SAADA KAMILI (KITABU CHA KIADA CHA MAADILI)
السعادة الكاملة
Kimeandikwa na: Muhammad Mahdi bin Abu Dharr al-Naraqi
Kimetarjumiwa na: Salman Shou
ترجمة
السعادة الكاملة
تأليف محمد مهدي ابن أبي ذر النراقي
من اللغة اإلنجليزية الى اللغة السواحلية
©Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 –17 – 067 – 8 Kimeandikwa na: Muhammad Mahdi bin Abu Dharr al-Naraqi Kimetarjumiwa na: Salman Shou Kimehaririwa na: Al-Hajj Ramadhani S. K. Shemahimbo Kimepitiwa na: Al-Hajj Hemedi Lubumba Selemani na Mbarak A. Nkanatila Kimepangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation Toleo la kwanza: Agosti, 2014 Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. - 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: www.alitrah.info
YALIYOMO Neno la Mchapishaji........................................................................1 Kuhusu Kitabu.................................................................................3 Sifa bainifu za mwili na Nafsi.........................................................4 Maana na Chimbuko la Tabia (Akhlaq)...........................................7 Utakaso na Upambaji wa Nafsi......................................................10 Nguvu ya Nafsi: Athari na Sifa zake Bainifu.................................12 Nafsi na Amri Zake........................................................................14 Furaha na Uchungu........................................................................17 Wema na Furaha............................................................................19 Tabia Njema na Mbaya..................................................................20 Wastani na Mkengeuko..................................................................22 Aina mbalimbali za Uovu..............................................................23 Umuhimu wa Haki.........................................................................31 Aina mbalimbali za Haki...............................................................32 Kujiendeleza Mwenyewe...............................................................35 Maradhi ya Nafsi na Tiba Zake......................................................36 Tiba ya Maradhi ya Nguvu ya Akili na Tiba yake.........................38
(a)
Hali ya Kupindukia:........................................................38
(b)
Hali ya Upungufu:..........................................................39
(c)
Hali ya Wastani...............................................................39 v
SAADA KAMILI
Uovu mwingine unaohusiana na nguvu ya Akili...........................44
(1)
Ujinga mchanganyiko:....................................................44
(2)
Mfadhaiko na Shaka:......................................................45
Ishara za Watu wenye kusadikisha.................................................45 Hatua za Yakini..............................................................................47 (3) Shirk (ushirikina)............................................................49
(4)
Vishawishi na ufahamu wa Kishetani.............................51
(5)
Udanganyifu na Hila.......................................................52
Maradhi ya Nguvu ya Hasira na Tiba Yake...................................53
(a)
Hali ya kuzidi kiasi.........................................................53
(b)
Hali ya Upungufu...........................................................54
(c)
Hali ya Wastani...............................................................54
Uovu mwingine wa Nguvu ya Hasira............................................55
1. Hofu.....................................................................................55
2. Kujidhalilisha au Kutojiamini..............................................58
3. Ukimya.................................................................................60
4. Kutokuwa na hisia za heshima.............................................60
5. Kufanya Jambo Kwa Pupa...................................................61
6. Chuki kwa Muumba na Viumbe Wake................................61
7. Hasira...................................................................................63
8. Vurugu..................................................................................65 vi
SAADA KAMILI
9. Chuki....................................................................................66
10. Tabia ya Kinyongo..........................................................66
11. Tabia ya majivuno na kiburi..........................................67
12. Ufidhuli...........................................................................69
13. Hali ya Uasi....................................................................71
14. Mtu kushindwa kuona dosari zake.................................72
15. Ushabiki..........................................................................72
16. Kuficha Haki...................................................................73
17. Usugu na Ukatili.............................................................74
Maovu ya Nguvu ya Matamanio....................................................75
1. Kupenda Dunia....................................................................75
2. Kupenda Mali na Utajiri......................................................76
3. Ukwasi na Utajiri.................................................................79
4. Ulafi (Hirs)...........................................................................80
5. Tamaa...................................................................................81
6. Ubakhili [Bukhl]...................................................................82
7. Kipato cha haramu...............................................................83
8. Usaliti [Khiyaanah]..............................................................85
9. Uasherati na Ufisadi.............................................................86
10. Kuchimba sana kwenye Mambo Machafu na Haramu......83 vii
SAADA KAMILI
Maradhi ya pamoja ya nguvu ya Akili, Hasira na Tamaa..............87
1. Husuda (Hasad)....................................................................88
2. Kubughudhi na Kutusi Watu Wengine. ...............................89
3. Kutishia na Kusumbua Waislamu........................................89
4. Kutojali Mambo ya Waislamu..............................................90
5. Uzembe katika Kutekeleza Wajibu wa.................................92
6. Kutopenda kuchanganyika na watu......................................92
7. Kuvunja uhusiano na familia na ndugu. ..............................93
8. Kutowajibika kwa Wazazi....................................................93
9. Kutafuta Dosari za Wengine na Kufichua Mapungufu yao au Makosa yao...........................................94
10. Kufichua Siri za Wengine...................................................94
11. Shamaatah [Kufurahia Mabalaa ya Wengine.] ..................95
12. Kudhihaki na Kuzua Mjadala [Ta‘n wa Mujaadalah] .......96
13. Kuwadhihaki na Kuwafanyia Mzaha Watu Wengine. .......96
14. Utani. .................................................................................96
15. Kusengenya [Ghi‘bah] ......................................................97
16. Kusema uwongo ................................................................97
17. Kujionyesha [Riyaa`] ........................................................97
18. Unafiki (Nifaq)...................................................................99
19. Majivuno.[Ghuruur]...........................................................99 viii
SAADA KAMILI
20. Kuwa na Matumaini na Matakwa Makubwa na ya Mbali kabisa................................................................101
21. Uasi [‘Isyaan]...................................................................102
22. Utovu wa Haya.................................................................102
23. Kung`ang`ania Kutenda Dhambi.....................................102
24. Uzembe [Ghaflah]............................................................103
25. Karaha [Karahah].............................................................104
26. Sakhat...............................................................................107 27. Huzn (Huzuni)..................................................................108
28. Kukosekana Imani kwa Allah..........................................108
29. Utovu wa Shukurani (Kufraan)........................................109
30. Kuwa na Wahaka (Jaza‘)................................................. 110
31. Uasi wa wazi.................................................................... 112
Dua ya Imam Ali bin Husain Zainul-Abidin (a.s.) katika kuomba Tabia Njema........................................................ 115
ix
SAADA KAMILI
بسم اهلل الرحمن الرحيم NENO LA MCHAPISHAJI
K
itabu ulichonacho mikononi mwako ambacho asili yake ni cha Kiarabu kinaitwa, Jami’u ‘s-Sa’aadah. Kitabu hiki, alhamdulillah, kimetarjumiwa kwa Kiswahili kutoka Kiingereza na tumekiita, Saada Kamili (Kitabu cha Kiada cha Maadili). Maudhui ya kitabu hiki yanahusu maadili katika karibu kila kipengee cha maisha ya mwanadamu. Mwandishi amejadili kwa mapana na marefu masuala ya kimaadili ambayo yanamwangusha au yanamfanikisha mwanadamu. Aidha, ameonyesha ufumbuzi na mwongozo kwa ajili ya kurekebisha au kuboresha maadili. Sisi kama wachapishaji, tunapenda kujulisha kitabu hiki kama kilivyo kwa wasomaji wetu na kuwashauri wayasome yaliyomo humu, wayafanyie kazi na kuyazingatia na kufaidika na hazina iliyomo ndani yake. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa makubwa hususan wakati huu wa sayansi na tekinolojia kubwa ambapo ngano, hadithi za kale na upotoshaji wa historia ni vitu ambavyo havina nafasi kwa watu wa sasa. Taasisi yetu ya Al-Itrah imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili. Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni chenye manufaa makubwa kwao. 1
SAADA KAMILI
Tunamshukuru ndugu yetu Salman Shou kwa kufanikisha tarjuma ya kitabu hiki katika lugha ya Kiswahili, pia na wale wote waliosaidia kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha toleo hili kuchapishwa na kuwa mikononi mwa wasomaji. Allah Mwenye kujazi awalipe wote malipo mema hapa duniani na huko Akhera pia. Amin! Mchapishaji: Al-Itrah Foundation
2
SAADA KAMILI
بسم اهلل الرحمن الرحيم Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.
KUHUSU KITABU
“M
aadili” ni mojawapo ya sayansi muhimu sana za Kislamu. Katika muda wote wa historia tukufu ya Uislamu, wanazuo wakubwa wa Kislamu wamebobea katika nyanja hii na kuandika vitabu muhimu na vya kuthaminiwa kuhusu somo hili. Kitabu kiitwacho Jami‘ al-Sadat (mkusanyaji wa elimu fasaha), ambacho kimeandikwa na mwanazuo mkubwa wa Kislamu aliyebobea katika uchaji Mungu, mtawa, na mwanafalsafa katika nyanja ya maadili, Muhammad Mahdi ibn Abi Zarr al-Naraq, ambaye alikuwa mfano wa matendo mema ya kimaadili, ni miongoni mwa vitabu vizuri sana vyenye maarifa mengi. Kitabu hiki kiliandikwa kwa lugha ya Kiarabu, halafu kikachapishwa katika juzuu tatu (kurasa 1200). AlNaraq alikuwa miongoni mwa wanazuo waliobobea katika nyanja ya tafakuri wa karne ya 12/18 hadi 13/19. Licha ya Jami‘al-Sadat, al-Naraq pia aliandika vitabu kadhaa muhimu Tukiwa katika jitihada za kuhuisha maadili ya Kislamu kwenye ulimwengu unaozama kwenye vurugu za anasa za kidunia na kuashiria kusahaulika kabisa thamani ya maisha ya binadamu ya milele Akhera, tulifikiria ni juhudi yenye manufaa kukusanya kazi hii ya kuthaminika katika makala chache kwa manufaa ya wale ambao hawatapata fursa ya kupata yote yaliyo katika lugha ya Kiarabu.
3
SAADA KAMILI
بسم اهلل الرحمن الرحيم SIFA BAINIFU ZA MWILI NA NAFSI
B
inadamu ana nafsi na mwili, kila kimoja ya vitu hivi kinatawaliwa na burudani zake na maradhi yake. Kinachodhuru mwili ni ugonjwa, na kile kinachoupatia mwili burudani kipo kwenye ustawi wake, yaani afya njema na chochote kile kinachoendana na maumbile yake. Sayansi inayoshughulikia afya na maradhi ya mwili ni sayansi ya tiba. Maradhi ya nafsi ni matendo maovu na kuridhia tamaa zinazoshusha daraja la binadamu hadi kuwa chini ya daraja la hayawani. Burudani za nafsi ni matendo mema na maadili, vitu ambavyo humnyanyua binadamu na kumpeleka karibu zaidi na ukamilifu na busara na kumfikisha karibu na Allah. Mafunzo yanayoshughulikia mambo hayo ni sayansi ya maadili (ilm al-akhlaq).
Kabla hatujaanza kuzungumzia mada kuu za somo letu, lazima tuthibitishe kwamba nafsi ya binadamu haina umbo, yenyewe si tegemezi kwa mwili, na haigusiki. Ili kuweza kuthibitisha usemi huu, zipo hoja kadhaa na miongoni mwao zinatajwa ifuatavyo: i.
Mojawapo ya sifa bainifu za miili ni kwamba wakati wowote sura na maumbo mapya yakiingia mwilini, mwili hukataa na huacha umbo lake la kawaida au sura yake ya kawaida. Hata hivyo, katika nafsi ya binadamu, maumbo mapya yanayoonekana kupitia milango ya fahamu au kiakili yanayoingia mfululizo hayafuti maumbo ya kwanza. Kwa hakika, kadiri maumbo mengi yanavyoingia akilini, ndivyo nafsi inavyokuwa imara. 4
SAADA KAMILI
ii. Elementi tatu: rangi, harufu na ladha zinapoonekana kwenye kitu; kitu hicho hubadilika. Lakini, nafsi ya binadamu huzipokea elementi hizo zote bila kuathiriwa kimwili. iii. Burudani ambazo binadamu huzipata kupitia utambuzi wa akili zinaweza kuwa kwa ajili ya nafsi tu, kwani mwili wa binadamu hauwajibiki kwa vyovyote ndani yake. iv. Maumbo ya kinadharia na dhana yanayotambuliwa na akili, bila shaka hayagusiki na hayagawanyiki. Kufuatana na hali hiyo, nafsi, ambamo ndimo maumbo hayo hupita, pia lazima isigawanyike, na kwa hiyo haigusiki. v.
Binadamu anao uwezo wa kupokea mambo kupitia milango mitano ya fahamu, ambapo nafsi ya binadamu hutambua vitu fulani bila msaada wa milango ya fahamu. Miongoni mwa vitu ambavyo nafsi ya binadamu huvitambua bila kutegemea milango ya fahamu ni kanuni ya ukinzani, fikra kwamba kitu kizima siku zote ni kikubwa kuliko moja ya sehemu yake, na kanuni zingine kama hizo ambazo zinajulikana ulimwenguni. Ukanushaji wa makosa yanayofanywa na milango ya fahamu unaofanywa na nafsi kama vile vitu vionekanavyo kwa macho, hufanywa kwa msaada wa nadharia ya kifikra, pamoja na kwamba vitu hivyo hupita kwenye milango ya fahamu.
Sasa kwa vile uwepo wa kujitegemea wa nafsi umethibitishwa, hebu na tuangalie vitu ambavyo huifanya nafsi iwe na ustawi na furaha, na ni vitu gani vinavyoifanya nafsi iuguwe na kukosa furaha. Afya na ukamilifu wa nafsi upo katika ufahamu wa uhalisia wa maumbile ya vitu, na uelewa huu unaweza kuipatia uhuru na kuitoa 5
SAADA KAMILI
kwenye jela finyu ya tamaa na ulafi na vizuizi vingine vyote vinavyozuia mageuzi na ujenzi wa maadili kuelekea kwenye hatua ya mwisho ya ukamilifu wa mwanadamu ambao umo kwenye ukaribu wa mtu na Allah. Hili ni lengo la “busara ya kinadharia” (al-hikmat al-nazariyyah). Wakati huo huo, nafsi ya binadamu lazima ijitakase ili isije ikakumbwa na tabia na sifa mbaya, na badala yake ikumbatie mwenendo na fikra za kimaadili. Hili ni lengo la “busara ya kimaumbile”(al-hikmat al-amalliyah). Busara ya kinadharia na busara ya kimaumbile zinahusiana kama vile ilivyo kwa kitu kinachogusika na umbo, haviwezi kuwepo bila kingine kuwepo. Kama jambo la kanuni, neno “falsafa” linarejelea “busara ya kinadharia” na “maadili” linarejelea “busara ya kimaumbile.” Mtu ambaye ni stadi wa busara ya kinadharia na busara ya kimaumbile ni kama mfano mdogo wa ulimwengu mpana kwa ujumla.
6
SAADA KAMILI
MAANA NA CHIMBUKO LA TABIA (AKHLAQ)
N
eno akhlaq ni wingi wa neno khulq ambalo maana yake ni tabia. “Tabia� ni ule uwezo (malakah) wa nafsi, ambayo ndio chanzo cha matendo yote ambayo binadamu huyafanya papo kwa papo bila kuyafikiria. Uwezo (malakah) ni rasilimali ya nafsi ambao kuwepo kwake husababishwa na mazoezi yanayofanyika kwa kurudiarudia na si rahisi kuiharibu. Tabia (malakah) ya pekee inaweza kujitokeza kwa binadamu kwa ajili ya mojawapo ya sababu zifuatazo: i.
Asili na muonekano wa kimaumbile: Imechunguzwa na kuonekana kwamba baadhi ya watu ni wavumilivu ambapo wengine wana hamaki na kiherehere. Wengine huvurugikiwa na kuhuzunika kwa urahisi ambapo wengine wanaonyesha kujizuia na kutulia kukubwa.
ii. Tabia: Ambayo hufanyizwa kwa sababu ya kufanya matendo fulani kwa mfululizo, kurudiarudia kwa muda mrefu na hivyo kusababisha kujitokeza kwa tabia fulani. iii. Dhamira ya makusudi ya kujizoeza: Ambayo kama ikiendelezwa kwa kipindi kirefu cha kutosha hatimaye itasababisha kujengeka kwa tabia. Hata hivyo, muonekano wa kimaumbile wa mtu husababisha mhusika kuwa na tabia fulani, kwa vyovyote vile si kweli kwamba binadamu hana hiari katika jambo analolifanya na kwamba analazimishwa kutii amri ya umbile lake. Kinyume chake ni kwamba, kwa 7
SAADA KAMILI
kuwa binadamu anao uwezo wa kuchagua, anaweza kukataa kutii amri ya asili ya umbile lake kupitia juhudi ya kujizoeza, na anaweza kupata tabia anayoitaka. Kama mambo yalivyo, ni vema kukiri kwamba tabia zinazosababishwa na uwezo wa ubongo kama vile akili, kumbukumbu, ukakamavu wa akili na mengine yafananayo na hayo, hazibadiliki. Hata hivyo, tabia zingine zote zinaweza kubadilika kafuatana na utashi wa mhusika. Binadamu anaweza kudhibiti tamaa yake, hasira na mihemko mingine na shauku na kuziweka kwenye mkondo wa kujirekebisha na kumfikisha kwenye njia ya ukamilifu na busara. Tunapozungumzia uwezo wa binadamu kufanya mabadiliko ya tabia zake, hatumaanishi kwamba aziharibu silika zake za uzazi au uhifadhi. Binadamu hangeweza kuwepo bila ya silika hizi. Tunachomaanisha ni kwamba mhusika anatakiwa aepuke kufika kwenye ncha zinazochupa mipaka, mhusika anatakiwa kuwa katika hali ya uwiano na kiasi ili silika hizi ziweze kufanya kazi zao inavyotakiwa. Kama vile mbegu ya mtende inavyoota na kuwa mti unaozaa matunda baada ya kupata matunzo mazuri, au farasi wa msituni anapofundishwa namna ya kumhudumia bwana wake, au mbwa anapofundishwa kuwa rafiki wa maisha wa binadamu, ndivyo pia binadamu anavyoweza kupata ukamilifu na busara kwa kujizoeza nidhamu na kuvumilia kiakili. Ukamilifu wa binadamu una viwango vingi. Ukubwa wa juhudi ya kujidhibiti kinidhamu unaofanywa na mhusika, ndivyo atakavyofanikiwa kufika kwenye kiwango cha juu zaidi cha ukamilifu. Kwa maneno mengine, mtu huyu atakuwa amesimama katikati ya ncha mbili zinazovuka mpaka wa kawaida, kiwango cha chini kabisa ni kile kinachokuwa chini ya kiwango cha hayawani na kiwango cha juu kabisa ni kile kinachopita kiwango cha malaika. Mwendo wa binadamu wa katikati ya hizi ncha mbili zinazovuka mpaka unazun8
SAADA KAMILI
gumuziwa na (ilm al-akhkaq) au sayansi ya maadili. Ni lengo la maadili kumnyanyua na kumuongoza binadamu kutoka kwenye hali ya hayawani wa chini kabisa hadi kwenye nafasi iliyotukuka kuzidi ile ya malaika. Umuhimu wa maadili unaonyeshwa namna hii. Na ni kwa ajili ya sababu zilizotajwa hapo juu kwamba sayansi ya maadili inafikiriwa kuwa tukufu na yenye thamani zaidi kuliko sayansi zingine, kwani thamani ya sayansi yoyote inahusishwa moja kwa moja na thamani ya somo husika, na kwa kuwa somo la sayansi ya maadili ni kuhusu binadamu na anavyoweza kupata ukamilifu. Zaidi ya hayo, tunajua kwamba binadamu ni kiumbe chenye daraja la juu sana kuliko viumbe vingine vyote, lengo lake la mwisho katika maisha yake ni kupata ukamilifu; kwa hiyo, maadili ni sayansi tukufu kuzidi sayansi zingine zote. Kwa hakika, wanafalsafa wa zamani hawakufikiria nyanja zingine za kusomea kwa kuwa waliona kwamba hazijitegemei. Waliamini kwamba bila ya sayansi ya maadili na utakaso wa kiroho, ustadi wa sayansi zingine zozote si tu kwamba usingekuwa na thamani yoyote, lakini pia kwa kweli ungewafanya wale wanaozisomea wasiwe na umaizi na hatimaye kuwaharibu kabisa. Ndio maana imesemwa kwamba
9
SAADA KAMILI
َ اب ْا ُ ال ِع ْل ُم ُه َو ْال ِح َج ال ْك َب ُر “Maarifa ni pazia nene sana”, ambalo humzuia binadamu asione uhalisia wa asili hasa wa vitu.
UTAKASO NA UPAMBAJI WA NAFSI
M
atendo mema humfanya binadamu apate furaha ya milele, ambapo matendo maovu humpeleka binadamu kwenye wasiwasi wa milele. Kwa hiyo ni muhimu kwa mwanadamu kujitakasa asiwe na tabia mbaya na aipambe nafsi yake kwa matendo yote mema ya uadilifu. Zaidi ya hayo, bila ya mtu kujisafisha ili asiwe na tabia zozote chafu, hataweza kustawisha na kuendeleza matendo mema. Nafsi ya binadamu inaweza kulinganishwa na kioo. Kama tunataka kuona kitu kizuri ambacho umbo lake linaakisiwa kwenye kioo, lazima kwanza tukisafishe kioo, ili kwamba vumbi na uchafu mwingine usivuruge nakisi ya umbo la kitu kile. Jaribio lolote la kutii amri za Allah linaweza kusababisha mafanikio na kufuzu pale tu ambapo mhusika amejitakasa na ameondokana na tabia mbaya, vinginevyo itakuwa sawa na kuuvisha pambo la vito mwili mchafu. Utakaso wa mtu unapokuwa umekamilika na mhusika anakuwa hana tabia ya fikira chafu katika matamshi na matendo yake, basi nafsi itakuwa tayari kupokea neema za Allah zisizo na ukomo. Mapokezi ya aina hiyo ndio yaliyosababisha binadamu kuumbwa. Kwa kweli, neema na miujiza ya Allah humfika binadamu wakati wowote. Ni binadamu ndiye anayetakiwa kuitakasa nafsi yake na akuze ndani mwake umuhimu wa mapokezi ili aweze kunufaika na baraka za Muumba wake zisizo na ukomo.
10
SAADA KAMILI
Kuna hadithi ya Mtume Muhammad (s.aw.w.) inayosema:
َ ال َت ْد ُخ ُل ْال َم َ . ال ِئ َك ُة َبي ًْتا ِف ْي ِه َك ْل ٌب “Malaika hawaingii nyumba anamofugwa mbwa.” Vipi basi iwezekane kwa miale ya baraka na nuru ya Kimungu iingie kwenye moyo uliojaa na kufurika matamanio ya kihayawani, ufisadi na uchoyo? Hadithi ya Mtume isemayo: “Msingi wa dini yangu ni tohara,” hii haimaanishi unadhifu wa nje peke yake; zaidi inamaanisha utakaso wa ndani ya nafsi. Ili kuweza kupata hitimisho na mwisho wa ukamilifu, ni muhimu kupita kwenye njia ya mapambano dhidi ya mielekeo ya uchoyo, ufisadi na uovu ambao unaweza kuwemo ndani ya nafsi, na kwa hiyo, kuitayarisha nafsi kupokea baraka za Allah. Kama binadamu atafuata njia ya kujitakasa, Allah atamsaidia na kumuongoza kwenye njia hiyo.
11
SAADA KAMILI
NGUVU YA NAFSI: ATHARI NA SIFA ZAKE BAINIFU
W
akati wa kuumbwa kwake, nafsi ya binadamu ipo kama tembe safi, inakuwa haina uwezo wowote wa tabia, zilizo nzuri au mbaya. Jinsi binadamu anavyoendelea na maisha, hukuza tabia ambazo huhusiana moja kwa moja na jinsi anavyoishi, anavyofikiri, na anavyotenda. Matamshi na matendo ya binadamu yanaporudiwa mara nyingi kwa muda mrefu, hutengeneza athari za kudumu katika nafsi ambazo hujulikana kama “tabia.� Tabia hizi hupenya kwenye nafsi ya binadamu na kutengeneza chimbuko na sababu ya matendo ya binadamu. Kwa maneno mengine, nafsi ya binadamu hupata mazoea ya tabia hizi, huanzisha mshikamano nazo, na hubainisha mwelekeo wa binadamu kufuatana na amri zao. Kama tabia (malaka) hizi ni njema, hujionyesha kwa matamshi na matendo ya mhusika.Kama kinyume chake, tabia hizi zinakuwa mbaya na ovu, na hujionyesha kwa matamshi na matendo ya mhusika. Tabia hizi ndizo zenye uwezo wa kuamua hatima ya mtu kuhusu maisha yake ya Akhera. Huko, nafsi itasindikizwa na baadhi ya tabia na kuunganishwa nazo katika dunia hii. Kama tabia hizi ni njema, nafsi itakuwa na furaha kamili ya milele, kama tabia hizi ni ovu, nafsi itapata laana ya milele. Jambo hili, malakat linatoa jibu kwa hao wasemao inawezekanaje Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu amlaani mtu kwenye laana ya milele kwa sababu ya dhambi ambayo imefanywa katika kipindi kifupi tu. Jambo la kuzingatia ni kwamba dhambi inapofanywa kwa kurudiwa tena na tena hustawi ndani ya nafsi ya mtu, kwani tabia hii mbaya huunganishwa na nafsi, kwa hiyo mhusika akipewa adhabu na mateso pia nafsi itaathirika. Qur`an inasema: 12
SAADA KAMILI
“Na kila mwanadamu tumemfungia matendo yake shingoni mwake, na tutamtolea Siku ya Kiyama daftari atakayoikuta imekunjuliwa, (Aambiwe) soma daftari lako. Nafsi yako inatosha leo kukuhesabia.(17:13-14)” Na: “Na daftari itawekwa (mbele yao) ndipo utawaona waovu wanaogopa kwa sababu ya yale yaliyomo, na watasema: Ole wetu! Kwa nini daftari hili haliachi dogo wala kubwa linahesabu yote. Na watakuta waliyoyafanya yamehudhurishwa, na Mola Wako hamdhulumu yeyote.” (18:49) Na: “Siku ambayo kila nafsi itakuta kheri iliyotenda imehudhurishwa, na shari iliyotenda (pia), itapenda lau kungekuwa na nafasi ndefu kati yake na kati ya hiyo (shari). Na mwenyezi Mungu Anakutahadharisheni naye, na Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa waja.(3:30)”
13
SAADA KAMILI
NAFSI NA AMRI ZAKE
N
afsi ni ile asili ya utukufu ambayo huutuma mwili na huvitumia viungo vyake mbalimbali katika kufanikisha malengo na makusudio yake, na inayo majina mengine yaani, roho (ruh), akili (aql), na moyo (qalb) lakini maneno haya yanayo matumizi mengine pia. Tabia muhimu sana za nafsi ni: i.
