Sunnah katika kitabu cha fiqhu al sunnah

Page 1

SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

Kimeandikwa na: Muhammad A. Bahsan

Kimehaririwa na: Alhaj Hemedi Lubumba

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 1

1/17/2017 12:44:39 PM


Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 – 9987 – 512 – 78–2 Kimeandikwa na: Ustadh Mohamed Alawy Bahsan Kimehaririwa na: Ustadh Hemedi Lubumba Selemani Kimesomwa-Prufu na: Al-Haji Ramadhani S. K. Shemahimbo Kimepitiwa na: Al-Haji Mujahid Rashid Kupangwa katika Kompyuta na: Al-Itrah Foundation Toleo la Kwanza, Octoba 2010 : Nakala 1000 Toleo la Pili: Mei, 2017 : Nakala 2000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Al-Itrah Foundation, S. L. P. 19701, Daressalaam. Tanzania. Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua pepe: alitrah@yahoo.com Tovuti: www.alitrah.info

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 2

1/17/2017 12:44:39 PM


‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu. Sifa zote njema zinamstahikia Mwenyezi Mungu, Mola wa Walimwengu. Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu. Mwenye Kumiliki Siku ya Malipo. Wewe tu ndiye tunayekuabudu, Na wewe tu ndiye tunayekuomba msaada. Tuongoze njia iliyonyooka. Njia ya wale uliowaneemesha, Siyo (ya wale) waliokasirikiwa, Wala ya wale waliopotea. vvvvv Ewe, Mwenyezi Mungu, Mtakie Rehema Bwana Wetu na Mtume wako ambaye ni wa Mwisho wa Mitume, Muhammad bin Abdillah na jamaa zake watukufu na watoharifu, Na watakie Rehema Mitume Wako na Mursalina wote.

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 3

1/17/2017 12:44:39 PM


Yaliyomo Dibaji ......................................................................................... vi Neno la Mchapishaji........................................................................ 1 Utangulizi wa toleo la kwanza......................................................... 3 Utangulizi wa toleo la pili................................................................ 6 Mambo yenye khitilafu.................................................................... 7 Ufumbuzi wa Khitilafu.................................................................. 12 Utohara wa manii........................................................................... 29 Kuelekea Kibla wakati wa kwenda haja........................................ 34 Kujisaidia wima............................................................................. 39 Kuoshamiguu................................................................................. 42 Viungo vya Sijda............................................................................ 45 Kumswalia Mtume ................................................................... 49 Dhikri na dua baada ya salamu...................................................... 55 Karaha ya kumfuata imamu muovu na mzushi.............................. 58 Kisimamo cha mwezi wa Ramadhani............................................ 62 Swala ya safari............................................................................... 65 Kuchanganya Swala....................................................................... 67 Wanaostahiki kupewa Zaka........................................................... 68

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 4

1/17/2017 12:44:39 PM


Mambo yanayomfaa Maiti............................................................. 71 Ndoa ya Muta (Muda).................................................................... 92 Wanawake walioharamu kuwaowa.............................................. 101 Kufunga ndoa katika hali ya kutaka kutaliki............................... 105 Ushahidi wakati wa talaka........................................................... 107 Idadi ya talaka.............................................................................. 113 Talaka ya kiSunnah...................................................................... 118 Talaka ya uzushi........................................................................... 120 Kutaliki kabla ya kufunga ndoa................................................... 122 Masahaba na Sunnah za Mtume.............................................. 124 Hitimisho..................................................................................... 127

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 5

1/17/2017 12:44:39 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬

DIBAJI

K

itabu hiki ni toleo la Kiswahili la taasisi ya Al Itrah Foundation. Chapisho lake limelenga kukidhi mahitaji ya kiroho ya zama hizi pamoja na Ubongo na fikra zinazokuwa za Muislam. Jitihada kubwa zimefanywa na Taasisi kuweka chapisho hili la Kiswahili katika msingi wa haki na wenye kukubalika katika Uislam. Unaombwa kwa Taadhima ukisome kitabu hiki katika malengo yaliyokusudiwa. Pia Unaombwa kuwasilisha kwetu maoni yako huru juu ya chapisho letu hili, jambo ambalo tutashukuru sana. Kutangaza ujumbe wa Uislam ni kazi ambayo inahitaji ushirikiano wetu sote. Taasisi inakuomba kuungana na kushirikiana kama ilivyoagizwa katika aya ya Qur’an: (Surat Saba’ 34:46). Na rehma za Allah ziwe juu yako. Wako katika Uislam Al Itrah Foundation Barua Pepe: alitrah@yahoo.com SMS: +255 778 300 140

vi

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 6

1/17/2017 12:44:40 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬

Neno la Mchapishaji

K

itabu kilichoko mikononi mwako ni mapitio yaliyofanywa na Ustadh Mohamed Alawy Bahsan juu ya kitabu maarufu kiitwacho, Fiqh al-Sunnah, kilichoandikwa na Sheikh Sayyid Sabiq. Kitabu hiki ni ufafanuzi wa baadhi ya hukumu za kisheria zilizoandikwa katika kitabu cha Fiqh al-Sunnah cha Sayyid Sabiq ambazo mwandishi anadai kuwa hukumu hizo zinatokana na Qur’ani Tujufu na Sunna za Bwana Mtume (s.a.w.w.). Ustadh Mohamed Alawy Bahsan amezifafanua kwa nia nzuri hukumu hizo ili watu wasichangayikiwe wakati wanapozisoma hukumu hizo. Katika kupitia na kutoa ufafanuzi, mwandishi amejaribu kuonesha lipi ni sahihi na lipi si sahihi, na katika kufanya hivyo amejitahidi sana kuthibitisha hoja zake kwa kurejea katika Qur’ani Tukufu na Sunna na vyanzo vingine vya kuaminika. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili za watu. Kutokana na ukweli huo, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili. Tunamshukuru ndugu yetu, Ustadh Mohamed Alawy Bahsan kwa kazi ya uandishi wa kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale 1

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 1

1/17/2017 12:44:40 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikishwa kwake. Â Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni changamoto kubwa kwa wasomaji wetu. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation Dar es Salaam

2

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 2

1/17/2017 12:44:40 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬

UTANGULIZI WA TOLEO LA ­KWANZA

S

ifa zote njema, ni za Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mola wa ­walimwengu wote, Rehema na Amani zimwendee Bwana wetu na mwombezi wetu, Muhammad ibn Abdillah pamoja na Jamaa zake wema waliotakaswa na kutoharishwa na kila aina ya uchafu, na kila anayefuata nyayo zao. Kitabu hiki kilichoko mikononi mwako, ewe ndugu msomaji, ni utafiti wa baadhi ya hukumu za kisharia zilizoandikwa katika kitabu cha ‘Fiqhu Sunnah’ cha Sheikh Sayyid Sabiq, (Mwenyezi Mungu amrehemu). Ni ukweli usiopingika ya kwamba kitabu cha ‘Fiqhi Sunnah’ ni miongoni mwa vitabu vilivyopata bahati ya kupendwa na kusomwa sana miongoni mwa Waislamu, si hapa petu tu Afrika ya Mashariki bali katika nchi nyingi ulimwenguni, inawezekana bahati hiyo imetokana na namna ya upangiliaji wa maudhui na jinsi alivyoyatolea dalili, na pia lugha aliyoitumia, kwani ametumia lugha nyepesi na fasaha, kiasi ambacho hata wale waliobahatika kujifunza Kiarabu wana uwezo wa kuyafahamu mengi yaliyomo ndani ya kitabu hicho. Baada ya utafiti tulioufanya kwenye kitabu hicho cha Sheikh Sayyid Sabiq, tumegundua ya kwamba kuna baadhi ya maudhui ambayo kwa vile tu yamezoeleka kutendwa yanaonekana ni Sunnah sahihi, na pia kinyume chake kuna baadhi yake ni Sunnah Sahihi, lakini kutokana na kutokutendwa na baadhi ya Waislamu, huonekana wale wanayoyatenda kuwa ni wazushi katika Dini. 3

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 3

1/17/2017 12:44:40 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

Kutokana na umuhimu na wajibu wa kila Mwislamu kufuata sharia za Mwenyezi Mungu na Sunnah za Mtume wetu  tumeamua kuandika kijitabu hiki ili kiwe ni mwongozo wa kulifikia lengo la kuletwa hapa duniani, lengo hilo si jingine bali ni kumwabudu Mwenyezi Mungu kama anavyotaka na anavyostahiki. Kila Mwislamu anatakiwa aelewe ya kwamba kila kitendo anachokitenda hakikosi hukumu ya kisharia kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kitendo hicho ama kitakuwa ni wajibu au haramu, au mustahabbu (Sunnah) au mubaha au makruhu. Kwa hivyo Mwislamu hana budi kuchukua tahadhari katika matendo yake ili asije akafanya kile ambacho hakimridhishi Mola Wake Muumba, kwani mwathirika wa mwanzo na wa mwisho ni mwanadamu ikiwa atakwenda kinyume na mafunzo ya Mwenyezi Mungu na Sunnah za Mtume . Mwenyezi Mungu anasema:

ّ‫للاِ َو َمن ي ُِط ِع ه‬ ّ‫ك ُح ُدو ُد ه‬ ‫ت تَجْ ِري ِمن تَحْ تِهَا األَ ْنهَا ُر‬ َ ‫تِ ْل‬ ٍ ‫للاَ َو َرسُولَهُ يُ ْد ِخ ْلهُ َجنَّا‬ ّ‫ْص ه‬ ُ‫للاَ َو َرسُولَهُ َويَتَ َع َّد ُح ُدو َدهُ يُ ْد ِخ ْله‬ َ ِ‫خَالِ ِدينَ فِيهَا َو َذل‬ ِ ‫ َو َمن يَع‬.‫ك ْالفَوْ ُز ْال َع ِظي ُم‬ ٌ ‫نَاراً خَالِداً فِيهَا َولَهُ َع َذابٌ ُّم ِه‬ ‫ين‬ “Hiyo ni mipaka ya Mwenyezi Mungu. Na anayemtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, Yeye atamtia katika Pepo zipitazo mito kati yake, wadumu humo. Na huko ndiko kufuzu kukubwa. Na anayemuasi Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na akaipindukia mipaka yake, (Mwenyezi Mungu) atamtia Motoni adumu humo, na atapata adhabu ya kudhalilisha.” (Qur’ani 4:13-14).

Kitu pekee kitakachomwokoa mwanadamu dhidi ya adhabu hiyo kali ya Moto wa Jahannam ni utii na kusalimu amri kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake . Napenda ieleweke ya kwamba neno ‘Sunnah’ lilimo katika kijitabu hiki linamaana ya kila hukumu 4

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 4

1/17/2017 12:44:40 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

ambayo si haramu, nadhani hata Sheikh Sayyid Sabiq amekusudia hivyo katika Fiqhi Sunnah yake. Nina matumaini makubwa ya kwamba baada ya kukisoma kijitabu hiki itakubainikia na kuitambua Sunnah Sahihi kutokana na Bidaa (uzushi) iliyoingizwa katika Dini yetu Tukufu kwa kutumia visingizio mbalimbali. Mwisho, napenda kueleza ya kwamba lengo letu la kuandika kijitabu hiki ni kutekeleza wito wa Mwenyezi Mungu wa kuamrisha mema na kukataza mabaya, ili Umma wa Kiislamu ushikamane na mafunzo sahihi aliyokuja nayo Mtume wetu , na kama kutakuwa na maneno yenye kumgusa mtu, basi ieleweke kwamba hiyo ndio tabia ya ukweli, na ndio pekee unastahiki kufuatwa. Ewe Mola! Tusaidie. Muhammad A. Bahsan.

5

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 5

1/17/2017 12:44:40 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬

UTANGULIZI WA TOLEO LA PILI

S

ifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mola wa walimwengu wote, Rehema na Amani zimwendee Bwana wetu na mwombezi wetu, Muhammad ibn Abdillah pamoja na Jamaa zake wema waliotakaswa na kutoharishwa na kila aina ya uchafu, na kila anayefuata nyayo zao. Baada kutoka kitabu hiki na kusambazwa kwa wasomaji, tumeamua kukitoa tena kwa mara ya pili. Katika toleo hili, tumefanya baadhi ya marekebisho na masahihisho yaliyojitokeza katika toleo la kwanza. Pia katika toleo hili tumeongeza kipengele kimoja kipya, kinachozungumzia wanawake walio haramu kuwaowa, na katika kipengele hiki, tumejadili juu ya uhalali wa kumnyonyesha mtu mzima. Kipengele hiki nilikumbushwa na mmoja wa wasomaji wa kitabu chetu cha mwanzo, kwani yeye alikuwa ni miongoni mwa watu waliokisoma kitabu cha ‘Fiqhu Sunnah,’ namshukuru sana msomaji huyo kwa mchango wake huo, kwani kwa kupitia ukumbushaji wake huo, itakuwa ni sababu ya Waislamu kuijua Sunnah iliyo sahihi. Napenda tena kuchukua nafasi hii kuwakumbusha Waislamu kwamba, lengo la kitabu hiki, ni kuwafahamisha Waislamu yale yaliyo sahihi katika Dini yao, na ikiwa kuna ibara yoyote yenye kumkera msomaji yeyote atambue kwamba lengo letu halikuwa hilo, bali huenda huo ukawa ndio ukweli na haki, na hiyo ndio tabia ya haki, lakini mwisho wa yote, haki ndio peke yake inayostahiki kufuatwa. Ewe Mola! Tusaidie Muhammad A. Bahsan. 6

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 6

1/17/2017 12:44:40 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

‫بسم هللا الرحمن الرحيم‬

MAMBO YENYE KHITILAFU

K

atika kipengele hiki alichokieleza Sheikh Sayyid Sabiq katika utangulizi wa kitabu chake ‘Fiqhi Sunnah’ juzuu ya kwanza amekitolea dalili kutoka katika Qur’ani Tukufu, zikiwaonesha Waislamu njia ya kuifuata iwapo watazozana juu ya jambo fulani katika dini yao. Aya alizozinakili kwa lengo la kutolea ushahidi ni kama zifuatazo:

ْ ‫للاَ َوأَ ِطيع‬ ْ ‫وا أَ ِطيع‬ ْ ُ‫يَا أَ ُّيهَا الَّ ِذينَ آ َمن‬ ّ‫ُوا ه‬ ‫ُوا ال َّرسُو َل َوأُوْ لِي األَ ْم ِر ِمن ُك ْم فَإِن‬ ّ‫ُول إِن ُكنتُ ْم تُ ْؤ ِمنُونَ بِ ه‬ ّ‫تَنَا َز ْعتُ ْم فِي َش ْي ٍء فَ ُر ُّدوهُ إِلَى ه‬ ‫اآلخ ِر‬ ِ ‫اللِ َو ْاليَوْ ِم‬ ِ ‫للاِ َوال َّرس‬ .ً‫ك َخ ْي ٌر َوأَحْ َس ُن تَأْ ِويال‬ َ ِ‫َذل‬ “Enyi mlioamini, mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume na wenye mamlaka miongoni mwemu. Na mkizozona katika jambo, basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake.” (Qur’ani, 4: 59).

ْ ‫َو َما‬ ...ِ َّ‫اختَلَ ْفتُ ْم فِي ِه ِمن َش ْي ٍء فَ ُح ْك ُمهُ إِلَى للاه‬ “Na kama mkikhitalifiana katika jambo lolote, basi hukumu yake iko kwa Mwenyezi Mungu....» (Qur’ani, 42:10).

..‫َاب تِ ْبيَانا ً لِّ ُكلِّ َش ْي ٍء‬ َ ‫ َونَ َّز ْلنَا َعلَ ْي‬... َ ‫ك ْال ِكت‬ “…Na tumekuteremshia Kitabu hiki kinachobainisha kila kitu…” (Qur’ani, 16: 89). 7

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 7

1/17/2017 12:44:40 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

ْ ‫َّما فَر‬ …...‫ب ِمن َش ْي ٍء‬ ِ ‫َّطنَا فِي ال ِكتَا‬ “Hatukupuuza kitabuni kitu chochote.” (Qur’ani, 6: 38).

...‫اس َما نُ ِّز َل إِلَ ْي ِه ْم‬ َ ‫َوأَنز َْلنَا إِلَ ْي‬ ِ َّ‫ك ال ِّذ ْك َر لِتُبَيِّنَ لِلن‬ “Na tumekuteremshia Qur’ani ili uwabainishie watu yaliyoteremshwa kwao.” (Qur’ani, 16:44).

ّ‫ك ه‬ ِّ ‫َاب بِ ْال َح‬ ...‫للا‬ َ ‫اس بِ َما أَ َرا‬ َ ‫إِنَّا أَنز َْلنَا إِلَ ْي‬ َ ‫ك ْال ِكت‬ ِ َّ‫ق لِتَحْ ُك َم بَ ْينَ الن‬ “Hakika tumekuteremshia Kitabu kwa haki ili upate kuhukumu baina ya watu kama alivyokufahamisha Mwenyezi Mungu.” (Qur’ani, 4: 105).

ً ‫اإل ْسالَ َم ِدينا‬ ُ ‫ض‬ ُ ‫ت لَ ُك ْم ِدينَ ُك ْم َوأَ ْت َم ْم‬ ُ ‫ْاليَوْ َم أَ ْك َم ْل‬ ِ ‫ت َعلَ ْي ُك ْم نِ ْع َمتِي َو َر‬ ِ ‫يت لَ ُك ُم‬ “Leo nimewakamilishieni dini yenu, na kuwatimizieni neema Yangu, na nimewapendeleeni Uislamu uwe dini yenu.” (Qur’ani, 5:3).

Baada ya mwandishi kunukuu Aya hizi Tukufu, anasema: “Kwa vile mambo ya kidini yameshaelezwa wazi wazi na pia kuelezwa pahala pa kupatia ufumbuzi wakati wa mzozo, basi hakuna sababu ya kukhitalifiana, Mwenyezi Mungu anasema:

ْ ُ‫اختَلَف‬ ْ َ‫َوإِ َّن الَّ ِذين‬ ….‫ق بَ ِعي ٍد‬ ِ ‫وا فِي ْال ِكتَا‬ ٍ ‫ب لَفِي ِشقَا‬ ‘Na wale walio khitalifiana katika Kitabu wamo katika upinzani ulio mbali na haki.’ (Qur’ani, (2: 176).

Na amesema tena:

8

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 8

1/17/2017 12:44:40 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

ْ ‫ك فِي َما َش َج َر بَ ْينَهُ ْم ثُ َّم الَ يَ ِج ُد‬ ‫وا فِي أَنفُ ِس ِه ْم‬ َ ‫ك الَ ي ُْؤ ِمنُونَ َحتَّ َى يُ َح ِّك ُمو‬ َ ِّ‫فَالَ َو َرب‬ ْ ‫ضيْتَ َويُ َسلِّ ُم‬ ً ‫وا تَ ْسلِيما‬ َ َ‫َح َرجا ً ِّم َّما ق‬ ‘Naapa kwa Mola Wako! Hawatoamini mpaka wakufanye wewe ndiye hakimu (wao) katika yale waliyokhitalifiana kati yao, kisha wasione dhiki nyoyoni mwao juu ya hukumu uliyotoa na wanyenyekee kabisa.’ (Qur’ani, 4: 65).”

Baada ya Sheikh Sayyid Sabiq kunakili Aya hizi Tukufu za Qur’ani anazitolea ufafanuzi zaidi na kueleza hali ilivyo hivi sasa katika hukumu mbali mbali za Kiislamu, anasema: “Kutokana na kanuni hizi zilizowekwa, Masahaba waliweza kuzifuata, na ni wenye kushuhudiwa kwa wema juu ya hilo, ama khitilafu hazikuwa kubwa baina yao, na sababu kubwa ya kutofautiana ilikuwa ni namna ya kufahamu nassi (Qur’ani na Sunnah za Mtume ) kwani wengine walikuwa ni wajuzi zaidi kuliko wengine. Na pale walipokuja maimamu wa madhehebu manne, (Abu Hanifa, Malik, Shafi na Ahmad) nao pia walifuata Sunnah za waliotangulia, isipokuwa baadhi yao walikuwa karibu zaidi na Sunnah kuliko wengine, mfano, watu waliokuwa zaidi na Sunnah ni watu wa Hijazi (leo inajulikana kwa jina la Saudi Arabia), kwani miongoni mwao mlikuwa na watu ambao walikuwa ni wabebaji na watendaji wa Sunnah, na pia walikuwa ni wapokeaji wa Hadithi za Bwana Mtume , na baadhi ya watu walikuwa karibu zaidi na kutumia rai zao katika masuala ya Dini, mfano wa watu hao ni Wairaki, kwani kulikuwa na wapokezi wachache wa Hadithi miongoni mwao, kwa vile nyumba zao zilikuwa mbali na pahala palipoteremshwa Wahyi (Makka na Madina). Walichokifanya zaidi hao maimamu wanne ni kuwafunza watu dini yao na kuwaongoa, na walikuwa wakiwakataza watu kuwafuata kwa kusema: Haifai kwa yeyote kusema jambo letu bila ya kujua dalili yetu. Walizungumza wazi wazi ya kwamba madhehebu 9

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 9

1/17/2017 12:44:40 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

yao yalikuwa ni Hadithi Sahihi, kwani walikuwa hawakusudii kufuatwa kama kwamba wao ni watu maasumu (wasio kosea) kama alivyo Bwana Mtume , bali lengo lao lilikuwa ni kuwasaidia watu katika kuzifahamu hukumu za Dini yao. Lakini watu waliokuja baada yao waliwafanya viongozi na maimamu na kuwafuata, na kila kundi likashika mwelekeo wake (madhehebu), na wakawa wanatoa kila wanachokimiliki kwa ajili ya kumnusuru na kumtetea imamu wao, na ikawa analolisema ni kama neno la Mwenyezi Mungu na Mtume Wake , na wakawa hawakubali kufuata lolote linalokwenda kinyume na yale aliyoyatolea fatwa imamu wao. Hali hii ya kuwaamini hao maimamu kupita kiasi ilikuwa mbaya na ya kupindukia mipaka, kwani ilimpelekea al-Karkhiy kusema: ‘Kila Aya au Hadithi inayokwenda kinyume na yale walioshikamana nayo watu wetu (maimamu), basi Aya hiyo au Hadithi hiyo itakuwa na maana nyingine au ni yenye kufutwa.’ Kufuata na kung'ang'ania madhehebu kibubusa kumepelekea umma wa Kiislamu kukosa uongofu wa Qur'ani na Hadithi. Palihimizwa kufungwa kwa mlango wa ijtihadi, na maneno ya wanafikihi yakawa ndio sharia ya Kiislamu, na sharia ya Kiislamu ikawa ni maneno ya wanafikihi, na palizingatiwa kila anayetoa fatwa kinyume na hao maimamu wanne ni mzushi, na fatwa zake hizo hazizingatiwi na hazipewi umuhimu wowote. Kitu kilichosaidia kuenea madhehebu haya ni ule mchango mkubwa walioutoa watawala na matajiri katika kuanzisha vyuo na majumba ya kufundishia, huku kila mtu akishikilia kusaidia madhehebu yake, hii ikawa sababu ya kukubaliwa madhebebu hayo (manne), na kuachana na mambo ya ijtihadi, ili kulinda kipato ambacho kiliwekwa kwa hao wanafikihi. Siku moja Abu Zar’at alimuuliza sheikh wake 'Albalqayniy' kwa kusema: Ni kasoro gani aliyonayo As-Sabakiy ya kutokuwa mujtahidi (mwenye kutoa fatwa) na 10

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 10

1/17/2017 12:44:40 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

ilhali ameshafikia daraja hiyo? Albalqayniy alinyamaza kimya, Abu Zar’at alisema: Mimi sina jawabu, isipokuwa kinachomzuia kuwa mujtahidi ni ajira ambayo wamepangiwa wanafikihi wa madhehebu manne, na yeyote atakaye toka katika ajira hiyo hatopata kipato na atazuiliwa kuwa kadhi na watu watazuiliwa kufuata fatwa zake, na ataambiwa ya kwamba yeye ni mzushi… Katika suala la kufungwa kwa mlango wa ijtihadi, umma wa Kiislamu umeingia katika shari na balaa, na pia umeingia katika shimo la nge, ambalo Mtume  alitutahadharisha nalo. Hali hii ilipelekea umma kukhitalifiana na kugawanyika katika makundi mbalimbali. Ilifika hadi ikawa wanakhitalifiana kuhusu ndoa kati ya mwanamke wa madhebebu ya Hanafi na mume wa madhehebu ya Shafi, baadhi yao walisema: Haifai, kwa vile mwanamke anatiliwa shaka katika imani yake. Na wengine walisema: Inafaa kumuowa kwa kumfananisha na mwanamke kafiri anayeishi katika himaya ya dola ya Kiislamu.” Ndugu msomaji haya ni machache tu niliyokunukulia katika kitabu hiki kutoka kwenye utangulizi wa kitabu cha ‘Fiqhi Sunnah,’ Nimeamua kuyanukuu maneno haya ya Sayyid Sabiq ili yawe ndiyo dira na mwongozo wa yale tunayotaka kuwafikishia Waislamu, hasa tukizingatia ya kwamba kitabu cha ‘Fiqhi Sunnah’ kimepata bahati ya kusomwa na kusomeshwa na Waislamu wengi, katika ulimwengu wa Kiislamu. Hii inatokana na umahiri wa mwandishi katika kazi yake hiyo nzito.

11

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 11

1/17/2017 12:44:40 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

UFUMBUZI WA KHITILAFU

B

ila ya shaka kila aliyeusoma utangulizi wa Sheikh Sayyid Sabiq kwa makini anaweza kusema ya kwamba tayari tumeshaoneshwa njia ya kuifuata pindi inapotokea khitilafu juu ya masuala kadhaa katika Dini, hasa katika Aya ya 59 ya Sura ya 4. Leo kila madhehebu miongoni mwa madhehebu za Kiislamu inazungumza kwa kinywa kipana ya kwamba wao ndio wafuasi wa Qur’ani na Hadithi za Bwana Mtume , na wengine wamefika hadi kujiita ni maanswari Sunnah, yote hayo ni kuonesha wazi ya kwamba ni namna gani Waislamu walivyo na shauku ya kutaka kuufuata Uislamu halisi ule aliokuja nao Mtume wao . Pamoja na yote hayo bado tunashuhudia baadhi ya tofauti miongoni mwa Waislamu licha ya kuchukuliwa juhudi kubwa za kuziondosha au kuzipunguza. Miongoni mwa sababu alizozitoa Sheikh Sayyid Sabiq, ambazo ziliwafanya watu kufuata mambo kibubusa, ni kushikamana na misimamo fulani bila ya kuangalia wengine wanachosema hasa baada ya pale walipoondoka maimamu wanne wa madhehebu ya kisunni. Lakini ukweli wa mambo ni kwamba mizizi ya khitilafu hazikuanzia mara baada ya kuondoka hao maimamu, bali ilianzia mbali na zikiwa na sababu tofauti, baadhi ya sababu hizo ni kama zifuatazo: Kwanza: Tukio La Kalamu na Karatasi: Mwenyezi Mungu anasema:

ُ ْ‫ض َر أَ َح َد ُك ُم ْال َمو‬ ‫صيَّةُ لِ ْلوالِ َدي ِْن‬ َ ‫ت إِ ْن تَ َر‬ َ ‫ب َعلَ ْي ُك ْم إِذا َح‬ َ ِ‫ُكت‬ ِ ‫ك َخيْراً ْال َو‬ . َ‫ُوف َحقًّا َعلَى ْال ُمتَّقِين‬ ِ ‫َواألَ ْق َربِينَ بِ ْال َم ْعر‬ 12

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 12

1/17/2017 12:44:40 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

“Mmelazimishwa, mmoja wenu anapofikwa na mauti, kama akiacha mali, kuwausia wazazi wawili na jamaa zake kwa uadilifu. Ni waajibu haya kwa wachamungu.” (Qur’ani, 2: 180).

Katika kulitekeleza agizo hili Mtume  aliagiza apelekewe kalamu na karatasi ili awausie Waislamu kile kilicho bora kuliko mali, kwani alitaka awaandikie kile ambacho wasingepotea baada ya yeye kuondoka duniani. Habari ya tukio hilo anaisimulia Bukhari na Muslim katika Sahihi zao kama ifuatavyo:

‫“ح ّدثنا يحيى بن سليمان قال حدثني بن وهب قال أخبرني يونس عن بن‬ ‫شهاب عن عبيد هللا بن عبد هللا عن بن عبّاس قال ثم ل ّما اشتد بالنّبي صلى‬ ‫ قال‬,‫هللا عليه وسلم وجعه قال ائتوني بكتاب أكتب لكم كتابا ً ال تضلّوا بعده‬ ّ ‫عمر‬ ‫إن النّبي صلّى هللا عليه وسلم غلبه الوجع وعندنا كتاب هللا حسبنا‬ ‫فاختلفوا وكثر اللّغط قال قوموا عنّي وال ينبغي عندي التّنازع فخرج بن‬ ‫عبّاس يقول إن الرّزية ك ّل الرّزية ما حال بين رسول هللا صلّى هللا عليه‬ ”.‫وسلّم وبين كتابه‬ “Ametusimulia Yahya ibn Sulayman, …kutoka kwa Ibn Abbas, amesema: Wakati maumivu ya ugonjwa wa Mtume  yalipozidi, alisema: Nileteeni karatasi, ili niwaandikie yale ambayo hamtopotea baada yake, Umar alisema: Hakika Mtume  amezidiwa na ugonjwa, na sisi tunacho Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kinatutosha. Basi walikhitalifiana na zogo likazidi, Mtume  alisema: Niondokeeni, na wala haifai kuzozana mbele yangu. Ibn Abbas alitoka nje huku akisema: Kwa hakika msiba wa kila msiba ni kule kuzuiliwa Mtume  kile alichotaka kukindika.”1

Kama ilivyo kawaida ya kuwatetea wakoseaji na kuonekana wao ni wenye kupatia zaidi kulikoni Mtume , Imamu Nawawiy anasema katika kuisherehesha hadithi hii: 1

Sahihi

Bukhari, Juz. 1, Kitabul- ilmi, Sahihi Tarkul-wasiyyah

Muslim, Juz. 5, Babu

13

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 13

1/17/2017 12:44:40 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

“Elewa ya kwamba Mtume  ni maasumu (hatendi makosa) kutokana na kusema uongo na kubadilisha kitu katika hukumu za kisheria katika hali ya uzima wake na ugonjwa wake, na hatendi kosa kwa kuacha kubainisha na kufikisha yale yaliyowajibishwa kwake kuyafikisha kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Na si mwenye kuzuiliwa na ugonjwa na maumivu yanayotokea katika viwiliwili vya wanadamu na mengineyo, ambayo hayazingatiwi kuwa ni upungufu wa utukufu wake…Maulamaa wametofautiana juu ya kile ambacho alitaka kukiandika, pamesemwa alikuwa akitaka kumteua mtu maalumu kuwa khalifa ili pasitokee mizozo na fitina, na pamesemwa ya kwamba alikuwa akitaka kubainisha kwa mukhtasari hukumu za kisheria zilizo muhimu, ili kuondosha mizozo na kupatikana makubaliano…” Baada ya maelezo hayo ya Imamu Nawawiy, pia anaeleza ­sababu iliyomfanya Umar kuchukua maamuzi ya kuzuia pasiandikwe, anasema: “Ama maneno ya Umar (r.a) wanachuoni wa elimu ya akida katika kuisherehesha hadithi hii, wamewafikiana ya kwamba ni dalili ya wazi juu ya maarifa ya Umar na utukufu wake na uoni wake wa hali ya juu, kwani alichelea Mtume  kuja kuandika mambo ambayo huenda watu wakaja kushindwa kuyatekeleza na hatima yake wakaja kuadhibiwa…"2 Tunasema, lau kama Mtume  katika maandishi yake angebainisha mtu wa kushika ukhalifa, au kufupisha hukumu zilizo muhimu, basi hilo lisingekuwa zito kwa Mwislamu yeyote. Leo tuna uzito mkubwa sana katika jamii ya Kiislamu, tunaona ni namna gani misikiti ilivyokuwa ni pahala pa mizozo, kwani kila mmoja anataka kufanya lile analoona ni sawa kwake. Umma umegawanyika kwa kukosa kiongozi. Ardhi za Waislamu ziko kwenye mikono ya makafiri, na tunashuhudia kila aina ya dhulma wanayofanyiwa Waislamu 2

An-Nawawiy, Sherehe ya Sahih Muslim, Juz. 11, Uk. 90. 14

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 14

1/17/2017 12:44:40 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

ulimwenguni kote. Bila ya shaka yeyote ile hii ni tija ya kuzuiliwa Mtume kuandika alichotaka kukiandika. Tija ya kuzuiliwa kuandika ilionekana mara tu baada ya kufariki Mtume  kwani wako waliotishiwa kukatwa vichwa vyao kwa sababu tu walisema Mtume  ameshafariki. Watu wanaoonekana kuwa ni wabora na wakaribu zaidi kwa Mtume  walishindwa kuhudhuria mazishi ya Mtume ! Vita mbali mbali vya umwagaji damu ya Waislamu vilitokea kati ya Bibi Aisha dhidi ya Sayyidna Ali  na pia Muawiya dhidi ya Sayyidna Ali , na mizozo mbalimbali pamoja na fitna kubwa kati ya Masahaba ni katika mambo yaliojitokeza. Kwa makini kabisa, ndugu msomaji naomba uangalie amri zilizomo katika Hadithi hiyo ya tukio la karatasi, kwanza, Mtume  alisema nileteeni kalamu na karatasi…, amri ya pili, aliwaambia wale waliokuwa wakizozana: Niondokeeni… Tunachokishuhudia ni kwamba amri ya kwanza ilipingwa na kukataliwa katakata, kwa madai ya kwamba amezidiwa na ugonjwa, kwa hivyo hakuna haja ya kusikilizwa ombi lake, lakini amri ya pili ilitekelezwa bila ya upinzani wowote. Sasa ikiwa madai ya kuzidiwa na ugonjwa au kuzimia yalikuwa ni ya kweli, ni kipi kilichowafanya kukubaliana na amri ya kuondoka na kuacha kuzozana mbele ya hadhara tukufu ya Mtume ! Ni ajabu ilioje ya kutii amri hiyo ya kuondoka na kumuacha mgonjwa peke yake, ambaye wameshuhudia na kukiri wenyewe kwamba maradhi yamezidi?! Madai ya Imamu Nawawiy ya kwamba, Umar kuzuia pasiandikwe ni kuonesha jitihada zake na upeo wa akili yake ili Mtume , asije akaandika mambo ambayo yatakuwa mazito kwa Waislamu, nadharia yake hii inapingana na kilio cha Ibn Abbas. Ikiwa Imamu Nawawiy linamfurahisha tendo la Umar na kulibariki, basi na aelewe ya kwamba tendo hilo hilo limemliza na kumsononesha sana Ibnu 15

