Shia na vyombo vya habari

Page 1

SHIA NA VYOMBO VYA HABARI ‫الشيعة ووسابل إلاعالم‬

Kimeandikwa na: Sheikh Ja’far Subhani

Kimetarjumiwa na: Amiri Mussa


‫الشيعة و وسابل إلاعالم‬

‫تأليف‬ ‫الشيخ جعفر السبحاني‬

‫من اللغة العربية إلى اللغة السواحلية‬


©Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 – 9987 – 17 – 002 – 9 Kimeandikwa na: Sheikh Ja‟far Subhani Kimetarjumiwa na: Ustadh Amiri Mussa Kimehaririwa na: Ustadh Hemedi Lubumba Kimesomwa Prufu na: Al-Haji Ramadhani S. K. Shemahimbo Kimepitiwa na: Al Haji Mujahid Rashid Kimepangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation Tole la kwanza: Novemba, 2017 Nakala: 2,000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Al-Itrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.alitrah.info Vitabu mtandaoni: www.alitrah.info/ebooks/ ILI KUSOMA QUR‟ANI MUBASHARA KWA NJIA YA MTANDAO, TEMBELEA www.somaquran.com


YALIYOMO Dibaji…………………………………………...

8

Neno la Mchapishaji…………………………… 9 Utangulizi………………………………………

17

Hukumu ya Swala katika Misikiti ya Shi‟a……

19

Hukumu ya ujengaji misikiti juu ya makaburi ya mawalii………………………………….

21

Namna ya utoaji wa Dalili……………………... 24 Utekelezaji Usiotakiwa Kusemwa……………..

27

Taawili Isiyokubalika ya Albaani……………...

30

Udunishaji wa Ahlul-Bayt  na Tabiina…….. 33 Uchambuzi juu ya Dalili za Wazuiaji....……….

38

Uwepo wa Misikiti katika sehemu za Mashahidi, hakuna mahusiano yoyote na Hadithi Hizo..................................................

50

Vipande vitatu katika maneno ya Uthmani Khamis......................………………………

51

Ukosoaji na Urekebishaji sio Kutukana ………

64


UKOSOAJI WA NADHARIA YA UTHMANI KHAMIS KATIKA UOMBAJI MSAADA NA TAWASULI

67

Maneno ya Sheikh Kuhusiana na Tawasuli …..

84

Uombaji wao wa Mvua kupitia kwa Abbasi; Baba mdogo wa Mtume  ………………..

92

MIRATHI YA MTUME  NA MAOMBI YA FATIMAH ZAHRA I JUU YA FADAK

102

Kwa nini Mtume  hakumfundisha Fatimah hukumu ya mirathi yake?........

102

Anajibiwa hilo kwa mambo mawili:...................

109

Barua Ya Maamun Abbas Hadi Kwa Qatham Bin Ja‟far Gavana Wake Katika Mji Wa Madina: ……………………………………. 113 Ukosoaji wa maneno ya Aluusi........................... 125 PAMOJA NA UTHMAN KHAMIIS KATIKA MAJIBU YAKE JUU YA SHI‟AH KUHUSIANA NA MADHUMUNI YA HADITHI YA KISHAMIYA

133


Jambo la Kwanza: Shi‟ah na Hadithi ya Kishamiya: …………...................................

136

Jambo la Pili: Hadithi ya Kishamiya haiwahusu Ahlul-Bayt  tu: ……………………….... 140 Kundi la Kwanza: Kutaja kinaga ubaga majina yao:…………………………………………

142

Kundi la Pili: Kuwaingiza hao katika Kishamiya:……………………....................

144

Kundi la Tatu: Kuwaainisha hao kwa Usomaji wa aya Mlangoni Kwao: ……………………… 145 Jambo la Tatu: Hadithi ya Kishamiya haiwahusishi Maimamu waliobaki miongoni mwa watoto wa Husein …….

149

Jambo la Nne: Hadithi ya Kishamiya na Umaasumu wa Maimamu 

151

1. Ushangaaji wa Uthmani Khamiis kuhusiana na kuwanasibisha Shi‟ah katika tawasuli ya Mtume :………………………………….

152

1. Shi‟ah na uchukuaji wa hadithi za AhlusSunnah:…………………………………….. 154 Mzaha wa Sheikh mwishoni mwa maneno yake: ……………………………………….

155

KISIMAMO KINGINE NA SHEIKH UTHMANI KHAMIIS Sheikh na Ukufurishaji wa Yazid …..................

157 157


Shi‟ah na Upotoshwaji wa Qur‟ani ……………

161

UTOKEZO NI UHAKIKA WA QUR‟ANI

165

Uhakika wa utokezo……………………………

168

Athari ya wale wenye kuamini utokezo……….

174

Matukio ambayo Mwenyezi Mungu (s.w.t) Amedokeza Kwayo.......................................

176

Nini maana ya: “Mwenyezi Mungu ametokewa" katika hadithi ya Mtume ?..............

181

Watu ni maadui kwa wasilolijua……………….

188


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬

DIBAJI Kitabu hiki ni toleo la Kiswahili la taasisi ya Al Itrah Foundation. Chapisho lake limelenga kukidhi mahitaji ya kiroho ya zama hizi pamoja na Ubongo na fikra zinazokuwa za Muislam. Jitihada kubwa zimefanywa na Taasisi kuweka chapisho hili la Kiswahili katika msingi wa haki na wenye kukubalika katika Uislam. Unaombwa kwa Taadhima ukisome kitabu hiki katika malengo yaliyokusudiwa. Pia Unaombwa kuwasilisha kwetu maoni yako huru juu ya chapisho letu hili, jambo ambalo tutashukuru sana. Kutangaza ujumbe wa Uislam ni kazi ambayo inahitaji ushirikiano wetu sote. Taasisi inakuomba kuungana na kushirikiana kama ilivyoagizwa katika aya ya Qur‟an: (Surat Saba‟ 34:46). Na rehma za Allah ziwe juu yako. Wako katika Uislam Al Itrah Foundation Barua Pepe: alitrah@yahoo.com SMS: +255 778 300 140 8


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬ NENO LA MCHAPISHAJI Kitabu ulichonacho mikononi mwako kimetarjumiwa kutoka kitabu cha Kiarabu kwa jina la, ash-Shi‟ah wa Wasa‟ilu „l-I‟lam, kilichoandikwa na Allamah Mhakiki Sheikh Ja'far Subhani. Sisi tumekiita, Shia na Vyombo vya Habari. Hiki ni kitabu kizuri na kinafaa sana kusomwa ili kujua ukweli wa mambo. Katika miaka ya hivi karibuni yamezuka makundi ambayo kazi yao ni kuwafarakisha Waislamu na kuwakufurisha wale wote ambao hawafuati itikadi yao na hatimaye kumwaga damu zao kwa madai kwamba ni makafiri. Kutokana na itikadi yao hiyo hakuna madhehebu iliyosalimika. Kwao Sunni, Shia na Ibadhi ambazo ndizo madhehebu kubwa za awali katika Kiislamu ni potofu na za kikafiri. Kwa kueneza itikadi yao hii wameanzisha vyombo vya habari sehemu mbalimbali ulimwenguni na kutumia vituo hivyo vya habari kueneza itikadi yao hiyo potofu. Kutokana na propaganda yao hii mwanachuoni maarufu, Sheikh Ja‟far Subhani, ameandika kitabu hiki ili kuikosoa itikadi hii potofu kwa kuelemisha 9


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Umma juu ya hatari ya itikadi hii katika jamii yote ya wanadamu. Allah Mwenyezi anasema: “Hakika zimepita desturi nyingi kabla yenu; basi tembeeni katika nchi na muone ilikuwaje mwisho wa wale waliokadhibisha. Huu ni ubainifu kwa watu na mwongozo na mawaidha kwa wenye takua.” (3:137138) Hapa itoshe tu kunukuu utangulizi ulioandikwa na Sayyid Murtadha al-Ridhwi katika tarjumi ya Kiswahili ya kitabu chake kiitwacho, al-Wahda (Umoja wa Waislamu): “Kwa kipindi kirefu kilichopita moto wa chuki umechochewa baina ya Waislamu ili kuleta hitilafu kati yao, na hilo ni kwa kuwashughulisha na tofauti ndogondogo kwanza, ndipo wenye roho dhaifu wakanunuliwa na kuzitumia kalamu zao kuvunja umoja wa Kiislamu, wakadhaniana vibaya Waislamu wenyewe kwa wenyewe hata kufikia kukufurishana na kumwaga damu zao. “Bado akili hazijasahau mauaji na fitina zilizotokea kati ya Shia na Sunni nchini Iraq na Afrika ya Kaskazini katika enzi ya utawala wa Bani Abbas mpaka kuishia kwa dola ya Fatimiya. 10


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

“„Je, siwaambii wale waliohasirika? Hao ni wale ambao amali zao zimepotea katika maisha ya duniani na wao wanadhani kuwa wanafanya mema.‟ Yote hayo ni kwa sababu ya upotoshaji wa habari kutoka kwa wale wanaonufaika na mfarakano wa Waislamu.” Mfano wa wanavyuoni hao wamekuwa kama kasuku wanakariri kile wanachoambiwa na mawakala wa utawala bila ya kuhakikisha au kuchunguza, na wanasahau kwamba yale wanayoandika hayaendi na wakati wa sasa ambao haukubali jambo kiholela tu bila ya kuthibiti ukweli wake. Ukweli wa hayo niyanenayo umekusanywa na Sayyid Murtadha alRidhwi aliyejitolea nafsi yake kwa bidii zote ili kuueneza ukweli wa Kiislamu, kuhakikisha umoja na kuunganisha Waislamu. Na haya tuyasomayo katika kitabu hiki ni natija ya juhudi za wanavyuoni katika kupekua, kuchunguza na kusoma vitabu vikubwa, ndipo kwa kuamua kusema ukweli kwa ushujaa wote na wakayaeneza ili wengine pia waelimike, huenda nyoyo zikakaribiana, ukaondoka na uchafu, na Umma wa Kiislamu kurudi kama ulivyokuwa mwanzo Umma bora ulioletwa kwa watu kama alivyosema Allah Mwenyezi: “Hakika umma wenu huu ni umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu, kwa hivyo niabuduni.” (21:92) 11


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Basi maji na yarudi kwenye mapitio yake, na ndugu wa Kiislamu wapeane mikono Mashariki na Magharibi mwa dunia na waungane katika kuondoa tofauti za zamani, wafungue ukurasa mpya - suluhusheni baina ya ndugu zenu, ili wavishinde vitimbi vya maadui. Vilevile mtazamo mmoja tu wa maneno ya wanavyuoni hao (yaliyomo kitabuni humu) yanayotokana na nasaha za Mwenyezi Mungu na Mtume wake (s.a.w.), unatosha kutambua hakika inayowapasa Waislamu wote waijue. “Hakika katika hayo kuna ukumbusho kwa mwenye moyo au akatega sikio naye ni shahidi.� (50:37) Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa makubwa hususan wakati huu wa sayansi na tekinolojia kubwa ambapo ngano, hadithi za kale na upotoshaji wa historia ni vitu ambavyo kwa sasa havina nafasi katika akili za watu. Taasisi yetu ya Al-Itrah imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili. Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni chenye manufaa makubwa kwao. 12


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Tunamshukuru ndugu yetu Sheikh Amiri Mussa kwa kufanikisha tarjuma ya kitabu hiki katika lugha ya Kiswahili, pia na wale wote waliosaidia kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha chapisho la toleo hili kuchapishwa na kuwa mikononi mwa wasomaji. Allah Mwenye kujazi awalipe wote malipo mema hapa duniani na huko Akhera pia. Amin!

Mchapishaji: Al-Itrah Foundation

13


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

 ‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬ Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu. Kwajina la Mwenyezi Mungu mwenye kuneemesha neema kubwa kubwa na neema ndogo ndogo. Sifa zote zinamstahili Mwenyezi Mungu, Mola wa viumbe wote, na rehema na amani zimfikie mbora wa viumbe wote, na mtakatifu wa viumbe wote, Nabii Muhammad na watu wake walio wasafi waliotakasika. Haifichiki ya kwamba hakika vyombo vya habari vina faida nyingi sana katika kueneza elimu na tamaduni na tabia, na ni mfano uliotukuka katika kuwalingania watu katika kuishi salama na kusaidiana kati ya mataifa na kuungana juu ya kutatua matatizo. Lakini mkabala na hayo, watu wenye malengo mabaya wanavitumia vyombo vya habari kama nyenzo ya kueneza fitna na kueneza fikra zenye sumu katika jamii, na kuwaingiza watu katika magomvi na mizozo. Hakuna shaka hakika anayetaka kutengeneza hufuata jambo la kwanza, lakini anayetaka kubomoa hufuata njia ya pili. Na wale wanaojishabihisha na wasomi wenye heshima na maarifa, ambao wamejitokeza katika ukumbi wa Kiislamu katika zama za mwisho, tunawashuhudia wakiweka juhudi zao kwa ajili ya kugombanisha na kuleta matatizo katika jamii ya Kiislamu katika njia hii, kana kwamba 14


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

hawana jambo lolote la muhimu isipokuwa kuleta chuki katika jamii. Na miongoni mwao katika njia ya mfano ni Sheikh Uthman Khamisi na anayepita pamoja naye katika njia hii yenye giza katika wandishi wa vitabu wa sasa, ambao wamenyanyua bendera ya vurugu ili waubomoe umma mmoja na kuusambaratisha kwa kuzingatia sehemu moja ya umma ni ya Kiislamu na nyingine ni ya kikafiri. Na wakati tulipoona kwamba uwanja huu wameachiwa wao, wanazunguka ndani yake na wanafanya kama wanavyotaka, tukagundua kuwa hiyo ndio nguvu yao na ni kuficha haki na kueneza uwongo, hivyo tulifuata kauli ya Mtume Muhammad rehema na amani ziwe juu yake, pale aliposema: “Utakapodhihiri uzushi ni juu ya msomi aidhihirishe elimu yake.� Na kwa ajili hiyo tumesimama kukosoa mihadhara yao wanayoieneza kupitia vyombo vya habari, na maneno yao wanayoyaweka na kuyasambaza kupitia Intaneti. Tumeamua kukosoa kwa uhalisia kwa kujiepusha mbali kabisa na vigezo vya tuhuma vya uwongo na uzushi dhalili, kinyume na wafanyavyo wao. Na sisi tunawasilisha sehemu ya kwanza ya majibu, ambamo ndani yake tutamjadili Khamisi kupitia mihadhara na maneno yake. Huenda kazi hii ikawa ni yenye manufaa kwa Waislamu wanaofahamu na wan15


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

aoizamisha batili, wale wanaoidhihirisha haki na hakika. Na Mwenyezi Mungu ndiye aliye nyuma ya makusudio yetu. Jaâ€&#x;fari Subhani.

16


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬ UTANGULIZI Sifa zote zinamstahiki Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mola wa viumbe vyote. Na rehema na amani zimfikie Mtume Muhammad , mwisho wa Mitume. Zimfikie yeye na watu wa nyumba yake waliotwaharika waliotakasika, na pia maswahaba zake wema na mataabiina, radhi za Mungu ziwe juu yao. Hakika Ijtihadi ni kujipa wasaa wa kung‟amua hukumu za kisheria kupitia Qur‟ani, hadithi, Ijmai na akili yenye utambuzi, ambayo kupitia akili hiyo tumemfahamu Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na Ijtihadi si halali kwa kila anayepokea sahihi na yasiyokuwa sahihi. Na hakika anaiweza mtu aliyejaa vipaji vya fikra na fani za kielimu katika maeneo tofauti ya elimu na fani. Na hakika baadhi ya watu wameizuia kwa watu wasiovuka kumi. Na kwa ajili ya ugumu wa kupanda hadi katika daraja ya Ijtihadi tunaona hakika mafakihi wakubwa katika wanavyuoni wanamuomba Mwenyezi Mungu awaruzuku Ijitihadi wakisema kwamba, ni ngumu kuliko jihadi yote. Hakika wamedhihiri katika wakati wetu wa leo, watu wanaokata na kutengua, wanaokaa wakikunja nne 17


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

katika meza ya kutoa fatwa, hali yakuwa hawana uwezo wala nguvu katika kutoa fatwa. Na kwa ajili hiyo wanaanguka mwanguko baada ya mwanguko, na wanateleza mtelezo baada ya mtelezo. Na huenda ukatulia na maneno yetu haya pale utakaposoma fatwa ya Sheikh Uthman Khamis, upande wa kuswali katika misikiti ya Shiâ€&#x;ah, na vipi alijaribu na akatoa fatwa ya kwamba harufu ya shirki inatoka ndani ya misikiti hii, na katika mambo mengine yasiyokuwa hayo yanayochukiza. Na kwa ajili ya kuweka wazi msimamo tumeanza kukosoa maneno yake kutokana na muda utakavyoruhusu, na Mungu ndiye Mwongozaji na anayewafikisha. Jaâ€&#x;far Subhani.

18


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬ HUKUMU YA SWALA KATIKA MISIKITI YA SHI‟AH Kupitia kipindi cha Liqaaul-Jumaa, kilichorushwa na Tv ya Alburhan, aliulizwa Sheikh Uthman Khamis kuhusu kuswali ndani ya misikiti ya Shi‟ah, akajibu: “Haifai kwa mwislamu kuingia ndani ya misikiti hii ili aswali ndani yake, kwa sababu misikiti hiyo haitoki nje ya maeneo ambayo mwislamu anazuiliwa kuswali ndani yake. Na mambo haya ni kama yafuatayo: 1. Hakika Shi‟ah wanapenda sana kutukuza makaburi, na hujenga misikiti juu ya makaburi hayo na pia huyaweka makaburi ndani ya misikiti, kwa maana ya kwamba huwazika maiti ndani yake, na haifai kuswali katika msikiti ambao ndani yake kuna kaburi. 2. Hakika harufu ya shirki inatoka ndani ya misikiti hii, na hutajwa humo asiyekuwa Mungu na huombwa msaada asiyekuwa Mungu, na wanamuita asiyekuwa Allah. Na wanawatukana humo vipenzi vya Allah miongoni mwa maswahaba kama khalifa wa Kiislamu. 3. Alitoa fatwa ya kielimu kwamba, kama mtu ataingia na akaswali ndani ya misikiti hii pamoja 19


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

na kujua kwake kwamba haifai, swala yake ni sahihi, lakini jambo la kwanza –nakusudia kutokufaa kuingia ndani ya miskiti hii- linabaki katika hali yake ile ile.” Haya ndiyo aliyosema Sheikh Uthman Khamis katika kipindi kinachoitwa Liqaaul-Jumaa, na hayo ameyajengea juu ya msingi anaouamini yeye, nao ni uharamu wa kujenga misikiti juu ya makaburi ya vipenzi vya Allah. Na juu ya haya amejengea yale aliyoyataja katika vipambanuzi vitatu. Na kwa ajili hiyo inatupasa sisi kusoma majengo ya maneno yake, kabla hatujaanza kuhoji vipengele vya majibu yake, na hapo kwa hakika tutakuwa tumeyakunjua maneno kwa kuyaweka wazi majengeko na yale ambayo ni haki ndani yake. Na kabla hatujasoma mada hii ya hukumu ya kujenga misikiti juu ya makaburi, tunatanguliza kitu, nacho ni kwamba, hakika Sheikh Uthman Khamis alisema: „Hakika Shi‟ah wanapendelea sana kutukuza makaburi, na hujenga misikiti juu ya makaburi, huyaweka makaburi ndani ya misikiti, yaani huwazika maiti ndani yake.‟ Sisi tunamuuliza habari hii ameipata wapi? Na hivi yeye ni mwenye kushuhudia jambo hilo katika misikiti yote ya Shi‟ah ambayo ni maelfu ya misikiti katika miji tofauti tofauti? Sidhani kama yeye amewahi kufanya utafiti juu ya jambo hilo. Pamoja na hayo, vipi ametoa hukumu hii ya pamoja? 20


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Nasema: Kila alichokitaja Sheikh katika upande huu ni uwongo ulio wazi na uzushi usiofichika. Ni uzushi unaotokana na kanuni waliojiwekea watu hawa (Mawahabi), nayo ni kwamba “Kila kitu kinahitaji dalili isipokuwa kuwazushiaShi‟ah (ndiko hakuhitaji dalili).” Lakini kila kitu kina mwisho wake isipokuwa uwongo juu ya Shi‟ah, na kana kwamba Mungu Mtakatifu amewalazimisha uwongo sehemu ya ukweli. Na kusema uwongo ni sehemu ya kutupa ukweli. Na tupitishe mjadala wa kuswihii kauli yake, na tusome hukumu ya mambo haya, nakusudia: kujenga misikiti juu ya makaburi, tuzungumzie hilo juu ya mwanga wa Qur‟ani uliotukuka na hadithi takatifu. Hukumu Ya Kujenga Misikiti Juu Ya Makaburi Ya Mawalii: Yale ambayo Sheikh ameyakanusha kuhusu kujenga misikiti juu ya makaburi ya wafu, hakika Mwenyezi Mungu Mwenye hekima ametamka kuhusiana na kufaa kwake. Na hiyo ni ikiwa wafu hao ni miongoni mwa mawalii, hivyo hakuna kizuizi chochote kuhusu kujenga msikiti juu ya makaburi yao kwa lengo la kutabaruku kupitia wao. Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema:

َ ٰ َ َ​َ َ َ َ َ َ​َ​َ ‫مش ِهم لنح ِخز َّن‬ ِ ‫َ… قال الزين غلجىا على أ‬..” َ َ ."‫سج ًذا‬ ِ ‫عل ِيهم م‬ 21


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

“Wakasema wale walioshinda katika shauri lao: Hakika tutajengamsikiti juu yao.”1 Hakika uzingatiaji katika kisa cha watu wa pangoniunafichua kwetu kwamba kujenga msikiti juu ya makaburi ya mawalii ni sunna iliyokuwa ikifuatwa na umma mbalimbali na ni sharia iliyotangulia. Na Qur‟ani tukufu inatoa ishara kuhusu sunna hiyo pasina kuipinga na kuikosoa. Hakika watu wa pangoni baada ya kugundulika habari yao, watu walitofautiana katika namna ya kuwapa thamani, kuwaheshimu na kuwatukuza hao, kwa hivyo waligawanyika makundi mawili: 1. Kundi lilisema: “Jengeni jengo juu yaoMolaWao mlezi anawajua zaidi hao.” Na uelezaji huu yaani “Mola wao mlezi anawajua zaidi hao” unafichua kwamba msemaji auwasemaji hawakuwa ni wenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu, namna ambayo walidogesha jambo lao kwa kauli yao: “Jengeni jengo juu yao, Mola wao anawajua zaidi hao” yaani Mola wetu mlezi anaijua hali yao ya heri au ya shari, wema au ubaya. 2. Na kundi lingine kulingana na msimamo wa mwisho, namna ambapo liliomba kujengwe msikiti juu ya pango ili kiwe kituo cha ibada ya Mwenyezi 1

Surat al-Kahf; 18:21.

22


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Mungu pembezoni mwa makaburi ya wale ambao walikataa ibada ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na wakatoka wakikimbia ukafiri na kuwa wakimbizi wa tawhidi ya Mwenyezi Mungu na utiifu Wake. Na hakika Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewaelezea hao kwa kauli yake: “Wakasema wale ambao walioshinda katika shauri lao: Hakika tutajenga msikiti juu yao” basi kiwakilishi katika kauli yake (s.w.t): “Wale walioshinda katika shauri lao” kinarejea kwa watu wa pangoni, yaani wamesimama juu ya cheo chao na wakaondoa pazia la uhakika wa jambo lao, wakasema: “Tutajenga msikiti juu yao.” Kwa hakika wafasiri wakubwawamekubaliana kwamba wale waliosema hilo ni wale wenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu, Twabari amesema: Washirikina wakasema: Tujenge jengo juu yao kwani hao ni watoto wa baba zetu, Waislamu wakasema: Bali sisi tuna haki zaidi juu yao, na wao wanatokana nasi, tujenge msikiti juu yao tuswali ndani yake na tumwabudu Mwenyezi Mungu humo.2 Na Raazi akasema: Na wengine wakasema: Bali kauli ya awali ya kujenga msikiti juu ya mlango wa pangoni, ni kauli inayojulisha kwamba watu hao walikuwa wenye kumjua Mwenyezi Mungu, wenye kukiri juu ya ibada na swala.3 2

Tafsiri Twabari,Juz. 15, uk. 149. Tafsiri Kashaf,Juz. 2, uk. 334.

3

23


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Na Zamakhshari amesema: “Wakasema wale walioshinda juu ya shauri lao” ni miongoni mwa Waislamu na mfalme wao walikuwa wenye kustahiki zaidi kujenga juu yao „Tujenge‟ juu ya mlango wa pango msikiti watakaoswali humo Waislamu na kutabaruku kwa sehemu yao.”4 Na Naysabuuri amesema: “Ambao walioshinda juu ya shauri lao” ni Waislamu na mfalme wao mwislamu; kwani wao walijenga juu yao msikiti Waislamu wakaswali humo, na wakitabaruku kwa sehemu yao, na walikuwa ni wenye kustahili zaidi kwao kujenga juu yao ili kuhifadhi udongo wao na zuio kwalo.5 Na yasiyokuwa hayo miongoni mwa maneno yaliyomo ndani ya vitabu vya tafsiri vya waheshimiwa. Na lile ambalo linaonekana hapa ni kwamba hakika ujengaji wa msikiti ulikuwa juu ya “mlango wa pango” au “mbele ya pango” ni tofauti ya dhahiri ya aya, hakika dhahiri yake inajulisha kwamba maoni yaliyotolewa ni juu ya ujengajiwa msikiti juu ya makaburi yao. Namna ya Utoaji wa Dalili Utoaji wa dalili kwa kutumia aya haukujengeka juu ya kukokoteza hukumu ya kisharia ya yule wa kabla 4

Tafsiri Raazi, Juz. 21, uk. 105. Gharaaibul-Qur‟an wa Gharaaibul-Furqaan, (Tafsir Naysabuuri) Juz. 7, uk. 283, chapa Maktabat Qayyimat Qairo.

5

24


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

yetu, bali umejengeka juu ya jambo lingine nalo ni kwamba sisi tunaona hakika Qur‟ani tukufu inataja maoni ya makundi mawili bila ya ukosoaji wala kujibu.Na ni vigumu sana Mwenyezi Mungu (s.w.t) kutaja maneno ya washirikina na kupita juu yake bila ukosoaji wa kijumla wala wa mapana na marefu, au bila kutaja maoni ya wenye tawhid. Na lilikuwa ni jambo la haramu katika sharia zetu pasi na haja ya kujibu hilo. Hakika ukadiriaji huu kutokana na Qur‟ani juu ya kusihi maoni ya wale ambao ni waumini, unajulisha kuwa sira na nyendo za waumini wapwekeshaji ulimwenguni kote ilikuwa ikijiri juu ya jambo hili, na ilikuwa ikizingatiwa kwao ni aina ya kumheshimu mwenye kaburi na kutabaruku kwalo. Hakika yule anayesoma Qur‟ani tukufu kwa uzingatiaji na uelewa na mwenye mwamko, anajua kwamba hakika yale anayoyanukuu kutoka kwa washirikina pale yanapokuwa ni jambo ambalo limebainishwa ubatili wake hulipita pasi na kujibu. Na ama ikiwa ubatili hauko wazi basi huwa na msimamo mwingine. Kwa mfano pale Firauni alipohisi hatari na akawa na yakini kwamba anaangamia akasema:

َ َ ٰ َ​َ َ​َ ُ َ َ ‫ءامند ِب ِه‬ ‫ءامند أّن ُه ال ِإلـ َه ِإال الزي‬ ‫… قال‬..” ُ َ ‫ٰ َ َ َ ۠ا‬ َ “‫َبنىا ِإسشءيل وأّنا ِمن اا ِل مّن‬ “Akasema: Nimeamini kwamba hakuna Mola isipokuwa yule wana25


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

yemwamini wana wa Israelinami ni miongoni mwa Waislam (walionyenyekea).”6 Basi Qur‟ani tukufu haikumwacha katika hali yake ili asije mjinga kufikiria kwamba huenda inatosha aina hii ya imani, kwa hivyo akamjibu kwa kauli yake:

ُ َ َ ُ َ ُ َ َ َ َ َ َ َ ٰ ‫ٔـ‬ َ ‫ذين‬ ‫ءال ـن وقذ ع د ق‬ ِ ‫جل ولند ِمن اا‬ “Hivi sasa! Na hali uliasi kabla yake na ukawa miongoni mwa wafisadi.”7 Hakika lengo la kutaja visa vya waliotangulia ni kuchukua mazingatio, mawaidha na tadaburi katika madhumuni yake na maana zake. Hakika Qur‟ani tukufu sio kitabu cha visa au historia inayoelezea maisha ya waliopita, hakika imeteremka kuwa katiba ya uhai wa watu, na kila mmoja anatoa fatwa kutokana na visa kwa yale ambayo yanayomfaa yeye. Basi mwana itikadi anafaidika kutokana na kisa cha watu wa pango kwa uwezekano wa ufufuo na kurudi upya maisha baada ya kupita karne kadhaa. Lakini mwanazuoni wa kifikihi anatoa hukumu anafaidika kutokana na kisa cha watu wa pango kufaa kujenga msikiti juu ya makaburi mawalii ili kutabaruku kwao. 6 7

Surat Yunus; 10:90. Surat Yunus; 10:91.

26


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Utelezaji Usiotakiwa Kusemwa: Hakika Sheikh Albaani (Mwenyezi Mungu atusamehe sisi na yeye) pindi aliposimama juu ya dalili ya wazi yenye nguvu, alijaribu kujadili katika kutoa dalili kwa lengo la kuhifadhi msimamo wake uliotangulia katika suala husika, akasema: Utoleaji dalili ni batili kwa sura mbili: Sura ya Kwanza: Hakika haifai kuzingatia kukosekana kuwajibu wao kuwa ni kukiri kwao isipokuwa ikithibiti kwamba, hakika wao walikuwa ni Waislamu na watu wema, wenye kushikamana na sharia ya Nabii wao, na hakuna katika aya yale yanayoashiria lau kwa uchache ishara ya kuwa watu hao walikuwa hivyo, bali inategemewa kwamba walikuwa makafiri au waovu, basi kukosekana kuwajibu hao haihesabiwi ni kukiri na kulipitisha hilo, bali ni ukanushaji. Hakika maelezo ya kauli kutoka kwa makafiri na waovu inatosha katika kujibu kwake na kuwasifia hao, haizingatiwi unyamazaji juu yake kuwa ni kukiri.8 Anajibiwa kuwa: Mosi: Hakika aya imetoa ishara kwamba, hakika kauli ya kwanza ni kauli isiyokuwa ya wenye 8

Tahdhiiru Saajid mani Takhadha Qubuur Masaajid, uk. 81-82.

27


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

kumpwekesha Mwenyezi Mungu ambao hawakuwa wenye kujishughulisha pamoja na watu wa pango. Na kauli ya pili ni kauli ya wenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu ambao kulikuwa na muunganiko wa kiroho kati yao, na linaloshuhudia juu ya hilo ni kuwa utoaji maoni wa kwanza umetajwa kwa mujibu wa kauli yao: “Jengeni jengo juu yao” kisha wakafuatilizia utoaji maoni kwa kauli yao: “Mola wao mlezi anawajua zaidi hao” yaani hatuwajui hao wala hatusemi kuhusu wao chochote na Mola wao mlezi anawajua hao zaidi.Na maneno haya ni ya yule asiyewajua watu wa pango na kazi yao, au hapendi wasifike na kitu cha wema na kufuzu, na kwa hivyo mafikio yao yanapelekwa kwa Mwenyezi Mungu. Na ama utoaji maoni wa pili wenyewe ni chimbuko kutokana na moyo wa mwenye maarifa kwa watu wa pango, namna ambayo wamesema: “Wakasema walioshinda juu ya shauri lao” waliwajua hao kwa umakini “Tutajenga msikiti juu yao” na je, inawezekana utoaji wa maoni haya ukawa unatoka kwa kafiri muovu?! Na juu ya hili iweje Sheikh aseme: Inategemewa kwamba walikuwa (watoaji maoni) ni waovu makafiri?!! Pili: Hakika utoaji dalili haukujengeka juu ya kuwa utoaji maoni unatoka kwa Waislamu na wapwekeshaji Mungu, bali imejengewa – kama ilivyo28


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

tangulia – juu ya mtazamo wa Qur‟ani, nao ni kwamba hataji lolote kutoka kwa mwingine, ikiwa litakuwa ni jambo lenye utata isipokuwa atataja na ukosoaji wake na kujibu. Na maudhui ipo katika hali hii. Kama utoaji maoni huu ungekuwa na harufu ya shirki kama anavyodai hilo yule anayezuia ujengaji wa misikiti hiyo, basi Qur‟ani isingelinyamazia. Sura ya Pili: Amesema: Utoaji wa dalili uliotajwa hakika umenyooka juu ya njia ya watu waliopotoka waliopita na wa hivi sasa, ambao wanatosheka nadini kwa kutumia Qur‟ani tu wala hawaipi Sunnah uzito wowote.9 Anajibiwa kuwa: Hakika mtoaji wa dalili kwa kutumia aya ambaye ni Sheikh Abu Faydh Sadiiq Ghumar katika kitabu chake kinachoitwa: “Ihyaaul-Maqbuur min Adillat Istihbaab binau masajid wal-Qubaab A‟lal-Qubuur” naye ni Sheikh wa hadithi katika nchi ya Morocco, na anazo shule na wanafunzi. Naye ni mwenye kuhuisha Sunnah katika kijiji chake, basi vipi anamtuhumu huyo kuwa ni miongoni mwa watu wa upotovu wapuuziaji wa sunna kwa kushikamana tu na Qur‟ani?! 9

Tahdhiiru Saajid mani Ttakhadha Qubuur Masajid, uk. 82.

29


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Na msemaji hebu ageuze jambo, atakuta maneno ya wale wenye kuzuia kuyafanya makaburi ya mawalii kuwa ni misikiti, ni maneno ya wapuuziaji wa Qur‟ani, na wenye kushikamana na sunna tu, hivi ndivyo ewe Sa‟ad unamfanyisha ngamia!! Na la kushangaza ni kwamba hakika katika baadhi ya maneno yake ananasibisha utoaji maoni wa kwanza kwa waumini, na anasema: “Na msemaji aseme: Hakika kundi la kwanza walikuwa waumini wenye kujua kutokuwepo sharia ya kujenga misikiti juu ya makaburi, basi wakaashiria kujenga juu ya mlango wa pango na kuziba mahali pake pia kuzuia upinzani wa watu wake, na hawakukubali watawala miongoni mwao na wakalifumbia macho hilo, wakaendelea kusisitiza mpaka wakaapa kujenga msikiti.”10 Anajibiwa kuwa: Hakika yale aliyoyasema ni kinyume na kauli ya wafasiri ambao tayari umeshasikia maneno yao. Huyu hapa Imam wa athari Sheikh Twabari: Ananasibisha kauli ya kwanza kwa makafiri na utoaji wa maoni wa pili kwa waumini. Hakika limetangulia neno lake na maneno ya wengine yasiyo na idadi. Taawili Isiyokubalika ya Albaani: Pindi Albaani alipojua kwamba yale aliyoyasema yeye hayaendani na andiko la Qur‟ani tukufu, 10

Tahdhiiru Saajid mani Ttakhadha Qubuur Masaajid, uk. 86.