Nguvu ya kiakili (al-aquwwah al-aqliyyah) - wa kimalaika.
ii. Nguvu ya hasira (al-quwwah al-ghadhabiyyah) - wa kikatili. iii. Nguvu ya kutamani (al-quwwah al-shahwiyyah) - wa uhayawani. iv. Nguvu ya kubuni (al-quwwah al-wahmiyyah aualamilah)* - wa kishetani. Kazi na thamani ya kila moja ya uwezo huu au nguvu hizi za nafsi zinajulikana sana. Kama binadamu hangekuwa na uwezo wa kufikiri, hangeweza kutambua zuri na baya, haki na batili, kweli na uwongo. Kama hangekuwa na tabia ya hasira, hangeweza kujilinda dhidi ya shambulizi na ushari. Kama binadamu hangekuwa na nguvu ya matamanio ya ngono hali hiyo ingehatarisha muendelezo wa kuzaliana kwake. Na hatimaye, kama binadamu hangekuwa na uwezo wa kubuni, hangeweza kupiga picha ya kitu chochote kichwani au picha halisi na hangeweza kutoa uamuzi kutokana na kuona. 14
SAADA KAMILI
Maelezo ya wazi na yanayoeleweka kuhusu sifa bainifu za kila mojawapo ya aina nne za uwezo wa binadamu yametolewa hapo juu. Akili ni malaika anayemuongoza binadamu. Nguvu ya hasira na ukali uliopo ndani ya binadamu husababisha ukatili na vurugu. Uwezo wake wa ashiki na hisia kali humpeleka kwenye tabia mbaya na uasherati. Na uwezo wa kubuni humpatia binadamu nyenzo za kutengeneza hila na njama za kishetani. Sasa, kama uwezo wa kiakili unapewa fursa ya kudhibiti aina nyingine za uwezo wa binadamu, bila shaka kila moja ya aina nyingine itakuwa mahali pake panapostahili na itaweza kupunguza utendaji wa kuvuka mpaka; aina zote zitafanya kazi kwa ustawi wa binadamu na zitafanya kazi zenye manufaa; kinyume chake, hakuna kingine kitakachotokea isipokuwa uovu na uharibifu. Uhusiano wa hizi aina nne za Nguvu ya nafsi ya binadamu kwa kila moja unazungumziwa kwa namna ya mfano unaoweza kutusaidia kuelewa kwa urahisi. Fikiria mtu aliyeko safarini, amepanda farasi na anaye mbwa na mtu ambaye kazi yake ni kupeleleza majambazi. Huyu msafiri aliyepanda farasi anawakilisha akili. Mito ya kukalia iliyoko mgongoni mwa farasi inawakilisha shauku na mapenzi makali. Mbwa anawakilisha Nguvu ya hasira na ukali. Na mpelelezi anawakilisha uwezo wa kubuni. Endapo msafiri aliyetajwa hapo juu atafaulu kudhibiti makalio yaliyoko kwenye mgongo wa farasi, mbwa, na mpelelezi, na kudumisha mamlaka katika safari yake, atafika aendako salama; kinyume chake, ataangamia. Kwa hiyo nafsi ya binadamu ni hatua au uwanja wa vita ambapo kuna mapambano yanayoendelea kwa mfululizo baina ya hizi aina nne za Nguvu ya nafsi. Aina na sifa bainifu na asili ya nafsi ya mhusika inayoweza kutawala aina zingine inategemea matokeo yote ya mapambano haya. Kwa maneno mengine, aina yoyote miongoni mwa hizi aina nne za Nguvu ya nafsi ikitokeza kuwa na nguvu zaidi, ndio 15
SAADA KAMILI
itakayoamua tabia na mwelekeo wa nafsi. Ndiyo maana baadhi ya nafsi ni za kimalaika, zingine za kihayawani na sumbufu na bado zingine ni za kishetani. Hadithi kutoka kwa Imam Ali (as) inasema;
َّ لك ب ْال َع ْق ِل ُد ْو َن َ ْ َّ اِ َّن اهللَ َخ َ الش ْه َو ِة َو ْال َغ ص َّ َو َخ. ض ِب ِ ص ال َم ْ ان باِ ْع َطا ِء ْ ف َ َو َش َّر. ات ِب ِه َما ُد ْو َن ُه َ ْال َح َي َوا َ .ْع ي م ج ال نس ال ا ن َ َ ِ ِ ِ ِ ِ َ ض ُل ِم َن ْال َم َ ار ْأف َ َفاِ ِن ا ْن َقا َدت َش ْه َوتُ ُه َو َغ آلئك ِة َص َ ضبُ ُه لِ َع ْقلِ ِه ْ ْ َ ْس ُ لِ ُو َ از ِع َو ْال َمآل ِئ َك ُة لَي ِ ص ْولِ ِه اِلى َه ِذ ِه ال َم ْر َت َب ِة َم َع ُو ُج ْو ِد ال ُم َن َ لَ ُه ْم م .اح ٌم ِ ُز “Hakika Allah amewapa malaika akili bila ya tamaa ya ngono na hasira, na hayawani wamepewa hasira na tamaa ya ngono lakini hawakupewa akili. Amempandisha daraja binadamu kwa kumpa sifa hizi zote. Kufuatana na hali hiyo,kama akili ikitawala tamaa ya binadamu na ukatili wa binadamu; binadamu hunyanyuliwa na kuvuka daraja la malaika; kwa sababu amelipata daraja hili pamoja na kuwepo kwa viunzi ambavyo havipo kwa malaika.”
16
SAADA KAMILI
FURAHA NA UCHUNGU
F
uraha ni hali inayopita kwenye nafsi pale ambapo hutambua kitu kinachoendana na asili yake. Maumivu na mateso husababishwa na pale nafsi inapokutana na hali isiyoendana na asili yake. Kwa kuwa nafsi inao uwezo wa aina nne, lifuatalo ni kwamba starehe na mateso ya nafsi pia lazima yagawanywe katika namna nne, kila moja ya aina hizi iendane na moja ya aina nne za tabia za nafsi. Furaha ya Nguvu ya akili imo katika kupata ujuzi kuhusu uhalisia wa asili ya vitu na maumivu yake yamo kwenye ujinga na kukosa ujuzi. Furaha ya Nguvu ya hasira na ukatili imo kwenye kuhisi ushindi na kuridhika kwa kushindwa adui na kuweza kulipiza kisasi ambapo maumivu yake yapo kwenye kuhisi kuzidiwa na kushindwa. Starehe ya kupenda na kutamani ni kufurahia vyakula, vinywaji na mahusiano ya ngono (halali) ambapo maumivu yake yamo kwenye kukataa mambo kama hayo. Raha ya Nguvu ya ubunifu imo kwenye upigaji picha akilini wa mambo ambayo hupelekea kujitokeza kwa tamaa ya ngono na mwelekeo wa kishetani, ambapo mateso yake yamo kwenye kujitokeza upungufu na kutotosheleza kwa maono hayo. Furaha yenye nguvu na yenye uhalisi sana kuzidi nyingine ni ile inayohisiwa na Nguvu ya akili. Hii ni aina ya furaha ambayo ni ya asili na ya kimaumbile kwa binadamu. Ni furaha inayoendelea, haitawaliwi na mabadiliko ya mambo yanayompata binadamu kila siku katika maisha yake. Ni tofauti na furaha nyingine, ambazo kwa sababu ni za kimwili na kinyama, zinazo tabia ya kupita na hazina thamani ya kudumu. Furaha hizi za unyama kwa kweli ni za daraja la chini sana na za 17
SAADA KAMILI
upuuzi hivyo kwamba binadamu huona aibu na hujaribu kuzificha. Endapo ingesemekana kwamba mtu fulani hufurahia sana kula chakula, kunywa na hujishughulisha sana na ngono, ataona aibu na kufadhaika. Ambapo, kama burudani na shughuli za aina hiyo zingekuwa na manufaa kwa binadamu, kwa kweli angefurahi kama jambo hilo lingechapishwa na kusababisha ajivune kwa hilo. Hivyo basi, tunaweza kuhitimisha kwamba aina ya furaha ambayo inamfaa binadamu na inayopendeza, na isiwe katika hali ya kuonekana tu, ni aina ya furaha inayopitiwa na Nguvu ya akili ya nafsi. Aina hii ya furaha inayo daraja nyingi, miongoni mwa daraja hizo ya juu sana ni ile ambayo binadamu anahisi kuwa yu karibu na Allah. Aina hii ya furaha ambayo ni tukufu sana hupatikana katika kumpenda Allah, na kuzingatia amri Zake kwa juhudi kwa lengo la kuwa karibu zaidi Naye. Juhudi zote za binadamu zinapoelekezwa kwenye kuipata furaha hii ya kweli na ya milele, furaha za kupenda anasa hufunikwa; huchukua nafasi iliyo stahili yao katika maisha ya binadamu, zikifuatiliwa kwa wastani.
18
SAADA KAMILI
WEMA NA FURAHA
L
engo la msingi la utakaso wa nafsi na kupata tabia njema na adilifu ni kufika kwenye upeo wa furaha kuu inayofaa. Furaha kuu iliyokamilika kabisa kwa ajili ya binadamu ni kuwa mfano unaoonekana wa sifa na tabia za Kimungu. Nafsi ya mtu mwenye furaha ya kweli huendelezwa kwa kumjua na kumpenda Allah; hutiwa nuru na mng`ao unaotoka kwa Allah. Linapotokea hilo, hakuna kingine tena isipokuwa uzuri utaonekana kutokea kwake; kwani uzuri huonekana kutoka kwenye kitu kilichopambwa. Ni vema izingatiwe kwamba furaha kuu ya kweli haiwezi kupatikana au kudumishwa isipokuwa aina zote za Nguvu ya nafsi na sifa bainifu za Nguvu ya nafsi zitakaswe na kurekebishwa. Furaha haitapatikana kama marekebisho ya baadhi ya aina za Nguvu ya nafsi, au aina zote yakifanyika kwa kipindi kifupi. Inafanana na afya ya mwili. Mwili unaweza kuwa na afya hapo tu ambapo miguu na mikono na viungo vingine vyote vinayo afya njema. Kwa hiyo, mtu anayejaribu kupata furaha ya mwisho iliyokamilika, lazima ajirekebishe kwa kuondokana na nguvu na mwelekeo wa kishetani na unyama na akanyage ngazi ya kuelekea juu zaidi.
19
SAADA KAMILI
TABIA NJEMA NA MBAYA
K
atika mazungumzo yetu ya mwisho, tulisema kwamba nafsi ya binadamu inayo aina nne tofauti za nguvu. Aina hizi ni: Akili, Hasira, Tamaa na ubunifu. Sasa, kitu tunachotakiwa kukiona ni kwamba katika utakaso na maelekezo sahihi ya kila mojawapo ya aina hizi za uwezo, patajitokeza tabia ya pekee kwa mhusika. Utakaso na maelekezo sahihi ya aina ya Nguvu ya akili matokeo yake ni maendeleo ya ujuzi na kwa hiyo busara, kwa binadamu. Utakaso wa Nguvu ya hasira utasababisha kujitokeza kwa tabia ya ujasiri na kwa hiyo ustahamilivu (hilm).Utakaso wa nguvu ya Tamaa na ashiki utasababisha maendeleo ya tabia ya usahili, na kwa hiyo ukarimu. Na utakaso wa Nguvu ya ubunifu utasababisha kujitokeza kwa tabia ya utendaji wa haki kwa mhusika. Kwa hiyo, tabia njema ni kama zifuatazo: busara, ujasiri, usahili, na utendaji haki. Kinyume cha sifa hizi ni kama zifuatazo: ujinga,* woga, ulafi, kutokutenda haki na udhalimu. Maana ya busara ni kuwa na uelewa wa mambo ya dunia, jambo ambalo linaendana na hali halisi. Uwepo wa ujasiri na usahili inamaanisha kwamba Nguvu ya hasira na ulafi vyote vinakuwa chini ya maamrisho ya akili na kuwa huru kabisa kwa kutokuwa kwenye utumwa wa matamanio na ubinafsi. Kuhusu haki, inarejelea kwenye hali ambapo Nguvu ya ubunifu unakuwa chini ya maamrisho ya Nguvu ya akili. Hii inamaanisha ulinganifu wa Nguvu ya nafsi unaofanywa na Nguvu ya akili. Kwa maneno mengine, kuwepo kwa tabia ya utendaji wa haki ndani ya nafsi hulazimisha kuwepo kwa tabia zingine tatu yaani - busara, ujasiri na usahili.
20
SAADA KAMILI
Lazima litamkwe jambo la muhimu hapa. Kwa mtazamo wa mabingwa wa maarifa ya maadili, mtu ambaye ameendeleza tabia nne katika nafsi yake, haiwezekani asifiwe isipokuwa tabia hizi ziwe na manufaa kwa wengine pia. Huu ndio ujumbe wa akili kwetu. Akili inatuambia kwamba mtu anaweza kuwa na tabia safi kabisa lakini kama hazionyeshi anaposhughulika na binadamu wenzake hazina thamani na mhusika hastahili kusifiwa.
21
SAADA KAMILI
WASTANI NA MKENGEUKO
K
ila moja ya aina nne za mfumo wa maadili mema inatakiwa kufanyiwa zoezi kwa kiwango fulani na katika mipaka iliyoainishwa, zoezi hilo likivuka mpaka, wema hutabadilika na kuwa uovu. Kama kila tabia njema ingefikiriwa kuwa kiini cha mduara, mwendo wowote ukivuka mduara ungekuwa uovu, na mwendo huu kila utakapokwenda mbali zaidi na kitovu cha mduara, ndivyo uovu utakavyokuwa mkubwa zaidi. Kwa hiyo, kwa kila jema kunakuwa na maovu yasiyo na idadi; kwani mduara una kitovu kimoja tu ambapo sehemu zote zinazokizunguka kitovu hicho ni nyingi mno kiidadi. Kuhusu mkengeuko, popote pale utakapoanzia ni mkengeuko tu, hauna tofauti yoyote ilhali umevuka mpaka wa mduara. Kuweza kupata kitovu cha katikati halisi cha mduara, zoezi ambalo linahitaji wastani kamili, ni vigumu kiasi kukipata. Kubaki kwenye kitovu hicho cha kati na kudumisha uwiano huu ni vigumu zaidi. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Surat Hud imenifanya mimi kuwa mzee kwa sababu ya aya hii, “Na uendelee kwa kudumu kama ulivyoamrishwa.”(42:15) Kama inavyopingana na kitovu halisi, kuna kile kitovu cha karibu sana ambacho kinafikika kwa urahisi. Watu wanaotakasa na kuendeleza nafsi zao kwa kawaida hufika kwenye kitovu hiki cha kweli hasa na hupata wastani unaofaa. Ni kwa sababu hii kwamba tabia njema hutofautiana kwa watu mbali mbali, mazingira na nyakati. Wastani unaohusika, kama ilivyo kwa mkengeuko, huathiri eneo pana hapo katikati kwenye kitovu ambapo ndipo ilipo sehemu ya uwiano na wastani kamili.
22
SAADA KAMILI
AINA MBALI MBALI ZA UOVU
T
ayari tumekwishasema kwamba mkengeuko kutoka kwenye wastani na kiasi husababisha uovu. Mkengeuko huu wa kuelekea kwenye miishilizio hiyo miwili ya kila upande wa kiasi, unao viwango visivyo na ukomo. Hapa tutataja mipaka miwili tu kwa kila tabia njema: (Tafriit)
(A‘tidaal)
(Ifraat)
Upungufu Upumbavu Woga Uvivu Unyongevu
Kiasi Busara Ujasiri Usahili Hak
Zaidi ya Kificho Ujasiri wa kijinga Enye tamaa Udhalimu
Kwa hiyo, zipo aina nane za uovu, na kila moja tutaitolea maelezo mafupi. i.
Upumbavu ni upungufu wa busara; ni kwamba mhusika hatumii Nguvu ya akili kuelewa hali ya mambo.
ii. Kificho au Udanganyifu ni kutumia akili kupita kiasi; yaani, kutumia Nguvu ya akili katika mambo yasiyofaa, au kutumia akili kuzidi kiasi katika mambo yanayofaa. iii. Woga ni upungufu wa ujasiri; yaani hofu na kutokufanya maamuzi ya mambo ambapo hayana sababu.
23
SAADA KAMILI
iv. Ujasiri wa kijinga ni ujasiri wa kuzidi kiasi, yaani, kufanya mambo kizembe katika mambo yasiyofaa. v.
Uvivu ni hali ya upungufu inayosababishwa na kushindwa kutumia vitu ambavyo mwili unavihitaji
vi. Tamaa ya kupindukia ni kinyume kingine cha uchovu; yaani kukithiri katika shughuli za ngono, kula na kunywa kupita kiasi na burudani zingine zinazoamsha ashiki. vii. Unyonge ni hali ya upungufu ambayo suala kiasi ni haki; yaani kuridhia uonevu na udhalimu. viii. ni upande mwingine katika upingaji wa unyonge, yaani, kujidhulumu wewe mwenyewe au kudhulumu watu wengine. Kila moja ya maovu haya lina matawi mengi sana na vijisehemu vingi, ambavyo vimeunganishwa na upande na kiwango cha mkengeuko kutoka kwenye wastani unaowakilishwa na aina nne za mema. Kwa kuwa mkengeuko unaweza kutokea katika idadi ya viwango isiyo na ukomo, si rahisi kuziorodhesha zote. Hata hivyo, tutazitaja baadhi ambazo zinajulikana sana, na baadaye tutazungumzia njia za jinsi ya kupambana nazo. Uovu umegawanywa kufuatana na nguvu ambazo zinahusishwa nao, yaani, Akili, Hasira, na shauku. i.
Nguvu ya akili inaweza kuwa na uovu wa aina mbili, ambao ni upumbavu na uchovu, aina hizi zinaweza kugawanywa tena katika vijisehemu kama ifuatavyo; Ujinga wa kawaida: kutokujua. Ujinga mkubwa: mtu kuwa mjinga lakini hajui kuwa yeye ni mjinga. 24
SAADA KAMILI
Mkanganyiko na shaka: ambao kinyume chake ni yakini na msimamo. Tamaa ya ngono: ambayo kinyume chake ni tafakuri juu ya uzuri wa maumbile ya Mungu. Ulaghai na hila: kufanikisha hatima zinazoamrishwa na Shauku na Hasira. Shirk (ushirikina): kinyume chake ni kuamini Upweke na Umoja wa Allah. ii. Nguvu ya Hasira inazo aina mbili za uovu: woga na ujasiri bila busara, mgawanyo wake wa vijisehemu ni: Woga: ni hali ya kisaikolojia ambayo husababishwa na matarajio ya kutokea jambo la kuumiza hisia, au kupotea kwa hali utulivu wa mambo. Kutokuwa na ustahamilivu na mtu kujishusha hadhi: hii ni mojawapo ya matokeo ya udhaifu wa moyo na inaonyesha kutokuwa na uwezo wa kukubiliana na matatizo. Kinyume cha tabia hii ni uvumilivu, maana yake ni kuwa na uwezo wa kukabiliana na shida na matatizo. Haya: hii husababishwa na kutokujiamini na udhaifu wa tabia, na huashiria kutokuwa na uwezo wa kupambana kwa ajilii ya kutimiza malengo yenye manufaa. Kinyume chake ni uvumilivu; yaani, ujasiri na kuwa tayari kujituma kwa bidii kupata furaha kuu na ukamilifu. Kutojiheshimu: pia hii husababishwa na udhaifu wa tabia na huashiria kushindwa kuwa muangalifu na kutazama mambo ambayo yanahitaji kuangaliwa na kusimamiwa kwa umakini. 25
SAADA KAMILI
Papara: hii ni ishara nyingine ya udhaifu wa tabia na maana yake ni kuchukua uamuzi na kufanya mambo bila kuyafikiria kwanza. Kinyume chake ni unyongevu ambao ni tabia ya mtu kuendekeza uzembe na kushindwa kuwa mwepesi katika kufanya jambo katika wakati unaotakiwa. Shaka juu ya Allah na waumini: huu ni udhihirishaji mwingine wa tabia dhaifu na kutojiamini. Kinyume chake ni kuwa mwaminifu kwa Allah na waumini, ambayo ni dalili ya ujasiri na kujiamini. Hasira: ambayo kinyume chake ni subira na uvumilivu. Ulipizaji wa kisasi: ambao kinyume chake ni sifa ya kusamehe. Ghasia: hii husababishwa na nguvu ya hasira na matumizi ya nguvu ili kufikia lengo. Kinyume chake upatanisho na huruma. Hamaki: kinyume chake ni moyo wa utulivu na upole. Wivu na kijicho: pia hutokana na nguvu ya Hasira. Uadui na uhasama: huu ni udhihirishaji wa nguvu ya hasira na kinyume chake ni urafiki; kwa maneno mengine, kufikiria na kuweka ustawi wa watu wengine moyoni mwako. Kiburi na majivuno: ambayo kinyume chake ni kuwa na hali ya kutojiamini kupita kiasi. Kupenda makuu:kinyume chake kutopenda makuu bali unyenyekevu. Majisifu: maana yake ni kusema sana kwa kujisifu kwa majivuno na kuridhika. Hali hii huletwa na kiburi na majivuno. Maasi: kukataa kumtii mtu anayestaki kutiiwa. Hali hii pia inasababishwa na kiburi na majivuno, na kinyume chake ni kutoa utiifu kwa mtu anayestahili kutiiwa. 26
SAADA KAMILI
Ushabiki: kupenda sana jambo bila ya kulihakiki. Dhulma na kuficha haki: kinyume chake ni kutenda haki na uimara katika kusimamia ukweli bila kutetereka. Ukatili: kutokuwa na huruma na upole pale ambapo sifa hizi zinahitajika. iii. Aina za uovu unaotokana na Nguvu wa Hisia Kali na matamanio ni uchovu na ulafi; na vijisehemu vyake ni hivi: Kutamani mambo ya dunia na mali: kinyume chake ni kujizuia (zuhd). Utajiri na ukwasi: ambavyo kinyume chake ni umasikini na ufukara. Tamaa: kinyume chake ni kutojali kutamani vitu vya wengine. Ulafi (hirs): kinyume chake ni kutosheka na kile ulichonacho. Kutamani vitu vilivyoharamishwa na dini, na kujihusisha na vitendo haramu: kinyume chake ni wara‘ (ucha-Mungu na tahadhari), kutojiingiza kwenye mambo na shughuli haramu. Usaliti: kinyume chake ni uaminifu. Aina zote za ufisadi wa kupindukia: yaani zinaa, liwati, unywaji wa vilevi, na aina zingine za tabia za kipuuzi. Kutumbukia kwenye uwongo na kuamini mambo ya uwongo. Kujiingiza kwenye mazungumzo ya kipuuzi na yasiyo na maana na kuyafanya majivuno kuwa tabia. Hivyo, tumefika mwishoni mwa maelezo ya aina za tabia njema na mbaya ambazo zinatokana tu na kila mojawapo ya aina tatu za nguvu. Sasa na tuangalie aina hizo za tabia njema na mbaya ambazo zinatokana kwa pamoja na aina mbili au tatu za Nguvu za nafsi. 27
SAADA KAMILI
Aina za tabia njema na mbaya ni kama zifuatazo: Wivu: Kwamba, unataka mtu mwingine asiwe na bahati ya kupata. Kuwafedhehesha na kushusha hadhi ya watu wengine: kinyume chake ni kuheshimu na kustahi watu. Kutowasikitikia na kuwasaidia wengine. Kumpa mtu sifa isiyo stahili yake. Kuvunja uhusiano wa familia na ndugu wengine. Kutowasaidia wazazi wako na hatimaye kulaaniwa nao. Kuingilia mambo ya wengine kwa lengo la kugundua mapungufu yao. Kutangaza siri za wengine: kinyume chake ni kulinda siri za wengine na kuzificha. Kusababisha misuguano na kutokuelewana miongoni mwa watu: kinyume chake ni kutengeneza mazingira ya amani na kuwapatanisha watu wengine. Kulaani. Majadiliano ya mdomo na uhasama. Kudhihaki na kukebehi watu wengine. Kusengenya. Kusema uwongo. Kutamani umaarufu na hadhi. Kupenda kusifiwa na kuchukia kukosolewa: kinyume chake ni kutokujali hayo yote. 28
SAADA KAMILI
Kujisingizia: ni kwamba mtu anafanya kitu kwa lengo la kutaka apendelewe. Unafiki: kinyume chake ni mtu kuonyesha vitendo vyake hapa nje kama alivyo ndani ya nafsi yake. Mtu kujidanganya mwenyewe: kinyume chake ni utambuzi, ujuzi na unyenyekevu. Maasi: kinyume chake ni utiifu. Ufidhuli na kutokuwa na aibu: kinyume chake ni staha na aibu. Kuwa na matarajio na tamaa zenye utata yaliyotupwa mbali sana Kudumu katika kufanya dhambi: kinyume chake ni toba. Kuzembea na kujitenga na nafsi: kinyume chake ni mtu kujijali na kutambua malengo yake. Utepetevu na kutojishughulisha kwa mtu juu ya furaha na faida yake. Chuki iliyoelekezwa pasipostahili: kinyume chake ni urafiki na upendo unaofaa. Kutofuata utaratibu na kutotii: kinyume chake ni utiifu. Upweke na kujitenga: kinyume chake ni uchagamfu na kuonyesha urafiki kwa watu. Hasira na maudhi: kinyume chake ni utulivu na umakini. Huzuni na majuto: kinyume chake ni uchangamfu na nderemo. Imani na mategemeo madogo juu ya Allah. Utovu wa shukrani na fadhila: kinyume chake ni kushukuru na kuridhia. Wasiwasi, hamaki na kukosa subira. 29
SAADA KAMILI
Kukufuru: kutomcha Allah na kukhalifu amri za Allah: kinyume chake ni uchaji Mungu na utekelezaji mtiifu wa wajibu uliowekwa na Allah na pia kutekeleza vitendo vilivyopendekezwa Naye.
30
SAADA KAMILI
UMUHIMU WA HAKI
S
asa basi, tumetoa maelezo ya aina zote za tabia njema na mbaya, ni muhimu kupata uelewa wa maana ya kweli ya ubora wa haki, kwa kuwa maadili mema yote chanzo chao ni haki hii bora, kama vile ilivyo kwa aina zote za uovu zinatokana na udhalimu, sifa ambayo inakinzana nayo. Plato mwanafalsafa wa Kiyunani anasema: “Pale ambapo welekevu wa haki hukuzwa na binadamu, huzitia nuru welekevu zingine zote ikiwa ni pamoja na aina zote za Nguvu ya nafsi, na welekevu zote na aina zote za Nguvu ya nafsi hutiliana nuru zenyewe kwa zenyewe. Hii ni hali ambayo nafsi ya binadamu huunda na kutenda kwa namna iliyo nzuri kabisa na inayostahili kadiri iwezekanavyo, huku ikipata mvuto na kuwa karibu na Chimbuko la Uumbaji.� Sifa ya utendaji wa haki humwokoa binadamu kutoka kwenye hatari ya mkengeuko unaoweza kumwelekeza kwenye kupinduka mipaka, ama katika mambo yake binafsi au mambo ya kijamii, na humwezesha pia kupata furaha kuu iliyo kamili na ya kudumu, Kama mambo yalivyo, lazima ifahamike kwamba mhusika akijenga mazoea ya kuitumia sifa hii atapata mafanikio endapo tu anajua maana ya kanuni ya kutovuka mpaka, na anaweza kuitofautisha kanuni hiyo na kuzidi kiasi pindi anapokutana nayo. Upambanuzi wa aina hii huwa si rahisi kuupata isipokuwa kwa njia ya mafundisho matakatifu ya Uislamu, ambayo maelekezo yake yamefafanuliwa kwa undani kuhusu vitu vyote anavyovihitaji binadamu ili aweze kupata furaha hapa duniani na furaha kuu Akhera.
31
SAADA KAMILI
AINA MBALIMBALI ZA HAKI
H
aki ni za aina tatu:
i.
