Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
Q U R ’ A N I YAT O A C H A N G A M O TO
Kimeandikwa na: Imam Sayyid Muhammad Husaini Shirazi
Kimetarjumiwa na: Abdul - Karim Juma Nkusui
11:42 AM
Page A
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
ŠHaki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: ISBN: 978 - 9987 - 427 - 67 - 3 Kimeandikwa na: Imam Sayyid Muhammad Husaini Shirazi
Kimetarjumiwa na: Abdul - Karim Juma Nkusui S. L. P. 970, Singida, Tanzania Kimehaririwa na: Ustadh Abdallah Mohamed Ustadh Hemedi Lubumba Selemani Kimepangwa katika Kompyuta na: Ukhti Pili Rajab Toleo la kwanza: Juni, 2008 Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Al-Itrah Foundation P. O. Box 19701. Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Fax: +255 22 2127555 Email: alitrah@raha.com Website: www.alitrah.org Online Website: www.alitrah.info
7/15/2011
11:42 AM
Page B
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
YALIYOMO FAHARASI 1. Neno la mtangazaji..................................................................................2 2. Utangulizi................................................................................................5 3. Manabii wa Mwenyeezi Mungu na vitabu vya mbinguni.....................11 4. Qur’ani tukufu na vitabu vingine vya mbinguni....................................18 5. Wasia wa Mtume (s.a.w.w.) juu ya Qur’ani tukufu na kizazi chake.......20 6. Muujiza wa Qur’ani...............................................................................26 7. Qur’ani inatoa changamoto...................................................................29 8. Aya ya changamoto................................................................................30 9. Nabii (s.a.w.w.) anaonya kaumu yake...................................................33 10. Aina za utawala katika zama ya Nabii (s.a.w.w.).................................34 11. Nabii na Walid bin Mughira.................................................................35 12. Qur’ani inawaonya wazushi................................................................38 13. Wazushi wa karne ya ishirini...............................................................40 14. Ulahid uliopangwa na kupiga vita vitu vitakatifu................................41
Page C
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
15. Mwanzo wa kupanga ulahidi...............................................................43 16. Wajibu wetu katika Qur’ani tukufu.....................................................46 17. Kujifunza Qur’ani na kuifundisha.......................................................49 18. Qur’ani ni chimbuko la maendeleo na ustaraabu................................50 19. Kutoka katika uongofu wa Qur’ani.....................................................53 20. Kuhifadhiwa Qur’ani kutokana na upotoshaji....................................55 21. Utafiti katika Qur’ani..........................................................................56 22. Kutoka katika uongofu wa Sunna tukufu............................................57 23. Qur’ani inatoa changamoto kwa vizazi...............................................58 24. Thawabu za kusoma Qur’ani...............................................................63
Page D
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
NENO LA MCHAPISHAJI Kitabu ulicho nacho mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kwa jina la al-Qur’an Yatahaddaa kilichoandikwa na Marehemu Ayatullah Sayyid Muhammad Husaini Shirazi. Sisi tumekiita Qur’ani Yatoa Changamoto. Kila Mtume au Nabii alikuja na muujiza wake na alipoondoka muujiza wake huo ulikoma kuwepo pia. Kwa mfano, Nabii Ibrahim (a.s.) muujiza wake mkubwa ilikuwa kwamba alipotupwa kwenye tanuri ya moto kwa nia ya kumteketeza, moto ule ukawa baridi juu yake. Fimbo ya Nabii (a.s.) ilikuwa ikitenda miujiza mingi – iliweza kugeuka kuwa joka kubwa la kutisha, ilipasua bahari na kutoa njia kwa Wana wa Israil kuweza kuvuka bahari kwa salama bila ya kutumia chombo, n.k. Nabii Isa (a.s.) alikuwa akiponya vipofu, wakoma na hata kufufua wafu kwa idhini ya Allah (Mwenye kuhuisha, Aliye Hai). Lakini Mitume hao walipoondoka na miujiza yao pia ikatoweka pamoja nao. Mtume Muhammad (s.a.w.) ambaye ni mwisho wa Mitume, naye kaja na miujiza mingi, lakini ulio mkubwa kabisa ni Qur’ani Tukufu ambayo ni muujiza ambao umebakia baada ya kuondoka kwake. Qur’ani ni muujiza kwa sababu inakwenda na wakati na inakubalika katika kila karne na kizazi. Kwa mfano, wanasayansi wa leo wanagundua mambo ambayo yalikuwa yameshaelezwa na Qur’ani Tukufu zaidi ya karne 14 zilizopita, na hapana shaka, wataendelea kila karne kugundua mambo ambayo tayari maelezo yake yamo katika Qur’ani. Hii ndio maana tunaposema kwamba Qur’ani ni muujiza ulio hai na utabakia kuwa hai mpaka mwisho wa dunia. Qur’ani yenyewe inatoa changamoto kwa usahi-
Page E
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
hi wake kwa wale wote wanaoitilia shaka, wakiwemo majini na wanadamu, kwamba watoe mfano wa hii Qur’ani. Hii ni karne ya 15 tangu Qur’ani Tukufu iteremshwe kutoka mbinguni, na hakutokea jini wala binadamu yeyote aliyeweza kutoa mfano wake. Mwandishi wa kitabu hiki amejitahidi kuonesha ni jinsi gani muujiza huu umehifadhiwa kwa kutoa dalili kutoka kwenye hiyohiyo Qur’ani na hadithi tukufu za Mtukufu Mtume (s.a.w.) Kutokana na umuhimu wa Qur’ani, tumeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa lengo letu lilelile la kuwahudumia ndungu zetu Waislamu wazungumzao Kiswahili. Tunamshukuru ndugu yetu Abdul Karim Juma Nkusui kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki katika kusahihisha na kukipitia hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni chenye manufaa kwa wasomaji wetu na kuzidisha upeo wao wa elimu katika dini. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation
F
Page F
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Page 1
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto
NENO LA MTANGAZAJI Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu. Qur’ani ni nuru isiyozimika mwanga wake, ni taa isiyokoma kuwaka kwake, ni bahari isiyofahamika kina chake, ni mfumo usiopotea njia yake, ni mshumaa usio na kiza katika mwanga wake, ni upambanuzi usiozimwa hoja yake, ni ubainifu usiovunjwa nguzo zake, ni nguvu wasioshindwa wafuasi wake. Umma wa Kiislam unamiliki desturi kuu na mfumo ambao wanadamu wameutambua katika historia yake kongwe, Qur’ani tukufu ni muujiza mkuu wa maisha wenye kudumu milele; yatosha kwa muujiza huu kuwa ni fahari na utukufu kwamba ni Kitabu kitokacho kwa Mwenyezi Mungu, na ni maneno Yake matukufu ambayo Aya zake zimeteremka katika vifua vitoharifu na nyoyo takatifu, basi zikawa ni nuru inayouangazia ulimwengu kwa maarifa mbali mbali na kuufanya upande daraja na kufikia ukamilifu. Ni uzuri ulioje wa herufi hizo kana kwamba unatoa sauti mbalimbali na kwa uzuri wa mvuto wake nyoyo zinapata uhai, herufi ambazo zimeandikwa kwa uwezo wa utukufu wa kiungu mtukufu athari zake zinashangaza, humo kunafafanuliwa elimu na maarifa mbali mbali na unabainika humo uvumbuzi wa kina, akili zinapanuka, zinatoa dira ya maendeleo na mwanadamu anavikwa taji tukufu la kiungu. Herufi za Qur’ani ni herufi za mapinduzi na changamoto, herufi ambazo kwazo Mwenyezi Mungu Muweza na Mtukufu ametoa changamoto kwa wanafasihi wa ulimwengu na werevu wa dunia, Ahlul Kitab na kila mwenye ubinafsi (umimi) wakashindwa kutoa changamoto na wakakiri kwa ukweli wake na utukufu wake, karne baada ya karne, elimu baada ya 2
Page 2
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto elimu, wamenyanyua bendera ya kushindwa na kujisalimisha na kunyenyekea, bado zingali zinaita hadi kesho mustakabala ambao mapambazuko yake yamechomoza kwa nuru ya Qur’ani tukufu na mwanga wa kizazi kitukufu cha Muhammad (s.a.w.w.). Yatosha kwa utukufu wa vizito hivi viwili kuwa vyenyewe ndivyo dhamana pekee katika kuongoka wanadamu katika mambo yao yote, vizazi vyao vyote na katika nyanja zao zote. Kushikamana navyo inamaanisha kutopotea na kutoporomoka katika matamanio ya shetani na kutotumbukia katika mashimo ya matamanio. Mwanadamu vyovyote atakapokimbilia katika hifadhi yeyote basi kuna siku ataporomoka isipokuwa kama atashikamana na nuru ya Qur’ani na kizazi kitukufu, katika hali hii atapata tumaini hivyo hataogopa kudidimia wala hatachelea udhalili kama atakuwa ni mkweli katika kushikamana kwake. Na matumaini haya hayatoweki katika maisha yake yote kwa sababu ameshikamana na ngome imara yenye nguvu haisogelewi na silaha ya adui na wala haishindwi na adui. Mwanadamu tangu zamani amechagua mfumo wake mahsusi ambao umewakilishwa na utawala, nguvu, hukumu na kupambana hadi akafikia katika lengo la msingi ambalo linasimama juu ya fikra sahihi, na hatua ya awali katika njia hii ni kupambana baina ya haki na batili, baina ya nuru na giza, na hatua hii ni muhimu katika kukidhi matakwa yake na kufikia malengo yake, hapana shaka kwamba njia hii inahitaji kuhakiki katika kiini cha mambo na ufafanuzi wake, hivyo ni lazima awe na mfumo atakaoufuata katika kumuongoza, na haujapatikana katika maisha mfumo mtukufu na njia ya sawa tukufu zaidi kuliko Kitabu kitukufu cha Mwenyezi Mungu.
3
Page 3
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto Ni fahari ya Uislamu ambao umetoa changamoto kwa ulimwengu, ambapo amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
“Sema kama watakusanyika wanadamu na majini ili walete mfano wa hii Qur’ani, hawataleta mfano wake hata kama watasaidiana baadhi yao kwa baadhi”Al-Israa: 88 Maadui wa Uislamu wamejaribu kutuhumu muujiza wa Qur’ani kwa kuidharau na wakati mwingine kwa kuitilia shaka, wamejaribu hila mbalimbali lakini hila zao hazijawa isipokuwa ni kama upepo katika dirisha na wamerejea hali ya kuwa ni wenye hasara. Imam Al-Marhum Ayatullah Al-Udhma As-Sayyid Muhammad As-Shirazi anatilia mkazo katika kitabu hiki umuhimu wa mas’ala haya na kuhimiza juu ya kuyatatua na kutanabahi juu ya ukubwa wa umuhimu wake katika jamii ya kiislam, kisha ameashiria juu ya muujiza mkuu wa Qur’ani tukufu ambao umewastaajabisha wanafasihi wote, watu wa elimu na maarifa, umeshangaza fikra zao na ukatatiza akili zao na ukamshangaza mwerevu wao na nyoyo zao. Muasastul Mujtabaa lilitahaqiqi wa nnashri Beirut Lebanon
4
Page 4
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto
UTANGULIZI Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu Shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa viumbe, rehema na amani zimwendee Nabii wetu Muhammad (s.a.w.w.) na kizazi chake chema kitoharifu, na laana za daima ziwashukie maadui zao wote hadi siku ya Kiyama. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Kitabu Chake kitukufu:
“Na Mola wako anajua zaidi katika yaliyo mbinguni na ardhini na tumeshawafadhilisha baadhi ya manabii kwa baadhi yao na tumempa Daud Zaburi.” Al-Israa: 55
5
Page 5
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto Tafsiri ya aya: “Na Mola wako” Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, “anajua zaidi walio mbinguni na ardhini,” wote wapo chini ya elimu yake pana, wawe ni malaika, wanadamu au majini, na kwa muktadha wa elimu yake pana kwa yaliofichikana amewafadhilisha baadhi ya manabii juu ya wengine, na kwayo inajulikana sababu ya kuwafadhilisha manabii juu ya watu wengine, na jambo hili limeletwa hapa kwa sababu ya mtiririko wa aya unahusu itikadi, msingi wake, ujumbe wake na siku yake ya mwisho.
“Tumewafadhilisha baadhi ya manabii kwa baadhi” ambapo nafsi zao zilikuwa tofauti baadhi yake zilikuwa na daraja la juu zaidi kuliko zingine “na tumempa Daud” Nabii (a.s.) Zaburi3” kama ambavyo tumekupa wewe Qur’ani, hivyo hakuna sababu ya makafiri kusema kwamba manabii wamekuja na miujiza ya ulimwengu, nini basi maana ya kuja kwako na Kitabu hiki? Je ilikuwa kama fimbo ya Musa (a.s.) au kuponya mbalanga na ukoma kama vile alivyofanya Nabii Isa (a.s.)?3 Kati ya manabii wa Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Daud (a.s.) naye ni kati ya manabii wa Bani Israil na miongoni mwao ni Suleiman bin Daud (a.s.) na wao ni kati ya manabii wakuu wa Mwenyezi Mungu ingawa wao sio katika Ulul-azmi, ambapo Ulul-azmi ni watano tu nao ni: Nabii wa Uislamu Muhammad (s.a.w.w.), Musa, Isa, Ibrahim na Nuh (a.s.), ama Manabii wengine ambao idadi yao inafikia 124,000 baina ya nabii na mitume kwa kauli mashuhuri wao sio Ulul-azmi. Na imepokewa kauli kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.): “Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ana manabii 124,000 na mimi ni bwana wao, mbora wao na mtukufu wao kwa Mwenyezi Mungu, na kila Nabii ana wasii wake aliyemuusia kwa amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na hakika wasii wangu Ali bin Abi Twalib, ni bwana wao, mbora wao na 3 Taqribul Qur'ani ilaaliadhihan Jz. 15 uk. 58; Suratul Israa 6
Page 6
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto mtukufu wao kwa Mwenyezi Mungu.” 4 Na imepokewa kutoka kwa Ibnu Abbas kwamba yeye amesema: “Nabii wa kwanza ni Adam (a.s.) na wa mwisho wao ni Muhammad (s.a.w.w.) na Manabii walikuwa 124,000 kati yao 305 ni Mitume na kati yao 5 ni Ululazmi nao ni: “Nuh, Ibrahim, Musa, Isa na Muhammad (a.s.).” Watano ni katika Waarabu: Hud, Swalehe, Shuaib, Ismail na Muhammad, na watano ni Waibrania: Adam, Shith, Idris, Nuh na Ibrahim, (a.s.). Nabii wa mwanzo kwa Bani Israil ni Musa na wa mwisho wao ni Isa (a.s.). Na vitabu vilivyoteremshwa kwa Manabii ni 104, kwa Adam sahifa 50, kwa Idrisa sahifa 30, kwa Ibrahim 20, kwa Musa Torati, kwa Daud Zaburi kwa Isa Injili na kwa Muhammad ni Qur’ani.”5 Pia imepokewa kwamba Manabii watano walikuwa Wasiriania Adam, Shith, Idris, Nuh na Ibrahim (a.s.) na lugha ya Adam ilikuwa ni kiarabu nayo ndio lugha ya Peponi, alipomwasi Mola wake akambadilishia Pepo na neema zake kwa ardhi na kilimo, na lugha ya kiarabu kwa lugha ya kisiriyania. Na amesema: “Watano walikuwa ni Waebrania Is’haq, Yaaqub, Musa, Daud na Isa (a.s.), na katika waarabu ni Hud, Swaleh, Shuaib, Ismail na Muhammad (a.s.), na watano walitumwa katika zama moja Ibrahim, Is’haq, Ismail, Yaaqub na Lut (a.s.). Mwenyezi Mungu alimtuma Ibrahim na Is’haq katika ardhi ya Quds, Yaaqub katika ardhi ya Misri, Ismail katika ardhi ya Jarham, Jarham ilikuwa karibu na Al-Ka’aba humo waliishi Amaaliqa na wameitwa Amaaliqa kwa sababu babu yao alikuwa ni Imlaaq bin Lud bin Sam bin Nuh (a.s.). 4 Man laa yahudhuruhul Faqiih Jz. 4, uk. 180 Babul wasiyya min ladun Adam (a.s.) Hadith Na. 5407 5 Al-Ikhitiswas, uk. 264 Hadith Ziyaaratil Muumin 7
Page 7
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto Lut alitumwa katika miji mine: Sodom, Amuur, Sanaa na Darumaa. Na watatu ni wafalme Yusuf, Daud na Suleiman. Na wametawala dunia waumini wawili na makafiri wawili, waumini wawili ni: “Dhul Qarnain na Suleiman, ama makafiri wawili ni Namrud bin Kushi bin Kan’an na Bakhti Nasri”.6 Na kati ya yanayoashiria katika idadi ya Manabii ni yaliyopokewa kutoka kwa Abu Abdillah (a.s.) amesema: “Anayetaka kupeana mkono na Manabii 124,000 basi azuru kaburi la Husein bin Ali (a.s.) katika nusu ya Shaaban kwani roho za Manabii (a.s.) zinataka idhini kwa Mwenyezi Mungu kwa
6 Al-Ikhitiswas, uk. 264 Hadith ziyaaratil muumin
8
Page 8
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto ajili ya kuzuru na huruhusiwa”7 7 Tahdhibul ahkaam, Juz. 6 uk. 48 mlango 16 Amesema Sheikh Al-Mufid katika mlango wa Al-itiqaad fi adadil anbiyaai wal auswiyaai: Amesema Sheikh Suduq “Itikadi yetu katika idadi yao ni kwamba wao ni 124,000 kila Nabii kati yao ana wasii aliyemuusia kwa amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na tunaitakidi kuwa walikuja kwa haki kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kwamba kauli yao ni kauli ya Mwenyezi Mungu na amri yao ni amri ya Mwenyezi Mungu na kuwatii wao ni kumtii Mwenyezi Mungu na kuwaasi wao ni kumwasi Mwenyezi Mungu na kwamba wao hawakutamka ila yatokayo kwa Mwenyezi Mungu na kwa wahyi wake, na kwamba mabwana wa Manabii ni watano ambao ndio wakuu na wao ndio walipewa sharia nao hao ni Ulul-Azmi: Nuh, Ibrahim, Musa, Isa na Muhammad (a.s.), na kwamba Muhammad ni bwana wao na mbora wao alikuja kwa haki na amesadikisha mitume na wale waliomkadhibisha wataonja adhabu iumizayo na wale waliomwamini wakamtukuza, wakamnusuru na wakafuata nuru iliyoteremshwa pamoja nae hao ndio wenye kufaulu. Na ni wajibu tuitakidi kuwa Mwenyezi Mungu hajaumba kiumbe bora kuliko Muhammad na Maimam na kwamba wao ni viumbe wanaopendwa zaidi na Mwenyezi Mungu na watukufu zaidi kwake, wao ndio wa mwanzo kumkubali pale Mwenyezi Mungu alipochukua ahadi kwa Manabiii akawahudhurisha katika nafsi zao: “Je, mimi si ndio Mola wenu?” wakasema ndio, na kwamba Mwenyezi Mungu alimtuma Nabii wake Muhammad (s.a.w.w.) kwa Manabii katika ulimwengu wa kiroho, na kwamba Mwenyezi Mungu alimpa kila Nabii katika aliyompa kwa kadri ya maarifa yake na kutangulia kwake katika kumkubali na kwamba Mwenyezi Mungu aliumba vyote kati ya alivyoviumba kwa ajili yake na Ahlul-bayt wake (a.s.), na kwamba kama sio wao Mwenyezi Mungu asingeumba mbingu, ardhi, pepo wala moto, Adam wala Hawa, Malaika wala kiumbe chochote. Na itikadi yetu ni kwamba makhalifa wa Mwenyezi Mungu kwa viumbe vyake baada ya Nabii wake ni Maimam kumi na wawili (a.s.) na wa mwanzo wao ni Amirul-Muuminina Ali bin Abi Twalib kisha Hasan, Husein, Ali bin Husein, Muhammad bin Ali, Ja’far bin Muhammad, Musa bin Ja’far, Ali bin Musa, Muhammad bin Ali, Ali bin Muhammad, Hasan bin Ali kisha Muhammad bin Hasan Al-Hujjatul Qaim Swahibuz-Zaman Khalifa wa Mwenyezi Mungu (a.s.). Itikadi yetu kwao ni kwamba wao ndio Ulul-Amri ambao Mwenyezi Mungu ameamuru kuwatii na kwamba wao ndio mashahidi kwa watu na wao ndio milango ya Mwenyezi Mungu na njia za kuendea Kwake na wenye kuionyesha ni wao, wao ndio hazina ya elimu Yake na wafasiri wa wahyi Wake na nguzo za tauhidi Yake na kwamba wao wamehifadhiwa kutokana na makosa na kuteleza na wao ndio ambao Mwenyezi Mungu amewatakasa kutokana na uchafu na akawatakasa kabisa, wao wana miujiza na hoja na wao ndio tumaini la watu wa ardhini kama ambavyo nyota ni tumaini la walio mbinguni na mfano wao katika Umma huu ni kama mfano wa safina ya Nuh au kama mfano wa mlango wa Hitwah “toba” na wao ndio waja wa Mwenyezi Mungu waliotukuzwa ambao hawatanguliwi kwa kauli na wanafanya kulingana na amri Yake. Na tunaitakidi kwamba kuwapenda wao ni imani na kuwachukia ni ukafiri, na kwamba amri yao ni amri ya Mwenyezi Mungu na makatazo yao ni makatazo ya Mwenyezi Mungu, kuwatii wao ni kumtii Mwenyezi Mungu, mwenye kuwatawalisha amemtawalisha Mwenyezi Mungu, adui yao ni adui wa Mwenyezi Mungu, kuwaasi wao ni kumwasi Mwenyezi Mungu, Na tunaitakidi kuwa ardhi haibaki bila ya Khalifa wa Mwenyezi Mungu kwa viumbe Vyake ama awe dhahiri anaonekana kwao na ama amefichikana kwa hofu na tunaitakidi kuwa Hujja ya Mwenyezi Mungu katika ardhi na Khalifa Wake kwa waja Wake katika zama zetu hizi ni Al-Qaim Al-Muntadhar Muhammad bin Al-Hasan bin Ali bin Muhamad bin Ali bin Musa bin Ja’far bin Muhammad bin Ali bin al-Husein bin Ali bin Abi Twalib (a.s.) naye ndiye ambaye Nabii wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alitoa habari kwa jina lake na nasaba yake, naye ndiye atakayeijaza ardhi uadilifu na usawa kama ilivyojazwa dhulma na ufisadi yeye ndiye ambaye Mwenyezi Mungu kwa yeye atadhihirisha dini Yake ili ishinde dini zote hata kama washirikina watachukia na kwamba yeye ndiye ambaye Mwenyezi Mungu atafungua kupitia kwake ardhi yote hadi isibaki sehemu katika ardhi ila kutaadhiniwa na dini yote itakuwa ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, yeye ndiye Mahdi ambaye Nabii (s.a.w.w.) ametoa habari kwamba atakapotokea Isa bin Mariam atateremka na kuswali nyuma yake na mwenye kuswali atakuwa kama aliyekuwa anaswali nyuma ya Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa sababu yeye ni Khalifa wake. Na tunaitakidi kuwa haijuzu Al-Qaim awe asiye kuwa yeye, abaki atakavyobaki katika ghaiba yake hata kama atabakia umri wote wa dunia Al-Qaim hatokuwa mwingine asiyekuwa yeye kwa sababu Nabii na Maimam wameeleza kuhusu yeye kwa jina lake na nasaba yake na kwayo wametoa tamko na kwaye wamebashiri (a.s.),
tazama Itiqadaat Suduq uk: 21 Babun Nubuwwah.
