Ndugu na jirani

Page 1

NDUGU NA JIRANI Kimeandikwa na:

Jumuiya ya Maarifa na Utamaduni wa Kiislamu

Kimetarjumiwa na:

Amiri Mussa Kea


B


Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 - 512 - 52 - 2 Kimeandikwa na:

Jumuiya ya Maarifa na Utamaduni wa Kiislamu Kimetarjumiwa na:

Amiri Mussa Kea Kimehaririwa na: Shaikh Haroon Pingili Kupangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation Toleo la kwanza: Novemba, 2013 Nakala:1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: w.w.w.alitrah.info


YALIYOMO Adabu za wanandugu..................................................................................2 Ibada za muunganisho.................................................................................4 Nchi za Magharibi na uvunja udugu...........................................................5 Mahusiano ya Kijamii katika jamii ya Kiislamu.........................................6 Sababu za uvunja udugu..............................................................................7 Baina ya Taasubi na Uungaji Udugu.........................................................11 Uungaji udugu kwa mujibu wa Qur’ani Tukufu........................................13 Uungaji udugu kwa mujibu wa Hadithi...................................................15 Kudumisha udugu na wazazi wawili.........................................................18 Kuwatendea wema wazazi wawili ............................................................20 Baadhi ya yale yaliyoelezwa na Hadithi kuhusu kuwatendea wema wazazi wawili........................................................................................................23 Ndugu ni Nani...........................................................................................26 Vipi tuunge Udugu....................................................................................28 Kuukimbia Uungaji udugu .......................................................................28 Adabu za majirani......................................................................................29 Haki za Jirani.............................................................................................32 Matokeo ya ujirani mwema.......................................................................38


Neno la Mchapishaji Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kiitwacho: al-Arhaam wa ‘l-Jiiraan. Sisi tumekiita: Ndugu na Jirani. Uislamu ni dini na ni mfumo wa maisha. Ni dini ambayo huzingatia maisha ya ulimwengu huu na ulimwengu ujao - Akhera. Hivyo, mfumo wake umesheheni mafundisho ya kiroho na ya kimwili. Mafundisho ya kimwili ni mafundisho ya maisha; jinsi mtu anavyotakiwa kuendesha maisha yake hapa duniani, ambayo ni pamoja na uhusiano mwema na wanadamu wenzake, wakiwemo ndugu na jirani zake. Na katika nukta hii, mafundisho ya Kiislamu hayakurudi nyuma kuhusiana nayo. Qur’ani ambayo ndiyo kiini na chimbuko la mafundisho na sheria zote za Uislamu, imejaa aya zinazozungumzia nukta hii ikifuatiwa na Sunna, ambayo ni mafundisho ya Mtukufu Mtume (saw). “Na mwabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote; na wafanyieni wema wazazi wawili na jamaa wa karibu, na mayatima na maskini na jirani wa karibu…” (Sura 4:36). Mtukufu Mtume anasema: “Nimetumwa ili nikamilishe mwenendo mwema.” Huo hapo juu ni mfano mdogo tu kutoka katika Qur’ani Tukufu na Hadithi (Sunna). Uislamu ni dini ya amani na inapenda kila mtu aishi kwa amani na uhuru wa kweli.

E


Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili za watu. Tunamshukuru ndugu yetu, Amiri Mussa Kea kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation

F


UTANGULIZI Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu Sifa zote njema anastahili Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa viumbe, na rehema na amani zimfikie mbora wa viumbe baba Qasim Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w.) na Aali zake watoharifu (a.s.). Kwa hakika Uislamu umetilia mkazo sana suala la ndugu na kuunga udugu kwa yale ambayo hayafichiki kwa mchunguzaji, kwa mujibu wa yale yaliyoelezwa na Hadithi mbalimbali zilizopokewa kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) pamoja na watu wa nyumbani kwake (a.s.), bila shaka kwazo kuna ishara ya jinsi suala la uungaji udugu lilivyo na nguvu katika kukuza mfumo wa ukaribu na muungano kati ya watu, katika jamii ya kiislamu yenye nidhamu, upendo, ushirikiano na mwamko. Pia Hadithi hizo huakisi yale yenye kuvunja udugu kutokana na hali halisi ya jamii iliyovurugika na iliyokosa upendo, kwani jamii hiyo hukosa mafungamano na pia watu huwa hawajali isipokuwa maslahi madogo ya kidunia ambayo umuhimu wake wote umesimama juu ya umimi na kutaka cheo, hadi umoja unakuwa ni jambo lisilokubalika, basi tunaona kila mmoja hukumbatia na hupenda dhati yake na huzama katika ubinafsi. Kwa hivyo Uislamu tunaoujua na tunaousoma – Aya na Hadithi – si huo (wa kila mtu kujali maslahi yake binafsi), hivyo tutaangazia namna Uislamu ulivyotilia umuhimu faradhi hii, kwa hivyo mpendwa msomaji mikononi mwako una kitabu hiki kidogo ambacho huangazia baadhi ya mambo ambayo yameelezwa katika Hadithi na Aya mbalimbali ambazo huifanya jamii kuwa kitu kimoja na kuinyanyua familia kwa kiwango cha juu kabisa.


Tunamuomba Mwenyezi Mungu atuwezeshe sisi na nyinyi kutekeleza faradhi na Sunna mbalimbali ili tutengeneze jamii iliyo bora na iliyo kamilika kwayo, hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anavyotaka jamii iwe.

Jumuiya ya Maarifa na Utamaduni wa Kiislamu


I



Ndugu na Jirani

ADABU ZA WANANDUGU Uislamu ni dini ya muungano: Hakika rejea za msingi za dini ya kiislamu ni Qur’ani tukufu na Hadithi takatifu, ambazo huonesha waziwazi uhakika wa kadhia hiyo, nayo ni: Kwa hakika usia mwingi kati ya wasia za kiislamu, wajibu wake na hukmu zake, hulingania katika kuondoa vizuizi vilivyopo baina ya watu kwa ujumla na kati ya mtu na mtu. Hakika Uislamu haujakuja kuvunja ubinadamu, isipokuwa umekuja kwa lengo la kuondoa vizuizi ambavyo kwa njia moja au nyingine humtenganisha mtu na mwingine, au mtu na ndugu yake katika imani, mfano taasubi, aina zake pamoja na majina yake, kama vile kiburi, kujiona, chuki, husda na dhana mbaya… huu ni mlolongo mrefu wa sifa mbaya ambazo Uislamu umekuja kuziondoa na kung’oa mizizi yake. Na huenda ukastaajabu kutokana na maneno ya Mtume (s.a.w.w.) amesema:

“Nimetumwa ili nikamilishe mwenendo mwema” Lakini jamii ambayo haina tabia njema na inayotenganisha wanajamii wake kwa husda, chuki na kiburi, na wala hakuna uaminifu kati ya mtu na ndugu yake, na ambayo haina msingi wa upendo, usafi na ikhlasi, jamii hiyo haiwezi kuendelea na kuwa na mafanikio, kwani jamii ambayo yenye kutengana, yenye husda, na chuki sio jamii ya kiislamu hata kama inaitwa hivyo…

2


Ndugu na Jirani Kwa hivyo Uislamu hulingania jamii yenye kupendana, yenye kuungana na kusaidiana na kuwa ndugu, na yawepo mapatano ya jamii, aidha kusiwepo ndani yake vipingamizi vya kinafsi na vya kijamii kati ya watu wake, na isiwe yenye machafuko ya ndani, na muda huo ndipo inawezekana kuwa jamii yenye uhalisia wa maneno ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.): “Na shikamaneni na kamba ya Mwenyezi Mungu wala msitofautiane” Na kuwa hivi:

“Na tumekufanyeni mataifa na makabila ili mjuane, hakika aliye mbora zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni yule aliye mchamungu zaidi katika nyinyi.” (Hujrat:13). Na kuwa hivi: “Mfano wa waumini katika kupendana kwao na kuhurumiana kwao ni kama mwili mmoja, kiungo kimoja kikipatwa na maumivu mwili wote hupatwa na maumivu na hukesha vyote kwa homa.” Na iwapo jamii itaungana kwa ndani na itasalimika kwa undani, hapo itakuwa rahisi kuwashinda maadui, ama ikiwa jamii imesambaratika, jamii hiyo haitakuwa na usalama na amani, na kwa hivyo haitaweza kukabiliana na maadui na kuwashinda. Na historia na hasa hasa Uislamu unatilia kwetu sisi mkazo kuhusiana na uhakika huu, waislamu walirudi nyuma pindi walipotengana, na ikiwa wanataka kurudi katika uongozi wa umma ni juu yao waungane na wapatane. Na muungano lazima uanze katika ngazi ya familia na ukoo, yaani kati ya wanandugu, ili ndani ya nyumba kuwe na amani kisha hapo yatakuja maneno ya umoja na maelewano katika jamii ya kiislamu mahsusi na kwa ubinadamu kwa ujumla. 3


Ndugu na Jirani

IBADA ZA MUUNGANISHO Kwa hakika hata ibada za kiislamu ambazo ni kidhahiri ni za mtu mmoja, huzikuta zinahusiana na jamii, chukua mfano wa Swala; wakati mwislamu anaposwali peke yake, je inamaanisha Swala hiyo ni Swala ya mtu mmoja? Hapana, hakika Swala hata kama ina sura ya kufanywa na mtu mmoja, isipokuwa madhumuni yake ni ya jamii nzima. Chukua mfano mwingine; wakati mwenye kuswali anaposoma Suratul Fat’ha hufikia Aya hizi:

“Mwenye kumiliki siku ya malipo. Wewe tu tunakuabudu, na kwako tu tunataka msaada.” (Sura Al-Fati’ha: 4 – 5). Hapa tunakuta tamko la wengi “tunakuabudu” na “tunataka msaada” na “tuongoze” na sio tamko la mtu mmoja binafsi, mfano wa ‘’ninakuabudu” “ninakuomba msaada” na “niongoze”. Achia mbali kwamba Uislamu umehimiza kusimamisha Swala ya jamaa na katika msikiti, na hili linatoa ishara juu ya umuhimu wa kuchanganyika jamii na iwe yenye maelewano katika Uislamu. Vivyo hivyo ibada ya Hija, kwa hakika sura yake ni sura ya jumuiya, kuanzia pale anapotoka katika mji wake hadi pale atakaporejea, Hija huambatana na makusudio ya kijamii na ishara za muungano. Vivyo hivyo Saumu na Zaka, unaona ndani ya hayo maana za kijamii, kwa hivyo Uislamu ni dini ya kijamii yenye kuleta mapatano, na hulingania upendo, kusaidiana na maelewano. Na miongoni mwa mambo ambayo 4


Ndugu na Jirani yametiliwa mkazo na dini hii tukufu ni suala la kuunganisha udugu, na hili tutalieleza muda mfupi ujao.

