Mwanamke na sharia

Page 1

MWANAMKE NA SHARIA ‫المرأة والشريعة‬ Kimeandikwa na: Allamah Sayyid Zeeshan Haider Jawadi

Kimetarjumiwa na: Alhaji Ramadhani S.K. Shemahimbo

Kimehaririwa na: Alhaji Hemedi Lubumba

Kimepitiwa na: Mbaraka A. Nkanatila


‫ترجمة‬

‫المرأة والشريعة‬

‫تأ ليف‬ ‫السيد ذي شأن حيدر الجواد‬

‫من اللغة اإلنجليزية الى اللغة السوا حلية‬


© Haki ya kunakili imehifadhiwa na: Al-Itrah Foundation ISBN No: 978 - 9987 – 17 – 058 – 6 Kimeandikwa na: Allamah Sayyid Zeeshan Haider Jawadi Kimetarjumiwa na: Alhaji Ramadhani S.K. Shemahimbo Kimehaririwa na: Alhaji Hemedi Lubumba Kimepitiwa na: Mbaraka A. Nkanatila Kimepangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation Toleo la kwanza: Julai, 2014 Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. - 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: www.alitrah.info



YALIYOMO Neno la Mchapishaji.......................................................................1 Balehe .............................................................................................3 Dalili za Balehe................................................................................7 Hukmu za Janaba...........................................................................10 Namna ya kuchukua josho ............................................................ 11 Mambo yasiyoeleweka vizuri .......................................................12 Mambo Yanayokatazwa Wakati wa Janaba ..................................13 Hedhi (Kipindi cha damu ya mwezi) ............................................16 Aina Za Hedhi ...............................................................................16 Yaliyoharamishwa (makatazo) Wakati wa Hedhi .........................20 Mukhtasari wa Kanuni za Hedhi ...................................................28 Istihadha.........................................................................................30 Kanuni za Istihadha .......................................................................32 Baadhi ya Kanuni za Kijumla .......................................................34 Nifaas (Damu baada ya Uzazi) .....................................................36 Baadhi Ya Kanuni Nyingine .........................................................40 Hijaab ............................................................................................40 v


Mwanamke Na Sharia

Hukmu za Maiti ............................................................................42 Kanuni za Swala ...........................................................................43 Saumu ...........................................................................................46 Khums na Zaka. ............................................................................48 Kanuni za Hijja .............................................................................48 Kanuni za Ndoa .............................................................................53 Kanuni za Kuangalia (kutupia macho) .........................................63 Baadhi ya Kanuni za Kijamii ........................................................67 Kanuni za Malezi (Unyonyeshaji) ................................................71 Matatizo ya Unyonyeshaji ............................................................73 Taratibu za Unyonyeshaji .............................................................76 Taratibu za Talaka .........................................................................78 Talaqa al-Khul’a ............................................................................82 Talaqa al-Mubarat .........................................................................83 Mas’ala Mbalimbali ya Talaka ......................................................83 Mirathi ...........................................................................................86 Mirathi Kutoka kwa Mke Aliyeolewa ...........................................88

vi


Mwanamke Na Sharia

‫بسم اهلل الرحمن الرحيم‬ NENO LA MCHAPISHAJI

M

wanamke na Sharia ni kitabu chenye maudhui yanayohusiana na sheria zinazowahusu wanawake kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu. Kama tunavyosema wakati wote kwamba Uislamu ni dini na mfumo kamili wa maisha, haukuacha lolote linalomhusu mwanadamu kimwili au kiroho na kuweka sheria ya kuyaendesha maisha hayo (kiroho na kimwili). Katika kitabu hiki mwanachuoni huyu anazungumzia kuhusu sheria zinazowahusu Wwanawake kwa mtazamo wa Kiislamu, kama vile ndoa, talaka, tohara, swala, saumu, Hija, zaka, sadaka, mirathi, umiliki wa mali, n.k. Sisi kama wachapishaji tunakuleteeni kitabu hiki kama kilivyo kwa wasomaji wetu na kuwashauri wasome yaliyomo humo, wayafanyie kazi na kuyazingatia na kufaidika na hazina iliyoko ndani yake. Hii ni moja kati ya kazi kubwa zilizofanywa na Taasisi ya AlItrah katika kuwahudumia kielimu wasomaji wake wazungumzaji wa Kiswahili. Na kwa maana hiyo hiyo imeamua kukichapisha kitabu hiki chenye manufaa makubwa kwa lugha ya Kiswahili kwa lengo lake lile lile la kuwahudumia Waislamu, hususan wanaozungumza Kiswahili. 1


Mwanamke Na Sharia

Tunamshukuru Ndugu yetu Alhaji Ramadhani S. K. Shemahimbo kwa kukitarjumi kwa Kiswahili kitabu hiki, insha’Allah Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jallah amlipe kila la kheri hapa duniani na huko Akhera pia; bila kuwasahau na wale wote waliochangia kwa namna mmoja au nyingine mpaka kufanikisha kuchapishwa kwake. Allah Mwenye kujazi awalipe wote malipo mema duniani na Akhera pia. Mchapishaji Al-Itrah Foundation.

2


Mwanamke Na Sharia

‫بسم اهلل الرحمن الرحيم‬ MWANAMKE NA SHARIA Kuanza kwa Maisha ya Mwanamke

BALEGHE

K

wa mujibu wa Sheria ya Kiislam (Sharia) pale umri wa msichana unapokuwa ni miaka tisa, anahesabiwa kuwa amefikia utu uzima (amebaleghe), kwa umbile anakuwa ama ni dhaifu au mwenye nguvu – anakuwa ni mrefu au mfupi wa kimo – na anakuwa miongoni mwa wasichana wanaocheza au mtu mwenye wajibu ndani ya nyumba. Athari ya kwanza kabisa ya kubaleghe kwake ni kwamba, Mwenyezi Mungu baada ya kuona ubora wa hali yake ya kimwili na kiroho anampamba na majukumu yote ya Amri Zake – ya wajibu yanafanywa kuwa wajibu juu yake – makatazo (haramu) yanaharamishwa, na kwa namna hii anamjaalia mwanamke hali ya hadhi ambayo mwanamume anaipata baada ya miaka sita. Katika nyakati za zamani, mwanamke alikuwa anachukuliwa kama kiumbe asiyetegemewa, na wala kumpa mafunzo hakukufikiriwa juu yake na wala hakupewa majukumu yoyote, na wakati wote wito huo huo ulisikika kwamba yeye ni mwenye akili yenye mapungufu na asije akapewa kazi yoyote ya wajibu na wala kazi ya akili au ya mawazo ya haraka isitakiwe kutoka kwake, ilichukuliwa kwamba 3


Mwanamke Na Sharia

umbile lake ni kwa ajili ya kufanya kazi nyumbani tu, na kupitisha maisha yake jikoni akibuni orodha mpya ya vyakula ili kuwaridhisha wanamume. Huu ulikuwa ndio ubora pekee ambao mwanamke alitambulika kuwa nao na vipaji vyake vilizungumziwa kwa mbali kwamba mwanamke fulani wa nyumbani anapika vyakula vizuri kabisa, na kababu za nyumba hiyo hazina kifani. Halijawahi kusikika hili la kusema kwamba wanawake wa nyumba fulani ijapokuwa hawana utaalamu katika mapishi na hawajui lolote isipokuwa dal na roti, lakini miongoni mwao kuna wanawake wema na bora wanaoweza kuonekana. Kinyume chake ni kwamba hata wanawake watu wazima katika nyumba vilevile wakati wanapochagua mkwe wa kike walikuwa wanasisitiza juu ya utaalamu wa jikoni kuliko uwezo wa kiakili, na kama, Mungu aepushilie mbali, licha ya kuwa na shahada za kisomi, hakuweza kuwapikia chakula kizuri, alikuwa anastahili hizaya kwamba, kuna faida gani ya shahada hizi wakati hawezi hata kupika chakula cha sawasawa. Kutoweza kupika kwa wanaume hakukuwa ni kasoro, lakini kulikuwa ni kasoro kubwa sana kwa wanawake, ambako kwa namna fulani kulikuwa ni tamko kwamba wanamume wameumbwa kwa ajili ya nyanja za kiutendaji na shule za elimu na maarifa, na wanawake wameumbwa kutumikia tumbo na jiko. Lakini maumbile vile vile hayawezi kuvumilia maonevu kwa muda mrefu, na zama zikageuka, na wasichana wakatoka nje ya jiko kuelekea kwenye Madrasa na mashule, matokeo yakawa kwamba wasichana wako mbele na wana mafanikio ya wastani kuliko ya wavulana, na hii sio kwa sababu wasichana hawana majukumu mengine mbali na kujisomea na wavulana nao wana majukumu ya kijamii – bali siri ya hili imejificha katika ule uwezo wa asili ambao unaonyeshwa na mwanamke mbele ya mwanamume, na kwa sababu 4


Mwanamke Na Sharia

ya hili Uislamu umeweka kubaleghe kwake kuwa miaka sita kabla ya mwanamume, na kumfanya aanze kuwajibika na maamrisho ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kabla ya mwanamume. Kwa kweli kutimiza miaka tisa, katika maisha ya mwanamke, ni siku ya namna ya furaha ambayo kamwe haijirudii yenyewe, hii ndio siku ambayo Mola wa ulimwengu anamtangazia yeye kuwa ana hadhi ya uwajibikaji, naye anathibitisha mawazo na hisia zake kama zilizopevuka. Hii ndio siku ambayo Uislamu unamfanya yeye kuwa mwenye kuwajibika na maamrisho yake ya mambo ya wajibu na makatazo yake, na unataka kutoka kwake usalama wa Sharia zake. Hii ndio siku ambayo vitendo vyake vinakubalika kwa ajili ya wengine, na kufanya kazi yoyote ya wajibu yenye ufanisi, basi inatosheleza kwa ajili ya wengine pia. Hii ndio siku ambayo shughuli zake zote zinastahili kutambulika, na kufanya biashara kwake na mahusiano mengine yanapata utambulikaji uliothubutu. Hivi ni vishawishi vya kishetani tu kule kusema kwamba, masikini mwanamke amefungwa kwenye kamba ya majukumu wakati ambapo mwanamume anazurura huru tu hadi umri wa miaka kumi na tano, vinginevyo kwa kweli hili ni tangazo la heshima na hadhi ya mwanamke, mtoto mdogo asiyejua lolote hapewi malaki ya rupia kwani atazipoteza na kuziharibu, hivyo Mwenyezi Mungu hatatoa amri Zake mpaka awe ameridhika kabisa juu ya mawazo na silika zake, na Yeye kwa hakika amemuona mwanamke huyo kuwa anao wepesi wa kuhisi na kufahamu. Ni muhimu kwamba mwanamke atambue utukufu wake katika Uislamu na ainamishe kichwa chake (kusujudu) kwa wingi wa 5


Mwanamke Na Sharia

shukurani kwa kuvuka katika mipaka ya upevu (kubaleghe), kwa vile Mwenyezi Mungu amemfanya yeye kuwa muwajibikaji katika amri Zake kabla ya wanamume na amemchukulia kuwa mpokeaji wa maneno Yake, na heshima ambayo si kila kiumbe huipata.

6


Mwanamke Na Sharia

DALILI ZA BALEGHE

B

aada ya kufikia baleghe mwili huwa umekamilisha hatua yake ya kwanza ya ubora, hivyo mwenendo wa awamu mpya unaanzishwa ndani yake, na ndani ya msichana huyo mnazaliwa tamaa ya mbali ambayo yeye hana uzoefu nayo na kwa hivyo anakuwa hana ufahamu hata wa jina lake, tamaa ambayo katika mazungumzo ya kawaida inaitwa ashiki au matamanio, utajo huu umekuwa sio maarufu sana kiasi kwamba hata maelezo yake yanamfanya mtu aone aibu, kwani hakuna mwanadamu katika ulimwengu huu ambaye anaweza kupatika asiyepatikana na tabia hii bainifu na wala ambaye maisha yake yameepukana na hawaa. Faida kubwa kabisa ya hawaa hii ni kwamba inaandaa na kuzalisha idadi ya watu duniani, na kama tutakaa mbali nayo hakutakuwa na zana yoyote ya kuongezea idadi ya watu duniani. Hawaa hii hii inamuita mtu atoke nje kwenye maisha ya jamii kutoka kwenye upweke na mtu ambaye alijifikiria kuwa mtu kamilifu, inamkumbusha juu ya udhaifu wake, na kumsimulia kwamba Mungu Muumba hakumuumba yeye peke yake kabisa bali amebuni kiumbe kingine pia kwa ajili ya ukamilifu wa maisha yake na amemfanya kuwa chombo cha kukamilishia utu wake. Silka hii ya upweke na udhaifu inazaliwa ndani ya kila mtu baada ya kufikia baleghe awe mwanamume au mwanamke, inaelekea kwamba ule udhaifu ambao mwanadamu amezaliwa nao unakuwa hauleti maana yoyote wakati wa utoto wake, bali zile silka zinapokomaa, udhaifu wa nafsi huzaliwa, na hii ndio rehma ya Mola Ambaye ametutunuku ile fursa ya kuhisi udhaifu ambao matokeo yake ni kwamba yale mawazo ya kuuondoa (udhaifu huo) pia hujitokeza, vinginevyo mtu ambaye haogopi maradhi hatoki kwenda 7


Mwanamke Na Sharia

hata kutafuta matibabu yake. Matamanio haya ya maisha ya kijamii na kuishi kwa pamoja yanapanuka kwa upande wa ndani, na hivyo kuna njia mbili za kuyaeleza: 1.

Wakati mwingine yanaandaliwa kihalali au kinyume chake, hivyo ili mtu kukidhi matamanio yake anakutanisha mwili wake na mwili wa mwingine, ambavyo kwa kawaida inaitwa kujamiiana, kuingiliana au wenza wa kitandani na kadhalika, ambako kwamba matamanio ya asili yanatimizwa pale kile kiini (maji) cha ndani kinachochemka kinapotoka.

2.

Na endapo hakuna maandalizi yanayopatikana kwa ajili ya kutimiza matamanio hayo, hapo basi kile kiini kinaendelea kuchemka huko ndani na hatimaye homa au joto la hali hii linaitawala akili kwa nguvu sana kiasi kwamba mtu anatimiza haja yake katika ndoto na anajihisi kwamba ameunganisha nafsi yake na sehemu yake mwenyewe ya ubora, ambayo matokeo yake kile kiini kinatoka, ambacho kilishambulia akili na kumlazimisha kupata ndoto kama hiyo.

Jambo hili huwa linajitokeza kwenye maisha ya mwanamume na ya mwanamke pia – kwa maana kwamba kwa vile kitendo cha kujamiiana kinatokea kwa wote wawili – na njia hii katika ulimwengu wa ndoto pia wote wanashiriki, na ndoto kama hizo zinaweza kuonekana kwa wote, wanamume na wanawake vilevile. Majimaji yale yanayotoka kwa sababu ya ndoto hii yanaitwa manii, yenye rangi kama nyeupe hivi na mnato na hali inayojitokeza kutokana na jambo hili inaitwa hali ya janaba ambayo inawapata wote, mwanamume na mwanamke. Jambo hili linaweza kutokea kihalali kama kwa kuota au kwa kujamiiana mtu na mke wake, na kwa kitendo cha zinaa 8


Mwanamke Na Sharia

au kupiga punyeto (kujikojoza), vitendo vyote hivi ni vibaya na vimeharamishwa, lakini kama mwenye bahati mbaya amehusika kwenye kitendo hiki, basi kwake yeye, mwanamume au mwanamke, vilevile ile hali ya janaba itamtokea. Na hali hii pia huwakuta wanamume kwenye mahusiano ya kuingiliana kinyume cha maumbile (homosexual) na kwa vitendo vya haramu na wanyama pia. Dunia hii haikosi mashetani na madhali Shetani aliyelaaniwa bado anaishi, wapenzi na wafuasi wake wataendelea kuzaana. Na ifahamike wazi kwamba hii hali ya janaba inayotokana na ndoto ni pamoja na masharti ya kutoka kwa manii, kwani kuona ndoto tu bila ya manii kutoka, hata kama yamesogea kutoka mahali pake, basi haiwezi kuitwa hali ya janaba, ambapo katika kujamiiana, kule kuingia tu kwa kiungo cha kiume kwenye njia ya mwanamke kunatosha, kutoka kwa manii sio sharti hata kidogo katika hali hiyo, hivyo hapo zile hukmu za janaba lazima kwa hali yoyote ile zitajitokeza. Hili ni lazima pia likumbukwe kwamba wakati wa baada ya kubaleghe katika maisha yake mtu, kuzaliwa kwa matamanio ni muhimu, na kunaweza kukamsukuma mtu kuelekea kwenye vitendo haramu vilevile, kisha ni wajibu wa kipaumbele kabisa kwa watu wazima wa familia yake kugundua njia za halali, vinginevyo utendaji wa vitendo haramu utamtia hatiani mtoto, na wale wazazi pia, waliomfanya awe mateka wa jamii lakini hawakuweza kuyafunga matamanio yake. Katika suala hili, mafunzo, umasikini, huduma au visingizio vingine vyovyote vile havifai kuviazima masikio, na mtu anapaswa kuwajibika kwa kila hali juu ya vitendo viovu.

9


Mwanamke Na Sharia

HUKMU ZA HALI YA JANABA

N

amna tatu za wajibu hujitokeza juu ya mtu baada ya kuwa katika hali ya janaba:

1.

Kama anatakiwa kuswali basi josho la janaba la kujitakasa na hali ya janaba lazima lifanyike kabla ya swala hiyo.

2.

Kama mtu anataka kutufu al-Ka’ba basi kwanza josho la janaba ni lazima lifanyike kabla.

3.

Kama mtu anataka kufunga saumu za mwezi wa Ramadhani na akaingia kwenye hali ya janaba kabla ya adhana ya asubuhi (mwito wa swala) basi ni lazima achukue josho kabla ya adhana, na endapo baada ya adhana hali ya janaba itajitokeza, basi anaweza kuchukua josho hilo wakati wowote.

10


Mwanamke Na Sharia

NAMNA ZA KUCHUKUA JOSHO

K

una njia mbili za kuchukua Josho hili:

1.

Tumbukia kwa kuchupa kwenye bwawa au mto kwa nia ya josho, mara mwili wote utakapokuwa umezama kwenye maji basi hapo josho litakuwa limekamilika.

2.

Baada ya kunuia, kwanza osha kichwa hadi shingoni, baada ya hapo uoshe mwili mzima, josho litakuwa limekamilika. Kwa kutahadhari, kwanza osha nusu ya kulia ya mwili wako, baada ya hapo utaosha hiyo nusu ya pili ya upande wa kushoto.

Kama hakuna muda uliosalia kwa ajili ya swala, saumu, tawaf na kadhalika basi kunuia hivi tu – nachukua josho la janaba kwa kujikurubisha kwa Allah – kufanyike, na kama kuna muda wa kutosha kwa ajili ya swala, saumu, au tawafu, hapo unaweza kufanya na manuizi ya wajibu pia.

11


Mwanamke Na Sharia

MAMBO YASIYOELEWEKA VIZURI 1.

Watu wengine wanadhani kwamba mwanamke hawezi kuchukua josho (ghusl) akiwa amesimama. Hakuna sheria kama hiyo katika Uislam.

2.

Wengine wanafikiri kwamba josho la Janaba haliwezi kuchukuliwa kwa kuvua nguo zote kabisa. Hakuna sheria kama hiyo katika Uislam, kama hakuna mtu wa kukuona au kama mume anamwangalia, basi katika kuwepo huyo mume, mke anaweza kuchukua josho akiwa amevua nguo zote kabisa.

3.