9
Page 9
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto Na katika kauli nyingine idadi ya Manabii ni 320, 000. Imepokewa kutoka kwa Abu Abdillah (a.s.) amesema, amesema Abu Dharr: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu ametuma Manabii (anbiyaa) wangapi?” Akasema: “Ametuma Manabii laki tatu na ishirini elfu.” Akasema: “Ewe Mtume, na Mitume (mursaluuna) ni wangapi?” Akasema: “Ni mia tatu na kumi na zaidi.” Akasema: “Mwenyezi Mungu ameteremsha vitabu vingapi?” Akasema: “Vitabu mia moja na ishirini na nne. Ameteremsha kwa Idris sahifah 50 naye ndiye Akhanukh naye ni wa mwanzo aliyeandika kwa kalamu, na ameteremsha kwa Nuh sahifah 10, kwa Ibrahim sahifah 10, ameteremsha kwa Musa Torati, Zaburi kwa Daud, Injili kwa Isa na Qur’ani kwa Muhammad (s.a.w.w.)”8 Na katika kauli nyingine idadi yao ni Manabii 144,000 kama ilivyopokelewa kutoka kwa Swafwan bin Mahram Al-Jamal kutoka kwa Abu Abdillah (a.s.) amesema: “Aliniambia ewe Swafwan! je, unajua Mwenyezi Mungu alituma manabii wangapi?” Nikasema sijui. Akasema: “Mwenyezi Mungu ametuma Manabii 144,000 na Mawasii ni idadi hiyo hiyo, wametumwa kusema kweli, kutekeleza amana na zuhudi katika dunia na Mwenyezi Mungu hakutuma Nabii bora kuliko Muhammad wala wasii bora kuliko wasii wake.”9 Hivyo kama ambavyo baadhi ya Manabii (a.s.) wamefadhilishwa kwa wengine kama alivyosema Mwenyezi Mungu: “Hao ni Mitume tumewafadhilisha baadhi yao kwa baadhi, kati yao kuna aliowasemesha Mwenyezi Mungu na baadhi yao amewanyanyua daraja.”10 Ambapo kuna wabora wao nao ni Ulul-Azim na hao ndio waliopewa sharia na azima kama ilivyopokewa katika riwaya. 8 Ikhitiswas, uk. 264 9 Biharul-Anwar: J: 11 Uk: 59 babu 1 hadith 67 10 Al-Baqara: 253 10
Page 10
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto Imepokewa kutoka kwa Abu Abdillah (a.s.) amesema: “Mabwana wa Manabii na Mitume ni watano nao ni Ulul-Azim baina ya Mitume na wao ndio kitovu: Nuh, Ibrahim, Musa, Isa na Muhammad (a.s.).”11 Ama sababu ya hawa watano kuitwa Ulul-Azim hayo yanabainishwa na riwaya tukufu zilizopokelewa kutoka kwa Ahlul-bayt (a.s.), imepokewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s.) amesema: “Hakika wameitwa Ulul-Azim kwa sababu wao walikuwa ni wenye azima na sharia na hiyo ni kwa kuwa kila Nabii aliyekuja baada ya Nuh alifuata sharia yake na mfumo wake na kufuata kitabu chake hadi zama za Ibrahim, na kila Nabii aliyekuwepo katika wakati wa Ibrahim na baada yake alikuwa katika sharia ya Ibrahim na mfumo wake na alifuata kitabu chake hadi zama za Nabii Musa. Kila Nabii aliyekuwepo wakati wa Musa na baada yake alikuwa katika sharia ya Musa na mfumo wake na kufuata kitabu chake hadi zama za Nabii Isa, na kila Nabii aliyekuwa katika wakati wa Isa na baada yake alikuwa katika sharia yake na kufuata kitabu chake hadi zama za Nabii wetu Muhammad (s.a.w.w.) hawa watano ndio Ulul-Azim na ndio Manabii na Mitume bora (a.s.) na sharia ya Muhammad haitofutwa hadi Siku ya Kiyama na atakayedai unabii baada ya Nabii wetu au kuleta Qur’ani basi damu yake ni halali kwa kila mwenye kusikia hilo kutoka kwake.”12
MANABII WA MWENYEZI MUNGU NA VITABU VYA MBINGUNI Kisha Manabii wako aina mbili: Kati yao kuna ambaye Mwenyezi Mungu amemteremshia kitabu cha sharia ambacho humo kuna hukmu za Mwenyezi Mungu na haddi zake, mfano: Adam, Ibrahim na Idris (a.s.) kama ilivyopokelewa katika tafsiri ya Aya tukufu “Sahifa za Ibrahim na Musa” (Al-A’laa: 19), katika Aya hii kuna 11 Al-Kafi, Jz: 1, uk: 175 Babu twabaqaatil Ambiyai wal Mursaliyna hadthi 13 12 Ilalu sharaiu Jz: 1, uk: 122 Babu 101 hadith 2
11
Page 11
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto ushahidi kwamba Ibrahim aliteremshiwa kitabu kinyume na anayedai hakuteremshiwa kitabu na suhfu umoja wake ni sahifah. Imepokewa kutoka kwa Abu Dharr kwamba amesema: “Nilisema, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, Manabii wako wangapi? Akasema: “Wako 124,000.” Nikasema: Ewe Mtume, na Mitume ni wangapi kati yao? Akasema: “Wako 313 na waliobaki ni Manabii.” Nikasema, Adam alikuwa Nabii? Akasema: “Ndio, Mwenyezi Mungu alimtereshia na amemuumba kwa uwezo wake ewe Abu Dharr, Manabii wanne ni Waarabu: Hud, Swaleh, Shuaib na Nabii wako.” Nikasema, Mwenyezi Mungu ameteremsha vitabu vingapi. Akasema: “Ameteremsha vitabu 104, 10 kwa Adam, kwa Shith 50, kwa Akhanukh naye ni Idris 30, naye ndio wa mwanzo kuandika, kwa Ibrahim 10, Torati, Injili, Zaburi na Qur’ani. Katika Hadith ni kwamba katika kitabu cha Ibrahim (a.s.) kulikuwa na “Inapasa kwa mwenye akili awe ni mwenye kuchunga ulimi wake, mwenye kujua zama yake, mwenye kukabili mambo yake, na inasemekana kuwa vitabu vyote vimeteremshwa katika mwezi wa Ramadhani, 13 na Torati kwa Musa14 13 Tafsiru Majmaul-Bayan, Jz. 10, Uk. 332 Suratul A’laa
14.Agano la Kale: ni jina mashuhuri la vitabu vya wayahudi na Torati ni sehemu tu katika agano la kale. “Torati” hutumika kwa vitabu vyote katika upande wa sehemu kupewa jina la jumla tu au kwa umuhimu wa torati na kunasibishwa kwake kwa Musa (a.s.) kwa sababu ni kati ya viongozi wakuu wa Bani Israil na kwake inaanzia historia yao halisi, na neno torati maana yake ni sharia au mafundisho ya dini na agano lake linatukuzwa kwa wayahudi na kwa manaswara ila vitabu vyake hawaafikiani, baadhi ya wachungaji wa kiyahudi huongeza vitabu wasivyovikubali wachungaji wengine na manaswara wana nakala ya kikatholiki inayozidi vitabu saba kwa nakala ya Kiprotestanti, na vinagawanyika vitabu vya agano la kale ambavyo wanavikubali waprotestanti sehemu tatu: Sehemu ya kwanza: Torati, nayo inajumuisha vitabu vya: Mwanzo, Kutoka, Mambo ya walawi, Hesabu, na Kumbukumbu la Torati, hivi ndivyo vinavyoitwa vitabu vya Musa. Kitabu cha kwanza: Mwanzo ni kitabu cha kuumba “Genesesis,” na kimeitwa kwa jina hili kwa sababu ya kujumuisha kwake kisa cha kuumba ulimwengu na binadamu wa mwanzo pia kinajumuisha kisa cha kosa alilolifanya baba wa wanadamu, kuteremshwa kwake ardhini kwa kuadhibiwa, maisha ya watoto wake na yaliyotokea baina yao, kisa cha tufani na kuenea watu baada ya hapo, kisa cha Ibrahim, safari zake na kizazi chake kwenda kwa Is’haq, Yaaqub na watoto wake na hasa Yusuf na yaliyomtokea hadi akawa na cheo kikubwa Misri na kuwaita baba yake na ndugu zake na kitabu hiki kinamalizikia na kifo cha Yusuf.
Inaendelea p.g 13
12
Page 12
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto Kitabu cha pili: ni Kutoka pia kinaitwa kwa kiyunani na kilatini “Exodus” yaani kutoka na kinaitwa hivyo kwa kuzungumzia kutoka kwa Bani Israil toka Misri, kitabu hiki kinaelezea kisa cha Bani Israil baada ya Yusufu na mateso waliyoyapata kwa Firauni, kudhihiri kwa Musa na kuwatoa Misri na hiki kinaendelea katika kisa cha historia ya Bani Israil hadi kuwafikisha mashariki ya Jordan, na katika kitabu hiki kuna amri kumi ambazo Mwenyezi Mungu alimpa Musa na humo kuna mas’ala mengi ya kisheria na mafunzo ya kidini hususan ya Yehova Mungu wa Bani Israil, wasifu wa hema, hekalu la makutano na tabuti la agano na yaliyotokea katika ghaiba ya Bani Israil. Kitabu cha tatu: Mambo ya walawi au wachungaji na kinaitwa kwa kilatini “Leviticus” kwa kunasibishwa na familia ya Lawiy au Lefiy kitabu hiki kimekusanya sharia, wasia na hukumu mfano: Kafara za dhambi, vyakula vilivyoharamishwa, ndoa zilizoharamishwa, sherehe, ibada, nadhiri na tohara, kama ambavyo kina mambo mengi yanayofungamana na ibada na amri za kidini ambazo zinampatia thawabu mwenye kuzifuata na adhabu kwa mwenye kuzikhalifu. Kitabu cha nne Hesabu: “Numeri” kimeitwa hivyo kwa sababu kimejaa hesabu na migawanyo ya koo za Bani Israil na kwayo zimepangwa daraja zao kulingana na koo na idadi ya wanaume kati yao na kwa ukuruba wa hesabu hii, kitabu hiki kimejumwisha kutembea kwa Bani Israil katika jangwa la Sinai na baada yake kwa hiyo ni mlolongo wa yaliyopokelewa kutoka katika kitabu cha Kutoka na humo kuna mafunzo ya kiibada, kikuhani, kijamii, utamaduni vilevile kuna maelezo ya vita vya Ban Israil dhidi ya Madayinina.
Kitabu cha tano Kumbukumbu la Torati: na maana yake ni kurudia na kukariri ili kuimarisha sharia na mafunzo na kwa kilatini inaitwa “Deuteronomim” yaani kurudia, katika kitabu hiki amri kumi zimeelezwa upya kama ambavyo yamerudiwa maelezo kuhusu vyakula vya halali na haramu, mfumo wa hukumu, na ufalme kwa Bani Israil, pia kitabu hiki kimezungumzia kuhusu Ukuhani na unabii kama ambavyo kimezungumzia kuhusu kuchaguliwa Yoshua bin Nun kuwa Khalifa wa Musa, kitabu hiki kinaishia kwa habari za kifo cha Musa na kuzikwa kwake katika mlima Moabu, tazama: Muqaranatul Adiyani Jz: 1, uk: 230 babu 4 maswadirul fikril yahud. Na inasemekana kuwa nakala mashuhuri kati ya Torati ni: Nakala ya kiibrania nayo ndio inazingatiwa na wayahudi, jopo la wachungaji wa kiprotestanti. Nakala ya kiyunani nayo ni ambayo ilikuwa kwa manaswara hadi karne ya kumi na tano nayo ndio yenye kuzingatiwa katika kanisa la kiyunani na makanisa ya mashariki. Nakala ya Samiriya nayo ni nakala ya kiebrania lakini ina vitabu saba, vitano vya Musa, kitabu cha Yoshua bin Nun na kitabu cha hukumu kwa sababu Samiriya hawatambui vitabu vingine. Na wachugaji wa kiprotestant wanasema: “Wayahudi wamepotosha nakala ya kiebrania na kuna ushahidi mwingi juu ya ikhitilafu zilizo wazi baina ya nakala tatu.” Amesema Dokta Ken: “Nakala za Agano la kale zilizopo zilikuwa zimeandikwa baina ya mwaka 1000 – 1400 na akatoa ushahidi kwa kusema: Hakika nakala zote ambazo ziliandikwa katika mwaka 700 au 800 ziliteketezwa kwa amri ya jopo la ushauri la kiyahudi kwa sababu zilikuwa zikikhalifu sana nakala ambazo zilikuwa zinategemewa kwao.” Warton amesema: “Hakika nakala ambayo imepita miaka 600 tangu iandikwe ni nadra kupatikana, ambayo imepita miaka 700 au 800 ni nadra sana kuipata.” Rejea Madkhalu Ilaa Dirasaati Al Adiyan wal Madhahib Jz. 1, uk.156 ya kiyahudi.
13
Page 13
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto na Injili ya Isa (a.s.).”15 15 Neno Injili “Gospels” ni neno la kiyunani maana yake ni “Pipi” nayo ni ambayo unampa anayekujia kwa habari njema, kisha ikakusudiwa bishara hasa, ama Isa alilitumia kwa maana ya “bishara ya ukombozi” ambayo amemletea mwanadamu na Mitume baada yake walilitumia kwa maana hiyo hiyo huenda pia wamelitumia kwa maana ya muhtasari wa mafunzo ya Isa (a.s.) kwa sababu humo kuna Ukombozi au sera ya maisha yake na kifo chake kwa sababu katika sera hii kuna maana ya ukombozi pia. Na Agano jipya “Injili” kati ya vitabu 27 tunaweza kuigawa katika sehemu tatu: 1. Sehemu ya vitabu vya historia: na sehemu hii inajumuisha Injili 4 Injili ya Mathayo, Marko, Luka na Injili ya Yohana, kama ambavyo inajumuisha nyaraka za matendo ya Mitume ambazo ameziandika Luka na vitabu hivi vitano vimeitwa vitabu vya historia kwa sababu vimekusanya visa vya kihistoria Injili ina kisa cha maisha ya Isa, historia yake, mawaidha yake, miujiza yake, na nyaraka za matendo ya mitume zina kisa cha mwalimu wa Ukristo na hasa Paulo. 2. Sehemu ya vitabu vya mafunzo na inajumuisha nyaraka 21 3. Ama sehemu ya tatu ni maneno ya Yohana ya kiungu na yanaitwa maono kwa sababu yanafanana na ndoto isipokuwa Yohana aliyaona akiwa macho na ufuatao ni muhtasari wa Injili zinazozingatiwa na wakristo: 1.Injili ya Mathayo: Mathayo ni mmoja wa wanafunzi wa Isa aliyefariki Ethiopia mwaka 79 ambapo aliifanya kuwa ni makazi ya mahubiri yake na wakristo wengi wanaafikiana kuwa Mathayo aliandika injili yake kwa lugha ya kiaramia lakini nakala ya kiaramia haipatikani, kitabu kilipatikana kwa lugha ya kiyunani na inasemekana kuwa tarjama ya Injili ya Mathayo mtarjumu hajulikani wala tarehe ya tarjama kama ambavyo haijulikani tarehe ya kuandikwa na inapopatikana shaka hii kwa kitabu chochote basi thamani yake inapungua au inakosekana kabisa. 2. Injili ya Marko: Marko ni kati ya wanafunzi waliozunguka katika miji akihubiri Ukristo kisha akaishi Misri na akauliwa mwaka 62, na haijulikani tarehe ya kuandikwa Injili hii kama ambavyo mwandishi wake ni mahala pa ikhitilafu, baadhi wanaona kuwa Marko ndiye aliyeiandika, wengine wanaona kuwa Petro mkuu wa wanafunzi na mwalimu wa Marko amekipokea kutoka kwa “Marko” na jambo hili lina mashaka, vipi mwalimu atapokea kutoka kwa mwanafunzi wake, lakini hivi ndivyo walivyosema baadhi ya wanahistoria wa kikristo kama vile Mwana wa Patric na imekuja katika kitabu cha “Murujul akhbari fiy tarajimil Abrar ” kwamba Marko na mwalimu wake Petro walikuwa wanapinga uungu wa Isa. 3. Injili ya Luka: Luka si miongoni mwa wanafunzi wa Yesu na wala si mwanafunzi wa wanafunzi wake,ila tu yeye ni mwanafunzi wa Paulo na hili limekaririwa kutajwa katika barua za Paulo.
