Shia asema haya,sunni asema haya, wewe wasemaje

Page 1

Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje?

Kimeandikwa na: Muhammad ar-Radhii ar-Radhawi

Kimetarjumiwa na: Hemedi Lubumba Selemani

7/15/2011

12:02 PM

Page A


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

B

7/15/2011

12:03 PM

Page B


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

Š Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 - 512 - 14 - 0 Kimeandikwa na: Muhammad Ar-Radhii Ar-Radhawi Kimetarjumiwa na: Hemedi Lubumba Selemani Kimehaririwa na: Abdallah Mohammed Kupangwa katika Kompyuta na: Ukhti Pili Rajab. Toleo la kwanza: Januari, 2011 Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info

7/15/2011

12:03 PM

Page C


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

YALIYOMO Shia Asema: Ni lazima waislamu wote kuwatii na kuwatawalisha maimamu..........................................................................4 Sunni Asema: Kauli ya Mwenyezi Mungu “Enyi mlioamini mtii Mwenyezi Mungu na Mtiini Mtume na wenye mamlaka katika nyinyi “wenye mamlaka ni Watawala na Wanachuoni”....................................................................6

Shia Asema: Hakika kumuweka Imam ni wajibu kutokana na uharibifu mkubwa.....................................................8 Sunni Asema: Kwetu sisi wafuasi wa madhehebu manne Imam wa haki baada ya Mtume wa Mwenyeezi Mungu (s.a.w.w) ni ............................................................20 Shia Asema:

Hakika Imam w ahaki baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.a.w.w).................................20

Sunni Asema: Sisi wafuasi wa madhehebu manne tunaamini kuwa Abu Bakr bin Quhafa ni Khalifa..........................24 Sunni Asema: Waislamu wote wamekubaliana juu ya Ukhalifa wa Abu Bakr na Uimamu wake..................................35 Shia Asema:

Hayajatimia makubaliano juu ya Ukhalifa wa Abu Bakr.......................................................................35

Sunni Asema: Amesema (s.a.w.w) aakayekufa ilihali shingoni mwake hana kiapo cha utii basi amekufa kifo cha kijahiliya...............................................................39 Shia Asema:

Hadithi hii ni dalili juu ya ubatilifu wa ukhalifa wa Abu Bakr bin Abu Quhafa....................................39

12:03 PM

Page D


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

Shia Asema:

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Ni sharti kwa Imam na Khalifa anayekaimu nafasi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu...........................42

Sunni Asema: Si sharti Imam na khalifa kuwa mtakasifu wala kutokana na kizazi cha Ali.....................................43 Sunni Asema: Bila shaka kiongozi wa wasema kweli na Rais wao ni Abu Bakr............................................................43 Sunni Asema: Kwa uhakika kabisa aliye mbora kuliko viumbe wote wa Mwenyezi Mungu baada ya Mtume .......45 Shia Asema:

|Kwa uhakika kabisa aliye mbora kuliko viumbe wote wa Mwenyezi Mungu baada ya mbora wa Manabii na Mitume (s.a.w.w) ni Imam kiongozi wa waumini ni Ali bin Abi Talib a.s...........................45

Sunni Asema: Masahaba walikuwa na adaub nzuri kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu.................................................48 Shia Asema:

Tunatamani As-Subki angetutajia angalau Hadith Moja..................................................................... 48

Sunni Asema: SisiSunni tunawaheshimu sahaba wote................59 Shia Asema:

Sisi Shia Imamiyya tunaamini Uimamu wa maimamu kumi na wawili.................................................61

Sunni Asema: Sahaba wote ni watu wa Peponi bila shaka yoyote72 Shia Asema: Si sahaba wote ni watu wa Peponi bila shaka.........72 Sunni Asema: Sisi Sunni wafuasi wa madhehebu manne...............73 Shia Asema: Sisi shia wafuasi wa Maimamu kumi na wawili.....73 Shia Asema: Uimamu na Ukhalifa Hauwi kwa mtu asiyekuwa

12:03 PM

Page E


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Mkuraishi................................................................76 Sunni Asema: Haina maana yoyote Ukhalifa kuwa Muhtasari kwa Makuraishi.............................................................76 Sunni Asema: Madheheu ya Kiislamu manne...............................77 Shia Asema:

Madhehebu yote manne ya Kisunni yalizuka........77

Sunni Asema: Sisi wafuasi wa madhehebu manne ndio wafuasi wa Sunna.....................................................................83 Shia Asema:

Sisi Shia Imamiyya wafuasi wa Maimamu kumi na wawili ndio wafuasi wa kweli...............................83

Sunni Asema: Baadhi ya wanachuoni wa sheria wameona ni lazima kuacha baadhi ya Sunna...................................85 Shia Asema:

Sisi tunaheshimu Sunna za Mtukufu Mtume (s.a.w.w)................................................................85

Sunni Asema: Mtume wa Mwenyezi Mungu anasema “ Uma wangu utagawika makundi sabini na tatu.............86 Shia Asema:

Sisi shia imamiyya wafuasi wa maimamu kumi na wawili ndio kundi lililookoka kati ya makundi haya.......................................................................86

Shia Asema:

Ndoa ya Mut’a yaani ndoa ya muda ni halali........ 89

Sunni Asema: Ndoa ya muda ni haramu kwetu............................89 Shia Asema:

Ni wajibu kwetu kuficha imani.............................94

12:03 PM

Page F


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

Sunni Asema:

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Ufichaji huo si chochote bali ni kuficha haki na kudhihirisha batili...............................................95

Shia Asema:

Swala ya Tarawehe ambayo Sunni huisali ndani ya Ramadhani............................................................96

Sunni Asema: Sisi Suni tunaswali swala ya Tarawehe.................96 Shia Asema:

Sisi Shia Imamiyya tunapaka juu ya nyayo zetu....97

Sunni Asema: Sisi tunaosha nyayo zetu wakati wa kutawadha....98 Sunni Asema: Katika kuosha mkono miwili ndani ya Udhuu.........98 Shia Asema: Sisi katika kuosha mikono ndani ya Udhuu.............98 Sunni Asema: Wake wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w) ni miongoni mwa watu wa nyumba yake .................................103 Shia Asema: Wake wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w) si miongoni mwa watu wa nyumba yake..................................103

12:03 PM

Page G


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Neno la Mchapishaji Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kiitwacho, ash-Shi’iyyu Yaquul, Wa ‘s-Sunniyyu Yaquul, Wa Anta MaaTaquul? kilichoandikwa na Sayyid Muhammad al-Radhii ar-Radhawi. Sisi tumekiita, Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Ewe msomaji mpendwa! Ndani ya kitabu hiki utasoma kauli mbalimbali zitakazokuelezea kuhusu imani za makundi mawili, kila moja kati ya hayo mawili likijinasibu kwenye Uislamu, huku likiona kuwa lenyewe pekee ndilo lililo kwenye haki na jingine liko kwenye upotofu. La kwanza ni: Shia[Imamia] Ithnaasharia, wafuasi wa madhehebu ya watu wa Nyumba ya Mtume (Ahlul Bait) wa Mwenyezi Mungu SAW (Sallallaahu ‘Alayhi Wa-aalih – rehema na baraka za Allah ziwe kwake na kwa Aali zake) na kizazi chake ambao ni Maimamu Watakatifu AS (‘Alayhimus Salaam - amani iwe juu yako). La pili ni: Sunni, wafuasi wa madhehebu nne zilizozuka baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu SAW, zilizojitenga na madhehebu ya kizazi chake na watu wa nyumba yake ambao ni Maimamu Watakatifu AS. Jambo ambalo Uislamu unakuwajibisha ikiwa kweli wewe ni Mwislamu, na akili inakulazimisha ikiwa kweli unatafiti na kutafakari, ni kuzamisha fikira zako ndani ya kile anachosema Shia, kile kinachokueleza kuhusu imani yake, na ndani ya kile anachosema Sunni, kile kinachokueleza kuhusu imani yake.

i

12:03 PM

Page i


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Kisha ufuate kile kinachokubaliana na akili yako, ambacho dini yako inakiwajibisha juu yako toka kwenye madhehebu hizi mwili zenye kuhitalifiana, na ndicho ukihukumu kuwa ndio haki, na kile kilichokhalifu ukihukumu kuwa ndio upotofu. Mwenyezi Mungu anasema: “…Tena ni nini baada ya haki isipokuwa upotevu? Basi mnageuzwa wapi.” (Yunus, 12:32) Na tena Mwenyezi Mungu anasema: “… Kundi moja litakuwa Peponi na kundi litakuwa Motoni.” (ash-Shuuraa, 42:7) Halahala jihadhari usiwe miongoni mwa wale ambao Mwenyezi Mungu amewaelezea kwa kusema: ”… Bali wanasema: ‘Hakika sisi tuliwakuta baba zetu juu ya desturi hii na tunafuata nyayo zao.’” (az-Zukhruf, 43:22) Tunamshukuru ndugu yetu, Hemedi Lubumba Selemani kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation S. L. P. 19701 Dar-es-Salaam, Tanzania.

ii

12:03 PM

Page ii


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

1

7/15/2011

12:03 PM

Page 1


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje?

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu. Mwenyezi Mungu asema:

“Basi wabashirie waja wangu ambao husikiliza kauli kisha wakafuata zilizo nzuri zaidi. Hao ndio aliowaongoza Mwenyezi Mungu, na hao ndio wenye akili. Sura Az-Zumar 39:18. Ewe msomaji mpendwa! Ndani ya kitabu hiki utasoma kauli mbalimbali zitakazokueleza kuhusu imani za makundi mawili, kila moja kati ya hayo mawili likijinasibu kwenye Uislam, huku likiona kuwa lenyewe pekee ndilo lililo kwenye haki, na jingine liko kwenye upotovu. La kwanza ni: Shia Imamiyya Ith’naashariyya, wafuasi wa madhehebu ya watu wa nyumba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na kizazi chake, ambao ni Maimamu watakasifu (a.s.). La pili ni: Sunni, wafuasi wa madhehebu manne yaliyozuka baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), yalilojitenga na madhehebu ya kizazi chake na watu wa nyumba yake, Maimamu watakasifu (a.s.). Jambo ambalo Uislam unakuwajibisha ikiwa kweli wewe ni mwisilamu, na akili inakulazimisha ikiwa kweli una sehemu fulani ya akili, ni kuzamisha 2

12:03 PM

Page 2


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? fikira zako ndani ya kile anachosema Shia, kile kinachokueleza kuhusu imani yake, na ndani ya kile anachosema Sunni, kile kinachokueleza kuhusu imani yake. Kisha ufuate kile kinachoungwa mkono na akili yako, ambacho dini yako inakiwajibisha juu yako toka kwenye madhehebu haya mawili yenye kupingana, na ndicho ukihukumu kuwa ndio haki, na kile kilichokhalifu ukihukumu kuwa ndio upotovu. Mwenyezi Mungu anasema:

“Tena ni nini baada ya haki isipokuwa upotovu? Basi mnageuzwa wapi.” Yunus: 32. Na tena Mwenyezi Mungu anasema:

“Kundi moja litakuwa Peponi na kundi litakuwa Motoni.”Shuraa: 7. Hala hala jihadhari usiwe miongoni mwa wale ambao Mwenyezi Mungu amewaelezea kwa kusema:

“Bali wanasema: Hakika sisi tuliwakuta baba zetu juu ya desturi hii na tunafuata nyayo zao.”Az-Zukhruf: 22. Hivyo ukaja kuwa miongoni mwa watu wa Motoni. Namuomba Mwenyezi Mungu akukinge na moto huo. Sayyid Muhammad Ar-Radhii Ar-Radhawi Mwandishi wa kitabu ‘Kwa nini sisi ni Shia?’ 3

12:03 PM

Page 3


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje?

Shia Asema: Ni lazima kwa waislamu wote kuwatii na kuwatawalisha Maimamu watakasifu wa nyumba ya Mtume (a.s.) na kuchukua kauli zao na kuwafuata, hilo ni kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume na wenye mamlaka katika nyinyi.”An-Nisai: 59. Na makusudio ya wenye mamlaka hapa ni Maimamu watakasifu wa nyumba ya Mtume, namaanisha Maimamu kumi na wawili (a.s.). Wa kwanza wao ni Imam kiongozi wa waumini Ali bin Abi Talib (a.s.) na wa mwisho wao ni Imam Al-Mahdi mwana wa Imam Al-Hasan Al-Askari (a.s.). Hawa ndio makhalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kwa mujibu wa kauli yake (s.a.w.w.): “Hakika makhalifa wangu na mawasii wangu na hoja wa Mwenyezi Mungu juu ya viumbe baada yangu ni kumi na wawili. Wa kwanza wao ni ndugu yangu na wa mwisho wao ni mwanangu. Akaulizwa: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni nani ndugu yako?” Akajibu: “Ali bin Abi Talib.” Akaulizwa: “Na ni nani mwanao?” Akasema: “Al-Mahdi ambaye ataijaza dunia usawa na uadilifu kama ilivyojaa ujeuri na dhulma…”. Chanzo: Faraidu As-Samtwayni: Juz. 2, Uk. 312. Hivyo wale ambao Mtukufu Mtume(s.a.w.w.) alitoa tamko kuhusu ukhalifa wao baada yake ndio waliokusudiwa kwenye “Wenye mamlaka” ndani ya Aya tukufu, na hivyo kuwatii na kuwatawalisha ni lazima kwa waisla4

12:03 PM

Page 4


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? mu wote. Hili ni la kwanza. Pili: Yule ambaye ni lazima kumtii, na utawala wake juu ya waislamu unasihi, na anafaa kuwa khalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na kaimu wake, ni lazima awe na sifa zilezile alizonazo Mtume (s.a.w.w.), ambazo mwisilamu mwingine yeyote hashiriki naye. Na iliyo muhimu sana miongoni mwa sifa hizo ni utakaso dhidi ya madhambi, na utohara dhidi ya kila dhambi na dosari. Na kwakuwa Mtukufu Mtumewetu (s.a.w.w.) alikuwa ni mtakasifu dhidi ya madhambi yote makubwa na madogo, na mtoharifu dhidi ya uchafu, basi ni lazima yule anayekaimu nafasi yake na kuchukua jukumu lake awe kama yeye. Na kwa kuwa Maimamu wetu (a.s.) wao ndio watu wa nyumba toharifu ya Mtume (s.a.w.w.), na wao ndio waliyoteremshiwa Aya tukufu

“Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu watu wa nyumba, na kukuutakaseni kabisa,� -Al-Ahzab: 33. Na Mtukufu Mtume(s.a.w.w.) akatoa tamko juu ya ukhalifa wao baada yake, basi hilo limethibitisha kuwa wao wana sifa ya utakaso na utohara dhidi ya uchafu na hivyo wakastahiki ukhalifa baada yake. Tatu: Maimamu wetu ndio watu wa karibu mno kwa Mtukufu Mtumewa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), hivyo wao ndio wajuao mno dini yake kuliko watu wengine, na wajuzi mno wa Sunna yake kuliko watu wa pembeni na wa nje (Na watu wa nyumbani ndio wajuao zaidi ya nyumbani) hivyo wao (a.s.) wakawa wanafaa zaidi kukaimu nafasi yake ya uongozi wa umma, na wala si wengine.

5

12:03 PM

Page 5


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Na Sunni Asema: Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Enyi mlioamini mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume na wenye mamlaka katika nyinyi.” Makusudio ya “wenye mamlaka” ni watawala na Wanachuoni1. Hayo yamesemwa na Sheikh Jamil Sadiq Az-Zahawi Al-Baghdad2 Wewe wasemaje?

Sunni Asema: Hakika Mtume (s.a.w.w.) hakuusia. Hilo limesemwa na imam At-Tirmidhi ndani ya kitabu As-Sunan, nacho ni moja ya Sahih zetu sita3 Na Hujatul-Islam imam Abu Hamid Al-Ghazali amesema: “Asilan hakuna tamko la Mtukufu Mtumewa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) juu ya Imam yeyote, kwani laiti yangekuwepo basi ni lazima yangedhihirika kuliko lile la kumpa mtu utawala na uongozi wa jeshi, ikiwa hilo hakulificha itakuwaje hili alifiche. Na kama lilidhihirika basi ilikuwaje likatoweka mpaka lisinukuliwe kwetu? Ama kitendo cha kukadiria kuwepo tamko juu ya mwingine (asiyekuwa Abu Bakr) ni kuwanasibisha sahaba wote na kitendo cha kumpinga Mtume wa Mwenyezi Mungu4 na ni kuondoa Ijimai,5 na hakuna yeyote mwenye ujasiri wa kuzusha kitendo hicho isipokuwa 1.Watawala ni madhalimu, mafasiki na waovu, hivyo haiwezekani Mwenyezi Mungu aamuru tuwatii wao, na tumtii mtu asiye mtakatifu, kwani wanavyuoni na watawala hukosea. (Utii unaokanushwa hapa ni ule utii wa ngazi ya mwisho baada ya Mtume. Hivyo hakanushi utii mfano wa ule wa mwana kwa mzazi au mwanafunzi kwa mwalimu, au mfano wa huo - Mtarjumi). 2 - Al-Fajru As-Sadiq: uk. 5, chapa ya mwaka 1323. 3 -As-Sunan: Juz 4, uk. 432. 4 -Haya ni maneno yasiyo na hadhi kabisa. 5 Ni Ijimai ipi hiyo ewe mwenye kuwapotosha Waisilamu?

6

12:03 PM

Page 6


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Marawafidhi6……. Na Ustadh Twaha Abdul-Baqi Saruri amesema: “Na ni huyu hapa (Yaani Mtukufu Mtumes.a.w.w.) ghafla anauacha uhubiri wake bila ya kumwacha khalifa atakayekaimu nafasi yake na kutawala mambo ya waislamu, atakayeongoza dini yao na dunia yao, atakayeunganisha malengo yao na atakayetimiza matarajio yao na ndoto zao7.” Na Al-Allamah Sadiq Jamil Az-Zahawi Al-Baghdad amesema: “Hakika kumuweka Imam ni wajibu ili asimamie masilahi ya waislamu, kama vile kulinda mipaka na kuandaa vikosi vya jeshi, kupambana na wahaini, wezi na majambazi, pia kuwakemea wavunjaji wa heshima za Mwenyezi Mungu, na kuondoa mizozo itokeayo baina ya wagomvi, na kulinda masilahi ya watu ya kidini na kidunia. Kwani laiti kama si Imam watu wasingejizuia kutenda dhulma na wala zisingetolewa hukumu zao, wala kutekelezwa adhabu juu yao. Na sahaba wote baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) walimuweka (khalifa) hadi wakafanya kitendo hicho kuwa miongoni mwa wajibu muhimu, na hivyo wakakitanguliza kabla ya kitendo cha kumzika Mtume (s.a.w.w.)…..”8 6 Ihyau ulumud-Din: Juz. 1 Uk. 99 chapa ya Misri 1316. (Jina hili hulitumia maadui wa Shia kuwatusi na kuwakashifu Shia, hivyo msemaji hapa anawakusudia Shia )– Mtarjumi. 7 Abu Ubaydah Bin Al-Jarahi: uk 82. 8 Al-Fajru As-Sadiq: uk 7, chapa ya mwaka 1323 Misri, chapa ya Al-Waidhu. Ar-Radhawi: Ewe Az-Zahawi, ikiwa kitendo cha kumuweka Imam kimefikia umuhimu wa kiwango hiki, na ni kweli hivyo ndivyo kilivyo, hivi kweli inaingia akilini kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu hakujua umuhimu huo ndio maana akakipuuzia, lakini sahaba wakaujua umuhimu wake na hivyo wakakitanguliza kabla ya kumzika Mtukufu Mtume(s.a.w.w.)? Ewe mwenye kuwapotosha waislamu, ni kweli kabisa bado haujamjua Mtukufu Mtume swa Mwenyezi Mungu vilivyo, na hivyo ndio maana umemshusha cheo na kumuweka chini kabisa kuliko sahaba zake.

7

12:03 PM

Page 7


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje?

Na Shia Asema: Hakika kumuweka Imam ni wajibu kutokana na uharibifu mkubwa utokanao na kitendo cha kuacha kumuweka, na uharibifu muhimu ni kule kutofautiana kwa waislamu na kufanyiana uadui wao kwa wao. Na hivyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alihangaikia sana kuwaunganisha pamoja na kuwafanya kitu kimoja, kwa ajili hiyo aliweka udugu kati yao huko Makka na mara nyingine huko Madina. Kitendo hicho kinaonyesha jinsi alivyojali mambo yao na kutengeneza mustakabali wao, na haiwezekani kabisa Mtukufu Mtume(s.a.w.w.) apuuzie wajibu huu wa kidini na kijamii, ambao haupuuzii hata Mkurugenzi wa shirika, au wa jumuiya yoyote ile ya kidini au kisiasa, wa dini yoyote ile au mwenye elimu ya kiwango chochote kile pindi anapotaka kuondoka hata kwa muda mfupi au siku chache. Itawezekanaje Mtume wetu (s.a.w.w.) auache umma wake holela ilihali yeye ndiye mbora wa wenye busara na kinara wa wajuzi, huku akijua fika kuwa ataondoka bila kurejea? Mwenyezi Mungu amemsifia ndani ya Kitabu chake kitukufu kuwa yeye ni rehema ya ujumla: “Na wala hatukukutuma ila uwe rehema kwa viumbe wote.” Na ni rehema mahususi kwa waumini, akasema:

“Bila shaka amekufikieni Mtume kutoka miongoni mwenu, yanamuhuzunisha yanayokutaabisheni, anakuhangaikieni, kwa waumini ni Mpole, Mwenye kurehemu.” Tawba: 128. 8

12:03 PM

Page 8


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Hivyo yule ambaye rehema imewafikia na kuwapata binadamu wote kupitia kwake, kiakili hawezi kuuacha umma wake holela bila ya kuuainishia mtu atakayekaimu nafasi yake baada yake, atakayetengeneza mambo yake na kuboresha mustakabali wa maisha ya umma. Sahaba zake walijue hilo na mpaka walifanye kuwa miongoni mwa wajibu muhimu, na walitangulize kabla ya kumzika, lakini yeye asilijue?! Basi iko wapi hiyo rehema mahususi kwa waumini, ukiachia mbali rehema yake ya ujumla? Tunajikinga kwa Mwenyezi Mungu dhidi ya upofu wa nyoyo

“Kwa hakika macho hayakupofuka, bali nyoyo ambazo zimo vifuani ndizo zinazopofuka.”Al-Haji: 46. Haki ambayo haina shaka yoyote ni kuwa Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alitoa tamko zaidi ya mara moja juu ya khalifa na Imam baada yake. Na alimuainisha kwa jina, naye ni mwana wa ami yake, Ali bin Abi Talib (a.s.), na miongoni mwa matukio mashuhuri ya kitendo hicho cha (s.a.w.w.) ni lile la siku ya bonde la Khum, alipokuwa akirejea kutoka kwenye Hijja yake ya kuaga, akasema huku akiwa ameushika mkono wa mwana wa ami yake Ali (a.s.) na ameuinua juu kuliko kundi kubwa la waislamu: “Yule ambaye mimi ni mtawala wake basi huyu Ali ni mtawala wake. Ewe Mwenyezi Mungu, mpende atakayempenda na mfanyie uadui atakayemfanyia uadui….” Al-Haythami amesema ndani ya kitabu Majmauz-Zawaid, Juzuu ya tisa: “Ameipokea Ahmad, na wapokezi wake ni wapokezi sahihi.” Al-Hakim amesema ndani ya kitabu Al-Mustadrak as-Sahihayni, Juzuu ya tatu: “Hadithi hii ni sahihi kwa mujibu wa sharti za Mashekhe wawili,9 na hawajaitoa kwa urefu wake.” 9 Bukhari na Muslim – Mtarjumi.

9

12:03 PM

Page 9


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Ibnu Hajar amesema: “Yenyewe ni Hadithi sahihi haina shaka yoyote, na imetolewa na At-Tirmidhi, An-Nasai na Ahmad, na njia zake ni nyingi sana. Na tena imepokewa na sahaba kumi na sita, na kwa mujibu wa riwaya ya Ahmad ni kuwa sahaba thelathini waliisikia moja kwa moja kutoka kwa Mtukufu Mtume(s.a.w.w.) na wakaitoa kama ushahidi kwa ajili ya Ali zama za ukhalifa wake pale aliponyang’anywa…….. Ama kauli ya baadhi kuwa: Kifungu “Ewe Mwenyezi Mungu mpende atakayempenda…..” kimeongezwa, kauli hiyo haikubaliki, kwani kifungu hicho kimepokewa kwa njia mbalimbali ambazo nyingi kati ya hizo Ad-Dhahabi amekiri kuwa ni sahihi.”10 Na ndani ya kitabu Ta’rikhul-Islam Ahadul-Khulafair-Rashidina: “Hadithi hii ni sahihi.” At-Turkamani amesema ndani ya kitabu chake Taarifu bimadh’habi-Shia al-Imamiyyah ukurasa wa ishirini na nane: “Hadithi hii ni sahihi, ameipokea imam Ahmad na mwanae Abdullah kwa njia sahihi ndani ya kitabu Al-Musnad. Na Al-Hafidhu na As-Suyutwi wameiweka kwenye Hadithi mutawatiri.”11 Ameipokea Ibnu Abu Hadid Al-Mu’utazil kwenye ufafanuzi wake wa Nahjul-Balagha, uk. 209, chapa ya mwaka 1329 Misri. Ameipokea Ahmad ndani ya Musnad yake, Juz. 1, uk. 84. Na ameipokea Ad-Dhahabi ndani ya Tarikhul-Islam Ahadul-Khulafai Ar-Rashidina, uk. 631. 10 As-Sawaiq Al-Muhriqah, uk. 25 na 28, chapa ya mwaka 1324 Misri, chapa ya Al-Maymaniyyah. Majmauz-Zawaid: Juz 9, uk. 104 na 106, chapa ya pili mwaka 11 An-Naswayihu Al-Kafiyah Liman Yatawala Mu’awiyah, uk. 66. (Na Mutawatiri ni Hadithi ambayo imepokewa na kusimuliwa kwa wingi kiasi ambacho usahihi wa Hadithi hiyo hautiliwi mashaka – Mtarjumi.)

