SHIA NA HADITH Majibu na Maelezo
الشيعة و الحديث
Abdilahi Nassir
© Haki ya kunakili imehifadhiwa na: Al-Itrah Foundation
ISBN No: 978 – 9987 – 17 – 090 – 6
Kimeandikwa na: Abdilahi Nassir
Kimehaririwa na: Alhajj Ramadhani S. K. Shemahimbo
Kimepitiwa na: Mbarak A. Tila
Kimepangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation
Toleo la kwanza 1995 – Nakala 2000 Toleo la pili 2001 – Nakala 5000 Toleo la tatu Januari 2015 – Nakala 2000
Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation
S.L.P. - 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: w.w.w.alitrah.info
SHIA NA HADITH
SHUKURANI Tunamshukuru Sheikh Abdilahi Nassir kwa kuturuhusu sisi Al-Itrah Foundation kuchapisha kitabu chake hiki “Shia na Hadith – Majibu na Maelezo” toleo la tatu nakala 2000. Ni matumaini yetu kwamba wasomaji wetu watanufaika na mtiririko huu wa majibu na maelezo juu ya kitabu al-Khututul Aridhwa cha Muhibbudin al-Khatib ambamo anapinga na kujaribu kukatisha tamaa juu ya uwezekano wa maelewano baina ya madhehebu mbalimbali za Kiislamu ambayo masheikhe wamejaribu kuushughulikia. Tunamshukuru sana Sheikh kwa kuandika kitabu hiki. Tunamombea kila la kheri, Allah Aza wa Jalah ampe tawfiq azidi kutuelemisha kwa kalamu yake ya maarifa na upole.
iv
Yaliyomo Neno la Mchapishaji ���������������������������������������������������������������������������������� 1
UTANGULIZI ������������������������������������������������������������������������������ 3 HADITH KWA SUNNI ��������������������������������������������������������������� 5
• Kutokhalifu Hadith Sahihi �������������������������������������������������������������� 7
• Mustwalalahul Hadith ������������������������������������������������������������������� 10
• Sharti ya Usahihi wa Hadith ��������������������������������������������������������� 11
• Tarekhe za Wapokezi wa Hadith ��������������������������������������������������� 12
• Hadith ya mwongo au asiyejulikana ��������������������������������������������� 13
HADITH KWA SHIA ���������������������������������������������������������������� 16
• Kwa nini kuchagua wapokezi? ����������������������������������������������������� 20
• Kuswihi sanad ������������������������������������������������������������������������������� 21
• Hadith zisizo sahihi ziko hata kwa Sunni. ������������������������������������ 22
• Za Mitume wengine ���������������������������������������������������������������������� 23
• Za Mtume Muhammad (s.a.w) ������������������������������������������������������ 28
• Za Mwenyezi Mungu (s.w.t) ��������������������������������������������������������� 33
• Mwisho ����������������������������������������������������������������������������������������� 46
v
SHIA NA HADITH
NENO LA MCHAPISHAJI
K
itabu ulichonacho mikononi mwako asili yake ni cha lugha ya Kiswahili kwa jina “SHIA NA HADITH” kilichoandikwa na Sheikh Abdilahi Nassir. Kitabu hiki ni majibu ya kitabu cha Wahhabi, “al-Khututul Aridhwa” (kwa lugha ya Kiarabu) cha Sheikh Muhibbudin al-Khatib wa Misr (mwaka wa 1930) na kufanyiwa tarjuma ya Kiswahili kwa jina la “Misingi Mikubwa lliyojengewa Dini ya Ushia” na taasisi ya Kianswari (Wahhabi) ya Mombasa Kenya katika mwaka wa 1988. Bahati mbaya kama ilivyo kawaida ya waandishi wa Kiwahhabi hawajishughulishi kuangalia majibu yanayotolewa na Mashia, waliendelea kutoa kitabu chao hicho “Misingi Mikubwa lliyojengwa Dini ya Ushia” kwa nia ya kuzidi kuwapotosha watu. Badala ya kutoa majibu kwa majibu ya Mashia, wanarudia yaleyale waliyoandika mwanzo. Huu ni msiba mkubwa kwa wasomi wa aina hii! Kutokana na hali hiyo kwa ruhusa ya Sheikh wetu tunatoa tena toleo lingine la kitabu hiki “Shia na HADITH” ambacho ni moja ya milolongo ya vitabu vyake vya majibu ya kitabu hicho. vingine ni ‘Shia na Qu’an’ ‘Shia na Swahaba’ na ‘Shia na Taqiyah’ Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa makubwa hususan wakati huu ambapo Waislamu wenye nia safi wanapigania umoja wa Waislamu baada ya kuona hatari inayouzunguka Uislamu na Waislamu. Tunawaomba wasomaji wetu wasome kitabu hiki kuanzia mwanzo mpaka mwisho ili wapate somo kutokana na yaliyomo humu na kuyafanyia kazi. 1
SHIA NA HADITH
Kwa mara nyingine tena tunamshukuru Sheikh wetu huyu kwa kutupa ruhusa hii ya kukichapisha tena kitabu hiki. Pia shukrani zetu ziwaendee wale wote waliosaidia kwa njia moja au nyingine mpaka kuwezesha kitabu hiki kuchapishwa. Allah (swt) awalipe wote malipo mema ya hapa duniani na Akhera pia. MCHAPISHAJI AL-ITRAH FOUNDATION
2
SHIA NA HADITH
UTANGULIZI
S
ifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehema na amani zimshukie bwana wetu na mwombezi wetu, Muhammad b. Abdillahi, na ali zake wema waliotakaswa wakatakasika, na wote wanaofuata nyayo zao.
Hiki ni kitabu cha pili katika mfululizo wa majibu yetu ya al-Khuutul Aridhwa kilichoandikwa na marehemu Sheikh M. al-Khatib kwa lugha ya Kiarabu, kiasi cha miaka thelathini iliyopita, na kufasiriwa kwa Kiswahili huku Kenya, hivi karibuni, kwa jina la Msingi Mikubwa iliyojengewa Dini ya Ushia. Katika kitabu hiki, tumejaribu kuyajadili yote yale ambayo Sheikh M.al-Khatib aliyaeleza dhidi ya Shia, kuhusu Hadith za Mtume Muhammad (s.a.w). Na kama tulivyofanya katika kitabu chetu cha kwanza, Shia na Qur’ani, tumeyalinganisha hayo na yale yanayopatikana katika vitabu vya Kisunni. Ni matumaini yetu kwamba, baada ya kukisoma kitabu hiki, itakudhihirikia kwamba hakuna hitilafu kubwa hivyo baina ya msimamao wa Sunni juu ya Hadith na ule wa ndugu zao, Shia, hata iwazuie wao kukurubiana na kuelewana kama alivyopendelea Sheikh M. al-Khatib. Kitu cha pekee kinachozuia ndugu wawili hao kuelewana ni zile chuki zinazojengwa baina yao na wale ambao watapata hasara lau ndugu hao watasikilizana na kuungana! Lli uweze kufaidika na majadiliano yaliyomo humu, na yale yaliyomo katika vitabu vyetu vingine katika mfululizo huu, ningependa uhakikishe kwamba:
3
SHIA NA HADITH
i.
Unayo nakala ya hicho kitabu cha Sheikh M. al-Khatib tunachokijibu. Kama huna, jaribu kukipata kutoka mojawapo ya anwani hizi: S.L.P. 70541/67971/48509 zote za Nairobi, Kenya. Hivi vyetu, unaweza kuvipata kwa kutuandikia kwenye S.L.P 86260, Mombasa, Kenya. ii. Tunapotaja kwamba maneno fulani ya Sheikh M. al-Khatib yamo kwenye ukurasa fulani wa kitabu chake, hakikisha umefungua ukurasa huo na kuyakinisha kwamba tumeyanukuu maneno haya vilivyo. Kama sivyo, tafadhali tuandikie utukosoe ili tuvveze kujisahihisha. Maana nia yetu si kumzulia marehemu Sheikh uwongo, bali ni kujenga umoja wa Waislamu kwa kujaribu kuondoa kutoelewana kulioko baina yao. iii. Tunapotoa ushahidi wa vitabu fulani, ujaribu kuangalia ushahidi huo katika vitabu hivyo, kwa lugha unayoielewa. Kama hakuna kwa lugha hiyo, basi mwendee shekhe yeyote aliye karibu nawe, na ambaye hayuko upange wowote katika mzozo huu, umwombe akuangalilie katika nuskha za Kiarabu alizonazo yeye ili uhakikishe kwamba tulivyonukuu ndivyo. Kama sivyo, tafadhali usisite vile vile kutujulisha ili tuweze kuelekezana. Mwisho, ningependa kurudia tena kwamba lengo letu katika kuandika majibu haya si kutafuta ubishi wala mizozo, bali ni kutaka tu kuonyesha kwamba vile vikwazo vya kuzuia uelewano na umoja baina ya Sunni na Shia, ambavyo Sheikh M. al-Khatib alidhania viko, haviko! Kama tutafaulu kulithibitisha hilo, tutakuwa tumepiga hatua kubwa kwa maslahi ya Waislamu wote. Ewe Mola! Tusaidie ABDILAHI NASSIR Nairobi, Kenya Rajab, 1409 Machi, 1989 4
SHIA NA HADITH
HADITH KWA SUNNI 1.
Katika uk.29 wa kitabu chike, Sheikh M. al-Khatib amesema: Hadith kwa Ahlil-sunnah ni tumbuko la pili la sharia, na ndizo zenye kuifasiri Qur’an tukufu.
Majibu: Hilo si kwa Sunni peke yao. Hata kwa Shia ni vivyo hivyo. Kwa mfano, unaposoma al-Kafi, Juzuu ya Kwanza, uk.69-70 utaona Hadith zifuatazo: a.
Imepokewa kwa Abu Abdillahi (a.s) kwamba amesema: ‘Kila kitu ni chenye kurejezwa kwenye Kitabu na Sunna; na kila Hadith ambayo haiwafikiani na Kitabu cha Mwenyezi Mungu basi (Hadith hiyo) ni uwongo.’
b.
Imepokewa kwa Ibn Abii Umayr... kwamba amemsikia Abu Abdillahi (a.s) akisema: ‘Yeyote anayekwenda kinyume na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya Muhammad (s.a.w.w) basi (huyo) amekufuru.’
c.
Imepokewa kwa Ali b.al-Husayn (a.s) kwamba: ‘Bora ya amali mbele za Mwenyezi Mungu ni ile iliyofanywa kwa kufuata Sunna, japo iwe ni kidogo.’
d.
Imepokewa kwa Amirul Mu’minina (a.s) kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) amesema: ‘Hakuna maneno (yanayokubaliwa) ila kwa vitendo; na hakuna maneno wala vitendo (vinavyokubaliwa) ila kwa nia; na hakuna maneno wala vitendo wala nia (inayokubaliwa) ila yawafikiane na Sunna.’
5
SHIA NA HADITH
e.
Imepokewa kwa Jabir kwamba Abu Ja’far (a.s) amesema: ‘Hakuna yeyote ila ana nishati na utulivu. Basi yule ambaye nishati yake imo katike sunna, huyo ameongoka. Na yule ambaye (nishati yake) imo katika bid’a (uzushi), huyo amepotea.
f.
Imepokewa kwa Abu Abdillahi (a.s) kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) amesema: ‘ Kila Haki ina hakika, na kila ta sawa lina nuru. Basi linalokubaliana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu, lichukeni; na linalopingana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu, liacheni.’
g.
Imepokewa kwamba Abu Abdillahi (a.s) amesema: ‘Hadith yoyote isiyowafikiana na Qur’ani uwongo.’
h.
Imepokewa kwamba Abu Abdillahi (a.s) kwamba Mtume (s.a.w) alihotubu Minaa akasema: ‘Enyi watu! Lolote linalowajia kutoka kwangu, linalowafikiana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu, basi mimi nimelisema. Lakini linalowajia likawa linapingana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu, basi hilo sikulisema.’
Kutokana na Hadith hizo, ambazo nimezitoa katika kitabu kimoja tu kati ya vitabu vingi vya Hadith vinavyokubaliwa na Shia, itadhihiri kwamba kama vile ambavyo Sunni wanaamini kwamba Sunna ya Mtume Muhammad (s.a.w) ni’chimbuko la pili la sheria’ na ndiyo inayoifasiri Qur’ani Tukufu, ndivyo vivyo hivyo wanavyoamini ndugu zao, Shia. Ili kuthibitisha hilo kwa vitendo tazama, kwa mfano, jinsi Shia wanavyosali. Jee, wamepata wapi, kama si katika sunna, ile idadi ya rakaa za swala zao?
6
SHIA NA HADITH
Wametoa wapi kurukuu, kusujudu na kukaa tahiyatu? Wameipata wapi Allahu Akbar au Samiallahu Liman Hamida au Rabbiyal Adhimu Wabihamdihi au Subhana Rabbiyal A’laa Wabihamdihi? Wamezipata wapi zote hizo hali hazimo katika Qur’ani? Bila shaka wamezipata katika Hadith za Mtume (s.a.w) kama walivyozipata ndugu zao, Sunni. Kwa hivyo kama Shia hawakubali kuwa Hadith za Mtume (s.a.w) ni chimbuko la pili la sheria, na kwamba ndizo zinazoifasiri Qur’an Tukufu, bila shaka wasingekuwa na mambo yote hayo katika swala zao. Ile kuwa wanayo yote hayo, na mengi mengine ambayo hatukuyataja, ni ushahidi tosha kwamba wanalikubali hilo. Juu ya yote hayo, mtu yeyote anayeweza kusoma ni kukielewa Kiarabu natazame, katika tafsiri yoyote ya Shia ya Qur’ani Tukufu, jinsi Sura 4:80, 16:44, 59:7 na nyingine kama hizo zilivyofafanuliwa ili aweze kuelewa vyema msimamo wa Shia kuhusu Hadith za Mtume (s.a.w) kama chimbuko la pili la sheria ya Kiislamu.
Kutokhalifu Hadith Sahihi 2.