Haki baina ya binadamu na Allah; hizo ni, adhabu na thawabu ambazo Allah humpa binadamu kufuatana na amali na vitendo vyake. Kwa maneno mengine, kwa vitendo vyovyote anavyofanya, ama vizuri au viovu, Allah humpa binadamu thawabu au adhabu. Kama ingekuwa kinyume chake, ingemaanisha udhalimu na ukiukwaji wa haki kwa upande wa Allah na kutowatendea sawa viumbe Wake - na hii ni tabia ambayo Allah hanayo.
ii. Haki baina ya binadamu, inayomaanisha kwamba kila mtu lazima aheshimu haki ya mtu mwingine na jamii na atende kufuatana na sheria tukufu za Uislamu. Hii inaitwa haki ya kijamii. Kwenye hadithi ya Mtume, haki za kijamii zimeorodheshwa ifuatavyo:
َّ ِال َب َرا َء َة لَ ُه ِم ْن َها ا َ ال ِب ْا َ ْن َح ًّقا ْ اِ َّن لِْلم َ أخ ْي ِه َثال ِثي ال َدا ِء ِ ُؤ ِم ِن َعلَى ُ َي ْغ ِف ُر َزلََّت ُه َو َي ْر َح ُم ُغ ْر َب َت ُه َو َي ْستُ ُر َع ْو َر َت ُه َويُ ِقي:أو ْال َع ْفو ْل ِ ِ ْح َت ُه َو َي ْح َف ُظ ِخلََت ُه َ صي ِ َع ْثر َت ُه و َي ْق َب ُل َم ْع ِذ َر َت ُه َو َي ُر ُد ِغ ْي َب َت ُه َويُ ِد ْي ُم َن ْ َ َو َي ْر َعى ِذ َّم َت ُه َو َيعُو ُد َم ْر ُ ُجي ْب َد ْع َو َت ُه ِ ض َت ُه َو َيش َه ُد َم ْي َتت ُه َوي َ َو َي ْق َب ُل َه ِديَّ َت ُه َوي ص َر َت ُه ْ صلََت ُه َو َي ْش ُك ُر ِن ْع َم َت ُه َوي ْ ُح ِس ُن َن ِ ُكا ِف ُئ ُس ِمُّت َع ْط َس َت ُه َ ض ْى َح َ اج َت ُه َو َي ْش َف ُع َم ْسألََت ُه َوي ِ َو َي ْح َف ُظ َحلِيْلََت ُه َو َي ْق 32
SAADA KAMILI
َ َ َ ُر ِش ُد َ ُطيُّب َ ُص ِّدُق ْ َوي َ كال َم ُه َوي ُِب ُّر اِ ْن َع ا َم ُه َوي ِ ضآلَّت ُه َو َي ُر ُّد َسال َم ُه َوي َ اِ ْق َسا َم ُه َويُ َوالِ ْي ِه َو ص ُر ُه َظالِمًا اَ ْو َم ْظلُ ْومًا َفيُ ِع ْينُ ُه ُ ال يُ َعا ِد ْي ِه َو َي ْن َ ال َي ْسأ ُم ُه َو َ أخ ِذ َح ِّقِه َو ْ أو يُ ِعيْن ُه َعلَ َى ُح ُّب لَ ُه ْ ُظ ْل َم ُه ِ ال َي ْخ ُذلُ ُه َوي ْ .ُح ُّب لَِن ْف ِس ِه َو َي ْك َر ُه لَ ُه ِم َن ْال َش ِّر َما َي ْك َر ُه لَِن ْف ِس ِه ِ ْر َما ي ِ ِم َن ال َخي “Kila muumini anazo wajibu thelathini kwa ndugu yake katika imani, ambazo lazima azifanye isipokuwa awe amesamehewa na ndugu yake katika imani. wajibu hizi ni kama zifuatazo:
“Kusamehe makosa yake; kumkirimu na kumhurumia akiwa ugenini; kuficha siri zake na kumsaidia anapokaribia kupata matatizo; kumkubalia anapoomba msamaha; kuzuia masengenyo kuhusu yeye; kusisitiza kumpa ushauri mzuri; kuthamini urafiki wake; kutekeleza amana yake; kumtembelea anapougua; kuwa karibu naye wakati wa kifo chake; kukubali mwaliko wake na zawadi zake; kumrudishia fadhila kama alivyokutendea; kumshukuru kwa fadhila zake hizo; kumshukuru kwa msaada wake; kulinda heshima na mali yake; kumsaidia kupata mahitaji yake; kufanya juhudi katika kutatua matatizo yake; kumwambia: “Allah Akurehemu” pale anapopiga chafya; kumwelekeza kwenye kitu alichopoteza; kujibu salam yake anapokusalimia ukichukulia maneno yake (usimtafsiri vibaya); kubali kupokea zawadi anazokupa; kuthibitisha anapoapa kuhusu jambo fulani; uwe mpole na rafiki kwake; kutokuwa mkosa huruma na mkali kwake; msaidie pale anapokuwa hatendi haki au ni muathiriwa wa udhalimu; (tunaposema umsaidie anapokuwa hatendi haki, tunamaanisha lazima aepushwe asije akafanya dhuluma; tunaposema kumpa msaada pale anapokuwa muathiriwa wa udhalimu, tunamaanisha kwamba asaidiwe kupata haki yake); kuepuka 33
SAADA KAMILI
kuhisi kukukera au kumchoka; kutomtelekeza katikati ya matatizo yake. Yale yote mazuri anayoyapendelea nafsi yake anapaswa pia kumpendelea ndugu yake katika imani; na yale yote anayoyachukia pia ayachukie kwa ndugu yake katika imani.� iii. Haki baina ya walio hai na marehemu. Hii ni haki ambayo inaamuru kwamba walio hai wanatakiwa kuwakumbuka marehemu kwa wema, kwa kulipa madeni yao, kutekeleza wosia wao, kuwaombea, kuwatolea sadaka, kuwaombea msamaha kwa Allah; kufanya vitendo vyenye hisani katika kuwakumbuka.
34
SAADA KAMILI
KUJIENDELEZA MWENYEWE
M
wishoni mwa sehemu hii tunahitimisha kwamba maana ya haki ni umahiri kamili kabisa wa akili juu ya hisi nyingine ikiwa ni pamoja na aina zote za Nguvu ya nafsi ya binadamu, hivyo kwamba vyote hivyo vinatumika kwenye mwelekeo wa lengo la mwisho la ukamilifu wa binadamu na mwisho wa kufikia kilele cha kupendwa na Allah. Kwa maneno mengine, akili hutawala mwili; kama haki ikiwemo ndani yake, pia itakuwepo kwenye eneo la mamlaka yake. Kama vile, endapo mtawala wa jamii atakuwa mwadilifu, haki itaenea kwenye jamii yote, ambapo kwamba, kama mtawala ni dhalimu, basi hapatakuwepo na haki nchini humo. Hii inaelezwa kwenye hadithi. “Pale mtawala anapokuwa mwadilifu, mtawala huyo hugawana thawabu na wema wa kazi nzuri iliyofanywa na raia wake; lakini kama mtawala ni dhalimu, atafahamika kama naye ameshiriki katika dhambi zao zote na vitendo vyao viovu.� Namna nyingine ya kuhitimisha ni kwamba mtu hataweza kuwarekebisha wengine endapo yeye mwenyewe hajajirekebisha. Kama mtu anashindwa kuifanya haki itawale nafsi yake, atawezaje kuifanya haki iwaathiri watu wengine alionao, watu wa familia yake, raia wenzake, na hatimaye, jamii yote kwa ujumla? Kwa hiyo, ni muhimu mtu ajiendeleze mwenyewe kabla ya mambo mengine yote, na hili haliwezi kufanikiwa bila kupitia elimu ya maadili.
35
SAADA KAMILI
MARADHI YA NAFSI NA TIBA ZAKE
K
atika utambuzi wa magonjwa ya mwili zipo kanuni na taratibu zinazotakiwa kufuatwa. Kwanza kabisa, ugonjwa lazima utambuliwe. Pili, njia ya kutibu ugonjwa lazima ibainishwe. Tatu, matibabu lazima yaanze kwa kutumia dawa zinazofaa, na kuepukana na mambo yanayoweza kusababisha madhara, na kisha kuendelea na matibabu hadi mtu apone. Maelezo yamekwishatolewa kwamba maradhi ya nafsi husababishwa pale ambapo nguvu zake zinavuka mipaka ya wastani, na kuelekea kwenye mwisho wa ama upungufu au kuzidi kiasi. Namna ambavyo magonjwa haya yanatakiwa kutibiwa ni sawa kama ile inayotumika kutibu maradhi ya mwili, na lazima zifuatwe hatua tatu zilizotajwa hapo juu hadi kupona. Tutaendelea na mazungumzo yetu, kuhusu kila aina ya ugonjwa, na kuonyesha tiba inayofaa. Magonjwa yatakayochunguzwa yatagawanywa katika makundi manne: i.
Maradhi ya Nguvu ya akili na tiba yake
ii. Maradhi ya Nguvu ya hasira na tiba yake iii. Maradhi ya Nguvu ya Tamaa na tiba yake iv. Maradhi yanayohusiana na muunganiko wa makundi yoyote mawili au yote matatu. Kabla hatujaanza mazungumzo yetu kuhusu maradhi ya haya makundi manne, lazima itamkwe kwamba kila moja ya nguvu hizi inaweza kuwepo kwenye yoyote kati ya hali tofauti hizi tatu za wastani,upungufu, au kuzidi kiasi.
36
SAADA KAMILI
Katika kuzungumzia kila mojawapo ya nguvu hizi, kwanza tutafikiria kukengeuka kwake kuelekea kuzidi kiasi, ambapo hiyo ni aina ya ugonjwa, na kuonyesha tiba yake inayofaa. Hii itafuatiwa na mazungumzo ya mkengeuko kuelekea kwenye hali ya upungufu na namna ya kutibu. Halafu tutafikiria hali yake ya wastani. Tutahitimisha uchunguzi wetu wa kila aina ya nguvu na kupima aina mbalimbali za ugonjwa wa tabia njema unaoweza kukumba aina hizi za nguvu na aina ya tiba yake.
37
SAADA KAMILI
TIBA YA MARADHI YA NGUVU YA ÂAKILI NA TIBA YAKE (a) Hali ya Kupindukia Ujanja: Ni mojawapo ya uovu wa Nguvu ya akili katika hali yake ya kuzidi kiasi au kuvuka kikomo. Akili ya binadamu inapopatwa na ugonjwa huu, huwa imezama sana kwenye uangalifu na uchambuzi sana wa mambo madogo madogo hivyo kwamba hupoteza tabia yake ya kawaida. Kwa maneno mengine, badala ya akili kumfikisha mhusika karibu na uelewa wa hali halisi, humsogeza mbali zaidi na zaidi kutoka kwenye hali halisi, na inawezekana ikampeleka mbali zaidi hadi kukanusha uhalisi wa mambo - kama walivyo wapotoshaji - na kusababisha mhusika kukwama kwenye shaka na kushindwa kutoa uamuzi kuhusu sheria za kidini na namna ya kuzitumia. Jinsi ya kutibu ugonjwa huu mbaya, ni kwamba mhusika lazima kwanza atambue hatari ya maradhi haya, atafakari sana, na halafu afanye jitihada ya kuilazimisha akili yake kuwa katika mipaka ya wastani. Akiwa anatumia maarifa ya kawaida kama muongozo wake na kufikiria na kutumia uamuzi wake kwa watu wa kawaida kama kigezo chake, atatakiwa ahakiki mfumo wake wa kufikiri na utoaji wa maamuzi, wakati wote akiwa na tahadhari hadi afike kwenye hali ya wastani.
38
SAADA KAMILI
(b) Hali ya Upungufu Ujinga wa Kawaida: Maradhi haya husababishwa na upungufu wa Nguvu ya akili ya mhusika, na inasemekana humkumba mhusika kwa sababu ya kukosa ujuzi na elimu, lakini anautambua ujinga wake. Hali hii ni tofauti na “ujinga mchanganyiko” - hali ambayo mhusika si tu kwamba hajui kwamba yeye ni mjinga lakini pia anafikiria kwamba yeye ameelimika. Ni wazi kwamba kutibu “ujinga wa kawaida” ni rahisi kuliko “ujinga mchanganyiko.” Ili kuweza kutibu “ujinga wa kawaida” jambo la muhimu ni kupima matokeo ya uovu wa ujinga, na kutambua ukweli kwamba tofauti ya binadamu na wanyama wengine imo kwenye elimu na kujifunza. Zaidi ya hili, lazima mhusika aelewe umuhimu wa elimu na ujuzi kama ilivyothibitishwa na akili na pia ufunuo. Matokeo ya tafakari na mawazo kama hayo yanaweza kumfanya mhusika apende kuelimika. Lazima afuatilie utashi huu kwa bidii sana, na asiruhusu namna yoyote ya kusitasita au shaka kuingia akilini mwake.
(c) Hali ya Wastani Elimu na hekima: Hali hii ipo katikati ya upeo wa “ujanja” na “ujinga wa kawaida.” Bila shaka, elimu na hekima ni sifa mbili tukufu sana ambazo binadamu anaweza kuwa nazo, kama vile ambavyo ni sifa muhimu na nzuri sana miongoni mwa Sifa za Uungu. Kwa kweli ni tabia hii ndio humsogeza binadamu kwa Allah. Ni hivyo kwa sababu jinsi mtu anavyozidi kuwa na ujuzi na elimu, ndivyo anavyokuwa na uwezo mkubwa wa kupambanua (tajarrud); kwani imeonyeshwa kwenye uchunguzi wa falsafa kwamba ujuzi na udhanifu huenda 39
SAADA KAMILI
pamoja. Kwa hiyo, jinsi mtu anavyozidi kuwa mdhanifu katika akili yake, ndivyo anavyokuwa karibu na Dhati ya Uungu, ambaye fikira yake katika akili ya binadamu ndiye kipambanuzi cha hali ya juu sana. Katika kusifu elimu na busara, Qur`an Tukufu inasema: “….. Na aliyepewa hekima bila shaka amepewa kheri……” (2:269)12 Na: “…….Na hiyo ndiyo mifano tunayoeleza kwa watu, na hawaifahamu ila wale wanaoijua.”(29:43)13 Mtume amenukuliwa akimwambia Abudhar:
ْ ُذا َِك َر ِة ْال ِع ُُجل َ اع ٍة ِع ْن َد م ْ أح ُّب اِلَى اهللِ َت َعالَى ِم ام ي ق ن م ـل س س و ُ َ ْ َ َ َ ِ ِ ِ ْ ْ َ َ وأح ُّب اِل ْي ِه ِم ْن أل َ ُصلِّ ْى ِف ْى ُك ِّل لَيْلَ ٍة ْأل ف َ ف َرك َع ٍة َ ف لَيْلَ ٍة ي ِ ْأل ُْ َ ف َم َّر ٍة ْر ِم ْن ٌ وخي ِ آن ُكلِِّه اِ ْث َن ْى َع َش َر ْأل ِ َغ ْز َو ٍة و ِم ْن ِق َرا َء ِة الق ْر س َ صا َم َن َه َ َو َم ْن َخ َر َج ِم ْن َب ْي ِت ِه لَِي ْل َت ِم.ار َها َو َقا َم لَيْلَ ِها َ ِع َبا َد ِة َس َن ٍة ّ ُ َ َّ ْ ْ ُ َ اب َن ِب ٍّى ِم َن ِ َبابًا ِم َن ال ِعـل ِم َك َت َب اهلل َع َّز َو َجل ل ُه ِبك ِل َق َد ٍم ث َو َ ْا ْ ف َش ِه ْي ٍد ِم ْن ُش َه َدآ ِء َب ْد ٍر وأع َطا ُه اهللُ ِب ُك ِّل َ ال ْن ِب َيا ِء َو َث َو ِ اب ْأل .أو َي ْكتُ ُب َم ِد ْي َن ًة ِفى ْال َجنَّ ِة ْ ف َي ْس َم ُع ٍ َح ْر “Mtu akikaa kwenye kundi la watu wenye elimu kwa muda wa saa moja anaonekana anafaa mbele ya Allah kuliko swala za usiku elfu moja ambapo kila usiku zimeswaliwa swala elfu moja, na vizuri zaidi kuliko kusoma Qur`ani yote mara elfu kumi na mbili, au vizuri zaidi kuliko ibada ya mwaka moja wakati ambapo anafunga saumu na 40
SAADA KAMILI
kuswali usiku kucha. Kama mtu akiondoka nyumbani kwake kwa nia ya kwenda kupata elimu, kwa kila hatua anayotembea, Allah atampa thawabu ambazo angepewa Mtume, na thawabu zinazolingana na thawabu za mashahidi elfu moja (wa vita vya) Badr. Na kwa kila neno ambalo anasikia au kuandika, jiji litatengwa kwa ajili yake Peponi……….”
Kwenye Uislamu kanuni fulani za adabu zimewekwa kwa ajili ya walimu na wanafunzi, zimeelezewa kwa kina kwenye vitabu vingine, na kizuri zaidi miongoni mwa vitabu hivyo labda ni “Adab al-muta‘allimiin” kilichoandikwa na Zayn al-Din ibn `Ali al‘Amili (1495-1559 AD). Hapa tutaandika mambo machache kuhusu mwenendo sahihi wa mwanafunzi na mwalimu: i.
Mwanafunzi lazima ajiepushe na tabia ya uchoyo na tamaa ya anasa na asikae kwenye makundi ya watu wa kidunia, kwa sababu, kama vile lilivyo pazia, humzuia mtu asifike kwenye nuru ya Uungu.
ii. Mwanafunzi lazima awe na lengo moja tu ambalo ni kupata radhi nzuri ya Allah na kupata furaha kuu ya Akhera; si kwa lengo la kupata utajiri wa dunia, umaarufu na heshima. iii. Mwanafunzi lazima atekeleze kwa vitendo yote yale anayojifunza na kuelewa, ili Allah aweze kumuongezea ujuzi wake. Mtume amenukuliwa akisema:
َ َم ْن ْ أخ َذ ْال ِع ْل َم ِم ْن أرا َد ِب ِه َ أهلِ ِه َو َع ِم َل ِب ِع ْل ِم ِه َن َجا َو َم ْن ّ ْال ُّد ْن َيا فهي .حظه 41
SAADA KAMILI
“Mtu anayepata ujuzi kutoka kwa mwanazuo, na vitendo vyake vikaendana na ujuzi wake ataokolewa, na mtu ambaye anapata ujuzi kwa lengo la kidunia atapata hayo tu (hatapata thawabu zozote huko Akhera)�
iv. Mwanafunzi lazima amheshimu mwalimu wake, awe mnyenyekevu na mtiifu kwa mwalimu wake. Mwenendo wa mwalimu unaofaa ni kama haya yafuatayo: i.
Ufundishaji uwe kwa ajili ya Allah, na si kwa ajili ya mambo ya kidunia.
ii. Mwalimu anatakiwa kumtia moyo na kumuongoza mwanafunzi wake, awe mkarimu kwake na awe anazungumza naye kufuatana na kiwango cha uelewa wake. iii. Mwalimu lazima auhamishie ujuzi wake kwa wale tu wanaoustahili; asiwafundishe wale wasiostahili na ambao wanaweza kuutumia ujuzi huo vibaya. iv. Mwalimu anatakiwa kufundisha yale tu anayoyajua, na akwepe mada ambazo hana ujuzi nazo. Hapa kuna umuhimu wa kutoa maelezo kuhusu maana ya elimu na kusoma na namna ya elimu tunayoizungumzia. Kwa maneno mengine, suala linalojitokeza ni ama heshima na hadhi kwa ajili ya elimu na ujuzi ambao unaainisha sifa ya Uislamu, inatumika kwa sayansi mbalimbali au kwa baadhi tu? Jibu ni kwamba nyanja za kujifunza zinaweza kugawanywa katika makundi mawili: kwanza, sayansi zinazohusu mambo ya dunia hii - kama vile tiba, jometri, muziki na kadhalika: pili, sayansi zinazohusu kuendeleza mambo ya 42
SAADA KAMILI
kiroho kwa binadamu. Ni hii aina ya pili ya kujifunza ambayo inaheshimiwa sana na mafundisho matakatifu ya Uislamu. Hata hivyo, baadhi ya sayansi zilizopo kwenye kundi la kwanza pia huwa zinafikiriwa kuwa muhimu, na ufuatiliaji wao ni wajibu (Wajib kifaa‘i) kwa Waislamu wote. Ni kwamba, Waislamu wote wanawajibika kufuatilia sayansi hizi hadi kwenye kiwango muhimu cha kukidhi mahitaji ya jamii ya Waislamu. Sayansi hizo ambazo kujifunza kwake ni muhimu kwa maendeleo ya kiroho kwa binadamu ni: elimu ya kanuni za kidini za Uislamu (usul al-din au misingi ya dini), maadili (akhlaq) - iliyoanzishwa kwa lengo la kumuongoza binadamu kwenye vitu vinavyoweza kumletea ukombozi, na kumwepusha kwenye vitu vinavyoweza kumpeleka kwenye kuangamia - na sayansi ya maarifa ya sheria (fiqh) - ambayo inahusu wajibu wa mtu binafsi na jamii kwa mtazamo wa Sharia ya Kislamu.
43
SAADA KAMILI
UOVU MWINGINE UNAOHUSIANA NA NGUVU YA AKILI (1) Ujinga mchanganyiko Ujinga mchanganyiko, kama ilivyotangulia kuelezwa, ni aina ya ujinga ambao mtu mwenye ujinga huu huwa hajui na hatambui kwamba yeye hajui. Huu ni ugonjwa mbaya sana ambao tiba yake ni ngumu mno. Hii ni kwa sababu mhusika mwenye maradhi ya “ujinga mchanganyiko� haoni kama anao upungufu huo, na kwa hiyo anakuwa hana msukumo wa kujikwamua kuhusu hilo. Kwa hiyo hubaki mjinga hadi mwisho wa maisha yake na athari zake mbaya humharibu yeye. Ili kuweza kutibu aina hii ya ujinga, lazima tutafute chanzo chake. Endapo sababu ya ujinga mchanganyiko wa mhusika ni muendelezo wa fikira potofu, tiba itakayomfaa sana ni kujifunza baadhi ya sayansi kamili kama jometri au hesabu ili akili yake iondokane na mkanganyo na utepetevu wa akili na kumwelekeza kwenye uimara, ubayana, na wastani. Matokeo ya haya, ujinga mchanganyiko hubadilika na kuwa ujinga wa kawaida, na mwenye ugonjwa huu anaweza kuchangamshwa na kuanza kutafuta elimu. Endapo sababu ya tatizo ni jinsi anavyotumia akili yake katika kufikiri, mhusika atahitaji kulinganisha namna anavyotumia akili yake katika kufikiri na ile ya watu wachunguzi na fikira zilizo wazi, hivyo kwamba anaweza kugundua kosa lake. Kama sababu ya ujinga wake ni vitu vingine kama vile kutumia akili kizembe na kuiga, atatakiwa kujaribu kuviondoa vitu hivyo.
44
SAADA KAMILI
(2) Mfadhaiko na Shaka Maradhi mengine ambayo yanaweza kutesa Nguvu ya akili ni tabia ya shaka na mfadhaiko, hali ambayo humfanya mhusika asiweze kutofautisha wema na uovu. Ugonjwa huu kwa kawaida husababishwa na kutokeza kwa vitu vingi mchanganyiko na vinavyotofautiana, ambavyo humchanganya, na kumfanya asiweze kutoa hitimisho sahihi. Ili kuweza kutibu ugonjwa huu, mhusika lazima kwanza afikirie kanuni za semi za mantiki, kama vile sheria ya ukinzani, kwamba kitu kizima wakati wote ni kikubwa kuzidi mojawapo ya sehemu yake, sheria ya utambulisho na kadhalika, na ategemeze fikira zake zote za nyuma, akitambua kwamba kweli ni moja tu kwa hiyo uamuzi mwingine wowote utakuwa si kweli. Kwa njia hii anaweza kuukata katikati ule utando wa mkanganyiko wa fikira unaomchanganya. Kinyume cha ujinga, mfadhaiko, na shaka ni yakini ambayo inadumu daima, yakini ya kusadikika, ambayo inaendana na ukweli, haiwezi kutikiswa na shaka hata kama shaka hiyo itakuwa na nguvu ya kiwango chochote. Hususani hii ni muhimu kuhusu theolojia na matawi yake mbalimbali. Kwa maneno mengine, imani ya kuwepo kwa Allah, sifa Zake zinazothibitika na zinazokanushika, Utume, Ufufuo, na lolote linalohusiana nazo, zinatakiwa kuwa madhubuti sana hivyo kwamba haziwezi kutikiswa na shaka yoyote. Hali ya yakini ni mojawapo ya hali za daraja la juu sana ambazo binadamu anaweza kuwa nazo, na wanadamu wachache sana huweza kuzipata. Ipo hadithi ya Mtume (s.a.w.w.) isemayo:
45
SAADA KAMILI
ُ ال ْي َم ُ ْال َي ِقي .ان ُكلُُّه ِ ْن ا “Yakini ni imani kamili.”
Imam Ja`far al-Sadiq (as) amenukuliwa akisema:
ْ َ َّ اِ َّن اهللَ َت َعالَى ب َع ْدلِ ِه َو ِق ْس ِط ِه َج َع َل ْال َّر ْو َح َو ْن َو ِ ِ الراَحة ِفى ال َي ِقي ِّ الح ْز َن ِفى ْال َّش .َّخط ُ َو َج َع َل ْال َه َّم َو. الرَّضا ِ اك َو الس ِ “Allah, Muweza wa yote, katika haki ya mamlaka Yake, ameshirikisha furaha na starehe pamoja na yakini na kutosheka [ni kwamba, kujisalimisha moja kwa moja kwenye radhi ya Allah], na ikaunganisha huzuni na maumivu pamoja na shaka na kero [kuhusiana na ridhaa ya Allah].
46
SAADA KAMILI
ISHARA ZA WATU WENYE KUSADIKISHA Zipo ishara fulani zinazohusishwa na hali ya yakini ambayo kwayo mtu anaweza kujipima ili aweze kutambua kiwango chake cha usadikishaji. Ishara hizi ni: (i) Mtu kumtegemea Allah katika mambo yake na kujihusisha na kuitafuta ridhaa ya Allah tu. Kwa ufupi, hii inatakiwa kuwa imani ya mtu iliyo thabiti kwamba:
َّ ِال ُق َوَّة ا َ ال َح ْو َل َو َ . الِبااهللِ ْال َع ِظي ِْم “Hapana nguvu au uwezo [hapa duniani] isipokuwa [uwe umetokana] na Allah, Aliyeko Juu sana, na Mkuu kabisa.”
(ii) Kunyenyekea kiroho na kimwili mbele ya Allah, wakati wote na katika kila hali, na utiifu kwa amri Zake hadi kwenye zile ndogo kabisa. (iii) Mtu kuwa na uwezo usio wa kawaida, ambao unakaribiana na muujiza -kwa sababu ya kuwa karibu na Allah - hali ambayo mtu huwa nayo baada ya kutambua uduni na udhalili wake mbele ya ukuu na utukufu Wake.
HATUA ZA YAKINI i.
(`Ilm al-Yaqin: Ambayo ni usadikisho yakini na wa kudumu. Ni sawa na usadikisho wa mtu ambaye anapoona moshi huamini kwa yakini kwamba lazima pawepo na moto pia. 47
SAADA KAMILI
ii.
` Ayn al-Yaqin: Ambayo ni kukiona kitu kwa jicho la kimwili ama jicho la kiroho. Kwa kutumia mfano huo hapo juu, ni usadikisho wa mtu ambaye hakuona moshi tu bali pia ameona moto.
iii.
Haqq al-Yaqin: hii ni hali ya yakini ambayo mtu huipata ambapo aina ya muungano wa kiroho ulio halisi unapokuwepo baina ya anayetambua kitu na kitu kinachotambuliwa. Kwa mafano; hali hii ingekuwa pale ambapo mtu angekuwa yumo katikati ya moto uliotajwa kwenye mfano wa hapo juu. Na hali hii inaitwa “muungano wa mtambuaji na kile kinachotambuliwa,� na hili limezungumziwa mahali pake panapofaa. Ili mtu aweze kupata haqq al-yaqin lazima atimize masharti fulani muhimu. Ambayo ni: i.
Nafsi ya mhusika lazima iwe na uwezo wa kupokea na kuelewa ukweli huu; mathalani, nafsi ya mtoto haiwezi kuelewa uhalisi wa vitu.
ii. Nafsi isiwe imekumbwa na ufisadi na dhambi. iii. Uzingativu kamili unatakiwa kuelekezwa kwenye kitu kinachohusika, lazima akili iwe salama kutokana na uchafu na uovu wa maslahi ya kidunia. iv. Mhusika asiwe mtu wa kuiga kibubusa na chuki. v.
Ili kuweza kufikia lengo, lazima ufanyike uchunguzi wa mwanzo kuhusu mambo muhimu na ya lazima.
48
SAADA KAMILI
(3) Shirk (ushirikina) Shirk ni maradhi mengine ya hatari kwa nafsi ya binadamu, na ni kitengo kingine cha ujinga. Imo katika misingi ya kuamini kwamba zipo nguvu zingine zaidi ya Allah ambazo zinafanya kazi ya kuongoza mambo ya dunia. Kama mtu akiabudu nguvu hizi, inaitwa ‘shirk ibadi’ – (ushirikina katika ibada), na kama mhusika atazitii nguvu hizi, ingeitwa “shirk ita`i” – (ushirikina katika utii). Ile aina ya kwanza pia inaitwa “shirk jali” – (ushirikina wa dhahiri), na aina ya pili pia inaitwa “shirk khafi” (ushirikina uliofichika). Inawezekana aya ya Qur’ani isemayo: “Na wengi wao hawamwamini Mwenyezi Mungu isipokuwa wao ni washirikina tu” (12:106), ni marejeo ya kwenye hii aina ya pili ya ushirikina. Kinyume cha shirk ni “tawhid” kumwamini Mungu Mmoja, na maana yake ni kwamba hapana nguvu nyingine yoyote ulimwenguni isipokuwa ile ya Allah Mwenye Enzi. Tawhid inayo hatua; nazo ni: i.