10

12:03 PM

Page 10


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Na ndani ya kitabu “Je, hizi ni Hadithi zetu au zenu?” Nimetaja vyanzo sitini vya Hadithi hii kutoka kwenye vitabu vya kisunni. Pamoja na kuthibiti tamko juu ya Imam (a.s.) kuwa ndio khalifa wa waislamu wote, lakini wenye tamaa walimzuia Imam Ali bin Abi Talib mwana wa ami ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na mkwe wake asikae nafasi ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimuweka kwa amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu, hivyo wakamtenga na kumtupilia mbali na watahesabiwa hesabu nzito kwa kitendo chao hiki

“Na siku dhalimu atajiuma mikono yake, akisema: Laiti ningelishika njia pamoja na Mtume. Ee Ole wangu! Nisingelimfanya fulani kuwa rafiki. Kwa hakika yeye alinipoteza nikaacha mawaidha baada ya kunifikia, na Shetani ndiye anayemtupa mwanadamu.”SuratulFurqan: 27-29 Na maelezo ya tamko la Mtukufu Mtume(s.a.w.w.) juu ya ukhalifa na uimamu wa Imam Ali bin Abi Talib ni mengi mno hayajafichika kwa yule mwenye kufuatilia kwenye vitabu vya Sunna katika maudhui mbalimbali. Na wala hayajatoweka kama alivyodai Abu Hamid Al-Ghazali ash-Shafi’i. Haya hapa leo mbele yetu na yanaweza kuchukuliwa na yeyote kati yetu, na yamethibitishwa na wasimulizi wa Hadithi wa kisunni ndani ya Sahih zao na Masanid zao, na yamenukuliwa kwetu na yataendelea kunukuliwa kwa wale watakaokuja baada yetu ili yawe hoja ya Mwenyezi Mungu yenye nguvu juu ya viumbe Wake mpaka Siku ya Kiyama. 11

12:03 PM

Page 11


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Sehemu kubwa ya maelezo hayo nimeyataja ndani ya kitabu (Je, hizi ni Hadithi zetu au zenu?) na hapa nitamtajia msomaji mpendwa sehemu ya maelezo hayo na kumwezesha kuyafahamu mengine ndani ya kitabu hiki. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwongozaji wa njia ya uongofu. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema huku akiwaambia waislamu: “Enyi watu, hakika Mwenyezi Mungu ni Mtawala wangu na mimi ni mtawala wa waumini, na mimi nina mamlaka kwao zaidi kuliko nafsi zao, basi yule ambaye mimi ni mtawala wake huyu Ali ni mtawala wake. Ewe Mwenyezi Mungu mpende atakayempenda Ali na mfanyie uadui yule atakayemfanyia uadui.” Chanzo: Al-Mu’ujam al-Kabir cha At-Twabarani: Juz 3, uk. 180, chapa ya mwaka 1404, chapa ya pili. Na pia ameipokea At-Twabarani kwa njia yake mpaka kwa Hudhayfa bin Asidu Al-Ghaffar amesema: “Pindi Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alipotoka kwenye Hijja ya kuaga…..alisimama akasema: “Enyi watu, hakika Mpole mtoa habari amenipa habari kuwa hakuna Nabii yeyote aliyepewa umri ila alipewa nusu ya umri wa kabla ya unabii wake, na bila shaka mimi nakaribia kuitwa na kujibu (nakaribia kufariki), na hakika mimi ni mwenye kuulizwa na nyinyi ni wenye kuulizwa, basi nyinyi mtajibu nini?” Wakasema: “Tunashuhudia kuwa wewe umefikisha na umejitahidi na umenasihi, tunamuomba Mwenyezi Mungu akulipe kheri.” Akasema: “Si mnakiri kwa moyo kuwa hapana Mola wa haki isipokuwa Allah, na kuwa Muhammad ni mja Wake na Mtume Wake, na kuwa pepo Yake ni haki na moto Wake ni haki, na kuwa kifo ni haki, na kuwa ufufuo baada ya kifo ni haki, na kuwa Kiyama kijacho hakina shaka, na kuwa Mwenyezi Mungu atawafufua waliyomo makaburini?” 12

12:03 PM

Page 12


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Wakasema: “Ndiyo, ni kweli kabisa tunakiri hivyo.” Akasema: “Ewe Mwenyezi Mungu, shuhudia.” Kisha akasema: “Enyi watu, hakika Mwenyezi Mungu ni Mtawala wangu na mimi ni mtawala wa waumini, na mimi nina mamlaka kwao zaidi kuliko nafsi zao, hivyo yule ambaye mimi ni mtawala wake basi huyu (Ali) ni mtawala wake. Ewe Mwenyezi Mungu mpende atakayempenda Ali na mfanyie uadui yule atakayemfanyia uadui. “Enyi watu, mimi ninawatangulia na nyinyi mtanikuta kwenye Hodhi, Hodhi ambayo upana wake ni kati ya Busra na Swunaau12, ndani yake mna idadi ya nyota zinazokaribia mng’ao wa fedha, na mimi nitawauliza kuhusu vizito viwili13 pindi mtakaponikuta. Basi angalieni ni vipi mtakavyonifuata ndani ya viwili hivyo. “Kizito kikubwa ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu aliyetakasika, nayo ni kamba ambayo ncha yake moja imo mikononi mwa Mwenyezi Mungu, na ncha nyingine imo mikononi mwenu, basi shikamaneni nayo hamtopotea.

12 Busra ni mji huko Sham. Na Sanaa ni eneo la huko Yemen, na ni kijiji cha mwanzo wa Damascus. 13 Az-Zarnadiyyu Al-Hanafiyyu amesema: “Ameviita Vizito Viwili kwa sababu kuvichukua, kuvifanyia kazi na kuvihifadhi ni jambo zito. Na amevifanya vizito kwa sababu kila cha thamani na cha hatari ni kizito, wakiwemo binadamu na majini ambao nao ni vizito viwili, kwa sababu wao wamekuwa bora kuliko wanyama. “Na kila kitu chenye heshima na hadhi ambayo inagombaniwa basi chenyewe ni kizito, na yeye ameviita kwa jina hilo kutukuza hadhi yake. Na baadhi wamefasiri kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo: “Hakika sisi tutakupa kauli nzito” kuwa ni amri za Mwenyezi Mungu, faradhi Zake na makatazo Yake kwa kuwa hayatekelezwi ila kwa kujilazimisha kuliko kuzito. Na inasemekana nzito, yaani ni yenye heshima (Nidham Duraru As-Samtwayni, uk. 232.

13

12:03 PM

Page 13


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? “Na kizazi changu, watu wa nyumba yangu, hakika Mpole mtoa habari amenipa habari kuwa hivyo viwili havitotoweka14 mpaka viniijie kwenye Hodhi.” Na katika riwaya nyingine: “Aliuchukua mkono wa Ali akauinua mpaka nywele za kwapani zikaonekana, kisha akasema: “Enyi watu, hivi mnajua kuwa mimi nina madaraka kwenu zaidi ya nafsi zenu? Basi yule ambaye mimi ni mtawala wake basi Ali ni mtawala wake…..” Chanzo: Usudul-Ghaba fi Ma’rifati As-Sahabah: Juz 1. Na katika riwaya nyingine: “Hivi mnajua kuwa mimi nina madaraka kwa waumini kuliko nafsi zao? Basi yule ambaye mimi ni mtawala wake basi Ali ni mtawala wake. Ewe Mwenyezi Mungu mpende ampendaye…..”. Chanzo: Ta’rikhul-Islam Ahadul-Khulafai Ar-Rashidina. Na katika riwaya nyingine kutoka kwa Aisha binti Saad amesema: “Nilimsikia baba yangu akisema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu siku ya Al-Jahfah, alimshika Ali mkono na kuanza kuhutubia, basi akamuhimidi Mwenyezi Mungu na kumsifu, kisha akasema: “Enyi watu, hakika mimi ni mtawala wenu.” Wakasema: “Umesema kweli ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu.” Kisha akauchukua mkono wa Ali akauinua na kusema: “Huyu ni Walii wangu na atanilipia deni langu, na mimi nampenda mwenye kumpenda na ni adui wa mwenye kumfanyia uadui.” 14 Hivyo ndivyo ilivyo kwenye riwaya ya At-Tabarani ndani ya kitabu AlMuujam Al-Kabir. Ama Hadithi zote za Vizito Viwili nilizoziona mimi zinatamka (Havitoachana) au (Havitofarakana) mpaka vinikute kwenye Hodhi. Na tamko hili ndilo sahihi.

14

12:03 PM

Page 14


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Chanzo: Khasaisu Amirul-Muuminin Ali bin Abi Talib cha An-Nasai, uk. 4, chapa ya mwaka 1348 Misri, chapa ya maendeleo ya kielimu. Na katika Hadithi nyingine: “Hivi mimi si mwenye mamlaka kwa kila aliyeamini kuliko nafsi yake?” Wakasema: “Ndiyo.” Akasema (baada ya kumwita Ali na kumshika mkono wake): Basi hakika huyu ni mtawala wa kila ambaye mimi ni mtawala wake. Ewe Mwenyezi Mungu mpende ampendaye Ali na kuwa adui wa mwenye kumfanyia uadui.” Ndipo Umar bin Al-Khattab akamwendea na kusema: “Hongera ewe Ali, umekuwa mtawala wa kila aliyeamini wa kiume na wa kike.” Na ndani ya kitabu Manaqib Sayyidina Ali cha Al-Ayni, ukurasa wa ishirini, chapa ya India….: “Abu Bakr na Umar waliingia kwa Ali na kumwambia: “Amani iwe juu yako na rehema za Mwenyezi Mungu na baraka zake, ewe Kiongozi wa waumini.” Ar-Radhawi: Ewe Abu Bakr na Umar, kwa nini mlimtangulia kwenye ukhalifa ilihali nyinyi mnajua kwa yakini kuwa yeye ndiye kiongozi wa waumini? Na mtamjibu nini Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama pindi atakapowaulizeni kuhusu hilo? Na Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Fahamuni nawajulisha jambo ambalo ikiwa mtaulizana kuhusu hilo hamtoangamia: Hakika mtawala wenu ni Mwenyezi Mungu, na hakika Imam wenu ni Ali bin Abi Talib, hivyo mpeni nasaha na msadikisheni, kwani hakika Jibril amenipa habari hiyo.” Chanzo: Sharhu Nahjul-Balagha cha Ibnu Abil Hadid. Juz 1, uk. 255, chapa ya mwaka 1329 Misri. Na akasema (s.a.w.w.): “Hakika ndugu yangu, waziri wangu, wasii wangu na mbora ninayemwachia nafasi yangu baada yangu ni Ali bin Abi Talib.” 15

12:03 PM

Page 15


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Chanzo: Manaqibus-Sayyidina Ali cha Al-Ayni, uk. 15, chapa ya Haydaru Abad, mwaka 1352. Na akasema (s.a.w.w.): “Namuusia aliyeniamini na kunisadikisha ashikamane na utawala wa Ali bin Abi Talib, atakayemtawalisha basi kanitawalisha, na atakayenitawalisha bila shaka atakuwa kamtawalisha Mwenyezi Mungu Mtakasifu. Na atakayempenda basi kanipenda na atakayenipenda bila shaka atakuwa amempenda Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na atakayemchukia basi kanichukia na atakayenichukia bila shaka atakuwa kamchukia Mwenyezi Mungu.” Chanzo: Kanzul-Ummal: Juz. 11, uk. 610, chapa ya mwaka 1399 Beirut. Muntakhabu Kanzul-Ummal, uk. 32, kwenye maelezo ya Musnad Ahmad: Juz. 5. Majmauz-Zawaid. Juz 9, uk. 108, chapa ya mwaka 1967 Beirut, chapa ya pili iliyosambazwa na Darul-Kitabi. Kifayatut-Twalib, uk. 32. Na akasema (s.a.w.w.): “Ali bin Abi Talib ni ndugu yangu na anatokana na mimi, na mimi natokana na Ali, yeye ni mlango wa elimu yangu na wasii wangu…..” Chanzo: Yanabiul-Mawaddah, uk. 263, chapa ya mwaka 1302 Istambul. Na akasema (s.a.w.w.): “Kila Nabii ana wasii na mrithi, na hakika Ali ndiye wasii wangu na mrithi wangu.” Chanzo: Dhakhairul-Uquba, uk. 71, chapa ya mwaka 1356 Misri. Al-Imam Jafar As-Sadiq cha Ustadhi Abdul-Halim Al-Jundiyyu, uk. 253, chapa ya mwaka 1397 Misri, chapa ya Darul-Ahrami At-Tijariyyah.

16

12:03 PM

Page 16


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Na akasema (s.a.w.w.): “Wasii wangu, mrithi wangu, atakayenilipia deni langu na kutimiza ahadi zangu ni Ali bin Abi Talib.” Chanzo: Dhakhairul-Uquba fi Mawadati Dhawil-Qurba, uk. 71, chapa ya Misri. Na akasema (s.a.w.w.): “Ewe Ali, wewe ni wasii wangu, mrithi wangu, baba wa kizazi changu na mume wa binti yangu. Amri yako ndiyo amri yangu na katazo lako ndio katazo langu, naapa kwa yule ambaye amenipa unabii na akanifanya kuwa mbora wa viumbe kuwa, hakika wewe ni hoja ya Mwenyezi Mungu juu ya viumbe Wake, na ni mwaminifu wa siri Yake na ni khalifa wa Mwenyezi Mungu juu ya viumbe Wake.” Chanzo: Yanabiul-Mawaddah, uk. 53, chapa ya mwaka 1302 Istambul. Na akasema (s.a.w.w.): “Hakika Imam Ali ni kiongozi wa waumini na bwana wa waislamu na Imam wa wachamungu na kiongozi wa kundi mashuhuri.” Chanzo: Al-Imam Ali bin Abi Talib cha Ustadhi Tawfiq Abu Ilmi, wakili mkuu wa wizara ya uadilifu huko Cairo Misri, uk. 70, chapa ya Misri iliyosambazwa na Darul-Ma’arifi. Na akasema (s.a.w.w.): “Hakika Ali ni bendera ya haki, Imam wa vipenzi vyangu na nuru ya mwenye kunitii.” Chanzo: Sharhu Nahjul-Balagha cha Ibnu Abil Hadid: Juz. 2, uk. 429, chapa ya mwaka 1329 Misri. Faraidus-Samtwayni: Juz. 1, uk. 151. KifayatutTwalib, uk. 73, chapa ya Tehrani. Manaqibu Sayyidina Ali, uk. 20, chapa ya India. 17

12:03 PM

Page 17


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Na akasema (s.a.w.w.): “Ali ni Imam wa watu wema, na muuaji wa waovu, atapata msaada atakayemsaidia na atatelekezwa atakayemtelekeza.” Chanzo: Isiafu Ar-Raghibina, uk. 158 kwenye maelezo ya Nurul-Absari, chapa ya mwaka 1312 Misri, chapa ya Al-Maymaniyyah. Nurul-Absari, uk. 73. AsSawaiqul-Muhriqah, uk. 75, chapa ya Misri. Faydhul-Qadiri: Juz. 4, uk. 356, chapa ya Beirut. Al-Jamius-Swaghir: Juz. 2, uk. 177, chapa ya mwaka 1401 Beirut, chapa ya Darul-Fikri. Al-Futuhatul-Islamiyyah: Juz 2, uk. 516, chapa ya Misri. Kanzul-Ummal: Juz. 11, uk. 602, chapa ya mwaka 1399 Beirut. Muntakhabu Kanzul-Ummal, uk. 30 kwenye maelezo ya Musnad Ahmad: Juz. 5, chapa ya Misri. Nadhamu Durarus-Simtwayni, uk. 67 na 87. Manaqibu Sayyidina Ali, uk. 37, chapa ya India. Na akasema (s.a.w.w.) kumwambia Ali: “Karibu ewe bwana wa waislamu na Imam wa wachamungu.” Chanzo: Hil’yatul-Awliyai: Juz 1, uk. 66, chapa ya Beirut. Sharhu Nahjul-Balagha: Juz 2, uk. 430. Kanzul-Ummal: Juz 11, uk. 619. Muntakhabu Kanzul-Ummal, uk. 55 kwenye maelezo ya Musnad Ahmad Juz. 5. Matwalibu As-Su’ul, uk. 49 na 57. Nadhmu Durarus-Samtwayni, uk. 115. Na akasema (s.a.w.w.): “Ali ni Imam wa mawalii.” Chanzo: Manaqibu Sayyidina Ali, uk. 37, chapa ya Haydaru Abad-Dukni. Abu Bakr bin Abdur-Rahmani bin Shihabi amesema katika beti zake: “Ali ni ndugu aliyeteuliwa, mwenye kunusuru dini yake na mila yake, yeye ni kiongozi wake mkuu na Imam wake.”

18

12:03 PM

Page 18


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Chanzo: Diwanu Ibnu Shahabi, uk. 30. Pamoja na maelezo haya ya Mtume yaliyotangulia yenye kutamka wazi ukhalifa wa Imam kiongozi wa waumini Ali bin Abi Talib, na pamoja na mengine yaliyomo ndani ya vitabu vya kisunni tu, pia pamoja na Wanachuoni wa kisunni tuliyowataja huko nyuma kutamka wazi kuwa maelezo hayo ni sahihi, lakini bado Abu Hamid Al-Ghazali As-Shafi’i anasema: “Asilan hakuna tamko la Mtukufu Mtumewa Mwenyezi Mungu juu ya Imam yeyote, kwani laiti lingekuwepo basi ni lazima lingedhihirika…..” Mpaka mwisho wa uzushi wake. Tunamuomba Mwenyezi Mungu atukinge dhidi ya kuipinga haki na wenye haki na dhidi ya kuwapotosha waja wa Mwenyezi Mungu, na mfano wa watu kama yeye ndiyo aliowasema Mwenyezi Mungu kwa kauli yake:

“Na wakaikataa kwa dhuluma na kujivuna ilihali nafsi zao zina yakini nayo, basi angalia ulikuwaje mwisho wa wenye kufanya ufisadi.”Sura Naml: 14. Ewe Abu Hamid, ikiwa asilan Mtume hakutoa tamko juu ya Imam yeyote, ilikuwaje Imam wako Abu Bakri bin Abu Quhafa aache tamko juu ya uimamu na ukhalifa wa Umar bin Al-Khattab baada yake, na kwa mujibu wa madai yako atakuwa kapinga Sunna ya Mtukufu Mtumewa Mwenyezi Mungu katika hilo, kisha wewe na wenzako mkamfuata katika hilo na mkaamini ukhalifa wake. Hivi hamuoni kuwa khalifa anayekaimu nafasi ya Mtukufu Mtume(s.a.w.w.) anatakiwa kufuata Sunna yake (s.a.w.w.) na afuate mwongozo wake? Kwa nini hamueliwi nyinyi?

Wewe Wasemaje? 19

12:03 PM

Page 19


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje?

Sunni Asema: Kwetu sisi wafuasi wa Madhehebu manne Imam wa haki baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ni Abu Bakri bin Abu Quhafa, kisha Umar bin Al-Khattab, kisha Uthman bin Affan, kisha Ali bin Abi Talib. Hayo yamesemwa na Hujatul-Islam Abu Hamid Al-Ghazali As-Shafi’i15. Imani hii ndiyo waliyokuwa nayo mashekhe zetu waliyotangulia na wazazi wetu waliyopita, na sisi tumewafuata, hivyo tumekubali waliyoyakubali na tumekataa waliyoyakataa. Hivyo ukhalifa wa hawa kwa utaratibu huu ni ukhalifa wa kisheria hatuna shaka nao.

Na Shia Asema: Hakika Imam wa haki baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ni mwana wa ami yake Ali bin Abi Talib (a.s.), kisha ni mwanae Al-Hasan Az-Zakiyyu (a.s.), kisha Al-Husaini bin Ali (a.s.), kisha Ali bin Al-Husaini Zaynul-Abidina (a.s.), kisha Muhammad bin Ali Al-Baqir (a.s.), kisha Jafar bin Muhammad As-Sadiq (a.s.), kisha Musa bin Jafar Al-Kadhim (a.s.), kisha Ali bin Musa Ar-Ridhaa (a.s.), kisha Muhammad bin Ali Al-Jawad (a.s.), kisha Ali bin Muhammad Al-Hadi (a.s.), kisha Al-Hasan bin Ali AlAskari (a.s.), kisha Muhammad bin Al-Hasan Al-Mahdi (a.s.). Hawa ndiyo Maimamu wetu, watawala wetu na viongozi wetu. Dalili yetu juu ya hilo ni kauli ya Mtukufu Mtume(s.a.w.w.) ambaye hatamki kwa matamanio yake ila ni kwa Wahyi uliofunuliwa: “Hakika makhalifa wangu, mawasii wangu na hoja wa Mwenyezi Mungu juu ya viumbe baada yangu ni kumi na wawili, wa kwanza wao ni ndugu yangu na wa mwisho wao ni mwanangu. Akaulizwa: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ndugu yako ni nani?” Akasema: “Ali bin Abi Talib.” Akaulizwa: 15. Ihyau ulumud-Din: Juz. 1 Uk. 99 chapa ya Misri 1316, chapa ya pili ya AlAzhariyyah.

20

12:03 PM

Page 20


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? “Na ni nani mwanao?” Akasema: “Al-Mahdi ambaye ataijaza ardhi usawa na uadilifu kama ilivyojazwa ujeuri na dhuluma.” Chanzo: Faraidus-Samtwayni: Juz. 2, uk. 312. Na akasema (s.a.w.w.): “Hakika mimi nawaachieni vizito viwili, cha kwanza ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu ndani yake mna uongofu na nuru, hivyo chukueni Kitabu cha Mwenyezi Mungu na shikamaneni nacho (hapo akahimiza juu ya kitabu cha Mwenyezi Mungu na kutamanisha yaliyomo ndani), kisha akasema: “Na watu wa nyumba yangu, nawakumbusheni Mwenyezi Mungu juu ya watu wa nyumba yangu. Nawakumbusheni Mwenyezi Mungu juu ya watu wa nyumba yangu, Nawakumbusheni Mwenyezi Mungu juu ya watu wa nyumba yangu.” Chanzo: Sahih Muslim: Juz. 2, uk. 238, chapa ya mwaka 1290 Misr. Na akasema (s.a.w.w.): “Hakika mimi nawaachieni vizito viwili: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu watu wa nyumba yangu, mkishikamana navyo hamtopotea,16 na hakika hivyo viwili havitoachana mpaka vitakaponikuta kwenye Hodhi, basi jifunzeni kutoka kwao (AhlulBayt) na wala msiwafunze, kwani wao wanajua kuliko ninyi.” Chanzo: Yanabiul-Mawaddah, uk. 35, chapa ya mwaka 1302 Istambul. Na Imam Ali bin Abi Talib (a.s.) yeye ni mwana wa ami ya Mtukufu Mtume(s.a.w.w.) na ni mkwe wake na baba wa kizazi chake na ndiye Imam wa kwanza katika maimamu kumi na mbili baada yake. 16 - Kutokana na maneno haya inafahamika kuwa asiyeshikamana navyo amekwenda nje ya haki. Na Mwenyezi Mungu anasema: “Baada ya haki hakuna chochote isipokuwa ni upotovu.”

21

12:03 PM

Page 21


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Ibrahim Shaybatul-Ansari amepokea kwa kusema: “Niliketi kwa AlAsbagh bin Nabatah, akasema: Je, nikusomee aliyoyaandika Ali bin Abi Talib, radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. Ndipo alipotoa sahifa iliyoandikwa: Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu. Haya ndiyo aliyowausia Muhammad watu wa nyumba yake na umma wake: Amewausia watu wa nyumba yake kumcha Mwenyezi Mungu na kutoachana na utiifu Wake. Na ameuusia umma wake kutoachana na watu wa nyumba yake, na kuwa watu wa nyumba yake wanachukua aliloshikamana nalo Mtume wao (s.a.w.w.), na kuwa wafuasi wao watawang’ang’ania Siku ya Kiyama, na hakika wao hawatowaingizeni kwenye mlango wa upotovu na wala hawatowatoeni kwenye mlango wa uongofu.” Chanzo: Nudhmu Duraru As-Samtwayn, uk. 24. Hakika watu wa nyumba ya Mtume wetu Muhammad ndio wanaostahiki nafasi ya ukhalifa baada yake (s.a.w.w.) na ndiyo wenye haki ya uimamu baada yake kuliko waislamu wote, kwa sababu wao ni kizazi chake na wasiri wake, na ndiyo wajuao zaidi Sheria yake na Sunna zake, hakuna yeyote miongoni mwa waislamu anaelingana nao katika sifa yoyote ya ubora na Uk.amilifu wa kibinadamu, si katika elimu wala matendo, si katika maadili wala dini wala siasa. Na hata ukifumbia macho maelezo ya Mtukufu Mtumeyanayoamuru kuwafuata na kuchukua Sheria kutoka kwao, bado akili salama inatuwajibisha kuwafuata wao na kuwafanya viongozi wetu ndani ya maisha yetu kwakuwa wao wanawashinda waislamu wote katika kila sifa ya ubora na ukamilifu wa kibinadamu, na kumtanguliza asiye mbora juu ya aliye mbora ni vibaya kiakili. Atakayesoma maisha yao na mahusiano yao na Mwenyezi Mungu ndani ya nyakati na hali mbalimbali, na mahusiano yao na jamii za tabaka mbalimbali atathibitisha hilo, hivyo kujitenga nao ni kujitenga na haki, na hakuna 22

12:03 PM

Page 22


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? baada ya haki isipokuwa upotovu. Mwenyezi Mungu anasema:

“Tena ni nini baada ya haki isipokuwa upotovu? Basi mnageuzwa wapi?”Sura Yunusu: 32. Ikiwa kweli sisi ni waislamu, waumini wa ujumbe wa Mtume wetu (s.a.w.w.) na utakaso wake, na kuwa hatamki kwa matamanio ila ni ufunuo anaofunuliwa, hivyo haweweseki katika maneno yake, na hawezi kufanya hivyo, basi hatuna njia isipokuwa baada yake ni kurejea kwa kizazi chake, watu wa nyumba yake na kuchukua Sheria kutoka kwao, na kuwafanya viongozi wetu ndani ya maisha yetu, tufuate uongofu wao na tuachane na wayakatazayo. Na tayari juu ya hilo Mtukufu Mtume(s.a.w.w.) ameshatuhakikishia amani dhidi ya upotovu. Tunajikinga kwa Mwenyezi Mungu tusiwafuate mashekhe zetu katika imani yao yoyote kabla ya kuichunguza na kuitafiti. Hilo ni baada ya Mwenyezi Mungu kuwatuhumu wenye kuwafuata mababu zao na wazazi wao na wengineo waliyotangulia, akasema:

“Na wakiambiwa: Fuateni aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, husema: “Bali tutafuata tuliyowakuta nayo baba zetu. Je, hata kama baba zao walikuwa hawafahamu chochote wala hawakuongoka?”Sura AlBaqara: 170.