Akasema tena (katika huo huo uk.29)
Na wala haifai kukukhalifu hukumu za Hadith yoyote iliyoswihi kutokamana na Mtume (s.a.w.w) Majibu: Hilo pia si kwa Sunni peke yao. Hata kwa Shia ni vivyo hivyo; na kama mtu ataikataa au ataikhalifu Hadith yoyote iliyoswihi, basi huyo ni kafiri. Taz.Hadith Na. (b) katika uk.3.humu. Lakini hata hivyo, tunapotazama vitabu vya Kisunni tunaona kwamba matendo yao ni kinyume na madai ya Sheikh M. al-Khatib hapo juu. Wao hukhalifu hukumu za Hadith hizo; na hapa chini tunatoa mifano miwili mitatu tu: 7
SHIA NA HADITH
i.
Talaka tatu: Tunaposoma vitabu vya Kisunni vya Hadith tunaona kwamba Bwana Mtume (s.a.w), alipoendewa na mtu aliyemwacha mke wake talaka tatu katika kikao kimoja, alimwambia: ‘Hiyo ni moja tu. Mrejee, ukipenda.’ Lakini Umar b.al-Khattab, alipokuwa Khalifa, akahukumu kinyume cha hivyo. Yeye akasema talaka tatu ni tatu!
Ukitaka kuyaona hayo, tazama Mlango wa Talaka katika vitabu vya Kisunni vya Hadith k.v. Sahih Muslim, al-Mustadrak, Sunan Abi Dawud, na hata Bulughul Maram ya Ibn Hajar as-Asqalani inayosomeshwa sana misikitini mwetu. Mote humo utaona imeandikwa kwamba talaka tatu zilikuwa ni moja katika enzi ya Bwana Mtume (s.a.w), na ya Abubakar, na miaka miwili ya kwanza ya Ukhalifa wa Umar. Lakini baadaye Umar akazifanya ni tatu! Na hivyo ndivyo ilivyo hadi leo katika madhehebu yote ya Kisunni! Jee, hapo ndugu zetu wa Kisunni watakuwa wamefuata Hadith ‘iliyoswihi kutokamanana Mtume (s.a.w)’ au watakuwa wamefuata sunna ya Khalifa Umar? Kwa wale wanaojua Kiingereza nawatazame Hadith Na.34913493 katika uk.759 wa Juzuu ya Pili ya Sahih Muslim, na Hadith Na. 2193-2194 katiak uk.593 wa Juzuu ya Pili ya Sunan Abi Dawud. ii. Swala ya Tarawehe: Swala hii haikiswaliwa jamaa; bali ikiswaliwa kila mtu peke yake. Hivyo ndivyo ilivyokuwa zama za Mtume (s.a.w), na hata zama za Ukhalifa wa Abubakar:mpaka alipofariki dunia mwaka 13H.Halafu akatawala Umar b.al-Khattab mwaka huo huo wa 13H, akafunga Ramadhan na asibadilishe chochote. Ilipotika Ramadhan ya mwaka 14H ndipo alipomteua Ubayy b. Ka’b aswalishe watu jamaa. Hata siku ya pili alipoona watu wakiswali hivyo, akasema: ‘Bora ya bid’a (uzushi) ni hii!’ 8
SHIA NA HADITH
Tazama hayo katika ‘Kitabus Sawm’ Mlango wa ‘Fadhl Man Qaama Ramadhan’ katika Sahih Muslim. Kwa wale wenye tafsiri za Kiingereza za vitabu hivyo, nawatazame Hadith Na.227 katika uk.126 wa Juzuu ya Tatu yaSahih Muslim, Hadith Na.1663 katika uk.366 wa Juzuu ya Kwanza ya Sahih Muslim, na hata Hadith Na.136 katika uk.358-359 wa Juzuu ya Kwanza ya Sunan Abi Dawud. Na hilo la kuwa Umar b. al-Khattab ndiye aliyeizua tarawehe hivi iswaliwavyo na Sunni leo, linakubaliwa na wanazuoni wakubwa wakubwa wa Hadith wa Kisunni. Kwa mfano, ukitazam uk.173 wa Juzuu ya Pili ya Subulus Salaam (sherehe ya Bulughul Maram) utamwona Imam as-Swan’ani asema: ‘Ama hii tarawehe, ilivyozowewa sasa, haikuwa hivi zama za Mtume (s.a.w). Kwa hakika aliyeizua ni Umar wakati wa Ukhalifa wake, akamwamrisha Ubayy aswalishe watu jamaa.’ Na kama hivyo ndivyo alivyosema Ibn Hajar al-Qastwalani katika Irshadus Saari (sherehe ya Sahih Bukhari alipofikia kile kipande cha maneno ya Umar b. al-Khattab kisemacho: ‘ Bora ya bid’ani hii.’. Yeye amesema: ‘(Umar) ameiita hiyo bi’da kwa sababu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) hakuwawekea sunna hiyo, wala haikuwako zama za as-Siddiq (r.a), wala mwanzo wa usiku, wala idadi hii!..’ Kwa hivyo ni wazi hapa vile vile kwamba, kinyume na anavyodai Sheikh M.al-Khatib, sio wakati wote Sunni hufuata Hadith iliyoswihi kutokamana na Mtume (s.a.w). 3.
Ndoa ya Muda (mut’a): Hii ni ndoa ya sheria iliyowekwa na Mwenyezi Mungu (s.w.t) kama ilivyo katika Sura 4:24. Ndoa hii ilikuwa ikitendeka zama za Bwana Mtume (s.a.w) ikatendeka zama za Khalifa Abubakar mpaka akafariki dunia. Ikaendelea 9
SHIA NA HADITH
katika enzi ya Umar b.al-Khattab mwanzo mwanzo; baadaye akaiharamisha! ‘Na tangu siku hiyo ikawa ni haramu kwa Sunni hadi hii leo!’ Ukitazama Sahih Muslim,‘Kitabun Nikah’. Mlango wa ‘Nikahul Mut’a’ utaona jinsi Jabir b. Abdillahi anavyosema kwamba walikioa mut’a zama za Mtume (s.a.w) na Abubakar na Umar; mpaka Umar alipokuja kuizuia kwa ajili ya Amr b.Hurayth. Pia tazama Musnad Ahmad, Juzuu ya Tatu, uk.380. Kwa wale wenye tafsiri ya Kiingereza, nawatazame Hadith Na. 3249-3250 katika uk.706 wa Juzuu ya pili Sahih Muslim... Kwa hivyo, na hapa pia, twaona sunna iliyowekwa na Mwenyezi Mungu na Mtume wake (s.a.w.w), ikaondolewa na Umar; na Sunni nao wakajiharamishia hadi leo! Kwa mifano mitatu hii (na kuna mingi mingine nimeiacha) itaonekana kwamba madai hayo ya Sheikh M. al-Khatib (yaliyomo uk.29 wa kitabu chake hicho) hayana mashiko!
Mustwalahul Hadith 4.
Akaendelea kusema, hapo hapo uk.29, kwamba:
Na kwa ajili ya kuswahihisha hadith kuna misingi ambayo wanavyoni wa Ummah wameafikana kuitegemea katika ilimu inayojulikana kwa jina la Mustwalahul Hadith. Majibu: Elimu hiyo haiko kwa Sunni peke yao. Iko hata kwa Shia; na vitabu imetungiwa k.v. ad-Diraya Fii llmi Mustwalahil Hadith ‘cha Zaynuddin b. Ali al-Amily, maarufu ‘as-Shahiduth Thani’. Qawa’idul Hadith cha Muhyiddin al-Musawil Ghurayf, na vinginevyo (taz.uk.8 humu) 10
SHIA NA HADITH
Sharti ya usahihi wa Hadith 5.
Akamalizia:
Na nia ya kutimiza hilo ni kuhakikisha kushikamana sawa nyororo ya wapokezi wa Hadith pasi na kubagua kati ya wanaume na wake isipokuwa kukhusu kuhakiksha kuwa ushahidi ni wa uadilifu. Majibu: Na vivyo hivyo ndivyo hasa ilivyo kwa Shia. Kwao wao vile vile Uislamu (sio madhehebu) na uadilifu wa mpokezi wa Hadith ni miongoni mwa sharti kubwa za kuhukumia usahihi wa Hadith yoyote. Kwa ajili hii utaona kwamba, pamoja na hitilafu zilizoko baina yao na Sunni, Shia huzikubali Hadith zilizopokewa kwa Sunni bora tu awe ni mwadilifu; kama anavyotweleza Sayyid Muhammad Taqiy al-Hakim katika uk.219 wa kitabu chake kitwacho al-Usulul Aammah (chapa ya kwanza): Shia Imamiyya huzizingatia habari za wapinzani wao katika akida (imani) kuwa ni hoja inapothubutu kwamba (watu hao) ni thuqaat (wanaoaminika): na habari zao hizo huziita muwaththaqaat (zenye kuaminika). Nazo (habari hizo) katika kuwa ni hoja. Ni kama habari nyinginezo (zilivyo). Na vitabu vyao yaani Shia) vimejaa hayo. Lakini pamoja na yote hayo, tunapotazama vitabu vya Kisunni vinavyohusu sanad (nyororo za wapokezi) twaona kwamba wao wakati mwingine humtia hila (aibu) mpokezi kwa sababu za kibinafsi; sio kwamba si mwadilifu! Kwa mfano, ukitazama Tahdhibut Tahdhib chini ya jina la Abdullah b. Sa’d Abu Qudama as-Sarkhasi, utaona kwamba Muhammad b.Yahya amekataa Hadith zake kwa sababu tu ‘Muhammad aliingia kwake, naye (Abdullah b. Sa’d) hakumsimamia’! 11
SHIA NA HADITH
Kadhalika ukitazama katika kitabu hicho, chini ya jina la Sa’d b. Ibrahim b. Abdulrahman b. Awf, utaona kwamba Imam Malik hakupokea Hadith zake kwa sababu ‘alimwaidhi’ kwa maneno yaliyomuudhi. Na vivyo hivyo ndivyo alivyosema Ibn Mu’in, humo humo, kwamba ‘Sa’d alisema kitu juu ya nasabu ya Malik ndiyo (Malik) akaacha kupokea kwake”!. Ukija kwenye Mizanul I’tidal, chini ya jina la Abdullah b. Dhakwan (maarufu Abuz Zanaad), utaona Rabia anasema kwamba si thiqah (wa kutegemeka). Kisha inaendelea: ‘Neno la Rabia kumhusu (huyu Abuz Zanaad) lisisikilizwe maana baina ya wawili hao palikuwa na uadui ulio dhahiri.’ Haya! Hiyo ni mifano miwili mitatu tu. Mingine nimeiacha. Kutokana na mifano hiyo tunaona kwamba lile dai la Sheikh M. al-Khatib, kwamba sharti kubwa katika kutimiza usahihi wa Hadith ni kuhakikisha uadilifu wa mpokezi, halitumiki wakati wote. Maana tumeona hapo juu kwamba kuna wapokezi ambao riwaya zao zimekataliwa kwa sababu za kibinafsi, sio kwamba si waadilifu! Jee, mambo yakiwa ni hivyo, tutakuwa na hakika gani kwamba Hadith nyingine hazikukataliwa kwa sababu hizo hizo za kibinafsi? Tarekhe za wapokezi wa Hadith 1.
Akaongeza shekhe wetu huyo (uk.30):
Na kila (mpokea) wa Hadith ana tarekhe inayojulikana, na Hadith maalumu zenye kudhibitiwa zilo swahihi au zilotaywa kwa kuwa si swahihi. Majibu: Na hili pia ndivyo lilivyo kwa Shia. Wao, kama ndugu zao Sunni, wana vitabu maalum vyenye tarekhe na habari za wapoke12
SHIA NA HADITH
zi wao wa Hadith pamoja na kudokeza usahihi au uwongo wa Hadith hizo. Miongoni mwa vitabu hivyo ni hivi vichache tunavyovitaja hapa chini: I.
At-Tustiri: Qamusur Rijal
II.
Al-Ardabili: Jamiur Ruwat
III.
Al-Khui: Mu’jamu Rijalil Hadith
IV.
Mamqani: Tanqihul Maqal
V.
An-Najjashi: Rijalun Najjashi
VI.
Allama Hilli: Khulaswatur Rijal
VII.
At-Twusi: Ikhtiyaru Ma’rifatir Rijal
VIII. Al-Muqmaqani: Miqyasul Hidaya IX.
Al-Amili: al-Bidaya Fi llmid Diraya
X.
Hasan as-Sadr: Sarhui Wajiza
Kwa hivyo, wenye vitabu vya aina hiyo si Sunni peke yao; bali na Shia pia wanavyo. Hadith ya mwongo au asiyejulikana 2.
Mwisho Sheikh M. al-Khatib akafunga maneno yake hayo kwa kusema (uk.30):
Haikubaliwi Hadith iliyopokewa na mrongo au asiyejulikana, wala kwa yeyote kwa sababu ya ujamaa tu au ya kizazi. Majibu: Hilo li wazi mno: halihitaji hata kusemwa! Hakuna mtu yeyote, sikwambii Mwislamu, anayeweza kukubali habari iliyosimuliwa na mwongo; seuze uwongo huo uwe amezuliwa Bwana Mtume (s.a.w)! 13
SHIA NA HADITH
Hata hivyo, tunapochunguza kwa makini baadhi ya vitabu vya Kisunni vya tarekhe za wapokezi wa Hadith tunaona kwamba, kinyume na alivyodai Sheikh M.al-Khatib, wanazuoni wa Kisunni hukubali Hadith zilizopokewa na ‘waongo’ na majhulul hali (wasiojulikana hali zao)! Ili kulithibitisha hilo, hapa chini nataja majina ya wapokezi kumi tu (ingawa tunayo zaidi ya hayo) walioelezwa hivyo katika Tahdhibut Tahdhib na/au Mizanul l’tidal; na wote hao wamo katika Sahih Bukhari na/au Sahih Muslim ambavyo ndivyo vitabu sahihi mno kwa Sunni: I.
