Sunan an nabi

Page 1

Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page i

SUNAN AN-NABI Kimeandikwa na:

Allamah Sayyid Muhammad Husayn Taba’taba’i.

Kimetarjumiwa na: Ramadhani Kanju Shemahimbo


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page ii


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page iii

Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 - 512 - 45 - 4

Kimeandikwa na: Allamah Sayyid Muhammad Husayn Taba’taba’i.

Kimetafsiriwa na: Ramadhani Kanju Shemahimbo

Kupangwa katika Kompyuta na: Hajat Pili Rajab Toleo la kwanza: Januari, 2009 Nakala:1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page i

YALIYOMO Mlango wa 1 Sifa na Tabia bainifu za Kimaadili za Mtukufu Mtume (s.a.w.w)..................2

Mlango wa 2 Uhusiano wake Mtukufu Mtume (s.a.w.w) na watu.....................................21

Mlango wa 3 Usafi na Kanuni za kujipamba......................................................................51

Mlango wa 4 Kusafiri na adabu zake..................................................................................61

Mlango wa 5 Adabu za mavazi na chochote kinachoambatana na jinsi ya kuyavaa..........67

Mlango wa 6 Sunnah yake katika mavazi..........................................................................75

Mlango wa 7 Adabu za kulala na kando ya kitanda............................................................78

Mlango wa 8 Adabu za ndoa na watoto..............................................................................82

Mlango wa 9 Vyakula, vinywaji na Adabu za Mezani........................................................90

Mlango wa 10 Adabu za Chooni........................................................................................100

Mlango wa 11 Wafu na chohote kinachohusiana (na kifo).................................................114

Mlango wa 12 Adabu za Matibatu......................................................................................122

Mlango wa 13 Kupiga Mswaki (Siwak).............................................................................126

Mlango wa 14 Adabu za Wudhuu......................................................................................128


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page ii

Mlango wa 15 Adabu za kuoga (Ghusl).............................................................................132

Mlango wa 16 Adabu za Swala..........................................................................................135

Mlango wa 17 Adabu za (kufunga) Swaumu.....................................................................168

Mlango wa 18 Adabu za Itikaf...........................................................................................175

Mlango wa 19 Adabu za kutoa Sadaka...............................................................................176

Mlango wa 20 Adabu za kusoma Qur’an Tukufu...............................................................178

Mlango wa 21 Maombi (Du’a) na adabu zake...................................................................183

Mlango wa 22 Hijja............................................................................................................249


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page iii

NENO LA MCHAPISHAJI Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza kwa jina la: “Sunan An-Nabi” Sisi tumekiita: "Sunnani-Nabii." Kitabu hiki, "Sunnani-Nabii" ni matokea ya kazi ya kielimu iliyofanywa na Mwanachuoni wa Kiislamu, Allamah Sayyid Muhammad Husayn Taba’taba’i. Kitabu hiki ni mkusanyiko wa matendo simulizi juu ya mwenendo na tabia ya mtukufu Mtume (saw). Matendo, simulizi na kunyamaza kwa Mtume hujulikana kama Sunna katika istilahi za Kiislamu. Kwa hiyo, kwa ujumla kitabu hiki huzungumzia maisha ya mtukufu Mtume (saw). Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote. Kutokana na ukweli huu, Taasisi yetu ya 'AlItrah Foundation' imeona ikitoe kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili, kwa madhumuni yake yale yale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili, ili kuongeza ujuzi wao katika masuala ya dini na ya kijamii. Tunamshukuru ndugu yetu, Al-Akh Ramadhani Kanju Shemahimbo kwa kukubali jukumu hili la kukifanyia tarjuma kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation S. L. P. 19701

Dar-es-Salaam, Tanzania.


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page iv

DIBAJI Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu, Mola wa ulimwengu, na rehma na amani juu ya bwana wetu Muhammad (s.a.w.w.) na kizazi chake kitakatifu. Said Muhammad Husein ibn Muhammad Husein al-Hasani al-Husein – Mwenyezi Mungu amsamehe makosa yake: Hiki ndio Mwenyezi Mungu alichokifanya kiwezekane kwa sisi kukusanya kutoka kwenye baadhi ya simulizi za wasimuliaji wa Kiislamu, za mwenendo wa bwana wetu, Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) katika muda mfupi na kipindi kidogo kilichopatikana. Tunamuomba Mwenyezi Mungu swt. atujaalie sisi uwezo wa kuzifuata Sunnah hizi kwa kiasi iwezekanavyo. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:

“Kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu ninyi mnacho kigezo chema,” (Surat Ahzab: 21). na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema katika ushauri wake kwa Ali (a.s.): “…..Na sita ni kufuata Sunnah zangu katika swala zangu na saumu na kutoa kwangu sadaka.”2 Na Imam Ali (a.s.) amesema: “Yeyote atakayejidhibiti mwenyewe kwa tabia ambayo Mwenyezi Mungu anataka mja wake awe nayo, yeye atajaaliwa ustawi wa kudumu.”3 Kwa nyongeza, Imam al-Sadiq (a.s.) amesema: “Nitachukia kwa mtu kufariki kabla hajatwaa tabia moja yoyote katika tabia za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).”4 Kwa hakika, kufuata nyayo zake na kutwaa tabia zake bainifu ndio ukamilifu wa kweli na lengo la mwisho, na ni kwa hili ambapo mtu anaweza kupata mafanikio katika dunia hii na ile dunia ya akhera. 2 al-Mahasin: 17, al-Kafi 8:66, al-Faqih 4:188, Majmu’at Warram 2:91, Da’aim al-Islam 2:347. 3 Tafsiir inayohusishwa na Imam al-Askari (a.s.):17, Adabu Qira’ati al-Qur’an namba. 3, Biharul Anwar 92:214. 4 Makarimul-Akhlaq: 39


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page v

Tumeacha kutaja mambo ya Makruhu (yenye kuchukiza), kwani ni sehemu ya imani yetu kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kamwe hakufanya makuruhu yoyote au vitendo vinavyoruhusiwa katika namna inayochukuliwa kuwa ni makuruhu au ruhusa, na hili hasa limethibitishwa kwa ushahidi wa hekima na kiroho. Tuliamua kuziondoa zile nyororo za wasimuliaji wa riwaya hizo kwa ajili ya kupunguza maneno, hata hivyo tumeyataja majina ya vitabu na waandishi wake, na tumetofautisha kati ya zile riwaya zenye nyororo kamili na zisizo na nyororo kamili ili kwamba yoyote anayetaka kukipata chanzo cha riwaya hizo anaweza kuzipata kwa urahisi. Tumeitaja pia tabia yake kwa sababu ya fadhila zake na kwa sababu inahusiana na hulka yake adilifu ingawaje haiingii kwenye maudhui ya kitabu hiki. Hatukutaja maelezo maalum ya matukio lakini badala yake tumeshughulika kwa umakini zaidi katika vipengele vya kawaida, na kwa Mwenyezi Mungu ndiko tunakotafuta msaada.s

Sayyid Muhammad Husein Taba’taba’i


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page vi

SUNAN-NABII

UTANGULIZI Tunaanza kwa jina la Mwenyezi Mungu ambaye kutoka Kwake mambo yote yalianzia na Kwake kila kitu kitarejea. Tunaomba msaada kutoka Kwake peke yake; Yeye ndio chanzo halisi, wingi na neema zote zinatoka Kwake. Sifa zote na shukrani ni Zake Mwenyezi Mungu, wa kwanza kabla ya yoyote yule, na wa mwisho ambaye baada Yake hakutakuwa na mwingine tena. Yeye ambaye macho hayawezi kumuona na sifa Zake haziwezi kufahamika kwa tafakari. Yeye aliuumba ulimwengu kwa utashi Wake, halafu akayageuza maumbile kama alivyotaka na akayajaalia mapenzi Yake. Ewe Allah! Mbariki Muhammad, mlezi wa wahyi Wako, mbora wa viumbe Wako, kiongozi wa wema, ufunguo wa neema tukufu na mwisho wa Mitume na Manabii Wako. Ewe Allah! Ibariki familia ya Muhammad na kizazi chake kitakatifu na wale kutoka miongoni mwao, ambao wako karibu sana na Wewe, kwa baraka na neema bora, na uwashushie rehema zinazojumuisha kila kitu na kamilifu juu yao, rehma ambazo hazina mwisho na zenye kuendelea. Amina – Rabbil-A’lamiina. Kwa hakika kuna nyanja za elimu ambazo ni makhsusi kwa wale ambao wako karibu na Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla., na hawa ni wale ambao wanatajwa kama Mitume wa Mwenyezi Mungu, na Mtume wa mwisho ambaye alitumwa na Mwenyezi Mungu kwa ajili ya mwongozo wa wanadamu alikuwa ni Mtukufu Mtume Muhammad ibn Abdillah (s.a.w.w.). Miongoni mwa mafunzo na masomo ambayo yametufikia sisi kwa kupitia kwake yeye, sehemu yake moja ni kile kilichoteremshwa katika muundo wa ile Qur’ani Adhim ambayo inajulikana kama ‘al-Kitab’ – Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na sehemu nyingine imetegemea kwenye vitendo na simulizi zake, na hii inajulikana kama ‘al-Sunnah.’ Kutoka miongoni mwa Sunnah hiyo ni vile vitendo ambavyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amevipa umuhimu na akavifanya wakati wote. Kitabu hiki – ambacho tunakiwakilisha kwa wale ambao wana shauku katika utafiti na uchunguzi wa kisomi – kina simulizi kuhusu vile vitendo ambavyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alivitilia mkazo sana juu yake, vile ambavyo wakati wote alikuwa akivitenda na vile ambavyo vinaelezea maisha yake, tabia na mwenendo wake. Katika utangulizi huu tutawasilisha baadhi ya mambo ya kawaida kwa lengo la kufafanua ile maudhui ambayo inajadiliwa katika kitabu hiki, na haya yamefanyiwa mukhtasari kama ifuatavyo: vi


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page vii

SUNAN-NABII Neno ‘Adab’ linalotumika kwenye Kiarabu fasaha na kile cha mazungumzo lina maana nyingi mbalimbali kama: Usanifu, uzuri na uangalifu sana katika mambo Kuungana kwa pamoja kwa jamii katika jambo Utii na heshima kwa watu wengine Elimu na ujuzi, mwenendo unaostahili na tabia njema Nguvu ya uhakika ambayo inamuwezesha mtu kujiepusha na vitendo viovu. Adabu vilevile inarejea kwenye elimu tangulizi kama vile uchunguzi wa lugha, sarufi (nahau), matumizi mazuri ya tashbihi na lahaja, ufasaha katika kuongea na ushairi. Inarejea pia kwenye utukufu wa tabia, usafi wa moyo na ukamilifu wa nafsi. Na kuhusu ‘Adiib’ inarejea kwa mwalimu, mwandishi na mzungumzaji. Hali kadhalika, inatumika kwa mtu ambaye ana ustadi sana juu ya ushairi na lugha, matumizi ya istiari, hotuba zenye mvuto na uwasilishaji wenye fasaha. Hili neno ‘Sunnah’ pia nalo lina maana nyingi miongoni mwa hizo ambazo ni: ukuaji, balehe, ubayana wa mazungumzo, mwendo wa shoti wa farasi wenye madaha, kupiga mswaki meno, kulia na kububujika (machozi). Sunnahtullah: Inaashiria kwenye amri za Mwenyezi Mungu, utashi Wake na maagizo ya kabla na vilevile adhabu na malipo Yake ya thawabu. Sunnah inatumika vilevile kwa kumaanisha: Mwenendo, tabia, asili, sheria tukufu, kuchagua njia maalum na kufuata matamanio na maoni. Hizi ndio maana tofauti za maneno ‘adabu’ na ‘Sunnah.’ Hata hivyo, ile ambayo inakubaliana na mjadala wetu hapa ni: Vile vitendo vyote ambavyo vinakubaliwa na akili na dini, kama vikitendwa kwa namna bora na nzuri zaidi, vitaweza kuitwa ‘adabu.’ Yule mtu ambaye ana adabu hufanya vitendo vyake na mishughuliko yake katika namna nzuri zaidi na sanifu. Na juu ya sifa ambazo zinahusiana na usafi wa moyo na ukamilifu wa nafsi na sehemu ya ndani kabisa ya mwanadamu – kama ukarimu, ujasiri haki na usamehevu, huruma na sifa zote nyingine za kiutu – hizi zinakuja chini ya jina la ‘akhlaq’ (hulka). Kuliweka hili kwa namna nyingine, adabu inaunda zile sifa za vitendo vya mtu kama vinavyotendwa katika dunia ‘halisi’ ambapo ‘akhlaq’ inajumuisha sifa za ile nafsi ya kina cha ndani kabisa. Maana hizi mbili kwa njia hii zimeunganishwa na kila mojawapo. vii


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page viii

SUNAN-NABII Kwa msingi huu, itakuwa ni makosa kutumia neno ‘Adab’1 kwa vitendo ambavyo havifai katika macho ya akili na dini kama vile: dhulma, ulaghai, uongo, kijicho na mfano wa hayo, na hili pia linahusika kwenye vitendo ambavyo viko nje ya udhibiti wa wanadamu. Kadhalika Sunnah inajumuisha zile sifa za vitendo vya kibinadamu kwa kuzingatia akilini kwamba maana ya Sunnah ni ya jumla zaidi kiliko ile ya adabu kwa vile Sunnah inahusiana na njia ya mema na maovu ambapo adab inatumika kumaanisha tu matendo mema ambayo yanastahili sifa katika maana ile maalum na ya jumla. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Adabu nzuri kabisa ni pambo la akili.”2 Imam Ali (a.s.) anasema: “Adabu ziko kama nguo mpya.”3 Imam Hasan al-Mujjtaba (a.s.) amesema: “Mtu ambaye hana akili, basi hana adabu pia.”4 Kwa hakika Hadith kuhusu Adabu ni nyingi mno. Mwanadamu – kwa msingi wa elimu yake, imani, mawazo na hisia zake – kwa kweli amefungwa na mnyororo wa adabu na Sunnah,5 ambao kwazo maisha huanzia na kuishia. Adabu na Sunnah hizo zinaonyesha kwa mfano yale mambo ya kiroho ya jamii na kudhihirisha mawazo ya watu na imani zao. Kuzidi na kushuka kwao, mafanikio na kushindwa, kuendelea na kurudi nyuma kwao, yote hayo yanategemea juu ya adabu zao na Sunnah. Kadhalika, njia pekee ya kumjua mtu binafsi ni kwa adabu na Sunnah ambazo ni makhsusi kwake na zinaonyesha mawazo na maoni yake. Adabu na Sunnah ambazo zimepatikana katika jamii mbalimbali hadi leo zinaweza kufanyiwa mukhtasari katika aina nne: 1. Adabu na Sunnah zilizo katika msingi wa ushirikina 2. Adabu na Sunnah ambazo zinakubaliwa kwa jumla na watu wengi 3. Adabu na Sunnah za wanachuoni na wale wenye hekima 4. Adabu na Sunnah za Manabii, Mitume na Maimam Ma’sum Sio rahisi juu yetu kutambua ule wakati hasa au kuonyesha mahali ambapo zile adabu na Sunnah zilizoko kwenye msingi wa ushirikina au zile zilizokuja kukuba1 Wingi wa neno Adabu (Mfasiri) 2 al-Bihar; 77:131 3 Nahjul-Balaghah; 469, Hotuba ya 5 4 Kashf al-Ghummah; 1: 571 5 Wingi wa Sunnah (Mfasiri) viii


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page ix

SUNAN-NABII lika kijumla na watu zilipoanzia. Tunaweza kusema kwa uhakika, hata hivyo, kwamba ilitokea miongoni mwa wale wenye kuamini juu ya Mungu mmoja kuwepo na mtindo mmoja wa adabu na Sunnah, kuanzia wakati wa Adam (a.s.) mpaka leo, ambao uko tofauti kabisa na mitindo mingine ya Sunnah. Aina hii ya Sunnah na adabu iko nje ya uwezo wa akili na ufahamu wa wanadamu, na mwanadamu hawezi kuifikia hiyo kwa akili au hisia zake. Iko nje ya upeo wa namna ya uelewa wake. Ni kikundi maalum tu cha watu wanaoitwa “Manabii” ambao wana uwezo wa kuipata hiyo kwa njia ya msukumo wa mbinguni na wahyi na halafu wao wanaipitisha na kuifikisha kwa watu wote. Aina hii ya Sunnah na adabu imeegemea kwenye mfumo wa ki-mungu ambao unahakikisha mafanikio ya wanadamu katika maisha haya na yale ya kesho akhera, kimaada na kiroho. Mwenyezi Mungu amependelea juu Yake Mwenyewe kuwaongoza Manabii katika Qur’ani Tukufu na ameidhinisha adabu na Sunnah zao na akauthibitisha uhusiano wao na watu. Katika Surat-al-An’am, baada ya kumsifu Nabii Ibrahim (a.s.), manabii wengine wote kutoka kwenye kizazi chake, na vilevile kutoka kwenye kizazi cha Nuhu (a.s.) wanatajwa. Yeye Mwenyezi Mungu anasema:

ix


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page x

SUNAN-NABII “Na tukampa (Ibrahim mtoto aitwaye) Is’haka na Yaakub, wote tukawaongoza, na Nuhu tulimuongoza zamani na katika kizazi chake, Daudi na Suleiman na Ayubu na Yusuf na Musa na Harun. Na hivyo ndivyo tuwalipavyo wafanya wema. Na Zakaria na Yahya na Isa na Ilyasa, wote walikuwa miongoni mwa watu wema. Na Ismail na Al-Yasaa na Yunus na Luti. Na wote tuliwafadhilisha juu ya walimwengu. Na kutoka miongoni mwa baba zao (baadhi ya) vizazi vyao na (baadhi ya) ndugu zao, na tukawachagua na kuwaongoza katika njia iliyonyooka. Huo ni mwongozo wa Mwenyezi Mungu amabao kwa huo humuongoza amtakaye katika waja Wake, na kama wao wangemshirikisha, bila shaka yangeliwaharibikia yale ambayo walikuwa wakiyatenda. Hao ndio tuliowapa Kitabu na hukumu na Utume, kama hawa wakiyakataa hayo, basi tumekwishayawekea watu ambao hawatayakataa. Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu amewaongoza, basi fuata muongozo wao. Sema: Sikuombeni malipo juu ya haya, hayakuwa haya ila ni mawaidha kwa watu. (al-An’am; 6: 84-90) Na Yeye anasema tena katika Surat al-Mumtahanah:

“Hakika ninyi mna mfano mzuri kwa Ibrahim na wale waliokuwa pamoja naye ……” 60: 4 na imesimuliwa katika Majma’al-Bayan kwamba maneno haya: ‘….. na wale waliokuwa pamoja naye’ yanaashiria kwa mitume wengine. Katika Surat al-Imran, Mwenyezi Mungu anasema:

“Hakika watu wanaomkurubia zaidi Ibrahim ni wale waliomfuata nabii huyu, na wale walioamini. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi wa waumini. 3:68.” Miongoni mwa Aya nyingine kama hizo. Imesimuliwa na al-Tabrasi katika Makarim al-Akhlaq na pia na Sharif al-Radhi katika Nahajul-Balaghah kwamba Imam Ali (a.s.) amesema katika moja ya hotuba zake: “Na kwa hakika Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa ni mfano wa kutosha juu yenu na ushahidi dhidi ya maovu ya dunia, kasoro zake, na wingi wa fedheha zake x


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page xi

SUNAN-NABII na maovu, kwa sababu sehemu zake zilikuwa zimezuiwa kwa upande wake, ambapo mapana yake yalikuwa yamesambazwa kwa ajili ya wengine; alinyimwa maziwa yake na akayapa mgongo mapambo yake. Kama ukitaka, kama mfano wa pili, nitakusimulia kuhusu Musa (a.s.), yule mshiriki katika mazungumzo na Mwenyezi Mungu, pale aliposema: “Ewe Mola! Hakika mimi ni mhitaji wa kila kheri utakayoniteremshia.”6 Wallah, yeye alimuomba Yeye mkate tu wa kula kwa sababu alikuwa amezoea kula majani ya mimea na ardhi, na kile kijani kibichi cha majani hayo kiliweza kuonekana katika ngozi yake dhaifu ya tumbo lake kutokana na wembamba na uhaba wa minofu yake. Kama ukitaka ninaweza nikatoa mfano wa tatu wa Daudi (a.s.). Yeye alikuwa ndiye mshika Zaburi na mwenye kughani miongoni mwa watu wa Peponi. Alikuwa akitengeneza vikapu makuti ya mitende kwa mikono yake mwenyewe na akiwaambia wafuasi wake: “Ni nani atakayenisaidia kwa kukinunua kikapu hiki?” Alikuwa akila mkate wa shayiri alionunua kutokana na mapato yake hayo. Kama ukitaka nitakueleza kuhusu Isa mwana wa Mariam (a.s.). Yeye alikuwa akitumia jiwe kama mto wake, akivaa nguo zilizochakaa na alikuwa akila chakula kikavu. Kikolezo chake kilikuwa ni njaa. Taa yake wakati wa usiku ilikuwa ni mwezi. Kinga yake wakati wa kipupwe ilikuwa ni upana wa ardhi kuelekea Mashariki na Magharibi. Matunda yake na maua yalikuwa ni yale tu yaliyoota kutoka ardhini kwa ajili ya ng’ombe. Hakuwa na mke wa kumtamanisha yeye, wala mtoto yoyote wa kiume wa kumhuzunikia, wala utajiri wa kumgeuza nadhari yake, wala mwenye tamaa ya kuweza kumfedhehesha. Miguu yake miwili ilikuwa ndio chombo chake cha usafiri na mikono yake miwili ilikuwa ndio watumishi wake.”7 Al-Daylami amemnukuu Imam Ali (a.s.) katika kitabu chake, Irshad al-Qulub akielezea umuhimu wa kufuata mifano ya maisha ya mitume (a.s.). Yeye alisema: “Na kuhusu Nuhu (a.s.) mbali na kuwa ndiye mtume mkubwa kwa umri kati ya mitume wote, ambaye aliishi kwa kipindi kirefu sana (katika baadhi ya riwaya imetajwa kwamba aliishi kwa miaka elfu mbili na mia tano), alifariki dunia akiwa bado hajajijengea nyumba yeye mwenyewe. Wakati alipokuwa akiuona mchana alikuwa akisema: ‘Ninaweza nisiuone usiku’ na alipokuwa akiuona usiku alikuwa akisema: ‘Huenda nisiuone mchana. “Kadhalika, Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w.) aliiaga dunia hii bila ya kubandika tofali juu ya tofali jingine. Wakati mmoja alimuona mtu akiwa anajenga nyumba 6 Surat al-Qasas; 28: 24 7 Nahajul-Balaghah; uk. 226, Hotuba ya 160 na pia imesimuliwa na al-Zamakhshari katika Rabi’al-Abrar sehemu ya kukata tamaa na uridhikaji. xi


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page xii

kwa matofali ya kuchoma na plasta, hivyo yeye Mtume (s.a.w.w.) akasema: ‘Jambo lenyewe ni la haraka sana kuliko hili.”’ Na kuhusu Ibrahim (a.s.), yule baba wa Mitume, nguo zake zilitengenezwa kwa sufi iliyo duni na chakula chake kilitengenezwa kutokana na shayiri. Yahya ibn Zakariyya (a.s.) alikuwa akitumia kuvaa nguo zilizotengenezwa na nyuzi za mtende na kula majani kutoka kwenye miti. Licha ya ufalme wake mkubwa, Suleiman (a.s.) alikuwa akivaa ngozi yenye manyoya chakavu na usiku ulipoingia, aliweza kuweka mikono yake shingoni na kulia, akibakia katika hali hii mpaka alfajiri. Chakula chake kilikuwa ni pamoja na majani ya mtende ambayo aliweza kuyaponda kwa mikono yake na alimuomba Mwenyezi Mungu tu juu ya ufalme huo kuweza kupata nguvu na kushinda zile falme za wasioamini na kuwatiisha. Inasemekana pia kwamba alimuomba Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kuweza kuridhika tu.” 8 Kuna hadith nyingi kama hizo. Kwa kuhitimisha, imetajwa katika hadith sahihi kwamba: “Sunnah iliyo bora kabisa ni ile Sunnah ya Mitume,9 na hususan Sunnah ya Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.) ambaye ndiye mwisho wa Mitume. Kwani mwenendo wake wa maisha ulikuwa ni mfano bora kwa wanadamu kuiga. Na vilevile imesimuliwa: “Bora ya Sunnah ni ile Sunnah ya Muhammad (s.a.w.w.)”10 Qur’ani Tukufu katika mifano mingi imesifia tabia, maadili, utaratibu wa kushughulika na watu na namna ya maisha ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Katika Surat-alImran imeelezwa:

“Basi kwa sababu ya rehema ya Mwenyezi Mungu umekuwa mpole kwao na kama ungekuwa mkali na mshupavu wa moyo wangekukimbia...”(al-Imran; 3: 159) Ameelezewa kuwa anayo tabia adhimu ndani ya Suratal-Qalam:

“Na bila shaka una tabia njema, tukufu ………....” (al-Qalam; 68: 4) Halafu katika Suratul-Ahzab, wanadamu wameagizwa kuchukua mwenendo wake wa maisha kama mfano wa kufuatwa. 8 Irshad al-Qulub; 1: 157 9 Man La Yahdhuruhu al-Faqih; 4: 402, namba 5868 10 al-Ikhtisas; 342


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page xiii

“Bila shaka mnao mfano mwema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu…..” (alAhzab; 33: 21) Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. anasema katika Surat-al-Imran:

“Sema: Ikiwa ninyi mnampenda Mwenyezi Mungu, basi nifuateni; Mwenyezi Mungu atawapenda na atawasamehe madhambi yenu, na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa msamaha, Mwenye kurehemu.” (3: 31) Vilevile anasema:

“Enyi mlioamini! Mwitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapokuiteni kwa yale yatakayokupeni uzima ……..” (Al-Anfal; 8:24) Sheikh Mufid amesimulia katika al-Amali yake kutoka kwake Imam al-Baqir (a.s.) kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema akiwa katika kitanda chake cha umauti: “Hakuna Mtume baada yangu, na hakuna Sunnah baada ya Sunnah yangu.”11 Imesimuliwa katika Jami’ al-Akhbar kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba alikuwa akisema: “Heshimuni kizazi changu na twaeni adabu zangu.”12 Katika hadith mashuhuri, imetajwa kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa kila mara akisema: “Mola wangu amenidhibitishia nidhamu bora kabisa.”13 Ibn Sha’bah al-Harrani amesimulia katika Tuhf al-‘Uqul kwamba Imam Ali (a.s.) amesema: “Fuateni mwongozo wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwani ndio mwongozo bora na twaeni Sunnah yake kwani ndio Sunnah tukufu zaidi.”14 Imetajwa katika hotuba iliyoelezwa mapema kutoka kwa Imam Ali (a.s.) kwamba yeye alisema: “Mnapaswa kumfuata Mtukufu Mtume, aliye mtakatifu na msafi, Mwenyezi Mungu ampe rehma yeye na kizazi chake. Kwake yeye kuna mfano kwa mfuasi na faraja kwa yule anayeitafuta faraja. Mwenye kupendwa sana mbele ya 11 Al-Amali ya Sheikh Mufid, uk.53 12 Jami’ al-Akhbar, uk. 140 13 al-Bihar, 16: 210 14 Tuhf al-‘Uqul, uk. 150


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page xiv

Mwenyezi Mungu ni yule anayemfuata Mtume wake na anayefuata nyayo zake. Yeye alichukua fungu dogo sana kutoka kwenye dunia hii na hakuitazama kikamilifu. Kati ya watu wote wa dunia, yeye alikuwa ndiye aliyekinai sana na kuwa na tumbo tupu sana. Yeye aliipewa dunia lakini alikataa kuipokea. Yeye alipojua kwamba Mwenyezi Mungu Mwenye kuenziwa, alilichukia jambo, yeye pia alilichukia; kwamba Mwenyezi Mungu anapolidharau jambo, na yeye pia hulidharau; kwamba Mwenyezi Mungu alipolishusha jambo, yeye pia alilishusha. Kama tunapenda kile anachokichukia Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na tukakishusha hilo litakuwa ni utenganisho wa kutosha na Mwenyezi Mungu na kuvunja amri Zake. Mtume alikuwa akila chakula juu ya ardhi, na alikaa kama mtumwa. Alirekebisha viatu vyake kwa mikono yake mwenyewe na akitia viraka kwenye nguo zake kwa mikono yake mwenyewe. Aliweza kupanda juu ya punda asiye na matandiko na akamuweka mtu mwingine nyuma yake. Kama kulikuwa na pazia lenye mapicha juu yake kwenye mlango wake angeweza kumwambia mmoja wa wake zake: “Oh, ewe fulani binti fulani! Liondoe pazia hilo kwenye macho yangu kwa sababu ninapolitazama, ninaikumbuka dunia na mapambo yake.” Hivyo aliuweka mbali moyo wake na dunia hii na kuondosha kumbukumbu zake kutoka akilini mwake. Alitamani kwamba mapambo yake yangebakia yamefichika katika macho yake ili asiweze kuchukua utajiri kutokana nayo, wala asipaone ni mahali pa kukaa na kutarajia kuishi ndani yake. Hivyo, aliitoa kabisa akilini mwake, akaiweka mbali na moyo wake na akaiweka imefichika kutoka machoni mwake. Kama vile tu ambavyo mwenye kukichukia kitu atakavyochukia kukitazama au kusikia kuhusu kitu hicho. Kwa hakika kwa Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kulikuwa na kila kitu ambacho kingeweza kukuarifu wewe juu ya maovu ya dunia hii na mapungufu yake, wakati alipokuwa na njaa duniani humu pamoja na masahaba wake maalum, na licha ya ukaribu wake kwavyo, vishawishi vya dunia hii vilibakia kuwa mbali naye. Hivyo basi acha mwenye kuhoji aweze kuhoji kwa akili yake; hivi Mwenyezi Mungu alimpa heshima hii Muhammad (s.a.w.w.) kwa matokeo ya hili au kumdhalilisha yeye? Kama atasema kwamba Mwenyezi Mungu alimdhalilisha, kwa hakika atakuwa anadanganya – Wallahi – na kueneza uwongo mkubwa. Iwapo atasema Mwenyezi Mungu amemtukuza yeye, basi anapaswa kujua kwamba Mungu amemdhalilisha yule mwingine wakati Yeye alipovitandaza vishawishi vya dunia hii kwa ajili yake, na kuviweka mbali na yule mja ambaye alikuwa wa karibu sana Kwake kati ya wanadamu wote. Kwa hiyo, mtu ni lazima amfuate Mtume wa Mwenyezi Mungu, apite kwenye nyayo zake na aingie kupitia mlango wake, vinginevyo hatakuwa salama kutokana na kuangamia. Kwa hakika Mwenyezi Mungu alimfanya Muhammad (s.a.w.w.) kuwa alama kwa ajili ya Muda Teule, muwasilishaji wa habari njema za Peponi na


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page xv

muonyaji wa adhabu. Aliiondoka dunia hii akiwa mwenye njaa lakini akaingia kwenye hiyo dunia nyingine kikamilifu. Hakuwahi kubandika jiwe moja juu ya jingine (ili kujenga nyumba) mpaka amefariki dunia na kuitikia mwito wa Mola Wake. Ni kubwa kiasi gani neema za Mwenyezi Mungu juu yetu ambazo ametuneemesha sisi kwa Mtume kama mtangulizi ambaye sisi tunamfuata na kiongozi ambaye tunamuigiza! “Wallahi, nilikuwa nikiweka viraka vingi sana kwenye shati langu hili kiasi kwamba ninaona aibu juu ya fundi wake. Mtu mmoja alinitaka mimi nilivue, lakini mimi nikasema: ‘Hebu niache – kwani ni wakati wa asubuhi tu ambapo watu huisifia ile safari ya usiku.”15 Imesimuliwa katika Makarimul-Akhlaq kutoka kwa as-Sadiq (a.s.): “Nitachukia kwa mtu kufariki dunia wakati akiwa bado hajatwaa yoyote kati ya tabia za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).16 Zipo hadith nyingi za namna kama hii. Ni muhimu sana kwa hiyo juu yetu sisi kutia mazingatio kwenye nukta moja muhimu, yaani Sunnah ambayo ndio maudhui ama somo la kitabu hiki, ni tofauti katika maana kulingana na kile kinachomaanishwa na wanahistoria, wale ambao wanajifunza sirah na hadith, na vilevile mafaqihi. Kwa mujibu wa wanahistoria na wale ambao wanaandika sirah, kwao Sunnah inachukuliwa kuzungumzia kwenye historia ya maisha ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kutoka kuzaliwa kwake hadi kwenye vita vyake, na historia ya kizazi chake, familia na masahaba na kadhalika. Kwa mujibu wa wale wanaosimulia hadith, Sunnah inarejea kwenye hadith, vitendo au kukubali kwa ukimya wa Ma’sum. Akina ‘Amma’17 wanamchukulia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) tu kuwa ndiye maasum, ambapo kwa kulingana na Shi’a, Maimam watoharifu (a.s.) wao pia wanaingia pamoja na Mtume (s.a.w.w.) katika hilo. Katika istilahi za mafaqihi, inahusiana na vitendo vilivyopendekezwa, ikilinganishwa na zile aina nyingine nne za vitendo; yaani: Wajib, Haramu, Makuruhu na Mubah (vinavyoruhusiwa). Katika hadith, Sunnah inajumuisha vitendo vyote na maagizo yaliyotajwa na kutendwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kama ile idadi ya rakaa katika swala za kila siku na visomo vyake tofauti, namna ya utekelezaji wa Hijja, ndoa na talaka, na kad15 Nahjul-Balaghah; uk. 227, Hotuba ya 160 16 Makarimul-Akhlaq; uk. 95, Hadithi ya 183. 17 Neno linalotumika kumaanisha Waislam wa Sunni (mfasiri)


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page xvi

halika. Sunnah inahusika kwenye maagizo na hukumu za kisheria katika simulizi na hadith. Na kuhusu istilahi ya Sunnah iliyotumika kwenye kitabu hiki – kama tulivyokwisha kuelezea hapo kabla – ina maana sahihi zaidi na yenye mipaka kutoka kwenye maana zote hizi ambayo ni: vitendo vyote vile vilivyopendekezwa ambavyo vilitendwa na kufundishwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika wakati wa uhai wake mwenyewe. Ni jambo linalofahamika kwa wanachuoni kwamba kulikuwa na sunna nyingi za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na hizi zimeandikwa kwenye mamia ya vitabu na maelfu ya hadith. Kila msimuliaji ametaja sehemu ya hizo kulingana na kile kinachohusiana na maudhui ya kitabu chake. Kadiri nijuavyo mimi ni nadra sana kuwepo kitabu chochote kutoka kwenye madhehebu zote mbili, Shi’a na Sunni – ambacho kina ukusanyaji kamili wa riwaya zote kuhusu Sunnah na adab za Mtukufu Mtume. Bali inaweza kusemekana kwamba hakuna hata mtu mmoja, hadi kufikia sasa, ambaye ameweza kutunga kitabu kama hicho, chenye maelezo haya. Ni dhahiri kabisa kwamba ukusanyaji wa simulizi ambazo zinahusiana na Sunnah na adab za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ungekuwa ni kazi muhimu sana ambayo ingesaidia kulinda thamani ya kiroho ya Uislamu, na aina hii ya kitabu inakuwa ni chanzo cha taarifa kuhusu mtindo wa maisha ya mwanadamu kutoka kwa mtu mbora na mkamilifu zaidi kati ya watu, ni cha umuhimu wa hali ya juu kabisa. Mtu pekee ambaye amefikiria juu ya jambo hili katika wakati wetu wa sasa alikuwa ni Allamah Taba’taba’i, mwandishi wa makala ya asili ya kitabu hiki. Yeye alizikusanya riwaya ambazo zinaelezea mienendo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kuzungumza juu ya adab na sunnah katika kitabu alichokiita ‘Sunan an-Nabi’ na hapo kufungua njia kwa ajili ya mtindo wa maisha wa kiadilifu kwa yule anayeutaka mtindo huo. Inafaa kusema kwamba kitabu hiki kimeziba pengo katika utamaduni wa Kiislamu wa kipindi chetu hiki cha sasa. Tunaweza kusema bila shaka kwamba kuna vitabu vichache sana kama hiki katika nyanja hii, bali ni kazi (kitabu) ya kisomi ambayo ni ya kwanza ya aina yake, kilichotungwa na mwandishi mwenye kuheshimika. Kitabu hiki cha kuvutia kiliandikwa na Allamah huyu takriban miaka arobaini iliyopita mnamo miaka ya hamsini (1350 H.A./1929 AD), yaani, wakati alipokuwa bado akijifunza sayansi (elimu) za kidini huko Najaf al-Ashraf na haikuwa mpaka baada ya mwezi wa Shaabani wa mwaka 1391 Hijiria, sawa na 1970 ambapo nilipata heshima ya kukutana naye huko Qum na nilimuuliza kama itakuwa sawa endapo ningeingia kwenye tafsiri ya kitabu hiki kwenye lugha ya ki-Fursi. Allamah alikubali pendekezo hili na akanipatia ruhusa – kwa maandishi – ya kuianza kazi hii. Katika wakati wa kuendelea na tafsiri yangu (ya kitabu kwa Ki-Fursi) na uthibitisho


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page xvii

wa vyanzo na rejea, nilikutana na baadhi ya hadith juu ya mada ya Sunnah ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambazo mheshimiwa mtunzi huyu alizikosa. Mimi nilizikusanya hadith hizi katika faili tofauti na nikaliwasilisha kwa mtukufu Allamah katika kukutana pamoja naye tena huko Mashad al-Ridha (a.s.) na baada ya kumaliza kuziangalia, aliomba kwamba hadith hizi ziingizwe katika kitabu hiki chini ya kichwa cha maneno cha “Nyongeza.” Kwa kulingana na maelekezo yake, niliweka ‘nyongeza’ katika kila mwisho wa sehemu ya kitabu, nikidumisha ule mpango wa asili isipokuwa hiyo nyongeza, kwenye “Tabia ya Mtume” ambayo niliiweka mwishoni mwa kitabu. Kadhalika niliongeza sehemu mbili mpya kwenye kazi ya asili, yaani sehemu juu ya Hijja na nyingine juu ya simulizi zisizofahamika kwa kawaida. Inafaa kueleza kwamba vyanzo vilivyorejelewa ndani ya kitabu hiki ni vya kutoka kwenye vitabu vya wanachuoni wa Ki-Shi’a na hakuna rejea zilizofanywa kwenye vitabu vya waandishi wa Sunni ukiacha kile ‘Ihya al-Ulum’ cha Ghazali na ‘adDurr al-Manthur’ cha Suyuti. Kitabu hiki kwa jumla kimegawanywa katika sehemu tatu juu ya misingi ya maisha ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): 1. Sunna na adab zake kwa Mola Wake, yaani, utaratibu wake wa ibada na du’a na maombi. 2. Sunna na adab zake kwa aina tofauti za watu, yaani adab yake katika maingiliano ya kijamii. 3. Sunna na adab zake nyingine zote, kama vile adabu zake anaposafiri, anapokula, anavyovaa na kadhalika, ambazo tutaziita adab binafsi na zake pekee. Tunamuomba Mwenyezi Mungu, Mola wa Ulimwengu wote atupe msukumo na dhamira ya kuweza kufuata katika nyayo, na kutwaa tabia bainishi za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Ewe Mwenyezi Mungu! jaalia neema Zako tukufu na fadhila Zako kubwa na nyingi juu ya Mtume Wako Muhammad (s.a.w.w.). Mjaalie nafasi ya juu kabisa iliyo karibu na Wewe, mjaze malipo maradufu kutoka kwenye rehma Zako, kamilisha juu yake ile nuru ya ukamilifu na utuweke pamoja naye huko Peponi. Ewe Mwenyezi Mungu! Tusaidie kutuwezesha kufuata sunna yake katika maisha yetu na tuwe wenye kunafaika na uombezi wake – Amin. Muhammad Hadi al-Fiqhi 20th Dhil-Qa’dah al-Haram, 1394 Hijri


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page xviii

WASIFU WA MWANDISHI Allamah Muhammad Husayn Taba’taba’i alizaliwa katika kijiji cha Shadabad karibu na Tabriz mnamo mwezi 29 Dhul-Hijjah 1321 A.H./16th Machi, 1904. Alimpoteza baba yake, Sayyid Muhammad Taba’taba’i akiwa na umri wa miaka mitano na mama yake alifariki miaka minne baadae wakati alipokuwa anamzaa ndugu yake, Sayyid Muhammad Hasan. Ile hali ya kuwa mayatima iliongeza ukaribu zaidi kati ya makaka hawa wawili na kuwaunganisha katika maisha yao yote. Malezi ya vijana wawili hawa yaliangukia kwenye mabega ya ami yao wa upande wa kiumeni kwao Sayyid Muhammad Ali Qadhi, na ilikuwa ni chini ya ulezi wake ambapo Allamah Taba’taba’i alianza elimu yake ya msingi. Kulingana na mfumo uliokuwepo kwa wakati huo, kwanza alianza kuhifadhi Qur’ani, akajifunza maandiko ya fasihi ya Kifarsi na akajifunza sanaa ya kuandika vizuri kabla ya kuendelea kwenye masomo ya kina zaidi ya elimu za lugha ya Kiarabu – sarufi, nahau na sintaksi (kupanga na kuhusisha vipasho na maneno kisarufi), masharti ya muhimu kabisa kwa ajili ya masomo ya daraja la juu ya mkusanyiko wa maandishi ya jadi ya Kiislamu. Allamah anasimulia uanzaji wake uliochelewa kiasi, wa kuingia kwenye ulimwengu wa uanachuoni na anaeleza kwamba yeye kimsingi alikuwa akiona karaha kusoma na kukatishwa tamaa na kutokuweza kwake kuelewa kikamilifu kile alichokuwa akikisoma, hali ambayo iliendelea kwa takriban miaka minne hivi. Kipindi muhimu hatimaye kilifikiwa pale wakati aliposhindwa mtihani katika tasnifu (maandiko) mashuhuri ya Suyuti juu ya sarufi na mwalimu wake aliyeghadhibika akamwambia: “Acha kupoteza muda wangu na wako!” Akiwa amefedheheka sana, aliondoka Tabriz kwa muda kiasi kwenda kujishughulisha na utekelezaji maalum wa kiibada ambao uliishia katika kupata kwake fadhila tukufu – uwezo wa kumudu somo lolote alilojifunza, na uwezo huu alibakia nao mpaka mwisho wa maisha yake. Sambamba na unyamavu wake wa kawaida juu ya masuala yake ya binafsi, hakudhihirisha kamwe ule utekelezaji huu wa kiibada husika. Baadae alikumbuka: “Nilikoma kabisa kushirikiana na mtu yoyote ambaye hakujitolea katika kusoma na nikaanza kujiridhisha mwenyewe kwa chakula kichache, usingizi na mahitaji ya kimaada machache, na kujitolea kila kitu changu kwenye masomo yangu. Ilitokea mara kwa mara wakati wa kipupwe na kiangazi kwamba ninabakia kuwa macho hadi alfajiri na wakati wote nikijiandaa kwa darasa la siku inayofu


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page xix

ata katika usiku uliopita. Kama nilikutana na tatizo, niliweza kutatua ugumu wowote niliokabiliana nao, kwa kiasi chochote cha jitihada kilichohitajika kuchukuliwa. Nilipokuja darasani, kila kitu mwalimu alichokuwa akiseme kilikuwa tayari kinaeleweka wazi kwangu; sikuwa na haja kamwe ya kutaka maelezo zaidi au kwa kosa lolote kusahihishwa. Baada ya kumaliza kiwango cha Sutuh cha mtaala wa Hauza mnamo mwaka 1925, Allamah Taba’taba’i pamoja na kaka waliondoka kwenda Najaf, kituo cha kielimu cha Shi’a ambacho kidesturi kiliteuliwa kama Darul’Ilm (Nyumba ya Elimu). Ilikuwa ni hapa ambapo alitumia miaka mingi akijifunza kiwango cha Kharij cha fiqh (Sheria za kiislam) pamoja na mabingwa kama Mirza Husein Na’ini (aliyefariki mwaka 1355A.H./1936A.D.). Ayatullah Abul Hasan Isfahani (aliyefariki mwaka 1365A.H./1946A.D.). Ayatullah Haji Mirza Ali Irvani na Ayatullah Mirza Ali Asgher. Alipata cheo cha Ijtihadi wakati akiwa Najaf, lakini kamwe hakutafuta kuwa Marja al-Taqlid. Ilikuwa ni fasili ya Qur’ani ikiambatana na falsafa ambayo ilikuja kumshughulisha kwa kiasi kikubwa cha masomo yake. Aliyekuwa na mvuto sana juu ya Allamah Taba’taba’i kuliko yoyote kati ya walimu wake wengine hapo Najaf alikuwa ni binamu yake, Haji Mirza Ali Qadhi Taba’taba’i (aliyefariki mwaka 1363A.H./1947A.D.). Alikuwa ni yeye ambaye, zaidi kuliko yoyote yule, aliyemsaidia kujenga haiba yake ya kiroho. Mvuto wake Sayyid Qadhi juu yake ulikuwa wa kina mno. Chini ya mwongozo wake yeye alianza kujishughulisha na kujizoesha matendo ya Irfan (maarifa ya kiroho), ukeshaji wa usiku na matendo ya hali ya juu ya ibada. Mnamo mwaka 1354A.H/1935A.D., Allamah Taba’taba’i alirudi tena Tibriz kutoka Najaf, akifuatana na kaka yake. Kurudi huku kuja Tibriz kulisababisha jambo la kutulia katika shughuli zake za kisomi kwa kiasi cha muongo mmoja (kipindi cha miaka kumi) ambacho ndani yake alijitolea kufanya shughuli za kulima mashamba ya familia. Licha ya kiwango cha elimu alichokuwa amekipata, alikuwa takriban ni kama mtu asiyejulikana kabisa hapo mjini. Mnamo mwaka 1946, yeye aliondoka kwenda Qum ambako alibakia kwa maisha yake yote yaliyobaki. Mji wa Qum ulikuwa umepata umaarufu kama kituo cha elimu tangu zile siku za awali kabisa za Ushi’a huko Iran, na ilikuwa ni hapa ambapo mandhari ya sehemu ya mafanikio makubwa ya kazi ya Allamah kama mwalimu na mtunzi inaweza kuonekana.


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page xx

Kwa yote yaliyotokea kwa nje, kifani hasa cha mwanachuoni aliyejinyima, aliyejitenga, Allamah Taba’taba’i kwa hali yoyote ile hakuwa akipuuza au kutotambua hali ya nyanja ya kisiasa. Hata hivyo alifanya wajibu mdogo kama ukitambulika katika juhudi kali na za muda mrefu zilizoongozwa na Imam Khomein na washirika wake ambazo zilifikia kilele katika mapinduzi ya Kiislam mnamo mwaka 1978 – 79 na kuanzishwa kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Irani. Wakati ule mapinduzi yalipoanza, yeye alikuwa dhaifu kiafya kuweza kushiriki japo kidogo. Hata hivyo ule wajibu mkubwa uliofanywa na wanafunzi wake wengi katika mapinduzi hayo unaonyesha kwamba mwelekeo na mafundisho aliyofundisha kwao yalikuwa kwa kiasi fulani yakikubaliana na uungaji mkono wa mpango mpya wa Kiislam. Akiwa amedhoofishwa kwa muda mrefu na matatizo ya moyo na jakamoyo – nyurolojia (matatizo ya mfumo wa neva), Allamah Taba’taba’i alijiondoa kabisa kwenye shughuli za ufundishaji na akawa amejishughulisha sana na ibada za faragha kiasi mwisho wa uhai wake ulivyokaribia. Mnamo mwaka wa 1405A.H./1981 A.D., alisimama kama kawaida yake hapo Damavand akiwa anarejea kwenda Qum kutoka kwenye ziara yake ya kiangazi huko Mashhad. Hapo aliugua sana na akapelekwa hospitalini huko Tehran. Matumaini ya kupata nafuu tena yalikuwa ni madogo sana na kwa hiyo alipelekwa nyumbani kwake Qum, ambako alitengwa vikali sana kwa wote isipokuwa kwa wanafunzi wake wa karibu sana. Baadaye kidogo, mnamo mwezi 18 Muharram, 1402A.H./Novemba, 1981 alifariki dunia na akalazwa mapumzikoni karibu na makaburi ya Sheikh Abd al-Karim Ha’iri na Ayatullah Khwansari; sala ya mazishi iliongozwa na Ayatullah al-Udhma Hajj Sayyid Muhammad Ridha Gulpaygani. Moja ya tabia za mtu huyu mashuhuri kama ilivyoonyeshwa kwa kauli moja na wanafunzi wake ilikuwa ni staha yake ya wastani na unyenyekevu. Allamah hajawahi kusikika akitamka neno “mimi” katika maisha yake yote imma kwa Kiarabu au Kifursi. Tofauti na wengi kama sio karibu nyota wote wa Qum, yeye hakuruhusu kamwe mkono wake kupigwa busu, akiurudisha kwenye mkono wa nguo yake kama mtu alijaribu kufanya hivyo. Wakati wote alikataa kumuongoza mtu yoyote kwenye swala ya jamaa hata wanafunzi wake mwenyewe. Wakati akifundisha, kamwe hakujiruhusu yeye mwenyewe kuchukua nafasi ya mamlaka yanayoonyeshwa na usomi juu ya kochi au kuegemea ukutani, badala yake akipendelea kukaa wima chini ardhini, kama vile tu walivyo wanafunzi wake. Alikuwa na subira na uvumilivu juu ya maswali na vipingamizi vilivyotolewa na wanafunzi wake, akitoa muda wake kwa ukarimu kabisa hata kwa wale ambao walikuwa bado wachanga miongoni mwao.


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page xxi

Mazingira ya kidunia ya Allamah hapo Qum yaliendana na ukosefu wa kutojipa kwake umuhimu kabisa yeye mwenyewe binafsi. Hakuwa na njia ya kwenye mafungu ya fedha yaliyotengwa kwa ajili ya wanafunzi na walimu wa fiqh, na wakati mwingine alikosa hata pesa za kuwashia taa yake katika nyumba yake ya wastani huko katika wilaya ya Yakhchal-i Qadhi ya Qum. Nyumba yake ilikuwa ndogo sana kiasi cha kutoweza kuyapatia nafasi ya kukaa yale makundi ya wanafunzi waliokuwa wanakuja kumtembelea, na kwa hiyo alikuwa akikaa kwenye ngazi zilizokuwa mbele ya nyumba ili kuwapokea. Tofauti na wanachuoni wengi, yeye hakukusanya maktaba kubwa binafsi, ingawaje alikuwa ameacha nyuma yake mkusanyiko mdogo wa miswada. Cha kutambulika, haikuwa ni wanafunzi wake peke yao tu walionufaika kutokana na kujistahi na tabia ya kutojitanguliza kwake. Huo ndio ulikuwa upendo wake kwa familia yake kwamba alikuwa kila mara akisimama wakati mke wake na watoto walipoingia hapo chumbani, na ilipokuwa lazima kuondoka hapo nyumbani na kwenda kununua mahitaji muhimu, Allamah alijitolea kulibeba jukumu hilo mwenyewe badala ya kulitupa kwa familia yake. Huo ndio uliokuwa mwenendo wa nje au adabu ya mtu, ambaye kwa maoni ya wafuasi wake, yeye alikuwa amegeuka kuwa kioo cha vivuli vya Ma’sumin, ambaye alikuwa amefikia kiwango cha mtengo kutoka kwenye dunia hii ambacho kilimruhusu kuangalia moja kwa moja kile kilichokuwa ni sehemu ya ufalme usioonekana. Baadhi ya vitabu ambavyo Allamah Taba’taba’i alijaaliwa kuweza kuviandika katika maisha yake mafupi ni pamoja na vitabu vifuatavyo: 1. Al-Mizan fi Tafsir al-Qur’an Munzal: Kazi moja muhimu sana ya Allamah, Sharhe ya mfano bora juu ya Qur’an iliyoandikwa katika juzuu ishirini kwa lugha ya Kiarabu. Tafsiri yake kwa lugha ya Kiingereza, ilikuwa ikifanywa na ambaye sasa ni marhum Sayyid Sa’id Akhtar Rizvi,18 imekwishafikia juzuu sita za mwanzo (zilizochapishwa katika mijaladi 12). 2. Usul-i-falsafah wa Rawish-i-ri’alism – Kanuni za Falsafa na Utaratibu wa Uhalisia: Hiki kiliandikwa katika juzuu tano na kimechapishwa pamoja na Sherhe ya Marhum Ayatullah Murtadha Mutahhari. 3. Hashiyahi Kifayah – Ufafanuzi wa Kifayah. Sherehe juu ya toleo jipya la AlAsfar cha Sadr al-Din Shirazi (Mullah Sadra), kilichokusanywa chini ya maeleke18 Ningependa ijulikane wazi kuwa huyu Akhtar Rizvi ndiye asasi na chimbuko la Mashia wa Kiafrika Tanzania, na huenda Afrika Mashariki.- Mhariri-


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page xxii

zo ya Allamah Taba’taba’i ambacho tayari juzuu saba zimekwisha kuchapishwa. 4. Musahabat ba Ustad Kurban – Mazungumzo pamoja na Profesa Corbin. Juzuu mbili zenye msingi juu ya mazungumzo yaliyofanyika kati ya Allamah Taba’taba’i na Henry Corbin. 5. Risalah dar Hukumat-I Islami – Tasnifu juu ya Serikali ya Kiislam. 6. Risalah dar Ithbat-i dha’t – Maandiko juu ya Ushahidi wa Dhati Tukufu. 7. Risalah dar Sifat – Maandiko juu ya Sifa Takatifu. 8. Risalah dar Insan Qabl Dunya – Tasnif juu ya Mwanadamu kabla ya (kuumbwa kwa) Dunia. 9. Risalah dar Insan fil Dunya – Maandiko juu ya Mwanadamu katika Dunia. 10. Risalah dar Insan ba’d Dunya – Maelezo juu ya Mwanadamu baada ya Dunia. 11. Risalah dar Nubuwwat – Makala juu ya Unabii. 12. Qur’an dar Islam – Qur’ani katika Uislamu: Tafsiri ya Kiingereza imekwishachapishwa. 13. Shi’ah dar Islam – Uislamu wa ki-Shi’ah: Tafsiri ya Kiingereza tayari imekwishachapishwa.


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 1

SUNAN-NABII

1


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 2

SUNAN-NABII

MLANGO WA 1 SIFA NA TABIA BAINIFU ZA KIMAADILI ZA MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.). 1. Kutoka kwa Ibn Shahr ndani ya al-Manaqib; Tirmidhi katika al-Shama’il; Tabari katika Ta’rikh; Zamakhshari ndani ya al-Fa’iq na al-Fattal katika al-Raudhah wote wamesimulia kuhusu sifa za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa riwaya mbalimbali. Kutoka miongoni mwa hizi ni: Imesimuliwa kutoka kwa Amirul-Mu’mini (a.s.), Ibn Abbas, Abu Huraira, Jabir ibn Samarah na Hindi ibn Abi Halah kwamba: Yeye Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akitukuzwa na kuheshimiwa, kuenziwa machoni mwa watu na kuheshimiwa kwenye nyozo za watu. Uso wake ungeweza kung’ara kama mwezi kamili, mwangavu na mweupe pamoja na dalili za wekundu. Yeye hakuwa mwembamba sana, wala mnene sana. Alikuwa na paji la uso jeupe na sura ya kupendeza. Ule weupe wa macho yake ulikuwa mweupe sana na weusi wa macho yake ulikuwa mweusi zaidi, kingo za vigubiko vya macho yake zilikuwa nyeusi, alikuwa na nyusi ndefu nyembamba, kichwa kikubwa cha wastani chenye uwiano na alikuwa na urefu wa wastani unaofaa. Alikuwa na komo la uso pana, mgongo wa pua yake ulikuwa umenyanyuka kiasi, wekundu kidogo ulikuwa unaweza kuonekana katika weupe wa macho yake, nyusi zake zilikuwa zimeungana, alikuwa na mashavu laini mazuri, vigasha vya mikono (forearms) virefu na vipana, viungo vya mabega vikubwa, mabega mapana, mikono yenye nguvu na miguu mikubwa ya wastani. Alikuwa hana nywele kifuani, nyayo za miguu yake zilikuwa zimejikunja katikati, mistari ilikuwa inaonekana kuzunguka kwenye misuli yake ya uti wa mgongo, alikuwa na kope ndefu, ndevu nyingi, masharubu yaliyojaa kikamilifu, mchanganyiko wa nywele nyeusi na nyeupe, kinywa na pua vilivyoumbwa vizuri, meno yaliyoachana maangavu na meupe, nywele nyembamba na ndefu, msitari wa nywele ndogo sana kutoka katikati ya kifua chake hadi kwenye kitovu na mwili unaowiana. Tumbo lake lilifungamana na kifua chake. Alikuwa na kifua kipana. Shingo yake ilikuwa nzuri kama picha ya fedha safi halisi. Alikuwa na vidole vilivyonyooka, visigino vya miguu yake vilikuwa vyembamba visivyo na nyama. Alikuwa na kidevu kifupi. Paji lake la uso liliinamia kidogo upande wa mbele, mapaja yake yalikuwa manene yenye misuli, na kulikuwa na uvimbe kidogo kwenye ubavu wake. Viungo vyake vilikuwa madhubuti. Alikuwa wa kimo cha wastani, hakuwa mrefu sana wala mfupi sana. Alikuwa na nywele zenye mawimbi sio za wazi zenye kuanguka. Uso wake haukuwa imma kondefu au 2


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 3

SUNAN-NABII nene na rangi yake haikuwa nyeupe kama ule weupe wa macho yake. Alikuwa na viungo vikubwa. Hapakuwa na nywele katika kifua au tumbo lake isipokuwa mstari wa nywele uliofikia kuanzia tumboni kwake hadi kwenye kitovu. Alikuwa na mgongo mkubwa kwa juu. Nywele nyeupe zilionekana pembeni mwa kichwa chake (s.a.w.w.) karibu na masikio yake (kama matokeo ya umri mkubwa – uzee). Mikono yake ilikuwa kama mikono ya muuza manukato – wakati wote ikiwa inanukia marashi. Alikuwa na viganja vipana. Mifupa ya mikono na miguu yake ilikuwa mirefu ya kuwiana. Alipokuwa mwenye furaha na kicheko, uso wake ulikuwa kama kioo kinachong’ara. Alitembea kwa kuinamia mbele,1 kwa mwendo wa unyenyekevu. Ataharakisha mbele ya watu katika kutenda matendo mema. Alipokuwa anatembea alinyanyua miguu yake kana kwamba anashuka kwenye mteremko. Alipotabasamu, meno yake yaling’ara yalipoonyeshwa kidogo tu, kabla ya kufunikwa na midomo. Alikuwa mtanashati anayevutia kwa sura, mwenye tabia njema, muungwana na mwenye urafiki. Wakati alipogeuka kuwaangalia watu, wao walihisi kana kwamba uso wake ulikuwa kama taa inayong’ara, na matone ya jasho usoni mwake yalikuwa kama lulu, na harufu ya pumzi zake ilikuwa nzuri zaidi kuliko misk iliyo bora kabisa. Alikuwa na muhuri wa utume katikati ya mabega yake.2 2. Abu Huraira anasema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa akigeuka kuona mbele au nyuma, aligeuka mwili mzima (sio kichwa chake peke yake)3 3. Jabir ibn Samarah anasema: Alikuwa mwembamba kwenye miundi.4 4. Abu Juhayfa anasema: Nywele nyeupe zilifunika ndevu zake kwa upande wa pepembeni na zile nywele kati ya kidevu chake na kingo za mdomo wake wa chini.5 5. Umm Hani: Nilimuona Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) misokoto minne ya nywele Ibn Shahr anasema: Kwa ukweli alikuwa na mafungu au misokoto miwili ya nywele na yule alianzisha (desturi hii ya kuweka nywele namna hii) alikuwa ni Hashim (babu yake Mtukufu Mtume).6 6. Anas: Sikuhesabu zaidi ya nywele nyeupe kumi na nne katika kichwa na ndevu 1 Hii inaashiria kuwa na nguvu (Mfasiri) 2 Manaqib Aale Abi Talib 1:155, Faid al-Qadir, 5: 76-79, Wa’sail al-Wusul Ila Shama’il alRasul: 37- 47 3 Manaqib Aale Abi Talib, 1:157 4 Manaqib Aale Abi Talib, 1:157; Fayd al-Qadir, 5:80 5 Manaqib Aale Abi Talib, 1:158 6 Ibid 3


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 4

SUNAN-NABII za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).7 7. Imesemekana kwamba: Alikuwa na nywele nyeupe kumi na saba.8 8. Ibn Umar: Dalili za uzee juu yake (s.a.w.w.) ni kule kuwepo kwa takriban nywele nyeupe ishirini.9 9. al-Bara’ ibn Azib: Nywele zake zilikuwa ndefu kufikia mabegani mwake.10 10. Anas: Yeye alikuwa na nywele zilizoshuka nyuma ya masikio yake mpaka kwenye ndewe za masikio.11 11. Aisha: Nywele zake zilirefuka kupita kwenye ndewe za masikio yake bali hazikufika kwenye mabega.12 12. Ndani ya Qisas al-Anbiya: Pasingekuwa na mahali ambapo kutoka hapo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angepita bali kwamba wale wote ambao wangepita hapo wangejua kwamba yeye (s.a.w.w.) alikuwa hapo kutokana na harufu ya jasho lake lenye manukato. Yeye hakupita kwenye jiwe au mti isipokuwa kwamba utasujudu mbele yake.13 13.Kutoka kwa al-Saffar ndani ya Basa’ir al-Darajat: Imesimuliwa kutoka kwa Zurarah kutoka kwa Abu Ja’far (a.s.) kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Kwa hakika sisi Mitume tunalala kwa macho yetu bali sio kwa mioyo yetu, na tunaona kile kilicho nyuma yetu kwa uwazi uleule kama vile tunavyoviona mbele yetu.14 14. Kutoka kwa al-Qutb ndani ya al-Khara’ij wa al-Jara’ih: Kutoka kati ya miujiza yake mingi Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambao umethibitishwa na vyanzo mbalimbali kwa idadi kubwa, na makafiri na waumini wameukubali, ni ule mhuri wa utume kwenye nywele ambao ulikuwa umejikusanya kati ya mabega yake.15 15. Ndani ya al-Manaqib: Kivuli chake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakikuanguka 7 Ibid 8 al-Faqih, 1:122; Manaqib Aale Abi Talib, 1:158 9 Manaqib Aali Abi Talib,1:158; Biharul-Anwar, 16:191 10 Manaqib Aale Abi Talib,1:158 11 Ibid. 12 al-Faqih, 1:129, Manaqib Aale Abi Talib, 1:158. 13 Biharul-Anwar, 16:172, ikinukuu kutoka kwenye Qisas al-Anbiya: 287, MakarimulAkhlaq: 24 14 Basa’ir al-Darajat: 420, Namba 8 15 al-Khara’ij wal-Jara’ih, 1:32; Namba 29, Biharul-Anwar 16:174, Kamal al-Din wa Tamam al-Ni’mah, 1:165 na ndani ya kitabu cha Abd al-Malik: 99. 4


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 5

SUNAN-NABII chini juu ya ardhi.16 16. Kutoka kwa al-Kulayni ndani ya al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Ali ibn Muhammad al-Nawfali, kutoka kwa Abi al-Hasan (a.s.), yeye amesema: Nilimtajia kuhusu sauti nzuri. Yeye akasema: Wakati Ali bin Husein (a.s.) alipokuwa akisoma (Qur’ani) na mtu akawa anapita karibu, angeweza kuzirai kwa sababu ya uzuri wa sauti yake, na kama Imam akidhihirisha kidogo ya sauti hii, watu wasingeweza kustahimili uzuri wake. Mimi nikasema: Kwani Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakuwaongoza watu kwenye swala, akinyanyua sauti yake katika kuisoma Qur’ani? Yeye (a.s.) akasema: Yeye alikuwa akisoma kwa sauti ambayo iliweza kustahimilika kwa watu waliokuwa nyuma yake.17 Kumbuka: Na hii imesimuliwa kwa nyororo nyingine nyingi za wasimuliaji. 17. Kutoka kwa as-Saduq katika Ma’ani al-Akhbar: Kupitia kwa Ibn Abi Halah alTamimi kutoka kwa al-Hasan ibn Ali (a.s.) na (katika riwaya nyingine) kwa njia ya ar-Ridha kutoka kwa baba zake, kutoka kwa Ali ibn al-Husein, kutoka kwa Husein ibn Ali (a.s.) na vilevile (katika riwaya nyingine tena) kupitia kwa mtu mmoja wa kizazi cha Abi Halah kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Hasan ibn Ali (a.s.) ambaye amesema: Nilimuomba mjomba wangu, Hind ibn Abi Halah – ambaye wakati wote alikuwa akizungumza kuhusu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) – anielezee jambo kuhusu yeye ili niweze kuongeza mahaba yangu juu yake. Hivyo akasema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliheshimiwa na kutukuzwa. Uso wake ulikuwa uking’ara kama mwezi kamili. Alikuwa mrefu kuliko wale waliokuwa wafupi, na alikuwa mfupi kuliko wale waliokuwa warefu (yaani alikuwa wa kimo cha wastani). Alikuwa na kichwa kikubwa cha wastani na nywele zenye mawimbi. Kama nywele zake zingechanwa angezichana vyovyote vile, kama aliziachia kukua, hakuweza kuziachia kurefuka kufikia urefu wa ndewe za masikio yake. Alikuwa na rangi nyepesi, paji la uso pana, nyusi ndefu nyembamba ambazo zilikuwa pana lakini hazikuungana, pamoja na vena iliyopita kati yao ambayo ilikuwa ikionekana wakati alipokuwa amekasirika. Kulikuwa na nuru ambayo ilimnyanyua kiasi kwamba kama mtu ambaye amemuona hakuitambua, angeweza kufikiri kwamba alikuwa ananyanyua kichwa chake kwa maringo. Ndevu zake zilikuwa fupi na nyingi, mashavu yake yalikuwa laini na mapana. Alikuwa na kinywa kipana chenye meno maangavu yaliyoachana. Alikuwa na nywele laini kifuani mwake. Shingo yake ilikuwa kama taswira nzuri ya fedha halisi. Mwili wake ulikuwa na uwiano mzuri (viungo vyake vyote vilikuwa vya kipi16 Manaqib Aale Abi Talib 1;124. Mengi zaidi kuhusu hili yanasimuliwa katika al-Khara’ij: 221. 17 Al-Kafi 2: 615, na al-Tabarsi amesimulia hilo hilo ndani ya al-Ihtijaj: 204 5


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 6

SUNAN-NABII mo kamilifu kuhusiana na mwili wake). Tumbo na kifua chake vilikuwa sawa kwa ukubwa. Alikuwa na mabega mapana. Viungo vyake vilikuwa vinene. Alikuwa na kifua kipana. Zile sehemu zake za mwili ambazo hazikufunikwa na nguo ziliwaka kwa ung’aavu. Alikuwa na mstari wa nywele ulianzia kifuani kwake hadi kwenye kitovu chake; mbali na hili, kifua na tumbo lake vilikuwa havina nywele. Vigasha vyake vya mikono, mabega na sehemu ya juu ya kifua vilikuwa na nywele. Alikuwa na vigasha vya mikono virefu na viganja vipana. Mikono na miguu yake ilikuwa minene na madhubuti. Alikuwa na vidole virefu na mifupa ambayo ilikuwa haina mibinuko yoyote katika vigasha na miundi. Sehemu ya katikati ya nyayo zake za miguu zilinyanyuka kutoka ardhini na makanyagio ya miguu yake yalikuwa mapana. Maji yalikuwa hayawezi kuyalowesha. Wakati alipokuwa akitembea alinyanyua miguu yake kutoka ardhini na kuinamia kwa mbele akikanyaga taratibu kwa hatua nyepesi. Alitembea kwa wepesi kana kwamba alikuwa akishuka kwenye mteremko. Alipokuwa akigeuka kumtazama mtu, alikuwa akigeuka mwili mzima (sio kichwa chake tu). Macho yake yalishuka chini; kuangalia kwake chini aridhini kulikuwa kurefu zaidi kuliko kuangalia kwake juu angani. Alikuwa akiangalia kwa mitazamo mifupi. Yeye alikuwa ndiye wa kwanza kusalimia (kutoa maamkuzi) kwa yeyote yule aliyekutana naye. Yeye (a.s.) halafu akasema: Nielezee kuhusu mazungumzo yake. Yeye akajibu: Yeye (s.a.w.w.) aliteseka kwa huzuni zisizokwisha, wakati wote akiwa kwenye mawazo mazito na kamwe hakuwa na starehe. Alikuwa mkimya kwa vipindi virefu vya muda. Hakuzungumza kamwe bila sababu ya maana. Alianza mazungumzo yake na kuyamaliza kwa ufasaha mkubwa. Hotuba yake ilikuwa muhimu na fupi, bila kuzidisha kiasi na kukosa maelezo muhimu. Alikuwa mwenye sauti nyororo na hakuwa fidhuli au mwenye kufedhehesha kamwe. Alikuwa akiziona neema kuwa kubwa sana hata kama zilikuwa ndogo kiasi gani, kamwe hakuzilalamikia. Hata hivyo, yeye hakushutumu wala kusifia kile alichokionja au kukila. Ulimwengu na kero zake kamwe haukumfanya achukie. Bali pale haki za mtu ziliponyang’anywa, yeye aliweza kukasirika sana kiasi kwamba hakuna aliyeweza kumtambua, na hapakuwa na chochote kilichoweza kuwa kikwazo cha kumzuia hadi alipokuwa ameweza kumsaidia kuirudisha haki yake. Aliponyooshea mkono kitu chochote, yeye alinyoosha mkono mzima na alipokuwa amepata mshangao, yeye aligeuza mkono wake chini juu. Wakati alipokuwa akiongea alikuwa akikusanya mikono yake yote pamoja, na akagonga mgongo wa dole gumba lake la kushoto kwa kiganja chake cha mkono wa kulia. Wakati alipokasirika aligeuzia uso wake kando na alipoudhiwa aliangalia chini. Kicheko chake kilidhihirishwa na 6


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 7

SUNAN-NABII tabasamu na (pale alipotabasamu) meno yake yalionekana kuwa kama vijiwe vya mvua ya mawe. As-Saduq (r.a.) amesema: Mpaka kufikia hapa imekuwa ni riwaya ya Qasim ibn alMuni’ kutoka kwa Ismail ibn Muhammad ibn Ishaq ibn Ja’far ibn Muhammad na wengine, hadi kufikia mwisho, ni riwaya ya Abd al-Rahman. Imam Hasan (a.s.) amesema: Nililificha hili kwa Husein (a.s.) kwa muda fulani halafu nikaja nikamwambia kuhusu hilo, lakini nikagundua kwamba alikuwa tayari amekwishalijua hili kabla yangu mimi, hivyo nikamuuliza kuhusu hilo na nikagundua kwamba yeye alikuwa amemuuliza baba yake kuhusu jinsi gani Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alivyokuwa, ndani ya nyumba yake na anapokuwa nje, ukaaji wake na muonekano wake; na yeye alikuwa hakuacha jambo lolote. Imam Husein (a.s.) amesema: Nilimuuliza baba yangu kuhusu tabia ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wakati alipoingia nyumbani kwake. Yeye alisema: Yeye (s.a.w.w.) aliingia nyumbani kwake alipokuwa anahitaji kufanya hivyo, na alipokuja nyumbani kwake, katika kuingia kwake, aliugawa muda wake katika sehemu tatu: Sehemu ya Mwenyezi Mungu, sehemu ya familia yake na sehemu kwa ajili yake mwenyewe. Halafu aliugawanya ule muda wake mwenyewe kati yake mwenyewe na watu, akiwetenga sehemu yake kwa ajili ya masahaba zake maalum na ile sehemu nyingine kwa watu wote kwa jumla; na hakutenga muda kwa ajili ya kazi zake binafsi. Ilikuwa ni kutoka katika desturi yake, katika ile sehemu aliyotenga kwa ajili ya (kukutana na) watu, kutoa kipaumbele na heshima kwa watu wa heshima maalum na angeweza kuwatofautisha kulingana na ubora wao katika dini. Kutoka miongoni mwao walikuwepo wale ambao walikuwa na haja moja na wale waliokuwa na haja mbili na pia wale waliokuwa na haja nyingi, hivyo alijishughulisha nao na aliwashughulisha kwa yale yaliyokuwa mazuri kwa ajili yao. Angewauliza kuhusu umma na katika kuwajulisha kuhusu ni nini kilikuwa muhimu angesema: “Wale ambao mpo miongoni mwenu wanapaswa kuwajulisha wale ambao hawapo hapa, na mnijulishe kuhusu haja za mtu yule ambaye hana uwezo wa kunijulisha mwenyewe juu ya shida yake. Kwani kwa hakika yule anayemjulisha mtu aliyeko kwenye mamlaka juu ya shida ya mtu ambaye hawezi kuielezea, Mwenyezi Mungu ataifanya miguu yake imara katika Siku ya Kiyama.” Hakuna kingine zaidi ya hiki ambacho kiliweza kutajwa mbele yake na asingeweza kukubali kutoka kwa mtu jambo jingine mbali na hili. Wangeweza kuja kutafuta elimu na hekima na wasingeweza kuondoka hapo hadi walipokuwa wameipata, na wangeondoka pale kama waongozaji kwa wengine. Niliuliza kuhusu tabia za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) nje ya nyumbani kwake – je ilikuwa vipi? Yeye (a.s.) alijibu: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angeweza kukaa kimya 7


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 8

SUNAN-NABII tu isipokuwa pale ambapo ilikuwa ni lazima azungumze, na alikuwa na uchangamfu kwa watu na asingeweza kuwatenga. Angewaheshimu wale wenye kuheshimiwa wa kila jamii na angeweza kuwafanya kuwa wasimamizi wa mambo yao. Alikuwa muangalifu sana na watu na angekuwa na tahadhari asije akawa mwenye kuwakosea staha au kuwageuzia au kuwakunjia sura. Angetafuta kujua kuhusu hali za masahaba wake na angewauliza watu kuhusu hali za watu wengine (kama ndugu na majirani zao). Alikuwa akiyapenda matendo mema na kuyahimiza wakati alipokuwa akiyakosoa matendo maovu na kuyavunja nguvu na kuyakataza. Alikuwa mwenye wastani wa kutokuyumba katika mambo yake. Hakuwa mwenye kutozingatia (kwa watu) kwa hofu ya kuja kuwa kwao wazembe na kukengeuka (kutoka kwenye njia iliyonyooka). Kamwe hakuweza kutoifikia haki na asingeweza kuikiuka. Wale waliokuwa karibu yake walitokana na wabora wa watu. Mbora zaidi kutoka miongoni mwao, kwa maoni yake, alikuwa yule mtu ambaye alitoa ushauri mwingi na muongozo kwa Waislamu na wale waliokuwa wa hadhi ya juu kabisa mbele ya macho yake walikuwa ni wale waliokuwa wakijali zaidi na wenye msaada kwao. Akasema: Kisha nilimuuliza yeye (a.s.) kuhusu tabia ya ukaaji wake, hivyo akasema: Yeye asingeweza kukaa au kusimama ila kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. Yeye kamwe hakujiwekea nafasi maalum kwa ajili yake na aliwakataza wengine kuwa na nafasi zilizohifadhiwa kwa ajili yao. Wakati yeye alipowasili mahali penye mkusanyiko, alikaa mahali popote palipokuwa na nafasi ya kukaa na aliwaagiza na wengine kufanya vivyo hivyo. Angetoa nafasi kwa wale wote waliokuwa wameketi pamoja naye, bila ya kutoa upendeleo kwa mmoja juu ya mwingine kwa sababu eti alikuwa anamheshimu sana. Pale mtu alipokuja kukaa naye angebakia ameketi mpaka mtu huyo atakaposimama na kuondoka. Kama mtu alimuomba kitu, basi yeye alimpatia kile alichokiomba hasa au kama alikuwa hanacho basi angempa maneno matamu. Watu walikuwa wamefurahishwa sana na tabia zake kiasi kwamba alikuwa kama baba kwao na wote walitendewa naye kama waliosawa. Hadhara zake zilikuwa ni hadhara za uvumilivu, heshima, uaminifu na imani. Hapakuwa na sauti zilizonyanyuliwa hapo wala hapakuwa na shutuma za uovu wowote ule. Makosa ya mtu yoyote yule hayakurudiwa nje ya mkusanyiko huo. Wale waliokuwepo kwenye mkutano huo walikuwa wema kwa kila mmoja wao, na walikuwa, katika hili, wameungana pamoja kwa uchamungu. Walikuwa wanyenyekevu, wenye heshima kwa waliowazidi umri na wenye huruma kwa wadogo, wenye hisani kwa wenye shida na wakarimu kwa wageni. Mimi nikasema: Mwingiliano wake na wale watu aliokuwa pamoja naye kwenye 8


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 9

SUNAN-NABII mkusanyiko ulikuwaje? Yeye (a.s.) akasema: Yeye wakati wote alikuwa mchangamfu, mtulivu wa tabia, mwepesi wa kuwasiliana na watu na mtaratibu wa kuzungumza. Yeye hakuwa fidhuli kamwe wala kuwa mkali. Kamwe hakucheka kwa sauti kubwa, hajawahi kuzungumza lugha chafu, hakutafuta kamwe makosa kwa watu na hakuwahi kumsifia mtu yoyote kwa kejeli. Alipuuza lile ambalo hakulipenda yeye kwa namna ambayo kwamba lisije likasababisha imma ukataji tamaa au mtu kujihisi kukosa matumaini. Aliweka mambo matatu mbali naye: kubishana, kuwa mwenye maneno mengi na kuzungumza kuhusu mambo ambayo yalikuwa hayamhusu yeye. Vilevile alijitenga na mambo matatu yanayohusiana na watu, yaani: asingeweza kumkaripia mtu yoyote, kamwe hakumlaumu na hawahi kutafuta makosa madogo madogo au hatia. Asingezungumza ila lile ambalo kwamba alitarajia kulipwa na Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. Wakati alipoongea, wale waliokuwa wamekaa pamoja naye walipumbaa na kutulia tuli na kimya kwa heshima na staha – kana kwamba walikuwepo ndege waliotulia juu ya vichwa vyao. Wakati aliponyamaza kimya wao walizungumza. Kamwe hawakujadiliana mbele zake; pale mmoja alipoweza kuongea, wale wengine wangeweza kumsikiliza mpaka alipokuwa amemaliza na wangechukua zamu za kuongea mbele yake. Yeye angecheka pale walipocheka wao na kuonyesha mshangao wao walipoonyesha mshangao. Alikuwa akionyesha uvumilivu kwa ufidhuli wa watu wa nje, wageni katika kuuliza na kuongea kwake, hata kama masahaba zake walipinga. Angesema: “Kama mnamuona mtu mwenye shida msaidieni.” Asingekubali kusifiwa isipokuwa kutoka kwa mtu mwaminifu katika kujitangaza mwenyewe kuwa ni Mwislamu. Hakuwa kamwe akiingilia mazungumzo ya mtu anapoongea mpaka akiwa amevuka mipaka, ambamo angemkatisha kwa kumtaka aache au kwa kusimama. Yeye akasema: Kisha nikamuuliza yeye (a.s.) kuhusu ukimya wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa hiyo yeye akasema: Kimya chake kilitegemea juu ya mambo manne: Uvumilivu, tahadhari, mazingatio na tafakari. Na kuhusu (ukimya wake katika) mazingatio, hiki kilikuwa ni ili aweze kuangalia na kumsikiliza kila mtu kwa usawa. Na kuhusu tafakari, ilikuwa ni kuhusu nini kinabakia na ni nini kinaangamia. Alikuwa na ulingano kamilifu wa uvumilivu na subira. Hakuna kilichoweza kumkasirisha au kumfadhaisha yeye. Alikuwa mwangalifu katika mambo manne: Katika kufanya kitendo chema ili kwamba wengine waweze kumuigiza yeye; katika kujitenga na maovu ili kwamba na wengine waweze kuyaacha; katika kujitahidi kufanya maamuzi bora kwa ajili ya kurekebisha umma wake, na katika kufanya kwake lile ambalo litampatia wema wa dunia hii na ile ya akhera.18 18 Ma’ani al-Akhbar: 83, Uyun Akhbar al-Rida, 1:246, as-Sirah al-Nabawiyyah ya Ibn Kathir 2:601 9


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 10

SUNAN-NABII Maelezo: Imesimuliwa vilevile ndani ya Makarimul-Akhlaq19 kwa kunukuu kutoka kwenye kitabu cha Muhammad ibn Ishaq ibn Ibrahim al-Talqani pamoja na ndani ya simulizi kutoka kwa wale ambao aliwachukulia kuwa waaminifu, kutoka kwa Hasan na Husein (a.s.). Anasema ndani ya Bihar: Na riwaya hii inatoka kwenye hadith maarufu ambazo zimetajwa na Aimmah (Maimam) ndani ya vitabu vyao vingi.20 18. Katika Makarimul-Akhlaq, at-Tabarasi anasimulia kutoka kwa Anas bin Malik ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na rangi nyeupe kama rangi ya lulu, na aliinamia mbele wakati alipotembea; na sio harufu ya marashi ya miski wala ya ambari yaliyoweza kuwa bora kuliko riha yake; na sio ulaini wa hariri iliyotariziwa wala wa hariri halisi ungekuwa mwororo kuugusa kuliko mkono wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).21 19. (Vile vile) kutoka kwake, kutoka kwa Ka’b ibn Malik ambaye alisema: Wakati jambo fulani lilipomfurahisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), uso wake uling’ara kama ule mwezi kamili.22 20. Kutoka kwa al-Ghazali katika al-Ihya’a: Kati ya wanadamu wote, yeye Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na mtindo na jinsi ya kuongea fasaha zaidi na maneno mazuri kupita kiasi. Alikuwa akisema: “Mimi ndiye fasaha zaidi wa Waarabu;” na watu wa peponi watakuja kuongea kwa lahaja ya Muhammad ….. na yeye (s.a.w.w.) aliongea kwa namna ya mkato, bila kuzidisha sana wala kutofikia lengo lake, kana kwamba kila neno lilifuatana na jingine; kulikuwa na mwanya kati ya maneno yake ambao ulimfanya msikilizaji kukumbuka kile alichokisema na kukielewa vema. Alikuwa na sauti yenye nguvu na ughani mtamu.23 21. Katika al-Manaqib, imesimuliwa kutoka kwa Aisha: Nikasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Nilikuona ukiingia (msalani) lakini sikukuta kitu chochote isipokuwa harufu ya miski?!” Yeye akasema: “Sisi jamii ya mitume tuna miili ambayo inatunzwa na viumbe wa ki-mbinguni, hivyo hakuna kinachotoka humo chochote bali ardhi inakimeza.”24 22. Katika al-Mahasin: Kutoka kwa Abdullah ibn al-Fadhil al-Nawfali, kutoka kwa 19 Makarimul-Akhlaq: 11 20 Biharul-Anwar; 16: 161 21 Makarimul-Akhlaq: 24, ‘Awarif al-Ma’arif: 224 22 Makarimul-Akhlaq: 19; Majmaul-Bayan 5:69 – Suratut-Tawbah (9) 23 Ihya’a Ulum al-Din, 2: 367 24 Manaqib Ali ibn Abi Talib 1: 125, Makarimul-Akhlaq: 24 10


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 11

SUNAN-NABII baba yake, kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye alisema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Mwenyezi Mungu aliiumba akili na akaiambia: Kimbia! Hivyo nayo ikakimbia. Halafu Yeye akaiambia: Songa mbele! Nayo ikasonga mbele. Kisha Yeye ‘Azza wa Jalla. akasema: Sijaumba kitu chochote ninachokipenda sana kuliko wewe. Mwenyezi Mungu akampa Muhammad (s.a.w.w.) sehemu zake (akili hiyo) tisini na tisa na akaigawanya ile sehemu moja iliyobakia miongoni mwa waja Wake waliobakia.25 23. Kutoka kwa Sheikh at-Tusi katika at-Tahdhib: Katika riwaya yake kutoka kwa Ishaq ibn Ja’far, kutoka kwa ndugu yake Musa, kutoka kwa wahenga wake, kutoka kwa Ali (a.s.) ambaye amesema: Nilimsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema: “Mimi nimetumwa kwa tabia tukufu na halisi zaidi.”26 24. Kutoka kwa as-Saduq katika al-Fiqh: Katika riwaya kutoka kwa Abdallah ibn Miskan kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. amemtofatisha Mtume Wake kwa tabia tukufu, hivyo jipimeni wenyewe, kama unayo hiyo nafsini mwako, basi mshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu na uombe kwa ajili ya ziada yake. Yeye alitaja mambo kumi (ya kupimwa): Yakini, kuridhika, subira, shukurani, uvumilivu, tabia njema, ukarimu, heshima na ujasiri.27 Maelezo: al-Kulaini ameisimulia hii, kama alivyosimulia as-Saduq katika vitabu vyake vingine vyote.28 25. Katika Makarimul-Akhlaq, kwa kunukuu kutoka katika kitabu cha alNubuwwah: Kutoka kwa Anas ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa ndiye mtu jasiri katika watu wote, na mpole wa watu wote, na mkarimu wa wanadamu wote. Usiku mmoja watu wa Madina walisikia kelele kubwa ambayo yiliwatishia, hivyo wao (wote) wakatoka kwenda kuelekea kule kelele hiyo ilikotokea. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akatukana nao; na alikuwa amewatangulia (na tayaru alikuwa amekwisha kuichunguza) na alikuwa akisema: “Msiwe na mshituko,” wakati alipokuwa juu ya farasi wa Abi Talha na alikuwa na upanga uliokuwa umefungwa shingoni mwake. Alianza kuwaelezea watu: “Msiogope, tuligundua kwamba ni kelele kubwa tu (isiyo na matokeo).29 26. Vilevile: Kutoka kwa Ali (a.s.) ambaye amesema: Katikati ya vita, wakati pande 25 al-Mahasin: 192, namba 8 26 Hatukuikuta hii katika Tahdhib, bali tumeipata katika Amali al-Sheikh at-Tusi, 2:209, al-Fiqh al-Rida: 353, Mishkat al-Anwar: 243, Awarif al-Ma’arif: 211 27 al-Faqih, 3:554 28 Ma’an al-Akhbar: 191, al-Khisal: 431, Tuhf al-Uqul: 362, al-Kafi 2:56 (na ni Yeye ambaye aliwatofautisha mitume Wake), Amal al-Saduq: 184. 29 Makarimul-Akhlaq:19 11


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 12

SUNAN-NABII mbili zimekuwa zikishambuliana, tulitafuta kimbilio kwa Mutukufu Mtume (s.a.w.w.) kwani (atakuwa yuko mbele kabisa ya vita na) hapakuwa na mtu aliyekuwa karibu sana na adui kuliko yeye.30 27. Vilevile: Kutoka kwa Abi Sa’id al-Khudri ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa mwenye haya sana kuliko msichana bikira aliyekuwa nyuma ya pazia. Alipokuwa hakukipenda kitu fulani angekiona kwenye uso wake.31 28. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Hafs ibn Ghiyath ambaye alisema: Abu Abdillah (a.s.) aliniambia: “Ewe Hafs, hakika yule ambaye alikuwa na subira alikuwa na subira kidogo sana na yule ambaye alikuwa mwenye kukosa subira alikuwa na ukosa subira mdogo sana.” Halafu akasema: “Lazima uwe mwenye subira katika mambo yako yote, kwani Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. alimtuma Muhammad (s.a.w.w.) na akamwagiza kuwa mwenye subira na mpole na halafu Yeye ‘Azza wa Jalla. akasema: ‘Na kuwa na subira kwa yale wanayosema na uwaepuke mwepuko mwema. Na niachie mimi wanaokadhibisha walioneemeka, na uwape muda kidogo.32 Na Yeye akasema: ‘….. Zuia ubaya kwa yaliyo mema zaidi, na mara yule ambaye baina yako na yeye pana uadui atakuwa kama rafiki mkubwa. Lakini (jambo hili) hawatapewa ila wale wanaosubiri, wala hawatapewa ila wenye bahati kubwa.33 Kwa hiyo alikuwa na subira mpaka wakamkashifu na wakamshutumu na makosa makubwa na hili likamfanya mwenye huzuni sana. Hivyo Mwenyezi Mungu akamfunulia haya: ‘Na kwa hakika Sisi tunajua kuwa kifua chako kinadhikika kwa yale wanayosema. Basi mtukuze Mola Wako kwa sifa njema, na uwe miongoni mwa wanaosujudu.34 Kisha wakamwita mwongo na wakamlaani, na yeye akahuzunika kwa hili. Hivyo Mwenyezi Mungu akamshushia: ‘Hakika tunajua kwamba yanakuhuzunisha yale wanayoyasema. Basi wao wala hawakukadhibishi wewe bali madhalimu wanakanusa hoja za Mwenyezi Mungu. Na hakika wamekadhibishwa Mitume kabla yako, bali wakavumilia kwa kule kukadhibishwa na kuudhiwa mpaka ukawafikia ushindi wetu. Na hakuna abadilishaye maneno ya Mwenyezi Mungu, na bila shaka zimekufikia baadhi ya habari za Mitume…..35 Hivyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akajiamrishia mwenyewe subira, lakini wao walivuka mipaka na wakati yeye alipomtaja Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. wao walimuita muongo. Hivyo yeye (s.a.w.w.) akasema: “Nimekuwa na subira kuhu30 Makarimul-Akhlaq: 18, Nahjul-Balaghah: 520, Kashf al-Ghummah, 1: 9 31 Makarimul-Akhlaq: 17 32 Suratul-Muzammil; 73: 10-11 33 Suratul-Fussilat; 41: 34-35 34 Suratal-Hijri; 15:97-98 35 Surat al-An’am; 6: 33-34 12


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 13

SUNAN-NABII siana na mimi mwenyewe, familia yangu na hadhi yangu, bali sina subira pale inapokuja kwenye kumkumbuka Mola wangu.” Hivyo Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. akashusha: “Basi vumilia hayo wasemayo …..”36 hivyo alibakia kuwa mvumilivu nyakati zote. Kisha habari njema za Uimamu zilitolewa kwa kizazi chake na walielezewa kuwa ni wenye subira, na Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. amesema: “Na tukawafanya miongoni mwao maimamu wanaoongoza kwa amri yetu waliposuburi na walikuwa wakiziyakinisha Aya zetu.”37 Kufikia hapa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Uvumilivu kwa upande wa imani ni kichwa kama ilivyo kwenye mwili” na akamshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema hii kubwa, hivyo Mwenyezi Mungu akashusha: “….. na likatimia neno jema la Mola wako kwa wana wa Israili kwa sababu walivumilia, na tukayaangamiza yale aliyokuwa ameyatengeneza Firauni na watu wake, na yale waliyokuwa wakiyajenga.”38 Ambayo juu yake Mtukufu Mtume akasema: “Hizi ni bishara njema na (ahadi ya) kisasi.” Na Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. alikuwa ameifanya ni ruhusa kwake yeye kupigana na washirikina, na Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. akateremsha haya: “Na miezi mitukufu itakapopita, basi waueni washirikina popote muwakutapo, na wakamateni na wazungukeni, na wakalieni katika kila njia (kuwashitukiza).”39 Na “Waueni kila mtakapokabiliana nao.”40 Hivyo Mwenyezu Mungu ‘Azza wa Jalla. akawaua mikononi mwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na masahaba zake wapendwa na akampa malipo kwa ajili ya subira yake kwa nyongeza ya tunu zilizohifadhiwa kwa ajili yake huko Akhera. Kwa hiyo, yule mwenye subira na kujihifadhi, na akayaachia mahesabu yake kwa Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla., hatauwacha ulimwengu huu mpaka Mwenyezi Mungu awe amemridhisha kwa kuwashinda maadui zake kwa ziada ya malipo ambayo atakuja kuyapata huko Akhera.’”41 29. Ndani ya al-Ma’ani al-Akhbar: Katika riwaya yake kutoka kwa Ahmad ibn Abi Abdillah kutoka kwa baba yake, katika hadithi iliyohusishwa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba yeye amesema: Jibril (a.s.) amenijia na kusema: “Ewe Mtume wa Allah! Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. amenituma kwako pamoja na zawadi ambayo Yeye hajawahi kumpa yeyote kabla yako.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Ni nini hiyo?” Jibril akasema: “Ni subira; na kitu kilicho bora kuliko 36 Surat Qaf; 50: 36 37 Suratul-Sajidah; 32: 24 38 Suratal-A’raf; 7:137 39 Surat-Tawba; 9: 5 40 Suratul-Baqarah 2 :191, Suratun-Nisa 4:91 41 al-Kafi; 2: 88 13


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 14

SUNAN-NABII hicho.” Yeye akasema: “Na hicho ni nini tena?” Jibril akasema: “Ni furaha; na kitu bora zaidi ya hicho.” Yeye akasema: “Na hicho ni nini?” Jibril akasema: “Ni kujizuia; na kile ambacho ni bora kuliko hicho.” Yeye akasema: “Na ni nini hicho?” Jibril akasema: “Ni unyofu; na kilicho bora kuliko hicho.” Yeye akasema: “Na hicho ni kitu gani?” Jibril akasema: “Ni uhakika; na bora kuliko hicho.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: Mimi nikasema: “Hicho ni kitu gani ewe Jibril!” Yeye Jibril akasema: “Njia ya kuvipata vyote hivyo ni kuwa na imani kwa Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla.” Mimi nikasema: “Ewe Jibril! Ni nini maana ya kuwa na imani kwa Allah?” Yeye akasema: “Kujua kwamba viumbe haviwezi ama kusababisha madhara wala manufaa na haviwezi imma kutoa au kuzuia (chochote), na kutokuwa na matumaini (ya kupata chochote) kwa viumbe. Wakati mja atakapofikia hali hii, basi hatafanya lolote isipokuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla., na atakuwa hamuombi au kumhofia mtu yoyote yule bali Mwenyezi Mungu na hayaweki matumaini yake juu ya yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. Hii ndio maana ya kuwa na imani kwa Mwenyezi Mungu.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Oh, Jibril! Ni nini maana ya subira?” Yeye akajibu: “Mtu lazima awe mvumilivu na mwenye subira katika wakati wa mateso kama anavyokuwa katika nyakati za furaha, na wakati wa umasikini kama anavyokuwa wakati akiwa kwenye utajiri, na kwenye matatizo kama anavyokuwa kwenye starehe; bila ya kulalamikia hali yake kwa sababu ya yale yaliyomfika.” Mimi nakasema: “Na ni nini maana ya kuridhika?” Yeye akasema: “Ni kutosheka na chochote kile kinachomfika katika dunia hii, kuridhika na chochote kile kidogo atakachokuwanacho na anapaswa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa ajili ya hilo.” Mimi nikasema: “Na nini maana ya furaha?” Jibril akasema: “Ina maana kwamba mtu kamwe asimkasirikie Mola wake, iwapo anapata chochote kile (starehe) cha dunia hii au la, na kutokuridhika na matendo mazuri yake mtu machache.” Mimi nikasema: “Na ni nini maana ya kujinyima?” Yeye akasema: “Kwamba mtu apende kila kile anachokipenda Muumba wake na kuchukia chochote Yeye anachokichukia na anakuwa mwangalifu sana kuhusu kile ambacho ni halali na wala haangalii kilicho haramu, kwani kile kilicho halali kitakuja kuhesabiwa na kilicho haramu kitafuatiwa na adhabu. Yeye awe ni mwenye huruma kwa Waislamu wote kama alivyo na huruma kwake mwenyewe. Anaepuka mazungumzo yasiyo na maana kama vile anavyoepuka mzoga wenye harufu mbaya sana. Anaepuka umiliki na mapambo ya dunia kama anavyojiweka mbali na moto – kwamba usije ukamfunika. Hana matumaini wala matamanio makubwa na wakati wote anakumbuka kifo chake.” 14