Wewe Wasemaje?

23

12:03 PM

Page 23


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje?

Sunni Asema: Sisi Sunni wafuasi wa madhehebu manne tunaamini kuwa Abu Bakr bin Quhafa ni khalifa baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu hata kama Mtume (s.a.w.w.) hakutoa tamko juu ya ukhalifa wake, kwa sababu sahaba walimchagua ili awe khalifa na wakampa kura ya ndiyo, hivyo ukhalifa wake ni sahihi kisheria. Hujatul-Islam Abu Hamid Al-Ghazali amesema: “Abu Bakr hakuwa Imam ila kwa kuchaguliwa na kupewa kiapo cha utii.”17 Na Shia Asema: Ukhalifa wa Abu Bakr si wa kisheria, kwa sababu ukhalifa wa kukaimu nafasi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu huthibiti kwa tamko lake (s.a.w.w.) juu ya ukhalifa huo kwa maelezo kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na wala hauthibiti kwa uchaguzi wa watu, kwa sababu huo ukhalifa si haki yao bali ni haki ya Mwenyezi Mungu ambayo hashirikiani na yeyote yule. Mwenyezi Mungu amesema:

“Na Mola Wako Mlezi huumba atakavyo na huchagua, kwao hakuna hiari. Mwenyezi Mungu ameepukana na upungufu, na ametakasika kabisa kuliko wale wawashirikishao.”29Sura Al-Qasas: 68. Hivyo kama ilivyo uteuzi wa Mtukufu Mtume (Muhammad)18 umo mikononi Mwake, vile vile uteuzi wa khalifa wake atakayekaimu nafasi yake katika kutekeleza jukumu lake nao umo mikononi Mwake, hivyo 17 Ihyau Ulumid-din: Juz. 1, uk. 99, chapa ya Misri, chapa ya pili ya AlAzhariyyah. 18Aya ya mwisho ya Suratul-Fat’hu.

24

12:03 PM

Page 24


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? hateuliwi isipokuwa kwa uteuzi Wake Yeye mtukufu na kwa maelezo kutoka Kwake Mtukufu kupitia Mtukufu Mtume(s.a.w.w.). Na kwa Ijimai ya waislamu wote ni kuwa Mtume (s.a.w.w.) hakutoa tamko juu ya ukhalifa wa Abu Bakr. Na ndani ya Qur’ani tukufu mna Aya nyingine zisizokuwa hiyo iliyotangulia zikionyesha kuwa uteuzi wa khalifa na Imam ni jukumu la Mwenyezi Mungu. Miongoni mwa Aya hizo ni kauli yake:

“Na pindi Mola Wako Mlezi alipowaambia Malaika: Mimi nitamuweka khalifa katika ardhi.” Sura Al-Baqara: 30. Na akasema:

“Ewe Daudi! Hakika tumekujaalia kuwa khalifa aridhini, basi uwahukumu watu kwa haki.”Sura Swadi: 26. Akasema tena:

“Na Ibrahim alipojaribiwa na Mola Wake Mlezi kwa matamko, na akayatimiza. Akasema: Hakika Mimi nitakufanya Imamu wa watu. Akasema: “Je, na katika kizazi changu?” Akasema: Ahadi yangu haiwafikii madhalimu. Sura Al-Baqara: 124.

25

12:03 PM

Page 25


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Hivyo Mwenyezi Mungu ndiye huchagua nani awe khalifa kwa ajili ya waja Wake, sawa awe Nabii au khalifa wa Nabii, katika hilo hamna tofauti. Kwa sababu utakaso ni sharti muhimu katika hilo, na hakuna aujuaye ila Yeye Mwenyezi Mungu Mjuzi wa mambo yaliyofichikana, na hakuwapa watu mamlaka ya uteuzi kwa sababu wao hawajui utakaso wake na hivyo uchaguzi wao utaangukia kwa mtu asiyefaa. Mwenyezi Mungu anasema:

“Na kama ukiwatii wengi katika waliomo ulimwenguni watakupoteza na njia ya Mwenyezi Mungu. Hawafuati ila dhana tu, hawana ila uongo tu.”Sura Al-An'ami: 116. Na tayari kabla ya Aya hiyo ameshasema:

“Haiwi kwa mwanaume aliyeamini wala kwa mwanamke aliyeamini, Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wanapokata shauri, wawe na hiari katika shauri lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume Wake hakika amepotea upotovu ulio wazi.” Sura Al-Ahzabi: 36. Kumchagua khalifa ambaye hajaainishwa na Mtukufu Mtumeni kukiasi Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu kama ulivyoona, hivyo ukhalifa wa yule wanayemchagua si wa kisheria, na hivyo kila kitendo atendacho na hukumu aitoayo na amri aitekelezayo ni batili, na Siku ya Kiyama, siku ya majuto na hasara atahukumiwa kwayo. Mwenyezi Mungu anasema: 26

12:03 PM

Page 26


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje?

“Na siku dhalimu atajiuma mikono yake, akisema: Laiti ningelishika njia pamoja na Mtume. Ee Ole wangu! Natamani nisengelimfanya fulani kuwa rafiki. Kwa hakika yeye alinipoteza nikaacha mawaidha baada ya kunifikia.”Sura Al-Furqan: 27 - 29. Ni wazi kuwa kubatilika kwa ukhalifa wa Abu Bakr kunabatilisha ukhalifa wa yule aliyemuweka yeye kwenye ukhalifa baada yake naye ni Umar bin Al-Khattabi, na baada yake Uthman bin Affan, hivyo atakayeamini ukhalifa wa hawa watatu atakuwa kaamini uongo na uzushi na atakuja kujuta na majuto yake hayatomnufaisha chochote ikiwa hatoacha imani hiyo na kumwomba Mwenyezi Mungu msamaha kutokana na dhambi yake hiyo. Na hata kama Sahaba wangekuwa na haki ya kuchagua lakini wamekosea kumchagua Abu Bakr kwa ajili ya ukhalifa kwa sababu hana sifa zinazofaa, ya kwanza ni utakaso nayo ni sifa ya lazima kwa khalifa, na mwenye sifa hii anastahiki kuwatangulia waislamu wote na kukaimu nafasi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), na Abu Bakr hana sifa hii. Na miongoni mwa sifa za mtu mwenye kukaimu nafasi ya Mtukufu Mtume(s.a.w.w.) ni kuwa mjuzi wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna za Mtukufu MtumeWake, na Abu Bakr alikuwa si mjuzi wa hivyo viwili. Na zifuatazo ni baadhi tu ya dalili kutoka kwenye vitabu vya wapenzi wake na marafiki zake juu ya hilo (la kutokuwa na elimu). As-Suyuti

amesema: “Kuna bedui mmoja alimjia Abu Bakr na kumwambia: “Nimeua mnyama ilihali nikiwa muhrimu, 27

12:03 PM

Page 27


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? malipo yangu ni nini?” Abu Bakr akamwambia Ubayya bin Kaab aliyekuwa amekaa naye: “Unaona malipo yake ni nini?” Bedui akasema: Nimekuijia wewe, na wewe ndiye khalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, nakuuliza tena na wewe unamuuliza mwingine?” Chanzo: Ad-Durul-Manthur fit-Tafsiri Bil-Maathur. Qubaysah bin Dhuaybu amesema: “Kuna bibi alikuja kwa Abu Bakr AsSwidiq akamuomba mirathi yake. Akasema: Ndani ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu hauna chochote, na wala ndani ya Sunna ya Mtume wa Mwenyezi Mungu sijui chochote kuhusu wewe, rejea mpaka niwaulize watu. Akawauliza watu, Mughirah bin Shuaybah akasema: Alikuja kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akampa sudusi. Basi ndipo Abu Bakr akamtekelezea…….” Chanzo: At-Taju Al-Jamiu Lil-Usuli fi Ahadithir-Rasul Juz. 2, uk. 259 na 263, chapa ya pili ya mwaka 1381. Ta’rikhul-Khulafai cha As-Suyuti, uk. 80, chapa ya India, na Uk. 92, chapa ya Beirut. Sheikh

Ali Mansur Nasif mwanazuoni wa Al-Azhari amesema: “Bibi, mama wa baba alimuijia Abu Bakr na kumuomba haki yake kutoka kwenye mirathi ya mwanae wa kiume. Basi akauliza na alipojua kuwa haki yake ni sudusi alimpa.”

Chanzo: At-Taju Al-Jamiu Lil-Usul: Juz. 2, uk. 260. Al-Qasim

bin Muhammad amesema: “Hakika bibi wawili 28

12:03 PM

Page 28


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? walimjia Abu Bakr wakitafuta mirathi yao, mmoja mzazi wa mama na mwingine mzazi wa baba. Basi akampa mzazi wa mama na kumnyima mzazi wa baba. Ndipo Abdurahman bin Sahlu Al-Ansari ambaye alikuwa miongoni mwa watu waliohudhuria vita vya Badri na ndiye kaka wa kizazi cha Haritha, akasema: Ewe khalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, umempa yule ambaye laiti kama yeye angefariki basi (huyu mrithiwa) asingerithi. Ndipo akaigawa mirathi kati yao wawili.” Chanzo: Usudul-Ghaba Fi maarifati As-Sahabah: Juz. 3, uk. 299. Ta’rikhulKhulafai, uk. 80, chapa ya India, na Uk. 92, chapa ya Beirut. Ar-Radhawi: “Ndipo akaigawa mirathi kati yao wawili,” inamaanisha akampa sehemu ya mirathi yule asiyestahiki, na kumdhulumu sehemu ya haki yake yule anayestahiki sehemu ya mirathi hiyo. Huyu

hapa Uyaynah bin Hasnu na Al-Aqrau bin Habisu walikuja kwa Abu Bakr na kumwomba ardhi isiyoendelezwa. Lakini alikuwa hajui kama hilo ni jukumu lake au sio lake, na mwisho akawakatia ardhi hiyo na kuwaandikia hati kwa ajili ya ardhi hiyo….

Chanzo: Manaqibu Amiril-Mu’minin Umar bin Al-Khattab, uk. 64. Muhammad bin Sirin amesema: “Abu Bakr alipatwa na kadhia ambayo asilan hakupata hukumu yake ndani ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu wala athari ndani ya Sunna, akasema: “Nitajitahidi kwa rai yangu, ikiwa nimepatia basi ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na ikiwa nimekosea basi ni kutoka kwangu na nitamuomba Mwenyezi Mungu msamaha.”

29

12:03 PM

Page 29


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Chanzo: Tabaqati ibnu Sa’ad: Juz. 3, sehemu ya kwanza, uk. 126. Ta’rikhul-Khulafai, uk. 84, chapa ya India. Amir bin Sharahilu amesema: “Abu Bakr aliulizwa kuhusu maana ya (Asiye na mtoto wala mzazi), akasema nitajibu kwa rai yangu, na ikiwa nimepatia basi ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu peke Yake hana mshirika, na ikiwa nimekosea basi ni kutoka kwangu na kutoka kwa Shetani.” Chanzo: Ad-Durrul-Manthur Juz. 2, uk. 329. Ta’rikhul-Khulafai, uk. 76. As-Suyuti amesema: “Aliulizwa kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na matunda na malisho.”19 Akasema: Ni mbingu ipi itakayonifunika, na ni ardhi ipi itakayoniinua iwapo nitasema kutoka ndani ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu nisichokijua.” Na katika riwaya nyingine: “Iwapo nitasema kutoka ndani ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu kitu ambacho Mwenyezi Mungu hajakileta.” Chanzo: Ta’rikhul-Khulafai, uk. 76, chapa ya India, na uk. 88, chapa ya Beirut. Jarida la chuo kikuu cha kiislamu cha Madina, toleo la 59 la mwaka 1403 la mwaka wa 15. Humo mna: Nisichokijua (badala ya): Ambacho Mwenyezi Mungu hajakileta. Ahmad amepokea kutoka kwa Ibnu Abbas kuwa alisema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema: Atakayetoa hukumu ndani ya Qur’ani bila elimu basi ayaandae makalio yake na moto.”

19. Suratul Abasa: 3.

30

12:03 PM

Page 30


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Chanzo: As-Sirajul-Munir: Juz. 1, uk. 3. Imepokewa kutoka kwa Abu Huraira kuwa: “Atakayetoa fatwa bila elimu basi Malaika wa mbinguni na ardhini humlani.” Chanzo: Muntakhabu Kanzul-Ummal, uk. 43 kwenye maelezo ya Musnad Ahmad Juz. 4. Ar-Radhawi: Ewe msomaji mpendwa umeona kauli ya Abu Bakr: “Nitajitahidi kwa rai yangu, na ikiwa nimepatia basi ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na ikiwa nimekosea basi ni kutoka kwangu na kutoka kwa Shetani na nitamwomba Mwenyezi Mungu msamaha.” Anatumia kauli yake kuhalalisha msimamo wake wa kutoa fatwa bila elimu yoyote na kutafsiri Kitabu cha Mwenyezi Mungu kwa rai yake. Na Mwenyezi Mungu anasema:

“Wala usifuate usiyo na elimu nayo, hakika masikio na macho na moyo, hivyo vyote vitaulizwa.” Sura Al-Israi: 36. Pia akasema:

“Waambie: Mola Wangu Mlezi ameharamisha mambo machafu, yaliyodhihirika na yaliyofichika, na dhambi na uasi pasipo haki, na kumshirikisha Mwenyezi Mungu na ambacho hakukiteremshia dalili, 31

12:03 PM

Page 31


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? na kusema juu ya Mwenyezi Mungu msiyoyajua.” Sura Aaraf: 33. Mwenyezi Mungu amefanya kusema bila elimu ni sawa na kumshirikisha Mwenyezi Mungu. Je, kuomba kwake msamaha kutamnufaisha baada ya kusema kutoka ndani ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya Mtume wa Mwenyezi Mungu bila elimu yoyote? Na miongoni mwa sifa za kupewa Ukhalifa ni khalifa awe shujaa. Huyu hapa Ustadh wa kimisri wa zama zetu Abdul-Karim Al-Khatibu anasema: “Abu Bakr hajulikani kwa ushujaa katika medali za vita. Na Hasan bin Thabiti radhi za Mwenyezi Mungu zimuendee hakuwa miongoni mwa wapiganaji wa kutegemewa katika medali za vita na mapambano, na si mmoja bali ni sahaba wengi wa Mtukufu Mtumekama Abu Bakr na Uthman.” Chanzo: Khilafah, uk. 130 mpaka wa 133, chapa ya mwaka 1386 Misri, chapa ya kwanza ya As-Sunnah Al-Muhamadiyyah. Abu Bakr alishindwa kwenye vita vya Khaybar, Al-Hakim amepokea kutoka kwa Ali kuwa amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu alimtuma Abu Bakr kwenda Khaybari akaenda na kikosi akashindwa na kukimbia.” AlHakim amesema: “Hadithi hii njia yake ni sahihi na mashekhe wawili hawajaitoa.”

Chanzo: Al-Mustadrak Alas-Sahihayn: Juz 3, Uk. 37. na Ad-Dhahabi amesema katika muhtasari wa Al-Mustadrak kuwa ni sahihi. Na katika riwaya ya Al-Muttaqi Al-Hindi kutoka kwenye Hadithi ya Abdur-Rahman bin Abi Layla ni kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu alimtuma Abu Bakr akaenda na kikosi akashindwa na kukimbia. Akamtuma 32

12:03 PM

Page 32


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Umar akakimbia akiwa na kikosi na akarejea kwa Mtume, ndipo Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Bila shaka nitampa bendera mtu ambaye anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume Wake,20 si mkimbiaji na Mwenyezi Mungu atampa ushindi.” Mwoga hafai kuwa khalifa wa Mtukufu Mtume(s.a.w.w.), na kauli ya Mtume kusema: “Si mkimbiaji” ni kuwaumbua Abu Bakr na Umar, kama ilivyo wazi. Ibnu Abu Hadid Al-Muutazil amewaumbua kwa kukimbia kwao kwenye vita vya Khaybar kwa kusema: “Nisilolisahau sisahau wawili ambao walikwenda kupambana na wakakimbia huku ardhi na bendera tukufu vimejaa huzuni. Wakarudi wakiwa wamefunikwa na mavazi na kanzu za udhalili21.” Na miongoni mwa sifa za khalifa anayekaimu nafasi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu ni asiwe mwongo. Na Abu Bakr hakuwa mtu wa namna hiyo, Bukhari amepokea kutoka kwa Aisha kuwa Fatima binti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu alituma barua kwa Abu Bakr akimuomba mirathi yake kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu miongoni mwa mali ambayo Mwenyezi Mungu alimpa Mtume Wake, hapo Fatima alikuwa akiomba mali ya Mtume iliyoko Madina, Fadak na Khumsi iliyobakia kutoka kwenye Khumsi ya Khaybari. Abu Bakr akasema: “Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa akisema: Hakika sisi kundi la Manabii haturithiwi, tuliyoyaacha ni sadaka….” Chanzo: Sahih Bukhari: Juz. 2, uk. 301, na Juz. 3, uk. 55, chapa ya Misri kwenye 20. Kipengele (Na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanampenda) kimeondolewa kwenye Hadithi hii, lakini kimo kwenye Hadithi nyingine, nacho kimetajwa kwenye riwaya ya Al-Haythami ndani ya kitabu Maj'mauz-Zawa'idi kutoka kwa Abu Layla. 21. Al-Qaswaidu As-Sab'u Al-Alawiyati, chapa ya mwaka 1340, chapa ya Swayda.

33

12:03 PM

Page 33


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? maelezo ya As-Sindi. At-Taju Al-Jamiu Lil-Usuli: Juz 3, uk. 33, na Juz. 4, uk. 381. Hivyo Abu Bakr akakataa kumpa Fatima, radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, chochote kutoka kwenye mirathi hiyo, hivyo Fatima akamkasirikia Abu Bakr na kujitenga naye, kuanzia hapo hakuzungumza naye mpaka alipokufa, na aliishi miezi sita baada ya kifo cha Mtume wa Mwenyezi Mungu. Alipofariki alizikwa usiku na mumewe na hakumpa ruhusa Abu Bakr ya kuhudhuria (mazishi), na Ali, radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, ndiye aliyemsalia na kumzika. Chanzo: Tarikhul-Madinah Al-Munawwarah: Juz. 1, uk. 196, uhakiki wa Fahim Muhammad Shaltuti. Ustadhi Abbas Mahmud Al-Aqad amesema: “Fatima alimtumia Abu Bakr barua akimuomba mirathi yake ikiwemo Fadak na Khumsi iliyobakia kutoka kwenye Khumsi ya Khaybar, Abu Bakr akasema hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa akisema: Hakika sisi kundi la Manabii haturithiwi, tunayoyaacha ni sadaka… Na inasemekana Az-Zahrau alimtolea dalili kwa kutumia kauli ya Mwenyezi Mungu kuhusu mmoja kati ya Manabii Wake - Zakariya:

“Atakayenirithi na awarithi ukoo wa Yakub.” Sura Mariyam: 6. Na kauli yake:

“Na Sulayman alimrithi Daudi.”43 Sura An-Naml: 16. 34

12:03 PM

Page 34


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Chanzo: Fatimah Az-Zahrau Wal-Fatimiyun, uk. 327, chapa ya mwaka 1974 Beirut, chapa ya Darul-Kitabi Al-Lubnaniyyu. Ar-Radhawi: Aya hii inatamka waziwazi kuwa Manabii (a.s.) wanarithiwa, hivyo inakadhibisha kauli ya: “Sisi kundi la Manabii haturithiwi,” Mwenyezi Mungu anasema:

“Na tuiweke laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie wenye kusema uongo.” Sura Al-Imran: 61.

Wewe wasemaje?

Sunni Asema: Waislamu wote wamekubaliana juu ya ukhalifa wa Abu Bakr na Uimamu wake isipokuwa marawafidhu (Shia), na kukhalifu kwao hakudhuru. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Umma wangu haukubaliani juu ya jambo la upotovu.”

Na Shia Asema: Hayajatimia makubaliano juu ya ukhalifa wa Abu Bakr, na dai lake hilo si hoja, na wala kauli ya Mtukufu Mtume haimuunga mkono, kwani tamko (Umma) linajumuisha kila mwisilamu, na kila mwislamu ni sehemu ya umma, na inajulikana wazi kwa yakini kabisa kuwa si kila mtu miongoni mwa waislamu aliamini ukhalifa wake. – (Na kwa upande mwingine, umma haukubaliani juu ya jambo la upotovu – na huu ulikuwa ni upotovu kiasi kwamba hata hao baadhi tu ya umma waliokuwepo hapo wakati huo, 35

12:03 PM

Page 35


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? hawakukubaliana kweli ili itimie kauli hiyo – Mtarjuma) Ahmad bin Hajar amesema: “Ansari walichukia kitendo cha kumchagua Abu Bakr.” Chanzo: As-Sawaiq Al-Muhriqah, uk. 12, chapa ya mwaka 1375. Saad bin Ubadah kiongozi wa watu wa Madina alikataa kwa nguvu zote kumpa Abu Bakr kiapo cha utii, akasema: “Naapa kwa Mwenyezi Mungu siwezi mpaka niwarushie mishale iliyomo kwenye fuko langu, nizipakaze damu ncha za mshale wangu, niwapige kwa upanga wangu kadiri utakavyonitii na nipigane na ninyi kutumia watu wa nyumba yangu na yule atakayenifuata. Na hata kama majini na wanadamu watajikusanya pamoja nanyi sintowapa kiapo cha utii mpaka nifike kwa Mola wangu Mlezi.” Chanzo: Ta’rikhul-Umami wal-Muluuki : Juz 3, uk. 210. Na Muhammad bin Jarir At-Tabari amesema: “Watu wa Madina wakasema, au baadhi ya watu wa Madina, hatumpi kiapo cha utii ila Ali tu.” Chanzo: Tarikhul-Umami Wal-Muluki: Juz 3, uk. 198. Abu Asuwad Ad-Duali amesema: “Baadhi ya watu wa Makka walichukizwa na kitendo cha Abu Bakr kupewa kiapo cha utii bila ushauri, na Ali na Zubayr walichukizwa……” Chanzo: Sharhu Nahjul-Balagha cha Ibnu Abil Hadid: Juz. 2, uk. 19, chapa ya mwaka 1329 Misri. Na kabila la Asad na Fazarah walisema: “Tunaapa kwa Mwenyezi Mungu abadan hatutompa Abu Fasilu (baba wa mwana wa ngamia) kiapo cha utii.” 36

12:03 PM

Page 36


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Chanzo: Ta’rikhul-Umami Wal-Muluki: Juz. 3, uk. 229. Na kabila la Twiu wakasema: “Tunaapa kwa Mwenyezi Mungu abadan hatutompa Abu Fasilu (baba wa mwana wa ngamia) kiapo cha utii.” Chanzo: Tarikhul-Umami Wal-Muluki: Juz. 3, uk. 228. Sheikh Muhammad Al-Arabiyyu At-Tabani Al-Jazairi amesema: “Watu walimpa Abu Bakr jina la Abu Fasili (baba wa mwana wa ngamia) kwa ajili ya kumdharau.” Chanzo: Tahdhirul-Abqariyyu Min Muhadharati Al-Khudhariyyu: Juz. 2, uk. 140. Kabila la Huwazini likasema: “Hatumpi kiapo cha utii mwenye nguo kuukuu (yaani Abu Bakr).” Chanzo: Sharhu Nahjul-Balagha: Juz. 2, uk. 17, chapa ya mwaka 1329 Misri. Ibnu Abil Hadid amesema: “Alikuwa na shuka la Fadak ambalo awapo juu ya kipando hujifunika na ateremkapo hulivaa, nalo ndilo walilomwaibishia watu wa Huwazini baada ya Mtume (s.a.w.w.).” Ahmad bin Muhammad bin Abdur-Rabih Al-Andalusi amesema: “Waliopinga uteuzi wa Abu Bakr ni Ali, Abbas, Zubayr na Sa’ad bin Ubadah. Ama Ali na Abbas wao waliendelea kukaa nyumbani kwa Fatima mpaka Abu Bakr alipowatumia Umar ili awatowe nyumbani mwa Fatima, na akamwambia: Iwapo wakikataa basi wauwe….” Chanzo: Al-Aqdu al-Farid: Juz. 2, uk. 197, na Juz. 4, uk. 259, chapa ya mwaka 1403 Misri, na Juz. 5, uk. 13, chapa ya mwaka 1407. 37

12:03 PM

Page 37


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Muhammad bin Muslim bin Shihabi Az-Zahri amesema: “Ali, wala yeyote miongoni mwa kizazi cha Hashim hawakumpa Abu Bakr kiapo cha utii muda wa miezi sita.” Chanzo: Ta’rikhul-Umami Wal-Muluki: Juz. 3, uk. 202. Umar bin Al-Khattab alisema: “Uchaguzi wa Abu Bakr ulikuwa ni vurugu tupu, Mwenyezi Mungu akazuia shari yake.”22 Chanzo: Ta’rikhul-Khulafai, uk. 56, chapa ya India. Na akaongezea kuwa: “Atakayerudia kutenda mfano wake muueni.” As-Sawaiq al-Muhriqah, uk. 21. Al-Milalu wan-Nihal, uk. 13, chapa ya mwaka 1332 Misri. Sharhu Nahjul-Balagha: Juz. 1, uk. 123, chapa ya mwaka 1329 Misri. Hivyo dai la kuwepo makubaliano juu ya ukhalifa wa Abu Bakr ni batili halina msingi wowote, na hata kimjadala tukijaalia kuwa yalitimia makubaliano, je ukhalifa unaopatikana kwa msingi wa dhuluma, kulazimisha na vitisho vya kuua ni ukhalifa wa kisheria? Ilihali Mwenyezi Mungu anasema:

“Hakuna kulazimisha katika dini.”Sura Baqara: 256. Hapana. Enyi wapotezaji, ni lini mtazinduka kutoka kwenye mghafala wenu na mkatae kuwafuata mashekhe zenu waliotangulia, mtumie akili zenu na mrudi kwenye uongofu wenu?

