Muhtasari wa sifa bainifu za mtume muhammad (saww)

Page 1

MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW) (A Glimpse of the Character Traits of the Prophet Muhammad [s])

Kimeandikwa na: Sayyid Abul Fadhl Mujtahid Zanjani

Kimetarjumiwa na: Salman Shou

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 1

6/18/2016 2:39:59 PM


©haki ya kunakili imehifadhiwa na: Al-Itrah Foundation ISBN: 978 - 9987 – 17 – 037 – 1 Kimeandikwa na: Sayyid Abul Fadhl Mujtahid Zanjani Kimetarjumiwa na: Salman Shou Kimeharirirwa na: Al Haj Ramadhani S. K. Shemahimbo Kimesomwa-Prufu na: Ustadh Hemedi Lubumba Selemani Kimepitiwa na: Al Haj Mujahid Rashid Kimepangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation Toleo la kwanza: Novemba, 2016 Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation
 S.L.P. - 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: www.alitrah.info

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 2

6/18/2016 2:39:59 PM


Yaliyomo Dibaji.............................................................................1 Neno la mchapishaji......................................................2 Utangulizi......................................................................4 Utoto.............................................................................5 Chini ya malezi ya Abdul-Muttalib...............................9 Chini ya malezi ya Abu Talib......................................11 Akifanya kazi kama mchunga kondoo........................14 Kuongoza msafara wa biashara..................................17 Msimamo wake kuhusu wanaokandamizwa...............19 Kuhusiana na familia yake..........................................22 Kuhusu watumwa wake..............................................29 Unadhifu.....................................................................34 Usamehevu..................................................................37

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 3

6/18/2016 2:39:59 PM


Mipaka ya Sharia........................................................40 Ibada............................................................................44 Kujinyima (Zuhd)........................................................54 Umadhubuti.................................................................57 Heshima juu ya maoni ya watu...................................66

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 4

6/18/2016 2:39:59 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬

DIBAJI

K

itabu hiki ni toleo la Kiswahili la taasisi ya Al Itrah Foundation. Chapisho lake limelenga kukidhi ­mahitaji ya kiroho ya zama hizi pamoja na Ubongo na fikra zinazokuwa za Muislam. Jitihada kubwa zimefanywa na Taasisi kuweka chapisho hili la Kiswahili katika msingi wa haki na wenye kukubalika katika Uislam. Unaombwa kwa Taadhima ukisome kitabu hiki katika malengo yaliyokusudiwa. Pia Unaombwa kuwasilisha kwetu maoni yako huru juu ya chapisho letu hili, jambo ambalo tutashukuru sana. Kutangaza ujumbe wa Uislam ni kazi ambayo inahitaji ushirikiano wetu sote. Taasisi inakuomba kuungana na kushirikiana kama ilivyoagizwa katika aya ya Qur’an: (Surat Saba’ 34:46). Na rehma za Allah ziwe juu yako. Wako katika Uislam Al Itrah Foundation Barua Pepe: alitrah@yahoo.com SMS: +255 778 300 140 1

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 1

6/18/2016 2:39:59 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬

NENO LA MCHAPISHAJI

K

itabu ulichonacho mikononi mwako chanzo chake ni makala kutoka kwenye jarida liitwalo, Message of Thaqalayn, toleo la 44, Majira ya Baridi 1432/2011 kwa la lugha ya Kiingereza.

Mwandishi wa makala hii anazungumzia kwa ufupi wasifu wa Mtukufu Mtume Muhammad 3 akijikita zaidi katika mwenendo wake. Kuna baadhi ya waandishi wasio Waslamu ambao kwa makusudi wamepotosha sio tu historia ya Uislamu bali hata historia ya maisha ya Mtume wetu Mtukufu. Hivyo, mwandishi wa makala hii anajaribu kuonesha udhaifu wa waandishi hao na kwa ufupi kuelezea mwendo halisi wa Mtukufu Mtume 3 na sifa zake bainifu. Tumeiona makala hii ni yenye manufaa makubwa, hivyo, tukaamua kuifanya kuwa kijitabu kwa ajili ya wasomaji wetu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili, kwani huu ni wakati wa sayansi na tekinolojia ambapo ngano, hadithi za kale na upotoshaji wa historia ni vitu ambavyo kwa sasa havina nafasi katika akili za watu. 2

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 2

6/18/2016 2:39:59 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

Tunamshukuru ndugu yetu Salman Shou kwa kutarjumi makala hii kwa lugha ya Kiswahili, pia tunawashukuru wale wote waliosaidia kwa njia moja au nyingine mpaka kuwezesha kitabu hiki kuchapishwa. Allah Mwenye kujazi awalipe wote malipo mema duniani na Akhera pia. MCHAPISHAJI AL-ITRAH FOUNDATIONL DAR ES SALAAM

3

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 3

6/18/2016 2:39:59 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬

Utangulizi

T

angu mwanzo wa Uislamu hadi sasa, waandishi wa wasifu, wanahistoria, na wasimuliaji wa hadithi wamekusanya taarifa zenye utondoti kuhusu maisha ya Mtukufu Mtume 4 katika maelfu ya vitabu vyao na makusanyo yao, na hivyo wameweka vyanzo vyenye taarifa nyingi na zenye thamani ambazo zinaweza kufikiwa na watafiti. Hata hivyo, ndani ya vingi ya vitabu hivi sifa za Mtukufu Mtume 4 hazikubainishwa katika mtiririko unaofaa bali badala yake ziko katika mpango usio mzuri hasa. Kwa hiyo, inakuwa sio rahisi kuzifahamu sifa hizi. Zaidi ya hayo, kwa kuwa kazi nyingi miongoni mwa kazi hizi zimeandikwa katika lugha ya Kiarabu, haiwezekani kwa wale wasiojua Kiarabu kuweza kuzifikia na kuzijua sifa na tabia hizi. Mtindo wa maisha wa kiteknolojia wa zama za leo unakuza tatizo hili kwa sababu badala ya kuweka muda na fursa zaidi kwa wanadamu, juu ya matarajio yote, umesababisha kipingamizi cha muda na umewazuia watu katika kutumia muda kwa kusoma vitabu hivi vyenye maelezo ya kina. Kwa sababu hii, na kwa kuthamini umuhimu wa 4

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 4

6/18/2016 2:39:59 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

mada hii iliyopo mkononi, mwandishi wa makala hii, wakati anapokiri mapungufu ya elimu yake, atatafuta kuweka muhtasari kwa ufupi, utakaoweza kufikiwa na wasomaji kuhusu namna Mtukufu Mtume 4 alivyoishi. Rumi anasema: “Kama huwezi kunywa maji ya bahari yote, kunywa kidogo chake ili kukata kiu yako.�

Juhudi zimefanywa kutumia taarifa ambazo zinaendana na yale ambayo yanakubaliwa na wote, au yanayojulikana kwa mapana miongoni mwa wanahistoria na wasimulizi wa hadithi wa kuaminika. 1.

Utoto

Baba yake Muhammad, `Abdullah, alifariki dunia akiwa bado kijana akiwa mbali na mahali alipozaliwa na mbali na ndugu zake, na bila kujua kwamba mke wake alikuwa anatarajia kujifungua na kwamba alikuwa anaacha urithi wenye thamani kwa ajili ya dunia ya wanadamu. Abdullah alikuwa mtoto anayependwa sana miongoni mwa watoto wanamume wa `Abd alMuttalib, ambaye alitoa sadaka ngamia mia moja kwa ajili yake na akagawa nyama miongoni mwa mafukara. Abdullah hakurudi kutoka kwenye safari yake ya kibiashara huko Syria. Alifariki dunia hapo Madina siku 5

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 5

6/18/2016 2:39:59 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

chache baada ya kuugua na alizikwa ndani ya nyumba ya mtu wa kabila la Banu Najjar (Daar al-Naabighah). Abd al-Muttalib alifadhaika sana juu ya msiba huu wa kuondokewa lakini huzuni yake kubwa na kuvunjika moyo kwake kulitulizwa kwa namna fulani na mjukuu wake aliyezaliwa kipindi hicho, kumbukumbu pekee ya Abdullah aliyobaki nayo. Alifarijika na kupata utulivu wa akili kwake huyo na alikuja kumpenda mtoto huyo kwa shauku kubwa. Mnamo siku ya saba baada ya kuzaliwa mtoto huyo, alimpa jina la Muhammad (mwenye kusifiwa). Jina hili lilikuwa la nadra miongoni mwa Waarabu wa zama hizo. Inataarifiwa kwamba baada ya Abdul-Muttalib kuulizwa kwamba kwa nini alimwita mjukuu wake jina hilo, alijibu: “Nilifanya hivyo kwa kutamani kwamba mjukuu wangu angetukuzwa na Mwenyezi Mungu huko Peponi na wanadamu hapa duniani.”1 Ilionekana kama vile alikuwa anajua kwa ndani hatima ya mjukuu wake, na jina la Muhammad, ambalo lilikuwa linamfaa mjukuu wake lilifunuliwa na Mungu. Ilikuwa ni desturi na kawaida ya Waarabu ambao waliishi mijini kuwapeleka watoto wao kwa wanawake wa Kibedui walioajiriwa kunyonyesha mtoto wa 1

Al-Sirah al-Halabiyyah, Ali bin Burhan al-Din al-Halabi, Juz. 1, uk. 93 6

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 6

6/18/2016 2:39:59 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

mwingine. Iliaminika kwamba mtoto akikulia kwenye mazingira ya jangwa yaliyo huru na ya kiafya yangeweza kuwa na athari kubwa katika kusaidia makuzi ya kimwili na kiakili na pia kuwa na ufasaha mzuri wa kujieleza na ujasiri kwa mtoto. Kwa hiyo, Abd al-Muttalib alimkabidhi Muhammad mdogo kwenye uangalizi wa Halimah binti wa Abdullah bin Harith, ambaye alikuwa wa kabila la kiungwana la Banu Sa`d. Muhammad 4 aliishi kwa takriban miaka 6 katika kabila hili, na jinsi wakati ulivyopita, ndivyo alivyopata makuzi mazuri ya kimwili na kiakili pia. Alikomaa zaidi katika kila hali kuliko wengine wenye umri kama wa kwake. Alikuwa msafi zaidi, mwenye furaha zaidi, na alikuwa na ukarimu zaidi kuliko watoto wengine wote. Akiwa na umri wa miaka sita, Halimah alimrudisha Muhammad kwa mama yake. Bibi huyu mtukufu alikuwa bado anaomboleza kifo cha mume wake mpendwa na kufikiria kuhusu mtoto wake mmoja tu ambaye ni yatima, ni hali iliyompa huzuni sana moyoni mwake. Ili kuweza kuonesha uthabiti, kwa lengo la kupunguza huzuni yake kubwa, na kuzuru tena kaburi la mume wake mpendwa, ambaye alimwacha siku chache tu baada ya ndoa yao, alisafiri safari ndefu ya kwenda

7

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 7

6/18/2016 2:39:59 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

Madina (wakati huo ikiitwa Yathrib), katika safari hiyo aliandamana na mwanawe mpendwa. Muhammad alikwenda na mama yake ili na yeye akaweze kutoa machozi kwenye kaburi la baba yake na kumhurumia mama yake, kwa kuwa alikwisha nyang`anywa mpapaso wa mahaba, tabasamu, na matunzo. Amina alikaa hapo Madina kwa mwezi mzima, na kila siku alikuwa anakaa karibu ya kaburi la mume wake na kuutuliza moyo wake uliokuwa unaumia kwa kupitia machozi yake. Mandhari hiyo ya kuhuzunisha ilikaa katika kumbukumbu ya Muhammad 4. Baadaye, wakati wa kuhama kutoka Makkah kwenda Madina, alipokuwa anapita kwenye mitaa ya Madina, aliitambua nyumba moja na akasema kwamba aliwahi kuwa humo akiwa na mama yake na ilikuwa ni hapo ambapo baba yake alizikwa.2 Huzuni kubwa na pigo zito alilolipata katika hatua ya mapema sana ya ndoa yake ilisababisha kifo cha mapema cha Amina. Akiwa safarini kurudi Makkah, aliugua na alifariki dunia akiwa sehemu iitwayo Abwa`. Sasa Muhammad alikuwa ni yatima kamili. Baada ya kifo cha mama yake, ambaye uwepo wake, upendo, na matunzo yake alivyokuwa anavihitaji sana, moyo laini na mwepesi kuhisi wa mtoto wa miaka sita ukawa wenye kuomboleza sana. Moyo wake mtambuzi ulizidiwa na   Al-Sirah al-Halabiyyah, Ali bin Burhan al-Din al-Halabi, Juz. 1, uk. 95

2

8

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 8

6/18/2016 2:39:59 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

huzuni isiyosahaulika. Imeandikwa kwamba baada ya miaka 55, akiwa katika safari ya kwenda kutekeleza Hijja ya fidia au Umra (Umrat al-qada), Muhammad alipita kaburini kwa mama yake, ambapo alisimama na akalia sana kiasi kwamba wale waliokuwepo hapo nao pia walilazimika kutoa machozi. Inasemekana kwamba hiyo ilikuwa ni kumbukumbu ya upendo wa mama yake ndiyo iliyomfanya alie sana.3 2.

Chini ya Malezi ya Abdul-Muttalib:

Umm Ayman (au Barakah, mwanamke mashuhuri Mwafrika ambaye aliheshimiwa sana na Mtume adhim), alimchukua na akampeleka Madina na akamwacha kwa Abdul-Muttalib. Kumuona mjukuu wake akiwa ameondokewa na mama; hali ya huruma, huba na mapenzi kwa mjukuu wake kwa Abdul-Muttalib iliongezeka. Akampenda Muhammad 4 zaidi kuliko hata watoto wake wote mwenyewe,4 na hakumwacha kamwe. Hata pale baraza la waungwana wa kabila la Quraysh lilipofanyika katika Msikiti Mtakatifu (Masjid al-Haraam), Abdul-Muttalib alikuwa akiketi sehemu iliyo mashuhuri na alimruhusu Muhammad 4 aketi kwenye kochi, na wakati wowote ami zake walipotaka   al-Sirah al-Nabawiyyah, Zaini Dahlan, Juz. 1, uk. 125   al-Sirah al-Nabawiyyah, Zaini Dahlan, Juz. 1, uk. 29

3 4

9

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 9

6/18/2016 2:39:59 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

kumfukuza mtoto kutoka kwenye kiti cha baba yake, alikuwa akiwakataza kwa kusema, “Mwacheni mwanangu.” Alitabiri, kutokana na msukumo au utambuzi wake, kwamba mjukuu wake atakuwa na mustakabali angavu sana baadaye.5 Hata hivyo, kile kiasi cha mapenzi na huba iliyooneshwa na babu yake haikuweza kujaza pengo lililoachwa na wazazi wake. Muhammad 4 alionesha huzuni yake mara nyingi sana katika muktadha wa somo la wema kama ifuatavyo: “Gonga vichwa vya mayatima na waheshimu wale ambao wapo mbali na makwao, kwa sababu mimi nilikuwa yatima nilipokuwa mtoto, na kama mtu mzima, nilipata mateso makali kwa maumivu ya kuwa mbali na nyumbani.”6

Ili kuweza kuwapa moyo wengine katika kulisaidia kundi hili la hali ya chini katika jamii, alisema: “Yeyote atakayemtunza yatima na akamlea hadi anakuwa mtu mzima atakuwa karibu nami peponi.”7

Iliamuriwa mapema bila utata kwamba hatua hii mpya ya maisha yake, ambamo takriban alipata amani na utulivu wa akili, isingedumu muda mrefu.   al-Sirah al-Nabawiyyah, Zaini Dahlan, Juz. 1, uk. 129   al-Sirah al-Halabiyyah, Juz. 1, uk. 129 7   Sahih al-Muslim, Abul Husayn Muslim bin al-Hallaj al-Qashayri alNisaburi, Juz. 8, uk. 222 5 6

10

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 10

6/18/2016 2:40:00 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

Alipokuwa na umri wa miaka minane, babu yake alifariki dunia, na Muhammad 4 akapatwa na huzuni zaidi. Aliusindikiza mwili wa Abdul-Muttalib kimyakimya huku akitokwa machozi.8 Hivyo Mtukufu Mtume 4 alijaaliwa uwezo wa kustahamili kiwango kikubwa cha matatizo na mateso ambayo yangemtokea wakati wa misheni yake ya kitume. Ilikuwa muhimu kwamba Mtume apaswe kuonja huzuni na maumivu tangu kipindi cha utoto wake ili akuze moyo wa uvumilivu na subira. 3.