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 15

SUNAN-NABII Mimi nikasema: “Ewe Jibril! Na ni nini maana ya uaminifu?” Yeye akasema: “Mtu mwaminifu ni yule ambaye haombi chochote kutoka kwa watu hadi akipate yeye mwenyewe na wakati wowote anapokipata, anakifurahia. Kama kitu chochote cha ziada kitabakia kwake, yeye anakitoa katika njia ya Mwenyezi Mungu. Kwa kule kutokuomba kitu kutoka kwa wengine, anakuwa ameonyesha kwamba kweli yeye kweli ni mtumishi wa Mwenyezi Mungu. Kama anakipata kile anachokitaka, anakuwa mwenye furaha, na anafuraha juu ya Mwenyezi Mungu, na Yeye Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. Mwenye enzi yote anamridhia yeye. Wakati anapotoa kutokana na hicho katika njia ya Mwenyezi Mungu, anakuwa amefikia hatua ya kutegemea kikamilifu kwa Mola Wake.” Mimi nikasema: “Na yakini ni nini?” Yeye akasema: “Mtu mwenye yakini anafanya vitendo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kana kwamba anamuona. Hata kama hamuoni Mwenyezi Mungu, yeye anajua kwamba Mwenyezi Mungu anamuona; na ana uhakika kwamba chochote kinachokuja kwake (kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu) hicho hakitampitia mbali, na kile ambacho hakukusudiwa yeye basi hakiwezi kumfika yeye. Haya yote ni matawi ya imani kwa Mwenyezi Mungu na kujizuia (kutokana na anasa za dunia).42 30. Ndani ya kitabu cha Asim ibn Hamid al-Hannat: Kutoka kwa Abi Basir ambaye amesema: Nilimsikia Aba Ja’far (a.s.) akisema: Malaika mmoja alikuja kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na akasema: “Oh, Muhammad! Mola Wako anakutumia salamu na Anasema: Kama ukipenda Mimi nitakuwekea vijiwe vya dhahabu katika sehemu yenye ukubwa kama eneo la Makka.” Hivyo yeye (s.a.w.w.) akanyanyua mikono yake juu kuelekea mbinguni na akasema: “Ewe Mola Wangu! Ninakula siku moja ili nikutukuze Wewe, na ninashinda na njaa siku moja ili kukuomba Wewe.”43 31. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Muhammad ibn Muslim ambaye amesema: Nilimsikia Abu Ja’far (a.s.) akitaja kwamba Malaika mmoja alikuja kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w) na akasema: “Mwenyezi Mungu amekupa hiari ya uchaguzi wa ama kuwa mja mnyenyekevu au mfalme tajiri.” Hivyo yeye (s.a.w.w.) akamwangalia Jibril (a.s.) ambaye alifanya ishara kwa mkono wake kwake kuchagua unyenyekevu. Hivyo yeye (s.a.w.w.) akasema: Mimi ninachagua kuwa mja mtumishi mnyenyekevu.” Hivyo yule Malaika aliyetumwa akasema: “Kama ungechagua kuwa mfalme, kwa hali yoyote ile ingekushushia hadhi yako mbele ya Mola Wako.” Yeye, Imam (a.s.) akasema: Na yeye alikuwa na funguo za kwenye hazina za dunia.44 42 Ma’an al-Akhbar: 260, Uddat al-Da’i: 94 43 al-Usul al-Sittat- Ashar: 37, Makarimul-Akhlaq: 24, al-Kafi, 8:131, Jami’al-Akhbar: 291, Amali al-Tusi, 2: 144, Bihar al-Anwar, 16: 283 na 70:318 44 al-Kafi 2:122 na 8:131, Amali as-Saduq: 365, Biharul-Anwar 18:334 15


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 16

SUNAN-NABII 32. Katika Nahjul-Balaghah: Yeye Imam (a.s.) akasema: “Hivyo mfuateni Mtume wenu, aliye mtukufu na safi ….. Yeye alichukua (fungu) kidogo sana kutoka kwenye dunia hii na hakuitazama kwa tazamo zima. Kati ya watu wote wa ulimwengu huu, yeye alikuwa ndiye aliyekinai sana na aliyekuwa na tumbo tupu zaidi. Dunia ilitolewa kwake lakini alikataa kuipokea. Wakati alipojua kwamba Mwenyezi Mungu Mtukuka alilichukia jambo, yeye pia alilichukia; kwamba Mungu alichukulia kitu kuwa duni, na yeye pia alikidunisha; kwamba Mungu alikichukulia kitu kuwa kidogo, yeye pia alikichukulia kuwa ni kidogo. Kama tukiyapenda yale ambayo Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wanayachukia, na kuyathamini yale ambayo wameyachukulia kuwa ni madogo, huko kutakuwa ni kujitenga kwa kutosha na Mwenyezi Mungu na uvunjaji wa amri Zake. Mtukufu Mtume alitumia kula chakula chake akiwa ameketi chini (sakafuni), na alikuwa akikaa kama mtumwa. Alitengeneza viatu vyake kwa mikono yake mwenyewe na kushona viraka vya nguo zake kwa mikono yake mwenyewe. Angeweza kupanda juu ya punda asiyekuwa na matandiko na angembeba mtu mwingine nyuma yake. Kama kulikuwa na pazia kwenye mlango wake lililokuwa na picha juu yake, angemwambia mmoja wa wake zake: “Ewe Fulani binti Fulani! Liondoe hili mbele ya macho yangu kwa sababu kama nikiliangalia ninaikumbuka dunia na vishawishi vyake.” Kwa hiyo, aliuweka moyo wake mbali na dunia hii na akaufuta ukumbusho wake kwenye akili yake. Alitamani kwamba vishawishi vyake vingebaki kufichika kutoka machoni mwake ili asiweze kuchukua mali yoyote kutoka humo, wala kuichukulia kama ni mahali pa kudumu na kutegemea kuishi ndani yake. Kwa sababu hiyo yeye aliiondoa kabisa kutoka akilini mwake, akaiweka mbali na moyo wake na akaificha kutoka machoni mwake, kama vile tu ambavyo mtu anayechukia kitu angechukia kukitazama au kusikia habari zake.45 33. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Talha ibn Zayd kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Hakukuwa na kitu chochote katika dunia hii ambacho kilimfurahisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) zaidi kuliko kubakia na njaa na kumuogopa Mwenyezi Mungu.46 Maelezo: Hili pia limesimuliwa kutoka Hisham na wengineo kutoka kwa Imam (a.s.). 47 34. Kutoka kwa Tabarsi ndani ya al-Ihtijaj: Kutoka kwa Musa ibn Ja’far, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa baba zake, kutoka kwa Husein ibn Ali (a.s.), katika riwaya ndefu akielezea hali ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): Alikuwa akilia kwa hofu ya Mwenyezi Mungu mpaka mkeka wake wa swala ukaweza kulowa (kutokana na 45 Nahjul-Balaghah: 227, Hotuba ya 160, Makarimul-Akhlaq: 9, Biharul-Anwar, 16:285 46 al-Kafi, 2: 129 47 Ibid; 8:129 16


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 17

SUNAN-NABII machozi yake) licha ya kwamba hajafanya kosa lolote.48 35. Katika al-Manaqib: Yeye (s.a.w.w.) angeweza kulia mpaka akakosa fahamu. Mtu mmoja akamuuliza: Kwani Mwenyezi Mungu hajakusamehe wewe dhambi zako zote, zilizopita na za baadae?” Yeye akajibu: “Hivi mimi nisewe mja mwenye shukurani?” Na hiyo hiyo ndio iliyokuwa hali ya Ali ibn Abi Talib (a.s.), mrithi wake, wakati alipokuwa akifanya ibada.49 36. Kutoka kwa al-Daylami katika al-Irshad: Imesimuliwa kwamba sauti ya kilio kama sauti ya mchemko kutoka kwenye chungu kinachochemka ingeweza kusikika kutoka kwa Nabii Ibrahim (a.s.) wakati alipokuwa akiomba – kwa hofu juu ya Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) naye alikuwa vivyo hivyo.50 37. Kutoka kwa Sheikh al-Fattuh katika Tafsiif yake: Kutoka kwa Abi Sa’id alKhudri ambaye amesema: Wakati aya hii, ‘…..mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi’51 iliposhuka, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alijishughulisha sana katika kumkumbuka Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. kiasi kwamba wale makafiri wakasema kwamba amekuwa mwendawazimu.52 38. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Abu Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuwa akiomba maghfira mara sabini kwa siku. Mimi nikauliza: Je, alikuwa akisema ‘Astaghfirullaha wa Atubu Ilayh’ yaani – Naomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu na ninatubia Kwake? Yeye alijibu: Hapana, bali akitumia kusema ‘Atubu Ilallah’ – Natubia kwa Mwenyezi Mungu. Mimi nikasema: Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa akitubia na bila kurudia na sisi tunatubia na kurudia (makosa yetu), hivyo yeye (a.s.) akasema: Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kutoa msaada.53 39. Vilevile: Imesimuliwa kutoka kwa Talha ibn Zayd kutoka Abi Abdillah (a.s.): Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kamwe hakuwa akisimama na kuondoka kwenye mkusanyiko wa watu, hata kama takriban watu wote wakiwa wamekwisha kuondoka, mpaka awe ameomba maghfira kutoka kwa Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. mara sabini na tano.54 48 Al-Ihtijaj: 223 – Katika majadiliano ya Imam Ali pamoja na Wayahudi. 49 Al-Mustadrak; 11: 247, Irshad al-Qulub: 91 na hatukuiona kwenye Manaqib. 50 Irshad al-Qulub: 105, Uddat al-Da’i: 137 51 Surat al-Ahzab; 33: 41 52 Rawhul-Jinan wa Ruhul-Jinan (Tafsir ya Abi al-Futtuh al-Radhi) 1: 375-SuratulBaqarah: 147 53 al-Kafi; 2: 438, Uddat al-Da’i: 250 54 al-Kafi, 2: 504, Uddat al-Da’i: 250 17


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 18

SUNAN-NABII 40. Katika Makarimul-Akhlaq, ikinukuu kutoka kwenye kile kitabu cha alNubuwwah: Kutoka kwa Amirul-Mu’minin (a.s.) ambaye, wakati alipokuwa akimweleza Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angeweza kusema: Yeye alikuwa ndiye mkarimu zaidi, jasiri sana, mkweli zaidi, mwaminifu zaidi katika kutimiza wajibu wake, mpole na mwenye huruma zaidi, na muungwana zaidi wa watu wote. Wakati mtu alipomuona yeye kwa mara ya kwanza aliingiwa na butwaa kwa kuwepo kwake, na wakati mtu alipochanganyika naye (mara ile tu) angempenda yeye. Sijawahi kumwona mtu yoyote yule kama yeye (s.a.w.w.) kabla na baada yake.55 41. Kutoka kwa as-Sheikh al-Tusi katika kitabu al-Amali: Imesimuliwa kutoka kwa Muhammad ibn Ali ibn al-Husein ibn Zayd ibn Ali kutoka kwa ar-Ridha kutoka kwa baba zake (a.s.) ambao wamesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Ni lazima mtwae tabia adhimu, kwani Allah ‘Azza wa Jalla. amenileta pamoja nayo hiyo. Kutokana na tabia adhimu hiyo ni juu ya mtu kuonyesha usamehevu kwa yule anayemkosea, kumpa yule anayemnyima yeye, kuwasiliana na yule anayevuja mahusiano naye na kumtembelea mgonjwa ambaye huwa hamtembelei yeye anapokuwa mgonjwa.56 42. Ndani ya al-Kafi: Kutoka kwa Isa ibn Abdillah ibn Umar ibn Ali kutoka kwa baba yake (a.s.) ambaye amesema: Ilikuwa ni kutoka kwenye uthibitisho wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kusema: Hapana, na ninaomba msamaha kutoka kwa Mwenyezi Mungu.57 43. Katika Makarimul-Akhlaq: Kutoka kwa Ibn Umar ambaye amesema: Furaha na kuchuckia kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) viliweza kuonekana usoni mwake. Wakati alipokuwa amefurahi ingeweza kudhihirika kwa ung’aavu wa uso wake, na wakati alipokasirika, rangi ya uso wake ilikwajuka na ukafifia.58 44. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Muhammad ibn Arafah kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema (akiwaambia masahaba wake): “Je, nisiwajulishe kuhusu mmoja kati yenu ambaye ndiye anayefanana zaidi sana na mimi? Wao wakasema: “Ndio; Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu!” Yeye akasema: “Yule ambaye ana tabia njema zaidi kati yenu, yule mwenye huruma zaidi kwa watu, yule aliye mkarimu zaidi kwa ndugu zake, mwenye subira zaidi kuhusiana na haki, yule ambaye anazuia hasira zake zaidi, mwenye kusamehe zaidi na mwenye kuzidi sana katika kushikilia kwake uadilifu, akiwa katika furaha na pia kwenye hasira.59 55 Makarimul-Akhlaq: 18, Biharul-Anwar, 16:194, sehemu ya 8 Hadithi ya 33. 56 Al-Amali ya Sheikh Tusi, 2:92 57 al-Kafi 7: 463 58 Makarimul-Akhlaq: 19 59 al-Kafi 2: 240, Tuhf al-Uqul: 48 18


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 19

SUNAN-NABII 45. Kutoka kwa Ghazali katika kitabu chake al-Ihya’: Wakati yeye (s.a.w.w.) alipokuwa ametaharuki angezishika ndevu zake tukufu kila mara.60 46. Vilevile: Yeye alisema: Na yeye (s.a.w.w.) alikuwa ndiye mkarimu zaidi wa wanadamu wote. Sio dinari wala dirham ambayo alibakia nayo hadi jioni. Na usiku ungeingia na akawa na kitu cha ziada ambacho amebakia nacho na akawa hajapata mtu wa kukitoa kwake, yeye hakurudi nyumbani kwake mpaka awe ameweza kukitoa kwa mtu mwenye kukihitaji. Hakuchukua kutoka kwenye kile alichopewa na Mwenyezi Mungu isipokuwa mahitaji yake ya mwaka, kutoka kwenye tende na shayiri ambavyo vilikuwa rahisi kwake kuvipata, na akatoa kilichobakia katika njia ya Mwenyezi Mungu. Hakuombwa kitu chochote kile bali alikitoa. Halafu (baada ya kutoa ili ziada) yeye aligeukia kwenye yale mahitaji yake ya mwaka na akapendelea kutoa kutoka humo. Hata pale ilipokuwa inawezekana kwamba angeweza kuyahitaji kabla ya mwisho wa mwaka huo, endapo kusingekuwa na kitu kingine chochote kitakachopatikana kwake – yeye angeitekeleza haki, hata kama ingekuwa na maana ya yeye ama masahaba zake kupata hasara – angetembea peke yake miongoni mwa maadui zake bila ya mlinzi binafsi – yeye hakuvutiwa na lolote kati ya mambo ya kidunia – alikaa na masikini na akala nao. Aliwaheshimu watu wenye maadili kwa sababu ya tabia zao njema na alizikonga nyoyo za watu waungwana kwa kuwaheshimu kwake. Aliweka karibu uhusiano wake na jamaa wa karibu yake bila ya kuwapendelea wao juu ya yule aliyekuwa mbora kuliko wao (katika maadili). Hakumuonea mtu yoyote na alikubali sababu za yule aliyeomba msamaha – na alikuwa na mtumwa wa kiume na wa kike lakini kamwe hakula chakula kizuri au kuvaa nguo nzuri kuliko wao. Hakuna muda katika wakati wake uliotumika bila ya kufanya kitendo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, au kufanya kile ambacho ni muhimu kwa ajili ya unyofu wa nafsi yake. Angetembelea bustani za masahaba zake. Hakumdharau kamwe mtu masikini kutokana na ufukara wake au taabu zake, wala hakumwogopa mfalme kwa sababu ya madaraka yake; (bali) angewasukuma wote sawasawa kwa Mwenyezi Mungu.61 47. Vilevile: Yeye amesema: Kati ya watu wote yeye (s.a.w.w.) ndiye aliyechukia kidogo sana na mwepesi wa kufurahisha. Alikuwa ndiye mwenye kujali zaidi, mshauri na mwenye msaada kwa watu.62

60 al-Ihya’ Ulum al-Din, 2:387 61 Ihya’ ‘Ulum al-Din 2:360, al-Manaqib 1: 145, al-Mahajjat al-Bayda’ 4: 123 62 Ihya’ ‘Ulum al-Din 2: 369 19


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 20

SUNAN-NABII 48. Vilevile: Yeye alisema: Wakati yeye Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa na shangwe na akawa amefurahi, alikuwa ndiye mbora wa wenye kufurahi. Kama alihutubia, basi alihutubia kwa makini sana; kama alikasirika, na kamwe hakukasirika isipokuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu – hakuna ambacho kingeweza kustamili hasira zake. Hivi ndivyo alivyokuwa katika mambo yake yote. Pale tatizo lolote lilipokuja kwake, alilikabidhi kwa Mwenyezi Mungu na alizikana nguvu zake mwenyewe na mamlaka, na akatafuta mwongozo kutoka kwa Mwenyezi Mungu.63 49. Ndani ya al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Salam ibn al-Mustanir kutoka kwa Abi Fa’far (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Kwa hakika kwa kila jambo la ibada kuna uchangamfu (hapo mwanzoni) halafu linakuwa legevu. Hivyo yule ambaye ibada yake imetekelezwa kwa uchangamfu kulingana na Sunna yangu amepata uongofu, na yule ambaye anatenda kinyume na Sunna yangu amepotoka na matendo yake yameharibika. Na kuhusu mimi, ninaswali na ninalala, ninafunga na kufuturu, ninacheka na ninalia. Kwa hiyo yule anayetelekeza mwenendo wangu na Sunna zangu, huyo hatokani na mimi.64 Maelezo: Riwaya kuhusu suala hili ni nyingi mno. Tumenukuu riwaya moja au mbili kutoka katika kila mada. Hata hivyo, kuna hadithi nyingi juu ya vipengele vilivyoelezwa kirefu (juu ya tabia yake Mtume (s.a.w.w.).

63 Ibid. – mwandishi ana maelezo juu ya hadith hii, rejea kwenye al-Mizan 6:311 – SuratulMaida; 3: 116-120 64 al-Kafi 2:85 20


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 21

SUNAN-NABII

MLANGO WA 2 UHUSIANO WAKE MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.) NA WATU 1. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwenye kitabu Bahr al-Siqa kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Abi Abdillah aliniambia: Ewe Bahr! Utukufu wa tabia huleta wepesi (na furaha) – kisha akasimulia hadith ambayo ilikuwa na maana kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na adabu nzuri.65 2. Kutoka kwa Imam as-Sadiq ndani ya kitabu al-Ilal: Kutoka kwa Husein ibn Musa, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa baba zake, kutoka kwa Amirul-Mu’minin (a.s.) ambaye amesema: Michango ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa jamii ilikuwa haikuthaminiwa; na yale mema aliyoyatenda kwa Maquraishi, Waarabu, na wasiokuwa Waarabu – na ni nani ambaye matendo yake yalikuwa bora kuliko yale ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kwa viumbe Wake? Vivyo hivyo inahusika kwetu sisi – Ahlul-Bayt; yale mema tunayoyafanya (kwa ajili ya Waislam) hayathaminiki na kadhalika wema wa waumini wa kweli pia hauthaminiki.66 3. Kutoka kwa Daylami ndani ya al-Irshad: Yeye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akishona viraka vya nguo zake yeye mwenyewe, akirekebisha viatu vyake mwenyewe, akikamua kondoo wake, na kula chakula na watumwa wake, akikaa chini ardhini, akipanda punda na kubeba mtu mwingine pamoja naye; asingeona aibu kubeba bidhaa zake za nyumbani yeye mwenyewe na vitu vingine kutoka sokoni kupelekea familia yake. Angepeana mikono na matajiri na masikini sawa sawa vilevile na asingeondoa mkono wake kutoka kwenye mkono wa mtu mwingine mpaka mtu huyo atakapoondoa huo mkono wake yeye mwenyewe. Angemsalimia yeyote aliyekuja kwake kutoka kwa matajiri hadi masikini, wazee au vijana. Asingekiangalia kwa dharau kitu chochote alichopewa hata kama kingekuwa ni tende kavu. Alimiliki vitu vichache, alikuwa na huruma kwa asili, mkunjufu, mchangamfu, akitabasamu wakati wote bila ya kucheka, wakati wote akisikitika lakini bila ya kukunja uso, mnyenyekevu bila ya kushusha au kupoteza heshima 65 al-Kafi; 2: 102 66 al-Ilal al-Shara’i: 560 21


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 22

SUNAN-NABII yake, mkaribu bila ya kuwa mbadhirifu, mkweli na mpole kwa kila Mwislam. Hakuteuka kutokana na kushiba na yeye kamwe hakunyooshea mkono wake (kitu chochote) alichokuwa hana haja (nacho) – abadan.67 4. Katika Makarimul-Akhlaq: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akitazama katika kioo na kuchana nywele zake, na wakati mwingine alikuwa akiangalia kivuli chake ndani ya maji na kupanga nywele zake. Angeweza kujinadhifisha mwenyewe kwa ajili ya (kukutana na) masahaba zake mbali na kujitunza kwa ajili ya familia yake; na akasema: “Mwenyezi Mungu anapenda mja wake ajinadhifishe mwenyewe na kujipuna na kujipamba wakati anapotoka kwenda kuwatembelea ndugu zake 68 5. Kutoka kwa al-Saduq ndani ya al-‘Ilal na Uyunal-Akhbar: Imesimuliwa kutoka kwa ar-Ridha, kutoka kwa baba zake (a.s.) ambao wamesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Kuna mambo matano ambayo sitayaacha mpaka kufariki kwangu: Kula juu ya ardhi (bila meza) pamoja na watumwa, kupanda juu ya mnyama wa kipando asiyekuwa na matandiko, kukamua mbuzi kwa mikono yangu, kuvaa nguo za sufi zinazokwaruza na kuwasalimia watoto – kiasi kwamba vitendo vyangu hivi viweze kuja kuwa ni Sunnah baada yangu.” Nyogeza: Hili vilevile limesimuliwa katika al-Majalis.69 6. Kutoka kwa al-Qutb ndani ya Lub al-Lubab: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angeweza kuwasalimia wadogo na wakubwa.70 7. Kutoka kwa al-Saduq ndani ya al-Faqih: Amirul-Mu’minin (a.s.) alimwambia mtu mmoja kutoka kabila la Bani Sa’d: Hivi nisikuambie kuhusu mimi binafsi na Fatimah? ….. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuja kwetu asubuhi tukiwa bado tumelala na akasema: ‘As-Salamu Alaykum’ (amani iwe juu yenu). Tulibakia kimya kwa sababu ya kuona haya kwa kule tulikokuwa wakati huo. Halafu akasema tena ‘AsSalamu Alaykum’ nasi tukabakia kimya. Kisha akasema tena ‘As-Salamu Alaykum’ hivyo tukahofia kwamba kama tungebakia kimya (kwa mara ya tatu) basi angeweza kuondoka. Hii ilikuwa ndio desturi yake – angeweza kusalimia mara tatu na kama akiwa ameruhusiwa kuingia basi angefanya hivyo, kinyume cha hayo yeye angeondoka. Kwa hiyo sisi tukasema: ‘Alaykas-Salam Yaa Rasulallah’ (Juu yako zikushukie rehma na amani Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu!) Tafadhali karibu 67 Irshad al-Qulub: 115 68 Makarimul-Akhlaq: 34 69 Amali al-Saduq: 68; al-Majlis al-Sabi’ Ashar, ‘Ilal al-Shara’i: 130, Uyun Akhbar arRidha 2: 81, al-Khisal: 271. 70 Akiinukuu kutoka kwenye al-Mustadrak 8:364 22


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 23

SUNAN-NABII ingia! Basi yeye akaingia.71 8. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Rab’i ibn Abdillah kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye alisema: Mtukufu Mume (s.a.w.w.) alikuwa akiwasalimia wanawake nao wangeweza kujibu salamu zake. Amirul-Mu’minin alikuwa akiwasalimia wanawake, lakini hakupenda kuwasalimia wale wadogo wa umri akisema: Nahofia kwamba sauti yake isije ikanivutia mimi na ikaishia kwa mimi kupata zaidi kuliko ninachotaka katika namna ya zawadi (kwa ajili ya hizo salamu).72 Maelezo: Naye al-Saduq ameisimulia hii pamoja na nyororo ya wasimulizi isiyokamilika.73 Kadhalika, mjukuu wa Tabarsi anaisimulia katika al-Mishkat akinukuu kutoka kwa al-Mahasin.74 9. Vilevile: Imesimuliwa kutoka kwa Abd al-Adhim ibn Abdillah ibn al-Hasan alAlawi akiihusisha na mmoja wa Ma’sum (a.s.), yeye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akikaa katika mikao namna tatu, al-Qurfusa – huu ni ule ambao miundi yake inakuwa imenyooka, katika hali ya kusimama, na mikono ikiwa imewekwa kuizunguka, na viganja vikiwa vimeshika kwenye sehemu ya mbele ya (kigasha cha) mkono wake. Angeweza (wakati mwingine) kukaa juu ya magoti yake. Yeye ageweza pia kukalia juu ya mguu mmoja na kunyoosha huo mwingine juu yake, na hajawahi kuonekana kamwe akiwa amekaa mkao mwingine wowote wa nne.75 10. Katika al-Makarim, kwa kunukuu kutoka kwenye kitabu cha al-Nubuwah: Kutoka kwa Ali (a.s.) ambaye amesema: Wakati Mtukufu Mtume alipokuwa akipeana mikono na mtu mwingine, asingeweza kuuondoa mkono wake mpaka huyo mtu mwingine aondoe wa kwake kwanza, na alipokuwa anashughulika na mtu katika kutatua matatizo yake au akizungumza naye, yeye asingeweza kuondoka kwanza mpaka mtu huyo atangulie kuondoka mwenyewe kwanza. Wakati mtu mwingine alipokuwa akiongea naye, yeye (s.a.w.w.) asingeweza kukaa kimya mpaka mtu huyo aliponyamaza kimya, na hakuonekana kwamwe akinyoosha mguu wake mbele ya yule mtu aliyekuwa amekaa naye. Yeye hakuchagua kati ya mambo mawili isipokuwa lile lililokuwa gumu zaidi kati ya mawili hayo. Asingeweza kujichukulia kisasi mwenyewe kwa ajili ya kukosewa kokote mpaka 71 al-Faqih 1:320 Hadithi ya 937, Ilal al-Shara’i: 366. 72 Al-Kafi 2: 648 na 5: 535; al-Mustadrak 8:373 73 al-Faqih, 3:469 74 Mishkat al-Anwar: 197 75 al-Kafi; 2: 661, Makarimul-Akhlaq; 26, al-Mustadrak; 7: 400, Fayd al-Qadir; 5: 85/145/233. 23


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 24

SUNAN-NABII kuwe kumevunja sheria tukufu ya Mwenyezi Mungu, ambapo hapo atakuwa amekasirika kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. Hakuwahi kamwe kula chochote huku akiwa ameegamia kwenye kitu chochote mpaka pale alipoiaga dunia hii. Hakuombwa kitu chochote kamwe ambapo akajibu kuwa “hapana,” na hakumrudisha muombaji mwenye haja bila ya kumpa kile alichohitaji, au (kama alikuwa hanacho) bila kumwambia maneno ya upole na huruma. Swala yake ilikuwa ndio nyepesi mno.76 Hotuba zake zilikuwa fupi mno na zisizokuwa na maneno yasiyo na muhimu wenye kupasa. Yeye angeweza kutambulika kwa riha ya manukato yake pale alipokaribia mahali. Alipokuwa akila chakula na kundi la watu, yeye alikuwa ndio wa kwanza kuanza kula na wa mwisho kuacha kula. Wakati alipokula angeweza kula kutoka kile kilichokuwa karibu mbele yake, na kama palikuwepo na tende kavu ama mbichi angenyoosha mkono wake (kuokota kutoka pale zilipo). Na kama angekuwa anakunywa chochote, alikunywa kwa funda tatu, na angekunywa maji kwa kuyakonga kidogo kidogo na asingeweza kuyameza kwa kuyagugumia kwa pupa. Yeye alikuwa akitumia mkono wake wa kulia kwa kula, na ule wa kushoto kwa jambo jingine lolote mbali na kula. Yeye alipendelea kuanza na upande wa kulia katika mambo yake yote, kuanzia kuvaa nguo mpaka kuvaa viatu na hata mpaka kuchana nywele zake. Pale alipokuwa akiita, aliita mara tatu. Alipokuwa akizungumza, alizungumza kwa kifupi na wakati yeye alipobisha hodi kuomba kuingia, alifanya hivyo mara tatu. Hutoba zake zilikuwa zenye kueleweka wazi na rahisi kiasi kwamba yeyote aliyezisikiliza alizielewa, na alipokuwa akizungumza, ingeweza kuwa kana kwamba nuru ilikuwa anatoka kutoka katikati ya meno yake ya mbele kiasi kwamba kama ungemuona, ungeweza kusema: Yeye ana uwazi katikati ya meno yake, lakini kwa kweli alikuwa hana. Angeweza kuangalia kwa kupepesa haraka haraka (bila ya kukodoa macho) na asingeweza kuongea na mtu jambo ambalo halipendi, na analolichukia. Alipokuwa akitembea angeweza kunyanyua miguu yake kana kwamba alikuwa akishuka kwenye mteremko. Angeweza kusema kwamba: “Wabora kutoka miongoni mwenu ni wale ambao wana akhlaq (tabia) njema.” Yeye asingeweza kukosoa ladha ya chakula au kukisifia. Masahaba zake wasingeweza kugombana wenyewe mbele yake. Yeyote aliyezungumza kuhusu yeye angesema, “Kamwe sijawahi kuona mtu kama yeye, imma kabla yake au baada yake.”77 76 Ikiwa na maana kwamba angekuwa akiweza kuwafikiria wale waliokuwa wakiswali katika jamaa hiyo nyuma yake na hivyo asingeirefusha hiyo Swala (Mfasiri). 77 Makarimul-Akhlaq; 23 24


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 25

SUNAN-NABII 11. Ndani ya al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Jamil ibn Darraj kutoka kwa Abu Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angeweza kugawanya fikra na mawazo yake kati ya masahaba zake: angeweza kuwaangalia wote kwa usawa. Yeye (pia) amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakuwahi kamwe kunyoosha miguu yake mbele ya masahaba zake. Wakati mtu alipopeana mikono naye, asingeweza kuuondoa mkono wake mpaka yule mtu mwingine alipoondoa mkono wake kwanza. Wakati watu walipolitambua hili, pale mtu yoyote alipopeana mkono naye, angeweza kuondoa mkono wake haraka sana kutoka mkononi mwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).78 Maelezo: Hili limesimuliwa katika njia mbili nyingine. Katika mojawapo (imeongezwa) ….. na asingeweza kamwe kumrudisha mwombaji – kama alikuwa na kitu cha kumpata, angeweza kumpatia, vinginevyo angesema: “Mwenyezi Mungu akijaalie kitu hicho juu yako.” 79 12. Kutoka kwa al-Ayyashi ndani ya kitabu chake cha Tafsiir: Kutoka kwa Safwan, kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) na kutoka kwa Sa’d al-Iskaf katika hadithi juu ya sifa na tabia za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): Alipokuwa ameketi (pamoja na mtu), asingeweza kusimama mpaka yule mtu aliyekuwa ameketi naye aliposimama kwanza.80 13. Katika al-Makarim: Amesema: Pale ambapo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angezungumza, angetabasamu huku akiwa anaongea.81 14.Vilevile: Kutoka kwa Yunus al-Shaybani ambaye amesema: Abu Abdillah (a.s.) aliniambia: “Unafanya vipi utani na mtu mwingine?” Mimi nikasema: “Kiasi kidogo tu.” Yeye akasema: “Wewe hulifanyi hilo? Kwa hakika masihara yanatokana na wema na ungeweza kumfanya ndugu yako awe mwenye furaha kutokana na masihara hayo. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akitumia kufanya masihara na mtu ili aweze kumfurahisha.82 15. Kutoka kwa Abi al-Qasim al-Kufi ndani ya kitabu cha Akhlaq: Kutoka kwa asSadiq (a.s.) ambaye amesema: Hakuna mtu muumini bali mpaka awe na hisia za ucheshi, na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akifanya masihara na alikuwa hasemi kamwe ili kweli tupu.83 78 al-Kafi; 2: 671, al-Mustadrak 8:437, Makarim al-Akhlaq: 17 na 23. 79 Al-Kafi 4:15 80 Tafseer al-Ayyashi 1: 204 – Surat al-Imran (3) 81 al-Makarimul-Akhlaq: 21 82 al-Kafi; 2: 663, Makarimul-Akhlaq: 21 83 al-Mustadrak, 8: 408 25


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 26

SUNAN-NABII 16. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Ma’mar ibn Khallad ambaye amesema: Nilimwambia Abul-Hasan (a.s.): “Mimi naniwe fidia yako. Wewe unasemaje juu ya mtu ambaye yuko pamoja na kundi la watu na likasemwa jambo la mzaha na wao wakacheka?” Yeye akasema: “Hakuna ubaya juu ya hilo kama sio ….. “ na nadhani kwamba alikuwa na maana kwamba kama halikuwa la uchafu, matusi – kisha yeye (a.s.) akasema: Kulikuwa na Bedui mmoja wa Kiarabu aliyekuwa akienda kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akileta zawadi kwa ajili yake na halafu akisema: “Tupatie thamani ya zawadi zetu,” hivyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angecheka, na wakati yeye (s.a.w.w.) alipokuwa na huzuni angeweza kusema: “Ni nini kimemtokea yule bedui? Laiti angetujia huku kwetu.”84 Maelezo: Kuna riwaya nyingi kama hizi.85 17. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Talha ibn Zayd kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa kawaida alikuwa akikaa kuelekea Qibla.86 18. Katika Makarimul-Akhlaq: Yeye amesema: Wakati kitoto kichanga kilipoletwa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ili kuweza kukiombea baraka, yeye (s.a.w.w.) angelikichukua mikononi mwake ili kuipa heshima hiyo familia ya kichanga hicho. Wakati mwingine kichanga hicho kingelikojoa mikononi mwake kiasi kwamba wale waliolishuhudia hilo wangetoa kelele ya sauti kubwa. Yeye (s.a.w.w.) angesema: “Msimkatishe mpaka awe amemaliza kukojoa.” Halafu akiwa amekwisha kumuombea mtoto huyo au kumpatia jina na familia yake ikawa imefurahia, basi yeye angemrudisha kwa familia yake, na wao wasingeweza kuona dalili za yeye kuwa amekasirishwa na mikojo ya yule mtoto wao mchanga. Walipokuwa wamekwisha kuondoka, yeye angeweza kuziosha nguo zake.87 19. Vilevile: Imesimuliwa kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) asingeweza kumruhusu mtu yoyote kuongozana naye wakati yeye akiwa kwenye kipando isipokuwa awe amembeba yeye pamoja naye, na kama angekataa (kupanda pamoja naye) angeweza kumwambia: “Basi tangulia ukaningojee sehemu ambayo umeichagua.”88

84 al-Kafi; 2: 663, Manaqib Ali ibn Abi Talib; 1: 149, Biharul-Anwar 16: 259. 85 Biharul-Anwar, 16: 294 86 Al-Kafi, 2: 661, Makarimul-Akhlaq: 26, al-Mustadrak, 8: 406 87 Makarimul-Akhlaq: 25 88 Ibid: 22 26


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 27

SUNAN-NABII 20. Kutoka kwa Abi al-Qasim al-Kufi katika kitabu cha ‘Akhlaq’: Na imesimuliwa kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) asingeweza kujilipizia kisasi kutoka kwa mtu yoyote, bali angemsamehe na kuondoka zake.89 21. Katika al-Makarim: Yeye amesema: Wakati mtu alipokuja kukaa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) yeye asingeweza kusimama kamwe (kutaka kuondoka) mpaka aliposimama mtu huyo.90 22. Vilevile: Yeye alisema: Kama Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakuwa amemuona mmoja wa ndugu zake kwa siku tatu, angemuulizia habari zake. Kama alikuwa hayupo (hapo mjini) basi angemuombea dua na kama alikuwa yupo angemtembelea, na kama alikuwa mgonjwa angemtembelea na kumliwaza.91 23. Vilevile: Kutoka kwa Anas ambaye amesema: Mimi nilimtumikia Mtukufu Mtume (.s.a.w.w.) kwa muda wa miaka tisa na kamwe mimi sikumbuki yeye kuniambia: “Kwa nini umefanya hivi?” na hakuwahi kunilaumu kwa jambo lolote lile.92 24. Kutoka kwa al-Ghazali ndani ya al-Ihya: Anas alisema: Naapa kwa yule ambaye amemtuma kwa haki! Yeye kamwe hajanizungumzia kuhusu jambo ambalo alikuwa halipendi: “Kwa nini umefanya hivi?” Na wakati wowote ule ambapo wake zake wangenilaumu, yeye angesema: “Mwacheni, hili lilikuwa limekwisha kuandaliwa na kuamuliwa kabla.”93 25. Vile ile kutoka kwake: Wakati yeye Mtume (s.a.w.w.) alipoitwa na masahaba zake au watu wengine, yeye angeweza kuitikia hivi, “Labbayka” (Nipo hapa).94 26. Pia alikuwa akiwaita masahaba zake kwa majina yao (ya heshima) ili kuwapa heshima na kufanya nyoyo zao zivutike kwake. Angeweza kutoa jina la hadhi kwa yule ambaye alikuwa hanalo na mtu huyo kuanzia hapo angeendelea kuitwa kwa jina hilo alilopewa. Angeweza pia kutoa majina ya hadhi kwa wanawake wenye watoto na wale ambao walikuwa hawana watoto, na angetoa majina kama hayo kwa watoto kutafuta kulainisha nyoyo zao kwa sababu ya hilo.95 89 Al-Mustadrak, 9: 7, Ihya ‘Ulum al-Din, 2: 365 90 Makarim al-Akhlaq: 17 91 Makarimul-Akhlaq: 19 92 Makarimul-Akhlaq: 16, na Ibn Abi Firas amesimulia hili katika Majmu’ah yake uk.46, kama alivyosimulia al-Suhrawardi katika Awarif al-Ma’arif: 224 (na katika vitabu hivi imetajwa ‘kwa muda wa miaka kumi’ badala ya tisa), Fayd al-Qadir 5: 152 93 Al-Ihya ‘Ulum al-Din, 2: 365 94 Ibid, 2: 381 95 Ibid, 2:366 27


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 28

SUNAN-NABII 27. Pia: Yeye Mtume (s.a.w.w.) alimpendelea zaidi mgeni wake (kuliko yeye mwenyewe) kwa kumpatia mto ambao angeegemea, na kama angekataa, yeye (s.a.w.w.) angamsisitizia hilo mpaka akawa ameukubali.96 28. Vilevile: Katika mwezi wa Ramadhani, yeye Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa kama “Upepo uliotumwa kwa wema”,97 bila kubakisha chochote (na kutoa kila kitu kuwapa wenye haja).98 29. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Ajlan ambaye amesema: Mimi nilikuwa pamoja na Abu Abdillah (a.s.) wakati muombaji mmoja alipokuja, hivyo alikiendea kikapu cha tende na akajaza mikono yake (kwa tende nyingi kiasi alivyoweza) na akampatia huyo muombaji, kisha akaja muombaji mwingine, hivyo akasimama tena akaijaza mikono yake kwa tende na akampatia huyo muombaji, halafu akafika mwingine tena, hivyo akasimama na akachukua tende ujazo wa mikono yake akampatia muombaji. Kisha bado akafika muombaji mwingine na hivyo yeye (a.s.) akasema: “Mwenyezi Mungu ndiye Mpaji wetu, kama alivyo Mpaji wako.” Halafu akasema: “Isingeweza kutokea kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliombwa kitu chochote kutoka kwenye milki zake za kidunia bali alikitoa kwa muombaji. Wakati fulani mwanamke mmoja alimtuma kijana wake kwake (s.a.w.w.) akisema: “Nenda kwa Mtume na umuombe, kama akisema: “Hakuna chochote cha kutoa” basi useme, “kwa hiyo nipe shati lako.” Kijana akaenda. Hivyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akavua shati lake na akampa yule kijana. Halafu Mwenyezi Mungu akamuelekeza katika njia ya sawa na akasema: “Usiuweke mkono wako ukiwa umefungwa nyororo shingoni mwako, wala usiuache wazi moja kwa moja, ama sivyo utabaki mwenye kulaumika, mwenye majuto.99 30. Vilevile: Imesimuliwa kutoka kwa Jabir kutoka kwa Abi Ja’far (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliweza kukubali zawadi, lakini hakuweza kukubali sadaka.100 31. Pia: Kutoka kwa Musa ibn Imran ibn Bazi’ ambaye amesema: Nilimwambia arRidha (a.s.): “Mimi niwe fidia yako! Watu wamesimulia kwamba wakati Mtukufu 96 Ibid. 97 Tazama Surat al-Mursalat; 77: 1 98 Ihya ‘Ulum al-Din, 2: 379, Sahih Muslim 4: 1803 99 Al-Kafi 4: 55, Tafsiir al-Ayyashi; 2: 289, namba 59, Tuhf al-’Uqul: 351 – Surat al-Isra’: 29 100 Al-Kafi, 5:143, Kamal al-Din wa Tamam al-Ni’mah 1:165, Fayd al-Qadir 5: 195, alKhisal: 62 no.88, Amal at-Tusi 1:231, Tafsiir al-Ayyashi 2: 93, no. 75, Basharat al-Mustafa: 765, Da’aim al-Islam 1: 246/258/259, al-Mustadrak 7: 122.

28


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 29

SUNAN-NABII Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa akienda kwa kutumia njia moja, angeweza kurejea kwa kutumia njia nyingine tofauti. Je, ilikuwa ni hivyo kweli hasa?” Yeye akasema: “Ndiyo, na nimefanya hivyo mimi mwenyewe binafsi kwa mara nyingi tu – kwa hiyo na wewe (pia) unapaswa kufanya hivyo.” Halafu akasema: “Kwa sababu hiyo itakuletea riziki nyingi zaidi.”101 32. Kutoka kwa Sayyid ibn Tawus katika al-Iqbal: Imesimuliwa kutoka kwa Abi Basir kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akitoka nje baada ya kuchomoza kwa jua.102 33. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Abdillah ibn al-Mughira kutoka kwa yule aliyemsimulia hilo kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipoweza kuingia mahali, angeweza kukaa sehemu iliyokuwa karibu zaidi ambayo ingepatikana wakati anaingia.103 Maelezo: Mjukuu wa al-Tabarsi vilevile analisimulia hili katika al-Mishkat akinukuu kutoka kwenye al-Mahasin na vinginevyo.104 34. Katika Awali al-La’ali: Imenukuliwa kwamba yeye (s.a.w.w.) alikuwa akikerwa na kutopendelea wengine kusimama kwa ajili yake, kwa hiyo yeye alipokuwa akiwajia watu, wasingeweza kusimama kwa sababu walijua kwamba yeye alilichukia hilo, na pale aliposimama, na wao walisimama pamoja naye (na wakabaki wamesimama hivyo) mpaka yeye atakapokuwa ameingia nyumbani kwake.105 35. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Ishaq ibn Ammar ambaye amesema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipotaka kutoka kwa ajili ya vita, angeweza kuwaita wake zake na kutaka ushauri kutoka kwao, halafu angeweza kutenda kinyume na ushauri wao.106 36. Ndani ya al-Manaqib: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akijipatia usingizi wake wa mchana katika nyumba ya Umm Salamah, hivyo bibi huyu alikuwa akikusanya jasho lake (s.a.w.w.) na kulichanganya na manukato.107 Maelezo: Hili limesimuliwa na wengine pia.108 101 al-Kafi, 5: 314 na 8: 147, al-Iqbal:283 102 al-Iqbal: 281 103 al-Kafi 2: 662, Makarim al-Akhlaq: 26, al-Mustadrak 8: 403 104 Mishkat al-Anwar: 204 105 Awali al-La’ali, 1: 141, al-Mustadrak, 9: 159 106 Al-Kafi 5:518, al-Faqih 3: 468, Makarimul-Akhlaq: 230 107 Manaqib Ali ibn Abi Talib, 1: 124 108 Majmu’at Warram: 23 29


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 30

SUNAN-NABII Nyongeza kwa sehemu hii: 1. Katika al-Kafi: Katika riwaya yake kutoka kwa Hasan ibn Ali ibn Fadhal kutoka kwa baadhi ya masahaba zake, yeye alisema: Abu Abdillah (a.s.) amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakuzungumza na watu kwa kiwango chake mwenyewe cha akili. Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: “Sisi Mitume tumeagizwa kuzungumza na watu kulingana na kiwango chao cha uelewa.”109 Maelezo: Hili limesimuliwa katika al-Mahasin, katika al-Amali cha as-Saduq na katika Tuhf al-Uqul.110 2. Ndani ya al-Amali at-Tusi: Katika riwaya yake kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye alisema: “Sisi, kundi la Mitume, tumeagizwa kuwa na uchangamfu na watu kama vile ambavyo tumeamriwa kufanya yale matendo ya wajibu.111 3. Katika al-Kafi: Katika hadithi yake kutoka kwa Abdillah ibn Sinan kutoka kwa Abu Abdillah (a.s.) ambaye amesema kwamba, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Mola Wangu ‘Azza wa Jalla. Ameniamuru mimi kuwa mwenye bashasha na watu kama vile alivyoniagiza kufanya vile vitendo vya wajibu.”112 Maelezo: Hii imesimuliwa katika Tuhf al-Uqul, al-Khisal na ndani ya Ma’ani alAkhbar.113 4. Katika kitabu al-Mahajjat al-Bayda cha al-Fayd; Sa’d ibn Hisham amesema: Nilikwenda kwa Aisha na nikamuuliza kuhusu tabia ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hivyo yeye akasema: “Kwani wewe husomi Qur’ani?” Mimi nikasema: “Ndio, kwa hakika mimi ninaisoma.” Yeye akasema: “Tabia ya Mtukufu Mtume ni Qur’ani.”114 Maelezo: Hili limesimuliwa pia katika Majmu’at Warram.115 5. Katika Tuhf al-Uqul: Kutoka Mtukufu Mtume (s.s.w.w.): “Mwendo wetu sisi, yaani mwendo wa Ahlul-Bayt (a.s.) ni: Kuwasamehe wale ambao wanatukosea, na kuwapa wale ambao wanatunyima sisi.”116 109 al-Kafi 1: 23 na 8: 223 110 Al-Mahasin: 195, Amali: 341, Tuhf al-Uqul: 37 111 Amali at-Tusi 2: 135 112 Al-Kafi 2: 117, Mishkat al-Anwar: 177 113 Tuhf al-Uqul: 46, al-Khisal: 82, Ma’ani al-Akhbar: 184 114 Al-Mahajjat al-Bayda 4: 120 115 Majmu’at Warram: 89 116 Tuhf al-Uqul: 38 30


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 31

SUNAN-NABII Maelezo: Sehemu ya mwanzo imesimuliwa ndani ya kitabu, al-Amali cha asSaduq.117 6. Katika al-Kafi: Katika simulizi yake kutoka kwa Isma’il ibn Mukhallad as-Sarraj kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) katika hadithi kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Mola Wangu ameniagiza kuwapenda wale wenye shida kutoka miongoni mwa Waislam.”118 7. Katika al-Irshad ya Daylami: Kutoka kwa as-Sadiq (a.s.) ambaye amesema: “Kwa hakika subira, haki, huruma na maadili mema yanatokana na akhlaq ya Mitume (a.s.)”119 8. Katika al-Mahajjat al-Bayda: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angekuwa wakati wote akitafuta na kuomba kwa Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. akizidi kumuomba ampambie tabia na sifa zake bainifu na amjaalie mwendo mtukufu. Alikuwa akisema katika dua zake: “Ewe Mola! Nifanyie maadili yangu kuwa mema” na tena “Ewe Mola! Niepushie sifa mbaya ziwe mbali nami.”120 9. Katika al-Majalis ya al-Saduq: Kutoka kwa Husein ibn Khalid, kutoka kwa Ali ibn Musa ar-Ridha, kutoka kwa baba yake (a.s.) katika hadithi: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Jibril, Malaika Mlezi, alinishukia (pamoja na ujumbe) kutoka kwa Mola wa ulimwengu na akasema: ‘Ewe Muhammad! Ni lazima utwae tabia njema, kwani tabia mbaya hufukuza mema ya dunia hii na ya akhera. Hakika wale wenye mfanano mkubwa kabisa na Mimi ni wale wenye tabia nzuri kabisa.”121 10. Katika kitabu Kashf al-Raibah cha Shahid al-Thani: Kutoka kwa Husein ibn Zayd ambaye amesema: Nilimwambia Ja’far ibn Muhammad (a.s.): “Mimi niwe fidia yako! Je, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na namna ya ucheshi?” Yeye akasema: “Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. Amemweleza kama mwenye maadili ya ubora wa hali ya juu. Mwenyezi Mungu amewatuma mitume na walikuwa na hali fulani ya umakini kuhusu wao wenyewe na Yeye alimtuma Muhammad (s.a.w.w.) pamoja na huruma na upendo. Katika upendo wake ulikuwemo ucheshi na kufanya masihara na watu kiasi kwamba wasije wakahisi kwamba yeye ni mkubwa sana hivyo kwamba hawamuangalii wala kumwendea yeye.” Halafu akasema: Abi Muhammad amenisimulia kutoka kwa baba yake Ali, kutoka kwa baba yake Husein, kutoka kwa baba yake Ali (a.s.) ambaye amesema: Wakati 117 Amali as-Saduq: 238 118 Al-Kafi 8: 8, Tuhf al-Uqul: 9 119 Irshad al-Qulub: 133, Tuhf al-Uqul: 9 120 Al-Mahajjat al-Bayda 4:119, Fayd al-Qadir 2: 110 - 120 121 Amali al-Saduq: 223 31


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 32

SUNAN-NABII Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipomuona mmoja wa masahaba zake yoyote anahuzunika angemchangamsha kwa ucheshi na yeye (s.a.w.w.) angesema: “Mwenyezi Mungu hampendi anayewakunjia uso ndugu zake.”122 11. Katika al-Makarim: Kutoka kwa Zayd ibn Thabit ambaye amesema: Wakati tulipokuwa tumekaa naye (s.a.w.w.), kama tulianza kuongea juu ya akhera, alianza kuizungumzia hiyo, na kama tulianza kuzungumzia kuhusu dunia hii, yeye pia alianza kuizungumzia, na kama tulizungumza kuhusu chakula na vinywaji, yeye pia angezungumza kuhusu hilo.123 12. Ndani ya al-Manaqib: Yeye (s.a.w.w.) hakuwa na ‘udanganyifu wa macho’ (yaani, kufanya ishara kwa macho au mkono ili kuashiria makosa ya wengine).124 13. Katika Kashf al-Ghummah: Yeye (s.a.w.w.) alimwambia mmoja wa wake zake: “Je, mimi sikukukataza kuhusu kubakisha kitu kwa ajili ya kesho? Kwani kwa hakika Mwenyezi Mungu huleta riziki ya kila kesho yake.”125 14. Katika Da’aim al-Islam: Kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba yeye alisema: Akhlaq tukufu zaidi ya mitume, wakweli, mashahidi na waadilifu ni kutembeleana kila mmoja wao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.126 15. Katika Majmu’at Warram: Kutoka kwa Jabir ibn Abdillah al-Ansari, kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): Ni kutoka katika maadili ya mitume na wale wakweli kuwa na nyuso changamfu wanapoonana na kupeana mikono wakati wanapokutana.127 16. Ndani ya al-Manaqib: Wakati yeye Mtume (s.a.w.w.) alipokutana na Mwislam, angeanza kwa kumpa mkono wake.128 17. Katika al-Ihya cha al-Ghazali: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa mara kwa mara akisema: “Yeyote kutoka miongoni mwenu asije akanijulisha juu ya jambo lolote (baya) kuhusu yeyote kati ya masahaba zangu, kwani ningependa nije kwenu kwa moyo mweupe, safi.”129 122 Kashf al-Riba: 119, ‘Arba’in Hadith cha Ibn Zahra al-Halabi: 82 123 Makarimul-Akhlaq: 20 124 Manaqib Ali ibn Abi Talib 1:144, Majmaul-Bayan 8: 360 – Suratul-Ahzab. 125 Kashf al-Ghummah 1:10 126 Da’aim al-Islam 2:106 127 Majmu’at Warram: 29 128 Manaqib Ali ibn Abi Talib, 1:147 129 Al-Ihya Ulum al-Din 2: 378 32


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 33

SUNAN-NABII Maelezo: at-Tabarsi ameisimulia hii katika al-Makarim.130 18. Katika Misbah al-Shari’ah: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Sisi, kundi la mitume, walezi na wale wachamungu, tuko huru kutokana na jitihada zisizo za mahali pake”131 19. Vilevile: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Mimi nilitumwa kama kitovu cha upole, chanzo cha elimu na makazi ya subira.”132 20. Ndani ya al-Makarim: Kutoka kwa Abu Dharr ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angeweza kukaa kwa adabu stahiki kati ya masahaba zake na wakati mtu wa nje alipokuja, huyo asingeweza kubaini Mtume alikuwa ni yupi kutoka miongoni mwao mpaka aulizie. Hivyo tulimuomba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuweka nafasi (kwa ajili yake binafsi) ili kwamba watu wa nje waweze kumtambua yeye pale walipokuja. Tulitengeneza kiti kwa ajili yake kutokana na udongo wa mfinyanzi na angekaa juu yake hicho na sisi wote tukakaa pande zote kandoni mwake.133 21. Katika Majmu’at Warram: Ni kutoka katika sunnah, wakati unapozungumza na kikundi cha watu, kwamba wewe humuangalii mtu mmoja tu katika mkusanyiko huo, bali uwaangalie wote kwa zamu.134 22. Vilevile: Yeye (s.a.w.w.) alikuwa akifuma mwenyewe nguo zake na kurekebisha viatu vyake, na kitendo ambacho alikifanya sana ndani ya nyumba yake kilikuwa ni kushona.135 23. Vilevile: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakuwahi kumpiga mtumwa wake – kamwe, na wala (kamwe hakupiga) mtu yoyote mwingine isipokuwa katika njia ya Mwenyezi Mungu. Hakulipiza kisasi kamwe kwa ajili yake mwenyewe isipokuwa pale alipokuwa anapaswa kutekeleza adhabu iliyoagizwa kisheria ambayo imeamriwa na Mwenyezi Mungu.136 24. Katika al-Kafi: Kutoka kwa Husein ibn Abi al-‘Ala kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Hakika Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. hakutuma 130 Makarimul-Akhla: 17 131 Misbah al-Shari’ah: 140, al-Kafi 6: 276, al-Ja’fariyat: 193 132 Misbah al-Shari’ah: 155 133 Makarimul-Akhlaq: 16 134 Majmu’at Warram: 26 135 Ibid: 34 136 Ibid: 278 33


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 34

SUNAN-NABII mtume bali kwamba alizungumza ukweli na alirudisha mali ya watu (ambayo ilikuwa imewekwa amana kwake) kwa wamiliki wake halali, wawe wachamungu au waovu.137 Maelezo: al-Ayyash ameisimulia hii katika Tafsiir yake.138 25. Katika Majmu’at Warram: Kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: “Rudisha kile ambacho kimewekwa chini ya dhamana yako, kwani kwa hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuwa akirudisha hata sindano ya kushonea na uzi wake (kwa mmiliki wake halali).”139 26. Katika al-Makarim: Kutoka kwa Abu Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa amemuahidi mtu mmoja (kwamba angekutana naye) karibu na jiwe moja kubwa naye akasema: “Nitakusubiri hapa mpaka utakapofika.” Kisha jua kali linalochoma likafanya iwe vigumu kwake kulihimili, hivyo masahaba zake wakamwambia: “Oh, ewe Mtume wa Allah! Kwa nini usije kukaa kwenye kivuli?” Yeye akasema: “Nilimuahidi kukutana naye hapa hapa hasa na kama hatakuja atawajibika kwa hili.”140 27. Katika al-Mahasin: Kutoka kwa Jabir, kutoka kwa Abi Ja’far (a.s.) ambaye amesema: Ali (a.s.) alikuwa akisema: “Sisi, Ahlul-Bayt, tumeamriwa kuwalisha wenye shida, kutoa hifadhi wakati wa huzuni na kuswali wakati watu wengine wakiwa wamelala.”141 Maelezo: Hii imesimuliwa vilevile katika al-Kafi.142 28. Katika al-Kafi: Kutoka kwa Ubayd ibn Abi Abdillah al-Baghdad kutoka kwa yule aliyemweleza kuhusu hilo, yeye alisema: Mgeni alikuja kwa Abu al-Hasan arRidha (a.s.) na akaketi pamoja naye, akizungumza naye mpaka sehemu ya usiku ikawa imepita. Halafu (ghafla) taa ikafifia mwanga na yule mtu akanyoosha mkono ili kuitengeneza, lakini Abul-Hasan akamzuia (kufanya hivyo) na akaharakisha kuitengeneza yeye mwenyewe. Kisha akamwambia: “Sisi ni jamii ambayo haipokei huduma kutoka kwa wageni wetu.”143 137.Al-Kafi 2:104, Mishkat al-Anwar: 171, al-Mustadrak 8: 455 138 Tafsiir al-Ayyash 1: 251 – Suratun-Nisa 139 Majmu’at Warram: 10, al-Kafi 2: 636 140 Makarimul-Akhlaq: 24. Katika hadithi nyingine, yeye alingojea hapo kwa muda wa siku tatu. 141 Al-Mahasin: 387 142 Al-Kafi 4: 50 143 Ibid, 6: 283 34


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 35

SUNAN-NABII 29. Katika Amali as-Saduq: Kutoka kwa Huraiz Ibn Abdillah au mtu mwingine mbali na yeye ambaye amesema: Kundi la watu kutoka Jahinah lilikuja kwa Abu Abdillah (a.s.) hivyo akawapokea kama wageni wake, na pale walipotaka kuondoka, yeye aliwapa mahitaji ya chakula na akawasindikiza na kuwapatia kila walichokihitaji. Halafu akawaambia watumishi wake: “Ondokeni muwaache na msiwasaidie (katika kufungasha mahitaji yao),” na walipokuwa wamemaliza kufungasha, walikuja kumuaga. Wao wakasema: Oh, ewe mwana wa Mtume wa Mwenyezi Mungu! Umetukaribisha na kutuweka kwa ukarimu mzuri sana, halafu uliwaagiza watumishi wako wasitusaidie katika kuondoka kwetu?!” Yeye akasema: “Sisi Ahlul-Bayt hatuwasaidii wageni wetu kututoka.”144 30. Katika al-Kafi: Katika riwaya yake kutoka kwa Ali ibn Ja’far, kutoka kwa kaka yake (a.s.): Wakati mgeni alipokuja kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), yeye angekula pamoja naye, na asingeacha kula mpaka mgeni huyo alipoacha kula.145 31. Ndani ya al-Ihya ya Ghazali: Ni katika sunnah kumuona mgeni kwamba anapaswa kusindikizwa mpaka kwenye mlango wa nyumba.146 32. Katika al-Kafi: Katika riwaya yake kutoka kwa ibn Bukayr, kutoka kwa baadhi ya masahaba, ambao wamesema: Abu Abdillah (a.s.) wakati mwingine alikuwa akitupatia sisi ‘al-Furani’ (aina ya mkate wa duara ambao umeokwa kisha ukapakazwa maziwa, siagi iliyosafishwa na sukari) na ‘al-Akhbasah’ (tamtamu iliyotengenezwa kwa tende na siagi iliyosafishwa) ili tule, na halafu mkate na mafuta. Ilisemwa kwake (a.s.): “Ungekuwa tu na wastani katika mambo yako.” Yeye (a.s.) akasema: “Sisi tunayamudu mambo yetu tu kwa amri ya Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla; hivyo kama akituneemesha, tunakuwa wakarimu zaidi, na kama akitufanya masikini, basi tunakuwa wenye kubana matumizi zaidi.”147 33. Katika Majmu’at Warram: Mas’adah amesema: Nilimsikia Aba Abdillah (a.s.) akisema kuwaambia wafuasi wake: “Msimlaumu yule anayekujieni kwa sababu ya upendo na msimuadhibu adhabu kali kwa vitendo vyake viovu kiasi kwamba akawa amedhalilika kwa hayo, kwani hii sio katika Akhlaq ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wala akhlaq ya wale walio karibu naye.”148

144 Amali as-Saduq: 437 145 Al-Kafi 6: 286 146 al-Ihya Ulumud-Din 2:18 147 al-Kafi 6: 280 148 Majmu’at Warram: 383, al-Kafi 7: 150 35


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 36

SUNAN-NABII 34. Ndani ya al-Faqih: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Kama ningekaribishwa (kula) makongoro ya kondoo ningekubali, na kama ningepewa zawadi ya makongoro ya kondoo ningeipokea.”149 Maelezo: Hicho kipande cha pili kimesimuliwa pia katika al-Kafi.150 35. Katika al-Mahasin: Katika riwaya yake kutoka kwa Ma’mar ibn Khallad ambaye amesema: Mmoja wa watumwa wa Imam ar-Ridha (a.s.) ambaye alikuwa akiitwa Sa’d alifariki. Yeye, ar-Ridha (a.s.) akaniambia: “Nipe ushauri juu ya mtu ambaye ana utukufu na ni mwaminifu.” Mimi nikasema: “Unanitaka mimi nikushauri wewe? Yeye akasema kwa ukali kabisa – kana kwamba alikuwa amekasirika: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikukuwa akitaka ushauri kwa sahaba zake, halafu angeweza kuamua kama alivyotaka mwenyewe.”151 36. Ndani ya al-Ihtijaj: Kutoka kwa Abi Muhammad al-Askari (a.s.) ambaye amesema: Nilimuuliza baba yangu, Ali ibn Muhammad (a.s.): Je, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alijadiliana na Wahayudi na wale washirikina pale walipompinga kikaidi na je, alihojiana nao (kwa kutumia hoja na ushahidi)?” Yeye akasema: “Ndiyo, mara nyingi tu.”152 Maelezo: Hili vilevile limesimuliwa katika Tafsiir al-Askari.153 37. Katika Amali as-Saduq: Katika riwaya yake kutoka kwa Muhammad ibn Muslim ndani ya hadithi kutoka kwa al-Sadiq (a.s.) kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): Kitu cha kwanza ambacho nilikatazwa na Mola Wangu ‘Azza wa Jalla. kilikuwa ……. na kubishana na watu.154 38. Katika al-Bihar kutoka kwa Da’awat al-Rawandi: Kutoka kwa AmirulMu’minin (a.s.) ambaye alisema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipoulizwa (kufanya) jambo, kama angetaka kulifanya angesema: “Ndiyo,” na kama alikuwa hataki kulifanya angebakia kimya tu. Asingeweza kusema “Hapana” kwa jambo lolote lile.155

149 al-Faqih 3: 299, Da’aim al-Islam 2: 107 na 325, al-Mustadrak 16: 237 150 al-Kafi 5: 141 151 al-Mahasin: 601 152 al-Ihtijaj 1: 26 153 Tafsiir al-Imam al-Askari (r.a.) 154 Amali al-Saduq: 339 155 Biharul-Anwar 93: 327 36


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 37

SUNAN-NABII 39. Katika al-Makarim: Kutoka kwa Anas ambaye amesema: Tulipokuwa tukija kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) tulikuwa tukikaa kumzunguka yeye katika mduara.156 40. Vilevile: Kutoka kwa Jabir ambaye amesema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipotoka nje, masahaba zake walitembea mbele yake na waliacha mgongoni kwake kwa ajili ya Malaika.157 41. Vilevile: Kutoka kwa Jabir ibn Abdillah katika hadithi ambamo yeye anaelezea adabu yake (s.a.w.w.) katika medani ya vita: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa miongoni mwa watu wa mwisho (kuja kwenye uwanja wa vita). Angemhimiza mpiganaji dhaifu (aliyebakia nyuma) na kumchukua pamoja naye na kumuelekeza lilikokuwa hilo jeshi.158 42. Ndani ya al-Majma’ al-Bayan: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) asingeangalia (kwa kupendezewa) kile kitu ambacho kilifikiriwa kwamba ni kizuri kutoka katika dunia hii.159 43. Vilevile: Wakati kitu chochote kilipomsikitisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) basi angekwenda kuswali.160 44. Vilevile: Yeye Mtume (s.a.w.w.) aliishi pamoja na watu kwa mahusiano yake mazuri lakini alikuwa ametengana nao kwa moyo wake; mwili wake ulikuwa dhahiri pamoja na watu lakini nafsi yake ilikuwa na al-Haq (Allah ‘Azza wa Jalla.).161 45. Katika al-Bihar: Kutoka kwa Abul-Hasan al-Bakri ndani ya kitabu chake alAnwar: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akipenda kukaa faraghani.162 46. Ndani ya Majma’ul-Bayan: Kutoka kwa Umm Salamah ambaye alisema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) imma asingesimama wala kukaa, kuja au kuondoka bali kwamba angesema: “Subhana’llahi wa Bihamdih. Astaghfirullaha wa Atubu ilayh” (Utukufu na sifa kwa Mwenyezi Mungu. Naomba maghfira kutoka kwa Allah na 156 Makarimul-Aklaq: 22 157 Ibid. 158 Makarimul-Akhlaq: 20 159 Majmaul-Bayan 6: 345 – Suratul-Hijr (15) 160 Majmaul-Bayan 6: 347 – Suratul-Hijr (15) 161 Majmaul-Bayan 1: 333 – Suratul-Qalam (68) 162 Biharul-Anwar 41: 16 37


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 38

SUNAN-NABII ninatubia Kwake). Kwa hiyo sisi tukamuuliza kuhusu hili na yeye akasema: “Mimi nimeamrishwa kulifanya hili,” halafu akasoma ‘Idha Ja’a Nasrullahi wal Fat’hu’ (Suratun-Nasr).163 47. Katika al-Bihar, kutoka kwenye Kanz al-Karajiki: Yeye (s.a.w.w.) amesema: Mola Wangu amenitaka mimi nitwae mambo saba: Amenitaka niwe mkweli sirini na dhahirini, kwamba nimsamehe yule anayenikosea mimi, nimpe yule anayeninyima, nirudishe uhusiano na yule anayenitenga mimi, na kwamba kimya changu kiwe kwenye tafakari na kuangalia kwangu kuwe katika kuelewa.164 48. Katika al-Manaqib: Yeye (s.a.w.w.) alikuwa akirekebisha viatu vyake yeye mwenyewe, kutia viraka kwenye nguo zake, kufungua mlango (wa nyumbani kwake kulipokuja mtu), akikamua kondoo jike wake, kumzuia ngamia ili aweze kumkamua na kusaga ngano (kuwa unga) na mtumishi wake alipokuwa amechoka. Angeweka maji yake kwa ajili ya wudhuu mwenyewe (pembeni mwa kitanda chake) wakati wa usiku. Hakuna mtu ambaye angetembea kwa hatua za haraka zaidi kuliko yeye. Yeye asingekaa na kuegemea kwenye kitu chochote. Angeweza kusaidia katika kazi ngumu za nyumbani na alikuwa akikatakata nyama. Alipokuwa akikaa kwa ajili ya kula, angekaa kwa unyenyekevu, na alilamba vidole vyake (baada ya kumaliza kula) na yeye hajawahi kuteuka – kamwe. Angeweza kupokea mwaliko wa mtu huru na ule wa mtumwa hali kadhalika, hata kama ilikuwa ni kwa sehemu ya mbele ya mguu au makongoro (ya kondoo). Angeweza kukubali zawadi yoyote ile. Hata kama ingekuwa ni kiasi kidogo tu cha maziwa, yeye angekinywa; bali alikuwa hakubali kupokea sadaka. Kamwe hakuweza kukodoa macho kuangalia uso wa mtu yoyote. Alikuwa akikasirika kwa ajili ya Mola Wake na sio kwa ajili yake mwenyewe binafsi. Alikuwa akijifunga jiwe tumboni mwake kutokana na njaa. Yeye alikula kile chochote kilichokuwepo na hakukikataa. Hakuwa akivaa nguo mbili (kwa wakati mmoja). Alivaa nguo ya Yemen ya miraba na (wakati mwingine) alivaa nguo ya sufi iliyotiwa matamvua, na wakati mwingine alivaa nguo zisizokuwa laini zilizotengenezwa kwa pamba na katani. Nyingi ya nguo zake zilikuwa nyeupe. Alikuwa akivaa kofia chini ya kilemba chake. Alikuwa akivaa shati lake kutokea upande wa kulia. Alikuwa na nguo maalum kwa ajili ya siku za Ijumaa na alipovaa nguo mpya, angezigawa zile za zamani kwa wenye shida. Alikuwa na joho ambalo lingeweza kukunjwa mara mbili na kulitandaza wakati wowote alipotaka kukaa. Alikuwa aki163 Majmaul-Bayan 10:554 – Suratun-Nasr (110) 164 Biharul-Anwar 77: 170, Tuhfal-Uqul: 36 38


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 39

SUNAN-NABII vaa pete ya fedha kwenye kidole kidogo cha mkono wake wa kulia. Alipenda sana matikiti maji na alichukia harufu mbaya. Alikuwa akiyasafisha meno yake kwa mswaki wakati alipokuwa akichukua wudhuu. Alipokuwa juu ya kipando, angemfanya mtumishi wake au mtu mwingine yoyote kukaa nyuma yake, na alipanda kipando chochote kilichokuwepo, iwe ni farasi, nyumbu au punda. Angeweza kupanda juu ya punda mwenye hatamu bila ya matandiko. Angeweza (wakati mwingine) kutembea miguu mitupu bila viatu, bila ya joho la kujifunika, kilemba au kofia. Alikuwa akishiriki katika shughuli za mazishi na alikuwa akiwatembelea wagonjwa kwenye pembe za mbali kabisa za mji. Angekaa na masikini na kula pamoja nao, na angewalisha kwa mkono wake mwenyewe. Alikuwa akiwaheshimu ambao walikuwa na tabia bora na ya kiadilifu kabisa. Yeye angeweza kufanya urafiki na watu wanaoheshimika na kushughulika nao kwa upendo. Alikuwa akiweka mahusiano ya karibu sana na ndugu zake wa karibu bila ya kuwapa upendeleo usiostahiki juu ya wengine, isipokuwa kama angeamriwa kufanya hivyo na Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. Yeye asingeweza kuwa mkali kwa mtu yoyote yule na angepokea maombi ya msamaha ya yule aliyeuomba toka kwake. Kati ya watu wote, yeye alikuwa akitabasamu zaidi – isipokuwa pale Qur’ani ilipokuwa ikiteremshwa kwake na wakati alipokuwa akiwahimiza au kuwaonya watu. Wakati mwingine angecheka (lakini) bila kuangua kicheko cha sauti kubwa. Asingeweza kula chakula kizuri au kuvaa nguo nzuri kuliko watumishi wake wa kiume au wa kike. Hakumkosea mtu yoyote kwa tusi wala hakumlaani mwanamke yoyote au mtumishi kwa maapizo. Watu hawakumlaumu mtu yoyote bali yeye akasema: “Muacheni huyo mtu.” Hakuja mtu yoyote kwake, imma muungwana ama mtumwa bali yeye angefanya kila jitihada ya kutatua haja yake. Yeye hakuwa mwenye kukosa staha au adabu, wala kuwa na makelele katika eneo la sokoni. Yeye kamwe hakujibu baya kwa ubaya bali angeweza kusamehe na kugeukia mbali. Angekuwa wa kwanza kumsalimia yeyote aliyekutana naye kwa maamkuzi ya ile salaam maalum. Yeye angeweza kuvumilia kwa subira na yoyote aliyekuja na kuelezea haja zake kwake (s.a.w.w.) mpaka mtu huyo alipoondoka. Asingeweza kamwe kuondoa mkono wake kutoka kwa yoyote aliyekuwa ameushika, mpaka mtu huyo alipouachia mkono wake mwenyewe na pale alipokutana na Mwislam angeanza kwa kupeana mikono. Yeye asingeweza kusimama au kukaa isipokuwa kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. Wakati mtu alipokuja kuketi naye yeye akiwa anaswali, basi 39


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 40

SUNAN-NABII angefupisha swala yake na kumgeukia akisema: “Je, unahitaji kitu chochote?” Wakati mwingi angekaa huku akiwa ameiweka miundi ya miguu yake yote wima (akiishikilia kwa mikono yake) Yeye angekaa kwenye nafasi ya kwanza iliyo wazi kwenye mkusanyiko, na zaidi hasa angekaa kuelekea Qibla. Yeye alimheshimu yule mtu aliyekuja kumtembelea, wakati mwingine hata kumtandikia joho lake kwa ajili yake au kumpa ule mto aliokuwa ameukalia yeye. Yeye wakati wote alisema kweli tu – akiwa katika furaha au hasira. Yeye alitumia kula tango pamoja na tende mpya na chumvi. Matunda ambayo aliyapenda sana yalikuwa ni matikiti maji na zabibu, na chakula chake zaidi kilikuwa ni maji na tende kavu. Angeweza wakati mwingine kula tende kavu na maziwa na aliviita hivi ‘virutuishi viwili vizuri.’ Chakula alichokipendelea sana kilikuwa ni nyama na angeweza kula ‘Thariid’ – bakuli la supu na mkale uliolowekwa ndani yake – pamoja na nyama. Vilevile yeye aliyapenda maboga. Yeye angeweza kula nyama ya wale wanyama waliowindwa bali yeye mwenyewe asingewinda. Wakati mwingine alikuwa akila mkate na siagi iliyosafishwa. Kutoka kwenye (nyama ya) kondoo yeye alipenda sana mguu wa mbele na bega. Kutoka kwenye vyakula vilivyopikwa yeye alipenda kitoma/mung’unye. Kutoka kwenye viungo vya kutia ladha yeye alipenda siki. Kutoka kwenye tende yeye alipenda ‘Ajwah’ (aina ya tende inayopandwa Madina) na kutoka kwenye mbogamboga yeye alipenda majani ya miti ya endive, chicory na purslane kama saladi.165 49. as-Sheikh Abu al-Fattuh al-Radhi katika Tafsiir yake: Yeye (s.a.w.w.) alizoea kusema: “Ewe Mungu Wangu! Nifanye mimi niishi kwenye ufukara na nife kwenye ufukara, na uje kunifufua miongoni mwa kundi la watu masikini.166 50. Vilevile: Kutoka kwa Abdillah ibn Abi Awfa ambaye alisema: Iwapo mtu alileta fedha (ili kutolewa) kwa ajili ya sadaka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), yeye angesema: “Ewe Mola! Shusha rehema zako juu ya familia ya fulani bin fulani.167 51. Katika al-Makarim: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipendelea kuwa na matumaini mema na alichukia ubashiri.168 52. Katika al-Ja’fariyat: Katika simulizi yake kutoka kwa Ali (a.s.) ambaye alisema: Kama mtu angezungumza uwongo mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) yeye 165 Manaqib Ali ibn Abi Talib 1: 147 166 al-Nuri ameinukuu hii katika al-Mustadrak 7: 203, Fayd al-Qadir 2: 103 167 al-Nuri ameinukuu hii katika al-Mustadrak 7: 136 168 Makarimul-Akhlaq: 350 40


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 41

SUNAN-NABII angeweza kutabasamu na kusema: “Kwa kweli yeye anazungumza kitu.”169 53. Katika al-Makarim: Kutoka kwa ibn Abbas ambaye amesema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipozungumza jambo au alipoulizwa kuhusu jambo fulani, angelirudia mara tatu ili kuhakikisha kwamba limeeleweka vizuri.170 54. Ali ibn Ibrahim ndani ya Tafsiir yake: Wakati masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walipokuja kwake, wangemwambia: “Kuwa na asubuhi njema na jioni njema pia” – na hizi zilikuwa ni salamu za Zama za Jahilia – hivyo Mwenyezi Mungu akateremsha haya: “…..Na wafikapo kwako wanakuamkia kwa maamkuzi asiyokuamkia nayo Mwenyezi Mungu…..” (al-Mujadilah; 58: 8). Hivyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akawaambia: “Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. Ameyabadilisha haya kwa yaliyo bora zaidi juu yetu: yale maamkuzi ya watu wa Peponi (ambayo ni) ‘As-Salaam Alaykum’”171 Maelezo: Imeelezwa katika sehemu ya tabia yake (s.a.w.w.) kutoka kwa as-Saduq katika Ma’ani al-Akhbar kwamba yeye Mtume (s.a.w.w.) angeharakisha kumsalimia yeyote yule aliyekutana naye.172 55. as-Sheikh Abu al-Fattuh katika Tafsiir yake kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba pale mtu kutoka miongoni mwa Waislam alipomsalimia yeye na kusema: ‘Salaamun Alayka’ yeye angejibu: ‘Wa Alaykas-Salaam wa Rahmatullah.’ Na iwapo alisema: As-Salam Alayka wa Rahmatullah,’ Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alijibu ‘Wa Alaykas-Salam wa Rahmatullah wa Barakatuh.’ Hivi ndivyo alivyokuwa akiongezea kitu zaidi kwenye majibu yake kwa yule aliyemsalimia.173 56. Katika al-Ja’fariyat: Katika simulizi yake kutoka kwa Ali (a.s.) ambaye amesema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipopewa habari njema za kuzaliwa kwa mtoto wa kike yeye alisema: “Hii ni rehma, na Mwenyezi Mungu ndiye Mdhamini wa riziki yake.”174 57. Ibn Abi al-Jamhur katika Durar al-La’ali: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Nimeamrishwa kuchukua sadaka kutoka kwa matajiri miongoni mwenu na kuigawa kwa masikini miongoni mwenu.”175 169 Al-Ja’fariyat: 169 170 Makarimul-Akhaq: 20 171 Tafsiir al-Qummi 2: 355 – Suratul-Mujadilah. 172 Ma’ani al-Akhbar: 81 173 An-Nuri anaisimulia hii katika al-Mustadrak 8: 371 174 Al-Ja’fariyat: 189 175 Hatunayo rejea hii kwa bahati mbaya. 41


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 42

SUNAN-NABII 58. Ndani ya al-Kafi: Katika riwaya yake kutoka kwa Abd al-Karim ibn Utbah alHashimi katika hadithi kutoka Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aligawa na kuisambaza sadaka ya watu wa jangwani kati ya watu masikini wa jangwani na sadaka ya watu wa hapo mjini kati ya watu masikini wa mjini hapo.176 Maelezo: Hii imesimuliwa kwa namna hiyo hiyo hasa na Ahmad ibn Ali ibn Abi Talib ndani ya al-Ihtijaj.177 59. Katika Makarimul-Akhlaq, kikinukuu kutoka kwenye kile kitabu cha alNubuwwah: Kutoka kwa ibn Abbas, kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye amesema: “Mimi nimeelimishwa na Mwenyezi Mungu, na Ali ameelimishwa nami. Mola Wangu ameniamuru kuwa mkarimu na mwadilifu na amenikataza kuwa bahili na ukatili.”178 60. as-Sheikh Abu al-Fattuh katika Tafsiir yake: Kutoka kwa Abu Sa’id al-Kudri katika hadithi kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Pale mtu atakapokuja kutuomba kitu, sisi hatutamficha chochote kile tulichonacho.”179 Maelezo: Hii pia imesimuliwa katika Fiqh al-Ridha.180 61. Katika al-Ja’fariyat: Katika riwaya yake kutoka kwa Ali (a.s.) ambaye amesema: Wakati wowote Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliposahau kitu angeweka kichwa chake katika kiganja cha mkono wake na kusema: “Allahumma laka al-Hamd, Ya Mudhakkir al-Shai wa Fa’ilahu, Dhakarni ma Nasitu” (Ewe Mungu! Himidi zote ni Zako. Ewe Mkumbushaji wa jambo na Mfanyaji wake, nikumbushe mimi hiki nilichokisahau).181 62. Katika al-Amali as-Saduq: Katika riwaya yake kutoka kwa Ghayath ibn Ibrahim, kutoka kwa as-Sadiq Ja’far ibn Muhammad, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa baba zake (amani iwashukie wote) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Allah ‘Azza wa Jalla. hakunipendelea mimi sifa sita nami sikuzipendelea juu ya waandamizi wangu kutoka kwenye kizazi changu na wafuasi wao baada yangu: Kucheza ndani ya Swala (yaani kuichukulia kwa wepesi), 176 Al-Kafi 5: 27 177 Al-Ihtijaj: 364 178 Makarimul-Akhlaq: 17 179 An-Nuri ameinukuu hii katika al-Mustadrak 7: 223 180 Fiqh al-Imam al-Ridha: 365 181 al-Ja’fariyat: 217 42


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 43

SUNAN-NABII kuongea mambo machafu wakati nimefunga, kupenda shukurani baada ya kutoa sadaka, kuja msikitini katika hali ya Janabah, kuchungulia kwenye nyumba za wengine na kucheka katikati ya makaburi.”182 63. Katika Tuhfal-Uqul: Kutoka kwa as-Sadiq (a.s.): Mambo manne ni kutoka kwenye akhlaq za mitume (a.s.): Uadilifu, ukarimu, subira nyakati za matatizo na kusimama imara kwa ajili ya haki za muumini.183 64. Katika Ja’fariyat: Katika riwaya yake kutoka kwa Ali (a.s.): Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alivaa pete yake pamoja na jiwe lake likiangalia kuelekea upande wa ndani wa mkono wake na alikuwa akiiangalia mara kwa mara.184 65. Ndani ya Tafsiir al-‘Ayashi: Kutoka kwa Sama’ah, kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) kutoka kwa baba yake: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akichukia kukata mitende wakati wa usiku na kuchuma mazao yake wakati wa usiku.185 66. Ndani ya al-Mahasin: Katika riwaya yake kutoka kwa Abdilla ibn al-Qasim alJa’fari kutoka kwa baba yake, ambaye amesema: Wakati matunda yalipokuwa yamekomaa, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliagiza kwamba uwazi utengenezwe katika ukuta wa bustani ili wengine nao waweze kunufaika nayo.186 67. Katika Qurb al-Isnad: Kutoka kwa Abi al-Bukhturi kutoka kwa Ja’far kutoka kwa baba yake (a.s.) ambaye amesema: Ali ibn Abi Talib (a.s.) alisema: Watu fulani walikuwa na mazoea ya kuja kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wakiwa hawana chochote katika milki yao, hivyo Ansar wakasema: “Kwa nini tusichangie kikutwa cha tende kutoka katika kila bustani kwa ajili ya watu hawa!” Hivyo hili likageuka kuwa Sunna hadi leo hii.187 68. Katika Awarif al-M’arif: Jibril (a.s.) amesema: Hakuna nyumba yoyote katika ardhi ambayo sijaichunguza, na sikumpata mtu yoyote mwenye shauku kubwa katika utoaji sadaka kutoka kwenye mali yake kuliko Mtume wa Allah ‘Azza wa Jalla. (s.a.w.w.).188 182 Amali al-Saduq: 60, al-Mahasin: 10, at-Tahdhib 4: 195 183 Tuhfal-Uqul: 375 184 Al-Ja’fariyat:185 185 Tafsiir al-‘Ayashi: 379 – Surat al-An’am (6) 186 Al-Mahasin: 528 187 Qurb al-Isnad: 66 188 Awarif al-Ma’arif: 239 43


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 44

SUNAN-NABII 69. Ndani ya al-Ja’fariyat. Katika riwaya yake kutoka kwa Ali ibn al-Husein, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Ali (a.s.) ambaye amesema: Iwapo muombaji angekuja kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), yeye angesema: “Hakuna kisingizio, hakuna kisingizio.”189 70. Ndani ya Awarif al-Ma’arif. Kutoka kwa Jabir ambaye alisema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakuwahi kuombwa kitu kamwe ambacho yeye alijibu: “Hapana.” Ibn Utaybah akasema: Kama alikuwa hanacho basi angeahidi kukipata.190 71. Vilevile: Kama yeye (s.a.w.w.) alitaka kutuma kikosi maalum (cha kijeshi), basi angekituma mapema kabisa wakati wa asubuhi.191 72. Katika al-Kafi. Katika riwaya yake kutoka kwa al-Sakuni, kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.): Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipotuma kikosi maalum cha jeshi, yeye angewaombea hao kupata mafanikio.192 73. Katika Qurb al-Isnad. Kutoka kwa al-Rayyan ibn al-Salt ambaye alisema: Nilimsikia Imam ar-Ridha (a.s.) akisema: Pale Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipotuma jeshi angechagua kamanda wake, halafu angemtuma pamoja naye mmoja wa masahaba wake waaminifu kumwangalia na kumchunga na kumrudishia yeye taarifa.193 74. Ndani ya al-Kafi. Katika riwaya yake kutoka kwa Mas’adah ibn Sadaqah, kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipotaka kutuma kikosi, angemuagiza kamanda kiongozi wake kumwogopa Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. kuhusu yeye mwenyewe binafsi na halafu kuhusu wafuasi wake. Kisha angesema: “Anzeni kwa jina la Allah ‘Azza wa Jalla. na muwapige makafiri katika njia ya Allah ‘Azza wa Jalla. Msiwe wasaliti na msifanye udanganyifu. Msiikatekate miili ya wafu na msimuue mtoto yoyote au mtu yeyote aliyejitenga mwenyewe katika milima. Msichome mtende wowote na wala msiifunike kwa mafuriko ya maji. Msikate mti wowote wenye kuzaa matunda, na msiyachome mazao kwa sababu hamuwezi kujua – mnaweza mkayahitaji baadae. Msikate ukano wa mnyama yoyote, ambaye nyama yake ni halali kuliwa isipokuwa kwa yule ambaye mtamhitaji kwa ajili ya chakula. Mnapokutana na maadui wa 189 Al-Ja’fariyat: 57 190 Awarif al-Ma’arif: 239 1911 Ibid: 126 192 Al-Kafi 29:5 193 Qurb al-Isnad: 148 44


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 45

SUNAN-NABII Uislam walinganieni kukubali moja ya mambo matatu ya kuchagua (kukubali Uislam, kukubali kulipa kodi ya Jizya au kurudi nyuma), na iwapo watalikubali hili basi liridhieni hilo kutoka kwao na muwaache.”194 Maelezo: Hili limesimuliwa pia katika at-Tahdhib, al-Mahasin na al-Da’aim.195 75. Katika al-Ja’fariyat. Katika riwaya yake kutoka kwa Ali ibn Abi Talib (a.s.): Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokutana uso kwa uso na maadui katika vita, yeye angewahamasisha wale askari wa miguu, wale waliokuwa kwenye migongo ya farasi, na wale waliopanda ngamia, halafu angesema: “Ewe Mungu! Wewe ndiye Mlinzi na Msaidizi na Mlezi wangu. Ewe Mola! Kwa matakwa Yako mimi ninashambulia na kwa ridhaa Yako mimi ninapigana.”196 Maelezo: Hiyo sehemu ya kwanza imesimuliwa vile vile katika al-Da’aim. 76. Katika al-Majma’. Qatadah amesema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliposhuhudia mapambano ya vita alisema: “Ewe Mola! Amua kwa haki.”197 77. Katika Nahjul-Balaghah. Katika barua yake Imam (a.s.) kwa Mu’awiyah: …..Pale mapigano yalipogeuka kuwa makali na watu wakaanza kukimbia, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angewatuma watu wa familia yake kwenye mstari wa mbele na kupitia kwa wao, masahaba wangeweza kulindwa kutoka na mashambulizi ya panga na mikuki.198 78. Katika al-Manaqib. Katika hadith ya kiapo cha utii cha Ma’mun, kutoka kwa arRidha (a.s.): “Hivi ndivyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alivyochukua kiapo cha utii kutoka kwa watu,” halafu yeye (a.s.) akapokea kiapo chao kwa kuweka mkono wake juu ya mikono yao.199 79. Katika al-Ja’fariyat. Katika riwaya yake kutoka kwa Ali (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) asingegusa mikono ya wanawake, hivyo pale alipotaka kuchukua kiapo chao, yeye alileta bakuli la maji kisha akatumbukiza mikono yake ndani yake halafu akaitoa. Kisha yeye akasema: “Tumbukizeni mikono yenu ndani yake halafu mtakuwa mmetoa kiapo chenu cha utii.”200 194 Al-Kafi 5:29 195 Tahdhib al-Ahkam 6: 138, al-Mahasin: 355, Da’aim al-Islam 1: 369 196 Al-Ja’fariyat: 217 197 Majma’ul-Bayan 7: 68 – Surat al-Anbiya’ (21) 198 Nahjul-Balaghah: 368 199 Manaqib Ali ibn Abi Talib 4:364 200 Al-Ja’fariyat: 80 45


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 46

SUNAN-NABII Maelezo: Ibn Sha’bah vilevile ameisimulia hii katika kitabu chake Tuhf al‘Uqul.201 80. Katika al-Da’aim. Kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba kutoka miongoni mwa masharti atakayoweka wakati anapochukua kiapo cha utii kutoka kwa wanawake lilikuwa kwamba wasingeongea na wanaume isipokuwa kwa wale ambao walikuwa ni Maharim kwao.202 81. Katika Jami’ al-Akhbar. Kutoka kwa ibn Abbas ambaye amesema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipomuona mtu ambaye alimvutia, yeye alisema: “Je, huyu anao ujuzi (ambao anapatia maisha yake)?” Kama walisema: “Hapana” yeye (s.a.w.w.) angesema: “Ameanguka kwenye macho yangu.” Mtu mmoja akauliza: “Hilo liko vipi, ewe Mtume wa Allah?” Yeye akajibu: “Kwa sababu kama mu’min hana ujuzi anatumia dini yake (kupata mahitaji yake ya maisha).203 82. Katika Da’aim al-Islam. Kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye alisema: Kutoa mikopo na kukirimu wageni ni katika Sunnah.204 83. Katika Maj’maul-Bahrain: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipopata dirham (sarafu za fedha) mbovu kwenye mkopo, yeye alilipa kwa dirham nzuri.205 84. Katika Tafsiir al-Ayyashi: Kutoka kwa Abi Jamilah, kutoka kwa baadhi ya wafuasi wake, kutoka kwa mmoja wale Ma’asum wawili (a.s.) ambao wamesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Allah ‘Azza wa Jalla. Amenidhihirishia mimi kwamba ninapaswa nipende (watu) wanne Ali, Abu Dharr, Salman na Miqdad.”206 Maelezo: at-Tabari amelisimulia hili katika kitabu cha al-Imamah.207 85. Ndani ya kitabu chake Ja’far ibn Muhammad ibn Shuraih al-Hadhrami: Kutoka kwa Jabir ambaye amesema: Abu Ja’far (a.s.) amesema: Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: Jibril alinijia na akasema: “Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. Anakuamuru kumpenda Ali na kuwaagiza wengine kumpenda na kufanya urafiki naye.”208 201 Tuhf al-‘Uqul: 457 202 Da’aim al-Islam 2: 214 203 Jami’ al-Akhbar: 390, al-Mustadrak 13:11 204 Da’aim al-Islam 2: 489, al-Mustadrak 13: 395 205 Maj’ma-ul-Bahrain 5: 439 206 Tafsiir al-Ayyashi,1: 328 – Suratul-Maidah (5) 207 Hatukuikuta hii humo, na tuliikuta ndani ya al-Ikhtisas 9-13 208 Al-Usul al-Sittata ‘Ashar: 62 46


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 47

SUNAN-NABII 86. Vilevile: Kutoka kwa Abdillah ibn Talha al-Nahdi kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.): Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Mola Wangu ameniamuru kutwaa sifa saba: Mapenzi kwa masikini na ukaribu kwao; kwamba niwe ninasema ‘La Hawla wa La Quwwata illa Billah’ mara kwa mara; kwamba nidumishe uhusiano na ndugu zangu wa karibu hata kama wakinitenga; kwamba niwaangalie wale walioko chini yangu na sio kuwaangalia wale walioko juu yangu; kwamba katika njia ya Allah, nisiathiriwe na lawama za mwenye kulaumu; kwamba niseme kweli hata kama ni chungu na kwamba nisimuombe mtu yoyote kitu chochote.”209 87. Katika Awarif al-Ma’arif: Kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w): Kama unao uwezo wa kuanza siku mpya na kuimaliza bila ya kuwa na chuki moyoni mwako juu ya mtu yoyote basi fanya hivyo. Hii ni miongoni mwa Sunnah, na yeyote mwenye kuhuisha Sunnah yangu atakuwa amenihuisha mimi, na yule anayenihuisha mimi atakuwa nami huko peponi.210 88. Wakati jamii ya watu ilipokuja kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) pamoja na sadaka zao yeye alisema: “Ewe Mungu Wangu! Shusha neema Zako juu ya familia ya fulani bin fulani.”211 89. al-Hasan (a.s.) amesema: “Wakati wowote wale As’hab al-Ukhdud (wachimba shimo) walipotajwa mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), yeye angeomba hifadhi kwa Mwenyezi Mungu kutokana na ile adhabu kali.”212 90. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwatokea watu nje pamoja na Amirul-Mu’minin (a.s.) kwa ajili ya Swala na vilevile katika ile siku ambayo aliwaonya jamaa zake (ili kutangaza kwamba yeye alikuwa ndio mwandamizi - mrithi - wake).213 91.Wakati Halima (yule mama mnyonyeshaji wa Mtume) alipokuja kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), yeye nabii alimheshimu sana na baada ya Hijrah, Mtume wa Allah ‘Azza wa Jalla. (s.a.w.w.) alikuwa akimpelekea nguo kama zawadi mpaka alipofariki baada ya vita vya Khaibar.”214 92. Yeye (s.a.w.w.) amesema: “Hapakuwa na nabii yeyote yule isipokuwa kwamba alikuwa amechunga kondoo.” Mtu mmoja akasema: “Pamoja na wewe, ewe Mtume wa Allah?” Yeye (s.a.w.w.) akasema: “Ndiyo. Pamoja na mimi.”215 209 Ibid, 75 210 Awarif al-Ma’arif: 47 211 ad-Durrul-Manthur 3: 275 – Surat-Tawbah (9) 212 Biharul-Anwar 14: 443 213 Al-Sirah al-Nabawiyyah cha ibn Hashim 1: 229 214 Biharul-Anwar 15: 384 215 Ibid, 64: 117 47


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 48

SUNAN-NABII 93. Abu Dawud amesimulia: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na kondoo mia moja na hakutaka kuwa na zaidi. Wakati wowote mwanakondoo alipozaliwa, yeye angechinja kondoo mahali pake.216 94. Katika al-Bihar: Kutoka kwa as-Sadiq (a.s.) ambaye amesema: “Sisi ni jamii ambayo tunamuomba Mwenyezi Mungu kwa ajili ya yale tunayoyapendelea juu ya tunaowapenda, hivyo Yeye hutupatia sisi hayo. Kama Yeye anapenda kile ambacho sisi hatukipendi kwa ajili ya wale tunaowapenda, sisi tunakifurahia.217 95. Kutoka ndani ya al-Kafi. Katika simulizi yake kutoka kwa Ma’mar ibn Khallad, kutoka kwa ar-Ridha (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akianza siku kwa kuwauliza masahaba zake: “Je, kuna habari njema zozote?” Na kwa hili alikuwa akimaanisha ndoto.218 96. Katika Mustatraf: Wakati habari za mtu zilipomfikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) yeye hakusema: “Fulani ibn fulani ana hali gani?” bali angesema: “Watu huko wana hali gani?” Wao wanasema hivi …..” ili kwamba asije akahuzunika mtu yoyote.219 97. Ndani ya Kashkul cha as-Sheikh al-Baha’i kutoka kwenye al-Ihya ndani ya Kitab al-’Uzla: Bwana wa Mitume (s.a.w.w.) alikuwa akitumia kununua kitu na kukibeba yeye mwenyewe hivyo masahaba zake wangemwambia: “Nipe mimi mzigo huu niubebe, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu!” na yeye angesema: “Mwenye mzigo wa bidhaa hizi anao wajibu zaidi wa kuubeba.220 98. Katika al-Majma’: Kutoka kwa Muqatil: Wakati Sura ya an-Nasr ilipoteremshwa, yeye (s.a.w.w.) aliwasomea masahaba zake na wao walifurahi na kushangilia, lakini pale al-Abbas alipoisikia, yeye alilia, hivyo yeye (s.a.w.w.) akauliza: “Ni nini kimekufanya mpaka ukalia, ewe ammi yangu?” Yeye akasema: “Nadhani umetangaza kifo chako mwenyewe, Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu!” Yeye Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Ni kama unavyosema.” Na aliishi kwa muda wa miaka miwili baada ya hili na hakuonekana akicheka au kufurahia hata mara moja.221 99. Katika al-Mizan: Imesimuliwa na madhehebu zote kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akibashiri kwa uhakika na angeweza kuwaagiza na wengine 216 Ibid, 64: 116 217 Ibid, 82:133 218 al-Kafi 8: 90 219 Al-Mustatrat 1: 116 220 Al-Kashkul li as-Sheikh al-Baha’i, 2: 308 221 Maj’ma’ul-Bayan 10: 554 – Suratun-Nasr (110) 48