Wewe wasemaje? 22. As-Suyuti amesema: Hakika Mwenyezi Mungu aliiweka haki kupitia ulimi wa Umar. Tarikhul-Khulafai, uk. 112, chapa ya Beirut.

38

12:03 PM

Page 38


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje?

Sunni Asema: Amesema (s.a.w.w.): “Atakayekufa ilihali shingoni mwake hana kiapo cha utii basi amekufa kifo cha kijahiliya”23

Na Shia asema: Hadithi hii ni dalili juu ya ubatilifu wa ukhalifa wa Abu Bakr bin Abu Qahafa khalifa wa kwanza wa Sunni, na kubatilika kwa ukhalifa wake kunabatilisha ukhalifa wa yule ambaye yeye alimpa ukhalifa baada yake naye ni Umar bin Al-Khattab, na hivyohivyo ukhalifa wa aliyekuja baada yake. Sunni wote wanakubaliana juu ya usahihi wa ukhalifa wao na ule ukhalifa wa mtu wa Ukoo wa Umayya Uthman bin Affan japokuwa hakuna hata mmoja kati yao ambaye Mtukufu Mtume alimsimika kwa ukhalifa. Na dalili ya kubatilika ukhalifa wa Abu Bakr kwa Hadithi hii ni kuwa: Hamna shaka kuwa Fatima binti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alifariki akiwa amemkasirikia. Na baada ya Abu Bakr kumtuma Umar bin Al-Khattab nyumbani kwa Fatima ili akachukue kiapo cha utii kwa nguvu kutoka kwa wale waliomo ndani ya nyumba hiyo, Fatima alimwambia: “Ewe Abu Bakr, mmeharakisha kujipa ujasiri juu ya AhlulBait wa Mtume wa Mwenyezi Mungu. Naapa kwa Mwenyezi Mungu sintomsemesha Umar mpaka nitakapokutana na Mwenyezi Mungu.” Chanzo: Sharhu Nahjul-Balagha cha Ibnu Abil Hadid: Juz. 1, uk. 19, chapa ya mwaka 1329 Misri. Pia akasema akiwa anamshitaki yeye na Umar kwa Mtukufu Mtumewa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.): “Ewe baba yangu mpendwa, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu tumepatwa na nini baada yako kutoka kwa mwana wa 23. Jahiliya ni hali na imani iliyokuwepo kabla ya Uislam - mtarjumi. Al-Fajru As-Sadiq, uk. 7, chapa ya mwaka 1323 Misri.

39

12:03 PM

Page 39


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Al-Khattab na mwana wa Abu Quhafa.” Chanzo: Al-Imamah Was-Siyasah cha Ibnu Qutaybah Ad-Daynuriyyu: Juz. 1, uk. 13, chapa ya mwaka 1388 Misri. Na akamwambia Umar: “Hakika mimi namfanya Mwenyezi Mungu na Malaika Wake kuwa shahidi, hakika nyinyi wawili mmenikasirisha na hamjaniridhisha, na nikikutana na Mtukufu Mtumebila shaka nitawashitaki kwake.” Chanzo: Al-Imamah Was-Siyasah: Juz. 1, uk. 14. Ibnu Abil Hadid amesema: “Na kilicho sahihi kwangu ni kuwa yeye alifariki akiwa amemkasirikia Abu Bakr na Umar, na yeye aliusia kuwa wao wawili wasimsalie….” Chanzo: Sharhu Nahjul-Balagha: Juz 2, uk. 20, chapa ya mwaka 1329 Misri. Na laiti yeye angeona kuwa Abu Bakr anastahiki kiapo cha utii basi asingelidhihirisha ghadhabu yake juu yake, na wala asingelimwambia yeye na rafiki yake: “Naapa kwa Mwenyezi Mungu bila shaka nitawashitaki kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, na wala asingeusia kuwa wasimsalie.” Hayo yote ni dalili ya kutokuutambua ukhalifa wake, hivyo atakayeamini ukhalifa wake na usahihi wa Hadithi hii ya kisunni: “Atakayekufa ilihali shingoni mwake hana kiapo cha utii basi amekufa kifo cha kijahiliya.” Analazimika kusema kuwa Fatima (a.s.) alikufa kifo cha ujahiliya, na bila shaka hakuna mwisilamu yeyote atakayesema hivyo, kwa sababu kusema hivyo bila shaka ni kufuru. Mwenyezi Mungu amesema:

40

12:03 PM

Page 40


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? “Na wale walioamini na wakafuatwa na vizazi vyao katika imani tutawakutanisha nao watoto wao.”Suratut-Tur: 21. Bila shaka Fatima binti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ni kinara wao, Mwenyezi Mungu amemkutanisha na baba yake (s.a.w.w.), na tayari alikuwa ameshamwambia kuwa: “Hakika wewe utakuwa mtu wa kwanza wa nyumba yangu kukutana na mimi.” Na Fatima ni miongoni mwa watu wa nyumba ya Mtume ambao walishukiwa na Aya ya Utakaso:

“Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu watu wa nyumba na kukutakaseni kabisa.” Surat Al-Ahzab: 33. Na ni miongoni mwa wale ambao bila shaka Mwenyezi Mungu alifaradhisha juu ya waislamu kuwapenda, akasema: “Sema: Kwa haya siombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi katika ndugu.”Surat AsShura: 23. Na kwa ajili yake Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema: “Fatima ni pande la nyama yangu yananiudhi yale yanayomuudhi.” Chanzo: Sahih Muslim: Juz. 2, uk. 339, chapa ya mwaka 1327 Misri. Na Mwenyezi Mungu akasema:

41

12:03 PM

Page 41


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? “Kwa hakika wale wanaomuudhi Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, Mwenyezi Mungu amewalaani duniani na Akhera, na amewaandalia adhabu yenye kufedhehesha. Na wale wanaowaudhi wanaume waumini na wanawake waumini pasipo wao kufanya kosa lolote, bila shaka wamebeba dhuluma kubwa na dhambi zilizo dhahiri.”AlAhzab; 33: 57-58

Wewe wasemaje?

Shia Asema: Ni sharti kwa Imam na khalifa anayekaimu nafasi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) awe na sifa ya utakaso, nayo ni hali ya dhati inayomzuia kutenda madhambi hata yale madogo, na dhidi ya kila upungufu na dosari ili afae kukaimu nafasi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) aliyemtakasifu dhidi ya kila dhambi na aliyeepukana na kila upungufu na dosari. Na laiti asipokuwa mtakasifu na akatenda yasiyotakiwa na yasiyofaa kutendwa na yeye ilihali yeye yuko kwenye nafasi aliyo nayo basi ni wajibu kwa waislamu kumpinga, na hapo hadhi yake itashuka na kudharaulika kwa watu, na hivyo atakuwa mtu asiyefaa kukaimu nafasi ya Mtukufu Mtume(s.a.w.w.), hivyo kwetu utakaso ni sharti kwa khalifa na Imam anayekaimu nafasi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.). Pia ni sharti khalifa awe anatokana na kizazi cha Ali kwa sababu Mtukufu Mtume(s.a.w.w.) aliufanya ukhalifa muhtasi kwa Imam Ali bin Abi Talib (a.s.) na Maimamu kumi na moja kutoka kwenye kizazi chake tu. Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Hakika makhalifa wangu, mawasii wangu na hoja wa Mwenyezi Mungu juu ya viumbe baada yangu ni kumi na wawili, wa kwanza wao ni ndugu yangu na wa mwisho wao ni mwanangu.” Akaulizwa: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ndugu yako ni nani” Akasema: “Ali bin Abi Talib.” Akaulizwa na ni nani mwanao? Akasema: 42

12:03 PM

Page 42


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? “Al-Mahdi ambaye ataijaza ardhi usawa na uadilifu kama ilivyojaa dhuluma na ujeuri.” Chanzo: Faraidus-Samtwayni: Juz. 2, uk. 312.

Na Sunni Asema: Si sharti Imam na Khalifa kuwa maasumu wala kutokana na kizazi cha Ali.24 Mpakistani Ihsan Dhahir amesema: “Wamenukuu (Shia) kutoka kwa Imam wao wa kwanza maasumu Ali bin Abi Talibi kama wanavyodai.”25

Wewe wasemaje?

Sunni Asema: Bila shaka kiongozi wa wasema kweli na Rais wao ni Abu Bakr (r.a). Hilo limesemwa na imam Fakhrud-Din Ar-Razi ndani ya Mafatihul-Ghayb26 Na Umar ndiye Mtenganishaji27 (al-Faruuq), Muhammad bin Shihabi AzZahri amesema: “Zimetufikia habari kuwa watu wa kitabu ndiyo waliokuwa wa kwanza kumwita Umar Mtenganishaji (Faaruuq), na wais24. Al-Fajrus-Sadiq fii raddi Alaa munkirit-Tawassul wal-karamati wal-khawariq, uk. 5, chapa ya mwaka 1323 Misri, chapa ya Al-Waidhu. 25. As-Shi'ah Was-Sunnah, uk. 157, chapa ya pili iliyosambazwa na Daru Taybatur-Riyadhi. 26. Juzuu la kwanza ukurasa wa 263, chapa ya mwaka 1401 Beirut, chapa ya Darul-Fikri. 27. Anayetenganisha kati ya haki na batili -Mtarjumi.

43

12:03 PM

Page 43


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? lamu walikuwa wakitanguliza hilo kuliko kauli yao na wala haijatufikia kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema chochote kuhusu hilo.” Chanzo: Ta’rikhul-Madinah: Juz. 2, uk. 662.

Na Shia Asema: Hakika Imam wetu kiongozi wa waumini Ali bin Abi Talib (a.s.) ndiye msema kweli mkubwa na ndiye Mtenganishaji ambaye anatenganisha kati ya haki na batili, na katika sahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) hakuna ambaye inasihi kumsifia kwa moja kati ya sifa hizi mbili isipokuwa yeye. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amemzungumzia kwa kusema: “Hakika huyu ndiye msema kweli mkubwa na mtenganishaji wa umma huu.”28 Chanzo: Manaqibu Sayyidina Ali cha Al-Ayni, uk. 20, chapa ya mwaka 1352 ya Haydar Abad. Na (s.a.w.w.) akamwambia Ali (a.s.): “Wewe ni msema kweli mkubwa, na wewe ni mtenganishi ambaye unatenganisha kati ya haki na batili na wewe ni kiongozi mkuu wa dini.” Chanzo: Dhakhairul-Uqba fi Mawadat Dhawil-Qurba, uk.56, chapa ya mwaka 1356 Misri. Manaqib Sayyyidina Ali, uk. 28 India. Na alisema (s.a.w.w.): “Wasema kweli ni watatu: Habibu seremala muumi28. Anayetenganisha kati ya haki na batili ndani ya umma huu.

44

12:03 PM

Page 44


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? ni wa watu wa Yasin ambaye alisema: “Enyi kaumu, wafuateni Mitume”. Na Hizqil muumini wa watu wa Firaun ambaye alisema: “Mnamuua mtu kwa kusema tu Mola Wangu Mlezi ni Mwenyezi Mungu.” Na Ali bin Abi Talib na yeye ndiye mbora wao.” Chanzo: Dhakhairul-Uqba, uk. 56. Al-Jamius-Saghir: Juz. 115, chapa ya mwaka 1401 Beirut, chapa ya Darul-Fikri. As-Sawaiqul-Muhriqah fii-Raddi Ala ahlil-Bidaa Waz-Zindiqah, uk. 74 na 75, chapa ya Misri. Faydhul-Qadir: Juz. 4, uk. 238. Kifayatut-Talib, uk. 47. Kanzul-Ummal: Juz. 11, uk. 601, chapa ya mwaka 1399 Beirut. Muntakhabu Kanzul-Ummal, uk. 31 kwenye maelezo ya Musnad Ahmad: Juz. 5, chapa ya Misri.

Wewe Wasemaje?

Sunni Asema: Kwa uhakika kabisa aliye mbora kuliko viumbe wote wa Mwenyezi Mungu baada ya Mitume ni Abu Bakr As-Swiddiq. Hilo limesemwa na Abdur-Rahman As-Safur ndani ya kitabu chake Mukhtasar Al-Mahasin AlMujtamiah Fii fadhail-Khulafai Al-Ar’baah.

Na Shia Asema: Kwa uhakika kabisa aliye mbora kuliko viumbe wote wa Mwenyezi Mungu baada ya mbora wa Manabii na Mitume (s.a.w.w.) ni Imam kiongozi wa waumini Ali bin Abi Talib (a.s.) mwana wa ami ya Mtukufu Mtume, mume wa binti yake Fatima Mtakasifu, Al-Batul mbora wa wanawake wote wa ulimwengu, na mzazi wa wajukuu wawili, Al-Hasan na Al-Huseini mabwana wawili wa vijana wa Peponi.

45

12:03 PM

Page 45


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Kwa sababu sifa zote za ubora wa kibinadamu na ukamilifu wa kibinadamu zimejikusanya kwake, kama vile elimu, utawa, udhibiti wa nafsi, uchaji, ushujaa, ukarimu, uadilifu na nyinginezo miongoni mwa sifa za ukamilifu. Na Abu Bakr hakuwa na hata sifa moja kati ya hizi, na hilo litathibitika ndani ya kitabu hiki. Zaidi ya hapo ni kuwa Ali ni miongoni mwa watu wa nyumba ya Mtukufu Mtume(s.a.w.w.) ambao walishushiwa Aya ya Utakaso:

“Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu watu wa nyumba na kukutakaseni kabisa.” Sura Al-Ahzab: 33. Na ni miongoni mwa wale ambao bila shaka Mwenyezi Mungu alifaradhisha juu ya waislamu kuwapenda, akasema:

“Sema: Kwa haya siombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi kwa ndugu zangu wa karibu.”Sura Shura: 23. Na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) aliapizana na wakristo wa Najran kupitia yeye, mkewe na wanawe wawili Hasan na Huseini (a.s.), Mwenyezi Mungu akasema:

“Na atakayebishana nawe katika hili baada ya ujuzi uliokujia, basi 46

12:03 PM

Page 46


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake wetu na wanawake wenu, na nafsi zetu na nafsi zenu, kisha tuombe kwa unyenyekevu na tuiweke laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie wenye kusema uongo.�Sura Imran: 61. Mwenyezi Mungu akampa nafasi ya nafsi ya Mtume Wake mbora kuliko viumbe vyote vya Mwenyezi Mungu, na hiyo inatosha kuwa mbora kuliko viumbe wote. Ali (a.s.) alizaliwa ndani ya Ka’aba tukufu ambayo ndiyo Kibla cha waislamu ndani ya nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu, na hakuna yeyote aliyezaliwa ndani ya eneo hilo kabla yake na hata baada yake. Alikulia ndani ya nyumba ya ufunuo na ujumbe, na akaadabika kwa maadili ya Mtukufu Mtumena kupambika kwa tabia zake tukufu za kupendeza tangu akiwa mchanga mpaka alipokua na kuvuka miaka ya balehe. Katu hajaabudu sanamu lolote wala kusujudia sanamu lolote ndani ya maisha yake hata kidogo, na kwa ajili hiyo ndiyo maana linapotajwa jina lake husemwa (Mwenyezi Mungu autakase uso wake) yaani asisujudie sanamu lolote. Ama Abu Bakr yeye alizaliwa ndani ya nyumba ambayo wazazi wake wanaabudu masanamu na akakulia mikononi mwa waabudu masanamu na kulelewa kwenye vifua vya Washirikina na watu wa jahiliya mpaka alipokuwa kijana. Mtukufu Mtume(s.a.w.w.) alimuoza Ali (a.s.) binti yake Fatima Az-Zahra mbora wa wanawake wote wa ulimwengu. Chanzo: As-Sawaiqul-Muhriqah, uk. 97 kutoka kwa Abu Daud As-Sajistani mwandishi wa kitabu As-Sunan, moja ya Sahih Sita za Sunni.

47

12:03 PM

Page 47


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Mtukufu Mtume(s.a.w.w.) aliunga udugu kati ya sahaba zake mara ya kwanza huko Makka na mara nyingine huko Madina, na ndani ya mara zote mbili alimwambia Ali (a.s.): “Wewe ni ndugu yangu duniani na Akhera.” Chanzo: Al-Mustadrak Alas-Sahihayni: Juz. 2, uk. 14. Talkhisul-Mustadrak: Juz. 3, uk. 14. Kwa ajili ya sifa hizi na ubora huu akawa amewapita na kuwashinda waislamu wote katika ubora na ndio maana sisi Shia Imamiyya tunasema kuwa yeye (a.s.) kwa uhakika ndiye mbora kuliko viumbe wote wa Mwenyezi Mungu baada ya mwana wa ami yake, Mtukufu Mtume(s.a.w.w.).

Wewe wasemaje?

Sunni Asema: Sahaba walikuwa na adabu nzuri kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu na wakimuheshimu na kuheshimu athari zake. Abu Hasan As-Subki amesema: “Laiti tukikusanya Hadithi sahihi ambazo humo mna maelezo ya jinsi sahaba walivyokuwa wakimuheshimu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na wakiheshimu athari zake na adabu yao nzuri kwake, tutapata juzuu nyingi.29

Na Shia Asema: Tunatamani As-Subki angetutajia angalau Hadithi moja tu miongoni mwa hizo Hadithi sahihi ambazo zinaonyesha jinsi sahaba walivyomuheshimu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na athari zake pamoja na heshima yao kwake ili athibitishe dai lake la fedheha. 29- At-Tawassul Bin-Nabiyyi Wabis-Swalihiyn: Uk. 14, chapa ya Istambul 1986.

48

12:03 PM

Page 48


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Lakini kamwe hawezi, tena kamwe hawezi, tena kamwe hawezi, ni wakati gani ataweza kuleta Hadithi hiyo, kwani hakika Hadithi zilizomo ndani ya vitabu vyao zinazoonyesha mwenendo wa sahaba pamoja na Mtukufu Mtume(s.a.w.w.) zinathibitisha hali iliyo kinyume na madai yake. Zinatamka waziwazi jinsi walivyomvunjia heshima Mtume na watu wa nyumba yake baada yake, zimebeba maelezo ya mambo ambayo mtu hawezi kudhani kuwa yanaweza kutoka kwa mwislamu anayeamini kweli utume wa Mtukufu Mtumewetu (s.a.w.w.), isipokuwa siasa yake yenye hekima na maadili yake bora yalikuwa yakimzuia kufichua wazi siri ya mambo yao. Tunamtajia msomaji mpendwa baadhi ya mambo waliyopokea Sunni kuhusu wapenzi wao ndani ya vitabu vyao na wakaviandika kwa ajili yao ili kudumisha utajo wao na kusheherekea mambo yao. Na tunachotaraji kutoka kwa msomaji ni kuyachunguza na kuzama kwa makini ili ukweli umbainikie. Na ifuatayo ni baadhi tu ya mifano na inatosha kuthibitisha hoja. Abu Hamid bin Marzuk amesema: “Kauli yake (s.a.w.w.) ndani ya Sahihi: “Ewe Abu Bakr, ni kitu gani kimekukataza usiwe thabiti nilipokuamrisha?” Chanzo: At-Tawassul bin-Nabiyyi wabis-Salihina, ukurasa wa 112. Ewe Sabki, hivi laiti Abu Bakr angetekeleza amri ya Mtume kwa kuwa thabiti na bila kumuasi na kukimbia vitani, kauli ya Mtukufu Mtume(s.a.w.w.) ingekuwa na maana yoyote kwake? Hivi unahesabu uasi huu na kukhalifu amri ya Mtukufu Mtumendiyo heshima ya Imam wako Abu Bakr kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu? Huyu hapa Ibnu Abdur-Rabih Al-Andalusi naye ni miongoni mwa vipenzi wa Abu Bakr anasema: “Abu Bakr alimtuma Umar bin Al-Khattab akawatowe nyumbani kwa Fatima (wale waliyokataa kumpa kiapo cha utii, aki49

12:03 PM

Page 49


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? wemo Ali bin Abi Talib), na akamwambia: Wakikataa wauwe, basi akaenda akiwa na kijinga cha moto ili awaunguze kwa kuwachomea nyumba, ndipo akakutana na Fatima na kumwambia: “Ewe mwana wa Al-Khattab hivi umekuja ili uchome nyumba yetu? Akajibu: Ndiyo, au muingie ulimoingia umma.” Chanzo: Al-Aqdul-Farid: Juz. 2, uk. 197, chapa ya mwaka 1403 na Juz. 5, uk. 13, chapa ya mwaka 1407. Kauli ya Umar: “Au muingie ulimoingia umma”, maana yake mumpe Abu Bakr kiapo cha utii kuwa yeye ni khalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, na kama sivyo basi nitawaunguza kwa kuwachomea nyumba yenu. Umar bin Shibbah An-Numayru amesema: “Umar alikwenda nyumbani kwa Fatima wakiwemo humo baadhi ya watu wa Madina na wachache miongoni mwa watu wa Makka, akasema: “Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu imo mikononi Mwake, mtatoka kwenda kutoa kiapo cha utii au nitawaunguza kwa kuwachomea nyumba.” Chanzo: Sharhu Nahjul-Balagha cha Ibnu Abil-Hadid Al-Muutazil: Juz. 2, uk. 19, chapa ya mwaka 1329 Misri. Ewe Subki, hivi unahesabu uadui huu juu ya watu wa nyumba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu ni heshima ya Umar juu ya athari za Mtume wa Mwenyezi Mungu!! Hivi Mtume wa Mwenyezi Mungu hajasema: “Hakika Fatima ni pande la nyama yangu, yananiudhi yanayomuudhi.”?!! Na Mwenyezi Mungu anasema:

“Na wale wanaomuudhi Mtume wa Mwenyezi Mungu watapata adhabu iumizayo.” Suratul Tawba: 61. 50

12:03 PM

Page 50


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Chanzo: Sahih Muslim: Juz. 2, uk. 339, chapa ya mwaka 1327 Misri. Ibrahim bin Sayyar An-Nidham amesema: “Hakika Umar alilipiga tumbo la Fatima siku ya kiapo cha utii mpaka akamporomosha Muhsin kutoka tumboni mwake.” Chanzo: Al-Wafi bil-Wafiyati: Juz. 2, uk. 17. Ewe Sabki, na hili ni miongoni mwa heshima ya Imam wako Umar kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na athari zake? Na Bukhari amepokea kutoka kwa Aisha binti wa Abu Bakr kuwa alisema: “Fatima binti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alituma barua kwa Abu Bakr (r.a.) akimuomba mirathi yake kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kutoka kwenye mali aliyompa Mwenyezi Mungu Mtume Wake, na hapo Fatima alikuwa akiomba mali ya Mtume (s.a.w.w.) iliyoko Madina, Fadaki na khumsi iliyobakia kwenye khumsi ya Khaybari. Abu Bakr akasema: Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema: Sisi haturithiwi tunayoyaacha ni sadaka.” Chanzo: Sahih Bukhari: Juz. 2, uk. 301, na Juz. 3, uk. 55, chapa ya Misri kwenye maelezo ya As-Sindi. Binti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu alimjibu na kupinga dai lake la kusema kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema haturithiwi….. Dai ambalo linapingwa na zaidi ya Aya moja miongoni mwa Aya za Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu anasema:

51

12:03 PM

Page 51


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje?