Ash’athb. Said al-Basry
II.
Suwayd b. Said Abu Mohammad al-Harawi
III.
Abdullah b. Swalih b. Muhammad b. Muslim
IV.
Abdulrahman b. Nu’man b. Ma’bad
V.
Abdulwahhab b. Atta al-Khafaf
VI.
Ali b. Abdillahi b. Ja’far
VII.
Muhammad b.Ishaq b. Yasar
VIII. Nu’aim b.Hammad al-Khuzai IX.
Asbat Abul Yasa’
X.
Ismail b. Abdillahi Abi Uwais b.Abdillahi al-Asbahi
Juu ya hao kuna watu kama: I.
Ismail b. Sami’ al-Kufi al-Hanafi ambaye, inaelezwa katika Mizanul I’tidal, kwamba alikuwa jirani na msikiti kwa miaka arobaini,lakini hakuonekana katika swala ya Ijumaa wala 14
SHIA NA HADITH
jamaa! Na bado mtu kama huyo mna riwaya zake katika Sahih Muslim! II. Hajjaj b. Artwaat ambaye, kwa mujibu wa Imam Shafi, alikuwa akisema kwamba murua wa mtu hautimii mpaka aache kuswali jamaa! Pia, kwa mujibu wa al-Aswma’i, mtu huyo ndiye Kadhi wa kwanza kupokea hongo Basra! Na alipoulizwa kwa nini hahudhurii swala ya jamaa msikitini, alijibu: ‘Nihudhurie msikitini kwenu ili wachukuzi na wauza mboga wasongamane nami?’ Yote hayo yamo katika Mizanul I’tidal chini ya jina lake; na bado mtu kama huyo riwaya zake zimo katika Sahih Muslim! Jee, watu kama hao watakuwa ni waadilifu kwa kipimo gani? Ewe ndugu yangu! Mpaka hapa nataraji ushaona kwamba yote yale ambayo Sheikh M. al-Khatib amewadaia Sunni kuhusu Hadith za Mtume (s.a.w) ndiyo yaliyoko kwa Shia. Kama kuna hitilafu yoyote (na ziko kama tutivyokwisha kuona), basi hitilafu hiyo si ya kuzuia makundi mawili hayo kukurubiana na kushirikiana kwa maslaha ya Uislamu, kama Sheikh M. al-Khatib alivyokusudia kuonyesha katika kitabu chake. Sasa tuyajadili yale aliyowasingizia Shia katika uk.30 wa kitabu chake hicho. Na kuwafikiwa ni kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t).
15
SHIA NA HADITH
HADITH KWA SHIA i.
Katika uk.30 wa kitabu chake, Sheikh M.al-Khatib amesema hivi:
Maisha hawazitegemei hadith zozote zisizo kutegemezwa kwa jamaa wa Mtume, na baadhi ya hadith za watu fulani waliokuwa pamoja na Ali (r.a) kwenye vita vyake vya kisiasa, na wanazikataa nyinginezo. Majibu: Si kweli kwamba Shia wanazikataa Hadith zisizotegemezwa kwa Ahlul Bayt (watu wa Nyumbani kwa Mtume s.a.w) na waliokuwa pamoja na Imam Ali (a.s). Ukweli ni kwamba wanazikubali bora tu ithubutu kwamba watu hao ni waadilifu na waaminifu. Likithubutu hilo, kama tulivyokwisha kuona uk.7 humu, hapana tatizo. Na si kwamba huzikubali tu, bali huzipa daraja ya muwath-thaq (yaani ‘zenye kutegemeka’) kama ilivyo wazi kwa yeyote anayesoma vitabu vya Kishia vya Mustwalahul Hadith. Hata hivyo, ni kweli kwamba Shia huzipa uzito mkubwa, na kwa hivyo huzitegemea zaidi, zile Hadith zilizotegemezwa kwa Ahlul Bayt na wale waliokuwa pamoja na Imam Ali (a.s) katika vita vyake.1 Na hilo ni kwa sababu zilizo wazi kueleweka kwa yeyote asiye na chuki. Shia huwapa Ahlul Bayt uzito mkubwa zaidi kwa sababu: i.
1
Mwenyezi Mungu amewaondolea uchafu (dhambi) na kuwatakasa kikamifu, kama ilivyodokezwa katika Sura 33:33;
Sheikh M.al-Khatib ameviita vita hivi “vya kisiasa”! Kwa kweli si vya kisiasa. Ni vya kidini hasa kama inavyoeleweka waziwazi kutokana na baadhi tu Hadith za Bwana Mtume (s.a.w) tulizozidokeza humu (uk, 12-13) 16
SHIA NA HADITH
ii. Kabla ya Mtume (s.a.w) kufariki dunia, aliwatangazia Waislamu kwamba anawaachia ‘vizito viwili’ ambavyo, wakishikamana navyo, hawatapotea baada yake kabisa: cha kwanza ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na cha pili ni Ahlul Bayt wake2 iii. Hadith iliyothubutu kwamba imetokana na Ahlul Bayt huwa haina mushkeli kwamba inatokana na Mtume (s.a.w) maana imepokawa kwamba, Imam Jar’far asSadiq (a.s) amesema: ‘Hadith yangu ni Hadith ya babangu, na Hadith ya babangu ni Hadith ya babu yangu, na Hadith ya babu yangu ni Hadith ya Husayn, na ya Husayn ni Hadith ya Hasan, na Hadith ya Hasan ni Hadith ya Amirul Mu’minina,3 na Hadith ya Amirul Mu’minina ni Hadith ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) na Hadith ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) ni Neno la Mwenyezi Mungu azza wajalla’. (taz Bihar, Juzuu ya Pili, ‘Kitabul llim.’) Hizo ni chache tu kati ya sababu kadhaa zinazowafaya Shia wazipe uzito mkubwa Hadith zinazotegemezwa kwa Ahlul Bayt. Pia Shia huzipa uzito mkubwa Hadith zilizopokewa kwa wale waliokuwa na Imam Ali (a.s) katika vita vyake kwa sababu: i.
Bwana Mtume (s.a.w) amesema kwamba hampendi Ali isipokuwa mu’mini, na hamchukii isipokuwa mnafiki.
Hadith ya ‘vizito viwili’ imenakiliwa katika vitabu vingi sana vya Kisunni vya Hadith k.v. Sunan at-Timidhi, Kanzul Ummal, Mishkatul Masaabih, Majma’uz Zawaid, na vinginevyo ambavyo nafasi hapa haituruhusu kuvitaja vyote. Kwa wale wanaotaka maelezo kamili, watayapata katika kanda za hotuba zangu za “Majlis ya Muharram ya mwaka 1410” ziwezazo kupatikana kwa: Bilal Muslim Mission, S.L.P 82508, Mombasa. Kenya. 3 Maksudio hapa ni Imam Ali b. Abi Twalib (a.s) 2
17
SHIA NA HADITH
Hadith hiyo unaweza kuiona katika Sahih Muslim ‘Kitabu Iman’, Mlango wa ‘ad-Dalilu Alaa Anna Hubbal Answaar Wa Ali r.a Minal Iman...’ Na kwa wale wenye tafsiri ya Kiingereza, nawatazame Hadith Na.141 katika uk.46-47 wa Juzuu ya Kwanza. Sasa basi, kama anayemchukia tu huwa mnafiki, jee anayechukuwa upanga na kumpiga vita huwaje? Jee aliyemlaani na kuamrisha watu wamlaani? Jee aliyeuwa watu waliokataa kumlaani? Wote hao nini hukumu yao? Na kama wanaompenda Imam Ali (a.s) ndio mu’mini, jee wale waliojitolea kumtetea na kumkinga na maafa wa vipi? Na kwa nini iwe ni aibu au kosa kwa Shia kuzikubali Hadith zilizopokewa kwa wapinzani wake? Pengine watetezi wa Sheikh M. al-Khatib watapendelea kutweleza! ii. Bwana Mtume (s.a.w) alimwonya Ammar b. Yasir kwamba atauliwa na ‘tapo (kundi) la waasi’; na inajulikana katika historia kwamba sahaba huyo mtukufu aliuwawa katika Vita vya Siffin mwaka 36H alipokuwa pamoja na Imam Ali (a.s) dhidi ya kundi la Muawiya b. Abi Sufyan. Onyo hilo imetajwa katika uk.114 wa Juzuu ya Pili ya Sirat Ibn Hisham; na hata katika uk.52-53 wa Masiha ya Imam Aly (a.s) cha Sheikh Muhammad Kasim Mazrui, aliyekuwa Kadhi Mkuu wa Kenya. Sasa basi, kama kundi lililomuuwa Ammar (r.a). ni ‘kundi la waasi’ (kama alivyotabiri Bwana Mtume s.a.w), ni wazi kwamba lile kundi alimokuwamo yeye lilikuwa ni la watiifu; nalo ni lile la Imam Ali (a.s) na kama ni hivyo, kwa nini basi Shia walaumiwe kwa kuzitegemea Hadith zilizopokewa kwa kundi tiifu, wasilaumiwe wale wanaotegemea Hadith zilizopokewa kwa ‘kundi la waasi’? Tungependa tuelezwe. 18
SHIA NA HADITH
i.
Bwana Mtume (s.a.w) aliwaonya wake zake wasibwekewe na mbwa wa Haw’ab; na katika baadhi ya riwaya, alimwelekea mkewe, Mw. Aisha, hasa! Hata palipotokea Vita vya Ngamia (mwaka 36H), ambapo Mw. Aisha (akiwa juu ya ngamia mwenye nywele nyingi, kama alivyotabiri Mtume s.a.w) aliongoza jeshi la kumpinga Imam Ali (a.s) alifika mahali hapo paitwapo Haw’ab na akabwekewa na mbwa hao! Papo hapo akakumbuka lile onyo la mumewe (Bwana Mtume s.a.w), na kwa kutambua kwamba hayuko upande wa haki, akataka aachwe arejee alikotoka! Kisa hicho kimeelezwa katika vitabu vingi vya historia, k.v. Tarikh at-Tabari. Al-Iqdul Farid; uk.237 wa Juzuu ya Saba ya Majmauz Zawaid; na uk.334 wa Juzuu ya Kumi na Moja ya Kanzul Ummal. Kwa hivyo, kutokana na maelezo ya kisa hicho na jinsi Bwana Mtume (sa.w.w) alivyowaonya wake zake nacho, ni dhahiri kwamba kila aliyekuwapo katika kundi la waliobwekewa na mbwa hao, alikuwa katika kundi “dhalimu’’ kama ilivyoashiriwa na Bwana Mtume s.a.w.w katika uk.283 wa juzuu ya pili ya al iqdul farid ; uk.237 wa juzuu ya saba ya majmauz Zawaid; na uk. 334 wa juzuu ya kumi na moja ya kanzul Ummal. Kwa hivyo, pale Sheikh M. al-Khatib anaposema (taz.uk.30 wa kitabu chake) kwamba Shia huzitegemea ‘baadhi ya hadithi za watu fulani waliokuwa pamoja na Ali (r.a) kwenye vita vyake vya kisiasa...’ amekusudia vita kama hivyo vya Siffin na Ngamia! Kwa maneno mingine, Shekhe wetu huyo anawalaumu Shia kwa kuzikataa Hadith za watu waliompinga Imam Ali (a.s) na kumpiga vita – hata baada ya Bwana Mtume (s.a.w) kusema alivoyasema! Basi mambo yakifika hapo, tusemeje? Bora mhukumu nyinyi, wasomaji watukufu. 19
SHIA NA HADITH
Lililo sawa, tukikumbuka maneno ya Bwana Mtume (s.a.w) juu ya Imam Ali (a.s), ni lipi? Ni kupokea Hadith zilizopokewa kwa watu Imam Ali (a.s) na kundi lake, au zile zilizopokewa kwa wapinzani wake? Hizo basi, vile vile, ni chache tu kati ya sababu nyingi zilizowafanya Shia wazipe uzito zaidi zile Hadith zilizopokewa kwa wale waliokuwa pamoja na Imam Ali (a.s), na kuzikataa za wale wapinzani wake. Nyingine tumeziacha kwa kuogopa kukirefusha kitabu hiki. Kwa nini kuchagua wapokezi Wala hili la watu fulani kuchagua habari zao kwa wale wanaoaminika zaidi kwao haliko kwa Shia peke yao. Liko kwa madhehebu yote. Kwa mfano: Ni jambo lijulikanalo, hata kwa wenye ujuzi mdogo, kwamba riwaya inayotegemeka ya Imam Malik ni ile ya Ibnul Qasim na Ash’hab; lakini ya Abdullah b.al-Hakam na mfano wake huwa haina mashiko kwa wafuasi wa madhehebu hayo. Hali kadhalika tukija kwa Mahanafi; wao hawakubali riwaya ya Abu Hanifa isipokuwa ile iliyosimuliwa na Abu Yusuf na Muhammad b. al-Hasan. Kama kuna riwaya, kinyume cha riwaya ya hao, iliyopokewa kwa al-Hasan b. Ziyad al-Lu’lui na wenziwe, basi Mahanafi huwa hawaikubali wala hawaitegemei. Vivyo hivyo ndivyo ilivyo kwa Mashafi. Wao hutegemea riwaya ya al-Muzani na ar-Rabi’b. Sulayman al-Muradi. Lakini riwaya ya al-Khuzayma na al-Jurumi, na mfano wao; hawazitegemei. Sasa basi, ikiwa mambo ni hivyo katika madhehehbu ya kifiqhi tu, ambayo hushughulika na furuu’ (matawi), jee inapokuja kwenye usul (mashina)? Kwa maneno mengine, ikiwa wafuasi wa madhehe20
SHIA NA HADITH
bu fulani hawakubali riwaya ya Imam wao ila iwe imepokewa kwa mtu anayeaminika kwao, kwa nini Sheikh M. al-Khatib ataka Shia wapokee Hadith za Bwana Mtume (s.a.w) kwa watu wasioaminika kwao? Lipi lililo muhimu zaidi kuhakikishwa? La Bwana Mtume (s.a.w), au la kina Abu Hanifa na Shafi? Kuswihi sanad 1.