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 49

SUNAN-NABII kufanya vivyo hivyo. Alikuwa akikataza utabiri (ramli) na akawaagiza watu kuachana nao na kuweka imani zao juu Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla.222 100. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kamwe hakuwahi kutabiri (kupiga ramli), na alikuwa akibashiri kwa uhakika. Alipokuwa ameondoka kwenda Madina, Maquraishi waliweka zawadi ya ngamia mia moja kwa mtu atakayeweza kumkamata na kumrudisha kwao. Hivyo Buraydah alitoka na watu sabini kati ya wafuasi wake kutoka Bani Sahm na wakakutana na Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na Mtukufu Mtume akamuuliza: “Wewe ni nani?” Yeye akasema: “Mimi ni Buraydah,” hivyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamgeukia Abu Bakr na akasema: “0h, Abu Bakr! Jambo letu limekuwa jepesi na zuri zaidi.” Halafu yeye (s.a.w.w.) akasema: “Wewe umetokea kwenye kabila gani?” Yeye akajibu: “Kutoka Aslam.” Yeye (s.a.w.w.): “Tuna usalama (amani).” Yeye (s.a.w.w.) kisha akamuuliza: “Umetoka kwenye ukoo gani wewe?” Yeye akasema: “Kutoka Bani Sahm.” Yeye (s.a.w.w.) akasema: “Ujaaliwe kupata fungu lako (sehemu) zuri.” Kisha Buraydah akamuuliza Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) “Kwani wewe ni nani?” Yeye akajibu: “Mimi ni Muhammad ibn Abdillah, Mtume wa Mwenyezi Mungu.” Buraydah akasema: “Nashuhudia kwamba hapana mungu ila Allah ‘Azza wa Jalla, na ninashuhudia kwamba Muhammad ni mja na mjumbe Wake.” Buraydah na wale wote aliokuwa nao wakawa Waislam. Siku iliyofuata (wakati walipokuwa wanakaribia Madina), Buraydah alimwambia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Usiingie Madina isipokuwa uwe pamoja na bendera …..”223 101. Ndani ya al-Maj’ma’: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akichukia kwamba pawepo na harufu mbaya inayotoka mwilini mwake kwa sababu Malaika walikuwa wakimtembelea kila mara.224 102. Kutoka ndani ya Ikmal al-Din: Katika riwaya yake kutoka kwa al-Sayrafi katika hadithi yake ndefu kutoka kwa as-Sadiq (a.s.) ….. (kuhusiana na aya ya):

“Akasema mimi nataka nikuoze mmojawapo katika binti zangu hawa kwa kunitumikia miaka minane, na kama ukitimiza kumi ni hiari yako, lakini mimi sitaki kukutaabisha, itanikuta Insha’allah miongoni mwa watu wema.” (alQasas; 28:27) 222 Tafsir al-Mizan; 6: 119 – Suratal-Ma’idah (5) 223 Biharul-Anwar 19: 40 224 Maj’ma’ul-Bayan 10: 313 – Suratut-Tahrim (66) 49


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 50

SUNAN-NABII imesimuliwa kwamba yeye alitimiza ule ukamilifu zaidi wa vipindi vyote viwili (yaani, miaka kumi) kwa sababu hao mitume (amani juu yao wote) hawafanyi tendo bali kwamba wao hulitekeleza kwa ubora na ukamilifu zaidi.225 103. Katika al-Kafi: Katika riwaya yake kutoka kwa Aban, kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) katika hadithi juu ya masharti ya kiapo cha utii kwa wanawake, yeye Mtume (s.a.w.w.) aliwaambia: “Msijipige kwenye mashavu yenu na msijikwaruze nyuso zenu. Msing’oe nywele zenu na wala msichane sehemu za mbele za mavazi yenu. Msizitie weusi nguo zenu na wala msilie kwa kupiga mayowe (katika nyakati za maafa) …..”226 104. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angejadiliana na Wayahudi na washirikina iwapo wangemshutumu na angewabainishia ukweli.227 105. Ndani ya al-Kafi. Katika hadithi yake kutoka kwa al-Rayyan ibn al-Salt ambaye amesema: Nilimsikia ar-Ridha (a.s.) akisema: Mwenyezi Mungu hakumtuma Mtume yeyote bali pamoja na ukatazaji wa mvinyo na uthibitisho wa (imani katika) al-Bada’228 kuhusiana na Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla.229 106. Ndani ya al-Kafi. Katika riwaya yake kutoka kwa Ma’mar ibn Khallad ambaye amesema: Nilimuuliza Abul-Hasan ar-Ridha (a.s): “Je, ninaweza kuwaombea wazazi wangu ikiwa tu wanajua (na kuifuata) haki?” Yeye (a.s.) akasema: “Omba dua kwa ajili yao na uwe mpole kwao, na kama wako hai na hawaifuati haki, basi waelekeze kwenye haki hiyo. Kwani Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. amenituma mimi pamoja na huruma sio na ukaidi (wa mtoto kwa wazazi wake).230

225 Kamal al-Din wa Tamam al-Ni’mah, 1: 151 226 al-Kafi 5: 527 227 Bihar al-Anwar 9:269 ikunukuu kutoka kwenye Tafsir al-Imam al-Askari (a.s.) 228 Kwamba Allah ‘Azza wa Jalla, anaweza kubadili matokeo yaliyoamuliwa kabla kwa mengine mapya (Tr.) 229 al-Kafi 1:148 230 Ibid, 2:159 50


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 51

SUNAN-NABII

MLANGO WA 3 USAFI NA KANUNI ZA KUJIPAMBA 1. Katika al-Makarim: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa akiosha kichwa chake na ndevu, huwa angeziosha kwa ‘Sidr’ (mkunazi au yungiyungi – Lotus jujube)231 2. Katika al-Ja’fariyat. Katika riwaya yake kutoka kwa Ja’far ibn Muhammad, kutoka kwa baba zake, kutoka kwa Ali (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akichana nywele zake na zaidi hasa akizichana na maji akisema: “Maji yanatosha kuwa manukato kwa muumin.”232 3. Kutoka kwa al-Saduq ndani ya al-Khisal: Imesimuliwa kutoka kwa Abdu Rahman ibn al-Hajjaj kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) katika (maelezo yake kuhusu) maneno ya Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. ‘Enyi wanadamu (Waislam), chukueni pambo lenu kila mahali wakati wa ibada…..,’233 amesema: “Ni kuchana nywele, kwani kuchana nywele kunaleta riziki, kunaboresha nywele zenyewe, kunatimiza haja, kunaongeza urijali na kunazuia kohozi. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitumia kuchana chini ya ndevu zake mara arobaini na kutokea juu yake mara saba na amesema: Inaongeza akili na kuzuia kohozi.”234 Maelezo: Hili limesimuliwa na al-Fattal ndani ya al-Rawdha kwa sanad isiyokamilika.235 4. Ndani ya al-Kafi. Imesimuliwa kutoka kwa al-Sakuni kutoka wa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Ni Sunnah kupunguza mashurubu mpaka juu ya ukingo wa mdomo wa juu.236

231 Makarimul-Akhlaq: 32 232 Al-Ja’fariyat: 156 233 Surat al-A’araf; 7:31 234 Al-Khisal 268, Makarimul-Akhlaq: 70 235 Rawdhat al-Wa’idhin: 308 236 Al-Kafi 6: 487, Tuhf al-’Uqul: 100, Makarimul-Akhlaq: 67, al-Khisal: Hadith Mia Nne

51


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 52

SUNAN-NABII 5. Ndani ya al-Faqih. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Majusi wanakata ndevu zao na kuachia sharubu zao kuwa ndefu zaidi, ambapo sisi tunakata sharubu zetu na kuachia ndevu zetu zikue.237 6. Vilevile. Imesimuliwa hivi: Kuzika nywele, kucha na damu ni kutoka kwenye Sunnah.238 7. Katika al-Kafi. Imesimuliwa kutoka kwa Ibn Uqbah kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: “Kupunguza kucha ni kutoka kwenye Sunnah.239 8. Katika al-Faqih. Katika hadith yake kutoka kwa Muhammad ibn Muslim ambaye alimuuliza Aba Ja’far (a.s.) kuhusu kule kutia nywele hina, hivyo yeye (a.s.) akasema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla., (s.a.w.w.) alikuwa akizitia rangi nywele zake, hapa kuna baadhi ya nywele zake (zilizotiwa hina) ambazo tunazo kwenye milki yetu.240 9. Vilevile. Yeye alisema: Mtukufu Mtume na Husein ibn Ali na Abu Ja’far Muhammad ibn Ali (a.s.) walitumia kutia nywele zao rangi kwa ‘Katm’ (aina ya rangi inayotengenezwa kutokana na mmea maalum) na Ali ibn al-Husein alitumia kupaka nywele zake hina na Katm.241 10. Ndani ya al-Makarim. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angenyoa nywele kutoka mwilini mwake. Mtu angefanya hivyo mpaka kwenye mzingo wa kiuno chake naye angemalizia mwenyewe sehemu iliyobakia.242 11. Katika al-Kafi. Kutoka kwa Hudhaifah ibn Mansur ambaye amesema: Nilimsika Abu Addillah (a.s.) akimesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akiondoa nywele za mbeleni na zile za kwenye sehemu za siri katika kila siku ya Ijumaa.243 12. Kutoka kwa al-Fattal ndani ya kitabu Rawdhat al-Wa’idhin: Abu Abdillah (a.s.) amesema: Iliyo Sunnah kuhusu matumizi ya kunyoa ni kutumia kila baada ya siku kumi na tano (kwa sababu ya kutokuwa na pesa) unapaswa kuchukua mkono, 237 al-Faqih 1:130, Makarimul-Akhlaq: 67 238 al-Faqih, 1: 128 239 al-Kafi: 490 240 al-Faqih, 1:122, Makarimul-Akhlaq: 84 241 al-Faqih, 1:122, Makarimul-Akhlaq: 80 242 Makarimul-Akhlaq: 35 243 al-Kafi: 6: 507 52


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 53

SUNAN-NABII ambao kwao Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. atakuwa ndiye Mdhamini, na kisha unyoe. Yule atakayepitisha siku arobaini bila ya kunyoa (zile nywele za ziada mwilini) yeye sio muumini wala sio kafiri, na hakuna heshima katika hili.244 13. Katika al-Faqih. Ali (a.s.) amesema: Uondoaji wa nywele kutoka kwenye makwapa unaondoa harufu mbaya na ni wa kiafya. Ni Sunnah ambayo yule mbora wa daraja (s.a.w.w.) ameagiza (wafuasi wake kuifanya).245 14. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Salim al-Fazari kutoka kwa mtu mmoja, kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akitumia kuhl - wanja pamoja na collyrium – aina nyingine za wanja – (kwenye macho yake yote) wakati alipopanda kitandani, moja baada ya jingine.246 15. Vilevile: Imesimuliwa kutoka kwa Zurarah kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akipaka Kuhl - wanja kwenye macho yake kabla ya hajakwenda kulala, mara nne katika jicho lake la kulia na mara tatu katika la kushoto.247 16. Ndani ya al-Makarim: Yeye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akipaka kuhl katika jicho lake la kulia mara tatu na katika la kushoto mara mbili ….. na alikuwa na chombo cha kuhifadhia kuhl ambacho alikuwa akikitumia wakati wa usiku. Hiyo kuhl aliyokuwa akitumia ilitengenezwa kutokana na wanja.248 17. Kutoka kwa al-Husayn ibn Bastam ndani ya Tibb al-A’immah: Imesimuliwa kutoka kwa Abdillah ibn Maimun kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na chombo cha kuhl ambacho yeye alichukua kuhl - wanja kutoka humo kila usiku na kuipaka kwenye mara tatu kwenye macho yake yote kabla ya kulala.249 Maelezo: Tofauti katika idadi ya upakaji (wa wanja) inadokeza kwenye tofauti ya kitendo chake (s.a.w.w.) katika nyakati tofauti. Lililo Sunnah hasa ni kile kitendo cha kupaka wanja kabla ya kwenda kulala bila ya kukifanya kwa idadi maalum upakaji.250 244 Rawdhat al-Wa’idhin: 308, al-Kafi 6: 506, al-Faqih 1:119 245 Al-Faqih, 1: 120; al-Khisal: Hadith Mia Nne, Makarimul-Akhlaq: 60 246 Al-Kafi 6: 493; Makarimul-Akhlaq, 46: 47 247 Al-Kafi 6: 493 248 Makarimul-Akhlaq: 34. 249 Tibb al-A’immah: 83 250 Biharul-Anwar, 76:95 53


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 54

SUNAN-NABII 18. Katika al-Faqih. as-Sadiq (a.s.) amesema: Manne (matendo) yanatokana na akhlaq ya mitume (a.s.): Kutumia manukato, kupunguza nywele (za kichwa) kwa wembe, kuondoa nywele zote za mwili kwa kinyoleo na kuwa mwandani na mke wake mtu mara nyingi.251 Maelezo: Kuna hadithi nyingi mno kama hizo. Nyingine tumekwisha zitaja na nyingine tutazitaja katika milango inayofuata. 19. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Abdillah ibn Sinan kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na chombo cha Miski na wakati alipochukua wudhuu angeweza kuichukua miski kwa mikono yake yenye unyevunyevu. Wakati alipotoka nje, kila mmoja alitambua kwamba ni Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kwa sababu ya manukato yake.252 20. Katika al-Makarim: Yeye (s.a.w.w.) asingepewa manukato yoyote bali angeyapokea na akatumia kiasi juu yake mwenyewe na angesema: “Yana harufu nzuri ambayo ni rahisi juu ya mvaaji.” Kama hakupenda kuyatumia, angeweka tu ncha ya kidole chake katika manukato hayo na kuyachukua kwa kiasi kidogo tu.253 21. Vilevile: Yeye (s.a.w.w.) angechoma ubani wa ‘Ud al-Qamari’ (aina maalum ya ubani).254 22. Ndani ya Dhakhirat al-Ma’ad: Miski ilikuwa ndiyo manukato ambayo yeye (s.a.w.w.) aliyapenda zaidi sana.255 23. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Ishaq al-Tawil al-Attar kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akitumia zaidi fedha kwenye manukato kuliko ambavyo angetumia kwenye chakula.256 24. Vilevile: Imesimuliwa kutoka kwa Abi Basir, kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Kuweka manukato katika sharubu ni katika Sunnah ya mitume (a.s.) na ni (njia ya kuonyesha) heshima kwa wale Malaika wawili ambao wanaandika kumbukumbu ya matendo yako.257 251 Al-Faqih, 1: 131, Makarimul-Akhlaq: 63; Tuhf al-Uqul: 442 252 Al-Kafi, 6: 515; Makarimul-Akhlaq: 42 253 Makarimul-Akhlaq:34 254 Ibid. 255 Hatukuiona hii katika Dhakhirat al-Ma’ad, hata hivyo al-Kulayni ameisimulia hii katika al-Kafi 6:515 256 Al-Kafi, 6: 512; al-Makarimul-Akhlaq: 43

257 Al-Kafi, 6: 510; al-Makarimul-Akhlaq: 42 54


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 55

SUNAN-NABII 25. Vilevile: Imesimuliwa kutoka kwa al-Sakan al-Khazzaz ambaye alisema: Nilimsikia Abu Abdillah (a.s.) akisema: “Ni lazima kwa kila muumini kukata kucha zake, kupunguza sharubu zake na kuweka manukato kila Ijumaa. Ilipokuwa ni Ijumaa, na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akawa hakuwa na manukato, yeye angeweza kuomba kiasi kidogo kutoka kwa wake zake, cha mafuta yenye marashi, ambayo aliyachanganya na maji na kuyapaka usoni mwake.”258 26. Katika al-Faqih: Ilipokuwa ni Ijumaa, kama Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakuwa na manukato yoyote, angeweza kuomba nguo ambayo imetiwa rangi ya zafarani na angeinyunyiza maji na kisha akafuta mikono yake juu yake na kupangusa uso wake kwayo.259 27. Ndani ya al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Ishaq ibn Ammar kutoka kwa Abi Abdillah (a.a.) ambaye amesema: Wakati manukato yalipoletwa kwa ajili ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika siku ya Idd al-Fitr, yeye angeanza kwa kugawa baadhi yake kwa wake zake (kabla hajayatumia yeye mwenyewe binafsi).260 28. Vilevile: Imesimuliwa kutoka kwa Isa ibn Abdillah, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake, kutoka kwa Ali (a.s.) ambaye alisema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) asingeweza kamwe kuyakataa manukato na tamutamu.261 29. Kutoka kwa al-Ghazali ndani ya al-Ihya, katika kukumbuka kwake ile akhlaq ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): Yeye alipenda sana manukato na alichukia harufu mbaya mbaya.262 Maelezo: Kutokana na idadi kubwa ya riwaya hizo inaweza kuonekana kwamba yeye Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akitumia jamii ya aina mbalimbali tofauti za manukato. 30. Katika al-Makarim: Yeye alisema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akipaka mafuta kwenye nywele zake na alichukia nywele chafu na zilizo timtim. Yeye angeweza kusema: “Kutumia kupaka mafuta kunaondoa wasiwasi.263

258 Al-Kafi, 6:511 259 Al-Faqih, 1: 465 260 Al-Kafi, 4:170 261 Ibid, 6:513 262 Al-Ihya Ulum al-Din, 2: 358 263 al-Makarimul-Akhlaq: 34

55


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 56

SUNAN-NABII 31. Pia: Yeye angetumia aina tofauti za mafuta, na angeweza kuanza kwa kupaka mafuta kichwani mwake kabla ya ndevu zake, akisema: “Kichwa kabla ya ndevu.”264 32. Vilevile: Angeweka nywele zake mafuta ya urujuani na angesema: “Ndio mafuta yaliyo mazuri zaidi katika mafuta yote.”265 33. Vilevile: Wakati alipopakaza mafuta, angeanza na nyusi, halafu sharubu zake, kisha angeweka kiasi kidogo kwenye pua yake na kuyanusa, halafu angeyapakaza mafuta hayo kwenye kichwa chake.266 34. Vilevile: Angeweza kupaka mafuta kwenye nyusi zake ili kupata ahuweni kutokana na maumivu ya kichwa. Alipaka mafuta tofauti katika sharubu zake mbali na yale aliyotumia kwenye ndevu zake.267

NYONGEZA KWA SEHEMU HII 1. Katika Tuhf al-Uqul: Kutoka kwa ar-Ridha (a.s.): Afya njema ni katika akhlaq ya manabii (a.s).268 2. Katika al-Faqih. As-Sadiq (a.s.) amesema: (Matendo) Manne yanatokana na Sunnah ya mitume (a.s.): Kutumia manukato, kupiga meno mswaki, kuwa karibu na wanawake na kutumia hinna.269 3. Katika al-Da’aim: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angetumia sana manukato kiasi kwamba yangeweza kubadilisha rangi ya ndevu na nywele zake kuwa na rangi ya kimanjano.270 Maelezo: Kuna hadithi kama hiyo ndani ya Qurb al-Isnad.271 4. Katika al-Makarim: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akichana nywele zake kwa ‘Midra’ (aina ya kitana) ….. na angeweza wakati mwingine kuchana ndevu 264 Ibid. 265 Ibid. 266 Ibid. 267 Ibid. 268 Tuhf al-Uqul: 442 269 Al-Faqih, 1: 52, al-Makarimul-Akhlaq: 49, al-Ja’fariyat: 16, Da’am al-Islam 1:119, Lubb al-Lubb 2: 521 270 Da’aim al-Islam 2:166

271 Qurb al-Isnad, 70 56


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 57

SUNAN-NABII zake mara mbili katika siku moja. Alikuwa akikiweka kitana hicho chini ya mto wake baada ya kumaliza kuchana nywele zake nacho.272 5. Ndani ya al-Kafi: Katika riwaya yake kutoka kwa Amr ibn Thabit kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.): Nilisema kumwambia yeye (a.s.): “Wanasimulia kwamba kupanga, au kupiga wei nywele ni kutoka kwenye Sunnah.” Yeye akasema: “Kutoka kwenye Sunnah?” Mimi nikasema: “Wanadai kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipiga wei nywele zake.” Yeye (a.s.) akasema: “Mtukufu Mtume hakupiga wei nywele zake na Mitume (a.s.) kamwe hawakuweka nywele zao katika mtindo huo.”273 Maelezo: Hadithi hii imesimuliwa pia katika al-Makarim.274 6. Vilevile: Kutoka kwa Ayyub ibn Harun: Nilimuuliza Abi Abdillah (a.s.): “Je, Mtukufu Mtume (s.a.ew.w.) alipiga wei nywele zake?” Yeye akasema: “Hapana, kwa sababu kama nywele za Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) zilikuwa ndefu, zingefikia kwenye ndewe za masikio (na asingeziruhusu zikue zaidi ya hapo kamwe).”275 Maelezo: at-Tabarsi ameisimulia hii katika al-Makarim.276 7. Ndani ya kitabu al-Ta’rif cha Safwani: Wakati alipokuwa akata nywele zake, yeye (s.a.w.w.) angeanzia kwenye sehemu ya mbele ya kichwa chake, kwani hii ilikuwa ni kutoka kwenye Sunnah ya mitume (a.s.)277 Maelezo: Zayd al-Narsi ameisimulia hii katika kitabu chake, Asl, kutoka kwa AbulHasan (a.s.).278 8. Katika al-Kafi. Ndani ya simulizi yake kutoka kwa Abi Basir ambaye amesema: Nilimuuliza Abi Abdillah (a.s.): “Huku kupanga wei nywele, hivi ni kutoka kwenye Sunnah?” Yeye akasema: “Hapana.” Nikasema: “Hivi Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwahi kupanga wei nywele zake?” Yeye akasema: “Ndio.” Nikasema: “Ni vipi Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipiga wei nywele zake na bado isiwe ni kutoka kwenye Sunnah?” Yeye akasema: “Kama mtu anapitia katika yale aliyopitia Mtukufu 272 Makarimul-Akhlaq: 33 273 Al-Kafi, 6: 486 274 Al-Makarimul-Akhlaq: 70 275 Al-Kafi, 6:485 276 Makarimul-Akhlaq:70 277 Al-Ta’rif: 4 278 Al-Usul al-Sittata ‘Ashar: 56 57


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 58

SUNAN-NABII Mtume (s.a.w.w.) basi mwache apange wei nywele zake kama Mtume alivyopiga wei nywele zake. Ni hapo ndio atakapokuwa ametekeleza Sunnah hiyo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) vinginevyo hajatekeleza.” Mimi nikasema: “Hili liko vipi?” Yeye akasema: “Pale Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa amegeuzwa mbali na Ka’bah licha ya kuwa alikuwa tayari ameleta kafara na akawa amevaa Ihram, Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. alimwonyesha ndoto kwamba Yeye alimjulisha ndani ya Kitabu Chake, pale aliposema:

“Kwa hakika Mwenyezi Mungu amemhakikishia Mtume Wake ndoto yake ya haki. Lazima ninyi mtaingia katika Msikiti Mtukufu Insha’allah kwa salama, mkinyoa vichwa vyenu na mkipunguza nywele, hamtaogopa, na Mwenyezi Mungu alijua msiyoyajua, na kabla ya haya alikupeni ushindi ulio karibu.” (Suratu-Fat’h; 48:27) Hivyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alijua kwamba Mwenyezi Mungu atamtimizia yeye yale aliyokwisha kumwonyesha. Ilikuwa ni baada ya hili kwamba aliachia nywele zake kwenye kichwa chake ziwe ndefu pale alipovaa Ihram, akisubiri kuzinyoa kabisa ndani ya Haram (ndani ya Makkah) kama Mwenyezi Mungu alivyomuahidi. Baada alipokuwa amezinyoa, hakuziruhusu tena nywele zake kukua na hakufanya hivyo hapo kabla vilevile.279 9. Pia: Katika riwaya yake kutoka kwa Hafs al-A’war ambaye amesema: Mimi nilimuuliza Abu Abdillah (a.s.) kuhusu kutia rangi kwenye ndevu na kichwa – ilikuwa ni kutoka kwenye Sunnah?” Yeye akasema: “Ndiyo.”280 Maelezo: at-Tabarsi ameisimulia hii katika al-Makarimu yake.281 10. Katika al-Khisal. Kutoka kwa Aisha: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angeagiza kuzikwa kwa vitu saba kutoka kwa mwanadamu: nywele, kucha, damu, damu ya hedhi, kondo la nyuma (baada ya kujifungua), meno na mabonge (ya mimba iliyoporomoka).282 279 Al-Kafi, 6: 486 280 Ibid, 6:481 281 Makarimul-Akhlaq: 83 282 Al-Khisal: 340 58


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 59

SUNAN-NABII 11. Katika al-Kafi. Katika riwaya yake kutoka kwa Abdillah ibn Abi Ya’fur ambaye amesema: Tulikuwa Madina tukijadili pamoja na Zurarah kuhusu kunyofoa na kunyoa nywele za makwapani. Mimi nikasema: “Kuzinyoa kabisa ni bora.” Zurarah akasema: “Kuzinyofoa ndio bora.” Hivyo tukatafuta ruhusa ya kuonana na Abi Abdillah (a.s.) na yeye akaturuhusu kumuona. Yeye alikuwa ndani ya nyumba ya kuogea kwa wakati huo, akinyoa makwapa yake. Nikamwambia Zurarah: “Je! Hii inatosha (kuwa kama ushahidi kwamba mimi niko sahihi)?” Yeye akasema: “Hapana, pengine yeye amefanya hivi ambapo huenda hairuhusiwi kwa mimi kufanya hivi.” Yeye Imam (a.s.) akauliza: “Kuna nini kinachotokea hapa kati yenu ninyi wawili?” Hivyo mimi nikajibu: “Zurarah alikuwa akihojiana nami kuhusiana na kunyofoa na kunyoa nywele kutoka kwenye makwapa. Mimi nilisema kwamba kuzinyoa ndio bora na yeye akasema kwamba kuzinyofoa ndio bora.” Yeye Imam (a.s.) akasema: “Wewe umefikia kwenye Sunnah na Zurarah ameikosa. Kuzipunguza ni bora kuliko kuzinyofoa na kuziondoa ni bora zaidi kuliko kuzipunguza.”283 12. Vilevile: Katika riwaya yake kutoka kwa Yasir kutoka kwa Abul-Hasan (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Mpendwa wangu Jibril aliniambia: “Tumia manukato kwa siku za kupishana na ni lazima utumie manukato kila Ijumaa bila kukosa.”284 13. Ndani ya al-Makarim: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimwambia Ali (a.s.): “Oh Ali! Ni lazima utumie manukato kila siku ya Ijumaa kwani hii ni kutoka katika Sunnah. Matendo mema yataandikwa kwa ajili yako alimuradi marashi ya manukato yanapatikana kutoka kwako.”285 14. Vilevile: Kutoka kwa Anas ambaye amesema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipopewa mti unaonukia marashi, yeye angeunusa manukato yake na kuurudisha, isipokuwa majorama ambao asingeurudisha.”286 15. Katika al-Bihar kutoka kwa Risalah al-Shahid al-Thanii: Yeye (s.a.w.w.) angekata kucha zake na kupunguza sharubu zake katika siku za Ijumaa kabla ya kutoka kwa ajili ya Swala ya Ijumaa.287 283 al-Kafi, 6: 508 284 Al-Kafi, 6: 511, al-Mustadrak 6:48 285 Makarimul-Akhlaq: 43 286 Ibid, 45 287 Bihar al-Anwar, 89:358, al-Mustadrak 6: 46

59


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 60

SUNAN-NABII 16. al-Sheikh Fakhr al-Din ndani ya al-Muntakhab, katika hadithi kutoka kwa Mkristo mmoja: Niliwauliza baadhi ya masahaba zake Mtume (s.a.w.w.): “Ni zawadi gani anayoipendelea zaidi?” Wao wakasema: “Manukato ndio kitu anachokipenda sana kuliko kitu kingine chochote na anao mvuto maalum juu ya hayo manukato.”288 17. Katika al-Khisal: Katika hadithi yake kutoka kwa al-Hasan ibn al-Jahm ambaye alisema: Abu al-Hasan Musa ibn Ja’far (a.s.) alisema: Mambo matano ni kutoka katika Sunnah kuhusiana na kichwa na matano kuhusiana na mwili. Na ile Sunnah kuhusu kichwa, ni: kupiga meno mswaki, kupunguza masharubu, kuchana nywele, kusukutua kinywa na kusafisha tundu za pua. Zile zinazohusiana na mwili ni: kutahiri, kunyoa nywele za mbeleni, kuondoa nywele kutoka makwapani, kukata kucha na kujisafisha na kila uchafu baada ya kutoka chooni.289 18. Fiqh ar-Ridha (a.s.): Kuwa mwangalifu katika kutekeleza Sunnah za Ijumaa, nazo hizi ziko saba: kujamiiana na mkeo, kuosha kichwa na ndevu kwa kinamasi zito (marsh mellow), kupunguza sharubu, kukata kucha, kubadilisha nguo na kutumia manukato.290 19. as-Shahid al-Thani katika Risalat A’mal Yawm al-Jumu’ah: Yeye (s.a.w.w.) alikuwa akitumia kukata kucha zake na kupunguza sharubu zake katika siku ya Ijumaa kabla ya kuja kwenye Swala ya Ijumaa.291 20. Ja’far ibn Ahmad katika kitabu ‘al-‘Arus’: Kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye alisema: Mpendwa wangu Jibril aliniambia: “Tumia manukato katika siku za kupishana, na katika siku za Ijumaa ni lazima kufanya hivyo.292 21. Vilevile: Kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye alisema: Ni kutoka katika Sunnah kutakia rehma (Salawat) juu ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kizazi chake kila Ijumaa kwa mara elfu moja, na katika siku nyingine zote mara mia moja.293 Maelezo: as-Sheikh al-Tusi ameisimulia hii ndani ya at-Tahdhib katika riwaya yake kutoka kwa Umar ibn Yazid kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.)294 288 al-Muntakhab: 64 289 Al-Khisal: 271 290 Fiqh ar-Ridha: 128 291 Al-Mustadrak, 6:45 292 Ibid, 6: 48 293 Ibid, 6: 71 294 at-Tahdhib, 3:4 60


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 61

SUNAN-NABII

MLANGO WA 4 KUSAFIRI NA ADABU ZAKE 1. Kutoka kwa al-Saduq katika al-Fiqh: Katika riwaya yake kutoka kwa Abdillah ibn Sulayman kutoka Abi Ja’far (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitumia kusafiri katika siku za Alhamisi.295 Maelezo: Zipo hadithi nyingi kama hii.296 2. Kutoka kwa Ibn Tawus katika Aman al-Akhbar na Misbah al-Za’ir: Mwandishi wa kitabu ‘Awarif al-Ma’arif amesimulia: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa akisafiri, angebeba pamoja naye vitu vitano: Kioo, chombo cha kuhl (aina ya wanja), kitana na mswaki. Katika hadithi nyingine ameongeza: na mkasi.297 Maelezo: Hadithi kama hizo zimetajwa katika al-Makarim al-Akhlaq na alJa’fariyat.298 3. Katika al-Makarim: Kutoka kwa ibn Abbas ambaye amesema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipotembea, ingeweza kujulikana kutokana na mwendo wake kwamba hakuwa mnyonge au mvivu.299 Maelezo: Imesimuliwa katika hadithi nyingi kwamba yeye (s.a.w.w.) alikuwa akitembea akiinamia mbele (akiashiria nguvu) kwa hatua nyepesi kana kwamba alikuwa anashuka kwenye mteremko. 4. Katika al-Makarim, kwa kunukuu kutoka Kitab al-Nubuwwah: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akipendelea kupanda kwenye punda asiyekuwa na matandiko (akitumia tu lile blanketi la tandiko).300 5. Katika al-Kafi. Imesimuliwa kutoka kwa Isma’il ibn Hammam kutoka kwa Abi 295 Al-Faqih 2: 266, Makarimul-Akhlaq: 240, Awarif al-Ma’arif: 126 296 ‘Uyun Akhbar al-Ridha 2: 37 297 al-Aman: 54, Misbah al-Za’ir: 28, Da’aim al-Islam 1:118 na 2: 165 298Makarimul-Akhlaq: 35, al-Ja’fariyat: 185 299Makarimul-Akhlaq: 22 300 ibid, 24 61


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 62

SUNAN-NABII al-Hasan (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angeichukua njia ya ‘Dhabb’ (ile njia ya mlimani ambako Masjid al-Khif ndiko uliko) akiwa njiani kutoka Mina na angerudia kutoka kwenye njia hiyo kati ya ‘Ma’zamayn’ (baina ya Mash’ar na Arafah). Na wakati wowote aliposafiri kwenda mahali kwa kutumia njia moja, basi asingerudi kwa kutumia njia hiyohiyo.301 Maelezo: Hii imesimuliwa pia na al-Saduq kwa sanadi ya wasimulizi isiyotimia.302 Amesimulia pia kitu kinachofanana na hicho kutoka kwa ar-Ridha (a.s.) 6. Ndani ya al-Bihar: Wakati yeye (s.a.w.w.) aliponuia kwenda vitani, angeificha nia yake kwa wengine.303 7. Katika al-Faqih. Ndani ya hadithi yake kutoka kwa Mu’awiyah ibn Ammar kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Wakati akiwa safarini, pale Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipoteremka (kutoka kwenye mwinuko) huwa angesoma tasbih “Subhana Allah” na wakati alipopanda, angesoma takbir “Allahu-Akbar.”304 8. Kutoka kwa al-Qutb ndani ya kitabu cha Lubb al-Lubab: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) asingeondoka kamwe kutoka mahali popote hadi awe ameswali rakaa mbili, na (alipoulizwa) alisema: “Ili kwamba mahali hapo pashuhudie kuhusu swala yangu.”305 9. Katika al-Faqih: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipotaka kuwaaga waumini alisema: “Mwenyezi Mungu akujaalieni na taqwa, akugeuzieni kwenye yote ambayo ni mazuri, akutimizieni kila haja zenu, akulindieni dini yenu na mali zenu, na akurudisheni kwangu salama.”306 10. Kutoka kwa al-Barq ndani ya al-Mahasin: Imesimuliwa kutoka kwa Ali ibn Asbat kutoka kwa yule aliyemsimulia hiyo: Abu Abdillah (a.s.) alimuaga mtu mmoja akisema: “Nakabidhi kwenye ulinzi wa Mwenyezi Mungu dini yako na usalama wako. Mwenyezi Mungu akujaalie na taqwa na akugeuzie kwenye mema popote unapogeukia.” Halafu Abu Abdillah akatugeukia sisi na akasema: “Huku ndio kuagana kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akimuaga Ali (a.s.) pale ambapo angemtuma mahali fulani.”307 301 al-Kafi, 4: 248, 8:147 302 al-Faqih, 2:237 303 al-Bihar al-Anwar, 13: 135 kwa kunukuu kutoka Ma’ani al-Akhbar: 386 304 al-Faqih, 2: 273, al-Kafi 4: 287, Makarimul-Akhlaq: 261 305 Awarif al-Ma’arif: 126 306 al-Faqih, 2: 276, Makarimul-Akhlaq: 249, ‘Awarif al-Ma’arif: 125, al-Mahasin: 354 307 al-Mahasin: 354, al-Mustadrak, 8: 208, Makarimul-Akhlaq: 249 62


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 63

SUNAN-NABII Maelezo: Riwaya kusuhu dua yake (s.a.w.w.) kwa ajili ya kuagana ni nyingi na zinatofautiana kimaana. Hata hivyo, licha ya tofauti hiyo, zote zinabeba maombi kwa ajili ya usalama na mafanikio. 11. Katika al-Ja’fariat: Katika hadithi yake kutoka kwa Ja’far ibn Muhammad kutoka kwa baba zake kutoka kwa Ali (a.s.): Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akimwambia mtu yoyote anayerudi kutoka Makka: “Mwenyezi Mungu aikubalie hijja yako, akusamehe madhambi yako na akufidie matumizi yako.”308

Nyongeza kwenye sehemu hii: 12. Ndani ya al-Mahasin: Kutoka kwa Muhammad ibn Abi al-Kiram, kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye alimwambia yeye: “Ningependa wewe uondoke siku ya Alhamisi. Hii ndio siku ambayo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angeondoka wakati alipokuwa akienda kwenye msafara wa kivita.”309 13. Katika Majmu’at Warram: Yeye (s.a.w.w.) angepiga kura kati ya wake zake wakati alipotaka kutoka kwenda safari.310 Maelezo: Hii pia imesimuliwa na at-Tabarsi katika Majma’ na al-Mufid katika alIkhtisas.311 14. Vilevile: Yeye (s.a.w.w.) hakupendezewa juu ya mtu kusafiri bila ya mwenzie.312 15. Katika al-Mahasin: Kutoka kwa al-Sakuni katika riwaya yake: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Ni kutoka katika Sunnah kwamba wakati kikundi cha watu kinapoondoka kwenda safari, wanapaswa kuchukua fedha kwa ajili ya matumizi yao. Hili ni bora kwa ajili ya nafsi zao na murua wao.313 Maelezo: Hii imesimuliwa vilvile na al-Saduq ndani ya al-Faqih. 314

308 al-Ja’fariyat: 75, al-Faqih, 2: 299, al-Mustadrak, 8: 232 309 al-Mahasin: 347, al-Faqih, 2: 266, al-Mahajjat al-Bayda’ 4: 65 310 Majmu’at Warram: 28 311 Majma’ul-Bayan, 7: 130 – Suratun-Nur, al-Ikhtisas: 118 312 Majmu’at Warram: 28 313 al-Mahasin: 359, al-Ja’fariyat: 170, Da’am al-Islam, 1: 346 314 al-Faqih, 2: 278 63


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 64

SUNAN-NABII 16. Katika al-Makarim: Kwenye safari zake, yeye (s.a.w.w.) wakati wote angebeba pamoja naye chupa ya mafuta, chombo cha wanja, mkasi, mswaki wa meno na kitana. Katika riwaya nyingine; yeye angechukua pamoja naye, nyuzi, sindano, msharasi na mikanda ya ngozi, na angeshona nguo zake (wakati zinapopasuka) na kutengeneza viatu vyake.315 17. Vilevile: Kutoka wa Anas ibn Malik ambaye amesema: Wakati yeye Mtume (s.a.w.w.) aliponuia kusafiri, angesema wakati wa kuondoka: “Ewe Mungu! Kwa Ridhaa Yako (na baraka Zako) mimi nimeanza safari hii, na Kwako ndio ninakoelekea, na ninatafuta hifadhi Kwako. Wewe ndiyo tegemeo langu na tumaini langu. Ewe Allah! Nitoshelezee mimi lile ambalo ni muhimu kwangu, na lile ambalo silitilii muhimu na ambalo Wewe unalijua zaidi kuliko mimi. Ewe Mungu Wangu! Nizidishie taqwa na unisamehe, na unielekeze kwenye mema kokote ninakoelekea.” – halafu ndio angeondoka.316 18. Katika Ma’ani al-Akhbar: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angesafiri kwa haraka sana na alipofika kwenye sehemu ya wazi angeongeza kasi yake.317 Maelezo: Hili limesimuliwa vilevile na al-Mufid katika al-Ikhtisas.318 19. Al-Barqi amesimulia ndani ya al-Mahasin, al-Saduq katika al-Faqih na atTabarsi katika al-Makarim: Katika riwaya yao kutoka kwa Abu Ja’far (a.s.): Wakati yeye (s.a.w.w.) alipotaka kumuaga msafiri, angemshika mkono na kumuombea yeye kama alivyopenda.319 20. Katika al-Ja’fariyat: Katika riwaya yake kutoka kwa Ali (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na fimbo fupi yenye ncha ya chuma ambayo alikuwa akiiegemea. Alikuwa akiitoa katika zile siku za ‘Iddi mbili na angeswali karibu nayo, na alipokuwa katika safari angeiweka katika mwelekeo wa Qiblah na kuswali.320 21. Katika al-Makarim: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Kubeba fimbo ni ishara ya muumini na Sunnah ya mitume (a.s.).321 315 Makarimul-Akhlaq: 35, al-Ja’fariyat: 185, Da’aim al-Islam 1:118, al-Mustadrak, 8: 217 316 Makarimul-Akhlaq: 246 317 Ma’ani al-Akhbar: 378 318 al-Ikhtisas: 120 319 al-Mahasin: 354, al-Faqih 2: 276, al-Makarimul-Akhlaq: 249 320 al-Ja’fariyat: 184, al-Faqih, 1: 509 321 Makarimul-Akhlaq: 244 64


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 65

SUNAN-NABII Maelezo: Hii imesimuliwa pia ndani ya ‘Awarif al-Ma’arif.322 22. Katika Awarif al-Ma’arif: Kuegemea katika fimbo ni katika akhlaq ya Mitume (a.s.)323 Maelezo: Hii imesimuliwa vilevile katika al-Faqih na Mahajjat al-Bayda.324 23. Vilevile: Ka’b ibn Malik amesimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) asingerudi kutoka safari isipokuwa katika wakati wa mchana, wakati wa alasiri.325 24. Katika Mahajjat al-Bayda: Yeye Mtume (s.a.w.w.) asingeteremka kwenye kipando mpaka pale kulipokuwa na joto sana kiasi cha kushindikana kusafiri katika wakati wa mchana, na hii ni kutoka kwenye Sunnah. Safari zake zaidi zilifanyika wakati wa usiku.326 25. Vilevile: Wakati alipolala akiwa safarini mwanzoni mwa usiku, angelala (akiweka kichwa chake) juu ya mkono wake na kama angelala baadae usiku sana, angenyanyua mkono wake na kulala akiwa ameweka kichwa chake kwenye kiganja cha mkono.327 26. Katika ‘Awarif al-Ma’arif: Iliyo Sunnah ni kuondoka kwenda safari mapema wakati wa asubuhi na kuanza (kusafiri) mnamo siku ya Alhamisi.328 27. Katika ‘Awarif al-Ma’arif: Kubeba mfuko wa maji pia ni katika Sunnah.329 28. Vilevile: Imesimuliwa kwamba wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa anarudi nyumbani kutoka vitani au kutoka Hijja, (akiwa njiani) angeweza kusoma Takbira (Allahh Akbar) mara tatu katika kila muinuko juu ya ardhi halafu akasema: “Hakuna mungu isipokuwa Allah, Yeye ni Mmoja tu – hana mshirika yoyote. Ufalme ni Wake na utukufu wote ni wa Kwake na anao uwezo juu ya kila kitu. (Tunakuja Kwake) tukifanya ibada, tukisujudu na kumtukuza Mola Wetu. Mwenyezi Mungu ameithibitisha ahadi Yake na amemsaidia mja Wake na akayatokomeza makundi (ya kiadui) peke yake.”330 322 Awarif al-Ma’arif: 127 323 Ibid. 324 al-Faqih, 2: 270, al-Mahajjat al-Bayda 4: 74 325 Awarif al-Ma’arif: 133 326 al-Mahajjat al-Bayda, 4: 67 327 al-Mahajjat al-Bayda, 4: 68 328‘Awarif al-Ma’arif: 126 329 Ibid, 127 330 ‘Awarif al-Ma’arif: 129 65


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 66

SUNAN-NABII Kidokezo: Al-Fayd vilevile ameisimulia hii katika al-Mahajjat.331 29. Vilevile: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa akirudi (kutoka kwenye safari yake) angeanza kuingia kwanza msikitini na kuswali rakaa mbili, halafu ndipo angeingia nyumbani kwake.332 Kidokezo: al-Fayd vile vile amelisimulia hili.333 30. Katika Durr al-Manthur: Kutoka kwa Jabir ibn Abdillah ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) asingeweza kupigana vita katika mwezi mtukufu ulioharamishwa mapigano isipokuwa kama angeshambuliwa, basi angepigana; na wakati ulipofika (mwezi huo), yeye angelidumisha hilo mpaka ulipokuwa umepita.334 31. Katika al-Makarim: Kutoka kwa Jabir ibn Abdillah ndani ya hadithi ambamo anaelezea baadhi ya adab za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wakati wa mapigano: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angekuwa miongoni mwa watu wa mwisho (kuja kwenye uwanja wa mapambano). Angehimiza mbele na kuwatia moyo wale wadhaifu, kupanda vipando pamoja nao na kuwaombea dua.335 32. Kutoka kwa al-Iqbal: Ndani ya riwaya yake kutoka kwa Abu Ja’far (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akiondoka nyumbani baada ya kuchomoza kwa jua.336 33. Katika Durr al-Manthur: Kutoka kwa Abu Musa kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akichukia kupiga makelele wakati wa mapambano ya vita. Wakati Mtume alipokuwa vitani, asingepigana mapema wakati wa asubuhi bali hasa angechelewesha kupambana mpaka jua lilipokuwa limepita upeo wa kati wa mchana (meridiani) na upepo ukawa umeanza kuvuma, na hadi kushuka kwa msaada wa ki-mbingu.337

331 Mahajjat al-Bayda, 4: 75 332 ‘Awarif al-Ma’arif: 130 333 Mahajjat al-Bayda, 4: 76 334 ad-Durr al-Manthur,1: 207 – Sura al-Baqarah (2) 335 Makarimul-Akhlaq: 20 336 Iqbal katika al-A’mal: 281 337 ad-Durr al-Manthur, 3: 189 – Suratal-Anfal (7) 66


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 67

SUNAN-NABII

MLANGO WA 5 ADAB ZA MAVAZI NA CHOCHOTE KINACHOAMBATANA NA JINSI YA KUYAVAA 1. Kutoka kwa Ghazali katika al-Ihya’: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akivaa chochote kilichopatina, kuanzia nguo ya kufunga kiunoni au shuka, shati refu au kanzu ya juu yenye mikono mizima au vazi lolote lile, na alikuwa akipendelea hususan nguo za kijani. Nyingi ya nguo zake zilikuwa nyeupe na angeweza kusema: “Jivisheni uhai wenu na mjivuni maiti zenu kwa vazi hilo hilo (jeupe).” Alivaa juba lisilo na mikono lililonakshiwa na vitu laini kwa ajili ya mapambano na nyakati nyinginezo. Yeye (s.a.w.w.) alikuwa na juba la tarizi ya hariri safi ambayo wakati mwingine alikuwa akiivaa na rangi yake ya kijani ilijipambanua vizuri sana na ngozi yake nyeupe. Nguo zake zote zilichomekewa juu ya vifundo vyake vya miguu na nguo yake ya kiunoni ingekuwa juu ya hili, ikifikia katikati ya miundi yake. Shati lake refu lilifungwa kwa vifungo, ambavyo wakati alivifungua wakati wa swala na katika nyakati nyinginezo. Alikuwa na shuka iliyotiwa rangi kwa zafarani ambayo wakati mwingine aliivaa alipokuwa akiongoza swala. Yeye wakati mwingine alivaa nguo ya kipande kimoja. Alikuwa na nguo ya kitambaa gandamizo (duni) ambayo alikuwa akiivaa akisema: “Mimi ni mtumwa tu. Ninavaa kama anavyovaa mtumwa.” Alikuwa na mavazi mawili maalum kwa ajili ya siku za Ijumaa, mbali na zile nguo ambazo alizivaa kwa nyakati nyinginezo. Wakati mwingine alivaa shuka ya kiunoni tu, akizifunga zile ncha zake mbili katikati ya mabega yake, na akiwa amevaa hivyo, wakati mwingine aliwaongoza watu katika swala ya jeneza. Wakati mwingine alikuwa akiswali nyumbani kwake akiwa amevaa shuka moja ya kiunoni, akizifunga ncha zake mbili kwa kupishana. Wakati mwingine aliswali nyakati za usiku akiwa na shuka ya kiunoni tu, akijivunika yeye mwenyewe na sehemu ya mwisho ya nguo, ambayo ilikuwa karibu yake, na kutandaza ile sehemu iliyobakia juu ya mke wake. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na shuka jeusi ambalo aliligawa. Papohapo Ummu Salama akasema: “Baba yangu na mama wawe fidia yako! Ni nini kilichotokea kwa lile shuka jeusi?” Yeye akajibu: “Nilimvisha nalo mtu fulani.” Kisha bibi huyu akasema: “Sijaona kamwe kitu kinachopendeza zaidi kuliko weupe wako dhidi ya weusi wake.” 67


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 68

SUNAN-NABII Anas amesema: “Wakati mwingine nilimuona yeye akituongoza katika swala ya Dhuhr akiwa amevaa shuka jeusi ambalo ncha zake mbili zilifungwa fundo.” Alikuwa akitumia kuvaa pete kwenye kidole chake ….. na wakati mwingine alitumia kuweka mhuri wake kwenye barua akisema: “Muhuri kwenye barua ni bora kuliko kutiliwa mashaka.” Alikuwa na matumizi ya kuvaa kofia chini ya kilemba chake na (wakati mwingine) hata bila kilemba. Nyakati nyingine aliivua kofia yake na kuifanya kama kinga mbele yake na aliswali kuielekea. Nyakati nyingine, alipokuwa hana kilemba, yeye alifunga nguo ya kichwa nyeusi juu ya kichwa chake na sehemu ya mbele ya kichwa chake. Alikuwa na kilemba kilichoitwa al-Sahab (wingu), ambacho alikitoa kama zawadi kwa Ali (a.s.). Wakati mwingine Ali (a.s.) alitoka akiwa amekivaa, na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angesema: “Ali huyo anakujieni akiwa ndani ya lile wingu.” Yeye alipokuwa anavaa, alianza kuvaa kuanzia upande wake wa kulia huku akisema: “Shukrani ni Zake Mwenyezi Mungu ambaye amenivisha mimi kile ambacho nausitiri utupu wangu na ambacho ninajipamba nacho katika watu.” Wakati alipokuwa akivua nguo zake, yeye alianza kuzivua kuanzia kushoto kwake. Alipovaa nguo mpya, alizigawa zile nguo zake za zamani kwa masikini huku akisema: “Hakuna Mwislamu anayemvisha Mwislam mwingine kwa nguo zake za zamani kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, bali kwamba huyo mtoaji anakuwa chini ya ulezi, hifadhi na ulinzi wa Mwenyezi Mungu, wakati akiwa hai au akiwa amefariki.” Alikuwa na matandiko ya kulalia ya ngozi, ambayo yalifutikwa na nyuzi za mitende. Urefu wake ulikuwa takriban dhiraa mbili na upana wake ni takriban dhiraa moja na unene (wa takriban inchi tisa). Alikuwa na shuka ambalo angeweza kulikunja mara mbili na kulitandika chini yake popote alipokuwa. Yeye (s.a.w.w.) alikuwa akitumia kulala chini ya mkeka bila kuwa na chochote chini yake. Moja ya sifa zake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ilikuwa kwamba angeweza kuwapa majina wanyama wake, silaha zake na vifaa vyake. Jina la bendera yake lilikuwa ni ‘al-Iqab’, jina la upanga wake ambao alikabiliana nao mapambano lilikuwa ‘DhulFiqar’. Alikuwa na upanga ambao uliitwa ‘al-Mikhdham’, mwingine ukiitwa ‘alRusub’ na mwingine uliitwa ‘al-Qadhib’. Mkono au kishikio cha upanga wake ulipambwa kwa fedha na yeye alikuwa akitumia kuvaa mkanda uliotengenezwa kwa 68


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 69

SUNAN-NABII ngozi ambao ulikuwa na pete tatu za fedha. Jina la upinde wake lilikuwa ‘alKatum’, na jina la pongono yake lilikuwa ‘al-Kafur’. Jina la ngamia jike wake lilikuwa ‘al-Qaswa’ na alikuwa ni ngamia huyu ambaye alikuwa akiitwa ‘alAdhba’. Jina la nyumbu jike wake lilikuwa ni ‘al-Duldul’. Jina la punda wake lilikuwa ni ‘Yafur’ na jina la kondoo jike wake ambaye alikuwa akitumia kunywa maziwa yake lilikuwa ‘Ainah’. Alikuwa na bakuli lililotengenezwa kwa udongo uliookwa ambalo alilitumia wakati anapokuwa anachukua wudhuu na angeweza (pia) kunywa ndani yake. Watu waliwapeleka watoto wao wadogo ambao ndio kwanza wamefikia umri wa kuelewa, hivyo walikuja kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na hawakuondoka kwake tena. Walipoyakuta maji kwenye bakuli hilo, walikunywa kutoka humo na wakafuta nyuso zao na miili kwalo, wakitegemea kupata baraka kwa kufanya hivi.338 2. Imesimuliwa kwamba kilemba chake kilikuwa na (urefu wa) mikunjo mitatu au mitano.339 3. Katika al-Awali: Imesimuliwa kwamba yeye (s.a.w.w.) alikuwa na kilemba cheusi ambacho alikivaa wakati alipokuwa anaswali.340 4. Katika al-Ja’fariyat: Katika riwaya yake kutoka kwa Ja’far ibn Muhammad, kutoka kwa baba zake, kutoka kwa Ali (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akivaa kofia yenye mistari – na alikuwa na vazi la deraya ya chuma liitwalo ‘Dhat al-Fudhul’ ambalo lilikuwa na pete za fedha, moja ikiwa mbele na mbili nyuma.341 5. Katika al-Makarim: Juu ya ubora wa nguo za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): Mtukufu Mtume angevaa ‘shamlah’ na ‘namirah’342 na ile rangi nyeusi ya hiyo ‘namirah’ ingechukuana vizuri sana na ule weupe wa miundi na nyayo zake.343 6. Katika al-Awali: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akitumia kuswali akiwa amevaa nguo pana.344 338 Ihya ‘Ulum al-Din, 2:374 - 377 339 Hatukuipata (rejea kwa ajili ya) hii 340 Awali al-La’ali: Sehemu juu ya Swala 2:214 341 al-Ja’fariat: 184, Da’aim al-Islam, 2:159, Makarimul-Akhlaq: 120. 342 Hizo shamlah na namirah zilikuwa ni nguo ambazo zilikuwa kwa kawaida zikivaliwa na Waarabu. (Mfasiri) 343Makarimul-Akhlaq: 35 344 al-Mustadrak 3: 213, Da’aim al-Islam 1: 176 69


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 70

SUNAN-NABII 7. Kutoka kwa al-Karajiki ndani ya Kanz al-Fawa’id: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na nguo mbili za kufumwa makhsusi kabisa kwa ajili ya Swala, ambazo asingeweza kizivaa katika nyakati nyingine zozote. Alikuwa (wakati wote) akiwasihi wafuasi wake na kuwaelekeza katika kudumisha usafi.345 8. Katika al-Kafi: Imepokewa kutoka kwa Abi Basir kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Amirul-Mu’minin (a.s.) amesema: “Vaeni nguo zilizotengenezwa kwa pamba, kwani haya yalikuwa ndio mavazi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) nayo ndio mavazi yetu (ya chaguo letu) sisi.”346 9. Kutoka kwa al-Saduq ndani ya al-Khisal: Katika riwaya yake kutoka kwa Ali (a.s.) ambaye amesema: “Vaeni nguo za pamba kwani hivi ndivyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alivyokuwa akivaa na hakuwa kamwe akivaa nguo za manyoya au sufi isipokuwa kama kulikuwa na sababu ya muhimu (ya kufanya hivyo).”347 Kidokezo: al-Saduq anasimulia hadithi hii katika al-Khisal bila kutaja sanadi ya wapokezi, kama afanyavyo al-Safwani ndani ya al-Ta’rif.348 Tumeona katika sehemu ya pili (juu ya uhusiano wake na watu) kwamba Mtume (s.a.w.w.) wakati mwingine angevaa nguo za manyoya lakini hadithi hii inafafanua vizuri kwamba angefanya hivyo kwa sababu nzuri muhimu (hivyo hakuna kukinzana). 10. Katika al-Manaqib: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na mkanda kwa ngozi iliyogeuzwa ambao ulikuwa na pete tatu na chuma chake na kingo zake vilikuwa pia vimetengenezwa kwa fedha. Alikuwa pia na kikombe cha kunywea ambacho kilikuwa kimepambwa na mapambo matatu ya fedha.349 11. Katika al-Ja’fariyat: Katika riwaya yake kutoka kwa Ja’far ibn Muhammad, kutoka kwa baba zake, kutoka kwa Ali (a.s.): Ile ala ya upanga wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ilikuwa (imetengenezwa) kutokana na fedha na mkono wake ulikuwa wa fedha na katikati yake kulikuwa na pete iliyotengenezwa kwa fedha.350 12. Katika al-Faqih: Katika riwaya yake kutoka kwa Isma’il ibn Muslim kutoka kwa as-Sadiq kutoka kwa baba yake (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume 345 Kanz al-Fawa’id: 285 346 al-Kafi 6: 446; Da’aim al-Islam 2: 155; Tuhf al-‘Uqul: 103; Makarimul-Akhlaq: 103. 347 al-Khisal: 613; Tuhf al-‘Uqul: 103; Makarimul-Akhlaq: 103; al-Kafi, 6: 445; Da’aim al-Islam, 2: 155 348 Imesimuliwa na mwandishi wa al-Mustadrak 3: 248 kutoka kwenye kitabu cha Safwani, al-Ta’riif; Tuhf al-‘Uqul: 103; Makarimul-Akhlaq: 103 349 Manaqib Ali ibn Abi Talib 1: 170 350 al-Ja’fariyat: 185; Da’aim al-Islam 2: 164; al-Kafi 6: 475; al-Mustadrak 3: 309 70


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 71

SUNAN-NABII (s.a.w.w.) alikuwa na fimbo fupi ambayo ilikuwa na ncha ya chuma katika mwisho wake wa chini. Angekuwa akiitumia kama fimbo ya kutembelea na kuegemea juu yake. Katika zile siku mbili za Iddi angetoka nayo na angeiweka mbele yake wakati anaswali.351 Kidokezo: Hii imetajwa pia katika al-Ja’fariyat.352 13. Katika al-Makarim: Imesimuliwa kutoka kwa Hashim ibn Salim kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Pete ya Mtukufu Mtume ilikuwa imetengenezwa kwa fedha.353 Kidokezo: Hadithi hii ina sanadi nyingine ya wasimulizi na imetajwa katika Qurb al-Isnad.354 14. Vilevile: Imesimuliwa kutoka kwa Abi Khadijah ambaye amesema: Jiwe ambalo linawekwa kwenye pete linapaswa kuwa la mviringo. Hivi ndivyo ilivyokuwa pete ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)355 15. Vilevile: Imesimuliwa kutoka kwa Abdillah ibn Sinan kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Yale maandishi yaliyokuwa yamechongwa juu ya pete ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) yalisomeka “Muhammad ni Mtume wa Allah”356 16. Kutoka kwa al-Saduq katika al-Khisal: Imesimuliwa kutoka kwa Abd alRahman ibn Abi al-Bilad kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na pete mbili. Moja ilikuwa imeandikwa ‘Hakuna mungu ila Allah na Muhammad ni Mtume wa Allah’ na juu ya hiyo nyingine mliandikwa ‘Allah amesema kweli.’357 17. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa al-Husein ibn Khalid kutoka kwa Abi al-Hasan al-Thani (a.s.) – katika hadithi – kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Amirul-Mu’minin, Hasan na Husein na Maimam (wote) a.s. walikuwa wakivaa pete zao katika mkono wa kulia.358 351 al-Faqih 1: 501 352 al-Ja’fariyat: 184 353 al-Makarim al-Akhlaq: 85 354 Qurb al-Isnad: 31 355 Vile vile tumeikuta kama hii hasa katika al-Kafi 6: 468 356 Makarim al-Akhlaq: 91; al-Kafi 6:473; Da’aim al-Islam 2:165. 357 al-Khisal: 61; Amali al-Saduq: 370. 358 al-Kafi, 6:474; ‘Ilal al-Shara’:158; al-Ja’fariyat:185; ‘Uyun al-Akhbar al-Ridha, 2:55 71


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 72

SUNAN-NABII Maelezo: Kuna riwaya kama hizi ndani ya al-Kafi kutoka kwenye sanadi mbalimbali tofauti za wasimuliaji, zikiwa na tofauti kidogo kuhusu yale maandishi juu ya pete. Al-Saduq na wengineo pia wameisimulia hadithi hii. Al-Kulain ameendelea kusimulia kwamba Ali, Hasan, Husein na baadhi ya Maimam wengine (a.s.) walivaa pete katika mkono wa kushoto.359Hakuna tatizo kwa kuhitimisha kwamba walikuwa wangeweza kuvaa pete kwenye mikono yote, au kwamba ingeweza kuvaliwa katika mikono tofauti kwa nyakati tofauti, lakini hii haijawahi kusimuliwa kuhusu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Hata hivyo, al-Kulayni amesimulia ndani ya al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Ali ibn Atiyya kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akivaa pete kwa muda tu na baadae angeweza kuivua.360 18. Katika al-Makarim: Kutoka kwa as-Sadiq (a.s.) kutoka kwa Ali (a.s.) ambaye amesema: Mitume walikuwa wakivaa mashati yao kabla ya kuvaa suruali zao.361 Kidokezo: Hii imesimuliwa vilevile katika al-Ja’fariyat.362

Nyongeza kwenye Sehemu hii 1. Katika al-Makarim: Kutoka kwa Ma’mar ibn Khallad kutoka kwa Abul-Hasan arRidha (a.s.) – Katika ushauri wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa Abu Dharr yeye alisema: “Oh, Abu Dharr! Mimi ninavaa nguo zilizo duni, ninaketi chini juu ya ardhi, ninalamba vidole vyangu (baada ya kula), ninapanda juu ya punda bila matandiko na ninabeba mtu pamoja nami, hivyo yule asiyeipenda Sunnah yangu huyo hatokani nami.”363 Kidokezo: Hii vilevile imesimuliwa na Sheikh Abu Faras ndani ya Majmu’at Warram.364 2. Vilevile kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akitumia kuvaa kofia nyeupe yenye miraba miraba. Wakati alipokuwa kwenye vita, yeye (s.a.w.w.) alivaa kofia yenye mapindo mawili.365 359 al-Kafi 6: 469 360 Ibid, 6:469 361 Makarim al-Akhlaq: 101 362 al-Ja’fariyat: 240 363Makarimul-Akhlaq: 115 364 Majmu’at Warram, 306 365 Makarim al-Akhlaq: 120; Da’aim al-Islam, 2: 159 72


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 73

SUNAN-NABII 3. Katika al-Khisal: Kutoka kwa Muhammad ibn Ahmad ibn Abi Abdillah al-Barqi ndani ya riwaya yake kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa hapendezewi na rangi nyeusi isipokuwa katika vitu vitatu: Katika kilemba, viatu na shuka.366 Kidokezo: Hii imesimuliwa pia na al-Kulayni katika al-Kafi na vilevile al-Saduq katika al-Fiqh na al’Ilal.367 4. Katika al-Makarim: Kutoka kwa Abi Ja’far (a.s.) ambaye amesema: Ni kutoka katika Sunnah kuvaa kiatu cha kulia kabla ya cha kushoto na kuanza kuvua kiatu cha kushoto kabla ya kile cha kulia.368 5. Vilevile: Kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Vueni viatu vyenu wakati mnapokula, kwani hii inapumzisha sana kwa ajili ya miguu yako na ni Sunnah nzuri ajabu kabisa.369 6. Vilevile kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Hii ni katika Sunnah kuvaa viatu vyeusi na kandambili za manjano.370 7. Vilevile: Kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Nguo ya kitani ni kutoka katika mavazi ya mitume (amani juu yao).371 8. Katika Da’aim al-Islam: Kutoka kwa Abi Abdillah kutoka kwa baba zake (amani juu yao wote) kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba yeye asingependezewa na rangi nyekundu kupakwa katika nguo zake.372 9. Katika al-Faqih: Kutoka kwa Muhammad ibn Qays, kutoka kwa Abi Ja’far Muhammad ibn Ali al-Baqir (a.s.) ambaye amesema: Yeye Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na hema lililoitwa ‘al-Kinn’ (hifadhi).373 10. Katika al-Manaqib: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angevaa vazi lake jekundu katika siku za Ijumaa na angevaa kile kilemba chake kinachoitwa ‘al-Sahab’. Wakati 366 al-Khisal: 148 367 al-Kafi 6: 449; al-Fiqh, 1: 251; al-Ilal al-Sharai’: 347 368 Makarim al-Akhlaq: 123 369 Ibid, 124 370 Ibid, 125 371 Ibid, 104 372 Da’aim al-Islam, 2:160 373al-Faqih, 4:178 73


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 74

SUNAN-NABII alipoingia Makkah ile siku ya kutekwa kwake, yeye alikuwa amevaa kilemba cheusi. Alikuwa na kisanduku ambacho ndani yake aliweka kitana cha pembe, chombo cha wanja, mkasi na mswaki – alifariki dunia akiwa katika nguo hafifu ya kujitandia ya kutoka Yemen na shuka linaloitwa ‘al-Malbadah’. Alikuwa na kitanda ambacho alikuwa amekipewa na Asad ibn Zurarah. Mimbari yake ilikuwa na ngazi tatu na ilitengenezwa kwa mbao za mkwaju (tamarind) na fundi seremali aliyeitwa Maymun. Msikiti wake ulikuwa hauna minara na Bilal alikuwa akiadhini huku akiwa amesimama chini juu ya ardhi.374 11. Katika al-Kafi: Kutoka kwa Ibn al-Qaddah, kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.): Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na vazi lililotiwa rangi ambalo yeye (kila mara) alilivaa alipokuwa nyumbani mpaka ili rangi ya nguo hiyo ikamuathiri mwili wake.375 12. Vilevile: Kutoka kwa Abi Ja’far (a.s.) ambaye amesema: “Tungeweza kuvaa mavazi yaliyonakshiwa kwa rangi ya kimanjano-nyekundu tukiwa nyumbani.”376 13. Katika al-Bihar: Kutoka kwenye Risalat al-Jumu’ah ya Shahid al-Thani: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na nguo maalum ambazo alizivaa kwenye zile Idd mbili na siku za Ijumaa, mbali na nguo zake nyingine za kawaida.377 14. Vilevile: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na nguo ya kijani kutoka Yemen ambayo yeye aliweza kulala ndani nayo.378 15. Katika al-Bihar kutoka kwenye al-Kafi: Ndani ya riwaya yake kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na nguo mbili kutoka Yemen ambazo angeweza kuzivaa kama Ihram na nguo hizi vilevile zilitumika kama sanda yake.379 16. Vilevile: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipoongoza ujumbe, angeweza kuvaa nguo zake nzuri kabisa na angewaambia masahaba zake wafanye kama vivyo hivyo.380 374 Manaqib Ali ibn Abi Talib, 1:171 375 al-Kafi 6:448 376 Ibid. 377Ibid, 89: 212 378 Ibid, 19:53 379 Ibid, 21: 401

380 Ibid, 21: 372 74


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 75

SUNAN-NABII

MLANGO WA 6 SUNNAH YAKE KATIKA MAKAZI 1. Kutoka kwa Ibn Fahd ndani ya Kitab al-Tahsin: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliondoka katika dunia hii bila ya kuweka tofali juu ya tofali.381 2. Katika Lubb al-Lubab: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Misikiti ni sehemu za kukutania za mitume (a.s.).382 3. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka al-Sakuni, kutoka kwa Abi Abdillah (a.s) ambaye amesema: Kama Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitaka kutoka nje ya nyumba yake wakati wa kiangazi, angetoka katika siku ya Alhamisi na wakati aliponuia kuingia kwenye majira ya kuchipua, angefanya hivyo katika siku ya Ijumaa.383 Kidokezo: Riwaya kama hii imesimuliwa katika al-Khisal.384 4. Katika kitabu al-‘Adab al-Qawiiyyah cha Sheikh Ali ibn al-Hasan ibn alMutahhar (ndugu yake Allamah): Kutoka kwa Khadijah – Mwenyezi Mungu awe radhi naye – ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliingia ndani ya nyumba, angeomba apewe beseni na kuchukua wudhuu kwa ajili ya swala. Halafu angeswali swala fupi ya rakaa mbili ambayo baada yake angekwenda kulala.385 5. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa al-Abbad ibn Suhaib ambaye amesema: Nilimsikia Aba Abdillah (a.s.) akisema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) asingeweza kamwe kuwavamia kwa kuwashitukiza maadui zake wakati wa usiku – abadan.386

Nyongeza juu ya sehemu hii 1. Katika al-Makarim: Kutoka kwa Anas ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Jogoo mweupe ni rafiki yangu, na adui yake ni adui wa Mwenyezi Mungu, Anamlinda mmiliki wake na (walioko) nyumba saba (za jirani).” Mtukufu Mtume (s.a.w.w) alikuwa akimfuga jogoo mweupe ndani ya nyumba 381 Vilevile imesimuliwa na al-Nuri katika al-Mustadrak 3:466, na ndani ya ‘Uddat alDa’i: 119 382 Imesimuliwa na an-Nuri katika al-Mustadrak 3: 323 383 al-Kafi 6: 532, ‘Uddat al-Da’i: 45, Makarim al-Akhlaq: 128 384 al-Khisal: 391 385 Imesimuliwa na al-Majlisi katika al-Bihar 16: 80 386 al-Kafi 5: 28, Tahdhib al-Ahkam 6: 174 75


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 76

SUNAN-NABII yake.387 2. Katika al-Khisal: Kutoka kwa Muhammad ibn Isa al-Yaqtini ambaye amesema: ar-Ridha (a.s.) amesema: “Jogoo mweupe anazo sifa tano kutoka kwenye sifa za mitume (amani juu yao): Utambuzi wa saa za swala, heshima, ukarimu, ujasiri na uhusiano wa ziada wa kuarifu.388 Kidokezo: Imesimuliwa pia katika al-‘Uyun.389 3. Katika al-Makarim: Kutoka Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mitume wote (a.s.) walikuwa na njiwa katika majumba yao, kwa sababu wale majini wapumbavu huwa wanacheza na watoto wa nyumba lakini panapokuwa na njiwa wao hucheza na njiwa na kuachana na watu.390 4. Katika al-Kafi: Kutoka kwa Aban, kutoka kwa mtu mmoja (aliyesikia) kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na jozi ya njiwa wekundu katika nyumba yake.391 5. Vilevile: Kutoka kwa Talha ibn Zayd, kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) asingependelea kuingia nyumba yenye giza isipokuwa awe na taa.392 6. Pia: Kutoka kwa Abdullah ibn Sinan kutoka Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angependelea kwamba katika wakati wa majira ya kuchipua, pale alipoingia au kutoka (nyumbani kwake) iwe ni katika siku ya Alhamisi usiku..393 7. Katika al-Da’aim: kutoka kwa Ali (a.s.) ambaye alisema: Ni katika Sunnah (kwamba) wakati unapoingia msikitini unapaswa ukae kuelekea Qibla.394 8. Katika al-Tahdhib: Katika riwaya yake kutoka kwa Jarrah al-Mada’ini kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: “Msichore mapicha kwenye mapaa ya nyumba zenu kwani Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alilichukia hili.395 387 al-Makarimul-Akhlaq: 130 388al-Khisal: 298 389 al-Uyun al-Akhbar ar-Ridha, 8: 277 390 Makarimul-Akhlaq: 131 391 al-Kafi 6: 548 392 Ibid, 6: 534 393 al-Kafi 3: 413, Tahdhib al-Ahkam 3:4 394 Da’aim al-Islam,1: 148, Katika al-Bihar al-Anwar; 83: 380 395 Tahdhib al-Ahkam 1: 461 76


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 77

SUNAN-NABII 9. Muhib al-Din at-Tabari amesimulia: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimiliki jogoo mweupe na masahaba walikuwa wakitembea na majogoo ili kuweza kutambua nyakati za Swala.396 10. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa nalo (jogoo) nyumbani kwake na msikitini.397 11. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akipendelea kuangali miti jamii ya michungwa na njiwa wekundu.398 12. Kutoka kwa Aisha: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipendelea kutazama majani ya kijani na njiwa wekundu.399 13. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akitembelea nyumba za kabila moja la Ansari lakini hakuwa akitembelea nyingine, hivyo waliongea naye kuhusu hili na yeye akasema: “Ni kwa sababu mnao mbwa majumbani mwenu.”400 14. Katika al-Kafi: Katika riwaya yake kutoka kwa Abdillah ibn al-Mughirah, kutoka kwa mtu mmoja ambaye alisema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipoingia kwenye nyumba, angeweza kuketi kwenye kiti (kilichokuwa) cha karibu kabisa.401 15. Kijalizo: Allamah amesema: Hii imesimuliwa na mjukuu wa Tabari katika alMishkat akinukuu kutoka kwenye al-Mahasin na wengine.402 16. Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipoamka kutoka usingizini mwake, alikuwa akitumia kumshukuru Mwenyezi Mungu.403 17. Kutoka kwa Fadhlah ibn Abid aba Barzah al-Aslami: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakupendelea kulala kabla ya swala ya ‘Isha, na kuongea na watu baada ya swala hiyo.404 396 Bihar al-Anwar 65:7 397 Ibid. 398 Bihar al-Anwar 65: 26 399 Ibid. 400 Bihar a-Anwar, 65: 67 401 al-Kafi, 2: 662 402 Mishkat al-Anwar: 204 403 Bihar al-Anwar, 15: 292 404 Bihar al-Anwar,76: 118; al-Khisal: 520 77


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 78

SUNAN-NABII

MLANGO WA 7 ADABU ZA KULALA NA KANDO YA KITANDA 1. Katika al-Makarim: Matandiko ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) yalikuwa ni shuka na mto wake ulitengenezwa kutokana na ngozi iliyojazwa nyuzi za mtende. Usiku mmoja shuka lake lilikuwa limekunjwa mara mbili na wakati alipoamka, yeye akasema: “Matandiko haya yamenizuia kuswali swala ya usiku.” Hivyo akaagiza kwamba litandikwe tabaka moja tu kwa ajili yake. Alikuwa na mto uliotengenezwa kutokana na ngozi na kufutikwa nyuzi za mitende, na alikuwa na shuka ambalo lingeweza kukunjwa mara mbili na alilolitumia kama matandiko alipokuwa ametoka nje ya nyumbani kwake.405 2. Vilevile: Yeye Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akitumia kulala kwenye mkeka bila kuwa na chochote chini yake.406 3. Vilevile: Kutoka kwa Abi Ja’far (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kamwe hakuwa akiamka kwenye usingizi wake bali kwamba mara tu angemsujudia Mwenyezi Mungu.407

Nyongeza juu ya sehemu hii Katika al-Khisal: Kutoka kwa Abi al-Qasim Abdillah ibn Ahmad ibn Amir al-Ta’i, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa ar-Ridha, kutoka kwa baba zake kutoka kwa Ali ibn Abi Talib (a.s) ambaye amesema: Mitume (amani juu yao) wanalala wakiwa wamelalia migongo yao.408 Kidokezo: Habari ndefu za hadithi hii zimesimuliwa katika al-‘Uyun na alFaqih.409 2. Katika Majmu’at Warram: Inasemekana kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na wake tisa na kati yao walichangia shuka la kitanda moja ambalo lilitiwa 405 Makarim al-Akhlaq: 38, Amali al-Saduq: 377, Bihar al-Anwar, 16: 217 406 Makarim al-Akhlaq: 38, Ihya al-‘Ulum al-Din 2:376 407 Makarim al-Akhlaq: 39, Muhasibat al-Nafs: 36 408al-Khisal: 263 409Uyun Akhbar ar-Ridha: 246; al-Faqih 4: 365 78


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 79

SUNAN-NABII rangi ama kwa ‘wurs410 au kwa zafarani. Pale ilipokuwa ni usiku wa mke mmoja, wangelipeleka shuka hilo kwake na maji kiasi yangenyunyizwa juu yake ili kwamba liweze kutoa harufu nzuri.411 3. Katika al-Khisal: Kutoka kwa Muhammad ibn Muslim, kutoka kwa Abi Abdillah, kutoka kwa Abi Ja’far, kutoka kwa baba zake kutoka kwa Ali (a.s.) ambaye amesema: “Kukaa macho katika (sehemu ya mwisho ya) usiku kuna afya kwa ajili ya mwili, kunamridhisha Mola Mwenye enzi, ni njia ya huruma ya kiungu na kushikamana na akhlaq ya mitume (amani juu yao wote).412 Maelezo: Hii imesimuliwa pia kutoka kwa ibn Shu’bah katika Tuhf al-‘Uqul na alBarqi katika al-Mahasin kutoka kwa Basir kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.). 413 4. Katika al-Kafi: Katika riwaya yake kutoka kwa ibn al-Qaddah kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokwenda kulala huwa angesema: “Ewe Mungu Wangu! Kwa jina Lako mimi ninaishi, na nitakufa kwa jina lako.” Na wakati alipoamka huwa angesema: “Utukufu na sifa zote ni za Mwenyezi Mungu aliyenipa mimi uhai baada ya kunifisha, na Kwake Yeye ndio marejeo.”414 Maelezo: Hii pia imesimuliwa na al-Saduq ndani ya al-Faqih na at-Tabarsi katika al-Makarim.415 5. Katika al-Kafi: Ndani ya riwaya yake kutoka kwa Muhammad ibn Marwan ambaye amesema: Abu Abdillah (a.s.) amesema “Je! Nisiwaambie kile ambacho Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alichokuwa akisema wakati alipokuwa akienda kulala?” Mimi nikasema: “Ndiyo, tuambie.” Yeye akasema: “Yeye Mtume (s.a.w.w.) angesoma Ayatul-Kursi416 na kisha angesema: 410 Wurs – Mti wa rangi ya manjano (unaofanana na ufuta) ambao unachanua mara tu baada ya majira ya kuchipua na unatumika kama rangi (tr.) 411 Majmu’at Warram: 266 412 al-Khisal: 121, Tahdhib al-Ahkam 2: 121 413 Tuhf al-‘Uqul: 101, al-Mahasin: 53 414al-Kafi 2: 539 415 al-Faqih 1: 480, Makarim al-Akhlaq: 39 416 Surat al-Baqarah; 2: 255-257 79


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 80

SUNAN-NABII “Kwa jina la Allah, mimi ninamuamini Mwenyezi Mungu na wala siamini miungu ya uwongo. Ewe Mungu Wangu! Nilinde nikiwa kwenye kulala kwangu na wakati ninapokuwa macho.”417 6. Katika al-Makarim: Yeye Mtume (s.a.w.w.) angepumzika mara nyingi kwenye mto uliotengenezwa kwa ngozi na kufutikwa na nyuzi za magome ya mtende na angekaa pia akiwa ameegemea juu yake huo.418 7. Vilevile: Kama Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angeona kitu ambacho kinatisha katika usingizi wake, basi yeye (angemkumbuka Mungu na) angesema: “Yeye ni Mwenyezi Mungu – aliye peke ambaye hana mshirika.” Na pale aliposimama kwa ajili ya kutaka kuswali angesema: “Alhamdu’lillahi nuuru samaawati wal-ardhi, wa Alhamdu’lillahi Qayuumus-Samaawaati wal-ardhi, wa Alhamdu’lillahi Rabussamaawaati wal-ardhi, wa man fiihinna. Antal-haqqu wa qaulukalhaqqu, wa liqaaukal-haqqu wal-jannatu haqqu wan-naaru haqqu, wa sa’atu haqqu. Allahuma laka aslamtu wa bika amantu wa a’alayka tawakal’tu, wa ilayka uniibu wa bika khaswamtu wa ilayka haakamtu. Faghfir liy maa qaddamtu wa maa akhar’tu wa maa asrar’tu wa maa aa’lantu. Anta ilaahiy laa ilaha illa anta.” “Utukufu wote unastahiki ni wake Allah, aliye nuru ya mbingu na ardhi na Msimamizi wa mbingu na ardhi. Sifa zote ni za Allah, Mola wa mbingu na ardhi na vyote vilivyomo. Wewe ni Haki na maneno yako ni kweli halisi, na kurejea kwako ni kweli, pepo ni kweli, na moto wa Jahannam ni kweli na ile saa iliyokadiriwa (Qiyamah) ni kweli. Ewe Mungu Wangu! Kwako nimesalim amri na ni Wewe ninayekuamini. Kwako ni mategemeo yangu na marejeo ni Kwako. Kwa ajili yako nagombana, na kwa ajili Yako nahukumu. Zako napigana na maadui zangu na ninatafuta haki kutoka Kwako. Nakuomba unisamehe madhambi yangu, niliyotanguliza na ya sasa, niliyoyafanya katika siri na niliyofanya kwa dhahiri. Wewe ni Mungu Wangu – hapana mungu ila ni Wewe.” Halafu apige mswaki kabla ya kuchukua wudhuu.419

417 al-Kafi; 2: 536 418 al-Makarim al-Akhlaq: 38 419 Makarimu al-Akhlaq: 292 80


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 81

SUNAN-NABII Maelezo: Kuna riwaya nyingine zitakazokuja katika sehemu ya Dua Mwenyezi Mungu akijaalia.

kama

8. Katika al-Falah al-Sa’il: Kutoka kwa al-Hasan ibn Ali al-Alawi, kutoka kwa Ali ibn Muhammad ibn Musa ar-Ridha (a.s.) ambaye amesema: Sisi, wana Ahlul-Bayt, tunazo tabia kumi wakati tunapolala: Kujitoharisha (kwa wudhuu), kulalia upande wa kulia, kusoma “Subhanallah” mara thelathini na tatu, na kusoma “Alhamdulillah” mara thelathini na tatu, kusoma “Allahu Akbar” mara thelathini na nne, kuelekea Qiblah, kusoma Fatihat al-Kitab (Surat al-Hamd) na Ayatul-Kursi na kushahidia kwa Allah kwamba hapana mungu ila Yeye ….. na yule atakayefanya matendo haya atakuwa amejipatia fungu lake la manufaa kutoka kwenye usiku huo.420 9. Katika al-Kafi: Katika riwaya yake kutoka kwa Muhammad ibn Marwan ambaye amesema: Abu Abdillah (a.s.) amesema: “Je, nisiwaambie kile ambacho Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alichokuwa akitumia kukisema wakati anapoingia kwenda kulala?” Mimi nikasema: “Ndiyo, tuambie.” Yeye akasema: “Yeye (s.a.w.w.) huwa angesoma Ayat al-Kursi421 na halafu angesema: “Kwa jina la Allah ‘Azza wa Jalla. Ninamuamini Mwenyezi Mungu na kuwakana miungu wa uwongo. Ewe Allah, nilinde katika usingizi wangu na wakati ninapokuwa macho.”422 10. Katika at-Tahdhib: Abu Abdillah (a.s.) amesema: Dumisheni zile swala za usiku kwani kwa hakika hilo ni katika Sunnah ya Mtume wenu (s.a.w.w.).423

420 Falah al-Sa’il: 280 421 Surat al-Baqarah; 2: 255-257. 422 al-Kafi, 2:536 423 Tahdhib al-Ahkam, 2: 120, Da’wat al-Rawandi: 272 81


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 82

SUNAN-NABII

MLANGO WA 8 ADABU ZA NDOA NA WATOTO 1. Katika al-Khisal: Katika riwaya yake kutoka kwa Ali (a.s.) ambaye amesema: Oaneni, kwani kwa hakika ndoa ni Sunnah ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na yeye angeweza kusema: “Yeyote yule anayependa kufuata Sunnah yangu anapaswa kufunga ndoa kwani ndoa ni kutoka kwenye Sunnah yangu.”424 2. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Ma’mar ibn Khallad ambaye amesema: Nilimsikia Ali ibn Musa ar-Ridha (a.s.) akisema: Mambo matatu ni kutoka kwenye Sunnah ya mitume (amani juu yao wote): Manukato, kuondoa nywele (zilizozidi) kutoka mwilini na kuzidisha uhusiano wa ndani na wake zao.425 Kidokezo: al-Saduq, at-Tusi, na wengine wamesimulia hadithi kama hizohizo kwa sanadi mbalimbali za wasimuliaji.426 3. Kutoka kwa al-Murtadha katika Risalat al-Muhkam wal-Mutashabih: Katika simulizi yake kutoka kwenye Tafsir al-Nu’mani kutoka kwa Ali (a.s) ambaye amesema: Kikundi cha masahaba kilijinyima chenyewe ukaribu wa ndani na wake zao, kula wakati wa mchana na kulala wakati wa usiku. Umm Salamah akamuarifu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuhusu hili hivyo yeye akaja kwa masahaba zake na akasema: “Je, mnajizuia kuhusiana na wake zenu ambapo mimi ninakwenda kwa wake zangu na ninakula wakati wa mchana na kulala usiku? Kwa hiyo, yeyote ambaye hatafuata Sunnah yangu, huyo hatokani na mimi.”427 Kidokezo: Riwaya kama hizo zimetajwa katika vitabu vingine kwa sanadi tofauti za wasimuliaji.428 4. Katika al-Kafi: Katika riwaya yake kutoka kwa Ishaq ibn Ammar kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Kutoka katika Akhlaq ya mitume (a.s.) ni mapenzi juu ya wanawake.429 5. Vilevile, imesimuliwa kutoka kwa Bakkar ibn Kurdam, bila ya msimuliaji mmoja, kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume 424 al-Khisal: 614 425 al-Kafi, 5: 350 426al-Faqih 3: 382, Tahdhib al-Ahkam 7: 403, Tuhf al-Uqul: 442 427 al-Muhkam wal-Mutashabih: 73 428 Da’aim al-Islam 2:191, Jami’ al-Akhbar: 271 429 al-Kafi 5: 32, Tahdhib al-Ahkam 7: 403, Makarim al-Akhlaq: 197

82


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 83

SUNAN-NABII (s.a.w.w.) amesema: Nuru ya macho yangu ilipatikana katika salah na furaha yangu (ilipatikana) kwa wanawake.430 Kidokezo: Hadithi kama hiyo inaweza kupatikana pamoja na sanadi nyingine za wasimuliaji. 6. Katika al-Faqih yeye alisema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipotaka kumuoa mwanamke, yeye angetuma mtu mwingine kwenda kumuona (kwanza).431 7. Katika Tafsir al-Ayyashi: Kutoka kwa al-Hasan ibn Bint Ilyas ambaye amesema: Nilimsikia Aba al-Hasan ar-Ridha (a.s.) akisema: Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. ameufanya usiku kuwa chanzo cha utulivu na amewafanya wanawake pia kuwa ni chanzo cha utulivu. Ni kutoka katika Sunnah kuoa wakati wa usiku na kuandaa chakula kwa watu (katika tukio la ndoa).432 8. Katika al-Faqih: Ndani ya riwaya yake kutoka kwa Harun ibn Muslim ambaye amesema: Nilimuandikia Sahib al-Dar (a.s.): Mimi nilipata kuzaliwa mtoto, kisha nikazinyoa nywele zake na kuzipima na dirham na nikatoa sadaka. Yeye (a.s.) akasema: Hairuhusiwi kuzipima isipokuwa dhidi ya dhahabu au fedha, na hii ndio Sunnah. 433 9. Katika al-Khisal: Ndani ya riwaya yake kutoka kwa Ali (a.s.) ambaye amesema: Mnamo siku ya saba, tekelezeni ile ‘aqiqah434 kwa ajili ya watoto wenu na toeni kinacholingana katika uzito wa nywele zao katika fedha kama sadaka kwa Mwislam. Hivi ndivyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alivyofanya kwa ajili ya Hasan na Husein (a.s.) na kwa watoto wake wengine wote.435

Nyongeza kwa sehemu hii 1. Katika al-Faqih: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Kwa hakika mbora kutoka miongoni mwenu ni yule ambaye ni mwema kwa wake zake, na mimi ndio mbora zaidi kutoka miongoni mwenu kwa kuwa mwema kwa wake zangu.436 430 al-Kafi, 5:321 431 al-Faqih 3:388, Tahdhib al-Ahkam 7: 402, Makarim al-Akhlaq: 199, al-Mustadrak 14: 180 432 Tafsir al-Ayyashi, 1: 371 – Surat al-An’am (6), Tahdhib al-Ahkam 7: 418, Tafsir alBurhan, 1:544 – Surat al-An’am (6), Tuhf al-Uqul: 445 433 al-Faqih 3:481 434 Uchinjaji wa mbuzi katika tukio la kuzaliwa kwa mtoto. (Mfasiri) 435 al-Khisal: 619, Tuhf al-‘Uqul: 109 436 al-Faqih, 4: 443 83


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 84

SUNAN-NABII 2. Katika al-Kafi: Katika riwaya yake kutoka kwa Ibn Mahbub, bila msimuliaji hata mmoja, kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Nabii Ibrahim (a.s.) alikuwa mwenye kupenda kulinda heshima yake na mimi ni mwenye kuilinda heshima yangu zaidi kuliko yeye alivyokuwa.437 Kidokezo: Hii imesimuliwa na al-Saduq ndani ya al-Faqih na al-Tabarsi ndani ya al-Makarim.438 3. Katika al-Da’aim: Kutoka kwa Ja’far ibn Muhammad (a.s.) – katika kisa cha nabii Musa (a.s.): Musa alisema (kumwambia binti yake Shu’aib, a.s.): “Tembea nyuma yangu na unionyeshe njia, kwani kwa hakika sisi (mitume) hatuwaangalii wanawake kwa nyuma kwao.”439 4. Katika al-Faqih: Bakr ibn Muhammad amesimulia kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) akisema: Nilimuuliza yeye kuhusu ile ndoa ya muda. Yeye akasema: “Mimi nisingependelea kwa mtu, kwamba aweze kuitoka dunia hii wakati akiwa hajatekeleza tendo ambalo lilifanywa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).440 5. Katika al-Makarim: Kutoka kwa Abi Qiladah kwamba wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipomuoa mwanamke bikra, angebakia naye kwa siku saba na pale alipomuoa mjane angeweza kubakia naye kwa muda wa siku tatu.441 6. Katika al-Mahasin: Kutoka kwa al-Hasan al-Washa’ kutoka kwa Abul-Hasan arRidha (a.s.): al-Najjashi alimtafuta mkono wa uchumba (kumchumbia) Umm Habiba binti Abi Sufyan kwa ajili ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na wakati alipomuoa yeye, aliwakaribisha watu kwa ajili ya chakula akisema: “Hakika ni kutoka kwenye Sunnah ya mitume kuwakaribisha watu kwenye chakula wakati wa harusi.”442 7. Katika Maj’ma’ul-Bayan: Kutoka kwa Abi Qilabah: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angegawa (sawa kwa sawa) miongoni mwa wake zake akisema: “Ewe Mungu Wangu! Huu ndio ugawaji wangu wa kile nilichonacho kwa hiyo naomba usinilaumu mimi kwa kile Wewe ulichonacho na mimi nikawa sinacho.443 437 al-Kafi, 5: 536; al-Mahasin, 1: 115 438 al-Faqih, 3: 444; Makarim al-Akhlaq: 239 439 Da’aim al-Islam, 2: 201 440 al-Faqih, 3: 463; al-Mustadrak, 14: 451; Bihar al-Anwar, 103: 305 441 Makarim al-Akhlaq: 213 442 al-Mahasin, 2: 418 443 Maj’ma’ul-Bayan, 3: 121 – Suratun-Nisa (4) 84


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 85

SUNAN-NABII 8. Katika al-Amali ya at-Tusi: Kutoka kwa Umm Salama, mke wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema kwamba, yeye alisema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikwenda hijja yake ya mwisho (Hijjatul-Wida’) akiwa ameandamana na wake zake na yeye angeweza kwenda kwa mke mmoja kila siku mchana na usiku, akitaka kuwa muadilifu kwao wote.444 9. Katika al-Maj’ma’: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipomaliza swala yake ya asubuhi, angeweza kuwatembelea wake zake wote, mmoja baada ya mmoja.445 10. Katika al-Ja’fariyat: Katika simulizi yake kutoka kwa Ali (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Nyakati zilizopita zote hazina maana isipokuwa kwa matatu: Matumizi ya utupaji mishale, kumfundisha na kumpa mazoezi farasi wako, na kucheza na kufurahi na familia yako, kwani hayo ni kutoka kwenye Sunnah.446 11. Katika Maj’ma’ul-Bayan: Kutoka kwa Ja’far as-Sadiq kutoka kwa baba zake (a.s.) kwamba hata wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa mgonjwa, angeweza kuomba apelekwe kwenye nyumba ya mke ambaye alikuwa ndiye mwenye zamu yake (ya kuwa naye Mtume).447 12. Katika al-Faqih: Kutoka kwa al-Halabi, kutoka kwa Abi Abdillah kutoka kwa baba zake (amani juu yao wote): Maymuna, mke wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akitumia kusema: “Pale nilipokuwa kwenye vipindi vyangu vya mwezi alikuwa akiniambia nifunge nguo na kujifunika na kwenda kulala naye kitandani.448 13. Katika al-Kafi: Kutoka kwa Hammad ibn Isa kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Baba yangu alisema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kamwe hajawahi kutaja zaidi ya ‘awqiyyah’ na ‘nash’ moja kwa ajili ya mahari ya binti zake na wake zake. ‘Awqiyyah’ moja ikiwa ni sawa na dirham arobaini na ‘nash’ moja sawa na dirham ishirini.449 Maelezo: al-Kulayni amesimulia riwaya kama hizo kwa sanadi nyingine za wasimuliaji na hii pia imesimuliwa na al-Saduq ndani ya al-Ma’ani, at-Tusi katika at-Tahdhib na ibn Shahr Ashib katika al-Manaqib.450 444 Amal at-Tusi, 2: 89 445 Maj’ma’ al-Bayan, 10: 313 – Suratut-Tahrim (66) 446 al-Ja’fariyat: 87 447 Maj’ma’ul-Bayan, 3: 121 – Suratun-Nisa (4) 448 al-Faqih, 1: 99 449 al-Kafi, 5: 376 450 Manaqib Ali ibn Abi Talib, 1: 161 85


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 86

SUNAN-NABII 14. Katika al-Makarim: Yeye Mtume (s.a.w.w.) angeomba dua: “Ewe Mungu Wangu! Najikinga Kwako dhidi ya mtoto ambaye atakuwa mtawala juu yangu, na dhidi ya mali ambayo itakuwa ndio chanzo cha kuangamia kwangu na dhidi ya mke ambaye atanifanya nizeeke kabla ya wakati wangu.451 Kidokezo: Riwaya nyingine inayofanana kama hii imesimuliwa na al-Kulayn kutoka kwa al-Sakuni kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.).452 15. Katika ‘Uddat al-Da’i: ar-Ridha (a.s.) amesema: “Wakati mtoto wa kiume alipozaliwa kwetu tungeweza kumpa jina la Muhammad na baada ya siku saba tungeweza kulibadili jina lake hilo kama tungependa, vinginevyo tungeweza kuliacha kama lilivyo.”453 16. Vilevile: Nyakati za asubuhi, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angeweza kupapasa papasa kwa mapenzi vichwa vya watoto na wajukuu zake.454 17. al-Sayyid Hashim at-Tawbali katika Madinat al-Ma’ajiz kutoka kitabu Musnad Fatima (a.s.) katika riwaya yake kutoka kwa Ali ibn Abdillah kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Wakati Fatima (a.s.) alivyohamia kwenye nyumba ya Ali (a.s.) katika usiku wa kwanza wa ndoa yao, Jibril, Mika’il na Israfil walishuka – na Jibril akatoa wito wa Takbir na vivyo hivyo akafanya Mika’il na Israfil, wakifuatiwa na malaika wengine na ikawa ni Sunnah (kusoma takbir) katika usiku ule wa kwanza, mpaka Siku ya Hesabu.455 Maelezo: Hadithi kama hiyohiyo inaweza kupatikana ndani ya al-Faqih na katika Amali ya Sheikh at-Tusi. Katika baadhi ya vyanzo (imesimuliwa hivi): ….. na Waislam wanaisoma takbir na ilikuwa ndio mara ya kwanza kusomwa takbir katika usiku wa kwanza wa harusi hivyo ikawa ni Sunnah (tangu hapo na kuendelea). 18. Katika al-Khisal kutoka kwa Ali (a.s.) ambaye amesema: Vitieni utamu vinywa vya watoto wenu wanaozaliwa kwa tende, na hivi ndivyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alivyofanya kwa Hasan na Husein (a.s.).456 451 Makarim al-Akhlaq: 203 452 al-Kafi, 5: 326 453 Uddat al-Da’i: 77 454 Uddat al-Da’i: 79; Bihar al-Anwar, 104: 99 455 Imesimuliwa na al-Nuri ndani ya al-Mustadrak, 14: 197, Dala’il al-Imamah: 25 456 al-Khisal: 637 86


