SHIA NA QUR’ANI Majibu na Maelezo
Abdilahi Nassir
© Haki ya kunakili imehifadhiwa na: Al-Itrah Foundation
ISBN No: 978 – 9987 – 17 – 076 - 0
Kimeandikwa na: Abdilahi Nassir
Kimehaririwa na: Alhajj Ramadhani S. K. Shemahimbo
Kimepitiwa na: Mbarak A. Tila
Kimepangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation
Toleo la kwanza 1995 – Nakala 2000 Toleo la pili 2001 – Nakala 5000 Toleo la tatu Agosti 2014 – Nakala 2000
Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. - 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: www.alitrah.info
SHUKURANI
T
unamshukuru Sheikh Abdilahi Nassir kwa kuturuhusu sisi Al-Itrah Foundation kuchapisha kitabu chake hiki “Shia na Qur’ani – Majibu na Maelezo” toleo la tatu nakala 2000. Ni matumaini yetu kwamba wasomaji wetu watanufaika na mtiririko huu wa majibu na maelezo juu ya kitabu al-Khututul Aridhwa cha Muhibbudin al-Khatib ambamo anapinga na kujaribu kukatisha tamaa juu ya uwezekano wa maelewano baina ya madhehebu mbalimbali za Kiislamu ambayo masheikhe wamejaribu kuushughulikia. Tunamshukuru sana Sheikh kwa kuandika kitabu hiki. Tunamombea kila la kheri, Allah Aza wa Jalah ampe tawfiq azidi kutuelemisha kwa kalamu yake ya maarifa na upole.
Yaliyomo Neno la Mchapishaji........................................................................1 UTANGULIZI.................................................................................3 SABABU ZAKE..............................................................................7 SUNNI NI NANI.............................................................................9 QUR’ANI TUKUFU.....................................................................13
• Kuawili aya..........................................................................21
• Faslul Khitab........................................................................22
• Surat-al- Wilaya...................................................................23
• Dabistan Madhhab...............................................................28
• Al-Kafi si Bukhari................................................................29
• Waja’alnaa Aliyyan Swihraka..............................................31
• Msahafu wa Fatima..............................................................32
• Zaidi ya hizo........................................................................37
• Bali Makubwa Zaidi............................................................39
• Mwisho................................................................................40
v
SHIA NA QUR’ANI
Neno la Mchapishaji
K
itabu ulichonacho mikononi mwako, Shia na Qur’ani, kimeandikwa na mwanachuoni na khatibu mashuhuri wa Afrika ya Mashariki, Sheikh Abdilahi Nassir. Kitabu hiki ni majibu ya kitabu cha Wahhabi kiitwacho, alKhututul Aridhwa, kilichoandikwa kwa Kiarabu na Sheikh Muhibbudin al-Khatib wa Misr (mwaka wa 1930) na kutarjumiwa kwa Kiswahili kwa jina la, Misingi Mikubwa lliyojengwa Dini ya Ushia; na kuchapishwa na taasisi ya Kianswari (Wahhabi) ya Mombasa Kenya katika mwaka wa 1988. Bahati mbaya, kama ilivyo kawaida ya waandishi wa Kiwahhabi, hawajishughulishi kuangalia majibu yanayotolewa na Mashia, bali waliendelea kutoa kitabu chao hicho Misingi Mikubwa lliyojengwa Dini ya Ushia kwa nia ya kuzidi kuwapotosha watu. Badala ya kutoa majibu kwa majibu ya Mashia, wanarudia yaleyale waliyoandika mwanzo. Huu ni msiba mkubwa kwa wasomi wa aina hii! Kutokana na hali hiyo, kwa ruhusa ya Sheikh wetu, tunatoa tena toleo lingine la kitabu hiki, Shia na Qur’ani, ambacho ni moja ya milolongo ya vitabu vyake vya majibu ya kitabu hicho, vingine ni: Shia na Hadithi; Shia na Swahaba na Shia na Taqiyah. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa makubwa hususan wakati huu ambapo Waislamu wenye nia safi wanapigania umoja wa Waislamu baada ya kuona hatari inayouzunguka Uislamu na Waislamu. Tunawaomba wasomaji wetu wasome kitabu hiki kwa makini kuanzia mwanzo mpaka mwisho ili wapate somo kutokana na yaliyomo humu na kuyafanyia kazi. 1
SHIA NA QUR’ANI
Kwa mara nyingine tena tunamshukuru Sheikh wetu huyu kwa kutupa ruhusa hii ya kukichapisha tena kitabu hiki. Pia shukrani zetu ziwaendee wale wote waliosaidia kwa njia moja au nyingine mpaka kuwezesha kitabu hiki kuchapishwa. Allah ‘Azza wa Jalla awalipe wote malipo mema ya hapa duniani na huko Akhera pia. Mchapishaji Al-Itrah Foundation
2
SHIA NA QUR’ANI
UTANGULIZI
S
ifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehema na amani zimshukie bwana wetu na mwombezi wetu, Muhammad b. Abdillahi, na ali zake wema waliotakaswa wakatakasika, na wote wanaofuata nyayo zao. Hitilafu baina ya Shia na Waislamu wengine wasio Shia haikuanza juzi na jana. Ilianza karne nyingi zilizopita; mara tu baada ya Mtume Muhammad (s.a.w) kufariki dunia. Hata hivyo, katika kipindi cha Makhalifa wawili wa kwanza, hitilafu hiyo haikuzusha zogo na fitina kubwa kama lile lililozuka katika kipindi cha Makhalifa wa tatu na wa nne. Na hilo ni kwa sababu ambazo, kwa kuwa ziko nje ya maudhui ya kitabu hiki, sikusudii kuzizungumzia humu. Itoshe tu, kwa hivi sasa, kujua kwamba ni baada ya Khalifa wa tatu (Khalifa Uthman) kuuliwa, na mtu aliyekiitwa Muawiya kuongoza upinzani dhidi ya Khalifa wa nne (Imam Ali), ndipo hitlafu hiyo ilipopaliliwa moto. Na kutokana na upinzani huo ndipo Imam Ali (a.s) alipolaaniwa, kwa amri ya Muawiya, katika hotuba zote za Ijumaa, kwa muda usiopungua miaka themanini. Ndipo wote wale waliokimtambua Imam Ali (a.s) kuwa ni Imamu wa haki (yaani Shia) walipokuwa wakisakwa kama nyoka na kuuawa! Ndipo Imam Hassan (a.s) mjukuu wa Mtume (s.a.w) alipouliwa kwa kutiliwa sumu chakulani mwake! Ndipo Imam Hussein (a.s) mjukuu mwingine wa Mtume (s.a.w), alipouliwa kinyama huko Karbalaa (Iraq) kwa kukatwa kichwa chake, kikatundikwa kwenye mkuki na kuchezwa ngoma, na kuliacha pingiti la mwili wake lishetweshetwe na farasi! Ndipo hofu il3
SHIA NA QUR’ANI
ipofika kiwango cha watu, chini ya Ufalme wa Muawiya, kuogopa kuwapa watoto waliowazaa jina la Ali! Ndipo hata mashekhe, kwa kuchelea kuadhibiwa na kuuawa, walipoogopa kulitaja jina la Imam Ali (a.s) katika riwaya za Hadith za Mtume (s.a.w) badala yake ikawa husema: ‘ Amesema Sheikh’! Hapo ndipo chuki baina ya Shia na wasio Shia ilipozidi na kuendelea kwa miaka mingi – mara inapanda, mara inashuka – hadi hii karne tuliyonayo. Katika karne hii, kiasi cha miaka thelathini hivi iliyopita , baadhi ya wanazuoni wa Kishia na wasio Shia huko Mashariki ya Kati wakaona la! Hali hii haifai kuachwa ikaendelea. Kwa hivyo wakakutana na kujadiliana jinsi yakuleta mkuruba na uelewanao baina ya madhehebu mbali mbali ya Kiislamu – hasa baina ya Shia na Sunni. Matokeo yake yakawa ni kuundwa chama kilichoitwa Darut Taqrib Baynal Madhahibil Islamiyya na kuweka jukwaa la pamoja la kuwawezesha wanazuoni hao wa madhehebu mbali mbali kueleza imani na misimamo ya madhehebu yao juu ya mada mbali mbali za kidini. Hatua hii ilisaidia sana kuleta uelewano kiasi cha kwamba, Sheikh Mahmud Shaltut (aliyekuwa Mufti wa Al-Azhar wakati huo) alitoa ile fatwa yake mashuhuri ya kusema kwamba madhehebu ya Ja’fari (yaani Shia Ithnaashari) ni madhehebu ya Kiislamu yanayojuzu kufuatwa katika kufanyia ibada kama madhehebu mengineo ya Sunni. Na kwa mara ya kwanza, akaruhusu madhehebu hayo yasomeshwe katika Chuo Kikuu cha Al-Azhar huko Misri. Hata hivyo, baadhi ya mashekhe wa wakati huo hawakupendezwa na hatua hiyo. Miongoni mwao ni mmoja aliyekuwa akiitwa Muhibbudin al-Khatib. Huyu aliandika kitabu kwa lugha ya Kiarabu kiitwacho al-Khututul Aridhwa kuonyesha kwamba ni muhali jaribio hilo la wanazuoni wenzake kufanikiwa - hasa inapokuja kwenye uelewano baina ya Sunni na Shia – na akatoa sababu zake. Sababu 4
SHIA NA QUR’ANI
hizo ndizo tutakazozijadili katika mfululizo wa vitabu vyangu hivi inshallah, kuanzia ile inayohusu Qur’ani Tukufu. Japokuwa kitabu hicho kishajibiwa kwa hiyo hiyo lugha ya Kiarabu, inaonekana kwamba wale wasiopendelea umoja baina ya Waislamu hawana habari ya majibu hayo, au labda hawapendi kuwa nayo! Maana kama si hivyo, wasingekuwa wakiendelea kukichapisha kitabu hicho mumo kwa mumo, na kukifasiri kwa lugha nyinginezo, bila ya kusema cho chote juu ya majibu yaliyokwisha kutolewa. Ilipofika 1983, miaka minne baada ya mapinduzi Kiislamu ya Iran, kitabu hicho kilifasiriwa kwa Kiingereza na kusambazwa ulimwengu mzima. Kwa nini? Kwa sababu ya waandamizi wa marehemu Sheikh M.al-Khatib kuona jinsi juhudi za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zilivyofanikiwa nje ya Ulimwengu wa Kiarabu, ambako lugha ya Kiingereza hueleweka zaidi, katika kuleta uelewano na umoja baina ya Waislamu. Huku kwetu Afrika Mashariki, tafsiri hiyo ya Kiingereza ilienezwa zaidi kuliko ile nuskha ya Kiarabu – hasa miongoni mwa wanafunzi wa mashule na vyuo vikuu. Hata hivyo, baada ya kuonekana kwamba athari ya nuskha hiyo ya Kiingereza haikuwa kama ilivyotarajiwa, bali Waislamu wamezidi kuvutiwa na maongozi ya Kiislamu ya Imam Khomeini na kutaka kujua zaidi Ushia, jamaa hao wakaonelea bora itolewe tafsiri ya Kiswahili: huenda ikaleta athari itakikanayo! Hivyo hivi majuzi (Disemba 1988) kukachapishwa tafsiri ya Kiswahili ya kitabu hicho kwa jina la Misingi Mikubwa lliyojengwa Dini ya Ushia ambayo kitabu hiki inshallah ndiyo mwanzo wa majibu yake. Katika kuandika majibu haya, napenda ieleweke kwamba sikuyaandika kwa hiari; nimelazimika! Sikuyaandika kwa hiari kwa sababu ninaamini kwamba sisi waandishi wa Kiislamu wa leo inatupasa kuyashughulikia. 5
SHIA NA QUR’ANI
Na nimelazimika kwa kuona hatari ya mfarakano baina ya Waislamu inayoweza kutokea kwa vitabu kama hicho cha Sheikh M. AlKhatib kuachwa bila ya kujibiwa – hasa hivi ambavyo idadi ya Shia wananchi, humu mwetu Afrika Mashariki, inavyozidi kukua, na hasa hivi ambavyo sababu zote alizozitoa shekhe wetu huyo katika kitabu chake hicho hazina mashiko. Hivyo nimeyaandika majibu haya ili kuuzuia mfarakano huo unaoweza kutokea; na kwa roho hiyo hiyo nakuomba, ewe ndugu msomaji, uyasome. Pengine, wakati mwingine, ushahidi utakaotolewa katika mfululizo wa majibu haya utaonekana mkali. Hilo ni kweli! Lakini huo ni ukali usioweza kuepukika! Ni kama daktari mpasuaji kulazimika kukikata kiungo kimoja cha mwili ili kuuhifadhi mwili mzima. Mwili hapa ni umoja wa Waislamu; na kiungo ni Sheikh M. Al-Khatib na wale wenye mawazo kama yake. Nataraji ndugu zangu mtayasoma majibu haya kwa ikhlasi na bila chuki, pamoja na kuyalinganisha na vitabu nilivyovitolea ushahidi, ili mweze kuufikia ukweli. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi. ABDILAHI NASSIR Nairobi, Kenya Rajab, 1409 Machi, 1989
6
SHIA NA QUR’ANI
SABABU ZAKE
K
atika kueleza kwa nini haiwezekani kuwako umoja na uelewano baina ya Sunni na Shia, Sheikh M. al-Khatib ametoa sababu nane kubwa: nazo ni: 1.