4. Injili ya Yohana: Ameiandika Yohana mwanafunzi ambaye Isa alikuwa anampenda na kumteua. Na vitabu vingi nya kikristo vinatilia mkazo kuwa Injili hii lazima itakuwa imeandikwa na Yohana mwingine ambaye hana uhusiano na Yohana mfuasi, na imepokewa katika duru za maarifa-Encyclopedia ya - kiingereza: “Ama Injili ya Yohana hakuna shaka ni kitabu cha uzushi mwandishi wake anataka kuwapinga wanafunzi wawili wao kwa wao nao ni watakatifu wawili, Yohana na Mathayo, na mwandishi huyu mzushi amedai katika kitabu kuwa yeye ni mfuasi ambaye Isa anampenda, kanisa linachukulia sentensi hii kuwa ni alama na kuthibitisha kuwa mwandishi ni Yohana mfuasi wake jina lake katika kitabu pamoja na kwamba mwandishi wake sio Yohana kwa yakini kitabu hiki hakitofautiani na kuwa mfano wa baadhi ya vitabu vya Torati ambazo hazina uhusiano baina yake na baina ya vilivyonasibishwa kwake. Sisi tunawahurumia sana wale
14
Page 14
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto ambao wanajitolea juhudi zao ili kunasibisha walau kwa uongo huyo mtu mwanafalsafa ambaye ameandika kitabu hiki katika kizazi cha pili kinachomfuatia Yohana mwanafuzi. Hakika kazi yao inapotea bure kwa kukanganyikiwa kwao bila ya uongofu. Amesema mwandishi wa kimagharibi kufuatana na utafiti wake katika Injili yafuatayo: “Hakika falsafa ya kigiriki na kanuni ya kiromania imeifanya Injili isiwakilishe ukweli wake kama ambavyo wameathiri katika kuandikwa kwake, na mtafiti mwadilifu katika historia ya kanisa hawezi hata kwa upande mmoja kupinga kwamba rai za uongo, malengo potofu na madhumuni ya makosa yalikuwa ndio sababu ya msingi yaliyokuwa yakitawala, mara nyingi ndio yaliyoleta msukumo wa mabadiliko ambayo yalitokea katika Injili. Uchaguzi wa Injili nne na kuacha zingine umefanyika katika karne ya pili na kanisa liliposhindwa kuwajua waandishi halisi wa Injili limelazimika kusema yale yaliyopo leo katika makanisa. Wanahistoria waliobobea wanaona kuwa Injili zote zinategemea nakala ya Arimia iliotoweka; wanaashiria kwayo kwa herufi “k” muhtasari wa neno “Copel” kwa maana ya asili, na kati yao kuna wanaoita “lujiya” kwa maana ya kauli. Ama Injili zilizopo sasa zote zimeandikwa kwa lugha ya kiyunan na imezingatiwa katika tarjama maandishi ya kiarmiya, na rai zimeafikiana juu ya kutokukusanya kwake aliyoyasema Isa (a.s.), kama ambavyo makanisa yameafikana kutojua waandishi wa Injili, kama ambavyo pia zimeafikiana kwamba nakala mbili kati yake wameziandika wakristo wawili ambao hawajakutana na Isa na wala hawajasikia kutoka kwake. Utaratibu unaokubalika kwa wanahistoria ni kwamba Injili ya “Marko” ndio Injili ya mwanzo, kisha inafuatiwa na Injili ya Mathayo na Injili ya Luka, nazo ni Injili tatu ambazo ni mashuhuri kwa “Injili zinazokubaliwa” kwa kuafikiana yaliyomo humo miongoni mwa habari na wasia pamoja na kutofautiana mpangilio, kisha inafuatia Injili ya Yohana, hii ni ya nne. Injili ya Barnaba: Injili hii inaweza kuzingatiwa kuwa ni kiungo baina ya Ukristo na Uislamu ni kiungo kilichokosekana baina ya dini hizi mbili, kanisa haliitambui wala haliipi umuhimu wowote, imetarjumiwa kwa lugha ya kiarabu mwanzoni mwa karne ya ishirini na “Barnaba” ni mmoja wa wanafunzi kumi na wawili naye yuko katika safu ya kwanza kati ya wanafunzi wa Isa (a.s.), na jina lake limepokelewa mara nyingi katika nyaraka za matendo ya mitume, naye yuko katika mitume 70, Injili hii imetoweka na kupotea nakala yake, nayo ndio Injili iliyokusudiwa kuharamishwa na “Baba Julius wa kwanza”, nayo ni kati ya vitabu vilivyopigwa marufuku kusomwa. Ama sababu ya kutofautiana baina ya Injili hii na Injili nne maarufu ni:1.Hakika Yesu amekataa uungu wake na kuwa yeye ni mtoto wa mungu na hiyo ni mbele ya kundi kubwa. 2. Kwamba mtoto aliyetolewa na Ibrahim kuchinjwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ni Ismail na sio Is’haka. 3. Kwamba Masihi anayengojewa sio Yesu bali ni Muhammad. 4. Masihi hakusulubiwa, aliyesulubiwa ni Yahudha msaliti na ambaye alifanana naye, rejea: Muqaranatul Adiyan al masihiyah Jz: 2, uk: 174 Al-Maswadirul haqiqiyati lil’imu’utaqaadatil masihiyah.
15
Page 15
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto Kitabu cha Majusi ambacho kinaitwa “Jamasib” kama ilivyopokewa kutoka kwenye baadhi ya riwaya ambapo imepokewa kutoka kwa Imam AlBaqir (a.s.): “Na Majusi inachukuliwa jizya kutoka kwao kwa sababu Nabii (s.a.w.w.) amesema: “Wafanyieni kama mnavyowafanyia Ahlulkitab, walikuwa na Nabii jina lake ni Damisab, wakamuua na kitabu kinachoitwa Jamasib kilikuwa na kurasa 12,000 katika ngozi ya ng’ombe wakakichoma.”16 Na katika riwaya nyingine kutoka kwake (a.s.) amesema: “Jizya (kodi) inachukuliwa kutoka kwa Majusi. Nabii (s.a.w.w.) amesema: “Wafanyieni kama mnavyowafanyia Ahlul-kitab, walikuwa na Nabii jina lake ni Damasat, wakamuua na kitabu kinachoitwa Jamasat kilikuwa na kurasa 12,000 katika ngozi ya ng’ombe wakakichoma moto.”17 Na huenda jina hili “Jamasat” lilikuwa kulingana na lugha ya kiarabu ni: “Austa” kwa lugha isiyokuwa ya kiarabu.18 Na sehemu nyingine ni ambao hawajapewa kitabu bali unabii wao ulikuwa ni mwendelezo wa Nabii aliyetangulia kama vile manabii waliokuja baada ya Nabii Isa (a.s.), ambapo walikuwa wanafanya kazi kufuatana na aliyokuja nayo Isa (a.s.), na wanatumia mafundisho yake kisha hali hiyo ikaendelea hivyo hadi Mwenyezi Mungu alipomtuma mwisho wa manabii, Muhammad bin Abdillah (s.a.w.w.), ambaye kwaye na kwa Kitabu chake amehitimisha dini na vitabu na kuiteua Qur’ani kuwa ndio Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kanuni ya mbinguni, sharia na mfumo wa maisha ambao umejumuisha kila kitu, kama alivyosema Mwenyezi Mungu 16 Man laa yahudhuruhul faqihi Jz. 2, uk. 53 babul kharaji waljiziya Hadith 1678. 17 Wasailus shia J: 13 Uk: 127 babu 79 Hadith 20135 18 Wamekhitalifiana katika jina la la nabii wa majusi na jina la kitabu chao kwa maelezo ya ziada rejea Jawahirul kalami J: 21 Uk: 227 Rukuni thalithi fiy ahkami Ahlul al-dhimma. Wa Madinatul-ma’ajiz Jz. 8, uk. 191, Hadith ya 160 na nyinginezo.
16
Page 16
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto Mtukufu:
“Na (waonye) siku tutapowainua mashahidi katika kila umma, wakishuhudia kwa yanayotokana na wao, na tutakuleta wewe uwe shahidi juu ya hao. Na tumekuteremshia Kitabu hiki kinachobainisha kila kitu, na ni uongofu, na rehema, na ni bishara kwa Waislam19.SuratulNah’l: 89 Na baada yake walikuja Maimam watoharifu (a.s.) wanaendeleza njia ya Nabii kwa Kitabu kile kile, sharia ile ile, tabia na mwendo uleule. Imepokewa kutoka kwa Abu Ja’far kutoka kwa baba yake (a.s.) amesema: Mwenyezi Mungu hakutuma Nabii isipokuwa alimpa baadhi ya elimu, isipokuwa Nabii Muhammad (s.a.w.w.) kwani yeye alimpa elimu yote na akasema: “Huu ni ubainifu wa kila kitu”20 na akasema: “Na tukamwandikia (Musa) kila kitu katika ubao.”21 Na “Akasema mwenye elimu ya kitabu”22 na hakusema kuwa yeye ana elimu ya kitabu, na neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu hazimwendei kila mtu na akamwambia Muhammad (s.a.w.w.): “Kisha tukawarithisha kitabu wale ambao tumewateua kati ya waja wetu.”23 Hii ni elimu yote na sisi ni wateule, Nabii (s.a.w.w.) amesema: “Mola nizidishie elimu” nayo ni ziada ambayo tunayo kati ya elimu ambapo haikuwepo kwa yeyote katika mawasii wa Manabii wala kizazi cha Manabii wasiokuwa sisi, elimu hii tumefundishwa balaaya, na manaaya na hekima.”24 19 Suratul-Nah’l: 89 20 Surat Nah’l : 89 21 al A’araf; 7: 145. 22 Surat: Namli; 27: 40 23 Surat Fatir: 32 24 Tafsirul furatil al-Kufiy uk. 145; Suratul A’raf
17
Page 17
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto
QUR’ANI TUKUFU NA VITABU VINGINE VYA MBINGUNI Haifichikani kwamba vitabu muhimu sana vya mbinguni kati ya vitabu vya manabii (a.s.) ni Qur’ani tukufu. Kisha kati ya Qur’ani na vitabu vingine kunatofauti ya msingi, nayo ni kwamba: Vitabu vyao vilikuja katika zama maalum na wakati maalum, kwa sababu vilikuwa katika zama za maandalizi na katika nyakati za utangulizi, ili kuje dini kamilifu ya mbinguni. Hadi ulipokuja Uislamu pamoja na Qur’ani Tukufu, nayo ndio dini ya milele na mfumo wa daima wa maisha kama ilivyokuja kauli yake (s.w.t.): “Na anayetaka dini isiyokuwa ya kiislam basi hatokubaliwa nayo, na katika akhera atakuwa katika wenye hasara.”25 Ndio, hakika Qur’ani tukufu ni Kitabu kikamilifu na muujiza wa mbinguni wa daima ni muongozo wa viumbe wote, ni muongozo kwa watu wote, zama zote na sehemu zote, ni kanuni thabiti ya Mwenyezi Mungu na mfumo wa mbinguni wa milele katika ardhi hadi siku ya Kiyama na kwa ajili hiyo Qur’ani haikuashiria kuhifadhiwa vitabu vya mbinguni vilivyotangulia kutokana na upotovu na kupotoshwa wala kubaki kwake bila ya kugeuzwa na kubadilishwa bali kinyume chake Qur’ani tukufu imesema wazi kwamba vitabu hivyo vimepotoshwa na kubadilishwa, kwani Zaburi, Torati na Injili vyote vimepotoshwa kama inavyoashiria hilo kauli yake (s.w.t.): “Wanapotosha maneno katika mahala pake na wamesahau nafasi waliyokumbushwa kwayo.” anakusudia “Al Kalim” maneno ni wingi wa kalimatu “neno” na “katika sehemu zake” kupotosha maneno kuko namna mbili: Kufuta baadhi ya Torati na kuandika mahala pake kitu kingine, na aina nyingine ni kupotosha kwa kuifanyia taawili kwa maana isiyokusudiwa.26 Na kauli yake (s.w.t.): “Hatuzifuti Aya au kuisahaul25 Surat Aali-Imran; 3: 85 26 Tazama Taqribul Qur’an ilal-adhihaan Jz. 6, uk. 63 Suratul-Maida na kwa kwa maelezo ya ziada kuhusu kupotoshwa Torati na Injili rejea kitabu cha Al-Huda ilaa dinil Mustafaa, Rihlatil-madrasiyah na Tauhid wa tathilithi cha Sheikh Jawad Al-Balaghiy
18
Page 18
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto isha ila tunaleta iliyo bora zaidi au mfano wake, je hujajua kwamba Mwenyezi Mungu ni muweza wa kila kitu.”27 Na makusudio ya kauli yake (s.w.t.): “Tunaisahaulisha” yaani tunakiacha kitabu hadi kinatoweka, kupotea, kinamalizika na kinasahaulika kwa wanadamu na kufuta inatokea wakati kinapoletwa kilicho mfano wake, kwa sababu kinachofanana ni bora zaidi kuliko kilichofutwa na kusahaulika kwa mfano: Fedha ikikosa thamani mtawala analeta fedha nyingine mfano wa ile katika thamani kama ambavyo anaweza kuchukua dirham “fedha” kwa Zaid ili ampe dinar “dhahabu” na “hukujua” ewe myahudi mwenye kupinga kufuta “kwamba Mwenyezi Mungu ni muweza wa kila kitu” kwani wayahudi walikuwa wanashutumu kwamba inawezekanaje kufuta kitabu chao kwa Qur’ani na kwamba kama kitabu chao kinafaa kwa nini kifutwe na kama hakifai kwa nini Mwenyezi Mungu alikiteremsha? Jawabu: Kufutwa ama kunakuwa kwa sababu ya kutopatikana kilicho mfano wake au kilicho bora zaidi na ama kwa Mwenyezi Mungu kutokuwa na uwezo wa kufuta na mambo yote mawili hayapo, kilicho mfano wake na kilicho bora zaidi kipo na Mwenyezi Mungu ni muweza wa kila kitu.28 Hivyo tamko la mwisho na kamilifu la mbinguni kuja ardhini, na mfumo kamili unaotosheleza nyanja zote za maisha na mabadiliko ya zama ni Qur’ani, na Mwenyezi Mungu kwa utukufu Wake ametaka kuihifadhi na kuifanya ibakie bila ya uharibufu na kubadilishwa ambapo amesema: “Hakika sisi tumeteremsha ukumbusho na sisi tutauhifadhi.”29 Qur’ani imeitwa ukumbusho kwa sababu inamkumbusha mwanadamu itikadi na mfumo katika yale ambayo ni maumbile yake, isipokuwa amekwisha yasahau “na hakika sisi tutauhifadhi” kutokana na upotovu, kubadilishwa, kuongezwa na kupunguzwa. Na ambacho naitakidi kuwa kimeafiki27 Suratul Baqara; 2: 106 28 Taqribul Qur’an ilal-adhihaan, Jz: 1, uk: 108; Suratul Baqarah 29 Suratul Hijr: 9 19
Page 19
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto wa na wengi kati ya maulamaa wetu wema ni kwamba Qur’ani tuliyonayo ndio ileile iliyoteremshwa bila ya kupungua au kubadilishwa, Aya na Sura zimepangwa kama alivyoamuru Mtume (s.a.w.w.) ingawa kushuka kwake kunatofautiana, na Mtume hakufanya hivyo isipokuwa kwa amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Hatamki kwa matamanio yake bali ni wahyi unaofunuliwa.” 30 Na hivi ndivyo ilivyokuwa itikadi ya mzazi wangu kama alivyoitaja katika toleo la “Ajiwibatul masailud-Diyniya” la Karbala na baadhi yake katika mwanzo wa toleo la “Akhlaqu wal-adab” la Karbala katika tafsiri ya Sura ya Al-Hamdu na baadhi ya Sura ya Baqara.31
WASIA WA MTUKUFU MTUME (SAWW) KUHUSU QUR’ANI NA KIZAZI CHAKE Mtume wa Uislamu ameusia juu ya Qur’ani tukufu na ameamuru kushikamana nayo na kuifanyia kazi kama mfumo wa kudumu unaofuatwa na watu wote hadi Siku ya Kiyama kama ambavyo ameusia juu ya Ahlul-Bayt wake, na akaamuru kushikamana na mwendo wao na kuwatii kwani wao ndio wafasiri wanaojua yale ambayo Qur’ani imekuja nayo kati ya hukumu na mafunzo, amesema Mtume (s.a.w.w.): “Hakika mimi ninawaachieni vitu vizito viwili kama mtashikamana navyo kamwe hamtapotea baada yangu, kimojawapo ni kitukufu zaidi kuliko kingine. nacho ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu, kamba inayotoka mbinguni hadi ardhini, na kizazi changu, watu wa nyumba yangu, viwili hivyo havitotengana hadi vitakaponifikia katika hodhi “birika” tazameni namna gani mtanifuata katika kizazi changu.”32 30 An-Najim: 3 – 4 31 Taqribul Qur’ani ilal-adhihaan J. 14, uk. 19; Suratul-Hijri 32 At-Taraif, Juz.1, uk. 115 Hadithu Thaqalayn 175
20
Page 20
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto Kwa hiyo mfumo wa Uislamu ndio wenye kutawala hadi Siku ya Kiyama, halali ya Muhammad ni halali hadi Siku ya Kiyama, na haramu yake ni haramu hadi Siku ya Kiyama. Imepokewa katika Hadithi tukufu kutoka kwa Imam Sadiq (a.s.) kwamba amesema: “Hakika Mwenyezi Mungu amemtuma Muhammad kuwa Nabii hivyo hakuna Nabii baada yake amemteremshia Kitabu akahitimisha kwacho hakuna tena kitabu baada yake, amehalalisha humo halali yake na akaharamisha humo haramu yake, hivyo halali yake ni halali hadi Siku ya Kiyama na haramu yake ni haramu hadi Siku ya Kiyama, humo ameeleza yaliyokuwa kabla yenu na amefafanua yaliyopo baina yenu, kisha akaashiria kwa mkono wake katika kifua chake akasema: “ Sisi tunaijua.”33 Imepokewa kutoka kwa Abu Muhammad Al-Askari (a.s.) kwamba amesema: “Makuraishi na wayahudi ambacho wamesema uongo juu ya Qur’ani wamesema: Ni uchawi ulio wazi ameuzua.” Mwenyezi Mungu akasema: “Alif lam miym hiki ni kitabu”34 Yaani Ewe Muhammad, Kitabu hiki tumekiteremsha kwako ni katika herufi moja moja ambazo ni Alif, lam, miym na kwa lugha yenu na herufi zenu za Hijai basi leteni mfano wake ikiwa nyinyi ni wakweli na saidianeni juu ya hilo na baadhi yenu kisha ikabainisha kwamba wao hawatoweza hilo kwa kusema: “Sema kama watakusanyika majini na wanadamu ili walete mfano wa hii Qur’ani hawatoleta mfano wake hata kama watasaidiana wao kwa wao.”35 Kisha akasema Mwenyezi Mungu mtukufu: “Alif lam miym” yaani Qur’ani ambayo imeanza na Alif lam miym ni “kitabu hiki” ambacho Musa ametoa habari kwacho na Manabii waliokuja baada yake, waliwapa habari Bani Israil kwamba mimi nitakiteremsha kwako Ewe Muhammad kitabu 33 Kashful Ghumma: Jz. 2, uk:197, amemtaja Imam wa sita Jafar bin Muhammad Al Baqara: 1-2 34 Suratul-Baqara: 1-2 35 Suratul Israi: 88 - 89
21
Page 21