NCHI ZA MAGHARIBI NA UVUNJA UDUGU Umekwishatambua na kujua mfumo wa Uislamu katika mahusiano na wengine na kwamba ni wa kijamii, elekeza mtazamo wako katika nchi za Kimagharibi ili uone jinsi Wamagharibi wanavyoishi kuhusiana na upande huu. Urejeaji wa ndani na wa makini katika jamii za Kimagharibi hukuwekea mkazo katika yale yasiyo na shaka, kwamba ni jamii ya kipweke na ubinafsi, haijui ila kujishughulisha na maslahi madogo, na mtu huangalia na hujali hali yake binafsi, na haulizwi kuhusu wengine, na kwa hivyo thamani na maslahi yote humhusu yeye tu binafsi, hawatumikii wala kutoa huduma za kibinadamu kwa wengine, kwa namna yoyote ile, iwe mbali au karibu, na wakati mwingine hata kama akiwa ni mwanawe, sio ajabu kuona kuwa humzingatia ni kati ya vitendea kazi na miongoni mwa vitega uchumi, haingii kwa maana ya binadamu, au ana ubinadamu na kwamba yeye ana hatma inayofaa. Na jambo la kuumiza ni kwamba dhamira za watu wa Magharibi zimetuhujumu, na imekuwa ndiyo mwelekeo wa waislamu na msingi wao, mielekeo potofu ya Kimagharibi ndiyo kioo cha waislamu, na hayo huhujumu utamaduni na huleta mabadiliko na mageuzi makubwa. Kwa hivyo yampasa kila mwislamu katika mapambano haya kuidhibiti dhati yake na kuzuia upotovu huu wa kitamaduni na kushikamana na misingi asilia ya Uislamu. Utakapotaka kujua uhakika wa jamii za Kimagharibi wawajibika kurejea magazeti mbalimbali na majarida tofauti tofauti ambayo huzungumzia suala la kutengana jamii zao, na hasa hasa kusambaratika kwa familia zao. 5


Ndugu na Jirani Umefanywa utafiti na sensa ya wahalifu 7598 huko Marekani waliopelekwa katika taasisi za marekebisho mwaka 1910, imedhihiri asilimia 50.7 walitokana na familia zenye migongano, na ni asilimia 50.5 ya wale waliopelekwa katika shule za marekebisho za Uingereza, na Scottland walikuja kutoka katika nyumba zenye migogoro na migongano. Na umefanywa utafiti Ufaransa mwaka 1942 katika mji wa Paris kuhusu matukio ya vijana wenye umri wa kubalehe waliopotoka, basi ikabainika kwamba asilimia 88 miongoni mwao walitoka katika familia zenye mizozo.1 Hakika jamii za Kimagharibi ziko hatarini kuanguka na sababu yake ni kuenea hali ya ubinafsi katika jamii hizo. Kutokana na maoni ya baadhi ya watafiti wa mambo ya kijamii ni kwamba jamii ya Kimarekani kwa dhati ni jamii iliyosambaratika, na kwa hivyo haina matarajio kwa ajili ya mustakabali wa kijamii, ikiwa hawatachukua hatua muafaka kabla ya kupitwa na wakati, kwa hivyo yahitajika yawepo mabadiliko kuanzia katika msingi wa mtazamo wa Wamarekani.2

MAHUSIANO YA KIJAMII KATIKA JAMII YA KIISLAMU Kwa hakika jamii za kiislamu pamoja na kukosa kushikamana na Uislamu mshikamano kamilifu, ila bado uhai wa kijamii hubakia na kuendelea. Kulingana na tafiti na majaribio yaliyofanywa katika jamii za Kiarabu – nazo ni sehemu ya jamii ya umma wa kiislamu – bado upo upendo, mafungamano na maingiliano mazuri katika jamii hizo za Kiarabu, nayo ni msimamo ambao huenda ukatoa sura halisi ya umuhimu wa wengi na sio wa mtu mmoja… 1. Kwa ufafanuzi zaidi rejea: Ahdathu Munharifiina Uk. 5 chapa ya Muasasat Jaamiiyya lil darasaat wa nashri wa tawzii, Beirut cha Dr. Ali Muhammad Ja’far 1984. 2. Kwa ufafanuzi zaidi rejea Majallat Fakr Arabi toleo la 54 Uk. 233. 6


Ndugu na Jirani Na utekelezaji kwa ajili ya matakwa ya familia na hofu kutokana na maneno ya watu, na umuhimu wa kuhifadhi sifa nzuri, na mahala pa hali ya juu ambapo huletwa na mambo mazuri ya jamii ya Kiarabu, si jingine ila ni kutilia mkazo umuhimu wa jamii kwa mtu mmoja. Mmoja wa watafiti ameeleza kwamba waarabu ni tofauti na watu wa Ulaya na Wamarekani, mara nyingi hufadhilisha usimamaji na ukaaji kwa ukaribiano mkubwa kati yao katika sehemu za umma.3

SABABU ZA UVUNJA UDUGU Baada ya kulinganisha kati ya jamii ya Kiislamu na thamani yake katika mwelekeo wa kijamii na kati ya jamii ile ya Kimagharibi yenye mtazamo wa umimi na ubinafsi, ni vizuri tujue sababu ambazo hupelekea watu kuwa kila mmoja kivyakevyake na kujitenga na wengine, na sababu hizi pia zinahusu uvunja udugu. Kutawaliwa na roho ya kimaada: Hali hii inakuwa kwa jamii na kwa watu pia, miongoni mwa sababu hizo ni kwamba kila binadamu hujali nafsi yake kwa namna ambayo hupelekea kujali wengine, na hilo tunaliona katika jamii za Kiarabu ambazo mahusiano yake na wengine hayana kipimo, isipokuwa kwa ulinganishaji wa kimaada, na hufupisha mahusiano yao kwa kipimo cha mfuko wa nguo na mali iliyopo. Na roho hii ya kimaada imekataliwa na dini ya kiislamu, na ikilingania katika kuipa kinyongo dunia pamoja na mali, kwani mawili hayo husababisha maovu mengi na kati ya hayo ni uvunja udugu. Sisi tunaona matajiri wengi wanapupia katika ukusanyaji wa mali, hawana mahusiano na ndugu zao, pamoja na hivyo wao ni mafakiri, hawafaidiki kutoka kwao 3. Majallat Fikra Arabi Uk. 17. 7


Ndugu na Jirani chochote, si kwa kiasi cha mfuko wa suruali na si maslahi mengi ya kimaada. Kiburi: Hali hii inahusiana na utawala wa roho kimaada, ambayo humpelekea binadamu ambaye aliyezidiwa na roho ya aina hii, kumfanya awafanyie kiburi wengine na kuwadharau. Mtume (s.a.w.w.) amesema:

“Haingii peponi mwenye punje ndogo ya kiburi moyoni mwake.”4 Ikiwa kiburi ni jambo baya katika Uislamu, kwa hakika kuwafanyia kiburi ndugu ni jambo baya zaidi, matajiri na wenye vyeo wangapi tunawaona ndugu yake fakiri hamfikii, au asiye na cheo hamfikii mwenye cheo, wala hawatambui bali huwafanyia kiburi, ama akimuona nduguye tajiri humwelekea kwa heshima, na kwa kweli uhakika huo hauungi udugu, bali huko ni kujali mali na maslahi madogo na sio utu na udugu, kwani huheshimu mali na kuwapuuza ndugu zake, je! hajui huyu mwenye kiburi kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anasema:

“Hampendi kila mwenye kujiona na mwenye kujifaharisha.” (Sura Luqman:18). Dhana mbaya: Nayo husababisha uadui mkubwa na chuki, ndugu wangapi wamekatiana udugu kwa sababu ya kudhaniana kwao vibaya, na familia nyingi zimesambaratika kwa sababu ya jambo hilo liangamizalo. Kwa mantiki hiyo 4. Usuulul-Kafiy Juz. 2 Kitabul-Imani Wal-Kufri, Hadithi namba 11. 8


Ndugu na Jirani basi Mwenyezi Mungu ametutahadharisha kuhusiana na tabia hiyo, anasema:

“Enyi mlioamini! Jiepusheni na dhana nyingi kwani baadhi ya dhana ni dhambi wakati mwingine…” (Sura Hujrat:12). Na zipo Hadithi chungu nzima zinazoelezea suala hili, Abu Abdillah asSadiq (a.s) amesema: Amirul-Mu’miniina Ali (a.s.) amesema: “Lichukulie jambo la ndugu yako kwa kheri hadi akuletee lile likushindalo kwake, wala usidhanie ubaya neno litokalo kwa ndugu yako, na yakupasa wewe ulichukulie kwa kheri.”5 Husda: Nalo ni miongoni mwa mambo ambayo huharibu dini, aidha linakata mahusiano baina ya vipenzi na waumini, kwa hakika sharia ya kiislamu imetutahadharisha kuhusiana na jambo hilo, Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anasema:

“Au wanawahusudu watu kwa yale aliyowapa Mwenyezi Mungu katika fadhila yake?” (Sura Nisai:54). Na anasema:

“Na shari ya hasidi anapohusudu.” (Sura Falaqi:5). Na Mtume (s.a.w.w.) amesema kuwaambia Masahaba: “Ah, hakika mme5. Usuul-Kaafiy mlango wa Tuhuma na dhana mbaya, amenukuu moyo uliyosalimika Dastaghiib Uk. 300 cha Kulaini. 9


Ndugu na Jirani fikwa na gonjwa lililowakumba watu waliokuweko kabla yenu, nalo ni husda, halinyoi nywele bali huharibu dini.”6 Je! Haikuwa husda ni sababu ya Qaabiil kumuua nduguye Haabiil, Imam as-Sadiq (a.s.) amesema: “Husda asili yake hutokana na upofu wa moyo… na husda humuingiza mtu kwenye hasara ya milele na humuangamiza na wala hanusuriki milele kwayo.”7 Na ndugu wa Nabii Yusuf (a.s.) walipopanga kumuua Yusuf (a.s.) ilikuwa ni kutokana na wao kuwa na sifa ya husda, na kisa chake ni mashuhuri.

