Safari ya kuelekea kwa mwenyezi mungu

Page 1

SAFARI YA KUELEKEA KWA MWENYEZI MUNGU ‫الرحلة إلى اهلل‬

Mtungaji: Mahdi Jaafar Sulail

Mtarjumi: Abdul-Karim Juma Nkusui

02_15_Safari ya kuelekea_3_Feb_2015.indd 1

2/3/2015 1:36:30 PM


‫الرحلة إلى اهلل‬

‫تأليف‬ ‫مهدي صليل‬

‫من اللغة العربية إلى اللغة السواحلية‬

‫‪2/3/2015 1:36:30 PM‬‬

‫‪02_15_Safari ya kuelekea_3_Feb_2015.indd 2‬‬


© Haki ya kunakili imehifadhiwa na: Al-Itrah Foundation ISBN No: 978 – 9987 – 17 – 030 – 2 Mtungaji: Mahdi Jaafar Sulail Mtarjumi: Abdul-Karim Juma Nkusui Kimehaririwa na: Alhajj Ramadhani S. K. Shemahimbo Na Alhajj Hemedi Lubumba Kimepitiwa na: Mbarak A. Tila Kimepangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation Toleo la kwanza: Julai 2015 Nakala: 2000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. - 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: www.alitrah.info

02_15_Safari ya kuelekea_3_Feb_2015.indd 3

2/3/2015 1:36:30 PM


02_15_Safari ya kuelekea_3_Feb_2015.indd 4

2/3/2015 1:36:30 PM


Yaliyomo Neno la Mchapishaji........................................................................ 1 Utangulizi......................................................................................... 3 Safari ya Kuelekea kwa Mwenyezi Mungu..................................... 4 Mwenye Kujitahidi Hupata.............................................................. 5 Kisimamo Pamoja na Nafsi............................................................. 6 Dhahiri na Batini.............................................................................. 8 Kulia .......................................................................................... 9 Hupita Kama Mawingu.................................................................. 10 Falsafa ya Ibada............................................................................. 11 Kupita Kwenda Kwenye Uhalisia.................................................. 12 Katika Safari ya Arafah.................................................................. 13 Kiini cha Maneno........................................................................... 15 Maombi ........................................................................................ 18 Hitimisho....................................................................................... 20

02_15_Safari ya kuelekea_3_Feb_2015.indd 5

2/3/2015 1:36:30 PM


SAFARI YA KUELEKEA KWA MWENYEZI MUNGU

َّ‫ب ْسم الله‬ ‫يم‬ ‫ح‬ ‫الر‬ ‫م‬ ‫ح‬ ‫ر‬ ‫ال‬ َّ ِ‫ن‬ ٰ ِ ِ َ ْ َّ ِ ِ ِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.

‫ار ًكا‬ ٍ ‫إِ َّن أَ َّو َل َبي‬ َ ‫اس لَلَّ ِذي ِب َب َّك َة ُم َب‬ ِ ‫ْت ُو‬ ِ َّ‫ض َع لِلن‬ َ ‫َو ُه ًدى لِْل َعالَ ِم‬ ‫ين‬ “Hakika nyumba ya kwanza waliyowekewa watu ni ambayo ile ­iliyoko Makka yenye kubarikiwa na mwongozo kwa viumbe.” (Suratu Aal –Imraan: 96).

َ ُ‫َوأَ ِّذ ْن ِفي النَّاس ب ْال َح ِّج َي ْأت‬ ‫وك ِر َج اًال َو َعلَىٰ ُك ِّل‬ ِ ِ ْ ‫ضامر َي‬ ِّ ُ ‫ين ِم ْن‬ َ َ ‫يق‬ ‫م‬ ‫ع‬ ‫ج‬ ‫ف‬ ‫ل‬ ‫ك‬ ‫ت‬ ‫أ‬ ٍّ َ ِ ِ ٍ ٍِ َ “Na watangazie watu Hijja watakujia kwa miguu na juu ya kila mnyama aliyekonda kutoka kila njia ya mbali. Ili washuhudie manufaa yao na walitaje jina la Mwenyezi Mungu katika siku maalumu juu ya wanyama hawa aliyowaruzuku Mwenyezi Mungu basi kuleni katika hao na mumlishe mwenye shida aliyefukara.” (Suratul- Hajji: 27).

vi

02_15_Safari ya kuelekea_3_Feb_2015.indd 6

2/3/2015 1:36:30 PM


SAFARI YA KUELEKEA KWA MWENYEZI MUNGU

ZAWADI Katika maana ya upendo, Na hisia za shauku, Uzuri wa kumbukumbu, Kwa anwani ya ukweli, Na uhalisia wa juhudi, Na ukweli wa kutoa, Kwako baba, mpendwa wa moyo wangu, Nakupa zawadi ya (kitabu hiki), “Safari ya kuelekea kwa Mwenyezi Mungu.”