30


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

amejaribu kufanya taawili ya aya, akasema: Na ikiwa utakataa isipokuwa kuchukua dhana ya kundi la pili, basi inakupasa kusema: Hakika ujengaji wao wa msikiti juu yao sio juu ya mtindo wa kujenga msikiti juu ya makaburi, na linalokatazwa kwalo, na hakika ni kujenga msikiti mbele yao na karibu ya pango lao na mfano huu usioepukika.11 Anajibiwa kuwa: Hakika msimamo uliotangulia wa Sheikh Albaani mwenye kufuata mfumo wa Ibn Taymiyya na anayefanana naye, alikokoteza mpaka katika taawili ya Qur‟ani, na hakuna aya ya Qur‟ani yenye lafudhi “mbele” bali ipo lafudhi “juu”ambapo wamesema: “Tutajenga juu yao” yaani juu ya makaburi yao na juu ya pango lao, namna ambayo makaburi yanakuwa ndani ya msikiti na sio nje. Kurejea Katika Maneno ya Uthman Khamis: Pindi Uthmani Khamis alipohisi kwamba ukatazaji wake wa kusimamisha swala kwenye msikiti ambao ndani yake limo kaburi, haukusanyiki pamoja na kuswali katika msikiti wa Mtume , wakati ambapo Waislamu kwa karne na karne waliswali ndani yake 11

Tahdhiiru Saajid mani Ttakhadha Qubuur Masaajid, uk. 7677.

31


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

na humo lipo kaburi la Mtume  na makaburi ya masheikh wawili. Alijaribu kujibu kuhusiana na matendo ya Waislamu kwa kauli yake: “Hakika Mtume  alikuwa hai pindi ulipojengwa msikiti, na pindi alipozikwa hakuzikwa ndani ya msikiti bali katika nyumba yake, na pindi ulipopanuliwa msikiti likawa kaburi tukufu ndani ya msikiti. Na hapa hukumu inatofautiana. Hapo msikiti ulijengwa juu ya uchamungu, basi hapo swala haitakuwa na tatizo lolote. Ama ujengwe msikiti juu ya kaburi au akizikwa maiti ndani ya msikiti, hakika hautakuwa umejengwa juu ya uchamungu, na hapo haifai kuswali ndani yake.” Ninasema: Hakika maneno yake yanaonesha upatiaji wa tendo la kuingiza kaburi la Mtume  ndani ya msikiti. Hiyo ni kutokana na ubainifu aliyoutaja, lakini anatofautiana na yale aliyoyasema Sheikh Albaani ambapo hakuridhia amali ya wale waliopita kwa kuingiza kaburi la Mtume msikitini, kwani hakuna tofauti kwamba walimzika yeye  msikitini pindi alipofariki, na kati ya lile walilolifanya wale wa baada yao la kuingiza kaburi lake ndani ya msikiti kwa kuupanua, kizuizi kipo kwa namna yoyote ile.12

12

Tahdhiiru saajid mani Ttakhadha Qubuur masaajid, uk. 89.

32


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

UDUNISHAJI WA AHLUL-BAYT  NA TABIINA Hakika Sheikh Albaani alikanusha amali ya Tabiina katika uingizaji wa kaburi la Mtume  ndani ya msikiti, na akasema: Hakika Umar bin Abdul-Aziz pindi alipokuwa naibu wa Walid katika mji wa Madina katika mwaka wa 91A.H, aliubomoa msikiti na akaujenga kwa mawe yenye nakshi, na akausakafia huo kwa msaji (mvule) na maji ya dhahabu. Pia akavunja vyumba vya wake wa Mtume  na akaviingiza msikitini na akaingiza kaburi ndani yake. Kisha akampinga kwa kauli yake: “Hakika kaburi tukufu kuingizwa ndani ya msikiti wa Nabii liliwekwa wakati ambapo hapakuwa na yeyote miongoni mwa Maswahaba katika mji wa Madina. Na hakika hilo lilikuwa linakwenda kinyume cha lengo lao, basi haifai kwa mwislamu aweke hoja kwa yale ambayo yametokea baada ya Maswahaba.”13 Ninasema: Amejua kutoka wapi kwamba kipindi hicho katika mji wa Madina hapakuwa na yeyote miongoni mwa Maswahaba? Je, huu sio usingiziaji wa jambo la ghaibu? Kwa hakika Mtume  alikuwa na Maswahaba wapatao laki moja, na historia imeandika majina ya karibia Maswahaba wapatao elfu kumi na tano, pamoja na kuwa hakika historia ya vifo vya wengi wao haijaandikwa. 13

Tahdhiirul-saajid mani Ttakhadha Qubuur masaajid, uk. 93.

33


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Kisha hakika maneno yake haya yamechukuliwa kutokana na maneno ya mwasisi wa madhehebu yake Ibn Taymiyya, ambapo amesema: “Hakika liliingizwa jiwe katika msikiti baada ya kutokuwepo Maswahaba.” Angalia kitabu chake “Jawabu litoshalo kwa wenye kuzuru makaburi” hakika kimechapishwa chapa ya zamani katika mji wa Cairo Misri kama anavyoeleza mwenyewe Albaani. Hebu na tujaalie kwamba hakukuwa na yeyote miongoni mwa Maswahaba katika mji wa Madina, lakini alikuwapo miongoni mwao yule aliyeishi miaka 93, yaani: Anas bin Malik (mpokezi wa hadithi za Mtume baada ya Abu Huraira) na huyu hapa Dhahabi katika tarjuma yake anasema: Na wakasema wengi nayo ni kauli iliyosahihi, kwamba alikufa mwaka wa 93; akasema hayo: Ibn Udayy, Said bin Aamir, Madaini, Abu Naiim, Falas na Qa‟nab.14 Na sio muhali kuwa Anas bin Malik aliishi na tukio hilo, sawa alikuwa Madina au sehemu nyingine, lakini pamoja na hivyo hakusema kwa usemaji wa mdomo, na haikunukuliwa kutoka kwake kwamba alipinga au alikanusha tendo hili. Na huyu hapa Abu Tufail wa mwisho kufa miongoni mwa Maswahaba. Hakika alikufa kama Dhahabi 14

Siirat Aalam Nubalaai, Juz. 3, uk. 406 na. 62.

34


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

anavyosema mwaka wa mia moja, na ikasemwa: Alikufa baada ya mwaka huo na aliishi Makkah.15 Je, inawezekana asijue chochote sahaba huyo na watu wa Madina walikuwa wakihiji kila mwaka na wakinukuu habari zake. Pamoja na hivyo haukunukuliwa kutoka kwake ukanushaji wowote ule?! Tujaalie kwamba hakukuwa na yeyote siku ambayo liliingizwa kaburi la Mtume  ndani ya msikiti, yaani sahaba, lakini Madina walikuwapo wanazuoni na watoa fatwa wengi na kiongozi wao alikuwa Imam Zaynul-Abidiina Ali bin Husein , ambaye aliwafunika wanahistoria na wanahadithi juu ya elimu yake na zuhudi yake. Na hakika idadi kubwa ya mafakihi na watoa fatwa walichukua kutoka kwake elimu mbalimbali, na aliasisi madrasat ya fikihi na hadithi. Na alikusanya zaidi ya mia na sitini ya taabiina miongoni mwa wale ambao walikuwa wakifaidika kutokana na chemchem yake, na wakipokea kutoka kwake. Hakika alipokea hadithi kutoka kwake: Saidi bin Musayyab, Said bin Jubair, Qasim bin Muhammad bin Abi Bakri, Abu Zinad, Yahya bin Ummu Twawiil, Umar bin Diinar, Zahriy, Zayd bin Aslam, Yahya bin Sa‟da Answari na kundi la wasomi. 15

Siirat Alaam Nubalaai, Juz. 3, uk. 470 na. 97.

35


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Imepokewa kutoka kwa Zahriy amesema: “Sijamuona yeyote aliyekuwa mwanafikihi zaidi yake.”16 Na lau ungelikuwa uingizaji wa kaburi la Mtume  ndani ya msikiti ni jambo lisilo sahihi basi Imam  asingelinyamazia hilo. Na aliponyamaza kwa hilo mtoto wake Imam Baqir  na yule wa baada yake ambaye ni Imam Swadiq  wasingelinyamazia. Hakika hivyo ndivyo ilivyokuwa. Kwa hakika Waislamu waliendelea kuswali tangu siku lilipoingizwa kaburi la Mtume  ndani ya msikiti kwa karne na karne hadi hivi leo, na wala halikusikika lolote kutoka kwa yule, yaani mtoto wamwanamke, kwamba alikanusha tendo hilo, bali Waislamu wote wanaswali katika msikiti na wanatabaruku kaburi lake tukufu hadi zama alipokuja Ibn Taymiyya na yule aliyemfuata yeye, basi wakadhihirisha chuki zao juu ya tendo hili!! Je, hawakukubaliana Waislamu au mafakihi na watoa fatwa katika karne moja juu ya tendo hilo, kwamba ni dalili ya uhalali wa amali hii na kuruhusu kwake? Hakika ijimai ya rai za wanazuoni juu ya jambo fulani ni miongoni mwa vyanzo vya sharia kama vile; Kitabu naSunnah. Basi kwa nini hatujaalii kwamba maafikiano kuwa ni dalili juu ya kufaa hilo bali ni mustahabu?! 16

Angalia: Siirat Nubalaai, Juz. 4, uk. 389 na Tarikh Madina Damishqi, Juz. 41, uk. 371.

36


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Na hii hapa miji ya Kiislamu katika Mashariki ya kati yote ikiwa na makaburi ya Manabii watukufu , na ndani yake ipo misikiti upande wa makaburi. Na hili sio ila ni lengo la kutabaruku mwenye kuswali kwenye makaburi ya Manabii watukufu ambao walipitisha uhai wao katika kueneza tawhid na kupambana na waabudu masanamu. Ni dhuluma ya wazi kuihesabu swala kwenye makaburi yao kwa lengo la kutabaruku kwao kuwa ni shirki au inafuka kutoka humo harufu ya shirki! Na kuanzia siku walipotawala Mawahabi katika sehemu ya miji hiyo walianza kutenganisha makaburi na misikiti yao na sehemu walipozikwa Mashahidi wao kwa kitu kinachohusiana na sitara. Na jambo la kustaajabisha na kushangaza ni kwamba kulingana na yale watu waliyo yapokea kutoka kwa Mtume  amesema: “Hakika heri ya umma wangu ni pembe yangu, kisha wale ambao wanaowafuata hao kisha wanao wafuata hao.17 Wakafanya karne hizi tatu ni karne zilizo bora zaidi, na ikawa ni kipimo baina ya ubainifu wa sunna kuhusiana na bidaa nayo ni yale yaliyodhihirika katika karne mbalimbali kulingana na jambo jipya kwa upande mmoja na yale yaliyodhihirika baada yake kwa upande mwingine. Basi juu ya hili kwa nini wamevunja ahadi yao ambapo kwa hakika limezuka jambo hili katika karne 17

Fat-hul-Baari, Juz. 7, uk. 3.

37


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

nzuri katika mikono ya tabiina? Na kwa nini limekuwa ni jambo lisiloridhiwa ewe muonaji?!! Ndio, limepatikana kaburi la Nabii Yunus  Mosuul nchini Iraq ndani ya msikiti, na vivyo hivyo kaburi la Nabii wa Mwenyezi Mungu Shiith . UCHAMBUZI JUU YA DALILI ZA WAZUIAJI Mawahabi wameshikamana na mkusanyiko wa hadithi nyingi juu ya uharamu wa kujenga msikiti kwenye makaburi ya watu wema, na sisi tunasoma lililo muhimu mno kuhusu hayo, na hakuna isipokuwa hadithi mbili. Hadithi ya Kwanza: Bukhari amepokea: Pindi alipofariki Hasan bin Hasan binAli, mkewe aliweka tungi juu ya kaburi lake mwaka mmoja, kisha akaliondoa. Basi ukasikika ukelele ukisema: Je, wamepata ambayo waliyoyakosa? Basi mwingine akamjibu yeye: Bali wamekata tamaa na wamekengeuka.18 Ninasema: Hadithi hii ambayo ameipokea Bukhari – nacho ni kitabu kilicho sahihi zaidi kwa Masuni – ni 18

Sahihi Bukhari: 314, kitabu Janaiz, mlango yale yanayochukiza kujenga misikiti juu ya makaburi, kabla ya na. 1330, chapa ya Daarul-Fikri, Beirut 1424H, utoaji na uchapishaji: Sadiqiy Jamiil Atwar.

38


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

dalili juu ya kufaa mambo mawili ambayo mawahabi wanayakanusha: 1. Uwekaji wa mwamvuli na kuba (tungi) juu ya kaburi, kwa sababu mwanamke wa Hasan aliweka tungi juu ya kaburi la mumewe,Tabiina walikuwa wakiona na wengine kusikia na kati ya hao ni mafakihi, watoaji fatwa na watu wa hadithi, na hakujulikana yeyote ambaye amelikanusha hilo. Na hilo ni dalili tosha ya wazi zaidi juu ya kufaa kuweka kuba (tungi) juu ya makaburi, na lilikuwa hili katika karne bora zaidi ambayo ni kitenganishi kati ya bidaa na sunna, kama Sunni wanavyosema. 2. Hakika kufaa kuswali kwenye makaburi ya mawalii, kwamba mkewe aliweka tungi kwa ajili ya kusimamisha swala kwenye kaburi lake na usomaji wa Qur‟ani tukufu. Na Hasan bin Hasan maarufu kwa jina la Muthanna, ni miongoni mwa wajukuu wa Mtume , na inatosha kuwa miongoni mwa fadhila zake ni kwamba alikuwa wasii wa baba yake na msimamizi mkweli wa Ali bin Abi Twalib . Na hakika amepokea kutoka kwa baba yake Hasan bin Ali bin Abi Twalib  na mtoto wa baba yake mdogo Abdullah bin Ja‟far bin Abi Twalib na wengineo. Na hakika Hajjaj wakati alipokuwa kiongozi wa Madina alimpa vitisho huyo kwa kumkamata 39


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

ikiwa hataingia mtu asiyekuwa mwema katika sadaka ya Ali, basi akasimama mbele yake akasema: Sibadilishi sharti juu yangu, wala simuingizi ndani yake yule asiyeingizwa.19 Na ama kauli ya mpokezi: Basi wakasikia ukelele ukisema: je, wamepata waliyoyakosa? Basi akamjibu mwingine: Bali wamekata tamaa na wakaenda zao. Hapa kuna mambo mawili: Mosi: Hakika yamefanana na maneno ya msemaji asiye mwema; kwa sababu maneno yake ni aina ya kuwakejeli watu waliopatwa na msiba, kwani ilikuwa ni juu yake aomboleze kwa kitu kwa ajili ya kifo cha mumewe kama ilivyo sunna, basi akawa anawatolea maneno yasiyofaa watu waliopatwa na msiba kwa lugha mbaya, nayo sio miongoni mwa tabia za watu wema. Na mfano wake katika hilo ni yale aliyoyajibu mpiga ukelele anayedaiwa. Pili: Hakika uwekaji huo wa tungi wa mwanamke juu ya kaburi la mumewe aliyefariki haukuwa na mategemeo ya kurejea kuishi tena hai hata isemwe hakika yeye amekata tamaa, bali ilikuwa ni kwa malengo matukufu tuliyoyaashiria. Hivyo mpiga ukelele kusema aliyoyasema na mwingine kujibu aliyoyajibu, yote 19

Tahdhiibul-Kamal, Juz. 6, uk. 92.

40


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

hayo si dalili ya kisharia, ikiwa hawakutegemea juu ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu wala Sunnah ya Mtume , bali walidhihirisha chuki zao na vinyongo vyao siku aliyojaribiwa mwanamke mwema kwa kifo cha mumewe. Hadithiya Pili: Bukhari amepokea kutoka kwa Ur‟wah, kutoka kwa Bibi Aisha, kwamba wakati wa maradhi yaliyopelekea kifo chake, Mtume  alisema: “Mwenyezi Mungu amewalaani Mayahudi na Manaswara kwa kuyafanya makaburi ya Manabii wao kuwa msikiti.” Bibi Aisha akasema: “Na lau sio hivyo wangelidhihirisha kaburi lake, lakini mimi ninahofia wasilifanye msikiti.”20 Hakika hadithi hii vyovyote itakavyokuwa sahihi sanad yake haiwezekani kukubali dhahiri yake, bali hapana budi kubainisha mradi wake kwa kitu, na hilo lina sababu zifuatazo: Ya kwanza: Hakika historia ya Mayahudi haikubaliani na madhumuni ya hadithi hii, kwani nyendo zao kwa hakika zimesimama katika kuua Manabii, kuwaghasi na kuwaudhi. Ni hayo na yasiyokuwa hayo miongoni mwa aina ya mabalaa ambayo 20

Sahihi Bukhari: 314, mlango yale yanayochukiza kujenga misikiti juu ya makaburi na. 1330.

41


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

walikuwa wakiwafanyia Manabii wao, na inatosha katika hilo kauli ya Mwenyezi Mungu (s.w.t):

َ َ َ َ َ َ​َ َ ‫الل ُـه َقى َل َال‬ ُ ‫قمر َو َّن‬ ٌ ‫الل َـه َف‬ ‫حن‬ ‫زين قالىا ِإّن‬ ‫لق ذ س ِ ع‬ َ َ َ َ َ َ ُ ّ َ َ ‫ياء َسننح ُب ما قالىا َوقحل ُه ُم ألاّنح‬ ُ ‫َأغ ِن‬ ‫ياء ِةغ ِمر ح ٍق َوّنقى ُل‬ ِ َ َ َ .‫شرق‬ ِ ‫روقىا عزاا اال‬ “Hakika Mwenyezi Mungu amekwisha sikia kauli ya wale waliosema: Mwenyezi Mungu ni fukara na sisi ni matajiri. Tutaandika yale waliyoyasema; na kuua kwao Mitume; na tutawaambia: Onjeni adhabu ya kuungua.”21 Na Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema:

ٰ َ َ َ ُ َُ ‫الج ِّ نـ ِد‬ ‫جاءلم ُس ُس ٌل ِمن قجلى ِب‬ ‫… قل قذ‬..” َ ٰ ُ ُ ُ ‫َوت َالزي ُق ُلحم َفل َم َق َح ُلح‬ ‫ىهم ِإّن لنحم ـ ِذقمّن‬ ِ ِ “Waambie: Bila shaka wamekuja kwenu Mitume kabla yangu na dalili zilizo wazi na kwa yale mliyoya sema; basi kwanini mliwaua ikiwa nyinyi ni wenye kusema kweli.”22 21 22

Surat Aali-Imran; 3:181. Surat Aali-Imran; 3:183.

42


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Na (s.w.t) anasema:

َ ُ َ​َ َ ٰ ‫ٔـ‬ َُ ُ َٰ َ َ َ ‫ألاّنح‬ ‫ياء‬ ِ ‫”ف ِج ا ّن‬ ِ ‫قض ِهم ميثـقهم ول ِش ِهم ِبـايـ ِد الل ِـه وق ِحل ِهم‬ َ ّ “…..‫ِةغ ِمر َح ٍق‬ “Basi kwa sababu ya kuvunja ahadi yao, na kuzikataa kwao dalili za Mwenyezi Mungu, na kuua kwao Manabii bila ya haki”23 Ya pili: Hakika huko kuna vielelezo vya ushahidi wa kwamba Manaswara walikuwa wakifanya makaburi ya Manabii wao Kibla chao, inawaondoa kuelekea Kibla cha wajibu. Hili lina uhusiano gani nakuswali katika msikiti wa Nabii au kuswali ndani ya msikiti ambao ndani yake limo kaburi la Walii wa Mwenyezi Mungu (s.w.t) huku mtu akiwa kaelekea Kaaba, akiswali kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (s.w.t), akisoma aya za Mwenyezi Mungu kwa lengo la kutabaruku ardhi takatifu?! Na ambalo linajulisha juu ya hilo ni mambo yafuatayo: 1. Yale aliyopokea Ummu Habiba na Ummu Salama, hadithi zilizotaja kanisa waliloliona Uhabeshi, ndani yake zikiwemo picha, Mtume  akasema: 23

Surat an-Nisa; 4:155.

43


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

“Hakika hao walikuwa na kawaida anapokuwa miongoni mwao yupo mtu mwema basi akifa walijenga juu ya kaburi lake msikiti, na wakachora picha zake ndani yake, hao ni watu wabaya kati ya viumbe mbele ya Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama.”24 2. Na lengo la uwekaji wa picha za watu wema pembezoni mwa makaburi yao, hakika ilikuwa ni kwa ajili ya kusujudu juu yake, au juu ya makaburi yao, namna ambayo kaburi linalokuwa na picha linakuwa ni Kibla chao, au zinakuwa ni mfano wa sanamu zikiabudiwa na kusujudiwa hizo.Na ushuhuda juu ya hilo ni kwamba Ahmad bn Hanbal katika “Musnad wake” na Malik bin Anas katika “Muwatwai” wamepokea hadithi hii: Hakika Mtume  amesema – baada ya kukataza kulifanya kaburi kuwa ni msikiti:- “Ewe Mwenyezi Mungu! Usilifanye kaburi langu sanamu lenye kuabudiwa.”25 Hakika hili linajulisha juu ya watu hao walikuwa wakilifanya kaburi na picha kuwa Kibla wakizielekea, bali ni sanamu lenye kuabudiwa, pasi na Mwenyezi Mungu (s.w.t). 3. Hakika uzingatiaji katika hadithi ya Aisha – hadithi ya pili – unaongeza uwazi wa uhakika 24

Sahihi Muslim, Juz. 2, uk. 66, kitabu masjid; angalia: Sunan Nasaai, Juz. 2, uk. 41. 25 Musnad Ahmad, Juz. 3, uk. 248, na Muwatwai, Juz. 1, uk. 172 na. 85.

44


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

huu, ambapo baada ya hadithi iliyopokewa kutoka kwa Mtume  akasema: “Na lau sio hivyo wangelidhihirisha kaburi lake, lakini mimi nahofia wasilifanye msikiti.” Yaani waliweka kizuizi. Tunajiuliza: Usimamishaji wa ukuta kuzunguka kaburi ni kuzuia kitu gani?! Na lililothibiti ni kwamba ukuta unazuia swala juu ya kaburi lenyewe na kulifanya sanamu lenye kuabudiwa, na kwa uchache haliwi Kibla kinachoelekewa. Ama kuswali pembezoni mwa kaburi – pasi na kuliabudu kaburi au kulifanya Kibla kwa ajili ya ibada – hilo halizuiliwi, kwa ushahidi kwamba hakika Waislamu – tangu karne kumi na nne – wanaswali pembezoni mwa kaburi la Mtume  katika kipindi ambacho walikuwa wakielekea Kibla na wakimwabudu Mwenyezi Mungu (s.w.t), na uwepo wa kizuizi haukuwazuia kuswali. Faida ya maneno: Hakika hitimisho la hadithi ya pili – ambayo inatokana na maneno ya Aisha – inaweka wazi maana ya hadithi, kwani hiyo imetaja sababu ambayo imezuia kudhihirisha kaburi la Mtume , kuwa ni kuzuia lisifanywe msikiti, na makusudio ya kufanya mahali alipozikwa kuwa ni msikiti yaani ni kufanywa Kibla kinachoelekewa wakati wa kuswali, kama utakavyokuja ubainifu kutoka kwa wafafanuzi 45


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

wa hadithi. Na kwa ajili hiyo ukawekwa ukuta kuwa ni kizuizi kwenye kaburi la mtukufu huyo. Basi kizuizi kinazuia vitu viwili: 1. Kaburi lisibadilishwe na kuwa sanamu, watu wakasimama mbele yake wakiliabudu hilo. Hivyo panapokuwepo kizuizi haiwezekani kuliona kaburi na haiwezekani kulifanya sanamu ili kuliabudu. 2. Ili lisifanywe kuwa Kibla, hiyo ni kwa sababu kulifanya kuwa Kibla ni sehemu ya kuliona. Na ama kuswali ndani ya msikiti ambao amezikwa humo ni dhahiri shahiri jambo hilo halijakatazwa, na hii ni dalili kwamba hakika hofu ya Mtume  – tukijaalia kusihi kwa hadithi – ilihusu kulifanya kaburi lake sanamu linaloabudiwa au linalosujudiwa. Kama msemaji atasema: Hakika kulifanya kaburi kuwa ni Kibla hakutegemei kuliona, kwa ushahidi kwamba Kaaba ni Kibla cha Waislamu katika kipindi ambacho Waislamu wengi zaidi hawaioni hiyo Kaaba wakati wa kufanya ibada. Jibu: Haipaswi kulinganisha baina ya Kaaba na kaburi, kwa sababu Kaaba ni kibla cha Waislamu wote katika sehemu zote za ardhi. Na si Kibla cha ibada tu, bali ni kwa ajili ya ibada na mambo 46


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

mengineyo kama vile; kuchinja na kuzika, na yanayofanana na hayo, basi hicho ni Kibla katika hali zote, wala hakuna uhusiano wa kukiona kwa aina yoyote ile. Ama kulifanya kaburi la Mtume  Kibla, hakika hilo linawezekana kwa wale ambao wanaokuwepo msikitini mwake na wanaosimamisha swala mbele yake, hivyo kulidhihirisha kaburi tukufu kunaandaa mazingira ya dhana hii –kwa mujibu wa rai ya Aisha – wakati ambapo kuweka sitara kunakuwa ni kizuizi chenye kuzuia hilo. Tatu: Vielelezo vinaonesha kwamba katazo la Mtume  hakika lilihusu kuabudu kaburi, na hakika watoaji maelezo wengi wa Sahihi Bukhari na Muslim wamefasiri hadithi kama tulivyoifasiri, na wamefahamu kama tulivyofahamu… kwa mfano Qastwalani - katika kitabu chake Irshaad Saari anasema: “Hakika wa mwanzo wao wameweka sura ili wajiliwaze kwayo na wanajikumbusha vitendo vyao vyema. Basi wanajitahidi kama vile walivyo jitahidi wao na wakamwabudu Mwenyezi Mungu mbele ya makaburi yao, kisha vikafuata vizazi baada yao. Watu hawa hawakujua mradi wao, na shetani akawashawishi hao kwamba mababu zao walikuwa wakiziabudu picha hizo na wakizitukuza. Basi Mtume  alihadharisha mfano wa hilo.” 47


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Hadi pale aliposema: Baydhawi amesema: “Pindi Mayahudi na Manaswara walipokuwa wakisujudia makaburi ya manabii wao kwa lengo la kutukuza jambo lao basi wakayafanya kuwa ni Kibla wakiyaelekea katika swala na mfano wa hiyo na wakayafanya masanamu, wakakatazwa Waislamu juu ya hilo. Na ama yule anayejenga msikiti pembezoni mwa mtu mwema ili kutabaruku na kujikurubisha kwalo – sio kwa ajili ya kutukuza wala kuelekea hilo – haingii katika kuahidiwa adhabu iliyotajwa.”26 Na Qastwalani sio peke yake katika utoaji wa maelezo haya, bali anasema hilo Sundiy – mtoaji maelezo wa kitabu Sunan Nasaai – anasema: “Kuyafanya makaburi ya manabii wao misikiti” yaani: Kibla kwa ajili ya swala wanayoiswali kuyaelekea hayo, au walijenga misikiti juu yake wakiswali humo. Na huenda kwa njia ya chukizo 26

Irshaad Saari katika Sharhu Sahihi Bukhari, Juz. 2, uk. 437, mlango wa kujenga misikiti juu ya makaburi. Na hakika Ibn Hajar imeelemea katika maana hii – katika kitabu Fat-hulBaari, Juz. 3, uk. 208 namna ambavyo amesema: Hakika katazo hakika hilo kutokana na yale ambayo yanapelekea kwa kaburi hadi yale ambayo juu yake watu wa kitabu, ama lisilokuwa hilo hakuna mushkeli kwalo.

48


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

kwamba hilo linahukumiwa kufikia hadi kuliabudu kaburi lenyewe.”27 Vile vile anasema: (Mtume) anauhadharisha umma wake kulifanya kaburi lake kama vile walivyofanya Mayahudi na Manaswara makaburi ya Manabii wao. Waliyafanya makaburi hayo misikiti, ama kwa kusujudu kuyaelekea hayo kwa kuyatukuza, au kuyafanya kuwa ni Kibla wanachokielekea wanaposwali.28 Na Nawawi anasema – katika maelezo ya Sahihi Muslim: Wanazuoni wamesema: Hakika katazo la Mtumekulifanya kaburi lake msikiti na kaburi la mwingine, ni kuhofia kule kuzidisha katika kumtukuza yeye na kuwa ni fitna kwalo. Basi huenda likapelekea hilo katika ukafiri, kama ilivyojiri katika umma zilizopita. Na pindi walipohitaji Maswahaba na taabiina kuongeza na kuupanua msikiti wa Mtume  wakati walipozidi Waislamu na ukapanuka na kuingia 27

Sunan Nasaai kwa sherehe ya Suyuut na mstari wa pambizo wa Sundiy, Juz.4 uk. 96, chapa ya Daaru Ihyaai Turathi Arabi Beirut. 28 Sunan Nasaai kwa sherehe ya Suyuut na mstari wa pambizo wa Sundiy, Juz.4 uk. 96, chapa ya Daaru Ihyaai Turathil-Arabi Beirut.

49


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

nyumba za mama wa waumini ndani yake, na kati ya hizo ni chumba cha Bibi Aisha, alimozikwa Bwana Mtume  na Maswahaba wake wawili, walijenga juu ya kaburi lake ukuta ulioinuka wenye kuzunguka pembezoni mwake, ili lisidhihiri katika msikiti na wale wasiojua wasije kuswali kwa kulielekea. Na hayo ameyasema Bibi Aisha katika hadithi, “Na lau sio hivyo wangelidhihirisha kaburi lake, lakini mimi nahofia wasilifanye msikiti.” 29 Ninasema: Pamoja na fuo la maneno hayo, pamoja na yale aliyoyafahamu mtoaji maelezo ya hadithi, hapana budi kusema hilo, wala haiwezekani kutoa natija isiyokuwa hiyo au kufutu kwa lisilokuwa hilo. Uwepo Wa Misikiti Katika Sehemu Za Mashahidi Hakuna Mahusiano Yoyote Na Hadithi Hizo Hakika ujumbe wa hadithi, ni ikiwa msikiti umejengwa juu ya kaburi, hivyo basi hakuna uhusiano baina ya hadithi hiyo na sehemu takatifu za mashahidi, kwani misikiti – katika sehemu za mashahidi – isiyokuwa msikiti wa Mtume  hakika ipo jirani yake na sio juu yake, kwa aina ambayo kimoja wapo kinatengana na kingine. Na ibara nyingine ni kwamba: Huko ipo Haram tukufu na upo msikiti. Basi Haram Tukufu ni mahsusi 29

Sharh Sahihi Muslim, Juz. 5, uk. 13-14.