Chini ya Malezi ya Abu Talib

Abdul-Mutallib alimkumbatia Mtukufu Mtume 4 akiwa kwenye kitanda alichofia, akilia, na akamgeukia mwanawe mkubwa Abu Talib, ambaye alikuwa aje kuwa mrithi wa baba yake na mtemi wa ukoo wa Hashim. Abu Talib alikuwa mtu mwenye kuheshimika sana miongoni mwa makabila ya Waarabu. Abd al-Mutallib alimpa maelekezo yake ya mwisho, akisema: “Kumbuka, mwanangu, kwamba baada yangu unatakiwa kumtunza na kumsaidia johari huyu ambaye alikosa uwepo wa baba yake na ambaye hakufaidi upendo wa mama yake. Mlinde kama wa kwako na umkinge mbali na madhara   al-Sirah al-Halabiyyah, Juz. 1, uk. 134

8

11

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 11

6/18/2016 2:40:00 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

yoyote. Simjui yeyote miongoni mwa Waarabu kama baba yake ambaye alifariki dunia akiwa katika ujana wake, akiwa mbali na nyumbani kwake na bila ya kutimiza matamanio yake ya ujana. Mama yake ambaye alifariki akiwa katika huzuni kubwa, kukata tamaa na simanzi, pia alimwacha peke yake. Utakubali wosia wangu wa mwisho?”

Abu Talib alikubali kwa kusema: “Ndiyo baba, na Mungu awe Shahidi.”

Kisha Abu Talib akaweka mkono wake juu ya mkono wa baba yake na akatoa kiapo cha utii kwa baba yake ambacho kwacho Abdul-Muttalib akajibu kwa kusema: “Sasa imekuwa rahisi kwangu mimi kufariki.” Katika kumuaga mjukuu wake, alimshikilia karibu na kifua chake, akamnusa na kumbusu na akavuta pumzi yake ya mwisho.9 Baada ya hapo, Abu Talib aliyekuwa mtu jasiri, alifanya kila jitihada kadiri alivyoweza kwa kipindi cha miaka arobaini katika kuhifadhi na kulinda heshima ya mpwa wake, hadi hapo na yeye alipofariki dunia. Abu Talib alimlinda Muhammad 4 kwa ujasiri, uaminifu, na kujitolea muhanga kwa namna ya kipekee. Mke wake 9

I`lam al-wara`, al-Tabarsi, uk. 23 12

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 12

6/18/2016 2:40:00 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

Fatimah, ambaye pia alikuwa mwanamke mwenye moyo kama wa simba miongoni mwa Makuraishi, yeye na mume wake walimtunza Muhammad, na kutokana na upendo wake wa kimama (ambao Mtukufu Mtume 4 kamwe hakuusahau), mama huyu hakuacha hata kitu kidogo katika kumpa Muhammad faraja zaidi kuliko watoto wake mwenyewe. Tabia ya Muhammad ndani ya nyumba ya Abu Talib ilivutia uzingativu wa kila mmoja wao humo na baada ya muda mfupi alipendwa na familia yote.10 Tofauti na watoto wengine wenye umri kama wa kwake ambao walionekana na nywele chafu timtimu na macho machafu, Mtukufu Mtume 4 siku zote aliziweka nywele zake safi na uso wake aliuweka katika hali ya usafi. Alikuwa na muonekano wa mtu mzima ambaye aliishi katika hali ya faraja. Hakuwa mlafi wa chakula hata kidogo. Watoto waliokuwa wanakula chakula na yeye kama ilivyo desturi ya watoto, walikula chakula harakaharaka na wakati mwingine walinyang’anyana matonge, lakini yeye alitosheka kwa chakula kidogo na aliepuka tabia ya kula kwa ulafi.11 Muhammad alikuwa na roho nzuri sana kushinda umri wake na katika mazingira yote. Wakati mwingine, mara tu aamkapo, alikuwa akienda kwenye kisima cha Zam Zam na kunywa maji kidogo   Ruh al-Islam, Sayyid Ameer Ali, uk. 19   al-Sirah al-Nabawiyyah, Zaini Dahlan, Juz. 1, uk. 80

10 11

13

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 13

6/18/2016 2:40:00 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

kutoka kwenye kisima hicho. Halafu, wakati mwingine alipoitwa kula chakula cha asubuhi, alisema hahisi njaa kwa hiyo hakutaka kula.12 Kamwe hakuwa na tabia ya kulalamika kuhisi njaa au kiu wakati wa utoto na utu uzima wake.13 Pia, Abu Talib siku zote alimwacha alale karibu na kitanda chake. Anasimulia: “Siku moja, nilimwambia (Mtukufu Mtume 4) avue nguo zake na aende kulala. Nilihisi kwamba hakupenda agizo langu lakini kwa kuwa hakutaka kukataa, alisema, ‘Ami yangu, geuka unipe kisogo ili nivue shati langu.’ Mimi nilistaajabu sana kusikia hivyo. Kamwe sikupata kusikia uongo wowote wala kuona kitendo chochote kisicho na adabu au kicheko kutoka kwa Muhammad. Yeye hakupenda michezo ya kitoto na alifurahia kujitenga faraghani na upweke, na siku zote alikuwa mnyenyekevu.”14 4.

Akifanya kazi kama mchunga kondoo.

Wakati mmoja, alipokuwa anaishi chini ya malezi ya Halimah, Muhammad 4 alimuuliza Halimah, “Hawa ndugu zangu huwa wanakwenda wapi?” Halimah akamjibu kwamba wanamume wengine huwapeleka   Imta` al-Asma`, Maqrirzi, Juz. 1, uk. 8   al-Sirah al-Halabiyyah, Juz. 1, uk. 111 14   Bihar al-Anwar, Allamah Muhammad Baqir al-Majlisi, Juz. 9 12 13

14

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 14

6/18/2016 2:40:00 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

kondoo wao machungani. Mtukufu Mtume 4 ndipo akasema, “Nitakuwa pamoja nao kuanzia leo na kuendelea.”15 Akiwa na umri wa miaka saba, alionekana akibeba udongo kwenye mikunjo ya shati lake refu akimsaidia Abdullah bin Ju`dan katika kujenga majumba. Muhammad hakuonekana akipitisha hata siku moja katika uzururaji katika maisha yake yote. Wakati akiomba, siku zote alisema: “Ewe Mungu, ninajikinga Kwako kutokana na uzembe, uvivu, na udhalili.”16 Aliwahimiza Waislamu kufanya kazi, na akasema: “Ibada ina sehemu sabini, miongoni mwa hizo iliyo bora kuliko zote ni kuchuma riziki kwa njia ya halali. Dua ya mtu anayekaa nyumbani na anayemwomba Mungu ampe riziki bila kufanya kazi haiwezi kujibiwa.”17

Na: “Ni bora zaidi yeyote miongoni mwenu akibeba mzigo wa kuni begani mwake, kuliko kumwomba mtu mwingine ambaye anaweza kukupa au asikupe.” 18   al-Sirah al-Halabiyyah, Juz. 1, uk. 111 na Bihar al-Anwar, Juz. 9, Bab fi Makarim al-akhlaqihi 16   Sahih al-Bukhari, Muhammad al-Bukhari, Juz. 8, uk. 79 17   Wasa`il al-Shi’ah, Muhammad bin Hasan al-Hun al-Amili, Bab al-Tijarah 18   Sahih al-Bukhari, Muhammad bin Isma`il al-Bukhari, Juz. 2, uk. 57 15

15

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 15

6/18/2016 2:40:00 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

Labda, ilikuwa ni kwa sababu ya moyo huu katika kazi na pia kwa sababu hakupenda kuishi miongoni mwa familia ya Abu Talib bila kuwajibika kwa namna moja au nyingine katika kutoa mchango katika njia zao za kupatia riziki, ndipo akaanza kuchunga kondoo wa Abu Talib.19 Zaidi ya hayo, tangu mwanzoni mwa kipindi cha utoto wake, Mtukufu Mtume 4 alipenda sehemu za wazi na majangwa mapana, na fikira ya kujitenga ilikuwa inapata nguvu katika akili yake. Ilikuwa kama vile ametiwa msukumo wa kuondoka kutoka kwenye mipaka na misongamano na pilikapilika za jiji ili aweze kutafakari juu ya dunia ya viumbe kwa umaizi sana na kufikiria sehemu zake kwa usahihi. Nguvu ya fikira huenea na kushamiri zaidi katika maeneo ya wazi, kama mawimbi mepesi ambayo hayakutani na kipingamizi chochote. Kwa upande mwingine, kuchunga wanyama wa kawaida, kuwalinda wasidhuriwe na wanyamapori, na kwenye magenge ya miporomoko na kuwazuia wasipigane wao kwa wao huo ulikuwa ni uzoefu mzuri kwa ajili ya misheni ya siku za usoni ya Mtukufu Mtume 4. Sababu ilikuwa kwamba siku zake za usoni angekutana na watu wajinga na wasio na mwongozo na wakaidi wenye vichwa vigumu na hivyo atapaswa kuwakomboa watu hao kutoka kwenye mazingira   al-Sirah al-Halabiyyah, Juz. 1, uk. 150

19

16

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 16

6/18/2016 2:40:00 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

hatarishi walimokuwemo. Kabla yake, pia Musa na Daudi walikuwa wachunga kondoo kwa vipindi vya muda fulani vilevile.20 Kwa hiyo, kuwa mchunga kondoo, haikuwa kazi ya aibu. 5.

Kuongoza msafara wa biashara.

Mtukufu Mtume 4 alisafiri katika misafara ya biashara ya kwenda Syria na Yemen. Safari yake ya kwanza ilikuwa pale alipofuatana na ami yake Abu Talib kwenda Basra, ambako alijifunza mbinu za biashara. Katika safari yake ya mwisho, alikodishwa na Khadija, ambaye alimkabidhi bidhaa zake na kuzipeleka Syria na akarudi akiwa amepata faida kubwa. Muhammad siku zote alizingatia haki na usawa wakati anafanya biashara na alijiepusha kusema uongo na hila, ambazo zilikuwa ni tabia za wafanyabiashara wengi. Muhammad 4 kamwe hakuwa mkali wakati anafanya biashara na wafanyabiashara wengine. Sa`ib ibn al-Sa`ib anasimulia: “Katika kipindi cha ujahiliya, mimi nilikuwa mwenza wake (Mtukufu Mtume 4) wa kibiashara, na nilimuona yeye kuwa bora zaidi miongoni mwa washirika wote katika kila jambo. Yeye hakubishana na mtu yeyote ama kuwa   al-Sirah al-Halabiyyah, Juz. 1, uk. 150

20

17

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 17

6/18/2016 2:40:00 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

mkaidi wala kumlaumu mwenzake kwa ajili ya kitu chochote.”21

Mtukufu Mtume 4 alijulikana sana kwa ukweli na uaminifu wake hivyo kwamba kila mtu aliyemjua yeye alithibitisha uaminifu wake na walimuita Muhammad al-Amin (mwaminifu).22 Wakati wa kazi yake ya utume, pale Makurayshi walipojitokeza kumpinga, lakini hata hivyo bado waliziaminisha rasilimali zao kwake. Mfano wa uaminifu wake unaweza kuonekana wakati alipohama kutoka Makkah kwenda Madina, na kumuagiza Ali abakie Makkah hasa ili aweze kuwarejeshea watu rasilimali zao ambazo waliziaminisha kwa Mtukufu Mtume 4. Yeye alichukulia ukweli na uaminifu kuwa ndiyo msingi wa maisha na akasema: “Tabia hizi mbili za (uadilifu) zimethibitishwa na kusisitizwa katika mafundisho yote ya Mitume na hutumika kwa yeyote ambaye ameaminishwa jukumu.”

Pia alisema: “Kila mmoja wenu ni kiongozi na anao wajibu kwa kile ambacho ameaminishwa kwacho.”23   al-Sirah al-Halabiyyah, Juz. 1, uk. 162   al-Sirah al-Halabiyyah, Juz. 1, uk. 172 23   Sahih al-Bukhari, Juz. 4, uk. 6 21 22

18

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 18

6/18/2016 2:40:00 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

6.

Msimamo wake kuhusu wanaokandamizwa:

Katika kipindi cha ujahiliya, hapakuwepo na mfumo wa kisheria au mamlaka ambayo ingeweza kulinda mipaka ya haki za mtu binafsi au ambako mtu angeweza kufungua madai na kufanyika hukumu. Ukiacha wale ambao walitegemea uwezo na ushawishi wao, au ufuasi wa kikabila, watu wengi waliosalia, mara kwa mara walifanyiwa aina zote za uvukaji mipaka, dhidi ya uhai wao, rasilimali, na familia zao. Tabia za kishenzi na kikatili na kanuni ya mwenye mabavu mpishe zilitawala. Katika jiji la Makkah, hali ilikuwa ya vurugu sana. Hususani wageni ndiyo waliofanyiwa ubaya. Mara kwa mara vitu vyao vilipokwa hadharani na wakati mwingine, wao wenyewe walichukuliwa mateka. Bila shaka, miongoni mwa umati huu usio na nidhamu, walikuwepo watu wachache ambao hawakuacha moja kwa moja kabisa maadili ya ubinadamu, na zilikuwepo dalili za hisia kubwa, huruma na uungwana katika nyoyo zao. Bila shaka, waliudhiwa na kuchoshwa na hali hii isiyo ya kawaida. Siku moja, lilitokea tukio ambalo liliashiria kuwahuzunisha sana, na katika kujibu kutokuridhishwa kwao na dhuluma waliyoiona, walichukua hatua kadhaa zinazofaa kwa uhakika. Mgeni kutoka kabila la Zubayd alikuja kuuza bidhaa zake mjini Makkah. Aas ibn Wa`il, mmojawapo

19

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 19

6/18/2016 2:40:00 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

wa machifu wa jadi wa Quraysh, alichukua bidhaa zote za mgeni huyo bila kulipa chochote. Matokeo yake, Zubayd aliwaendea viongozi kadhaa mashuhuri wa kabila la Quraysh lakini hakufanikiwa. Walikataa kumsikiliza. Katika hali ya kukata tamaa alikwenda kileleni mwa Mlima Abu Qubays na akaomba kwa sauti kubwa atendewe haki, akasema: “Enyi familia ya Fahr! (Fahr alikuwa mhenga wa Quraysh, ni kwamba, ndiye Quraysh mwenyewe. Alikuwa mtu ambaye kabila lote lilikuwa na limenasibishwa naye na alijulikana sana kwa uungwana wake.) Mimi ni mgeni katika jiji lako na bado sijatekeleza ibada ya Umra (Hijja ndogo). Sijaheshimiwa na bidhaa zangu zimemilikiwa kidhulma. Wako wapi wale watu jasiri ambao wanaweza kunikomboa na kulinda haki yangu?�

Mvumo wa sauti ya yule mtu aliyeonewa ulisikika ukijirudia hewani na ukazigusa nyoyo za watu wa Makka wasioridhika na hali hiyo. Muhammad akifuatana na ami yake Zubayr bin Abdul-Muttalib, alisimama na akisaidiwa na baadhi ya viongozi wengine wa koo za ki-Quraysh walikusanyika nyumbani kwa Abdullah bin Jud`an al-Taymi. Kwa pamoja walifanya mkataba kwa ajili ya uzuiaji wa vitendo vya uhalifu na kurejesha haki kwa wanyonge na wakandamizwao. 20

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 20

6/18/2016 2:40:00 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

Halafu wale wote waliofanya makubaliano walimwendea Aas bin Wa`il kwa pamoja. Hakuweza kuwazuia watu hao waliokuwa wamekasirika na kusikitishwa na dhulma hiyo na alilazimishwa kunywea na kurudisha bidhaa hizo kwa mwenyewe.24 Mtukufu Mtume 4 alikumbuka tukio hili baadaye na akasema: “Nilikuwepo wakati makubaliano yalipokuwa yanafanyika nyumbani kwa Abdullah bin Jud`an, na sitavunja makubaliano hayo kwa hali yoyote ile. Hata sasa hivi nipo tayari kushiriki katika makubaliano kama hayo.”25

Kufuatana na mtazamo wa Muhammad 4, watu wote wa jamii wanao wajibu wa kuzuia wakandamizaji na wasije wakaridhika na kuwa watazamaji tu. Pia amenukuliwa akisema: “Msaidie nduguyo hata kama ni mkandamizaji au ndiye anayekandamizwa.”