“Mwenyezi Mungu anawausia kwa watoto wenu, mwanamume apate sawa na fungu la wanawake wawili…..” Sura An-Nisa: 11 Na pia akasema:

“Na Sulayman alimrithi Daudi…” Sura Nahli: 16. Aya hizi mbili zinatamka waziwazi kuthibitisha urithi kwa wana wa Manabii na wengineo, na je, mwisilamu atakubali kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) anapingana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Haiwezekani. Na Fatima binti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) yeye ni miongoni mwa watu wa nyumba ya Mtume walioshushiwa ‘Aya ya Utakaso’:

“Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu watu wa nyumba, na kukutakaseni kabisa.”61 Sura Al-Ahzab: 33. Ustadhi wa zama zetu mwandishi wa kimisri Khalid Muhammad Khalid anasema: “Bibi Fatima, radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake aliposikia tu jibu la Abu Bakr juu ya matakwa yake, uso wake ulijaa huzuni na uchungu.” Chanzo: Wajaa Abu Bakr, uk. 135, chapa ya Misri. Na kwa ajili ya Fatima Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: 52

12:03 PM

Page 52


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? “Fatima ni kipande cha nyama yangu, atakayemkasirisha kanikasirisha, na atakayemuudhi kaniudhi.” Chanzo: Al-Jamiu As-Saghir: Juz. 2, uk. 609. Nadhmu Duraru As-Samtwayn, uk. 176. As-Suyuti amesema: Hadithi ni sahihi, na imeondolewa (Atakayemuudhi ameniudhi). Na pia (s.a.w.w.) amesema: “Ridhaa ya Fatima ndio ridhaa yangu na kuchukia kwa Fatima ndio kuchukia kwangu, basi atakayempenda Fatima binti yangu atakuwa kanipenda na atakayemridhisha Fatima basi kaniridhisha, na atakayemchukiza Fatima basi kanichukiza.” Chanzo: Al-Imamah was-Siyasah: Juz. 1, uk. 13, chapa ya mwaka 1388 Misri. Jarida la kimisri Mimbarul-Islam, toleo la 7, mwaka 1388, la mwaka wa 26. Ustadhi Ahmad As-Shahawi Saad Sharafud-Din amesema: “Fatima alikuwa hajamaliza uchungu wa huzuni juu ya baba yake, ghafla akapatwa na uchungu wa mirathi yake ya kisheria…. Kama alivyopatwa na uchungu wa tatu nao ni mumewe kunyimwa haki yake ya ukhalifa, na ilikuwa ni lazima amuombe khalifa wa kwanza (Abu Bakr) haki hizi mbili pamoja. Bwana wetu Abu Bakr akamwambia: “Ama kuhusu mirathi yako kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu ni kuwa mimi nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akisema: ‘Sisi kundi la Manabii haturithiwi, tunayoyaacha ni sadaka.’ Hakika bibi Fatima aliendelea kulia juu ya haki hii na aliendelea kuumia na kupata uchungu kutokana na msimamo wa khalifa wa kwanza na waislamu waliokuwa pamoja naye. Na baada ya baba yake kufariki hakuzidi miezi sita naye kifo chake kikafika na muda wake ukatimia, hivyo akakutana na Mtume wa Mwenyezi Mungu.” 53

12:03 PM

Page 53


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Chanzo: Al-Batlah al-Mujahidah as-Sayyidah Zaynabu Karramallah Wajihahu, uk. 37, chapa ya Misri.

bintul-Imam Ali

Abu Hamid Al-Ghazali As-Shafi’i amesema: “Alipofariki Mtume kabla ya kufariki kwake alisema: Nileteeni kalamu na karatasi ili niwaondoleeni utata wa jambo na niwatajieni nani anayestahiki kwalo (Ukahlifa) baada yangu, Umar akasema: Mwacheni hakika yeye anaweweseka.” Chanzo: Makala ya nne ya Sirrul-Alamina, chapa ya Misri. Ewe Sabki, na hili ni miongoni mwa adabu ya Imam wako Umar na heshima yake kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, kumnasibisha na uwewesekaji ilihali yeye (s.a.w.w.) ndiye aliyethibitishwa na Mwenyezi Mungu kuwa hatamki kwa matamanio bali ni ufunuo anaofunuliwa? Aidhu bin Rabia amesema: “Sharih bin Harith aliendelea kuwa kiongozi mwakilishi wa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa kaumu yake na kiongozi mwakilishi wa Abu Bakr, Umar alipochukua utawala alimletea hati ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, basi akaichukua na kuiweka chini ya nyayo zake na kusema: Yeye si chochote isipokuwa ni mfalme ameshapita.” Chanzo: Ta’rikhul-Madinah al-Munawwarah: Juz. 2, uk. 596, chapa ya mwaka 1410 Beirut, chapa ya Darut-Turathi Al-Islamiyyah. Ewe Sabki, hivi unahesabu kitendo cha Imam wako Umar kuikanyaga barua ya Mtukufu Mtumena kuidharau hati ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ni kumuheshimu Mtukufu Mtumena athari zake?!! Enyi kina Sabki, acheni uongo na kupotosha, kwani hakika Mwenyezi Mungu atawauliza kuhusu matendo yenu na kauli zenu Siku ya Kiyama, wewe si umesema kuwa: “Hakika atakayeporomosha hadhi ya cheo cha 54

12:03 PM

Page 54


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Mtukufu Mtumekuhusu yale yaliyo ya lazima kwake bila shaka kakufuru?” Ewe Sabki, sasa unasemaje kuhusu Imam wako Umar na tayari ameshaporomosha hadhi ya Mtukufu Mtume(s.a.w.w.). Chanzo: At-Tawassul bin-Nabiyyi wabis-Salihin, ukurasa wa 125, chapa ya mwaka 1407 Misri. Al-Hasan amesema: “Abdullah bin Ubayya alimuomba Mtukufu Mtumekanzu yake ili iwe sanda ya baba yake, Mtume akampa. Umar (r.a.) akasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, unampa huyu mnafiki kanzu yako ili afanyiwe sanda.” Mtume akasema: “Ole wako ewe mwana wa Al-Khattab, kuna ubaya gani mimi kuungana na wana wa Najari kupitia kanzu yangu.” Chanzo: Ta’rikhul-Madinah: Juz. 1, uk. 370. Abdullah bin Umar amesema: “Alipofariki Ubayya alikuja mwanae Abdullah kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akamuomba ampe kanzu yake ili akamvishie sanda baba yake, akampa, kisha akamuomba amsalie, Mtume wa Mwenyezi Mungu akasimama ili amsalie. Umar akasimama na kukamata nguo ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na kumwambia: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu unamsalia ilihali Mola Wako Mlezi amekukataza usimsalie?....” Chanzo: Sahih Bukhari: Juz. 3, uk. 137. Ibnu Shibah amesema: “Kisha akasimama ili amsalie, ndipo Umar (r.a.) akamshika mkono wake na kumwambia: Unamsalia ilihali yeye ni mnafiki na Mola Wako Mlezi amekukataza?.....” 55

12:03 PM

Page 55


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Chanzo: Ta’rikhul-Madinah: Juz. 1, uk. 373. Ar-Radhawi: Inamaanisha vipi: unakhalifu amri ya Mola Wako Mlezi na unamuasi kwa wewe kumsalia. Nasiru bin Sulayman Al-Ammar amesema: “Hakika Umar alipojua kuwa Mtukufu Mtumeameazimia kufanya suluhu ya Hudaybiyya na haijabakia ila kuandika hati ya suluhu alikasirika sana, na akaenda kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na kumwambia: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hivi sisi si waislamu na wao si mushirikina? Akasema: “Ndiyo, sisi ni waislamu na wao ni mushirikina.” Akasema: “Juu ya lipi tuwe dhalili katika dini yetu?” Mtume akasema: “Mimi ni mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, sitokhalifu amri Yake na wala hatonitupa.” Chanzo: Haqiqatul-Ansar, uk. 92, chapa ya mwaka 1412 Riyadhi, chapa ya DarulWatan. Ar-Radhawi: Inamaanisha; inakuwaje unafanya suluhu kati ya waislamu na mushirikina na kuleta udhalili ndani ya dini ilihali wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akamwambia: Sikufanya hivyo ila ni kwa amri kutoka kwa Mola Wangu Mlezi na kamwe sitoasi amri Yake. Imran bin Husni Al-Khazai (Abu Nujid) amesema: “Kuna mwanamke kutoka Juhaynah alikwenda kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ilihali akiwa mjamzito kutokana na zinaa, akamwambia: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu nimepata adhabu nitekelezee”, basi Mtume wa Mwenyezi Mungu akaita wanawake wakamfunga nguo zake kisha akaamuru wakampopoa mawe, kisha akamsalia.”

56

12:03 PM

Page 56


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Umar akasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, unamsalia ilihali amezini?” Ameipokea Muslim. Chanzo: Al-Mustatrafu: Juz. 2, uk. 289. Ar-Radhawi: Inamaanisha; mzinifu wa kike haifai kuswaliwa hata kama ni mwislamu, inakuwaje wewe unamsalia ilihali wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Sheikh mmoja kutoka Basra alimuuliza Yahya bin Akthami: “Unamfuata nani katika ndoa ya Mut’a?” Akajibu: “Umar bin Al-Khattab (r.a.).” Akasema: “Vipi, ilhali Umar alikuwa miongoni mwa watu wanaoipiga sana vita?” Akasema: “Ndiyo, imesihi Hadithi kuwa alipanda mimbari na kusema: “Enyi watu, Mut’a mbili alizihalalisha Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mimi naziharamisha kwenu na nitatoa adhabu juu yake.” Hivyo tumekubali ushahidi wake na hatujakubali uharamishaji wake.” Chanzo: Islam bilaa madhaahibi chapa ya tano, uk. 200. Mufti wa kishafi’i wa Makka tukufu Ahmad Zayni Dahlani amesema: “Kuna mtu alikwenda kwa Mtukufu Mtume(s.a.w.w.) na kumuomba, Mtume akamwambia: “Sina kitu lakini kopa kwa niaba yangu nikipata kitu nitalipa.” Umar akasema: ‘Mwenyezi Mungu hajakulazimisha usiloliweza.’ Hapo Mtume akakasirishwa na hilo.’” Chanzo: Al-Futuhatul-Islamiyyah: Juz. 2, uk. 354. Ar-Radhawi: Ewe Sabki, unaona Imam wako Umar kumwambia haya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ni kumuheshimu? Hivyo akamtamkia kauli chafu mpaka (s.a.w.w.) akadhihirisha kuchukizwa kwake. Je, 57

12:03 PM

Page 57


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa hajui kuwa Mwenyezi Mungu hajamlazimisha hilo ndio maana akamuahidi mtu huyo na Umar alikuwa anajua ndio maana akaona ni wajibu kwake kumzindua Mtukufu Mtumejuu ya kosa lake? Muhibud-dini Al-Khatibu katika kumsifia Umar amesema: “Hakika roho yake ilichanganyikana na Sunna ya Mtume, na maisha yake yakachanganyikana na imani ya Uislam, kana kwamba Wahyi na Ufunuo vinaafiki ufahamu wake na imani yake.” Chanzo: Al-Awasim wal-Qawasim Al-Muutamidah Alal-Muwatai: Juz. 2, uk. 1007, chapa ya mwaka 1370 Misri, chapa ya Daru Ihyail-Kutubi Al-Arabiyyah. Kwa sifa hizi za uongo mmewapoteza watu dhidi ya dini ya Mwenyezi Mungu, na adhabu itawapata. Ewe Sabki, tazama misimamo ya mama yenu na binti wa Imam wenu wa kwanza, Aisha mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.). Huyu hapa Ahmad Zayni Dahlan anasema: “Kuna siku ulitokea mzozo kati ya Aisha na Mtume mpaka Abu Bakr akaingilia ili ahukumu. Mtume wa Mwenyezi Mungu akamwambia Aisha: “Unaelezea wewe au nielezee mimi?” Akajibu: “Elezea na wala usiseme ila lililo haki……” Na mara nyingine akamkasirikia Mtume katika mazungumzo na kumtamkia: “Wewe ndiye ambaye unadai eti wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu …… Na akamwambia tena: Hakika jina lako baya.” Chanzo: Al-Futuhatil-Islamiyyah: Juz. 2, uk. 478, chapa ya mwaka 1354 Misri, chapa ya Mustafa Muhammad.

58

12:03 PM

Page 58


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Ewe Sabki, unaona maneno yake haya kumwambia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ambaye hatamki kwa matamanio kama Mwenyezi Mungu alivyomsifia kwa hilo ndani ya Kitabu Chake ni kumuheshimu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) au ni kutaka kutia dosari utume wake? Laiti angekuwa anaamini unabii wake na kuwa yeye hatamki kwa matamanio bali ni kwa Wahyi anaofunuliwa, hivi kumwambia: “Elezea na wala usiseme ila lililo haki.” Na kumwambia: “Wewe ndiye ambaye unadai eti wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu.” Kungekuwa na maana yoyote? Ni lini mtaamka kutoka kwenye usingizi wenu enyi wafuasi wa Umar, ni lini mtarejea kwenye akili zenu enyi mliopotea wenye kuwapoteza watu.

Wewe wasemaje?

Sunni Asema: Sisi Sunni tunaweheshimu sahaba wote wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na tunawatakasa dhidi ya kila dosari na upungufu, na tunawafanya bora kuliko waislamu wote na wala hatuwahukumu vibaya kwa chochote walichokitenda, vyovyote vile watakavyotenda. Hujatul-Islam Abu Hamid Al-Ghazali As-Shafi’i amesema: “Imani ya Sunni ni kuwatakasa swahaba wote na kuwasifia kwa mazuri, kama ambavyo Mwenyezi Mungu na Mtume Wake walivyowasifia kwa mazuri.”30 Ar-Radhawi: Hilo ni dai lisilo na dalili, bali dalili inathibitisha hali kinyume na hiyo, hivyo huo ni uongo wa wazi kwani Mwenyezi Mungu 30. Ihyau Ulumid-Din: Juz. 1, uk. 99, chapa ya mwaka 1316 Misri.

59

12:03 PM

Page 59


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? hajawasifia kwa mazuri, na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwatia dosari kama utakavyoona. Na Ahmad bin Hajar Al-Haytham amesema: “Jua kuwa walilokubaliana kwalo Sunni ni kuwa ni wajibu kwa kila mwislamu kuwatakasa sahaba wote kwa kuthibitisha uadilifu wao, kuwasifia kwa mazuri na kuacha kuwatia dosari.”31 Na pia Akasema: “Na ni haki ambayo ni lazima kuiamini kutokana na heshima ya sahaba na kuepukika kwao na kila upungufu.”32 Ar-Radhawi: Makubaliano anayodai Ibnu Hajar ya watu wa madhahebu yake ya Sunni juu ya wajibu wa kila mwislamu kuwatakasa sahaba wote hayathibitishi wajibu, kwani hayo ni madai matupu yasiyo na dalili, kwani wajibu wowote ule ni faradhi itokayo kwa Mwenyezi Mungu kupitia habari anayotupa Mtukufu Mtume(s.a.w.w.) na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) yeye mwenyewe amewatia dosari sahaba, kama utakavyosoma hilo ndani ya kitabu hiki. Mkaguzi wa elimu ya dini huko Misri Hasan Mutawal amesema: “Si halali kufuatilia yaliyotokea kati ya sahaba……”33 Ibnu Saleh na An-Nanawi wamesema: “Sahaba wote ni waadilifu, na Mtume wakati wa kifo chake alikuwa na sahaba laki moja na kumi na nne elfu. Na Qur’ani na riwaya zinatamka wazi bila tuhuma, na yale yaliy31.As-Sawaiqul-Muhriqah, uk. 206, chapa ya mwaka 1375 Misri. 32. As-Sawaiqul-Muhriqah, uk. 222. Madai haya ni uongo wa wazi kwani atakayefuatilia kitabu hiki na kufuatilia kwa makini baadhi ya vipengele vyake itambainikia kwa wazi kabisa uongo wa Ibnu Hajar katika kuwapamba sahaba kwa sifa hii. 33. Moduli ya Tauhid kwa ajili ya kidato cha tatu, uk. 62. Hii ni fatwa ya rai binafsi isiyokuwa na nguvu yoyote ya kisheria.

60

12:03 PM

Page 60


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? otokea kati yao yana tafsiri mbalimbali……”34

Na Shia Asema: Sisi Shia Imamiyya tunaoamini Uimamu wa Maimamu kumi na wawili hatumuheshimu eti kila swahaba na wala hatuwatakasi kwa kauli moja bila mipaka. Kwa sababu miongoni mwao yumo aliye dhalimu, mnafiki, fasiki na aliyeritadi, na hawa ni lazima kujitenga nao. Bali tunawaheshimu wale walio waumini na wachamungu miongoni mwao. Mwenyezi Mungu anasema:

“Basi anayefanya wema sawa na chembe atauona.* Na anayefanya uovu sawa na chembe atauona.”68 Surat Al-Zilzalah: 4. Na hili ni jambo la mjumuisho linamjumuisha kila mwisilamu, sawa awe sahaba au asiwe sahaba. Hivyo kauli ya Abu Hamid Al-Ghazal ahs-Shafi’i kuwa itikadi ya Sunni ni kuwatakasa sahaba wote na kuwasifia kwa mazuri, na pia kauli ya aliyemfuata katika kupenda huko kulikovuka mipa34. As-Sawaiqul-Muhriqah. Atakayefatilia maneno ya hawa wanaowapenda sahaba hadi kupita kipimo, na akafatilia mwenendo wa sahaba, vitendo vyao na kauli zao utambainikia uongo wao katika kuwapamba sahaba. Na ndani ya kitabu hiki tutapata mwenendo wao wa aibu ambao ndani yake walikhalifu Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na kutafsiri vitendo vyao hivyo vibaya kuwa ni juhudi za kielimu. Bidaa hii waliyoizusha inaonyesha uchache wa akili zao, pale wanapodai kuwa wao wamefanya juhudi za kielimu lakini wamekosea, hivyo mwenye kupatia miongoni mwao hupata thawabu mbili na mwenye kukosea hupata thawabu moja. Hiyo inamaanisha kuwa Mu'awiyya atapata thawabu kwa kupigana vita na Imam wa zama zake, kwani yeye alitumia juhudi za kielimu lakini akakosea. Hii ni kwa mujibu wa akili zao.

61

12:03 PM

Page 61


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? ka, inapingana na tamko la wazi la Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Na kutokana na kupenda huku kwa aibu wamewapoteza watu wa kawaida dhidi ya haki na kuwapofua macho yao dhidi ya uongofu, na watapata adhabu kali. Na kuhusu sahaba wanafiki Mwenyezi Mungu amesema mwanzo tu wa Suratul-Munafiquun: “Wanapokujia wanafiki husema: Tunashuhudia ya kuwa, kwa hakika wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu anajua kwa hakika wewe ni Mtume Wake, na Mwenyezi Mungu anashuhudia ya kuwa, kwa hakika wanafiki ni waongo hasa. Wamevifanya viapo vyao ngao, wakaiacha njia ya Mwenyezi Mungu, kwa hakika ni mabaya waliyokuwa wakifanya.” Na akasema:

“Hakika Wanafiki watakuwa katika tabaka ya chini kabisa Motoni.” Suratun-Nisai: 145. Na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akasema: “Mimi nitawatangulia kufika kwenye Hodhi, na watu miongoni mwa sahaba zangu watanikimbilia lakini hawatanifikia. Kisha nitaambiwa: Hakika wewe hujui waliyoyazusha baada yako.” Chanzo: Musnad Ahmad: Juz. 1, uk. 406, chapa ya Misri. Na katika Hadithi nyingine: “Mimi nitawatangulia kufika kwenye Hodhi, na watu miongoni mwenu watainuliwa kuelekezwa upande wangu, lakini nitakapowafuata ili niwanyweshe watasogezwa mbali na mimi. Nitasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Hawa ni sahaba zangu! Nitaambiwa: Hujui waliyoyazusha baada yako.” 62

12:03 PM

Page 62


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Chanzo: Sahih Bukhari: Juz. 4, uk. 221, chapa ya Misri kwenye maelezo ya AsSindi. Na katika Hadithi nyingine: “Watu miongoni mwa sahaba zangu watachukuliwa na kuelekezwa upande wa kushoto,35 kisha mimi nitasema: sahaba zangu! sahaba zangu! Nitaambiwa: Hakika wao hawakuacha kurudi nyuma tangu ulipowaacha…..” Chanzo: Sahih Bukhari: Juz 2, uk. 233, chapa ya Misri kwenye maelezo ya AsSindi. Na Mwenyezi Mungu ametupa habari za kuritadi kwao baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ndani ya Kitabu Chake kitukufu kwa kusema:

“Na hakuwa Muhammad ila ni Mtume aliyepitiwa na Mitume kabla yake. Basi je, akifa au akiuliwa mtarudi nyuma kwa visigino vyenu? Na atakayerudi nyuma kwa visigino vyake hatamdhuru kitu Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu atawalipa wanaoshukuru.”Sura Imran: 144. 35. Ili wafikishiwe sehemu inayowafaa wao, Mwenyezi Mungu anasema: "Na watu wa kushoto, watakuwa vipi watu wa kushoto. Watakuwa katika upepo wa moto na maji yachemkayo. Na kivuli cha moshi mweusi sana. Si baridi wala si starehe."- Sura Waqia: 41.

63

12:03 PM

Page 63


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Ni wajibu kwa kila mwislamu kujitenga na sahaba wanafiki na wenye kuritadi baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ili isihi imani yake kwa Mtume na awe mkweli wa imani. Mwenyezi Mungu anasema: “Hupati watu wanaomuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, kuwa wanawapenda wale wanaompinga Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, hata wakiwa ni baba zao au watoto wao au ndugu zao au jamaa zao….” 36 Mkaguzi wa elimu ya dini huko Misri Hasan Mutawal amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: ‘Msiwatusi sahaba zangu, atakayewatusi basi laana ya Mwenyezi Mungu na Malaika na watu wote itakuwa juu yake, na Mwenyezi Mungu hakubali badala wala fidia kutoka kwao.’” Ar-Radhawi: Hadithi hii ni uzushi wa wale wanaowapenda sahaba kupita mipaka, na dalili juu ya uongo wake ni ile riwaya aliyoipokea Ahmad bin Hanbal mmoja wa maimamu wanne kuwa: “Mtu mmoja alimtukana Abu Bakr ilihali Mtukufu Mtumeakiwa ameketi, basi Mtume akawa anamshangaa na akitabasamu.” Chanzo: Musnad Ahmad: Juz. 2, uk. 436. Hayatus-Sahabah: Juz. 2, uk. 154. Na laiti yangesihi aliyoyanasibisha Hasan Mutawal kwa Mtume, kuwa alikataza kuwatukana sahaba basi (s.a.w.w.) angemkataza mtu huyo hilo na wala asingestaajabu na kufurahi. Na hawa wanaowapenda swahaba kupita mipaka hawajajidhibiti na uongo katika kuwapamba na kuwatakasa sahaba kwa kauli moja bila mipaka, bali wameendelea kuwathibitishia wote uadilifu bila kujali yote mabaya waliyoyatenda, na madhambi makubwa waliyoyafanya. 36.Mwishoni mwa Suratul Mujadalah

64

12:03 PM

Page 64


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Na wapo ambao tayari umeshajua hali yao miongoni mwa sahaba ambao sira yao imechafua uso wa historia ya Uislamu kwa kukhalifu Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya Mtume Wake (s.a.w.w.) pamoja na viongozi wa waislamu, wa kwanza wao Mtukufu Mtumena watu wa nyumba yake watakasifu ambao Mwenyezi Mungu amewaondolea uchafu na kuwatakasa kabisa, ambao Mwenyezi Mungu amefaradhisha mapenzi juu yao kwa waislamu kwa kusema:

“Sema: Kwa haya siombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi kwa ndugu zangu wa karibu.” Surat Shura: 23. Huyu hapa Muhammad bin Abdul-Wahab An-Najdi anasema: “Hakika kundi moja miongoni mwa sahaba walikuwa wakipigana bega kwa bega pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu, na wakiswali pamoja naye, wakitoa Zaka na kufunga na kuhiji, lakini pamoja na hayo yote walikuwa makafiri wenye kujitenga na Uislamu.” Chanzo: Risalatu Kashfu-Shubhat, uk. 120, kutoka kwenye Ar-Rasailu AlAlamiyyah At-Tisaa cha Muhammad bin Abdul-Wahabi. Adh-Dhahabi amesema: “Baadhi ya sahaba walikufurishana wao kwa wao.” Chanzo: Ma’rifatu ar-Ruwat, uk. 45, chapa ya Darul-Fikri Beirut. Na miongoni mwa sahaba yupo aliyetoka kwenda kumpiga vita Imam wa zama zao Imam Ali bin Abi Talib (a.s.) mwana wa ami ya Mtume wa Mwenyezi Mungu na khalifa wake, akatoka kumpiga vita huku akihalal65

12:03 PM

Page 65


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? isha damu yake na damu ya sahaba wa Mtukufu Mtume waliokuwa naye, bila kujali kauli ya Mtukufu Mtume: “Ewe Ali, kukupiga vita wewe ni kunipiga vita mimi…” Chanzo: Yanabiul-Mawaddah cha Al-Qanduzi Al-Hanaf, uk. 55, na uk. 71, chapa ya mwaka 1302 Istambul. Na kwa imani yetu ni kuwa mwenye kumpiga vita Mtukufu Mtume ni kafiri. Na kwa ajili hiyo sisi Shia Imamiyya wafuasi wa Maimamu kumi na wawili tunawaheshimu wachamungu na waumini miongoni mwa sahaba na tunawatukuza, na tunajitenga na wale waliomuasi Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wakavuka mipaka ya Uislamu na kuvunja heshima yake. Mwenyezi Mungu anasema: “Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni aliye mchamungu zaidi katika nyinyi.” Hivyo mwislamu atakayekuwa mchamungu mno kuliko mwingine ndiye mwenye hadhi mbele ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mbele yetu sisi Shia Imamiyya na wala si mwingine. Mkaguzi wa elimu ya dini huko Misri Hasan Mutawal, katika hali ya kuwatakasa sahaba waliokwenda kinyume na Uislamu na waliovuka mipaka yake amesema: “Ugomvi uliyotokea kati yao kama vile suala la Ali na Mu’awiya, umetafsiriwa kuwa ni juhudi zao za kielimu, hivyo aliyepatia ana thawabu mbili na aliyekosea ana thawabu moja.” Chanzo: Moduli ya Tauhidi ya kidato cha tatu, ukurasa wa 82. Maana ya maneno haya ya upuuzi ni kuwa Mu’awiya aliyelaniwa aliyempiga vita khalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) wa kisheria na mwana wa ami yake ambaye Mwenyezi Mungu aliwaamuru waislamu wampende kwa ushahidi wa Aya: 66

12:03 PM

Page 66


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje?