Akaendela kusema (katika huo huo uk.30):
Wala hawafajishughulishi na kuswihi sanad (tegemezo) wala maelezo ya kiilimu! Kwani mara nyingi wanasema kwa mfano: ‘ Kumepokewa kwa Muhammad bin Ismail kutoka kwa baadhi ya watu wetu, kutoka kwa mtu mmoja, kutoka kwake kwamba alisema...!! Majibu: Si kweli kwamba Shia hawajishughulishi na kuswihi sanad ya Hadith. Ukweli ni kwamba,kama ndugu zao Sunni, wanakishughulisha kama tulivyoeleza uk.8 humu. Kama hawajishughulishi, kwa nini wawe na somo la mustwalahul Hadith4? Kwa nini wawe na somo la al-Jar’h wat Ta’dil5? Kwa nini wawe na vigawanyo vya Hadith? Kwa nini wawe na Kutubur Rijal6? Na ni kwa sababu Shia huchunguza sasa uadilifu na kutegemeka kwa watu ambao Hadith za Mtume hutegemezwa kwao ndio
Hii ni fani inayohusika na vigawanyo mbalimbali vya usahihi na udhaifu wa Hadith Hii ni somo linalohusika na kuchunguza saifa na ila za wapokezi wa Hadith. 6 Hivi ni vitabu ambavyo kwavyo hujulikana habari za wapokezi wa Hadith. 4 5
21
SHIA NA HADITH
ikawa wao hawawategemei watu kama Abu Hureira7, Ka’bil Al.bar8, Muawiya b. Abi Sufyan9, Abul Ghadiya Yasar b. Sab’i as-Sulami10, Abdulrahman b. Muljam11 Imran b. Hittan12, Yazid b. Muawiya13, na wengineo kama hao ambao hutegemewa na ndugu zao, Sunni! Hadith zisizo sahihi ziko hata kwa Sunni 1.
Akasema tena (ukurasa huo huo wa 30):
Huyu ndiye aliyepokea Hadith nyingi za Mtume (s.a.w) kuliko sahaba yeyote. Jumla ya Hadith zilizopokewa kwake ni 5374. Ukilinganisha idadi hiyo na ile idadi ya Hadith zilizopokewa, kwa mfano, kwa Khalifa Abubakar (142) au kwa Khalifa Umar (kiasi 50) au kwa Imam Ali (kiasi 50) au hata Mw. Aisha (2210). Utaweza kuelewa kwa nini Shia wana wasiwasi na riwaya za bwana huyu – hasa inapokumbukwa kwamba muda aliowahi kukaa na Bwana Mtume (s.a.w) tukimpa muda mrefu sana, ni miaka mitatu tu maana yeye alisilimu miaka mitatu tu kabla ya Bwana Mtume kufariki dunia! Pia unapotambua kwamba nyingi sana ya Hadith tulizozitaja katika uk.16-31 humu zimepokewa kwake! Mbali na sababu nyingine kadha wa kadha. 8 Kabla ya kusilimu kwae. Alikuwa ni miongoni mwa wanazuoni wakubwa wa Kiyahudi. Yeye hakuwa sahaba maana hakusilimu zama za Bwana Mtume (s.a.w) Alisilimu zama za Ukhalifa wa Umar b.al-Khattab. Kupita kwake. Hadith nyingi za uwongo (Israilyyaat) zimepokewa! 9 Huyu ndiye aliyempinga Imam Ali (a.s) pale alipochaguliwa kuwa Khalifa, akasababisha roho za sahaba wengi sana wakubwa wakubwa kutilifu...Yeye ndiye aliyetoa amri ya Imam Ali (a.s) alaaniwe katika hotuba za Ijumaa na Idd. Akawa huwapa tunzo wanaofanya hivyo na kuwaadhibu wanaokataa! Ndiye yeye aliyeanzisha Ufalme katika Uislamu, baada ya Imam Ali (a.s) kuuwawa kwa kuwalazimisha Waislamu wambai mwanawe, Yazid, kuwa Khalifa baada yake. Na ni yeye aliyemshawishi mke wa Sayyidnal Hasan (a.s) amtilie sumu kumuua! Mbali visa vya sahaba wengine k.w.k. waliouliwa na yeye. 10 Huyu ndiye aliyemuua Ammar b. Yasir ambaye kisa chake tumekidokeza katika uk.12 humu. 11 Huyu ndiye aliyemuua Imam Ali (a.s) 12 Huyu alisherehekea kuuwawa kwa Imam Ali (a.s) kwa kutunga shairi la kumsifu Ibn Muljama aliyetajwa chini yakidokezo Na.11 hapo juu. 13 Huyu ni mtoto wa Muawiya ambaye habari zake zimeelezwa chini ya kidokezo Na.9 hapo juu. Yeye ndiye aiyebandikwa kimabavu na babake kuwa Khalifa wa Sita (kwa kweli, ni Mfalme wa pili) wa Waislamu japokuwa alijulikana kuwa mlevi, mzinifu, mbali na maovu mengine aliyokuwa nayo! na 7
22
SHIA NA HADITH
Na vitabu vyao vi tele hadithi ambazo haimkini kuthibitisha uswahihi wazo Majibu: Ni imani ya Shia kwamba, katika ulimwengu huu, hakuna kitabu chochote kilicho sahihi chote isipokuwa Qur’ani Tukufu. Vingine vyote, hata visifike kwa ukubwa wa kadiri gani, lazima viwe na kweli na ya uwongo ndani yake. Kwa sababu hii ndio ikapokewa kwa Maimamu wa Shia (taz.uk. 3-4 humu) kwamba lolote lidaiwalo kwamba limesemwa na wao, na likawa ni kinyume na Qur’ani Tukufu, basi ni uwongo na ndio pia ikasemwa, kama tulivyoeleza katika uk.16 wa kitabu chetu, Shia na Qur’ani, kwamba kati ya Hadith 16199 zilizomo katika al-Kafi (ambacho ni kitabu kikubwa cha Hadith kwa Shia) zaidi ya asilimia hamsini si sahihi. Kwa hivyo, shekhe wetu M. al-Khatib hapo hakusema lolote jipya ambalo Shia wao wenyewe hawajalisema. La kushangaza ni kwamba alipoandika Hadithi kwa Ahlil-Sunnah’ (taz.uk.29-30 wa kitabu chake), hakutaja kwamba na vitabu vyao pia ‘vi tele hadith ambazo haimkini kuthibitisha uswahihi wazo’. Au hakulijua hilo? Kama hakulijua hilo, basi hapa chini twazitaja baadhi tu ya Hadith za aina hiyo; na ni juu ya waliokiswahilisha hicho kitabu chake, kama hawa kubaliani na sisi, watukinaishie usahihi wazo. Kwanza tuanze na zile zinazowahusu mitume wengine wasiokuwa Mtume Muhammad (s.a.w): Za Mitume wengine 1.
Imepokewa kwa Abu Hureira kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) alisema kwamba Suleimaan b. Dawud, Mtume wa Mwenyezi Mungu, alisema: Nitawajamii wake (zangu) 23
SHIA NA HADITH
sabini usiku; kila mwanamke kati yao atazaa mtoto wa kiume atakayepigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Akaambiwa: Sema Inshallah. Lakini hakusema. Basi akawajamii; lakini hakuzaa yeyote kati yao isipokuwa mke mmoja tu, tena nusu mtu! Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) akasema: Lau angalisema Inshallah asingalishindwa, na haja yake ingalitimia. Hiyo ni Hadith iliyomo katika Sahih Muslim, ‘Kitabul Aymaani’. Mlango wa al-istihnaa Filyamini Waghayrihaa’. Kuna na Hadith nyingine mbili hapo hapo isipokuwa, badala ya wake sabini kama ilivyo katika Hadith tuliyoitaja hapo juu, zimetaja ‘wake sitini na tisni’! Kwa wale wenye Sahih Muslim kwa Kiingereza, nawatazame Hadith Na. 4066,4067 na 4070 katika uk.880-881 wa Juzuu ya Tatu. Vile vile Hadith kama hiyo unaweza kuipata katika Sahih Bukhari, ‘Kitabu Bad’il Khalqi’, Mlango wa ‘Wawahabnaa Li Dawuda Sulaymana...’; pia ‘Kitabun Nikah’, Mlango wa ‘Qawlur Rajuli La –atufannal Laylata Alaa Nisaaii’; na ‘Kitabul Aymaani Wan Nudhuur’, Mlango wa ‘al-Istithnaa Fil Aymaani’ isipokuwa humo idadi ya wake wa Nabii Sulaiman (a.s) imetajwa kuwa ‘sabini’ na ‘tisini’ na ‘mia’; na wote akawaingilia kwa usiku mmoja!! Kwa wale wenye Sahih Bukhari kwa Kiingereza, nawatazame Hadith Na.635 katika uk.421 wa Juzuu ya Nne, Hadith Na. 169 katika uk. 122-123 wa Juzuu ya Saba, na Hadith Na. 711 katika uk.466467 wa Juzzu ya Nane. Ewe ndugu yangu! Tafadhali zizingatie kwa makini riwaya zote hizo, na ujiulize: kweli mwanamume, hata awe Mtume wa Mwenyezi Mungu, anaweza kuwaingilia wanawake wengi kama hao kwa usiku mmoja? Na kwa nini awe na uchu hivyo? Ataka kuonyesha nini? Miujiza ya kujamii?! Au jee, inawezekana Mtume wa Mwenyezi Mungu, kama alivyokuwa Nabii Sulaiman (a.s), akatae’kusema 24
SHIA NA HADITH
Inshallah hata baada ya kukumbushwa na malaika wa Mwenyezi Mungu, kama riwaya nyingine isemavyo? 2.
Imepokewa kwa Abu Hureira kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) amesema: Malaika wa mauti alimjia Musa(a.s), akamwambia: Mwitikie Mola wako. Musa (as.) akalipiga ngumi jicho la Malaika wa mauti, akalikoboa! Malaika akarejea kwa Mwenyezi Mungu akamrejeshea jicho lake, na akamwambia: Rejea kwa mja Wangu, na umwambie: Utakayo ni maisha? Kama wataka maisha, basi weka mkono wako juu ya mwili wa gombe dume. Kadiri ya nywele ambazo mkono wako utazifunika, ndiyo idadi ya miaka utakayoishi: Musa (a.s) akasema: Kisha (Malaika) akamjibu: Kisha utakufa...
Hadith hiyo, na nyingine kama hiyo, utaiona katika Sahih Muslim, ‘Kitabul Fadhail’, Mlango wa ‘Fadhailu Musa (a.s)’. Kwa wale wenye tafsiri ya Kiingereza kitabu hicho, nawatazame Hadith Na. 5851-5852 katika uk.1264 wa Juzuu ya Nne. Pia tazama ‘Kitabu Ahaadithil Aniyaa’, Mlango wa ‘Wafaati Musa’ katika Sahih Bukhari, na Mlango wa ‘Man Ahabbad Dafna Fil Ardhil Muqaddasah’ katika ‘Abwaabil Janaiz.’ Na katika tafsiri ya Kiingereza, tazama Juzuu ya pili, uk.236237, Hadith Na.423; na Juzuu za Nne, uk.409, Hadith Na. 619. Na kwa mujibu wa Juzuu ya Kwanza ya Tarikhul Umami Wal Muluki ya Ibn Jarir at-Tabari, pale palipotajwa ‘Kifo cha Musa’, imepokewa kwa Abu Hureira vile vile kwamba Malaika wa mauti alikuwa akiwajia watu wazi wazi; mpaka alipomwendea Musa (a.s) kufariki, ikawa huwajia watu kwa uficho! Haya! Hiyo ndiyo Hadith yenyewe. Jee, ewe ndugu yangu, waionaje? Si vituko hivyo? 25
SHIA NA HADITH
Hivi kweli binadamu, hata awe ni mtume wa Mwenyezi Mungu, aweza kumpiga ngumi Malaika aliyepewa mamlaka ya kutoa roho za watu, na alikoboe jicho lake? Kwani Malaika huyo alikwenda kuifanya kazi hiyo kwa hiari yake, au ilikuwa ni amri ya Mwenyezi Mungu? Bila shaka, ilikuwa ni amri ya Mwenyezi Mungu. Maana, kwa mujibu wa Qur’ani Tukufu, Malaika ‘hawamwasi Mwenyezi Mungu kwa alilowaamrisha, na hufanya wanayoamrishwa.’ (Sura 66:6). Kama ilikuwa ni amri ya Mwenyezi Mungu, basi nini kosa la Malaika huyo hata ajeruhiwe hivyo? Kama hakuwa na kosa, basi si wazi hapo kwamba Nabii Musa (a.s) alimdhulumu kwa kumpiga bure bure? Jee, Mtume wa Mwenyezi Mungu aweza kufanya dhuluma hivyo? Na jee, badala ya Mwenyezi Mungu kumwadhibu yule aliyemdhulumu mwenzake, ni sawa ampe bahashishi ya kuridhia kumwongezea umri? Jee, huyo Malaika alipomwendea Musa (a.s), ilikuwa ajali yake ishafika au bado? Kama ilikuwa ishafika, kwa nini akiondoka bila ya kutekeleza wajibu wake hali Mwenyezi Mungu anatwambia katika Qur’ani Tukufu (Sura 7:34) kwamba ‘inapowafikia ajali yao hawatachelewa (hata) saa moja, wala hawatatangulia’? Au ndiyo tusema Musa (a.s) ambaye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, alikiogopa kufa? Hata baada ya kuambiwa na Malaika amwitikie Mola wake? Kweli inawezekana Mtume wa Mwenyezi Mungu awe asi hivyo? Yote hayo ni maswali muhimu ambayo inataka, ewe ndugu Mwislamu, ujiulize. Na bila shaka majibu yatakayojitokeza, yatakudhihirishia wazi kwamba haiwezekani kuthibitisha usahihi wa Hadith hiyo. Au wale waliomsaidia kazi Sheikh M. al-Khatib wataweza kututhibitishia hilo? Kwamba wataweza, tutashukuru. 3.