Kukiri au kukubali kwa ulimi “tawhid” yaani kusema;
ُال اهلل َّ ِال اِلَ َه ا َ “Hapana mungu ila Mwenyezi Mungu” bila kuamini moyoni.
ii. Kuamini moyoni pale ambapo tamko la hapo juu kuhusu kumwamini Mwenyezi Mungu linapotamkwa kwa ulimi. iii. Kutambua Upekee wa Allah kupitia nguvu kali ya uelewa na hisia ya uwepo karibu wa Mungu kimuujiza. Kwa maneno mengine, mtu anagundua kwamba mkusanyiko huu mkubwa wa viumbe, kuwepo kwao kunatokana 49
SAADA KAMILI
na Allah - wa Pekee, na anatambua kwamba hapana uwezo mwingine unaofanya kazi katika ulimwengu huu isipokuwa uwezo wa Allah. iv. (iv) Mtu haoni kingine chochote hapa duniani isipokuwa Mungu wa mbinguni na hutambua kwamba viumbe vyote ni kutoka Kwake na ni uakisi wa Mungu huyo. Hatua hizi za imani katika tawhid hutuongoza katika kutambua sababu ya maradhi ya shirk. Sababu ya msingi ya shirk ni kuzama sana kwenye anasa za dunia na kuwa wasahaulifu katika kumgeukia Allah. Ili kuweza kutibu ugonjwa huu, mhusika lazima atafakari kwa kina kuhusu kuumbwa kwa mbingu na dunia na wingi wa viumbe wa Allah. Hatua hii inaweza kuamsha hali ya kukubali utukufu wa Allah. Jinsi mtu atakavyozidi kutafakari na kutaamali kuhusu uzuri wa ulimwengu na muujiza wa maumbile, ndivyo imani ya mhusika itakavyokuwa inaongezeka na kuwa kubwa katika kuwepo kwa Upekee wa Allah. Qur`ani inasema: “Ambao humkumbuka Mwenyezi Mungu wakiwa wima na wakikaa na wakilala na wanafikiri katika umbo la mbingu na nchi (wakisema) Mola wetu! Hukuviumba hivi bure, utukufu ni wako, basi tuepushe na adhabu ya Moto.” (3:191) . Imam al-Ridha (as) imenukuliwa akisema:
اَِنَّما ْال ِع َبا َد ُة َك ْث َر ُة ال َت َف ُّكِر,َّل َو ِة الص َ َّيام َو َ لَي ِ ْس ِت ْال ِع َبا َد ُة َك ْث َر ُة ْال ِ ص .ِْر اهلل ِ ِفى أم “Ibada haimaanishi kuswali na kufunga saumu, lakini zaidi ipo katika kiasi cha tafakuri kuhusu uumbaji wa Allah.” 50
SAADA KAMILI
(4) V ishawishi na ufahamu wa Kishetani Chochote kinachoingia kwenye ufahamu wa binadamu ni ama kwa njia ya uwakala wa malaika wa rehema au shetani. Kama kitu hicho ni cha kimungu, huitwa msukumo (ilham), na kama kimesababishwa na shetani, huitwa kishawishi (waswaas). Nafsi ya binadamu ni uwanja wa mapambano ambamo jeshi la malaika na jeshi la mashetani yapo vitani, na binadamu anayo hiari ya kuthibitisha moja ya hayo majeshi. Kama jeshi la shetani linatiwa nguvu, atatawaliwa na vishawishi vya kishetani, na vitendo vyake vya nje vitaakisi yalioko ndani mwake. Lakini kama majeshi ya Kimungu yakitiwa nguvu, mhusika anakuwa mfano wa Sifa na Tabia za Kimungu. Qur`ani Tukufu inaeleza jinsi shetani (iblis) alivyoapa kuwapotosha wanadamu na kuwapeleka katika dhambi; “Akasema: Kwa sababu umenihukumu mpotovu kwa hakika nitawakalia (waja wako) katika njia yako iliyonyooka. Kisha nitawafikia kwa mbele yao na nyuma yao na kuliyani kwao na kushotoni kwao, wengi katika wao hutawakuta ni wenye kukushukuru.” (7:16-17) Kuhusu watu wanaoshindwa na shetani, Qur`ani Tukufu inasema: “…..Na bila shaka tumewaumbia Moto wa Jahannam wengi katika majinni na wanadamu. Nyoyo wanazo lakini hawafahamu kwazo, na macho wanayo lakini hawaoni kwayo, na masikio wanayo lakini hawasikii kwayo, hao ni kama wanyama, basi wao ni wapotovu zaidi, hao ndio walioghafilika.”(7;179) Na kuhusu wale ambao hawashawishiwi na shetani, Qur`ani inasema: “Ama wale waliomwamini Mwenyezi Mungu na wakashikamana naye, atawatia katika rehema itokayo kwake na fadhila (Yake) na atawaongoza kwake kwa njia iliyonyooka.”(4:175) 51
SAADA KAMILI
Njia ya kupigana na majaribu ya kishetani ni kuikusudia Akhera. Kama mtu anataamali matokeo ya kufuata ushauri wa shetani na ya wakati ujao, utiifu wa aina hiyo hautakua na nafasi kwake, kwani ataiona njia iliyonyooka na kuwa huru kutokana na vishawishi vya kishetani. Atakapoiona njia ya haki, pia atapata msaada toka kwa Allah na atamuongoza hadi kwenye furaha kuu na shangwe - kama ambavyo imetamkwa wazi wazi kwenye aya hapo juu.
(5) Udanganyifu na Hila Hila ni uovu mwingine uliopo kwenye Nguvu ya akili, na hutokeza kupitia matakwa ya kishetani na uovu wa Nguvu ya Matamanio na Hasira. Hila na udanganyifu vinafafanuwa kama ni upangaji njama dhidi ya wengine na kutengeneza mipango kiundani zaidi ya kuwadhuru. Uovu huu ni mbaya sana, kwa sababu mtu aliyekumbwa nao anahesabika kama mmoja miongoni mwa kundi la shetani. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema:
َ ْس ِمنَّا َم ْن َم .ُسلِمًا ْ اك َر م َ لَي “Yeyote anayemfanyia njama Muislamu, si katika sisi.”
Njia ya kutibu ugonjwa huu mbaya sana ni mhusika anatakiwa awe mwangalifu kuhusu matokeo mabaya ya uovu huu, na atambue kwamba mtu anayewachimbia mashimo wengine mwishoni atatumbukia mwenyewe, akitapata adhabu yake hapa hapa duniani. Anatakiwa pia ajiulize, kwa nini, badala ya kuwa mpole na mwema kwa wengine, anawafanyia njama wengine.
52
SAADA KAMILI
MARADHI YA NGUVU YA HASIRA NA TIBA YAKE Kama ambavyo imetamkwa hapo juu, Nguvu ya hasira ina hali tatu: upungufu, wastani na kuzidi kiasi; ambazo kila mojawapo tutaipatia maelezo ya kina kama ifuatavyo.
Hali ya kuzidi kiasi Ujasiri wa kipumbavu: Ujasiri wa kipumbavu, ugonjwa wa Nguvu ya hasira, ni kujiingiza kwenye hali za hatari na mbaya sana licha ya tahadhari zote za akili na dini. Qur`ani Tukufu inakataza waziwazi inaposema: “…….wala msizitie nafsi zenu katika maangamizo……”(2-195)
Njia ya kutibu ujasiri wa kipumbavu ni kufikiri kwa uangalifu kabla ya kuchukua mwelekeo wowote wa kiutendaji ili kuona endapo akili na dini. Kama kibali kitatolewa na akili na dini vinakiidhinisha au hapana. Kama kikipata idhini yao, mtu anaweza kutekeleza kitendo hicho, vinginevyo ajiepushe nacho kama hakikuidhinishwa na kimojawapo ya hivyo. Pia inaweza kuwa muhimu kwake kujiepusha na vitendo ambamo kiwango cha hatari inayoweza kusababishwa ni ndogo, kwa lengo la kupunguza hulka yake ya ujasiri wa kipumbavu. Mhusika lazima adumishe mwelekeo huu hadi hapo atakapokuwa na uhakika kwamba amepona ugonjwa wa uovu huo, na hadi hapo hali ya wastani, yaani ujasiri, itakapokuwa imefikiwa. Akishafika katika hali hii, lazima ajaribu kuihifadhi na kuidumisha.
53
SAADA KAMILI
(b) Hali ya Upungufu Woga: Woga ni hali ya kutishika haraka dhidi ya tukio linaloamuru kitendo cha ukali wa haraka. Woga, kinyume cha hamaki ya hasira na ukali, huishia kwenye hisia za udhalili, kusitasita, huzuni, na kukosa kujiamini. Hadithi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) inasema:
ْ َ ُ ُ ُخ ِل َو ْ أع ْو ُذ ِب َك ِم َن ْالب ُ الل ُه َم اَِنّ ْى ْن ِ أع ْوذ ِبك ِم َن ال ُجب “Ee Mola, najikinga Kwako kutokana na ubakhili na woga.”
Njia ya kutibu ugonjwa wa woga ni kuamsha hasira na hali ya ukali ndani ya mhusika, na kuchukua hatua ya kutumia ukali mwingi katika utekelezaji wa kitendo pale ambapo haitasababisha hatari kufanya hivyo, hadi hapo nafsi itakapofika kwenye hali ya ujasiri, ambayo ni hali ya wastani ya Nguvu ya hasira. Mhusika lazima basi awe na tahadhari asije akatoka nje ya hali ya wastani na kuielekea hali ya kuzidi kiasi. © Hali ya Wastani Ujasiri: Ujasiri ni udhihirisho wa Nguvu ya hasira katika hali yake ya wastani, na inaelezwa kama yenye kutii Nguvu ya hasira na kutumikia Nguvu ya akili. Utiifu huu ni tabia inayopendeza sana, na ni chanzo cha maadili mengi ya kiroho. Hali hii hupatikana baada ya ushindi wa mapambano dhidi ya ujasiri wa kipumbavu na woga kama matokeo ya uvumilivu na mazoezi ya mfululizo.
54
SAADA KAMILI
UOVU MWINGINE WA NGUVU YA HASIRA Nguvu ya hasira inaweza kukumbwa na uovu wa aina mbalimbali kumi na saba, yafuatayo ni maelezo mafupi ya kila moja ya maovu hayo kumi na saba.
1. Hofu Hofu ni dhana ya matarajio ya kitu kibaya kinachoweza kutokea wakati wowote. Mathalani, mtu anaweza kuogopa kupanda meli au kulala peke yake kwenye nyumba. Ni wazi kwamba kuna tofauti baina ya woga na hofu. Kuna aina mbili za hofu. Kwanza, kuna kumhofia Allah, na hofu juu ya dhambi na adhabu ya Kimungu. Pili, kuna kuhofia vitu visivyokuwa Allah. Aina ya kwanza ya hofu ni ya kustahiki kusifiwa, na humuongoza mtu kwenye ukamilifu; ambapo aina ya pili ya hofu ni uovu usiopendeza ambao husababishwa na maradhi ya woga. Hofu isiyofaa huwa inasababishwa na uwezekano kwamba kitu fulani kisichopendeza kinaweza kutokea ama kwa mtu binafsi au kwa kitu fulani au mtu fulani anayependwa. Mathalani, mtu anaweza akaogopa kifo, hatari mbaya, maiti za binadamu, mashetani, na kadhalika. Kiini cha aina hizi za hofu ni udhaifu wa kiroho, ambao unaweza kuondoshwa kwa mtu kujipima mwenyewe. Mathalani, kama anatambua kwamba hawezi kufanya kitu ili kuzuia hatari fulani au uwezekano wa kutokea hatari ya kifo na anaona kwamba hofu haitamsaidia katika kuizuia hatari hiyo, polepole atapoteza hofu yake. Kama hofu yake ya kifo husababishwa na kupenda kwake sana dunia na vitu vyake, lazima apunguze mwambatano huu.
55
SAADA KAMILI
Aina zingine za hofu zinasababishwa na dhana, kama vile kuogopa giza na maiti za binadamu. Mhusika anatakiwa aweke pembeni mawazo yake anapokutana na matukio kama hayo na aiimarishe nafsi yake. Hofu inayofaa na inayostahili kusifiwa ni ile ya kumhofu Allah, utukufu na ukuu Wake. Hofu hii pia inaitwa “khashyah” au “rahbah.” Pia ni hofu ya dhambi ambazo mtu amezitenda na adhabu zake. Jinsi hofu hiyo inavyozidi kuwa kubwa ndivyo mchango wake wa kuelekea kwenye maendeleo ya kiroho na ukamilifu unavyozidi kuwa mkubwa. Zaidi ya hayo, jinsi ya uelewa na kina cha kumwelewa na kumjua Allah, ndivyo atakavyozidi kuhofu uwezo Wake. Qur`ani Tukufu inasema: “….Kwa hakika wanaomuogopa Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja wake ni wale tu wenye ujuzi ……” (35:28) Kuhusu maelezo ya maisha ya mitume, tunaona kwamba mara kwa mara walikuwa wakipoteza fahamu kwa sababu ya khofu yao kubwa sana juu ya Allah. Khofu kubwa sana juu ya Allah ndio nguvu nzuri sana ya kudhibiti roho ya binadamu; kwa sababu inadhoofisha matamanio mabaya na uchoyo, humwepusha mhusika na maasi na dhambi, na hutiisha moyo wa binadamu na kujisalimisha kwenye amri za Kimungu. Zaidi ya hayo, unapomhofu Allah, huwezi kukumbwa na aina zingine za hofu, na humfanya mtu kuwa na nguvu za kupambana na batili, udhalimu, na ukandamizaji. Qur`ani inasema hivi kuhusu watu kama hao: “Wale walioamini na hawakuchanganya imani yao na dhulma, hao ndio watakaopata amani, nao ndio walioongoka.”(6:82) Na: 56
SAADA KAMILI
“…..Basi msiwaogope watu, bali niogopeni [Mimi]….” (5:44)
Na: “………Mwenyezi Mungu amewaridhia nao wamemridhia (malipo) hayo ni kwa yule anayemuogopa Mola wake. (98:8). Na: “Na ama yule anayeogopa kusimama mbele ya Mola wake, na akaikataza nafsi matamanio (maovu); basi kwa hakika Pepo ndiyo makazi (yake).” (79:40-41) Na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amenukuliwa akisema:
َف اهلل َ أخ َ َم ْن َخ َ َاف اهلل ِ اف اهللُ ِم ْن ُه ُك َّل َش ْى ٍء َو َم ْن ل ْم َي َخ َ .أخ َاف ُه اهللُ ِم ْن ُك ِّل َشى ٍء “Yeyote anayemuogopa Allah, Yeye (Allah) atavifanya vitu vyote vimuogope yeye; yeyote ambaye hamuogopi Allah, Yeye (Allah) atasababisha aviogope vitu vyote.”
Zipo aya nyingi za Qur`ani na pia hadithi zinazozungumzia kuhusu sifa za kumuogopa Allah; hata hivyo, kwa sababu ya ufinyu wa nafasi, hatutazitaja zote hapa. Lazima izingatiwe kwamba hata katika kumuogopa Allah, mhusika lazima azingatie masharti ya kufanya hivyo kwa wastani, ili kwamba isije kumfanya mhusika akakata tamaa juu ya huruma ya Allah; kwani mtu kukata tamaa kwa ajili ya rehema na huruma ya 57
SAADA KAMILI
Allah, nayo ni dhambi kuu. Qur`ani inasema: “….Na nani anayekata tamaa ya rehema ya Mola wake isipokuwa wale waliopotea?” (15;56). Endapo binadamu anamuogopa Allah kupita kiasi ni muhimu hali hiyo isawazishwe kwa rajaa’ au matumaini ya rehema ya Allah; kwani, kwa msaada wa mbawa mbili za matumaini na hofu mhusika anaweza kupaa na kufika mbali sana katika kiwango cha ukamilifu wa binadamu. Qur`ani inarejelea jambo hili kwa maneno haya: “Waambie waja wangu kwamba: Mimi ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu. Na hakika adhabu yangu ni adhabu yenye kuumiza.” (15:49-50).
2. Kujidhalilisha au Kutojiamni Uovu huu, unaosababishwa na woga, ni hali ambayo hujitokeza pale ambapo mtu anakuwa hana ujasiri wa kuingilia mambo muhimu kwa uhakika na hushindwa kutimiza wajibu wake wa kijamii kama vile kuwashawishi binadamu wenzake kutenda mema na kuwakataza wasijiingize kwenye uovu. Tiba ya maradhi haya ni sawa na ile iliyoainishwa kwenye tiba ya woga. Mtu ambaye amekumbwa na maradhi haya ya kimaadili lazima atambue kwamba muumini wa kweli wa Allah kamwe hawezi kupatwa na fedheha, na kwamba Allah amempa muumini heshima na hadhi. Qur`ani Tukufu inasema: “…….utukufu ni wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na waumini Wake ……..” (63:8). Ipo hadithi isemayo:
58
SAADA KAMILI
ْ َ َ أن اهللَ َف َّو ّ ُؤ ِمن ُك َّل َشى ٍء َ إال اِ ْذ َّ .الل َن ْف ِس ِه ِ ْ ض اِلى الم “Allah amempangia muumini wajibu wa kupatwa na kila adha isipokuwa fedheha juu ya nafsi yake.”
Kinyume cha sifa ya kujidhalilisha ni kuwa na tabia madhubuti na kujiheshimu; ni kwamba, mtu anatakiwa awe na tabia ambayo haiathiriwi na kitu chochote cha kufurahisha au kutesa, ama kusifiwa au kulaumiwa. Imam al-Baqir (as) amenukuliwa akisema;
ْ الم .أصلَ ُب ِم َن ْال َج َب ِل ْ ُؤ ِم ُن “Muumini wa kweli hatetereki kama mlima.”
Kwenye hadithi nyingine, amenukuliwa akisema:
َ ُؤ ِم َن َث َ ْال ِع َّز ِفى ْال ُد ْن َيا َو ْا:ال ْ أع َطى ْالم ْ َاِ َّن اهلل ال ِخ َر ِة َ ال َث ِخ ٍص َ َو ْال َف َ ال َح ِفى ْال ُد ْن َيا َو ْا .ص ُد ْو ِر ْال َّظاِل ِميْن ُ ال ِخ َر ِة َو ْال َم َها َب َة ِفى “Allah amempa muumini sifa tatu: fadhila hapa duniani na Akhera, wokovu hapa duniani na Akhera, na yeye kuogopwa katika nyoyo za madhalimu.”
59
SAADA KAMILI
3. Ukimya Maana yake ni hisia za kutojiamini ambazo husababisha mhusika kushindwa kufanya jitihada ya kufika kwenye upeo wa ukamilifu ambao upo wazi kwa binadamu, na kuridhika na hali ya kiwango cha chini na kisichokamilika. Kinyume chake ni tabia ya kujiamini, ambayo humfanya mhusika kuwa radhi kujitahidi ili aweze kupata furaha kuu hapa duniani, Akhera na hatimaye ukamilifu. Tabia ya kujiamini husababishwa na sifa za kiroho ambazo ni: uimara, ujasiri na kujiheshimu. Tiba yake ni saidizi ya ile ya maradhi ya woga ambayo ni maradhi makubwa zaidi kuliko mengine yote katika daraja hili.
4. Kutokuwa na hisia za heshima Uovu huu ni pamoja na kutokuwa na uzingativu wa kutosha na kushindwa kushughulikia mambo yanayohitaji kuangaliwa na tahadhari, kama vile, heshima, watoto, na mali. Uovu huu husababishwa na udhaifu wa tabia na hali ya kutojiamini. Kinyume chake ni kuwa na hisia za heshima raghba juu ya hilo, ambazo ni tabia zinazostahili kusifiwa mtu kuwa nazo. Kuhusu dini, inahitajika jitihada za kuifanya isije ikaathiriwa na mikengeuko, kuwa na moyo katika kuitangaza, jitihada za mtu kufuata sheria za kidini na pia kuwafanya wengine wazifuate. Kuhusu heshima ya mtu, inamaanisha mhusika kuilinda heshima yake na kufanya jitihada ya kuihifadhi. Kuhusu watoto, maana yake mhusika lazima awahudumie watoto wake kufuatana na haki za kuwalea na katika kuwaendeleza kwenye maadili na utamaduni mwema ili waweze kupata mafunzo ya maadili mema wakiwa bado 60
SAADA KAMILI
wadogo ambayo yatakuwa ni sehemu ya utu wao. Uislamu umeweka kipaumbele muhimu kwa wajibu wa wazazi kwa watoto katika kuwafundisha na kuwalea. Hili limezungumziwa kwa kina kwenye vitabu vya hadithi. Kuhusu mali na vitu vingine vilivyo katika milki ya mtu, ina maana kwamba wakati wote avichukulie kuwa hivyo ni sehemu ya neema za Allah na kama amana ambayo amepewa na Allah. Lazima asiitumie kuzidi kiasi na kuifuja, atekeleze wajibu wake wa kidini, na asisahau kuwasaidia mafukara.
5. Kufanya Jambo Kwa Pupa Hii ni hali inayomlazimisha mtu kufanya uamuzi na kutekeleza jambo haraka bila wazo stahiki. Hali hii pia husababishwa na mhusika kuwa mdhaifu kitabia pamoja na kutojiamini. Kinyume chake ni tabia ya mtu kuwa makini katika utendaji na kauli. Matokeo ya kufanya jambo kwa pupa ni hasara kwa maslahi yetu ikifuatiwa na majuto na toba. Mara nyingi, madhara yanayosababishwa na vitendo vya pupa huwa hayarekebishiki. Ili kuweza kutibu madhara ya uovu unaosababishwa na pupa, mhusika lazima aelewe matokeo yake ya kutisha, na ajizoeze na tabia inayoheshimika na kuwa makini.
6. Chuki kwa Muumba na Viumbe Wake Hii ni hali ambayo hujitokeza pale ambapo mtu anakuwa na fikra za kutokumwamini na kumbeza Allah, viumbe vyake, na shughuli zao, na kutafsiri kila kitu katika namna ya kukanusha. Pia ni matokeo 61
SAADA KAMILI
ya woga na kutojiamini; kwa sababu mtu mwenye udhaifu wa tabia njema vitendo vyake huongozwa na maoni yanayotokana na dhana zake. Kinyume cha tabia hii ni kuonyesha nia njema na kumwamini Allah na binadamu; yaani kuwa na msimamo wa kupenda kila kitu isipokuwa panapokuwa na ushahidi wa kutosha wa kinyume chake. Qur`ani inasema: “………na mlidhania dhana mbaya, na mmekuwa watu wanaoangamia”(48:12). Imam Ali (a.s.) anasema:
َ أح َس ِن ِه َحتَّى َي ْا ِت َي َك َما َي ْغلِب َ أخي َ ُك ِم ْن ُه َو َ ال ْ ْك َعلَ َى َ ض ْع أم ِ ْر ْ َ َ ِ َت ُظ َنّ ّن ب َكلِ َم ٍة َخ َر َج ْت ِم ْن ْ ْر ِ ِ أخيْك ُس ْو ًءا َوأن َت َت ِج ُد ل َها ِم َن ال َخي ً َم ْح َم .ال “Uwe na fikra za kupenda kile anachokifanya nduguyo, isipokuwa pale unapogundua kitu ambacho ni kinyume chake; amini kile anachokisema nduguyo wakati uwezekano upo wa wewe kuweza kuamua kama ni sahihi na kizuri.”
Jinsi ya kupambana na uovu huu ni mtu kupuuza chochote anachoona au kusikia kuhusu ndugu yake katika imani, na aweke dhana nzuri moyoni mwake kuhusu nduguye katika imani, kujenga dhana njema moyoni juu yake na adumishe msimamo wa kumheshimu na kumpenda.
62
SAADA KAMILI
7. Hasira Hasira ni mojawapo ya athari za nafsi na ina hali za aina tatu: a.
Aina ya kuzidi kiasi, ambayo imeelezewa kama kile ambacho kinaweza kumtupa mhusika nje ya mipaka ya dini na sheria zake.
b. Aina ya upungufu, ambayo imefafanuliwa kama hali ambayo mhusika hushindwa kuchukua kitendo cha kutumia nguvu nyingi hata kama kufanya hivyo ni muhimu ili ajitetee. c.
Aina ya wastani, ambapo hasira huamshwa kwenye mazingira yanayofaa na yanayoruhusu. Kwa hiyo ni wazi kwamba aina ya kwanza na ya pili ni miongoni mwa maovu yanayoikumba nafsi, ambapo ile ya tatu ni miongoni mwa tabia za uadilifu zinazotokana na ujasiri.
Hasira ya kuzidi kiasi ni maradhi mabaya, ambayo inaweza kuchukuliwa kuwa ni kichaa cha muda mfupi. Maradhi haya yanapopungua, haraka sana hufuatiwa na majuto na toba, hali ambayo huwakilisha miitikio mizuri ya mtu mwenye busara. Imam Ali (a.s.) amesema:
َ ض ْر ٌب ِم َن ْال ُجنُ ْون َ الح ّدُة اح َب َها َي ْن َد ُم َفاِ ْن لَ ْم َي ْن َد ْم َف ُجنُ ْونُ ُه َ ال َّن ِ ص ِ .ُس َت ْح َك ٌم ْم “Hasira ni pigo la kichaa, kwa kuwa mtu aliyekumbwa na hali hiyo baadaye huhisi majuto na masikitiko. Kama mtu hawezi kuhisi majuto baada ya hasira, ina maana kwamba kichaa chake kimekuwa cha kudumu.” 63
SAADA KAMILI
Zaidi ya hayo, kutokuwa na hasira kabisa pia ni uovu, ambao humburuza mhusika kwenye fedheha, kutiishwa na kutokuwa na uwezo wa kupigania haki zake. Ili kuweza kutibu hasira ya kupita kiasi, mhusika analazimika kuondoa visababishi vyake. Visababishi hivi vinaweza kuwa majivuno, uchoyo, jeuri, ulafi na uovu mwingine ufananao na huo. Pia mtu lazima atambue kwamba hasira ya kupita kiasi ikoje, na matokeo ya uovu wake yakoje. Pili, mhusika lazima apime manufaa ya uvumilivu na kujizuia, na aambatane na watu wenye sifa hizi. Lazima pia mhusika atambue kwamba uwezo wa Allah ni mkubwa sana, na kila kitu kipo chini ya amri Yake, ambapo mhusika anaweza kutambua udhaifu wake ukilinganishwa na uwezo wa Allah usio na mpaka. Tatu, atatakiwa atambue kwamba mtu aliyeko kwenye hali ya hasira hapendwi na Allah; zaidi ya hayo, anaweza akafanya kitu wakati yu ana hasira, hatimaye akaaibika. Kinyume cha hasira ni upole na uvumilivu - tabia ambazo ni miongoni mwa sifa kamilifu za nafsi. Sifa hizi humfanya mtu kuwa msamehevu na mwenye huruma, ingawaje anaweza kuwa na uwezo kamili wa kulipa kisasi. Qur`ani Tukufu inasema: “Shikamana na kusamehe na amrisha mema na wapuuze wajinga.” (7:199). Na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema:
ُاع ُفوا يُ ِع ُز ُك ْم اهلل َّ ِال َيز ْي ُد ْال َع ْب َد ا َ ْ ْ ْ ال ِع ًّزا َف ِ ال َعف ُو “Usamehevu hunyanyua daraja la mtu; samehe ili Allah akuheshimu.”
