Nashuhudia kwamba mimi nimemsikia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akisema: Mwenye kumpenda Ali atakuwa amenipenda mimi, na mwenye kunipenda mimi atakuwa amempenda Mwenyezi Mungu, na mwenye kumchukia Ali, atakuwa amenichukia mimi na mwenye kunichukia mimi atakuwa amemchukia Mwenyezi Mungu.”280 Baada ya kunakiliwa hadithi hii, al-Haythamiy amesema: “Sanadi yake ni nzuri.”281 Na kauli hiyo ya Mtume (s.a.w.w.) inatiwa nguvu zaidi kutokana na riwaya aliyoipokea Muslim kutoka kwa Ali (a.s.), amesema: “Naapa kwa Ambaye ameipasua mbegu na kuumba viumbe! Kwa hakika ni maneno madhubuti ya Mtume (s.a.w.w.) kuhusiana nami: Kwa kweli hanipendi mimi isipokuwa Muumini na wala hanichukii isipokuwa mnafiki.’’282 Basi Ibn Taymiya achukue tahadhari sana, ili asije akawa ni miongoni mwa wale wasiompenda Imam Ali (a.s.), kwani ibara nyingi katika vitabu vyake zinaashiria ya kwamba hana mapenzi naye, bali katika moyo wake kuna kitu fulani, zaidi ya hayo anadhihirisha chuki dhidi yake, si tu anadhihirisha Almustadrak Juz. 3, uk. 130. Al-Mu’jamul Kabir Juz. 23, uk. 380. 281 Majmau’ Zawaid Juz. 9, uk. 132. 282 Sahih Muslim, Kitabul- Iman, Mlango: Kuwapenda Maanswari na Ali ni miongoni mwa imani na ni alama yake, na kuwachukia ni katika alama za unafiki. 279 280

154

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 154

11/25/2014 3:00:42 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

chuki kwa Imam Ali (a.s.), bali pia kwa wafuasi wake, kwani amesema kuhusiana na Abu Dharr: “Ama Abu Dharr kuwa ni mkweli zaidi wa watu, hiyo haimaanishi ya kwamba yeye ni bora kuliko wengine…, na ni hadithi ambayo wameisimulia Mashia, ni hadithi dhaifu, bali ni ya kuzushwa, na wala haina sanadi inayoitia nguvu.”283 Ninasema: “Tirmidhiy amesimulia kwa sanadi yake kutoka kwa Abdillah ibn Umar, amesema: “Nilimsikia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu akisema: “Hakuna mtu yeyote aliyebebwa na ardhi na kufunikwa na mbingu, aliye na lahaja ya kweli zaidi kuliko Abu Dharr.” Tirmidhiy baada ya kuinakili riwaya hii amesema: “Hadithi hii ni nzuri, na katika mlango huu kuna hadithi iliyosimuliwa kutoka kwa Abu Dardai na Abu Dharr.”284 Kisha Tirmidhiy amepokea hadithi ambayo ni ndefu kutoka kwa Abu Dharr, kisha akasema: “Hadithi hii ni nzuri iliyo ngeni katika mfumo huu.”285 al-Baniy ameisahihisha hadithi hii (amekubaliana juu ya usahihi wake) na kuiona ni nzuri hadithi hiyo ndefu,286 na katika hadithi hiyo ndefu kuna maneno haya: “Hakuna mtu yeyote aliyebebwa na ardhi na kufunikwa na mbingu, aliye na lahaja ya kweli zaidi kuliko Abu Dharr…” Na Hakim amepokea kutoka kwa Abdur-Rahman ibn Ghanam, amesema: “Nilikuwa pamoja na Abu Dardai, mara akaja mtu kutoka Madina, Abu Dardai akamuuliza yule mtu, akamwambia ya kwamba Abu Dharr amefukuzwa kupelekwa Rabdha, Abu Dardai akasema: Hakika sisi tunatoka kwa MweNinhaju Sunna Juz. 6, uk. 275-276. Sunan Tirmithiy baabu Manaqib Abu Dharr al-Ghaffariy, Hadithi Na. 3827. 285 Kitabu kilichotangulia: Hadithi Na. 3828. 286 Sahihul-Jami’I Aswaghir Juz. 5,uk.124. 283 284

155

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 155

11/25/2014 3:00:42 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

nyezi Mungu, na kwa hakika sisi ni wenye kurejea Kwake, lau kama Abu Dharr angenikata kiungo au mkono, basi nisingemlipizia kisasi baada ya kumsikia Mtume (s.a.w.w.) akisema: “Hakuna mtu yeyote aliyebebwa na ardhi na kufunikwa na mbingu, aliye na lahaja ya kweli zaidi kuliko Abu Dharr.” Dhahabiy amesema: Sanadi yake ni nzuri.”287 Pia ni kwamba hadithi imesimuliwa na wapokeaji mbalimbali, akiwemo Ibn Sa’d,288 Ibn Majah,289 Ahmad ibn Hanbal 290 na wengineo miongoni mwa wale walioisimulia hadithi hii kwa njia mbalimbali na kwa matamshi tofauti. Na Allamah al-Amin amezinakili njia na matamshi ya hadithi hii, basi ambaye ataziangalia njia hizo na wapokezi wake walio wengi atagundua kwamba ni hadithi iliyo sahihi na makini kabisa, ila chuki za kibanu Umayya zilizoko kwa Ibn Taymiya zimempofua macho yake na kumfanya asione ukweli wa hadithi, na kuishia kusema: “Na wala haina sanadi inayoitia nguvu.”