Imepokewa kwa Abu Hureira kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) amesema: Wana wa Israeli walikuwa na des26
SHIA NA HADITH
turi ya kuoga uchi pamoja, wakitazamana nyuchi zao! Lakini Musa (a.s) akawa huoga peke yake. (Wana wa Israeli) wakasema: Wallahi! Hakuna kinachomzuia Musa kuoga pamoja nasi isipokuwa ni kwa sababu ana mshipa! Hata siku moja akaenda kuoga. Akaziweka nguo zake juu ya jiwe. Lile jiwe likakimbia na zile nguo zake! Musa (a.s) akalifukuzia huku akisema: Nguo zangu, jiwe! Nguo zangu, jiwe! Mpaka Wana wa Israeli wakautazama uchi wa Musa. Wakasema: Wallahi Musa hana ubaya wowote. Jiwe likasimama baada ya (Musa) kuonekana (uchi wake). Hapo akazichukua nguo zake, na akalipigilia mbali lile jiwe! Abu Hureira akasema: Naapa kwamba jiwe lenyewe likawa na kovu sita au saba kwa sababu ya kupigwa na Musa (a.s)! Hadith hiyo, na yingine kama hiyo, utaiona katika Sahih Muslim kabla ya Hadith mbili tulizozitaja katika Na.2 hapo juu. Na kwa wale wenye tafsiri ya Kiingereza, ni Hadith Na. 5849-5850 katika hiyo hiyo Juzuu ya Nne (uk.1263-1264). Katika Sahih Bukhari, Hadith hizo utazipata katika ‘Kitabu Bad’il Khalqi’ kwenye Mlango ulioko baada ya Hadith ya Khidhr, na katika ‘Kitabul Ghusi’, Mlango wa Ightasala Aryaanan’. Kwa wale wenye tafsiri ya Kiingereza, nawatazame Hadith Na. 277 katika uk. 168-170 wa Juzuu ya Kwanza, na Hadith Na. 616 katika uk.407 wa Juzuu ya Nne. Haya! Bismillah! Jee, ewe ndugu Mwislamu, kabla ya hata kuuliza maswali yetu, waweza kukubali kuwa Hadith hizo ni sahihi? Mwenyezi Mungu aliamrishe jiwe (maana jiwe, kwa hiari yake, halina uwezo wa kufanya hilo) likimbie na nguo za Mtume Wake (a.s) ili uchi wake uonekane na watu kwa sababu tu wajue kwamba hana mshipa? Au Mtume wa Mwenyezi Mungu afukuzanie na jiwe uchi huku akisema nalo kama kwamba lasikia au laona? Na akili27
SHIA NA HADITH
pata alipige, bado akiwa uchi, na watu wakiendelea kumtazama! Jee, Mtume huyo hakuwa na akili ya kubaki pale alipokuwapo na kupigia watu ukelele wamletee nguo nyingine? Au jiwe limehiti nini hata lipigwe hali haliwezi kufanya lililofanya isipokuwa kwa amri ya Mwenyezi Mungu? Na hata kama Nabi Musa (a.s) angekuwa na mshipa kweli, ndiyo nini? Ni aibu? Ni ila? Kwani ni aibu Mtume wa Mungu kuwa na maradhi? Kama ni hivyo, jee Nabii Shuaib (a.s) hakupotea macho (Sura 12:84) Nabii Ayub (a.s) hakuugua (Sura 21:83)? Sasa huo mshipa ungempunguzia nini Nabi Musa utume wake? Mwisho, jambo la kushangaza ni kwamba Hadith hizo, katika Sahih Muslim, zimo katika mlango wa ‘Fadhila za Musa (a.s)’. Sasa fadhila hapo ni ipi? Ni Nabii Musa (a.s), kumpiga ngumi Malaika wa Mwenyezi Mungu na kulikoboa jicho lake? Au ni kuogopa kufa? Au ni kufukuzana na jiwe uchi? Au ni huko kulipiga na kulitia kovu? Twangojea majibu. Mpaka hapa tushaona baadhi ya Hadith zinazohusu mitume wengine ambazo, kwa maoni ya Shia, ‘haimkini kuthibitisha uswahihi wazo.’ Sasa tutazame zile zinazohusu Mtume Muhammad (s.a.w). Za Mtume Muhammad (s.a.w) 4.
Abdullah b. Burayda alisema kwamba amemsikia Burayda akisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) alitoka kwenda katika baadhi ya vita vyake. Aliporejea, alikuja kijakazi mmoja mweusi. Akasema : Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Mimi nilikuwa nimeweka nadhiri kwamba, Mwenyezi Mungu akikurejesha salama, nipige dufu mbele zako na niimbe. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) akamwambia: Kama umenadhiria 28
SHIA NA HADITH
(hiyo), piga. Kama hukunadhiria, usipige. Akawa anapiga. Akaingia Abubakar, naye anapiga. Kisha akaingia Ali,akawa vile vile apiga. Kisha akaingia Uthman; akaendelea kupiga. Kisha akaingia Umar; akaliweka lile dufu chini ya makalio yake, akalikalia. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) akasema: Hakika Shetani anakuogopa, ewe Umar! Mimi nilikuwa nimekaa, akawa anapiga. Abubakar akaingia, naye anapiga. Kisha akaingia Ali, naye anapiga. Kisha akaingia Uthman, naye anapiga. Hata ulipoingia wewe, ewe Umar, akaliweka dufu (lake)! Hiyo ni Hadith Na. 3773 katika Mlango Na.71 wa Sunan at-Tirmidhi. Hadith hiyo vile vile waweza kuiona katika uk.353 wa Juzuu ya Tano ya Musnad Ahmad. Sasa, kama kupiga dufu na kuimba ni haramu (kama tuambiwavyo mara nyingi humu mwetu Afrika Mashariki), basi vipi itakuwa ni halali kwa nadhiri na Bwana Mtume (s.a.w) aruhusu? Jee, inaingia akilini kwamba Bwana Mtume (s.a.w) aweza kuhalalisha haramu k.m. kamari au kunywa pombe au uzinifu, kwa kuwekea nadhiri? Hasha! Kama ni halali, au tujaalie ni haramu iliyohalalishwa kwa kuwekea nadhiri, basi kwa nini huyo mjakazi alifiche dufu lake chini ya makalio yake? Jee, halali hufichwa? Na kwa nini ifichwe alipoingia Umar tu? Kwani yeye peke yake ndiye aliyekiijua halali na haramu kuliko hao wengine? Kuliko hata Mtume (s.a.w)? Na kwa nini Bwana Mtume (s.a.w) asema: Hakika Shetani anakuogopa, ewe Umar? Kwa nini, kama ni halali, amwite mwanamke huyo Shetani? Jee, mtu anayefanya kitendo cha halali huitwa ‘Shetani’? Mwisho, jee inaingia akilini Shetani kumwogopa Umar, na kumkimbia, na asimwogope Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) bali aendelee kupiga dufu mbele zake na kumghania? Kweli inaweza Hadith hii kuwa sahihi? Twangojea majibu. 29
SHIA NA HADITH
5.
Imepokewa kwa Udhaifa kwamba Mtume (s.a.w) alifika kwenye jalala la watu fulani, akakojoa kwa kusimama! ‘Kisha akasema aletewe maji. Nikamletea, akatawadha.’
Hiyo ni Hadith iliyomo katika ‘Kitabul Wudhuu’, Mlango wa ‘al-Bawli Qaaimaa’, katika Sahih Bukhari. Kwa wale wenye tafsiri ya Kiingereza, nawatazame Hadith Na. 224, uk.144 wa Juzuu ya Kwanza. Katika kuieleza Hadith kama hiyo, Hammad b. Abi Sulaiman amesema kwamba Bwana Mtume (s.a.w) ‘alipanua miguu yake’ akakojoa kwa kusimama! Taz. Musnad Ahmad, uk.246 wa Juzuu ya Nne. Jee, ewe ndugu Mwislamu, yawezekana Mtume wa Mwenyezi Mungu kusimama jalani, apanue miguu yake kama mnyama (ambapo itambidi asege nguo zake), na akojoe hivyo? Mwache Bwana Mtume (s.a.w), mtu wa kawaida tu, mwenye heshima yake na murua wake, aweza kufanya hivyo? 6.
Imepokewa kwa Humaid b. Nafi’ kwamba alimsikia Zinab binti Abi Salama akisema: Nimemsikia Ummu Salama, mke wa Mtume (s.a.w), akimwambia Aisha: Wallahi, sipendi kuonekana na kijana ambaye ashaacha kunyonya. (Aisha) akasema: Kwa nini? Sahla binti Suhail alikuja kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Mimi naona (hasira) katika uso wa Abu. Hudhaifa pindi anapoingia Saalim (nyumbani kwetu). Mtume (s.a.w) akamwambia: Mnyonyeshe. (Sahla) akasema: (Yeye) ana ndevu! Lakini (Mtume s.a.w.) akamwambia (tena): Mnyonyeshe, na (hasira) iliyomo juu ya uso wa Abu Hudhaifa itaondoka. (Sahla) akasema: (Nikamnyonyesha) na wallahi, sikuona (hasira yoyote) juu ya uso wa Abu Hudhaifa.
30
SHIA NA HADITH
Hadith hii imo katika Sahih Muslim, ‘Kitabur Radhai,’ Mlango wa Radha’ il. Kabir’. Kwa wale wenye tafsiri ya Kiingereza, ni Hadith Na. 3428 iliyoko uk.742 wa Juzuu ya Pili. Katika Hadith nyingine14 iliyopokewa kwa Mw, Aisha, katika Mlango huo huo, inatweleza kwamba, alipoambiwa amnyonyeshe, Sahla aliuliza: Nitamnyonyesha naye ni mtu mzima? Mtume (s.a.w) akakenya. Akasema: Kwa hakika najua kwamba ya mtu mzima15... Na kwa riwaya ya Ibn Umar: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) atacheka. Na katika Hadith nyingine, katika Mlango huo huo tena, iliyopokewa kwa Ibn Abu Mulaika16 yeye (Ibn Abu Mulaika) akasema: Nimekaa mwaka (mzima) au karibu yake siitoi Hadith hii, kwa kuogopa. Ewe ndugu Mwislamu! Hebu zisome tena riwaya zote hizo, na ujiulize: Kweli Mtume Muhammad (s.a.w), au mtu yeyote yule, aweza kumwamrisha mke wa watu atoe ziwa lake ili amnyonyeshe mtu mzima mwenye ndevu zake? Na mwanamke anapoonyesha kushangazwa na amri hiyo, Mtume (s.a.w) akenye/acheke na kusema kwamba yeye ajua kuwa huyo mtu mzima? Hebu fikiria kama ni wewe uliyeamrishiwa mke wako hivyo, ungehisi vipi? Na kwa nini Ibn Abu Mulaika ajizuie kuitoa Hadith hiyo kwa mwaka mzima kama si kwa sababu ya kuona aibu? Hivi Ibn Abu Mulaika alikuwa na haya zaidi kuliko Mtume (s.a.w)? kweli wasaidizi wa Sheikh M. al-Khatib wanaweza kututhibitisha usahihi wa Hadith hii? Tunangojea majibu yao Inshallah. Yaani Hadith Na.3424 Neno la Kiarabu katika Hadith hii tulilolifasiri kwa ‘mtu mzima’, ni rajulun kabir. Jambo la kushangaza hapa ni kwamba, katika uk.741 wa tafsiri ya Kiingereza, neno hilo limefasiriwa kwa ‘ a young man’ badala ya ‘ a big man’ au ‘a grown-up man au ‘an adult’. Hata kwenye kichwa cha Hadith hiyo, neno lililotumiwa ni ‘ a young (boy)!’ Sijui kosa hilo ni kwa kughafilika au ni makusudi Allahu a’lamu! 16 Hiyo ni Hadith Na.3428 katika uk.742. 14
15
31
SHIA NA HADITH
Baadhi ya wanazuoni ili isieleweke vibaya Hadith hii, wamejaribu kutoa maelezo. Wengine17 wamesema kwamba, sio amnyonyeshe ziwa, bali atoe u hayo maziwa yake na amnyweshe! Na wengine18 wamesema kwamba ni kumnyonyesha hasa; lakini hiyo ilikuwa ni amri maaluum kwa huyo Salim peke yake! Lakini yote maelezo mawili hayo hayakubaliki, kwa sababu zifuatazo: i.
Neno ardhi’ihi lililotumiwa katika Hadith hizi ndio lile lile alilotumiliwa mamake Nabii Musa katika Sura 28:7, na kwa maana hiyo hiyo ya kuynyonyesha.
Kwa hivyo kulifasiri neno hilo kwa maana ya ‘mnyweshe’ ni kulinyumbua mno19 Hapo, haliwezi kuwa na maana hiyo asilan! ii. Kwa sheria ya Kislamu, mtu hawi maharimu ya mwanamke kwa kunywa maziwa yake nje ya ziwa lake. Huwa tu hivyo kwa kulinyonya hasa na iii. Kama amri hiyo ilikuwa nk kwa Salim peke yake, mbona Mw. Aisha haonekani kuwa ameielewa hivyo? Maana tunaposoma Muwatta’a ya Imam Malik katika ‘Kitabur Radha’i’, Mlango wa ‘Maa jaa-a Fir Radha’ati Ba’adal Kibari’, tunaona kwamba Mw. Aisha, alipokitaka mtu awe maharimu yake, alikimwamrisha20 dadake, Ummu Kulthum binti Abubakar, na binti ya ndugu yale (yaani Kama Sheikh Abdul Hamid Siddiqi katika kidokezo Na.1905 kilichoko mwisho wa uk.741 wa hiyo Juzuu ya Pili ya Kiingereza ya Sahih Muslim. 18 Kama Sheikh Muhammad as-Zurqani katika uk.91 wa Juzuu ya Tatu ya sherehe yake ya Muwatta’a Malik. 19 Hata katiak tafsiri ya Kiingereza ya Muwatt’a Mulik badala ya kulifasiri neno hilo kwa neno ‘suckle’, kama lilivyofasiriwa ndivyo katika Sahih Muslim, limefasiriwa kwa ‘feed him with their milk’.(Taz, mstari wa tano kutoka juu uk.275) Kufanya hivyo, kwa yeyote anayejua Kiingereza, ni Kulinyumbua mno! 20 Taz Hadith Na. 1242 katika uk. 274 wa tafsiri yake ya Kiingereza. 17
32
SHIA NA HADITH
Abdulrahman) wamnyonyesha! Jee, hiyo si fedheha nyingine? Sasa tuzitazame Hadith zinazomhusu Mwenyewe Mwenyezi Mungu (s.w.t). Za Mwenyezi Mungu (s.w.t) 7.