50


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

kwa kuzuru na kufanya tawasuli kwa kumwelekea Mwenyezi Mungu (s.w.t) kupitia walii huyo mwema, na msikiti – pembezoni mwake – kwa ajili ya kuswali na kufanya ibada. Basi sehemu takatifu za mashahidi – katika hali hii – ziko nje ya kile kinachofaidisha hadithi na maana yake – ikiwa madhumuni yake ni kama wanavyodai mawahabi. Na kwa hivyo inadhihiri faidisho la hadithi alizozikusanya Sheikh Albaani katika kitabu chake “Tahdhiirul-saajid mani ttakhadha kubuura masaajid” ambapo imefikia idadi yake hadithi 14. Na nyingi kati ya hizo zinazungumzia amali ya manaswara wale waliofanya makaburi kuwa sehemu ya kusujudu juu yake. Na ama kuswali tu ili kutataburu mahali hapo ambapo lipo kaburi la Mtume  mwana tawhid, hilo lipo nje ya yale yanayofaidisha hadithi hizo. Mpaka hapa yametimia yale tuliyotaka kubainisha kuhusiana na hukumu ya kujenga misikiti juu ya makaburi ya mawalii, ambayo ndio msingi wa ukosoaji wa maneno ya Uthmani Khamis. VIPANDE VITATU KATIKA MANENO YA UTHMANI KHAMIS Ikiwa imebainika hivyo basi na turejee katika vipande vitatu katika maneno yake. 51


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Mjadala katika kipande cha kwanza: Uthmani Khamis amezuia kuswali katika misikiti ya Shi‟ah kwa mambo mawili: 1. Kwa sababu Shi‟ah wanatukuza zaidi makaburi, wanajenga misikiti juu ya makaburi au wanafanya makaburi ndani ya misikiti, yaani wanazika maiti ndani yake, basi haifai kuswali katika msikiti ambao ndani yake limo kaburi. Na sisi tuna baadhi ya maswali ya kumuuliza Sheikh kuhusiana na maneno yake hayo: Moja: Hakika Sheikh amefutu katika maneno yake kwamba hakika haifai kwa Mwislamu kuingia kwenye misikiti ya Shi‟ah nakuswali humo kwani yamo makaburi. Tunamuuliza: Hakika utoaji wake wa fatwa wa jumla ni dhamana inayotegemea Sheikh awe alishaiona misikiti yote ya Shi‟ah au zaidi yake iliyoenea ulimwenguni kote, ndipo aweze kutoa hukumu ya ujumla, je, Sheikh alishafanya hivyo, na ameshuhudia misikiti yote ya Shi‟ah kwa jicho lake mwenyewe mpaka ahukumu kwa hukumu hii?! Hakika Shi‟ah wana misikiti inayokadiriwa kufikia maelfu katika nchi ya Iran, Iraq, Lebanoni, Pakistani, India, Afghanistani na penginepo katika miji ya 52


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Kiislamu, napia katika nchi za kimagharibi, je, inasihi kufutu mas‟ala ya ujumla pasi na kushuhudia misikiti hiyo na kuona kwa jicho lake mwenyewe kuwa wamezikwa humo maiti? Na hakika imepokewa kutoka kwa Mtume  kwamba aliulizwa kuhusiana na suala la kutoa ushuhuda? Akasema: “Je, unaliona jua? Basi mfano wake huo ndio ushuhudie au acha.”30 Wala sidhani hakika Sheikh wala wafuasi wake ambao wanachukua yale aliyoyataja Ibn Taymiyya na Muhammad bin AbdulWahab, kuwa wamefanya kazi hii lau kwa kiwango kidogo. Na hakika umepita utajo wa hilo mwanzo wa maneno. Pili: Vipi anawatuhumu Shi‟ah kwamba wao wanazika maiti misikitini mwao, ilihali wanazuoni wa Kishi‟ah wamesema kinaga ubaga ndani ya vitabu vyao vya kifikihi uharamu wa suala hilo. Na huyu hapa Sayyid Twabatwabai katika kitabu chake “Urwatul-Uthqa” ameweka mlango wa baadhi ya hukumu za msikiti na akasema: Haifai kuzika maiti ndani ya msikiti, kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na wakfu.31 Hivyo yule atakayekuwa na ardhi na akatenga mahsusi kwa ajili ya kujengwa msikiti, hakika miliki yake 30

Kanzul-Ummal, Juz. 7, uk. 23, hadith namba 17782. Urwatul-Uthqa, Juz. 2, uk. 407, mlango baadhi ya hukumu za msikiti. 31

53


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

itaondoka kutoka kwake na kuwa miliki ya Mwenyezi Mungu (s.w.t), na hivyo vipi anatumia miliki ya Mwenyezi Mungu, je, amesoma Sheikh kurasa zinazohusiana na fikihi ya Shi‟ah, na akatoa fatwa hii kutokana na elimu na uonaji? Ndio ni haramu kuzika maiti baada ya kujenga misikiti, na ama kujenga misikiti juu ya makaburi yao hakuna muunganiko kwa yale ambayo tuliyoyataja kuhusiana na uharamu, na kwa hivyo inadhihirika kwamba suala la kuswali katika sehemu takatifu walimozikwa Maimamu wa Ahlul-Bayt ambazo miili yao mitakatifu imo humo, halina muunganiko na suala la kuzikwa maiti ndani ya misikiti, bali sehemu walimozikwa wao zimejengewa baada ya kuzikwa kwao, kama vile hakika sehemu walimozikwa watukufu hao kwa Shi‟ah hawazihesabu kuwa ni misikiti. Ndiyo huenda ikapatikana katika baadhi ya majengo kwa hali ya nadra, kwamba mwekaji wakfu anajitengea chumba maalum nje ya msikiti chenye kuungana na msikiti ili azikwe ndani yake, kwa ajili ya kutaka kuombewa msamaha na wale wenye kuswali na kusomewa Surat Fatiha na thawabu zake kupelekwa kwake, na wala haupatikani mfano huu ila kwa nadra. Tatu: Hakika uzuiaji kutoka kwa Ustadhi wake ni kuhusu kaburi lililo dhahiri. Ama kaburi lisilo dhihi54


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

rika basi inafaa ndani yake kuswali. Na huyu hapa Albaani anasema: Hakika mazingatio katika suala hili la makaburi ni yaliyopo dhahiri na ama yale ambayo yamo katika tumbo la ardhi miongoni mwa makaburi hayafungamani na hukumu ya kisharia kwa dhahiri, bali sharia inatembea kutokana na mfano wa hukumu hii, kwa sababu sisi tunajua kwa udharura na kushuhudia hakika ardhi yote ni makaburi ya walio hai, kama vile Mwenyezi Mungu anavyosema:

َ َ َ َ​َ ًٰ َ​َ ً َ ً َ ‫ألا‬ ‫مىثا‬ ‫سض ِل اثا أحياء وأ‬ ‫ألم ّنجع ِل‬ “Je, hatukuifanya ardhi ni chombo? Kwa walio hai na wafu.”32‟33 Basi makaburi katika misikiti ya Shi‟ah kwa kujaalia sio sahihi hayako dhahiri, vipi anafutu kuwa haifai kuswali ndani yake?! Mjadala wa kipande cha pili: Sheikh ameweka wazi sababu ya pili ya uzuiaji wa kuingia ndani ya misikiti ya Shi‟ah: Hakika harufu ya shirki inatoka ndani ya misikiti hii. 1. Humo anatajwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu. 2. Na anaombwa msaada asiyekuwa Mwenyezi Mungu. 32

Surat al-Mursalat; 77:25-26. Tahdhiirul-Saajid mani Ttakhadha Kubuur Masaajid, uk. 113.

33

55


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

3. Na wanamuita asiyekuwa Mwenyezi Mungu. 4. Na wanatukanwa Mawalii wa Mwenyezi Mungu miongoni mwa Maswahaba na makhalifa. Kwa hakika ametaja katika maneno yake haya mambo manne: Mosi: Wanamtaja asiyekuwa Mwenyezi Mungu: Basi tunamuuliza: Je, kumtaja asiyekuwa Mwenyezi Mungu msikitini ni kumwabudu mwingine asiyekuwa Mwenyezi Mungu?! Na lau kitakuwa hicho ni kigezo cha tawhid na shirki basi hakuna binadamu yeyote ardhini mwenye tawhid, kwani makhatibu wanamtaja Mtume wa Mwenyezi Mungu na wapokezi wa hadithi na majina ya ulamaa na yasiyokuwa hayo. Na huenda mtoaji waadhi akataja majina ya watu wema na waovu na visa vyao na hali zao. Pili: Na wanamuomba msaada asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Na hili ndio la umuhimu katika maneno ya Sheikh, tunasema: Je, kumuomba msaada asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni jambo la haramu? Basi Qur‟ani hii inataja kisa cha mtu ambaye alimuomba msaada Nabii Musa  kama ilivyokuja katika kauli ya Mwenyezi Mungu (s.w.t):

َ َ َ َ ٰ َ َ​َ َ َ َ َ​َ ‫هلها ف َى َج َذ فيها‬ ِ ‫حمّن غ ل ٍة ِمن ٰأ‬ ِ ‫ود َخل ااذينة ع ٰلى‬ َ َ ُ َ َ ‫قححالّن هـزا من‬ ‫شيع ِح ِه َوهـزا ِمن‬ ِ ِ ِ ‫سجل ِمّن ي‬ 56


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

َ َ َ َ َ ‫اسحغٰـ َث ُه َالزي من‬ ‫شيع ِح ِه َعلى الزي ِمن‬ ‫ف‬ ِ َ​َ ٰ َ َ ٰ َ​َ​َ َ ُ “….. ‫فىلض مىوس فق س عل ِيه‬

َُّ ِ ‫عذ ِو‬ َُّ ِ ‫عذ ِو‬

“Na aliingia mjini wakati wenyeji wake wako kwenyemghafala. Akakuta humo watu wawili wanapigana, huyu ni katika kundi lake na huyu ni katika adui zake. Yule aliye katika kundi lake alimtaka msaada dhidiya yule aliye katika adui zake. Musa akampiga, akammaliza…..”34 Na lau ungelikuwa uombaji msaada ni jambo la ushirikina basi kwa nini yeye alimuomba Musa  na hakumkataza hilo. Na huenda Uthmani Khamis na mabwana zake watajibu kwa kusema, hilo ni kama vile kumuomba msaada yule aliyehai. Na maneno yetu yanahusu kumuomba msaada mtu aliyekufa. Lakini mtoa jibu hakujua kwamba uhai na kifo sio vigezo viwili vya tawhid na shirki, bali vigezo hivyo viwili havina faida katika uwepo wake na kutokuweko kwake. Lakini bado anang‟ang‟ania kuwa kumuomba msaada aliyekufa ni shirki. Je, inawezekana kuwa amali moja ni tawhid katika hali moja na shirki katika hali nyingine?! – Na ama kumuomba msaada maiti ni utukuzaji au hapana? Basi hilo lipo nje ya maneno yetu. 34

Surat al-Qasas; 28:15.

57


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Tatu: Na wanamuita asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Basi tunamuuliza: Anakusudia nini kumuita mwingine? Je, anakusudia dua kwa maana ya kilugha, yaani mtu kumuomba kitu mtu mwingine? Sidhani yupo yeyote anayeharamisha hilo, huyu hapa Mtume  katika vita vya Uhudi aliwaita Maswahaba wake ambao waliacha uwanja wa vita na wakakengeuka na kukimbia. Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema:

ُٰ ُ ُ َ ‫لى َأ َح ٍذ َو‬ ٰ ‫"إر ُث ِعذو َّن َوال َثلى َۥّن َع‬ “….. ‫خشًنم‬ ‫الشسى ُل َيذعىلم فى أ‬ ِ “(Kumbukeni) mlipotoka mbio wala hamumtizami yeyote, na hali Mtume anawaita nyuma yenu.”35 Na ikiwa anakusudia kumwabudu mwingine basi huo ni usingiziaji mkubwa. Hakika ibada ni ibara ya unyenyekevu mbele ya muumba au mpangaji wa mambo ambaye mkononi Mwake kuna mafikio ya waja. Na Shi‟ah kwa ujumla – wanaafikiana na Waislamu wote – wakiitakidi tawhid katika uumbaji na Mungu Mlezi. Hakika mambo yote yako mkononi mwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) wala hamiliki yeyote hata kwa nafsi yake wala mwingine kitu isipokuwa dua kwa nafsi yake au kwa mwingine kwa idhini kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t). 35

Surat Aali-Imran; 3:153.

58


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Hakika kumuomba dua mwingine na kuomba msaada hili ni jambo ambalo wanakubaliana Waislamu juu ya kufaa kwake ila wachache mno. Na huyu hapa Tirmidhi anapokea kutoka kwa Anas bin Malik amesema: Nilimuomba Mtume  aniombee mimi uombezi Siku ya Kiyama, akasema: “Mimi nitafanya hivyo” nikasema: Basi wapi nitakuomba, akasema: “Juu ya njia.”36 Na huyu hapa Suwaad bin Qaarib alikwenda kwa Mtume  na kumuomba yeye uombezi katika ubeti wa kaswida, kati ya beti hizo ni: “Na uwe kwangu mimi muombezi siku ambayo hakuna mwenye uombezi katika njia ya utambi kwa Sawaad bin Qaarib.”37 Wala haihusishi kuomba uombezi kutoka kwa aliye hai tu bali inaenea kuomba uombezi kutoka kwa maiti pia. Basi huyu hapa Ibn Abbasi anasema: Pindi Amirul-Muuminina  alipomaliza kumuosha Mtume  alisema: “Naapa kwako kwa baba na mama yangu ewe Mtume! Hakika kifo chako kimekata yale ambayo hayakukatika kwa kifo cha mwingine, ikiwa 36

Sunan Tirmidhi,Juz. 4, uk. 42, mlango wa yale yaliyokuja katika suala la (Swiraat) njia. 37 Durarul-Saniyya, uk. 29 cha Zayniy Dahlaan.

59


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

ni pamoja na utume na habari ya mbinguni – hadi aliposema: Tutaje sisi mbele ya Mola Wako Mlezi, na tujaalie kutokana na jambo lako!...”38 Pia imepokewa kwamba pindi alipofariki Bwana Mtume  Abu Bakri aliufunua uso wake kisha akamwelekea yeye na akambusu na kisha akasema: Naapa kwa baba na mama yangu, ama kifo ambacho Mwenyezi Mungu amekuandikia juu yako hakika umekionja, kisha hakitakusibu wewe kifo kamwe.”39 Hakika hadithi hizi mbili – na zinazofanana na hizo – zinajulisha kwamba hakuna tofauti kati ya kuomba uombezi kutoka kwa muombezi katika uhai wake na baada ya kifo chake. Hakika Maswahaba walikuwa wakiomba dua kutoka kwa Mtume  baada ya kifo chake. Na kama uombaji dua kutoka kwake ni sahihi baada ya kifo chake, hakika kuomba uombezi – ambao huo ni aina ya uombaji wa dua – pia utakuwa ni sahihi. Na haipatikani ndani ya misikiti ya Shi‟ah kitu miongoni mwa yale ambayo ameyataja Sheikh ila kuomba uombezi, yaani kumuomba dua Mtume  na Aali zake. Hakika aya na hadithi zimejulisha juu ya uhai wao na uwepo wao kati yetu na wao. Na hata 38

Nahjul-Balaghah, Qiswarul-Kalaam na. 235. Siirat Nabawiyya,Juz. 2, uk. 655-656.

39

60


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

tukijaalia – ujaaliaji ambao ni batili – kuwa hawako hai, na wao hawasikii maneno yetu, basi kubwa linaloweza kusemwa ni kuwa hakuna faida yoyote katika uombaji dua kutoka kwa mja ambaye hasikii, wala haliwezi kuwa hilo ni dalili juu ya Shirki. Nne: Kuwatukana mawalii wa Mwenyezi Mungu miongoni mwa Maswahaba na Makhalifa. Hakika Shi‟ah hufuata athari ya Maimamu wa AhlulBayt katika kuwatukuza Maswahaba. Huyu hapa Imam wa wachamungu na kiigizo cha wanatawhid Amirul-Muuminina Ali bin Abi Twalib , na sisi tunanukuu kitu miongoni mwa maneno yake kuhusu Maswahaba: “Wapo wapi ndugu zangu ambao wamepanda njia, na wamepita juu ya haki? Na yuko wapi Ammar? Na yuko wapi Tayihan? Na yuko wapi mwenye shahada mbili? Na wako wapi walinzi wao miongoni mwa ndugu zao, ambao walikubaliana juu ya kifo, na wakavipozesha vichwa vyao kuukabili uovu!” Mpokezi anasema: Kisha akapiga ndevu zake tukufu kwa mkono wake, basi akalia sana, kisha akasema: “Oh! Juu ya ndugu zangu ambao wamesoma Qur‟ani na wakaitekeleza, na wakazingatia faradhi na wakaisimamisha Sunnah na wakaiua bidaa. Waliitwa kwa ajili ya jihadi basi wakaitikia, na 61


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

wakaharakisha na wakamkubali kiongozi na wakamfuata.”40 Na huyu hapa Imam Zaynul-Abidiina Ali bin Husein  anawaombea Maswahaba wa Mtume  anasema: “Ewe Mwenyezi Mungu! Na Maswahaba wa Muhammad  mahsusi ambao wamefanya usahaba mzuri, na ambao wamejaribiwa kwa balaa zuri katika kumnusuru yeye. Wakamkinga yeye na wakaharakisha kumfidia yeye. Na wakashindana kuelekea kwenye ulinganio wake – hadi aliposema – Ewe Mwenyezi Mungu wala usiwasahau hao kwa yale waliyoacha kwa ajili Yako, na waridhie hao kutokana na ridhaa Yako, na kwa yale ambayo wamewazuia viumbe Kwako. Na wakawa pamoja na Mtume Wako waitaji kwa ajili Yako na wenye kuelekea Kwako.Na washukuru hao juu ya kuhama kwao majumba ya watu wao kuja Kwako.” Kisha akasema: “Ewe Mwenyezi Mungu! Waunganishe waliowafuata wao kwa wema ambao wanasema: Ewe Mola Wetu Mlezi! Tusamehe sisi.”41 Haya ni maneno ya Maimamu na viongozi wa Shi‟ah na Waislamu, na Waislamu wote wenye kupita juu yake. Na la kushangaza ni kwamba wanatuhumiwa Shi‟ah kwa kuwatukana Maswahaba katika misikiti 40

Nahjul-Balaaghah, khutba ya 182. Sahifatu Sajjadiyya: Dua nambari 4, amani iwe juu ya wenye kuwasadikisha mitume. 41

62


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

yao na kwa hivyo anamzuia yule anayeingia katika misikiti hiyo. Pamoja na hayo yote tunaona katika kitabu chao sahihi zaidi nacho ni Sahihi Bukhari, baadhi ya Maswahaba wamewatusi Maswahabawenzao na kuwabughudhi katika kikao cha Mtume  na mbele ya hadhira yake. Na ikiwa wewe una shaka basi tukusomee hadithi aliyoinukuu Bukhari katika Sahihi yake kwa ufupi: Mtume  katika kisa cha Ifki alisema: “Ni nani atakayenipumzisha na mtu huyu. Yamenifikia kutoka kwake maudhi yake kuhusu mke wangu. Wallahi sijui lolote juu ya mke wangu isipokuwa kheri. Na wamemtaja mwanamume ambaye sijui lolote juu yake isipokuwa kheri. Na wala huwa haingii nyumbani kwangu isipokuwa pamoja nami.‟ Akasimama Saad bin Muadh ndugu wa Bani Abdul-Ash‟hal, akasema: „Mimi hapa ewe Mtume wa Allah nitakupumzisha naye. Ikiwa mtu huyo ni miongoni mwa Awsi basi nitaikata shingo yake. Na kama ni miongoni mwa ndugu zetu Khazraj utatuamrisha cha kufanya nasi tutatekeleza amri yako.‟ Akasimama Saad bin Ubadah chifu wa Khazraj, na kabla ya hapo alikuwa ni mtu mwema lakini aliyeelemewa na hasira za kijinga, akasema kumwambia Saad: „Wallahi umeongopa, hutamuua wala huna uwezo wa kumuua. Na kama angekuwa ni kutoka katika kabila lako usingependa auwawe.‟ Akasimama Asidu bin Hudhayru ambaye ni binamu wa Saad bin Muadh, akasema kumwambia Saad bin Ubadah: „Wallahi umeongopa 63


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

nitamuua. Hakika wewe ni mnafiki unajadili kwa niaba ya wanafiki.‟” Ukazuka mzozo baina ya makabila mawili Awsi na Khazraji mpaka wakakaribia kupigana. Wakati huo Mtume wa Allah alikuwa juu ya mimbari, Mtume wa Allah  aliendelea kuwatuliza mpaka wakanyamaza naye akanyamaza. 42 UKOSOAJI NA UREKEBISHAJI SIO KUTUKANA Hakika ni ukosoaji uliosimama juu ya msingi sahihi na vipimo vilivyo salama, nao ndio mwelekeo wa watafutaji wa uhakika, na wenye kuhangaika katika kupata fadhila. Na ama utukanaji na utoaji matusi basi hilo ni zao la kasumba na matokeo ya chuki, kinyongo na upotovu. Na kwa ibara nyingine: Utukanaji ni uchafuzi dhidi ya heshima ya mtu kwa maneno machafu na ulimi mbaya wenye lengo la kuvunja heshima yake. Na ama chuki, ni somo la maisha ya mtu kutokana na mtazamo wa kimaudhui na ubainifu ambao una fadhila na utukufu, au yale aliyochuma kutokana na dhambi na makosa. Basi linasifiwa la kwanza na linachukiwa la pili. Basi ambalo limo ndani ya vitabu vya Shi‟ah kwa mapitio ya aya mbalimbali na utajo wa Mola Hakimu, 42

Sahihi Bukhari, 1192, kitabu Tafsiri Qur‟an (Surat Nuur) nambari 4750.

64


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

ni ukosoaji na urekebishaji na sio utukanaji. Na lau lingelikuwa hili ni tusi basi vitabu vya Masunni ndio vilivyofungua mlango huu mbele ya uso wa Waislamu. Huyu hapa Bukhari na Muslim wamepokea katika Sahihi zao hadithi nyingi kuhusiana na kuritadi Maswahaba baada ya Mtume , na sisi tunanukuu kati ya hizo hadithi moja tu: Amepokea Abu Huraira kwamba hakika Mtume  amesema: “Siku ya Kiyama litakuja kwangu kundi miongoni mwa Maswahaba wangu – au akasema: Miongoni mwa umma wangu – basi wataondolewa kutoka katika hodhi, basi nitasema: Ewe Mola Wangu Mlezi! Maswahaba wangu, basi atasema: Hujui yale waliyoyazusha baada yako, hakika wao waliritadi juu ya visigino vyao kwa kurudi nyuma.”43 Mjadala wa kipande cha tatu: Pamoja na kuwa Mufti amefutu uharamu wa kuswali katika misikiti ya Shi‟ah isipokuwa yeye mwishoni amefutu kwamba, kama mtu ataingia na kuswali katika misikiti hii – hata akiwa na elimu kuwa haijuzu kuingia – basi swala yake ni sahihi. Ninasema: Vipi anafutu kusihi kwa swala, wakati mwenye kuswali ndani yake – kulingana na riwaya 43

Sahihi Bukhari 1655, kitabu Riqaaq, mlango katika Hodhi, nambari 6576, angalia hadithi zilizobakia katika nambari 6582, 6583, 6584, 6585, 6586, 6587.

65


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

yao – amelaaniwa kwa amali yake hiyo. Basi vipi unaoana uharamu wa amali pamoja na kusihi kwake, na vipi mwenye kuswali awe mlaaniwa pamoja na swala yake kuwa ni yenye kukubaliwa?! Na vipi kukusudia kujikurubisha na utekelezaji wa amri kuoane na hali ya kufukuzwa kutoka katika rehema ya Mwenyezi Mungu?! Naapa kwa haki, ni rahisi kiasi gani ijitihadi hii ambayo haihitaji kuelewa kwa yakini misingi na mambo matakatifu ya lazima. Kana kwamba utoaji wa fatwa kwa watu hawa hakuhitajii misingi na matakatifu ambayo yatamuandalia mazingira mazuri Mufti kutoa hukumu ya kisharia kutoka katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah ya Mtume , basi anafutu mas‟ala bila dalili juu ya uharamu wa uingiaji kwenye misikiti ya Shi‟ah, kisha anavunja aliyoyaeleza, bila dalili wala hoja! Haya ndiyo yaliyotupa sisi nafasi katika upitiaji na usomaji huu wa fatwa na ukosoaji wa kielimu. Na hakika imedhihirika kwetu udhaifu wa hilo na kwamba mambo hayo ni upuuzi mtupu. Sifa zote njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu.

66


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

UKOSOAJI WA NADHARIA YA UTHMANI KHAMIS KATIKA UOMBAJI MSAADA NA TAWASULI Hakika imani na ukafiri ni mambo mawili yaliyo wazi ndani ya Kitabu (Qurâ€&#x;ani) na Sunnah, na hayakuachiwa mtu mambo hayo mawili hadi mtu amkufurishe amtakaye na amhesabu muumini yule amtakaye.Na hakika inafuatwa katika wasifu wa mtu kwa imani au ukafiri. Hivyo ndivyo vigezo ambavyo vimepatikana katika vyanzo viwili vya msingi, na kukithiri kutajwa katika vitabu vya wanazuoni wa kifikihi na tafsiri na wana itikadi. Lakini jambo la kusikitisha ni kuwaona wale wanaojiita wasomi na wenye ijitihadi wanaukufurisha umma mkubwa miongoni mwa Waislamu bila dalili wala hoja yoyote ile. Hakika ukufurishaji unaofuata matamanio unapelekea kuusambaratisha umma wa Kiislamu, na kuwadhoofisha Waislamu, hadi kufikia kuenea kwa fujo na ukosefu wa amani ambayo ni miongoni mwa haja muhimu mno ya kimaumbile. Wala hakuna shaka kwamba hakika dhihiriko la ukufurishaji humea na kustawi katika jamii ya wajinga na yenye ufahamu mbaya wa hukumu za sharia takatifu. Nayo ni kati ya mambo ya hatari zaidi 67


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

juu ya Uislamu na mabaya zaidi katika njia ya kuchafua sura ya Uislamu kwa dhuluma na uadui. Na miongoni mwa wale waliopandisha bendera yake katika wakati wa sasa ni Sheikh Uthmani Khamiis – Mwenyezi Mungu atusamehe sisi na yeye. – Hakika utamkuta anamkufurisha yule anayeomba msaada kwa aliye hai katika jambo ambalo hawezi yeyote ila Mwenyezi Mungu, na anatoa hukumu kwamba huko ni kumkufuru na kumshirikisha Mwenyezi Mungu (s.w.t). Na msemaji akimuuliza Sheikh: Hakika kinachoombwa kikiwa hakiwezi kutimizwa isipokuwa na Mwenyezi Mungu, vipi mtu timamu amuombe kitu hicho asiyekuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t)?! Ilihali anajua maudhui ilivyo? Ndiyo, kama hajui hapo atakuwa na udhuru. Na kwa kuwa Sheikh hakutofautisha baina ya uwezo unaojitegemea na uwezo unaochumwa, alihukumu juu ya vigao viwili kwa hukumu moja!! Na kwa ajili ya kuweka wazi maudhui kama vile ilivyo tangulia – na kabla hatujaleta ufafanuzi wake katikati ya jibu – tunasema: Kwa mfano, hakuna shaka kwamba kuhuisha na kufisha ni vitendo viwili miongoni mwa vitendo vya Mwenyezi Mungu (s.w.t), wala hasimami kwa kuvitekeleza yeyote asiyekuwa Yeye. Na hakika zimejulisha aya chungu tele juu ya kujihusisha 68


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Mwenyezi Mungu (s.w.t) tu na matendo hayo mawili, anasema:

ٰ

َ​َ

ُ َ

َ

ُ

َ ّ

ُ ‫”إّنا ّن‬ ٰ ‫حن ّنحى اا‬ “…..‫ىجى َوّننح ُب ما قذمىا َوءارـ َش ُهم‬ ِ ِ “Hakika Sisi tunawahuisha wafu, na tunayaandika wanayoyatanguliza na athari zao.”44 Na anasema (s.w.t):

َ َ ٰ​ٰ َ ُ ُ َُ ُ ‫سض ُيحح َو ُر يد‬ ِ ‫له ملك ال ـى ِت وألا‬

“Yeye Ndiye Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi. Anahuisha na anafisha.”45 Na zisizokuwa hizo miongoni mwa aya ambazo zinahusisha suala la kuhuisha na kufisha kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) tu. Lakini wakati huo huo tunaona kwamba hakika Masihi Nabii Isa  anatoa habari kuhusiana na suala la kuhuisha kwake na kufisha kwake, anasema:

َُ َ َ َ َ َ َ َ ُ َُ َ ٰ َ “…..‫رّن الل ِـه‬ ِ ‫… وأ ِبشا ألال ه وألابش وأ ِى ااىجى ِب ِئ‬..” “…..Na niwaponye vipofu na wenye mbalanga. Niwafufue wafu kwa idhini ya Mwenyezi Mungu…..”46 44 45

Surat Yaasin; 36:12. Surat al-Hadid; 57:2.

69


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Hadi Mola Manani anamsemesha yeye  kwa kumwambia yeye kuwa anahuisha na anafisha, anasema:

َ َ َ َ َ ُ َُ ٰ َ‫ألا َبش َ بئرنى َوإر ُثخش ُج اا‬ “…..‫ىجى ِب ِئرنى‬ ‫… وث ِبرا ألال ه و‬..” ِ​ِ ِ ِ “Na ulipowaponyesha vipofu na wenye mbalanga kwa idhini Yangu, na ulipowatoa wafu kwa idhini yangu.”47 Na yeyote mwenye maarifa angalau duni zaidi kuhusu tafsiri ya Qur‟ani tukufu anajua kwamba hakuna mpingano kati ya makundi mawili ya aya. Hakika kundi la kwanza linaangalia uwezo usiokuwa na mipaka usiochumwa wa kuhuisha maiti na kila ambalo asiloliweza mwingine. Na hili linahusika tu na Mwenyezi Mungu (s.w.t). Basi yule atakayemsifu mwingine kwa uwezo huo na kudhani kwamba kwa nafasi yake na bila ya uwezo wa kuchuma anaweza kuhuisha na kufisha, kwa hakika amekufuru. Bali lau kama atadai hilo hata katika vitendo vya kawaida ambavyo anavitenda asiyekuwa Yeye (s.w.t) kama vile kusimama na kukaa, na akadhani hakika yeye mwenyewe ndiye ana uwezo wa kujitegemea usiotoka 46 47

Surat Aali-Imran; 3:49. Surat Aali-Imran; 5:110.

70


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

kwa Mwenyezi Mungu, kwa maana akadai kwamba anasimama na anakaa kwa uwezo wake binafsi tu bila kuingiliwa na uwezo wa Mwenyezi Mungu, kwa hakika atakuwa amekufuru, basi muda huo anakuwa ni Mungu wa pili. Na ama kundi la pili, lenyewe linaangalia yule anayefanya miujiza na karama mbalimbali ambazo sio katika matendo ya watu wengi, lakini ni kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) na nikwa uwezo wenye kuchumwa kutoka Kwake, na hili ni tawhiid halisi. Na kwa kuwa Sheikh hakutaja kigezo cha imani na ukafiri, amedai kwamba “Hakika yule aliyefanya tawasuli kwa maiti katika jambo ambalo hana uwezo juu yake isipokuwa Mwenyezi Mungu hakika amekufuru.” Wakati ambapo hakika mwenye akili timamu hafanyi tawasuli kwa mtu katika sehemu ambayo anajua haliwezi hilo isipokuwa tu Mwenyezi Mungu, bali hakika anafanya tawasuli kwa taswira ya kwamba Yeye (s.w.t) ni Mwenye uwezo zaidi juu ya hilo na ndiye aliyempatia mtu uwezo juu yake. Kisha hakika yeye – kwa hilo – huenda anakuwa ni mwenye kupatia na huenda ni mwenye kukosea. Na kosa katika maudhui hizo halipelekei ukafiri. Anasema (s.w.t):

ٰ ُ َ​َ َ َ​َ ُ َ َ ٌ ‫ينم ُج‬ ‫ناح في ا أخطأثم ِب ِه َولـ ِنن‬ ‫… ول س عل‬..” َ َ َ ُ ُ ‫ما َج َع َ َذت ُق‬ ً ‫لىت ُنم َوماّن اللـه غ‬ “‫ىسا َسحي ً ا‬ 71


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

“Si vibaya kwenu kwa mlivyokosea, lakini kwa yale ziliyoyakusudia nyoyo zenu.Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.”48 Na pima juu ya hili maudhui nyingine, na tofautisha kati ya uwezo usio na kikomo na uwezo unaochumwa. Basi yule anayetafuta kitu miongoni mwa karama na yasiyo ya kawaida, hakika anaomba hayo kutoka kwa mawalii kwa kuamini kwamba (s.w.t) amempatia walii uwezo huo, na hana uwezo wa kujitegemea juu ya hilo isipokuwa Mwenyezi Mungu. Na huyu hapa Ibn Taymiyya – Imam wa Sheikh na Marjaa wake katika mizizi na matawi – anasema: Watu wa sunna hawatakiwi kumkufurisha kila yule ambaye amesema kauli na akakosea, kwani hakika Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema: “Ewe Mola Wetu! Usituadhibu tukisahau au tukikosea.”49 Na sisi hatuna haja ya fatwa hii na ile, basi Kitabu kitukufu, Sunnah ya Mtume na ijimai ya Waislamu ni dalili kubwa zaidi juu ya kumpambanua muumini na kafiri. 48

Surat al-Ahzaab; 33:5. Majmuuatul-Fatawa, Juz. 7, uk. 684 cha Ibn Taymiyya.

49

72


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Na mwisho wa hili tunageukia mtazamo wa Sheikh kuelekea hatari inayopatikana kwa kile ambacho alicho kitaja Imam Abu Abdillah Muhammad bin Idrisa Shaafii, ambapo amesema: “Hakika sisi tumekuta umwagaji wa damu ndio dhambi kubwa zaidi anayoasiwanayo Mwenyezi Mungu (s.w.t) baada ya shirki.”50 Maana yake ni kwamba ukufurishaji utakapotokea katika sehemu isiyo yake basiunakuwa ni maasi makubwa zaidi baada ya kumshirikisha Mwenyezi Mungu (s.w.t). Hivyo tunamuusia asiuachie ulimi wake moja kwa moja bila ya kutadaburi katika Kitabu na Sunnah na yale ambayo wamekusanyika Waislamu juu yake, katika ukufurishaji wa Waislamu wengine wasiokuwa Mawahabi. Kinyume na hivyo atakuwa anatenda jambo linalotoa picha mbaya kwa Uislamu mbele ya wasiokuwa Waislamu, jambo linalozuia kuenea kwa Uislamu pande zote za dunia, bali inapaswa iwe kaulimbiu yake ni kauli ya msemaji: “Hakika sisi ni umma mmoja, inatukusanya itikadi yetu. Na dini ya uongofu inatukusanya sisi wafuataji. Na Uislamu unaleta upendo nyoyoni mwetu, popote tutakapokwenda kwenye uongofu hata tukiwa makundi makundi.”51 50

Al-Ummu, Juz. , uk. 205. LIl-Adiib Shaai‟r, mwandishi Muhammad Abdul-Ghanii Hasan Mmisri, (amekufa mwaka 1405H). 51

73


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Chaneli ya Wuswal ilirusha kipindi cha Sheikh Uthmani Khamiis, na aliulizwa katika kipindi hicho maswali kuhusu tofauti baina ya uombaji msaada na tawasuli? Basi akasema katika jibu lake – baada ya tafsiri ya uombaji msaada kwa dua: “Hakika hilo linafaa ikiwa mwingine ni muweza juu ya utekelezaji wa maombi ya muombaji msaada, kama vile katika kauli Yake (s.w.t) inayosema: „Yule aliye katika kundi lake alimtaka msaada dhidi ya yule aliye katika adui zake.‟”52 Na ama akiwa sio muweza basi akataja hapo aina mbalimbali, nazo ni: 1. Amuombe msaada mtu katika jambo ambalo hana uwezo juu yake ila Mwenyezi Mungu (s.w.t), basi huyo amefanya shirki na amemkufuru Mwenyezi Mungu (s.w.t). 2. Amuombe msaada asiyekuwepo kana kwamba yeye anasema: Huyu ni yule ambaye hakifichiki kwake kitu cha uficho. 3. Amuombe msaada maiti kana kwamba anasema huyu ni yule yu hai ambaye hafi. Na pindi anapomuomba msaada juu ya kitu ambacho hana uwezo nacho ila Mwenyezi Mungu, ni kama vile yeye anasema: Huyu ni yule ambaye ni muweza juu ya kila kitu. Basi tusome yale ambayo aliyoyataja moja baada ya lingine. 52

Surat al-Qasas; 28:15.