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 15

1/17/2017 12:44:40 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

Abbas ambaye alilizwa na kitendo cha Umar cha kumzuilia Mtume kuandika alichotaka kukiandika, Ibn Abbas alilia mpaka machozi yake yaliweza kuzilowesha changarawe zilizo chini ya miguu yake.3 Tuna yakini kwamba amri ya Mtume  ya kutaka apelekewe kalamu na karatasi ingetekelezwa, basi umma huu usingeingizwa katika mambo ya bidaa na uzushi, kwani Mtume  aliweka sharti la kutokupotea baada yake ambalo ni kupelekewa karatasi na kalamu, na kwa vile amri hiyo haikutekelezwa tija haikupatikana, na badala yake ni umma wa Kiislamu kufikishwa hapa ulipofikishwa! Leo kumezuka namna nyingine ya kuwatetea wakoseaji kwa kutoa taswira kwamba haiwezekani watu kama hao kufanya kitendo cha kumzuilia Mtume  kuandika usia wake. Wasomi na watayarishaji wa mitaala ya elimu ya Dini hapa Tanzania (Islamic Education Panel), pamoja na kukiri waziwazi ya kwamba tukio la karatasi limenakiliwa na Bukhari na Muslim katika Sahihi zao, wasomi hao wanasema kwa kinywa kipana ya kwamba halikutokea, katika kitabu chao ' Elimu ya Dini ya Kiislamu, Shule za Sekondari, Kitabu cha Nne, uk. 323, wamenakili haya: “Pamoja na kuwepo maandishi juu ya tukio hili na wanahistoria kuwa na mifano na tafsiri tofauti, hakuna ushahidi wa kutosha kama tukio hili limetokea kweli au ni maandishi tu yenyewe yaliyopachikwa ili kukidhi haja ya waliyobuni tamko hili…”

Tunaamini ya kwamba wasomi wao wameyaandika haya waliyoyaandika kwa lengo tu la kumtetea yule aliyezuia pasiandikwe, 3

Nawawiy anataka kwa maneno yake haya kutuonesha kwamba, Umar aliona mbali zaidi kuliko Mtukufu Mtume ! Ambapo yeye mwenyewe amekiri kwamba kuzidiwa maradhi au kuzimia kwa Mtume hakumtoi katika uwezo wa kufikisha alichotumwa! Na Qur’ani imethibitisha kwamba Mtume hasemi kwa matamanio yake ila ni wahyi! Huku ni kuwachanganya Waislamu kwa makusudi kabisa. Na hiki ndicho kilichomliza Ibn Abbas kuona Mtume anafanywa anazidiwa elimu na hekima na Umar, mtu ambaye hapokei wahyi! Hivi ni kweli Qur’ani inatutosha Waislamu bila ya msimamizi mteuliwa?!!! 16

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 16

1/17/2017 12:44:40 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

huku wakiwa na imani thabiti ya kutokea tukio hilo, hasa kwa vile tukio hilo limenakiliwa katika vitabu ambavyo wao wanaitakidi ya kwamba havikuandikwa ndani yake isipokuwa hadithi sahihi tu (Sahihi Bukhari na Sahihi Muslim). Madai yao ya kutokutokea tukio la karatasi wanatupa taswira ya kwamba wanataka kuwaambia Waislamu ya kwamba si kila hadithi iliyomo kwenye Sahihi Bukhari na Sahihi Muslim ni Sahihi, na hili litakuwa ni kwenda kinyume na makubaliano ya wanachuoni juu usahihi wa kitabu cha Bukhari na Muslim. Ukweli wa mambo ni kwamba hakuna mwanachuoni yeyote wa fani ya hadithi au historia aliyethubutu kusema ya kwamba tukio la katatasi halikutokea. Walilolifanya wanachuoni hao ni kuleta dhana mbalimbali zinazoonesha uhodari, umahiri na jitihada za hali ya juu za yule aliyetamka ya kwamba Mtume  alikuwa amezidiwa na ugonjwa au alikuwa akiweweseka! Hali halisi ya Waislamu tokea kufariki kwa Mtume  hadi sasa ni dalili tosha ya kuthibiti kutokea tukio hilo, kwani Mtume aliweka sharti la watu kutokupotea ikiwa tu kile alichotaka kukiandika kingeandikwa, lakini wanachuoni waliokuja kuisherehesha hadithi ya tukio hilo wanaona kinyume na uoni wa Mtume , kwa maana lau kama Mtume  angeliandika Waislamu wangelilazimishwa kufanya wajibu ambao ungewashinda kuutekeleza! Pili: Kuzuiwa kuandikwa Hadithi za Bwana Mtume 3 Hadithi za Mtume  ambazo ni tegemeo na marejeo ya pili katika kutolea hukumu za kisheria katika Uislamu baada ya Qur'ani Tukufu, zilizuiwa kuandikwa katika kipindi kisichopungua miaka mia moja, na hata zile zilizoandikwa zilichomwa moto, Adhahbiy anasema: 17

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 17

1/17/2017 12:44:40 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

ّ “ ‫إن أبا بكر جمع أحاديث النبي (ص) في كتاب فبلغ عددها خمسمائة‬ ”.‫ فأحرقها‬, ‫ ث ّم دعا بنار‬,‫حديث‬ “Abu Bakri alikusanya Hadithi za Mtume  zipatazo mia tano katika kitabu, kisha aliomba apewe moto, alipopewa alizichoma.”4

Katika maudhui haya kuna riwaya nyingi zinazoashiria kukatazwa kuandikwa Hadithi kutokana na hoja mbalimbali zilizotajwa. Hapa si pahala pa kuzitaja riwaya hizo ili tusije tukatoka katika maudhui, lakini tunachoweza kusema, ni kwamba riwaya hizo ni mbinu tu iliyotumika katika kuufunika ukweli na mwenendo mzima wa Sunnah za Mtume . Si hivyo tu, bali ni kuficha mafunzo sahihi ya Uislamu kwa ujumla, kwani miongoni mwa majukumu ya Mtume  yalikuwa ni kuwabainishia Waislamu yale yaliyoteremshwa kwao kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Sasa ikiwa maneno yake yatakatazwa yasiandikwe, hii ina maana kwamba, mafunzo ya Aya mbalimbali za Qur’ani hayatojulikana, na hali hii ndio tunayoishi nayo katika Dini yetu. Je, ni kweli inawezekana Mtume  awakataze Masahaba kuyaandika mafunzo hayo matakatifu kutoka kwake kama inavyodaiwa! Kwa kweli jambo hilo halikufanywa na Mtume  ambaye alipelekwa kwa watu wa zama zote. Kuna Hadithi mbalimbali zinazopingana na zile zinazoeleza ya kwamba Mtume  aliwakataza Masahaba kuandika maneno yake, baadhi ya Hadithi hizo ni kama zifuatazo:

‫عن عقيل عن المغيرة بن حكيم سمع أبا هريرة قال ما كان أحد أعلم‬...“ ‫بحديث رسول هللا صلى هللا عليه وسلم منّي اال عبد هللا بن عمرو فإنه كان‬ ‫يكتب استأذن رسول هللا صلى هللا عليه وسلم أن يكتب بيده ما سمع منه فأذن‬ ”.‫له الحديث‬ 4

Adhahabiy,Tadhkiratul hufadh: Juz. Uk. 5. 18

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 18

1/17/2017 12:44:40 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

“…Kutoka kwa Aqil, kutoka kwa Mughira bin Hakim, alimsikia Abu Hurayra akisema: “Kulikuwa hakuna yeyote aliyekuwa mjuzi zaidi wa Hadithi za Mtume wa Mwenyezi Mungu  kuliko mimi, isipokuwa tu Abdallah ibn Amru alikuwa akiandika. Alimuomba ruhusa Mtume wa Mwenyezi Mungu  ya kuandika kwa mkono wake na akamruhusu.”5�

Hadithi nyingine anaisimulia mwenyewe Aballah ibn Amru kwa kusema:

‫“ كنت أكتب شيء أسمعه من رسول هللا صلى هللا عليه وسلّم وأريد حفظه‬ ‫فنهتني قريش عن ذلك قالوا تكتب كل شيء تسمعه من رسول هللا صلى هللا‬ ‫عليه وسلم ورسول هللا صلى هللا عليه وسلّم يتكلم في الرضى والغضب قال‬ ‫فأمسكت فذكرت ذلك للنّبي صلى هللا عليه وسلم فأشار بيده إلى فيه فقال‬ ”.‫أكتب فوالّذي نفسي بيده ما يخرج منه إال حق‬ “Nilikuwa nikiandika kila kitu nilichokuwa nikikisikia kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu , lakini Makureish walinikataza na kusema: Wewe unaandika kila kitu unachokisikia kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu  na hali ya kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu  huzungumza katika hali ya hasira na furaha (kuridhika), basi nikajizuia kuandika, na nikamweleza Mtume wa Mwenyezi Mungu  kutokana na hayo, Mtume  aliweka kidole chake katika kinywa chake na kusema: Andika, naapa kwa Yule ambaye nafsi yangu imo Mikononi Mwake, hamtoki humu (kinywani mwangu) isipokuwa haki.”6

Watu waliokuwa mstari wa mbele katika kukataza kuandikwa Hadithi za Mtume  pia walikataza hata kuzisimulia, kama anavyoeleza Dhahabiy ya kwamba: “Siddiq (Abu Bakri) aliwakusanya   Fat-hul Barri, Mlango: Kitabatul-ilmi, Juz.1, Uk. 182. Sunan Abi Daud, Mlango: Kitabatul-ilmi, Juz. 2, Uk. 176. Mustadrakal- Hakim, Mlango: Qayyidul – ilma bilkitaba, Juz. 2, Uk. 106. 6   Kitabu kilichotangulia. 5

19

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 19

1/17/2017 12:44:40 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

watu baada ya kufariki Mtume wa Mwenyezi Mungu  na akasema:

,‫“ إنّكم تح ّدثون عن رسول هللا صلى هللا عليه وسلم أحاديث تختلفون فيها‬ ‫ فمن سألكم‬,ً‫ فال تح ّدثو عن رسول هللا شييئا‬,ً‫والنّاس بعدكم أش ّد اختالفا‬ ً”.‫ فاستحلّوا حالله وحرّموا حرامه‬,‫ نيننا وبينكم كتاب هللا‬:‫فقولوا‬ “Hakika nyinyi mnasimulia Hadithi kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu  mtakhitalifiana ndani yake, na watu baada yenu watakuwa na khitilafu kubwa zaidi, basi msisimulie chochote kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu .”7

Hapo zilipofikishwa Hadithi za Mtume  ni dalili tosha ya Utume wake, kwani alieleza wazi ya kwamba suala la kukataliwa maneno yake ni jambo litakalofanywa na baadhi ya watu, amesema:

‫“ يوشك الرّجل متكئا على أريكته يحدث بحديث من حديثي فيقول بيننا‬ ‫وبينكم كتاب هللا عز وج ّل فما وجدنا فيه من حالل استحللناه وما وجدنا فيه‬ ‫من حرام حرمناه أال وإن ما حرم رسول هللا صلّى هللا عليه وسلم ملث ما‬ ”.‫حرّم هللا‬ “Karibuni hivi mmoja wenu atakuwa ameegemea katika kochi lake na kusimuliwa Hadithi yangu, atasema: Baina yetu na baina yenu ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu, halali tutakayoikuta humo tutaihalalisha, na haramu tutakayoikuta tutaiharamisha. Tambueni ya kwamba, aliyoyaharamisha Mtume wa Mwenyezi Mungu ni kama aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu.”8

Hadithi ya Mtume  inatuonesha wazi umuhimu wa kushikamana na Hadithi zake, sambamba na Qur'ani. Na pia Hadithi aliyoin7 8

Dhahabiy, Tadhkiratul hufadh, Juz.1, Uk.3.   Sunanu Daramiy, Juz.1,Uk. 144. Sunan Ibnu Majah, Juz. 1, uk. 7. Sunan Abi Daud, Juz. 2. uk. 392.Musnad Ahmad, Juz. 4, uk. 131 Fiqhi Sunnah, Juz. 3, uk. 254. 20

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 20

1/17/2017 12:44:40 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

akili Sheikh Sayyid Sabiq, Mtume  anasema: “Nimepewa Qur'ani na mfano wake…” Basi kulikuwa na haja gani ya mafunzo matakatifu ya Mtume  yazuiliwe kuandikwa, kusimuliwa na hatima yake kuchomwa moto! Njama za watu kuzuiliwa kufaidika na Hadithi za Mtume  zilifanywa tangu katika uhai wake, kama tulivyoona katika tukio la karatasi. Basi ikiwa ni kweli Hadithi zilizuiliwa kuandikwa kutokana na amri ya Mtume  kama wanavyoamini baadhi ya watu, je, wale walioziandika si watakuwa wamekwenda kinyume na amri yake? Kutokana na hujuma hii kubwa iliyofanyiwa Hadithi za Mtume  imewafanya baadhi ya Waislamu kukoseshwa mafunzo sahihi ya Uislamu, kwani pengo lililokuwepo la Hadithi za Mtume  lilijazwa hadithi nyingi za uongo. Ushahidi wa hili uko wazi, kwani leo idadi ya hadithi dhaifu ni nyingi zaidi kuliko Hadithi sahihi, na hata hizo ambazo zinazoitwa sahihi zina udhaifu uliyo wazi. Tatu: Kushikamana na hadithi dhaifu: Tija nyingine ya kuzuiliwa kuandikwa hadithi za Mtume  ni kupatikana hadithi nyingi zilizo dhaifu, na kwa masikitiko baadhi ya hadithi hizo zimo katika vitabu ambavyo vinadaiwa ya kwamba ni sahihi kila kilichomo ndani yake, wanafikihi wamechukua mengi kutoka humo kama ni dalili na mategeo ya yale waliyoyaeleza katika vipengele mbalimbali vya fikihi, hata Sheikh Sayyid Sabiq mwenyewe ameingia katika mfumo huu, kama tutakavyoona huko mbele. Nne: Kurejea kwa watu ambao si hoja kwa wengine: Baadhi ya wakati wanafikihi wanapokosa dalili ya wazi juu masuala fulani, hutafuta mtu ambaye aliishi katika zama za Mtume  na 21

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 21

1/17/2017 12:44:40 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

wakigundua kama kuna yeyote aliyelifanya jambo hilo, basi hiyo huifanya kuwa ni dalili, hata kama mtu huyo alikuwa fasiki, mlevi au mpungufu wa maarifa, haya pia tunayashuhudia katika kitabu cha Sheikh Sayyid Sabiq. Haya yatakubainikia ndugu msomaji katika baadhi ya maudhui tuliyoyajadili katika kitabu chetu hiki. Tukirudi katika Aya ya 59 ya Surat Nisai, ni wazi kwamba Mwenyezi Mungu anawataka Waislamu warudi Kwake na kwa Mtume Wake pindi panapotokea mzozo juu ya jambo lolote linalohusiana na Dini yao. Bila ya shaka Waislamu walioishi katika zama zake walifanya hivyo, lakini suala linalojitokeza ni kwa mtu au watu gani wanatakiwa Waislamu warejee kwao baada ya kuondoka Mtume  kwa ajili ya kutatuliwa mizozo yao? Hapa ndipo palipougawa umma wa Kiislamu na kuwafanya wafuasi wake waelekee katika mitazamo tofauti katika baadhi ya hukumu za kisharia, kwani wako wanaoona wa kushika nafasi ya marejeo baada ya Mtume  ni kila ambaye amekalia kiti cha ukhalifa, hata kama wako wanaomzidi kielimu. Watu wanaounga mkono hoja hii wanategemea riwaya isemayo:

‫عليكم بسنتي وسنة الخلفاء الراشدين من بعدي‬ “Shikamaneni na Sunnah zangu na Sunnah za makhalifa wangu waongofu wenye kuongoa baada yangu.” 9

Riwaya nyingine inasema:

“ ”.‫اقتدوا بالذين من بعدي أبو بكر وعمر‬ “Fuateni mwenendo wa watu wawili baada yangu, Abu Bakri na Umar...”10 9

Fat-hul Barriy: Juz. 1, uk. 286.   Musnad Ahmad: Juz. 5 Uk. 382

10

22

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 22

1/17/2017 12:44:40 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

Kuhusiana na riwaya hizi Muhammad ibn Ismail katika kitabu chake. ‘Subulus Salaam’ juzuu ya pili anasema: “Hakika Masahaba  waliwakhalifu mashekhe wawili (Abu Bakri na Umar) katika baadhi ya mambo, hii ni dalili kwamba hawakuichukulia hadithi kwa maana ya kwamba kile walichokisema na kukifanya kuwa ni hoja.11” Itakuwa Masahaba hao walifanya hivyo kwa kutokuona ulazima wa kufuata Sunnah za hao masheikh wawili, au walikhalifu amri ya Mtume . Na hata pale Imam Ali  alipopewa sharti la kufuata Sunnah za Abu Bakri na Umar, ili akabidhiwe ukhalifa, alilikataa sharti hilo. Na pia wako wanaoona ulazima wa kushikamana na Sunnah ya kila Sahaba, dalili ya watu hao ni riwaya inayonasibishwa na Mtume , riwaya hiyo inasema:

‫أصحابي كالنّجوم بأيذهم اقتديتم اهتديتم‬ “Masahaba wangu ni kama nyota, yeyote mtakayemfuata basi mtaongoka.”

Kwa masikitiko baadhi ya maulamaa mara nyingi hutolea ushahidi juu ya mambo kadhaa wakadhaa kwa kutumia riwaya hii iliyo dhaifu mno. Tunapokisoma kitabu cha Fiqhi Sunnah tunamuona mwandishi akiwa ni miongoni mwa wanaoikubali hadithi hiyo dhaifu, kwani baadhi ya dalili zake ni matendo ya baadhi ya Masahaba, hata kama Sahaba huyo ana sifa isiyokubalika katika Uislamu, kufanya kitendo kinyume na sharia ya Mwenyezi Mungu. Na vilevile kuna kundi linaloona ya kwamba Mtume  aliweka watu maalumu wa kuweza kushika nafasi yake ya kuwa ni marejeo   Subulus Salaam: Juz. 2. Uk. 11

11

23

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 23

1/17/2017 12:44:41 PM


‫‪SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH‬‬

‫‪ya kila jambo linalowatatiza Waislamu, dalili ya watetezi wa fikra hii‬‬ ‫‪ni Hadithi Sahihi isemayo:‬‬

‫حدثني زهير بن حرب وشجاع بن مخلد جميعا عن بن علية قال زهير حدثنا‬ ‫إسماعيل بن إبراهيم حدثني أبو حيان حدثني يزيد بن حيان قال ثم انطلقت‬ ‫أنا وحصين بن سبرة وعمر بن مسلم إلى زيد بن أرقم فلما جلسنا إليه قال‬ ‫له حصين لقد لقيت يا زيد خيرا كثيرا رأيت رسول هللا صلى هللا عليه وسلم‬ ‫وسمعت حديثه وغزوت معه وصليت خلفه لقد لقيت يا زيد خيرا كثيرا حدثنا‬ ‫يا زيد ما سمعت من رسول هللا صلى هللا عليه وسلم قال يا بن أخي وهللا لقد‬ ‫كبرت سني وقدم عهدي ونسيت بعض الذي كنت أعي من رسول هللا صلى‬ ‫هللا عليه وسلم فما حدثتكم فاقبلوا وما ال فال تكلفونيه ثم قال قام رسول هللا‬ ‫صلى هللا عليه وسلم يوما فينا خطيبا بماء يدعى خما بين مكة والمدينة فحمد‬ ‫هللا وأثنى عليه ووعظ وذكر ثم قال أما بعد أال أيها الناس فإنما أنا بشر يوشك‬ ‫أن يأتي رسول ربي فأجيب وأنا ثقلين أولهما كتاب هللا فيه الهدى والنور‬ ‫فخذوا بكتاب هللا واستمسكوا به فحث على كتاب هللا ورغب فيه ثم قال وأهل‬ ‫بيتي أذكركم هللا في أهل بيتي أذكركم هللا في أهل بيتي أذكركم هللا في أهل‬ ‫بيتي…‪.‬‬ ‫‪“Katuhadithia Zuhair ibn Harb na Shujaa ibn Makhlad wote kutoka kwa‬‬ ‫‪ibn Uliyyah. Kasema Zuhair: Katuhadithia Ismail ibn Ibrahim, kaniha‬‬‫‪dithia Abu Hayyan, kanihadithia Yazid ibn Hayyan kasema: Niliondoka‬‬ ‫‪mimi na Husain ibn Sabra na Umar ibn Muslim kwenda kwa Zaid bin‬‬ ‫‪Arqam. Tulipokaa naye, Husain akamwambia: Ewe Zaid! Kwa hakika‬‬ ‫‪umekuta kheri nyingi: umemuona Mtume  na umesikia Hadithi zake‬‬ ‫‪na umekwenda vitani pamoja naye, na ukaswali nyuma yake: kwa hakika‬‬ ‫‪umekuta kheri nyingi ewe Zaid! Tuhadithie ewe Zaid yale ulioyasikia‬‬ ‫‪kutoka kwa Mtume  Akasema (Zaid bin Arqam) ewe mwana wa ndugu‬‬ ‫‪yangu! Wallahi, miaka yangu imekuwa mikubwa (nimeshakonga), na‬‬ ‫‪24‬‬

‫‪1/17/2017 12:44:41 PM‬‬

‫‪15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 24‬‬


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

umri wangu umekuwa mkongwe, na nimesahau baadhi ya yale niliokuwa nimeyahifadhi, basi nitachokusimulieni kikubalini na nisicho (kusimulieni) basi msinikalifishe. Kisha akasema: “Alisimama Mtume  siku moja pamoja nasi akahutubia katika (sehemu yenye) maji yanayoitwa ‘Khumman’ baina ya Makka na Madina. Basi akamuhimidi Mwenyezi Mungu na kumsifu na akatoa mawaidha na kukumbusha. Kisha akasema: Baada ya hayo, Enyi watu! Hakika yangu mimi ni mtu (ambaye) amekaribia kunijia Mjumbe wa Mola Wangu (Malaika wa kutoa roho) nami nitaitika. Nami nakuachieni vizito viwili. Cha kwanza: Ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu, Ndani yake kuna uongofu na nuru, basi kishikeni Kitabu cha Mwenyezi Mungu na mshikamane nacho. Basi akahimiza juu ya (kushikamana na) Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kuwataka (watu) wakipende. Kisha akasema: Na Ahlu Bayti wangu (watu wa nyumba yangu), nakukumbusheni Mwenyezi Mungu kuhusu watu wa nyumba yangu, nakukumbusheni Mwenyezi Mungu kuhusu watu wa nyumba yangu, nakukumbusheni Mwenyezi Mungu kuhusu watu wa nyumba yangu…” 12

Katika kuthibitisha zaidi maneno haya ya Mtume  mfasiri maarufu wa Qur’ani, ibn Kathir anasema: Hakika imethibiti katika kitabu sahihi ya kwamba Mtume  alisema katika khutba yake aliyoitoa Ghadir Khum, ya kwamba:

‫“ إنّي تاركم فيكم الثقلين كتاب هللا وعترتي وإنّهما لم يفترقا حتى يردا على‬ ”.‫الحوض‬ “Hakika mimi ninawaachieni vizito viwili, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Kizazi changu, na viwili hivyo havitaachana mpaka vitakaponifika katika Hodhi.”13

Lau kama umma wa Kiislamu ungefanya uadilifu kwa kushikamana na Aya ya 59 ya Sura ya 4, inayowataka kushikamana na maneno pamoja na vitendo vya Mtume Mtukufu  bila ya shaka tusingelikuwa katika hali hii tuliyonayo leo, kwani katika yale ali12 13

Sahihi Muslim Juz. 7, uk. 123.   Tafsir Ibnu Kathir, Juz. 4, uk. 122. 25

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 25

1/17/2017 12:44:41 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

yokuja nayo Mtume wetu  yanapatikana katika Hadithi hii inayotutaka kushikamana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na watu wa nyumba ya Mtume , kwa kweli hili ndilo hakikisho kubwa la kutokupotea njia. Sheikh Sayyid Sabiq amesikitishwa mno kutokana na watu kuwakalidi (kuwafuata) maimamu ambao wenyewe hawakutaka kufuatwa, kama alivyosema katika utangulizi wa kitabu chake. Lakini tunaloliona ni kwamba yeye mwenyewe ni mfuasi wa hao maimamu wanne. Na pia amesononeshwa na kuingia majonzi kwa kufungwa mlango wa ijtihadi, lakini kwa bahati mbaya sana yeye ameshindwa kuufungua, na kama aliufungua basi hata kuchungulia hakuchungulia ili kutaka kujua kilichoko ndani. Watu ambao tuliachiwa na Mtume wetu  kwa lengo la kuiendeleza kazi aliyoiacha, na kutuelekeza katika mfumo sahihi wa maisha, ni watu wa nyumbani kwake, waliotakaswa na kutoharishwa barabara na Mwenyezi Mungu Mtukufu. Mtume  hakutosheka na kuyasema hayo tu, bali ametutajia idadi ya hao Makhalifa kwa kusema:

‫ال يزال اإلسالم عزيزاً إلى اثنى عشر خليفة‬ “Uislamu hauachi kuwa na nguvu, mpaka watawale Makhalifa kumi na mbili.”14

Maulamaa wote wa madhehebu manne pamoja na wataalamu wa elimu ya Hadithi wanakubaliana na usahihi wa Hadithi hizi, lakini kilichowashinda ni kuainisha majina ya hao Makhalifa, kiasi ambacho leo imezoeleka ya kwamba Makhalifa waongofu ni wanne tu, na mara nyengine husemwa ni watano baada ya kuingizwa Umar ibn Adbul Aziz. Ninachoamini ni kwamba lau kama mwandishi an14

Sahih Muslim Juz. 6, uk. 3. 26

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 26

1/17/2017 12:44:41 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

geufungua mlango wa ijtihadi na kuingia ndani ya vitabu vinavyotegemewa na madhehebu manne, bila ya shaka angeuelekeza umma katika Sunnah sahihi, kwani angechukua kutoka kwao mafundisho mazuri na sahihi kutoka kwa watu watoharifu wa nyumba ya Bwana Mtume . Waislamu wanapaswa kuelewa ya kwamba wale wanaoitwa ‘Ithnaasharia’ au ‘Maithnaashir’ wameitwa hivyo kutokana na kuiamini na kushikamana na Hadithi hiyo sahihi iliyomo kwenye kitabu cha Sahihi Muslim na vitabu vingine. Na wewe pia ndugu msomaji ungeikubali Hadithi hiyo pia nawe ungeitwa hivyo. Leo ni madhehebu moja tu kati ya madhehebu za Kiislamu yanayoamini ya kuwa Makhalifa baada ya Mtume ni kumi na mbili, na Makhalifa hao wanatokana na watu wa nyumba ya Mtume  sambamba na Hadithi tuliyoiyeleza, inayotutaka tushikamane na vizito viwili, sasa wewe ndugu msomaji, ni kipi kinachokukwaza hata uyakatae haya yaliyothibiti katika vitabu sahih?! Mtume  ametukataza kuwafundisha watu hao pamoja na Qur'ani au kuwatangulia, kwa kutanguliza jambo letu, amesema:

”.‫ فال تق ّدموهما لتهلكوا وال تعلّموهما فإنّهما أعلم منكم‬...“ “Msivitangulie (vizito hivyo viwili), mtaangamia na wala musivifundishe kwani vitu hivyo vinajua zaidi kuliko nyinyi»15

Tano: Ikhitilafu za Masahaba. Taswira wanayopewa Waislamu katika zama mbalimbali, ni kuoneshwa ya kwamba, baada ya Mtume  kufariki dunia, Masahaba wote waliishi kwa wema, amani utulivu, kupendana na kusaidiana. Lakini hali halisi ni tofauti kabisa, khitilafu na kupingana kuli15

Addurul Manthur Juz. 2, uk. 60. 27

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 27

1/17/2017 12:44:41 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

jitokeza mara tu baada ya kufariki Bwana Mtume  bali walipigana vita mbali mbali na kuimwaga damu yao katika njia isiyo sahihi. Bila ya shaka wale waliodhulumiwa walikuwa na haki ya kujihami nafsi zao kwa mujibu wa sharia. Huku kutofautiana kwao kumewafanya baadhi ya Waislamu washikamane na kundi fulani na kuachana na kundi fulani, kwa mfano, leo kwa sababu ya mapenzi juu ya sahaba fulani kunawafanya baadhi ya Waislamu kushikamana na hukumu alizozitoa hata kama hukumu hizo zinakwenda kinyume na Qur'ani pamoja na mwenendo wa Mtume . Ukweli wa haya utaweza kuuona huko mbele katika vipengele tulivyovichagua kutoka katika kitabu Fiqhi Sunnah.

28

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 28

1/17/2017 12:44:41 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

UTOHARA WA MANII

K

atika Mlango wa Najisi Sheikh Sayyid Sabiq ameeleza ya kwamba manii sio najisi, pamoja na kuwepo baadhi ya maulamaa kupingana na uoni wake, amesema: “Baadhi ya maulamaa wameona ya kwamba manii ni najisi, lakini dhahiri yake ni tohara, pamoja na hayo ni mustahabu (ni vizuri zaidi) kuyaosha pindi yanapokuwa ni rutuba. Bibi Aisha  amesema: “Nilikuwa nikiyakwangua manii pale yalipokuwa makavu, na nilikuwa nikiyaosha pale yanapokuwa ni rutuba. Hadithi hii kaipokea Addaruqutniy, Abu Awanat na Albazzaz.” Pia Sheikh Sayyid Sabiq amenukuu hadithi nyingine inayosema: Kutoka kwa Ibn Abbas  “Mtume  aliulizwa kuhusiana na manii yanayoingia katika nguo? Mtume alijibu: Hakika hayo (manii) ni kama mafua na mate, basi inakutosha kufuta (kupangusa) kwa kitambaa au majani.” “Imepokewa na Addaruqutniy, Albahyhaqiy na Atwahawiy.” Sasa tuangalie nafasi ya hadithi hizi mbili, tukianzia na hadithi ya pili ya Ibn Abbas, ni kwamba Sheikh Sayyid Sabiq ameeleza wazi ya kwamba, hadithi hiyo ama ni 'Marfuu' au ' Mawquf,’ basi hatuna haja ya kuijadili kwani imekosa sifa ya kukubalika. Ama kuhusiana na Hadithi ya kwanza, amesema Allamatul-Hilliy katika kitabu chake ‘Almu-utabar’ ya kwamba aliyokuwa akiyafanya Aisha kwa nguo ya Mtume  ilikuwa si kwa amri ya Mtume  na matendo yake (Aisha) si hoja (mategemeo) kwa mwingine.” Kila Mwislamu atakapoiweka vizuri akili yake mbele ya riwaya hizi mbili, atapata jawabu jingine. Tumeona ya kwamba manii yamefananishwa na mafua na mate, kama tulivyoona katika riwaya, suala lin29

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 29

1/17/2017 12:44:41 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

akuja, je! Mtu akitokwa na mate au mafua ana wajibu wa kuoga josho la wajibu kama anavyotokwa na manii? Bila ya shaka hana wajibu huo na wala si mustahabu kamwe seuze kuwa wajibu. Ikiwa hali yenyewe ndio hii, ni kipengele gani kilicho shabihishwa manii na mate au mafua? Je, ni katika rangi yake (weupe wake), utelezi wake au… Hapa inanikumbusha masuala aliyoulizwa Abu Hanifa na mwalimu wake, Imam Ja’far bin Muhammad Sadiq, miongoni mwa masuala hayo yalikuwa ni kama ifuatavyo: “Ni kitu gani ambacho ni uchafu (najisi) zaidi kati ya manii na mkojo?” Abu Hanifa alijibu: “Ni mkojo.” Imam Sadiq  akamwambia: "Kutokana na kipimo chako (kiasi), inaonesha ya kwamba ni wajibu kuoga baada ya mtu kukojoa na sio baada ya kutokwa na manii, na hali ya kuwa Mwenyezi Mungu amewajibisha kuoga baada ya kutokwa na manii na sio baada ya kukojoa.” Abu Hanifa alisema: “Hakika mimi ni mtu wa kutumia kiasi (rai).” Abu Hanifa baada ya kuulizwa masuala mengi ambayo hakuyapatia jawabu, aliamua kufunga safari na kuelekea Madina katika msikiti wa Bwana Mtume  na akapinda goti mbele ya mwalimu wake huyo na kuchukua maarifa sahihi kutoka kwake, hata akawa na msemo wake maarufu ulionukuliwa kutoka katika kinywa chake akisema: “Lau kama si miaka miwili angaliangamia Annu-uman (Abu Hanifa).” Hapa anakusudia ile miaka miwili aliyosoma kwa Imam Ja’far Sadiq . Abu Hanifa hakuwa mtu wa mwanzo kuyasema maneno hayo aliyoyasema, wako waliomtangulia, Khalifa wa pili alipokuwa aki30

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 30

1/17/2017 12:44:41 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

toa hukumu ambazo zilikuwa kinyume na mafunzo ya Uislamu au kuulizwa masuala ambayo alishindwa kuyajibu alikuwa akielekea kwa yule aliye mjuzi zaidi miongoni mwa Masahaba, naye ni Imamu Ali  na baada ya kupata jawabu sahihi alikuwa akisema: “Lau kama si Ali, angeliangamia Umar.”16 Na pia alikuwa akijikinga kwa Mwenyezi Mungu ili asipate masuala magumu iwapo Imam Ali  hayuko naye.17 Hivi ndivyo ilivyokuwa mwenendo wa wale waliotangulia. Alichokifanya Khalifa wa pili ni kutekeleza maagizo ya Mtume  kama alivyosema kuhusiana na watu wa nyumba yake (Ahlulbayt a.s.) ambao ndani yake mnapatikana wale Makhalifa kumi na mbili. Mtume  anasema kuhusiana na nafasi ya watu hao katika Uislamu:

»‫” مثل أهل بيتي فيكم‬.‫مثل سفينة نوح من ركبها نجا ومن تخلف عنها غرق‬ “Mfano wa watu wa nyumbani kwangu ni kama jahazi ya Nuhu, mwenye kuipanda ameokoka na aliyeiwacha alighariki na kupotea.”18

Lau kama Sunnah ya kweli ingelifuatwa, basi watu wasingediriki kusimama mbele ya Mola Wao Muumba kwa kuswali hali ya kuwa nguo zao zina najisi ambayo inampasa kuoga yule aliyetokwa na najisi hiyo (manii) kutokana na uzito wa najisi hiyo, nasema haya kwani wako ambao huswali na najisi hiyo wakitegemea maandiko yasiyo na mashiko! Ikiwa hoja ni kwamba manii si najisi kwa sababu ndio chanzo cha mwanadamu, bila shaka tunaelewa ya kwamba baada ya mwanamke   Tafsir Raziy Juz. 21, uk. 22.   Tahdhibut-Tahdhib Juz.7,uk. 927. Asadul Ghabah Juz.4, uk. 23. Tajul-urus Juz.15, uk. 494. 18   Taz. Al-Haythamiy, Majmau Zawa’id, Juz.9, uk. 168. al-Hakim, al-Mustadrik alaa Swahihayn, Juz. 2, uk. 373. 16 17

31

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 31

1/17/2017 12:44:41 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

kutunga mimba, mimba hiyo hupita katika hali mbalimbali, miongoni mwake ni kuwa damu, lakini hakuna anayesema ya kwamba damu hiyo ni tohara ikiwa itatoka ndani ya mwili wa mwanadamu! Suala la kuoga baada ya kutokwa na manii na kuitoharisha nguo au sehemu ya mwili iliyogusa najisi hiyo liko hata katika kitabu cha Bibilia, inasema: “Kama mwanamume yeyote akitokwa na shahawa yake, ni lazima aoge mwili mzima kwa maji, naye atakuwa najisi mpaka jioni. Vazi lililodondokewa shahawa au ngozi yeyote iliyoguswa na shahawa hiyo ni lazima ioshwe kwa maji, na itakuwa najisi mpaka jioni. Kama mwanamume akilala na mwanamke akatokwa na shahawa, basi ni lazima wote wawili wakoge kwa maji, nao watakuwa najisi mpaka jioni.”19 Pamoja ya kwamba kitabu cha Bibilia ni katika vitabu vilivyopoteza usahihi na ukweli lakini bado kina baadhi ya mambo yanayokubaliana na sharia za Kiislamu, moja kati ya hayo ni unajisi wa manii, na njia ya kuitoharisha nguo au pahala paliposibiwa na manii. Tunawaomba ndugu Waislamu wasiwe kama Wakristo, ambao wanajiona kutokuwa na ulazima wa kufuata mafunzo kama haya pamoja na kitabu chao kuwataka kufanya hivyo, kwani kubwa kwao ni kumwamini Yesu (Nabii Issa ) kuwa ni mtoto wa Mungu, na kwamba kasulubiwa, imani hiyo inatosha kumfikisha mtu kwenye ufalme wa mbinguni! Ama sisi Waislamu mafunzo yetu ni kinyume kabisa na ya Wakristo, hatuna budi kufanya matendo mema baada ya imani ili 19

Mambo ya Walawi 15: 16-18. 32

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 32

1/17/2017 12:44:41 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

tuepukane na adhabu ya Mwenyezi Mungu, hayo tutayafikia iwapo kila mmoja wetu atajilazimisha kufuata yale aliyokuja nayo Mtume wetu  ikiwemo Hadidhi yake aliyotutaka tushikamane na vizito viwili, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na watu wa nyumbani kwake. Kwa kufanya hivyo itakuwa ndio njia pekee ya kuzifikia Sunnah sahihi za Mtume wetu  na hatimaye kupata radhi za Mola Wetu Mtukufu.