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 87

SUNAN-NABII Kidokezo: Hii imesimuliwa vilevile na Tabarsi ndani ya al-Makarim na ibn Sha’bah katika Tuhf al-‘Uqul.457 19. Katika al-Makarim: as-Sadiq (a.s.) amesema: Kuna matendo saba ambayo ni Sunnah kuyatenda wakati mtoto wa kiume anapozaliwa. Kwanza apewe jina. Pili, kichwa chake kinanyolewa. Tatu, sadaka inatolewa kwa kiwango kinacholingana na uzito wa nywele zake kwa fedha au dhahabu ikiwezekana. Nne, ile ‘aqiqah inafanyika. Tano, kichwa chake kinapakazwa zafarani. Sita, anatoharishwa kwa kutahiriwa. Saba, majirani wanagawiwa ile nyama inayotokana na ‘aqiqah.458 20. Vilevile: Kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): Kutahiriwa ni Sunnah kwa mwanaume na ni heshima kwa wanawake.459 21. Katika al-Kafi: Ndani ya riwaya yake kutoka kwa Mus’ada ibn Sadaqah kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Kutoboa sikio la mvulana ni kutoka katika Sunnah na kutahiriwa baada ya siku saba (vilevile) ni katika Sunnah.460 Kidokezo: al-Kulayni ameisimulia hii kwa sanadi nyingine ya wasimulizi na atTabarsi anasimulia riwaya kama hiyo hiyo ndani ya al-Makarim.461 22. Katika Ikmal al-Din: Kutoka kwa Abi Ahmad Muhammad ibn Ziyad al-Azadi: Wakati ar-Ridha (a.s.) alipozaliwa, mimi nilimsikia Abul-Hasan Musa ibn Ja’far (a.s.) akisema: Mtoto wangu huyu alizaliwa akiwa ametahiriwa, tohara na aliyetakaswa, na Maimam wote walizaliwa wakiwa wametahiriwa, tohara na waliotakaswa, lakini bado nitampitia kwa wembe ili kutimiza ile Sunnah na kufuata kanuni ya al-Hanafiyyah.462 Kidokezo: Hadithi kama hiihii imetajwa katika al-Makarim.463 23. Katika al-Kafi: Katika riwaya yake kutoka kwa Ma’mar ibn Khathim katika hadithi kutoka kwa Abi Ja’far (a.s.): Sisi tunatoa majina kwa watoto wetu wakiwa bado ni wadogo wasijekuwa wakapewa majina yasiyopendeza baadae.464 457 Makarim al-Akhlaq: 229; Tuhf al-‘Uqul: 124 458 Makarim al-Akhlaq: 228, Bihar al-Anwar, 104:122 459 Makarim al-Akhlaq: 229; al-Da’awat: 283; al-Mustadrak, 15: 149, Tahdhib al-Ahkam, 2: 445 460 al-Kafi, 6: 35 461 al-Kafi, 6: 36; Makarim al-Akhlaq: 230 462 Kamal al-Din wa Tamam al-Ni’mah; 2: 433 463 Makarimu al-Akhlaq: 230 464 al-Kafi, 6: 20; Tahdhib al-Ahkam, 7: 438 87


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 88

SUNAN-NABII 24. Katika al-Kafi: Katika riwaya yake kutoka kwa al-Sakuni, kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: “Ni Sunnah na uadilifu kwa mtu kutumia kuitwa pamoja na jina la baba yake.” Na katika nakala zingine: “kwa jina la mwanawe wa kiume.”465 25. Vilevile: Katika riwaya yake kutoka kwa Al-Halabi, kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Sisi tunawaelekeza watoto wetu wa kiume kuswali wanapofikia umri wa miaka mitano, hivyo waelekezeni vijana wenu kuswali wanapofikia umri wa miaka saba. Tunawaambia vijana wetu kufunga wanapokuwa na umri wa miaka saba – kwa kiasi chochote cha kutwa moja wanachoweza – iwe ni nusu ya mchana au zaidi ya hapo au pungufu yake, na kama wakizidiwa na kiu wangeweza kuvunja saumu zao, mpaka wanaifanya kuwa ni tabia na kupata uwezo wa kufunga kwa siku nzima. Kwa hivyo, vijana wenu wanapokuwa na umri wa miaka tisa, wafundisheni kufunga kwa kiasi chochote katika siku nzima watakachoweza kuhimili, na iwapo watazidiwa na kiu, waruhusuni kuvunja funga zao.466 Kidokezo: Hii imesimuliwa vilevile na al-Saduq katika al-Faqih.467 26. Katika Majmu’at Warram: Imesimuliwa kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba wakati familia yake ilipokumbwa na ufukara au dhiki, yeye alisema: “Simameni kwa ajili ya swala.” Na angeweza kusema: “Hiki ndio ambacho Mola Wangu ameniamuru kufanya.” Allah ‘Azza wa Jalla. amesema: “Na waamrishe watu wako kuswali, na uendelee kwa hayo, hatukuombi riziki bali sisi tunakuruzuku, na mwisho mwema ni kwa mchamungu.”468 27. Katika al-Muqni’: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipotaka kuoa mwanamke angetuma (mwanamke) kwake akisema: “Nusa kwenye shina la shingo yake, kwani kama shingo yake itanukia vizuri, kadhalika na jasho lake litanukia vizuri, na kama tindi za miguu yake ni nene vizuri, basi atakuwa na ashiki kubwa.469 28. Kutoka ndani ya ad-Durr al-Manthur: Kutoka kwa al-Mughira ibn Shu’bah ambaye alisema: Sa’d ibn Ibadah amesema: “Kama ningekuwa nimuone mtu na mke wangu, ningempiga kwa upanga wangu.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alijulishwa kuhusu hili na akasema: “Je, unashangazwa kuhusu hali ya heshima ya Sa’d? 465 al-Kafi, 2: 162; al-Ja’fariyat: 189; al-Mustadrak; 15: 131; Bihar al-Anwar, 104: 131 466 al-Kafi, 3: 409; Tahdhib al-Ahkam, 2: 380 467 al-Faqih, 1: 280 468 Majmu’at Warram, 1: 184, Musakkin al-Fawa’id: 50, al-Mustadrak, 6: 395, Surat Taha; 20: 132 469 al-Muqni’: 100; al-Faqih; 3: 388; Tahdhib al-Ahkam; 7:402; Mustadrak; 14: 180 88


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 89

SUNAN-NABII Wallah mimi nina hali bora kabisa ya heshima kuliko Sa’d, na Mwenyezi Mungu anayo hali bora zaidi ya heshima kuliko mimi, na ni kwa sababu ya hili kwamba amekataza matendo maovu, ya dhahiri yote na siri, na hakuna kwenye hadhi bora zaidi kuliko Mwenyezi Mungu.”470 29. Bibi Khadija (amani iwe juu yake) alikuwa ndiye mtu wa kwanza kumuamini Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. Na Mtume Wake (s.a.w.w.) na alikikubali kile alichokileta kutoka kwa Mwenyezi Mungu na akamsaidia katika kazi yake na kwake bibi huyu, Mwenyezi Mungu aliufanya wepesi uzito wa mzigo wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Yeye (s.a.w.w.) kwa kweli angeweza kuwa mwenye kukata tamaa pale watu walipomgeuzia masikio viziwi au walipojaribu kumsingizia na hili lingeweza kumfanya ahuzunike sana. Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. alimfariji kwa yeye. Wakati alipokuwa akirudi nyumbani kwa bibi huyu, yeye angemsaidia, kumliwaza yeye na kumpunguzia fadhaa ya watu – mpaka alipofariki bibi huyu, Mwenyezi Mungu amrehemu.471 30. Wakati wowote yeye (s.a.w.w.) alipomkumbuka Khadija (a.s.), asingeweza kuchoka kumsifia yeye na kumuombea msamaha kwa Mwenyezi Mungu.472 31. Nawadir ar-Rawandi: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Sisi Ahlul-Bayt tumebarikiwa na sifa bainifu saba ambazo hakuna yoyote aliyekuwa nazo kabla yetu wala yeyote baada yetu atakayekuwa nazo: Neema, ufasaha, ukarimu, ujasiri, elimu, uungwana na upendo kwa wanawake.473

470 ad-Durr al-Manthur; 3: 81 – Surat al-A’raf (7) 471 Bihar al-Anwar; 16: 10 472 Bihar al-Anwar, 16: 14 473 Nawadir al-Rawandi: 15; Bihar al-Anwar; 103:228

89


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 90

SUNAN-NABII

MLANGO WA 9 VYAKULA, VINYWAJI NA ADABU ZA MEZANI 1. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Hisham ibn Salim na wengineo, kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Hakuna jambo lililopendwa sana na Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) kuliko kubakia na njaa na hofu juu ya Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla.474 2. Kutoka kwa al-Saduq katika al-Amali: Kutoka kwa al-‘Ays ibn al-Qasim ambaye amesema: Nilimuuliza as-Sadiq (a.s.): Kuna hadithi imesimuliwa kutoka kwa baba yako kwamba yeye amesema: “Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) hakuwahi kamwe kukinai kula mkate wa ngano,” je, hii ni kweli? Yeye akajibu: Hapana, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakula mkate wa ngano kamwe, na hakuwahi kuwa amekinahishwa na mkate uliotengenezwa kwa shayiri.475 3. Katika al-Ihtijaj ya at-Tabarsi: Katika riwaya yake kutoka kwa Musa ibn Ja’far, kutoka kwa baba zake, kutoka kwa Husein ibn Ali (a.s.) katika hadithi ndefu juu ya maswali ya Myahudi mmoja kutoka Damascus aliyomuuliza Amirul-Mu’minin (a.s): Myahudi huyo alimwambia: “Wanadai kwamba Isa (a.s.) alikuwa mwenye kujinyima raha na anasa, je ni kweli?” Ali (a.s.) akamwambia: “Hivyo ndivyo alivyokuwa; na Muhammad (s.a.w.w.) alikuwa mwenye kujihini sana kuliko mitume wengine wote. Yeye alikuwa na wake kumi na watatu mbali na idadi kadhaa ya vijakazi, lakini hakuna hata mara moja ambapo mabaki yaliokotwa kutoka kwenye tandiko la meza yake ya chakula. Yeye hakula mkate wa ngano kabisa na hajawahi kukinai kwa mkate wa shayiri kwa siku tatu usiku mfululizo.”476 4. Katika Nahjul-Balaghah: Yeye (a.s.) amesema: Unapaswa kumfuata Mtume wako, yule halisi na mtakatifu wa watu wote wa dunia hii, yeye alitosheka kwa kidogo sana na aliyekuwa na tumbo tupu zaidi. Yeye aliiaga dunia hii akiwa mwenye njaa lakini akaingia kwenye hiyo dunia nyingine mkamilifu kabisa.477 474 al-Kafi, 8: 129 na 163 475 ‘Amali al-Saduq:263; Makarimu al-Akhlaq: 28 476 al-Ihtijaj: 225 477 Nahjul-Balaghah: 227 90


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 91

SUNAN-NABII 5. Kutoka kwa al-Qutb katika Da’awat yake, yeye amesema: Imesimuliwa kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kamwe hakuwa kula katika hali ya kuegemea mahali isipokuwa mara moja tu, kisha (baada ya kulitambua hilo) alikaa wima na akasema: “Ewe Mungu Wangu! Mimi ni mja na mtume Wako.”478 Maelezo: Hii imesimuliwa pia na al-Kulayni na at-Tusi kwa sanadi za wasimuliaji nyingi tofauti; na kadhalika na al-Saduq al-Barqi; na al-Husein ibn Sa’id katika kitabu chake, al-Zuhd.479 6. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Zayd al-Shahham kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakuwahi kula akiwa amekaa mkao wa kuegemea, kuanzia wakati alipotumwa na Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. hadi wakati pale alipomchukua kutoka dunia hii. Alikuwa akitumia kula kama mtumwa na kukaa kama mtumwa vilevile. Mimi nikauliza: “Kwa nini ilikuwa hivyo?” Yeye akasema: “Kutokana na unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla.”480 7. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Abi Khadijah ambaye amesema: Bashi al-Dahhan alimuuliza Abi Abdillah (a.s.) wakati mimi nikiwepo: “Je, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akila huku akiwa ameegemea kulia na kushoto kwake?” Yeye akajibu: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) hakuegemea kulia kwake au kushoto kwake, bali alikaa kama mtumwa.” Mimi nikauliza: “Kwa nini ilikuwa hivi?” Yeye akajibu kwamba: “Ni kutokana na unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla.”481 8. Vile ile: Imesimuliwa kutoka kwa Jabir kutoka kwa Abi Ja’far (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akila kama mtumwa na kukaa kama mtumwa. Angeweza kula amekaa chini na kulala chini.482 Kidokezo: Wale wanachuoni watatu wa kuheshimika, al-Barqi, al-Husein ibn Sa’id na at-Tabarsi wamesimulia riwaya nyingi zenye kufanana kama hizi.483 478 al-Da’awat: 138; al-Mustadrak 16: 225 479 al-Kafi, 6: 272; Tahdhib al-Ahkam, 9: 93; al-Faqih, 3: 354; al-Mahasin, 456-457; alZuhd ya ibn Sa’id al-Ahwazi: 39 480 al-Kafi, 6: 270; al-Makarim al-Akhlaq: 27; Da’aim al-Islam, 2: 119; Faydh al-Qadir, 5:181. 481 al-Kafi, 6:271, al-Mahasin: 457 482 al-Kafi, 6: 271 483 al-Kafi 6:27; al-Faqih 3:354; Tahdhib al-Ahkam 9:93; al-Mahasin: 457; Makarim alAkhlaq: 27 91


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 92

SUNAN-NABII 9. Kutoka kwa al-Ghazali ndani ya al-Ihya: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokaa kwa ajili ya kula, angekaa kwa kupiga magoti yake na nyayo pamoja kama vile mtu anayeswali anavyokaa, isipokuwa kwamba goti moja lingekuwa juu ya jingine, na mguu mmoja juu ya mwingine, na angesema: “Mimi ni mtumwa tu, ninakula kama vile anavyokula mtumwa na ninakaa kama vile mtumwa anavyokaa.484 10. Katika al-Ta’rif cha al-Safwani: Kutoka kwa Amirul-Mu’minin (a.s.): Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokaa chini kwenye tandiko la mezani (ili kula), yeye alikaa kama vile anavyokaa mtumwa na angekaa akiegemea kwenye paja lake la kushoto.485 11. Katika al-Makarim: Kutoka kwa ibn Abbas ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akikaa chini juu ya ardhi na angemzuia kondoo jike (ili kumkamua), na kukubali mwaliko wa mtumwa kujiunga naye katika kula mkate wa shayiri.486 12. Kutoka kwa al-Barqi ndani ya al-Mahasin: Imesimuliwa kutoka kwa Abi Khadijah kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.): Yeye, (s.a.w.w.) angekaa kama vile anavyokaa mtumwa na kuweka mkono wake chini na kula kwa vidole vitatu. Abi Abdillah (a.s.) amesema: Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alikuwa akila kama hivyo na sio kama wale wenye kiburi wanavyokula.487 Maelezo: Ni dhahiri kutokana na hili kwamba pale inaposemwa kuwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakutumia kuegemea kamwe, haijumuishi na kuegemea kwenye mkono ambao umewekwa chini, bali inaashiria kwenye kuegemea kwenye mto au kiti na mambo kama haya yalikuwa yamezoeleka kutendwa na wafalme na wengineo. Hili linaweza kuonekana kwenye maneno ya as-Sadiq (a.s.) kwa yule mtu ambaye alimwambia asiegemee kwenye mkono wake (wakati wa kula). Aliposema hivyo kwa mara ya tatu, Imam (a.s.) akamwambia: “Wallahi! Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakulikataza hili – kamwe.”488 13. Vilevile: Imesimuliwa kutoka kwa Hammad ibn Uthman kutoka kwa Abi Abdillah kutoka kwa baba yake (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na mazoea ya kulamba vidole vyake baada ya kula.489 484 Ihya ‘Ulum al-Din 2: 369; Makarim al-Akhlaq: 27 485 al-Nuri ameisimulia hii katika al-Mustadrak 16: 228 486 Makarim al-Akhlaq: 16; Amali al-Tusi 2:7 487 al-Mahasin: 441; al-Kafi 6: 297; al-Fayd al-Qadir 5: 196 488 al-Kafi 6: 271; Fayd al-Qadir 5: 128 489 al-Mahasin: 443 92


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 93

SUNAN-NABII Kidokezo: Hii imesimuliwa vilevile kwa sanadi nyingine ya wasimulizi na atTabarsi pia ameisimulia katika al-Makarim kwa sanadi kamili ya wasimuliaji.490 14. Katika al-Makarim: Wakati yeye Mtume (s.a.w.w.) alipokula komamanga, yeye alikuwa hashirikiani na mtu yoyote.491 15. Katika al-Makarim, akinukuu kutoka kwenye Mawalid al-Sadiqin, yeye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akitumia kula aina mbalimbali za vyakula. Yeye alikula kile ambacho Mwenyezi Mungu amemfanyia kuwa halali, pamoja na familia yake na watumishi, na pamoja na yule ambaye amemkaribisha yeye kutoka miongoni mwa Waislam, akiwa amekaa chini au katika kile ambacho wao walikuwa wamekalia juu yake kwa ajili ya chakula, na kula kutoka katika kile walichokula, isipokuwa wakati mgeni angeweza kuwasili, hali ambayo angeweza kula na mgeni wake na chakula alichokuwa anakipenda zaidi kilikuwa ni kile ambacho watu wengi walikuwa wakila.492 16. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa ibn al-Qaddah kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa anakula na watu, yeye alikuwa ndiye wa kwanza kuanza kula na wa mwisho kuacha kula, ili kwamba watu waweze kula bila ya kujihisi kutahayari.493 17. Katika al-Ja’fariyat: Katika simulizi yake kutoka kwa Ja’far ibn Muhammad, kutoka kwa baba zake, kutoka kwa Ali (a.s.) ambaye amesema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipofuturu pamoja na kikundi cha watu, angeweza kuwaambia: “Wale ambao walikuwa wamefunga wamefuturu pamoja nawe na wale wachamungu wamekula chakula chako na wale wateuliwa wamemuomba Mwenyezi Mungu akushushie rehma juu yako.”494

490 al-Makarim al-Akhlaq: 30; al-Mahasin: 443; al-Kafi 6: 297 491 Makarim al-Akhlaq: 171; al-Mahasin 541, ‘Uyun Akhbar al-Ridha 2: 43 492 Makarim al-Akhlaq: 23 Kidokezo: Allamah Tabatabai anasema: Kisha at-Tabarsi anataja zile aina za chakula ambazo yeye (s.a.w.w.) alikuwa akila, kama vile mkate na nyama za aina tofauti, matikiti maji, zabibu, komamanga, tende, maziwa, siagi, siki, sukari, kabichi na kadhalika. Imesimuliwa kwamba alikuwa akipendelea sana tende na kwamba yeye alipenda asali. Imesimuliwa pia kwamba tunda alilokuwa analipendea sana lilikuwa ni komamanga. (rejea kwenye al-Mizan 6:326) 493 al-Kafi 6: 285; al-Mahasin: 448 494 al-Ja’fariyat: 60; Makarim al-Akhlaq: 27; Tahdhib al-Ahkam 6: 99; Nawadir alRawandi: 35. 93


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 94

SUNAN-NABII Kidokezo: Hii imesimuliwa pia na al-Kulayni katika riwaya kutoka kwa al-Sakuni kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.)495 18. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka Muhammad ibn Muslim kutoka kwa Abi Ja’far (a.s.) ambaye amesema: Amirul-Mu’minin (a.s.) amesema: Mitume walikula chakula chao cha usiku baada ya swala ya Isha kwa hiyo msiitelekeze tabia hiyo, kwani kutokula chakula cha usiku kuna madhara kwenye mwili.496 19. Vilevile: Imesimuliwa kutoka wa Ansabah ibn Bajad kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Hapakuwa na chakula kamwe ambacho kilijumuisha tende ndani yake, ambacho kiliandaliwa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) bali kwamba yeye alianza kwa kula hizo tende.497 20. Katika al-Iqbal: Kutoka kwenye juzuu ya pili ya Ta’rikh al-Naishaburi katika maelezo ya Hasan ibn Bashir ambaye, katika riwaya yake amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angemshukuru Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. baina ya kila matonge mawili ya chakula.498 21. Katika Sahifah ar-Ridha kutoka kwa baba zake (a.s.) ambao wamesema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa anakula tende, angeziweka kokwa za tende nyuma ya mkono wake na halafu akazirusha (ili kuzitupa kabisa).499 Kidokezo: al-Kulayni vilevile ameisimulia katika al-Kafi.500 22. Vilevile: Katika riwaya yake kutoka kwa baba zake (a.s.) ambao wamesema: Wakati Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alipokunywa na maziwa angesuuza kinywa chake huku akisema: “Yalikuwa na mafuta.”501 23. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Wahab ibn Abd al-Rabbih ambaye amesema: Nilimuona Aba Abdillah (a.s.) akichokoa meno yake nami nikamtazama, hivyo akasema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akitumia kuchokoa meno yake, na hii inakipa kinywa harufu nzuri.502 495 al-Kafi 6: 294 496 al-Kafi 6:288; al-Mahasin: 420 (na katika vyanzo hivi viwili imesimuliwa kutoka kwa Abi Abdillah (.a.s.), Makarim al-Akhlaq: 194; Tuhf al-‘Uqul: 110. 497 al-Kafi 6: 345 498 al-Iqbal al-A’mal: 116 499 Sahifa al-Imam al-Ridha: 75; Makarim al-Akhlaq: 169, ‘Uyun Akhbar al-Ridha 2: 41. 500 Hii hatukuipata rejea yake. 501 Sahifah al-Imam al-Ridha: 69; Makarim al-Akhlaq: 193, al-Mustadrak 16: 373 502 al-Kafi 6: 376; al-Mahasin: 559; Makarim al-Akhlaq 152; al-Faqih 3: 357 94


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 95

SUNAN-NABII 24. Katika al-Makarim: Akinukuu kutoka kwenye Tibb al-a’immah yeye anasema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alichokoa meno yake kwa chochote alichoweza kutumia, isipokuwa majani ya mtende na matete.503 25. Vilevile: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokunywa maji, alianza kwa jina la Allah ‘Azza wa Jalla. Aliyachukua maji kwa funda moja moja na wala asingeyagugumia, na angesema: “Maradhi ya ini yanasababishwa na kugugumia maji.”504 26. Vilevile: Kutoka kwa Abdallah ibn Mas’ud: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angekunywa maji kutoka kwenye bakuli kwa mivuto mitatu, akimtaja Mwenyezi Mungu mwanzoni mwa kila mvuto na kumshukuru mwisho wa kila mvuto.505 27. Vilevile: Kutoka kwa Ibn Abbas ambaye amesema: Mimi nilimuona Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akinywa maji na akipumzika mara mbili baina ya mivuto.506 28. Katika al-Ja’fariyat: Katika riwaya yake kutoka kwa Ja’far ibn Muhammad kutoka kwa baba zake kutoka kwa Ali (a.s.) ambaye amesema: Nilimuona Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) zaidi ya mara moja wakati alipokuwa akinywa maji, yeye angechukua kutu tatu, na kwa kila kutu, yeye angeanza na jina la Allah ‘Azza wa Jalla. na kumtukuza na kumshukuru wakati alipomaliza, hivyo nikamuuliza kuhusu hili na yeye akasema: “Kumshukuru Mwenyezi Mungu kunafanywa kwa kumtukuza Yeye, na kuanza kwa jina Lake ni ulinzi kutokana na maradhi.”507 29. Katika al-Makarim: Yeye (s.a.w.w.) asingepumulia kwenye chombo au kikombe wakati alipokuwa anakunywa, na kama alitaka kuhema, angekisogeza mbali kikombe hicho na kisha ndipo avute pumzi.508 30. Katika al-Ja’fariyat: Katika riwaya yake kutoka kwa Ja’far ibn Muhammad kutoka kwa baba zake kutoka kwa Ali (a.s.): Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipotaka kuyaombea maji (kwa madhumuni ya kuyatumia kama tiba), yeye angelileta lile bakuli karibu na kwenye kinywa chake na kuomba kiasi ambacho Mwenyezi Mungu angeridhia bila kutemea mate ndani yake.509

503 Makarim al-Akhlaq 153; al-Kafi 6: 377; al-Mahasin 564 504 Makarim al-Akhlaq: 31 505 Ibid, 151 506 Ibid. 507 al-Ja’fariyat: 161; Da’aim al-Islam 2: 130; al-Mustadrak 17: 12 508 Makarim al-Akhlaq: 31 509 al-Ja’fariyat: 217 95


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 96

SUNAN-NABII 31. Katika al-Mahasin: Imesimuliwa kutoka kwa Hatim ibn Isma’il, kutoka kwa Abi Abdillah kutoka kwa baba yake (a.s.) kwamba Amirul-Mu’minin Ali (a.s.) alitumia kunywa huku akiwa amesimama. Siku moja alikunywa maji yaliyokuwa yamezidi katika kuchukua wudhuu kwake wakati akiwa amesimama, kisha alimgeukia Hasan (a.s.) na kusema: “Ewe mwanangu! Mimi nilimuona babu yako, Mtume wa Allah ‘Azza wa Jalla. akifanya hivi.”510 32. Kutoka kwa al-Saduq katika al-‘Uyun: Imesimuliwa kutoka kwa Darim ibn Qabisah, kutoka kwa ar-Ridha kutoka kwa baba zake (a.s.): Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akila mashuke ya maua na ule moyo laini wa mti wa mtende pamoja na tende akisema: Ibilisi – Mwenyezi Mungu amlaani – huwa anachukia na kusema: “Mwana wa Adam (a.s.) ameishi (muda mrefu sana) kiasi kwamba amekula vilivyozeeka na vipya.”511 33. Kutoka kwa al-Ghazali katika Ihya: Wakati yeye (s.a.w.w.) alipokula nyama, hakuiinamishia kichwa chake, bali aliileta mdomoni kwake kwa kuinyanyua na kisha akaing’ata kipande – na hususan alipokula nyama, angeosha sana mikono yake, halafu, kwa maji yaliyobakia, angepangusia uso wake.512 34. Vilevile: Yeye (s.a.w.w.) angeweza kula chochote kile kilichoweza kupatikana.513 35. Katika al-Makarim: Kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba yeye alikuwa akila aina tofauti za vyakula ….. alikuwa akila matango na tende mbivu, na alipendelea kupata matikitimaji na zabibu, na angekula tikitimaji na tikititamu na wakati mwingine kwa sukari. Wakati mwingine alikula tikitimaji na tende ….. na alipokuwa amefunga, angefuturu kwa tende mbivu zilipokuwa kwenye msimu. Wakati mwingine alikula zabibu moja baada ya nyingine, na alitumia kula jibini ….. angekula tende na akanywa maji; na hizo tende na maji ndivyo alivyokuwa akila sana muda mwingi. Alikuwa akitumia kunywa maziwa, kula tende na al-Harisah (chakula kilichotengenezwa kwa kuchanganya bulga – ngano iliyochemshwa kidogo na kuanikwa – na nyama). Chakula alichokuwa akikipenda sana ni nyama. Alipenda sana aina za maboga na alikuwa akiokota kutoka kwenye bakuli kubwa (la matunda). Alikuwa akitumia kula nyama ya kuku na ndege wa kufugwa, nyama ya wanyama pori (wenye kula majani) na ndege, mkate na siagi safi, siki, majani yaliyojikunja yanayotumika kama saladi, ‘al-Badhruj’ (majani kama ya mrihani mtamu) na kabichi.514 510 al-Mahasin: 580; al-Kafi: 383 511 Uyun al-Akhbar al-Ridha 2: 72 512 Ihya ‘Ulum al-Din 2: 371; Makarim al-Akhlaq: 30: 31 513 Ihya ‘Ulum al-Din 2: 361 514 Makarim al-Akhlaq: 29 - 30 96


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 97

SUNAN-NABII Maelezo: Hii imesimuliwa mara nyingi na wengi wa ulamaa wa Shi’a na vilevile na Maimamu pamoja na sanadi nyingi tofauti za wasimuliaji. Tumeliacha hili kwa kupunguza maneno (kwa sababu ya nafasi). 36. Kutoka kwa al-Shahid katika al-Durus: Yeye (s.a.w.w.) alikuwa akila matango na chumvi.515 37. Kutoka kwa al-Ghazali katika al-Ihya: Yeye (s.a.w.w.) alikuwa akila nyama ya ndege waliowindwa, bali hakuwahi kutega au kuwinda yeye mwenyewe binafsi. Yeye alipendelea awindwe kwa ajili yake na aletwe kwake ili amle.516 38. Kutoka kwa Husein ibn Hamadan al-Husayni katika al-Hidayah: Kutoka kwa Abi Abdillah, kutoka kwa baba zake, kutoka kwake Amirul-Mu’minin Ali (a.s.) katika hadithi: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akipendelea kula kutoka kwenye nyama ya mfupa wa mkono (ile sehemu ya juu ya mguu wa mbele wa mnyama).517 Kidokezo: at-Tabarsi na wengineo wameisimulia hadithi hii.518 39. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Hisham ibn Salim kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akipenda asali.519 Kidokezo: Hii vilevile imesimuliwa na yeye na wengineo kwa sanadi nyingine za wasimuliaji.520 40. Vilevile: Imesimuliwa kutoka kwa Sulayman ibn Ja’far al-Ja’fari ambaye amesema: Nilikwenda kwa Abi al-Hasan ar-Ridha (a.s.) na alikuwa na tende za ‘Burni’521 mbele yake na alikuwa anazila kwa starehe sana na hamu. Yeye akasema: “Oh, Sulayman! Njoo ule,” hivyo mimi nikala pamoja naye. Nikamwambia: “Mimi naniwe kafara yako! Ninakuona unakula tende hizi kwa hamu sana?” Yeye akasema: “Naam, kwa kweli ninazipenda sana hizi.” Mimi nikamuuliza: “Kwa 515 al-Durus al-Shar’iyyah 3: 46; al-Mahasin: 558; Makarim al-Akhlaq: 185; al-Kafi 6: 373 516 Ihya ‘Ulum al-Din 2:371; Makarimu al-Akhlaq: 30 517 an-Nuri ameisimulia hii katika al-Mustadrak 16: 350 – akinukuu kutoka kwenye alHidayah. 518 Makarim al-Akhlaq: 30; al-Kafi 6:315; Da’aim al-Islam 2: 110 519 al-Kafi 6: 332, Makarim al-Akhlaq: 165 520 al-Kafi 5: 320 na 6:332; Makarim al-Akhlaq: 165 521 Jamii fulani ya tende nyekundu na manjano ambayo ilikuwa ikichukuliwa kuwa ndio ya daraja bora zaidi (Mfasiri). 97


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 98

SUNAN-NABII nini?” Yeye akasema: “Kwa sababu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alikuwa akipenda tende, Amirul-Mu’minin alikuwa akipenda tende, al-Hasan (a.s.) alikuwa akipenda tende, Abu Abdillah al-Husein (a.s.) alikuwa akipenda tende, Sayyid al-Abidiin (a.s.) alikuwa akipenda tende, Abu Ja’far (a.s.) alikuwa akipenda tende, Abu Abdillah (a.s.) alikuwa akipenda tende, baba yangu (a.s.) alikuwa akipenda tende, na mimi pia napenda tende. Shi’ah wetu wanapenda tende kwa sababu walikuwa wameumbwa kutokana na udongo (ufinyanzi) wetu, ambapo maadui zetu, Ewe Sulayman, wao wanapenda vilevi kwa sababu wao wameumbwa kutokana na miali ya moto.”522 41. Kutoka kwa al-Tusi katika al-Amali: Imesimuliwa kutoka kwa Abi Usamah523 kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Chakula cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kilikuwa mkate wa shayiri kama alikuwa nao, na kitindamlo chake kilikuwa ni tende, na kuni zake zilikuwa ni matawi ya mtende.524 42. Kutoka kwa al-Kulayni: Imesimuliwa kutoka kwa Umar ibn Aban al-Kalbi ambaye amesema: Nilimsikia Aba Ja’far na Abi Abdillah, amani juu yao, wakisema: Hapakuwa na tunda katika dunia hii ambalo lilipendwa sana na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) zaidi kuliko komamanga. Na Wallahi! Alipokuwa akilila hakutaka mtu yoyote ashirikiane naye katika kulila.525 43. Katika al-Makarim: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakuwa akitumia kamwe kula chakula cha moto mpaka kilipokuwa kimepoa na angesema: “Mwenyezi Mungu hakulisha sisi na moto. Kwa hakika chakula cha moto hakina baraka kwa hiyo kiacheni kipoe kabla ya kula chakula hicho.” Wakati alipokula, alianza kwa ‘bismillah.’ Yeye alikuwa anakula kwa kutumia vidole vitatu, kutoka kwenye kile kilichokuwa mbele yake, na alikuwa hali kutoka kwenye kilichokuwa mbele yaw engine. Wakati chakula kilipoletwa, yeye alikuwa wa mwanzo kuanza kula ndipo watu wengine wangeanza kula. Yeye angekula kwa vidole vitatu, dole gumba, na kile kilichofuatia (yaani kidole cha shahada) na kidole cha kati na wakati mwingine alivisaidia na kile kidole cha nne. Angekula wakati mwingine kwa mkono mzima (kutumia vidole vyote) na hakuwahi kula kwa vidole viwili tu kamwe akisema: “Kwa hakika kule kula kwa vidole viwili ni ulaji wa shetani.” Siku moja masahaba zake walikuja na kiasi cha ‘Fadhulaj’ (aina fulani ya chakula kitamu) hivyo akakila pamoja nao na akauliza: “Chakula hiki kimetengenezwa kwa 522 al-Kafi 6: 346 523 Katika chanzo cha habari: Imesimuliwa kutoka kwa Amr ibn Sa’id ibn Hilal 524 Amali at-Tusi 2: 294; al-Kafi 2: 137; Amali al-Mufid: 195 525 al-Kafi 6: 352; al-Mahasin: 541 98


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 99

SUNAN-NABII kitu gani?” Wao wakasema: “Tunachanganya siagi iliyosafishwa pamoja na asali na inageuka na kuwa kama unavyoona sasa hivi,” hivyo yeye akasema: “Chakula hiki ni kizuri.” Yeye (s.a.w.w.) alikuwa akila mkate uliotengenezwa kutokana na shayiri isiyopetwa wala kuchekechwa, na kamwe hakuwahi kula mkate wa ngano – asilan. Yeye hakuwahi kula juu ya meza (iliyosheheni aina mbalimbali za vyakula) mpaka siku alipofariki. Yeye alikuwa akila tikitimaji na zabibu, na angeweza kula tende na kuwalisha kondoo kwa kokwa zake. Hakutumia kamwe kula kitunguu saumu, vitunguu, liki au asali ambayo ilikuwa na nta ndani yake – nta hiyo ni kile kinachobakia kutoka kwenye miti ndani ya nyuki, ambacho inakidondosha kwenye asali; na inaacha harufu mdomoni (pale inapoliwa). Daima yeye hajashutumu chakula – kamwe. Iwapo alikipenda basi alikila na kama hakukipenda basi aliacha kukila, lakini hakuwazuia wengine kukila. Yeye angelifuta bakuli ili kulisafisha huku akisema: “Chini ya bakuli ndiko kuna chakula kilichobarikiwa sana,” na pale alipokuwa amemaliza kula, angevilamba vile vidole vyake vitatu ambavyo alikuwa amevitumia wakati wa kula, kimoja kimoja, na angeosha mikono yake mpaka iwe imeng’aa na kuwa safi kabisa. Yeye (s.a.w.w.) asingeweza kula akiwa peke yake.526 44. Katika al-Mahasin: Imesimuliwa kutoka kwa Ya’qub ibn Shu’aib kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Amirul-Mu’minin Ali (a.s.) alikuwa na baadhi ya wafuasi wake huko Rahbah wakati lilipoletwa bakuli la ‘Faludhaj’ kwa ajili yake. Yeye aliwaambia wafuasi wake: “Chukueni kutoka humo na mle,” hivyo wakachota humo na yeye pia akachukua kiasi (kwa ajili ya kula), halafu akaacha ghafla na akasema: “Nilikumbuka kwamba Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) hakukila hicho hivyo sikupenda kwamba niweze kukila.527 526 Makarim al-Akhlaq: 28-30 Allamah Tabatabai anasema katika al-Mizan: Yale maneno yake “Kidole gumba na kile kilichofuatia na kidole cha kati …..” yanaonyesha ufasaha wa msimuliaji kwa vile hakusema: “….. na kidole cha shahada…..” katika kumheshimu yeye (s.a.w.w.) kwa kutokutaja ‘shahada’ kuashiria kwenye kidole chake kitukufu wakati dole gumba limetajwa. Kisha Allamah anasema: Na yule anayesimulia kule kulak wake (s.a.w.w.) ile Faludhaj amepingana na kilichomo kwenye al-Mahasin, kilichosimuliwa kutoka kwa Ya’qub ibn Shu’aib kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.)….. (tazama hadithi inayofuata) [Rejea kwenye alMizan 6: 326] 527 al-Mahasin: 410; Manaqib Ali ibn Abi Talib 2: 99; Kashif al-Ghummah 1: 163; Katika al-Da’aim: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akipenda hiyo Faludhaj na wakati alipotaka kuila angeweza kusema: Ichukueni na muipunguze. Halafu al-Qadhi al-Nu’mani amesema: Nadhani yeye aliepuka kuichukua kwa wingi isije ikamletea madhara.(Da’aim al-Islalm 2: 111) 99


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 100

SUNAN-NABII 45. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa al-Sakuni kutoka kwa Ja’far kutoka kwa baba zake (a.s.) ambao wamesema: Wakati yeye (s.a.w.w.) alipokula (chakula chochote chenye) mafuta, angepunguza kipimo chake cha maji ya kunywa; hivyo yeye alipoulizwa: “Ewe Mtume wa Allah! Mbona umepunguza kiwango cha maji unayokunywa?” Yeye alisema: “Hili linakuwa na afya zaidi kwa (kumeng’enyua) chakula changu.”528 Kidokezo: Riwaya kama hiyohiyo imetajwa katika al-Ja’fariyat.529 46. Vilevile: Imesimuliwa kutoka kwa Talha ibn Zayd kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akipenda kunywa kutoka kwenye al-Qadah al-Shami530 na alikuwa akisema: “Hiki ndio kisafi zaidi kati ya vyombo vyenu.”531 Kidokezo: Hii imesimuliwa na al-Barqi na al-Kulayhi pamoja na sanadi tofauti za wasimuliaji.532 47. Katika al-Makarim: Yeye amesema: Yeye (s.a.w.w.) alikuwa akitumia kunywa kutoka kwenye vikombe vya kunywea vilivyotengenezwa kwa kioo ambavyo vililetwa kutoka Damascus, na angeweza (pia) kunywa kutoka kwenye vikombe vya kunywea vilivyotengenezwa kwa miti, ngozi na ufinyanzi.533 48. Vilevile: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akitumia kunywa kwa mikono yake, akiimwagia maji ndani yake na akisema: “Hakuna chombo bora zaidi kuliko mkono.”534 49. Vilevile: Yeye (s.a.w.w.) alikuwa akinywa kutoka kwenye mdomo wa mfuko wa ngozi mkubwa au mfuko mdogo na yeye asingeukunjua kwa nje akisema: “Kuukunjua kwa nje kunayafanya maji yawe na harufu mbaya.535 50. Kutoka kwa Ibn Tawus katika al-Muhaj akinukuu kutoka kwa Zad al-Abidin kwenye hadithi ndefu: Katika sehemu yake inayoelezea jinsi maji ya ‘Naisan’536 528 Hatukiliona hili katika al-Kafi bali limesimuliwa katika al-Makarim al-Akhlaq: 157. 529 al-Ja’fariyat:161 530 Kikombe au bakuli la kunywea lililotengenezwa huko Damascus (Mfasiri). 531 al-Kafi 6: 386 532 al-Kafi 6: 385’ Al-Mahasin: 577 533 Makarim al-Akhlaq: 31 534 Ibid. 535 Ibid. 536 Maji ya mvua inayonyesha kwenye mwezi wa saba wa kalenda ya Roman Catholic yanakuwa na vitu maalum [Rejea: Taj al-‘Arus, Jz. 9, uk. 28] (Mfasiri). 100


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 101

SUNAN-NABII yanavyokusanywa, inaelezea pia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akiyatumia.537 51. Katika al-‘Uyun: Katika riwaya yake kutoka kwa al-Tamimi ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angetoa kafara (katika siku ya Idd al-Udh’ha) kondoo dume wawili wenye pembe nene.538 52. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Abdillah ibn Sinan ambaye amesema: Katika siku ya Udh’ha, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alichinja kondoo dume wawili, mmoja kutoka kwake mwenyewe na huyo mwingine kwa niaba ya masikini kutoka miongoni mwa umma wake.539 Kidokezo: Hii imesimuliwa kutoka kwa Ahlul-Bayt (a.s.) kwa idadi kubwa ya sanadi za wasimuliaji.

Nyongeza kwenye sehemu hii 1. Katika utangulizi wa Tibb al-Nabi: Katika hadithi, yeye (s.a.w.w.) amesema: Sisi ni jamii ambayo hatuli mpaka tujisikie kuwa na njaa, na pale tunapokula hatuli tukashiba.540 2. Katika Majmu’at Warram: Kutoka kwake ibn Abbas ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angeweza kwenda (wakati mwingine) kulala wakati wa usiku akiwa mwenye njaa, bila ya chakula cha usiku kwa ajili yake au familia yake; na kile chakula ambacho kwa kawaida huwa alikula ni mkate wa shayiri.541 3. Vilevile: Kutoka kwa Aishah: Kwa Yule ambaye alimtuma Muhammad (s.a.w.w.) kwa haki! Sisi tulikuwa hatuna chungio na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakula mkate uliotengenezwa kutokana na shayiri iliyochekechwa tangu mwanzo wa utume wake hadi pale alipofariki.542 4. Katika al-Makarim: Kutoka kwa Anas ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakula juu ya meza (au jukwaa) na yeye hakula kutoka kwenye ‘Sukurrajah’ (bakuli inayofanana na sahani) na yeye hakula mkate wa unga 537 Muhaj al-Da’awat: 355-356 538 ‘Uyun al-Akhbar ar-Ridha 2: 63 539 al-Kafi, 4: 495 540 Tibb al-Nabi (s.a.w.w.) – Utangulizi. 541 Majmu’at Warram: 39 542 ibid. 101


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 102

SUNAN-NABII uliochekechwa mwembamba. Hivyo Anas aliulizwa: “Je! Wao walikuwa wakila kwenye nini?” Yeye akasema: “Juu ya kitambaa cha meza (kilichotandikwa chini).”543 5. Katika Majmu’at Warram: Aishah alikuwa akisema: Mtukufu Mtume hakuwa akila mpaka akashiba – daima.544 6. Katika Amali al-Tusi: Katika riwaya kutoka kwa Muhammad ibn Muslim ndani ya hadithi kutoka kwa Abi Ja’far (a.s.) ambaye amesema: “Oh, Muhammad! Unaweza ukawa unafikiri kwamba mtu mmoja lazima atakuwa amemuona Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akiwa anakula huku ameegemea angalau mara moja, kuanzia ule wakati ambapo Mwenyezi Mungu alimtuma (kama mtume kwa watu) mpaka kwenye kufa kwake?” Halafu akasema: “Ewe Muhammad! Unaweza ukadhani kwamba lazima alikuwa anajishibisha kwa kula mkate wa ngano kwa siku tatu mfululizo ingawa mara moja, kati ya wakati Mwenyezi Mungu alipomtuma kama mtume mpaka alipofariki?” Kisha yeye (a.s.) akajibu mwenyewe na akasema: “La hasha, Wallahi! Yeye hakuwahi kujishibisha mwenyewe kwa mkate wa ngano kwa siku tatu mfululizo mpaka Mwenyezi Mungu alipomchukua (kutoka kwenye ulimwengu huu). Lakini sisemi kwamba yeye (s.a.w.w.) hakuweza kuupata mkate huo. Angeweza wakati mwingine kumzawadia mtu mmoja ngamia mia moja, na kama angetaka kuula angeula. Jibril alikuwa amemletea funguo za hazina za ulimwengu mara tatu na akampa yeye fursa hiyo, akimhakikishia kwamba Mwenyezi Mungu asingempunguzia malipo yoyote kati ya yale aliyokuwa amemuahidi katika Siku ya Hukumu (iwapo angechukua funguo hizo). Lakini alichagua kuwa mnyonge mbele ya Mola Wake na yeye kamwe hakuomba kitu chochote. Daima hakusema ‘Hapana’ pale alipoombwa kitu chochote. Kama alikuwa nacho angeweza kukitoa na kama hakuwa nacho angesema: ‘Mungu akipenda utakipata kitu hicho.’”545 7. Katika al-‘Uyun: Katika riwaya yake kutoka kwa al-Tamimi, kutoka kwa arRidha kutoka kwa baba zake, kutoka kwa Ali (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakujishibisha kwa mkate wa ngano kwa siku tatu mfululizo mpaka alipofariki dunia.546 8. Katika Majmu’at Warram: Kutoka kwa Abu Huraira: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na familia yake hawakupata kushiba kwa mkate wa ngano kwa siku tatu mfululizo 543 Makarim al-Akhlaq: 149. 544 Majmu’at Warram: 82 545 Amali al-Tusi 2: 303 546 ‘Uyun al-Akhbar al-Ridha 2: 64 102


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 103

SUNAN-NABII mpaka alipoiaga dunia.547 9. Vilevile: Aishah amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakupata kushiba kwa siku tatu mfululizo mpaka alipofariki dunia. Kama angetaka yeye angeweza kujishibisha, lakini yeye alipendelea kukigawa chakula chake kwa wengine kuliko (kula) yeye binafsi.548 10. Vilevile: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakuwahi kuchanganya chakula cha rangi mbili tofauti katika funda moja mdomoni mwake; kama ilikuwa ni nyama ilikuwa sio mkate na kama ilikuwa ni mkate ilikuwa sio nyama.549 11. Vilevile: Haikuwahi kutokea kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na aina mbili za chakula lakini kwamba angeweza kula aina moja na kutoa ile nyingine kwenye sadaka.550 12. Katika al-Makarim: Ibn Khauli alileta kwa ajili ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) bakuli lilikuwa na asali na maziwa, lakini yeye alikataa kunywa na akasema: “Hivi ni vinywaji viwili vimechanganywa kama kimoja na kile ambacho kingekuwa kwenye mabakuli mawili kimewekwa kwenye bakuli moja,” hivyo hakukinywa kinywaji hicho. Kisha akasema: “Mimi sikukatazeni kunywa kinywaji hiki, bali nachukia fahari na kuogopa kuwajibika kwa ziada za dunia hii kesho (akhera); na ninapenda udhalili, kwani kwa kweli yule ambaye ni mnyenyekevu mbele ya Mungu atakuja kufufuliwa katika hadhi na Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla.551 13. Katika al-Bihar: Kutoka kwa Lut ibn Yahya kutoka kwa wakubwa zake na watangulizi – katika hadithi ndefu juu ya jinsi Ali (a.s.) alivyouawa shahidi mpaka pale alipomwambia binti yake Umm Kulthum (amani iwe juu yake): “Nataka kufuata mwendo wa ndugu na binamu yangu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.). Hakujakuwa na aina mbili za chakula kilicholetwa kwake katika sahani moja mpaka wakati Mwenyezi Mungu alipoichukua roho yake.552 Kidokezo: Hii imesimuliwa pia katika al-Manaqib.553 547 Majmu’at Warram: 39 548 Ibid: 141 549 Majmu’at Warram: 39 550Ibid. 551 Makarim al-Akhlaq: 32 552 Bihar al-Anwar 42: 276 553 Manaqib Ali ibn Abi Talib 2: 99 103


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 104

SUNAN-NABII 14. Katika al-Makarim: Kwa kiasi kama ilivyowezekana, yeye (s.a.w.w.) asingekula peke yake kamwe.554 15. Katika al-Bihar: Kutoka ndani ya Bisharat al-Mustafa – katika hadithi juu ya ushauri wa Ali (a.s.) kwa Kumayl ibn Ziyad mpaka pale yeye aliposema: “Oh, Kumayl! Usihangaike sana kuhusu chakula chako, kwani Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakuwa mwenye kuchagua sana kuhusu chakula.” 555 16. Katika al-Kafi: Katika riwaya yake kutoka kwa Ali ibn Asbat kutoka kwa baba yake: Aba Abdillah (a.s.) aliulizwa: “Je! Mtukufu Mtume aliilisha familia yake kwa chakula chenye afya na virutubisho?” Yeye akasema: “Ndio. Wakati mtu anapokula chakula ambacho kina afya na virutubisho, yeye anapata hisia ya kuridhika na misuli yake huanza kukua.”556 17. Katika al-Mahasin: Katika riwaya yake kutoka kwa Amr ibn Jami’ kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akilikomba bakuli la chakula mpaka likasafika.557 18. Katika al-Mahasin: Kutoka kwa baadhi ya masahaba wetu kutoka kwa al-Hasan ibn Ali (a.s.) ambaye amesema: Kuna tabia kumi na mbili ambazo mtu ni lazima ajifunze kuzitumia wakati anapokula chakula. Nne kati ya hizo ni wajibu, nne ni (kutoka kwenye) Sunnah na nne ni adabu (za misingi ya mezani)….. ama kwa hizo za Sunnah, inajumuisha na kukaa juu ya mguu wa kushoto, kula kwa vidole vitatu, na kwa mtu kula kutoka kwenye kile kilicho mbele yake.558 Maelezo: Hii imesimuliwa na al-Saduq katika al-Khisal na al-Faqih, pia na atTabarsi katika al-Makarim, na as-Sayyid katika al-Iqbal – na ndani yake (imeongezwa) “Na kuhusu hizo za Sunnah inajumuisha mtu kuosha mikono yake kabla ya kula ….. na kulamba vidole …..”559 19. Katika al-Mustadrak: Kutoka kwa Abi al-Qasim al-Kufi katika hadithi juu ya matendo ambayo ni kutoka katika Sunnah wakati wa kula: Sunnah katika hili ni kuosha mikono yake mtu kabla na baada ya kula chakula.560 554 Makarim al-Akhlaq: 31 555 Bihar al-Anwar 77: 268; Bisharat al-Mustafa: 25 556 al-Kafi 4: 12 557 al-Mahasin: 443 558 Ibid; 459 559al-Khisal: 485; al-Faqih 3: 3359; al-Makarim al-Akhlaq:141; Iqbal al-A’mal: 113 560 al-Mustadrak 16: 269 104


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 105

SUNAN-NABII 20. Katika al-Kafi: Katika riwaya yake kutoka kwa Muhammad ibn al-Fadhil ambaye anaihusisha kwao (Ma’sum a.s.) kwamba wao wamesema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokula, angeweka chakula kwa ajili ya yule mtu aliyekuwa upande wa pili mkabala naye na alipokuwa anakunywa maji angeyatoa kiasi kwa yule mtu aliyekaa kulia kwake.561 21. Katika al-Makarim: Yeye (s.a.w.w.) alikuwa akitumia kunywa akiwa amesimama na wakati mwingine angekunywa akiwa amepanda mnyama, na wakati mwingine angemsimamisha na kunywa – kutoka kwenye mfuko wa maji (wa ngozi) au kwenye kiriba cha udongo au kutoka kwenye chombo kingine chochote ambacho kilikuwa kinapatikana, na wakati mwingine kwa mikono yake.562 22. Katika al-Ihya: Yeye (s.a.w.w.) alitumia kunywa funda tatu, akimtukuza Mwenyezi Mungu mwisho wa kila funda na kuanza kila funda kwa ‘bismillah …..’ Baada ya kumaliza ile funda ya kwanza agesema ‘Alhamulillah’ na baada ya ile ya pili angeongeza: ‘Rabil-‘Alamin’ na katika ile ya tatu yeye angeongeza: ‘arRahmanir-Rahim.’563 23. Katika al-Irshad ya al-Daylami: Wakati yeye (s.a.w.w.) alipokunywa maji angesema: “Alhamdulillah al-ladhyi lam yaj’alhu ujaajan bidhunuubina wa ja’alahu ‘Adhbaan furaatan bini’imatihi.” “Utukufu ni Wake Allah, Mpweke ambaye hakuyafanya maji haya kuwa machungu kama adhabu kwa ajili ya dhambi zetu, na ameyafanya matamu na yenye kutoa kiu kwa neema Zake.”564 Kidokezo: Al-Kulayni ameitaja hii katika al-Kafi na al-Ghazali katika al-Ihya.565 24. Katika al-Iqbal: Kutoka kwa as-Sayyid Yahya ibn al-Husein ibn Harun alHasayni katika Amali yake: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa amekula funda chache, yeye angesema: “Allahuma lakal-hamdu ‘Atwa’amta wa sakayta wa arwayta falakalhamdu ghayra makfuurin wa laa muwadda’iin wa laa mustaghniya ‘anka. 561 al-Kafi 6: 299; al-Mustadrak 16: 287 562 Makarim al-Akhlaq: 31-32 563 Ihya al-‘Ulum al-Din 2:6 564 Hatukuiona rejea hii katika al-Irshad, bali tumeikuta katika al-Wasa’il, 17: 204 565 al-Kafi, 6: 384; al-Ihya ‘Ulum al-Din, 2: 6; Qurb al-Isnad: 12 105


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 106

SUNAN-NABII “Ewe Mungu Wangu! Sifa tukufu zote ni Zako. Wewe umelisha na kunywesha na kupoza kiu; hivyo shukurani zote ni Zako, Haukufuriwi (kuto shukriwa), na bila mapumziko, na bila (kutafuta) kutokutegemea kutoka Kwako.”563 25. Katika al-Makarim: Yeye (s.a.w.w.) amesema: Kiungo kizuri kabisa ni siki – Ewe Mungu Wangu! Ifanye siki kuwa ni baraka kwa ajili yetu – kwani ndio kiungo cha mitume kabla yangu.564 26. Katika al-Kafi: Katika riwaya yake kutoka kwa al-Sakuni kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Viungo vilivyokuwa vikipendwa sana na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) vilikuwa ni siki na mafuta ya zeituni, na amesema: “Hiki ndio chakula cha mitume (a.s.)”565 27. Katika al-‘Uyun: Katika riwaya yake kutoka kwa al-Ridha, kutoka kwa baba zake kutoka kwa Ali (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakuwahi kula figo (za wanyama) kamwe, ingawa hakuzikataza, na yeye angesema: “ ….. kwa sababu ya ukaribu wake na kwenye mkojo.”566 28. Katika al-Kafi: Katika riwaya yake kutoka kwa Abd al-Rahman ibn al-Hajjaj katika hadithi kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.): Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliletewa bakuli la wali kama zawadi kutoka kwa Ansari, hivyo akawaita Salman, Miqdad na Abu Dharr – Mwenyezi Mungu awaridhie – waje kuungana naye. Wakaanza kutoa visingizio baada ya kula kidogo sana, hivyo yeye (s.a.w.w.) akasema: “Hamjala chochote! Yule anayetupenda sana sisi kutoka miongoni mwenu ni yule atakayekula sana na sisi.”567 29. Vilevile: Katika riwaya yake kutoka kwa Ibrahim al-Karkhi ambaye amesema: Abu Abdillah (a.s.) amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Kama muumini angekuwa anikaribishe mimi kula nyama ya mfupa wa mkono wa kondoo, nitakubali; na hii ni sehemu ya dini. Kama mshirikina au mnafiki angekuwa anikaribishe kula nyama ya ngamia, mimi ningekataa, na hili linatoka kwenye dini. Mwenyezi Mungu amenifanyia kutokubalika juu yangu, zawadi za washirikina na wanafiki na chakula chao.568 563 Iqbal al-A’mal: 116 564 Makarim al-Akhlaq: 190, ‘Awarif al-Ma’arif: 314 565 al-Kafi 6: 328; al-Mahasin: 483 566 ‘Uyun al-Akhbar al-Ridha 2: 41 567 al-Kafi, 6: 278 568 al-Kafi, 6: 274; al-Mahasin: 411 106


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 107

SUNAN-NABII 30. Katika al-Bihar, kutoka kwa Allamah ndani ya al-Tadhkirah: Yeye (s.a.w.w.) hakuwa akitumia kula kitunguu saumu, vitunguu na liki (mmea kama kitunguu, wenye tumba laini).569 31. Katika al-Mahasin: Kutoka kwa al-Nawfali katika riwaya yake: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Vueni viatu vyenu wakati mnapokula, kwani ni Sunnah ya ajabu sana na kitulizo kwa miguu.570 32. Katika al-Kafi: Katika riwaya yake kutoka kwa ibn al-Qaddah kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ndani ya hadithi: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alizoea kupenda nyama ya mfupa wa mkono na bega, na hakupendelea ile (nyama) ya mfupa wa nyonga kwa sababu ya ukaribu wake na njia ya mikojo.571 Kidokezo: Hii imesimuliwa na al-Barqi ndani ya al-Mahasin na al-Saduq katika alIlal.572 33. Katika ‘Awarif al-Ma’arif: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakukosoa chakula kamwe – asilan. Kama alikuwa na hamu nacho, basi alikila, vinginevyo angekiacha tu.573 34. Vilevile: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakuwa akitumia kupuliza chakula asilani au kupumulia pumzi ndani ya kikombe (wakati anapokunywa).574 35. Vilevile: Kuwa na siki na mboga za majani mezani ni kutoka kwenye Sunnah.575 36. Katika al-Mahasin: Katika riwaya kutoka kwa Ibn al-Qaddah kutoka kwa Ja’far (a.s.) ambaye amesema: Wakati mmoja ‘Khabis’ (chakula kilichotengenezwa kutokana na tende, zabibu kavu na siagi safi) ililetwa kwa ajili ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) lakini yeye akakataa kuila, hivyo akaulizwa: “Je, unakikataza chakula hiki?” Yeye akasema: “Hapana, bali nisingependa kujizoesha mwenyewe na aina hii ya chakula.” Kisha akasoma ile aya isemayo: “….. Mlipoteza vitu vyenu vizuri katika maisha yenu ya dunia …..”576 (46:20) 569 Bihar al-Anwar, 16: 387 570 al- Mahasin: 449 571 al-Kafi, 6: 315 572 al-Mahasin: 470; hatukuiona hii ndani ya al-Ilal. 573 ‘Awarif al-Ma’arif: 313 574 ‘Awarif al-Ma’arif: 314; Ihya ‘Ulum al-Din 2: 5-6 575 ‘Awarif al-Ma’arif: 314 576 al-Mahasin: 409; Surat al-Ahqaf; 46: 20 107


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 108

SUNAN-NABII 37. Katika al-Majma’: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akitumia kuliinamisha upande bakuli kwa ajili ya paka (akifanya iwe rahisi kwa paka kunywa humo).577 38. Katika al-Da’aim: Kutoka kwa Ja’far ibn Muhammad (a.s.) kwamba alikuwa na mazoea ya kula kwa kutumia vidole vitano huku akisema: Hivi ndivyo Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alivyokuwa amezoea kula, sio kama vile wanavyokula watu wenye kiburi na majivuno.578 39. Vilevile: Kutoka kwa Ali (a.s.) kwamba amesema: Tulikuwa tukiloweka zabibu kavu na tende katika maji safi ili kuyafanya yawe matamu kwa ajili ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na kama zingepita siku moja au mbili yeye angeyanywa maji hayo, lakini pale yalipokuwa yamebadilika (katika ladha) basi angeagizia kwamba yamwagwe.579 40. Kutoka kwenye al-Da’aim: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w) alipokuwa anakula, angekaa kwa mguu mmoja wima na mwingine ukiwa umetulizana chini.580 41. Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa anakula au kunywa huwa akisema: “Alhamdu-lillahi al-ladhii atu’ama wa saqaa wasawwaghahu waja’ala lahu makhrajaan.” “Utukufu wote ni wake Mwenyezi Mungu, aliyelisha na kunywesha, na kukiruhusu kitumike mwilini, na kukifanyia njia ya kupitia na ya kutokea.” 581 42.Katika al-Majma’: Katika simulizi ya vita vya Khandaq baada ya kutaja kuuliwa kwa Nawfal ibn Abd al-Ghazza, hadi pale aliposema: Makafiri walituma dirham ishirini elfu kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ili kununua maiti yake, hivyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Maiti huyu ni wenu; kwa sababu sisi hatuchukui pesa kwa ajili ya wafu.582 43. Katika al-Makarim al-Akhlaq: Kutoka kwenye sanadi ya wasimuliaji isiyokamilika kutoka kwa ar-Ridha (a.s.) ambaye amesema: Tunda moja aina ya pera lililetwa kwa ajili ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hivyo akaligawa kwa mikono yake, naye 577 Majma’ul-Bayan 4: 352 – Surat al-An’am 578 Da’aim al-Islam 2: 119 579 Ibid, 2: 128 580 Da’aim al-Islam 2: 118; Biharul-Anwar 66: 389. 581 Sunan Abi Dawud 3:366 582 Majma’ al-Bayan, 8:343 – Surat al-Ahzab. 108


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 109

SUNAN-NABII (s.a.w.w.) alikuwa na mazoea ya kulipenda hasa, hivyo alilila na akatoa sehemu kwa wale baadhi ya masahaba zake ambao walikuwa pamoja naye, halafu yeye akasema: “Muwe mnakula tunda hili, kwani huwa linasafisha moyo na linaondosha utando (wa kohozi) kutoka kifuani.”583 44. Katika Makarim al-Akhlaq: Katika riwaya yake kutoka kwa al-Ridha (a.s.) kwa nyororo ya wasimuliaji isiyokamilika: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. ameifanya asali kuwa ni baraka. Hiyo ni tiba ya maumivu na mitume sabini wameibariki.584 45. Katika ‘Uyun al-Akhbar: Katika riwaya yake kutoka kwa al-Ridha kutoka kwa Ali ibn Abi Talib (a.s.) ambaye amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) aliniambia: “Ewe Ali! Uwe unakula dengu kwani ni chakula kilichobarikiwa na kitukufu. Kinalainisha moyo na kinaongeza mwelekeo wa mtu katika kulia (kumlilia Mungu), na mitume sabini wamekibariki, wa mwisho wao akiwa ni Isa ibn Maryam (a.s.).585 46. Kutoka kwa Abi Umar: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipotaka kula kuku, angeagiza kwamba aletwe na angemuweka kwa kumfunga kamba (na kumlisha) kwa muda wa siku kadhaa ambazo baadae angemchinja na kumla.586 47. Katika al-Mahasin: Katika riwaya kutoka kwa Adim ‘Bayya’ al-Harwi kutoka kwa as-Sadiq (a.s.) katika hadithi: …..Yeye (s.a.w.w.) alikuwa akipendelea kula nyama.587 48. Katika al-Kafi: Katika riwaya ya Ali kuhusu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): Yeye hakuwahi kukataa manukato na tamtamu kamwe.588

583 Makarim al-Akhlaq: 172; Musnad al-Imam ar-Ridha: 342 584 Makarim al-Akhlaq: 166, Musnad al-Imam al-Ridha: 351 585 ‘Uyun al-Akhbar al-Ridha (a.s.) 2: 40; Musnad al-Imam ar-Ridha: 342 586 Bihar al-Anwar 65: 6 587 al-Mahasin: 460 588 al-Kafi 6: 513; Wasa’il al-Shi’ah 1: 444 109


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 110

SUNAN-NABII

MLANGO WA 10 ADAB ZA CHOONI 1. Kutoka kwa Shahid al-Thani katika Sharh al-Nafliyyah: Hakuna hata mtu mmoja aliyewahi kumuona kamwe Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akienda haja ndogo au kujisaidia (haja kubwa).589 2. Katika al-Ja’fariyat: Katika riwaya yake kutoka kwa Ja’far ibn Muhammad, kutoka kwa baba zake, kutoka kwa Ali (a.s.): Wakati wowote Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipotaka kutema makohozi, angejifunika kichwa chake kwanza na kisha (baada ya kutema) angezika makohozi hayo. Na wakati alipokwenda chooni, (vilevile) angefunika kichwa chake.590 3. Katika al-Majalis al-Akhbar: Imesimuliwa kutoka kwa Abu Dharr kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba katika ushauri wake, yeye alisema: Oh, Abu Dharr! Ona haya mbele ya Mwenyezi Mungu, kwani Wallahi ninapokwenda kujisaidia, huwa ninajificha na kujifunika kwa nguo zangu kwa aibu na Malaika ambao wako pamoja nami.591 4. Kutoka kwa al-Mufid ndani ya al-Muqni’ah: Kujifunika kichwa, kama kiko wazi, ni Sunnah katika Sunnah za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).592 5. Katika al-Ja’fariyat: Katika riwaya yake kutoka kwa Ja’far ibn Muhammad, kutoka kwa baba zake, kutoka kwa Ali (a.s.): Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angelikamua njia ya mkojo mara tatu baada ya kwenda haja ndogo.593 6. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa al-Husein ibn Khalid kutoka kwa alHasan al-Thani (a.s.) akisema: “Imesimuliwa kwetu ndani ya hadithi kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angejitakasa mwenyewe (baada ya kujisaidia) wakati ambapo pete yake ikiwa bado kwenye kidole chake, na hivi ndivyo ilivyokuwa pia kwa Amirul-Mu’minin (a.s.); na ile michoro ya maandishi juu ya pete ya Mtukufu 589 Fawa’id al-Milliyyah fi Sharh al-Nafliyyah:17; ‘Awarif al-Ma’arif:261; Da’aim alIslam 1: 104 590 al-Ja’fariyat: 30; Da’aim al-Islam 1: 104; al-Mustadrak 1:248 591 Amali at-Tusi 2: 147; Majmu’at Warram: 307; Makarim al-Akhlaq: 465 592 al-Muqni’ah: 39; Tahdhib al-Ahkam 1:24 593 al-Ja’fariyat: 12; al-Mustadrak 1: 260 110


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 111

SUNAN-NABII Mtume (s.a.w.w.) yalikuwa maneno ‘Muhammad ni Mtume wa Allah’ (je, haya ni kweli)? Yeye (a.s.) akasema: “Wao wamesema kweli.” Mimi nikasema: “Je, na sisi tufanye vivyo hivyo?” Yeye akajibu: “Wao walikuwa wakivaa pete zao katika mkono wa kulia ambapo ninyi mnavaa pete zenu juu ya mkono wa kushoto.”594 Kidokezo: Hadithi kama hiyo inapatikana ndani ya al-Makarim akinukuu kutoka kwenye Kitab al-Libas cha al-Ayyashi kutoka kwa al-Hasayn ibn Sa’id kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.), na vilevile ndani ya al-Ja’fariyat.595 7. Katika al-Khisal: Imesimuliwa kutoka kwa al-Husein ibn Mus’ab kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mambo matatu ambayo yalikuwa yakifanywa na al-Barra’ ibn Ma’rur al-Ansari yalikuja kuwa ni sehemu ya Sunnah: Hapo mwanzoni, watu walitumia kujisafisha wenyewe kwa mawe hivyo al-Barra’ ibn Ma’rur alikula boga ambalo lililainisha matumbo yake na akajisafisha kwa maji; na Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. akajulisha kuhusu yeye: “ ….. Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda sana wale wanaotubu na wale wanaojitakasa.” (2: 222) Na ikawa ni Sunnah mtu kujisafisha mwenyewe kwa maji. Alipokuwa kwenye kitanda chake cha umauti, alikuwa nje ya Madina, hivyo aliagiza kwamba uso wake ugeuziwe kumuelekea Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) (ambaye alikuwa Makka) na akausia moja ya tatu ya mali yake; hivyo ikawa kwamba ile sheria ya kuhusu kuelekea Qibla ilipitishwa na kuusia moja ya tatu ya mali yake mtu ikawa ndio Sunnah.596 8. Katika al-Tahdhib: Katika riwaya yake kutoka kwa Abdullah ibn Maskan kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa mwangalifu sana kuhusu mikojo. Wakati alipotaka kwenda haja ndogo, yeye angetafuta mahali ambapo pamenyanyuka kutoka ardhini, au eneo ambapo palikuwa na udongo mwingi, kwa kuchukia kurukiwa na mkojo.597 9. Ndani ya al-Ja’fariyat: Katika riwaya yake kutoka kwa Ja’far ibn Muhammad, kutoka kwa baba yake (amani juu yao wote), ambaye amesema: Baba yangu (Ali ibn Husein a.s.) amesema: “Ewe mwanangu! Nipatie nguo kwa ajili ya (matumizi ya) chooni. Mimi nilimuona inzi ametua juu ya kitu kichafu na kisha akaja akatua mwilini mwangu.” Yeye akasema: Nilimletea nguo hiyo halafu akasema: “Sio Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wala masahaba zake, wote hawana nguo (kwa ajili ya 594 al-Kafi 6: 373; ‘Uyun al-Akhbar al-Ridha 2: 55 595 Makarim al-Akhlaq: 92, al-Ja’fariyat: 186 596 al-Khisal: 192 597 Tahdhib al-Ahkam, 1: 33; Ilal al-Shara’i: 278; al-Faqih 1: 22 111


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 112

SUNAN-NABII madhumuni haya) nyingine mbali na nguo zao za kawaida,” hivyo yeye hakuichukua nguo hiyo tena.”598

Nyongeza kwa sehemu hii 1. Katika al-Hidayah: Sunnah ya kuingilia chooni ni kwamba mtu aingie kwa mguu wake wa kushoto kabla ya ule wa kulia na anapaswa kufunika kichwa chake na kumkumbuka Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla.599 2. Katika al-Kafi: Katika riwaya yake kutoka kwa Abi Usamah ndani ya hadithi kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.): Mtu mmoja alimuuliza yeye, (miongoni mwa mambo mengine): “Ni ipi Sunnah kuhusu kuingia chooni?” Yeye (a.s.) akasema: “Mkumbuke Mwenyezi Mungu, omba ulinzi Kwake dhidi ya Shetani aliyelaaniwa na pale utakapokuwa umemaliza kujisaidia, basi sema: “Alhamduli-llahi ‘alaa maa akhraja minniy minal-‘adhaa fiy yusrin wa ‘aafiytin.” “Utukufu wote na sifa ni Zake Mwenyezi Mungu kwa kile alichoondoa kutoka kwangu ambacho ni chenye madhara (kwa mwili wangu) kwa urahisi na kunibakisha mwenye afya njema.”600 Kidokezo: al-Barqi ameisimulia hadithi hii katika al-Mahasin kama vile alivyofanya al-Saduq katika al-‘Ilal.601 3. Katika at-Tahdhib: Katika riwaya yake Zurarah kutoka kwa Abi Ja’far (a.s.) ambaye amesema: Hakuna swala isipokuwa mpaka wudhuu. Inaruhusiwa wewe kujisafisha kwa mawe matatu (baada ya kujisaidia) kwani hii ilikuwa ni katika Sunnah ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Na kwa kwenda haja ndogo hata hivyo, ni lazima kwa mtu kujisafisha kwa maji baada ya kukojoa.602 Kidokezo: Yeye ameisimulia pia ndani ya al-Istibsar.603

598 al-Ja’fariyat: 14 599 al-Hidayah: 15 600 al-Kafi, 3: 69 601 al-Ilal al-Shara’i: 276, hatukuipata hadithi hii katika al-Mahasin. 602 Tahdhib al-Ahkam, 1:50 603 al-Istibsar, 1: 55

112


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 113

SUNAN-NABII 4. Katika at-Tahdhib: Kutoka kwa Ahmad ibn Muhammad, kutoka kwa baadhi ya masahaba wetu wakisimulia kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Ilikuwa ni kutoka katika Sunnah kutumia mawe matatu masafi kwa ajili ya kujisafishia mtu (baada ya kwenda haja) ikifuatiwa na kusafisha kwa maji.604 5. Katika al-Da’aim: Ali (a.s.) amesema: Sunnah ya kuhusiana na kujisafisha mwenyewe mtu kwa maji ni ya kuanza na (kuondosha) huo mkojo na halafu mabaki ya haja kubwa na sio kuosha vyote mara moja kwa wakati mmoja.605 6. Vilevile: Wakati yeye (s.a.w.w.) alipotaka kujisaidia mwenyewe wakati akiwa safarini, angejisogeza mbali sana (na walipo watu) na kujitafutia sehemu iliyojificha. 606 7. Vilevile: Wao (Maimam – a.s.) wamesimulia: Pale Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa akiingia chooni, angefunika kichwa chake na kujificha mwenyewe na hakuna hata mtu mmoja aliyewahi kumuona asilani.607

604 Tahdhib al-Ahkam, 1: 46 605 Da’aim al-Islam, 1: 106 606 Da’aim al-Islam, 1: 104; al-Mstadrak, 1:249; ‘Awarif al-Ma’arif: 261 607 Da’aim al-Islam, 1: 104 113


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 114

SUNAN-NABII

MLANGO WA 11 WAFU NA CHOCHOTE KINACHOHUSIANA (NA KIFO) 1. Katika al-Makarim: Kila wakati pale Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipoona kipele kwenye mwili wake, yeye alikuwa akikimbilia kwa Mwenyezi Mungu na kujisalimisha Kwake na kumwomba kwa unyenyekevu. Alikuwa akiulizwa: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Ni nini sababu ya huzuni yako hii?” Yeye angejibu: “Kama Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. akipenda (jambo) dogo kuwa kubwa, litakuwa kubwa na kama akipenda jambo kubwa liwe dogo, basi litakuwa dogo.608 2. Katika kitabu al-Tamhis: Kutoka kwa Abi Sa’id al-Khudri (ambaye amesema) kwamba yeye aliweka mkono wake juu ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w) naye akaona kwamba alikuwa na homa, na aliligundua hili (wakati mkono wake ukiwa) juu ya blanketi, hivyo yeye akasema: “Ni kwa ukali kiasi gani (homa) limekuathiri, Ewe Mtume wa Allah?!” Yeye (s.a.w.w.) akasema: “Hivi ndivyo ambavyo tumefanywa kupitiwa na mitihani mikubwa na malipo yetu (hapo) ni maradufu.”609 3. Kaktika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Jabir kutoka kwa Abi Ja’far (a.s.) ambaye amesema: Iliyo Sunnah ni kwamba jeneza linapaswa kubebwa kwa pande zake zote nne na lolote la nyongeza zaidi ya hili ni hiari.610 4. Vilevile: Imesimuliwa kutoka kwa al-Fadhl ibn Yunus kutoka kwa Musa ibn Ja’far (a.s.): Utaratibu wa kubeba jeneza lenye mwili wa marehemu, kwa mujibu wa Sunnah iliyozoeleka, ulikuwa ni kuanza kwa kunyanyua upande wa mkono wa kulia (wa mwili wa marehemu), halafu mguu wa kulia, kisha mguu wa kushoto, na mwishowe ule mkono wa kushoto, mpaka liwe limenyanyuliwa juu kutoka pande zote.611 5. Kutoka kwa Abdillah ibn Ja’far katika Qurb al-Isnad: Kutoka kwa al-Hasan ibn Dharif kutoka kwa al-Husein ibn ‘Alwan kutoka kwa Ja’far kutoka kwa baba yake (a.s.): al-Hasan ibn Ali (a.s.) alikuwa amekaa na wafuasi wake wakati maandamano 608 Makarim al-Akhlaq: 357 609 al-Tamhis: 34; Bihar al-Anwar, 16: 275 610 al-Kafi, 3:168; Tahdhib al-Ahkam, 16: 275 611 Ibid. 114


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 115

SUNAN-NABII ya mazishi yalipopita karibu yao, hivyo baadhi ya watu walisimama lakini Hasan (a.s) yeye hakusimama, na pale msafara huo ulipokwisha kupita, baadhi yao wakasema: “Kwa nini wewe hukusimama – Mwenyezi Mungu akujaalie afya njema – wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akisimama kwa ajili ya jeneza lilipokuwa linapitishwa?” Hasan (a.s.) akasema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisimama mara moja tu na hii ilikuwa pale wakati jeneza la Myahudi mmoja lilipokuwa limebebwa na sehemu hiyo ilikuwa finyu, kwa hiyo Mtume alisimama kwa sababu alikuwa hakupenda kwamba jeneza hilo lipite juu ya kichwa chake.”612 6. Kutoka kwa al-Qutb ndani ya Da’awat yake: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipofuata msafara wa mazishi, angezidiwa na huzuni na angetafakari zaidi na kuongea kidogo.613 7. Katika al-Ja’fariyat: Katika riwaya yake kutoka kwa Ja’far ibn Muhammad kutoka kwa baba zake, kutoka kwa Ali (a.s): Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa amezoea kutupa mafumba matatu ya udongo kwenye kaburi (la muumini).614 8. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Zurarah kutoka kwa Abi Ja’far (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angefanya jambo maalum pale mtu kutoka Bani Hashim alipofariki; jambo ambalo hakulifanya kwa Mwislam mwingine yoyote. Baada ya kuswali ile salat al-mayyit kwa ajili ya huyo Bani Hashim na kunyunyiza maji juu ya kaburi lake, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliweka mkono wake juu ya kaburi hilo mpaka vidole vyake vikawa vinaonekana kuwa ndani ya udongo, na pale ambapo mtu angerejea nyumbani (kutoka safarini) au msafiri kutoka Madina (angekuja), angeona kaburi mpya yenye chapa ya mkono wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kusema: “Ni nani aliyekufa kutoka kwenye familia ya Muhammad (s.a.w.w.)?”615 9. Vilevile: Imesimuliwa kutoka kwa Abd al-Rahman ibn Abi Abdillah ambaye alisema: Nilimuuliza yeye kuhusu kule mtu kuweka mkono juu ya kaburi – ni kitu gani na kwa nini kinafanyika? Yeye alijibu: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alilifanya hili juu kaburi la mwanawe baada ya kunyunyizia maji (juu ya kaburi hilo). Nilimuuliza yeye tena: Nitaweka vipi mkono wangu juu ya makaburi ya Waislam? Yeye alinionyesha kwa kuweka mkono wake juu ya ardhi na kisha akaunyanyua (na hili lilikuwa) wakati akiwa ameelekea Qiblah.616 612 Qurb al-Isnad: 42 at-Tahdhib, 1: 456 (pamoja na sanadi nyingine ya wasimuliaji akiitaja kutoka Husein a.s.) 613 Da’awat: 256 614 al-Ja’fariyat: 202 615 al-Kafi, 3: 200; Tahdhib al-Ahkam 1: 460 616 al-Kafi, 3: 200 115


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 116

SUNAN-NABII 10. Kutoka kwa Shahid al-Thani katika Musakkin al-Fu’ad: Kutoka kwa Ali (a.s.): Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipotoa rambirambi angesema: “Ajarakumu-llahu wa rahimakum.” “Mwenyezi Mungu akulipeni na akurehemuni nyie.” Na wakati alipokuwa anampongeza mtu yeyote, yeye angesema: “Baraka llahu lakum wa baraka lahu alaykum.” “Mwenyezi Mungu akubariki na akudumishe katika kubarikiwa.” 11. Kutoka kwenye al-Qurb ndani ya Da’awat yake: Zayn al-Abidin (a.s.) amesema: Hapakuwa kamwe na wakati ambapo Amirul-Mu’minin (a.s.) alipatwa na huzuni bali kwamba angeswali rakaa elfu moja siku hiyo, kutoa sadaka kwa waombaji sitini na kufunga kwa siku tatu. Yeye (a.s.) aliwaambia wanawe: “Wakati huzuni yoyote inapokufikeni, basi fanyeni kama ninavyofanya mimi, kwani nilimuona Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akifanya hivi, kwa hiyo fuateni mwenendo (nyayo) wa Mtume wenu na msiuvunje kwani Mwenyezi Mungu atakuwa (kwa ajili ya hilo) dhidi yenu. Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. amesema:

“Na anayesubiri na kusamehe, bila shaka hilo ni katika mambo makubwa.” (Suratul-Shuraa; 42: 43)

Zayn al-Abidin (a.s.) akasema: “Mimi bado ninafanya kitendo hiki cha AmirulMu’minin (a.s.).617

Nyongeza kwenye sehemu hii 1. Katika al-Makarim: Kutoka kwa Anas ibn Malik ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akitumia kuwatembelea wagonjwa na kuhudhuria mikusanyiko ya mazishi.618

617 al-Da’awat: Mustadrak al-Da’awat: 287 618 Makarim al-Akhlaq: 15; al-Manaqib, 1: 146 116


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 117

SUNAN-NABII 2. Katika al-Majalis ya Sheikh al-Tusi: Katika riwaya yake kutoka kwa al-Harith kutoka kwa Ali (a.s.) ambaye amesema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipotembelea mtu mgonjwa, yeye angesema: “Adh’hibil-ba’asa rabal-ba’asi wa-ashfi anta-shaafiy laa shaafiya ila anta.” “Ondoa huzuni hii Ewe Bwana wa huzuni, na ponya kwani Wewe ndiwe Mponyaji, hakuna mponyaji mwingine ila ni Wewe.”619 Kidokezo: Hadithi nyingine kama hii inatajwa na al-Tabarsi katika al-Makarim.620 3. Katika Tibb al-A’immah: Kutoka kwa Jabir kutoka kwa al-Baqir (a.s.) ambaye amesema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) au mtu yoyote kutoka kwenye familia yake, au kati ya masahaba (wa karibu) alipokuwa anateswa na muwasho kwenye macho yake, yeye angesoma dua ifuatayo: “Allahumma mati’iniy bi sam’iy wa baswariy waj’alhumaa alwarithayni miniy wansurniy ‘alaa man dhwalamaniy wa ariniy fiyhi tha’ariy.” “Ewe Mungu Wangu! Nifanye nifaidi kusikia kwangu na kuona kwangu na vifanye viendelee pamoja nami hadi ile siku nitakapokufa, na nisaidie (kupata ushindi) juu ya yule anayenionea mimi na unilipizie kisasi changu toka kwake.”621 4. Katika al-Makarim: Kutoka kwa ibn Abbas ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akitufundisha sisi kusoma hii kwa ajili ya aina zote za maumivu, homa na kuumwa na kichwa: “Bismillahi al-Kabiir. ‘Audhu billahi’l-‘Adhwiimi min sharri kulli ‘irqin na‘arin wa min sharri harrin-naari.” “Kwa jina la Mwenyezi Mungu aliye Mkubwa. Najikinga kwa Mungu Mwenye Enzi dhidi ya ubaya wa kila kinacho bubujika mishipani na kutokana na ubaya wa joto la Moto wa Jahannam.”622 619 Amali al-Tusi, 2: 252 620 Makarim al-Akhlaq: 401 621 Tibb al-A’immah: 83 622 Makarim al-Akhlaq: 401 117


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 118

SUNAN-NABII 5. Katika Majmu’at Warram: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa amehuzunishwa na jambo, angechukua kimbilio kwenye kufunga na swala.”623 6. Al-Shahid al-Thani katika Musakkin al-Fu’ad: Wakati wowote huzuni ilipomfika Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), yeye angesimama, akachukua wudhuu, akaswali rakaa mbili na kusema: Allahumma qad fa’altu maa ‘amartanaa fa’anjizlana maa wa ‘adtanaa.” “Ewe Mungu wangu! Nimefanya kama ulivyotuamuru, hivyo tutimizie ambacho ulikuwa umetuahidi.”624 7. Katika al-Kafi: Kutoka kwa ‘Ala’ ibn Kamil ambaye amesema: Nilikuwa nimeketi mbele ya Abi Abdillah (a.s.) wakati ambapo (ghafla) ukelele wa mwanamke ulisikika kutoka ndani nyumba hiyo, hivyo Abu Abdillah (a.s.) akasimama halafu tena akakaa chini na akarejea kwenye umakini wake na akaendelea na mazungumzo yake mpaka alipoyamaliza, halafu akasema: “Sisi (Ahlul-Bayt) tunapenda ustawi wetu, wa watoto wetu na mali zetu, lakini kunapokuwa na amri ya ki-ungu, sio juu yetu sisi kupenda jambo ambalo Mwenyezi Mungu hatutaki juu yetu sisi.”625 Kidokezo: al-Kulayni amesimulia hadithi nyingine mbili zenye maana hiyo hiyo na al-Saduq vilevile ameisimulia hii katika al-Faqih na Ikmal al-Din.626 8. Katika al-Kafi: Kutoka kwa Ali ibn Ibrahim kutoka kwa baba yake, kutoka kwa (Imam A.S.) ambaye amesema: Ile Sunnah kuhusu ‘Hunut’ (kafuri inayotumika katika kuhifadhi maiti – wakati wa kuosha) ni (kutumia) kiasi sawa na (uzito wa) dirham kumi na tatu na theluthi moja. Halafu yeye (a.s.) akasema: Jibril alimshukia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na ‘Hunut’ yenye uzito sawa na dirham arobaini, hivyo Mtukufu Mtume akaigawanya katika sehemu (zinazolingana) tatu, moja ya kwake yeye mwenyewe, sehemu kwa ajili ya Ali (a.s.) na sehemu kwa ajili ya Fatimah (a.s.)627

623 Majmu’at Warram: 255 624 Musakkin al-Fu’ad: 56 625 al-Kafi 3:226 626 al-Kafi 3:225-226, al-Faqih 1: 187, Kamal al-Din wa Tamam al-Ni’mah 1:73 627 al-Kafi 3:151

118


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 119

SUNAN-NABII Kijalizo: Hii imesimuliwa vilevile na Sheikh at-Tusi katika al-Tahdhib pia na alSaduq katika al-‘Ilal, al-Faqih, Fiqh al-Ridha na al-Hidayah.628 9. Vilevile: Katika simulizi yake kutoka kwa Zurarah na Muhammad ibn Muslim ambao wamesema: Tulimuuliza Abu Ja’far (a.s.): “Je kilemba cha mwili wa marehemu ni sehemu ya sanda?” Yeye akasema: “Hapana. Sanda ya wajibu inatengenezwa na vipande vitatu vya nguo au kwa kima cha chini sana, (kama hivyo haviwezi kupatikana) nguo moja kamili ambayo inafunika mwili mzima. Kitu chochote zaidi ya hicho ni Sunnah mpaka ifikie nguo tano, na chochote zaidi ya hicho ni bid’a na hicho kilemba ni Sunnah.629 10. Katika al-Tahdhib: Kutumia ‘Jarid’ (matawi ya mtende – yaliyoondolewa majani – ambayo yanazikwa pamoja na maiti) pia ni kutoka katika Sunnah.630 11. Sheikh Tusi katika ‘Ghaybah’: Kutoka kwa Muhammad ibn al-Hasan al’-Alawi na wengineo katika hadithi ndefu kutoka kwa Musa ibn Ja’far (a.s.) ambaye alisema: Sisi Ahlul-Bayt – mahari kwa ajili ya wanawake zetu, hijja ya wale kutoka miongoni mwetu ambao hawajakwenda hijji, na sanda za marehemu zetu (zote) zinatoka kwenye mali yetu safi halisi kabisa; na mimi ninayo sanda yangu kabisa…..631 12. Katika Ja’fariyat: Katika riwaya yake kutoka kwa Ali (a.s.): Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa akiswalia mwili wa marehemu, kama alikuwa ni mwanaume, basi angesimama karibu na kifua chake, na kama alikuwa ni mwanamke, angesimama karibu na kichwa chake.632 Kidokezo: Hii imesimuliwa pia katika al-Da’aim, na vilevile katika at-Tahdhib kutoka kwa Jabir kutoka kwa Abi Ja’far (a.s.)633 13. Katika ‘Awali al-La’ali: Kutoka kwa Abi Sa’id al-Khudri: Yeye (s.a.w.w.) kamwe hakupanda kipando (kwenye siku ya) Iddi au (wakati akihudhuria) kwenye mazishi – asilan.364 628 Tahdhib al-Ahkam 1:290, ‘Ilal al-Shara’i: 302, Fiqh al-Imam ar-Ridha: 168, al-Faqih 1:149 629 al-Kafi 3: 144, Tahdhib al-Ahkam 1: 292 630 Tahdhib al-Ahkam 1: 326, al-Muqni’:18, al-Faqih 1:144 631 al-Ghayba: 23, al-Mustadrak 2: 231, Tuhf al-‘Uqul: 412 632 al-Ja’fariyat: 210 633 Da’aim al-Islam 1:125, Tahdhib al-Ahkam 3:190 634 ‘Awali al-La’ali 2;220, al-Mustadrak 2: 300 119


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 120

SUNAN-NABII 14. Katika al-Kafi: Katika riwaya kutoka kwa al-Sakuni kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye alisema: Amir al-Mu’min (a.s.) amesema: Iligeuka kuwa Sunnah kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba mtu yoyote asije akaingia kwenye kaburi ya mwanamke isipokuwa wale waliokuwa wanaruhusiwa kumuona wakati wa uhai wake.635 15. Vilevile: Katika riwaya yake kutoka kwa Ali ibn Yaqtin ambaye alisema: Nilimsikia Aba al-Hasan (a.s.) akisema: Usishuke ndani ya kaburi ukiwa umevaa kilemba, kofia, skafu au viatu, na ufungue vifungo vyako (kabla ya kuingia ndani) kwani hii ilikuwa ni Sunnah ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.); na utafute hifadhi kwa Mola Wako kutokana na Shetani aliyelaaniwa na usome ‘Fatihal-Kitab’ (SuratulHamd); al-Mawaidhatain (Suratun-Nas na Suratul-Falaq): ‘Qul huwa-llahu Ahad’ na Ayatul-Qursi.636 Kidokezo: Hii imesimuliwa vilevile na as-Saduq katika al-‘Ilal na Sheikh at-Tusi katika at-Tahdhib.637 16. Vilevile: Katika simulizi yake kutoka kwa Umar ibn Udhaynah ambaye amesema: Nilimuona Aba Abdillah (a.s.) akirushia udongo kwenye mwili wa marehemu (ndani ya kaburi). Aliushikilia udongo huo mkononi mwake kwa muda kiasi na halafu akaurusha na hakuwahi kurusha zaidi ya mafumba matatu. Hivyo nikamuuliza kuhusu hili. Yeye akajibu: “Ewe Umar! Mimi nilikuwa nikisema hivi: “‘Iymaanan wa tasidiiqan biba’athika haadhaa maa wa’ada’llahu wa rasuuluhu wa swadaqa’llahu wa rasuuluhu wa maa zaadahum ila iymaanan wa tasliiman.” “(Ewe Mola Wangu!) Ninaamini na kuthibitisha kwamba utawafufua (wanadamu wote); ….. Haya ndio Mwenyezi Mungu na Mtume Wake waliyoyaahidi na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wamesema kweli – na haikuwaongezea ila imani na utii.”638 Hivi ndivyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w) alivyokuwa akifanya na kwa hiyo ikawa ni Sunnah.”639

635 al-Kafi 3:194, Tahdhib al-Ahkam 1:325, al-Ja’fariyat: 203 636 al-Kafi 3:192 637 Ilal al-Sharai’: 305, Tahdhib al-Ahkam 1:313 638 Suratu’al-Ahzab; 33:22 639 al-Kafi 3:198 120


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 121

SUNAN-NABII 17. Katika Qurb al-Isnad: Kutoka kwa Ali (a.s.): Ni (kutoka katika) Sunnah kumwagia maji kidogo juu ya kaburi.640 18. Katika al-Tahdhib: Katika riwaya yake kutoka kwa Musa ibn Ikil al-Numayri kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Iliyo Sunnah kuhusu kumwagia maji juu ya kaburi ni kwamba mtu lazima aelekee Qibla na aanze kumwagia maji kuanzia upande wa kichwani kwenda upande wa miguuni, halafu alizunguuke kaburi kwenda kwenye upande ule mwingine, halafu amwagie maji katikati ya kaburi; na hii ndio Sunnah yenyewe.641 19. Katika al-Fiqh al-Ridha: Iliyo Sunnah ni kaburi kunyanyuliwa (kwenye urefu wa) vidole vinne vilivyotanuliwa kutoka ardhini, na kama imenyanyuliwa zaidi ya hivi hakuna tatizo na kaburi lazima lisawazishwe bali lisifanywe duara.642 20. Katika al-Kafi: Katika riwaya yake kutoka kwa Hashim ibn Salim kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Wakati Ja’far ibn Abi Talib (a.s.) alipouawa shahidi, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimwambia Fatimah (a.s.) apeleke chakula kwa Asma’ binti ‘Umays kwa muda wa siku tatu na aende na wanawake wa familia yake na wakakae naye kwa siku tatu, hivyo ikajakuwa ni Sunnah kutoa chakula kwa ile familia yenye kuhuzunika.643 Kidokezo: Riwaya kama hii imesimuliwa pia na al-Barqi katika al-Mahasin na pia al-Saduq katika al-Faqih na katika al-Faqih ar-Ridha, na vilevile Sheikh at-Tusi katika al-Amali.644 21. Vilevile: Katika riwaya yake kutoka Hariz au mtu mwingine ambaye amesema: Abu Ja’far (a.s.) aliusia dirham mia nane kwa ajili ya mazishi yake na aliliona hili kuwa ni kutoka kwenye Sunnah kwa sababu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Chukueni chakula kwa ajili ya familia ya Ja’far ibn Abi Talib kwani wameshughulishwa (katika maombolezo).”645 22. Katika al-Faqih: as-Sadiq (a.s.) amesema: Kula kwenye nyumba ya (familia) wenye huzuni ni desturi tangu zama za jahilia na iliyo Sunnah ni kupeleka chakula kwa ajili yao.646 640 Qurb al-Isnad: 72, al-Ja’fariyat: 203 641 Tahdhib al-Ahkam 1:320 642 al-Fiqh al-Mansub li al-Imam ar-Ridha: 175, al-Mustadrak 2:335 643 al-Kafi 3:217 644 al-Mahasin: 419; al-Faqih 1:182; al-Fiqh al-Imam ar-Ridha: 172; ‘Amali at-Tusi 2: 642 645 al-Kafi 3:217 646 al-Faqih 1:182 121


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 122

SUNAN-NABII

MLANGO WA 12 ADAB ZA MATIBABU 1. Katika Qurb al-Isnad: Katika riwaya yake kutoka kwa Husein ibn Dhariif kutoka kwa al-Husein ibn ‘Alwan, kutoka kwa Ja’far kutoka kwa baba yake (amani juu yao wote): Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikifanya kichwa chake kiumikwe647 sehemu ya kati yake. Abu Dhabiyyah alifanya huo uumikaji kwa vyombo vyake maalum na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimpa sa’ moja (kilo tatu) ya tende. Yeye (pia) alisema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angeweza kuvuta mafuta ya mbegu za ufuta kwa pumzi (akiyaweka ndani ya pua yake) wakati alipokuwa na maumivu ya kichwa.648 Maelezo: al-Kulayni amesimulia vilevile hadithi kama hiyo.649 Kama ilivyokuwa imetajwa kwenye sehemu juu ya usafi, yeye (s.a.w.w.) angeweka (pia) mafuta kwenye kope za macho yake ili kupata nafuu kutokana na maumivu ya kichwa. 2. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Bakr ibn Salih al-Nawfal na wengine, wakiihusisha kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakutumia dawa kwa ajili ya baridi ya homa za kawaida, akisema: “Hakuna mtu yoyote ambaye ana hali ya kutoweza kuambukizwa ukoma, hivyo pale anapopatwa na homa, huwa linadhibiti ukoma huo.650 3. Vilevile: Imesimuliwa kutoka kwa Muhammad ibn Al-Fayd ambaye amesema: Nilimwambia Abi Abdillah (a.s.): “Mtu kutoka miongoni mwetu alipatwa na ugonjwa hivyo akaamriwa na waganga ashikilie kwenye chakula maalum.” Yeye akasema: “Lakini sisi, Ahlul-Bayt, hatujiwekei utaratibu wa chakula maalum isipokuwa tende, na tunatumia tufaha na maji baridi kama tiba.” Mimi nikasema: “Na kwa nini mnachunga ulaji kwa tende?” Yeye akajibu: “Kwa sababu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliagiza chakula hiki kwa ajili ya Ali (a.s.) wakati alipokuwa mgonjwa.651