Wakati masahaba wake walipomuuliza ni kwa jinsi gani wangemsaidia mkandamizaji, yeye akajibu: “Kwa kumzuia yeye asiwaonee wengine.”26   al-Sirah al-Halabiyyah, Juz. 1, uk. 157   al-Sirah al-Halabiyyah, Juz. 1, uk. 156; na al-Sirah al-Nabawiyyah, Zaini Dahlan, Juz. 1, uk. 101 26   Sahih al-Bukhari, Juz. 2, uk. 128 24 25

21

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 21

6/18/2016 2:40:00 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

7.

Kuhusiana na familia yake:

Licha ya uhodari na uchangamfu wa ujana wake, Mtukufu Mtume Muhammad 4 hakuathiriwa na tamaa na shauku zake kama matokeo ya maadili ya usafi na ukarimu aliokuwa nao. Kabla ya ndoa yake, kamwe alikuwa hajaonekana akiwa na Khadija wala hata kusikika au kusemwa kwamba alikuwa na urafiki wa karibu na wanawake. Mathalani, hata wakati alipohamia Madina, katika umri wake wa uzeeni, alioa wanawake kadhaa, lakini kila ndoa ilifungwa katika msingi wa kuangalia manufaa. Kama angedhamiria kutafuta kujifurahisha, asingewaoa wanawake wanaomzidi umri. Ilikuwa ni rahisi sana yeye kuoa wasichana wazuri ili apate kustarehe, lakini aliwashutumu na kuwalaani wale waliochukulia ndoa kama ni njia ya kupata kujistarehesha tu.27 Mke wa kwanza wa Mtukufu Mtume 4 alikuwa Khadija, binti wa Khuwaylid bin al-Asad, ambaye alitoka kwenye familia mashuhuri. Khadija mwenyewe alikuwa anaheshimiwa kama Bibi Wa Nafasi ya Kwanza kwa heshima ya Quraysh. Yeye alijaaliwa kuwa msafi (asiye mzinifu) na mwaminifu, na kwa tofauti hii, aliitwa al-Tahirah (aliye safi).28 Alikuwa mmoja wa   al-Islam Ruh al-Madaniyyah, Sheikh Mustafa al-Ghalayini, uk. 182   al-Sirah al-Halabiyyah, Juz. 1 uk. 163

27 28

22

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 22

6/18/2016 2:40:00 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

wafanyabiashara matajiri sana mjini Makkah, Khadija alikataa kuchumbiwa na watu kadhaa mashuhuri wa kabila la Quraysh waliotaka kumuoa, akiamini kwamba wao walikuwa wanatamani utajiri wake. Maadili mema ya Muhammad 4 Mwaminifu ambayo yalijulikana sana yalimvutia Khadija. Aliona kwake zile sifa alizokuwa akizitafuta kwa muda mrefu na akakubali kuolewa naye. Tofauti na ndoa zingine nyingi zilizofanyika wakati huo, ndoa yao haikufanyika kwa sababu ya mapenzi ya hadhi, uzuri wa sura, uwezo wa kipato cha fedha na umiliki wa rasilimali, au kwa ajili ya kujionesha. Hasa zaidi ni ndoa ambayo msingi wake ulikuwa juu ya ulinganifu wa maadili, kupenda wema, mfungamano wa kiroho na mapenzi ya wote wawili yakiipatia hali ya kudumu. Muunganiko huu wa kindoa ulichukua nafasi ya mfano wenye athari ya mvuto na yenye kufaa sana katika kueneza wito wa Uislamu na kumtia moyo mjumbe wa Mungu. Khadija, mwanamke mwadilifu na mwenye kujitolea, siku zote alikuwa akishiriki katika maumivu na starehe za mume wake na alikuwa akimfariji alipopatwa na matatizo. Khadija alitoa mali yake yote kwa mafukara kwa ajili ya kuinua tangazo la Tawhid ya Mungu. Alikuwa mwanamke wa kwanza kuingia katika Uislamu na alikuwa akiswali nyuma ya mume wake. Mtume 23

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 23

6/18/2016 2:40:00 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

Mtukufu 4 hakuoa mwanamke mwingine kipindi chote alipokuwa bado yu hai. Baada ya kifo cha Khadija, alioa tena na aliwafanyia wema na haki bila upendeleo wa ubora juu ya yeyote kati ya wake zake wote. Wakati Mtukufu Mtume 4 alipotaka kwenda safari, alikuwa na kawaida ya kupiga kura kati ya wake zake ya kuokota karatasi na yule ambaye kura ilimwangukia ndiye aliyesafiri naye.29 Hakuwa mkatili kimaadili lakini hususani alikuwa mwema na mvumilivu. Aliwavumilia hasira mbaya na lugha chafu za wake zake, hata wakati baadhi yao walipokuwa washupavu sana na kutoa siri zake za ndani na kumkasirisha yeye kwa kupanga kula njama na kushirikiana, hadi kufika kwenye hatua ambapo aya za Qur`ani ziliteremshwa kwa lengo la kuwaonya na kuwakaripia.30 Baada ya vita baina ya Banu Nadir na Banu Qurayzah (makabila mawili ya Kiyahudi), baadhi ya wake zake waliwaza kuhusu maisha ya kikubwa na ya anasa na wakadai wapewe mapambo ya vito kwani walikwishajua kwamba hazina za Wayahudi zilikuwa katika miliki ya Mtukufu Mtume 4. Mtukufu Mtume 4, ambaye hakutaka kutoa muhanga haki ya jamii kwa sababu ya mawazo ya ghafla ya wake zake na   Sahih al-Bukhari, Juz. 4, uk. 34   Sura al-Tahrim; 66: 3-5

29 30

24

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 24

6/18/2016 2:40:00 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

aruhusu hazina ya Waislamu itumike kibinafsi, alikataa kutekeleza madai yao na hakuzingatia maneno yao ya fujo. Abu Bakr na `Umar, ambao walipewa taarifa ya jambo hili, waliamua kuwaadhibu mabinti zao Aisha na Hafsa, lakini Mtukufu Mtume 4 aliwazuia wasifanye hivyo.31 Yeye aliridhika tu na kujitenga mbali nao. Baada ya mwezi moja, aliamriwa, katika msingi wa aya za Qur`ani zilizoteremshwa katika tukio hilo kwamba alitakiwa awaruhusu wake zake kuchagua moja kati mambo mawili: kama mmojawao yeyote alikuwa bado anataka kuwa mke wake, aachane na madai ya kutaka ongezeko la utajiri, aishi maisha rahisi na ya kuridhika, na awe na matumaini ya thawabu nyingi zaidi. Hata hivyo, endapo yeyote miongoni mwao anapenda anasa na mng`aro wa dunia hii, basi Mtukufu Mtume 4 amwache katika namna inayofaa.32 Mtukufu Mtume 4 alipandisha hadhi ya wanawake hadi kwenye kiwango cha wanadamu kamili ambao walikuwa na haki ya kumiliki maisha yao na rasilimali. Siku zote, hata wakati wa dakika za mwisho wa uhai wake, alipendekeza kuwa na mke mmoja; yaani, kuzingatia dharura za asili ya maumbile ya mwanamke na alitolea mfano wa jambo hili kwa ifuatayo:   Sahih al-Muslim, cha Abul Husayn Muslim bin al-Hajjal Qushayri alNisaburi, Juz. 4, uk. 187 32   Surat al-Ahzab; 33: 28-29 31

25

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 25

6/18/2016 2:40:00 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

“Mwanamke yu kama ubavu ambao unaweza kuvunjika kama utajaribu kuunyoosha. Unaweza kunufaika nao kama ubavu huo utabaki kama ulivyoumbwa (na Mwenyezi Mungu Mtukufu).”33

Mpango wa uumbaji na mipaka ya asili ya binadamu ni vitu ambavyo haviwezi kubadilishwa, na mambo fulani ambayo yanaweza kufanywa na wanamume hayawezi kufanywa na wanawake, na ndani ya mpango wa uumbaji kila mmoja –mwanamume/mwanamke anayo nafasi yake na vipaji vyake. Mtukufu Mtume 4 alisisitiza kwamba wanawake wanatakiwa kuwatendea kwa upole na akasema: “Watu wote wana tabia nzuri na mbaya na mume asizifikirie zile sifa mbaya tu za mke wake na akamchukia, kwa sababu wakati anapokuwa hakufurahishwa na sifa moja mbaya ya mke wake, anafurahishwa na sifa nyingine nzuri ya mke wake na nukta hizi mbili zinatakiwa kufikiriwa kwa pamoja.”34

Pia Mtukufu Mtume Muhammad 4 aliwalaani wale wanaoshindwa kufanya jitihada kwa ajili ya hali njema ya familia zao, akisema:   Sahih al-Bukhari, Juz. 7, uk. 26   Sahih al-Muslim, Juz. 4, uk. 178

33 34

26

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 26

6/18/2016 2:40:00 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

“Mtu asiyetilia maanani familia yake na akawaacha peke yao anakoseshwa rehema za Mwenyezi Mungu.”35

Alikuwa mwema kwa watoto wake akielezea kwamba: “Watoto wetu ni sehemu muhimu yetu sisi.” Alikuwa mwangalifu katika kuwalea watoto wake na aliwafundisha adabu za Kiislamu. Alikuwa na desturi ya kusema: “Fatimah ni sehemu yangu, na ni moyo wangu na roho yangu na yeyote atakayemuudhi atakuwa ameniudhi mimi.”36

Na: “Hasan na Husayn wanatokana na mimi, na mimi natokana na wao.”

Ilikuwa inatokea kwamba wakati Mtukufu Mtume 4 akiwa kwenye sijida, Hasan na Husayn walikuwa wakipanda mabegani kwake na ama alirefusha sijida hadi hapo waliposhuka, au alikuwa akiwashusha chini polepole ndipo ananyanyuka tena kutoka kwenye sijida. Alikuwa akiwakumbatia na kubusu mashavu yao na nyuso zao. Siku moja, mtu mmoja alikuwepo pamoja na Mtukufu Mtume 4 aliona tukio hili linatokea na   Wasa`il al-Shi`ah, Bab al-`afw`an al-Zaujah   Nur al-Absar, Muhammad bin Mu`min al-Shablanji, uk. 27

35 36

27

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 27

6/18/2016 2:40:00 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

akasema: “Kamwe sisi huwa hatuwabusu watoto wetu.” Mtukufu Mtume 4 akajibu: “Mimi niwafanyieni nini kama Mungu ameondosha hisia za huruma kutoka katika nyoyo zenu?”

Siku nyingine, alipomketisha Hasan kwenye goti lake na akabusu uso wa mtoto huyo. Aqra`bin Habis akasema: “Ninao watoto kumi, na kamwe sijambusu hata mmoja wao.” Mtukufu Mtume 4 akasema: “Mtu asiye na huruma kwa wengine hastahili kupata huruma (kutoka kwa Mungu)”37

Mtukufu Mtume 4 sio kwamba aliwapapasa kimahaba watoto wake tu bali pia alikuwa anawapenda watoto wa wengine na alikuwa anawakumbatia na kuwasalimia.38 Zaidi ya hayo, mapenzi na upendo wa Mtukufu Mtume 4 haukuishia hapo. Pia alikuwa anawakumbatia watumishi wake. Anas ibn Malik anasimulia:   Sahih al-Muslim, Juz. 7, uk. 77   Nur al-Absar, uk. 28

37 38

28

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 28

6/18/2016 2:40:00 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

“Nilimtumikia Mtukufu Mtume 4 mchana na usiku katika nyumba yake kwa kipindi cha miaka kumi na kamwe hakupata kuniambia ‘kwa nini umefanya hivi?’ baada ya kufanya kitu fulani au ‘Kwa nini hukufanya hivi?’ baada ya kufanya uzembe wa kutokufanya kitu fulani. Kamwe hakusema neno lolote la dharau kwangu.”39

Kwa ufupi, alikuwa akiifanyia huruma familia yake, sio kwa ukali au kuwakalifu na akasema 4: “Mtu aliye bora sana miongoni mwenu ni yule ambaye ni mbora sana kwa familia yake na mimi ni mbora zaidi miongoni mwenu kwa familia yangu.”40

8.

Kuhusu watumwa wake:

Utumwa ni mojawapo ya tabia mbaya ya kutisha ya binadamu na inaashiria ukatili wake. Utumwa umekuwepo tangu kwenye historia ya zamani ya binadamu, polepole ikawa sehemu ya haki ya mabwana na kanuni za kijamii zisizokanushika. Katika hali hiyo imepenya kwenye jamii zote za binadamu kwa kiwango kwamba hata watu wasomi na wanazuoni wa mataifa mengi walifikiria kuwa utumwa ni jambo linalofaa na sahihi. Katika ustaarabu huu sio tu kwamba hazikuchukuliwa   Sahih al-Muslim, Juz. 7   Wasa`il al-Shia`ah, Bab al-`afw`an al-Zaujah

39 40

29

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 29

6/18/2016 2:40:00 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

hatua zozote za kufuta utumwa lakini pia hapakuwepo na hatua zozote za kuurekebisha. Wanafalsafa wa Kigiriki waliamini kwamba aina mbili za binadamu ziliumbwa: binadamu huru na binadamu watumwa, na kwamba binadamu watumwa waliumbwa kwa ajili ya kuwatumikia binadamu huru. Aristotle alichukulia mfumo wa utumwa kuwa ni mfumo muhimu katika jamii ya binadamu. Alisema kwamba kuhusu kazi, wakati nguvukazi kubwa inapohitajika, serikali inapaswa kutumia watumwa, lakini uzingativu unatakiwa kuelekezwa katika kuendeleza maisha yao. Mtukufu Mtume 4 alielewa kwa hekima zake komavu na dhamiri yake timamu kwamba wanadamu wapo sawa katika asili yao ya kimaumbile na vipaji vyao vya kimaumbile. Alijua kwamba wanadamu wote wanazo roho, hiari, hisia na michomo ya moyo. Pia alielewa kwamba tofauti katika mbari, rangi ya ngozi, lugha, utaifa, na hata fadhila za ucha Mungu na elimu haviwezi kuwa sababu ya kubaguana wao kwa wao na haki zao. Kwa nini baadhi ya wanadamu wanawafanya wanadamu wengine kuwa watumwa, na kuwanyang`anya uhuru wao na stahili ya heshima zao? Mtukufu Mtume 4 alikuwa anatambua vema kwamba kufutilia mbali fikira ambayo imepenya kwenye kina cha akili za wamiliki wa watumwa 30

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 30

6/18/2016 2:40:01 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

na watumwa kwa miaka 1000 haingewezekana, isipokuwa kwa kubadili mtindo wa fikira ya kijamii. Endapo sheria ingepitishwa bila ya msukumo wa kiutendaji au dhamana ya kutiisha kutoka ndani ya nafsi za mabwana na watumwa, mfumo huu wa kitabaka ambao ulikwishakuwa na mizizi mirefu kamwe haungeweza kuondolewa. Hata hivyo, hao mabwana walifikiri kwamba dhuluma ya dhahiri kama hiyo ilikuwa ni sehemu muhimu ya haki yao. Kwa nguvu ya tabia, katika hali ya polepole watumwa nao pia walikwisha kuwa dhaifu sana kuweza kutumia nguvu ya hiari yao na hawakuweza kutenda kwa uhuru. Matokeo ya kukosa kwao kuwa na hisia za uhuru na kuishi maisha huru, watumwa waliamini kwamba haki ya maisha yao ilikuwamo kwenye mipaka hali ile hasa ya ukatili mno ambamo walikwishanaswa. Kwa hiyo, hali ya kijamii ilipaswa kurekebishwa sambamba na kukua polepole kwa hali ya kijamii. Hapa ilihitajika fikira na hekima nyingi wakati wa kuchukua hatua za kuliweka hili katika utekelezaji. Kama hatua ya kwanza, Mtukufu Mtume 4 aliwashauri mabwana na watumwa wenyewe kuchukuliana wao kwa wao kama ndugu katika matukio