Al-Mustadrak Juz. 3, uk. 344. Tabaqatul Kubra Juz. 4, uk. 228. 289 Sunan ibn Majah Hadihi Na. 156. 290 Musnad Ahmad Juz. 3, uk. 163 na 175. 287 288

156

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 156

11/25/2014 3:00:42 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

IBN TAYMIYA NA KUSHUKA SURA ‘HAL ATAA’ KWA AHLUL-BAYT (A.S.)

I

bn Taymiya amesema: “Miongoni mwa hizo (Hadithi zilizozushwa) ni kauli yake (Allamatul Hilliy): Sura ya Hal-Ataa imeshuka kwa ajili yao (Ahlul-bayt), kwani Sura ya Hal-Ataa ni Sura iliyoteremka Makka kwa mujibu wa makubaliano ya wanachuoni, na Ali alimuoa Fatima baada ya Waislamu kuhamia Madina, na wala hakukutana naye kimwili ila baada ya vita vya Badr, na alimzaa Hasan katika mwaka wa pili wa Hijiria, na akamzaa Husein mwaka wa nne wa Hijiria baada ya kuteremka Sura Hal-Ataa kwa miaka mingi, basi mwenye kusema kwamba imeteremka kwa ajili yao, huo ni uongo ambao haufichiki kwa yeyote yule mwenye elimu ya ushukaji wa Qur’ani na elimu ya kutambua hali za mabwana hawa wakubwa.”291 Na sasa ni wakati wa kujadili maneno yake, kwa nukta zifuatazo: Kwanza: Dai la Ibn Taymiya ya kwamba hiyo ni Sura iliyoteremka Makka kwa mujibu wa makubaliano ya wanachuoni. Hii ni dalili ya wazi kwamba ujinga wake katika maandiko umepita mipaka, au anazungumza uongo kwa makusudi, kwani kwa mujibu wa kauli za wanachuoni walio wengi ni wazi kwamba hakuna makubaliano juu ya Sura hiyo kushuka Makka bali wanasema kwamba ni ya Madina, kwani kuna riwaya mbalimbali za Ahlu Sunna: Amesimulia Mujahid kutoka kwa Ibn Abbas: Ni kwamba 291

Minhaju Sunna Juz. 4, uk. 20. 157

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 157

11/25/2014 3:00:42 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

ni Sura iliyoteremka Madina. Na kauli hii ni ya Mujahid, Qutada, Ikrima, Hasan al-Baswariy al-Kalbiyy na Jabir ibn Zayd.292 Ama kuhusiana na riwaya za Ahlu-Bayt (a.s.), kwa ujumla wake zinasema kwamba iliteremka Madina. Basi hiyo kauli ya pamoja ya wanachuoni ya kwamba imeteremka Makka, iko wapi, ewe sheikh wa Kiislamu wa kibanu Umayya?!! Pili: Tamko ‘Asiira’ linalopatikana katika Sura (au aya zinazozungumzia tukio la ulishaji chakula), ni dalili tosha kwamba Sura iliteremka Madina, kwani kuna maana tatu za wafasiri wa Qur’ani kuhusiana na neno ‘Asiira’: 1. Mateka miongoni mwa washirikina, na kwa maelezo ya Tabariy, maana yake ni mateka wa kivita katika uwanja wa mapambano, huchukuliwa kwa nguvu kwa sababu ya kushindwa kwake, kauli hii ni ya Ibn Abbas, Hasan al-Baswariy, Qutada na Ikrima. Kwa kweli kauli hii inanasibiana na neno ‘Asiir.’ 2. Mfungwa miongoni mwa Waislamu, hii ni kauli ya Mujahid, Atwai na Said ibn Jubair.293 3. Mtumwa, kauli hii ni ya Suddiy.294 Allamatul Alusiy amesema: “Mfungwa kuitwa mateka ni majazi (tawria), kwa sababu ya kule kuzuiliwa kwake kutokutoka, pia ni majazi kuitwa mtumwa, kutokana na hali aliyokuwa nayo hapo mwanzo, na pia pamesemwa ni kwa sababu ya kufanana naye (mtumwa) kwa sababu ya kulazimishwa mambo, na kukosa kufanya kile akitakacho.295 Tafsirul Baghwiy Juz. 5, uk.188. Tafsir ibn Ashur Juz. 29, uk. 343-344. Tafsiru Tabariy Juz.14, uk. 254-255 294 Tafsirul Kabir Lifakhr-Raziy Juz. 30, uk. 245. 295 Ruhul Maaniy Juz. 29, uk. 156.Ruhul Maaniy Juz. 29, uk. 156. 292 293