647 Kuumika kulikuwa ni taratibu ya matibabu ya kienyeji yaliyokuwa yakitumika kuongeza mgao wa damu kwenye sehemu ya mwili. (Mfasiri) 648 Qurb al-Isnad: 52 na 53 649 al-Kafi 6:524 650 Ibid, 8:382 651 Ibid, 8: 291 122


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 123

SUNAN-NABII Kidokezo: al-Saduq ameisimulia hii ndani ya al-‘Ilal,652 na riwaya kama hizi zimesimuliwa na wengine pia.653

Nyongeza kwenye sehemu hii 1. Katika Ma’ani al-Akhbar: Kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angefanya uumikaji kwenye kichwa chake na angeuita uumikaji huo ‘al-Mughithah’ (kitulizo) au ‘al-Munqidhah’ (kiokozi).654 2. Katika al-Makarim: Kutoka kwa as-Sadiq (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angefanya uumikaji katika siku za Jumatatu baada ya swala ya Alasiri.655 Kidokezo: Hii vilevile inasimuliwa na al-Saduq katika al-Khisal.656 3. Katika al-Bihar: Zayd an-Nursi amesema: Nilimsikia Abul-Hasan (a.s.) akisema: Kuosha kichwa kwa kinamasi nyororo (marsh mallow) katika siku za Ijumaa ni kutoka katika Sunnah. Kunaleta wingi katika riziki na kunazuia umasikini. Kunaboresha nywele na ngozi na kunakinga maumivu ya kichwa.657 4. Vilevile: Kutoka kwa mmoja wa masahaba wetu ambaye amesema: Nilimsikia Abi Abdillah (a.s.) akisema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angeosha kichwa chake kwa sidr, akisema: “Yule atakayeosha kichwa chake kwa sidri Mwenyezi Mungu atamuepusha na vishawishi vya Shetani; na yule ambaye hasumbuliwi na vishawishi vya Shetani huwa hafanyi dhambi, na yule ambaye hafanyi dhambi ataingia Peponi.658 Kidokezo: Kipande hicho cha mwanzoni kimesimuliwa na al-Saduq katika Thawab al-A’mal.659 5. Ibn Bastam katika Tibb al-A’immah: Imesimuliwa kutoka kwenye sanadi ya ‘Ammar kutoka kwa Fudhayl al-Rassan ambaye amesema: Abu Abdillah (a.s.) amesema: Kutoka kwenye tiba na dawa za Mitume (a.s.) kuna pamoja na kuumika, 652 ‘Ilal al-Shara’i: 464 653 al-Mustadrak 16: 452, al-Ja’fariyat: 199 654 Ma’ani al-Akhbar: 74 655 Makarim al-Akhlaq: 74 656 al-Khisal: 384 657 Bihar al-Anwar 76: 88 658 Ibid, 76: 88 659 Thawab al-A’mal: 37 123


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 124

SUNAN-NABII kuondoa nywele na ugoro (wa ki-dawa)660 6. al-Qurb al-Rawandi katika kitabu chake, Da’awat: Kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye amesema: “Hivi nisiwafundishe kuhusu ile dawa ambayo mimi nilifundishwa na Jibril – ambayo baada yake hamtahitaji mganga yoyote au tiba?” Wao wakasema: “Ndio, tufundishe, Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu!” Yeye akasema: “Chukua maji ya mvua na uyasomee Fatihat al-Kitab (Suratul-Hamd) mara sabini; ‘Qul A’udhu Birabbi an-Nas’ (Suratun-Nas) mara sabini; ‘Qul A’udhu Birabbil-Falaq’ (Suratul-Falaq) mara sabini, Salawat mara Sabina na Subhana-llah mara sabini na kisha kunywa kutoka kwenye maji haya asubuni na wakati wa usiku kwa siku saba mfululizo.661 7. Katika al-Kafi: Katika simulizi yake kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimlalamikia Mola Wake ‘Azza wa Jalla. juu ya maumivu ya mgongo, hivyo Yeye akamuagiza kula nafaka pamoja na nyama – kwa maana ya ‘al-Harisah’ (chakula kinachotengenezwa kwa kuchanganya bulga na nyama).662 8. Katika al-Ja’fariyat: Katika riwaya yake kutoka kwa Ali (a.s.): Wakati wowote Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipoteseka kutokana na maumivu yoyote yale (ndani ya mwili wake) angefanya uumikaji.663 9. Ibna Bastam ndani ya Tibb al-A’immah katika riwaya yake kutoka kwa Abi Usama ambaye amesema: Nilimsikia Abi Abdillah (a.s.) akisema: Babu yetu hakuwa akitumia kitu chochote bali sukari ya uzito wa dirham kumi iliyochanganywa na maji ya baridi (kuyanywa) – kwenye tumbo tupu – kutibia homa.664 Kidokezo: Ni dhahiri kwamba wakati aliposema ‘babu yetu’ alikuwa akiashiria kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). 10. Katika Tibb al-A’immah: Katika riwaya yake kutoka kwa Abi Basir, kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akifanya uumikaji kwenye (mishipa ya) shingo yake, hivyo Jibril akatumwa kwake na Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. pamoja na maagizo kwamba anapaswa kuumika 660 Tibb al-A’immah: 57 661 al-Da’awat: 183 662 al-Kafi 6: 320 663 al-Ja’fariyat: 162, al-Mustadrak 13: 77 664Tibb al-A’immah: 50 124


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 125

SUNAN-NABII sehemu ya juu ya mgongo badala yake.665 11. Vilevile: Katika simulizi yake kutoka kwa Shu’aib ambaye amesema: Niliitaja ile hadithi (kuhusu Amirul-Mu’minin (a.s.) ya kuoga baada ya kufanya ndumiko) kwa Abi Abdillah (a.s.). Yeye akasema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipofanya ndumiko, damu yake ilitikisika kwa hiyo alioga maji baridi, na wakati Amirul-Mu’minin (a.s) alipoingia kwenye mabafu ya umma, joto la mwili wake lilipanda hivyo alijimwagia maji ya baridi ili kulipoza.666

665Ibid, 58 666 Ibid, 125


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 126

SUNAN-NABII

MLANGO WA 13 KUPIGA MSWAKI (SIWAK) 1. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Ishaq ibn Ammar kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Kupiga mswaki – kusafisha meno – ni kutoka katika Sunnah ya Mitume (a.s.).667 2. Katika al-Khisal: Katika riwaya yake kutoka kwa Ali (a.s.): Kupiga mswaki kunapendwa sana na Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla na ni Sunnah ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na namna ya kusafisha kinywa.668 Kidokezo: Kuna riwaya kama hiyo zisizo na idadi kutoka kwenye vyanzo mbalimbali. 3. Katika al-Makarim: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angepiga mswaki meno yake mara tatu kwa kila usiku. Mara moja kabla hajakwenda kulala, mara moja wakati alipoamka kwa ajili ya ibada za usiku na mara moja kabla ya kuondoka kwenda kwenye swala ya Alfajiri.669 4. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Ibn Abi Umayr kutoka kwa Hammad kutoka kwa al-Halabi kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokwisha kuswali swala ya Isha, angeomba beseni la kuchukulia wudhuu na mswaki wake na (vilipokwishaletwa) angevifunika na kuviweka karibu naye na kulala kwa muda kiasi – mpaka pale alipotaka Mwenyezi Mungu – halafu angeamka na kusafisha meno yake, akachukua wudhuu na kuswali rakaa nne ambazo baada yake angerudi kulala. Kisha angeamka tena na kupiga mswaki meno yake na kuchukua wudhuu na kuswali. Halafu yeye Imam (a.s.) akasema: “Kwa hakika mnacho kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kigezo chema.”670 Mwishoni mwa hadithi hiyo akasema kwamba yeye (s.a.w.w.) angepiga meno yake mswaki kila wakati alipoamka kutoka usingizini.671 667 al-Kafi 6: 495 668 al-Khisal 2: 611, al-Makarim al-Akhlaq: 51, al-Kafi 6:495, al-Ja’fariyat: 15, alMahasin: 562, Tuhf al-Uqul: 101 669 Makarim al-Akhlaq: 39 670 Surat al-Ahzab; 33: 21 671 al-Kafi 3: 445, Majmaul-Bayan 2: 555, Tahdhib al-Ahkam: 35 126


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 127

SUNAN-NABII 5. Kutoka kwa al-Saduq katika Muqni’: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angepiga meno yake mswaki kabla ya kila swala.672 6. Katika al-Makarim: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipopiga meno yake mswaki, angeyapiga kwa mapana.673 7. Vilevile: Yeye (s.a.w.w.) angeyapiga meno yake mswaki kwa (mswaki wa) ‘alArak674 kwani hivi ndivyo ambavyo Jibril alimwambia afanye.675

Nyongeza kwenye sehemu hii 1. Katika al-Mahasin: Kutoka kwa Muhammad al-Halabi kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akiyapiga sana mswaki meno yake.676 Kidokezo: Hadithi hii imesimuliwa na al-Saduq katika al-Faqih, ibn Abi Jamhur katika Lubb al-Lubab na al-Qadhi katika al-Da’aim.677 2. Katika al-Faqih: Kupiga meno mswaki wakati wa sahar (saa za mwisho za usiku) kabla ya kuchukua wudhuu ni kutoka katika Sunnah.678 3. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kwamba ni (kutoka katika) Sunnah mtu kupiga mswaki meno yake wakati wa sahar.679 4. Kutoka al-Qurb ar-Rawandi katika Lubb al-Lubab kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye amesema: “Mswaki bora ni ule wa mti uliobarikiwa wa mzeituni. Unaifanya pumzi kuwa nzuri na inazuia kutoboka kwa meno; na ndio mswaki wangu na mswaki wa mitume wote wa kabla yangu.”680 5. Katika Jami’ al-Akhbar: Katika hadithi kutoka kwa Ali (a.s.), kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): Yule anayepiga mswaki meno yake mara mbili kwa siku ameendeleza na kudumisha Sunnah ya mitume (a.s.).681 672 al-Muqni’: 8 673 Makarim al-Akhlaq: 35 674 al-Arak ni aina ya mti (Mfasiri) 675 Makarim al-Akhlaq: 39 676 al-Mahasin: 563 677 al-Faqih 1: 53 678 Ibid, 1: 481 679 al-Kafi, 3: 23 680 Imenukuliwa na al-Nuri katika al-Mustadrak 1:369 kutoka kwenye Lubb al-Lubab. 681 Jami’ al-Akhbar: 68 127


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 128

SUNAN-NABII

MLANGO WA 14 ADABU ZA WUDHUU 1. Katika al-Faqih: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angechukua wudhuu upya kwa kila tendo la ibada ya faradhi na katika kila swala ya wajibu.682 2. Kutoka kwa al-Qurb katika Ayat al-Ahkam: Kutoka kwa Sulayman ibn Buraydah kutoka kwa baba yake: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angechukua wudhuu kwa kila swala na wakati mwaka wa kutekwa Makka ulipofika, yeye angetekeleza swala kadhaa kwa wudhuu mmoja hivyo Umar akasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Mbona umefanya jambo ambalo hujawahi kulifanya kabla?” Yeye (s.a.w.w) akajibu: “Nimelifanya huku nikijua ninachokifanya.”683 3. Katika al-Ja’fariyat: Katika riwaya yake kutoka kwa Ja’far ibn Muhammad kutoka kwa baba zake (amani juu yao wote) ambao wamesema: Ali ibn Abi Talib (a.s.) alikuwa akichukua wudhuu kwa kila swala na angesoma Aya ya: ‘Mnaposimama kwa ajili ya swala, osheni nyuso zenu …..’684 Ja’far ibn Muhammad as-Sadiq (a.s.) amesema kwamba yeye alikuwa akifanya hivi ili kupata ubora. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angekusanya pia swala kwa wudhuu mmoja.685 4. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Zurarah ambaye amesema: Abu Ja’far (a.s.) amesema: “Hivi nisiwaambie kuhusu wudhuu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)?” Sisi tukajibu: “Ndiyo, tuambie.” Yeye akasema: “Nileteeni bakuli na maji.” Halafu akaliweka mbele yake na akakunja mikono ya shati lake. Kisha akatumbukiza mkono wake (ndani ya bakuli) na akasema: “Hili (linafanywa) kama mkono wako ni tohara (umesafika kutokana na kinachoonekana ni najisi).” Kisha akachota ujazo wa kiganja kimoja cha maji akauweka kwenye paji lake la uso na akasema ‘Bismillah’ na akayaacha maji hayo kudondoka mpaka kwenye kingo za ndevu zake. Kisha akapitisha kiganja cha mkono wake juu ya uso wake na paji la uso wake mara moja. Kisha akatumbukiza mkono wake wa kushoto na akachota ukufi mmoja wa maji na akayaweka kwenye kiwiko cha mkono wake wa kulia na akapitisha kiganja cha mkono wake wa kushoto juu ya mkono wake wa kulia mpaka 682 al-Faqih 1:39; Da’aim al-Islam 1:100; al-Mustadrak, 1:294 683 Fiqh al-Qur’an, 1: 12 684 Suratul-Ma’idah 5:6 685 al-Ja’fariyat: 17; al-Mustadrak 1:295 128


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 129

SUNAN-NABII maji yakafika kwenye ncha za vidole vyake. Kisha akachota ukufi mmoja wa maji kwa mkono wake wa kulia na akayaweka kwenye kiwiko cha mkono wake wa kushoto na akapitisha kiganja chake juu ya mkono wake wa kushoto mpaka maji yakafika kwenye ncha za vidole vyake. Kisha yeye akapaka maji kwenye sehemu ya mbele ya kichwa chake na kwenye miguu yake kwa unyevunyevu wa kiganja chake cha kushoto na unyevu uliobakia kwenye kiganja cha kulia. Abi Ja’far (a.s.) amesema: Kwa hakika Mwenyezi Mungu yu peke na anapenda upweke. Inatosha kabisa kufanya wudhuu kwa kufi tatu za maji, moja kwa ajili ya uso, na mbili kwa ajili ya mikono, na kisha pakaza sehemu ya mbele ya kichwa chako kwa unyevunyevu wa mkono wako wa kulia, na kile kilichobakia katika unyevu wa mkono wako wa kulia paka juu ya mguu wako wa kulia na kwa unyevu wa mkono wako wa kushoto paka juu ya mguu wako wa kushoto. Zurarah amesema: Abu Ja’far (a.s.) alisema: Mtu mmoja alimuuliza AmirulMu’minin Ali (a.s.) kuhusu wudhuu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hivyo akauelezea kwake kwa namna hii.686 Kijalizo: Kuna riwaya nyingi zinazofanana na hii kutoka kwa Zurarah na Bukair. Hizi zimesimuliwa na al-Saduq, at-Tusi, al-‘Ayyashi, al-Mufid, al-Karajiki na wengineo, na Hadithi kutoka kwa Ahlul-Bayt kuhusu hili ni nyingi mno.687 5. Kutoka kwa Mufid al-Din al-Tusi katika Amali yake: Imesimuliwa kutoka kwa Abu Hurayrah (kwamba): Wakati ambapo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angechukua wudhuu, wakati wote angeanza na upande wake wa kulia (kabla ya ule wa kushoto).680 6. Katika al-Tahdhib: Ndani ya riwaya yake kutoka kwa al-Husayn ibn Sa’id, kutoka kwa ibn Sinan, kutoka kwa Miskan kutoka kwa Abi Basir ambaye amesema: Nilimuuliza Abi Abdillah (a.s.) kuhusu wudhuu naye akasema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alichukua wudhuu kwa Mudd (la maji) na alifanya ghusli (kuoga) kwa Sa’689 ya maji.690 686 al-Kafi, 3:25 687 al-Faqih, 1:36, Tahdhib al-Ahkam, 1:55, al-Istibsar 1:58, Tafsir al-Ayyashi 1:298 – Suratul-Ma’idah, Kanz al-Fawa’id: 69 688 Amali at-Tusi 1:397 689 Vipimo vya zamani – Mudd ni sawa na takrban milimita 750 na Sa’ ni sawa na lita 3 (Tr.) 690 Tahdhib al-Ahkam 1:136, al-Istibsar 1:121, al-Ja’fariyat: 16 129


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 130

SUNAN-NABII Kidokezo: Kuna riwaya kama hiyo kutoka kwa Abi Ja’far (a.s.) pamoja na nyororo tofauti ya wasimuliaji. 691 7. Katika al-‘Uyun: Imesimuliwa kwa sanad mbili za wasimuliaji, kutoka kwa arRidhaa kutoka kwa baba zake (a.s.) – katika hadithi ndefu: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Hairuhusiwi kwetu sisi – Ahlul-Bayt – kupokea sadaka, na tumeamrishwa kutengeneza ibada ya wudhuu kikamilifu kabisa, na hatupandishi (kuzalisha) punda kwenye farasi jike.692 8. Katika at-Tahdhib: Katika riwaya yake kutoka kwa Husayn ibn Sa’id kutoka kwa Qasim ibn Urwah kutoka kwa Abdillah ibn Sinan kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Kusukutua mdomo na kuvuta maji puani (wakati wa kuchukua wudhuu) vilikuwa na kutoka kwenye Sunnah ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).693

Nyongeza kwenye sehemu hii 1. Ndani ya al-Khisal: Kutoka kwa al-Sakuni, kutoka kwa Abi Abdillah, kutoka kwa baba zake kutoka, kwa Ali (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Kuna mambo mawili ambayo nisingependa mtu yoyote ayashiriki pamoja nami – Wudhuu wangu kwani ni sehemu ya swala yangu na sadaka yangu kwani inawekwa kwenye mikono ya Mwenye Huruma.694 2. Katika al-Manaqib: Yeye (s.a.w.w.) angeyahifadhi maji yake ya wudhuu mwenyewe wakati wa usiku.695 3. Katika al-Ikhtisas: Kutoka kwa Abdillah ibn Abi Rafi’, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake ambaye amesema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipochukua wudhuu kwa ajili ya swala, alisogeza pete zake mara tatu.696 4. Katika Majma’ul-Bayan: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angepaka sehemu ya mbele ya kichwa chake (wakati akichukua wudhuu) na hii ingekuwa takriban moja ya nne 691 Tahdhib al-Ahkam 1:136 692 Uyun Akhbar ar-Ridha 2:28, Sahifat al-Imam ar-Ridha: 46 693 Tahdhib al-Ahkam 1:79, al-Ikhtisas: 36, Usul al-Sittata Ashar: 157 694 al-Khisal 1:33, Tafsir al-Ayyashi 2:108 – Surat at-Tawbah, al-Ja’fariyat: 17 695 al-Manaqib 1:146 696 al-Ikhtisas: 160 130


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 131

SUNAN-NABII – robo – ya kichwa (upana).697 5. Katika Amali ya Sheikh at-Tusi: Kutoka kwa Abu Ishaq al-Hamadani katika Hadithi kutoka kwa Ali (a.s.) ambaye amesema: Sukutua kinywa chako mara tatu, weka maji kwenye pua yako mara tatu, osha uso wako, halafu mkono wako wa kulia na kisha mkono wako wa kushoto, halafu paka kichwa na miguu yako, kwani nilimuona Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akifanya hivi.698

697 Majma’ul-Bayan 3:164 – Surat al-Maidah (5) 698 ‘Amali at-Tusi 1:29 131


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 132

SUNAN-NABII

MLANGO WA 15 ADABU ZA KUOGA (GHUSL)699 1. Katika at-Tahdhib: Katika simulizi yake kutoka kwa Husayn ibn Sa’id, kutoka kwa an-Nadhr, kutoka kwa Muhammad ibn Abi Ja’far, kutoka kwa Mu’awiyah ibn Ammar ambaye amesema: Nilimsikia Abi Abdillah (a.s.) akisema: Mtikufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akioga kwa kutumia Sa’700 moja na wakati alipokuwa amefuatana na mmoja wa wake zake, yeye angeoga kwa kutumia Sa’ moja na mudd701 moja (ya maji).702 Kijalizo: Kulayni ameitaja vilevile kutoka kwa Muhammad ibn Muslim, akiongezea: ‘Wote walioga kutoka katika chombo kimoja.’ Kadhalika (imesimuliwa) na Sheikh at-Tusi kwa sanadi nyingine (ya wasimuliaji).703 2. Katika al-Ja’fariyat: Katika riwaya yake kutoka kwa Ja’far ibn Muhammad, kutoka kwa baba yake (amani iwe juu yao wote) ambaye amesema: Hasan ibn Muhammad alimuuliza Jabir ibn Abdillah kuhusu josho la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hivyo Jabir akasema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angejimwagia maji kwenye kichwa chake mara tatu.” Hasan ibn Muhammad akasema: “Nywele katika kichwa changu ni nyingi sana, kama unavyoweza kuona,” ambapo Jabir alimjibu: “Ewe Hur704usiseme hivyo, kwa sababu Mtukufu Mtume alikuwa na nywele nyingi na bora zaidi.705 Kidokezo: Hadithi kama hiyo hiyo imesimuliwa pia kutoka kwa Ja’far, kutoka kwa baba yake (r.a.) kutoka kwa Jabir. 3. Kutoka kwa Ibn Shu’bah ndani ya Tuhf al-Uqul: Kutoka kwa Ali (a.s.): Josho katika siku za Idd ni utakazo kwa wale ambao wangetaka haja zao kutimizwa na (namna ya) kufuata Sunnah.706 699 Kuoga kwa taratibu ya kiibada (Josho) 700 Kipimo cha kizamani – takriban lita 3 (Tr.) 701 Kipimo cha kizamani – takriban mililita 750 (Tr.) 702 Tahdhib al-Ahkam 1:137 703 al-Kafi 22:3, Tahdhib al-Ahkam 1:137 704 Mtu huru kinyume na mtumwa (Tr.) 705 al-Ja’fariyat: 22 706 Tuhf al-Uqul: 101 132


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 133

SUNAN-NABII Kidokezo: Riwaya kama hii inaweza kupatikana ndani ya al-Bihar.707 4. Kutoka kwa al-Saduq ndani ya al-Hidayah: as-Sadiq (a.s.) amesema: Josho (ghusl) la siku ya Ijumaa ni Sunnah ya lazima kwa wanaume na wanawake, wakati wanapokuwa safarini na wanapokuwa nyumbani pia – na yeye (a.s.) amesema: Lile josho la siku ya Ijumaa ni utakaso na ni malipo kwa ajili ya dhambi zinazotendwa Ijumaa hadi Ijumaa. Na sababu ya ghusl ya Ijumaa ilikuwa ni kwa sababu Ansari walikuwa wakifanya kazi ya kuchunga ngamia na ng’ombe wao, na siku za Ijumaa wangekuja msikitini na watu wangebughudhiwa na ile harufu ya miili yao. Hivyo Allah ‘Azza wa Jalla. akamuagiza Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuchukua josho katika siku za Ijumaa na hapo kuifanya kuwa ni Sunnah.708 Kidokezo: Hadithi inayofanana na hiyo inaweza kupatikana ndani ya al-Muqni.709 5. Kutoka kwa Sayyid ibn Tawus katika al-Iqbal: Katika riwaya yake kutoka kwa Ibn Sinan, kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Kuchukua josho katika siku ya al-Fitr ni Sunnah.710 6. Katika kitabu hicho hicho, anasimulia: Kutoka kwenye sehemu ya aghsal 711 za Ahmad ibn Muhammad Ibn Ayyashi al-Jawhari katika riwaya yake kutoka kwa Ali (a.s.): Wakati zile siku kumi za mwisho za mwezi wa Ramadhani zilipoingia, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angejiandaa kuondoka nyumbani kwake kwenda kufanya I’tikaf712 ndani ya Msikiti. Yeye angekesha usiku mzima na angechukua josho kati ya swala za Magharibi na Isha kila usiku.713 Kidokezo: Hadithi sawa kama hii imenukuliwa pamoja na nyororo nyingine mbili za wasimuliaji.714 Aghsal nyingine zitatajwa katika sehemu juu ya swala – kama Mungu akipenda.

707 Bihar al-Anwar 3:81 708 al-Hidayah: 22-23, Ilal al-Sharai’i: 285, at-Tahdhib al-Ahkam 3:9 709 al-Muqni: 45 710 Iqbal al-A’mal: 279, Da’aim al-Islam 1:187 711 Wingi wa ghusl (majosho) 712 Kitendo cha ibada ambamo mtu anakaa ndani ya msikiti kwa muda wa siku 3 – 10 (Tr.) 713 Tuliikuta Hadithi hii ndani ya Da’aim al-Islam 1:286 714 Iqbal al-A’mal:195 133


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 134

SUNAN-NABII

Nyongeza kwenye sehemu hii 1. Katika al-Ja’fariyat: Kwenye riwaya yake kutoka kwa Ali (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Jibril aliniambia nisogeze sogeze pete yangu wakati ninapochukua wudhuu na josho la janaba.”715 2. Vilevile: Kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Jibril aliniambia niweke kidole changu kwenye kitovu changu na kioshe wakati ninapochukua josho la janaba.”716 3. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angechukua josho katika siku zifuatazo: Ijumaa, siku ya A’rafah, siku ya Fitr na siku ya Idd al-Udh’ha.717

715 al-Ja’fariyat: 18 716 ibid 18 717Musnad Ahmad, 4:78; Da’aim al-Islam 1:319 na Sunan ibn Majah 1:418 134


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 135

SUNAN-NABII

MLANGO WA 16 ADABU ZA SWALA 1. Ndani ya al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa al-Fudhail ibn Yasar na Abdul Malik na Bukayr ambao wamesema: Tulimsikia Aba Abdillah (a.s.) akisema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akiswali swala za suna mara mbili zaidi ya kama zile swala za wajib na alikuwa akifunga suna mara mbili zaidi ya funga ya wajib.718 Kidokezo: Hii imesimuliwa pia na Sheikh at-Tusi.719 2. Vilevile: Imesimuliwa kutoka kwa Hannan ambaye amesema: Amr ibn Harith alimuuliza Aba Abdillah (a.s.) nikiwa mimi nimekaa hapo: “Naniwe fidia yako! Hebu niambie kuhusu swala ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)” Yeye (a.s.) akasema: “Mtukufu Mtume alikuwa akiswali rakaa nane wakati wa mchana na rakaa nne katika swala ya kwanza (yaani swala ya Adhuhuri), halafu rakaa nane baada ya hii na rakaa nne katika swala ya Alasiri. Rakaa tatu katika swala ya Magharibi na rakaa nne baada ya Magharibi, na halafu rakaa nne katika swala ya Isha na nane kwa ajili ya swala ya usiku na rakaa tatu za swala ya Witri. Na aliswali rakaa mbili wa mapambazuko na mbili kwa ajili ya swala ya Alfajiri.” Mimi nikasema: “Mimi niwe kafara yako! Ni vipi kama nitakuwa na uwezo wa kuswali zaidi ya hizo – je, Mwenyezi Mungu ataniadhibu mimi kwa kuswali zaidi?” Yeye akajibu: “Hapana, bali atakuadhibu kwa kuitelekeza Sunnah.”720 3. Katika at-Tahdhib: Katika riwaya yake kutoka kwa Husayn ibn Sa’id, kutoka kwa Muhammad ibn Abi Umayr kutoka kwa Hammad ibn Uthman, kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angeswali ile swala ya Utmah721 na halafu angeingia kulala.722 Maelezo: Kuna Hadithi nyingi kama hii lakini tutatosheka na hii moja. Ni dhahiri kutokana na riwaya hii kwamba utmah inachukuliwa kuwa ni tofauti na zile swala hamsini zenye kujumuisha na swala za wajib za kila siku na swala za nawafil. Rakaa 718 al-Kafi 3:344 719 Tahdhib al-Ahkam 2:4, al-Istibsar 1:218 720 Ibid 721 Waarabu walikuwa wakikiita kile kiza cha usiku ‘utmah’ na vile vile walitumia hili kuashiria ile swala inayoswaliwa usiku (Tr.) 722 Tahdhib al-Ahkam 2:5 135


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 136

SUNAN-NABII zake mbili (zinazoswaliwa ukiwa umekaa) zinahesabiwa kama rakaa moja na zimeshauriwa kuwa kama tahadhari mbadala – endapo mtu atafariki katika usingizi wake kabla hajawa na uwezo wa kuswali hiyo witri. Al-Saduq amesimulia katika al-Ilal: Akisimulia kutoka kwa Abi Basir, kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mtu anayemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Hesabu asilale mpaka baada ya kuwa ameiswali swala ya Witri. Mimi nikauliza: “Kwa maana ya zile rakaa mbili zinazoswaliwa baada ya swala ya Isha?” Yeye akajibu: “Ndiyo, nazo zinachukuliwa kuwa kama rakaa moja; na yeyote anayeiswali kisha akafariki, inakuwa kana kwamba amekufa akiwa ameswali swala ya Witri, na kama hatafariki, anapaswa kuswali ile swala ya witri katika sehemu ya mwisho ya usiku.” Mimi nikamuuliza tena: “Je, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliziswali rakaa hizi mbili?” Akasema: “Hapana.” Nikamuuliza: “Je, ni kwa nini hakuziswali?” Akajibu: “Kwa sababu Wahyi ungeshuka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) naye angejua kama angekufa usiku huo au hapana, lakini wengine hawalitambui hili na hii ndio sababu ya kwa nini hakuziswali bali aliwaambia wafuasi wake wafanye hivyo.”723 Maana ya kauli ya muulizaji: ‘Je, yeye aliziswali hizi rakaa mbili?’ ni – je, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliifanya hii kuwa ni Sunnah kwa kuifanya kila wakati? 4. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka Zurarah, kutoka kwa Abi Ja’far (a.s.) ambaye alisema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angeswali rakaa kumi na tatu wakati wa usiku, ambazo zilijumuisha na swala ya witri na rakaa mbili kwa ajili ya sunnah ya swala ya Alfajiri, akiwa yuko safarini au nyumbani.724 5. Katika al-Khisal: Imesimuliwa kutoka kwa Muhammad ibn Isa ibn Ubayd kutoka kwa ar-Ridhaa (a.s.) ambaye amesema: Ndani ya jogoo mweupe kuna sifa tano kutoka kwenye sifa za Mitume (a.s.) mojawapo ikiwa ni kutambua nyakati za swala.725 6. Ndani ya al-Faqih: Katika riwaya yake kutoka kwa Zurarah, kutoka kwa Abi Ja’far (a.s.): Nilimuuliza kuhusu wakati wa swala ya Dhuhri. Yeye akasema: “Ni wakati kivuli kinapokuwa urefu wa dhiraa moja baada ya jua kuwa limevuka nusu ya mzingo wa dunia (meridian), na wakati kwa ajili ya swala ya Alasiri ni wakati kivuli kikiwa na urefu wa dhiraa mbili kuanzia wakati wa swala ya Dhuhri. Hii ni sawa na futi nne baada ya jua kuvuka meridiani.” Halafu yeye 723 al-Ilal al-Shara’i: 331 724 al-Kafi 3:446 725 al-Khisal: 298, ‘Uyun al-Akhbar ar-Ridha 1:277, pia imesimuliwa na al-Kulayni 6:550 136


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 137

SUNAN-NABII akasema: “Ukuta wa msikiti wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ulikuwa takriban sawa na urefu wa mtu na wakati kivuli chake kilipopita dhiraa moja yeye aliswali Dhuhri na zilipokuwa zimepita dhiraa mbili aliswali swala ya Alasiri.” Kisha yeye akauliza: “Je unajua ni kwa nini dhiraa moja na dhiraa mbili zimewekwa kama sharti?” Mimi nikasema: “Kwa nini zimewekwa hivyo? Yeye akasema: “Kwa ajili ya nafasi ya swala ya sunnah (nafilah). Unapaswa kuswali sunnah kuanzia wakati jua linapovuka nusu mzingo mpaka kufikia dhiraa moja, hivyo pale kivuli chako kinapofikia urefu wa dhiraa moja unapaswa kuanza kuswali ile swala ya wajib (Dhuhri) na kuiacha hiyo Sunnah, na wakati kivuli chako kikifikia ridhaa mbili unapaswa kuswali ile swala ya wajib (Alasiri) na kuiacha hiyo Sunnah.726 Kidokezo: Hii imesimuliwa vilevile na at-Tusi na al-Kulayni ndani ya al-Kafi.727 7. Katika al-Tahdhib: Katika riwaya yake kutoka kwa Husayn ibn Sa’id, kutoka kwa Nadhr, kutoka kwa Musa ibn Bakr, kutoka kwa Zurarah ambaye alisema: Nilimsikia Abi Ja’far (a.s.) akisema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) asingeswali wakati wa mchana mpaka jua lilipovuka nusu mzingo; na wakati lilipokuwa limekwisha kupita kwenye hiyo nusu mzingo (meridian) kwa kutupa kivuli urefu wa nusu kidole, angeswali rakaa nane, na pale kivuli kilipofikia urefu wa dhiraa moja, yeye angeswali swala ya Dhuhri. Halafu aliswali rakaa mbili baada ya Dhuhri, na kabla ya wakati wa Alasiri aliswa rakaa nyingine mbili, na pale kivuli kilipofikia urefu wa dhiraa mbili, yeye aliswali swala ya Alasiri. Wakati jua lilipozama, yeye aliswali swala ya Magharibi, na wakati wa Isha uliingia pale utusitusi wa jioni ulipokuwa umepita. Mwisho wa swala ya Magharibi ni wakati wa kuingia usiku. Ndipo wakati wa Isha unapoingia na unaendelea hadi kwenye theluthi moja ya usiku huo. Baada ya swala ya Isha, yeye (s.a.w.w.) asingeswali tena mpaka usiku wa manane. Kisha baada ya usiku wa manane (nusu ya usiku) yeye angeswali rakaa kumi na tatu, ambazo zinajumuisha na Witri na rakaa mbili kwa ajili ya sunnah ya ya Alfajir kabla swala ya Asubuhi haijaingia. Na wakati wa mapambazuko, pale mwanga unapoanza kuonekana, yeye aliswali swala ya Asubuhi.728 Maelezo: Wapokezi wametaja riwaya zingine kuhusu wakati wa ile swala ya usiku. Kadhalika, al-Ayyashi amesimulia hadithi zingine juu ya wakati wa sunnah ya 726 al-Faqih 1:217 727 Tahdhib al-Ahkam 2:20, al-Kafi 3:288, al-Ilal al-Shara’i 2:349 728 Tahdhib al-Ahkam 2:262 - 263

137


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 138

SUNAN-NABII Adhuhuri kama alivyosimulia al-Saduq na wengine.729 Inapasa ieleweke kwamba rakaa zote za sunnah ya Alasiri zilikuwa hazikutajwa katika hadithi hii. Inavyoonekana, yale maelezo ‘….. na kabla ya wakati wa swala ya Alasiri yeye aliswali …..’ ni yenye kujieleza tu juu ya kile kinachoitangulia hiyo. 8. Katika al-Tahdhib: Ndani ya simulizi yake kutoka kwa Muhammad ibn Ali ibn Mahhub, kutoka kwa Abbas ibn Ma’ruf, kutoka kwa kwa Abdillah ibn Mughirah kutoka kwa Mu’awiyah ibn Wahab ambaye alisema: Nilimsikia Abi Abdillah (a.s.) akisema – kama alivyoikumbuka swala ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): Yeye angeyachukua maji yake ya wudhuu, akayafunika na kuyaweka karibu naye, na angeuweka mswaki wake chini ya kitanda chake halafu angelala kwa muda kiasi ambacho Mwenyezi Mungu angependa. Wakati alipoamka, yeye angekaa, akageuza macho yake kuelekea angani na angesoma aya kutoka Suratul-al-Imran: “Hakika katika kuumba mbingu na ardhi na kutofautiana kwa usiku na mchana ni dalili kwa wenye akili.” (3:190), hapo alipiga mswaki meno yake na akachukua wudhuu na baada ya hapo alikwenda kwenye sehemu yake ya kuswalia na akaswali rakaa nne na muda wake wa rukuu ukawa sawa na wa kisomo chake (wakati akiwa amesimama) na muda wake wa sajidah ukawa sawa na ule wa rukuu. Angeinama katika rukuu mpaka ingeulizwa kuwa: “Ni wakati gani atakapoamsha kichwa chake?” Na angekaa kwenye sajidah mpaka ingeulizwa: “Ni lini atanyanyua kichwa chake?” Halafu yeye alirudi kitandani kwake na kulala kwa kiasi Mwenyezi Mungu atakachopenda. Halafu aliamka na kukaa na akasoma ile aya ya Suratal-Imran na akaangalia kuelekea mbinguni. Kisha alipiga mswaki meno yake, akachukua wudhuu na akaenda kwenye sehemu yake ya kuswalia ambako aliswali swala ya witri na rakaa nyingine mbili (yaani sunnah ya al-Fajr) na kisha alitoka nyumbani kwake (kuelekea msikitini) kwa ajili ya swala ya al-Fajr.730 Kidokezo: al-Kulayni amesimulia pia hadithi hii pamoja na nyororo mbili tofauti za wasimuliaji.731 9. Imesimuliwa vilevile kwamba yeye Mtume (s.a.w.w.) angefupisha swala yake ya sunnah na akaja kuifanya baadae mwanzoni mwa mawio, halafu angetoka (nyumbani kwake kuelekea msikitini) kwenda kuswali swala ya al-Fajr.732 10. Kutoka kwa Sheikh at-Tusi ndani ya Mishab al-Mutahajjid: Swala ya Mtukufu Mtume inajumuisha rakaa mbili: Katika kila rakaa inasomwa al-Hamd mara moja na Inna Anzalnahu mara kumi na tano wakati ukiwa umesimama, mara kumi na 729 Tahdhib al-Ahkam 2:118, al-Hidayah: 30 730 Tahdhib al-Ahkam 2:334, Majmaul-Bayan 2:555 731al-Kafi 3:445 732 Hatukupata rejea kwa ajili ya riwaya hii. 138


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 139

SUNAN-NABII tano ndani ya rukuu, mara kumi na tano unaposimama baada ya rukuu, mara kumi na tano, mara kumi na tano wakati unaposujudu, mara kumi na tano wakati unaponyanyua kichwa chako, mara kumi na tano unaposujudu mara ya pili na mara kumi na tano unaponyanyua kichwa chako kwa mara ya pili. Kisha unasimama na kuswali rakaa ya pili kwa namna ileile kama ile ya rakaa ya kwanza na unapokuwa umemaliza kuswali swala hiyo na kufanya vitendo vingine vyovyote vya kiibada unavyotaka vinavyohusiana nayo, hakutakuwa na dhambi yoyote ambayo utakuwa umeifanya bali kwamba Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. atakuwa amekwisha kuisamehe.733 Kijalizo: Sayyid Ibn Tawus naye pia ameisimulia hadithi hii katika Jamal al-Usbu – kutoka kwa Yunus ibn Hashim kutoka kwa ar-Ridhaa (a.s.).734 11. Katika al-Tahdhib: Ndani ya riwaya yake kutoka Ali ibn al-Hatim, kutoka kwa Hamid ibn Ziyad kutoka kwa Abdillah, kutoka kwa Abi Khadijah, kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Wakati Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ulipokuwa umewadia, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alizidisha swala yake na mimi pia nilizidisha (ndani ya Ramadhani) hivyo mnapaswa vilevile kuizidisha.735 12. Vilevile: Katika riwaya yake kutoka kwa Ali ibn al-Hasan ibn Faddhal, kutoka kwa Isma’il ibn Mirhan, kutoka kwa Hasan ibn Muhsin al-Mirwazi, kutoka kwa Yunus ibn Abd al-Rahman, kutoka kwa Muhammad ibn Yahya ambaye alisema: Nilikuwa na Abi Abdillah (a.s.) wakati alipoulizwa: “Je, swala za sunnah zinazidishwa katika mwezi wa Ramadhani?” Yeye akajibu akasema: “Ndiyo, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akitumia kuswali (swala za sunnah) baada ya swala ya Isha na alifanya hivyo kwa wingi sana. Na watu wangekusanyika nyuma yake ili kuswali kama alivyokuwa akiswali yeye, na wakati kundi lilipozidi nyuma yake, yeye aliwaacha na akaingia nyumbani kwake. Baada ya watu kuwa wametawanyika, yeye alirudia kwenye sehemu yake ya kuswalia na akaendelea kuswali kama alivyokuwa akiswali, na wakati lile kundi lilipokusanyika nyuma yake tena, aliliacha na kuingia nyumbani kwake, na alifanya hivi kwa kukariri mara nyingi.736 Kidokezo: Zipo hadithi nyingi kama hii.737 13. Vilevile: Katika riwaya yake kutoka kwa Ali ibn Hatim, kutoka kwa Ahmad ibn 733 Misbah al-Mutahajjid: 255 734 Jamal al-Usbu: 246 735 Tahdhib al-Ahkam 3:60 736 Ibid. 737 al-Kafi 4:155, at-Tahdhib al-Ahkam 3:613 139


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 140

SUNAN-NABII Ali kutoka kwa Muhammad ibn Abi Sahban, kutoka kwa Muhammad ibn Sulayman ambaye amesema: Baadhi ya masahaba wetu walikubaliana juu ya hadithi hii; miongoni mwao walikuwa: Yunus ibn Abd al-Rahman kutoka kwa Abdillah ibn Sinan kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) na Sabbah ibn Hadha’ kutoka kwa Ishaq ibn Ammar kutoka kwa Abul-Hasan (a.s.) na Suma’ah ibn Mihran kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.). (Kisha) Muhammad ibn Sulalyman alisema: Nilimuuliza ar-Ridha (a.s.) kuhusu hadithi hii hivyo alinifahamisha mimi kuihusu hiyo. Hawa (masahaba) wote walisema: Tuliuliza kuhusu swala katika wakati wa mwezi wa Ramadhani – ni vipi ilivyokuwa ikifanyika na ilifanywa vipi na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)? Wote walisema (wakisimulia majibu ya Imam a.s.): Wakati mwezi wa Ramadhani ulipokuwa ukiwadia, kwenye ule usiku wa kwanza Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angeswali swala ya Magharibi na kisha akaswali zile rakaa nne ambazo siku zote alikuwa akiziswali baada ya swala ya Magharibi kila usiku. Halafu aliswali rakaa nane (zaidi) na wakati alipokuwa amekwishaswali Isha, aliswali rakaa mbili ambazo alikuwa kwa kawaida akiswali huku amekaa baada ya swala ya Isha. Kisha alisimama na akaswali rakaa kumi na mbili ambazo baada yake aliingia nyumbani kwake. Wakati watu walipoliona hili na walipogundua kwamba vile mwezi wa Ramadhani ulipowadia Mtukufu Mtume alizidisha swala yake, walimuuliza kuhusu hilo, hivyo alifafanua kuwaelezea watu hao akisema: “Niliswali swala hizi kwa sababu ya ubora wa mwezi wa Ramadhani (na utofauti wake) kutokana na miezi mingine.” Pale yeye (s.a.w.w.) aliposimama kuswali wakati wa usiku, watu walijipanga nyuma yake, hivyo aliwageukia na kusema: “Enyi watu! Hii ni swala ya sunnah, na hakuna jamaa kwa ajili ya swala za sunnah, hivyo kila mmoja anapaswa kuswali peke yake na kusoma kutokana na kile alichofundishwa yeye na Mwenyezi Mungu ndani ya Kitabu Chake, na tambueni kwamba hakuna jamaa katika swala za sunnah.” Hivyo watu wakatawanyika na kila mtu akaswali peke yake. Katika usiku wa mwezi kumi na tisa, yeye Mtume (s.a.w.w.) alichukua josho wakati wa machweo ya jua na akaswali swala ya Magharibi. Baada ya kumaliza kuswali Magharibi na zile rakaa nne ambazo alikuwa akiziswali siku zote baada ya Magharibi aliingia nyumbani kwake. Wakati Bilal alipoadhini kwa ajili ya swala ya Isha, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitoka na akaswali pamoja na watu. Baada ya hapo aliswali rakaa mbili akiwa amekaa chini kamba ambavyo angeswali kila usiku. Halafu alisimama na akaswali rakaa mia moja, akisoma katika kila rakaa ‘Fatihat al-Kitab’ na Qul Huwallahu Ahad mara kumi na alipomaliza hili aliswali ile swala ambayo aliiswali siku zote katika sehemu ya mwisho ya usiku na kisha (akaswali) swala ya witri. Kwenye usiku wa mwezi ishirini wa mwezi wa Ramadhani, yeye Mtume (s.a.w.w.) 140


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 141

SUNAN-NABII alifanya kama alivyokuwa amefanya kila usiku wa siku zilizopita wa mwezi mtukufu, (aliswali) rakaa nane baada ya Magharibi na kumi na mbili baada ya swala ya Isha. Katika usiku wa mwenzi ishirini na moja alichukua josho (ghusl) wakati wa macheo ya jua na akaswali kama alivyofanya kwenye usiku wa mwezi kumi na tisa. Kwenye usiku wa mwezi ishirini na mbili, alizidisha swala zake akiswali rakaa nane baada ya Magharibi na rakaa ishirini na mbili baada ya swala ya Isha. Na kwenye usiku wa mwezi ishirini na tatu alifanya ghusl kama alivyofanya kwenye usiku wa mwezi kumi na tisa na mwezi ishirini na moja na akafanya kama yale aliyofanya katika usiku wa siku hizo mbili. Hao wapokezi wamesema: Na walimuuliza yeye kuhusu zile (rakaa hamsini za swala) – ni nini kinatokea kwenye hizo katika mwezi wa Ramadhani? Yeye alisema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliswali hizi na akaswali hizo rakaa hamsini kama alivyokuwa akiziswali katika miezi mingine na wala asingepunguza chochote kutoka kwenye hizo.738 Maelezo: Tunaona katika riwaya nyingine kwamba katika ile mikesha baada ya ule usiku wa mwezi ishirini na tatu, hadi mwisho wa mwezi huo, yeye angefanya kama vile alivyofanya katika mkesha wa mwezi ishirini na mbili.739 14. Kutoka wa as-Sayyid Ibn Tawus katika al-Iqbal: Akisimulia kutoka kwa Muhammad ibn Fudhayl al-Sayrafi ambaye alisema: Ali ibn Musa ar-Ridha (a.s.) alitusimulia kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake, kutoka kwa baba zake (a.s.) ambao wamesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akitumia kuswali swala ya rakaa mbili katika siku ya kwanza ya mwezi wa Muharram.740 15. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Yazid ibn Khalifah ambaye amesema: Nilimuuliza Abi Abdillah (a.s.): “Umar ibn Handhala alikuja kwetu (na akatusimulia) kutoka kwako kuhusiana na nyakati za swala.” Yeye akasema: “Yeye hatuhusishii uongo kwetu sisi….” Mimi nikasema: “Yeye alisema kwamba wakati wa swala ya Magharibi ni pale wakati jua linapozama na kutoweka (kutoka kwenye upeo), hata hivyo, wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa anasafiri kwa haraka, angeahirisha swala ya Magharibi na akaichanganya na swala ya Isha.” Yeye (a.s.) akasema: “Huyo amesema kweli.”741 16. Katika at-Tahdhib: Katika riwaya yake kutoka kwa Ahmad ibn Muhammad ibn Isa, kutoka kwa Muhammad ibn Yahya, kutoka kwa Talha ibn Zayd kutoka kwa 738 Tahdhib al-Ahkam 3:64-66 739 al-Kafi 4:155 740 Iqbal al-A’mal:553 741 al-Kafi 3:279, al-Tahdhib al-Ahkam 2:31 141


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 142

SUNAN-NABII Ja’far, kutoka kwa baba yake (a.s.): Katika kila usiku wa nyakati za mvua, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angechelewesha swala ya Magharibi na kuharakisha ile ya Isha, akiziswali zote kwa pamoja na akisema: “Mtu ambaye haonyeshi huruma yoyote ile na yeye pia hataonyeshwa huruma.”742 17. Vilevile: Katika riwaya yake kutoka kwa Ali ibn Ibrahim, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abi Umayr, kutoka kwa Hammad, kutoka kwa al-Halabi, kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa safarini au kama jambo la muhimu lilijitokeza, yeye angekusanya swala ya Dhuhr na Alasiri na swala ya Magharibi na Isha.743 Kidokezo: Kuna hadithi nyingi kama hii kutoka kwa Kulayni, Sheikh at-Tusi na mwanawe, na as-Shahid al-Awwal.744 18. Katika al-Faqih: Katika riwaya yake kutoka kwa Mu’awiyah ibn Wahab, kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.): Pale Mwadhini alipokuja kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika siku za joto kali sana (kuomba idhini ya kuita Adhana) kwa ajili ya swala ya Adhuhuri, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angesema: “Abrid! Abrid! (ngojea kupoe japo kidogo).745 Maelezo: al-Saduq anasema: Hii Abrid! Abrid! maana yake ni “Haraka! Haraka!” Na yeye ameichukua kwenye nomino al-Barid. Analitaja hili katika kitabu Madinat al-Ilm.746 Maana ya dhahiri (ya neno hili) ni kuchelewesha jambo mpaka lile joto lililozidi lipungue, kama inavyoweza kuonekana katika kitabu al-‘Ala’ kutoka kwa Muhammad ibn Muslim ambaye amesema: Abu Ja’far (a.s.) aliniona mimi nikiswali katika msikiti wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na wakati nilipokuwa nimemaliza swala hiyo alikutana nami na akasema: “Unapaswa kuswali ile swala ya wajib katika wakati ule (wa baadae), unaswali swala yako katika joto kali (kama hili)?” Mimi nikasema: “Nilikuwa nikiswali ile ya sunnah.”747 19. Kutoka kwa al-Ghazali ndani ya al-Ihya: Wakati wowote mtu alipokuja kuketi kando ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wakati alipokuwa anaswali, yeye angeharakisha swala yake na kumpokea akisema: “Je, unahitaji kitu chochote?” Na baada ya kuwa amekwisha kumtimizia haja yake yeye (s.a.w.w.) angerudia kwenye swala 742 Tahdhib al-Ahkam 2:32 743 Tahdhib al-Ahkam 3:233, al-Ilal al-Sharai’: 321 744 al-Kafi 3:431, Tahdhib al-Ahkam 3:234, Dhikra al-Shi’ah: 118 745 al-Faqih 1:223 746 Muntaha al-Matlub 1:200 – akinukuu kutoka kwenye kitabu Madinat al-Ilm, alMustadrak 3:212, Bihar al-Anwar 44:83. 747 al-Usul al-Sittata ‘Ashar: 154, Taz. al-Mustadrak 6:19 kwa ajili ya riwaya inayohusiana na hii. 142


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 143

SUNAN-NABII yake.748 20. Kutoka kwa Ja’far ibn Ahmad al-Qummi katika kitabu Zuhd al-Nabi: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliposimama kwa ajili ya swala, uso wake ungepauka kwa ajili ya hofu juu ya Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. na sauti ya kilio ingesikika kutoka kwake, sawa na sauti ya mchemko kutoka kwenye chungu cha kupikia.749 21. Vilevile: Katika riwaya nyingine yeye amesema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa akisimama kwa ajili ya swala, angekuwa kama nguo ambayo imeanguka kwenye sakafu (akiwa ametulia kabisa – na mnyenyekevu mbele ya Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla.).750 22. Katika al-Bihar: ‘Aisha amesema: Mtume wa Allah (s.a.w.w.) angeongea na sisi nasi tungeweza kuongea naye, lakini ulipoingia wakati wa swala, ingekuwa kana kwamba alikuwa hatufahamu na sisi pia tulikuwa hatumfahamu yeye.751 23. Katika al-Awali: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliangalia kulia na kushoto ndani ya swala lakini hakugeuza kichwa chake nyuma.752 24. Kutoka kwa Mufid al-Din at-Tusi katika al-Majalis: Katika riwaya yake kutoka kwa Imam Ali (a.s.) katika barua yake kwa Muhammad ibn Abi Bakr wakati alipomteua yeye kama gavana wa Misri: ….. Halafu chunga rukuu na sajidah yako kwani Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa ndiye mkamilifu zaidi kabisa katika swala yake na mwepesi sana katika vitendo vyake753 ndani yake.754 25. Katika al-Tahdhib: Imesimuliwa kutoka kwa Ammar al-Sabati, kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.): Mtukkufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akiswali hata bila ya kuwa ameosha mikono yake baada ya kula nyama lakini alipokuwa amekunywa maziwa, yeye asingeweza kuswali mpaka awe ameosha mikono yake na kusukutua mdomo wake.755 748 Ihya ‘Ulum al-Din 2:365 749 Falah al-Sa’il: 161 – akinukuu kutoka kwenye Zuhd al-Nabi, al-Mustadrak 4:93, Bihar al-Anwar 84:248, Uddat al-Da’i: 151. 750 Falah al-Sa’il: 161, al-Mustadrak 4:93, Bihar al-Anwar 44:248. 751 Bihar al-Anwar 84:258, Uddat al-Da’i: 152, al-Mustadrak 3:100. 752 al-Awali al-La’ali 1:175, al-Mustadrak 4:114 753 Kwa maana kwamba yeye (s.a.w.w.) alikuwa muangalifu sana asije akarefusha swala yake ili wale wazee, wanyonge na kadhalika wawe wanaweza kirahisi kujiunga katika swala ya jamaa. (Tr.) 754 Amali at-Tusi1:29, Amali al-Saduq: 267. 755 Tahdhib al-Ahkam 1:350, al-Istibsar 1:97 143


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 144

SUNAN-NABII 26. Vilevile: Katika riwaya yake kutoka kwa Huseini ibn Sa’id, kutoka kwa alNadhr kutoka kwa Ibn Sinan ambaye alisema: Nilimwambia: “Tunaye Mwadhini ambaye anaadhini (ikiwa bado ni) wakati wa usiku.” Yeye akasema: “Hiyo inaweza kuwa ni yenye manufaa kwa majirani ili kuwaamsha kwa ajili ya swala ya al-Fajr, hata hivyo, iliyo sunnah ni kwamba Adhana ifanyike wakati wa mapambazuko na pengo baina ya adhana na iqamah lisizidi wakati unaochukuliwa kwa kuswali rakaa mbili.756 27. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Abdillah ibn Sinan kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Wakati wa swala ulipoingia, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angemwambia Bilal: “Ewe Bilal! Panda kwenye ukuta na uadhini kwa sauti kubwa.”757 28. Katika al-Faqih: Katika riwaya yake kutoka kwa Zurarah, kutoka kwa Abi Ja’far (a.s.) ambaye amesema: al-Husein (a.s.) alikuwa mtaratibu katika kuongea (wakati alipokuwa mdogo), mpaka ikahofiwa kwamba hataweza kuja kuongea. Wakati mmoja Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikwenda msikitini kwa ajili ya swala akiwa amembeba katikati ya mabega yake na akamfanya asimame upande wa kulia kwake. Watu wakajipanga nyuma ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa ajili ya swala. Vile alipoanza tu swala hiyo (kwa kutamka Takbir), Husein (a.s.) naye pia akatamka takbir. Pale Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) aliposikia hivyo, yeye akairudia tena takbir, hivyo Husein naye akairudia tena hiyo takbir. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alirudia hivi mara saba na Husein (a.s.) akaisoma takbir mara saba na hii ikawa imesimamishwa kama sunnah.758 Maelezo: Hii imesimuliwa katika al-‘Ilal, na Sheikh Tusi na katika at-Tahdhib na ibn Tawus katika Falah al-Sa’il na wengineo.759 Katika baadhi ya riwaya, al-Hasan anatajwa badala ya Husein, hata hivyo iliyo kawaida zaidi ni utajo wa Husein. 29. Katika al-Da’aim: Kutoka kwa Ja’far ibn Muhammad, kutoka kwa baba zake, kutoka kwa Ali (a.s.): Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akinyanyua mikono yake hadi kwenye masikio yake alipokuwa akitamka ‘Takbiratul-Ihram’ (takbir ya kwanza ndani ya swala) na wakati alipotamka takbir kabla ya rukuu na wakati alipotamka takbir pale aliponyanyua kichwa chake kutoka kwenye rukuu.760 756 Tahdhib al-Ahkam 2:53 757 al-Kafi 3:307, Tahdhib al-Ahkam 2:58 758 al-Faqih 1:305 759 al-Ilal al-Sharai’: 332, Tahdhib al-Ahkam 2:67, al-Falah al-Sa’il: 130, al-Manaqib 4:73 760 Da’aim al-Islam 1:162, al-Mustadrak 4:144 144


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 145

SUNAN-NABII 30. Kutoka kwa al-Sayyari ndani ya kitabu chake at-Tanzil wal-Tahrif: Kutoka kwa Muhammad ibn Ali kutoka kwa Muhammad ibn Fudhayl al-Azadi kutoka kwa Abi Ja’far (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akitamka ‘Bismillahi-Rahmanir-Rahim’ kwa sauti kubwa ndani ya swala na angenyanyua sauti yake wakati akiitamka.761 31. Kutoka kwa al-Ayyashi ndani ya Tafsiir yake: Kutoka kwa Mansur ibn Hazim, kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliposwali pamoja na watu, angetamka ‘Bismillahi-Rahmanir-Rahim’ kwa sauti.762 32. Katika al-Ja’fariyat: Katika riwaya yake kutoka kwa Ja’far ibn Muhammad, kutoka kwa baba zake, kutoka kwa Ali (a.s.) ambaye amesema: Kila mara Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipopiga mwayo ndani ya swala huwa angefunika kinywa chake kwa mkono wake wa kulia.763 33. Vilevile: Katika riwaya yake kutoka kwa Ali (a.s.) ambaye amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) wakati mwingine angezigusa ndevu zake ndani ya swala. Hivyo tukamwambia: “Ewe Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu! Mboma tunakuona ukigusa ndevu zako ndani ya swala?” Yeye akasema: “Wakati huzuni yangu inapozidi mimi hufanya hivyo.764 34. Kutoka kwa al-Shahid al-Awwal katika al-Dhikra: Kutoka kwa Abi Sa’id alKhudri kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba alikuwa akisema ‘A’udhu Billahi min al-Shaytani ar-Rajim’ kabla ya kisomo katika swala.765 35. Katika al-Faqih: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa ndiye mkamilifu zaidi katika swala yake kutoka miongoni mwa watu wote. Wakati alipoanza swala yake angesema: Allahu Akbar. Bismillahi-Rahmani-Rahim.766 36. Katika at-Tahdhib: Imesimuliwa kutoka kwa Ishaq ibn Ammar kutoka kwa Ja’far kutoka kwa baba yake (a.s.): Watu wawili kutoka miongoni mwa masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walitofautiana katika swala ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hivyo walimuandikia Ubay ibn Ka’b: Ni mara ngapi Mtukufu Mtume 761 Imesimuliwa ndani ya al-Mustadrak 4:185, Tafsir al-Ayyashi 2:295 – Surat al-Isra’a 762Tafsiir al-Ayyashi 2:295 – Surat al-Isra’a 763 al-Ja’fariyat: 36, al-Mustadrak 5:416, Da’aim al-Islam 1:175 764 al-Ja’fariyat: 39, al-Mustadrak 5:416 765 Dhikra al-Shi’ah:191, Bihar al-Anwar 85:5 766 al-Faqih 1:306 145


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 146

SUNAN-NABII (s.a.w.w.) alipumzika (ndani ya swala yake)? Yeye alijibu akasema: Kulikuwa na sehemu mbili ambazo yeye alikuwa kimya (kitambo kidogo). Sehemu ya kwanza ni wakati alipokuwa amemaliza kusoma ‘Umm al-Kitab’ (Surat al-Hamd) na ya pili ni pale alipomaliza kusoma ile surah nyingine.767 Maelezo: al-Saduq ameisimulia hii kwa kirefu na (ametaja) kwamba kimya chake cha kwanza kilikuwa baada ya takbir na cha pili kilikuwa baada ya kusoma sura zote – kabla ya kurukuu.768 37. Kutoka kwa al-Shahid ndani ya al-Dhikra: Ibn al-Junayd amesema: Samarah na Ubay ibn Ka’b wamesimulia kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba kimya chake cha kwanza kilikuwa ni baada ya takbir ya kwanza na cha pili ni baada ya (kusoma) al-Hamd.769 38. Katika al-Tahdhib: Imesimuliwa kutoka kwa Isa ibn Abdillah al-Qummi, kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Katika swala ya al-Fajr, Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisoma sura kama ‘Amma Yatasa’alun (SuratunNaba), Hal Atakal Hadithul Ghashiyah (Surat al-Ghashiyah), Hal Ata’alal Insan (Surat ad-Dahr) na La Uqsimu bi Yaumil Qiyamah (Suratul-Qiyamah). Katika swala ya Dhuhr alisoma sura kama Sabbihisma (Surat al-A’la), Washamsi wa Dhuhaha (Suratush-Shams) na Hal Ataka Hadithul Ghashiyah (Surat alGhashiyah). Yeye angesoma katika swala ya Magharibi sura kama Qul Huwallahu Ahad (Surat al-Ikhlas), Idha Ja’a Nasrullah (Suratun-Nasr) na Idha Zulzilat. Katika swala ya Isha angesoma kile alichokisoma kwenye swala ya Dhuhr; na katika swala ya Alasiri angesoma kile ambacho angesoma katika swala ya Magharibi.770 39. Vilevile: Imesimuliwa kutoka kwa Ibn Abi Umayr kutoka kwa Abi Mas’ud alTa’i kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.): Katika rakaa ya mwisho ya swala ya usiku, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akitumia kusoma sura Hal Ata’alal Insan (Surat ad-Dahr).771 40. Katika al-Misbah: Imesimuliwa kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akisoma sura tisa katika rakaa tatu (za mwisho) za swala ya usiku. Katika rakaa ya kwanza: Alhakumu al-Takathur (Surat at-Takathur), Inna Anzalna (Suratul767 Tahdhib al-Ahkam 2:297 768 al-Khisal:74 769 Dhikra al-Shi’ah:192, Bihar al-Anwar 84:189 770 Tahdhib al-Ahkam 2:95 771 Ibid 2:124 146


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 147

SUNAN-NABII Qadr) na Idha Zulzilat (Surat al-Zilzal). Katika rakaa ya pili: al-Hamd (SuratulFat’hah), Wal Asr (Surat al-Asr) na Idha Ja’a Nasrullah (Suratun-Nasr). Na katika ile rakaa moja ya swala ya Witr: Qul Ya Ayyuhal Kafirun (Surat al-Kafirun), Tabbar (Surat al-Lahab) na Qul Huwallah Ahad (Surat al-Ikhlas).772 41. Katika al-Khisal: Imesimuliwa kutoka kwa al-Amash kutoka kwa Ja’far ibn Muhammad (a.s.) ambaye amesema: Qunut ni Sunnah inayotakiwa katika kila swala – katika rakaa ya pili kabla ya kurukuu na baada ya kisomo (cha sura zote).773 42. Katika al-‘Awali: al-Barra’ ibn ‘Azib amesimulia ifuatavyo: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) hakuswali swala yoyote ya wajibu kamwe bila kuleta Qunut ndani yake.774 Kidokezo: Hii imesimuliwa pia kutoka kwa al-Hasan (a.s.).775 43. Kutoka kwa Husayn ibn Hamdan al-Hasini katika al-Hidayah, kutoka kwa Isa ibn Mahdi al-Jawhari, kutoka kwa Askar yule mtumwa wa Abu Ja’far, al-Rayyan mtumwa wa ar-Ridhaa (a.s.) na kundi la wapokezi wengine – wanaokisiwa kuwa zaidi ya watu sabini – kutoka kwa al-Askari (a.s.) ambaye, katika hadithi moja ndefu, yeye amesema: Hakika Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. amemfunulia babu yangu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) yafuatayo: “Nimekutofautisha wewe na Ali na hujja Wangu (Maimam kumi na wawili – a.s.) kutoka kwenye kizazi chake hadi Siku ya Kiyama kwa sifa kumi ….. na moja ya sifa hizo ni kusoma Qunut katika kila rakaa ya pili.776 44. Katika al-Ma’ani al-Akhbar: Imesimuliwa kutoka kwa Qasim ibn Salam ambaye amesema: Rukuu ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ilikuwa kwa namna kwamba kama maji yangemwagwa mgongoni mwake basi yangetulia (bila kutiririka).777 45. Katika al-Ilal: Imesimuliwa kutoka kwa Hisham ibn al-Hakam kutoka kwa Abi al-Hasan Musa (a.s.), yeye alisema: Nilimuuliza yeye: “Ni nini sababu ya kusema ‘Subhana Rabbiyal Adhim wa Bihamdihi’ ndani ya rukuu na kusema katika sajidah ‘Subhana Rabbiyal A’la wa Bihamdihi’?” Yeye akasema: “Ewe Hisham! Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipochukuliwa (kwenda mbinguni kwenye Mi’raji) na 772 Misbah al-Mutahajjid: 132 773 al-Khisal: 604, ‘Uyun Akhbar al-Ridha 2:122 774 ‘Awali al-La’ali 2:42, al-Mustadrak 4:396 775 ‘Awali al-La’ali 2:219 (pia kutoka kwa al-Hasan), al-Mustadrak 4:396 776 al-Mustadrak 4:395 777 Ma’ani al-Akhbar: 280, Da’aim al-Islam 1:162 147


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 148

SUNAN-NABII alimswalia Mola Wake na akakumbuka kile alichoshuhudia katika utukufu Wake, mwili wake ulitetemeka (kwa hofu) na aliinama pamoja na mikono yake juu ya magoti yake na akaanza kusema ‘Subhana Rabbiyal Adhim wa Bihamdihi’ na pale aliposimama kutoka kwenye rukuu alimtazama Yeye kutoka kwenye sehemu iliyonyanyuka zaidi (ya kiroho), hivyo akaanguka kwenye kumsujudia Yeye huku akisema‘Subhana Rabbiyal A’la wa Bihamdihi’, na alipokuwa amekwisha kusema hivi mara saba, ile hofu (aliyokuwa nayo) ilitulizwa. Kuanzia hapo na kuendelea hii ikawa imesimamishwa kama ndio sunnah.”778 46. Kutoka kwa al-Thaqafi katika kitabu al-Gharat: Imesimuliwa kutoka kwa Ubayah ambaye alisema: Amirul-Mu’minin Ali (a.s.) alimwandikia Muhammad ibn Abi Bakr: “Chunga rukuu na sajjidah zako kwani Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa ndiye mkamilifu zaidi katika swala yake na pia mnyenyevu zaidi ndani yake. Na wakati alipokwenda rukuu alisema: ‘Subhana Rabbiyal Adhimi wa Bihamdihi’ mara tatu ….. na alipofanya sajjidah alisema ‘Subhana Rabbiyal A’la wa Bihamdihi’779 Kidokezo: Hii imesimuliwa pia katika hadithi nyingine.780 47. Katika al-Ja’fariyat: Katika riwaya yake kutoka kwa Ja’far ibn Muhammad, kutoka kwa baba zake, kutoka kwa Ali (a.s.) ambaye amesema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokwenda sajidah angeshusha magoti yake chini sakafuni kabla ya mikono yake.781 Maelezo: Katika riwaya nyingi kutoka kwa Ahlul-Bayt (a.s.) tunakuta kwamba imependekezwa kuweka mikono chini ardhini kabla ya magoti wakati wa kwenda sajidah.782 Inawezekana kwamba riwaya hiyo hapo juu inaelekeza kwenye kuleta magoti karibu na ardhi bila kuyaweka kabisa juu yake. 48. Vilevile: Katika simulizi kutoka kwa al-Husein kutoka kwa Ali (a.s.) ambaye amesema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipofanya sajidah, angesujudu na viganja vyake vikiwa juu ya ardhi na angepanua mikono yake mpaka ingewezekana kwa yule mtu aliyekuwa nyuma yake kuona makwapa yake.783 778al-Ilal al-Sharai’ 2:332 779 al-Ghayat 1;246 780 al-Faqih 1:300 781 al-Ja’fariyat: 246 782 al-Mustadrak 4:445 783 al-Ja’fariyat: 41 148


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:11 PM

Page 149

SUNAN-NABII 49. Kutoka kwa Sayyid Radhi katika al-Majazat al-Nabawiyyah: Ilikuwa imesimuliwa kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angefanya sajidah juu ya Khumra, ambayo ni kipande cha mkeka kilichotengenezwa kwa matawi ya mtende.784 50. Katika al-Ja’fariyat: Muhammad alitufahamisha hivi: Musa aliniambia kwamba baba yangu alituambia kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake, Ja’far ibn Muhammad, kutoka kwa baba yake (a.s.) ambaye alisema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akimwagia maji kwenye sehemu ambayo alisujudia juu yake.785 51. Katika al-Faqih: Ndani ya riwaya yake kutoka kwa Isma’il ibn Muslim, kutoka kwa al-Sadiq kutoka kwa baba yake (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na fimbo fupi, ambayo ilikuwa na kichungi cha chuma mwishoni kwake, ambayo angeweza kuiegemea juu yake. Angekuja nayo kwenye zile siku mbili za Idd na angeswali karibu nayo.786 52. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Mu’awiyah ibn Wahab kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angeiweka ile fimbo fupi mbele yake wakati alipokuwa anaswali.787 53. Katika al-Ja’fariyat: Katika riwaya yake kutoka kwa Ja’far ibn Muhammad, kutoka kwa baba zake, kutoka kwa Ali (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angesoma takbira katika swala za zile Idd mbili na katika Istisqa’ (swala ya mvua) – katika rakaa ya kwanza mara saba (mara moja kwa ajili ya TakbiratulIhram, mara tano kwa ajili ya zile Qunut tano na mara moja kabla ya kurukuu), na katika rakaa ya pili mara tano (mara nne kwa ajili ya Qunut nne na mara moja kabla ya kurukuu).788 Kidokezo: Hii imesimuliwa ndani ya al-Manaqib pamoja na maelezo marefu.789 54. Vilevile: Katika riwaya yake kutoka kwa Ali (a.s.): Katika swala za Idd mbili Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akisoma Sabbihisma Rabbikal ‘A’la (Surat al‘A’la) na Hal Ataka Hadith al-Ghashiyah (Surat al-Ghashiyah).790 784 al-Majazat al-Nabawiyyah: 255 (na katika hii ni Humrah badala ya Khumrah), alMustadrak 4:10 785 al-Ja’fariyat: 17, al-Mustadrak 1:356 786 al-Faqih 1:509, al-Ja’fariyat: 184 787 al-Kafi 3:296, Tahdhib al-Ahkam 2:322, al-Mustadrak 3:335 788 al-Ja’fariyat: 45 789 al-Manaqib 4:15 790 al-Ja’fariyat: 40 149


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 150

SUNAN-NABII 55. Katika al-Faqih: Katika riwaya yake kutoka kwa Abi Ja’far (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akiswali rakaa mbili wakati alipokuwa salat al-Istisqa’ na angemuomba Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. anyesheshe mvua na angeomba Du’a akiwa ameketi chini. Yeye (a.s.) vilevile alisema: Yeye Mtume (s.a.w.w.) alianza na swala kabla ya hotuba na alizisoma hizo surah kwa sauti kubwa.791 56. Kutoka wa al-Saduq katika al-Hidayat: Abu Ja’far (a.s.) amesema: Ni katika Sunnah kwa watu wanaokaa mijini kutoka nje ya miji yao kwenda kwenye uwanja wa wazi kwa ajili ya swala ya zile Idd mbili – isipokuwa kwa watu wa Makka, kwani wao wanaswali swala za Idd ndani ya Masjid al-Haram.792 Kidokezo: Kuna hadithi nyingi mno zinazofanana na hii.793 57. Katika al-Ja’fariyat: Katika riwaya yake kutoka kwa Ja’far ibn Muhammad kutoka kwa baba zake (a.s.) ambao wamesema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipotoka nyumbani kwake kwenda kwenye mahali pa swala, angekwenda kwa kutumia njia ya al-Shajarah na katika njia yake ya kurudia angepitia al-Mu’arrish. Yeye alikusudia kuondoka kwa kutumia ile njia ya mbali kati ya njia hizo mbili na akakusudia kurudi kwa kutumia ile ya karibu zaidi kati ya hizo mbili.794 58. Kutoka kwa al-Saduq ndani ya al-Hidayah: Amirul-Mu’minin Ali (a.s.) amesema: Iliyo Sunnah ni kwamba swala ya Istisqa’ inapaswa kufanyika katika mawanda ya wazi ambako watu wanaweza kuiona mbingu. Hiyo swala ya Istisqa’ haiswaliwi ndani ya misikiti – isipokuwa msikiti wa Makka. 795 59. Kutoka kwa Sheikh Warram ibn Abi Firas katika Tanbih al-Khawatir: Kutoka kwa Nu’man ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akitupanga sisi katika namna ambayo kwamba tuwe tumesimama katika mistari iliyonyooka – kunyooka kama mishale – na angetoa umuhimu mkubwa zaidi katika hili hususan wakati alipoona kwamba sisi tumelipurukusha hilo. Siku moja alikuja na akasimama (kwa ajili ya swala) na alipokuwa akitaka kusoma takbira, alimuona mtu mmoja ambaye kifua chake kilikuwa mbele ya wengine hivyo akasema: “Enyi waja wa Mwenyezi Mungu! Nyoosheni safu zenu vinginevyo mtapingana wenyewe kwa wenyewe.”796 791 al-Faqih 1:535, Qurb al-Isnad: 54, al-Ja’fariyat: 45 792 al-Hidayah: 53 793 al-Kafi 3:461, al-Faqih 1:508, Tahdhib al-Ahkam 3:138, al-Mustadrak 6:135 794 Awali al-La’ali 2:221, al-Mustadrak 6:149, al-Ja’fariyat: 47 795 al-Hidayah: 37, Tahdhib al-Ahkam 3:150, Qurb al-Isnad: 64, Bihar al-Anwar 91:321 796 Majmu’at al-Warram: 267 150


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 151

SUNAN-NABII 60. Vilevile: Kutoka kwa Ibn Mas’ud ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angeweka mkono wake juu ya mabega yetu kabla ya swala na kusema: “Simameni katika mistari iliyonyooka na msihitilafiane kwani (kama mtafanya hivyo) nyoyo zenu zitapingana.798

Nyongeza kwenye sehemu hii 61. Katika Astar al-Salah cha as-Shahid al-Thani: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akisubiria wakati wa swala na angekuwa anaionea shauku kubwa sana. Yeye angekuwa mwenye kuzingatia juu ya kuingia kwa wakati wa swala na angemwambia Bilal, muadhini wake: “Tufurahishe Ewe Bilal! (kwa kutangaza kwamba ni wakati wa swala).799 62. Katika Majmu’at Warram: Kutoka kwa Amir al-Mu’minina (a.s.) ambaye amesema: Sio kula chakula cha jioni wala kitu kingine chochote ambacho kamwe kilimuondoa mawazo Mtukufu Mtume (kutoka kwenye swala) na pale wakati wa swala ulipoingia, ilikuwa ni kana kwamba alikuwa hamjui mtu yoyote wa familia yake wala rafiki wa karibu kabisa.800 63. Katika al-Ilal: Kutoka kwa Layth, kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Hakuna kilichomtoa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwenye swala ya Magharibi wakati jua lilipokuwa limezama, (na asingeshughulika na jingine lolote) mpaka alipokuwa amekwisha kuswali swala hiyo.801 64. Katika al-Makarim: Yeye (s.a.w.w.) alikuwa akisema: Kutulia kwa macho yangu kuliwekwa katika swala na saumu.802 65. Katika Amali ya Sheikh at-Tusi: Kutoka kwa Abi Harb ibn Abi Al-Aswad alDuwali, kutoka kwa baba yake Abi al-Aswad, kutoka kwa Abu Dharr katika hadithi ndefu kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye amesema: “Ewe Abu Dharr! Allah ‘Azza wa Jalla. aliweka utulivu wa macho yangu katika swala na ameifanya ipendeke kwangu kama chakula kinavyopendwa na wenye njaa na maji yanavyopendwa na wenye kiu, na wakati mwenye njaa atakapokula chakula hushiba, na mwenye kiu akinywa maji hukata kiu yake lakini mimi kamwe sitosheki na swala (na wakati wote ninakuwa na tamaa ya ziada).”803 798 Majmu’at al-Warram: 266, Usul al-Sittata ‘Ashar: 66 na 152 799 Astar al-Salah: 120 800 Majmu’at Warram: 323, ‘Uddat al-Da’i: 139 801 Ilal al-Sharai’: 350 802 Makarim al-Akhlaq: 34 803 Amali at-Tusi 2:141 151


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 152

SUNAN-NABII Kidokezo: Hii imesimuliwa pia na at-Tabarsi katika al-Makarim na Sheikh Warram katika al-Majmu’ah yake.804 66. Katika Jami’ al-Akhbar: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa kwenye swala, ile hali ya moyo wake ilikuwa kama ni chungu kinachochemka – kutokana na hofu ya Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla.805 Kidokezo: Hii imesimuliwa pia katika vitabu vinginevyo.806 67. Katika al-Bihar: Kutoka katika Bayan al-Tanzil cha Ibn Shahr Ashub: Inasemekana kwamba wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa anaswali, angenyanyua macho yake (akiangalia) mbinguni lakini aya hii: “….. ambao ni wanyenyekevu katika swala zao…..” (23:2) iliposhuka, aliinamisha kichwa chake na akalenga kule kutazama kwake juu ya ardhi.807 68. Katika al-Faqih: Ni Sunnah kusoma ile tawjjuh808 katika swala sita – nazo ni: ile rakaa ya kwanza ya swala ya usiku, ile swala ya witri, ya kwanza kati ya zile rakaa mbili swala ya mchana (sunnah ya Dhuhr), rakaa ya kwanza ya zile rakaa mbili za swala ya Ihram, rakaa ya kwanza ya sunnah ya Magharibi na rakaa ya kwanza ya swala (zote) za wajib.809 Kidokezo: Ameisimulia pia katika al-Khisal, al-Hidayah na al-Muqni’.810 69. Katika al-Ihtijaj: Kutoka kwa Muhammad ibn Abdillah ibn al-Humayri – katika hadithi juu ya majibu ya kwenye maswali kutoka kwa mtu ambaye amehifadhiwa ki-ungu: …..Hivyo yeye (a.s.) akamjibu: Tawajjuh (mwelekeo) moja kwa moja sio wajib, na ile sunnah ambayo imekokotezwa sana ambayo imekubaliwa ni (kwa mtu kusoma): “Wajjahatu wajihiya lilladhi Fatwaras-Samaawati wal ardhi haniyfan musliman wa maa anaa minal-mushrikiina. Inna swalatiy wa nusukiy wa mahyaaya wa mamaatiy lillahi Rabbil-‘Alamiin laa sharika-lahu, wabidhaalika umirtu wa anaa minal muslimiina. Allahummaj’alniy 804Makarim al-Akhlaq: 461, Majmu’at Warram: 303 805 Jami’ al-Akhbar: 96 806 Bihar al-Anwar 84:248, Falah al-Sa’il: 161 807 Bihar al-Anwar 84:256 808 Ni kile kisomo: ‘Wajjahtu Wajhiya Lilladhi Fatwaras-Samaawati wal-Ardhi…..’ (Tr.) 809 al-Faqih 1:484 810 al-Khisal: 333, al-Hidayah: 38 152


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 153

SUNAN-NABII minal Muslimiina. A’udhu billahi samiy’i al-‘Aliim mina shaytaanirRajiim. Bismillahi ar-Rahmanir-Rahiim.” “Nimejielekeza mzima mzima kwa Yule ambaye ameumba mbingu na ardhi na mimi si miongoni mwa washirikina. Hakika swala yangu na kafara yangu na maisha yangu na umauti wangu ni kwa ajili ya Allah, Mola wa ulimwengu wote – Yeye hana mshirika, na hili ndilo nililoamriwa nami ni miongoni mwa wale wanaonyenyekea. Ewe Allah! Niweke miongoni mwa wale wanaonyenyekea. Naomba hifadhi kwa Mola Wangu dhidi ya Shetani aliyelaaniwa. Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu ….. na kisha soma Suratul-Hamd. 70. Katika al-Khisal: Kutoka wa Abi al-Hasan ibn Rashid ambaye amesema: Nilimuuliza ar-Ridha (a.s.) kuhusu zile takbira za ufunguzi. Yeye (a.s.) akasema: “Zenyewe ziko saba.” Mimi nikasema: “Imesimuliwa kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akisoma takbira moja.” Yeye akasema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisoma takbira moja kwa sauti kubwa na sita kwa sauti ya polepole.”811 Kidokezo: al-Saduq ameisimulia hii katika al-Uyun.812 71. Katika al-Falah al-Sa’il: Kutoka kwa Kurdin ibn Masma’ katika kitabu chake mashuhuri, ndani ya hadithi yake kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): ….. Halafu angetamka takbira tatu (baada ya kumaliza swala), akinyanyua mikono yake hadi kwenye masikio yake, na hii ni Sunnah iliyokokotezwa sana ambayo imeagizwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wakati alipopokea bishara njema.813 72. Katika al-Amal ya Sheikh at-Tusi: Kutoka kwa Zurayq ambaye amesema: Nilimsikia Abi Abdillah (a.s.) akisema: Ni katika Sunnah kubakia umekaa wakati baina ya Adhana na Iqamah katika swala ya al-Fajr na Magharibi na Isha – hakuna swala ya sunnah baina ya adhana na iqamah katika swala hizi. Na ni sunnah kuswali rakaa mbili za sunnah baina ya adhana na iqamah ya swala za Adhuhuri na Alasiri.814 73. Katika al-Makarim: Kutoka kwa Zurarah, kutoka kwa Abi Ja’far (a.s.) katika hadithi: Imeagizwa kama sunnah kwamba wanawake wasinyanyue vichwa vyao kutoka kwenye rukuu na kwenye sajidah mpaka pale wanaume watakapokuwa wamenyanyua wao vichwa vyao.815 811 al-Khisal: 347 812 Uyun al-Akhbar ar-Ridha 1:217 813 Falah al-Sa’il: 135 814 Amali at-Tusi 2:306 815 Makarim al-Akhlaq: 95, Qurb al-Isnad: 10, Ilal al-Sharai’: 344 153


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 154

SUNAN-NABII 74. Katika al-Ma’ani al-Akhbar: Kutoka kwa Qasim ibn Salam katika hadithi (kutoka kwa Ma’sum mmojawapo): “Wakati yeye (s.a.w.w.) alipokwenda rukuu hakushusha kichwa chake moja kwa moja wala kukinyanyua mpaka kikawa kiko juu zaidi ya mwili wake, bali alikiweka katika nafasi moja baina ya viwili hivi. 816 75. Katika al-‘Ilal: Kutoka kwa Abdillah ibn Maimun kutoka wa Ja’far ibn Muhammad kutoka kwa baba yake ambaye amesema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliposikia sauti ya mtoto mchanga anayelia wakati yeye akiwa katika swala, basi angeiharakisha swala yake hiyo ili kwamba mama yake kichanga hicho aweze kumshughulikia mwanawe.817 76. Katika al-Kafi: Kutoka kwa Abi Basir, kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Urefu wa tandiko (la kipando) la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ulikuwa ni dhiraa moja na aliposwali (akiwa safarini) angeliweka mbele yake ili liweze kuwa kama kizuizi kwa mtu yoyote aliyepita mbele yake.818 77. Vilevile: Kutoka kwa Aban ibn Taghlub ambaye amesema: Nilimuuliza Abi Abdillah (a.s.): “Ni wakati gani hasa ambapo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliswali ile swala ya Witri?” Yeye akasema: “Kama ule wakati baina ya kuzama jua na swala ya Magharibi (yaani muda mfupi sana kabla ya swala ya al-Fajr).”819 78. Katika al-Faqih: Kutoka kwa al-Halabi, kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Iliagizwa kama sunnah kwamba mtu katika ile siku ya Idd al-Fitr ale kabla ya kwenda kuswali Idd hiyo na asile kitu katika siku ya Idd ul-Udh’ha mpaka baada ya swala ya Idd.820 79. Katika al-Kafi: Kutoka kwa Fudhayl ibn Yasar kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mkeka mdogo (kwa ajili ya kusujudia) uliletwa kwa ajili ya baba yangu katika siku ya Idd al-Fitr lakini akaomba uondolewe pale, halafu akasema: “Katika siku hii Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akitumia kuangalia kwenye upeo wa macho na kuweka paji lake la uso juu ya ardhi.”821 Kidokezo: Hii imesimuliwa ndani ya al-Da’aim na kwenye al-Faqih, na ndani yake ile siku ya Udh’ha pia imetajwa baada ya siku ya Fitr.822 816 Ma’ani al-Akhbar: 280 817 Ilal al-Sharai’: 344 818al-Kafi 3:296, Tahdhib al-Ahkam 2:322 819 al-Kafi 3:448 820 al-Faqih 1:508, al-Hidayah:53 821 al-Kafi 3:461 822 Da’aim al-Islam 1:185, al-Faqih 1:508 154


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 155

SUNAN-NABII 80. Vilevile: Kutoka kwa Layth al-Muradi kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.): Ilisemwa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika siku ya Fitr au siku ya Udh’ha: “Laiti ungeswali (hiyo Idd) ndani ya msikiti wako!” Yeye akajibu: “Mimi napendelea kuja kwenye mazingira haya anga la wazi.823 81. Katika al-Muqni’ah: Imesimuliwa kwamba katika zile Idd mbili, Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuwa akivaa Burda (aina ya nguo ya mistari) na kilemba – iwe ni wakati wa kipupwe ama kiangazi.824 82. Katika an-Nihayah ya Allamah: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angetoka siku ya Idd huku akisoma takbira kwa sauti kubwa.825 83. Katika al-Kafi: Kutoka kwa Muhammad al-Fadhl al-Hashimi kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Kuna swala ya rakaa mbili ambayo ni sunnah ya kufanya ndani ya Madina tu na sio mahali pengine popote, na ni ya kufanywa ndani ya msikiti wa Mtukufu Mtume katika zile siku za Idd mbili kabla ya kwenda kwenye swala yenyewe ya Idd. Sunnah hii haifanywi mahali pengine popote isipokuwa Madina tu kwa sababu hivi ndivyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alivyoifanya.826 84. Katika al-Uyun: Kutoka kwa Yasir al-Khadim na kutoka kwa Rayyan ibn Salt na wengineo kutoka kwa wale walioisimulia kutoka kwa Abul-Hasan ar-Ridha (a.s.) katika hadithi: Wakati siku ya Idd ilipowadia, Ma’mun alimtumia ar-Ridha (a.s.) mtu akimuomba aende kwenye swala ya Idd na akatoe hotuba ….. na pale Ma’mun aliposisitiza, yeye (a.s.) alisema: “Oh Amir al-Mu’minin,827 endapo utanisamehe katika hili basi itakuwa ni furaha sana kwangu mimi, bali kama hutanisamehe, basi nitatoka kwa ajili ya swala ya Idd kama Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alivyokuwa akitoka, na kama Amirul-Mu’minin Ali ibn Abi Talib (a.s.) alivyotoka … hivyo wakati jua lilipochomoza, Imam ar-Ridha alichukua ghusl na akavaa kilemba cheupe kilichotengenezwa kwa pamba, akiweka ncha yake moja juu ya kifua chake na ncha nyingine kati ya mabega yake na akawaambia watumwa wake wote: “Fanyeni kama mimi nilivyofanya.” Kisha alichukua fimbo fupi mkononi mwake na akatoka nje na tulikuwa pamoja naye. Yeye (a.s.) alikuwa miguu mitupu bila viatu, akiwa amekunja suruali yake 823 al-Kafi 3:460 824 al-Muqni’ah: 202, Tahdhib al-Ahkam 3:130 825 Nihayat al-Ahkam 2:66 826 al-Kafi 1:461, Tahdhib al-Ahkam 3:137, al-Faqih 1:509 827 Cheo hiki kimehifadhiwa kihalali kwa ajili ya Imam Ali (a.s.) lakini Imam ar-Ridha (a.s.) alilazimika kutumia cheo hicho kwa Ma’mun kama namna ya kughilibu. 155


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 156

SUNAN-NABII hadi nusu ya muundi wake. Aliposimama na sisi tukatembea mbele yake, yeye alinyanyua kichwa chake kuelekea juu mbinguni na akasoma takbira mara nne – na alipofika mlangoni alisimama kidogo na akasema: “Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, ‘Alaa maa hadaanaa, Allahu Akbar, ‘Alaa maa razaqanaa min bahiimati al-an’aami, walhamdu lillahi ‘Alaa maa ablaanaa.” “Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, kwa kile ambacho ametuongoza kwacho, Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, kwa rizki aliotujaalia miongoni mwa wanyama, na sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu kwa kile alichokikusudia kwa ajili yetu sisi.” Alisoma hivi kwa sauti na sisi pia tuliitikia kwa sauti – na yeye alisema hivi mara tatu ….. na Abu al-Hasan (a.s.) angetembea na kusimama kidogo baada ya kila hatua kumi, akiisoma takbira mara nne.828 85. Katika al-Faqih: Ndani ya riwaya ya al-Sakuni: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokwenda kwenye swala ya Idd, yeye hakurejea kwa kufuata njia ileile ambayo alikuwa amechukua wakati alipoanza, bali angechukua njia nyingine.829 Kidokezo: Hii imesimuliwa vilevile ndani ya al-Da’aim.830 86. Katika at-Tahdhib: Katika riwaya yake kutoka kwa Isa ibn Abdillah, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake, kutoka kwa Ali (a.s.) ambaye alisema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kamwe hakuwa akisoma zaidi ya takbira moja ndani ya swala za Idd mbili mpaka pale Husein (a.s.) alipokuwa amechelewa kuongea (alipokuwa mtoto mchanga). Siku moja, mama yake (a.s.) alimvalisha na akampeleka kwa babu yake na wakati yeye (s.a.w.w.) alipotamka takbir, na al-Husein (a.s.) pia akatamka takbir, alifuatisha baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na alifanya hivi mara saba. Kisha katika rakaa ya pili, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliitamka takbir na al-Husein akafuatisha baada yake mara tano. Kuanzia hapo na kuendelea, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliifanya kuwa ni Sunnah na sunnah hii inaendelea kutumika hadi leo hii.831

828 ‘Uyun al-Akhbar ar-Ridha 2:149 829 al-Faqih 1:510 830Da’aim al-Islam 1:186 831 Tahdhib al-Ahkam 3:286 156


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 157

SUNAN-NABII Kidokezo: Hii imesimuliwa pia katika al-Manaqib.832 87. Katika Nawadir al-Rawandi: Katika riwaya yake kutoka kwa Musa ibn Ja’far kutoka kwa baba zake, kutoka kwa Imam Ali (a.s.) ambaye amesema: Ilikuwa ni sunnah katika swala ya Istisqa kwamba Imam lazima asimame na kuswali rakaa mbili na kisha anyooshe mikono yake na amuombe Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. (Dua kwa ajili ya mvua).833 88. Katika al-Ilal: Katika riwaya yake kutoka kwa Abi Hamzah Anas ibn ‘Ayyad alLaythi kutoka kwa Ja’far ibn Muhammad, kutoka kwa baba yake (a.s.): Wakati Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alipokuwa akiomba kwa ajili ya mvua, aliangalia juu mbinguni na akageuza shuka yake kutoka kulia kwenda kushoto na kutoka kushoto kwenda kulia (nje-ndani). Yeye akasema: Mimi nilimuuliza: Ni nini maana ya (kufanya) hilo? Yeye (a.s.) akasema: Ilikuwa ni ishara kati yake yeye na masahaba zake ya kugeuza ukame kuwa neema (ya chakula tele).834 Kidokezo: Hii imesimuliwa pia katika al-Kafi, al-Tahdhib, al-Faqih na Da’aim.835 89. Katika al-Faqih: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipoomba dua kwa ajili ya mvua, angesoma: “Allahuma asqi ‘ibaadaka wa bahaa’imaka, wa anshur rahmataka, wa ahyii bilaadakal mayitata.” “Ewe Mola Wangu! Wanyweshe waja Wako na wanyama Wako, na eneza rehma Zako, na ihuishe ardhi yako iliyokufa.” Na angeyarudia haya mara tatu.836 90. Katika al-Ja’fariyat: Kutoka kwa Ali ibn Abi Talib (a.s.) ambaye amesema: Ile mvua ambayo kwayo huja riziki ya wanyama inatoka chini ya ‘Arsh.’837 Ni kwa sababu hii ambapo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angetoka nje pale mara ya kwanza mvua inapanza kunyesha na angesimama hapo mpaka kichwa na ndevu zake viwe vimetota na kudondoka maji.838

832 al-Manaqib 4:13 833 Nawadir al-Rawandi: 29, Bihar al-Anwar 91:315, al-Ja’fariyat: 49. 834 Ilal al-Sharai’: 246 835 al-Kafi 3:463, Tahdhib al-Ahkam 3:149-150, al-Faqih 1:535, Da’aim al-Islam 1:203 836 al-Faqih 1:527 837 Kiti Kitukufu cha Enzi cha Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. (Tr.) 838 al-Ja’fariyat: 241, al-Mustadrak 6:191 157


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 158

SUNAN-NABII Kidokezo: Hii imesimuliwa na al-Rawandi katika Nawadir pamoja na tofauti kidogo.839 91. Vilevile katika al-Ja’fariyat: Kutoka kwa Ali (a.s.): Wakati Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alipoiona mvua alisema: “Ewe Mola Wangu! Ifanye iwe mvua yenye manufaa.”840 92. Katika at-Tahdhib: Katika riwaya yake kutoka kwa Abdillah ibn Maimun kutoka kwa Ja’far kutoka kwa baba yake (a.s.) ambaye amesema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipotoka kwenda kwenye swala ya Ijumaa, alikaa juu ya mimbari hadi mwadhini alipomaliza kuadhini.841 93. Katika at-Tahdhib: Kutoka kwa Amr ibn Jami’ akisimulia kutoka kwa Ali (a.s.) ambaye amesema: Ni kutoka kwenye Sunnah kwamba wakati Imam anapopanda juu ya mimbari, anapaswa kuwasalimia watu (kwa kusema ‘salaamun ‘alaykum’) wakati anapowageukia kuwaangalia.842 94. Katika al-Ja’fariyat: Katika riwaya yake kutoka kwa Ja’far ibn Muhammad kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake (a.s.) kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akitoa hotuba mbili akizitenganisha kwa kuketi chini kidogo na kisha akasimama.843 95. Vilevile: Katika riwaya yake kutoka kwa Ja’far ibn Muhammad, kutoka kwa baba yake (a.s.) ambaye alisema: Fanyeni usomaji wenu wa zile surah wenye kusikika katika swala za Ijumaa kwani hii ndio sunnah.844 96. Vilevile: Katika riwaya yake kutoka kwa Ja’far ibn Muhammad, kutoka kwa baba yake (a.s.) ambaye alisema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitumia kuswali swala ya Ijumaa wakati jua lilipovuka sehemu ya kati ya mbingu.845 97. Vilevile: Katika riwaya yake kutoka kwa Ali ibn al-Husein (a.s.) ambaye amesema: Kuleta Qunut (dua) ndani ya swala ya Ijumaa ni kutoka katika sunnah.846 839 Nawadir al-Rawandi: 41 840al-Ja’fariyat: 217 841 al-Tahdhib al-Ahkam 3:244 842 Ibid. 843 al-Ja’fariyat: 43 844 Ibid. 845 al-Ja’fariyat: 44 846 Ibid. 43 158