31

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 31

6/18/2016 2:40:01 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

kadhaa. Alianza kwa kuwaaminisha kwamba wote wao walikuwa mbari moja na wote waliumbwa kutokana na udongo.41 Alisema: “Weupe hawana fursa zaidi kimaumbile kuliko Weusi, na watu waovu sana mbele ya Mungu ni wafanya biashara ya utumwa.42 Watumwa ni ndugu zenu. Wamewekwa chini ya amri zenu na wao wanazo haki zao wenyewe. Mnapaswa kuwalisha chakula kile ambacho nyinyi mnakula na kuwapa nguo kama zile mnazovaa nyinyi. Msiwaamuru kufanya mambo yaliyo nje ya uwezo wao na muwasaidie kufanya mambo mnayowatuma kufanya.43 Mnapowaita, waiteni kwa upole na msiwaambie, ‘Ewe Mtumwa wangu’ au ‘Ewe Kijakazi wangu.’ Badala yake, mnatakiwa kusema, ‘kijana wangu’ au ‘msichana wangu’ au ‘mvulana wangu.’ Wanamume wenu wote na wanawake wenu wote ni waja wake Mungu, na Yeye ndiye Bwana (Mola) wa Kweli wa watu wote.”44

Mantiki hii yenye kujieleza na inayofaa, ambayo ilitoka kwenye kina cha moyo wa mwanahuruma wa kweli katika muundo wa ujumbe wa kimbinguni,   Man la-Yahdhuruh al-Faqih, Sheikhe al-Saduq Muhammad bin Babuyah al-Qummi, uk. 575 42   Man la-Yahdhuruh al-Faqih, Sheikhe al-Saduq Muhammad bin Babuyah al-Qummi, uk. 354 43   Sahih al-Bukhari, Juz. 3, uk. 149 44   Sahih al-Muslim, Juz. 7, uk. 48 41

32

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 32

6/18/2016 2:40:01 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

ulichukua jukumu kubwa katika kuvunja kiburi cha mabwana wa watumwa, na katika kufutilia mbali hisia za udhalili kutoka kwenye nyoyo za watumwa, na katika mabadiliko ya kisomi kwa watu wengi, na katika kusababisha shaka kuhusu jambo ambalo lilikuwa linachukuliwa kama kanuni isiyopingika kwa kipindi cha karne nyingi. Bila shaka, ujumbe huo uliwafanya watu wafikirie upya hali zao na polepole walihitimisha kwamba ndugu hapaswi kumtumikisha ndugu yake. Baada ya hapo, Mtukufu Mtume 4 kupitia hatua zake za kivitendo, aliandaa njia kwa ajili ya kuwapa uhuru watumwa, ama kwa kuwahamasisha watu kufanya hivyo na kuwaahidi thawabu: kwamba dhambi zao zitafidiwa na toba yao ingekubaliwa; au watumwa wangeachiwa huru kwa njia ya fidia (kununuliwa tena upya) ili waweze kuwalipa wamiliki wao kiasi fulani cha fedha kutoka kwenye mishahara yao kidogokidogo, au kwamba fidia hiyo ingelipwa kutoka kwenye hazina ya Waislamu (Bayt al-Mal) hadi hapo watakapokuwa huru. Katika njia hii, Mtukufu Mtume 4 alizuia takribani njia zote zinazoelekea kwenye utumwa kwa lengo la kuua utumwa polepole. Yeye mwenyewe alikuwa mstari wa mbele, akionesha kwa mfano wa kivitendo hasa,

33

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 33

6/18/2016 2:40:01 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

na akamuacha huru mtumwa wake Zayd bin Haritha, ambaye mke wake Khadija alikuwa amemzawadia Mtukufu Mtume 4. Zaidi ya hayo, ili kufuta hisia za udhalili na utumwa kutoka katika akili ya Zayd, Mtukufu Mtume 4 alimuita Zayd ‘mtoto wake wa kupanga’ hadharani. Mara tu Zayd alipofika umri wa balehe, Mtukufu Mtume 4 alimuoza Zayd binamu yake, ili kuondoa ubora wa kimbari ambamo dunia ya wakati huo, hususani dunia ya ukabila wa Kiarabu, ilikuwa ikiutegemea sana. Hivyo, Mtukufu Mtume 4 aliasisi kanuni ya usawa. 9.

Unadhifu:

Kama ilivyotajwa hapo kabla, Mtukufu Mtume 4 alipenda sana unadhifu tangu siku za utoto wake na alikuwa wa kipekee katika kuzingatia unadhifu wa mwili na nguo. Kwa nyongeza zaidi ya kuchunga adabu za wudhu, alikuwa anajisafisha na kuoga mara nyingi na alihamasisha hayo yote kama ni vitendo vya ibada. Alikuwa akiosha nywele zake ambazo zilining`inia hadi kwenye ndewe za masikio yake kwa kutumia majani ya mti wa Lote (sidr) na alizichana nywele na kupaka mafuta ya urujuani. Alikuwa anajifukiza manukato ya miski (musk) na ubani wa ambari kiasi kwamba alipopita watu walipata mnuso wa marashi yake. Alisafisha 34

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 34

6/18/2016 2:40:01 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

meno yake kwa mswaki wa asili kwa uangalifu sana mara kadhaa kwa siku, hususani kabla ya kulala na baada ya kuamka asubuhi. Nguo yake nyeupe, ambayo ilifunika magoti yake, siku zote ilikuwa safi. Kabla na baada ya kula chakula, alikuwa na desturi ya kunawa mikono na kusukutua mdomo wake na alikuwa akijiepusha kula majani ya miti yenye harufu mbaya au mboga zenye harufu mbaya. Kitana kilichotengenezwa kwa meno ya tembo, dawa tepetepe ya kubandika kwenye macho, kiwekeo, mkasi, kioo na mswaki wa asili ni vitu ambavyo vilikuwa sehemu ya mzigo wake popote alipokwenda. Siku zote nyumba yake ilikuwa safi licha ya urahisi wake na kukosa vitu vya anasa. Alisisitiza kwamba takataka zinatakiwa kuondolewa wakati wa mchana na hazitakiwi kuachwa hadi usiku. Usafi wake wa kimwili uliendana na utakatifu wa usafi wake wa kiroho. Aliwashauri masahaba na wafuasi wake kuweka vichwa vyao, miili yao, nguo zao na nyumba zao katika hali ya usafi na hususani aliwashawishi kuoga na kujifukiza manukato mnamo siku za Ijumaa ili kwamba wasije wakawa na harufu mbaya wakati wakihudhuria swala ya Ijumaa.45 Mtukufu Mtume 4 aliwaamuru wafuasi wake wasijisaidie haja yoyote karibu na makaburi, ukingoni   Yaliomo katika sura hii yamo katika vitabu vyote vya Sirah na Hadithi

45

35

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 35

6/18/2016 2:40:01 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

mwa mito, au katika vivuli vya miti. Alisisitiza kwamba tahadhari ichukuliwe ya kutokuchafua maji kwa kiasi kwamba hata wakati wa kuoga ni bora zaidi kuoga nje ya maji badala ya kuingia ndani ya maji.46 10. Adabu za maingiliano ya kijamii: Mtukufu Mtume 4 alikuwa mchangamfu na mwenye furaha katika hadhara lakini alikuwa na hali ya huzuni na mazingatio wakati akiwa katika faragha. Kamwe hakuwa na desturi ya kumkodolea macho mtu usoni na mara nyingi alikuwa akitazama chini zaidi ya kunyanyua kichwa chake juu. Alikuwa mwangalifu katika kutangulia kumsalimia kila mtu, hata watumwa na watoto. Mara nyingi yeye alikuwa na kawaida ya kuketi kwa kupiga magoti na alikuwa hanyooshi miguu yake mbele ya wengine. Wakati wowote alipoingia kwenye mkutano, alikuwa na tabia ya kuketi kwenye nafasi ya wazi iliyo karibu sana na yeye na kamwe hakumruhusu mtu kusimama kwa ajili yake au kusogea kwa ajili ya kumpa yeye nafasi. Wakati anaelezewa kitu, hakujaribu kumkata kauli mtu anaposema na alimchukulia kwa namna ambayo kwamba mtu huyo anapomaliza kuongea aliondoka akijifikiria kwamba na yeye alikuwa kipenzi sana cha Mjumbe wa Mungu. Hakuwa na   Sahih al-Muslim, Juz. 1, uk. 163

46

36

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 36

6/18/2016 2:40:01 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

mazoea ya kuzungumza isipokuwa kama kuna ulazima wa kufanya hivyo. Usemaji wake ulikuwa wa polepole na dhahiri na kamwe hakutumia lugha chafu. Yeye alikuwa mfano kamili wa staha na soni. Kamwe alikuwa hakasirishwi na tabia ya mtu lakini katika matukio fulani, hali ya kukasirika ilionekana usoni mwake. Kamwe hakuwa na desturi ya kulalamika na kukataa. Alikuwa anawatembelea wagonjwa mara kwa mara na alikuwa anashiriki katika maandamano ya mazishi. Hakumruhusu mtu yeyote kumsema vibaya mtu mwingine isipokuwa wakati anapotoa maeleza ya kudai haki. Katika tukio moja, kundi la Wayahudi lilikuja kwa Mtukufu Mtume 4 na wakasema: “as-Saamu-Alaykum” (kifo kiwe juu yako), ambapo Mtukufu Mtume 4 akajibu: “Wa alaikum.” `A`isha alielewa maana ya salaam hiyo na akawalaani lakini Mtukufu Mtume 4 akamwambia, “A`isha usifanye hivyo, kwani Mwenyezi Mungu hapendi matumizi ya maneno makali.” 47 11. Usamehevu. Siku zote Mtukufu Mtume 4 alisamehe uonevu na ufidhuli aliofanyiwa. Hakuwa na kinyongo dhidi ya mtu yeyote na kamwe hakutafuta kulipa kisasi. Moyo wake   Sahih al-Muslim, Juz. 7, uk. 4

47

37

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 37

6/18/2016 2:40:01 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

wenye nguvu, ambao ulivuka mipaka ya changamani ya kutoonesha hisia na akili, alikuwa anapendelea zaidi kusamehe badala ya kulipa kisasi. Kiwango chake cha hisia kwa mikasa hakikuvukia kwenye huzuni. Katika Vita vya Uhud, licha ya kiwango cha ukatili na utovu wa heshima ulivyofanyiwa mwili wa Hamza bin `Abdul-Muttalib, jambo ambalo lilimuumiza sana Mtukufu Mtume 4 na kumhuzunisha sana, yeye 4 hakulipa kisasi dhidi ya maiti za wapiganaji wa Quraysh. Hata baadaye, wakati alipopata kuwafikia wale waliofanya kitendo hicho pamoja na Hind, mke wa Abu Sufyan, Mtume 4 hakulipa kisasi. Kwa kweli, wakati Abu Qutadah al-Ansari alipokuwa karibu ya kuwalaani watu hao, Mtukufu Mtume 4 alimzuia asifanye hivyo.48 Tukio lingine linalofanana na hilo lilitokea baada ya ushindi wa Khaybar, wakati kundi la Wayahudi ambao walikwisha jisalimisha lilipompelekea Mtukufu Mtume 4 chakula chenye sumu. Mtukufu Mtume 4 alipewa taarifa kuhusu jaribio lao hilo la kutaka kumuua, lakini aliwasamehe.49 Na kwenye tukio jingine tena, pia alimsamehe mwanamke mmoja Myahudi ambaye alikuwa na hatia katika mpango wa kumpa chakula chenye sumu. 50   Imta`al-Asma`, Ahmad bin Ali al-Maqrizi, Juz. 1, uk. 425   Sahih al-Bukhari, Juz. 4, uk. 100 50   Sahih al-Muslim, Juz. 7, uk. 14 48 49

38

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 38

6/18/2016 2:40:01 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

Abdullah bin Ubayy, ambaye alikuwa kiongozi wa wanafiki, ambao walipewa kinga kwa kutamka Shahadah (tangazo la Waislamu la kuamini katika Upweke wa Mungu na kukubali kwamba Muhammad 4 ni Mtume Wake), na ambaye alikuwa analea uadui moyoni mwake dhidi ya Mtukufu Mtume 4, alidhani kwamba baada ya Mtukufu Mtume 4 kuhamia Madina basi huo ndiyo utakuwa mwisho wa serikali yake. Mtu huyu alikuwa anakula njama na Wayahudi ambao walikuwa na uadui na alikuwa mashughuli katika kumkashifu Mtukufu Mtume 4, kuchochea uadui dhidi yake na kueneza uzushi kuhusu yeye. Ni yeye huyo ambaye katika Vita vya Bani al-Mustaliq, alisema: “Tutakaporudi Madina, wale wenye heshima zao watawafukuza wale wasioheshimika, yaani wahamiaji (muhaajirin).�

Masahaba wa Mtukufu Mtume 4 ambao walikuwa na chuki iliyoota mizizi juu ya Abdullah bin Ubayy, walikuwa wakimwomba Mtukufu Mtume 4 mara kwa mara amwadhibu mtu huyo. Hata hivyo, sio tu kwamba Mtukufu Mtume 4 aliwakataza kufanya hivyo, lakini pia alikuwa anamvumilia sana Abdullah. Wakati Abdullah bin Ubayy alipokuwa mgonjwa, Mtukufu 39

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 39

6/18/2016 2:40:01 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

Mtume 4 alimtembelea. Alihudhuria mazishi yake na pia aliiswalia maiti yake.51 Pia imesimuliwa kwamba wakati fulani kundi la wanafiki lilikula njama ya kumuua Mtukufu Mtume 4 wakati alipokuwa anarudi kutoka kwenye Vita vya Tabuk. Walipanga kumwogofya ngamia wake ili hapo kumfanya aangukie kwenye bonde hilo alipokuwa anapita kwenye barabara ya mlimani. Walikuwa wamefunika nyuso zao, lakini Mtukufu Mtume 4 aliwatambua. Hata hivyo, hakufichua majina yao licha ya msisitizo wa masahaba wake na hakutilia maanani ushauri wao wa kuwaadhibu watu hao.52 12. Mipaka ya sheria. Mtukufu Mtume 4 alikuwa anasamehe usumbuvu wowote wa utu wake mtakatifu bila kusita, lakini hakuwapuuzia wale waliovunja sheria ya kimungu. Wakati wa kutekeleza haki na kuwaadhibu wakosaji ulipofika, hakuwa na huruma kabisa kwa sababu sheria za haki hulinda usalama wa jamii na ni muhimu sana kwa uwepo wenyewe hasa wa jamii. Kwa hiyo sheria hizi hazitakiwi kuchezewa na watu vigeugeu wa ajabu vinginevyo jamii itatolewa kafara kwa ajili ya mtu binafsi.   Imta`al-Asma`, Ahmad bin Ali al-Muqrizi, Juz. 1, uk. 496   Imta`al-Asma`, Ahmad bin Ali al-Muqrizi, Juz. 1, uk. 479

51 52

40

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 40

6/18/2016 2:40:01 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

Katika mwaka wa kuiteka Makka, mwanamke mmoja wa kabila mashuhuri la Makhzum alifanya uhalifu wa kuiba na kitendo hicho kilithibitishwa kisheria. Ndugu zake mwanamke huyo, ambao bado walikuwa wanakumbatia mfumo wa kitabaka wa kabla ya Uislamu (ujahiliya), walihisi kwamba adhabu ambayo mwanamke huyo angeadhibiwa ingewafedhehesha wao pia. Walijaribu kumshawishi Mtukufu Mtume 4 asimwadhibu mwanamke huyo kwa uhalifu wa wizi aliofanya. Usamah bin Zaid, ambaye alikuwa akipendwa sana na Mtukufu Mtume 4, aliteuliwa kuingilia kati kwa ajili ya mwanamke huyo ili adhabu hiyo ipuuzwe na Mtukufu Mtume 4. Alipokuwa anajitayarisha kujaribu kuingilia kati, Mtukufu Mtume 4 akasema: “Unajaribu kuingilia kati ili kumtetea mtu katika kesi ambayo inayohusika na Adhabu Zilizoamriwa na Mwenyezi Mungu?”