158

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 158

11/25/2014 3:00:42 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Kwa upande wa Tabariy yeye ametosheka na kutaja kauli mbili za mwanzo, na imepokewa kwa sanadi yake kutoka kwa Hasan al-Baswariy, ni kwamba amesema: “Hawakuwa mateka wao isipokuwa washirikina.”296 Na pia hiyo ndio msimamo wa Sheikh Tusiy ambaye ni miongoni mwa wafasiri wa madhehebu ya Shia Ithna-Asharia.297 Tabraniy yeye amesema: ‘Asiir’ ni kafiri aliyetekwa na mikono ya Waumini, na inasemwa: ‘Asiir’ ni mtumwa.298 Ewe ndugu msomaji, umejionea kwamba makusudio ya ‘Asiir’ ni mshirikina aliyetekwa katika uwanja wa mapambano, kwa kweli kauli hii ndio kauli sahihi zaidi kwa mujibu wa dhahiri ya neno, basi hapa tunamuuliza Ibn Taymiya pamoja na wafuasi wake: - Ni wakati gani Waislamu waliweza kuwashika mateka washirikina? Ilikuwa ni Makka ambapo Waislamu walikuwa wakiteswa, kuonewa na kufukuzwa, au ilikuwa ni Madina, sehemu ambayo walikuwa na nguvu baada ya kuunda dola ya Kiislamu? Ama tukichukua kauli ya wale wanaosema kwamba, maana ya ‘Asiir’ ni mateka waliokuwa Waislamu, maana hii itakuwa sahihi ikiwa kutakuwa na hoja yenye kukubalika ya kwamba ilitokea kulishwa chakula mateka aliyetekwa na maadui, kama alivyosema Tayyibiy.299 Na ni jambo lililo wazi kwamba, hakuna Mwislamu aliyetekwa na washirikina huko Makka, na kujitokeza Mwislamu kutoa chakula chake chote na kumpa yeye. Jamiul Bayan Juz. 14, uk. 255 At-Tibyan fii Tafsiril Qur’an Juz. 10, uk.210. 298 Tafsirul Kabir Lit-Tabariy Juz.6, uk.206. 299 Ruhul Maaniy Juz. 29, uk.155. 296 297

159

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 159

11/25/2014 3:00:42 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Baada ya yote haya, ni vipi isemwe kwamba sura hii kwa ujumla wake imeteremka Makka! Kutokana na hali hii Allamah Tabatabai ameashiria kwa kusema: “Huku kutajwa mateka kuwa ni miongoni mwa waliolishwa na watukufu hawa, ni dalili ya wazi kwamba Sura hii imeteremka Madina, kwani mateka walipatikana baada ya Mtume (s.a.w.w.) pamoja na Waislamu kuhamia Madina, na Uislamu kuweza kuushinda ushirikina, na sio kabla yake.” Tatu: Kuteremka aya hizi juu ya Imam Ali (a.s.) pamoja na Ahlul-Bayt wake kutokana na ukarimu wao wa hali ya juu wa kuwakirimu masikini, yatima na mateka, ni jambo lilitotajwa na wanachuoni wengi wa Kiahlu Sunna na Mu’tazila, achilia mbali wanachuoni wa Kishia, miongoni mwao ni Abu Ja’far al-Iskafiy al-Mu’taziliy, aliyefariki mwaka 240A.H., Ibn Abdu Rabbah, al-Andalusiy al-Malikiy,300 aliyefariki mwaka 328A.H., Abu Bakr ibn Mardawayh,301 aliyefariki mwaka 416A.H., Abu Is’haka Tha’labiy,302 aliyefariki mwaka 428A.H., Abul Hasan alWahidiy,303 aliyefariki mwaka 468A.H., Husein ibn Mas’ud alBaghwiy Shafiy, aliyefariki mwaka 516A.H., Abul Qasim Zamakhshariy al-Mu’taziliy,304 aliyefariki mwaka 538A.H., Fakhru Diyn Raziy Shafiy, aliyefariki mwaka 606A.H., Kadhi Nasru Diyn al-Baydhawiy Shafiy,305 aliyefariki mwaka 685A.H. na Hafidhu Diyn Abdullah ibn Ahmad An-Nasafiy al-Hanafiy,306 aliyefariki mwaka 701A.H. Al-Aqdul Farid Juz. 5, uk. 354. Ad-Durrul Mathur As-Suyutiy Juz. 8, uk. 371. 302 Tafsiru Tha’labiy Juz. 10, uk. 98-102. 303 Asbabun Nuzuli uk. 296. 304 Tafsirul Kashaf Juz.4, uk.670. 305 Tafsirul Kashaf Juz.4, uk.670. 306 Tafsirun Nasafiy Juz. 4,uk. 318. 300 301