Imepokewa kwa Abu Hureira kwamba Mwenyezi Mungu Aliyetukuka alimwumba Adam kwa sura Zake, urefu wake ukiwa dhiraa sitini. Alipokwisha kumwumba, alimwambia: Nenda kawaamkie kundi lile – nalo lilikuwa ni kundi la malaika limekaa - usikilize watakujbu nini. Maana hayo ndiyo yatakayokuwa maamkizi yako na maamkizi ya kizazi chako. Akaenda, akasema: Amani iwe juu yenu! Nao wakasema: Amani iwe juu yako, na rehma za Mwenyezi Mungu. Wakaongeza ‘na rehema za Mwenyezi Mungu.’ Kwa hivyo, kila atakayeingia Peponi ataingia kwa sura za Adam, urefu wake ukiwa dhiraa sitini. Na watu hawakwacha kupungua (urefu wao) baada yake, mpaka sasa.
Hadith hii unaweza kuiona katika Sahih Bukhari, Hadith ya kwanza katika ‘Kitabul Isti’dhan’. Vile vile utaiona katika ‘ Kitabul Jannati Wasifatu Na’imihaa’, Mlango wa ‘Yadkhulul Jannata Aqwaamun Af-idatuhum Mithlu Af-idatit Twayr’ katika Sahih Muslim. Kwa Kiingereza, tazama Hadith Na.246, uk. 160-161 wa Juzuu ya Nane ya Sahih Bukhari; na Hadith Na.6809, uk.1481 wa Juzuu ya Nne ya Sahih Muslim. Hata hivyo, kabla hatujasema lolote kuhusu Hadith hii, tafadhali ilinganishe na yale maneno ya MWANZO 1:27 katika Biblia yase33
SHIA NA HADITH
mayo: Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. Jee, inawezekana sura za Adam ziwe ndizo sura ya Mwenyezi Mungu hali Qur’ani Tukufu inatwambia kwamba Yeye hana mfano? Hivi kweli Hadith hii nii Sahihi? Ili Hadith hii isiwe imemfananisha Mwenyezi Mungu ni kiumbe Chake, na kwa hivyo ionekane ni sahihi, baadhi ya wanazuoni husema kwamba dhamiri ‘Zake’ katika neno: alimwumba Adam kwa sura Zake, yarejea kwa Adam, sio kwa Mwenyezi Mungu! Yaani Mwenyezi Mungu alimwumba Adam kwa sura za Adam! Lakini taawili hiyo haikubaliki; maana tunapozitazama Hadith nyingine, zilizopokewa kwa yuyo huyo Abu Hureira tunaona kwamba dhamiri hiyo inamrejelea Mwenyezi Mungu, sio Adam! Kwa mfano: I.
Ukitazama uk.491 wa Juzuu ya Kumi ya Irshaadus Saari, sherehe ya Sahih Bukhari, utamwona Ibn Hajar al-Qastwalani anavyoirejeza dhamiri hiyo kwa Mwenyezi Mungu (sio Adam) kwa kuitaja Hadith nyingine iliyopokewa kwa Abu Hureira isemayo: Mwenyezi Mungu alimwumba Adam kwa sura za Rahman (Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema). Na hiyo ndiyo sababu ikapokewa tena Abu Hureira kwamba:
II. ‘Mmoja wenu anapopigana na ndugu yake na ajiepushe na (kumpiga) uso; maana Mwenyezi Mungu alimwumba Adam kwa sura Zake.’ Hadith Na. (ii) itakutunukia zaidi unapoilinganisha na: III. ile iliyoko uk.434 wa Juzuu ya Pili ya Musnad Ahmad isemayo: Yeyote kati yenu anapompiga (mwenzake) najiepushe na uso: 34
SHIA NA HADITH
wala asiseme: Mwenyezi Mungu aufanye’ mbovu uso wako, na uso wa anayeushabihi uso wako! Maana Mwenyezi Mungu amemwumba Adam kwa sura Zake. Jee, si wazi hapo kwamba sababu ya sisi kuzuiwa tusipigane nyuso, na tusigoane, ni kwamba nyuso zetu zimeshabihiana na uso wa Mola wetu? Jee, Hadith hiyo bado yaweza kuwa ni sahihi? Pia itakutunukia zaidi unapo ilinganisha na ile iliyotajwa na Ibn Qutayba21 katika uk.280 wa kitabu chake, Ta’wilu Mukhtalafi Hadith, isemayo kwamba: IV. Musa (a.s) alilipiga jiwe la Wana wa Israeli likabubujika (maji). Akasema: Kunyweni, enyi punda. Mwenyezi Mungu akamteremshia wahyi (kumwambia): Umewatukana viumbe niliowaumba kwa sura Zangu kwa kuwafananisha na punda... Jee, si wazi hapo kwamba Hadith zote tulizozitaja hapo juu zathibitisha kwamba Adam aliumbwa kwa sura za Mola wake? Bila shaka! Na hivyo ndivyo walivyoelewa hata wale waliofasiri Sahih Bukhari na Sahih Muslim; maana wanapofasiri neno alaa (kwa sura Zake) huliandika ‘in His image’ (kwa H kubwa, sio ndogo) ambavyo ndivyo inavyoandikwa kwa Kiingereza inapokusudiwa Mwenyezi Mungu. Hiyo ni Hadith ya kwanza inayomhusu Mwenyezi Mungu, na ambavyo haiwezekani kuwa sahihi. Sasa tuiangalie nyingine: 8.
21
Imepokewa kwa Abu Hureira kwamba watu walimwambia (Mtume s.a.w.): Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Jee tutamwona Mola wetu Siku ya Kiyama? (Mtume s.a.w.) akasema: Jee,
Kama ilivyonakiliwa katika uk.61 wa Abu Huraira ya Imam Abdul Husein Sharafuddin al-Musawi 35
SHIA NA HADITH
mna shida yoyote ya kuuona mwezi usiku wa arbatashara22, panapokuwa hakuna mawingu? Wakasema: La, wewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Akasema : Basi na nyinyi mtamwona Yeye Siku ya Kiyama kama hivyo (mnavyouona mwezi na jua). Mwenyei Mungu atawakusanya watu Siku ya Kiyama, aseme: Yeyote aliyekuwa akikiabudu kitu, nakifuate. Basi aliyekuwa akiliabudu jua, atalifuata jua; aliyekuwa akiliabudu mwezi, ataufuata mwezi; na aliyekuwa akiabudu mashetani, atawafuata mashetani. Ubaki umma huu (wa Kiislamu) ukiwa na wanafiki (miongoni mwao). Hapo Mwenyezi Mungu Aliyetukuka atawajia kwa sura isiyokuwa sura Yake wanayoijua. Aseme: Mimi ndiye Mola wenu. Nao waseme: Tunajilinda kwa Mwenyezi Mungu, na wewe. Tutakaa hapa mpaka Mola wetu atujie. Atakapotujia Mola wetu, tutamjua. Hapo, Mwenyezi Mungu Aliyetukuka atawajia kwa sura Yake wanayoijua. Aseme: Mimi ndiye Mola wenu. Nao waseme: Wewe ndiye Mola wetu. Hapo wamfuate: na sirati (njia) itatandikwa juu ya Moto. Mimi (Mtume s.a.w.), na umma wangu, niwe wa kwanza kupita; na siku hiyo hakuna atakayesema isipokuwa Mitume, na dua ya Mitume, siku hiyo itakuwa: Ewe Mola! Tupe salama, tupe salama... Hadith hiyo utaipata katika Sahih Muslim, ‘Kitabul Iman’, Mlango wa ‘Ithbaatu Ru’yatil Mu’minana Rabbahum Fil Akhira.’ Kwa tafsiri ya Kiingereza, ni Hadith Na.349, iliyoko uk.115 wa Juzuu ya Kwanza. Na hadith kama hiyo utaipata katika Sahih Bukhari, ‘Kitabu Abwaabi Swifatis Swalaa; na ‘Kitabur Riqaaq’, Mlango wa ‘asSwiraatwi Jisri Jahannam’. Kwa Kiingereza, ni Hadith Na.770 katika Juzuu ya Kwanza (uk.427-430); na Hadith Na.577 katika Juzuu ya Nane (uk.374-375)... 22
Huu ni usiku wa tarehe kumi na nne ambapo mwezi hung’ara sana. 36
SHIA NA HADITH
Na katika Hadith nyingine ilivyopokewa kwa Abu Said al-Khudri, inasema: ‘ Baadhi ya watu, katika zama za Mtume (s.a.w) , walisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Jee, tutamwona Mola wetu Siku ya Kiyama? Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) akasema: Ndiyo na akaongeza: Jee, mna shida yoyote ya kuliona jua adhuhuri, panapokuwa hapana mawingu? Na jee, mna shida yoyote ya kuuona mwezi usiku wa arbatashara, panapokuwa hapana mawingu? Wakasema: La, Mtume wa Mwenyezi Mungu. Naye akasema: Hamtakuwa na shida ya kumwona Mwenyezi Mungu aliyetukuka Siku ya Kiyama kama msivyo na shida ya kuuona mwezi na jua. Itakapokuwa Siku ya Kiyama mtangazaji atatangaza: Kila umma maukifuate kile walichokuwa wakikiabudu. Hapo hatobakia yeyote aliyekuwa akiabudu masanamu na mawe badala ya Mwenyezi Mungu aliyetakasika (na mawi) isipokuwa ataangukia Motoni. Wabaki wale wema na waovu waliokimwabudu Mwenyezi Mungu, na baadhi ya Watu wa Kitabu. Hapo waitwe Mayahudi waambiwe: Nyinyi mlikuwa mkiabudu nini? Waseme: Tulikimwabudu Uzayr Mwana wa Mungu! Waambiwe: Mwasema uwongo; Mwenyezi Mungu hakupata kuwa na mke wala mtoto. Mnataka nini (sasa)? Watasema: Tuna kiu, ewe Mola wetui Tunyweshe. Hapo wataelekezwa (upande fulani), waulizwe: Mbona hamchoti? Ndipo wasukumizwe Motoni (wautambue) kuwa ni mangati23, unakutana wenyewe kwa wenyewe na wao waangukie humo. Kisha waitwe Wakristo. Waulizwe: Mlikuwa mkiabudu nini? Waseme: Tulikuwa tukimwabudu Masihi Mwana wa Mungu! Waambiwe: Mwasema uwongo; Mwenyezi Mungu hakupata kuwa na mke wala mtoto. Mnataka nini (sasa)? Watasema: Tuna kiu, ewe Mola wetu! Tunyweshe. Hapo wataelekezwa (upande fulani), waulizwe: Mbona hamchoti? Ndipo wasukumizwe Motoni (wautambue) 23
Pia huitwa ‘mlenga’ au ‘mzigazi’. Kwa Kiingereza ni mirage. 37
SHIA NA HADITH
kuwa ni mangati, unakulana wenyewe kwa wenyewe, na wao waangukie humo. Hata panapokuwa hapakubaki yeyote isipokuwa yule aliyekimwabudu Mwenyezi Mungu aliyetukuka, awe mwema au mwovu, ndipo Bwana wa viumbe vyote (s.w.t) awajie kwa sura waliokimjulia, asema: Mnatafuta nini? Kila umma na ukifuate kile walichokuwa wakikiabudu. Waseme: Ewe Mola wetu! Tulijitenga na watu duniani japokuwa tulikuwa na haja nao sana; hata hivyo, hatukuandamana nao. Hapo (Mwenyezi Mungu) aseme: Mimi ndiye Mola wenu. Na wao waseme: Tunajilinda kwa Mwenyezi Mungu na wewe! Hatumshirikishi Mwenyezi Mungu na chochote. Watasema hivyo mara mbili au tatu hata wengine wakaribie kugeuka (na kurejea). (Mwenyezi Mungu) aulize: Jee kuna alama yoyote baina yenu na Yeye ambayo kwayo mtamjua? Watajibu Ndio. Hapa pafunuliwe muundi; na hapatabaki yeyote aliyekimsujudia Mwenyezi Mungu kwa hiari yake isipokuwa Mwenyezi Mungu atamruhusu kusujudu. Wala hapatabakia yeyote aliyekisujudu kwa kuogopa (watu) au kujionyesha isipokuwa Mwenyezi Mungu ataufanya mgongo wake kuwa tabaka moja; kila akitaka kusujudu, ataangukia mgngo wake. Kisha watainua vichwa vyao, na Yeye atarudia sura Yake waliyomwonea mara ya kwanza Awaambie: Mimi ndiye Mola wenu. Nao waseme: Wewe ndiye Mola wetu... Hiyo ni Hadith ya tatu, katika Sahih Muslim, baada ya ile tuliyoitaja kabla hapo juu. Kwa Kiingereza, ni Hadith Na.352 iliyoko uk.117-119 wa Juzuu ya Kwanza. Na katika Sahih Bukhari, Hadith kama hiyo utaiona katika ‘Kitabut Tafsir’ Mlango wa ‘innallaha Laa Yadhlimu Mithqaala Dharratin’. Kwa Kiingereza, ni Hadith Na.105 katika Juzuu ya Sita (uk.85-87) Jee, Hadith hizo zaweza kuwa sahihi? Hadith zinazosema kwamba tutamwona Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama kama tunavy38
SHIA NA HADITH
ouona mwezi na jua panapokuwa hakuna mawingu! Swali hapa ni: vipi tutaweza kumwona hivyo bila ya Yeye kuwa na umbo? Na vipi ataweza kuwa na umbo bila ya kuwa na mipaka? Na jee, tunaweza kuamini kuwa ana sifa hizo na tukabaki kuwa Waislamu? Au vipi Mwenyezi Mungu atatujia kwa sura mbalimbali – tunayoijua na tusiyoijua? Kwa ana sura ngapi? Na hiyo Yake hasa ikoje? Na jee Mwenyezi Mungu ana muundi wenye alama? Yote hayo ni maswali yanayojitokeza katika Hadith hizo; nani muhali kuyajibu bila ya kuingia kufuruni. Kwa hivyo haiwezekani Hadith hizo kuwa ni sahih ila ikiwa wasaidizi wa Sheikh M. al-Khatib watauthibitishia hilo! 9.