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto kitukufu ambacho “hakipatwi na batili kimeteremshwa kutoka kwa Mwenye hekima Mtukufu”36, “hakuna shaka ndani yake humo”37 hakuna shaka katika kudhihirika kwake kwao kama walivyowapa habari Manabii wao kwamba Muhammad atateremshiwa kitabu ambacho kwamba hakitopatwa na batili; atakisoma yeye na umma wake katika hali zao zote, “uongofu” ni ubainifu kutokana na upotofu “kwa wachamungu” ambao wanaogopa madhambi na wanaogopa kutawalisha ujinga katika nafsi zao wanapojua yale yaliyo wajibu kwao kuyajua wanafanya yale ambayo humo kuna ridhaa ya Mola wao, amesema: Amesema Imam Swadiq (a.s.) kisha Alif ni herufi katika kauli yako “Allah” imeashiria Alif na kauli yako lam inaonyesha Al-Malkul-adhim “Mfalme mkuu muweza kwa viumbe vyake vyote” na miym inaonyesha kuwa yeye ni Majiydu Hamiydu “Mtukufu, mwenye kuhimidiwa” katika vitendo vyake vyote. Na akaifanya kauli hii kuwa ni hoja kwa wayahudi na hiyo ni pale Mwenyezi Mungu alipomtuma Musa bin Imran kisha baada yake Manabii katika Bani Israil hawakuwepo na kaumu isipokuwa walichukua ahadi kwao na mafungamano kwamba; watamwamini Muhammad, Nabii wa Kiarabu atakayetumwa katika mji wa Makka, ambaye atahamia Madina na atakuja na kitabu ambacho herufi zake ni herufi za hijai ndio ufunguzi wa Sura zake, umma wake watakihifadhi watakisoma katika hali zote kwa kusimama, kukaa na kutembea. Mwenyezi Mungu atafanya wepesi katika kukihifadhi kwao na watamwambatanisha Muhammad (s.a.w.w.) na ndugu yake wasii wake Ali bin Abi Twalib (a.s.) mwenye kuchukua elimu yake ambaye amemfundisha na mwenye kushikamana na uaminifu wake ambao amemfundisha mwenye kumdhalilisha kila mwenye kumpinga kwa upanga wake na mwenye kumshinda kila anayejadiliana naye kwa hoja yenye nguvu na atapambana na waja wa Mwenyezi Mungu kwa kitabu cha Mwenyezi Mungu mpaka awaongoe kwa kukubali kwa hiyari au kwa kulazimishwa, kisha 36 Suratu Fuswilat: 42 37 Suratul Baqara; 2: 12
22
Page 22
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto Muhammad (s.a.w.w.) akienda kwa Mola wake na wengi kuritadi kati ya wale waliodhihirisha imani wakapotosha taawili zake na wakabadilisha maana zake wakaziweka pasipo mahala pake atawapiga vita kwa kuwa mbali na taawili yake ili Iblisi mwenye kuwapotosha awe ni mwenye hasara, dhalili, mwenye kufukuzwa na mwenye kushindwa. Akasema Mwenyezi Mungu alipomtuma Muhammad akamdhihirisha Makka kisha akahamia Madina na akampa ushindi huko kisha akamteremshia kitabu akafanya ufunguzi wa Sura yake kuwa ni Alif lam miym yaani “Alif lam miym - hiki ni kitabu” nacho ni kile kitabu ambacho manabii wangu waliotangulia walitoa habari kwamba mimi nitakiteremsha kwako ewe Muhammad “hakina shaka ndani yake” kimeshadhihiri kama walivyowapa habari manabii wao kwamba Muhammad atateremshiwa kitabu kitukufu chenye baraka hakitopatwa na batili atakisoma yeye na umma wake katika hali zao zote kisha wayahudi watapotosha mwelekeo kutoka kwake na kufanya taawili kwa upande usiokuwa wake, na watasaidiana kufikia elimu ambayo Mwenyezi Mungu ameshaifunga kwao juu ya muda wa umma huu na muda wa utume wake. Lilikuja kundi kati yao kwa Mtume, Mtume akamwacha Ali azungumze nao, akasema msemaji wao: “Hakika kama anayoyasema Muhammad ni ya kweli basi tumeshajua muda wa ufalme wa umma wake ni miaka 71, alif ni moja lam ni thelathini na miym ni arobaini. Ali (a.s.) akasema: “Mtafanyaje katika ‘Alif lam miym swad’38 nayo imeteremshwa kwake?” Wakasema: “Hii ni miaka 161.” Ali akasema: “Mtafanyaje kwa Alif lam raa 39 nayo imeteremshwa kwake.” Wakasema hii ni zaidi ni miaka 231.” Ali akasema: “Mtasemaje kwa yaliyoteremshwa “Alaf lam miym raa.”40 38 Suratul A ‘Araf: 1 39 Suratu Yunus: 1 40 Suratu Raad: 1 23
Page 23
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto Wakasema: “Hii ni miaka 271.” Ali akasema: “Moja kati ya hii ni yake au yote ni yake?” Maneno yao yakatofautiana, baadhi yao wakasema ana moja kati ya hiyo; na wengine wakasema bali ni yake yote; hivyo ni miaka 704, kisha ufalme utarejea kwetu yaani kwa wayahudi.” Ali akasema: “Ni kitabu kati ya vitabu vya Mwenyezi Mungu vimesema hivyo au ni rai zenu ndio zinasema hivyo?” Baadhi wakasema: Kitabu kimesema hayo; na wengine wakasema bali ni rai zetu ndio zimesema hayo. Ali akasema: “Leteni kitabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu kinacho sema hivyo.” Wakashindwa kuleta, akawaambia wengine: “Tuonyesheni ushahihi wa rai hii.” Wakasema: “Usahihi wa rai yetu ni hoja yake, hii hesabu ya sentensi.” Ali akasema: “Vipi imeonyesha juu ya mnayoyasema? Katika herufi hizi hakuna isipokuwa rai mliyoisema bila ya ubainifu. Mtaonaje kama mtaambiwa kuwa hesabu haionyeshi muda wa ufamle wa umma wa Muhammad (s.a.w.w.), lakini kila mmoja wenu amelaaniwa kwa idadi ya hesabu hii, au kwa idadi hiyo kila mmoja kati yetu na yenu kwa idadi ya hesabu hiyo ana dinar, au dirham, au Ali anamdai kila mmoja wenu katika mali yake mfano wa hesabu hii?” Wakasema: “Ewe Abul Hasan hakuna kitu kati ya uliyoyataja kimezungumzwa katika Alif lam miym, Alif lam miym swad, Alif lam raa na Alif lam miym raa, kama kauli yetu itabatikilika katika tuliyoyasema yako pia itabatilika katika uliyoyasema.” Msemaji wao akasema: “Usifurahi ewe Ali kama tutashindwa kusimamisha hoja kwa yale unayoyasema juu ya madai yetu, ni ipi basi hoja yako juu ya madai yako? Ila kufanya hoja yako kuwa ni kushindwa kwetu, sisi hatuna hoja katika tunayosema wala nyinyi hamna hoja katika mnayosema.” Ali akasema: Sio kweli, hakika sisi tuna hoja, nayo ni muujiza wenye kushangaza.” Kisha akawaita ngamia wa wayahudi: “Enyi ngamia shuhudieni kwa Muhammad na wasii wake.” 24
Page 24
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto Ngamia wakaanza kushuhudia: “Umesema kweli ewe wasii wa Muhammad, wamesema uongo hawa wayahudi.” Ali (a s) akasema: “Enyi nguo za wayahudi, shuhudieni kwa Muhammad na wasii wake, nguo zao zote zikatamka: “Umesema kweli umesema kweli ewe Ali tunashuhudia kwamba Muhammad ni Mtume wa haki na hakika wewe; ewe Ali, ni wasii wake wa haki. Muhammad hajapata fadhila ila na wewe umepata mfano wake. Nyinyi ndugu wawili ni kati ya nuru bora za Mwenyezi Mungu, ni utukufu wenu nyinyi wawili na nyinyi katika fadhila mnashirikiana isipokuwa hakuna Nabii baada ya Muhammad (s.a.w.w.).” Hapo huyo myahudi akanyamaza na baadhi yao wakamwamini Mtume papohapo. Chuki ikazidi kwa baadhi yao na kwa wayahudi wengine, hivyo Mwenyezi Mungu akasema: “Hakina shaka ndani yake” na kwamba ni kama alivyosema Muhammad (s.a.w.w.) na wasii wa Muhammad, kutoka katika kauli ya Muhammad (s.a.w.w.), kutoka katika kauli ya Mola wa walimwengu, kisha akasema: “ni uongofu” ubainifu na ponyo “kwa wale wachamungu” katika wafuasi wa Muhammad na Ali, hakika wao wameogopa aina za ukafiri, hivyo wakaziacha na wameziogopa dhambi wakazipinga, wameogopa kudhihirisha siri za Mwenyezi Mungu na siri za wema kati ya waja na mawasii baada ya Muhammad (s.a.w.w.), hivyo wakazificha. Na wameogopa kuficha elimu kwa watu wake wanaostahiki na kwao wameisambaza.41 Ndio hakika Qur’ani tukufu na kizazi kitukufu ni vizito viwili ambavyo aliviacha Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) katika umma wake, na Mwenyezi Mungu Mtukufu ameshatoa changamoto kwayo kwa watu wote, hivyo haiwezekani kwa yeyote kuleta mfano wa Qur’ani wala mfano wa Ahlul-Bayt (a.s.).
41 Biharul Anwar, Jz. 89, uk. 377 Babu 127 hadith 10
25
Page 25
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto
MUUJIZA WA QUR’ANI Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
“Haikuwa hii Qur’ani ni yenye kuzuliwa pasipo kutoka kwa Mwenyezi Mungu; lakini ni ukweli ambao uko mikononi mwake na ufafanuzi, ni Kitabu kisicho na shaka ndani yake kutoka kwa Mola wa walimwengu, au wanasema amekizua, sema, basi leteni Sura mfano wake na waiteni muwezao wasiokuwa Mwenyezi Mungu kama nyinyi ni wa kweli, bali wao wamesema uongo kwa yale wasiyoyajua na wala haijawajia taawili yake, vivyo hivyo walisema uongo waliokuwa kabla yao, tazama ulikuwaje mwisho wa madhalimu.” Suratu Yunus: 37 - 39 Qur’ani tukufu tangu mwanzo wa kushuka kwake ni Kitabu cha muujiza, kinatoa changamoto kwa wanadamu hadi Siku ya Kiyama walete angalau Sura moja tu mfano wake, na imeendelea hivyo hadi leo hii, na itabaki hivyo. Ni muujiza wa milele na wala sio kama miujiza mingine inayodhihiri muda baada ya muda mwingine, kisha inatoweka. Na wala sio kama uvumbuzi ambao unakuja kwa muda kisha kinakuja kitu kingine ambacho ni bora zaidi yake. Mfano: Wamarekani walipovumbua mashine ya hesabu, mwanzo lilikuwa ni jambo la kushangaza lakini baada ya muda mchache wajapani wakavumbua mashine ya hesabu bora zaidi kuliko mashine ya hesabu ya wamarekani. Vivyo hivyo, ulimwengu leo unashindana katika nyanja hii ili 26
Page 26
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto kuleta kilicho bora zaidi, na kisha kinapokuja kitu kipya, huwa kinatofautiana na kilichotangulia kwa sifa, umaridadi na ukisasa unafanya kilichotangulia kuwa duni kwa kilicho kipya. Bomu la Atomiki alipolivumbua mtaalamu wa kijerumani, kilikuwa ni kitu cha ajabu katika wakati wake, baadae wakatengeneza bomu la Haidrojeni, ambalo ni hatari zaidi kuliko bomu la Atomiki na baada ya hapo wakatengeneza bomu la Nitrojeni.42 42 Jaribio la kwanza la bomu la nyuklia lilianza mwaka 1945 katika jangwa la New Mexco Amerika, na fikra ya bomu la nyuklia inategemea mchanganyiko wa madini ya “Urenium 235” au “Protonium 239” bila ya msaada wa Neutron. Kwa kuanza msuguano wa mfululizo zikichukuliwa kilogram 4 – 8 za madini haya kisha yakapata mbinyo wa ghafla kwa muda mchache, inafikia vijisehemu milioni kwa sekunde, kwani mkusanyiko wake umesinyaa katika sehemu ndogondogo, unatokea myeyuko otomatiki, na inatokea nguvu kubwa inayotosha kuzaa mlipuko unaoweza kulipua madini ya “TNT” yenye mlipuko mkali zaidi. Bomu la nyuklia la kwanza, ambalo lilitupwa katika mji wa Heroshima wa Japani wakati wa vita kuu ya pili ya dunia, lilikuwa na uwezo wakuteketeza tani 20,000 za madini ya “TNT” na mabomu haya hutumiwa kama silaha ya kushambulia sehemu kubwa kama vile miji, ama bomu la Hydrogen mlipuko wake unazidi mlipuko wa bomu la Atomic mara mia moja hadi elfu moja, na bomu la Hydrogen hutiwa joto kwa sababu mchemko wa nyuklia ni mchanganyiko wa mchemko wa nyuklia, hauanzi isipokuwa kiwango cha joto kinapofikia kiasi cha joto daraja la juu kabisa, na ambacho hufanya mchemko huu uendelee hadi umalizike huu. Ni kwamba mchemko huu wenyewe unazidisha joto. Aina ya mwisho ya bomu la “Nitrogen” ni bomu dogo la Hydrogen isipokuwa muundo wake na athari yake inatofautiana na bomu la Hydrogen ambapo mwingi kati ya mlipuko wa bomu la nitrogen unakuwa kwa mionzi ya nitrogen unaounguza viwiliwili hai na kusababisha kifo chake mara moja, wakati ambapo huathiri katika asili kinyume na aina zingin,e na kuna bomu la kikemia nayo ni kutumia mada za sumu katika vita kwa lengo la kuuwa au kuharibu wanadamu, wanyama na kuleta madhara kwa mimea kwa kuvuta hewa au kwa kula au kwa kugusa kwake kwa kuingia sumu hii katika mwili. Sumu hii wakati mwingine inakuwa ni gesi au rojorojo inayoyeyuka na kugeuka kuwa moshi kwa haraka, na mara chache huwa ni kitu kigumu. Na kati ya mada za sumu zilizotumiwa katika vita kuu vya kwanza vya dunia ni gesi ya khardali, siyndi ya hydrogen. Ama katika wakati huu kuna aina nyingi baadhi yake zinaziba pumzi, zingine zinatia sumu katika damu na kutoa machozi, gesi ya kutapisha, sumu ya halusaa na gesi ya mishipa. Na kuna bomu la baiolojia ambapo uhatari wake ni kutumia vijidudu au sumu yake katika vita, navyo ni viumbe hai havionekani kwa macho bali kwa darubini inayokuza umbo lake, na mfano wake ni bakteria na fitriyat na kati ya vinavyozidisha hatari ya silaha ya baiolojia ni kwamba unaweza kubadilisha sifa maalumu ya mazingira, mfano kubadilisha kinga na umbo la vijidudu kama ambavyo kutumia mchanganyiko wa aina mbali mbali za vijidudu kunavyozidisha hatari ya silaha hii, ambapo inakuwa vigumu kujua maradhi yake, na silaha ya baiolojia inaweza kusambazwa kwa umbo la Ukungu wa moshi, kwa kuwekwa katika risasi, au kwa kurushwa moja kwa moja kutoka katika chombo cha kufyatulia kwa njia ya ndege, kama ambavyo inaweza kusambazwa kwa njia ya kunyunyizwa katika chakula au kinywaji kwa vijidudu au kwa njia ya kuumwa na wadudu wanaobeba vijidudu hivyo.
27
Page 27
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto Vivyo hivyo katika ulimwengu wa nadharia za kielimu, kitabibu, kiuchumi n.k, kati ya elimu zingine hakika zinakua kila siku, na wataalamu wanakuja na kitu kipya na nadharia bora. Hivyo kila uvumbuzi mpya unafuta uliotangulia kati ya uvumbuzi, vivyo hivyo nadharia mpya inaondoa nadharia ya zamani isipokuwa Qur’ani; kwani yenyewe daima ni mpya haichakai wala kumalizika, hadi siku ya Kiyama na yeyote hataweza kuleta mfano wake itawezekanaje kuleta kilichobora zaidi yake? Ndio, Qur’ani tukufu imebakia kuwa mpya haichakai wala haimaliziki, vyovyote muda utakavyorefuka na zama kuwa ndefu, kwa sababu ni muujiza mkuu wa milele. Viumbe wote wa mwanzo na wajao kati ya wanadamu na majini hata kama watasaidiana na baadhi yao, hawatoweza kuleta changamoto katika Qur’ani tukufu, hawatoleta mfano wake wala hawatoondoa utukufu wake na muujiza wake kwa kupotosha na kuharibu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
“Sema, kama watakusanyika wanadamu na majini ili walete mfano wa hii Qur’ani, hawataleta mfano wake hata kama watasaidiana wao kwa wao,” na “na tumetoa kila mfano katika hii Qur’ani lakini watu wengi wamekataa isipokuwa ukafiri.”Suratul Israi: 88 - 89
28
Page 28
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto
QUR’ANI INATOA CHANGAMOTO KWA WOTE Hakika Qur’ani ni muujiza katika pande zote na nyanja zote, vipi isiwe hivyo na ilihali ni muujiza wa Mwenyezi Mungu wa milele, na muujiza uko wazi hauhitaji dalili na hoja, muujiza uko wazi katika kila tamko kati ya matamshi yake, na katika kila maana kati ya maana zake, mvuto katika ubainifu wake na fasihi yake, mvuto katika mfumo wake na mtiririko wake, mvuto katika kila kitu na muujiza wake umo humo. Ndio hakika kati ya muujiza wa Qur’ani ni mshangao wa kila anayeisoma au kuisikia naye anafahamu lugha ya kiarabu, na hiyo ni kila wakati na kila sehemu na kwa kiwango chochote kile, muujiza wa Qur’ani ni muujiza unaoendelea kuwa mpya milele, umewashangaza wanafasihi, na watu wote wa balagha na maulamaa wote wa fasihi, umestaajabisha fikra zao, umetatiza akili zao umewashangaza werevu wao na nyoyo zao. Ndio, Qur’ani imetoa changamoto tangu mwanzo wa kuteremka kwake na changamoto hii imebakia kama ilivyokuwa hadi leo hii, hajaweza mtu yeyote kukabiliana nayo, na hilo kama litaashiria jambo, basi linaonyesha kudumu muujiza wa Qur’ani milele ambapo haujawashangaza waarabu tangu mwanzo wa kushuka kwake tu, bali umewastaajabisha watu katika kila mji na kila zama, na wamebakia katika mshangao bila ya kuweza chochote katika kukabiliana nayo na hali wao wanaisikia aya ya changamoto.
29
Page 29
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto
AYA YA CHANGAMOTO Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
“Sema, kama watajikusanya wanadamu na majini ili walete mfano wa hii Qur’an hawataleta mfano wake hata kama watasaidiana wao kwa wao, na tumetoa kila mfano katika hii Qur’ani lakini watu wengi wamekataa ila ukafiri.” Suratul Israi: 88 -89 Qur’ani sio maneno ya kawaida anayoweza kila mtu kuleta mfano wake kwa kauli yake (s.w.t.): “Sema, yaani Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, kwa hawa “kama wanadamu na majini watajikusanya kwa kusaidiana wao kwa wao ili walete mfano wa hii Qur’ani”kwa sifa zao zote za balagha, mfumo wa kielimu na sifa zingine zinazopatikana katika muujiza katika vitabu vya elimu ya mantiki “hawataleta mfano wake” kwa sababu iko nje ya upeo wao na uwezo wao “hata kama baadhi watasaidiana na baadhi” yaani wakisaidiana wao kwa wao. Qur’ani imeshatimiza miaka elfu moja mia nne na zaidi na hajatokeza mwenye kuleta mfano wa hii Qur’ani, ndio alikuja Musailamah kwa kichekesho kama vile “wanisaa dhatul furuuj” na Papa alileta yanayoliza kwa kusema: “Innaa jaalika khauswana khawiswa lilikhawiswiyna.” Ama mwanafalsafa mkongwe kati ya washirikina alifikiri na akaamua kisha akasema: “Hii si kingine bali ni uchawi wenye kuathiri.”