Usamah alitambua kosa lake, akaomba msamaha, na akaomba msamaha kwa Mungu. Halafu Mtukufu Mtume 4 alisimama akatoa hotuba ambamo alielezea jambo hilo kwa namna ifuatayo: “Kile kilichoangamiza umati za kabla yenu ilikuwa kwamba kama mtu mashuhuri miongoni mwao aliiba, walimsamehe, na kama mtu fukara miongoni mwao 41

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 41

6/18/2016 2:40:01 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

aliiba, walimwadhibu kwa kufuata hukumu ya Sheria ya Mungu. Naapa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ambaye uhai wangu upo Mikononi Mwake, sitakuwa na huruma katika kutekeleza haki kwa yeyote, hata kama muhalifu awe ni ndugu yangu wa karibu sana.”53 Zaidi ya hayo, Muhammad 4 hakujitoa au kujifikiria kwamba yeye yupo juu ya sheria. Siku moja, alikwenda msikitini na akapanda kwenye mimbari ambapo aliwahutubia watu. Wakati wa hotuba yake alisema: “Mungu Aliyetukuka kabisa ameapa kwamba Yeye atatilia maanani vitendo vyovyote vya dhuluma au ukandamizaji kwa hiyo kwa jina la Mungu ninaomba sana yeyote ambaye ameteseka kutokana na dhuluma ya mikono ya Muhammad asimame na kulipa kisasi, kwani adhabu ya hapa duniani inapendeza zaidi kwangu mimi kuliko adhabu ya akhera, mbele ya malaika wa Mwenyezi Mungu na Mitume.”

Sawaadah ibn Qays akasimama na kusema: “Mama yangu na baba yangu wawe fidia kwa ajili yako ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Ulipokuwa unarudi kutoka Ta`if, mimi nilikuja   Sahih al-Bukhari, Juz. 5, uk. 152

53

42

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 42

6/18/2016 2:40:01 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

kukusalimia na wewe ulikuwa umepanda ngamia jike wako ukiwa umeshika fimbo mkononi mwako na ulipoinyanyua fimbo hiyo ilinipiga tumboni mwangu. Sikujua kama ulifanya hivyo kwa kukusudia au bila kukusudia.”

Mtukufu Mtume 4 akajibu: “Mungu na apishe mbali kwamba mimi niweze kufanya hivyo kwa kukusudia.”

Kisha Mtukufu Mtume 4 aliagiza fimbo yake iletwe na akamwambia Sawaadah alipe kisasi kwa kumpiga fimbo, kwa mfanano uleule. Sawaadah alisimama na akamwendea Mtukufu Mtume 4, lakini alimpofikia Mtukufu Mtume 4 alianza kuubusu mwili wake 4. Mtukufu Mtume 4 akamuuliza: “Hivi unalipa kisasi au unatoa msamaha wako?”

Ambapo Sawadah akasema: “Ninakusamehe.”

Halafu Mtukufu Mtume 4 akamwombea, akasema: “Mwenyezi Mungu na akusamehe na wewe pia.”54   Bihar al-Anwar, Bab fi Wafat al-Nabi

54

43

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 43

6/18/2016 2:40:01 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

Hiyo ndiyo ilikuwa tabia ya kiongozi huyu wa kidini na siasa ambaye alipewa uwezo wote wa kusimamia haki na kulinda sheria. 13. Ibada. Tangu mapema maishani mwake, alipokuwa anachunga kondoo mahali paitwapo al-Ajyad, Mtukufu Mtume 4 alikuwa anapenda upweke na faragha na alitumia saa nyingi akitafakari katika usalama wa jangwani. Alikuwa na desturi ya kutafakari na kuwaza juu ya mambo yote ya maumbile yaliyomzunguka. Alikuwa katika dunia nyingine tofauti kabisa na ile ya kabila lake na kamwe alikuwa hahudhurii mikusanyiko yao ya burudani na shamrashamra. Zaidi ya hayo, hakuwa akishiriki katika maadhimisho ya kipagani, wala hakuchafua mikono yake na mdomo wake kwa kula nyama ya kafara iliyotolewa kwa ajili ya masanamu.55 Alikamilisha safari yake ya tafakuri kwa haraka kupitia na hatua ya kwanza ya imani; Upweke wa Mungu (Tawhid). Ni kwamba, yeye alivikana vitu vyote, kwa kutumia hekima na tafakuri, isipokuwa Mungu Mmoja wa kipekee. Aliyachukia sana masanamu na alikuwa na desturi ya kusema, “Sichukii kitu kingine zaidi kama ninavyoyachukia masanamu haya.”56 Ili kuweza kupita   al-Sirah al-Nabawiyyah, Zaini Dahlan, uk. 95   al-Sirah al-Halabiyyah, Juz. 1, uk. 270

55 56

44

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 44

6/18/2016 2:40:01 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

kwenda hatua ya pili ya kutangaza Ummoja wa Mungu (Tawhidi), hatua ya uthibitishaji, moyo wake bora aliopewa na Mungu na fikira zinazotiririka kwa wingi vilipaa juu zaidi ya dunia ionekanayo. Nje ya mipaka ya dunia ionekanayo na katika jambo la kushangaza, na la mpito wa kasi sana, alimtafakari Muumba Mwenye enzi na wa Milele. Alikuwa na tabia ya kukiri hili moyoni mwake:

“Hakika mimi nimeuelekeza uso wangu kwa Yule Aliyeziumba mbingu na ardhi. Hali ya kuwa nimeacha dini za upotevu, tena mimi si katika washirikina.” (6:79)

Kuanzia hapo na kuendelea, mwambatano wake na upweke na kujitenga uliongezeka na akauona Mlima Hira kuwa mahali panapofaa kwa lengo lake. Alikuwa akitumia muda wake mwingi akiwa mahali hapo na mara kwa mara alikuwa akikimbilia hapo na kujipwekesha kwa usiku wa siku kadhaa mfululizo, akiwa na mahitaji kidogo, kwa lengo tu la kumwabudu Mungu Mmoja.57 Jambo la kusikitisha ni kwamba tabia yake ya kufanya ibada akiwa ndani ya pango la Mlima   Sahih al-Muslim, Juz. 1 uk. 97

57

45

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 45

6/18/2016 2:40:02 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

wa Hira limesahaulika na kwa hiyo limenyamaziwa kimya katika historia na hivyo ni sehemu ndogo sana inayoweza kuzungumziwa. Hapana mtu mwingine ambaye aliweza kupata kufika kwenye sehemu hiyo ya kimbilio na haijulikani kama Mtukufu Mtume 4 alikuwa akipiga magoti au alikuwa ananyanyua mikono yake kuelekea juu wakati wa dua au alikuwa akisujudu katika nyakati alizotumia ndani ya pango hilo. Inawezekana alikuwa anafanya yote haya. Kwa vyovyote vile, aliutambua uhalisia wa ibada. Kwa kweli, ibada haina maana nyingine zaidi ya kujikana, kuzingatia, kuwa tayari kuridhia (ridhaa), na kujisalimisha (taslim) kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye Kutukuka. Baada ya kuanza misheni yake ya Kitume, malaika Jibra`il alimfundisha kununi na taratibu za udhu na swala kama ambavyo zimeainishwa katika Sheria za Kiislamu (Shari`ah), na tangu hapo na kuendelea akaanza kuswali swala kwa masharti yale yale na vijenzi hivyohivyo kama vinavyozingatiwa leo hii, pamoja na utambuzi na uhudhurishaji wa moyo. Mtukufu Mtume 4 alikuwa na desturi ya kutumia muda mwingi wa usiku kila siku katika swala, dua, na minong’ono ya maombi (munaajaat) kwa kiasi kwamba miguu yake ilikuwa inavimba kwa sababu ya kusimama kwa muda mrefu. Aliichukulia ibada 46

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 46

6/18/2016 2:40:02 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

kwamba ni wajibu wa mja, na alikuwa akifanya ibada kwa shauku kubwa. Hakumuabudu Mwenyezi Mungu kwa matumaini ya kupata thawabu au kutokana na kuogopa adhabu. Wale ambao walikuwa wakizembea na kutojua kuhusu hali yake walikuwa wakimwambia kwa huruma kabisa: “Kwa nini unafanya hivi ambapo wewe uko huru kutokana na dhambi.” Na yeye alikuwa akijibu, “Hivi nisiwe mja mwenye kushukuru?” 58 Kwa nyongeza ya mwezi wa Ramadhani na sehemu kubwa ya mwezi wa Sha`ban, Mtukufu Mtume 4 alikuwa na desturi ya kufunga saumu kila baada ya siku moja katika kipindi cha mwaka mzima uliobakia.59 Alikuwa anakaa na kujitenga msikitini kwa muda wa siku kumi za mwisho za mwezi wa Ramadhani.60 Kwa upande mwingine, alikuwa na huruma kwa wengine. Alikuwa anasema: “Inatosha kwenu ninyi kufunga saumu kwa siku tatu katika kila mwezi. Fanyeni matendo mema mengi kwa kadiri muwezavyo. Kitendo kinachopendwa sana na Mwenyezi Mungu ni kile ambacho anayekifanya huambatana nacho kwa mfululizo, hata kama ni kidogo.”61   Sahih al-Bukhari, Juz. 2, uk. 50 na Sahih al-Muslim, Juz. 8, uk. 141   Sahih al-Bukhari, Juz. 2, uk. 50 60   Sahih al-Bukhari, Juz. 3, uk. 48 61   Sahih al-Muslim, Juz. 3, uk. 161 na 162 58 59

47

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 47

6/18/2016 2:40:02 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

Ingawa kwamba alifanya usahihisho au ubora wa baadhi ya vitendo vya ibada kuwa vyenye masharti, kutegemea juu ya hali mahususi ilivyo na wakati, kwa ujumla alikuwa na muono mpana wa matendo ya ibada na hakuweka mipaka katika kumwabudu Mungu mahali fulani mahususi au kwenye sherehe fulani au kwa maelekezo ya watu fulani. Yeye alichukulia kila sehemu hapa duniani kuwa ni msikiti - masjid (sehemu ya kufanyia sajida), aliwachukulia waja wote kuwa na uwezo wa kuunganika na Mwenyezi Mungu bila ya upatanishi wa yeyote, na alichukulia kila kitendo kizuri kuwa ni kitendo cha ibada kwa sharti kwamba kitendo hicho kilikuwa kitendo halali na chenye nia ya uaminifu. Mtukufu Mtume 4 alidhihirisha hili kwa uwazi katika miaka ya mwanzo ya kazi yake ya Utume wakati agizo la kuhamia Madina alipotolewa kwa ajili ya kuweka msingi wa Uislamu kwa kutangaza: “Yeyote ambaye kuhama kwake ni kwa ajili ya kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu na Mjumbe Wake, basi kuhama kwao ni kwa Mwenyezi Mungu na Mjumbe Wake; lakini mtu ambaye kuhama kwake ni kwa ajili ya jambo la kidunia, au kwa ajili ya kuoa mke, uhamaji wake ni kwa kile ambacho kwacho anahamia.� 48

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 48

6/18/2016 2:40:02 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

Alitegemeza kigezo kwa ajili ya kuamua usahihi wa vitendo vya watu kwa maelezo yafuatayo: “Vitendo hupimwa kufuatana na nia, na kila mtu atalipwa kufuatana na kile alichokinuia.” 62

Kitendo chochote, hata shughuli ya kila siku, ambayo kinatokana na nia nyofu kitachukuliwa kama ni kitendo cha ibada. Kama mume anaweka tonge la chakula kwenye mdomo wa mke wake,63 au akifanya tendo la ndoa na mke wake kwa lengo la kulinda usahili wake na asijiachie kuruhusu kujichafua kwa kutenda dhambi, basi yote haya ni ibada pia.64 Kama hakuna nia safi, basi hata swala na kufunga saumu ni vitendo ambavyo havitalipwa thawabu na Mwenyezi Mungu, pamoja na kwamba vinaweza kuonekana kuwa ni halali. Muhammad 4 pia aliona kwamba ni muhimu kulinda usawa kati ya maisha ya kimaada na kiroho na alikataza kuvuka mipaka. Alilaani kujitenga kwenye maisha ya kijamii, lakini pia alilaani kujiingiza kwenye ashiki za kinyama katika kiwango kilekile. Alionesha njia ya kati na kati baina ya hizo njia mbili kwa maneno   Sahih al-Muslim, Juz. 3, uk. 144   Sahih al-Bukhari, Juz. 7, uk. 62 64   Sahih al-Muslim, Juz. 3, uk. 82 62 63

49

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 49

6/18/2016 2:40:02 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

yake na vitendo vyake na aliwazuia wale ambao walitumia muda wao wote katika swala na saumu na wale ambao walikuwa wanapuuza mambo ya maisha ya kidunia kutokana ukengeukaji kwa kuwakumbusha kwamba: “Familia yako ina haki juu yako, mgeni wako anayo haki juu yako, na mwili wako una haki juu yako.”65

Wakati mmoja, alipokuwa kwenye moja ya safari zake, baadhi ya masahaba waliokuwa wameandamana naye walikuwa wamefunga na wengine hawakufunga. Wale waliokuwa wana swaumu walianguka kwa sababu ya kudhoofika kwao. Masahaba waliokuwa hawakufunga walisimika mahema na kuwanywesha maji vipando vyao. Kuona hivyo, Mtukufu Mtume 4 akasema: “Waliofungua saumu leo wamepokea thawabu.”66

Kwenye ukimya wa usiku, alikuwa na desturi ya kutumia muda mwingi akikesha na akiswali swala za usiku na nyuradi, lakini alipokuwa anaswalisha swala ya jamaa siku zote alikuwa mwangalifu kuhusu watu wengine na alikuwa akisema:   Sahih al-Muslim, Juz. 3, uk. 163   Sahih al-Muslim, Juz. 3, uk. 144

65 66

50

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 50

6/18/2016 2:40:02 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

“Ninaposimama kwenye swala huwa ninadhamiria kuirefusha, lakini ninaposikia sauti ya mtoto anayelia, huifupisha swala, kwani sipendi kumsumbua mama wa mtoto anayelia.”67

Katika tukio lingine, mtu mmoja alikuwa anawaongoza ngamia wawili waliotumika kwa malengo ya kilimo wakati usiku ulipoingia. Alimkuta mtu mmoja aitwaye Mu`adh anaswali kwa hiyo na yeye aliwasimamisha ngamia wake akajiunga katika swala. Mu`adh akasoma Surat al-Baqarah (Sura ya Ngo`mbe) na, kutokana na urefu wa Surah hiyo, yule msafiri akajitenga na swala hiyo ya jamaa na akaanza kuswali peke yake. Mu`adh alipewa taarifa ya jambo hili, na akasema kwamba mtu huyo alikuwa mnafiki. Wakati maneno hayo yalipofikishwa kwa msafiri huyo, mtu huyo alifadhaika na akaenda kwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu 4 kumtaarifu kile alichosema Mu`adh. Baada ya kusikia kile kilichotokea, Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu 4 alihuzunika na akamshauri Mu`adh: “Unawaogopesha na kuwafukuza watu. Ingekuwa bora kama ungesoma surah fupi, kwani nyuma yako wapo watu dhaifu, wazee, na watu wenye biashara zao za kushughulikia. Katika   Sahih al-Bukhari, Juz. 1, uk. 139

67

51

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 51

6/18/2016 2:40:02 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

swala ya jamaa, unatakiwa kuwafikiria wazee na watu dhaifu.”68

Mtukufu Mtume 4 alikuwa hapendi sauti ya juu katika dua kama ambavyo hufanywa mara nyingi na watu wapendao kujishaua. Wakati wa safari, wakati wowote masahaba wake walipopanda sehemu ya juu, walikuwa wakinyanyua sauti zao katika Takbir (kumtukuza Mwenyezi Mungu). Mtukufu Mtume 4 alikuwa na tabia ya kwenda karibu nao na kuwaeleza: “Enyi watu! Msitumie nguvu kubwa kwani mnamuita Yule ambaye sio kiziwi au ambaye hayupo. Mnamuita Yule Ambaye Husikia na Yu Karibu.”

Na katika maneno mengine: “……na yupo karibu nanyi kuliko shingo ya mnyama ambaye umemfanya kipando chenu.”