Shia wana Qur’ani iliyo tofauti na Sunni
2.
Misingi ya Hadith inayotegemewa na Shia ni tofauti na ile inayotegemewa na Sunni
3.
Shia hawawaheshimu sahaba wa Mtume (s.a.w), bali wanawatukana na kuwalaani
4.
Shia wanaamini taqiyya ambayo kwayo hujitokeza kwa Sunni ‘kwa yasiyokuwa yale wanayoyaficha.’ Kwa hivyo huwezi kujua ukweli wao
5.
Shia hawawatambui Makhalifa watatu wa kwanza wanaotambuliwa na Sunni. Wao wanawatambua Maimamu wao kumi na mbili tu
6.
Imani ya Shia juu ya upweke na ujuzi wa Mwenyezi Mungu, na kwamba Mwenyezi Mungu aonekana au haonekani, ni tofauti na ile ya Sunni
7.
Misingi ya dini na fiqhi kwa Shia ni tofauti na ile ya kwa Sunni na
8.
Kinyume na Sunni, Shia wanaamini raj’ah; nayo ni imani kwamba mwisho mwisho wa dunia atakuja Mahdi (a.s) ‘awachinje watesi wake wote wa kisiasa. Na atawarejeshea Mashia haki zao walizonyang’anywa na watu wa madhehebu mengine miaka mingi iliyopita’. 7
SHIA NA QUR’ANI
Hizo, kwa jumla, ndizo sababu kubwa zilizompelekea Sheikh M.al-Khatib kuandika kitabu chake hicho ili kuwaonya Sunni hatari ya kuitikia mwito wowote wa kuleta umoja na uelewano baina yao na ndugu zao wa Kishia. Na bila shaka ndizo sababu pia za waandamizi wake kuitoa tafsiri yake kwa Kiswahili. Zaidi ya hayo, kuna tuhuma nyingine ndogo ndogo zilizopachikwa pachikwa na kurudiwarudiwa hapa na pale katika kitabu hicho. Ni nia yangu Inshallah kuzijibu na kuzieleza zote hizo kadiri nitakavyoweza. Na kuwafikiwa ni kwa Mwenyezi Mungu. ba:
Katika majibu yangu haya nitajaribu Inshallah kuonyesha kwami.
Baadhi ya mambo yaliyosemwa na Sheikh M. al-Khatib ni kinyume na Ushia ulivyo
ii. Imani yoyote ya kidini ambayo Shia wanayo ina mategemeo yake katika Qur’ani Tukufu na Sunna ya Mtume Muhammad (s.a.w) iii. Karibu katika kila tuhuma ambayo Sheikh M. al-Khatib amewafanyia Shia, tuhuma kama hiyo inaweza kufanyiwa Sunni kutokana na yaliyomo katika vitabu vya Kisunni na mila zao; na kwa hivyo iv. Hititafu zilizoko baina ya Sunni na Shia si kubwa hivyo hata zizuie umoja na uelewano baina yao. Na Mwenyezi Mungu ndiye wa wa kuombwa msaada. Ewe Mola! Tuonyeshe Haki kuwa ni Haki, uturuzuku kuifuata, tuonyeshe batili kuwa ni batili, uturuzuku kuiepuka.
8
SHIA NA QUR’ANI
SUNNI NI NANI
K
wa kuwa kitabu cha Sheikh M. al-Khatib kimeandikiwa Sunni kuwatahadharisha na hatari ya Ushia, nimeona kwamba itakuwa vizuri Sunni ajijue yeye mwenyewe kabla ya kumzungumza Shia. Maana ionekanavyo, Sunni wengi sana hawajijui wao ni nani; na kama wakijijua, hujijuwa kimakosa! Kwa mfano, baadhi ya wale walisoma miongoni mwa Sunni hudhania kwamba wameitwa hivyo kwa sababu wao tu ndio wanaoiamini na kuifuata sunna ya Mtume Muhammad (s.a.w) – kama kwamba madhehebu mingine ya Kiislamu (k.v. Shia Ithnaashari, Zaydiyya au Ibadhi) hayafuati! Wengine hudhani wameitwa hivyo kwa kuwa madhehebu yao yalikuwako tangu zama za Mtume (s.a.w)! Kumbe zote fikira mbili hizo ni kinyume na mambo yalivyo. Ukweli ni kwamba Sunni ni wale ambao, katika mambo ya sheria, hufuata maoni ya mmoja wapo wa maimamu wanne (Abu Hanifa, Malik, Shafi au Hanbal) au wanafunzi wao; na katika mambo ya akida (imani), hufuata maoni ya Abul Hassan al-Ash’ari. Bila ya kufanya hivyo – kwa mfano, kama mtu atafuata maoni ya wasiokuwa hao katika sheria na/au katika imani - hawi ni Sunni. Kwa hivyo, ili mtu aelewe ni lini hasa ulipoanza Usunni, itambidi ajue (japo kidogo) historia ya maimamu hao. Nayo ni kama ifuatavyo:
•
Abu Hanifa ndiye wa kwanza. Yeye alizaliwa Kufah mwaka 80H na kufariki Baghdad mwaka 150H. Miongoni mwa walimu aliosoma kwao ni Imam Ja’far as-Sadiq (a.s) (aliyekuwa Imam wa Sita wa Shia Itnaashari) hata akasema kwamba, kama si miaka miwili aliyojifunza kwake, basi angeangamia. 9
SHIA NA QUR’ANI
•
• •
Malik ndiye wa pili. Yeye alizaliwa Madina mwaka 93H na kufariki huko huko Madina mwaka 179H. Yeye pia, kama Abu Hanifa, alisoma kwa Imam Ja’far as-Sadiq (a.s) miongoni mwa walimu wengine. Wa tatu ni Imam Shafi. Yeye alizaliwa Gaza mwaka 150H na kufariki Misri mwaka 204H. Na wa mwisho ni Imam Hanbali aliyezaliwa Baghdad mwaka 164H na kufariki huko huko Baghdad mwaka 241H.
Hao ni wa upande wa sheria. Kwa upande wa akida (imani), Sunni humfuata Abul Hassan al-Ash’ari ambaye alizaliwa Basra mwaka 260 H na kufariki Baghdad mwa 333H. Sasa, unapotazama tarehe za maimamu hao utaona kwamba wa kwanza kabisa ni Abu Hanifa aliyezaliwa mwaka 80H. Hii ina maana kwamba yeye alikuja duniani miaka sabini hivi baada ya Mtume Muhammad (s.a.w) (ambaye alifariki dunia mwaka 10H). Jee basi, kama ni hivyo, wale Waislamu walioishi baina ya kufa Mtume (s.a.w) na yeye kuwa Imamu (kipindi cha zaidi ya miaka 70) walikuwa wakimfuata nani? Hawakuwa na wafuasi? Jee, wale walimu waliomsomesha yeye hawakuwa na wafuasi? Wafuasi hao walitowekea wapi? Jee, anayefuata maoni ya walimu hao hawi Mwislamu bali anayefuata maoni ya wanafunzi wao huwa? Kama hawi Mwislamu, basi ni kwa hoja gani? Kama huwa, basi kwa nini Sunni wa kawaida kupawa fikra kwamba wao tu ndio Waislamu wa haki? Japokuwa hayo ni maswali ambayo majibu yake yangehitajia kitabu chake peke yake, maana ni hadithi ndefu yenye undani mwingi, ningependelea ewe ndugu msomaji ujiulize au umuulize anaye10
SHIA NA QUR’ANI
jua zaidi yako, na uyazingatie majibu yake kwa makini. Maana, kwa kupata majibu ya kuridhisha ya maswali hayo, ndipo utakapoweza kutatua kitendawili hiki cha mfarakano na kutoelewana baina ya waislamu. Tukija upande wa akida (imani), itaonekana kwamba Sunni hufuata mawazo ya mtu aliyekuja duniani miaka 19 baada ya imamu wa mwisho wa Kisunni kufariki, yaani Imam Hanbali! Maana yeye alifariki mwaka 241 H hali Abul Hassan al-Ash’ari alizaliwa mwaka 260H! Kwa hivyo al-Ash’ari hakukutana na yeyote kati ya maimamu wa Kisunni wa sheria! Kama ni hivyo basi, hao maimamu wanne, kabla ya kufariki kwao, walifuata imani gani? Ya al-Ash’ari, ambaye alikuwa bado hajazaliwa, au imani nyingine iliyokuwako kabla ya kuzaliwa al-Ash’ari? Kama ni nyingine, ni ipi? Na je!, walikuwa ni Waislamu kwa kuamini hivyo? Kama walikuwa ni Waislamu – na sidhani kuwa yuko yeyote anayeweza kujasiri kusema kuwa maimamu hao walikuwa makafiri – basi kwa nini iwe ni wao tu? Kwa nini mtu mwingine, anapofuata maoni ya asiyekuwa al-Ash’ari, awe si Mwislamu? Kwani yeye al-Ash’ari alipozaliwa, alizaliwa na hayo maoni yake? Jee hakuwa akifuata maoni ya wataalamu aliowakuta kabla ya yeye kuzuka na maoni yake? Kama alikifuata mawazo ya wengine – na ukweli ni kwamba alikifuata – jee, wakati huo yeye alikuwa si Mwislamu? Kama alikuwa ni Mwislamu, pamoja na kwamba alikuwa akifuata maoni yasiyokuwa yake, kwa nini leo mtu mwingine awe si Mwislamu kwa kufanya vivyo hivyo? Hayo nayo pia ni maswali ambayo, ewe ndugu msomaji, inataka ujiulize (au umuulize anayekuzidi elimu) na uyazingatie majibu yake kwa makini. Maana majibu sahihi utakayoyapata ndiyo yata11
SHIA NA QUR’ANI
kayokusaidia kuelewa kiini cha mzozo huu tunaoujadili katika mfululizo wa vitabu hivi. Kutokana na maelezo mafupi haya, na majibu sahihi utakayoweza kuyapata ya maswali machache tuliyoyauliza, nataraji Inshallah kila aliye Sunni ataweza kujijua yeye ni nani. Na Mwenyezi Mungu ndiye wa kuombwa msaada.