“Sema: Kwa haya siombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi katika ndugu,” Surat Shura: 23. atalipwa thawabu mbele ya Mwenyezi Mungu kwa kitendo cha kumpiga vita (Ali) hata kama Mtukufu Mtume alimwambia Ali: “Kukupiga vita wewe ni kunipiga vita mimi…” Mwenyezi Mungu amlaani yule aliyewahalalishieni kauli ya juhudi za kielimu, hivyo kwa kauli hiyo mkafanya makusudi kuvuka mipaka ya Mwenyezi Mungu na kuvunja heshima zake, enyi wenye kuwapoteza wajinga ndani ya umma wa Muhammad (s.a.w.w.). Na kauli ya Al-Ghazali aliye dalili ya Uislam wenu kuwa: “Yaliyotokea kati ya Mu’awiya na Ali (r.a.) yalitokana na juhudi za kielimu, na wanachuoni wakubwa wamesema: Kila mwenye kufanya juhudi za kielimu amepatia.” Ndiyo iliyowapa ujasiri wa kutamka maneno duni yasiyo na maana. Basi ikiwa fatwa za wanachuoni wenu wakubwa kama alivyosema AlGhazali aliye dalili ya Uislam wenu wa makosa ni sahihi kwenu, na ndio tegemeo lenu katika kumtetea yule sahaba aliyetenda haramu na kuvuka mipaka ya Mwenyezi Mungu, kwa nini basi Aisha binti wa khalifa wenu wa kwanza alisema kuhusu Uthman khalifa wenu wa tatu baada ya waislamu kuhalalisha damu yake na kumuuwa walipoona amekwenda kinyume na Uislam na amevuka mipaka yake: “Ewe Mwenyezi Mungu mtenge mbali, hilo ni kutokana na matendo yake, na Mwenyezi Mungu si mwenye kumdhulumu mja.” Chanzo: Sharhu Nahjul-Balagha cha Ibnu Abu Hadid Al-Muutazil: Juz. 2, uk. 77, chapa ya mwaka 1329 Misri. Na wala Aisha hakutafsiri uendaji kinyume wa Uthman dhidi ya Uislam 67

12:03 PM

Page 67


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? katika vitendo vyake kuwa ni juhudi za kielimu ambazo zitamuhakikishia thawabu moja kwa kila kosa alilolitenda na baya alilolifanya, na ndiyo maana akamuombea dua mbaya. Na kwa nini Fatima (a.s.) binti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimkasirikia Abu Bakr Imam wenu wa kwanza alipomuomba haki yake na mirathi yake kutoka kwa baba yake baada ya Abu Bakr kumnyima huku akitoa hoja kutumia kauli aliyomzushia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), nayo ni kuwa: “Sisi kundi la Manabii haturithiwi, tunayoyaacha ni sadaka.” Kauli ambayo inapingwa na zaidi ya Aya moja toka kwenye Aya za Kitabu cha Mwenyezi Mungu, kati ya hizo ni:

“Na Sulaymani alimrithi Daudi.” Suratun-Naml: 16. Na Fatima akamjibu: “Naapa kwa Mwenyezi Mungu, nitakuombea dua mbaya ndani ya kila Swala ninayosali.” Chanzo: Al-Imamah was-Siyasah: Juz. 1, uk. 14. Na akamwambia yeye na Umar: “Naapa kwa Mwenyezi Mungu, kamwe sitowasemesha.” Na akafariki ilihali hawasemeshi. Chanzo: Sahih At-Tirmidhi: Juz 1, Uk. 303, mlango unaohusu mirathi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na pia akawaambia wao wawili: “Hakika mimi namfanya Mwenyezi Mungu na Malaika Wake kuwa shahidi, bila shaka nyinyi wawili mmenichukiza na hamjaniridhisha, na nikikutana na Mtukufu Mtume nitawashitakia kwake.” 68

12:03 PM

Page 68


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Chanzo: Fatimah az-Zahrau wal-Fatimiyun, uk. 328, chapa ya mwaka 1974 Beirut, chapa ya Darul-Kitabi Al-Lubnan. Je, kitendo cha kuzuia haki yake na mirathi yake kutoka kwa baba yake umetafsiri kuwa ni juhudi za kielimu ambazo Mwenyezi Mungu kwazo atamlipa thawabu hata kama amekosea, kama mnavyodai nyinyi? Na je, Fatima (a.s.) hakufa ilihali amemkasirikia? Mkaguzi wa elimu ya dini huko Misri Hasan Mutawal, katika hali ya kumtetea Imam wake Abu Bakr kwa kitendo cha kumnyima Fatima (a.s.) haki yake na mirathi yake kutoka kwa baba yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Ama mzozo wa bibi Fatima binti wa Mtukufu Mtume pamoja na Abu Bakr unatafsiriwa kuwa yeye (a.s.) hakufikiwa na Hadithi hii: Sisi kundi la Manabii haturithiwi, tunayoyaacha ni sadaka.” Chanzo: Moduli ya Tauhidi ya kidato cha tatu. Kweli mtu huyu ni juha sana na mpotevu sana dhidi ya haki, yeye kwa tafsiri yake hii duni ya makosa ananasibisha ujinga kwa Fatima binti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) aliyelelewa ndani ya nyumba ya Wahyi na utume, ili tu amtetee Imam wake mwenye kumzushia uongo Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kwa kumnasibishia kauli ya: “Sisi kundi la Manabii haturithiwi, tunayoyaacha ni sadaka….”. Kauli ambayo inapingwa na kauli ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu:

69

12:03 PM

Page 69


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje?

“Na Sulaymani alimrithi Daudi.”Suratun-Naml: 16. Na kauli Yake kuhusu Zakariya:

“Basi nipe mrithi kutoka kwako. Atakayenirithi…”Surat Maryam: 5. Na kauli ya Mwenyezi Mungu:

Mwenyezi Mungu anawausia kwa watoto wenu, mwanamume apate sawa na fungu la wanawake wawili…”.Suratun-Nisai: 11. Na kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Wanaume wana fungu katika yale waliyoyaacha wazazi na jamaa waliowakaribia, na wanawake wana fungu katika yale waliyoyaacha wazazi na jamaa waliowakaribia, ikiwa kidogo au kingi, fungu lililofaradhishwa.”Suratun-Nisai: 7. Ewe juha, ikiwa kwa mujibu wa kauli yako haijamfikia Hadithi hii, yaani aliyozushiwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), je, yeye (a.s.) alikuwa hazijui Aya za urithi, jumuishi na husishi, ilihali ndani ya nyumba aliyozaliwa 70

12:03 PM

Page 70


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? ndimo zilimoteremkia? Alikuwa anazijua ndiyo maana akatoka nyumbani kwake mpaka msikitini kwenda kumuomba Abu Bakr haki yake. Na je, Imam Ali bin Abi Talib naye alikuwa hajui kuwa yeye (a.s.) hana haki, hivyo akashindwa kumzuia asiende kwa Abu Bakr kutafuta haki yake? Au alitoka ndani ya nyumba yake bila kupewa idhini na Imam? Ni kweli kabisa mmepotea dhidi ya uongofu na macho yenu yamepofuka dhidi ya haki, na kwa ajili hiyo hamjaongokewa njia. Ni kwa nini basi alikata mahusiano na Abu Bakr na hakumsemesha mpaka anafariki akiwa amemkasirikia, na akaacha usia azikwe usiku na kaburi lake lifichwe ili yeye na rafiki yake Umar wasihudhurie mazishi yake, na ili waislamu wajue kuwa yeye (a.s.) amefariki huku akiwa ni mwenye kumchukia Abu Bakr kwa sababu alimdhulumu haki yake na akamnyima urithi wake kutoka kwa baba yake, na dhalimu hafai kuwa khalifa wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), hivyo huenda waislamu watazindiukana kutoka kwenye mghafala wao ikiwa wameghafilika, na warejee kwenye uongofu wao na hivyo wabadili mwenendo wao. Bado mpaka leo kaburi lake halijulikani, hata kwa wanae na wajukuu zake,37 na watajua madhalimu ni mgeuko gani watakaogeuka.

Wewe Wasemaje? 37.Hakuna anayelijua kaburi la kipenzi cha Mtukufu Mtumena binti yake mpendwa aliyekuwa mke wa kipenzi chake, khalifa wake, mrithi wa elimu yake na jemedari wa jeshi lake Ali bin Abi Talib, kaburi la binti aliyemzalia Mtukufu Mtume wajukuu wawili, manukato yake mawili na mabwana wawili wa vijana wa peponi Hasan na Huseini, hakuna anayelijua ila watu wa nyumba ya Mtukufu Mtume ambao ni Maimamu watakatifu, akiwemo Imam wa zama hizi, faraja inayongojewa na matumaini yanayosubiriwa, mkombozi aliyehifadhiwa na ushindi unaokaribia, Imam Mahdi (a.s.) - Mtarjumi.

71

12:03 PM

Page 71


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje?

Sunni Asema: Masahaba wote ni watu wa Peponi bila shaka yoyote. Hilo limesemwa na Ibnu Hazmi38, na mfano wa kauli hiyo imesemwa na wanazuoni wengine wa kisunni.

Na Shia Asema: Si masahaba wote ni watu wa Peponi bila shaka. Kwani hali yao ni sawa na hali ya watu wengine wa zama zote, yumo aliye muumini wa kweli na aliye mnafiki, mwema mchamungu na fasiki muovu, na Peponi hawaingii wanafiki. Mwenyezi Mungu amesema mwanzoni mwa Sura ya Munafiquun: “Wanapokujia wanafiki husema: Tunashuhudia ya kuwa, kwa hakika wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu anajua kwa hakika wewe ni Mtume Wake, na Mwenyezi Mungu anashuhudia ya kuwa, kwa hakika wanafiki ni waongo hasa.* Wamevifanya viapo vyao ngao, wakaiacha njia ya Mwenyezi Mungu, kwa hakika ni mabaya waliyokuwa wakifanya.” Aya hii inatamka waziwazi kuwa miongoni mwa sahaba wa Mtukufu Mtume wamo wanafiki, Mwenyezi Mungu awalaani, walikuwa wakihudhuria pamoja naye kwenye Swala na wanamfuata ndani ya Swala hiyo, isipokuwa kwa ajili ya kutokuamini kwao na ubovu wa imani yao walikuwa wakitanguliza dunia kuliko dini, hivyo walikuwa wakikata Swala na kwenda kwenye mchezo na biashara, kama Mwenyezi Mungu alivyofichua habari zao kwa kusema: “Na wanapoiona biashara au mchezo wanavikimbilia na wanakuacha umesimama, sema: Yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu ni bora kuliko mchezo na biashara, na Mwenyezi Mungu ni Mbora wa watoa riziki.39 38. Al-Isabah fi-m'arifatis-Sahabah, uk. 10. 39.”Mwishoni mwa Suratul-Jumua.

72

12:03 PM

Page 72


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Na akasema tena:

“Hakika wanafiki watakuwa katika tabaka ya chini kabisa Motoni.” Suratun-Nisai: 145. Na kauli ya kusema wao wote ni watu wa Peponi ni uongo mtupu na kuwapenda kupita kiasi na ni kuwapoteza wasiojua. Na ni kuipinga Qur’ani tukufu ambayo imetamka wazi kuwa sahaba wanafiki wapo na ni watu wa tabaka la chini kabisa la Motoni, na huo ni ukafiri wa wazi. Ad-Dhahabi amesema: “Baadhi ya sahaba walikufurishana wao kwa wao.40” Itakuwaje aliyekufurishwa awe miongoni mwa watu wa Peponi? Kwa nini hamuwi na akili?

Wewe wasemaje?

Sunni Asema: Sisi Sunni wafuasi wa madhehebu manne tunawapenda watu wa nyumba ya Mtume, radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao.

Na Shia Asema: Sisi Shia wafuasi wa Maimamu kumi na wawili tunawapenda watu wa nyumba ya Mtume wetu, amani iwe juu yao, na tuna mapenzi ya dhati kwao. Dalili ya Ukweli wa dai letu la kuwapenda wao ni kuwafuata na kuwapa mgongo wasiyokuwa wao, na kuwapenda vipenzi vyao na kuwapiga vita 40. Ma'rifatur-Ruwat, uk. 45, chapa ya Darul-Maarifah Beirut.

73

12:03 PM

Page 73


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? maadui zao na kujitenga na yule aliyewadhulumu. Hivyo sisi hufurahishwa na kile kinachowafurahisha na huhuzunishwa na kile kinachowahuzunisha, na wala hatujali chochote tunachokumbana nacho kutoka kwa maadui zetu katika njia hii. Mwenyezi Mungu anasema:

“Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu, basi nifuateni Mwenyezi Mungu atawapenda na atawasamehe madhambi yenu.”Surat al-Imran: 31. Aya hii tukufu inatufidisha kuwa ili tumpende Mwenyezi Mungu Mtukufu ni lazima tumfuate Mtume Wake (s.a.w.w.), na yeye ametuamuru zaidi ya mara moja kukifuata kizazi chake, watu wa nyumba yake baada yake, huku akihimiza hilo kwa mkazo wa hali ya juu. Muslim amepokea kutoka kwake (s.a.w.w.) kuwa alisema: “Hakika mimi nimewaachieni vizito viwili: Kimoja ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu, humo mna uongofu na nuru, basi kichukueni Kitabu cha Mwenyezi Mungu na mshikamanane nacho. (Akahimiza juu ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kutamanisha yaliyomo humo), kisha akasema: Na watu wa nyumba yangu, nawakumbusheni Mwenyezi Mungu juu ya watu wa nyumba yangu, nawakumbusheni Mwenyezi Mungu juu ya watu wa nyumba yangu, nawakumbusheni Mwenyezi Mungu juu ya watu wa nyumba yangu.” Chanzo: Sahih Muslim: Juz 2, uk. 238, chapa ya mwaka 1290 Misri.

74

12:03 PM

Page 74


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Na kuwapenda kwao (a.s.) kunalazimu kuwapenda vipenzi wao na kujitenga na maadui zao, wapinzani wao na wale waliyowadhulumu. Mwenyezi Mungu anasema: “Hupati watu wanaomuamini Mwenyezi Mungu na siku ya Mwisho, kuwa wanawapenda wale wanaompinga Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, hata wakiwa ni baba zao au watoto wao au ndugu zao au jamaa zao….”41 Hivyo tunachukua hukumu za dini yetu, tafsiri ya kitabu cha Mola wetu Mlezi na Sunna ya Mtume wetu kutoka kwao, hiyo ni kwa amri ya kauli yake (s.a.w.w.): “Jifunzeni kutoka kwao, na wala msiwafunze, kwani hakika wao ni wajuzi kuliko nyinyi.” Chanzo: Yanabiul-Mawadah, uk. 35, chapa ya mwaka 1302 Istambul. Hivyo kudai mnawapenda bila kuwafuata na bila kuchukua hukumu za dini kutoka kwao wala kujitenga na maadui zao na wale waliyowadhulumu hakunufaishi chochote. Mshairi anasema: “Unampenda adui yangu kisha unadai eti mimi ni rafiki yako Hakika rai (yangu) iko mbali na wewe.” Muhammad Ali As-Sabun anapotafisiri Aya: “Wenye kuamini wasiwafanye makafiri kuwa viongozi badala ya wenye kuamini.” ndani ya tafsiri yake Safuwatu-tafasir anasema: “Haingii akilini (uwezekano wa) mwadamu kukusanya kati ya mapenzi ya Mwenyezi Mungu na mapenzi ya adui zake.” Na sisi Shia Imamiyya tunasema: Pia haiingii akilini mwislamu kudai kuwa anawapenda watu wa nyumba ya Mtume (a.s.) ilihali yeye anawapenda adui zao na waliowadhulumu. Na makosa yote waliyotendewa (a.s.) na adui zao anayatafsiri kuwa ni juhudi za kielimu.

Wewe Wasemaje? 41. Mwishoni mwa Suratul Mujadalah

75

12:03 PM

Page 75


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje?

Shia Asema: Uimamu na ukhalifa hauwi kwa mtu asiyekuwa mkuraishi, wenyewe ni muhtasi kwao tu, hauvuki kwenda kwa wengine, hilo ni kwa mujibu wa kauli ya Mtukufu Mtume: “Maimamu ni kutoka kwa makuraish.” Chanzo: Al-Fajrus-Sadiq fii radi ala-munkirit-tawasul wal-karamati wal-khawariq, uk. 6, chapa ya mwaka 1323 Misri.

Na Sunni Asema: Haina maana yoyote ukhalifa kuwa muhtasi kwa Makuraish, kinyume na hivyo itakuwa ni kuwanyima haki sehemu kubwa ya waislamu, na Uislamu umewafanya wote ni ndugu. Mwenyezi Mungu anasema:

“Kwa hakika wenye kuamini tu ndio ndugu.”Surat al-Hujirat: 10. Undugu huo hautimii ila kwa kuwa sawa katika haki zao na zilizo juu yao. Hakika uimamu na ukhalifa ni niaba ya unabii, hivyo kama ilivyo unabii ni haki ya wanadamu wote, Mwenyezi Mungu Mtukufu hajaufanya mahususi kwa baadhi ya watu fulani na kuwaacha wengine, hivyo hivyo uimamu si mahususi kwa kundi fulani la waislamu bila kuwahusu wengine. Hilo limesemwa na Mufti wa Baghdad Sheikh Jamil Sadqi Az-Zahawi42.

Wewe wasemaje? 42. Al-Fajrus-Sadiq, uk. 5.

76

12:03 PM

Page 76


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje?

Sunni Asema: Madhehebu ya kiisilamu ni manne: Madhehebu ya Hanafiyya, na kiongozi wake ni Abu Hanifa An-Nu’man bin Thabiti aliyezaliwa mwaka 80 A.H. na madhehebu ya Malikiyya, na kiongozi wake ni Maliki bin Anas aliyezaliwa mwaka 95 A.H. na madhehebu ya Shafi’yya, na kiongozi wake ni Muhammad bin Idiris aliyezaliwa mwaka 150 A.H. na madhehebu ya Hanbaliyya, na kiongozi wake ni Ahmad bin Hanbal As-Shayban aliyezaliwa mwaka 164 A.H. Na madhehebu yote haya ni sahihi kisheria, hivyo madhehebu yoyote atakayoichagua mwislamu kati ya hayo na akatenda kwa mujibu wa rai za kiongozi wake na juhudi zake za kielimu basi matendo yake ni sahihi, hivyo hakuna madhehebu isiyokuwa hayo.

Na Shia Asema: Madhehebu yote manne ya kisunni yalizuka baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kama ilivyo wazi, hivyo yenyewe ni madhehebu yaliyozushwa na kisheria haipasi kutenda kwa kufuata hata moja kati ya madhehebu hayo, hivyo yeyote atakayemfuata mmoja wa viongozi wa madhehebu hayo, akamfuata katika rai zake na akatenda kwa mujibu wa fatwa zake atakuwa kapotea kwa kuicha haki na amejitenga na njia iliyonyooka, kwani hakuna hata mmoja kati ya viongozi hao anayerejea kwa Maimamu wa nyumba ya Mtume, ambao ni kizazi cha Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ambao Mtukufu Mtume aliamuru turejee kwao na tuchukue kanuni za sheria kutoka kwao, na akawa amehimiza hilo kwa kusema: “Hakika mimi nimewaachieni vizito viwili: Kimoja ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu, humo mna uongofu na nuru, basi kichukueni Kitabu cha Mwenyezi Mungu na mshikamanane nacho. (Akahimiza juu ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kutamanisha yaliyomo humo), kisha akasema: Na watu wa nyumba yangu, nawakumbusheni Mwenyezi Mungu juu ya 77

12:03 PM

Page 77


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? watu wa nyumba yangu, nawakumbusheni Mwenyezi Mungu juu ya watu wa nyumba yangu, nawakumbusheni Mwenyezi Mungu juu ya watu wa nyumba yangu.” Chanzo: Sahih Muslim: Juz. 2, uk. 238, chapa ya mwaka 1290 Misri. Na katika Hadithi nyingine (s.a.w.w.) alisema: “Hakika mimi nimewaachieni vizito viwili: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu watu wa nyumba yangu, mkishikamana na hivyo viwili hamtopotea kamwe, na hakika hivyo viwili havitotengana mpaka vitakaponifikia kwenye Hodhi, basi jifunzeni kutoka kwao (Ahlul-Bayt) na wala msiwafunze, kwani hakika wao ni wajuzi kuliko nyinyi.” Chanzo: Yanabiul-Mawaddah, uk. 35, chapa ya mwaka 1302 Istambul. Na katika Hadithi nyingine akasema: “Enyi watu, hakika mimi nimewaachieni jambo ambalo laiti mkishikamana nalo kamwe hamtopotea: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu watu wa nyumba yangu.” Chanzo: Al-Jamius-Sahih (As-Sunan At-Tirmidhi): Juz. 5, uk. 662, chapa ya Daru Ihyait-Turathi Al-Arabi Beirut, uhakiki wa Ibrahim At’wah. Hivyo bila muhali wowote ni kuwa atakayejitenga na njia aliyoonyesha na kulingania Mtukufu Mtume bila shaka kajitenga na haki na ameingia kwenye bonde la upotovu, kama inavyofahamika kutoka kwenye Hadithi hizi sahihi zisizokuwa na shaka yoyote. Mwenyezi Mungu anasema: “Tena ni nini baada ya haki isipokuwa upotovu, basi mnageuzwa wapi?” Hamna maana yoyote ya kuwa na madhehebu mengi ndani ya dini moja, 78

12:03 PM

Page 78


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Uislam pekee ndio dini yetu na Allah peke Yake asiye na mshirika ndiye Mola Wetu Mlezi na Muhammad ndiye Mtume wetu hakuna Nabii mwingine asiyekuwa yeye, na Ali bin Abi Talib ni wasii wake na khalifa wake hatuna Imam asiyekuwa yeye mara tu baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Na baada yake ni mwanae Hasan (a.s.) ndiye Imam wetu, na baada yake ni Husein bin Ali (a.s.) ndiye Imam wetu, na baada yake ni Ali bin Husein Zainul-Abadina (a.s.) ndiye Imam wetu, na baada yake ni Muhammad bin Ali Al-Baqir (a.s.) ndiye Imam wetu, na baada yake ni Ja’far bin Muhammad As-Sadiq (a.s.) ndiye Imam wetu, na baada yake ni Musa bin Ja’far Al-Kadhim (a.s.) ndiye Imam wetu, na baada yake ni Ali bin Musa Ar-Ridha (a.s.) ndiye Imam wetu, na baada yake ni Muhammad bin Ali AlJawad (a.s.) ndiye Imam wetu, na baada yake ni Ali bin Muhammad AlHadi (a.s.) ndiye Imam wetu, na baada yake ni Hasan bin Ali Al-Askari (a.s.) ndiye Imam wetu, na baada yake ni mwanae Imam Al-Mahdi AlMuntadhar (a.s.) Imam wa kumi na mbili kwenye orodha ya Maimamu wa nyumba ya Mtume (a.s.) ndiye Imam wetu. Na yeye ndiye Imam wa zama zetu asiyeonekana kwa macho, tunamuomba Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) aliwasimika kwa ukhalifa na uimamu baada yake kwa kuwataja majina mmoja baada ya mwingine (ingawa wengine walikuwa bado hawajazaliwa). Ibnu Hajar amepokea kutoka kwa Mtukufu Mtume ndani ya kitabu chake As-Sawaiqul-Muhriqah kuwa alisema: “Jambo hili litaendelea kuwa na nguvu wakilinusuru wale aliyowakusudia juu ya jambo hili mpaka Makhalifa kumi na mbili, wote ni kutoka kwa Makuraish.” Ibnu Hajar ameongeza: “Ameipokea Abdullah bin Ahmad kwa njia sahihi.” Na hawa Maimamu wetu kumi na wawili ndio Makhalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu na wote ni kutoka kwa Makuraishi. 79

12:03 PM

Page 79


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Na katika riwaya ya Muslim aliyopokea kutoka kwake (s.a.w.w.): “Uislam utaendelea kuwa na nguvu imara mpaka wafike Makhalifa kumi na mbili.” Na nyingine kama hizo zilizopokewa na Sunni kutoka kwa (s.a.w.w.) zenye maana hiyo na idadi hiyo. Idadi hii haioani ila na Maimamu wetu kumi na mbili kutoka nyumba ya Mtume wetu (a.s.) na kizazi chake kitoharifu ambao sisi Shia Imamiyya tunaamini uimamu wao. Na wote wako katika madhehebu moja, hawana rai zao binafsi wala juhudi zao binafsi katika hukumu za Mwenyezi Mungu, bali mmoja wao anapokea Hadithi kutoka kwa baba yake ambaye ni Imam wa kabla yake, na huyu pia anapokea kutoka kwa baba yake ambaye ni Imam wa kabla yake, hivyo hivyo mpaka Hadithi inakomea kwa kiongozi wa waumini Ali (a.s.) ambaye ni Imam wa kabla yake kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.). Imamu wetu wa tano Muhammad bin Ali Al-Baqir anasema: “Nikiwasimulia Hadithi bila kutaja njia yake basi jueni njia yake ni kutoka kwa baba yangu Zaynul-Abidina kutoka kwa baba yake Husein asShahidu kutoka kwa baba yake Ali bin Abi Talib kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kutoka kwa Jibril kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.”43 Pia akasema (a.s.): “Naapa kwa Mwenyezi Mungu laiti tungekuwa au tungeliwasimulia kwa rai zetu tungekuwa miongoni mwa waliyohiliki, lakini sisi tunawasimulia kwa athari tulizonazo kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ambazo Imam huzirithi kutoka kwa Imam.”44 Na Abdur-Rahman bin Umar Al-Laythiyyu alipomuomba fatwa kuhusu ndoa ya muda (Mut’a), Imam alimpa fatwa ya kuruhusu kwa kutegemea ushahidi wa kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya Mtume Wake (s.a.w.w.), lakini Umar Al-Laythiyyu akasema Umar aliiharamisha, ndipo 43. Iilamul-wara biaalamil-huda. 44. Biharul-Anwari: Juz. 1.