Imepokewa kwa Abu Hureira kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) amesema: Mola wetu Aliyetukuka kila usiku, inapobaki thuluthi ya mwisho ya usiku huo, hushuka mpaka kwenye uwingu wa chini kabisa, akasema: Ni nani atakayeniomba maghfira, nimghufirie?
Hadith hiyo unaweza kuiona katika Sahih Bukhari, ‘Kitabud Da’awaat’ Mlango wa ‘ad-Du’a Nisful Layli’; vile vile katika ‘Kitabu kusufi,’ Mlango wa ‘ad-Du’a Was Swalatu Min Akhiril Layli’. Na katika Sahih Muslim utaiona katika ‘Kitabus Swalat’, Mlango wa ‘at Targhibu Fid Du’ai Wadh Dhikhri Fii Akhiril Layli’. Kwa Kiingereza, ni Hadith Na.333 iliyoko uk.225 wa Juzuu ya Nane ya Sahih Bukhari na pia Hadith Na. 246 iliyoko uk. 136 wa Juzuu ya Pili. Na katika Sahih Muslim, ni Hadith Na.1656 iliyoko uk.365 wa Juzuu ya Kwanza. Na katika Jami’ut Tirmidhi, Mlango Na.324 ‘Fii Nuzulir Rabbi Tabaraka Wata’ala Ilas Samaaid Dunyaa Kullu Laylatin’ mna Hadith (Na. 445) isemayo: Imepokewa kwa Abu Hureira kwamba Mtume 39
SHIA NA HADITH
wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) amesema: Mola wetu Aliyetukuka kila usiku hushuka mpaka kwenye uwingu wa chini kabisa, inapokuwa thuluthiya kwanza ya usiku imepita, akasema: Mimi ndimi Mfalme. Ni nani atakayenilingana, nimwitikie? Ni nani atakayeniomba, nimpe? Ni nani atakayeniomba maghfira, nimghulfirie? Basi huwa vivyo hivyo mpaka alfajiri iangaze. Na katika Musnad Ahmad, Juzuu ya Kwanza (uk. 120) mna Hadith isemayo kwamba imepokewa kwa Ali (a.s) kwamba amemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) akisema: Lau kwamba si kwa kuhofia kuwapa mashaka ummu wangu, basi ningaliwaamrisha kupiga mswaki wakati wa kila swala, na ningaliiakhirisha Ishaa ya mwisho mpaka thuluthi ya kwanza ya usiku. Maana inapopita thuluthi ya kwanza ya usiku, Mwenyezi Mungu Aliyetukuka hushuka mpaka kwenye uwingu wa chini kabisa: na hubaki huko mpaka alfajiri inapochomoza. Hizo basi ni baadhi tu ya Hadith zinazohusu kushuka kwa Mwenyezi Mungu mpaka uwingu wa chini kabisa! Jee, ni sawa Mwenyezi Mungu kuhama kutoka mahali pamoja mpaka pengine? Hiyo si sifa ya mwili? Jee, Mwenyezi Mungu ni mwili? Kisha isitoshe! Ati Mwenyezi Mungu hubaki kwenye huo uwingu wa chini kabisa mpaka alfajiri inapochomoza! Hilo, bila shaka, halikubaliki. Maana kama tutalikubali – itamaanisha kwamba Mola wetu siku zote yuko kwenye uwingu huo. Maana, kwa mfano, alfajiri inapochomoza huku wetu Afrika Mashariki, huwa bado haujawachomozea wenzangu walioko upande wa magharibi. Na inapowachomozea, wao baada ya saa hivi, huwa bado haujawachomozea wengine walioko magharibi yao zaidi. Na ni vivyo hivyo mpaka iturejelee sisi huku. Kwa hivyo kila wakati humu ulimwenguni huwa kuna jimbo lenye alfajiri yake. Na hili li40
SHIA NA HADITH
namaanisha kwamba nyakati zote hizo Mwenyezi Mungu huwako kwenye huo uwingu wa chini kabisa. Jee, ni wakati gani ambao hupanda na kurejea kwenye uwingu iliko Arshi Yake? Jee, baada ya maelezo na maswali yetu hapo juu, bado wale waliokiswahilisha kitabu cha Sheikh M. al-Khatib watatwambia kuwa Hadith hizo ni sahihi? Uko wapi hapo usahihi wake? Tunangojea majibu yao! 10. Katika ‘Kitabul Iman’ ya Sahih Muslim, mna Hadith k.w.k zinazozungumzia Mwenyezi Mungu kucheka! Moja ni ile Hadith ndefu iliyomo katika Mlango wa ‘Akhiru Ahlil Jannati Dukhulan al-Jannah’ ambayo ina kipande kisemacho hivi ‘...Mwenyezi Mungu Aliyetukuka atasema: Jee, hukutoa ahadi na mithaki kwamba hutaomba chochote kingine zaidi ya nilichokupa? Ole wako, ewe mwana wa Adam! Uhaini ulioje! Naye atasema: Ewe Mola wangu! Sitakuwa mwovu wa viumbe Vyako! Hapo ataendelea kumlingana Mwenyezi Mungu mpaka Mwenyezi Mungu Aliyetukuka amcheke! Basi atakapochekwa na Mwenyezi Mungu, atamwambia: Ingia Peponi...’ Ya pili ni ile iliyomo katika Mlango wa Ithbatus Shafa’a..’ yenye kipande kisemacho: ‘...Mwenyezi Mungu atamwambia: Nenda uingie Peponi, maana utapata mfano wa dunia na mara kumi mfano wake, au utapata mara kumi mfano wa dunia... (Yule mtu) atasema: Jee, unanifanyia maskhara, au unanicheka na Wewe ndiye Mfalme?...’ Ya tatu ni ile iliyomo katika mlango wa ‘Akhiru Ahlin Nari Khurujan’ ambayo kipande chake cha mwisho chasema hivi: ‘... Ibn Mas’ud akacheka. Akasema: Mbona hamniulizi ninacheka nini wakasema: Unacheka nini? Akasema: Hivyo Ndivyo alivyocheka 41
SHIA NA HADITH
Mtume na Mwenyezi Mungu (s.a.w) (Mashaba) wakamwuliza: Unacheka nini, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: (Ninacheka) kwa ajili ya kicheko cha mola wa viumbe vyote alipoambiwa (na mtaka pepo): Jee, unanifanyia stihzai na wewe ni mola wa viumbe vyote? Naya atasema: Mimi sikufanyi stihzai, ila ni Mweza wa kila kitu. Ya nne ni ile iliyomo katika mlango huo huo, yenye kipande kisemacho:... Kisha atatujia Mola wetu, aseme: Mnamngojea nani? Watasema: Tunamngojea Mola wetu. Atasema: Mimi ndiye Mola wenu. Nao watasema Mpaka tukutazame! Hapo (Mwenyezi Mungu) atawatokea huku anacheka! Na ataondoka nao huku wakimfuata; na kila mtu miongoni mwao, awe mnafiki au mu’mini, atapewa nuru...’ Mbali nyingine nyingi tulizoziacha. Hizo tulizozitaja hapo juu, katika Sahih Muslim kwa Kiingereza, ni Hadith Na.349 (uk. 115-116), Na 359 (uk 120-121), Na 361 (uk. 121’122), na Na. 367 (uk.123-124) wa Juzuu ya Kwanza. Jee, Hadith kama hizo zinaweza kuthibitishwa usahihi wazo? Mwenyezi Mungu kucheka? Bila shaka hilo haliwezekani. Maana tunapozungumzia kucheka huwa tunazungumzia kukunjua uso na kufunua mdomo kwa namna ambayo, ghalibu, meno ya mchekaji yatadhihiri, na sauti ya kicheko chake kutokeza. Ikiwa ni hivyo basi, jee Mwenyezi Mungu anao uso na mdomo? Ukoje? Na jee, meno Yake yakoje? Astaghfirullah! 11. Imepokewa kwa Abu Hureira kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) amesema: Pepo ilihojiana na Moto. Moto ukasema: Mimi nimeheshimiwa kwa kupokea wenye kiburi, na majabari. Na pepo ikasema: nina nini mimi, hakuna anayeniingia 42
SHIA NA HADITH
isipokuwa madhaifu na watu wa chini na wasiojiweza? Hapo Mwenyezi Mungu Aliyetukuka akaiambia Pepo: Wewe ndiye Rehema Yangu. Kwawe humrehemu nimtakaye kati ya waja Wangu. Akauambia na Moto: Hakika wewe ni adhabu. Kwawe humwadhibu nimtakaye kati ya waja Wangu. Na kila mmoja kati yenu atajaa. Moto hautajaa mpaka Mwenyezi Mungu aweke mguu Wake (juu yake), nao useme: Basi! Basi! Hapo utajaa na ushikamanishwe. Hiyo ni Hadith unayoweza kuiona katika Sahih Bukhari, ‘Kitabul Tafsiril Qur’an,’ Mlango wa ‘Surat Oaf; na katika Sahih Muslim, ‘Kitabul Jannati Waswifati Naimihaa Wa Ahlihaa’, Mlango wa ‘Jahannam A’adhanallahu Minhaa’. Kwa Kiingereza, tazama Hadith Na.373 iliyoko uk.354 wa Juzuu ya Sita ya Sahih Bukhari; na Hadith Na 6819 iliyoko uk.1483 wa Juzuu Nne ya Sahih Muslim. Jee, wale waliomsaidia Sheikh M. al-Khatib katika kukiswahilisha kitabu chake wanaweza kututhibitishia usahih wa Hadith hiyo hapo juu? Mwenyezi Mungu ana mguu? Umekaaje mguu huo? Tena auweke juu ya Moto ndipo moto ujae! Nini hekima yake? Jee, Mtoto kuingiwa na wenye kiburi na majabari ni jambo la kujivunia? Kwa fadhila gani walizonazo watu hao, hali wao siku hiyo watakuwa chini ya walio chini (Sura 95:5)? Au vipi Pepo itawadhania wale walioiingia kwamba ni watu wa chini na madhaifu hali wao ni miongoni mwa wale ambao Mwenyezi Mungu amewaneemesha manabii, masiddiki, mashahidi na watu wema’ (Sura 4:69) 12. Abu Hureira amasema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) alinishika mkono wangu akasema: Mwenyezi Mungu aliumba 43
SHIA NA HADITH
mchanga siku ya Jumamosi. Akaumba na majabali humo siku ya Jumapili. Akaumba na miti siku ya Jumatatu. Akaumba vya kuendesha maisha siku ya Jumanne. Akaumba na nuru siku ya Jumatano. Akaeneza wanyama humo siku ya Alkhamisi. Akamwumba na Adam (a.s) baada ya alasiri, siku ya Ijumaa; kiumbe cha mwisho, katika saa ya mwisho kati ya saa za Ijumaa: baina ya alasiri mpaka usiku. Hadith hiyo utaipata katika Sahih Muslim, ‘Kitabu Swifatil Qiyamati Waijannati Wannari’, Mlango wa ‘Ibtidaul Khalqi Wakhalqi Adam (a.s).’ Kwa Kiingereza, ni Hadith Na.6707 (uk. 146) katika Juzuu ya Nne: Sasa hapa tushike lipi? La Qur’ani kwamba mbingu na ardhi ziliumbwa kwa siku sita, au la Hadith hiyo kwamba ardhi (na vinginevyo visivyokuwa ardhi) viliumbwa kwa siku saba? Na jee, hapo zikiumbwa mbingu na ardhi, siku hizo zikijulikana kwa haya majina (ya Jumamosi na Jumapili) tuyajuayo sisi leo? Kila siku ilikuwa ni saa 24? Jua na mwezi vilikuwa vishaumbwa? Na jee, siku moja kwa Mwenyezi Mungu ni kama hii yetu, au ni ‘kama miaka efu’ (Sura 22:47)? Jee usahihi wa Hadith hiyo unaweza kuthibitishwa? Tunangojea tuone. Sasa tutazame ya vioja vingine. Na vioja vingine 13. Abu Hureira amesema kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) amesema: Mtu mmoja alikuwa akimchunga ng’ombe aliyekuwa amembebea mzigo. Mara yule ng’ombe akamgeukia na kusema Mimi sikuumbiwa hili (la kubeba mizigo) bali nimeumbiwa konde (kunyweshea mashamba). Watu wakasema kwa mshangao na fazaa: Subhanallah! Ng’ombe anasema?! 44
SHIA NA HADITH
Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) akasema: Mimi naamini hilo, na Abubakar na Umar. Akasema Abu Hureira kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) alisema: Mchunga mmoja alikuwa akichunga mifugo yake. Mara akaja mbwa mwitu akamchukua mbuzi wake mmoja. Yule mchunga akamfukuza yule mbwa mwitu mpaka akampokonya (yule mbuzi wake), Mbwa mwitu akamgeukia (yule mtu) na kumwambia: Ni nani atakayemwokoa (mbuzi wako) siku ambayo hapatakuwa na mchunga isipokuwa mimi?! Hapo watu wakasema: Subhanallahi Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) naye akasema: Mimi naamini hilo; mimi na Abubakar na Umar. Hadith hiyo unaweza kuiona katika Sahih Bukhari, ‘Kitabu Fadhailis Swahaba’, Mlango wa ‘Law Kuntu Muttakhidhan Khalilan’; na katika Sahih Muslim. ‘Kitabu Fadhailis Swahaba’ vile vile, Mlango wa ‘Fadhaili Abibakar as Siddiq’. Kwa Kiingereza, ni Hadith Na.15 iliyoko uk.10-11 wa Juzuu ya Tano ya Sahih Bukhari; na Hadith Na.5881 iliyoko uk. 1276 -1277 wa Juzuu ya Nne ya Sahih Muslim. Haya! Mambo hayo! Ng’ombe na mbwa mwitu wanazungumza Kiarabu! Tangu lini? Kwa kuthibitisha jambo gani hapo? Pengine tutaelezwa hapo tutakapojibiwa, na tuthibitishwe usahihi wa Hadith Hiyo inshallah. 14. Imepokewa kwa Abu Hureira kwamba Mtume (s.a.w) amesema: Ayub alikuwa akioga uchi. Mara akaangukiwa na nzige wa dhahabu! Ayub akawakusanya katika nguo yake. Mola wake akamlingana: Ewe Ayub! Jee sikukukwasisha24 na unavyoviona? Akasema: Kwani; kwa Utukufu Wako! Lakini mimi sikwasiki na baraka Zako. ‘Kumkwasisha mtu’ kumfanya atosheke na kitu fulani.