30
Page 30
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto Kama ambavyo hajaleta yeyote mfano wa fimbo ya Musa, Isa kuhuisha wafu, tufani ya Nuh, vivyo hivyo hajaja yeyote na mfano wa Qur’ani ya Muhammad (s.a.w.w.) na “tumeshatoa kila mfano katika hii Qur’ani” ubainifu kwa watu na tumeleta mifano mbali mbali na aina tofauti “watu wengi wamekataa isipokuwa ukafiri” yaani kukanusha haki pamoja na kwamba hoja imeshatimia kwao. Hakika Mwenyezi Mungu amempa mwanadamu Qur’ani muujiza kwa Mtume (s.a.w.w.) na mfano wa maisha mema na neno lenye kubakia kwayo watu wamepata nuru na kuongoka katika njia lakini makafiri wao wamekataa isipokuwa kukanusha na kung’ang’ania ukaidi wameifumbia macho na wakawa wanataka miujiza ya kimada kuwanufaisha katika maisha wala haibakii pamoja na vizazi bali wameitaka kwa ukaidi baada ya kuwadhihirikia hoja43 Ndio, imeshapita katika changamoto hii miaka elfu moja na mia nne na zaidi bado ipo inaelea katika anga inapenya katika masikio na viumbe vyote vinasikia changamoto hii vinanyenyekea, vimesalimu amri, na kutii kwa udhalili na kushindwa havinabudi kutii na kujisalimisha kwayo. Hii haifichikani kwamba wenye kuelewa zaidi na kufahamu muujiza wa Qur’ani tukufu ni maulamaa, watu wabalagha na fasihi wanafikira wanapolinganisha baina yake na maneno ya viumbe wanasema: “Udongo na nyota ni wapi na wapi”44
43 Taqriybul Qur’ani ilaa liadhihan Jz.15, Uk. 86, Suratul Israi 44 Thuraa: Ni mchanga nao ni ambao uko juu ya ardhi kama si hivyo basi ni udongo. Majmaul Bahrayni Jz. 1, uk: 73 Maddatu tharaa Na thuraya: Ni miongoni mwa sayari imeitwa hivyo kwa wingi wa mwanga wake na inasemekana imeitwa hivyo kutokana na wingi wa sayari zake pamoja na udogo wa mwanga wake inasemekana kuwa ni nyota ambayo ni tharuwa, na kutokana na kudhihiri sana mwanga wake kwake sayari nyingi hazionekani. Tazama Lisanul Arab Jz. 14, uk. 112 maddatu thuraya na Majmaul bahrayni Jz. 1 uk. 73 Maddatu tharaa 31
Page 31
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto Ndio, Waarabu walioishi wakati wa kushuka Qur’ani, pamoja na balagha na fasihi waliokuwa nayo, walijiona kuwa hawana uwezo mbele ya Qur’ani tukufu, tangu mwanzo wa kudhihiri Qur’ani na wakapata yakini kwamba wao kamwe hawataweza kuleta mfano wa hii Qur’ani, na sio tu mfano wa Qur’ani bali hata kuleta Sura moja mfano wa Qur’ani tukufu na Mwenyezi Mungu amesema:
“Kama mna shaka kwa yale tuliyoyateremsha kwa mja wetu basi leteni Sura moja mfano wake.” Suratul Baqara: 23 Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Aya nyingine:
“Wanasema ameizua; basi leteni Sura moja mfano wake” Suratu Yunus: 38 Ni maarufu kwamba katika Qur’ani kuna Sura ndefu na fupi, fupi kati yake kuna ambazo zina mstari mmoja tu, mfano wa Suratul Ikhlas, Suratul Kawthar kama ilivyo katika kauli yake (s.w.t.): “Bisimillahi Rahmani Rahiym, Innaa a’twainakal kawthara, faswalili Rabbika wan har inna shaanika huwal abtar.”45
45 Suratul Kawthar: 1 -3 32
Page 32
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto
NABII ANAONYA KAUMU YAKE Hakika Mtume wa Uislamu Muhammad bin Abdillah (s.a.w.w.) alikuwa ni mtukufu wa makuraishi kwa nasaba na kabila, alitokana na kabila la Bani Hashim ambalo watu wake wanajulikana kwamba wao ni mabwana wa Makka lakini pamoja na utukufu na cheo hicho hawakuwa ni wenye pato na utajiri wala wenye mali na ardhi, na tabia ya jamii hiyo ya ukabila aliyokuwa anaishi humo Mtume (s.a.w.w.) ni jamii yenye muamala mgumu haiamini isipokuwa misingi ya kimaada na haithamini isipokuwa mali na utajiri. Katika jamii hii ngumu yenye muamala mbaya, Mtume (s.a.w.w.) alitangaza muujiza wa milele, Qur’ani tukufu na akawalingania kwenye kuiamini lakini makuraishi wakakuta nafsi zao zinashindwa kuelewa Qur’ani na utukufu wake. Qur’ani imewapa changamoto kwa kitu ambacho ni balagha na fasihi, wakaikabili kwa uadui na wakamwandama kwa hila za tuhuma na kujaribu kwa kila njia kuzima nuru yake, na kufuta athari yake kwa ukaidi na ufedhuli. Na ukaidi na ufedhuli huo kutoka kwao ulikuwa kwa sababu wao waliposikiliza Qur’ani wakajua ukweli wa muujiza wake, na wakapata yakini ya utukufu wa ubainifu wake, na muujiza wa balagha yake, wakajisalimisha mbele ya changamoto yake na wakakiri udhalili wa kushindwa kwao katika kukabiliana nayo, lakini pamoja na hayo hawakuiamini.
33
Page 33
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto
AINA ZA TAWALA KATIKA ZAMA ZA NABII (S.A.W.W.) Katika kubainisha msimamo aliouchukua Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) kwa makuraishi na tawala zao wakati ule hakuna budi kuzungumzia kwa kifupi aina za tawala: 1 - Tawala za kidikiteta: Nazo ni ambazo zinajengeka katika udikiteta wa mtawala, mtu mmoja anahukumu kwa mabavu au kwa mapinduzi ya kijeshi au kwa kurithi au kwa njia zingine za udikiteta ambazo madikiteta wanazifuata ili kufikia katika utawala, naye hutumia kanuni kama mtumishi wa malengo yake bila ya kuwa mtumishi wa haki, malengo matukufu na kulinda wananchi. 2 – Tawala za kikabila: Nazo ni ambazo zinajulikana kama utawala za kibwanyenye, kama tukijaalia kuwa katika nchi kuna makabila mengi na kila kabila lina kiongozi, hawa viongozi wanakaa sehemu maalumu katika nchi na wanahukumu baina yao, hakuna bunge, Rais wa nchi wala kiongozi anayehukumu bali wanahukumu hawa viongozi wa makabila au koo, na nyinginezo kati ya aina za tawala.46
46 Rejea Fiqhi Siyasah uk: 276 mas’ala 29 juu ya aina za tawala 34
Page 34
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto
NABII (S.A.W.W.) NA AL-WALID BIN MUGHIRA Utawala wa Makka ulikuwa ni wa mamwinyi humo kulikuwa na koo arobaini kubwa na ndogo, kila moja kati yake kuna mkuu, hawa wakuu wanakusanyika sehemu maalum inayoitwa “Darun-Naduwah.”47 Na kati ya wakuu hawa kulikuwa na mwanaume anayeitwa Al-Walid bin Al47 Nayo ni nyumba aliyoijenga Qusay bin Kilab bin Murrah hapo Makka pembezoni mwa Al-Ka’aba tukufu alipojenga upya Al-Ka’aba katika karne ya pili kabla ya hijira, na makuraishi walikuwa wanakusanyika humo kwa ajili ya mashauriano, utawala na kutoa hukumu. Hivyo ilikuwa haolewi mwanamke wala hakiundwi kikosi, haonywi kijana wala hakanywi kijakazi isipokuwa humo, na imeitwa “Nadwah” kwa sababu wao walikuwa wanaitwa humo kwa ajili ya kheri na shari. Na tamko hili limechukuliwa katika neno “nadaa, naadiy na muntadaa” nayo ni majilisi ya kaumu wanaokaa pembezoni mwake, yaani wanaokwenda karibu kisha wanarejea na inasemekana ni nyumba ya dawaa wanaitwa kwa ajili ya chakula, kupanga mambo n.k. na nyumba hii ipo karibu na masjid tukufu, nyumba hii baada ya kufa Qusay bin Kilab ilihamia kwa mtoto wake mkubwa Abdu Dar kisha haikuacha kuwa mikononi mwa watoto wake hadi ikawa chini ya Hakim bin Hazim bin Khuwailid bin Asad bin Abdul Uzza bin Qusay, yeye akaiuza kwa Muawiya kwa diriham laki moja, Muawiya akamlaumu kwa hilo na akasema: “Umeuza utukufu na heshima ya baba zako.” Akasema: “Utukufu umekwenda kwenye uchamungu, naapa kwa Mwenyezi Mungu niliinunua wakati wa ujahiliya kwa machicha ya pombe, na nimeiuza kwa laki moja na ninawashuhudilisha kwamba thamani yake ni katika njia ya Mwenyezi Mungu, wako wapi walioghibu, na katika nyumba hii washirikina wa Makka waliazimia kuwatenga Bani Hashim na humo pia washirikina walipanga njama ya kumuua Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.). Tazama Muujamul-Buldan Jz. 2, uk. 423 Babu dali na alif na yanayofuatia na Jz. 5, uk. 179 - 186. 35
Page 35
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto Mughira48 pamoja na cheo chake alikuwa na ukoo mkubwa, watoto wengi na mali nyingi sana na wakati huo huo alikuwa ni mwanafasihi mkubwa wa waarabu na alikuwa na mashairi mazuri sana na maridadi, aliambiwa kuwa kuna mtu anadai kuwa ametumwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu, akauliza ametoka kwa akina nani? Akaambiwa kutoka kwa makuraishi, akasema ni nani huyo? Wakasema ni Muhammad bin Abdillah, kisha Walid akakutana na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), akamuuliza: “Unadai kuwa wewe ni Nabii? Mtume kasema ndio, Walid akasema kama Mwenyezi Mungu angetuma mtume basi angenituma mimi kwa sababu mimi ninamiliki mali, watoto na haiba kubwa. Mtume (s.a.w.w.) hakumjibu kitu akamwacha. Wakuu wa kikuraishi wakakusanyika katika Daru Naduwah wakasema: “Unasemaje ewe Walid katika kutatua suala hili?” Walid akasema: “Nini hoja ya Muhammad juu ya unabii?” Wakasema “Hoja yake ni Qur’ani.” Akasema: “Qur’ani ni nini?” Wakasema ni maneno anakuja nayo na kuyasoma na anasema: Nyinyi nyote hamuwezi kuleta mfano wa maneno haya.” Walid akataka wamletee baadhi ya Aya zake, akaja mmoja wa aliyesikia Qur’ani na akamsomea Walid. Aliposikia akashangaa na akavutwa na utamu wa Qur’ani kwa sababu mfano wa Walid naye ni mwenye balagha na fasihi, mjuzi wa fasihi na balgha na muweza wa kutambua muujiza wa Qur’ani kuliko asiyekuwa yeye, hivyo alisema rudieni tena kwangu maneno haya kwani sijawahi kusikia maneno kama haya katika maisha 48 Ni Walid bin Mughira bin Abdillah bin Amr bin Makhuzum, Abu Abdu Sham ni kati ya makadhi wa kiarabu wakati wa ujahiliya, na ni kati ya wakuu wa kikuraishi na viongozi wake, alifikiwa na Uislamu hali ya kuwa ni kikongwe akaufanyia uadui na akaipinga daawa yake, na imetajwa kuwa ndiye ambaye alikusanya makuraishi na akasema: “Hakika watu wanawajieni siku ya Hijja wanawaulizeni kuhusu Muhammad, kauli zenu zinatofautiana kwaye, mnasema huyu ni kuhani, wengine wanasema mshairi, wengine wanasema huyu ni kichaa na wala hakuna hata moja kati ya hayo, lakini yanayofaa kati ya yaliyosemwa ni mchawi kwa sababu anafarakanisha baina ya mtu na ndugu yake, mke na mume. Walid bin Mughira alikufa baada ya Hijra kwa miezi mitatu na akazikwa Hajun, Walid bin Mughira alikuwa kati ya wazee wakubwa, mzoefu kati ya werevu wa kiarabu, waarabu walikuwa wanamfanya kuwa ni mwamuzi wao na wanamsomea mashairi yao na analolichagua kati ya mashairi basi linakuwa ni teule, naye ni kati ya watu watano wacheza shere ambao Mwenyezi Mungu alizima shari zao. Tazama Al-ilaam Jz: 8 uk. 122, Zakuliy na Al-kunaa wal Al Qaab Jz. 1, uk. 40 36
Page 36
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto yangu. Wakayarejea tena maneno hayo, akawa anafikiri kwa muda kisha akawaambia: “Mnasemaje enyi wakuu wa makuraishi?” Wakasema: “Tunasema ni kuhani.” Akasema: “Hapana, wallahi sio kuhani kwa sababu kuhani anazungumza maneno yasiyosikika.” Wakasema: “Basi tunasema ni kichaa.” Akasema: “Sio kichaa, tumekwishaona vichaa na tumeshawajua na Muhamaad hana harakati za kichaa na wala hatembei njiani kama kichaa wala hapatwi na wasiwasi na mengineyo kati ya alama za kichaa.” Wakasema: “Tunasema ni mshairi.” Akasema: “Sio mshairi, tumeshayajua mashairi yote na aina zake zote hivyo sio mashairi.” Wakasema: “Tunasema ni mchawi.” Akasema: “Sio mchawi, tumeshaona wachawi na uchawi wao sio katika pulizo zao wala mafundo yao.” Wakasema: “Sasa unasemaje ewe Walid?” Akasema: “Hakika kauli yake ina mvuto, na shina lake lina utamu na tawi lake lina matunda.” Hivyo kafananisha maneno yake na mtende ambao shina lake ni thabiti na lina nguvu na tawi lake ni zuri linapokuwa na matunda; lakini wakuu wa kikuraishi wakamtaka Walid aseme chochote kuhusu Mtume wa Mwenyezi Mungu na Qur’ani yake ili wakipeleke kwa watu na kwacho wawaweke mbali na Nabii na Qur’ani yake. Walid akasema: “Hakika maneno yaliyo karibu ni kusema kuwa ni mchawi.” Mwenyezi Mungu akateremsha Aya kumhusu Walid bin Mughira:
37
Page 37
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto “Niache na niliyemuumba peke yangu, na nikamjaalia mali nyingi na watoto wanaoonekana, na nikampangia mpango, hakika yeye alifikiri na akapimia basi ameangamia, alipimiaje…… Nitamwingiza katika moto wa Jahannam.” Suratul-Muddathir: 11 – 26
QUR’ANI INAWAONYA WAONGO Allamma Tabrasiy amenukuu katika Tafsiir yake Majmaul Bayan sababu ya kushuka Aya hizi za Suratul-Mudathir ni kwamba; wao makuraishi walipomwambia Walid tunasema ni mchawi, akasema mchawi ni nani? Wakasema: “Ni watu wanaotia mapenzi baina ya wanaochukiana na wanatia chuki baina ya wanaopendana.” Akasema: “Basi ni mchawi.” Wakatoka, basi ikawa yeyote kati yao hakutani na Nabii (s.a.w.w.) isipokuwa anasema: “Ewe mchawi!” Hilo likazidi sana kwake, ndipo basi Mwenyezi Mungu akateremsha “Yaa ayyuhal Muddatthir.” 49 Nabii (s.a.w.) baada ya kubainisha haya kwa Masahaba wake na kusema: “Hakika Aya hii imeteremka kwa Walid bin Mughira” kundi lilikwenda kwa Walid likamwambia kwamba Muhammad anasema kuna Aya zimeshuka kwa ajili yako, akataka azisikilize, wala hakuenda mwenyewe kwa Nabii kwa sababu ilimuwia uzito kwake na akataka kulinda heshima yake kwa wakuu wa kikuraishi, wakaja nayo Aya na wakamsomea. Wanahistoria wanasema Walid alipozisikiliza aliogopa sana, akasimama na kutetemeka sana kwa woga, kana kwamba amepatwa na ugonjwa wa moyo na akazimia kutokana na Aya zilizoshuka kwa ajili yake, na hazikupita siku tatu akafa, akafariki dunia hali ya kuwa amefanya vitendo viovu na kupoteza watu kutoka katika haki, na Mwenyezi Mungu ameahidi kumwingiza katika moto wa chini kabisa wa Jahanamu, nao ni moto wa “Saqar” na hali hii ilimpata Walid baada ya kusikiliza Aya zilizotajwa kwa 49 Tazama Majmaul-Bayan, Juz. 10, uk. 178, Shajaratu Tubaa Jz. 2, uk: 230 38
Page 38
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto sababu yeye ni fasihi anajua balagha na ni mjuzi wa mashairi na lugha, hivyo ni jambo la kawaida kwamba alijua kuwa ni maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, isipokuwa yeye hakuweza kuvumilia maneno kama hayo hivyo hakuamini.50 50 Tazama Tafsirul-Qumi Jz. 2, uk. 186 babu 1 hadith 16, pia imepokewa katika kitabu cha Ihtijaj sababu nyingine ya kufa kwa Mughira, ambapo imepokewa kuwa Myahudi alimwambia AmirulMuuminina (a.s.) katika mazungumzo: “Hakika Musa bin Imran Mwenyezi Mungu alimtuma kwa Firaun na akampa muujiza mkubwa.” Amirul-Muuminina akasema: “Ndio ilikuwa hivyo, na Muhammad alitumwa kwa mafirauni mbali mbali mfano: Abu Jahal bin Hisham, Utbah bin Rabi’ah, Shaibah, Abu Bakhtar, Nadhir bin Harthi, Ubayya bin Khalaf, Munabbihi na Nabiyh watoto wa Hajaj, na wacheza shere watano; Walid bin Mughira Al- Makhuzumiy, Asi bin Wail As-Sahamiy, As’wad bin Abdu Yaghuth Az-Zahariy, Aswad bin Abdil-Muttalib, na Hariy bin Abi Twalala, basi akawaonyesha miujiza ya angani na katika nafsi zao hadi ikabainika haki kwao. Myahudi akamwambia: “Mwenyezi Mungu alilipiza kisasi kwa ajili ya Musa.” Ali akamwambia: “Ilikuwa hivyo na Mwenyezi Mungu alilipiza kisasi kwa ajili ya Muhammad kwa mafirauni, ama kwa wacheza shere Mwenyezi Mungu amesema: “Hakika sisi tumekutosheleza kutokana na wacheza shere.” (Suratul-Haj: 95). Mwenyezi Mungu akawauwa wote watano, kila mmoja kati yao kwa kifo tofauti na cha mwenzake kwa siku moja. Ama Walid bin Mughira alipitia katika mtego wa mwanaume wakikhuzay, alikuwa ameshautega na akauweka njiani, basi ukapata baadhi ya sehemu za mboni zake na zikatoka damu, na akafa hali anasema ameniua Mola wa Muhammad. Ama Asi bin Wail bin As-Sahamiy alitoka kwa ajili ya haja zake, sehemu fulani akajikwaa katika jiwe chini, akaanguka na kukatikakatika vipande vipande na akafa naye anasema ameniua Mola wa Muhammad. Aswad bin Abdil Yaghuth alitoka kwenda kumpokea mtoto wake Zam’ah, akasimama katika kivuli cha mti, Jibril akamjia akamshika kichwa chake na kumpigiza kwenye mti akamwambia kijana wake mzuie huyu kwangu. Akasema: “Sioni yeyote anayefanya kitu isipokuwa wewe mwenyewe.” Basi akamuua hali akisema ameniua Mola wa Muhammad. Ama Aswad bin Hariyth, Nabii (s.a.w.w.) alimuomba Mwenyezi Mungu apofushe macho yake na amuuwe mtoto wake basi siku hiyo alitoka hadi alipofika mahala, Jibril alimwendea na jani la kijani na akampiga kwalo usoni mwake akapofuka, na akabaki hai hadi Mwenyezi Mungu alipomfisha mtoto wake. Ama Harith bin Abi Twalalah alitoka nyumbani katika wakati wa joto kali basi akabadilika na kuwa mweusi kama mhabeshi, akarejea kwa watu wake akasema: “Mimi ni Harith.” Wakakasirika wakamuua naye anasema ameniua Mola wa Muhammad; na imepokewa kuwa Aswad bin Harith alikula samaki akapatwa na ugonjwa wa kiu hakuacha kuwa anakunywa maji hadi tumbo lake likapasuka akafa, naye anasema ameniuwa Mola wa Muhammad, yote hayo kwa muda wa saa moja na hiyo ni kwamba wao walikuwa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu wakamwambia: “Ewe Muhammad, tunakusubiri hadi adhuhuri kama utarejea katika kauli yako, vinginevyo tutakuua.” Nabii (s.a.w.w.) akaingia katika nyumba yake akafunga mlango kwa huzuni kutokana na maneno yao. Jibril akamjia kutoka kwa Mwenyezi Mungu wakati ule ule akasema: “Ewe Muhammad, Mwenyezi Mungu amekuteremshia amani na anakuambia kwamba tangaza unayoamrishwa na achana na washirikina” (Suratul-Hijr: 94) yaani dhihirisha jambo lako kwa watu wa Makka na waite katika imani. Akasema: “Ewe Jibril, nitawafanyaje wacheza shere na waliyonitishia?” Akamwambia: “Sisi tutakutosheleza na wacheza shere.” (Suratul Hijur: 95). Akasema: “Walikuwa kwangu punde.” Akasema: “Nimewatosheleza,” na akadhihirisha jambo lao wakati ule, ama mafirauni waliobaki waliuliwa siku ya Badri kwa upanga wa Mwenyezi Mungu, akawashinda wote na wakakimbia. Tazama AlIhtijaj, Jz. 1, uk. 216 katika hoja zake kwa wayahudi.