160

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 160

11/25/2014 3:00:42 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Na sasa tutaje angalau kauli za wanachuoni watatu kati yao: Ja’far al-Iskafiy amesema pale alipokuwa akitaja fadhila za Imam Ali (a.s): “Yeye ndiye ambaye aliwalisha chakula masikini, yatima na mateka hali ya kuwa akikipenda chakula hicho, na ikamteremkia yeye na mke wake na watoto wake Sura kamili katika Qur’ani.”307 Al-Baghwiy naye amesema: “Imepokewa kutoka kwa Mujahid na Atwai, kutoka kwa Ibn Abbas: (Aya ya ulishaji chakula) imeteremka kwa Ali ibn Abi Talib (a.s.), ni pale alipofanya kazi kwa Myahudi kwa ujira wa shairi, baada ya kukabidhiwa aliisaga thuluthi yake, na kuitayarisha kwa ajili ya chakula, baada ya kuiva na kujitayarisha kula, waliendewa na masikini na kuomba chakula, walitoka na kumpa chakula, kisha wakatayarisha thuluthi ya pili, ilipofikia wakati wa kuiva waliendewa na yatima, akawaomba chakula, basi walimpa, kisha wakatayarisha thuluthi iliyobakia, baada ya kuiva waliendewa na mateka miongoni mwa washirikina, akaomba chakula, na wakampa, basi walishinda na njaa katika siku yao hiyo.’’308 (kwa maoni yake Baghwiy). Na Fakhru Raziy amesema: “Na al-Wahidiy ambaye ni mwenzetu (ni katika Ahlus-Sunna) ameeleza katika kitabu ‘Albaswit’ kwamba iliteremka juu ya Ali (a.s.) na mwenye ‘alKashaf’ miongoni mwa Mu’tazila amekitaja kisa hiki, amepokea kutoka kwa Ibn Abbas r.a., kwamba Hasan na Husein walipata ugonjwa na Mtume (s.a.w.w.) alikwenda kuwajulia hali akiwa pamoja na watu, wakasema: Ewe baba Hasan! Lau kama ungeweka nadhiri kwa watoto wako. Basi Ali, Fatima 307 308

Sharhu Nahjul Balaghah Libn Hadid: Juz. 13, uk. 276, Khutba Na. 238. Tafsirul Baghwiy Juz. 5, uk. 191-192. 161

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 161

11/25/2014 3:00:42 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

na mfanyakazi wao aliyekuwa akiitwa Fidha waliweka nadhiri kwa ajili yao (Hasan na Husein)…, basi Jibril aliteremka na kusema: Ewe Muhammad! Mwenyezi Mungu anakupongeza juu ya watu wako, na hapo akamsomea Sura hii (Hal-Ataa)”309 Suala la kushuka Aya hii kwa Imam Ali pamoja na familia yake ni jambo lililo mashuhuri sana kwa wanachuoni, kwani wameweka bayana juu ya hilo. Mfasiri wa Qur’ani; al-Alusiy baada ya kutaja sababu ya kushuka Sura hii amenakili beti za mashairi yenye kumsifu Imam Ali (a.s): “Ni kwa nini, na mpaka lini, ninalaumiwa kwa sababu ya kumpenda kijana huyu, je Fatimah ameolewa na mwingine asiyekuwa yeye, na asiyekuwa yeye imemteremkia Hal-Ataa?’’310 Ewe ndugu msomaji mpendwa! Baada ya kuyapitia haya na mengineyo, utabainikiwa na kile ambacho Ibn Taymiya kimempelekea kukanusha Sura hii kumteremkia Imam Ali (a.s.) na wanafamilia wake, si kingine, bali chuki iliyoko moyoni mwake, ambayo imemzuia kukubali hoja zilizo wazi, Mwenyezi Mungu anasema:

‫ور‬ ُّ ‫ْصا ُر َو ٰلَ ِكنْ َتعْ َمى ْالقُلُوبُ الَّتِي فِي ال‬ َ ‫َفإِ َّن َھا َال َتعْ َمى ْاألَب‬ ِ ‫ص ُد‬ “Kwani hakika si macho yanayopofuka, lakini zinazopofuka ni nyoyo ziliyomo vifuani.” (Qur’an, 22:46).

309 310

Tafsiru Raziy Juz. 30, uk. 243-244. Ruhul Maaniy Juz. 29, uk. 157. 162

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 162

11/25/2014 3:00:42 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

MJADALA WA IBN TAYMIYA JUU YA SIFA ZA KIPEKEE ZA IMAM ‘ALI (A.S.)

P

indi Ibn Taymiya anaposhindwa kukataa usahihi wa hadithi zinazoelezea fadhila za Imam Ali (a.s.) kutokana na uthabiti wa sanadi zake na wingi wa njia zake, huzua kauli isemayo kwamba, yaliyokuja katika hadithi hizo ni katika fadhila za Ali na si katika mambo yanayomhusu yeye peke yake. Miongoni mwa hadithi hizo ni hii ifuatayo Muslim amepokea kutoka kwa Sa’d ibn Abi Waqqas, amesema: “Muawiya ibn Abi Sufiyan alimuamrisha Sa’d, kwa kusema: Ni kitu gani kinachokuzuia usimtukane Abu Turab (Ali ibn Abi Talib)? Alisema: “Kutokana na kukumbuka mambo matatu aliyomwambia Mtume (s.a.w.w.), katu sitomtukana, kwani kama nitakuwa na jambo moja kati ya hayo napendezeshwa zaidi nalo kuliko kuwa na ngamia mwekundu; nilimsikia Mtume (s.a.w.w.) akimwambia pale alipomuacha asiende vitani, Ali alimwambia Mtume (s.a.w.w): Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Umeniacha pamoja na wanawake na watoto? Mtume (s.a.w.w.) akamwambia: Je, huridhiki kuwa na daraja kwangu, kama vile Harun alivyokuwa kwa Mussa, isipokuwa hakuna Unabii baada yangu? Na nilimsikia akisema siku ya (vita vya) Khaybar: Nitampa bendera mtu anayempenda Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na anayependwa na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Basi tukawa tunasubiria, mara akasema: Niitieni Ali; 163