Hakuna haja ya jagi, kata na kadhalika kwa ajili ya ghusli, kama kichwa na shingo vikioshwa kwa bomba na kadhalika, basi josho hilo litakamilika.

4.

Hakuna haja ya kusoma Kalimah, Suratul-Hamd au Inna an zalnaahu pamoja na niyyat ya ghusli.

5.

Inatosha kuosha kichwa au mwili mara moja wakati wa ghusli, hakuna haja ya kuosha mara tatu.

6.

Hakuna haja ya wudhuu kabla au baada ya ghusli. Ghusli hiyo peke yake inatosha kwa ajili ya Swala.

12


Mwanamke Na Sharia

YANAYOKATAZWA WAKATI WA HALI YA JANABA

M

ambo yafuatayo yanakatazwa wakati wa kuwa katika hali ya janaba:

1.

Kugusa neno Allah au majina mengine ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, au kugusa herufi za Qur’ani tukufu.

2.

Zile Sura nne ambazo ndani yake mnapatikana zile aya za sajida ya wajibu, miongoni mwa hizi kule kusoma zile aya za sajida ndio kunakokatazwa tu, kusoma Sura yote iliyobakia haikatazwi.

3.

Kuingia ndani ya Msikiti na kukaa humo kunakatazwa, hakuna madhara kwa kuingia kupitia mlango mmoja na kutoka kwenye mlango mwingine isipokuwa kwenye Masjidul-Haraam na Masjidun-Nabi.

4.

Kuingia ndani ya msikiti na kuchukua kitu ndani yake kunakatazwa.

5.

Kuweka kitu chochote msikitini, hata kiwe tohara au hata kukirusha kutokea nje pia kumekatazwa.

6.

Kama vile tu kwa msikiti, pia imekatazwa kuingia kwenye makuba ya Maasu’miina (a.s.), lakini hakukukatazwa kuingia kwenye uwanja wake na kadhalika sehemu yake nyingine yoyote ile.

7.

Haikatazwi kula, kunywa, kusoma Qur’ani au kumdhukuru Mwenyezi Mungu. Yaani itakuwa ni makuruhu (isiyopendeza) yenye kupunguza thawabu, lakini haikatazwi kama yenye kuleta adhabu. 13


Mwanamke Na Sharia

Na iwe yenye kueleweka wazi kwamba mbali na manii, kuna umajimaji mwingine pia huwa unatoka kwenye sehemu za siri za mtu ambao una namna ya mnatonato lakini ambao hakuna mhemko unaopatikana wakati wa kutoka kwake kama katika suala la manii, badala yake, kwa sababu ya matukio ya hisia kali tu au kwa sababu ya mabadiliko ya hali unatoka, hivyo umajimaji huu sio najisi na hakuna ghusli yoyote ya wajibu inayohitajika hapo kwa sababu yake, wala wudhuu unaoharibiwa nao, kama ukitoka baada ya kuchukua wudhuu. Tofauti ya kawaida ya umajimaji huu na manii ni kwamba, manii yanatoka wakati wa kudinda kwa dhakari na umajimaji huu unatoka baada ya hali ya kudinda kutoweka na uchovu kuchukua nafasi. Ni muhimu kuelewa tofauti ya viwili hivi, vinginevyo mtu ataharibu mengi ya matendo yake.

14


Mwanamke Na Sharia

HEDHI (KIPINDI CHA DAMU YA MWEZI)

K

wa kawaida baada ya miaka 9 na katika baadhi ya hali zingine, mapema kidogo ya hapo, damu huanza kuchuruzika kutoka kwenye sehemu za siri za mwanamke ambayo inaitwa damu ya hedhi au kipindi cha mwezi, kwa vile inajitokeza katika tarehe maalum za kila mwezi, dalili za hili ni kwamba damu hii ni nyekundu nzito yenye weusi na ina hali ya kuunguza kwa kiasi fulani. Damu hii ni zawadi kwa mwanamke kutoka asili, ambayo inasawiri kwamba sasa mwanamke amekuwa katika hali ya kutoa kizazi kipya, na amedhihirikiwa na uwezo mpya ndani yake wa kuzaa mtu mpya, vinginevyo kulingana na sheria asili ya kawaida, mwanamke akiwa mbali na hali hii anakuwa hana uwezo wa kupata mtoto. Kuna hali tatu za damu hii kuwa ni damu ya hedhi: 1.

Umri wa mwanamke lazima usiwe chini ya miaka tisa (9) na zaidi ya miaka sitini (60), vinginevyo haitaitwa damu ya hedhi.

2.

Mtiririko wa damu unapaswa usiwe chini ya siku tatu, vinginevyo itaitwa damu ya Istihadha na sio hedhi.

3.

Damu isije ikaonekana kwa zaidi ya siku kumi, vinginevyo sehemu yake moja itakuwa chini ya amri ya hedhi na sehemu nyingine kuwa ya Istihadha. Kipindi kati ya damu za hedhi mbili pia hakiwezi kuwa chini ya siku kumi, vinginevyo kipindi kimoja kitakuwa ni hedhi na kingine kuwa Istihadha. 15


Mwanamke Na Sharia

AINA ZA HEDHI

B

aada ya kuanza kwa damu ya hedhi, mwanamke anakuwa na hatua tofauti tofauti:

Mwenye kuanza (Mubtadiya) Huyu ni mwanamke ambaye ameiona damu yake ya hedhi ya mara ya kwanza kabisa. Kanuni juu ya hili ni kwamba, kama damu hii ina wekundu mweusi na ina hali ya kuchoma basi itachukuliwa kama ni damu ya hedhi na lazima ajiepushe na swala na saumu kwani swala na saumu vimekatazwa chini ya hali hii, na kama damu hiyo ikisimama kabla ya siku tatu basi haitakuwa ni hedhi na atapaswa kufanya kadha ya swala na saumu zilizompita (Saumu ni kama ikiwa ni katika mwezi wa Ramadhani). Na kwa namna hiyo hiyo, kama hali hii ikiendelea kwa zaidi ya siku kumi basi atapaswa kuwaona wanawake wa familia yake, na kujua kama ni kwa muda wa siku ngapi ambazo walikuwa kwa kawaida wakiziona hedhi zao, na kutokana na hizo apange idadi ya siku za hedhi, na kwa zile zilizobakia afanye kadha ya swala na saumu zilizompita, na kama desturi yao haifahamiki na damu ikawa ni ya namna mbili, basi ile rangi ya hedhi itaitwa kipindi cha hedhi na iliyobakia kuwa ni Istihadha, na kama yote ni ya namna moja ileile, basi kuanzia ile siku ya tatu hadi ya kumi kwa kiasi hicho inaweza kuchukuliwa kama hedhi na iliyobakia kuitwa Istihadha. Kwa hali ya tahadhari ni bora kuchukulia siku saba kwa ajili ya hedhi na zinazobakia kama Istihadha.

16


Mwanamke Na Sharia

Kwa kweli hali hujitokeza mara moja tu katika maisha ya mwanamke, na baada ya mwezi wa pili tabia fulani huamuliwa na yeye kuwa ni katika ipi kati ya hizo namna tatu: 1.

Ada ya Muda Tu:

Kama muda umekuwa ni ule ule katika miezi yote, yaani kwa maana kwamba, umeanza katika tarehe zilezile au siku moja au mbili kabla au baada. Hivyo ni jukumu la mwanamke kama huyo kwamba wakati wa kuanza kwa kuvuja kwa damu hiyo ajiepushe na swala na saumu, baada ya hili kama itasimama kabla ya siku tatu, basi afanye kadhaa, na kama ikizidi siku hii ya tatu angalia kama kuna idadi yoyote ya siku zilizojipanga katika miezi miwili hiyo au hapana na uamue kulingana na jinsi inavyojitokeza. 2.

Ada ya Kiidadi Tu:

Endapo katika miezi yote miwili tarehe hizo zilitofautiana zilikuwa ni siku tano tu. Wajibu wa mwanamke huyu ni kwamba ikiwa damu imtokayo ni kama damu ya hedhi basi aanze kuzitii amri hizo mara tu inapoanza, vinginevyo, subiri endapo uwezekano wa kubaki kwake ni wa siku tatu kisha aanze kutekeleza kanuni za hedhi. Baada ya hili, ikiwa kama itasimama kabla ya siku kumi basi zote zitaitwa hedhi, vinginevyo zile siku za mazoea ya kawaida zitachukuliwa kama hedhi na zinazobakia kama Istihadha. 3.

Ada Zote – Ya Muda na ya Kiidadi:

Kama kwa miezi miwili hedhi ikianza katika tarehe zile zile na imebakia kwa idadi ile ile, yaani, ilianza katika tarehe ya kwanza na 17


Mwanamke Na Sharia

imeendelea kwa muda wa siku saba, hivyo mara tu damu inapoonekana inapaswa kuchukuliwa kama hedhi na kama itasimama ndani ya siku kumi basi yote ni hedhi, vinginevyo kulingana na mazoea itakuwa ni hedhi na zinazobaki ni Istihadha, kama itakuwa kabla au baada ya muda uliopangwa.

ISIYOFUATA KANUNI MAALUM (MUDH’TARIB) Katika hatua hii, kunaweza kuwa na namna ambapo desturi haiwezi kuamuliwa, na kila mwezi tarehe vilevile zinabadilika na siku pia, ni wajibu wa mwanamke kama huyo, wakati wowote damu ya hedhi inapoonekana, basi aanze kutekeleza zile kanuni za hedhi, na kama baada ya hapo itaendelea kwa zaidi ya siku kumi, na kama kati ya siku hizo kuna nyingine hazikuwa na sifa ya hedhi basi azichukulie kama Istihadha, na kama zote zina sifa za hedhi basi awafanye wanawake wa familia kuwa ni kigezo cha kufuata, na apange muda wa hedhi kulingana na siku zao na zinazobaki azizingatie kuwa ni Istihadha, na kama hali yao wote ni moja ileile, basi achukue idadi yoyote anayotaka kutoka siku ya tatu hadi ya kumi na afanye kadhaa kwa ajili ya siku zinazobakia. Kama suala la tahadhari siku saba zichukuliwe kama hedhi na ashughulike na hizo nyingine kwa mujibu wa amri za Istihadha. Iwe wazi kwamba tofauti ya msingi ya hedhi na Istihadha ni kwamba, swala na saumu haiwezi kutekelezeka katika hedhi lakini hizo ni wajibu katika hali ya Istihadha, hivyo wakati wowote ule Istihadha inapofikiriwa kuwa ni hedhi basi kadhaa ni wajibu kwa hali yoyote ile.

18


Mwanamke Na Sharia

Na njia iliyo bora ni kwamba, wakati wowote kunapokuwa na mashaka kuhusu damu kuwa ya hedhi basi tekeleza njia ya kati na kati, tekeleza swala na saumu kulingana na Istihadha, na jiepushe kutokana na yale mambo yote ambayo yanakatazwa katika hali ya hedhi. Kwa hali ya mambo ikiwa hivi, ni muhimu kufahamu yale mambo ambayo yanakatazwa katika hali ya hedhi na pia zile amri za Istihadha ni muhimu kufahamika.

19


Mwanamke Na Sharia

YALIYOHARAMISHWA WAKATI WA HEDHI

M 1.

wanamke haruhusiwi wakati akiwa katika hedhi mambo haya yafuatayo: Hawezi kuswali swala yoyote ya faradhi au mustahabu. Lakini ni bora kuja kukaa kwenye mkeka wake wa swala unapoingia wakati wa swala na akajishughulisha na utajo (dhikr) ama nyuradi za kumkumbuka Mwenyezi Mungu kwa kiasi kile cha muda ambao alikuwa akiutumia kwa kawaida kwa ajili ya swala, ili kwamba mafundisho kwa ajili ya watoto yasije yakaathiriwa vibaya, vinginevyo mara moja watakuja kudhani kwamba swala ni jambo ambalo kwamba linatekelezwa wakati fulani na wakati fulani linaweza kuachwa kutekelezwa, na kwa namna hii ile hisia ya umuhimu wa swala itatoka kwenye akili za watoto. Na watakuwa na wasiwasi kuhusu wanawake wa familia, kwa vile ambavyo mara wanaswali na wakati mwingine hawaswali, hawatatambua kwamba kuswali kwao hadi jana tu kulikuwa ni ibada na kuacha kuswali leo ni ibada vile vile.

Naiwe wazi kwamba mwanamke ambaye ameacha swala zake za wajibu wakati wa kipindi cha hedhi, kadhaa kwa ajili ya swala hizo sio wajibu pia. Na kwa namna hii, kama baada ya kifo cha mwanamke huyo, warithi wake wakitaka kufanya kadhaa kwa niaba yake basi ni lazima wakumbuke kwamba kwa upande wa mama kanuni hiyo haitumiki kama inavyotumika kwa upande wa baba. Kadhaa kwa ajili ya siku zote thelethini itakuwa ni wajibu kwa ajili ya baba kama alikuwa muacha swala (tarikus-Swalat). Lakini kama 20


Mwanamke Na Sharia

na mama naye ni tarikus-Swalat, basi sio muhimu kwa kiasi hicho kadhaa kwa ajili yake. Mola Wake amempunguzia wajibu wa kidini zaidi ya mwanamume, na huenda hili likawa ndio jibu kwa lile swali ambalo linaulizwa sana na watu, kwamba, kwa nini Uislam umeweka majukumu ya wajibu juu ya tabaka hili dhaifu (wanawake) miaka sita kabla, na kwa nini mwanamume mwenye nguvu na uwezo mwingi awe huru hadi kufikia miaka kumi na tano? Jibu fupi kwa ajili ya hili ni kwamba, kwanza kabisa hii ni kutokana na ukamilikaji wa umbile la mwanamke kimwili na kiakili ambao unatokeza kabla ya ule wa wanaume, na pili upungufu huu unakuja kuwekwa sawa katika kipindi cha baadaye cha maisha yake. Na kila mwezi uhuru wa siku kuanzia tatu hadi kumi unatolewa kwake, kwa njia hii uhuru kwa mwaka wa kiwango cha chini siku 36 na kiwango cha juu kabisa siku120 unapatikana kwake, na kwa njia hii katika miaka kumi swala za mwaka mmoja au miaka tisa zinasamehewa, na bila shaka upungufu ule ambao aliuhisi wakati wa mwanzo wa balekhe umekamilishwa. Elimu na ujuzi wote viko mikononi mwa Mwenyezi Mungu! 2.

Kufunga wakati wa kipindi cha hedhi pia hakuruhusiwi, bali ni jambo tofauti kwamba kadhaa kwa ajili ya saumu hizi itakuwa ni lazima. Siri ya kwanza ikiwa ni hii kwamba tukio hili litatokea katika mwaka ndani ya mwezi wa Ramadhani tu, na katika mwaka mzima wote kadhaa ya saumu ya siku tatu hadi kumi tu ndio itakayofanyika, ambayo pia inaweza kufanyika wakati wa kipindi cha siku kipupwe kukiwa na baridi, na hii ni fursa mpya ambayo uhuru unatolewa wakati wa siku za kiangazi na kadhaa ya wakati wa baridi imekubaliwa.

Sababu ya pili inaweza kuwa kwamba, sambamba na kungojwa na kadhaa ya swala, majukumu mengine ya maisha vilevile hayawezi 21


Mwanamke Na Sharia

kutekelezwa (akiwa katika hedhi), lakini wakati wa kufunga saumu shule zinaweza kuhudhuriwa, kazi za kiofisi zinaweza kufanyika, mambo ya nyumbani pia yanaweza kuangaliwa, mume pia anaweza kuhudumiwa, malezi ya watoto pia yanawezekana na kwa njia hii, isipokuwa kwa matatizo binafsi, jamii na shughuli za kijamii haziathiriki na maumivu binafsi yanafidiwa kwa njia ya malipo ya thawabu. 3. Mahusiano ya kujamiiana na mumeo pia hayaruhusiwi hata kwa kiwango cha kupenyeza tu, bali mbali na kupenyeza, hakuna madhara kwa mambo mengine na ari, na kama hisia zikimlazimisha mtu kutaka kupenyeza basi kwa ridhaa ya mkewe, njia na namna nyingine zinaweza kuchukuliwa, lakini kutoka kwenye sehemu inayotoka damu matumizi yoyote hayawezekani kufanyika kwani kiafya na kijinsia ni hatari pia, kwa vile haja ya damu ni kutoka nje, na kujamiiana kunadai ufyonzaji wa kiini hicho (manii) ndani, hivyo kwa namna hii, mgongano wa tamaa mbili hizi unaweza kusababisha maradhi yoyote yale. Kuingilia kunaweza kufanyika baada ya kusimama kwa kutoka damu hata kama mke hajaoga ghusl ya hedhi kwani hakuna sharti kama hilo la tohara kwa ajili ya kuingilia. Naieleweke wazi kwamba kutwaa njia nyingine hakuwezi kulaumiwa kwamba ni liwati kisharia, ambayo hairuhusiwi katika Uislam, kwa sababu liwati ya kisharia maana yake ni kujamiiana mwanaume kwa mwanaume, kitendo hiki pamoja na mwanamke hakiwezi kupewa jina la kipuuzi kama hilo, vinginevyo baadaye hili litakuja kusemwa kwamba baada ya ndoa tendo la kujamiiana ni kama zinaa tu, hivyo hilo nalo linakatazwa. Kwakweli hakuna 22


Mwanamke Na Sharia

mtu yoyote mkweli anayeweza kusema hili, na kila mtu anatambua kwamba zinaa ni jina la kitendo cha haramu. Hivyo kujamiiana baada ya ndoa, ni kitendo cha halali na kwa namna hiyo hiyo liwati ni kitendo cha haramu, hivyo kushiriki kwa mume na mke hakuwezi kufikia hapo au kuamuliwa hivyo.1 Suala lao ni tofauti kabisa na watu wote, wanaweza kukaa uchi mbele ya kila mmoja wao na wanaweza kuoga pamoja katika hali hiyo hiyo, tendo la ponyeto kama likifanywa na mwanaume linakatazwa, lakini tendo hilohilo kama likifanywa na mke kwa ajili ya mumewe (yaani kumfanya amwage manii), hilo linakuwa halina madhara. Baada ya kufariki, mume anaweza kufanya josho (ghuslilMayt) kwa kumfanyia mkewe, ambapo kwa ajili ya josho sharia ni mwanaume kwa mwanaume, na mwanamke kwa mwanamke, hilo ni lazima. Hivyo ulimwengu wa mume na mke ni ulimwengu tofauti kabisa, na Uislam umeuzawadia ulimwengu huo fursa nyingi mno ambazo haujazizawadia kwenye njia nyingine yoyote ya maisha. Na ni dhahiri kabisa kwamba Uislam sio dini ya uchamungu mkavukavu tu, kinyume chake mazuri yote ya kila namna juu ya maisha yanapatikana ndani yake, lakini yana mipaka yake, na kuivuka mipaka hiyo kunajulikana kama ni ukatili na sio ubinadamu.

1

A ngalizo: Suala hili tulichukulie kama lile suala la ruksa ya kula nyama ya nguruwe kwa udhuru wa kujiokoa na njaa, fursa ambayo kwa zama hizi haina nafasi kwani sio rahisi mtu kukosa kabisa chakula na ipatikane tu nyama ya nguruwe. Kadhalika suala hili kwa vile linahitaji ridhaa hasa ya mke na sio la kulazimishana, sio rahisi kumpata mke mwenye kuridhia jambo hilo hasa kwa waumini, na dharura kama hiyo sio rahisi kupatikana hivyo inaweza kubakia ni ruksa isiyotekelezeka – kwani kuna riwaya zinazoonyesha kwamba jambo hili limefanyika bila ya kushutumika. 23


Mwanamke Na Sharia

4.