vii

02_15_Safari ya kuelekea_3_Feb_2015.indd 7

2/3/2015 1:36:30 PM


02_15_Safari ya kuelekea_3_Feb_2015.indd 8

2/3/2015 1:36:30 PM


SAFARI YA KUELEKEA KWA MWENYEZI MUNGU

NENO LA MCHAPISHAJI

K

itabu ulichonacho mikononi mwako asili yake ni cha lugha ya Kiarabu kwa jina la, ar-Rihlatu ila ‘l-Laah, kilichoandikwa na Sheikh Mahdi Ja’far Sulail. Sisi tumekiita, Safari Kuelekea kwa Mwenyezi Mungu. Kitabu hiki kinahusu safari ya Hija, hivyo mwandishi ameelezea kwa ufupi historia ya Hija, kisha akaelezea maana, faida na matokeo kwa mwenye kufanya safari hii. Sisi kama wachapishaji tumekiona kitabu hiki kuwa ni chenye manufaa sana kwa wasomaji wetu, hususan wale ambao wanafanya maandalizi ya safari hii tukufu na pia kuwahamasisha wale ambao tayari wana uwezo wa kufanya safari hii wafanye hima kuiendea Nyumba ya Allah ‘Azza wa Jallah na kuitekeleza ibada hii tukufu. Hii ni moja kati ya kazi kubwa zilizofanywa na Taasisi ya AlItrah katika kuwahudumia kielimu wasomaji wake wazungumzaji wa Kiswahili. Na kwa maana hiyohiyo, imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa lengo lake lilelile la kuwahudumia Waislamu, hususan wanaozungumza Kiswahili ili nao waweze kunufaika na yaliyomo ndani yake.

Tunamshukuru mwandishi wa kitabu hiki, Sheikh Mahdi Ja’far Sulail kwa kazi kubwa aliyoifanya kwa ajili ya Umma huu wa Waislamu, Allah ‘Azza wa Jallah amlipe kila kheri na amuingize Peponi kwa salama na amani insha’Allah. Halikadhalika tunamshukuru Ustadh Abdul-Karim Juma Nkusui kwa kukitarjumi kwa Kiswahili kitabu hiki, insha’Allah na yeye Allah Mwenye kujazi amlipe kila kheri hapa duniani na Akhera pia, bila kuwasahau na wale wote waliochangia kwa namna mmoja au nyingine mpaka kufanikisha 1

02_15_Safari ya kuelekea_3_Feb_2015.indd 1

2/3/2015 1:36:30 PM


SAFARI YA KUELEKEA KWA MWENYEZI MUNGU

kuchapishwa kwa kitabu hiki. Allah awalipe wote malipo mema hapa duniani na kesho Akhera pia. Mchapishaji Al-Itrah Foundation.

2

02_15_Safari ya kuelekea_3_Feb_2015.indd 2

2/3/2015 1:36:30 PM


SAFARI YA KUELEKEA KWA MWENYEZI MUNGU

UTANGULIZI Wito wa kwenda huko: Ewe nafsi vua nguo za uzembe hapa, Umeshawadia wakati wa kuondoka kwenda huko, Pamoja na waendaji waliotangulia kwenda peponi, Na kuwasili bila ya kikwazo, katika mapito ya machozi, na sauti ya upole, na mapito ya Husein kuelekea Karbalaa, Huko utakunywa maji ya uzima bila kukatika, Na utaonja ladha ya ukaribu kwa utamu wa mapenzi hakuna ­mashaka. Ni mara ngapi imevuma sauti ya mbinguni kwa waliokaa baina ya kona za uzembe, Na mara ngapi umefululiza wito wa Manabii, Unatamani kwa waenda mbio nyuma ya mazigazigazi warudi nyuma, Roho yangu akuongoze Mwenyezi ewe tumaini langu, Katika maji ya Zamzam, kunywa kisha oga, Na omba msamaha katika mlango wa Mkarim na wala isikuzuie ­kukata tamaa, Vunja kizuizi cha haya.

3

02_15_Safari ya kuelekea_3_Feb_2015.indd 3

2/3/2015 1:36:30 PM


SAFARI YA KUELEKEA KWA MWENYEZI MUNGU

SAFARI YA KUELEKEA KWA MWENYEZI MUNGU

H

ii ndio anwani kubwa zaidi ambayo ni wajibu ihudhurishwe kila sekunde kati ya sekunde za uwepo wetu. Na inatiliwa mkazo anwani hii wakati wa uhudhuriaji wetu ilihali tumevaa nguo mbili za ihram na kuzunguka nyumba tukufu na kutekeleza ibada karibu na Mwenyezi Mungu. Anwani nyingine zitajaribu kusonga makusudio yetu, na kudhihiri mbele yetu wazo la kununua, kupata chakula na kuandamana na marafiki, na yote hayo ni kheri, lakini mwenye kuwa macho na lengo la hatima atayaweka hayo kando katika mazingatio yake ili aonje ladha ya kujongea kwa Mwenyezi Mungu na katika dua: “Na unipe ukamilifu wa kujongea Kwako.” Ni siku chache kisha tunazoea na kurejea katika maisha ya kawaida ambayo yanamiliki fikira ya mwanadamu na kumzamisha katika yale ambayo hawezi kuepukana nayo, na ziwe siku hizi ni hazina ya uchamungu na uhudhuriaji wa fikira katika ulimwengu wa ghaibu uliofichikana katika siku za maisha yetu. Hii inahitajia kwetu azma na kung’ang’ania kufikia kwenye uhalisia wa Hija na kufaidika na muda wa kuwa karibu na Mwenyezi Mungu Mtukufu.

4

02_15_Safari ya kuelekea_3_Feb_2015.indd 4

2/3/2015 1:36:31 PM


SAFARI YA KUELEKEA KWA MWENYEZI MUNGU

MWENYE KUJITAHIDI HUPATA

M

abadiliko makubwa katika ratiba ya maisha yetu ambayo tumeyazoea, ni kozi yenye masomo mengi ya elimu, kusajili upya uhusiano wa kijamii, na mazingira yenye kujaa huruma za Mwenyezi Mungu. Na baada ya siku kadhaa tunarejea kutoka kwenye kozi hii yenye masomo huku tukiwa tumebeba pamoja nasi zawadi na hidaya ambazo tumezipata huko. Unadhani ni wote watapata zawadi na hidaya ya aina moja? Au kutakuwa na tofauti katika matokeo? Kila mmoja aiulize nafsi yake: Ni tija ipi ambayo nitaipata? Je, nitakuwa wa kwanza, katika kilele cha orodha? Au mimi nitatoka kwenye ushindani na mikono mitupu? Au nitakuwa baina ya haya na yale? Kama mtu atazinduka na manufaa ya Hija na kuyaweka mbele ya macho yake ataweza kunufaika. Fursa iko mbele yetu na sisi tuko mwanzo wa safari, tufanye juhudi na tujitahidi, na tukusanye kiasi kikubwa miongoni mwa zawadi zinazotushukia kutoka katika rehema za Mwenyezi Mungu.