Usengenyaji: Tabia ya kusengenya ni miongoni mwa tabia mbaya ambazo husababisha mpasuko katika familia, na Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ametukataza hilo kwa maslahi yetu, anasema:

“Wala baadhi yenu msiwatete wengine, je! Mmoja wenu anapenda kula nyama ya nduguye aliyekufa? Mnalichukia hilo…”(49:12)8

Utetaji: Na kusema maneno machafu, ukosefu wa heshima na chuki iliyopo ndani ya nafsi, seuze vita vya kitamaduni za Kimagharibi kwetu sisi, kwa namna ambayo tunakaribia kuwa na tabia kama zile za watu wa Kimagharibi, mwenendo na mwelekeo wao. 6. Al-Wasail, mada Jahad, mlango 54, amenukuu moyo uliyosalimika Dastaghiib Uk. 402 cha Hurru A’mili. 7. Mustadrakul- Wasail, amenukuu moyo uliyo salimika Dastaghiib Uk. 402. 8 Arbaini Hadithi Uk. 173 cha Imam Khomeini. 10


Ndugu na Jirani Na sababu hizo na zisizo kuwa hizo hatukuzieleza kwa urefu na mapana kuchelea mada hii kuwa ndefu, kwa ufafanuzi zaidi ni vyema kurejea vitabu vinavyohusiana na tabia, ambavyo huelezea mada hii kwa urefu zaidi, hali kadhalika hutoa tiba kwa tabia hizi mbaya, na katika kutatua na kuponya maradhi hayo vivyo hivyo hutibu suala la uvunja udugu, na tabia nyingi kati ya tabia mbaya pamoja na chuki.

BAINA YA TAASUBI NA UUNGAJI UDUGU Ni sahihi kwamba Uislamu unalingania umoja na kuhurumiana, kama vile itavyokuja katika Hadithi mbalimbali na Aya za Qur’ani, lakini Uislamu umekataza suala la taasubi pofu kwa ajili ya familia na jamaa. Imam Khomeni amesema: “Taasubi ni moja ya sifa iliyo ndani ya nafsi, na miongoni mwa athari yake ni kuwatetea na kuwahami ndugu na jamaa na wale wote anaohusiana nao, liwe hilo linafungamana kidini au kimadhehabu au mwelekeo wao kuwa mmoja, vivyo hivyo mafungamano yawe ya kinchi na kikanda…Na taasubi ni miongoni mwa tabia za kifisadi na sifa isiyopendwa na kusifiwa, kwa hivyo hilo husababisha ufisadi katika tabia na matendo…Mtu anapofanya taasubi kwa ajili ya ndugu zake, au wapendwa wake na akawatetea, akiwa anakusudia kudhihirisha haki na kuindoa batili, basi taasubi hiyo ni nzuri, kwani hutetea haki na ukweli… “Ama iwapo atashughulishwa kwa lengo la kutetea uzalendo, bila shaka taasubi yake itakuwa kutetea taifa lake na wapendwa wake katika ubatili wao na mambo yao, kwa hivyo mtu huyo atakuwa ametawaliwa na tabia mbaya, kwani sifa ya taasubi ni sifa ya kijahili, aidha ni kiungo na nyenzo mbaya katika jamii… Nayo ilikuwa ni nembo ya waarabu wa zama za ujinga…” Imekuja katika kitabu Al-Kafiy kutoka kwa Abu Abdillah as-Sadiq (a.s) amesema: “Mwenye kufanya taasubi au akafanyiwa yeye taasubi kwa 11


Ndugu na Jirani hakika huvuliwa imani kutoka shingoni mwake.”9 Na imepokewa Hadithi kutoka kwa Abu Abdillah as-Sadiq (a.s.) amesema: “Mwenye kufanya taasubi Mwenyezi Mungu atamtia motoni kadiri ya taasubi yake.”10 Kwa hivyo kuunga udugu na jamaa wa karibu, kusaidiana nao na kuishi nao vizuri ni mambo yatakiwayo na Uislamu, na haikubaliki kabisa kusaidiana nao katika batili na dhulma, Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anasema:

“Na saidianeni katika wema na taq’wa wala msisaidiane katika dhambi na uadui.” (Sura Maida:2). Na Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ametuamrisha katika Kitabu chake kitukufu tusiwe wenye taasubi kwa yule ambaye ana karaba na udugu nasi, na ugunduzi wetu uwe ni haki na uadilifu, na tuseme haki japo iwe dhidi ya ndugu zetu, Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anasema:

“Na msemapo, basi semeni kwa insafu ingawa ni jamaa wa karibu” (Sura An’aam:152).

9. Al-Kaafiy Juz. 2, Uk. 307. 10. Al-Kaafiy Juz. 2, Uk. 308. 12


Ndugu na Jirani

UUNGAJI UDUGU KWA MUJIBU WA QUR’ANI TUKUFU Miongoni mwa masuala ambayo yametiliwa umuhimu sana na Qur’ani tukufu ni suala la udugu, na kwa ufafanuzi ni jamaa wa karibu, hususani tutakapofuatilia Aya za Qur’ani tunaona kwa uwazi namna Qur’ani tukufu ilivyojali na kutilia umuhimu suala hilo, hapa tunataja baadhi ya Aya kuhusiana na kadhia hiyo: Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anasema:

“Na mwabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote na wafanyieni wema wazazi wawili na jamaa wa karibu, na mayatima na masikini na jirani wa karibu….” (Sura Nisai:36). Aya hiyo tukufu inatoa ishara ya kuwatendea haki wazazi wawili, aidha inausia kuwatendea wema, na tukichunguza tunaona uhusiano uliopo wa kutomshirikisha Mwenyezi Mungu na kuwatendea wema wazazi wawili, na vivyo hivyo inatupia macho mafungamano yaliyopo kati ya masuala hayo mawili, kwa namna ambayo inakuwa kuacha kuwatendea wema wazazi wawili na kutozizingatia haki zao ni katika kumshirikisha Mwenyezi Mungu (s.w.t.), kisha inausia kuwatendea wema jamaa, na mwisho wa Aya hiyo Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anamalizia kwa kusema: “Hakika Mwenyezi Mungu hampendi mwenye kiburi, ajivunaye.” (Sura Nisai:36). Hapo inatoa ishara kwamba sababu ya uvunja udugu au miongoni mwa sababu zake ni kiburi, ambacho kimeelezwa kwa ibara ya kujivuna na kujifaharisha. 13


Ndugu na Jirani Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anasema:

“Kwa hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha uadilifu na hisani na kuwapa jamaa wa karibu…” (Sura Nahli: 90). Kwa hakika kuna idadi kubwa ya Aya ambazo zinazoamrisha kuwatendea wema jamaa wa karibu, vyovyote wema utakavyo kuwa, kuwatendea ndugu na jamaa ni vizuri na bora zaidi. Mwenye kurejea vitabu vya Fiq’hi (sharia za kiislamu) ataona fatwa ambazo zinatoa ishara namna ambavyo Uislamu unavyotilia umuhimu mkubwa suala la kuwatendea wema jamaa wa karibu, kwa mfano ni mustahabu kuwapa ndugu na jamaa wa karibu sadaka, zaka na zawadi, na hukmu zinginezo. Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anasema:

“Na (kumbukeni) tulipofunga ahadi na wana wa Israeli, hamtamwabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu tu, na muwatendee wema wazazi wawili na jamaa wa karibu na mayatima na masikini, na mseme na watu kwa wema, na simamisheni Swala na toeni Zaka, kisha mkakengeuka isipokuwa wachache tu katika nyinyi, na nyinyi mnapuuza.” (Sura Baqara:83). Aya tukufu inawakemea wana wa Israeli kutokana na kupuuza hukumu 14


Ndugu na Jirani zilizopo katika Aya hiyo, kati ya hizo ni kuwafanyia wema jamaa wa karibu, na hilo linaashiria juu ya umuhimu wa jambo hilo mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.). Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anasema:

“Na wasiape wale wenye utajiri na wenye wasaa (kujizuia) kuwapa walio jamaa…” (Sura Nuru:22). Imeelezwa kwamba Aya hiyo iliteremshwa kwa baadhi ya watu ambao walikuwa wamewaudhi jamaa zao wa karibu, wakaapa kutounga nao udugu, lakini Mwenyezi Mungu (s.w.t.) akawakataza jambo hilo. Na hilo linatupa fikra iliyo muhimu kwamba hata kama tumeudhiwa na jamaa zetu wa karibu na wakakata udugu na sisi kwa sura yoyote ile basi ni juu yetu tusikate nao udugu.