Kumtaliki mke wakati wa kipindi cha hedhi vilevile sio sahihi, wakati ambapo kumuoa wakati wa hedhi kulikuwa ni sawa na sahihi, na tena huu ni ushahidi pia kwamba Uislam sio dini kavukavu, kwani ndani yake, wakati wa hedhi raha na starehe zote zinaruhusiwa isipokuwa kuingiliana. Pia moja ya sababu za kizuizi juu ya talaka inaweza kuwa ni hii, kwani kwa njia hii mume anapata fursa na wasaa wa kuliangalia upya hilo kwa muda wa siku tatu hadi siku kumi na huenda ndani ya wakati huu akajirudi na kuokoa maisha ya watu wawili kutokana na kuangamia. Kwani talaka imefanywa halali chini ya hali ya kulazimu, vinginevyo Uislam hauridhii kitendo hiki kwa hali yoyote ile, na ndio maana inasemekana kwamba, pale roho mbili zinapotengana na hati ya talaka ikatolewa, Arshi ya Mwenyezi Mungu inatikisika, kwani Mola ameamuru kuziunganisha roho hizi mbili wala hakuagiza utengano wao. Mambo kama yalivyo, endapo kioo kikivunjika kama hivyo, kwa vile kukiunga sio jambo linalowezekana hivyo badala ya kukiweka ndani kwa masikitiko, ni bora kukitoa na kukitupa nje ya nyumba. Lakini huenda kioo kilichovunjika kikawa na matumizi fulani kwa moyo uliovunjika kwani watu wote hawafanani na mahitaji ya wote vilevile hayafanani.

5.

Katika hali ya hedhi kugusa herufi za Qur’ani tukufu, majina ya Allah na sifa Zake makhsusi pia kumekatazwa. Lakini hakuna madhara wala ubaya katika kuisoma, ni kwamba tu malipo yake ya thawabu yatakuwa machache, na hali hii hii anakuja wakati wa kuisoma bila wudhuu kwani ni dhahiri malipo yake ni madogo zaidi kuliko yapatikanayo inaposomwa pamoja na wudhuu.

6.

Kutembelea msikitini wakati wa kipindi cha hedhi na ku24


Mwanamke Na Sharia

kaa humo, na kuweka kitu ndani yake pia kumekatazwa hata kama kitu hicho kiwe tohara. Kwa hili sio kwamba ina maana kwamba ndani ya hali hii mwanamke amegeuka kuwa kiumbe najisi kabisa moja kwa moja, kwa kweli hili peke yake linakuwa ni heshima ya msikiti wenyewe, hili kwa hali yoyote ile halihusiani na uchafu wa mwanamke, hali kama hiyo ni kama wanaume wanapokuwa kwenye hali zao za janaba, kwani wote wanatekeleza kazi zao nyingine zilizobakia za kimaisha, mwanamke anapika chakula nyumbani katika siku hizi hasa na mume anakila akiwa katika hali ya janaba na Uislam haukuweka vipingamizi juu ya kupika kwake wala kwa mume kula kwake chakula. Cha kushangaza kabisa, watu wanawaona wanawake walio kwenye nyumba zao kuwa dhalili na wanaostahili kudharauliwa na kwamba hawana faida yoyote kwenye dini, na wakati huo huo wanapoleta vitu kutoka nje kamwe hawafikirii kwamba tamtamu walizonunua kutoka dukani au vyakula walivyonunua kwenye hoteli nimeandaliwa na watumishi wanaopaswa kuoga josho la janaba, na ni kwa kiasi gani wanawake wale walio majumbani wako tohara kutokana na hedhi na nifasi. Kwa kweli haya yote ni itikadi za kidhana na vishawishi ambavyo havina thamani katika ulimwengu wa hali halisi ya mambo, ni wajibu juu ya kila mtu kuziandama kanuni za dini na asijaribu kujifanyia kanuni zake mwenyewe, vinginevyo watakusanywa pamoja na wale ambao kuanzia siku ya mwanzo kabisa walikuwa wameanza kufanya mlolongo wa halali zote za Muhammad (saww) kuwa haramu, na wafuasi wao hadi hata leo hii wameujengea mlolongo huu na kuuambatanisha kwenye vizingiti vyao. 7.

Kusoma zile aya nne kumekatazwa katika kipindi cha hedhi, zile ambazo sajida ni wajibu ndani yake. Hakuna 25


Mwanamke Na Sharia

dhambi katika kusoma Qur’ani tukufu yote iliyobakia bali kuna thawabu ndani yake, hakuna ajabu hata zikiwa chache kidogo. 8.

Kama vile ilivyo kwa misikiti, pia kuingia kwenye makuba ya maasumina kumekatazwa wakati wa kipindi cha hedhi. Kama hali hiyo inajitokeza basi ni bora kwenda kwenye hicho kiwanja cha kiuchamungu (kinachozunguka Kuba) na usome ziyara ukielekea kwenye kuba hiyo badala ya kurudi ukiwa umekosa kitu, kwa vile wanachuoni wasomi wakubwa hawakuweka wajibu wowote katika kiwango hiki.

9.

Kama mwanamke anataka kufanya Hijja kwenye Nyumba ya Mwenyezi Mungu wakati wa kipindi cha hedhi basi hawezi kuvaa Ihraam (vazi la Hijja linalokataza utaratibu wa kawaida kama huo) ndani ya msikiti, lakini anaweza kuvalia nje kutokea kwenye Kituo chochote cha Kuvalia ihramu (kuingia Makka ni pale tu baada ya kuvaa Ihraam). Baada ya hili katika tendo lolote la Hijja, isipokuwa kwenye tawafu na swala yake tu, hakuna masharti ya kuwa na tohara, hivyo anaweza kutekeleza Hijja yote kwa kujiamini, ila tu anapaswa kusubiri kuwa tohara kwa ajili ya tawaf, au ampange mtu kumwakilisha kama akilazimika kufanya hivyo.

Naieleweke wazi kwamba josho la hedhi linafanyika kwa namna mbili kama vile josho la Janaba: a.

Mwanamke atazama mara moja kwenye maji pamoja na nia, hapo josho litakuwa limekamilika.

b.

Baada ya nia, ataosha kichwa chake na shingo kwanza na baada ya hapo aoge mwili mzima, josho litakuwa 26


Mwanamke Na Sharia

limekamilika. Hili linaweza kufanyika akiwa amesimama au akiwa amekaa, akiwa amevaa nguo ya ndani au kuvua nguo zote, likifanyika nje ya uoni wa dunia au mbele ya mume wake. Hili pia lieleweke wazi kwamba mwanamke anaweza kukaa uchi kabisa mbele ya mumewe tu, kujitokeza mbele ya wanawake wengine pia kumekatazwa kwa vile kuficha sehemu za siri ni wajibu katika hali yoyote ile na kuzionyesha sehemu hizo hakuruhusiwi si kwa wanaume tu bali hata kwa wanawake pia. Ni jambo la kipekee tofauti kwamba Mwenyezi Mungu Mwenye hekima ameliumba umbile la mwanamke kiasi kwa asili ya kuzifunika sehemu zake za siri, basi na kuzionyesha kwake mbele ya mtu yeyote, mwanaume au mwanamke hakuruhusiwi. Huu ndio umahususia wa maisha ya mume na mke kwamba Qur’ani tukufu imewafanya kuwa ni vazi la kila mmoja wao kwa mwingine, umahususi wa nguo ni kwamba zinaficha mwili machoni mwa watu wengine, bali hakuna la kuficha kutokana na hili (la mume na mke). Hili na lijulikane pia kwamba, kwa vile hakuna haja ya wudhuu kwa ajili ya swala baada ya josho la janaba, kwa njia hiyo hiyo hakuna haja ya wudhuu baada ya josho la hedhi, tofauti iliyopo tu ni kwamba kwa josho la janaba haja ya kuchukua wudhuu hutoweka, lakini hapa kwenye hedhi ni bora na vizuri ufanywe ama kabla ya kuoga au baada ya kuoga josho lenyewe, bali tohara halisi inapatikana kwa josho tu.

27


Mwanamke Na Sharia

MUKHTASARI WA KANUNI ZA ­HEDHI

P

ale wakati wa baleghe katika maisha ya mwanamke, mlolongo wa damu za mwezi unapoanza, basi ni wajibu wake mara tu anapoona katika mwezi wa kwanza ile damu nyekundu yenye weusi weusi ya hedhi yenye hali ya kuchoma choma, basi aachane na ibada na abakie katika hali hiyo hiyo mpaka damu iendelee kutoka na baada ya hapo kadhaa ya swala sio lazima, lakini kama itatokea katika mwezi wa Ramadhani basi kadhaa ya saumu kwa hali yoyote ile lazima ifanyike. Baada ya hapo, katika mwezi wa pili ikiwa damu itatoka katika tarehe zilezile basi tarehe itakuwa imejipanga, na baadaye kama itaanza katika tarehe hii hii au siku moja au mbili kabla au baada, basi atafanya kulingana na kanuni za hedhi na endapo jambo hilo litasimama kabla ya siku tatu basi atapasika kufanya kadhaa ya swala na saumu vyote kwa siku hizo. Baada ya hapo, ikiwa katika mwezi wa pili tarehe zimebadilika lakini idadi ya siku ni ile ile kama ya mwezi uliopita, kwa mfano, katika miezi yote ilikuwa ni kwa siku tano au saba, kwa hiyo wakati wowote damu itakapoanza anapaswa kujihesabu kuwa yuko kwenye hedhi, baadae kama itazidi zile siku zilizojipanga, na dalili zinafanana kama za hedhi, basi hadi siku kumi ichukuliwe kwamba ni hedhi, lakini dalili zikiwa ni tofauti basi zile siku zinazojulikana zichukuliwe kama hedhi na zinazozidi zihesabiwe kama Istihadhaa na zishughulikiwe ipasavyo. Kama kuna mwanamke kama huyo ambaye siku zake hazikupangika na tarehe za kila mwezi ni tofauti pia, na idadi yake pia inatofautiana, basi mara tu baada ya kuiona damu aichukulie 28


Mwanamke Na Sharia

kama hedhi. Kama baada ya hapo ikisimama ndani ya kipindi cha siku kumi basi damu yote itahesabiwa kama hedhi, na kama ikizidi siku kumi basi ile damu yenye dalili za hedhi itahesabiwa kuwa ni hedhi na zinazozidi kuchukuliwa kama Istihadha.

29


Mwanamke Na Sharia

ISTIHADHA (VIPINDI VISIVYO NA ADA MAALUM)

I

le damu mbali na hedhi ambayo inatoka kwenye sehemu za siri za mwanamke inaitwa Istihadha inayotembea pamoja na hedhi, kabla yake au baada, kwa kawaida rangi ya damu hii ni ya manjano manjano na inatoka bila ya muwasho au hali ya kuchoma na pia sio nzito sana. Damu hii iko ya namna tatu: 1. Pamba itawekwa kwenye sehemu inayotoka damu hiyo kwa ajili ya uchunguzi, na kama pamba hiyo ikilowa na nguo inayoshikilia pamba hiyo pia ikilowana basi itaitwa Istihadha Nyingi (Kathiri), katika hali hii mwanamke atapaswa kuchukua majosho matatu, kwa josho moja ataswali swala ya al-Fajri, na kwa josho la pili ataswali adh-Dhur na al-Asri bila kuweka mwanya kati yake, na kwa josho la tatu ataswali swala ya Magharibi na Isha bila ya kuweka mwanya kati yake, hapa hakuna haja ya wudhuu, hiyo ghusl inatosha kwa ajili ya swala. 2.

Kama pamba italowana lakini ile nguo inayoishikilia haikufikwa na damu basi itaitwa Istihadha ya Wastani (Mutawassita), na kwa ajili ya hii josho moja kwa siku litakuwa ni lazima na wudhuu lazima uchukuliwe kwa kila swala. Kama damu hii Istihadha ya Wastani (Mutawassita) itatoka kabla ya swala ya al-Fajr, basi josho litakuwa kwa ajili 30


Mwanamke Na Sharia

ya swala ya Asubuhi na kwa swala zilizobakia ni wudhuu tu utachukuliwa. Na kama imeanza wakati wa swala ya Dhuhri, basi josho litakuwa kwa ajili ya swala ya Dhuhri na swala zinazobakia ni wudhu tu, na kama ikitokea kabla ya Maghrib basi josho litakuwa kwa ajili ya swala ya Maghribi na kwa zilizobakia atachukua wudhuu, lakini pamoja na josho wudhuu pia utalazimika kufanyika kwa wajibu, na kwa njia hii wudhuu mara tano utafanyika na josho lifanyike wakati wowote. 3.

Kama damu ni chache kuliko hicho kiwango kilichoelezwa hapo juu na ipo kwenye sehemu tu ya pamba basi hakuna haja ya josho lolote lile, ni wudhu tu utakaotosha kwa ajili ya swala na pamoja na wudhu huo pamba au nguo iliyopata doa la damu lazima itoharishwe au kubadilishwa, ambapo kufanya hivyo ni lazima katika Istihadha Nyingi (Kathiri) kwa mujibu wa tahadhari, na ni mustahabu katika Istihadha Chache (Qaliilah) au ya Wastani (Mustawassita).

Pia ieleweke wazi kwamba katika kipindi cha Istihadha Chache (Qaliilah), kama ilivyo lazima kuchukua wudhu kila baada ya swala, pia ni muhimu kuchukua wudhu kila baada ya swala ya sunna vilevile. Na kwa wudhu mmoja haiwezekani kuswali swala mbili au kufanya aina mbili za ibada. Hili vilevile linapasa likumbukwe kwamba wakati wowote inapokuwa hakuna uwezekano wa kuchukua josho, kwa mwanaume au mwanamke, hapo badala ya josho Tayammum itafanywa, na ibada haiwezi kuachwa kutekelezwa.

31


Mwanamke Na Sharia

KANUNI ZA ISTIHADHA

I

stihadha ikiwa chache (qaliil), ya wastani (mutawassita) au nyingi (kathiir), katika hali zote tatu ugusaji wa herufi za Qur’ani tukufu umekatazwa, bali hakuna madhara katika kugusa jalada la juu au pambizo. Mbali na hili vile vitendo vyote vinavyokatazwa kwenye hedhi kwenye hili havikatazwi na mfumo wa maisha ya mwanamke hautibuliwi. Wakati wa Istihadha vilevile talaka inawezekana kutolewa na mwanamke anaweza kuingia msikitini pia na anaweza akaketi humo. Anaweza akasoma zile aya za wajibu wa sajida na kufunga na kuswali pia, badala yake swala na saumu ni wajibu kwa masharti kwamba kama josho lolote ni wajibu juu yake, basi ibada zote hizi zitafanyika baada ya josho na asije akazifanya moja kwa moja katika hali ya kukosa tohara. Hakuna madhara ya kujamiiana wakati wa Istihadha na kipindi chake sio cha urefu kama wa hedhi. Kwa uangalifu zaidi, kama damu yoyote itatoka kabla au baada ya hedhi, na wala sio ile damu ya baada ya uzazi (nifas) na pia sio ile damu ya bikira na hakuna majeraha katika sehemu zake za siri, basi hiyo itaitwa damu ya Istihadha, ambayo wakati mwingine inakuwa chache na wakati mwingine ya kiwango cha wastani na wakati mwingine inakuwa nyingi. Wakati wa hatua ya uchache atachukua wudhu baada ya kila swala na hana wajibu wa josho. Katika aina ya wastani, josho moja kwa siku litafanyika na wudhu kwa ajili ya kila swala. Katika suala la ile inayokuwa nyingi (kathiir), josho kwa ajili ya swala ya Asubuhi, josho moja kwa ajili ya swala za mchana (Dhuhri na Laasiri) na josho moja kwa ajili 32


Mwanamke Na Sharia

ya swala za jioni (Maghrib na Isha), hapa hakuna haja ya wudhuu lakini pia ni bora kuuchukua. Katika hatua ya mwisho (Kathiir) ni muhimu ama kuosha au kubadilisha ile pamba au nguo iliyochafuliwa na damu hiyo lakini katika hatua zake za nyuma hili pia sio muhimu na bila hilo swala inaweza kutekelezwa bali swala haiwezi kuachwa kwa hali yoyote ile. Swala inaachwa tu wakati wa hedhi, mbali na hiyo hakuna uruhusiwaji wa kuacha swala katika hali na wakati wowote ule maishani, ambalo linaonyesha ukweli huu kwamba, uwezekano wa kuacha swala upo kwenye maisha ya mwanamke tu na kamwe haupatikani katika maisha ya mwanamume. Sasa kama mwanaume ataacha swala anaweza akahesabiwa kuwa miongoni mwa wanawake, na vilevile aina ya mwanamke asiye na tohara. Hawezi hata akahesabiwa kuwa miongoni mwa wanawake tohara na wasafi kwani mwanamke mwenye tabia njema anaacha swala katika kutii amri ya Mola Wake na wanamume wanapuuza swala tu katika misingi ya nia zao mbaya na majivuno.

33


Mwanamke Na Sharia

BAADHI YA KANUNI ZA KIJUMLA 1.

Kama hali ya Istihadha ikibadilika na kuwa Chache, au kuwa ya Wastani au kuwa Nyingi, basi utekelezaji utakuwa kulingana na hali iliyopo wakati huo wa swala, kwa mfano, kama wakati wa swala za mchana Istihadha ya Wastani (mutawassita) itabadilika na kuwa Istihadha Chache (qaliila) basi atachukua josho la Istihadha ya Wastani, na baadaye achukua wudhuu wa Istihadha Chache (qaliilah), baada ya hapo hakuna haja ya josho lolote lile kwa ajili ya swala za Magharib na Isha.

2.

Kwa namna nyingine, kama Istihadha Chache inapokuwa ya Wastani, basi kanuni za Wastani lazima zitumike, na hakuna jingine linalohitajika zaidi ya hilo.

3.

Namna ya kuchukua josho wakati wa Istihadha itakuwa sawa sawa na namna ya kuchukua josho wakati hedhi na janaba, tofauti pekee ni kwamba, katika hedhi josho linachukuliwa baada ya kusimama kutoka kwa damu, na hapa damu inaendelea kutoka na josho linaendelea, jambo ambalo linaonyesha ukweli huu kwamba Uislam ni utawala wa Mwenyezi Mungu, ambao kuutii ni wajibu wa kila mtu katika wanadamu, na hakuna uingiliaji kati katika hili wa elimu ya mtu yoyote au mawazo yenye kupendeza au yenye kuchukiza.

4.

Katika Istihadha vilevile kama haiwezekani kufanya ghusl, basi inapaswa ifanywe tayammam badala yake, na hata kama uwezekano wa kuchukua wudhuu unakuwa haupo, tayammam inaweza kufanyika badala yake. 34


Mwanamke Na Sharia

5.

Mbali na rangi na tabia, hedhi na Istihadha zinaweza kutofautishwa kwa njia tatu: a.

Kwa kawaida muda wa hedhi umejipanga bali hakuna muda wa Istihadha.

b.

Hedhi sio chini ya siku tatu (3) au zaidi ya siku kumi (10) lakini Istihadha inaweza kuwa chini ya hapo au zaidi yake.

c.

Hedhi haipatikani kabla ya baleghe na baada ya miaka sitini (60) lakini Istihadha inaweza kuwapo katika nyakati hizi pia.

35


Mwanamke Na Sharia

NIFAS (Damu baada ya uzazi)

K

wa kawaida wakati mwanamke anapozaa mtoto kisha baada ya hapo damu inamwagika kutoka kwenye tumbo la uzazi, damu hii inaitwa Nifas katika sharia ya dini, na baada ya hii pia josho linakuwa ni lazima, lakini lina kanuni na khususia ambazo ni lazima kuzizingatia akilini. 1.