74


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

1. Kuomba msaada mtu aliye hai: Sheikh amegawa uombaji msaada kwa aliye hai katika sehemu mbili: i. Yale ambayo anaweza kuyatekeleza mtu aliye hai: Sheikh amehukumu kufaa kwake kwa kutoa ushuhuda wa aya, nasi hatuna maneno juu yake. ii. Yale ambayo hawezi kuyatekeleza ila Mwenyezi Mungu: Sheikh amehukumu kwamba kufanya hivyo ni shirki na ni kumkufuru Mwenyezi Mungu (s.w.t). Ninasema: Hakika muombaji msaada katika jambo ambalo hana uwezo nalo ila Mwenyezi Mungu (s.w.t), lakini kwa kuamini kwamba huyo walii ni muweza juu ya hilo kwa uwezo kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) na uwezesho kutoka Kwake, je, hilo linakuwa ni kumkufuru na kumshirikisha Mwenyezi Mungu? Jibu ni hapana, kwa sura mbili, nazo ni: Ya kwanza: Hakika Nabii Suleiman bin Daud ď „ alimuomba mmoja wa wale waliohudhuria katika hadhara yake amletee kiti cha enzi cha Balqiis, kama ilivyo katika kauli yake (s.w.t), anasema: 75


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

َ َ َ َ َ ُ ُ َ ۟ ُ َ​َ َ ُ َٰ َ ” ‫جل أّن‬ ‫ششها ق‬ ِ ‫قال يـأّيها االؤا أينم يأثين ِةع‬ ‫َ ۠ا‬ َ َ ٌ ُ َ َ ‫ااج ِ ّن أّنا ءاثيك ِب ِه‬ ‫َي‬ ِ ‫أثىنى م ِل مّن قال ِع شرد ِمن‬ َ َ ّ َ َ َ َ َ َ َ ‫َو ِإنى َعل ِيه ل َق ِى ٌي‬ ‫قامك‬ ِ ‫قجل أّن ثقىم ِمن م‬ ‫ٰ َ ۠ا‬ َ َ ٌ َ َ َ َ ٌ ‫نذ ُ ع‬ ‫النحـ ِب أّنا ءاثيك ِب ِه‬ ‫قال الزي ِع‬ ‫أممّن‬ ِ ‫لم ِمن‬ ِ َ ُ َ َ َ َ​َ َ َ َ َ “…..‫قجل أّن يشثذ ِإليك شفك‬ “Akasema: Enyi wakuu wa baraza! Ni nani kati yenu atakayeniletea kiti chake cha enzi kabla hawajanijia nao wamekwisha salimu amri? Akasema Afriti katika majini: Mimi nitakuletea kabla hujainuka mahali pako. Na mimi hakika ninanguvu, mwaminifu. Akasema mwenye elimu ya Kitabu: Mimi nitakuletea kabla ya kupepesa jicho lako…..”53 Basi tunamuuliza Sheikh: Hakika uletaji wa kiti cha enzi cha Balqiis kwa njia mbili zilizotajwa katika aya uko nje ya uwezo wa viumbe, basi vipi Nabii Suleiman  amuombe jambo hilo ambalo hana uwezo juu yake ila Mwenyezi Mungu (s.w.t)?! Ikiwa Sheikh atasema: Hakika Nabii Suleiman  alikuwa anajua kwamba hakika Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewapa hao uwezo huo na kwa hivyo 53

Surat an-Naml; 27:38-40

76


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

akawaomba kutoka kwao. Tunasema: Basi na hapa ndivyo ilivyo, muombaji msaada anajua kwa yakini kwamba hakika muombwa msaada ni miongoni mwa wale waliowezeshwa na Mwenyezi Mungu (s.w.t), na ni Yeye (s.w.t) Ndiye aliyempa uwezo mtu huyo juu ya utekelezaji wa yale ambayo ameomba. Hivyo inakuwa ni sawa na ombi la Suleiman, ila hakika yeye Sheikh anatofautisha kwa kuona kuwa Suleiman  alikuwa ni mwenye kupatia katika itikadi yake, lakini huyu muombaji msaada ni mwenye kukosea, ilihali msingi wa maombi hayo mawili ni jambo moja, basi ni vipi moja ya mambo mawili ni tawhid na jingine ni shirki? Umma wa Kiislamu umekubaliana kwamba muujiza ni dalili yakinifu juu ya ukweli wa mwenye kudai unabii. Hakuna shaka hakika watu walikuwa wakimuomba yule anayejidai kuwa ni Nabii, alete na kutenda yale ambayo hana uwezo nayo ila Mwenyezi Mungu (s.w.t), je, ombi lao lilikuwa – kwa lengo la kupata uhakika – linapelekea ukafiri? Hakuna shaka kwamba hakika Manabii wamepewa uwezo na Mwenyezi Mungu (s.w.t) wakufanya mambo ambayo hayafanyi hayo ila Mwenyezi Mungu (s.w.t), kama vile ubadilishaji wa fimbo kuwa nyoka, na kupasua bahari katika sehemu mbili, na uponyaji wa ukoma na mbalanga, na ufufuaji wa wafu, hadi hakika Masih  alikuwa akinadi hilo akisema: 77


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

‫ُ ُ ٔـ‬ َ َّ ُ َ ُ َ َّ ُ ‫…أنى قذ ِجئحنم ِبـ َاي ٍة ِمن َسِّتنم أنى أخل ُق لنم‬..” َٔ َ ّ َ ً َ ُ َ َ ِ ‫الطمر َف َأّن ُ ُخ‬ ‫رّن‬ ‫ِم َن الط ِمّن ل َهيـ ِة‬ ِ ‫فيه فينىّن مرا ِب ِئ‬ ِ َُ َ َ َ َ َ َ َ ُ َُ َ َ ٰ َ ‫رّن الل ِـه‬ ِ ‫الل ِـه وأ ِبشا ألال ه وألابش وأ ِى ااىجى ِب ِئ‬ “…..

“Mimi nimewajia na ishara kutoka kwa Mola Wenu, hakika mimi nitawafanyia kama namna ya ndegekatika udongo; kisha nimpulizie awe ndege kwa idhini ya Mwenyezi Mungu na niwaponye vipofu na wenye mbalanga. Niwafufue wafu kwa idhini ya Mwenyezi Mungu...”54 Na lau tutajaalia hakika mtu miongoni mwa wana wa Israeli alipata uhakika na akamuomba Masih  moja ya mambo haya, je, analaumiwa juu ya elimu yake hii, au je Masihi alimsifu kuwa ameritadi?! YA PILI Hakika muombaji msaada kwa mtu katika kitendo ambacho hana uwezo nacho ila Mwenyezi Mungu (s.w.t), kama atajua kuwa mtu huyo hawezi kamwe hatamuomba, lakini anamuomba kwa kuwa anajua fika kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) amemwezesha 54

Surat Aali-Imran; 3:49.

78


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

juu ya hilo, na amemneemesha kwa utukufu huo, na kwahiyo ndio maana anamuomba hilo. Lakini anaweza kuwa amekosea sehemu ya kuomba msaada, je, kwa kukosea huko kinasifiwa kitendo chake hiki kuwa ni ukafiri, pamoja na kuwa yeye katika undani wa dhati yake anajua hakika vitendo vimegawanyika sehemu mbili, nazo ni: i. Yale ambayo hana uwezo nayo ila Mwenyezi Mungu. ii. Yale ambayo hana uwezo nayo mwingine ila kwa kupewa uwezo na Mwenyezi Mungu. Na yeye anaitakidi kwamba hakika hapa ni sehemu kati ya sehemu ambazo Mwenyezi Mungu amemwezesha walii muombwa msaada, kama vile uponyaji wa maradhi na ufufuaji wa maiti. Na wakati huo anamuomba amali hiyo yule walii aliye hai. Hata kama yeye ni mwenye kukosea sehemu ya kuomba, lakini yeye kwa ujumla ni mwenye kupatia kwa kujua kuwa yale ambayo hana uwezo nayo ila Mwenyezi Mungu haombwi mwingine asiyekuwa Yeye. 2. Kumuomba msaada asiyekuwepo: Sheikh amesema: Mtu anapomuomba msaada mtu asiyekuwepo, ni kana kwamba yeye anasema: Huyu ni yule ambaye hakifichikani kwake chochote kilichojificha. 79


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Ninasema: Vipi Sheikh aseme hakika kumuomba msaada asiyekuwepo katika mambo maalum inalazimu kuitakidi kwamba asiyekuwepo hakifichikani chochote kwake? Je, anayo dalili juu ya ulazima huo miongoni mwa sharia au akili? Hakika maana ya yule ambaye hakifichikani kwake chochote, ni kwamba yeye ni mjuzi wa mambo yote yaliyojificha na yale yanayoonekanaardhini, mbinguni na angani na yale yaliyopo chini ya mchanga na juu ya mbingu. Na ama yule anayemuomba asiyekuwepo aliye hai, hakika huwa anaamini kuwa huyu asiyekuwepo anasikia maneno yake haya katika hali maluum, na iwapo litasihi hilo basi ni vizuri, na iwapo atakuwa ni mwenye kukosea basi hukumu yake ni kosa. Na ama kufanya hivyo kuwa kunalazimiana na hali ya muombwa msaada kuwa hakifichikani kwake chochote, hilo ni dhana yake tu, wala hakuna ulazima huo. Kisha yule anayeitakidi kwamba asiyekuwepo anasikia maneno yake, anaitakidi kwamba hakika Mwenyezi Mungu (s.w.t) ndiye aliyempa uwezo huo. Amemzawadia uwezo wa kusikia maneno ya yule anayemuomba. Basi huyu hapa Mtukufu Mtume  anawazungumzisha wanafiki kwa kauli yake (s.w.t):

ُ

َ

َُ

َ​َ َ َ

َ “…..‫خجاسلم‬ ِ ‫… قذ ّنجأّنا اللـه ِمن أ‬..” 80


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

“…..Hakika Mwenyezi Mungu amekwishatueleza habari zenu.”55 Kama vile Mtume  alivyowapa habari baadhi ya wakeze na akasema:

َ َ

َ

َ ‫… ّن َجأن َى‬..” ُ ‫الع‬ ُ ‫ليم اال‬ “‫جمر‬ ِ “Kaniambia Mjuzi Mwenye habari.”56 Na lau tutajaalia kwamba hakika walii miongoni mwa mawalii wake ameombwa msaada na mtu kwa itikadi kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) amempatia uwezo wa kusikia maneno yake, je, mwenye kuitakidi hilo anatoka katika wigo wa Uislamu? Na je amemshirikisha Mwenyezi Mungu? Je, amemjaalia walii muombwa msaada ni mshirika wa Mwenyezi Mungu, ambaye hafichikani na chochote kilichojificha? Basi mna nini nyinyi, vipi mnahukumu? Na huko kuna jambo lingine tunataka msomaji alitupie jicho, nalo nikwamba, suala la kuwepo mtu mwenye kusemeshwa na Malaika ni miongoni mwa yale ambayo umekubaliana umma wa Kiislamu juu ya uwepo wake katika umma huu. Yaani uwepo wa wale wasemezwao na malaika bila ya utume wala uonaji 55

Surat-Tawba; 9:94. Surat-Tahrim; 66:3.

56

81


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

wa sura, au kwa kupewa ilhamu na kuingiziwa katika akili yake kitu kutokana na elimu kwa njia ya ilhamu. Au anamuingizia yeye moyoni mwake hakika zilizojificha juu ya mwingine. Ushahidi juu ya hilo ni yale aliyoeleza Bukhari katika Sahihi yake katika mlango wa sifa za Umar bin Khatwab.Imepokewa kutoka kwa Abu Huraira amesema: Mtume  amesema: “Hakika kati ya wale waliokuwa kabla yenu miongoni mwa wana wa Israeli walikuwemo watu wanaozungumzishwa na hawakuwa Manabii. Kama miongoni mwa umma wangu yupo mtu wa namna hiyo basi ni Umar.”57 Na lau tutajaalia kwamba muombwaji ni miongoni mwa waliosemeshwa na Malaika katika umma wa Kiislamu, naye akawa amejua kupitia moja ya njia zilizotajwa hapa kabla, je, maana ya hilo ni kuwa yeye ni mjuzi wa mambo yote ya ghaibu (yasiyoonekana) na yanayoonekana, wala hakifichikani kwake chochote kilichojificha? 3. Kumuomba msaada maiti: Sheikh amesema: Mtu anapomuomba msaada maiti ni kama vile anasema: Huyu ni aliye hai ambaye hafi, na pale anapomuomba kitu ambacho hana uwezo nacho 57

Sahihi Bukhari: 901, kitabu fadhila za masahaba, nambari 3989, angalia katika tafsiri ya hadithi: Kitabu Irshaadu Saari sharhu Sahihi Bukhari, Juz. 6, uk. 99.

82


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

ila Mwenyezi Mungu, ni kana kwamba anasema: Huyu ni yule ambaye ni muweza juu ya kila kitu. Ninasema: Hakika amepangilia juu ya uombaji msaada kwa maiti, mambo mawili, nayo ni: i. Hakika yeye ni yu hai ambaye hafi. ii. Huyu ni yule ambaye ni muweza juu ya kila kitu. Na ulazima katika yote mambo mawili umekosekana, na inadhihirika sura hiyo kwa yale yafuatayo: La kwanza: Basi hakuna ulazima kuwa muombwa msaada yu hai na ni ambaye hafi. Na hilo ni kwamba muombaji msaada wakati wa kuomba anaitakidi kwamba yeye muombwa yu hai katika maisha ya baada ya kufa na kabla ya ufufuo, lakini anakufa wakati wa kupulizwa parapanda la kwanza, basi uko wapi ushirikiano kati yake na Mwenyezi Mungu? Hakika Mola Manani (s.w.t) anawasifu wale ambao wameuawa katika njia ya Mwenyezi Mungu kwamba wao: “Ni hai na wanaruzukiwa na Mola wao mlezi� na dhahiri ya aya ni kwamba watu hao ni hai katika uhai wa barzakh hadi siku aitakayo Mwenyezi Mungu. Je, huko ni kuitakidi kuwa wao wako hai hawafi abadani? La pili: Hakika uombaji wa msaada kwa kitu ambacho hana uwezo nacho ila Mwenyezi Mungu 83


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

hailazimu kusema kwamba yeye ni muweza juu ya kila kitu. Kwani hakika kadhia ni ya kipengele kimoja – ninamaanisha: Kuwa na uwezo juu ya uponyaji maradhi haulazimu kuwa ni muweza juu ya kuumba viumbe wa mbinguni na ardhini. Je, itikadi ya uwezo juu ya jambo mahsusi ni dalili juu ya itikadi ya uwezo juu ya kila kitu? Kisha hakika muombaji katika jambo ambalo hana uwezo nalo juu yake isipokuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t), anaitakidi kwamba walii aliye hai amepewa na Mwenyezi Mungu (s.w.t) uwezo juu ya jambo hilo. Na lau atakuwa ni mwenye kukosea katika kuitakidi basi atahesabiwa ni mwenye udhuru katika jambo, lakini mwenye kupatia katika jambo la ujumla, nalo ni kujua kwamba jambo husika ni miongoni mwa yale ambayo hana uwezo nayo ila Mwenyezi Mungu. Ikiwa Mwenyezi Mungu hakumpatia uwezo huo yeyote miongoni mwa waja wake, hivyo haliombwi ila kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t). MANENO YA SHEIKH KUHUSIANA NA TAWASULI Sheikh ameigawa tawasuli – kufuatana na wale waliomtangulia - katika makundi mawili: Mosi: Tawasuli sahihi, nayo ni ibara ya vigawanyo vitatu vifuatavyo: 84


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

i. Tawasuli kuelekea kwa Mwenyezi Mungu kwa kutumia majina Yake na sifa Zake. ii. Tawasuli kuelekea kwa Mwenyezi Mungu kupitia matendo mema. iii. Tawasuli kuelekea kwa Mwenyezi Mungu kwa dua za watu wema. Na hapa hatuna maneno kwalo. Na hakika imepokewa tawasuli kwa mambo haya matatu katika hadithi mbalimbali za Maimamu wa Ahlul-Bayt . Tunatamani Sheikh awe amepitia hayo. Pili: Tawasuli isiyokuwa sahihi, nayo ameitaja katika mambo mawili: i. Tawasuli kwa dhati ya maiti, kana kwamba anasema: Ewe Mwenyezi Mungu! Hakika mimi ninakuomba kupitia kwa Muhammad. Akasema hili ni jambo la haramu na sio ukafiri. ii. Tawasuli kwa cheo cha Mtume  kwa ajili ya ukaribu wake kwa Mwenyezi Mungu, hakika amehukumu pia uharamu wake. Ninasema: Ama ya kwanza inaruhusiwa kwa kupokewa kwake, sio katika hadithi moja tu bali katika hadithi chungu nzima, na hapa tunataja kwa ufupi hadithi mbili: Hadithi ya mlemavu wa macho: Wanahadithi wamekubaliana juu ya kusihi kwa hadithi ya kipofu – 85


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

hata Ibn Taymiyya: Na tunakuletea andiko lake, ni juu yako kulisoma na kupitia sanad yake pamoja na dalili yake. Imepokewa kutoka kwa Uthmani bin Hunayf amesema: Hakika mtu mmoja kipofu alikuja kwa Mtume  akasema: Niombee mimi ili nipone. Mtume  akasema: “Ukitaka nitaomba, na ikiwa utataka utasubiri, nalo ni heri zaidi.” Akasema: Basi omba. Hapo Bwana Mtume  akamwamrisha mtu huyo atie wudhuu vizuri na aswali rakaa mbili na aombe dua hii: “Allahumma inni asaluka wa atawajjahu ilayka binabiyyika nabiyyi rahmat, ya Muhammad inni atawajjahu bika ila rabbi fi haajati lituqdha, Allahumma shaffi‟hu fiyya.” Maana yake: Ewe Mwenyezi Mungu! Hakika mimi ninakuomba na ninaelekea kwako kupitia Nabii Wako, Nabii mwenye rehema, ewe Muhammad! Hakika mimi ninapitia kwako kuelekea kwa Mola Wangu Mlezi katika haja zangu ili zikidhiwe, ewe Mwenyezi Mungu! Mshufaiye kwangu.” Ibn Hunayf akasema: Naapa kwa Mwenyezi Mungu hatukutawanyika sisi na wala kikao hakikuwa kirefu, hadi akaingia kwetu kana kwamba hakuwa na madhara yoyote. 86


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Upitiaji wa hadithi kisanadi na kidalili: Hakuna maneno katika usahihi wa sanad ya hadithi hii, hata Imam na kiongozi wa mawahabi - Ibn Taymiyya – ameizingatia hadithi hii kuwa ni sahihi na akakata shauri kuwa aliyekusudiwa hapo ni (Abu Ja‟far) aliyekuwepo katika sanad ya hadithi, naye ni Abu Ja‟far Khutwami ambaye ni mkweli mwaminifu.58 Muhammadi Nasiib Rifaa‟ – mwandishi wa kiwahabi wa zama hizi ambaye daima anajitahidi kudhoofisha hadithi mbalimbali zinazohusiana na tawasuli – kuhusu hadithi hii anasema: “Basi juu ya hili hadithi inakuwa hapana shaka ni sahihi kabisa.”59 Na anasema: Hakika Nasaai amepokea hadithi hii pia Bayhaqi, Twabarani, Tirmidhi na Hakim katika kitabu chake Mustadrak, lakini Tirmidhi na Hakim wametaja sentensi hii “Allahumma shaffi‟ni fiihi” sentensi inajulisha “Shaffi‟hu fiyya”60 58

Imekuja katika kitabu Musnad Ahmad: “Abu Ja‟far Khutwami” ama katika kitabu Sunan ibn Maaja mwanafiqhi “Abu Ja‟far” tu. 59 Tawasuli ilal-Haqiiqat Tawasuli, uk. 228-229, chapa ya Beirut mwaka 1394H. 60 Tawaswul ilal-Haqiiqat Tawasuli, uk. 228-229, chapa ya Beirut mwaka 1394H.

87


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Baada ya hayo yote… hakuna sehemu ya mjadala kuhusiana na sanad ya hadithi au kuiponda hiyo. Na ama dalili ya hadithi, lau ningelitanguliza hadithi hii kwa yule anayeijua vizuri lugha ya kiarabu na akili yake iko safi. Yuko mbali na majarida ya kiwahabi na utata wao kuhusiana na suala la tawasuli, kisha ningelimuuliza: Hivi ni kitu gani Mtume  alimwamrisha yule kipofu wakati alipomfundisha dua ile? Basi jibu lake linakuwa – kwa haraka – hakika Mtume  alimfundisha yeye amuombe Mwenyezi Mungu (s.w.t) na katika dua yake afanye tawasuli kuelekea kwa Mwenyezi Mungu kupitia Nabii Wake Muhammad, Nabii mwenye rehema, na amuombe Mwenyezi Mungu amponye kwayo. Na maana hii ni kidhibiti ambacho kinafahamika kutokana na maneno ya hadithi iliyokwishatajwa hapo kabla. Na katika maelezo yafuatayo tunaigawa hadithi katika sentensi kadhaa ili kuzidisha uwazi zaidi: i. “Allahumma inni as-aluka wa atawajjahu ilayka binabiyyika” Maana yake: “Ewe Mwenyezi Mungu! Hakika mimi ninakuomba na ninakuelekea Kwako kupitia Nabii wako.” Hakika neno “nabiyyika” linafungamana na 88


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

yale ambayo yaliyopo kabla yake, yaani “As-aluka” (Ninakuomba) kupitia nabii Wako na “Atawajjahu ilayka” (ninaelekea Kwako) kupitia Nabii Wako. Kwa ibara ya wazi zaidi: Hakika alimuomba Mwenyezi Mungu (s.w.t) kupitia Nabii , na makusudio ya “Nabii” ni nafsi iliyotakasika na sio dua ya Mtume. Ama yule anayekadiria neno “dua” katika kauli yake, “Ninakuomba kupitia kwa nabii Wako” yaani kwa dua ya nabii wako, basi huko ni kuhukumu bila dalili na madai yaliyo tofauti na dhahiri. Na mdai katika taawili hii, ni kwamba mwenye kuawili haitakidi kufaa kwa tawasuli kwa nafsi ya Nabii, basi analazimisha katika ukadiriaji wa neno “dua” ili isemwe: Hakika tawasuli kwa dua ya Nabii hakuna mushkeli kwayo. Na hili linahalalisha rai iliyotangulia. Na la kushangaza ni kwamba hakika watu hawa wanafasiri kwa tafsiri sisisi, zile sifa zilizotajwa katika maandiko, wala hawatumii taawili katika kauli ya Mwenyezi Mungu (s.w.t): “Na mbingu tulizozijenga kwa mikono.” Lakini wao pindi lilipobana koo juu yao katika sehemu husika wanaibadilisha hadithi na wanaiawili hiyo kwa kwenda mbali zaidi ya yale yanayowezekana. ii. “Muhammad nabii mwenye rehema.” 89


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Ili yawe wazi makusudio yake ya kumuomba Mwenyezi Mungu kupitia Nabii na shakhsia yake na utukufu wake, kwa hakika imekuja baada ya neno “Nabii Wako” sentensi “Muhammad Nabii mwenye rehema” ili lengo liwe wazi zaidi. iii. “Ewe Muhammad! Hakika mimi ninaelekea kwa MolaWangu mlezi kupitia kwako.” Paragrafu hii inajulisha kwamba hakika mtu ameifanya nafsi ya Nabii ni njia ya dua yake, sio dua yake  yaani: Hakika hiyo ni tawasuli kwa dhati ya Nabii na sio kwa dua yake. Hakika yamekuwa wazi yale ambayo tuliyoyataja kwamba, kitovu katika dua yote ni utu wa Mtume  na nafsi yake tukufu, na hakuna dalili ya kutawasali kwa dua yake  kiasili. Na kila yule anayedhani kuwa kipofu alitawasali kwa dua ya Nabii na si kwa utu wake, kwa hakika ameghafilika na paragrafu za hadithi. Na wewe kama utachunguza kauli yake: “Ewe Mwenyezi Mungu! Hakika mimi ninakuomba na ninaelekea Kwako kupitia Nabii Wako, Nabii mwenye rehema” na kauli yake: “Ewe Muhammad! Hakika mimi ninapitia kwako kuelekea kwa Mola Wangu Mlezi” itadhihirika kwako kwa uwazi kabisa kwamba, alikazia hilo juu ya utu wa Mtume . Na lau 90


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

lingelikuwa lengo ni dua ya Nabii ingelikuwa ni sahihi aseme: Ninakuomba kwa dua ya Nabii. Yamebakia maneno katika kauli yake: “Na mshufaiye kwangu” basi huenda akafikiria kwamba fuo la maneno ni kwamba kipofu alifanya tawasuli kwa dua ya Nabii, katika hali ambayo maana yake ni kwamba alitaka kuifanya dua ya Nabii  ni wajibu, lakini dai hilo ni batili kwa sura mbili: Mosi: Inadhaniwa kuwa hakika maana yake ni mfanye Nabii kuwa muombezi wangu na ukubalie uombezi wake katika haki yangu, kama vile tunasema: Na ukubalie uombezi wake na liinue daraja lake. Pili: Basi tujaalie kuwa maana ya kipengele hiki ni: Itikia dua yake kwa haki yangu, lakini hayathibiti yale waliyoyataka, kwani hakuna kizuizi Mtume  kuwa aliomba dua na wakati huo huo mlemavu wa macho awe aliomba dua aliyofundishwa na Mtume  akifanya tawasuli kwa dhati ya Mtume , basi hakuna msigano wowote baina ya amali mbili hizo. Na kwa ibara nyingine: Mtume  alifanya amali mbili: i. Alimfundisha kipofu dua ambayo ndani yake ipo tawasuli ya Mtume . 91


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

ii. Mtume  alisimama kwa kumuombea yeye dua, na hakuna msigano kati ya mambo hayo mawili. Na juu ya ukadiriaji wowote ule, sisi tunajikita juu ya matini ya dua ambayo Mtume  alimfundisha yule kipofu na kwayo zipo dalili nyingi za wazi kwamba tawasuli ilikuwa ni kupitia kwa Mtume . Uombaji Wao Wa Mvua Kupitia Kwa Abbasi; Baba Mdogo Wa Mtume : Bukhari ameeleza kwa sanad yake hadi kwa Anas bin Malik, amesema: Hakika ilikuwa pindi wanapokumbwa na ukame, Umar bin Khatwab alikuwa akiomba mvua kupitia kwa Abbas bin AbdulMutwalib, akisema: “Allahumma inna kunna natawassalu ilayka binabiyyika , wa inna natawassalu ilayka bi‟ammi nabiyyina fas-qinaa.” Maana yake: Ewe Mwenyezi Mungu! Hakika sisi tulikuwa tunafanya tawasuli kupitia Nabii Wako , na hakika sisi tunafanya tawasuli kwako kupitia baba mdogo wa Mtume wetu, tuletee mvua.” Basi wanapata mvua.61 Na wewe ukimpelekea mwarabu yeyote hadithi hii, ambaye hajakumbana na mijadala ya kiwahabi na 61

Sahihi Bukhari: 238, nambari 1010, kitabu Istisqaa, mlango; watu kumuomba imam pindi ukame ulipowapata.

92


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

malumbano yao kuhusiana na tawasuli kwa kupitia nafsi zilizotakasika, atahukumu kwa kukata shauri kwamba, hakika khalifa Umar bin Khatwab pindi alipofanya tawasuli kwa dhati ya Abbas ni kwa kuwa ni baba mdogo wa Mtume , na hakika kutawasuli kwake kwa baba mdogo wa Mtume  ilikuwa ni sababu yakutawasuli kwa dhati ya Mtume , kwa uwepo ukaribu baina ya Abbas na Mtume . Na kwa hivyo akamchagua yeye, na kama si hivyo alikuwepo miongoni mwa Maswahaba yule ambaye ni bora zaidi ya Abbas kwa nyanja mbalimbali. Kisha hakika Albaani yule muwahabi mwenye msimamo mkali, pindi ilipowekwa mbele yake dalili hii yenye kukata shauri, alijaribu kufanya taawili ya hadithi kwa namna ambayo kama mwingine asiyekuwa yeye angefanya taawili katika sehemu isiyokuwa hii, basi angetuhumiwa kwa Ujahiliyyah, alisema: “Hakika makusudio yake ni„kwa dua ya baba mdogo wa Nabii Wako‟wakati ambapo lililozoeleka kwa Maswahaba ni desturi yao ya kwenda kwa Mtume  na kumuomba dua ya kupata mvua. Na Sunnah inafasiri baadhi yake kwa baadhi. Basi yanakuwa makusudio ni kutawasuli kwa dua, na sio tawasuli kwa dhati yake, kwani tawasuli kwa dhati yake haipo katika Sunnah ya Mtume.”62 62

Tawasuli, uk. 51 cha Arbanu, kimechapwa na maktabatul maarif.

93


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Anajibiwa kwa Mambo Yafuatayo: Moja: Hakika lau tawasuli hapa ingelikuwa ni kwa dua ya baba mdogo wa Mtume  kwa kuwa ni dua ya Mwislamu, ingelikuwa ni lazima kutawasuli kwa dua ya aliye bora zaidi kuliko Abbas, kwani hakika dua ya aliye bora zaidi ndio iliyo karibu zaidi kukubaliwa kuliko dua ya mwingine. Na linalozingatiwa na mwandishi ni kwamba hakika Umar ni mbora zaidi katika watu baada ya Mtume , na Abu Bakri naye anasahihisha hadithi “lau angelikuwepo Nabii (baada ya Muhammad ) basi angekuwa Umar.”63 Na zao la maneno ni: Hakika lau ingelikuwa makusudio ya tawasuli ni kwa dua, ingelikuwa ni juu ya khalifa achague mbora zaidi ya Maswahaba, na wa mwanzo wao ni yeye mwenyewe. Na kama aliacha kufanya tawasuli kupitia kwake mwenyewe, kutokana na unyenyekevu, basi ni kwa nini aliwaacha waliobora zaidi –ninamaanisha wale ambao waliotangulia katika Uislamu kwa imani na jihadi – kushinda baba mdogo wa Mtume . Yote hayo yanajulisha ya kwamba hakika khalifa alifanya tawasuli kwa baba mdogo wa Mtume  kwa kuwepo ukaribu kati yao, na ama tawasuli kwa dua haikuwa katika akili ya khalifa wala Waislamu. 63

Silsilatul-ahadith sahiha, Juz.1, uk. 646 kimechapwa na maktabatul maarif.

94


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Pili: Hakika wafafanuzi wa Bukhari hawakufahamu kuhusiana na hadithi isipokuwa tawasuli kwa dhati; basi huyu hapa Ibnu Hajar Asqalani amesema: “Na linalofaidisha kutokana na kisa cha Abbasi, ni kwamba ni sunna kuomba dua ya mvua kupitia watu wa heri na wema na watu wa nyumba ya Mtume. Na kwa hilo kuna fadhila ya Abbasi na fadhila ya Umar kwa unyenyekevu wake kwa Abbasi na kutambua kwake haki yake.”64 Na Badru Dini Aynii Hanafi katika sherehe ya hadithi amesema: “Kauli yake: Aliomba mvua kupitia Abbasi” yaani: Alifanya tawasuli kwake ambapo alisema: “Ewe Mwenyezi Mungu! Hakika sisi tulikuwa…” hadi mwisho wake… na kwa hilo kuna faida zifuatazo: Ni sunna kuomba mvua kupitia watu wa heri, wema na ndugu wa Mtume , na kwa hilo kuna fadhila ya Abbasi na fadhila ya Umar kwa unyenyekevu wake kwa Abbasi pia kumjua yeye na haki yake.”65 Na wengineo miongoni mwa wale walioitaja hadithi na ufafanuzi wake.66 Wote wanaona kuwa tawasuli 64

Fat-hul-Baari,Juz. 2, uk. 413, chapa ya Daarul-Maarifa Beirut. Umdatul-Qaari, Juz. 7, uk. 33, chapa ya Daarul-Ihyaai Turath Beirut. 66 Angalia Adhkar Nabawiya, uk. 178, miongoni mwa machapisho ya Daarul-Fikr, na Mad-khalJuz.1, uk. 254 cha Abdariy Maliki. 65

95


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

ilikuwa kwa nafsi ya Abbasi kutokana na mahusiano yake na Mtume. Hakika imepokewa na Muhammad bin Numan Maliki (aliyekufa mwaka 683H) katika kitabu chake “Misbahul-Dhwalam fil-Mustaghithiina bikhayrilAnaam” namna ya kufanya tawasuli, aliyofanya Umar kupitia kwa Abbasi, amesema: “Allahumma inna nastasqi bika biammi nabiyyika wa nastashfia‟ ilayka bishaybatihi” maana yake: “Ewe Mwenyezi Mungu! Hakika sisi tunakuomba mvua kupitia baba mdogo wa Nabii Wako. Na tunakuomba uombezi wako kwa mvi zake.” Basi wakapata mvua, na kwa hilo Abbasi bin Utba bin Abi Lahabi anasema: “Kupitia baba mdogo wangu Mwenyezi Mungu akaleta jioni mvua katika mji wa Hijaz (Saudia) na watu wake, basi Umar alikuwa akiomba mvua kupitia mvi zake.” Vivyo hivyo Hasan aliimba ubeti wa shairi akasema: “Basi mbingu ikanyesha mvua kwa utukufu wa Abbas.” Tatu: Hakika kati ya mambo ya kuchekesha ni kudai: “Hakika tawasuli kupitia dhati haipo katika Sunnah ya Mtume .” Kwa hakika mtoa madai huyu amefanya hilo kuwa ni sababu ya kufanya taawili ya hadithi kwa kukadiria dua kama alivyofanya hivyokatika taawili ya hadithi ya kipofu. 96


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Nne: Pindi ulipokuwa mfumo wa watu hawa “(Mawahabi) ni kushusha vyeo vya Manabii na daraja zao na kuwafanya wao baada ya kufariki kwao wapo pamoja na watu katika sifa moja, waliamua kujikita katika kufanya taawili ya hadithi na kuipotosha, Albaani akasema: “Lau ingelikuwa kutawasuli kwa dhati imeruhusiwa basi isingeli kuwepo sababu ya kuhama kutoka kutawasali kwa Mtume  hadi kutawasuli kwa Abbasi. Uhamaji wao huo umejulisha kuwa walikuwa wakifanya tawasuli kwa dua ya Mtume , na pindi alipofariki bwana Mtume  haikuwezekana kufanya tawasuli kwa dua yake, hivyo basi wakakimbilia kwa Abbas na wakafanya tawasuli kwa dua yake.”67 Ninasema: Hakika kauli yake: “Na pindi alipofariki Bwana Mtume  haikuwezekana kufanya tawasuli kwa dua yake, hivyo basi wakakimbilia kwa Abbas na wakafanya tawasuli kwa dua yake.” ni maneno yanayopingana na mfumo wake. Vipi iwepo hali ya kulazimiana baina ya kutofanya tawasuli kwa dua ya Mtume  na tawasuli kwa dua ya mtu baki kama vile Abbas, isipokuwa ni kwa sababu Abbas ana cheo kwa kuzingatia nasaba yake kwa Mtume . Basi kutawasuli hata kwa dua yake inakuwa nikutawasuli kupitia kwa Mtume . Kinyume na hivyo ni kwamba, kutoweza kufanya tawasuli kupitia dua ya 67

Tawassul, uk. 56 cha Albaani.