39
Page 39
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto Hii ndio Qur’ani; inatoa changamoto kwa mkubwa na mdogo, na kwa kila mwenye balagha na fasaha tangu wakati huo hadi leo hii, pamoja na kuongeza kwamba Qur’ani imekusanya elimu mbali mbali na mengi yaliyofichikana ambayo mwanadamu anayahitaji kwa ajili ya maisha yake ya duniani na akhera, hivyo ni muujiza katika matamko yake na maana zake, na tangu siku hiyo hadi leo hii, na hata baadae hajaweza wala hatoweza mwenye kukanusha na wengineo, kutoa changamoto kwa Qur’ani na kuleta mfano wake hata kwa Sura kumi, bali hata Sura moja, hata kama watasaidiana wao kwa wao.
WAZUSHI WA KARNE YA ISHIRINI Ujahili wa zamani ulishikamana na kasumba za itikadi za baba zao waliotangulia; wakaizulia Qur’ani kwa ukaidi na ujeuri na hawakuiamini, miaka ikapita ukaja ujahili mwingine watoto wao wakawa na kasumba kama za baba zao waliotangulia, wakaizulia Qur’ani kwa ukaidi na ujeuri na kuuzidi ujahili wa mwanzo. Ujahili wa mwanzo ulitokana na maneno tu, na hawa wapya wameandika vitabu juu ya hayo, wakataka kusambaza shubuhati kuhusu Qur’ani tukufu, dini ya Kiislam na Mtume Mtukufu (s.a.w.w.). Mimi nawalingania watunzi wote, wale wenye kuhakiki na wachambuzi, kurejea kwenye vitabu hivyo ambavyo havijaacha shutuma ila wameipakazia juu ya Uislamu na Waislam, na wala uongo ila wameunasibisha na Qur’ani tukufu na Nabii Mtukufu (s.a.w.w.), na kati ya vitabu hivyo ni ambavyo vimetokea katika nchi za kikafiri na wasimamizi wake walikuwa ni makafiri. Na kwa kawaida makafiri huwa wanapinga hata mambo ambayo yako wazi kabisa, nayo ni kuwepo muumba wa ulimwengu huu, muumbaji wa dunia hii pamoja na kwamba ni muhali kupatikana kitu bila muumbaji, au mtengenezaji, wala mwenye kukileta. Itakuwaje liwezekane hilo katika ulimwengu huu mpana na dunia kubwa yenye 40
Page 40
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto kupangika kwa umakini? Mwenye kukanusha kuwepo muumba hana kizuizi cha kuikanusha Qur’ani na kuizulia uongo. Yeye haamini ukweli, anaona kila kitu ni uongo na upuzi, lakini Qur’ani tukufu imebaki kuwa ni muujiza, wote wanashindwa kuleta mfano wake au hata sehemu yake tu. Ndio, baadhi ya wakanushaji wamepanda hadi kwenye mwezi na wametengeneza Satelaiti, ndege na vitu vingine, lakini wao katika mambo ya kiroho wako nyuma sana, bali wanayakanusha na kuyapiga vita na wanawapiga vita wale wanaoyalingania hayo. Walipojikuta kuwa ni wenye kushindwa kusimama dhidi ya Qur’ani wakasema ni upuuzi na maneno yasiyo na maana, yasiyo na hoja wala dalili za kimaudhui, na yaliyo mbali na mantiki na fikra sahihi. Na hii inazingatiwa kuwa ni uadui kwa hisia za Waislam na kuvunja heshima ya dini yao, na kitendo hiki hakionyeshi ubinadamu na kuheshimu haki za wengine, si kwa karibu wala kwa mbali, bali ni kitendo cha majahili wenye chuki.
UKANUSHAJI ULIOPANGWA NA VITA VYA VITU VITAKATIFU Hakika wanaokanusha kuwepo kwa Mwenyezi Mungu na wanaopinga Qur’ani bila shaka walikuwepo muda wote wa historia ya ulimwengu lakini walikuwa wamesambaratika na hawakuwa na mpangilio, tablighi na propaganda kama tunavyoona leo ukafiri wa kikomonisti katika umoja wa Soviet.51 Wakaanzisha vituo na wakafungua shule kwa ajili ya kuwaingiza 51 Yaani Urusi, wakati wa kuandikwa kitabu hiki ilikuwa chini ya himaya ya wakanushaji na ilikuwa inaitwa "Soviet Union" na humo imetoka fikra ya kupinga kuwepo Mungu hadi katika nchi za Kiislam. Na kati yake ni Iraki ambayo ilijipenyeza kwa pazia la kijamaa baina ya watu wepesi kati ya wananchi, kupitia kwa mamluki wa ukoloni ambao walizipigia ngoma na zumari sana fikra hizo potovu, na nembo za kipuuzi. Baadhi ya wajinga na wepesi baina ya watu wakazichukulia usahihi wa misingi yake, na kutokana na hayo, kuna beti za shairi za Imam Shirazi ambaye wakati huo umri wake ulikuwa haujavuka miaka thelathini. Na wengi kati ya Maulamaa wakachukua majukumu yao dhidi ya fikra hizo mbovu na rai potovu, wakapambana nazo kwa njia mbali mbali, kwa kuweka wazi kwamba ni Uislamu tu ndio unaweza kuleta uadilifu wa kijamii. Na Imam ametaja baadhi ya njia hizo ambazo alizifuata katika kukabiliana na ujamaa katika kitabu chake "Tilkal Ayyaam," akaelezea baadhi ya ambayo yamepita katika jamii kutokana na kuenea fikra hizo akasema:
41
Page 41
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto "Qasim alipofanya mapinduzi ya kijeshi na akaangusha ufalme, akaruhusu chama cha kijamaa kufanya kazi na harakati kwa uhuru, basi wajamaa wakaenea kila sehemu na wakaijaza nchi kwa kelele na vilio, wakawatoa wanawake katika majumba na wakawataka wajidhihirishe kwa wanaume. Na walikuwa hawaogopi kufanya kosa lolote kwa ajili ya kueneza fikra zao za kupinga kuwepo Mungu. Na kati ya njia zao walikuwa wanaweka magari mawili katika sehemu mbili tofauti, wanafunga miguu ya mpinzani wao, au yule ambaye wanashuku kuwa ni mpinzani wao kwenye gari mbili, mguu moja katika gari moja na mwingine katika gari nyingine kisha magari yanaondoka kwa mwelekeo tofauti basi anapasuka akiwa yuko hai vipande viwili. Na hayo yalikuwa yanatokea katika sehemu takatifu. Katika Karbalaa tukufu tuliunda kikundi ili kutembelea maulamaa katika mji wa Najaf tukufu, kwa ajili ya kufanya maafikiano na maulamaa watukufu, kusimama dhidi ya ujamaa muovu ambao unaingia katika nchi, na nilikuwa nafuatana na Sayid Swadiq Al-Qazuwini, Sheikh Ja'ar Rashta, Sayid Murtadha Al-Qazuwini na maulamaa wengineo karibia ishirini, na wa kwanza tuliyekutana naye ni Sheikh Muhammad Ridhaa Al-Mudhafar na alikuwa ni mtu mtoaji mzuri wa moyo mtukufu, anaependa kuwatumikia wengine, naye ndiye aliyeasisi "Kitivo cha Fiqih" na rai ya Sheikh ilikuwa ni kwamba tuwaite na wengine katika majilisi kubwa basi tukaafikiana na uamuzi wake. Al-Allammah alifanya haraka na kuandaa sehemu ya kufanyia kikao, na ambacho kilihudhuriwa na maulamaa mbali mbali takriban arobaini. Miongoni mwa maulamaa na mafaqih, wakiwemo Masayyid kutoka familia ya Bahrul Ulumi, familia ya Sayyid Swadr, familia ya Sayyid Ridhaa n.k. Majadilianao yalikuwa ni marefu katika kikao hicho kuhusu kupambana na mashambulizi ya kijamaa, na kwamba kunyamaza kimya juu ya hilo kutaacha athari mbaya, kwa sababu wajamaa wanakanusha mambo matano, dini, utukufu, umilkaji binafsi, hakuna familia wala hakuna uhuru. Kama hatutosimama imara dhidi yao basi watafanya waliyoyafanya Moscow, kwa sababu ujamaa wa Iraki ni tawi la Moscow. Wajamaa wa Iraki hawakuwa na mamlaka bali walikuwa ni bendera, haya aliyathibitisha balozi wa Uingereza baada ya kumalizika utawala wa Abdul-Karim Qasim, ambapo balozi aliandika makala katika gazeti la "AlHayatu" la Lebanoni akisema: "Hakika sisi tuliruhusu ujamaa kuenea. Ama utawala wa asili ulikuwa mikononi mwetu." Nayo ni kazi ile ile, waliyoyafanya Waingereza katika baadhi ya nchi za kiislam, yaliyotokea Afghanistan, yalikuwa ni mfano wa yaliyotokea Iraki. Na wajamaa walitakiwa kutumia nguvu zao kubomoa nguvu ya Iraki na koo za ki-Iraki zilikuwa na nguvu ambazo hazipuuziki, Hauza za kielimu, maulamaa, na wanafikra wao walikuwa na nguvu na walikuwa na sauti kwa wananchi. Wanafikra wakiislam walikuwa na nguvu vile vile. Kikao hicho kilichofanyika Najaf kilizaa matunda; mwisho kiliafikiana kuunda jopo la maulamaa, na wote walikuwa katika daraja la pili na la tatu, na maulamaa katika daraja la kwanza wakafanya haraka kuwaunga mkono, kwa mfano mzazi wangu, Sayid Al-Hakim, na Marajiu wengine wakubwa. Jopo hili lilianza kazi yake dhidi ya ujamaa kwa kutoa makala kila siku na kutoa matangazo katika magazeti mbalimbali, na kwa mukabala wake serikali ikaanza kujibu haraka. Abdul-Karim Qasim akaasisi jopo la maulamaa huru chini ya uongozi wa Sheikh AbdulKarim Al-Mashtah, na alikuwa na uhusiano mzuri na wajamaa na akakusanya kundi la wenye mandhar na wala sio dini, ambao wana upungufu wa uchamungu na elimu. Kundi hili lilitoweka na baadhi wakakimbia baada ya kupinduliwa Abdul-Karim Qasim. Mawasiliano yetu yaliendelea kwa Marjaa. Tulikuwa tunawazuru na kuwapa habari za kazi zetu, na tunataka kwao msaada wa kusimamisha kuenea kwa ujamaa. Safari moja tulikuwa na ziara kwa Marjiu kama vile Sayyid Muhsin Al-Hakim, Sayid Al-Hamamiy, Al-Mirzaa Abdul Hadiy Shiraziy na wengineo na maulamaa hawa walikuwa wanazidiana kwa hamasa dhidi ya ujamaa. Kati yao kuna waliozingatia hamasa na wengine hawakuitilia umuhimu. Baadhi yao walikuwa wanasema ujamaa ni chombo cha wamagharibi na watamalizika upesi na rai yetu ilikuwa ni kuendelea na wajibu wetu wa kisheria na majukumu yetu ya kidini kupambana na uovu, vyovyote zitakavyokuwa sababu zake na msukumo wake, tazama "Tilkal ayaam" cha Imam Shiraziy uk: 125, pia rejea kitabu "Fiqih Siyasa" Jz. 106 katika mlango huu, na kitabu "Mubahathatu ma'a Shuyu'iyyina, Al-Qaumiyat fiy khamsiyni sanah na "Markis yanhazim" n.k.
42
Page 42
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto watu katika ukafiri. Kwa sababu hii tunawaomba vijana kuwa waangalifu, watambue, wawe macho na waamke ili waone ukweli, na watambue hila za makafiri na wasimame kidete dhidi ya mbinu za kutangaza ukafiri ili wasalimike katika mitego yao, bali watengue mitego yao ya kikafiri na wawaokoe watu kutokana na mitego yao. Hakika makafiri katika zama hizi na kwa wakati usiozidi miaka mitatu wameweza kuongeza katika harakati zao za kikafiri, na taasisi zao za kikafiri, katika kueneza fikra zao za kikafiri. Na wamechapisha zaidi ya vitabu 217 katika kumkanusha Mwenyezi Mungu, kuwakanusha Manabii na mawasii (a.s.) na kuvizulia uongo vitabu vya dini hususan Qur’ani tukufu. Na hatari hii ni tishio kwa akili na wenye akili, binadamu na ubinadamu ni lazima tuizuie na kuisimamisha katika mpaka wake, kuifichua na kuaibisha.