5

02_15_Safari ya kuelekea_3_Feb_2015.indd 5

2/3/2015 1:36:31 PM


SAFARI YA KUELEKEA KWA MWENYEZI MUNGU

KISIMAMO PAMOJA NA NAFSI

M

wanadamu hukesha kwa kupiga ukelele wa dhamiri wakati unapomlingania kubadilisha baadhi ya sifa zake. Na anakiri ukweli, na anatamani kuondoa sifa mbaya moyoni mwake, lakini anaona gurudumu la siku linakwenda bila ya kumwachia fursa ya kutibu magonjwa haya na kuyang’oa! Anatamani mmoja wetu kubadili nafsi yake na kujinasua na baaadhi ya sifa zake, lakini kila siku kazi za mfululizo na matukio hayamwachii fursa na kukaa faragha na nafsi yake na kutafakari katika dhati na kujinasua na makosa ya maisha ambayo yamegandamana na nafsi. Nafsi ya kwanza ni safi tumezaliwa nayo, nafsi ya utotoni isiyo na hatia ambayo inafanya kazi otomatiki na bila ya hatia, ingawa kunarundikana kwake uchafu wa matamanio na utelezi wa ugomvi. Ni lini tutakabilina nayo na kuanza kazi ya marekebisho ya ndani? Hakika sisi tunasimama kwa muda mrefu mbele ya kioo kwa ajili ya kurekebisha mandhari yetu ya nje na tunakuwa makini kwa kila dogo na kubwa katika sura zetu, kope zetu, nyusi zetu na magamba ya midomo yetu, lakini sisi tunaghafilika na ukweli na uhalisia! Tunachagua chakula chetu na vinywaji vyetu kwa umakini mkubwa, tunahakiki usalama wa chakula na tunaangalia usafi wa samaki na nyama na tunaosha matunda na mboga mboga kabla ya kula, lakini mukabala wa hilo tunaacha nafsi zetu ziko wazi katika uwanja wake na tunaingiza humo kila tunachokiona! Picha ambayo jicho linaiona inaenda katika nafsi “na moyo ni karatasi ya macho” unaandika kila kinachoonwa na jicho. Sisi tunabagua baina ya matunda mazuri na matunda mabovu, lakini sisi tunaghafilika na sura iliyoharibika ambayo tunaiingiza ndani 6

02_15_Safari ya kuelekea_3_Feb_2015.indd 6

2/3/2015 1:36:31 PM


SAFARI YA KUELEKEA KWA MWENYEZI MUNGU

mwetu na inafanya kazi ya virusi vinavyoharibu sifa nzuri zilizomo ndani mwetu. Tunasikiliza kila mazungumzo na tunazungumza kila neno na tunaacha maneno haya yanatengeneza dhati na kujenga sifa. Utu wa kila mtu miongoni mwetu umeundwa na sehemu ndogo ndogo za harakati na kutulizana ambazo tunazifanya, na maneno tunayoyatamka, na picha na mandhari ambayo tunayakubali au tunayakataa, na baada ya miaka mambo haya yanatengeneza shakhisiya ambayo haitengani na ada na sifa ambazo zinageuka na kuwa gamba gumu katika ukuta wa nafsi, na kadiri siku zinavyoendelea ndivyo ada zinazidi kuwa ngumu zaidi na sifa zinajikita na kuwa vigumu kuzibadilisha. Hapa unakuja umuhimu wa huruma za Mwenyezi Mungu katika misimu ya kidini. Leo sisi tuko katika msimu wa Hija, nafsi inajiandaa kwa mabadiliko na moyo unalainika kwa mawaidha na roho inaelea katika anga la fadhila. Je, tutanufaika na fursa hii tukufu ili tuanze mabadiliko?

7

02_15_Safari ya kuelekea_3_Feb_2015.indd 7

2/3/2015 1:36:31 PM


SAFARI YA KUELEKEA KWA MWENYEZI MUNGU

DHAHIRI NA BATINI

M

tu anasimama sana akiangalia nafsi yake kwenye kioo, anasawazisha mwonekano wake na anaweka vizuri mavazi yake, akiona kasoro anaisawazisha au dosari anairekebisha. Kama anavyokwenda mbio aonekane kwa mandhari nzuri mbele ya watu, vilevile anatamani awe na sifa nzuri kimwenendo na umashuhuri, na hivyo hafanyi kitendo anachoona kinamtia ila na kasoro. Mwonekano mzuri, mwenendo mzuri na kisha sifa nzuri na umashuhuri. Nalo ni jambo analoliafiki kila mwenye akili na wanaafikiana juu yake watu wote, lakini ukweli ambao ni wajibu uwe ni kigezo mbele yetu ni kwamba, huu ni urekebishaji wa nje tu, hautakuwa na maana ikiwa haukuambatana na marekebisho ya ndani. Na hapa ni lazima kusema: Hakika Uislamu unahimiza juu ya kuwapima watu kulingana na mwonekano wao na kutopekua undani wao na mwelekeo wao. Ama katika upande wa mwanadamu kupima nafsi yake anatakiwa kuingia ndani katika nafsi yake ili aigundue na airekebishe, jicho la nje ni kwa ajili ya watu na macho ya ndani ni kwa ajili ya nafsi yake. “Ni ubaya ulioje kwa mwanadamu nje ni mzuri na ndani ni mnafiki” “Ambaye dhahiri yake ni nzuri zaidi kuliko undani wake basi mizani yake itakuwa nyepesi.” Amesema Imam al-Baqir A. Na siku za Hija ni fursa bora ambayo anaipata mwanadamu ili kujua ukweli wa nafsi yake na kuirekebisha.