24
45
SHIA NA HADITH
Hadith hiyo utaipata katika Sahih Bukhari, ‘Kitabul Ghusli’, Mlango wa ‘at-Tasattur Fil Ghuslli Indan Nasi’. Kwa Kiingereza, ni Hadith Na. 277 iliyoko uk. 170 wa Juzuu ya Kwanza. Hapa hatukatai kwamba Mwenyezi Mungu hashindwi kufanya miujiza yoyote – ya kuumba nzige wa dhahabu, na zaidi ya hilo. Lakini ni sharti pawe na dharura ya kuleta miujiza kama hiyo. Jee, hapo pa Nabii Ayub (a.s) kuoga faraghani peke yake, palikuwa na dharura gani ya kuteremshiwa nzige wa dhahabu? Awafanye nini? Hizo basi, tulizozidondoa hapo juu (uk, 16-32) ni baadhi tu ya Hadith nyingi zilizomo katika vitabu vya Kisunni (na nyingi yazo tumezitoa katika Sahih Bukhari na Sahih Muslim) ambazo haiwezekani kuthibitisha usahihi wazo. Maana zinzapingana na Qur’ani Tukufu, Hadith nyingine za Mtume (s.a.w) zilizo sahihi, na hata akili. Kwa hivyo, sio vitabu vya Kishia peke yake vilivyo na Hadith kama hizo, bali hata vya Kisunni ni hali kadhalika. Mwisho Kutokana na majibu na maelezo yetu yaiyomo humu, tumeona kwamba wote wawili (Sunni na Shia) wanakubaliana kwamba: i.
Hadith za Mtume Muhammad (s.a.w) ndilo chimbuko la pili la sheria ya Kiislamu, na ndizo zenye kuifasiri Qur’ani Tukufu. Yeyote asiyeamini hivyo ni kafiri
ii. Haifai kukhalifu hukumu za Hadith yoyote iliyosihi kutokamana na Bwana Mtume (s.a.w) Kufanya hivyo ni kukufuru vile vile iii. Katika kuthibitisha usahihi wa Hadith yoyote, ni lazima pathibitishwe ukweli na uadilifu wa kila mmoja kati ya 46
SHIA NA HADITH
wapokezi wake. Na hilo huwezekana tu kwa kupitia fani makhususi ya Mustwalahul Hadith. Fani hii inakubaliwa na pande zote mbili, na kila upande umeitungia vitabu na kuvichapisha iv. Hadith yoyote iliyopokewa kwa mwongo au mtu asiyejulikana, haifai kukubaliwa. Hata hivyo, pamoja na hadhari yote iliyochukuliwa kuhakikisha kwamba ni Hadith sahihi tu zitakazochapishwa vitabuni: v.
Baadhi ya Hadith, ambazo haiwezekani kuthibitisha usahih wazo, zimepenya na kuchapishwa katika vitabu vya pande zote mbili. Lakini ni uamuzi wa wote kwamba popote pale inapothibiti kwamba Hadith kama hizo si sahihi, basi zikataliwe.
Kwa hivyo, ikiwa mambo ni kama hivyo, kwa nini Sunni wazuiwe kukurubiana na kuelewana na ndugu zao, Shia? Ikiwa Wakatoliki na Waprotestanti, pamoja na kuwa Biblia zao ni tofauti, wanaweza kukurubiana na kuelewana, kwa nini sisi Waislamu tusiweze hali Âyanayotuunganisha ni mengi zaidi kuliko yale yanayotutenganisha?? Majibu ninawaachia nyinyi, ndugu Waislamu, wa madhehebu yote. Inshallah, katika kitabu kijacho, tutatazama msimamo wa Shia juu ya masahaba wa Mtume Muhammad (s.a.w).
47
SHIA NA HADITH
ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24. 25. 26. 27. 28. 29.
i) Qur’ani Tukufu – Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili ii) Qur’an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thelathini Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudhar Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur’an na Hadithi Elimu ya Nafsi Yajue Madhehebu ya Shia Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur’an Tukufu Al-Wahda Ponyo kutoka katika Qur’an Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii 48
SHIA NA HADITH
30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39. 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52. 53. 54. 55. 56. 57. 58. 59. 60. 61. 62. 63. 64. 65.
Mashukio ya Akhera Al Amali Dua kwa Mujibu wa Ahlulbayt (a.s) Udhuu kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyezi Mungu na sifa zake Kumswalia Mtume (s) Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana Upendo katika Ukristo na Uislamu Qur’ani na Kuhifadhiwa Kwake Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu Kupaka juu ya khofu Kukusanya Sala Mbili Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kusujudu juu ya udongo Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) Tarawehe Malumbano baina ya Sunni na Shia Kupunguza Swala safarini Kufungua safarini Umaasumu wa Manabii Qur’an Yatoa Changamoto as-Salaatu Khayrun Mina -’n Nawm Uadilifu wa Masahaba Dua e Kumayl Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mtume Muhammad (s) Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili Kuzuru Makaburi Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili 49
SHIA NA HADITH
66. 67. 68. 69. 70. 71. 72. 73. 74. 75. 76. 77. 78. 79. 80. 81. 82. 83. 84. 85. 86. 87. 88. 89. 90. 91. 92. 93. 94. 95. 96. 97. 98. 99. 100. 101.
Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita Tujifunze Misingi Ya Dini Sala ni Nguzo ya Dini Mikesha Ya Peshawar Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu Ubora wa Imam ‘Ali na Ushia ndio njia iliyonyooka Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake Liqaa-u-llaah Muhammad (s) Mtume wa Allah Amani na Jihadi Katika Uislamu Uislamu Ulienea Vipi? Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) Dhana ya Ndoa ya Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) Urejeo (al-Raj’ah) Mazingira Utokezo (al - Badau) Hukumu ya kujenga juu ya makaburi Swala ya maiti na kumlilia maiti Uislamu na Uwingi wa Dini Mtoto mwema Adabu za Sokoni Na Njiani Johari za hekima kwa vijana Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu Tawasali (AT- TAWASSUL) Imam Mahdi katika Usunni na Ushia Hukumu za Mgonjwa Sadaka yenye kuendelea Msahafu wa Imam Ali Maimamu wa Ahlul Bait – Ujumbe na Jihadi Idi Al-Ghadir Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu 50
SHIA NA HADITH
102. 103. 104. 105. 106. 107. 108. 109. 110. 111. 112. 113. 114. 115. 116. 117. 118. 119. 120. 121. 122. 123. 124. 125. 126. 127. 128. 129. 130. 131. 132. 133. 134. 135. 136. 137.
Hukumu zinazomuhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi Huduma ya Afya katika Uislamu Sunna za Nabii Muhammad (saww) Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) Shahiid Mfiadini Mwanamke Na Sharia Ujumbe -Sehemu ya Kwanza Ujumbe - Sehemu ya Pili Ujumbe - Sehemu ya Tatu Ujumbe - Sehemu ya Nne Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu Hadithi ya Thaqalain Ndoa ya Mutaa Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza Ukweli uliopotea sehemu ya Pili Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu Ukweli uliopotea sehemu ya Nne Ukweli uliopotea sehemu ya Tano Mkutano wa Maulamaa wa Baghdad Safari ya kuifuata Nuru Fatima al-Zahra Myahudi wa Kimataifa Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi Visa vya kweli sehemu ya Kwanza Visa vya kweli sehemu ya Pili Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Mwanadamu na Mustakabali wake Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) Khairul l’Bariyyah Uislamu na mafunzo ya kimalezi Vijana ni Hazina ya Uislamu Adhana ni Ndoto au ni Wahyi? Tabaruku Saada Kamili – Kitabu cha Kiada cha Maadili 51
SHIA NA HADITH
138. 139. 140. 141. 142. 143. 144. 145. 146. 147. 148. 149. 150. 151. 152. 153. 154. 155. 156. 157. 158. 159. 160. 161. 162. 163. 164. 165. 166. 167. 168. 169. 170. 171. 172. 173.
Vikao vya furaha Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? Visa vya wachamungu Falsafa ya Dini Kuhuzunika na Kuomboleza Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah Mjadala wa Kiitikadi Kuonekana kwa Allah Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) Ndugu na Jirani Ushia ndani ya Usunni Maswali na Majibu Mafunzo ya hukmu za ibada Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1 Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2 Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 Abu Huraira Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. Mazingatio kutoka katika Qur’an - Sehemu ya Kwanza Mazingatio kutoka kaitka Qur’an - Sehemu ya Pili Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili Shia na Qur’ani – Majibu na Maelezo Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu Uislamu Safi Majlisi za Imam Husein Majumbani Je, Kufunga Mikono Uislam wa Shia Amali za Makka Amali za Madina Asili ya Madhehebu katika Uislamu Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi Ukweli uliofichika katika neno la Allah 52
SHIA NA HADITH
174. 175. 176. 177. 178. 179. 180. 181. 182. 183. 184. 185. 186. 187. 188. 189. 190. 191. 192. 193. 194. 195. 196. 197. 198. 199. 200. 201. 202. 203. 204. 205. 206. 207. 208. 209.
Uislamu na Mifumo ya Uchumi Umoja wa Kiislamu na Furaha Mas’ala ya Kifiqhi Jifunze kusoma Qur’ani as-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah Hayya ‘Alaa Khayri’l-’Amal Katika Adhana Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na Ramadhani) Uadilifu katika Uislamu Mahdi katika Sunna Maswali Ya Uchunguzi Kuhusu Uislam Kazi na Bidii ni njia ya maendeleo Abu Talib – Jabali Imara la Imani Ujenzi na Utakaso wa Nafsi Vijana na Matarajio ya Baadaye Historia maana na lengo la Usalafi Ushia – Hoja na Majibu Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) Maombolezo – Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu Takwa Upotoshaji Dhahiri katika (Turathi) Hazina ya Kiislamu Amirul Muuminina (‘as) na Makhalifa Tawheed Na Shirki Kuvunja hoja iliyotumika kutetea Uimamu wa AbuBakr Adabu za vikao na mazungumzo Hija ya Kuaga Uwazi baina ya Maslahi na Vikwazo Fadhila za watukufu watano katika Sahih Sita Mdahalo baina ya Mwanachuoni wa Kisunni na Kishia (Al- Muraja’aat) Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (as) Imam Husain ni Mfumo wa Marekebisho na Mageuzi Mtazamo kuhusu msuguano wa Kimadhehebu Nchi na Uraia – Haki na wajibu kwa Taifa Mtazamo wa Ibn Taymiyyah juu ya Imam Ali (as) Uongozi wa Kidini – Maelekezo na Utekelezaji wa Kijamii 53
SHIA NA HADITH
210. Maadili ya Ashura 211. Mshumaa – Shahidi na Kifo cha Kishahidi 212. Mizani ya Hekima – Hadithi za Ahlul Bait (as) – Sehemu ya Kwanza 213. Imam Ali na Mambo ya Umma 214. Imam Ali na Mfumo wa Usawa 215. Uimamu na Tamko la Kutawazwa 216. Mfumo wa Wilaya 217. Vipi Tutaishinda Hofu? 218. Kumswalia Mtume ni Ufunguo wa Utatuzi wa Matatizo 219. Maeneo ya Umma na Mali Zake 220. Nahju ‘L-Balagha – Majmua ya Khutba, Amri, Barua, Risala, Mawaidha na Semi za Amirul-Muuminin Ali bin Abu Talib (a.s.) 221. Mukhtar – Shujaa aliyelipiza kisasi dhidi ya wauaji a Imam Husein (as) hapo Karbala 222. Mazingatio Katika Swala 223. Imam Hasan na Mfumo wa Kujenga Jamii 224. Vyakula Na Vinywaji 225. Kuelewa Rehema ya Mwenyezi Mungu 226. Tiba ya Maradhi ya Kimaadili 227. Yafaayo kijamii 228. Shia Na Hadith - Majibu na Maelezo 229. Mkakati wa Kupambanana Ufakiri 230. Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu 231. Taqiyya Kwa Mujibu Wa Sheria Ya Kiislamu 232. Imam Mahdi Na Bishara Ya Matumaini 233. Jihadi 234. Majanga Na Jukumu La Jamii 235. Muhadhara wa Maulamaa 236. Mashairi ya Kijamii 237. Ngano ya kwamba Qur’ani imebadilishwa 238. Mwanamke Katika Harakati Za Mageuzi 239. Shia Na Sahaba - Majibu na Maelezo 240. Yusuf Mkweli 241. Hotuba Za Kiislamu Juu ya Haki Za Binadamu
54
SHIA NA HADITH
KOPI NNE ZIFUATAZO ZIMETAFSIRIWA KWA LUGHA KINYARWANDA 1. 2. 3. 4.
Amateka Ya Muhammadi (s.a.w.w) Na Aba’ Khalifa Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya Shiya na Hadithi
ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION KWA LUGHA YA KIFARANSA 1.
Livre Islamique
55