Na vile vile katika maneno mengine: “…..na Yeye yupo karibu zaidi nanyi kuliko mshipa mkubwa wa shingo zenu.”69

Sahih al-Muslim, Juz. 2, uk. 42   Sahih al-Bukhari, Juz. 4, uk. 57

68 69

52

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 52

6/18/2016 2:40:02 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

UFUPISHO: Katika sehemu ya kwanza ya makala hii iliyochapishwa katika toleo la nyuma, Ayatollah Zanjani alitoa maelezo mafupi kuhusu tabia njema alizozionesha Mtukufu Mtume Muhammad 4, wakati wote wa utoto wake, wakati akiwa kwenye matunzo ya walezi wake, na wakati wa ajira yake. Mtukufu Mtume 4 pia alionesha upendo na moyo wa kujitolea kwa mintarafu ya wasiojiweza, wakandamizwao, na watumwa. Katika kutoa maelezo haya, Zanjani amezipatia umuhimu tabia nzuri zinazopendeza ambazo Mtukufu Mtume 4 alizozitenda kwa ukamilifu mkubwa, baadhi ya hizo zikiwa ni usafi, usamehevu, ibada, na usuhubiano. Sehemu ya pili inaendelea na maelezo haya juu ya kajinyima, uimara, na kuheshimu kwake maoni ya watu. Katika kukamilisha misheni yake Mtukufu Mtume 4 aliwakomboa Waislamu kutokana na haja zao wenyewe, hivyo alithibitisha kwamba kujinyima ni tabia muhimu. Licha ya vikwazo vyote, alibaki kuwa mtu asiyeyumba katika imani yake. Zaidi ya hayo, alikuwa anathamini maoni ya watu na alionya dhidi ya kuingilia mambo ya watu wengine. Mtukufu Mtume Muhammad 4 aliishi maisha bora na ya uadilifu na aliweka mfano kwa wanadamu wote. Makala hii inazungumzia baadhi ya tabia bainifu za Mtukufu Mtume 4, ambazo tunaweza kujifunza 53

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 53

6/18/2016 2:40:02 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

kutoka kwenye aya za Qur`ani na kutoka kwenye mwenendo wa maisha yake alivyoishi. Kujinyima (zuhd): Mtukufu Mtume 4 aliondosha vitu vyote vya anasa na visivyo na umuhimu kutoka katika maisha yake na akaweka mfano wa uadilifu. Alikuwa na desturi ya kuketi chini, alikuwa akilala` kwenye mkeka uliotengenezwa kwa majani ya mtende70 na alikuwa akiegemeza kichwa chake juu ya mto wa ngozi iliyojazwa nyuzi za mtende.71 Chakula chake kikuu kilikuwa shayiri, mkate na tende. Kamwe hakushutumu chakula ambacho hakukipenda,72 alikuwa hali chakula hadi ajaze tumbo lake na wakati mwingine alikuwa akila mkate wa shayiri kwa muda wa siku tatu mfululizo.73 Alikuwa anafuturu kwa kula kiasi kidogo cha tende, na kama tende hazikuwepo, alikuwa akinywa tu funda chache za maji.74 Mke wake Aisha alisimulia hadithi kwamba wakati mwingine jiko lilikuwa haliwashwi moto kwa mwezi mzima.75 Alipopanda kipando cha farasi, aliku  Nur al-Absar, Juz. 26, uk. 26 na Bihar al-Anwar, Bab fi Makarim Akhlaq al-Nabi 71   Sahih al-Muslim, Juz. 6, uk. 145 72   Sahih al-Muslim, Juz. 8, uk. 217 73   Bihar al-Anwar, Bab fi Makarim Akhlaq al-Nabi 74   Sahih al-Muslim, Juz. 8, uk. 218 75   Sahih al-Bukhari, Juz. 4, uk. 190 70

54

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 54

6/18/2016 2:40:02 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

wa haweki mto wa kukalia na alikuwa akimwachia mtu mwingine apande farasi nyuma yake, kama haingesababisha madhara kwa mnyama. Alikuwa na tabia ya kushona viraka kwenye nguo zake yeye mwenyewe, alikuwa akishona viatu vyake yeye mwenyewe, alikuwa akimkamua kondoo wake yeye mwenyewe na alikuwa akisaga unga wake mwenyewe.76 Zaidi ya hayo, alikuwa anaisaidia famila yake kufanya kazi zingine za nyumbani. Na juu ya hayo, alikuwa akiisaidia familia yake katika kazi nyingine za nyumbani. Aidha alikuwa akienda msikitini kuswali mara tu aliposikia adhana ya mwadhini.77 Kwa kuwa lengo la Mtukufu Mtume 4 na masahaba wake lilikuwa ni kuwakomboa wanadamu kutoka kwenye uozo na kufutilia mbali kuabudu sanamu na kuwafanya huru, ingewezekanaje wao kuwa wabinafsi na watumwa wa matamanio yao? Kama wangekuwa na mojawapo ya tabia hizi, isingewezekana wao kuweza kuvumilia mateso kwa kipindi cha miaka mitatu kwenye bonde la mlima (shi`b) la Abu Talib, mahali ambapo waasi waliwazingira na kuwazuia wasipate chakula na bidhaa zingine.78 Vivyo hivyo, watu wa Makka wasio na makazi (as’haab al-suffah – maana yake ni watu wa   Nur al-Absar, uk. 27   Sahih al-Bukhari, Juz. 8 uk. 14 78   Imta` al-Asma`, Miqrirzi, Juz. 1, uk. 25 76 77

55

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 55

6/18/2016 2:40:02 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

varanda yenye matao na nguzo) wasingeweza kuishi kwenye jukwaa lililonyanyuliwa pembezoni mwa msikiti bila ya chakula, nguo, au hifadhi ya nyumba na bado wakavumilia shinikizo dhidi yao. Au katika vita vya Tabuk, kama wao wangekuwa watumwa wa matamanio yao, ingekuwa vigumu kwao kustahamili kwa subira mateso makubwa kupindukia, njaa, na kiu katika joto la Rasi ya Arabuni.79 Hata hapo shinikizo lilipopunguzwa, masahaba wa kweli waliendelea kuishi kama miti ya jangwa ambayo inapaswa kuishi kwa kutumia maji kidogo. Kwa vyovyote vile, tamaa ya makuu ya watawala waadilifu na wenye huruma hawakuwaruhusu wao kuishi maisha ya starehe na anasa almuradi umasikini na dhiki vilikuwepo na mahitaji ya msingi ya watu yalikuwa hayajatimizwa. Hiyo sio kusema kwamba Mtukufu Mtume 4, kwa hakika, alikuwa anapinga mtu kutajirika na kutumia utajiri huo kwa njia ya haki na halali. Kwa kweli, Mtukufu Mtume 4 aliunga mkono kwa hakika suala hili aliposema: “Msaada bora zaidi katika kujikinga dhidi ya uovu (kuwa na takua) ni ukwasi (ghinaa)”80 Yeye alichukulia utajiri kuwa ni njia ya namna ya kuishi 81 na alifundisha kwamba hakuna njia ambayo   Imta` al-Asma`, Miqrirzi, Juz. 1, uk. 472   Wasa`il al-Shi`ah, Bab al-Tijarah 81   Sura al-Nisa`; 4:5 79 80

56

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 56

6/18/2016 2:40:02 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

ni yenye kuleta matokeo yanayotarajiwa kuliko utajiri katika kufikia malengo ya mtu. Umadhubuti: Muhammad 4 hakupelekwa kwa uongozi wa kabila au taifa lakini pia alikuwa amepewa kazi ya ulimwengu wote “…..ili awe muonyaji kwa walimwengu wote.”82 Ilikuwa muhimu kwa Mtukufu Mtume 4 kuwakomboa wanadamu kutoka kwenye giza la tamaa na ujinga, kutoka katika ibada ya viumbe vyenye uhai na masanamu yasiyo na uhai, kutoka kwenye udhalimu na mamlaka ya watawala madikteta na madhalimu, kutoka kwenye uigaji usio na masharti wa watabiri na walaghai, kutoka kwenye upendeleo wa kimbari na tabaka, na kutoka kwenye umasikini wa mambo ya kidunia na kiroho. Pia alipelekwa kuwafanya huru wanadamu kutoka kwenye minyororo mingi ambayo ilikuwa imewafunga na iliyomomonyoa nafsi na miili yao na kubatilisha v­ igezo bandia na vya udanganyifu ambavyo vilikubaliwa na wao kwa karne nyingi na kama njia ya kutathimini tabia na sifa bainifu na kwamba kwa hakika hali hiyo ilionesha ubaya kama ndiyo uzuri, udanganyifu kama ndiyo ukweli, na uovu kama wema. Kwa ufupi, alitakiwa kubomoa dunia iliyofisadika na kuijenga tena dunia mpya bora zaidi.   Surat al-Furqan; 25:1

82

57

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 57

6/18/2016 2:40:02 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

Mwanzoni, wakati ambapo amri kwa ajili ya wito wa wazi kwenye Uislamu ilikuwa haijateremshwa na ambapo watu wachache tu ndio ambao walikwishageuka kuwa Waislamu, Makuraysh walifikiri kwamba Mtukufu Mtume 4 naye pia alikuwa mmojawapo wa hunafaa (waumini wa kweli, waumini katika imani ya Ibrahim) pamoja na Zayd bin Amr ibn Kufayl, Uthman ibn Huwayrith, na Waraqahb in Nawfal, ambao wakati mwingine walikuwa wakitoa maoni yao kuhusu mambo fulani ya theolojia, lakini kwa jumla hawakuwapa watu changamoto. Uhusiano baina ya walioingia dini ya Uislamu na Mtukufu Mtume 4 ulifikiriwa kuwa sawa na uhusiano wa mkuu wa kiroho na mwanafunzi wa utawa. Pamoja na kwamba hawakusababisha usumbufu, baadhi ya watu waliwaangalia kwa wasiwasi na kuwakasirikia.83 Mtukufu Mtume 4 hakuogopa kuswali na/au kufanya ibada hadharani kama alivyoonekana mara nyingi akiwa amesimama katika swala na Ali na mke wake, Khadija, pembezoni mwa Ka`bah. Siku moja, Afif al-Kindi aliwaona na akamuuliza Abbas bin Abdul-Mutallib, “Ewe `Abbas dini hii ni dini gani?” `Abbas akamjibu: “Huyu ni Muhammad bin Abdullah, ambaye anadai kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu   Imta` al-Asma`, Miqrirzi, Juz. 1, uk. 18

83

58

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 58

6/18/2016 2:40:02 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

amemuita kuwa mtume, na kwamba hazina za Kisra (Khusraw, Mfalme wa Sassanid wa Ajemi) na Qaysar (Kaisari, Mfalme wa Binzantini (Byzantine) zitafunguliwa kwa ajili yake. Huyu ni mke wake Khadija, binti Khuwaylid, ambaye amemwamini. Na yule kijana ni Ali bin Abi Talib ambaye ni binamu yake.”84

Miaka mitatu baada ya tukio hili, Mtukufu Mtume 4 alianza kufungua mwaliko kwenye Uislamu chini ya amri ya Mungu. Mwaliko wake umefupishwa kama ifuatavo: “Nimeleta kitu bora zaidi cha dunia hii na akhera. Ninyi mnaoabudu masanamu mpo kwenye upotofu, kwa sababu mnafuata nyayo za baba zenu na wahenga wenu. Masanamu haya hayana uwezo wa kipato na hasara. Ni Muumba wa dunia tu Ambaye Anastahili kutukuzwa na Ambaye anaweza kuwapeni thawabu kwa matendo yenu mema na kukuadhibuni kwa matendo yenu maovu. Ninawaonyeni dhidi ya njia ile mnayoifuata ambayo itasababisha ninyi kuadhibiwa adhabu inayoumiza.”

Maneno haya yalisikika kwa uzito masikioni mwa washirikina na yakawachanganya. Abu Lahab ambaye   Al-Sirah al-Halabiyyah, Juz. 1, uk. 334-337

84

59

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 59

6/18/2016 2:40:02 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

ni ami yake ndiye alikuwa wa kwanza kukataa mwaliko huo wa Mtume kwa sauti ya shari. Kuanzia siku hiyo na kuendelea, yeye na washirikina walisimama na kupinga na walipinga uenezaji wa Uisalmu. Upinzani wao haukuwa tu kwa sababu ya upendeleo juu ya imani zao za kidini na sehemu zake takatifu, lakini pia waliona dunia yao yote ikitishiwa na ujio wa hii dini mpya. Manufaa yao na hadhi yao ya kijamii vilitegemea hali ilivyokuwa katika bara Arabu wakati huo. Endapo mapinduzi au mabadiliko yangetokea, bila shaka mazingira yangebadilika na mamlaka yao ya juu na fursa zao vingetoweka. Washirikina walikuwa wameweka masanamu 360 ndani ya Ka`bah,85 na kila kabila la Kiarabu liliabudu sanamu moja au zaidi miongoni mwa masanamu hayo. Pia washirikina hao waliizingatia Ka`bah kuwa ni nyumba ya Mungu na aliwaweka kama walezi wake na kwa hiyo alilazimisha mamlaka yao juu ya makabila yote ya Waarabu. Wao walidhani kwamba wamekusanya kwa pamoja miungu ya mbinguni na ile ya hapa duniani ili kwamba kila mtu angeabudu sanamu lake analotaka kuliabudu. Kama wangeyatelekeza masanamu yao, wangeachilia fursa zote na manufaa ambayo walikuwa wanayapata kutoka kwenye ziara za kila wakati, utoaji sadaka na viapo vya mahujaji.   Sahih al-Bukhari, Juz. 5, uk. 45 na 46

85

60

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 60

6/18/2016 2:40:02 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

Zaidi ya hayo, kiburi na wivu ni vitu ambavyo viliwapofua na viliacha athari juu ya uzito wa nguvu ya upinzani wao. Abu Jahl alidhihirisha hili pale aliposema: “Tumeshindana na ukoo wa `Abd Manaf kwa ajili ya heshima na hadhi na wakatushinda katika uwanja wa mashindano ya mbio. Sasa wanadai kwamba mtume ametumwa kutoka miongoni mwao na wanataka kutushinda sisi. Kamwe hilo halitatokea.”86

Kuanzia hapo na kuendelea, Mtukufu Mtume 4 na wafuasi wake walikuwa katika shinikizo kubwa na walizuiwa kutekeleza ibada zao za kidini. Walilazimishwa kwenda kwenye bonde lililopo nje ya Makka ambako waliweza kuswali pamoja bila ya kuonekana.87 Waliteswa kwa kiwango kisichopimika na waabudu masanamu, ambao waliwalaza chini na kuweka mawe mazito yenye joto juu ya migongo yao na vifua vyao vya wazi wakati wakijaribu kuwalazimisha kuachana na dini ya Muhammad 4 na kukiri kwamba al-Lat na al-Uzzaa walikuwa ndio miungu wao.88 Waliwafunga kamba waumini kwenye shingo zao na kuwaburuza   Sirah ya Ibn Hisham, Juz. 1, uk. 388   Sirah ya Ibn Hisham, Juz. 1, uk. 275 88   Imta` al-Asma`, Miqrirzi, Juz. 1, uk. 18 86 87

61

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 61

6/18/2016 2:40:03 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

kwenye mabonde. Waliivisha miili yao iliyokuwa uchi mavazi ya kivita na kuwalaza kwenye jua kali. Baadhi yao walipigwa, walifungwa jela bila kupewa chakula na maji ya kunywa. Mtukufu Mtume 4 alihuzunishwa sana na kiwango hicho cha ukatili walichokuwa wanafanyiwa wafuasi wake. Siku moja, alimuona Ammar na mama yake Sumayyah, ambao walikaribia kukosa fahamu kama matokeo ya mateso ambayo waliyapata na akasema “Enyi familia ya Yasir, kuweni na subira! Hatima yenu ni peponi.” Baada ya muda, Yasir na mkewe Sumayyah waliuawa kishahidi,89 na kuwafanya wafia dini wa kwanza katika historia ya Uislamu. Makafiri wa ki-Kuraysh hawakuacha kumtukana na kumfedhesha Mtukufu Mtume 4 popote pale walipomkuta. Siku moja, wakati Mtukufu Mtume 4 alipokuwa kwenye sijida, Uqbah ibn Abi Mu`it aliweka majani yaliyotoka kwenye tumbo la ngamia mgongoni mwa Mtukufu Mtume 4 katikati ya mabega yake. Mtukufu Mtume 4 hakunyanyua kichwa chake hadi pale binti yake Fatimah (a) alipokuja na kuyaondoa. Katika tukio jingine, wakati Mtukufu Mtume 4 alipokuwa anaswali katika uwanja wa Ka`bah, mtu huyohuyo alikuja na akamkamata mabegani, akaikunja nguo yake kwenye shingo yake na akaanza   Al-Sirah al-Halabiyyah, Juz. 1, uk. 334-337