8

02_15_Safari ya kuelekea_3_Feb_2015.indd 8

2/3/2015 1:36:31 PM


SAFARI YA KUELEKEA KWA MWENYEZI MUNGU

KULIA

M

achozi ambayo yanadondoka kwenye macho yako sio maji yanayotiririka kwenye mashavu yako! Bali kwa hakika ni nuru inayoondoa giza la moyo ambalo linazuia uoni. Na ni dawa ya kuponya ugonjwa sugu unaoua. Kulia ni kujikomboa na umateka wa matamanio na kujiweka huru na pingu za matamanio. Kulia ni nuru ya moyo ambayo inakuonyesha uhalisia wa mambo. Kulia ni anwani ya kujuta, na dalili ya kuporomoka mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Muumini anakaa faragha na nafsi yake usiku wa manane, anamnong’oneza Mola Wake, na moyo wake unashughulika na yanatiririka machozi yake na kusafisha makosa ambayo yamezuia nuru. Amesema Mtukufu Mtume 5: “Mambo manne ni alama ya uovu: Ugumu wa macho, ugumu wa moyo, kupupia kuitafuta dunia na kung’ang’ania dhambi.” Na amesema 5: “Ewe Ali! Mambo matatu yanaokoa: Zuia ulimi wako, lia kutokana na makosa yako na ikutoshe nyumba yako.” “Ewe Ali! Kila jicho litalia siku ya Kiyama ila macho matatu: Jicho lililokesha katika njia ya Mwenyezi Mungu, na jicho lililofumba katika aliyoharamisha Mwenyezi Mungu na jicho lililolia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.” “Ewe Ali! Mafanikio ni kwa sura ile aliyoiangalia Mwenyezi Mungu akaikuta inalia kutokana na dhambi ambayo hakuiona dhambi hiyo yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu.” “Ewe Ali! Mambo manne ni katika uovu: Jicho gumu, ugumu wa moyo, matumaini ya mbali na kuipenda dunia.” Amesema Imamu Ali A: “Kulia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kunatia nuru katika moyo na kunazuia kurudia dhambi.” 9

02_15_Safari ya kuelekea_3_Feb_2015.indd 9

2/3/2015 1:36:31 PM


SAFARI YA KUELEKEA KWA MWENYEZI MUNGU

HUPITA KAMA WINGU

S

iku hizi zitapita haraka, je tutaweza kuutangulia wakati?

Hakika ni swali gumu, na muhimu sana! Tulikuwa tunasubiri kuwadia mazingira haya ya kiroho hatimaye tumeshafika. Je, tutajitolea kuutumia wakati mchache katika saa za mwaka? Katika miaka iliyopita niliiambia nafsi yangu: Ni wajibu wako kujitolea kabla ya kupitwa na muda. Na sijakaa mara naona siku hizi zimeshapita haraka, naikuta nafsi yangu mbele ya Arafah. Siku ya Arafah, na nini Arafah! Inahitajia maandalizi makubwa ya kiroho ili tuweze kuelewa kheri zake na baraka zake. Hakika kila mmoja atachuma kwa kadri ya maandalizi yake ili kupata rehema za Mwenyezi Mungu. Na maandalizi yanahitajia kuituliza nafsi na kuidhalilisha “kwani mmea unaota katika ardhi tambarare na wala hauoti katika jabali.” Je unadhani nitakuwa na fungu katika rehema hizo? Leo, kuna fursa na saa bado hazijamalizika, basi na tumimine maji ya unyenyekevu katika bustani za nyoyo zetu ili ichipue na kuota miti ya unyenyekevu na tushuhudie matunda ya kukubaliwa. Na hapo tutavaa nguo za ridhaa, na tutaneemeka na huruma ya upendo. Kutoka kwa Imamu Ali A hakika amesema: “Fursa inapita kama yanavyopita mawingu, basi itumieni fursa katika kheri.” “Fursa inapita haraka na ni yenye kurejea taratibu.”

10

02_15_Safari ya kuelekea_3_Feb_2015.indd 10

2/3/2015 1:36:31 PM


SAFARI YA KUELEKEA KWA MWENYEZI MUNGU

FALSAFA YA IBADA

K

utufu, Kutembea baina ya Swafa na Marwa, Swala, Rukuu na Sijda, ni vitendo tunavyovifanya, na kila mmoja wetu anataraji kupitia katika vitendo hivyo ili kutimiza jambo ambalo lipo katika nafsi yake. Mmoja wetu anahisi uzito wa jukumu lake (jukumu la wajibu) na anataka kuliondoa katika mgongo wake. Baada ya kumaliza kazi anahisi raha kwa sababu ametekeleza wajibu wake, na mtu mwingine anafanya vitendo vya ibada kwa msukumo wa kupata thawabu na malipo. Kwa hakika wa kwanza anaenda mbio kwa ajili ya kupata malipo vile vile, lakini lengo la awali kwake ni kutekeleza (wajibu wake). Na kuna daraja la juu zaidi kuliko hili na lile, hakika ni raghaba ya kuilea nafsi na kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Vitendo hivi ambavyo tunavifanya ndani vinakusanya twahara ya moyo, kuitakasa nafsi na kutukuka kwa roho. Na wala hatupati natija hii ila tukinoa azma ya kuzama ndani ya kina cha ibada, na hata tunapovumbua thamani yetu tunafanya haraka kuishikilia kabla ya kuharibika kwake na tunaimimina kama dawa ya maradhi yetu.