33

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 33

1/17/2017 12:44:41 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

KUELEKEA KIBLA WAKATI WA KWENDA HAJA

K

atika kipengele hiki mwandishi wa kitabu cha Fiqhi Sunnah, hakuona ubaya wowote wa mtu kujisaidia hali ameelekea Kibla! Pamoja na kueleza Hadithi inayokataza kufanya hivyo. Anasema Sheikh Sayyid Sabiq: “Na mwenye kwenda haja anatakiwa akiheshimu Kibla, kwa kutokielekea au kukipa mgongo. Kutokana na Hadithi ya Abu Hureira  ni kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu  amesema: “Wakati mmoja wenu atakapokaa kwa ajili ya kwenda haja, basi asikielekee Kibla na wala asikipe mgongo.” Hadithi hii kaipokea Ahmad na Muslim. Baada ya mwandishi kunakili Hadithi hii yenye mafunzo bora kabisa katika Dini yetu, amesema: “Katazo hili ni kuonesha karaha tu (si haramu), kutokana na hadithi ya Ibn Umar  aliposema: “Siku moja niliparamia nyumba ya Hafsa, nilimuona Mtume  akijisaidia hali ya kuelekea Shamu na huku amekipa mgongo Kibla. Imepokewa na jamaa.” Na baada ya kunakili riwaya hii, ametoa rai nyingine kwa kuse-

ma:

“Au inawezekana kukusanya mambo yote mawili, kwa maana uharamu wa kuelekea au kukipa mgongo Kibla ni pale mtu anapojisaidia akiwa katika jangwa, na inajuzu wakati anapokuwa ndani ya jengo.” Hoja yake hii ya pili ameitegemezea riwaya isemayo: “'Kutoka kwa Maruwan Asghar, amesema: “Nilimuona Ibn Umar akimsimamisha mnyama wake, kisha akakojoa hali ya kuele34

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 34

1/17/2017 12:44:41 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

kea Kibla, nikamwita na kumuuliza, ewe! Abdurrahman… Je! Jambo hilo halikukatazwa? Alijibu, limekatazwa… (lakini) jambo hili limekatazwa ukiwa unajisaidia na ilhali uko katika jangwa hakuna majumba), ama ikiwa kati yako na Kibla kuna kitu kinachokuzuia usikione Kibla (Alqaaba), basi hakuna ubaya wowote. Imepokewa na Abu Daud, Ibn Khuzayma na Hakim, na sanadi yake ni nzuri…” Tukianza kuangalia matini ya Hadithi aliyoisimulia Abu Huraira tunaona wazi namna Bwana Mtume  alivyokuwa akiiheshimu nyumba ya kwanza ya Mwenyezi Mungu iliyowekwa kwa ajili ya watu, ili wapate manufaa yao, nyumba iliyoasisiwa na Baba wa Mitume, nyumba ambayo Swala ya mtu yeyote haikubaliwi bila ya kuielekea, na wala ibada ya Hijja na Umra hazikamiliki bila ya kuizunguka. Kwa utukufu huo aliwakataza Waislamu wasiielekee na wala wasiipe mgongo pindi wanapojisaidia. Lakini katika riwaya ya pili tunaona mambo ni kinyume na yale aliyoyasema, baada ya huyo aliyeparamia nyumba yake alimuona akikhalifu maneno yake!! Na watu wakapata hoja ya kukivunjia heshima Kibla chao kwa kujisaidia huku wakikielekea au kukipa mgongo, kama ilivyo hata katika misikiti mingi, vyoo vimejengwa bila ya kuzingatia heshima ya Kibla. Je! Wale walionakili tendo la Ibn Umar la kuparamia ukuta wa nyumba ya Mtume  hawaoni ya kwamba wamempaka matope kwa tabia hiyo mbaya ya kupiga bodi (chabo) nyumba ya mtu Mtukufu  ambaye pia alikuwa ni shemeji yake?! Ikiwa ni kweli alifanya kitendo hicho kibaya mno, vipi mtu kama huyo asadikiwe maneno yake? Na lau kama wakati wa kupiga kwake bodi angemuona dada yake (Hafsa) angesimulia?! Kwa kweli ni Sunnah za kusikitisha na zenye kumdhalilisha Mtume wetu! Tendo hilo linalonasibishwa na Ibn Umar ni vigumu kukubalika kutokea kwake, na lingelitokea basi maonyo makali na lawama nzito 35

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 35

1/17/2017 12:44:41 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

zingemteremkia, kama zilivyowateremkia wale waliomvunjia heshima Bwana Mtume  kwa kumwita na hali wako nje ya nyumba yake. Mwenyezi Mungu anasema:

‫صبَرُوا‬ َ َ‫إِ َّن الَّ ِذينَ يُنَا ُدون‬ َ ‫ َولَوْ أَنَّهُ ْم‬. َ‫ت أَ ْكثَ ُرهُ ْم لاَ يَ ْعقِلُون‬ ِ ‫ك ِمن َو َراء ْال ُح ُج َرا‬ ...‫َحتَّى ت َْخ ُر َج إِلَ ْي ِه ْم لَ َكانَ َخيْراً لَّهُم‬ “Hakika wale wanaokuita nyuma ya vyumba, wengi wao hawana akili. Na kama wangalingoja mpaka uwatokee, ingelikuwa kheri kwao…” (Qur’ani, 49: 4-5).

Na hata pale baadhi ya Masahaba walipokuwa wakiingia nyumbani kwa Mtume bila ya kuomba ruhusa, au kuingia wakati wa mlo, na baadaye kupiga soga, na wako wengine walikuwa wakikaa na kujipangia ni nani atawaowa wake wa Mtume  baada ya yeye kufariki, Mwenyezi Mungu hakuyanyamazia kimya mambo hayo, ili kuilinda na kuitetea heshima na hadhi ya kipenzi Chake, aliteremsha Aya ili kuwataka waachane na tabia hizo mbaya, anasema:

‫يَا أَيُّهَا الَّ ِذينَ آ َمنُوا لاَ تَ ْد ُخلُوا بُيُوتَ النَّبِ ِّي إِلاَّ أَن ي ُْؤ َذنَ لَ ُك ْم إِلَى طَ َع ٍام َغ ْي َر‬ َ‫َاظ ِرينَ إِنَاهُ َولَ ِك ْن إِ َذا ُد ِعيتُ ْم فَا ْد ُخلُوا فَإِ َذا طَ ِع ْمتُ ْم فَانت َِشرُوا َولاَ ُم ْستَأْنِ ِسين‬ ِ ‫ن‬ ِّ ‫ي فَيَ ْستَحْ يِي ِمن ُك ْم َوللاهَّ ُ ال يَ ْستَحْ يِي ِمنَ ْال َح‬ ‫ق‬ ٍ ‫لِ َح ِدي‬ َّ ِ‫ث إِ َّن َذلِ ُك ْم َكانَ ي ُْؤ ِذي النَّب‬ ْ َ‫ب َذلِ ُك ْم أ‬ ‫طهَ ُر لِقُلُوبِ ُك ْم َوقُلُوبِ ِه َّن‬ ٍ ‫َوإِ َذا َسأ َ ْلتُ ُموهُ َّن َمتَاعا ً فَاسْأَلُوهُ َّن ِمن َو َراء ِح َجا‬ ‫َو َما َكانَ لَ ُك ْم أَن تُ ْؤ ُذوا َرسُو َل للاهَّ ِ َوال أَن تَن ِكحُوا أَ ْز َوا َجهُ ِمن بَ ْع ِد ِه أَبَداً إِ َّن َذلِ ُك ْم‬ .ً‫َظيما‬ ِ ‫َكانَ ِعن َد للاهَّ ِ ع‬ “Enyi mlioamini! Msiingie nyumba za Nabii ila mpewe ruhusa kwenda kula, sio kungojea kiwive. Lakini mtakapoitwa basi ingieni, na mkishakula tawanyikeni, wala msiweke mazungumzo. Hakika hayo yanamuudhi Nabii naye anakustahini, lakini Mwenyezi Mungu hastahi kwa jambo la haki. Na mnapowauliza wakeze kitu waulizeni 36

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 36

1/17/2017 12:44:41 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

nyuma ya mapazia. Hivyo ndio usafi zaidi kwa nyoyo zenu na nyoyo zao. Wala haikufalieni kumuudhi Mtume wa Mwenyezi Mungu, wala kuwaoa wake zake baada yake kabisa. Hakika jambo hilo ni kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu.” (Qur’ani, 33:53).

Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu anavyowafunza Waislamu jinsi ya kukaa na kuamiliana na Mtume wao. Na hakuchelea kumpasha yeyote aliyeivunjia heshima yake. Na kama wako wanaokubali ya kwamba Ibn Umar kafanya hayo aliyoyafanya basi hukumu yake wanaijua wao, na Sunnah hiyo naibakie kwake, kosa lake hilo isiwe ni sababu ya wengine kuingizwa makosani. Mtume  hakuwa na tabia ya kukataza jambo kisha yeye akawa ni wa mwanzo kulitenda jambo hilo, kwani kufanya hivyo ni ukosefu wa akili na ni kuingia katika makosa makubwa kama anavyosema Mwenyezi Mungu:

َ‫َاب أَفَالَ تَ ْعقِلُون‬ َ ‫اس بِ ْالبِ ِّر َوتَن َسوْ نَ أَنفُ َس ُك ْم َوأَنتُ ْم تَ ْتلُونَ ْال ِكت‬ َ َّ‫أَتَأْ ُمرُونَ الن‬ “Je! Mnawaamrisha watu mema na mnajisahau nafsi zenu, na hali nyinyi mnasoma Kitabu, basi hamfahamu.” (Qur’ani, 2: 44).

‫ َكبُ َر َم ْقتا ً ِعن َد للاهَّ ِ أَن تَقُولُوا َما ال‬. َ‫يَا أَيُّهَا الَّ ِذينَ آَ َمنُوا لِ َم تَقُولُونَ َما ال تَ ْف َعلُون‬ َ‫تَ ْف َعلُون‬ “Enyi mlioamini mbona mnasema msiyoyatenda? Ni kosa kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu kusema msiyoyatenda.” (Qur’ani, 61:23.).

Ama riwaya ya tatu inatuonesha watu waliokuwa wakiishi na Mtume  namna walivyokuwa wakijisaidia, walikuwa wakijisaidia hali ya kuelekea Kibla tena bila ya kujificha. Tendo hilo la Ibn Umar si hoja kwa wengine, hoja alizozitoa na kukubaliwa na Sheikh Sayy37

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 37

1/17/2017 12:44:41 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

id Sabiq, hazikubaliani na akili iliyotimia, eti mtu akijisaidia bila ya kuwepo kizuizi kati yake na Kibla, atakuwa amefanya makosa, na kama kutakuwa na kizuizi itakuwa si kosa! Suala linakuja, iwapo mtu ameswali bila ya kukielekea Kibla (Alqaaba) moja kwa moja, kwa mfano, kuswali ndani ya nyumba yake, je! Swala yake itakuwa si sahihi? Ndugu Mwislamu, tufuate mwenendo wa Mtume wetu  kwani alipowakataza Masahaba kutokielekea au kutokipa mgongo Kibla wakati wa kwenda haja, alikuwa yuko Madina, ambako ni mbali mno na Makka iliko na hiyo nyumba tukufu ya Kaaba. Sunnah sahihi ni kutokielekea na kutokipa mgongo Kibla popote mtu anapojisaidia, ili kulinda heshima ya nyumba ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

38

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 38

1/17/2017 12:44:41 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

KUJISAIDIA WIMA

K

wa mara nyingine mwandishi amefanya kila aliloweza ili kusimamisha dalili ya kuhalalisha kujisaidia wima, aliyetolewa muhanga katika kitendo hiki kwa mara nyingine ni Bwana Mtume  Sheikh Sayyid Sabiq anasema: “Na anayejisaidia asikojowe wima, kwani kufanya hivyo (kukojoa wima) kunaondosha utulivu na tabia nzuri, na huenda akarukiwa na cheche za mkojo, lakini ikiwa mtu ataepukana nazo (chachizo za mkojo) itajuzu kukojoa wima, Bibi Aisha amesema: Atakayewasimulia ya kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu  amekojoa wima, basi msimwamini, alikuwa hakojoi isipokuwa katika hali ya kukaa. Imepokewa na wapokezi watano… Attirmidhiy amesema: Riwaya hii ni nzuri zaidi na sahihi zaidi katika mlango huu… Na maneno ya Aisha amesimamia yale aliyokuwa akiyajua yeye, kwa hivyo hayapingani na yale yaliyopokewa kutoka kwa Hudhayfa  ya kwamba Mtume  alifika katika jaa (jalala) la watu fulani, na akakojoa wima, kisha akasema aletewe maji, nikampelekea na akatawadha na akapangusa khofu zake. Imepokewa na jamaa. “ Baada ya kuwepo riwaya hizo mbili zenye kupingana, Imamu Nawawiy ameamua kuzikubali riwaya zote kama Sheikh Sayyid Sabiq alivyomnukuu, anasema: “Kukojoa hali ya kukaa kunanipendezesha zaidi, na kukojoa wima ni mubaha (inafaa), na yote hayo yamethibiti (yametendwa) kwa Mtume .” Haya ndio aliyoyanakili Sheikh Sayyidi Sabiq, na anatuambia kujisaidia wima ni katika mwenendo na Sunnah ya Mtume wetu Mtukufu ! Alichokifanya ni kunukuu riwaya na maneno ya Nawawiy, huku 39

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 39

1/17/2017 12:44:41 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

akiifumbia macho shakhsiyya ya Bwana Mtume . Ameshindwa kumsafisha Mtume  kwa lengo la kuvilinda vitabu vilivyonukuu riwaya hiyo, kwani angelisema riwaya hiyo si sahihi, ingelimaanisha ya kwamba si kila riwaya iliyomo kwenye Sahihi Bukhari na Muslim ni sahihi. Bibi Aisha alipotutaka kutomwamini yeyote anayedai ya kwamba Mtume  alijisaidia wima, bila ya shaka aliyanena hayo kutokana na kufahamu fika tabia nzuri alizokuwa nazo, kabla na baada ya kupewa Utume, Bibi Aisha aliyafahamu vyema maneno ya Mwenyezi Mungu kuhusiana na Mtume Wake, pale aliposema:

‫ُول للاهَّ ِ أُ ْس َوةٌ َح َسنَةٌ لِّ َمن َكانَ يَرْ جُو للاهَّ َ َو ْاليَوْ َم الآْ ِخ َر َو َذ َك َر‬ ِ ‫لَقَ ْد َكانَ لَ ُك ْم فِي َرس‬ ً‫للاهَّ َ َكثِيرا‬ “Hakika nyinyi mnayo ruwaza (kigezo) njema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa anayemtaraji Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na akamkumbuka Mwenyezi Mungu sana.” (Qur’ani, 33:21).

‫َظ ٍيم‬ َ َّ‫َوإِن‬ ِ ‫قع‬ ٍ ُ‫ك لَ َعلى ُخل‬ “Na hakika wewe una tabiya tukufu” (68: 4).

Hivi ndivyo Bibi Aisha alivyomwelewa Mtume Mtukufu wa daraja  kwa kupitia Qur’ani, na hata wale waliokuja baada yake wanamwelewa hivyo, Ja’far Barazanji katika kitabu chake kinachoelezea mazazi ya Mtume  na maisha yake kwa ujumla (Kitabu cha Maulidi) anasema:

.‫وكان صلى هللا عليه وسلَم أكمل الناس خَلقا و ُخلقا ذا ذات وصفات سنيّة‬ “Mtume, rehema za Mwenyezi Mungu na amani zimshukie juu yake, alikuwa mkamilifu zaidi wa watu, kwa umbile na tabia na mwenye tabia njema.” 40

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 40

1/17/2017 12:44:41 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

Je! Ni kweli iliwezekana kwa mtu kama Muhammad ibn Abdillahi  kufanya kitendo hicho katika hali ambayo alikuwa na miaka zaidi ya arobaini! Kitendo ambacho hakifanywi na mtu wa kawaida mwenye muruwa na heshima yake! Wakoloni walipoanzisha shule, wazee wengi wa mwambao wa Afrika Mashariki waliwazuia watoto wao kusoma, miongoni mwa hoja zao ni kwamba huko walikuwa wakifundishwa kukojoa wima. Riwaya kama hizi ndizo zinazowapa fursa maadui wa Uislamu kumkashifu Mtume wetu, na kubwa tunalolifanya ni kuzijaza barabra kwa maandamano ya hamasa pale wanapomkashifu, wakati huku maktaba zetu zikikosa wasomaji na watafiti wa mambo yanayohusiana na Dini yetu, kwa lengo la kuzipatia ufumbuzi riwaya kama hizi na nyinginezo zinazomshusha hadhi Mtume wetu . Vitabu hivyo vimeweza kutunga filamu za kumdhalilisha Mtume , na kuwarahisishia maadui kuzicheza filamu hizo! Si mwenendo wala Sunnah ya Mtume  kujisaidia wima. Na kila mwenye uchu wa kufuata Sunnah za Mtume  asitosheke na kujiita ya kwamba yeye ni mtu wa Sunnah, bali hana budi kuanza kubadili miundo ya sehemu za kujisaidia, kwani tunashuhudia hata katika misikiti mingi vyoo vyake vimeelekezwa Kibla, hata hiyo misikiti ya wale wanaojiita Answaru Sunnah pamoja na Masalafi. Hapa tunaungana na Bibi Aisha kwa kutoiamini riwaya hii na mfano wa hii zenye kumdhalilisha na kumvunjia heshima kipenzi cha Mwenyezi Mungu Mtukufu . Kuikubali riwaya ya Hudhayfa, ni kukubali ya kwamba Mtume  alikuwa hajisitiri (hajifichi) wakati wa kujisaidia! Hasha jambo hilo kufanywa na mtu wa kawaida seuze Mtu bora kuliko watu wote.

41

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 41

1/17/2017 12:44:41 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

KUOSHA MIGUU

W

aislamu wengi huosha miguu yao wakati wanapotawadha, la kuelewa hapa ni kwamba pia wako Waislamu wanaopaka miguu yao badala ya kuiosha, kila upande unatoa dalili ya Aya ya sita ya Suratul-Maida, inayosema:

ْ ُ‫وا إِ َذا قُ ْمتُ ْم إِلَى الصَّال ِة فا ْغ ِسل‬ ْ ُ‫يَا أَيُّهَا الَّ ِذينَ آ َمن‬ ‫ق‬ ِ ِ‫وا ُوجُوهَ ُك ْم َوأَ ْي ِديَ ُك ْم إِلَى ْال َم َراف‬ ْ ‫ين َوإِن ُكنتُ ْم ُجنُبا ً فَاطَّهَّر‬ ْ ‫َوا ْم َسح‬ ‫ُوا َوإِن ُكنتُم‬ ِ ‫ُوا بِ ُر ُؤ‬ ِ َ‫وس ُك ْم َوأَرْ ُجلَ ُك ْم إِلَى ْال َك ْعب‬ ْ ‫ضى أَوْ َعلَى َسفَ ٍر أَوْ َجاء أَ َح ٌد َّمن ُكم ِّمنَ ْالغَائِ ِط أَوْ الَ َم ْستُ ُم النِّ َساء فَلَ ْم ت َِج ُد‬ ‫وا‬ َ ْ‫َّمر‬ ْ ‫ص ِعيداً طَيِّبا ً فَا ْم َسح‬ ْ ‫َماء فَتَيَ َّم ُم‬ ّ‫ُوا بِ ُوجُو ِه ُك ْم َوأَ ْي ِدي ُكم ِّم ْنهُ َما ي ُِري ُد ه‬ ‫للاُ لِيَجْ َع َل‬ َ ‫وا‬ َ‫ج َولَـ ِكن ي ُِري ُد لِيُطَهَّ َر ُك ْم َولِيُتِ َّم نِ ْع َمتَهُ َعلَ ْي ُك ْم لَ َعلَّ ُك ْم تَ ْش ُكرُون‬ ٍ ‫َعلَ ْي ُكم ِّم ْن َح َر‬ “Enyi mlioamini! Mnaposimama kwa ajili ya Swala basi osheni nyuso zenu, na mikono yenu mpaka vifundoni, na mpake vichwa vyenu, na miguu yenu mpaka vifundoni. Na mkiwa na janaba basi ogeni. Na mkiwa wagonjwa au mmo safarini, au mmoja wenu ametoka chooni au mmewagusa wanawake, na hamkupata maji, basi tayamamuni vumbi lililo safi, na mpake nyuso zenu na mikono yenu. Hapendi Mwenyezi Mungu kukutieni katika taabu; bali anataka kukutakaseni na kutimiza neema Yake juu yenu ili mpate kushukuru.” (Qur’ani, 5:6).

Tukirudi katika tafsiri ya marehemu Sheikh Addalla Saleh Alfarsy, tunaona neno ‘kuosha’ amelitia katika mabano, wakati wa kutafsiri Aya hiyo, hii ni dalili ya wazi ya kwamba miguu imeunganishwa na kichwa na sio na uso. La muhimu hapa si kuingia katika mjadala mrefu kwani unahitaji maelezo mengi yakiwemo ya kinahau ili kusimamisha hoja ya kupaka miguu kwa wale wanaopinga hukumu hii, licha ya kwamba Aya iko wazi ikiwataka 42

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 42

1/17/2017 12:44:41 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

Waumini wapake miguu yao badala ya kuiosha. Pamoja na hayo ninachotaka kueleza si sahihi ya kwamba Masahaba wote wa Mtume  wameungana na kukubaliana juu ya kuosha miguu, kama Sheikh Sayyid Sabiq alivyomnukuu Abdurrahman ibn Abi Layl. Kuna miongoni mwa Masahaba wanaoona wajibu ni kupaka miguu na sio kuiosha, na pia kuna baadhi ya Matabiina waliopita mwendo wa Masahaba hao. Mfasiri wa Qur'ani, al-Alusiy anasema: “'Watu wamekhitalifiana kuhusu kuosha miguu na kupaka. Amesema Imamu Raaziy: "Kutoka kwa ibn Abbas, Anas ibn Malik, Iqrima, Ash-sha-abiy, na Abu Ja’far Muhammad ibn Ali al-Baqir  ya kwamba, wajibu katika miguu ni kupakwa…” Pia amenukuu maneno ya Hassan al-Baswariy na Muhammad ibn Jarir Attabary ya kwamba: “Mukallafi (mtu aliye baleghe) ana hiyari kati ya kuiosha miguu au kuipaka.” Lakini ibn Taymiya anawaona wale wanaopaka, wakiwemo hao Masahaba na Matabiina aliowataja al-Alusiy kuwa ni wazushi na wenye kukhalifu Sunnah pamoja na Qur'an!20 Ni vyema Waislamu waelewe ya kwamba pale wanapowaona Waislamu wengine wanapaka miguu yao ni kwamba wana dalili, tena dalili ambayo haivunji heshima ya Bwana Mtume  Na pia wasomeshaji wa kitabu cha Fiqhi Sunnah wasitosheke na maamuzi yaliyomo humo, bila ya kurudi katika vitabu vingine. Na la kushangaza katika mlango wa ‘Almas-hi Alal khuffayni.’ pamejuzishwa kupaka juu ya ngozi ya mnyama inayovaliwa miguuni (khofu) au soksi, kama mtu ni msafiri au si msafiri, lakini kupaka katika ngozi ya mguu inaonekana ni kosa na uzushi! 20

Daqaiq Tafsir Juz. 2, uk. 28. 43

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 43

1/17/2017 12:44:41 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

Bado kwa wale wanaopenda kumfuata Mtume  katika mambo yanayohusiana na ibada zao, wanalazimika kufanya juhudi za kuutafuta ukweli katika hili na mengineyo ili Sunnah sahihi itawale katika ibada zao na maisha yao yote kwa ujumla.

44

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 44

1/17/2017 12:44:41 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

VIUNGO VYA SIJDA

K

abla ya kuangalia yale aliyoyanakili Sheikh Sayyid Sabiq, kwa faida ya msomaji na mwenye kutafuta Sunnah sahihi, napenda kutoa maana ya neno ‘Sajada’ ambalo chimbuko lake ni ‘Sujuud.’ Katika kamusi zote za Kiarabu zinasema: Neno ‘Sajada’ ni kuweka paji la uso juu ya ardhi. Hii ndio maana khalisi ya neno hilo. Tukirudi katika kitabu tunachokwenda nacho ‘Fiqhi Sunnah,’ tunamwona mwandishi akitoa Hadithi zinazoashiria maana hii.

Hadithi ya kwanza inasema: Mtume  amesema: “Nimeamrishwa nisujudu juu ya viungo saba: juu ya paji la uso – aliashiria kwa mkono wake kwenye pua yake – na mikono miwili, magoti mawili na ncha (pembezoni) za miguu miwili. Wapokezi wote wamewafikiana juu ya Hadithi hii.” Hadithi ya pili: "Nimeamrishwa nisujudu juu viungo saba na wala nisikusanye nywele wala nguo, (viungo hivyo ni) paji la uso, pua, mikono miwili, magoti mawili na miguu miwili." Imepokewa na Muslim na Annasaai. Hadithi ya tatu: Kutoka kwa Abi Humeid: “Mtume  alipokuwa akisujudu alikuwa akimakinisha (akiambatanisha) pua yake na paji la uso wake juu ya ardhi.” Imepokewa na Abu Daud na kusahihishwa na Attirmidhiy. Riwaya hizi alizozitaja Sheikh Sayyid Sabiq, zinatueleza ni jinsi gani Mtume  alivyokuwa akisujudu, na jambo la kuzingatia katika maudhui haya ni kule kuweka paji la uso juu ya ardhi kama riwaya zinavyoeleza.

45

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 45

1/17/2017 12:44:41 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

Katika ulimwengu wa Kiislamu ni wafuasi wa madhehebu ya Ahlulbayt  peke yao wanaoitekeleza Sunnah ya kusujudu juu ardhi, na kitendo chao hicho kimeleta maneno yasio na mwisho dhidi yao, kama kwamba wanachokifanya ni uzushi, basi kama kuna shaka juu hadithi hizi, basi na tuangalie fatwa ya yule ambaye maneno yake hayapingwi, na aliyefanywa na baadhi ya watu kuwa ni kigezo cha Sunnah katika zama zetu hizi, mtu huyo ni Ibn Taymiya. Ibn Taymiya aliulizwa kuhusiana na mtu ambaye hutandika zulia katika msikiti na kuswalia (kusujudia) juu yake, je, kitendo chake hicho ni bidaa au si bidaa? Jawabu lake lilikuwa ni kama ifuatavyo: “…ama Swala juu ya zulia kiasi ambacho mwenye kuswali imekuwa ni ada yake kufanya hivyo, basi na atambue ya kwamba jambo hilo si katika Sunnah za waliotangulia miongoni mwa Muhajirina na Ansaar katika zama za Mtume  na wale waliokuja baada yao na kuwafuata kwa wema, bali walikuwa wakiswali katika msikiti wa Mtume  juu ya ardhi na wala hakuna yeyote aliyekuwa akiswali juu ya zulia maalumu kwa ajili ya Swala”. Imepokewa ya kwamba Abdurrahman ibn Mahdi alipofika Madina, alitandika zulia, Malik aliamrisha awekwe mahabusu, Malik aliambiwa huyo ni Abdurrahman ibn Mahdi. Malik alisema: Je, huelewi ya kwamba kutandika zulia katika msikiti wetu ni bidaa? Na katika Sahihi, kutoka kwa Abi Saidil Khudriy kuhusiana na Hadithi ya itikafu ya Mtume , alisema: Tulikaa itikafu pamoja na Mtume  basi alitukumbusha Hadithi, katika Hadithi hiyo alisema: Mwenye kukaa itikafu na arejee katika itikafu yake, kwani mimi nimeona katika usiku huu na umeniona nasujudu juu ya udongo na maji, na mwishowe umeona – akimaanisha asubuhi ya mwezi ishirini na moja - kwa wote wawili athari ya maji na udongo. Hii ni dalili ya wazi ya kwamba alikuwa akisujudu juu ya udongo, na msikiti 46

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 46

1/17/2017 12:44:41 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

wake ulikuwa umeezekwa kwa makuti ya mtende, wakati mvua ilipokuwa inanyesha ilikuwa ikiingia ndani, msikiti wake ulikuwa ni ardhi (haukutandikwa). Na huenda ikawa waliweka changarawe, kama ilivyopokewa katika Sunnah ya Abu Daud kutoka kwa Abdillah ibn Harith alisema: Nilimuuliza Ibn Umar  kuhusiana na changarawe zilizokuwemo msikitini, alijibu: Usiku mmoja tulinyeshewa na mvua, na ardhi ilikuwa imelowana, ikawa mtu anakuja na changarawe katika nguo yake na kisha kuzitawanya mbele yake, Mtume  alipomaliza Swala yake alisema: Ni uzuri ulioje huu (mliofanya)…” Ama suala la kusujudu juu ya nguo, Ibn Taymiya analiona ni ruhusa pale tu mtu atakaposhindwa kuweka paji la uso wake katika ardhi pindi ardhi itakapokuwa ya moto sana, dalili ya hilo ni Hadithi iliyopokewa na Bukhari, Muslim na wapokezi wengineo, Hadithi hiyo inasema: “Tulikuwa tukiswali pamoja na Mtume  wakati wa jua kali, pale ambapo mmoja wetu hawezi kuweka paji lake katika ardhi alikuwa akitandika nguo yake na kusujudu juu yake.” Ibn Taymiya anamalizia kwa kusema: “Hili ni jambo lililo wazi ya kwamba walikuwa hawasujudu juu ya mazulia, wala juu ya kizuizi baina ya vipaji vyao na ardhi…” Pia Umar ibn Abdul Aziz (mmoja kati ya makhalifa wa kibanu Umayya), alikuwa hasujudu isipokuwa juu ya udongo. 21 Ibn Taymiya pamoja na Umar ibn Abdul Aziz, ambaye amepandishwa daraja la Makhalifa waongofu, watu hawa wameungana na Mashia Ithnaasharia katika kuitekeleza Sunnah ya Mtume  kwa kusujudu juu ya ardhi. Na kule kufinyanga kipande cha udongo na kusujudu juu yake si jambo la kuzua katika Dini. Tumewaona Masahaba walivyokuwa wakichukua changarawe na kuzitandaza chini ki21

Ahyau Ulumi ddiyn Juz.1, uk. 177. 47

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 47

1/17/2017 12:44:42 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

sha wakisujudu juu yake. Hii ndio Sunnah ya Mtume wetu  na kutendwa na Masahaba, lakini leo yale yalioingizwa katika Dini ndio yanayoonekana ni sawa, na Sunnah kuonekana ni uzushi na viroja! Na katika kuitolea tafsiri ibara ya Aya isemayo:

‫ِسيماهُ ْم فِي ُوجُو ِه ِه ْم ِم ْن أَثَ ِر ال ُّسجُو ِد‬ “Alama zao zi katika nyuso zao, kwa athari ya kusujudu…” (Qur’ani, 48:29).

Ikrima na Said ibn Jubeyr wanasema: “Hiyo ni alama ya mchanga iliopo katika vipaji vyao vya uso.” Na Abu Aaliya naye akaongezea kusema: “Wanasujudu juu ya udongo na wala sio juu ya nguo.”22 Kwa kuweka bayana zaidi fatwa ya Ibn Taymiyya, fatwa hiyo tumeinakili kwa lugha ya Kiarabu mwishoni mwa kitabu hiki.

22

Tafsiru Tha’labiy: Juz. 9, uk. 25. 48

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 48

1/17/2017 12:44:42 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

KUMSWALIA MTUME .

K

utokana na dalili mbalimbali alizozinukuu Sheikh Sayyid Sabiq amefikia tija ya kuona kumswalia Bwana Mtume  katika Swala ni jambo la mustahabu (Sunnah) na siyo wajibu, ingawa wako maulamaa wanaoona jambo hilo tukufu linalotendwa na Mwenyezi Mungu pamoja na Malaika wake kuwa ni wajibu, kama anavyosema Imam Shafi:

‫يا آل بيت رسول هللا حبّكم فرض من هللا في القرآن أنزله‬ ‫كفاكم من فضل القدر أنّكم من لم يص ّل عليكم ال صالة له‬ “Enyi watu wa nyumba ya Mtume, kupendwa kwenu ni faradhi (lazima) kutoka kwa Mwenyezi Mungu kama alivyoteremsha katika Qur›ani (42:23), inatosha kwenu kuwa ni heshima kubwa mliyonayo, yeyote asiyewaswalia nyinyi (asiyewatakia rehema), mtu huyo hana Swala.”