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 159

SUNAN-NABII 98. Katika al-Da’aim: Kutoka kwa Ja’far ibn Muhammad (a.s.): Iliyo sunnah ni kwa Imam kusoma, katika rakaa ya kwanza ya swala ya Ijumaa, Surat al-Jumu’ah na katika rakaa ya pili asome Surat al-Munafiqun.847 99. Katika al-Tahdhib: Katika riwaya yake kutoka kwa al-Sakuni kutoka kwa Ja’far, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa baba zake, kutoka kwa Ali (a.s.): Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipoingia msikitini, Bilal alikuwa anakimu swala, yeye alikaa chini (na hakufanya swala yoyote ya sunnah).848 100. ash-Shahid al-Thani katika al-Dhikra: Kutoka kwa Sahl al-Sa’idi ambaye alisema: Baina ya sehemu ya swala ya Mtukufu Mtume na ukuta, palikuwa na njia kwa ajili ya kondoo.849 101. Katika at-Tahdhib: Katika riwaya yake kutoka kwa Hisham ibn Salim ambaye alimuuliza Aba Abdillah (a.s.) kuhusu ile tasbihi (inayosomwa kwenye swala), hivyo yeye akasema: Unasema, ‘Subhana Rabbiyal Adhim’ ndani ya rukuu na katika Sajidah unasema, ‘Subhana Rabbiyal ‘A’la,’ halafu akasema: Usomaji wa wajib wa tasbihi hii ni mara moja na iliyo sunnah ni kusoma mara tatu na ubora (mustahab) ni kusoma mara saba.850 102. Vilevile: Katika riwaya yake kutoka kwa Muhammad ibn Abi Hamzah kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akisoma aya kumi na tano za Qur’ani tukufu katika kila rakaa, na rukuu yake ilikuwa ya muda huohuo kama kisimamo (Qiyam) chake, na sajidah yake ilikuwa kwa muda ule ule kama rukuu yake; na muda baada ya kunyanyua kichwa chake kutoka kwenye rukuu na baada ya kukinyanyua kutoka kwenye sajidah ulikuwa unalingana.851 Kidokezo: Imesimuliwa kwa tofauti ndani ya al-Kafi.852 103. Vilevile: Katika riwaya yake kutoka kwa Zurarah kutoka kwa Abi Ja’far (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akiswali rakaa mbili za Subh – yaani ile swala ya al-Fajr – wakati yalipoingia mawio na mwanga wa mchana ukianza kuonekana.853 847 Da’aim al-Ahkam 2:281 848 Tahdhib al-Ahkam 2:281 849 Dhikra al-Shi’ah: 153, al-Mustadrak 3:336 850 Tahdhib al-Ahkam 2:81 851Ibid, 2:123 852 al-Kafi 3:329 853 Tahdhib al-Ahkam 2:36 159


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 160

SUNAN-NABII Kidokezo: Hii imesimuliwa vilevile katika al-Gharat ya al-Thaqafi.854 104. Vilevile: Katika riwaya yake kutoka kwa Ishaq ibn al-Fadhl ambaye amesema kwamba yeye alimuuliza Aba Abdillah (a.s.) kuhusu utekelezaji wa Sajidah juu ya mikeka na matete yaliyosukwa. Yeye (a.s.) akasema: “Hapo hakuna matatizo, bali ningependelea kwamba mtu asujudu juu ya ardhi, kwani Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipenda sana kuweka paji la uso wake juu ya ardhi – hivyo mimi ninakutakieni (kufanya) yale ambayo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipendelea kuyafanya.855 105. Vilevile: Katika riwaya yake kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) – kuhusu swala za sunnah – yeye akasema: Sunnah kuhusiana na zile swala za mchana ni kwamba inaswaliwa kwa kimya kimya na sunnah kuhusiana na swala za usiku ni kwamba inapaswa kuswaliwa kwa sauti.856 106. Vilevile: al-Harith amesema: Nilimsikia yeye akisema: ‘Qul Huwallahu Ahad’ (Surat al-Ikhlas) ni sawa na theluthi ya Qur’ani na ‘Qul Ya Ayyuhal-Kafirun’ (Surat al-Kafirun) ni sawasawa na robo (ya Qur’ani); na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akirudia kusoma ‘Qul Huwallahu Ahad’ katika swala ya Witri mara tatu ili aweze kupata thawabu za kisomo cha Qur’ani nzima.857 107. Katika al-Faqih: Kutoka kwa Zurarah ambaye amesema: Nilimsikia Aba Ja’far (a.s.) akisema: Ile dua inayosomwa baada ya swala ni bora kuliko swala ya sunnah; na hivi ndivyo sunnah ilivyoelekezwa.858 108. Katika at-Tahdhib: Katika riwaya yake kutoka kwa Abi Harun al-Makfuf kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye alisema: “Ewe Aba Harun! Sisi (Ahlul-Bayt) tunawaelekeza watoto wetu kusoma ile tasbih ya Fatima Zaharah (a.s.) kama vile tu tunavyowaamrisha kushikamana na swala, hivyo wakati wote isome hiyo, kwani mtu anayeisoma hiyo kamwe hatakuwa mnyonge.859 109. Katika al-Qurb al-Isnad: Kutoka kwa Husein ibn ‘Alwan kutoka kwa Ja’far kutoka kwa baba yake (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimwambia Ali (a.s.): “Ewe Ali! Ni lazima usome Ayatul-Kursi kila baada ya swala ya wajib, kwani kwa hakika hakuna atakayeweza kushikilia katika kufanya hivyo isipokuwa mtume, mtu ambaye ni mkweli au shahidi.”860 854 al-Gharat 1:246 855 at-Tahdhib al-Ahkam 2:311 856 Ibid, 2:289 857 Tahdhib al-Ahkam 2:124 858 al-Faqih 1:328 859 Tahdhib al-Ahkam 2:124 860 Qurb al-Isnad: 56 160


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 161

SUNAN-NABII Kidokezo: Hii imesimuliwa pia katika al-Da’aim.861 110. Katika al-Da’aim: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akisoma (ifuatayo) katika rakaa mbili za mwanzo kabla ya swala ya Witri: Katika rakaa ya kwanza, ‘Sabihisma Rabbikal ‘A’la’ (Surat al-‘A’la), katika rakaa ya pili, ‘Qul Ya Ayyuhal Kafirun’ (Surat al-Kafirun), na katika rakaa ya tatu, ambamo inasomwa Qunuti, yeye alitumia kusoma ‘Qul Huwallahu ‘Ahad’ (Surat al-Ikhlas); na yote haya ni baada ya kusoma ‘Fatihat al-Kitab’ (Surat al-Hamd).862 111. Katika ‘Awarif al-Ma’arif: Amirul-Mu’minin (a.s.) alisimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akisema katika sajidah yake: “Allahuma laka sajadtu wa bika amantu wa laka aslamtu, sajada wajhiya lilladhiy khalaqahu wa swawarahu washaqa sam’ahu wabaswarahu, fatabaaraka llahu ahsanul-khaaliqiina.” “Ewe Mungu wangu! Kwa ajili Yako nimesujudu, na Wewe nimekuamini na nimesalimu amri kwako. Uso wangu umemsujudia Yule ambaye ameuumba na kuutengeneza vizuri na kuupa nguvu na uwezo wa kusikia na kuona, hivyo Ametukuka Mwenyezi Mungu, Mbora wa Waumbaji.863 112. Ndani ya kitabu al-Gharat cha al-Thaqafi: Kutoka kwa Ubayah ambaye amesema: Amirul-Mu’minin Ali (a.s.) alimwandikia Muhammad ibn Abi Bakr: Chunga rukuu zako ….. na wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa akisimama kutoka kwenye rukuu alisema: “Sami’a llahu liman hamidahu, Allahuma lakal-Hamdu mil’a samawaatika, wa mil’a ardhika, wa mil’a maa shi’ita min shay’in.” “Mwenyezi Mungu amemsikia yule anayemtukuza Yeye. Ewe Mola wangu! Utukufu ni Wako, (utukufu ambao) unaojaa mbingu Zako, na unaoijaa ardhi Yako, na unaojaa ukitakacho miongoni mwa vitu.”864 113. Katika al-Bihar kutoka kwenye al-Dhikra: Kwenye dua inayosomwa baina ya sajidah mbili – imesimuliwa kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba alikuwa akitumia kusema baina yake hizo: 861 Da’aim al-Islam 1:168 862 Ibid, 1:205 863Awarif al-Ma’arif: 284 864 al-Gharat 1:246 161


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 162

SUNAN-NABII “Allahuma ighfirliy warhamniy wa ajirniy wa afiiniy inniy limaa anzalta ilay’ya min khairin faqiirun. Tabaaraka llahu Rabul-‘Alamiyna.” “Ewe Mungu Wangu! Nisamehe mimi, na unihurumie, na uniweke salama na unijaalie afya njema. Mimi ni mhitaji wa yale mema ambayo umenishushia. Ametukuka Mwenyezi Mungu, Mola wa ulimwengu.”865 114. Katika al-‘Awarif al-Ma’arif: Maimunah, mke wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesimulia: Khumrah866 ingetandikwa msikitini kwa ajili ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuswalia juu yake.867 115. Katika al-Hidayah ya Husein ibn Hamdan al-Hasini: Kutoka kwa Isa ibn Mahdi al-Jawhari na wengine wengi, katika hadithi kutoka kwa Abi Muhammad alAskari (a.s.): Allah ‘Azza wa Jalla. alimshushia wahyi babu yangu, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): Nimewatofautisha wewe na Ali, na hujja Zangu kutokana na yeye (yaani kutoka kwenye kizazi chake) mpaka Siku ya Kiyama, na wafuasi wako kwa sifa kumi: - ….. na (kufanya) ta’fir 868 baada ya kila swala.869 116. Katika al-Majma’: Wakati yeye (s.a.w.w.) alipokuwa akiswali, angekuwa imara sana katika swala yake.870 117. Katika Durr al-La’ali ya Ibn Jamhur, katika hadithi: Swala zilizopendwa sana machoni mwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) zilikuwa ni zile ambazo ziliswaliwa wakati wote, hata kama zilikuwa chache. Na wakati aliposwali swala yoyote katika swala hizo, angefanya hivyo wakati wote.871 118. Katika ‘Ilal al-Sharai’: Katika simulizi yake kutoka kwa Anas ibn Malik ambaye amesema: Nilimsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema: “Rakaa mbili zinazoswaliwa katikati ya usiku kwa hakika zina thamani sana kwangu kuliko dunia na kile kilichomo ndani yake.”872

865 Bihar al-Anwar 85:137 866 Ni mkeka uliotengenezwa kutokana na makuti ya mtende (Tr.) 867 ‘Awarif al-Ma’arif: 103 868 Kile kitendo cha kusugua mashavu yake mtu kwenye udongo wakati akisujudu (Tr.) 869 al-Mustadrak 3:290 Hadith namba 7. 870 Hatukuiona hii katika al-Majma’ 871 al-Nuri ameisimulia hii katika al-Mustadrak 7:539 akinukuu kutoka kwenye Durr alLa’ali. 872 ‘Ilal al-Sharai’: 363 162


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 163

SUNAN-NABII 119. al-Saduq katika al-Fadha’il al-Ash’hur: Katika simulizi yake kutoka kwa Abdillah ibn Mas’ud, kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye amesema: Naapa kwa Yule ambaye amenituma mimi kwa Haki – Jibril amenifahamisha kutoka kwa Israfil, kutoka kwa Mola Wake Mtukufu kwamba Yeye ‘Azza wa Jalla. amesema: Yule atakayeswali katika usiku wa mwisho wa mwezi wa Ramadhan rakaa kumi, akisoma katika kila rakaa ‘Fatihat al-Kitab’ (Surat al-Hamd) mara moja na ‘Qul Huwallahu Ahad’ (Surat al-Ikhlas) mara kumi na kusoma katika rukuu yake na sajidah: “Subhaana llahi wal-hamdu lilahi wa laa ilaha ila-llahu Wallahu Akbar.” Na akasoma tashahudi na salam baada ya kila rakaa mbili. Na wakati anapomaliza ile rakaa ya mwisho kati ya hizo kumi, baada ya salam anasoma ‘Astaghfirullah’ mara elfu moja ambapo baada yake hizo anakwenda sajidah na anasema: “Yaa hayyu yaa qayuumu, Yaa dhaal-Jalaali wal-ikraami, Yaa Rahmaanu al-Duniyaa wal-Aakhirati wa rahiimahumaa, Yaa arhamarRahimiin, Yaa ilahal-awaliina wal-akhiriina, ighfir lanaa dhunuubanaa, wataqabal minaa swalaatanaa wa swiyaamanaa waqiyaamanaa.” “Ewe Uliye hai! Ewe Qayyum! = Mwenye kuwepo kwa kujitegamea! Ewe Mwenye utukufu na heshma! Ewe Mwenye kurehemu katika dunia hii na akhera na mwenye huruma katika zote hizo! Ewe Mwenye kurehemu mno kuliko wenye kurehemu wote! Ewe Mungu wa wa mwanzo na wa mwisho! Tusamehe sisi dhambi zetu na tukubalie swala zetu na swaumu zetu na kisimamo chetu.” Yaani cha swala za usiku. ….. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Hii ilikuwa ni zawadi makhsusi kwangu mimi na wanaume na wanawake wa ummah wangu ambao Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. hakumpa yeyote yule kabla yangu, kutoka katika mitume na hata wengineo.873 120. Katika Awarif al-Ma’arif: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akitumia kuswali wakati anapoingia nyumbani kwake, kabla ya kukaa chini, rakaa nne. Na katika rakaa hizi nne alisoma Surat Luqman, Yaasin, al-Dukhan na al-Mulk.874 873 Fadha’il al-Ash’hur al-Thalathah: 134-135 874 Awarif al-Ma’arif: 335

163


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 164

SUNAN-NABII 121. Kutoka kwenye at-Tahdhib: Katika simulizi yake kutoka kwa Ibn Sinan kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Sunnah kuhusiana na adhana mnamo siku ya Arafah ni kwamba mtu aadhini ikifuatiwa na Iqamah kwa ajili ya swala ya Adhuhuri, na halafu swala inaswaliwa. Kisha mtu asimame kwa ajili ya iqamah ya Alasri bila ya Adhana, na ifanyike vivyo hivyo kwa swala ya Magharibi na Isha huko Muzdalifah.875 122. Kutoka kwenye al-Kafi: Katika riwaya yake kutoka kwa Muhammad ibn Muslim kutoka kwa Abi Ja’far (a.s.) ambaye amesema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipomsikia Mwadhini akiadhini, yeye alirudia kumfuatisha (akitamka) kila kitu ambacho alikuwa akikisema Mwadhini huyo.876 123. Katika at-Tahdhib na al-Istibsar: Katika riwaya yake kutoka kwa Zurarah na Fudhayl ibn Yasar, kutoka kwa Abi Ja’far (a.s.) ambaye amesema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliponyanyuliwa (kwenda Mi’raj), pale alipofika Baytul-Ma’mur wakati wa swala ukaingia. Hivyo Jibril akaadhini na kukimu swala na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akapita mbele na malaika na mitume wakapanga safu nyuma ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.). Yeye akasema: Tulimuuliza: Je, aliisomaje hiyo Adhana? Yeye (s.a.w.w.) akasema: (Aliadhini hivi): “Allahu Akbar, Allahu Akbar, Ash’hadu an laa ilaha ila-llah, Ash’hadu an laa ilaha ila-llah, Ash’hadu anna Muhammadan rasulu-llah, Ash’hadu anna Muhammadan rasulu-llah, Hai’yaala al-Swala, Hai’yaala al-Swala, Hai’yaalal-falaah, Hai’yaala-falaah, Hai’yaalaa khairil-amal, Hai’yaalaa khairil-amal, Allahu Akbar, Allahu Akbar, laa ilaha ila-llahu, laa ilaha ila-llah.” Na Iqamah ilikuwa kama vivyo hivyo isipokuwa iliongezeka “Qad qaamati swalaat, qad qaamat swalat,” ambayo ilisomwa katikati ya “Hayi’alaa khairil-amal, hayi’alaa khairil-amal” – na – “Allahu Akbar.” Na Mtukufu Mtume akamwelekeza Bilal (kuisoma Adhana kama hivyo), na aliendelea kuadhini kama hivyo mpaka Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipofariki dunia.877

875 at-Tahdhib al-Ahkam 2:282, Wasa’il ash-Shi’ah 4:665 876 al-Kafi 3:307, Wasa’il al-Shi’ah 4:671 877 Tahdhib al-Ahkam 2:60, al-Istibsar 1:305, Wasa’il al-Shi’ah 4:644 164


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 165

SUNAN-NABII na 878 124. Katika Majma’ul-Bayan: Katika riwaya yake, Anas ibn Malik amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akitoa kafara (la Udh’ha) kabla ya kuswali, kwa hiyo aliamrishwa na Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. kuswali kwanza halafu ndipo atoe kafara.879 125. Katika al-Majma’ ya at-Tabarsi: Katika riwaya yake kutoka Jabir ibn Samarah: Sikumuona Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akitoa hotuba bali kwamba angefanya hivyo huku akiwa amesimama,, hivyo yoyote atakayekwambia kwamba alitoa hotuba huku akiwa amekaa, huyo atakuwa anadanganya.880 Kidokezo: Hii imesimuliwa pia kutoka kwa Abdillah ibn Mas’ud.881 126. Katika al-Khisal: Katika riwaya yake kutoka kwa Aishah kwamba amesema: “Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa na mimi, alikukwa akitumia kuswali rakaa mbili baada ya swala ya Alasiri.882 127. Katika al-Ikhtisas: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa anatoa hotuba, mwishoni angeweza kusema: “Pepo ni kwa yule ambaye sifa zake ni nzuri, ambaye tabia yake ni njema, ambaye matendo yake yaliyofanywa kwa siri ni ya kiuchamungu, ambaye vitendo vyake vilivyotendwa hadharani ni vya kiadilifu, ambaye anatoa mali yake bora kama sadaka, anayejiepusha na mazungumzo yasiyo 878 Adhana kama ilivyotajwa kwenye Hadithi hii na ambayo inaonekana kwenye makusanyo mbalimbali ya Hadithi ikiwa ni pamoja na al-Bihar al-Anwar “haikukamilika” kulingana na hadithi inayokubalika kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Maimam (a.s.) ambao wametufundisha sisi namna ambayo adhana lazima ifanyike na kama ilivyoelezwa kirefu na wanachuoni katika vitabu mbalimbali vya fiqh. Nakala mbali mbali za Bihar alAnwar zilipitiwa na zote zimesimulia tukio hilo kwa njia moja hiyo hiyo. Kwa hiyo, inawezekana kwamba hadithi yote haikusimuliwa kikamilifu kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) au kwa sababu vitabu vya hadithi vya Ahlul-Bayt (a.s.) vimekuwa wakati wote vikishambuliwa na kuharamishwa huko nyuma na hivyo, hadithi yote nzima inaweza kuwa imepotea. (Mh. – kama ilivyojibiwa na ofisi ya Ayatullah al-Uzma Hajj Sheikh Nasir Makarim Shirazi) 879 Majmaul-Bayan 10:549 – Surat al-Kawthar (108) 880 Majmaul-Bayan 10:289 – Surat al-Jumu’ah (62) 881 Ibid. 882 al-Khisal 1:71, Bihar al-Anwar 83:148

165


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 166

SUNAN-NABII na maana na anayewatendea watu kwa wema kuliko anavyojitendea yeye mwenyewe.”883 128. Katika Uyun Akhbar al-Ridha (a.s.): Pamoja na nyororo tofauti za wasimuliaji kutoka kwa Fadhl ibn Shadhan, kutoka kwa ar-Ridha (a.s.) ambaye, katika barua yake kwa Ma’mun, alisema: Kusoma ‘Bismillahir-Rahmanir-Rahim’ kwa sauti kubwa katika swala zote ni kutoka katika Sunnah.884 Kidokezo: Hii ina maana kwamba ni sunnah kufanya hivi katika swala zote wakati wa mchana na wa usiku, iwe ni wajibu au za hiari. 129. Katika Majma’ul-Bayan: Katika riwaya yake kutoka kwa Asbagh ibn Nubatah, kutoka kwa Amirul-Mu’minin Ali (a.s.) ambaye amesema: Wakati Sura – alKawthar – ilipoteremshwa, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuuliza Jibril: “Ni kafara gani hili ambalo Mola Wangu ananitaka nitoe?” Yeye akasema: “Sio kafara, bali anakuamuru kwamba pale unapoianza swala unapaswa kunyanyua mikono yako vile unapotamka takbir, na (tena) wakati unapokwenda rukuu, na pale unaponyanyua kichwa chako kutoka kwenye rukuu, na wakati unapokwenda sajidah – kwani hii ndio swala yetu na swala ya Malaika walioko kwenye zile mbingu saba. Kwa hakika kuna mapambo kwa ajili ya kila kitu, na pambo la swala ni kunyanyua mikono sambamba na kutamka kila takbir.”885 Kidokezo: Hii imesimuliwa vilevile katika ad-Durr al-Manthur.886 130. Kutoka kwenye at-Tahdhib: Katika riwaya yake kutoka Ali ibn Ja’far ambaye amesema: Nilimuuliza Aba al-Hasan (a.s.) kuhusu usomaji wa adhana kutoka kwenye minara – kwamba je, ni sunnah? Yeye alinijibu: Katika wakati wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) adhana ilikuwa ikiadhiniwa chini na kulikuwa hakuna minara katika siku zile.887 131. Kutoka katika al-Faqih: Katika riwaya kutoka kwa Hasan ibn al-Sirri kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Ni kutoka katika sunnah kwa mtu kuweka vidole vyake ndani ya masikio yake wakati anapoadhini.888 883 al-Ikhtisas: 228, al-Mustadrak 11: 309 884 Uyun al-Akhbar al-Ridha 2:122, Wasa’il al-Shi’ah 4:758 885 Majma’ al-Bayan 10:550 – Surat al-Kawthar (108) 886 al-Durr al-Manthur 6:403 – Surat al-Kawthar (108) 887 At-Tahdhib al-Ahkam 2:284, Wasa’il al-Shi’ah 4:640 888 al-Faqih 1:284, Wasa’il al-Shi’ah 4:641 166


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 167

SUNAN-NABII Kidokezo: Hii imesimuliwa pia katika at-Tahdhib.889 132. Katika al-Tahdhib: Katika riwaya yake kutoka kwa Ibn Sinan ambaye amesema: Nilimuuliza yeye kuhusu mwito wa adhana kabla ya mawio, (- je, inaruhusiwa?) Yeye akasema: Hakuna tatizo, hata hivyo iliyo sunnah ni (kuadhini) pamoja na mawio.890 133. Katika al-Da’aim: Kutoka kwa Abi Abdillah Ja’far ibn Muhammad (a.s.) kwamba amesema: Katika tukio la kupatwa kwa jua au kupatwa kwa mwezi, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angewaambia watu: “Nendeni misikitini kwenu haraka sana.”891 134. Vilevile: ….. Iliyo sunnah ni kuswali (Swalat al-Ayat) swala ya matukio ndani ya msikiti kama wanaswali katika swala ya jamaa.892

889 Tahdhib al-Ahkam 2:284 890 Tahdhib al-Ahkam 2:53 891 Da’aim al-Islam 1:200 892 Ibid., 1:202 167


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 168

SUNAN-NABII

MLANGO WA 17 ADABU ZA (KUFUNGA) SWAUMU 1. Katika al-Faqih: Imesimuliwa kutoka kwa Muhammad ibn Marwan ambaye amesema: Nilimsikia Abi Abdillah (a.s.) akisema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angefunga kiasi kwamba ingeweza kusemekana kwamba alikuwa havunji (kufuturu) swaumu yake, na angeweza kusimama kufunga kwa muda mrefu kiasi kwamba ingeweza kusemwa kwamba alikuwa hafungi. Kisha alifunga swaumu siku za Jumatatu na Alhamisi. Mwishoni aligeukia kufunga siku tatu kwa mwezi; ile Alhamisi ya mwanzoni mwa mwezi, Jumatano ya katikati ya mwezi na Alhamisi ya mwishoni mwa mwezi; na yeye (s.a.w.w.) angesema: “Huu ndio ufungaji wa kipindi cha uhai.” Yeye (Abu Abdillah) (a.s.) vilevile alisema: Baba yangu (a.s.) alikuwa akisema: “Hakuna anayechukiwa na Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. kuliko mtu anayeambiwa: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angefanya hili na lile” na akajibu: “Allah ‘Azza wa Jalla. hatoniadhibu kwa juhudi zangu katika (kutekeleza kwa wingi) swala na kufunga kwangu” – kana kwamba anadhani kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliacha jambo ambalo lilikuwa bora zaidi kwa sababu alikuwa hana uwezo wa kulitenda.893 2. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Muhammad ibn Muslim kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.): Mwanzoni mwa kazi yake ya utume, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akitumia kufunga sana kiasi kwamba ingeweza kusemwa alikuwa havunji swaumu yake kamwe, na yeye angeacha kufunga kwa muda mrefu kwamba ingesemwa yeye alikuwa hafungi. Halafu aliacha (mwendo huu) na akaanza kufunga siku za kupishana – na huu ulikuwa ndio ufungaji wa Nabii Dawud (a.s.). Kisha akaliacha hili na akafunga katika siku tatu za al-Ghurr (siku ya 13, 14 na 15 ya kila mwezi). Yeye halafu akaacha (mwenendo huu) vilevile na akatenganisha swaumu hizo kwa siku kumi, (akifunga) kwenye Alhamisi mbili pamoja na Jumatano moja katikati yake, na yeye (s.a.w.w.) aliliendeleza hili mpaka kufariki kwake.894 3. Katika Hadith al-Arba’mia: Yeye (a.s.) amesema: Kufunga katika siku tatu kila mwezi, katika Alhamisi mbili na Jumatano katikati, na kufunga katika mwezi wa 893 al-Faqih 2:81; Makarim al-Akhlaq: 138, al-Kafi 4:90, Qurb al-Isnad: 43 Tahdhib alAhkam 4:302 894 al-Kafi 4:90 168


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 169

SUNAN-NABII Sha’ban, kunaondoa mipenyezo ya kiovu na wasiwasi kutoka moyoni – na sisi (Ahlul-Bayt) tunafunga katika Alhamisi mbili na Jumatano moja katikati yao.895 4. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Anbasah al-Abidi ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alifariki huku (akiendeleza mwendo wa) akiwa anafunga katika mwezi wa Sha’ban na Ramadhani na siku tatu katika kila mwezi mwingine.896 5. Kutoka kwa al-Saduq ndani ya vitabu vyake viwili, al-Ma’ani na kile cha alMajalis: Imesimuliwa kutoka kwa Abi Basir kutoka kwa as-Sadiq kutoka kwa baba zake (a.s.): Siku moja, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwauliza masahaba zake: “Ni nani miongoni mwenu anayefunga muda wa uhai wake (wote)?” Salman akasema: “Mimi ninafanya hivyo, ewe Mtume wa Allah.” Mtu mmoja akamwambia Salman: “Nimekuona ukila katika takriban siku zote!” Yeye akasema: “Sio kama unavyodhania wewe. Mimi ninafunga katika siku tatu kila mwezi na Allah amesema: ‘Yeyote anayefanya tendo jema atapata mara kumi kama hilo …..’897 na mimi ninaunganisha Sha’ban na Ramadhani, hivyo huku ni kufunga kwa maisha yote.” Vilevile (imeelezwa kwamba) Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimwambia mtu huyo: “Ni wapi tena utakapoona anayefanana na Luqman mwenye hekima? Muulize huyo na atakwambia.”898 6. Kutoka kwa Ahmad ibn Muhammad ibn Isa katika Nawadir yake: Kutoka kwa Ali ibn Nu’man kutoka kwa Zur’ah ambaye amesema: Nilimuuliza Abi Abdillah (a.s.) iwapo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akifunga katika mwezi wa Sha’ban. Yeye alijibu: “Ndiyo, bali hakuufunga mwezi wote mzima.” Mimi nikasema: “Ni siku ngapi alizokuwa akifunga yeye?” Yeye akanijibu kwa kusema: “Alikatisha kuendelea kufunga katika baadhi ya siku (za mwezi wa Sha’ban).” Nilimuuliza swali hili mara tatu naye alinipa jibu hilohilo, bila kuongezea chochote zaidi kwenye ‘alikatisha kufunga katika baadhi ya siku.’ Nilimuuliza tena swali hili baada ya mwaka mmoja naye alinijibu kwa namna ileile.899 7. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Amr Ibn Khalid kutoka kwa Abi Ja’far (a.s.): Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akifunga Sha’ban na Ramadhani, akiziunganisha zote pamoja, bali akiwaelekeza watu kutoziunganisha, yeye (s.a.w.w.) angesema: “Yote ni miezi ya Allah, na yote ni fidia kwa ajili ya dhambi za wakati ulio895al-Khisal 2:612 896 Surat al-‘An’am; 6:160 897 Ma’ani al-Akhbar: 234, Amali al-Saduq: 37 898 Hatunayo hiyo Nawadir ya Ahmad ibn Muhammad ibn Isa, 899 Wasa’il al-Shi’ah 7:367 169


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 170

SUNAN-NABII pita na wa baadaye.”900 Kijalizo: Inawezekana kwamba maelekezo ya kutoiunganisha funga ya miezi hiyo miwili yanaashiria kutofunga mfululizo kwa miezi yote miwili, kama ilivyoelezwa katika baadhi ya hadithi zetu ambamo mna maelekezo ya kuikatisha (miwili hiyo) japo iwe ni kwa kutofunga siku moja katikati ya mwezi.901 8. Katika al-Makarim: Kutoka kwa Anas ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na kinywaji ambacho angevunjia swaumu nacho na kinywaji kwa ajili ya sahr -daku. Wakati mwingine angeweza kuwa na kinywaji kimoja – wakati mwingine ingekuwa ni maziwa na wakati mwingine ingekuwa ni kinywaji chenye mkate uliolowekwa ndani yake.902 9. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Ibn al-Qaddah kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Kitu cha mwanzo ambacho Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alivunja nacho swaumu yake katika msimu wa tende mbivu kilikuwa ni tende mbivu safi na katika msimu wa tende kavu kilikuwa ni tende kavu.903 10. Vilevile: Imesimuliwa kutoka kwa al-Sakuni kutoka kwa Ja’far kutoka kwa baba zake (a.s.): Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipofunga na akawa hakuweza kupata kitu chochote kitamu (kwa ajili ya kuvunjia swaumu yake kwacho), angefungua kwa maji.904 11. Katika baadhi ya hadithi: Yeye (s.a.w.w.) wakati mwingine angevunja swaumu yake kwa zabibu kavu.905 12. Kutoka kwa al-Mufid ndani ya al-Muqni’ah: Imesimuliwa kutoka kwenye familia ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): Imependekezwa kuchukua suhur 906 hata kama ni bilauri ya maji tu. Vilevile imesimuliwa kwamba ni bora kula tende kavu na Sawiq907 kwa sababu hivi ndivyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alivyokuwa akila katika daku (suhur) lake.908 900 al-Kafi 4:92, al-Faqih 2:93, Tahdhib al-Ahkam 4:307, al-Khisal: 606 901 Wasa’il al-Shi’ah 7:387-390 902 Makarim al-Akhlaq: 32 903 al-Kafi 4:153, Da’aim al-Islam 2:111 904 al-Kafi 4:152 905 Tahdhib al-Ahkam 4:198 906 Chakula cha mwisho kabla ya mawio katika mwezi wa Ramadhani – Daku. (Tr.) 907 Chakula kinachotengenezwa kwa ngano au shayiri iliyochanganywa na sukari na tende.(Tr.) 908 al-Muqni’ah: 316 170


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 171

SUNAN-NABII 13. Katika al-Makarim: Kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba yeye alikuwa akitumia kula al-Harisah910 zaidi kuliko chakula kingine chochote na angekitumia hicho pia kwa daku lake.911 14. Katika al-Faqih: Wakati mwezi wa Ramadhani ulipowadia, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwaachia huru wafungwa wote na alitoa kitu (chochote) kwa wenye kuomba wote.912 15. Katika al-Da’aim: Kutoka kwa Imam Ali (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angekunja godoro lake na kukithirisha ibada zake katika siku kumi za mwisho za mwezi wa Ramadhani. Yeye alikuwa akiiamsha familia yake katika usiku wa mwezi ishirini na tatu na angezinyunyizia maji nyuso za wale waliokuwa wamelala kwenye usiku huu. Na Fatimah (a.s.) hakumruhusu yeyote katika familia yake kulala kwenye usiku huu, na ili kuwawezesha kubakia macho, aliwapa chakula kichache na kuwaandaa tangu asubuhi akisema: “Yule ambaye hanufaiki na neema za usiku huu kwa hakika amenyimwa (fadhila).913 16. Katika al-Ja’fariyat: Katika riwaya yake kutoka kwa Ja’far kutoka kwa baba zake, kutoka kwa Ali (a.s.): Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipotaka kwenda kwenye swala katika siku ya Idd el-Fitr, (kwanza) angepata kifungua kinywa cha tende na zabibu kavu.914 17. Kutoka kwa al-Saduq ndani ya al-Muqni’ah: Iliyo sunnah ni kwamba mtu anapaswa kula baada ya swala kwenye siku ya Idd al-‘Adh’ha na kabla ya kuswali kwenye siku ya Idd al-Fitr.915

Nyongeza kwenye sehemu hii 1. Katika Durar al-La’ali: Kutoka kwa mmoja wa wake za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye amesema kwamba yeye angefunga katika mwezi tisa ya Dhul Hijjah na katika siku tatu za kila mwezi.916 2. Katika al-Iqbal: Katika juzuu ya pili ya Ta’rikh al-Nisabur, kutoka kwa Khalf ibn 910 Chakula kinachotengenezwa kwa kuchanganya bulga na nyama (Tr.) 911al-Makarim al-Akhlaq: 29 912 al-Faqih 2:99, Amali al-Saduq: 57 913 al-Da’aim al-Islam 1:282 914 al-Ja’fariyat: 40, Nawadir al-Rawandi: 39, Bihar al-Anwar 91:122 915 al-Muqni’: 46, al-Faqih 1:508 916 Imesimuliwa na al-Nuri katika al-Mustadrak 7:520 171


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 172

SUNAN-NABII Ayyub al-‘Amiri katika riwaya yake kuhusu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): Wakati mwezi wa Ramadhani ulipoingia, yeye angesawajika na swala zake zingeongezeka na yeye angeomba dua na angemuomba Mwenyezi Mungu kwa kumsihi sana.917 3. Katika Majmu’at Warram: Pale jambo fulani lilipomhuzunisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), yeye angetafuta kimbilio kwenye kufunga na swala.918 4. Katika al-‘Uyun: Kutoka kwa Darim ibn Qabisah kutoka kwa ar-Ridha kutoka kwa baba zake kutoka kwa Ali (a.s.) ambaye amesema: Wakati mwezi wa Sha’ban ulipoingia, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angefunga kwa siku tatu mwanzoni mwa mwezi, siku tatu katikati ya mwezi na siku tatu mwishoni mwa mwezi, na angesimama kufunga kabla mwezi wa Ramadhani haujaingia, akiacha pengo la siku mbili kabla, na kisha akaanza kufunga (tena).919 5. Katika al-Kafi: Kutoka kwa Abdillah ibn Maskan, kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipofungua swaumu yake, alianza kwa chakula kitamu, na endapo hakuwa nacho, angekula sukari kiasi au tende kavu na kama alikuwa hana chochote kati ya hivi, basi angefungulia kwa maji yenye vuguvugu.920 6. Katika al-Iqbal: Kutoka kwa Jabir, kutoka kwa Abi Ja’far (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angefuturu kwa vile ‘vyakula vyeusi viwili.’ Mimi nikauliza: “Mwenyezi Mungu ashushe rehma Zake juu yako – ni nini hivyo ‘vyakula vyeusi viwili’?” Yeye akasema: “Ni tende kavu na maji, na tende mbichi na maji.”921 7. Katika al-Makarim: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akifuturu kwa tende kavu na pale sukari ilikuwepo, angefuturu kwayo.922 8. Katika al-Kafi: Katika riwaya yake kutoka kwa Abi Basr ambaye amesema: Wakati ile mikesha kumi ya mwisho (ya mwezi wa Ramadhani) ilipowadia, yeye (s.a.w.w.) angejiandaa mwenyewe, akiwaacha wake zake, akabakia macho akikesha usiku na kujishughulisha na ibada.923 Kidokezo: Hii imesimuliwa vilevile na al-Saduq katika al-Faqih na at-Tabarsi kati917 Iqbal al-A’mal: 20 918 Majmu’at Warram: 255 919 Uyun al-Akhbar al-Ridha 2:70 920 al-Kafi 4:153 921 Iqbal al-A’mal: 114 922 Makatim al-Akhlaq: 27 923 al-Kafi 4:155 172


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 173

SUNAN-NABII ka al-Majma’.924 9. Katika at-Tahdhib: Kutoka kwenye kile kilichothibitishwa kwamba kinatoka kwenye sunnah: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angeuatafuta mwezi mwandamo na kuchukua wajibu wake wa kujaribu kuuona huo mwezi mpya yeye mwenyewe.925 10. Katika al-Da’aim: Kutoka kwa Ali (a.s.) ambaye amesema: Kulipa ile sadaka (ya wajib) ya Fitr kabla ya swala ya Idd al-Fitr inatoka kwenye sunnah.926 11. al-Saduq katika al-Muqni’: Ni kutoka katika sunnah kusoma takbir katika usiku wa Fitr na kwenye siku ya Idd al-Fitr baada ya swala kumi (kati ya zile za wajib), na kusoma takbir katika siku ya Idd al-Adh’ha kwa wale ambao hawakwenda Hijja – kuanzia ile swala ya Dhuhr mpaka swala ya al-Fajr ya siku ya pili (12 Dhul Hajj) – baada ya swala kumi za wajibu.927 12. Katika at-Tahdhib: Katika riwaya yake kutoka kwa Sayyed al-Naqqash ambaye alisema: Abu Abdillah (a.s.) aliniambia: “Kuna takbir katika siku ya Idd al-Fitr lakini imeagizwa kama sunnah.” Mimi nikauliza: “Inasomwa wakati gani?” Yeye akajibu: “Kwenye usiku wa Fitr ndani ya swala ya Magharibi na Isha, na katika swala ya al-Fajr na ile swala ya Idd siku ya Fitr kisha inasimamishwa…..”928 13. Katika al-Da’aim: Tumesimuliwa kutoka kwa Ali (a.s.) ambaye amesema: Ni katika sunnah kuharakisha katika kufuturu na kuchelewesha kula Daku hadi sehemu ya mwisho ya usiku, na kuanza na swala – kwa maana ya Magharibi – kabla ya kufuturu.929 14. Katika al-Tahdhib: Katika riwaya yake kutoka kwa Mu’awiyah ibn Wahab ambaye amesema: Nilimsikia Aba Abidillah (a.s.) akisema: Katika suala la Zakat alFitr, sunnah ilikuwa ni kutoa sa moja (sawa na kilo 3) ya tende, sa moja ya zabibu kavu au sa moja ya shayiri.930 15. Vilevile: Katika riwaya yake kutoka kwa Ishaq ibn Ammar, kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. hakupendelea mimi niwe na sifa sita nami sikuzipendelea 324 al-Faqih 2:156, Majma’ al-Bayan 10:518 – Surat al-Qadr (97) 925Tahdhib al-Ahkam 4:155 926 Da’aim al-Islam 1:267 927 al-Muqni’: 46 928 Tahdhib al-Ahkam 3:138 929 Da’aim al-Islam 1:280 930 Tahdhib al-Ahkam 4:83 173


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 174

SUNAN-NABII sifa hizi juu wa warithi wangu kutokana na kizazi changu na wafuasi wao baada yangu: (moja ya sifa hizo ni) kujamiiana wakati ukiwa katika swaumu.931 Kidokezo: Hii imesimuliwa pia na al-Saduq katika al-Amali yake ndani ya riwaya yake kutoka kwa Ghiyath ibn Ibrahim.932 16. Katika Tuhf al-Uqul: Mtu mmoja alikuja kwa Imam ar-Ridha (a.s.) mnamo siku ya Fitr na akasema: “Kwa futari yangu leo, nikula tende kavu na udongo wa kaburi.” Yeye (a.s.) akasema: “Wewe umechanganya sunnah pamoja na rehma.”933 17. Katika al-Awarif al-Ma’arif: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akitumia kufuturu kwa kunywa maji, maziwa kidogo na tende kavu.934

931 Ibid, 4:195 932 Amali al-Saduq: 60 933 Tuhf al-Uqul: 448 934 ‘Awarif al-Ma’arif: 304 174


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 175

SUNAN-NABII

MLANGO WA 18 ADABU ZA ITIKAF 935 1. Katika al-Faqih: Ndani ya simulizi yake kutoka kwake Dawud ibn al-Hasin kutoka kwa Abi Abbas, kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alifanya Itikafu katika mwezi wa Ramadhani kwenye siku kumi za mwanzo, halafu alifanya Itikafu katika mwaka uliofuatia kwenye siku kumi za katikati na katika mwaka wa tatu, yeye alifanya Itikafu kwenye siku kumi za mwisho – na kuanzia hapo wakati wote alikuwa akifanya Itikafu yake kwenye siku kumi za mwisho za mwezi wa Ramadhani.936 2. Vilevile: Abu Abdillah (a.s.) amesema: Vita vya Badr vilitokea ndani ya mwezi wa Ramadhani hivyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakufanya Itikafu na mwaka uliofuatia alifanya Itikafu kwa muda wa siku ishirini, kumi kwa ajili ya mwaka ule na kumi kwa ajili ya kulipizia ule mwaka uliopita ambao alikosa kuifanya.937 Kidokezo: Hadithi hii imetajwa vilevile na al-Kulayni.938 3. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa al-Halabi kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Wakati zile siku kumi za mwisho zilipowadia, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angefanya Itikafu ndani ya msikiti na hema ndogo iliyotengenezwa kwa manyoya ilisimamishwa kwa ajili yake, na alikusanya matandiko yake. Mtu mmoja aliuliza: “Je, alijitenga na wake zake?” Yeye (a.s.) akajibu: “La hasha, hakujitenga na wake zake.”940 Kidokezo: Zipo hadithi nyingi kama hii na baadhi yake zimetajwa hapo mapema na zimeelezea kwamba maana ya mtu kujitenga na wake zake wakati wa Itikafu inaelekezea kwenye ruhusa ya kuchanganyika nao bila ya kujamiiana nao.941

935 Itikaf – Kitendo cha ibada ambamo mtu anakaa ndani ya msikiti kwa muda kati ya siku 3 hadi 10, anafunga swaumu mchana na anafanya ibada wakati wa usiku (Mfasiri). 936 al-Faqih 2:189, Da’aim al-Islam 1:286, al-Kafi 4:175, al-Mustadrak 7:560 937 al-Faqih 2:183 938 al-Kafi 4:175, al-Mustadrak 7:560 940 al-Kafi 4:175 941 al-Faqih 2:184, Tahdhib al-Ahkam 4:287, al-Usul al-Sittata ‘Ashar: 112 175


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 176

SUNAN-NABII

MLANGO WA 19 ADABU ZA KUTOA SADAKA 1. Katika al-Mahasin: Katika ushauri wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa Imam Ali (a.s.) – mpaka pale aliposema: “….. Na la sita, fuata sunnah yangu kuhusiana na swala, swaumu na kutoa sadaka … Na kuhusu sadaka sisitiza katika kutoa mpaka uje useme kujiambia mwenyewe: ‘Sasa nimekuwa mbadhilifu.’”942 2. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Zayd al-Shahham kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakuwahi kumrudisha muombaji – kamwe. Kama alikuwa ana kitu chochote angekitoa, vinginevyo angesema: “Mwenyezi Mungu akujaalie nacho.”943 Kidokezo: Hii imesimuliwa katika vitabu vingi vya madhehebu zote, Shi’ah na Sunni944 Baadhi ya hadithi kama hiyo zimetajwa katika sehemu ya pili ya kitabu hiki. 3. Kutoka kwa Sayyid ibn Tawus katika al-Muhaj ndani ya hadithi ambamo yeye, kwa maana ya as-Sadiq (a.s.) amesema: “Sisi Ahlul-Bayt hatuchukui tena kitu ambacho tumekwisha kukitoa katika njia ya Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla.”945

Nyongeza kwenye sehemu hii: 1. Katika al-Makarim: Kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Kamwe sitaviacha vitu vitatu: kupanda punda asiye na matandiko, 946 kula juu ya mkeka pamoja na watumwa na kumlisha muombaji kwa mikono yangu mwenyewe.”947

2. Katika Tuhf al-‘Uqul: Kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): Huruma yetu sisi 942 al-Mahasin: 17, al-Kafi 8:89, al-Faqih 4:189, Majmu’at Warram 2:299 943 al-Kafi 4:15 944 Tafsir al-Ayyashi 1:261, al-Mustadrak 7:204 945 Muhaj al-Da’awat: 196 946 ….. kwa kutumia blanketi lilitotandikwa tu (Mfasiri). 947 Makarim al-Akhlaq: 24 176


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 177

SUNAN-NABII – Ahlul-Bayt – ni ya kiasi kwamba tunawasamehe wale wanaotukosea na tunawapa wale wanaotunyima.948 3. Katika Kashf al-Ghummah: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa ndiye mtu mkarimu zaidi ya watu wote. Yeye alitoa bila ubakhili na alichangia bila kusita.949 4. Katika ‘Uddat al-Da’i: Yeye (a.s.) amesema: Sisi tunawapa wale wasiostahili kwa kuhofia kuwafukuza wale wanaostahili.950 5. Katika al-Bihar, kutoka kwenye Da’awat ar-Rawandi: Kutoka kwa AmirulMu’minin (a.s.) ambaye amesema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipoombwa kufanya jambo, kama alipenda kulifanya angesema: ‘Ndio’ na kama hakutaka kulifanya angebakia kimya, na asingesema ‘Hapana’ kwa jambo lolote lile.951 6. Katika al-Ilal: Kutoka kwa Ali ibn al-Hasan ibn Ali ibn Fadhdhal, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abul-Hasan (a.s.), yeye amesema: Nilimuuliza yeye kuhusu Amirul-Mu’minin (a.s.): “Kwa nini hakuitwaa tena Fadak pale alikuwa ndiye Khalifa?” Yeye akajibu akasema: “Kwa sababu sisi ni Ahlul-Bayt na hakuna kati yetu anayechukua tena kitu cha haki yetu kutoka kwa mtu aliyetudhulumu sisi isipokuwa Yeye Allah ‘Azza wa Jalla. Sisi ni viongozi wa waumini, tunahukumu tu kwa faida yao na kuzirudisha haki zao kutoka kwa wale waliowadhulumu na hatuchukui kitu kwa ajili yetu wenyewe.952 Kidokezo: Hii imesimuliwa pia na al-Irbili ndani ya Kashf al-Ghummah kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).953

948 Tuhf al-‘Uqul: 33 949 Kashf al-Ghummah 1:10 950 Uddat al-Da’i: 101 951 Bihar al-Anwar 93:327 952‘Ilal al-Shara’i: 155 953 Kashf al-Ghummah 1:494 177


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 178

SUNAN-NABII

MLANGO WA 20 ADABU ZA KUSOMA QUR’ANI TUKUFU 1. Kutoka kwa Sheikh ndani ya al-Majalis: Imesimuliwa kutoka kwa Abi al-Dunya kutoka kwa Amirul-Mu’minin (a.s.) ambaye amesema: Hakuna ambacho kingemzuia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kusoma Qur’ani tukufu isipokuwa Janabah (kukosa tohara).954 2. al-Tabarsi katika Majma’ul-Bayan: Kutoka kwa Umm Salamah ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angepumzisha usomaji wake Aya baada ya Aya.955 3. Kutoka kwa Sheikh Abi al-Fattuh katika Sharhe yake: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) asingelala mpaka awe amezisoma ‘Musabbihat’ akisema: “Katika Sura hizi kuna aya ambayo ni bora kuliko aya elfu moja.” Watu wakamuuliza: “Na hizo ‘Musabbihat’ ni zipi?” Yeye akasema: “Ni Suratul-Hadid, al-Hashr, al-Saff, alJumu’ah na al-Taghabun.”956 Kidokezo: Hadithi kama hii inaweza kupatikana ndani ya Majma’ul-Bayan kutoka kwa al-Irbas ibn Sariyah.957 4. Kutoka kwa Ibn Abi Jamhur katika Durar al-La’ali kutoka kwa Jabir ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) asingeweza kwenda kulala mpaka awe amesoma ‘Tabarak’ (Suratul-Mulk) na ‘Alif Lam Mim al-Tanzil’ (Surat al-Sajdah).958 5. Katika Majma’ul-Bayan: Imesimuliwa kutoka kwa Ai ibn Abi Talib (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akiipenda Surah hii – ‘Sabbihisma Rabbikal A’alaa’ (Surat al-‘A’alaa), na mtu wa kwanza kusema ‘Sabhana Rabbiyal A’alaa’ (Utukufu ni wa Mola Wangu aliye Juu) alikuwa ni malaika Mika’il (a.s.)959 Kidokezo: Kile kipande cha mwanzo (cha hadithi hii) kimesimuliwa pia katika alBihar na kutoka kwa Suyuti ndani ya Durr al-Manthur.960

954 Bihar al-Anwar 81:68 na 92:216, al-Mustadrak 1:465 955 Majma’ul-Bayan 10:378 – Surat al-Muzammil, Fayd al-Qadir 5:238 956 Ruh al-Jinan ya Abu Fattuh al-Radhi 11:30 – Surat al-Hadid (57), ad-Durr al-Manthur 6:170 – Suratal-Hadid (57), Bihar al-Anwar 92:312 957 Majma’ul-Bayan 9:229 – Suratul-Hadid (57) 958 Tumeiona rejea hii kwenye Majma’ul-Bayan 8:325 na Bihar al-Anwar 92:316 959 Majma’ul-Bayan 10:472-473 – Surat al-‘A’alaa (87) 960 Bihar al-Anwar 92:322, ad-Durr al-Manthur 6:337 178


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 179

SUNAN-NABII 6. Vilevile: Kutoka kwa Ibn Abbas: Kila wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliposoma ‘Sabbihisma Rabbikal A’alaa’ huwa angesema “Sabhana Rabbiyal A’ala.” Hii imesimuliwa pia na Imam Ali (a.s.).961 7. Katika ad-Durr al-Manthur ya Suyuti: Kutoka kwa Abi Umamah ambaye amesema: Niliswali pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) baada ya hijja yake ya mwisho na alikuwa mara kwa mara akisoma ‘La Uqsimu bi Yawmil-Qiyamah’ (Suratul-Qiyamah) na alipokuwa akisoma:

“Je, Yeye huyo hana uwezo wa kuhuisha wafu?” (75:40) nilimsikia akisema: “Ndio kwa hakika, na mimi ni shahidi juu ya hili.”962 Kidokezo: Kuna hadithi nyingine kama hii ambazo zinaashiria kwamba yeye (s.a.w.w.) alisema kitu tofauti – na kile kilichosemwa kwenye hadithi hii.963 8. Vilevile: Kutoka kwa Ibn Abbas ambaye amesema: Wakati Mtukufu Mtume alipokuwa akiisoma aya hii:

“Na kwa nafsi na kwa yule aliyeifanya iwe kamili, kisha akaifahamisha uovu wake na taqwa yake.” (91; 7-8) yeye hapo husimama na kusema: Allahuma ati nafsiy taqwaahaa wa zakihaa anta khairu man zakaahaa anta waliiyuhaa wa mawlaahaa.” “Ewe Mungu Wangu! Ipe nafsi yangu taqwa yake na uitakase, Wewe ndiye Mbora wa wale wanaoitakasa, Wewe ndiye Mola na Mlezi. Yeye akasema: Na hufanya hivi wakati akiwa ndani ya swala.964 961 Majma’ul-Bayan 10:473 – Surat al-‘A’ala (87) 962 ad-Durr al-Manthur 6:296 – Suratul-Qiyamah (75) na kutoka kwake ndani ya Bihar al-Anwar 92:219 963 Bihar al-Anwar 92:291-220 964 ad-Durr al-Manthur 6:356 – Surat al-Shams (91), Bihar al-Anwar 92:220 179


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 180

SUNAN-NABII Nyogeza kwenye sehemu hii 1. Katika al-Bihar kutoka kwenye al-Dhikra: Kutoka kwa Abi Sa’id al-Khudhri: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) huesema: “A’udhubillahi mina Shaitwanir-Rajiim.” “Najikinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani aliyelaaniwa” – kabla ya kusoma Qur’ani tukufu.965 2. Katika Tafsiir al-Ayyashi: Kutoka kwa Zayd ibn Ali, kutoka kwa Abi Ja’far (a.s.) ambaye amesema kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliisoma Qur’ani kwa sauti nzuri zaidi kati ya watu wote.966 3. Katika al-Da’awat al-Rawandi: Kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye amesema: Jibril aliniambia nisome Qur’ani wakati nikiwa nimesimama.967 4. Katika al-Majma’ul-Bayan: Kutoka kwa Anas ambaye alisema: Yeye Mtume (s.a.w.w.) angevuta sauti yake wakati akisoma Qur’ani tukufu.968 5. Katika al-Kafi: Kutoka kwa Abdullah ibn Farqad na al-Mu’alla ibn al-Khunays, kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: “Na kuhusu sisi, tunaisoma Qur’ani kulingana na usomaji wa Ubay.”969 Kidokezo: Kuna hadithi nyingine zinazoashiria uruhusiwaji wa kusoma kwa mujibu wa visomo vya wale wasomaji wengine saba wanaojulikana, kama ilivyoelezwa ndani ya al-Khisal.970 6. Katika Majma’ul-Bayan kwenye sherhe ya Suratut-Tiin, kutoka kwa Muqatil: Qatadah amesema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipomaliza Surah, huwa angesema: “Hakika ndivyo, na mimi ni shahidi juu ya hili.”971 965 Bihar al-Anwar 85:5 966 Tafsir al-Ayyashi 2:295 –Surat al-Isra’ (17), Bihar al-Anwar 92:326, Tafsir Furat alKufi: 85 na kutoka kwake ndani ya al-Mustadrak 4:185 967 al-Da’awat al-Rawandi 47 na kutoka kwake ndani ya al-Mustadrak 4:427 968 Majma’ul-Bayan 10:378 – Surat al-Muzammil. 969 al-Kafi 2:634 970 al-Khisal: 358 971 Majma’ul-Bayan 10:512 180


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 181

SUNAN-NABII 7. Katika Durr al-Manthur: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipoisoma aya ya: “Je huyo hana uwezo wa kuhuisha wafu?” (75:40) yeye Mtume angesema:“Subhaanaka Allahumma balaa.” – Utukufu ni Wako Mwenyezi Mungu, hakika ndivyo.972 Kidokezo: Hii imesimuliwa na Sheikh at-Tusi katika Sharh yake at-Tibyan, kutoka kwa Abi Ja’far na Abi Abdillah (a.s.).973 8. Katika Majma’ul-Bayan, katika sherehe juu ya aya:

“Na hushughuliki na jambo lolote, wala husomi humo katika Qur’ani, wala hamfanyi kitendo chochote, isipokuwa sisi tunakuwa mashahidi juu yenu mnapoingia-kwenye hicho kitendo-. Wala haufichiki mbali na Mola wako uzito wa chembe ardhini au mbinguni, wala kidogo kuliko hicho wala kikubwa, isipokuwa kimo katika Kitabu kilicho bayana.” (Yunus;10:61). Alisema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipoisoma aya hii alilia daima.974 9. Katika Majma’ul-Bayan, chini ya maelezo ya Suratul-Ikhlas: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa yu asimama mwisho wa kila aya ya Surah hii.975 10. Katika ad-Durr al-Manthur: Kutoka kwa Ahmad, ibn al-Dhariis na al-Bayhaqi kutoka kwa Ayisha ambaye amesema: Ningeweza kuamka usiku pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na yeye angesoma kutoka Suratul-Baqarah, Aali Imran na an-Nisa na wakati alipoifikia aya yenye kutoa habari njema (kwa waumini) yeye angeomba dua na kuweka matumaini, na alipoifikia aya yenye kuwatishia waumini, yeye angeomba dua na kutafuta hifadhi.976 972 ad-Durr al-Manthur 6:296 – Suratul-Qiyamah (75) na kutoka kwake ndani ya Bihar al-Anwar 92:219 973 at-Tibyan 10:203 –Suratul-Qiyamah (75). 974Majma’ul-Bayan 5:116 – Surat Yunus (10) 975 Majma’ul-Bayan 10:567 – Suratul-Ikhlas (112) 976 ad-Durr al-Manthur 1:18 – Suratul-Baqarah (2) 181


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 182

SUNAN-NABII 11. Katika Thawab al-Amal ndani ya simulizi kutoka kwa Husayn ibn Abi al-Ula’ kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Yeyote mwenye kusoma SuratutTalaq na at-Tahrim katika swala zake za wajib yeye atalindwa na Mwenyezi Mungu kutokana na kuwa miongoni mwa wale ambao wana hofu na huzuni katika Siku ya Kiyama, ataokolewa na Moto wa Jahhannam na Mwenyezi Mungu atamuingiza Peponi kwa sababu ya kisomo cha Surah hizi mbili na kule kuzishughulikia kwake; kwa sababu Surah hizi ni kwa ajili ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).977 12. Katika al-Mizan kutoka kwenye ad-Durr al-Manthur: Kutoka kwa Ibn Abbas ambaye amesema: Wakati Qur’ani iliposhushwa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), yeye angeharakisha katika kuisoma ili kuihifadhi, hivyo ile aya:

“Usiutikise ulimi wako ili uharakie kuisoma. (Suratul-Qiyamah 75:16) ndipo ikashushwa.978 13. Vilevile: Baada ya hii, wakati wowote Jibril alipokuja kwa Mtukufu Mtume, yeye (s.a.w.w.) angeisoma aya kama ilivyoteremshwa kwake na Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla.979 14. Vilevile: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) asingejua mwisho wa Surah mpaka iliposhushwa kwake ‘Bismillahi Rahmanir-Rahim.’980 15. Katika Tafsir al-Qummi: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angekaa chumbani kwake na kusoma Qur’ani tukufu.981

977 Thawab al-Amal: 146 978ad-Durr al-Manthur 6:289 – Suratul-Qiyamah; 75:16, al-Mizan 20:116 – SuratulWaqi’ah (56) 979 Ibid. 980 Ibid. 981 Tafsir al-Qummi 2:393 – Surat al-Mudathir (74), Bihar al-Anwar 9:245

182


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 183

SUNAN-NABII

MLANGO WA 21 MAOMBI (DU’A) NA ADABU ZAKE 1. Kutoka kwa al-Qutbi ndani ya al-Da’awat: Kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye amesema: Jibril amenielekeza kusoma Qur’ani wakati nikiwa nimesimama, na kumtukuza Mwenyezi Mungu katika hali ya rukuu, na kumsifu na kumshukuru nikiwa katika Sajidah na kumuomba Yeye nikiwa katika hali ya kukaa.982 2. Kutoka kwa Ahmad ibn al-Fahd katika ‘Uddat al-Da’i: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angenyoosha mikono yake wakati alipokuwa akiomba na kusihi kwa Mwenyezi Mungu kama vile tu anavyofanya ombaomba anapoomba chakula.983 Kidokezo: Hii imesimuliwa pia na Sheikh at-Tusi katika al-Majalis na al-Akhbar kutoka kwa Muhammad na Zayd – wale watoto wawili wa Ali ibn al-Husein (a.s.), kutoka kwa baba yao kutoka kwa Husein (a.s.).984

DU’A YAKE WAKATI ALIPOANGALIA KWENYE KIOO 3. Katika al-Ja’fariyat: Katika riwaya yake kutoka kwa Ja’far ibn Muhammad kutoka kwa baba zake kutoka kwa Ali (a.s.) kwamba wakati wowote Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipoangalia kwenye kioo, yeye alisema: “Alhamdulillahi al-Ladhii akmala khalqiy, wa ahsana suuratiy, wa zaana minniy maashaana min ghairiy, wahadaaniy lil-Islaami wa munna ‘alaiya bin-Nubuuwati.” “Utukufu na shukurani ni zake Allah ambaye ameniumba mimi kikamilifu, na akalifanya umbo langu kuwa zuri, na akakipamba kutokana nami kile ambacho alikifanya kiwe kibaya kwa wengine, na akaniongoza kwenye Uislam, na akanineemesha na Unabii.”985 982 al-Da’awat: 47, al-Mustadrak 4:427 983 Uddat al-Da’i: 196 984Amali al-Tusi 2:198 (hapa haikusimuliwa kutoka kwa Husein a.s.), Makarim al-Akhlaq: 267, Majmu’at Warram: 320 985 al-Ja’fariyat: 186 183


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 184

SUNAN-NABII 4. Kutoka kwa Sheikh Abi al-Futtuh ndani ya Tafsir yake: Kutoka kwa as-Sadiq (a.s.) ambaye amesema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipoangalia kwenye kioo alisema: “Alhamdulillah al-Ladhii ahsana khalqiy wa khulqiy, wa zaana minniy maa shaana min ghairiy.” “Shukrani zote ni zake Allah ‘Azza wa Jalla. aliyefanya uzuri umbo langu, na hulka yangu, na akakipamba kutokana na mimi kile alichokifanya kiwe kibaya kwa wengine.”986

DU’A YAKE ANAPOKUWA JUU YA KIPANDO CHAKE 5. Katika Awali al-La’ali: Kuhusu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba: Wakati wowote alipokaa juu ya kipando chake alivyokuwa akiondoka kwenda safari, angesoma takbir mara tatu kisha akasema: “Subhaana al-ladhiy sakhara lana haadha wamaa kuna lahu muqriniina, wa inna ilaa rabina lamunqalibuuna. Allahuma inna nas’aluka fiy safarinaa hadhaa al-birra wa taqwaa wa minal-amali maa tardwaa. Allahuma hawwin alaynaa safaranaa wa atwwi ‘anaa bu’udahu. Allahuma anta swaahibu fiy as-safari wal khaliifatu fiy al-ahli. Allahuma inniy a’udhubika min wa’athaai as-safari wa kaabati almunqalabi wasuuil-mandhari fiy al-ahli wal-maali.” “Sifa njema ziwe kwa Mwenyezi Mungu ambaye amemfanya (mnyama) huyu kuwa mtiifu kwetu na sisi tusingeweza kumfanya hivyo wenyewe na hakika kwa Mola Wetu tutarejea. Ewe Mungu! Tunakuomba kwamba safari hii iandamane na wema na uchamungu na pamoja na vitendo ambavyo vinakupendeza Wewe. Ewe Mungu! Ifanye safari hii kuwa nyepesi kwetu na tufupishiye umbali wake. Ewe Mungu! Wewe ndiwe Mwenza katika safari na Mlinzi juu ya familia. Ewe Mungu! Naomba ulinzi Kwako kutokana na matatizo ya safari hii na kutokana na uzito wa moyo wa kuwa katika mahali tofauti na kutokana na kushuhudia jambo lolote baya katika familia na mali.”

986 Tafsir Ruh al-Jinan 1:36, naye an-Nuri ameisimulia hii katika al-Mustadrak 5:307 184


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 185

SUNAN-NABII Na alipokuwa anarejea, yeye alisema: “Aaibuuna taaibuuna ‘aabiduuna lirabbinaa haamiduuna.” – “Tunarejea (nyumbani tukiwa) wenye kutubia, wenye kuabudu na wenye kumtukuza Mola Wetu.”987

DU’A YAKE WAKATI WA USIKU ANAPOSAFIRI 6. Katika al-Awali: Kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): Wakati alipokuwa anasafiri na usiku ukaingia, yeye alisema: “Ardhu rabbiy wa rabbuki-llahu. A’udhu min sharriki wa sharri maa fiyki wa sharri maa yadubu ‘alayki wa a’udhu billahi min asadin wa as’wadin wa minal-hayatin wal’aqrabi wa min saakini al-baladi wa waalidi wa maa walada.” “Ewe ardhi! Mola Wangu na Mola Wako ni Allah ‘Azza wa Jalla. Najikinga na shari za maovu yako na maovu ya kile kinachoishi juu yako, na shari ya kile kinachotembea juu yako. Na najikinga kwa Mwenyezi Mungu na kila mnyama muwindaji aliyejificha na kutokana na nyoka na nge na kutokana na wakazi wa mahali hapa – wao wenyewe na watoto wao.”988

DU’A YAKE ALIPOVAA NGUO MPYA 7. Katika al-Makarim: Kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba wakati alipokuwa anavaa nguo mpya yeye alisema: “Alhamdu-lillahi al-ladhiy kasaaniy maa yuwaariy ‘auratiy wa atajammalu bihi fiy an-naasi.” “Sifa njema ni Zake Allah ‘Azza wa Jalla. ambaye amenivisha mimi na kile kinachofunika hali ya utupu wangu na kile ambacho ninajipamba nacho mwenyewe miongoni mwa watu.”989

987 Awali al-La’ali 1:145, al-Mustadrak 8:137, Majma’ul-Bayan 9:41 – SuratulZukhruf, Bihar al-Anwar 76:293 988 al-Awali al-La’ali 1:156 989 Makarim al-Akhlaq: 36, Da’aim al-Islam 2:157, Kashf al-Ghummah 1:164 185


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 186

SUNAN-NABII Kidokezo: Mufid al-Din at-Tusi amesimulia kitu kama hiki ndani ya al-Amali kutoka kwa Abi Matar, na kadhalika imesimuliwa ndani ya al-Bihar (kwa kunukuu) kutoka kwenye al-Manaqib kutoka kwa Abi Matar.990 8. Vilevile: Wakati yeye (s.a.w.w.) alipokuwa akivua nguo zake, angezivua kutoka upande wake wa kushoto kwanza; na ulikuwa ni mwenendo wake kwamba alipokuwa anavaa nguo mpya angemshukuru Mwenyezi Mungu na kisha akamuita masikini muombaji ili kumpa zile nguo zake za zamani. Halafu angesema: “Hakuna Mwislam anayemvisha muhitaji Mwislam kwa nguo zake chakavu – na hakuna anayemvisha yeye isipokuwa Allah ‘Azza wa Jalla – bali kwamba yeye anakuwa chini ya ulezi, ulinzi na rehema za Mwenyezi Mungu muda wote nguo hizo zikiwa kwenye mwili wa huyo mhitaji, awe mtoaji yuko hai ama amekwishafariki.”991 9. Vilevile: Wakati wowote yeye (s.a.w.w.) alipovaa nguo mpya na akasimama, na akawa yuko karibu kuondoka (nyumbani kwake), yeye alisema: “Allahumma bika istatartu wa ilayka tawajahtu wa bika‘I’itaswamtu wa alayka tawakaltu. Allahumma anta thiqatiy wa anta rajaaiy. Allahumma akfiniy maa ahammaniy wa maa laa ahtammu bihi wa maa anta a’alamu bihi minnniy ‘azza jaaruka wajalan thanaauka wa laa ilaaha ghayiruka. Allahumma zawwidniy at-taqwaa waghfir liy dhanbiy wawajjihniy lil-khayiri haythu maa tawajahtu.” “Ee Mungu wangu! Kwa Wewe nimejisitiri na Kwako Wewe nimeelekea na kwako nimejihifadhi na kwako nimetegemea. Ewe Allah Wewe ndio tegemeo langu na Wewe ndio tarajio langu. Ee Mungu! Nitosheleze ambalo lenye umuhimu kwangu na lile ambalo silitilii umuhimu na lile ambalo Wewe walijua mno kuliko mimi.Amekuwa na enzi mwenye kuwa karibu na Wewe, na umetukuka utukufu Wako wala hapana mungu ghairi Yako. Ee Mungu! Nipe taqwa na unisamehe dhambi zangu na unielekeze kwenye wema kila nitakakoelekea.” Halafu angeendelea na kile alichotaka kukifanya.992

990 Amali al-Tusi 1:398, Bihar al-Anwar 16:251 991 Makarim al-Akhlaq: 36 992 Ibid. 186


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 187

SUNAN-NABII

DU’A YAKE ALIPOSIMAMA KUTOKA PALE ALIPOKUWA AMEKAA 10. Kutoka kwa al-Ghazali ndani ya al-Ihya’: Pale ambapo yeye (s.a.w.w.) husimama kutoka pale alipokuwa amekaa na husema: “Subhaanaka Allahumma wabihamdika ash’hadu anlaa ilaha ila anta, ‘astaghfiruka wa atuubu ilayka.” “Sifa ziwe juu Yako Ewe Mungu! na kwa utukufu Wako! Nashuhudia kuwa hapana mungu ila ni Wewe. Naomba msamaha Kwako na ninatubu Kwako.”993

DU’A YAKE ANAPOINGIA NA KUTOKA MSIKITINI 11. Kutoka kwa Sheikh at-Tusi ndani ya al-Majalis: Imesimuliwa kutoka kwa Abdillah ibn al-Hasan kutoka kwa mama yake, Fatimah bint al-Husein kutoka kwa baba yake kutoka kwa Ali (a.s.): Kila wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aingiapo msikitini husema: “Allahumma iftahliy abuwaaba rahmatika.” “Ewe Allah! Nifungulie milango ya neema zako.” Na alipokuwa akitoka msikitini alikuwa akisema: “Allahumma iftahliy abuwaaba rizqika.” “Ewe Allah! Nifungulie milango ya riziki Yako.” 12. Kutoka kwa at-Tabari ndani ya al-Imamah: Imesimuliwa kutoka kwa Abdillah ibn al-Hasan kutoka kwa Fatimah as-Sughra, kutoka kwa baba yake, al-Husein, kutoka kwa Fatimah al-Kubra bint Rasulillah amani iwe juu yao wote: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipoingia msikitini, yeye huwa anasema: 993 Ihya’ ‘Ulum al-Din 2:367

187


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 188

SUNAN-NABII “Bismillahi, Allahumma swali ‘alaa Muhammadin wa aali Muhammad waghfirliy dhunuubiy waftahliy abuwaaba rahmatika. “Kwa jina la Allah, Ee Mungu! Mpe rehma na amani Muhammad na kizazi cha Muhammad na unisamehe dhambi zangu na unifungulie milango ya rehma Zako.” Na wakati alipokuwa akitoka nje alikuwa akisema: “Bismillahi, Allahumma swali ‘alaa Muhammadin wa aali Muhammad waghfirliy dhunuubiy waftah’liy abuwaaba fadhiilika.” “Kwa jina la Allah, Ee Mungu! Mpe rehma na amani Muhammad na kizazi cha Muhammad na unisamehe dhambi zangu na unifungulie milango ya fadhila Zako.” 994

DU’A YAKE WAKATI ALIPOKUWA AKIENDA KITANDANI KWAKE 13. Katika al-Makarim: Wakati yeye (s.a.w.w.) alipokuwa akipanda kitandani kwake, yeye alikuwa akilalia upande wake wa kulia na kuweka mkono wake wa kulia chini ya shavu lake la kulia, halafu husema: “Allahumma qiniy ‘adhaabaka yawma tab’athu ‘ibaadaka.” “Ewe Mola wangu! Niepushe na adhabu Yako siku ile ambayo utakayowafufua waja Wako.”995 14. Vilevile: Yeye (s.a.w.w.) alikuwa na aina tofauti za dua ambazo angezisoma wakati alipopanda kitandani kulala … na wakati alipokaribia kupatwa na usingizi angesema: “Bismillah amuutu wa ahyaa wa ila llahil-maswiiru. Allahumma amin raw‘atiy wa astur ‘auratiy wa adi ‘aniy amaanatiy. “Kwa jina la Allah mimi ninafariki na kuishi na kwa Allah ndio marejeo. Ee Mungu Wangu! Niondoshee hofu yangu na unifichie makosa yangu na (nisaidie) nirudishe kile kilichowekwa amana kwangu.”996 994 Dala’il al-Imamah: 7, Bihar al-Anwar 83:23, al-Mustadrak 3:394 995 Makarim al-Akhalq: 38, al-Mustadrak 5:36 996 al-Makarim al-Aklaq: 38 188


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 189

SUNAN-NABII 15. Vilevile: Yeye (s.a.w.w.) alikuwa akitumia kusoma Ayat al-Kursi kabla ya kulala, akisema: Jibril (a.s.) alinijia na kusema: “Ewe Muhammad! Hakika kuna jinni muovu ambaye anakudanganya katika usingizi wako hivyo ni lazima usome ayat al-Kursi (ili kufukuza uovu wake huo).”997

DU’A YAKE WAKATI KITANGA CHA CHAKULA KILIPOTANDIKWA 16. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Ahmad ibn al-Hasan al-Maythami ambaye ameihusisha kwa Ma’sum mmojawapo; yeye alisema: Wakati kitambaa cha meza kilipotandikwa mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) yeye alisema: “Subhaanaka Allahumma maa ahsana maa tabtaliynaa, Subhaanaka maa akthara maa tu‘utwiinaa, Subhaanaka maa akthara maa tu‘aafiynaa. Allahumma awsi‘i ‘alaynna wa ‘alaa fuqaraail-mu’uminiina walmu’uminaati wal-muslimiina wal-muslimaati.” “Kutakasika ni Kwako Ewe Allah! Ni uzuri ulioje wa kile ulichotujaribu nacho. Kutakasika ni kwako Ewe Mola, ni cha wingi kiasi gani kile ulichotupatia sisi. Kutakasika ni kwako Ewe Mola, ni wingi kiasi gani wa kile ulichotujaalia nacho juu yetu. Ewe Mola! Tuzidishie sisi riziki zetu na juu ya wale waumini masikini wanaume kwa wanawake na waumini na juu ya waislam wanaume kwa wanawake.998 17. Katika al-Makarim: Wakati kitambaa cha meza (ya chakula) kilipotandikwa mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) yeye alisema: “Bismillahi. Allahumma aj‘alhaa ni’matan mashkuuratan taswilu bihaa ni’matan al-Jannati.” “Kwa jina la Allah. Ewe Mola! Ijaalie iwe ni neema yenye kushukuriwa kwa njia ambayo fadhila zako za peponi zinavyopatikana.”999

997 Makarim al-Akhlaq: 38, al-Kafi 2:536 998 al-Kafi 6:293 999 Makarim al-Akhlaq: 27 189


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 190

SUNAN-NABII

DU’A YAKE WAKATI ALIPOKIGUSA CHAKULA 18. Katika al-Makarim: Wakati yeye (s.a.w.w.) alipoweka mkono wake kwenye chakula alisema: “Bismillah, baarik lanaa fiymaa razaqtanaa wa’alayka khalfahu.” “Kwa jina la Allah! Ewe Allah kibariki kwa ajili yetu kile ulichotupa sisi miongoni mwa riziki na kwako Wewe tunatarajia kwa ajili ya kutujazia tena.”1000

DU’A YAKE WAKATI KITANGA KILIPOONDOLEWA 19. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Ibrahim ibn Mahzam kutoka kwa mtu mmoja kutoka kwa Abi Ja’far (a.s.) ambaye amesema: Wakati kile Kitanga cha chakula kilipoondolewa, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Allahumma aktharta wa atwabta wa baarakta fa’ashba’ta wa ar’waita. Alhamduli-llahi al-ladhiy yut’imu walaa yut’ama.” “Ewe Mola! Umekithirisha na umefanya vyema na umebariki, hivo umeshibisha na kukoza kiu. Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, ambaye analisha naye halishwi.”1001

DU’A YAKE ANAPOKULA NA KUNYWA MAZIWA 20. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Abdullah ibn Suleiman kutoka kwa Abi Ja’far (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) asingekula chakula chochote wala kunywa kinywaji bali kwamba yeye angesema: 1000 Makarim al-Akhlaq: 27 na 143 1001 al-Kafi 6:294, al-Mahasin: 436 190


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 191

SUNAN-NABII “Allahumma barik-lanaa fiyhi wa abdilnaa bihi khayran minhu.” “Ewe Mungu Wangu! Kibariki kinywaji hiki juu yetu na ukibadili kwa kile kilicho bora zaidi.” isipokuwa kama akinywa maziwa, hapo angesema: “Allahumma barik-lanaa fiiyhi wazidnaa minhu.” “Ewe Mola! Yabariki haya juu yetu na uyaongeze kwa ajili yetu.”1002 Kidokezo: Hii imesimuliwa pia na yeye, vilevile na al-Barqi kwa tofauti ya nyororo ya wasimuliaji.1003 21. Katika al-Iqbal: Katika kula funda au tonge, yeye Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angesema: “Allahumma lakal-hamdu atw’amta wa asqayta warawayta. falakalhamdu ghairu makfuurin walaa muwada’in walaa mustaghnaa ‘anka.” “Ewe Mola Wangu! Sifa zote njema ni Zako. Wewe umelisha na kunywesha. Hivyo sifa njema ni zako Hukufuriwi– kuto shukuriwa-, na huachwi wala kujitosheleza bila ya Wewe.”1004

DU’A YAKE WAKATI ALIPOONA MATUNDA SAFI (YALIYOIVA) 22. Kutoka kwa al-Saduq ndani ya al-Majalis: Imesimuliwa kutoka kwa Wahab kutoka kwa Ja’far ibn Muhammad kutoka kwa baba zake kutoka kwa Imam Ali (a.s.) ambaye amesema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipoona tunda lililowiva, yeye angelibusu na kuliweka machoni mwake na mdomoni, halafu angesema: “Allahumma kamaa araayitanaa awwalahaa fiy ‘aafiytin faarinaa akhirahaa fiy ‘aafiytin.” “Ewe Allah! Kama vile ulivyotuonyesha sisi mwanzo wake katika afya njema, basi tuonyeshe mwisho wake katika afya njema.”1005 1002 al-Kafi 6:336, Uyun al-Akhbar al-Ridhaa 2:38 1003 al-Mahasin: 437 1004Iqbal al-Amal: 116 1005 Amali al-Saduq: 219 191


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 192

SUNAN-NABII Kidokezo: at-Tabarsi ameisimulia hii katika al-Makarim bila (yale maneno) ‘na mdomo wake’ na pia katika kitabu cha Ma’adh al-Jawhari, imesimuliwa kutoka kwa Ibn Umayr kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.), humo mna hadithi kama hiyo lakini bila ya maneno ya mwanzo ‘katika afya njema.’1006

DU’A YAKE WAKATI ANAPOINGIA BAFUNI 23. Katika al-Faqih: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipotaka kuingia bafuni alisema: “Allahumma inniy a’udhubika minal-rijsi an-najisil-khabiythi almukhbathi ashaitwaani, Allahumma amtwi ‘anniy al-adhaa wa a’izaniy mina shaitwaani rajiimi.” “Ewe Mungu! Najikinga kwako kutokana na uchafu wa najisi ya uovu wa shetani aliyelaaniwa. Ewe Mungu! Niondolee kila uchafu na unilinde kutokana na shetani aliyelaaniwa.” Na pale alipochuchumaa ili kujisaidia, yeye alisema: “Allahumma adh’hib ‘anniy al-kadhaa wal-adhaa, waj’alniy mina almutatwahiriina.” “Ewe Allah! Niondolee mimi uchafu na najisi na unifanye niwe miongoni mwa wale wanaojitoharisha.” Na anaposhikwa na tumbo la kuendesha yeye alisema: “Allahumma kamaa atw’amtaniyhi twayyibaan fiy ‘aafiyatin fa akhrijhu minniy khabiythan fiy ‘aafiyatihi.” “Ewe Allah! Kama vile tu ulivyonilisha mimi kwa ubora wake katika afya njema, basi uondoe uchafu wake mwilini mwangu kwa hali njema.” Na wakati yeye (s.a.w.w.) alipokuwa akiingia chooni angesema: “Alhamdulillahi al-haafidwi al-muwadiy.” 1006 Makarim al-Akhlaq: 170 192


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 193

SUNAN-NABII “Sifa njema zote ni zake Allah, Mlinzi na Mtimizaji (wa haja).” Wakati alipokuwa akitoka chooni yeye alipitisha mkono wake juu ya tumbo lake na akasema: “Alhamdulillahi al-ladhiy akhraja ‘aniy adhaahu wa anqiy fiyya quwwatahu, fayaalahaa min ni’imatin laa yuqadiru al-qaadiruuna qadrahaa.” “Sifa zote ni zake Allah, wa pekee ambaye ameniondolea mimi uchafu wake (tumbo) na kuniachia nguvu zake. Ni neema kubwa iliyoje – ambayo thamani yake halisi haiwezi kukadiriwa kikamilifu na yeyote.” 1007

DU’A YAKE WAKATI ALIPOYAPITA MAKABURI 24. Kutoka kwa Ibn Qulawayh ndani ya al-Kamil: Katika riwaya yake kutoka kwa Muhammad ibn Muslim kutoka kwa Abi Ja’far (a.s.) ambaye amesema: Nilimsikia yeye akisema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipopita karibu na makaburi ya kikundi cha waumini alisema: “As-salaamu ‘alaykum min diyaari qaumin mu’miniina wa innaa insha’allah bikum laahiquuna.” “Amani iwe juu yenu kutoka kwenye makazi ya jamii ya waumini na tutajiunga nanyi - Mungu akipenda.”1008

DU’A YAKE WAKATI ALIPOTEMBELEA MAKABURI 25. Kutoka kwa Ibn Qulawayh katika al-Kamil: Katika riwaya yake kutoka kwa Safwan al-Jammal ambaye amesema: Nilimsikia Abi Abdillah (a.s.) akisema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akitumia kuondoka kwa watu pamoja na baadhi ya masahaba zake kila Alhamisi jioni na kwenda kwenye makaburi ya Baqi huko Madina na kusema mara tatu:

1007 al-Faqih 1:23 na 25 1008 Kamil al-Ziyarat: 322, al-Faqih 1:179 193


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 194

SUNAN-NABII “As-salaam ‘alaykum yaa ahli-diyaari. “Amani iwe juu yenu enyi watu wa makazi haya” – mara tatu “Rahimakumu-llahu.” “Mwenyezi Mungu akurehemuni.”1009

DU’A YAKE WAKATI ANAPOFIKWA NA JAMBO LA KUFURAHISHA AU LA KUHUZUNISHA 26. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Muhammad ibn Hannat kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Wakati jambo la kufurahisha lilipomfika Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), yeye angesema: “Alhamdulillahi ‘alaa hadhihi an-ni’matin.” “Shukurani kwa Mwenyezi Mungu juu ya neema hii.” Na jambo la kuhuzunisha lilipomfika, yeye angesema: “Alhamdulillahi ‘alaa kuli haalin.” “Mwenyezi Mungu ashukuriwe katika kila hali.”