11

02_15_Safari ya kuelekea_3_Feb_2015.indd 11

2/3/2015 1:36:31 PM


SAFARI YA KUELEKEA KWA MWENYEZI MUNGU

KUPITA KWENDA KWENYE ­UHALISIA

A

likuwa anaongea na mume wake na macho yake yanabubujika machozi, anaangalia Kaaba na wakati mwingine anamwangalia mume wake naye hasadiki anachokiona. Allahu Akbar! sisi tuko wapi? Hii ni Kaaba mbele yetu? Shauku kubwa, na hisia ambayo haielezeki kwa maneno, kila ninapokumbuka mandhari hayo naihurumia nafsi yangu. Nautukuza moyo huo ambao uliyeyuka kwa mapenzi katika maana ya utukufu wa Kaaba Tukufu. Sehemu takatifu na kitovu cha tawafu kando ya rehema ya Mwenyezi Mungu na ukamilifu wa faragha. Je, tunaweza kufika kwenye kiini cha uhalisia kwa Tawafu zetu na Swala zetu? Au hatua zetu zitakuwa ni kwenda mbio ili kuondoa wajibu wetu tu? Ibada ambazo tunazifanya na amali ambazo tunazifanya zinabeba maana tukufu, na madhumuni matukufu yanahitajia usafi wa moyo na unadhifu wa roho, na kutafakari kwa fikra ili tupite kupitia kwayo hadi kwenye uhalisia.

12

02_15_Safari ya kuelekea_3_Feb_2015.indd 12

2/3/2015 1:36:31 PM


SAFARI YA KUELEKEA KWA MWENYEZI MUNGU

KATIKA SAFARI YA ARAFAH

M

vua inaponyesha pande za ardhi zinatofautiana katika kuipokea kwake na kuathirika kwake, maji ni ya aina moja yanateremka juu ya sehemu hizi, ardhi inatikisika na maua yanaota, na nyingine inapasuka na kutoa miba. Na sehemu ya pili haiwezi kusema: Hakika mvua ndio sababu. Na sisi tunapokea bishara za kheri katika siku hii ambayo haifanani na siku nyingine yoyote. Ardhi yetu ni ipi? Ni ardhi ya miba au ardhi ya maua? Yatafanya nini maji ya baraka ya Arafah katika moyo huu? Hili ndio swali muhimu sana katika siku hii. Je, mimi niko tayari kupokea wito wa Mwenyezi Mungu? Swali muhimu ni lazima tufikirie humo ili tutimize katika nafsi zetu maandalizi ya kupokea rehema za siku hii. Siku hii sio mahala pa dua na nyuradi za dhahiri tu, siku hii sio ya kukariri maneno ya kufungua milango ya pepo! Hakika ni siku ya kung’oa miba iliyojikita katika moyo, kiburi, husuda, chuki, uadui, ugumu, miiba inayozuia mmea wa kheri kuota. Hakika ni siku ya kupanda miche ya kheri ambayo inazalisha kukubaliwa, kujikurubisha na ridhaa. Unyenyekevu, uchamungu, kulia, huruma ni maneno ambayo ni wajibu yawe katika daraja la kwanza kwetu. Hakika kutoka kwetu Arafah kwa maneno haya tutakuwa tumeshaweka nyayo zetu katika njia ya peponi, na tumeshazalisha utajo huu ambao tunataabisha miili yetu, vinginevyo utakuwa ni utajo usio na maana, hautozalisha maua bali – Mungu aepushie mbali – utaotesha miba!!

13

02_15_Safari ya kuelekea_3_Feb_2015.indd 13

2/3/2015 1:36:31 PM


SAFARI YA KUELEKEA KWA MWENYEZI MUNGU

Hakika siku hii ndio inayofaa sana kuwa ni kituo cha kusimama ili mtu achukue humo utulivu madhubuti, ang’oe humo ada mbaya na achume ada nzuri.

14

02_15_Safari ya kuelekea_3_Feb_2015.indd 14

2/3/2015 1:36:31 PM


SAFARI YA KUELEKEA KWA MWENYEZI MUNGU

KIINI CHA MANENO 1.

Faida za Hija:

Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu 5: “Ewe Ali mambo matatu thawabu zake ni katika dunia na Akhera: Hija inaondoa ufakiri, sadaka inazuia balaa na kuunga udugu kunaongeza umri.” “ Mwenye kutaka dunia na Akhera basi akusudie nyumba hii, hajaiendea mja na akaomba dunia isipokuwa atapewa kwayo au akaomba Akhera ila atapewa kwayo. Enyi watu ni juu yenu kuhiji na kufanya Umra, basi zifatanisheni, hakika zinasafisha dhambi kama yanavyosafisha maji uchafu na zinaondoa ufakiri kama unavyoondoa moto uchafu wa chuma.” Amesema Imamu as-Sadiq A: “Hija na Umra ni masoko mawili kati ya masoko ya Akhera.” Na kutoka kwa Imamu Sajad A: “Nendeni Hija na fanyeni Umra mtapata afya ya miili yenu na zitapanuka riziki zenu na mtatosheleza mahitaji ya familia zenu.” Na kutoka kwake A: “Haji ni mwenye kusamehewa, ni mwenye kuwajibishiwa pepo, ni mwenye kurudifiwa amali na ni mwenye kuhifadhiwa ahali yake na mali yake.”