Maneno haya ya Imam Shafi yanamaanisha utukufu wa watu wa nyumba ya Mtume  kiasi kwamba hata yule anayeona kumswalia Mtume  si jambo la wajibu, basi malipo ya amali hiyo hayatokamilika bila ya kumswalia Mtume  pamoja na jamaa zake ­(Ahlulbayt). Sheikh Sayyid Sabiq anasema: “Ni mustahabu kwa mwenye kuswali kumtakia rehema Mtume  katika tashahhud (tahiyya) ya mwisho, kwa kusoma moja kati ya namna zifuatazo: Kutoka kwa Abu Masoud Albadry amesema: “Bashir Ibn Said alisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu 49

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 49

1/17/2017 12:44:42 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

ametuamrisha tukuswalie wewe, basi tukuswalie vipi? Mtume alikaa kimya, kisha akasema: Ewe Mwenyezi Mungu mtakie rehema Muhammad na jamaa wa Muhammad, kama ulivyowarehemu jamaa wa (Nabii) Ibrahim, na mbariki Muhammad pamoja na jamaa zake kama ulivyowabariki jamaa wa Ibrahim…” Namna ya pili aliyoitaja Sheikh Sayyid Sabiq sitoinukuu kwa vile haina tofauti sana na hii ya kwanza. Jambo la msingi linalojitokeza hapa ni kufikiri na kuyatia akilini yote tunayotamka katika Swala zetu, tumeona ni namna gani Sheikh Sayyid Sabiq alivyotunukulia namna ya kumswalia Bwana Mtume , sawa iwe mtu anaitikadi kuwa ni Sunnah au ni wajibu, vyovyote vile iwavyo, swala hiyo haikamiliki pasi na kuwajumuisha watu wa nyumba ya Bwana Mtume , ambao ndio wale ambao Mtume  aliotuachia pamoja na Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu. Anasema Mtume :

‫ اللهم‬:‫ تقولون‬:‫ وما الصالة البتراء ؟ قال‬, ‫ال تصلّوا عل ّي الصالة البتراء‬ .‫ اللهم ص ّل على مح ّمد وآل مح ّمد‬:‫ بل قولوا‬,‫ص ّل على مح ّمد وتمسكتون‬ “Msinisalie swala kibutu (iliyokatika)”, Masahaba wakamuuliza: Ni ipi hiyo swala iliyokatika ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Mtume aliwajibu: “Ni kusema, Allahumma swali alaa Muhammad kisha mkanyamaza, lakini semeni: Allahumma swali alaa Muhammad wa alaa Aali Muhammad.”23

Hivi ndivyo anavyotakiwa kila Mwislamu kuitekeleza Sunnah hii, akiwa katika Swala au nje ya Swala. Ikiwa watu wa nyumba ya Mtume ndio wanaoikamilisha Swala ya Mtume , basi ni kitu gani kinachowafanya Waislamu wengi kutowafuata na kutowafanya kuwa ndio marejeo yao baada ya Mtume , au zile Hadithi Sahihi 23

Yanabiihul Mawaddah Juz. 1, uk. 37. 50

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 50

1/17/2017 12:44:42 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

kutoka kwa Mtume  zina shaka yeyote juu ya usahihi wake? Au ni kukubaliana na dhana ya kwamba jamaa wa Mtume  hawana haki ya kuwa viongozi kwa vile Uislamu si dini ya kiukoo? Suala hili la mwisho jawabu lake liko ndani ya hiyo Swala ya Mtume , kwani pia jamaa wa Nabii Ibrahim  pia nao walikuwa Mitume. Pengine jambo lililopo ni choyo na husda iliyojengeka katika nafsi za baadhi ya watu dhidi ya watu wa nyumba ya Mtume  na si jambo jingine lolote. Mwenyezi Mungu anasema:

ّ‫اس َعلَى َما آتَاهُ ُم ه‬ ‫َاب‬ َ ‫للاُ ِمن فَضْ لِ ِه فَقَ ْد آتَ ْينَا آ َل إِ ْب َرا ِهي َم ْال ِكت‬ َ َّ‫أَ ْم يَحْ ُس ُدونَ الن‬ ً ‫َظيما‬ ِ ‫َو ْال ِح ْك َمةَ َوآتَ ْينَاهُم ُّم ْلكا ً ع‬ “Au wanawahusudu watu kwa yale aliyowapa Mwenyezi Mungu kwa fadhila Yake? Basi tuliwapa ukoo wa Ibrahim Kitabu na hikima na tukawapa mamlaka makubwa.” (Qur’ani, 4:54).

Ni Sunnah ya Mwenyezi Mungu kuiteua nyumba fulani, kwa kuipa majukumu ya kuwaongoza wengine, na wala si bidaa (uzushi) kufanya hivyo, Mwenyezi Mungu alimteua Nabii Ibrahim  na kisha kuwateua watoto wake, wajukuu wake, vitukuu, vilembwe n.k. kuwa Mitume. Basi kuteuliwa watu katika kizazi cha Mtume  kwa ajili ya kushika majukumu ya kuwaongoza watu halikuwa jambo geni katika historia ya Uislamu, hasa tukizingatia ya kwamba watu hao wana sifa ya kutoharishwa na Mwenyezi Mungu kabla ya kupewa majukumu, kama anavyosema Mwenyezi Mungu:

ْ ‫ت َويُطَهِّ َر ُك ْم ت‬ ً‫َط ِهيرا‬ َ ْ‫ب عَن ُك ُم ال ِّرج‬ َ ‫إِنَّ َما ي ُِري ُد للاهَّ ُ لِي ُْذ ِه‬ ِ ‫س أَ ْه َل ْالبَ ْي‬ 51

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 51

1/17/2017 12:44:42 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

“Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu, enyi Watu wa Nyumba ya Mtume, na kukusafisheni baraabara.” (Qur’ani, 33:33).

Bibi Aisha anathibitisha ya kwamba Aya hii inawahusu watu wa nyumba ya Mtume  na si wengineo, anasema:

‫“ خرج النبي صلى هللا عليه وسلم غداة و عليه مرط مرحل من شعر أسود‬ ‫فجاء الحسن بن علي فأدخله ثم جاء الحسين فدخل معه ثم جائت فاطمة‬ ‫ “إنما يريد هللا ليذهب عنكم الرجس أهل‬:‫فأدخلها ثم جاء علي فأدخله ثم قال‬ ”.‫البيت و يطهركم تطهيرا‬ “Mtume  alitoka asubuhi naye akiwa na shuka yenye nakshi za matandiko (ya ngamia) imefanywa (shuka hilo) kutokana na manyoya meusi, basi akaja Hasan ibn Ali akamwingiza, kisha akaja Husain akaingia pamoja naye, kisha akaja Fatimah akamuingiza kisha akaja Ali akamuingiza kisha akasema: “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu, enyi Watu wa Nyumba ya Mtume na kukusafisheni baarabara.”

Iwapo Sunnah ya Mwislamu ni kuwafuata watukufu hawa waliotoharishwa na Mola Wao Muumba kutokana na kila aina ya uchafu, basi mafanikio ya dunia na akhera yatapatikana bila ya shaka yeyote. Ni ukweli usiopingika ya kwamba Waislamu walio wengi wanamswalia Mtume  pamoja na jamaa zake ndani ya Swala zao, lakini la kusikitisha ni kwamba jambo hilo halifanywi nje ya Swala au katika maandishi yao, isipokuwa wachache tu ndio wanaofanya hivyo. Historia ya Kiislamu inatuonesha ya kwamba kabla ya Waturuki kushika hatamu za dola na kuanzisha ufalme wa Kiothmania (Otman Empire), vitabu vya Kiislamu vilivyokuwa vimeandikwa vilikuwa vikitaja Saala ya Mtume pamoja na Ahlulbayti wake, kwa 52

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 52

1/17/2017 12:44:42 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

kuandika Swalla Llahu Alayhi Waalihi. Lakini watawala hao kwa vile hawakuridhishwa na hilo waliweza kubadilisha usemi huo na kuweka ibara inayotumiwa na Waislamu wengi hivi sasa, ibara hiyo ni Swalla Llahu Alayhi Wasallam. Ibara hii mpya waliyoiweka watawala hao wa Kituruki wamejaribu kuwapotosha Waislamu kwa makusudi ili wawe mbali na watu wa nyumba ya Mtume . Katika kulithibitisha hili na tuangalie neno Wassalimuu Tasliimaa lililoko katika Aya ya 56 ya sura ya 33, Aya hiyo inasema:

‫صلُّوا َعلَ ْي ِه َو َسلِّ ُموا‬ َ ‫صلُّونَ َعلَى النَّبِ ِّي يَا أَيُّهَا الَّ ِذينَ آ َمنُوا‬ َ ُ‫إِ َّن للاهَّ َ َو َمالئِ َكتَهُ ي‬ ً ‫تَ ْسلِيما‬ Wafasiri wengi wa Qur›ani wameyafasiri maneno Wassalimuu Tasliima kwa maana ya ‘Msalieni (Mtume ) na muombeeni amani'. Lakini pia maneno hayo mawili katika Aya hii yana maana ya Kusalimu amri barabara. Na lau kama Mwenyezi Mungu alikusudia kuwaamrisha Waumini wamsalimie na kumuombea amani, angelitumia neno ‘Wassalimuu Salaamaa’ Katika kuuweka wazi ukweli huu basi na tuangalie maana ya maneno hayo hayo yaliyoko katika Aya ya 65 ya sura ya 4. Mwenyezi Mungu anasema:

ْ ‫ك فِي َما َش َج َر بَ ْينَهُ ْم ثُ َّم الَ يَ ِج ُد‬ ‫وا فِي أَنفُ ِس ِه ْم‬ َ ‫ك الَ ي ُْؤ ِمنُونَ َحتَّ َى يُ َح ِّك ُمو‬ َ ِّ‫فَالَ َو َرب‬ ْ ‫ضيْتَ َويُ َسلِّ ُم‬ ً ‫وا تَ ْسلِيما‬ َ َ‫َح َرجا ً ِّم َّما ق‬ “Naapa kwa mola Wako! Hawataamini mpaka wakufanye wewe ndiye hakimu katika yale wanayohitilafiana baina yao. Kisha wasione dhiki katika nyoyo zao kwa uliyohukumu na wanyenyekee kabisa kabisa.” (4:65) 53

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 53

1/17/2017 12:44:42 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

Maneno hayo mawili katika Aya hii yamefasiriwa kwa maana tofauti na yale yaliyoko katika Aya iliyotangulia, hapa wamefasiri hivi: “…na wanyenyekee kabisa.” Bila shaka suala la kumsalimia na kumuombea amani Bwana Mtume  ni katika mambo yanayoonesha mapenzi makubwa juu yake, na pia ni katika mambo yanayomkurubisha mja kwa Mola Wake, kwa hivyo Masahaba walikuwa na tabia ya kumsalimia Mtume  kwa maamkizi mazuri kwa kumuambia “Assalamu Alayka Ayyuhan Nabiyy Warahmatu Llahi Wabarakaatuh”. Kutokana na umuhimu na ubora wa jambo hili pia limewekwa ndani ya Swala zetu kila tunapokaa kitako cha Attashahud (Tahiyyat). Kila Mwislamu mwenye ghera na mapenzi juu ya Mtume wake, inampasa kufuata na kutekeleza vyema mafunzo yote aliyokuja nayo Mtume wetu  katika kila kipengele cha maisha yake, ikiwa ni kauli au vitendo, kwa kufanya hivyo itakuwa amejihakikishia kujiweka mbali na kila bidaa na uzushi.

54

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 54

1/17/2017 12:44:42 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

DHIKRI NA DUA BAADA YA SALAMU

M

wandishi wa Kitabu cha Fiqhi Sunnah katika mlango huu ametaja riwaya mbalimbali zinazohimiza kuleta dhikri, kusoma dua na kusoma baadhi ya Sura katika Qur’ani mara baada ya kutoa salamu katika swala. Bila ya shaka Waislamu wengi wanaitekeleza Sunnah hii tukufu na mafunzo haya mazuri ya Mtume  ila wengine wanakatishwa moyo kutokana na baadhi ya watu kudai ya kwamba kuomba dua kwa pamoja ni jambo lisilofaa na ni uzushi, hata tumewasikia baadhi yao wakidiriki kusema ya kwamba wale wanaomswalia Mtume  baada ya Swala kuwa wanacheza mchezo wa majani ya mndimu saaga...sagasaga! Mchezo unaochezwa na watoto wadogo. Sijui ni dalili gani waliyonayo hadi jambo hilo linalofanywa na Mwenyezi Mungu pamoja na Malaika W ake, kisha kuwaamrisha Waumini kulifanya, Waumini walioitikia wito huo kuambiwa wanacheza mchezo wa majani ya mndimu! Kwa kweli ni majonzi na masikitiko kutokana na maneno yao hayo dhidi ya Waumini. Ikiwa kumswalia Mtume  baada ya kuswali au kuomba dua kwa sauti haifai na ni bidaa, kwa nini wao wamekuwa ni waombaji wa dua ndefu na kwa sauti kubwa katika Swala ya witri ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani? Au ni kwamba Bee yao tu ndiyo inayojarisha (inalifanya neno la Kiarabu kuwa na Kisra wakati linapotanguliwa na Bee) na Bee ya wengine haijarishi?! Katika mada hii napenda kuwafahamisha Waislamu na wapenda Sunnah za Mtume  ya kwamba kuna Sunnah ambayo Mtume alikuwa akiifanya mara baada ya kutoa salamu, Sunnah ambayo imethibiti juu ya usahihi wake, lakini Waislamu wengi wameghafilika 55

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 55

1/17/2017 12:44:42 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

nayo ila wachache. Sunnah hiyo ni kutoa Takbira mara baada ya kutoa salamu. Ibnu Abbas amesema:

‫كنّا نعرف انتهاء صالة النب ّي صلى هللا عليه وسلَم بالتّكبير‬ “Tulikuwa tukijua kumalizika kwa Swala ya Mtume  kwa Takbiri.”24

Huu ndiyo uliokuwa mwenendo wa Mtume wetu  ambaye alikuwa na tabia ya kumkabiri Mwenyezi kwa kusema: Allahu Akbar mara tu baada ya kutoa salamu. Imamu Nawawiy katika kuisherehesha Hadithi hii ya Ibn Abbas, anasema: Hakika kunyanyua sauti wakati wa kuleta dhikri mara baada ya watu kumaliza Swala za faradhi ni jambo lililokuwepo wakati wa zama za Mtume …Baadhi ya maulamaa wa zamani (masalafia) wamesema: Ni mustahabbu (Sunnah) kunyanyua sauti wakati wa kusoma takbir na dhikri baada ya kumaliza Swala ya faradhi… Sunnah hii ni kama baadhi ya Sunnah nyingine, nayo imetolewa hoja mbalimbali ili isiwe kama vile ilivyokuwa katika zama za Mtume , au kuachwa kabisa, Imamu Nawawiy analizungumzia hilo kwa kusema: “Ibn Battal na maulamaa wengine wamenukuu ya kwamba watu wa madhehebu yanayofuatwa na wengineo wamewafikiana kutokuwa mustahabbu kunyanyua sauti wakati wa Takbiri na dhikri…”25 Masikitiko na majonzi ni kwa wale walioamua kuiacha Sunnah hii kisha wakawazushia uongo wale wanaoitekeleza ya kwamba huwa wananyanyua mikono na kusema: ‘Khaanal Amin, Khaanal Amin,’ kila wanapomaliza kuswali!! Hivi ndivyo Sunnah ya Mtume  na wafuasi wake walivyofiki24 25

Sahih Bukhar Juz.1 Uk. 204. Sahih Muslim Juz.2 Uk. 91.  Annawawiy, Sharhu Sahih Muslim, Juz. 5, uk.83 56

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 56

1/17/2017 12:44:42 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

shwa kwa kusingiziwa mambo mbalimbali yasiyokuwa na mwisho, hata katika zama hizi za utandawazi wa kila kitu ikiwemo elimu, tuhuma hizo bado zinaendelea. Maneno ya Imamu Nawawiy pia ni hoja na dalili dhidi ya wale wanaodai ya kwamba ni bidaa kusoma dua au dhikri kwa sauti baada ya kumaliza kuswali. Ndugu Mwislamu rehani ya nafsi yako ni kufuata kikamilifu mwenendo wa Mtume wako  na kujiepusha na yale yanayokwenda kinyume na mafunzo yake sahihi.

57

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 57

1/17/2017 12:44:42 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

KARAHA YA KUMFUATA IMAMU ­MUOVO NA MZUSHI

S

heikh Sayyid Sabiq hakuona ubaya wowote kwa ibada tukufu ya Swala kuongozwa na mtu mwenye sifa ya ufasiki na uzushi, anasema:

“Imepokewa kutoka kwa Bukhari ya kwamba, Ibn Umar alikuwa akiswali nyuma ya Hajjaj. Na Muslim amepokea ya kwamba Abu Saidil-Khudriy, aliswali Swala ya Idi nyuma ya Mar’wan, na Ibn Masuud aliswali nyuma ya Walid ibn Uqba ibn Abi Muiit –Walid alikuwa akinywa ulevi, na siku moja aliwaswalisha watu Swala ya Asubuhi rakaa nne, Uthman ibn Affan alimpiga Haddi (bakora) kwa kosa hilo la ulevi. Masahaba na Tabiina walikuwa wakiswali nyuma ya Abu Ubaydi, ambaye alikuwa akituhumiwa kwa kuukanusha Uislamu na akiwalingania watu kwenye upotofu. Asili ya haya ni kauli ya wanachuoni isemayo: “Kila ambaye Swala yake ni sahihi kwa mujibu wa nafsi yake, basi pia Swala ya mwenye kuswali nyuma yake pia itakuwa sahihi. Lakini pamoja na hayo wameona ni karaha (jambo lenye kuchukiza) kuswali nyuma ya fasiki (muovu) na mwenye kuzua mambo katika dini, kwa yale aliyoyapokea Abu Daud na Ibn Habban… kutoka kwa Saib ibn Khalaad, ya kwamba siku moja mtu mmoja aliwaswalisha watu, na akatema mate Kiblani, na huku Mtume  akimwangalia mtu huyo, hapo Mtume  akasema: Mtu huyu asiwaswalishe. Baada ya hapo akataka kuwaswalisha, wale watu walimzuia na wakamkumbusha maneno ya Mtume , alipomwambia: Ndiyo hakika wewe umemuudhi Mwenyezi Mungu na Mtume Wake.” Haya ndio aliyotunukulia Sheikh Sayyid Sabiq, na kama kichwa cha habari alichokipa maudhui haya, ni kwamba si kosa mtu kuswali 58

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 58

1/17/2017 12:44:42 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

nyuma ya mlevi, fasiki, au katili yeyote alimradi ametamka shahada mbili! Ni ipi Sunnah ya kufuatwa? Ya Masahaba au ya Mtume  ambaye alimzuia aliekivunjia heshima Kibla kwa kutema mate asiwaswalishe watu?! Ikiwa huyo aliyetema mate alimuudhi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, Je! Mtu katili kama Hajjaj ambaye kwa siku moja alidiriki kuuwa mamia ya Waislamu wasiokuwa na hatia, na kufikia idadi ya watu wanaozidi laki moja aliowauwa katika maisha yake akiwemo Said ibn Jubeir? Hajjaj anatambulika kuwa ni mtu anayesifika kwa uovu na kuwashinda waovu wengine, Hasan Al- Basariy amesema: “Lau kama kila ummah watamleta khabithi (muovu) wao na sisi tukamleta Abu Muhammad (Hajjaj), basi tutawashinda." Huyo ndiye aliyekuwa imamu wa Ibn Umar! Au Walid ibn Utba aliyekuwa jilevi la kupindukia, na kuitwa fasiki na Mwenyezi Mungu, kama ilivyo katika Aya ya 6 ya Sura ya 49, au Marwan aliyeitwa na Mtume  mjusi mtoto wa mjusi na maluuni mtoto wa maluuni (mwenye kulaaniwa)."26 Marwan ni mtu aliyechangia kiasi kikubwa kuuliwa kwa Khalifa wa tatu, na hiyo ikawa ni sababu kubwa ya Waislamu kupigana wenyewe kwa wenyewe na kusababisha maelfu kwa maelfu ya roho kupotea bure. Je haya yote hayamuudhi Mwenyezi Mungu? Naamini haya yanamuudhi kila binadamu mwenye akili timamu kabla ya kumuudhi Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Kuna riwaya moja iliyotengenezwa kwa lengo la kuwahifadhi na kuwalinda wale waliothubutu kukaa nyuma ya watu waovu na kuwaachia waziongoze Swala zao, riwaya hiyo inasema: “Swalluu khalfa kulli barri wa fajir.” Maana yake ni: “Swalini nyuma ya kila mwema na muovu.” Bila ya kujisumbua sana kwa kuangalia usahihi au udhaifu wa riwaya hiyo, kwa wepesi na haraka sana, basi natuyaangalie maneno 26

Kitabul Fitan: uk. 73. 59

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 59

1/17/2017 12:44:42 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

mawili yaliyomo katika riwaya hiyo, maneno hayo ni ‘Barri’ (Mwema) na ‘Fajir ‘ (Muovu), na kisha tuitazame Qur’ani inasemaje juu ya malipo ya wawili hao. Mwenyezi Mungu anasema:

‫ َوإِ َّن ْالفُجَّا َر لَفِي َج ِح ٍيم‬.‫إِ َّن األ ْب َرا َر لَفِي نَ ِع ٍيم‬ “Kwa hakika watu wema watakuwa katika neema. Na kwa hakika waovu watakuwa Motoni.” (Qur’ani, 82: 13-14).

Bila ya shaka yamekubainikia malipo ya wale ambao Sheikh Sayyid Sabiq amesema kuswali nyuma yao inafaa isipokuwa kufanya hivyo ni makuruhu tu!! Ni kipi kilichotufikisha katika hali hii ya kuruhusiwa waovu wa sampuli mbalimbali wasiokuwa na hata chembe ya ubinadamu na wasiomuogopa Mwenyezi Mungu, mfano wa Hajjaj kuongoza ibada ambayo ndiyo ibada tukufu kwa kila Mwislamu. Ibada ambayo kukubaliwa kwake Siku ya Kiyama itakuwa ni sababu ya kukubaliwa amali nyingine, na itakaporejeshwa, na ibada nyingine zitarejeshwa. Vipi aachiwe kuongoza Swala yule ambaye Swala yake haimkatazi maovu?! Mtume  anasema:

”.ً‫“ من لم تنته صالته عن الفحشاء والمنكر لم يزدد من هللا إالّ بعدا‬ “Mtu ambaye Swala yake haimkatazi mabaya na maovu, basi haimzidishii kwa Mwenyezi Mungu isipokuwa umbali. “27

Sunnah na mwenendo sahihi ni ule aliokuwa nao Bwana Mtume  katika maisha yake, kwani alikuwa haondoki Madina isipokuwa akimuacha mtu mwema ili asimamie mambo yote yaliyokuwa yakiwahusu watu wake, ikiwa ni mambo yanayohusu dunia yao na akhera, likiwemo suala la kuongoza Swala za jamaa. 27

Ahyau Ulumi ddin Juz. 1, uk. 150. 60

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 60

1/17/2017 12:44:42 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

Ni Mtume  aliyewakataza Masahaba zake wasikubali kuswalishwa na aliyetema mate Kiblani (Mihrabuni), vipi iwe inafaa kuswali nyuma ya mtu ambaye hajijui wala hajitambui kutokana ulevi uliomo kichwani mwake. Tunaamini fika hata mlevi mwenyewe hakubaliani na hoja ya maulamaa waliyoibuni katika kuhalalisha kuswali nyuma ya watu waovu, hoja hiyo aliyoinakili Sheikh Sayyid Sabiq inasema: “Kila ambaye Swala yake ni sahihi kwa mujibu wa nafsi yake, basi pia Swala ya mwenye kuswali nyuma yake pia itakuwa sahihi.” Ikiwa kuna Masahaba walikubali kuswalishwa na mafasiki, walevi, makatili na waovu wengine, basi kosa hilo libakie kwao na iwe ni Sunnah yao, na wala pasitafutwe sababu ya kujuzishwa, kwa kuonekana kufanya hivyo si dhambi. Mtu mwenye akili timamu hayuko tayari kupakiwa na mlevi katika gari, hata kama ni bure. Sasa iweje ibada hii tukufu wapewe walevi na makatili usukani wa kuiongoza!

61

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 61

1/17/2017 12:44:42 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

KISIMAMO CHA MWEZI WA ­RAMADHANI (TARAWEHE)

S

heikh Sayyid Sabiq anasema ya kwamba:

“Kisimamo cha mwezi wa Ramadhani (Swala ya Tarawehe) ni Sunnah kwa wanaume na wanawake, Sunnah ambayo hutekelezwa baada ya Swala ya Isha na kabla ya Swala ya Witri, na huswaliwa rakaa mbili mbili, na pia inafaa kuiswali baada ya Swala ya Witri, lakini ni kukosa ubora, na wakati wake huendelea hadi usiku.” Baada ya maelezo yake haya amenukuu Hadithi aliyoisimulia Abu Hureira kama alivyosema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa akihimiza juu ya kisimamo cha usiku wa Ramadhani lakini bila kulazimisha, alikuwa akisema: ‘Mwenye kusimamisha kisimamo cha Ramadhani kwa imani na kwa kutarajia malipo, atasamehewa madhambi yake yaliyopita na yajayo.’” Na wapokezi wote wamepokea isipokuwa Attirmidhiy, kutoka kwa Aisha pale aliposema: “Mtume  aliswali msikitini na watu wengi waliswali Swala yake (waliswali nyuma yake), kisha akaswali siku ya pili, pia watu wakazidi, siku ya tatu watu walipokusanyika, Mtume  hakwenda kuwaswalisha, asubuhi yake alisema: Hakika niliona mlivyofanya, na hakuna kilichonizuia kuwajieni isipokuwa nilichelea ikaja ikafaradhishwa…” Hii ndiyo hali halisi ya asili ya Swala ya tarawehe, iliswaliwa siku mbili katika uhai wa Mtume  katika hali ya jamaa, tena jamaa ambayo haikuhimizwa na Mtume , bali ni Waislamu wenyewe waliamua kufanya hivyo, na hatima yake Mtume  alijizuia na ikawa kila mmoja anajiswalia peke yake. 62

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 62

1/17/2017 12:44:42 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

Kuswaliwa Jamaa: Anasema Sheikh Sayyid Sabiq: “Swala ya usiku wa Ramadhani inafaa kuswaliwa kwa jamaa, kama inavyofaa kuswaliwa kila mtu peke yake, lakini Swala ya jamaa katika msikiti ni bora zaidi kwa mujibu wa (kauli ya) jamhuri, na imetangulia habari yenye kumaanisha ya kwamba Mtume  aliwasalisha Waislamu Swala ya usiku wa Ramadhani, na hakudumu kufanya hivyo akikhofia kuja kufaradhishiwa juu yao. Kisha Umar akawakusanya na kuwateulia imamu wa kuwaswalisha. Abdurrahman bin Abdu al-Qaariyy (amesema): Siku moja katika mwezi wa Ramadhani nilitoka pamoja na Umar ibn Khattab kwenda msikitini, tulipofika tuliwakuta watu wametawanyika; kila mmoja akiswali peke yake, na wengine wakimfuata mtu, hapo Umar alisema: mimi naona lau kama watu hawa wangelikusanyika kwa msomaji (imamu) mmoja, basi ingekuwa ni vizuri zaidi, kisha aliazimia kufanya hivyo, na aliwakusanya na kumchagua Ubayy ibn Kaab kuwa imamu wao. Kisha nikatoka naye usiku mwingine, na watu wakawa wanasoma kwa kisomo cha msomaji (imamu) wao, Umar alisema: Niimatul-bid-atu hadhihi. (Maana yake ni: Uzushi ulio mzuri ni huu, na wale wanaolala (na kuja kuswali usiku wa manane), ni bora kuliko wanaoswali hivi sasa, kawaida watu walikuwa wakiswali mwanzoni mwa usiku (mara baada ya Swala ya Isha). Imepokewa na Bukhari, ibn Khuzayma, Bayhaqiy na wengineo. Bila ya shaka Khalifa Umar alikuwa mtambuzi mzuri wa Sunnah za Mtume , kwani amekiita kitendo chake hicho cha kuwakusanya watu katika jamaa ya Swala ya Tarawehe kuwa ni bidaa (uzushi) nzuri, akijua fika kwamba Swala hiyo ya jamaa ilisitishwa wakati wa maisha ya Mtume  na ndio maana yeye Umar hakupata kuiswali, alilolifanya ni kwenda kuwakagua watu kama wanatekeleza agizo lake aliloagiza, alipoona mambo yanakwenda kama alivyoagiza aliondoka hali ya kuwa ameridhika na uzushi huo. 63

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 63

1/17/2017 12:44:42 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

Pia tukirejea riwaya ya Bibi Aisha, inatuonesha wazi ya kwamba Mtume  alikuwa akiiswali mwishoni mwa usiku, khalifa Umar pia alilielewa hilo, ndio akasema: “Yule anayelala na akaja akaswali mwishoni mwa usiku ni bora kuliko yule anayeswali sasa hivi.” Khalifa Umar hakupata kuongoza uzushi huo mzuri katika maisha yake yote, na badala yake alimteua Ubbay bin Kaab kuifanya kazi hiyo. Ndugu msomaji nadhani umeshakubainikia mwenendo na Sunnah sahihi unayopaswa kuifuata. Kuacha kuiswali katika hali ya jamaa utakuwa umefuata Sunnah ya Mtume  na ya Khalifa Umar, kwani pia yeye hajaiswali kwa namna hivi ilivyo leo, licha ya kuwataka wengine wafanye hivyo.

64

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 64

1/17/2017 12:44:42 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

SWALA YA SAFARI

M

wandishi ameanza kuyafungua maudhui haya kwa Aya ya Qur’ani Tukufu isemayo:

ْ ‫صر‬ َّ ‫ُوا ِمنَ ال‬ ‫صالَ ِة إِ ْن ِخ ْفتُ ْم‬ ُ ‫ْس َعلَ ْي ُك ْم ُجنَا ٌح أَن تَ ْق‬ َ ‫ض فَلَي‬ َ ‫َوإِ َذا‬ ِ ْ‫ض َر ْبتُ ْم فِي األَر‬ ْ ُ‫ُوا إِ َّن ْال َكافِ ِرينَ َكان‬ ْ ‫أَن يَ ْفتِنَ ُك ُم الَّ ِذينَ َكفَر‬ ً ‫وا لَ ُك ْم َع ُد ّواً ُّمبِينا‬ “Na mnaposafiri katika nchi si vibaya kwenu kama mkifupisha Swala, iwapo mnachelea wasije wale waliokufuru wakakuleteeni maudhi. Hakika makafiri ni maadui zenu walio wazi wazi.” (Qur’ani, 4:101).

Sheikh Sayyid Sabiq anaendelea kusema ya kwamba: “Suala la kuchelea maudhi ya makafiri si jambo la kutegemewa kuwa ndio sharti la kupunguza Swala, kama ilivyopokewa kutoka kwa Yaali ibn Umayya, amesema: “Nilimwambia Umar ibn Khattab, je umeona upunguzaji wa Swala unaofaywa na watu, na ilhali Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: “Iwapo mnachelea wasije wale waliokufuru wakakuleteeni maudhi.” Bila shaka siku hiyo ya kuwachelea makafiri imeshapita? Umar alisema: Nilishangazwa kama wewe ulivyoshangazwa, basi nilimuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu kuhusiana na jambo hilo, Mtume alinijibu: Ni sadaka ambayo Mwenyezi Mungu aliitoa kwenu basi ikubalini (ipokeeni) sadaka hiyo. Imepokelewa na jamaa.” Na amesimulia Ibn Jariir kutoka kwa Abi Mubiib al-Jarshiy ya kwamba Ibn Umar aliulizwa kuhusiana na Aya, “Na mnaposafiri katika nchi,’ ya kwamba sisi hivi sasa tuko katika usalama na hatuna khofu tena, mbona bado tunapunguza Swala? Alijibu kwa kusema: “Hakika nyinyi mnayo ruwaza (kigezo) njema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu…” 65

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 65

1/17/2017 12:44:42 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

Na kutoka kwa Aisha amesema: Swala zilikuwa zimefaradhishwa rakaa mbili mbili wakati wa Makkah, na pindi Mtume  alipohamia Madina alizidisha rakaa mbili kwa kila zile rakaa mbili isipokuwa Swala ya Magharibi, kwani hiyo ni witri wa mchana, na Swala ya Alfajiri kutokana na urefu wa kisomo chake, basi wakati alipokuwa katika safari alikuwa akiswali kwa Swala ya mwanzo (Swala ya Makkah - rakaa mbili). Imepokewa na Ahmad, Bayhaqiy, Ibn Habban, na Ibn Khuzayma, na wapokezi wake ni wakweli.” Baada ya riwaya hizi, Sheikh Sayyid Sabiq amemnukuu ibn Qayyim, akisema: “Mtume  alikuwa akipunguza Swala zenye rakaa nne na kuziswali rakaa mbilimbili pale alipokuwa ametoka Madina na mpaka aliporejea ndipo aliswali kamili, na haijathibiti ya kwamba yeye Mtume  alitimiza Swala (aliswali rakaa nne wakati akiwa safarini), na wanachuoni hawakukhitalifiana kwa hilo, ila wamekhitalifiana juu ya hukumu ya kisheria ya kupunguza Swala, wako wanaosema ya kwamba ni wajibu. Wenye kauli hii ni Umar, Ali, ibn Abbas, Ibn Umar na Jabir. Hii ndio rai (mwenendo) ya madhebebu ya Kihanafi. Ama watu wa madhehebu ya Kimaliki, wanasema: Kupunguza Swala ni Sunnah iliyotiliwa mkazo, na pia imetiliwa mkazo kuiswali jamaa, iwapo msafiri hakupata msafiri mwenzake wa kumfuata (kumfanya imamu), basi aswali peke yake katika hali ya kupunguza, na ni makuruhu kwa msafiri anayepunguza swala kumfuata mkaazi (asiye punguza swala). Na kwa madhehebu ya kihanbali, kupunguza Swala ni jambo linalofaa na ni bora zaidi kuliko kutimiza. Hukumu ni hiyo hiyo kwa upande wa madhehebu ya Kishafi, pindi msafiri atakapofika masafa maalumu, atakuwa na ruhusa ya kupunguza Swala.” Ndugu Mwislamu, maneno haya yaliyomo katika kitabu cha Sheikh Sayyid Sabiq ‘Fiqhi Sunnah ‘ yanayohusiana na suala zima 66

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 66

1/17/2017 12:44:42 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

la kupunguza Swala zenye rakaa nne kwa msafiri, ikiwa umeyasoma kwa makini na kwa akili iliyo huru, utakuwa umeshaujua wajibu wako wa kufanya pale unapokuwa safarini. Nadhani tayari umeshaijua Sunnah (mwenendo) sahihi ya Mtume  na iliyokuwa ikifuatwa na Masahaba wake. Na hata wale walioufumbia macho mwenendo bora wa Mtume  kwa kudai kupunguza Swala si jambo la lazima, wanakiri wazi wazi ya kwamba kupunguza Swala kwa msafiri ni bora kuliko kuswali kamili. Lakini leo tunalolishuhudia wakati tunapokuwa safarini, ni kuwaona Waislamu wengi wakiikataa katakata sadaka hii kutoka kwa Mola Wao, kama alivyosema Mtume  katika Hadithi yake iliyopita. Utawaona wakiswali rakaa nne badala ya mbili. Lakini pale tunaposikia kuwa kuna mkopo wa Rais au kutoka katika benki fulani utaona namma watu watakavyokimbilia, hata kama mkopo huo una masharti magumu, lakini sadaka ya Mwenyezi Mungu hatuitaki! Kwa kufuata mwenendo wa Mtume wetu katika kila jambo ndio njia pekee ya kupata mafanikio ya dunia na Akhera. Masafa ya kupunguza Swala: Katika jambo lenye utata mkubwa katika madhehebu manne ya kisunni ni suala hili la masafa ya kisheria ambayo kwayo msafiri atalazimika kupunguza Swala, kwani kuna kauli zaidi ya ishirini zinazoelezea kiwango cha masafa. Sheikh Sayyid Sabiq anasema: “Kitu kinachofahamika katika Aya (4:101) ni kila safari kilugha, safari hiyo iwe ni ndefu au fupi, basi Swala itapunguzwa na kukusanywa. Na pia inafaa kutokufunga Swaumu, na haikupokewa hadithi inayobainisha masafa maalumu. Ibn Mandhur na wengineo wamenakili kauli zaidi ya ishirini…” 67