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 163

11/25/2014 3:00:42 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Alipelekewa huku akiwa na ugonjwa wa macho, basi Mtume (s.a.w.w.) alimtemea mate katika macho yake, na kisha akamkabidhi bendera. Na wakati ilipoteremka aya hii: “Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu.” Mtume (s.a.w.w.) alimuita Ali, Fatima, Hasan na Husein, akasema: Ewe Mola Wangu! Hawa ni Ahlul-Bayt wangu.”311 Ibn Taymiya amesema: “Hadithi hii ya Muslim ni hadithi sahihi, ndani yake kuna fadhila tatu za Ali, lakini si katika mambo yanayowahusu Maimam peke yao, na wala yanayomhusu Ali peke yake, kwani kauli yake pale alipomuacha nyuma kati ya moja ya vita vyake, Ali alimwambia Mtume (s.a.w.w): Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Unaniacha pamoja na wanawake na watoto? Na Mtume (s.a.w.w.) akamwambia Ali: Je, huridhiki kuwa na daraja kwangu, kama vile alivyokuwa Harun kwa Musa, isipokuwa hakuna Unabii baada yangu? Jambo hili si katika mambo yanayomhusu Ali peke yake, kwani Mtume (s.a.w.w.) aliwaacha watu mbalimbali katika mji wa Madina, na hayo madaraka aliyopewa (kubakishwa pamoja na wanawake na watoto) hayakuwa bora zaidi kuliko ya wengine.’’312 Ninasema: Matini ya hadithi hii ni dalili tosha kwamba yale yaliyomo humo yanazingatiwa kuwa ni katika fadhila zake na pia ni katika mambo yanayomhusu yeye peke yake, kwani lau kama si hivyo, basi Sa’d asingetamani kuwa na jambo moja kati ya hayo. Je, hii haimaanishi ya kwamba hakukuwa na Swahaba yeyote aliyekuwa akisifika na sifa S ahihi Muslim Juz. 4, uk. 1871, Hadithi Na. 2404, Kitabu Fadhail Swahaba; Sunan Tirmidhiy Juz. 5, uk. 638, Hadithi Na. 3724, Kitabul Fadhail; Al-Mustadrak Juz. 3, uk. 116. 312 Minhaju Sunna Juz. 5, uk. 24. 311

164

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 164

11/25/2014 3:00:42 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

hizo? Na dalili ya wazi zaidi ni kutokana na maneno ya Mtume (s.a.w.w.) ya kumpa daraja kama ile aliyokuwa nayo Nabii Harun kwa Musa (a.s.), hii inamaanisha kwamba Imam Ali (a.s.) ana sifa zote za Mtume (s.a.w.w.) isipokuwa sifa moja tu, nayo ni Unabii, na hakuna yeyote kati ya Maswahaba mwenye kusifika na sifa hii isipokuwa Imam Ali (a.s.). Ni kweli Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwaachia madaraka Maswahaba mbalimbali katika mji wa Madina pale alipokuwa akienda safari zake, kama alivyosema Ibn Taymiaya, lakini hakuna yeyote aliyepata nafasi na daraja ya kipekee kama aliyoipata Imam Ali (a.s.). Kwa hivyo fadhila hii inazingatiwa kuwa ni katika mambo yanayomhusu Imam Ali peke yake, na hakuna mwingine yeyote anayeshirikiana naye, lakini Ibn Taymiya hafahamu maana hii, au hataki kufahamu kutokana na bahati yake mbaya ya kuamua kuwafuata wale wenye upofu katika ufahamu wao.313 Kwa hivyo Ibn Taymiya amejaribu kwa nguvu zake zote kupotosha maana ya hadithi kwa makusudi yeye mwenyewe na wale wanaomfuata, inashangaza namna anavyodai kwamba fadhila hizo zimezuliwa, au kuzitilia shaka, au kuzishusha daraja yake! (Madai aliyoshindwa kuyatolea ushahidi wala hoja ya msingi!) Upofu wake juu ya Qur’an Kutokana na Mashia kuwa na imani kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ameeleza bayana ya kwamba wenye kustahiki 313

S iku moja Muawiya ibn Abi Sufiyan alimwambia Aqil ibn Abi Talib baada ya kupata upofu wa macho: “Nyini Bani Hashim ni wenye upofu katika macho yenu.” Aqil naye akasema: “Na nyinyi Banu Umayya mna upofu katika ufahamu wenu: al-Aqdul Farid Libn Abd Rabbah al-Andalusiy Juz. 91. 165