64
SAADA KAMILI
8. Vurugu Vurugu ni matumizi ya nguvu kwa hasira na uharibifu wake ni ama kwa kauli au kitendo, na hayo ni mojawapo ya matokeo ya hasira. Kinyume chake ni tabia ya upole, ambayo inatokana na uvumilivu. Ikimtahadharisha Mtume, Qur`ani Tukufu inasema kuhusu tabia hii: “…….kama ungekuwa mkali mshupavu wa moyo, wangekukimbia……”[3:159]. Na hadithi ya Mtume inasema:
ْ أح َّب اهللُ َع ْب ًدا ُحر ِم َّ ُح َر ِم ِّ ُأع َطا ُه اهلل ْ الر ْف َق َو َم ْن ي َ الر ْف َق ي َ اِ َذا َّْر ُكل َ َ الخي “Allah akimpenda mmojawapo wa waja wake, humbariki kwa kumpa tabia ya kirafiki, na yeyote anayepungukiwa na tabia hii, hupungukiwa na baraka zingine zote.”
Mahali pengine: ipo hadithi ya Mtume ambayo inasema:
ال ْي َمان َ ْال ُم َد ِ ارا ُة ِنصف ا “Kuwafikiria na kuwahurumia watu wengine ni nusu ya imani.”
65
SAADA KAMILI
9. Chuki Uovu huu husababishwa na hasira, na kinyume chake ni tabia ya upole. Uovu huu husababisha watu kuwaepuka wale wenye tabia hii, na humsababishia maangamizi mhusika hapa duniani na Akhera. Pia huharibu kazi zote nzuri za mhusika. Mtume amenukuliwa akisema:
ُس ْو ُء ْال ُخ ْل ِق ي ُْف ِس ُد ْالع َم َل َك َما ي ُْف ِس ُد ْال َخ ُّل ْال َع َس َل “Tabia ya chuki huharibu kazi nzuri, kama vile siki inavyoharibu asali.”
Ikiongea na Mtume (s.a.w.w.), Qur`ani inasema: “Na bila shaka una tabia njema, Tukufu.” (68:4).
10. Tabia ya Kinyongo Pia kinyongo husababishwa na hasira, na ni changamani inayotengenezwa baada ya kwisha hasira. Inayo matokeo machafu kama vile wivu na kukata uhusiano na mtu ambaye kinyongo hicho kinamwelekea, na kinaweza kusababisha ugomvi wa kupigana, na kutoa maneno machafu dhidi ya mtu mwingine, kusema uwongo, kusengenya, kumkashifu mtu mwingine, kutangaza siri zake. Wakati mwingine kinyongo hutokeza nje na hujionyesha kuwa uadui kabisa, na matokeo yake ni kupigana, kutoa maneno ya laana dhidi ya adui na kumuita majina mabaya - yote haya ni maovu mabaya..
66
SAADA KAMILI
Njia za kutibu ugonjwa huu wa kiroho ni kwamba mhusika lazima kwanza atambue kwamba kinyongo humuumiza zaidi yule mwenye kukihodhi moyoni mwake kuliko yule ambaye huelekezewa. Pili, lazima mhusika aamue kuchukua msimamo wa kirafiki na kimsaada kwa mtu ambaye anamchukia, kumfanyia mambo mazuri hata kama hisia zake zinamvuta na kumkataza asifanye hivyo na aendelee na msimamo huo wa kirafiki hadi apone ugonjwa huu.
11. Tabia ya majivuno na kiburi Huu ni uovu mwingine unaotokana na Nguvu ya Hasira - hali ambayo mwenye nayo hujifikiria yeye kuwa mtu wa juu sana kwa sababu ya manufaa fulani ya kweli au ya kudhania. Kwa upande mwingine, mhusika hushindwa kukubali sifa za ukamilifu wa Allah, Ambaye ndiye chanzo cha vitu vyote. Hadithi nyingi sana zinasema kuhusu uovu wa tabia hii. Hadithi moja ya Mtume (s.a.w.w.) inasema:
ْ لَ ْو لَ ْم ُ ْت َعلَي ُ تذ ِنبُوا لَ َخ ِشي ُجب؛ َ ْك ْم ما ُه َو اَ ْك َب ُر ِم ْن َذلِ َك؛ ْالع .ُج َب ْ ْالع “Hata kama hamtendi dhambi yoyote, ninahofia kwamba mnaweza kuangukia kwenye kitu ambacho ni kibaya zaidi: Majivuno! Majivuno!”
Uovu ambao ni matokeo ya tabia ya majivuno na kiburi ni: ufidhuli, usahaulifu, mhusika kutokujali mapungufu yake mwenyewe, na, kwa hiyo, kushindwa kuyasahihisha; kuanguka kwa thamani ya matendo ya mhusika mbele ya macho ya binadamu na Allah; ku67
SAADA KAMILI
tokumshukuru Allah kwa neema Zake, na kwa hiyo kuwa na hatari ya kuzipoteza; kushindwa kuuliza maswali kuhusu vitu asivyovijua mhusika, na kwa hiyo, anabaki na ujinga wake; na mwisho, kuamini na kutangaza maoni yasiyo sahihi na yasiyo na msingi. Ili kuweza kumtibu mtu mwenye ugonjwa huu, ni muhimu kwa mhusika kurejesha fikra zake kwa Allah na kumjua Yeye. Anapotambua kwamba ni Muumba Mwenye kudura ndiye anayestahili kuabudiwa na kutukuzwa, na kwamba yeye si chochote akilinganishwa na utukufu wa Allah, na kwamba hakuna kitu chochote anachoweza kukiita kuwa ni cha kwake, na kwamba hata viumbe wengine watukufu zaidi kwake kama mitume na malaika, sio chochote kulinganishwa na Allah, atakuwa ameamka kuhusu ukweli kwamba ni upuuzi kujivuna na kuwa na kiburi, na kwamba lazima ajifikirie yeye kwamba vile alivyo kwa ukweli: ni kiumbe mdogo mno wa Allah. Binadamu anapotafakari juu ya mwanzo wake duni kama tone la manii, mwisho wake kama vumbi linalojaa kwenye kiganja, na muda mfupi wa maisha yake kama kiumbe dhalili kinachoweza kushambuliwa na magonjwa na kutawaliwa na tamaa na silka, si tu kwamba atasahau kiburi chake bali pia atajisahau nafsi yake yeye mwenyewe, na kutumia uhai wake wote katika kumwabudu Allah. Qur`ani Tukufu inasema: “Ameangamia mwanadamu, mbona anakufuru sana! Kwa kitu gani amemuumba? Kwa tone la manii amemuumba, na kumuwezesha. Kisha akamfanyia njia nyepesi. Kisha akamuua akamuweka kaburini. Kisha atakapotaka atamfufua.” (80:17-22). Na tunayo beti ifuatayo kutoka kwenye mashairi ya Kiajemi: “Usijivunie utajiri wako, nguvu na madaha, kwani mojawapo ya hayo linaweza, katika usiku moja tu 68
SAADA KAMILI
likachukuliwa na wezi, na lingine kwa pigo moja tu la homa likaweza kutoweka.” Lazima izingatiwe akilini kwamba kiburi na majivuno vinaweza kusababishwa pia pale ambapo mtu anapendelewa na akapata neema za Kimungu kama: ujuzi, kujitoa kwa mambo mema, uchaji Mungu, imani, ujasiri, ukarimu, subira, ukoo bora, uzuri, utajiri, nguvu, daraja kubwa, akili na kadhalika. Ili kuweza kuepuka matokeo ya aina hii, mtu lazima wakati wote akumbuke mapungufu yake na dosari zake; kumbukumbu ya aina hii humsaidia mhusika kuepuka majivuno. Kinyume cha majivuno na kiburi ni staha, ambayo ni tabia yenye thamani sana yenye kujenga maadili ya nafsi na ukamilifu wa mhusika.
12. Ufidhuli Ufidhuli ni mojawapo ya matokeo ya kiburi na majivuno. Pale ambapo mhusika anapojikweza mwenyewe sana; hayo ni majivuno binafsi na pale anapokuwa na kawaida ya kuwaona wenzake kuwa ni watu wa chini wakilinganishwa na yeye; huo ni ufidhuli. Kinyume na hali hizi, mtu anapojifikiria yeye kuwa mdogo na asiye na thamani, hii huitwa staha; na kwa nyongeza ya hili, anapowafikiria wengine kuwa ni wabora kuliko yeye, huo ni unyenyekevu. Kwa vyovyote vile, ufidhuli ni mojawapo ya uovu mbaya sana wa kimaadili. Ni hivyo kwa sababu ufidhuli ni pazia zito ambalo huficha dosari za mhusika kwa kushindwa kujigundua kwamba anazo dosari, na katika hali hiyo hushindwa kuziondosha na kuweza kupata ukamilifu. Qur`ani Tukufu inasema: “……..hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyopiga muhuri juu ya kila moyo wa jeuri, ajitukuzaye.” (40:35). 69
SAADA KAMILI
Na: “Nitawaepusha na Aya zangu wale wanaotakabari katika nchi pasipo haki….” (7:146). Na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema:
ُ َْ َ ال َي ْد ُخ ُل ْالجنّة َم ْن ْر ٍ كان ِفى قل ِب ِه مثقال َحبٍّة ِم ْن ِكب “Mtu mwenye japo chembe ndogo tu ya majivuno moyoni mwake, hataweza kuingia Peponi.”
Nabii Isa (as) amesema: “Kama vile mmea unavyoota kwenye ardhi iliyo laini, na si kwenye mwamba mgumu, ndivyo pia busara inavyostawi na kukua kwenye moyo mnyenyekevu na laini, si kwenye mioyo migumu ya watu mafidhuli. Huoni kwamba mtu anayenyanyua kichwa chake juu hugonga dari, ambapo yule anayeinamisha kichwa chake, dari inakuwa rafiki yake na inamhifadhi?” Tiba ya ufidhuli ni kama ile ya uovu wa majivuno. Tiba nyingine ni kujifunza aya mbalimbali za Qur`ani na hadithi ambazo zinazungumzia na kulaani uovu huu. Pia mhusika lazima avumilie katika kujizoesha unyenyekevu mbele ya Allah na binadamu wenzake, awe karibu na mafukara na wanyonge, aepukane kuvaa nguo za kujishaua badala yake avae nguo za kawaida, aelewane vizuri na watu fukara na matajiri, amsalimie kila mtu bila kujali umri wake, na ajiepushe na kutaka kukaa kwenye meza kuu kwenye hafla mbalimbali. Kwa ufupi, lazima ajizuie kuyaendea matamanio ya ubinafsi kwani ndio yanayochangia kumfanya awe na tabia ya ufidhuli. Kinyume cha ufidhuli ni unyenyekevu, ambayo ni mojawapo ya tabia njema zinazosifika sana. Qur`ani Tukufu inasema hivi kuhusu 70
SAADA KAMILI
tabia ya unyenyekevu: “Na waja wa Rahmani ni wale wanaotembea ardhini kwa unyenyekevu na wajinga wakisema nao, husema: Amani.” (25:63). Na: “Na uinamishe bawa lako kwa yule anayekufuata katika wale walioamini” (26:215). Ni lazima izingatiwe kwamba unyenyekevu ni uwanja wa katikati baina ya ufidhuli na unyonge kabisa, na kama vile ufidhuli ni uovu, ndivyo ilivyo uovu kwa unyonge kabisa. Tofauti baina ya unyonge kabisa na unyenyekevu pia inajulikana wazi. Kwa hiyo, pale ambapo ni sifa nzuri kwa mtu kuwa mnyenyekevu, ni uovu kuwa mnyonge wa kupindukia.
13. Hali ya Uasi Ni aina ya ufidhuli, pia ni uovu mbaya sana. Unafafanuliwa kama uasi dhidi ya wale wote ambao ni muhimu watiiwe, kama vile: mitume na manaibu wao, serikali zenye kukubalika kimaadili, walimu, wazazi na kadhalika. Hadithi ya Mtume (s.a.w.w.) inasema:
َ أع َج َل ْ اِ َّن الش ِّر ُع ُق ْو َب ُة ال َبغى “Dhambi inayoadhibiwa haraka sana ni ile ya maasi.”
Pia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema:
َّ ِلى َش ْى ٍء ا َّ َوج َّل ا ال اَ َذلَُّه اهلل َ َح ٌّق َعلَى اهلل َع َّز َ ال َي ْب ِغ ْى َش ْى ٌء َع 71
SAADA KAMILI
“Ni haki ya Allah swt. kukishusha hadhi kitu chochote kinachoasi dhidi ya kitu kingine chochote.”
Imam Ali amesema:
َّ َ ِص َحا َب ُه ا ار ْ َاِ َّن ْال َب ْغ َى َي ُق ْو ُد ا ِ لى الن “Maasi humsukumiza mhusika kwenye Moto”
Namna ya kutibu uovu wa maasi ni mhusika kutafakuri juu ya hali yake ya kiroho na arejelee hadithi ambamo utiifu sahihi umeamriwa, na wakati huohuo ajitahidi kuendeleza moyo wa unyenyekevu kwenye nafsi yake.
14. Mtu kushindwa kuona dosari zake Haya ni matokeo mengine ya kiburi na majivuno. Kinyume chake ni mhusika kutambua dosari zake na mapungufu yake.
15. Ushabiki Ushabiki ni uovu mwingine wa kimaadili ambao huielekeza akili na uelewa wa mhusika kwenye uharibifu wa tabia. Hisia za mapenzi zinaweza kuwepo kuhusu imani ya mhusika kidini, taifa, kabila, familia, au mambo mengine kama hayo, na hali hii inaweza kuonekana kwa namna ya kauli au matendo. Inapokuwa hisia kali ni kuhusu vitu vyenye manufaa, huitwa shauku na ghera, na ni hali inayostahii kusifiwa sana. Kama kwa upande mwingine hisia kali zinakuwepo kwenye vitu visivyofaa, inakuwa ni uovu. 72
SAADA KAMILI
Hadithi ya Mtume (s.a.w.w.) inasema:
ص ِبية َب َع َث ُه اهلل َي ْو َم َ َم ْن كاَ َن ِف ْى َق ْل ِب ِه َحبٌّة ِم ْن َخ ْر َد ٍل ِم ْن َع اهلَِي ِة ِ اب ْال َج ِ ال ِق َيا َم ِة َم َع اَ ْع َر “Yeyote mwenye chembe ndogo tu ya ushabiki moyoni mwake, Siku ya Ufufuo, Allah atamfufua akiwa na Waarabu wapagani wa enzi za Ujahilia.”
Namna ya kutibu uovu wa ushabiki ni mhusika mwenyewe afanye zoezi la kujichunguza, na atambue ukweli kwamba ushabiki huziba maendeleo ya mtu na hufifisha uelewa wa mtu kuhusu ukweli wa mambo. Hivyo basi, endapo anataka kujua ukweli, ni lazima aepukane na ushabiki wenye kupofusha akili yake, na aweze kupima mambo bila upendeleo na bila kutekwa na hisia kali.
16. Kuficha Haki Uovu wa kutafsiri vibaya na kuficha haki husababishwa na ushabiki, woga au hofu. Pia inaweza kusababisha na matamanio ya mali au malengo yanayofanana na hayo. Kwa vyovyote vile, uovu huu humwelekeza mtu kwenye kupotoka kutoka kwenye Njia Iliyonyooka, na kuleta uharibifu wa tabia. Kinyume chake ni kudhihirisha na umadhubuti kwenye njia ya haki. Kuna hadithi nyingi na aya za Qur`ani zinazolaani kuficha ukweli na kuwasifu wakweli. Baadhi ya aya ambazo zinasema waziwazi na moja kwa moja kuhusu jambo hili ni kama zifuatazo: “…..kwa nini mnachanganya haki na batili, na mnaificha haki na hali mnajua?” (3:71) 73
SAADA KAMILI
Na “…..Na ni nani dhalimu mno kuliko yule afichaye ushahidi alionao utokao kwa Mwenyezi Mungu…..?” [2:140] Na “Hakika wale wanaoficha tuliyoyateremsha katika dalili zilizo wazi na muongozo, baada ya sisi kuzibainisha kwa watu Kitabuni hao hulaaniwa na Mwenyezi Mungu na hulaaniwa na wenye kulaani (pia).” (2:159). Kuhusu kujitibu maradhi haya, mtu anatakiwa afahamu ukweli kwamba tabia hii huvuna hasira ya Mungu na inaweza kumuelekeza mtu kwenye ukafiri (kufr). Zaidi ya haya, mhusika anatakiwa kutafakari kuhusu manufaa ya kusema kweli, na halafu ajilazimishe kufuata kweli hii katika matendo.
17. Usugu na Ukatili Mtu anapokumbwa na uovu huu; usugu na ukatili, haathiriwi au kuhuzunishwa na maumivu na mateso ya binadamu wenzake. Kinyume chake ni tabia ya wema na huruma. Zipo aya kadhaa za Qur`ani zinazokemea uovu huu, na kusifu huruma na upendo. Tiba na uponyaji wa maradhi haya ni ngumu sana, kwa sababu ukatili na usugu huzama kwenye tabia ya mhusika, na kuwa sugu na kuwa ngumu kupona. Tiba iliyo nzuri sana ya ugonjwa huu ni mhusika kuepuka, kwanza kabisa, matendo ya kikatili, ambayo huonekana kimwili. Halafu, lazima afanye jitihada ya kujali mateso na matatizo yanayowakumba wengine, na kuyafikiria matatizo hayo kuwa ya kwake. Zaidi ya haya, mhusika anatakiwa kuathirika kwa namna inayofaa kwa hali kama hiyo, hadi, polepole aanze kuonja ladha ya huruma na hatimaye kuwa ni tabia yake moja kwa moja.
74
SAADA KAMILI
MAOVU YA NGUVU YA MATAMANIO Moja ya tatu kati ya sehemu nne za kitabu hiki inazungumzia magonjwa ya Nguvu ya Hisia Kali na tiba yake. Kuna aina kumi za maradhi haya, na tutatoa maelezo mafupi kuhusu kila moja ya maradhi husika:
1. Kupenda Dunia Maana nzuri sana ya uovu huu na “dunia” iliyolaaniwa humo, inaonekana kwenye aya ifuatayo ya Qur`ani Tukufu: “Watu wamepambiwa kupenda matamanio ya wanawake, na vijana wa kiume, na mali mengi ya dhahabu na fedha na farasi wazuri wazuri, na wanyama na mimea. Hivyo ni vitu vya kustarehea katika uhai wa ulimwenguni, na kwa Mwenyezi Mungu ndiko kwenye marejeo mazuri.” (3:14). Lazima izingatiwe kwamba vitu vyote vilivyotajwa kwenye aya hii ya Qur`ani ambavyo ni neema za Mwenyezi Mungu, vinaweza visilaaniwe. Juu ya haya, matumizi yanayofaa ya neema ya Mungu pia ni jambo la kuthaminiwa. Hata hivyo, jambo lisilopendeza ni mtu kuambatana na vitu hivi sana, na kuvipatia umuhimu mkubwa katika maisha yake - msisitizo ambao unaweza kuzidi hata ule anaopewa Allah. Lakini kama vitu hivi havitachukua nafasi ya Allah na vingetumika kama namna ya kupata maendeleo na kupata ukaribu kwa Allah, si tu kwamba hali hii haikatazwi bali inapendeza sana. Kwa hiyo, laana na sifa ya dunia ambayo tunakutana nayo ndani ya Qur`ani au hadithi inahusu namna ya jinsi ya kuvitumia vitu hivi hapa duniani. Kama mtu anaifanya dunia kuwa kijimungu chake, na anamezwa na matumaini ya kidunia kwa kiwango kwamba anamsa75
SAADA KAMILI
hau hata Allah na Akhera basi tunaweza kusema kwamba mtu kama huyu amekuwa majeruhi wa ugonjwa wa “kupenda dunia.” Hadithi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) inaeleza kinagaubaga jinsi walivyoshindwa wale wanaopenda dunia kwa maneno haya:
ُّ صبح َو الد ْن َيا اَ ْك َب ُر َه ِمِّه َفلَيْس ِم َن اهلل ِفى َش ْي ٍء واَْل َز ِم اهلل ْ ََم ْن ا ًفرُغ ِم ْن ُه اََبدا ً ال َي ْن َق ِط ُع أ َب ًدا َو ُش َ َهمّا:ال ّ غال ال َي َت َ َق ْل َب ُه اَ ْر َب َع ِخ ٍص ُ ال َي َن ً ال ِغ َنا ُه اََب ًدا َواَ َم َ ال َ َو َف ْق ًرا .ال َيبْلُغ ُم ْن َت َها ُه اََب ًدا “Mtu anayeamka na fikra zake zikiwa zimeelekezwa kwenye anasa za dunia, hutengwa na Allah, na Allah Atatengeneza sifa nne kwa ajili yake: masikitiko yasiyo na ukomo, kufanya kazi zisizokwisha, mahitaji yasiyotimizwa, na matumaini ambayo hayapatikani.”
Ili kuweza kutibu ugonjwa huu, mhusika lazima atafakari juu ya ukweli kwamba vitu vizuri vya hapa duniani ni vya kupita, na kile kinachobaki kwa ajili ya mwanadamu ni mafao ya kiroho, kuwa karibu na Allah, na juhudi zinazofanywa kwa ajili ya maandalizi ya Akhera.
2. Kupenda Mali na Utajiri Uovu huu ni tawi la maradhi ya kuipenda dunia, na yote yale yaliyosemwa katika kusifia au kulaani mambo ya dunia yanaweza kusemwa kuhusu kukusanya mali nyingi. Baadhi ya aya za Qur`ani na hadithi zimesifia mali na utajiri, ambapo aya zingine zinalaani. Hata hivyo hakuna mkanganyiko baina yao; kwa sababu aya na ha76
SAADA KAMILI
dithi hizo ambazo zinalaani, zinakusudiwa kulaani ukusanyaji wa mali nyingi ambayo humtenganisha mhusika na Allah na Akhera; ambapo zile zinazosifia mali na utajiri, zinarejelea ukwasi unaotumika kunyanyua tabia ya binadamu na kumfikisha binadamu karibu zaidi na Allah. Kwenye aya ya Qur`ani tunasoma: “Enyi mlioamini! yasikusahaulisheni mali yenu wala watoto wenu kumkumbuka Mwenyezi Mungu, na wafanyao hayo, basi hao ndio wenye khasara.” (63:9). Na kwenye aya nyingine, ummah unatakiwa kuomba toba kwa Allah na kuahidiwa rehema zifuatazo: “Na atakupeni mali na watoto, na atakupeni mabustani, na atakufanyieni mito.” (71:12). Kwa mujibu wa hadith Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amenukuliwa akisifu na kulaani mali:
َّ ال َو َ ان ال ِن .َّفاق َك َما يُ ْن ِب ُت ال َما ُء ْال َب ْق َل ِ الش َر ِ ُح ُّب ال َم ِ ف يُ ْن ِب َت “Kupenda mali na umaarufu hustawisha unafiki kama ambavyo mimea hustawishwa na maji.”
ُ ِن ْع َم ْال َم .الصالِ ِح َّ ِصالِ ُح ل َّ ال ْال َ لر ُج ِل ”Ni uzuri wa kiasi gani kwa mali iliyopatikana kwa njia ya haki kumilikiwa na mtu mwadilifu.”
Kwa vyovyote vile, aina ya ukwasi unaofaa na wa haki ni ule ambao umepatikana kwa njia ya halali, na unaotumika kwa kumfurahisha Allah -kama vile (hajj) kwenda kuhiji Maka, (jihad) kupi77
SAADA KAMILI
gana katika njia ya Allah, kuwasaidia mafukara, na aina zingine zote za sadaka zenye lengo la ustawi wa ummah. Kujizuia (Zuhd): Kinyume cha kupenda anasa za dunia ni (zuhd), yaani kujizuia kupenda mambo ya dunia, kimwili na kiroho isipokuwa kwa vitu ambavyo ni muhimu kwa lengo la kupata neema za Akhera, na kupata ukaribu zaidi kwa Allah. Zuhd imesifiwa sana ndani ya Qur`ani na hadithi: Zuhd inafikiriwa kuwa mojawapo ya tabia za Mitume na watakatifu. Zipo daraja mbalimbali za kujizuia (zuhd), nazo ni: i.
Kujizuia kutenda dhambi.
ii. Kujizuia kufanya vitu “mushtabah” ambavyo havijulikani kwa uhakika endapo vimeharamishwa, bali vinadhaniwa tu. iii. Kujizuia kutokana na kilicho zaidi ya mahitaji yako. iv. Kujizuia kufuatilia matamanio binafsi. v.
Kujizuia na kila kitu isipokuwa Allah; yaani kuelekeza mazingatio yako yote kwa Muumba, kutosheka na kiasi kidogo kinachokidhi mahitaji ya kimaumbile na kilichobaki kitolewe kwa ajili ya Allah.
Watu hutekeleza Zuhd kwa sababu tofauti tatu: i.
Kwa ajili ya kuukwepa Moto wa Jahannam. Aina hii ya zuhd inaitwa “Zuhd al-kha ifin,” au “kujizuia kwa wenye hofu” 78
SAADA KAMILI
ii. Ili kuweza kupata radhi za Allah na kupata furaha ya Pepo. Aina hii ya zuhd inaitwa “Zuhd al-rajin” au “kujizuia kwa wenye matumaini.” iii. Kujizuia kwa ajili ya kupata imani kali ya kimbingu (ifran). Hili ni lengo la juu zaidi na aina ya zuhd yenye kuthaminiwa sana, ambayo hutekelezwa bila ya kuogopa Moto wa jahannam wala kutamani furaha ya Peponi.
3. Ukwasi na Utajiri Maana yake ni kuwa navyo vitu muhimu vya maisha na zipo daraja nyingi, wakati mwingine humfikisha mtu kwenye utajiri mkubwa na kuhodhi mali. Kinyume chake ni umasikini na ufukara, yaani kupungukiwa na vitu muhimu vya maisha. Ukwasi na umasikini ama vinaweza kunyanyua tabia ya mtu au kumharibu. Kama ukwasi umepatikana kwa njia ya halali, na unaobaki ukatumika kwa ajili ya Allah na kuwahudumia viumbe wake, inafikiriwa kuwa mojawapo ya tabia njema. Endapo, kama mambo yalivyo, utajiri umepatikana kwa njia isiyo halali, kupitia udhalimu na unyonyaji, na tajiri hajali kutoa msaada kwa fukara na masikini, hali hiyo itamwelekeza na kumfikisha kwenye kuharibikiwa. Qur`ani inasema: “Sivyo, hakika mwanadamu anaasi sana. Kwa kujiona ametosha.” (96:6-7). Kwa njia ileile, umasikini pia kama unakwenda sambamba na uvumilivu, kukubali matokeo ya maisha na kutosheka humpeleka mtu kwenye ukamilifu wa kiroho, vinginevyo, pia unaweza kumharibu mtu kiroho. Hivyo, kama tunaona kwenye aya za Qur`ani na 79
SAADA KAMILI
hadithi ukwasi na umasikini ni hali zinazosifiwa na wakati mwingine kulaaniwa ni kwa sababu kama hali hizi zinakwenda sambamba na masharti yanayotakiwa hupendeza, vinginevyo, hazipendezi na huchukiza.
4. Ulafi (Hirs) Ulafi ni hali ambayo humfanya mtu asitosheke na chochote anachomiliki na humfanya atamani kupata zaidi. Ulafi ni mojawapo ya maovu mabaya sana yenye kusababisha uharibifu, na haukuwekewa mipaka kwenye umiliki wa mali wa kidunia tu, bali pia vitendo viovu kama vile; kupenda kula kupita kiasi, kupenda ngono sana, na mambo mengine. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema:
ُ ص َو ُط َ ْ ْن اَ َد َم َو َت ُش ُب ِف ْي ِه َخ َ ول ُ ْب اِب ُ َي ِشي اال َم ِل ُ ْال ِح ْر:ان ِ صل َت “Jinsi mtu anavyoongezeka umri na kuelekea uzeeni , tabia zake mbili zinakuwa katika umri wa ujana: ulafi na matumaini yasiyo na uhakika.”
Imam al-Baqir (as) amesema;
َُ َ َ ْ ُّ الحريْص َعلَى َ ْ ُكلََّما:الق ّز از َدا َد ْت َعلَى ِ ِ َ َمثل ِ الدن َيا ك َمث ِل ُد ْو َد ِة ًّ ََن ْف ِس َها ل ُ ان اَ ْب َعد ُلَ َها ِم َن َ ف َك .ُو َت َغمًّا ْ الخ ُر ْو ِج َحتَّى َتم 80
SAADA KAMILI
“Mtu mlafi katika kuipenda dunia yu kama kiwavi cha hariri: jinsi mdudu huyu anavyozidi kujizungusha kwenye kifukofuko chake ndivyo anavyozidi kukosa mwanya wa kutoka humo, hadi anakufa kwa uchungu.”