Kama baada ya kujifungua hakuna damu inayotoka hata kidogo, basi mwanamke huyu hana masharti ya nifas, na baada ya kujifungua wakati wowote wa swala unaowadia, swala hiyo lazima iswaliwe mara moja.

2.

Kama mtoto atazaliwa baada ya adhana ya mchana, na kutoka damu kukasimama baada ya saa moja, basi anapaswa kuchukua josho mara moja na kuswali swala ya Dhuhr, kwa sababu hakuna kiwango cha chini kilichowekwa kwa ajili ya nifas.

3.

Kama wakati wa nifas ukiendelea, na damu ikaendelea kutoka hata baada ya siku kumi, iwapo siku zake za hedhi ni za kawaida ya kudumu, basi kiasi cha siku hizo kitachukuliwa kama nifas na zinazobakia kama Istihadha kwa mfano kwa kawaida siku za kudumu hedhi ni saba, hivyo baada ya siku saba atachukua josho na kuanza kuswali au kufunga. Na kama siku za hedhi hazina kawaida ya kudumu basi atachukua josho baada ya kungoja kwa siku kumi na kuanza kuswali au kufunga, na siku zinazobakia zitakuwa kwa kanuni ya Istihadha, hazitahusishwa kwa namna yoyote ile na nifas. 36


Mwanamke Na Sharia

4.

Kadhaa kwa ajili ya swala zilizoachwa wakati wa nifas, hizi sio wajibu lakini wakati wa mwezi wa Ramadhani kama mtu akiwa katika hali ya nifas basi kadhaa ya saumu lazima ifanyike.

5.

Kiwango cha hali ya juu kabisa cha nifas ni siku kumi, na hizi zinahesabiwa kuanzia damu inapoonekana baada ya uzazi, na inahesabiwa kuanzia siku hiyo hata kama damu itatoka wakati wa usiku, na kuhusu damu ina maana ya damu inayotoka baada ya kuzaa, vinginevyo ile damu inayotoka wakati wa kuzaa ni ya nifas, lakini haiingii katika hesabu ya siku.

6.

Kujamiiana hakuruhusiwi wakati wa nifas, starehe nyinginezo zinaweza kufanyika, hakuna wajibu juu yake hizo.

7.

Wakati wa nifas vilevile talaka haiwezi kutolewa kwa mke.

8.

Kama tahadhari ya wajibu, wakati wa nifas pia zile aya zenye sijida haziwezi kusomwa ,kuingia msikitini na kukaa humo, kuweka kitu chochote ndani ya msikiti au kupita ndani ya msikiti wa Masjidul-Haraam na Msikiti wa Mtukufu Mtume (saww) yote haya yamekatazwa.

9.

Josho la Nifas pia ni kama majosho mengine linaweza kufanywa kwa njia moja kati ya namna mbili, kwa kuzama katika dimbwi, mto au bahari na kwa kuosha kichwa, shingo na mwili mzima.

10. Kwa hali yoyote ile kipindi cha nifas sio zaidi ya siku kumi, hivyo endapo mwanamke yeyote hakuswali kwa siku arobaini kulingana na utaratibu wa ukosefu wa elimu wa tangu dahari, basi anapaswa mara moja afanye Kadhaa ya angalau swala za siku thelathini vinginevyo kwenye Siku 37


Mwanamke Na Sharia

ya Kiyama atakabiliwa na matokeo mazito na ile furaha ya kuwahi kuwa mama wa mtoto itatoweka mavumbini. Na kama watoto wakitambua kwamba, kwa misingi ya ukosefu wa elimu, mama yao aliacha swala kwa siku arobaini (40) wakati wa kuzaliwa kwao, basi ni jukumu la uhisani wao kutekeleza kadhaa za swala hizo kwa niaba ya mama yao baada ya kifo chake. Isije ikawa kwamba mnamo Siku ya Kiyama yeye mtoto akahesabiwa miongoni mwa dhambi za kukosa shukurani, kwani mama yake kwa ajili ya uzazi alihatarisha maisha yake na kuvumilia matatizo yote ya ujauzito na mtoto huyu asiye na maana wala hakufidia kosa la mama yake, kuuacha wajibu wa mama yake wazi kwa stahili Moto wa Jahannam. Wenye kutenda matendo mema kwa ajili ya wazazi wao wanapaswa kuzingatia akilini mambo haya kwamba wengi wa akina mama wameacha swala zao kutokana na ujinga wa kutojua au wameziswali kwa makosa, basi huku sio kuonyesha huruma kwao kwamba mtu amepika biriyani kwa kutumia maelfu ya fedha na kuwalisha ndugu zake, bali huruma halisi na ya kweli juu yao ni kutekeleza wajibu wao (wa mwisho), ili waokolewe na adhabu ya Moto wa Jahannam, na watoto wenyewe nao wahesabiwe miongoni mwa wenye wema na hisani. Hali ni kama hiyo hiyo kwa ajili ya swala za kimakosa za baba, kwa vile kuzitekeleza upya ni wajibu wa kidini na kimaadili wa watoto, wajibu ambao mtu hapaswi kupuuza. Na ieleweke wazi kwamba, endapo baada ya kuzaa mwili wa mwanamke au nguo vinakuwa sio tohara, basi, kwanza vifanywe kuwa tohara na kisha ndipo swala itekelezwe, na kama kuviosha kuwa tohara au kubadilisha haiwezekani, na damu ikawa imesimama, basi baada ya kuchukua josho husika anapaswa kuswali na nguo zake zilezile 38


Mwanamke Na Sharia

zisizo tohara, na swala haiwezi kuachwa kwa gharama yoyote ile kwani kuacha swala kwa hali yoyote ile kumekatazwa, na tendo hili, la kuacha swala, kwa upande mmoja linaporomosha hisia za kidini na kwa upande mwingine linamfanya mtu kuwa na haki ya kumiliki Jahannam.

39


Mwanamke Na Sharia

BAADHI YA KANUNI NYINGINEZO

K

wa vile katika hukmu muhimu za wanawake ni hedhi, Istihadha na nifas tu ndizo zinazohesabiwa, lakini kwa kuhisi umuhimu, zimeelezewa hukmu za janaba pia, kwa vile suala hili ni la kawaida kwa wanaume na wanawake, lakini kutokana na utambuzi wa wanawake imekuwa muhimu kugusia baadhi ya masuala nyeti, baada ya hili, chini ya maudhui hii hii, baadhi ya matatizo mengine yanagusiwa.

HIJAB

H

ii takriban ni moja ya hukmu muhimu juu ya wanawake, kwani ni wajibu wa kila mwanamke kuhifadhi na kuuficha mwili wake wote, isipokuwa mbele ya wale watu ambao kuoana nao kumeharamishwa kabisa, ambao katika sharia ya kidini wanaitwa mahrim, ama mbele ya watu wengine wote mwanamke anapaswa kuhifadhi na kuuficha mwili wake wote, ni uso na mikono hadi mwisho wa viganja tu vinaweza kuwa wazi (bila mapambo), kwa masharti kwamba hakuna hali chochezi au ya kichokozi inayoweza kujitokeza katika jamii, na jamii yenyewe isiwe na dhamira mbaya, roho mbaya na mawazo ya kiovu. Lakini katika kuweka uso wazi, nywele kukaa wazi kunakatazwa na kufunika kila unywele mmoja ni wajibu, vinginevyo hata angalau unywele mmoja utaonekana kupitia hijabu angavu, basi swala 40


Mwanamke Na Sharia

inakuwa batili na adhabu itakuwa lazima, haikwepeki, kwani katika Uislam ushungi (purdah) ni wajibu sio inapaswa iwe kama kitambaa cha kufunika nywele dupatta – dupatta, vinginevyo kuwepo kwake au kutokuwepo vyote ni sawa tu, kama alivyosema AmirulMu’minin Ali (a.s.): “Utafika wakati ambapo wanawake watakuwa wanaonekana kama wako uchi japo wawe wamevaa nguo zao, na matokeo yao yatakuwa si chochote bali ni Moto wa Jahannam.” Ni wajibu katika mazingira yoyote yale mtu kuficha sehemu zake za siri hata mbele ya maharimu (mwanaume mbele ya mwanamke, na mwanamke mbele ya mwanaume), kutokuwa na nguo kabisa kunaruhusiwa mbele ya mume na mke tu na sio mbele ya mtu mwingine yoyote. Na katika shughuli zote, vitendo vya kijamii vya kichochezi au uchokozi visije vikafikiriwa akilini kwa njia yoyote ile, vinginevyo kuna uwezekano wa uchochezi kuenea katika jamii. Hivyo wanawake kufunua miili yao mbele ya wanawake, na wanaume kuwa uchi mbele ya wanaume kumekatazwa, hata kwa kiasi cha kuficha sehemu zao za siri. Ndio maana Qur’ani Tukufu imewadokeza wanawake kwamba msionyeshe hata sehemu za mapambo mbele ya wanawake makafiri, kwani huenda wakaelezea uzuri na sifa zenu kwa waume zao na wanafamilia wao, hatimaye kuhatarisha heshima na hadhi ya wanawake wa Kiislam.

41


Mwanamke Na Sharia

HUKMU ZA MAITI

K

ama maiti ni ya mwanamke basi josho (ghusl) na kukafini lazima kufanywe na mwanamke tu, mwanaume hawezi kufanya hivyo, isipokuwa kama umri wa msichana ni chini ya miaka mitatu au asiwe chini ya umri wa utambuzi na upambanuzi wa mambo, kwani chini ya masharti haya hata mwanamume anaweza kumpa josho, vinginevyo chini ya masharti ya kawaida ni mwanamke tu ndiye atakayeosha maiti ya mwanamke. Upambanuzi huu unakuwa kwa mwanamume tu kwamba anaweza kumuosha marehemu mke wake, kwa vile hajakuwa sio maharimu kutokana na kifo, na wala uhusiano wake na mkewe haujavunjika moja kwa moja, vinginevyo hii ingekuwa hivyo, basi isingekuwa ni wajibu kumuombolezea mke na isingewezekana hata kumrithi pia, kwani ni ndugu tu wanaopata urithi. Baada ya kuondolewa kwa uhusiano hakuna yoyote ambaye anakuwa mrithi.

42


Mwanamke Na Sharia

KANUNI ZA SWALA 1.

Swala ya Ijumaa ni wajibu kwa wanaume pamoja na swala nyinginezo, lakini sio wajibu kwa wanawake, bali kama mwanamke akitaka kujiunga basi anaweza kufanya hivyo, na kama ataswali swala ya Ijumaa hatakuwa na haja ya kuswali swala ya Adhuhuri.

2.

Swala ya Idd pia ni kwa ajili ya wanaume na hailazimishwi kutoka kwa wanawake.

3.

Ni wajibu kwa wanaume kusoma katika rakaa mbili za awali za swala ya Asubuhi, Magharibi na Isha kwa sauti, lakini sio wajibu kwa mwanamke kusoma kwa sauti. Kama kuna mtu asiye maharimu anayesikiliza, basi anaweza mwanamke akasoma kwa sauti.

4.

Mwanaume anaweza kusimama mbele na kuswali, bali mwanamke hawezi imma kusimama mbele au ubavuni – bali anapaswa kusimama nyuma kidogo ili mwenza wake awe na usalama naye aibu na staha yake visije kubadilika mbele ya maharimu wake.

5.

Swala za jamaa na swala za misikitini sio maalum kwa wanaume tu, wanawake pia wanayo haki ya kujiunga lakini kama hakuna mipango ya jamaa katika msikiti, na hakuna fursa ya kujifunza sheria za Kiislam basi ni bora mwanamke akaswali nyumbani, kwani kwa ajili ya hili nyumba yenyewe imepewa 43


Mwanamke Na Sharia

hadhi ya msikiti na yeye atapata malipo ya kuswali msikitini ndani ya kuta nne za nyumba yake mwanamke huyo. Na kwa ajili ya jamaa, mwanamke anaweza kuswali katika jamaa na anaweza pia akaongoza swala, ila tofauti iliyopo tu ni kwamba ni wanawake tu wanaoweza kuswali pamoja naye, wanaume hawatakuwepo hapo na ni mwanamke tu atakayesimama kwenye safu pamoja naye, hatasimama mbele hata ya wanawake wenzie, kwa vile Uislam unahifadhi staha na aibu ya mwanamke hata mbele ya mwanamke mwenzie pia. 6.

Endapo mwanaume anapendelea kuvaa dhahabu na hariri na kuswali, basi swala yake inakuwa batili, lakini mwanamke anaweza akavaa dhahabu na hariri wakati wa kuswali.

7.

Adhana na Iqamah zinapendekezwa (ni mustahabu) kwa mwanamke, lakini ni muhimu kwa mwanamke kwamba asipaze sauti yake ili asije akaisikia asiye maharimu wake. Ieleweke wazi kwamba Adhana na Iqamah hazikulengewa wanaume peke yao, bali zinahusika kwa wote, wanaume na wanawake, ni jambo tofauti tu kwamba, kwa upande wa mwanamke masharti yaliyotajwa hapo juu hayana budi kukumbukwa.

8.

Mwanamke anaweza kujiunga katika swala ya jamaa na kusimama nyuma ya pazia, ambapo ni wajibu juu ya wanaume kwamba kisiwepo kitu chochote cha kuingia kati ya Imam na maamuma wake, na kati ya Maamuma na Imam, vinginevyo swala ya jamaa itakuwa ni batili, haiswihi.

9.

Kama swala za kadhaa zikiwa zimestahilia kwa upande wa baba na yeye akawa hakupata fursa ya kuzitekeleza, basi huo 44


Mwanamke Na Sharia

utakuwa ni wajibu kwa mtoto wake mkubwa wa kiume kuzitekeleza kwa niaba yake, lakini kama swala za kadhaa zimestahili juu ya mama, basi hizo sio wajibu wa mtoto mkubwa wa kiume kuzitekeleza, hivyo ni juu ya mwanamke mwenyewe kukamilisha swala zake kisha aondoke, na madai haya juu yao ni ya haki ya sawa kabisa kwani swala zilifanywa pungufu kwao kwa kila mwezi swala za siku nne hadi sita zilikuwa zikisamehewa juu yao. 10. Kama ilivyo kwa wanaume, na kwa wanawake pia swala za matukio (Salat al-Aayaat) kama za kupatwa kwa jua, kupatwa kwa mwezi, tetemeko la ardhi na kadhalika ni wajibu, lakini katika muda huo kama akiwa kwenye hedhi au nifas yeye hawezi akaswali chini ya hali hii na ni bora zaidi juu yake kuleta kadhaa yake baada ya kuondokana na hali hii (kama tahadhari).

45


Mwanamke Na Sharia

SAUMU 1.

Sio wajibu kwa mwanamke kufunga wakati akiwa kwenye kipindi chake cha mwezi (hedhi) na hawezi akafanya hivyo, bali baadaye kadhaa yake ni lazima ifanyike kwa hali na mazingira yoyote yale.

2.

Kama mwanamke akiwa mjamzito katika mwezi wa Ramadhani, na kama kuna uwezekano wa madhara kwa mwanamke huyo ama kwa mtoto, basi anapaswa kuakhirisha kufunga, na baadaye aje kufanya kadhaa yake, na sambamba na kadhaa hiyo aandae kulisha mtu mmoja masikini mwenye haja kwa kila saumu moja.

3.

Kama mwanamke ananyonyesha mwanawe mwenyewe au mtoto wa mwenzie na hakuna mtu mwingine wa kuweza kumlisha mtoto huyo, na kwa kufunga kuna uwezekano wa madhara kwake yeye mwenyewe au kwa mtoto, basi anayo haki ya kuacha kufunga, na kisha pamoja na kadhaa alishe masikini mmoja mwenye haja kwa kila saumu moja.

4.

Kama mfululizo wa siku za hedhi ama nifas umekwisha katika usiku wa mwezi wa Ramadhani, basi ni wajibu wake kuchukua josho kabla ya adhana ya swala ya Asubuhi na kuanza kufunga, vinginevyo kama josho halitachukuliwa kabla ya alfajiri basi saumu itakuwa batili, sharti kama hilo hilo linakuja kutumika kwenye suala la kadhaa ya saumu kwa mwezi wa Ramadhani. 46


Mwanamke Na Sharia

5.

Kama mwanamke yuko kwenye hali ya kipindi cha Istihadha Nyingi, basi ni wajibu wake kuwahi kwa wakati kuchukua josho kwa ajili ya kufunga saumu, vinginevyo, kama tahadhari, saumu yake itakuwa haisihi na itabidi kurudiwa, lakini kwa sharti la kuchukua josho pia, tahadhari inakuwa hii, kwamba mara moja anapaswa kuchukua josho kwa ajili ya saumu kabla ya adhana ya Asubuhi na tena baada ya adhana achukue josho kwa ajili ya swala ya Alfajiri.

6.

Kama mwanamume atakuwa amemlazimisha mkewe kujamiiana katika mwezi wa Ramadhani, basi jukumu la wajibu la kuifidia pia litakuwa juu ya mume, na endapo na mke pia alihiari basi atafidia yeye mwenyewe, na wote watachapwa viboko, kulingana na ulazima, kwa hukumu ya mwenye mamlaka ya juu (Hakim al-Shari’ah), kwa vile usiku mzima umewekwa huru juu ya hilo, basi iwapi ruksa yake kwa mchana huo.

47


Mwanamke Na Sharia

KHUMS NA ZAKA 1.

Kama mwanamke ni tajiri na anamiliki mapato yake mwenyewe basi yeye pia anapaswa kulipa Khums (1/5 ya akiba), au Zaka (kodi ya Kiislam) kwa wakati uliokadiriwa, na hahusishwi kwa hali yoyote ile na Khums au Zaka ya mume wake.

2.

Kama mume hampatii mke huyo matumizi ya lazima, basi kama mwanamke huyo akiwa ni Saiydani (kutoka kwenye kizazi cha Fatimah s.a.) anaweza kuchukua Khums na vinginevyo achukue Zaka, na hana haja ya kupondeka kwa huzuni ya ufidhuli wa mumewe.

KANUNI ZA HIJJA 1.

Kama mwanamke anazo fedha za kutosha kwendea Makka na kutekeleza ibada ya Hijja, basi ni wajibu wake kwenda kuhiji Nyumba ya Allah (Hajj al-Baitullah), hata kama mumewe anao uwezo wa kwenda au hapana.

2.

Kama mwanamke anavyo vito vya thamani vinavyozidi mahitaji yake muhimu, na kwa kuviuza hivyo anaweza akafanya Hijja, basi ni wajibu wake kuviuza na kwenda kuhiji.

48


Mwanamke Na Sharia

3.

Kama vito hivyo vya mwanamke huyo vimekuwa havina maana kutokana na umri wa uzeeni wa mwanamke huyo, na vikawa sasa havitumiki, basi inakatazwa na ni haramu kuvihifadhi kwa ajili ya vizazi vijavyo, ni wajibu wake wa kwanza na wa mbele kabisa kwamba endapo kwa kuviuza Hijja inawezekana kuendwa, basi aviuze na kwenda kuhiji. Mwenyezi Mungu ni huyo huyo kwa ajili ya vizazi vijavyo kama alivyokuwa kwa ajili yake yeye.

4.

Kama mume wa mwanamke hawezi kwenda Hijja na mke huyo amekuwa na uwezo wa hali, basi ni wajibu wake kwenda kuhiji, hakuna sharti la kufuatana na mtu maharimu iwapo hadhi na heshima yake binafsi havipo hatarini, jambo ambalo kwa kawaida huwa halitokei katika umri huu.

5.

Mwanamke anaweza kuwakilisha mwanamke mwenzie katika Hijja na anaweza pia kuwakilisha mwanaume, na kwa namna hiyo hiyo yeye anaweza akawakilishwa na mwanaume au mwanamke pia.

6.