UUNGAJI UDUGU KWA MUJIBU WA HADITHI Kama ilivyo Qur’ani tukufu inavyojali na kutilia umuhimu suala la udugu, vivyo hivyo zimepokewa Hadithi chungu nzima kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w.) na Ahli bayt wake (a.s.) kusisitizia zaidi umuhimu huo, hapa tunataja baadhi ya Hadithi hizo: Himizo la kuunga udugu: Imam Ali (a.s.) amesema: “Hatosheki mtu na jamaa zake hata kama ana mali, kwa utetezi wao kwake kwa mikono yao na ndimi zao, na wao ni watukufu zaidi ambao wapo nyuma yake na machungu yao huwa juu yake, ni wapole zaidi kwake pindi anapofikwa na matatizo, na kwa kauli ya 15


Ndugu na Jirani ukweli Mwenyezi Mungu humjaalia mtu huyo kuwa mbora kwa watu kuliko mali anayoirithi mwingine, wala asijitenge mmoja wenu na jamaa zake…”11 Vile vile amesema: “Watukuze ndugu zako kwani wao ni ubawa wako ambao kwa huo huruka, na asili yako ambayo huifikia, na mkono wako ambao kwake unapata kitu.”12 Matokeo ya uungaji udugu: Kwa hakika uungaji udugu ni jambo zuri na linalomnyanyua mtu hapa duniani na akhera, na zimepokewa Hadithi nyingi zinazohusiana na suala hilo, hapa tunataja baadhi ya hizo: Imam as-Sadiq (a.s.) amesema: “Uungaji udugu unatakasa matendo, huongeza mali, hukinga balaa, hufanya wepesi hesabu na hurefusha umri.”13 Aidha (a.s.) amesema: “Kuunga udugu husababisha tabia nzuri, huruhusu kipokeo, hupendezesha nafsi, huongeza riziki na hurefusha umri.”14 Na imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s.) amesema: “Hakika kuunga udugu na kutenda wema hufanya wepesi hesabu na hukinga madhambi.”15 Na lau mtu angelijua malipo makubwa atakayoyapata huko akhera achilia mbali yale ayapatayo hapa duniani wala asingelivunja udugu katu katika umri wake wote. Na kwa umri wangu! hivi ni rehema ngapi za Mwenyezi Mungu, na ukarimu Wake ulioje kwa kutoa rehema hizo, mara nyingi binadamu huzembea kwalo. 11. Miizanul-Hikma Juz. 2, Uk. 54 cha Muhammad Muhammadi Ray Shahri. 12. Miizanul-Hikma Juz. 2, Uk. 54 cha Muhammad Muhammadi Ray Shahri. 13. Miizanul-Hikma Juz. 2, Uk. 54 cha Muhammad Muhammadi Ray Shahri. 14. Miizanul-Hikma Juz. 2, Uk. 54 cha Muhammad Muhammadi Ray Shahri. 15. Miizanul-Hikma Juz. 2, Uk. 54 cha Muhammad Muhammadi Ray Shahri. 16


Ndugu na Jirani Kama ilivyo kuunga udugu ni jambo zuri na linalotakiwa kikawaida, na uvunja udugu ni jambo baya na lisilofaa, aidha lina madhara mengi duniani na akhera, na zifuatazo ni baadhi ya Hadithi zinazohusiana na kadhia hiyo, nazo ni: Uvunja udugu ni miongoni mwa matendo yamchukizayo mno Mwenyezi Mungu: Mtu mmoja alikwenda kwa Bwana Mtume (s.a.w.w.) akauliza: “Ni matendo gani yamchukizayo sana Mwenyezi Mungu?” Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Kumshirikisha Mwenyezi Mungu.” Akauliza: Kisha nini? Akasema (s.a.w.w.): “Kuvuja udugu.”16 Husababisha umri kupungua: Amiirul-Mu’miniina Ali (a.s.) katika Khutba yake amesema: “Ninajilinda kwa Mwenyezi Mungu na dhambi ambayo huharakisha kifo.” hapo akasimama Abdallah bin Kuwai akasema: “Ewe Amiirul-Mu’miniina je! kuna dhambi ambayo huharakisha kifo?” Akasema: “Ndio, ni uvunja udugu, ikiwa wanandugu wanapokuwa pamoja na wanaelewana na wao ni wamoja basi Mwenyezi Mungu huwaruzuku hao, na pindi wanandugu wanafarikiana na baadhi yao kukatiana udugu Mwenyezi Mungu huwanyima wao riziki hata kama wakiwa wachamungu.”17 Usivunje udugu hata ikiwa wao watauvunja udugu: Mtu mmoja alikwenda kwa Imam Abu Abdillah as-Sadiq (a.s.) akiwashitaki ndugu zake, Imam (a.s.) akamwambia: “Zuia ghadhabu zako na watendee wema.” Akasema: Hakika wananifanyia mabaya mbali mbali, Imam (a.s.) akamwambia: “Je! Unataka kuwa kama walivyo wao, 16. Dhunubul-Kabiira Juz. 1, Uk. 164 cha Dastaghiib. 17. Dhunubul-Kabiira Juz. 1, Uk. 165 cha Dastaghiib. 17


Ndugu na Jirani Mwenyezi Mungu hatawaangalia nyote.”18 Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Usivunje udugu hata kama ikiwa ndugu yako amekata udugu nawe.”19 Uvunjaji udugu unazuia maombi kujibiwa, na pia kupata harufu ya Peponi: Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Jibrail amenipa habari kwamba hakika harufu ya Pepo hupatikana umbali wa mwendo wa miaka elfu mbili, haipati harufu hiyo mwenye kuwakosea wazazi wake na mvunjaji udugu.”20 Vile vile Mtume (s.a.w.w) amesema:

“Kuvunja udugu kunazuia kujibiwa maombi.”21

KUDUMISHA UDUGU NA WAZAZI WAWILI Ikiwa kuunga udugu na jamaa ni jambo la wajibu na kuvunja udugu nao ni jambo la haramu, kwa hiyo hutiliwa mkazo zaidi katika kudumisha udugu na wazazi wawili, na kuwepo kemeo kali juu ya kukata udugu nao, kwa hakika kutowatendea wema wazazi wawili huhesabiwa ni miongoni mwa madhambi makubwa, kama lilivyoelezwa hilo kinaga ubaga na Hadithi chungu nzima. Imepokewa Hadithi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) amesema: 18. Dhunubul-Kabiira Juz. 1, Uk. 165 cha Dastaghiib. 19. Dhunubul-Kabiira Juz. 1 Uk. 165 cha Dastaghiib. 20. Dhunubul-Kabiira Juz. 1 Uk. 166 cha Dastaghiib. 21. Dhunubul-Kabiira Juz. 1 Uk. 166 cha Dastaghiib. 18


Ndugu na Jirani

“Mwenye kuwachukiza wazazi wake wawili kwa hakika amemchukiza Mwenyezi Mungu, na mwenye kuwaghadhibisha hao amemghadhibisha Mwenyezi Mungu.”22 Vile vile amesema:

“Mwenye kuwaudhi wazazi wawili kwa hakika ameniudhi mimi, na mwenye kuniudhi mimi kwa hakika amemuudhi Mwenyezi Mungu, na mwenye kumuudhi Mwenyezi Mungu mtu huyo ni mwenye kulaaniwa.”23 Aidha (s.a.w.w.) amesema:

“Mwenye kuwaudhi wazazi wake atende apendalo kutenda, asilani hatoingia peponi.”24 Na imepokewa kutoka kwa Imam Swadiq (a.s) amesema:

“Mwenye kuwaangalia wazazi wake kwa jicho la chuki hali ya kuwa wamemdhulumu yeye, haitokubaliwa Swala yake.”25

22. Dhunubul-Kabiira Juz. 1, Uk. 144 cha Dastaghiib. 23. Dhunubul-Kabiira Juz. 1 Uk. 144 cha Dastaghiib. 24. Dhunubul-Kabiira Juz. 1 Uk. 144 cha Dastaghiib. 25. Dhunubul-Kabiira Juz. 1 Uk. 144 cha Dastaghiib. 19


Ndugu na Jirani Hiyo ni hali ambapo wao ndio wamemdhulumu, je, hali itakuwaje iwapo atakuwa yeye ni mwenye kuwadhulumu.

KUWATENDEA WEMA WAZAZI WAWILI Kwa mujibu wa Qur’ani tukufu na Hadithi za Mtume (s.a.w.w.) pamoja na za Ahlul-bayt (a.s.) tunafaidika kwamba kuwatendea wazazi wawili ndivyo sivyo haimaaanishi tu kuwaudhi, kuwakera na kuwasumbua kuwa ndio haramu na miongoni mwa madhambi makubwa, la hasha, bali pamoja na kutokuwafanyia hayo, kuwatendea wema na kutekeleza haki zao ni wajibu na kuacha kufanya hivyo ni haramu kisharia. Ama Aya zinazoelezea suala la kuwatendea wema wazazi wawili nazo ni: “Na muwatendee wema wazazi wawili” (Sura Baqara:83). Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na tumemuusia mwanadamu (afanye) wema kwa wazazi wake.” (Sura Ankabut:8). Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Unishukuru mimi na wazazi wako.” (Sura Luqman:14). Namna ambayo kuwashukuru wazazi wawili kumekuja baada ya kumshukuru Mwenyezi Mungu (s.w.t.), na hakuna shaka kiakili kwamba ni lazima kumshukuru Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa viumbe, kwa mantiki hiyo kama ilivyo lazima kumshukuru Mola Manani vivyo hivyo ni 20


Ndugu na Jirani lazima kuwashukuru wazazi wawili. Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anasema:

“Na Mola wako Mlezi ameamuru kuwa msimuabudu (yeyote) ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema, mmoja wao akifikia uzee naye yuko kwako, au wote wawili, basi usiwaambie Akh! Wala usiwakemee, na useme nao kwa msemo wa heshima, na uwainamishie bawa la uyenyekevu kwa huruma, na useme: Mola wangu Mlezi! Warehemu (wazazi wangu) kama walivyonilea katika utoto.” (Sura Israi: 23-24). Kwa hivyo kutenda wema kunakabiliana na kutenda ubaya, kwa hali hiyo kuwatendea wema wazazi wawili ni wajibu ulio mkubwa baada ya kumpwekesha Mweyezi Mungu (s.w.t.), aidha kuwatendea vibaya ni miongoni mwa madhambi makubwa baada ya kumshirikisha Mwenyezi Mungu (s.w.t.). Na kwa mantiki hiyo baada ya hukmu ya tawhiid na kufuatia na hukmu zinginezo zilizotajwa, kuhusiana na mchakato huu Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amelieleza suala hili sehemu mbali mbali ndani ya Qur’ani tukufu. Na imekwishatangulia hapo kabla mfano wa Aya hiyo katika Aya ya 151 ya Surat An’aam, kwa hakika mahusiano na mafungamano ya kiupendo 21


Ndugu na Jirani mama na baba kwa upande mmoja na kwa mtoto kwa upande mwingine ni makubwa zaidi, kulingana na yale ambayo hufanywa katika jamii ya kibinadamu, nayo ni hali ya kimaumbile ambayo wanandoa hushirikiana kwayo ndani ya jamii husika, kwa hivyo kwa mujibu wa kanuni za kijamii na hali ya kimaumbile ni wajibu kwa mwanadamu kuwaheshimu wazazi wake wawili, kwa kuwakirimu, kuwatukuza na kuwatendea wema, na lau kama isingelijiri hukmu hii, na jamii ya kibinadamu ikaihama na kuiacha, bila shaka ungelibatilika upendo na mafungamano yaliyopo kati ya watoto na wazazi wao, na kwa hivyo ingelienea chuki katika jamii.26 Iwapo mmoja wao akifikia umri wa uzee naye yuko kwako au wote wawili: Kwa hivyo basi kuhusisha hali ya uzee kwa kuitaja, hii inajulisha kwamba hali hiyo ambayo huipitia wazazi wawili ni tete na ngumu, ambapo huwa na haja kubwa ya usaidizi kutoka kwa watoto wao, na kusimamia wajibu mbalimbali wa maisha yao wawili ambayo wao hushindwa kuutekeleza, na kwa hivyo ni matarajio ya wazazi wawili kupata wajibu huo kutoka kwa watoto wao, kama vile wazazi walivyoshughulikia malezi yao katika hali ya utoto, wakati ambao hawakuwa na nguvu wala uwezo wowote wa kujipatia mahitaji ya maisha yao. Kwa hiyo Aya inajulisha ni wajibu wa watoto kuwatukuza wazazi na kuchunga adabu kikamilifu tunapoishi na kuamiliana nao, vilevile yatupasa kuzungumza nao vizuri wakati wote, hususan wakati ambao mmoja wao anapofikia umri wa uzee au wote wawili, na hapo huwa na haja zaidi kutoka kwa mtoto wao...”27

26. Miizan Fii Tafsiiril-Qur’an Juz. 13, Uk. 79 - 80 cha Muhammad Husein Tabatabai. 27. Miizan Fii Tafsiiril-Qur’an Juz. 13, Uk. 80 cha Muhammad Husein Tabatabai. 22


Ndugu na Jirani

BAADHI YA YALE YALIYOELEZWA NA HADITHI KUHUSU KUWATENDEA WEMA WAZAZI WAWILI Ni bora zaidi kuliko Jihadi: Mtu mmoja alikwenda kwa Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu mimi naipenda Jihadi na ni mchangamfu.” Mtume (s.a.w.w.) akamwambia: “Pigana katika njia ya Mwenyezi Mungu hakika ikiwa wewe utauawa utakuwa hai unaruzukiwa na Mola wako, lakini malipo yako yatakuwa kwa Mwenyezi Mungu, na ukirudi salama utarejea hali ya kuwa huna dhambi kama vile ulivyozaliwa.” Akasema: “Ewe Mtume! hakika mimi nina wazazi wawili wazee hufarijika kwa kuwepo kwangu na wanakarahika kwa kutokuwepo kwangu.” Mtume (s.a.w.w.)

akasema: “Bakia pamoja na wazazi wako, naapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, farijiko lao kwako mchana na usiku ni bora zaidi kuliko Jihadi ya mwaka mzima.”28

28. Dhunubul-Kabiira Juz. 1, Uk. 147 cha Dastaghiib. 23


Ndugu na Jirani Athari mbaya zitokanazo na kuwakosea wazazi: Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Dhambi tatu huharakisha adhabu wala haichelewi kumfikia mhusika hadi akhera, kuwakosea wazazi wawili, kuwafanyia uovu watu na kukufuru ihsani.”29 Kuwatendea wema wazazi wawili hurefusha umri: Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s.) amesema:

“Swadaka ya siri huzuia ghadhabu za Mola, kuwatendea wema wazazi wawili na kuunga udugu hurefusha umri.”30 Kuwatendea wema wazazi wawili huleta utajiri: Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Mwenye kunidhamini mimi kwa kuwatendea wema wazazi wawili na kuunga udugu, nitamdhamini yeye utajiri, umri mrefu na kupendwa na jamaa.”31 Hizo ni baadhi ya Hadithi zinazoelezea suala la wema na kuwatendea wema wazazi wawili, zipo Hadithi chungu nzima lakini tunakomea hapa: Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Hakika mtu anaunga udugu hali ya kuwa umri wake hujabaki ila siku tatu tu, basi Mwenyezi Mungu ataurefusha hadi miaka thelathini, na mtu anakata udugu umri wake ukiwa umebaki miaka thelathini, basi Mwenyezi Mungu ataupunguza hadi siku tatu.”32 29. Dhunubul-Kabiira Juz. 1, Uk. 148 cha Dastaghiib. 30. Dhunubul-Kabiira Juz. 1, Uk. 148 cha Dastaghiib. 31. Dhunubul-Kabiira Juz. 1, Uk. 149 cha Dastaghiib. 32. Dhunubul-Kabiira Juz. 1, Uk. 1056 cha Dastaghiib. 24


Ndugu na Jirani Daraja la Peponi la muunga udugu: Imam Abu Abdillah as-Sadiq (a.) amesema: “Mtume (s.a.w.w.) amesema:

“Hakika peponi kuna daraja halifikiwi na yeyote isipokuwa na Imamu mwadilifu, au muunga udugu na mwenye familia kubwa mwenye subira.” Uvunja udugu ni miongoni mwa madhambi makubwa: Imam Khomeini katika kuelezea madhambi ambayo ni miongoni mwa madhambi makubwa amesema: “Ama madhambi makubwa ni kila maasi ambayo mtendaji wake ameahidiwa moto au adhabu kali, au ipo dalili inayojulisha kuwa hilo ni miongoni mwa madhambi makubwa, au yapo maandiko yanayojulisha kwamba hayo ni miongoni mwa madhambi makubwa, nayo ni mengi …na uvunja udugu…”33 Ni Sunna kuwapa kitu ndugu na jamaa wa karibu katika wale ambao Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ameamrisha kupewa (sadaka au zaka), na amekataza na kukemea vikali kuvunja udugu nao, imepokewa kutoka kwa kiongozi wetu Imam as-Sadiq (a.s.) amesema: “Katika kitabu cha AmiirulMu’miniina Ali (a.s.) mna: Mambo matatu hafi mtendaji wake hadi aone matokeo yake; dhulma, uvunja udugu na yamini ya uongo ambayo anajipambanisha kwayo na Mwenyezi Mungu, kwa hakika utiifu ambao una harakisha zaidi thawabu ni uungaji udugu, na watu wanakuwa waovu na wanaungana basi mali zao huongezeka na huwa matajiri, na yamini ya uongo pamoja na uvunja udugu huporomosha majumba kutokana na kuachwa na watu wake, kwani huondoa kizazi, na kizazi kikiondoka uzazi huisha.” 33. Dhunubul-Kabiira Juz. 1, Uk. 1056 cha Dastaghiib. 25


Ndugu na Jirani Na walio bora zaidi wa hilo ni wazazi wawili ambao Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ameamrisha kuwatendea wema, imepokewa kutoka kwa Imam asSadiq (a.s.) amesema: “Mtu mmoja alikwenda kwa Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Niusie.” Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Usimshirikishe Mwenyezi Mungu na chochote hata ikiwa wachomwa moto na hadi kuungua ila moyo wako umetulia ukiwa na imani, wazazi wako wawili watii na watendee wema wakiwa hai au wamekufa, na wakikuamrisha utoke uache familia yako na mali zako fanya, kwani kufanya hivyo ni katika imani.” Na aliye bora zaidi kati ya hao wawili ni mama, kwani umetiliwa mkazo na msisitizo zaidi juu ya mama kumtendea wema na kuunga naye udugu kuliko baba. Imepokewa Hadithi kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s.) amesema: “Mtu mmoja alikwenda kwa Mtume (s.a.w.w.) akauliza: “Ewe Mtume! nani nimtendee wema zaidi?” Akasema (s.a.w.w): “Mama yako.” Akauliza tena: Kisha nani? Akasema (s.a.w.w.): “Mama yako.” Akauliza tena: Kisha nani? Akasema (s.a.w.w): “Mama yako.” Akauliza tena: Kisha nani? Akasema (s.a.w.w): “Baba yako.” Zipo habari chungu tele kuhusiana na maana hii, na zitafutwe kwenye mahali pake.34

NDUGU NI NANI Tunapozungumzia suala la uungaji udugu hapana budi waeleweke kwanza wanandugu, na je! Kila anayehusiana na binadamu kwa ukaraba au ujamaa ana kuwa ni ndugu?