Kinyume cha ulafi ni tabia ya kutosheka, ambayo humwezesha mtu kudhibiti matamanio yake na kutosheka na kuwa na vitu muhimu vya maisha. Mtu mwenye tabia hii wakati wote huishi maisha ya kuheshimika, kama mtu huru; yeye anakinga ya kutokuathiriwa na uovu wa ukwasi hapa duniani na matokeo ya kuadhibiwa Akhera. Ili mtu aweze kujinasua kutoka kwenye uovu wa ulafi lazima mhusika atafakari matokeo yake yanayoumiza na atambue kwamba ulafi ni tabia ya wanyama, ambao hawatambui mipaka katika kukidhi haja ya ngono, na hutumia kila njia ili waweze kifanikisha, Kwa hiyo ni muhimu kwa mtu kujinasua kwenye uovu huu na kudhibiti nafsi yake yenye kuasi.
5. Tamaa Husababishwa na kupenda dunia, tamaa ni aina nyingine ya tabia ya uovu, na inafafanuliwa kuwa mtu anatamani vitu vilivyomilikiwa na wengine. Kinyume chake ni kutokuwategemea wengine na kutokutamani vile vinavyomilikiwa na wengine. Zipo hadithi nyingi zinazosifia mtu kutokutegemea wengine na kulaani tamaa ya mali. Hapa tutanukuu hadithi mbili zinazosifia mtu kutosheka, ambazo pia zinalaani ulafi wa mali. Imam Baqir (as) amesema:
س ال َع ْب ُد َع ْب ٌد لَه َرغ َب ٌة َ َو ِب ْئ.ُس ال َع ْب ُد َع ْب ٌد له َط َم ٌع َي ُق ْو ُده َ ِب ْئ .تُ ِذلُ ُه 81
SAADA KAMILI
“Ni kiumbe muovu jinsi gani yule anayeongozwa na tamaa ya mali. Ni kiumbe muovu kiasi gani yule ambaye tamaa yake humletea fedheha.”
Imam Ali (as) amesema:
ْ اِ ْس َت ْغ ِن َعم ار َغ ْب اِلَى َم ْن ِش ْئت َت ُك ْن ْ َو, ْر ُه َ َّن ِش ْئ َت َت ُك ْن َن ِظي َ ْر ُه َواَ ْح ِس ْب اِلَى َم ْن ِش ْر ُه َ ئت َت ُك ْن اَ ِمي َ اَ ِسي “Kama unaweza kufanya mambo yako bila kumtegemea yeyote yule, unaweza kuwa mwenzi wake. Yeyote yule ambaye unapenda kuwa karibu naye, wewe utakuwa mateka wake. Yeyote ambaye unamuonea huruma, unaweza kuwa juu yake”
6. Ubakhili [Bukhl] Ubahili unaelezewa kama mtu kuwa mbaniaji pale ambapo anatakiwa kuwa mkarimu, kama vile ubadhirifu, ambao ni kinyume chake, unavyoelezewa kama ni tabia ambayo mtu anakuwa na ukarimu wa fahari badala ya kuwa muwekevu. Njia ya katikati baina ya hizi ncha mbili zilizovuka mipaka ya kiasi huitwa sakhaa’; hii ni kuwa mkarimu pale ambapo ukarimu unahitajika. Qur`ani inaelezea tabia za waumini, ambao pia huitwa [ibaad al-Rahman] au “waja wa Mwenye rehema,” inasema: “……..Na wale ambao wanapotumia hawatumii kwa fujo, wala hawafanyi ubakhili na wanakuwa waadilifu baina ya hayo.”[25:67]. Kama ambapo ubakhili (bukhl) husababishwa na kupenda mambo ya dunia sana, ukarimu (sakhaa’) ni matokeo ya zuhd. Aya nyingi 82
SAADA KAMILI
sana za Qur`ani na hadithi zinasifu na kulaani sifa hizi mbili, ambazo hatutazitaja kwa sababu ya uchache wa nafasi. Daraja la juu kabisa la ukarimu ni muhanga; yaani kuwa tayari kuwapa wengine kile unachokihitaji. Ikiwaelezea waumini wa aina hii, Qur`ani inasema: “.…. na wanawapendelea wengine kuliko nafsi zao ingawa wenyewe wana hali duni……” (59:9). Ili mtu aweze kujitibu ugonjwa huu wa ubakhili, ni muhimu kwa mhusika kuzingatia aya za Qur`ani na hadithi ambamo uovu huu umelaaniwa, na kutafakari kwa kina kuhusu matokeo yake mabaya. Kama hiyo haitoshi, mhusika ajilazimishe kuwa mkarimu na mpaji, hata kama ukarimu huo unakuwa wa bandia; na zoezi hili lazima liendelee hadi hapo ukarimu unakuwa tabia ya mhusika. Ukarimu ni muhimu mtu anapofanya vitendo vya wajiba kama vile kulipa khums na zakat, kuwatunza watoto na mke wake, kugharamia safari ya kwenda (hajj) kuhiji Kaaba Takatifu) na mengineyo. Pia ni muhimu kufanya wajibu uliopendekezwa (mustahabbat), kama vile kuwasaidia masikini, kutoa zawadi, kufanyiza hafla za chakula ili kuweza kutengeneza au kuimarisha mshikamano wa kirafiki au undugu, kukopesha, kuwapa wadeni muda mrefu zaidi wa kulipa madeni, kuwapa nyumba na nguo mafukara, kutumia kilicho muhimu ili kudumisha heshima au kuondoa batili, na kutoa michango kwa huduma za jamii kama misikiti, shule, hospitali barabara, madaraja, visima na kadhalika.
7. Kipato cha haramu Binadamu anapomiliki rasilimali ya aina yoyote bila kufuata utaratibu uliowekwa na Uislamu, kipato hicho ni cha haramu kwa hiyo ni uovu unaosababishwa na ulafi na kupenda dunia, na matokeo yake ni 83
SAADA KAMILI
kumomonyoka kwa maadili na kupotea kwa heshima ya binadamu. Aya kadhaa za Qur`ani Tukufu na hadithi nyingi zinatuonya vikali tusimiliki mali zilizopatikana kwa njia za haramu na kutukumbusha kuhusu matokeo yake mabaya. Lazima izingatiwe kwamba utajiri ni wa aina tatu: i.
Utajiri uliopatikana kwa njia ya halali kabisa.
ii. Utajiri uliopatikana kwa njia ya haramu iii. Utajiri uliopatikana kwa mchanganyiko wa mapato ya halali na haramu. Kitu chochote cha halali ni halali kutumika, na kitu kilichopatikana kwa njia ya haramu au ya mashaka (mushtabah) lazima tuepukane nacho. Vitu vya haramu ni vya aina nyingi, kama vile nyama ya nguruwe au mbwa, vinywaji vyenye kilevi, kitu chochote ambacho matumizi yake yanaweza kusababisha madhara kwa mwili, kitu chochote kilichopatikana kwa matumizi ya mabavu (unyang`anyi), dhuluma, au wizi, mali iliyopatikana kinyume cha sheria yaani kudanganya kwa kutumia kipimo cha mizani au mtu kulipwa ujira kwa saa ambazo hakufanya kazi, mali iliyolimbikizwa wakati kuna uhaba wa mali, mali iliyopatikana kwa njia ya rushwa, mali iliyopatikana kwa njia ya riba, na njia zingine zote za haramu ambazo zimeelezewa kwenye vitabu vya fiqh ya Kislamu. Kinyume cha kuchuma mali kwa njia za haramu ni kujizuia – yaani kutojihusisha na shughuli zozote za haramu (wara‘ ‘anil-haram). Tabia hii inaweza kuwa mazoea kwa mtu kudhamiria kujizoesha kujizuia, hivyo kwamba hatimaye ataweza kujizuia hata katika vile vitu ambavyo ni mushtabah (uhalali wenye shaka). Hadithi ya Mtume (s.a.w.w.) inasema: 84
SAADA KAMILI
َ الح َ ال َل اَ ْر َب ِع واج َرى َي َن ِابيْع ْ ين َي ْومًا َن َّو َر اهلل َق ْل ِب ِه َ َم ْن اَ َك َل الح ْك َم ِة ِم ْن َق ْل ِب ِه َعلَى لِ َسا ِن ِه ِ “Mtu yeyote anayeishi kwa kipato cha halali kwa siku arobaini, Allah atauongoa moyo wake na kusababisha chemchem ya busara kuanzia moyoni mwake na kutiririka hadi kwenye ulimi wake.”
8. Usaliti [Khiyaanah] Usaliti ni aina nyingine ya uovu unaoanzia kwenye Nguvu ya Tamaa. Usaliti unaweza kutokea kuhusu pesa au kuvunjika kwa uaminifu. Unaweza kutokea kuhusu heshima, mamlaka au cheo. Kinyume cha usaliti ni uaminifu, ambao pia unatumika katika vitu vyote vilivyotajwa kwenye usaliti; yaani mali yake ambayo ni amana kutoka kwa Mungu, familia ya mtu, cheo chake, madaraka na mamlaka anayotumia mtu. Wakati wote mtu lazima akumbuke kwamba vitu vyote vilivyotajwa ni rehema za Allah, zinazokwenda sambamba na wajibu maalum, anayevunja mpangilio huo tayari anakuwa msaliti. Luqman, yule mwenye Hekima, amenukuliwa kwa kusema:
َّ َِما َبلَ ْغ ُت اِلَى َما َبلَ ْغ ُت اِلَ ْي ِه ِم َن ْال ِح ْك َم ِة ا ْث ِ ص ْد ِق ْال َح ِدي ِ ال ِب َ َوا َداَ ِء اال َما َن ِة “Sikupata daraja langu la hekima isipokuwa kwa kuwa mkweli na mwaminifu”
85
SAADA KAMILI
9. Uasherati na Ufisadi Haya yanajumuisha mzunguko wa maovu kama; ufuska, uzinzi, liwati, ulevi na mambo mengine yote ya aina ya ubadhirifu - yote haya hutokana na Nguvu ya Tamaa, na humburuza mtu na kumfikisha kwenye maisha ya uhayawani. Zipo aya nyingi za Qur`ani, hadithi na simulizi ambazo zinalaani aina ya tabia hii, si lazima zitajwe hapa kwani zinajulikana sana.
10. Kuchimba sana kwenye Mambo Machafu na Haramu Uovu huu upo katika mazungumzo yanayovuka mpaka wa kisheria na matendo ya haramu, kupenda kujiingiza kwenye mazungumzo kama hayo, na kufanyiana utani na kusimuliana hadithi zisizoendana na heshima na daraja la binadamu. Kwa kuwa mambo haramu na machafu ni ya aina nyingi, kuchimba sana kwenye mambo hayo pia kunaweza kuainishwa kwa njia mbalimbali. Ili kuweza kuondokana na uovu huu mhusika anatakiwa lazima ayadhibiti na kuyawekea mipaka mazungumzo yake, na mazungumzo yake yawe yale tu ambayo yanamfurahisha Allah. Qur`ani Tukufu inawanukuu wakazi wa Jahannam wakisema: “Na tulikuwa tukipiga porojo na wale wapigao porojo” [74:45]. Na kwenye aya nyingine, inaonya dhidi ya kuandaa makundi mbalimbali kwa ajili madhumuni kama hayo: “…..usikae nao [ambao hawaamini na kudhihaki] hadi watakapoanza mazungumzo mengine. [1:140]. Mojawapo ya aina ya uovu huu ni kujiingiza kwenye uchunguzi wa mambo yasiyo na maana – mazungumzo ambayo hayana faida 86
SAADA KAMILI
kabisa ama kwa hapa duniani au kwa Akhera. Zaidi ya haya mazungumzo ya aina hiyo humpotezea mtu wakati wake na ni kipingamizi kwa tafakuri na mawazo ya maana. Ndiyo maana tabia ya kimya imechukuliwa kama kinyume cha uovu huu. Na maana ya “kimya” hapa haimaanishi kwamba mtu awe kimya moja kwa moja, lakini mtu anatakiwa kuchunga ulimi wake na masikio yake asiseme wala kusikiliza maneno ya upuuzi. Kwa maneno mengine, mtu anatakiwa kuwa mwangalifu na maneno yake, aseme yale tu yenye manufaa kwa maisha yetu hapa duniani na Akhera. Wenye busara wamesema: “Vitu viwili vinaweza kumharibu binadamu: utajiri mwingi na ufahari.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema:
ْ ض َل ِم ْن لِ َسا ِن ِه َوا ْن َف َق ال َف ْ ْس َك ال َف ض َل ِم ْن َمالِ ِه َ ُط ْوبى لِ َم ْن اَم “Ameneemeka ambaye ni mwangalifu katika mazungumzo yake na ni mkarimu katika mali yake.”
MARADHI YA PAMOJA YA NGUVU YA AKILI, HASIRA NA TAMAA Sehemu ya nne ya kitabu hiki inashughulika na uovu utokanao na muunganiko wa nguvu zote mbili za, Akili, Hasira, na Tamaa au zote tatu, na namna ya kuyatibu. Yapo maovu thelathini na moja ya aina hii. Mazungumzo haya yanayoshughulika na idadi kubwa ya maovu na wema na yanayotoa mchango kwa somo la vitabu vingi vya maadili, yanaenea nusu ya jumla ya urefu wa kitabu Jami al-Sa‘adaat. Ili tuweze kujiweka kwenye mipaka inayofaa kwa mukhtasari huu, tutashughulika na maelezo mafupi ya nukta zilizojitokeza kwenye sehemu hii ya kitabu. 87
SAADA KAMILI
1. Husuda (Hasad) Ni kutamani mtu mwingine anyang`anywe manufaa yake au neema zake. Kama mtu anawania kupata manufaa kama ya mtu mwingine, huu huitwa wivu (ghibtah), na kama mtu anatamani kuona mtu mwingine aendelee kufurahia manufaa au baraka, ambazo anastahili, hii itakuwa ni nasihah. Katika hali hizi tatu ile yenye daraja la uovu ni hasad, ambayo humfanya mtu astahili kuadhibiwa hapa duniani na Akhera. Mtu mwenye husda hajui amani, na wakati wote anaungua kwenye moto wa husda. Zaidi ya hayo, husda yake huharibu thamani ya amali zake zote nzuri kama ilivyotamkwa kwenye hadithi ya Mtume inayosema:
ُ ات َك َما َت . الح َط َب ُ َّاك ُل الن َ ار َ الح َس ُد َي ْا ُك ُل َ ِ الح َس َن “Husda huunguza matendo mema kama vile moto unavyounguza kuni.”
Hata hivyo, vyote ghibtah na nasihah ni matendo mema, ambayo lazima yastawishwe kwa kuisafisha nafsi iondokane na uovu unaosababishwa na husda. Ugonjwa mbaya wa husda unaweza ukatokana na ama Nguvu ya Tamaa au Nguvu ya hasira au zote kwa pamoja, kutegemea ni kitu gani kilichohamasisha. Hivyo, ili kuweza kutibu uovu huu, lazima tuelekeze fikra zetu kwenye aina hizi mbili za nguvu, na yale ambayo tayari yamekwishasemwa kuhusu maradhi mbalimbali yenye uhusiano na aina hizi za nguvu pia zinatumika kwenye ugonjwa wa husda.
88
SAADA KAMILI
Kinachoweza kumsaidia mtu katika kujitibu mwenyewe maradhi haya ni kutafakari sana kuhusu athari zenye mwelekeo hasi za kisaikolojia na kiroho za husda, ambazo zinamuathiri yeye tu mwenye husda, si yule ambaye husda huelekezwa kwake. Zaidi ya haya, mtu mwenye maradhi ya husda anatakiwa kutengeneza ndani mwake tabia ya nasihah (kuwatakia mema wenzake), ambayo ni kinyume cha husda. Mwanzoni, inawezekana iwe lazima yeye kuulazimisha msimamo unaohimizwa na tabia hii ya nasihah, bila kujali kwamba ndani ya nafsi yake anasumbuliwa na husda, hadi hapo tabia ya husda itakapotoweka na tabia ya nasihah kushika nafasi yake.
2. Kubughudhi na Kutusi Watu Wengine Tabia ya aina hii kwa kawaida husababishwa na hasad (husda) na uadui, ingawaje pia inaweza kutokana na ulafi (hirs), tamaa, kiburi (takabbur), na kadhalika. Kwa hiyo, chanzo chake ni ama Nguvu ya hasira au Nguvu ya Tamaa, au aina zote mbili zilizotajwa hapo juu. Kwa vyovyote vile, kubughudhi na kutukana au kukashifu Waislamu ni dhambi kuu, na imelaaniwa mara kwa mara kwenye aya za Qur`ani na hadithi: “Na wale wanaowaudhi wanaume waumini na wanawake waumini pasipo wao kufanya kosa lolote, bila shaka wamebeba dhulma kubwa na dhambi zilizo dhahiri” [33:58]. Na katika hadithi kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) inasema:
َُؤ ِم ًنا َف َق ْد اَ َذا ِنى َو َم ْن اذا ِنى َف َق ْد َاذى اهلل َو َم ْن َاذى اهلل ْ َم ْن اَ َذى م َ ُ َّ ِ ال ْنجي . ان ْ َف ُه َو َم ْلع ِ ُو ٌن ِفى التَّ ْو َرا ِة َو ْا ِ ُور َوالف ْرق ِ ْل والزب 89
SAADA KAMILI
“Yeyote anayemuudhi muumini, ameniudhi mimi, yeyote anayeniudhi mimi amemuudhi Allah; na yeyote anayemuudhi Allah amelaaniwa kwenye Torati, Injili, Zaburi, na Qur`ani. (Angalia: Jami al-Akhbaar)”
Kwa upande mwingine, kumzuia mtu asiwabughudhi na kuwatukana watu wengine ni kitendo kizuri ambacho kimesifiwa na hadithi kadhaa, miongoni mwao hadithi ifuatayo ni mfano wake;
َ ْ ْن َشي ًْئا ي َ ُسلِ ِمي ْه ْم َك َت َب اهللُ لَ ُه ِب ِه ْ ئق ْالم ِ ُؤ ِذي ِ َِم ْن َز ْح َز َح ِم ْن طرا . َح َس َن ًة اَ ْو َج َب لَه ِب ِه ْال َجنَّ َة “Yeyote anayeondosha kihunzi kinachoudhi kwenye njia ya Waislamu, Allah atamwandikia jema, na malipo yake ni Peponi” (Ihya al-ulum al-din, Juz. 11, uk. 172)
3. Kutishia na Kusumbua Waislamu Tabia ya aina hii ni tawi la uovu uliotajwa hapo juu, na inasababishwa na ama hasira au kuhamaki au ulafi. Kinyume chake ni kuwafanya watu wengine wafurahi na kuondoa mambo yanayoweza kuwasababishia huzuni au wasiwasi. Zipo hadithi nyingi zinazosifia tabia hii, kama hii ya Bwana Mtume isemayo:
ُ اال ْع َمال اِلَى اهللِ َع َّز َو َج َّل اِ ْد َخ رو ِر َعلَى ُ ال ْ الس ِ َ اِ َّن اَ َح َّب َ المُؤ ِم ِني . ْن 90
SAADA KAMILI
“Kwa hakika kitendo kinachompendeza sana Allah, Mwenye Uwezo Usio Wezwa, ni kuwafurahisha waumini”
4. Kutojali Mambo ya Waislamu Kutojihusisha na mambo ya Waislamu ni tabia mbaya inayosababishwa na uchovu, udhaifu wa kiroho, au ubahili. Uovu huu umelaumiwa kwenye hadithi nyingi, mfano wake ni kauli maarufu ya Bwana Mtume ifuatayo:
َ اص َب َح َ ُسلِ ِمي َو َم ْن َس ِم َع.ْس ِم ْن ُه ْم ْ َم ْن ْ ُو ِر الم ْ ال َي ْه َت ُّم ِباُم َ ْن َفلَي ً َر ُج َ َ مسلِ ِمي .ُسلِ ٍم ْ ْس ِبم ْ ال يُ َنا ِد ْى َيا ْلل َ ُج ْب ُه َفلَي ِ ْن َفل ْم ي “Mtu anayeamka na akawa hataki kujihusisha na mambo ya Waislamu, na yule anayesikia, “Enyi Waislamu” bila ya kuitikia; si Muislamu.”
Kinyume chake, kutosheleza mahitaji ya Waislamu na kutatua matatizo yao hufikiriwa kuwa ni mojawapo ya namna nzuri sana ya ibada. Mtume anasema:
َ ٍ اع ًة ِم ْن لَي َ ار َق َض اهاَ اَو ل ْم َ اج ِة اَ ِخ ْي ِه َس َ َم ْن َم َشى ِفى َح ٍ ْل ا ْو َن َه َ ض َها َك .ْن ً ان َخي َ اف َشه ِ ْرا لَ ُه ِمن اع ِت َك ِ َي ْق ِ ْري “Mtu kutembea kwa mguu kwa muda wa saa moja, wakati wa usiku au mchana, katika jitihada za kumsaidia Muislamu mwenzake, ni 91
SAADA KAMILI
bora zaidi kuliko i`tikaaf ya miezi miwili (itikafu), bila kujali kama mafanikio yamepatikana au hapana.”
5. Uzembe katika Kutekeleza Wajibu wa:“Kuamrisha mema na Kukataza maovu” Kushindwa kutekeleza wajibu wa kuamrisha mema na kukataza maovu ni dhambi isiyosameheka inayosababishwa na ama udhaifu wa uadilifu au mtu kutokuwa msikivu kwa mambo ya kidini na matokeo yake ni kusambaa kwa uovu, rushwa, dhulma, na aina zingine za uchafu katika jamii yote. Ni wajibu wa kila Muislamu “kuamrisha mema na kukataza mabaya.” Wajibu huu unazo hatua na masharti kama ambavyo imekwishaainishwa kwa kina kwenye vitabu vinavyozungumzia Fiqh ya Kiislamu. Kwa kuwa hapa tunajihusisha zaidi na kazi za mtu mmoja mmoja kuhusu uhusiano wake na wenzake, maelezo haya mafupi kuhusu kazi hii inatosha.
6. Kutopenda kuchanganyika na watu Uovu huu husababishwa ama na uadui, kutaka kulipa kisasi, husda, au ubahili na, kwa hiyo, ipo ama kwenye Nguvu ya Tamaa au Nguvu ya Hasira. Uovu huu umeshutumiwa ndani ya hadithi nyingi. Kinyume cha uovu huu ni tabia ya kuwa na muamala mzuri na watu; ukarimu, na urafiki, ambayo inasaidia kupanua uhusiano wa kindugu katika jamii yote. Tabia hii inakokotezwa sana na Uislamu. 92
SAADA KAMILI
7. Kuvunja uhusiano na familia na ndugu Uovu huu ni tawi la kutokupenda kukaa na watu, lakini uovu huu ni mbaya zaidi na unayo madhara zaidi. Kiyume cha uovu huu ni tabia ya kudumisha uhusiano wa karibu wa kifamilia. Idadi kubwa ya riwaya zinazoweza kupatikana kwenye vitabu vya hadithi, zinashughulika na somo hili.
8. Kutowajibika kwa Wazazi Huu ni uovu mbaya zaidi kuzidi uovu wa kuvunja uhusiano wa kifamilia na kindugu na kufuatana na hadithi zinazozungumzia kwa ukali kuhusu uovu huu, ni sababu ya mhusika kupata adhabu kali sana hapa duniani na Akhera. Kinyume chake ni tabia ya kuhurumia na kuipenda familia ambayo inafahamika kuwa mojawapo ya tabia ya juu sana katika tabia za binadamu. Imam al-Sadiq (a.s.) aliulizwa: “Ni kitendo kipi chenye thamani kubwa zaidi mbele ya Allah?” Jibu: “Swala inayoswaliwa katika wakati wake uliowekwa, mtu kuwahurumia wazazi wake, na kupigana jihadi kwa ajili ya Allah.” Kauli hii ya kuwahurumia wazazi na kufuatiwa na swala na jihadi, ambazo ni nguzo mbili muhimu sana za Uislamu, inaonyesha umuhimu wake kwa wazi. Pia ni muhimu kusisitiza hapa wajibu wa mtu kwa jirani zake na haki zao, kwani pia upo kwenye kundi la uhusiano wa mtu na mtu ambao umezungumziwa kwa ufupi hapo juu, na zipo hadithi nyingi zinazolaani mtu kuwabughudhi jirani zake na kuwafanyia tabia mbaya.
93
SAADA KAMILI
9. Kutafuta Dosari za Wengine na Kufichua Mapungufu yao au Makosa yao Uovu huu husababishwa na ama husda au uadui, na huelekeza kwenye uchafu, chuki, na uharibifu wa uhusiano mzuri baina ya watu. Kinyume cha uovu huu ni tabia ya kuficha dosari na makosa ya watu wengine. Tabia hii inazo sifa nyingi zisizopimika, na hapa tutataja aya moja na hadithi moja kuhusiana na tabia hii. “Kwa hakika wale wanaopenda uenee uchafu kwa wale walioamini, watapata adhabu yenye kuumiza katika dunia na Akhera…….” [24:19]. Na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema:
.آلخ َر ِة ْ َم ْن َس َت َر َعلى م ِ ُسلِ ٍم َس َت َر ُه اهللُ ِفى ْال ُّد ْن َيا َو ْا “Yule anayeficha (aibu za) Muislamu, Allah ataficha aibu zake hapa duniani na kesho akhera.”
10. Kufichua Siri za Wengine. Kuzungumzia siri za watu wengine husababisha mgongano wa kijamii na wakati mwingine chuki. Kwa hiyo, huu unafahamika kuwa ni uovu na umeshutumiwa na idadi kubwa ya hadithi. Uovu huu unaweza kuwa wa aina mbalimbali, mojawapo ni mtu kumwambia mtu maneno ya kumshusha hadhi yaliyosemwa na mtu mwingine, na kwa hiyo kusababisha kutokuelewana na chuki baina yao. Aina nyingine ni kutoa maelezo kwa mtu mwenye uwezo na mamlaka jambo ambalo mtu mwingine inaweza kuwa amesema au kufanya dhidi yake 94
SAADA KAMILI
kwa hiyo anamshawishi amfanyie madhara huyo mhusika. Kwa ujumla, uovu wa kutengeneza migongano na kutokuelewana baina ya watu na kusababisha vurugu na uadui baina ya watu unaweza kuwa wa aina mbalimbali na kufichua siri za watu ni aina mojawapo. Kinyume cha uovu huu ni tabia ya kutengeneza hali ambayo itasababisha watu wengine wahisi vizuri, maelewano, na upendo miongoni mwa watu, ambayo ni sifa yenye thamani sana. Kinyume cha uovu wa kufichua siri za watu ni tabia ya kulinda siri zao na kuzihifadhi. Kwa vyovyote vile, aina zote za kuchafua uhusiano mzuri baina ya watu zinafahamika kuwa ni dhambi na zimeshutumiwa kwenye aya nyingi za Qur`ani na hadithi.
11. Shamaatah [Kufurahia Mabalaa ya Wengine] Uovu huu unajumuisha kuhusisha mabalaa anayopata mtu na matendo yake yasiyofurahisha, kufurahia mabalaa hayo na kumlaumu juu ya mabalaa hayo ni tabia iitwayo Shamaatah ambayo ni uovu. Uovu huu kwa kawaida husababishwa na husda [hasad] au Nguvu ya Tamaa. “Shamaatah� ni uovu ambao umelaumiwa kwenye hadithi nyingi, inasemekana kwamba, kwanza, shamaatah husababisha mtu anayefurahia mabalaa ya mwenzake baadaye naye hukumbwa na mabalaa kama hayo; pili, hiyo tabia yake ya shamaatah huumiza hisia za ndugu yake katika imani na kwa hiyo ni sababu ya yeye kupata adhabu ya Kimungu. Tatu, ukweli kwamba mtu ambaye amekumbwa na mabalaa si lazima awe amefanya matendo mabaya; hiyo inaweza kuwa ni mtihani wa Kimungu ambao unaweza kuwatokea hata wale ambao wapo karibu sana na Allah. 95
SAADA KAMILI
12. Kudhihaki na Kuzua Mjadala [Ta‘n wa Mujaadalah] Kudhihaki [ta‘n] maana yake ni kusema jambo kwa kejeli kwa lengo la kumshushia mtu hadhi, na uzuaji mijadala huelekeza watu kwenye mabishano yasiyo na maana bila ya kuwa na nia hasa ya kuutafuta ukweli wenyewe. Tabia hizi mbili zanachukuliwa kuwa ni uovu wa kimaadili, na huelekeza wahusika kwenye kutokuelewana na kuwa na hisia mbaya miongoni mwa marafiki. Kinyume cha uovu huo ni tabia ya kusema maneno yaliyonyooka yenye lengo la kugundua ukweli kwa mazungumzo ya upole, uaminifu, na kirafiki.