97


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Mtume  hakulazimishi kumchagua aliyembora kwa ajili ya dua wakati yule aliyebora zaidi yupo, kwani aliyebora zaidi ya baba mdogo wa Mtume  alikuwepo. Kisha ni kwamba uhamaji wao kutoka kutawasuli kwa Mtume  hadi kutawasuli kwa Abbas na kumchagua yeye, ni kwa kuwa baba mdogo wa Mtume  alikuwa anashirikiana na watu katika shida na raha. Kwa hivyo wakahama kutoka katika kufanya tawasuli kupitia Mtume  hadi kwa baba yake mdogo. Basi wakatawasuli kwa yule ambaye ananufaisha kwa kuomba mvua na uteremkaji wa rehema kwake kwa lengo kwamba ili wengine wanufaike pia. Kisha hakika yale ambayo yanajulisha juu ya kufaa kufanya tawasuli kwa dhati ni zaidi kuliko hayo, basi tumefupisha kwa kutaja hadithi mbili ambazo dalili yake ipo juu ya mkusudiwa, ni mfano wa jua katikati ya mchana. Tawasuli Kwa Cheo Cha Mtume : Hii ni sehemu ya pili ambayo ameizuia Sheikh Uthmani Khamis, na anakusudia daraja la Mtume  mbele ya Mwenyezi Mungu na haki zake alizopatiwa na Mwenyezi Mungu (s.w.t) kwa fadhila Yake na karama Yake, basi akawa ni mwenye haki. Hakika zipo hapa hadithi chungu tele tunatosheka kwa kutaja moja tu kati ya hizo: 98


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Hadithi ya Atwiya bin Awfi kutoka kwa Abu Said Khudri, kwamba hakika Mtume  alisema: “Yule anayetoka nyumbani kwake kwenda kuswali na akasema: Ewe Mwenyezi Mungu! Hakika mimi ninakuomba kwa haki ya wale wanaokuomba Wewe, na ninakuomba kwa haki ya utembeaji wangu huu. Hakika mimi sikutoka kwa uovu wala kwa ubaya wala kujionesha wala kusifiwa. Na nimetoka ili kujikinga na ghadhabu Zako na kutafuta radhi Zako. Basi ninakuomba unikinge mimi na moto na unisamehe mimi dhambi zangu, kwani hakuna anayesamehe ila ni Wewe, basi Mwenyezi Mungu atakutana naye kwa uso Wake, na watamuombea yeye msamaha Malaika sabini elfu.”68 Hakika haki ya wenye kumuomba ni ibara ya vyeo vyao mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w.t), ambavyo wamepatiwa wao, ambavyo ni fadhila na karama. Ndiyo, huenda ikajadiliwa sanad ya Atwiya bin Awfi, na hana dhambi yoyote isipokuwa Ushia wake. Huyu hapa Dhahabi anasema: “Lau itarudishwa hadithi kwa ajili ya watu hawa (Shia) basi zingelipotea athari za Mtume , na hilo ni ufisadi na uovu wa wazi wazi.”69 68

Sunan Ibn Maaja, Juz. 1, uk. 256, nambari 778. Miizanul-Iitidaal, Juz. 1, uk. 5.

69

99


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Ibn Sa‟ad katika kitabu Twabaqaat amesema: “Na alikuwa ni mtu mkweli mwaminifu kwa utashi wa Mwenyezi Mungu, na anazo hadithi nyingi nzuri.”70 Na Tarmidhi katika uwekaji wa maelezo yake juu ya baadhi ya yale ambayo yameelezwa na Atwiya amesema: “Hadithi ni hasan ngeni, hatumjui yeye ila kutokana na aina hii.”71 Na akaifanya ni nzuri kwake katika sehemu mbalimbali katika kitabu chake.72 Na Ajaliy akasema: “Atwiya bin Awfi: Ni mtu wa Kuufa, ni tabiina, mkweli na sio mwenye nguvu.”73 Na Mula Ali Qaari amesema: “Naye ni kati ya watu watukufu na waheshimiwa miongoni mwa tabiina.”74 Kisha hakika hadithi sahihi zinazojulisha juu ya kufaa kufanya tawasuli kwa haki ya Mtume , daraja lake na cheo chake, zipo chungu tele hatuna muda wa kuzinukuu ila chache kati ya hizo. Na lau Sheikh atataka kuzijua hizo basi arejee kitabu chetu kiitwacho “Al-Wahabiyyatu fil-Miizan.” 70

Twabaqaatul-Kubra, Juz. 6, uk. 304 cha Ibn Sa‟ad, chapa ya Daaru Swadir Beirut. 71 Sunan Tirmidhi, Juz. 2, uk. 394, chapa ya Daarul-Fikr Beirut. 72 Sunan Tirmidhi, Juz. 1, uk. 296 na Juz. 3, uk. 228 na Juz. 4, uk. 7-8, 46, 96, 260 na 261. 73 Maarifatul-Thiqaat, Juz. 2, uk. 140, chapa ya Madinat Munawwarat mwaka 1405H. 74 Sharhu Musnad Abi Haniifa, uk. 292, chapa ya Beirut.

100


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Na mwishowe tunaunganisha mtazamo wa Sheikh Uthmani bin Khamis hadi kwenye kauli iliyo juu baina ya wale wanazuoni mashuhuri wa Ahlu Sunna. Hakika imekuja katika kitabu Mawsu‟atul-Fiqihiyyacha Kuwait kama ifuatavyo: Wanazuoni wa kifikihi (Maliki, Shafii na wale Mahanafi waliokuja baadaye, na haya ndiyo madhehebu kwa Mahanbali) wanaona kuwa inaruhusiwa aina hii ya TAWASULI; „Ewe Mwenyezi Mungu! Hakika mimi ninakuomba kupitia Nabii Wako au cheo cha Nabii Wako au kwa haki ya Nabii Wako.” Sawa katika uhai wa Mtume  au baada ya kufariki kwake.75 Kisha hakika Sheikh ana mhadhara mwingine kuhusiana na yale ambayo yaliyopokewa kutoka kwa Mtume , kwamba yeye harithiwi, na sisi tunasoma hadithi kwa sanad na matini na tutailinganisha na Kitabu na Sunnah siku nyingine Mwenyezi Mungu akipenda, kwa sharti kwamba Sheikh ajibu maswali mawili yafuatayo, nayo ni: 1. Je, Abu Bakri aliifunua nyumba ya bibi Fatimah au hapana? 2. Je, alijuta wakati wa kufa kwake kutokana na kitendo chake hiki au hapana? 75

Mawsuu‟at Fiqhiyya Kuwaytiyya, kitolea na wizara ya waqfu na mambo ya Kiislamu katika Kuwait Juz. 14 uk. 156.

101


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Na lau Sheikh atajibu kuhusiana na maswali hayo mawili basi, utakuwa umeshatangulia utangulizi wetu kuhusiana na mhadhara wake, na itadhihirika kwake hali halisi. Basi Sheikh afaidike na fursa hii. MIRATHI YA MTUME NA MAOMBI YA FATIMAH ZAHRA  JUU YA FADAK Katika kipindi kingine cha “Majibu na Maswali,” Sheikh Uthmani Khamis aliuliza maswali matatu kuhusu kuzuiwa Fatimah urithi wa baba yake, na kwa hivyo akajaribu kuzuia urithi wa Mitume wa vile walivyoviacha miongoni mwa mali zao binafsi, kisha akajibu maswali hayo. Na hapa sisi tunajadili yale aliyoyataja Sheikh juu ya utaratibu ambao yamekuja mazungumzo yake: Swali La Kwanza: Kwa Nini Mtume  Hakumfundisha Fatimah  Hukumu Ya Mirathi Yake? Akasema: Hakika pindi alipofariki Mtume , Fatimah  alikuja kwa Abu Bakri. Basi akamuomba ampatie urithi wake kutoka kwa Mtume , kwa sababu Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema:

َ ُ ّ ُ َ ُ َ​َ ُ ٰ َ “…..‫ثل َح ِ ألاّنن َي ِمّن‬ ‫”يى ين ُم الل ُـه فى أولـ ِذلم ِللزل ِش ِم‬ 102


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

“Mwenyezi Mungu wanawausia juu ya watoto wenu; fungu la mwanaume ni kama fungu la wanawake wawili.”76 Basi Abu Bakri akasema: Nilimsikia Mtume  akisema: “Haturithiwi, kile tunachokiacha ni sadaka” basi Fatimah akarudi wala hakupewa chochote. Kisha akajibu swali: Ilikuwaje Abu Bakri akajua kwamba Mtume  harithiwi na Fatimah halijui hilo? Kwa kauli yake: “Mushkeli upo wapi katika hili. Na je, ni lazima Fatimah aijue sharia kwa marefu na mapana? Anayejua kila sharia kwa marefu na mapana ni Mtume .” Ninasema: Katika maneno yake yapo maangalizo mawili: La kwanza: Hakika yeye alikata mahojiano ambayo yalitokea baina yake na Abu Bakri, na hakunukuu kwa ukamilifu wake, kwa kuwa yaliyopo mwishoni mwake hayaambatani na fikra yake na madhehebu yake. Na yafuatayo ni mahojiano kwa ukamilifu wake: Bukhari amepokea kutoka kwa Aisha, kwamba hakika Fatimah binti wa Mtume  alimtuma kwa 76

Surat an-Nisa; 4:11.

103


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Abu Bakri amuulizie mirathi yake, basi Abu Bakri akamjibu: Mtume  amesema: “Haturithiwi kile tunachokiacha ni sadaka.” Hadi aliposema: “Basi Abu Bakri akakataa kumpatia Fatimah chochote. Basi akamghadhibikia Abu Bakri na hakusema naye kwa lolote mpaka alipofariki.Na aliishi baada ya Mtume  miezi sita. Na pindi alipofariki alizikwa usiku na mumewe Ali, na wala hakumruhusu Abu Bakri kushiriki katika mazishi yake wala kumswalia.”77 Unaona kwamba kwa hakika Uthmani Khamiis hakutaja kauli yake: “Na akamghadhibikia yeye.” Je, ghadhabu ya Fatimah bibi wa wanawake wa ulimwenguni inakuwa bila sababu? Na je, kuzikwa kwake usiku hakuna sababu?! Na ilikuwa ni vizuri khalifa akumbuke katika hali hii kauli ya Mtume  kuhusiana na binti yake: “Fatimah ni sehemu ya pande la nyama yangu, basi atakayemghadhibisha yeye kwa hakika amenighadhibisha mimi.”78 Na yule anayesoma tukio hili na akatakafari katika hadithi iliyopokewa kutoka kwa Mtume  kuhusiana na pande lake la nyama , atajua nafasi ya mtu huyu kwa Mtume !! Kwa nini Sheikh hajapitia mambo haya na kusema hayo kwa mdomo. 77

Sahihi Bukhari, 1036, nambari 4240-4241, kitabu Maghaziy. Sahihi Bukhari; 910, nambari 361, kitabu Fadhail Sahaba.

78

104


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

La Pili: Hakika Sheikh amejibu swali la muulizaji: Vipi Abu Bakri amejua kwamba hakika Mtume  harithiwi na Fatimah hakulijua hilo, kwa kauli yake: “Mushkeli upo wapi katika hili. Na je, ni lazima Fatimah aijue sharia kwa marefu na mapana? Anayejua kila sharia kwa marefu na mapana ni Mtume .” Hakika muulizaji akakubali kwamba hakika Fatimah sio wajibu kujua ufafanuzi wa sharia, lakini katika kamusi ya sharia ni wajibu Fatimah ajifunze wajibu wake mahsusi kwake, nayo ni kwamba yeye hamrithi baba yake. Basi ni juu ya Mtume  amfundishe hayo ili asikosee uhakika katika suala hilo, na ili asishikamane na uelezaji wa moja kwa moja wa aya katika kuijibu hadithi inayodhaniwa. Swali La Pili: Hakika Nabii Suleiman  alimrithi baba yake Nabii Daud  Akasema: Vipi unasema: Mtume  harithiwi hali ya kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) katika Kitabu chake kitakatifu anasema: “Na Suleiman alimrithi Daud.”79 Jibu: Hakika Suleiman  alirithi utume baada ya Daud , na Daud  alikuwa na idadi kubwa ya 79

Surat an-Naml; 27:16.

105


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

watoto, hakika hadithi zinasema Nabii Daud  alikuwa na wake mia tatu, yaani alikuwa na watoto wengi, kwa hivyo kumtaja Nabii Suleiman  peke yake hakuna maana yoyote, hivyo basi makusudio yake ni kurithi elimu na utume. Nasema: Daud  alikuwa akifaidika na mambo manne, nayo ni: 1. Elimu 2. Utume 3. Ufalme 4. Mali Ama la kwanza; Suleiman hakumrithi Daud kwa mujibu wa mambo mawili, nayo ni: i. Hakika elimu sio yenye kurithiwa. ii. Hakika Aya iliyotangulia iko wazi kwamba, Mwenyezi Mungu (s.w.t) aliwapatia hao wawili elimu pasi na mmoja kumrithi mwingine, akasema: “Bila shaka tuliwapa Daudi na Suleiman elimu.”80 Wala baada ya hili hakuna maana yoyote ya kubebesha urithi juu ya elimu. Na ama la pili – yaani utume – nao pia sio wenye kurithiwa, kwani ni dhamana ya tabia na uwezo 80

Surat an-Naml; 27:15.

106


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

maalum ili Mwenyezi Mungu (s.w.t) amchague mtu kwa ajili ya utume, hivyo kama mtu atakosa sifa husika itazuilika yeye kuwa Mtume, na kama atakuwa nazo basi Mwenyezi Mungu atamchagua kwa utume bila kuwepo haja ya kumrithi mwingine. Na ama la tatu – yaani ufalme – hakika kama unaokusudiwa ni ule uendeshaji wa mamlaka, basi wenyewe unakubali kurithiwa. Na ama la nne – yaani – mali, hakika hili ni mfano dhahiri miongoni mwa mifano halisi ya urithi.Na kila linapotajwa neno urithi akili huelekea huko kwenye mali. Na linapotumika neno hilo kwenye maana nyingine huwa ni kwaufananishaji, kama vile kauli ya Mwenyezi Mungu (s.w.t):

َ َ َُ​َ َ َ َ ُ ‫أوس ُرح ىها ِب ا ل ُنحم جع َ لىّن‬ ‫ااجنة ال‬ ‫و ِثلك‬ ِ “Na hiyo ni bustani (Pepo) mliyorithishwa kwa hayo mliyokuwa mkiyafanya.”81 Na kwa mujibu huu, hakika utajaji wa Aya unajulisha kwamba hakika Daud  alimrithisha Suleiman ufalme na mali. Na ama yale aliyoyataja mwenye kujibu, kwamba “Hakika Daud alikuwa na watoto wengi, kwa hivyo 81

Surat az-Zukhruf 43:72.

107


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

kumtaja Nabii Suleiman  peke yake hakuna maana yoyote.” Jibu lake liko wazi, kwani Suleiman  alimiliki mamlaka na mali pamoja, na ama watoto wengine wasiokuwa yeye kwa hakika walirithi mali pasi na ufalme na uongozi. Na miongoni mwa yale ambayo yanatoa jasho la paji la uso ni yale yaliyonukuliwa kutoka katika hadithi, kwamba Daud  alikuwa na wake mia tatu.Kwa hakika ni miongoni mwa yaliyozushwa na kubuniwa na wazushi kwa lengo la kuupotosha ukweli, jambo ambalo halina thamani yoyote ile. Na maana ya hilo ni kwamba Daud  ni mwanaume mwenye matamanio mengi, mwenye kujishughulisha na wakeze na wajakazi wake na kuacha kila kitu. Na liko wapi hili mbele ya yale ambayo Qur‟ani tukufu inaeleza kwa kauli ya Mwenyezi Mungu (s.w.t):

ُ َ َ َ ّ ٌ َّ َُ َ َ َ ‫ارلش َع‬ ‫اا ِإّنا َسلشّنا‬ ‫جذّنا داوۥد را ِإّنه أو‬ ‫…و‬..” ُ َ ُ َ َ َ َ ّ َ َ ّ “‫ششاا‬ ِ ِ ‫ااججال معه ِجحن ِبالع ِ س ِ و ِإلا‬ “Na umkumbuke mja wetu Daudi, mwenye nguvu. Hakika yeye alikuwa mwingi wakutubia. Hakika tuliidhalilisha milima iwe pamoja naye, ikimtukuza jioni na asubuhi.”82 82

Surat Swad; 38:17-18.

108


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Kisha hakika Uthman bin Khamiis amesema: Hakika Bibi Fatimah hakuwa anafungamana na dunia, ni kana kwamba katika kauli yake hii anafuata kauli ya Raaghib ambapo amesema: “Hakika mali haina thamani yoyote mbele ya Mitume.”83 Anajibiwa hilo kwa mambo mawili: Mosi: Hakika Mwenyezi Mungu (s.w.t) anaelezea mali kuwa ni heri na anasema:

َ َ َ َ َ ٰ َُ َ ً َ َ َ​َ ‫قشتمّن‬ ‫… ِإّن ثشك خمرا الى ِ ية ِللى ِلذ ِين وألا‬..” َ “.‫عشوو‬ ‫ِباا‬ ِ “Kama akiacha mali, kuwausia kitu wazazi wawilina akraba kwa namna nzuri (inayokubalika).”84 basi mali ni heri ikiwa mikononi mwa watu wema, na ni shari ikiwa mikononi mwa watu wabaya.Na ni maneno mazuri yale ambayo ameyaeleza Imam Ali  kuhusu dunia na yaliyo ndani yake: “Yule atakayeona kwayo itamuonesha, na yule atakayeikodolea macho itampofusha.”85 83

Al-Mufradaat, mada ya “urithi” cha Raaghib. Surat al-Baqara; 2:180. 85 Sharhu Nahjul-Balaaghah, khutba ya 82. 84

109


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Pili: Hakika binti wa Mustafa pindi nafsi yake ilipoghadhibika kwa kudhulumiwa, na akapata hukumu ya mhukumu aliyetoa hukumu tofauti na Kitabu na Sunnah, alisimama mbele ya uso wa hakimu, kwani ni jukumu la kila Mwislamu huru kutoogopa lawama za mwenye kulaumu katika jambo la Mwenyezi Mungu. Vipi lisiwe hilo na huyu hapa ni Mtume  anasema: “Yule ambaye atauawa akitetea mali yake basi huyo amekufa shahidi.”86 Basi Mtume  anamweleza yule ambaye anayetafuta haki yake na hata ikimpelekea kuuwawa, kuwa huyo ni shahidi, ama Uthman bin Khamiis anamweleza yeye kuwa ni mtafutaji wa dunia. Ndiyo wamepokea Ahlu Sunna kutoka kwa Mtume  kwamba hakika amesema: “Sisi kongamano la Mitume haturithiwi dhahabu wala fedha, wala ardhi wala shamba wala nyumba, lakini tunarithiwa imani, hekima, elimu na sunna.”87 Na Kulayni amepokea kwa sanad yake kutoka kwa Abu Bakhtari kutoka kwa Abu Abdillah , akasema: “Hakika wanazuoni ni warithi wa Mitume. Na hilo ni kwamba hakika Mitume hawakurithiwa mali 86

Sahihi Bukhari: 595, nambari 2480, kitabu Madhalim walGhadhab. 87 Sharh Nahjul-Balaaghah, Juz. 16, uk. 223.

110


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

wala dinari, na hakika wamerithiwa hadithi kutokana na hadithi zao.â€?88 Lakini makusudio ni kwamba hadhi ya Mitume ni kurithisha imani, hekima, elimu na sunna na sio mali. Lakini hii haimaanishi kuwa kama akiacha mkeka au chombo au elimu na mswala au nyumba basi mali hizo zinahamia kwa umma na sio kwa wanawe. Kwani msimamo wa hadithi hii nikutofautisha kati ya lengo la Mtume na Wafalme wengine watafutaji wa dunia ambao wanaacha lundo la mali na hazina iliyojaa. Na ambalo linajulisha juu ya yale tuliyoyataja, ni kwamba alitaja mirathi ya imani, hekima na hadithi, na inajulikana kwamba mambo hayo sio mirathi ya warithi wake bali ni mirathi ya umma. Basi msimamo wa hadithi ni kuutahadharisha umma kuwa wasitarajie kuwa Mitume watawarithisha hazina na mali lukuki. Wala makusudio ya hadithi hizi si kuzuia Mitume kumiliki mahitaji ya msingi kibinadamu. Na miongoni mwa yale yanayopelekea mtu kustaajabu na kushangaani kwamba, khalifa alitabikisha kwa Fatimah ď Š tu yale aliyodai kuwa ameyasikia kutoka kwa Mtukufu Mtume, kwa kumzuia Fatimah asirithi mali kutoka kwa Mtume, lakini aliacha mali 88

Kaafi, Juz. 1, uk. 32, mlango wa sifa ya elimu‌

111


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

nyingine za Mtume mkononi mwa yule aliyemrithi. Hizi hapa nyumba za Mtume zilibakia mikononi mwa wakeze bila ya kunyang‟anywa!! Na huu hapa upanga wa Mtume , pete yake na baadhi ya vile ambavyo vinahusiana naye, hakuviomba na hakuvitwaa!! Na hakika alizuia Fadak ambayo ilikuwa ni kitegauchumi chenye kuzalisha zaidi. Na ukhalifa wakati huo ulikuwa na haja nayo. Na hakika Fadak imekuwa ni jambo la kisiasa baada ya zama za khalifa. Na ushahidi juu ya hilo ni kwamba imetofautiana sira na nyendo za makhalifa kuihusu, yupo yule aliyeirudisha kwa watoto wa Fatimah na yule aliyeichukua: Anasema Ibn Abi Hadiid: “Na pindi alipotawala Muawiya bin Abi Sufyan alipomkatia Marwan bin Hakam theluthi yake, na akamkatia Amru bin Uthman bin Affan theluthi yake, na akamkatia Yazid bin Muawiya theluthi yake. Na hilo lilitokea baada ya kifo cha Hasan bin Ali .Waliendelea kupeana hiyo hadi ikaishia kwa Marwan bin Hakam katika zama za ukhalifa wake. Basi akampatia hiyo mwanawe Abdul-Aziz, na Abdul-Aziz akampatia mwanawe Umar bin AbdulAziz. Na pindi alipotawala Umar bin Abdul-Aziz kuwa khalifa, alikuwa ni wa mwanzo aliyeirudisha dhulma. Alimwita Hasan bin Ali bin Abi Twalib , bali akamwita Ali bin Husein , basi akairudisha hiyo kwake, na ilikuwa mikononi mwa watoto wa 112


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Fatimah muda wa utawala wa Umar bin AbdulAziz. Na pindi alipotawala Yazid bin Atika akaichukua kutoka kwao, na jambo lilikuwa juu ya aina hii hadi lilipofika katika ukoo wa Abbas. Ama katika zama za Bani Abbas, ilikuwa ikizunguka baina ya Makhalifa na watoto wa Fatimah Zahra . Hakika Saffah aliirudisha kwa Abdullah bin Hasan, na baada ya kufa kwake ikarudishwa kwa Mansuur, na ilikuwa mikononi mwake hadi alipokufa. Basi akasimama mwanawe Mahdi sehemu yake akairudisha hiyo kwa watoto wa Fatimah , hadi jambo likafikia kwa Maamuni. Basi akairudisha hiyo na akaandika barua hadi kwa gavana wa mji wa Madina, na kwa hili Daabal Khazaaiy, anasema: “Muonekano wa zama kwa hakika ukawa ni wenye kuchekesha – kwa kurudisha Maamuni Fadak kwa Hashim.”89 Barua Ya Maamun Abbas Hadi Kwa Qatham Bin Ja‟far Gavana Wake Katika Mji Wa Madina: Baladhuri amesema: Na pindi ulipokuwa mwaka wa mia mbili na kumi Maamuni aliamrisha, basi akampatia (yaani Fadak) mtoto wa Fatimah na 89

Sharhu Nahjul-Balaaghah; Juz. 16, uk. 21.

113


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

akamwandikia hilo Qatham bin Ja‟far Gavana wake katika mji wa Madina: “Ama baada, hakika Amirul-Muuminina kutokana na mahali pake katika dini ya Mwenyezi Mungu. Na katika ukhalifa wa Mtume Wake na ukaribu wake kwake, ndiye anayefaa zaidi kufuata sunna yake, na kutekeleza jambo lake, kumpa yule aliyempa, na kumpa sadaka aliyempa sadaka. Naapa kwa Mwenyezi Mungu kwa uwezeshaji wa AmirulMuminina na isma yake, na amali ambayo inamkurubisha kwake na katika utashi wake. Hakika Mtume  alimpatia Fatimah binti Rasuli  Fadak na akaitoa sadaka kwake. Na hilo lilikuwa ni jambo shahiri dhahiri lililojulikana bila kuwepo ikhtilafu baina ya ndugu wa Mtume . Na akaendelea kudai kupitia hilo yale ambayo ni bora zaidi kwake kuliko sadaka. Hivyo basi, Amirul-Muuminina ameona airudishe hiyo kwa warithi wake na awapatie hao ili kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t), kwa kusimamisha haki yake na uadilifu wake hadi kwa Mtume  kwa utekelezaji wa jambo lake na sadaka yake. Basi anaamrisha kuifanyia ithibati katika vitabu vyao vya kumbukumbu na kitabu chake mpaka kwa magavana wake. “Na ikiwa atanadi katika kila msimu wa Hijja baada ya kufariki Mtume wake , kwamba kila yule 114


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

aliyekuwa na sadaka au zawadi au zana ya kazi basi aitaje ili kauli yake ikubaliwe na itekelezwe, hakika Fatimah  ndiye anayefaa zaidi kusadikishwa maneno yake kuhusu yale ambayo amejaalia Mtume  kwake. Na hakika ameandika (Amirul-Muuminina) barua kwenda kwa Mbaraka Twabari, Gavana wa Amirul-Muuminina akimwamrisha kuirudisha Fadak kwenye urithi wa Fatimah binti Rasuli  kwa mipaka yake na wingi wa haki zake zilizowekwa juu yake. Na yale ambayo yananasibishwa kwake kutokana na watumwa na mazao na visivyokuwa hivyo, na kuzikabidhi hizo kwa Muhammad bin Yahya bin Hasan bin Zayd bin Ali bin Husein bin Ali bin Abi Twalib, na Muhammad bin Abdullah bin Hasan bin Ali bin Husein bin Ali bin Abi Twalib, ili (Amirul-Muuminina) kuweka hiyo katika usimamizi na uangalizi wa hao wawili ili iweze kuwasaidia katika masuala ya kiuchumi kwa manufaa ya watu wake. Basi tambua kuwa hilo linatokana na rai ya Amirul-Muuminina na yale ambayo Mwenyezi Mungu aliyompa ilhamu kuhusiana na kumtii Yeye na akamwezesha yeye kujikurubisha Kwake na kwa Mtume . Pia akamfundisha yeye yule wa kabla yako. Na amiliana na Muhammad bin Yahya na Muhammad bin Abdullah kwa yale ambayo ulikuwa ukiamiliana na Mubaraka Twabari, na wasaidie yale 115


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

ambayo yataimarisha na kutengeneza na kujaza mazao kwa utashi wa Mwenyezi Mungu, na amani. Imeandikwa siku ya jumatano, siku mbili baada ya kuingia mfungo pili, mwaka wa mia mbili na kumi.” Na pindi alipochukua ukhalifa Mutawakili, aliamrisha ikarudishwa hiyo kwa waliyokuwa nayo kabla ya Maamuni.90 Swali La Tatu: Hakika Zakaria  Alimuomba Mwenyezi Mungu (s.w.t) Ampatie Mtoto Wa Kumrithi: Vipi unasema hakika Manabii hawarithiwi, na sisi tunaona hakika Zakaria  alimuomba Mwenyezi Mungu (s.w.t) amruzuku mtoto wa kiume ili amrithi, akasema:

ُ َ​َ ُ َ ً َ َ ُ َ َ​َ ‫ءال‬ ِ ‫… فهب لى ِمن لذّنك و ِليا ي ِشرن ور ِشذ ِمن‬..” َ َ “‫عقىا‬ “Basi nipe mrithi kutoka Kwako. Atakayenirithi mimi na arithi ukoo wa Ya‟qub.”91

90

Futuhul-Buldaan, uk. 46-47. Surat Maryam; 19:5-6.

91

116


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Akajibu Uthmani Khamiis kwa majibu yafuatayo: 1. Lau tutaangalia katika uhalisia ni kwamba, hakika Yahya  alikufa wakati wa uhai wa baba yake, na aliuawa ndani ya kipindi hicho na hakumrithi Zakaria. Na hii inamaanisha kwamba, Mwenyezi Mungu (s.w.t) aliikubali dua ya Zakaria  na Yahya akarithi utume. 2. Hakika Zakaria  alikufa fukara, na hakuwa na mali yoyote. 3. Yuko wapi Yahya mbele ya ndugu wa Yakub, basi yeye ni mwenye kuzuiwa kwa mamia, nalo ni kundi, wala harithi chochote kutokana na ndugu wa Yakub. Ninasema: Kabla hatujasoma aina tatu alizozitumia kama dalili, tunataja namna ya dalili ya maswahiba zetu Imamiyyah walioitumia kuthibitisha kuwa makusudio ya kurithi hapa ni mali, na hivyo ni kwa aina mbili: Ya kwanza: Hakika uombaji wa mtoto ni miongoni mwa aliyoumba Mwenyezi Mungu kwa aina ya binadamu, sawa awe ni mtu mwema au muovu, awe Nabii au mwingine. Na kila mwanadamu ikiwa hatakengeuka maumbile yake, basi ataambatana na maombi ya kupata mtoto na ataona uwepo wa mtoto baada yake ni kubakia kwa nafsi yake. Na sharia za 117


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

kiungu hazikubatilisha hukumu hii ya kimaumbile, wala hazikulaumu na kukemea ombi hilo la kimhemko bali ziliisifu hiyo. Na yatosha katika hilo kauli ya Nabii Ibrahim :

َ ٰ ‫َس ِ ّا َهب لى ِم َن ال ّ ـ ِ لمّن‬ “Ewe MolaWangu! Nitunukie aliye miongoni mwa watenda mema.”92 Na kauli yake (s.w.t) akielezea kuhusiana na waumini:

ُ ‫… َسَتنا َهب َلنا من َأ ٰصوجنا َو ُر ّسّرٰـخنا ُق َش َ َأ‬..” “…..‫عم ٍّن‬ ِ ِ ِ ِ “…..Mola Wetu! Tupe katika wake zetu na wanetu wetu yaburudishayo macho.”93 Ya pili: Zakaria alikuwa akipelekewa mali kutoka kwa wana wa Israeli bali kutoka kwa makuhani, na alikuwa Zakaria ni Rais wao. Kwa hivyo alihofia kufariki bila kuacha mtu wa kusimamia mali hizo na kubakia mikononi mwa wasimamizi ambao hawakuwa ni watu wema. Basi akamuomba (s.w.t) mtoto wa kiume asimamie mahali pake na agawe mali za 92

Surat as-Saffat; 37:100. Surat al-Furqan; 25:74.

93

118


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

watu kulingana na vipimo vya kiungu. Katika tafsiri ya Ali bin Ibrahim imeandikwa: “Hakuwa Zakaria muda huo na mtoto wa kiume atayesimamia mahali pake na atakayemrithi yeye. Na ilikuwa ni zawadi za wana wa Israeil na nadhiri za makuhani, na alikuwa Zakaria ni Rais wa makuhani.” Hadi mwisho.94 Ukijua yale tuliyoyataja basi tambua pia, katika aya yenyewe kuna dalili mbili zilizo wazi juu ya makusudio ya kurithi, nazo ni urithi katika mali: Mosi: Hakika kauli yake:

َ

ُ

ّ

“…..‫” َو ِإنى ِخ د اا ٰى ِل َى ِمن َوساءي‬ “Na hakika mimi nawahofia jamaa zangu baada yangu”95 Ni dhahiri shahiri kwamba kulikuwa na jambo analohofia. Basi lau atamruzuku mtoto, hofu ya Zakaria itaondoka, na lau atakufa bila kuacha mrithi ingeliendelea hofu yake, na kwa mwangaza huu tunasema: Lau hofu inayokusudiwa ni hofu ya urithi wa mali, basi hii ndio inayoondoka kwauwepo wa mtoto, kwani jamaa wakati huo hawamrithi yeye 94

Tafsir Qummi, Jz. 2, uk. 48 na Tafsir Nurul-Thaqalayn, Juz. 3, uk. 323. 95 Surat Maryam; 19:5.

119


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

pamoja na uwepo wa mtoto. Na hili ni tofauti na pale ambapo urithi unaokusudiwa utakuwa ni urithi wa utume au elimu au yale ambayo yanafanana nayo. Hakika hayo hayazuki wala hayazuiliki iwapo mtu atakufa bila mtoto. Hakika utume na elimu sio miongoni mwa mambo ya kurithi, sawa awe na mtoto au hapana, sio kati ya yale ambayo anahofia kwayo, hakika Mwenyezi Mungu (s.w.t) ni mjuzi zaidi pale anapojaalia utume wake. Pili: Hakika yeye alimuomba Mwenyezi Mungu (s.w.t) amrukuzu mtoto wa kiume ili awe mridhiwa mbele yake, kama anavyosema: “Ewe Mola Wangu mjaalie mwenye kuridhisha.”96 Na katika aya nyingine amesema: “Ewe Mola Wangu mlezi! Nipe mimi kutoka kwako kizazi kizuri, hakika wewe ni msikivu wa maombi." Na lau yangelikuwa makusudio ni kwamba Yeye (s.w.t) amruzuku yeye mtoto atakayemrithi katika utume na hekima, basi ombi la kutaka mtoto awe ni mzuri kwake, litakuwa ni jambo lisilo na faida; kwani hakika utume unalazimu mwenye kupewa awe ni mwenye kuridhiwa mbele ya Mwenyezi Mungu. Na hakika kama watu wangelizingatia mambo mawili haya wasingeangukia katika tafsiri ya aya kwa kudai kuwa makusudio yake ni urithi wa hekima na utume. 96

Surat Maryam; 19:6.