12
SHIA NA QUR’ANI
QUR’ANI TUKUFU
M
wenyezi Mungu (s.w.t) amesema:
ِّ إنَّا َن ْح ُن َن َّز ْل َنا َ الذ ْك َر َوإِنَّا لَ ُه لَ َحا ِف ُظ ون ِ
“Hakika Sisi ndio tuliouteremsha Ukumbusho (huu), na hakika Sisi ndio Wenye kuulinda.” (Sura 15:9)
ُ اط ْ يز اَل َي ْأ ِتي ِه ََوإنَّ ُه ل ٌ اب َعز َ ْ ٌ ْن َي َد ْي ِه ي ب ن م ل ب ال ت ك َ َ ِ ِ ِ ِ ِ ِ ٌ ْ َا َْ َ ْ ْ يم َح ِمي ٍد ٍ َول ِمن خل ِف ِه تن ِزيل ِمن َح ِك “Bila shaka hicho ni Kitabu Kitukufu. Hakitajiliwa na batili mbele yake wala nyuma yake; ni wahyi utokao kwa Mwenye hekima, Asifiwaye.” (Sura 41:41-42)
Hayo ni maneno ya Mwenyezi Mungu yanayotuthubutishia kwamba Qur’ani ni kitabu kilichohifadhiwa na kila aina ya nyongeza, upungufu au mabadiliko. Waislamu wote – wa zama zote na nchi zote – wanaamini kwamba hii Qur’ani tuliyonayo leo ndiyo ile ile iliyokuwako zama za Mtume (s.a.w), chapa kwa ya pili, na ndiyo hii hii itakayokuwako mpaka Siku ya Kiyama. Kwa hivyo, mtu ye yote atakayeamini kinyume cha hivyo, huyo si Mwislamu. Kwa kuwa Sheikh M. al-Khatib, katika kitabu chake hicho (uk. 4), amedai kuwa Shia hawaamini hivyo, nimeona ni bora nianze majibu yangu haya kwa madondoo ya wanazuoni mbalimbali wa 13
SHIA NA QUR’ANI
Kishia, wa nyakati mbalimbali, yanayobatilisha madai yake hayo. Baada ya hapo ndipo niendelee na madai yake mengine: 1.
Al-Fadhl b, Shaadhaan: Huyu ni kati ya wanazuoni wakubwa wa Kishia aliyeishi katika karne ya tatu ya Hijria. Katika kitabu chake kiitwacho al-lidhaah katika kukataa baadhi ya maoni ya wanazuoni wa Kisunni wa zama zake kwamba Qur’ani Tukufu imepotolewa, amesema: “Lakini wale ambao, kwa kutaja Hadith kama hizo, wadhania kwamba nassi ya Qur’ani imepotolewa, bila shaka wanakosea.”
2.
Abu Ja’far Muhammad b. Ali b. Baabawayh al-Qummi: Mwanachuoni huyu ni maarufu zaidi kwa jina la al-Shaykh as-Saduq na alifariki dunia katika mwaka 381H. Yeye amesema hivi katika kitabu chake kiitwacho al-i’tiqaadaat: “Imani yetu ni kwamba Qur’ani ambayo Mwenyezi Mungu (s.w.t) amemteremshia Mtume Wake Muhammad (s.a.w) ni hii hii iliyo baina ya majalada mawili na iliyomo mikononi mwa watu; si zaidi ya hiyo... Na yeyote anayetusingizia kwamba twasema zaidi ya hivyo, basi huyo ni mwongo.”
3.
Sayyid al-Murtadhaa Ali b. Al-Husayn al-Muusawi al-Alawi: Huyu ni mwanachuoni mwingine mkubwa wa Kishia aliyefariki dunia katika mwaka 436H. Yeye, katika kujibu maswali ya Taraabultisiyyaat, amesema: “Ujuzi wa kwamba mapokezi ya Qur’ani ni sahihi ni kama ujuzi wa nchi na miji, matukio makubwa makubwa ya kihistoria, vitabu mashuhuri, na mashairi yaliyoandikwa na Waarabu. Hili ni kwa sababu hamu na sababu za kuinakili na kuihifadhi Qur’ani zilishitadi na kufikia kiwango am14
SHIA NA QUR’ANI
bacho hakikufikiwa na hayo mengine tuliyoyataja...katika zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) Qur’ani ilikuwa ni mkusanyo uliotungamanishwa kama uliyo hivi sasa. Mtume (s.a.w) alikuwa hata ametua masahaba wa kuihifadhi kwa moyo na kuilinda. Pia ilikuwa ni desturi (ya baadhi ya masahaba) kuisoma mbele zake ili kuhakikisha kuwa ndivyo. Kikundi cha masahaba, kama vile Abdullah b. Mas’ud , Ubayy b. Ka’b na wengineo walikiihitimisha Qur’ani mbele za Mtume (s.a.w) hitima kadha wa kadha. Na yote haya yaonyesha, hata kwa taamuli ndogo, kwamba Qur’ani ilikuwa ni mkusanyo uliopangwa; haukukatika kipande wala haukutawanyika... Na kwamba yeyote katika Imamiyya (Shia ithnaashari) au Hashwiyya (wasiokuwa Shia), anayeamini kinyume cha hivyo, basi kinyume hicho chatokana na watu wa Hadith walionakili Hadith dhaifu wakidhania ni sahihi; hali Hadith dhaifu kama hizo haziwezi kulirud’ – Jambo ambalo usahihi wake unajulikana kwa njia isiyo na shaka.” Maneno hayo unaweza kuyaona katika Majma’ul Bayaan, Juzuu ya Kwanza, uk. 15. 4.
Shaykh at-Taifah Abu Ja’far Muhammad b. al-Hasan atTusi: Huyu alifariki katika mwaka 461H. Yeye amesema, kama ilivyo katika uk. 48-49 wa Juzuu ya Kwanza ya Tafsirus Swaafi: “Ama neno la kwamba (Qur’ani) imezidi au imepungua; hilo si jambo lililo laiki yake. Maana (kusema) kuwa imezidi, kuna kongamano (la wanazuoni kwamba fikira hiyo) ni batili. Ama kuwa imepungua, hilo dhahiri vile vile katika madhehebu yote ya Kiislamu ni kinyume chake. Na ndilo lililo sahihi katika madhehebu yetu. Na hii ndiyo (imani) ili15
SHIA NA QUR’ANI
youngwa mkono na Sayyid al-Murtadhaa r.a, na ndiyo iliyo dhahiri katika riwaya mbalimbali. Hata hivyo, kuna riwaya nyingi za kwa upande wa Shia na Sunni kuhusu kupungua kwa aya nyingi za Qur’ani na kuhusu baadhi ya aya kuwa mahali pa aya nyingine. Lakini riwaya zote hizo ni za aahaad (si mutawaatir) zisizo na yakini. Kwa hivyo lililo bora ni kujiepusha na riwaya kama hizo na kutoshughulika nazo. Maana yamkinika kuziawili (riwaya kama) hizo. Na lau kama riwaya hizo zingalikuwa sahihi zisingaliweza kuyatia doa yale yaliyomo baina ya majalada mawili (ya’ Qur’ani) kwa kuwa yajulikana kuwa yote ni sahihi isiyopingwa wala kukataliwa na yeyote katika umma wa Kislamu.” 5.
Abu Ali at-Tabarsi: Huyu alifariki katika mwaka 548H. Yeye amesema katika Juzuu ya Kwanza ya tafsiri yake iitwayo Majma’ul Bayaan: (uk. 15). “Kuna kongamano la Waislamu kwamba hakuna kilichozidi katika Qur’ani. Ama kuwa imepungua; baadhi ya watu wetu na baadhi ya Hashwiyya (yaani Sunni) wamesema kuwa kuna mabadiliko na upungufu katika Qur’ani. Lakini lililo sahihi katika madhehebu ya watu wetu ni kinyume chake.”
6.
Sayyid Ibn Twaawus: Huyu alifariki katika mwaka 664H. Yeye amesema: “Maoni ya immamiyya ni kwamba Qur’ani haikupotolewa.” Kisha akaendelea kusema, katika kuwarudi Sunni: “Mimi nawastaajabia wale ambao hutoa ushahidi kwamba Qur’ani imehifadhiwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu 16
SHIA NA QUR’ANI
(s.a.w) na kwamba yeye mwenyewe ndiye aliyeikusanya, kisha wakataja hitilafu iliyoko baina ya watu wa Makka na Madina, na watu wa Kufah na Basra. Na wakaamini kwamba Bismillahir Rahmanir Rahim si sehemu ya sura! Bali lililo la ajabu zaidi ni kule kutoa hoja kwao kwamba lau ingelikuwa ni sehemu ya sura, basi pangelitajwa kifunguzi chengine kabla yake. Ajabu iliyoje! Kama Qur’ani imehifadhiwa na ziada na upungufu wowote, kama inavyokubaliwa na akili na sheria, basi vipi itawezekana kuwa na aya kabla yake ambayo haimo ndani yake? Vipi itawezekana hivyo?” Hayo ndiyo maneno ya mwanachuoni huyo yaliyomo katika uk.144-145 na 192-193 wa kitabu chake kiitwacho Sa’dus Su’ud. Kwa kuwa hatukusudii kuyafanya mambo marefu katika majibu haya (ingawa tutakuwa tayari kufanya hivyo iwapo dharura), hatuna haja ya kuendelea kuyadondoa yote yaliyosemwa na wanazuoni wa Kishia juu ya jambo hili. Twadhani hayo tuliyoyataja yatatosha kwa sasa. Lakini, kwa faida ya wasomaji wetu. Tunawatajia hapa chini baadhi ya majina ya wanazuoni wengine wa Kishia (sio wote) waliosema kuwa Qur’ani Tukufu iliyokuwako zama za Mtume (s.a.w) ndiyo hii hii waliyonayo Waislamu leo; haikuzidi, haikupungua: 1.
Mulla Fathullah al-Kashani (aliyefariki mwaka 988H) katika tafsiri yake Manhajus Sadiqin.
2.
Al-Muhaqqiq Zaynuddin al-Bayadhi (aliyefariki mwaka 877H) katika kitabu chake as-Swiratum Mustaqim.
3.
Muhammad Bahauddin al-Amili, maarufu Shaykh al-Bahai (aliyefariki mwaka 103H), kama alivyonakiliwa katika Tafsiri ya Aalaair Rahman.
4.
Mulla Muhsin, maarufu kwa jina la-al Faydhul Kashani (al17
SHIA NA QUR’ANI
iyefariki mwaka 109H) katika tafsiri yake iitwayo Tafsirus Swafi. 5.
Muhammad b. al-Hassan al-Hurrul Amili (aliyefariki mwaka 1104H) katika risala yake kwa Kifarsi Risala Fi Ithbati Adamit Tahrif.
6.
Al-Qadhi Sayyid Nurullah as-Shustari (aliyefariki 1091H) kama alivyonakiliwa katika Alair Rahman.
7.
Sayyid Muhammad Mahdi b. Sayyid Murtadha at-Tabatabai, ajulikanaye kama Bahrul Ulum (aliyefariki 1212H) katika kitabu chake kiitwacho Fawaidul Usul.
8.
Ja’far b. Shaykh Khidhr aj-Janahi an-Najafi, ajulikanaye kama Kashiful Ghitaa (aliyefariki 1228H) katika kitabu chake kiitwacho Kashful Ghitaa An Mubhamatis Shariatil Gharraa.
9.
Muhammad Hasan b. al Mawla Abdullah al-Mamaqani (aliyefariki 1323H) katika kitabu chake kiitwacho Tanqihul Maqal.