13. Kuwadhihaki na Kuwafanyia Mzaha Watu Wengine Uovu huu unayo athari mbaya kama ile tabia ya kukejeli na msimamo wa ubishani usiokuwa na maana.
14. Utani Utani pia ni lazima uepukwe kama desturi ya kawaida, kwani unaweza kusababisha hisia mbaya na uadui kwa baadhi ya watu. Hata hivyo, lazima izingatiwe kwamba utani ulio mbaya ni ule wa kuvuka mpaka wa wastani; vinginevyo aina ya kichekesho ambacho hufurahisha nafsi na kuchangamsha akili bila kukimbilia kusema uwongo na kuteta, na bila ya kusababisha maudhi kwa wengine, huo unaruhusiwa.
96
SAADA KAMILI
15. Kusengenya [Ghi‘bah] Kusengenya ni kusema jambo kuhusu mtu fulani ambalo mwenyewe asingelipenda. Masengenyo ni mojawapo ya dhambi kuu, ambayo mambo mengi yameandikwa kuhusu dhambi hii, na ambayo imeshutumiwa kwenye hadithi nyingi na aya za Qur`ani. Mazungumzo ya kina kuhusu mipaka yake, sifa zake bainifu, na mambo yake yasiyokuwa ya kawaida yameandikwa kwenye kitabu. Hata hivyo, ili kuweza kubakia kwenye mipaka iliyowekwa na hali ya ufupi wa mazungumzo yetu, hatutatoa maelezo marefu. Kilicho kibaya zaidi kuliko kusengenya [ghi‘bah] ni kusingizia [buhtaan], ambayo ni mashitaka ya kubambikiza. Kinyume cha kusengenya ni kuwasifu watu wengine, na kinyume cha kusingizia – ambako kunajumuisha na uongo pia – ni kusema ukweli wa zile sifa nzuri hasa za mtu.
16. Kusema uwongo Kusema uwongo ni dhambi inayoaibisha na dhambi kuu, ambayo huelekeza kwenye ufisadi wa mtu mmoja na jamii. Zipo hadithi nyingi na aya za Qur`ani zinazozungumzia uovu wa uwongo, na yapo maandiko mengi yanayolaani uovu huu. Kinyume cha uovu huu ni tabia ya mtu kuwa mkweli [swidq]. Ukweli ni mojawapo ya sifa nzuri sana za binadamu na neno swidq [ukweli] limeonekana mara nyingi sana ndani ya Qur`ani Tukufu.
17. Kujionyesha [Riyaa`] Maana yake ni kufanya kitu kwa lengo la kuonyesha ufahari badala ya kuwa ni kwa ajili ya Allah. Ni dhambi kuu, na husababisha kud97
SAADA KAMILI
hoofu kiroho na kifo. Na Qur`ani inasema: “Basi ole wao wanaoswali. Ambao wanapuuza swala zao. Ambao wao hujionyesha. Wakazuilia (watu) manufaa.” (107:4-7). Kwenye aya nyingine tunasoma: “……Na wanaposimama kuswali, husimama kwa uvivu, kujionyesha kwa watu, wala hawamtaji Mwenyezi Mungu ila kidogo tu.” (4:142). Ifuatayo ni hadithi ya Mtume kuhusu uovu wa riya: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema:
ُ الش ُ اف َعلَي ِِّ َو َما: َقالُ ْوا.ص َغ ُر ِّ ْك ُم ُ ف َماَ اَ َخ َ رك ْا َ اِ َّن اَ ْخ َو الش ْر ُك ْ ال َ َ َ َ ُرا ِئ ين ْ ْا َ َي ُق ْو ُل اهللُ َع َّز َو َج َّل َي ْو َم ال ِق َيا َم ِة لِلم.لرَّيا ُء ِ ا:الص َغ ُر؟ قال َ اِ َذا َج َ اِ ْذ َهبُوا اِلَى ال ِذي:از ال ِع َباد ِباَ ْع َمالِ ِه ْم ْن ُك ْنتُم تُ َرا ُء ْو َن لَ ُه ْم َ ون ِع ْن َد ُهم ُّ فى َ الد ْن َيا َفا ْن ُظ ُروا َهل َت ِج ُد الجزا َء ِ Kitu muhimu ninacho kihofia kuhusu nyinyi ni ‘shirki ndogo.’ Wakauliza, ‘Shirki ndogo’ ni nini?” Akajibu: “Kujionyesha! Mnamo Siku ya Hukumu, ambapo Allah, Mwenye Enzi atakuwa anapima matendo ya viumbe Wake, atasema kwa wajionyeshao, ‘Nendeni kwa wale ambao mlikuwa mnajionyesha kwao wakati mnaishi duniani na waombeni wao malipo yenu.’
Zipo aina nyingi za riya: riya katika ibada, kwa namna yoyote ile iwayo, wakati wote ni mbaya; riya katika mambo mengine, ambayo wakati mwingine hulaumika, lakini wakati mwingine huruhusiwa (mubah) na hata hupendekezwa. Mathalani, kama mtu anakuwa mkarimu kwa njia ya wazi akiwa na nia ya kutaka kuwatia moyo watu wengine wawe wakarimu pia, kitendo chake hicho si tu kwam98
SAADA KAMILI
ba hakilaumiki, bali kwa kweli kinastahili kusifiwa sana. Umuhimu wa kujionyesha katika mifano yote miwili hutegemea nia ya mhusika. Kinyume cha riya ni ikhlas (uaminifu), kwa maana kwamba kufanya kila kitu kwa ajili ya Allah tu, bila ya kutegemea thawabu yoyote kutoka popote kwa kile alichokifanya. Daraja la ikhlas ni mojawapo ya madaraja ya juu sana ambalo muumini anaweza kulipata, lakini linaweza kufikiwa kwa njia ya kujizoeza kwa mfululizo na uvumilivu.
18. Unafiki (Nifaq) Unafiki ni kujifanya kuwa wa hali fulani kumbe sivyo au kujifanya kuamini kitu kumbe sivyo, katika uhusiano wa dini au kijamii, ni mojawapo ya uovu mharibifu sana. Katika Qur`ani Tukufu wanafiki wamelaaniwa kwa ukali sana. Pia, zipo hadithi nyingi zinazolaani uovu huu. Kinyume cha unafiki ni kuwa sawasawa vile mtu aonekanavyo kimwili na ndani ya nafsi yake iwe vivyo, au bora zaidi, mtu kuwa safi zaidi ndani ya nafsi yake kuliko anavyoonekana kimwili. Hii aina ya pili ni tabia ya mtu anayeamini (muumini) na wale walio karibu na Allah (awliyaa’ Allah)
19. Majivuno.[Ghuruur] Majivuno ni kuwa na kiburi kutokana na mtu kuwa na fikira za ubinafsi na njozi, inaweza kuwa inahusu mambo yake ya kidunia au Akhera. Mtu anaweza kuwa anajivunia ucha Mungu wake, au wato99
SAADA KAMILI
to wake wa kiume, utajiri wake, cheo na mamlaka, au vitu vingine. Vitu vyote hivi vinaweza kumwelekeza mtu kwenye majivuno, na matokeo yake mhusika anaanguka kimaadili na kiroho. Kwa hiyo, tunaona Qur`ani Tukufu inamuonya binadamu dhidi ya aina zote za majivuno, ambayo ni aina ya njozi na mtu kujidanganya mwenyewe “…….basi yasikudanganyeni maisha ya dunia hii, wala asikudanganyeni mdanganyifu katika [mambo ya] Mwenyezi Mungu (31:33) Watu namna mbalimbali wanaweza kukumbwa na uovu huu wa majivuno. Wanaweza kuwa waumini au makafiri, wanazuo, wachaMungu, wenye irfaan na kadhalika na kila mmojawao anaweza kuwa anajivunia kitu fulani. Hivyo, tunaona kwamba majivuno yanaweza kuwa ya aina nyingi. Majivuno yanaweza kusababishwa na Nguvu ya akili, Nguvu ya Tamaa, Nguvu ya hasira au aina zote tatu za nguvu. Kinyume cha majivuno - ambayo kama yalivyoelezwa, ni aina ya mtu kujidanganya mwenyewe - ni elimu, hekima, utambuzi, na zuhd; kwa sababu jinsi mtu anavyotambua ukweli ndivyo itakavyo kuwa vigumu yeye kukumbwa na majivuno. Hadithi ya Imam alSadiq ifuatayo inatoa nasaha kuhusu tiba ya kweli ya uovu wa majivuno:
َّ ات ْال ُغ ُر ْور َوال َت َم ِنّى ْ َو ص ْد ِق ِ اال ِب ِ اعلَ ْم أنَّ َك لَ ْن َت ْخ ُر َج ِم ْن ُظلُ َم ِ ُ أح َوالِ َك ِم ْن َحي َ ِ ال ْخ َب ْث ْ ُو ِب ْ ْر َف ِة ُعي ِ ْاال َنا َب ِة اِلَى اهللِ َو ْا ِ َو َمع.ات ل ُه َّ ين َو َ ال يُ َوا ِف ُق ْال َع ْق َل َو ْال ِع ْل َم َو َ ُ الد ِّ ال َي ْح َت ِملُ ُه الش ِري َع ُة َو ُس َن ُن أح ٌد َ اضيًا ِب َما أ ْن َت ِفي ِه َف َما ِ َواِ ْن ُك ْن َت َر.ْال ُق ْد َو ِة َوأ ِئ َّم ِة ْالهُدى ْ ْ أش َقى ِب َع َملِ َك ِم ْن َك َو . َفاَ ْو َر ْث َت َح ْس َر ًة َي ْو َم ْال ِقيا َم ِة.ْرا ً أض َيع ُعم 100
SAADA KAMILI
“Tambua kwamba hautakuwa huru kutoka kwenye giza la majivuno na matamanio isipokuwa pale utakaporejea kweli kweli kwa Allah kwa unyenyekevu na majuto, na uzitambue dosari zako na mapungufu yako - kwamba, yale mambo ambayo hayaendani na mantiki na akili, na hayakubaliwi na dini, Sheria ya Mungu, na kanuni za viongozi wa muongozo. Na kama unaridhika na hali uliyonayo, uwe na uhakika kwamba hapana yeyote aliye sugu na muovu kulingana na matendo yako mwenyewe na hapana ambaye hajali zaidi kupotea bure miaka ya maisha yako kukuzidi wewe, na msimamo huu hatimaye utakuacha kwenye urithi wa maumivu ya kukata tamaa mnamo Siku ya Ufufuo.â€? [Misbah al-Shari`ah, Ů?Sura ya 36]
20. Kuwa na Matumaini na Matakwa Makubwa na ya Mbali kabisa Uovu huu husababishwa na Nguvu ya akili na Tamaa, na unatokana na ujinga na kupenda dunia. Uovu huu humuumiza mhusika kwa kumweka akiwa anajishughulisha sana na mambo ya dunia na kudumaza maendeleo yake ya kiroho. Ili mtu ajitibu maradhi haya, lazima awe anafikiria kifo na Akhera kila wakati kwa mfululizo, awe anatambua kwamba dunia na maisha yake ni vitu vya kupita, na chochote anachokipata mtu, iko siku mtu huyo atalazimika kukiacha nyuma kitu hicho na kufa. Binadamu lazima atambue jambo hili wakati wote kwamba kitu ambacho ndicho tu atachoondoka nacho baada ya kufa ni matendo yake mema.
101
SAADA KAMILI
21. Uasi [‘Isyaan] Maana ya uasi ni kutotii amri za Allah. Uovu huu upo katika Nguvu ya hasira na Matamanio, kinyume chake ni utiifu na uchaji Mungu [taqwa].
22. Utovu wa Haya Uovu huu upo kwenye Nguvu ya hasira na Matamanio, una ufidhuli na utovu wa haya katika kufanya mambo yaliyoharamishwa. Kinyume chake ni kuwa na staha na kuona haya [hayaa`] ambayo ni sehemu ya imani. Imam al-Sadiq (a.s.) amesema:
ُ ال ِي َم ان ِفى ْال َجنَّ ِة ِ ان َوا ِ ْال َح َيا ُء ِم َن ا ِ ال ْي َم “Staha ipo ndani ya imani na imani ipo ndani ya Pepo”
23. Kung`ang`ania Kutenda Dhambi Hii ni hali ya uovu, na kinyume chake ni toba [tawbah]. Kurudia rudia kufanya dhambi huzifanya zionekane kama ni jambo la kawaida, lisilokuwa na muhimu na kuwa katika mambo ya kila siku. Kwa hiyo, kabla hali hii haijamtokea mtu, ni muhimu mtu huyu atafakari matokeo mabaya ya kufanya dhambi na kupima madhara yake ya hapa duniani na Akhera. Tafakuri ya aina hii inaweza kumwelekeza kwenye kutubu dhambi zake na kujuta na kuona haya kweli kwamba alifanya dhambi hizo. Kwa upande mwingine tawbah au kutubu ni 102
SAADA KAMILI
hali ya kurudi kutoka kwenye utendaji dhambi. Ipo hali ya juu zaidi ya kutubia nayo ni “inaabah.” Ni kurudi kutoka kwenye kutenda dhambi na kuacha kabisa hata yale yaliyoruhusiwa [mubaah]. Katika hali hii ya toba ya juu zaidi mhusika hutafuta kumridhisha Allah tu kwa kauli na matendo na kumkumbuka Allah wakati wote. Kiungo muhimu cha toba ni muhaasabah na muraaqabah, yaani mhusika anayetubu kwa kweli wakati wote huangalia matendo yake yote na kutafakari hali ya uadilifu ya matendo yake. Ipo hadithi isemayo:
َ ُوا أ ْن ُف َس ُك ْم َقب ْ ْل .ُوا ْ اسب ْ اسب َ أن تُ َح ِ َح “Jihesabuni nafsi zenu wenyewe kabla ya kuhesabiwa.”
24. Uzembe [Ghaflah] Maana ya ghaflah ni uzembe na kutokujali; kinyume chake ni kuzingatia na kuazimia. Kama kilichofanyiwa uzembe ni hatima ya furaha yetu kuu na ustawi wetu, huu ni uovu. Hata hivyo, kama kinachofanyiwa uzembe na kutokujaliwa ni ubaya na uovu basi hii ni tabia njema. Kwamba, kujali ufisadi na mambo mabaya ni uovu, ambapo kinyume chake ni tabia njema. Uzembe na nia au uangalifu, ni tabia zinazotokana na ama Nguvu ya Tamaa au Nguvu ya hasira. Mathalani kama mtu amenuia kuoa, msukumo wa nia hiyo unatokana na Nguvu ya Tamaa, na ni tabia njema. Kama mtu ananuia kujihami kutokana na adui, nia hiyo inatokana na Nguvu ya hasira na hii pia ni tabia njema. Haya yalikuwa ni maelezo ya jumla ya uzembe na uangalifu au nia. Hata hivyo, Kama msamiati ulivyotumika kwenye aya za 103
SAADA KAMILI
Qur`ani na hadithi, kwa kawaida uzembe unarejelea tabia ya kutokujali malengo halisi ya uhai wa binadamu hapa duniani na uwakala wa ustawi na furaha hapa duniani na Akhera; na kinyume chake, dhamira, hutafsiriwa kama uwazi wa nia na lengo katika maana ile ile. Katika maana hiyo hiyo, kwa hiyo, wakati wote uzembe ni mbaya na nia ni nzuri. Qur`ani inatoa tamko kuhusu uzembe: “Na bila shaka tumewaumbia Moto wa Jahannam wengi katika majinni na wanadamu. Nyoyo wanazo lakini hawafahamu kwazo, na macho wanayo lakini hawaoni kwayo, na masikio wanayo lakini hawasikii kwayo, hao ni kama wanyama, basi wao ni wapotovu zaidi, hao ndio walioghafilika.� [7:179].
25. Karaha [Karahah] Karaha inarejelea hali ya kujenga kero kubwa sana dhidi ya mambo yote yanayoingiza shida na kazi. Hali ya kero iliyovuka mpaka ni maqt au chuki. Kinyume cha karaha ni hubb au kupenda. Hubb hutokana na nafsi kupenda vitu vizuri na vyenye manufaa. Aina ya mapenzi, hubb yaliyovuka mpaka ni `ishq (ashiki). Karaha inaweza kuwa nzuri au mbaya: mathalani, endapo mtu anaona karaha kupigana jihad kwa ajili ya Allah au kujihami, tabia hii haipendezi kabisa na inalaumika sana. Hata hivyo, endapo, mtu anayo tabia ya kukerwa na matendo mabaya na dhambi, ni vema na inapendeza sana. Kanuni ileile inatumika kwa tabia ya hubb, yaani endapo mtu anapenda vitu vizuri na vyenye manufaa ni tabia njema; lakini si hivyo kama mtu anapenda vitu viovu. Jambo linalofaa kuzingatia ni kwamba hubb ni muhimu kimsingi ielekezwe kwa Allah tu na kila chochote kinachohusiana Naye. Hii ni aina ya mapenzi (hubb) ya juu sana. Lazima izingatiwe kwam104
SAADA KAMILI
ba wa Kupendwa Hasa ni Allah, na ni hapo tu ambapo mtu anapompoteza yule wa Kumpenda Hasa hujikuta ameelekeza mapenzi yake kwa vitu vingine, kama vile mke, watoto, ukwasi, hadhi, au kitu kingine chochote cha kidunia. Endapo mtu angeweza kumpata yule wa Kumpenda Hasa tena, pia atakuwa amepata wokovu kutoka kwenye uzururaji wake usio na ukomo, na makusudio. Ili kuweza kumpata yule wa Kupendwa Kweli, kwanza lazima tujue aina mbalimbali za mapenzi (hubb). Kimsingi hubb inaweza kuelekezwa kwenye vitu tofauti tisa: i.
Mtu kujipenda mwenyewe; haya ni mojawapo ya aina ya mapenzi mazito sana.
ii. Mapenzi ya mtu kwa vitu vilivyoko nje ya nafsi yake kwa lengo la kujifurahisha kimwili, mathalani aina mbalimbali za vyakula, nguo, na vitu vingine vinavyohudumia mahitaji ya kimwili na matamanio yake. iii. Mtu kumpenda mtu mwingine kwa sababu ya ukarimu au huduma ambazo mtu mwingine atakuwa amemfanyia. iv. Mtu kupenda kitu fulani kwa sababu ya uzuri wa kitu hicho, kama vile urembo, na kukubalika kimaadili. v.
Mtu kumpenda mtu mwingine bila ya sababu yoyote; si kwamba mtu huyo anayependwa anao uzuri, ukwasi au mamlaka au kitu kinachofanana na hicho, lakini ni kwa sababu tu ya kuwepo kwa uhusiano fulani wa kiroho usioonekana baina yao.
vi. Mtu kumpenda mtu mwingine ambaye amekuja kutoka mbali sana, au ambaye amefuzu kuonana naye wakati wa safari ndefu. 105
SAADA KAMILI
vii. Mapenzi ya mtu kwa wafanyakazi wenzake au wataalam wenzake, kama vile, mwanazuo kumpenda mwanazuo mwenzake, au mfanyabiashara kumpenda mfanyabiashara mwenzake, na kadhalika. viii. Mapenzi yanayosababishwa na athari ya (udugu), na kinyume chake. ix. Mapenzi ya athari ya kawaida ya sababu moja ya mtu kwa mtu, kama vile mapenzi baina ya watu wa familia moja. Kama tukitafakari juu ya jambo hili, tutahitimisha kwamba kwa kuwa Uwepo wa Allah Hauna Mpaka na vingine vyote humtegemea Yeye, kitu kingine chochote ambacho binadamu atakipenda hakiwezi kuwa na uwepo wa kujitosheleza chenyewe. Kwa maneno mengine ni kwamba, kwa kuwa Allah ni Msingi wa Ukweli, kwa kweli Yeye ni wa mwisho katika mapenzi ya kweli, na aina zote za mapenzi yanayoelekezwa kwa vitu vingine ni ya kitamthilia na kudhania. Kwa hiyo mtu lazima atakase mapenzi yake na kugundua kitu chenyewe cha kweli; na hili haliwezekani isipokuwa hali zifuatazo zionekane ndani mwake: i.
Mhusika awe na shauku ya kutamani kukutana na Allah (liqaa`Allah); kwa maneno mengine, asihofu kifo. Matendo yake lazima yawe yenye kuakisi uthibitisho wake kwamba atakutana na Allah baada ya kifo chake.
ii. Mtu awe na kipaumbele cha matamanio ya kukutana na Allah na si vinginevyo, kwa kuwa hili ni mojawapo ya masharti ya mapenzi. iii. Mhusika amkumbuke Allah wakati wote, kama vile 106
SAADA KAMILI
mwenye mpenzi huwa hamsahau mpenzi wake hata kwa muda kidogo. iv. Mhusika lazima asifurahi anapopata kitu, au ahuzunike anapokosa kitu, kwa kuwa kama mazingatio yake yote yanaelekea kwa Allah vitu vingine havitakuwa na umuhimu kwake. v.
Mhusika lazima awe mkarimu na kuvipenda viumbe vyake Allah, kwa kuwa yeyote anayempenda Allah, atavipenda na viumbe Vyake pia.
vi. Mhusika anatakiwa awe na hofu juu ya Allah na wakati uleule ampende Allah, kwani masharti hayo mawili hayakinzani. vii. Mhusika anatakiwa ayaweke mapenzi yake kwa Allah kuwa siri. Chini ya masharti kama hayo Allah pia atampenda mja Wake na kutekeleza ahadi Yake: “Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu, basi nifuateni, Mwenyezi Mungu atawapenda na atawasamehe madhambi yenu,…….”[3:31].
26. Sakhat Sakhat ni kusikitika wakati wa shida na mabalaa ambayo yanaweza kumpata mtu hadi kulalamika. Kinyume cha uovu huu wa sakhat ni tabia njema ya ridhaa ambayo ni tabia ya kutosheka na kuridhika na chochote ambacho Allah ameruzuku. Sakhat ni aina ya karaha, na kuwa na ridhaa ni aina ya hubb. 107
SAADA KAMILI
Zipo hadithi nyingi zinazoshutumu sakhat na kuwaasa watu kuwa wavumilivu wakati wanapopatwa na shida na mabalaa; kwani hiyo ni mitihani iliyopangwa Kimungu. Kimsingi lazima tutambue kwamba maisha ya hapa duniani yamechanganyikana na maumivu, matatizo, maradhi na kifo, na bila shaka kila mmoja atakumbwa na mambo haya. Kwa hiyo, lazima tujifunze namna ya kuyashughulikia matatizo kama haya. Kujitayarisha kwa namna hii kunaitwa ridhaa, na kiwango chake cha juu sana ni kutosheka kikamilifu na kile anachoruzuku Mungu. Hivi ndivyo Qur`ani inavyowazungumzia watu kama hao: “….Mwenyezi Mungu amewawia radhi, nao wamekuwa radhi naye, huko ndiko kufuzu kukubwa.” [5:119]. Na hivi ndivyo Qur`ani inavyowazungumzia wale wasio kuwa na sifa hii: “…..na wamekuwa radhi na maisha ya dunia na kutulia kwa hiyo, ….” [10:7] . Ni muhimu kuzingatia kwamba taslim (kukubali matokeo) na ridhaa (kuridhika) kwa kawaida hutumika kama maneno yanayokaribiana sana katika maana kwenye vitabu vya maadili. Hii ni kwa sababu ya maana zao kuwa karibu sana; kwa sababu yule aliyeridhika na kile anachojaaliwa, anakuwa amejitoa moja kwa moja kwa Allah katika kila kipengele cha maisha.
27. Huzn (Huzuni) Maana yake ni kuhuzunika na kuhisi majuto kwa sababu ya kupoteza au kushindwa kupata kitu unachokipenda. Huzn kama ilivyo sakhat huja baada ya karaha.
28. Kukosekana Imani kwa Allah Uovu huu ni wa aina ya mtu kukiamini kitu kingine katikati yake na Allah, kwa ajili ya kutatua matatizo ya mhusika. Husababishwa 108
SAADA KAMILI
na upungufu wa imani, na chanzo chake ni Nguvu ya akili na ya Tamaa. Kutegemea na kuamini sana njia ya kati na kati ni aina ya ushirikina. Kinyume cha uovu huu ni tawakkul (imani) kwa Allah katika vipengele vyote vya maisha ya mtu, akiamini kwamba ni Allah peke yake ndiye nguvu inayofaa Ulimwenguni. Hii ndio maana ya lile tamko maarufu: “Hakuna nguvu au uwezo isipokuwa [uwe umepatikana] kutoka kwa Allah.”. Na Qur`ani inasema wazi wazi: “…….na anayemtegemea Mwenyezi Mungu basi yeye humtoshea,…..” [65:3]. Na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema:
َم ِن ا ْن َق َط َع اِلَى اهللِ َك َفا ُه اهللُ ُك َّل َمؤ َن ٍة “Yeyote anayeweka matumaini yake yote kwa Allah, atamtimizia mambo yake yote katika maisha yake.”
Ni muhimu izingatiwe kwamba tawakkul haipingani na fikira kwamba binadamu anatakiwa kufanya jitihada katika kutafuta fadhila za Allah ili aweze kunufaika nazo. Ndio maana Uislamu unaona ni wajibu kwa kila mtu kujitahidi kutafuta riziki kwa ajili yake na familia yake, kujihami yeye mwenyewe, na kupigania haki zake. Jambo la muhimu ni kuona kwamba njia zote hizi za usuluhishi wa kati kuwa zipo chini ya mamlaka na uwezo wa Allah, bila kuwa na wajibu wa kujitegemea zenyewe.
29. Utovu wa Shukurani (Kufraan) Uovu huu unatokana na mtu kutokushukuru juu ya rehema za Mungu, na kinyume chake ni shukr (kushukuru). Tabia ya kushukuru (shukr) ina elementi zifuatazo: 109
SAADA KAMILI
i.
Kuzitambua neema na chanzo chao, ambacho ni Ukarimu wa Mungu.
ii. Kufurahi kwa sababu ya neema hizo – si kwa thamani yao ya kidunia au kwa sababu ya kuzipata, bali ni kwa ajili ya thamani yao katika kutufikisha sisi karibu zaidi kwa Allah. iii. Katika kufurahia hali hiyo tunatakiwa kufanya hivyo kwa maneno na matendo kwa lengo la kumridhisha Mpaji. iv. Kumsifu Mpaji wa neema hizi. v.
Kutumia neema hizi tulizopewa katika njia ambayo itamfurahisha Yeye.
Tunaposema “neema” tanamaanisha vitu vyote vinavyofurahisha, vyenye manufaa, na furaha kuu, ama hapa duniani au Akhera. Qur`ani Tukufu inasema: “……. kama mkishukuru bila shaka nitakuzidishieni, na kama mkikufuru, hakika adhabu yangu ni kali sana.” [14:7]. Na katika kufafanua zaidi sehemu ya pili ya aya hiyo hapo juu, Qur`ani inasema: “Na Mwenyezi Mungu amepiga mfano wa mji uliokuwa na amani na utulivu, riziki yake ikaufikia kwa wingi kutoka kila mahala, lakini ukazikufuru neema za Mwenyezi Mungu kwa hiyo Mwenyezi Mungu akauonjesha vazi la njaa na khofu kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyafanya.” [16:112].