15

02_15_Safari ya kuelekea_3_Feb_2015.indd 15

2/3/2015 1:36:31 PM


SAFARI YA KUELEKEA KWA MWENYEZI MUNGU

2.

Ihramu: Kutoka kwa Imamu as-Sadiq A amesema: “ Unapohirimia ni juu yako kumcha Mungu, kumtaja Mwenyezi Mungu, kupunguza maneno isipokuwa kwa kheri, hakika katika ukamilifu wa Hija na Umra ni mtu kuhifadhi ulimi wake isipokuwa katika kheri.”

3.

Kuiangalia Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu “ Mnapohiji basi kithirisheni kuiangalia nyumba ya Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu ana huruma 124 katika nyumba yake tukufu, miongoni mwayo 60 ni kwa ajili ya wenye kufanya tawafu, na 40 ni kwa ajili ya wenye kuswali, na 20 ni kwa ajili ya wenye kuiangalia.” “Mwenye kuiangalia Kaaba hatoacha kuwa ni mwenye kuandikiwa mema na kusamehewa maovu hadi atakapoacha kuiangalia.” “Kuiangalia Kaaba kwa kuipenda kunateketeza kabisa maovu.”

4.

Kuungama Dhambi: “ Ungameni katika Nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu yale mliyoyahifadhi katika madhambi na ambayo hamjayahifadhi na semeni: ‘Uliyoyahifadhi ewe Mola dhidi yetu nasi tumeyasahau tunaomba utusamehe.” “ Hakika mwenye kukiri madhambi yake katika sehemu hiyo na akazihesabu na kuzitaja na akamtaka Mwenyezi Mungu msamaha, ni haki ya Mwenyezi Mungu kumsamehe.”

5.

Kusimama Arafah: utoka kwa Nabii 5: “Katika madhambi kuna madhambi K yasiyosamehewa ila katika Arafah.” 16

02_15_Safari ya kuelekea_3_Feb_2015.indd 16

2/3/2015 1:36:31 PM


SAFARI YA KUELEKEA KWA MWENYEZI MUNGU

Kutoka kwa Nabii 5: “Inapofika jioni ya siku ya Arafah Mwenyezi Mungu Mtukufu anawaambia malaika: Tazameni waja wangu na vijakazi wangu wamechakaa wana vumbi, wamenijia toka sehemu za mbali, hawajaona rehema Zangu wala adhabu Yangu, na kuweni mashahidi malaika Wangu kwamba hakika Mimi nimemsamehe aliyehiji na asiyehiji, haitaonekana siku yenye kukombolewa watu kwa wingi dhidi ya moto kama siku ya Arafah na usiku wake.” Na kutoka kwa Ridhaa A amesema: “Abu Ja’far A alikuwa anasema: ‘Hakuna mwema wala muovu anayesimama katika vilima vya Arafa na kumuomba Mwenyezi Mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu anamkubalia.” 6.

Kutupa Vijimawe: Mmoja wao alimuuliza Imamu Musa bin Ja’far A: Anasema: “ Nilimuuliza: Kuhusu kutupa vijimawe kwa nini imewekwa sharia hiyo? Akasema: “Hakika Ibilisi aliyelaaniwa, alikuwa anajidhihirisha kwa Ibrahimu A katika sehemu hiyo ya kutupa vijimawe basi Ibrahim A akampiga mawe, basi hilo likawa ni sunnah.” Na kutoka kwa as-Sadiq A: “Na utupilie mbali uovu na ubaya katika kutupa kwako mawe.”

17

02_15_Safari ya kuelekea_3_Feb_2015.indd 17

2/3/2015 1:36:31 PM


SAFARI YA KUELEKEA KWA MWENYEZI MUNGU

MAOMBI

K

utoka kwa Asmaiy: Nilikuwa natufu Kaaba usiku, nikamuona kijana mzuri wa tabia amejitanda nguo mbili ameng’ang’ania pazia la Kaaba na anasema: “ Macho yamelala, na nyota zimeangaza na wewe ni Mfalme uliyehai msimamizi, wafalme wamefunga milango yao na wameweka walinzi wao lakini mlango wako uko wazi kwa wenye kuomba, nimekujia ili uniangalie kwa huruma yako ewe mwenye huruma mno kuliko wenye kuhurumia.” Kisha akaanza kusema: “Ewe Mwenye kujibu dua ya Mwenye shida katika giza, Ewe Mwenye kuondoa madhara na balaa pamoja na maradhi, wameshalala wajumbe wako wote kando ya nyumba, Na Wewe peke Yako ewe Msimamizi hujalala, Nakuomba ewe Mola dua ambayo ulishaamuru, Hurumia kilio changu kwa haki ya Nyumba na utukufu, Ikiwa msamaha Wako hawautarajii wenye madhambi, Ni nani atawakirimu waasi wa neema.” Akasema: “Nikaangalia nikakuta ni Zainul-Abidin A.’” Kutoka kwa Tawusi al-Yamaniy amesema: Niliona katika usiku wa manane mtu ameng’ang’ania pazia la Kaaba naye anasema: “ Ewe Mwenye kutarajiwa katika kila haja, nimeshitakia Kwako madhara basi sikiliza malalamiko yangu, Ewe tegemeo langu, wewe ndio utakayeondoa tatizo langu, Nisamehe dhambi zangu zote na nikidhie haja zangu, Akiba yangu ni chache sioni kama itanifikisha. 18

02_15_Safari ya kuelekea_3_Feb_2015.indd 18

2/3/2015 1:36:31 PM


SAFARI YA KUELEKEA KWA MWENYEZI MUNGU

Je, nilie kwa akiba yangu au kwa urefu wa masafa yangu. Nimekuja kwa amali zangu mbaya na mbovu. Hakuna katika ardhi mja aliyefanya dhambi kama dhambi zangu, Je, utanichoma kwa moto ewe kilele cha matarajio? Yako wapi matumaini yangu kisha iko wapi hofu yangu?� Akasema: Nikaangalia nikakuta ni Ali bin al-Husain A.