34. Tahriirul-Wasiilat Juz. 1, Uk. 274 cha Imam Khomeini.

26


Ndugu na Jirani Ndugu hawana madaraja na matabaka kama vile matabaka ya urithi, kwa hakika ndugu ambao tunaowakusudia hapa ni kila yule ambaye hujulikana kuwa ni ndugu, kwa mfano baba, mama, kaka, mjomba, baba mdogo, babu na bibi. Huenda baadhi ya watu wakauliza: Je! Wajibu wa kuunga udugu unawahusu ndugu wa baba, aidha wajibu huo waenea pia hata kwa upande wa ndugu na jamaa wa mama? Katika kujibu swali hilo ni kwamba: Wajibu wa kuunga udugu unawahusu ndugu wa baba na mama, kama vile ni wajibu kuwazuru na kuwatembelea jamaa wa baba, vivyo hivyo inawajibika kwa jamaa wa mama,35 kwa mantiki hiyo wajibu wa kuunga udugu unamhusu shangazi wa baba na wa mama pia, vilevile mama zao wadogo, kwani wote ni ndugu zao na wote unawahusu wajibu huo.36 Na huenda wakadhani baadhi kwamba inafaa kuvunja udugu katika baadhi ya sehemu, je, zipo sehemu hizo? Na je, inafaa kuvunja udugu? Ni dhahiri shahiri kwamba haifai kuvunja udugu kwa hali yoyote ile hata kwa mambo madogo, hata kama ikiwa upande mmoja wa wanandugu wamevunja udugu, bali wajibu wa kuunga udugu unabaki palepale. Malipo ya suala hilo huongezeka mara dufu hasa hasa pale inapoambatana na jihadi ya nafsi na kutokuwa na umimi na ubinafsi. Ndio zipo baadhi ya hali ambazo ni nadra sana kutokea ambapo hufaa kuvunja udugu kwazo, ni mara chache sana na nadra sana kutokea hilo. Na huenda ikatokea mume kumzuia mkewe kuunga udugu na jamaa zake, je inafaa kwake kufanya hivyo? 35. Tahriirul-Wasiilat Juz. 1, Uk. 60-61 cha Imam Khomeini. 36. Istiftaat cha Sayyid Kiongozi Khamenei 27


Ndugu na Jirani Ni dhahiri shahiri kwamba kulingana na fatwa za kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, yeye hamruhusu mume kumzuia mkewe kuunga udugu, kwani suala hilo ni la wajibu, ndio, anatoa ruhusa kumzuia kwa baadhi ya mambo katika uungaji udugu, kama vile kuwatembelea kila siku, lakini haifai amzuie daima, kwani hilo hupelekea kuvunja udugu.

VIPI TUUNGE UDUGU Hakuna madaraja wala matabaka katika kuunga udugu katika sharia, kama vile sharia iseme kwa mfano: Ni wajibu kufanya ziara, bali namna ya kuunga udugu ni suala la kawaida za kijamii, kulingana na hali iliyotambulika na kuzoeleka na jamii husika, jamii husika ndiyo ambayo inahukumu wakati gani binadamu anakuwa ameunga udugu au kuukata, hiyo ni kulingana na matendo ambayo kwao wao ni kuunga udugu, muradi tu hayatoki nje ya sheria tukufu. Kwa hivyo kufanya ziara ni kiungo kati ya viungo vya uungaji udugu, na sio sawa kwamba wajibu wa kuunga udugu unahusiana na hilo tu, inawezekana muumini msafiri akaunga udugu na jamaa zake kwa njia ya barua, simu au njia zinginezo za mawasiliano, kwa hivyo kwa yule aliye mbali atatumia njia inayoeleweka katika mchakato huo wa kuunga udugu, anaweza kumuulizia yeye na kujua hali yake, na hiyo ikawa ni sababu ya kupatikana utulivu, nayo huzingatiwa ni katika uungaji udugu.

KUUKIMBIA UUNGAJI UDUGU Huenda wakawepo baadhi ya watu ambao hawajakutana na ndugu zao wala hawajaonana nao maishani mwao asilani, je inalazimu kwao kuunga udugu nao, na je ina lazimu juu ya baba zao na jamaa wengine wawakusanye pamoja nao ili udugu upate kuungika? Ni lazima ifahamike kwamba hakuna mwanya wala upenyo wa kukimbia kutokana na uungaji udugu, lau kama kukusanyika pamoja wanandugu 28


Ndugu na Jirani ikiwa wazazi, watoto na jamaa wengine ni utangulizi wa uungaji udugu, na kwamba wanandugu wataungana kwalo, basi itawajibika kwa wazazi kuharakisha suala hilo la kuwakusanya wao pamoja na jamaa zao ili uthibiti wajibu wa uungaji udugu.37

ADABU ZA MAJIRANI Uislamu unatilia muhimu sana suala la ujirani pamoja na jirani, kwa namna ambayo umelazimisha haki kadhaa, na wajibu mbalimbali ambazo yapaswa kufanyiwa yeye, na huenda mtu akashangaa kutokana na kukithiri kwake, inahitajika muhusika azielewe, azizingatie, afanyie mazoezi utekelezaji wake na hatimae kuzitenda kivitendo. Yote hayo ni kutokana na sharia ya kiislamu katika kuhuisha mahusiano baina ya jamii ya kiislamu iliyo moja na kutilia mkazo mshikamano kupitia mafungamano na mahusiano mazuri ya wanajamii husika. Imam Sajjad (a.s.) ametaja na kueleza masuala hayo katika kitabu Risalatul-Huquuq, humo zipo haki za jirani, na zimepokewa Hadithi chungu nzima ambazo zinahimiza juu ya utekelezaji wa haki zake, na Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amemtaja jirani katika Kitabu chake pale anaposema:

“Na mwabuduni Mwenyezi Mungu wala usimshirikishe na chochote, na wafanyieni wema wazazi wawili na jamaa wa karibu, na mayatima na masikini na majirani wa karibu (katika ukoo) na majirani wa mbali, na rafiki wa ubavuni…” (Sura Nisai:36). 37. Al-Istiftaat kilichoelezwa na kitabu hiki. 29


Ndugu na Jirani Na imepokewa Hadithi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) amesema:

“Utakatifu alionao jirani kwa mtu ni kama vile utukufu wa mama yake.”38 Na mara nyingi Bwana Mtume (s.a.w.w.) aliusiwa na Jibril kuhusiana na jirani, amesema: “Jibril hakuacha kuniusia kuhusu jirani hadi nikadhani kwamba atarithi, mwenye kupuuza haki yake kwa uadui au kwa ubakhili basi atakuwa mwenye kupata dhambi.”39 Muda mfupi ujao tutaeleza kuhusu ujirani, wigo wa jirani na aina za jirani, na baadhi ya haki za jirani ambazo zimeelezwa na Hadithi mbalimbali za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na za Maimamu (a.s.). Wigo wa jirani: Dini ya kiislamu huwazingatia jirani kuwa ni wale watu waliopo katika nyumba arobaini wanao karibiana na nyumba yake kwa kila upande. Imepokewa Hadithi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Jirani ni nyumba arobaini.”40 Na imepokewa kutoka kwa Amiirul-Mu’miniina Ali (a.s.) amesema:

“Haramu ya msikiti ni dhiraa arobaini na ujirani ni nyumba arobaini kila upande.”41 38. Miizanul-Hikma Hadithi ya 3008. 39. Sherhu Risaalatul-Huquq, Juz. 2 Uk. 172. 40. Miizanul-Hikma, Hadithi ya 3028. 41. Miizanul-Hikma, Hadithi ya 3027. 30


Ndugu na Jirani Yaani upande wa Mashariki, Magharibi, Kaskazini na Kusini ni nyumba arobaini kila upande, zote hizo ni majirani wa mwislamu, kwa hivyo inawajibika kwa mwislamu kutekeleza haki za kila jirani. Umuhimu wa kuchagua jirani: Kabla mtu hajaweka makazi yake mahala fulani ni muhimu sana kuchagua watu ambao watakuwa majirani zake, ili asifikwe na balaa la jirani muovu, kwa hivyo ni vyema mtu afuate sera na mwenendo wa Bwana Mtume (s.a.w.w.), yaelezwa kwamba siku moja mtu mmoja alimuuliza Bwana Mtume (.s.a.w.w.): “Ni sehemu gani inafaa anunue nyumba atakayoishi?” Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Jirani kabla ya nyumba.”42 Mara nyingi mtu hujuta kutokana na kuchagua sehemu mbaya ya makazi yake ya kuishi, basi ni juu yake kuchunguza majirani wenye kupambika na sifa nzuri, dini yao na tabia njema, Luqman Hakiim alimuusia mwanawe akimwambia:

“Ewe mwanangu! Nimebeba jiwe zito na chuma kizito sikuona uzito wowote kuliko kuishi na jirani muovu.”43 Aina za majirani: Mtume (s.a.w.w.) amewagawanya majirani katika makundi matatu kulingana na haki zao. Imepokewa Hadithi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Majirani wako wa aina tatu: Jirani mwenye haki tatu, jirani mwenye haki mbili na jirani mwenye haki moja. Ama mwenye haki tatu ni jirani ambaye ni karaba na ni mwislamu, ana haki ya ujirani, haki ya ukara42. Miizanul-Hikma Hadithi ya 3010. 43. Sherhu Risaalaul-Huquq Juz. 2 Uk. 176 31


Ndugu na Jirani ba na haki ya Uislamu. Ama jirani mwenye haki mbili ni jirani mwislamu, ana haki ya Uislamu na ya ujirani. Na ama jirani mwenye haki moja ni kafiri ambaye ana haki ya ujirani.” Na tanabahisho hilo la Mtume (s.a.w.w.) kwetu sisi lina lengo kwamba tusipuuze hata kidogo suala la jirani aliye kafiri, kwani kuamiliana vizuri na jirani kafiri kwa tabia njema kunamfanya awe karibu na Uislamu na avutiwe nao. Imepokewa Hadithi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) kwamba alikuwa na jirani Myahudi ambaye kila siku alikuwa akimtupia uchafu karibu ya nyumba yake, siku moja hakumuona basi akaenda kumtembelea ili kumjulia hali kwani yule Myahudi alikuwa mgonjwa, kwa hivyo akasilimu kwa tabia njema za Bwana Mtume (s.a.w.w.) na kuamiliana naye vizuri.