89

62

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 62

6/18/2016 2:40:03 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

kumkaba koo kikatili kabisa. Wakati huo, Abu Bakr akafika, akamkwida Uqbah mabegani na kumtupa mbali. Mtukufu Mtume 4 alikabiliana na mateso haya magumu kwa subira kabisa na aliendelea kuwalingania wafuasi wake kuwa na uvumilivu. Khabbab ibn Arat anasimulia: “Nilimlalamikia Mtukufu Mtume 4 (kuhusu mateso tuliyokuwa tunayapata kutoka kwa makafiri) alipokuwa kwenye kivuli cha ukuta wa Ka`bah. Nilisema, ‘Kwanini hutuombei msaada kwa Mwenyezi Mungu atunusuru?’ Aliketi chini huku uso wake umesawajika na akasema, ‘Muumini miongoni mwa waumini waliokuwepo kabla yenu alichanwa kwa chanuo la chuma kiasi kwamba haikubakia misuli au mishipa ya neva kwenye mifupa yake, lakini kamwe hilo halikumfanya aache dini yake. Msumeno ungeweza kuwekwa katikati ya kichwa chake na kichwa chake kupasuliwa vipande viwili, lakini yote hayo yasingemfanya aitelekeze dini yake. Wallahi! Dini hii itakamilishwa na kupata ushindi.’” 90

Katika tukio lingine, Mtukufu Mtume 4 aliambiwa “Waombee laana washirikina,” ambapo yeye akajibu, “Mimi sikutumwa kama mwombaji wa laana, bali mimi nimetumwa kama rehema.”91   Sahih al-Bukhari, Juz. 5, uk. 45 na 46   Sahih al-Muslim, Juz. 8, uk. 24

90 91

63

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 63

6/18/2016 2:40:03 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

Katika kupinga waziwazi umadhubuti wa Mtukufu Mtume 4, wapinzani wake kutoka kabila la Quraysh walizidisha ukaidi wao na wakadhamiria kubatilisha mwaliko wake kwa kuchafua jina lake na heshima yake nzuri na wakawa wanajaribu kutafuta madhaifu yake. Aliitwa mwendawazimu (majnuun, kwa maana ya mtu aliyetawaliwa na majini), mshairi, mtabiri, au mchawi kila mahali alipopita. Pia tetesi zilienezwa kwamba aliwatenganisha baba na watoto wao wanamume, au kuwatenganisha wake na waume zao kwa kutumia uchawi. Wakati wa msimu wa hijja, waliwashawishi wageni na wahujjaji kwa maneno ya upuuzi kwa lengo la kuwakatisha tamaa wasiwasiliane naye.92 Mwanzoni, Quraysh walimwendea Mtukufu Mtume 4 kwa namna ya kumtishia. Halafu, wakamwendea Abu Talib ambaye, miongoni mwa kundi lao alikuwa ndiye mtu pekee aliyekuwa anamuunga mkono Mtukufu Mtume 4 kwa dhati. Walifanya hivyo kwa lengo la kumshawishi asiendelee kumuunga mkono mpwa wake ingawa hakukubaliana nao. Mara Quraysh walipogundua kwamba vitisho vyao havikuleta matokeo waliyotarajia, walikimbilia kwenye hongo. Walimtuma `Utbah bin Rabi`ah kumwambia Mtukufu Mtume 4 kama alitaka utajiri wao walikuwa tayari   Sirah ya Ibn Hisham, Juz. 1, uk. 284

92

64

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 64

6/18/2016 2:40:03 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

kumfanya yeye kuwa mtu tajiri sana nchini hapo. Kama Mtukufu Mtume 4 alitaka mamlaka na utawala, wangemfanya yeye kuwa mtawala wao almuradi aache mwaliko wake kwenye Uislamu. Hata hivyo, Mtukufu Mtume 4 akajibu, kwa kukataa kwa namna ya dhahiri inayostahili daraja la Mitume waliotumwa kimungu: “Ninaapa kwa Jina la Mungu kwamba kama wakiweka jua kwenye mkono wangu wa kuume na mwezi kwenye mkono wangu wa kushoto iwe kama fidia ya mimi kuachilia mbali jambo hili (la kuwalingania watu kwenye Uislamu), kamwe sitaacha mpaka ama Mungu alifanye jambo hili lifuzu au mimi niangamie nikiwa katika kulitetea.”93

Kwa kifupi, wala sio vitisho ama hongo ama kashifa ama kule kuzingirwa kwa miaka mitatu kwenye bonde la Shi`b Abi Talib, ama njaa ama unyimwaji ama kutokuwa na makazi, ni mambo ambayo hayakuweza kuvunja umadhubuti wa Mtukufu Mtume 4. Baada ya miaka ishirini na tatu ya mapambano, alifanikisha lengo lake katika kufikisha ujumbe wa Uislamu kwa dunia nzima. Heshima juu ya maoni ya watu. Kuhusu masomo (mawdhuu) na hukumu (hukm) mambo ambayo yanaamuliwa na wahyi wa uhakika na   Sirah ya Ibn Hisham, Juz. 1, uk. 278

93

65

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 65

6/18/2016 2:40:03 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

maelezo yaliyo dhahiri (nass), pamoja na vitendo vya ibada na amali vilivyotungiwa sheria kimungu, Mtukufu Mtume 4 hakujipa haki yeye na mwingine yeyote kuingilia na kutoa maoni kuhusu mambo hayo. Kundi hili, hukumu, linapaswa kutekelezwa bila sharti, na ukiukaji wa hukumu hizo huchukuliwa kama kutokumwamini Mwenyezi Mungu kama ambavyo imetamkwa katika Qur`ani Tukufu: “Na wasiohukumu kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri.” (al-Maida; 5:44). Hata hivyo, wakati ilipokuja kwenye mambo yanayohusu maisha ya mtu binafsi na shughuli zake, kwa kuwa haya yaliruhusiwa, Waislamu walikuwa na haki ya kutoa maoni yao na uhuru wa kutenda. Hakuna aliyekuwa na haki ya kuingilia mambo binafsi ya watu wengine.94 Wakati ambapo mambo yalihusu jamii, Mtukufu Mtume 4 aliamini kwamba kila mtu alikuwa na haki sawa ya kutoa maoni yake. Pamoja na kwamba mawazo yake safi dhahiri na akili isiyokuwa ya kawaida vilizidi vya wengine katika kutambua maslahi ya umma, kamwe hakuwa na tabia ya udikiteta au kifalme na hakuonesha kutojali maoni ya umma. Siku zote alichukua maoni ya watu wengine na kuyazingatia wakati akitekeleza amri za Qur`ani na   Sahih al-Muslim, Juz. 8, uk. 10

94

66

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 66

6/18/2016 2:40:03 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

yeye alitaka tu Waislamu kuzingatia mwenendo huu wa kitume. Yalikuwepo matukio matatu katika Vita vya Badr ambapo Mtukufu Mtume Muhammad 4 aliwalingania masahaba wake kushauriana kwa pamoja na aliwaambia watoe maoni yao. Wakati wa tukio la kwanza, aliwataka masahaba wake wamshauri yeye kwamba wapigane vita na Quraysh au wasipigane nao na warudi Madina. Masahaba wake wote kwa pamoja walipendelea kupigana, kwa hiyo na yeye alikubaliana nao.95 Tukio la pili, alitaka ushauri wa masahaba wake kuhusu mahali pa kuweka kambi yao. Katika tukio hili Mtukufu Mtume 4 alikubaliana na ushauri wa Hubaab ibn al-Mundhir. Katika tukio la tatu, alitaka ushauri wa masahaba na wafuasi wake kwamba mateka wa kivita watendewe vipi. Baadhi yao walisema wauawe, wengine wakasema kwamba mateka waachiwe huru kwa malipo ya fidia. Mtukufu Mtume 4 alikubaliana na ushauri wa kundi la pili.96 Katika Vita vya Uhud, Mtukufu Mtume 4 aliwataka masahaba wake ushauri kuhusu stratejia (mbinu) bora zaidi ya kufuata. Alikubaliana na stratejia iliyopendelewa na wengi ya kutoka nje ya Madina na   Sirah ya Ibn Hisham, Juz. 2, uk. 253   Imta` al-Asma`, Miqrirzi, Juz. 1, uk. 78 na 97

95 96

67

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 67

6/18/2016 2:40:03 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

kukutana na majeshi ya Qur`aysh kuliko kubakia ndani ya ngome na kupigana humo.97 Katika vita ya Ahzab, Mtukufu Mtume 4 alifanya mashauriano ya haraka ya iwapo kama ama wayakusanye majeshi yao na kuyapanga nje ya Madina au wajihami wakiwa ndani ya jiji la Madina. Baada ya mashauriano hayo, ilikubalika kwamba Mlima wa Sal` utumike kama makao makuu ya jeshi la Uislamu na handaki lichimbwe kuwa kama kizuizi kwa lengo la kuwazuia maadui kuwashambulia.98 Wakati wa vita ya Tabuk, mfalme wa Rumi alitishika wakati jeshi la Uislamu lilipokaribia mpaka wa Syria. Hakuanzisha mashambulizi kwa sababu hakuliamini jeshi lake. Katika hali hii, Mtukufu Mtume 4 aliwakusanya maofisa wake wasifika na kwa kufuata kanunia za Kiislamu zilizowekwa kwa ajili ya ushauriano, aliwataka wampe maoni yao kama waingie kwenye nchi ya adui au warudi Madina. Kwa matokeo ya ushauriano huu wa kijeshi, iliamuliwa kwamba jeshi la Uislamu lirudi Madina.99 Inajulikana kwamba Waislamu wote wanaamini katika umaasumu wa Mtukufu Mtume 4 na hawaoni   Sirah ya Ibn Hisham, Juz. 3, uk. 7   Imta` al-Asma`, Miqrirzi, Juz. 1, uk. 220 99   Imta` al-Asma`, Miqrirzi, Juz. 1, uk. 463 97 98

68

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 68

6/18/2016 2:40:03 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

kitendo chake chochote kama ni cha kupingwa.100 Hata hivyo, Mtukufu Mtume 4 alikuwa mvumilivu kama akikosolewa hata kama ukosoaji huo haukuwa na umuhimu na kutokuwa na msingi, na alikuwa mwangalifu wa kutokuwaweka watu katika mazingira ya kuwabana. Badala yake, alikuwa na desturi ya kumfanya mkosoaji atambue kosa lake kwa kutumia hoja zenye nguvu alizozieleza kwa sauti ya chini na kwa namna ya uungwana. Alikuwa na desturi ya kuambatana na sheria ya kimaumbile ambayo Muumbaji wa dunia amewapa wanadamu wote uwezo wa kufikiri na kukosoa, na alikuwa anakubaliana kwa wazi kwamba uwezo huo haukuwa wa pekee kwa wale wenye ushawishi na mamlaka. Hakuruhusu kuwanyima watu  Inapaswa ifahamike kwamba Waislamu wote wanaamini katika umaasumu wa Mtukufu Mtume 4 kuhusu ujumbe wake, lakini kuhusiana na maisha yake binafsi kabla au baada ya misheni yake, kuna tofauti miongoni mwa madhehebu ya Uislamu. Shia wanaamini katika umaasumu wa Mtukufu Mtume 4 katika nyakati zote, kabla na baada ya misheni yake katika uwasilishaji wake wa ujumbe na pia katika maisha yake binafsi. Sunni wamegawanyika katika jambo hili. Kimsingi wao wanakubaliana katika umaasumu katika uwasilishaji wa ujumbe, lakini kuhusu maisha yake binafsi baadhi wanaamini katika uwezekano wa kutenda dhambi bila kukusudia na wengine wanaamini katika uwezekano wa kutenda dhambi ndogo ndogo. Kuhusu kipindi cha kabla ya kuanza kwa misheni yake kwa kawaida hawaamini katika umuhimu wa umaasumu. Kwa maelezo zaidi Tazama, Shomali, Mohammad Ali, katika kitabu chake kiitwacho Shi`i Islam: Origins, Faith &Practices (2001&2010), uk. wa 97 na 106. – (Mhariri -kitabu cha Kiingereza).

100

69

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 69

6/18/2016 2:40:03 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

uhuru wa kujieleza na kukosoa. Hususani aliwaagiza wafuasi wake kutumia uhuru kukabiliana na mtawala ambaye alifanya kitu kinyume cha sheria za haki kwa kukataa na kupinga kitu hicho. Katika tukio jingine, Mtukufu Mtume 4 alituma jeshi kufanya mapambano. Alimteua mtu kutoka miongoni mwa Ansar kuwa kamanda wa jeshi hilo na aliwaamuru wapiganaji kumtii kamanda huyo. Wakati wa mapambano, kamanda aliwakasirikia wapiganaji wake na akasema: “Hivi Mtukufu Mtume 4 hakuwaamuru ninyi kunitii mimi?” Wakajibu kwa kukubali. Halafu akasema: “Ninawaamuru mkusanye kuni na kukoka moto na halafu mjitupe ndani ya moto huo ninyi wenyewe.” Hivyo wanajeshi hao wakakusanya kuni na wakakoka moto, lakini walipotaka kuanza kujitupa kwenye moto, walianza kuwa na fikira tofauti. Wakaanza kutazamana na wakajiuliza: “Tulimfuata Mtukufu Mtume 4 ili kukwepa moto. Tulikubali Uislamu ili kujiokoa na ‘moto’ sasa kwa nini sisi tuuingie moto?” Walipokuwa katika hali ya kuchanganyikiwa, moto ulizimika na ulikwenda na hasira ya kamanda. Tukio hili lilifikishwa kwa Mtukufu Mtume 4 ambaye alisema: “Kama wangeingia kwenye moto kamwe hawangetoka humo (yaani kutoka kwenye moto wa dhuluma), kwani utii 70

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 70

6/18/2016 2:40:03 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

(kwenye amri ya mtu) unatakiwa pale tu anapoamuru yaliyo mema.”101

Katika vita vya Hunayn, Mtukufu Mtume 4 aliona ni jambo linalofaa kuwapa sehemu kubwa ya ngawira watu wa Makka ambao walikuwa wapya katika kuingia Uislamu. Sa`d ibn Ubaadah na baadhi ya Ansari kutoka Madina ambao walikuwa miongoni mwa mashujaa waliokuwa mstari wa mbele wakaonesha hisia zao za kutokuridhika na uamuzi wa Mtukufu Mtume 4 wa kugawa ngawira kwa upendeleo. Mtukufu Mtume 4 alipopata taarifa ya kutokuridhika kwao, aliwakusanya hao Ansari waliovunjika moyo pamoja, na kwa namna ya kujieleza yenye fasaha na ya kupendeza, aliwafanya watambue kuhusu sababu zilizopelekea yeye kufanya upendeleo huo na kutambua pia kosa lao wenyewe. Waliposikia maneno ya Mtukufu Mtume 4, Ansari waliokuwepo hapo waliangua kilio na kumwomba radhi.102 Katika tukio jingine ambalo lilitokea baada ya Vita vya Hunayn, mtu mmoja aitwaye Hurqus wa kabila la Tamim, (ambaye baadaye alipata kuwa mmojawapo wa wakuu wa Khawariji), alimlaumu Mtukufu Mtume 4 kwa kusema: “Kuwa mwadilifu katika ugawaji   Sahih al-Muslim, Juz. 6, uk. 16   Imta` al-Asma`, Miqrirzi, Juz. 1, uk. 431