Ni lazima kwa Ihraam ya mwanaume kwamba nguo yake hiyo isishonwe, lakini mwanamke anaweza akavaa Ihraam iliyoshonwa, ni bora kwamba nguo ya Ihraam iwe nyeupe.

7.

Kama mwanamke yuko kwenye damu ya hedhi wakati wa Hijja au Umra, basi hawezi kuingia humo msikitini, na ni wajibu wake kufanya niya ya Ihraam nje ya msikiti lakini hakuna madhara katika Ihraam, kwani kuwa tohara sio sharti kwa ajili ya Ihraam.

49


Mwanamke Na Sharia

8.

Kwa vile mwanamke anaweza kuswali akiwa amevaa hariri, lakini kwa ajili ya nguo ya Ihraam kama tahadhari isiwe ni ya hariri, kwa sababu kanuni za swala ni tofauti na kanuni za Ihraam, na katika Uislam hakuna nafasi ya kubuni.

9.

Kama mume atamlazimisha mke wake kujamiiana wakati wakiwa kwenye Ihraam basi wajibu wa kufidia (kaffarah) unakuwa juu ya mume wake na sio wa mwanamke huyo, na fidia hiyo ni kafara ya ngamia mmoja na wala sio mbuzi.

10. Mwanamke anaweza kuvaa soksi na viatu wakati wa Ihraam kwani vitu hivi vimeharamishwa kwa wanaume. 11. Ni wajibu kwa mwanamke kuhifadhi kabisa kichwa chake katika Ihraam na hilo limekatazwa kwa wanaume. 12. Imeharamishwa kwa mwanamke kujifunika ushungi kwenye uso wake katika Ihraam, kwani kuna umati wa malaki ya watu na kwa njia hii mtu anajaribiwa kwamba, ushungi (purdah) wake ni wa kawaida za kijamii au ameegemea kwenye amri za Mwenyezi Mungu, kama ni kwa mujibu wa amri za Mwenyezi Mungu, basi kila pale amri inapobadilika na mtindo unapaswa kubadilika. 13. Mwanamke anaweza kusafiri katika gari iliyofungwa au chini ya kivuli cha gari iliyofunikwa juu katika Ihraam ambapo imeharamishwa kwa wanaume na fidia yake pia ni wajibu. 14. Mwanamke hawezi kufanya tawafu (kuzunguka Ka’aba) wakati wa hedhi, au nifas kwani anakatazwa kuingia ndani 50


Mwanamke Na Sharia

ya Masjidul-Haraam, kama baada ya kuvaa Ihraam damu ya hedhi ikaanza basi asubiri uwe tohara, na kama hili limetokea wakati wa Umra, basi baada ya kumaliza zile kanuni za ibada zilizobakia, avae Ihraam kwa ajili ya Hijja na kufanya kadhaa ya tawafu na swala za Umra baada ya ibada za Hijja, na kama itakuwa haiwezekani kusubiri mpaka baada Hijja basi amfanye mtu mwingine kuwa mwakilishi kwa ajili ya tawafu na swala na yeye mwenyewe kutekeleza matendo yaliyobakia. 15. Kama mwanamke yumo katika kipindi cha Istihadha Chache, basi kwa wudhuu mmoja atafanya tawafu na kwa wudhuu mwingine ataswali na kama akiwa kwenye Istihadha ya Wastani basi afanye josho moja kwa ajili ya yote (tawafu na swala) na wudhu mara mbili tofauti, na kama ni Istihadha Nyingi basi kwa ajili ya matendo yote, majosho mawili yatachukuliwa na hakuna haja ya wudhu. 16. Kama mwanamke hawezi kurusha vijiwe kumpiga yule Shetani mkubwa (Shaitan al-Akbar) wakati wa mchana na kama kuna uwezekano wa kuongezeka kwa umati wa watu, basi anaweza kufanya hivyo katika usiku wa Idd. 17. Inaruhusiwa kwa mwanaume kunyoa nywele zake zote za kichwa au kuzipunguza lakini hairuhusiwi kwa wanawake kunyoa vichwa vyao, na kwao wao inatosha kupunguza baadhi ya nywele zao. 18. Baada ya kafara na kunyoa nywele ingawaje makatazo mengi sasa yanakuwa halali lakini mume hawezi kupata starehe za matamanio yake kutoka kwa mkewe hadi atakapofanya ­tawafun - Nisaa. 51


Mwanamke Na Sharia

19. Kama mwanamke akihofia kwamba wakati wa Hijja anaweza akafikwa na damu ya hedhi, basi yuko huru kufanya Tawaf ya Hijja, swala ya tawafu na Tawafun-Nisaa na swala yake kabla ya kuelekea Arafa na Muzdalifah baada ya kuvaa Ihraam ya Hijja ili watu kwenye msafara wasije wakasumbuliwa, na kama ikijitokeza ghafla basi kama watu wa msafara wake wanaweza kusubiri, basi baada ya kuwa tohara anapaswa kufanya Tawafu ya Hijja na Tawafun-Nisaa, vinginevyo amteue mtu kwa ajili ya tawafu na swala na yeye mwenyewe atafanya Sa’ii (kitendo cha kukimbia mara saba baina ya Safwa na Marwah), kwani inatekelezwa nje ya Masjidul-Haraam. 20. Katika Makka Tukufu, ndani ya uwanja kama mwanamke anapata nafasi mbele ya wanaume na kukawa na umati mkubwa, basi anaweza akaswali mahali hapo hapo na hakuna ubaya katika hilo, kwani katika sehemu nyingine mwanamke hawezi kuswali mbele za wanaume (Hii ni kwa mujibu wa fatwa ya Sayyid Siistani). 21. Kama mwanamke amekunywa vidonge ili kuzuia kutokwa na damu wakati wa Hijja au katika mwezi wa Ramadhani, na badala ya damu kutoka kwa mfululizo ikatoka kwa tone moja moja, basi haitachukuliwa kwamba ni hedhi na matendo yake yote yatakuwa ni sahihi, hata kama ikihukumiwa kwamba kama asingekula vidonge, ilikuwa ni kipindi cha hedhi na kwa wakati huo damu ingekuwa inatoka mfululizo. 22. Inatosha kwa mwanamke kupita Muzdalifah, hakuna haja ya kupitisha usiku mzima.

52


Mwanamke Na Sharia

KANUNI ZA NDOA 1. Katika tamko la ndoa (Sigha al-Nikaah) uthibitisho wa kukubali ni kutoka upande wa mwanamke na anajiwasilisha yeye mwenyewe kwenye kuwa mke, hivyo ni wajibu wake kuchunguza juu ya hali za baadaye na kupata msimamo, na kama kuna tishio la kuzidi na kukosekana uangalifu kutoka upande wa mwanaume, basi liweke sharti hili katika ikbali yenyewe kwamba iwapo kukiwa na matatizo ya kuzidi kiasi kutoka kwa mume, mamlaka ya talaka yatakuwa mikononi mwa mke. Na yeye atasimamia maelezo ya hati ya talaka chini ya utetezi wa mumewe, na kisha mume hatakuwa na haki ya kuingilia kati. 2.

Upangaji wa mahari pia uko mikononi mwa mwanamke, kwa vile ni kitendo cha kutendewa usawa katika kujitoa kwake, hivyo kuhudumia sehemu ya makubaliano yake ya ndoa (mahari) pia ni haki yake binafsi.

3.

Kama msichana katika kubaleghe kwake na kuwa na busara akiwa ni bikira pia, basi kama tahadhari anapaswa kupata ruhusa kutoka kwa baba yake au babu yake kwa ajili ya ndoa yake, na asiwe na uhuru wa kuolewa bila ruhusa hii. Lakini kama sio bikira, basi anaweza akaolewa bila ya ruhusa kwa sababu anajua njia na namna za maisha na hategemei juu ya ulezi wowote. Hakuna haja ya ruhusa zaidi ya ile ya baba au babu hata kama mama au kaka watakuwepo.

53


Mwanamke Na Sharia

4.

Kama mume akija kutambua kwamba mke alikuwa mwendawazimu kabla ya ndoa, ama alikuwa na ugonjwa wa ukoma au alikuwa kipofu au kilema, alikuwa na nyama ya ziada au mfupa na kadhalika katika sehemu yake ya siri, basi ana uhuru wa kukatisha uhusiano wao bila ya talaka na kusema kwamba simkubali mwanamke huyu, kwa njia hii uhusiano huo utakoma mara moja. Lakini kama mapungufu yote haya yatagundulika baada ya kufunga ndoa, basi hakuna njia ya kutengana isipokuwa kwa talaka, kwa vile hata hivyo maisha hayako huru kutokana na ajali.

5.

Kama mwanamke anakuja kujua kwamba mumewe hana dhakari ama hana nguvu ya kusimika basi na yeye pia anao uhuru wa kukatisha uhusiano wake mara moja, hakuna haja ya kupata talaka. Lakini katika suala la ukhanithi, kwanza suala hilo litawekwa mbele ya mtu mwenye mamlaka ya juu ya kidini (Hakim al-Shari’ah) naye ataliakhirisha kutoa nafasi ya matibabu, na kama katika kipindi hicho atakuwa hana nguvu za urijali, basi mwanamke huyo ana uhuru wa kukatisha ndoa hiyo.

6.

Endapo kutokana na dosari yoyote ya mwanamke huyo mume amevunja ndoa na hata kama mara moja amepenyeza dhakari yake (kwenye uke wake bila ya kumwaga manii), basi anapaswa kumpa kiasi chote cha mahari, na kama hilo lilitokea kabla ya kupenyeza huko, basi wala yeye hana wajibu wa kutoa mahari na wala mwanamke hana wajibu wa eda (kipindi cha muda ambacho mwanamke aliyeachwa au aliyefiwa na mume hawezi kuolewa na mume mwingine). Lakini ikiwa mwanamke ameikatisha ndoa kwa sababu ya udhaifu wa mwanaume, basi ukatishaji baada ya mpenyezo utampatia yeye mahari kamili, 54


Mwanamke Na Sharia

na katika suala la ukatishaji kabla ya mpenyezo, yeye hatapata chochote. Ni pale tu kama kwa msingi wa ukhanithi ndipo mke alipokatisha ndoa, basi hapo kwa hakika atapata nusu ya mahari iliyokadiriwa, kwani pale ambapo mwanaume alikuwa hana uwezo wa chochote basi iko wapi haja ya kumchukulia yeye kama mwanamke aliyeolewa. 7.

Kama mwanaume amemuoa mwanamke kwa sharti kuwa awe bikira na baadaye akaja akagundua kwamba amepoteza ubikira wake, basi na mwanaume naye anayo haki ya kufuta ndoa hiyo, na hata wakati ndoa kama ikiendelea, yeye anayo haki ya kurudishiwa ile tofauti ya mahari inayozidi, kati ya ile ya mwenye bikira na asiye bikira.

8.

Kama mtu amemuoa tu mwanamke mama wa mke wake atakuwa maharimu (kwa kumuoa) wake pia daima milele. Lakini kama alianza kumuoa mama wa binti, basi binti huyo hatakuwa ni maharimu kwake wakati akiwa hajamuingilia mke wake, kwani kabla ya kumwingilia anaweza akamtaliki huyo mama na akamuoa binti yake.

9.

Kama mtu amemuoa mwanamke, basi kumuoa dada wa mke huyo imekatazwa, ni haram kwake maadamu dada huyu yuko kwenye ndoa yake, na kisha kama atamtaliki mke wake basi hawezi kumuoa dada yake mpaka eda yake ikamilike, na kama hakuna eda juu ya mke huyo kama katika mas’ala ya ndoa ya Mut’a (ndoa ya muda maalum), basi hawezi kumuoa dada huyo mpaka kwisha kwa ule muda wa eda.

10. Yeye hawezi kumuoa binti ya dada au binti ya kaka wa mke ali55


Mwanamke Na Sharia

yekuwa amemuoa bila ruksa ya mkewe huyo, bali kuoa mwanamke mwingine yoyote yule hakuna haja ya ruhusa kutoka kwa mke wake. 11. Endapo mtu atakuwa amefanya zinaa na mwanamke, basi kama tahadhari hapaswi kumuoa binti ya mwanamke huyo, na kama baada ya ndoa atafanya zinaa na mama yake mkewe, basi kwa hali yoyote ile huyo mkewe hawezi kuharamishwa kwake. 12. Mwanamke wa Kiislam hawezi kuolewa na mume kafiri (mwenye kumkana Allah), si kwa ndoa ya Mut’a au ndoa ya kudumu, bali Mwislamu mwanaume anaweza kufanya Mut’a na mwanamke atokanaye na Ahlul-Kitaab (waliopewa kitabu). 13. Yale madhehebu ya Kiislam yaliyochukuliwa kama ya kikafiri, kama vile madhehebu ya Ghali, Naasibi na Khawarij na kadhalika, ndoa ya Mut’a au ile ya kudumu na wanawake wao hairuhusiwi. 14. Kama mtu amefanya zinaa na mwanamke aliyeolewa au aliye katika eda ya Talaka Rejea (Talaka ambayo baada yake mume anaweza kumwendea mkewe), basi mwanamke huyo ameharamishwa kwake milele, hata baada ya kufariki kwa mumewe, au kama mwanamke huyo ni kafiri kisha baadaye akawa Mwislamu, hakuna uwezekano wa mwanamke huyo kuwa halali kwa mwanaume huyo. 15. Kama zinaa inafanyika pamoja na mwanamke asiyeolewa, au mwanamke asiye na eda ya Talaka Rejea, basi anaweza akamuoa baadaye, lakini kama yuko kwenye eda basi amuoe baada 56


Mwanamke Na Sharia

ya eda hiyo na kama hakuna eda basi kama tahadhari amuoe baada ya kutubia kwa ajili ya zinaa hiyo, mtu mwingine wa tatu anaweza kumuoa bila ya kutubia kokote pia kwa masharti kwamba mwanamke huyo sio maarufu wa zinaa, vinginevyo, kama tahadhari, toba ni lazima ifanyike. 16. Endapo mtu, kwa makusudi kabisa, amemuoa mwanamke ambaye tayari ameolewa, basi mwanamke huyo ataharamishwa kwake daima, hata ikiwa amepenya au hapana. Lakini kama alimuoa bila kujua na akawa hajamwingilia basi hatakuwa haramu kwake hata kama mwanamke huyo alikuwa anatambua kuhusu kuwa kwake ameolewa, lakini kama kwa masharti hayo hayo hapo juu pia kupenyeza kumefanyika, basi hakuna namna ya yeye kuwa halali kwa kuolewa na mwanaume huyo. 17. Kama mwanamke yeyote atafanya zinaa basi hataharamishwa kwa mume wake, lakini ni bora kwa mumewe kumtaliki mke huyo kama hatatubia. 18. Kama mtu aliyekuwa muovu amefanya liwati na kijana mdogo wa kiume, basi hawezi kumuoa mama yake na dada wa kijana huyo mpaka Siku ya Kiyama, hata kama huyo mtendaji na mtendewa wamebalehe au hawajabalehe. 19. Kama baada ya kumuoa mwanamke, mume wake atafanya liwati na baba wa mke, kaka yake au mwanawe, basi na mke huyo pia, kama tahadhari atakuwa ni haramu kwa mumewe huyo.

57


Mwanamke Na Sharia

20. Kama mtu anamuoa mwanamke aliye katika Ihraam, basi mwanamke huyo atakuwa haramu kuoana naye daima, hata kama mwanaume alikuwa hayuko kwenye hali ya Ihraam. Na katika hali hiyo hiyo kama mwanamke anaolewa na mwanaume aliye katika Ihraam, basi yeye pia atakuwa haram kuolewa na mume huyo daima, hata kama mwanaume huyo akiwa hayuko kwenye hali ya Ihraam. 21. Kama mwanaume hakufanya Tawafun-Nisaa, basi wanawake wote akiwemo pamoja na mke wake watakuwa wameharamishwa kwake, na kama mwanamke yeyote atakuwa hakufanya Tawafun-Nisaa, basi wanaume wote, pamoja na mume wake watakuwa ni haramu kwake, lakini kama baadaye watafanya hiyo Tawafun-Nisaa, basi wote watakuwa ni halali kwa kila mmoja wao. 22. Ndoa inaweza kufanyika na msichana wa chini ya miaka tisa, lakini kuingilia hakuwezi kufanyika, kama mwanaume yeyote atamuingilia mke wake ambaye hajabalehe bado, basi kitendo hicho kitachukuliwa kama haramu, lakini msichana huyo hataharamishwa kwa mume wake, hata kama kwa kitendo hicho cha kuingiliwa sehemu yake ya siri itakuwa imechanika. 23. Ni wajibu wa mwanamke kwamba wakati wowote mume wake atakapoelemea tamaa ya kujamiiana, yeye lazima awe tayari kwa ajili yake na asimkatalie bila sababu ya maana, na asije akatoka nje ya nyumba yake bila ruhusa ya mumewe hususan pale ambapo kwa kutoka kwake kuna hatari ya matakwa yake kukanyagwa. Kama Hijja imekuwa ni wajibu juu ya mke huyo basi bila ya ridhaa ya mumewe yeye hawezi kujiunga na msa58


Mwanamke Na Sharia

fara wa kwanza kwenda Hijja, na atakwenda na ule msafara ambao Hijja inaweza kufanyika na matamanio ya kujamiiana ya mume wake yakiwa hayakukanyagwa. 24. Kama mwanamke atashughulikia haki za kujamiiana za mumewe, basi matumizi yake yote (ya halali) yatakuwa ni wajibu juu ya mumewe, na kama akimkatalia vivi hivi basi atakuwa hana haki yoyote, hata kama atakaa ndani ya nyumba ya mume wake. Lakini endapo wakati mwingine anakuwa yuko tayari na wakati mwingine anamkatalia bila sababu ya msingi, basi ni dhahiri kwamba atakuwa mkosaji mwenye dhambi lakini haki yake ya riziki haitakoma, na mahari lazima itolewe kwa hali zote hizo, kwani mahari inahusika na yote, ndoa na kupenyeza kwa mara moja. Kwa hili utayari na uendelevu sio muhimu. 25. Mwanaume hana haki ya kumlazimisha mke wake kufanya kazi ndani ya nyumba, bali kubeba matumizi yake ni wajibu kwa mazingira yoyote yale, hata kama mume atamchukua mkewe kwenye safari, au mke akisafiri kwa idhini yake basi anapaswa kubeba gharama hiyo hata kama ikiwa ni zaidi ya matumizi ya nyumbani. Lakini kama mume ametoa ruhusa kwa masharti kwamba hatabeba gharama hizo basi hatakuwa na wajibu juu ya hilo. 26. Kama mume atakataa kutoa mahitaji muhimu kwa mke wake, basi mke ana haki ya kutumia kutoka kwenye mali ya mumewe, na kama hilo halitawezekana basi atatoa malalamiko kwa kiongozi mwenye mamlaka ya juu ya kidini, na kama yeye pia hawezi kufanya lolote, basi mke anaweza kutafuta kazi ya kufanya na mume atakuwa hana haki ya kumzuia kutoka nje kwa ajili ya kazi hiyo. 59