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 67

1/17/2017 12:44:42 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

Baada ya hapo Sheikh Sayyid Sabiq ametaja rai ambazo anaona ni sahihi zaidi, lakini baada ya kuzitaja inawia vigumu kwa mwenye kuzisoma kutokana na jawabu la kukinaisha, kwani kuna rai inayosema ni safari ya maili tatu, na kuna rai inayoshurutisha safari kuwa ndefu yenye vituo viwili na wengine wakasema vituo vitatu… Ufumbuzi wa suala hili si jingine bali ni kurejea pale Bwana Mtume  alipotutaka turejee na kushikamana napo, ili mambo yetu yaweze kunyooka na ibada zetu kuwa sahihi na kutokuwa ni wenye kupotea njia. Hayo tutayafikia iwapo tutashikamana na vizito viwili alivyotuachia Mtume wetu  kama ilivyo katika Hadithi iliyopokelewa na Muslim. Naiusia nafsi yangu na kila Mwislamu msikivu wa maneno ya Mtume wake, arejee katika vitabu vya wafuasi wa Qur'ani na watu wa nyumba ya Mtume  kwa lengo la kulipatia ufumbuzi suala hili, au awaulize wanavyuoni wao, kwani vitabu vyao vina maelezo ya kina katika masuala yanayowahusu Waislamu katika ibada zao na maisha yao ya kila siku. Ni wakati gani msafiri hutimiza Swala? Tumetangulia kusema ya kwamba wengi miongoni mwa wafuasi wa madhebebu manne hawafuati Sunnah ya kupunguza Swala wanapokuwa katika safari kama tunavyowashuhudia. Pamoja na hayo wapo wanaofurutu ada katika kupunguza, kwani wanachozingatia ni mtu kuwa anaishi ugenini hata kama amekusudia kukaa hapo kwa miaka mingi, alimradi ametia nia ya kurudi kwao siku za baadae! Sheikh Sayyid Sabiq anasema: “Msafiri atapunguza Swala, madamu ni msafiri, ikiwa amesafiri kwa shughuli maalum, basi wakati wa kusubiri kukamilika kwake atapunguza Swala kwa vile yeye anazingatiwa kuwa ni msafiri, na 68

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 68

1/17/2017 12:44:42 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

hata kama ni miaka mingi, ikiwa tu alinuia kukaa muda maalumu.” Kisha Sheikh Sayyid Sabiq amenukuu maneno ya Ibn Qayyim yasemayo kwamba: “Ukaazi haumtoi msafiri katika hukumu ya safari, ni sawa mtu kama atakaa muda mrefu au mfupi, ikiwa hapo anapokaa hajafanya makaazi ya kudumu.” Watu wenye mtazamo huu wanatolea dalili ya safari mbalimbali za Mtume  na pia safari za baadhi ya Masababa ambao baadhi yao walipunguza Swala kwa muda wa miaka miwili pale walipokuwa safarini, kama alivyoeleza mwandishi wa kitabu cha Fiqhi Sunnah. Kwa ufafanuzi zaidi unaweza kurejea katika kipengele kisemacho ‘Mataa Yattimu l-Musaafir.’ Maimamu wa madhebebu ya Kisuni nao wakaja na rai zao tofauti, anasema Sheikh Sayyid Sabiq: “Na amesema Malik na Shafi: Ikiwa amenuia kukaa zaidi ya siku nne basi ataswali kamili, na akinuia chini ya hapo basi atapunguza. Na amesema Abu Hanifa r.a: Ikiwa amenuia kukaa siku kumi na tano ataswali kamili na kama ni chini ya hapo, basi atapunguza.” Kwa mara nyingine natoa nasaha zangu kwa Waislamu kurudi kwenye maandiko matukufu yaliyonakiliwa kutoka kwa Mtume wetu Mtukufu , ni yale yale aliotutaka kurudi kwenye Kitabu cha Mwenyezi Mungu pamoja na Watu wa nyumbani kwake (Ahlulbayti a.s.) na si kwa wengineo, hasa katika hali hii ya kila mtu kuingiza rai zake katika Dini, kwa kufuata kanuni isemayo: 'Pinga ili ujulikane.' Tumeona ni namna gani walivyoshindwa kuwa na kauli moja juu ya suala hili, tena ndani ya madhehebu moja kubwa ya Kisuni. Kwa kweli khitilafu hizi zinamweka njia panda yule ambaye tayari ameshakinai juu ya wajibu wa kupunguza Swala wakati anapokuwa safirini, lakini atakuwa na tatizo la kuelewa ni muda gani anapaswa kupunguza Swala. 69

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 69

1/17/2017 12:44:42 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

Basi ni kwa nini Ummah unaacha kauli ya mtu aliye mjuzi zaidi wa Sunnah za Mtume  na badala yake kushika maneno ya wasiofikia hata tone moja la maji ya bahari ukilinganisha na elimu yake. Huyo si mwingine bali ni yule yule Imamu Ali bin Abu Talib . Yeye ndio tegemeo na makimbilio ya kila mwenye kutaka kuujua ukweli katika Dini hii Tukufu ya Kiislamu, hasa wakati watu wanapotofautiana, kwani analolisema au alitendalo ndilo jambo linalowafikiana na hukumu sahihi na mwenendo wa Mtume . Mwenendo wa Khalifa Umar ulikuwa ni kurejea kwa Imamu Ali  katika masuala mazito yanayohusiana na Dini kama tulivyokwishaona huko nyuma. Basi kwa nini Waislamu wamejitenga na Sunnah hiyo ya Khalifa Umar?! Sheikh Sayyid Sabiq anasema: “Na Ali ibn Abi Talib r.a. amesema: Ikiwa msafiri atakaa siku kumi, basi atatimiza Swala.” Maneno haya ya Sayyidna Ali  ndiyo yanayofuatwa na wafuasi wake (Mashia). Maneno hayo yanatupa funzo ya kwamba msafiri ana wajibu wa kupunguza Swala ikiwa amenuia kukaa si zaidi ya siku tisa, kinyume chake ataswali kamili. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na namna ya Swala hii ya safari utayapata katika vitabu vyote vya fikihi vya wafuasi hao wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Watu wa nyumba ya Bwana Mtume . Ndugu msomaji hii ndio Sunnah sahihi ambayo haina shaka ndani yake, na itakuwa ni kosa kubwa kwa Mwislamu kuacha kauli ya Imam Ali  na akaamua kushikamana na maneno ya imamu wa madhehebu yake.

70

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 70

1/17/2017 12:44:42 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

KUCHANGANYA SWALA

K

atika maudhui haya anasema Sheikh Sayyid Sabiq:

“Inafaa kwa mwenye kuswali kuchanganya kati ya Swala ya Adhuhuri na Laasiri, na kati ya Swala ya Magharibi na Swala ya Isha, kwa kutanguliza au kuchelewesha.” Kisha mwandishi alitaja hali ambazo zikimtokea mtu ataruhusika kufanya hivyo, hali zenyewe ni kama zifuatazo: Kuchanganya sehemu ya Arafah na Muzdalifa. Anasema Sheikh Sayyid Sabiq: “Wamekubaliana maulamaa juu ya kuchanganya kati ya Swala ya Adhuhuri na Swala ya Laasiri, mchanganyo wa kutanguliza (Jam-u taqdiim) sehemu ya Arafah, na kati ya Swala ya Magharibi na Swala Isha kwa kuzichelewesha (Jam-u taakhiir) sehemu ya Muzdalifa, kufanya hivyo ni Sunnah ya Mtume wa Mwenyezi Mungu 3 Kuchanganya katika safari: Suala la kuchanganya Swala katika safari ni suala ambalo halina khitilafu kwa Waislamu wa madhehebu yote, na jambo hili tumelidokeza kidogo katika Swala ya safari, ili kulijengea hoja zaidi hapa ninakunukulia riwaya moja kutoka katika kitabu tunachokwenda nacho, ‘Fiqhi Sunnah’ anasema Sheikh Sayyid Sabiq: “Kuchanganya kati ya Swala mbili wakati wa safari kwa kuziswali wakati wa moja kati ya Swala mbili ni jambo linalofaa kwa mujibu wa kauli za wanachuoni walio wengi. Ni sawa kama mtu bado hajaanza kuondoka au akiwepo kwenye mwendo. Kutoka kwa Muadh, ni kwamba Mtume  alipokuwa katika vita vya Tabut, baa71

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 71

1/17/2017 12:44:43 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

da ya kupinduka jua na kabla ya kuanza safari alichanganya kati ya Swala ya Adhuhuri na Laasiri, na ilipokuwa kabla ya kupinduka jua aliichelewesha Swala ya Adhuhuri hadi ilipoingia Swala ya Laasiri. Na Swala ya Magharibi ilikuwa kama hivyo, lilipozama jua kabla ya kuanza safari, alichanganya kati ya Swala ya Magharibi na Swala ya Isha, na alipokuwa akianza safari kabla ya kuzama jua alikuwa akiichelewesha Swala ya Magharibi hadi itakapoingia Swala ya Isha, kisha alikuwa akishuka kutoka katika mnyama wake na kuziswali wakati mmoja.” Imepokelewa na Abu Daud na Attirmidhiy, na akasema hadithi hii ni nzuri.” Katika maudhui haya, riwaya alizozitaja Sheikh Sayyid Sabiq si tu zinaonesha ya kwamba Mtume  alikuwa akichanganya Swala baada ya kuondoka nyumbani kwake, bali alikuwa akichanganya hata kabla ya kuondoka. Sheikh Sayyid Sabiq anasema: “Amesema Dayyid: Kutoka kwa Kureib, kutoka kwa Ibn Abbas, amesema: Je, nikuelezeni Swala ya Mtume  katika safari? Tukamjibu: Ndio, alisema: Alikuwa pindi jua linapopinduka na yeye yuko nyumbani kwake, alikuwa akichanganya kati ya Swala ya Adhuhuri na Laasiri kabla hajaanza kupanda mnyama wake, na pale ambapo jua halijazama na ilhali yuko nyumbani kwake, akisafiri, na ulipofika wakati wa Swala ya Laasiri, akishuka kutoka katika mnyama wake na akichanganya kati ya Swala ya Adhuhuri na Laasiri…" Na ni hivyo hivyo alikuwa akifanya kwa Swala ya Magharibi na Isha. Hadithi hii kaipokea Bayhaqiy kwa sanadi iliyo nzuri.” Jambo hili ni katika Sunnah za Mtume  na Masahaba zake, kama anavyoeleza Sheikh Sayyid Sabiq kwa kusema: “Kuchanganya kati ya Swala mbili kwasababu ya udhuru wa safari ni jambo lililotendwa na kuwa maarufu kati ya Masahaba.” 72

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 72

1/17/2017 12:44:43 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

Faida nyingine inayopatikana kutokana na riwaya tulizizitaja ni kwamba, katika kipengele hiki alichokitaja Sheikh Sayyid Sabiq hakina uhusiano na kipengele kilichozoeleka cha kuchangnya na kupunguza Swala, kama tulivyoona maelezo yake hapo nyuma, kwani Swala ya safari huanza kupunguzwa na kuchanganywa mara baada ya msafiri kukata masafa maalumu ya kisharia. Lakini hapa tumeona riwaya inatuonesha ni jinsi gani ilivyokuwa Sunnah ya Mtume  alivyokuwa akichanganya Swala hata kabla ya kuanza safari yake. Kuchanganya wakati wa mvua: Anasema Sheikh Sayyid Sabiq: “Al-Athram, amepokea katika kitabu chake kutoka kwa Abi Salama ibn Abdirrahman, amesema: Miongoni mwa Sunnah ni kuchanganya Swala kati ya Swala ya Magharibi na Swala ya Isha itakapokuwa ni siku ya mvua. Na Bukhari amepokea ya kwamba Mtume  alichanganya kati ya Swala ya Magharibi na Swala ya Isha katika usiku wa mvua.” Sheikh Sayyid Sabiq anaendelea kwa kuchambua rai za wanafikihi kwa kusema: “Kiufupi, kwa mujibu wa rai za madhebebu katika hili ni kwamba, watu wa madhehebu ya kishafi wanajuzisha kwa mkaazi kuchanganya kati ya Swala ya Magharibi na Swala ya Isha tu, kwa mchanganyo wa kutanguliza, kwa sharti kuwe na mvua mwanzoni mwa takbira ya kwanza ya kufungulia Swala, na kuendelea mpaka katika takbira ya Swala ya pili. Na kwa mujibu wa Malik inafaa kuchanganya kwa kutanguliza kati ya Swala ya Magharibi na Swala ya Isha katika msikiti kwa sababu ya mvua inayonyesha wakati huo wa Swala au mvua inayotarajiwa kutokea, au kwa sababu ya udongo (tope) wenye kuambatana na giza, itakapokuwa udongo huo ni mwingi kiasi ambacho unawazuilia watu kuvaa viatu, ama kuchanganya kati 73

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 73

1/17/2017 12:44:43 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

ya Swala ya Adhuhuri na Swala ya Laasiri kwa sababu ya mvua amekirihisha. Na kwa upande wa madhehebu ya Hanbali, inafaa kuchanganya kati ya Swala ya Magharibi na Swala ya Isha tu kwa kutanguliza au kuchelewesaha kwa sababu ya theluji, tope, baridi kali na mvua inayolowesha nguo, na ruhusa hii inamhusu yule tu anayeswali Swala ya jamaa katika msikiti na ilhali anakaa mbali na msikiti, kiasi ambacho atapatwa na madhara njiani kutokana na mvua. Ama yule ambaye anakaa msikitini au anayeswali Swala ya jamaa nyumbani kwake au anayekwenda msikitini kwa kujisitiri na kitu, au ambaye nyumba yake iko karibu na msikiti, mtu huyo haimpasi kuchanganya.” Kuchanganya kwa sababu ya ugonjwa au udhuru: Sheikh Sayyid Sabiq anasema: “Imam Ahmad, Kadhi Husein, Khatabiy na Mtawala ambaye ni miongoni mwa wafuasi wa kishafi, wanajuzisha kuchanganya kwa kutanguliza au kuchelewesha kwa sababu ya udhuru wa maradhi, kwani mashaka ya ugonjwa ni makubwa zaidi kuliko ya mvua. Annawawiy amesema: Hiyo ni dalili yenye nguvu. Na katika kitabu kinachoitwa ‘Al-mughniy’ kumeandikwa haya: Na maradhi ambayo kwayo inafaa kuchanganya ni yale ambayo yatamsabibishia mashaka na udhia mgonjwa ikiwa ataswali kila Swala katika wakati wake. Wanachuoni wa kihanbali wao wamekwenda mbali zaidi kwa kujuzisha kuchanganya kwa kutanguliza na kuchelewesha kwa wenye udhuru na khofu, pia wamejuzisha kwa mwenye kunyonyesha pindi anapoona mashaka kuosha nguo kila wakati wa Swala, na pia mwenye kuhofia juu ya nafsi yake au mali yake au nyumba yake (watu wake) na mwenye kuhofia madhara ambayo yanaweza yakamsibu kwa sababu ya kuacha kuchanganya Swala. 74

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 74

1/17/2017 12:44:43 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

Ibn Taymiyya naye amesema: “Na madhehebu yaliyokwenda mbali zaidi, ni madhehebu ya Ahmad, kwani yeye amejuzisha kuchanganya Swala kama ikiwa mtu ana shughuli, kama alivyopokea Annasai kuhusiana na hayo katika riwaya isiyo na sanadi ya wapokezi, amesema Mtume  “Inafaa vilevile kuchanganya Swala kwa mpishi, muokaji mikate na mfano wa wawili hao miongoni mwa watu kwa anayehofia kuharibika kwa mali yake.” Kuchanganya kwa haja: Ndugu msomaji, kabla ya kukunakilia yale aliyoyaeleza mwandishi katika kipengele hiki, ni kwamba kwa kweli kichwa cha habari alichokiandika mwandishi, hakiendani na maelezo aliyoyaeleza, hilo utaligundua punde tu baada ya kuyasoma yale aliyoyaandika. Sheikh Sayyid Sabiq anasema: “Annawawiy amesema katika sherehe ya Sahihi Muslim: Kundi miongoni mwa maimamu, limeona ya kwamba inafaa kuchanganya Swala katika hali ya ukazi (kwa asiye msafiri) kwa ajili ya haja, kwa yule anayefanya hivyo (kuchanganya) kuwa ni ada yake, na hiyo ni kauli ya Ibn Sayriin na Ash’hab ambao ni katika wanachuoni wa Kimalik, pia amesema hivyo hivyo al-Khitabiy kutoka kwa al-Qaffal na Ashashiy Kabir katika wafuasi wa Imamu Shafi, na pia kutoka kwa Abu Is’haq al-Maruziy, na vilevile kutoka kwa kundi miongoni mwa wana hadithi, na kauli hii ameichagua Ibn Mundhir. Na kuna kauli ya Ibn Abbas inayotilia nguvu hoja hii pale aliposema: Alitaka asiutie mashakani umma wake. Ibn Abbas hakutoa sababu ya ugonjwa wala kitu chenginecho… Na hadithi ya Ibnu Abbas inayoashiria jambo hilo la kuchanganya Swala ni ile aliyoisimulia Muslim kutoka kwake (ibn Abbas), anasema: Mtume wa Mwenyezi Mungu  alipokuwa Madina alichang75

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 75

1/17/2017 12:44:43 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

anya kati ya Swala ya Adhuhuri na Swala ya Laasir na Maghaaribi na Isha bila ya kuwa na hofu au mvua. Ibn Abbas aliulizwa: Ni kitu gani alitaka Mtume  kutokana na kufanya kwake hivyo? Alijibu: Alitaka asiupatishe mashaka umma wake. Pia Bukhari na Muslim wamepokea kutoka kwa huyo Ibn Abbas: Mtume  alipokuwa Madina aliswali rakaa nane (kwa wakati mmoja) na saba (kwa wakati mmoja): Adhuhuri pamoja na Laasiri, Magharibi pamoja Isha. Na kutoka kwa Muslim, kutoka kwa Abdillahi bin Shaqiiq, amesema: Siku moja Ibn Abbas alitukhutubia baada ya Laasiri mpaka wakati wa kuzama jua, na nyota zikaanza kudhihiri, watu wakaanza kusema: Swala, Swala, Ibn Abbas alisema: Unanifundisha mimi Sunnah? Usiye na mama wee! Kisha akasema: Nilimuona Mtume  akichanganya kati ya Swala ya Adhuhuri na Laasiri, na Magharibi na Isha. Abdallah ibn Shaqiq akasema: Hilo lilinitia shaka moyoni mwangu, basi nilimwendea Abu Hureira na nikamuuliza kuhusiana na jambo hilo, basi Abu Hureira alithibitisha ya kwamba aliyoyasema Ibn Abbas ni ya kweli.” Kipengele hiki cha mwisho kinavunja vikwazo vyote vilivyowekwa na watu mbalimbali dhidi ya suala zima la kuchanganya Swala. Hadithi zilizopokewa kutoka kwa Ibn Abbas ni ushahidi tosha kwa kila mwenye kuitanguliza akili yake mbele, ya kwamba kuchanganya Swala bila ya sababu ni Sunnah ya Mtume  na kufuatwa na Masahaba wake, seuze watu wenye nyudhuru mbalimbali. Kwa bahati mbaya pamoja na kitabu cha Fiqhi Sunnah kusomwa na kusomeshwa sehemu mbalimbali, bado watu hawajawafafanuliwa kwa uwazi Sunnah hii, leo tunawashahudia watu wanaokwenda kwenye maeneo yaliyo mbali na maeneo yao wanapata wasaa wa kuswali Adhuhuri wakati wa mchana, lakini kwa 76

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 76

1/17/2017 12:44:43 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

masikitiko makubwa, Swala ya Laasiri wanakuja kuiswali kadhaa wakati wa usiku! Na masikitiko zaidi ni baadhi ya Waislamu kuwaona wale wanaoshikamana na Sunnah hii, kuwa wako nje ya mafunzo ya Uislamu! Uzito uliopo kwa baadhi ya Waislamu katika kuikubali Sunnah hii unatokana na fikra ya kwamba kufanya hivyo ni kuziswali baadhi ya Swala nje ya wakati. Wenye mawazo haya hutoa dalili ya Aya isemayo:

ْ ‫صالَةَ َكان‬ َّ ‫إِ َّن ال‬ .‫َت َعلَى ْال ُم ْؤ ِمنِينَ ِكتَابا ً َّموْ قُوتا‬ “…Hakika Swala kwa wenye kuamini ni faradhi iliyo na wakati maalumu.” (Qur’ani, 4: 103).

Tunasema jambo hilo ni kweli, lakini inawezekana pamoja na wajibu wa kuziswali katika wakati wake kwa mujibu wa watetezi wa rai hii, kisha Mtume  awe halijui hilo! Na kwa nini msafiri anayechanganya kwa kutanguliza au kuchelewesha haambiwi anaswali nje ya wakati? Sasa hivi tunawasikia baadhi ya watu wakikubaliana na Sunnah hii, lakini bado nyoyoni mwao mna shaka, wanasema: Ni kweli jambo hili limethibiti kutendwa na Mtume  lakini alilifanya mara moja tu katika maisha yake! Nasi tunauliza: Ili jambo lithibiti kuwa Sunnah linahitaji kutendwa mara ngapi na Mtume ? Na ikiwa Mtume alifanya jambo fulani mara moja na bila ya kulikataza, baadaye huwa si Sunnah tena? Suala la mwisho watu waliswali mara ngapi Swala ya tarawehe nyuma ya Mtume ? Tukirudi nyuma kidogo kuhusiana na wakati wa Swala, Qur'ani Tukufu imeliweka wazi jambo hilo, Mwenyezi Mungu anasema:

77

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 77

1/17/2017 12:44:43 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

َّ ‫أَقِ ِم ال‬ َ‫ق اللَّي ِْل َوقُرْ آنَ ْالفَجْ ِر إِ َّن قُرْ آنَ ْالفَجْ ِر َكان‬ ِ ُ‫صالَةَ لِ ُدل‬ ِ ‫س إِلَى َغ َس‬ ِ ‫وك ال َّش ْم‬ ً‫َم ْشهُودا‬ “Simamisha Swala linapopinduka jua mpaka giza la usiku, na Qur’ani ya alfajiri. Hakika (kusoma) Qur’ani ya alfajiri imekuwa ni yenye kushuhudiwa.” (Qur’ani, 17:78).

Ni hizi nyakati tatu za Swala zilizomo katika Qur’ani, ndio ikawa suala la kuchanganya Swala ni jambo la kawaida katika maisha ya Mtume  kama alivyotusimulia Ibn Abbas ambaye anatambulika kwa elimu yake aliyokuwa nayo, na yeye alikuwa mkali pale watu walipotaka kumfundisha yeye Sunnah za Mtume . Kila ninapoupitia mlango huu ‘Kuchanganya Swala,’ huwasikitikia baadhi ya masheikh, kwani siku moja walitutaka tujadiliane kuhusiana na mambo mbalimbali yanayoaminiwa na kutendwa na wafuasi wa Ahlulbayt , na moja kati ya mada walizozichagua wao wenyewe ni suala hili la kuchanganya Swala na ilhali masheikh hao ni walimu wa kitabu cha Fiqhi Sunnah! Basi kutokana na kijitabu hiki hata wale wasioelewa Kiarabu nadhani watakuwa ni wenye kuzifahamu vyema Sunnah sahihi za Mtume wetu .

78

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 78

1/17/2017 12:44:43 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

WANAOSTAHIKI KUPEWA ZAKA

K

wa uwazi kabisa Qur’ani Tukufu imeeleza aina ya watu wanaostahiki kupewa Zaka, kama Mwenyezi Mungu anavyosema:

ُ َ‫ص َدق‬ َّ ‫إِنَّ َما ال‬ ‫ين َو ْال َعا ِملِينَ َعلَ ْيهَا َو ْال ُمؤَلَّفَ ِة قُلُوبُهُ ْم َوفِي‬ ِ ‫ات لِ ْلفُقَ َراء َو ْال َم َسا ِك‬ ّ‫للاِ َو ه‬ ّ‫ضةً ِّمنَ ه‬ ّ‫يل ه‬ ‫للاُ َعلِي ٌم َح ِكي ٌم‬ َ ‫يل فَ ِري‬ ِ ‫الرِّ قَا‬ ِ ِ‫للاِ َواب ِْن ال َّسب‬ ِ ِ‫َار ِمينَ َوفِي َسب‬ ِ ‫ب َو ْالغ‬ “Hakika Sadaka (Zaka) ni kwa (watu hawa) tu; Mafakiri, na masikini, na wanaozitumikia Zaka, na wanaotiwa nguvu nyoyo zao, na katika kuwapa uhuru watumwa, na wenye deni, na katika njia ya Mwenyezi Mungu na msafiri. Ni faradhi kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye hekima.” (Qur’ani, 9:60).

Hivi ndivyo Mola Muumba anavyotaka mali Yake igaiwe kwa watu wenye sifa hizi nane tu, na hakuna haki kwa yeyote kuanzisha Sunnah yake juu ya hukumu hii. Lakini kwa masikitiko makubwa wako baadhi ya Masahaba walioivunja Sunnah hii na baadaye wakatokea watu wakahiyari kuwafuata hao Masahaba na kuifumbia macho Aya hii, na pia kuacha mwenendo na Sunnah sahihi ya Mtume  katika kuitekeleza Aya hii Tukufu. Katika kuwaeleza ‘Muallafat Quluubuhum’ Sheikh Sayyid Sabiq anasema: “Watu wanaotiwa nguvu nyoyo zao ni wale waliokusudiwa kuzoweshwa nyoyo zao na kuzikusanya katika Uislamu na kuzifanya ziwe thabiti, hii ni kwa sababu ya udhaifu wa Uislamu wao, au kwa ajili ya kuzizuia shari zao dhidi ya Waislamu, au kuvutiwa na hayo manufaa na ikawa ni sababu ya kuwatetea Waislamu.” 79

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 79

1/17/2017 12:44:43 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

Baada ya maelezo hayo Sayyid Sabiq anatunukuliwa namna gani Mtume  alivyokuwa akiitekeleza Qur'ani kwa kumpa kila mwenye haki, haki yake bila ya kinyongo wakiwemo watu wanaotiwa nguvu nyoyo zao. Ibn Abbas amesema: “Hakika watu walikuwa wakimwendea Mtume, pindi Mtume  anapowapa (kitu) wakiusifu Uislamu kwa kusema: Dini hii ni nzuri. Na alipojizuia kuwapa walikuwa wakiulaumu na kuutia aibu. Miongoni mwa hao alikuwa Abu Sufiani ibn Harb, Aqraa ibn Habis na Iyaynatu ibn Husni, Mtume  aliwapa kila mmoja kati ya watu hawa ngamia mia moja.” Alichokifanya Sheikh Sayyid Sabiq baada ya kuthibitisha Sunnah hiyo iliyotendwa na Mtume wetu, ni kututajia majina ya wale waliokwenda kinyume nayo, nao ni Abu Hanifa na wafuasi wake, na chimbuko la dalili yao ni Sunnah za baadhi ya Masahaba, anasema Sheikh Sayyid Sabiq: “Mahanafi wamepita na kuona ya kwamba fungu la watu wanaotiwa nguvu nyoyo zao limeanguka (halipo tena) kwa vile Mwenyezi Mungu ameshaitia nguvu Dini yake. “Hakika Iyaynatu ibn Husni, Aqra-a ibn Habis na Abbas ibn Murdaas walikwenda kwa Abu Bakri kutaka wapatiwe sehemu ya Zaka yao, Abu Bakri aliwaandikia hati, baada ya kuandikiwa walikwenda kwa Umar na wakamkabidhi ile hati, Umar baada ya kupewa aliichanachana, kisha akasema: Fungu hili alikuwa Mtume  akikupeni ili kukuzoesheni katika Uislamu na amekutajirisheni kwa hilo, basi ikiwa mmeshathibiti katika Uislamu ni vyema, na kama bado basi kati yetu sisi na nyinyi ni upanga tu, (akasoma Aya ifuatayo): “Na sema ukweli unatoka kwa Mola wako, basi anayependa akubali na anayependa akatae.” (Qur’ani,18: 29). 80

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 80

1/17/2017 12:44:43 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

Wale watu walirejea kwa Abu Bakri  na kumuuliza: Khalifa ni wewe au ni Umar? Kwani wewe ulitupa hati na Umar akaichanachana, Abu Bakri akawajibu: Khalifa ni yeye akipenda.” Ndugu msomaji hivi ndivyo Sunnah sahihi zilivyochezewa na bidaa (uzushi) kupata nafasi katika Dini yetu! La kushukuru ni kwamba hata Sheikh Sayyid Sabiq hakubaliani na Sunnah hii mpya, lakini ameshindwa kusema yule aliyeizua kuwa amekosea, na badala yake amedai kuwa jambo hilo ni katika jitihada zake Umar! Istilahi ya neno ‘kukosea’ imefutwa katika Dini yetu pale inapothibiti kwamba sahaba fulani amefanya kosa, na kimbilio limekuwa ni kwa kila anayekosea miongoni mwa Masahaba hudaiwa kuwa amejitahidi! Mwenyezi Mungu anajua ya kwamba waja Wake wana tabia ya kukosea, kwa hivyo ametufunza dua ya kusoma baada ya kukosea:

‫َاخ ْذنَا إِن نَّ ِسينَا أَوْ أَ ْخطَأْنَا‬ ِ ‫َربَّنَا الَ تُؤ‬ “…Ewe Mola wetu, usitupatilize pale tunaposahau au kukosea… “ (Qur’ani, 2: 286).

Na Mtume  ameeleza wazi katika Hadithi iliyo maarufu ya kwamba:

”.‫“ ك ّل بن آدم خطّاء وخير الخطّائين التّ ّوابون‬ “Kila mwanadamu ni mwenye kukosea na wabora wa wakoseaji ni wale wenye kutubia. “28

Na hata baba yetu Nabii Adam  pamoja na mama Hawa walipoukaribia mti ambao walikatazwa wasiukaribie na hatima yake wakatolewa peponi, hawakukaa na kujifariji au kujipa matumaini ya 28

Mustadrakul Hakim Juz. 4, uk. 244. 81

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 81

1/17/2017 12:44:43 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

kwamba wamejitahidi, kwa hivyo watapewa ujira (malipo) mmoja, bali walilia kilio kikubwa na kumnyenyekea Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kutaka msamaha, huku wakikiri kosa lao kwa kusema:

َ‫َاس ِرين‬ ِ ‫قَاالَ َربَّنَا ظَلَ ْمنَا أَنفُ َسنَا َوإِن لَّ ْم تَ ْغفِرْ لَنَا َوتَرْ َح ْمنَا لَنَ ُكون ََّن ِمنَ ْالخ‬ “Mola wetu Mlezi! tumejidhulumu nafsi zetu, na kama hutatusamehe na kuturehemu, hakika tutakuwa katika wenye kukhasirika.” (Qur’ani; 7:23).

Kama kweli mtu ana mapenzi na hao waliokwenda kinyume na hukumu za Mwenyezi Mungu, basi ni vyema awatakie msamaha kwa Mwenyezi Mungu kutokana na makosa yao, huenda Mwenyezi Mungu akawatakabalia dua zao na kuwasamehe makosa yao, ama kudai ya kwamba wamejitahidi na watapata ujira kutokana na juhudi zao, jambo hili halimsaidii, halisaidii mtu yeyote yule, bali lina madhara makubwa kwa Waislamu na Uislamu. Si aibu wala matusi kusema fulani amekosea pindi tu ikiwa kweli amekosea, bali hiyo ndio haki na uadilifu, kwani kunawafanya wengine wasitumbukie katika makosa kama yake, kama tunavyowaona watu wa madhebebu ya Hanafi walivyojitolea kwa dhati kabisa kushikamama na Sunnah ya Khalifa wa kwanza na wa pili, na kuthubutu kuiacha Sunnah ya Mtume wa Mwenyezi Mungu na Aya ya Qur’ani Tukufu! Khalifa Umar mwenyewe alikuwa hajui suala la kuwepo na uhuru wa mtu kubadilisha hukumu ya Mwenyezi Mungu na kuingiza yake, na yeye alipokuwa akikosea na kukumbushwa alikuwa akikubali makosa na kutubia kwa Mwenyezi Mungu, na wala alikuwa hasemi amejitahidi na atalipwa ujira mmoja. Kisa maarufu wakati wa utawala wake aliwataka watu wasiozeshe mabinti wao kwa mahari makubwa, alisimama mwanamke mmoja na kumwambia: 82

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 82

1/17/2017 12:44:43 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

“Je hujamsikia Mwenyezi Mungu akisema: …na hali mmoja wao mmempa chungu ya mali… 4: 20. Baada ya Umar kukumbushwa Aya hiyo alipanda mimbari na kusema: Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe, watu wote ni wajuzi (wanaelewa) zaidi kuliko Umar…29 Katika kuitetea na kuipigania Sunnah ya Mwenyezi Mungu na mwenendo wa Mtume Wake  tunamuona mwanachuoni mkubwa wa kisunni akiipa mgongo Sunnah ya Khalifa wa pili na kushikamana na Sunnah ya Mtume . Mwanachuoni huyo ni Abdullah ibn Qudama, anasema: “Ashu-ubiy, Malik, Shafi na watu wanaofuata rai zao wanasema: Sehemu ya Zaka ya wale wanaotaka kutiwa nguvu nyoyo zao imekatika baada ya Mtume  na kwa hakika Mwenyezi Mungu ameshautia nguvu Uislamu na hana haja ya kuwatia nguvu watu katika kuukubali Uislamu. Basi kwa hali yoyote ile asipewe mshirikina kwa lengo la kutiwa nguvu moyo wake. Habari hii imepokewa kutoka kwa Umar." Baada ya hukumu hiyo ya kuwazuilia kundi moja haki yao kati ya yanayostahiki kupewa Zaka kama ilivyobainishwa na Mwenyezi Mungu na kutekelezwa na Mtume Wake  na kwa bahati mbaya sana kukatokea watu kwa makusudi wakaamua kuipa mgongo hukumu hiyo, ibn Qudama ana msimamo na uoni unaokwenda sambamba na Qur'ani na Sunnah ya Mtume  yeye anasema: “Sisi tuna Kitabu na mwenendo wa Mtume . Hakika Mwenyezi Mungu amewataja wale wanaotaka kutiwa nguvu nyoyo zao katika kundi linalostahiki kupewa Zaka, na Mtume  amesema: Hakika Mwenyezi Mungu ametoa hukumu katika Zaka na kutaka wapewe watu wa aina nane, na Mtume  alikuwa akiwapa wenye kutiwa nguvu nyoyo zao mara nyingi, kama ilivyo katika habari iliyo mashuhuri, na alikuwa akifanya hivyo mpaka alipofariki. Na wala haifai kuacha Kitabu cha Mwenyezi Mungu na mwenendo wa 29

Fiqhi Sunnah Juz. 2, mlango wa mahari. 83

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 83

1/17/2017 12:44:43 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

Mtume Wake isipokuwa baada ya kufutwa (Naskh). Na kufutwa hukumu hakufanyiki kwa dhana, na pia kufutwa hukumu kunakuwa wakati wa uhai wa Mtume  kwani kufutwa hukumu kunakuwa kwa maandiko matakatifu (Nassi), na wala hakuna maandiko matakatifu baada ya kufariki Mtume  na kumalizika zama za kushuka Wahyi. Kisha Qur'ani haifutwi isipokuwa kwa Qur'ani, na katika Qur’ani na Sunnah hakuna ufutwaji wa hukumu hiyo (kuzuiliwa zaka wenye kutiwa nguvu nyoyo zao), basi ni vipi Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah ya Mtume  vinaachwa kwa sababu tu ya rai za watu na hukumu zao, au kwa sababu ya kauli ya Sahaba au mwengineo.”30 Laiti Masababa na wanachuoni wa Kiislamu wangekuwa na mtazamo kama huu aliokuwa nao Ibn Qudama, bila ya shaka umma usingetoka au kutolewa katika njia ya sawa tuliyowekewa na Mtume wetu  lakini wapi! Rai za watu na bidaa zao zimeuweka umma wa Kiislamu mbali na mafunzo sahihi ya Uislamu. Katika utangulizi wa Sheikh Sayyid Sabiq tumeshuhudia ni kiasi gani umma wa Kiislamu ulivyopindishwa njia kutokana na kufungwa mlango wa ijtihadi, tunaungana naye mkono katika kilio chake hicho, lakini wito wetu kwa wale wanaotaka kuufungua, iwe ni kwa lengo la kuwarudisha watu katika mafunzo sahihi ya Uislamu na Sunnah za Bwana Mtume . Ewe Mola tuongoze katika kukifuata Kitabu Chako na Sunnah za Mtume Wako .