MWANZO WA KUPANGA “ULAHIDI” UKANUSHAJI Walikutana watu watatu katika walahidi huko Makka wakati wa Hijja kuipinga Qur’ani, nao ni kama ilivyopokelewa katika kitabu cha Al-Ihtijaj “Abdillah bin Al-Muqafaa, Abu Shakir Daysan na Ibun Abi Al-Aujau.” Wakajipenyeza miongoni mwa mahujaji ili kusambaza fikra zao zenye sumu miongoni mwao. Walifikiria kuitengua Hijja kupitia katika kuitengua Qur’ani kwa sababu ni msingi wa Uislamu na sharia, utume na Mtume, Makka na Hijja na kila kinachofungamana na Uislamu. Na hawa wakanushaji watatu walikuwa ni fasaha na wenye kujua balagha na kati ya waliojifunza elimu mbali mbali. Wakapanga wakutane mwaka uliofuata, na kila mmoja wao alete mfano wa Qur’ani kwa kiasi cha theluthi moja, yaani juzuu kumi. Kisha waonyeshe kitabu chao hichi kipya ambacho kinatoa changamoto kwa Qur’ani ya Nabii Muhammad (s.a.w.w.) kwa viongozi wa Waislam Makka, na waseme kuwa wao wametoa changamoto ya Qur’ani na wameleta mfano wake. Lakini ulipofika msimu wa Hijja mwaka uliofuata, wakakutana na wakawa hawakuleta hata Aya moja 43
Page 43
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto mfano wa Aya za Qur’ani. Mmoja wao akasema: “Mimi niliposoma Qur’ani kwa makini nikajua kuwa mimi siwezi kuleta mfano wake, na hiyo ni kwa sababu nimekuta Aya katika Qur’ani kuwa ni muhali mwanadamu kuleta mfano wa Qur’ani, nayo inasema: “Walipokata tamaa wakaishia kwenye kunong’onezana.”52 Na Aya hii tukufu imekuja katika kisa cha Yusuf (a.s.) na ndugu zake, walipotaka kumbadilisha na Benjamin ambaye walimzuia kwa mmoja wao, lakini akakataa pendekezo lao na hakusalimu amri kwa ombi lao, hivyo Aya inasema: “Walipokata tamaa kumchukua ndugu yao pamoja nao Benjamin wakajitenga kunong’ona,” yaani wakatoka kwa watu bila ya kuwa na yeyote asiyekuwa katika wao ili walete baina yao ambayo yanapasa kuyaandaa kati ya nyudhuru watakapokwenda kwa baba yao peke yao bila ya ndugu yao, na ili wachukue uamuzi wa mwisho kwamba watarejea au watabaki. Muhtsari: Hakika wao walijitenga na watu ili wanong’onezane, na tamko hili ni kati ya matamko ya Qur’ani tukufu ambayo ni kati ya lengo la fasaha na kilele cha balagha. Hakika inakusanya muujiza katika tamko moja pamoja na wingi wa maana;53 hivyo huyo mlahidi mtaalam, mwanafasihi na mwanabalagha hakuweza kutoa changamoto kwa Aya moja ya Qur’ani. Sasa itakuwaje alete mfano wa Qur’ani, bali ikawa ni jambo la muhali kwake kwa sababu amepata yakini kuwa ni muujiza, na akatoa uamuzi kuwa hawezi kuleta mfano wa Qur’ani pamoja na kuwepo mfano wa aya hii. Ama mtu wa pili akasema: “Hakika mimi pamoja na kupata muda katika mwaka kila nilipoibinya fikra yangu, na nikatilia maanani jambo langu, sikuweza kuleta kitu chochote mfano wa Qur’ani kwa sababu katika Qur’ani nilipata ambayo siwezi kuleta mfano wake, kwani nilipitia katika kisa cha Nuh katika kauli yake (s.w.t.): “Na ikasemwa, ewe ardhi meza maji yako na ewe mbingu zuia maji yako, na mambo yakahukumiwa na ikatua juu ya mlima, na ikasemwa wawe mbali watu madhal52 Suratu Yusuf: 8
53 Taz. Tafsir Majma’ul-Bayan Jz. 5, uk. 440, Surat Yusuf 44
Page 44
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto imu.”54 Aya hii tukufu imekuja katika kisa cha Nuh (a.s.) na katika tufani. Nayo vilevile ni katika Aya za miujiza katika balagha na fasaha, na ambayo inakusanya maana nyingi katika matamko machache. Ama yule watatu alisema: “Mimi ni kama nyie vilevile, hakika mimi sijaweza kuleta mfano wake kwa sababu nimekuta katika Qur’ani tukufu Aya kuhusu mama yake Musa, ambayo imenifanya nishindwe kuleta changamoto, nayo ni kauli yake (s.w.t.): “Tukamfunulia mama yake Musa kwamba mnyonyeshe, na ukiwa na hofu juu yake basi mtupie kwenye bahari, usiogope wala usihuzunike, hakika sisi tutamrejesha kwako na tutamjaalia kuwa kati ya Mitume.” 55 Aya hii tukufu inabainisha kisa cha Musa na namna ya kuzaliwa kwake, kunyonyeshwa kwake, kutupwa kwake katika bahari na kurejeshwa kwake kwa mama yake kisha kupewa utume na kutumwa kwake kwa Firaun. Nayo vilevile ni katika Aya ambazo zimekusanya maneno machache yenye fasaha na maana nyingi na kubwa. Na katika wakati huu na wakati hawa walioshindwa wamekaa wanazungumza, alipita kwao Imam Sadiq (a.s.) akawasomea kauli yake (s.w.t.): “Sema kama watakusanyika wanadamu na majini ili kuleta mfano wa hii Qur’ani hawataweza kuleta mfano wake hata kama watasaidiana baadhi ya wao kwa wao.”56 na 57 Na kwa kusoma kwake Aya hii tukufu kwao, ikafichua njama yao ya kutoa changamoto ambayo wameafikiana kwa siri baina yao, pia akawapa habari ya kutoweza kwao kuleta Sura angalau moja mfano wa Qur’ani. 54 Surat Hud: 44 55 Suratul-Qisas: 7 56 Suratul-Israi: 88 57 Tazama Ihtijaji; Jz. 2, uk. 377 katika ihtijaji za Abi Abdillah (a.s.), Swiratwal Mustaqiym Jz. 1, uk. 42 babu 31 45
Page 45
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto
WAJIBU WETU KATIKA QUR’ANI TUKUFU Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.): “Mwenye kusoma Qur’ani mpaka akafahamu na kuihifadhi Mwenyezi Mungu atamwingiza peponi na atampa uombezi kwa watu kumi katika familia yake ambao wote walikuwa tayari wamestahili kuingia motoni.”58 Amesema Amirul-Mu’minin (a.s.): “Allah Allah katika Qur’ani wasije wakawatangulia wasiokuwa nyinyi kuifanyia kazi.” 59 Hakika Qur’ani tukufu ni Kitabu cha dini ya Mwenyezi Mungu, amekiteremsha kwa ajili ya kuongoza wanadamu hivyo ni wajibu kwa Waislam wote kukisoma na kutafakari Aya zake na kujifunza hukumu zake na kuzitekeleza katika maisha yao ili warejeshe heshima yao na utukufu wao na kuteremsha rehema za Mola wao kwao, lakini kinachosikitisha ni kuona Qur’ani imehamwa katika jamii yetu na hasa miongoni mwa vijana kwa kiasi kwamba baadhi yao hawawezi hata kuisoma Qur’ani tukiachilia mbali kufanya utafiti humo, kusoma tafsiri yake na kushikaimana na sharia zake, na kinachosikitisha pia ni kuona kwamba baadhi wametosheka na kutabaruku na Qur’ani tu, utawaona wanaiandika kwa hati nzuri kwa wino wa rangi nzuri kisha wanaiweka katika moja ya sehemu za nyumba. Wengine tunawaona wanajilazimisha kujifunza Suratul Fatiha na Suratul Ikhlasi vizuri ili kuzisoma kwake katika Swala kwa njia sahihi, ama zaidi ya hapo hazingatii, hivyo ni wajibu kuhuisha visomo vya kujifunza Qur’ani tukufu na kuisimamia visomo vya tajwid katika misikiti, majumbani, Huseiniya na hata katika mashule na vyuo vikuu ili tulee vizazi vyetu malezi mazuri ya Kiislam na tuwashibishe malezi ya Qur’ani kwani cha kwanza walichokuwa wanajifunza wazazi wetu zamani ni Qur’ani tukufu. Na sisi pia yalitujumuisha mafunzo haya ambapo tulikuwa tunakwenda 58 Wasailush-Shi'ah, Jz. 6, uk. 169 babu 1 hadith 7649 59 Nahajul Balagha; khutuba: 47 wasia wake kwa Hasan na Husein ( as) alipopigwa na Ibnu Muljim mlaaniwa 46
Page 46
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto katika Madrasa na mwalimu anatufundisha tangu siku ya kwanza herufi za hijai “Alif, bee, tee….” kisha anatufundisha Suratul Hamdu na Suratul Ikhilasi, kisha juzuu Amma kisha juzuu ya Tabaraka kisha Dhariyat kisha tunasogea darasa hili hadi darasa jingine. Na mmoja wetu anapohitimu Qur’ani yote familia yake ilikuwa inajifakharisha sana juu yake na wanamfanyia hafla kwa ajili ya kumpongeza na kumkirimu na wanawaalika watu katika hafla hiyo. Na hii ilikuwa ni desturi ya Kiislamu inayofuatwa katika nchi za Kiislamu inayompa moyo mtu kujifunza, kuhifadhi na kuitekeleza Qur’ani kwa vitendo.60 60 Desturi hii ilikuwa imeenea Iraki, Kuwait, na nchi zingine za Kiislamu. Mwenye kuhifadhi Qur’ani alikuwa anavaa nguo nzuri, na anakuwa na kundi la vijana wanamshangilia kutoka katika madrasa ile ambayo amejifunza humo. Wanamnyunyizia maji ya waridi, wanabeba mishumaa, na chetezo za udi. Na walikuwa wanachanganya maji ya waridi na ambari, na mmoja wao anasoma Qur’ani kwa sauti ya juu. Sayid Suleiman ametaja sherehe za kuhitimu Qur’ani katika moja ya vitabu vyake akasema: “Jukumu la kufundisha Qur’ani lilikuwa ni la Madrasa, au chuo cha Kiislamu kinakuwa na nafasi muhimu katika kutengeneza utamaduni wa Qur’ani, ambapo madrasa hizi zinakusanya makundi ya watoto wenye umri kati ya miaka mitano hadi kumi na tano. Mwanafunzi anapovuka hatua ya kujifunza Qur’ani na kuihifadhi, basi anafanyiwa sherehe maalumu inayojulikana kama sherehe ya kuhitimu Qur’ani, hizo ni katika ada maarufu za wananchi zilizorithiwa. Katika mji mtukufu wa Karbala, sherehe za kuhitimu kuhifadhi Qur’ani zilikuwa zinafanywa kwa muundo wa makundi, ambapo wanafunzi wanakusanyika sehemu maalum kwa utaratibu, wakubwa kati yao wanatangulia wanabeba taa za kandili, watoto wanabeba chetezo za udi na mishumaa katika visahani maalum. Ama mwanafunzi aliyehitimu Qur’ani tukufu, yeye anavaa egali katika kichwa chake, kikoi cheupe na anavaa joho maalum kisha maandamano yanaanzia mlangoni mwa aliyehitimu Qur’ani, na wote wanasoma kasida kwa shangwe. Mwalimu anawatangulia pamoja na mbebaji ambaye anabeba Hamal ambayo inaitwa “Hajjah,” nayo ni sahani humo huwekwa waridi na maua na mishumaa, na inakuwa
47
Page 47
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto midogo inang’aa na kutoa mwanga. Kila watoto watatu wanatembea kwa utaratibu maalum, na juu ya vichwa vyao kuna kofia maalum inayojulikana kwa “Al-araaqijynah,” na wanafunga mikanda mipana katika matumbo yao, na wote wanaelekea katika Haram ya Imamu Husein (a.s.). Na miongoni mwa kasida hizi ni: “Hubbu Aliyi bin Abi Twalib, ahlaa minas shahd ilaa sharibi, lau fatashuu qalbiy rau ausatahu, satwarayn qad khutwaa bilaa kaatib, al adilu watawhiyd, wahubbu Ahlil bayti fiy janib.” Na wanapowasili katika uwanja wa harram ya Imam Husein, wanasimama kwa mstari mmoja mbele ya moja wa waalimu na wanaimba: “Salaamun salaamun salaamun salaamu, salaamun alaykum farudus salaam. kisha mwalimu anaitikia na baadhi ya wanafunzi wanaowapokea kwa kusema: Hanian marian lakum jamu’ukum, burika yaumu waas’ad aam.” Ila maneno ya kupokea ni marefu zaidi kuliko tuliyoyataja. Kisha wanafunzi wanahamia kwenye uwanja wa harram tukufu ya Abbas na wanasimama mbele ya mmoja wa waalimu na wanakariri baadhi ya kasida. Kisha wote wanaelekea katika nyumba ya aliyehitimu Qur’ani ili wakapate chakula. Na watoto wanakusanya zawadi, fedha n.k. zinawekwa katika sahani na wanapewa familia ya mwanafunzi aliyehitimu Qur’ani tukufu. Na hapa Sheikh anasimama na kumwimbia mwenye nyumba baadhi ya kasida kwa sauti nzuri, na anapokaribia kumaliza anapewa zawadi, nayo ni kiasi cha fedha au kitu kingine. Kisha wote wanaondoka, na mchana wake kunakuwa ni mapumziko. Tazama: Karbala fiy Dhaakraat: uk. 148 (Zafatu khatamil Qur’ani).
48
Page 48
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto Amesema Abu Abdillah (a.s.): “Mwenye kusoma Qur’ani naye ni kijana muumini, Qur’ani inakuwa kwenye mwili wake na damu yake, na Mwenyezi Mungu anamjaalia pamoja na malaika watukufu na Qur’ani itakuwa ni kinga yake siku ya Kiyama itasema: ‘Ewe Mola! hakika kila mtendaji amepata malipo ya amali yake isipokuwa mtendaji wangu, basi nifikishie malipo yako mema.’ Akasema, “Basi Mwenyezi Mungu Mtukfu atamvisha nguo mbili katika nguo za peponi, na atamvika taji la utukufu kichwani mwake kisha ataambiwa je, umeridhika? Qur’ani itasema: ‘Ewe Mola; nilikuwa namtakia yaliyo bora kuliko hayo.’ Atapewa amani kwa mkono wake wa kulia na kuishi milele kwa mkono wake wa kushoto kisha ataingia peponi na ataambiwa: ‘soma Aya upande daraja.’ Kisha ataambiwa je, tumefikia na tumekuridhisha? Itasema: ‘Ndio na mwenye kuisoma kwa wingi na kujifunza kwa taabu kutokana na kuihifadhi kwake Mwenyezi Mungu atampa malipo haya mara mbili.61
KUJIFUNZA QUR’ANI NA KUIFUNDISHA Zimepokewa riwaya nyingi zinazohimiza kujifunza Qur’ani na kuifundisha, kuihifadhi na kuitekeleza kwa vitendo. Imepokewa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kwamba amesema: “Ibada bora ni kusoma Qur’ani.”62 na imepokewa kutoka kwa Amirul-Mu’minina (a.s.) kwamba amesema: “Jifunzeni Qur’ani hakika ni mazungumzo mazuri na ifahamuni hakika ni bustani ya nyoyo na jiponyeni kwa nuru yake hakika ni ponyo la roho na jifunzeni kuisoma vizuri hakika ni visa vyenye manufaa.”63 Na kutoka kwa Imam Sadiq (a.s.) amesema: “Mwenye kuihifadhi Qur’ani na mwenye kuitekeleza kwa kivitendo atakuwa pamoja na malaika wema.”64 61Al-Kafi, Jz. 2. uk. 603, Babu fadhili hamilil-Qur’ani hadith ya 4 62 Wasailus-Shi’a, Jz. 6, uk: 168 Babu I hadith 7645 63 Nahjul-Balaghah, khutuba ya 110 fiy arkani diyni 64 Al-Kafi, Jz. 2, uk: 603 Babu fadhailul Qur’ani hadith 3
49
Page 49
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto Ama leo hatuoni ila kinyume cha hayo, mtoto anaingia katika shule ya msingi anaendelea hatua kwa hatua hadi anahitimu chuo kikuu hali ya kuwa hajasoma Qur’ani kama manhaji ya masomo, na baadhi wanakuwa hawajasoma Qur’ani hata nyumbani, wala katika kazi yake. Na wengine hawaisomi vizuri bali hata kuisoma kabisa, na hii ni kwa manufaa ya mbinu za maadui wa Uislamu, za kuwaweka waislamu mbali na Qur’ani na kufahamu fikra zake, na kutafakari hukumu zake. Na inaonyesha juu ya hayo yaliyosambazwa katika vitabu vyao, katika kauli ya mmoja wao katika kauli yake: “Hakika sisi tumeona kwamba wale walioongoza mapambano dhidi yetu sisi wakoloni walikuwa ni wenye kufuata uongozi wa maulamaa wao, na tumekuta kuwa njia bora kwa hilo ni kuasisi shule ambazo hazifundishwi Qur’ani na dini.” Kwa hilo wameweza kuwaweka vijana wa kiislamu mbali na Qur’ani na dini. Ndio, kuna baadhi ya vijana wetu wanasoma Qur’ani vizuri na wanafuata mafunzo yake, lakini wao hawajajifunza kuisoma wala hawakujifunza kwa njia ya madrasa bali ni kwa njia ya wazazi wao au jamaa zao wenye kushikamana na dini, au kupitia taasisi za kufundisha Qur’ani tukufu, miskitini na shuleni, Mwenyezi Mungu awalipe kheri.
QUR’ANI NI CHANZO CHA KUSONGA MBELE NA KUENDELEA Aliulizwa Abu Al-Hasan (a.s.): “Mwenyezi Mungu anijaalie niwe fidia kwako, nieleze Nabii (s.a.w.w.) aliwarithi Manabii wote?” Akasema: “Ndio,” nikasema “Kuanzia Adam hadi akamalizia kwake?” Akasema: “Mwenyezi Mungu hakutuma Mtume ila Muhammad (s.a.w.w.) ni mjuzi zaidi kuliko yeye.” Nikasema: “Isa bin Mariam alikuwa anahuisha wafu kwa idhini ya Mwenyezi Mungu?” Akasema: “Kweli, na Suleimani bin Daud alikuwa anafahamu milio ya ndege, na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuwa anaweza yote hayo.” 50
Page 50
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto Akasema: “Hakika Suleiman bin Daud alisema kuhusu Hud hud alipomkosa na kushuku katika jambo lake: “Vipi, mbona simuoni Hudi hud au ni kati ya wasio kuwepo.”65 Alipomkosa akakasirika akasema: “Nitamwadhibu adhabu kali au nitamchinja au anipe hoja iliyo wazi.”66 Alikasirika kwa sababu alikuwa anamuonyesha maji, huyu ndiye ndege ambaye alipewa asiyopewa Suleiman. Japo kuwa upepo, mdudu chungu, Majini, mashetani na wanadamu vyote vilikuwa vikimtii lakini havikuwa vikijua maji yalipo chini ya anga na ndege huyu ndiye alikuwa akijua. Mwenyezi Mungu anasema katika kitabu chake: “Kama Qur’ani ingekuwa ndiyo inayoendeshewa mlima na kupasuliwa ardhi na kusemeshwa wafu.”67 Bila shaka sisi tumerithi Qur’ani hii, ambayo humo yamo yanayopeperusha majabali na kukata masafa ya nchi na kwayo wafu wanafufuliwa na sisi tunajua maji yapo chini ya anga. Ndani ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu kuna Aya ambazo haombwi kwazo jambo ila Mwenyezi Mungu huruhusu. Japo kwamba Mwenyezi Mungu anaweza kuruhusu aliyowaandikia waliotangulia ameyajaalia kwetu katika Umul-Kitab, kwani Mwenyezi Mungu anasema: “Hakuna ghaibu katika mbingu wala katika ardhi ila ipo katika kitabu kilicho wazi.”68 Kisha akasema: “Tumewarithisha kitabu wale ambao tumewateua katika waja wetu.” 69 Sisi ndio aliotuteua Mwenyezi Mungu Mtukufu na ameturithisha kitabu hiki ambacho humo umo ubainifu wa kila kitu.”70 Hivyo Qur’ani tukufu ni chanzo cha msingi wa maendeleo, kusonga mbele na kufaulu duniani na akhera. Na tukitaka kujua chochote katika hila za 65 Suratun-Namli: 20 66 Suratun-Namli: 21 67 Suratur-Raad: 31 68 Suratun-Namli: 75 69 Suratul Fatwir: 32 70 Al-Kafi Jz. 1, uk: 226 Babu annal Aimmata warathuu ilman nabiyi wa jami’il ambiyai, hadith ya 7
51
Page 51
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto maadui wa Uislamu na mbinu zao za kishetani dhidi ya Uislamu, tutaona ni namna gani wao wanaipiga vita Qur’ani; na wanakwenda mbio kuuweka umma mbali nayo. Tunanukuu maneno haya kutoka kwa mmoja wa viongozi wao ili vijana wetu waelewe umuhimu wa Qur’ani tukufu na ulazima wa kufanya tadaburi humo na kuifanyia kazi ili kuamsha umma wetu wa Kiislam ambapo Qur’ani ni chimbuko la siri ya nguvu yetu na maendeleo yetu. Huyu anasema katika moja ya vikao vyao vya kupanga njama na Qur’ani ipo mkononi mwake: “Mkitaka kuimarisha utawala wenu katika nchi za Kiislamu basi ni juu yenu kuchukua kitabu hiki kutoka katika mikono ya waislam kwa sababu kitabu hiki ndio chimbuko la uchumi, uongozi, azma, jamii, familia, malezi na ukamilifu wa fikra za waislamu.” Ndio, maadui wa Uislamu wametambua kuwa Qur’ani tukufu ni chimbuko la nguvu yetu, ni alama ya ustaarabu wetu na maendeleo yetu. Wakapanga kwa umakini wa hali ya juu ili kutuweka mbali na Qur’ani. Hivyo ni wajibu wetu umma wa Kiislamu kurejea kwenye Qur’ani tukufu, tufanye bidii kujifunza na kutekeleza hukumu zake, kuiingiza katika mitaala yetu ya kufundishia katika kila hatua za masomo, kuhuisha hafla za Qur’ani katika miskiti, kwenye Huseiniya, majumbani na kutoa umuhimu mkubwa katika kusoma Qur’ani, tajwid, kuhifadhi, kuisoma vizuri, kuijua, kufanya tadabur, kujua hukumu zake na kuzitekeleza kwa sababu Qur’ani ni kitabu cha maisha, maendeleo, utukufu na ni muongozo katika dunia na akhera. Imepokewa kutoka kwa Imam Amirul-Mu’minin (a.s.) kwamba amesema: “Allah allah katika Qur’ani, wasikutangulieni watu wengine kuifanyia kazi.”71 Ewe Mwenyezi Mungu tunufaishe kwa Qur’ani tukufu, ee Mwenyezi Mungu tujaalie katika wale wanaoamini ukweli wake na kufuata njia yake, 71 Nahjul-Balaghah, khutuba ya 37
52
Page 52
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto na kuchunga haki zake na kufuata amri zake, na kuogopa makatazo yake na kuongoka kwa muongozo wake, na kutosheka na malipo ya hazina yake, kwa rehema zako, ewe Mwingi wa rehema.”72