10. Muhammad Jawad al-Balaghi (aliyefariki 1352H) katika tafsiri yake iitwayo Aalair Rahman. 11. Ayatullah Sayyid Husayn Kuhkamari (aliyefariki 1299H), kama ilivyoelezwa na mwanafunzi wake katika Bushral Wasul lla llmil Usul. 12. Mirza Hasan al-Ashtlyani (aliyefariki 1319H), katika kitabu chake kiitwacho Bahrut Fawaid. 13. Sayyid Abdul Husayn Sharafuddin al-Musawai-al-Amili (aliyefariki 1377H) katika kitabu chake kiitwacho Ajwibatu Masaili Musa Jarullah. 18
SHIA NA QUR’ANI
14. Ayatullahi Udhmaa Sayyid Abul Qasim al-Khui (ambaye alikuja kufariki 1412 Najaf - Iraq) katika tafsiri yake iitwayo al-Bayan. 15. Al-Imamal-Khumayni katika kitabu chake kiitwacho Kashful Asrar. 16. Muhammad an-Nahawandi katika tafsiri yake iitwayo Nafahatur Rahman. 17. Sayyid Al Naqi al-Hindi katika utangulizi wa kitabu chake kiitwacho Tafsirul Qur’an. Hayo basi ndiyo maneno ya baadhi ya wanazuoni wakubwa wakubwa wa Kishia - kuanzia karne ya tatu hadi hii tuliyonayo! Unapoyasoma maneno yao unaona wazi kwamba imani ya Shia kuhusu Qur’ani Tukufu ni kama ile ya Waislamu wote – kwamba tangu ilipoteremshwa hadi leo hajiabadilika hata kitone. Lakini, kwa sababu anazozijua yeye mwenyewe, Sheikh M. al-Khatib hakupendelea kuujulisha umma wa Waislamu maneno hayo. Badala yake amependelea kuwaambia yafuatayo: i.
Misingi ya dini kwa Shia imesimama ‘juu ya kutaawili aya kuyapindua maana yake zifahamike kinyume na walivyozifahamu maswahaba kutoka kwa Mtume (s.a.w) kinyume na walivyozifahamu wale watu wa mwanzo ambao Qur’ani iliteremka kwao’ (tazama uk. 4 wa kitabu chake hicho).
ii. ‘Qur’ani imezidishwa na imepuunguzwa’, na kwamba ushahidi wa hilo umo katika kitabu kitwacho Fasl ulKhitab Fi ithbati Tahriffi Kitabi rabbil Arbab cha Haji Mirza Husayn at-Twabarsy. (uk.4). 19
SHIA NA QUR’ANI
iii. Miongoni mwa ushahidi kwamba Qur’ani imepungua ni Surat al-Wilaya ambayo ati Shia wanadai kwamba imetolewa katika misahafu tuliyonayo; na kwamba sura hiyo imethibitishwa katika hicho kitabu cha at-Twabarsy tulichokitaja hapo (ii) juu. (uk.5). iv. Sura hiyo vile vile iko kwenye kitabu chao (Dabistan Madhhab) kwa lugha ya Kifursi kilichoandikwa na Muhsin Faniy al-Kashmiri. (uk.6). v.
Hali kadhalika, kama alivyotoa ushahidi kwa Surat alWilaya kuthibitisha kwamba Qur’ani imabadilishwa, atTwabarsy ametoa ushahidi ‘kwa yaliyo kwenye ukurasa wa 289 wa kitabu cha (al-Kafi) chapa ya mwaka wa 1278H, Iran’. Kitabu hicho kwa Shia, anavyodai Sheikh M. al-Khatib, ‘ni Swahihi ya Bukhari kwa Waislamu.’ (uk.6).
vi. ‘Miongoni mwa aya wanazozidai Mashia kuwa zimeondolewa wenye Qur’ani’ ni ile aya isemayo: Waja’alnaa Aliyyan swihraka, yaani: ‘Na tukamfanya Ali kuwa ni mkwe wako.’ (uk.7) vii. Shia wana Mswahafu wa Fatima ambao ‘ndani yake kuna kama Qur’ani yenu hii mara tatu. Hakuna ndani yake herufi moja ya Qur’ani yenu!’ (uk.9). Kwa hivyo, hebu tuyachambue na kuyajibu madai hayo moja baada ya moja:
20
SHIA NA QUR’ANI
Kuawili aya Hilo ndilo dai la kwanza la Sheikh M. al-Khatib kwamba Shia, wanapoifasiri Qur’ani, huziawili aya na kuzipindua maana yake ili ‘zifahamike kinyume na walivyozifahamu masahaba kutoka kwa Mtume (s.a.w), na kinyume na walivyozifahamu wale watu wa mwanzo ambao Qur’ani iliteremka kwao.’ (taz. uk. 4). Hapa, jambo la kushangaza ni kwamba shekhe wetu huyo hakutupa angalau mfano wa aya mbili tatu tu zilizoawiliwa hivyo ili kuthibitisha dai lake hilo. Pengine wale walioko hai sasa, waliomshikia kazi yake, watatufanyia wema wa hilo pindi itakapowapendeza kutujibu. Kwa hivi sasa ningependa wasomaji wetu watukufu waelewe kwamba baadhi ya tafsiri za Qur’ani za Shia, kama zilivyo zile za Waislamu wa madhehebu mengine, zimekusanya riwaya zilizo sahihi na zisizo sahihi. Na mtu anaposoma vitabu vya wafasiri na wahadithi wa Kishia ataona jinsi mabingwa hao walivyozichambua – ama kwa kuzikubali au kuzikataa – riwaya kama hizo. Na hivi hivi ndivyo ilivyo kwa Sunni. Lakini kama Sheikh M. al-Khatib ana lazima Shia wote wawe makosani kwa sababu tu baadhi ya masheke wao wameziawili baadhi ya aya - hata kama taawili hizo si zenye kukubaliwa na Shia wote – jee na Shia nao wasemeje kuhusu taawili kama hizo kwa upande wa Sunni? Au shekhe wetu huyo, na wengine wenye fikira kama zake, hawazijui taawili zilizomo katika vitabu cya Kisunni vya tafsiri - kama vile ad-Durrul Manthur ya Suyuti, Gharaibul Qur’an ya an-Nishaburi, Tafsirul Qur’anil Adhim ya at-Tustari, Araisul Bayan ya as-Shirazi, Tafsir ya ibn Arabi, na nyinginezo? Au akataa kwamba hao wote ni Sunni, si Shia? 21
SHIA NA QUR’ANI
Kwa hivyo, ndugu yangu, hiyo ya taawili ya aya si hoja ya kuzuia Sunni na Shia kukurubiana na kushirikiana kwa maslaha ya Uislamu. Maana lidaiwalo liko kwa Shia, na kwa Sunni nako liko!
Faslul Khitab Dai la pili la shekhe wetu M. al-Khatib ni la kitabu kiitwacho Faslul Khitab Fi Ithbati Tahrifi Kitabi Rabbil Arbab cha Haji Mirza Husein at-Twabarsy. Katika uk. 4 wa kitabu chake, Sheikh M. alKhatib amesema kwamba ndani ya kitabu hicho cha Faslul Khitab mna ushahidi kwamba, kwa imani ya Kishia, Qur’ani imezidishwa na imepunguzwa.’ Kuhusu dai hilo, tazama uk. 9-11 wa kitabu hiki uone jinsi wanazuoni mbalimbali wa Kishia walivyokanusha jambo hilo. Pia tazama uk. 19-22 uone kwamba fikira hiyo ya Qur’ani kuzidishwa na kupunguzwa iko hata kwa Sunni – tena katika vitabu vyao vikubwavikubwa vinavyotegemewa kuwa ndivyo ‘sahihi mno baada ya Qur’ani! Sasa basi, kama mambo ni hivyo, kwa nini zani iwachukie Shia peke yao? Tukija kwenye hicho kitabu chenyewe, Faslul Khitab; ni kweli, kama alivyosema Sheikh M. al-Khatib, kilichapishwa Iran katika 1298. Lakini si kweli kwamba kimekusanya ushahidi wa wanavyuoni wa Kishia na wanaijitihadi wao’ peke yao! Bali ukweli ni kwamba kitabu hicho kimekusanya ushahidi wa hata Sunni – tena kwa wingi zaidi! Hata hivyo, lililo muhimu hapa ni kujua kwamba, baada ya kitabu hicho kuchapishwa, palitokea wanazuoni wa Kishia walioandika vitabu kukirudi. Nao ni Sayyid Muhammad Husein Shahristani kwa kitabu chake: Risalatu Hifdhil Kitabis Sharifi An Shubhatil Qawli 22
SHIA NA QUR’ANI
Bii Tahrif na Sheikh Mahmud at-Tahrani kwa kitabu chake: Kashful Irtiyabi. Jee, shekhe wetu huyo hakuyajua hayo? Juu ya yote hayo, ieleweke kwamba mwandishi huyo wa Faslul Khitab, kabla ya kufariki dunia, alikiri kosa lake la kukiita kitabu hicho hivyo alivyokiita. Bali akasema kwamba lililokuwa bora ni kukiita kitabu hicho Faslul Khitab Fi Adami Tahrifil Kitab maana katika kitabu chake hicho amethibitisha kwamba sura na aya zote za Qur’ani Tukufu, iliyomo baina ya majalada mawili na kuenea pande (zote) za ulimwengu, ni wahyi wa Mwenyezi Mungu ambao haukuingiliwa na mageuzo wala mabadiliko, ziada wala upungufu – tangu ilipokusanywa hadi leo... Lakini hata kama tutakubali kuwa yote yaliyomo katika Faslul Khitab yatoka katika riwaya za Kishia, na hata kama tutakataa ripoti ya Sheikh at-Twabarsy kukiri kosa lake. Sheikh M. al-Khatib atatwambiaje kuhusu baadhi ya zile riwaya zilizomo katika Juzuu ya Pili ya Al-Itqan ya Suyuti ambazo ni sawa na zile zilizomo katika hiyo Faslul Khitab? Jee kwa hilo, yeye au wale wenye fikira kama zake, yu tayari kuwahukumu Sunni kama alivyowahukumu Shia kwa Faslul Khitab? Kama hawatakuwa tayari, basi wasomaji wetu watukufu watakuwa na haki ya kutaka kujua kwa nini.