19

02_15_Safari ya kuelekea_3_Feb_2015.indd 19

2/3/2015 1:36:31 PM


SAFARI YA KUELEKEA KWA MWENYEZI MUNGU

HITIMISHO Mambo matatu: Atanufaika nini ambaye anakusudia Nyumba hii ikiwa hana mambo matatu: Uchamungu unaomzuia na maasi ya Mwenyezi Mungu, upole ambao kwao anadhibiti hasira yake, na usuhuba mzuri kwa anayesuhubiana naye. Mazuri zaidi ambayo tunaweza kutoka nayo katika msimu wa Hija:

• • •

Uchamungu katika aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu Kudhibiti hisia Muamala mzuri pamoja na watu.

Na mwisho wa ulingano wetu, shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola mlezi wa viumbe, na rehema na amani zimshukie Muhammad na kizazi chake kitwaharifu.

20

02_15_Safari ya kuelekea_3_Feb_2015.indd 20

2/3/2015 1:36:31 PM


SAFARI YA KUELEKEA KWA MWENYEZI MUNGU

ORODHA YA VITABU VILIVYO ­CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1. Qur’an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thelathini 2. Uharamisho wa Riba 3. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza 4. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili 5. Hekaya za Bahlul 6. Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) 7. Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) 8. Hijab vazi Bora 9. Ukweli wa Shia Ithnaashari 10. Madhambi Makuu 11. Mbingu imenikirimu 12. Abdallah Ibn Saba 13. Khadijatul Kubra 14. Utumwa 15. Umakini katika Swala 16. Misingi ya Maarifa 17. Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia 18. Bilal wa Afrika 19. Abudharr 20. Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu 21. Salman Farsi 22. Ammar Yasir 23. Qur’an na Hadithi 24. Elimu ya Nafsi 25. Yajue Madhehebu ya Shia 26. Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur’an Tukufu 27. Al-Wahda 28. Ponyo kutoka katika Qur’an 29. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii 30. Mashukio ya Akhera 31. Al Amali 32. Dua Indal Ahlul Bayt 33. Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. 34. Haki za wanawake katika Uislamu 35. Mwenyezi Mungu na sifa zake 36. Kumswalia Mtume (s) 37. Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) 38. Adhana 39 Upendo katika Ukristo na Uislamu 40. Tiba ya Maradhi ya Kimaadili 41. Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu 42. Kupaka juu ya khofu 43. Kukusanya swala mbili 44. Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara 45. Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya 46. Kusujudu juu ya udongo 47. Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) 48. Tarawehe 49. Malumbano baina ya Sunni na Shia 50. Kupunguza Swala safarini 51. Kufungua safarini 52. Umaasumu wa Manabii 53. Qur’an inatoa changamoto 54. as-Salaatu Khayrun Mina -’n Nawm 55. Uadilifu wa Masahaba 56. Dua e Kumayl 57. Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu

21

02_15_Safari ya kuelekea_3_Feb_2015.indd 21

2/3/2015 1:36:31 PM


SAFARI YA KUELEKEA KWA MWENYEZI MUNGU

58. Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake 59. Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata 60. Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mtume Muhammad (s) 61. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza 62. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili 63. Kuzuru Makaburi 64. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza 65. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili 66. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu 67. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne 68. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano 69. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita 70. Tujifunze Misingi Ya Dini 71. Sala ni Nguzo ya Dini 72. Mikesha Ya Peshawar 73. Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu 74. Ubora wa Imam ‘Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliyonyooka 75. Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake 76. Liqaa-u-llaah 77. Muhammad (s) Mtume wa Allah 78. Amani na Jihadi Katika Uislamu 79. Uislamu Ulienea Vipi? 80. Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) 81. Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) 82. Urejeo (al-Raja’a ) 83. Mazingira 84. Utokezo (al - Badau) 85. Hukumu ya kujenga juu ya makaburi 86. Swala ya maiti na kumlilia maiti 87. Uislamu na Uwingi wa Dini 88. Mtoto mwema 89. Adabu za Sokoni 90. Johari za hekima kwa vijana 91. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza 92. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili 93. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu 94. Tawasali 95. Imam Mahdi katika Usunni na Ushia 96. Hukumu za Mgonjwa 97. Sadaka yenye kuendelea 98. Msahafu wa Imam Ali 99. Ngano ya kwamba Qur’ani imebadilishwa 100. Idi Al-Ghadir 101. Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu 102 Hukumu zinazomhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi 103. Huduma ya Afya katika Uislamu 104. Sunan an-Nabii 105. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) 106. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) 107. Shahiid Mfiadini 108. Kumsalia Nabii (s.a.w) 109. Ujumbe -Sehemu ya Kwanza 110. Ujumbe - Sehemu ya Pili 111. Ujumbe - Sehemu ya Tatu 112. Ujumbe - Sehemu ya Nne 113. Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu 114. Hadithi ya Thaqalain 115. Ndoa ya Mutaa 116. Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza 117. Ukweli uliopotea sehemu ya Pili 118. Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu 119. Ukweli uliopotea sehemu ya Nne