120


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Baada ya kujua hilo, sasa basi turejee katika dalili alizotoa Uthman Khamiis na huenda zote kazichukua kutoka katika tafsiri ya Aluusi. Ama ya kwanza: Ninamaanisha kauli yake: Hakika Yahya ď „ alikufa katika uhai wa baba yake basi hakumrithi baba yake. Anajibiwa kuwa: Mosi: Hakika swali linaelekezwa kwa nadharia zote mbili, urithi wa utume na urithi wa mali. Hakika urithi kwa maana zote mbili unafikiriwa baada ya Zakaria kuaga dunia na kukutana na Mwenyezi Mungu.Na hakika angekufa Yahya kabla yake basi isingelikuwa na maana yoyote, kuwa Yahya Nabii katika wakati huo huo ambao alikuwa Zakaria hai. Kama vile hakuna maana ya kuwa kwake ni mrithi wa baba yake, kwani hakuna haja ya kutumwa Manabii wawili (Zakaria na Yahya) katika umma mmoja na jumuiya maalum kama vile wana wa Israeli. Ndiyo, huenda mazingira ya ujumbe yakapelekea kutuma Manabii wawili katika sehemu mbili tofauti, na katika umma mbili tofauti, kama vile kumtuma Nabii Lut kwa kaumu yake, na Nabii Ibrahim katika kaumu nyingine. Na huenda mazingira yakapelekea uwepo wa Manabii wawili katika sehemu moja na 121


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

umma mmoja kwa haja ya Nabii aliyetangulia, ili kuchangia na kumuunga mkono Nabii aliyetangulia, kama vile utume wa Harun ambapo Musa  alimuomba Mola Wake amtume ndugu yake kuwa Nabii na Waziri na msaidizi wake. Pili: Hakika hilo halijathibiti kwa dalili ya kukata shauri, kwamba Yahya aliuawa katika uhai wa baba yake, na haikuthibiti kinyume na hivyo. Huyu hapa Jalalu Diin Suyuut ananukuu kutoka kwa Ali bin Abi Twalib  katika kauli ya Mwenyezi Mungu (s.w.t), inayosema: “Bila shaka mtafanya uharibifu katika nchi mara mbili”97 Akasema: Uharibifuwa kwanza: Kuuawa Zakaria na mwingine ni kuuawa Yahya .98 Na Ibn Jariir amepokea kutoka kwa Ibn Zayd amesema: “Ulikuwa uharibifu wao ambao wakiufanya katika nchi mara mbili: Kumuua Zakaria  na Yahya bin Zakaria ”99 ni dhahiri shahir kwamba mzazi alimtangulia mtoto. Amepokea Kulayni kutoka kwa Abu Ja‟far Baqir  kwamba yeye alifariki baada ya kufariki Zakaria.100 97

Sura Israa; 17: 4. Tafsiri Durrul-Manthuur, Juz. 5, uk. 235. 99 Tafsiri Durrul-Manthuur, Juz. 5, uk. 243. 100 Kaafi, Juz. 1, uk. 382, mlango wa hali za Maimamu  katika umri. 98

122


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Basi dhahiri hiyo inatokana na hadithi kuwa kilitangulia kifo cha mzazi (Zakaria) na kufuatiwa cha mwanawe (Yahya). Ama ya pili – ninamaanisha kauli yake: Hakika Zakaria  alikufa fukara na hakuwa na mali. Anajibiwa kuwa: Kama tulivyotaja huko nyuma, kuwa tuliyoyataja kuwa Zakaria alikuwa akipelekewa mali kutoka kwa wana wa Israeli bali kutoka kwa makuhani, na alikuwa Zakaria ni Rais wao, kwa hivyo alihofia kufariki bila kuacha mtu wa kusimamia mali hizo na kubakia mikononi mwa wasimamizi ambao hawakuwa ni watu wema, basi akamuomba (s.w.t) mtoto wa kiume asimamie mahali pake na agawe mali za watu kulingana na vipimo vya kiungu. Na ya tatu – yaani urithi wa Yahya wa mali kutoka kwa jamaa wa Yakubu, kuwa unazuiwa kwa mamia, nalo ni kundi, na hivyo wala harithi chochote kutoka katika ndugu wa Yakub. Anajibiwa kuwa: Hakika hilo la kundi kuzuia lipo katika kitabu Fiqhi Sunnah, na haijulikani kuwa hilo lilikuwepo katika sharia ya Musa au ya Isa, kama vile hakika kundi sio 123


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

kizuizi katika Fiqhi ya Imamiyya. Ukiongezea kwamba makusudio ya kauli yake (s.w.t): “Amrithi kutokana na ndugu wa Yakub” sio urithi kwa watu wote wa ndugu wa Yakub, hakika huo ni urithi kutoka kwa baadhi yao. Na inatosha katika hilo urithi wa mama yake au mtu mwingine baki kutokana na ndugu wa Yakub, ambaye ana mafungamano naye kinasaba au kisababu. Ukosoaji Wa Maneno Ya Aluusi Na hadi hapa yamekamilika maneno yetu. Sasa tunataja yale ambayo aliyoyataja ndugu Aluusi kuhusiana na hilo, naye ni miongoni mwa wale wenye kukumbatia rai kwamba urithi sio urithi wa mali na kwa hilo lina sura tatu: Mosi: Anasema: Miongoni mwa yale yanayounga mkono ubebaji wa urithi hapa ni kwa maana ya urithi wa elimu na si wa mali, ni kwamba sio katika maono ya hali ya juu na muhimu, ya wale waliojuu wenye nafsi takatifu ambazo zimekata mafungamano na ulimwengu huu wenye kubadilika wenye kuisha, na kuungana na ulimwengu wenye kubaki, kuelemea katika starehe za dunia hata kwa mfano wa kiwango cha ukubwa wa bawa la mbu. Na hasa mheshimiwa Zakaria , hakika yeye alikuwa ni mtu mashuhuri kwa ukamilifu wa kukata mafungamano ya dunia, na kuwa katika hali ya upweke. Basi inakuwa ni muhali 124


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

kwa ada na desturi kuhofia kurithisha mali na starehe, vitu ambavyo kwake yeye katika mtazamo wa juu wa ukadiriaji wake ni vitu duni zaidi.Wala kuomba kutokana na hadhara ya Haki (s.w.t) mfano wa uombaji huo. Nalo linajulisha juu ya ukamilifu wa mapenzi na moyo kufungamana na dunia.101 Anajibiwa kuwa: Hakika hofu ya Zakaria  kuhusiana na urithi wa watu wa pembeni haikuwa ni kwa sababu nafsi yake imefungamana na mali, mpaka isemwe, hakika azma ya hali ya juu ya nafsi takatifu haina mafungamano na ulimwengu huu. Na hakika hofu yake ilikuwa kwamba mali hizi ambazo kila uchao zinamfikia zisije kuangukia mikononi mwa watu waovu, na basi wasije wakazitumia pasipo mahali pake. Na kwa hivyo imepokewa katika sira ya Mtukufu Mtume , kwamba alikuwa akikitumia kile kilichokuwa kinapatikana katika mkono wake kutokana na ngawira katika wakati mfupi zaidi. Na hii aina ya hofu sio dalili juu ya kufungamana na dunia na starehe zake, bali ni dalili juu ya uchamungu wake na takwa yake na kuzuia kutumia mali katika sehemu zisizo za kisharia. Pili: Hakika hilo haliogopwi, kwani ikiwa mtu akifa na amali zake zikahamia kwa warithi, basi mali 101

Ruuhul-Ma‟ani, Juz. 16, uk. 64.

125


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

zitakuwa ni za mtu mwingine, na matumizi yake yapo juu ya dhima yake, sawa amepatia au amekosea, wala maiti hagombezwi wala kuadhibiwa kuhusiana na matumizi ya mtu mwingine, bali hana hatia yoyote.102 Anajibiwa kuwa: Kwa hakika binadamu mshika dini akihisi kwamba yale yaliyopo mikononi mwake miongoni mwa mali yataangukia mikononi mwa watu waovu, na wataitumia sio mahali pake pa kisharia, basi anaweka mipango kuhusu hizo ili zisiangukie mikononi mwao. Basi kauli ya kusema: “Hakika mali ni mali yao na dhambi ni yao” ni kauli ya yule asiyehisi majukumu kuelekea yale ambayo wanayamiliki watu waovu kuhusiana na mali ambayo ipo mikononi mwake. Tatu: Hakika ilikuwa katika uwezekano wa Zakaria  kutumia vile anavyovimiliki kabla ya kufa kwake, kwakutoa sadaka vyote katika dini ya Mwenyezi Mungu (s.w.t), na awaache mikono mitupu watoto waovu wa baba yake mdogo.103 Ninasema: Maneno haya ni ya kushangaza sana kuliko hata kwa wale waliomtangulia. Naye anamaanisha kwamba hakika Zakaria  alikuwa anajua 102

Ruuhul-Ma‟ani, Juz. 16, uk. 65 Ruuhul-Ma‟ani, Juz. 16, uk. 65.

103

126


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

kifo chake wakati gani atakufa, basi atoe sadaka mali yake mwaka mmoja kabla ya kumfika hilo, mfano; hakika imeshetangulia kwamba mali zilikuwa zikimfikia wakati baada ya wakati. Naapa kwa umri wangu hakika mtoaji madai ameweka sura hizo na akaiondoa aya kutokana na dhahiri yake. Nayo ni sahihi kwa mujibu wa yale aliyoyapokea Abu Bakri kuhusiana na kadhia hii, na lau sio hili wala isingeingia akilini mwa yeyote kitu kati ya aina hizi za dalili. Na katika kuhitimisha tunasema yale aliyotolea dalili kwayo binti wa Mtume , bibi wa wanawake wote wa ulimwengu katika hutuba yake tukufu juu ya kukosea kwa Abu Bakri katika uchukuaji wa Fadak na kuwatoa watumishi wake humo. Wamepokea wanahistoria na wanahadithi kwamba pindi Abu Bakri na Umar walipojikusanya kumzuia Fatimah bint wa Mtume  asiimiliki Fadak, lilimfanya hilo Fatimah afunge kitambaa juu ya kichwa chake na kujitanda juba lake, na akaelekea katika mkusanyiko kutokana na uharaka wake akiwa na wanawake wa kaumu yake. Hadi alipoingia kwa Abu Bakri naye akiwa katika kundi la Muhajiriina na Answari. Basi akalia kwa masikitiko katika hali ya utoaji wa lawama zake na akaanza maneno yake kwa kusema: “Sifa njema zote zinamstahiki Yule aliyetuneemesha, na shukurani ni Zake kwa yale aliyowapa ilhamu…” 127


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

hadi aliposema: “Enyi watu! Mnapaswa kujua kwamba hakika mimi ni Fatimah na baba yangu ni Muhammad.Ninasema waziwazi nawala sisemi kwa makosa wala sifanyi ambayo hayafai…” hadi aliposema: “Ewe mtoto wa Abu Quhafa! Je, ndani ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu unamrithi baba yako wala simrithi baba yangu, hakika umekuja na kitu cha uzushi?! Je, mmeacha kwa makusudi Kitabu cha Mwenyezi Mungu na mkakiweka nyuma ya migongo yenu? Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema:

ُ َ​َ ُ َ ً َ َ ُ َ َ​َ ‫ءال‬ ِ ‫… فهب لى ِمن لذّنك و ِليا ي ِشرن ور ِشذ ِمن‬..” ُ َ ‫عقىا َو‬ َ َ “‫اجعله َس ِ ّا َس ِض ًيا‬ “Basi nipe mrithi kutoka Kwako. Atakayenirithi mimi na arithi ukoo wa Ya‟qub. Ewe Mola Wangu mjaalie mwenye kuridhisha.”104 Na (s.w.t) anasema:

َ

َ

ٰ

ُ

َ

ُ ُ

َ ٰ َ ُ َ “…. ‫عع فى ِلحـ ِب الل ِـه‬ ِ ‫… وأولىا ألا‬..” ٍ ‫سحام ةعضهم أولى ِبج‬ “Na ndugu wa tumbo, wanastahikiana wenyewe kwa wenyewe katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu.‟105 104

Surat Maryam; 19:5-6. Surat al-Anfal; 8:75.

105

128


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Pia (s.w.t) anasema: “Mwenyezi Mungu anawausia juu ya watoto wenu; fungu la mwanaume ni kama fungu la wanawake wawili.”106 Vile vile anasema: “..Kama akiacha mali, kuwausia kitu wazazi wawili na akraba kwa namna nzuri (inayokubalika). Ni haki (haya) kwa wenye takua.‟107 Na mmedhani: Sina cheo wala daraja lolote mimi wala urithi kutoka kwa baba yangu wala undugu baina yetu. Je, Mwenyezi Mungu amewahusisha nyinyi kwa aya (iliyopo ndani ya Qur‟ani) lakini amemvua baba yagu [Muhammad ] kwayo? Au je, mnasema: Hakika watu wa dini mbili hawarithiani? Au sio mimi na baba yangu ni miongoni mwa watu wa dini moja? Au nyinyi ni wajuzi zaidi wa kuielewa Qur‟anikwa umahsusi wake na ujumla wake kuliko baba yangu na mtoto wa baba yangu mdogo?”108 106

Surat an-Nisa; 4:11. Surat al-Baqara; 2:180. 108 Angalia kitabu Nisaai uk. 23-33 cha Muhammad bin Abi Twahir (amezaliwa mwaka 204 na kufa mwaka 280H), kitabu Saqiifat, uk. 97-101 cha Abi Bakar Jawhari (amekufa mwaka 323H), Shafii fil-Imaamat, Juz. 4, uk. 69-77 cha Sayyid Murtadha (amekufa mwaka 436H), Maa‟ni Ahbaar, uk. 354 cha Sheikh Saduuq (amekufa mwaka 381H), Aamali, uk. 384 cha Tuusi, Al-Majlis, uk. 13 cha Sheikh Tuusi (amekufa mwaka 460H), Sharhu Nahjul-Balaaghah, Juz. 16, uk. 211 cha Abi Hadidi (amekufa mwaka 655H), Kashful-Ghummat, Juz. 1, uk. 116 cha Abi Hasan Urdubiili 107

129


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Hapa yamebakia mambo mawili, nayo ni: 1. Hakika imekwishatangulia hapo kabla kwamba, makhalifa wa ukoo wa Umayya na Abbasi walikuwa wakiichezea Fadak, mara wakiichukua na wakati mwingine wakiirudisha kwa wenyewe. Na hakika Sheikh Uthmani Khamiis ametaja kisa cha kuzunguka juu ya aina ambayo hatujaikuta hiyo katika vitabu rejea, na hakika tumetaja yale ambayo yaliyopo katika kitabu “Futuhul-Buldaan” cha Baladhuri. 2. Hakika yeye amesema: “Aliniuliza mmoja kati ya Shi‟ah basi akasema: „Hakika Abu Bakri amedhulumu, kwani amemzuia Fatimah  urithi wake.‟ Nikasema: Abu Bakri amedhulumu, nikasema: Yule aliyekuwa baada yake? Akasema: „Umar‟, nikasema: Naye pia amedhulumu.” Hadithi iliendelea hadi kwa Ali, basi yeye pia amedhulumu kwani hakuwapa haki wahusika wake, hadi aliposema: Vipi kitendo ni kimoja lakini baadhi ni madhalimu na wengine sio madhalimu? Anajibiwa kuwa: Hakika mwenye kujibu imejificha kwake sababu iliyompelekea Ali kuitumia Fadak, na ametaja sababu (amekufa mwaka 936H) na vingi vinginevyo miongoni mwa vitabu rejea.

130


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

katika baadhi ya hutuba zake. Basi akasema katika barua yake aliyoiandika kwa Gavana wake Uthman bin Hunayf wa Basra, amesema: “Ndiyo hivyo, Ni kweli, mikononi mwetu mulikuwa na Fadak109 iliyokuwa na vyote vilivyo chini ya kivuli cha mbingu (ilikuwa na mazao mbalimbali), lakini kikundi cha watu kiliionea uroho, na kingine nyoyo zilididimia mbali nayo. Na hakimu aliye bora zaidi ni Mwenyezi Mungu. Niifanye nini Fadak na mali nyingine isiyokuwa Fadak, hali ikiwa nafsi mahali pake kesho ni kaburi, ambalo ndani ya giza lake athari yake itakatika, na kutoweka habari yake. Ni shimo ambalo lau lingezidishwa nafasi yake, na mikono ya mchimbaji wake kufanya wasaa (uwezo wa kulizidisha), basi jiwe na udongo vitalikandamiza, na myanya yake kuzibwa na mchanga uliorundikana!”110 Ibn Abi Hadiid anasema katika kujibu utata huu ambao Uthmani Khamiis ameutegemea na akaunukuu 109

Fadak ni shamba ambalo lilikuwa na mazao mbali mbali, shamba ambalo Mtume  alimzawadia mtoto wake; Bibi Fatimah , na hili lilitokea baada ya Mwenyezi Mungu kuteremsha Aya isemayo: „‟Na mpe jamaa (yako) haki yake…‟‟ (Qur‟an, 17:26). Lakini jambo la kusikitisha ni kwamba baada ya kufariki Mtume , Khalifa Abu Bakar alilitaifisha shamba hilo na kutoka kwa Bibi Fatimah kwa madai ya kwamba Mitume ya Mwenyezi Mungu hairthiwi.

110

Nahjul-Balaaghah, sehemu ya barua, na. 45.

131


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

kwa aina ambayo ni kana kwamba yeye ndiye wa awali kuutaja, anasema: “Ama yale ambayo yametajwa kuhusiana na uachaji wa Amirul-Muuminina  Fadak pindi lilipopelekwa jambo kwake, na ikafanywa kuwa ni dalili, ni kwamba, sababu iliyopelekea aache kuirudisha Fadak ni kukiri kwake hukumu za watu, na kujizuia kuzivunja nakuzibadilisha. Na hakika tumebainisha hilo katika yale ambayo tuliyokwishayasema hapo kabla, kwamba hakika yeye alikuwa katika taqiyya yenye nguvu mno katika mambo mengine.111 Na hukumu ngapi za kibidaa ziliwekwa katika siku za Makhalifa, kama vile usimamishaji wa Swala ya tarawehe jamaa na yasiyokuwa hayo, Imam  hakuweza kurudisha katika sehemu yake mpaka hakika yeye  pindi alipomtuma mwanawe Hasan  msikitini, ili kuwazuia watu kusimamisha Swala ya sunna jamaa katika mwezi wa Ramadhani, zilisikika sauti za wenye kuswali kuzipaza kwa kusema: “Eee sunna ya Umar mmeiacha.”Na lau haki-ka Imam Ali  angelisimama kurudisha ardhi ya Fadak kwa watoto wa Fatimah basi sauti zingelipazwa ili kuwafuata Makhalifa, kama vile zilivyokuwa katika mambo mengine. Basi Imam alipendelea kuicha hiyo katika hali yake na anywe111

Sharhu Nahjul-Balaaghah, Juz. 16, uk. 278.

132


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

shwe wa mwisho wake kikombe cha wa mwanzo wake. Haya ndiyo tunayoyatanguliza kwa yule anayesikiliza na kuangalia vipindi hivyo vya luninga, na afuate kauli ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) inayosema: “Wale ambao wanasikiliza maneno basi wakafuata yaliyomema.” PAMOJA NA UTHMAN KHAMIIS KATIKA MAJIBU YAKE JUU YA SHI‟AH KUHUSIANA NA MADHUMUNI YA HADITHI YA KISHAMIYA Chaneli ya Wisal ilirusha kipindi kipya kilichobeba mada isemayo „Utata uliopo” na maudhui ya kipindi kulingana na maelezo yao ni kujibu hoja za Shi‟ah kuhusiana na Hadithi ya Kishamiya. Na alikuwa Sheikh Uthmani Khamiis ni mmoja wa wazungumzaji katika kipindi hicho.Na hakika Sheikh amenukuu hadithi ya kishamiya kutoka katika kitabu Sahihi Muslim, akasema: “Hakika Mtume  alimwita Ali na Fatimah na akawaingiza kwenye kishamiya, kisha akaja Hasan akaingia kwenye kishamiya, kisha akaja Husein naye akaingia pamoja nao kwenye kishamiya.” Na akasema: “Pindi walipokusanyika watu watano kwenye kishamiya, Mtume  akainua mkono wake 133


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

mbinguni akasema: „Ewe Mwenyezi Mungu! Hakika hawa ni watu wangu wa karibu basi waondolee hao uchafu. Ewe Mwenyezi Mungu watoharishe hao kabisa kabisa.‟” Kisha akaelekeza upinzani wake juu ya mambo manne: 1. Hakika Shi‟ah wanashindwa kutoa sanad sahihi kuhusiana na hadithi hii, wala haipatikani hadithi kwao inayopokea kisa hiki, basi hadithi imethibiti kwetu sisi Ahlu Sunnat wal-jamaa. 2. Shi‟ah wamesema kwamba hakika hadithi hii imemuhusisha Bibi Fatimah, Imam Ali, Hasan na Husein , hakika hao ni watu wa nyumba ya Mtume, na wasiokuwa hao wako nje kuhusiana na watu wa nyumba ya Mtume, wala haingii yeyote mwingine katika maana ya wale wanaokusudiwa miongoni mwa watu wa nyumba ya Mtume . Kisha akajibu hilo kwamba, hakika jambo hili sio sahihi, na kama mfano tu katika kuweka wazi jambo hili, mimi ninapo sema: „Hakika hawa ni wanafunzi wangu,‟ na mimi ninakusudia wale waliohudhuria miongoni mwao, hili haliwatoi wanafunzi wasiokuwepo kuhusiana na ukweli wa kauli yangu: Wanafunzi wangu. Na hili limethibiti kwa andiko kwamba wapo Ahlulbayt wa Mtume ambao inasadikika juu yao kauli hii, lakini wao 134


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

hawakuwa pamoja na Mtume  kwenye kashamiya. 3. Hakika Shi‟ah wanawaingiza Maimamu wengine miongoni mwa kizazi cha Husein , (pamoja na wao) hawakuwa pamoja na Mtume  kwenye kishamiya. 4. Shi‟ah wanasema: Hakika Ahlulbayt ni maasumiina tangu kuzaliwa, na lau wangelikuwa hivyo vipi aseme Mtume  katika dua yake: “Watoharishe hao kabisa kabisa.” Na je, hili sio katika hali ya kukifanya kitu kiwepo hali ya kuwa kipo? Na natija ya maneno yake yanafupishwa katika mambo manne: i. Hakuna hadithi sahihi kwa Shi‟ah kuhusiana na watu wa kishamiya. ii. Hakika hadithi hii haijulishi kuwa watu wa kishamiya ndiyo tu Ahlulbayt. iii. Na lau itajaaliwa kuwa watu wa kishamiya ndiyo tu Ahlulbayti, basi hilo linalazimu kutoka wengine waliobakia miongoni mwa Maimamu. iv. Lau wangelikuwa Maimamu maasumiina basi vipi Mtume  awaombee hao kutoharishwa kutokana na dhambi? Na kabla ya kujibu maswali yake tata, ambayo anayarudia kipindi baada ya kipindi, katika hali tete na mazingira haya, ni kana kwamba Sheikh hana 135


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

jambo la muhimu na la msingi la kufanya isipokuwa kukabiliana na Shi‟ah, na wakati mwingine kuwazushia wao?! Tunasema: Mheshimiwa Sheikh anasoma Qur‟ani tukufu na Mwenyezi Mungu (s.w.t) analaumu kati ya Waislamu kuitana kwa majina mabaya, anasema: “Wala msiitane kwa majina mabaya (ya kejeli).”112 Je kuuita umma mkubwa miongoni mwa Waislamu ambao wanampwekesha Mwenyezi Mungu (s.w.t) Muumbaji, Mpangiliaji wa mambo na Mwekaji sharia, na wanashuhudia kwa utume wa Mtume , na kuwa yeye ni Nabii wa mwisho, na wanaswali na wanafunga na wanahiji – unawaita watu hawa - ni Raafidha si kuwaita kwa majina mabaya, nalo ni jambo la haramu? Basi ilikuwa ni lazima juu ya Sheikh awaite Shi‟a kwa jina la Shi‟ah Imamiyya au wafuasi wa Maimamu wa Ahlul-Bayt, kama ilivyo katikati ya maneno yake. Basi ukishajua hilo, rejea kusoma mambo manne kutokana na maneno yake. Jambo la Kwanza: Shi‟ah na Hadithi ya Kishamiya: Anasema: Hakika Shi‟ah wanashindwa kutoa sanad sahihi kuhusiana na hadithi hii. 112

Sura 49 aya 11.

136


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Ninasema: Sisi tunamuuliza Sheikh je, amevisoma vitabu vyote vya Shi‟ah na hadithi zao na akazichunguza kisha hakuikuta ndani yake hadithi sahihi inayohusiana na watu wa kishamiya?! Sidhani hakika Sheikh atajibu ndiyo, na kwa ukadiriaji wowote ule basi ni tofauti kabisa na dhana ya Sheikh, bali uhalisia ni kwamba,Shia wamejali kunukuu hadithi hii tangu karne ya kwanza hadi leo hii. Hakika Sheikh Kulayni (aliyekufa mwaka 329 A.H) ameweka mlango ambao amenukuu ndani yake hadithi ya kishamiya kwa sanad sahihi,113 na wakaendelea kulitilia umuhimu kwa kunukuu hadithi hii wale waliokuja baada yake. Basi Hafidh bin Batriiq Hully (aliyeishi kati ya mwaka 523-600 A.H) amenukuu kitabu cha athari ya zamani kiitwacho “Umdatu Uyuun Sihahil-Akhbaar” katika moja ya faslu zake, amenukuu ndani yake hadithi zipatazo 37 kutoka kwa wasomi wakubwa wa hadithi.114 Kama vile alivyonukuu mwanahadithi Sayyid Hashim Bahraani katika kitabu chake kiitwacho “GhaayatulMaraam” zaidi ya hadithi arobaini kutoka katika vitabu vya Ahlu SunnatWal-jamaa, na hadithi 34 kutoka katika vitabu vya Shi‟ah.115 113

Al-Kaafi, Juz. 1, uk. 276, mlango wa yale ambayo Mwenyezi Mungu (aza wa jalla) aliyomhusisha Mtume Wake juu ya Maimamu mmoja baada ya mwingine. 114 Umdatu, uk. 75-90. 115 Ghaayatul-Maraam wa hujjatul-Khiswaam, Juz. 3, uk. 193211, chapa ya Beirut.

137


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Na amepokea Shahid Sayyid Nurullah Qaadhi katika kitabu chake “Ihqaaqul-Haqqi” hadithi ya kishamiya kutoka katika vitabu vya Ahlu Sunnat wal-jamaa (kihadithi, kitafsiri na kihistoria), na utakuta katika mstari wa pambizo wa kitabu ameweka yale mengi ambayo yaliachwa kuandikwa katika yale ambayo yamempitia mwandishi.116 Na sisi tuna barua yenye jina la “Ahlul-Bayt Simaatuhum wa huquuqihim fil-Qur‟ani kariim” tumekifanyia uhakiki, ndani yake kuna yale yanayofaidisha kuhusiana na aya ya utoharifu, na tumenukuu ndani yake hadithi zinazokaribia 35 kati ya zile ambazo wamezipokea wanazuoni na wasomi wakubwa wa Ahlu Sunnah. Na hakika mwanetu sayyid Ali Muwahid Abtahi amefanya zoezi la kukusanya kila ambalo walilolipokea wanazuoni na wasomi wa Ahlu Sunna na Shi‟ah kuhusiana na aya ya utoharifu, na kuchapisha katika juzuu mbili, kwa jina la: “Ayatul-Tat-hiir fi Ahadiithi fariiqayni.” Na kwa mwangaza huo basi hadithi hii ni mutawatiri kwa makundi yote mawili, hakuna haja ya kunakili hadithi sahihi pembezoni mwake. Pamoja na uwepo wa vitabu sahihi vinavyofungamana na jambo hilo, 116

Angalia: Tafsiri Nuru Thaqalayni, Juz. 4, uk. 270-277.

138


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

vipi Sheikh anaomba kutoka kwetu hadithi sahihi kuhusiana na hadithi ya kishamiya, na hakika maudhui imefikia kiwango cha kusihi kusema: Amezima taa na limewaka jua, pamoja na hivyo sisi kwa mapenzi ya Sheikh tunataja hadithi moja sahihi, tunasema: Amepokea Kulayni, kutoka kwa Muhammad bin Yahya, kutoka kwa Ahmad bin Muhammad bin Isa, kutoka kwa Muhammad bin Khalid na Husein bin Said, kutoka kwa Nadhru bin Swed, kutoka kwa Yahya bin Imran Halabi, kutoka kwa Ayub bin Hurri. Kutoka kwa Imran bin Ali Halabi, kutoka kwa Abu Baswiir kutoka kwa Abu Abdillah , katika hadithi… amesema: Lakini Mwenyezi Mungu (s.w.t) aliiteremsha hiyo ndani ya Kitabu Chake kumsadikisha Nabii Wake:

َ ُ ُ َ َ ‫جس َأ‬ َ ‫الش‬ ّ ُ ُ َ َ ‫الل ُـه ِل ُي‬ ‫هل‬ ‫… ِإّن ا يشرذ‬..” ِ ِ ‫زهب عننم‬ َ َُ َّ َُ َ ً “‫الج ِد ورط ِهشلم ثطهمرا‬ “Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kukuondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.”117 117

Surat al-Ahzaab; 33:33.

139


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Walikuwa ni Ali, Hasan, Husein na Fatimah , Mtume  aliwaingiza hao kwenye kishamiya katika nyumba ya Ummu Salama, kisha akasema: Ewe Mwenyezi Mungu! Hakika kila Nabii ana watu wake wa karibu na kizito chake, na hawa ndio watu wangu na kizito changu.” Basi Ummu Salama akasema: Je, mimi sio miongoni mwa watu wako wa karibu? Mtume  akasema: “Hakika wewe una kheri, lakini hawa ni watu wangu wa karibu na kizito changu…”118 Vile vile Kulayni amenukuu – katika mlango huo huo – njia mbili sahihi kuhusiana na hadithi hii, tumeiacha kuitaja kwa lengo la kufupisha. Jambo la Pili: Hadithi ya Kishamiya haiwahusu Ahlul-Bayt tu: Anasema: Hakika hadithi hii haijulishi kuwa AhlulBayt ni wale tu watu wa kishamiya, akitolea ushahidi mfano uliousikia. Ninasema: Lau Sheikh angezijua na kuzielewa njia zote za hadithi ambazo wanazuoni wa hadithi, wa historia na wa tafsiri wamezinukuu, angelitambua 118

Kaafi, Juz. 1, uk. 288, hadithi ya kwanza, mlango wa yale ambayo Mwenyezi Mungu (s.w.t) amemhusisha Mtume Wake juu ya Maimamu mmoja baada ya mwingine.

140


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

kwamba Mtume  aliwatambulisha Ahlul-Bayt kwa njia tatu, na lengo la kuchukua njia hizi tatu tofauti ilikuwa ni kuonesha wao tu ndio Ahlulbayti: Kuna wakati alitaja kinaga ubaga majina ya yule ambaye imeshuka aya kwa haki yake. Na kuna wakati aliwaingiza chini ya kishamiya wote ambao Aya ilishuka kwa ajili yao, na akamzuia kuingia yule asiyehusika naona akainua mkono wake mbinguni akasema: Ewe Mwenyezi Mungu! Hakika kila Nabii alikuwa na watu wake wa karibu, na hawa ndio watu wangu wa karibu.” Tatu: Alikuwa akipita kwenye nyumba ya Fatimah kwa miezi kadhaa, pindi alipokuwa akitoka kuelekea msikitini kwa ajili ya swala ya alfajiri, akisema: Swala enyi watu wangu wa karibu: “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu enyi watu wa nyumba na anataka kukutakaseni kabisa kabisa.” Na kwa njia hizi tatu ameeleza watu wa karibu wa nyumba yake na akaainisha uhalisia wa watu hao katika sura yenye kuwakusanya haona kuwazuia wengine wasiohusika. Na kwakuwa hadithi za kila njia kati ya njia hizi ni nyingi, basi tunafupisha katika kila sehemu yale aliyoyanukuu Twabari katika Tafsiir yake, na Suyuutwi katika kitabu chake Duraru. Na ndani ya hivyo viwili kuna utoshelezo wa yale yaliyotajwa na 141


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

vitabu rejea vingine miongoni mwa vitabu rejea vya Ahlu Sunna na Musnad, na hatutataja yote waliyopokea wasomi hao wawili katika tafsiri zao ili kutosheka na ufupi, na huu ni ubainifu wake: Kundi la Kwanza: Kutaja kinaga ubaga majina yao: 1. Amepokea Twabari kutoka kwa Said Khudri, amesema: Mtume  amesema: Aya hii iliteremka kuwahusu watu watano: Kwangu mimi , kwa Ali , Hasan , Husein  na Fatimah : “Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kukuondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.”119 2. Na amepokea Abu Said kutoka kwa Ummu Salama, mke wa Mtume : Hakika aya hii iliteremka nyumbani kwangu: “Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kukuondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.” Akasema: Wakati huo mimi nilikuwa nimekaa kwenye mlango wa nyumba, basi nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Je, mimi sio miongoni mwa Ahlul-Bayt? Akasema: “Hakika wewe upo katika kheri, wewe ni miongoni 119

Tafsiri Twabari, Juz. 22, uk. 5, chapa ya Daarul-Maarifat Beirut mwaka 1400H.

142


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

mwa wake wa Mtume .” Anasema: Na nyumbani kwangu alikuwamo Mjumbe wa Mwenyezi Mungu , Ali , Fatimah, Hasan  na Husein .120 3. Amepokea Suyuutwi kutoka kwa Ibn Murduwayh, kutoka kwa Ummu Salama amesema: Aya hii iliteremka nyumbani kwangu: “Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kukuondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.” Na nyumbani kwangu walikuwa saba: Jibrail, Mikail, Mtume, Ali, Fatimah, Hasan na Husein ; na mimi nikiwa mlangoni. Basi nikasema: Ewe Mtume! Je, mimi sio miongoni mwa Ahlul-Bayt? Akasema: Hakika wewe upo katika kheri, na hakika wewe ni miongoni mwa wake wa Mtume .”121 4. Imenukuliwa kutoka kwa Ibn Jariri, Ibn Abi Hatam na Twabaraani kutoka kwa Abu Said Khudri , amesema: Mtume  amesema: “Aya hii iliteremka kuhusiana na watu watano; kwangu mimi, Ali, Fatimah, Hasan na Husein: “Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kukuondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.”122 120

Tafsiri Twabari, Juz. 22, uk. 7. Tafsir Durrul-Manthuur, Juz. 6, uk. 604, chapa ya Daarul-Fikr Beirut mwaka 1403H. 122 Tafsiri Durrul-Muthuur, Juz. 6, uk. 604. 121

143


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Kundi la Pili: Kuwaingiza hao katika Kishamiya: Kuwaingiza hao katika kishamiya au guo au joho: Hakika imepokewa kuhusu hilo hadithi hizi: 5. Ameeleza Twabari amesema: Aisha amesema: Mtume  alitoka siku moja mchana na akiwa na guo lenye nywele nyeusi, basi akaja Hasan akamwingiza na kuwa pamoja naye, kisha akaja Ali akamwingiza na akawa pamoja naye, kisha akasema: “Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kukuondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.”123 6. Ameeleza Twabari amesema: Imepokewa kutoka kwa Ummu Salama amesema: Alikuwa kwangu Mtume , Ali, Fatimah, Hasan na Husein, basi nikawaandalia chakula wakala na wakalala na akawafunika joho kisha akasema: Ewe Mwenyezi Mungu! Hawa ni Ahlul-Bayt wangu basi waondolee uchafu na watoharishe kabisa kabisa.”124 7. Ameeleza Twabari: Imepokewa kutoka kwa Abu Ammar amesema: Hakika mimi nilikuwa nimekaa mbele ya Waathilat bin Asqaa wakati walipomtaja Ali basi wakamshutumu, waliposimama akasema: 123

Tafsir Twabari, Juz. 22 uk. 5 Tafsir Twabari, Juz. 22 uk. 6.