Almughniy Juz. 2, uk. 528.

30

84

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 84

1/17/2017 12:44:43 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

MAMBO YANAYOMFAA MAITI

K

atika mambo yanayoleta mizozo miongoni mwa Waislamu ni suala la mambo wanayoyafanya baadhi ya Waislamu kwa ajili ya kuwazawadia thawabu za mambo mema ndugu zao waliotangulia mbele ya haki. Jambo hili linaonekana na wengine kuwa ni uzushi na bidaa katika Dini. Mategemeo ya wale wanaoona kuwa ni uzushi ni Hadithi ya Mtume  isemayo: "Pindi mwanadamu anapokufa, amali zake hukatika, isipokuwa mambo matatu: Sadaka yenye kuendelea, au elimu yenye manufaa, au mtoto mwema mwenye kumuombea dua (mzazi) wake.” Ufahamu usio sahihi wa maneno haya ya Mtume  ndio uliowapelekea baadhi ya watu kugombana na wenzao, kwa kisingizio kuwa wao si watu wa Sunnah, kwa vile mtu anapokufa hanufaiki na chochote zaidi ya mambo hayo matatu aliyoyataja Mtume . Inshaallah tutaona ni namna gani Mwenyezi Mungu na Mtume Wake  walivyotueleza mambo mengine yenye kuwafaa watu baada ya kufariki dunia tukiachilia hayo matatu. Kabla ya kuendelea katika kipengele hiki, kwanza naturudi nyuma kidogo katika kipengele nambari kumi katika mlango wa ‘Maziko’. Kichwa cha habari cha kipengele hicho ni ‘Istihbaabud Dua-a baadal Faraaghi Minad Dafni.’ Kama Sheikh Sayyid Sabiq alivyokipa jina hilo. Kwenye kipengele hicho Sheikh Sayyid Sabiq anasema: “Ni mustahabbu (jambo zuri) kumuombea msamaha maiti mara tu baada ya kuzikwa, na kumuombea uthabiti, kwani wakati huo huwa anaulizwa masuala. Dalili ya hayo ni kutoka kwa Uthman, amesema: Mtume  alikuwa mara tu baada ya kumzika maiti husimama mbele ya kaburi 85

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 85

1/17/2017 12:44:43 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

lake na kusema: Muombeeni msamaha ndugu yenu, na kumuombea uthabiti, kwani hivi sasa anaulizwa. Imepokewa na Abu Daudi na kusahihishwa na Hakim na al-Bazzaz, na amesema: Na haikupokewa kutoka kwa Mtume  isipokua namna hii. Na imepokewa kutoka kwa Ruzeyn, kutoka kwa Ali, ni kwamba alipokuwa akimaliza kuzika maiti alikuwa akisema: Ewe Mola Wangu, huyu mja Wako ameshuka Kwako na Wewe ni Mbora wa kushukiwa na yeye, basi msamehe na mpanulie maingilio yake.” Sheikh Sayyid Sabiq anaendelea kusema: “Na Ibn Umar ameona kuwa ni mustahabbu kusoma mwanzoni mwa Suratul Baqara na mwishoni mwake, kwenye kaburi mara baada ya kuzika. Imepokewa na Bayhaqii kwa sanadi iliyo nzuri.” Hapa tumeona wazi ya kwamba kuna mambo zaidi ya matatu yanayomfaa maiti, tumeona ni namna gani Waislamu wasiokuwa watoto wa maiti walivyotakiwa kumuombea ndugu yao katika imani. Kama ni yale mambo matatu tu ndiyo yanayomfaa maiti, basi Mtume  asingewaamrisha Masahaba wake kumtakia maghfira. Na wale wenye fikra za kuwaambia wengine ya kwamba ni wazushi kwa kuwasomea maiti Qur'ani, je Ibn Umar watamweka kwenye kundi gani? Tukirudi kule tulikoanzia, baada ya Sheikh Sayyid Sabiq kutaja mambo yaliyoasisiwa na maiti mwenyewe wakati wa uhai wake, kama vile kujenga kisima, msikiti, hospitali na mengineyo miongoni mwa mambo ya kheri, au kuwafunza wengine elimu yenye manufaa kwa jamii, au kumlea mtoto katika malezi ya Kiislamu na baada ya kufa bila ya shaka yeyote mtoto huyo haachi kumuombea dua mzazi wake, au ikiwa mtu ameanzisha mwenendo mzuri wenye kuleta tija na manufaa kwa jamii, mtu huyo atafaidika kuendelea kupata thawabu za amali zake hizo. 86

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 86

1/17/2017 12:44:43 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

Baada ya hapo Sheikh Sayyid Sabiq ameeleza manufaa na thawabu atakazozipata maiti kutokana na vitendo vya wengine, anasema: “Ama yale atakayofaidika nayo kutokana na vitendo vizuri vinavyofanywa na wengine, maelezo yake ni kama ifuatavyo: Dua na Maghfira: Jambo hili ni kutokana na kauli yake Mwenyezi Mungu, pale aliposema:

‫َوالَّ ِذينَ َجا ُؤوا ِمن بَ ْع ِد ِه ْم يَقُولُونَ َربَّنَا ا ْغفِرْ لَنَا َولإِ ِ ْخ َوانِنَا الَّ ِذينَ َسبَقُونَا‬ ٌ ‫ك َر ُؤ‬ ‫َّحي ٌم‬ َ َّ‫ان َولاَ تَجْ َعلْ فِي قُلُوبِنَا ِغلاّ ً لِّلَّ ِذينَ آ َمنُوا َربَّنَا إِن‬ ِ ‫وف ر‬ ِ ‫بِالإْ ِ ي َم‬ “Na waliokuja baada yao wanasema: Mola Wetu! Tusamehe sisi na ndugu zetu waliotutangulia katika imani, na wala usiweke fundo katika nyoyo zetu kwa walioamini, Mola Wetu! Hakika Wewe ni Mpole sana.” (Qur’ani,59 :10).

Sadaka: An-Nawawiy amesema ya kwamba, kuna Ijmai (makubaliano ya wanachuoni) ya kwamba Sadaka pindi inapotolewa kwa niaba ya maiti inakubalika, na kumfikia thawabu zake, ni sawa kama imetolewa na mtoto wa marehemu au mtu mwingine, kutokana na yale yaliyopokewa na Ahmad, Muslim na wengineo, kutoka kwa Abu Hureira: Ni kwamba kuna mtu alisema kumwambia Mtume  ya kwamba baba yangu amefariki na ameacha mali, bila ya kuacha wasia, je nimtolee kafara kwa kutoa Sadaka kwenye hiyo mali aliyoiacha? Mtume  alisema: Ndio. Na kutoka kwa Hassan, kutoka kwa Saad ibn Ubada: Ni kwamba mama yake alifariki, na akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mun87

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 87

1/17/2017 12:44:43 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

gu! Hakika mama yangu amefariki, je nitoe Sadaka kwa ajili yake? Alisema: Ndio. Nikasema: Ni Sadaka gani iliyo bora zaidi? Alisema: Ni kunywesha maji. Funga: Kutokana na yale aliyopokea Bukhari na Muslim, kutoka kwa Ibn Abbas, amesema: Mtu mmoja alikwenda kwa Mtume  na akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Hakika mama yangu amefariki na ana kadhaa (deni) ya funga ya mwezi wa Ramadhani, je! nimlipie? Mtume  alisema: Lau kama mama yako angelikuwa na deni, je ungemlipia? Alisema: Ndio. Mtume  alisema: Deni la Mwenyezi Mungu ni haki zaidi kulipwa. Hijja: Kutokana na yale aliyopokea Bukhari, kutoka kwa Ibn Abbas: Mtu mmoja mwanamke kutoka Juhaynat, alikwenda kwa Mtume  na akasema: Hakika mama yangu aliweka nadhiri ya kwenda kuhiji, lakini hakuhiji mpaka akafariki, je nimhijie? Mtume  alisema mhijie, unaonaje lau kama mama yako angekuwa na deni, je ungemlipia? Walipieni, kwani Mwenyezi Mungu ana haki zaidi ya kulipwa. Swala: Kutokana na yale aliyopokea Dar Qutuniy, ya kwamba mtu alisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Mimi nilikuwa na wazazi wawili ambao nilikuwa nikiwafanyia wema katika uhai wao, basi vipi niwafanyie wema baada ya mauti yao? Mtume  alisema: Hakika miongoni mwa wema baada ya mauti yao ni kuswali kwa niaba yao pamoja na Swala yako na kufunga (Saumu) kwa ajili yao pamoja na funga yako. 88

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 88

1/17/2017 12:44:43 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

Kusoma Qur’ani: Hii ni rai ya Jamhuri ya Ahlus-Sunnah, amesema An-Nawawiy: Lililo mashuhuri kwa madhehebu ya Kishafi ni kwamba Qur’ani haimfikii maiti, Na Ahmad ibn Hanbal na kundi miongoni mwa wafuasi wa Kishafi wamepitisha ya kwamba Qur’ani inamfikia maiti. Kinachotakiwa kwa msomaji wa Qur’ani ni kusema baada ya kumaliza kusoma: Ewe Mola! Thawabu za kile nilichokisoma katika Qur’ani zifikishe kwa fulani. Na katika kitabu ‘Almughniy’ cha Ibn Qudama, Ahmad amenukuliwa akisema: Maiti anafikiwa na kila jambo la kheri, kutokana na nassi (maandiko) iliyopokelewa inayohusiana na jambo hilo, na kwa vile Waislamu wanakusanyika kila pahala na kuwazawadia thawabu maiti wao bila ya kuwa na upingaji, hii ni dalili tosha kuwa kuna Ijmai (makubaliano) katika jambo hili…” Katika kuthibitisha zaidi ukweli wa jambo hili, Sheikh Sayyid Sabiq amenakili maneno ya Ibn Qayyim juu ya kile kilicho bora cha kuzawadiwa maiti, anasema: “Ibn Qayyim amesema: Imesemwa, kitu kilicho na manufaa zaidi katika nafsi yake (nafsi ya maiti) ni kuacha mtumwa huru kwa ajili ya maiti, na Sadaka ni bora zaidi kuliko kumfungia Swaumu, na Sadaka iliyo bora zaidi ni ile yenye kukidhi shida ya mwenye kupewa na ambayo itakuwa ni yenye kudumu na kuendelea, na hili (la Sadaka) ni kutokana na kauli ya Mtume : “Sadaka iliyo bora zaidi ni kunywesha maji.” Ubora wa Sadaka hii ni pale ambapo kuna uhaba wa maji na kukithiri kiu, kinyume chake kunywesha maji kutoka mitoni na michirizi, hakutokuwa bora zaidi kuliko kulisha chakula wakati wa shida, pia (mambo yenye kumfaa maiti) ni kumuombea dua na kumtakia msamaha, ikiwa muombaji atafanya hivyo kwa ikhlasi na unyenyekevu…” 89

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 89

1/17/2017 12:44:43 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

Sheikh Sayyid Sabiq anamalizia kufupisha maneno ya Ibn Qayyim kwa kusema: “Kwa ujumla, Kilicho bora zaidi kuzawadiwa maiti ni kuacha mtumwa huru kwa niaba yake, kumtolea Sadaka, kumtakia msamaha, kumuombea dua, na kumfanyia ibada ya Hijja.� Haya ndiyo yaliyomo katika kitabu cha Sheikh Sayyid Sabiq, kitabu ambacho wasomaji wake wengi ni wale wanaojiita Maanswari Sunnah. La kushangaza ni kwamba kitabu chao kinasema hivi lakini wao wanawahubiria watu kinyume na kitabu chao. Wao wanakataa kujumuika na wenzao katika kuwasomea Qur'ani wale waliofariki, na baya zaidi wanawakataza wengine wasifanye hivyo, wakidai kuwa ni uzushi. Basi kwa nini hawatangazi waziwazi ya kwamba Imam Ahmad bin Hanbali alikuwa katika hao! Naelewa wazi kuwa hilo hawalifanyi kamwe, basi ni kwa nini wanalionea tumba (sega) na kuwaacha nyuki? Badala ya Waislamu kufunzwa namna ya kujishughulisha na maiti wao kama walivyokuwa wakifanya wakati wa uhai wao, kinachofanywa ni kuenezwa kasumba ya kutengana nao mara tu baada ya kuzikwa. Kikubwa familia ya marehemu huuliza kama kuna mtu anayemdai marehemu, huku wakilisahau deni la Mwenyezi Mungu. Hawashughuliki kama alikuwa na wajibu wa ibada fulani ambao hakuweza kuutekeleza au kumzawadia thawabu za matendo mema, ikiwemo kumsomea hitma. Ama Hadithi inayoeleza ya kwamba, mtu akifariki amali yake hukatika isipokuwa mambo matatu, kwa mujibu wa maelezo ya Sayyid Sabiq ni kwamba mtu huyo hatoendelea kupata malipo ya yale aliyokuwa akiyatenda mwenyewe katika uhai wake, isipokuwa mambo matatu. Ama mambo ya kheri ambayo watu watayafanya na kutaka thawabu za amali hizo zimfikie, thawabu hizo zitamfika, au kumuombea msamaha kwa Mwenyezi Mungu, bila ya shaka maombi hayo yatamfikia, kama tulivyoona katika Aya ya Qur'ani tulioitaja 90

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 90

1/17/2017 12:44:43 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

ikielezea umuhimu wa Mwislamu kumtakia msamaha Mwislamu mwenzake hata kama hawahusiani kwa ndewe wala sikio. Pia hapa napenda kuwakumbusha wasomaji ya kwamba kuna msemo unaotumiwa na wataalamu wa elimu ya Usulul Fiqh usemao: 'Kutaja kitu hakuzuii kuingia kitu kingine.' Kwa mfano, mtu akitaja siku ya Jumamosi, Jumapili na Jumatatu, kisha akasema siku hizi ni siku za wiki, hiyo haimaanishi ya kwamba Jumanne, Jumatano na siku nyingine si siku za wiki. Kwa msingi, pale Mtume  alipotaja mambo matatu yanayomfaa maiti, haimaanishi kutokuwepo mambo mengine yenye hukumu kama hayo mambo matatu, na zaidi mpenzi msomaji umejionea mwenyewe hakuna haja ya kutafuta mifano zaidi. Huu ndio mwenendo sahihi uliothibiti katika Qur'ani na Sunnah ya Mtume wetu  namna ya kujishughulisha na wale waliotangulia mbele ya haki, bila ya kuangalia uhusiano wa kidamu thawabu za matendo ya wengine zinawafikia.

91

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 91

1/17/2017 12:44:43 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

NDOA YA MUTA (MUDA)

K

uhusiana na ndoa hii Sheikh Sayyid Sabiq anasema:

“Ndoa hii ya Muta pia inaitwa ndoa ya Muda. Ndoa ya Muda ni mwanamme kufunga akdi (mkataba) ya ndoa pamoja na mwanamke kwa muda wa siku moja au wiki au mwezi. Na imeitwa Muta kwa vile mwanamme ananufaika kwa kustarehe na mwanamke ndani ya ule muda aliyouweka.” Baada ya Sheikh Sayyid Sabiq kueleza maana ya Muta, anaeleza hukumu yake kwa mujibu wa sharia, anasema: “Ni ndoa ambayo maimamu wamewafikiana juu ya uharamu wake. Na wakasema pindi tu inapofungwa basi huwa ni batili, na wametolea dalili zifuatazo: Kwanza: Ndoa hii haifungamani na hukumu zilizomo katika Qur’ani katika masuala ya ndoa yenyewe, talaka, eda na mirathi, kwa hivyo inakuwa batili kama zilivyo ndoa nyingine zilizo batili. Pili: Hadithi za wazi zimekuja kuharamisha: Kutoka kwa Saburat al-Jahniy: Ni kwamba yeye alipigana vita pamoja na Mtume  katika kuikomboa Makka, Mtume  aliwaruhusu kufanya ndoa ya Muda na wanawake, na Mtume hakutoka humu (Makka) mpaka alipoiharamisha. Na katika tamko alilolipokea ibn Majah: “Ni kwamba Mtume  aliharamisha Muta, kwa kusema: Enyi watu, mimi nilikuhalalishieni kustarehe na wanawake kwa muda maalumu, basi tambueni ya kwamba Mwenyezi Mungu ameiharamisha hadi siku ya Kiyama.

92

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 92

1/17/2017 12:44:43 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

Na kutoka kwa Ali : Ni kwamba Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ameharamisha Muta ya wanawake siku ya Khaybar, na pia ameharamisha nyama ya punda wanaofugwa.” Kabla ya kuendelea na nukta nyingine alizozitaja Sayyid, akili yangu imeniamrisha nisimame kidogo na kuzifikiri kwa makini hizi sababu mbili alizozitaja Sheikh Sayyid Sabiq. 1.

Hao maimamu waliposema kuwa ndoa ya Muta ni haramu kwa sababu ya kukosekana vipengele vinavyohusiana na ndoa katika Qur'ani, suala langu ni hili, je, pale Mtume  alipowaruhusu Masahaba kufanya Muta alikuwa halijui jambo hilo? Na je, ni lazima kila sheria iwemo katika Qur'ani? 2. Ndoa hii iliharamishwa Makka na baadaye Khaybar, kama tulivyoelezwa. Inamaanisha ya kwamba Mtume  aliwaruhusu Waislamu kufanya Muta kisha akawakataza, na ilipofika siku ya Khaybar akawaruhusu, sasa hamuoni kuwa huu ni kama mchezo wa kitoto! Sheikh Sayyid Sabiq amemnukuu Imam Sahafi akisema: “Sijui kitu ambacho Mwenyezi Mungu amekihalalisha kisha akakiharamisha, kisha akakihalalisha kisha akakiharamisha, isipokuwa Muta.” Kila mwenye akili ayapime maneno haya na aangalie mwenyewe pakushika. 3. Sheikh Sayyid Sabiq anaendelea na kutaja sababu nyingine ya uharamu wa ndoa hii anasema: “Umar r.a. aliiharamisha wakati alipokuwa katika mimbari zama za ukhalifa wake, na Masahaba  walikubaliana naye, na lau kama alikuwa amekosea basi wasingekubaliana naye.”31

31

Hili peke yake linatosha kubatilisha hadithi za uzushi alizozinukuu Sayyid humu kwamba ndoa hii iliharamishwa na Mtukufu Mtume wakati wa uhai wake! Kama ilikuwa hivyo ndio ukweli, basi hii anayoiharamisha Umar ni ipi tena? Na anaharamisha kwa wahyi gani? 93

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 93

1/17/2017 12:44:43 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

Katika nukta hii ya tatu inaanza kutupa mwanga ya kwamba ndoa hii ya Muta iliyohalalishwa na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake  na kutekelezwa kivitendo na Masahaba wake, ni kwamba baadaye kulijitokeza watu walioiharamisha. Ni wazi kwamba Khalifa wa pili ndiye aliyejitwika jukumu lisilokuwa lake – kuhalalisha na kuharamisha. Ama Masahaba kunyamaza na kutomrudi Khalifa, hiyo si hoja ya kuwa Khalifa Umar alikuwa amepatia katika kuiharamisha Muta. Tusisahau ya kwamba Khalifa Umar alikuwa na sifa ya ukali na kutaka lake tu lisikilizwe na baadhi wakati akimtishia kila anayempinga kukifweka kichwa chake kwa upanga, kwa hivyo waliona bora wanyamaze. Ikiwa Masahaba waliamua kukaa kimya pale Khalifa alipoiharamisha Muta, pia walikaa kimya kama vile wameridhia pale Khalifa alipoharamisha Hajji Tamattui. Ni wazi kwamba siku aliyoiharamisha Muta ni siku hiyo hiyo na wakati huo huo na kikao hicho hicho aliyoiharamisha Hajji Tamattui, alisema:

”.‫“ متعتان كانتا على عهد رسول هللا صلى هللا عليه وسلّم وأنا أحرّمهما‬ “Muta mbili (Muta ya wanawake na Muta ya Hajji) zilikuwepo wakati wa zama za Mtume na mimi naziharamisha na nitamwadhibu mwenye kufanya mambo hayo mawili” 32

Wanachuoni na Maimamu wa fikihi walio wengi wamekubaliana na Khalifa Umar juu ya kuharamisha Muta ya wanawake, lakini hakuna mwanachuoni hata mmoja aliyekubaliana naye ya kwamba Hajji Tamattui ni haramu. Kwa hivyo kunyamaza kwa Masahaba pale Khalifa alipoiharamisha Muta si sababu ya kuridhika na kukubaliana na uwamuzi wake. 32

Tafsirul Kabir, Juz. 2, uk. 528. Sunanul Bayhaqiy Juz.6, uk. 206. 94

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 94

1/17/2017 12:44:43 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

Sayyidna Ali  ambaye waharamishaji wa ndoa hii wanamsingizia ya kwamba amesema eti Mtukufu Mtume  aliiharamisha Muta, tunamuona akituthibitishia hayo aliyoyasema Sayyid Sabiq ya kwamba, khalifa Umar ndiye aliyeiharamisha, anasema:

ّ ‫“ لوال‬ ”.‫أن عمر نهى عن المتعة ما زنى إالّ شق ّي‬ “Lau kama si Umar kuikataza ndoa ya Muta asingelizini isipokuwa mtu muovu.” 33

Naye Jabir ibn Abdillahi anaeleza waziwazi ya kwamba Khalifa Umar ndiye aliyechukua uamuzi wa kuiharamisha, anasema:

‫“ كنا نستمتع بالقبضة من الدقيق والتمر األيام على عهد رسول هللا صلى هللا‬ ‫عليه وآله وسلم وأبي بكر وصدرا من خالفة عمرحتى نهانا عنها عمر في‬ ”.‫شأن حديث عمرو بن حريث‬ “Tulikuwa tukifanya Muta kwa gao la tende na nguo kwa siku nyingi katika zama za Mtume  na zama za Abu Bakri mpaka Umar alipoikataza katika tukio (la kuoa Muta) la Amru bin Hurayth.” 34 4.

Al-Khitabiy:

“Uharamu wa Muta ni kama Ijmai (makubaliano ya wanachuoni wote) isipokuwa baadhi ya Mashia.” Sayyid Sabiq katika kuunga kwake mkono maneno ya Al-Khitabiy, anasema: “Na wala haisihi katika kanuni za Mashia kurejea kwa asiyekuwa Ali katika mambo yenye mzozo na ikhtilafu, kwani imesihi kutoka kwa Ali ya kwamba ndoa ya Muta ilifutwa. Na Bayhaqiy amenukuu 33 34

Tafsiru Tha’labiy, Juz. 3, uk. 286. Almuharrirul Wajiz, Juz. 2, uk.36.   Sahih Muslim Juz. 2, uk. 1023. Naylul-Awtar, Juz. 6, uk. 274. Sharhu Maanil-Athar, Juz. 3, uk. 26. 95

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 95

1/17/2017 12:44:44 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

kutoka kwa Ja’far ibn Muhammad, pale alipoulizwa kuhusu Muta, alijibu hiyo ni zinaa ya wazi.” Kwanza hatuna budi kumpongeza Sheikh Sayyid Sabiq kwa kuwaelezea watu ukweli, kwamba marejeo ya Mashia ni kwa Imamu Ali . Jambo hili la kurudi kwake si la Mashia peke yao, bali hata Makhalifa, mfano wa Umar na Uthman pia nao walikuwa wakirudi wa Imamu Ali . Ama kuhusiana na tuhuma hii ya kwamba Imamu Ali  amesema kwamba ndoa hii ilishafutwa, kwa kweli tumeshalitolea maelezo. Ama hili kuhusiana na kauli hii inayonasibishwa na Imamu Ja’far Sadiq , ambaye ni mmoja kati ya Maimamu kumi na wawili wanaotoka katika nyumba ya Mtume , Imam huyu ndiye yule tuliyemueleza ya kwamba ni mwalimu wa Abu Hanifa. Kwa kweli Imam huyu pia naye amesingiziwa kama alivyosingiziwa babu yake (Imam Ali ), kwani ni muhali kwa mtu kusema Muta ni zina ya wazi, kwani kusema hivyo ni kumaanisha ya kwamba pale Mtume  alipoihalalisha Muta alihalalisha zinaa, na tumeona si mara moja kuihalalisha Muta kwa mujibu wa riwaya na pia maneno ya Imamu Shafi! 5.

“Mwenye kuoa ndoa hii ana lengo la kukidhi shahawa (matamaniyo ya kimwili) na wala hakusudii kupata kizazi, na pia hakusudii kuwahifadhi watoto, kwani haya ndiyo malengo ya msingi ya ndoa, basi inashabihiana na zinaa, kwani zinaa haina lengo lolote zaidi ya kustarehe. Kisha mwanamke huwa ni kama bidhaa inayokwenda huku na kule, na inawadhuru watoto kwani wanakosa nyumba ya kuwahifadhi na kufunzwa malezi na adabu nzuri."

Katika dalili yao hii, watatuambiaje pale Mtume  alipowaruhusu Masahaba wake kuoa Muta. Dalili yao hii ingekuwa na uzito lau kama ikhtilafu ya wanazuoni ni juu ya kutokea na kutendwa au haikutendwa, na tunalolishuhudia ni kwamba mzozo wao ni juu ya 96

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 96

1/17/2017 12:44:44 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

kuendelea uhalali wake au kuharamishwa. Je! Mtume  alipoiamrisha alikuwa hayajui hayo yanayokosekana katika ndoa hii na madhara yanayopatikana? Ile dhana ya Ash-shaukaniy ya kwamba ndoa hii ni haramu, kwa vile ilipata baraka ya jamhuri ya Masababa na wao walilinda uharamu huo na kuufanyia kazi, naneno yake hayo yanapingana na ya Sheikh Sayyid Sabiq pale aliposema: “Na hakika imepokewa kutoka kwa baadhi ya Masahaba na baadhi ya Tabiina ya kwamba ndoa ya Muta ni halali, na aliye mashuhuri katika hilo ni Ibu Abbas . Katika kitabu ‘Tahdhibu Sunan.’ “Ama ibnu Abbas, amepita mapito haya ya kuhalalisha Muta iwe ni wakati wa haja na dharura, na hakuihalalisha moja kwa moja, basi pale maneno ya watu yalipozidi alibadili rai. Na alikuwa akiiharamisha kwa yule asiyekuwa na ulazima wa kufanya hivyo.” Ibnu Jureij na ndoa ya Muta: Sheikh Sayyid Sabiq katika utangulizi wake alituambia ya kwamba watu wa Hijazi (Leo inaitwa Saudi Arabia) walikuwa ni wafuasi zaidi wa Sunnah sahihi ukilinganisha na watu wa Iraq, ambao walikuwa ni watu wa kutumia rai zao katika masuala ya Dini. Ibn Jureij alikuwa ni mwanachuoni mkubwa miongoni mwa wanachuoni wa Makka, yeye ni miongoni mwa watu waliotoa mchango mkubwa wa kuandikwa Hadithi baada ya kupita muda mrefu wa kizuizi hicho cha uandishi, jina lake linadhihirika katika sanadi za wapokezi takriban katika vitabu vyote vya Hadithi, vikiwemo vitabu sita vilivyo sahihi kwa mujibu wa itikadi ya kissuni. Bwana huyo siku za mwisho wa uhai wake aliwaita watoto wake na kuwausia, miongoni mwa usia wake alitaja majina ya wanawake sitini, na kuwaambia watoto wake kuwa hao ni mama zao wa kambo kwa hivyo wasiwaowe. 97

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 97

1/17/2017 12:44:44 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

Dhahabiy katika tarjuma ya mwanachuoni huyo ametaja kama ifuatavyo: “Ibn Jureij ni Imamu na mwenye kuhifadhi, ni mwanachuoni wa Haram (Makka), pia anajulikana kwa Abul Walid na Abu Khalid, Abdul Malik ibn Abdul Aziz ibn Jureij… ni mkazi wa Makka, ni mwanchuoni, ni mtu aliyeandika vitabu vingi na ni mmoja wa wataalamu wa Hadithi.” Katika kuendelea kumzungumzia habari zake, Dhahabiy amemnukuu Imamu Ahmad akisema: “Ibn Jureij alikuwa ni chombo cha elimu, na ni wa kwanza kuandika vitabu.” Ama kuhusiana na ndoa hii ya Muta Dhahabiy anasema: “Amesema Jariir: Ibnu Jureij alikuwa akiona uhalali wa ndoa ya Muta, na alioa wanawake sitini.”35 Imam Shafi naye amenukuliwa akisema: “Ibn Jureij alifanya Muta na wanawake tisini, na wakati wa usiku alikuwa akitumia dawa za kuongeza nguvu za kiume.” 36 Pia Ibn Jureij katika kujipendezesha zaidi kwa akina mama, alikuwa akizitia rangi nyeusi nywele zake na kuvaa mavazi yenye thamani.37 Imamu Shafi ambaye ameonesha msimamo wa wazi wa kuharamishwa Muta, kisha ametueleza namna gani mwanachuoni huyo mkubwa wa Makka (ibn Jureij) alivyojikusanyia mabibi kwa kupitia ndoa ambayo kwa mtazamo wa Imamu Shafi ni haramu, kisha wakati huo huo tunaviona vitabu vyake kikiwemo kitabu chake maarufu ‘Al-ummu’ vikisheheni riwaya za mtu aliyetembea na wanawake wengi zaidi kwa ndoa ya Muta baada ya kuharamishwa, - kama wanavyodai - je! Mzinifu naye pia anakuwa na nafasi ya kukubaliwa riwaya zake na mafunzo yake katika Uislamu? Tukirudi kwa wale walioifananisha ndoa ya Muta na zinaa, bila ya shaka tija yake itakuwa mwanachuoni huyo amezini (na siyo ijti  Tadhkiratul Hufadh, Juz. 1, uk. 170.   Sayru A›alami Nnubalai Juz. 6, 37   Taz. Kitabu kilichotangulia. 35 36

98

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 98

1/17/2017 12:44:44 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

hadi) tena vibaya mno. Sasa watatueleza nini kuhusu kukubaliwa Hadithi ambazo amezipokea yeye, tena Hadithi hizo si kidogo ni kwa mamia kwa maelfu, au mzinifu si kikwazo cha kukubalika Hadithi? Katika maudhui ya ‘Ushahidi wakati wa kutoa talaka’, ambayo Sheikh Sayyid Sabiq ameyaeleza katika kitabu chake cha Fiqhi Sunnah, wakati alipowataja Masahaba na Maulamaa wanaoona ya kwamba talaka haisihi bila ya kuweka mashahidi wawili, miongoni mwao ni Ibn Jureij, na wote kwa pamoja baada ya kuwataja majina yao amewatakia rehema kwa Mwenyezi Mungu. Je! Ikiwa Ibn Jureij ni katika waliotenda zinaa kwa kufanya Muta anastahiki rehema hizo kutoka kwa Sayyid Sabiq? Maudhui haya pia tumeyajadili katika kitabu hiki kama utakavyoona. Mwisho kabisa wa suala hili tunapenda kuwaeleza wasomi wa kitabu hiki kwamba, wale wanaoihalalisha Muta tegemeo lao la kwanza ni Aya Tukufu ya Qur’ani pale Mwenyezi Mungu aliposema:

ً‫ضة‬ َ ‫فَ َما ا ْستَ ْمتَ ْعتُم بِ ِه ِم ْنه َُّن فَآتُوهُ َّن أُجُو َرهُ َّن فَ ِري‬ “ … Ambao mmestarehe nao katika wao (wanawake), basi wapeni mahari yao yaliyo lazimu…” (Qur’ani, 4: 24.).

Wafasiri wa Qur’ani wameeleza bayana kwamba Aya hii imeteremka kwa ajili ya ndoa ya Muta. Baadhi ya tafsiri hizo ni kama zifuatazo: Tafsirut Tabariy, Tafsir ibn Kathir, Tafsirul Qurtubiy, Tafsirul Kash-shaf, Tafsirul Kabir, Tafsirul Maraghi, Tafsirul Khazin, Tafsirul Baghawiy, al-Bahril Muhiit, Fat-hul Qadiir Ahkamul Qur’ani ya Ibnu Arabiy, Mukhtasar Tafsir Ibnu Kathir, Addurul Manthur, Ahkamul Qur’ani ya al-Jassas. Sikutaja juzuu wala namba ya ukurasa wa 99

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 99

1/17/2017 12:44:44 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

hizo tafsiri nilizoziainisha kwa kuchelea kumsumbua yule anayetaka kufanya utafiti juu ya suala hili. La kufanya ni kuangalia Aya hiyo tulioitaja. (4: 24). Wale maulamaa walioharamisha ndoa ya Muta, wote kwa sauti moja wamekubaliana ya kwamba hakuna adhabu yeyote anayostahiki kuadhibiwa yule aliyefanya ndoa hiyo, katika kitabu cha Fiqhi Sunnah, juzuu ya tatu, mlango unaoelezea Haddi (adhabu), kwenye kipengele cha saba, Sayyid Sabiq anasema: “Si wajibu kutoa adhabu katika ndoa ambayo ina ikhtilafu katika kusihi kwake, mfano, ni ndoa ya Muta…” Naamini lau kama wale maimamu wa kifikihi walikuwa na uhakika katika fatwa yao ya kuharamisha ndoa ya Muta, basi vilevile wasingelisita kuwajibisha kuadhibiwa kwa kupigwa bakora mia au kupigwa mawe mwenye kufanya Muta, kwani walifika hadi hata kusema kuwa ni zina iliyo wazi kabisa. Lakini lisikushangaze sana, la kushangaza zaidi ni pale wakati wa zama za Khalifa wa pili, Amru ibn Hureith alipofunga ndoa ya Muta, Khalifa hakumpa adhabu yeyote. Hii ni dalili nyingine ya kwamba Mtume  hakuikataza ndoa hiyo. Bila ya shaka yeyote lau kama ndoa hiyo iliharamishwa kikweli kweli basi Khalifa angemwadhibu mtu huyo, lakini alichokifanya yeye ni kuchukua uamuzi wa kuiharamisha tu.