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 165

11/25/2014 3:00:42 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

kuwa Makhalifa baada yake ni Imam Ali (a.s.) na kisha watoto wake (a.s.), basi Ibn Taymiya amedai kwamba mwenye kuitakidi kwamba Ukhalifa ni haki ya Ahlul-Bayt (a.s.) peke yao, basi hiyo ni itikadi ya kijahilia ya Kiarabu au Kiajemi. Na sasa yasikilize maneno yake: “Hakuna yeyote aliyesema ya kwamba, mimi nina haki zaidi juu ya jambo hili (Ukhalifa) kuliko Abu Bakr, na wala hakuna aliyesema ya kwamba, fulani ana haki zaidi ya jambo hili kuliko Abu Bakr, bali wale walioathirika na ujahili wa Kiarabu au Kiajemi wamesema: ‘Walio na haki ya kutawala ni watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w.)’, hii ni kwa sababu Waarabu katika zama za kijahilia walikuwa wakiwatawalisha watu wa nyumba za viongozi wao, na hivyo hivyo ndivyo walivyokuwa wakifanya Waajemi, wakiwatawalisha wana wa mfalme.”314 Jambo la kuzingatia hapa, ni kufahamu maana ya Ukhalifa au Uimam, maana yake ni mamlaka ya Mwenyezi Mungu Mtukufu anayompa mja Wake amtakaye, kutokana na uwezo wa mtu huyo. Ndio maana wakati Nabii Ibrahim (a.s.) alipomuomba Mola Wake awajaalie watoto wake wawe Maimam (Viongozi) kama Qur’an inavyosema:

‫اس إِ َمام ًۖا َقا َل َو ِمنْ ُذرِّ َّي ِت ۖي َقا َل‬ ِ ‫َقا َل إِ ِّني َج‬ َ ُ‫اعل‬ ِ ‫ك لِل َّن‬ َّ ‫َال َي َنا ُل َع ْھ ِدي‬ ‫ين‬ َ ‫الظالِ ِم‬ “Hakika Mimi nitakufanya uwe kiongozi wa watu. Akase-

ma: Je, na katika vizazi vyangu pia? Akasema: Ahadi yangu haitawafikia wenye kudhulumu.” (Qur’ani, 2:124). 314

Minhaju Sunna Juz. 6, uk. 455-456. 166

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 166

11/25/2014 3:00:43 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Mwenyezi Mungu hakumkatalia ombi lake hilo isipokuwa kwa wale madhalimu. Kutokana na hali hii kuna suala limejitokeza: Je, inafaa kwa yeyote kusema kwamba Nabii Ibrahim (a.s.) wakati alipomuomba Mwenyezi Mungu awafanye watoto wake kuwa Maimam, ni kwa sababu ya kuathiriwa na athari za kijahilia za Kibebiloni au za Kimisri? Na kama ambavyo tunaona Mwenyezi Mungu Mtukufu anavyoelezea namna anavyowateua Mitume kutoka A.katika A. kizazi cha baadhi ya Mitume, anasema:

ُ‫اق َ ُو َيعْ ق‬ ‫اب‬ ‫وب َج َ​َعو ْل َن َجا َع ْلف َناِي ف ُذِيرِّ َّي ُ ِذت ِرِّه َّي ِتال ُِّنهبُوَّال ُّ َنةب َّ َُوو َة ْال َ ِكو َت ْال ِك َ َت‬ َ ‫اب‬ َ ‫وب َو‬ َ ْ‫َو َو َھ َ ْبو َ َنوا َھ َل ْب ُ َهناإِ َلسْ ُه َحإِس‬ َ ‫اق َح َو َ​َيعْ ق‬ “Na tulimtunukia (Ibrahim) Is’haq na Ya’qub. Na tukajaalia katika kizazi chake Unabii na Kitabu…” (Qur’ani, 29:27).

Na amesema tena katika aya nyingine:

B. B.

َ ْ ْ‫َ َ ْ َر‬ ‫وحً ُنوحً ا َوإِب َْراھِي َم َو ْ َ َج َع ْل َنا ف ُِي ُذرِّ َّيت ِ​ِھ َم ُّا ال ُّنَب َُّو َة‬ ‫َو َل َق ْد َوأَلقرْد َسأ ْل َنا َس ُنلنا ا َوإِب َْراھِي َم َو َج َعلنا فِي ذرِّ َّيت ِ​ِھ َما النبُوَّ ة‬ ۖ ‫اب‬ ‫ْ َ َو ْال ِك‬ َ ۖ ‫اب َت‬ َ ‫َوال ِكت‬ “Na bila ya shaka tulimpeleka Nuh na Ibrahim, na tukaweka katika kizazi chao Unabii na Kitabu…” (Qur’ani, 57:26).

Na pia amesema:

167

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 167

11/25/2014 3:00:43 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

‫ُف‬ َ ‫ُّوب َويُوس‬ َ ‫ان َوأَي‬ َ ‫َو ِمنْ ُذرِّ َّي ِت ِه دَاوُ و َد َو ُس َل ْي َم‬ ۚ ‫ُون‬ َ ‫ُوس ٰى َو َھار‬ َ ‫َوم‬ “Na katika kizazi chake (Nuh) ni Daudi na Sulayman Na Ayub na Yusuf na Musa na Harun.” (Qur’an, 6:84).