124

144


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

“Keti ili nikueleze kuhusu huyu waliyemshutumu. Hakika mimi nilikuwa na Mtume  pindi alipomjia Ali, Fatimah, Hasan na Husein basi akawafunika kishamiya chake kisha akasema: Ewe Mwenyezi Mungu! Hawa ni Ahlul-Bayt wangu, Ewe Mwenyezi Mungu waondolee uchafu na watoharishe kabisa kabisa.”125 8. Ameeleza Twabari: Imepokewa kutoka kwa Abu Ammar amesema: Nilimsikia Waathilat bin Asqaa akisimulia hadithi, akasema: Nilimuulizia Ali bin Abi Twalib nyumbani kwake, basi Fatimah akasema: „Hakika ametoka. Punde atakuja na Mtume ‟, pindi alipokuja, basi Mtume  akaingia na nikaingia, basi Mtume  akakaa juu ya godoro na akamkalisha Fatimah kuliani mwake, Ali kushotoni mwake, Hasan na Husein mbele yake, akawafunika kwa nguo yake, na akasema: „Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu…‟ Ewe Mwenyezi Mungu hawa ndio watu wangu wa karibu.”126 Kundi la Tatu: Kuwaainisha hao kwa Usomaji wa aya Mlangoni Kwao: 9. Ameeleza Twabari: Imepokewa kutoka kwa Anas bin Malik, hakika Mtume  alikuwa akipita kwenye 125

Tafsir Twabari, Juz. 22, uk. 6. Tafsir Twabari, Juz. 22, uk. 6.

126

145


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

nyumba ya Fatimah kwa muda wa miezi sita kila alipotoka akielekea kuswali, akisema: Swala enyi Ahlul-Bayt: “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu…”127 10. Ameeleza Twabari: Amepokea kutoka kwa Abu Hamraa amesema: Nilikaa Madina kwa muda wa miezi sita katika zama za Mtume . Akasema: Nilikuwa nikimuona Mtume  alipokuwa akienda kuswali swala ya alfajiri akisimama kwenye mlango wa Ali na Fatimah basi akisema: Swala swala: Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu enyi watu wa nyumba na kukutakaseni kabisa kabisa.”128 11. Amepokea Suyutwi: Ameeleza Ibn Abi Shayba, Ahmad na Tirmidhi na akasema hadithi hii ni hasan. Na Ibn Jarir, Ibn Mandhur, Twabarani na Hakim alisema hadithi hiyo ni sahihi.Imepokewa kutoka kwa Anas bin Malik hakika Mtume  alikuwa akipita kwenye mlango wa Fatimah alipokuwa akitoka kwenda kuswali swala ya alfajiri akisema: “Swala enyi Ahlul-Bayt: Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu enyi watu wa nyumba na kukutakaseni kabisa kabisa.”129 127

Tafsir Twabari, Juz. 22, uk. 5-6. Tafsir Twabari, Juz. 22, uk. 6 129 Tafsir Durrul-Manthuur, Juz. 6, uk. 605. 128

146


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

12. Amepokea Suyutwi: Ameeleza Ibn Mardawayh, kutoka kwa Abu Said Khudri  amesema: Pindi Ali alipoingia kwa Fatimah Mtume  alikuja asubuhi arobaini kwenye mlango wake akisema: “Rehema na amani ya Mwenyezi Mungu ziwe juu yenu enyi Ahlul-Bayt, swala swala Mwenyezi Mungu awarehemu nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu… mimi ninampiga vita yule anayewapiga vita hao, mimi ninampa usalama yule anayewapa usalama hao.”130 13. Amepokea Suyutwi: Ameeleza Ibn Jariri na Ibn Mardawayh, kutoka kwa Abu Hamraa amesema: Nilimuona Mtume  miezi sita Madina sio mara moja, akitoka kwenda kuswali swala ya alfajiri, alikuwa akija kwenye mlango wa Ali na akiweka mkono wake juu ya upande wa mlango kisha akisema: “Swala swala: Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu enyi watu wa nyumba na kukutakaseni kabisa kabisa.”131 14. Amepokea Suyutwi: Ameeleza ibn Mardawayh, kutoka kwa ibn Abbas  amesema: Tulimshuhudia Mtume  miezi tisa akija kila siku kwenye mlango 130

Tafsir Durrul-Manthuur, Juz. 6, uk. 606. Tafsir Durrul-Manthuur, Juz. 6, uk. 606.

131

147


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

wa Ali bin Abi Twalib kila wakati wa swala, akisema: “Rehema na amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yenu enyi watu wa nyumba. Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu enyi watu wa nyumbana kukutoharisheni kabisa kabisa. Mwenyezi Mungu awarehemu, swala.”Kila siku mara tano.132 15. Amepokea Suyutwi: Ameeleza Twabarani kutoka kwa Abu Hamraa , amesema: Nilimuona Mtume  akija kwenye mlango wa Ali na Fatimah kwa muda wa miezi sita na akisema: “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu enyi watu wa nyumba na kukutoharisheni kabisa kabisa.”133 Je mambo haya matatu hayajulishi kuwa Mtume  alitilia umuhimu suala la kuonesha kuwa aya hii ni makhususi kwa watu hawa wema watano? Na kuna umbali kiasi gani baina ya maudhui ya aya na mfano ambao ameshikamana nao Sheikh, wala haturefushi maneno katika kubainisha tofauti, hasa kwa kuzingatia kwamba yeye  alimzuia Ummu Salama kuingia kwenye kishamiya akimwambia hakika yeye ni mke miongoni mwa wake za Mtume, na sio miongoni mwa Ahlul-Bayt wake walioelezwa katika aya. 132

Tafsir Durrul-Manthuur, Juz. 6, uk. 606. Tafsir Durrul-Manthuur, Juz. 6, uk. 607.

133

148


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Jambo la Tatu: Hadithi ya Kishamiya haiwahusishi Maimamu waliobaki miongoni mwa watoto wa Husein : Huu ni utata mwingine usio na mashiko ambao anaueneza Sheikh Uthman Khamiis, na hilo lina sura mbili: 1. Hakika Shi‟ah wanaitakidi uimamu wa maimamu wengine waliobakia wanaotokana na kizazi cha Husein , kwani hiyo imekuwa ni hadithi mutawatiri. Pia zipo hadithi chungu tele zinazoelezea juu ya ukhalifa wa makhalifa kumi na mbili. Hakika wameipokea hiyo wasomi wakubwa wa Ahlu Sunna na Shi‟ah. Amepokea Muslim katika Sahih yake kutoka kwa Jabir bin Samrat amesema: Niliingia pamoja na baba yangu kwa Mtume  basi nikamsikia akisema: “Hakika jambo hili halitotimia mpaka watimie makhalifa kumi na mbili.” akasema: Kisha akazungumza maneno sikuyasikia mimi, akasema: Basi nikamuuliza baba yangu: Amesemaje? Akajibu: Amesema: “Wote wanatokana na Kuraish.”134 134

Sahihi Muslim, Juz. 6, uk. 3, kitabu cha Uongozi, mlango wa watu wamewafuata Kuraish, kwa hakika ameileza hiyo isiyokuwa njia moja, angalia: Sahihi Bukhari: 1812, na. 7223, chapa ya Daarul-Fikr, Beirut mwaka 1424H.

149


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Na miongoni mwa ya yale yanayojulikana ni kwamba, Maimamu kumi na mbili ambao Mtume  ametoa habari kuhusu dini kutiliwa nguvu kupitia kwao, katika zaidi ya hadithi moja, si wale wanaojidai kwa ukhalifa miongoni mwa ukoo wa Umayya na ukoo wa Abbasi; kwani wao wamemwaga damu na wameua wajukuu wa Mtume . Wakawadhulumu Maimamu wa Kiislamu na wakafanya mambo ya haramu. Na hakuna mfano halisi wa Maimamu kumi na wawili waliotajwa na Mtume isipokuwa Maimamu wa Ahlul-Bayt ambao limekubaliana neno la Waislamu wote juu ya utukufu wao, tohara yao, elimu zao na kujitolea kwao kufa katika kunyanyua bendera ya dini. 1. Kama ambavyo pia hakika umausumu umethibiti kwao , kwani umaasumu wa Imam umethibiti kwake kwa andiko kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) katika utajo wa Mwenyezi Mungu Hakim.135 Pia unajulishwa na akili iliyosafi. Basi sifa zote mbili zimethibiti katika haki ya Maimamu waliobakia bila ya haja ya kuwa kwao ni wenye kuingia katika yale yanayojulisha aya, au hakika wao walikuwa kwenye kishamiya. 135

Angalia: Sura 2 aya 124.

150


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Jambo la Nne: Hadithi ya Kishamiya na Umaasumu wa Maimamu : Anasema: Shi‟ah Imamiyya wanasema kuhusu umaasumu wa Maimamu, kama walikuwa ni maasumu kwa nini Nabii awaombee huo umaasumu. Hili sio lolote ila ni uombaji wa kitu kilichokuwepo?! Ninasema: Hakika mushkeli huu si wa Uthmani Khamiis pekee, bali una mizizi katika historia. Huyu hapa Allamah Majlisi ananukuu mushkeli na anajibu mushkeli huo. Ama mushkeli wenyewe ni kwamba: Hakika uondoaji wa uchafu hautokuwa ila baada ya kuthibiti kwake, na nyinyi mmesema kuhusu umaasumu wao tangu mwanzo wa umri hadi mwisho wao. Na ama jibu la hilo ni kwamba: Hakika uondoaji na utumiaji kama vile unavyotumiwa katika uondoaji wa jambo lililopo, hutumiwa pia katika uzuiaji wakutokea jambo mahali linapowezekana kutokea, kama vile kauli ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) inavyosema:

َ

ُ

َ

َ َ ٰ َ

َ َ ّ ‫… لزلك لن شو َعنه ال‬..” “…..‫حشاء‬ ‫ىء َوال‬ ِ ِ ِ “Hivyo ndivyo ilivyokuwa ili tumuepushie uovu na uchafu.”136 136

Surat Yusuf; 12: 24.

151


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Na unasema katika dua: Mwenyezi Mungu amekuondolea wewe kila uovu na akakuondolea wewe kila lisilofaa.137 Ninasema: Imekuwaje Sheikh ameghafilika kuhusiana na mushkeli alioutaja, kuwa kwa dhana yake hiyo utawarudia Waislamu wote, ambapo huomba kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) katika swala tano, uongofu wao katika njia iliyonyooka, na wanasema: “Tuongoze katika njia iliyonyooka,” je wao hawako juu ya njia iliyonyooka, au ombi hili si kama vile uombaji wa kitu kilichopo?! Na jibu katika daraja zote ni moja, nalo ni ombi la kuomba kuendelea kuwa juu ya njia iliyonyooka. Basi akaomba Mtume  waendelee kubakia katika umaasumu na tohara. Hakika waja wote wa Mwenyezi Mungu wanahitaji uthibitisho wa Mwenyezi Mungu wa kuwa juu ya uongofu na kuendelea nao katika uhai wao. Kisha hakika Sheikh ameelezea mwishoni mwa maneno yake mambo mawili, nayo ni: 1. Ushangaaji wa Uthmani Khamiis kuhusiana na kuwanasibisha Shi‟ah katika tawasuli ya Mtume : 137

Mir-atul-U‟quul, Juz. 3, uk. 245-246.

152


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Amasema: Mimi sishangai maneno haya kutoka kwa Shi‟ah, kwani wao hudai mambo mengi ambayo hayana msingi wowote ule wakusihi kwake. Miongoni mwa mambo hayo ni kudai kwao usharifu na nasaba hadi kizazi cha Mtume . Na mimi ninasema daima vipi Mtume  awe Mwarabu katika hali ambayo hakika wengi wa watoto wake hao wanatokana na Waajemi na wasiokuwa Waarabu? Ninasema: Yale aliyoyataja Sheikh kuhusiana na kuenea masharifu na nasaba hadi kwa Mtume  baina ya Waajemi, chimbuko lake ni ujinga wake wa kutojua nasaba ya kizazi kitakatifu katika miji yote ya Kiislamu na mingineyo.Kwa hakika ametoa habari Mwenyezi Mungu (s.w.t) katika Kitabu Chake kitukufu kuhusiana na kumfadhilishaMtume Wake  kwa kauli yake (s.w.t): “Hakika sisi tumekupa kauthari.” akafasiri kauthari kuwa ni watoto wengi kwa ushahidi wa kauli yake iliyopo mwisho wa sura: “Hakika anayekuchukia wewe basi yeye ndiye aliyekatikiwa na kizazi.” Na hakika amejumuisha nasaba hadi kwenye mti wa utume katika miji mbalimbali. Basi nyumba ngapi ambazo wamo watu wanaonasibiana na Mtume  katika Yemeni, Morocco, Misri na nchi nyinginezo, na wao wana shajara ya nasaba iliyowazi juu ya nasaba zao. Na hakika nimezuru miji ya Magharibi nimewakuta huko masharifu wengi wenye kunasibiana na Mtume 153


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

, lakini madai ya kuenea nasaba hiyo baina ya Iran na uajemi amedanganya asili yake. Na hakika takwimu zimejulisha juu ya uwepo wa zaidi ya watu milioni sitini ambao ni ukoo wa Hashimu katika nchi za Kiislamu, wengi wao ni kizazi cha Mtume . 2. Shi‟ah na uchukuaji wa hadithi za AhlusSunnah: Hakika Shi‟ah Imamiyya hawachukui hadithi za Ahlu Sunnah isipokuwa iwapo wao watakuta jambo kuwahusu wao na lina maslahi na wao, basi wanalichukua hilo na wanalitolea hoja kwalo, basi uko wapi uungwana? Ninasema: Ni dhahiri shahiri kwamba Sheikh hakusoma vitabu vya utoaji dalili vya Shi‟ah Imamiyya katika nyanja za kifikihi na itikadi. Hakika hoja kwao wao ni kauli ya mkweli na mwaminifu pasi na kutofautisha baina ya suala husika liwe la Shi‟ah au asiyekuwa Shi‟ah, na kwa hivyo wanatolea hoja sehemu ya hadithi zilizopokewa katika vitabu sahihi na musnad, akiwa mpokeaji ni mkweli mwaminifu au zimejulisha fuo mbalimbali za maneno juu ya chimbuko la hadithi. Na la kushangaza kutoka kwake ni kwamba maneno yake mengine: „Hakika Shi‟ah hawatolei hoja hadithi za Ahlu Sunna lakini iwapo watapata hadithi inahudumia maslahi yao basi wanaitolea hoja kwayo.‟ 154


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Ninasema: Hivi ni aibu gani kwa hilo na wao wanafanya matendo yao haya kutokana na kauli ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) inayosema:

ٰ َ َ َ َ َ َ َ َ ّ ُ ” ‫اال َ ن ِة َوجـ ِذ ُلهم ِبال ِه َى‬ ‫ىعظ ِة‬ ‫ادع ِإ ٰلى َس‬ ِ ‫االن ِة واا‬ ِ ‫حيل َسِتك ِب‬ ِ َ “…..‫أح َ ُن‬ “Waite (watu) kwenye njia ya Mola Wako kwa hekima na mawaidha mazuri, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora.”138 Au sio mjadala kwa yale ambayo ni mazuri zaidi miongoni mwa yale ambayo Kitabu na Sunnah vimelingania juu yake, na imejiri sera ya wanazuoni wa Kiislamu katika miji yote? Mzaha wa Sheikh mwishoni mwa maneno yake: Kisha Sheikh Uthman Khamiis anaitakidi uwepo wa chuki nyoyoni mwa Shi‟ah juu ya Waarabu, kama alivyosema kinaga ubaga katika maneno yake: “Hakika jambo hili haliingii akilini. Hakika chuki ambazo zipo nyoyoni mwa Shi‟ah kwa Waarabu, ndizo zinazowafanya wao wadai mfano wa madai hayo.” Ninasema: Kwanza; hakika Sheikh amewahesabu Shi‟ah kuwa ni wale tu waliopo katika nchi ya Iran na uajemi, kana kwamba hawapo Uturuki, Iraq, Syria, 138

Surat an-Nahl; 16:125.

155


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Yemen, Misri, Lebanoni, Moroco, Aljeria (na Saudia pia)…., kwamba hakuna Shi‟ah anayetokana na asili ya Uarabu, kana kwamba Shi‟ah kwake yeye ni Waajemi tu. Iweje hivyo ikiwa Shi‟ah wanafikia robo ya Waislamu, na wanapatikana katika nchi za Kiislamu kwa makundi?! Pili: Hakika amewazulia Shi‟ah wa Iran, kwa madai ya uwepo wa chuki nyoyoni mwao juu ya Waarabu. Na tunamuuliza Sheikh lau angelikuwa mwenye kusoma na kupitia habari za Ghaza katika siku za mwisho, angelijua yule ambaye aliyewanusuru na akawapatia makombora ambayo yameteketeza Israeli na kubomoa tungi la Fuladhiya, ambalo lilikuwa wakijifaharisha kwalo kuwa haliwezi kuharibiwa? Je, wamewanusuru katika hilo watu watukufu au Marais wa nchi za Kiarabu au viongozi wao ambao walikuwa wakijifariji juu ya kuchinjwa kwa vichanga na kutengwa wanawake na wanaume wao, na wao wakiwa ndani ya Ikulu zao wakistarehe, na watoaji mawaidha wa masulutani wakiwasifu na kuwatukuza katika hutuba zao. Ewe Sheikh wetu! Una uchache wa insafu, uungwana na murua katika hukumu unazozitoa!!

156


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

KISIMAMO KINGINE NA SHEIKH UTHMANI KHAMIIS Hakika Sheikh Uthmani Khamiis – na katika kipindi chake kingine cha luninga cha Wuswal– anasema: Hakika alikutana na Shi‟ah akisema kwa kumkufurisha Yazid bin Muawiya kwa ajili ya kumuua Husein , basi akamjibu yeye kwamba Husein ni kizito kidogo kati ya vizito viwili, na Qur‟ani tukufu ni kizito kikubwa, basi iweje asimkufurishe yule aliyesema kupotoshwa kwa Qur‟ani (kizito kikubwa) na akaweka shaka kwayo, na ambayo lipo andiko kwamba imehifadhiwa wala haiwezekani kupotoshwa. Sheikh na Ukufurishaji wa Yazid: Ninasema: Sijui vipi zimejiri hoja baina yake na Shi‟ah huyu, lakini Shi‟ah ni mwenye kujua historia na sira, anajua kwa hakika kwamba Yazid chapombe amekufuru kwa kuritadi kwake katika dini, na uadui wake kwa Mtume . Huyu hapa kiongozi wetu Imam Husein , mjukuu wa Mtume  alimwambia Muawiya pindi alipotaka achukue kiapo cha utii kwake: “Unataka kuwachanganya watu kana kwamba unasifu kitu kilichojificha, au unamsifu asiyekuwapo, au unatoa habari kutokana na yale ambayo yamezingira elimu 157


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

yake maalum. Na hakika Yazid amejulisha kwa nafsi yake juu ya msimamo wa rai yake. Basi mchukue Yazid katika yale ambayo amechukua kutokana na utafutaji wake, wa kujua jambo la mbwa wakati wa kuparua, na njiwa anapotangulia mchanga wake, na wale wachezaji mziki nawafanyastarehe za aina mbalimbali,hapo utamkuta ni muonaji. Acha yale unayojaribu, …...”139 Na haya yanatosha kwa yule ambaye ametega sikio kusikiliza, naye ni shahidi. Na tunaongeza ubainifu kwa yale aliyoyataja Twabari katika kitabu chake cha historia (Taarikh Tabari), amesema: “Na katika mwaka huu [yaani mwaka 284 A.H] Muutadhidubillah aliazimia kumlaani Muawiya bin Abi Sufyan juu ya mimbari, na akaamrisha uanzishwaji wa kitabu ambacho kitasomwa kwa watu, na yafuatayo ndiyo ambayo yamekuja katika kitabu ambacho alikianzisha Muutadhidubillah. „Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu. Sifa zote njema ni za Yule wa juu zaidi aliyetukuka, Mwenye hekima, Mtukufu Mwenye huruma… hadi aliposema katika haki ya mwanawe Yazid: 139

Imamat wa Siyaasat, Juz. 1, uk. 161 cha Ibn Qutayba, chapa ya Muassasat Hulba na vitabu rejea vinginevyo.

158


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

„Na kwa hivyo ameiharibu dini ya Mwenyezi Mungu, yule mchezaji na majogoo, duma na tumbili. Na akachukua kiapo cha utii kwa nguvu kwa wabora wa Waislamu, pia kwa mabavu, vitisho, hofu, ubabe na utishaji; naye anajua upumbavu wake, na anajua ukhabithi wake na kubwabwaja kwake. Na anamsaidia unywaji wake wa pombe na uovu wake na ukafiri. Na pindi alipoweza yale aliyoweza, akamuasi Allah na Mtume Wake kwayo. Akaomba kwa kuomboleza juu ya washirikina, na kuwaghasi Waislamu. Basi akawafanyia tukio baya watu wa Hurri, tukio ambalo halijatokea katika Uislamu, tukio baya zaidi kuliko hilo, wala ovu zaidi kutokana na yale ambayo aliyowatendea watu wema. Na nafsi yake ikapona na shauku yake, na akadhani hakika amelipiza ubaya kwa mawalii wa Mwenyezi Mungu. Na ukafikia kiwango cha uadui wake kwa Mwenyezi Mungu, basi akasema akidhihirisha ukafiri wake na kuonesha ushirikina wake: „Laiti mababu zangu wa Badri wangelishuhudia – huzuni ya khazraj kutokana na lililotokea lililoenda kasi. Hakika tumewaua watu miongoni mwa wabora wenu – na tukarudisha uelemeaji wa upande mmoja wa Badri basi ukalingana. 159


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Basi mfurahi na mpongeze kwa furaha – huko wakasema ewe Yazid acha kukumbusha hayo. Sikuwa katika vita vya handaki sasa nimelipiza – kutokana na ukoo wa Ahmed kile ambacho alichokifanya Bani Hashim wamecheza na ufalme, hakuna habari iliyokuja wala wahyi uliyoteremka.140 “Huu ni uchopokaji kutoka kwenye dini, na kauli ya yule asiyerejea kwa Mwenyezi Mungu wala kwenye dini Yake wala kwenye Kitabu Chake wala kwa Mtume Wake. Wala hamwamini Mwenyezi Mungu wala yale yaliyokuja kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Kisha miongoni mwa mazito aliyotenda katika uvunjaji wa heshima ni umwagaji wa damu ya Husein bin Ali, ambaye ni mtoto wa Fatimah binti wa Mtume , bila kujali nasaba yake kwa Mtume  na cheo chake na daraja lake katika dini. Ubora na ushahadi wa Mtume  kwake na kwa kaka yake kwamba, ni mabwana wa vijana wa peponi. Kufanya hivyo ni 140

Uthmani Khamiis anadai, na wale wa mfano wake kwamba hakika Shi‟ah – kwa ajili ya kuichafua sura ya Yazid katika akili – wananasibisha kwake shairi hili. Ninasema: Je, hakika Muudhad au Twabari ni Shi‟ah na kwa hivyo wakati waliposema: (Basi akasema hali ya kudhihirisha ukafiri wake na kuonesha ushirikina wake), na lau itasihi kwambba beti hizo ni mtu mwingine, basi kuzisoma hizo pia husababisha ukafiri wake.

160


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

kuthubutu dhidi ya Mwenyezi Mungu, na ni ukafiri kwa dini Yake, na uadui kwa Mtume  na kupambana na kukipiga vita kizazi chake na ni kuondoa heshima yake. Alipokuwa akimuuwa yeye na watu wa nyumba yake ni kana kwamba alikuwa anamuuwa mtu miongoni mwa makafiri wa Uturuki na Daylam. Haogopi kabisa adhabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na wala hachukui hadhari hata kidogo. Basi Mwenyezi Mungu akaufupisha umri wake, na akang‟oa mzizi wake na tawi lake. Akayaondoa yale yaliyo chini ya mkono wake, na akamwandalia adhabu yake kwa yale ambayo anayostahiki kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa maasi yake.”141 Shi‟ah na Upotoshwaji wa Qur‟ani: Na ama yale ambayo yanapatikana katika baadhi ya hadithi kuhusiana na kaulimbiu ya upotoshwaji wa Qur‟ani, basi ama ni yenye kuletewa tafsiri nyingine, au ni yenye kukataliwa yenye kwenda kinyume na Qur‟ani tukufu na ijimai ya Waislamu. Na lau Sheikh anataka kuzisoma rai za Shi‟ah katika suala la upotoshwaji wa Qur‟ani tukufu basi arejee katika vitabu vifuatavyo: 141

Tarikh Twabari, Juz. 8, uk. 187-188, chapa ya Muassasat A‟lami Beirut.

161


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

1. Tahqiiq fi nafii tahriif cha Sayyid Ali Maylaani. 2. Swiyaanatul-Qur‟ani mina Tahriif cha Sheikh Muhammad Hadi Ma‟rifat. 3. Al-Bayaan fi Tafsiril-Qur‟ani cha Sayyid Khuui. 4. Miizan fi tafsir Qur‟ani (Juz. 12) cha Sayyid Twabatwabai. 5. An-Nassu Khalid lam walan yuharrifa Abadan cha Sayyid Ali Musawiy Daraaby (kimetolewa na Majmau Buhuuth Islamiyya fi Mashhad – Iran, mwaka 1433H). Na hakika ametaja mtunzi wa kitabu cha mwisho miongoni mwa maandiko ya Ahlul-Bayt hadi kwa Imam Askary , yale ambayo yanajulisha juu ya kukataa kwao suala la upotoshwaji. Kisha akataja maandiko 114 kutoka kwa wanazuoni wa Kishi‟ah yenye kujulisha juu ya ukataaji upotoshwaji. Vilevile ametaja maandiko 11 miongoni mwa wanazuoni wa Ahlus-Sunnah ambao wamesema kinaga ubaga kuwa Shi‟ah wako mbali kuhusiana na kauli ya upotoshwaji. Na lau utasihi ukufurishaji wa yule anayesema upotoshwaji wa Qur‟ani, basi Sheikh atamkufurisha kila yule ambaye amesema kuhusu usomaji uliofutwa kulingana na aya.Hakika kauli hiyo ni ibara nyingine kuhusiana na upotoshwaji na uwekaji wa pazia juu ya uchongo wa kauli hii yenye kupingana na Kitabu kitukufu cha Mwenyezi Mungu. Basi inaulizwa kwa 162


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

nini umefutwa usomaji wa aya hizi na umebakia usomaji wa aya zingine zilizofutwa? Na je, umefutwa kwa ajili ya mapungufu ya uhifadhi wake au katika yaliyomo? Na Mwenyezi Mungu (s.w.t) ametakasika na ameepukana na kuteremsha aya pasi na mpaka wa kuifanya ishindikane, na yale yaliyomo ndani yake baada ya zilizobakia kama vile aya ya upigaji mawe. Na je, Sheikh anamkufurisha yule aliyekuwa akisema: „Ole wenu msiipuuze Aya ya kupopoa mawe mzinifu, asiseme msemaji: Hatukuti adhabu mbili katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu, kwa hakika Mtume  alipiga mawe na sisi tukapiga. Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi Mwake, kama si kuhofia watu watasema kuwa: Umar alizidisha katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu (s.w.t) ningeliiandika hiyo: „Mzee wa kiume na mzee wa kike wakizini basi wapigeni mawe hao wawili.‟ Na hakika sisi tuliisoma hiyo.‟142 Na katika Sahihi Bukhari, amesema: Nilichelea muda urefuke kwa watu mpaka msemaji aseme: Hatukuti upigaji mawe katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu, basi wanapotoka kwa kuacha faradhi ambayo Mwenyezi Mungu ameiteremsha.143 142

. Fat-hul-Baari juz. 12 uk. 127. . Sahihi Bukhari: 1712, na. 6829, mlango wa kukiri kwa uzinifu, kitabu cha adhabu za kisharia. 143

163


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Au je, anamkufurisha yule aliyesema: Hakika sisi tulikuwa tukisoma katika yale ambayo tunasoma katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu: Ala hamuwapendi baba zenu, hakikani ukafiri kwenu nyinyi kutowapenda baba zenu. Au hakika ni ukafiri kutowapenda baba zenu.144 Au je, anamkufurisha yule aliyesema kumwambia Ubay bin Ka‟ab: Au hatukuwa sisi tunasoma: „Mtoto wa kitanda na mzinifu wapigwe mawe.‟ Ni katika tuliyoyakosa katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu? Ubay bin Ka‟ab akasema: Ndivyo hivyo.145 Na msemaji katika sehemu hizi tatu sio mwingine bali ni Umar bin Khatwab? Au je, anamkufurisha yule aliyesema: Yalikuwa katika yale ambayo yaliyoteremshwa katika Qur‟ani ni: “Manyonyesho kumi yenye kujulikana yanaharamisha” kisha yakafutwa kwa yale matano yanayojulikana. Basi akafariki bwana Mtume  na wao wakisoma kutokana na Qur‟ani.146 Na msemaji wa hilo ni Bibi Aisha mama wa waumini? 144

. Sahihi Bukhari: 1713, mkiani mwa hadithi 6830, mlango wa kumpiga mawe mja mzito kwa uzinifu akiwa wenye kuolewa. 145 . Tafsir Durrul-Manthuur juz. 1 uk. 106. 146 Sahihi Muslim, Juz. 4, uk. 167, mlango wa uharamisho kwa manyonyesho matano.

164


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Ewe Mwenyezi Mungu! Hakika sisi tunashuhudia hakika aya hizi zilinasibishwa na Qur‟ani tukufu, na sio miongoni mwake. Na yule anayechunguza katika undani wa sentensi zake na uhifadhi wake, anasimama juu ya kwamba hayo ni maneno ya kiumbe wala hayana mahusiano yoyote na Qur‟ani tukufu. Na kwa hivyo tukasema mwanzoni mwa maelezo haya: Hakika jamhuri ya Waislamu wanaafikiana juu ya kutokuwapo na upotoshwaji. Na lau watakwenda wachache waliotoka nje ya utaratibu miongoni mwa makundi mawili, basi hilo ni suala la tafsiri au limeelezwa na yule anayetofautiana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na makubaliano ya Waislamu.

َ ُ ُ َ َ ٍ ‫َفج َأ ّي َح‬ ‫ؤمنىّن‬ ِ ‫ذيي ةعذ ي‬ ِ ِ “Basi ni mazungumzo gani baada yake watakayoyaamini”147 SUALA LA TANO UTOKEZO NI UHAKIKA WA QUR‟ANI Katika Tovuti ya Burhan kuliwekwa makala iliyobeba anwani isemayo “utokezo kwa Imamiyya.” Na miongoni mwa yale ambayo yamekuja katika utangulizi wa maneno haya, ni kauli yake: 147

Surat al-Mursalat; 77:50.

165


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

[Suala la utokezo huchukua nafasi ya juu katika itikadi ya Imamiyya Ithnaashariyya, mpaka hufikia kwamba halikosekani katika vitabu vyao vya itikadi. Na zimekuja hadithi chungu tele ndani ya vitabu vyao vya kisasa zikitukuza itikadi hii. Na mkabala wake, hakika itikadi hii imekutana na upingwaji mkali na ukosoaji mkubwa kutoka kwa watukufu wa makundi ya Waislamu, na wakashutumu hilo juu ya Shi‟ah Imamiyya. Kutokana na hatari tuionayo katika upinzani wamakundi haya mawili kuhusu itikadi hii, na kwamba makundi mawili yako pande mbili za upinzani, tumeona kuna umuhimu wa kuchukua nafasi ya kudhihirisha ukweli ili tuelezee uhakika wa suala hilo, katika njia ya uchunguzaji wa upande kauli zote mbili na insafu inayolazimu kuacha taasubi na king‟ang‟anizi, nayo ni njia ya haki na njia maridhawa yenye kuridhiwa.] Huenda msomaji akafikiria kwamba maneno ya mwandishi yanaitafuta haki au ukweli, na kwamba amechunguza maudhui hii bila taasubi na chuki. Lakini kwa hakika ameandika makala bila kuwa na chembe ya insafu na uungwana. Kwa ushahidi kwamba hakika yeye hajabainisha uhakika wa utokezo kwa mtazamo wa Shi‟ah Imamiyya, na hakika amependelea uangaliaji wa masuala ya nje. Na lau kama yeye angeliangalia yale ambayo yame166


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

semwa na wanazuoni wa Kishi‟ah au yale tuliyosema katika kitabu chetu: “Al-Badaau fi dhaw-il-Kitabi wa Sunnah” angelielewa - kama vile walivyoelewa baadhi ya Ahlus-Sunnah – kwamba, utokezo kwa maana ambayo wanaitakidi Shi‟ahImamiyya, ni uhakika wa Qur‟ani na ni itikadi yenye mashiko ambayo imesimama juu ya andiko kutoka kwa Mtume  kati ya maandiko mengi yanayotokana na kauli ya Bwana Mtume . Na inasikitisha kuona wale wanaoipinga itikadi ya utokezo wamejikita juu ya lafudhi yake ambayo kwa maana ya dhahiri, ambayo ni kudhihiri baada ya kufichika lile lisilowezekana kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t), na wakaghafilika kuhusiana na uhakika na uhalisia wake. Hakika matumizi ya neno utokezo hapa si kwa maana yake ya halisi, na hakika limetumiwa kwa njia ya kinaya mahsusi, kufuatana na yale yaliyokuja katika maneno ya Mtume  ambaye alitumia ibara ya “Mwenyezi Mungu amedokeza” katika hadithi ya mwenye ukoma, mwenye upara na kipofu, akasema: “Mwenyezi Mungu amedokeza kwa mwenye ukoma, mwenye upara na kipofu.” Na hakika ameipokea hiyo Bukhari katika Sahih yake, na tutataja yale ambayo yamekuja baada ya andiko la hadithi.148 148

Angalia: Sahih Bukhari: 852, na. 3464, kitabu Anbiyaa, mlango wa hadithi ya mwenye ukoma, kipofu na mwenye upara miongoni mwa wana wa Israeli.