KATIKA UONGOFU WA QUR’ANI Kutumwa kwa Manabii na malengo yake amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Tulikwisha kuwatuma Mitume wetu kwa ubainifu na tumeteremsha pamoja nao kitabu na mizani ili wawaongoze watu kwa haki”73 Na amesema (s.w.t.): “Mimi sitaki ila kutengeneza kwa kadri niwezavyo na taufiki ni ya Mwenyezi Mungu, kwake nimetegemea na kwake narejea.”74 Na amesema (s.w.t.): “Mtume anawasomea Aya za Mwenyezi Mungu zilizo wazi ili awatoe walioamini na kutenda mema kutoka kwenye giza na kwenda kwenye nuru.” 75
QUR’ANI INATOA CHANGA MOTO KWA WANADAMU NA MAJINI Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Au wanasema ameizua, waambie walete Sura kumi mfano wake za kuzua na waiteni muwezao asiyekuwa Mwenyezi Mungu kama nyinyi ni wa kweli, kama hawataleta basi jueni kuwa imeteremshwa kwa elimu ya Mwenyezi Mungu, na hakuna mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu; je, mtakiri ?”76 72 Mustadrakul-Wasa’il, Jz. 4, uk. 379, Babu 45 hadith 4983 73 Suratul Hadid: 25 74 Suratul Hud: 88 75 Surat-Twalaqa:11 76 Suratu Hud: 13 - 14
53
Page 53
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto Na amesema (s.w.t.):
“Sema kama watakusanyika wanadamu na majini ili walete mfano wa hii Qur’ani, hawataleta mfano wake hata kama watasaidiana baadhi kwa baadhi yao.”Suratul Israi: 88 Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
“Au wanasema ameizua bali hawaamini, basi walete maneno mfano wake kama wao ni wakweli.Surat-Tur: 33 -34 Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
“Au wanasema ameizua! Sema: Basi leteni Sura mfano wake, na waiteni muwezao asiyekuwa Mwenyezi Mungu kama nyinyi ni wakweli” Suratul-Yunus : 38 Na akasema (s.w.t.):
“Kama mna shaka kwa tuliyoyateremsha kwa mja Wetu basi leteni Sura mfano wake na waiteni mashahidi wenu asiyekuwa Mwenyezi Mungu kama nyinyi ni wakweli.”Suratul-Baqara: 23 54
Page 54
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto
QUR’ANI IMEHIFADHIWA KUTOKANA NA UPOTOFU Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Hakika sisi tumeteremsha Qur’ani na sisi ni wenye kuihifadhi.” Suratul-Hijir: 9
“Na hakika ni Kitabu kitukufu hakipatwi na batili mbele yake wala nyumba yake. Kimeshuka kutoka kwa Mwenye hekima, Mwenye kuhimidiwa.”Suratul-Fuswilat: 41 - 42 Na amesema (s.w.t.):
“Na kama ingetoka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu wangekuta humo ikhtilafu nyingi.”Suratun-Nisai: 82
55
Page 55
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto “Tumeshawajia na Kitabu, tumekibainisha kwa elimu na uongofu, na ni rehema kwa watu wenye kuamini je, hawasubiri ila taawili yake, siku itakapokuja taawili yake watasema wale walioisahau: kabla yake walikuja Mitume wa Mola wetu kwa haki.” Suratul-A’araf: 52 -53
UTAFITI KATIKA QUR’ANI Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
“Imekujieni kutoka kwa Mwenyezi Mungu nuru na Kitabu kilicho wazi, kwacho Mwenyezi Mungu anamuongoza mwenye kufuata radhi zake njia ya sawa, na anawatoa katika giza kwenda kwenye nuru kwa idhini yake na kuwaongoza kwenye njia iliyonyooka” SuratalMaidah: 15-16 Na amesema:
“Kitabu tumekiteremsha kwako kimebainishwa ili watafakari Aya zake na ili wakumbuke wenye akili.” Suratu Swad: 29 Na amesema:
56
Page 56
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto
“Je! Hawaitafakari Qur’ani, au nyoyo zao zimetiwa kufuli.” Suratu Muhammad: 24
KATIKA UBAINIFU WA SUNNA Kutosheleza na ukamilifu katika Qur’ani Amesema Imam Ali (a.s.): “….. jueni kuwa hii Qur’ani ni mtoa nasaha asiyedanganya, muongozaji asiyepoteza na msemaji asiyesema uongo.”77 Na amesema Imam Baqir (a.s.) katika kauli yake (s.w.t.): “Hakika wale waliokufuru kitabu kilipowajia,”78 yaani Qur’ani haipatwi na batili mbele yake “akasema haipatwi na batili kutoka katika Torati, Injili na Zaburi” na nyuma yake yaani hakitakuja kitabu baada yake kuitengua.79 Na amesema Abu Abdillah (a.s.) alipoulizwa na mwanaume mmoja; akasema: “Qur’ani ina nini haiongezeki wakati wa kuitangaza na kuifundisha isipokuwa upya?” Akasema: “Kwa sababu Mwenyezi Mungu hakuiteremsha kwa ajili ya zama fulani tu bila ya zama nyingine wala kwa kaumu fulani bila ya kaumu nyingine, katika kila zama ni mpya na kwa kila kaumu ni mpya hadi siku 77 Mustadrakul wasail: J: 4 Uk: 239 babu 3 hadith 4594 78 Suratu Fuswilat: 41 79 Tafsir Nuru Thaqalayni: Jz. 4, uk. 553, hadith ya 67
57
Page 57
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto ya Kiyama”80 Na amesema Imam Ridha (a.s.) katika kuitaja Qur’ani tukufu kuwa ukubwa wa hoja humo na Aya za muujiza ni katika mpangilio wake: “Hakika hii Qur’ani ni kamba ya Mwenyezi Mungu madhubuti hadi aliposema “haijaletwa kwa zama fulani wala kwa lugha fulani tu, kwani haijafanywa ni mahusus kwa ajili ya zama fulani bila ya zama zingine, bali imefanywa kuwa ni hoja na dalili, ni hoja kwa kila binadamu, haipatwi na batili mbele yake wala nyuma yake, imeteremka kutoka kwa Mwenye hekima, Mtukufu.”81
QUR’ANI INATOA CHANGAMOTO KWA VIZAZI Amesema Imam Musa bin Ja’far (a.s.) katika kauli yake (s.w.t.):
80Uyunil-Akhbar-Ridhaa, Jz. 2, uk. 87, Babu 22 hadith ya 32 81 Uyunul-Akhbar, Jz. 2, uk: 130, Babu 35 hadith ya 9
58
Page 58
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto “Kama mna shaka kwa yale tuliyomteremshia mja Wetu basi leteni Sura moja mfano wake; na waiteni mashahidi wenu asiyekuwa Mwenyezi Mungu kama nyinyi ni wa kweli, kama hamtaleta basi hamtoleta, basi ogopeni moto ambao kuni zake ni watu na mawe, umeandaliwa kwa makafiri. Wabashirie walioamini na kufanya mema kwamba wanayo Pepo inayopita mito chini yake, kila wanapopewa riziki katika matunda wanasema: haya ni ambayo tuliruzukiwa kabla, na wamepewa mfano wake, na humo kuna wanawake watoharifu, watakaa humo milele.” Suratul-Baqarah: 23 - 25 Mwenyezi Mungu alipopiga mfano wa makafiri wanaopinga utume wa Muhammad (s.a.w.w.), maadui na wanafiki kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, wenye kupinga aliyoyasema Muhammad kwa ndugu yake Ali (a.s.), na wanapinga kuwa aliyoyasema hayatoki kwa Mwenyezi Mungu, nazo ni Aya za Muhammad na miujiza yake kwa kuongezea Aya zake ambazo amezibainisha kwa Ali (a.s.) Makka na Madina, hawakuzidisha isipokuwa uadui na uasi, Mwenyezi Mungu akasema kwa wajeuri wa Makka na waasi wa Madina: “Kama mna shaka kwa yale tuliyomteremshia mja wetu” hadi mpinge kuwa Muhammad si Mtume wa Mwenyezi Mungu na kwamba haya yaliyoteremshwa sio maneno Yangu; pamoja na kudhihiri miujiza yenye kushangaza Makka, kama vile mawingu yaliyokuwa yakimfunika wakati wa safari zake na vitu viliyokuwa vikimsalimia kama vile milima, mawe, changarawe na miti. Na kama vile kuwazuia wanaotaka kumuua Mtume na kuwaua, na mfano wa miti miwili iliyo mbalimbali iliyoungana naye akakaa nyuma yake na kukidhi haja yake, kisha ikarejea sehemu zake kama ilivyokuwa. Na mfano wa kuuita kwake mti na ukaja kwa kuitika wito hali yakuwa ni wenye kunyenyekea na dhalili, kisha akauamrisha ukarejea kwa utiifu “ leteni” enyi Makuraishi na wayahudi na enyi wakanushaji na wanafiki wanaodai kuwa ni waislam na ambao wako mbali nao na enyi waarabu wenye balagha na fasaha ya lugha “Sura moja tu mfano wake,” mfano wa aliyoleta Muhammad (s.a.w.w.) kati ya wanaume 59
Page 59
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto mfano wenu asiyejua kusoma wala kuandika na wala hajasoma kitabu chochote na hajakutana na wanachuoni wala hajajifunza kwa yeyote, nanyi mnamjua katika safari zake na pasipokuwa na safari. Amebakia hivyo kwa miaka arobaini, kisha akapewa elimu yote hadi akajua elimu ya waliotangulia na wajao, kama mna shaka katika aya hizi basi leteni mfano wa mtu huyu na mfano wa maneno haya ili ibainike kuwa yeye ni muongo kama mnavyodai; kwa sababu kila ambacho hakitoki kwa Mwenyezi Mungu basi utapata mfano wake katika viumbe vya Mwenyezi Mungu. Na kama mkiwa na shaka; enyi wasomaji wa vitabu vya wayahudi na manaswara, katika yale aliyokuja nayo Muhammad (s.a.w.w.) kati ya sharia zake na kumsimika ndugu yake kuwa bwana wa mawasii kuwa wasii baada ya kudhihiri kwenu miujiza yake ambayo kati yake ni kwamba, nyama ya mkono yenye sumu ilimsemesha, mbwa mwitu alimsemesha na kijiti kilimnyenyekea naye yuko katika mimbari na Mwenyezi Mungu alimkinga kutokana na sumu aliyolishwa na myahudi katika chakula chake na kuwageuzia kuwa balaa kwao ikawaangamiza na kukifanya chakula kichache kuwa kingi, “basi leteni Sura moja mfano wake.” Yaani mfano wa hii Qur’ani kutoka katika Torati, Injili, Zaburi kitabu cha Ibrahim na vitabu kumi na nne; hakika hamtopata katika vitabu vingine vya Mwenyezi Mungu, Sura mfano wa Sura za hii Qur’ani, itakuwaje maneno ya Muhammad ya kuzua yawe bora kuliko maneno mengine ya Mwenyezi Mungu na vitabu vyake, enyi wayahudi na manaswara? Kisha akawaambia jamaa zao, “waleteni mashahidi wasiokuwa Mwenyezi Mungu,” yaiteni masanamu yenu mnayoyaabudu enyi washirikina, na waiteni mashetani wenu enyi wayahudi na manaswara, na waiteni ndugu zenu kati ya walahidi enyi wanafiki wa kiislam kati ya maadui wa kizazi cha Muhammad kitukufu na wasaidizi wenu katika rai zenu “kama nyinyi ni wa kweli.” Kwamba Muhammad amezua hii Qur’ani yeye mwenyewe na wala hakuiteremsha Mwenyezi Mungu kwake, na kwamba aliyoyasema katika fadhila za Ali (a.s.) kwa umma wake wote, na akampa uongozi wao sio kutoka kwa Mwenyezi Mungu. 60
Page 60
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto Kisha akasema (s.w.t.): “Kama hamtafanya” yaani hamtaleta enyi mlioshindwa kwa hoja ya Mola wa walimwengu “na wala hamtaleta,” yaani hili halitawezekana kwenu abadan, “basi uogopeni moto ambao kuni zake ni watu na mawe,” utawashwa na utakuwa, ni adhabu kwa watu wake, “umeandaliwa kwa makafiri,” wenye kukanusha maneno ya Mwenyezi Mungu na Nabii wake, wenye kumfanyia uadui walii wake na wasii wake, akasema: “Basi tambueni kushindwa kwenu juu ya hilo, kwamba ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu; na kama ingetoka kwa viumbe mngeweza kuipinga. Waliposhindwa baada ya kuonywa, wakapewa changamoto, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Sema kama watakusanyika majini na wanadamu ili kuleta mfano wa hii Qur’ani hawatoleta mfano wake hata kama watasaidiana baadhi kwa baadhi yao.”82 na.83
QUR’ANI IMEHIFADHIWA KUTOKANA NA KUPOTOSHWA Amesema Amirul muuminina (a.s.): “Litamjia mmoja wenu jambo katika hukumu kati ya hukumu; atahukumu kwa rai yake, kisha jambo hilo hilo litamjia mwingine, atahukumu kinyume na kauli yake. Kisha makadhi watakusanyika kwa Imam aliyewapa ukadhi na atasahihisha rai zao zote, Mola wao ni mmoja, Nabii wao ni mmoja kitabu chao ni kimoja, je! Mwenyezi Mungu amewaamuru kutofautiana hivyo wakamtii, au amewakataza nao wakamwasi, au walishirikiana naye hivyo ni juu yao kusema, naye ni lazima aridhie au Mwenyezi Mungu ameteremsha dini kamilifu ila Nabii akazembea kufikisha na kuitekeleza? 82 Suratul-Israi: 88 83 Biharul-Anwar, Jz. 89, uk. 28; Babu 1 hadith ya 33
61
Page 61
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto Na Mwenyezi Mungu anasema: “Hatujaacha kitu chochote katika Kitabu.”84 Humo kuna ubainifu wa kila kitu na kitabu kinasadikisha baadhi yake na kwamba hakuna ikhitilifu humo, amesema (s.w.t.): “Kama kingetoka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu wangekuta humo ikhitilafu nyingi.” 85 Na kwamba dhahiri ya Qur’ani ni nzuri na undani wake ni mpana, maajabu yake hayaishi na upya wake haumaliziki na wala giza haliondolewi ila kwayo.86 Na amesema (a.s.): “Ni ambayo matamanio hayaipotoshi na wala haifunikwi na shaka na rai.”87 Na amesema Imam Baqir (a.s.): “Hakika Qur’ani ni moja, imeteremka kutoka kwa mmoja lakini ikhitilafu zinatoka kwa wapokezi.”88
KUIZINGATIA QUR’ANI Amesema Amirul-Mu’minina (a.s.): “Ee hakuna kheri katika kisomo kisichokuwa na kutafakari.”89 Na amesema Imam Ali (a.s.): “Zitafakarini aya za Qur’ani na zingatieni kwayo hakika ni mawaidha yenye mazingatio.”90Na amesema Imam Swadiq (a.s.): “Inampasa muumini asife hadi ajifunze Qur’ani au awe katika kujifunza.”91
84 Suratul An’am: 38 85 Suratul Nisai: 82 86 Al-Ihtijaj Jz. 1, uk. 261; Ihtiajjhi alaa man qala birayi fiy shar’i wal ikhitilaf fiy fat’wa 87 Ghurarul-Hikam wa durarul Kalim, uk. 110 Q 1 b4 f 4 hadith 1968 88 Al-Kafi, Jz. 2, uk. 630, Babun-Nawadir hadith 12 89 Al-Kafi, Jz. 1, uk. 36, Babu swifatil Ulamaa hadith 3 90 Ghurarul-Ahkam wa durarul Kalim, uk: 111 Q1 b 4 f4 hadith 1985 91 Al-Kafi, Jz. 2, uk. 607 Babu man yata’alamul Qur’ani bimashaqati hadith 3
62
Page 62
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto
THAWABU ZA KUSOMA QUR’ANI Amesema Imamul-Husein (a.s.): “Amesema Mtume (s.a.w.w.): “Hakika hii Qur’ani ni adabu za Mwenyezi Mungu Mtukufu; basi jifunzeni kutoka katika adabu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kadri muwezavyo, kwani ni nuru iliyo wazi na ponyo lenye manufaa hivyo jifundisheni, hakika Mwenyezi Mungu anawapokeeni kwa kujifunza Qur’ani jifunzeni SuratulBaqarah na Al-Imran, kuzichukua ni baraka na kuiacha ni hasara, nazo zitakuja siku ya Kiyama kana kwamba ni mawingu mawili au milima miwili au makundi mawili ya ndege waliojipanga safu, zitatoa hoja kwa msomaji wake na Mola wa walimwengu atasikia hoja zao, zitasema: “Ewe Mola, hakika mja wako huyu ametusoma na tumempa kiu mchana wake na tumemfanya akeshe usiku wake, tumeuchokesha mwili wake.” Hadi aliposema (a.s.): Amesema Mtume (s.a.w.w.), ‘hakika wazazi wa msomaji watavikwa taji la utukufu, nuru yake itaangaza kwa umbali wa mwendo wa miaka elfu kumi, na watafunikwa kwa nguo ambayo haiwezi kunyanyuliwa na watu wachache, na ni maradufu ya laki moja kwa yaliyopo duniani, kwa kujumuisha kwake kheri zote, kisha msomaji huyu atapewa ufalme kuliani kwake katika kitabu na kuishi milele kushotoni kwake katika kitabu, atasoma kutoka katika kitabu chake kuliani mwake, “umejaaliwa kuwa kati ya wafalme watukufu wa Peponi na kuwa kati ya marafiki wa Muhammad bwana wa Manabii na Ali bwana wa mawasii na Maimam baada yao ni mabwana wa wachamungu na atasoma kushotoni kwake katika kitabu, umehakikishiwa kutoondoka wala kuhama katika ufalme huu na umekingwa kutokana na mauti na magonjwa na umeepushwa na maradhi na magonjwa na umeepushwa na husuda za wenye husuda na hila za wenye hila.
63
Page 63
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto Kisha ataambiwa, soma na ukeshe, na makazi yako yapo mwisho wa Aya utakayoisoma, wazazi wake watakapotazama kwenye nguo zao na mataji yao watasema: “Mola wetu, utukufu wetu huu umetoka wapi na wala amali zetu hazijaufikia?” Wataambiwa na malaika watukufu: ‘Haya ni yenu kwa kumsomesha mtoto wenu Qur’ani kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: Alif laam miiym, hiki ni kitabu hakina shaka ndani yake, ni uongofu kwa wachamungu” 92na.93
92 Suratul-Baqarah: 1 -2 93 Tafsiru Imamul Askari (a.s.) uk: 60 Sura inayo elezea Suratul Baqarah hadith 31
64
Page 64
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto
ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION: 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24. 25. 26. 27. 28.
Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Ishirini Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo Juzuu ya kwanza Uharamisho wa uwongo Juzuu ya pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudharr Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur'an na Hadithi Elimu ya Nafsi Yajue Madhehebu ya Shia Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu Al-Wahda Ponyo kutoka katika Qur'an. 65
Page 65
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto 29. 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52. 53. 54. 55. 56. 57. 58. 59. 60. 61.
Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii Mashukio ya Akhera Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyeezi Mungu na sifa zake Amateka Na Aba'Khalifa Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana. Upendo katika Ukristo na Uislamu Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya Kupaka juu ya khofu Kukusanya swala mbili Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kusujudu juu ya udongo Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) Tarawehe Malumbano baina ya Sunni na Shia Kupunguza Swala safarini Kufungua safarini Umaasumu wa Manabii Qur’an inatoa changamoto as-Salaatu Khayrun Mina -'n Nawm Uadilifu wa Masahaba Dua e Kumayl Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mitume Muhammad (s) Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza 66
Page 66
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
Qur’ani Yatoa Changamoto 62. 63. 64. 65. 66. 67. 68. 69. 70. 71. 72. 73. 74. 75. 76. 77. 78.
Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili Kuzuru Makaburi Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu Tujifunze Misingi Ya Dini Sala ni Nguzo ya Dini Mikesha Ya Peshawar Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliy onyooka Shia asema haya, Sunni asema haya, Wewe wasemaje? Liqaa-u-llaah Muhammad (s) Mtume wa Allah Amani na Jihadi Katika Uislamu Uislamu Ulienea Vipi? Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s)
67
11:42 AM
Page 67
Qur_an_inatoa_changa_moto[1]..EDITED.doc final edit Lubumba.qxd
7/15/2011
11:42 AM
Qur’ani Yatoa Changamoto
BACK COVER Qur’ani Tukufu ni nuru isiyozimika mwanga wake, ni taa isiyokoma kuwaka kwake, ni bahari isiyofahamika kina chake, ni mfumo usiopotea njia yake, ni mshumaa usio na kiza katika mwanga wake, ni upambanuzi usiozimwa hoja yake, ni ubainifu usiovunjwa nguzo zake, na ni nguvu wasioshindwa wafuasi wake. Umma wa Kiislamu unamiliki desturi kuu na mfumo ambao wanadamu wameutambua katika historia yake kongwe. Qur’ani Tukufu ni muujiza mkuu wa maisha wenye kudumu milele. Yatosha kwa muujiza huu kuwa ni fahari na utukufu kwamba ni Kitabu kitokacho kwa Mwenyezi Mungu, na ni maneno Yake matukufu ambayo aya zake zimeteremka katika vifua vitoharifu na nyoyo takatifu, basi zikawa ni nuru inayouangazia ulimwengu kwa maarifa mbalimbali na kuufanya upande daraja na kufikia ukamilifu. Kimetolewa na kuchapishwa na: Al-Itrah Foundation S.L.P - 19701. Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu / Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info
68
Page 68