80

12:03 PM

Page 80


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Imam (a.s.) akamwambia: “Mimi nimeleta kauli ya Mtume wa Mwenyezi Mungu na wewe ilete kupitia kwao, hakika haki ni ile aliyoisema Mtume wa Mwenyezi Mungu na batili ni ile aliyoisema rafiki yako (Umar bin AlKhattab).”45 Na akasema (a.s.): “Fuateni athari za Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na Sunna zake, hivyo zichukueni na wala msifuate matamanio yenu mtapotea.”46 Imam wetu wa sita Ja’far bin Muhammad As-Sadiq (a.s.): “Hadithi yangu ni Hadithi ya baba yangu na Hadithi ya baba yangu ni Hadithi ya babu yangu, na Hadithi ya babu yangu ni Hadithi ya Husein, na Hadithi ya Husein ni Hadithi ya Hasan, na Hadithi ya Hasan ni Hadithi ya kiongozi wa waumini, na Hadithi ya kiongozi wa waumini ni Hadithi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), na Hadithi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.47 Na amesema (a.s.): “Sisi ni watu tunaofuata athari. Naapa kwa Mwenyezi Mungu hatusemi kwa matamanio yetu na wala hatusemi kwa rai zetu na wala hatusemi ila alilosema Mola wetu Mlezi.”48 Na akasema (a.s.): “Msikubali kutoka kwetu ila yale yanayoafikiana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna….. Mcheni Mwenyezi Mungu, na wala msikubali kuhusu sisi yale yanayopingana na kauli ya Mola Wetu Mlezi na Sunna ya Mtume wetu (s.a.w.w.).”49 Hadithii kama hizi na zenye maana hii zimepokewa pia kutoka kwa Maimamu wetu wengine, na tumezifafanua kwa undani ndani ya kitabu chetu Al-Itrah Maas-Sunnah Layaftariqan (Kizazi na Sunna haviachani). Ama viongozi wa madhehebu manne katika fatwa hutegemea rai zao na 45. Al-Wafi: Juz. 12. 46. Al-Fusulul-Muhimmah fii Usulil-A'immah. 47. Al-Kafi: Juz. 1. 48. Biharul-Anwar: Juz. 1. 49.Al-Hadaiqun-Nadhirah Fii Ahkamil-Itratit-Tahirah: Juz. 1.

81

12:03 PM

Page 81


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? juhudi zao za kielimu, kwa ajili hiyo ndio maana unaona tofauti nyingi kati yao katika kanuni za Sheria. Utamkuta huyu anaharamisha jambo lililo halali kwa mwingine miongoni mwao, na yule anahalalisha lililo haramu kwa mwenzake, kana kwamba dini ni mchezo wa kuigiza ulio chini ya miliki yao, na unaotegemea rai zao, hivyo wanachotaka kukiharamisha wanakiharamisha na wanachotaka kukihalalisha wanakihalalisha. Kwa ajili hiyo, ndio maana Al-Allamah Sheikh Mariiyyu Amin Al-Antaki As-Shafi’i aliyakana madhehebu yake na madhehebu mengine manne na akachagua madhehebu ya Shia Imamiyya, na akaandika kitabu alichokiita (Kwa nini nimechagua madhehebu la Shia, madhehebu la watu wa nyumba ya Mtume?). Ndani ya kitabu hicho ametaja kwa undani sana tofauti za viongozi wa madhehebu manne, na tayari kitabu hiki kimeshachapwa, nakuomba ewe Sunni ukisome huenda Mwenyezi Mungu atakuongoza kwenye haki na njia iliyonyooka kama alivyomuongoza Al-Antaki na kaka yake Sheikh Ahmad Amin Al-Antaki, na yeye aliandika kitabu alichokiita (Njia ya kuelekea kwenye ufuasi wa nyumba ya Mtume), nacho kisome na Mwenyezi Mungu ndiye mtoa taufiki. Ama tofauti zao katika masuala ya kiimani huku kila mmoja akimtia dosari mwenzake, dosari ambazo hufikia kiwango cha kumkufurisha, ni nyingi. Daktari wa kisunni Ahmad Afghani anasema: “Madhehebu manne yenye kupondana.”50 Ukitaka kujua tofauti hizo kwa undani soma kitabu chetu “Muhatarat bayna at’bai madhahibil-Ar’baah” (Kashfa chafu kati ya wafuasi wa madhehebu manne) humo utakuta msiba mkubwa. Na tofauti hiyo iliyofikia kiwango hiki haisababishwi na chochote ila ni kule tu kujitenga na watu wa nyumba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na kizazi chake, Maimamu waon50. Sirabu fi Iran, uk. 58.

82

12:03 PM

Page 82


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? gozaji watakasifu (a.s.), ambao Mtume wa Mwenyezi Mungu ameamuru tushikamane nao na tuchukue kutoka kwao ili waislamu wasalimike na upotovu.

Wewe Wasemaje?

Sunni Asema: Sisi wafuasi wa madhehebu manne ndio wafuasi wa Sunna ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Na Shia Asema: Sisi Shia Imamiyya, wafuasi wa Maimamu kumi na wawili ndio wafuasi wa kweli wa Sunna ya Mtukufu Mtume. Dalili yetu juu ya usahihi wa kauli yetu na dai letu ni kuwa sisi tunafuata amri zote za Mtukufu Mtume wetu na tunaacha aliyokataza, na miongoni mwa amri zake ni kauli yake: “Hakika mimi nimewaachieni vizito viwili: Kimoja ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu, humo mna uongofu na nuru, basi kichukueni Kitabu cha Mwenyezi Mungu na mshikamanane nacho. (Akahimiza juu ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kutamanisha yaliyomo humo), kisha akasema: Na watu wa nyumba yangu, nawakumbusheni Mwenyezi Mungu juu ya watu wa nyumba yangu, nawakumbusheni Mwenyezi Mungu juu ya watu wa nyumba yangu, nawakumbusheni Mwenyezi Mungu juu ya watu wa nyumba yangu.” Chanzo: Sahih Muslim: Juz. 2, uk. 238, chapa ya mwaka 1290 Misri. Na katika Hadithi nyingine (s.a.w.w.) alisema: “Hakika mimi nimewaachieni vizito viwili: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu, watu wa nyumba yangu, mkishikamana na hivyo viwili hamtopotea, na hakika hivyo viwili havitotengana mpaka vitakaponifikia kwenye Hodhi, basi jifunzeni kutoka kwao (Ahlul-Bayt) na wala msiwafunze kwani hakika wao ni wajuzi kuliko ninyi.” 83

12:03 PM

Page 83


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Chanzo: Yanabiul-Mawaddah, uk. 35, chapa ya mwaka 1302 Istambul. Na akasema (s.a.w.w.): “Hakika Imam Ali ni kiongozi wa waumini na bwana wa waislamu na Imam wa wachamungu na kiongozi wa kundi mashuhuri.” Chanzo: Al-Imam Ali bin Abu Twalib cha Ustadhi Tawfiq Abu Alam, wakili mkuu wa wizara ya uadilifu Cairo, Misri, uk. 70, chapa ya Misri iliyosambazwa na Darul-Ma’arif. Na akasema (s.a.w.w.): “Hakika Ali ni bendera ya haki, Imam wa vipenzi vyangu na nuru ya mwenye kunitii.” Chanzo: Sharhu Nahjul-Balagha cha Ibnu Abil Hadid: Juz. 2, uk. 429, chapa ya mwaka 1329 Misri. Faraidus-Samtwayni, Juz. 1, uk. 151. Kifayatu AtTwalib, uk. 73, chapa ya Tehran. Manaqib Sayyidina Ali, uk. 20, chapa ya India. Na akasema: “Asiyeamini kuwa Ali ni mbora kuliko watu wote bila shaka kakufuru.” Chanzo: Kanzul-Ammali: Juz. 11, uk. 625. Muntakhabu Kanzul-Ammal, uk. 35 kwenye maelezo ya Musnad Ahmad: Juz 5, chapa ya Misri. Ar-Radhawi: Kauli ya Mtukufu Mtume: “Ali ni mbora kuliko watu wote” maana yake ni baada yake (s.a.w.w.) kwani linaloaminika kwa kila mwislamu ni kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu ni mbora kuliko watu wote na ndiye mwenye fadhila kuliko wote. Na inapokuwa hivyo basi khalifa wake Imam anayekaimu nafasi yake anakuwa kama yeye, mbora kuliko watu wote baada yake na mwenye fadhila kuliko wote, na yeye (a.s.) ana nafasi ya nafsi ya Mtukufu Mtume kama ilivyo kwenye Aya ya maapizano. 84

12:03 PM

Page 84


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Na kwa kutegemea Hadithi hizi tukufu za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambazo zinaungwa mkono na Hadithi zilizopokewa kutoka kwa watu wa nyumba ya Mtume ndio maana tumeamini uimamu wa Imam Ali bin Abi Talib baada yake (s.a.w.w.) na uimamu wa Maimamu wengine kumi na moja kutoka kizazi chake (s.a.w.w.) na tumeshikamana na kitabu cha Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kuamini kauli yake (s.a.w.w.): “Mkishikamana navyo kamwe hamtopotea.” Na hakuna Sunna ila ni kutenda kwa mujibu wa kauli za Mtukufu Mtume(s.a.w.w.).

Wewe wasemaje?

Sunni Asema: Baadhi ya Wanachuoni wa Sheria wameona ni lazima kuacha baadhi ya Sunna zitakapokuwa ni alama za Shia, ili kutofautisha kati ya Sunni na Shia. Hilo limesimuliwa na Ahmad bin Taymiyyah Al-Haran kutoka kwa Wanachuoni wa kisunni, na yeye mwenyewe akaunga mkono hilo kwa kusema: “Na masilahi ya kutofautisha ni makubwa na muhimu kuliko Sunna yenyewe.”51 Ar-Radhawi: Kweli nyuso zenu hazina haya enyi mnaojiita wafuasi wa Sunna ya Mtukufu Mtume.52

Na Shia Asema: Sisi tunaheshimu Sunna za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na wala hatumpingi hata kwenye jambo la Sunna hata kama tukiona Sunni analitenda jambo hilo.

Wewe wasemaje? 51. Minihajus-Sunnatil-Muhammadiyyah: Juz. 2, uk. 147. 52. Inashangaza sana anayejiita mfuasi wa Sunna ya Mtukufu Mtume anaacha ibada ya Sunna kwa kuwa tu kuna mwislamu mfuasi wa kweli wa Sunna ya Mtukufu Mtume anaifuata na kuitenda ibada hiyo hadi kawa mashuhuri kwayo - Mtarjumi.

85

12:03 PM

Page 85


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje?

Sunni Asema: Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: “Umma wangu utagawika makundi sabini na tatu, na yote yataenda motoni ila kundi moja tu.” Ameipokea Muhammad bin Umar Fakhrud-Din Ar-Razi,53 hivyo sisi Sunni ndio kundi lililookoka kati ya makundi hayo.

Na Shia Asema: Sisi Shia Imamiyya wafuasi wa Maimamu kumi na wawili ndio kundi lililookoka kati ya makundi haya sabini na tatu ambayo Mtukufu Mtume alitoa habari kuwa yataingia motoni ila kundi moja tu. Dalili yetu juu ya hilo ni kauli ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Wafuasi wa Ali ndiyo wenye kufuzu Siku ya Kiyama.” Chanzo: Yanabiul-Mawaddah cha Qanduzi Al-Hanafi, uk. 55, chapa ya mwaka 1302 Istambul. Manaqib Sayyidina Ali, uk. 37, chapa ya Haydar Abad na mna: “Ali na wafuasi wake ndiyo wenye kufuzu Siku ya Kiyama.” Na akasema (s.a.w.w.) kumwambia Ali: “Wewe utakuja kwa Mwenyezi Mungu huku wafuasi wako wakiwa wameridhia wenye kuridhiwa.” Chanzo: Manaqib Sayyidina Ali, uk. 25. Na akamwambia (s.a.w.w.): “Wewe na wafuasi wako ni watu wa Peponi mtanikuta kwenye Hodhi mkiwa mmekunywa na kunyweshwa huku nyuso zenu ziking’ara, na adui zenu watanikuta kwenye Hodhi wakiwa na kiu kali wamezuiwa kunywa.” 53. At-Tafsirul-Kabir: Juz. 1, uk. 12, chapa ya mwaka 1401chapa ya Darul-Fikri Beirut. Al-Imlau, uk. 31, chapa ya mwaka 1357 Misri, kimeunganishwa na kitabu Ihyau UlumidDin cha Al-Ghazali.

86

12:03 PM

Page 86


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Chanzo: Al-Ishaah Li-ashrati As-Saah, uk. 64, chapa ya mwaka 13125, chapa ya As-Saadah Misri. Majmau Az-Zawaid: Juz. 9, uk. 131, chapa ya mwaka 1967 Beirut. Nurul-Absar, uk. 70, chapa ya mwaka 1312 Misri. ArRiyadhu An-Nadhirah: Juz. 1, uk. 58, na mna: “Ewe Ali jibashirie, wewe na wafuasi wako ni watu wa Peponi.” Manaqib Sayyidina Ali, uk. 29, na mna: “Wewe na wafuasi wako ni watu wa Peponi.” Na akasema (s.a.w.w.) huku akimuashiria Ali: “Huyu na wafuasi wake ndiyo wenye kufuzu Siku ya Kiyama.” Chanzo: Kifayatut-Talib, uk. 313, chapa ya mwaka 1404 Tehran. Na akasema (s.a.w.w.): “Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu imo mikononi Mwake kuwa, huyu (Ali) na wafuasi wake ndio wenye kufuzu Siku ya Kiyama.” Chanzo: Tarjamatu Ali bin Abi Talib kutoka kwenye Ta’rikhu Damishq, uk. 442. AdDurrul-Manthur Fit-Tafsir Bil-Maathur: Juz. 6, uk. 379, chapa ya Misri. Shawahidut-Tanzil: Juz. 2, uk. 362, chapa ya mwaka 1393 Beirut. Yanabiul-Mawaddah, uk. 62 na 72, chapa ya mwaka 1302 Istambul. AlManaqib cha Al-Khawarzami, uk. 62, chapa ya mwaka 1965, Najaf. Na akasema (s.a.w.w.): “Ewe Ali, wewe na sahaba zako ni watu wa Peponi, wewe na wafuasi wako ni watu wa Peponi, fahamu miongoni mwa watu wanaodai eti wanakupenda ni kundi la watu wanaoudharau Uislam, wanausema kwa ndimi tu, wanasoma Qur’ani lakini haivuki mitulinga yao.” Chanzo: As-Sawaiqul-Muhriqa, uk. 96, chapa ya mwaka 1324 Misri, chapa ya AlMaymaniyyah. 87

12:03 PM

Page 87


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Na dalili nyingine kuwa sisi ndio kundi lililookoka ni kuwa sisi tumeshikamana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi cha Mtume wetu Maimamu kumi na wawili wa nyumba yake, na kwa ajili hiyo Mtume wetu ametuhakikishia usalama dhidi ya upotovu, na mwenye kusalimika na upotovu ndiye mwenye kufuzu Siku ya Kiyama bila kizuizi chochote. Amesema (s.a.w.w.): “Hakika mimi nimewaachieni vizito viwili: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu, watu wa nyumba yangu, mkishikamana na hivyo viwili kamwe hamtopotea, na hakika hivyo viwili havitotengana mpaka vitakapinifikia kwenye Hodhi, basi jifunzeni kutoka kwao (Ahlul-Bayt) na wala msiwafunze kwani hakika wao ni wajuzi kuliko nyinyi.” Chanzo: Yanabiul-Mawaddah, uk. 35, chapa ya mwaka 1302 Istambul. Na Sunni ni makundi mbalimbali na madhehebu mengi na kila kundi lina mwenendo wake na kiongozi wake. Hivyo madhehebu ya Hanafiyya kiongozi wake Abu Hanifa An-Nu’man bin Thabiti, na Shafiiyya kiongozi wake ni Muhammad bin Idiris, na Malikiyya kiongozi wake ni Malik bin Anas, na Hambaliyya kiongozi wake ni Ahmad bin Hambal. Na baina ya makundi haya kuna tofauti nyingi, huku yakitiana dosari yenyewe kwa yenyewe mpaka kiwango cha kukufurishana. Daktari Ahmad Al-Afghan amesema: “Madhehebu manne yenye kupondana.”54 Hivyo kudai kuwa haya madhehebu yenye kupondana yote ni kundi moja ni kichekesho miongoni mwa vichekesho vinavyoonyesha udhaifu wa akili za wanaodai hivyo, kama ilivyo wazi.

Wewe wasemaje? 54.Sirabu fi Iran: uk. 58.

88

12:03 PM

Page 88


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje?

Shia Asema: Ndoa ya Mut’a, yaani ndoa ya muda ni halali ndani ya Uislam, hivyo yenyewe inaruhusiwa kwetu. Mwenyezi Mungu amesema: “Ambao mmestarehe nao katika wao, basi wapeni mahari yao yaliyolazimu, wala si vibaya kwenu katika yale mliyokubaliyana baada ya mahari, hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye hekima.”55 Na hakuna Aya yoyote ndani ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu iliyokuja kuondoa hukumu yake, hivyo yenyewe ni halali mpaka Siku ya Kiyama.

Na Sunni Asema: Ndoa ya muda ni haramu kwetu kwa sababu Umar bin Al-Khattab aliikataza kwa ukali sana, akasema: “Mut’a mbili zilikuwepo zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu, na zama za Abu Bakr, na mimi naziharamisha na ninatoa adhabu juu yake: Ndoa ya muda na Mut’a ya Hijja.” Ameipokea Ar-Razi ndani ya kitabu Mafatihul-Ghaybi56. Na katika riwaya nyingine imepokewa kutoka kwake kuwa alisema: “Enyi watu, Mut’a mbili alizihalalisha Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na mimi naziharamisha na natoa adhabu juu yake.”57 Na Abshihiyyu amepokea ndani ya kitabu Al-Mustatrafu58 kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) kuwa alisema: “Laiti kungekuwa na Nabii baada yangu basi angekuwa Umar!” Al-Fuyumi amesema ndani ya kitabu Al-Misbahul-Muniru: “Ndoa ya Mut’a ni mapatano ya muda.” Kisha akaitaja Aya tukufu (Ambayo Shia 55. Suratun-Nisai: 24. 56. Juz. 1, uk. 51, na Juz. 5, uk. 165. Ibnu Abu Hadid ndani ya Sharhu Nahjul-Balagha: Juz , uk. 61, chapa ya mwaka 1329 Misri. 57. Islamu Bilaa Madhahibu, uk. 200, chapa ya tano. 58. Juz. 1, uk. 137. Faydhul-Qadir: Juz. 5, uk. 325.

89

12:03 PM

Page 89


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? wanaitumia kama dalili juu ya uhalali wa ndoa hiyo ya Mut’a), kisha akasema: “Na Aya hii bado hukumu yake ipo, na Wanachuoni wa kisunni wanaharamisha ndoa ya Mut’a ili kuwapinga Shia.” Muhammad Mansur aliingia kwa Al-Ma’mun huku (Al-Ma’mun) akiwa anapiga mswaki na yeye akiwa amechukia na akisema: “Mut’a mbili zilikuwepo zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na zama za Abu Bakr (r.a), na mimi nazipiga marufuku. Ewe mende, wewe ni nani mpaka niache lile alilolitenda Mtume wa Mwenyezi Mungu au Abu Bakr?”59 Ufafanuzi: Al-Isbahan amepokea ndani ya kitabu At-Targhibi kutoka kwa Ibnu Umar kuwa alisema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema: Imani ya muumini haitokamilika mpaka matamanio yake yatakapokuwa yanafuata kile nilichowaletea.” (Ad-Durrul-Manthur: Juz. 2, uk. 17). Ar-Radhawi: Hivyo Umar kusema “Mut’a mbili zilikuwepo zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), na mimi naziharamisha” katika kauli hiyo amefuata matamanio yake au amefuata yale aliyoyaleta Mtume wa Mwenyezi Mungu kutoka kwa Mwenyezi Mungu? Na Mtukufu Mtume amesema: “Atakayejitenga na Sunna yangu si mfuasi wangu.” Kisha Mtume akasoma Aya hii: “Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu, basi nifuateni, na Mwenyezi Mungu atawapenda na atawasamehe madhambi yenu, na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa msamaha, Mwenye kurehemu.” Ibnu Abu Hatim ametoa kwa njia ya Hushibu kutoka kwa Hasan kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu “Basi nifuateni na Mwenyezi Mungu atawapenda” kuwa amesema: “Hivyo alama ya kumpenda Yeye ilikuwa ni kufuata Sunna za Mtume Wake. (Ad-Durul-Manthur: Juz. 2). Na Al-Yafi 59. Mir-atul-Janani Waibratul-Yaqidhani: Juz. 2, uk. 137.

90

12:03 PM

Page 90


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? amenukuu kutoka kwa Mmisri Dhun-Nun kuwa alisema: “Alama ya mwenye kumpenda Mwenyezi Mungu ni kumfuata kipenzi cha Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) katika maadili yake, vitendo vyake, amri zake na Sunna zake (Mir’atul-Jinan: Juz. 2, uk. 151). As-Sabuni anapotafsiri kauli ya Mwenyezi Mungu: “Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu, basi nifuateni, na Mwenyezi Mungu atawapenda na atawasamehe madhambi yenu, na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa msamaha, Mwenye kurehemu;” amesema huku akinukuu kutoka kwa Ibnu Kathir (Mukhtasar Ibnu Kathir): “Aya hii inamuhukumu kila anayedai kuwa anampenda Mwenyezi Mungu ilihali yeye si mfuasi wa Muhammad, hakika yeye ni mwongo katika dai lake hilo mpaka pale atakapofuata Sheria ya Muhammad katika kauli zake zote na vitendo vyake vyote” (Safuwat-Tafasiri, sehemu ya kwanza, uk. 17). Na Daktari Ali bin Muhammad Nasiru Al-Fiqihiyyu mhariri mkuu wa jarida la chuo kikuu cha kiislamu huko Madina tukufu amesema: “Na Mola Mlezi ndio Muumba Mmiliki Mwenye kuwatendea viumbe atakavyo Yeye, na Yeye ndiye mwenye kuwawekea sheria, Yeye ndiye ajuaye ni lipi litakalotengeneza hali ya waja Wake katika hali zao na matarajio yao (Je, asijue aliyeumba? Naye ndiye aonaye visivyoonekana Mwenye khabari).” Na tayari Mwenyezi Mungu ameshamsifu mwenye kuingilia jukumu hilo kuwa ni mwongo mwenye kumzushia Mwenyezi Mungu uongo, kwa sababu suala la kuhalalisha na kuharamisha ni jukumu la Mwenyezi Mungu pekee

“Wala msiseme, kwa sababu ya uongo usemao ndimi zenu, hii ni halali na hii ni haramu, msije mkamzulia uongo Mwenyezi Mungu. Hakika wale wamzuliao uongo Mwenyezi Mungu hawatafaulu.” (SuratunNahl: 116). 91

12:03 PM

Page 91


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Hivyo hii ni haki ya Mwenyezi Mungu hairuhusiwi kwa kiumbe yeyote kumwingilia Mwenyezi Mungu na kuweka sheria kwa waja Wake bila kutoka Kwake, kwani kufanya hivyo ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu katika mambo yanayomhusu Yeye tu. Na wale wanaokubali sheria hii na kuridhika nayo na kuifanyia kazi ni Mushirikina wanamshirikisha Mwenyezi Mungu” (Jarida la chuo kikuu cha kiisilamu huko Madina tukufu, toleo la 58, uk. 112, mwaka 1403, la mwaka wa 15). Hivyo bila shaka Daktari Al-Fiqhiyyu amemhukumu Imam wake Umar kuwa amemshirikisha Mwenyezi Mungu, baada ya Al-Ghazali, Al-Hanbal kumhukumu kuwa ametoka ndani ya Uislam, kwa sababu yeye aliweka sheria ya uharamu wa Mut’a mbili akasema: “Mut’a mbili zilikuwepo zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu, na mimi naziharamisha na ninatoa adhabu juu yake: Ndoa ya muda na ndoa ya Hijja.” Kwani kuweka sheria ni miongoni mwa mambo mahususi kwa Mwenyezi Mungu. Na amemhukumu kwa shirki yule aliyekubali sheria hii miongoni mwa Sunni. Al-Fuyumi amesema ndani ya kitabu Al-Misbahul-Muniru baada ya kutaja Aya inayohalalisha ndoa ya muda: “Wanazuoni wa kisunni wanaharamisha ndoa ya Mut’a.” Na hili linatuthibitishia kuwa Uislam wao ni Uislam wa Umar, wao wanamwabudu yeye na hawamwabudu Mwenyezi Mungu kwa chochote. Ahmad bin Taymiyyah Al-Harran amesema: “Mwenyezi Mungu amesema:

“Wamewafanya makasisi wao na watawa wao kuwa ni miungu badala ya Mwenyezi Mungu na Masihi mwana wa Mariam, hali hawakuam92

12:03 PM

Page 92


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? rishwa isipokuwa kumwabudu Mwenyezi Mungu Mmoja, hakuna aabudiwaye ila Yeye tu, ametakasika na yale wanayomshirikisha nayo.” (Sura Tawba: 31.). Na imeshathibiti ndani ya Sahih At-Tirmidhi na ndani ya vitabu vingine kwa Hadithi ya Adi bin Hatim kuwa alisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni upi huo uungu wao? Akasema: “Hakika wao waliwahalalishia haramu na wakawaharamishia halali, na wao wakawatii, huko ndiko kulikokuwa kuwaabudu kwao (Minihaju As-Sunnah An-Nabawiyyah: Juz. 1, uk. 11). Ar-Radhawi: Hivi Sunni anahisi kuwa kukubali kwake kitendo cha Umar kuharamisha Mut’a mbili kunaingia ndani ya Aya hii “Wamewafanya makasisi wao na watawa wao kuwa ni miungu” na kuwa ni miongoni mwa mifano yake halisi, au hahisi? Abu Hamid Al-Ghazali Ash-Shafi’i amesema: “Nabii Maasumu dhidi ya makosa ambaye imani haithibiti ila kwa kumuafiki na ukafiri hauthibiti ila kwa kumkhalifu.” (Ihyau Ulumid-Din) Wahabi Sulayman Al-Banni amesema: “Uislam ambao umesimamia msingi wa kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kumtii Yeye na Mtume Wake (s.a.w.w.), na ambao haumruhusu mtu kubadili hukumu yake, sawa awe kasisi au mwanachuoni, awe kiongozi au mtu wa kawaida, iwe kwa ajili ya maslahi au siasa.” (Jarida la Ad-Daa’watul-Islamiyyah, toleo la 612 mwaka 1397). Ustadhi Khalid Muhammad mwandishi wa kimisri wa zama zetu amesema: “Hakika Umar bin Al-Khattab aliacha maelezo matakatifu ya kidini yaliyomo ndani ya Qur’an na Sunna pale masilahi yalipomtaka, hivyo akayaitikia.” (Ad-Damuqiratiyyah Abada, uk. 155, chapa ya tatu ya mwaka 1958, chapa ya Al-Umumiyyah, Damascus). Kisha akataja mifano mbalimbali ambayo Umar alikhalifu maelezo matakasifu. 93

12:03 PM

Page 93


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Umar An-Nasaf amesema: “Na kupinga maelezo matukufu ni Ukafiri.” (Aqaidu An-Nasafi). Ar-Radhawi: Umeshasikia maneno ya Al-Banni kuwa Uislam haumruhusu mtu yeyote kubadili sheria yoyote ile hata awe na cheo gani, si katika hali ya masilahi wala kwa ajili ya siasa. Lakini Imam wa Sunni na khalifa wao wa pili Umar bin Al-Khattab anaona ni lazima aharamishe hukumu ya Mwenyezi Mungu anayoitaka Yeye (swt). Na ahalalishe ile aitakayo yeye, bila kuhisi uzito wowote katika kutenda hilo. Ahmad Ibnu Taymiyyah Al-Haran amesema: “Hakika Umar ana makosa mengi na matukio mengi makubwa na mabaya zaidi.” (Tatuhirul-Fuadi Minad-Danasil-Iitiqad, uk. 11, chapa ya mwaka 1318 Misri). Ar-Radhawi: Tunamuomba Mwenyezi Mungu atulinde dhidi ya kukhalifu dini ya Mwenyezi Mungu na kwa fadhila Zake na neema Yake, atuwafikishe tuwafuate Maimamu wetu maasumu (a.s.) waliotakasika na makosa katika kauli na vitendo.