100

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 100

1/17/2017 12:44:44 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

WANAWAKE WALIO HARAMU ­KUWAOA

K

atika mlango huu Sheikh Sayyid Sabiq ametaja sababu tatu ambazo mojawapo ikipatikana itasababisha kusiwepo hukumu ya kuoana kati ya mume na mke, sababu hizo ni: Nasaba, Ukwe na Kunyonya: Kati ya sababu hizi tatu, tutajadili sababu moja tu, ambayo ni uharamu unaotokana na kunyonya. Kipengele hiki nacho kinavipengele vidogo vidogo, ambavyo hatutovijadili vyote, bali tutatosheka na kipengele kinachozungumzia juu ya ‘Kunyonywesha mtu mzima.’ Kwani tunaona Sunnah sahihi ni ile inayokwenda kinyume na yale aliyoyaandika Sayyid Sabiq kama utakavyoona. Sheikh Sayyid Sabiq anasema katika maudhui haya (Kunyonywesha mtu mzima): “Kwa hivyo, kunyonyeshwa mtu akiwa mtu mzima (akisha baleghe), hakusababishi uharamu wa kuoana kwa mujibu wa rai ya jamhuri ya wanachuoni kutokana na dalili zilizotangulia.” Dalili alizoziorodhesha Sheikh Sayyid Sabiq zinatokana na Aya ya Qur’ani, isemayo: “Wazazi wa kike wawanyonyeshe watoto wao kwa muda wa miaka miwili kamili…” Pia Hadithi za Mtume  zinazotilia mkazo Aya hii, na hakuishia hapo amenukuu maneno ya Maswahaba pamoja na ya wanachuoni, kama vile Imamu Malik. Baada ya kueleza msimamo wa wanachuoni hao ambao wanategemea Aya ya Qur’ani na Hadithi za Mtume , Sayyid Sabiq ametaja rai nyingine yenye kukinzana na hiyo ya mwanzo, anasema: 101

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 101

1/17/2017 12:44:44 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

“Kundi miongoni mwa wanachuoni wa kale linaona ya kwamba kunyonyeshwa kunasababisha uharamu wa kuoana, hata kama mwenye kunyonyeshwa ni mtu aliyezeeka sana, kama ambavyo inaharamisha kwa kunyonyeshwa mtoto mdogo (ambaye hajafikia miaka miwili), na hii ni rai ya Aisha . Sheikh Sayyid Sabiq anaeleza dalili ya wale wenye kushikamana na rai hii. Ni kwamba Shihab aliulizwa juu ya kumnyonyesha mtu mzima, alisema: Ur-watu ibn Zubeir alinisimulia hadithi ifuatayo: “Mtume wa Mwenyezi Mungu alimuamrisha Sahlatu binti Suheyli amnyonyeshe Salim, naye Sahlatu akafanya hivyo, na ikawa anamuona ni mwanawe.” Ur-watu akasema: “Kutokana na hayo, ikawa Aisha, mama wa Waumini  anamchukua mtu miongoni mwa watu wazima na kuwataka waingie kwake, na kumuamrisha dada yake, Ummu Kulthum na mabinti wa kaka yake wawanyonyeshe anaowapenda miongoni mwa wanaume, ili waweze kuingia kwake (bila kizuizi).” Kuna maelezo mengi ambayo Sheikh Sayyid Sabiq kayaeleza juu ya kadhia hii, maelezo ambayo yanamaanisha kwamba Mtume  aliamuru mke wa Abu Hudhayfa amnyonyeshe huria wake, baada ya mke huyo kupeleka malalamiko kwa Mtume  kwamba huria huyo aliyekuwa akijulikana kwa jina la Salim, akiingia ndani mwake, na katika nafsi ya Abu Hudhayfa mlikuwa na kitu. Waungaji mkono wa hukumu hii hawakuzingatia udhaifu wa hoja hii (kunyonyesha mtu mzima), hasa ikizingatiwa kwamba unyonyeshaji unaosababisha uharamu ni ule wa mtoto aliye chini ya miaka miwili, kama Aya ilivyosema. Pili: Uislamu unaharamisha kwa mwanamke kufunua kifua chake na matiti yake kwa mwanaume wa kando aliye balenge. Tatu: Uislamu umeharamisha kugusana kati ya mwanamke na mwanaume wa kando au wasio wanandoa. Nne: 102

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 102

1/17/2017 12:44:44 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

Uislamu si tu kwamba umekataza zinaa, bali umekataza vishawishi na vitangulizi vya maasia hayo machafu. Ingekuwa vyema na uadilifu kwa wanachuoni wote kuikataa Sunnah hii inayodaiwa kuwa ni Sunnah, kwa vile inapingana na mafunzo adhimu ya Uislamu, lakini baadhi yao wameshindwa kufanya hivyo, nadhani sababu yao kubwa, ni kwamba riwaya hii imeelezwa na Muslim katika sahihi yake, na kuikataa riwaya hii ni kukitia dosari kitabu hicho kinachoonekana kwamba kila kilichomo humo ni sahihi! Miongoni mwa waungaji mkono wa riwaya hii ni Sheikh Sayyid Sabiq mwenyewe, anasema: “Na kauli teule kati ya kauli hizi mbili (kauli ya kupinga na kukubali) ni ile iliyohakikiwa na ibn Qayyim, alisema: Hakika hadithi ya Sahlatu si yenye kufutwa, wala makhsusi, wala hukumu yake haimhusu kila mtu, bali ni ruhusa iliyotolewa kwa dharura kwa yule asiyekuwa na njia ya kutojizuia kuingia kwa mwanamke, na inakuwa mashaka kwa mwanamke kuvaa hijabu, kama hali ilivyokuwa kwa Salim pamoja na mke wa Abu Hudhayfa. Kwa hivyo, mwanamke mwenye kumnyonyesha mwanamme huyu mkubwa, maziwa yake yataleta athari (atakuwa maharimu wake), ama kinyume na hivyo, haitokuwa na athari, isipokuwa kwa kumnyonyesha mtoto mdogo, na mapito haya ndiyo mapito ya sheikhul-Islamu, ibn Taymiya, Mwenyezi Mungu amrehemu.� Haya ndio aliyoyanakili Sheikh Sayyid Sabiq kwenye Fiqhi Sunnah yake. Kwa kweli Sunnah hii haiendani na mafunzo ya Dini ya Kiislamu. Na ubaya zaidi ni kujitokeza baadhi ya wanachuoni katika zama hizi kuunga mkono jambo hili na kulitolea fatwa ya kujuzu kwake. Haya ameyafanya Dokta Izzat Atiyya, Mkuu wa Kitengo cha Hadithi, katika Chuo Kikuu cha al-Azhar. Lakini licha ya kuite103

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 103

1/17/2017 12:44:44 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

tea fatwa yake hiyo, ilipata upinzani mkubwa katika Bunge la Misri wakati wa kujadiliwa fatwa yake hii. La kushangaza zaidi, ni kwamba Dokta Izzat Atiyya ameeleza mambo mapya, ambayo hayamo katika asili ya riwaya alizozinakili Sheikh Sayyid Sabiq. Baada ya kubanwa sana, alisema kwamba, unyonyeshaji wa mtu mzima hauharamishi ndoa. Wito wetu: Ni wajibu wa Waislamu kuvitoharisha vitabu vyetu kutokana na riwaya zenye kuishusha hadhi Dini ya Kiislamu, Dini ambayo imeshuhudiwa juu ya umakinifu wake na hata na wasiokuwa Waislamu. Filamu hizi zilizotungwa na kuingizwa katika vitabu vyetu, pindi maadui wanapozicheza, sisi hupandwa na hasira na jazba za hali ya juu. Basi jazba zetu na hasira zetu zianzie dhidi ya vitabu vyetu wenyewe vilivyosheheni hadithi za uongo, na baya zaidi hadithi hizo kuonekana kuwa ni dalili na mashiko ya baadhi ya mambo yenye kwenda kinyume na sharia takatifu za Mwenyezi Mungu.

104

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 104

1/17/2017 12:44:44 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

KUFUNGA NDOA KATIKA HALI YA KUTAKA KUTALIKI

W

ale waliowafikiana juu ya uharamu wa ndoa ya Muta, hapa wanawafikiana juu uhalali wa ndoa ya kughushi, kwa maana mwanamume kufunga ndoa na mwanamke huku mwanamume akiwa na nia ya kumuacha mke wake mara tu baada ya kumaliza haja (shughuli) zake. Zaidi anasema Sheikh Sayyid Sabiq: “Wamewafikiana maulamaa wa fikihi juu ya uhalali wa ndoa kwa yule aliyemuowa mwanamke bila ya kuweka masharti ya muda (kama ilivyo katika ndoa ya Muta) na ilhali mwamamme ameweka nia ya kumtaliki baada ya muda fulani au baada ya kumaliza shughuli zake katika mji ambao yeye amekwenda.� Tukiiangalia ndoa hii na ndoa ya Muta, tunaiona ndoa hii ina madhara makubwa zaidi kuliko yale madhara waliyoyadai kupatikana katika ndoa ya Muta. Matatizo makubwa ya kisaikolojia yanaweza kumpata mwanammke pale ambapo ameshatia tamaa ya kuishi na mume wake huyo ndani ya maisha yao yote, mara anaona ameshakimbiwa na kutelekezwa baada ya muda mfupi tu baada ya ndoa na bila kutokea khitafu yeyote kati ya wadau hao wawili wa ndoa. Madada zetu wa Kizanzibari wao ni miongoni mwa wahanga wakubwa wa ndoa hii, pale baadhi ya watu wanaotoka Arabuni kwenda Visiwani kwa ajili ya kupata upepo mwanana wa bahari ya Hindi, hufunga ndoa na mabinti hao. Mara baada ya mume huyo kumaliza likizo yake, huamua kuondoka peke yake, na kumuahidi mke wake ya kwamba atamletea tiketi ya kwenda Arabuni ili naye akanufaike na neema ya petrol. Wengi wao tunawaona wakisubiri na kusubiri na mwisho wake hukata tamaa, kumbe masikini hawajui 105

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 105

1/17/2017 12:44:44 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

kama hao waume zao tokea mwanzo hawakuwa na nia ya kuidumisha ndoa hiyo. La kushukuru ni kwamba hivi sasa baadhi ya watu wameshaubaini ujanja huo. Ndugu Mwislamu, jijuwe kwamba una wajibu wa kuutafuta ukweli na kuufuata, ili uwe ni mwenye kuridhiwa na Mola Wako, hasa katika wakati huu ambao tunashuhudia mambo mbalimbali yakitokea katika maisha ya Waislamu, ikiwa ni ndani ya misikiti na nje yake. Ewe Mola, tuoneshe haki kuwa ni haki na uturuzuku kuifuata, na tuoneshe batili kuwa ni batili na uturuzuku kuiacha, Amin, Amin ya Rabbal-alamiin.

106

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 106

1/17/2017 12:44:44 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

USHAHIDI WAKATI WA TALAKA

K

atika suala hili nyeti katika maisha ya wanadamu pia nalo lina khitilafu baina ya wanachuoni, lakini pindi msomaji atakapoyasoma maelezo ya Sheikh Sayyid Sabiq atapata suluhisho la ikhitilafu hizo na hatimaye kushikamana na Sunnah sahihi, anasema: “Jamuhuri ya wanachuoni wa fikihi wa zamani na wa sasa wamepita ya kwamba talaka inasihi bila ya kushuhudilisha, kwa vile talaka ni miongoni mwa haki za mume, na wala hahitaji ushahidi wa kutekeleza haki yake, na haikupokewa kutoka kwa Mtume  wala kwa Sahaba dalili inayoashiria wajibu wa kuweka mashahidi. Wanachuoni wa fikihi wa madhehebu ya Shia Imamiya wamekhalifu hukumu hiyo, wanasema: Ushahidi ni sharti katika kusihi kwa talaka. Na wametolea dalili kwa tamko lake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

ِ َّ‫َوأَ ْش ِه ُدوا َذ َويْ َع ْد ٍل ِّمن ُك ْم َوأَقِي ُموا ال َّشهَا َدةَ للِه‬ “…Na mshuhudishe mashahidi wawili waadilifu miongoni mwenu, na simamisheni ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu…” (Qur’ani, 65: 2).”

Baada ya maneno hayo ya Sheikh Sayyid Sabiq anaeleza majina ya wale wanaoshurutisha ushahidi katika talaka, na hapa ndugu msomaji nakuomba uwe makini sana na hayo aliyoyaeleza ili nawe uwe ni miongoni mwa wafuasi wa Sunnah sahihi, anasema: “Na miongoni mwa waliopita kwa kuona kuwa ni wajibu kuweka mashahidi, na kuwa kufanya hivyo ni sharti la kusihi talaka, mionngoni mwa Masahaba ni Amiri wa Waumini Ali ibn Abi Talib, na Imran bin Huswayn r.a. na katika tabiina ni Imam Muhammad 107

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 107

1/17/2017 12:44:44 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

al-Baqir, Imam Ja’far Sadiq na watoto wao hao ambao ni Maimam wa nyumba ya Mtume , na pia Itwaau, Ibn Jureij na Ibn Sayrin Mwenyezi Mungu awarehemu. “ Kabla ya kuendelea na maneno ya Sayyid, hapa pamejitokeza suali ambalo nalielekeza kwa kila aliyetoa fatwa inayojuzisha kutaliki bila ya mashahidi kwa kisingiziyo eti haikupokewa kutoka kwa Mtume  wala kwa Sahaba anayeshurutisha mashahidi, kama alivyoeleza Sheikh Sayyid Sabiq katika maudhui haya. Je Ali ibn Abi Talib  pamoja na Huswayn si miongoni mwa Masahaba?! Hapa napenda kuwakumbusha ikiwa mlihukumu hivyo mlivyohukumu kwa kukosa dalili kutoka kwa Mtume  au Sahaba, basi Masahaba hao wawili wa Mtume  hukumu yao mmeshaiona, ni juu yenu kubatilisha maamuzi yenu ya kwanza na kufuata Sunnah sahihi. Ni masikitiko makubwa kuona kuna kauli mbili zinazopingana katika suala la ushahidi wakati wa kutaliki mke, kauli ya kwanza inatoka kwa Sahaba mtukufu na mjuzi zaidi kuliko Sahaba yeyote (Imamu Ali ), na kauli ya pili ni ya wanachuoni wa elimu ya Fikihi, kisha mtu akasalimu amri juu yao na kuipa mgongo kauli ya Sahaba ambaye tumeona baadhi ya sifa zake katika kitabu chetu hiki. Kwa kweli ni masikitiko na majonzi makubwa, kwani kufanya hivyo ni kujitenga na kujiweka mbali sana na Sunnah sahihi! Tukirudi tena katika kitabu cha Sheikh Sayyid Sabiq tunamuona akitueleza namna gani Imam Ali  alivyotoa hukumu kwa yule aliyemtaliki mke wake bila ya kuweka mashahidi: "Kutoka kwa Ali  alisema kumwambia yule ambaye aliuliza kuhusiana na talaka, Imamu alimuuliza: Je umeshuhudilisha mashahidi wawili waadilifu kama alivyoamrisha Mwenyezi Mungu Mtukufu…? Alijibu: Hapana, Imamu Ali  akamwambia: Nenda kwani talaka yako si talaka sahihi." 108

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 108

1/17/2017 12:44:44 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

Tunamshuhudia Imamu Ali  jinsi alivyoifahamu vyema Aya ya Qur’ani inavyowalazimisha wanaotaka kutoa talaka kuhakikisha kuwa wanatekeleza sharti la kuweka mashihidi wawili walio waadilifu, kinyume chake talaka haitosihi. Pia Sheikh Sayyid Sabiq ametoa dalili za kuthibitisha suala la mashahidi wakati wa talaka kutoka kwa Huswayni na Imamu Ja’far Sadiq, lakini hayo aliyoyaeleza Imam Ali  yanatosha, na hasa kwa vile Sayyidna Ali  ni Imamu anayekubaliwa na Waislamu wa madhehebu mbalimbali, kwa hivyo wale wenye wasiwasi juu ya jambo hilo wajue kwamba dalili yake imethibiti katika Qur'ani, na katika matendo ya Sayyidna Ali . Naamini ya kwamba hivi alivyopita Imamu Ali  katika hukumu hii, ingekuwa ni khalifa mwingine ndiye aliyepita hivi, huku kuweka mashahidi wakati wa talaka ingekuwa leo ndio inayokubalika na kufuatwa na Waislamu wengi, lakini wapi! Sababu tu ni Ali . Ama sababu ya kudai talaka ni haki ya mume, kwa hivyo haina ulazima wa kushuhudilisha wakati wa mtu kutekeleza haki yake. Katika hili tunasema ni kweli hiyo ni haki yake, lakini si kila mtu anapotekeleza haki yake hana haki ya kuwashuhudilisha wengine. Tukichukua mfano wa suala la kukopeshana, ni haki ya mtu kukubali kumkopesha mwingine au laa, sheria haimlazimishi, lakini anachotakiwa ni kuweka mashahidi wakati anapokopesha. Katika Qur'ani tunaiona Aya iliyo ndefu zaidi kuliko nyingine, ikielezea namna ya kuweka mashahidi wakati wa kukopeshana, lakini nayo ni katika Aya zilizopuuzwa na Waislamu wengi, Mwenyezi Mungu anasema:

ْ ُ‫يَا أَيُّهَا الَّ ِذينَ آ َمن‬ ٌ‫وا إِ َذا تَدَايَنتُم بِ َدي ٍْن إِلَى أَ َج ٍل ُّم َس ًّمى فَا ْكتُبُوهُ َو ْليَ ْكتُب بَّ ْينَ ُك ْم َكاتِب‬ ّ‫ب َك َما َعلَّ َمهُ ه‬ ُّ ‫للاُ فَ ْليَ ْكتُبْ َو ْليُ ْملِ ِل الَّ ِذي َعلَ ْي ِه ْال َح‬ ‫ق‬ َ ُ‫ب َكاتِبٌ أَ ْن يَ ْكت‬ َ ْ‫بِ ْال َع ْد ِل َوالَ يَأ‬ 109

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 109

1/17/2017 12:44:44 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

ّ‫ق ه‬ ً ‫ض ِعيفا‬ ُّ ‫للاَ َربَّهُ َوالَ يَ ْبخَسْ ِم ْنهُ َشيْئا ً فَإن َكانَ الَّ ِذي َعلَ ْي ِه ْال َح‬ َ ْ‫ق َسفِيها ً أَو‬ ِ َّ‫َو ْليَت‬ ْ ‫أَوْ الَ يَ ْست َِطي ُع أَن يُ ِم َّل هُ َو فَ ْليُ ْملِلْ َولِيُّهُ بِ ْال َع ْد ِل َوا ْستَ ْش ِه ُد‬ ‫وا َش ِهي َدي ِْن من رِّ َجالِ ُك ْم‬ ‫َض َّل‬ َ ْ‫َان ِم َّمن تَر‬ ِ ‫ضوْ نَ ِمنَ ال ُّشهَدَاء أَن ت‬ ِ ‫فَإِن لَّ ْم يَ ُكونَا َر ُجلَي ِْن فَ َر ُج ٌل َوا ْم َرأَت‬ ْ ‫ب ال ُّشهَدَاء إِ َذا َما ُد ُع‬ ‫وا َوالَ تَسْأ َ ُموْ ْا أَن‬ َ ْ‫ْإحْ دَاهُ َما فَتُ َذ ِّك َر إِحْ دَاهُ َما األُ ْخ َرى َوالَ يَأ‬ ّ‫ص ِغيراً أَو َكبِيراً إِلَى أَ َجلِ ِه َذلِ ُك ْم أَ ْق َسطُ ِعن َد ه‬ ‫للاِ َوأَ ْقو ُم لِل َّشهَا َد ِة َوأَ ْدنَى‬ َ ُ‫تَ ْكتُبُوْ ه‬ ْ ‫أَالَّ تَرْ تَاب‬ َّ‫ْس َعلَ ْي ُك ْم ُجنَا ٌح أَال‬ َ ‫اض َرةً تُ ِديرُونَهَا بَ ْينَ ُك ْم فَلَي‬ ِ ‫ُوا إِالَّ أَن تَ ُكونَ تِ َجا َرةً َح‬ ْ ُ‫ضآ َّر َكاتِبٌ َوالَ َش ِهي ٌد َوإِن تَ ْف َعل‬ ٌ ‫وا فَإِنَّهُ فُسُو‬ ‫ق‬ َ ُ‫تَ ْكتُبُوهَا َوأَ ْش ِه ُدوْ ْا إِ َذا تَبَايَ ْعتُ ْم َوالَ ي‬ ْ ُ‫بِ ُك ْم َواتَّق‬ ّ‫للاُ َو ه‬ ّ‫للاَ َويُ َعلِّ ُم ُك ُم ه‬ ّ‫وا ه‬ .‫للاُ بِ ُك ِّل َش ْي ٍء َعلِي ٌم‬ “Enyi mlioamini! Mnapokopeshana deni kwa muda uliowekwa, basi andikeni. Na mwandishi aandike baina yenu kwa uadilifu, wala mwandishi asikatae kuandika. Aandike kama alivyomfunza Mwenyezi Mungu. Na mwenye deni juu yake aandikishe; naye amche Mwenyezi Mungu, Mola Wake Mlezi. Wala asipunguze chochote ndani yake. Na akiwa mwenye kudaiwa ni mtu aliyepumbaa au mnyonge au hawezi kuandikisha mwenyewe, basi aandikishe mlinzi wake kwa uadilifu. Na mshuhudilishe mashahidi wawili katika wanaume wenu. Ikiwa hapana wanaume wawili, basi mwanamume mmoja na wanawake wawili katika mnaowaridhia kuwa mashahidi. Ili ikiwa mmoja wao akipotea, mmoja wao amkumbushe mwingine. Na mashahidi wasikatae waitwapo. Wala msipuuze kuliandika deni likiwa dogo au kubwa mpaka muda wake. Hayo ndiyo haki zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu, na ndiyo sawa zaidi kwa ushahidi, na vyema zaidi ili msiwe na shaka. Ila ikiwa ni biashara ya mkono-kwamkono baina yenu, basi hapo si vibaya kwenu msipoiandika. Lakini mnapouziana wekeni mashahidi. Wala asitiwe matatani mwandishi wala shahidi. Na mkifanya hivyo basi hakika hilo ni kosa kwenu. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.” (Qur’ani, 2: 282).

Ikiwa masuala ya vijisenti tunatakiwa kufuata utaratibu huu, basi kwa nini linapokuja suala la kutaka kuvunja nyumba na kuiten110

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 110

1/17/2017 12:44:44 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

ganisha familia, ionekane suala la kuweka mashahidi halina ulazima wowote. Mwenyezi Mungu ametutaka kuweka mashahidi wakati wa kutoa talaka ili tusiitingishe Arshi Yake na wala tusimghadhibishe, kwani imekuja katika riwaya ya kwamba: “Halali inayomghadhibisha Mwenyezi Mungu ni talaka. Talaka inaitingisha Arshi ya Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema.” Haya yanaweza kuzuilika pindi mtu atakapowaita mashahidi wawili waadilifu na kuwaelezea alilowaitia kabla ya kutamka talaka, hapo bila ya shaka hao mashahidi watataka kujua lililotokea mpaka pakachukuliwa uwamuzi huo. Baada ya maelezo watatoa nasaha zao ili jambo hilo lisitendeke, na ikiwa hakuna budi wao watakuwa mashahidi wa kuangalia haki, hasa pale ambapo mmoja kati ya wanandoa hao wawili amefariki katika kipindi cha eda au hata baada ya eda. Na pia hao mashahidi watakuwa ni wenye kuwaangalia hao walioachana wasiingie katika mambo ya haramu katika kipindi cha eda, kama mwanamme kuoa mke mwingine iwapo atakuwa na wake wanne, kwani haifai kufanya hivyo mpaka eda imalizike. Na vilevile watakuwa ni wenye kumwangalia mwanamke asiolewe na mume mwingine kabla ya kumaliza eda yake. Kwa kweli kuna hekima kubwa na faida nyingi katika kutekeleza agizo la Mwenyezi Mungu katika suala hili na masuala mengine yote. Sunnah sahihi ni kuifuata Qur’ani Tukufu na mwenendo wa Mtume wake , na si vinginevyo. Mwenyezi Mungu amehalalisha talaka, lakini wakati huo huo ameweka masharti mbalimbali ili jambo hilo lisifanyike kirahisi. Siku moja niliambiwa ya kwamba katika kipindi cha maswali na majibu katika Redio ya Sauti ya Tanzania, Zanzibar, Sheikh aliulizwa ikiwa mtu aliandika talaka na kuiweka katika mfuko wa suruali yake, wakati mke wake alipotaka kufua nguo za mume wake alitia mkono mfukoni mwa suruali na aliona karatasi yenye maandishi, yakimanisha ya kwamba mwanamke 111

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 111

1/17/2017 12:44:44 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

huyo ameshaachwa tokea siku zilizopita. Jawabu la Sheikh lilikuwa ni kwamba talaka hiyo ni sahihi na imeanza kufanya kazi tokea siku iliyoandikwa! Ndugu Waislamu hivi ndivyo namna talaka ilivyorahisishwa baada ya kuwekewa vikwazo mbalimbali na masharti mbalimbali ili lisiwe ni jambo rahisi kutekelezwa kwake. Katika suala hili tunawausia Waislamu wawe makini zaidi, kwani ikiwa mwanamke ambaye ameachwa kwa talaka isiyo sahihi, kisheria bado anakuwa ni mke wa mtu, kama tulivyoona. Sasa fikiria mwanamke huyo ambaye talaka aliyopewa haikuwa sahihi na baada ya kumalizika eda akaolewa na mume mwingine, je huko si kutakuwa ni kupalilia uzinzi katika jamii! Tunawaomba wanachuoni wawe makini katika jambo hili na mambo mengine yanayohusiana na Dini yetu ili Sunnah sahihi iwe na nafasi katika maisha yetu ya kila siku.

112

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 112

1/17/2017 12:44:44 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

IDADI YA TALAKA

K

atika zama zetu hizi tunasikia habari za wanaume kuwaacha wake zao talaka tatu katika kikao kimoja. Sheikh Sayyid Sabiq ni miongoni mwa wale wanaopinga uzushi huu, lakini pamoja na hayo hakuacha kumtetea aliyeuzua, kwa kusema hiyo ilikuwa ni jitihadi zake na sio katika makosa yake, kama kwamba bwana huyo ni maasumu (hakosei), anasema Sheikh Sayyid Sabiq: “Wakati mume atakapokutana kimapenzi na mke wake atakuwa amemiliki talaka tatu juu yake. Maulamaa wameafikiana ya kwamba ni haramu kumuacha mwanamke talaka tatu kwa tamko moja, au kwa matamko matatu kwa wakati tofauti ndani ya tahara moja (kabla ya kumalizika eda). Na wakatoa sababu ya uharamu huo wa talaka tatu kwa pamoja, kuwa ni kufunga mlango wa kurejeana tena baada ya kujuta. Na Mwenyezi Mungu amelipinga hilo, kwani ameweka talaka tatu kuwa mara tatu ili waweze kurudiana baada ya kujuta, na zaidi ya hayo inamdhuru mwanamke kwani atakuwa amepoteza uhalali wake kwa huyo mume wake. Annasai amepokea Hadithi inayotoka kwa Mahmud ibn Labib, amesema: Mtume  aliambiwa habari ya mtu aliyemuacha mke wake talaka tatu kwa pamoja, Mtume  alisimama huku amekasirika, na akasema: ‘Je, Kitabu cha Mwenyezi Mungu kinachezewa na mimi bado niko pamoja na nyinyi?’ Kuna mtu alisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, je nisimuuwe?... Ibn Qayyim amesema katika kitabu ‘Ighathatu llahafaat’ (Katika kusherehesha maneno ya Mtume  pale aliposema: Anakichezea Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Kwa vile ni kukhalifu mfumo wa talaka, na alitaka vile ambavyo Mwenyezi Mungu hakutaka, kwani 113

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 113

1/17/2017 12:44:44 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

Yeye Mwenyezi Mungu alitaka amtaliki talaka ambayo atakuwa na fursa ya kumrejea mwanamke pindi atakapohitaji kufanya hivyo, lakini alimtaliki talaka ambazo hana uwezo tena wa kumrejea. Na vile vile kutaliki talaka tatu kwa pamoja ni kwenda kinyume na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu pale aliposema:

ُ َ‫الطَّال‬ ...‫َان‬ ِ ‫ق َم َّرت‬ “Talaka ni mara mbili…» (Qur’an, 2: 229).

Na ‘mara mbili’ na ‘mara nyingi’ katika lugha ya Qur’ani na Sunnah, bali na katika lugha ya Waarabu na ya watu wengine, inamaana ya mara baada ya mara ya kwanza. Wakati mara mbili na mara nyingi zitakapokusanywa katika mara moja itakuwa ni kuchupa mipaka ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na yale yaliyothibitishwa na Kitabu Chake. Vipi basi mtu anataka hukumu iliyo kinyume na ile aliyoikusudia Mwenyezi Mungu kwa kupitia tamko alilolipanga Mwenyezi Mungu!” Haya ndiyo maneno mazuri aliyotuandalia Sheikh Sayyid Sabiq, maneno ambayo ndiyo mwongozo sahihi wa kuifikia Sunnah ya kweli, na hakuna hukumu nyingine badala ya hii isipokuwa itakuwa ni upotofu, bidaa na uzushi ulio wazi, na zaidi ya hayo ni kukichezea Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu kama Mtume  alivyobainisha. Lakini pamoja na maulamaa kuwafikiana juu uharamu wake tunawashuhudia wakitofautiana juu ya kuthibiti au kutothibiti baada ya mtu kumtamkia mke wake! Kisha wakatofautiana ikiwa itathibiti itakuwa ni tatu au moja? Hivi ndivyo umma huu ulivyofikishwa na watu waliojibebesha majukumu yasiyokuwa yao. Haya yote ndugu msomaji utayakuta katika kitabu cha Fifqi Sunnah.

114

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 114

1/17/2017 12:44:44 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

Khitilafu hizi za maulamaa zimekuja kwa ajili ya kumlinda yule aliyekuja na sera na hukumu mpya ya talaka, kwa maana iwapo mtu atamtaliki mke wake talaka tatu kwa pamoja zitakuwa ni tatu, na huyo mume hatoruhusika kumuowa mwanamke huyo mpaka atakapoachwa na mume atakayemuowa baada ya kuachwa na huyo mume wa mwanzo. Kwa bahati nzuri Sheikh Sayyid Sabiq ametutajia huyo aliyekuja na hukumu hii mpya, kwakusema: “Hakika Abu Swahbaa alimwambia Ibn Abbas: Je! hujui ya kwamba talaka tatu kwa pamoja zilikuwa ni moja katika zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu na Abu Bakri na kipindi kifupi (riwaya nyingine inasema: miaka miwili) katika Ukhalifa wa Umar? Ibn Abbas alisema: Ndio.” Katika kule kuwaita kwao baadhi ya wakoseaji kuwa ni wenye kujitahidi, hata kama wameipindisha Aya iliyo bayana na kuleta hukumu mbadala inayopingana na Qur’ani, Sheikh Sayyid Sabiq ameendelea kulifanya hilo kwa kusema: “Umar  aliona akubaliane na fikra ya kwamba talaka tatu kwa pamoja ni tatu, kwa lengo la kuwaadhibu (watu) kutokana na kukanusha kwao, na jambo hili ni ijtihadi kutoka kwake , lengo lake ni kutaka kutekelezwa hukumu hiyo kutokana na maslahi aliyoyaona yeye. " Baada ya hapo Sheikh Sayyid Sabiq ametoa msimamo wake, na kwa kweli ni msimamo unaotakiwa kufuatwa na kila mpenda Sunnah sahihi katika maisha yake, anasema: “Haifai kuacha yale aliyoyatolea fatwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, na hivi ndivyo walivyokuwa Masahaba wake na katika zama zake na zama za khalifa wake (Abu Bakr). Na pindi ukweli utakapodhihiri kila mmoja naaseme atakalo. Na kwa Mwenyezi Mungu ndiko kwenye tawfiki.” 115

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 115

1/17/2017 12:44:44 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

Hapa sina haja ya kuongeza langu baada ya ukweli huu ulio wazi kutoka kwa Sheikh Sayyid Sabiq, kwani nakhofia nikitia langu nitapunguza ladha ya maneno yake yaliyojaa ukweli. Ila nazidi kusisitiza ya kwamba ni wajibu wetu kufuata Sunnah sahihi na kuachana na uzushi ambao leo ndio ulioenea na kushika hatamu ndani ya Dini yetu Tukufu kwa hoja ya kwamba fulani katika Masahaba amesema hivyo au amefanya hivi, hata kama jambo hilo ni kinyume na Qur'ani au mwenendo wa Mtume . Ndugu Mwislamu unayependa kufuata Sunnah za Mtume wako, napenda nikunukulie maandishi yaliyomo katika kitabu cha somo la Dini, kitabu kinachofundishwa katika shule za sekondari, hapa kwetu, Tanzania: “Ni kinyume kabisa na sheria ya Kiislamu kutoa talaka tatu mfululizo katika kikao kimoja au katika twahara moja kwa matamshi au kwa maandishi. Wanachuoni wengi wamekubaliana kuwa talaka ya namna hiyo itahesabiwa kuwa ni talaka moja. Waislamu wanaofanya hivyo, wajue kuwa huko ni kuzifanyia mzaha Aya za Mwenyezi Mungu na kuvuka mipaka ya Mwenyezi Mungu. “…na anyeiruka mipaka ya Mwenyezi Mungu basi amejidhulumu nafsi yake… (Qur’ani; 65:1). Uislamu umekataza vikali mchezo wa kutoa talaka tatu kwa mpigo kama tunavyojifunza katika hadithi ifuatayo: Mahmud bin Labiid ameeleza kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu alielezwa juu ya mtu aliyetoa talaka tatu mfululizo kwa mkewe. Kisha Mtume alisimama akiwa amechukizwa sana na akasema: “Unacheza na Kitabu cha Mwenyezi Mungu (swt) nikiwa bado tupo pamoja (nikiwa bado sijafa)?” (Mtume alikasirika) kwa kiasi ambacho mtu mmoja alisimama akauliza: Je, siwezi kumuua?”38 Baada ya maelezo haya, ndugu Mwislamu nadhani sasa utakuwa 38

Elimu ya Dini ya Kiislamu, Shule za Sekondari, Kitabu cha 4. uk. 113-114. 116

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 116

1/17/2017 12:44:44 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

tayari kuchukua maamuzi mazito ya kufuata Sunnah sahihi za Mtume wako  hata kama maamuzi yako hayo yatamkasirisha mwasisi na mwanzilishi wa talaka tatu za papo kwa hapo na wafuasi wake, na nina yakini ya kwamba unalielewa jina kamili la mwasisi huyo.