Watu wote wanashuhudia kwamba Utume na Uimam vikitoka kwa Mtume huenda kwa kizazi chake kilicho chema. Baada ya haya, inafaa kwa Mwislamu kusema ya kwamba, Mwenyezi Mungu amefanya hivyo kwa kufuata mwenendo wa kijahilia?! Na kitu kingine cha kuzingatia katika nadharia ya ibn Taymiya ni kwamba, Mwenyezi Mungu kujaalia Utume na Uimam kwa vizazi vya Mitume, na kwa Nabii wa Mwisho (s.a.w.w.), ni jambo linalokwenda kinyume na mwenendo wa kijahilia wa Waarabu na Waajemi, kwani Mwenyezi Mungu humpa mamlaka Yake yule ambaye ana uwezo na sifa za kuwa Khalifa, kwa kufanya hivyo ni kipingamizi kwa madhalimu kupewa mamlaka na Mwenyezi Mungu. Kwa maana nyingine ni kwamba, kule mtu kupewa Utume au Ukhalifa kutoka kwa kizazi cha Mtume, haimaanishi mamlaka hayo ameyapata kwa njia ya kurithishana mmoja baada ya mwingine, mfumo huu unatofautiana sana na mfumo wa kurithishana unaofanywa na maraisi na wafalme wa Kiarabu na Wakiajemi, kwani wao mtoto wa mfalme naye huwa mfalme, akiwa ni mwema au muovu. Naapa kwa Mwenyezi Mungu - Na kwa hakika ni kiapo kikubwa lau kama mnajua! Kwa hakika mtu huyu (Ibn 168

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 168

11/25/2014 3:00:43 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

Taymiya), lau angezingatia ujumbe uliomo katika maneno yake, angebainikiwa ya kwamba amekwenda kinyume dhidi ya aya za Qur’ani na hadithi za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na alichokifanya ni kutanguliza rai yake juu ya viwili hivyo (Qur’ani na hadithi), basi akawa ni miongoni mwa walengwa wa aya hii:

‫ﷲ َو َرسُولِ ِه ۖ َوا َّتقُوا‬ ِ َّ ِ‫ِين آ َم ُنوا َال ُت َق ِّدمُوا َبي َْن َي َدي‬ َ ‫َيا أَ ُّي َھا الَّذ‬ ‫ﷲ َّ َسمِي ٌع َعلِي ٌم‬ َ َّ‫ﷲ ۚ إِن‬ َ َّ “Enyi mlio amini! Msitangulie mbele ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na mcheni Mwenyezi Mungu, hakika ­Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona. (Qur’ani 49:1).

169

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 169

11/25/2014 3:00:43 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1.

Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thelathini

2.

Uharamisho wa Riba

3.

Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza

4.

Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili

5.

Hekaya za Bahlul

6.

Muhanga wa Imamu Husein (A.S.)

7.

Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.)

8.

Hijab vazi Bora

9.

Ukweli wa Shia Ithnaashari

10. Madhambi Makuu 11.

Mbingu imenikirimu

12. Abdallah Ibn Saba 13. Khadijatul Kubra 14. Utumwa 15. Umakini katika Swala 16. Misingi ya Maarifa 170

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 170

11/25/2014 3:00:43 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

17. Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia 18. Bilal wa Afrika 19. Abudharr 20. Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu 21. Salman Farsi 22. Ammar Yasir 23. Qur'an na Hadithi 24. Elimu ya Nafsi 25. Yajue Madhehebu ya Shia 26. Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu 27. Al-Wahda 28. Ponyo kutoka katika Qur'an. 29. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii 30. Mashukio ya Akhera 31. Al Amali 32. Dua Indal Ahlul Bayt 33. Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. 34. Haki za wanawake katika Uislamu 35. Mwenyeezi Mungu na sifa zake 36. Kumswalia Mtume (s) 37. Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) 38. Adhana. 171

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 171

11/25/2014 3:00:43 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

39. Upendo katika Ukristo na Uislamu 40. Tiba ya Maradhi ya Kimaadili 41. Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu 42. Kupaka juu ya khofu 43. Kukusanya swala mbili 44. Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara 45. Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya 46. Kusujudu juu ya udongo 47. Kusherehekea Maulidi Ya Mtume (s) 48. Tarawehe 49. Malumbano baina ya Sunni na Shia 50. Kupunguza Swala safarini 51. Kufungua safarini 52. Umaasumu wa Manabii 53. Qur’an inatoa changamoto 54. as-Salaatu Khayrun Mina -'n Nawm 55. Uadilifu wa Masahaba 56. Dua e Kumayl 57. Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu 58. Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake 59. Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata

172

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 172

11/25/2014 3:00:43 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

60. Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mtume ­Muhammad (s) 61. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza 62. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili 63. Kuzuru Makaburi 64. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza 65. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili 66. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu 67. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne 68. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano 69. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita 70. Tujifunze Misingi Ya Dini 71. Sala ni Nguzo ya Dini 72. Mikesha Ya Peshawar 73. Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu 74. Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliyonyooka 75. Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake 76. Liqaa-u-llaah 77. Muhammad (s) Mtume wa Allah 78. Amani na Jihadi Katika Uislamu 79. Uislamu Ulienea Vipi? 80. Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) 173