30. Kuwa na Wahaka (Jaza‘). Wahaka humfanya mtu apige mayoe, apige uso wake, kupasua nguo, na kupiga kelele mhusika anapokumbwa na balaa au janga. Jaza‘ ni 110
SAADA KAMILI
mojawapo ya uovu ambao chanzo chake ni Nguvu ya hasira. Kinyume chake ni Swabr (subira) ambayo ni mojawapo ya tabia njema. Kwa vyovyote vile, wahaka‘ ni mojawapo ya uovu ambao humwelekeza mtu kwenye anguko, kwa kuwa kimsingi inakuwa ni malalamiko dhidi ya Allah na kukataa amri Zake. Subira, kinyume chake, ni pamoja na kuhifadhi hali ya utulivu katika mazingira yoyote na mtu kufanya kazi katika hali zote. Subira ina kazi tofauti katika hali tofauti; mathalani, subira katika uwanja wa vita ipo katika mtu kuvumilia na kufanya wajibu wake; kwa maneno mengine, ni aina ya ujasiri. Subira katika hali ya hasira ni kujidhibiti na maana yake ni hilm (ustahimilivu). Subira mtu anapokumbwa na matamanio na ashiki hiyo ni ‘iffah (utawa). Kujiepusha na maisha ya starehe na ufahari hii ni subira iitwayo zuhd (kujizuia). Kwa ujumla subira ni tabia inayohusiana na zile aina zote nne za Nguvu. Subira ni tabia ambayo imesifiwa sana katika hadithi za Kislamu, na Qur`ani Tukufu inaisifu tabia hii, sifa zake na thawabu zake katika sehemu tofauti sabini. Mathalani, Qur`ani inasema: “….. nawe wape habari ya furaha wenye kusubiri. Ambao ukiwafikia msiba, husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mwenyezi Mungu na sisi tu wenye kurejea Kwake. Hao juu yao ziko baraka na rehema kutoka kwa Mola wao, wao ndio wenye kuongoka.” [2:155-157]. Na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema:
َ َ َو,الر ْاس ِم َن ْال َج َس ِد ال َج َس َد لِ َم ْن ُ الصب َّ ِ ْر ِمن َا ِ َّ ان ِب َم ْن ِزل ِة ِ ال ْي َم َ َو, س لَ ُه .ْر لَ ُه َ صب َ ال َر ْا َ ال إيمان لمن ال 111
SAADA KAMILI
“Uhusiano wa subira na imani ni sawa kama ule wa kichwa na mwili; kama vile ambavyo mwili hauwezi kuishi bila ya kichwa, ndivyo pia ilivyo kwa imani ambayo haiwezi kuwepo bila subira.”
Zipo aina tano za subira kuhusiana na Sheria ya Kislamu: waajibu, haraam, mustahabb, makruh, na mubaaha. Mfano wa “subira iliyoharamishwa” ni uvumilivu wakati mtu anaponyimwa haki yake kama vile ukandamizaji au ukatili. Subira inayopendeza ni kufanya mambo yanayopendeza kwa uadilifu, ambapo subira inayochukiza inahusu kustahamili mambo ya kulaumika. Mwisho, mubaaha au subira iliyoruhusiwa inahusu mambo yaliyohalalishwa. Sasa basi, ni muhimu ieleweke kwamba subira si kila wakati ni tabia njema, na thamani yake, au pungufu yake, hutegemea kusudio lake. Kwa ujumla, kigezo ambacho hutumika katika kupima aina mbalimbali za subira ni kilekile ambacho kinatumika kupima matendo mengine yote na tabia zingine zote, yaani, matendo yote ambayo humsaidia mtu kuendeleza mambo yake ya kiroho yanathaminiwa na kusifiwa, ambapo matendo mengine yote na tabia zingine zote zinaonekana kuwa mbaya na zenye madhara hulaumiwa.
31. Uasi wa wazi Fisq kama neno maana yake ni kuasi kutii amri za kiwajibu za Shariah ya Kislamu au uasi wa wazi wa kufanya matendo ambayo yameharamishwa; na kinyume chake ni ita`ah [utii] kwenye amri za Allah, Mwenye mamlaka yote. Sehemu kubwa ya amri za Mungu zinajumuisha pamoja na aina maalum za ibada ambazo zinachukuliwa kama ama wajibu au mustahabb [zinazopendekezwa] katika Uislamu. Nazo ni: taharah [utakaso], swala, du’a, dhikiri (utajo wa kumkumbuka Mwenyezi 112
SAADA KAMILI
Mungu), qiraa‘ah [kusoma Qur`ani Tukufu], kufunga saumu, kwenda Makka kwenye Ka`aba Tukufu Kuhiji], Ziyarat [Kuzuru Makaburi ya Mtukufu Mtume na dhuria wake], jihad katika njia ya Allah, adaa`al-ma‘ruuf [Kutekeleza wajibat za kifedha kama zilivyowekwa na Sharia ya Kislamu; yaani khums, zakaat na sadaqah - ambayo ni msaada wa fedha unaotolewa kwa hiari. Baada ya kufika hapa, al-Naraqi mwandishi wa kitabu hiki ameingia kwenye mazungumzo yake ya mwisho kuhusu namna ya kuzitendea amri za Mungu zilizotajwa hapo juu, sababu zao za msingi na mchango wao wa manufaa kwa maendeleo ya kiroho ya mwanadamu. Kwa kuwa mazungumzo haya yanahusu zaidi fiqh, kwa sababu ya ufinyu wa nafasi, hatutayaandika hapa. Uislamu unapendekeza kwamba watu waende kuzuru makaburi hususani ya wazazi wao, makaburi ya watu ambao wamefanya mambo mema kwa jamii [kama vile kifo cha kishahidi, wanazuo, waalimu, wenye kuleta mageuzi na kadhalika]. Katika kuhitimisha, tunatumaini kwamba Allah atujaalie nguvu kimaadili ili tujiendeleze kwa kutekeleza kivitendo ushauri ambao umetolewa kwenye sura nne za kitabu hiki. Pia ni jambo la kutumainiwa kwamba uchunguzi wa kina na kipimo cha kina cha maelezo haya mafupi kuhusu Maadili ya Kislamu utatuhamasisha kushikilia kanuni zake, kwa hiyo kuleta furaha na kuridhika kwa moyo wa mwandishi wake. Wal-hamdu lillah. MWISHO.
113
SAADA KAMILI
DUA YA IMAM ALI BIN HUSAIN ÂZAINUL-ABIDIN (A.S.) KATIKA KUOMBA TABIA NJEMA 1.
Ewe Mwenyezi Mungu! Msalie Muhammad na Aali zake na ifikishe imani yangu katika daraja ya ukamilifu zaidi. Ifanye yakini yangu iwe yakini bora, nia yangu iwe nia bora na matendo yangu yawe matendo mema zaidi.
2.
Ewe Mwenyezi Mungu! kwa huruma Yako ipe nia yangu ukamilifu, ipe yakini yangu usahihi wa yale uliyonayo na kwa uwezo Wako sawazisha kile kilicho haribika toka kwangu.
3.
Ewe Mwenyezi Mungu! Msalie Muhammad na Aali zake na niepushe na hima inizuwiayo kujali yale yatokayo kwangu. Nishughulishe katika yale ambayo utaniuliza kesho. Ziache siku zangu zitumike kwenye yale ambayo kwa ajili yake uliniumba. Nitosheleze na unipanulie riziki Yako. Usiniweke majaribuni kwa kutokuwa na shukurani. Nipe hishima na wala usinijaribu kwa kiburi. Nifanye niwe mwenye kukuabudu Wewe na wala usiiharibu ibada yangu kwa majivuno. Ipitishe kheri ya watu mikononi mwangu na wala usiifute kwa masimbulizi yangu kwao. Nipe tabia njema tukufu na niepushe na fakhari.
4.
Ewe Mwenyezi Mungu! Msalie Muhammad na Aali zake na wala usinipandishe daraja kwa watu ila uwe umenishusha nafsini mwangu kwa kadiri ileile. Usinipe utukufu wa wazi 114
SAADA KAMILI
isipokuwa uwe umenipa udhalili nafsini mwangu kwa kadiri ileile. 5.
Ewe Mwenyezi Mungu! Msalie Muhammad na Aali zake na unistareheshe kwa mwongozo mwema ambao sitaubadilisha. Na kwa njia ya haki ambayo sitapotoka na nia ongofu ambayo sitakuwa na shaka nayo. Nipe uhai iwapo uhai wangu utakuwa ni juhudi niitoayo katika kukutii Wewe. Ama endapo uhai wangu utakuwa ni malisho ya shetani basi nichukuwe Kwako kabla hasira Yako haijanifika au kabla ghadhabu Yako haijaimarika juu yangu.
6.
Ewe Mwenyezi Mungu! usiiache sifa yoyote yenye kunitia dosari isipokuwa uwe umeisawazisha. Au aibu yenye kunitia lawamani ila uwe umeisawazisha. Wala sifa njema pungufu ila uwe umeikamilisha.
7.
Ewe Mwenyezi Mungu! Msalie Muhammad na Aali zake na badilisha kwa ajili yangu bughudha ya watu wenye chuki kuwa upendo, husda ya mafedhuli kuwa mapenzi, dhana ya watu wema kuwa uaminifu, uadui wa makaraba kuwa urafiki, uvunjaji wa haki za ndugu wa damu kuwa wema, kutelekezwa na ndugu wa karibu kuwa msaada, upendo wa wabembe kuwa upendo wa dhati, kukataliwa na wenzi kuwa hishima, uchungu wa kuwaogopa madhalimu kuwa utamu wa amani.
8.
Ewe Mwenyezi Mungu! Msalie Muhammad na Aali zake na nipe uwezo dhidi ya anayenidhulumu, ufasaha dhidi ya anayenihasimu na ushindi dhidi ya anayenifanyia ukaidi. Nipe mbinu dhidi ya anayenifanyia hila, uwezo dhidi ya anayenikandamiza, 115
SAADA KAMILI
jibu dhidi ya anayenikebehi, usalama dhidi ya anayenikamia, na nipe taufiki ya kumtii anayeniweka sawa na kumfuata anayeniongoza. 9.
Ewe Mwenyezi Mungu! Msalie Muhammad na Aali zake na niweke sawa ili nimpinge anayenighushi kwa nasaha, nimlipe wema yule anayejitenga nami, nimjazi yule mwenye kuninyima, niendeleze mahusiano na yule mwenye kuvunja mahusiano nami, nimpinge mwenye kunisengenya kwa kumtaja kwa mema, nishukuru mema na kufumbia macho maovu.
10. Ewe Mwenyezi Mungu! Msalie Muhammad na Aali zake na nipambe kwa mapambo ya watu wema, nivishe pambo la wachamungu kwa kueneza uadilifu, kujizuia na ghadhabu, kuuzima moto wa chuki, kuleta umoja kati ya watu waliofarakiana, kusuluhisha mizozo ya wasiopatana, kueneza mema, kusitiri aibu, kuwa na tabia ya upole, kuwa mnyenyekevu, kuwa na mwendo mwema, uvumilivu, tabia njema, kuharakia maadili mema, kuchagua fadhila, kuacha kufedhehesha na kumfadhili asiyestahiki, kusema yaliyo haki japo ni machungu, kuuona wema ni mchache kwa kauli yangu au kitendo changu japo uwe ni mwingi, kuuona uovu ni mwingi kwa kauli yangu au kitendo changu japo uwe ni mchache. Na nikamilishie hayo kwa utii wenye kudumu, kujiambatanisha na jamaa na kuwakataa wazushi na wale watumiao rai zao za kubuni. 11. Ewe Mwenyezi Mungu! Msalie Muhammad na Aali zake na jaalia riziki yangu iwe wasaa mno kwangu pindi nitakapofikia utu uzima. Niwe mwenye nguvu sana kupitia nguvu Zako pindi nitakapoishiwa nguvu. Usinipe majaribu ya kuwa mvivu katika 116
SAADA KAMILI
ibada Yako, kuwa kipofu wa kutoiona njia Yako, kujihusisha na lile linalopingana na mapenzi Yako, kujiunga na yule ambaye amejitenga na Wewe wala kujitenga na yule aliyejiambatanisha na Wewe. 12. Ewe Mwenyezi Mungu! nijaalie niwe nakimbilia Kwako wakati wa dharura, nakuomba wakati wa haja na niwe nanyenyekea Kwako wakati wa shida. Usinipe majaribu ya kumwomba mwingine msaada mbali na Wewe ninapodharurika, wala kumnyenyekea mwingine kwa maombi mbali na Wewe niwapo fakiri, wala kumnyenyekea yule aliye chini Yako nipatwapo na woga, kwani kwa kufanya hivyo nitastahiki kutelekezwa na Wewe, kunyimwa na Wewe na kupewa kisogo na Wewe. Ewe Mwenye kurehemu kushinda wote wenye kurehemu. 13. Ewe Mwenyezi Mungu! Badali kile anachonitupia shetani moyoni miongoni mwa tamaa, dhana mbaya na husuda kuwa kumbukumbu ya utukufu Wako, tafakari ya nguvu Yako na mpango dhidi ya adui Yako. Na badili yale ayapitishayo ulimini mwangu miongoni mwa maneno machafu, au kebehi, au shutuma, au ushahidi batili, au kumsengenya muumini asiyekuwapo au kumtukana aliyopo au yaliyo mfano wa hayo, kuwa tamko la kukuhimidi Wewe, kufukizia katika kukusifu Wewe, matembezi katika kukuenzi Wewe, shukurani kwa ajili ya neema Zako, utambuzi wa ihisani Yako na ni kuhisabu huruma Yako. 14. Ewe Mwenyezi Mungu! Msalie Muhammad na Aali zake na nisidhulumiwe na hali Wewe ni Muweza wa kunilinda, wala nisidhulumu na hali Wewe waweza kunizuia, usiache nipotee na hali Wewe waweza kuniongoza, usiniache katika umasikini 117
SAADA KAMILI
na hali Kwako kuna kile kiwezacho kunitosheleza na wala nisivuke mipaka hali utajiri wangu upo Kwako. 15. Ewe Mwenyezi Mungu! Nimekuja kwenye maghufira Yako, nauelekea msamaha Wako, nina shauku ya ustahimilivu Wako na nina imani na fadhila Zako. Sina kinachoweza kuwajibisha msamaha Wako kwangu, wala katika matendo yangu hakuna kinachoweza kunifanya nistahiki msamaha Wako na sina chochote kinifaacho baada ya kujihukumu mwenyewe dhidi ya nafsi yangu ila fadhila Zako, hivyo msalie Muhammad na Aali zake na nipe fadhila Zako. 16. Ewe Mwenyezi Mungu! Nitamkishe uongofu, tia moyoni mwangu uchamungu, nipe taufiki ya kile ambacho ni safi mno, na nishughulishe katika lile ambalo waliridhia mno. 17. Ewe Mwenyezi Mungu! Nipitishe njia bora na niwezeshe nifie na kuishi katika mila Yako. 18. Ewe Mwenyezi Mungu! Msalie Muhammad na Aali zake na nistareheshe kwa iktisadi na nijaalie niwe miongoni mwa watu wa sawa, wanyoofu, waongofu na waja wema. Na niruzuku nifuzu Marejeo Kwako na usalama kwenye mavizio unayowavizia. 19. Ewe Mwenyezi Mungu! Chukua kwa ajili Yako toka nafsini mwangu kile kitachoiokoa, na bakisha kwa ajili yangu toka nafsini mwangu kile kitakachoifanya iwe njema, kwani nafsi yangu ni yenye kuangamia isipokuwa ukiilinda.
118
SAADA KAMILI
20. Ewe Mwenyezi Mungu! Wewe ndio kifao changu nihuzunikapo, Wewe ndio kimbilio langu ninyimwapo, Kwako ndipo niombapo msaada wakati wa taabu, na Kwako kuna badala ya kile kilichopotea, utengemao wa kile kilichoharibika na mabadiliko ya kile ulichokikataa. Hivyo nihurumie kwa kunipa afya kabla ya maradhi, mali kabla ya kuomba, na uongofu kabla ya kupotea. Nikinge na fedheha mbele ya waja, nipe amani siku ya marejeo na nipe mwongozo mwema. 21. Ewe Mwenyezi Mungu! Msalie Muhammad na Aali zake na nilinde kwa rehema Yako, nilishe kwa neema Zako, nifanikishie kwa ukarimu Wako, nitibu kwa wema Wako, nikinge kwa kivuli Chako, niweke katika himaya ya ridhaa Zako. Niwafikishe nichague lililo bora zaidi pindi mambo yatakaponichanganya, amali njema zaidi pindi amali zitakaposhabihiyana na itikadi uiridhiayo sana pindi itikadi zitakapopingana. 22. Ewe Mwenyezi Mungu! Msalie Muhammad na Aali zake na nivishe taji la kutosheka, nipe ulinzi mwema, nipe mwongozo sahihi, usiniingize majaribuni kwa maridhawa, nipe maisha mema na usiyafanye maisha yangu kuwa ya taabu na shida, na wala usiirudishe dua yangu kwangu kwa kuikataa. Kwani hakika mimi simfanyi yeyote kuwa dhidi Yako wala simwombi yeyote pamoja na Wewe. 23. Ewe Mwenyezi Mungu! Msalie Muhammad na Aali zake na nikinge na ubadhirifu, ilinde riziki yangu na uharibifu, iongezee mali yangu baraka, na nifanikishie njia ya mwongozo kwa kupata wema katika yale nitoayo.
119
SAADA KAMILI
24. Ewe Mwenyezi Mungu! Msalie Muhammad na Aali zake na niepushe na taabu za uchumaji, na nipe riziki bila ya hisabu, kutafuta riziki kusinizuie kukuabudu na wala nisiwajibike na matokeo mabaya ya uchumaji. 25. Ewe Mwenyezi Mungu! nipe niyatafutayo kwa uwezo Wako na niepushe kwa nguvu Zako dhidi ya lile ninalolikhofu. 26. Ewe Mwenyezi Mungu! Msalie Muhammad na Aali zake na uhifadhi uso wangu kwa kunipa maisha bora, wala usiishushe hishima yangu kwa ufakiri, ili nisije waomba riziki wale uliowaruzuku au kuwaomba kipawa wale waovu miongoni mwa viumbe Wako. Kwani kwa kufanya hivyo nitaingia katika majaribu ya kumsifu atakayenipa na kumlaumu atakayeninyima, na hali Wewe ndio Mtoaji na Mnyimaji na wala si wao. 27. Ewe Mwenyezi Mungu! Msalie Muhammad na Aali zake na unipe siha njema katika ibada, faragha katika utawa, ilimu katika matendo na kujiepusha katika kipimo. 28. Ewe Mwenyezi Mungu! Hitimisha muda wangu kwa msamaha Wako, timiza matarajio yangu kwa kuwa na matarajio juu ya rehema Zako, rahisisha njia zangu za kuifikia ridhaa Yako na zikuze amali zangu katika hali zote. 29. Ewe Mwenyezi Mungu! Msalie Muhammad na Aali zake na nizindue nyakati za mghafala ili niweze kukukumbuka. Nishughulishe katika kukutii Wewe siku za raha. Nirahisishie njia ya kuelekea kwenye mapenzi Yako. Na kwa njia hiyo nikamilishie kheri ya Dunia na Akhera. 120
SAADA KAMILI
30. Ewe Mwenyezi Mungu! Msalie Muhammad na Aali zake kwa ubora ule ule uliowahi kumsalia yeyote katika viumbe Vyako kabla yake, na kwa ubora ule ule utakao msalia yeyote baada yake. “Tupe Duniani mema na Akhera mema. Na kwa rehema Zako unilinde na adhabu ya Moto.� (2:201).
121
SAADA KAMILI
ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1. Qur’an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thelathini 2.
Uharamisho wa Riba
3.
Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza
4.
Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili
5.
Hekaya za Bahlul
6.
Muhanga wa Imamu Husein (A.S.)
7.
Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.)
8.
Hijab vazi Bora
9.
Ukweli wa Shia Ithnaashari
10. Madhambi Makuu 11. Mbingu imenikirimu 12. Abdallah Ibn Saba 13. Khadijatul Kubra 14. Utumwa 15. Umakini katika Swala 16. Misingi ya Maarifa 17. Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia 122
SAADA KAMILI
18. Bilal wa Afrika 19. Abudharr 20. Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu 21. Salman Farsi 22. Ammar Yasir 23. Qur’an na Hadithi 24. Elimu ya Nafsi 25. Yajue Madhehebu ya Shia 26. Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur’an Tukufu 27. Al-Wahda 28. Ponyo kutoka katika Qur’an 29. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii 30. Mashukio ya Akhera 31. Al Amali 32. Dua Indal Ahlul Bayt 33. Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. 34. Haki za wanawake katika Uislamu 35. Mwenyezi Mungu na sifa zake 36. Kumswalia Mtume (s) 37. Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) 38. Adhana 39
Upendo katika Ukristo na Uislamu 123
SAADA KAMILI
40. Tiba ya Maradhi ya Kimaadili 41. Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu 42. Kupaka juu ya khofu 43. Kukusanya swala mbili 44. Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara 45. Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya 46. Kusujudu juu ya udongo 47. Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) 48. Tarawehe 49. Malumbano baina ya Sunni na Shia 50. Kupunguza Swala safarini 51. Kufungua safarini 52. Umaasumu wa Manabii 53. Qur’an inatoa changamoto 54. as-Salaatu Khayrun Mina -’n Nawm 55. Uadilifu wa Masahaba 56. Dua e Kumayl 57. Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu 58. Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake 59. Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata 60. Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mtume Muhammad (s) 61. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza 124
SAADA KAMILI
62. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili 63. Kuzuru Makaburi 64. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza 65. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili 66. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu 67. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne 68. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano 69. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita 70. Tujifunze Misingi Ya Dini 71. Sala ni Nguzo ya Dini 72. Mikesha Ya Peshawar 73. Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu 74. Ubora wa Imam ‘Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliyonyooka 75. Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake 76. Liqaa-u-llaah 77. Muhammad (s) Mtume wa Allah 78. Amani na Jihadi Katika Uislamu 79. Uislamu Ulienea Vipi? 80. Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) 81. Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) 82. Urejeo (al-Raja’a )
125
SAADA KAMILI
83. Mazingira 84. Utokezo (al - Badau) 85. Hukumu ya kujenga juu ya makaburi 86. Swala ya maiti na kumlilia maiti 87. Uislamu na Uwingi wa Dini 88. Mtoto mwema 89. Adabu za Sokoni 90. Johari za hekima kwa vijana 91. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza 92. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili 93. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu 94. Tawasali 95. Imam Mahdi katika Usunni na Ushia 96. Hukumu za Mgonjwa 97. Sadaka yenye kuendelea 98. Msahafu wa Imam Ali 99. Ngano ya kwamba Qur’ani imebadilishwa 100. Idil Ghadiri 101. Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu 102 Hukumu zinazomuhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi 103. Huduma ya Afya katika Uislamu 104. Sunan an-Nabii 126
SAADA KAMILI
105. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) 106. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) 107. Shahiid Mfiadini 108. Kumsalia Nabii (s.a.w) 109. Ujumbe -Sehemu ya Kwanza 110. Ujumbe - Sehemu ya Pili 111. Ujumbe - Sehemu ya Tatu 112. Ujumbe - Sehemu ya Nne 113. Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu 114. Hadithi ya Thaqalain 115. Ndoa ya Mutaa 116. Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza 117. Ukweli uliopotea sehemu ya Pili 118. Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu 119. Ukweli uliopotea sehemu ya Nne 120. Ukweli uliopotea sehemu ya Tano 121. Mkutano wa Maulamaa wa Baghdad 122. Safari ya kuifuata Nuru 123. Fatima al-Zahra 124. Myahudi wa Kimataifa 125. Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi 126. Visa vya kweli sehemu ya Kwanza 127
SAADA KAMILI
127. Visa vya kweli sehemu ya Pili 128. Elimu ya Ghaibu ya Maimamu 129. Mwanadamu na Mustakabali wake 130. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) 131. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) 132. Khairul Bariyyah 133. Uislamu na mafunzo ya kimalezi 134. Vijana ni Hazina ya Uislamu 135. Yafaayo kijamii 136. Tabaruku 137. Taqiyya 138. Vikao vya furaha 139. Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 140. Visa vya wachamungu 141. Falsafa ya Dini 142. Azadari-Kuhuzunika na Kuomboleza 143. Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah 144. Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu 145. Kuonekana kwa Allah 146. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) 147. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) 128
SAADA KAMILI
148. Ndugu na Jirani 149. Ushia ndani ya Usunni 150. Maswali na Majibu 151. Mafunzo ya hukmu za ibada 152. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1 153 Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2 154. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 155. Abu Huraira 156. Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. 157. Mazingatio kutoka katika Qur’an - Sehemu ya Kwanza 158. Mazingatio kutoka kaitka Qur’an - Sehemu ya Pili 159. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza 160. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili 161. Qur’ani Tukufu – Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili 162. Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) 163. Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani 164. Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu 165. Uislamu Safi 166. Majlisi za Imam Husein Majumbani 167. Je, Kufunga Mikono 168. Uislam wa Shia 169. Amali za Makka 129
SAADA KAMILI
170. Amali za Madina 171. Asili ya Madhehebu katika Uislamu 172. Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi 173. Ukweli uliofichika katika neno la Allah 174. Uislamu na Mifumo ya Uchumi 175. Umoja wa Kiislamu na Furaha 176. Mas’ala ya Kifiqhi 177. Jifunze kusoma Qur’ani 178. As-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah 179. Hayya ‘Alaa Khayri’l-’Amal Katika Adhana 180. Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura 181. Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na Ramadhani) 182. Uadilifu katika Uislamu 183. Mahdi katika Sunna 184. Maswali Ya Uchunguzi Kuhusu Uislam 185. Kazi na Bidii ni njia ya maendeleo 186. Abu Talib – Jabali Imara la Imani 187. Ujenzi na Utakaso wa Nafsi 188. Vijana na Matarajio ya Baadaye 189. Usalafi – Historia yake, maana yake na lengo lake 190. Ushia – Hoja na Majibu 191. Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) 130
SAADA KAMILI
192. Maombolezo – Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) 193. Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu 194. Takwa 195. Upotoshaji dhahiri katika Turathi (Hazina) ya Kiislamu 196. Amirul Muuminina (‘as) na Makhalifa 197. Uongozi na Utawala katika Mwenendo wa Imam ‘Ali (‘a) 198. Kuvunja hoja iliyotumika kutetea Uimamu wa AbuBakr 199. Adabu za vikao na mazungumzo 200. Hija ya Kuaga 201. Uwazi baina ya Maslahi na Vikwazo 202. Fadhila za watukufu watano katika Sahih Sita 203. Mdahalo baina ya Mwanachuoni wa Kisunni na Mwanachuoni wa Kishia (Al-Muraja’aat) 204. Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (as) 205. Mjadala wa Kiitikadi 206. Mtazamo kuhusu msuguano wa Kimadhehebu 207. Nchi na Uraia – Haki na wajibu kwa Taifa 208. Mtazamo wa Ibn Taymiyyah juu ya Imam Ali (as) 209. Uongozi wa Kidini – Maelekezo na Utekelezaji wa Kijamii 210. Maadili ya Ashura 211. Mshumaa – Shahidi na Kifo cha Kishahidi 212. Mizani ya Hekima – Hadithi za Ahlul Bait (as) – Sehemu ya Kwanza 131
SAADA KAMILI
213. Imam Ali na Mambo ya Umma 214. Imam Ali na Mfumo wa Usawa 215. Mwanamke na Sharia 216. Mfumo wa Wilaya 217. Vipi Tutaishinda Hofu? 218. Kumswalia Mtume ni Ufunguo wa Utatuzi wa Matatizo
219. Mahali na Mali za Umma 220. Nahjul-Balagha – Majmua ya Khutba, Amri, Barua, Risala, Mawaidha na Semi za Amirul-Muuminin Ali bin Abu Talib (a.s.) 221. Mukhtar – Shujaa aliyelipiza kisasi dhidi ya wauaji wa Imam Husein (as) hapo Karbala 222. Uimamu na Tamko la Kutawazwa 223. Imam Husain ni Mfumo wa Marekebisho na Mageuzi 224. Saada Kamili – Kitabu cha Kiada cha Maadili
132
SAADA KAMILI
KOPI NNE ZIFUATAZO ZIMETAFSIRIWA KWA LUGHA KINYARWANDA 1.
Amateka Na Aba’Khalifa
2.
Nyuma yaho naje kuyoboka
3.
Amavu n’amavuko by’ubushiya
4.
Shiya na Hadithi
133
SAADA KAMILI
ORODHA YA VITABU VILIVYO ÂCHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION KWA LUGHA YA KIFARANSA 1.
Livre Islamique
134