Surat al-Wilaya Hii ndiyo sura inayochezwa mno ngoma na wapinzani wa Shia. Kwa mujibu wa Sheikh M. al-Khatib (uk. 5) sura hiyo imetajwa katika uk. 180 wa Faslul Khitab. Hali kadhalika, mwanachuoni mmoja ‘mwenye kuaminika’ aitwaye Muhammad Ali Saudiy na aliyekuwa mshauri mkubwa wa Wizara ya Sheria ya Misri, aliuona msahafu wa Kiirani kwa al-Mustashriq Brown akaweza kuinakili sura hiyo kwa picha! Haya ndiyo anayotwambia shekhe wetu huyo! 23
SHIA NA QUR’ANI
Jambo la kushangaza mno kuhusu dai hili ni kwamba kila anayelitolea ushahidi hutoa nakala hiyo hiyo aliyoipata Ustadh Muhammad Ali Saudiy kwa Mr Brown! Kwa nini iwe hivyo? Au ndiyo tuseme kuwa ulimwengu mzima hakuna nakala nyingine ya msahafu huo isipokuwa ya Mzungu huyo, Mr Brown? Mzungu huyo aliwezaje kuipata nakala hiyo, shekhe wetu na wenzake wakashindwa kuipata? Na kwa nini Shia waifiche sura hiyo, kama wanaamini ni mojawapo ya sura za Qur’ani, hali inazungumzia wilaya ya Imam Ali (a.s) ambayo ni kati ya nguzo kubwa ya imani ya Shia? Kama Shia hutoa ushahidi wa wilaya ya Imam Ali (a.s) kwa aya mbalimbali za Qur’ani, kwa nini basi waifiche sura hiyo? Na kwa nini tunapotazama tafsiri zote za Shia za Qur’ani za lugha zote, hatuioni sura hiyo? Yote hayo ni maswali ambayo inataka ujiulize, ewe ndugu yangu, ili usizuzuliwe na uzuzi huo. Hilo la kwamba nakala hiyo ilipatikana kwa mustashriq peke yake ni sababu tosha ya kumfanya Mwislamu yeyote, aliye na insafi na dini yake, kutokubali uzuzi huo. Maana mustashriqin – (au orientalists kwa Kiingereza) ni maadui wakubwa wa Uislamu. Hawa ni wale Wazungu na Mayahudi waliounda taaluma hii ya istishraq (orientalism) kwa malengo ya kuudhoofisha na kuuvunja umoja wa Waislamu, kuupalilia njia ukoloni uingie katika nchi za Kiislamu, na kuwanyonya Waislamu pamoja na kuwahujumu kwa kuupinga Ukristo katika Zama za Kati. lli kutekeleza malengo yao hayo, walianzisha majarida na vyuo mbalimbali, wakafanya mikutano na kutunga vitabu mbalimbali vya kuhujumu Qur’ani Tukufu, Mtume Muhammad (s.a.w), na Uislamu kwa jumla – tena kwa njia ya hila sana. Kama watu hao ni hivyo, vipi basi Sheikh M. al-Khatib atatosheka na ushahidi wa nakala moja tu iliyopatikana kwa watu kama hao? Au kwa nini aone hilo la sura hiyo tu ndilo kubwa? Kwa nini asiya24
SHIA NA QUR’ANI
kumbuke na yale yaliyomo katika vitabu vya Kisunni, ya sura zenye aya nyingi zaidi kuliko hizo saba za Surat al-Wilaya, zilizopungua katika Qur’ani? Hapa chini tutatoa mifano miwili tu; iliyobaki itazame kwenye uk. 19-22 humu: i.
Katika uk. 152 wa Juzuu ya Saba ya Majma’uz Zawaid imeandikwa kwamba Abdulrahman b. Yazid, yaani anNakhai, amesema kwamba Abdallah alikuwa akizifuta muawwidhataini katika misahafu yake, na akisema kwamba hizo si katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu (s.w.t). Kisha imeendelea: ‘Imepokewa na Abdallah b. Ahmad na Tabrani. Na watu wa Abdallah ni watu sahihi, na watu wa Tabrani ni waaminfu.’
Kwa hivyo, kutokana na Hadith hiyo, sura mbili hizo (Sura 113 na 114) zilizomo katika misahafu tuliyonayo, zimeongezwa! Kama ni hivyo, jee Shia hawatakuwa na haki ya kuwashutumu ndugu zao Sunni kuwa Qur’ani yao imeongezwa? ii. Ukija kwenye al-Itiqan ya Imam Suyuti (Juzuu ya Kwanza, uk. 87), imeandikwa kwamba katika msahafu wa Ibn aAbbas na Ubayy b. Ka’b mlikuwa na sura mbili, AlKhala na Al-Hafd zisemazo:
َ اَللُّه ّم إنّا َن ْس َت ِع ْينُك َو َن ْس َت ْغ ِف ُر َك ونُ ْث ِن ْي َعلَي ْك وال َن ْك ُف ُرك ِ اَللُّه ّم إيّاَك َن ْعبُ ُد ولَ َك.و َن ْخلَ ُع ونـَــت ْـ ُر ُك َم ْن َي ْف ُج ُرك َ صلِّي و َن ْس ُج ُد َوإلَي ْك َن ْس َعى و َن ْح ِف ُد َن ْر ُج ْو َر ْح َم َتك َ ُن ِ َ و َن ْخ َشى َع َذا َب َك إن َع َذ ْا َب َك ِب َ الكا ِف ِر ين م ُْل ِح ٌق ِ 25
SHIA NA QUR’ANI
Jee? Leo ukiuangalia msahafu wako, zimo sura zenye majina hayo? Majibu ni: hamna! Jee, zimo aya kama hizo msahafuni? Majibu vile vile ni: hamna! Jee mtu akisema, kwa maneno hayo ya Imam Suyuti, kwamba Qur’ani imepungua sura mbili, atakuwa amekosea? Jee Sheikh M. al-Khatib atazilinganisha vipi sura mbili hizo kwa ile moja ya al-Wilaya? iii. Ukija kwenye Sahih Muslim (taz. ‘Kitab az-Zakaf Mlango wa ‘Law Anna Libni Adama Waadiyayni Labtaghaa Thalithan’) twaambia kwamba Abu Musa al-Ash’ari amesema kwamba walikisoma sura ambayo urefu wake ulikuwa ni kama wa Sura Bara’ah, lakini sasa ameisahau isipokuwa aya moja tu isemayo:
َ لَ ْو َك ال اَل ْب َت َغى َوا ِديا َثالًِثا َو اَل ٍ ان ِم ْن َم ِ ْن آ َد َم َوا ِد َي ِ ان اِلب ُ ََيم أ ُّ ف ابْن آ َد َم إ اَّل َ ُ الت َر اب و ج ْل ْ َ ِ ِ Akasema vile vile kwamba walikiisoma sura waliyokiilinganisha na mojawapo ya musabbihaat (sura zianzazo kwa sabbaha au yusabbihu) lakini ameisahau isipokuwa aya moja tu aikumbukayo:
َ ُون َما اَل َت ْف َعل َ ُين آ َمنُوا لِ َم َت ُقول َ َيا أَيَُّها ال ِذ ون َفتُ ْك َت ُب َ َُش َها َد ًة ِفي أَ ْع َنا ِق ُك ْم َفتُ ْسأَل ون َع ْن َها َي ْو َم ْال ِق َيا َم ِة 26
SHIA NA QUR’ANI
Ewe ndugu yangu! Ukumbuke kwamba Sura Bara’ah ni ile Sura ya 9 katika Juzuu ya 10 ya Qur’ani ambayo vile vile huitwa Sura at-Tawba. Sura hiyo ina jumla ya aya 129. Kwa hivyo, kutokana na Hadith hiyo tuliyoitaja hapo juu, hii Qur’ani tuliyonayo imepungukiwa na sura yenye aya 129. Maana ukiiangalia hata hiyo aya aliyokiikumbuka Abu Musa al-Ash’ari, hivi leo huioni katika misahafu iliyoko! Jee, bado Sheikh M. al-Khatib ataka kuwashutumu Shia kwa kupungukiwa na aya saba za Surat al-Wilaya, lakini Shia wasiwashutumu wao kwa kupungukiwa na aya 129? Tukiangalia musabbihaat; hizi jumla ni sura sita: Sura ya 57, 59, 61, 62, 64 na 87. Kati ya hizo, iliyo fupi mno ni ile ya 62 (Sura alJumu’a) yenye aya kumi na moja. Lakini unapoiangalia sura hiyo, bali na hata hizo nyingine zote, huioni hiyo aya aliyokiikumbuka Abu Musa al-Ash’ari isipokuwa kipande cha kwanza tu ambacho ni aya ya pili ya Sura ya 61 (as-Saff). Jee, yakifika hapo, tusemeje? Jee, wale waliojitolea kumsaidia Sheikh M. al-Khatib, kwa kukifasiri kitabu chake na kukieneza, watatwambiaje? Bado wataka tukubali kwamba wasemao kuwa Qur’ani imepungua ni Shia peke yao? Kwa wale wenye Sahih Muslim ya Kiingereza, na waitazame Hadith Na. 2286 iliyo kwenye uk. 500-501 wa Juzuu ya pili. Mwisho, anesema shekhe wetu huyo (uk. 5) kwamba Sheikh atTwabarsy ameiandika hiyo Surat al-Wilaya katika uk.180 wa hicho kitabu chake, Faslul Khitab. Lakini Sheikh Lutful Lahi as-Swafi amelikataa hilo katika uk. 62 wa Ma’al Khatib Fi Khututihil Aridhwa, Akasema: ‘ Hamna katika Faslul Khitab - si katika uk. 180 wala mwingineo – tangu mwanzo wa kitabu hadi mwisho wake, mahali palipotajwa sura hiyo (al-Wilaya) ya uwongo...!’ Jee?
27
SHIA NA QUR’ANI
Dabistan Madhhab Dai la nne la Sheikh M. al-Khatib (uk. 6) ni kwamba sura hiyo ya alWilaya vile vile iko kwenye kitabu cha Kishia kiitwacho Dabistan Mathhab kilichoandikwa kwa lugha ya Kifursi na Muhsin Fani alKashmiri, na kuchapishwa chapa nyingi huko Iran. Majibu yetu hapa ni: (i) Kitabu hicho si cha Kishia (ii) Hakuna uhakika kwamba mwandishi wake ni huyo aliyetajwa na Sheikh M. al-Khatib (iii) Si kweli kwamba kimechapishwa chapa nyingi huko Iran; na, lililo muhimu sana, (iv) Katika kitabu hicho hamkutajwa hiyo Surat al-Wilaya! Hivyo ndivyo asemavyo Sheikh Lutful Lahras-Swafi, aliyelifanyia utafiti dai hilo na anayeielewa vizuri lugha ya Kifursi, katika kitabu chake Ma’al Khatib Fi Khututihil Aridhwa (uk. 64-66) – maneno ambayo hapa chini twayaeleza kwa muhtasari tu: Kitabu hicho hakihusu Ushia. Kinahusu mambo ya mila mbali mbali – ya kweli na ya uwongo. Kimejaa visa ambavyo akili haiwezi kukubali kuwa ni vya kweli; na vingi ya visa hivyo vimenakiliwa kwa watu wasiojulikana ingawa, kwa dhahiri ya majina yao, yaonekana ni madarweshi wa Kibaniani! Kitabu chenyewe pia hakina jina la mwandishi wala la madhehebu yake. Bali pana hitilafu juu ya ni nani hasa mwandishi wa kitabu hicho. Wengine wasema ni Muhsin al-Kashmiri. Wengine, ni Dhul Fikar. Wengine, ni Muhammad Fani. Wengine, ni Mobed Shah. Wengine, ni Mobed Afraseyab. Na wengine, ni Kykhosro Ibn Azar Kywan. alimuradi, hakuna uhakika kwamba huyo Muhsin Fani alKashmiri ndiye mwandishi wa kitabu hicho. Kuhusu dai kwamba kitabu hicho kimechapishwa ‘chapa nyingi huko Iran’, Sheikh Lutful Lahi as-Swaafi amesema (uk. 66) kwam28
SHIA NA QUR’ANI
ba, baada ya utafiti mkubwa sana wa maktaba zote kubwa kubwa, ameweza kupata nakala tatu tu za kitabu hicho: kimoja ni chapa ya kwanza iliyochapishwa Bombay, mwaka 1262. Cha pili ni chapa ya pili iliyochapishwa mwaka 1268, lakini haikutajwa mahali ilipochapishwa. Na cha tatu ni chapa ya tatu iliyochapishwa Bombay vile vile katika mwaka 1277. Jee, hizo ndizo ‘chapa nyingi’? Na Jee, Bombay iko Iran?