DU’A YAKE WAKATI ALIPOKIONA KITU ANACHOKIPENDA 27. Katika al-Makarim: Kutoka kwa Amirul-Mu’minin Ali (a.s.) ambaye amesema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokiona alichokipenda, yeye alisema: “Alhamdulillahi al-ladhiy bini’matihi tatimmu swaalihaatu.” “Sifa njema ni za Mwenyezi Mungu ambaye anatimiza (na kukamilisha) yote yale ambayo ni mema kwa neema Zake.”1010 1009al-Kafi 2:97, habari inayofanana na hii imesimuliwa katika al-Amali at-Tusi 1:49 1010 Makarim al-Akhlaq: 19

194


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 195

SUNAN-NABII Kidokezo: Hii imetajwa pia na Sheikh at-Tusi ndani ya al-Amali – ikisimuliwa na al-Farra’ kutoka kwa ar-Ridha kutoka kwa baba zake kutoka kwa Ali (a.s.).1011

DHIKIRI YAKE WAKATI ALIPOSIKIA ADHANA 28. Katika al-Da’aim: Imesimuliwa kwetu kutoka kwa Ali ibn al-Husayn (a.s.) kwamba wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliposikia adhana, yeye angekariri kile mwadhini alichokisema, na alipofikia kusema: “Hayya ‘alaa swalati, hayya ‘alaal-falaahi, hayya ‘alaa khayrilamali.” “Harakisha kwenye swala, harakisha kwenye mafanikio, harakisha kwenye matendo mema,” yeye angesema: “Laa haula wa laa quwwata ila billahi.” “Hakuna hila wala nguvu ila kwa (mapenzi ya) Mwenyezi Mungu.” Na wakati pale mwenye kuadhini alipomaliza adhana, yeye alisema: “Allahumma raba haadhihi da’awatit-taamati wa swalaatil-qaaimati a‘ati Muhammadan su’ulahu yawmal-Qiyaamati wa baligh’hu darajatal-wasiylati minal-jannati wa taqabal shafaa’atahu fiy ummatihi.” “Ewe Mungu Wangu! Mola wa wito huu mkamilifu na swala iliyosimama, mtimizie Muhammad maombi yake katika Siku ya Kiyama, na umfikishie daraja ya kuwa kiungo cha kufikia peponi na umtakabalie uombezi wake kwa ajili ya umati wake.”1012

DHIKIRI YAKE MWISHONI MWA SWALA YA MAGHARIBI 29. Katika al-Ja’fariyat: Ndani ya simulizi yake kutoka kwa Ja’far ibn Muhammad kutoka kwa baba zake kutoka kwa Ali (a.s.) kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alizoea kusoma (yafuatayo) katika rakaa ya tatu ya swala ya Magharibi: 1011 al-Amali at-Tusi 1:49 1012 Da’aim al-Islam 1:145, Fayd al-Qadir 5:145

195


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 196

SUNAN-NABII “Rabbanaa laa tuzigh quluubanaa ba’ada idh’hadaytanaa wa hablanaa min la dunka rahmatan innaka antal-wahhaabu.” “Ewe Mola Wetu! Usiziachie nyoyo zetu zipotoke baada ya Wewe kuwa umetuongoza na utupe rehema kutoka kwako, hakika Wewe ndiye Mpaji wa yote.”1013

DHIKRI NA DU’A YAKE KATIKA QUNUTI YA SWALA YA WITRI 30. Katika al-Faqih: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akitumia kuomba maghfira mara sabini ndani ya swala ya Witri na kisha akasema kwa mara sabini: “Haadha maqaamu al-‘aidhibika minan-naari.” “Hapa ndipo mahali pa yule mwenye kuomba ulinzi Kwako dhidi ya Moto wa Jahannam.” 1014 31. Vilevile: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akisema yafuatayo katika Qunuti ya swala ya Witri: “Alahumma ihdiniy fiyman hadayta, wa ‘aafiniy fiiyman ‘aafayita watawallaniy fiyman tawalayta, wabarikliy fiyman a‘atwaita, waqiniy sharra maa qadhwaita innaka taqdhwiy wa laa yuq’lwa ‘alayka subhaanaka rabbal-bayti astaghfiruka wa atuubu ilayka wa uumin bika wa tawakalu ‘alayka wa laa hawla wa laa quwwata ilaa bika yaa rahiymi.” “Ewe Mungu! Niongoze kama wale ambao umewongoza, na unijaalie afya njema kama wale uliowapa afya njema, na unitengenezee mambo yangu kama wale ambao umewatengenezea mambo yao, na unibariki katika kile ulichotoa, na unilinde dhidi ya shari ya kile ulichohukumia, hakika Wewe unahukumu wala hauhukumiwi. Utukufu ni Wako Ewe Mola wa Nyumba hii! Naomba msamaha kutoka Kwako na ninatubu Kwako, na ninaomba hifadhi Kwako na kukutegemea Wewe, na hapana uwezo wala nguvu bali kwa utashi Wako, Ewe Mwingi wa rehema!”1015 1013 al-Ja’fariyat: 41, Surat al-Imran; 3:8 1014al-Faqih 1:489, Tafsiir al-Ayyashi 1:165 – Surat al-Imran (3) 1015 al-Faqih 1:487, Bihar al-Anwar 87:205 196


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 197

SUNAN-NABII DU’A YAKE WAKATI ANAPOFUTURU 32. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa al-Sakuni kutoka Ja’far kutoka kwa mababu zake (a.s.): Wakati wowote Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipovunja saumu yake kwa kufuturu, yeye angesema: “Allahumma laka swumnaa wa ‘alaa rizqika aftwarnaa, fataqabalhu minaa, dhahaba al-dhwamau wa abtalati al-‘uruuqu wa baqiyal-ajru.” “Ewe Mola Wangu! Kwa ajili Yako sisi tumefunga, na kwa riziki Yako tumefuturu kuvunja saumu zetu, hivyo utukubalie hayo kutoka kwetu. Kiu zimetutoka na mifereji ya chakula imejaa na zimebakia (tu) thawabu (kwa ajili ya funga hiyo.”1016 Kidokezo: Kuna hadithi nyingi sana ambazo zinafanana na hii.1017

DU’A YAKE BAADA YA KUSWALI 33. Katika Majmu’at al-Shahiid, ikinukuu kutoka kwenye kitabu cha Fadhl ibn Muhammad al-Ash’ari: Kutoka kwa Masma’ kutoka kwa Abi Bakr al-Hadhrami kutoka kwa Abi Ja’far (a.s.) ambaye amesema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa amemaliza kusoma zile tashahudi mbili na salam, yeye angekaa chini akiwa amekunja miguu na kuweka mkono wake wa kulia kwenye paji lake la uso na halafu akasema: “Bismillahi ladhiy laa ilaha illa huwa ‘aalimul-ghaybi wa shaadati arrahmaanir-rahiimu, swali ‘alaa Muhammadin wa aali Muhammad wa adh’hib ‘aniy al-hamma wal-huzna.” “Kwa jina la Allah, hapana mungu ila Yeye, Mjuzi wa yaliyo ghaibu na ya dhahiri Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu. Ee Allah! Rehma na amani Yako iwe juu ya Muhammad na kizazi cha Muhammad na uniondolee mimi dhiki na huzuni zote.”1018 1016 al-Kafi 4:95, Tahdhib al-Ahkam 4:200, al-Faqih 2:106, Makarim al-Akhlaq:27, alJa’fariyat: 60, Fayd al-Qadir 5:107 1017Rejea kwenye Wasa’il al-Shi’ah 7:106 1018 al-Nuri anainukuu hii kutoka ndani ya al-Mustadrak 5:52

197


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 198

SUNAN-NABII 34. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Muhammad ibn al-Faraj ambaye amesema: Abu Ja’far ibn ar-Ridha (a.s.) aliniandikia hivi: ….. Na wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa amemaliza swala yake, yeye angesema: “Allahumma ighfirliy maa qadamtu wa maa akhartu wa maa asrartu wamaa a’alantu, wa israafiy ‘alaa amriy (nafsiy) wa maa anta a’alamu bihi minniy. Allahumma antal-muqadimu wal-muwakhiru laa ilaha ila anta bi’ilmikal-ghaiba wa biqudratika ‘alaa al-khalqi ajma’iina maa ‘alimtal-hayaata khairan liy fa ahyi, watawafaniy idhaa ‘alimtalwafaata khairaanliy. Allahumma inniy as’aluka khashyaataka fiy assirri wal ‘alaaniyati, wa kalimatal-haqqi fiy ghalwabi wa ar-rilwaa, wal qaswda fiy faqri wal-ghinaa. Wa as’aluka naiiman layanfadu, waqurrata ‘ayini laa yanqatwi’u. wa as’aluka ridhwaa bilqadhwaai, wa barakatal-mauti ba’adal’aiishiy, wa bardal-‘ayishi ba’adal-mauti, wa ladhatan-nadhari ilaa wajhika, wa shawkaan ilaa ru’uyatika waliqaaika, min ghairi dhwarraa’a mudhwirratin wa laa fitnatin mudhwilatin. Allahumma zayyinna biziynatil’ iyimaana, waj’alnaa hudaatan muhdiyiina. Allahumma ihdinaa fiyman hadayta. Wa as’aluka shukra ni’amika, wa husna ‘aafiyatika, wa adaa’a haqika. Wa as’aluka yaa rabbi qalban saliiman, wa lisaanan swaadiqaan, wa astaghfiruka limaa ta’alamu waas’aluka khaira maa ta’alamu, wa a’udhubika min sharri maa ta’alamu, fainaka ta’alamu wa laa na’alamu, wa anta ‘alaamul-ghuyuubi. “Ee Mungu! Nisamehe mimi kwa makosa yangu ya wakati uliopita na ule ujao, yale niliyofanya kwa siri na kwa dhahiri, na ubadhilifu wangu katika mambo yangu, na yale ambayo unayatambua vema kuliko mimi mwenyewe. Ee Mungu! Wewe ni wa Mwanzo na wa Mwisho hapana mungu ila Wewe kwa Elimu Yako ya ghaibu na Uwezo Wako juu ya viumbe Wako, endapo unajua kwamba maisha ni bora kwangu mimi basi nifanye niishi na kama kifo ndio bora kwangu basi nifanye nife. Ee Mungu! Nakuomba uwezo wa kukuogopa Wewe sirini na hadharani, na kutamka yaliyo kweli kwenye hasira ama furaha, na niwe mwenye wastani katika ufukara na kwenye utajiri; na nakuomba neema ambayo haikatiki, na nuru ya macho yangu ambayo haikomi; na nakuomba unifanye niridhie na kile kilichohukumiwa, na unijaalie ile neema ya kifo baada ya uhai, na maisha mazuri baada ya kifo, na kufurahia katika kushuhudia hadhira mbele ya usoWako, na shauku ya kukuona na kukutana Nawe, bila ya mitihani migumu na matamanio yenye kupotosha. Ee Mungu! Tupambe sisi kwa mapambo ya imani na tujaalie kuwa viongozi walioongozwa vema. 198


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 199

SUNAN-NABII “Ee Mungu! Tuongoze kama wale uliowaongoza. Ewe Mungu! Nakuomba Wewe juu ya utashi wa kufuata njia iliyonyooka na kuwa imara juu yake, nakuomba unisaidie katika kukushukuru kwa neema Zako na afya njema uliyoniruzuku mimi, na kutimiza wajibu wangu Kwako. Na ninakuomba, Ewe Mola Wangu juu ya kuwa na moyo uliosalimika na ulimi mkweli, na ninaomba maghfira kwa yale unayoyajua (katika madhambi yangu), na nakuomba wema kwa yale unayoyajua (kuwa ni mema juu yangu); na najikinga Kwako juu ya uovu wa kile unachokijua, kwani kwa hakika Wewe unajua na sisi hatujui, na Wewe ni Mjuzi wa yaliyo ghaibu.” 1019

DU’A YAKE BAADA YA SUNNA YA SWALA YA AL-FAJR 35. Katika al-Ja’fariyat: Katika simulizi yake kutoka kwa Ja’far ibn Muhammad kutoka kwa baba zake kutoka kwa Ali (a.s.) kwamba wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa ameswali rakaa mbili kabla ya swala ya asubuhi, alilala chini juu ya upande wake wa kulia na kuweka mkono wake wa kulia chini ya shavu lake la kulia, kisha akasema: “Istamsaktu bi’ur’wati-llahi al-wuthqa latii laa anfiswaama lahaa, wasta’aswamtu bi habli-llahil’ matiini. A’udhu bi-llahi min fawrati alarabi wal’ajami, wa a’udhu bi-llahi min sharri shayaatwiini al-insiy wal-jinni. Tawakaltu ‘ala-llahi, twalabtu haajatiy mina-llahi, hasbiyallahu wa ni’imal-wakiylu, laa hawla walaa quwwta ila bi-llahil-‘aliyil‘adhwiimi.” “Nimeshikilia kwenye mpini wa Allah ambao hautavunjika na nimejihifadhi na kamba madhubuti ya Allah. Najikinga Kwake Allah dhidi ya hasira za waarabu na wasiokuwa waarabu, na najikinga kwa Allah dhidi ya shari ya shetani miongoni mwa watu na majinni. Natawakali kwa Allah. Naomba utimilivu wa haja zangu kutoka kwa Allah. Ananitosha mimi Allah na Yeye ndiye wakili bora, hapana hila wa nguvu ili kwa utashi wa Allah, Aliye juu –kwa daraja- na Mwenye adhwama.”1020

1019 al-Kafi 2:548, Bihar al-Anwar 86:2 1020 al-Ja’fariyat: 34, al-Mustadrak 5:106

199


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 200

SUNAN-NABII

DU’A YAKE BAADA YA SWALA YA AL-FAJR 36. Kutoka kwa al-Mufid ad-Din ndani ya al-Majalis: Imesimuliwa kutoka kwa Abi Barzah al-Aslami kutoka kwa baba yake ambaye amesema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa amekwisha kuswali al-Fajr, yeye alinyanyua sauti yake mpaka masahaba zake wangeweza kumsikia, na kusema: “Allahumma aswlih liy diiniy al-ladhii ja’altahu liy ‘ismatan. Allahumma aslih liy duniyayaal-latii ja’alta fiyhaa ma’ashiy. Allahumma aslih liy aakhiratiy al-latii ja’alta ilayhaa marja’ii. Allahumma inniy a’uudhu biridhwaaka min sakhatwika, wa a’uudhu bi’afwika min niqmatika. Allahumma inniy a’udhubika laa mani’a limaa a’atwaita walaa mu’utwiya limaa mana’ata walaa yanfa’u dhaljaddi minkal-jaddu.” “Ee Mungu! Ifanye nzuri dini yangu ambayo umeijaalia kuwa hifadhi. kwa ajili yangu (mara tatu). Ee Mungu! Ifanye nzuri akhera yangu ambayo umeijaalia kuwa marejeo yangu (mara tatu). Ee Mungu! Najikinga kwa ridhaa Yako dhidi ya ghadhabu Yako, na ninajikinga kwa msamaha Wako dhidi ya hasira Zako (mara tatu). Ee Mungu! Najikinga Kwako, hakuna awezaye kumziwia uliyempa, na hakuna awezaye kumpa uliye mnyima, na hakuna juhudi ya mtu yoyote inayoweza kumnufaisha bila Wewe.”1021 37. Kutoka kwa al-Qutb ndani ya Da’awat yake: Wakati Mtukufu Mume (s.a.w.w.) alipokuwa ameswali swala ya asubuhi alisema: “Allahumma mati’iniy bisam’iy wa baswariy waj’alhumaa waarithayni minniy wa arinaa thaariy min ‘aduwiy. “Ee Mungu! Nijaalie matumizi ya kusikia kwangu na kuona kwangu na uvijaalie viwili hivyo kubakia nami mpaka kufa kwangu na unionyeshe kuangamia kwa maadui zangu.”1022

1021Amali at-Tusi 1:158, Bihar al-Anwar 86:134 1022 al-Majilis ananukuu kutoka kwenye Bihar al-Anwar 86:130

200


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 201

SUNAN-NABII DHIKIRI YAKE BAADA YA SWALA YA AL-FAJR 38. Kutoka kwa Sayyid ibn Tawus ndani ya al-Iqbal: Imesimuliwa kutoka kwa Ja’far ibn Muhammad kutoka kwa baba yake (a.s.), ambaye amesema katika hadithi: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa amemaliza swala ya asubuhi, yeye angeendelea kuelekea Qibla mpaka kuchomoza kwa jua akimuomba Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. Wakati huu Ali ibn Abi Talib (a.s.) angekuja na kuketi nyuma yake Mtume na watu wangekuja kuomba ruhusa ya kuomba haja zao, na hiki ndio Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alichowaelekeza kufanya:1023

DU’A YAKE BAADA YA SWALA YA DHUHRI 39. Kutoka kwa Sayyid Ibn Tawus katika al-Iqbal: Imesimuliwa kutoka kwa alHadi kutoka kwa baba zake kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) kutoka kwa AmirulMu’minin (a.s.) kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): Kutoka miongoni mwa maombi yake baada ya swala ya adhuhuri ilikuwa ni hii: “La ilaha ila-llahu al-‘adhwiimul-‘al’haliimu, laa ilaha ila-llahu rabbul-‘arshil‘adhwiimi, wal-hamdulillah rabbil-‘aalamiina. Allahumma inniy as’aluka muujibati rahmatika wa’azaaima maghfiratika wal-ghaniimata min kuli khairi wa salaamata min kuli ithmin. Allahumma laa tada’aliy dhanban ilaa ghafartahu, walaa hamman ilaa farrajtahu, walaa karban ilaa kashaftahu, walaa suquman ilaa shafaytahu, walaa ‘aiban ilaa satartahu, walaa rizqan ilaa basat’tahu, walaa khawfan ilaa amantahu (walaa dhanban ilaa qadhwaitahu) walaa suu’an ilaa swaraftahu, walaa haajatan hiya laka ridhwaan waliy fiyhaa swalaahu ilaa qadhwaitahaa, yaa arhamar-raahimiina, aamina rabbil-‘aalamiina.” “Hapana mungu ila Allah Mtukufu Mpole. Hapana mungu ila Allah, Mola wa Arshi adhiimu. Na sifa zote ni za Allah, Mola wa ulimwengu wote. Ee Mungu! Nakuomba yale yote yanayowajibisha Rehma Zako, na yale yanayolazimu maghfira Yako; na uninufaishe kwa kila wema na kusalimika kwa kila dhambi. Ewe Mungu! Usiniacha na dhambi yoyote ila uwe umenisamehe, wala hangaiko ila uwe umeniondolea, wala maradhi yoyote ila niponye, wala aibu yoyote ile ila unisitiri, wala riziki yoyote ila uniongezee, wala hofu yoyote ila unipe amani mbali nayo, wala uovu wowote ila uniepushe nao, na haja yoyote ambayo wairidhia na ni njema kwangu niqidhiye; Ewe Mwingi wa Rehma! Nikubalie maombi yangu, iwe Ee we Mola wa Ulimwengu.” 1024 1023 Iqbal al-A‘mal: 320, Bihar al-Anwar 35:289 1024 Hii hatukuikuta kwenye Iqbal bali imesimuliwa ndani ya Falah al-Sa’il: 171, alMustadrak 5:94 201


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 202

SUNAN-NABII

DU’A YAKE KATIKA SIJDAH 40. Katika al-Bihar: Imesimuliea kutoka kwa Abdillah ibn Sinan kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema kwamba wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipoweka uso wake kwenye ardhi kwa ajili ya kusujudu angesema: “Allahumma maghfiratuka ausa’u min dhunuubiy wa rahmatuka arjaa ‘indiy min ‘amaliy, faghfir liy dhunuubiy yaa hayaan laa yamuutu.” “Ee Mungu! Msamaha Wako ni mkubwa kuliko dhambi zangu na rehema zako ndio matarajio yangu makubwa kuliko amali zangu, hivyo nisamehe dhambi zangu Ewe Uliye Hai ambaye kamwe hafi.”1025

DU’A YAKE ALIPOTAKA KUONDOKA (BAADA YA KUMALIZA SWALA) 41. Katika al-Ja’fariyat: Katika simulizi yake kutoka kwa Ja’far ibn Muhammad kutoka kwa baba zake kutoka kwa Ali (a.s.), kwamba wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipotaka kuondoka baada ya kumaliza kuswali, yeye angepitisha mkono wake wa kulia juu ya paji lake la uso halafu akasema: “Allahumma lakal-hamdu laa ilaha ila anta ‘aalimul-ghaibi wa shahaadati. Allahumma adh’hab ‘annaa al-hamma wal-huzna maa dhwahara minhaa wa maa batwana.” “Ee Mungu! Sifa njema zote ni Zako, hapana mungu ila ni Wewe, Mjuzi wa yaliyo ghaibu na ya dhahiri. Ewe Allah! Tuondolee sisi mashaka, huzuni na mitihani yote, iliyo dhahiri na ya siri.” Na amesema: Hakuna yoyote katika ummah wangu ambaye anafanya hivi bali kwamba Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. atampa kile anachokiomba.1026 Kidokezo: Sayyid Ibn Tawus anasimulia hadithi kama hii ndani ya kitabu chake, Falah al-Sa’il.1027 1025 Bihar al-Anwar 86:217 1026 al-Ja’fariyat: 40 1027 Falah al-Sa’il: 287 202


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 203

SUNAN-NABII DU’A YAKE BAADA YA SWALA 42. Katika Kanz ya al-Karajiki: Imesimuliwa kutoka kwa Anas ambaye amesema: Baada ya swala, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angeomba dua akisema: “Allahumma inniy a’udhubika min ‘ilmin laa yanfa’u wa qalbin laa yakhsha’u wa nafsin la tashba’u wa du’aai la yusma’u. Allahumma inniy a’udhubika min haulaail-arba’i. “Ee Mungu! Najikinga Kwako dhidi ya elimu isiyo na manufaa, na moyo ambao hauna unyenyekevu, na nafsi ambayo haitosheki, na dua ambayo haisikilizwi. Ewe Mungu Wangu! Najikinga Kwako dhidi ya hayo manne.”1028

SWALA NA DU‘A YAKE MWANZONI MWA MWAKA MPYA 43. Kutoka kwa Sayyid Ibn Tawus ndani ya Iqbal: Imesimuliwa kutoka kwa Muhammad ibn al-Fudhayl al-Sayrafi ambaye amesema: Ilisimuliwa kwetu kutoka kwa Ali ibn Musa ar-Ridhaa kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake, kutoka kwa baba zake (a.s.), ambao wamesema: Katika siku ya kwanza ya mwezi wa Muharrami, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angeswali rakaa mbili ambazo baada yake angenyanyua mikono na kuomba mara tatu kwa dua ifuatayo: “Allahumma anta ilaahul-qadiimu, wa haadhihi sanatun jadiidatun, fa-as’aluka fiihal’ismatan mina shaitwaani, wal-quwwata ‘alaa haadhihin-nafsil-ammaarati bis’suui, wal ishtighaala bimaa yuqarribuniy ilayka, yaa kariimu, yaa dhal-jalaali wal-ikrami, yaa ‘imaada man laa ‘imaada-lahu, yaa dhakhiirata man laa dhakhiirata lahu, yaa hirza man laa hirza lahu, yaa ghiyaatha man laa ghiyaatha lahu, yaa sanada man laa sanada lahu, yaa kanza man laa kanza lahu, yaa hasanal-balaai, yaa ‘adhwimar-rajaai, yaa ‘iza dhuafaai, yaa munqidhal-gharqa, yaa mun’jiyal-halaka, yaa mun’imu, yaa mujmilu, yaa muf’dhwilu, yaa muhsinu, antaladhii sajada laka sawaadul-layli, wa nuurun-nahaari, wa dhwau’ul-qamari, wa shu’aa’u sh-shamsi wa dawiyyul-maai, wa hafiyfush-shajari, yaa Allahu laa shariyka laka, Allahummaj’alnaa khairaan min maa yadhunnuuna, waghfir’lanaa maa laa ya’alamuuna, hasbia-llahu laa ilaha ila huwa ‘alayhi tawakkaltu wa huwa rabbul-‘arshil-‘adhwiimi, amannaa bihi, kullun min ‘indiy rabbinaa, , wamaa yadhdhakkaru illa uuluul-albaabi, Rabbanaa laa tuzigh quluubanaa wa hablanaa min 1028 Kanz al-Fawa’id 1:385, Bihar al-Anwar 86:18 203


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 204

SUNAN-NABII ladunka rahmatan innaka antal-wahabu. “Ee Mungu! Wewe ndiye Mola wa milele, na huu ni mwaka mpya, hivyo nakuomba unijaalie kinga dhidi ya shetani, na nguvu juu ya nafsi hii inayo amrisha maovu, na nijishughulishe na yanayonisogeza karibu Nawe, Ewe Mkariim! Ewe Mwenye jalali na ukariimu! Ewe Tegemeo la asiye na tegemeo, Ewe akiba kwa asiye kuwa na akiba, Ewe hirizi kwa asiye na hirizi, Ewe Msaidizi wa asiye kuwa na msaidizi, Ewe Tegemeo la asiye na tegemeo, Ewe Hazina ya yule asiye kuwa na hazina, Ewe Balaa njema.Ewe tarajio adhwiim, Ewe Utukufu wa wanyonge. Ewe Muokozi wa wazamao. Ewe Muokozi wa wanaohiliki, Ewe Mneemeshaji, Ewe Mtenda mema, Ewe Mfadhili, Ewe Mwema, Wewe ndiye ambaye limenyenyekea giza la usiku na nuru ya mchana, na mwanga wa mwezi, na mionzi ya jua, na wangu wa maji na sauti ya mchakariko wa miti; Ee Allah! Wewe hauna mshirika. Ee Allah! Tufanye bora kuliko wanavyodhania, na utusamehe yale ambayo hawayajui. Mtoshelezi wangu ni Mwenyezi Mungu, hapana mungu ila ni Yeye; Kwake Yeye ninategemea naye ndiye Mola wa Arshi adhiim. Tunaiamini – Arsh – yote ni kutoka kwa Mola Wetu, na hakuna anaye onyeka ila wale wenye akili. Mola Wetu! Usiziachie nyoyo zetu zipotoke na tupe rehma kutoka kwako, hakika Wewe ni Mpaji sana .” 1029

DU’A YAKE KATIKA USIKU WA MWEZI KUMI NA TANO SHA’BANI 44. Kutoka kwa Seyyid Ibn Tawus ndani ya al-Iqbal: Miongoni mwa matendo ya kufanywa mnamo usiku wa mwezi kumi na tano Sha’aban ni: ….. na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitumia kuomba dua katika usiku huu na kusema: “Allahumma-iq’sim-lanaa min khash’yatika maa yahuulu baynanaa wa bayna ma’aswiyatika, wa min twaa’atika maa tuballighunaa bihi ridh’waanaka, wa minal-yaqiini maa yahuunu ‘alaynaa bihi muswiybatid-dun’yaa. Allahumma matti’inaa bi asmaa’inaa wa abswaarina wa quwwatinaa maa ah’yaytanaa, waj’alhulwaaritha minnaa, waj’al thaaranaa ‘alaa man dhwalamana, wansur’naa ‘alaa man ‘aadaanaa, walaa taj’al muswiybatanaa fiy diyninaa, walaa taj’alid-dun’yaa akbara hammanaa, walaa mablaghaa ‘ilminaa, walaa tusallitw’ ‘alaynaa man laa yarhamunaa, birahmatika yaa arhamar-rahimiina.” “Ee Mungu! Tupe sisi hofu nyingi juu Yako kiasi kwamba ituzuie kutokana na kutokukutii, na utujaalie utii kwa kiasi kwamba utatufanya kuzipata radhi Zako, na uhakika kiasi ambacho kitatufanya tuivumilie misiba ya dunia hii. Ee Mola Wetu! 1029 Iqbal al-A’mal: 553 204


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 205

SUNAN-NABII Tujaalie kutumia kusikia kwetu na kuona kwetu na nguvu zetu katika uhai uliotupa sisi, na uvijaalie kubakia hadi tutakapofariki, na kuwalipiza kisasi wale waliotudhulumu, na utunusuru dhidi ya wale ambao wamekuwa maadui zetu, na usitujaalie misiba katika dini yetu, wala usiijalie dunia hii kutushughulisha sana, wala kikomo cha elimu yetu, wala usimfanye mtawala juu yetu yule ambaye hana huruma na sisi, kwa Huruma Zako Ewe Mwingi wa Huruma zaid ya wenye huruma.”1030 45. Katika al-Iqbal: Ndani ya riwaya kutoka kwa babu yake Abi Ja’far at-Tusi, kutoka kwa mmoja wa wake za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye amesema: Katika usiku ambao Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alikuwa pamoja nami, alitoka taratibu kwenye shuka yangu (ili asiniamshe) lakini nililitambua hilo. Nilianza kujihisi wivu ule wanaouhisi wanawake na nikadhani kwamba yupo kwenye chumba cha mmoja kati ya wake zake wengine lakini hapo nilipomkuta alikuwa kana nguo iliyoanguka chini juu ya ardhi, akisujudu na ncha za vidole vyake vya miguu juu ya ardhi na akisema: “As’bahtu ilayka faqiyran khaaifan mustajiyran falaa tubadil ismiy walaa tughair jismiy walaa tajtahid balaaiy waghfirliy.” Naja Kwako kama fukara mwenye kuomba, mwenye hofu nyingi, nikiomba hifadhi, hivyo usiibadili hali yangu, wala usiugeuze mwili wangu, wala usiifanye bisiba yangu kuwa mizito, na unisamehe.” Kisha alinyanyua kichwa chake na akasujudu tena nami nikamsikia yeye akisema: “Sajada laka sawaadiy wa khiyaaliy wa aamina bidhaalika fu’aadiy. Haadhihi yadayaa bimaa janaytu ‘alaa nafsiy, yaa ‘adhwiymu turjaa likuli ‘adhwiymin ighfirliy dhanbiyal-‘adhwiyma fainnahu laa yaghfiru dhanbal-‘adhwiyma illal‘adhwiymu.” “Mwili wangu na akili vimekusujudia Wewe, na kwa hili moyo wangu umepata imani. Hii hapa mikono yangu ambayo kwayo nimeidhulumu nafsi yangu, Ewe Mkuu ambaye juu Yako kuna matumaini makubwa, nisamehe mimi madhambi yangu makuu, kwani hakuna awezaye kusamehe madhambi makuu ila yule Mkuu.” Kisha akanyanyua kichwa chake na akasujudu kwa mara ya tatu na nikamsikia akisema:

1030 Ibid , 699 -700

205


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 206

SUNAN-NABII “A’udhu bi’af’wika min ‘iqaabika, wa a’udhu biridhwaaka min sakhatwika, wa a’udhu bimu’aafatika min ‘uquubatika, wa a’udhubika minka, anta kamaa athnayta ‘alaa nafsika wa fawqa maa ya quulul-qaailuuna.” “Najikinga adhabu yako kwa msamaha Wako, na ninajikinga dhidi ya hasira zako kwa ridhaa Yako, na ninajikinga kwa msamaha wako dhidi ya adhabu yako. Na ninaomba hifadhi kwako dhidi ya adhabu Yako. Wewe upo kama ulivyojieleza Mwenyewe na uko juu zaidi ya wanayosema wenye kusema.” Kisha akanyanyua kichwa chake na akasujudu kwa mara nyingine tena, kwa mara ya nne na akasema: “Allahumma inniy a’udhu binuuri waj’hika ladhiy ashraqat lahus-samaawatu wal ardhu, wa qasha’at bihi dhulumaatu, waswaluha bihi amrul-awwaliyna walakhiriyna, an yahilla ‘alay’ya ghadhwabuka au yanzila ‘alay’ya sakhatuka. A’udhu min zawaali ni’imatika wa faja’ati niqmatika watah’wili ‘aafiyatika wajamiy’i sakhatwika. Lakal-‘utbaa fiymaa statwa’atu walaa hawla walaa quwwata illa bika.” “Ee Mungu! Mimi najikinga kwa nuru yako ambayo kwayo mbingu na ardhi zime’ngara, na kwyo giza limetoweka, na kwayo mambo ya wa mwanzo na wa mwisho yameboreka ili nisipatwe na ghadhabu yako au kushukiwa na hasira Zako. Najikinga zisitoweke neema Zako, na kusitukizwa na adhabu Yako na kubadilika kwa afya njema uliyonipa, na makasiriko yako yote. Una haki ya lawama kwa yale ambayo niliyo yaweza, wala hapana hila wala nguvu ila kwa - kukutegemea Wewe.” Mama wa waumini aliendelea: “Nilipoyaona haya kutoka kwake, nilimuacha na kikaondoka kuelekea nyumbani kwani hali ya wasiwasi ilinishika. Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akanifuata na kusema: “Kwa nini huna raha?” Mimi nikasema: “Nilikuwa nawe ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu.” Yeye akasema: “Je unaujua ni usiku gani huu? Huu ni usiku wa nusu ya Sha’aban. Ndani yake mna matendo yaliyoamuliwa, na hugawanywa riziki humo, na muda wa uhai unakadiriwa; na Allah anawasamehe wote isipokuwa washirikina au wale maadui wa dhahiri, au mtu ambae amevunja uhusiano na familia yake ya karibu, au mnywaji wa pombe, au yule anayeng’ang’ania katika kutenda dhambi, au mshairi wa mzaha mzaha au mtabiri..” 1031

1031Ibid, 702 206


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 207

SUNAN-NABII Kidokezo: Hii imesimuliwa katika al-Iqbal kutoka kwa babu yake Abi Ja’far atTusi kutoka kwa Hammad kutoka kwa Aban kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ndani ya hadith inayofanana na hii bali ambamo dua hiyo inatofautiana kabisa na ile dua iliyoko katika hadith hii.1032 al-Zamakhshari pia anaisimulia hii ndani ya al-Faqih bila kutaja dua yenyewe.1033

DU’A YAKE KATIKA KUUONA MWEZI MPYA 46. Kutoka kwa Sheikh Tusi ndani ya al-Amali: Imesimuliwa kutoka kwa Muhammad ibn Hanafiyya kutoka kwa Ali (a.s.) ambaye amesema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipouangalia mwezi mwandamo, yeye angenyanyua mikono yake na kusema: “Bismillahi, Allahumma ahilahu ‘alaynaa bil-amni wal-iimani was-salaamat walIslaami Rabbiy warabbuka-llahi.” “Kwa jina la Allah. Ewe Mungu! Uandamishe kwetu kwa amani na imani, kwa salama na unyenyekevu. Mola wangu na Mola wako ni Allah.”1034 Kidokezo: Zipo hadith nyingi kama hii.1035

DU’A YAKE ALIPOUONA MWEZI MWANDAMO WA RAMADHANI 47. Kutoka kwa Sayyid ibn Tawus katika mlango wa matendo ya kufanywa ndani ya mwezi wa Ramadhani: Kutoka kwa Muhammad ibn Hanafiyya kutoka kwa Amirul-Mu’minin Ali (a.s.) ambaye amesema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipouona mwezi mwandamo wa Ramadhani, yeye aligeuzia uso wake kuelekea Qiblah na kusema: “Allahumma ahilahu ‘alaynaa bil-amni wal-iimaani was-salaamati wal-islaami, wal-‘aafiyati mujallalati, wadifaa’i al-asqaami, wal-‘awni ‘alaa swalaati was-swiyaami watilaawatil-Qur’ani. Allahumma salimnaa lishahri Ramadhana, watusalimhu minnaa, wasalimnaa fiyhi, 1032 Ibid. 1033 Hatukuikuta ndani ya al-Faqih. 1034 Amali al-Tusi 2:109 1035 Taz. al-Wasa’il ash-Shi’ah 7:233-235

207


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 208

SUNAN-NABII hataa yanqadhwiya ‘an’naa shahru Ramadhana waqad ‘afawta ‘annaa waghafarta lanaa warahimtanaa.” “Ee Mungu! Uandamishe kwetu kwa amani na imani, salama na unyenyekevu, afya njema na kinga ya maradhi, na- iwe - msaada wa swala, saumu na kusoma Qur’ani. Ee Mungu! Tujaalie tuuelekee mwezi wa Ramadhani na uufanye utupokee, na tuwe wanyenyekevu ndani yake, mpaka utakapokwisha mwezi wa Ramadhani uwe umetusamehe dhambi zetu na umetughofiria na umetuhurumia.”1036

URADI (DHIKR) WAKE WA KILA SIKU 48. Katika al-Kafi: Imesimuliwa kutoka kwa Abil-Hasan al-Anbari kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akimsifu Mwenyezi Mungu mara mia tatu na sitini kwa siku, idadi (sawa na ile) ya mifereji ndani ya mwili, huku akisema: “Alhamdulillahi Rabbil-‘Aalamiina kathiiran ‘alaa kuli haalin.” “Sifa njema ni za Mwenyezi Mungu Mola wa ulimwengu nyingi kwa kila hali.” 1037 49. Vilevile: Imesimuliwa kutoka kwa Ya’qub ibn Shu’aib ambaye amesema: Nilimsikia Abi Abdillah (a.s.) akisema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Kwa hakika kuna (mifereji) mishipa mia tatu na sitini katika mwili wa mwanadamu, ambayo kati ya hiyo, mia na themanini inatiririka na mia na themanini imetulia. Kama mshipa wa kutiririka ukigeuka na kutulia, unakuwa haukui na kama ule wa kutulia ukianza kutiririka hauongezeki kukua. Na Mtukufu Mtume akasema: “Alhamdulillahi kathiiran ‘alaa kuli haali. “Sifa nyingi ni zake Mwenyezi Mungu kwa kila hali” ……. mara mia tatu na sitini wakati alipoamka asubuhi na (halafu tena) wakati usiku unapoingia.1038 50. Kutoka kwa Sheikh Tusi ndani ya Majalis na al-Akhbar: Imesimuliwa kutoka kwa Sariyya ibn Ya’qub kutoka kwa baba yake, kutoka kwa as-Sadiq, kutoka kwa baba zake (a.s.) katika hadith hii: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipoamka 1036 Iqbal al-Amal: 17, al-Kafi 4:70, al-Faqih 2:100, Tahdhib al-Ahkam 4:196 1037 al-Kafi 2:503 1038 Ibid. 208


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 209

SUNAN-NABII muda wa asubuhi, wakati jua lilipochomoza, yeye huwa angesema: “Alhamdulillahi rabbil-‘aalamina kathiiran twayiban ‘alaa kuli haalin.” “Sifa nyingi njema ni za Allah ‘Azza wa Jalla. – Mola wa ulimwengu katika kila hali.” Na angeonyesha shukurani zake Kwake ‘Azza wa Jalla. mara mia tatu na sitini.1039

URADI (DHIKR) WAKE WAKATI WA ASUBUHI NA JIONI 51. Kutoka katika al-Qurb al-Rawandi: Imesimuliwa kwamba wakati Ali ibn alHusein (a.s.) alipopelekwa kwa Yazid alitaka kumuua hivyo akamfanya Imam huyo kusimama mbele yake na kuzungumza naye, akijaribu kutaka kupata jibu litakalompa kisingizio cha kumuua yeye. Na Imam (a.s.) alimjibu, na wakati alipokuwa anaongea alikuwa na shanga ndogondogo za dua 1040mkononi mwake ambazo alikuwa akizigeuza kwa vidole vyake vile alivyokuwa anaongea. Hivyo Yazid akamwambia: “Mimi ninaongea na wewe nawe unanijibu huku ukigeuza geuza hizo shanga za dua katika vidole vyako; hivi hiyo inawezekanaje?” Yeye (a.s.) akasema: “Baba yangu amenisimulia kutoka kwa babu yangu kwamba wakati yeye alipomaliza swala yake ya asubuhi asingeongea hadi awe ameshika shanga zake za dua mkononi mwake na akasema: “Allahumma inniy as’bahtu usabbahuka wa umajidduka wa uhammiduka wa uhalliluka bi’adadi maa udiyru-bihi subhatiy.” “Ee Mungu Wangu! Ninaianza siku yangu kwa kukusabihi na kukutukuza Wewe kwa idadi kiasi cha niigeuzavyo tasbihi zangu. ….. na angezichukua shanga hizo za dua na kuanza kuzizungusha huku akiongea kile chochote alichopenda kuongea, mbali na kuvuta uradi, na alisema kwamba kugeuza shanga za dua kungehesabiwa (kama kuvuta uradi) na kungekuwa kama kinga mpaka alivyopanda kitandani kwake (wakati wa usiku) na pale alipopanda kitandani kwake, angesema kama vile alivyosema wakati wa asubuhi na angeziweka shanga zake za dua chini ya mto wake na hivyo ingehesabiwa kama ni dhikr kutoka wakati mmoja hadi mwingine – kwa hiyo nilifanya hivi kufuata nyayo za 1039Amali at-Tusi 2:210, Majmu’al Warram: 322, Biharul-Anwar 86:266 na 93:216 1040 Zile zinazojulikana kwa kawaida kama Tas’bih kwa Kiajemi, ki-Urdu n.k. (Mfasiri) 209


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 210

SUNAN-NABII babu yangu.” Yazid akasema – kwa kukariri mara kwa mara: “Hakuna yeyote kutoka miongoni mwenu ninayeongea naye bali kwamba ananijibu kwa kile ambacho kwacho kufanikiwa kwake kunaonekana,” na akaachana na ile dhamira yake ya kutaka kumuua na akaagiza kwamba afunguliwe pingu zake.1041 Kidokezo: Ni dhahiri kutokana na riwaya hii kwamba kwa neno ‘babu’ alimaanisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

TIBA YAKE KWA AJILI YA MAUMIVU YA KICHWA 52. Katika Tibb al-A’immah: Kutoka kwa Ahmad ibn Ziyad kutoka kwa Fadhalah kutoka kwa Isma’il ibn Ziyad kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Wakati wowote Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliposhikwa na uzito au kuumwa na kichwa, yeye angenyoosha mikono yake na kusoma Suratul-Fatihah na Mu’awwadhatain 1042 na angepona kutokana na kile alichokuwa amesibiwa nacho yeye.1043

KUOMBA KWAKE KINGA YA HOMA NA MAGONJWA MENGINE 53. Katika Da’awat al-Rawandi: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angeomba kinga ya homa na maumivu mengine kwa kusema: “Allahumma a’uudhubika min sharri ‘irqin na’aarin wamin sharri harrin-naari.” “Ewe Mola Wangu! Najikinga Kwako dhidi ya madhara ya mishipa itowayo damu kwa kufoka na dhidi ya shari ya ukali wa moto wa Jahannam.1044

MAOMBI YAKE KWA AJILI YA KINGA YA HOMA 54. Katika Tibb al-A’immah: Imesimuliwa kutoka kwa Amr Dhi Qurrah na Tha’alabi al-Jammal ambaye amesema: Tulimsikia Amirul-Mu’minin (a.s.) akise1041 al-Da’awat: 61, al-Mustadrak 5:124 1042 Suratun-Nas (114) na Suratul-Falaq (113) 1043Tibb al-A’immah (a.s.): 39, Bihar al-Anwar 7:95 na al-Ja’fariyat: 216 1044 al-Da’awat: 208 na Bihar al-Anwaar 95:31 210


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 211

SUNAN-NABII ma: Homa kali sana ilikuja kumshika Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hivyo Jibril alimshukia na akamsomea dua ifuatayo: “Bismillahi urqiyka, Bismillahi ashfiyka min kulli daa’in yu’udhiika, wallahu shaafiiyka, bismillahi khudh’haa faltuhanniyka. Bismillahi arrahmaanir-rahiimi. Walaa uqsimu bimawaaqi’in-nujuumi, wa ilahu laqasamun law ta’alamuuna ‘adhwiymun, latabarra anna bi-idhnillah ‘azza wajalla.” “Kwa jina la Allah – naomba kwa ajili yako. Kwa jina la Allah – nakutibia kwa kila maradhi yale yanayokufika na Allah ndiye Mponyaji wako. Kwa jina la Allah – ichukue kwani inakuletea afya njema. Kwa jina la Allah, Mwingi wa rehma Mwenye kurehemu – naapa kwa mahali pa nyota. Na kwa hakika hicho ni kiapo chenye nguvu kama mungejua. Kwa kweli wewe utapona kwa utashi wa Allah Mwenye nguvu zote.” Na kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasimama akiwa amepona kutokana na kile kilichokuwa kimemfunga na yeye akasema: “Oh, Jibril! Hii kwa hakika ni dua kubwa!” Yeye akajibu: “Inatoka kwenye hazina ya kwenye mbingu saba.”1045

MAOMBI KWA AJILI YA KINGA KUTOKANA NA UCHAWI 55. Katika al-Bihar: Kutoka kwa Ibn Abbas ambaye amesema: Lubaid ibn A’sam alimfinga Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kisha akalitega (fingo hilo) kwenye kisima kilichokuwa mali ya Bani Zurayq. Hivyo Mtume (s.a.w.w.) aliugua na wakati akiwa usingizini, malaika wawili walimjia, mmoja akakaa karibu na kichwa chake ambapo yule mwingine akakaa karibu na miguu yake na wakamjulisha kuhusu uchawi huo na kusema: “Fingo hilo limo kwenye kisima cha Dharwan, ndani ya shuke la maua ya mti wa mtende chini ya jiwe chini ya kisima hicho.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliamka na kuwatuma Ali (a.s.), Zubayr na Ammar (kwenda kuliongoa fingo hilo). Waliyaondoa maji kutoka kwenye kisima hicho na wakalinyanyua jiwe na wakaondo hilo shuke la maua. Ndani yake mlikuwa na nywele kidogo za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) pamoja na kiasi fulani cha njiti kadhaa zilizovunjika kutoka kwenye kitana chake zilizokuwa zimefungwa katika mafundo kumi na moja pamoja na sindano. Ndipo Surah hizi mbili zikateremshwa. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akaanza kuzisoma Surah hizo mbili na kwa kisomo cha 1045Tibb al-A’immah (a.s.): 37, Bihar al-Anwar 95:20, Qurb al-Isnad: 46, al-Kafi 8:109. 211


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 212

SUNAN-NABII kila aya moja, lilifunguka moja kati ya mafundo hayo, na baada ya mafundo yote kufunguka, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alionekana kama mtu aliyekuwa hivi punde tu amebeba mzigo mzito ambao umeondolewa kutoka kwake, na Jibril akaanza kusema: “Bismillahi urqiyka min kulli shay’in yuudhiyika min haasidin wa ‘ay nin wallahu yashfiyika.” “Kwa jina la Allah ninakukinga wewe dhidi ya kila kitu kinacho kuudhi – miongoni mwa hasidi na mwenye kijicho – na Mwenyezi Mungu atakuponya maradhi yako.” Kidokezo: Sura hizo mbili zinazotajwa hapa ni zile Mawa’idhatain – Surat alFalaq na an-Nas – kama ilivyoelezwa kwenye hadithi nyinginezo.1046

MOJA YA DU’A ZAKE NYINGINE 56. Katika al-Bihar kutoka kwenye Tafsiir ya Imam: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliweka mkono wake kwenye nyama ya mfupa wa mkono na akasema: “Bismillahi sh-Shaafiy, bismillahi al-kaafiy, bismillahi al-mu’aafiy, bismillahi al-ladhiy laa yadhurru ma’a ismihi shay un fil’-ardhi walaa fiyis-samaai wa huwas-sami’ul-‘aliimu.” “Kwa jina la Allah Mponyaji, kwa jina la Allah Mwenye Kutosheleza, kwa jina la Allah Mwenye kustawisha, kwa jina la Allah ambaye kwa jina Lake hakuna chochote katika ardhi au mbingu kinachoweza kusababisha madhara juu yetu na Yeye ni Mwenye kusikia Mwenye kujua.” Halafu akasema: “Kula kwa jina la Allah,” na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akala, na wote wakala mpaka wakatosheka, na (sumu hiyo) haikuwadhuru japo kidogo.1047

DU’A YAKE ALIPOHUZUNIKA AU KUSUMBUKA 57. Kutoka kwa Sheikh at-Tusi ndani ya al-Amali: Imesimuliwa kutoka kwa Zayd, kutoka kwa baba zake, kutoka kwa Ali (a.s.) ambaye amesema: Wakati wowote 1046 Bihar al-Anwar 95:126, Tibb al-A’immah: 114, Majma’al-Bayan 10:568 Da’aim alIslam 2:138 1047 Bihar al-Anwar 95:144, Tafsiir iliyohusishwa kwa Imam al-Askari (a.s.): 178 212


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 213

SUNAN-NABII Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa amehuzunika au kusumbuka huwa angesoma dua ifuatayo: “Yaa hayyu yaa qayyuumu, yaa hayyaan laa yamuutu, yaa hayyu laa ilaha illa anta, kaashifal-hammi, mujiibata da’awatil-mudh’twarriina. As’aluka bi anna lakal-hamda laa ilaha illa anta al-manaanu, badiy’us-samaawaati wal-ardhi dhuul-jalaali wal ikraami, rahmaanad-dunyaa wal aakhirati wa rahiimahumaa, rabbi’rhamniy rahmata tughniiniy bihaa ‘an rahmati man siwaaka, yaa arhamar-rahimiyna.” “Ewe wa Milele! Ewe Wa Kudumu! Ewe Uliye Hai daima ambaye hafi! Ewe Uliye Hai daima hapana mungu ila Wewe. Muondoshaji wa masumbufu! Mwenye kujibu wito wa walio na dharura! Nakuomba, kwakuwa sifa zote njema ni Zako Wewe – hapana mungu ila ni Wewe – Ewe Mpaji wa fadhila! Muanzishi wa mbingu na ardhi! Mwenye Uwezo na Utukufu! Mwenye kurehemu katika dunia hii na ile ya Akhera na Mwenye huruma katika dunia zote! Ewe Mola Wangu! Ni rehemu rehema ambayo itanitosha sitohitajia rehema kutoka kwa mwingine mbali na Wewe, Ewe Mwingi wa Rehema Mwenye kurehemu.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Yeyote yule, kutoka miongoni mwa Waislam atakayesoma dua hii mara tatu anahakikishiwa kupata kile anachoomba isipokuwa kama anachokiomba ni dhambi au kama atakuwa amevunja uhusiano na ndugu zake wa karibu.”1048

DU’A YAKE KWA AJILI YA KUHIFADHI QUR’ANI TUKUFU 58. Katika Qurb al-Isnad: Kutoka kwa Mas’adah ibn Sadaqah: Nilisimuliwa na Ja’far kutoka kwa baba zake (a.s.) kwamba ifuatayo ilikuwa ni moja ya dua za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Allahumma irhamniy bi tarki ma’aaswiyka maa abqaiytaniy, warzukniy husnan-nadhwari fiymaa yurdhwiyka ‘anniy wa alzim qalbiy hifdhwa kitaabika kamaa ‘allamtaniy, waj’alniy atluuhu ‘alaannahwi al-ladhii yurdhwiyka ‘anniy. Allahumma nawwir bikitaabika baswariy, washrah bihi swadriy, wa farrih bihi qalbiy, wa atwliq bihi 1048Amali al-Tusi 2:125 213


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 214

SUNAN-NABII lisaaniy, waasta’amil bihi badaniy, wa qawwiniy ‘alaa dhaalika, fainnahu laa hawla wa laa quwwata illa bika.” “Ewe Mungu! Nihurumiye kwa kuacha kukuasi muda wote utakao nibakisha, na niruzuku kuwa na mtizamo mwema katika yakuridishayo kwangu; Ubidishe moyo wangu kuhifadhi kitabu chako kama ulivyo nifundisha; na uniwezeshe kukisoma kwa namna nitakayokuridhisha. Ee Mungu Wangu! Kwa kitabu chako yatiye nuru macho yangu, na kwayo ukunjue kifua changu, na kwayo ufurahishe moyo wangu, na kwayo ufanye ulimi wangu fasaha, – kwa kitabu chako - utumikishe mwili wangu, na nipe nguvu kwa hilo, kwa kuwa hapana hila wala guvu ila - kupitia – wewe.”1049

KINGA YAKE 59. Katika al-Muhaj: Hijab (kinga) ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) – yaani dua au maombi ya kujilinda kutokana na maadui – ilikuwa:

“….. Na tumezitia pazia nyoyo zao wasije kuyafahamu, na mnauziwi masikiono mwao…..” (An’aam; 6:25)

“….. Na unapomtaja Mola Wako katika Qur’ani peke yake, basi wao hugeuza migongo yao kwa chuki.” (Bani Isra’il; 17:46). “Ewe Allah! Kwa kile ambacho Nguvu na Enzi Yako zilichofunika, na kwa kile ambacho kimezingirwa na ukamilifu wa Mamlaka Yako, na kwa heshima ambayo inatokana na Elimu Yako isiyo na kikomo, na kwa kile ambacho kimezungukwa na Milki Yako; Ewe Mmoja ambaye amri yake haiwezi kubatilishwa na ambaye hukumu yake haiwezi kupinduliwa! weka baina yangu na adui yangu kinga ambayo haiwezi kuodolewa hata kwa upepo wenye nguvu, wala isiyoweza kukatwa na mabapa makali, wala isiyoweza kuchomwa na mkuki. Ewe Mmoja ambaye Nguvu yake ni kuu! Nilinde kutokana na yule ambaye amenilenga kwa mishale yake na yule 1049 Qurb al-Isnad: 4, Bihar al-Anwar 95:341 214


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 215

SUNAN-NABII anayenifanya shabaha ya mashambulizi yake; na uniondolee kila huzuni na shida. Ewe muondoaji wa huzuni ya Ya’qub! Niondolee huzuni yangu. Ewe Muondoshaji wa dhiki za Ayyub! Niondoshee shida zangu; na mshinde kwa ajili yangu yule aliyenishinda. Ewe Mshindi usiyeshindika.” …..

“Na wale waliokufuru Mwenyezi Mungu amewarudisha na ghadhabu yao, hawakupata chochote katika kheri, na Mwenyezi Mungu amewatoshea waumini katika mapigano yao, Mwenyezi Mungu ni Mwenye uwezo, Mwenye nguvu.” (33:25)

“…..Ndipo tukawasaidia wale walioamini juu ya maadui zao na wakawa wenye kushinda.” (61:14) 1050

Nyongeza kwenye sehemu hii 1. Katika al-Manaqib: Yeye (s.a.w.w.) asingekaa wala kusimama ila kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu.1051 Kidokezo: Hii imesimuliwa vilevile katika Majma’ul-Bayan.1052 2. Katika al-Kafi: Ndani ya simulizi yake kutoka kwa Ibn Fadhal kutoka kwa mfuasi mmojawapo wa kutoka kwa Imam Ridha (a.s.) kwamba yeye alikuwa akitumia kusema kuwaambia wafuasi wake: “Twaeni ile silaha ya Mitume.” Ikasemwa: “Na ni ipi hiyo silaha ya mitume?” Yeye akajibu: “Ni dua.”1053 3. Katika Da’awat al-Rawandi: Yeye (s.a.w.w.) angesihi sana wakati alipokuwa akiomba hadi ikaonekana kana kwamba joho lake lilikaribia kuanguka.1054 1050 Muhaj al-Da’awat: 296 1051 Manaqib Ali ibn Abi Talib 1:147 1052 Majma’ul-Bayan 2:554 1053 al-Kafi 2:468 1054 al-Da’awat: 22, Bihar al-Anwar 93:339 215


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 216

SUNAN-NABII 4. Katika Kashf al-Ghummah: Ahmad ibn Hamdun amesema ndani ya Tadhkirah yake: Muhammad ibn Ali ibn Husein (a.s.) amesema: “Sisi (Ahlul-Bayt) tunamuomba Mwenyezi Mungu kwa kile ambacho tunakipenda, na kama litatokea tusilolipenda badala yake, huwa hatuendi kinyume na alilotupendelea Mwenyezi Mungu.1055

DU’A YAKE WAKATI WA ASUBUHI 5. Katika al-Kafi: Katika riwaya yake kutoka kwa al-Fadhl ibn Abi Qurrah kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Sentensi tatu zilitamkwa na mitume wote, mmoja baada ya mwingine, kuanzia Adam (a.s.) hadi waliposhuka mpaka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kila asubuhi angekuwa akisema: “Allahumma inniy as’aluka iyimaanan tubaashiru bihi qalbiy, wa taqiynan hattaa a‘alamu annahu laa yuswiybuniy illa maa katabtaliy, wa radhwiy bimaa qasamtaliy. “Ewe Mungu! Nakuomba imani ambayo inayoleta furaha kwenye moyo wangu, na yakini ili niweze kujua kwamba hakuna la kunikuta mimi isipokuwa lile ambalo Wewe umelikadiria juu yangu, na nifanye niridhie na kile ambacho umekipanga kwa ajili yangu.1056 6. Katika al-Khisal: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimfundisha Ali (a.s.) ile dua ambayo Jibril aliileta kutoka kwa Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. na akamuelekeza Mtume kuisoma wakati wa shida na matatizo: “Yaa ‘imaada man la imada lahu, wa yaa hirza min laa hirzalahu, wa yaa dhukhra man laa dhukhura lahu, wa yaa sanada man laa sanada lahu, wa yaa ghiyaatha man laa ghiyaatha lahu, wa yaa kariymal‘afwi, wa yaa hasanal-balaai, wa yaa ‘adhwiymar-rajaai, wayaa ‘awna dhu’afaai, wa yaa munqidhal-gharqa, wa yaa mun’jiyaal-halaka, yaa muhsinu, yaa mujmilu, yaa mun’iimu, yaa mufdhwilu, antalladhiy sajada laka sawaadul-layli, wa nuurun-nahaari wadhwauulqamari, wa shu’aa’ush-shamsi, wadawiyyul-maai, wa hafiyfush-shajari, yaa Allahu, yaa Allahu, yaa Allahu, anta wahdaka laa shariyka laka. Thumma taquulu: Allahumma if’aliy kadhaa wa kadhaa …..” 1055Kashf al-Ghummah 2:150 – 151. 1056 al-Kafi 2:524, Bihar al-Anwar 86:289 216


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 217

SUNAN-NABII “Ewe Tegemeo la asiyekuwa na wa kumtegemea! Ewe Mlinzi wa yule asiye na wa kumlinda! Ewe Hazina wa yule asiyekuwa na hazina! Ewe Msaidizi wa yule asiye na wa kumsaidia! Ewe Mwenye kusikia maombi yasiyosikilizwa! Ewe Mkarimu katika kusamehe! Ewe Ambaye mitihani yako ni mizuri! Ewe Mtoaji wa matumaini makubwa! Ewe Msaidizi wa wanyonge! Ewe Muokoji wa wanaozama! Ewe Muomkozi wa wanaoteketea! Ewe Mfadhili! Ewe Muumba wa uzuri! Ewe Mtoaji wa neema! Ewe Mpaji wa mema mazuri! Wewe Ndiwe ambaye kwako lakusujudia giza la usiku, na nuru ya mchana, na mwanga wa mwezi, miyonzi ya jua, sauti ya maji (yanayotiririka) na mvumo wa miti. Ewe Allah! Ewe Allah! Ewe Allah! Wewe ni wa Pekee na huna mshirika.” Halafu sema: “Ewe Mungu! Nijaalie hiki na kile,” na hautosimama kutoka pale ulipokaa bali dua yako itakuwa imejibiwa Mungu akipenda1057

MAOMBI YAKE 7. Katika al-Muhaj: Katika riwaya yake kutoka kwa Abi Basir na Muhammad ibn Muslim ambao wamesema: Ametusimulia Ja’far ibn Muhammad as-Sadiq kutoka kwa baba yake, kutoka kwa baba zake kutoka kwa Amirul-Mu’minin Ali ibn Abi Talib (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angemuomba Allah ‘Azza wa Jalla. kwa ajili ya usalama wa Hasan na Husein (a.s.) kwa dua hii, na angewaagiza masahaba zake kuisoma, nayo ni: “Bismillahi ar-Rahmaanir-Rahiim. U’iydhu nafsiy wa diini wa ahliy wa maaliy wa wuldiy wa khawaatiyma ‘amaliy wa maa razaqaniy Rabbiy wa khawalaniy bi’izzati-llahi wa ‘adhwamati-llahi wa jabaruuti-llahi wa sultwaani-llahi wa rahmati-llahi wa raufati-llahi wa ghufraani-llahi wa quwwati-llahi wa qudrati-llahi wa bialai-llahi wa bisun’i- llahi wa bi arkaani-llahi wa bijam’ii-llahi ‘azza wajalla wa bi rasuuli-llahi (s.a.w.w.) wa qudrati-llahi ‘alaa maa yashaau, min sharris-saammaati wal haammat, wa min sharril-jinni wal insi, wa min sharri maa dabba fiil-ardhi, wa min sharri maa yakhruju minhaa, wa min sharri maa yanzilu minas-samaai, wa maa ya’araju fiyhaa, wa min sharri kuli daabbati rabbiy aakhidhu bi naaswiyatihaa, inna rabbi ‘alaa swiraatwi mustaqiymin, wahuwa ‘alaa kulli shaiyin qadiyrun, wa laa hawla walaa quwwata illa bi-llahil-‘aliyi al’adhwiym, wa swalallahu ‘alaa sayyidinaa Muhammadin wa aalihi.”

1057 al-Khisal 2:510 217


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 218

SUNAN-NABII “Kwa jina la Allah, Mwingi wa rehma, Mwenye kurehemu, Ninajikinga binafsi, dini yangu, familia yangu, mali yangu na matokeo ya amali zangu, na kile ambacho Mola wangu ameniruzuku na kunitunukia, kwa utukufu wa Mungu na adhwama ya Mungu chini ya ulinzi wa Heshima, Utukufu, Enzi, Ukarimu, Huruma, Upole, Msamaha, Uwezo, Nguvu na Rehma za Allah; kwa nguzo ya Allah ‘Azza wa Jalla., Mtume wa Allah (s.a.w.w.) na Uwezo wa Allah juu ya kila kitu akitakacho, kutokana na shari ya viumbe wenye sumu na wasio na sumu, kutokana na shari ya majinni na watu, kutokana na shari ya vyenye kutambaa juu ya ardhi na shari ya vinavyotoka humo, na shari inayoshuka kutoka angani na chenye kupaa kutoka humo na shari ya kila kiumbe ambacho Mola wangu anakishika kwa kishungi chake, hakika Mola wangu yuko kwenye njia iliyonyooka na anao uwezo juu ya kila kitu; na hapana nguvu wala uwezo bali ule wa Allah Mtukufu Mwenye Nguvu – na rehma na amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu ya bwana wetu Muhammad na kizazi chake.”1058

DU’A YAKE ANAPOKUWA NA MATATIZO AU HUZUNI KUBWA 8. Katika kitabu al-Mujtabah cha Tawus: Ndani ya simulizi yake kutoka kwa Jabir ambaye amesema: Wakati jambo lilipomhuzunisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) au kama wale wasioamini wamemsumbua sana, yeye angefunga mkono wake na akasema: “Zuilika (halafu) achiliwa.” Kisha akaelekea Qibla na akanyanyua mikono yake akasema: “Bismillahir -Rahmaanir-Rahiimi, laa hawla walaa quwwata illa bi-llahil-‘aliyi al’adhwiymi, Allahumma iyaaka na’abudu wa iyaaka nasta’iinu, Allahumma kuffa baasal-ladhiyna kafaruu fainnaka ashaddu ba’asan wa ashaddu tankiylan.” “Kwa jina la Allah, Mwingi wa rehma, Mwenye kurehemu, hapana nguvu wala uwezo bali ule wa Allah Mtukufu Mwenye Nguvu. Ewe Allah! Ni Wewe peke Yako tunayekuabudu na Kwako peke Yako tunaomba msaada. Ewe Allah! Zuia shari ya wale waliokufuru kwani kwa hakika Wewe Ndiwe Mwenye nguvu zaidi katika Uwezo na Mwenye ukali zaidi katika kuadhibu.” ….. na Wallahi, kabla hajafungua mkono wake matatizo yake yangekuwa yamekwisha kutatuliwa.1059 1058 Muhaj al-Da’awat: 10 1059al-Mujtabah: 2 218


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 219

SUNAN-NABII

DU’A YAKE ALIPOKASIRISHWA NA JAMBO 9. Katika al-Bihar: Ndani ya Hadith kutoka kwa as-Sadiq (a.s.) ambaye alisema: Wakati wowote jambo lilipomtatiza Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) yeye angesoma dua ifuatayo – na waliitaja dua hii kwa jina la Du’a al-Faraj: “Allahumma-ihrusniy bi’ainikal-lattiy laa tanaamu, waknufniy bi rukbikal-ladhiy laa yuraamu, warhamniy biqudratika ‘alayya, walaa ahlaku wa anta rajaaiy, fakam min ni’imatin an’amta bihaa ‘alaiyya qalla lahaa shukriy, wa kam min balliyatin ibtalaytaniy qalla laka bihaa swabriy, fayaa man qalla ‘inda ni’imatihi shukriy falam yahrimniy, wayaa man qalla inda baliyyatihi swabriy falam yakhdhulniy, wayaa man raaniy ‘alaal-khatwaayaa falam yafdhwahniy, as’aluka an tuswaliy ‘alaa Muhammadin wa aali Muhammad. Allahumma a’aniy ‘alaa diiniy biddun’yaa, wa ‘alaal-aakhirati bi taqwaa, wahfadhniy fiymaa ghibtu ‘anhu, walaa takilniy ilaa nafsiy fiymaa hadhwartuhu, yaa man laa tadhwuuruhu dhunuubu, walaa tanqusuhul-maghfiratu, habliy ma laa yanqusuka, waghfirliy maa laa yahdhurruka, innaka rabbun wahaabun. As’aluka farajan qariyban, wa swabran jamiylan, warizqan waasi’an, wal’afiyata min jamiy’i al-balaai, washukra li’aafiyati.” “Ewe Mungu! Nilinde kwa uoni Wako ambao hauchoki, nikinge kwa ulinzi Wako ambao hauwezi kushindwa, nihurumie kwa mamlaka Yako juu yangu, na wala usiniangamize hali mimi nakutegemea Wewe. Ni neema ngapi ulizonineemesha mimi ambazo kushukuru kwangu kumekuwa kudogo, na ni mitihani mingapi uliyonijaribu nayo ambayo subira yangu kwa ajili Yako imekuwa ndogo? Ewe ambaye kwa neema Zako kushukuru kwangu kumekuwa ni kudogo lakini hakuninyima! Ewe ambaye kwenye mitihani Yake subira yangu imekuwa ndogo lakini hakunitelekeza! Ewe ambaye ameyaona makosa yangu lakini hakunifedhehesha! Nakuomba umshushie rehema na amani Muhammad na kizazi cha Muhammad. Ee Mungu! Ifanye dunia hii iwe ni njia kwa ajili ya dini yangu, na uchamungu kuwa njia kwa ajili ya akhera yangu. Nihifadhi kwa kile ambacho kimefichika kwangu na usiniache peke yangu katika kukabiliana na kilicho mbele yangu. Ewe ambaye hadhuriwi na madhambi na ambaye hapungukiwi na chochote kwa kutoa msamaha wake! Niruzuku na kile ambacho kwacho hupotezi chochote na msamaha ambao haukudhuru Wewe kitu! Wewe ni Mola Mpaji. Nakuomba faraja ya karibu, subira nzuri, na riziki yenye wasaa, afya njema mbele ya mitihani yote na shukurani juu ya neeme Zako zote.”1060

1060 Bihar al-Anwar 95:197 219


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 220

SUNAN-NABII

DU’A YAKE ALIPOUONA MWEZI MPYA 10. Katika al-‘Uyun: Kutoka kwa Darim ibn Qabisah kutoka kwa Ali ibn Musa arRidhaa kutoka kwa baba zake kutoka kwa Ali (a.s.) ambaye alisema: Wakati Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alipouona mwezi mpya angesema: “Ayyuha al-khalqul-mutwii’u ad-daaibus-sarii’u al-mutaswarrifu fiy malakuutiljabaruuti bit-Taqdiiri! Rabbiy wa Rabbuka llahu. Allahumma ahilahu ‘alaynaa bilamni wal iymaani wa salaamati wal ihsaani, wa kamaa balaghtanaa awwalahu fa balighnaa aakhirahu, waj’alhu shahraan mubaarakaan tamhuw fiyhis-sayiaati wa tarfa’u lanaa fiyhid-darajaati, yaa ‘adhwiimil-khaiyraati.” “Ewe kiumbe mtiifu – usiyechoka, kiumbe wa mbinguni mwenda-mbio unayezunguka kwa utashi Wake Allah! Mola Wangu na Mola Wako ni Allah. Ewe Allah! Ufanye mwezi huu mpya uje kwetu kwa utulivu na imani, na amani na wema. Kama ulivyotufikisha mwanzo wake, tuufikishe mwisho wake. Na ujaalie kuwa mwezi uliobarikiwa ambao ndani yake Wewe unafuta vitendo viovu na kunyanyua humo daraja zetu, Ewe Mtoaji mkuu wa kila mazuri.”1061 Kidokezo: Simulizi nyingine kama hii inapatikana ndani ya al-Mustadrak kutoka kwenye al-Iqbal. 1062

DU’A YAKE WAKATI WA MWEZI MPYA – WA RAJAB NA MIEZI MINGINE 11. Katika al-Iqbal: Dua kwa ajili ya mwezi mpya wa Rajabu kama inavyopatikana ndani ya al-Da’awat: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitumia kusema: “Allahumma ahillahu ‘alaynaa bil-amni wal-imaani was-salaamati wal-islaami, rabbi wa rabbuka-llahu ‘azzwajalla.” “Ee Mungu! Ufanye (mwezi mpya huu) utujie sisi na utulivu na imani na amani na unyenyekevu (kwenye utashi Wako). Mola Wangu na Mola wako ni Allah ‘Azza wa Jalla.”1063 1061 ‘Uyun al-Akhbar ar-Ridhaa 2:70 1062 al-Mustadrak 7:440, al-Iqbal al-A’mal: 17 1063al-Iqbal al-A’mal: 627-628, Bihar al-Anwar 98:376 220


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 221

SUNAN-NABII 12. Vilevile: Imesimuliwa kwamba wakati yeye (s.a.w.w.) alipouona mwezi mpya wa Rajab, yeye alisema: “Allahumma baarik lanaa fiy rajabin wa sha’baana, wabalighnaa shahra ramadhaana, wa a’innaa ‘alaas-swiyaami wal-qiyaami, wa hifdhwi lisaani wa ghadhwa al-baswari, walaa taj’al hadhwaana minhu al-juu’a wal’atwasha.” “Ewe Mungu! Tubariki sisi katika mwezi wa Sha’aban na tufanye tuufikie mwezi wa Ramadhan; na utusaidie katika kufunga na kusimamisha swala na uzihifadhi ndimi zetu na kushusha chini macho, na usilifanye fungu letu ndani yake kuwa ni njaa na kiu.”1064 13. Vilevile: Imesimuliwa kwamba, wakati yeye Mtume (s.a.w.w.) alipoona mwezi mpya, alisoma takbira (Allahu Akbar) mara tatu, na tahlil (Laa ilaha illa-llahu) mara tatu, kisha akasema: “Alhamdulillahi al-ladhiy adh’haba shahri kadhaa wa jaa-a bishahri kadhaa.” “Kila sifa njema ni Zake Allah ‘Azza wa Jalla. aliyefanya mwezi kadhaa kupita na akaleta mwezi kadhaa.”1065

DU’A YAKE BAADA YA SWALA YA DHUHRI 14. Katika Falah al-Sa’ail: Katika riwaya yake kutoka kwa Muhammad ibn Abi Abdillah ibn Muhammad al-Tamim, kutoka kwa Abi al-Hasan Ali ibn Muhammad, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa baba zake, kutoka kwa Abi Abdillah, kutoka kwa Amirul-Mu’minin (a.s.) kuhusu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), yeye alisema: Dua yake baada ya swala ya Adhuhuri ilikuwa: “Laa ilaha ila-llahu al’adhwiymul-haliyim, laa ilaha illa-llahu Rabbul‘Arshil-kariymi. Alhamdulillahi rabbil’alamiyna. Allahumma inniy as’aluka muujibati rahmatika wa’azaima maghfiratika, wal-ghaniymata min kuli khairi, was-salaamata min kulli ithmi. Allahumma laa tada’aliy dhanban illa ghafartahu wala hammaan illa farajtahu, walaa sukmaan illa shafaytahu, walaa ‘aibaan illa satartahu, walaa rizkaan illa basatwtahu, walaa khaufan illa aamantahu, walaa suuan illa swaraftahu, walaa haajatan hiyaa laka ridhwaan waliy swalaahun illaa qadhwaitahaa, yaa arhamar-rahimiyna, aamiyna rabbil1064 Iqbal al-A’mal: 628, Bihar al-Anwar 98:176 1065 Ibid. 221


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 222

SUNAN-NABII ‘aalamiyna.” “Hapana mungu ila Allah, Mkuu, Mpole. Hapana mungu ila Allah, Mola wa Arsh ya Ukarimu. Sifa zote ni zake Allah ‘Azza wa Jalla. Mola wa ulimwengu wote. Ewe Mungu! Nakuomba kwa kile ambacho ni chanzo cha rehema Zako, na kile ambacho kinahakikishia msamaha Wako, na kunufaika kutokana na kila jema, na usalama kutokana na kila dhambi. Ewe Mungu! Usiniachie dhambi yoyote bali uwe umeisamehe, madhara yoyote bali Wewe uwe umeyaondoa, na maradhi yoyote ila uwe umeyaponya, na aibu yoyote ila uwe umeisitiri, na riziki bali iwe umeizidisha, na hofu yoyote ile bali uwe umenilinda nayo, na uovu wowote bali uwe umeuepishilia mbali, na haja yangu yoyote ile ambayo ndani yake mna radhi Yako na ambayo ina manufaa kwangu bali kwamba uwe umenijaalia kwayo; Ewe Mwingi wa rehema! Nikubalie du’a yangu hii, Ewe Mola wa ulimwengu.” 1066

DU’A YAKE BAADA YA KILA RAKAA MBILI ZA SUNA YA DHUHRI 15. Katika al-Falah al-Sa’il: Katika riwaya yake kutoka kwa Fatimah bint al-Hasan, kutoka kwa baba yake Hasan bin Ali (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akitumia kusoma dua hii baina ya kila rakaa mbili za suna ya Dhuhri: “Allahumma anta akramu maatiyyi, wa akramu mazuurin, wa khayru man tulibat ilayhil-haajaati, wa ajwadu man a’atwii, wa arham man starhama, wa ar-afu man ‘afaa, wa a‘aazzu man a’atumida ‘alayhi. Allahumma biy ilayka faaqatun, wa liy ilayka haajaatun, wa laka ‘indiy twalibatun, min dhunuubin inaa bihaa murtahanun qad awqarat dhwahriy wa awbaqatniy, wailla tarhamniy wa taghfirliy akun minalkhaasiriina. Allahumma ’atamadtuka fiyhaa taaiban ilayka, faswalli ‘alaa Muhammadin wa aalihi, wa ghfirliy dhunuubi kullihaa qadiymahaa wa hadiythahaa sirrahaa wa’alaaniyatahaa, khatwaa-ahaa wa ‘amdahaa, swaghiirahaa wa kabiirahaa, wa kulli dhanbin adhnabtuhu wa anaa mudhnibuhu, maghfirata jazmaan, laa tughaadiru dhanban waahidan, walaa aktasibu ba’adahaa muharraman abadan, waaqbal minniy al-yasiira min twaa’atika wa tajaawazliy ‘anil-kabiyri min ma’aswiyatika, yaa ‘adhwiymu innahu laa yaghfirul-‘adhwiyma illal‘adhwiymu, yas-aluhu man fiy samaawaati wal-ardhi kulli yawmin 1066 Falah al-Sa’il: 171-172 222


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 223

SUNAN-NABII huwa fiy shaanin, yaa man huwa kulli yawmin fiy shaanin, swalli ‘alaa muhammadin wa aalih waj’al-liy fiy shaanika shaana haajatiy, wa haajatiy hiya fakaaku raqabatiy minan-naari, wal-amaanu min sakhatwika, wal fauzu bi ridhiwaanika wajannatika, wa swalli ‘alaa muhammadin wa aali muhammadin, waamnun bi dhaalika ‘alaiyya wa bi kulli maa fiyhi swalaahiy. As-aluka binuurikas-satwi’i fiy dhulumaati an tuswalli ‘alaa muhammadin wa aali muhammadin, wala tufarriq bayini wa bayinahum fiy dunyaa wal aakhirati innaka ‘alaa kulli shayin qadiyrun. Allahumma wa-aktub liy ‘itqaan minan-nari mabtuulan, waj’alniy minal-muniybiyna ilayka at-tabi’iina-liamrika, al-mukhbitiyna al-ladhiyna idhaa dhukirta wajilat quluubuhum, wal-mustakmiliyna manaasikahum, was-swabiriyna fiyl-balaai, wash-shaakiriyna fiy rakhaai, wal-mutwi’iyna liamrika fiymaa amartahum bihi, walmuqiymiinas-swalaata, wal-muwtiyna zakaata, wal-mutawakiliyna ‘alayka. Allahumma adh’ifniy yaa kariimu karaamataka wa-ajzil’liy ‘atwiyyataka wal-fadhwiylata ladayka war-rahaata minka, wal wasiylata ilayka wal-manzilata ‘indaka maa takfiyni bihi kulli hawlin duunal-jannat watudhwillaniy fiy dhwilli ‘arshika yawma laa dhwilla ilaa dhwilluka, watu’adhwima nuuriy, watu’utwiniy kitaabiy bi yamiyniy, watudh’ifa hasanaaniy, watahshuraniy fiy afdhwali al-waafidiyna ilayka minal-muttaqiina, watuskinaniy fiy ‘illiyyina, waj’alniy mimman tandhuru ilayhi biwajhikal-kariymi, watatawaffanii wa anta ‘anniy raadhwin, walhiqniy bi’ibaadikas-swalihiyna. Allahumma swali ‘alaa Muhammadin wa aalihi, waqlibniy bidhaalika kullihi muflihaan munjihaan qad ghafarta liy khatwa yaya wa dhunubiy kulaha,wakafarta anniy sayyiaatiy,wa hatwat’ ta ‘anniy wizriy, shaffa’ataniy fiy jami’i hawaaijid-dunyaa wal-aakhirat fiy yusrin minka wa ‘aafiyatin. Allahumma swali ‘alaa muhammadin wa aalihi, walaa takhlut bishay’in min ‘amaliy walaa bimaa taqarabtu bihi ilayka riyaa’an walaa sum’atan walaa ashiran walaa batwiran, waj’alniy minalkhaashiyna laka. Allahummas-swalli ‘alaa muhammadin wa aalihi, wa’atiniy as-sa’aata fiy rizqiy, was-swihata fiy jismiy, wal-qunua wal’ismata, walhuda war rahmata,wal’afwa wal’aafiata, wal’yaqiina wal’maghfirata wash shukra war ridhwa waswabra,wal’ilma waswidqa,wal’bira wat taqwa,wal’hilma wat tawadhua, walyusra wat tawfiiqa. fiy badaniy, alaa twa’atika wa’ibaadatika, wa’atwiniy min rahmatika wa ridh’waanika wa ‘aafiyatika maa tusallimniy bihi min kulli balaail-aakhirati wad-dunyaa, warzukniy rahbata minka, warraghbata ilayka, wal khushuu’a laka, wal waqaara wal haya’a minka, wat-ta’adhwiyma lidhikrika, wat-taqdiysa limajdika ayyama hayaatiy hat’taa tatawaf ’faniy wa anta ‘anniy radhwiyn, Allahumma wa 223


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 224

SUNAN-NABII as’alukas-sa’ata wa al-da’ata, wal-amna wal-kifaayata, was-salaamata wasw-swaahata, wal-qunuu’a wal-‘iswmata, wal-hudaa war-rahmata, wal-yaqiyna wal-maghfirata, wa-shukra war-ridhwaa was-swabra, wal-‘ilma was-swidqa, wal-birra wat-taqwaa, wal-hilma wat-tawaadhu’a wal-yusra wat-tawfiyqa. Allahumma swalli ‘alaa muhammadin wa aalihi, wa’aswim bidhaalika ahla baytiy waqurbatiy wa ikhwaaniy fiyka wa man ahbabtu wa ahabbaniy fiyka au walaytuhu wa waladaniy min jamiy’il-mu’minina wal-mu’minaati wal-muslimiyna wal-muslimaati, wa as’aluka yaa rabbi husna dhwanna bika was-swidqa fiy attawakkali ‘alayka wa a’uudhubika yaa rabbi an tabtaliyaniy bibayyati tahmilniy dhwaruuratuhaa alaa at-taghawwuthi bishaiyn min ma’aaswiyka, wa a’uudhubika yaa rabbi an akuwna fiy haali ‘usriy au yusrin adhunna an ma’aaswiyka anjahu fiy twalibatiy min twa’atika, wa a’uudhubika min takallufi maa lam tuqadirliy fiyhi rizqan, wa maa qad’darta liy min rizqin, faswalli ‘alaa muhammadin wa aalihi wa aatiniy bihi fiy yusrin minka wa ‘aafiyatin yaa ar-rahhaamar-rahimiyna.” “Ewe Mungu! Wewe ndiye Mtukufu zaidi ambaye unakabiliwa, uliye Mkarimu zaidi unayetembelewa, Mbora ambaye kutoka kwake utimiaji wa haja unatafutwa, Mkarimu katika Upaji (utoaji), Mwenye huruma zaidi ya waonyeshao huruma, Mpole zaidi ya wale wanaosamehe na Mkuu wa wale wanaotegemewa. Ee Mungu! Mimi ni mhitaji Kwako, ninazo haja ambazo nakuomba unitimizie na ninao wajibu Kwako kwa sababu ya dhambi ambazo zimeuvunja mgongo wangu na kunishusha hadhi yangu, na kama hutakuwa na huruma juu yangu na kunisamehe basi kwa hakika nitakuwa miongoni mwa wenye hasara. Ewe Mola Wangu! Mimi nakutegemea Wewe na ninatubia Kwako, basi shusha rehma na amani juu ya Muhammad na kizazi chake, na unisamehe makosa yangu yote, yaliyopita, yaliyotendwa sirini na dhahirini, kwa kukosea kwangu au kwa makusudi, madogo na makubwa, na madhambi yangu yote ambayo nimeyatenda na ni mkosaji kwayo – msamaha ambao unayafuta kabisa, bila kubakisha hata dhambi moja; na baada yake ambapo sitatenda kamwe yale yaliyoharamishwa. Na uyakubali matendo yangu madogo ya ibada wakati sitilii maanani ukosefu wangu mkubwa juu ya kutozitii amri Zako. Ewe uliye Mkuu! Hakuna awezaye kusamehe madhambi makubwa isipokuwa Yule Mkuu. Wote wale walioko mbinguni na ardhini wanaomba kutoka Kwake; kila wakati Yuko kwenye hali ya Utukufu. 224


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 225

SUNAN-NABII Ewe uliye katika hali ya Utukufu kila siku! Mpe rehma na amani Muhammad na kizazi chake, na ziweke haja zangu katika Utukufu Wako, na haja yangu ni uhuru kutokana na Moto wa Jahannam, usalama kutokana na ghadhabu Yako na ustawi kutokana na radhi Zako na Pepo Yako; na mbariki Muhammad na kizazi cha Muhammad, na unijaalie mimi kwa hili kila lililo jema kwa ajili yangu. Nakuomba kwa nuru Yako inayoangaza katika giza, kwamba umrehemu Muhammad na kizazi chake Muhammad na usinitenganishe nao katika dunia hii na akhera, hakika Wewe unao uwezo juu ya kila kitu. Ewe Allah! Jaalia juu yangu kuachwa huru na Moto wa Jahannam milele na milele, na nifanye niwe miongoni mwa wenye kutubia, wale wanaofuata maagizo na amri Zako, wale wanyenyekevu ambao nyoyo zao zinatetemeka kwa hofu pale unapotajwa, wale ambao wamekamilisha ibada zao takatifu, wale ambao ni wenye subira wakati wa kukabiliana na mitihani, wale wenye kushukuru wanapokuwa kwenye faraja, wale ambao wanasimamisha swala, wanatoa zakat na wale wanaoweka mategemeo yao Kwako. Ewe Mkarimu! Nisidishie ukarimu Wako, na unifanyie wingi wa neema Zako, wema na faraja nyingi, na usuluhisho Kwako na daraja mbele Yako na nifanyie hili lenye kutosheleza mbele ya vitisho vyote; mbali na pepo. Na nifunike kwa kivuli cha Nguvu Yako katika siku ambayo hakutakuwa na kivuli bali Chako tu; na ifanye nuru yangu ing’are, na unipe kitabu changu kwa mkono wa kulia, na uyazidishe matendo yangu mema, na unifufue miongoni mwa makundi bora ya wachamungu, na nikae miongoni mwa wale waliotukuzwa, nifanye miongoni mwa wale unaowaangalia kwa ihsani Zako, na uichukue roho yangu ukiwa umeniridhia na nifanye niungane na waja Wako wema. Ewe Allah! Mrehemu Muhammad na kizazi cha Muhammad, na nibadilishe kwa mafanikio na ustawi, ukiwa umenisamehe makosa na dhambi zangu, na umenifutia matendo mabaya yangu yote, na umeniondolea mzigo wangu, na ukiwa umenitekelezea haja zangu zote katika dunia hii nay a akhera, katika starehe na afya njema. Ewe Allah! Mpe rehma Muhammad na kizazi chake na usivichanganye vitendo vyangu vyovyote, na vile ambavyo nimeomba kuwa karibu na Wewe, pamoja na dhamira ya kuonekana au kusikiwa na watu ambapo hapo nikawa mwenye majivuno na kiburi, na unifanye kuwa miongoni mwa wale wanyenyekevu Kwako.

225


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 226

SUNAN-NABII Ewe Allah! Mpe rehma na amani Muhammad na kizazi chake, na nijaalie wingi wa riziki yangu, na afya njema katika kiwiliwili changu, na nguvu za mwili ambazo kwazo niweze kukuabudu na kukutii Wewe; na ujaalie juu yangu rehma Yako, radhi na afya njema, ambavyo vitaniweka salama kutokana mitihani yote ya akhera na ya dunia hii; na unijaalie hofu juu Yako, na kuelekea Kwako, unyenyekevu Kwako, hadhi na haya kutoka Kwako, heshima juu ya utajo Wako, utakaso kwa ajili ya utukufu Wako – siku zote za maisha yangu, mpaka pale utakapoichukua roho yangu ukiwa uko radhi nami. Ewe Allah! Nakuomba wingi na utulivu, usalama na utoshelevu, uzima na afya, uridhikaji na staha, mwongozo na rehma, msamaha na afya njema, yakini na kusamehe, shukurani na kuridhia na subira, elimu na ukweli, wema na uchamungu, upole na taadhima, wepesi na msukumo (katika kutenda mema). Ewe Allah! Rehma na amani ziwe juu ya Muhammad na kizazi chake, na uilinde kwa hili familia yangu, jamaa wa karibu, ndugu zangu katika imani na wale niwapendao na wanaonipenda mimi kwa ajili Yako, kutoka katika waumini wote, wanaume na wanawake. Na ninakuoma Ee Mola wangu niwe na fikra njema juu Yako na uwezo wa kukuamini Wewe kikamilifu; na ninajikinga Kwako kutokana na mtihani wowote utakaonijaribu nao ambao sina uwezo wa kuuhimili na hivyo ukageuka kuwa dhambi; na najikinga Kwako. Ewe Mola Wangu, kutokana na – imma nikiwa kwenye matatizo au kwenye wepesi – kamwe kufukiria kwamba kutenda dhambi kutakuwa na manufaa zaidi katika njia yangu kuliko kukutii Wewe; na ninajikinga Kwako kutokana na kupituka mipaka kuhusiana na riziki ambayo hukunikadiria, na kutokana na ile riziki uliyonikadiria mimi; basi mshushie rehma na amani Muhammad na kizazi chake na unijaalie katika lililo jepesi kutoka Kwako na afya njema, Ewe Mwingi wa rehma.”1067

1067 Ibid, 138-141 226


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 227

SUNAN-NABII DU’A YAKE BAADA YA SWALA YA AL-FAJRI 16. Katika al-Faqih: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitumia kusema baada ya swala ya al-Fajri: “Allahumma inniy a’uudhubika minal-hammi wal-huzani, wal’ajzi wal-kasli, wal-bukhli wal-jubni, wa dhwal’i-d-diini wal-ghalabatirrijaali, wa bawaaril-ayyami wal-ghaflati, wa dhillati wal-qas’wati, wal’aylati wal-maskanati. Wa a’uudhubika min nafsin laa tashba’u, wa min qalbin laa yakhsha’u, wa min ‘aynin laa tadma’u, wa min du’aain laa yusma’u, wa min swalaatin laa tanfa’u (laa turfa’u), wa a’uudhubika min imraatin tushayyibuniy qabla awaana mashiyibiy, wa a’uudhubika min waladin yakuunu ‘alayya rabba, wa a’uudhubika min maalin yakuunu ‘alayya ‘adhaaban, wa a’uudhubika min swaahibi khadiy’atin, in raa-a hasanatan dafanahaa, wa in raa-a sayyiatan afshaahaa. Allahumma laa taj’al lifaajirin ‘alayya (‘indiy) yadan wa laa minnatan.” “Ewe Allah! Najikinga Kwako kutokana na masononeko na huzuni, ajizi na uvivu, ubakhili na woga, uzito wa deni na kuwashinda watu haki na mazungumzo yasiyo na maana ya watu, kupoteza wakati na uzembe, upotovu na ukatili, ufukara na umasikini. Na ninajikinga Kwako kutokana na nafsi isiyotosheka, na moyo usionyenyekea, na jicho ambalo halitoi machozi, na dua isiyosikiwa, na swala isiyo na manufaa (isiyonyanyuliwa juu). Najikinga Kwako kutokana na mwanamke anayenizeesha kabla ya wakati wangu, na najikinga Kwako kutokana na mtoto anayenitiisha mimi, na ninajikinga Kwako kutokana na mali ambayo ni adhabu kwangu, na ninajikinga Kwako na rafiki mwenye hadaa, anaficha kila wema anaouona na anayetangaza kila ubaya anaouona. Ewe Mungu Wangu! Usijaalie jeuri mwenye dharau kunifanyia mimi wema na usimfanye atazamie chochote kutoka kwangu mimi.”1068

1068 al-Faqih 1:335, Bihar al-Anwar 86:186

227


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 228

SUNAN-NABII

DU’A YAKE KATIKA USIKU WA KWANZA WA RAMADHANI 17. Katika al-Mustadrak kutoka kwenye al-Iqbal: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angeomba katika usiku wa kwanza wa mwezi wa Ramadhani kwa du’a hii ifuatayo: “Alhamdulillahi al-ladhiy akramaniy bika ayyuhaal-shahrulmubaaraku, Allahumma faqawwinaa ‘alaa swiyaaminaa wa qiyaamanaa wathabbit aqdaamanaa wansurnaa ‘alaal-qawmil-kaafiriina. Allahumma antal-waahidu falaa walada laka, wa antal-‘aziyzu falaa yu’izzuka shayan, wa antal-ghaniyyu wa anaal-faqiyru, wa antalmawla wa anaal-‘abdu, wa antal-ghafuuru wa anaal-mudhnibu, wa antar-rahiimu wa anaal-mukhtwiyu, wa antal-khaaliqu wa anaalmakhluuqu, wa antal-hayyu wa anaal-mayyitu, as’aluka birahmatika an taghfirliy watarhamniy watajaawaz ‘anniy, innaka ‘alaa kulli shaiyn qadiyrun.” “Sifa zote ni kwa ajili ya Allah, ambaye kwa wewe amenikarimu, ewe mwezi uliobarikiwa. Ewe Mungu Wangu! Tupe nguvu katika swaumu yetu na swala zetu, na utufanye madhubuti miguu yetu na utunusuru dhidi ya kaumu ya waliokufuru. Ewe Mungu! Wewe ni Mmoja na huna mtoto; na ni wa Pekee ambaye hakuna anayefanana nawe; na Mwenye Nguvu hakuna kinachokufanya uwe na nguvu. Mkwasi na mimi ni masikini; Wewe ndiye Mola na mimi ni mja Wako; Wewe ndiye Mwenye kusamehe na mimi ni mwenye dhambi; Wewe Mwingi wa huruma nami ni makosani; Wewe ni Muumba na mimi ni kiumbe; Wewe uko hai na mimi ni mfu; nakuomba kwa rehma Zako, unisamehe na unihurumie na uzipuuze dhambi zangu, hakika Wewe ni Mwenye uwezo juu ya kila kitu.”1069

1069 al-Mustadrak 7:446, Bihar al-Anwar 98:74, Iqbal al-A’mal: 63. 228


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 229

SUNAN-NABII

DU’A YAKE WAKATI WA ASUBUHI NA JIONI 18. Ndani ya Tafsiir ya Ali ibn Ibrahim: Katika riwaya yake kutoka kwa Hashim ibn Salim kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) katika Hadith ya Mi’raj. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Ewe Mungu! Umetoa ubora kwa mitume Wako, hivyo nipe na mimi ubora.” Hivyo Mwenyezi Mungu akasema: “Ninakupa maneno mawili kutoka chini ya Arshi Yangu.” “Laa hawla wa laa quwwata illa billahi wa laa man’jaa-a minka illa ilayka.” “Hapana uwezo na hakuna nguvu ila Mwenyezi Mungu na hakuna usalama kutoka kwako bali pamoja na Wewe.” Yeye Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Malaika wamenifundisha cha kusema wakati wa asubuhi na wa jioni: ‘Allahumma inna dhulmiy asbaha mustajiiran bi’af-wika, wa dhanbiy asbaha mustajiiran bimaghfiratika, wa dhulliy asbaha mustajiiran bi’izzatika, wafaqriy asbaha mustajiiran bighinaaka, wa wajhiy albaliyl-faaniy asbaha mustajiiran biwajhikad-daaimil-baqiyl-ladhiy laa yafniy.’ ‘Ee Mungu! Dhulma yangu imetafuta kimbilio kwenye huruma Yako, na dhambi yangu imetafuta kimbilio kwenye msamaha Wako, na udhaifu wangu umetafuta kimbilio kwenye Ukubwa Wako, na ufakiri wangu umetafuta hifadhi kwenye utajiri Wako, na kuwepo kwangu kwa mpito kumetafuta hifadhi kwenye Umilele Wako usiofutika.’ ….. na ninasema vivi hivi na jioni pia.’” 1070

1070 Tafsiir al-Qummi 2:11, Bihar al-Anwar 86: 238 na 18: 329

229


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 230

SUNAN-NABII DU’A YAKE WAKATI WA MAWIO YA JUA 19. Katika Muhasabat al-Nafsi ya Ibn Tawus, kutoka kwenye kitabu cha al-Rabi kutoka kwa Muhammad al-Mustakin: Katika simulizi yake kutoka kwa Abi Ja’far (a.s.) ambaye amesema: Pale wekundu wa jua ulipofikia kwenye kilele cha mlima (wakati wa asubuhi), machozi yangetiririka machoni mwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na angesema: “Allahumma amsiy dhulmiy mustajiiran bi’af’wika, wa amsat dhunuubiy mustajiiran bimaghfiratika, wa amsiy khawfan mustajiiran biamnika, wa amsii dhwa’ifiy mustajiiran biquwwatika, wa amsii wajhiyalbaaliyal-faaniy mustajiiran biwajhikal-daaimil-baqiy, albisniy ‘aafiyataka, wa ghashniy birahmatika, wajalilniy karaamataka, waqiniy sharra khalqika minal-jinni wal-insiy yaa Allahu yaa rahmaanu yaa rahiymu.” “Ewe Mungu! Siku imewadia wakati dhulma yangu imetegemea kwenye Msamaha Wako, na dhambi yangu imetegemea kwenye Maghfira Yako, hofu yangu imetegemea kwenye Usalama Wako, udhaifu wangu umetegemea kwenye Nguvu Zako na uhai wangu wa mpito umetegemea kwenye Uhai Wako wa Milele usiokatika. Nipe afya njema na unifunike kwa rehma Zako, na unitukuze kwa Utukufu Wako na unikinge na shari ya viumbe Wako, miongoni mwa majinni na watu. Ewe Mungu Mwingi wa rehma Mwenye kurehemu.” 1071

KUTOKA KWENYE MAOMBI YAKE YA KAWAIDA 20. Ndani ya al-Bihar, kutoka kwenye al-Da’awat al-Rawandi: Kutoka kwenye dua za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ilikuweko: “Yaa man adh’haral-jamiyla wa sataral-qabiyha, yaa man yahtikalsitra wa lam yuwaaghidh bil-jariyrati, yaa adhwiymal-‘af’wi, yaa hasanat-tajaawuzi, yaa waasi’al-maghfirati, yaa basitwal-yadayini birahmatika, yaa swaahiba kulliy najwiy, wa muntahaa kulli shak’waa, yaa muqiylal-‘asharaati, yaa kariymas-swafhi, yaa ‘adhwiimal-manna, yaa mubtadiaan bin-na’aami qabla istihqaaqihaa, yaa rabbaahu, yaa 1071 Muhasabat al-Nafsi: 30 230


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 231

SUNAN-NABII sayyidaahu, yaa amlaahu, yaa ghaayata raghbataahu. As’aaluka bika yaa Allahu an laa tushawwihu khalqiy bin-naari, wa an taqdhwiya liy hawaaija aakhiratiy wa dunyaaya, wataf’alniy kadhaa wa kadha, watuswalli ‘alaa muhammadin wa aali muhammadin.” “Ewe unayedhihirisha mazuri na kusitiri (matendo) mabaya! Ewe ambaye hukufichua siri na hukumuadhibu mkosaji! Ewe Mwingi wa Msamaha! Ewe Mbora wa kusamehe! Ewe Mwingi wa wasaa wa maghfira! Ewe ambaye mikono yake iko wazi kwa huruma! Ewe Mwenye kusikia minong’ono yote! Ewe ambaye malalamiko yote yaja kwake! Ewe Mkamilifu katika kusamehe! Ewe Mwingi wa ukarimu! Ewe Mtoaji wa rehma hata kabla hazijastahili! Ee Mungu! Ewe Mola! Ewe Mlezi! Ewe Mkusudiwa wa matamanio yangu! Nakusihi, Ewe Allah! Usiniteketeze na kuniharibu kwa moto wa Jahannam, na unitimizie tamaa zangu za akhera na za dunia hii na ufanye hili na lile kwa ajili yangu ….. rehma na amani zimshukie Muhammad na juu ya kizazi cha Muhammad.”1072 21. Sheikh al-Mufid ndani ya al-Amali: Kutoka kwa Jabir al-Ju’fi, kutoka kwa Abi Ja’far Muhammad ibn Ali (a.s.), kutoka kwa Jabir ibn Abdillah Ansari, kutoka kwa Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) ambaye amesema katika hadith: Jibril alisema: “Ewe Muhammad! Sema haya wakati wote: “Alhamdulillah rabbil-‘aalamiyna – Sifa zote ni za Allah, Mola wa ulimwengu wote.”1073 22. Katika al-Muhaj: Kutoka kwenye dua na maombi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) imo ile dua iitwayo Du’a al-faraj ambayo ni hii ifuatayo: “Bismillahir-Rahmaanir-Rahiimi. Allahumma inniy as’aluka Yaa Allah, Yaa Allah, Yaa Allah, yaa man ‘alaa faqahara, wa yaa man batwana fakhabara, wa yaa man malaka faqadara, yaa man ‘ubida fashakara, wa yaa man ‘uswiyaa faghafara, yaa man laa yuhiytu bihilfikaru, yaa man laa yudrikuhu baswaru, wa yaa man laa yakhfii ‘alayhi athara, yaa ‘aaliyal-makaani, yaa shadiydal-arkaani, yaa munzila al-qur’aani, yaa mubaddila zamaani, yaa qaabilal-qurbaani, yaa nayyiral-burhaani yaa ‘adhwiima shaa-ana, yaa dhaal-manni walihsaani, wayaa dhaal-‘izzi was-sultwaani, yaa rahiimu yaa rahmaanu, yaa rabbil-arbaabi, yaa tawwaabu yaa wahhaabu, yaa mu’utiqarriqaabi, yaa munshia sahaabi, yaa man haythu maa du’iya ajaaba, yaa 1072 Bihar al-Anwar 95:164 1073 Amali ash-Sheikh al-Mufid: 347 231


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 232

SUNAN-NABII murakhiswal-as’aari, yaa munaazzilal-amtwaari, yaa munbital-ashjaari fiyl-ardhi al-qifaari, yaa mukhrijan-nabaati, yaa muhiiyalam’waati, yaa muqiylal-‘atharaati, yaa kaashifal-kurubaati, yaa man laa tadhjuruhul-as’waatu, walaa tushabbihu ‘alayhi al-lughaatu, walaa taghshaahu dhulumaatu, yaa mu’utwiya suulaati, yaa waliyyalhasanaati, yaa daafi’al-baliyaati, yaa qaabila swadaqaati, yaa qaabila taubaati, ya ‘aalimal-khafiyyaati, yaa mujiybad-da’awaati, yaa raafi’a, yaa raafi’a darajaati, yaa qaadhwiyal-haajaati, yaa raahimal’aabarati, yaa munjiha twalibaati, yaa munzilal-barakaati, yaa jaami’ash-shataati, yaa raadda maa kaana faata, yaa jamaalal-ardhiina wa samaawaati, yaa saabighan-ni’aami, yaa kaashifal-alami, yaa shaafiyas-saqami, yaa ma’adinal-juwdi wal-karami, yaa aj’wadalaj’wadiina, yaa akramal-akramiyna, yaa asma’as-saami’iina, yaa abswaran-naadhiriyna, yaa arhamar-rahiimiyna, yaa akrabal-akrabiyna, yaa ilaahal-‘aalamiina, yaa ghiyaathal-mustaghithiina, yaa jaaralmustajiriina, yaa mutajaawizan ‘anil-musiyiina, yaa man laa ya’aajalu ‘alaal-khaatwiyina, yaa fakaakal-ma-asuwriina, yaa mufarrija ghammi lam ghamuumiina, yaa jaami’a limutafariqiina, yaa mudrikal-haaribiina, yaa ghaayata twalibiina, yaa swaahiba kulli ghariibin, yaa muwnisa kulli wahiydin, yaa raahima shaykhil-kabiiri, yaa raazika twifli swaghiiri, yaa jaabaral-‘adhwiimi al-kasiyri, yaa ‘iswmatalkhaaifil-mustajiiri, yaa man lahut-tadbiiru wa ilayhi takdiiru, yaa manil-‘asiiru ‘alayhi sahlun yasiirun, yaa man huwa bikulli shaiin khabiirun, yaa man huwa ‘alaa kulli shaiin qadiirun, yaa khaaliqa samaai wal-qamaril-muniiiri, yaa faaliqal-isbaahi, yaa mursila riyaahi, yaa baa’ithal-arwaahi, yaa dhaal-juudi wa samaahi, yaa man biyadihi kullu miftaahi, yaa ‘imaada man laa ‘imaada lahu, yaa sanada man laa sanada lahu, yaa dhukhra man laa dhukhra lahu, yaa ‘izza man laa ‘izza lahu, yaa kanza man laa kanza lahu, yaa hirza man laa hirza lahu, yaa ‘auna man laa ‘auna lahu, yaa rukna man laa rukna lahu, yaa ghiyaatha man laa ghiyaatha lahu, yaa ‘adhwiimal-manni, yaa kariimal-‘af’wi, yaa hasanat-tajaawuzi, yaa waasi’al-maghfirati, yaa baasitwal-yadayni bir-rahmati, yaa mubtadaan bin-ni’ami qabla istihqaaqihaa, yaa dhaal-hujjatil-baalighati, yaa dhaal-mulki walmalakuuti, yaa dhaal’izzi wal-jabaruuti, yaa man huwa hayyun laa yamuutu. As-aluka bi’ilmikal-ghuyuuba, wa bima’arifatika maa fiy dhwamaairil-quluubi, wa bikulli ismin huwa laka stafaiytuhu linafsika, aw anzaltuhu fiy kitaabin min kutubika, aw staatharta bihi fiy ‘ilmilghaiybi ‘indaka, wa biasmaaikal-husna kullihaa hattaa-ntahi ilaa ismikal-adhwiimil-a’adhwami al-ladhiy fadhaltahu ‘alaa jamii’i asmaaika. As-aluka bihi, as-aluka bihi, as-aluka bihi an tuswali ‘alaa 232


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 233

SUNAN-NABII muhammadin wa aalihi, wa an tuyassira liy min amriy maa akhaafu ‘usrahu, watufarrij ‘anniyl-hamma wal-ghamma wal-karba, wamaa dhwaqa bihi swadriy, wa ‘iyla bihi swabriy, fainnahu laa yaqdiru ‘alaa farajiy siwaaka waf’alniy maa anta ahluhu, yaa ahlan-naqwaa wa ahlal-maghfirati, yaa man laa yakshiful-karba ghairuhu, wa laa yujaliyl-huzna siwaahu, wa laa yufarrij ‘anniy illa huwa, ikfiniy sharra nafsiy khaaswatan, washarran-naasi ‘aammatan, waaswlih liy shaa’niy kullahu, wa aswlih umuuriy, waqdhwi liy hawaaijiy, waj’al liy min amriy farajaan wa makhrajaan, fainaka ta’alamu wa laa a’aalamu, watuqaddiru walaa uqaddiri, wa anta ‘alaa kulli shaiyn qadiyrun, birahmatika yaa arhamar-rahimiyna.” “Kwa jina la Allah, Mwingi wa rehma, Mwenye kurehemu. Ee Allah! Nakuoma Ee Allah! Ee Allah! Ee Allah! Ewe Yule ambaye ametukuka na anamiliki! Ewe Yule ambaye amefichika na Mtambuzi! Ewe Yule ambaye Bwana na mwenye kukadiria! Ewe ambaye unaabudiwa na utoaye malipo! Ewe Yule ambaye hatiiwi na bado anasamehe! Ewe Yule ambaye hazingatiwi na fikra! Ewe Yule ambaye hatambuliwi na uoni! Ewe Yule ambaye hakuna alama inayobaki kufichika! Ewe Uliye juu zaidi! Ewe thabiti katika kusaidia! Ewe Ambaye Umeishusha Qur’ani! Ewe Mpitishaji wa wakati! Ewe Mkubali makafara! Ewe Hujja ya dhahiri! Ewe Mbora wa sifa! Ewe Mwenye fadhila na neema! Ewe Mwenye nguvu na mamlaka! Ewe Mwingi wa rehma! Ewe Mwenye huruma! Ewe Bwana wa mabwana! Ewe Mwenye kusamehe! Ewe Mpaji! Ewe Mfunguaji wa pingu! Ewe Mwenye kunyanyua mawingu! Ewe Muitikiaji kila anapoitwa! Ewe Mpunguzaji wa gharama! Ewe Mnyeshaji wa mvua! Ewe Mpanzi wa miti kwenye ardhi kame! Ewe mchipuaji wa mimea (kutoka ardhini)! Ewe Mhuishaji wa wafu! Ewe Mfutaji wa makosa madogo! Ewe Mwondoshaji wa matatizo! Ewe ambaye hukasirishwi na sauti (za wale wanaokuomba), wala ambaye maneno kamwe hayafichiki Kwake, wala ambaye giza halimfuniki Yeye. Oh Mtimizaji wa maombi! Msimamiaji wa mema! Ewe mwondoshaji wa shida na dhiki! Ewe Mwenye kukubali sadaka! Ewe Mwenye kukubali toba! Ewe Mjuzi wa yaliyojificha! Ewe Mwenye kujibu du’a! Ewe Mnyanyuaji wa hadhi! Ewe mtimizaji wa haja na mahitaji! Ewe Mwenye huruma juu ya wale wanaotokwa na machozi! Ewe Mtimizaji wa maombi! Ewe Mtoaji wa neema! Ewe Mkusanyaji wa vitu vyote vilivyotawanyika! Ewe ambaye unavihuisha 233


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 234

SUNAN-NABII vile vilibyokwishakufa! Ewe Mpambaji wa ardhi na mbingu! Ewe Mwingi wa neema! Ewe Muondoshaji wa maumivu! Ewe Mponyaji wa maradhi! Ewe Chanzo cha ukarimu na upaji! Ewe Mpaji zaidi ya wapaji! Ewe Mkarimu zaidi ya wakarimu! Ewe Msikivu zaidi ya wasikivu! Ewe Mwenye kuona zaidi ya waonaji! Ewe Mwenye huruma zaidi ya wenye huruma! Ewe wa karibu zaidi ya walio karibu! Ewe Mola wa ulimwengu! Ewe Msaidizi wa wale wanaotafuta msaada! Ewe Mlinzi wa wale wanaotafuta ulinzi! Ewe Msamehevu wa wale walio na makosa! Ewe ambaye hafanyi haraka katika kuwaadhibu wahalifu! Ewe Muacha huru watumwa! Ewe Mfariji wa huzuni za wenye huzuni! Ewe Muunganishaji wa wale waliotengana! Ewe Mwangalizi wa wale wanaokimbia! Ewe Lengo la watafutaji! Ewe Sahiba wa kila mgeni! Ewe Mwenza wa kila mpweke! Ewe Mwenye huruma kwa wazee! Ewe Mfadhili kwa watoto wadogo! Ewe Muungaji wa mifupa iliyovunjika! Ewe Ngome kwa mtafutaji kinga mwenye hofu! Ewe Ambaye anatawala na kukadiria! Ewe Ambaye kwa ajili yake lile gumu huwa jepesi na rahisi! Ewe Ambaye anatambua vitu vyote! Ewe Ambaye ana uwezo juu ya kila kitu! Ewe Muumba wa mbingu na mwezi unaong’ara! Ewe Mpasuaji wa mawio! Ewe Mpeperushaji wa upepo! Ewe Mhuishaji wa roho! Ewe Ambaye anamiliki ukarimu na uvumilivu! Ewe Ambaye mikononi Mweke zimo funguo zote! Ewe Nguzo kwa yule ambaye hana msaada! Ewe Ngao kwa yule ambaye hana wa kumlinda! Ewe Mwenye kumruzuku yule ambaye hana riziki! Ewe Muweza kwa ajili ya yule asiye na uwezo! Ewe Hazina kwa yule asiye na kitu! Ewe Hifadhi kwa yule asiye na kimbilio! Ewe Msaidizi kwa ajili ya yule asiye na msaidizi! Ewe Msingi kwa asiyekuwa na msingi! Ewe Mhudumiaji kwa yule asiye na wa kumhudumia! Ewe Mtoa matumaini makuu! Ewe Mkarimu katika kusamehe! Ewe Mbora wa kukubali makosa! Ewe Mwingi wa msamaha! Ewe ambaye mikono yake iko wazi kwa rehema! Ewe Mtoaji wa neema kabla hazijahitajiwa! Ewe Mwenye huja isiyopingika! Ewe Mmiliki wa Ufalme na mamlaka! Ewe Mwenye nguvu na uwezo! Ewe Uliye hai na ambaye hutakufa kamwe! Nakuomba kwa elimu yako ya ghaibu, na kwa kujua Kwako yale yaliyo kwenye vina vya nyoyo, na kwa kila jina ambalo umejichagulia Mwenyewe au ulilolionyesha ndani 234