101 102

71

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 71

6/18/2016 2:40:03 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

wako, Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Mtukufu.” Umari ibn Khattab alighadhibishwa na maneno hayo ya kijeuri na akamuomba Mtukufu Mtume 4 ampe ruhusa ya kumkata shingo Hurqus. Mtukufu Mtume 4 akasema: “Mwache!” Halafu Mtukufu Mtume 4 akamgeukia Hurqus na akasema kiungwana: “Ni nani basi anayeweza kuitwa mwadilifu kama mimi sio mwadilifu?”103 Kuhusu mikataba ya amani, Umari ibn Khattab alimkatalia kabisa Mtukufu Mtume 4 kuhusu masharti yasiyolingana ya mkataba wa Hudaybiyyah yaliofanywa na Mtukufu Mtume 4 na kabila la Quraysh. Mtukufu Mtume 4 hakumkasirikia sahaba huyo, badala yake alimshawishi kwa hoja yenye nguvu ya ushawishi.104 Bado katika tukio jingine, mtu mmoja alidai madeni yake kutoka kwa Mtukufu Mtume 4 katika namna ya kifidhuli hivyo kwamba masahaba wa Mtukufu Mtume 4 walitaka kumdhuru mtu huyo, lakini Mtukufu Mtume 4 akasema: “Mwacheni kwani yeye (mdai) anayo haki ya kudai. Nunueni ngamia wa umri wa ngamia anayedai na mpeni.” Masahaba wakatoa changamoto, “Lakini ngamia aliyopo ana   Sahih al-Bukhari, Juz. 4, uk. 200   Imta` al-Amsa`, Miqrirzi, Juz. 1, uk. 296

103 104

72

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 72

6/18/2016 2:40:03 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

umri mkubwa zaidi kuliko ngamia anayedai,” na Mtukufu Mtume 4 akajibu: “Mnunueni ngamia huyo halafu mpeni, kwani mbora zaidi miongoni mwenu ni wale wanaolipa madeni yao katika namna ya wema mkarimu zaidi.”105

Mtukufu Mtume 4 alikuwa amejaa moyoni mwake uadilifu wa haki na huruma. Katika njia hii, aliwafundisha watawala wa dunia hii jinsi ya kutawala ili watambue kwamba vyeo vyao na hadhi yao katika jamii ni kama sawa na baba mwenye huruma badala ya bwana mwenye amri zote, na kwamba siku zote wanapaswa kuzingatia maslahi bora zaidi ya raia wao badala ya kulazimisha matakwa na matamanio yao juu yao. Mtukufu Mtume 4 akasema: “Mimi ni mwenye kuzingatia zaidi na mwenye huruma kuhusu maslahi bora zaidi ya waumini kuliko walivyo wao wenyewe.” Pia alisema: “Qur`ani Tukufu inaeleza cheo na hadhi yangu katika maneno haya: ‘Nabii ni aula kwa waumini kuliko nafsi zao…’ (33:6). Kwa hiyo, ikiwa muumini wa kweli akifariki dunia na kuacha duniani rasilimali kadhaa, urithi wake utatolewa kwa warithi wake (kutoka uzao   Sahih al-Bukhari, Juz. 3, uk. 116

105

73

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 73

6/18/2016 2:40:03 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

wa baba), na kama akiacha deni ambalo linatakiwa kulipwa au watoto mafukara, basi mimi ndiye mlezi wao.�106 Taarifa na uzoefu wa tabia nzuri na sifa bainifu za uadilifu wa kiwango cha juu za Mtukufu Mtume 4 zilienea kwa mapana sana katika kipindi cha muda mfupi na zikaota mizizi ya kina katika nyoyo za Waislamu wa mwanzo kabisa hivyo kwamba walibadilisha kila kitu katika muundo ulio bora kadiri ilivyowezekana. Kupitia kwa Waislamu hao, Mtukufu Mtume 4 aliweza kubadili majivuno ya Waarabu na kuwa unyenyekevu, ukatili na kuwa huruma, kutokuwa na umoja na kuwa na umoja, kutoka kwenye ukafiri na kuwa na dini, kutoka kwenye uabudu masanamu na kuamini Mungu Mmoja, kutoka kwenye utengano na kuwa na mshikamano, kutoka kwenye ufisadi na kuwa safi, kutoka kwenye ulipizaji kisasi na kuwa wasemehevu, kutoka kwenye uzembe na kuwa katika kujishughulisha, kutoka kwenye ubinafsi na kuwa wenye kufikiria wengine, kutoka kwenye ukatili na kuwa wapole, kutoka kwenye uchoyo na kuwa katika kutojipendelea, na kuacha upumbavu na kuwa na busara na akili. Kwa kweli, njia ya maisha ya Mtukufu 4 ilikuwa ndio tafsiri kamili ya kivitendo ya Kitabu cha   Sahih al-Bukhari, Juz. 3, uk. 118

106

74

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 74

6/18/2016 2:40:03 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

Mwenyezi Mungu; Qur`ani Tukufu, ambayo aliipamba katika hatua zote mbalimbali za maisha yake.

75

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 75

6/18/2016 2:40:03 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

Orodha Ya Vitabu Vilivyo ­Chapishwa Na Al-Itrah Foundation 1.

i) Qur’ani Tukufu – Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili ii) Qur’an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thelathini 2. Uharamisho wa Riba 3. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza 4. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili 5. Hekaya za Bahlul 6. Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) 7. Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (a.s.) 8. Hijab vazi Bora 9. Ukweli wa Shia Ithnaashari 10. Madhambi Makuu 11. Mbingu imenikirimu 12. Abdallah Ibn Saba 13. Khadijatul Kubra 14. Utumwa 15. Umakini katika Swala 16. Misingi ya Maarifa 17. Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia 18. Bilal wa Afrika 19. Abudhar 20. Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu 76

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 76

6/18/2016 2:40:03 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

21. Salman Farsi 22. Ammar Yasir 23. Qur’an na Hadithi 24. Elimu ya Nafsi 25. Yajue Madhehebu ya Shia 26. Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur’an Tukufu 27. Al-Wahda 28. Ponyo kutoka katika Qur’an 29. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii 30. Mashukio ya Akhera 31. Al Amali 32. Dua kwa Mujibu wa Ahlulbayt (a.s) 33. Udhuu kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna 34. Haki za wanawake katika Uislamu 35. Mwenyezi Mungu na sifa zake 36. Kumswalia Mtume (s) 37. Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) 38. Adhana 39. Upendo katika Ukristo na Uislamu 40. Qur’ani na Kuhifadhiwa Kwake 41. Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu 42. Kupaka juu ya khofu 43. Kukusanya Sala Mbili 44. Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara 77

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 77

6/18/2016 2:40:03 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

45. Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya 46. Kusujudu juu ya udongo 47. Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) 48. Tarawehe 49. Malumbano baina ya Sunni na Shia 50. Kupunguza Swala safarini 51. Kufungua safarini 52. Umaasumu wa Manabii 53. Qur’an Yatoa Changamoto 54. as-Salaatu Khayrun Mina -’n Nawm 55. Uadilifu wa Masahaba 56. Dua e Kumayl 57. Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu 58. Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake 59. Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata 60. Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mtume Muhammad (s) 61. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza 62. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili 63. Kuzuru Makaburi 64. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza 65. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili 66. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu 67. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne 68. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano 69. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita 78

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 78

6/18/2016 2:40:03 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

70. Tujifunze Misingi Ya Dini 71. Sala ni Nguzo ya Dini 72. Mikesha Ya Peshawar 73. Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu 74. Ubora wa Imam ‘Ali na Ushia ndio njia iliyonyooka 75. Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake 76. Liqaa-u-llaah 77. Muhammad (s) Mtume wa Allah 78. Amani na Jihadi Katika Uislamu 79. Uislamu Ulienea Vipi? 80. Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) 81. Dhana ya Ndoa ya Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) 82. Urejeo (al-Raj’ah) 83. Mazingira 84. Utokezo (al - Badau) 85. Hukumu ya kujenga juu ya makaburi 86. Swala ya maiti na kumlilia maiti 87. Uislamu na Uwingi wa Dini 88. Mtoto mwema 89. Adabu za Sokoni Na Njiani 90. Johari za hekima kwa vijana 91. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza 92. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili 93. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu 94. Tawasali (AT- TAWASSUL) 79

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 79

6/18/2016 2:40:03 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

95. 96. 97. 98. 99. 100. 101. 102. 103. 104. 105. 106. 107. 108. 109. 110. 111. 112. 113. 114. 115. 116. 117. 118. 119.

Imam Mahdi katika Usunni na Ushia Hukumu za Mgonjwa Sadaka yenye kuendelea Msahafu wa Imam Ali Maimamu wa Ahlul Bait – Ujumbe na Jihadi Idi Al-Ghadir Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu Hukumu zinazomuhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi Huduma ya Afya katika Uislamu Sunna za Nabii Muhammad (saww) Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) Shahiid Mfiadini Mwanamke Na Sharia Ujumbe -Sehemu ya Kwanza Ujumbe - Sehemu ya Pili Ujumbe - Sehemu ya Tatu Ujumbe - Sehemu ya Nne Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu Hadithi ya Thaqalain Ndoa ya Mutaa Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza Ukweli uliopotea sehemu ya Pili Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu Ukweli uliopotea sehemu ya Nne

80

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 80

6/18/2016 2:40:04 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

120. Ukweli uliopotea sehemu ya Tano 121. Mkutano wa Maulamaa wa Baghdad 122. Safari ya kuifuata Nuru 123. Fatima al-Zahra 124. Myahudi wa Kimataifa 125. Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi 126. Visa vya kweli sehemu ya Kwanza 127. Visa vya kweli sehemu ya Pili 128. Elimu ya Ghaibu ya Maimamu 129. Mwanadamu na Mustakabali wake 130. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) 131. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) 132. Khairul l’Bariyyah 133. Uislamu na mafunzo ya kimalezi 134. Vijana ni Hazina ya Uislamu 135. Adhana ni Ndoto au ni Wahyi? 136. Tabaruku 137. Saada Kamili – Kitabu cha Kiada cha Maadili 138. Vikao vya furaha 139. Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 140. Visa vya wachamungu 141. Falsafa ya Dini 142. Kuhuzunika na Kuomboleza 143. Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah 81

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 81

6/18/2016 2:40:04 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

144. Mjadala wa Kiitikadi 145. Kuonekana kwa Allah 146. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) 147. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) 148. Ndugu na Jirani 149. Ushia ndani ya Usunni 150. Maswali na Majibu 151. Mafunzo ya hukmu za ibada 152. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1 153. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2 154. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 155. Abu Huraira 156. Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. 157. Mazingatio kutoka katika Qur’an - Sehemu ya Kwanza 158. Mazingatio kutoka kaitka Qur’an - Sehemu ya Pili 159. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza 160. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili 161. Shia na Qur’ani – Majibu na Maelezo 162. Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) 163. Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani 164. Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu 165. Uislamu Safi 166. Majlisi za Imam Husein Majumbani 167. Je, Kufunga Mikono 168. Uislam wa Shia 82

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 82

6/18/2016 2:40:04 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

169. Amali za Makka 170. Amali za Madina 171. Asili ya Madhehebu katika Uislamu 172. Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi 173. Ukweli uliofichika katika neno la Allah 174. Uislamu na Mifumo ya Uchumi 175. Umoja wa Kiislamu na Furaha 176. Mas’ala ya Kifiqhi 177. Jifunze kusoma Qur’ani 178. as-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah 179. Hayya ‘Alaa Khayri’l-’Amal Katika Adhana 180. Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura 181. Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na Ramadhani) 182. Uadilifu katika Uislamu 183. Mahdi katika Sunna 184. Maswali Ya Uchunguzi Kuhusu Uislam 185. Kazi na Bidii ni njia ya maendeleo 186. Abu Talib – Jabali Imara la Imani 187. Ujenzi na Utakaso wa Nafsi 188. Vijana na Matarajio ya Baadaye 189. Historia maana na lengo la Usalafi 190. Ushia – Hoja na Majibu 191. Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) 192. Maombolezo – Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) 193. Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu 83

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 83

6/18/2016 2:40:04 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

194. Takwa 195. Upotoshaji Dhahiri katika (Turathi) Hazina ya Kiislamu 196. Amirul Muuminina (as) na Makhalifa 197. Tawheed Na Shirki 198. Kuvunja hoja iliyotumika kutetea Uimamu wa AbuBakr 199. Adabu za vikao na mazungumzo 200. Hija ya Kuaga 201. Uwazi baina ya Maslahi na Vikwazo 202. Fadhila za watukufu watano katika Sahih Sita 203. Mdahalo baina ya Mwanachuoni waKisunni na Kishia (Al- Muraja’aat) 204. Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (as) 205. Imam Husain ni Mfumo wa Marekebisho na Mageuzi 206. Mtazamo kuhusu msuguano wa Kimadhehebu 207. Nchi na Uraia – Haki na wajibu kwa Taifa 208. Mtazamo wa Ibn Taymiyyah juu ya Imam Ali (as) 209. Uongozi wa Kidini – Maelekezo na Utekelezaji wa Kijamii 210. Maadili ya Ashura 211. Mshumaa – Shahidi na Kifo cha Kishahidi 212. Mizani ya Hekima – Hadithi za Ahlul Bait (as) – Sehemu ya Kwanza 213. Imam Ali na Mambo ya Umma 214. Imam Ali na Mfumo wa Usawa 215. Uimamu na Tamko la Kutawazwa 216. Mfumo wa Wilaya 217. Vipi Tutaishinda Hofu? 84

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 84

6/18/2016 2:40:04 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

218. Kumswalia Mtume ni Ufunguo wa Utatuzi wa Matatizo 219. Maeneo ya Umma na Mali Zake 220. Nahju ‘L-Balagha– Majmua ya Khutba, Amri, Barua, ­Risala, Mawaidha na Semi za Amirul-Muuminin Ali bin Abu Talib (a.s.) 221. Mukhtar – Shujaa aliyelipiza kisasi dhidi ya wauaji wa Imam Husein (as) hapo Karbala 222. Mazingatio Katika Swala 223. Imam Hasan na Mfumo wa Kujenga Jamii 224. Vyakula Na Vinywaji 225. Kuelewa Rehema ya Mwenyezi Mungu 226. Imam Mahdi na Bishara ya Matumaini 227. Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu 228. Shia Na Sahaba - Majibu na Maelezo 229. Majanga Na Jukumu la Jamii 230. Shia Na Hadith - Majibu na Maelezo 231. Upotofu Ndani ya Kitabu cha Mitaala kwa Shule za Sekondari 232. Ugaidi Wa Kifikra Katika Medani Ya Kidini 233. Yafaayo kijamii 234. Uswalihina Dhahiri Na Batini Yake 235. Mkakati wa Kupambana na Ufakiri 236. Mwanamke Katika Harakati Za Mageuzi 237. Jihadi 238. Hija Katika Maneno Na Ujumbe Wa Imam Khomeini (R.A) 239. Tiba Ya Maradhi Ya Kimaadili 85

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 85

6/18/2016 2:40:04 PM


MUHTASARI WA SIFA BAINIFU ZA MTUME MUHAMMAD (SAWW)

240. Yusuf Mkweli 241. Taqiyya Kwa Mujibu Wa Sheria Ya KIISLAMU 242. Imam Mahdi (A.S) Imam Wa Zama Hizi Na Kiongozi Wa Dunia 243. Talaka Tatu 244. Safari Ya Kuelekea Kwa Mwenyezi Mungu 245. Hotuba Za Kiislamu Juu Ya Haki Za Binadamu 246. Mashairi Ya Kijamii 247. Ngano Ya Kwamba Qur’ani Imebadilishwa 248. Wito Kwa Waumini: “Enyi Mlioamini” 249. Imam Husain (a.s) ni Utu na Kadhia 250. Imam Husain ni Kielelezo cha Kujitoa Muhanga na Fidia 251. Imam Mahdi ni Tumaini la Mataifa 252. Kuchagua Mchumba 253. Mazungumzo ya Umoja – Ukosoaji na Usahihishaji 254. Utamaduni wa Mwamko wa Kijamii 255. Hekima za kina za Swala 256. Kanuni za Sharia za Kiislamu 257. Utamaduni kufuatana na Qur’ani na Utekelezaji wa Kivitendo (Sehemu ya Kwanza) 258. Kauli sahihi zaidi katika kufafanua Hadithi

86

14_16_Muhtasari wa Sifa_(4-75 inch x 7 inch)_18_June_2016 .indd 86

6/18/2016 2:40:04 PM


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.