HAKI ZA JIRANI Tunaporejea na kudurusu Hadithi mbalimbali za Mtume (s.a.w.w.) pamoja na za Ahlul-bayt (a.s.) tunaona kwamba jirani ana haki chungu nzima, hapa tunataja baadhi, nazo ni: Kumhifadhi anapokuwa hayupo: Inampasa mwislamu kumhifadhi jirani yake kutokana na ndimi za watu, hususani anapokuwa hayupo, na amtetee pindi anaposengenywa au kusemwa vibaya. Imepokewa Hadithi kutoka kwa Imam Sajjad (a.s.) amesema:

“Wala usiache kuwa mlinzi wake, unamkinga na ulimi wa mwenye kumsema vibaya.”44 44. Risaalul-Huquq Juz. 2, Uk. 169.

32


Ndugu na Jirani Na Imam Sajjad (a.s.) ameusia katika kitabu Risalatul-Huquuq mtu amhifadhi jirani yake pindi anapokuwa hayupo amesema:

“Ni haki ya jirani yako kumuhifadhi asipokuwepo.”45 Kumtukuza unapokuwa naye: Ni miongoni mwa haki za jirani yako anapokuwa na wewe uamiliane naye kwa moyo mkunjufu na uso wa bashasha, na usiwe uzito kwake, mkirimu, mtukuze na mpe hadhi yake, kama vile uwafanyiavyo waislamu wenzako. Na imekuja katika kitabu Risalatul-Huquuq hivi: “Basi mtukuze jirani yako unapokuwa naye.”46 Imepokewa Hadithi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Hana imani, hana imani, hana imani.” Masahaba wakauliza: Nani? Akasema: “Yule ambaye jirani yake hasalimiki na dhulma na uovu wake.”47

Kumnusuru anapodhulumiwa: Kwa hakika kumnusuru aliyedhulumiwa ni sifa miongoni mwa sifa za muumini ambaye huwajali wengine, aidha ni miongoni mwa haki za jirani yako kumnusuru pindi anapofanyiwa tendo la uadui na kudhulumiwa na wengine, hasa hasa anapokuwa ni miongoni mwa waumini, kwa hivyo yakupasa umsaidie kwa hali na mali dhidi ya yale ambayo yanamtia maumivu kutokana na misukosuko na taabu za maisha, pamoja na dhulma ya wababe na mafisadi. 45. Risaalatul-Ququq Juz. 2, Uk. 169. 46. Risaalatul-Ququq Juz. 2 , Uk. 169. 47. Risaalatul-Ququq Juz. 2, Uk. 173. 33


Ndugu na Jirani Imam Sajjad (a.s.) amesema:

“Ni haki yake juu yako kumnusuru anapodhulumiwa.”48 Kumnasihi kwa anayoyakusudia: Kwa hakika tendo la muumini la kumnasihi ndugu yake huonesha jinsi gani anavyomjali na anavyompa yeye kipaumbele na uangalizi mahsusi, lakini nasaha hapana budi ilingane na kwenda sanjari na masharti na tabia njema, wala haifai kwa muumini kumnasihi nduguye mbele ya watu wengine au kwa kupaza sauti. Imepokewa katoka kwa Imam Sajjad (a.s.) amesema:

“Ukijua kwamba atakubali nasaha yako basi mnasihi mkiwa wawili wewe na yeye.”49 Na upo msisitizo katika baadhi ya Hadithi kwamba unasihi na uelezaji inabidi uwe kwa siri na faraghani. Imepokewa kutoka kwa AmiirulMu’miniina Ali (a.s.) amesema:

“Mwenye kumpa nduguye waadhi faraghani kwa hakika amempamba, na mwenye kumpa waadhi hadharani huyo amemchafua.”50 48. Risaalatul-Ququq Juz. 2, Uk. 169. 49. Risaalatul-Ququq Juz. 2, Uk. 169. 50. I’laamud Dini Fii Swifaatil-Mu’miniina Uk. 179. 34


Ndugu na Jirani

Kumfariji: Hakika tendo la kufariji huzingatiwa ni miongoni mwa mambo ambayo yameota mizizi ndani ya jamii ya kiislamu, kwani hilo huimarisha mahusiano baina ya watu, na kwa hivyo zipo Hadithi chungu nzima zinazotilia mkazo suala hili la kufariji, hasa hasa baina ya majirani, na ni miongoni mwa haki za jirani ambapo mtu hufurahika kwa furaha yake, kwa mfano pale anapoozesha mwanawe au anapofanya karamu au anapojaaliwa kupata mtoto n.k, vivyo hivyo hapana budi kuhuzunika kwa huzuni yake, kwa mfano anapofiwa na kipenzi chake au mpendwa wake, hali kadhalika amtembelee pindi anapoumwa kwa lengo la kumfariji na kumfanyia tahfifu machungu na maumivu yake. Imepokewa Hadithi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Na anapoumwa waenda kumjulia hali, anapokufa wasindikiza jeneza lake, anapopatwa na jambo la kheri hufurahi na humpongeza, na anapofikwa na msiba hukosa furaha na humfariji.”51

Kumsamehe: Miongoni mwa haki za jirani kwako ni kumsamehe na kukubali kukiri kwake makosa pindi anapokujia kukuomba msamaha, kwa hakika kutokubali udhuru wa mwingine ni uovu wa nafsi, na hilo linajulisha kuwa mtendaji wa hilo ni mtu mwenye kiburi. Imeelezwa katika kitabu Risalatul-Huquuq kuhusiana na haki za jirani kwamba: “Na unakubali utelezaji wake na wamsamehe makosa yake.”52

51. Risaalatul-Ququq Juz. 2, Uk. 175. 52. Risaalatul-Ququq Juz. 2, Uk. 169. 35


Ndugu na Jirani

Kumkopesha anapoomba mkopo: Hakika suala la ukopeshaji ni jambo lililosuniwa, na ni miongoni mwa masuala muhimu ambayo hudhamini uboreshaji maelewano baina ya waumini, kwa hivyo mkopo hufanya tahfifu ukata mkali wa maisha kwa mafukara, kwa mantiki hiyo ni Sunna mtu kumkopesha jirani yake anapomjia ili kumkopa. Imepokewa Hadithi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) amesema:

“Ikiwa atakuomba mkopo mkopeshe, akikuomba msaada msaidie, na akihitaji mkidhie haja yake.”53

Kutomchunguza chunguza ili kujua siri zake: Miongoni mwa tabia njema ni mtu kuchunga mambo mahsusi ya nduguye na jirani yake mwislamu, asichungulie kulia na kushoto ili kuona mambo ya siri ya mwenziwe, hapaswi hata kidogo kuchungilia wala kutegea sikio mambo ya nyumba ya mtu mwingine, bali awe katika uhalisia wa maneno ya mshairi pale aliposema: “Nakuwa kipofu kwa yale ambayo hudhihirika kwa jirani yangu wa kike hadi atakapojitanda ushungi.” Imepokewa Hadithi kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w.) amesema:

“Usirefushe jengo ili kuona kwake na kumzuia hewa ila kwa idhini yake.”54 53. Risaalatul-Ququq Juz. 2, Uk. 175. 54. Risaalatul-Ququq Juz. 2, Uk. 175. 36


Ndugu na Jirani Kwani kufanya hivyo ni kupora uhuru wa mwingine na kuingilia mambo yake binafsi. Imepokewa kutoka kwa Imam Sajjad (a.s.) amesema:

“Usifuatilie undani wa mwingine, na iwapo utajua ubaya wowote basi mstiri.”55 Na aina mbaya zaidi ya ufuatiliaji na uchunguzaji ni ule ambao una lengo la kumfedhehesha, kumwaibisha, kufichua siri zake na kuzieneza kwa watu.

Kutomuudhi: Muumini ana utukufu na hadhi kubwa, haifai hata kidogo kumuudhi seuze kumfanyia hivyo jirani wa karibu! Yafaa ieleweke kwamba kufanya hivyo ni miongoni mwa madhambi makubwa, bali ni dhambi kubwa zaidi, na tabia hiyo imekemewa na Bwana Mtume (s.a.w.w.), amesema:

“Mwenye kumuudhi jirani yake ameniudhi mimi, na mwenye kuniudhi mimi kwa hakika amemuudhi Mwenyezi Mungu.”56 Kutomfanyia ubakhili wa chakula: Miongoni mwa haki ya jirani utakapopika chakula mpelekee, kwani harufu ya chakula chako inamfikia yeye, kwa hivyo inakubidi kumpelekea

55. Risaalatul-Ququq Juz. 2, Uk. 169. 56. Risaalatul-Ququq Juz. 2, Uk. 178. 37


Ndugu na Jirani chakula hicho, imepokewa kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w.) amesema:

“Ewe Abu Dharri! utakapopika mchuzi zidisha maji, na ukishapika wapelekee majirani zako.”57 Mshairi mmoja kuhusu utukufu wa jirani amesema: “Moto wangu na moto wa jirani yangu ni mmoja. Na kwenye moto huo kabla yangu anaweka chungu.” Na Mtume (s.a.w.w.) ametuamrisha tumpe jirani zawadi ya tunda, na kama hatukuweza kumpa zawadi ya tunda basi hatuna budi tukija nalo nyumbani tuliingize ndani kwa uficho na siri ili asituone nalo, kwani huenda hana uwezo wa kulinunua, aidha tuchunge na tuchukue tahadhari sana juu ya watoto wake wasiwaone watoto wetu wakila. Imepokewa Hadithi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Utakaponunua matunda basi mgawiye jirani yako, na kama si hivyo yaingize ndani kwa siri, watoto wako wasitoe kitu nje ambacho kitawafanya watoto wake wachukie! Je! Mnafahamu ninayowaambia?! Kwa hakika watu wengi hawatekelezi haki za jirani ila wachache ambao wamerehemewa na Mwenyezi Mungu.”58