Mwanamke Na Sharia

27. Mwanamke anayo haki ya kusamehe masurufu ya baada ya kuachika kwake, hata kwa maisha yake yote. 28. Mahitaji muhimu ya mke yana kipaumbele zaidi juu ya matumizi ya ndugu wa mume, kama mume anayo mikate miwili basi anaweza kushirikiana mkate wake yeye pamoja na wazazi wake lakini hawezi kuzuia mkate wa mkewe, kwani sheria ya dini imefanya ni wajibu kutumia kwa ajili ya wazazi, na ameoa na kuchukua wajibu wa matumizi ya mke wake, hivyo anapaswa kuyatimiza hayo kwanza kisha ndipo zifuate haki nyinginezo, na kama mume hawezi kufanya hivyo basi kiongozi mwenye mamlaka ya juu ya kidini atawasaidia na asije akawaacha wafe kwa njaa. 29. Kwa muda mume anaweza akashindwa kumpatia mke mahitaji yake basi wajibu huu haujafikia mwisho, bali haki hii itakuwepo juu yake kwamba wakati wowote atakapokuwa tajiri atapaswa kutoa haki zote zilizokuwepo, kinyume chake kama kwa wakati huu yeye hawezi kutoa matumizi ya wazazi wake basi sio wajibu wake kuja kuyatoa baadaye kwa njia ya kuyafidia. 30. Ni bora kupitisha usiku wa siku moja kati ya siku nne pamoja na mke, lakini kama mtu anao wake wawili na amepitisha usiku mmoja na mke mmojawapo, basi na huyo mke mwingine lazima naye apate usiku mmoja kati ya siku nne, hata kama watadumisha mahusiano ya kimwili au hapana. 31. Kama mtu hatajamiiana na mke wake kijana kwa zaidi ya miezi minne chini ya ulazimikaji wa namna fulani au alikuwa katika makubaliano naye kabla ya hapo basi hakuna pingamizi, ving60


Mwanamke Na Sharia

inevyo hii ni dhulma kwa mwanamke nayo imeharamishwa, iwe kwa mke wa kudumu au wa muda maalum na mume kuwa nyumbani au safarini, hakuna ubaya katika kuchelewa baada ya kupata ruhusa kutoka kwa mke wake. 32. Kama mtu ameoa bila ya kupanga kiwango cha mahari, basi ndoa hiyo ni sahihi, bali ni lazima atoe kile kiwango cha mahari kinachotolewa kwa kawaida kwa wanawake kama hao. 33. Endapo masharti ni kwamba mahari yatatolewa mara tu, basi mwanamke anayo haki kamili ya kukataa kumilikiwa kwake na mumewe bila kuchukua mahari yake, lakini kama hakuna masharti kama hayo, na kuna uwezekano wa kuyapata siku za baadaye, basi kukataa hakuruhusiwi. 34. Hakuna haja ya silika za kiashiki tu kwa ndoa ya muda na mwanamke, lakini kunaweza kuwa na sababu nyingi nyingine kwa ajili yake na ndoa ya Mut’a inaweza kufanyika kwa ajili ya kumfanya mwanamke huyo kuwa maharimu (kuzoeana kidini). 35. Katika suala la Mut’a ni lazima kupanga kiwango fulani cha mahari, iwe ni rupia moja, shilingi ngapi, na kwa namna hiyo hiyo ni lazima kupanga muda wake, uwe ni mfupi kwa kiasi kiwacho chochote. 36. Kama mwanamke ataweka sharti katika ndoa ya Mut’a kwamba hakutakuwa na kuingilia basi mwanaume anapaswa kulishika na kuliheshimu sharti hilo, lakini kama mke atakubaliana juu ya kuingilia baadaye, basi hiyo haitakuwa ni zinaa, na hata hivyo, mke ni mke tu. 61


Mwanamke Na Sharia

37. Katika Mut’a mwanamke hana haki ya matumizi, hiyo ndio sababu ya kwa nini mume hana haki ya kumzuia kufanya kazi kabla haki yake haijakanyagwa, na kwa njia hiyo hiyo hakuna mirathi katika Mut’a, bali kama atazaliwa mtoto basi katika kipindi cha uhai wake wote matumizi yake ni wajibu wa baba yake, na baada ya kifo chake baba, mtoto atamrithi baba yake vile vile kwa vile muda ni kati ya mume na mke, hakuna muda kati ya uhusiano wa baba na mtoto. 38. Kama mume atasamehe muda katika Mut’a, na akawa amemwingilia mke huyo, basi atalazimika kutoa mahari yote, na endapo hakumuingilia basi atapaswa kutoa nusu ya mahari kwa namna yoyote ile. 39. Kama mwanamke yuko kwenye eda yake mwenyewe baada ya kumaliza muda wa Mut’a, basi mume huyo anaweza akafanya Mut’a au ndoa ya kudumu pamoja naye tena, lakini kama muda wenyewe utakuwa bado haujaisha basi hawezi kufanya aina yoyote ya ndoa mpaka kipindi hicho kimalizike. 40. Baba au babu wanayo mamlaka ya kufanya ndoa ya muda mfupi ya kijana wao au msichana ambao hawajabalehe kwa kudumisha kuzoena kidini tu (Mahramiyat), lakini kama tahadhari wakipanga kipindi ambacho uwezekano wa namna yoyote ya hawaa hauwezi kupatikana, na kisha pasiwe na kishawishi chochote cha kijamii au hasara kutokana na ndoa hii, vinginevyo sababu ya malezi kwa ajili ya mtoto asiyebalehe ni kwa faida yake.

62


Mwanamke Na Sharia

KANUNI ZA KUANGALIA (KUTUPIA MACHO)

U

tazamaji kwa kawaida unasemekana ni kwa ajili ya kuona kitu fulani, lakini sababu zake na nia zake zinatofautiana, na kwa msingi wa sababu na nia hizi hizi zinakadiriwa kuwa njema au mbaya. Utazamaji wa mama juu ya mtoto wake unaitwa ni huruma na upendo, na utazamaji wa adui kwa adui yake unaitwa ni utazamaji mbaya, kwa sababu nia na madhumuni ya yote mawili ni mbalimbali, vinginevyo macho ni yale yale na uwezo wa kuona pia ni wa namna moja hiyo hiyo. Katika mifano na vitendo vya utazamaji huu huu hasa, ni muonekano wa hisia za kimapenzi au upeo wa furaha, ambao ndio unaoelekeza kutazama kwa sababu kwa kupitia utazamaji huo maandalizi kwa ajili ya kukidhi haja ya kijinsia hufanyika, ambao katika msemo wa kawaida huitwa joto la macho, ambao njia yake ni uzuri wa mwanamke na mvuto wa mashavu yake, ambao katika lugha ya kidini ni kitia ashiki. Mtu wakati wowote anapomtazama mtu mwingine, mbali na mke wake au mtumwa wake wa kike, kwa utazamaji kama huo, hivyo utazamaji wake unaitwa ni wa haramu, ama shabaha yake iwe ni mwanaume au mwanamke, kijana au mzee, mwanadamu au mnyama, kwa kushangaza sana, anatazama pia picha kwa utazamaji huo na kunakuwa na hatari ya kujiingiza kwenye kitendo kiovu na vitendo vya kujifurahisha mwenyewe na kadhalika, ambavyo pia vimeharamishwa. Mbali na hili, aina za utazamaji mwingine sio haramu ambapo hakuna hatari yoyote ya mtu kuangukia kwenye umalaya, na namna 63


Mwanamke Na Sharia

za utazamaji huu hasa hatimaye huitwa utazamaji halisi. Ni jambo tofauti kwamba anaweza tu kuweka wazi uso wake na viganja mbele ya mtu asiye maharimu, lakini kuonyesha nywele zake za kichwa na sehemu nyingine za mwili kwa hali yoyote ile kumekatazwa. Taratibu zifuatazo kuhusiana na hili zinafaa kuzingatiwa: 1.

Kumwangalia mwanamke asiyejulikana bila ya kutamani hakukatazwi, kama macho yake yameangalia usoni na mikono tu, mbali na hivi, kuangalia sehemu za mwili zilizobakia kunakatazwa, na kule kuangalia kwa tamaa kwenye uso na mikono pia kunakatazwa.

2.

Inaruhusiwa kuangalia zile sehemu za mwili za wanaume na wanawake wasiojuana, ambazo kwa kawaida zinaachwa wazi, kama vile kichwa, mikono yote, miguu yote na kadhalika, kwa sharti kwamba nia yake pia sio ashiki ya kijinsia.

3.

Aina ya wanawake wazururaji wasio washika dini ambao hawako tayari kukubali kanuni za sheria za kidini, zile sehemu zao za mwili zinaweza kuangaliwa, ambazo kwa kawaida wanatii kuziweka wazi kwa sharti la kutokuwa na matamanio, na mwanamke huyo sio mwanachama wa ukumbi wa wakaa uchi, vinginevyo miili ya wanawake kama hao iko wazi kabisa na vipimo kama hivyo havipatikani katika uruhusikaji katika utazamaji.

Sababu ya uruhusiwaji huu juu ya utazamaji pia ni huu kwamba, kukataza utazamaji kama huu kwa kweli ni heshima ya mwanamke, na yule mwanamke ambaye hajiheshimu mwenyewe hana heshima katika dini pia, na kwa sababu hii wakati mwanamke anapotengana na mumewe basi mwanaume mwingine hawezi kumuoa mpaka 64


Mwanamke Na Sharia

amalize eda yake, kwani ni lazima kuheshimu maisha yake ya ndoa ya hapo kabla. Lakini kama mwanamke ni mzinifu na sasa hivi tu ametenda zinaa na mtu mwingine anataka kumuoa na hakuna haja ya kungojea kwa miezi mitatu, hivyo ambapo yeye mwenyewe hakuyaweka maisha yake kwa usafi, basi kuheshimu mahusiano yake machafu sio wajibu juu yetu. 4.

Kutupia macho kwenye sehemu za siri za mtu yoyote kumeharamishwa hata kama ni kafiri au hajabalehe kwa kuelewa kabisa ama ametazama moja kwa moja au kupitia kwenye kioo au maji angavu, ni mke na mume tu wanaoweza kuangaliana miili yao mizima.

5.

Mtu anaweza akaangalia mwili wa mwanamke maharimu wake, lakini sio kwenye sehemu zake za siri, na sio katika zile sehemu za mwili ambazo kuna uwezekano wa kusambaza mawazo maovu kwani utazamaji wa kitamaa umeharamishwa kwa hali yoyote ile.

6.

Mwanamke hawezi kuangalia mwili wa mwanamke mwingine na mwanaume hawezi kuangalia mwili wa mwanaume mwingine kwa matamanio, na hili ni jambo limeharamishwa pia.

7.

Kuangalia picha ya mwanamke ambaye si maharimu, ambaye mtu anamfahamu kumekatazwa, lakini kama ni uso na mikono tu vilivyo wazi, na utazamaji sio wa kitamaa basi hakuna madhara katika hilo.

8.

Katika nyakati za mahitaji, kama vile huduma ya matibabu na kadhalika, mwanaume anaweza kumwangalia mwanamke ambaye si maharimu, na mwanamke anaweza kumwangalia mwanaume ambaye si maharimu lakini sharti la kwanza ni kwamba, hakuna njia nyingineyo ya matibabu 65


Mwanamke Na Sharia

inayopatikana na sharti la mwisho ni kwamba matibabu kupitia kioo na kadhalika pia hayawezekani. Masharti kama hayohayo pia ni kwa ajili ya kuugusa mwili kwani kumekatazwa kwa nguvu zaidi kuliko kule kuangalia.

66


Mwanamke Na Sharia

BAADHI YA TARATIBU ZA KIJAMII 1.

Mtu ambaye hawezi kuidhibiti Nafsi yake, na kuna uwezekano wa yeye kufanya yale yaliyoharamishwa, basi ni wajibu wake kuoa au kuolewa haraka iwezekanavyo na kuiweka nafsi yake katika usalama kutokana na yale yaliyoharamishwa, awe ni mwanaume au mwanamke.

2.

Imeharamishwa kwa mwanaume na mwanamke wasio maharimu kukutana mahali ambapo kuna uwezekano wa kujiingiza kwenye tendo linalokatazwa kisheria, hata kama mtu wa tatu anayo nafasi ya kuweza kufika hapo.

3.

Kama mtu akioa kwa nia ya kutotoa mahari, basi ndoa hiyo ni sahihi, bali kwa hali yoyote ile ni lazima atoe kiasi kile cha mahari ambacho kwa kawaida kinatolewa kwa wanawake kama hao.

4.

Kama mume wa mwanamke mwislam akiritadi na kuwa kafiri, basi uhusiano wao umevunjika na ni wajibu wa mwanamke huyo kukaa eda ya miezi minne (Iddat al-wafaat) na kujitenga kabisa na uwanandoa, kwani mume kama huyo ni sawa na mtu aliyekufa tu. Uhai ni sehemu ya Uislam, kuuondoa huo kila imani ni kifo cha ubinadamu. Kama mume amekuwa mwislam kutoka kwenye ukafiri na kisha akawa kafiri tena, na hili limetokea baada ya kuingiliana, na mwanamke mwenyewe sio wa miaka sitini, basi anapaswa kuchunga eda ya talaka (Iddat al-Talaaq) kwa muda wa miezi mitatu na katika kipindi cha 67


Mwanamke Na Sharia

muda huo mwanaume awe mwislam tena ndipo amkubali kama mumewe tena. 5.

Kama mwanamke ameweka sharti katika ndoa yenyewe kwamba yeye hataondoka mjini hapo, basi mume hana haki ya kumlazimisha, bali kama yeye mwenyewe atahiari baadaye, basi hakuna madhara.

6.

Kama mke wa mtu anaye binti wa mume mwingine, na mume naye anaye kijana kutokana na mke mwingine, basi anaweza kumuoza binti huyo kwa kijana huyo, ambapo uhusiano utakuwa umekithiri ndani ya nyumba, baba ameoana na mama wa binti na kijana ameoana na binti ya mama huyo, bali kwa hakika wao sio kaka na dada, vinginevyo uhusiano huo ungeharamishwa moja kwa moja kabisa.

7.

Kama mtu amefanya zinaa na mwanamke na baadae wakaoana, na wakawa hawawezi kupambanua kama mtoto aliyezaliwa alikuwa ni wa kipindi cha haramu au cha halali (yaani wa baada ya kuoana) hivyo kisheria itapaswa kufikiriwa kwamba ni halali tu.

8.

Kama mwanamke atadai kwamba yeye ni mwenye umri wa miaka zaidi ya sitini (ambapo damu ya hedhi husimama), hivyo madai haya yanahitaji ushahidi kwani hakuwa hivyo tangu siku ile ya mwanzo, lakini kama akisema kwamba hana mume, basi madai yake haya yatakubalika, kwani kwa kuzaliwa, kila mwanamke hana mume.

9.

Kama mwanamke akisema kwamba yeye hana mume na mtu akamuoa huyo, na baadaye mtu akaja kudai kwamba yeye ni 68


Mwanamke Na Sharia

mume wa mwanamke huyo, hivyo mpaka pale kuwa kwake mumewe kutakapothibitishwa, kauli ya mwanamke huyo kuhusu yeye mwenyewe itakubaliwa. 10. Hairuhusiwi kwa baba kumtenganisha mtoto (anayenyonya) na mama yake kabla ya miaka miwili, na kama suala la tahadhari, asiuchukue msimamo huu kwa muda wa miaka saba. 11. Kama mtu ataleta posa (kwa ajili ya kuoa) kwa mtu ambaye dini yake pia ni sahihi na tabia ni nzuri pia, basi anapaswa kumuoza binti huyo mara moja haraka sana, vinginevyo Mtukufu Mtume (saww) amesema kwamba, kwa kutokufanya hivyo kunakuwa na uwezekano wa ufisadi na ufuska kuenea katika jamii. 12. Kama mwanamke anakuja kuelewana na mumewe kwenye suala la kwamba yeye hatodai mahari kutoka kwake kwa sharti mume hataiendea ndoa ya pili, basi ni wajibu wa mume huyo kutokuoa mke wa pili, na ni wajibu wa mke huyo kutokudai mahari hiyo. 13. Endapo baba wa mtu fulani alizaliwa nje ya ndoa (kwa zinaa) na yeye mwenyewe akazaliwa baada ya ndoa ya baba yake huyo, basi yeye atachukuliwa kama amezaliwa kwa njia halali, na sio kwa njia haramu kwani mtoto wa haramu ni matokeo ya uzinifu, sio ukoo wala jamii. 14. Kama mtu atakuwa amejamiiana na mkewe wakati wa mchana wa Ramadhani au wakati wa damu ya hedhi na mtoto akazaliwa, basi mtoto huyo ataitwa ni mtoto wa halali kwa sababu mwanamke wakati wa mwezi wa Ramadhani au akiwa katika 69


Mwanamke Na Sharia

hedhi bado ni mke tu, na hawi maharimu, ni kujamiiana na mumewe wakati huo tu ndio kumeharamishwa, ambako adhabu yake itabidi kuzingatiwe kwa hali yoyote ile. 15. Kama mwanamke yoyote anayo hakika juu ya kifo cha mumewe aliyepotea na akaingia kwenye ndoa nyingine ya pili, na baadaye yule mumewe akapatikana akiwa hai, basi mara moja atatengana na mume huyu aliyenaye na kurudi kwa mumewe wa kwanza, na atarudisha mahari kamili kutoka kwa huyu mume wa pili endapo kuingilia kulifanyika, lakini hawezi kuendeleza mahusiano ya kimapenzi na mume wake wa kwanza mpaka awe amezingatia eda wakati wa kutengana na mume wa pili, na matumizi yake katika kipindi hicho cha eda pia lazima yatokane na mumewe wa kwanza na sio huyu wa pili. Falsafa juu ya mwanamke huyu ni kwamba, kwa vile yeye alifanya jambo la ndoa sahihi chini ya mazingira (ya matukio) danganyifu, na wala hakufanya uzinifu, na kwamba katika ndoa eda ni lazima kwa namna yoyote ile, na kuiheshimu ni wajibu, masuala mengine yote mbali na kujamiiana kwa hiyo yanaruhusiwa pamoja na mumewe wa kwanza, na mume anaweza kukaa naye kama mumewe na yeye kama mke, bali hawezi kujamiiana na mkewe huyo wakati wa kipindi cha eda.

70


Mwanamke Na Sharia

KANUNI ZA MALEZI (UNYONYESHAJI)

M

asharti yafuatayo ni lazima, kwa masharti haya udugu wa kunyonya unajengeka, na bila ya hayo hakuna uhusiano unaoweza kuundika: 1.

Mwanamke anayenyonyesha maziwa lazima awe hai, vinginevyo kama mtu amenyonya maziwa ya mwanamke aliyekufa basi hakuna matokeo yoyote juu ya hili.

2.

Maziwa lazima yawe ni matunda ya njia halali, vinginevyo maziwa yaliyotengenezwa kwa njia ya zinaa hayaleti athari yoyote ya uhusiano.

3.

Mtoto huyo ni lazima anyonye maziwa kupitia kwenye chuchu za matiti ya mwanamke, maziwa ya kufanya kukamuliwa hayatakuwa na athari yoyote (kiuhusiano).

4.

Maziwa lazima yawe halisi yasiyochanganywa, vinginevyo kama kitu kingine chochote kitawekwa mdomoni kwa mtoto huyo, basi yatakuwa hayaathiri kitu.

5.

Maziwa yote yawe yanatokana na matunda ya mume mmoja, vinginevyo kama wakati mmoja ni ya mume huyu na wakati mwingine maziwa ya mume mwingine yakinyonyeshwa basi itakuwa hakuna athari yoyote.

6.

Mtoto lazima ayamengenye maziwa tumboni mwake, vinginevyo maziwa yaliyotapikwa hayatahesabika chochote.

7.

Maziwa yenyewe ayanyonye kwa kiwango ambacho kwamba minofu inatengenezwa na mifupa kufanywa kuwa 71


Mwanamke Na Sharia

na nguvu, dalili ya hili ni kiasi kwamba mtoto anapaswa kunyonyeshwa siku moja na usiku mmoja mfululizo, au katika muda mwingine tofauti, angalau anapaswa kunyonya na kushibisha tumbo kwa mara kumi na tano. 8.