167


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Na sisi tunajikita katika suala hili juu ya mambo mawili, tunaacha masuala ya nje yasiyohusika ambayo ameyataja msemaji kuhusiana na nyanja nyingine, na hakika tumejibu hayo yote katika barua yetu yenye anwani: “Utokezo katika Kitabu na Sunnah.”149 Uhakika wa Utokezo: Uhakika wa utokezo kwa Shi‟ahImamiyya ni neno moja, nalo ni uwezekano wa kubadilisha mwelekeo wa amali nzuri au amali mbaya. Na kwamba binadamu hana ukadiriaji mmoja uliyothabiti usiobadilika, bali uko mikononi mwake ubadilishaji na ukadiriaji unaochukua sehemu na nafasi ya ukadiriaji mwingine, lakini kwa mwangaza wa amali ambazo anazifanya, sawa akiwa mwema au muovu. Huu ndiyo uhalisia wa utokezo pasi na kuongeza au kupunguza, na yule anayetaka kuiunga mkono itikadi hiyo au kuijibu na kuipinga, basi ajaalie maana hiyo kuwa ni chanzo cha kuanzia uungaji mkono wake au upinzani wake na asitoke nje ya hayo. Na dalili inayoonesha kuwa binadamu ni muweza katika kubadilisha mwelekeo wake, zipo aya nyingi za Qur‟ani tukufu ambazo amefanya makusudi 149

Imechapishwa mwaka 1430H, kulingana na mlolongo; mfano wa usomaji mpya wa itikadi.

168


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

kutozitaja mhusika katika maneno hayo, kati ya aya hizo ni: 1. Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema:

َ َ َ َُ ً ُ ُ ُ َ َ َ​َ​َ ُ ‫شي َأّن َيأث َي ُهم َب‬ ٰ ‫الق‬ ‫لعجىّن‬ ‫أسنا ضحى وهم ي‬ ‫أوأ ِمن أهل‬ ِ “Au watu wa miji wameaminisha kuwa adhabu Yetu haitawafikia mchana, hali wanacheza?”150 2. Anasema:

َ ُ َُ ُ َّ َ َُ َُ ‫شس ِل‬ ِ ‫… فقلد اسحغ ِ شوا َستنم ِإّنه ماّن غ ًاسا ي‬..” ُ ُ َ​َ َ َ َ َُ ً ٰ ‫دلم ب َأ‬ ‫مى ٍل َو َتنمّن َو‬ ِ ٰ َ ‫ال اء علين ٰم ِمذساسا ور ِذ‬ ُ َ َ َ​َ ّ َ ُ َ َ َ “ ‫جعل لنم أنهـ ًشا‬ ‫يجعل لنم جنـ ٍد ور‬ “…Ombeni maghufira kwa Mola Wenu, hakika Yeye ni Mwingi wa kusamehe. Atawaletea mvua nyingi. Na atawapa mali na wana, na atawapa mabustani, na atawafanyia mito.”151 3. Anasema:

َ ّ َ ُ َ َُّ ُ َ َ َ “…..ۗ ‫ىم َح ٰ ُ غ ِّمروا ما ِبأّن ِ ِهم‬ ٍ ‫… ِإّن اللـه ال غ ِمر ما ِبق‬..” 150

Surat al-A‟Araf; 7:98. Surat Nuh; 71:10-12.

151

169


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

“Hakika Mwenyezi Mungu habadilishi yaliyoko kwa watu mpaka wabadilishe yaliyo katika nafsi zao.”152 4. Anasema:

َ ٰ َ َ َ َ ً َ ًَّ ُ ُ َ َ َ َ َ َ َ ٰ ‫ىم‬ ٍ ‫”ر ِلك ِبأّن اللـه لم يك مغ َ ِمرا ِنع ة أنع ها على ق‬ َ ّ ُ “…..ۙ ‫َح ٰ ُ غ ِّمروا ما ِبأّن ِ ِهم‬ “Hiyo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu habadilishi kabisa neema aliyowaneemesha watu, mpaka wao wabadilishe yaliyomo nafsinimwao….”153 5. Anasema:

ُ َ​َ ً َ َ ُ َ َ َ َ َ َ​َ َ َ ُ ‫شص‬ ‫قه ِمن‬ ‫…ومن يح ِق اللـه يجعل له مخشجا ور‬..” َ ُ “ ‫َحيي ال َيحخ ِ ُب‬ “..Na anayemcha Mwenyezi Mungu, Yeye humtengezea njia ya kutokea. Na humruzuku kwa upande asiotazamia…..”154 152

Surat ar-Ra‟d; 13 :11. Surat al-Anfal; 8:53. 154 Surat at-Talaq; 65:2-3. 153

170


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

6. Anasema:

ُ َ َ َ​َ ُ َ َ َ ُ َ َ َ​َ ُ َ​َ َ ‫” َو ِإر ثأرّن َسُتنم ل ِئّن شنشثم َلصرذّننم َول ِئّن ل شثم‬ َ ٌ َ َ “ ‫ِإّن َعزاثى لشذيذ‬ “Na (kumbukeni) alipotangaza Mola Wenu: mkishukuru nitawazidishia, na mkikufuru, basi adhabu Yangu ni kali sana.”155 7. Anasema:

ٰ َ​َ َ َ َ ُ َ ً ‫” َو‬ ٰ ‫ّنىحا إر‬ ‫جل فاسح َججنا ل ُه فن َجينـ ُه‬ ‫ّنادي ِمن ق‬ ِ َ َ ُ َ َ​َ َ “‫ظيم‬ ِ ‫شا الع‬ ِ ‫وأهله ِمن الن‬ “Na Nuhu alipoita zamani, Nasi tukamwitikia, na tukamwokoa yeye na watu wake kutokana na shida kubwa.”156 8. Anasema:

َ َ​َ ُ ُ َ َ َ َّ ُ َ​َ ٰ َ ‫ّند َأ‬ َ ‫” َو َأ ّي‬ ‫سح ُم‬ ‫ىا ِإر ّنادي سته أنى م ِن الضش وأ‬ َ َ َ ‫ّٰر‬ ُ ‫اسح َججنا َل ُه َف َن َش نا ما به من‬ “…..‫ض ٍّش‬ ‫الش ِح مّن ف‬ ِ ِ​ِ 155 156

Surat Ibrahim; 14:7 Surat al-Anbiyaa; 21:76.

171


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

“Na Ayub alipomlingania Mola Wake: hakika mbimiimenigusa dhara, Nawe ndiye unayerehemu zaidi kuliko wanaorehemu. Basi tukamwitikia na tukamuondolea dhara …..”157 9. Anasema:

َ ٰ َ َ َ َ َ ّ َ ُ َ َ ‫” َف َلىال َأ َّن ُه‬ ‫ىم‬ ِ ‫ماّن ِمن اا ِجحمّن لل ِجي فى ب َط ِن ِه ِإلى ي‬ َ َ ُٰ َ​َ​َ َ َ ُ ٌ ‫شاء َو ُه َى َس‬ ‫قيم َوأ َّنجخنا َعل ِيه‬ ِ ‫يجعثىّن فنجزّنـه ِبالع‬ ًَ َ َ َ “‫قطمّن‬ ٍ ‫جش ِمن ي‬ “Na lau asingelikuwa ni katika wanaomtakasa Mwenyezi Mungu, bila shaka angelikaa tumboni mwake mpaka siku yakufufuliwa. Kisha tulimtupa ufukweni patupu, hali ya kuwa mgonjwa. Na tukamuoteshea mmea wa mung‟unye.”158 Hakika aya hizo zinaelezea kuhusiana na amali njema zenye athari katika mwelekeo wa binadamu, na kwamba yeye anaweza kwa amali yake nzuri akabadilisha makadirio na ubadilishaji wa jambo lililopangwa. Kwani hilo sio katika matendo ya 157 158

Surat al-Anbiyaa; 21:83-84. Surat 37 aya 143-146.

172


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

binadamu ya hiari yenye kukadiriwa ya lazima, mpaka mja awe katika kukabiliana nalo ni mwenye kufungwa mikono na miguu. Na yale ambayo tuliyoyataja kuhusiana na uhakika wa Qur‟ani, tunaona mfano wake katika Sunnah ya Bwana Mtume , kwani hadithi zinaunga mkono kwamba binadamu anauwezo wa kubadilisha makadirio kwa ukadiriaji mwingine kwa matendo mema, na tunafupisha kwa kutaja machache kati ya mengi. 1. Ameeleza Hakim kutoka kwa Ibn Abbas amesema: Mtume  amesema: “Tahadhari hainufaishi mbele ya kadari, lakini Mwenyezi Mungu anafuta kwa dua yale ayapendayo kutokana na kadari.”159 2. Ameeleza Ibn Saa‟d, Ibn Hazm na Ibn Mardawayh kutoka kwa Kalbi katika aya hii:

َ ُ ُ َ ‫الل ُـه ما‬ “….. ‫شاء َو ُر ِثحد‬ ‫” َي ُحىا‬ “Mwenyezi Mungu hufuta na huimarisha ayatakayo…..”160 Akasema: “Anafuta riziki na anaongeza, na anafuta umri na anaongeza.” Basi ikaulizwa: Ni nani amekuhadithia hili? Akasema: Abu Saleh kutoka kwa Jabir bin Abdillah Answari, kutoka kwa Mtume . 159

Tafsir Durrul-Manthuur, Juz. 13, uk. 660, chapa ya DaarulFikr Beirut mwaka 1403H. 160 Surat ar-Ra‟d; 13:39.

173


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

3. Na ameeleza Ibn Mardawayh na Ibn Asakir kutoka kwa Ali kwamba alimuuliza bwana Mtume  kuhusiana na aya hiyo akamwambia: “Nitatuliza macho yako kwa tafsiri yake, na nitatuliza jicho la umma wangu baada yangu kwa tafsiri yake. Sadaka sahihi, kuwatendea wema wazazi wawili na kufanya mema, hubadilisha uovu kuwa wema, na huongeza katika umri na hukinga ubaya.”161 Na zisizokuwa hizo miongoni mwa hadithi zilizotapakaa katika vitabu vya tafsiri na hadithi hususan katika athari za dua na urejeo. Huu ndio uhakika wa utokezo katika Kitabu na Sunnah, na hii ndio itikadi ya Shi‟ahImamiyya kuhusu utokezo. Je, inawezekana kwa Mwislamu muumini wa Qur‟ani na Sunnah akanushe uhakika huu na aitakidi tofauti na hivyo, mpaka aangukie katika hesabu ya Mayahudi ambao wamekanusha utokezo kwa maana hii na wakasema: “Mkono wa Mwenyezi Mungu umefumba,”162 basi Mwenyezi Mungu (s.w.t) akawajibu hao kwa kauli yake: “Mikono yao ndio iliyofumba”163 Athari ya wale wenye kuamini Utokezo Hakika itikadi ya utokezo ina athari chanya ya kimalezi. Hakika binadamu iwapo ataitakidi kwamba 161

Tafsir Durrul-Manthuur, Juz. 13, uk. 661. Surat al-Maida; 5:64 163 Surat al-Maida; 5:64 162

174


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

akaisi na kuhukumiwa kuingia motoni basi hatojali kuitengeneza hali yake katika mustakabali wa siku za usoni za umri wake, na hivyo kwa itikadi yake hakika ukadirio wa kwanza unatekeleza katika haki yake, sawa amefanya mema au maovu.Na hili linapelekea kuzama kwake katika maasi katika maisha yake yote. Na ama ikiwa ataitakidi kwamba hakika Mwenyezi Mungu (s.w.t) ni Mpole Mwenye huruma, na lau ataitengeneza hali yake katika mustakabali, basi Mwenyezi Mungu (s.w.t) atamtengenezea yeye ukadirio wake na atambadilishia yeye kwa aina inayolingana na amali yake nzuri, basi ataitengeneza na kuibadili hali yake. Na kuhusu hilo Mwenyezi Mungu (s.w.t) ananadi kwa waja Wake kwa kauli yake:

ُ َ ٰ َ َ ‫” ُقل ٰـعجاد َي َال‬ َ ‫زين َأ‬ ‫لى أّن ِ ِهم ال‬ ‫سشفىا ع‬ ِ ِ َ َ َ ُ ُ َ َ​َ َ َ َ َ‫الزّنىا‬ ‫ثقنطىا ِمن سح ِة الل ِـه ِإّن اللـه غ ِ ش‬ ً ‫َج‬ “…..‫يعا‬ “Sema: Enyi waja Wangu waliozifanyia israfu nafsi zao! Msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu husamehe dhambi zote…..”164

164

Surat az-Zumar; 39:53.

175


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Matukio Ambayo Mwenyezi Mungu Amedokeza Kwayo: Huenda Manabii wa Mwenyezi Mungu wametoa habari kuhusiana na utokeaji wa tukio katika mustakabali lakini halikutokea. Na mfano wa hilo ni masuala mbalimbali ambayo tunaona kwamba mawalii walitoa habari za kutotokea kwake lakini hayakutokea. Na hakuna kilichozuia hayo isipokuwa amali nzuri, na lau si amali hizo basi lingelitokea ambalo Nabii amelitolea habari. Na hapa tunatolea ishara baadhi ya mambo hayo: 1. Uondoaji wa adhabu kwa watu wa Nabii Yunus : Nabii Yunus alitoa habari ya uteremkaji wa adhabu kisha akawaacha watu wake na wakawa katika ahadi yake, hali ya kuwa ni mkweli na mwenye kutegemea juu ya muktadha wa adhabu ambayo aliyoelezwa. Lakini ushukaji wa adhabu ulikuwa wenye masharti ya kutokuwepo kizuizi, ninamaanisha; toba na unyenyekevu. Ikiwa kitakuwepo kizuizi hapo haitakusanyika sababu iliyotimia ya adhabu, Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema:

َ​َ َ َ ‫ءام َند َف َن َ َعها إي ٰـ ُنها إ ّال َق‬ َ ‫ماّند َق َشر ٌة‬ ‫ىم‬ ‫فلىال‬ ِ َ َ َ َّ َ ُ َ َ َ ‫ضي ِفى‬ ‫يىن‬ ِ ‫س اا ءامنىا لش نا ع ُنهم عزاا‬ ِ ‫اال‬ ٰ َ ُ ٰ َ ٰ ُ َ​َ ‫حمّن‬ ٍ ‫االيى ِ الذّنيا ومحعنـهم ِإلى‬ 176


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

“Kwa nini usiweko mji ulioamini na imani yake ikawafaa, isipokuwakaumu ya Yunus? Walipoamini tuliwaondolea adhabu ya hizaya katika maisha ya dunia na tukawastarehesha kwa muda.”165 2. Ubadilikaji kuhusiana nakuchinjwa kwa Ismail: Qur‟ani tukufu imetaja kwamba hakika Nabii Ibrahim aliona usingizini anamchinja mwanawe Ismail, na akamjulisha hilo, ili liwe jepesi juu yake, na ili aijaribu subira yake na azma yake juu ya utiifu kwa Mwenyezi Mungu na utiifu kwa baba yake. Na akasema kama Qur‟ani tukufu inavyonukuu: “Hakika mimi ninakuchinja.” Na hii ni kauli inayoelezea kuhusiana na uhakika uliothabiti na utokeaji uliyotokea. Isipokuwa hakika jambo hilo halikutokea na likafutwa ufutwaji wa kisharia, kama vile hakukutokea uchinjaji wa Ismail katika hali ya nje basi ukawa ufutaji ni wa kimaumbile. Na hili ndilo limeelezwa katika Surat Swafaat.166 165

Surat Yunus; 10: 98, angalia yale yaliyotajwa kuhusu kisa cha nabii Yunus  katika tafsiri ya Durrul-Manthuur, Juz. 7, uk. 121 na 122. 166 Angalia Sura 37 aya 101-111.

177


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

3. Kukamilika kwa miadi ya Musa : Wafasiri wametaja kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) alimwahidi katika miadiya Nabii Musa usiku 30 ili kuchukua Taurat. Basi Musa  akafunga na kushinda bila kula na kunywa. Na pindi ilipotimia miadi Mwenyezi Mungu (s.w.t) akamwamrisha akamilishe kwa usiku kumi, akasema (s.w.t):

َ​َ َ ٰ َ َ​َ ً َ َ َ ٰ َ ٰ َ َٰ ‫شش فح َم‬ ٍ ‫”و ٰوعذّنا َمىوس رلـثمّن ليلة وأث نـها ِةع‬ ًَ َ َ ُ “…..‫ميقـد َسِّت ِه أ َسثعمّن ليلة‬ “Na tulimwahidi Musa masiku thelathini na tukayatimiza kwa kumi; ndipo ikatimia miadi ya Mola Wake siku arobaini”167 Basi katika kisa hicho yapo maelezo ya aina mbili: Hakika yeye alikaa katika miadi usiku 30, kisha akafuta hilo kwa habari nyingine kwamba atakaa usiku 40. Na akakaa Musa  mkweli katika maelezo yote mawili, ambapo ilikuwa habari ya kwanza ikitegemea sababu iliyopelekea kukaa usiku 30, kama kusingekuwepo sababu nyingine ambayo ilipelekea kukaa zaidi ya usiku 30.168 167

Surat al-A‟araf; 7:142. Angalia: Tafsir Durrul-Manthuur, Juz. 3 uk. 335.

168

178


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Hayo ni jumla ya matukio ambayo walipewa habari Manabii wa Mwenyezi Mungu juu ya utokeaji wake, na habari yake imekuja katika utajo wa Mwenyezi Mungu Hakimu, isipokuwa hakika hayo hayakutokea. Na haya ndio ambayo yanatajwa kwamba Mwenyezi Mungu ametokewa nayo, na utakujia ufafanuzi wa aina ya matumizi ya matamshi haya katika sehemu husika, basi ngojea. Haya yamo ndani ya Qur‟ani tukufu. Na ama yale ambayo yameelezwa na hadithi sahihi kutoka kwa Bwana Mtume , basi ni vyema haya kidogo uyajue. i. Myahudi mmoja alipita kwa Mtume  akasema: Saamu Alayka (mangamio yawe juu yako). Mtume  akamwambia: “Na yawe juu yako.” Maswahaba wake wakasema: Hakika amekusalimia kwa kukuombea kifo, akasema: Mauti yawe juu yako? Basi Mtume  akasema: “Na vivyo hivyo nimerudisha” kisha Mtume  akawaambia Maswahaba zake: “Hakika yahudi huyu atang‟atwa na mdudu mweusi mgongoni kwake na atauawa kwa sumu yake.” Basi yule yahudi akaondoka akaokota kuni nyingi, kisha haukupita muda akaondoka. Mtume  akamwambia: “Ziweke chini hizo kuni.” Akaziweka, basi ghafla mdudu mweusi akaonekana ndani ya kuni ameng‟ata juu ya kijiti, Mtume  akamwambia: “Ewe yahudi! Kitu gani umekifanya 179


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

leo?” akajibu: “Sikufanya amali yoyote ila kuni hizi ambazo nimezibeba na nikaja nazo, lakini nilikuwa na biskuti mbili basi nikala moja na nikatoa sadaka moja kwa masikini.” Basi Mtume  akasema: “Mwenyezi Mungu amekuepusha naye kwayo,” akasema: “Hakika sadaka inamkinga mwanadamu na kifo kibaya.”169 ii. Alipita Masihi Isa  kwa watu wenye kufurahika na mwanamke, basi akasema: Wana nini hawa? Ikasemwa: Ewe roho wa Mwenyezi Mungu! Fulani bint fulan anapelekwa kwa fulani katika usiku wake huu. Basi akasema: Wanamfurahia leo na watalia kesho. Msemaji miongoni mwao akasema: Kwa nini ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: Kwa sababu mtu wao atakufa usiku huu. Na wakati walipoamka wakamkuta katika hali yake, hana yeye kitu chochote.Wakasema: Ewe roho wa Mwenyezi Mungu! Hakika ambaye ulitupa habari jana kwamba yeye ni mfu bado hajafa. Basi akaingia Masihi nyumbani kwake akamuuliza: Umefanya nini usiku wa leo? Akasema: “Sijafanya chochote isipokuwa nilichokuwa ninakifanya katika siku zilizopita. Hakika alikuwa akitujia muombaji kila usiku wa ijumaa, basi tunampa yale aliyoyakosa.” Masihi akasema: “Inuka mahali ulipokaa na kaa kando.” Basi chini ya nguo yake akaonekana nyoka mfano wa 169

Biharul-Anwaar, Juz. 4, uk. 121.

180


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

shina la mti, ameng‟ata mkia wake. Akasema : “Kwa kitu ambacho umekifanya ndio umeepushwa na huyu.”170 Nini maana ya: “Mwenyezi Mungu ametokewa katika hadithi ya Mtume ? Hili ni jambo la pili ambalo tumetaka kulipitia, nayo ni sababu ya uelezaji wa utokezo kulingana na uhakika wa Qur‟ani ulio dhahiri. Hakuna shaka kwamba utumiaji wa neno utokezo kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) pasi na masharti, kwa maana ya kudhihirika baada ya kufichika, ni jambo halitumii wala kulifanyia kazi hilo ila mjinga. Hakika Mwenyezi Mungu (s.w.t) ni Mjuzi wa kila kitu kabla ya uumbaji, wakati wa uumbaji na baada ya uumbaji wake, na inakuwa ni muhali asifike Mwenyezi Mungu kwamba ametokezewa, yaani limedhihirika Kwake baada ya kujificha. Na ama aina ya uelezaji kuhusu uhakika huu kwa lafudhi ambayo inazuia kusifika kwa MolaManani, kwa maana ya hakika basi hapa kuna mambo mawili: 1. Hakika Shi‟ah Imamiyya wamefuata athari ya Mtume  kuhusiana na suala la utokezo kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t), ambapo ameeleza Bukhari 170

Biharul-Anwaar, Juz. 4, uk. 94.

181


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

katika Sahih yake kutoka kwa Abu Huraira: Hakika alisikia kutoka kwa Mtume  kuhusiana na watu watatu wa wana wa Israeli; mwenye ukoma, mwenye upara na kipofu, basi Mwenyezi Mungu akafanya utokezo kuwa awajaribu hao. Basi akawatumia malaika akaenda kwa mwenye ukoma, kwa mwenye upara na kwa kipofu. Akamwambia mwenye ukoma: Ni kitu gani kinapendeza zaidi kwako? Akajibu: Rangi nzuri na ngozi nzuri, na hakika watu wameniona kuwa ni mchafu. Akasema: Basi akamfuta yeye na ikamuondokea hali hiyo na akapatiwa rangi nzuri na ngozi nzuri. Akasema: Ni mali gani unaipenda zaidi? Akasema: Ngamia au akasema: Ng‟ombe – akapewa ngamia jike, na akamwambia: Allah atakutilia baraka kwake. Akamwendea mwenye upara akasema: Ni kitu gani unakipenda zaidi wewe? Akajibu: Nywele nzuri na iniondokee mimi hali hii, hakika watu wameniona mchafu, akasema: Akamfuta, hali ya upara ikaondoka, na akampatia nywele nzuri, akasema: Ni mali gani unaipenda zaidi? Akasema: Ng‟ombe. Akasema: Basi akampatia yeye ng‟ombe jike mwenye mimba, akasema: Ubarikiwe kwa hilo. Na akamjia kipofu akamwambai: Ni kitu gani unakipenda zaidi? Akasema: Mwenyezi Mungu anirudishie macho yangu, ili nione watu kwayo, akasema: Basi akamfuta yeye na Mwenyezi Mungu akamrudishia 182


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

macho yake. Akasema: Ni mali gani unaipenda zaidi? Akasema: Mifugo, basi akampatia yeye mbuzi jike mzazi. Basi ikapatikana mifugo mingi. Basi bonde likawa na ngamia, na bonde jingine limejaa ngâ€&#x;ombe na bonde lingine limejaa mbuzi. Kisha akamjia mwenye ukoma katika sura yake na umbo lake, akasema: Mimi mtu masikini nimeishiwa na masurufi katika safari yangu, wala leo siwezi kufika ila kwa msaada wa Mwenyezi Mungu na kisha msaada wako. Ninakuomba kwa kile ambacho amekupa Mwenyezi Mungu rangi nzuri, ngozi nzuri na nyumbu na ngamia, uniwezeshe mimi nifike safari yangu. Akamwambia: Hakika haki ziko nyingi. Naye akamwambia: Kana kwamba mimi ninakujua je, hukuwa wewe mwenye ukoma watu wakakuona ni uchafu. Ulikuwa fukara basi Mwenyezi Mungu akakupatia mali? Akasema: Hakika nimerithi kutoka kwa mzazi wangu? Akasema: Ikiwa wewe ni muongo basi Mwenyezi Mungu akubadilishe na uwe kama ulivyokuwa hapo kabla. Basi akamwendea mwenye upara katika sura yake na umbo lake, akamwambia mfano wa yale aliyomwambia yule. Basi akamjibu mfano wa yale aliyomjibu wa kwanza, basi akasema: Ikiwa wewe ni muongo basi Mwenyezi Mungu akufanye kama ulivyokuwa. 183


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Akaenda kwa kipofu katika sura yake na umbo lake, akasema: Mimi ni mtu masikini ni msafiri nimeishiwa na masurufu ya safari yangu, na sina pa kupata ila kwa Mwenyezi Mungu na kwako. Ninakuomba kwa haki ya yule aliyekurudishia macho yako, na akakupatia mbuzi uniwezeshe nifike safari yangu. Akasema: Hakika nilikuwa ni kipofu na Mwenyezi Mungu akanirudishia macho yangu. Na nilikuwa fukara na akanitajirisha, basi chukua kile ukipendacho. Naapa kwa Mwenyezi Mungu sitokunyima leo chochote utakachochukua kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Akasema: Chukua mali yako hakika Mwenyezi Mungu amewajaribu nyinyi na kwa hakika Mwenyezi Mungu amekuridhia wewe na ghadhabu ipo juu ya marafiki zako.171 Haya ndiyo maelezo ya Mtume  na Waislamu wote wameamrishwa kumfuata yeye, kulingana na kauli ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) aliposema:

َُ َ َ ٌَ ٌَ ُ َ ‫َ ل‬ َ​َ َ ‫سى َح َ نة ِان ماّن‬ ‫لقذ ماّن لنم فى سسى ِ الل ِـه أ‬ َ َ َ َ َ َ ‫َ َ َ َ َ ٔـ‬ ُ َ ً ‫الل َـه َل‬ ‫ثمرا‬ ‫اخش ورلش‬ ِ ‫يشجىا اللـه واليىم الـ‬ “Hakika ninyi mna ruwaza njema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 171

Sahihi Bukhari: 852 na. 3464, kitabu Anbiyaa, mlango wa hadithi ya mwenye ukoma, mwenye upara na kipofu katika wana wa Israeli.

184


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

kwa mwenye kumtarajia Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho, na akamkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi.”172 Hakika uwezo usio na mipaka wa kauli hii unakuja kutokana na mlango wa mishkeli mbalimbali, nao ni mlango mpana katika maneno ya Waarabu, kwani Mwenyezi Mungu (s.w.t) katika nyanja nyingi mahsusi anaelezea kuhusiana na kitendo chake kwa lile ambalo watu wanalielezea kuhusiana na vitendo vyao. Na sio hilo ila kwa ajili ya mishkeli ya dhahiri, na haya ni yale tunayoyasoma ndani ya Qur‟ani tukufu kama ifuatavyo: Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema:

ٰ ٰ َ ُٰ َ َ ‫ِإ َّن اانـ ِ قمّن ُيخـ ِذعىّن الل َـه َو ُه َى خـ ِذ ُع ُهم‬ “Hakika wanafiki wanamdanganya Mwenyezi Mungu, naye atawaadhibu kwa sababu ya udanganyifu wao.”173 Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema:

َ َ َُ َ َ َ​َ َ َ ‫الل ُـه َخ ُمر ااٰـن‬ ‫شرن‬ ‫َو َمنشوا ومنش اللـه و‬ ِ 172

Surat al-Ahzab; 33:21. Sura 4 aya 142.

173

185


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

“Na wakapanga njama; na Mwenyezi Mungu akapanga njama, na Mwenyezi Mungu ndiye mbora wa kupanga njama.”174 Na Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema:

ٰ

ُ

ُ

َ

َ

ُ

َ

َ َ َ َ َ َ ٰ “…..‫ىمنم هـزا‬ ِ ‫”وقيل اليىم ّنن ىنم ل ا ن حم ِلقاء ي‬ “Na itasemwa: Leo tunawasahau kama mlivyosahau mkutano wa siku yenu hii…..”175 Hakuna shaka kwamba Mola Manani (s.w.t) hafanyi udanganyifu wala vitimbi wala hasahau, kwa sababu hizo ni sifa za binadamu dhaifu. Ila yeye (s.w.t) anavisifu vitendo vyake kwa vile ambavyo watu husifika navyo kutokana na mlango wa mushkeli, na yote ni kinaya kutokana na ubatilishaji wa udanganyifu wao, vitimbi vyao na kunyimwa kwao msamaha wa Mwenyezi Mungu (s.w.t), na kwa hivyo kukosa pepo Yake na neema Zake. Hakika Laam (L) katika kauli ya Mtume : “Mwenyezi Mungu katokezewa” hiyo ina maana ya (min) kutoka, yaani utokezo kutoka kwa Mwenyezi 174

Sura 3 aya 54. Sura 45 aya 34.

175

186


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

Mungu kwa ajili ya watu. Waarabu husema: Hakika fulani ametokezewa na amali sahihi, au ametokezewa na maneno ya ufasaha, kama vile wanavyosema: fulani ametokezewa hivi, basi wanajaalia Laam (L) kuwa sehemu ya min (kutoka) basi kauli yao: Mwenyezi Mungu ametokezewa, yaani utokezo kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) kwa ajili ya watu. Basi juu ya mwangaza wa pande hizi inasihi kulitamka neno (utokezo) bila kuliwekea mipaka juu ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) na sifa zake. Huu ndiyo uhakika wa utokezo na athari yake ya ujengaji katika malezi ya binadamu juu ya mfumo wa Kiislamu sahihi, na yamekuwa wazi kwa mpendwa msomaji matumizi ya lafudhi kwa ubainifu wa uhakika huu. Kama vile tulivyosema yule ambaye anayetaka kupinga au kuunga mkono uhakika wa suala hili basi afanye utafiti kuhusiana na mchakato huu na aachane na mambo ya nje yasiyofungamana na maudhui. Na hilo limekuwa ni gumu zaidi kwa yule anayeweka mushkeli.Vyovyote itakavyokuwa lau itasihi sanad yake, kati ya hadithi za utokezo ni: 1. Ile ambayo inanasibishwa kwa Imam Swadiq  kuwa alisema: “Mwenyezi Mungu hakufanya utokezo kama vile alivyofanya utokezo wake kuhusiana na Ismail.” 187


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

2. Ile ambayo inanasibishwa kwa Imam AmirulMuuminina Ali  ambapo alitoa habari kupatikana kwa raha baada ya miaka 70 na halikutokea hilo. Na hakika tumezisoma hadithi hizo kisanad na kidalili katika mihadhara yetu kuhusaina na suala la “utokezo” ambao ameuandika Allamah Alhaji Sheikh Ja‟far Hadi. Basi ni juu ya mwandishi arejee barua hiyo ambayo haitupi nafasi kuielezea hapa kuchelea kuwachosha wasomaji. WATU NI MAADUI KWA WASILOLIJUA Na miongoni mwa yale ya kushangaza zaidi niliyoyaona kuhusiana na suala la utokezo sehemu nyingine Sheikh Ibrahim Junadi ameandika kwa kusema: Utokezo kwa Shi‟ah ni fikra iliyoanzishwa na Mayahudi. Na haki isemwe: Hakika watu ni maadui wa wasilolijua, na masikini huyu hajuwi kwamba imani ya utokezo iko upande wa upinzani dhidi ya itikadi ya Mayahudi, ambapo hakika wao wamekanusha ufutaji kabisa. Na linalojulikana ni kwamba utokezo katika maumbile ni kama vile ufutaji katika sharia, basi wao wanakanusha haya mawili yote.Na lau akitaka mwandishi kwa marefu na mapana basi arejee katika 188


SHIA NA VYOMBO VYA HABARI

tafsiri ya kauli ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) inayosema:

َ َُ ٌ َ َ َ ُ َ ُ َ َ َ ُ ‫يذّيهم َول ِعنىا ِب ا‬ ِ ‫وقال ِد اليهىد يذ الل ِـه مغلىلة غلد أ‬ َ َ ُ ُ َ َ َ َ ُ َ َ ُ َ ‫يف‬ ‫شاء َول َمزيذ َّن‬ ‫حاّن ين ِ ق ل‬ ِ ‫قالىا بل يذا ُ مح ى‬ َ ٰ ُ ً ُ َ َ َ َ ً ‫َل‬ ‫ثمرا ِم ُنهم ما أ ِّنض َل ِإليك ِمن َسِّتك غيـنا َول ًشا َوألقينا‬ ٰ َ َ َُ َ ‫َب َين ُه ُم‬ َ ‫الع ٰذ َو َ َو‬ َ ‫القيـ َ ِة مل ا أوقذوا‬ ‫غضاء ِإ ٰلى َي‬ ‫الج‬ ِ ‫ىم‬ ِ َ َ َ َ َ َ َ​َ َ َ ً ‫سض‬ ‫شا أ أ َها الل ُـه‬ ِ ‫ّناسا ِل ل‬ ِ ‫وي عىّن ِفى ألا‬ ُ َ ُ َُ َ ً َ ‫ذين‬ ِ ‫ف ادا واللـه ال ي ِح ُب اا‬ “Walisema Mayahudi: Mkono wa Mwenyezi Mungu umefumba. Mikono yao ndiyo iliyofumba, na wamelaaniwa kwa waliyo yasema. Bali mikono Yake iko wazi hutoa apendavyo. Kwa hakika yaliyo teremshwa kwako kutoka kwa Mola Wako yatawazidisha wengi katika wao uasi na kufuru. Na tumewatilia uadui baina yao na chuki mpaka Siku ya Kiyama. Kila mara wanapowasha moto wa vita Mwenyezi Mungu anauzima. Na wanajitahidi kuleta ufisadi katika ardhi. Na Mwenyezi Mungu hawapendi wafisadi.”176 176

Surat al-Maidah; 5:64.

189


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.