MATOKEO YA UJIRANI MWEMA Kwa hakika tumekwishajua haki za jirani, tunamuomba Mwenyezi Mungu atuwezeshe kuzitekeleza ipasavyo, na lililobakia juu yetu kujua matokeo ya ujirani mwema duniani na akhera. 57. Risaalatul-Ququq Juz. 2, Uk. 175. 58. Risaalatul-Ququq Juz. 2, Uk. 175 38


Ndugu na Jirani Huongeza umri: Imepokewa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s.) amesema: “Ujirani mwema huzidisha umri.”59 Huongeza riziki: Imepokewa kutoka kwa Amiirul-Mu’miniina Ali bin Abi Twalib (a.s.) amesema: “Ujirani mwema huongeza riziki.”60 Huimarisha makazi: Nyumba hubakia muda mrefu, hudumu pamoja na kuongeza humo baraka, pia wakazi wake hupata mafanikio na kheri nyingi kwayo. Imepokewa kutoka kwa Amiirul-Mu’miniina Ali (a.s.) amesema:

“Ujirani mwema huimarisha majumba na huzidisha umri”61

59. Sherhu Risaalatul-Ququq Juz. 2, Uk. 187. 60. Miizanul-Hikma Hadithi ya 2999. 61. Miizanul-Hikma Hadithi ya 3000. 39


Ndugu na Jirani

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24.

Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thelathini Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudharr Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur'an na Hadithi Elimu ya Nafsi 40


Ndugu na Jirani 25. 26. 27. 28. 29. 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52. 53.

Yajue Madhehebu ya Shia Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu Al-Wahda Ponyo kutoka katika Qur'an. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii Mashukio ya Akhera Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyeezi Mungu na sifa zake Kumswalia Mtume (s) Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana. Upendo katika Ukristo na Uislamu Tiba ya Maradhi ya Kimaadili Maana ya laana na kutukana katika Qur'ani Tukufu Kupaka juu ya khofu Kukusanya swala mbili Bismillah ni sehemu ya Qur'ani na husomwa kwa Jahara Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kusujudu juu ya udongo Kusherehekea Maulidi Ya Mtume (s) Tarawehe Malumbano baina ya Sunni na Shia Kupunguza Swala safarini Kufungua safarini Umaasumu wa Manabii Qur'an inatoa changamoto 41


Ndugu na Jirani 54. 55. 56. 57. 58. 59. 60. 61. 62. 63. 64. 65. 66. 67. 68. 69. 70. 71. 72. 73. 74. 75. 76. 77. 78. 79. 80. 81.

as-Salaatu Khayrun Mina -'n Nawm Uadilifu wa Masahaba Dua e Kumayl Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mtume Muhammad (s) Nahju'l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza Nahju'l-Balaghah - Juzuu ya Pili Kuzuru Makaburi Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita Tujifunze Misingi Ya Dini Sala ni Nguzo ya Dini Mikesha Ya Peshawar Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliyonyooka Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake Liqaa-u-llaah Muhammad (s) Mtume wa Allah Amani na Jihadi Katika Uislamu Uislamu Ulienea Vipi? Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) 42


Ndugu na Jirani 82. 83. 84. 85. 86. 87. 88. 89. 90. 91. 92. 93. 94. 95. 96. 97. 98. 99. 100. 101. 102 103. 104. 105. 106. 107. 108. 109. 110.

Urejeo (al-Raja'a ) Mazingira Utokezo (al - Badau) Hukumu ya kujenga juu ya makaburi Swala ya maiti na kumlilia maiti Uislamu na Uwingi wa Dini Mtoto mwema Adabu za Sokoni Johari za hekima kwa vijana Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu Tawasali Imam Mahdi katika Usunni na Ushia Hukumu za Mgonjwa Sadaka yenye kuendelea Msahafu wa Imam Ali Ngano ya kwamba Qur'ani imebadilishwa Idil Ghadiri Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu Hukumu zinazomuhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi Huduma ya Afya katika Uislamu Sunan an-Nabii Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) Shahiid Mfiadini Kumswalia Nabii (s.a.w) Ujumbe - Sehemu ya Kwanza Ujumbe - Sehemu ya Pili 43


Ndugu na Jirani 111. 112. 113. 114. 115. 116. 117. 118. 119. 120. 121. 122. 123. 124. 125. 126. 127. 128. 129. 130. 131. 132. 133. 134. 135. 136. 137.

Ujumbe - Sehemu ya Tatu Ujumbe - Sehemu ya Nne Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu Hadithi ya Thaqalain Maarifa ya Kiislamu Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza Ukweli uliopotea sehemu ya Pili Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu Ukweli uliopotea sehemu ya Nne Ukweli uliopotea sehemu ya Tano Safari ya kuifuata Nuru Fatima al-Zahra Myahudi wa Kimataifa Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi Visa vya kweli sehemu ya Kwanza Visa vya kweli sehemu ya Pili Muhadhara wa Maulamaa Mwanadamu na Mustakabali wake Imam Ali ('a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) Imam Ali ('a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) Khairul Bariyyah Uislamu na mafunzo ya kimalezi Vijana ni Hazina ya Uislamu. Yafaayo kijamii Tabaruku Taqiyya Vikao vya furaha 44


Ndugu na Jirani 138. 139. 140. 141. 142. 143. 144. 145. 146. 147. 148. 149. 150. 151. 152 153. 154. 155. 156. 157. 158. 159. 160. 161. 162. 163. 164. 165. 166.

Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? Visa vya wachamungu Falsafa ya Dini Kuhuzunika na Kuomboleza - Azadari Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu Kuonekana kwa Allah Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) Ndugu na Jirani Ushia ndani ya Usunni Maswali na Majibu Mafunzo ya hukmu za ibada Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1 Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2 Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 Abu Huraira Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. Mazingatio kutoka katika Qur'an - Sehemu ya Kwanza Mazingatio kutoka kaitka Qur'an - Sehemu ya Pili Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili Qur'ani Tukufu - Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu Uislamu Safi Majlisi za Imam Husein Majumbani Mshumaa 45


Ndugu na Jirani 167. 168. 169. 170. 171. 172. 173. 174. 175. 176. 177. 178. 179. 180. 181. 182. 183. 184. 185. 186. 187. 188. 189. 190. 191. 192. 193. 194. 195.

Uislam wa Shia Amali za Makka Amali za Madina Asili ya Madhehebu katika Uislamu Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi Ukweli uliofichika katika neno la Allah Uislamu na Mifumo ya Uchumi Umoja wa Kiislamu na Furaha Mas'ala ya Kifiqhi Jifunze kusoma Qur'ani As-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah Hayya 'Alaa Khayri'l-'Amal Katika Adhana Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na Ramadhani) Uadilifu katika Uislamu Mahdi katika Sunna Jihadi ya Imam Hussein ('as) Kazi na Bidii ni njia ya maendeleo Abu Talib - Jabali Imara la Imani Ujenzi na Utakaso wa Nafsi Vijana na Matarajio ya Baadaye Usalafi - Historia yake, maana yake na lengo lake Ushia - Hoja na Majibu Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) Maombolezo - Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu Takwa Amirul Muuminina ('as) na Makhalifa Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (a.s.) 46


Ndugu na Jirani 196. 197. 198. 199. 200. 201.

Kuelewa Rehma ya Mwenyezi Mungu Mtazamo kuhusu msuguano wa kimadhehebu Upotoshaji Dhahiri katika Turathi (Hazina) ya Kiislamu Nchi na Uraia - Haki na wajibu kwa Taifa Mtazamo wa Ibn Taymiyyah kwa Imam Ali (a.s.) Uongozi wa kidini - Maelekezo na utekelezaji wa Kijamii

KOPI NNE ZIFUATAZO ZIMETAFSIRIWA KWA LUGHA KINYARWANDA 1. 2. 3. 4.

Amateka Na Aba'Khalifa Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n'amavuko by'ubushiya Shiya na Hadithi

47


Ndugu na Jirani

BACK COVER Uislamu ni dini na ni mfumo wa maisha. NI dini ambayo huzingatia maisha ya ulimwengu huu na ulimwengu ujao - Akhera. Hivyo, mfumo wake umesheheni mafundisho ya kiroho na ya kimwili. Mafundisho ya kimwili ni mafundisho ya maisha; jinsi mtu anavyotakiwa kuendesha maisha yake hapa duniani, ambayo ni pamoja na uhusiano mwema na wanadamu wenzake, wakiwemo ndugu na jirani zake. Na katika nukta hii, mafundisho ya Kiislamu hayakurudi nyuma kuhusiana nayo. Qur’ani ambayo ndiyo kiini na chimbuko la mafundisho na sheria zote za Uislamu, imejaa aya zinazozungumzia nukta hii ikifuatiwa na Sunna, ambayo ni mafundisho ya Mtukufu Mtume (saw). “Na mwabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote; na wafanyieni wema wazazi wawili na jamaa wa karibu, na mayatima na maskini na jirani wa karibu…” (Sura 4:36). Mtukufu Mtume anasema: “Nimetumwa ili nikamilishe mwenendo mwema.” Huo hapo juu ni mfano mdogo tu kutoka katika Qur’ani Tukufu na Hadithi (Sunna). Uislamu ni dini ya amani na inapenda kila mtu aishi kwa amani na uhuru wa kweli. Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: w.w.w.alitrah.info

48


Ndugu na Jirani

49


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.