Yote haya yanapaswa yawe ndani ya miaka miwili ya umri, vinginevyo baada ya hapo kunyonya maziwa hakuleti athari kwa namna yoyote ile, na kwa sababu ya hili kama mume akinyonya maziwa ya mke wake hatakuwa ni mwanawe, kwani kitendo chake hiki kwa usawa kabisa kitaitwa ni makuruhu – cha kuchukiza.

72


Mwanamke Na Sharia

MATATIZO YA UNYONYESHAJI 1.

Mtoto yoyote wa kiume ambaye amenyonya maziwa ya mwanamke kwa mujibu wa masharti (yaliyotajwa), basi wanawake wafuatao watakuwa ni haramu kwake kuwaoa: a.

Mwanamke yule aliyemnyonyesha kwa vile amekwisha kuwa ni mama yake.

b.

Mama wa mnyonyeshaji, sawa awe wa nasaba au wa kunyonyesha, kwani hadhi yake itakuwa kama bibi.

c.

Watoto wake mama huyo wa nasaba au wa kunyonyesha, kwani wote wamekuwa ni dada zake.

d.

Mabinti za watoto wake kwani mtu huyu aliyenyweshwa maziwa amekuwa mjomba au baba yao mdogo/mkubwa.

e.

Dada zake, hata kama wakiwa ni wa kunyonya, kwani ni shangazi za watoto wake.

f.

Shangazi zake na mama zake wadogo na wakubwa, kwani nao pia wamekuwa mashangazi na mama zake mtoto huyu.

g.

Yule mtu ambaye alinyonya maziwa kutoka kwa mwanamke huyo, mabinti zake ama wa damu au wa kunyonya kwani wote hao ni dada zake.

h.

Mama wa yule mwenye kumiliki maziwa, sawa awe wa nasaba au wa kunyonya kwani wote wamekuwa ni nyanya (bibi) zake. 73


Mwanamke Na Sharia

2.

i.

Dada za mmiliki maziwa sawa wawe wa nasaba au wa kunyonya kwani wote wamekuwa ni shangazi zake.

j.

Akina mama wa upande wa kikeni na shangazi za mmiliki maziwa, au shangazi za wazazi wake kwani wote ni mabibi wa mtoto huyo.

k.

Wake za mmiliki wa maziwa kwani wao ni wake za baba yake na wako katika nafasi ya mama yake.

Kama mtoto yoyote wa kike amekunywa maziwa ya mwanamke kulingana na masharti, basi wanaume wafuatao watakuwa ni haramu kumuoa yeye: a.

Mmiliki wa maziwa hayo, maziwa ambayo yametengenezwa kutoka kwake, ambayo yeye ameyanyonya, kwani amekuwa ni baba yake.

b.

Baba na babu wa mmiliki wa maziwa kwani wamejiunga na wahenga wake.

c.

Watoto wa damu au wa kunyonya wa mmiliki wa maziwa kwani wamekuwa ni ndugu zake.

d.

Ndugu wa kiume wa mmiliki wa maziwa kwani wamekuwa ni Ami zake.

e.

Shangazi na mama wadogo wa mmiliki wa maziwa au wa wazazi wake, kwani wote wamekuwa mababu zake wa kiumeni na kikeni.

74


Mwanamke Na Sharia

3.

Baba wa mtoto wa kiume au wa kike hawezi kuwaoa mabinti wa mwanamke anayewanyonyesha maziwa watoto wake.

4.

Baba wa watoto wanaokunywa maziwa hawezi kuwaoa mabinti wa mmiliki wa maziwa yanayolishwa kwa watoto wake.

5.

Mama aliyepewa unyonyeshaji au mabinti zake hawazuiliwi kuolewa na ndugu wa mtoto anayenyonyeshwa maziwa.

6.

Sharti la msingi la kuanzisha undugu kati ya watoto ni kwamba, wote wawe wamenyonya maziwa yaliyozalishwa kutoka kwa mwanaume mmoja huyo huyo, vinginevyo kama mwanamke ameolewa mara mbili, na akawa amewalisha watoto wote kwa maziwa ya wanaume wote wawili basi hawatakuwa kaka na dada wa kunyonya.

7.

Undugu unaanzishwa, na kuoana kunaharamishwa, vyote kutokana na kunyonya, lakini hakuna kurithiana, kwani urithi upo kwenye uhusiano wa undugu halisi (wa damu) na hakuna mwingine zaidi ya hao mwenye haki hii.

75


Mwanamke Na Sharia

TARATIBU ZA UNYONYESHAJI 1.

Kwa vile kumnyonyesha maziwa mtoto sio jukumu la wajibu kwa mama, na wajibu wa kumlisha mama pamoja na mtoto unabakia juu ya baba, lakini bado haki ya kumnyonyesha mtoto maziwa kimsingi na kirasmi iko juu ya mama mwenyewe ukilinganisha na wanawake wengine. Kama wanawake wengine pia wataomba ujira au tuzo hiyo hiyo au mama akiwa tayari kunyonyesha bila malipo, basi baba huyo hana haki ya kumtenganisha mtoto huyo na mama yake na kumtoa kwa mwanamke mwingine. Kwa sababu maumbile yameweka upatanifu kati yao wote, na hata pale ambapo mtoto anapotimiza miezi tisa, bado hali huwa ni hiyo hiyo, hivyo hapawezi kuwepo na chakula kinachofaa zaidi kwa mtoto kuliko hiki.

2.

Mtu anapaswa kuchagua mwanamke wa kumnyonyesha mtoto wake ambaye lazima awe ni mwislamu, muumin, mwenye akili timamu na mwenye sifa na tabia njema, kwani katika maziwa zile athari za maisha zinakuja kujitokeza kwa hali yoyote ile, hivyo kumwachia jukumu hili mwanamke kafiri, mpumbavu, mwenye tabia mbaya na ovu haifai kabisa na inachukiza, ni makruhu.

3.

Inafaa kwamba mtoto anyonyeshwe kwa miezi ishirini na moja (21) na asitengwe na mama huyo kabla ya hapo, kama vile ambavyo kumnyonyesha mtoto baada ya miaka miwili hakufai, lakini hakukatazwi.

76


Mwanamke Na Sharia

4.

Ni bora kutowaacha huru wale wanawake wanaonyonyesha kiasi cha kwamba wanaweza kumnyonyesha yeyote wanayetaka kumnyonyesha, kwani kutapelekea watoto wanaonyonya kutokujua uhusiano wao, na hivyo baadaye kuhusika katika dhambi kubwa ya kuwachukulia mama wa kunyonyesha au dada wa kunyonya kama wake zao.

5.

Kama kwa kumnyonyesha mtoto wa mtu mwingine haki za mume zinaathirika,basi mwanamke haruhusiwi hata kidogo kwa kazi hii nzuri (yenye malipo ya thawabu).

6.

Kuna njia mbili za kuthibitisha unyonyaji: a.

Kama kupitia mtu mmoja au wengi, imani na uaminifu vinapatikana.

b.

Watu wawili waadilifu wapaswe kusimama kama mashahidi kwamba wamewahi kumuona mtoto huyo akinyonya, lakini hili haliwezi kuthibitishwa kwa ushahidi wa mwanaume mmoja au wanawake wawili au wanawake wanne.

77


Mwanamke Na Sharia

TARATIBU ZA TALAKA 1.

Kama mwanamke yuko kwenye hedhi au nifas basi talaka yake haiwezi kuwa sahihi, lakini kama hakuna kuingiliana kulikofanyika, au kama mimba yake iko dhahiri, au mume wake yuko sehemu ya mbali kiasi kwamba kutoka pale alipo hali ya mwanamke haiwezi kufahamika na mwezi umepita tangu alipotengana na mumewe, basi chini ya hali yoyote ile talaka inaweza kutolewa.

2.

Kama hedhi na nifas, mwanamke hawezi kutalikiwa katika wakati wa kuanza kuwa kwake katika hali ya tohara, wakati ambapo mume amekwisha kujamiiana naye, inaelekea kuwa muhimu kwamba kwa ajili ya talaka kipindi hiki cha tohara kinapaswa kipite, na baada ya hili ije kupita hedhi, baada ya hiyo anaweza akapewa talaka, ili kwamba katika wakati huo mume anapata fursa ya kufikiri tena na tena juu ya uamuzi wake, huenda Mwenyezi Mungu akamtengenezea njia mpya kwa ajilli ya masikilizano.

3.

Hakuna haja ya kumtaliki mwanamke ambaye umefanya naye ndoa ya muda maalum, katika ile siku (iliyopangwa) kipindi cha mkataba kinapokwisha, moja kwa moja uhusiano wake umekwisha, na kama akitaka kukatisha kabla ya siku hiyo basi samehe kipindi kilichobakia kwa mwanamke na uhusiano wenyewe utakuwa umefikia mwisho.

4.

Kama mwanamke ana umri chini ya miaka tisa au zaidi ya miaka sitini au hapakuwa na kuingilia, basi hakuna haja ya eda 78


Mwanamke Na Sharia

baada ya talaka yake, na anaweza kuolewa tena mara tu baada ya talaka. Lakini kama bila kuingiliana uchi wake umenyonya manii ya mwanaume basi kwa kigezo hiki anapaswa kukaa eda. 5.

Kama hakuna mimba iliyopo, basi kipindi cha eda kinakuwa cha hali tatu (tofauti) za tohara, kama siku moja baada ya talaka damu ikianza, basi siku hii moja itahesabiwa katika hali ya tohara ya kwanza, baada ya hapo kama hedhi ikibakia kwa siku tatu, na baada ya kupita siku kumi za tohara (ambayo itakuwa ni ya pili) akaiona hedhi tena kwa siku tatu, na baada ya kupita siku kumi za tohara (ambayo itakuwa ni ya tatu) kama hedhi itaonekana, kipindi cha eda kitakuwa kimekamilika ndani ya siku 27, hivyo jumla ya siku za na kipindi cha hali tatu za tohara itakuwa ni takriban siku 26 – 27.

Lakini kama mwanamke ni mjamzito, basi anapaswa kubakia ndani ya eda mpaka atakapozaliwa mtoto na hawezi kuolewa ndoa ya pili. Kama mwanamke yeyote hapati siku zake za hedhi wakati kikawaida wanawake wengine wa umri huo wanaiona hedhi, basi anapaswa kupitisha miezi mitatu ya eda. 6.

Baada ya kumaliza Mut’a yake mke wa muda anapaswa kungoja apate kuona hedhi mbili kamili kama kujamiiana kulifanyika, na kama mfululizo wa hedhi haupatikani hapo basi anapaswa kungojea kwa siku arobaini na tano. Na kama akiwa na mimba, basi yeye pia anapaswa kungoja mpaka atakapozaliwa mtoto, kwani mtoto wa Mut’a ni mtoto hasa, heshima yake haipaswi kupuuzwa.

7.

Eda ya talaka inaanza mara tu baada ya talaka, lakini kama mwanamke anakuja kujua juu ya talaka baada ya kupita kwa 79


Mwanamke Na Sharia

eda, hivyo anaweza akaolewa ndoa ya pili siku hiyo hiyo (aliyotambulia). 8.

Mwanamke ambaye mume wake amefariki anapaswa kukaa eda ya miezi minne na siku kumi, awe ama amebalehe au hapana, chini ya umri wa miaka sitini au zaidi, ndoa ya kudumu au ya (muda maalum) Mut’a, wameingiliana au hapana, na katika kipindi hiki hana ruhusa ya kujipamba kwani ile huzuni ya mume wake imeagizwa pia katika wajibu wake. Lakini kwa huzuni hii haina maana ya kutelekeza shughuli zake binafsi na mapendekezo na maagizo ya kidini. Na kuhusu mahitaji anaweza kutoka nje ya nyumba pia, na anaweza kujiunga na swala za jamaa pia na kadhalika.

9.

Talaka ya mwanamke iko ya namna mbili: Talaka isiyo na Rejea. Na Talaka Rejea:

Talaka isiyo na Rejea: Hii ni aina ya talaka ambamo wakati wa eda pia hakuna haki ya kumrudia mwanamke pale ambapo ndoa ya pili haijafanyika, nayo ni talaka ya mwanamke ambaye hajabalehe, au mwanamke ambaye mzunguko wake wa hedhi umekoma, au talaka ya bila kuingiliana, kwani katika zote hizo hakuna eda. Pia ni talaka baada ya mke kurudi kwa mumewe mara mbili, yaani ile talaka ya tatu, kwa vile sasa ni muhimu hapa kumwoza mwanamke huyo kwa mume wa pili. Pia ni ile talaka ya mwanamke mwenyewe kujivua, na ile talaka ambayo wote wamechukiana, na ile ambayo kwa kutokutoa mahitaji kwa mwanamke talaka ikawa imetolewa na Kadhi, hapa eda haipo bali hakuna haki ya kurudi kwa mumewe bali anapaswa kuolewa tena. Ukiachilia mbali hali zote hizi, talaka zilizobakia zinarejelewa tena na ni Talaka Rejea, kwani mume anayo haki ya kumrudia mkewe bila ya ndoa wakati wa eda, na hakuna kizuizi cha kidini 80


Mwanamke Na Sharia

kinachomfanya mwanamke achukuliwe kuwa si mke wakati wa kipindi hiki, bali huendelea kuwa chini ya utaratibu wa mke wa mtu, kwa vile kuna uwezekano wa kuimarisha hali hii ya uke wa mtu iliyotingishika. 10. Wajibu wa chakula na makazi wakati wa eda ya Talaka Rejea (kipindi cha rejea) utakuwa juu ya mume, na mwanamke haruhusiwi kutoka nje ya nyumba kama hajaruhusiwa na mumewe, na mume hana haki ya kumtoa hadi atakapokuwa mwanamke huyo ametenda dhambi au kosa kubwa mno, kwani kukaa hivi pamoja kuna uwezekano wa mume kubadili mawazo, na hili ndilo lengo pekee la sheria hii tukufu ya kidini. 11. Kwa kumrejea (Rujuu) hakuna neno maalum linalohitajika wala mashahidi waadilifu hawana lazima kuwepo na wala sio lazima mwanamke kujulishwa, lakini katika nafsi yake yenyewe hili linasemwa kwamba mimi nimekurejea, hiyo inatosha. Lakini ni lazima lithibitishwe mbele ya mwanamke mwenyewe, na njia bora ya rejea ni kupinga au kukatisha tamaa jambo kama hilo ambalo haliruhusiwi kwa mtu yoyote isipokuwa mume mwenyewe. 12. Kama mtu yoyote ametoa Talaka Rejea kwa mke wake na akamrudia baada ya talaka hiyo, au baada ya eda akamuoa tena na baada ya muda kidogo akawa amemtaliki tena kisha akamrejea tena au baada ya eda akamuoa tena kwa mara ya pili, basi baada ya kumtaliki tena mara ya tatu hawezi akamrejea tena kabla mwanamke huyo hajaolewa na mtu mwingine, hivyo ili kumuoa tena ni lazima kwanza awe ameolewa kwa ndoa ya kudumu na kuingiliana na mume huyo kumefanyika na kisha mume huyo amemtaliki au amefariki na eda yake pia imekamilika. 81


Mwanamke Na Sharia

TALAQ AL-KHUL’A

I

fahamike wazi kwamba haki ya kutoa talaka iko mikononi mwa mume tu, haihusiki chochote na mwanamke, kama vile tu kuchukua uamuzi wa kuikubali ndoa kulivyokuwa ni haki ya mwanamke tu, na mwanaume hakuwa na haki ya namna yoyote ya ulazimishaji wa jambo hilo. Mwenyezi Mungu ameweka jukumu la kuunganisha mahusiano juu ya mwanamke kwani katika hili hisia za upendo zinahitajika zaidi, na akaacha jukumu la kuvunja uhusiano kwa mwanaume kwani katika hili subira za hali ya juu na uvumilivu vinahitajika zaidi kuliko hisia za upendo, na sifa muhimu hii inajionyesha zaidi katika maisha ya mwanaume kuliko yale ya mwanamke. Maana ya Talaq al-Khul’a ni ile ambayo madai ya talaka yanatoka upande wa mwanamke naye anaonyesha kuchukia kwake, chini ya hali kama hii kama mume atakubali kumtaliki kwa mahari kusamehewa basi inatosha kwa maelezo haya, lakini kama madai ni zaidi ya haya, basi hayo pia yanapasa kutolewa, na hakuna uwezekano wa talaka bila ya ridhaa ya mume. Ni jambo tofauti kwamba kama maonevu ya mume yatathibitishwa, kwamba hatoi hata mahitaji ya riziki na hatoi talaka pia, basi Kadhi anaweza yeye akatoa talaka hiyo, kwani mume anaweza kuwa mmiliki wa haki kabisa kuliko mwingine yeyote lakini hawezi kuwa juu ya mmiliki wa Sheria Tukufu, na jukumu hili linaweza kutekelezwa tu na Kadhi kwa kumwakilisha mume huyo.

82


Mwanamke Na Sharia

TALAQ AL-MUBARAAT

K

atika talaka hii, chuki inakuwa iko kwenye pande zote na hakuna anayemtaka mwenzie, licha ya hili mwanamke anatoa mali kiasi na kuomba talaka na mwanaume anachukua kiasi cha mali na kumwacha huru mwanamke huyo kama vile tu alivyofanya kwa kutoa mali nyingi katika harakati za sherehe za harusi, wakati ambapo jambo hilo lilianza kwa maandamano ya shangwe, linaishia na utengano wa amani wenye huzuni. Mwenyezi Mungu atunusuru.

MAS’ALA MBALIMBALI YA TALAKA 1.

Kama mtu atajamiiana na mwanamke mwingine bila ya kujua akidhania kwamba ni mke wake, mwanamke huyo anapaswa kukaa eda baada ya talaka kwa hali yoyote ile, hata kama alikuwa akitambua tayari kwamba hakuwa ni mume wake, lakini kama wote walijua na wakafanya zinaa basi hakuna eda katika suala la zinaa. Kwa hili adhabu ya Jahannam na viboko inatosha. Lakini kama uzinzi ni kutoka upande wa mwanaume na kwamba yule mwanamke alikuwa akimfikiria yeye kuwa ni mumewe basi anapaswa kukaa eda hiyo (kama tahadhari).

2.

Kama mtu amemchochea mwanamke aliyeolewa na akamuandaa kuchukua talaka, na akaichukua talaka na baadaye yeye akamuoa vilevile, kwa hiyo talaka hiyo na ndoa yao hiyo vitakuwa ni sahihi, bali adhabu ya uhaini huu italazimu kubebwa na mwanaume huyu kwa hali yoyote ile. 83


Mwanamke Na Sharia

3.

Kama mwanamke akiweka sharti wakati ule wa ndoa kwamba atakuwa na haki ya kutoa talaka, sharti hilo ni batili kwa vile haki ya talaka haiwezi kuhamishwa, bali kama akishikilia sharti hili kwamba atakuwa mtetezi kwenye talaka na kwa matakwa yake, chini ya masharti maalum atakuwa wakili kwa ajili ya maandishi ya talaka yatakavyosomeka, hivyo katika uwakili kama huo hakuna madhara kwa sababu katika talaka utetezi unakubalika, uwe wa mke au mtu mwinginewe.

4.

Kama mume wa mwanamke ametoweka na hakuna dalili ya yeye kuweza kupatikana, basi mwanamke apeleke suala lake kwa mwanachuoni mwaminifu (mujtahid) na kisha afanye kulingana na hukmu zilizowekwa naye huyo, asije akajaribu kujiua mwenyewe kwa huzuni juu ya mumewe wala asije akachukua hatua potovu katika masuala ya kijinsia.

5.

Kama mwanaume atapatwa na wendawazimu, basi maelezo ya talaka yanaweza yakasomwa kwa niaba yake na baba yake au babu yake.

6.