22

02_15_Safari ya kuelekea_3_Feb_2015.indd 22

2/3/2015 1:36:31 PM


SAFARI YA KUELEKEA KWA MWENYEZI MUNGU

120. Ukweli uliopotea sehemu ya Tano 121. Mkutano wa Maulamaa wa Baghdad 122. Safari ya kuifuata Nuru 123. Fatima al-Zahra 124. Myahudi wa Kimataifa 125. Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi 126. Visa vya kweli sehemu ya Kwanza 127. Visa vya kweli sehemu ya Pili 128. Elimu ya Ghaibu ya Maimamu 129. Mwanadamu na Mustakabali wake 130. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) 131. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) 132. Khairul Bariyyah 133. Uislamu na mafunzo ya kimalezi 134. Vijana ni Hazina ya Uislamu 135. Yafaayo kijamii 136. Tabaruku 137. Taqiyya 138. Vikao vya furaha 139. Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 140. Visa vya wachamungu 141. Falsafa ya Dini 142. Azadari-Kuhuzunika na Kuomboleza 143. Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah 144. Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu 145. Kuonekana kwa Allah 146. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) 147. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) 148. Ndugu na Jirani 149. Ushia ndani ya Usunni 150. Maswali na Majibu 151. Mafunzo ya hukmu za ibada 152. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1 153 Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2 154. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 155. Abu Huraira 156. Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. 157. Mazingatio kutoka katika Qur’an - Sehemu ya Kwanza 158. Mazingatio kutoka kaitka Qur’an - Sehemu ya Pili 159. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza 160. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili 161. Qur’ani Tukufu – Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili 162. Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) 163. Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani 164. Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu 165. Uislamu Safi 166. Majlisi za Imam Husein Majumbani 167. Je, Kufunga Mikono 168. Uislam wa Shia 169. Amali za Makka 170. Amali za Madina 171. Asili ya Madhehebu katika Uislamu 172. Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi 173. Ukweli uliofichika katika neno la Allah 174. Uislamu na Mifumo ya Uchumi 175. Umoja wa Kiislamu na Furaha 176. Mas’ala ya Kifiqhi 177. Jifunze kusoma Qur’ani 178. As-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah 179. Hayya ‘Alaa Khayri’l-’Amal Katika Adhana 180. Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura 181. Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na R ­ amadhani)

23

02_15_Safari ya kuelekea_3_Feb_2015.indd 23

2/3/2015 1:36:31 PM


SAFARI YA KUELEKEA KWA MWENYEZI MUNGU

182. Uadilifu katika Uislamu 183. Mahdi katika Sunna 184. Maswali Ya Uchunguzi Kuhusu Uislam 185. Kazi na Bidii ni njia ya maendeleo 186. Abu Talib – Jabali Imara la Imani 187. Ujenzi na Utakaso wa Nafsi 188. Vijana na Matarajio ya Baadaye 189. Usalafi – Historia yake, maana yake na lengo lake 190. Ushia – Hoja na Majibu 191. Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) 192. Maombolezo – Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) 193. Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu 194. Takwa 195. Upotoshaji dhahiri katika Turathi (Hazina) ya Kiislamu 196. Amirul Muuminina (‘as) na Makhalifa 197. Uongozi na Utawala katika Mwenendo wa Imam ‘Ali (‘a) 198. Kuvunja hoja iliyotumika kutetea Uimamu wa AbuBakr 199. Adabu za vikao na mazungumzo 200. Hija ya Kuaga 201. Uwazi baina ya Maslahi na Vikwazo 202. Fadhila za watukufu watano katika Sahih Sita 203. Mdahalo baina ya Mwanachuoni wa Kisunni na Mwanachuoni wa Kishia (Al-Muraja’aat) 204. Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (as) 205. Mjadala wa Kiitikadi 206. Mtazamo kuhusu msuguano wa Kimadhehebu 207. Nchi na Uraia – Haki na wajibu kwa Taifa 208. Mtazamo wa Ibn Taymiyyah juu ya Imam Ali (as) 209. Uongozi wa Kidini – Maelekezo na Utekelezaji wa Kijamii 210. Maadili ya Ashura 211. Mshumaa – Shahidi na Kifo cha Kishahidi 212. Mizani ya Hekima – Hadithi za Ahlul Bait (as) – Sehemu ya Kwanza 213. Imam Ali na Mambo ya Umma 214. Imam Ali na Mfumo wa Usawa 215. Mwanamke na Sharia 216. Mfumo wa Wilaya 217. Vipi Tutaishinda Hofu? 218. Kumswalia Mtume ni Ufunguo wa Utatuzi wa Matatizo 219. Mahali na Mali za Umma 220. Nahjul-Balagha – Majmua ya Khutba, Amri, Barua, Risala, Mawaidha na Semi za Amirul-Muuminin Ali bin Abu Talib (a.s.) 221. Mukhtar – Shujaa aliyelipiza kisasi dhidi ya wauaji wa Imam Husein (as) hapo Karbala 222. Uimamu na Tamko la Kutawazwa 223. Imam Husain ni Mfumo wa Marekebisho na Mageuzi 224. Saada Kamili – Kitabu cha Kiada cha Maadili 225. Maeneo ya Umma na Mali Zake 226. Imam Hasan na Mfumo wa Kujenga Jamii 227. Adhana ni Ndoto au ni Wahyi? 228. Maimamu wa Ahlul Bait – Ujumbe na Jihadi KOPI NNE ZIFUATAZO ZIMETAFSIRIWA KWA LUGHA KINYARWANDA 1. 2. 3. 4.

Amateka Na Aba’Khalifa Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya Shiya na Hadithi.

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION KWA LUGHA YA KIFARANSA 1.

Livre Islamique

24

02_15_Safari ya kuelekea_3_Feb_2015.indd 24

2/3/2015 1:36:31 PM


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.