Al-Kafi si Bukhari Dai la tano la Sheikh M. al-Khatib (uk. 6) ni kwamba at-Twabarsy ametoa ushahidi kuwa Qur’ani imebadilisha ‘kwa yaliyo kwenye ukurasa wa 289 wa kitabu cha (al-kafi).....’ na kwamba kitabu hicho kwa Shia ‘ni Swahihi ya Bukhari kwa Waislamu!’ Kama kwamba Shia si Waislamu!! Ili kuweza kulijibu dai hilo, hebu tuangalie wanavyosema Shia juu ya al-Kafi, na wanavyosema Sunni juu ya al-Bukhari; Jee vitabu viwili hivyo vinalingana? - Amesema Sayyid Hashim Ma’ruf alHasani, katika uk.132 na 134 wa kitabu chake kiitwacho Diraasaatun Fil Hadith Walmuhaddithin kwamba (wanazuoni) waliotangulia hawakukongamana katika kuzitegemea riwaya zake (yaani, za alkafi) zote – kwa jumla na kwa tafsiri’. Kisha akasema: (Katika) Hadith za al-kafi ambazo zimefikia Hadith 16199 (elfu kumi na sita, mia moja na tisini na tisa), Hadith 5072 (elfu tano na sabini na mbili) ndizo sahihi. 144 ni hasan, 1128 ni muwath-thaq, 302 ni qawiy, na 9553 ni dhaif’. Kutokana na maelezo hayo basi, itaonekana kwamba zaidi ya 50% (asilimia hamsini) ya Hadith za al-Kafi si sahihi! Hivyo ni wasemavyo Shia wao wenyewe juu ya kitabu chao hicho. Sasa tutazame wasemavyo Sunni nao juu ya chao, al-Bukhari. 29
SHIA NA QUR’ANI
Amesema Imam Dhahabi kwamba al-Bukhari ‘ndicho kitabu kikubwa na bora kuliko vitabu vyote vya Kiislamu baada ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu (s.w.t)’ Na wanazuoni wakubwa wakubwa wa Hadith wamepokea kwamba Imam Bukhari amesema: ‘Nimekifanya (kitabu changu hiki) ni hoja baina yangu na Mwenyezi Mungu (s.w.t) Na sikuzitia humo isipokuwa (Hadith) sahihi tupu. Na nilizoziacha katika (Hadith) sahihi ni nyingi zaidi ili (kitabuche) kisiwe kikubwa mno.’ (taz. uk. 379 wa al-Hadith Wal Muhaddithun cha Muhammad Abu Zahw). Zaidi ya hayo, hivi karibuni (katika Februari 1966) jarida moja lichapishwalo huko Kuwait, na liitwalo Majallatul Arabiy, lilichapishwa (Katika Toleo lake Na. 87) makala ya Abdul Warith Kabir yenye kichwa cha habari: ‘Si Kila Kilichomo Katika Sahih Bukhari ni Sahihi, Bali Yamo ya Uzuzi na Munkar’. Makala hayo yaliudhi mashekhe wengi wa Kisunni wakiwamo, miongoni mwao, Sheikh Muhammad Abu Zahra na Sheikh Yusuf al-Qardhawi. Hata wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Damascus, wapatao 21, wakaandika ardhilhali kali kwa Mfalme wa Kuwait kupinga makala hayo, na kumtaka Mfalme huyo atumie uwezo wake kuzuia uchapishaji wa makala ya aina hiyo. Kwa upande mwingine, chama kimoja cha Kuwait kiitwacho Jumuiyyatul Islahil Ijitmaiy kikakusanya makala mbalimbali, yalioandikwa na mashekhe mbalimbali kumtetea Bukhari, na kuyachapishia kijitabu kiitacho Kulla Maa Fil Bukhari Sahih (Kila Kilichomo Katika Bukhari ni Sahihi). Kwa hivyo, mpaka katika hii karne tuliyonayo, Sunni bado wanaamini kwamba yote yaliyomo katika al-Bukhari ni sahih! Sasa basi, ewe ndugu yangu, kama Shia waamini kwamba zaidi ya asilimia hamsini (50) ya Hadith zote zilizomo katika al-Kafi si sahihi; na kama Sunni waamini kwamba Hadith zote zilizomo katika al-Bukhari ni sahihi, vipi al-Kahfi itakuwa ni kama al-Bukhari? 30
SHIA NA QUR’ANI
Kwa mantiki gani? Pengine wale wanaokubaliana na mawazo ya marehemu Sheikh M. al-Khatib watajaribu kutueleza, itakapowapendeza kutujibu. Kwa maelezo haya mafupi, itadhihirika kwamba huo ushahidi anaosema Sheikh M. al-Khatib kuwa umo katika uk. 29 wa al-Kafi utakuwa ni wa hizo Hadith zisizo sahihi. Na hilo lishasemwa na wanazuoni wa Kishia wa Hadith katika vitabu vyao mbalimbali – kwa mfano, Rijaalun Najjaashi; Qaamusur Rijaal; Mu’jam Rijaal al-Hadith; Khulaasatur Rijaal; na Diraasaatun Fil Hadith Wal Muhaddithin. Hayo ndiyo majibu yetu, kwa ufupi, juu ya al-Kafi na yaliyomo humo.
Waja’alnaa Aliyyan Swihraka Hilo ni dai la sita la shekhe wetu, M. al-Khatib – kuwa maneno hayo ni aya iliyokuwamo katika Qur’ani, lakini sasa Shia wadai imeondolewa! Majibu: Baada ya kuelewa msimamo wa Shia juu ya Qur’ani (kwamba i vile vile kama alivyoteremshiwa Mtume Muhammad (s.a.w), na maneno ya wanazuoni wao wa Hadith juu ya Hadith zinazogusia kupungua au kuzidishwa kwa Qur’ani (kuwa si sahihi), bila shaka hiyo ‘aya’ iliyotajwa hapo juu itakuwa ni miongoni mwa riwaya hizo hizo zisizo sahihi. Na kupatikana riwaya kama hizo katika vitabu vya Shia si bina. Maana hata katika vitabu vya Sunni zimo! Kwa mfano, tazama Sahih Bukhari: ‘Kitab at-Tafsir.’ Mlango wa ‘Tabbat Yadaa Abi Lahabin Watabba,’ utaona kwamba Ibn Abbas amesema: ‘lliposhuka: 31
SHIA NA QUR’ANI
َ ير َت َك َ األ ْق َر ِب ين ( َو َر ْه َط َك من ُه ْم َ َوأَ ْن ِذ ْر َع ِش ْ َ المخ )لصين Jee, tusemeje na hiyo ni Sahih Bukhari ambayo usahihi wake tushaona ulivyotetewa (taz. uk. 17)? Jee hicho kipande cha mwisho kisemacho warahtwaka minhumul mukhlasswiin kimo ‘katika Qur’ani tuliyonayo? Hebu hakikisha kwa kutazama Sura 26:214 ambapo utakiona hicho kipande cha kwanza tu! Je hicho kipande cha pili cha aya hiyo kimekwenda wapi? Kwa wale wenye Sahih Bukhari kwa lugha ya Kiingereza, nawatazame Hadith Na. 495 iliyoko kwenye ukurasa 467 wa Juzuu ya Sita, wataliona hilo tunalolisema. Hata hivyo, inahuzunisha kuona kwamba ingawa Hadith hiyo, katika hiyo nuksha ya Kiingereza, imeandikwa kama tuliivyoinukuu hapo juu kwa Kiarabu, kipande cha warahtwaka minhumul mukhlasswiin hakikuandikiwa tafsiri yake kwa Kiingereza! Kwa hivyo yeyote atakayeisoma Hadith hiyo kwa Kiingereza, kama hajui Kiarabu, hatajua kwamba pameachwa kitu! Swali hapa ni, jee, tafsiri ya kipande hicho imeachwa kwa mghafala au makusudi?
Msahafu wa Fatima Hili ni dai la saba la Sheikh M. al-Khatib – kwamba Shia wana msahafu uitwao Msahafu wa Fatima, na ambao ni tofauti na misahafu waliyonayo Waislamu! – Na hilo ni kweli! Lakini neno msahafu hapo halina maana ya Qur’ani. Maana humo humo, katika hiyo hiyo al-Kafi aliyoitaja shekhe wetu huyo (taz. uk. 237-242) wa Juzuu 32
SHIA NA QUR’ANI
ya Kwanza), mna Hadith zinazoeleza kwamba katika msahafu huo hamna chochote cha Qur’ani. Kwa mfano, hiyo Hadith aliyotaja yeye ni Hadith Na. 1 katika mlango uitwao Fiihi Dhikrus Swahifa Wal Jafr Wal Jami’a Wamaswhaf Fatima a.s. Lakini mbona hakuitaja na ile Na. 3 isemayo wazi kwamba ‘huyo huyo Abu Abdillahi aliyetajwa katika Hadith Na. 1, katika hiyo Hadith Na. 3 amesema: ‘Sidai kwamba katika (msahafu) huo mna Qur’ani? Au kwa nini hakuitaja na ile Hadith Na. 4 isemayo kuwa liliomo humo ni ‘wasia wa Fatima (a.s)? Kwa hivyo ni kwamba, kutokana na Hadith hizo zilizomo katika al-Kafi, ‘Msahafu wa Fatima’ si msahafu wa Qur’ani. Maana hamna aya yoyote humo, wala maneno yoyote, yaliyofanana na aya yoyote ya Qur’ani. Neno msahafu hapo limetumiwa tu kwa maana ya ‘mkusanyo wa suhuf (kurasa)’; si kwa maana ya Qur’ani. Maana si kila msahafu ni Qur’ani kama ambavyo si kila Jami’i ni msikiti. Kwa majibu haya mafupi, kuhusu madai muhimu ya Sheikh M. al-Khatib dhidi ya Shia juu ya Qur’ani, nataraji nimeweza kuwaondolea ndugu zangu Waislamu tashwishi yoyote ambayo wangekuwa nayo dhidi ya ndugu zao Shia baada ya kusoma madai ya shekhe wetu huyo. Sasa tuangalie yaliyomo katika vitabu vya Kisunni ya kuonyesha kwamba Qur’ani imepungua, tungojee majibu na maelezo ya wenye mawazo kama ya Sheikh M. al-Khatib maana yeye mwenyewe, kwa bahati mbaya, amefariki. 1.
Hadith ya kwanza ni ile ya Sahih Bukhari tuliyoitaja uk. 18 humu
2.
Ya pili ni ile ya Sahih Muslim tuliyoitaja uk. 15 humu vile vile. 33
SHIA NA QUR’ANI
3.
Ya tatu ni ile ya Majma ‘uz Zawaid tuliyoitaja uk. 14
4.
Ya nne ni ile ya al-Itqan, ya sura mbili, tuliyoitaja uk. 14
Zote hizo ni Hadith zinzoonyesha kwamba hii Qur’ani tuliyonayo ama imezidi au imepungua! Juu ya hizo, tutazame Hadith zifuatazo: 5.
Ukitazama Sahih Bukhari, Mlango wa ‘ash-Shahada Takunu Indal Hakimi Fil Wilayatihi Qadhaa, katika ‘Kitabu al-Ahkaami’, utaona Hadith isemayo kwamba Umar b. Khattab amesema: ‘Lau kwamba si kwa kuogopa watu kusema kuwa Umar amezidisha (kitu) katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu, ningeliiandika aya ya rajm kwa mikono yangu mwenyewe!’
Na katika Sahih Muslim ‘Kitabu al-Hududi’ Mlango wa ‘Rajmuth Thayb Fiz Zinaa’, imenakiliwa kwamba Umar b. Khattab huyo huyo amesema kwamba hiyo aya ya rajm ilikuwa ‘ni miongoni mwa aya alizoteremshiwa (Mtume Muhammad (s.a.w)’ Kisha akasema: ‘Tulikiisoma na kuihifadhi kwa moyo na kuielewa.’ Kwa wale wenye tafsiri za Kiingereza za vitabu viwili hivyo, nawatazame Hadith Na. 21 iliyoko kwenye uk. 212 wa Juzuu ya Tisa ya Sahih Bukhari, na Hadith Na. 4194 iliyoko kwenye uk. 912 wa Juzuu ya Tatu ya Sahih Muslim. Na kwa wale wasioijua hiyo aya ya rajm kwa Kiarabu ni hii:
َّ يخ َّ إن َ الش َ والشي َّ ُ ار ُج موهما ال َبتَّة ْ ْخ َة َإذا َز َن َيا َف Ambayo maana yake ni: ‘Mzee mwanamume na mzee mwanamke, wanapozini, wapigeni mawe wote.’ 34
SHIA NA QUR’ANI
Hapa tuna maswali mawili matatu ya kuuliza. Kwanza; hiyo ni aya ya Qur’ani au si aya? Kama ni aya, kwa nini Umar b. Khattab aacha kuiandika kwa kuogopa watu, asimwogope Mola wake? Kwa nini ikawa haimo katika hii Qur’ani tuliyonayo sisi hii leo? Na kama si aya, kwa nini Umar b. Khattab atamani kuiandika lakini aiacha kwa kuogopa watu? Kwa nini atamani kuiandika aya katika Qur’ani ambayo haikuteremshwa na Mwenyezi Mungu? Na jee, Hadith kama hizo zinakwacha na fikira gani, ewe ndugu yangu? 6.