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 173

11/25/2014 3:00:44 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

81. Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) 82. Urejeo (al-Raja’a ) 83. Mazingira 84. Utokezo (al - Badau) 85. Hukumu ya kujenga juu ya makaburi 86. Swala ya maiti na kumlilia maiti 87. Uislamu na Uwingi wa Dini 88. Mtoto mwema 89. Adabu za Sokoni 90. Johari za hekima kwa vijana 91. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza 92. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili 93. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu 94. Tawasali 95. Imam Mahdi katika Usunni na Ushia 96. Hukumu za Mgonjwa 97. Sadaka yenye kuendelea 98. Msahafu wa Imam Ali 99. Ngano ya kwamba Qur’ani imebadilishwa 100. Idil Ghadiri 101. Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu 102. Hukumu zinazomhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi 174

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 174

11/25/2014 3:00:44 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

103. Huduma ya Afya katika Uislamu 104. Sunan an-Nabii 105. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) 106. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) 107. Shahiid Mfiadini 108. Kumswalia Nabii (s.a.w) 109. Ujumbe -Sehemu ya Kwanza 110. Ujumbe - Sehemu ya Pili 111. Ujumbe - Sehemu ya Tatu 112. Ujumbe - Sehemu ya Nne 113. Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu 114. Hadithi ya Thaqalain 115. Maarifa ya Kiislamu 116. Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza 117. Ukweli uliopotea sehemu ya Pili 118. Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu 119. Ukweli uliopotea sehemu ya Nne 120. Ukweli uliopotea sehemu ya Tano 121. Johari zenye hekima kwa vijana 122. Safari ya kuifuata Nuru 123. Fatima al-Zahra 124. Myahudi wa Kimataifa 175

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 175

11/25/2014 3:00:44 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

125. Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi 126. Visa vya kweli sehemu ya Kwanza 127. Visa vya kweli sehemu ya Pili 128. Muhadhara wa Maulamaa 129. Mwanadamu na Mustakabali wake 130. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) 131. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) 132. Khairul Bariyyah 133. Uislamu na mafunzo ya kimalezi 134. Vijana ni Hazina ya Uislamu. 135. Yafaayo kijamii 136. Tabaruku 137. Taqiyya 138. Vikao vya furaha 139. Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 140. Visa vya wachamungu 141. Falsafa ya Dini 142. Azadari-Kuhuzunika na Kuomboleza 143. Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah 144. Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu 145. Kuonekana kwa Allah 176

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 176

11/25/2014 3:00:44 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

146. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) 147. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) 148. Ndugu na Jirani 149. Ushia ndani ya Usunni 150. Maswali na Majibu 151. Mafunzo ya hukmu za ibada 152. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1 153. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2 154. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 155. Abu Huraira 156. Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. 157. Mazingatio kutoka katika Qur’an - Sehemu ya Kwanza 158. Mazingatio kutoka kaitka Qur’an - Sehemu ya Pili 159. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza 160. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili 161. Qur’ani Tukufu – Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili 162. Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) 163. Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani 164. Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu 165. Uislamu Safi 166. Majlisi za Imam Husein Majumbani 177

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 177

11/25/2014 3:00:44 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

167. Mshumaa. 168. Uislam wa Shia 169. Amali za Makka 170. Amali za Madina 171. Asili ya Madhehebu katika Uislamu 172. Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi 173. Ukweli uliofichika katika neno la Allah 174. Uislamu na Mifumo ya Uchumi 175. Umoja wa Kiislamu na Furaha 176. Mas’ala ya Kifiqhi 177. Jifunze kusoma Qur’ani 178. As-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah 179. Hayya ‘Alaa Khayri’l-’Amal Katika Adhana 180. Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura 181. Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na Ramadhani) 182. Uadilifu katika Uislamu 183. Mahdi katika Sunna 184. Jihadi ya Imam Hussein (‘as) 185. Kazi na Bidii ni njia ya maendeleo 186. Abu Talib – Jabali Imara la Imani 187. Ujenzi na Utakaso wa Nafsi

178

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 178

11/25/2014 3:00:44 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

188. Vijana na Matarajio ya Baadaye 189. Usalafi – Historia yake, maana yake na lengo lake 190. Ushia – Hoja na Majibu 191. Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) 192. Maombolezo – Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) 193. Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu 194. Takwa 195. Mwonekano wa Upotoshaji katika Hazina ya Kiislamu 196. Amirul Muuminina (‘as) na Makhalifa 197. Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.) 198. Kuelewa Rehma ya Mwenyezi Mungu 199. Mtazamo kuhusu msuguano wa kimadhehebu 200. Upotoshaji Dhahiri katika Turathi ya Kiislamu 201. Nchi na Uraia – Haki na wajibu kwa Taifa 202. Mtazamo wa Ibn Taymiyyah kwa Imam Ali (a.s.) 203. Uongozi wa kidini – Maelekezo na utekelezaji wa Kijamii

179

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 179

11/25/2014 3:00:44 PM


Mtazamo wa Ibn Taymiyyah Juu ya Imam Ali (a.s.)

KOPI NNE ZIFUATAZO ZIMETAFSIRIWA KWA LUGHA KINYARWANDA 1.

Amateka Na Aba'Khalifa

2.

Nyuma yaho naje kuyoboka

3.

Amavu n’amavuko by’ubushiya

4.

Shiya na Hadithi

180

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 180

11/25/2014 3:00:44 PM


MUHTASARI

181

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 181

11/25/2014 3:00:44 PM


MUHTASARI

182

01_IBN TAYMIYYAH_25_Nov_2014.indd 182

11/25/2014 3:00:44 PM


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.