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 235

SUNAN-NABII ya Kitabu kutoka miongoni mwa Vitabu Vyako au ulilolificha kwenye elimu yako ya ghaib; na kwa majina Yako yote mazuri hadi kufikia kwenye Jina Lako kubwa kabisa na la juu mno ambalo umelinyanyua juu ya majina Yako yote mengine. Nakuomba kwalo hilo! Nakuomba kwalo hilo! Nakuomba kwalo hilo! Kwamba umshushie rehma na amani juu yake Muhammad na juu ya kizazi cha Muhammad, na kwamba uniwepesishie lile ambalo nalihofia kwamba litakuwa gumu, na kwamba uniondolee huzuni, masononeko na shida, na kwa kila chenye kunitia wasiwasi na kudhoofisha subira yangu, kwani kwa hakika hakuna mwenye uwezo wa kunifariji katika hayo kuliko Wewe; na unifanyie kwa namna inayokupendeza Wewe, Ewe Mwenye kustahili kuogopwa na Mwenye kustahiki (kutoa) msamaha! Ewe ambaye mwingine zaidi Yako hawezi kuyaondoa matatizo na hakuna anayeweza kuondoa huzuni, na hakuna anayeweza kuniokoa mimi ila Yeye! Nilinde kutokana na uovu wa nafsi yangu hasa na kutokana na uovu wa watu kwa jumla; na niwepesishie mambo na uninyooshee masuala yangu yote, na unitimizie haja zangu, na unipe kimbilio na wokovu katika hali yangu; kwani hakika Wewe unajua na mimi sijui, na Wewe una uwezo mimi sina uwezo, na Wewe unao uwezo juu ya kila kitu – kwa Rehema Zako Ewe Mwingi wa Rehma wa wenye rehema.1074 23. Vilevile katika Muhaj al-Da’awat: Kutoka kwa Muhammad ibn al-Hasan alSaffar: Katika riwaya yake kutoka kwa as-Sadiq (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akiomba kwa du’a hii: “Allahumma j’alniy swabuuran, waj’alniy shakuuran, waj’alniy fiy amaanika.” “Ewe Allah! Nijaalie kuwa mwenye subira, na unijaalie kuwa mwenye kushukuru, na unijaalie kuwa kwenye amani Yako.”1075 24. Katika al-irshad ya ad-Daylami: Yeye Mtume (s.a.w.w.) angeomba dua na kusema: 1074 Muhaj al-Da’awat: 90 1075 Ibid, 70 235


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 236

SUNAN-NABII “Allahumma’qsim lanaa min khashyatika maa yahuulu baiynanaa wa baiyna ma’aswiyatika, wa min twaa’atika maa tubalighnaa bihi jannataka wa minal-yaqiini maa yuhawwinu ‘alaynaa min maswaaibidduniyaa, wamatti’naa bi-asmaa’inaa wa abswaarinaa wansurnaa ‘alaa man ‘aadaanaa, walaa taj’ali duniya akthara hamminaa, walaa tusalitw ‘alaynaa man laa yarhamunaa, Allahumma lakal-hamdu wa ilaykal-mushtakaa wa antal-musta’anu, wa fiymaa ‘indaka minarraghabati wa ladaiyka ghayaatul-twalibati. Allahumma aamin raw’atii wastur ‘awratii. Allahumma aswlih diynanaal-ladhiy huwa ‘ismatu amrinaa, wa aswlihlanaa duniyaanaal-latiy fiyhaa ma’ashunaa, wa aswlih aakhiratanaal-latiy ilayhaa munqalabunaa waaj’alil-hayaata ziyaadata lanaa fiy kulli khaiyrin, wal wafaata raahata lanaa min kulli suuin. Allahumma inna nas-aluka mujibaati rahmatika wa ‘azaaima maghfiratika wal ghaniymata min kulli birri wa salaamata min kulli ithmi, yaa mawlwi’a kulli shakwaa, wa shaahida kulli najwaa, wa kaashifa kulli bal’waa, fainaka taraa walaa turaa, wa anta bil-mandharil-a’alaa. As’alukal-jannataa wa maa yuqarribu ilayhaa min qawlin aw fi’ilin. Wa a’udhubika minan-nari wa maa yuqaribu ilayhaa min qawlin aw fi’ilin. Allahumma inniy as-aluka khaiyral-khaiyri ridhwaanaka wal jannata, wa a’uudhubika min sharril-sharri sakhatuka wan-naaru. Allahumma inniy as-aluka khaiyra maa ta’alamu wa a’udhubika min sharri maa ta’alamu, fainnaka anta ‘allamul-ghuyuubi.” “Ewe Allah kutoka kwenye hofu juu Yako kile ambacho kitaweza kutuondoa sisi kutoka kwenye maasia Yako na (utugawie) kutoka kwenye utii Wako kile ambacho kitaweza kutupatia pepo, na kutoka kwenye yakini ambayo itaweza kurahisisha matatizo ya dunia hii; na utupe sisi matumizi endelevu ya kusikia na kuona kwetu, na utusaidie dhidi ya maadui zetu, na usiifanye dunia hii kuwa yenye kutushughulisha kukubwa, na usitoe utawala juu yetu kwa wale ambao hawana huruma juu yetu. Ewe Allah! Sifa njema zote ni Zako. Kwako Wewe ndiko anakorejelea mlalamikaji na Wewe ndiwe Msaidizi; Wewe unacho kile kinachohitajiwa na Kwako ndiko ulikolala mwisho wa matakwa yetu yote. Ewe Allah! Itulize hofu yangu na uyafiche makosa yangu. Ewe Allah! Tunyooshee dini yetu ambayo ndio kinga juu ya mambo yetu, na utuwepesishie dunia yetu kwani ndimo mahali tunamoishi, na ututengenezee akhera yetu kwani ndiyo hatima yetu ya mwisho; na yafanye maisha (ya dunia hii) zaidi kwetu kwa kila jema, na kifanye kifo kuwa ni nafuu kwetu sisi juu ya kila uovu. Ewe Allah! Nakuomba Wewe kila kile ambacho kimo kwenye njia ya 236


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 237

SUNAN-NABII Rehma Zako, na kile kinachohakikishia Msamaha Wako, na mafanikio katika kila jema, na usalama kutokana na kila dhambi. Ewe ambaye Kwako wote ndiko wanakolalamikia! Ewe Shahidi wa kila mahusiano ya siri! Ewe Muondoshaji wa kila balaa! Hakika Wewe unaona bali huwezi kuonekana, na Wewe uko juu ya kila mandhari; mimi ninakuomba pepo na kila kinachonisogeza karibu nayo kutokana na maneno na vitendo, na ninajikinga Kwako kutokana na moto wa Jahannam na chochote kinachonisogeza karibu nao kutokana na maneno na vitendo. Ewe Allah! Nakuomba ubora wa radhi Yako njema na pepo, na najikinga na Kwako kutokana na ubaya wa ghadhabu Yako na moto wa Jahannam. Ewe Allah! Nakuomba lile jema unalolijua Wewe na naomba kinga kutokana na lile ovu baya unalolijua Wewe; kwani kwa hakika Wewe ni Mjuzi wa yaliyo ghaib.” 1076 25. Katika Jami’ al-Akhbar: Ni du’a iliyosimuliwa kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Allahumma inniy a’udhubika min suw-il-qadhwaai wa suw-il-qadari, wa suw-il-mandhari fiy ahli wal-maali wal-waladi.” “Ewe Allah! Najikinga Kwako na baya ulilonikadiria na hatima mbaya na jicho baya lenye madhara kwa familia yangu, mali na wanangu.”1077 26. Vilevile kutoka kwenye dua zake yeye (s.a.w.w.): “Allahumma inniy a’udhubika min ghiynan yut’ghiniy, wa faqrin yunsiyniy, wa hawaa yurdiyniy, wa ‘amalin yukhziyniy, wa jaarin yuwdhiyniy.” “Ewe Allah! Najikinga Kwako kutokana na mali itakayonifanya nipituke mipaka, na kutokana na umasikini utakaonifanya nisahau (neema Zako), na kutokana na tamaa itakayoniangamiza, na kutokana na kitendo kitakachoniaibisha na kutokana na jirani mwenye kuniudhi mimi.” 1078

27. Vile vile kutoka kwenye dua zake Mtume (s.a.w.w.): 1076 al-Irshad ad-Daylami: 82 1077 Jami’ al-Akhbar: 132 1078 Ibid, 237


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 238

SUNAN-NABII “Allahummaj’alnaa mash’ghuuliyna bi-amrika, aaminiiyna bi-wa’adika, ayisiyna min khalqika, aanisiyna bika, mustawhishiina min ghayrika, raadhiyna bi-qadhwaaika, swaabiriyna ‘alaa balalaika, shaakiriyna ‘alaa ni’amaaika, mutaladdhidhiyna bi-dhikrika, farihiyna bikitaabika, munaajiyna iyyaaka aanaa-a layli wa atwraafan-nahaari, musta’iddiyna lilmauti, mushtaaqiyna ilaa liqaaika, mubghidhwiyna lil-duniyaa, muhibbiyna lil-aakhirati, wa aatinaa maa wa’adtanaa ‘alaa rusuulika, walaa tukhzinaa yawmal-qiyaamati innaka laa tukhliful-mi’aadi.” “Ewe Allah! Tufanye tuwe wenye kushughulika katika kufuata amri Zako, kuamini katika ahadi Yako, kutopoteza matumaini katika maumbile Yako, kuwa karibu Nawe, kuhisi kukataliwa na wengine wasiokuwa Wewe, tuwe tumeridhishwa na Wewe pamoja na hukumu Zako, wenye subira kwa mitihani Yako, wenye shukurani juu ya neema Zako, wenye kufurahia utajo Wako, na furaha kwa Kitabu Chako, kunong’ona nawe katika giza la usiku na mwanga wa mchana, kuwa tayari kwa kifo, kuwa na shauku ya kukutana Nawe, kuichukia dunia hii na kuipenda ya akhera, na utupe kile ulichotuahidi kupitia kwa Mtume Wako na usituhuzunishe sisi katika Siku ya Kiyama, hakika Wewe si Mwenye kuvunja ahadi.”1079 28. Katika al-Kafi: Katika riwaya yake kutoka kwa Ahmad ibn Muhammad ibn Khalid ambayo aliihusisha kwa mmoja wa Ma’asum ambaye amesema: Jibril (a.s.) alikuja kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na akamwambia: “Mola Wako anakwambia: Kama unataka kuniabudu Mimi wakati wa mchana na usiku kama ninavyostahiki kuabudiwa, basi nyanyua mikono yako juu, Kwangu na useme: “Allahumma lakal-hamdu hamdan khaalidan ma’a khuluudika, wa lakal-hamdu hamdan laa muntahaa lahu duwna ‘ilmika, wa lakalhamdu hamdan laa amada lahu duwna mashiyyatika, wa lakal-hamdu hamdan laa jazaa-a liqaailihi illaa ridhaaka. Allahumma lakal-hamdu kulluhu wa lakal-mannu kulluhu, wa lakal-fakhru kulluhu, wa lakalbahaau kulluhu, wa lakan-nuuru kulluhu, wa lakal-‘izzatu kulluhaa, wa lakal-jabaarutu kulluhaa, wa lakal-‘adhaamatu kulluhaa, wa lakalduniyaa kulluhaa, wa lakal-aakhiratu kulluhaa, wa lakallaylu wannahaaru kulluhu, wa lakal-khalqu kulluhu, wabiyadikal-khaiyru kulluhu, wa ilayka yarji’ul-amru kulluhu, ‘alaaniyyatuhu wasirruhu. 1079 Ibid

238


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 239

SUNAN-NABII Allahumma lakal-hamdu hamdan abadaan, anta hasanul-balaai, jaliylu thanaai, saabighul-na’amaai, ‘adlull-qadhwaaai, jaziylul-‘atwaai, hasanul-aalaai, ilaahu man fiyl-ardhi wa ilaahuman fiys-samaai. Allahumma lakal-hamdu fiys-sab’i shidaadi, wa lakal-hamdu fiyl-ardhil-mihaadi, wa lakal-hamdu twaaqatal-‘ibaadi, wa lakal-hamdu sa’atal-balaadi, wa lakal-hamdu fiyl-jibaalil-awtaadi, wa lakal-hamdu fiyl-layli idhaa yaghshaa, wa lakal-hamdu fiyn-nahaari idhaa tajallaa, wa lakal-hamdu fiyl-aakhirati wal-uwlaa, wa lakal-hamdu fiy mathaaniy wal-qur’aanil-‘adhiimi. Wa subhaanaka llahu wa bihamdihi wal-ardhu jamiy’aan qabdhwatuhu yawmal-qiyaamati was-samaawaatu matw’wiyyatun biyamiynihi, subhaanahu wata’alaa ‘ammaa yushrikuuna, subhaana llahu wabihamdihi, kullu shaiyn haaliku illa wajhahu. Subhaanaka rabbanaa wata’aalayta watabaarakta wataqaddasta, khalaqtu kulli shaiyn biqudratika, waqaharta kulli shaiyn bi’izzatika, wa’alwata fawqa kulli shaiyn bi-irtifaa’ika, waghalabta kulli shaiyn biquwwatika, wabtada’ata kulli shaiyn bihikmatika wa’ilmika, waba’ath’tar-rusula bikutubika, wahadaiytas-swaalihiyna bi’idhnika, wa ayyadtal-mu’miniina binaswrika, waqahartal-khakqa bi-sultwaanika, laa ilaha illa anta, wahdaka laa shariyka laka, laa na’abudu ghaiyraka, walaa nas’alu illa iyyaaka, wa laa narghabu illa ilayka, anta mawdhwi’u shak’waanaa, wa muntahaa raghbatinaa, wailaahunaa wa maliykunaa.” “Ewe Allah! Sifa zote ziwe juu Yako – sifa ambazo ni za daima na Umilele Wako. Sifa zote ziwe juu Yako – sifa ambazo hazikatiki bali kwa elimu Yako. Sifa zote ziwe juu Yako – sifa ambazo hazina ukomo katika kudumu bali kwa Utashi Wako. Sifa zote ziwe juu Yako – sifa ambazo hazitoi malipo kwa mtamkaji mbali na radhi Yako, Ee Allah! Sifa zote ni kwa ajili Yako, na fadhila zote zinatoka Kwako, na fahari yote ni Yako, na utukufu wote ni Wako, na nuru yote ni Yako, na heshima yote ni Yako, na uwezo wote ni Wako, na nguvu zote ni Zako, na ulimwengu wote ni Wako, na akhera yote ni Yako, na usiku na mchana vyote ni Vyako, na viumbe vyote ni Vyako, na mikononi Mwako yamo mazuri yote, na Kwako ndiko yanarejea mambo yote, ya dhahiri na ya siri. Ewe Allah! Sifa zote ni kwa ajili Yako – sifa za milele. Wewe ndiye Mbora wa kutoa Mitihani, Mwenye kustahiki sifa zaidi, Mwenye wasaa katika rehema, Muadilifu katika kuhukumu, Mkarimu katika upaji, Mtoaji bora wa neema, Mola wa vyote vilivyomo duniani na Mola wa 239


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 240

SUNAN-NABII vilivyo mbinguni. Ee Allah! Sifa zote ni kwa ajili Yako katika miaka saba ya matatizo na Kwako Wewe sifa zote katika upeo wote mpana wa dunia, na sifa zote ni kwa ajili Yako kwa kiasi chote cha uwezo wa waja Wako, na sifa zote ni kwa ajili Yako hadi kwenye mipaka ya ardhi, na sifa zote ni kwa ajili Yako katika milima ambayo imesimama kama vigingi, na sifa zote ni kwa ajili Yako katika ule usiku wakati unaposhusha utaji (pazia), na sifa zote ni kwa ajili Yako katika siku inapong’ara kwa mwangaza, na sifa zote ni kwa ajili Yako katika dunia ya akhera na ile ya kabla, na sifa zote ni kwa ajili Yako katika zile Aya Saba Zinazorudiwa mara kwa mara na Qur’ani Tukufu. Utukufu na Sifa kwa Allah, na ardhi yote itakuwa kwenye mshiko Wake katika Siku ya Kiyama na mbingu itakunjwa mkono Wake wa kulia. Utukufu uwe Kwake, na Yeye ameapukana na washirika wanaomshirikisha Naye; Utukufu na sifa ziwe kwa Allah, kila kitu kitatoweka isipokuwa Yeye. Utukufu uwe Kwako Mola Wetu, uliye Adhimu, Mtakatifu, Mtukufu; Uliyeumba kila kitu kwa Uwezo Wako na unakizidi kila kitu kwa mamlaka Yako, na umepanda juu ya kila kitu kwa ukuu Wako, na umekishinda kila kitu kwa nguvu Zako, na umekianzisha kila kitu kwa hekima Zako na elimu, na umetuma mitume pamoja na Vitabu Vyako, na umewaongoza wachamungu kwa ruhusa Yako, na umewasaidia waumini kwa msaada Wako mtukufu, na umetawala juu ya maumbile kwa mamlaka Yako. Hakuna mungu ila Wewe – peke Yako bila mshirika; hatumuabudu yeyote mbali ya Wewe, na hatumuombi yeyote ila Wewe, na hatutamani chochote ila kuwa karibu na Wewe. Ni Wewe tunayekulalamikia, na Wewe ndio tumaini la haja zetu, na Mola wetu na Bwana Wetu.” 1080 29. Katika al-Ja’fariat: Ndani ya simulizi yake kutoka kwa Ja’far ibn Muhammad, kutoka kwa baba zake, kutoka kwa Ali (a.s.) ambaye amesema: Wakati mkeka wa chakula ulipotandikwa mbele ya Mtukufu Mtume, yeye angesema: “Allahummaj’alhaa ni’amatan mahswuratan mashkuuratan mawsuulatan bil-jannati.” “Ewe Allah! Kifanye kiwe ni neema ambayo haina ukomo, inayokubalika na iliyounganishwa na peponi.”1081 1080 al-Kafi 2:571 1081 al-Ja’fariat: 216 240


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 241

SUNAN-NABII 30. Katika Awarif al-Ma’arif: Kutoka kwa al-Irbas ibn Sariyah ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akitumia kuomba hivi: “Allahumma j’al hubbaka ahabbu ilayyaa min nafsiy wa sam’iy wa baswariy wa ihliy wa maaliy waminal-maai al-baridi.” “Ewe Allah! Yafanye mapenzi Yako yapendeke kwangu zaidi kuliko nafsi yangu, kusikia kwangu, kuona kwangu, familia yangu, mali zangu na maji baridi.”1082 31. Katika al-Faqih: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipendelea kusema katika dua yake: “Allahumma inniy a’udhubika min waladin yakuunu ‘alayya ribba, wa min maali yakuunu alayya dhwiya’aan, wa min zawjatin tushayyibaniy qabla awaani mashiyabiniy, wa min khaliylin maakirin ‘aynaahu taraaniy wa qalbuhu yar’aaniy, in ra-aa khayraan dafanahu, wa in raaa sharaan adhaa’ahu, wa a’udhubika min waj’il-batwni.” “Ee Allah! Najikinga Kwako kutokana na mtoto wa kiume anayenishinda, na kutokana na mali itakayokuwa chanzo cha kuangamia kwangu, na kutokana na mke atakayenizeesha kabla ya wakati wangu, na kutokana na rafiki mwenye mhaini ambaye jicho lake linaniangalia lakini moyo wake unanionea kijicho – endapo akiona wema wowote (kitendo changu) anauficha na kama akiona ubaya wowote anaueneza; na najikinga Kwako kutokana na maumivu ya tumbo.” 1083 Kidokezo: Tabarsi ameisimulia hii pia katika al-Makarim.1084 32. Katika al-Muhaj: Kutoka kwenye dua za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Allahumma inniy a’udhubika an aftaqiru fiy ghinaaka, au adhwilla fiy hudaaka, au adhila fiy ‘izzaka, au udhwaama fiy sultaanika, au adhwtwahida wal-amru ilayka. Allahumma inniy a’udhubika an aquula zuuraan, au aghshiya fujuuraan, au akuuna bika maghruuraan.” “Ewe Allah! Najikinga Kwako kutokana na kuwa fukara katika Utajiri Wako, au kupotoka katika Muongozo Wako, au kudhalilika katika hali ya Utukufu Wako, au kutendewa dhulma katika Miliki Yako, au 1082 Awarif al-Ma’arif: 454 1083 al-Faqih 3:558 1084 Makarim al-Akhlaq: 203 241


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 242

SUNAN-NABII kuteswa wakati mambo yote yanarejeshwa Kwako. Ewe Allah! Najikinga Kwako kutokana na kusema uwongo, au kukosa uadilifu, au kuwa na kiburi mbele Yako.” 1085

HIJABU (PAZIA) YAKE: 33. Katika al-Bihar kutoka al-Khara’ij: Imesimuliwa kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akiswali mbele ya Hajr al-Aswad, akielekea Ka’aba na akielekea Bayt al-Maqdis; na angekuwa haonekani hadi pale alipomaliza swala yake, na angekuwa amefichwa kwa aya hii:

“Na unapoisoma Qur’ani tunaweka pazia lenye kusitiri baina yako na baina ya wale wasioamini Akhera” (Al-Israa; 17:45) na aya ifuatayo:

“Hao ndio Mwenyezi Mungu amepiga muhuri juu ya nyoyo zao …..” (SuratunNahl; 16:108, na Surat Muhammad; 47:16) na aya ifuatayo:

“Na tumetia vifuniko katika nyoyo zao na uziwi katika masikio yao ili wasije wakaifahamu …..” (Surat al-Israa 17:46) Na aya ifuatayo:

“Je, umemuona yule aliyeifanya tamaa yake kuwa mungu wake, na Mwenyezi Mungu alimwacha apotee akiwa yuajua na akapiga muhuri juu ya masikio yake na moyo wake, na kumtia kitanga machoni mwake ….. (Surat alJaathiya; 45:23). 1086 1085Muhaj al-Da’awat: 102 1086 Bihar al-Anwar; 95:218 242


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 243

SUNAN-NABII Kidokezo: Ni dhahiri kwamba zile dua ambazo zimesimuliwa kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni nyingi na kuzinukuu zote kusingeendana na malengo ya kitabu hiki, hivyo yeyote anayetaka anaweza kurejea kwenye vyanzo hivyo. Yeye Mtume (s.a.w.w.) anayo dua ndefu ambayo alitumia kuisoma baina ya swala ya wajibu na ya sunna ya al-Fajr, hivyo yeyote yule anayetaka anaweza kurejea kwenye kitabu cha Awarif al-Ma’arif. 1087 Yeye Mtume (s.a.w.w.) vilevile anazo dua ambazo alikukwa akitumia kuzisoma nyakati za usiku katika mwezi wa Ramadhani ambazo al-Kaf’ami amezitaja katika kitabu chake, al-Balad al-Amin1088 kama alivyozitaja Allamah Majlisi ndani ya alBihar. 1089 34. Katika al-Khisal: Kwenye riwaya yake kutoka kwa Abdillah ibn Sinan kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angejikinga kutokana na mambo sita kila siku: kutokana na mashaka, ushirikina, makuu, hasira, kuingilia jambo bila ya ruhusa na kijicho. 1090 35. Katika al-Iqbal: Kutoka kwa Ja’far ibn Babawayh, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, ndani ya Thawab al-Amal, katika simulizi yake kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), yeye anasema: Wakati Mtukufu Mtume alipokuwa anataja fadhail za mwezi wa Sha’ban kwa masahaba zake, yeye alisema: “Huu ni mwezi uliobarikiwa na ni mwezi wangu mimi.” 1091 36. Vilevile: Kutoka kwa as-Sadiq (a.s.) ambaye amesema: Baba yangu amenisimulia kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake (a.s.) ambao wamesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Mwezi wa Sha’ban ni mwezi wangu na Ramadhani ni mwezi wa Allah ‘Azza wa Jalla.” 1092 37. Vilevile: Katika riwaya yake kutoka kwa Abbas ibn Mujahid kutoka kwa baba yake ambaye amesema: Ali ibn Husein (a.s.) alikuwa akitumia kusoma dua ifuatayo wakati wa mchana kila siku katika mwezi wa Sha’ban na kwenye usiku wa mwezi kumi na tano wa mwezi huo; na angemswalia Mtume (s.a.w.w.) hivi:

1087 Awarif al-Ma’arif: 344 1088 al-Balad al-Amin: 195 1089al-Bihar al-Anwar 98:74 1090 al-Khisal 329, Bihar al-Anwar 72:191 1091 al-Iqbal al-Amal: 684 1092 Ibid, 684-685 243


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 244

SUNAN-NABII “Allahumma swalli ‘alaa Muhammadin wa aali Muhammad, shajaratin-Nubuwwati wa mawdhwi’i risaalati ….. wa haadha shahru nabiyika sayyidi rasulika swalawaatuka ‘aliyhi wa aalihi, sha’abaanul-ladhiy hafaftahu minka bir-rahmati wa ridhwaani, al-ladhiy kaana rasuuluka swalawaatuka ‘alayhi wa aalihi yad-abu fiy swiyaamihi wa qiyaamihi fiy layaalihi wa ayyaamihi bukhuu’an laka fiy ikraamihi wa i’idhwaamihi ila mahalli himaamihi. Allahumma fa-a’inna ‘alaal-istinaani bisunnatihi fiyhi wa nayli shafaa’ati ladayhi …..” “Ewe Allah! Mpe rehma na amani Muhammad na kizazi chake Muhammad, ule mti wa kijani daima wa utume, mafikio ya ule Ujumbe Mtakatifu ….. na huu ni mwezi wa Mtume Wako, mkuu wa mitume Wako, rehema na amani iwe juu yake na juu ya kizazi chake – mwezi wa Sha’ban, ambao umeuzingira rehma na radhi; mwezi ambamo Mtume Wako atakuwa hachoki katika kufunga kwake na swala, katika nyakati zake za usiku na mchana, akijitiisha mwenyewe mbele Yako katika kukutukuza na kukuadhimisha hadi alipofariki dunia. Ewe Allah! Tusaidie tuweze kwenda na Sunna zake katika mwezi huu ili tupate shufaa yake …..” 1093 38. Katika Kashkul ya Sheikh Bahai: Kwenye maandiko ya baba yangu, Mungu amrehemu: ‘Ata’ aliulizwa kuhusu maana ya hadithi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Dua iliyo bora ni dua yangu na dua ya mitume wa kabla yangu, nayo ni: “Laa ilaha illal-lahu wahadahu, wahdahu, wahdahu, laa sharika lahu, lahul-mulku, wa lahul-hamdu, yuhiiy wayumiitu wahuwa hayyun laa yamuutu biyadihil-khairu wahuwa ‘alaa kulli shaiyin qadiyrun.” “Hapana mungu ila Allah, wa Pekee, wa Pekee, wa Pekee, hana washirika, mamlaka yote ni Yake, na Kwake Yeye zinastahiki sifa zote, Yeye anahuisha na anafisha; Yu hai na kamwe hatakufa, mikononi Mwake zimo kheri zote na Anao uwezo juu ya mambo yote.” Halafu yeye akasema: Hii sio dua (kama hivyo), bali ni utukuzaji na utoaji sifa.1094

1093 Ibid, 687 1094 al-Kashkul 2:209 244


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 245

SUNAN-NABII DU’A YAKE ANAPOCHOMA UBANI 39. Katika al-Bihar, kutoka kwa Aman al-Akhtar: Imesimuliwa kwamba wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa akichoma ubani alikuwa akisema: “Alhamdu lillahil-ladhiy bini’imatihi tatimmu swaalihaatu. Allahumma twayyib ‘urfanaa, wazakki rawaaihanaa, wa-ahsin munqalabanaa, wa aj’alit-taqwaa zaadanaa, wal-jannata ma’aadanaa, walaa tufarriq baynanaa wa bayna ‘aafiyatinaa iyyaanaa wa karaamatika lanaa innaka ‘alaa kulli shaiyn qadiyrun.” “Sifa zote ni zake Allah, aliye Mmoja, ambaye kwa neema Zake mema yote yanatimia. Ewe Allah! Zifanye harufu zetu zinukie vizuri, na tuongezee manukato yetu, na yafanye marejeo yetu kuwa mazuri, na ufanye uchamungu wetu kuzidi, na peponi kuwa ndio mashukio yetu ya mwisho, na usitutenganishe na afya zetu nzuri na rehema Zako, hakika Wewe una uwezo juu ya kila kitu.” 1095

DHIKRI YAKE YA KILA SIKU Sehemu iliyopita ina maelezo kuhusu kile yeye Mtume (s.a.w.w.) alichokuwa akisoma kila siku. 40. Katika ‘Awarif al-Ma’arif: Kutoka kwa Anas ibn Malik ambaye amesema: Mtu mmoja alikuja kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na akasema: Ewe Mtukufu Mtume wa Allah! Mimi ni mtu mwenye ulimi mkali na zaidi hasa kwa familia yangu.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Uko wapi katika suala la kuomba maghfira? Kwani kwa hakika mimi ninaomba maghfira kwa Allah mara mia moja kwa siku.” 1096

Kidokezo: Ameisimulia katika al-Mizan kutoka kwenye al-Majma’. 1097 41. Vilevile: Kwa sanadi nyingine ya wasimuliaji: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Kwa hakika hunijia moyoni mwangu hivyo naomba msamaha kwa Allah ‘Azza wa Jalla. mara mia moja kwa siku.” 1098 1095 Bihar al-Anwar 76:143 1096Awarif al-Ma’arif 428 1097 al-Mizan 18:245 – Surat Muhammad (47) 1098 ‘Awarif al-Ma’arif 428 245


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 246

SUNAN-NABII Kidokezo: Ameisimulia katika al-Mizan. 1099 42. Katika al-Ikhtisas: Katika hadith ndefu kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Hapakuwa na mtume yoyote bali kwamba aliomba dua kwa Mwenyezi Mungu dhidi ya watu wake, na mimi nimechagua kuiweka dua yangu kwa ajili ya shufaa ya ummah wangu katika Siku ya Kiyama .....” 2000 43. Katika kitabu Munyat al-Murid: Imesimuliwa kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akimaliza mikutano yake kwa dua. 2001 44. Vilevile: Wakati yeye Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa amemaliza mazungumzo yake na akataka kusimama kutoka pale alipokuwa ameketi, yeye angesema: “Allahumma ghfirlanaa maa akkhtwaa-anaa wa maa ta’ammaddanaa wa maa asrarnaa wamaa anta a’alamu bihi minnaaa, antal-muqaddimu wa antal-muwaakharu laa ilaha illa anta.” “Ewe Allah! Tusamehe sisi kwa yale tuliyotenda kwa makosa na yale tuliyotenda kwa makusudi, na yale tuliyoyaficha na yale unayoyajua zaidi kuliko sisi. Wewe ndiwe wa Awali kabisa na Wewe ni wa Mwisho, hakuna mungu ila Wewe.” 2002 45. Katika ad-Durr al-Manthur: Kutoka kwa Umm Salamah kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angesema mara kwa mara katika dua yake: “Allahumma muqallibal-quluubi thabit qalbiy ‘alaa diynika.” “Ewe Allah – Mrekebishaji wa nyoyo! Ufanye moyo wangu kuwa thabiti katika dini Yako.” Nikasema: “Ewe Mtume wa Allah! Na nyoyo zinarekebishwa?” Yeye akasema: “Ndiyo. Mwenyezi Mungu hakumuumba mwanadamu bali kwamba moyo wake uko baini ya vidole viwili kutoka kwenye vidole vya Mwenyezi Mungu, hivyo kama akitaka ataufanya kuwa mnyofu na kama akitaka anaweza kuufanya upotoke.” 2003 1099 al-Mizan 18:245 – Surat Muhammad (47) 2000 al-Ikhtisas: 30 2001Munyat al-Murad: 107 2002 Ibid. 2003 ad-Durr al-Manthur 2:8 – Surat al-Imran (3) 246


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 247

SUNAN-NABII 46. Katika Majma’ul-Bayan: Na wakati yeye Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliposikia mngurumo wa radi alisema: “Subhaanahu minhu yusabbihur-ra’ada bihamdihi.” “Sifa zote ni Zake Mwenyezi Mungu – radi inatangaza utukufu Wake.” 2004

47. Vilevile: Salim ibn Abdillah anasimulia kutoka kwa baba yake ambaye amesema: Wakati wowote Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliposikia radi na mingurumo yake, yeye alisema: “Allahumma laa taqtalnaa bi ghadhaabika, walaa tuhaliknaa bi’adhaabika, wa ‘aafinaa qabla dhaalika.” “Ewe Allah! Usituue kwa ghadhabu Yako, na usitukhalikishe kwa adhabu Yako, na utupe msamaha kabla ya hayo.”2005 48. Vilevile: Wakati wale ‘As’habil-Ukhdud’ (wale wachimba handaki) walipotajwa mbele yake, yeye angetafuta kujikinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na ukali wa adhabu.2006 49. Katika ile al-Amali ya Sheikh at-Tusi: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipoona wingu jeusi, yeye angeacha kila kitu na kusema: “Allahumma inniy a’udhubika min sharri maa fiyhi.” “Ewe Mwenyezi Mungu! Najikinga Kwako na shari yoyote iliyomo ndani yake.” Na kama wingu hilo likipita, yeye angemshukuru Mwenyezi Mungu, na kama ilinyesha mvua yeye angesema: “Allahumma nashiaan nafi’aan” “Ewe Mwenyezi Mungu! Lifanye kuwa wingu lenye manufaa.” 2007 2004 Majma’ul-Bayan 6:283, Bihar al-Anwar 59:356 2005 Majma’ul-Bayan 6:283, Bihar al-Anwar 59:357 2006Majma’ul-Bayan 10:465 – Suratul-Buruj (85) 2007 Amali at-Tusi 1:128

247


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 248

SUNAN-NABII 50. Katika al-Faqih: Imam Ali (a.s.) amesema: Kuna aina tano za upepo, mojawapo ikiwa ni upepo wa al-Aqeem (ule upepo mharibifu) na tunaomba kinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na ubaya na uovu wake.2008 51. Katika al-Bihar: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipoona kwamba upepo umekuwa wenye nguvu kali sana, yeye angesema: “Allahumma j’alhaa riyaaha walaa taj’alhaa riyhan.” “Ewe Allah! Ufanye uwe kutokana na pepo nyinginezo na usiufanye kuwa upepo mharibifu.”2009 52. Katika Muhaj al-Da’awat: Kutoka kwa Jabir, kutoka kwa Abi Ja’far (a.s.) ambaye amesema: Jibril alisema: “Ewe Mtukufu Mtume wa Allah! Tambua kwamba mimi sijampenda mtume yoyote kama kiasi ninavyokupenda wewe, hivyo sema hivi mara kwa mara: “Allahumma innaka taraa walaa turaa, wa anta bil-mandharil-a’alaa, wa anna ilaykal-muntahaa war-ruj’aa, wa anna lakal-aakhirata waluwlaa, wa anna lakal-mamaata wal-mahyaa, rabbi a’udhubika an adhila wa akhzaa.” “Ewe Allah! Wewe unaona lakini huonekani, Upo kwenye mandhari yaliyo juu kabisa, na Kwako ndio marejeo ya mwisho, na ni Yako yote ya mwisho na ya mwanzo, na ni Pako mahali pa kufia na pa uhai. Ewe Mola! Najikinga Kwako kutokana na kutoheshimiwa na kuhuzunishwa.”2010

2008 al-Faqih 1:547 2009 Bihar al-Anwar 60:17 2010 Muhaj al-Da’awat: 172, Bihar al-Anwar 94:268 248


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 249

SUNAN-NABII

MLANGO WA 22 HIJJA NYONGEZA JUU YA HIJJA 1. Katika al-Kafi: Katika riwaya yake kutoka kwa Abi al-Faraj ambaye amesema: Aaban alimuuliza Abi Abdillah (a.s.): “Je, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na Tawafu maalum?” Yeye akajibu akasema: “Mtume wa Allah (s.a.w.w.) angefanya Tawaf mara kumi (kila mara moja akiizunguka al-Ka’ba mara saba) wakati wa usiku na wakati wa mchana; mara tatu katika sehemu ya kwanza ya usiku, mara tatu katika sehemu ya mwisho ya usiku, mara mbili wakati wa asubuhi na mara mbili wakati wa Adhuhuri, na katikati ya hizi angepumzika. 2011 Kidokezo: Sheikh Saduq ameisimulia hii katika al-Faqih na al-Khisal.2012 2. Vilevile: Kutoka kwa Abd al-Rahman ibn al-Hajjaj kutoka kwa Abi Abdullah (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angeligusa lile Jiwe Jeusi (Hajr) kila mara alipofanya Tawafu (kama ilikuwa) ya wajibu au ya sunnah.2013 3. Vilevile: Kutoka kwa Ghiyath ibn Ibrahim, kutoka kwa Ja’far kutoka kwa baba yake (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angeligusa lile Hajr alAswad na Rukn al-Yaman na halafu angeyabusu na kuweka shavu lake juu yao, nami nilimuona baba yangu akifanya kama hivyo hivyo.2014 Kidokezo: Sheikh at-Tusi anaisimulia hii ndani ya al-Tahdhib na al-Istibsar.2015 4. Katika al-Da’aim: Kutoka kwa Abi Ja’far (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akizigusa zile pembe mbili; pembe ambamo lilikuwemo Hajr al-Aswad na pembe ya al-Yamani, wakati wowote alipopita karibu nayo wakati wa Tawafu. 2016 2011 al-Kafi 4:428 2012 al-Faqih 2:411, al-Khisal: 449 2013 al-Kafi 4:404 2014 al-Kafi 4:408 2015 Tahdhib al-Ahkam 5:105, al-Istibsar 2:216 2016 Da’aim al-Islam 1:312 249


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 250

SUNAN-NABII 5. Katika al-Mahasin: Katika riwaya yake kutoka kwa Ja’far, kutoka kwa Ibn alQataddah kutoka kwa Abi Abdillah, kutoka kwa baba yake (a.s.): Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akipenda kupata maji ya Zamzam yakiletwa kwa ajili yake (kama zawadi) wakati alipokuwa yuko Madina.2017 Kidokezo: al-Saduq ameisimulia hii katika al-Faqih kama alivyoisimulia at-Tusi ndani ya al-Tahdhib.2018 6. Katika al-Kafi: Katika riwaya yake kutoka kwa Abdillah Ibn Sinan ndani ya hadithi kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.): Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akitumia kusoma ile Dhil-Ma’arij mara kwa mara , na angesoma Talbiya2019 kila mara alipomuona mwenye kupanda mnyama, au wakati wowote alipopanda kilima au aliposhuka kwenye bonde, na katika sehemu ya mwisho ya usiku na baada ya swala.2020 7. Katika al-Ja’fariyat: Ja’far ibn Muhammad as-Sadiq (a.s.) amesema: Baba yangu alinifahamisha kutoka kwa Jabir ibn Abdillah kwamba talbiya ya Mtukufu Mtume ilikuwa: “Labayka Allahumma labayka laa shariyka laka labayka innal-hamda wan-ni’amata laka wal-mulka laa shariyka laka.” “Mimi hapa, Ewe Mola! Mimi hapa, mimi hapa, Wewe huna mshirika. Mimi hapa. Hakika sifa, utukufu na neema ni Zako na mamlaka, Wewe huna mshirika.”2021 8. Katika Tahdhib: Kutoka kwa Muhammad ibn Muslim katika hadith kutoka kwa mmoja wao (yaani, al-Baqir au as-Sadiq – a.s.): Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angetoa kafara ya kondoo dume mkubwa, mnene mwenye afya, mwenye pembe ambaye alikuwa na mdomo mweusi na macho meusi.2022 Kidokezo: Hadith kama hii inapatikana ndani ya al-Da’aim.2023 2017 al-Mahasin: 574 2018 al-Faqih 2:218, at-Tahdhib al-Ahkam 5:372 2019 Mwito maalum unaotamkwa wakati wa kutekeleza Hijja (Mfasiri) 2020 al-Kafi 4:250 2021 al-Ja’fariyat: 64 2022 Tahdhib al-Ahkam 5:205, Faydh al-Qadiir 5:227 2023 Da’aim al-Islam 1:326 250


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 251

SUNAN-NABII 9. Katika al-Kafi: Katika simulizi yake kutoka kwa Abd al-Rahman ibn Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Katika siku ya kutoa kafara, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angenyoa kichwa chake, kukata kucha, na kupunguza nywele kutoka kwenye sharubu zake na kingo za ndevu zake.2024 10. Katika al-Muqni’: Sunnah katika Ihram ni: kukata kucha, kupunguza sharubu na kunyoa nywele za sehemu za siri.2025 11. Vilevile: Ni kutoka katika sunnah kwamba watu wakusanyike kutoka miji mbalimbali katika siku ya Arafa, bila ya kiongozi, na kumuomba Mwenyezi Mungu.2026

Nyongeza kwenye sehemu hii 1. Kutoka al-Kafi: Katika simulizi yake kutoka kwa Abi Maryam, kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Ilikuwa ni desturi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba kama alidaiwa na mtu ngamia wa miaka miwili, angemrudishia ngamia wa miaka saba na kama alidaiwa dirham mbili, yeye angelipa nne.2027 Kidokezo: Hii imesimuliwa pia katika Qurb al-Isnad.2028 2. Katika al-Ihtijaj: Katika hadith ndefu kutoka kwa Musa ibn Ja’far kutoka kwa Ali (a.s.): Wakati wowote Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipotaja wema wake wowote, yeye angesema: “Na hakuna fahari yoyote (kwangu mimi kwa sababu ya hili).” 2029 Kidokezo: al-Majlisi ametaja hadith kama hii katika al-Bihar kutoka kwenye Irshad al-Qulub. 2030 3. Katika al-Bihar: Kutoka kwenye maandishi ya Shahid Muhammad ibn Makki ambaye amesema: Imesimuliwa kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba inatokana na sunnah kwa muumini kusema mara mia moja katika siku ya Ghadiir: “Alhamdulillahi ladhiy ja’aala kamaala diynihi wa tamaama ni’imatihi biwilaayati amiyril-mu’minina ‘Aliy ibn Abi Talibi.” Sifa zote ni Zake Allah ambaye amejaalia ukamilifu wa dini Yake na kukamilisha neema Yake kwa wilayat (mamlaka) ya Amirul-Mu’minin 2024 al-Kafi 4:502, al-Faqih 2:507 2025 al-Muqni’: 70 2026 al-Muqni’: 46 2027al-Kafi 5:254 2028 Qurb al-Isnad: 44 2029 al-Ihtijaj 1:211 2030 Bihar al-Anwar 16:341 251


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 252

SUNAN-NABII Ali ibn Abi Talib.” 2031 4. Vilevile: Kutoka kwa Musa ibn Isma’il ibn Musa ibn Ja’far, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa baba zake (a.s.) ambao wamesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Kuwaombea wagonjwa ambao wanatokana na Bani Hashim ni wajibu, na kuwatembelea (kwa heshima) ni sunnah.2032 5. Katika al-Da’aim: Kutoka kwa Ja’far ibn Muhammad (a.s.): Wakati alipoulizwa kama kondoo ni wa kuchinjwa akiwa amesimama, yeye akasema: Haifai kufanya hivyo. Iliyo sunnah ni kwamba anapaswa kuchinjwa akiwa amelala chini kuelekea Qiblah.2033 6. Katika Tuhf al-Uqul: Kutoka kwa ar-Ridha (a.s.) ambaye amesema: “Sisi tunazichukulia ahadi zetu kuwa kama deni ambalo tunadaiwa, kama vile tu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alivyofanya.”2034 Kidokezo: Hii imesimuliwa vilevile na an-Nuri katika al-Mustadrak na pia Tabarsi katika al-Mishkat.2035 7. Katika Majma’ul-Bayan: Wakati wowote Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliposikia radi angesema: “Subhaana man yusabihur-ra’adu bihamdihi, “Sifa zote ni Zake Allah ambaye utukufu Wake unatangazwa na radi.”2036 8. Vilevile: Salim ibn Abdillah anasimulia kutoka kwa baba yake ambaye amesema: Kila pale ambapo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipoiona mianga ya radi, yeye angesema: “Allahumma laa taqtulnaa bighadhaabika wa laa tuhlilnaa bi’adhaabika wa ‘aafinaa qabla dhaalilka.” 2031 Bihar al-Anwar, 98:321 2032 Bihar al-Anwar, 98:234 2033 Da’aim al-Islam 2:179 2034 Tuhf al-Uqul: 446 2035 al-Mustadrak 8:458, Mishkat al-Anwar: 173 2036 Majma’ul-Bayan 6:283 252


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 253

SUNAN-NABII “Ewe Mwenyezi Mungu! Usitufishe kwa ghadhabu Zako, na usituangamize kwa adhabu Yako; na utusamehe kabla ya hayo.”2037 9. Vilevile: Kila mara wale As’habi al-Ukhdud (wachimbaji wa Handaki) walipotajwa mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), yeye angeomba kinga kutoka kwa Mwenyezi Mungu kutokana na ukali wa adhabu.”2038 10. Katika al-Faqih: Kila mara zile pepo za manjano, nyekundu au nyeusi zilipoanza kuvuma, uso wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ungebadilika na kuwa wa manjano, kama ule wa mtu ambaye ameogofywa, hadi matone ya mvua yalipodondoka kutoka kwenye anga, halafu angerudia kwenye hali yake ya kawaida na kusema: “Imekujieni kwenu pamoja na huruma.”2039 11. Katika Amali ya Sheikh Tusi: Kila wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipoona wingu jeusi, yeye aliacha kila kitu na akasema: “Ewe Allah! Najikinga Kwako kutokana na ubaya uliomo ndani yake.” Na kama limepita basi yeye angemshukuru Mwenyezi Mungu, na kama ikinyesha, yeye angesema: “Ewe Allah! Ifanye kuwa mvua yenye manufaa.”2040 12. Katika al-Da’aim: Kutoka kwa Abi Abdillah Ja’far ibn Muhhamad (a.s.): Kila kulipokuwa na kushikwa kwa jua au mwezi, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angesema: “Kimbilieni ndani ya msikiti wenu.”2041 13. Pia: Iliyokuwa sunnah ni kuswali ndani ya msikiti, endapo wanaswali swala ya tukio (Salat al-Ayat) kwa jamaa.2042 14. Katika al-Bihar: Katika simulizi yake kutoka kwa Ali (a.s.) ambaye amesema: Rafiki yangu mkubwa, Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) hakutumia kamwe kuweka jambo kiporo kwa ajili ya kesho, na Abu Bakr alikuwa akifanya hivi, na Umar ibn al-Khattab alikuwa akiyaweka madaftari ya fedha na kuzuiya kutoka mwaka hadi mwaka mwingine, na kuhusu mimi mwenyewe, ninafanya kama rafiki yangu mpenzi, Mtume wa Allah ‘Azza wa Jalla. alivyokuwa akifanya. Yeye (Bihar) akasema: “Na Ali alikuwa akiwagawia (mafungu yao) kila siku ya Ijumaa …..” 2043 2037 Majma’ul-Bayan 6:283 2038 Majma’ul-Bayan 10:465 2039 Man La Yahdhuruhu al-Faqih 1:547 2040Amali al-Tusi 1:128 2041 Da’aim al-Islam 1:200 2042 Da’aim al-Islam 1:202 2043 Bihar al-Anwar 100:60, al-Gharat 1:47 253


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 254

SUNAN-NABII 15. Katika al-Bihar: Kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): Sisi ni Ahlul-Bayt – Mwenyezi Mungu ametuondolea sisi tabia mbaya zote, za dhahiri na zilizofichika.2044 16. Vilevile: Kutoka kwake yeye Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): Sisi ni Ahlul-Bayt – Mwenyezi Mungu ameichagua akhera kwa ajili yetu juu ya dunia hii (ya mpito).2045 17. Tafsir al-Furat katika simulizi yake kutoka kwa Abi Ja’far (a.s.) ambaye amesema: Mwenyezi Mungu hakumtuma mtume yeyote bali kwamba alisema kuwaambia watu wake: “Sema: Siwaombeni malipo yoyote kwa ajili hii bali mapenzi kwa jamaa zangu wa karibu.”2046 18. Katika al-Bihar: Wakati Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alipomuonyesha mtu huruma maalum na kumuombea msamaha, basi mtu yule atapata kifo cha shahidi.2047

* * * * * Maelezo kutoka kwa mkusanyaji: Hii ndio inatufikisha mwisho wa kitabu hiki, kwa baraka na rehema za Mwenyezi Mungu. Hata hivyo, yule Allamah mashuhuri – Mwenyezi Mungu ampe cheo cha juu – alikuwa amejumuisha sehemu juu ya tabia na maadili bainifu ya Mtukufu Mtume mwanzoni mwa kitabu hiki, kwa sababu ya fadhila zake, hivyo tumeweka nyongeza kwenye sehemu hii mwishoni mwa kitabu hiki katika kufuata mwendo wa Allamah na kwa sababu ya manufaa yake, wakati tukihakikisha kwamba tunadumisha kufupisha maneno (kwa kubana matumizi ya nafasi).

* * * * * Nyongeza kwenye sehemu ya kwanza: Juu ya Tabia yake na Maadili Bainifu 1. Katika al-Bihar, kutoka kwenye Riyadh al-Jinan ya Fadhillah ibn Mahmud alFarsi: Kutoka kwa Jabir ibn Abdillah ambaye amesema: Nilimuuliza Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Ni kitu gani cha kwanza ambacho Mwenyezi Mungu alikiumba?” Yeye (s.a.w.w.) akajibu akasema: “Ni nuru ya Mtume wako, Ewe Jabir! Aliiumba hiyo halafu kutokana nayo akaumba vyote vile ambavyo ni vizuri.2048 2044 Bihar al-Anwar 23:116 2045 Bihar al-Anwar 23:116 2046 Tafsir al-Furat al-Kufi: 139, Bihar al-Anwar 23:248 2047 Bihar al-Anwar 82:148 2048 Bihar al-Anwar, 15:24 254


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 255

SUNAN-NABII 2. Vilevile: Kutoka kwa Jabir ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Kitu cha kwanza alichokiumba Mwenyezi Mungu ni nuru yangu.”2049 3. Katika Basair al-Darajat: Kutoka kwa Bishr ibn Abi Uqbah, kutoka kwa Abi Ja’far na Abi Abdillah (a.s.) ambao wamesema: “Hakika Mwenyezi Mungu alimuumba Muhammad (s.a.w.w.) kutokana na kito kilichokuwa chini ya Arshi Tukufu.”2050 4. Ndani ya Tafsir al-Furat: Kutoka kwa Abdillah ibn Abbas katika hadithi kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ambaye amesema: “Yeye ‘Azza wa Jalla. aliniumba mimi na kizazi changu kutokana na udongo ambao kutoka humo hakuna tena kitu kingine kamwe kilichoumbwa mbali na sisi, na tulikuwa wa kwanza wa viumbe Wake.”2051 5. Katika al-Kafi: Kwenye simulizi yake kutoka kwa Ishaq ibn Ghalib kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) katika moja ya hotuba zake ambamo anaelezea hali ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Maimam wa Ahlul-Bayt (a.s.) na sifa zao: “Na Mola Wetu, kutokana na huruma Yake, ukarimu na upole Wake hakuacha makosa na vitendo vyao viovu vimzuie Yeye kuwachagulia juu yao Kipenzi chake na Mtukufu Mtume, Muhammad ibn Abdillah (s.a.w.w.) – ambaye alizaliwa katika familia tukufu ya kuheshimika, aliyekuwa na nasaba tukufu bila ya upungufu katika utukufu wake, na aliyekuwa na jadi ambayo haikuchanganyika (na wasioamini). Sifa zake hazikuwa zisizojulikana kwa wasomi. Manabii walikuwa wametoa bishara njema za kuja kwake katika vitabu vyao, wanachuoni wamezungumza kuhusu sifa na tabia zake, na wanafalsafa wametafakari juu ya sifa bainifu zake bora. Alikuwa mwenye tabia njema mno na mtakatifu – kamwe hakuwa na akili duni; Bani Hashim ambaye hakuweza kulinganishwa, na ambaye umashuhuri wake haukuweza kupata ushindani, silika yake ilikuwa ni ya kujistahi sana na tabia yake ilikuwa ya ukarimu. Alitambulika kwa hadhi ya utume na sifa zake bainifu na aliainishwa kwa tabia za utume na misukumo yake. Hadi zile sheria tukufu za ki-mbingu zilipopatikana na maandalizi yakatayarishwa kwa ajili ya kuwasili kwake. Mataifa yote baada ya hayo yalipewa bishara njema (za kuja kwake) na yale yaliyoyatangulia kuzipata. Alipita kutoka baba mmoja hadi mwingine, kiuno kwenda kiuno kingine, bila ya kuchanganyika kamwe na uchafu wa zinaa, na hakuchanganywa kamwe na muungano mchafu kuanzia kwa Adam (a.s.) 2049Rejea ya hapo juu. 2050 Basair al-Darajat: 14 2051 Tafsir al-Furat al-Kufi: 110, Bihar al-Anwar 16:375 255


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 256

SUNAN-NABII mpaka kwa baba yake, Abdillah. Alikuwa kutoka kwenye ukoo bora, kabila tukufu kabisa, familia maarufu sana, tumbo lililolindwa sana na alilelewa katika mapaja salama. Mwenyezi Mungu alimchagua yeye, alimpendelea na kumteua, na akampa funguo za ilimu na chemchemi za hekima …..” 2052 6. Katika al-Ihtijaj: Kutoka kwa Musa ibn Ja’far, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa baba zake, kutoka kwa Husein ibn Ali, kutoka kwa Ali ibn Abi Talib (amani juu yao wote) katika hadithi: Wakati Muhammad (s.a.w.w.) alivyotoka tumboni mwa mama yake, aliweka mkono wake wa kushoto juu ya ardhi na akanyanyua mkono wake wa kulia angani wakati ambapo midomo yake ikicheza alipokuwa anatamka kalimah tawhid (kutamka kwamba kuna Mungu mmoja tu) ….. 2053 7. Katika al-Bihar: Kutoka kwa Abul-Hasan al-Bakri katika al-Anwar, kutoka kwa Aminah (a.s.) mama yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) – katika hadithi – yeye amesema: “Na wakati alipotoka tumboni, alianguka kusujudu kuelekea Ka’aba na kisha akanyanyua mikono yake juu mbinguni kama vile tu mtu anavyomuomba Mola Wake …..”2054 8. Katika Ikmal al-Din: Katika simulizi yake kutoka kwa Aban ibn Uthman, akiihusisha na hadithi kutoka kwa Aminah bint Wahab al-Zuhri (a.s.) kwamba alisema: “Wakati nilipokuwa mjamzito wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), sikujisikia kwamba nilikuwa mjamzito, na sikupatwa na kile kinachowapata wanawake wengine kwenye matatizo ya ujauzito …..”2055 9. Vilevile: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikua kwa siku moja kama wanavyokua watu wengine kwa wiki nzima, na alikua kwa wiki kama ambavyo wangekua watu katika mwezi mmoja.2056 Kidokezo: Hii imesimuliwa vilevile kutoka kwa Bibi Halima, mama mnyonyeshaji wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).2057 10. Katika al-Manaqib: Mwezi ulisababisha susu lake kusogea wakati alipokuwa mtoto mchanga.2058 11. Katika al-Bihar: Kutoka kwa al-Waqidi: Walikuwa wakisikia sauti za shukurani, kumsifia, kumtukuza Mwenyezi Mungu kutoka kwenye susu lake.2059 2052 al-Kafi 1:444 2053al-Ihtijaj: 223 2055 Kamal al-Din: 196 2058 Manaqib Ali ibn Abi Talib 1:126 2059Bihar al-Anwar 15:293 256


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 257

SUNAN-NABII 12. Katika Majma’ al-Bayan: Yeye Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alizaliwa akiwa ametahiriwa.2060 Kidokezo: Hii imesimuliwa pia katika al-Manaqib, na al-‘Uyun, al-Khisal, al-Ilal na ndani ya al-Bihar.2061 13. Katika al-Bihar: Halimah amesema: “Mimi sikuwahi kumtoa kwamwe kwenye jua bali pale kulipokuwepo na kijiwingu kidogo kilichompa kivuli na kamwe sikumtoa kwenye mvua bali pale palipokuwepo na kiwingu kidogo kilichomkinga kutokana na mvua hiyo.2062 14. Katika Ihtijaj: Kutoka kwa Musa ibn Ja’far, kutoka kwa baba zake, kutoka kwa Ali (a.s.) katika hadithi: Mawingu yalimpatia kivuli tangu siku ya kuzaliwa kwake hadi siku alipofariki dunia, alipokuwa anasafiri au laa – yeye alijaaliwa hekima na uelewa kama mtoto wakati alipokuwa akiishi na waabudu masanamu na wafuasi wa Shetani. Kamwe hakuelekea kwenye masanamu (yao) – abadan. Yeye hakusherehekea kamwe yoyote kati ya sikukuu zao na hakuna upotovu wowote uliowahi kupata kuonekana kutoka kwake.2063 15. Katika al-Manaqib: Kutoka kwa Abi Talib ambaye alisema: “Mimi sikuwahi kuona upotofu wowote kutoka kwake Mtume (s.a.w.w.), wala tendo lolote la kijahiliya. Sikuwahi kumuona kamwe akicheka wakati watu wengine walipocheka (bila ya sababu ya maana), au kujiunga na watoto katika michezo au kuwazingatia wakicheza. Alipendelea kuwa peke yake na wakati wote alikuwa mnyenyekevu.2064 16. Katika al-Bihar: Halimah amesema: “Sikupata kuungalia uso wa Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) wakati alipokuwa amelala bali kwamba niliyaona macho yake yako wazi kana kwamba alikuwa anacheka, na sio joto wala baridi iliyowahi kumsababishia matatizo yoyote kamwe.2065 17. Katika Nahjul-Balaghah kutoka kwa Ali ibn Abi Talib (a.s.): Kutoka wakati alipoacha kunyonya, Mwenyezi Mungu alimuweka Malaika mwenye nguvu kutoka miongoni mwa Malaika Zake kuwa pamoja naye, kumpitisha katika njia za utukufu na ubora wa tabia katika usiku wake na mchana, ambapo nilikuwa nikitumia 2060 Majma’ul-Bayan 2:481, Surat Aali Imran (3) 2061 Manaqib Ali ibn Abi Talib 1:23, Bihar al-Anwar 17:299 2062 Bihar al-Anwar 15:341 2063 al-Ihtijaj: 219 na 223 2064 Manaqib Ali ibn Abi Talib 1:37 2065Bihar al-Anwaar 15: 341 257


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 258

SUNAN-NABII kumfuata kama ngamia mdogo anayefuata nyayo za mama yake. Kila siku angenionyesha moja ya tabia zake bainifu na kuniambia niitwae. Kila mwaka alikuwa akijitenga kwenye Jabal al-Hira, ambako mimi nilimuona lakini hakuna mwingine tena aliyemuona ….. Na niliisikia milio ya kite cha Sheitani wakati wahyi ulipokuwa ukishuka kwake Mtume (s.a.w.w.). Nikasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Hiki ni kite gani ninachokisikia?” Yeye akajibu akasema: “Huyo ni Shetani. Amepoteza matumaini yote ya kuabudiwa. Ewe Ali! Wewe unasikia kile ninachokisikia na kuona kile ninachoona mimi, isipokuwa tu kwamba wewe sio mtume …..”2066 18. Katika al-Bihar: Kutoka kwa Abd al-Hamid ibn Abi al-Hadid, kutoka kwa Abi Ja’far Muhammad ibn Ali al-Baqir (a.s.) katika maelezo yake juu ya aya:

“Isipokuwa Mtume aliyemridhia, basi hakika yeye humuwekea walinzi mbele yake na nyuma yake.” (Surat Jinn; 72:27) Yeye (a.s.) amesema: Mwenyezi Mungu anaweka kwa mitume Wake Malaika ambao wanawalindia matendo yao (kutokana na makosa) na kuwasaidia katika kuutangaza ule Ujumbe Mtukufu. Na kwa Muhammad (s.a.w.w.) aliwekwa Malaika mkuu, kuanzia wakati alipokuwa mtoto anayenyonya, ambaye alimuongoza kuelekea kwenye wema na tabia tukufu na alimzuia kutokana na tabia bainifu zilizokuwa mbaya na za kiovu.2067 19. Katika al-Ilal al-Shara’: Katika simulizi yake kutoka kwa al-Mughirah, kutoka kwa yule aliyeitaja, kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Bi. Zulaykha aliomba idhini kutoka kwa Yusuf (a.s.) ….. Yeye alimwambia: “Oh, Zulaykha! Ni kilichokufanya uwe hivi (kwangu mimi)?” Yeye Zulaykha akasema: “Ni uzuri wa sura yako, Ewe Yusufu!” Yeye (a.s.) akasema: “Basi ingekuwa vipi (hali yako) kama ungemuona yule mtume anayeitwa Muhammad, ambaye atakuja katika zama zijazo baadae na atakuwa mzuri zaidi kuliko mimi na atakuwa na tabia bora na kuwa mkarimu zaidi kuliko mimi?2068” Kidokezo: Hii imesimuliwa vilevile katika ‘Uddat al-Da’i.2069 2066 Nahjul-Balaghah: Hotuba ya 192 2067 Bihar al-Anwar 15:361 2068 ‘Ilal al-Sharai’: 55 2069 ‘Uddat al-Da’i: 164 258


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 259

SUNAN-NABII 20. Katika al-Manaqib: Yeye Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Yusuf alikuwa mzuri zaidi kuliko mimi, lakini mimi ni maridhia, mpole zaidi.”2070 21. Katika Mahajjat al-Bayda: Yeye Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na mwili wenye uwiano na imara na alikujakuwa mnene kidogo katika miaka yake ya mwishoni, lakini alibakia kuwa na misuli – kana kwamba miaka haikuchukua kitu, au kugonga kengele juu yake japo kidogo.2071 22. Katika al-Khisal: Katika simulizi yake kutoka kwa Abdillah ibn Abbas katika hadithi kutoka kwa Ali (a.s.) katika jibu lake kwa Myahudi mmoja kutoka kwenye viongozi wa kiyahudi: Yeye alikuwa na muhuri wa utume baina ya mabega yake ambao ulikuwa mistari miwili iliyoandikwa, wa kwanza ukiwa: ‘Hakuna mungu isipokuwa Allah’, na wa pili ulikuwa: ‘Muhammad ni Mjumbe wa Allah’ ….. 2072 23. Katika al-Manaqib: Kulikuwa na mhuri wa utume katikati ya mabega yake, (na) kila mara alipoudhihirisha, mng’aro wake ungezidi mwanga wa jua. Ulikuwa umeandikwa: Hakuna mungu ila Allah, peke Yake, hana mshirika. Nenda popote unapotaka kwani kwa hakika unaruzukiwa (na Allah).’2073 24. Katika al-Mahajjat al-Bayda: Yeye Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na mabega mapana na kulikuwa na mhuri wa utume katikati ya mabega yake – karibu kidogo na bega la upande wa kulia (kuliko upande wa kushoto). Ndani yake kulikuwa na alama asilia nyeusi, yenye umanjano kidogo, ambayo ilikuwa na msitari wa nywele kuuzunguka ….. 2074 25. Katika al-Kafi: Katika riwaya yake kutoka kwa Abi Basir, kutoka kwa Abi Ja’far (a.s.) katika hadithi: Juu yake alikuwa na alama asilia ambayo ilikuwa ya hariri ya rangi ya utusitusi mweusi.2075 26. Katika al-Bihar: Kutoka kwa Jabir ibn Samarah ambaye amesema: Ule muhuri wa Utume uliokuwa mabegani mwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ulikuwa na ukubwa sawa na yai la njiwa.2076 2070Manaqib Ali ibn Abi Talib 1:218 2071 al-Mahajjat al-Bayda 4:157 2072 al-Khisal: 599 2073 Manaqib Ali ibn Abi Talib 1:124 2074 al-Mahajjat al-Bayda 4:156 2075 al-Kafi 8:249 2076 Bihar al-Anwar 16:190 259


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 260

SUNAN-NABII 27. Katika al-‘Uyun: Kutoka kwa at-Tamimi, kutoka kwa ar-Ridhaa, kutoka kwa baba zake kutoka kwa Ali (a.s.): Mimi sijamuona mtu mwenye mabega mapana kuliko Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.).2077 28. Katika Mahajjat al-Bayda: Yeye Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na shingo nzuri zaidi kutoka miongoni mwa waja wa Mwenyezi Mungu, haikuwa ndefu sana wala kuwa fupi sana.2078 29. Katika al-Amali ya Sheikh at-Tusi: Katika simulizi yake kutoka kwa Muhammad ibn Isa al-Mu’idi ambaye amesema: Bwana wetu, Ali ibn Musa, alitusimulia kutoka kwa baba zake kutoka kwa Ali (a.s.), ambaye amesema katika hadithi: Kulikuwa na namna ya mduara katika uso wake Mtume (s.a.w.w.)…..2079 Kidokezo: al-Majlisi vilevile anaisimulia hii katika al-Bihar kutoka kwa Ibrahim al-Thaqafi ndani ya kitabu chake al-Gharat.2080 30. Katika al-Bihar: Kutoka kwa al-Kazruni katika hadithi kutoka kwa Ali (a.s.): Kulikuwa na baka jeusi katika mdomo wake wa chini…..2081 Kidokezo: ‘Ayyashi vilevile ameisimulia hii katika Tafsiir yake kutoka kwa Safwan al-Jammal kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.).2082 31. Vilevile: Kutoka kwa al-Kazruni kutoka kwa Ali (a.s.) katika hadithi: Yeye Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na macho meusi.2083 32. Vilevile: Jabir ibn Samarah aliulizwa: “Je, kulikuwepo na nywele nyeupe katika kichwa cha Mtukufu Mtume?” Yeye akajibu akasema: “Hakukuwa na nywele nyeupe kichwani mwake isipokuwa katikati ya kichwa chake, na hizi pia zingefichika wakati alipoweka mafuta kwenye nywele zake.”2084 33. Katika al-Mahajjat al-Bayda: Yeye Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na mikunjo kwenye tumbo lake, mmojawapo ambao ungefunikwa na shuka yake ya kiunoni na mingine ingejionyesha.2085 2077 ‘Uyun al-Akhbar ar-Ridhaa 2:62 2078 Mahajjat al-Bayda 4:155 2079 Amali al-Tusi 1:351 2080 Bihar al-Anwar 16:194 2081 Bihar al-Anwar 16:186 2082Tafsiir al-Ayyashi 1:203; Surat Aali Imran (3) 2083 Bihar al-Anwar 16:190 2084 Bihar al-Anwar 16:191 2085 al-Mahajjat al-Bayda 4:156 260


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 261

SUNAN-NABII 34. Katika Kashf al-Ghummah: Kutoka kwenye Manaqib al-Kharazmi katika hadithi kutoka kwa Ali (a.s.) ambaye amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na fahari na heshima.2086 35. Katika Manaqib: Yeye Mtume (s.a.w.w.) alikuwa ametukuka sana na mwenye msukumo wa kuheshimika.2087 Kidokezo: Zaidi ya msimuliaji mmoja wameisimulia hii.2088 36. Katika al-Ihtijaj: Kutoka kwa Musa ibn Ja’far, kutoka kwa baba zake, kutoka kwa Ali (a.s.) kwenye hadithi katika majibu juu swali la Myahudi (yeye alisema): Alipokaa chini, mwanga uling’ara kutoka upande wake wa kulia na kutoka kushoto kwake, kiasi kwamba watu waliweza kuuona …..2089 Kidokezo: Hii imesimuliwa vilevile katika al-Manaqib.2090 37. Katika al-Kafi: Katika riwaya yake kutoka kwa Isma’il ibn Ammar, kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye alisema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipoonekana katika usiku wa giza, angeonekana na nuru inayong’ara sana, kiasi kwamba alionekana kama kipande cha mwezi.2091 Kidokezo: Hii imesimuliwa pia katika al-Makarim, al-Manaqib na Majma’ulBayan. 2092 38. Katika al-Bihar: Kutoka kwa Abil-Hasan al-Bakri: Ilikuwa ni kawaida kwamba kila wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipotaka kutembelea jumuiya fulani, alitanguliwa na nuru ambayo iliingia hadi majumbani mwao.2093 39. Katika al-Makarim: Kutoka kwa Ibn Umar ambaye amesema: Sikumuona mtu ambaye ni mkarimu zaidi, msaidizi zaidi, mwenye ujasiri zaidi au mnyenyekevu zaidi kuliko Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.).2094 2086Kashf al-Ghummah 1:348 2087 Manaqib Ali ibn Abi Talib 1:126 2088 Bihar al-Anwar 16:179 2089 al-Ihtijaj 1:128 2090 Manaqib Ali ibn Abi Talib 1:220 2091 al-Kafi 1:446 2092 Makarim al-Akhlaq: 23, Manaqib Ali ibn Abi Talib 1:123, Majma’ul-Bayan 2:481 2093 Bihar al-Anwar 16:27 2094 Makarim al-Akhalq:18

261


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 262

SUNAN-NABII 40. Katika al-Kafi: Ndani ya riwaya yake kutoka kwa Salim ibn Abi Hafsah, kutoka kwa Abi Ja’far (a.s.) ambaye amesema: Kulikuwa na tabia au sifa tatu kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambazo hazikuwepo kwa mtu mwingine yeyote yule. Yeye alikuwa hana kivuli, asingeweza kupita mahali bali kwamba kwa muda wa siku mbili au tatu zilizofuatia, yeyote aliyepita njia hiyo angeweza kujua kwamba yeye Mtume alikuwa amepita hapo kwa sababu ya harufu ya jasho lake lenye manukato, na asingeweza kupita karibu na jiwe au mti bali kwamba vingemsujudia (kumwinamia kwa heshima).2095 Kidokezo: Tabarsi ameisimulia hii katika al-Makarim.2096 41.Katika al-Makarim: Yeye Mtume (s.a.w.w.) angeweza kutambulika katika usiku wa giza, kabla ya kuonekana, kwa manukato yake, na ingesemwa kwamba: “Huyo ni Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).” 2097 42. Katika al-Bihar: Kutoka kwa Jabir ambaye alisema: Ishaq ibn Rahawayh ameeleza kwamba hii ilikuwa ndio harufu (ya kawaida) ya Mtume (s.a.w.w.), bila ya kuwa ametumia manukato yoyote.2098 43. Katika al-Manaqib: Yeye Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angesukutua na kutema ndani ya chungu na wangekuta kwamba ilinukia vizuri zaidi kuliko miski.2099 44. Katika al-Makarim: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Yeyote anayetaka kunusa harufu yangu anapaswa kunusa waridi jekundu.3000 45. Katika Majmu’at Warram: Kutoka kwa Anas ibn Malik na kutoka kwa Sulayman ambao wamesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuja (kututembelea) na wakati alipochukua usingizi wake wa mchana, mama yangu alikuja na chupa na akaanza kukusanya jasho lake ndani ya chupa hiyo. Mara, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akaamka na kuuliza: “Ewe Umm Salamah! Unafanya nini?” Akasema: “Hili ni jasho lako ambalo tunalichanganya katika manukato yetu, na ni manukato mazuri sana kati ya manukato.” Yeye (s.a.w.w.) akasema: “Uko sawa sawa.”3001 2095 al-Kafi 1:442 2096 Makarim al-Akhlaq: 34

2097 Makarim al-Akhlaq: 34 2098 Bihar al-Anwar 16:192 2099Manaqib Ali ibn Abi Talib 16:192 3000 Makarim al-Akhlaq: 44 3001Majmu’at Warram: 23 262


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 263

SUNAN-NABII 46. Katika al-Manaqib: Wakati wowote alipotembea na mtu yoyote, yeye angeonekana kuwa mrefu zaidi kuliko mtu huyo, hata kama mtu huyo alikuwa ni mrefu.3002 Kidokezo: Tabarsi ameisimulia hii katika al-Majma’.3003 47. Katika al-Bihar: Kutoka kwa Abi al-Hasan al-Bakri katika kitabu cha al-Anwar: Wakati yeye Mtume (s.a.w.w.) alipovaa nguo ambazo zilikuwa fupi, zingekuwa ndefu na wakati alipovaa nguo ambazo zilikuwa ndefu, zingekuwa fupi (na kumuenea sawasawa kabisa), kana kwamba zilishonwa rasmi kwa ajili yake.3004 48. Katika al-Manaqib: Wakati yeye (s.a.w.w.) alipotembea kwenye ardhi ambayo ilikuwa laini sana, nyayo zake zisingeonekana na wakati alipotembea juu ya ardhi ngumu nyayo zake zilionekana wazi kabisa.3005 49. Katika Majma’ul-Bayan: Yeye (s.a.w.w.) macho yake yangelala lakini moyo wake usingelala.3006 50. Katika al-Manaqib: Hakuna ndege ambaye angeruka juu yake (s.a.w.w.). 3007 51. Vilevile: Hakuna inzi ambaye angetua na kukaa mwilini mwake, na hakuna mdudu, awe ana sumu au vinginevyo, ambaye angesogea karibu yake.3008 Kidokezo: Sehemu ya kwanza imesimuliwa vilevile katika al-Majma’ulBayan.3009 52. Vilevile: Yeye (s.a.w.w.) angekitazama kilichokuwa nyuma yake kama vile alivyoweza kukitazama kilichokuwa mbele yake, na angemuona yule mtu aliyekuwa nyuma yake kama vile tu alivyomuona aliyekuwa mbele yake.3010

3002 Manaqib Ali ibn Abi Talib 1:124 3003 Majma’ul-Bayan 2:481, Surat al-Imran (3) 3004 Bihar al-Anwar 16:28 3005 Manaqib Ali ibn Abi Talib 1:126 3006 Majma’ul-Bayan 2:481, Surat al-Imran (3) 3007 Manaqib Ali ibn Abi Talib 1:124 3008 Manaqib Ali ibn Abi Talib 1:126 3009 Majma’ul-Bayan 2:481, Surat al-Imran (3) 3010 Manaqib Ali ibn Abi Talib 1:124 263


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 264

SUNAN-NABII Kidokezo: Hii imesimuliwa katika Basa’ir al-Darajat kutoka kwa Abi Ja’far (a.s.).3011 53. Vilevile: Yeye (s.a.w.w.) alisikiliza akiwa usingizini mwake kama ambavyo angesikiliza wakati akiwa macho3012 54. Vilevile: Hakuna harufu mbaya yoyote iliyowahi kuhisika kutoka kwake kutoka wakati yeye (s.a.w.w.) alipoumbwa.3013 Kidokezo: Hii imesimuliwa pia na Halimah katika al-Bihar.3014 55. Vilevile: Yeye hakuwahi kamwe kupata ndoto ya kimapenzi ya kumsababishia janaba – daima.3015 56. Vilevile: Mnyama yoyote ambaye Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimpanda, alikuwa asingeweza kuzeeka kamwe na angebakia katika hali hiyo hiyo.3016 57. Katika al-Bihar, kutoka kwenye Tadhkirah: Watu wangetafuta dawa na tiba kutoka kwake Mtume (s.a.w.w.)3017 58. Katika Manaqib: Hakuna mtu ambaye angeweza kulingana nguvu na zile za Mtukufu Mtume.3018 59. Katika Tafsiir al-Ayyashi: Katika riwaya yake kutoka kwa Sulayman ibn Khalid ambaye amesema: Nilimuuliza Abi Abdillah (a.s.) kuhusu watu walichokuwa wakisema juu ya Ali (a.s.): ‘Kama alikuwa na haki (kwenye ukhalifa) basi ni nini kilichomzuia kusimamia haki yake?’ Yeye (a.s.) akasema: “Mwenyezi Mungu hakufanya ni wajibu (juu ya mtu yoyote) kusimama au kupigania peke yake isipokuwa kwa Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.). Yeye ‘Azza wa Jalla. amesema:

3011 Basair al-Darajat: 420 3012 Manaqib Ali ibn Abi Talib 1:124 3013 Manaqib Ali ibn Abi Talib 1:124 3014Bihar al-Anwar 15:347 3015 Manaqib Ali ibn Abi Talib 1:125 3016 (Ibid) - Rejea ya hapo juu. 3017 Bihar al-Anwar 16:401 3018 Manaqib Ali ibn Abi Talib 1:125 264


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 265

SUNAN-NABII

“Basi pigana katika njia ya Mwenyezi Mungu, wewe hukulazimishwa ila kwa ajili ya nafsi yako, na uwahimize wenye kuaminis…..” (an-Nisaa; 4:84) hivyo hii haitumiki kwa mtu yoyote bali kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Na Yeye alisema kwa wengine mbali na yeye (s.a.w.w.):

“….. Isipokuwa kama amegeuka kwa kushambulia au kageuka kwa kuungana na jeshi …..” (8:16). Na kwa wakati huo hapakuwa na kundi ambalo lilikuwa tayari kumsaidia yeye (Ali – a.s.) katika suala hili.3019 Kidokezo: Hii imesimuliwa pia katika al-Kafi na al-Bihar.3020 60. Katika al-Manaqib: Hapakuwa na mtu yoyote aliyekuwa na elimu kuliko yeye Mtume (s.a.w.w.) juu ya uso wa dunia.3021 61. Vilevile: Kila mara wahyi mtukufu ulipokuwa ungeshuka kwake (s.a.w.w.), yeye angelemewa nao na rangi ya uso wake ingebadilika na kichwa chake kingeinamia chini.3022 62. Katika Ikmal al-Din: Ndani ya simulizi yake kutoka kwa Amr ibn Thabit ambaye amesema: Nilimuuliza Imam as-Sadiq (s.a.) kuhusu lile duwazo la kuzimia ambalo lingempata Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Je, ilikuwa ni pale Jibril aliposhuka”? Yeye (a.s.) akasema: “Hapana. Hakika Jibril asingekuja mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mpaka awe ameomba ruhusa ya kufanya hivyo, na alipofika mbele ya Mtume angekaa kama vile mtumwa anavyokaa; bali hili (duwazo la kuzimia) lingemjia juu yake wakati alipokuwa akizungumza na Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. moja kwa moja bila ya wasta kati yao.3023 3019 Tafsiir al-Ayyashi 1:126 – Suratun-Nisaa (4) 3020 al-Kafi 8:274, Bihar al-Anwar 16:340 3021 Manaqib Ali ibn Abi Talib 1:124 3022 Ibid – Rejea ya hapo juu, 1:43

3023 Kamalud-Din wa Tamam al-Ni’mah: 85 265


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 266

SUNAN-NABII Kidokezo: Hii imesimuliwa katika al-Tawhid, al-I’tiqadat na al-Ilal kwa sanadi nyingine ya wasimulizi.3024 63. Katika al-Amali al-Tusi: Katika simulizi yake kutoka kwa Hashim ibn Salim kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.), yeye amesema: Baadhi ya masahaba waliuliza: “Hivi ni kweli kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akisema: ‘Jibril ameniambia …..’ au “Huyu hapa Jibril akiniambia …..’ na kisha nyakati nyingine angezimia?” Abu Abdillah (a.s.) akasema: “Wakati kulipokuwa na Wahyi kutoka kwa Allah ‘Azza wa Jalla. ambao ulikuja kwake pale Jibril alipokuwa hayupo, hii (hali ya kuzimia) ingemfika yeye kwa sababu ya uzito wa Wahyi wa moja kwa moja kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Na kama Jibril alikuwa yupo kama wasti baina yao, hili lisingemkuta yeye, na hapa ndipo ambapo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angesema: ‘Jibril ameniambia …..’ na ‘Huyu hapa Jibril …..’”3025 64. Katika Manaqib: Imesimuliwa kwamba kila pale ambapo wahyi uliposhuka juu yake (s.a.w.w.), sauti kama mlio wa nyuki ingesikika kutoka kwake. Na wakati kama wahyi huo ungemshukia katika siku yenye baridi sana, mara tu ulipokwisha, paji lake la uso lingekuwa likivuja jasho.3026 65. Vilevile: Jibril alimshukia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) mara sitini elfu.3027 66. Katika Irshad al-Qulub ya ad-Daylami: Yeye (s.a.w.w.) amesema: “Jibril angenijia na kunionyesha Qur’ani mara moja katika kila mwaka, na mwaka huu ameinionyesha mara mbili.3028 67. Katika al-Kafi: Katika riwaya yake kutoka kwa Mufadhal ibn Umar kutoka Abi Abdillah (a.s.), yeye amesema: Nilimuuliza yeye kuhusu elimu ya Imam juu ya ni nini kinachotokea katika pembe za ardhi wakati ambapo yeye akiwa nyumbani kwake na amekingwa (kutoka kwenye kile kinachotokea). Yeye (a.s.) akasema: Oh ewe Mufadhal! Kwa hakika Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. aliweka roho tano ndani ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), roho ya uhai ambayo anatembea na kukua nayo, roho ya nguvu ambayo kwayo alifanya kazi na kupambana, roho ya matamanio ambayo kwayo alikula na kunywa na akawajia wale wanawake ambao walikuwa halali juu yake, roho ya imani ambayo kwayo aliamini na kutendea haki, 3024 al-Ilal al-Sharai’: 7, Bihar al-Anwar 18:256 kwa kunukuu kutoka kwenye alTawhiid na al-Ilal. 3025 Bihar al-Anwar 18:268 3026 Manaqib Ali ibn Abi Talib 1:43 3027 Rejea ya hapo juu, uk. 44 3028 Irshad al-Qulub: 33 266


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 267

SUNAN-NABII na ile Royo Takatifu ambayo kwa hiyo aliubebea (wajibu wa) utume. Pale Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipofariki dunia, ile Roho Takatifu ilihamia kwa Imam. Na hiyo Roho Takatifu yenyewe hailali au kuwa sahaulifu, au kufanya jambo bila ulazima au kwa ajili ya kujifurahisha tu. Hizi roho nyingine nne zinalala, zinasahau, na zinafanya mambo bila ulazima na kwa ajili ya kujifurahisha. Ni kwa hii Roho Takatifu ambapo kwamba yale matukio (yanayopita katika sehemu za mbali) yanaweza kuonekana.3029 Kidokezo: Hii imesimuliwa pia na al-Kulayni kwa nyororo nyingine ya wasimuliaji, pia na al-Saffar katika Basa’ir al-Darajat, na al-Mufid katika al-Ikhtisas na wasimuliaji wengineo.3030 68. Vilevile: Katika riwaya yake kutoka kwa Abi Basir ambaye amesema: Nilimuuliza Abi Abdillah (a.s.) kuhusu maneno ya Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla:

“Na hivyo ndivyo tulivyokufunulia Wahyi kwa amri Yetu, ulikuwa hujuoKitabu ni nini wala imani …..” (ash-Shuraa; 42:52).

Yeye (a.s.) akasema: “Ni kiumbe kutoka kwenye viumbe vya Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla. maarufu kuliko Jibril na Mikaili. Ni roho iliyokuwa ikitembea na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ikimfahamisha na kumsaidia yeye, na ilikuwa kwa Maimam baada yake.”3031 Kidokezo: al-Kashshi ameitaja hii ndani ya kitabu chake, ar-Rijal, kutoka kwa Abdillah ibn Tawus kutoka kwa ar-Ridhaa (a.s.), kama alivyotaja al-Qummi katika Tafsiir yake na al-Saffar ndani ya Basair al-Darajat.3032 69. Vilevile: Katika simulizi yake kutoka kwa Abi Basir kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.): Hiyo (Roho Takatifu) ilikuwa haiko kwa mtume mwingine yeyote kati ya waliopita, mbali na Mtume Muhammad (s.a.w.w.)3032 3029 al-Kafi 1:372 3030 Basair al-Darajat: 454, al-Bihar al-Anwar kwa kunukuu kutoka kwenye al-Ikhtisas 17:106 3031al-Kafi 1:273 3032Rijal Kashshi: 604, Tafsiir al-Qummi 2:279, Basair al-Darajat: 455 3032 al-Kafi 1:273 267


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 268

SUNAN-NABII 70. Katika al-Kafi: Ndani ya simulizi yake kutoka kwa Abi Basir, kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Pale Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipopaishwa kwenda mbinguni,3033 Jibril alifuatana naye hadi mahali fulani na kisha akabakia nyuma, hivyo yeye (s.a.w.w.) akamwambia: “Ewe Jibril! Unaniacha mimi kwenye hali hii?” Yeye akajibu: “Wewe endelea tu, kwani Wallahi umeingia mahali ambapo hakuna mwanadamu amewahi kuingia kamwe na hakuna aliyeipita hiyo kabla yako.”3034 71. Katika al-Bihar: Kutoka kwenye kitabu al-Muhtadhar cha al-Hasan ibn Sulayman: Kutoka kwa Salman Farsi (r.a), katika hadithi ndefu: (Jibril alisema) “Naapa kwa Yule ambaye amekutuma wewe kwa haki kama nabii, hakika njia hii haijapitwa na nabii yoyote wala malaika yoyote yule.3035 72. Katika Sahifat al-Ridhaa: Kutoka kwa Imam ar-Ridhaa, kutoka kwa baba zake, kutoka kwa Ali (a.s.), ndani ya hadithi kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye amesema: Nilimpanda juu yake (al-Buraq) hadi nilipofika kwenye hilo pazia ambalo lilikuwa mbele ya Mwingi wa Rehma ‘Azza wa Jalla. …..3036 73. Katika al-Tawhid: Katika riwaya yake kutoka kwa Muhammad ibn al-Fudhayl ambaye alisema: Nilimuuliza Abul-Hasan (a.s.): “Je, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuona Mola Wake?” Yeye akasema: “Ndiyo, alimuona kwa moyo wake. Wewe hujasikia kwamba Mwenyezi Mungu amesema:

“Moyo haukusema uongo kwa yale uliyoyaona.” (an-Najm; 53:11). Hii ina maana kwamba yeye hakumuona Yeye kwa macho yake bali alimuona kwa moyo.”3037 74. Katika Tafsiir al-Qummi: Katika simulizi yake kutoka kwa Isma’il al-Jufi kutoka kwa Abi Ja’far (a.s.), katika hadithi kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye amesema: “Halafu nikamuona Mola Wangu na kitu pekee kilichokuwa baina yangu mimi na Yeye kilikuwa ni Utukufu Wake. ….. 3038 3033 Akiashiria kwenye Mi’raj. (Mfasiri) 3034 al-Kafi 1:442 3035Bihar al-Anwar 18:313 3036 Sahifah al-Imam ar-Ridhaa: 65, Bihar al-Anwar 18:378 3037 al-Tawhid: 116 3038 Tafsiir al-Qummi 2:243, Bihar al-Anwar 18:373 268


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 269

SUNAN-NABII 75. Katika al-Bihar: Kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye amesema: “Nimekuwa na muda na Mwenyezi Mungu ambao hakuna malaika, hakuna nabii na hakuna mja yoyote ambaye moyo wake umejazwa imani na Mwenyezi Mungu.3039 76. Katika Kashf al-Yaqin: Katika ile hadithi ya Mi’raaj kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye amesema: “Wakati nilipofika kwenye wingu wa saba, malaika wote ambao walikuwa wakifuatana nami waliniacha peke yangu, na Jibril vilevile na kile kikundi miongoni mwa malaika, na niliyafikia yale mapazia ya Mola Wangu. Niliingia kupitia mapazia elfu sabini, na kati ya kila mapazia mawili kulikuwepo na mapazia ya Heshima, Mamlaka, Sharafu, Hadhi, Utukufu, Fahari, Nuru, Giza na Wangavu, mpaka nilipofika kwenye pazia la Utukufu ambako nilinong’ona kwa Mola Wangu Mwenye Enzi na nikasimama mbele Zake …..3040 77. Katika al-Kafi: Katika riwaya yake kutoka kwa Mu’awiyah ibn Ammar kutoka kwa Abi Abdillah (a.s.), katika hadithi kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ambaye amesema: “Hakuna siku au hakuna usiku bali kwamba huwa ninapokea zawadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu ndani yake …..3041 78. Katika al-Kafi: Katika simulizi kutoka kwa Harun ibn al-Jahm, kutoka kwa mmoja wa wafuasi wa Abi Abdillah (a.s.) ambaye amesema: Nilimsikia Aba Abdillah (a.s.) akisema: Hakika Isa ibn Maryam alipewa herufi mbili ambazo alifanya kazi nazo, na Musa alipewa herufi nne, na Ibrahim alipewa herufi nane, na Nuh alipewa kumi na tano, na Adam alipewa herufi ishirini na tano, na hakika Mwenyezi Mungu alizikusanya zote hizi kwa ajili ya Muhammad (s.a.w.w.). Hakika lile Jina Kubwa kabisa la Mwenyezi Mungu (Ism al-Adham) lina herufi sabini na tatu ambazo kwazo alimpa Muhammad (s.a.w.w.) herufi sabini na mbili na akaifunika pazia herufi moja tu kwake.3042 Kidokezo: Hii imesimuliwa katika Tafsiir al-Ayyashi na Basair al-Darajat.3043 79. Katika Safinat al-Bihar: al-Qadhi anasema ndani ya al-Shifa: Imesimuliwa kwamba wakati yeye (s.a.w.w.) alipokuwa amejeuruhiwa katika vita vya Uhud, masahaba zake waliingiwa na wasiwasi sana juu ya hili na wakasema: “Kwa nini usiombe dhidi yao kwa Mwenyezi Mungu.” Yeye (s.a.w.w.) akasema: “Sikutumwa 3039 Bihar al-Anwar 18:360 3040 al-Yaqin: 157, Bihar al-Anwar 18:398 3041 al-Kafi 8:49 3042 al-Kafi 1:230 3043 Basair al-Darajat: 228, Tafsiir al-Ayyashi 1:352 269


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 270

SUNAN-NABII kuja kulaani, lakini hasa nilitumwa kama muonyaji na rehema. Ewe Allah! Uongoze umma wangu kwani kwa hakika hawajui kitu.”3044 80. Katika al-Majma’: Hali yake (s.a.w.w.) ingebadilika wakati wahyi uliposhuka na angetoka jasho. Na kama alikuwa kwenye kipando, basi kipando chake kingepiga magoti na kisingeweza kutembea.3045 81. Katika al-Bihar: Ikinukuu kutoka kwenye Kanz al-Karajiki: Imesimuliwa kutoka kwa Halima al-Sa’diyyah ambaye amesema: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa na umri wa mwaka mmoja, aliongea maneno mazuri kiasi kwamba, maneno kama hayo sijawahi kuyasikika kabla. Nilimsikia akisema: “Ewe Mtukufu kabisa! Ewe Mtukufu kabisa! Macho yamelala wakati ambapo Mwingi wa Rehema hachoki wala hapatwi na usingizi.” Wakati mmoja, mwanamke mmoja alinipa kiasi cha tende kutoka kwenye sadaka na mimi nikazitoa kumpa yeye (s.a.w.w.) ili azile – na alikuwa na umri wa miaka mitatu tu wakati huo – lakini alizirudisha kwangu na akasema: “Ewe mama yangu! Usile kutokana na sadaka kwani neema yako ni kubwa na mema yako ni mengi. Na hakika mimi sili kutokana na sadaka.” Bi Halima akasema: “Wallahi sikupokea kamwe sadaka baada ya hili.”3046

3044 al-Shifa bi Ta’rif Huquq al-Mustafa: 105 3045 Majma’ul-Bayan 10:378, Surat al-Muzammil (75) 3046 Bihar al-Anwar 15:401 270


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 271

SUNAN-NABII ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL ITRAH FOUNDATION: 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24. 25. 26. 27. 28. 29. 30. 31. 32.

Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Ishirini na mbili Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo - Juzuu ya kwanza Uharamisho wa uwongo - Juzuu ya pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudharr Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur'an na Hadithi Elimu ya Nafsi Yajue Madhehebu ya Shia Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu Al-Wahda Ponyo kutoka katika Qur'an. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii Mashukio ya Akhera Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt 271


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 272

SUNAN-NABII 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52. 53. 54. 55. 56. 57. 58. 59. 60. 61. 62. 63. 64. 65. 66. 67. 68. 69.

Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyezi Mungu na sifa zake Amateka Na Aba'Khalifa - Kinyarwanda Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana. Upendo katika Ukristo na Uislamu Nyuma yaho naje kuyoboka - Kinyarwanda Amavu n’amavuko by’ubushiya - Kinyarwanda Kupaka juu ya khofu Kukusanya swala mbili Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kusujudu juu ya udongo Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) Tarawehe Malumbano baina ya Sunni na Shia Kupunguza Swala safarini Kufungua safarini Umaasumu wa Manabii Qur’ani inatoa changamoto as-Salaatu Khayrun Mina'n-Nawm Uadilifu wa Masahaba Dua e Kumayl Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mitume Muhammad (s) Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili Kuzuru Makaburi Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu Tujifunze Misingi Ya Dini Sala ni Nguzo ya Dini Mikesha Ya Peshawar 272


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 273

SUNAN-NABII 70. 71. 72. 73. 74. 75. 76. 77. 78. 79.

Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliy onyooka Shia asema haya, Sunni asema haya, Wewe wasemaje? Liqaa-u-llaah Muhammad (s) Mtume wa Allah Amani na Jihadi Katika Uislamu Uislamu Ulienea Vipi? Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) Amali za Ramadhani

82.

Ujumbe Sehemu ya Kwanza

83.

Ujumbe sehemu ya Tatu

84.

Swala ya Maiti na Kumlilia Maiti

85.

Amali za Ramadhani

86.

Ujumbe sehemu ya Pili

87.

Al-Mahdi katika Sunna

88.

Tabarruku

89.

Ukweli wa Shia

90.

Mariam, Yesu na Ukristo kwa Mtazamo wa Kiislamu

91.

Amali za Ramadhani

92.

Hadithi Thaqalain

273


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 274

SUNAN-NABII

BACK COVER Kwa hakika kuna nyanja za elimu ambazo ni makhsusi kwa wale ambao wako karibu na Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jalla., na hawa ni wale ambao wanatajwa kama Mitume wa Mwenyezi Mungu, na Mtume wa mwisho ambaye alitumwa na Mwenyezi Mungu kwa ajili ya mwongozo wa wanadamu alikuwa ni Mtukufu Mtume Muhammad ibn Abdillah (s.a.w.w.). Miongoni mwa mafunzo na masomo ambayo yametufikia sisi kwa kupitia kwake yeye, sehemu yake moja ni kile kilichoteremshwa katika muundo wa ile Qur’ani Adhim ambayo inajulikana kama ‘al-Kitab’ – Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na sehemu nyingine imetegemea kwenye vitendo na simulizi zake, na hii inajulikana kama ‘al-Sunnah.’ Kutoka miongoni mwa Sunnah hiyo ni vile vitendo ambavyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amevipa umuhimu na akavifanya wakati wote. Kitabu hiki – ambacho tunakiwakilisha kwa wale ambao wana shauku katika utafiti na uchunguzi wa kisomi – kina simulizi kuhusu vile vitendo ambavyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alivitilia mkazo sana juu yake, vile ambavyo wakati wote alikuwa akivitenda na vile ambavyo vinaelezea maisha yake, tabia na mwenendo wake.

Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info

274


Sunnani-Nabii final - D.Kanju.qxd

7/15/2011

12:12 PM

Page 275

SUNAN-NABII

275


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.