Kama baba au babu wa kijana wa umri mdogo ambaye hajabalehe amesoma khutba ya Mut’a na mwanamke fulani, basi na wao wana uhuru vilevile wa kusamehe kile kipindi kilichopangwa kwa ajili ya Mut’a, lakini kama imefungwa ndoa ya kudumu basi haki ya talaka itakuwa juu ya mume peke yake tu.

7.

Kama mwanaume yoyote amewafikiria watu wawili kuwa ni waadilifu na akasoma hati ya talaka mbele yao, basi mtu wa tatu anayo haki ya kumuoa mke huyo, hata kama mashahidi hao hawakuwa waadilifu machoni mwake yeye, lakini kwa kuhu84


Mwanamke Na Sharia

su mume hili ni bora zaidi kwamba wakati ambapo uadilifu wao haujathibitishwa asiwafanye watu hao kuwa mashahidi na asitekeleze uandishi wa talaka mbele yao. 8.

Kama mtu yeyote amemtaliki mwanamke na hakumjulisha hilo, na hata akampatia mahitaji ya muhimu kwa muda unaotakiwa, na akamjulisha baada ya muda wa eda ulipokuwa umekwisha, basi hana haki ya kurudishiwa yale matumizi aliyotumia katika kipindi cha eda, bali kama kutakuwa na kitu kinachobaki baada ya eda basi anaweza kukichukua, kwani baada ya eda wajibu wa matumizi hauwi juu ya mume tena, na kuhusu talaka, kumjulisha au kumridhisha mwanamke katika siku ile ya kwanza sio wajibu wake mume huyo.

Hii ni kanuni ya wazi ya Uislam kwamba haki kamili ya talaka imo mikononi mwa mume tu, hivyo kama mwanamke yeyote anakuwa hakuridhishwa na kanuni hii ya Kiislam, basi hakuna haja ya yeye kufunga ndoa ya kudumu, siku hiyo hiyo ya kwanza anapaswa kuingia kwenye ndoa ya muda maalum ili kupunguza matatizo au kuweka utetezi wa talaka mikononi mwake ili kwamba wakati itakapohitajika anaweza kuutumia, au vinginevyo aweze kujidhibiti mwenyewe na ajiweke mbali na huru na mahusiano ya namna hiyo ambamo namna yoyote ya majukumu ya ziada ichukuliwe kwa sharti kwamba anaweza kusalimisha heshima na utu wake, vinginevyo bila ya hili hakuna thamani ya binadamu katika ubinadamu.

85


Mwanamke Na Sharia

MIRATHI

N

i rehema ya Mola wa Ulimwengu kwamba hata baada ya kifo cha mtu, Yeye hakukata uhusiano kutokana na mali yake, na ameigawanya mali yake ndani ya ndugu zake mwenyewe, ugawaji ambao maelezo yake mafupi ni kama yafuatavyo: Kundi la kwanza linajumuisha mama mzazi, baba na binti na mtoto wa kiume na kadhalika, kwani wakati wa uhai wao hakuna anayeweza kuwa mrithi, uhusiano wao na marehemu ni wa moja kwa moja na usiokatizika. Kundi la pili linawahusu ndugu wa kiume, makaka, madada, mabibi na mababu wa kiumeni na kikeni na kadhalika, kwani wanahusiana kupitia wazazi wao, watoto wao na wanaitwa makaka na madada na wazazi wao wanaitwa mababu na mabibi. Kundi la tatu linajumuisha wajomba na akina ami, mashangazi na mama wadogo na wakubwa, kwani wanahusiana kupitia mababu wa kiumeni na kikeni, watoto wa babu wa kiumeni wanaitwa ami na shangazi na watoto wa babu wa kikeni wanaitwa wajomba na mama wadogo au wakubwa. Mume na mke hawana uhusiano wa undugu wa kinasaba, hivyo mfumo wao wa mirathi unatofautiana, na wao pamoja na warithi wao wote watakuwa wamiliki halali wa haki zao wenyewe na hakuna atakayeweza kuwazuia kwenye haki zao. 1.

Kama marehemu ameacha watoto wa kiume na wakike pamoja, basi kila mtoto wa kiume atapata fungu la mali sawa na la mabinti wawili kwa vile majukumu ya wajibu ya watoto wa kiume ni mengi, wao wana matumizi yao binafsi na mahitaji ya wake 86


Mwanamke Na Sharia

zao na watoto pia ni katika wajibu wao, lakini hakuna ambaye mahitaji ya binti yamo mikononi mwake, kwani mahitaji yake yapo ama kwa baba yake au kwa mume wake. 2.

Endapo miongoni mwa warithi ni wazazi tu waliopo, basi fungu la mama limekadiriwa kama ni theluthi moja, na fungu jingine lote lililobakia litatolewa kwa baba kwa vile hakuna mrithi mwingine aliyebakia.

3.

Kama miongoni mwa warithi wa marehemu ni binti na wazazi wa marehemu basi mali hiyo itagawanywa mafungu matano yanayolingana, wazazi watapewa moja moja kila mmoja na yale mafungu matatu yaliyobakia yatatolewa kwa huyo binti, kwa sharti la wakati mama hana msimamizi mkuu. (Lakushangaza ajabu Uislam unachukulia haki ya binti kwa heshima zaidi kuliko ya wazazi, na kuna Waislam ambao wamemnyima kabisa haki yake binti ya Mtukufu Mtume (saww) ya kurithi).

4.

Kama kuna kaka na dada miongoni mwa warithi wa marehemu, basi mafungu mawili yatakuwa ni ya kaka na moja litakuwa ni la dada, kwa vile majukumu ya kaka ni mengi kwa hakika kuliko ya dada.

5.

Wakati ndugu wa marehemu wakiwa ni wote wa kiumeni na kikeni, basi fungu la mwanaume litakuwa mara mbili ya fungu la mwanamke, lakini kama ni ndugu wa kikeni tu waliopo basi wote wanaume na wanawake watapata mafungu yanayolingana.

87


Mwanamke Na Sharia

MIRATHI KUTOKA KWA MKE ­ALIYEOLEWA 1.

Kama mume hana watoto wowote basi fungu la mke litakuwa moja ya nne, na kama mume anao watoto hata kama ni kwa mke mwingine, basi vilevile fungu la mke litakuwa ni moja ya nane.

2.

Kama mke hana watoto basi fungu la mume litakuwa nusu ya mali, na kama anaye mtoto wake mwenyewe yoyote yule, basi fungu la mume litakuwa ni moja ya nne (robo) tu ya mali, inayobakia itakwenda kwa watoto wake.

3.

Mke hawezi kupata fungu lolote kutoka kwenye ardhi inayomilikiwa na mume wake, lakini atapewa fungu lake kutokana na miti, bustani, mimea, nyumba na kadhalika, tofauti pekee ni kwamba hatachukuliwa kama mwanahisa katika mali halisi (isiyohamishika) bali kiwango kitakadiriwa cha mali hiyo na kutokana na hicho yeye atapata robo au moja ya nane kulingana na hali halisi na thamani yake itaamuliwa mnamo siku ya ugawaji. Kama baada ya hapo, warithi waliobakia watataka kumpa fungu lake hata kwenye mali isiyohamishika basi ni wajibu wake kukubali na asije akalazimisha kudai kuuzwa kwake au kiasi cha bei yake.

4.

Wakati wa kupanga bei ni lazima ikumbukwe kwamba fungu la mwanamke liko kwenye bustani na sio kwenye ardhi yenyewe, na humo kwenye bustani pia, kama ilivyo sharti, na sio kati88


Mwanamke Na Sharia

ka ile miti inayokatwa na kuangushwa, hivyo bei ya shamba, bustani, au nyumba itapangwa kwa namna ambayo ardhi haiingizwi katika bei hii wala kutengwa moja kwa moja kabisa, kwa mfano, kama bustani hii imo kwenye ardhi hii na kodi ya ardhi hiyo (iliyotumika) imelipwa, au mwenye kumiliki hiyo ardhi akapewa uhuru kwamba wakati wowote atakapopenda anaweza kukata mimea na kuondoka kwenye ardhi hiyo, basi katika hali kama hii bei yoyote itakayokuwa kutokana na ardhi hiyo, robo au moja ya nane yake itatolewa kwa mke. Kwa nyumba itakuwa vivyo hivyo pia, kama vyombo vyote vya nyumba bila ardhi yenyewe bali sio kwa kuitenga moja kwa moja na hiyo ardhi, kwa kuzingatia mambo yote hayo akilini, bei yoyote itakayokuwa kutokana na hiyo, robo au moja ya nane yake itatolewa kwa mke na bustani au nyumba itagawanywa miongoni mwa warithi wengine. 5.

Kabla haki za mke hazijatolewa au ruhusa yake haijapatikana, umiliki kwa warithi waliobakia wa bustani au nyumba hauruhusiwi.

6.

Kama mtu anao wake wengi basi hiyo moja ya nne (robo) au moja ya nane itagawanywa sawa sawa miongoni mwao, wakiwa ni wale alioingiliana nao au hapana, au wake wa aina nyingine yoyote.

7.

Kama mtu wakati akiwa kwenye maradhi ya umahututi kisha akawa ameoa mwanamke na akafariki akiwa katika maradhi na hali hiyo hiyo, basi ndoa hiyo imetanguka na kuwa batili na haki ya mwanamke haitakuwepo imma kwenye mahari wala kwenye mirathi, lakini kama alikuwa kwenye maradhi makali na akafariki basi kwa hakika mumewe atamrithi. 89


Mwanamke Na Sharia

8.

Kama mwanamke alikuwa kwenye eda ya talaka rejea (kipindi anachoweza kurejewa baada ya talaka), na mmoja wao akafariki, basi yule aliye hai miongoni mwao kwa hakika atarithi kwani eda hii ni aina ya uke wa mtu pia.

9.

Kama mtu yeyote amemtaliki mwanamke akiwa katika hali ya maradhi makali na akafariki ndani ya mwaka mmoja kwa maradhi yao hayo, na mwanamke pia alikuwa hakudai talaka, na hakufanya ndoa nyingine yoyote ya pili ndani ya mwaka huo hadi kifo cha mume wake, basi na yeye pia atachukuliwa kama mrithi.

10. Vifaa ambavyo mume amemzawadia mke wake vinakuwa ni mali yake mke huyo, haina uhusiano na warithi wengine, lakini vile vifaa vilivyomo ndani ya nyumba ambavyo vilikuwa ni kwa ajili ya matumizi yake, hivyo vitachukuliwa kama vilivyoachwa (tarka) baada ya kifo cha mume na wadai wake watakuwa ni warithi wake wote, na mke peke yake hatakuwa ndiye mrithi wa vifaa hivyo.

90


Mwanamke Na Sharia

ORODHA YA VITABU VILIVYO ­CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1.

Qur’an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thelathini

2.

Uharamisho wa Riba

3.

Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza

4.

Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili

5.

Hekaya za Bahlul

6.

Muhanga wa Imamu Husein (A.S.)

7.

Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.)

8.

Hijab vazi Bora

9.

Ukweli wa Shia Ithnaashari

10. Madhambi Makuu 11. Mbingu imenikirimu 12. Abdallah Ibn Saba 13. Khadijatul Kubra 14. Utumwa 15. Umakini katika Swala 91


Mwanamke Na Sharia

16. Misingi ya Maarifa 17. Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia 18. Bilal wa Afrika 19. Abudharr 20. Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu 21. Salman Farsi 22. Ammar Yasir 23. Qur’an na Hadithi 24. Elimu ya Nafsi 25. Yajue Madhehebu ya Shia 26. Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur’an Tukufu 27. Al-Wahda 28. Ponyo kutoka katika Qur’an 29. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii 30. Mashukio ya Akhera 31. Al Amali 32. Dua Indal Ahlul Bayt 33. Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. 34. Haki za wanawake katika Uislamu 35. Mwenyezi Mungu na sifa zake 36. Kumswalia Mtume (s) 92


Mwanamke Na Sharia

37. Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) 38. Adhana 39 Upendo katika Ukristo na Uislamu 40. Tiba ya Maradhi ya Kimaadili 41. Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu 42. Kupaka juu ya khofu 43. Kukusanya swala mbili 44. Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara 45. Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya 46. Kusujudu juu ya udongo 47. Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) 48. Tarawehe 49. Malumbano baina ya Sunni na Shia 50. Kupunguza Swala safarini 51. Kufungua safarini 52. Umaasumu wa Manabii 53. Qur’an inatoa changamoto 54. as-Salaatu Khayrun Mina -’n Nawm 55. Uadilifu wa Masahaba 56. Dua e Kumayl 57. Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu 93


Mwanamke Na Sharia

58. Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake 59. Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata 60. Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mtume Muhammad (s) 61. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza 62. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili 63. Kuzuru Makaburi 64. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza 65. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili 66. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu 67. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne 68. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano 69. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita 70. Tujifunze Misingi Ya Dini 71. Sala ni Nguzo ya Dini 72. Mikesha Ya Peshawar 73. Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu 74. Ubora wa Imam ‘Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliyonyooka 75. Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake 76. Liqaa-u-llaah 77. Muhammad (s) Mtume wa Allah 94


Mwanamke Na Sharia

78. Amani na Jihadi Katika Uislamu 79. Uislamu Ulienea Vipi? 80. Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) 81. Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) 82. Urejeo (al-Raja’a ) 83. Mazingira 84. Utokezo (al - Badau) 85. Hukumu ya kujenga juu ya makaburi 86. Swala ya maiti na kumlilia maiti 87. Uislamu na Uwingi wa Dini 88. Mtoto mwema 89. Adabu za Sokoni 90. Johari za hekima kwa vijana 91. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza 92. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili 93. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu 94. Tawasali 95. Imam Mahdi katika Usunni na Ushia 96. Hukumu za Mgonjwa 97. Sadaka yenye kuendelea 98. Msahafu wa Imam Ali 95


Mwanamke Na Sharia

99. Ngano ya kwamba Qur’ani imebadilishwa 100. Idil Ghadiri 101. Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu 102 Hukumu zinazomuhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi 103. Huduma ya Afya katika Uislamu 104. Sunan an-Nabii 105. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) 106. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) 107. Shahiid Mfiadini 108. Kumsalia Nabii (s.a.w) 109. Ujumbe -Sehemu ya Kwanza 110. Ujumbe - Sehemu ya Pili 111. Ujumbe - Sehemu ya Tatu 112. Ujumbe - Sehemu ya Nne 113. Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu 114. Hadithi ya Thaqalain 115. Ndoa ya Mutaa 116. Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza 117. Ukweli uliopotea sehemu ya Pili 118. Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu 119. Ukweli uliopotea sehemu ya Nne 96


Mwanamke Na Sharia

120. Ukweli uliopotea sehemu ya Tano 121. Mkutano wa Maulamaa wa Baghdad 122. Safari ya kuifuata Nuru 123. Fatima al-Zahra 124. Myahudi wa Kimataifa 125. Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi 126. Visa vya kweli sehemu ya Kwanza 127. Visa vya kweli sehemu ya Pili 128. Elimu ya Ghaibu ya Maimamu 129. Mwanadamu na Mustakabali wake 130. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) 131. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) 132. Khairul Bariyyah 133. Uislamu na mafunzo ya kimalezi 134. Vijana ni Hazina ya Uislamu 135. Yafaayo kijamii 136. Tabaruku 137. Taqiyya 138. Vikao vya furaha 139. Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 97


Mwanamke Na Sharia

140. Visa vya wachamungu 141. Falsafa ya Dini 142. Azadari-Kuhuzunika na Kuomboleza 143. Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah 144. Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu 145. Kuonekana kwa Allah 146. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) 147. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) 148. Ndugu na Jirani 149. Ushia ndani ya Usunni 150. Maswali na Majibu 151. Mafunzo ya hukmu za ibada 152. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1 153 Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2 154. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 155. Abu Huraira 156. Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. 157. Mazingatio kutoka katika Qur’an - Sehemu ya Kwanza 158. Mazingatio kutoka kaitka Qur’an - Sehemu ya Pili 159. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza

98


Mwanamke Na Sharia

160. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili 161. Qur’ani Tukufu – Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili 162. Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) 163. Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani 164. Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu 165. Uislamu Safi 166. Majlisi za Imam Husein Majumbani 167. Je, Kufunga Mikono 168. Uislam wa Shia 169. Amali za Makka 170. Amali za Madina 171. Asili ya Madhehebu katika Uislamu 172. Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi 173. Ukweli uliofichika katika neno la Allah 174. Uislamu na Mifumo ya Uchumi 175. Umoja wa Kiislamu na Furaha 176. Mas’ala ya Kifiqhi 177. Jifunze kusoma Qur’ani 178. As-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah 179. Hayya ‘Alaa Khayri’l-’Amal Katika Adhana 180. Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura 99


Mwanamke Na Sharia

181. Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na Ramadhani) 182. Uadilifu katika Uislamu 183. Mahdi katika Sunna 184. Maswali Ya Uchunguzi Kuhusu Uislam 185. Kazi na Bidii ni njia ya maendeleo 186. Abu Talib – Jabali Imara la Imani 187. Ujenzi na Utakaso wa Nafsi 188. Vijana na Matarajio ya Baadaye 189. Usalafi – Historia yake, maana yake na lengo lake 190. Ushia – Hoja na Majibu 191. Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) 192. Maombolezo – Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) 193. Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu 194. Takwa 195. Upotoshaji dhahiri katika Turathi (Hazina) ya Kiislamu 196. Amirul Muuminina (‘as) na Makhalifa 197. Uongozi na Utawala katika Mwenendo wa Imam ‘Ali (‘a) 198. Kuvunja hoja iliyotumika kutetea Uimamu wa AbuBakr 199. Adabu za vikao na mazungumzo 200. Hija ya Kuaga 100


Mwanamke Na Sharia

201. Uwazi baina ya Maslahi na Vikwazo 202. Fadhila za watukufu watano katika Sahih Sita 203. Mdahalo baina ya Mwanachuoni wa Kisunni na Mwanachuoni wa Kishia (Al-Muraja’aat) 204. Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (as) 205. Mjadala wa Kiitikadi 206. Mtazamo kuhusu msuguano wa Kimadhehebu 207. Nchi na Uraia – Haki na wajibu kwa Taifa 208. Mtazamo wa Ibn Taymiyyah juu ya Imam Ali (as) 209. Uongozi wa Kidini – Maelekezo na Utekelezaji wa Kijamii 210. Maadili ya Ashura 211. Mshumaa – Shahidi na Kifo cha Kishahidi 212. Mizani ya Hekima – Hadithi za Ahlul Bait (as) – Sehemu ya Kwanza 213. Imam Ali na Mambo ya Umma 214. Imam Ali na Mfumo wa Usawa 215. Mwanamke na Sharia 216. Mfumo wa Wilaya 217. Vipi Tutaishinda Hofu? 218. Kumswalia Mtume ni Ufunguo wa Utatuzi wa Matatizo 219. Maeneo ya Umma na Mali Zake 101


Mwanamke Na Sharia

220. Nahjul-Balagha – Majmua ya Khutba, Amri, Barua, Risala, Mawaidha na Semi za Amirul-Muuminin Ali bin Abu Talib (a.s.) 221. Mukhtar – Shujaa aliyelipiza kisasi dhidi ya wauaji wa Imam Husein (as) hapo Karbala 222. Uimamu na Tamko la Kutawazwa 223. Imam Husain ni Mfumo wa Marekebisho na Mageuzi

102


Mwanamke Na Sharia

KOPI NNE ZIFUATAZO ­ZIMETAFSIRIWA KWA LUGHA KINYARWANDA 1.

Amateka Na Aba’Khalifa

2.

Nyuma yaho naje kuyoboka

3.

Amavu n’amavuko by’ubushiya

4.

Shiya na Hadithi

103


Mwanamke Na Sharia

ORODHA YA VITABU VILIVYO ­CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION KWA LUGHA YA KIFARANSA 1.

Livre Islamique

104


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.