Ukitazama tena Sahih Bukhari, Mlango wa ‘Wamaa Khalakadh Dhakara Wal Unthaa’ katika ‘Kitabut Tafsir’ (au, katika tafsiri yaka ya Kiingereza, Hadith Na. 468 iliyoko kwenye ukurasa 441-442 wa Juzuu ya Sita) utaona kwamba Alqama alikiisoma Sura 92:3 sio kama tunavyoisoma sisi leo, wala sio kama ilivyo misahafuni mwetu, bali hivi: Wadh dhakari Wal Unthaa! Kisha akasema: ‘Ninashuhudia kwamba nimesikia Mtume (s.a.w) akisoma hivi. Na hawa (yaani baadhi ya masahaba) wananitaka nisome: Wamaa Khalaqadh dhakara wa unthaa. Naapa kwa Mwenyezi Mungu! Sitawafuata.’
Jee, kwa mujibu wa Hadith hiyo, si wazi kwamba neno wamaa khalaqa, lililomo katika misahafu yetu yote, limeongezwa katika hiyo Sura 92:3? Kisha tazama hapo jinsi Alqama anavyoapa kuwa hivyo ndivyo alivyokimsikia Mtume (s.a.w) akisoma, na kwamba hatawafuata hao watu wengine waliokimtaka asisome hivyo. Hapa ni vyema tujue kwamba si Alqama peke yake aliyesema hivyo; bali ukiitazama Hadith nyingine iliyoitangulia hiyo tuliyoitaja hapo juu (Hadith Na. 467) utamwona Abud Dardaa asema kwamba na yeye pia alikimsikia Mtume (s.a.w) akiisoma aya hiyo kama alivyosikiwa na Alqama. Lakini naye pia akakataliwa! 35
SHIA NA QUR’ANI
7.
Ukija kwenye al-Itqan Fii Ulumil Qur’an ya Imam Suyuti (uk. 33 wa Juzuu ya Pili, chapa ya nne iliyochapishwa 1398H) utaona imeandikwa kwamba Abu Sufyan al-Kala’i amesema kwamba Muslima b. Mukhallad al-Ansari aliwaambia siku moja: ‘Hebu nielezeni habari ya zile aya mbili za Qur’ani ambazo hazikuandikwa msahafuni! Hakuna aliyemweleza japokuwa Abul Kanud Sa’d b. Malik alikuwapo hapo. Basi Ibn Muslima akasoma:
َ إِ َّن الَّ ِذ َ ين آ َمنُوا َو َه ِيل اهلل ِ اج ُروا َو َج ِ اه ُدوا ِفي َس ِب َ ْش ُروا أَ ْنتُ ُم ْال ُم ْفلِ ُح ،ون ِ ِبأَ ْم َوالِ ِه ْم َوأَ ْن ُف ِس ِه ْم أَ اَل أَب ُ ص ُر ُ ين آ ُو َ َوالَّ ِذ وه ْم َو َجا َدلُوا َع ْن ُه ُم ْال َق ْو َم َ وه ْم َو َن َ َُّين َغ ِ لله َ ْه ْم أُولَِئ َك َ الَّ ِذ س َما ٌ ال َتعْلَ ُم َن ْف ِ ض َب ا َعلي َأُ ْخ ِفي لَ ُه ْم ِم ْن ُق َّر ِة أ َ ُُن َج َزا ًء ِب َما َكانُوا َي ْع َمل ْ ون ي ع َ ٍ Jee? Leo waweza kuzipata aya hizo, hivyo zilivyo, katika misahafu tulionayo? Bila shaka huzipati! Zilizo karibu sana nazo ni Sura 8:72 na 9:20 na 32:17. Hebu zilinganishe uone jinsi zinvyotofautiana! Jee, bado Sheikh M. al-Khatib na wenye fikira kama zake wanashikilia kuwa Shia peke yao ndio wenye Hadith za kuonyesha kuwa Qur’ani imepungua?
36
SHIA NA QUR’ANI
Zaidi ya hizo Mpaka hapa tumetaja Hadith chache tu zinazozungumzia kupungua aya mbili tatu katika Qur’ani. Sasa tuangalie zile zinazozungumzia kupungua sehemu kubwa kubwa: 8.
Ukiiangali al-Itqan, Uk. 32 wa hiyo hiyo Juzuu ya Pili, utaona kwamba imepokewa kwa Mwana Aisha kwamba amesema: ‘Sura al-Ahzab ilikuwa ikisomwa zama za Mtume (s.a.w) aya 200 (mia mbili). Lakini Uthman alipoandika misahafu, hatukupata isipokuwa hivi ilivyo sasa!’ Na hivi sasa, ilivyo katika misahafu yote tuliyonayo, ni aya 73 (sabini na tatu). Jee, kama Sheikh M, al-Khatib, au wale wenye fikira kama zake, wataulizwa ziko wapi aya 127 zilizopungua, watajibuje?
9.
Isitoshe! Katika hiyo hiyo al-Itqan, ukurasa huo huo wa 32, na mara tu baada ya Hadith tuliyoitaja hapo juu, imeandikwa kwamba Dharr b. Hubaysh aliulizwa na Ubayy b. Ka’b: ‘Sura al-Ahzab ina aya ngapi?’ Akajibu: ‘Aya sabini na mbili au sabini na tatu.’ Ubayy akasema: ‘Japokuwa ilikuwa sawa na Sura al-Baqarah – au zaidi yake!’
Haya! Sura al-Baqarah, Kama tujuavyo, ina aya 286. Jee tukishazitoa hizo aya 73 zilizomo misahafuni mwetu, hizo 213 zilizobaki zimepotelea wapi? Jee, utalinganishaje kutokuwamo aya saba za Sura al-Wilaya katika Qur’ani na hizo 213 za Sura al-Azhab? Hadith tuliyoitaja hapo juu vile vile waweza kuipata katika Muntakhab Kanzil Ummal iliyoko pambizoni mwa Musnad Ahmad. Juzuu ya Pili, uk.1. 37
SHIA NA QUR’ANI
10. Tukija kwenye Sura Bara’ah, ambayo ina aya 129 katika misahafu tuliyonayo, twaambiwa la! Ni sawa na Sura alBaqarah, yenye aya 286! (taz. uk. 80 wa Juzuu ya Kwanza ya al-Itqan). Jee tusemeje? Hizo aya 157 zilizopungua zimekwenda wapi? 11. Bali na zaidi ya hayo! Katika hiyo hiyo al-Itqan, uk. 34 wa Juzuu ya Pili, twaambiwa kwamba imepokewa wa Hudhayfa (katika al-Mustadrak) kwamba hii Sura Bara’rah tunayoisoma ni roboo yake! Kutokana na Hadith hiyo, kwa hivyo, robo tatu hazijulikani ziliko! Na hizo ni aya 387! Jee, Sheikh M. al-Khattab atatwambiaje? Hadith hiyo vile vile unaweza kuiona katika uk. 31 wa Juzuu ya Saba ya Majmauz Zawaid ambamo imesemwa kwamba wapokezi wake ni thuqaat (wa kutegemeka). 12. Zaidi ya yote hayo: kwa mujibu wa Umar b. Khattab, kama ilivyonakiliwa katika uk. 93 wa Juzuu ya Kwanza ya alItqan, Qur’ani ina herufi 1,027,000 (millioni moja na elfu ishirini na saba). Na kama hivyo imeelezwa katika uk. 517 wa Juzuu ya Kwanza ya Kanzul Ummal (Hadith Na. 2308). Lakini lijulikano ni kwamba idadi ya ya herufi za Qur’ani ni thuluthi (sehemu moja ya tatu) tu ya idadi hiyo! Hii, kwa hivyo, ina maana kwamba idadi ya herufi ambayo ni sawa na misahafu miwili kama huu tulionao imepotea; haijulikanj ilipo! Kwa maneno mengine, Qur’ani anayokusudia Umar b. Khattab ni mara tatu ya Qur’ani tuliyonayo. Kwa hivi sasa sisi tuna thuluthi moja tu! Tafadhali linganisha msahafu huo na ule wa Mwana Fatima ambao Sheikh M. al-Khattab alitutajia katika uk. 9 wa kitabu chake, na 38
SHIA NA QUR’ANI
majibu yetu yaliyomo humu ukurasa 18. Jee, wenye Qur’ani iliyo mara tatu ya hii tuliyonayo ni Shia au Sunni?
Bali makubwa zaidi Mpaka hapa tumezitaja Hadith zinazotufahamisha ni aya ngapi zilizopungua, kutokana na vitabu vya Kisunni. Lakini pia kuna zenye habari kubwa zaidi; za kutojulikana ni aya ngapi zilizopotea. Kwa mfano: 13. Ukiangalia al-Itqan (Juzuu ya Pili, uk. 32) utaona imeandikwa kwamba imepokewa kwa Nafi’ kwamba Ibn Umar amesema: ‘Huenda mmoja wenu akasema kwamba ameichukua Qur’ani yote, lakini ni nini kitakachomjulisha hiyo yote ni ipi? (Ukweli ni kwamba) Qur’ani nyingi imetoweka. Lakini naseme: Nimechukua ile sehemu iliyodhihiri.’ Ewe ndugu msomaji! Hebu isome tena riwaya hiyo, na uitafakari. Utaona kwamba Ibn Umar alikizuia watu wasiseme kwamba wameichukua Qur’ani yote. Maana hakuna anayeijua Qur’ani yote. Kwa hivyo mtu aseme tu kwamba aliyoichukua yeye ni ile aliyoipata! Jee, hiyo ambayo haikupatikana ni kadiri gani? 14. Mbali ile sehemu iliyoliwa na mnyama wa kufugwa, na isipatikane! Ukitazama Musnad Ahmad (Juzuu ya Sita, uk. 269) utaona kwamba Mwana Aisha amesema kwamba ukurasa uliokuwa chini ya kitanda chake, uliliwa na mnyama wa kufugwa; na kwamba kitendo hicho kilitendeka pale alipokufa Mtume (s.a.w) ambapo kina Mwana Aisha walikuwa wameshughulika na kifo chake. 39
SHIA NA QUR’ANI
Kwa hivyo, kutokana na riwaya hiyo, ni wazi kwamba hiyo aya ya rajm, na hiyo ya kumnyonyesha mtu mzima mara kumi, zilikuwamo katika huo ukurasa ulioliwa na mnyama huyo. Swali lililopo hapa ni: Sasa aya hizo ziko wapi? Mbona hazimo katika hii misahafu tuliyonayo? Kama Mwana Aisha amesema kwamba aya hizo zilikuwamo katika ukurasa huo hadi Mtume (s.a.w) alipofariki dunia, ni nani huyo aliyezitoa baada ya Mtume (s.a.w) kufariki? Kwa idhini ya nani? 15. Mwisho ni swala la misahafu ya masahaba. Katika uk. 9 wa kitabu chake hicho, Sheikh M. al-Khatib ametaja ‘msahafu wa Fatima. Lakini hakukumbuka kwamba vile vile kulikuwa na misahafu ya masahaba ni aya za Qur’ani. Na humo waziona aya ambazo, zilivyoandikwa humo, sivyo zilivyoandikwa katika hii misahafu tuliyonayo! Jee? Ipi ndiyo sahihi? Misahafu ya hao mashaba, au hii tuliyonayo? Kwa wale wanaojua Kiarabu, nawatazame kitabu kiitwacho alMasahif cha Abu Dawud, watayaona hayo tunayoyasema.