117

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 117

1/17/2017 12:44:44 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

TALAKA YA KISUNNAH

S

heikh Sayyid anaeleza maana ya talaka ya ki-Sunnah kwa kusema:

“Talaka ya ki-Sunnah ni ile ambayo inatekelezwa katika mfumo ambao sharia imeelekeza, nayo ni kumuacha mke aliyeingiliwa talaka moja katika tohara ambayo hakuingiliwa, hayo ni kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

ٌ ‫َان فَإِ ْم َسا‬ ُ َ‫الطَّال‬ ...‫ان‬ ٍ ‫ك بِ َم ْعر‬ ٍ ‫ْري ٌح بِإِحْ َس‬ ِ ‫ق َم َّرت‬ ِ ‫ُوف أَوْ تَس‬ “Talaka ni mara mbili, basi ni kushikamama kwa wema au kuachana kwa ihisani…» (Qur’ani, 2: 229).

Maana yake ni kwamba talaka ya kisharia ni kuacha mara moja na kupata fursa ya kurejea, kisha mara nyingine moja na kukawa na fursa ya kurejea, kisha baada ya hapo huyo aliyeacha ana hiyari ya kukaa naye kwa wema au kumuacha kwa ihisani. Na pia anasema tena Mwenyezi Mungu Mtukufu:

...‫يَا أَيُّهَا النَّبِ ُّي إِ َذا طَلَّ ْقتُ ُم النِّ َساء فَطَلِّقُوهُ َّن لِ ِع َّدتِ ِه َّن‬ “Ewe Nabii! Mnapowaacha wanawake, basi waacheni katika wakati wa eda zao…” (Qur’ani, 65:1).

Anamaanisha ya kwamba, mnapotaka kuwaacha wanawake, basi waacheni katika hali ambayo watakaa eda, na hali hiyo hupatikana iwapo ataachwa baada ya kutoharika na hedhi au nifasi na kabla ya kukutana na mume wake. Na hekima ya hukumu hii ni kwamba iwapo mwanamke ataachwa akiwa katika hedhi eda yake itarefuka, kwani siku za hedhi zilizobakia hazitohesabiwa, basi atakuwa ni 118

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 118

1/17/2017 12:44:44 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

mwenye kudhurika. Na ikiwa ataachwa katika tohara ambayo amekutana na mume wake itakuwa haijulikani kama ana mimba au hana, kwa hivyo atakuwa hajui ya kwamba akae eda ya tohara tatu au eda ya mwenye mimba. Na kutoka kwa Nafii, kutoka kwa Abdallah ibn Umar , ni kwamba yeye alimuacha mke wake akiwa katika hedhi wakati wa zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu , Umar ibn Khattab alimuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu , kuhusiana na jambo hilo, Mtume wa Mwenyezi Mungu  alisema: “Mwamrishe amrudie mke wake, kisha akae naye mpaka atakapotoharika, kisha aingie kwenye hedhi kisha atoharike, kisha baada ya hapo akitaka atakaa naye, na akitaka atamuacha, lakini kabla ya kumwingilia, hiyo ndiyo eda ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu ameamrisha atalikiwe mwanamke.” Maneno ya Sheikh Sayyid yako wazi kama jua, ndugu Mwislamu hiyo ndiyo Sunnah sahihi ya kuifuata iwapo mtu imembidi kutengana na mpenzi wake, vinginevyo ni kuingia katika uharamu na uzushi.

119

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 119

1/17/2017 12:44:44 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

TALAKA YA UZUSHI (BIDAA)

A

nasema Sheikh Sayyid Sabiq:

“Ama talaka ya uzushi ni talaka inayokwenda kinyume na sharia, kama vile mtu kumuacha mke wake talaka tatu kwa tamko moja, au kumuacha talaka tatu mara tatu tofauti katika kikao kimoja, kama kusema: wewe nimekuacha, wewe nimekuacha, wewe nimekuacha, au kumuacha katika hedhi au nifasi au katika tohara ambayo alilala naye. Maulamaa wamekubaliana ya kwamba talaka iliyozushwa ni haramu, na mwenye kuifanya hupata dhambi.” Jambo walilolifanya hao walioafikiana juu ya talaka ya uzushi na kusema mtendaji wake hupata dhambi, ni kule kusema “pamoja na uharamu wa talaka hiyo ya kizushi, inathibiti pindi itolewapo”, sijui wamejisahau ya kwamba Mtume  aliibatilisha talaka ya ibn Umar kwa vile talaka yake ilikuwa ni ya kizushi! Au kuna Sahaha yeyote aliyehalalisha uzushi huo?... Pamoja na hivyo Sheikh Sayyid Sabiq ametunukulia baadhi ya majina ya Masahaba pamoja na maulamaa wanaoona kuwa talaka hiyo ya kizushi ni haramu na haithibiti kwa vile si talaka iliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu, bali ni talaka ambayo Mwenyezi Mungu ameamrisha ipingwe na kukataliwa. Watu hao ni Abdallah ibn Umar, Said ibn Musib, Tausi – ambaye alikuwa ni miongoni mwa wafuasi wa ibn Abbas, Khulas ibn Umar, Abu Qulaabat - ni miongoni mwa tabiina, pia Imam ibn Aqil miongoni mwa wafuasi wa Kihanbal, Maimam wanaotoka katika nyumba ya Mtume  (Ahlulbayt a.s.), watu wa madhehebu ya Adhahiriyya… na ibn Taymiyya. Bila ya shaka yeyote hukumu ya kushika ni hii ambayo Maimamu wanaotoka katika nyumba ya Mtume  wameshikamana nayo, 120

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 120

1/17/2017 12:44:45 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

kwani hakuna yeyote anayefahamu Sunnah za Mtume  zaidi kuliko wao. Hukumu yeyote ambayo tunakiri ni ya kizushi ni wajibu wetu kuikataa na kutoipa nafasi katika Dini yetu Tukufu.

121

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 121

1/17/2017 12:44:45 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

KUTALIKI KABLA YA KUFUNGA NDOA

S

uala la kusihi kumtaliki mwanamke kabla ya kumuoa ni katika mambo ambayo hayazungumzwi katika jamii yetu, lakini ni jambo ambalo lipo katika vitabu mbalimbali vya kifikihi. Tumeamua kulizungumza suala hili kwa ufupi kwa ajili ya kuwatanabahisha ndugu Waislamu ili wasije kuingizwa katika mambo yanayokwenda kinyume na Dini yetu, kwani suala hili huenda huko mbeleni likaletwa katika jamii yetu na kuanza kuleta migongano mingine. Sheikh Sayyid Sabiq anasema ya kwamba: “Haitothibiti talaka kwa kuweka sharti katika kumuoa mwanamke, kama vile kusema: Nitakapomuoa mwanamke fulani, basi atakuwa ameshaachika.” Ametaja dalili ya kutokusihi kwa talaka hiyo kwa kusema: “Hii ni kutokana na yale aliyoyapokea Attirmidhiy, kutoka kwa Amru ibn Shuayb, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake, amesema: Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu : Hakuna nadhiri kwa mwanadamu kwa kitu asichokimiliki, na hakuna kuacha mtumwa huru kwa asiyemmiliki na hakuna talaka kwa asiyemiliki (mke). Attirmidhiy amesema: Hadithi hii ni nzuri, na ni Hadithi nzuri iliyopokewa katika mlango huu, na ndio msimamo wa wanachuoni wengi miongoni mwa Masahaba wa Mtume . Na pia yamepokewa hayo kutoka kwa Ali ibn Abi Talib (karamallahu wajihah), ibn Abbas, Jabir ibn Zayd na wengineo, na pia miongoni mwa wanachuoni wa kifikihi, mwenye mtazamo huu ni Imam Shafi. “

122

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 122

1/17/2017 12:44:45 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

Baada ya Sheikh Sayyid Sabiq kusimamisha dalili za wazi dhidi ya talaka hii, ametufafanulia ya kwamba kuna watu wanaoikubali talaka hii ya kizushi, anasema: “Abu Hanifa amesema: Kuhusiana na talaka hii: Inathibiti pindi tu sharti litakapopatikana (kufungwa ndoa), ni sawa sawa ikiwa atajumuisha kuwaacha wanawake wote, au kumkusudia kumuacha mwanamke maalumu. Malik na wafuasi wake wanasema: Akiwajumuisha wanawake wote haitothibiti, na kama akimkusudia mwanamke maalumu itathibiti, na mfano wa kujumuisha wanawake wote ni kusema: Nikimuoa mwanamke yeyote atakuwa ameshaachika. Na mfano wa kumkusudia mwanamke maalumu ni kusema: Nikimuoa mwanamke fulani (kwa kumtaja jina), basi atakuwa ameshaachika.” Ndugu Mwislamu, hatuna budi kufanya kila liwezekanalo kuuzuia uzushi huu kupata nafasi katika jamii yetu, kwani utatusababishia matatizo makubwa ya kifamilia, na ni wajibu wetu kujipamba na Sunnah za Mtume wetu  kwani huko ndiko kwenye uongofu na mafanikio ya dunia na Akhera.

123

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 123

1/17/2017 12:44:45 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

MASAHABA NA SUNNAH ZA MTUME 

K

atika maudhui mbalimbali tumeshuhudia baadhi ya Masahaba wakiacha Sunnah Sahihi za Mtume  na kuanzisha Sunnah zao, na baadhi ya wakati walikuwa wakizipa mgongo Aya za Qur'ani kwa kuacha kutekeleza hukumu zilizoelezwa na Mwenyezi Mungu kwa kupitia Kitabu chake Kitukufu, au kuleta hukumu mbadala kinyume na ile iliyoelezwa na Mwenyezi Mungu. Pamoja na kuwepo baadhi ya Masahaba waliokuwa na mwenendo huu, kulikuwepo baadhi yao waliokuwa wakishikamana na maandiko ya Qur'ani na kufuata Sunnah za Mtume  kikamilifu, huku wakiachana na yale yaliyozushwa na baadhi yao. Katika kulithibitisha hili na tuangalie mfano huu. Katika mambo yalioingizwa katika Dini ni kuharamishwa Hajji Tamattui, na kabla ya kuingia ndani ya maudhui na tuangalie maana yake. Hajji Tamattui ni mtu kuhirimia Umra katika moja ya miezi ya Hijja (mfunguo mosi, mfunguo pili au mfunguo tatu ), na baada ya hapo ni kusoma Talbiya katika kituo maalumu, na halafu atakwenda Makkah na kufanya tawafu (kuizunguka) Kaaba mara saba, atakwenda baina ya Swafa na Marwa mara saba na mwisho atakata nywele zake, kwa kufanya hivyo atakuwa yuko huru kufanya yale yote yaliyokuwa amezuiliwa kuyafanya kisheria. Hapo atasubiri mpaka siku ya mwezi nane mfunguo nne na atavaa ihramu mara nyingine katika mji wa Makkah kwa ajili ya ibada ya Hijja… Ibada hii iliyothibiti katika Qur'ani Tukufu na kutendwa na Bwana Mtume  pamoja na Masahaba wake iliweza kuharamishwa na Khalifa wa pili pale aliposema: “Muta mbili (Muta ya wanawake na Muta ya Hajji) zilikuwepo wakati wa zama za Mtume na mimi 124

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 124

1/17/2017 12:44:45 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

naziharamisha, na nitatoa adhabu kwa (mwenye kufanya) mambo hayo mawili.”39 Khalifa wa tatu ambaye alijilazimisha kutekeleza Sunnah za Makhalifa wawili waliomtangulia, naye alikuwa mstari wa mbele katika kuwazuia watu wasifanye Hajji Tamattui, lakini siku moja alikumbana na upinzani wa mhuwishaji Sunnah za Bwana Mtume  naye ni Imam Ali  kama anavyosimulia Muslimu katika Sahih yake kutoka kwa Said ibn Musib: “Ali na Uthman  walikusanyika Asfan, Uthman alikuwa akikataza Muta ya Hajji au Umra, Ali alisema: Je, hutaki jambo ambalo Mtume  alilifanya, (naona) unalikataza? Uthman alisema: Hebu achana nasi. Alisema (Imamu Ali Ba.s.): Mimi siwezi nikakuachia. Ali alipoona hivyo (upinzani) alihirimia Umra pamoja na Hajji (Hajju Tamattui).40 Katika Sahihi Bukhari, Imamu Ali baada ya kuhirimia na kusoma Talbiya alimwambia Uthman: “Mimi siwezi kuacha Sunnah ya Mtume  kutokana na maneno ya mtu.”41 Mtoto wa Umar, Abdullah ibn Umar, alikuwa ni miongoni mwa wale walioshikamana na Aya ya Qur’ani na Sunnah ya Mtume  juu ya Hajji Tamattui. Alipokuwa akiwatolea watu Fatwa ya kujuzu kufanya Hajji Tamattui, watu walimjia juu na kumwambia: “Vipi unamkhalifu baba yako kwani yeye alilikataza jambo hili?” Aliwajibu kwa kusema: “Je Sunnah ya Mtume  ni bora zaidi kuifuata au Sunnah ya Umar?!”42 Msimamo wa Imam Ali  na Ibn Umar ndiyo misimamo ya kuigwa na kila Mwislamu wa kweli anayetaka radhi za Mwenyezi Mungu, kwani kuzifumbia macho hukumu zilizothibiti katika  Al-Bayhaqiy, Maarifatus Sunani wal-Athari: Juz.5, uk. 345.   Sahihi Muslim, Juz. 4, uk. 47, Kitabul Hajji, Babu Jawazi Tamattui. 41   Sahihil Bukhari, Juz. 2,uk. 152, Kitabul Hajji, Babu Tamattui. 42   Musnad Imam Ahmad, Juz. 2, uk. 95. Sunan Tirmidhiy, Juz. 2, uk. 160, Hadithi ya 823. 39 40

125

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 125

1/17/2017 12:44:45 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

Qur’ani na Hadithi Sahihi na badala yake kushikamana na watu wengine hakumbashirii mtu kheri, kama anavyosema Mwenyezi Mungu:

ْ ‫ك فِي َما َش َج َر بَ ْينَهُ ْم ثُ َّم الَ يَ ِج ُد‬ ‫وا فِي أَنفُ ِس ِه ْم‬ َ ‫ك الَ ي ُْؤ ِمنُونَ َحتَّ َى يُ َح ِّك ُمو‬ َ ِّ‫فَالَ َو َرب‬ ْ ‫ضيْتَ َويُ َسلِّ ُم‬ ً ‫وا تَ ْسلِيما‬ َ َ‫َح َرجا ً ِّم َّما ق‬ “Naapa kwa Mola wako! Hawatoamini mpaka wakufanye wewe ndiye hakimu (wao) katika yale waliokhitalifiana kati yao, kisha wasione dhiki nyoyoni mwao juu ya hukumu uliyotoa na wanyenyekee kabisa.” (4: 65).

ُ‫ضى للاهَّ ُ َو َرسُولُهُ أَ ْمراً أَن يَ ُكونَ لَهُ ُم ْال ِخيَ َرة‬ َ َ‫َو َما َكانَ لِ ُم ْؤ ِم ٍن َولاَ ُم ْؤ ِمنَ ٍة إِ َذا ق‬ ً ‫ضلاَ الً ُّمبِينا‬ َ ‫ض َّل‬ َ ‫ْص للاهَّ َ َو َرسُولَهُ فَقَ ْد‬ ِ ‫ِم ْن أَ ْم ِر ِه ْم َو َمن يَع‬ “Haiwi kwa Muumini mwanamume wala Muumini mwanamke, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapoamua jambo, kuwa na khiari katika jambo lao. Na yeyote mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi hakika amepotea upotofu ulio wazi.” (Qur’ani, 33: 36).

126

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 126

1/17/2017 12:44:45 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

HITIMISHO

B

aada ya mukhtasari huu nadhani ya kwamba Sunnah sahihi itakuwa imebainika na uzushi utakimbiwa na kutengwa mbali, kwani hauna nafasi yeyote katika Uislamu. Kwa hivyo ile Sunnah iliyoanzishwa katika awamu ya pili na leo ndio iliyoshika nafasi ya Sunnah sahihi ya Mtume , na kuna haja ya Sunnah hiyo kukataliwa na kila Mwislamu, na badala yake ni kuiweka Qur'ani Tukufu mbele ya macho yetu na kukubali ituhukumu katika yale yote tunayokhitalifiana. Iwapo tutakubaliana na hili tutapiga hatua nyingi sana mbele katika kuinusuru Dini yetu tukufu. Miongoni mwa mambo ambayo Mwenyezi Mungu amewakataza Waislamu wote, hata wale walioishi na Bwana Mtume , tunayakuta katika Aya zifuatazo:

‫َي للاهَّ ِ َو َرسُولِ ِه َواتَّقُوا للاهَّ َ إِ َّن للاهَّ َ َس ِمي ٌع َعلِي ٌم‬ ِ ‫يَا أَيُّهَا الَّ ِذينَ آ َمنُوا لاَ تُقَ ِّد ُموا بَ ْينَ يَد‬ “Enyi mlioamini! Msitangulize (kusema lenu) mbele ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na mcheni Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia Mwenye kujua.” (Qur’ani, 49:1).

ْ ‫ب هَـ َذا َحالَ ٌل َوهَـ َذا َح َرا ٌم لِّتَ ْفتَر‬ ْ ُ‫َوالَ تَقُول‬ ّ‫ُوا َعلَى ه‬ ُ ‫َص‬ َ ‫ف أَ ْل ِسنَتُ ُك ُم ْال َك ِذ‬ ِ‫للا‬ ِ ‫وا لِ َما ت‬ ّ‫ب إِ َّن الَّ ِذينَ يَ ْفتَرُونَ َعلَى ه‬ َ‫ب الَ يُ ْفلِحُون‬ َ ‫للاِ ْال َك ِذ‬ َ ‫ْال َك ِذ‬ “Wala msiseme uwongo, kwa kuropokwa na ndimi zenu: Hiki halali, na hiki haramu - mkimzulia uwongo Mwenyezi Mungu. Hakika wanaomzulia uwongo Mwenyezi Mungu hawatafanikiwa.” (Qur’ani, 16:116).

127

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 127

1/17/2017 12:44:45 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

ْ ‫اطي ُم ْستَقِيما ً فَاتَّبِعُوهُ َوالَ تَتَّبِع‬ ‫ق بِ ُك ْم عَن َسبِيلِ ِه‬ َ ‫ُوا ال ُّسبُ َل فَتَفَ َّر‬ ِ ‫ص َر‬ ِ ‫َوأَ َّن هَـ َذا‬ َ‫َذلِ ُك ْم َوصَّا ُكم بِ ِه لَ َعلَّ ُك ْم تَتَّقُون‬ “Na kwa hakika hii ndiyo njia Yangu iliyonyooka, basi ifuateni, na wala musifuate njia nyingine, zikakutengeni na njia Yake. Haya amekuusieni ili mpate kumcha Mwenyezi Mungu.” (Qur’ani, 6: 153).

Tunamuomba Mwenyezi Mungu atuthibitishe katika kuyafuata mafunzo sahihi ya Dini yetu, na atuepushe na kila uzushi.

128

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 128

1/17/2017 12:44:45 PM


‫‪SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH‬‬

‫‪FATWA YA IBN TAYMIYA YA‬‬ ‫‪­KUSUJUDU JUU YA ARDHI‬‬ ‫وسئل عمن يبسط سجادة فى الجامع ويصلى عليها هل ما فعله بدعة أم ال؟‬ ‫‪:‬باجأف‬

‫“الحمد هلل رب العالمين أما الصالة على السجادة بحيث يتحرى المصلى ذلك‬ ‫فلم تكن هذه سنة السلف من المهاجرين واألنصار ومن بعدهم من التابعين‬ ‫لهم بإحسان على عهد رسول هللا بل كانوا يصلون فى مسجده على األرض‬ ‫ال يتخذ أحدهم سجادة يختص بالصالة عليها وقد روى ان عبدالرحمن بن‬ ‫مهدى لما قدم المدينة بسط سجادة فأمر مالك بحبسه‪ .‬فقيل‪ :‬له إنه عبدالرحمن‬ ‫بن مهدى‪ .‬فقال‪ :‬أما علمت أن بسط السجادة فى مسجدنا بدعة‬ ‫وفى الصحيح (البخاري ومسلم) عن أبى سعيد الخدرى فى حديث إعتكاف‬ ‫النبى صلى هللا عليه وسلم قال إعتكفنا مع رسول هللا صلى هللا عليه وسلم‬ ‫فذكر الحديث وفيه قال من اعتكف فليرجع إلى معتكفه فإنى رأيت هذه الليلة‬ ‫ورأيتنى أسجد فى ماء وطين وفى آخره فلقد رأيت يعنى صبيحة إحدى‬ ‫وعشرين على كالهما وأرنبته أثر الماء والطين فهذا بين أن سجوده كان‬ ‫على الطين وكان مسجده مسقوفا بجريد النخل ينزل منه المطر فكان مسجده‬ ‫من جنس األرض‬ ‫وربما وضعوا فيه الحصى كما فى سنن أبى داود عن عبدهللا بن الحارث‬ ‫قال سألت إبن عمر رضى هللا عنهما عن الحصى الذى كان فى المسجد فقال‬ ‫‪129‬‬

‫‪1/17/2017 12:44:45 PM‬‬

‫‪15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 129‬‬


‫‪SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH‬‬

‫مطرنا ذات ليلة فأصبحت األرض مبتلة فجعل الرجل ياتى بالحصى فى‬ ‫ثوبه فيبسطه تحته فلما قضى رسول هللا الصالة قال ما احسن هذا‬ ‫وفى سنن أبى داود أيضا عن أبى بدر شجاع بن الوليد عن شريك عن أبى‬ ‫حصين عن أبى صالح عن أبى هريرة قال أبو قد رفعه إلى النبى قال إن‬ ‫الحصاة تناشد الذى يخرجها من المسجد ولهذا فى السنن والمسند عن أبى ذر‬ ‫قال‪ :‬قال رسول هللا‪ :‬إذا قام أحدكم إلى الصالة فال يمسح الحصى فإن الرحمة‬ ‫تواجهه وفى لفظ فى مسند أحمد قال سألت النبى صلى هللا عليه وسلم عن‬ ‫كل شىء حتى سألته عن مسحالحصى فقال واحدة أودع وفى المسند ايضا‬ ‫عن جابر قال قال رسول هللا صلى هللا عليه وسلم ألن يمسك أحدكم يده عن‬ ‫الحصى خير له من مائة ناقة كلها سود الحدق فإن غلب أحدكم الشيطان‬ ‫فليمسح واحدة وهذا كما فى الصحيحين عن معيقيب أن النبى قال فى الرجل‬ ‫يسوى التراب حيث يسجد قال إن كنت فاعال فواحدة‬ ‫فهذا بين أنهم كانوا يسجدون على التراب والحصى فكان أحدهم يسوى بيده‬ ‫موضع سجوده فكره لهم النبى صلى هللا عليه وسلم ذلك العبث ورخص فى‬ ‫المرة الواحدة للحاجة وإن تركها كان أحسن‪ .‬وعن يروي بن مالك رضى هللا‬ ‫عنه قال كنا نصلى مع رسول هللا فى شدة الحر فإذا لم يستطع أحدنا ان يمكن‬ ‫جبهته من األرض بسط ثوبه فسجد عليه أخرجه صاحب الصحاح كالبخارى‬ ‫ومسلم وأهل السنن وغيرهم وفى هذا الحديث بيان أن أحدهم إنما كان يتقى‬ ‫شدة الحر بأن يبسط ثوبه المتصل كإزاره وردائه وقميصه فيسجد عليه‬ ‫”‪...‬لئاح ىلع الو لب تاداجس ىلع نولصي اونوكي مل مهنأ نيب اذهو‬

‫‪130‬‬

‫‪1/17/2017 12:44:45 PM‬‬

‫‪15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 130‬‬


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

Orodha Ya Vitabu Vilivyo ­Chapishwa Na Al-Itrah Foundation 1. i) Qur’ani Tukufu – Pamoja na Tarjuma ya Kiswahili ii) Qur’an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thelathini 2. Uharamisho wa Riba 3. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza 4. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili 5. Hekaya za Bahlul 6. Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) 7. Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (a.s.) 8. Hijab vazi Bora 9. Ukweli wa Shia Ithnaashari 10. Madhambi Makuu 11. Mbingu imenikirimu 12. Abdallah Ibn Saba 13. Khadijatul Kubra 14. Utumwa 15. Umakini katika Swala 16. Misingi ya Maarifa 17. Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia 18. Bilal wa Afrika 19. Abudhar 20. Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu 21. Salman Farsi 22. Ammar Yasir 23. Qur’an na Hadithi 24. Elimu ya Nafsi 25. Yajue Madhehebu ya Shia

131

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 131

1/17/2017 12:44:45 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

26. Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur’an Tukufu 27. Al-Wahda 28. Ponyo kutoka katika Qur’an 29. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii 30. Mashukio ya Akhera 31. Al Amali 32. Dua kwa Mujibu wa Ahlulbayt (a.s) 33. Udhuu kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna 34. Haki za wanawake katika Uislamu 35. Mwenyezi Mungu na sifa zake 36. Kumswalia Mtume (s) 37. Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) 38. Adhana 39. Upendo katika Ukristo na Uislamu 40. Qur’ani na Kuhifadhiwa Kwake 41. Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu 42. Kupaka juu ya khofu 43. Kukusanya Sala Mbili 44. Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara 45. Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya 46. Kusujudu juu ya udongo 47. Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) 48. Tarawehe 49. Malumbano baina ya Sunni na Shia 50. Kupunguza Swala safarini 51. Kufungua safarini 52. Umaasumu wa Manabii 53. Qur’an Yatoa Changamoto 54. as-Salaatu Khayrun Mina -’n Nawm 55. Uadilifu wa Masahaba 56. Dua e Kumayl 132

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 132

1/17/2017 12:44:45 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

57. Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu 58. Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake 59. Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata 60. Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mtume Muhammad (s) 61. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza 62. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili 63. Kuzuru Makaburi 64. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza 65. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili 66. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu 67. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne 68. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano 69. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita 70. Tujifunze Misingi Ya Dini 71. Sala ni Nguzo ya Dini 72. Mikesha Ya Peshawar 73. Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu 74. Ubora wa Imam ‘Ali na Ushia ndio njia iliyonyooka 75. Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake 76. Liqaa-u-llaah 77. Muhammad (s) Mtume wa Allah 78. Amani na Jihadi Katika Uislamu 79. Uislamu Ulienea Vipi? 80. Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) 81. Dhana ya Ndoa ya Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) 82. Urejeo (al-Raj’ah) 83. Mazingira 84. Utokezo (al - Badau) 85. Hukumu ya kujenga juu ya makaburi 86. Swala ya maiti na kumlilia maiti 87. Uislamu na Uwingi wa Dini 133

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 133

1/17/2017 12:44:45 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

88. 89. 90. 91. 92. 93. 94. 95. 96. 97. 98. 99. 100. 101. 102. 103. 104. 105. 106. 107. 108. 109. 110. 111. 112. 113. 114. 115. 116. 117. 118.

Mtoto mwema Adabu za Sokoni Na Njiani Johari za hekima kwa vijana Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu Tawasali (AT- TAWASSUL) Imam Mahdi katika Usunni na Ushia Hukumu za Mgonjwa Sadaka yenye kuendelea Msahafu wa Imam Ali Maimamu wa Ahlul Bait – Ujumbe na Jihadi Idi Al-Ghadir Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu Hukumu zinazomuhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi Huduma ya Afya katika Uislamu Sunna za Nabii Muhammad (saww) Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) Shahiid Mfiadini Mwanamke Na Sharia Ujumbe -Sehemu ya Kwanza Ujumbe - Sehemu ya Pili Ujumbe - Sehemu ya Tatu Ujumbe - Sehemu ya Nne Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu Hadithi ya Thaqalain Ndoa ya Mutaa Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza Ukweli uliopotea sehemu ya Pili Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu 134

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 134

1/17/2017 12:44:45 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

119. Ukweli uliopotea sehemu ya Nne 120. Ukweli uliopotea sehemu ya Tano 121. Mkutano wa Maulamaa wa Baghdad 122. Safari ya kuifuata Nuru 123. Fatima al-Zahra 124. Myahudi wa Kimataifa 125. Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi 126. Visa vya kweli sehemu ya Kwanza 127. Visa vya kweli sehemu ya Pili 128. Elimu ya Ghaibu ya Maimamu 129. Mwanadamu na Mustakabali wake 130. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Kwanza) 131. Imam Ali (‘a) Ndugu wa Mtume Muhammad (s) (Sehemu ya Pili) 132. Khairul l’Bariyyah 133. Uislamu na mafunzo ya kimalezi 134. Vijana ni Hazina ya Uislamu 135. Adhana ni Ndoto au ni Wahyi? 136. Tabaruku 137. Saada Kamili – Kitabu cha Kiada cha Maadili 138. Vikao vya furaha 139. Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 140. Visa vya wachamungu 141. Falsafa ya Dini 142. Kuhuzunika na Kuomboleza 143. Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah 144. Mjadala wa Kiitikadi 145. Kuonekana kwa Allah 146. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) 147. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) 148. Ndugu na Jirani 149. Ushia ndani ya Usunni 135

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 135

1/17/2017 12:44:45 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

150. 151. 152. 153. 154. 155. 156. 157. 158. 159. 160. 161. 162. 163. 164. 165. 166. 167. 168. 169. 170. 171. 172. 173. 174. 175. 176. 177. 178. 179. 180.

Maswali na Majibu Mafunzo ya hukmu za ibada Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 1 Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 2 Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni No 3 Abu Huraira Vipengee kadhaa katika Swala ya Jamaa na Msikiti. Mazingatio kutoka katika Qur’an - Sehemu ya Kwanza Mazingatio kutoka kaitka Qur’an - Sehemu ya Pili Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya kwanza Mazingatio kutoka katika Uislamu - Sehemu ya Pili Shia na Qur’ani – Majibu na Maelezo Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein (a.s) Amali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Elimu ya Tiba za Kiislamu - Matibabu ya Maimamu Uislamu Safi Majlisi za Imam Husein Majumbani Je, Kufunga Mikono Uislam wa Shia Amali za Makka Amali za Madina Asili ya Madhehebu katika Uislamu Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi Ukweli uliofichika katika neno la Allah Uislamu na Mifumo ya Uchumi Umoja wa Kiislamu na Furaha Mas’ala ya Kifiqhi Jifunze kusoma Qur’ani as-Sahifatul Kamilah as-Sajjadiyyah Hayya ‘Alaa Khayri’l-’Amal Katika Adhana Ukweli kuhusu Funga ya Siku ya Ashura 136

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 136

1/17/2017 12:44:45 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

181. Dua za Miezi Mitatu Mitukufu (Rajabu, Shaabani na Ramadhani) 182. Uadilifu katika Uislamu 183. Mahdi katika Sunna 184. Maswali Ya Uchunguzi Kuhusu Uislam 185. Kazi na Bidii ni njia ya maendeleo 186. Abu Talib – Jabali Imara la Imani 187. Ujenzi na Utakaso wa Nafsi 188. Vijana na Matarajio ya Baadaye 189. Historia maana na lengo la Usalafi 190. Ushia – Hoja na Majibu 191. Mateso ya Dhuria wa Mtume (saww) 192. Maombolezo – Msiba wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) 193. Shahidi kwa Ajili ya Ubinadamu 194. Takwa 195. Upotoshaji Dhahiri katika (Turathi) Hazina ya Kiislamu 196. Amirul Muuminina (as) na Makhalifa 197. Tawheed Na Shirki 198. Kuvunja hoja iliyotumika kutetea Uimamu wa AbuBakr 199. Adabu za vikao na mazungumzo 200. Hija ya Kuaga 201. Uwazi baina ya Maslahi na Vikwazo 202. Fadhila za watukufu watano katika Sahih Sita 203. Mdahalo baina ya Mwanachuoni waKisunni na Kishia (Al- Muraja’aat) 204. Utawala na Uendeshaji katika Sera ya Imam Ali (as) 205. Imam Husain ni Mfumo wa Marekebisho na Mageuzi 206. Mtazamo kuhusu msuguano wa Kimadhehebu 207. Nchi na Uraia – Haki na wajibu kwa Taifa 208. Mtazamo wa Ibn Taymiyyah juu ya Imam Ali (as) 209. Uongozi wa Kidini – Maelekezo na Utekelezaji wa Kijamii 210. Maadili ya Ashura 211. Mshumaa – Shahidi na Kifo cha Kishahidi 137

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 137

1/17/2017 12:44:45 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

212. Mizani ya Hekima – Hadithi za Ahlul Bait (as) – Sehemu ya Kwanza 213. Imam Ali na Mambo ya Umma 214. Imam Ali na Mfumo wa Usawa 215. Uimamu na Tamko la Kutawazwa 216. Mfumo wa Wilaya 217. Vipi Tutaishinda Hofu? 218. Kumswalia Mtume ni Ufunguo wa Utatuzi wa Matatizo 219. Maeneo ya Umma na Mali Zake 220. Nahju ‘L-Balagha– Majmua ya Khutba, Amri, Barua, Risala, Mawaidha na Semi za Amirul-Muuminin Ali bin Abu Talib (a.s.) 221. Mukhtar – Shujaa aliyelipiza kisasi dhidi ya wauaji wa Imam Husein (as) hapo Karbala 222. Mazingatio Katika Swala 223. Imam Hasan na Mfumo wa Kujenga Jamii 224. Vyakula Na Vinywaji 225. Kuelewa Rehema ya Mwenyezi Mungu 226. Imam Mahdi na Bishara ya Matumaini 227. Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu 228. Shia Na Sahaba - Majibu na Maelezo 229. Majanga Na Jukumu la Jamii 230. Shia Na Hadith - Majibu na Maelezo 231. Upotofu Ndani ya Kitabu cha Mitaala kwa Shule za Sekondari 232. Ugaidi Wa Kifikra Katika Medani Ya Kidini 233. Yafaayo kijamii 234. Uswalihina Dhahiri Na Batini Yake 235. Mkakati wa Kupambana na Ufakiri 236. Mwanamke Katika Harakati Za Mageuzi 237. Jihadi 238. Hija Katika Maneno Na Ujumbe Wa Imam Khomeini (R.A) 239. Tiba Ya Maradhi Ya Kimaadili 240. Yusuf Mkweli

138

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 138

1/17/2017 12:44:45 PM


SUNNAH KATIKA KITABU CHA: FIQHU AL-SUNNAH

241. Taqiyya Kwa Mujibu Wa Sheria Ya KIISLAMU 242. Imam Mahdi (A.S) Imam Wa Zama Hizi Na Kiongozi Wa Dunia 243. Talaka Tatu 244. Safari Ya Kuelekea Kwa Mwenyezi Mungu 245. Hotuba Za Kiislamu Juu Ya Haki Za Binadamu 246. Mashairi Ya Kijamii 247. Ngano Ya Kwamba Qur’ani Imebadilishwa 248. Wito Kwa Waumini: “Enyi Mlioamini” 249. Imam Husain (a.s) ni Utu na Kadhia 250. Imam Husain ni Kielelezo cha Kujitoa Muhanga na Fidia 251. Imam Mahdi ni Tumaini la Mataifa 252. Kuchagua Mchumba 253. Mazungumzo ya Umoja – Ukosoaji na Usahihishaji 254. Utamaduni wa Mwamko wa Kijamii 255. Hekima za kina za Swala 256. Kanuni za Sharia za Kiislamu 257. Utamaduni kufuatana na Qur’ani na Utekelezaji wa Kivitendo (Sehemu ya Kwanza) 258. Kauli sahihi zaidi katika kufafanua Hadithi

139

15_16_Sunna Katika Fiqhu_17_January_2017.indd 139

1/17/2017 12:44:45 PM


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.