Wewe wasemaje?

Shia Asema: Ni wajibu kwetu kuficha imani pindi tunapohisi madhara juu ya nafsi zetu kutoka kwa wapinzani wa imani zetu, hiyo ni kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu:

94

12:03 PM

Page 94


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? “Wenye kuamini wasiwafanye makafiri kuwa viongozi badala ya wenye kuamini, na atakayefanya hivyo basi hana chochote kwa Mwenyezi Mungu, ila mtakapojilinda nao kwa kujihifadhi.� Surat alImran: 28. Hivyo ni wajibu kwa mwislamu kuficha matendo yake na imani yake pindi anapohisi madhara juu ya nafsi yake, hivyo asali kama anavyosali mpinzani wake na atende anavyotenda ili kujilinda na shari yake na kuihifadhi nafsi yake dhidi ya hatari. Na kuna Hadithi zimepokewa kutoka kwa Maimamu wetu watakasifu zinazowajibisha pindi unapohisi madhara ya lazima juu ya nafsi, hivyo tunategemea riwaya hizo na kitabu cha Mwenyezi Mungu kuthibitisha hilo.60

Na Sunni Asema: Ufichaji huo si chochote bali ni kuficha haki na kudhihirisha batili. Hilo limesemwa na Ihsan Dhahir Al-Pakistan huku akiwashutumu Shia juu ya imani yao hiyo.

Wewe wasemaje? 60. Ufichaji huu hujulikana kwa jina la (Taqiyyah), yaani unaficha haki na unadhihirisha batili, kwa maana hii ni kinyume na Unafiki ambao wenyewe ni kujifanya kudhihirisha haki na kuficha batili. Taqiyya ina hukumu tofauti kulingana na mazingira halisi yanayomfika mhusika, hivyo kuna kipindi kuficha imani inakuwa ni Wajibu, hapo ni pale udhihirishaji utakapomletea madhara makubwa mhusika, kama vile kuuwawa yeye au familia yake, kupoteza mali zake, madhara ya kiafya na mfano wa hayo. Na kuna mazingira mengine Taqiyyah huwa haramu, hapo ni pale ufichaji huo wa imani utakapokuwa sababu ya Mwenyezi Mungu, au Mitume, au Maimamu, au Qur'ani na dini kwa ujumla kuvunjiwa heshima na kudharaulika, au kutukanwa na kukashifiwa, basi katika mazingira kama hayo na mfano wa hayo ni haramu Mwislamu kuficha imani yake bali ni Wajibu adhihirishe na aitetee kwa kila alicho nacho ikiwemo nafsi yake hata kama ataidhuru nafsi yake. Ufafanuzi zaidi rejea vitabu vya Matendo ya Kiibada vya Wanachuoni wetu Wakuu -Mtarjumi.

95

12:03 PM

Page 95


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje?

Shia Asema: Swala ya Tarawehe ambayo Sunni huisali ndani ya Mfungo wa Ramadhani haikuwepo zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu na wala yenyewe si miongoni mwa Sunna zake, hivyo kuisali ni kuleta bidaa ndani ya dini, Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.): “Hakika uongofu bora ni uongofu wa Muhammad, na mambo ya shari mno ni yale yanayozushwa, na kila linalozushwa ni bidaa na kila bidaa ni upotovu na kila upotovu ni jambo la motoni.” Chanzo: Al-Jamiu As-Saghiru fi AHadithil-Bashir An-Nadhir: Juz. 1, uk. 243. Na akasema: “Jiepusheni na mambo yanayozushwa, kwani hakika mambo ya shari mno ni yale yazushwayo, na kila lizushwalo ni bidaa na kila bidaa ni upotovu.” Chanzo: As-Sunan cha Ibnu Majah: Juz 1, uk. 18.

Na Sunni Asema: Sisi Sunni tunaswali Swala ya Tarawehe, na tunaona kuwa imeruhusiwa kisheria japokuwa haikuwepo zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), kwani Umar bin Al-Khattab khalifa wa pili aliamuru Swala hiyo, na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Laiti kungekuwa na Nabii baada yangu basi angekuwa Umar.”61 Bukhari ametoa ndani ya Sahih yake kutoka kwa Abdur-Rahmani bin Abdul-Qadir kuwa alisema: “Nilitoka nikiwa pamoja na Umar bin AlKhattab (r.a.) usiku ndani ya Mfungo wa Ramadhani kuelekea msikitini, 61. Faydhul-Qadir: Juz. 5, uk. 325. Al-Mustatraf: Juz. 1, uk. 137.

96

12:03 PM

Page 96


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? basi tukawakuta watu wametawanyika kila mmoja akisali peke yake, kila mmoja akisali Swala yake na kabila lake likisali Swala yake. Umar akasema: “Mimi naona laiti nikiwakusanya hawa kwa msomaji mmoja ni bora zaidi.” Kisha akaazimia na akawakusanya kwa Ubayya bin Ka’ab. Kisha nikatoka naye usiku mwingine tukawakuta watu wakisali Swala ya msomaji wao, Umar akasema: “Hii ni bidaa nzuri, na ile ambayo kwayo wanalala (wakaiacha) ni bora kuliko ambayo kwayo wanasimama (kuisali).”62

Wewe Wasemaje?

Shia Asema: Sisi Shia Imamiyya tunapaka juu ya nyayo zetu wakati wa kutawadha, hilo ni kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na mpake vichwa vyenu na miguu yenu mpaka kwenye nguyo mbili.”111 Surat al-Maidah: 6. Na tunaamini udhu kinyume na utaratibu huu ni batili kwa kuwa unapingana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Na unapobatilika udhu ambao wenyewe ni sharti la kusihi kwa Swala kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Enyi mlioamini mnaposimama kwa Swala, basi osheni nyuso zenu, 62. Fat'hul-Bari Bisharhi Sahih Bukhari: Juz. 3, uk. 204, chapa ya mwaka 1348 Misri.

97

12:03 PM

Page 97


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? na mikono yenu mpaka kwenye nguyo mbili, na mpake vichwa vyenu na miguu yenu mpaka kwenye nguyu mbili.” Surat al-Maidah: 6. Basi Swala nayo inabatilika, kwa kuwa chenye sharti hakitimii lisipotimia sharti. Na Swala inapobatilika basi hakuna ibada yoyote inayokubalika kutoka kwa mwisilamu, hilo ni kwa mujibu wa Hadithi tukufu ya Mtume: “Swala ndio nguzo ya dini, ikikubaliwa zinakubaliwa ibada nyingine, na ikikataliwa zinakataliwa nyingine.”

Na Sunni Asema: Sisi tunaosha nyayo zetu wakati wa kutawadha, na utaratibu huo ndio mwenendo wa Wanachuoni wetu na viongozi wetu wa sasa na wa zamani, na laiti udhu ungekuwa hausihi basi wasingefanya hivyo.

Wewe wasemaje?

Sunni Asema: Katika kuosha mikono miwili ndani ya udhu sisi huanzia kwenye vidole na kuishia kwenye fundo, Mwenyezi Mungu anasema:

“Basi osheni nyuso zenu, na mikono yenu mpaka vifundoni.” Surat alMaidah: 6. Na (mpaka) iliyopo hapa inaonyesha kikomo na mwisho.

Na Shia Asema: Sisi katika kuosha mikono ndani ya udhu tunaanzia kwenye fundo na tunaishia kwenye vichwa vya vidole, kwa sababu muradi wa Aya ni kubainisha mipaka ya eneo la kuoshwa katika mikono miwili, nalo ni eneo la kati ya fundo na vidole, si zaidi ya hapo wala si chini ya hapo. 98

12:03 PM

Page 98


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Wala (mpaka) hapa haina maana ya kikomo na mwisho hata tuseme inawajibika kuanzia kwenye vichwa vya vidole na tukomee kwenye fundo. Dalili yetu tegemeo juu ya hilo ni zile Hadithi zilizopatikana kutoka kwa kizazi kitakasifu, watu wa nyumba ya Mtume (a.s.), Maimamu wetu watakasifu wanapofundisha udhu wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), na udhu wa kiongozi wa waumini. Na watu wa nyumba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu ndio wajuzi zaidi wa utaratibu wa babu yao Mtume wa Mwenyezi Mungu kuliko watu wa pembeni na wageni.

Wewe wasemaje?

Sunni Asema: Sahaba wote ni waadilifu. Abdur-Rauf Al-Munawi As-Shafi’i amesema: “Sunni wote wamekubaliana kuwa sahaba wote ni waadilifu.”63 Na Abdul-Malik Al-Juniyyu As-Shafi’i amesema: “Wakubwa kwa wadogo wote wamekubaliana juu ya uadilifu wa sahaba wote.”64 Sheikh Muhammad Al-Arabiyyu At-Taban Al-Jazair amesema: “Uadilifu wa sahaba Mwenyezi Mungu awe radhi nao umethibiti na unajulikana kwa kila mwislamu kwa mujibu wa Kitabu, Sunna na Ijimai.”65

Na Shia Asema: Sahaba wapo walio wachamungu waumini wa kweli, na wapo walio wanafiki na mafasiki waliyo madhalimu waovu. Mwenyezi Mungu anasema: 63. Faydhul-Qadir: Juz. 1, uk. 263. 64. Tahdhirul-Abqariyyu min muhadharati Al-Hadhariyyu: Juz. 1, uk. 12, chapa ya mwaka 1404 Beirut. 65.Tahdhirul-Abqariyyu: Juz. 1, uk. 180.

99

12:03 PM

Page 99


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? “Wanapokujia wanafiki husema: Tunashuhudia ya kuwa kwa hakika wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu anajua kwa hakika wewe ni Mtume Wake, na Mwenyezi Mungu anashuhudia ya kuwa, kwa hakika wanafiki ni waongo hasa. Wamevifanya viapo vyao ngao, wakaiacha njia ya Mwenyezi Mungu, kwa hakika ni mabaya waliyokuwa wakifanya.”66 Na pia akasema: “Na wanapoiona biashara au mchezo wanavikimbilia na wanakuacha umesimama, sema: Yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu ni bora kuliko mchezo na biashara, na Mwenyezi Mungu ni Mbora wa watoa riziki.”67 Na wapo wenye kuritadi na kutoka kwenye Uislamu baada ya kifo cha Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.). Mwenyezi Mungu anasema: “Na hakuwa Muhammad ila ni Mtume aliyepitiwa na Mitume kabla yake. Basi je, akifa au kuuliwa mtarudi nyuma kwa visigino vyenu?” Hivyo sisi Shia Imamiyya hatuwatakasi sahaba wote kwa kauli moja bila mipaka na wala hatuhukumu kuwa wote ni waadilifu, katika hilo tunategemea Kitabu cha Mwenyezi Mungu kwa kuwa aliwasifu wengine kwa sifa ulizosikia. Bukhari ndani ya Sahih yake Juzuu ya nne, ukurasa 221, chapa ya Misri kwenye maelezo ya As-Sindi amepokea kuwa Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Mimi nitawatangulia kufika kwenye Hodhi, na watu miongoni mwenu watainuliwa kuelekezwa upande wangu, lakini nitakapowafuata ili niwanyweshe watasogezwa mbali na mimi. Nitasema: Ewe Mola Wangu Mlezi! Hawa ni sahaba zangu! Nitaambiwa: Hujui waliyoyazusha baada yako.” Na akasema (s.a.w.w.): “Watu miongoni mwa sahaba zangu watachukuliwa na kuelekezwa upande wa kushoto, kisha mimi nitasema: sahaba zangu! sahaba zangu! Nitaambiwa: Hakika wao hawakuacha kurudi 66. Mwanzoni wa Suratul-Munafiquun. 67. Mishoni mwa Surat Al-Jumua.

100

12:03 PM

Page 100


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? nyuma tangu ulipowaacha…..”68 Na akasema (s.a.w.w.): “Miongoni mwa sahaba zangu kuna kumi na wawili wanafiki, kati yao kuna wanane hawatoingia Peponi mpaka ngamia apite kwenye tundu ya sindano.69 Hivyo Kitabu na Sunna iliyopokewa kwa njia za kisunni zinawapinga hawa wenye kuwapenda sahaba hadi kuvuka mipaka. Ijimai iko kwingine na Kitabu na Sunna viko kwingine juu ya sahaba. Ewe At-Tabari kwa nini unaleta uongo huu na upotovu wa fedheha? Hivi hujasoma kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na tuiweke laana ya Mwenyezi Mungu iwashUk.ie wenye kusema uongo.”70 Ni jambo baya sana ulilojichagulia, na utakuja kujuta muda ambao majuto hayatokusaidia chochote. Zaidi ya hapo ni kuwa sahaba walikuwa wakitiana dosari wao kwa wao, dosari ambazo si kwamba zinawatoa kwenye uadilifu tu, bali zinawaingiza kwenye orodha ya Makafiri. Sheikh Mahmud Aburiyyah mwanachuoni wa kisunni wa zama zetu anasema: “Sahaba wao kwa wao walitiana dosari, na wakakufurishana.”71 Na At-Taftazani anasema: “Hakika sahaba walikuwa wakiuana kwa ncha za silaha, na wakikashifiana.”72 Ikiwa hii ndio hali kati yao itakuwaje isihi kuwasifu kuwa ni waadilifu? Hili ndilo analolikataa Shia kwa nguvu zote, na ili kuthibitisha usahihi wa kauli ya Aburiyyah na At-Taftazani tunakutajia utiaji dosari wa Aisha binti Abu Bakr dhidi ya sahaba mmoja tu, na bila shaka unakutosha. Alisema akiwa anamtia dosari Uthman bin Affan Al-Amawi khalifa wa 68. Sahih Bukhari: Juz. 2, uk. 225, chapa ya Misri kwenye maelezo ya AsSindi.69. Al-Jamiu As-Saghir: Juz. 2, uk. 225, chapa ya mwaka 1401 Beirut. 70. Surat al-Imran: 61. 71.Adhuwau Alas-Sunnatu Al-Muhammadyyah, chapa ya pili, uk. 342. 72. Sharhul-Maqasid, uk. 106, chapa ya mwaka 1305 Istambul.

101

12:03 PM

Page 101


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? tatu wa kisunni: “Mwenyezi Mungu amlaani Naathal73, muuweni Naathal bila shaka amekuwa muovu!74Muuweni Naathal kwani bila shaka amekufuru!.”75 Ustadh Abdul-Karim khatibu wa kimisri wa zama hizi anasema: “Naathal ni Myahudi aliyekuwepo Madina aliyefanana na Uthman.”76 Sheikh Muhammad Al-Arabii At-Tabani Al-Jazair anasema: “Watu walimpa Uthman (r.a.) lakabu ya Naathal.”77 Ukitaka kuona jinsi sahaba walivyotiana dosari wao kwa wao soma kitabu “Muhatarati Bayna Sahabati Rasulillah” ambacho tumekiandika ili kuwajibu wenye kuvuka mipaka katika kuwapenda sahaba. Kwa kuwa sahaba hivyo ndivyo walivyo wengine Mwenyezi Mungu ndani ya Kitabu Chake kawasifu kwa ubaya kama ulivyoona, na pia Mtukufu Mtume (s.aw.w.) kawatia dosari, itawezekanaje tena sisi Shia Imamiyya wafuasi wa kizazi cha Mtume kitakasifu tuhukumu kuwa wote kwa ujumla ni waadilifu na tuwe tumekipinga Kitabu cha Mola Wetu Mlezi na Sunna ya Mtume wetu na akili zetu kwa imani hiyo? Na huo ndio upotovu wa wazi kabisa.

Wewe Wasemaje?

73. Sharhu Nahjul-Balagha: Juz. 4, uk. 456, chapa ya mwaka 1329 Misri. 74. Al-Imamah Was-Siyasah: Juz. 1, 52, chapa ya mwaka 1388, Misri. 75. Al-Imam Ali Sawtul-Adalah Al-Insaniyyah: Juz. 4. 76. Aliyyu bin Abi Talib baqiyyatun-nubuwwah wa khatamul-kKhilafah, uk. 235, chapa ya Misri. 77. Tahdhirul-abqariyyu min muhadharatil-hadhariyyu: Juz. 2, uk. 142.

102

12:03 PM

Page 102


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje?

Sunni Asema: Wake wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni miongoni mwa watu wa nyumba yake.

Na Shia Asema: Wake wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) si miongoni wa watu wa nyumba yake, na imani yetu hii inaungwa mkono na kauli ya As-Shablanji ndani ya kitabu Nurul-Absar78, na As-Sabban ndani ya kitabu Is’afur-Raghibin79: “Imepokewa kwa njia mbalimbali sahihi kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuja akiwa na Ali, Fatima, Hasan na Husein, kisha akamshika kila mmoja kati ya hao wawili (Hasan na Husein) mkono wake na kuingia, akawaita Ali na Fatima na kuwaketisha mbele yake huku Hasan na Husein kila mmoja akiketi juu ya paja lake, kisha akawafunika shuka na kusoma Aya hii: “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu watu wa nyumba na kukutakaseni kabisa.” Na akasema: “Hawa ni watu wa nyumba yangu, waondolee uchafu na uwatakase kabisa.” Na wao wawili wameongeza kuwa: “Na ndani ya riwaya ya Ummu Salamah alisema: Nikafunua shuka ili niingie niwe pamoja nao lakini (s.a.w.w.) akaivuta toka mikononi mwangu. Nikasema: Na mimi nipo pamoja nanyi ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: “Hakika wewe ni miongoni mwa wake wa Mtume upo juu ya kheri.” Laiti wakeze wangekuwa wanaingia miongoni mwa watu wa nyumba yake basi (s.a.w.w.) asingemnyang’anya Ummu Salamah shuka toka mikononi mwake na kumzuia kuingia ilihali yeye ndiye mkewe bora kuliko wengine.80

Wewe Wasemaje? 78. Ukurasa wa 101, chapa ya Misri, Mwaka 1312, chapa ya Al-Maymaniyyah. 79. Ukurasa wa 109, kwenye maelezo ya Nurul-Absar. 80. Baada ya Khadija.

103

12:03 PM

Page 103


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje?

Mwisho Haya ndiyo niliyoweza kuyakusanya ndani ya kitabu hiki, na kazi hii ni fadhila kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu Mtoaji. Namuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amuongoze msomaji wake kwenye njia ya haki na ya sawa, na anilipe juu ya kazi hii kheri nitarajiayo kutoka kwake Siku ya hesabu, siku ambayo, “Imani haitoisaidia nafsi chochote ikiwa nafsi haikuiamini tangu mwanzo, au haikuchuma katika imani hiyo kheri yoyote.�

104

12:03 PM

Page 104


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje?

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION: 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24. 25.

Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thalathini Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudharr Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur'an na Hadithi Elimu ya Nafsi Yajue Madhehebu ya Shia 105

12:03 PM

Page 105


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? 26. 27. 28. 29. 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52. 53. 54. 55. 56.

Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu Al-Wahda Ponyo kutoka katika Qur'an. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii Mashukio ya Akhera Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyeezi Mungu na sifa zake Amateka Na Aba'Khalifa Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana. Upendo katika Ukristo na Uislamu Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya Kupaka juu ya khofu Kukusanya swala mbili Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kusujudu juu ya udongo Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) Tarawehe Malumbano baina ya Sunni na Shia Kupunguza Swala safarini Kufungua safarini Umaasumu wa Manabii Qur’an inatoa changamoto as-Salaatu Khayrun Mina -'n Nawm Uadilifu wa Masahaba Dua e Kumayl 106

12:03 PM

Page 106


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? 57. 58. 59. 60. 61. 62. 63. 64. 65. 66. 67. 68. 69. 70. 71. 72. 73. 74. 75. 76. 77. 78. 79. 80. 81. 82. 83. 84. 85.

Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mitume Muhammad (s) Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili Kuzuru Makaburi Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita Tujifunze Misingi Ya Dini Sala ni Nguzo ya Dini Mikesha Ya Peshawar Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliyonyooka Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake Liqaa-u-llaah Muhammad (s) Mtume wa Allah Amani na Jihadi Katika Uislamu Uislamu Ulienea Vipi? Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) Urejeo (al-Raja’a ) Mazingira Utokezo (al - Badau) Sadaka yenye kuendelea 107

12:03 PM

Page 107


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? 86. 87. 88. 89. 90. 91. 92. 93. 94. 95.

Msahafu wa Imam Ali Uislamu na dhana Mtoto mwema Adabu za Sokoni Johari za hekima kwa vijana Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu Tawasali Imam Mahdi katika Usunni na Ushia

96.

Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu

97.

Hukumu ya kujenga juu ya makaburi

98.

Swala ya maiti na kumlilia maiti

99.

Shiya na Hadithi (kinyarwanda)

100.

Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu

101.

Hadithi ya Thaqalain

102

Fatima al-Zahra

103.

Tabaruku

104.

Sunan an-Nabii

105.

Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza)

106.

Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili)

107.

Mahdi katika sunna

108.

Kusalia Nabii (s.a.w)

109.

Ujumbe -Sehemu ya Kwanza

110.

Ujumbe - Sehemu ya Pili

111.

Ujumbe - Sehemu ya Tatu

112.

Ujumbe - Sehemu ya Nne 108

12:03 PM

Page 108


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? 113.

Ngano ya kwamba Qur’ani imebadilishwa

114.

Iduwa ya Kumayili

115.

Maarifa ya Kiislamu.

116.

Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza

117.

Ukweli uliopotea sehemu ya Pili

118.

Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu

119.

Ukweli uliopotea sehmu ya Nne

120.

Ukweli uliopotea sehmu ya Tano

121.

Johari zenye hekima kwa vijana

122.

Safari ya kuifuata Nuru

123.

Idil Ghadiri

124.

Myahudi wa Kimataifa

125.

Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi

126.

Visa vya kweli sehemu ya Kwanza

127.

Visa vya kweli sehemu ya Pili

128.

Muhadhara wa Maulamaa

129.

Mwanadamu na Mustakabali wake

130.

Imam Ali binamu ya Mtume Sehemu ya Kwanza

131.

Imam Ali binamu ya Mtume Sehemu ya Pili

132.

Khairul Bariyyah

133.

Uislamu na mafunzo ya kimalezi

134.

Vijana ni Hazina ya Uislamu.

135.

Yafaayo kijamii

136.

Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu

137.

Taqiyya

138.

Vikao vya furaha 109

12:03 PM

Page 109


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? 139.

Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje?

140.

Uislamu na Mazingatio Sehemu ya Kwanza

141.

Uislamu na Mazingatio Sehemu ya Pili

142.

Azadari-Kuhuzunika na Kuomboleza

143.

Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah

144.

Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu

145.

Kuonekana kwa Allah

146.

Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza)

147.

Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili)

148.

Ndugu na Jirani

149.

Ushia ndani ya Usunni

150.

Maswali na Majibu

151.

Mafunzo ya hukmu za ibada

152

Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisusunni No 1

153.

Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisusunni No 2

154.

Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisusunni No 3

155.

Abu Huraira

156.

Kati ya Alama kuu za dini ni swala ya Jamaa na Adabu za Msikiti na Taratibu zake

157.

Uadilifu katika Uislamu

110

12:03 PM

Page 110


Shia asema haya,Sunni asema haya, wewe

wasemaje final Lubumba.qxd

7/15/2011

Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje?

BACK COVER Shia Asema Haya, Sunni Asema Haya, Wewe Wasemaje? Msomaji mpendwa!

Ewe

Ndani ya kitabu hiki utasoma kauli mbalimbali zitakazokuelezea kuhusu imani za makundi mawili, kila moja kati ya hayo mawili likijinasibu kwenye Uislamu, huku likiona kuwa lenyewe pekee ndilo lililo kwenye haki, na jingine liko kwenye upotofu. La kwanza ni: Shia[Imamia] Ithnaasharia, wafuasi wa madhehebu ya watu wa Nyumba ya Mtume (Ahlul Bait) wa Mwenyezi Mungu SAW (Sallallaahu ‘Alayhi Wa-aalih – rehema na baraka za Allah ziwe kwake na kwa Aali zake) na kizazi chake ambao ni Maimamu Watakatifu AS (‘Alayhimus Salaam - amani iwe juu yao). La pili ni: Sunni, wafuasi wa madhehebu nne zilizozuka baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu SAW, zilizojitenga na madhehebu ya kizazi chake na watu wa nyumba yake ambao ni Maimamu Watakatifu AS. Jambo ambalo Uislamu unakuwajibisha ikiwa kweli wewe ni Mwislamu, na akili inakulazimisha ikiwa kweli unatafiti na kutafakari, ni kuzamisha fikira zako ndani ya kile anachosema Shia, kile kinachokueleza kuhusu imani yake, na ndani ya kile anachosema Sunni, kile kinachokueleza kuhusu imani yake. Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation

111

12:03 PM

Page 111


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.