Mwisho Ewe ndugu msomaji! Hizo ni baadhi tu ya Hadith zilizomo katika vitabu vya Kisunni. Zote, kama inavyoonekana, zinaonyesha kwamba Qur’ani Tukufu imepungua! Sikuzinakili Hadith hizo kwa kuwa ninazikubali; hasha! Mimi sizikubali, wala Mwislamu yeyote hawezi kuzikubali, kwa sababu zinapingana na Qur’ani (Sura 15:9 na 41:41-42). Nimezinakili tu ili kuonyesha kwamba, kama vile ambavyo katika vitabu vya Kishia hupatikana Hadith ziwezazo kueleweka 40
SHIA NA QUR’ANI
kwamba Qur’ani imezidi au imepungua, kadhalika Hadith kama hizo hupatikana katika vitabu vya Kisunni. Kwa hivyo, kama, Sunni atakuwa na haki ya kumshutumu Shia kwamba ana Qur’ani isiyokuwa hii tuliyonayo, Shia naye - kwa hoja hiyo hiyo – atakuwa na haki kama hiyo dhidi ya Sunni. Kutokana na yote yaliyotangulia, itaonekana kwamba Qur’ani inayoaminiwa na Shia ndiyo ile ile inayoaminiwa wa Sunni – chapa kwa ya pili. Kwa hivyo, katika hilo, ndugu wawili hao hawana la kugombania. Inshallah, katika kitabu kijacho, tutatazama msimamo wa Shia juu ya Hadith za Mtume Muhammad (s.a.w).
41
SHIA NA QUR’ANI
ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1. Qur’an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thelathini 2.
Uharamisho wa Riba
3.
Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza
4.
Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili
5.
Hekaya za Bahlul
6.
Muhanga wa Imamu Husein (A.S.)
7.
Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.)
8.
Hijab vazi Bora
9.
Ukweli wa Shia Ithnaashari
10. Madhambi Makuu 11. Mbingu imenikirimu 12. Abdallah Ibn Saba 13. Khadijatul Kubra 14. Utumwa 15. Umakini katika Swala 16. Misingi ya Maarifa 17. Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia 42
SHIA NA QUR’ANI
18. Bilal wa Afrika 19. Abudharr 20. Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu 21. Salman Farsi 22. Ammar Yasir 23. Qur’an na Hadithi 24. Elimu ya Nafsi 25. Yajue Madhehebu ya Shia 26. Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur’an Tukufu 27. Al-Wahda 28. Ponyo kutoka katika Qur’an 29. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii 30. Mashukio ya Akhera 31. Al Amali 32. Dua Indal Ahlul Bayt 33. Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. 34. Haki za wanawake katika Uislamu 35. Mwenyezi Mungu na sifa zake 36. Kumswalia Mtume (s) 37. Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) 38. Adhana 39
Upendo katika Ukristo na Uislamu 43
SHIA NA QUR’ANI
40. Tiba ya Maradhi ya Kimaadili 41. Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu 42. Kupaka juu ya khofu 43. Kukusanya swala mbili 44. Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara 45. Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya 46. Kusujudu juu ya udongo 47. Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) 48. Tarawehe 49. Malumbano baina ya Sunni na Shia 50. Kupunguza Swala safarini 51. Kufungua safarini 52. Umaasumu wa Manabii 53. Qur’an inatoa changamoto 54. as-Salaatu Khayrun Mina -’n Nawm 55. Uadilifu wa Masahaba 56. Dua e Kumayl 57. Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu 58. Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake 59. Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata 60. Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mtume Muhammad (s)
44
SHIA NA QUR’ANI
61. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza 62. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili 63. Kuzuru Makaburi 64. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza 65. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili 66. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu 67. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne 68. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano 69. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita 70. Tujifunze Misingi Ya Dini 71. Sala ni Nguzo ya Dini 72. Mikesha Ya Peshawar 73. Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu 74. Ubora wa Imam ‘Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliyonyooka 75. Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake 76. Liqaa-u-llaah 77. Muhammad (s) Mtume wa Allah 78. Amani na Jihadi Katika Uislamu 79. Uislamu Ulienea Vipi? 80. Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) 81. Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s)
45
SHIA NA QUR’ANI
82. Urejeo (al-Raja’a ) 83. Mazingira 84. Utokezo (al - Badau) 85. Hukumu ya kujenga juu ya makaburi 86. Swala ya maiti na kumlilia maiti 87. Uislamu na Uwingi wa Dini 88. Mtoto mwema 89. Adabu za Sokoni 90. Johari za hekima kwa vijana 91. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza 92. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili 93. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu 94. Tawasali 95. Imam Mahdi katika Usunni na Ushia 96. Hukumu za Mgonjwa 97. Sadaka yenye kuendelea 98. Msahafu wa Imam Ali 99. Ngano ya kwamba Qur’ani imebadilishwa 100. Idi Al-Ghadir 101. Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu 102 Hukumu zinazomhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi 103. Huduma ya Afya katika Uislamu 46
SHIA NA QUR’ANI
104. Sunan an-Nabii 105. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) 106. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) 107. Shahiid Mfiadini 108. Kumsalia Nabii (s.a.w) 109. Ujumbe -Sehemu ya Kwanza 110. Ujumbe - Sehemu ya Pili 111. Ujumbe - Sehemu ya Tatu 112. Ujumbe - Sehemu ya Nne 113. Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu 114. Hadithi ya Thaqalain 115. Ndoa ya Mutaa 116. Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza 117. Ukweli uliopotea sehemu ya Pili 118. Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu 119. Ukweli uliopotea sehemu ya Nne 120. Ukweli uliopotea sehemu ya Tano 121. Mkutano wa Maulamaa wa Baghdad 122. Safari ya kuifuata Nuru 123. Fatima al-Zahra 124. Myahudi wa Kimataifa 125. Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi 47
SHIA NA QUR’ANI
126. Visa vya kweli sehemu ya Kwanza 127. Visa vya kweli sehemu ya Pili 128. Elimu ya Ghaibu ya Maimamu 129. Mwanadamu na Mustakabali wake 130. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) 131. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) 132. Khairul Bariyyah 133. Uislamu na mafunzo ya kimalezi 134. Vijana ni Hazina ya Uislamu 135. Yafaayo kijamii 136. Tabaruku 137. Taqiyya 138. Vikao vya furaha 139. Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 140. Visa vya wachamungu 141. Falsafa ya Dini 142. Azadari-Kuhuzunika na Kuomboleza 143. Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah 144. Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu 145. Kuonekana kwa Allah 146. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) 48
SHIA NA QUR’ANI
147. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) 148. Ndugu na Jirani 149. Ushia ndani ya Usunni 150. Maswali na Majibu 151. Mafunzo ya hukmu za ibada 152. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1 153 Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2 154. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 155. Abu Huraira 156. Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. 157. Mazingatio kutoka katika Qur’an - Sehemu ya Kwanza 158. Mazingatio kutoka kaitka Qur’an - Sehemu ya Pili 159. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza 160. Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili 161. Qur’ani Tukufu – Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili 162. Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) 163. Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani 164. Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu 165. Uislamu Safi 166. Majlisi za Imam Husein Majumbani 167. Je, Kufunga Mikono 168. Uislam wa Shia 49
SHIA NA QUR’ANI
169. Amali za Makka 170. Amali za Madina 171. Asili ya Madhehebu katika Uislamu 172. Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi 173. Ukweli uliofichika katika neno la Allah 174. Uislamu na Mifumo ya Uchumi 175. Umoja wa Kiislamu na Furaha 176. Mas’ala ya Kifiqhi 177. Jifunze kusoma Qur’ani 178. As-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah 179. Hayya ‘Alaa Khayri’l-’Amal Katika Adhana 180. Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura 181. Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na Ramadhani) 182. Uadilifu katika Uislamu 183. Mahdi katika Sunna 184. Maswali Ya Uchunguzi Kuhusu Uislam 185. Kazi na Bidii ni njia ya maendeleo 186. Abu Talib – Jabali Imara la Imani 187. Ujenzi na Utakaso wa Nafsi 188. Vijana na Matarajio ya Baadaye 189. Usalafi – Historia yake, maana yake na lengo lake
50
SHIA NA QUR’ANI
190. Ushia – Hoja na Majibu 191. Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) 192. Maombolezo – Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) 193. Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu 194. Takwa 195. Upotoshaji dhahiri katika Turathi (Hazina) ya Kiislamu 196. Amirul Muuminina (‘as) na Makhalifa 197. Uongozi na Utawala katika Mwenendo wa Imam ‘Ali (‘a) 198. Kuvunja hoja iliyotumika kutetea Uimamu wa AbuBakr 199. Adabu za vikao na mazungumzo 200. Hija ya Kuaga 201. Uwazi baina ya Maslahi na Vikwazo 202. Fadhila za watukufu watano katika Sahih Sita 203. Mdahalo baina ya Mwanachuoni wa Kisunni na Mwanachuoni wa Kishia (Al Muraja’aat) 204. Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (as) 205. Mjadala wa Kiitikadi 206. Mtazamo kuhusu msuguano wa Kimadhehebu 207. Nchi na Uraia – Haki na wajibu kwa Taifa 208. Mtazamo wa Ibn Taymiyyah juu ya Imam Ali (as) 209. Uongozi wa Kidini – Maelekezo na Utekelezaji wa Kijamii
51
SHIA NA QUR’ANI
210. Maadili ya Ashura 211. Mshumaa – Shahidi na Kifo cha Kishahidi 212. Mizani ya Hekima – Hadithi za Ahlul Bait (as) – Sehemu ya Kwanza 213. Imam Ali na Mambo ya Umma 214. Imam Ali na Mfumo wa Usawa 215. Mwanamke na Sharia 216. Mfumo wa Wilaya 217. Vipi Tutaishinda Hofu? 218. Kumswalia Mtume ni Ufunguo wa Utatuzi wa Matatizo 219. Mahali na Mali za Umma 220. Nahjul-Balagha – Majmua ya Khutba, Amri, Barua, Risala, Mawaidha na Semi za Amirul-Muuminin Ali bin Abu Talib (a.s.) 221. Mukhtar – Shujaa aliyelipiza kisasi dhidi ya wauaji wa Imam Husein (as) hapo Karbala 222. Uimamu na Tamko la Kutawazwa 223. Imam Husain ni Mfumo wa Marekebisho na Mageuzi 224. Saada Kamili – Kitabu cha Kiada cha Maadili 225. Maeneo ya Umma na Mali Zake 226. Imam Hasan na Mfumo wa Kujenga Jamii 227. Adhana ni Ndoto au ni Wahyi? 228. Maimamu wa Ahlul Bait – Ujumbe na Jihadi 52
SHIA NA QUR’ANI
229. Qur’ani na Kuhifadhiwa Kwake 230. Shia na Qur’ani – Majibu na Maelezo
53
SHIA NA QUR’ANI
KOPI NNE ZIFUATAZO ZIMETAFSIRIWA KWA LUGHA KINYARWANDA 1.
Amateka Na Aba’Khalifa
2.
Nyuma yaho naje kuyoboka
3.
Amavu n’amavuko by’ubushiya
4.
Shiya na Hadithi
54
SHIA NA QUR’ANI
ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION KWA LUGHA YA KIFARANSA 1.
Livre Islamique
55